Simulizi : Red Butterfly
Sehemu Ya Tatu (3)
Walikubaliana. Kutoka Uwanja wa ndege moja kwa moja walienda Mikocheni ilipo hospitali ya Hurbert Kairuki. IGP John Rondo mwenyewe ndiye aliyemueleza Daniel kila kitu kilichotokea kule uwanja wa ndege. Daniel akiwa kitandani aliwaza sana, kisha akauliza.
"Mnadhani mke wangu atakuwa wapi?"
"Kusema kweli hatuelewi kabisa. Tumeona tuje kukwambia wewe kilichotokea kule uwanja wa ndege labda utakuwa na mawazo yoyote" IGP John Rondo alisema.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kufikiria kidogo Daniel alisema "Hapo cha kufanya ni kuwasiliana na watu wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China watueleza je Elizabeth Neville alipanda katika hiyo ndege?" Daniel alisema.
"Wazo zuri sana Daniel. Tutafanya hivyo sasahivi tujue kama Elizabeth Neville alipanda ile ndege" IGP John Rondo alisema.
"Na endapo kama hakupanda basi kuna mchezo fulani umechezwa. Kama alikuwepo basi utakuwa ni mtihani wa mwaka, iweje Elizabeth apotelee hewani?" Daniel alisema.
"Ngoja tufatilie hilo tujue. Nitakuja tena hapa kukwambia majibu ya huko China" IGP John Rondo alisema.
IGP John Rondo aliaga kwa miadi ya kurudi baada tu ya kupata majibu.
Nusu saa baadae IGP John Rondo alirudi wodini kwa Daniel Mwaseba. Sura yake ikiwa yenye wingi wa mawazo. Daniel aliiona sura ya IGP John Rondo tangu kule mlangoni. Sura yake ilimwambia kuna kitu.
Baada ya salamu John Rondo alisema.
"Tumewasiliana na watu wa uwanja wa ndege kule China. Hata wao wameoneshwa kushangazwa sana na tukio hili. Hata huko China jina la Elizabeth Neville limeonekana katika orodha ya watu waliotakiwa kuondoka kutoka leo kule China kuja Dar es salaam, lakini Elizabeth Neville mwenyewe hakuwepo, nao bado wanafanya uchunguzi kimetokea nini.." Wakati anaongea mara siku yake iliita.
"Kuna taarifa mpaya tumeipata mkuu" Simu kutoka China ilisema "Ndege yetu ilitakiwa kuondoka na watu sitini na nne, na kweli iliondoka na watu sitini na nne, lakini cha kushangaza katika orodha yetu ina watu sitini na tano. Kwa mantiki hiyo inaonesha kuna mfanyakazi wetu aliongeza jina la mtu ambaye hajasafiri, na huku akiirudia namba ishirini mbili mara mbili katika orodha, na bila shaka mtu huyo ni Elizabeth Neville. Bado tunafanya uchunguzi ni nani kafanya hivyo na kwa malengo gani?" Yule mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China alisema.
"Nimekuelewa Maxi Lee. Fanyeni uchunguzi, nasi twachunguza huku tujue kitu gani kimetokea. Ukipata lolote usisite kuwasiliana na mimi" IGP John Rondo alisema.
"Sawa mkuu" Maxi Lee alijibu na siku ikakatwa.
"Daniel haya mambo yanazidi kuwa na utata. Yule mtu wetu anayetupa taarifa kutoka kule anasema ndege ilitakiwa kuondoka na abiria sitini na nne. Lakini katika orodha kulikuwa na abiria sitini na tano ila kuna namba moja ilirudiwa mara mbili. Hivyo kwa mwonekano wa kawaida inaonekana kama orodha ni ileile sitini nne kumbe wamezidi. Kwahiyo ndege ilikuja na abiria sitini na nne ila mkeo aliyekuwa anatengeneza idadi ya watu sitini na tano hakuwepo ndani ya ndege. Swali la kujiuliza ni, Yuko wapi?" IGP John Rondo alisema.
"Natamani ningekuwa mzima nitegue hiko kitendawili. Huwa naburudika sana kufumbua mafumbo ya utata kama hayo" Daniel Mwaseba alisema kwa majonzi.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ni kweli Daniel. Lakini safari hii yametokea hayo pengine kuwapa nafasi wengine waoneshe uwezo wao. Usisikitike sana, kuna kijana mmoja anaitwa Adrian namuona anakuja vizuri sana. Mwanzoni alikuwa kule Mkuranga kabla ya kuhamishwa na kuletwa makao makuu. Naona tumpe nafasi ya kufumbua fumbo hili, hata siku Daniel usipokuwepo tutajua tuna Adrian" IGP John Rondo alisema.
"Adriiiian" Daniel alisema akikuna kichwa. "Si ni yule aliyefanya kazi ya kufumbua fumbo la Briefcase akiwa na Inspekta Jasmin?" Daniel aliuliza.
"Ndo huyohuyo, Adrian Kaanan, yupo vizuri sana kijana. Na nilikuwa nae kule uwanja wa ndege hivyo anafahamu kidogo nini tunafatilia. Kwakuwa Elizabeth Neville hayupo tumpe Adrian kazi ya kumtafuta Elizabeth Neville pamoja na Red butterfly" IGP John Rondo alisema.
"Kwakuwa ni askari siwezi kumkatalia kwakuwa ni moja ya majukumu yake. Lakini kiukweli hii kazi ni ngumu sana na ni hatari pia. Yupo wapi huyo Adrian?"
IGP John Rondo alitoka nje, akimwita Adrian na kuingia naye ndani. Wakaongea wakiwa watatu na Adrian kupewa kazi mbili, moja kumsaka Red Butterfly pia kumtafuta Elizabeth Neville yupo wapi. IGP alimwambia Adrian kuwa miongozo yote itatoka kwake na kwa Daniel Mwaseba. Adrian alipokea kazi hiyo kwa mikono miwili. Ilikuwa ndio kazi yake kubwa baada ile ya Briefcase ambayo akiifanya akiwa chini ya Inspekta Jasmin.
Mfupa huu mgumu unaelekea kwa Adrian Kaanan..je atauweza? Itaendelea kesho Mungu akipenda...
Ilikuwa siku ya tatu tangu wakina Daniel washambuliwe. Hayakutokea mauaji yoyote kutoka kwa Red butterfly wala Elizabeth Neville hakujulikana alipo. Adrian Kaanan alikuwa anaendeleza upelelezi wake kwa umakini mkubwa sana. Alikuwa ameshapita katika familia za marehemu wote saba na kugundua mambo kadhaa ambayo alikuwa anaamini yatamsaidia katika upelelezi wake. Siku hiyo asubuhi na mapema alienda wodini kwa Daniel Mwaseba kumueleza wapi uchunguzi wake ulipofikia.
"Habari yako kaka Daniel?" Adrian alimsalimu Daniel.
"Nzuri aisee. Ninaendelea poa. Kidonda kinaendelea kukauka na maumivu yamepungua sana. Daktari amenambia kinapona haraka tofauti kabisa na matarajio yao" Daniel Mwaseba alisema.
"Tunakuombea sana Daniel upone haraka. Taifa linakusubiri katika harakati za kulijenga" Adrian alisema.
"Eeeh vipi ishu ya kumtafuta mke wangu imeishia wapi?" Daniel aliuliza.
"Bado naendelea kuchunguza mahali alipo shemeji. Nawasiliana mara kwa mara na watu wa kule China, kwa sasa wamemtambua na kumkamata mtu aliyeliingiza jina la Elizabeth Neville katika orodha ya watu walioondoka na ndege ile juzi. Bado wanamfanyia mahojiano. Maxi Lee amesema jioni atanipigia anipe nini amejibu katika hayo mahojiano. Tukipata sababu ya kuongezwa jina la Elizabeth Neville katika orodha ya abiria waliokuja juzi ndipo tunaweza kupata kiini cha mahali alipo. Kwa vyovyote vile huyo mtu aliyeliongeza jina la mkeo kule China anajua mahali mkeo alipo" Adrian alijibu.
"Umepiga hatua nzuri sana Adrian. Nashukuru umeenda vizuri sana kuhakikisha mke wangu anapatikana. Na vipi kuhusu suala la Red butterfly? Umefikia wapi?" Daniel aliuliza tena.
"Hapo ndipo kwenye utata kaka. Suala la Red butterfly ni suala tata sana. Baada ya kupewa kazi hii ya kuchunguza kuhusu Red butterfly nilienda katika familia zote za wafiwa. Nilianza katika familia ya kwanza ya Mzee Matojo. Nilifanya mahojiano na mjane wa marehemu. Hakuwa na mengi ya kusaidia katika kumpata Red butterfly, kikubwa kilichoganda kichwani kwangu kwamba mzee Matojo alikuwa anafanya kazi katika kiwanda cha Urafiki kabla ya kazi yake ya sasa. Nilipotoka pale nikaenda katika familia ya mzee Mahenge, kule niliongea na mdogo wa marehemu, naye alinisimulia mengi ingawa hayakunisaidia sana katika msako wa Red butterfly, lakini kubwa nililoondoka nalo pale mzee Mahenge naye ashawahi kufanya kazi katika kiwanda cha nguo cha urafiki. Nikahoji familia zingine nne, majibu yalifanana. Wote walifanya kazi kabla katika kiwanda cha urafiki. Mwishowe nikaenda kwa mjane wa mheshimiwa Elisha Ngwena..."
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Najua mzee Ngwena ashawahi kuwa meneja pale kiwanda cha urafiki" Daniel Mwaseba akadakia.
"Na hilo ndilo lilinivuruga kaka Daniel, kwanini marehemu wote saba wawe wamewahi kufanya kazi katika kiwanda cha Urafiki?"
"Uliyonieleza hapa yote nayafaham Adrian. Upelelezi wangu ulinifikisha hapo ulipofika wewe. Na nilikomea hapo kabla ya kupigwa hii risasi ya mguuni. Nafurahi sana kwakuwa umegundua kitu ambacho niligundua mimi awali. Sikutaka kukwambia kuhusu kiwanda cha urafiki kwakuwa nilitaka kujua kama nawe utafika hapo? Sasa hapo ndio mwanzo wa upelelezi wako Adrian. Hadi hapo ulipofikia nimeweka imani kubwa sana kwako kama utafumbua fumbo hilo" Daniel Mwaseba alisema.
"Usiwe na shaka na mimi kaka Daniel, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha nayafumbua mafumbo haya mawili" Adrian alisema.
Waliongea kama nusu saa huku Daniel akimpa maelekezo Adrian. Walielewana, walikubaliana. Na Adrian alienda kuyafanyia kazi.
***
Saa nne kamili asubuhi ilimkuta Adrian Kaanan nje ya kiwanda cha nguo cha Urafiki. Alipaki gari yake na kuingia kwa meneja wa kiwanda cha Urafiki.
"Kwa majina ninaitwa Adrian Kaanan. Ni askari Polisi ambaye nachunguza vifo vya watu saba akiwemo mheshimiwa Elisha Ngwena. Nimeamua kuja hapa ofisini kwako kutokana na utata wa vifo vya watu hao. Katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa watu wote saba waliouwawa wamewahi kufanya kazi hapa. Na hiyo ndio sababu ya mimi kuwa hapa" Adrian alisema.
"Karibu sana Adrian. Mimi ndiye meneja wa kiwanda hiki. Ninaitwa Christopher Mbulu. Umeongea jambo ambalo hata hapa tulikuwa hatujaligundua bado juu ya marehemu wote saba kuwahi kufanya kazi katika kiwanda chetu" Christopher alisema.
"Ndio hivyo meneja. Marehemu wote waliwahi kufanya kazi hapa kwenu. Sasa hapo ndipo tunapopata mashaka na kuhisi labda kuna kitu kilitokea hapa miaka hiyo ambacho kinaweza kuwa pengine ndio sababu ya vifo vya watu hao?" Adrian alisema na kuuliza swali.
"Nimekuelewa vizuri sana Adrian. Sasa nini msaada wetu hapa. Mana mauaji haya yanatishia sana usalama wa nchi yetu" Meneja Christopher alisema.
"Hapa nimekuja kufata kitu kidogo sana. Najua huwa mnatunza rekodi muhimu hapa. Sasa nilikuwa ninataka safu ya uongozi wa kiwanda hiki wa mwaka 1954 hadi 1957. Watu waliofariki inaonesha wamefanya kazi hapa miaka hiyo" Adrian akasema.
"Hizo rekodi lazima zitakuwepo. Ngoja nimwite mtu wa records atutafutie" Meneja alisema na kutoka nje. Baada ya kama dakika kumi alirudi na karatasi nne mkononi.
"Nimezipata Adrian. Hii hapa ni safu ya uongozi ya mwaka 1954, hii ni ya 55, hii ni ya 56 na hii ndio ya 57" Meneja alisema huku akimkabidhi Adrian karatasi moja moja.
"Nashukuru sana meneja. Bila shaka katika karatasi hizi ninaweza kugundua jambo la kunisaidia katika uchunguzi wangu. Mimi ninaenda..nitakapohitaji chochote tunawasiliana" Adrian alisema na kupeana mkono na meneja. Akaondoka.
Ni dakika kumi na tatu tu tangu Adrian aondoke mle ofisini aliingia mgeni mwengine ofisini kwa meneja wa kiwanda cha Urafiki. Mgeni huyo alikuwa mwanamke mrembo sana. Aliingia ofisini kwa madaha. Harufu ya marashi yake yaliimeza ile ofisi ya meneja wa kiwanda cha nguo cha Urafiki.
Baada ya salamu na kukaribishwa kitini mwanamke aliuliza swali.
"Yule Kijana aliyetoka hapa dakika kumi na nne zilizopita alikuwa amefata nini?"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni dakika kumi na tatu tu tangu Adrian aondoke mle ofisini aliingia mgeni mwengine ofisini kwa meneja wa kiwanda cha Urafiki. Mgeni huyo alikuwa mwanamke mrembo sana. Aliingia ofisini kwa madaha. Harufu ya marashi yake yaliimeza ile ofisi ya meneja wa kiwanda cha nguo cha Urafiki.
Baada ya salamu na kukaribishwa kitini mwanamke aliuliza swali.
"Yule Kijana aliyetoka hapa dakika kumi na nne zilizopita alikuwa amefata nini?"
Meneja alibaki na mshangao maana halikuwa swali alilolitarajia hata kidogo kutoka kwa mwanamke yule mrembo sana. Kilichomshangaza zaidi ni hali ya kujiamini ya mrembo yule.
"Nina mambo mengi ya kufanya Christopher, naomba nijibu swali langu niondoke" Mwanamke alisema huku akiuweka mkongojo wake juu ya meza alipoona meneja Christopher akichelewa kujibu.
"Huyu ni Red butterfly anayetafutwa. Na huu ndio mkongojo ambao niliusoma katika gazeti akitumia kuwashambulia wakina Daniel Mwaseba..." Meneja alikuwa akiwaza huku hofu dhahiri akijijenga usoni mwake.
"Alifa..." Kabla meneja hajaongea, mlango wa ofisi ulifunguliwa kwa pupa, alitokea Adrian akiwa kashika bastola imara mkononi mwake, bastola ilikuwa imeelekea katika kichwa cha yule mwanamke.
Yule mwanamke alistuka sana. Hakuutegemea ujio wa yule kijana aliyekuwa anamfatilia tangu alivyotoka katika hospitali ya Kairuki alipolazwa Daniel Mwaseba.
"Nyoosha mikono juu kabla sijapasua kichwa chako!!" Adrian alisema kwa ukali.
Siwezi kukamatwa na kitoto kama hiki, lazima nifanye kitu hapa. Iam a butterfly" Yule mwanamke aliwaza.
Sekunde ileile aliruka juu ya meza kimaajabu na kusimama nyuma ya mgongo meneja wa kiwanda. Mkongojo wake ulikuwa mkononi Iakini sasa ulikuwa mfupi mithili ya bastola. Mdomo wa bastola ulikuwa umegusana na shingo ya Meneja Christopher. Yule mwanamke alifanya kitendo kile kwa kasi ya ajabu. Kasi ambayo haijawahi hata kufikiriwa hata siku moja na Adrian Kaanan.
"Ni Red butterfly mwenyewe. Kasi yake ni ileile" Adrian alisema kwa sauti ndogo.
"Ukifanya ujanja wowote Adrian namuua huyu meneja!" Yule mwanamke alisema kwa sauti kubwa.
Meneja alikuwa anatetemeka sana. Ubaridi wa mdomo wa bastola ulimwogopesha sana. Ilikuwa mara yake ya kwanza kukaribiana na kifo katika maisha yake.
"Umekwisha Red butterfly, leo ni mwisho wako ..." Adrian alijisemea kimoyomoyo.
"R.B on target" Adrian alisema kwa sauti ndogo. Sekunde ileile waliingia wanajeshi watano wakiongozwa na Idd. Wanajeshi walikuwa katika gwanda za jeshi la Wananchi wa Tanzania. Na silaha zao mkononi.
Yule mwanamke hakuamini macho yake. Alihisi kuwa amekamatwa kirahisi sana.
"Wameniweza hawa wajinga. Sikuliwaza hili hata kidogo. Bila shaka hii itakuwa ni mipango ya Daniel Mwaseba tu. Hakika yule mwanaume sio binadamu wa kawaida. Sasa nitajiokoaje hapa?"
"Weka bastola yako chini!!" Idd alisema kwa ukali.
"Nikiweka bastola chini hapa nitakuwa nimejikamatisha mwenyewe. Siweki" Yule mwanamke aliwaza.
"Bastola sita za wanaume wenye mafunzo ya kijeshi umeelekezwa wewe. Huna ujanja wa kutoka hapa tena Red butterfly. Hapo ni kutii amri tu. Weka silaha yako chini" Adrian alisema akimrai yule mwanamke wa ajabu.
"Hamuwezi kunikamata mimi nyinyi. Na mkifanya ujanja wowote nitaondoka na roho ya huyu meneja!!" Yule mwanamke alisema kwa ukali.
Yule mwanamke akauangalia ule mkongojo wake. Akatabssamu. Wakati huo risasi alikuwa ameshaisogeza katika chemba kwa maana akitomasa kidogo tu triga ya mkongojo ule wa ajabu ilikuwa risasi inadidimia shingoni mwa meneja kiwanda cha urafiki. Christopher alikuwa anatetemeka huku akiamini ni miujiza tu ya Mungu ndiyo itakayomuacha salama.
Yule mwanamke akamnyanyua kwa nguvu Christopher kwa kutumia mkono wa kulia, sasa walikuwa wamesimama sambamba. Meneja Christopher mbele, yule Mwanamke wa mwenye kasi ya ajabu na shabsha ambaye walikuwa wanamtambua kwa jina la Red butterfly alikuwa nyuma.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Niseme tena tu uhai wa huyu fala ninao mimi. Hata mkinipiga risasi roho yangu haitoenda motoni kabla sijaichakaza vibaya san shingo ya huyu mjinga. Sasa ombi ni moja tu kwenu, wekeni silaha chini na mnipishe hapo mlangoni. La sivyo nitakufa lakini nitakuwa nimeuwa..." Yule mwanamke alisema kwa kujiamini na woga wote uliomvaa awali ulikuwa umemtoka. Alijua ile ni karata yake pekee ambayo ilimpasa kuitumia vizuri kujiokoa. Maneno aliyoyasema yaliingia vizuri kwa wale askari. Na walijua kwamba mwanamke alikuwa anasema kweli. Alikuwa na uwezo wa kuuwa kabla hajafa. Na dhamira yao kama askari ilikuwa kumlinda meneja Christopher na sio kusababisha kifo chake. Ilikuwa dhima kuu ya askari, kulinda raia.
"Nakuuwaaa mwanaume.." Yule mwanamke alisema kwa sauti ndogo sikioni mwa meneja Christopher.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment