Simulizi : Binti Wa Raisi
Sehemu Ya Tatu (3)
Giza nene lililoifunika anga likasababisha watu wake waanze kufanya maovu ambayo yaliwekwa kando majira yote ya mchana.
Aidan akiwa amepakia pombe kama tereko la kupikia,alibwabwaja maneno ya ajabu huku mkono wake wa kulia akiwa ameshikilia chupa ya bia,mkono wa kushoto ulikuwa juu ya kalio la msichana ambaye alionesha na yeye amelewa kupita kiasi.Mziki pekee wa baa ndio uliokuwa unawayumbisha,walijaribu kuucheza bila ya kufuata mapigo ya mdundo,hapo ndipo wakaleta vicheko kwa wateja wengine.
"Ina maana wale wanacheza ngoma ya mganda au Sindimba? Maana mmh ni hatari tupu" mnong'ono ya watu ikaanza kutoka kwa wateja hao lakini haikuweza kuwanyamazisha wawili wasicheze mziki huo.
Baada ya robo saa mbele Aidan akajikongoja mpaka kaunta na kulipia vinywaji alivyotumia na msichana huyo.
"Una...nidai shilingi ngapi?" Aidan akauliza kwa sauti iliyo na mikwaruzp iliyosababishwa na pombe.
"Elfu tisini na saba" mhudumu huyo akasema.Aidan akaingia mfukoni na kutoa walet baada mbaya hakuiona.Haikumuingia akilini akaacha kwanza funguo ya gari pembeni kisha akaanza kujisachi upya,kweli jibu ni lilelile.Haja ndogo kubwa ikaanza kumkaba ghafla na kutaka kutoka nje,pochi yake iliyokuwa na pesa zake amekwishaiangusha,hakuwa na hata shilingi mia,sasa atalipaje mtoto wa Mburahati anaumbuka mbele ya kadamnasi.
"Mungu wangu,pochi yangu.." Aidan akahamaki huku taratibu pombe ikianza kumtoka.
"Pochi yako?" mhudumu akauliza kwa mshangao "kwani imefanyaje?".
"Wameiba" Aidan akasema.Wakati anaendelea kujisachi,msichana ambaye alikuwa anakunywa nae akazitoa pesa zote za kwenye pochi ya Aidan na kuitupa,zaidi ya laki moja na nusu zilizopo kwenye pochi hilo akazibana vizuri kwenye mkoba wake.
"Sasa dada naomba niingie bank mara moja nitarudi sasa hivi" Aidan akajitetea.
"Nyooo! bwege nazi wewe,tena lipa hela sasa hivi kabla sijakuitia walinzi" majibu ya mlinzi yakamfanya aanze kuogopa,pombe kichwani imekwishamruka.
"Noo basi usifanye hivyo" akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya ghalama.
"Chukua hii simu ina thamani ya laki tano,naomba nikuachie mimi nitakuja kesho hapa kugomboa" Aidan akazungumza na kumkabidhi simu mhudumu.
*****
Siku zikapita Rayana akaridi katika hali yake ya kawaida,mawazo juu ya Aidan yakamuisha.Akaanza maisha mapya akiwa na familia yake.Ile pesa aliyotumiwa na Aidan hakuitumia ovyo,akafungua mgahawa mdogo wa kuuza chakula pamoja na chai.Watu wakaanza kumzoea na mwisho wake wakaanza kujaa katika mgahawa huo,hakuwa na kitu kingine anachojivumia kwa wateja wake zaidi ya ukarimu pamoja na heshima kwa kila mteja wake.
" Unajua Rayana we ni mtu wa ajabu sana?"
"Kwa nini?"
"Hivi kwa nini unanikataa mimi,ungelikuwa na mimi ningelikuongeza mtaji hapa,hujui kama wateja wanapenda sana hapa kukiwa na vyakula vizuri zaidi ya hivi.."
"Babuu achama na mimi,kwanza we mume wa mtu,hata sitaki huo mtaji kampelekee mke wako akaanzishe biashara yake sio kwangu"
Mazungumzo hayo yalikuwa kati ya Rayana na Mr Mwanjilo.Mr Mwanjilo anamsumbua sana Rayana kila siku ziendazo kwa Mungu ili ampate kimapenzi lakini kama ulivyokuwa msimamo wa Rayana,hakupenda mwanaume wowote kwani aliona kila mmoja ni msaliti tu.
"Aaah Rayana mke wangu hata jipya,kwana yupo Kitunda kwa mama yake"
"Kampe huko huko huo mtaji wako,hivi wewe mzee unadhani mi mrahisi eeh" Rayana akaendelea kuwa mkali mno.Majira hayo ya saa mbili ndio ulikuwa muda muafaka kwa Rayana kujaziwa na wateja.Akaanza kuosha vyombo vizuri ili isiwe tabu endapo akianza kuhudumia.
Ghafla akajikuta akijimwaga maji ya ukoko kwenye gari jeupe linalopita kando.
"Na nyie mnazidi hampigi honi makusudi aah " Rayana akahamaki.Gari hiyo ikasimama na dereva akashuka.Sura ya Swedy ikatoka huku akiwa na mikunjo ya hasira kwenye paji lake la uso.Wakajikuta wanatazamana kwa mshangao wa aina yake,Rayana akajiziba kinywa chake,macho kayatoa kwa wasiwasi,akajihisi ni mkosaji wa hali ya juu.
"Samahani kaka angu" Rayana akajitetea huku akipiga magoti lakini hakufika chini kabla ya kudakwa na Swedy.
"USIJALI" akasema maneno hayo na kuingia ndani ya gari lake.
Hakutegemea kabisa kama atakuwa ni mfadhili wake ambaye alijitolewa kwa pesa zake mwenyewe ili mradi aponye uhai wake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kumaliza biashara ya siku hiyo,akakusanya na kuweka vyombo vyake sawa baadae akaondoka kuelekea nyumbani.Huko aliwakuta baba na mama yake wakiwa nje wakisikiliza redio yao ambayo imetengenezwa kwa kutumia mbao za miti lakini wao mwenyewe wanaipenda kuiita REDIO MKULIMA,walitunukiwa enzi hizo kwa ukulima bora kabla hawajaama kijijini na kuhamia mjini.
"Hii redio ina miaka kumi na mitano hii"Mzee Gwamiro akazungumza kwa sauti ya mkwaluzo ikamuoneshwa zaidi kuwa umri wake ulikwishapiga hatua za kutosha.Mara baada ya kuwasalimia wazazi wake akaingia ndani kisha akarudi akiwa amebadilisha nguo zake.
"Mama hivi yule mkaka aliyetusaidia kunipeleka hospitali anaitwa nani vilee?"
"Nani Swedy au nani?"
"Ehee huyo huyo,leo si nimemwagia maji ya ukoko gari yake...mmh nimejisikia vibaya sana"
"Kwa nini?"
"Sikuliona,ila nataka kwenda kumuomba msamaha kwake wapi?"
"Kumuomba msamaha mpaka uende kwake?"
"Sasa ulitaka nimfuate wapi?" Rayana akahoji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmh we ntoto wewe usije ukatafuta mengine huko,kama ukimkuta na mchumba ake" mama Rayana akasema na kumuacha Rayana akitafakali jambo fulani.
"Basi mama nawe"
"Aaah mimi sio nakukataza nenda hapo mbele q kwa Mama Mou utaliona geti jeusi,ndio hapo hapo ila angalia sana mwanangu"
"Usiwe na wasiwasi mama"
"Mdogo wako yupo wapi?" Mama Rayana akauliza huku akitazama njiani.
"Mmh siku ya pili hii sijamuona,ngoja aje kupigwa huko na wenzake atambue kama kuna nyumbani".
Baada ya maongezi ya muda mfupi Rayana akaingia ndani na kuvaa khanga yake kisha akachukua ndoo ya maji,akaingia bafuni na kuanza kuoga.Burudani ya maji ya baridi akajikuta akipandwa na hisia kwa mbali za ngono kwa sababu tu hajapata kuingiliwa kwa muda mrefu na mwanaume yoyote.
"Mi mwezi sasa umekatika sijagindwa" akajisemea kwa kichwa chake.Alipomaliza akarudi chumbani na kupata mafuta yake ya mgando kisha akavaa nguo zake.Akajichomoa nyumbani hapo na kuanza kupita hatua ndogo ndogo kuelekea kwa mfadhili wake.
Kwa Mama mou akapita na hapo ndipo alipokutana na geti jeusi.Akalisogelea na kuanza kuligonga.Punde akatokea msichana mmoja aliyevalia tenge la bluu.
"Habari yako"
"Safi mambo" Rayana akaitikia
"Poa nikusaidie nini?" Msichana huyo akauliza.
"Samahani namuulizia Swedy yupo?"
Swali hilo likamfanya binti huyo amtazame Rayana kuanzia chini mpaka juu kwa dharau kisha akasema " we wa nini labda?"
"Ni kaka yangu"
"Swedy tangia lini ana dada?" Msichana huyo akaanza kuuliza maswali yaliyoanza kumchosha Rayana.
"Dada kama hutaki kuniruhusu niambie sio unipige maswali kama nimeiba gunia la mkaa" Rayana akarusha kiwembe na hapo ndipo urushaji wa makombola ya maneno kati yao yalipoanza.
****
Maneno ya hekima ya Inspekta Makurumla yakamuweka sawa Bosco ambaye alikuwa akiviruhusu vyupa vya pombe vipishane kwenye kunywa yake.
"Sikiliza ndugu yangu Bosco kunywa pombe sio suluhisho kabisa la wewe kumsahau Dayana,kumbuka yule ni Binti wa Raisi,huwezi kumuendesha hata siku moja,hizi pesa zako haziwezi kumfanya adate kwako,ni sawa na kusukuma ukuta ulioimalishwa kwa zege,mawazo yako ya kumkomeshwa mtu anayempenda sio sahihi kabisa.." Inspekta Makurumla akakohoa kidogo na kuchukua glasi yake ya pombe na kujimimia halafu akaendelea kumwaga maneno " Kumtoa mtu uhai wake ni sawa na kupakia zambi zote alizonazo yeye,Je ulikwisha wahi kujiuliza ni maovu mangapi ambao ameyafanya,lakini isitoshe ukichukua jukumu la kuua haha unadhani utaachwa hivi hivi na chombo cha dolla?, hata mimi nitakuwa wa kwanza kuendesha oparesheni hiyo ya kukusaka USIUE" Inspekta Makurumla akazungumza mengi sana.Bosco akaacha kabisa kunywa pombe yake,macho yake yakaanza kuikazia sura ya Inspekta Makurumla.
"Una Logic sana kaka mkubwa na ndio maana nikakualika wewe katika hili najua una ushauri mzuri" Bosco akazungumza huku akilalia upande wa kuafiki maneno ya Inspekta Makurumla.
"Anyway ila nataka tuifume ishu ya kupiga pesa ndefu,mimi naona wakati huu sio wa kutafuatana kwa sababu ya mademu kwani wapo wangapi?"
"Wengi sana" Bosco akajibu.
"Unaona eeh,yaani mchongo huu ukikaa sawa si chini ya dolla milioni hamsini tutainyaka" Inspekta akamuacha Bosco mdomo wazi.
"Dolla Milioni hamisi!" Akashangaa mno.
"Acha kubweka basi huoni kuna watu hapa?"
"Ehee hebu nipange mkuu"
"Kwanza hebu tuondoke hapa,hii ishu ni siri sana la sivyo tutajikuta tunaingia jela bila kutarajia.Maneno yakatoka mdomoni mwa Inspekta Makurumla ambaye aliwahi kuendeshwa oparesheni ya kumsaka gaiki aliyeitwa Mzee Kibangara.Pia alipewa jukumu zito la kumsaka mharifu mahiri anayeitwa Ramso lakini mwisho wake wakajikuta wanasakana kama mtu na ndugu yake.
KIMARA MBEZI JIJINI DAR ES SALAAM.
"Hapa ndio nyumbani kwangu,niliwahi kuingiliwa na majambazi hapa na kumteka mke wangu.." Inspekta Makurumla akamkaribisha Bosco huku akimuonesha baadhi ya mazingira ya nyumba yake.
"Aiseee pole sana"
"Yaani tabu tupu na kesho yake kazini mtuhumiwa akakimbia na kujeruhi askari mmoja" Inspekta Makurumla akazidi kumuelezea Bosco.Wakaingia ndani na kuketi kwenye sofa.Mama Karimu na pili akaingia sebleni akiwa amejitanda vizuri kama dini ya kiislamu inavyoruhusu.
"Huyu ni mke wangu kipenzi,ni mama wa watoto wangu wawili Karimu na Pili..nampenda sana" Inspekta Makurumla akasema.Mama Karimu akamuuliza Bosko kinywaji gani anatumia.
"Aaah kwa kuwa nimekunywa sana pombe nipatie maji tu shemeji" Bosco akaeleza.
Mipango madhubuti ya kusaka mamilioni ya dolla ikaanza.
*****
Ugeni wa familia ya raisi wa Rwanda ukagonga hodi ikulu ya Tanzania.Ugeni huo uliambatana na raisi wenyewe,mke wake,watoto wawili ambao mmoja wa kiume pamoja mwenye miaka ipatayo kumi pamoja ya mtoto wa kwanza wa kike mwenye miaka ishirini.Wakakaribishwa safi na kupewa hadhi kama wageni.Furaha ilikuja vizuri kwa Dayana kwani alipata rafiki yake wa kubadilishana mawazo.
"Naitwa Dayana Noel"
"Mercela ndio jina langu"
"Nice name (jina zuri)"
"You too(na we pia)"
Maongezi mafupi baina yao yakaendelea chumbani kwa Dayana huku wakitazama TV kwa pamoja.Wazo la kuomba ruhusa ya kutembea likamjia Dayana na huku akiamini kabisa wazazi wake hawataweza kukataa kutoa ruhusa.Wakajiandaa vizuri baada ya kumshawishi na kuondoka chumbani humo.Breki ya kwanza ilikuwa kwa Mama wa Dayana haswa ndiye anayemjulia kwa ruhusa kama hizo.Baada ya ridhaa ya wazazi wa pande mbili zote wakaingia garini huku wakiwa na mlinzi wao.Kitu cha kwanza kukifanya Dayana ni kumpigia simu Aidan.Akamjulisha wapi wakutane ili kwa pamoja wajumuike katika msafara huo.Gari hiyo inayoendeshwa na dereva pamoja na mlinzi mahiri anayefuata maelezo ya bosi wake ikaingia sehemu moja yenye bustani safi ya maua pamoja na miti ya kifuri yenye kutoa hewa safi na salama.Katika sehemu hiyo ikaoneshwa wazi kuwa ni sehemu ambayo hutumiwa sana na watu wenye uwezo wa juu,hali hiyo ilijidhihikisha pale tu walipofika getini na kuambiwa kuwa kiingilio ni elfu hamsini na pamoja na ada ya kuingia na gari ndani.Mlinzi akatoa kadi ya Dayana na kuingiza kwenye mashine ya kulipia kisha geti likafunguliwa.
Walipofika tu ndani tabasamu zikaanza kuchanua usoni mwao kwani kulikuwa na mvuto wa ajabu sana,maua yakiyokatiwa na kutengenezwa kwa umahiri yakaleta picha ya upendo na furaha katika mioyo ya wateja waliopata kuja eneo hilo.
"Waooh nimeipenda hii sehemu"
"Kweli yaani hii sehemu huwa sichoki kabisa kutembelea" Dayana akaeleza huku wakivuta viti na kuketi.Baada ya dakika chache wakalakiwa na mhudumu nadhifu kisha wakapewa menyu ya huduma zinazopatikana.
DENMARK RESTAULANT
Pilau......................Tsh 5000/=
Wali mweupe....... Tsh 3500/=
Kuku .....................Tsh 15000/=
Menyu hiyo yenye vyakula vya aina mbalimbali ikasome hivyo na kitu ambacho kiliwashangaza kidogo ni baada ya kusoma maelezo ya chini yaliyoandikwa kwa herufi kubwa na kukolezwa kwa wino mweusi 'SELFIE PICTURE TSH 10000' yaani kupicha picha za selfi ni elfu kumi za kitanzania,hakukuwa na mtu anayepiga picha katika eneo lile bila kulipia pesa.
Baada ya dakika kama kumi mbele akatokea Aidan na kuketi kitini,jasho jingi likiwa linamtoka huku akihema kwa nguvu hali ambayo ikamfanya Dayana ashangae na kumuuliza kitu gani nimemfanya awe katika hali ile.
"Jamani mbona unasweat namna hiyo?"
"Haaa! Si huyu boya wa getini eti mara ooh kuingia ni elfu ishirini na gari ni elfu hamsini,nikaanza kumpandishia anadhani mimi ni mshamba eeh" Aidan akaeleza.
"Aidan sasa tatizo lilikuwa nini pesa huna au?"
"Zimeisha mpaka sasa sina hata laki" Aidan akasema kwa sauti ya kudeka huku mtego wake ukitega kuingiza pesa kutoka kwa Dayana binti wa raisi.
"Ok anyway nitakupatia...vipi unatumia kinywaji gani?" Dayana akauliza.
"Aaaah sinywi chochote nataka burger na kuku wa kizungu wawili" Aidan akaeleza.
"Eeeeh tangia lini umeanza kula Burger?"
"Haaaa! Baby kwani hujui kuwa ndio napenda misosi kama hiyo?,hivyo ndivyo vyakula vya kijanja hapa town"
"Looh haya ila nipendi ule kuanzia leo,nakuagizia mara ya mwisho"
"Dayana kwani kuna ubaya gani mimi kula burger?"
"Nitakuelezea madhara yake"
Wakato maongezi ya wawili hao yanaendelea msichana Mercela alikuwa kimya akifuatilia maongezi hayo,hakupenda kutia neno kabisa.Dayana akachukua nafasi hiyo kutambulisha.
*****
"Mambo jamni Swedy"
"Poa"
"Safi mbona uko hivyo?"
"Niko vipi?"
"Inaitikia kimkato"
" kimkato ndio vipi?"
Maongezi hayo kati ya Swedy na Veronica yakafungua mjadala mpya wa malumbano chumbani kwa Swedy.Haukuchukua muda mrefu Veronica akaondoka huku akiwa anatokwa na machozi,kitu ambacho hakukijari kabiasa Swedy.
"Watu tumeona machozi ya damu sembuse hayo machozi yako.Nakupenda! Nakupenda! humpende nani pumbavu zako" Swedy akazungumza peke yake tena kwa sauti.Jumapili hiyo hakwenda kazini zaidi ya kukaa tu nyumbani huku akipata viburudisho vya hapa na pale.Kiburudisho kikubwa kwake ni kutazama movie za kimarekani huku akipiga vita movie za Kikorea zile za Misimu(season).Wakati anaendelea kutazama movie ya LONDON HAS FALL,akasikia mlango wako ukigongwa,akapunguza sauti na kuitikia hodi hiyo.
"Ingia" akaruhusu.
Mlango ukafunguliwa,sura ya Dynamo ikaingia ndani huku ikiwa na furaha mno.Dynamo ni rafiki mkubwa wa Swedy anayeishi katika mtaa huo wa Mburahati kisiwani.
"Vipi tena ndugu mbona una furaha sana leo?" Swedy akauliza.
"Aaah unajua leo sikujua kabisa kama ni jumapili,baada ya kusikia leo jumapili nikafurahi sana na nikajua kabisa Kijana wangu utakuwa upo kwenye movie sasa hivi haha"Dynamo akazungumza huku akimalizia na kicheko.
" Ndio unafurahi namna hiyo?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sio hivyo nimefurahi kwa sababu nimesikia sauti ya kilio huko nje huku jina lako likitajwa" Dynamo akaeleza.
"Achana nao ndio walivyo wasichana"
"Kwani umemfanya nini maana yupo na mama yake"
"Nimemchapa kwa maneno tu ndio hivyo analia,hebu una movie gani mpya?" Akauliza.Dynamo akachomoa flash na kumpatia Swedy kisha akaenda kuchomeka kwenye TV na hapo ndipo walipoanza kutazama.
Wakati wapo katikati ya Movie mlango ukagongwa kwa fujo sana.Swedy akapandwa na hasira na kuhamaki,akainuka na kupiga hatua kubwa kubwa,akaufungua mlango lakini akakutana na msukuno mkubwa.Mama Veronica akaingia akiwa na jazba za hali ya juu.Swedy akabaki akishangaa kwa nini Mama Vero amemsukuma namna ile.
"Mwanaizama mkubwa wewe,utaniambia kwanini umeniumizia mwanangu leo" Mama Vero akazungumza rangi yake ya macho imebadilika kutoka kwenye rangi yake ya kawaida na kuwa mekundu,ni wazi kabisa alikuwa na hasira sana.
"Nimekuumizia mwana...." Hapo hajafakiwa kumalizia sentensi hiyo kabla hajarukiwa na Mama Vero na kulambwa kibao kimoja cha adabu.Dynamo alipoonda hali tete akaingilia kati na kuanza kumgandua Mama Vero aliyemkandamiza Swedy chini.
"Mama Vero usataarabu haununuliwi,nina uwezo wa kukushtaki kwa kosa la kunifanyia fujo katika nyumba yangu haijalishi kama hii nyumba ya mume wako.Niache" akalalamika huku akijaribu kujinasua kutoka mwilini mwa Mama Vero.
Fedheha kubwa sana kwa Swedy,hakuna kitu kikubwa anachokichukua duniani kama ugomvi wa kushikana mashati.Vulumai likaendelea mpaka alipoingia Veronica.
"Mamaaaa!" Akagoma
"Nini na wewe unataka kumchekea! angelikuua" Mama Vero akazungumza huku akimuachia Swedy.Swedy akamkazia jicho Vero mpaka akahisi kitu fulani kibaya,ndio kuna ubaya mkubwa sana na sio wa kujificha,chuki za Swedy zikajionesha wazi haswa.
******
Gari aina ya Toyota Mark II yenye nambari za usajiri T CBA 547 ikakata pacha la fesitini na kuiacha barabara iendayo Mabibo,sasa ikawa imeshika barabara ya kwenda Manzese.Ndani ya gari hakuwa mwingine zaidi ya Aidan akiwa na msichana wake anayeitwa Debora.Wakaingiza gari mtaa mrefu na kuanza kuiendesha taratibu sana huku macho yakicheza nje na kuangaza huku na kule.Kama ilivyo kawaida ya macho,sifa yake kuu kwanza ni kuona.Aidan akabahatika kumuona Rayana akiwa anachakalika kwenye kibanda kuukuu,wateja waliokuwa wanatoka na kuingia wakamfanya awe bize zaidi kuliko kawaida.Akasimamasha gari na kutoka nje,akaingia kwenye mgahawa huo lakini mpaka dakika hiyo Rayana hakugundua kabisa kama kuna ujio wa Aidan katika mgahawa wake.Sura na mwili kwa ujumla alikuwa amebadilika sana,uso wake ule wenye vipele pamoja na mabaka meusi haikuwa hiyo tena zaidi ya kutawaliwa na unyororo na weupe.Tisheti iliyomkaa vizuri na kumchora kifua chake ikampendezesha zaidi lakini sio hivyo tu ambavyo vilimfanya Rayana asimjue vizuri Aidan kwani kichwani alifunika macho yake kwa miwani miyeusi pamoja na kofia.
"Wali maharage wapi?" Rayana akauliza.
"Hapa bana hunioni?" Mteja mmoja aliyekuwa na ndefu zilizochakaa na kufumuka akafoka.
Wakati Rayana anaendelea na huduma Aidan akavua miwani pamoja miwani na hapo ndipo Rayana alipopata na mshangao na kwa dakika kadhaa kisha akajikuta anamtazama kwa macho yaliyojawa huruma.
"Wapatie wanachotaka pesa nalipa mimi" Aidan akazungumza kwa madaha huku akichomoa waleti yake,akatoka elfu hamsini na kutoka nje.Rayana akabaki na mfadhaiko wa kipekee.
Akageuza gari palepale na kuanza kurudi alikotoka,safari hii alipanga aende kariakoo hakujua anaenda kufanya nini ni kutokana na halmashauri ya kichwa chake yanavyomtuma.Utanuzi wa wasichana tofauti ndio ulikuwa mtindo wa maisha yake ya kila siku,hakuwa na silaha nyingine kwao bali ni pesa anazoingiziwa kila wiki kwenye akaunti yake.
Aidan akaifunga breki yake nje ya duka moja la nguo mjini Katiakoo,wakaingia ndani na kumwambia Debora achague nguo aitakayo.Bila kusita mtoto huyu mwenye sura ya utaperi wa wazi akaanza kuchagua nguo za bei kali na Aidan akalipia,wakatoka na kuanza kuzunguka kwenye maduka mengine.
"Baby tuingie pale" Debora akazungumza kwa sauti ya kudeka.Kweli ile kauli inayosema AKIPENDACHO BINTI,MWANAUME LAZIMA ATANUNUA',wakaingia kwenye mlango huo ulioandikwa SONARA.Ndani kila pembe ya chumba hicho kilijaa vito vya dhahabu vyenye thamani tofauti.Debora akaanza kuchagua mikufu yenye vipande vya dhahabu,akachagua na pete pamoja na bangili za dhahabu.
"Shilingi ngapi hapo mkuu?" Aidan akauliza.
"Ahaa hapo kwanza Mkufu laki mbili na nusu,pete laki na ishirini..."Sonara akaorodhesha thamani ya vito vyote na Aidan akachomoa pochi,akatema pesa zote kisha wakaondoka.Mizunguko yao ikamfanya Aidan akumbuke kitu fulani cha nyuma,ni tukio moja alilofanyiwa na binti mmoja wa kihindi.Harakaharaka akajongea kwenye hilo na bahati mzuri alikuwepo binti huyo wa siku za nyumba.
"Mambo" Aidan akasalimia na kumfanya binti huyo ainue kuchwa chake na kumtazama.
"Poa karibu kaka angu" akajibu kwa uchangamfu.
"Unanikumbuka?"
"No! Sijakupata"
"Haha naitwa Aidan,nilishawahi kubeba mzigo wa viazi hapa ukanipa shilingi jero" maneno hayo yakamfanya binti awe kinywa wazi huku akihisi aibu kumtazama Aidan.
"Ndio weye kumbe naona maisha sio mabaya" Aidan hakuongea kitu chochote akachomoa simu yake na kumpatia binti huyo wa kihindi.
"Chora namba yako hapo basi"
Akaipokea simu huku akimtazama Aidan kwa uso wa kutabasamu,macho yake makubwa akayalembua na kuongeza uzuri wake.
'Unanilembulia mimacho nitakudinya mpaka uombe poo!' Akajisemea kimoyomoyo huku akisave namba hiyo,akachomoa noti ya elfu kumi na kumtupia binti huyo kwa dharau ya aina yake.
*******
"Nakuomba tukutane kwenye ile baa ya siku ile majira ya saa mbili usiku tafadhali,narudia tena nakuomba tukutane kwenye ile baa ya siku ile majira ya saa mbili tafadhali usikose.." Inspekta Makurumla akazungumza kwa sauti mzito ya chini huku akirudia kwa msisitizo ili anayeongea naye upande wa pili wa simu achukulie jambo kwa uzito sana.Baada ya kumaliza kazi saa kumi hiyo Inspekta Makurumla akaingia garini na kuondoka zake.Safari hiyo ikaongoza mpaka Tabata,akasimamisha gari yake nje ya geti jeusi na kuanza kulifuata.Akabonyeza kitufe cha alam ya geti na baada ya dakika tatu mlango ukafunguliwa na binti mmoja ambaye alionekana sio wa kisasa sana hivyo tu Inspekta Makurumla akabaini kuwa yule binti alikuwa mfanyakazi wa jumba hilo.
"Habari yako!" Inspekta Makurumla akazungumza.
"Salama shikamoo"
"Marhaba,baba mwenye nyumba yupo?"
"Ndio wapo wote karibu"
Inspekta Makurumla akakaribishwa,akaingia ndani na kufikia sebleni.Sebule kubwa haswa iliyosheheni kila aina ya vitu vinavyopaswa kuwepo katika eneo kama hilo.Sauti ya kufunguliwa kwa mlango ikasikiwa na punde akatokea mwanamke mwenye mtoto mdogo aliyembeba mikononi mwake.
"Oooh shemeji karibu sana" mwanamke huyo akamkaribisha Inspekta Makurumla kwa ukarimu.
"Shemeji asante sana hebu niletee mama yangu nami nimbebe kidogo" Inspekta Makurumla akapewa mtoto huyo na kuanza kucjeza nae.Akacheza nae kwa dakika mbili tatu mara kabla ya mlango wa chumba kingine kufunguliwa.Wakabaki wakimtazama mtu anayetoka chumbani humo.Ni mwanaume mrefu mwenye umbo jembamba.
"Habari kaka" jamaa huyo akauliza
"Salama tu,vipi ndugu yangu unalala jioni yote hii?" Inspekta Makurumla akahoji.
"Kaka uchovu tu,leo nimerudi ofisini mapema sana nilichoka mno"
"Sawa Ramso ila Gadna simuoni yupo wapi?" Swali la Inspekta likampa tabasamu fupi Ramso na hapo akajibu " leo baada ya kurudi shuleni kaja kuchukuliwa na mama yake mdogo Zulfa" Ramso akajibu kwa ufasaha.
"Kwa hiyo yupo Mbezi mwisho eti!"
"Ndio"
"Anaoenda ubwabwa yule utadhani kazaliwa pwani" Insepkta Makurumla akatania na wote wakacheka.
Familia ya Ramadhani au anavyopenda kujiita Ramso ikarejewa na furaha sana baada ya kupitiwa na matatizo mengi sana miaka ya nyuma ikiwemo kutafutwa kama jambazi sugu pamoja na kuiba katika mabenki mbalimbali.Maisha hayo yakatokomea na kuja kuwa ya furaha za kupitiliza huku akijisifu kwa kupambana vya kutosha katika kila tatizo lililomkuta.Sasa amebahatika kupata mtoto wa pili wa kike na mke wake Christina anayeitwa Leila.Ramso pia amefanikiwa kufungua hotel zake mbili za kufahari huku akisaidiana na dada yake Zulfa,ni hatua kubwa sana ya kimaisha aliyoifikia.
Ilipohitimu saa kumi na moja Inspekta Makurumla akaaga na kuondoka zake.Akawa anaelekea nyumbani kwake Mbezi huku kichwani akiona majira hayasogei hata kidogo ili akutane na Bosco wapange mikakati ya mwisho ya kuvuta pesa ndefu.Alitamani sana kumueleza juu ya kitu kipya alichokiwaza.Kadri mawazo yake yanavyozidi kugongana kichwani mwake ndio safari yake ya Mbezi ikazidi kuonekana fupi.Hatimaye akafika nyumbani kwake,akakutana na kelele za watoto wake waliokuwa wanacheza sebleni.
Akaingia chumbani kwake na kibadilisha nguo kisha akaingia bafuni,akajimwagia maji haraka na kurudi kitandani, akafungua kabatoli lake la nguo na kutoa nguo ambazo zitampendezesha jioni hiyo.Alipomaliza kuzivaa akatoka na kumuaga mke wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
'CHELEWA CHELEWA UTAKUTA MWANA SI WAKO' ndio yalikuwa mawazo ya Inspekta Mkaurumla yaliyogongana kuchwani mwake,akachomeka funguo ya gari kwenye swichi na kuliwasha.Akaondoka huku kila baada ya dakika mbili akubadilisha gia za gari yake.
Saa yake ya mkononi ikasomeka kama ni saa moja na dakika arobaini na tano.Maeneo ya ubungo ndipo foleni ilipoanza,ikamlazimu achukue muda na kukaa kwenye foleni hiyo.Mpaka gari zinaruhusiwa ilishatimia saa mbili kamili.Akawa na zoezi ka kufika kwenye baa ambayo walipanga wakutane na Bosco.
"Nimekuweka sana au?" Inspekta Makurumla akahoji.
"Hapana ndio kwanza naanza bia ya kwanza aaaah umekuja muafaka kabisa" Bosco akajibu kwa utulivu.
"Ok sasa mipango yetu ianze,nina habari mpya leo" Inspekta Makurumla akazungumza kwa sauti ya chini.Bia zikaletwa na wote wakaanza kunywa taratibu.Kila mmoja baada ya kupata bia mbili mbili maongezi yakaanza rasmi.Inspekta Mkaurumla akakohoa na kumeza kikohozi kisha akaanza kwa kusema.
"Nimenasa taarifa kuwa Ikulu ya raisi kuna ufeni wa raisi kutoka Rwanda,lakini ule ugeni unafaidi ya pili kwetu"Inspekta Makurumla akazungumza na kumuacha mdomo wazi pamoja na maswali mengi kichwani mwa Bosco.
"Sijakuelewa kaka unamaanisha nini"
"Tunaenda taratibu utanielewa tu.Ugeni ule wa raisi kuna binti yake na huyo tunaweza kumtia nguvuni maana wanapenda sana kufuatana"
"Achaa bana hahaha" Bosco akafurahi kidogo kisha akasema "unajua nafurahia nini?"
"Sijui"
"Navuta picha nikiwatia nguvuni si nitajilia uroda wote wawili" Bosco akazungumza.
"Hahah we dogo huna akili" Inspekta Makurumka akatania.Maongezi yakaendelea na kilichobaki ni kupanga vikosi maalumu vya watu wachache vitakavyowawezesha kuwateka mabinti hao.
"Mimi nitaongea na askari wangu wawili vinaowaamini tutasaidiana nao kikamilifu sawa!"
"Sawa mkuu"
Inspekta akatoa bahasha ndogo kisha akazitoa picha mbili za mabinti hao.
" Huyu ndio mtoto wa raisi wa Rwanda"
"Ohooo daah kazuri namna hii"
"Achana na mapenzi kwanza katika kazi utafeli katika maisha yako" inspekta akasema na kumfanya Bosco atulie.Hakika Inspekta Makurumla alidhamilia sana kuwateka mabinti hao kwa nguvu zake zote na akili pia.
"Unadhani bila kufanya hivi tutakuwa matajiri miaka gani?" Swali hilo la Inspekta likamuingia vizuri Bosco.
"Unaona eeh" akakili maneno hayo.
Wakati wanaendelea na mkakati huo simu ya Inspekta ikaanza kuita.Akaitoa mfukoni na kuipikea.
"Nipe mpya Zakaria" Inspekta akaitika.
"Ndio sasa kaka wiki ijayo hawa watoto wanasafiri kuelekea hifadhi ya SADANI kutazama wanyama lakini watakuwa na walinzi watatu wenye uzoefu sana,safari itahusisha watu kama saba wakiwemo hao mabinti,kwa hiyo fanya kila linalowezekana mutekeleze kazi yenu,lakini kumbukeni pesa yangu iwepo palepale" Sauti toka upande wa pili ikaeleza vizuri na kwa mchanganuo usio na swali lolote.
"Usijari dogo kila kitu kinachoendelea utatutonya,utakaa ikulu kupika mpaka lini?" Inspekta akahoji lakini swali halikupata kujibiwa kabla ya simu kukatwa.
"Unasikia mchongo huo dogo Mapenzi?"
"Haha kaka jina gani hilo" Bosco akajibu kwa utani na wote wakacheka.
******
"Hivi baby utaniongezea lini mzigo maana nguo zenyewe zimebaki chache tu,jana sijafungua na leo pia" msichana huyo mwembamba akalalamika huku akiwa kifuani mwa Aidan.Kikubwa anachotaka kwa Aidan ni kuongezewa mtaji wake wa duka la nguo alilofunguliwa na kijana huyu mpenda wanawake Aidan.
"Ahaaa nina mambo mengi baby nitaingiza kwenye akaunti yako kesho" Aidan akazungumza hivyo.Mabusu ya wizi yakaanza kumwagikia Aidan kwa maneno ya ushujaa mbele ya binti huyo.
"Ndio maana nakupenda sana Aidan wangu" msichana huyo akasema.Wakaanza kuvutana na kupapasana,hatimaye wakajikuta wanavuana nguo zao na kuingia kwenye mchezo wa kikubwa.
Baada ya masaa matatu wakiwa wamelala kila mtu kwake wako hoi bin taabani,simu ya Aidan ikaita,jina likasomeka Dayana.Ilikuwa saa tatu za usiku,ndipo simu ikapokelewa na wakaanza kuongea.
"Baby nakutakia safari njema mimi nitaendelea kukutunzia penzi lako nakupenda sana" Aidan akazungumza kwa sauti ya chini ili asimwage mchele kwenye kuku wengi.
"Sawa nimemisi sana pigo zako" Dayana akazungumza.
"Nitakupa ukisharudi usiwaze"
"Sawa"
Maongezi hayo yakaisha na Aidan akageuka na kumtazama msichana wake ambaye amelala fofofo!.Akavuta shuka na kumkumbatia usingizi ukaendelea.
*****
"Nisamehe mimi jamani Swedy,nimekukosea najua ila naomba unisamehe" Veronica akalalamika huku akipiga magoti mbele ya Swedy.
"Katika Maisha hata siku moja usije kufanya kosa ukajivunia msamaha,kumbuka kuwa hapa duniani tupo watu tofauti na kila mmoja ana muono wake juu ya jambo fulani.." Swedy akazungumza kwa hisia huku akimuachia maswali kadha wa kadha Veronica.
"Una maana gani "
"Mapenzi hayalazimishwi,mapenzi hayatumii nguvu,mapenzi hayahiyaji hasira na mapenzi ni maridhiano baina ya watu wawili...nadhani umenielewa"
"No! Swedy I love you"
"No one love me but myself" baada ya Swedy kusema maneno hayo akafungua mlango wa nje na kuondoka zake huku akimuacha Vero akibubujikwa na machozi.Lawama zote akawa anazitupa kwa mama yake baada ya kumvamia Swedy na kuanza kumpiga wakati kwa kawaida sio sahihi kabisa.
"Why mama umenifukuzia ndege wangu why" akazungumza peke yake huku akijaribu kujifuta machozi kwa kutumia kanga yake.Akatoka nje na kutazama huku na huko lakini hakumuona Swedy.Akalitazama gari lake na kubaini lipo na hapo ndipo alibaini kuwa yupo katika mazingira yaleyale.Akaingia ndani na kukaa chini peke yake huku sura yake ikiwa imetowekwa na furaha.
Mara Swedy akaingia ndani akiwa na Rayana.Jicho lake la kwanza likatua kwa Rayana,akakumbuka siku moja walishawahi kutupiana vita ya maneno na msichana huyo.
"Ahaa kumbe kinyamkela huyu anayenifukuzia mali yangu" Vero akajisemea mwenyewe huku akiwasindikiza wawili hao mpaka walipozama chumbani.Baada ya dakika tano Rayana akatoka huku akiwa na furaha mno kitendo ambacho kilimfanya Veronica aanze kuumia moyoni mwake.
'Hapana lazima nimuoneshe huyu malaya wa uswazi' akasemea tena Veronica kisha akainuka na kuanza kumsindikiza Rayana kwa jicho baya.
*****
Gari tatu zenye rangi nyeusi zikajazwa mafuta katika vituo tofauti kisha zikawa zimepaki ndani ya jumba la Bosco huku kila gari kukiwa na watu wawili wenye silaha kali.Inspekta Makurumla alikwishawapata vijana wake watatu ambao walishirikiana moja kwa moja na Bosco.
Mavazi meusi yaliyoambatani sawia na mask za usoni yakawakaa vizuri huku kila mmoja akiwa ameshikilia SMG.
"Hakikisha mnabeba na kamba zote" Inspekta Makurumla akatoa agizo.
"Sawa mkuu"
"Kila mmoja ana pistal?"
"Bila shaka"
Hawakataka kupoteza muda ndipo walipoingia kwenye gari zao na msafara ukaanza.Wakafika kwenye barabara kuu iendayo Bagamoto,hapo wakaongeza mwendo ili kuwahi misheni yao.
'TUTAKUWA LINI MATAJIRI HAPA DUNIANI' maneno haya yalijirudia kichwani mwa Bosco mara tatu tatu.Ikamuongeza uchungu na hasira mno.
"Yeah Money is first" Bosco akakili.Mwendo wa nusu saa mzima bado walikuwa njiani kuelekea kwenye eneo la tukio.
Hatimaye wakafunga breki katikati kabisa ya msitu mdogo ambao ulitenganisha nyumba za raia wa upande wa Dar es Salaam na wa Bagamoyo.Wakaingiza gari zao ndani ya pori na kutoa silaha zao.Wakaanza kujivesha nguo zao maalumu kiasi kwamba kwa haraka huwezi kuwatambua hata kidogo.Wakashika SMG zao na kuzishika mikononi kikamilifu.Mmoja wao akatoa Lap top na kuiwasha kisha akaunganisha na kifaa alichoweka sikioni ni kama kinasa sauti lakini hiki kilisaidia upatikanaji wa mawasiliano baina ya pande mbili.Kila mmoja alikuwa fiti na hakuna aliyeonekana hata rangi ya ngozi yake.
"We are going to make money my friends,so we need more care.Tukishindwa basi tambueni tutaenda kufia jela sisi wote.." Bosco akatoa maneno machache kisha akachuku kisu na kukichomeka kwenye kiatu chake.Akachukua na bastola iliyokwisha wekwa magazini na kuipachika kiunoni mwake.
"Wamekwisha toka tayari na sasa wako Bunju,nawaomba muwe makini sana kuna gari tatu kwenye safari hiyo moja ya mbele ina vibaraka tu na ya pili ndio ina wahusika wake" Sauti ya Inspekta Makurumla ikaeleza kutoka kwenye vifaa vya mawasiliano.Bosco punde akaanza kuwagawa,wachache wakaenda upande wa pili wa barabara na wengine wakabaki upande uleule.
'Wananikumbusha mbali sana haya mambo haha' Bosco akajisemea mwenyewe huku akiweka vuzuri SMG yake.
Baada ya nusu saa mbele milio ya gari ikaanza kusikika ikivuma kwa sauti ya juu,hapo ndipo wakajikuta wakijiweka sawa na kuwa tayari kwa jambo lolote mbele yao.
"Hizo ni Audi kama sikosei" mmoja akasema.
"Kwa nini?"
"Milio yake naipata vizuri sana"
"Sawa jiweke tayari"
Wakaanza kuyaona magari hayo yakiwa mwendo kasi mno hapo ndipo akili ya kila mmoja ikaanza kucheza.
Kitendo cha ghfla mno,gari ya mbele ikaanza kuyumba na kupoteza muelekeo,ikaelekea porini kwa kasi ya ajabu mpaka ilipokita kwenye mti mkubwa.Risasi iliyofyatuliwa na mmoja wa askari hao ikapelekea kupasuka kwa tairi ya mbele ya gari hiyo.Gari ya kwanza na ya pili zilipoona tukio hilo zikafunga breki za haraka na jamaa wawili wakachomoka huku mikononi wamekamata bastola zao.Hofu zikaanza kutanda katika msafara huo.Mara na wao wakajikuta wanaanguka chini na damu zikaanza kuwavuja.
Hawakuchukua dakika nyingi mara jamaa hao wenye silaha kali wakaanza kuwashambulia waliobakia na hatimaye wakajikuta wanawafikia mabinti hao.Wakawachomoa garini kisha wakaziba vitambaa vyeusi na kuzama nao msituni.Haraka gari zikageuzwa na kuifuata barabara hiyo ya Bagamoyo huku wakiwa na furaha mno.
"Kazi imemalizika ndani ya dakika mbili tu mkuu" Bosco akaeleza kupitia simu yake kwa sauti kubwa tofauti na siku zote.
"Safi sana,sasa nimekwishamtaarifu kijana wangu huko Bagamoyo atakupokeeni hapo kwake"
"Sawa"
******
Damu zikaendelea kumvuja kufuatia na kipigo kikali cha mbwa mwizi kilichotembezwa na Veronica pamoja na rafiki zake dhidi ya Rayana.Ulikuwa ni usiku wa saa nne mara baada ya Rayana kufunga mgahawa wake na hapo ndipo alipokutana na Veronica akiwa na wenzake.
"Leo utakoma malaya wewe mpalamia wanaume za watu.." Veronica akazungumza kwa ghazabu huku akivuta masikio ya Rayana kwa nguvu.
"Lakini mnanionea bure tu sina mwanaume wa mtu unanionea buree" Rayana akazungumza kwa sauti yenye kwikwi iliyokuwa inashindana na kilio.Wasichana wanne waliokuwa wanachangia kipigo hiko walifanya kitendo hiko kama jambo hilo linawagusa wao.Walipohakikisha kipigo kimemuingua vizuri na kuamini kabisa hatothubutu kumsogelea mwanaume wanaempigania wakakimbia zao.Rayana akabakia chini huku machozi yakimtoka.Akajiinua na kuanza kurudi nyumbani kwake.
Hakuna kitu kingine kinachomfanya Rayana apatwe na maswaibu ya kila aina zaidi ya Mapenzi.Sehemu anayodhani kuna hafueni mwisho wake huambulia patumu.Akiwa katika mawazo njia mzima akashtushwa na mlio wa honi ya gari,alipogeuka akakutana na gari ya Swedy ndipo machozi yalipozidi kumbubujika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unalia nini Rayana?" Swedy akauliza kwa mshangao kwa sababu ni ghafla na ni ajabu kumkuta Rayana akilia kama mtoto mdogo.
"Kwe...li Swedy unanifanyia hivyoo,ni wewe wa kuwatuma wanawake zako waje kunipiga mimi ,niambie nimetoka na wewe lini Swedy ni...ambie" Rayana akalalamika huku akiwa amelikunja shati la Swedy,kwa hasira na uchungu akawa analia na kamasi jembamba linamchuruzika.
"Hebu tulia Rayana una nini?"
" si unajifanya hujui,sawa " Rayana akaendelea kulalamika kwa uchungu lakini bado haikumzuia kuficha hasira zake.
"Unajua hasira haziwezi kusolve jambo,tafadhali naomba unyamaze kisha uniambie kitu gani unalia..."Swedy akaeleza.Akamchukua Rayana na kumuingiza ndani ya gari,akaanza kuiendesha gari mpaka kwa akina Rayana.
"Nyamaza tafadhali"
Wakashuka na kuingia ndani,mzee Gwamiro na mke wake tayari wakikwisha pumzika kwani muda ulikwishakwenda vilivyo.
"Yaani sijui kitu gani nimefanya mpaka nahazibiwa kiasi hichi..kweli kaka yangu,mfadhili wangu niliyekutumai lakini leo unamtuma yule msichana wako wa kule kwenu!" Akaeleza kwa hisia kali.
"Nani Vero?" Swedy akaulizwa kwa sauti ya juu iliyojaa hasira.
"Sijui huyo labda"
Hapohapo Swedy akageuka haraka na kuingia garini,akatoka kwa kasi huku akiamini kuwa Verpnica ndiye aliyefanya tukio hilo kwa binti wa watu.
******
"Baby hii laki tano haitoshi naomba uniongeze laki mbili nipate hata kufungua mradi,si unajua mwanamke mpaka awezeshwe?" Sauti nyororo ya mrembo ikapenya ndani ya ngoma za sikio la Aidan.Bado mdudu wa ngono unamsumbua kupita kiasi,zile pesa anazoingiziwa na binti wa raisi Dayana zinampandisha ukichaa wa hali ya juu.
"Ahaaa usijari navyokupenda mpenzi sidhani kama nitakuja kukutosa,nakutumia kwenye akanti yako sawa baby?"
"Sawa baby uko wapi sasa hivi nije huko,nimemisi joto lako" sauti ikaendelea kumlaghai.
"Nipo klabu fulani hapa hapa Kawe ila baada ya dakika ishirini nitakuwa home,kama vipi nikukute funguo zipo palepale".
"Sawa baby mwaaah" busu la ukuda likapigwa na simu ikakatwa.
Aidan yupo kaunta chupa kadhaa za bia zikiwa zinelazwa kwenye ubao huku chupa kama tatu zikimsubiri.Mziki laini ndio uliokuwa unamchanganya zaidi,akaanza kukichezesha kinywa na mguu mmoja akiurusha kufuata mdundo wa mziki huo.Ghafla macho yakamfikia msichana ambaye alikuwa akizungusha kiuno taratibu,ni mziki pekee ndio unaompagawisha.
"Cheki mtoto kiuno kinachotweki loooh wallah Aidan mwaka wangu huu" Aidan akazungumza peke yake huku akiendelea kunywa bia yake taratibu.Kadri dakika zinavyoenda ndipo Aidan anapoona faraja kumtazama binti yule anayecheza mbele ya mboni zake,akaichukua chupa moja na kuinuka nayo kisha akaanza kuyumba yumba huku akimfuata msichana huyo. Kwa kuwa alikuwa anacheza peke yake ikawa rahisi kwa Aidan kumfuata na kumuomba acheze naye.Bila kipingamizi chochote akaanza kucheza naye.Akafika hadi hatua ya kuwa karibu nae mno hapo ndipo Aidan alipoanza kuongea nae.
"Mambo mrembo"
"Poa"
"We ni mzuri sana unalijua hilo"
"Hapana sijui"
Majibizano yaliyotawaliwa kwa majibu ya mikato kwa wawili haya yaliendelea huku wakiyumbayumba kwa pombe ambazo zimepakiwa kwenye vichwa vyao.
"Naomba nitoke na wewe leo sawa" Aidan akachombeza.Binti akaanza kutabasamu huku akinyakua bega la kushoto kuashilia hayupo tayari.
"Mmmh mrembo unaniangusha"
"Nimekuja na mtu wangu hapa"
"Sasa mimi nyani,mimi ni mtu kama huyo mtu wako" Aidan akaendelea kuimbisha pasi kuchoka.
"Your non sense" kauli kali ikatoka kwa msichana huyo,akageuka na kumtumbulia macho.
"Tazama mfukoni" Aidan akafungua mfuko wake wa shati.
"Waoooh"akafurahia baada ya kuona pesa zikiwa zimejipanga kwenye mfuko.
"Twende home basi" akazungumza huku akimvuta msichana huyo.Kichwani mwake alisahau kabisa kama alipigiwa simu na msichana mwingine na kumpa ahadi ya kukutana kwake,sasa hivi anamchukua msichana mwingine na kuingia nae kwenye gari kisha safari ya kwenda nyumbani kwake.
Mapenzi hayana nguvu kabisa kwenye pesa kwa dunia ya sasa na ndio kila siku udhinifu unazidi yote kisa NGUVU YA PESA.
Aidan hakukawia kuondoka na msichana huyo huku kila mmoja yupo vizuri kichwani mwake.
"Nataka nikakuoneshe mambo mtoto mzuri" Aidan akajitapa kwa sauti ya kilevi.
"Huwezi kitu wewe,leo ndio utanijua kama mimi PAIN KILLER ya wanaume wote wa mjini.."akazungumza kwa madoido kisha akaivuta sketi yake juu mapaja yake yakamwagika nje,akatabamu na kusema "Unajua kitu kinaitwa KANTELELO? " Msichana huyu aliyegubikwa na pombe kichwani akasema kwa upole.
"KANTELELO!" Aidan akastaajabu.
"Ndio"
"Kilugha gani hiko?"
"Jibu swali langu unajua KANTELELO?"
"Walaa sijui mwenzako jina lenyewe tabu tupu"
"Heheeee sasa mwenzetu unajua mambo kweli kama hujui KANTELELO" akacheka kwa mkwala huku akiyalegeza macho yake.
"Mmmh"
"Sasa basi nitaenda kukuonesha KANTELELO leo,ila kama sio mvumilivu naomba usiniruhusu kukupa hii kitu"
"Kwa nini?"
"Kantelelo ni nguvu kuvumilika na inavumilika kwa wanaume nashabab tu" akamtisha.
"Acha zako wewe mimi mwenyewe Shabab,kwanza sio shabab tu mimi zaidi ya Al-kaida" Aidan akatamba.Maongezi yote yakafanyika wakiwa katikati ya safari ya kuelekea Kawe.Maneno ya Mrembo huyo yakamuweka katika pumbazo la ajabu huku akiwa na hamu kubwa ya kupewa huo mchezo unaojulikana kwa jina la KANTELELO.Hakuwapa kulisikia jina hili hata siku moja lakini siku hiyo ndio rasmi katika masikio yake.
Mpaka inahitimu saa nne na dakika zake kumi na sita,gari ndogo ya Aidan ikafunga breki nje ya nyumba yake.Akashuka na kumfungulia mlango.
"Twende Mama ukanioneshe Kantelelo"Aidan akazungumza na kumshika kiuno,wakawa wanavutiana kuelekea mlangoni.Kabla hajaufikia mlango akakumbuka kuwa ana kawaida ya kuweka funguo sehemu fulani,aliposogea na kupapasa akashtuka kidogo.Akabaini kuwa funguo yake kuna mtu kaichukua.Akawa akavuta kumbukumbu lakini zikashindana na pombe zilizo kichwani.Akatekenya kitasa na mlango ukafunguka,akaingia nae ndani kisha akaurudisha mlango.
Ndani hawakuamini kabisa kama kuna mtu,hapo ndipo kasheshe likaanza.
"Ehee Aidan lazima uniambie huyu ni nani yako.." Msichana huyo ambaye alijilaza juu ya sofa akazungumza kwa hasira huku akiinuka.
"Kwani wewe nani na umeingiaje humu ndani?" Aidan akauliza kuwa kama haelewi kinachoendelea.Ghafla msichana akaruka na kumshika shingoni msichana ambaye alikuwa amejishikilia kwenye mwili Aidan,wakaanza kuvilingishana huku na kule ili mradi wa kila mmoja amshinde mwenzake.
Purukushani zikaanza huku Aidan akashindwa kabisa kuamua ugomvi huo.
"Piganeni atakae kuwa mshindi ndio mali yangu leo pumbavuu" Aidan akatokwa na maneno mabovu kutokana na pombe aliyoifakamia kwa pupa.
*****
Gari hizo zenye uwezo wa aina yake zikafunga breki nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.Wakawatoa binti hao na kuwaingiza ndani.
"Mmmh mmmmh" sauti toka nyuma ikasikika ikilalamika na kuwashtua baadhi ya jamaa huyo.
"Oyaa kidudu gani hiko mbona kama kuna mtu mwenye buti" mmoja akahoji.
"Hahaha kumbe hamjaniona wakati namfanyia huyo jamaa?" Bosco akacheka kisha akaendelea kusema "kuna mlinzi wa wale mabinti namjua vizuri sana huyu atatusaidia katika mambo kadha wa kadha" Bosco akazunguka nyuma ya gari na kumtoa mlinzi wa Dayana.
"Sasa huyu umembeba wa nini atatutoroka huyu alafu aharibu mipango" jamaa mmoja akafoka na kutoa bastola yake.
"Aaaah acha ufala unataka kufanya nini sasa?" Bosco akafoka kwa ghazabu huku akimuoneshea bastola jamaa aliyekuwa anabishana naye.
"Eeeh eeeh upumbavu gani mnaufanya au mnataka niwafukuze hapa maskani,watu mnakuwa kama watoto wadogo akili zenu kama mavi..." Mwenyeji wao akazungumza kwa hasira kufuatia utovu wa nidhani wa wawili hao.
"Kama hamna nidhamu na kazi nitawatimua tu...ingia ndani wote mabwiga nyie" jamaa huyo akakoroma kiasi kwamba wakina Bosco wakaanza kuogopa.Mwenyeji huyo mwenye sura ngumu na mwenye mwili mkubwa,Mabega yote yalikuwa na tatoo zenye michoro ya ajabu na ya kutisha.Upande wa Shavu lake kulikuwa na mstari,mstari ambao ulibainika kama kovu lililotokana na kushonwa kwake.Hakika jamaa huyo akitisha mno.
"Kaeni pale"akaamulu na wakina Bosco wakafanya hivyo kwa haraka mno.Akaanza kutembea huku na huko huku sura yake ameikaza na kuwa mbaya kama ya mnyama.Taratibu kila mmoja wao akaanza kutetemeka kwa hofu .
"Sikilizeni kwa makini madogo" akaanza kusema hivyo kisha akachomoa sigara yake,akaiwasha na kuvuta fundo moja kisha akatoa moshi mwingi puani "Wananiita MK nina maana ya Master Killer.Kuua kwangu ni kama chakula cha siku mzima,So huu ujinga unaoufanya nitampoteza mtu dakika sifuri,sitaki ujinga katika kazi,naweza kuwaua na nikamwambua Inspekta wenu aje kuzoa mizoga yenu.Nina miaka takribani kumi katika kazi hizi lakini naona nyie maboya ndio mnajifunza.Sasa basi lazima mtafata kile nachokisema Sawa...?" Jamaa huyo anayeiita MK akaeleza kwa sauti kubwa sana iliyojaa vitisho.Alipowapa maneno hayo akawaita kwenye chumba kimoja chenye giza mno.Alipowasha taa wakastaajabu kuwakuta mabinti hao wakiwa na mlinzi,wamefungwa mikono yao kisha ikatundikwa juu.Usoni hawakuonekana zaidi ya mizula waliofukwa nayo.MK akawasogelea Dayana na kumtoa mzula wake.Akaanza kumkazia jicho kana kwamba anamtishia na jinsi lile kovu lilivyokuwa kubwa likamuogopesha sana Dayana hapo hapo kaanza kulia kwa sauti.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Shiiiii"MK akamnyamazisha kwa kumuwekea kisu shingoni.Dayana akanyamaza na kubaki akimtazama,mwili wake ukashindwa kabisa kuzuia jasho,likaanza kumlowesha na mtetemo ukawa unasumbua mwili wake.MK akamfunika na kumfuata binti wa pili,nae akamfanyia kama alivyomfanyia Dayana halafu akamalizia na mlinzi lakini huyu akamtishia kitofauti kabisa.Akaanza kwa kumtupia ngumi ya tumbo na hapo ndipo alipotapika.MK akasimama vizuri na kuanza kumtupia maswali.
"Unafanya kazu gani"Akauliza kwa sauti ya chini sana iliyojaa uzito kama mtu aliyefunikwa kwenye chungu.
"Mimi?" Mlinzi akauliza na hapo ndipo alipokaribishwa kwa kichwa kigumu cha MK.
"Sipendi kuulizwa maswali,nataka ujibu swali rafiki yangu" MK akazungumza kwa upole.
"BodyGuard wa mtoto wa Raisi" akazungumza kwa shida huku akiipikicha mikono yake kwa lengo la kujishika sehemu alipopigwa kwa kichwa cha MK.Mlinzi huyo ambaye ameanza kuyajua machungu kubeba dhamana ya kuwa mlinzi akaanza kujutia nini kilichomfanya aingie katika kazi ile.
'Why me! ningelisoma na kuwa mwalimu si ningelikula pesa mzuri tu aaah ona sasa nakufa leo...eeeeh Mungu nisaidie sana nisife mja wako bado familia inanitegemea" mlinzi huyo akaomba kimoyomoyo kisha dhamana yote ya kuwa katika mikono salama akamuachia Mungu.
Master Killer au kama anavyopenda kijiita MK,akawaita Bosco na wenzake mpaka kwenye chumba kidogo,huko wakamkuta mtu mmoja akiwa anachezea kompyuta na mitambo mingine iliyomjazia mezani kwake.
MK akaketi juu ya kiti na kumtaka jamaa huyo aingize namba ya Inspekta katika mashine moja.
"Nimewapokea vijana mzee ila wanaonekana ni wageni wa kazi mno" MK akazungumza kupitia mashine hiyo inayotoa sauti bila bughuza ya aina yoyote.
"Wavumilie wazazoea tu anko" Inspekta Makurumla akajibu
"Ok sasa baadae tuwasiliane kwa mtandao wetu wa siri"
"Sawa MK usiwe na shaka"
MK akakata simu na kuwatazama wakina Bosco kisha akasema " Kuanzia sasa hakuna kuzungumza na simu zenu za kawaida,mtakuwa mnazungumza kwa kutumia hii mashine hapa" MK akasema.
"Kwa nini kaka?" Bosco akauliza kwa sauti ya upole.
"Nina maana kwamba hizo namba zenu sijua za Voda nini Tigo,airtel na zingine zinanasa maongezi yetu na hii kazi yetu kama mnavyoijua" MK akaelezea kisha akasimama.
******
Taarifa ya kwanza ambayo ilishtuwa umati wa watu nchini ni juu ya ajali kubwa ambayo imetokea katikati ya msitu mdogo barabara ya kwenda Bagamoyo lakini taarifa zingine ambazo ziliwaacha hoi zaidi watu ni juu ya kutekwa kwa mabinti wawili na maraisi.Taarifa hii iliwafikia na kuwachukiza kikali familia ya raisi wa Tanzania pamoja na raisi wa Rwanda.Noel Mkwakwacha alichanganyikiwa vilivyo kufuata utekwaji wa binti yake na mbaya zaidi hakukua na taarifa zozote zilizosikika juu ya upotevu huo.
James Goba nae akazipekea kwa uzuni mkubwa sana juu ya taarifa hizi kwani kutokana tu na upendo aliokuwa nao kwa binti huyo.Mawazo ya kumtafuta Aidan yakamjia vizuri akiamini kabisa kuwa lazima Aidan atakuwa anachangia kwa namna moja ama nyingine.Siku hiyo hakupenda ipite hivihivi akaingia ndani ya Hammer na kuanza safari ya kwenda Kawe kwani alikumbuka siku moja aliambiwa na Dayana kuwa amempangia nyumba mzima mtu huyo.Akakanyaga mafuta kwa haraka sana.Hatimaye akafanikiwa kufika Lugalo ndipo alipokutana na foleni.Ikamlazimu asimame ili kusubiri foleni hiyo.Akachokoa sigara na kuiwasha.Baada ya dakika tano gari zikaanza kuruhusiwa.James Goba akaendesha kwa kasi huku akiovertake baadhi ya gari mpaka akaifikia kona iendayo Kawe.
James Goba akafika nyumbani kwa Aidan na kusimamisha gari yake.Akaanza kupiga hatua ndogondogo kulifuata geti.Akawa anagonga geti zaidi ya mara tano lakini ukimya ukatanda kwa muda mrefu,James Goba akagundua kuwa lazima tu Aidan atakuwa anahusika katika tukio hilo.Akaingia garini huku kichwani akiwa na imani na Aidan,akapania kwenda kumueleza mheshimiwa raisi.
"Kwanini hasipatikane?" Goba akajiualiza swali ambalo likamuwia ugumu katika kulipatia ufumbuzi.
Vituo mbalimbali vya habari vilikuwa na kazi kubwa ya kuripoti kila kitu kufuatia na tukio hilo.
******
Taarifa hizo hazikuumiza vichwa vya maraisi hao tu bali hata kwa kijana ambaye kwa mtazamo wa haraka hakuwa wa kisasa sana,sura yake ngumu ikamuonesha wazi kuwa usasa wa sasa haukuchukua nafasi katika kichwa chake.Kijana huyo hupenda sana kufuatilia magazeti mbalimbali likiwemo Mwananchi ,humo alipenda kusoma riwaya zinazotungwa na waandishi mbalimbali pamoja na matukio kadha wa kadha lakini leo aliposoma kichwa cha habari cha gazeti hilo pendwa akajikuta ana hamasa kubwa ya kutoa shilingi elfu moja na kulinunua kabisa.
Alipotoa pesa na kupatiwa gazeti lake akalikunja na kuondoka zake mpaka katika chumba anachoishi.Chumba chake hakikuwa kimekaa vizuri kwani vipande vingi vya magazeti vilisambaa chumba kizima.Akatabasamu na kuketi kwenye kitanda huku akilifungua gazeti hilo.
"Hahaha hebu subiri nisome kwanza hadithi" akatabasamu na kuzungumza peke yake huku akifungua gazeti hilo kuanzia upande wa kulia kwenda kushoto.Ndipo alipokuta hadithi aipendayo ikiwa sehemu ya tano,akaanza kuisoma kwa umakini huku kila msitari akiutafakari na kuuchambua kwa undani,akatabasamu tena na kusema "Hahaha kuna watu wana upeo mpana wa kufikiria mmh" akazungumza peke yake huku akifurahi mno.Mara machale yakampanda,akajikuta anageuza upande wa kushoto wa gazeti na kuanza kwa kusoma kuchwa habari 'UTEKWAJI WA BINTI WA RAISI KIZUNGUMKUTI' Kichwa hiko kikampa uchizi msomaji huyo na kuanza kufunua kurasa moja baada ya nyingine mpaka akaikuta habari kamili....
Akaanza kuisoma huku kadri anavyoendelea kushuka anajikuta anakunja sura na kuongeza umakini wa usomaji.Chanzo cha kutekwa kwa mabinti hao haikumuingia akilini kabisa kijana huyo,akajikuta anashindwa kumalizia na kuachana na gazeti lake,hii mara baada ya kupandwa na hasira za ghafla.
"Watanzania sio watu kabisa,iwaje wawateke hawa mabinti?,tena hawana utu yaani hata mtoto wa mgeni wanamteka,huu sio uungwana kabisa" jamaa huyu akazungumza peke yake.
"Lazima niwavalie njuga hawa wapuuzi labda sio mimi Geza" jamaa huyu akajitaja jina lake kwa mtindo wa kula kiapo katika kulitafutia ufumbuzi jambo hilo.Anaitwa Geza Ulole ni msukuma halisi kabisa anayetokea mkoa wa Mwanza,kwake suala la kuingilia mambo yasiyomhusu ili tu usawa na amani iwepo katika jamii yake ni kama kutumia dozi ya ugonjwa wa UKIMWI.Tukio baya lolote lazima alitafutie ufumbuzi na kuwakomesha wahusika kwa kuwapeleka mbele ya sheria.Akachukua simu yake na kutafuta namba iliyohifadhiwa kwa jina la Iron,akaipiga na kuanza kuisikiliza.
"Habari yako kaka Geza" sauti ya Iron ikazungumza mara baada ya kupokea simu kutoka kwa Geza.
"Safi dogo,umesoma gazeti la Mwananchi la leo?" Geza akauliza huku akisubiri jibu la Iron.
"Ndio nimesoma kaka"
"Safi sana,umeitazamaje hii habari ya kutekwa kwa hivi vitoto vya maraisi?" Geza akauliza tena swali la pili kwa utulivu kabisa.
"Nimelitazama tukio hili kwa jicho la tatu na kubaini kuwa watanzania hawana uungwana au labda tu mizimu ya pesa inawachanganya..."Iron akajieleza vizuri.
"Sasa tunafanyaje?" Swali la tatu la Geza likampa wakati mgumu katika kulijibu na hapo Iron aliposhukwa na kigugumizi kulijibu swali la Geza "Tunafanyaje!"
"Aaah dogo unataka kuharibu maongezi,nimekuuliza swali unaniuliza swali za wapi hizo?" Geza Ulole akakoroma kidogo kama simba dume.
"Sijakuelewa kabisa kaka Geza ndio maana nikauliza" Iron akajutetea.
"Sawa nina maana ya kuwa tunaliunda lipi kuwakomesha hawa watekaji?"
"Kaka mimi usinihusishe kabisa kwa hilo,we maliza mwenyewe,siwezi kuiga mambo yako kwa kweli"
"Kwa hiyo unanisaliti sio?"
"Hapana sikusaliti ila nitakusaidia kitu kimoja kwa kuanzia" Iron akazungumza na kumpa Geza umakini wa kusikiliza maneno yatakayosemwa.
"Kuna dogo anaitwa Swedy,jana alinipigia akanipa maneno mawili matatu ambayo yalinifungua ubongo wangu kuhusiana na hili tukio..."Iron akaeleza kile alichonacho.
"Huyo dogo anapatikana wapi?"
"Anaishi Mburahati Kisiwani"
"Nipe namba zake" Geza akazungumza na kupewa namba za Swedy.
*****
James Goba akaeleza kila kitu anachokihisi kwa Aidan na uhusiano wake kwa mtoto wake,Aidan akajikuta akiingia ndani ya mkumbo wa kutafutwa huku akihisiwa kama mtu ambaye amehusika kwa namna moja ama nyingine katika utekaji na uuaji katika msafara wa Dayana.Uhusiano wa Aidan na Dayana ukawa unamtilia mashaka sana,ndipo wapelelezi wawili wakaagizwa kuifanya kazi hiyo ya kumchunguza kijana huyo.Wakapewa ramani ya nyumba yake pamoja na taarifa zake muhimu huku bila kusahau picha ya mhusika huyo.
Walimsaka zaidi ya siku mbili mzima ila hawajaambulia kitu,siku ya tatu akapatikana akiwa amejilaza chumbani kwake huku akiwa na msichana wake.Wakampeleka moja kwa moja kwenye nyumba ndogo.Huko akakutana na James Goba akiwa anamsubiria hamu sana.Baada ya kuhakikisha wamemtia mbaloni,wakavuta kiti na kumkalisha.Aidan akatokwa na macho ya kushangaa huku mbele akiwa amekabiliana na sura komavu ya James Goba.
"Habari yako Mr Aidan" James Goba akamtupia swali Aidan lakini halikujibiwa kwani bado Aidan alikuwa kwenye butwaa kubwa mno,njemba mbili zilizosimama nyuma yake hazikumpa uhuru kabisa wa kujiamini kusema kitu chochote.
"Narudia tena kijana wangu,habari yako!" James Goba akarudia tena kwa utulivu.
"Mbaya kwani vipi mzee mbona umenikamata?" Aidan akauliza kwa wasiwasi.
"Taratibu basi kelele za nini?"
"Sawa ila nataka kujua kwanini mmenifanyia kitendo hiki?"
"Utajua tu bwana mdogo.Unaweza kuniambia Dayana yuko wapi?" Goba akauliza na kunyamaza kimya huku akisubiri jibu kutoka kwa Aidan.
"Dayana mimi sina naye nilishaachana tangia zamani,sasa nashangaa kwa nini unanikamata bila kuniuliza" Aidan akasema.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndugu yangu bora useme ukweli hapa hapa ama sivyo itakuja kula kwako" Jamea Goba kazungumza kwa utulivu mkubwa mno hakuangaika hata kidogo.
"Ukweli ndio huo,naomba mnifungie kamba zenu nikalale zangu na sio kuniuliza maswali ya kifa...." Kosa kubwa alilolifanya Aidan,kutoa lugha ya matusi mbele ya James Goba ni sawa na kujichanjia pilipili machoni ,hapo ndipo akakutana na kichwa kikali cha James Goba na kumuangusha chini kama mzigo.
"Ujasiri wa kutoa matusi umeutoa wapi?,nataka uniambie tu Dayana umempeleka wapi" James Goba akauliza tena huku akimfuata pale chini.
"Lakini unanionea bure kaka mimi sijui kabisa suala hilo"
"Hutaki kutaja eeeh!" Goba akaingia mlango wa chumbani kisha akurudi na kufuri ya mnyororo.
"Dayana yuko wapi"
"Sijui"
Ghafla kufuri hilo likaanza kutua tumboni mwa Aidan mfululizo na kumfanya atoe yowe la maumivu.
"Inamtosha kwanza kaka" njemba mmoja akasema ndipo James Goba alipositisha mkong'oto.Akaitupa kufuri na kuchomoa jamvia.Aidan alipoona hivyo akaanza upya kupiga kelele zake.
"Nasema mzee nasemaa usiniueee" Aidan akaropoka na huo hilo ndio lilikuwa kosa kubwa kwake.Hakuwa na ukweli wowote anaoujua kuhusu Dayana bali alitamka maneno hayo ili aokoe maisha yake mwenyewe.
Wakamuinua na kumkalisha vizuri,James Goba akaketi mbele yake kama alivyofanya awali.
"Tuambie sasa"
"Kwa kweli mimi sijui ila kuna mtu namhisi,maana miezi ya nyuma alilumbana naye..." Aidan akasema kisha akairuhusu chafya itoke ndipo alipoendelea kuzungumza "Anaitwa Rayana,msichana mmoja mbaya sana,mi ninahisi atakuwa huyo" Aidan akasema hayo huku akijua fika kitu alichokiongea hakina ukweli ndani yake.James Goba aliposikia hivyo akawatazama wale jamaa wawili,akatikisa kichwa kidogo kisha akarudisha uso kwa Aidan.
"Huyo Rayana ndio nani hebu fafanua" akazungumza Goba.Aidan akaanza kufunguka mambo mengi ya uongo kuhusiana na Rayana mpaka walipofikia muafaka na kuamua kumsaka Rayana wamkamate ili akaeleze vizuri.
*****
MBULAHATI KISIWANI.
Geza ulole akafanya hima baada ya kupata mambo machache kutoka kwa Iron kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mabinti wa raisi.Akafunga safari ya kuelekea kwa kijana huyo aliyetambulishwa kwa jina Swedy.Akafika mpaka mtaa huo na kuanza kutembea taratibu huku akihesabu nyumba kutoka pale barabarani.
"Nyumba ya hamsini na tatu kutoka barabarani upande wa kushoto" Geza ulole akazungumza peke yake na kuendelea kuhesabu nyumba hizo zilizo upande wa kushoto "Ina geti jeusi" akajisemea.Baada ya hatua nyingi akajikuta akitua mbele ya nyumba kubwa iliyo na geti jeusi na ndipo nambari hamsini na tatu ilipoishia kuhesabu.Geza akatabasamu na kujongea kwenyw geti hilo.Akalifikia na kuanza kugonga bila kukawia na baada ya dakika chache geti hilo likafunguliwa na msichana mmoja,bila shaka aliyefungua geti ni Veronica.Akamtazama Geza kuanzia chini mpaka juu huku akili yake ikimpa kuwa itakuwa amepotea kugonga nyumba hiyo au anaweza kuwa kuchaa kutokana tu na mawazi yake pamoja ana ile sura yake ambayo inaonesha wazi haikuwa na mng'aro wa aina yoyote.
"Nikusaidie nini?" Vero akauliza bila kuanza hata na salamu kitu ambacho kikamfanya Geza akunje sura na kumtazama kwa umakini binti huyo anayecheza na mboni za macho yake.
"Naongea na wewe chizi...." Hakuweza kabisa kumalizia maneno yale kwani kichwa cha Geza kilikwishatua kifuani mwa Vero na kumuangusha chini.Akaingia na kufunga geti.
"Dharau kama hizi sizipendi kabisa" Geza akazungumza peke yake huku akimuacha Vero akilia kwa maumivu pale chini.Akawa anaswaga mguu wake kuelekea ndani lakini kabla ya kuufikia mlango akakutana na mama Veronica akiwa ameshika wiko mkononi....
"Wewe nani na mwanangu umemfanya nini?" Mama Veronica akazingumza kwa hasira lakini Geza hakuonesha kuwa na wasiwasi hata kidogo.
"Kamuulize" Geza akajibu kwa mkato huku akiendelea kuingia ndani.Mama Veronica alipoona hivyo akarusha wiko na kumpata Geza mgongoni hapo ndipo alipokutana na wiko wa ugongo uliorushwa na Mama Veronica,akageuka kwa kasi na kumtulisha chini mama Vero kwa teke kubwa na lenye nguvu.Kutokana na kelele kuwa nyingi ikamlazimu Swedy asitishe kazi zake na kutoka nje.Alipofungua mlango tu akakutana na Sura ngeni machoni mwake,hakuelewa ni mtu wa aina gani.
"Dogo nakuhitaji"Geza akanguruma kwa sauti kubwa na kumfanya Swedy apatwe na hofu.
"We nani?"
"Utanijua tu" Geza akasema na kumvutia Swedy ndani.
******
Mwendo wa muda mfupi Inspekta Makurumla akawasiri Bagamoyo huku akiwa amedhamilia kukamilisha kila kitu.Picha za pesa zikaanza kujijenga ndani ya kichwa chake na ndipo alizidiwa na hamu ya kufanya jambo hilo kwa haraka sana.
Akafunga breki nje ya ngome hiyo kisha akaingia ndani mara baada kufunguliwa geti.Alipoingia ndani cha kwanza alifunga simu yake na kuiweka mfukoni,alifanya hivyo ili kuzuia mawasiliano yasisambae.
"Niambie anko" Inspekta Makurumla akamsalimia MK.
"Safi anko tumewaficha huku" MK akazungumza huku akipiga hatua ndogondogo kuelekea katika kile chumba kidogo.
"Wamepiga msosi?"
"Yaah wamepiga kiaina"
"Sawa,sasa tusipoteze muda tuwarushe hewani kama vipi" Inspekta Makurumla akashauri.
"Hapana hebu subiri kidogo kuna kitu nakifikiria nikifanikisha nitakueleza na itakuwa bora zaidi.
"Kitu gani hiko?"
"Nitakueleza mkuu ila hawa vijana wako ni waoga sana"
"Wazoee anko watajua kila kitu kwa sababu tukifanikisha hili tutakuwa na misheni zingine tatu zenye pesa zaidi ya hii ishu" Inspekta akazungumza kwa utulivu.Majira ya saa kumi na mbili za jioni Inspekta akaingia garini na kuanza safari yake ya kurudi Dar es Salaam huku akiacha ahadi ya kurudi tena siku inayofuata.
Ilipofika saa mbili za usiku katika ngome hiyo,gari aina ya Murano nyeusi ikafinya breki.Zikashuka njemba mbili pamoja na msichana aliyevalia buti kubwa zaidi ya zile njemba,mikononi wamekamata silaha.Mmoja akafungua buti na kumtoa mtoto mwenye umri wa makadilio ya miaka nane.Alikuwa amefungwa kitambaa chekundu usoni,mdomoni alishindiliwa kitambaa kikubwa ambacho hakikumpa nafasi ya kupiga kelele kabisa.Wakambeba begani na kuingia nae ndani,huko walipokelewa na MK kwa furaha na sifa kemkem zisizo na kikomo.
"Mnaona nyie maboya jinsi watu wanavyofanya kazi kiubunifu" MK akasema huku akiwatupia macho wakina Bosco.
"Sasa huyu mtoto tunapiga cheji ndefu alafu tunaenda kula bata ughaibuni" MK akaendelea kuzungumza.Ngome hiyo ambayo inamilikisa na MK huku kazi yake kubwa ni utekaji wa watoto wa matajiri pamoja na watu muhimu katika nchi kama njia yao ya kujipatia pesa.Siku hiyo waliingua jamaa hao wakiwa na mtoto wa tajiri mkubwa sana.Baada ya kuhakikisha wamejijengea hali ya kupata pesa kwa urahisi wakamchukua mtoto huyo na kumuingiza ndani ya chumba kitumikacho kwa mawasiliano.Wakachukua simu na kuingiza namba ya tajiri huyo na kuipiga,aliyeshika simu ni MK,simu ikaita na kupokelewa.
"Mr.Lwayo habari yako"
"Safi nani wewe?"
"Unaongea na Master Killer"
"Ndio nani?"
"Haha utanijua tu.Kwanza mpaka unaongea dakika hii unajua mtoto wako yupo wapi?" MK akauliza kisha akanyamaza kimya ili maneno yaliyomtoka yamuingue vizuri tajiri huyo.
"Ooooh mtoto wangu yuko wapi...naimba mnipe mtoto wangu tafadhali,tangia asubuhi simuoni jamani naomb......"Mr Lwayo akazungumza kwa hofu huku akihema juu juu kufuatia na maneno ya MK.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Aaaah polepole Mr mtoto wako yupo mzima kabisa ila unaomba ufuate hiki tutakachokisema"
"Kipi hiko jamani niambieni namuitaji mtoto wangu haraka sana"
"Sawa unatakiwa utusikize sisi la zivyo tutang'oa shingo ya mwanao"MK akapaza sauti na kumpa hofu kubwa Mr Lwayo.Akabaki kimya kwa muda kisha akaanza kuongea huku wazi ikisikika sauti ya kilio cha kwikwi.
"Unalia nini sasa mtu mzima kama wewe?" MK akauliza.
"My son,tafadhili naomba mnirudishie" Lwayo akalalamika.
"Tuma milioni arobaini upewe mtoto wako na tunakupa siku tatu tu" MK akazungumza kwa ukali sana kisha akakata simu yake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment