Simulizi : Plata O Plomo Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja [ Pablo Escobar]
Sehemu Ya Tano (5)
Moja ya mali muhimu za Pablo ilikuwa ni 'pepo' yake ya Hancienda Nápoles (rejea kwenye makala) Familia yake iliwahi kufungua kesi mahakama kuu ya Colombia kuzuia serikalini isichukue makazi hayo kwani si kitega uchumi bali ni makazi wanayoishi kama familia. Kesi hii iliunguruma kwa miaka mingi lakini hatimae mwaka 2006 mahakama ikawaruhusu serikali kuchukua Hacienda Nápoles.
Aina ya pili: wafanyabiashara wengi wa mihadarati (hasa America ya kusini) wana kitu kinaitwa Guacas/Caletas. Hizi huwa ni nyumba za siri zilizoko milimani ambako malundo ya fedha tasilimu huwa yanatunzwa. Yani unaweza ukaingia kwenye nyumba ukaikuta imejaa pesa tasilimu.
Pablo pia alikuwa na hizi Caletas. Na inasemekana kuwa kipindi yuko hai alikuwa anatupa au kuchoma moto kila mwaka karibia dola bilioni mbili (zaidi ya trilioni nne fedha ya kitanzania) kutokana na kuliwa na panya au kuharibika (kuoza kwa mfano) katika Caletas hizi za kuhifadhi pesa pasilimu.
Kutokana na mtoto wake wa kiume Juan kutoshiriki kwenye biashara za haramu za baba yake Caletas zote za Pablo zilikuwa zinafahamika na wapambe wake wa karibu pekee. Hivyo baada ya kifo cha Pablo wakatumia mwanya huo kuchukua fedha zote kwenye Caletas kama mali yao.
Aina ya tatu: fedha zinazo takatishwa
Mabilioni mengi ya Pablo yalikuwa yanainginzwa katika mamia ya akauti za siri kwenye nchi maarufu zinazojulikana kwa utakatishaji fedha ambazo huitwa 'tax havens' (mfano Uswisi, Canyon Islands, Mauritius n.k).
Marekani imeingia mkataba maalumu na Colombia ambapo kuna kikosi kazi maalumu cha kupeleleza na kuzigundua hizi akaunti za siri za Pablo na huwa zikigundulika fedha inatolewa na inagawanywa kwa serikali ya Colombia na Marekani.
----------------------------------------
UZALISHAJU WA COCAINE
Mkuu Mlatinoh king,
Nijibu swali lako kwa juu juu pasipo kuingia ndani sana kuepusha kufundishana uharamia..
Tahadhali: reader's discretion is advised
Cocaine inatengenezwa kutoka katika majani ya mmea wa Coca ambao unalimwa sana huko Amerika ya kusini. Kama umewahi kuona mti wa mkahawa basi unafanana kimuonekana kwa asilimia kubwa na mmea huu wa Coca.
Baada ya majani kuchumwa kutoka katika mmea wa Coca yanapelekwa maabara na kisha yanakatwa vipande vidogo vidogo sana na kunyunyuziwa chumvi ya carbonate na kiasi kidogo cha maji. Baada ya hapo mchanganyiko huu unaongezewa mafuta ya taa au dizeli.
Kisha baada ya hapo mchanganyiko huu (majani ya coca, chumvi ya carbonate na dizeli/mafuta ya taa) unakorogwa kwa siku tatu mfululizo. Watengenezaji wengi wanatumia mashine ya kufulia au mashine ya kuchanganya zege kukoroga huu mchanganyiko kwa siku tatu mfululizo pasipo kuacha.
Hii inasaidia kutenganisha Cocaine yenyewe kitoka katika majani ya Coca. (Kwa waliopitia masomo ya kemia nadhani wanakumbuka kuhusu Solvent extraction, na hicho ndicho kinachofanyika hapo)
Baada ya hatua hiyo kimiminika kinachopatikana kinachemshwa ili kuondoa nta inayotoka kwenye majani ya Coca. Watu watabora nadhani watanielewa zaidi hapa maana inakuwa ni kama vile unapochemsha asali mbichi kuondoa nta na takataka nyingine.
Baada ya mchanganyiko kuchemshwa kuondoa nta inachujwa na kisha kuchanganywa na Sulphuric acid ili kubadili vimelea/vinasaba huru vya Cocaine (Cocaine free base) vilivyopo kwenye mchanganyiko na kuvifanya kuwa Cocaine sulphate.
Baada ya hapo mchanganyiko huu unaachwa utulie na baada ya muda Cocaine sulphate inatuama chini.
Kisha Cocaine sulphate iliyotuama chini inaondolewa na kuchanganywa na chokaa pamoja na unga wa soda. Hii inafanyika ili kufifisha sulphuric acid iliyowekwa mwanzoni.
Baada ya hatua hii kufanyika kinapatikana kitu kigumu lakini kilaini laini kama bazoka chenye rangi ya njano. Hiki kinakaushwa na kusindikwa tayari kusafirishwa kwa wauzaji wa jumla. Hii ndio Cocaine unayoionaga kwenye runinga maarufu kama 'Pipi' ambazo watu tuliozoea kuwaita 'punda' huwa wamekamatwa nayo kwenye viwanja vya ndege wakiwa wamezimeza.
Baada ya 'Pipi' kumfikia muuzaji wa jumla inambidi aibadilishe iwe katika hali inayoweza kutumiwa na 'mlaji'.
Hapa wanaichanganya na tindikalii hafifu (diluted sulphuric acid) na kuongezea potassium permanganate. Kemikali hii ina uwezo mkubwa wa kuunguza (oxdizing) ambapo inaunguza taka taka ndogo ndogo zote zilizopo kwenye 'pipi' na kuibadilisha kutoka rangi ya njano kuuu kuu (yellow-brown) na kuwa kitu kisicho na rangi kabisa au weupe kwa mbali.
Baada ya hapo inachujwa tena na kuchanganywa na ammonia ili kufifisha acid iliyowekwa na kisha inaachwa ikauke.
Ikisha kaushwa unapatikana unga mweupe, wenye ladha chungu, wenye kuyeyuka ukiwekwa maji.
Hii ndio bidhaa inayouzwa mtaani na kuharibu vijana, watu wanaiita ngada, poda, unga na majina lukuki lakini kiuhalisia yenyewe katika hali hii inaitwa Cocaine Hydrochloride.
---------------------------------------
PABLO NA AFFAIRS..
Mkuu ngaboru,
Pablo alikuwa na michepuko mingi kiasi kwamba hata inashangaza ni kwanini mkewe Maria Gavaria aliendelea kuishi nae. Ni kwasababu alimpenda kwa dhati na alikuwa tayari kumvumilia udhaifu wake??? Au Maria alikubaliana na yote ili aendelee kuishi maisha ya anasa na utajiri??? Labda..
Hata kipindi ambacho Pablo alikuwa gerezani La Catedral, bado kulikuwa na 'oda' maalumu ya kumpelekea wanawake wa kumburudisha.. Kwa kifupi Pablo alikuwa 'mzee wa totoz'..
Lakini mchepuko wake wa muhimu zaidi alikuwa ni Virginia Vallejo. Huyu ndiye ambaye Nifah umemuongelea hapo juu..
Mwanamama huyu licha ya kuwa mchepuko lakini alimpenda kwa dhati Pablo. Huyu ndiye aliyesema msemo ambao nimeunukuu pale mwishoni mwa makala, "Amando a Pablo, Odiando a Escobar" (Nampenda Pablo, Namchukia Escobar).
Mapenzi yao yalikuwa moto moto kiasi kwamba Virginia alikuwa ni moja ya wa wasiri walioaminika na Pablo.
Kuna kisa kinasema kuwa Virginia aliwahi kunasa mimba kwa makusudi ili amzalie mtoto Pablo kutokana na kumpenda sana. Hicho kisa kinaeleza kuwa Pablo kutokana na kumpenda mwanae Manuella kupitiliza alishajiapiza kuwa hatozaa tena mtoto mwingine na mwanamke yeyeto yule.
Baada ya Pablo kugundua Virginia ana mimba akmwambia atoe lakini Virginia akakataa. Pablo akatuma walinzi wake wakamkamta wakaenda kumtoa kwa lazima.
Baada ya kifo cha Pablo Virginia alitumika sana na serikali ya Marekani na Colombia ili kuvujisha siri nyingi zilizohusu maisha ya Pablo hasa hasa vibaraka aliokuwa amewapandikiza serikalini.
Virginia Vallejo ndiye alikuwa shahidi Mkuu katika kesi ambayo Seneta Alberto Santofimio alishtakiwa akituhumiwa kutumiwa na kushirikiana na Pablo Escobar kumuua mgombea urais wa Colombia Carlos Gálan.
Mwaka 2006 Virginia Vallejo alitoa chapisho lake la kwamza (makala) iliyoitwa 'Polla Bianca' (White Dick) ambayo alieleza kwa ufupi mahusiano yake ya kimapenzi na Pablo. Mwaka uliofuata, yaani 2007 akatoa kitabu cha 'Amando a Pablo, Odiando a Escobar' ambapo ameelezea kwa kina uhusiano wake na Pablo, jinsi Pablo alivyowatumia viongozi na watendaji wakuu wa serikali na ugomvi wake na Cali Cartel.
--------------------------------------------
MAMA YAKE MZAZI NA TUKIO LZ ULIPUAJI NDEGE..
Mkuu lolypop,
Mama mzazi wa Pablo Escobar alifariki mwaka 2006 nchini Colombia jina lake aliitwa Hermilda de los Gaviria.
Mpaka kipindi anafariki alikuwa haivi chungu kimoja na mke na watoto wa Pablo kwasababu walikuwa wanamshutumu yeye (mama mzazi wa Pablo) pamoja na kaka yake Pablo aliyeitwa Roberto Escobar kuwa waliifanya makubaliano na kikundi cha Los Pepes ili waendelee kuishi Colombia. Mke na watoto wa Pablo wanaona kitendo hiki ni kama usaliti kwa Pablo kwani kikundi cha Los Pepes kinahusika kwa asilimia kubwa na kifo cha Pablo pamoja na zaidi ya watu 300 waliokuwa marafiki, washirika na ndugu wa Pablo Escobar.
Pia wanamshutumu kuwa alishirikiana na dada yake Pablo aliyeitwa Alba Marina kuwa baada ya kifo cha Pablo walijinufaisha kinyemela na sehemu ya fedha za zilifichwa kwenye moja ya Caletas.
Nikijibu swali lako kuhusu Pablo kulipua ndege; ni kweli Pablo aliwahi kufanya hili tukio siku ya tarehe 27 Novemba 1989 na ndege hii ilikuwa ni ya abiria ya kampuni ya Avianca Airlines (Flight 203) ambapo siku hii ya tukio ilikuwa inaruka kutoka mji wa Bogota kuelekea mji wa Cali.
Sababu kubwa ya Pablo kuilipua ni kwamba alipewa taarifa kuwa ndege hiyo imembeba mgombea urais aliyeitwa César Gaviria Trujjilo ambaye alikuwa na mafungamano na mahasimu wake wa Cali Cartel. Kwa bahati mbaya taarifa hii haikuwa ya kweli kwani César hakuwepo katika ndege hiyo.
Abiria wote 107 walikuwepo kwenye ndege pamoja na marubani na wahudumu walipoteza maisha katika ajali hii pamoja na watu watatu waliokuwa ardhini ambao waliangukiwa na mabaki ya mlipuko huo.
Hili lilikuwa ni moja kati ya matukio ambayo yalichochea zaidi hasira za Marekani dhidi ya Pablo kwani katika ndege hiyo pia walikuwepo Wamarekani watatu.
Miezi michache baadae muuji mkuu (chief assassin) wa Medellín Cartel aliyeitwa Dandeny Muñoz Mosquera alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kumi likiwemo la ulipuaji wa ndege hii. Muñoz alikutwa na hatia katika mashtaka yote na akahukumiwa kifungo cha maisha jela.
Join my exclusive whatsapp group kusoma makala na simulizikila siku – 0718 096 811 (kuna “subscription fee")
The Bold.
0 comments:
Post a Comment