Search This Blog

Tuesday 20 December 2022

TUKIO LA UJAMBAZI LILILOFANIKIWA ZAIDI, KUSISIMUA NA KUUSHANGAZA ULIMWENGU - 1

 


http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/tukio-la-ujambazi-lililofanikiwa-zaidi_10.html

IMEANDIKWA NA THE BOLD

************************************************************************

Simulizi : Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi,  Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu 

Sehemu Ya Kwanza (1)



Mwaka 2003 lilitokea tukio kubwa zaidi la ujambazi ambalo labda ndio lililotumia akili na maarifa zaidi pengine kushinda tukio lolote la ujambazi kwa miaka 50 iliyopita.. Tukio hili lilishuhudia wahusika wakitokomea na vitu vyenye thamani ya zaidi ya Bilioni 200 (100 mln USD)!

Uthubutu, ubunifu, akili na maarifa yaliyotumika kutekeleza tukio hili limefanya mpaka kampuni ya utengenezaji filamu ya Paramount Pictures kununua haki za hadithi ya tukio hili ili watengeneze filamu itakayo husu mkasa mzima wa tukio hili..


TUKIO LENYEWE


Mwanzoni mwa mwaka 2000 mfanyabiashara wa madini (almasi) Leonardo Natarbartolo alifungua ofisi mjini Antwerp nchini ubelgiji, mji ambao ndio kituo cha biashara ya madini ya almasi ulimwenguni.. Ofisi yake ilikuwa katikati kabisa ya kitovu cha mitaa ambayo ndio hasa biashara ya almasi hufanyika. Natarbartolo alijihusisha hasa katika manunuzi ya kiwangi cha kawaida cha almasi (small deals) lakini jambo ambalo watu hawakulifahamu ni kwamba walikuwa wamemkaribisha moja kati ya manguli wa wizi wa almasi ulimwenguni!

Kutokana na kujitambulisha kama mfanya biashara mwenzao, Natarbartolo alipata fursa ya kuingia katika Kuba (vault) za wafanyabiashara wengine ili aweze kukagua mali kabla ya kuinunua na aliutumia fursa hii kuyasoma mazingira ya Ofisi hizo zilizo hifadhi madini na kuja kufanya uhalifu kesho yake..

Natarbatolo aliishi hivi mjini Antwerp kwa miezi kadhaa kabla hajakutana na mfanyabiashara ya almasi Myahudi ambaye kukutana kwao kulipelekea kufanikisha tukio ambalo liliushangaza ulimwengu na limeendelea kuushangaza ulimwengu mpaka leo hii..




MAANDALIZI


Mwaka mmoja baada ya Natarbatolo kuingia Antwerp, siku hiyo akiwa kwenye mgahawa akinywa kahawa alifuatwa na Mfanyabiashara wa Kiyahudi ambaye alimuomba wazungumze faragha kuhusu biashara muhimu. Baada ya kukaa nae chemba Myahudi akamueleza amza yake kuwa anataka amshirikishe katika tukio la ujambazi na alimuuliza kama anahisi Vault ya Antwerp Diamond Center inaweza kuibiwa... Natarbartolo akamjibu kwa kifupi kuwa atamjibu swali hilo kama yuko tayari kumlipa dola laki moja! Na Myahudi huyo akakubali


Siku mbili baadae Natarbatolo alielekea ilipo Main Vault ya Antwerp Diamond Center (kumbuka kutokana na yeye kujitanabaisha kama mfanyabiashara ya almasi kwa mwaka mmoja aliokaa Antwerp hivyo alifanikiwa kujisajili ili aweze kuhifadhi almasi zake katika Main Vault ya Antwerp)..

Kitu ambacho watu wote wakiwepo walinzi hawakikugundua ni kwamba katika mfuko wa pembeni wa suti yake aliweka peni ambayo inaonekana kama peni ya kawaida lakini ilikuwa ni peni maalumu iliyokuwa na kamera ndogo ya siri.. Kamera hii ilimsaidia Notarbartolo kurekodi mandhali yote ya ndani ya vault na jinsi ulinzi ulivyo...



    0 comments:

    Post a Comment

    Blog