IMEANDIKWA NA : HALFANI SUDY
*********************************************************************************
Simulizi : Red Butterfly
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ulikuwa ni usiku wa saa nane kamili. Usiku tulivu huku kelele za miti na ndege ndizo zikizosikika nje ya nyumba aliyolala mpelelezi Daniel Mwaseba maeneo ya Masaki.
Mara simu maalum ya Daniel Mwaseba ilianza kuita kwa nguvu, mlio wake maalum alioutega kwa sababu maalum. Mlio ambao haukuwa ule wa mtu kupiga. Sekunde hiyohiyo harakaharaka Daniel aliamka toka usingizini na kuitoa simu yake iliyokuwa chini ya mto. Simu ilikuwa inaita kwa nguvu na kuwaka taa nyekundu na kuzimika karibu na sehemu ilipo spika, inawaka na kuzimika.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ina maana ameua tena?" Daniel Mwaseba alisema huku akiangalia saa katika simu yake. Simu maalum ya Daniel ilikuwa imeunganishwa moja kwa moja na geti lake. Ilikuwa mtu yoyote akigusa geti lazima taarifa zipelekwe katika simu yake. Na alitega hivyo baada ya visa vya Red butterfly.
Harakaharaka Daniel aliinuka kitandani. Alitoka na kwenda katika chumba chake maalum. Alikuta kompyuta zake zote nne zikiwa zinawaka. Kompyuta moja iliyokuwa karibu na dirisha ndiyo iliyokuwa inaonesha picha za geti la nyumba yake. Daniel aliisogelea ile kompyuta na kuanza kuiangalia kwa umakini.
Kompyuta ilionesha nje ya geti kulikuwa na mwanamke mmoja mtu nzima akiwa na mkongojo. Mwanamke alikuwa anatumia mkongojo wake kugonga geti la Daniel Mwaseba kidogokidogo. Daniel alimwangalia kwa makini yule mwanamke mtu mzima.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Red Butterfly umenifata tena nyumbani kwangu kama kawaida yako? Inamaana umeua tena?Safari hii nitakuonesha mimi ni nani?" Daniel alisema huku akichukua bastola iliyokuwa juu ya meza na kutoka nje harakaharaka.
"Red Butterfly ama zangu ama zako" Daniel aliwaza akiwa katika uwanja mpana sasa wa uwa wake, alikuwa anakimbilia nje kwa tahadhari kubwa sana. Bastola yake ikiwa mkononi, kidole chake cha shahada kikiwa katika triga tayari kumlipua Red Butterfly au yeyote yule atakayejipendekeza mbele yake. Daniel alipania kumaliza michezo ya kijinga anayoicheza Red butterfly kila anapofanya mauaji.
Alipolikaribia geti alipunguza mwendo. Sasa alikuwa anakwenda kwa tahadhari kubwa zaidi ili kumstukiza Red Butterfly. Kwa mkono wa kushoto alikuwa anafungua geti taratibu huku mkono wake wa kulia akiwa kaishika imara bastola fupi nyeusi huku kidole cha shahada kikiwa palepale kwenye triga. Taratibu geti lilifunguka. Daniel aliruka samasoti huku bastola yake akiielekeza pale alipokuwa Red Butterfly. Daniel alibaki mdomo wazi, hakukuwa na Red Butterfly. Alikuwa kalionesha bastola geti lake. Red Butterfly alikuwa ameruka tena kama kawaida yake.
"Kwa mara nyingine tena nimemkosa Red butterfly. Bila shaka na leo nitasikia taarifa za mtu kuuwawa na kubandikwa stika ya kipepeo mwekundu katika paji lake la uso ama tumboni. Huyu kibibi kizee mwenye mkongojo ni nani haswa? kila anapokuja kugonga hapa lazima auwe mtu na kumbandika stika ya kipepeo mwekundu" Daniel alijiuliza huku akiangaza huku na kule kwa kasi na umakini. Ilikuwa vilevile alibaki peke yake na bastola yake mkononi.
Red Butterfly hakuwepo.
Daniel alirudi sebuleni kwake. Alikaa juu ya sofa huku akiwa na mawazo lukuki.
"Huyu mwanamke ambaye nimepachika jina la Red Butterfly kutokana na kuja kugonga geti langu kisha yanatokea mauaji ya mtu aliyebandikwa stika ya kipepeo mwekundu usoni kwake ama tumboni ananiumiza sana kichwa changu. Hii ni mara ya sita anakuja kugonga katika geti langu na nikienda tu getini anayeyuka. Nini lengo la kuja kunigongea geti baada tu ya kufanya mauaji yake ya kinyama. Nusu saa mfululizo Daniel aliwaza na kuwazua. Afanye nini ili kumdhibiti mwanamke yule mwenye umbo la kizee. Anaua, anakuja kugonga kwangu na kuyeyuka. She is a red butterfly, tutaonana laki..."
Wakati Daniel akiwa katikati ya mawazo alisikia mlio wa simu yake ikiita. Alinyanyuka pale katika sofa na kuelekea chumbani kwake. Alijua tu ni nani aliyekuwa anampigia, pia alijua kwa vyovyote vile Red butterfly tayari kashafanya mauaji.
Aliichukua simu yake Kitandani ili kujua tu safari hii kamuua nani?. Hisia zake zilikuwa sahihi. Simu ilikuwa imepigwa na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP John Rondo. Akaipokea na kusikiliza Red butterfly itakuwa kamuua nani?
" Hallo Daniel?" IGP Rondo aliita simuni.
"Habari afande?" Daniel aliita kwa sauti ya uwoga.
"Kuna mauaji yametokea..." IGP John Rondo alisema.
"Nani kauwawa?" Daniel alimkatisha IGP John Rondo kwa swali.
"Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Elisha Ngwena ameuwawa usiku wa saa saba. Amepigwa risasi ya tumbo na mtu asiyejulikana. Nakuomba uende sasahivi kujua nini chanzo cha kifo chake. Ukitoka hapo njoo moja kwa moja ofisini kwangu nitakuwa na kikao na wewe" IGP John Rondo alisema.
"Sawa mkuu. Nitakuwa nyumbani kwa waziri wa mambo ya ndani muda mfupi tu na nikimaliza mahojiano yangu nitakuwa ofisini kwako" Daniel alisema.
Simu ilikatwa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Elisha Ngwena ameuwawa usiku wa saa saba. Amepigwa risasi ya tumbo na mtu asiyejulikana. Nakuomba uende sasahivi kujua nini chanzo cha kifo chake. Ukitoka hapo njoo moja kwa moja ofisini kwangu nitakuwa na kikao na wewe" IGP John Rondo alisema.
"Sawa mkuu. Nitakuwa nyumbani kwa waziri wa mambo ya ndani muda mfupi tu na nikimaliza mahojiano yangu nitakuwa ofisini kwako" Daniel alisema.
Simu ilikatwa
Daniel alikaa kitandani. Alishika tama, mawazo yalikuwa kwa yule mwanamke bibi kizee, Red Butterfly.
"Red Butterfly kaweza kumuua Mheshimiwa Elisha Ngwena. Kapitaje getini kwa Mheshimiwa waziri kwenye ulinzi mkali na kwenda kumuua? Ngoja niende nikapate majibu" Daniel alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga. Alipomaliza kuoga alivaa nguo. Akachukua bastola na zana zake za kazi. Alielekea Mikocheni nyumbani kwa Mheshimiwa Elisha Ngwena, ambaye sasa alikuwa ni marehemu.
Alitoka nje, aliingia katika gari lake na kuelekea Mikocheni.
"Red Butterfly, iwe isiwe lazima anahusika na kifo cha waziri wa mambo ya ndani. Haya yatakuwa mauaji yake ya mwisho, nitahakikisha haui tena" Daniel alikuwa anawaza akiwa ndani ya gari yake.
Daniel Mwaseba alifika Mikocheni saa moja kasoro dakika ishirini na tano asubuhi. Alikuta ummati wa watu umejaa. Viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo, wabunge na mawaziri na viongozi kadhaa wa dini. Daniel alipaki gari yake 'parking' ambapo kulikuwa kumejaa magari mengi sana. Alishuka na kuelekea sehemu ambapo kulikuwa na waombelezaji wengi, wengine walikuwa wakilia na wengine wakiwa katika majonzi makuu.
"Red Butterfly rafiki yangu bila shaka popote ulipo umefurahi sana. Najua furaha yako ni kuwaona watu wakiwa katika majonzi namna hii. Lakini, sasa zamu yako ya kulia wewe imefika" Daniel Mwaseba alikuwa anawaza wakati akielekea kwa wale waombolezaji. Aliwasalimia mmojammoja kwa kuwapa mkono. Alikuwa akitoa pole. Kisha akaingia ndani.
Sebuleni alikutana na watu kumi, miongoni mwao kulikuwa na mjane wa marehemu na ndugu zake wengine. Mke wa marehemu alikuwa ni msichana mdogo sana kiumri. Daniel alijitambulisha na kuomba nafasi ya kuongea faragha na mjane wa marehemu. Watu wengine waliokuwa pale sebuleni walitoka nje huku wakilia kwa maumivu makali sana. Hali iliyosababisha mjane wa marehemu nae kuwapokea kwa kilio. Daniel alipata kazi ya kumbembeleza mjane wa marehemu, kazi iliyodumu kwa dakika tano.
"Naitwa Daniel Mwaseba. Ni mpelelezi wa siri wa kifo cha marehemu Mme wako. Watakuja pia Polisi kukuhoji, wape pia ushirikiano nao watafanya upelelezi wao, lakini mimi ni mpelelezi maalum kutoka ikulu" Daniel alisema.
Mjane wa marehemu aliitikia kwa kichwa huku akifuta mafua kwa kanga.
"Kwanza pole sana kwa msiba, la msingi naomba unijibu maswali yangu ili yatusaidie kumjua muuaji wa mume wako ni nani?" Daniel Mwaseba alisema.
"Sawa kaka" Daniel kwa mara ya kwanza aliisikia sauti ya mjane wa marehemu.
"Unaitwa nani?" Daniel aliuliza.
"Naitwa Ilham Mshana. Mke wa marehemu Elisha Ngwena aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani"
"Mliooana lini na marehemu, na mna watoto wangapi?" Daniel aliuliza tena.
"Tuna mwaka mmoja katika ndoa, bado hatujajaaliwa kupata watoto" Ilham alijibu.
"Pole sana kwa msiba wa mumeo Ilham. Najua jinsi inavyoumiza pale unapoondokewa na mtu wa karibu. Nishawahi kupitia mazingira kama haya" Daniel alimpa pole mjane wa marehemu.
"Ahsante sana kaka. Ingawa naumia sana na hiki kifo cha mume wangu. Yeye ndio alikuwa tegemeo letu katika kila kitu. Lakini leo kazimika kama mshumaaa" Ilham akaanza kulia tena.
"Yalikuwaje mazingira ya kifo chake?" Daniel aliuliza bila kujali kama Ilham alikuwa analia.
Ilham alijitahidi kufuta machozi huku akiongea "Hakuna anayejua muuaji aliingia vipi na saa ngapi? Hakuna anayeelewa alipita vipi kule getini ambako kuna walinzi wanne wakiolinda nyumba hii. Muuaji alipita mote huko na kuja kugonga mlango wa chumba chetu. Kwa jinsi sauti ikivyosikika bila shaka hakuwa anagonga na mkono, ulikuwa ni mti au bastola. Mume wangu aliamka na kwenda kufungua akijua labda ni ndugu zetu tunaoishi nao humu. Alikuwa anajiamini kwakuwa haikuwa rahisi kwa mtu mwengine kuweza kuingia humu ndani kwakuwa kuna walinzi kule getini. Alipofungua tu, muuaji hakusema kitu alifyatua bastola yake na kudumbukia katika tumbo la mume wanguuu, nimekuwaaaa mjanee mimi Ilhaaaaam" Baada ya maelezo ilikuwa tafrani. Ilham hakuongea tena, alilia mfululizo akimlilia marehemu mumewe. Daniel akaona pale hatapata la maana. Aliwaita ndugu wa marehemu na kuwahoji, wote walikuwa na maelezo sawa na ya Ilham.
Baadae akaenda chumbani kuuona mwili wa marehemu. Aliufunua, ilikuwa mithili ya miili saba aliyokutana nayo katika kadhia hii. Na mwili wa marehemu Elisha Ngwena ulikuwa na stika ndogo sana ya kipepeo mwekundu tumboni mwake. Daniel aliibandua ile stika na kuiweka mfukoni mwake.
Saa kumi na mbili asubuhi Daniel alitoka Mikocheni nyumbani kwa Mheshimiwa Elisha Ngwena na kuelekea makao makuu ya Polisi Posta kuitikia wito wa IGP John Rondo. Huku kichwani akiwa na mawazo lukuki kuhusu Red Butterfly.
Alipofika kwa katibu mahsusi wa IGP John Rondo moja kwa moja aliruhusiwa aingie. Daniel aliingia ofisini, alipofungua tu mlango alisita.
"Karibu Daniel..." IGP John Rondo alisema.
Daniel alisogea taratibu. Mle ndani kulikuwa na viti sita. Viti vitano vilikaliwa kasoro kimoja tu, akajua kile kimeachwa kwa ajili yake. Alienda kwenye kile kiti na kukaa.
"Karibu sana Daniel. Najua umestuka baada ya kuwakuta watu usiowategemea katika ofisi yangu. Tangu saa tisa usiku tupo hapa baada tu ya kusikia kifo cha Mheshimiwa Elisha Ngwena"
Daniel aliitikia kwa kutingisha kichwa chini juu.
"Mheshimiwa Rais, naona kijana tayari kashafika. Tunaweza kuendelea na kikao chetu" IGP John Rondo alisema.
Daniel aliwaeleza kila kitu kuhusu ile stika yenye kipepeo mwekundu kukutwa katika miili ya marehemu yote. Baada ya maongezi yaliyodumu kwa muda wa saa zima kikao kifungwa huku wakiwa wamekubaliana namna ya kumkamata Red butterfly. Kila mmoja aliondoka akiwa na matumaini tele. Kwamba ule ulikuwa mwisho wa Red butterfly...http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
Wiki ya pili sasa, nyumba ya Daniel Mwaseba ilikuwa inalindwa na wanajeshi watano toka jeshi la Wananchi wa Tanzania. Pikipiki tano zilifichwa mahali huku wanajeshi wakipewa ruhusa kuomba helicopter ya jeshi muda wowote ule watakaohitaji.
Ndani ya wiki hizo mbili Red butterfly hakufika katika nyumba ya Daniel Mwaseba, na mauaji hayakutokea pia. Hii iliwapa imani kubwa sana Red butterfly ndiye alikuwa muuaji mwenyewe. Pamoja na kutotokea kwa Red butterfly hakukuwafanya wanajeshi kusahau kazi yao. Walikuwa wanailinda kwa zamu nyumba ya Daniel usiku na mchana.
Waliilinda, na kulinda, mpaka ikaja ile siku ambayo Red butterfly alienda kugonga katika geti la nyumba ya Daniel Mwaseba.
Ilikuwa usiku wa saa sita usiku. Wanajeshi wawili walikuwa macho lindoni huku watatu wakiwa wamelala. Ilikuwa ni kawaida yao kupeana zamu muda wa kulala wakati wengine wakiendelea kulinda. Kipindi hiko Daniel Mwaseba alikuwa ndani ya nyumba yake akiwa amelala ndipo aliposikia mlio wa simu yake. Daniel alikurupuka na kuelekea nje, hakwenda kuangalia kwenye kompyuta kama alikuwa Red butterfly mwenyewe, kwa mlio aliutega katika simu alikuwa na asilimia zote kuwa Red butterfly alikuwa anagonga geti lake nje.
Kule nje mwanajeshi akiyeitwa Mosha ndiye aliyemuona Red butterfly pale getini. Alimstua mwanajeshi mwenzake kisha wakawaamsha wale wengine watatu. Wanajeshi wote watano wakawa macho na silaha zao mkononi tayari kumkamata Red butterfly. Walikumbuka maneno ya mkuu wa jeshi.
"Itakuwa vyema zaidi mkimkamata akiwa hai, ila hata mkimuua sio mbaya sana"
Wanajeshi walikuwa wanataka kufanya vyema zaidi, wamkamate Red butterfly akiwa hai.
Mosha ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa wale wanajeshi watano aliwapanga vizuri wenzake. Wakaweka vizuri 'earphone' zao kwa ajili ya mawasiliano. Mosha mwenyewe alikuwa anashambulia kutokea kati, Idd alikuwa anashambulia kutoka upande wa kulia, Haji alikuwa anashambulia kutokea kushoto. Imma na Adrian walipanda katika pikipiki zao endapo Red butterfly akikimbia tu waanze kumfukuza. Kumbuka Daniel Mwaseba nae alikuwa anakuja wakawaka akitokea kwa ndani. Red butterfly aligonga mlango kwa mara ya pili kisha akaanza kuondoka.
"Wee bibi simama hapohapoooo!!" Mosha alisema kwa ukali.
Nukta ileile Red butterfly aligeuka mithili ya mzimu na risasi moja iliingia katika bega la Mosha. Ilikuwa ni shabaha kali sana gizani, cha kushangaza risasi ilitoka katika mkongojo wa Red butterfly!!
Sekunde ileile Idd na Haji walianza kumshambulia Red butterfly. Red butterfly alilala chini huku naye akijibu mashambulio yale kwa ule mkongojo wake. Risasi yake ya pili iliingia katika paja la kulia la Haji. Yowe la nguvu lilimtoka Haji huku akianguka chini kama mzigo akiiacha silaha yake mita kadhaa mbele.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sekunde tatu baada ya kupigwa risasi Haji, Daniel Mwaseba nae alitokea kule getini.
Alikutana nayo!
Mkongojo wa Red butterfly ulifanya kazi yake, mguu wa Daniel ulikuwa unavuja damu! Risasi kutoka kwa Red butterfly ilipenya chini kidogo ya goti. Daniel alianguka palepale getini huku akipiga kelele za maumivu.
Idd alikuwa anapiga risasi hovyo wakati Red butterfly akikimbia zigzag na zile risasi kumkosa gizani. Aliingia katika uchochoro pembeni ya nyumba ya Daniel, alirukia katika pikipiki alilolihifadhi pale na kuondoka kwa kasi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment