Search This Blog

Friday, 18 November 2022

BINTI WA RAISI - 2

 






Simulizi : Binti Wa Raisi 
Sehemu Ya Pili (2)






Kwa kweli alijihisi kama mtoto,kitendo cha haja ndogo kumtoka kikamfanya awe hofu zaidi.Wakati wanaishangaa pikipiki hiyo mara gari mbili za polisi zikapiga kwa kasi na kuzuia mbele.Gari zote zikasimama na kuwafanya watu washuke na kutazama nini kinachoendelea mbele yao.Aidan akashuka haraka na kuanza kutambaa chini mpaka alipofanikiwa kufika upande wa pili bila ya askari kuona kitu chochote.Akaanza kukimbia kwa nguvu huku akipita nje kabisa ya barabara.Mpaka anafika Mazense Tip Top ikahitimu saa sita na nusu usiku,akaongeza kasi ya mwendo japokuwa alivujwa na damu nyingi lakini hakuwa na njia nyingine zaidi ya kujikaza mpaka anakuja kufika Madoto akawa hoi mno,akaanza kutembea na kufika chumbani kwake,akachukua maji na kuanza kuoga,ndipo alipobaini kuwa alikuwa ameumizwa sehemu ndogo na Bosco.



'Kwani mimi lakini,nilishajua kuwa itakuja kuwa hivi,lakini Dayana mbishi,sasa nataka kufa jaman aaaah..' Aidan akajisemea huku akiwa amejilaza chali,mapigo ya moyo yakimtulia taratibu.



******

"Mambo vipi Raiya?"

"Poa vipi?"

"Rayana kwanini unanifanyia hivi,nakupenda Rayana na ndio maana nikakuambia kuwa nataka kukuoa,sitokuchezea hata kidogo niamini" sauti ya mwanaume anayejulikana kwa jina la Hibu akatamka huku akiwa amepiga magoti chini ya Rayana.Rayana akamtazama kwa dharau na kumchambua kuanzia chini hadi juu kisha akabinua midomo na kusema.

"Huwezi kuwa na mtoto kama mimi samahani eeeh" Rayana akasema hayo na kuondoka zake huku akimuacha Hibu akiwa haamini kama kweli ametemwa na Rayana.Kiburi hiki cha Rayana kimesababushwa sana na Aidan kutokana tu na mapenzi alionayo Rayana kwa Aidan.Orodha kubwa ya wanaume,walikatawaliwa pale tu walipojaribu kumtongoza.Haikuaa rahisi kabisa ya kukaimu nafasi ya Aidan.



Baada ya kumaliza mapishi ya jioni,akaweka chakula kwenye hotpot na kuondoka zake kuelekea Barafu kwa mpenzi wake huyo.Akamkuta akiwa amelala huku kwenye paji lake la uso akiwa ameziba na bandeji.Kitu cha kwanza kuhoji ni juu ya ile bandeji.

"Mpenzi vipi mbona bendeji jamaniii?" Rayana akauliza huku akimsogelea Aidan,akamtazama usoni na taratibu akashindwa kuzuia machozi yaliyoanza kumtiririka.

"Usilie dear,hii ni kwa sababu ya Kazi zetu" akasema Aidan na kumpunguza machungu Rayana.

"Unajua sipendi kukuona ukiwa katika hali kama hii Aidan wangu,sipendi kukuona ukiwa na shida yoyote ile,nitajitahidi kadri ya uwezo wangu ili tu niweze kukuburudisha mpenzi wangu nakupenda sana Aidan Wangu.."

"Nakupenda pia wangu" maneno yenye hisia kali za mapenzi yakatoka vinywani mwa wawili hao na kuwafanya wote watabasamu na kukumbatiana.



****

Dayana akapata wakati ngumu sana,hakujua aanzie wapi kumuomba msamaha.Akainuka na kuingia chumbani kweke,akachukua simu na kutafuta namba ya Bosco kisha akaipiga.

"Nakuambia lazimu unitambie na nitakusemea kwa baba,kwanini umpige mtoto wa watu kakukosea nini....tena lazima nikuoneshee ehee unijui vizuri,nakuchukia sana Bosco" Dayana akaongea kwa hasira sana.

"Nisikize basi mpenzi wangu please Dayana nakupenda mwenzio,nilifanya vile kwa sababu ya pombe tu sikua na dhamira nayo" Bosco akaongea kwa upole na kumfanya Dayana aanze kutukana matusi makubwa.Katika siku ambayo Dayana aliwahibkukasilika basi hii ndio siku ya kwanza yenye hasira zaidi,alijua fika kuwa Aidan hawezi kumpata tena na hata akimpata basi hatokubali tena kuwa naye katika mahusiano,wasiwasi juu ya usalama wake,ulikwishatamkwa kwa kinywa yake na hapo ndipo ilipojidhihirisha mbele yake katika ukumbi wa Mlimani City.Siku mbili zikakatika bila ya Dayana kupokelewa simu kwa Aidan.Akajikuta anakosa raha kabisa.Akachukua gari bila ya mlinzi wake na kutoka nayo nje.Safari ya kwenda Mbezi beach kwa Bosco ikaanza,kuchwani akaapa kabisa lazima amkomeshe.Akafika barabara kuu iendayo Bagamoyo na sasa akapita mataa ya mwenge ksa mwendo kasi,akaongeza kasi ya gari.Baada y dakika kama kumi na tano alikwishafika kwenye nyumba ambayo imezungukwa na bustan ya maua.Akapiga hodi na akafunguliwa na mlinzi,hakuonge akaingia moja kwa moja hadi ndani na kumkuta Bosco akiwa amejilaza kwwnye sofa huku pembeni akiwa na chupa yake kubwa ya pombe aina ya Wisk.Akamrukia na kuanza kumpiga makofi kwa fujo huku akilia kwa uchungu.Vibao hivyo havikuweza kumuwasha Bosco ipasavyo kwa sababu tu ya Dayana kuwa na mikono laini.Bosco alivyoona vile akamgeuza na sasa Dayana akawa chini.Akaanza kumtomasa maungo yake na kumchezea atakavyo,kwa vile alimshika kwa nguvu,Dayana hakuweza kumdhibiti Bosco kufanya kitendo kama kile,akajikuta ameingia katika penzi bila kutarajia,Kutokana na kushikwashikwa sana hatimaye na yeye akajikuta akimuachia Bosco afanye anachotaka kwenye mwili wake.



******

Heka heka za kariakoo huanza mapema sana pale tu dunia inapoanza kuingiwa na mwanga hafifu huku ukisaidiwa na mwanga wa taa mbalimbali.Wafanyabiashara hudamka asubuhi na mapema na kufungua maduka yao,hapo huanza kujipatia mateja kwa mgawanyo.Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kwa jina la machinga,wakamwaga bidhaa zao na kuzitangaza.Hali ikawa tofauti kwa makabwela ambao hufanya kazi ngumu zaidi ya kipato wakipatacho kwa siku,kazi ya kusukuma mkokoteni pamoja na kubeba mizigo ni kazi ambayo inahitaji nguvu za aina yake.

Aidan kama kawaida yake,alifika mjini kariakoo majira la saa kumi na mbili na nusu,hapo ndipo hupata dayworker nyingi mara kabla hawajaja wenzake wengine.



"Oyaa Kijeba eeeh" muuza duka la viazi akaita jina hilo na kumfanya Aidan amyazame muitaji.Jina hilo lilokuwa maarufu sana hapo kariakoo,kutoakana tu Aidan kuwa na nguvu za kubeba mizigo mikubwa na mizito.

"Niambie Charii yangu ya Arusha" Aidan akazungumza huku akitembea hatua ndefu kuelekea alipoitwa.Hapo akapewa mzigo wa gunia la viazi na kuambia apeleke sehemu husika.

"Ahaa huu mzigo cha mtoto sana,hebu unanipa bei gani hapa?" Aidan akauliza.

"Utapewa hukohuko"

Aidan akabeba gunio hilo lenye uzito upatao kilo mia moja na kuendelea,akaanza kukwepana na watu na kuelekea alipoelekezwa.Akatumia muda wa dakika nne mpaka kufika kwenye duka hilo.Hapo akakutana msichana wa kihindi akiwa anawahudumia baadhi ya wateja.Sura ya msichana huyo,ikaonekana vyema kutokana na kutofunga ijabu usoni kama wengi wao wanavyovaa,pua yake kubwa iliyonakishiwa na kipini kidogo kilichong'aa,ikamuonesha wazi uzuri wake.Aidan akatupa mzigo na kumuendea msichana huyo.



"Bosi kamzigo ketu haka kametua,nipasuliw mbumba nitambae basi"Aidan akasema huku akijichekesha bila kuchekeshwa.

"Nataka shingapi wewe" msichana huyo akauliza kwa kiswahili kibovu.

"Ahahaa ni buku tu"

"Na ukome..buku gani menipa kuweka hiyo buku?" Akafoka kidogo na hapo ndipo sura yake ilipozidi kuwa mzuri zaidi ya mara ya kwanza.

"Eeeeeh acha utani bana hebu lete buku" Aidan akachukulia utani lakini hakujua kama binti yule anachokisema anakimaanisha.Binti akachomoa mia tano na kumpatia Aidan.Halikuwa tegemeo lake la kupewa mia tano ya Kitanzania,akabaki akiitazama tu kwenye mikono yake,akamtazama binti huyo ambaye hana habari na yeye,akajikuta akitikisa kichwa na kuiweka pesa mfukoni.Akafika sehemu na kukaa huku akitweta kwa kazi ngumu anazozifanya tofauti yabpesa anayoipata,akakumbuka siku za nyuma jinsi alivyopatiwa pesa na Dayana pamoja na Mama Grace.Akapiga muhayo wa nguvu na kuinuka.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Majila ya saa kumi na mbili jioni,akapanda gari la Mazense na safari ya kurudi nyumbani kwake Barafu ikaanza.Safari ipo katikati akakumbuka kuwa mtaa wa Kigogo mwisho kuna rafiki yake anayeitwa Gomesa,huyu ni rafiki yake ambaye alikuwa anajishughulisha na kazi ya udalali.Akajikuta anashuka katika kituo hicho na kuanza kupandisha juu mpaka alipoufikia mlango wa chumba cha Gomesa.Akagonga hodi zaidi ya mara tatu lakini hakukuwa na muitiko wa aina yoyote.Akaamua kugeuza na kuanza kupiga hatua ndogo ndogo,ila kabla hajafika mbali akakutana na Gomesa akiwa amebeba mfuko laini.



"Ohooo ndugu yangu za siku nyingi aisee" Gomesa akamsalimia Aidan na Aidan akaitikia.

"Salama rafiki maisha yanaendaje?"

"Maisha ndio hivi rafiki yangu yanasonga,vipi wewe uko wapi siku hizi mwanagu huonekani?" Akauliza Gomesa.

"Daah kaka nipo hapo Barafu ndipo ninapopata shida"

"Aahaaa ila usiseme hivyo bwana shida mbona zitaisha tu"

"Sasa zinaisha vipi na usawa wenyewe kama huu"

"Anyway,sasa rafiki yangu Aidan kuna ishu nataka tuongee mimi na wewe" Gomesa akasema na kumfanya Aidan ajiweke vizuri kupata mpya kutoka kwa Gomesa.

"Ehee ndio nachokupendea wewe man yangu la A chuga hebu nipe mchongo" Aidan akasema.

"Sio hapa hebu njoo kwanza gheto"

Wakaingia ndani na kukaa kwenye kitandan,kwa kuwa hakukuwa na umeme katika chumba hicho cha Gomesa,ukawashwa mshumaa na mwanga mdogo ukaanza kulipeperusha giza kimtindo.Idadi ya mbu ikaanza kuongezeka kila baada ya sekunde,sasa kila mmoja akawa na jukumu la kufukuza mbu hao wanaopiga kelele bila kuchoka





"Ebana kuna rafiki yangu mmoja yupo Arusha,sasa kule kuna kampuni mpya ya kutengeneza madawati ya plastiki....,Gomesa akakohoa kadogo na kuendelea "unaona eeeh sasa wanahitaji chupa hizi za maji na juisi ili zitumike....tena mzigo ukiwa mkubwa linakuja lori wanabeba si wahuni tunadaka mshiko wetu au sio mwana" Gomesa akasema na kunyamaza,akamuua mbu ambaye alikuwa anamnyonya damu yake kwenye paji la uso kisha akaketi sawa na kujitayarisha kwa kumsikiliza Aidan.



"Ahaaa kweli nilisikia suala hilo la masawati ya plastiki,poa ila wanalipa shilingi ngapi kwa kilo?" Aidan akauliza

"Ngoja niwasiliane nae halafu nitakupa taarifa kesho,ila hili dili mwanangu limetulia sana"

Aidan na Gomesa,baada ya kukubaliana,Aidan akaanza kutembea kwa mguu mpaka barafu.



******

Kwa mara ya pili sasa Dayana akawafuata rafiki zake na kuwaomba waende Mburahati kwa Aidan,moyo ukamsukuma kufanya hivyo na ile nafasi ya Baba yake kuwa na ziara za nje,basi akatumia fursa hiyo kufanya kila kitu akitakacho,Mama yake hakuwa na kipingamizi chochote.Hakupenda kutembea tena na Mlinzi wake tangia ile siku ya kumtoa kwenye tamasha kule Mlimani City na kumuacha Aidan akipigwa.

akafika kwa Salmaya na kumkuta akiwa na mama yake,akamsalimia na kumuomba atoke na Salmaya,kweli akakubaliwa na Wote wakaondoka,wakafika tena kwa Angel,baada ya kumchukua wakaingua garini na kuondoka zao.

Njiani wakawa wanahadithiana mambo mbalimbali hususani kuhusu wanaume zao.



"Yaani niwaambie kitu,Seif jana kanikuna mpaka nikahisi nataka kutapika mmmh" Angel akasema na kuwafanya Dayana na Salmaya kutwga masikio yao waupate ubuyu wa Angel kwa umakini.

"Ehee mwaya tupe stori" Salmaya akazungumza na Angel akaendelea "Nyie acheni tu hawa vijana wa uswazi wanapiga kazi ile mbaya..."Angel akaeleza jinsi alivyokutana na Mpenzi wake Seif.Mazungumzo hayo yakamwongeza kasi ya kumuhutaji Aidan huku akiamini pekee kuwa na mwanaume ambaye atakuja kumpa kitu ambacho amekikosa kwa muda mrefu.

"Kumbe! Hawa wasichana wanaoishi huku uswazi wanapata raha eeeh? Dayana akauliza swali.

"Aaah tatizo hawa wa uswazi wanawapenda wenye pesa,ndio maana wanakimbilia kwa hawa wenzetu na sisi" Angel akaeleza.



Wakajikuta wanaingia njia Panda ya Kigogo na kuchukua barabara iendayo Mabibo au Manzese.Moaka wanafika Mburahati Kigogo,ikahitimu saa kumi na moja na nusu,hawakujua kabisa waanze wapi kumuulizia Aidan,kwa maana kuwa hawakukujua kabisa nyumbani kwake,wakawndesha gari mpaka kwa Mazuu na kusimamisha kando.Sasa wakawa na kazi ya kumuulizia Aidan kwa kila mtu anayepita.Bahati yao haikuwepo kwa siku ile,wakakata tamaa kabisa,wakachukua uamuzi wa kuingia garini na kurudi kwao.Wakaanza safari yao huku Dayana akiwa hawa raha hata kidogo,ika wanaifikia barabara wakamuona Aidan anashuka kwenye daladala akiwa amechafuka kupita kiasi,mkononi ameshika mfuko mdogo na chini akiwa na viatu vilivyochakaa,muonekano wake kwa ujumla ukamchora moja kwa moja ufukara aliokuwa nao.Dayana akapiga oni ya gari na kushusha kioo,akafungua mlango na kuanza kupiga hatua ndefu kumfuata Aidan,hakujari kama kuna watu wanamtazama,hilo akalifumbia macho.Baada ya hatua kadhaa akamfikia Aidan ambaye bado alikuwa anatembea.

"Aidaan...jamani simama basi,nisamehe mimi lakini mbona unakua hivyo?" Dayana akalalamika lakini Aidan hakusimama,hasira na chuki zikampanda kichwani na kumtema Dayana binti wa Raisi.

"Sitaki matatizo na wewe sawa eeh " Aidan akatamka na kuendelea kutembea.Vuta nikuvute,wakajikuwa wanaishia kwenye sura ya Rayana ambaye amebeba poti la chakula.

"Waoooh mpenzi!" Aidan akadakia na kumshika Rayana.

"Huyu nani Aidan?" Rayana akauliza huku akimuonesha kidole Dayana ambaye amejishika kichwani,wivu ukaanza kumzonga na kutamani arushe ngumi.

"Aaah huyu achana naye bwana" Aidan akasema huku akimvuta Rayana na kaunza kuondoka,Rayana hakusita kuntazama Dayana kwa umakini sana.

Moyo wa Dayana ukamuuma sana,kItendo cha kumuona mtu anayempenda akiwa na mtu mwingine ni maumivu tosha zaidi ya sindano ya kidonda.Akakimbia na kurudi ndani ya gari ambapo aliwakuta Salmaya na Angel wakimsubiri kwa hamu.Kilio cha kwikwi cha Dayana kikawachanganya sana.

"Vipi best kakufanya nini Aidan?" Salmaya akauliza huku akiwa na wasiwasi sana.Angel akaketi kwenye siti ya dereva na kuiondoa gari.Dayana akawasimulia wenzake kitu gani kinachomliza.



****

"Sitaki kazima uniambie ni nani yule?" Rayana akafoka kwa hasira sana huku akimpigapiga kifuani kwa Aidan,hakutaka kumuelewa kabisa,anajua fika madhara ya Aidan kuwa na mwanamke mwenye hadhi kama yule,tena kwa mtazamo wa machoni inamuonesha wazi kuwa binti yule kwao ni watu wenye uwezo wa kifedha,kwa vyovyote akajua lazima atanyang'anywa tonge mdomoni tu.

"Hamna sio hivyo Raya,mimi nakupenda wewe,tafadhali nielewe,yule simjui kabisa" Aidan akajitahidi kumbembeleza Rayana bila ya matumaini ya kumtuliza.

"Haiwezekani kabisa,mtu umesimama naye tena unaongea nae huku akitokwa na machozi,mimi sio mtoto mdogo Aidan,usinidanganye kabisa" Rayana hakuelewa na hapo ndipo Aidan alipokasirika na kutoka nje.Akaketi kwenye msingi wa nyumba na kuanza kuwaza kitu fulani,mara akatoka Rayana na kumpita alipokaa,akatoka nje kwa kasi,ni wazi alikuwa amekasilika mno.

"Sasa unaenda wapi Rayana eeeh" Aidan akamuita Rayana lakini hakuambulia kitu zaidi ya kushuhudia kisigino chake kikizama kwenye uchochoro.

"Jamani sasa mtu gani asiyeelewa khaaa!" Aidan akajisemea huku akiingia ndani.Hata yeye hakupenda lile jambo litokee kabisa,kwani kuwa na mahusiano na mtoto wa raisi,ni wazi kuwa lazima uhai wake utawekwa rehani muda wowote,wazo la kuchukua simu na kumpigia Dayana ili ampige marufuku kumfuatilia likamjia,simu ikaita mara ila haikupokelewa,akajaribu zaidi ya mara tatu lakini jibu ni lile lile.Akaamua kumpigia Rayana ili amuombe msamaha lakini huku simu yake ikawa haipatikani kabisa,akabaki njia panda.

"Aaah jamani kila kitu shida tuuu! Mapenzi shindaa!,Maisha ni shidaa,sehemu ya kulala ni shida,kula shida..." Aidan akajisemea mwenyewe.Matatizo anayaopitia Aidan kila siku katika maisha yake ni matatizo ambayo hajana mfano,ukabwela unamfanya ashinde kuheshimika mtaani,anashindwa kufanya mambo anayoyataka kisa pesa,kwa upande mwengine anajiona kama mpumbavu kwani kama anahitaji matatizo aondokane nayo,kwanini asimkubali Dayana binti wa raisi?,kitu anachokihofia ni kuuza maisha yake kwa watu hatari wanaomzunguka Raisi.



****

"Hivi inaingia akilini kwa jambo ambalo hauilihisi katika kichwa chako kuliachia lipite?" Bosco akamuuliza mmoja wa rafiki zake kwenye moja ya hotel ya kifahamu iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaaam.

"Sijakuelewa Bosco unamaanisha kitu gani?" Jamaa huyo akauliza.

"Kwa mfano wewe una demu halafu huyo demu akakutema ghafla na siku ya siku unamkuta akiwa na jamaa mwingine tena wakilana mate kabisa...mtu kama huyo utamfanyaje?"

Bosco akauliza na kuchukua glasi ya kinywaji,akavuta fundo moja na kuiweka glasi.

"Kwanza ndugu yangi Bosco,hakuna kitu cha kijinga kama kuvumilia jambo kama hilo na hukumu ya huyo boya ni kuitenganisha shingo yake na kukiacha kichwa kwake na kiwiliwili kwake,nadhani hapo utakuwa umeua mchezo,sasa hapo unajua nini kitatokea?" Jamaa huyo anayemoa ushauri Bosco akamswalika na swali Bosco kisha akavuta pafu la sigara,akatpa moshi puani mithili ya gari moshi.

"Ehee ndugu yangu kitatokea nini?" Bosco akauliza kwa hamu sana.

"Hapo lazima demu aje na kukurudia tena,maana hatakuwa na jamaa yake tena,sasa wapi atoe mzuka wake,lazima ajirudishe" jamaa huyo akaishia hapo.

"Daah ndio maana nakuaminia sana mwana,huwa uharibu hata siku moja" Bosco akachukua glasi na kugonganishana kwa pamoja.

Wakamaliza maongezi yao.Bosco akaondoka zake kuelekea nyumbani kwake Mbezi Beach,na baada ya kufika akaanza kujipanga na kutafuta njia gani anaweza kumnasa Aidan ili amalize kabisa kwa lengo la kulinda penzi lake kwa Dayana.Akafungua droo yake na kutoa bastola yake na kuiweka juu ya kitanda,akaiweka magazini kisha akaitega na kuitegua akatoa magazini na kuhifadhi,akasimama na kuliendea kabati lake la nguo na kuanza kutafuta mavazi ambayo yatamsaidia katika kazi hiyo ya kutoa roho ya mtu.

"Hakuja haja ya kuchukua mavazi ya kininja,hapa ni kupiga suti na moka kwisha kazi" Bosco akaongea peke yake huku akitoa suti nyeusi.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



*****

NDANI YA IKULU YA MR. NOEL MKWAKWACHA.



"James nakuomba ukaniombee msamaha kwa mtu wangu,nashindwa kula mimi nampe...nda sana Aidan jamanii" Dayana akalalamika sana huku mbele yake kukiwa na mwanaume mwenye ndevu zilizotengenezwa mithili ya herufi O,anaitwa James Goba,ni mfanyakazi wa ikulu ya raisi.Kutokana kuwa na ukaribu sana na binti huyo basi kila tatizo gumu alipatalo binti huyo,James huchukua nafasi hiyo na kusimama kama ushauri pamoja ja kutoa msaada.Chozi ambalo linamtoka Dayana juu ya penzi la mvulana ambaye hakuwahi hata kufanya nae mapenzi japo siku moja,likamfanya James amuonee huruma Dayana na sasa akawa na kazi ya kumbeleza pamoja na kumtia moyo katika kusuluhisha tatizo lake.



"Usilie basi,hili ni tatizo ndogo sana,nalimaliza mwenyewe,nyamaza Mama anakuja sawa,futa machozi"James akambeleza na hatimaye Dayana akafuta machozi yake.Dayana anaumuzwa na mapenzi ya hisia,hisia ambazo zinampa shida usiku kucha,chakula kwake ni kama sumu,kilio kikawa kama kitendo cha ulazima katika maisha yake,Aidan anamtesa Dayana.



****

Katika jumba kubwa lililojengwa na kujengeka ndani ya Mtaa wa Mbezi kwa Suka,kelele nyingi zikaendelea kusambaa kwa kasi,mziki wenye sauti ya juu ukavuma na kuvumika,glasi na chupa zikasikika zikigongana na watu wake wakicheza kwa kufuata mdundo wa wimbo huo.Ndani humo pia kulikuwa na wasichana ambao wamevalia nguo fupi sana,lakini kwa hao wote,mmoja wao ndio alifunga kazi kwa vazi lake alilovaa,ni wazi kabisa tamaduni ya mwafrika imegeuka na sasa uwigo wa utandawazi unaathiri jamii yetu na kuletwa ule wa kigeni,msichana huyo mnene amevalia sidilia na chupi aina ya Bikini,huku uzi wake ukiwa umepita katikati ya mpunyenye wake.

Kwa harakaharaka huwezi kushangaa kabisa kama watu hawa wapo katika fulani ya kitu fulani,kwani haikuwa siku maalumu kama wikiendi au sikukuu yoyote.

"Ongezaa bia wewe...yaani hapa kunywa halafu mambo mengine baadae" jamaa umoja wapo akazungumza kwa sauti ya kukwaluza kwa sababu ya pombe zilizomtawala kichwani.

"Namwaga lazi..." Hakuwa mtu mwingine bali ni msichana ambaye amevalia siketi fupi kupita maelezo,iliishia juu ya mapaja yake.Watu wote wakaikia kwa sauti ya kilevi.

"Mwagaaaaa!"

Mara akaanza kuvua blauzia yake na kuitupa chini.

"Nataka kumwaga lazii"

"Mwagaaaa!"

Bibie akasaula na sidilia,sasa akabaki na maziwa nje,maziwa yaliolala kiaina,akayatingisha na kuyalamba,pombe kichwani imemtawala kwa asilimia mia,hakuwa anajitambua kabisa.

"Na...mwaga laziii!"

"Oyooo mwagaaa!"

Akavuta sketi yake na kuitupa chini,akawa amebakiwa na kufuri lake,akalitoa na hilo.La haula,msichana huyo akabakiwa mtupu kabisa hana kitu,kama alivyozaliwa akaanza kukata nyonga zake kwa fujo na kuwafanya wenzake waanze kushangilia,wakagongeshana glasi ya pombe na kuendelea kufurahia siku hiyo.

Wakati wanaendelea kutazama shoo ile isiyo na kiingilia,mara akaongia Bosco akiwa amevalia T sheti yenye rangi ya zambarau huku chini akiwa amevalia jinzi,akaingia na kufunga mlango bila ya kubisha hodi.Akafikia kwenye redio na kuipunguza sauti mpaka ilipofika namba tano.

"Aaaaaah boya gani unatukata stimu sasa hivi..." Wote wakaanza kuhamaki na kuanza kutukana matusi ya nguoni.

"Tulieni nyie vikaragosi" Bosco akasema kwa sauti ya juu na hapo wote wakaa kimya.Bosco akasogea na kutoa bahasha,akaitupa juu ya meza na kumkodolea macho jamaa ambaye alikuwa anavuta sigara huku akiwa kifua wazi.Jamaa huyo akainama na kuichukua ile bahasha,alipochomoa kitu kilicho ndani akakutana na picha ya Aidan ambaye yupo katika tabasamu,jamaa huyo akainua kichwa chake na kumtazama Bosco,akakutana na mkono wa Bosco ukipita shingoni kama ishara ya kuondoa uhai wa mtu huyo anayeonekana kwenye picha.



"How much to kill this fucking boy?(Shilingi ngapi kuua huyu mpumbavu?)" akauliza jamaa huyo kwa sauti kubwa.

"Probability five milioni(kwa makadilia ni milioni tano)" Bosco akasema.

"Go and kill yourself(nenda kaue mwenyewe)"

"Noo my friend,so how much you need(Hapana rafiki,kwa hiyo unahitaji kiasi gani?)"

"About eight and half(kama milioni nane na nusu)" jamaa akasema na kuichukua glasi ya bia,akavuta fundo moja na kuiweka chini.

"Ok nice,we will talk on tommorow(sawa tutaongea kesho)" Bosco akazungumza na kutoka zake.Kazi ya kutoa uhai wa Aidan ambayo kazi hiyo aliipanga mwenyewe Bosco aimalize,sasa ipo mezani kwa kundi hatari la uharifu lililojificha mbali Mbezi Kwa Suka.



****



Mtaa wa Mburahati hususani maeneo ya Barafu,ukapata mshangao siku hiyo baada ya kuishuhudia gari aina ya Hammer ikiwa inaelekea mbele kabisa katika mtaa huo wa Barafu.

"Eeeh hii Hammer wapi huku mbona makubwa haya au Platnum anaingia Mazuu?" Maswali kadhaa yaanza kutoka kwa watu wakiwa hawajua majawabu yao.Gari hiyo ambao imekaliwa na James Goba,ikasimama kando ya uwanja wa Barafu kisha akashuka,akatazama huku na huko kisha akaona kuna bar pembeni.Akatumia fursa hiyo na kwenda sehemu hiyo kwani kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kupata kile kitu anachokihitaji katika mtaa ule,akafika na kuketi kwenye kiti,ndani ya sekunde tatu akaja mhudumu.Wakati anaendelea kunywa kinywaji chake akamuomba mhudumu wa kike aketi nae,kweli akatii wito kisha akapewa ofa ya bia mbili,hapo ndipo mwanamke huyo alipoanza kujilegeza kwa Mr.James Goba,mara aamze kuivuta sketi yake juu na kuacja mapaja yake nje,kidole kimoja akakibana mdomoni na macho akawa anayalegeza.



"Sorry! Unamjua huyu?" James Goba akatoa picha ya Aidan na kumuonesha mhudumu huyo.

"Yes...huyu namuona sana hapa Barafu ila sijui jina lake.." Akaeleza.

"Anapokaa unapajua?"

"Aaah naona tu anatokea nyumba ileee" mhudumu huyu akaonesha kidole nyumba husika na James Goba akageuka na kutizama.Baada ya maelekezo hayo James Goba akainuka na kitaka kuondoka,lakini akakimbuka kuwa hajalipa pesa za bia,akatoa noti tatu za elfu kumi na kumpatia mhudumu kisha akaanza kupiga hatua ndogondogo.

"Sasa kaka kwa hiyo ndio basi tena?" Mhudumu akahoji lakini James Goba hakuonesha ushirikiano wowote.

Akaikaribia nyumba hiyo na kupiga mlango taratibu,akagonga zaidi ya mara tatu lakini bado hakukuwa na mwitiko.Akagonga tena kwa mara ya sita na hapo ndipo alipokutana na sura ya msichana akiwa amevaa kanga moja iliyoishia kifuani,mabega yake yalio nje na kuusanifu mwili wake.

"Karibu ndani"

"Hapana hapahapa inatosha" James Goba akasema na ndipo alipoana kuongea.

"Samahani naomba kumuulizia huyu mtu hapa kama anaishi hapa" James Goba akatoa picha na kumuonesha msichana huyo.Akaitazama na kumtazam usoni James Goba,akaanza kumtazama tena kuanzia chini hadi juu,suti ambayo imemkaa vizuri pamoja na funguo ya gari zilizoning'inizwa mkononi mwake.

"Ndio namfahamu anaishi hapa" akajibu

"Anaweza kuwepo?"

"Sidhani hebu subiri nimtizame" akatoka huku nyuma akimuacha James Goba akitazama wimbi la makalio la msichana huyo yakitingishika kwa kupishana.

"Uswahilini dot com Loooh" akajisemea James Goba huku akimeza mate ya uchu.Baada ya dakika mbili msichana huyo akarudi huku nyuma yake anafuatwa na Aidan.Kitu kilichompa wasiwasi ni juu ya ujio wa James Goba,hakuwahi kuwa na ufahamiano kabisa na mtu huyo wala kuonana sehemu yoyote.Mawazo ya haraka yakamjia na kuanza kuhisi kama anatafutwa na polisi,lakini akajua hakuna baya lolote alilowahi kulifanya.

"Aaah samahani wewe ni Aidan eeh" James Goba akamuuliza Aidan,akaitikia kwa kutikisa kichwa huku wasiwasi mwingi umemjaa.

"Nakuomba mara moja tafadhali" James Goba akazungumza na kumfanya Aidan atoke nje kabisa,wakawa wanatembea kuelekea kwenye gari.Wakaingia na kufunga mlango,kwa kuwa vioo vya gari hilo viliwekwa tintedi basi hakukuwa hata na mtu yoyote angeliweza kuona nini kinachoendelea ndani humo.



"Kwanza kabisa,samahani kwa usumbufu najua muda huu ni wa kupumzika,lakini sitofanya haki kama sitakueleza haya niliyoagizwa..." James Goba akaanza kwa kusema hivyo huku akiwa na utulivu mno.Wakati huo wote Aidan alikuwa anatazama gari hilo bila kulimaliza,ndani mlikuwa na vitu vyenye thamani mno.James Goba alimchapa kwa maneno yenye hisia huku akitumia njia yake ya siasa ili tu amshawishi Aidan akubaliane na Dayana.



******



******

Mziki aina ya blues ukaendelea kukita katika redio kubwa ndani ya chumba kilicho na kutanda cha futi sita kwa sita,taa ya rangi nyekundu ikaangaza chumba hicho na kuwafanya watu waliomo waburudike mara duf.Chumba kilitawala mihemo ya huba na kwa haraka mtu apitaye nje,basi hawezi shangaa kitu gani kinaendelea ndani ya chumba hicho.Aidan na Dayana ndio walio juu ya kitanda wakiwa uchi wa mnyama kabisa,mpaka dakika hiyo aliyekuwa anatawala mchezo alikuwa ni Aidan ambaye amemuweka Dayana kwa juu huku Aidan amekishika kiuno cha binti huyo.Nywele ndefu za Dayana zilizofumuliwa na Aidan zikawa zinakokota mgongoni mwake pale tu anapoelekeza shingo yake kwa nyuma na nywele hizo pia huelekea kifuani mwa Aidan pale tu Dayana anapoinamisha kichwa chake.Kitendo hicho cha nywele kulala kwa mbele na kulala kwa nyuma ni dhahiri kulikuwa na mkuno ambao unamfanya Dayana asitulize kichwa chake.Wote wakahema kwa ngumu lakini mihemo ya Dayana ikazidi mara tatu zaidi ya mihemo ya Aidan,raha ambazo alikuwa anazihisi hazikuelezeka,japokuwa wameenda safari mbili ila bado mkuyati wa Aidan ulikuwa umesimama imara kama simba wa nyika,kila ulipochimba madini hayo ya ikulu ikaendelea kuimarika mara dufu na hapo ndipo Dayana alipoanza kuchanganyikiwa na mapigo ya kijana Aidan.



Ni moja ya faida kubwa sana ya kula vyakula vya asili kama mihogo,ugali wa dona,karanga na vyakula vingine tofauti na wale wanaokula vyakula vya kisasa hasa vya Supamaketi kama Chipsi kuku,Burger na kadhalika.Usimamaji imara wa mtalimbo huitaji uangalifu mkubwa sana hasa katika matumizi ya vyakula vya kila siku.



Aidan akapiga makasia kuhakikisha kuwa anaweka heshima kwa mara ya kwanza kwa binti huyo ili hata akihitaji kitu chochote anachotaka basi atimiziwe bila maswali.Ghafla akamgeuza Dayana kwa kasi bila hata Dayana kujijua kama yupo chini,akaendelea kumsurubu huyo kuku wa kizungu japokuwa hakuweza kuimudu ile hali ila aliapia haswa lazima amtambue.

Aidan hakuishia hapo akainuka na Dayana,akasimama naye na kuanza kumvuta juu na kumshusha chini,haikuwa tofauti na mtu anayetwanga nafaka fulani ndani ya kinu.Mpaka wanakuja kumaliza mzunguko wa tatu Dayana akashindwa kabisa kusimama,kila alipojaribu kusimama miguu ikamtetemeka na kuangukia kitandani.



"Beee! naomba pochi yangu" Dayana akazungumza kwa sauti ndogo,Aidan akamsaidia kuchukua pochi na kumpatia.Dayana akafungua na kutoa kitita cha shilingi laki moja na kumpatia Aidan kisha akasema "Hiyo kanunue nguo zako" akatoa bunda lingine kubwa zaidi ya lile la kwanza "Hii ni laki tano nataka unanunue fanicha za ndani kesho kutwa nakuamisha kule kwenu baby" Aidan akashangaa sana jinsi Dayana anavyotoa pesa kuwa kama anatoa pipi kwenye pochi.Alipotazama mlingoti wa Aidan hakuwa na dalili kabisa ya kulala hapo ndipo alipotokwa na macho na kuamini kabisa kuwa Wanaume wa Uswazi ni bora kuliko wa mijini.Akajikuta tu mwenyewe anafungua tena pochi na kutoa noti tano za elfu kumi kisha akamtupia Aidan.

"Na hizi za nini sasa?"

"Hazina sababu"

Aidan akamsaidia Dayana kumfikisha bafuni kisha wakaanza kuoga pamoja.



****

Siku ya pili sasa,Rayana anamtafuta Aidan kwenye simu lakini hampati hewani,maisha ya mapenzi yakaana kumuwia magumu haswa,akajutia sana kumkasirikia siku ile aliyomkuta na msichana kule Barafu.Akiwa amejifungia ndani akilia akasikia sauti ya mama yake ikimuita lakini hakutaka kuitika kabisa,haikuwa jadi ya yake ni kutokana na donge la mapenzi lililomkaa kwenye koo lake.

"Sasa mwanangu unalia nini mama eeh,Baba yako ana njaa naomba umpikir mwanangu..." Mama Rayana akalalamika lakini hakuitikia katakata.



Mausha ya mapenzi ni magumu sana hasa kwa wale wasio na kifua cha kuhimili kama yanavyomtesa Rayana,alimkabidhi moyo wake Aidan na kuamini siku moja atakuja kupanga nae famili kama mume wake lakini ndoto hizo zikaanza kufifia taratibu mfano wa mshumaa unaoishia.Katika kufurahia mapenzi basi lazima ukubaliane na changamoto zake mpaka mwisho lakini sio kwa Rayana mtoto wa kifukara aliyefifia kwa urembo sababu tu ya umasikini wake,hata hivyo kitu kizuri anachokufanya Rayana cha kumpenda mmoja tena masikini mwenzake japokuwa ni mara nyingi sana alifuata na wenye pesa lakini akabaki na msimamo wake wa kukataa na kumuenzi Aidan peke yake.Wakati anaendelea kulia kwa kwikwi,mara simu yake ikaanza kuita,alipotazama akabaini kuwa ni Aidan anayepiga,akakificha kilio chake na kuipokea simu kwa sauti ndogo iliyojaa huba.

"Hello darling jamani ulikuwa wapi sasa siku zote nakutafuta hewani hupatikani..." Rayana akazungumza kwa upole na kwa heshima.

"Haha haha haa" Aidan badala ya kujibu akawa anacheka tu kitu ambacho kilimshangaza sana,haikuwa kawaida ya Aidan anapopokea simu yake aanze kucheka.

"Sasa mbona unacheka Aidan eeeh" akahoji.

"Siku hizi umekuwa Comedian(mchekeshaji)?,maana unaniambia umenitafuta hewani kwani nimekuwa popo siku hizi?" Majibu ya Aidan yakamvunja moyo sana Rayana.

"Sawa tuachane na hayo niambie uko wapi mpenzi wangu?"

"Mimi nipo mbali sana na Dar es Salaam" Aidan akajibu na Rayana akashindwa kuongea akaanza kulia tena kwa uchungu.

"Kwa..nini hujaniaga Ai...dan eeh nime...kukosea ni..ni mimi,umeamua kuniacha pe..ke yangu why Aidan..." Rayana akalia sana.Aidan baada ya kuona hivyo akakata simu na kuamua kuzima kabisa.



*****

Jitihata za kumsaka Aidan kwa wale jamaa waliotumwa na Bosco zikaendelea ila siku hadi siku zikaelekea kugonga mwamba,walijaribu kila sehemu ya ambayo wanaweza kumpata lakini haikuwa rahisi kumpata.Wakiwa kwenye gari,watu wapatao tano wenye silaha za moto pamoja na visu wakakata kona ya Mabibo na kuingia barabara iendayo Mburahati.Wakakanyaga mafuta huku wakiwa wamechukia kwa kitendo cha kuunguza mafuta bila mafanikio.Mara nyingine wakajiona wao hawana akili,wanaendesha misheni pasi kuwa na ramani maalumu ya kuonesha japo mtaa anaokaa wanaemsaka.Wakajikuta wanaachia misonyo mikali kwa pamoja.

"Sasa tunatalii mji ili iweje jamani,mtu mwenye hatujui mahali anapokaa.." Akasema mmoja wao kisha akatulia kimya huku akisubiri oni lolote kutoka kwa wenzake.

"Turudi mbezi bwana" mmoja akashauri.

"Acheni ujinga...aya aliyechoka na kazi mlango uko wazi ashuke haraka aondoke" sauti ya jamaa huyo ikawakalisha kimya wenzake.



Wakafika kituo kimoja kinachoitwa saluni na kusimamisha gari yao nje ya duka moja la nguo.Wakashuka wawili na kuingia ndani ya duka hilo.Huko wakakutana na wateja wachache pamoja na wahudumu wawili,nao wakajifanya kuchagua nguo huku wakikonyezana macho,kwa ya ishara,mmoja wao akaenda kusimama mlangoni na mmoja akabaki ndani.

"Mikono juu haraka" sauti kutoka kwa jamaa huyo wa mlangoni ikasikika,mikononi akiwa ameshika bastola mbili akazielekeza kwa wateja hao na kitendo cha haraka wakafanya kama walivyoelekezwa.Wakanyoosha mikono juu.

"Lala chini fasta"

Wote wakalala haraka na hapo ndipo walipoanza kusachiwa,wakachukua kila kitu walichokiona kinafaa na kuondoka zao kwa kasi.

"Mgaa na upwa hali wali mkavu" jamaa mmoja akasema na hapo ndipo alipofungua midomo ya wenzake waanze kuorodhesha methali zao kufuatia na tukio walilolifanya.



***



"Aaah baby sio nguo hizo kabadilishe,kavae hizi" Dayana akazungumza na Aidan akachukua nguo zake na kuelekea sehemu ya majaribio,akarudi tena,mpaka walipolidhika wakawasha gari na kuondoka zao maeneo hayo ya Kinondoni.Safari hii walipanda waende Don Beach Hotel.Aidan anazivuna raha huku akiwa na binti wa raisi.Wakaingia Msasani majira ya saa nane na nusu,ndipo walipoingia mapokezi na kukabidhiwa chumba chao katika ghorofa ya tatu.

Wakaingia na kuweka nguo zao kutandani kisha wakabalisha na kuzivaa nguo za kuogelea,wakatoka nje na kuanza kuogelea katika swimming pool la hotel hiyo ya kifahari.Michezo mbalimbali wakaanza kucheza na kufurahia uhusiano wao,hata siku moja Dayana hakujuta kuwa na Aidan,mwanaume ambaye amekamilika kwa kila idara kama mtazamo wake unavyompa.

Wakati wanaendelea kucheza ndani ya maji hayo,Aidan akashtushwa kidogo na mkonyezo wa msichana ambaye yupo pembeni yake mita chache kutoka pale walipo.Msichana huyo mwenye sura ya urembo,macho malaini,lipsi za haja kiasi kwamba kwa mwanaume lijari basi hatakuwa na budi ya kumkodolea macho,maungo ya chini sasa,msichana huyo alijaaliwa sawa kupewa makalio makubwa,hipsi limevimba utadhani mlima kilimanjaro.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Akamkonjeza tena kwa uchokozi kisha akageuka nyuma na kumpa mgongo Aidan,akawa anatingisha makalio yake na kuyafanya maji yarukeruke.Taratibu mkuyati wa Aidan ukashindwa kuwa na stamina,ukaanza kuleta purukushani ndani ya nguo yake.

"Baby tushindane kuogelea" Dayana akasema lakini Aidan hakuitikia.

"Baby! wee Aidan" akarudia tena.

"Eeeeeh eeeh!" Akazinguka kutoka kwenye mawazo yake.

"Hee! unafikiria kitu gani sasa?"

"Hamna nipo sawa unasemaje?" Aidan akazuga kwa kumrushia maji Dayana huku akuchia tabasamu pana.

"Tushindane kuogelea"

"Sawa!"

Aidan akili yake yote ikaamia kwa Msichana yule anayemtamanisha wakati wote.Safari hii msichana huyo alikwishaiweka upande wa sidilia na kuanza kujilamba chuchu zake huku akilainisha macho yake kwa mrembuo,kitu ambacho kikamfanya Aidan aanze kuhisi msisimko wa aina yake ndani ya mwili.

Walipomaliza kuoga na kucheza wakatoka na kuingia chumbani kwao huku mara kadhaa Aidan akixhungulia dilishani ili aweze kumuona msichana yule aliyekuwa akimtega kwa makusudi.

"Ehee sasa kesho si unaenda kuhama kule uswazi kwenu,nimekulipia nyumba mzima ipo Kawe,kwa hiyo bado wewe tu" Dayana akazungumza.

"Whaaat!yaani mimi umenipangia nyumba mzima?" Aidan akajikuta ana furaha isiyo na mfano,akamkumbatia Dayana na kumbusu kwa furaha.

"Mbona kawaida tu,tena nitakuzawadia na gari la kutembelea"

"Oooh my God,upo siriazi kweli Dayana?"

"Yaah i'm serious baby"

Aidan akamkubatia tena na kumbusu lakini safari hii wakagandana kabisa,wakawa wanabusiana kwa mtindo wa kubadilishana mate,wazungu hupenda kuita FRENCH KISS,akamlaza chini na kuendelea na zoezi hilo.Mara simu ya Aidan ikaanza kuita,ikawalazimu wasitishe zoezi hilo,Aidan akatazama simu na kusonya kisha akaikata.

"Nani huyo?" Dayana akauliza

"Huyu ni bwege mmoja wa kitaa ananidai elfu kumi yake,ndio ananisumbua sana"

"Si ukamlipe" Dayana akashauri.

"Sawa achana nae" wakaendelea na zoezi lao lakini haijafika sekunde tano simu ikaita tena.Mpigaji wa simu hiyo alionesha kuwa na juhudi za kupiga labda kuna jambo muhimu sana la kumwambia lakini Aidan akapuuzia.

"Lete niongee nae kama unaogopa" Dayana akasema.

"Aaah hakuna haja baby tua..." Kabla hajamalizia Dayana akaichukua simu haraka na kuipokea,japokuwa Aidan alijaribu kumnyang'a lakini hakuambulia kitu.

"Hallooo sema shida yako,mbona unatunyima raha wenzio..." Dayana akazungumza na kukaa kimya huku akisubiri majibu toka upande wa pili.





"Haaa yaani mpenzi wangu Aidan umefikia hatua hii?" Sauti toka upande wa pili wa simu,Dayana akamtazama Aidan na kuiweka raudi spika.

"Sawa Aidan,Mungu anaona,kweli niliokufanyia leo hii ndio malipo yake haya,sawa Aidan sawa ila aliyekupa wewe naamini nami atanipa" Rayana akasema hayo na kuokata simu.Dayana akamtazama Aidan kisha akameza mate.

"Aidan" Dayana akaita kwa upole.

"Naam!"

"Bado huyu kikaragosi anakusumbua?"

"Ndio kama ulivyomsikia hapo" Aidan akajibu.

"Okay nitajua cha kufanya" Dayana akasema.



****

Rayana hakika akaumia sana.Moyo wake ukatamani sana kutoweka duniani,ingelikuwa kuna uwezekano wa ardhi kufunuka basi wa kwanza kuingia chini alikuwa yeye,hakutamani tena kuishi.

Majira ya saa mbili na nusu usiku,Rayana akaamua kutoka nje na kuanza kutembea kwa mguu kuelekea kwenye duka moja la hapo Mburahati kisiwani,mkononi ameshika shilingi mia tano.Hakukuwa na kingine cha kwenda kununua zaidi ya sumu,kaona muda wa kuishi kwa mateso umekwisha ni bora afanye hima ajitoe na unyonge wake katika mapenzi.Ni uamuzi mgumu sana lakini haikuwa kitu kigumu kwake.



Alipofika dukan akanunua sumu ya shiling mia tatu kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani,alipanga akainywe chumbani kwake pamoja na kuacha ujumbe.



****

Dayana akiwa amevalia gauni fupi,nywele zake kazibana vizuri,weupe wa mng'aro ukawaka vizuri,akajipakia kwenye gari lake huku akiwa na mlinzi wake.Mizunguko ya Dayana huwa inapamba moto pale baba yake anapokuwa na ziara za muda mrefu kama hizi za sasa,nyumbani akabaki yeye na wafanyakazi wa ikulu,kila kitu akakipanga mwenyewe na ratiba yake ikwa ni ya kutoka kila siku.

Wakafika Sinza na gari hiyo ikaingia barabara ya vumbi na kuanza kuisaka mitaa ya uswahilini.Hatimaye akafanikiwa kufika na wote wakashuka,kitu cha kwanza kukifanya ni kugonga mlango uliotengenezwa kwa chuma.

"Una uhakika kama wapo?" Dayana akauliza.

"Yaah nilishawaambia jana kama nitakuja"

"Sasa mbona hawafungui?"

Mlinzi huyo akasoge na kugonga kwa nguvu na baada ya dakika mbili geti likafunguliwa.Jitu nene likaonekana limekaa,sura yake huwezi kuitazama mara mbili na kuhisi kama kweli ni mtu mwema,mwili wake umejaa tatoo zenye michoro mbalimbali ya ajabu,alama kubwa ambayo ilionekana bila mficho ni ile iliyoandikwa G Killer na kumaliziwa kwa namba moja ya GKILLER1.



"Kama tulivyoongea jana tukamalize kazi basi" Mlinzi akasema.

"Ok pesa ipo kabisa?"

"Yes"

Jitu hilo likawachagua watu wawili na kuondoka.Lengo moja kuu la Dayana ni kwenda kumkomesha Rayana ili asimfuatilie tena Aidan.Ramani ya kumpata Rayana ilishakamilika na kilichobaki ni kumtia nguvuni tu.

Wakaimaliza Sinza kisha wakaingia ubungo baada ya kukata kona ya Shakelango,wakaanza kuifuata barabara kuu ya Ubungo mpaka wakafika Magomeni,wakakunja kona ya kuelekea njiapanda ya Kigogo,safari ikapamba moto kweli kweli,Dayana alidhamilia haswa kwenda kumfundisha adabu Rayana.Mizunguko yote wakaikamilisha huku ikiwachukua masaa mawili toka saa moja mpaka saa mbili za usiku.Hatimaye wakafika Mburahati Kisiwani,wakapunguza mwendo na kuanza kutembe taratibu huku wakitazama pembeni kwa umakini mno.



"Eeeh ni yule pale au namfananisha?" Mlinzi akazungumza na Dayana akamtazama binti huyo aliyekuwa katika mwendo wa haraka.

"Yaah huyo huyo..." Dayana akasema.Kwa kuwa ilikuwa sehemu ya uwazi na giza kubwa lililoifunika anga ikawawia uwepesi wa kumdaka na kumuingiza garini.Wakageuza gari haraka na kurudi walikotoka.Wakaishika barabara iendayo Mazense,wakaifuata mpaka wakakata kona ya kituo cha Madoto.

"Nyie wakina nani..?" Rayana akauliza kwa ukali lakini hajapata jibu lolote kutoka kwa jamaa hao.

"Nyie wakina nani nauli...." hajamalizia maneno yake akatulizwa kwa ngumi ya puani,Rayana akaachia ukelele wa maumivu sana lakini haukufanikiwa kutoka nje kutokana na vioo vya gari.Damu zikaanza kumvuja puani kwa wingi huku akiwa katika taharuki ya namna yake,akatafakari mara mbili lakini hajapata jawabu kamili,hakujua nini kilichomfanya atekwe na kupigwa namna ile.Gari ikasimama pembeni ya uwanja wa Mazense.



"Jamanii nimefanya ni..ni mimi mnaniua buree tuu!"sauti ya kike iliyojaa Simanzi na huruma ikalalamika kutoka katika gari aina ya Verosa lenye namba ya usajiri T 347 DFP.Wanaume wawili waliomuweka kati binti huyo huku wakiwa wamezuia vyuso zao kwa minajili ya kutotaka kufahamika na binti huyo.



"Nimekosa nini jamani mnaniuaa Mamaaaaa nakufaaa!" kwa hakika binti alilalamika sana kufuatia na kipigo kikali kutoka kwa njemba hizo.Mmoja wao akachomoa kitambaa na kumfunga usoni na ndipo msichama mrembo kutoka mbele upande wa kushoto kutoka upande wa dereva akagauka nyumba na kumtazama binti huyo,akatabasamu na sasa uso wake ukamchora vyema jinsi Mungu alivyoamisha halmashauri ya kichwa chake na kumuumba msichana huyo.Akamtazama tena na kunena "HUWEZI KUFA ILA CHA MOTO UTAKIONA,SASA BASI MIMI NI RAIA MWEMA SANA LAKINI NITAKUA MKALI KAMA HUTAFUATA HIKI NACHOKISEMA.KUANZIA SASA NAVYOONGEA SITAKI KUKUONA UKIWA NA AIDAN SAWA!" akamaliza kwa ukali sana.



"Sawaa!"binti huyo akaitikia kwa haraka mno.Ndipo walipomtoa kitambaa na kumrusha nje ya gari hiyo.Gari ikaondoka na kumuacha binti akitokwa na machozi.Akajinyakuwa na kujivuta vumbi kisha akaanza kukimbia nyumbani kwao.

Rayana hakuamini kama kweli katoka mikononi mwa wale watu,akakimbia sana huku kilio hakikumkauka mdomoni mwake.

Ukimbiaji wake haukuwa wa kutazama mbele wala nyuma,alichokijari yeye ni kuifuata barabara ya kurudia Mburahati kisiwani,ndipo alipofika kona ya madogo na kutaka kuvuka kwenda upande wa pili.



'Paaah!' Mlio mkali wa gari ukasikika,Rayana akaanguka chini na kutulia tulii,damu zikaanza kumwagika na kuipaka rangi barabara hiyo.Ni gari aina ya DCM inayofanya route zake Buguruni kwenda Mazense,ikiwa kwenye mwendo kasi ikamgonga Rayana ambaye alikuwa akivuka bila kutazama upande wowote.Watu wakaanza kumiminika na kujaa katika eneo la tukio.Dereva alikwishatokomea gizani na kuwaacha abiria ndani ya gari hilo.Raia wakazidi kujisogeza ili wasisimuliwe tukio hilo.



****

Jumba alilopangiwa Aidan na mpenzi wake Dayana lilikuwa lenye ufahari mno,kila aina na samani zikang'ara ndani kuanzia sebleni mpaka vyumbani.Aidan hakuwa na shida tena,shida sasa zikawa kama hadithi za wakoloni.Umila wake wa kukaa bila kutumia kilevi cha aina yoyote ukapotea ,kwa sasa ana uwezo wa kupakia bia hata tano mpaka sita kichwani mwake.

"Zalii la me..ntali lilitokea...wakati mi nna nja...a,nikapendwa na demu kale..na kuwaacha watu wote wakinishangaa katika mitaa...." Aidan akaimba wimbo wa msanii nguli wa kizazi kipya Profesa J huku mkononi ameshika glasi iliyojaa pombe,dhahiri kuwa amelewa kwa zile pombe anazokunywa.Wakati anaendelea kuimba mara simu yake ikaita,akaitazama na kuichukua,namba ngeni ukamfanya abinue kinywa kwa dharau kisha akaipokea.

"Helloo wee una...shida ga..ni unaongea na mk...we wa rais ha..pa" Aidan mdomo ukawa mzito katika kukamilisha maneno yake kutokana na pombe alizokuwa nazo.

"Rafiki yangu shemeji kapata ajari hapa,amegongwa na gari wewe uko wapi?" aliyepiga simu akaeleza.

"Shemeji yako gani?"

"Rayana kaka kwani una mademu wangapi?"

"Aaaah na afe tu,mwache afee bana" Aidan akazungumza na kukata simu.Akaingia kwenye majina na kuibonyeza namba iliyohifadhiwa kwa jina la Queen bonge,akaipiga na baada ya sekunde chache ikapokelewa.

"Queen wangu uko wapi?" Aidan akauliza kwa sauti ya kilevi

"Nipo kiwalani baby uko wapi mpenzi wangu?" Queen Bonge akajibu na kuuliza.

"Ni..po ghe..to njoo fasta"

"Sawa dakika sifuri"

Aidan akaanza mchezo wa kubadilisha wasichana wa kila aina huku akitumia pesa anazopewa na Dayana.Baada ya robo saa,mlango ukagongwa na ndipo Aidan alipoufungua.Queen bonge akaingia huku akiwa amevaa nusu uchi,makalio yake makubwa yaliyovimba yakamsisimua Aidan na bila ajizi akajikuta anathubutu kunyanyua mkono wake na kupiga makalio hayo mara mbili,Queen bonge akatabasamu na kumvuta Aidan,akavutika kwa urahisi mpaka kifuani kwa Queen na kuanza kubadilishana ndimi zao.Maisha ya namna hii ndio aliokuwa anayatafuta kwa hamu sana,mademu ambao alikuwa anawakosa sasa walianza kumtambua mmoja wapo ni Queen Bonge kwa jina lake la kawaida aliitwa Farida,jina la Queen Bonge limetokana kwa sababu tu ya unene wake,anaishi Kigogo maeneo ya Luanga huku akiwa na shughuli ya saluni.



Siku moja Aidan akiwa katika harakati zake za kutafuta riziki kabla hajaingiwa na zari la kupendwa na Dayana,alipita maeneo ya Luanga huku akiwa na toroli lililojaa mananasi kama tenda yake ya kupeleka kwenye genge moja la hapo Luanga.Akajikuta anakosea kumsukuma dada huyo anayeitwa Farida,hapo ndipo alipouchokoza moto wa bonge huyo.Watu wengi wakaelekeza macho yao kule walipo Aidan na Farida,walijua fika mtiti wa Farida pale anapoharibiwa tena ilikuwa asubuhi kabisa.

"Samahani dada ni bahati mbaya" Aidan akajaribu kuomba msamaha lakini Farida hakuelewa kabisa.Farida akamshika shati Aodan na kuanza kumburuka kama mtoto mdogo na kuwafanya watu watazamao waanze kucheka na kupiga kelele.

"Ndio kibonge mpe huyoooo!" Kelele hizi zikampa kichwa Farida,akawa anaongeza kipigo kwa Aidan.Mfadhaiko mkubwa mno kwa Aidan,aliomba ardhi ipasuke ili ajifukie kuliko fedheha ile anayoipata.Mbali na yote leo Aidan amethubutu kumpa moyo wake na kuwa mpenzi wake baada ya Dayana.Ndani ya dakika kumi wakajikuta wanaburuzana kuelekea chumbani.



******

KITUO CHA AFYA CHA MBULAHATIhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Mama Rayana pamoja na mtoto wake wa kiume hakujua kabisa kinachoendelea kwa mwanae,kitu gani nimempata mpaka akifikia hatua ya kupatwa na ajari kama ile.Rayana bado yupo hoi kitandani,chupa ya kwanza damu imeishia na sasa amewekewa ya pili,gharama zinakuwa kubwa na hata kwa kulipa hawapajui.Siku mbili zimekatika,Rayana ana majeraha mengi sehemu mbalimbali za mwili wake.Manesi ambao wanafanya kazi katika kituo hiko wakajitahidi kadri ya uwezo lakini kwa bahati mbaya wakashindwa kabisa kutoa huduma stahiki,ikawalazimu waende kwenye hosptali ya taifa ya Muimbili ila swali kinakuja hapo Je? wana pesa ya kuwaruhusu kwenda Muimbili?,jibu hawana,miguu wao na njia mpaka nyumbani kwao Mburahati Kisiwani,Rayana akakosa kabisa msaada wa kifedha kilichobaki ni kukaa nyumbani huku wakiuguzana kienyeji.

Siku moja Rayana akamkubuka sana Mpenzi wake Aidan,mema mengi sana amemfanyia na imani yake kwake si rahisi kusahau.Akiwa kitandani akapapasa pembeni na kuikamata simu yake,akatafuta jina la Aidan na kupiga,simu ikaita na kupokelewa.

"Haloo Darling ni mimi Rayana mpenzi wako,uko wapi jamani nafia kitandani.." Rayana akazungumza na kushindwa kuyazuia machozi yasimbubujike mashavuni,lakini kilio kikaongezeka baada ya kusikia majibu ya Aidan.

"Aaaah mi nilijua umekufa,kumbe bado unavuta pumzi,sasa sikio iwe mwanzo na mwisho kupiga simu hii.." Aidan akasema kwa dharau kubwa.

"Sa...wa kwa yote Mungu akubariki,hivi unasahau kabisa kama nilikuwa naiba pesa kwa mama yangu kwa ajiri yako...uko wapi wema wangu kwako Aidan eeeh ..." Rayana akalia kwa uchungu sana,mapenzi yake ya dhati leo yanamponza.

"Bwa...na eeeh usinichulie kama unataka pesa zako nakurushia tena sasa hivi,kwani nilikutuma uibe?"

Rayana hakujibu zaidi ya kutokwa na machozi tu.Mara baada ya dakika tano ujumbe mfupi wa pesa ukaingia.Ni laki moja na nusu,simu ikapigwa tena na Rayana akapokea,kabla hajaongea chochote akasikia maneno makali kutoka kwa Aidan.

"Sikupendi na hii iwe mara ya mwisho kunitafuta,mimi sio type yako" simu ikakatwa na kumuacha Rayana katika huruma mno.Japokuwa aliumia sana katika moyo wake lakini kwa namna moja ama nyingine alifarijika baada ya kuiona pesa,matumaini ya kurudi hospitalini yakalejea upya.Wakati anaendelea kutafakari hayo yote mara mlango wa chumba chake ukafunguliwa na mama yake akaingia akiwa na mgeni.

"Karibu baba karibu sana"

"Asante sana mama" Mgeni huyu akaingia mpaka ndani.Ugeni kama huo ukamshangaza kidogo Rayana lakini hakutaka kuuliza zaidi ya kikaa kimya huku akitazama nini kinaendelea mbele yake.Kijana mtanashati,alivalia tisheti ambayo imemkaba vizuri mwilini,shingoni akiwa amevaa cheni za rangi ka dhahabu,saa yenye mng'aro,kapero aina ya Dope imepachikwa vizuri kichwani na kuustawisha vyema utanashati wake.

"Mwanangu Rayana huyu anaitwa Swedy,mfanyabiashara mdogo anaishi hapo mbele,nimemuelezea tatizo lako na kwa bahati mzuri ameguswa,amesema atatusaidia kutulipia gharama za matibabu na kila kitu..." Mama Rayana akaeleza na wakati wote huo Swedy alikuwa anatikisa kichwa kukubaliana na maneno ya Mama Rayana,akatabasamu na hapo ndipo mashavu yake yakaonekana wazi kuwa yana mponyeo yaani DIMPOZ.

"Shikamoo yako kaka!" Rayana akamsalimia Swedy.

"Marhaba pole sana Rayana"

"Asante"

"Ok mama bila kupoteza muda twendeni hosptali nikawaache kisha niende ofisini kwangu" Swedy akaeleza kwa utulivu na upole kama kawaida yake.Wakamsaidia Rayana kumtoa nje na kumuingiza ndani ya gari la Swedy.Safari ikaanza huku Mzee Gwamiro akibakia nyumbani.

"Mama ulisema amepata ajari maeneo gani?" Swedy akauliza huku akiwa bize na msukani,siti za nyuma walikaa Bi.Chiku na mtoto wa Rayana.

"Madoto pale"

"Aaah yaani pale kuna wahuni wengi sana,kila mtu anajifanya dereva" Swedy akazungumza ila akatishwa na mlio wa simu yake.Akasitisha maongezi na kuipokea simu.

"Naam bosi wangu" Swedy akaitikia simu.

"Yes chief Swedy upo wapi wewe?" Sauti kutoka simuni ikauliza.

"Yaah nipo hapa njia panda ya Kigogo ninaelekea Muhimbili kidogo,vipi tena kuna kazi mpya bosi Kway?"

"Ahaa sasa ukitoka huko utapitia hapa ofisini kwangu kuna mzigo nataka nikuagizie upeleke M&K Publisher kwa bosi Eddy" Kway akazungumza na baada ya kukubaliana simu ikakatwa na safari ikaendelea.Mwendo wa dakika ishirini wakafika mnazi mmoja,wakatumia dakika kama kumi mpaka walipofika hospitali hiyo ya Muhimbili.Swedy akasaidia na Mama Rayana wakamshusha Rayana na kuanza kusonga nae ndani,manesi wakawaona na wao wakasogeza kitanda,wakamsukuma Rayana mpaka ndani.Swedy akatoka na kuingia ofisi moja ya hosptali hiyo.

"Ohoo bwana mkubwa umenenepa naona mambo sio mabaya aiseee" Daktari huyo huku akimpigapiga begani Swedy.

"Haha acha hizo kijana,sasa nina mgonjwa wangu hapo nje,naomba ndugu uniangalizie atibiwe safi bila matatizo" Akaeleza kisha akaingia mfukoni na kutoa pochi yake,akazitoa noti za elfu kumi kumi na kumkabidhi Daktari.

"Hilo ondoa shaka ndugu ,hapa ndio amefika kila kitu kitaenda sawa" Daktari akasema.

"Sawa hebu njoo uwaone maana sio unaongea tu wee kijana vipi bana" wakaongozana mpaka kwenye wodi hiyo.Baada ya kukamilisha utaratibu mzima Swedy akatoa pesa shilingi elfu hamsini na kumkabidhi mama Rayana kwa ajiri ya chakula na mahitaji yao muhimu.



"Asante sana baba Mungu akunyooshee kila kitu kiwe safi mwanangu ubarikiwe sana looh Mungu anipe nini mimi" Mama Rayana akazungumza kwa hisia,hakuwa na budi kumshuruku Swedy kwa msaada kama ule kwani ni watu wachache sana katika dunia ya sasa.



*****

"Kazi yangu ina maana imeishindwa?" Bosco akahoji vikali huku akiwa katika hali ya paniku mno,simuni lilisomeka jina la GKiller1.

"Hapana mkuu,tumeshindwa kujua ramani kamili ya kumnasa mtu huyo kabisa"

"Si ndio kushindwa huko?" Swali la Bosco likamnyamazisha GK1 kwa muda kisha akaanza kujing'atang'ata kwa maneno yasiyoeleweka.Hasira za ghafla zikampanda Bosco na ndio hapo alipoamua kuruka toka kitandani usiku huo na kutoa nguo zake maalumu kwenye kabati,akajipachika mavazi na kuiweka bastola yake kiunoni,gloves za mikono zikawa bayana na maski ya kitambaa cha usoni.Akatoka kwenye chumba chake hicho na kuingia ndani ya gari yake ndogo.Akatoka Mbezi Beach majira la saa mbili usiku,akapitia kituo cha mafuta na kujaza mafuta(full tank).Wakati yupo njiani akajikuta akipatwa na maswali mengi mfululizo,ni nampata nitamuona huyu mtu,sehemu gani anaishi?.Maswali hayo lukuki yakampunguza hasira zake na kuwa mpole,akaamua kusimamisha gari.Akajiinamia kwenye msukani wake,taratibu machozi yakaanza kumtoka huku akilitaja jina la Dayana.Wakati anaendelea kulia akashtushwa baada ya kugongwa kioo chake.Alipotazama akakutana na mtu aliyevalia nguo za kijeshi,kwenyw ukoni wake kulikuwa na kitambaa kidogo kilichoandikwa MP,hapo ndipo akahisi kuwa siku ya kufa imewadia,hakufahamu kabisa kama amepaki gari kwenye kambi ya jeshi ya Makongo.

"Kwanini umepaki gari hapa?" MP akauliza.

"Kaka samahani nimekosea kupaki hapa"

"Hujajibu swali kijana wangi,kwanini umepaki gari hapa"

Bosco hakuwa na jibu lolote la kumjibu mbaya zaidi akakumbuka ana silaha ya moto,endapo atatolewa nje na mwanajeshi hiyo akaiona silaha hiyo,litakuwa tatizo kubwa tena sana.Hasira zake zikazua maafa mengine ambayo kwa haraka haraka hayawezi kuzuilika,akakumbuka sana jinsi wanajeshi wanavyosifika kwa kuwasurubu wachafuzi wa kanuni na taratibu zao,hata alipopitia mafunzo ya kijeshi mkoani Musoma aliwafahamu vizuri sana wanajeshi hao.

"Mtoto wa kiume nikipoteza time hapa nimeingia choo cha kike" Bosko akawaza huku akipiga mahesabu ya haraka.Wazo jipya la kumsukuma mwanajeshi huyo kwa msukani likamjia,ndipo kwa kasi akatoa roki ya mlango na kuusukuma kwa nguvu sana huku akitumia bega lake,Mp akaanguka chini na kutoa sauti ya ukelele wa maumivu.Bosco akaiseti gari na kumuachia vumbi kubwa MP huyo.



*****

*****

Ujio wa raisi Noel Mkwakwacha kutoka kwenye ziara ya ndani ya nchi,zikaanza kumnyima uhuru Dayana,kutoka kwake kulikuwa ni kwa kuhesabika mno.Hakuwa anafaidi tena raha ya Aidan.Ndani ya wiki anaweza kutoka mara mbili tu na Aidan kitu ambacho hakikumpendeza binti huyo.Kila wakati alikuwa ni wa kupiga simu na kuchat kwa wingi na Aidan huku mara nyingine wakimaliza hamu ya mapenzi yao kwa kuchat sms za mahaba zenye msisimko.Kwa Aidan hakukumpa shida sana kwani aliona kama bahati ya mtende.Akabadilisha wasichana awatamaniao huku kila alipoishiwa pesa za matumizi basi alitatuliwa matatizo aliyokuwa nayo.

Jumapili tulivu kabisa huku mji mzima ukiwa na shamrashamra za kila aina,siku hiyo ikawaonesha watu katika matabaka yao mbalimbali.Matajiri walitumia muda kama huo kutulia na familia zao sehemu mbalimbali,wafanyakazi wakaitumia siku hiyo kuburudika katika kumbi mbalimbali mara baada ya kufanya kazi kwa muda wa siku sita ndani ya wiki,wasakatonge hawakuacha kujipatia kipato siku kama hizo kwani wafanyakazi wengi walitumia muda mwingi kununua bidhaa zinazouzwa na wasakatonge hapo ni wazi matabaka katika jamii hutegemeana kwa kiasi kikubwa.Je hawa waitwao mafukara wanaitumia siku kama hii namna gani?.

Mama yake Dayana pamoja na Dayana siku hiyo waliipanga kuitumia kwenye sherehe ya ndoa ya mtoto wa kiume wa Bi Simba Mwajimba.Sherehe hiyo ilipagwa kufanyika ukumbi mmoja uliopo Afrikana.Dayana akampigia simu Aidan wakutane huko.Kweli safari ikapangwa na kupangika,gari ya kifahari itumiwayo na raisi katika ziara ndogondogo za jiji ikaandaliwa na dereva mahiri akapanda garini ,baada ya wahusika kujiandaa vyema wakaingia garini na safari ikaanza.Njia mzima walikuwa kimya,hakukuwa na hata mmoja aliyethubutu kumsemesha mwenzake mpaka walipofika mataa ya mwenge,ndipo wakakutana na foleni kubwa,ikawalazimu wasubiri wakati gari zingine zinaruhusiwa.

Baada ya mwendo wa dakika kama ishirini mbele wakafika Afrikana,wakashuka na kuingia ukumbini.

Ukumbi mkubwa ulipambwa vizuri mno inaonrsha wazi wapambaji walikuwa makini mno na kazi.Macho ya Dayana yakaanza kuzunguka huku na huko kama antena,anatafuta sehemu gani alipo mpenzi wake Aidan,baada ya dakika mbili mbele akamuona akiwa amekaa pembeni kabisa ya ukumbi huo,wakati huo kila mmoja alikuwa bize na vinywaji vyake,kila mgeni aliyeingia alikaribishwa na kinywaji chake.Dayana akainuka na kuelekea alipo Aidan.

"Sijakuweka lakini?"

"Hapana baby ni kawaida tu,nimefika muda si mrefu"

"Sawa ila hujasumbuliwa getini?"

"Walihitaji Coupon yao sijui"

"Ehee ukawapa nini sasa?"

"Aaah si unajua mi mtu wa uswazi,nikawapiga kiswahili wakaelewa".

"Haha haa baby mbaya sana wewe" Dayana akafurahi kwa kuachia kicheko cha chinichini.Wakaletewa vinywaji na wahudumu wa sherehe hiyo na kuanza kunywa.Wakati wanaendelea kunywa huku wakitupiana stori mbili tatu,mara Aidan akajikuta akigandisha macho kwa msichana aliyevalia nguo fupi sana,kichwani alikuwa na nywele ndefu zenye rangi ya dhahabu huku zikinakshiwa kwa maua madogomadogo,ukaaji wake ukampa msisimko wa ajabu Aidan,alikaa kwa kukibinua kiuno chake na kuacha makalio yake wakiwa yamevula vizuri nyuma.Aidan akameza mate ya uchu kisha akameza mate.Akawa anamtathimini msichana huyo kwa umakini,akagundua kuwa ana lips nene yaani ni zile KISS LIPS zililowana kwa lip stick ya rangi nyekundu aliyopaka,alikuwa akichezea simu yake huku pembeni akiwa na unywaji wake.

"Baby Aidan unajua nina hamu sana?" Dayana akachokoza mada mpya kwa Aidan.

"Sasa tunafanyaje na tupo kwenye sherehe?"

"Kwani hatuwezi fanya,kule kuna choo,kule kuna maua mengi huoni kunafaa? Please nahitaji joto lako,unadhani nina siku ngapi sijafanya kitu hiki na wewe?" Dayana akalalamika sana huku akiomba haki yake apewe.

"Mmh nakuomba tuvute subira"

"Noo baby now" Dayana akasisitiza.

"Mmh ok sasa tufanye kitu kimoja,hapo nje kuna gest tunaweza kukimbia haraka halafu turudi,mimi natangulia sawa!" Aidan akasema na Dayana akatabasamu.Aidan akatoka zake nje huku mahesabu yake yalikuwa juu ya yule msichana aliyemuona awali.Baada ya dakika tano walikutana kwenye gest ya jilani,wakaingia chumbani na hapo sasa kila mmoja akawa anacheza na mwili wa mwenzake mpaka walipopandwa na mzuka wa aina yake,wakajikuta wanavunja amri ya sita.



****

Mama Rayana alifurahi sana siku hadi siku,Rayana alianza kurudi katika hali yake ya kawaida.Kutokana na matibabu yenye uhakika ndipo wakajikuta wakiruhusiwa kurudi nyumbani huku wakipewa maelekezo juu ya matumizi ya dawa.Wakaingia ndani ya gari la Swedy na safari ikaanza.Majira ya saa kumi na nusu jioni ndio majira ambayo Mr swedy hurudi toka ofisini kwake.Wakapitia sokoni kariakoo na kununua baadhi ya mboga pamoja na matunda kwa wingi.Hakika Mama Rayana na Rayana hawakujua kabisa kijana huyo ana wema wa aina gani.Wakafika nyumbani na Swedy akawaaga kisha naye akaenda kupaki gari yake nyumbani kwake.Katika mtaa huo wa Mburahati Kisiwani,Swedy alifanikiwa kupanda upande mmoja wa nyumba,hakuwa na mke zaidi ya kuishi peke yake.Hakuwa mtu wa kupenda wanawake japokuwa wanawake kadhaa walijaribu kujisogeza karibu yake lakini waliambuliwa patupu,maneno ya chinichini yakaanza kuongelewa kuwa inaweza Swedy akawa na matatizo fulani ya kiafya,kila mmoja alijitwisha swali lake lakini hata siku moja hawakupata majibu.



Baada ya kuoga,akarudi chumbani kwake na kufungua jokofu lake,akatazama idadi ya vinywaji vilivyosalia ndani ya jokofu hilo.Akabadilisha nguo na kuvaa bukta pamoja na T shirt,akatoka nje na kuanza kuelekea kwenye kibanda cha kuuza chipsi.Alipohakikisha amenunua chakula kinachomtosha,akatoka na kuingia dukani,akanunua vinywaji kisha akarudi zake chumbani.Akafungulia TV na kumtazama habari huku akishushia chakula chake taratibu.Wakati anaendelea kupata chakula na burudani mlango wake ukagongwa.Akapunguza sauti ya TV na kumruhusu apigaji hodi aingie.Akaingia binti wa makamo akiwa amevalia gauni ndefu huku mkononi ameshika glasi kubwa ya juisi.

"Oooh karibu Veronica" Swedy akamkaribisha binti huyo ambaye anajulikana kwa jina la Veronica.

"Nimekuletea juisi ya parachichi ni tamu hiyo" Veronica akazingumza kwa sauti ya utulivu huku tabasamu pana likichanua usoni kwake.

"Asante karibu tule tu Vero" akamkaribisha.

"Aka! nimeshakula mie,unadhani mpaka saa tatu hii niwe nimekaa tu?"

"Sawa wacha mi nikifinye lakini hutaki japo hata kapaja haka" Swedy akazungumza kwa utani huku akimtishia kumlisha paja la kuku.Bila kutarajia akajikuta anadakwa mkono na Vero akaupeleka mnofu huo mdomoni.

"Ha haha haha nilidhani utakataa"Swedy akatania.

"Hahaha umenilengesha makusudi bana" Vero akatabasamu tena.Waziwazi Veronica akaanza kujilainisha kwa Swedy lakini Swedy kama kawaida yake,akajifanya hana muda na Vero.Alipomaliza kula akatoa chombo chake na kukiweka pembeni kisha akarudi tena sehemu aliyokuwa ameketi na kuanza kunywa juisi.Veronica macho kayalegeza,zipu ya kifuani akailegeza pia ili mradi amshawishi Swedy kufanya kitu fulani kwenye mwili wake.Mara sauti ya kuitwa kwa Veronica kukasikika,ndipo Swedy akapata afadhali.Veronica akafungua mlango huku akijiweka sawa zipu ya kifuani kwake.

Muda wa saa nne usiku akachukua Lap top yake na kuiwasha,akaenda kwenye kazi aliyoiachia mchana na kuanza kuiendeleza.Ni kazi ya riwaya yake mpya ambayo anatarajia kuitoa katika mfumo wa kitabu,akaanza kuandika kwa umakini sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Aaah hizi kazi jamani ni adhabu tupu,yaani mtu unakesha kuandika halafu anatokea mtu huko anakuja kuikopi ya kuiua daah,halafu shabiki sasa,yaani hata shilingi buku jero anaiona nyingi,wangelijua jinsi tunavyopata shida wasingelilalamika namna hii" Swedy akalaani huku akiendelea kufanya kazi.

"Mtu hata mia mbili na hamsini ya kitanzania ya kulipia kipande kimoja anaona kama anatoa milioni sabini...,kweli hii kazi inahitaji moyo na uvumilivu" Swedy akaendelea kuongea peke yake juu ya wadau wa simulizi wanavyowakatili watunzi wa waandiashi ya hadithi za mitandaoni.



****


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog