Search This Blog

Friday, 18 November 2022

BINTI WA RAISI - 4

 






Simulizi : Binti Wa Raisi 
Sehemu Ya Nne (4)




****

Rayana hakutazama nyuma kabisa,mbio ambazo amezianzisha kufuatia na kufuatwa kwa watu wasiojukikana kamwe hazikupata kuelezeka.Usiku huo mara baada ya kuvamiwa katika kibanda chake,akakimbilia mabondeni japokuwa alijikwaa matofali lakini hakujari kabisa,akainuka na kuendelea kukimbia.Akafika kwenye mfereji wa maji taka na kuanza kupanda kivuko kilichotengenezwa kwa mbao.Kwa kuwa alikuwa katika mwendo mkali wa kukimbia ghafla akajikuta akiteleza na kutumbukia katika maji hayo machafu yenye rangi nyeusi.Akaanza kutapatapa huku akishindana na kasi ya maji hayo mpaka pale alipofanikiwa kutoka.

Akafika nyumbani ikiwa ni saa tano na nusu usiku,hakuwa na pesa yoyote ambayo aliibeba hii ni kutokana na kuhofia uhai wake.



"Mamaaa! Wanataka kuniua" Rayana akazungumza kwa uchungu huku akiwalaani wale watu asiowajua.

"Kweeh nani wenyee hao mwanangu?" Mama Rayana akalalamika huku akutafuta kiberiti ili awashe kandili lake.Aghalabu machozi yakawa yanamtoka,hakuelewa ni kitu gani kakosa mpaka afikie hatua ya kufukuzwa na kutaka kuuawa.

"Siwajui mama wamenifukuza"

"Uwiiii! Jamani mwanangu umekosa nini sasa"

"Sielewi"

Rayana akiwa amechafuka na tope la maji taka,mwili wake wote umebadilika rangi na kuwa mweusi,akachukua ndoo na kuijaza maji kisha akaingia bafuni na kuanza kuoga.Aliporudi akaivuta shuka yake huku pembeni ya kitanda chake amekaa mama yake Bi Chiku,akawa anambembeza mpaka walipoagana na Rayana akalala fofofo!.

Asubuhi na mapema alikuwa wa kwanza kuamka,akajiandaa na kwenda kwenye biashara.Kwa bahati mbaya alikuta mlango wake upo vilevile kama alivyoufungua jana yake.Hakukuta pesa,hakukuwa na chakula alichokiacha jana zaidi ya kuingia hasara kubwa katika biashara yake.Wakati yupo katika msongo wa mawazo,akaiona gari ya Swedy ikija kwa mbali,haraka akajifuta machozi yaliyokuwa yanamkenga kisha akasimama sehemu ya wazi ili iwe rahisi kuonekana.Kama ilivyoada gari ikasimama na kijana Swedy akashuka.

"Mambo Rayana" akasalimia.

"Sio salama kaka jana nilifukuzwa na watu nisiowajua,wanataka kuniua" Rayana akazungumza kwa uchungu sana.

"Wanataka kukuua?" Swedy akashtuka na kumtupia swali.

"Ndio"

"Wakina nani hao?"

"Sasa nimekuambia siwajui kabisa"

Swedy akabaki katika hali ya sintofahamu kabisa na upande mwingine alisumbuliwa sana na mtu anayeitwa Geza ulole,mtu ambaye amemhusisha moja kwa moja katika kufuatilia utekwaji wa binti wa raisi.Akili ya Swedy ikaanza kuchemka kwa kasi huku mara kadhaa alijaribu kutatua kitu kinachomkwamza lakini bado haikuwa rahisi kwa hilo.



"Hebu funga mlango wako halafu ingine kwenye gari ukanieleze vizuri zaidi" Swedy akazungumza na kuingia garini.Baada ya Rayana kufunga mlango wake akaingia ndani ya gari na kuondoka zake.Kitu cha kwanza alichokiwaza swedy ni kuifikisha gari mpaka nje ya mgahawa wa S&J reustaulant.Akafunga breki hapo na wote wakashuka kisha wakavuta kiti na kuagiza supu pamoja na chapati za nguvu.Bila kuzungumza wakaanza kuvamia chai hiyo.Rayana akiwa na tabasamu zito akamtazama Swedy cha jicho la kuiba kisha akainamisha sura yake na kuendelea kunywa chai.Hakuwa kuingia katika sehemu kama hiyo,alifurahia sana.

"Ehee Rayana hebu niambie vizuri unasema kuna watu wanataka kukuua?"

"Ndio walivalia suti lakini mikononi walishika bastola,wakaniita kando lakini kabla sijawafikia nikamuona mmoja akiikoki bast......" Kabla Rayana hajamalizia kisa chake simu ya Swedy ikaita,akaichukua na kuitazama.Alikuwa Geza anayepiga,akatoa pumzi ndefu huku akijua kabisa kuongea na mtu huyo kulihitaji umakini wa hali ya juu,endapo utaenda ndivyo sivyo basi utambulia na maneno yenye ukali mno.

"Vipi Swedy hupokei simu?" Rayana akauliza baada ya kumuona Swedy akiitazama simu bila kuipokea.

"Mmmh huyu mtu we acha tu" Swedy akasema hayo kisha akapokea simu.

"Naam kaka"

"Dogo napiga simu muda wote huu umeanza dharau" Geza akazungumza kwa ukali.

"Kaka samahani nilikuwa bafuni kidogo" Swedy akajitetea huku akiwa mpole kama mtu aliyemwagiwa maji ya baridi ama kama maji ya mtungini.Alipohakikisha amemalizana na Geza akakata simu na kuiweka mfukoni,akaachia tena pumzi ndefu huku akiikabili sura ya Rayana iliyo mbele yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Rayana nitaongea na wewe badae sasa hivi kuna mtu naenda kukutana nae na nikichelewa hata dakika mbili tu lazima anifokee"

"Bosi wako nini?" Rayana akatupa swali kwa Swedy.

"Hapana ni jamaa mmoja hivi ana sheria kama mzungu,ila chukua hii utafanyia nauli ya kurudi pia inatakiwa kuwa makini sana maana siku hizi watu wanateka muda wowote sijui wana nini haswa" Swedy akazungumza machache kisha akampatia fedha Rayana na yeye akaanza safari ya kwenda sehemu ambayo akiweka miadi na Geza Ulole.

Baada ya dakika kumi na tano akajikutana anasimamisha gari yake nje ya nyumba iliyo kuukuu na kuingia ndani,humo akamkuta Geza ulole akiwa na kalamu na karatasi yake juu ya meza.Alipomsalimia hakuitikia kabisa,macho ya Geza yalikuwa kwenye saa aliyoivaa mkononi mwake huku sura kaikunja.

"Umechelewa dakika tano dogo,umeshaniharibia ratibu yangu leo" Geza akanung'unika sana huku akidaika amepotezewa muda wake.

"Kaka dakika tano tu nimeharibu ratiba yako?" Swedy akashangaa sana kusikia maneno hayo.

"Ndio maana Waafrika hatuendelei kabisa,tatizo letu sisi ni mapuuza wa muda" Geza akaeleza kwa ufafanuzi mpana.Akaanza kuzungumza na Swedy jinsi ya utumizi wa muda katika maisha ya kila siku.Uchanganuzi huo wa Geza kuhusu muda ukamuacha mdomo wazi sana Swedy,hapo ndipo alipoamini kuwa Geza Ulole ana upeo mpana wa kuchanganua mambo japokuwa hakuwa na usasa wowote katika mwili wake zaidi ya usasa wa kifikra uliopo kichwani mwake.





Baada ya Geza kumaliza ufafanuzi juu ya matumizi ya muda akamruhusu Swedy aketi kitini ili kazi yao ianze.Geza akachomoa kipande cha gazeti kilichobeba habari kuhusiana na utekaji huo kisha akakiweka mezani.Sasa sura zao zikabaki kuitazama picha ya mtoto wa raisi Dayana akiwa na tabasamu pana usoni,Geza akatabasamu kisha akasema.

"Unajua nashindwa kuelewa kabisa,mtoto uzuri kama huyu unamteka huyu,si uonevu huu.Wangelikuwa wanatuteka watu kaka sisi,huwezi kujua kama huko waliko wanawaacha hivihivi bila kuwabaka hawa" Geza akazungumza kwa utulivu kisha akabaki kimya kwa muda.

"Sikia dogo hawa ni mademu na mademu hawakosi wapenzi si ndio?" Geza akamtupia swali Swedy.

"Ndio!"

"Safi,sasa unafikiri hao wapenzi wao hawawezi kujihusisha katika huu utekaji?,kama sio hivyo lazima kutakuwa na mkono wa mtu wa karibu yao ambao wamefanya tukio hili unadhani kutafuta pesa ni mchezo eeeh " Geza akaendelea kuzungumza watu anaowahisi kujihusisha katika tukio hilo.



******

Ung'ang'anizi wa James Goba juu wa uongo wa Aidan ukampa uchizi mno.Hakumuachia uhuru Aidan mpaka pale atakapopatikana Rayana mtu ambaye anahusiwa kwa namna moja ama nyingine.James Goba akiwa na wenzake wawili huku wakiwa wamemshikilia Aidan mpaka pale atakapopatikana Rayana,wakaendelea kusogeza bia katika makoo yao huku wakijipatia burudani kutoka kwenye kituo maarufu cha rununga.

Ghafla burudani ikakata na baada ya hapo zikabaki chenga zilizodumu kwa sekunde chache kabla haijaingia rangi nyeusi.Hapo ndipo video fupi ilipoanza kuwaonesha mabinti wa maraisi wakiwa na mlinzi wao,video hiyo iliyojionesha kwa sekunde kumi kisha ikakata na vipindi vya kawaida vikaendelea.Pigo kubwa sana likawapata wakina Goba,pombe walizokuwa nazo kuchwani zikapotea haraka hii ni kutokana na kipande cha video hiyo.

"Inaonesha wazi kuwa kuna watu wamewashikilia lakini hawa watu gani?" Goba akajiuliza mara nyingi bila ya kupata jibu.Akawatazama wenzake na kuwakazia macho.

"Tukamsake leo leo huyu binti mpaka tumpate!" Goba akazungumza kwa msisitizo.Wakamchukua Aidan akiwa na kuondika nae,safari ya pili ya kuelekea Mburahati kisiwani ikaanza.Lengo lao kuu ni kumsaka Rayana ili waweze kukamilisha uchunguzi wao.

Kweli wakaingia barabara ya Moroko na kuanza kuisaka njia panda kigogo baada ya kufika Magomeni.Hatimaye wakafika Kigogo mwisho.

Wakashuka kwenye gari na kutulia kidogo huku kila mmoja wao akichezesha akili namna gani wanaweza kumnasa binti huyo.Baada ya kutaharuki kwa mawazo ya kila mmoja ndipo James Goba akamtazama kijana ambaye amebeba boksi ndogo mkononi,akamuita na kumsalimia na hapo ndipo alipomuelezea shida yake "naomba uniitie yule binti pale mwambie kuna mzigo wake hapa" Goba akanena na kijana huyo akafanya kama alivyoagizwa,baada ya dakika chache Rayana akawa anajongea taratibu kuelekea kwenye gari hiyo ya akina James Goba.Kosa kubwa kwa Rayana kutia mguu kwenye eneo lile kwani Goba ndiye aliyekuwa wa kwanza kumrukia na kuingia nae garini.



******

Chimbo hilo lililogubikwa na kiza likawafanya watatu hawa wajawe na woga na hofu kubwa ndani yake.Hakikuwa kingine kinachowaogopesha zaidi ya sauti mbalimbali za wadudu wa ajabu waiokuwa wakifurahia kiza hiko.Miguu yao yote iliunganishwa na mnyororo mkubwa huku mikono yao ikiwa imebetuliwa kwa nyuma na kuunganisha kwa mnyororo pia,hakukuwa na hata mmoja aliyejaribu kujinusura katika chumba hiko.Sura zao zinaonesha wazi kuwa hawana furaha kabisa,majuto yakaanza kuwaandama na kila mmoja akajaribu kuhiukumu nasfi yake pasi kuwepo na hakimu "Kwanini nilikubali kuja Tanzania" sauti kali yenye ulegevu wa uchovu ikasikika kwa kulaani kitendo alichokikubali mwenyewe mwanzoni.

"Usiseme hivyo Mercela utakuwa unakosea" Sauti ya Dayana ikamsihi Mercela asitamke kauli kama hizo lakini hakuweza kuinyamazisha sauti hiyo zaidi ya kuendelea kuikanyaga Tanzania kwa maneno makali.Haikupita muda mlango ukafunguliwa na mwanga mkali wa tochi ukapenya ndani ya mboni zao.Watu hao wakaingia kwa kelele za hapa na pale zilizowapa shida za kuwasikiliza.Mmoja wao akatoa funguo na kuwafungua minyororo yao kisha wakawatoa nje.Huko wakakutana uso kwa uso na mtu ambaye siku zote walimchukia mno, anaitwa MK.

Siku hiyo waliamua kabisa kuweka wazi kuwa mabinti hao pamoja na mlinzi wao wamewashirikia wao na wahusika watapewa siku chache kuweza kuwakomboa mabinti zao.Kweli wale watu wakawapeleka kwenye chumba husika chenye mitambo mingi kisha wakawaweka sehemu moja,jamaa mmoja akachukua mashine moja aliyoundwa mfumo wa kioo kisha akaitazamisha mbele yao.Mtaalamu wa kompyuta akaiwasha mashine yake na kuanza kubonyeza bonyeza vitu anavyovijua kisha yakatokea maneno yaliyoandikwa kwa jina la kiingereza yaliyosomeka kama 'HACK' alipolifikia neno hilo akaliruhusu kisha akabonyeza button ya ENTER ndipo vituo vyote vya runinga vikakatwa mawasiliano na kuwaonesha mabinti wale.MK akaanza kujinadi na kutamba mbele ya kioo hicho.Ufafanuzi wa MK kwa kadamnasi ikajieleza kabisa kuwa hana mchezo katika hilo,alipania haswa kwa hilo.Baada ya kutamba kwa maneno mengi MK akamsigeza mmoja wapo audhihilishie umma kuwa wapo matatani na wanahitaji okolewa.



"Dady tunakuomba utuokoe tutakufa huku tunaomba utusaidi....."MK hakumpa muda mwingi wa kujimwayamwaya mbele ya kioo hicho,akamvuta na kumrudisha nyuma kisha akachomoa kisu kilicho na mng'aro kama ishara ya ukali wake.

"Two days to ago,hivi viumbe mje kuvitoa kabla hatujatenganisha shingo zao....ni rahisi sana kukata hizo shingo" MK akaongezea kisha akazitaja namba za mawasiliano.



NDANI YA MJI WA BAGAMOYO.



Sehemu ya nyumba tulivu kabisa iliyopokea upepo mwanana uvumao toka baharini.Uzio mkubwa uliozunguka nyumba hizo ikaonesha picha halisi kuwa mkaaji wa eneo hilo ni wazi kuwa ana pesa za kutosha.Miti ya mvuto iliyumba huku na huko kutokana na uelekezo wa upepo huo.Utulivu wa eneo hilo likawavutia sana ndege aina mbalimbali na wenye rangi tofauti waje kwa wingi na kufurahia hali ya hewa hiyo.Lakini japokuwa hali yote ya hewa kuwa hivyo haikumuweka sawa kabisa mtu aliye katika jumba hilo.Mtu huyo mwenye mvi kwa mbali,sura ya uviringo,mwili wake ulivimba kidogo na kutengeneza jina kwa watu la Miraba minne,ndefu zake zilizichongwa vizuri na kutengeneza umbo na O.Miwani yake ambao alizoea kuipachika chini ya macho yake yaani juu ya pua haikuwepo tena mahala pake zaidi ya kuiweka kwenye meza iliyo pembeni,sura yake inaonekana wazi haikuwa na tumaini la furaha kama ilivyo kawaida yake hapo nyuma.Mawazo tele ndio kitu pekee kilichochukua nafasi katika upeo wa ubungo wake.Wakati jamaa huyo anaendelea kuteseka kwa mawazo yasiyokatika mara akashtuliwa na mlio wa simu yake toka mfukoni.Naam ni mlio mfupi wa ujumbe ulioshtuwa kwa mvuto mzito.Akavaa miwani yake ambayo ilisaliti sehemu yake muda mchache uliopita,akaufungua ujumbe huo na kuanza kuusoma.Ni kama alimwagiwa maji ya baridi jinsi alivyosoma ujumbe huo,ni ujumbe mzito mno haukuwa wa kawaida kabisa katika serikali ya kichwa chake.Hali ya kuteswa ikamuongezeka mara dufu.Wakati anaendelea kuiumizia kichwa meseji hiyo mlio wa gari ukawa unavuma toka nje ya geti.Mlinzi wa nyumba hiyo akachukua nafasi yake kulifungua geti na kuiruhusu gari hiyo iingine ndani.Murano nyeusi iliyo na mng'aro ikaegeshwa ndani na sura ya mwanamke ukashuka huku nae akiwa hana furaha hata kiduchu.Akafunga mlango wa gari lake na kuanza kujongea alipo yule jamaa aliyeachwa hoi na ujumbe ulioingia katika meseji yake.Hatua hizo za mwanamke huyo hazikukinzana sana na zile za kinyonga,kwani zilikuwa ndogo mno ila utofauti wa hatuo zake na za kinyonga zilitenganishwa na kitu kimoja yaani mwendo wa kinyonga ni mdogo na wenye maringo lakini hatua za huyu mwanamke zilikuwa za upole zisizo na maringo zaidi ya uzuni pekee.Akamfikia jamaa huyo na kuketi pembeni bila kuongea chochote,sasa akawa anashindana na chozi ambalo lilikuwa linamlengalenga usoni mwake lakini jitihaza zake hazikuzaa matunda kabisa,machozi yakaanza kumvuja na kulowanisha mashavu yake huku bila sauti ya kilio kusikika.Ni kilio kilichojaa uchungu mno kitu ambacho kilichomfanya jamaa hiyo nae aanze kuitoa miwani yake na kuanza kutokwa machozi kidogokidogo hatimaye yakamjaa lakini hakukuwa na kilio cha sauti.Akamvuta mwanamke huyo na kuanza kumbembeleza.Hawajatulia ukaingia ujumbe ungine kwa namba ileile ikisisitiza jambo fulani.Jamaa huyu akafungua tena ujumbe huo hapo akahisi kunyong'onyea kabisa,hajapata kusema neno lolote ujumbe ungine ukaingia,ulikutwa kwa njia ya mtandao wa 'whatsapp'.Alipoufungua akaona kuna picha zilizoanza kujipakua zenyewe.Macho yakamtoka akaiweka simu mezani na ndipo mwanamke huyu akapata kutia macho katika jumbe ile.Na yeye akaanza kuhisi maluweluwe kichwani mwake akajikuta anaachia ukelele mkali mpaka baadhi ya ndege waliokuwa wakifurahia upepo wa eneo hilo wakawa anakimbia wakihisi kuna kitu kibaya kinawawinda.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/







'TUNAKUPA MASAA KUMI NA MBILI,SALIO LETU LIWE LIMEONGEZEKA,FANYA HIMA KABLA SHINGO YA MWANAO HATUJAIONDOA SEHEMU YAKE'

moja ya jumbe hizo zilisomeka katika simu ya Jamaa huyo.Ni ujumbe wa kuogopesha.Mbaya zaidi ukaingia ujumbe wa picha iliyomuonesha mtoto wao anatokwa na damu puani.Vichwa vikaanza kuwagonga na hisia za kufariki kwa mwanao zikaanza kutanda,muda mfupi baadae wakiwa wenye simanzi simu ya jamaa huyo ikaanza kuita.Wakasita kulia na kila mmoja akawa anakodoa macho yake kwenye kioo cha simu.

"Namba ngeni hii" jamaa huyo yakamtoka maneno bila kujitambua.Akaisogeza simu na kuipachika kiganjani,akabonyeza sehemu ya kupokelea kisha akaivuta taratibu mpaka sikioni.

"Halloo" sauti ya chinichini ikamtoka jamaa huyo.

"Umebakiwa na masaa sita tu fanya ima usipofanya...." Sauti ya kiume kutoka jamaa wa upande wa pili wa simu akazungumza.



********



Wasaa matata kwa kila mja hapa duniani,wasaa ambayo hata siku moja haukuwahi kuwa mzuri kwa usalama wa binadamu.Usiku! Usiku wa giza kabisa.Lakini giza hilo halikuwazuia vijana watatu walio ndani ya gari jeusi pembezoni mwa uwanja.Mmoja kati yao alikuwa na mwili mkubwa,mikono yake yote ilitapakaa michoro ya tatoo utadhani ni ubao watumiao watoto wa chekechea kuandikia,pua yake iliyochukua nafasi kubwa kwenye sura yake ikaonekana dhahiri kabisa,midomo miyeusi iliyo mipana unaweza sema ana undugu kabisa na kiboko.Macho yake yenye rangi nyekundu hayakuweka kutofautishwa na mlaji ulaji mmea haramu.Sura lake liliogopesha haswa.Mtu wa pili kutoka kwa hili jamaa lililokaa upande wa siti za nyumba kulikuwa na sura ya kike mwenye umbo la haja mno,kifua chake kilituna kwa mbele kutokana na ujengefu wa matiti yake yalio ya wastani.Macho yake makubwa na yenye ulegevu kwa haraka tu umuonapo unaweza kusema alikuwa kapakia pombe tena zile ziitwazo SAVANA.Kichwani alikuwa na nywele fupi zilizokatwa kwa mtindo wa Panki.Hakuwa na heleni hata kipini kama ilivyo kawaida kwa wasichana wengi.Chini alivaa raba nyeusi zilizoendana sawa na jinzi aliyoivaa,tisheti isiyo ya maandishi ama kwa majina mengine ya vijana hupenda sana kuita 'MANGA' ilimkaa sawa msichana huyo.Lakini japokuwa alikuwa kapendeza sana na kuwashinda baadhi ya wasichana wenzake,alikuwa na tabia tofauti kabisa na wenzake,huyu alikuwa fundi wa kuvuta moshi wa mmea haramu,ni fundi haswa wa kutupia pombe zenye ukali wa hali ya juu.Pembeni ya gari hilo kulikuwa na mtoto mwenye mwili mnene akiwa amelala fofofo kabisa,hakuelewa chochote kinachoendelea kwenye dunia hii zaidi ya usingizi uliompeleka kuwa nusu mauti.Alichomwa sindano ya usingizi kila alipojaribu kufungua kope zake.Gari lote kimya,mihemo ya pumzi tu ndio ilichukua nafasi yake.Kwa mbali mwanga wa taa ukawa unaangaza kiwanjani hapo huku ikipunguza mwendo taratibu

hatimaye ikasimama mida kadhaa kutoka kwenye ile gari ya wale jamaa wenye mtoto ndani yake.Jamaa huyu mwenye pua kubwa akaitoa simu iliyokuwa inanguruma.Akaipokea huku akitoa tabasamu pana lenye furaha.Baada ya kuongea maneno machache,msichana huyo akatoa bastola yake na kuishikilia mkononi vizuri,akamvuta mtoto yule ambaye kwa muda alianza kutikisika kuashiria kuwa anaenda kuamka.Kwa umakini msichana huyo akawa akanyata huku amemshika mtoto hiyo akisonga kuelekea sehemu ulipo mwanga wa gari ile.



Kazi hiyo haikuwa ngumu kwao, kwani walishakabidhi mtoto wa tajiri yule na kupokea pesa nyingi mno.Wakaingia kwenye gari yao na kutoka kwa kasi ya ajabu.Breki ya kwanza ilikuwa kwenye ngome yao ya MK,wakaingia mpaka ndani na kuwakuta wakina Bosco pamoja na wenzake wakifanya mazoezi.Wakapitiliza mpaka sehemu yao husika.



"Eeeh bwana eeeh hii mishe mbona inakuwa ngumu hivi?" Bosco akawauliza wenzake huku akinyanyua chumba kizito juu.

"Ngumu namna gani?" Akauliza mmoja wao na Bosco akajibu kuwa ugumu wa kazi yao unatokana na kuchukua muda mrefu tofauti na walivyotegemea.

"Mvumilivu hula mbivu mzee"

"Sio kihivyo" wakaendeleza mjadala huo huku hakuna hata mmoja aliyesaliti mazoezi hayo na kujikita katika maongezi



*****

Kipande cha video kilichorushwa kupitia katika vituo vyote vya runinga ikiwaoneshwa watekaji waliowateka mabinti wa wawili pamoja na mlinzi wao iliwaacha hoi sana watazamaji.Raisi nae alipoiona video hiyo alihisi kupagawa kwani tu kamwe watalaamu wa kompyuta hawakuweza kabisa kugundua sehemu ambayo watekaji hao wanapatikana.



Kwa upande wa James Goba na wenzake walimshikulia Rayana huku akimpa adhabu kali wakimtaka ataje wapi walipo mabinti hao lakini ukweli wake ulisimama palepale kuwa hakujua chochote kinachoendelea.

Kosa!



Wakaanza kumpatia kisago cha uhakika mpaka alipolegea kabisa.Wakafungua chumba kidogo na kumtupia kisha wakarudi na kuketi kwenye sofa.Wakawa wanajadili na kutafakari nini wakifanye mpaka msichana huyu aweze kueleza ukweli bayana.

"Unajua kaka Goba hawa watekaji kamwe hawawezi kutaja sehemu ambayo walipo na ni ngumu sana!,sijui wamelishwa kidudu gani hawa" mmoja wao akahamaki kwa jazba.

"Wanawake wauaji sana hawa!" Goba akafoka kwa hasira.Akachomoa simu yake na kuipiga.Ni Aidan anayepigiwa ambaye ameachiwa huru mara baada ya kumtaja mmoja wa wahusika.

"Dogo mbona kiumbe chenyewe hakiongei ukweli?" akauliza Goba na Aidan akajibu kwa sauti ya kubabaika

"Huyo nunda kaka we mtembezee mkong'oto kwanza atataja tu" Aidan akamchoma tena Rayana kwa mara ya pili.Simu ikakatwa na ukimya ukatawala kwa dakika kadhaa.Wazo jipya likaingia kichwani mwa jamaa mwingine.

"Tumefanya makosa kumuachia huyu dogo,itakuwaje anamtaja huyu demu kajuaje?...itakuwa na yeye anahusika kwa namna moja ama nyingine na yeye tumfinye aseme ukweli unaoeleweka" Jamaa huyo akatoa cheche za maneno yaliyoanza kuwakuna Goba na mwenzake.Kuna kitu kipya wanakiwaza na baada ya sekunde chache Goba akaja na maneno mapya,maneno ya kuafikiana na maneno ya jamaa aliyenena maneno ya kumfanya Goba aafiki.

"Naaam!" James Goba akatikisa kichwa chache na kukubali maneno hayo " Hebu nipige simu nimuite" Goba akasema.

"Mmmh unadhani atakuja tena yule jinsi tulivyomfinya?" Jamaa mmoja akauliza.

"Subiri natumia ubongo wangu uliodumu kwenye siasa kwa miaka sita sasa" Goba akajitamba kwa maneno yake kuntu.Akaichomoa simu kwa mara ya pili tena akaipiga namba ya Aidan.

"Ayaaaaaaaaaaaaah!" Goba akajikuta anajipiga konde la kichwa kama mtu aliyechanganikiwa.

"Vipi mkuu?"

"Hapatikani"

Wakapigwa na bumbuazi kwa dakika kama tano kisha wakaendelea kumjadili Aidan juu ya watu anaowataja! Kwa nini asiwemo na yeye katika hilo.

"Ndugu zangu tufanye kweli ili tufakinishe hili la sivyo mshahara wetu utapungua mno kutokana tu watu hawa wanahitaji pesa ili kuwatoa mabinti hao"Goba akashauri

"Lakini si kuna shirika la kijasusi limetumwa liperereze jambo hili?"

"Majasusi ni wao kivyao na sisi kivyetu,hebu fikiri kama tukimpata Dayana unadhani tutalipwa shiling ngapi au tutavishwa cheo gani kule White House?" Swali la James Goba likawapa tabasamu wawili hao na hapo ndipo bongo zao zikaanza kuchemka kwa kasi.



*********

********

Video fupi ya watekaji haikuteka akili ya raisi peke yake bali hata mtu anayependa usawa na haki siku zote anayeitwa Geza Ulole alipatwa na mshangao kidogo huku akijiuliza ni raia wa nchi gani mwenye sura mbaya kama ile.

"Mmmh si heri mimi nimependa kuliko huyu Jinamizi!..." Akazungumza peke yake huku akitabasamu.Sura ile ya jamaa aliyeonekana kwenye ile video fupi iliyowaonesha mabinti wa raisi ilimfurahisha sana sio tu kwa kifurahia ule utekaji la hasha! ni jinsi sura lile la jamaa lilivyochongwa vibaya na kuifanisha kama sura ya beberu linusalo haja ndogo.Lile kovu lake na weusi ukawa unamfanya Geza atabasamu kila wakati.Ghafla Geza akaingiwa na ghadhabu na hapohapo akaacha kucheka na kutabasamu,sura ya hasira dhidi ya yule jamaa aliyemuona kwenye video fupi.

Wakati anaendelea kugonganisha mawazo kichwani mwake akahisi kuna kitu kinalia,akatulia kwanza kimya huku likitazama sehemu inayolia.

"Nini hicho?" Akajiswalika na swali lisilo na mjibuji "ahaaaa hahaha kumbe unagongwa mlango" akazungumza huku akicheka kicheko chepesi.Akainuka na kufuata mlango.Sura ya kijana Swedy ikiwa katika taharuki na huzuni,ikamlaki Geza Ulole aliyekuwa ametimkiwa na unywele uliosaliti kichanio kwa muda mrefu,macho yake yalioiva na kuwa mekundu yakamtazama Swedy na mdomo wake ukapiga konde na kumtwanga swali Swedy.

"Vipi dogo umekuja na shari hivyo?" Geza akauliza na Swedy akatiririka kujibu kama atakavyo Geza.

"Kaka kuna tatizo limetokea" Swedy akazungumza kwa uchungu.Alichokifanya Geza ni kumkaribisha kwanza swedy ndani.Wakaketi kwenye meza kuukuu iliyo katika chumba cha Geza.

"Hebu niambie kuna tatizo gani dogo?" Geza alitupa swali lingine kwa Swedy linalohitaji majibu yaliyoshiba na ndio dhumuni kuu la Swedy kufika nyumbani kwa Geza Ulole.



Swedy akapiga chafya ndogo kisha akavuta pumzi na kuzishusha.Sasa yupo tayari kwa kutoa mfafanuzi wa tatizo.Katika maelezo yake akajikuza zaidi kuelezea jinsi wazazi wa Rayana wanavyolalama siku ya tatu sasa hawajamuona Rayana nyumbani kwao.

"Hofu yangu kubwa atakuwa amefariki maskini Rayana" Swedy akafafanua.

"Kwanini una hofu kama hiyo?"

"Kwa sababu siku chache zilizopita yule binti nilimkuta analia,nilipomuuliza nini kimemsibu akanijibu kuna watu wanamkimbiza wamuue" Swedy akaelezea kila kitu kilichompata Rayana.



*****

Noel Mkwakwacha pamoja na raisi mwenzake hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na mateka kulipa kiasi kile cha pesa.Japokuwa kilikuwa kiasi kikubwa lakini hawakuwa na budi kulitekeleza.



"Lakini sio kirahisi namna hii.Kama kulipa tulipe kwa shida" mshauri mkuu wa raisi akatoa wazo.

"Kwanini?"

"Pesa nyingi sana hizi mheshimiwa eeh lazima tuhakikishe tunalitatua hili suala" mshauri huyo akaongea mengi huku akisisitiza kutolipa pesa kwa jamaa hao.

"Kwa hiyo tunafanyaje?" Akauliza.

"Niachie mimi na Kabneti yangu nitamaliza hili tatizo" akazungumza mshari wa raisi bwana Noel Mkwakwacha.

Kazi ikakabidhiwa kwa mshauri huyu wa raisi anayeitwa George Mbasho.Mfupi kiasi mwenye ngozi nyeusi kabisa,ndefu zake za juu zilizorefuka sentimeta kadhaa kwenda mbele na kutengeneza Mustachi,chini ya kidevu chake kuliambatana na ndevu ndogondogo ambazo zilichanganyika na vijipere vidogo vidogo vilivyotokana na ukwanguaji wa ndevu hizo.Vazi la suti alilolivaa lilimpa heshima kubwa hata kama akitoka nje ya ikulu bado watu watatambua kuwa lazima mtu huyu atakuwa ana wadhifa fulani katika serikali.Akatoka pale kwenye meza na kuwapisha maraisi hao walio katika simanzi la kutekwa kwa mabinti zao.Moja kwa moja akaingia kwenye gari yake na kutoka nalo mpaka alipofika kwake masaki.Akaingia ndani na kulakiwa na familia yake kama ilivyo kawaida yake ya kila siku.Akachana na familia,akaingia chumbani kisha akabadilisha nguo zake na kuingia bafuni,alipomaliza kujimwagia maji na uchovu wake uliomkaba hapo awali ukawa umepunguzwa kwa kiasi kikubwa sana.Sasa amepata nguvu mpya.

Akalifungua kabati lake na kutoa kijibegi cha wastani,akaitoa lap top yake na kuiwasha.Akaingia moja kwa moja mpaka kwenye mtandao huitwao Skype kisha akabonyeza 'button' na ndipo alipotokea jamaa mmoja wa kizungu.Walizungumza kiingereza kukidhi mawasiliano yao na baadae wakamalizana kabisa.Akaufunga mtandao huo na kusimama kisha akatoka nje.



________________

SIKU MBILI MBELE KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA MWL JULIAS NYERERE DAR.



Ndege kubwa iliyo na chapa kubwa ya kampuni yao ikawa inapiga kelele nyingi haswa.Ni kutokana na kuwa karibu sana ardhi ikiashiria kuwa ni zamu yake ya kutua katika ardhi iliyo na amani ya nchini Tanzania.Baada ya ukelele wa dakika kadhaa hatimaye ndege hiyo ikathubutu kugusa ardhi kwa tairi zake za mbele na kumalizia za nyuma,ikaanza kukimbia kwa kasi lakini kadri sekunde zilivyoyoyoma ndipo ndege ile ikawa inapungua kasi yake mpaka iliposimama.Mlango mkuu uliofunguliwa tu,abiria mmoja mmoja akaanza kuchomoka na kutoka ndani ya ndege hiyo.

Bwana George Mbasho pamoja na vijana wake watatu walikuwa uwanjani hapo wakimsuburia kuwa mgeni wao aoneshe tu pua yake ili wampokee na kuondoka naye.Kichwa cha George Mbasho kilikuwa na kazi ya kuhesabu abiria watokao kwenye ndege kama mhudumu afanyaye ukaguzi uwanjani hapo.Hakuwa anahesabu abiria ili ajue idadi yake hapana! alihesabu abiria ili aweze kumnasa mgeni wake kwa urahisi sana kwani kuhesababu watu ina maana kuwa lazima upitishe macho kwa kila mtu unayemuhesabu.Kama yalivyo mahesabu yake.Jamaa mmoja wa kizungu aliyekuwa na ndefu nyingi kiasi kwamba zingine zilijazama shingoni.Pua yake ilichongoa na kuwa ndefu zaidi huku chini yake kulikuwa na ndefu almaarufu kwa jina la mustachi zikiyakinga matundu ya pua yasishambuliwe na vumbe au wadudu wadogo wadogo.Kofia yake ya Pama iliyokuwa na uzi uliopita chini ya kidevu chake ukijaribu kuingiza kofia hiyo isipatwe na dhuruba ya kupeperushwa na upepo kwa hilo ulifanikiwa kwani haikuwa na dalili ya kuanguka kabisa.Mzungu huyo ambaye alivaa shati laini,lilionekana likipepea na kujidhihirisha ulaini wake,alivalia pensi ya jinzi.

Akaanza kushusha ngazi taratibu huku akitazama huku na kule mpaka alipoikuta sura ya mwenyeji wake akiwa anampungia mkono.Akachomoka mpaka kwa George Mbasho.Hawakupoteza muda,wakaingia garini na safari ya Masaki kwa George ikaiva.



Mzungu huyo aliyefahamika kwa jina la Alexnder Bulton,mtaalamu wa masuala ya kompyuta atokae Urusi.Amealikwa na George Mbasho katika kazi maalumu ambayo atakabidhiwa.Alexnder Bulton ana sifa kadha wa kadha za kufichua siri zilizojificha katika mtandao akitumia programu yake aliyoitengeneza kwa akili yake.Anatumia masaa mengi sana kucheza na kompyuta akigundua njia mbalimbali za kunasa uharifu au mambo yaliyofichwa na sio rahisi.Huko kwao Urusi aliweza kujua kiasi cha fedha katika mabenki.Aidha mtu huyu alifanikiwa kuiba pesa kutoka katika moja huko Urusi akitumia programu yake hiyo na bila kutambulika.Leo ameingia Tanzania akiwa na kazi moja tu,kuwagundua watekaji wa mabinti wa raisi Dayana na Mercela.

Wakafika Masaki katika nyumba ya George Mbasho na mikakati madhubuti ikaanza kufanyika kwa haraka.Cha kwanza kukifanya Alexnder Bulton ni kuitoa mashine yake na kuipachika chaji,akakitoa kifaa kingine ambacho hata mmoja hakuwahi kukiona kabisa,ni kifaa kidogo lakini kiliwastaajabisha wakina George.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

*******

Harakati na juhudi za kuwaokoa mabinti hao kamwe hazikusimama hata dakika moja.Kila wakati unavyozidi kwenda ndipo mbinu na hisia mpya zikawa zinakuja vichwani mwa wahusika wa mabinti hao.Kama ilivyokuwa kwa James Goba pamoja na wenzake,waliendesha upelelezi wa chini kwa chini.Walihisi kuna vitu vinaelekea kuwa na uhusiano mkubwa na utekwaji wa binti.Ni kutokana na Aidan kuhisi watu mbalimbali.Siku hiyo waliamua kumsaka Aidan kwa uwezo wao wote ule.Walitumia siku mzima kumtafuta katika sehemu anazopenda kuwepo lakini wakamkosa.Baada ya kuwaza sana James Goba akaja na wazo la kumtumia msichana kuongea nae ili waweze kimnasa vizuri japokuwa hawakuwa na uhakika wa asilimia mia lakini walijipa moyo.



"Sijui kama tutamnasa huyu.Inawezekana kakimbia mji huyu" Jamaa mmoja akanena na kuwafanya wenzake wamtazame kwa dakika chache kidogo.

"Hapana mi naona tujaribu kwanza hii njia aliyosema Mkuu hapa,tumtumie msichana kwanza" jamaa mwingine akadakia na kutoa simu yake kisha akashuka ndani ya gari.Akawa na kazi ya kuwasimisha wasichana wapitao kando yake.





Uelekeo wa macho yake yakafika katika ukingo wa sura msichana aliyekuwa katika mwendo wa upole.Akachukua jukumu la kumuita na bila ajizi msichana huyo akasogea huku akiwa katika mshangao.Jamaa huyu akamsalimia msichana yule na kumueleza shida yake.Baada ya mwanamke huyo kukubali wakaingia garini na kukabidhiwa simu iliyokuwa na namba ya Aidan.Uzuri wa msicahana huyo alikuwa na sauti laini,sauti ambayo ingelikuwa chanzo kikubwa cha mvuto kwa msikilizaji yeyote wa kiume atakayekabiliana na sauti hiyo.Kama ilivyokuwa kwa Aidan kwani baada ya kusikia tu sauti ya kike toka upande wa pili akajikuta anapatwa na msisimko wa ajabu.Hapo ndipo akipoanza kufunguka.

"Nimesikia sifa zao sana my hapa nilipo natamani kukuona mno Aidan" msichana huyo akaendelea kumsomesha Aidan ambaye kwa muda huo alikuwa amelewa kabisa na sauti ile itokayo puani.

"Napenda sana kifua chako hasa ile picha yako ya profile ya whatsap..." Sifa kemkem zikamtoka msichana huyo kuwa kama aliwahi kumuona au hata kumsikia Aidan walau siku moja lakini kiukweli hakuwahi kumsikia kabisa mtu anayeitwa Aidan.

"Naitwa Veronica" msichana huyo akalitaja jina lake,ni wazi Aidan alitaka kujua jina la msichana huyo.Alipomaliza kuongea Msichana huyo aitwaye Vero akatolewa maelezo juu ya yale yaliyosemwa.

"Amesema anataka kuniona kwanza!"

"Haina shida ndio tunachokitaka,hebu tupe namba yako ya simu ili iwe rahisi zaidi kutujulisha" Veronica akazitaja namba zake na kupewa pesa taslimu shilingi elfu sabini kama pesa ya vocha ndivyo alivyozungumza James Goba.

Gari yao ikageuzwa haraka na kuanza kuelekea makao yao huku kila mmoka akiwa mwenye mawazo mengi sana juu ya lile suala.

Walipofika tu katika hiyo nyumba moja kwa moja wakaingia chumbani.Chumba alicholazwa Rayana.Wakamkuta amelala kabisa huku macho yamemtoka,hayakumtoka kwa ukodoaji macho La hasha!,ni vile viini vyeusi havikuonekana kabisa.Damu iliyotapaa pale chini ikawaogopesha sana kupita maelezo.Kila mmoja alicjanganyikiwa huku kesi ya mauaji ikigonga na kurudi katika bongo zao.

Maskini Rayana..

Alikuwa amekakamaa pale chini sakafuni hajitambui kabisa,sijui kakutwa na kitu gani masikini.

Mioyo ya hawa majamaa ikaanza kuwapitwa kwa kasi wasiamini kama kweli msichana yule wanaomdhania kahusika katika utekwaji wa Dayana huko njia ya Bagamoyo.

"Eeeeh kakufanye huyi!!?" James Goba akauliza kwa jazba huku akiwatazama wale jamaa wenzake kwa mshangao.

Kilikuwa kitendo cha kuogofya kabisa mle ndani.Hawakutaka kuugusa mwili ule badala yake yake wakawa wanatazama kila kona ya chumba kile.Mara ya kwanza hawakuona kitu chochote ambacho kingeweza kumfanya binti huyo awe katika hali ile ya uvujaji damu.

Nini sasa huyu!

Alam ya hatari ikaanza kugonga kichwani mwa James Goba na hapo akasogea karibu na mwili wa Rayana pale sakafuni na kuutazama kwa umakini sana.Ndipo alipogundua kitu kipya,kitu ambacho kilimfanya ainuke kwa kasi na kuwatazama wenzake mara baada ya kumguza kifuani.



_____________



Nyumbani kwa mh.George Mbasho,mtaalamu wa kompyuta kutoka Urusi bwana Alexnder Bulton aliendelea na kazi.Kazi ambayo kwake haikuwa ngumu sana kutokana tu na uwezo wa vifaa vyake pamoja na utaalamu aliokuwa nao.Sasa walikuwa sambamba mezani kati yake na George Mbasho.Waliketi hapo huku Alexnder akifanya yakd katika kuhakikisha anainasa ngome ya waasi hao wabaya wenye uthubutu wa kuwateka mabinti wapendwa wa Maraisi.

Kazi ilikuwa pevu!

Alexnder akavuta kitambaa cheupe kilicho pembeni yake na kujifuta lile jasho jembamba lililompa shida usoni kwake kisha akaendelea.

Kwenye kioo cha kompyuta yake kulitawaliwa na ramani ambapo sehemu ya ramani hiyo iliandikwa kwa herufi kubwa BAGAMOYO.Akaendelea kuidadavua eneo lile huku akitumia ujuzi wake katika kazi hiyo.

Akakohoa kidogo na kuacha kubofya ile kompyuta,akachukua glasi ya maji na kujimiminia kisha akageuza sura yake na kumtazama George aliyeonekana wazi kitofahamu nini kinaendelea mbele yake.Wakatazamana ma wote wakatabasamu.

"Are you ok George?"mzungu huyu anayeutwa Alexnder Bulton akazungumza kwa bashasha,George akajibu..

"Yeah i'm ok"

"Worry out my brother"

Kazi ikaendelea pale mezani.Akawa anabonyeza tena zile "Keypad" na hapo ndipo alipocheka kicheko cha furaha kisicho na sauti.George Mbasho alipoona hivyo akatabasamu na yeye halafu akatupa swali kwa mtaalamu huyu wa kizungu.

"Are you ok?"

"Catch!" Akazungumza Alexnder Bulton kwa furaha.George Mbasho akaachwa njia panda asijue pa kuanzia kumuuliza tena kulikoni ucheko mwingi namna ile?

Kuna kitu kipya nini?

Sasa si angelisema hapahapa?

Akaacha kuwaza hayo akaendelea kumtumbulia macho tu jamaa huyu mcheka peke yake.



Baada ya dakika kadhaa Alexnder akaanza kufafanua kitu alichokigundua kwa wakati ule.Ndipo George alipomakinika kwa maneno yale ya Alexnder Bulton,gwiji la kugundua vitu vilivyofichwa kwa njia ya mitambo akitumia programu yake mahususi isiyokuwa na utambuliko wa watu.



Alexnder Bulton alizaliwa mwaka 1965 nchini Ufaransa katika hospitali moja kubwa nchini humo.Alizaliwa akiwa na kilo tano kitu ambacho kiliwapa furaha sana wazazi wake ambao kwa miaka hiyo walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja katika kitengo cha mawasiliano.Walikuwa wajuzi wakubwa sana kitu ambacho kiliwapa sifa kubwa na uaminifu kazini kwao kiasi kwamba kampuni hiyo iliwazawadia,wakapandishindwa mshahara pamoja na makazi yao kubadilishiwa.

Miaka mitano baada ya kufunga ndoa waliingiwa na simanzi kubwa sana,simanzi ambalo hawatokaa na kulisahau katika maisha yao.Mke wa Bulton alipatwa na maswaibu ambayo yalimfanya ajisikie mnyonge na mtu asiyekuwa na mafanikio katika maisha yake japokuwa aliishi katika Maisha mazuri na yenye thamani ya juu.Kisanga cha kumpoteza mtoto wake mpendwa ambaye alifariki masaa machache tu baada ya kuzaliwa.Hawakuwa na budi na kukubaliana na hali kama hiyo kwani tu ni mipango ya Mungu na siku zote haina makosa.

Iliwachukua miezi mingi sana mpaka kuja kusahau matatizo yaliyokawaandama hapo awali.Wakapiga moyo konde na kuendelea na maisha yao huku akifanya kazi kwa juhudi mno.Kama ilivyoada Mungu hamtupi mja wake.Mke wa Bulton akashika Mimba kwa mara ya pili,mimba ya miezi mitatu.Hakika furaha yao ikawachunua tena.Furaha ambayo ilikosekana kwa muda mrefu mara baada ya kisanga kile cha hapo mwanzo.Wakapendana sana,Bulton Gheikan akaapa kabisa kuitunza mimba ile pamoja na kumtunza mke wake.Bahati mzuri mke wa Bulton Gheikan akapatiwa likizo ya kujiangalizia mimba yake katika kampuni ile.

Kitu kimoja tu ambacho alikifanya Bulton Gheikan kwa mke wake,alikuwa akirudi tu kazini kwake humchukua mke wake na kumfanyisha mazoezi madogomadogo ili tu amjengee uimara pamoja na kuijenga afya ya mtoto aliye tumboni.vyakula vyenye ujengefu mwilini vikachukua nafasi yake katika nyumba hii ya Bulton.Alisimamia kila aina ya mapishi nyumbani kwake.



Siku hazigandi na mshale wa saa haurudi nyuma.Usiku wa saa sita Mke wa Bulton akiwa amejulaza kitandani huku mume wake akiwa hajielewi kabisa kutokana na usingizi mzito uliochanganyika na uchovu.Akaanza kuhisi tumbo linamsokota huku kitu kama uchungu kinamjia kwa mbalii.Alichukulia kawaida kwa dakika kumi za mwanzo lakini ghafla hali ile ikazidi.Akaanza kulalamika huku akimpiga mume wake makofi ya kumuamsha.Bulton Gheikan akainuka kwa kasi na kuiwasha taa yake ili amsaidie mke wake.Kwa kuwa ulikuwa usiku sana hakufanya ajizi kabisa,akaikimbilia simu yake ya mezani na kuwa kuwapigia wahusika wa hosptali ya kati iliyo katikati ya mji nchini humo.Kweli ndani ya dakika chache king'ora cha gari la wagonjwa kikaanza kulia nje ya mjengo wa Bulton Gheikan.Akakimbia haraka na kuwafungulia mlango na wauguzi wanne wakaingia ndani wakiwa na kitanda chenye magurudumu.Ndipo walipomuweka Mke mpendwa wa Bulton Gheikan juu ya kitanda na kuanza kukivuta hadi ndani ya gari hili la wagonjwa.

Majira ya saa nane na nusu usiku ndipo mke wa Bulton akajifungua mtoto wa kiume,mtoto aliyekuwa na uzito wenye shehena kubwa ya uzito katika mwili wake.Bulton hakutulia kabisa nje ya hospitali ile,kila muuguzi aliyepita alikuwa harali yake kumuuliza kuhusiana na maendeleo ya mke wake.

Maskini mke wangu sijui atakuwa katika hali gani huko?

Sijui ndio itakuwa kama awali....eeeh Mungu naomba uniepushe na haya maswaibu..

Mawazo hasi na chanya yenye kila aina ya viulizo ndani yake.Hapo ndipo alipomuona daktari ambaye alikuwa akimshughulikia mke wake.Alikuwa harali yake,akamvamia na kumshika koti lake kwa nguvu huku akimtolea macho kama tumbusi.

"Dokta niambie sasa hivi na usiniambie kama mke wangu hajajifungua salama dokta talk to me....." Bulton Gheikan alihamaki kwa hali ya juu.Alipaniki kwa sababu alimpenda sana mke wake.Daktari huyu akamshika mabegani Bulton kwa upole na kumtumbulia jicho la unyonge hali ambayo ilimpa wasiwasi mkubwa sana Bulton.Hata hajasema kitu chochote ndipo waliposikia sauti,sauti ya kilio.





Sauti ambayo ilimfanya Bulton Gheikan aliachie koti la daktari.Akamtengeneza vizuri kora na kumtazama kwa umakini huku mikono yake akiwa ameifunga mbele kama mkasi.

"Dokta pole sana,ehee hiyo sauti ndio mtoto wangu au?" Gheikan akauliza kwa utulivu mno kama sio yeye aliyekuwa akitia vurugu kwa daktari aliye mbele yake.

'Usijari njoo umtazame mwanao!" Daktari akasema na kuelekea chumba alicholazwa mke wake,naye Bulton Gheikan akafuata nyuma kwa kasi kosakosa amgonge daktari kwa nyuma.

Sura ya mke wake ilikuwa pale kitandani ikiwa na tabasamu hafifu kwa uchungu uliokamuwinda kwa muda mrefu sana,sasa haupo tena.Pembeni yake kulikuwa na mtoto,mtoto wa kiume ambaye alinenepa kwa kiasi kikubwa sana,Bulton Gheikan hakuamini kabisa akaruka juu na kuyakita magoti yake chini kwa nguvu bila ya kuyajari maumivu yaliyompata kwa wakati ule.Akanyoosha mikono juu na kumshukuru Muumba kwa muujiza ule aliouonesha kwa mke wake.Akasogea na kumuinua mtoto wake.Kisha akazungunza maneno machache kisha akamtazama mke wake.Wakatazama na kukumbatiana kwa furaha.

Ndipo maisha ya Alexnder Bulton Gheikan ikawa imeanza rasmi hapa duniani.Wazazi wake wakamtumza vizuri sana huku wakimtimizia kila kitu alichokihitaji.Akiwa na miaka kumi,Bulton Gheikan akawa anamkalisha chini na kumuelekeza mambo mengi kuhusiana na kompyuta.Akiwa na miaka kumi na nane alishamaliza masomo yake ya ngazi ya kati nchini humo huku akiwa maarufu mkubwa sana shuleni kwao kwa utumiaji wa kompyuta.Aliwashindwa hata baadhi ya waalimu wa kompyuta,Alexnder alikuwa mtu wa ajabu sana.

Pigo!

Pigo kubwa likachukua nafasi kwa mara ya kwanza kwa Alexnder Bulton Gheikan akiwa na miaka ishirini tu.

Ilikuwa kama saa sita kamili za mchana,mama na baba yake Alexnder akiwa wanatoka kazini kwao kuelekea shuleni anakosoma mwanao.Wakiwa ndani ya gari moja wapo lililo zuri na lenye thamani ya hali ya juu,ndipo walipogongana uso kwa uso na gari kubwa iliyobeba taka toka mjini.Dereva wa lori hilo alikuwa katika mwendo kasi sana kiasi kwamba alishindwa kuulimili msukani wake na kujikuta akilivaa gari la Bulton Gheikan.Hapohapo likabetuka na kurushwa kando ya barabara likiwa limejifunika.

Kifo!

Kifo kikawachukuwa wanafamilia hawa aliokuwa katika kiini cha furaha kwa kipindi kile,sasa furaha yao ya duniani ilikwishatoweka ghafla.

Alexnder alilia sana tena sana.Ukurasa wake wa peke yake katika nchi ya Ufaransa ikaanza lakini haikudumu hata kidogo.Shule ikamuwia chungu kabisa,akawa haendi kabisa.Mawazo yake yalikuwa ni kuhama na kwenda mbali na nchi hiyo.

Siku moja akiwa nje ya nyumba yao upweke ukimtawala,magoti yake yalikuwa sawa sawia na kidevu chake kilichoegemezwa juu ya magoti yake.Akainuka na kuingia ndani chumbani kwake.Akatoa albamu yake ya picha na kuanza kufunua picha moja badala ya nyingine,ndipo akakutana na picha ambayo ilimtoa machozi upya.Picha hiyo ilipigwa wakati Alexnder akiwa na umri wa miaka mitatu tu.Alishikwa na baba yake kipenzi ambaye ametangulia mbele ya haki huku mama yake akiwa ameachia tabasamu la nguvu sana.Machozi yakamtoka kwa wingi.Akapita haraka pichani hapo na kufungua kurasa nyingine na kukutana na picha ya Bi kizee aliyefanana sana na sura ya baba yake.Akaitoa kutoka sehemu ile na kuitazama kwa umakini.Akaigeuza nyuma na hapo alipoyakuta maandishi yenye kuelezea ile picha. " ....My Mother 12/september/1941 RUSSIA." maandishi yakasoma namna hiyo huku akitoa ufafanuzi wa picha hiyo kuwa ilipigwamiaka hiyo na kuhifadhiwa.

Hakuwa na budi ya kuachana na jiji la Ufaransa na kumfuata bibi yake huko Russia kwani upweke ulimzidi sana.Kwa kuwa aliachiwa pesa nyingi sana katika akaunti ya wazazi wake akafanikiwa kupata Visa pamoja na hati zote za kusafiria.Katikati ya juma akawa amepanga mizigo yake na kwenda moja kwa moja uwanja wa ndege na kuchukua usafiri utakaomfikisha huko kwa bibi yake.

Mungu akampa njia nyoofu,akafanikiwa kumpata bibi yake.

Maisha yakaanza upya huko akiwa anajishughulisha na utengenezaji wa kompyuta za watu na hatimaye akakubalika na makampuni mengi sana yaliyohaidi kumlipa pesa nyingi sana.

Kuanzia hapo akawa mtaalamu wa kujitegemea nchini humo huku akiwa na utajiri wa kutisha kabisa.Akiwa na miaka arobaini na mbili akakutana na mtu mwenye asili ya Kiafrika aliyejitambulisha kwa jina la George Mbasho.Alikuwa akishugulika na shughuli za kiserikali kama kaimu wa balozi wa Tanzania baada ya balozi mkuu kufariki ghafla nchini humo.Wakafahamiana sana haswa ukizingatia Alexnder Bulton Gheikan ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta,alikuwa na kila sababu ya kujuana na George Mbasho kwani aliwahi kumfanyia kazi nyingi sana kule ubalozini.



Baada ya kutazama kwa makini wa aina yake Alexnder Bulton Gheikan akafanikiwa kuzijua code(namba za siri) za mtandao wa watekaji wa binti wa raisi.Akamtazama tena George Mbasho na kumtajia zile namba zilizo kwenye kioo cha kompyuta yake japokuwa George hakuelewa zile namba anazotajiwa zina kazi gani,akatega sikio na kumsikiliza kwa umakini sana.

"Code number B27693-P29768-00 discovered area at outside Bagamoyo Block 246" Alexnder Bulton akazungumza kwa umakini sana bila kukosea zile namba na kuanza kuzitolea mfafanuzi wa kina na hapo ndipo George alipofunguka kichwa kutoka kwenye viulizo vya zile namba za siri(code).

Alexnder Bulton Gheikan akazungumza kwa lugja ya kimombo...

"Namba hizi za siri ni namba ambazo zinaonesha muelekeo wa hawa jamaa walipo na ngome yao pia,pia hii B mwanzoni mwa hizi namba zinamaanisha kuwa ni eneo lenyewe,linautwa Bagamoyo,umenipata sijui...." alexnder akazungumza kisha akatulia ili maneno aliyoyatupa yaingie vizuri kichwani mwa George.

"......hizi namba ukizitia kwenye GPS zitakuonesha kabisa eneo zima kwa uwazi kabisa na zitakucholea ramani za barabara zitakazowafikisha mpaka eneo hili." Akamaliza na kumtazama George ambaye hakuwa na lolote la kusema kabisa.

Alexnder Gheikan akabonyeza tena zile "Button" na picha za jumba kubwa ikaoneshwa pale kiooni.

Ndio yenyewe kabisa!

Nyumba ile ambayo ilikuwa imekaliwa na watekaki wakubwa wakiongozwa na Master killer(MK) kama ana anavyopenda kujiita.

Anajisifu kwa kuua...

Kazi ya Alexnder Bulton Gheikan ikaishia pale huku akisubiri donge nono kutoka kwa George Bulton.Safari yake ya kutoka Russia mpaka Tanzania.Kazi iliyokuwa mezani kwa wakati ule ilikuwa ni ya kumtia mikononi mtekaji.



___________http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Ukimya mkubwa ukakifunika chumba chenye mitambo mingi,chumba ambacho kilikuwa kinaashiria kabisa ni chumba cha wagonjwa.Kilikuwa kimepoa sana.Madaktari wawili walihangaika sana kujaribu kuinusuru roho iliyolazwa kitandani.Macho mgonjwa huyo yalikuwa yamefumba kabisa.

Huruma...

Kitanda kile kilichokua mle chumbani kilikuwa tayari kinahimili mzigo ulio juu.Mzigo wa mgonjwa aliyepiteza fahamu.Huyu huyu alikuwa ni wa kike mwenye ngozi nyeusi ya asili.Ripoti ya waketaji mgonjwa huyo haikuwa nyoofu zaidi ya kuelezea kuwa amekutwa ameanguka ghafla na kupoteza fahamu.

Rayana amepoteza fahamu zake na sasa ni saa ya kumi na tatu,kitu kilichomkuta chumbani kwa akina James hakikujulikana mpaka hapo mwenyewe atakapozinduka aeleze nini kilimkuta.

Lakini bado madaktari hawakuwa na matumaini kabisa ya kuuponya uhai kwani ile mashine kupumulia haikusaidia kwa kiasi kikubwa sana.Madaktari wakachanganyikiwa sana.Rayana akaanza kujinyonganyonga pale juu ya kitanda kwa shida sana,hakuwa tofauti na mtu ambaye anaelekea kutaka roho.

Aliogopesha mno...





Katika chumba kile alichofungiwa Rayana,kilitawaliwa na vitu mbalimbali isipokuwa kitanda.Hakukuwa na kitanda chumba hiki,mwanga wa taa ulikuwa hafifu wenye rangi inayofanana na kandili.Rayana akiwa analia machozi huku asiamini kama kweli mambo yote haya chanzo chake ni Aidan.Mwanaume ambaye alikuwa wa ndoto yake,mwanaume ambaye alidhani atakuja kuwa nae maisha yake yote.Aidan ameyageuza maisha yake na kuwa kitu kingine kabisa alisochotalaji.

Akiwa pembe mojawapo ya chumba kile huku kidevu chake amekiweka katikati ya magoti yake aliyoyakunja,mikono yake ikapita uvunguni mwa magoti haya na kujikunyata,machozi yalimtiririka mashavuni pamoja na makamasi mepesi.Analia kwa uchungu sana.Baada ya kukaa pale chini kwa muda mrefu huku kila alipojaribu kuyawaza yale yanayomtokea bado hakupata muafaka.

Kuishi na ghasia kama hizi za maksudi haiwezekanani kabisa,ni kheri uepukane na hawa walimwengu tu..

Akajinyakua pale chini na kutazama tazama huku na kule.Akachambua viti vilivyo mle ndani kwa fujo mpaka alikupokuta bomba za sindano zipatazo sita mpya.Hakutaka kujua zina kazi gani alichokufanya yeye ni kuifanya kazi yake tu.

'Sipaswi kuendelea kuvumilia mateso haya ni bora niondokane hayo'

Akafikiria kwa dakika chache kabla hajaichomoa sindano moja kati ya zile sita na kuichukua chupa ya dawa ndogo..

Eeeh chupa ya supu!

Rayana anaitikiza ile chupa iliyokuwa na alama ya fuvu na mifupa (toxic) ikiwa kama ishara ya hatari kwa mtumiaji akiingiza kwenye mwili wake.Bila kujari kitu kama hicho ndipo alipoitosa ile sindano na kuinyonya simu ile kwa wingi.Akatazama juu huku akiomba Mungu ampokee vizuri yake.

Akajifinya mkono wake wa kushoto na msuli ukamtutumuka na kutokeza dhahiri.Akaitazama tena ile sindano ya sumu kisha akaipeleka pale mshipani kwa uchungu.Akawa anaisukuma sumu ile mpaka akafanikiwa kuifisha nusu,miguno ya maumivu ikamtoka na hapo hapo akaanza kuchezesha miguu yake kwa ghadhabu,sumu ikaanza kuingia mwilini taratibu ikianzia pale mshipa wa mkononi.Akainuka kwa tabu sana lakini akaonesha kutokuwa na nguvu kabisa.Akaanguka chini kama mzigo.Kilio cha kwikwi kikaanza kumtoka huku akilitaja jina la mama yake Bi Chiku.



Sura ya mdogo wake ikamjia kichwani ikiwa na tabasamu pana lenye uzito wa aina yake,isitoshe kuziona sura hizo za mama na mdogo wake lakini hata ile ya baba yake ikamjia pia.

Akajijuta akitumbua macho na kupiga yowe kali sana,alihisi kupona tena baada ya kuiona sura ya Swedy kichwani kwake ikimpa tabasamu murua halisi la mapendo.Akatahamaki na kuita jina la Swedy mara kadhaa akidhani kuwa anaweza kumsikia lakini ukweli kwamba zilikuwa hisia zake tu.Akajuta kuchukua uamuzi kama ule wa kujidunga sindano ya sumu kwa minajiri ya kuondoa uhai wake bila kufikiri mara mbili.

Ama kweli majuto ni Mjukuu...

Baada ya kujivilingisha pale chini kwa muda,akaanguka chini na kulala chali huku macho yamemtoka pinaaa!

Akavipigiza miguu yake sakafuni huku mikono yake ikiwa imeshika tumbo lake kwa nguvu,meno yake yakaumana na kutafunana kwa ghadhabu mno,ni wazi kifo kilianza kumjia na anachokifanya pale ni kupigana na hali ile kuinusuru roho yake isimuache mpweke.

Ndipo hapo sasa James Goba na wenzake walipoingia na kumkuta Rayana akiwa ameganda pale chini macho yakiwa wamemtoka,misuli ya shingoni imemtutumka na kuvimba kwa kiasi chake.Walionesha kupagawa sana na hapo James Goba alipoinama na kumshika Rayana kifuani na kugundua kuwa alikuwa katika hatua za mwisho sana kabla ya kuaga dunia,alipotazama pembeni yake akakuta chupa ndogo ya sumu iliyoambatana na sindano iliyokuwa na mabaki ya sumu ile.

Aaah!

Akahamaki kuona hali ile.Wakati James Goba anamgusa pale kifuani akashtuka kusikia mapigo ya moyo yakipiga kwa upole sana.

"Hajakufa huyu anapumua kwa mbali"

James Goba akazungumza kwa pupa muda huo huo wakambeba Rayana na kuingia nae garini.Safari ya kwenda hospitali ya taifa ikaanza mara moja.



…..

Daktari mmoja aliyehusika na chumba kile alicholazwa Rayana kilichoandikwa ICU kwa maandishi yenye mng'aro akatoka nje na hapo akavaana na maswali mengi toka kwa James Goba na wenzake.Pupa zikawajia juu na kutaka kufahamu nini kinachojiri.Wakaitwa na kuingia ofisini kwa dokta huyo.

"Kwanza kabisa niwaulize swali.." Daktari akazungumza huku akikabiliana na sura za wale watu watatu ambao ni James Goba na wenzake wawili.Wakatazama na kutikisa vichwa vyao kwa pamoja wakiafiki kauli ya daktari.

"Kwanini huyu binti amekutwa na hili tatizo?" Akauliza na kwa mara nyingine wakatazamana tena.

"Aaah tumemkuta tu ghafla ameanguka sa..sa hatujajua amekutwa na kitu gani dokta.." James Goba akazungumza kwa papara.

Daktari hakusema kitu chochote kwa maana kuwa alitambua fika kuna kitu wanaficha,vyuso zao zilizo na wasiwasi zingelimfanya mtu yeyote kuwagundua kuwa hawapo sawa kwa muda ule.Daktari akawazama na kuwaambia..

"Mgonjwa wenu amejidunga sindano yenye sumu kali na kama msingelimuwaisha mapema hapa kwetu angelikwishapoteza maisha kabisa...kwa sasa tunaendelea na matibabu ma bado yupo ICU amezimia...." Daktari akazunguma na kuweka kituo kisha akawatazama tena wale jamaa.

Hawakuwa na jibu.

Wakamalizana na kutoka nje ya ofisi hii ya daktari.Kitu kilichowaumiza kichwa endapo Rayana akifariki.

Watakuwa katika kundi gani?

Hawakujua Rayana hana hatia kabisa na lile swala la kutekwa kwa Dayana au ni maamuzi yao ya pupa bila kufikiria?

Walipotoka nje na kuendelea kuwepo pale nje mara wakagongana macho na jamaa mmoja wasiyemjua kwa jina,sio mara ya kwanza,aliwatazana kabla ya muda huo alafu akigundulika kuwa anawatazama huwa anakwepesha macho na kuyaelekeza kwenye simu yake.Jamaa huyo alifanya hivyo kila muda pasi kuonekana na wakina James Goba.

Wakahisi kitu fulani.

"Huyu jamaa mbona anatutumbulia mimacho sana?" Jamaa mmoja akazungumza kwa mshangao huku akitupa macho yake kwa yule jamaa ila wenzake hawakujari hata kidogo,walikuwa bize na mambo yao.

Naye akaamua kutomtilia maanani.

Wakaketi pale kitini.

"Unajua hapa tunaharibu muda wetu bure kwa sababu ya huyu mwanamke,hivi ni upumbavu wa aina gani huu?" James Goba akaliacha swali lake lielee vichwani mwa wenzake.

Wakatazamana tena kwa pamoja ila hawakuongea kitu kabisa.

Mara akaingia mtu.alikuwa na hofu kubwa mno huku akitazama huku na kule kama mtu aliyekuwa akikimbizwa na sasa amekuta njia panda na kujiuliza wapi aelekee.Kijana wa makamo kabisa,alipotazama kwa makini eneo lile ndipo alipomuona.Alimuona yule jamaa aliyekuwa akiwatazama wakina James Goba pale pembeni.Akaanza kuzivuta hatua ndefu kuelekea eneo hilo huku jasho likimtiririka.

"Ehee niambie jamaa Rayana yupo wapi?" Jamaa huyo akauliza kwa jazba sana.

"Tulia basi Swedy,ebu kaa kwanza hapa usiwe na papara" akazungumza jamaa yule mtulivu kwa utulivu sana.Akaketi na kutazama na wale akina James Goba.Baada ya dakika tano tu wakina James Goba wakainuka na kutoka eneo lile kwa kasi sana,walipofika kwenye maegesho wakaingia garini mwao na kutimua mbio sehemu isiyofahamika.

Wakabaki yule jamaa mtulivu na Swedy pale hosptali.Ndipo walipochukua uamuzi wa kuenda kwa dokta na kuuliza kama kuna mgonjwa wa kike aliletwa pale hosptali.

Rayana ampata mkombozi.



__________



Bwana George Mbasho hakufanya ajizi mara baada ya kugundua ngome ya watekaji ilipo kwa kumtumia yule mtaalamu wa kizungu.Japokuwa alitumia pesa nyingi kumuita na kukamilisha kazi lakini kwa namna moja ama nyingine ingeliweza kurahisisha kazi hiyo.Kitu kilichomsaidia sana George Mbasho ni kufikiri,alikuwa tofauti na wenzake kama akina Goba ambao huendesha kazi yao kwa kufikirika pekee yake.George Mbasho ana kawaida ya kufikiria jambo mara tatu na kulitafutia ufumbuzi kabambe.

Ndio sifa ya muungwana.



IKULU

Wafanyakazi wa karibu kabisa wa Raisi,siku hiyo waliita kikao kikubwa cha kujadili suala hili la utekaji ambalo linawaumiza vichwa sana maraisi.George Mbasho ndiye aliyeitisha kikao hiko kifupi kama mshauri wa raisi.

Saa tatu na dakika zake kadhaa za asubuhi ndipo kikao kilipoanza na mikakati ya nguvu yenye mashiko ya hoja ikajadiliwa.

Bila kupoteza muda wao George Mbasho akakisema kile alichokigundua mtalaamu alexnder Bulton Gheikan.Ugunduzi huo ukapita na kupewa nafasi katika kikao hiko pamoja na askari kadhaa walichaguliwa wakishirikiana na jeshi la polisi kanda ya Dar es salaam ambalo liliendeshwa na RPC Crispin Yanke.

Safari ya kuelekea Bagamoyo ikitakiwa ifanyike haraka sana kabla ya hawa jamaa hawajafanya kitu chochote kabisa.Wakiwa wametulia katika fomu zao huku wakivuta umakini kwa maneno ya George Mbasho,wakati huo Televisheni inaonesha matangazo yake kama kawaida.Lakini umakini ule ulikatishwa ghafla.Hata mzungumzaji hakuongea tena zaidi ya kukodoa macho yake kwa mshangao sana.

Wakaitazama ile televisheni kwa muda haswa sio tu kwa matangazo yake La hasha! bali ni kutokana na ile video fupi.

Haikuwa video ingine bali ni ya ile ya wale watekaji kutoka Bagamoyo.Ilionesha jinsi watoto hao na mlinzi wao walivyokuwa wanateswa kufuatia na ucheleweshaji wa kukabidhi pesa.Mwisho wa video hiyo wakajikuta wote wanaziba mdomo wao huku kelele za woga zikiwatoka bila kutegemea.

Mlinzi ambaye aliwekwa mbele ya kioo huku akiwa anavuja damu kwa wingi usoni,akatandikwa ngumi la nguvu na yule jamaa anayejiita MK kisha akachukua bastola na kuikoki,kabla hajairuhusu akazungumza kitu kwa msisitizo sana.

"Kuua kwangu ni jambo rahisi sana..." Akazungumza na kutulia kidogo "....kuua kwangu ni jambo dogo sana,kama mnawahitaji hivi viumbe vyenu viendelee kuishi basi fanyeni huo ujinga muufanyao" MK akajitutumua vilivyo na hapo akamalizia kwa kumtandika ngumi tena mzito yule mlinzi,ukelele ukasikika ukumbi mzima na hapo ndipo video ilipokata ghafla.

Huyu MK kajuaje kama kuna mpango wa siri?

Wakapuuzia ile video na kikao kikaendelea mpaka kilivyofika mwisho huku wakiwa wamekubaliana kabisa kuwa kutakuwa na kikosi cha anga pamoja na cha aridhini.

Kikosi hiko cha anga kitatumia helkopta za kivita kulizingila eneo hilo na huku kikosi cha ardhi kikitumia magari yenye kasi na uwezo wa juu.Hivi vyote viliendeshwa kwa umakini wa George Mbasho pamoja na RPC Crispin Yanke kanda ya Dar es Salaam.



MPANGO WA KAZI

Jua likazama na giza likachukua nafasi yake.Jiji zima liliongezeka hekeheka za watu zaidi tofauti na mchana.Hekaheka hizo zikawapa wakati murua wakina George Mbasho na wenzake.Walipanga kuvamia kambi ile usiku uleule wa manane,ramani na maelekezo aliyopewa George na yule mtaalamu Alexnder aliyafikisha mezani sasa na RPC akawa anaifanyia kazi kwa umakini mno.Mpaka wanakuja kukamilisha mipango ilihitimu saa sita za usiku na wakawa tayari kwa kila jambo.Gari zipatazo tano zilizojaa askari wenye silaha mzito zilipaki nje ya ikulu,wakati huo helkopta kama mbili zilikwishakuwa angani zinatalii anga ya Dar tayari kwa ukombozi wa binti wa raisi.

Ilipohitimu saa saba wakaanza safari huku wakitokea pale ikulu.

Kazi imeanza kwa kishindo na lengo lao kuu ni moja tu ni kumkomesha MK anayesadikika kumteka binti huyo bila kujua mipango hiyo inafanywa na Inspekta mkubwa wa jeshi la polisi wa Dar es salaam.





Gari ya kwanza ilikuwa na askari wanne wenye silaha za kutosha huku wamevaa kikinga risasi "Bullet proof",vichwa vyao vilizuia na element ngumu sana,gari hiyo iliendeshwa na dereva mahiri "Porter" Boyanka.Gari ya pili hii ilikuwa na askari tano wenye silaha mzito na ile gari ya mwisho ilikaliwa na askari wanne.Kikosi cha anga kilikwishapasua anga ya kuchukua uelekeo wa upwa wa pwani wa habari ya hindi.

Walitumia muda mchache sana kuifikia Bagamoyo,wakalozingilia lile jengo kwa umbali wa aina yake.Baada ya kupeana nikakati ya kuvamia kambi hiyo kwa upande kabisa wa magharibi.Hawakuzitumia zile helkopta kwanza kwa sababu ya kuhofia kuwashtua wale waasi.

Sasa walichanganya miguu kwa kasi kuelekea kule ngomeni huku wakiwa waangalifu mno.

Wale askari wa upande wa kushoto na ndio waliokuwa wanatazamana na ile ngome walishatembea kwa umbali mrefu na ndipo walipokutana na mwanga mkali wa taa kubwa likimulika kuelekea nje ya ngome ile.Walipotazama kwa makini hawakuona mtu yeyote pale nje zaidi ya ile taa peke yake.Wakaswaga mbele wakitumia ile njia ya kutambaa kwa tumbo.Silaha zao zikiwa mbele ya mikono yao wakaanza kutambaa kwa kasi kukwepa ule mwanga mpaka walipopata eneo lenye kiza kidogo na ndipo walipokaa na kupumzika kwa sekunde chache sana.

Askari wa upande wa nyuma walikwishafanikiwa kulifikia lile jengo na kukutana na mwanga mkali kama ule wa mbele ya ngome hiyo ya MK.Nao walichunguza kwa makini hawakuona mtu yeyote zaidi ya lile taa kubwa.Wakatumia mtindo uleule wa kutambaa.Na wale wa ubavuni mwa jengo walikwishaswaga viguru vyao na kulifikia jengo.

Sasa wakawa wamelikurubia kabisa jengo lile ila kilichowachanga zaidi katika ngome ile hakuna ulinzi zaidi ya zile tochi tu.

Walipagawa..

Askari wa awali wa upande wa mbele wa jengo,wakafanikiwa kuupata mlango mdogo wa kuingilia ndani,walipotaka kuingia tu wakasita,wakastaajabu sana.

Mlango ule ulikiwa wazi kabisa.

Nini tena hiki?

Wakatazama na kuutazama mlango kwa mara ya pili.

"Afande usalama upo kweli?" Askari mmoja akamuhoji mwenzake ila jamaa akauchuna.Hakuzungumza kitu zaidi ya kumuarisha mwenzake atangulie kuingia.Kweli akafanya kama alivyoeleza.Wakaingia na kuanza kunyata kwenye giza.Wakafika kwenye eneo lenye taa yenye mwanga hafifu,wakaifuata ile taa huku wakiburuza migongo yao ukutani kwa umakini.

Walipomaliza kuupita mwanga ule hafifu ndipo walipokuja kutokea kwenye kordo ndogo lilikuwa na umbali wa mita kadhaa kutoka pale walipo.Napo kulikuwa na mwanga hafifu sana kama ule wa mwanzo.Wakaona matone ya damu.Damu ambayo ilianza kukauka pale koridoni.

Wakashtuka na mapigo yao ya moyo yakaanza kuwaenda mbio.

Damu!!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakayaangalia matone yale yaliyoelekea mwisho wa kordo lile na kukata kona.Nao wakaanza kuyafuatilia kwa umakini sana.Ndipo walipoyamaliza yale matone,walikoma kwenye giza nene la chumba kilichokuwa upande wa kulia wa kordo hilo.Wakati wanaendelea kutahatuki katika chumba kile mara vishindo toka upande wa pili vikasikika.Vishindo hivyo vilikuwa vinakuja kwa kasi sana kuelekea pale walipo.

Wakagwaya ghafla kwa woga..

Wakajikuta wanajibanza pale gizani huku wakitulia tulii!!

Vishindo vilitulia na jumba lile likatawaliwa na ukimya mwingi,wakashusha pumzi ndefu na kutaka kutoka eneo lile,mara wakajiamiza tena pale mafichoni huku wakivitazama vivuli vya watu wapatao watatu vikija kwa mwendo wa madaha.Wakatazama tena kwa woga kisha wakapeana ishara,ishara hiyo imawafanya wafyatuke ghafla kuwaweka chini ya ulinzi wale jamaa walio kwenye mwanga hafifu.

Mara wakanywea na kuwa wadogo,walipotazama mbele yao wakakutana na mkubwa wao.

Wakashusha silaha zao na kukaa pembeni.Wale askari watatu mmoja wao akatoa tochi na kumulika chumbani mle.Hawakuona kitu zaidi ya matone ya damu tu.Wakaendelea kuyafuta na kukutana geti la chumba kabla hawajafika chumba kingine.Na mlango ule ulikuwa wazi kabisa.

Wakavuta hatua kwa uangalifu huku wakizikwepa zile damu.Wakawa wamefika kwenye chumba hicho chenye giza zaidi ya kile cha kwanza.Harufu kali ya damu iliyoanza kutoa harufu ikawafanya jamaa hawa wazibe pua zao kwa kujivisha vitambaa.Wasiwasi ukaanza kuwajia huku fikra zao zikiwapeleka kuwa huenda binti wa raisi na wenzake walikwishauawa.Yule mkuu wao akawatazama wenzake usoni kwa zamu zamu kisha akatazama pale chini kwenye matone ya damu.

" ....kuua kwangu ni jambo dogo sana,kama mnawahitaji hivi viumbe vyenu viendelee kuishi basi fanyeni huo ujinga muufanyao" maneno haya ya MK yalimtoka askari yule huku hisia za kuuawa kwa Dayana na wenzake ikampanda.Maneno ambayo ya kuogopesha sana.

"Inawezekana huyu jamaa kaua kama alivyosema kwenye kile kipande cha video yake" akahamaki na kusonya.Muda ule ule yule mmulikaji aliyekuwa anaangazaangaza mle ndani akatoa sauti ya mguno wa mshangao uliowashtua wenzake.Walimgeukia bila kusema kitu lakini hawakufikisha macho yao usoni kwa mmulikaji badala yake wakaelekeza macho yao kunako uelekeo wa ule mwanga.

Wakapiga yowe kama watoto wadogo...

Hawakuamini walichokiona katika eneo lile,hakika ni cha kuogofya.

MK na wenzake waligundua ujio wa askari katika ngome yao,ndipo walipoamua kufungasha vilago vyao na kutimua mbio mbali na jumba lao huku nyuma wakiacha mwili mmoja uliokuwa mfu mle chumbani "chumba cha mateso".

Askari wale walipoutazama ule mwili kwa umakini wakagundua kuwa wauaji walitumia visu vikali sana katika kutekeleza azma yao.Kwanza kabisa maiti ile ililowa damu ambazo zilianza kuganda mwilini,pia maiti haikuwa na kiganja cha mkono wa kulia.

Hiyo haikuwatisha kabisa lakini walijikuta wanagumia sauti ya hofu huku kila askari akitokwa na jasho pamoja na mtetemeko wa woga.Hakika yalikuwa ni mauaji ya kutisha.Kitu kikubwa kilichowaogopesha ni baada ya kuigeuza ile maiti,wakakuta haina macho kabisa.

Oooh shiit!

Maiti ya mlinzi wa Dayana(Bodyguard),haikuwa na macho zaidi ya matundu ya macho tupu.

"Wameua hawa!'" Mmoja wao akahamaki.Wakageuka na kuanza kurudi nyuma kwa mwendo wa kasi sana.Hawakujijua kwanini wanarudi kasi namna ile ila walichoamini kwa muda ule ni kurudi walikotoka lengo ni kuuponya uhai wao.

Mtego!

Ile maiti ya yule mlinzi ilikuwa imetegewa bomu lililokuwa linasoma namba na muda wa kulipuka ulikaribia mno na ndio maana wakajikuta wanaanza kukimbizana mle ndani kwa kasi.

Wakakimbia kwa kasi mpaka alipojikuta wapo gizani ghafla.

Wote tano wakaingia kwenye chimbo la giza bila kutarajia,hawakuweza kuona mbele wala nyuma tena.Wakati wamesimama pale gizani huku mihemo ya woga inawafuka wakajikuta wanauliza uwepo wao katika eneo lile.

"Afande Pius upo?"

"Ndio Afande"

"Afande Kipwaro nawe"

"Ndio Mkuu"

"Kiweru pia?"

"Ndio Afande"

"Na na......" Akakatiswa na mwanga mkali wa tochi toka mbele yao,wakakodoa macho kwa taharuki.Hazikuwa tochi mbili au tatu,zilikuwa zaidi ya tochi tano kabisa.Wakapata faraja huku wakiwa na imani kubwa ya kudhani wale wamulikaji ni askari wenzao.

La haula!

Hawakujua kabisa kuwa wameingia kwenye chimbo la MK(Master Killer).

Wakawa wanapiga hatua na kuanza kuelekea kule zilipo zile tochi.Mara wakafunga breki ya ghafla.Taa kubwa ikawaka toka juu na wote wakaonana.Wakaanza kuogopa baada ya kuwaona watu sio walivyowadhania.

Wakaanza kuingiwa na hofu.

"Ndio yule yule" askari mmoja ambaye ni mkubwa wa wale wengine.

Mbele yao kulikuwa na watu kama tano hivi,katikati alisimama mtu mwenye koti refu lililoburuza chini kwa ule ukubwa wake,mikononi mwa huyu bwana kulivaa glovusi nyeusi huku bastola ndogo ikiwa mkononi mwake.Alivaa jinzi kubwa lililodakwa na buti kubwa nyeusi mithili ya zile za wanajeshi,ndani ya koti lile ndefu alivaa T shirt iliyombana vilivyo.Uso wake ulijawa na chuki sana,ile miwani yake tu ilimuonesha ni katili kiasi gani kwa sababu ilikuwa ya jicho moja tu huku ule uzi wa ile miwani ukiwa umezunguka kichwa chake.

Master Killer a.k.a MK ndiye aliyekuwa kati amekunja sura kupita maelezo.Kilichowaogopesha sana askari ni baada ya kuwaona wale watu wa MK wamevalia nguo za polisi,ni wazi walianza kuwaua wale askari wa nje na ndio maana wakaingia pale chini,hawakuweza kuwafahamu kwani walizuia vyuso zao kwa mask za vitambaa vyeusi.

Wakalegea miguu kabisa na kujikuta wananyoosha mikono juu huku silaha zao zikitua chini.

Wameshikwa kiutamu..

MK na jamaa zake wakajongea pale walipo wale askari na kuziteka silaha zao.Kwa jicho baya MK akaitoa ile miwani yake na lile kovu lake la kudumu likaonekana vizuri.Wale askari wakatazama kwa woga.

Akhaa kovu baya..

Wakaogopa sana sura ile ilikuwa ya kuogofya zaidi.Ni heri kuitazama ile maiti iliyotolewa macho lakini ya MK ilikuwa ya kutisha sana.

MK akawatazama mmoja mmoja kwa ghadhabu,alipofika kwa yule askari mkubwa akaganda kama dakika tatu mzima,akatabasamu kwa kejeli kama anatania,tabasamu baya sana halikuwa mahali pake.Akatoa lile sura lake usoni kwa askari yule na kwenda begani kwake.Akakutana na vyota moja begani,akatabasamu tena kwa kejeli.Akaichukua bastola yake na kuikoki kisha akamuwekea kwenye paji la uso.

"Wewe ndio mkubwa wa hawa eeeh?" Hatimaye MK akauliza kwa dharau ila askari yule hakujibu zaidi ya kutetemeka kwa hofu.

Huyu jamaa hana mzaha kabisa.Akamtwaga ngumi kali sana iliyomfikisha pale sakafuni,akamuinua tena na kumtazama kwa ukali.

"Wee ndio mwenye mbwa hawa?" Akauliza tena safari hii yule askari akajibu kwa uharaka sana.Hapo ndipo MK akatabasamu tena kwa bashasha.

"Ndio umetumwa na raisi ama yule anayeitwa George Mbasho eeeh?"akauliza kwa kukazia.

Askari akaduwaaa kwanza!

Huyu jamaa kajuaje?

Kumbe MK alikwishajua mikakati yao ya kuja katika ngome yake.

Kuna mpango wa siri umefanyika sio bure kabisa.

Kimya kikatanda pale kwa dakika kadhaa na badae MK akawaamrisha wenzake wawachukue wale askari na kuwaweka chini ya ulinzi.Sasa mateka yakaongezeka kutoka wawili yaani wale mabinti wa raisi na wale askari tano.Mikono yao ikiwa vichogoni wakaamrishwa kisonga mbele kwa ukali hawakuwa na namna tena zaidi ya kuafiki matakwa ya wale watekaji.

Walipofika nje wakastaajabu sana,hawakuamini kabisa kama kweli MK ndiye aliyefanya kitu kama kile.

Nguvu zikawaisha kabisa na kubaki wakigumia kwa hofu ya kuuawa na yule mtu mwenye sura mbaya MK.







Wakawaingiza garini na kutimua eneo lile na kwenda kusikofahamika.



_______



Hali ya Rayana pale hosptali ilikuwa ni mshikemshike zaidi ya siku mbili mzima mara baada ya madaktari kufanya juhudi za nguvu na hatimaye kumnusuru Rayana kutoka kwenye chimbo la umauti.Akatolewa kwenye kile chumba cha wagonjwa mahututi na kuingizwa kwenye wodi za kawaida.Mamlaka yote kuhusu Rayana yalibaki kwa Swedy baada ya wale waliomleta kutoweka bila kuaga pale hosptalini.

...

Saa tatu na nusu asubuhi wauguzi na madaktari waliendelea kufanya kazi zao kama kawaida.Msongamano wa ndugu katika hosptali hiyo ulikuwa mkubwa mno,kila mmoja alikuwa na nia yake,wengine walikuja kutazama wagonjwa wao na wengine kuja kujitibia wenyewe.Lakini hosptali hii haikuacha kuzuia kelele za ndugu waliokuja kuwatazama ndugu zao na kukuta wamekwishafariki kutokana na maradhi mbalimbali.Hakika ilikuwa hekaheka mtindo mmoja.

Muda muafaka wa kutazama wagonjwa kila ndugu alipata wasaa huo kwrnda wodini huku wakiwa na vyakula vyao mikononi.Mmoja wapo alikuwa ni Bi chiku,mama mzazi wa Rayana akiwa na mtoto wa wake wa kiume ambaye ni mdogo wa Rayana.Wakaingia wodi ambayo alilazwa Rayana huku wakiwa na chupa ya chai pamoja na mfuko wenye vitafunwa.Rayana alikuwa kwenye usingizi mwepesi ambayo ulielekea kumtoka asubuhi ile,alipofumbua macho akakutana na sura pembeni yake,sura ambayo kwa haraka alizitambuahazikuwa ngeni machoni mwake na ndipo alipoachia yowe kali.

"Mamaaaa!"

Taratibu machozi yakaanza kumtoka bila kutegemea baada ya kumuona mama yake yupo mbele yake.Bi Chiku hakuweza kuyavumilia machozi yake yasimuanguke na akajikuta anatiririkwa na machozi mfululizo kwa sababu tu upendo ulichukua nafasi katika mioyo yao.Taratibu akachukua khanga yake kuukuu na kuivuta mpaka usoni,akajifuta yale matone ya machozi huku akimtazama mwanae pale kitandani kwa uchungu mkubwa.

Kweli uchungu wa mwana ajuaye mzazi...

Akainama na kumshika Rayana utosini na kumbusu kwa uchungu sana.

"Pole mwanagu hivi haya matatizo mpaka lini jamani?" Alihamaki kwa huruma lakini hakujibiwa swali lake.

Wakati wanaendelea kusalimia mlango ukafunguliwa na daktari akaingia akiwa na Swedy.

Wakakutanisha macho kwa pamoja Rayana akatabasamu huku akimtazama Swedy.

"Kama unavyomuona hali yake inaridhisha kwa kiasi kikubwa na hata leo naweza nikawapa ruhusa leo leo." Daktari yule mwenye ndefu zilizokatwa vizuri mithili ya "O" akazungumza.

"Asante sana dokta"

Wakasalimia na baada ya hapo daktari akaondoka na Swedy kwenye ofisi ya malipo.



……

"Kwa sasa ndio nakaa hapa Rayana,kule nimehama kwa sababu ya wale wenye nyumba ni watu wa ajabu sana" Swedy akazungumza kwa upole na mbele yake kukiwa na Rayana wakutazama huku tabasamu zikiwatoka.

Swedy alichukua uamuzi wa kuhama kwa wakina Veronica na kuhamia maeneo ya Moroko na siku hiyo alimuarika Rayana kwenye "lunch".Ni siku ya kwanza kumkaribisha Rayana katika makazi yake mapya wakitokea Mburahati.

"Asante Swedy yaani sina cha kukupa ila..." Rayana akazungumza ila akashindwa kusema machozi kwa mbali yakaanza kumlenga.

"Noo usilie kawaida tu,ndio maisha ya mwanadamu haya Rayana usilie jikaze" swedy akasema.Baada ya kuketi pale sebleni kwa muda mchache hatimaye Swedy akainuka na kuingia jikoni ili atayalishe chakula cha mchana.Kama ilivyo kawaida yake alianza kuangaika kwa kasi sana na baada ya dakika kama hamnsini alikwishakamilisha kila kitu.Akachukua matikiti na maparachichi akayamega vipande na kuyaweka katika sahani.

Wakiwa mezani kila mmoja akimtazama mwenzake kwa jicho la uchokozi lenye uwashiliaji wa matamanio,hakika walifichana kitu fulani chenye upendo ndani za mioyo yao.Kila mmoja alikula kwa furaha huku kila baada ya sekunde mbili walitazamana kwa kuibiana,hatimaye Rayana akashindwa kuvumilia mtazamo ule na kuanza kunena.

"Unapika vizuri! Sana dear"

"Kweli?"

"Yeah tena sanaaaaa"

"Haha asante Rayana"

"Ila kuna kitu nataka nikuulize lakini sio kigeni nadhani,je unaniruhusu?" Rayana akazungumza na ndipo Swedy alipokiacha kijiko kisha akamtazama kwa umakini binti aliye mbele yake.

Swali gani huyu anataka kuniuliza?

"Niulize tu usijari!"

Rayana akasimamisha zoezi lake la kula na kumtazama Swedy kwa sura ya aibu sana.Wakabaki walitazama zaidi ya sekunde kumi,Swedy akamshtua kwa kumpiga swali.

"Vipi Rayana niulize"

"Sawa hivi Swedy kwa...ni..ni?...." Akanyamaza na kukohoa kidogo kisha akaendelea "kwanini huna mchumba siku zote hizi wakati una maisha mazuri kama hivi?" Hatimaye akauliza.

Swedy akajikoholesha na kutabasamu kidogo.Tabasamu ambalo lilimpa mapigo ya moyo Rayana huku akisubiri jibu kwa hamu kubwa.Kiukweli Rayana alipigwa na homa ya mapenzi kwa Swedy na dawa ya homa hiyo alikuwa nayo Swedy peke yake kwa kipindi kile mara baada ya kutoswa na Mpenziwe Aidan.

Ilimchukua muda kidogo mpaka kuja kupona jeraha la penzi la Aidan na sasa anataka kulipoteza kabisa jeraha hilo kwa kumtumia Swedy.

Kwanza amenisaidia sana mpaka dakika hii,kwanini nisimpende?

Au kuna ubaya jamani kumpenda mtu mwenye msaada mkubwa kwangu?

Mawazo mfululizo yaligongana kichwani mwa Rayana ndani ya sekunde moja tu na ndipo alipokuja kushtushwa na sauti ya chinichini ya Swedy.

"Aaah nimeteswa sana na mapenzi Rayana hapo nyuma,hakika wanawake wamenitoa kutoka kwenye sehemu mzuri mpaka hapa tena.Huwezi amini kabisa kuwa nilikuwa namiliki jumba kubwa mwenyewe na huo msaliti wangu..lakini mmh nikaja kuambulia maumivu makali nafsini mape...." Akaacha kuzungumza na kuchukua kitambaa chake toka mfukoni.Akajifuta matone madogomadogo ya machozi yaliyoanza kumtoka.

"Pole jamani kumbe haukuwa hivi?"

"Yeah of course Rayana,ni hadithi ndefu sana" Swedy akazungumza kwa uchungu.Rayana akabaki akimtazama kwa huruma mno hasa pale alipodondosha chozi,ni wazi Swedy alikuwa na hadithi ndefu ya maisha yake tena ni ya huruma zaidi.Na ndio maana huwa anaingiwa na uchungu asikiapo mtu ana matatizo kama yake.

"Na ndio maana sitaki kuwa na wanawake...wanawake nyie ni wauaji kabisa" akamalizia na kukaa kimya huku akimtazama Rayana ambaye alikuwa ameduwaa pale mbele ya macho yake.

"Mmh ila sio wote Swedy"

"Mimi naamini hilo...wengi wenu wauaji"

kimya kikaingia tena pale mezani.Hawakuwa na mazungumzo mengine zaidi ya kutazamana tu huku chakula kikiwa kichungu kwao.



_____



Kama mwendo wa masaa manne hivi kutokea saa saba na nusu kule kwenye ngome ya MK.Sasa walikuwa kwenye gari zao huku wakiwa na mateka wao.Msafara wao ulikuwa na magari kama matatu aina ya Nissan Murano zilizosheheni watu.Safari ya kuelekea Dar es salaam ilikiwa imepamba moto.Hawakupenda kutimua mbia kuelekea mbali kabisa ili tu wajihakikishie usalama.

Lazima watatafutwa tu! Tena watasakwa maeneo ya msata au Tanga kabisa maana ndio sehemu mzuri za maficho,hawakutaka litokee hilo kabisa.

Mpaka wakati huo Dayana hakuweza kufahamu uwepo wa Bosco katika kikundi kile cha watekaji.Ndani ya gari hizo mateka wote walifunikwa na vitambaa vyeusi vizito kwa minajiri ya kutobaini wapi wanaelekea.

Saa kumi ndipo gari hizo tatu zilikanyaga ardhi ya Tegeta Dar es Salaam,Hapo ndipo mawasiliano yalipoanza rasmi na Inspekta Makurumla.

Baada ya kufanya kila linalowezekana ndipo wakakubaliana waingia nyumbani kwa Bosco Mbezi Beach.

Wakakurubia katika nyumba hiyo.Sasa wakawa nje gari tatu zote zikinguruma kwa sauti ya chini kabisa.

Bosco akashuka na kupiga mguu kuelekea kwenye geti.Alikuta mlango upo kama alivyouacha,akasogea pembeni upande wa kulia kwenye ua kubwa pale nje na kupapasapapasa kisha akatoa ufunguo wa geti lile.Akafungua na kulisukuna geti na kuruhusu gari zote tatu ziingie ndani halafu geti likarudishwa na kufungwa.Mateka yakaingizwa ndani haraka sana.Katika nyumba hiyo ya Bosco iliyozungushiwa fence,ilikuwa na nyumba vitatu,sebule moja kubwa sana pamoja na ukumbi mmoja wa kulia chakula huku eneo lingine likitengwa kwa niaba ya mazoezi,mateka wale wakaingizwa kwenye chumba kimoja ambacho hakikuwa na kitanda zaidi ya sakafu pekee lililotanda mle ndani.Kila mateka alifukwa mikono yao kwa nyuma pamoja na kufungwa vile vitambaa vyeusi.

Wahakuona kitu..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Masaa yakaziti kuondoka na sasa yalielekea kukurubia kwenye saa kumi na moja za alfajiri.

MK akajibweteka kwenye sofa za pale sebleni huku akiwa na ghadhabu sana.Walitumaini mchezo ule utawaingizia pesa kwa muda mchache sana lakini haikuwa kama walivyotegemea,na sasa walikuwa wanasakwa kila kona baada ya kuharibu kule kambini.

Aliwaza anafanya kitu gani ili aweze kuondokana na hadha ile?

Hawezi tena kujionesha kwenye televisheni kama afanyavyo ilhali mitambo yake imebaki kule ngomeni.

Akawaza bila ya kupata jibu..



Hatimaye ikawasili saa kumi na mbili ya asubuhi.Wafuasi kadhaa wa MK walikuwa wamepitiwa na usingizi mzito lakini MK peke yake ndiye aliyekuwa macho,alikuwa na msokoto mkubwa wa sigara huku pembeni akiwa na pombe kali sana zilizokuwa ndani ya jokofu la Bosco.

Akashtushwa na mngurumo wa gari toka nje.Hapo ndipo aliposimama na kuitoa ile bastola yake,akaishika mikononi kikamilifu na kuelekea dilishani,akachukungulia na kuiona gari kwa mbali ikiwa imepaki nje ya nyumba ile.

Ukimya ukatawala.MK akaruka toka pale dilishani na kuwatikisa jamaa zake na hao pamoja na Bosco wakakurumpuka toka kwenye usingizi mzito pale sebleni.

"Kuna gari imepaki hapo nje" MK akafoka kwa sauti ya chini sana.Kabla hawajaendelea na mjadala huo simu yake ikanguruma toka mfukoni.

Inspekta alipiga simu kutoka pale nje alipoegesha gari na kuomba afunguliwe geti,nao wakafanya hivyo haraka.

Hawakutaka kupoteza muda sana,Inspekta akazingumza machache na kumuachia kazi mzima MK huku akihaidi kuimalisha usalama kila kona.

"Tutatuna tena picha za hawa mateka wote kwenye ikulu ya raisi na kumpa masharti ndani ya masaa 48.Kama hataki kucheua huu mpunga tutawafyekelea mbali hawa vidudu wake..." Inspekta Makurumla akazungumza kwa ghadhabu huku jasho jembamba likimtoka haswaa.

Wakafanya kama walivyopewa maelekezo yao.Waliwachukua mateka wote na kuwapiga picha za pamoja kisha zikakumwa kupitia email huku zikiambatana na ujumbe mzito wenye vitisho zaidi.

Mchana ukapita kwa kasi sana,giza likaingia,wafuasi wa MK wakaaga kwenda baa ya jirani kwa lengo la kupoteza uchovu wa mikikimikiki ya mle ndani,MK naye alipanda gari ya binafsi na kuelekea Mbezi kwa Inspekta Makurumla kwa maongezi.Pale kwenye nyumba ya Bosco alibaki Bosco mwenyewe na wale mateka.Saa mbili za usiku zikatimia,Bosco anapiga miayo pale sebleni huku chupa ya konyaji ikisindikizwa na ya Safari ikawa inamburudisha.Baada ya kupiga fundo moja la glasi ya kinywaji cha konyagi akashushia na Safari kisha akamimina tena konyagi glasini na kuinuka,akawa anaelekea kule kwenye chumba waliko mateka huku kichwa chake kikitawaliwa na pombe kwa muda ule.Akaufungua mlango taratibu na kuiwasha taa ya chumba kile,hapo ndipo alipoiona miili ya mateka ikiwa imejilaza pale sakafuni.Akatabasamu na sura yake ikajikunyata na kuwa kama ya kilevi zaidi.Katika kitendo kisicho cha kawaida akaanza kurusha mateke ya ovyo kwa wale mateka huku akitoa matusi ya nguoni.Lakini mateke yale hayakuendelea kabisa aliposikia tu sauti ambayo aliwahi kuisikia sehemu.

Akahamanika na kuacha kurusha yake mateke ya ovyo.Sasa anamuendelea yule mateka aliyemfanaisha kwa sauti pale chini huku akiwa na glasi yake mkononi

Eeeeh***

Akalipukwa na mapigo ya moyo..



Glasi ikamtika na kutawanyika pale chini kwa kasi ya ajabu.

Akashindwa kujua kwanini imekuwa vile? Na isiwe siku za nyuma?

Akamvuta Dayana na kumtoa pale sakafuni,alidhoofu kupita maelezo.Tangu jana mateka wale hawakupata kutia kitu chochote mdomoni na njaa sasa zilikuwa zikiwatafuna kwa fujo mno.Hata pale alipojaribu kumtingisha hakuwa na dalili ya kuamka,alizimia kabisa kutokana na kukosa chakula kwa muda mrefu.

Bosco akatoka mle chumbani kama mtu aliyechanganyikiwa vile kisha akarudi na bilauri la maji,akayachota kwa kiganja kumwagia Dayana usoni mara tatu lakini bado hakuamka.Alifanya hivyo zaidi ya mara tano bado hakufanikiwa...

Akayasikiliza mapigo ya moyo na kubaini yakidunda kwa mbali sana.



_______



Katika hali ya kutoamini kabisa katika Maisha ya Aidan ni pale alipoishiwa pesa kwenye akaunti yake,nyumba ambayo alipangiwa na Dayana mkataba ule uliishia na alitakiwa alipe kiasi kingine cha pesa.

Akiwa ndani ya mashine ya ATM,ndipo hapo alipopagawa na kushindwa kuamini kabisa kile alichokiona kwenye akaunti yake.

Tsh elfu ishirini na saba mia mbili?

Alishabwetuka kimyakimya mle ndani huku bila kutarajia machozi yakaanza kumtoka kwa mbali.Akiwa ameduwaa pale ndani kwa muda mrefu ndipo askari anayehusika na ulinzi pale nje alipomshtua na kumtaarifu juu ya ujio wa wateja wengine.Kwa ghadhabu akatoka mle ndani na kuingia garini kisha akaitoa kwa kasi al manusura awachukue watu walio karibu na eneo lile,akasindikizwa na matusi mazito yasiyo kifani lakini hakusikia kitu chochote zaidi ya kukanyaga moto.Halmashauri ya kichwa chake ilimwambia atembee mpaka Kinondoni kwa mpenzi wake.

Akakanyaga moto na baada ya dakika kadhaa akaifikia kinondoni nje kabisa ya duka kubwa la nguo za kike.Akashuka kwa kasi na kuingia mle ndani huku akitupa jicho kila mahali mle ndani huku akimsaka mpenzi wake.

Ni huyu huyu ndiye niliyewahi kumuachia kadi yangu ya benk siku moja leo ataisoma namba!..

Aidan akapata kumuona mhudumu msaidizi wa duka lile na kukurubiana zaidi na yule binti jasho likiwa linamvuja kwa kasi japokuwa duka lile lilitawakiwa na hewa murua ya kiyoyozi.

"Eeeeeeh! Shem vipi?" Hatimaye binti yule akatokwa na swali la hamaniko kwa Aidan.

"Huyu malaya yupo wapi?" akauliza kwa ghadhabu ilahali misuli ya kichwa ikiwa imemtutumuka kwa hasira.

"Malaya!?"

"Ndio tena ehee yaani hapa patachimbika kabisa leo.Niambie yupo wapi?"

"Mhmmm unajua sikuelewi kabisa shem..." Binti yule hajamalizia maneno yake na ndipo Aidan akadakia kwa ghadhabu na kumfokea.

"Wacha maneno yako wewe,sema huyu kahaba yupo wapi?"

Wakati wanaendelea kuzozana pale wateja watatu waliokuwa wanachagua nguo mle ndani walimshangaa Aidan huku wakiwa na maswali lukuki vichwani mwao.

Huyu ni kichaa au mwehu?

Hapana sio bure yaani mpaka kwenye ofisi za watu?

Aidan akageuka kule ufunguliwapo mlango na kukutana na sura ya mpenzi wake akiwa ameshikana mikono na mwanaume mmoja mwenye mwili wa kujazia wenye hazina pekee ya mazoezi.

"Eheee nilikuwa nakusubiri sana kwa hamu wee malaya.." Akavuta hatua na kuwafikia wale watu ambao sasa waliuachia mlango ule wa kioo ukijifunga.Wakakirubiana zaidi na hapo Aidan alipopandwa na hasira za hali ya juu kabisa.

Bila kutegemea maamuzi yake ndipo alipojikuta anaiachia ngumi moja takatifu ambayo ilidakwa kwa uzuri na yule jamaa mwenye mwili wa kujazia.

Khaa!

Akaituma ngumi ya pili nayo ikachezwa kwa utamu na kumpandisha hasira zaidi ma zaidi.Hajakaa vizuri akatuma ya tatu na hii ndio ilimfanya imfikishe chini kwa kishindo sana.

Kaangukaje?

Wakati ile ngumi ya tatu inatumwa kwa yule njemba ndipo ilipompata vyema tumboni lakini kutokana na ukomavu wake yule jamaa hakutingishika hata kidogo,ndipo alipoachia ngwala la nguvu iliyomfikisha Aidan chini.Alipotaka kuinuka ndipo alipokutana na ngumi mbili za pua na yule jamaa.

Damu ikamtoka.

Alipoona sasa damu inamvuja puani ndipo alipohamaki na kujiinua kwa kasi na kujirusha kwenye shevu ya nguo zilizopangwa mle dukani na nguo zote zikaanguka chini huku ule mlingoni wa kututindikia zile nguo ukiwa umevunjia.

Kelele zikaanza kusikika mle ndani.Aidan hakuishia hapo,akajiinua tena na kujirusha kwa mara ya pili na hapo ndipo alipodakwa na yule jamaa na kukandamizwa chini kwa nguvu.Muda huohuo wakaingia watu wawili mmoja akiwa na mavazi maalum ya polisi na yule mwingine akiwa na nguo za kiraia.

Aidan matatani.

Lile vurumai baina ya Aidan na yule jamaa na ule uharibifu wa Aidan wa maksudi ukiendelea ndipo yule mpenzi wake Aidan kama anavyodai mwenyewe aliyemwibia pesa zote benk,akaichomoa simu yake huku akitoa kilio cha hofu,akapiga simu kituo cha polisi cha karibu pale Kinondini.Ndipo askari wale walipompiga pingu na kuondoka nae.

Hata hivyo Aidan hakuamini kama kile kinachomtokea maishani mwake ni kweli au ndoto,akang'amua macho na kubaini ile haikuwa ndoto bali ni mkweli mtupu.

Akaanza kulia kwa kwiwkwi huku akitokwa na maneno ya porojo.

"Jamani yule ni mchumba wangu na lile duka nimemgharamia mimi sasa mnanipeleka wapi?" Akahamaki na swali.

"Aisee sisi hatujui kabisa hilo utaenda kujibia kituoni" polisi mmoja akazungumza kwa ghadhabu.Wakafika nae kituoni,maelezo yalipochukuliwa Aidan akawekwa rumande kwa muda wa kama nusu saa mzima kabla hajarudishwa tena na kuanza kuhojiwa.

"Kwanini unaleta vurugu kwenye maofisi ya watu?" Polisi yule mwenye nguo za kiraia akamuuliza Aidan ambae yupo mbele yake anatoa chozi la huruma.

"Mimi afande yule mwanamke kaniibia pesa yangu nyingi sana na ile ofisi nimegharamikia mimi mwenyewe..." Aidana akashinda kuendelea kuzungumza na hasa pale alipokumbuka kipigo cha yule jamaa ambayo dhahiri anaonekana ni mpenzi wa msichana yule ambaye Aidana anadaia ndio mpenzi wake.

Amaa!!

Mahojiano yake hayakuduma zaidi maana yule polisi alitambua kuwa ile kesi haina macho wala migui zaidi ya kupotezea muda buree.

"Sikiza sasa hebu tuwezeshe uondoke,huu ujinga mtamalizana wenyewe bana alaaa" akafoka na kumuacha mdomo wazi Aidan.Alipojitahidi sana kung'amua maneno ya yule askari ndipo alipobaini kuwa anataka kitu gani.

Pesa tu hakuna kingine..

Akaingia mfukoni na kutoa ile elfu ishirini na kuitupa pale mezani kisha akamtazama yule polisi.

Polisi akamtazama na kutabasamu kwa kejeli.

"Hii nini sasa?"Polisi muhojaji akauliza kwa dharau huku mdomo wake ukiwa pembeni.Akampagawisha Aidan.

Eboo hawa jamaa wanataka nini sasa?

"Nina hiyo braza"

Bila kusema kitu polisi yule akainuka na kuanza kupiga hatua kuelekea ule mlango wa kutokea nje huku akimuacha Aidan akimtazama lwa mshangao ma sura yenye huruma.

Kabla hajaufikia ule mlango ndipo alipogeuka na kumtazama Aidan.

Machozi sasa yalikuwa yakimtoka.Akamtazama kwa dakika chache na kumuamrisha askari mwenzake amtoe pale kitini aondoke zake.Kweli akafanya hivyo.

Alipofika pale kaunta akakabidhiwa ufunguo wa gari yake na kuondoka zake huku mawazo yakivytana kwa kasi kichwani mwake.

Hakuwa na sehemu vyingine ya kwenda zaidi ya nyumbani kwake Kawe lakini hakujua maskini.

Baada ya kukatakata kona kadhaa za jiji,akafanikiwa kuikamata barabara kuu ya Bagamoyo na sasa alikuwa kwenye mataa Mwenge akisubiri gari za upande wake ziruhusiwe,hawakukawia,zikaruhusiwa na yeye akavuta moto mpaka Kawe nyumbani kwake.

Hali aliyoikuta nayo huko nyumbani kwake ni nora ile ya kule kwenye mashine ya ATM,lakini hii ya kwake ilimchanganya zaidi.

Alikuta mlango wa nyumba yake umepigwa "Lock" tofauti na ile ya kwake.Akiwa katika hali ya sintofahamu ndipo mzee wa makamo alipotokea akiwa amebeba makaratasi kadhaa mikononi mwake pamoja na funguo.

Baba mwenyenyumba!!

Akahamanika na kukumbuka kuwa mkataba wake wa nyumba umekwisha na ilimlazimu afunge mwingine.

Lakini atafungaje na pesa zimekauka?

Yule bosi wake wa kumtupia pesa hayupo tena..

Akanyong'onyea na kuelegea miguu hata kabla mzee yule hajazungumza kitu.

Jua hiloo lilikuwa linalimbia kwa kasi ya ajabu sana.Akashindwa kulipa tena pesa za nyumba ile ndipo alipoingia garini na kugeuza huku akitoa ahadi kwa yule mzee,ahadi ya kuja kulipia tena akipata pesa.

Loooo!!

Usiku umeingia kabisa na hana hata dalili ya kupata sehemu ya kulala,hana pesa ya chakula kwa muda ule japokuwa likuwa ana gari mziri.

Ndipo alipokumbuka kuna mpenzi wake anaitwa Queen Bonge,huyu alimpangoshia nyumba upande mmoja na kumpatia pesa ya mtaji.

Hana sehemu nyingine ya haraka ya kujihifadhi zaidi ya Queen bonge.

Hakujua kabisa anachokwenda kukikuta kule kwa Bonge.

Akavuta moto na kuanza safari ya kwenda kwa Queen bonge huku akihafiki kwa asilimia mia kabisa kuwa ndipo atapata mahali pa kujiegesha kwa usiku ule.Kama mwendo wa dakika kama arobaini hivi akajikuta anafunga breki Magomeni Mapipa nje ya nyumba ambayo haikuisha kwa nje kwani ilikuwa inejengwa kwa tofari za block huku zikiachwa wazi bila kuzuia na 'Plasta'.Akatoka garini na kuelekea mlangoni.Kwa kuwa alizoea pale kwenye ile nyumba,akaingia bila kubisha hodi na kuurudisha mlango ule Sasa akawa anaenda mlango wa mlengwa wa sebleni.

Sauti ya mziki ilisikika toka mle ndani huku pangaboy lililojizungusha kwa kuwekwa kwenye speed namba tatu ikasikika pia masikioni mwa Aidan.Hakutaka kuchelewa ndipo aliposukuma lango na kuufungua.

Laaah!!!

Queen Bonge alikuwa kifuani kwa jamaa ambaye na yeye alikuwa na mwili mkubwa tena kushinda yule aliyewahi kukutana naye mchana kule Kinondoni kwenye duka la nguo la msaliti wake.Jamaa huyu alikuwa na nywele tele kifuani pamoja na tumboni huku akiwa na bukta peke yake anachezewa zile vywele "GARDEN LOVE" na Queen Bonge kwa upole.Wakati huo yule jamaa alikuwa amemshika Queen Bonge kwa nyuma akidhibiti ile khanga ya Bonge isiachane na mwili.Miguu ya jamaa ilikuwa juu ya meza nayo ikiwa imetawaliwa na vivyweleo vingi.

Kile anachokiona pale mbele yake ni Mubashra kabisa na wala sio ndoto.

Kichwa kikaanza kumpiga huku akihisi maumivu mno utosini.

Kinachomuumiza zaidi si yale mahaba wanayoyaoneshwa mbele yake La hasha bali ni pesa alizotumia kumpangia nyumba upande mzima ilhali mwenye hana hata kibanda,lakini pia akiachana na hayo Aidan alimpatia Queen Bonge pesa ya mtaji ya kufungua saloon yake kwa kiasi kikubwa ilhali yeye mwenyewe hata hata mradi wa kufuga kuku.

Akhaaaa!! hii kali sasa





Queen Bonge kuiona sura ya Aidan tu pale mlangoni akaruka toka kifuani kwa yule jamaa na kujiweka pembeni huku akihema kwa hofu sana.Alichokuwa akikijua kufuatia hali ile ni kupoteza buzi lenye pesa zake (Aidan) kumbe hakujua kabisa.Akajifanya anatembea kwa magoti kwa unyenyekevu wa hali ya juu huku akilia kilio cha kinafiki.Yule jamaa akamtazama Aidan kwa ghadhabu mno huku mikundo utosini kwake ikimtuna kwa hasira zisizoelezeka kabisa.

Ghafla akajikuta anabamiza mlango na kutoka pale mlangoni.Akapnda gari na kuishia zake asijue wapi kwa kufikia na usiku ulikwishasonga sana.

Saa tatu na dakika arobaini na nne(09:44P.M)

Machozi yakaanza kumtoka bila kutegemea.



________



Mapenzi yalipopandikizwa yakamea na kukua, hatimaye yakaota mizizi na kubeba shehena kubwa ya matawi,haikutosha na ndipo lilipoanza kuzaa matunda,matunda ambayo kamwe hayajawahi kutoke kupendwa na binadamu wawili hawa.Kila mmoja alitamani kula nduta lile lilimea katika mti mzuri uliokuwa na ustawi wa kipekee.

Penzi likamea na matunda kuzaa.

Si lingine ni penzi la Swedy na Rayana,japokuwa zilipita apizo kali kwa Swedy huku akijitutumua na kusema hatopenda tena,sasa zikawa hadithi za abunuwazi.

Never say never... kama wazungu waalalishavyo.

Kwenye ndio usiweke hapana kwani ni kama kujipa shughuli ya kutafuta jibu ambalo liko wazi tu.

Ilikuwa siku ya jumamosi katila ufukwe wa Coco Beach,wapenda nao hawa walivalia nguo matata zenye kufanana sawia huku kila mmoja akiwa ana uso wa furaha sana.

Siku hiyo walipanga waje kuitumia kule Coco Beach pamoja na kufurahia penzi lao ambalo lina siku chache tu tangu lianze rasmi.

T shirt lenye rangi nyekundu lenye ishara tosha kwa wapenda nao,ilitupiwa na Swedy huku pale maeneo ya kifuani kukiwa na andishi lenye mkato lililosomeka " She Love Me" likiwa na maana ya ananipenda huku Rayana akiwa amevalia T shirt kama ileile aliyoivaa Swedy lakini hiyo ilisomeka "He Love Me" pamoja na alama ya kopa katika T shirt zote.Hakika walipendeza mno hawa kwa watu waliopata kuwaona siku ile pale ufukweni iliwavutia kwa kiasi kikubwa.

Michezo yao pale ufukweni ikawasisimua wengi sana lakini sio tu watazamaji wale ndio walioshuhudia tukio lile bali hata jamaa mmoja aliyekuwa ameketi chini mchangani,alionekana kuwa mwingi wa mawazo huku akihituhumu dunia kwa kumgeuzia kisogo.Alikuwa ameketi pale mchangani lakini kadri alivyopepesa macho yake ndipo alipowaona.

Akainuka muda ule ule na kuwatazama vizuri.

Hapana hakuwaona kwa ukaribu,akajongea na kuwakurubia zaidi na ghafla akaghadhibika bila kutegemea.

Aidan alipomuona Rayana akiwa na Swedy pale ufukweni punde akahisi hasira zinamjia,wivu ukachukua sehemu yake.

Duh!

Iweje awe na wivu wakati alimsaliti hapo awali na kumchomea tambi kwa watu wabaya?

Khaa.Jambo lisilo la kawaida Aidan akawasogelea kwa kasi mithili ya wapiganaji mieleka.Akamtazama Rayana kwa hasira.

"Rayana huyu nani?" Hatimaye maneno ya kukereka yakamtoka bila kuvuta kumbukumbu za awali akiwa na Rayana.

Sio bure huyu!

Rayana na Swedy wakashangaa sana.Aidan hakuwa tofauti na mwehu kabisa.

"What!!!!" Rayana akabwata kwa jazba.Hasira zenye chuki zikaanza kumpanda taratibu.Hakutegemea uwepo wa Aidan katika mandhari ile na hakuprnda kusikia swali kama lile kutoka mdomoni mwa Aidan.

"Kumbuka tulikotoka Raya...." Maneno ya Aidan yakakatwa ghafla baada ya mkono wa Rayana kutua shavuni mwake kwa utamu sana.

"Mwanaharamu mkubwa wee tena nitokee hapa nani akumbuke mimi nani yako?,tena niondokee mbali" Rayana akapayuka kwa hasira.Watu wa pale ufukweni wakaanza kusogea karibu kuutazama lile picha mubashara.Wakati wote huo Swedy alikuwa ametumbua macho asielewe nini kinaendelea.Ni kama anayeota hivi hata pale alipojaribu kutoa neno koo lilikuwa kavu sana.

Hasira zikamjia juu...

"Vipi mpenzi mbona siwaelewi? Huyu ni nani?"

"Wee fala kele...." Aidan akadakwa na kofi la pili la Rayana.Safari hii ukelele wa maumivu ukamtoka huku Rayana akijipuliza mkono wake alioutumia kumtandika Aidan.Maneno ya dharau na kejeli ni vitu ambavyo hata siku moja hakuweza kuvumilia Swedy na ndipo aliporuka na kumtwaga ngumi ya kifuani Aidan huku akitoa tusi la nguoni kwa hasira.Aidan akatupwa chini huku akilia kama mtoto mdogo.Uwezo wa kupambana alikuwa nao ila kile kitendo alichokifanya Rayana kiliashiria wazi haitajiki tena.

Majonzi..

Wakati Aidan bado anaendelea kugalagala pale chini Swedy na Rayana wakakimbilia kwenye gari yao na kutoka kasi ufukweni pale huku wakiacha maneno mengi kwa watu.Safari yao iliishia Moroko.Swedy kavula mno hataka kuzungumza kabisa na hapo ndipo alipokumbuka ule usemebwake wa wanawake wauaji!

Kila anapojaribu kupapasa mapenzi yanamrusha nje ya mstari na kujikuta akihaha hewani.



……

Kule ufukweni,ufukwe wa Coco Beach mara baada ya Aidan kupokea kichapo cha makofi mawilli ya Rayana pamoja na ngumi moja kali ya Swedy ndipo alipojivuta na kuingia garini na kuanza kuifuata gari aliyopanda Rayana kwa nyuma huku akiwa makini sana.Alichotaka kujua ni wapi ile gari inapoishia?

Kweli akafanikiwa kupajua sehemu ambayo wanaishi.Ni Moroko.Akageuza na kuondoka zake.Siku zote alizokosa hifadhi yaani sehemu ya kulala ndipo alipopata wazo la kwenda kule Kigogo mwisho kwa rafiki yake yule wa dili la kusafirisha makopo Arusha Gomesa.Walijifika pale kwenye kibanda chake huku akiwa na ile gari yake.

Alipofika tu pale kibandani kwao akaingia moja kwa moja ndani huku ghadhabu zimemkaa kooni haswa.

Chumba kilikuwa kimya kabisa,si Gomesa ambaye ndiyo mwenye kile chumba,hakuwepo kwa muda ule.Akajikuta anajilaza pale kitandani huku akizongwa na mawazo.Anajuta kufanya ujinga kama ule maishani mwake hasa ukizingatia Dayana anayemtegemea hakuwa huru tena kutoka mikononi mwa watekaji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakati yupo kwenye msongo ule wa mawazo ndipo alipotokea Gomesa akiwa amechafuka sana kutokana na kazi zake azifanyazo.

Kazi ngumu zenye malipo hafifu..

"Vipi wee jamaa!?" Akauliza huku akiketi kwenye kigoda kidogo kilicho pale ndani.Aidan hakulemba ndipo alipomuelezea kilichomkuta kule ufukweni jioni ile.Gomesa akahamaki pale pale huku akimshutumu Aidan kwa kuwa mnyonge kiasi kile.

"Yaani unamuacha mwanaume kama wewe tena anayekuchukulia mali yako akupe kisago?,yaani rafiki yangu we ni fala wa mwisho.Ingelikuwa mimi hapo eheee pangechimbika sekunde mbili,sasa we unawaacha tu kama boya fulani,na hili likifua lako lina kazi gani sasa?" Gomesa akafoka kwa ghadhabu huku akimkemea Aidan kitendo cha kuwaacha mahasimu wake.Ndipo walipopanga mikakati sasa.



__________


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog