IMEANDIKWA NA : SWEDI SHAURY
*********************************************************************************
Simulizi : Binti Wa Raisi
*********************************************************************************
Simulizi : Binti Wa Raisi
Sehemu Ya Kwanza (1)
Taratibu kigiza cha usoni kinaanza kuinyemelea mbingu na kuwafanya raia waanze kuwasha taa zao za majumbani na wale wenye uwezo hafifu basi walilazimika kuwasha vibatali vyao ili mradi tu wakabiliane na lile guza linaloingia kwa kasi katika nyumba zao.Hekaheka zinazidi kuongezeka na kulichangamsha jiji.Wasaa kama huu basi hupendwa na watu wengi sana hata humu mijini,mathalani, vibaka hutumia muda huo kujibatia bidhaa za watu kwa kupora,wasichana hutumua muda huo pia kujisogeza sehemu ambazo kwa namna moja ama nyingine wanaweza kujipatia pesa kwa njia ya kujiuza kwa wanaume.Muda kaa huo pia hutumika kufanyia maovu ya kila aina kwani tu giza kuficha kitu kisionekane.
MBULAHATI KIGOGO JIJINI DAR ES SALAAM.
Saa mbili kamili ya usiku,mtaa wa Mbulahati kisiwani,wakazi wamechachawa kufanya shughuli zao zinazowahusu,kila mmoja alijitahidi kila linalowezekana ili waweze kupata kitu chochite kile cha kupeleka kinywani.Madereva pikipiki wana kazi moja tu,ni ya kuwashawishi abiria na kuwasafirisha sehemu watakazo kwenda.Wakina mama ntilie ndio kwanza wanaongezewa kasi ya kuwahudumia wateja wanaomiminika katika vibanda vyao.
Rayana au Raiya kama wanavyopenda kutuita,sasa yupo jikoni anatayarisha chakula cha usiku.Machozi yanamtoka na kikohozi kinamnyemelea na ghafla anapiga chafya tatu mfululizo,hii tu ni kutokana na mkaa ambao anatumia kutoa moshi mwingi kupita kiasi,inaonesha dhahiri bado ulikuwa mbichi,lakini wauzaji wakale wapi na wenyewe wanatafuta pesa ya kula na familia zao?.Rayana akachukua khanga yake na kujifuta machozi yaliyosababishwa na moshi kisha akaendelea na mapishi yake.Baada ya kumaliza kupika wali,akauipua na kuweka chungu kidogo,akamimia mafuta kiasi na kisha akayaacha yapate moto,mara baada ya kupata moto akamiminia vitunguu na mafuta hayo yakaruka juu kidogo kisha baada ya sekunde chache vitunguu vikaanza kunukia na kuwaumiza pua watu wapitao njiani.
"Mmmh mambo matamu hayo...looooh" ni moja ya wapitanjia ambao hutumua mpenyo huo ulio kando na jiko analopikia Rayana,wanakili kuwa mtu aliyepo ndani anaweza kuunga barabara kabisa.Vitunguu vilivyoita vizuri,akamiminia nyanya na sasa kasi ya kunukia ikaongezeka.
Mzee Gwamiro ambaye ni baba yake mzazi wa Rayana,yupo nje akiwa na mke wake Bi.Chiku Gwamiro wanatazama watu wapitao njiani huku mara kadhaa wakizungumzia masuala yao ya kifamilia.Mzee Gwamiro kama kawaida yake ifikapo mida ya usiku kama hiyo,huchukua kiti chake cha uvivu na kutayarishiwa kahawa kisha anaanza kuifurahia dunia bila wasiwasi wowote.Siku hiyo Mzee Gwamiro alisubiri kwa hamu sana chakula aina ya Wali na mboga samaki ambacho kilikuwa kinatayarishwa na bintiye Rayana.Harufu nzuri inayotoka jikoni,inamvutia sana Mzee huyo mwenye mvi nyingi,anaamua kuchukua kikombe chake cha kahawa na kumeza fundo moja kisha anakiweka chini,anamtazama mke wake,anaachia tabasamu hafifu kisha anatazama njiani,anamuona Mzee Wajihi akimasalimia kwa kumpungia mkono.
"Habari yako Mzee Gwamiroo?" Mzee Wajihi anamsalimia Mzee kwa Gwamiro akiwa mbali nae.
"Swalamaa mzee mwenzangu za mihangaiko?"
"Safi tuu mke wetu anasemaje?"
"Yupo mzima anakusikia"
"Haya mpe salamu zangu"
"Sawa Wajihi" wanamaliza mazungumzo Mzee wajihi anaishia gizani.Anaingia Rayana akiwa na bilika ya maji,anatua chini na kuingia ndani tena,anarudi akiwa na sinia la wali huku pembeni akiwa ameshika bakuri lenye samaki.
Kwa heshima,Rayana akawanawisha wazazi wake na baadae akamalizia mwenyewe.
"Mdogo wako yuko wapi?" Mama Rayana akauliza huku akimtazama binti yake.
"Hata mimi sijui,kaondoka tangia asubuhi hapa" Rayana akajibu.
"Lijitu likiondoka hakuna haja ya kuliukizia,kwani yeye hajui kama muda huu ni wa kuwepo nyumbani!" Mzee Gwamiro akafoka kwa ukali akipinga kile kitu kinachoongelewa na mke wake.Baada ya kumaliza kula,Rayana akatoa vyombo na kuvihifadhi sehemu sitahiri.Akachukua ndoo na kujaza maji,hapo ndipo alipoingia bafuni na kuvua nguo zake zote.Uzuri aliokuwa nao hakuweza kumzuia kujikagua kila aendapo bafuni,alifurahi sana hasa pale alipojitazama akiwa uchi wa mnyama,akatabasamu na kukiri kuwa yeye ni mzuri,tena ule uzuri wa asili sio wa kununua kama wafanyavyo wasichana wengine.
Akajimwagia kopo la kwanza la maji na kuongeza la pili mpaka la tatu kisha akachukua sabuni na kuanza kujipaka maongoni mwake.Baada ya dakika kama kumi akatoka akiwa amejifunga khanga yake na kuingia chumbani.Akafungua begi lake na kutoa nguo ambazo zingemfaa kwa usiku huo na kuziweka pembeni,akachuku mafuta ya mgando aina ya BABY CARE na kujipaka akianza sehemu ya miguu yake mpaka mwili wote ukaisha.Akatoa simu yake ndogo al maarufu kwa jina la Jicho moja,akaiwasha na hapo meseji zaidi ya tatu zikaingia,alipozifungua akakuta moja kutoka kwa rafiki yake Jack na zilizobaki zilitumwa kutoka kwa Aidan ambaye ni mpenzi wake anayempenda sana.Akafungua ujumbe wa Aidan na kuusoma.
'Mpenzi mi naumwa na kichwa,sina hata mia ya dawa ,naomba unisaidia mke wangu nitakufa mimi' ujumbe huo ukamshtua sana Rayana.Mtu anayempenda kwa dhati anaumwa na pesa hana,lakini alipojifikiria akagundua na yeye hana pesa hata kidogo.Moyo ukawa unapwita kwa kasi na kuhofia afya ya mpenzi wake Aidan.
Wakati anajifikiria jinsi gani ya kupata pesa ndipo alipokumbuka kuwa kuna sehemu ambayo mama yake huwa anaifadhi pesa.Akatabasamu kisha akavaa nguo zake haraka,akaanza kunyata naelekea chumbani kwa mama yake.Bahati mzuri akakuta wazazi wake hawapo,akafungua mlango na kuingia ndani.Akafungua droo ndogo na kutoa shilingi elfu mbili na mia tano.Akafunga na kutoka nje kwa uangalifu.
Akatoka na kuufunga mlango,akatokea mlango wa nyuma na kuondoka kwenda kwa mpenzi wake Aidan sehemu moja iitwayo Barafu.Akatumia dakika chache sana mpaka kufika chumbani kwa mpenzi wake huyo.Akamkuta akiwa amejilaza kitandani huku akitazama mlangoni.
"Jamaniii mpenzi kichwa kimeanza lini?" Rayana akauliza kwa shauku,akamkumbatia Aidan na kumuweka kifuani kwa hisia kali.
"Sipendi kukuona ukiwa katika hali hii jamanii nakupenda sana Aidan wangu" Rayana akazungumza na machozi yakaanza kumlengalenga.Aidan ni kijana mwembamba mwenye sura ndefu kidogo,kidovu chake kilichojaa ndevu wengi hupenda kuziita UCHEBE zikamfanya aonekane mzuri hasa kwa wasichana wa pale mtaani,kifua chake ambacho kimetuna wastani kikawachanyanga sana mabinti wengi.Aidan akainuka na kukaa,akamtazama Rayana na kumbusu mdomoni.
"Nakupenda pia,vipi umekuja na dawa?" akauliza.
"Subiri nikakununulie hapo nje nakuja sasa hivi"
"Sasa unajua natumia dawa gani?" Aidan akuliza.
"Eheee unatumia dawa gani?"
"Kanunue Hedon za mia mbili na Panadol za mia tatu"Aidan akazungumza na Rayana akafungua mlango na kutoka nje.Baada ya dakika mbili akarudi na dawa hizo na kumpatia Aidan.Aidan akameza na kujilaza kutandani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Aidan leo nataka kulala hapa" Rayana akasema huku akimtazama Aidan,akazing'ata lipsi zake pana na kuzilowesha na mate yake.Sasa zikawa zimenona.
"Kweli eeeh" Aidan akauliza kwa mshangao.
"Yaah nataka kulala nawe hubby!"
"Sawa,hebu njoo kidogo hapa juu kwangu" Aidan akasema,jidudu la mahaba likaanza kumvizia na sasa likawa na nguvu kubwa mwilini mwake.Rayana akainuka na kulala kifuani mwa Aidan.Ndipo Aidan alipohisi kichwa kumtulia kabisa,akajibebesha mkono wake na kutuulisha juu ya mabomu mawili ya Rayana yaliyotegwa nyuma ya mwili wake.Hisia zikaanza kuwachezea kama watoto wadogo.
*****
"Mamy leo nataka kwenda kumuwatch Ali Kiba pale Solomon hall,naweza kwenda?" Sauti mzuri ya binti mweupe ambaye anamfumua nywele mama yake ikapenya vizuri kwenye ngoma ya masikio ya mama huyo.
"Sasa Dayana mwanangu si ukamuombe baba yako,kwani unamuogopea nini?" Mama huyo akazungunmza.
"Mmmh unataka ninaswe kibao cha nguvu eeeh sitaki mie,kama hutaki kunipa ruhusa natoroka leo" msichana huyo anayeitwa Dayana akazungumza.
"Umesahau walinzi wa getini eeh?"
"Aaah wale wakipewa laki tu wamenywea"
"Haha acha kunifurahisha na yule Timothy alivyo mnaa,unadhani atakubali hilo laki lako?"
"Basi yaishe mama,kwa hiyo utaniruhusu au nikaushie?"
"Hebu nifumue mie hayo tutazungumza baadae".
Mazungumzo hayo na mama na mtoto wake yakakomea hapo.Dayana ambaye ni mtoto wa pekee wa Mheshimiwa Raisi Bwana Joel Mkwakwacha,akaingia ndani ya bafu na kufungulia maji na kuanza kuoga huku akiwa na furaha sana ya kupewa ruhusa na mama yake ya kwenda kwenye Show ambayo itahisishwa wasanii wakubwa wa nchini Tanzania akiwemo Ali Kiba,Baraka De Prince,Mr Blue,Ruby na wengine wengi wakivamia Solomon hall.Dayana akamaliza kuoga na kurudi chumbani kwake.Akachukua taulo laini jeupe na kulivaa,akaketi kwenye dressing table.Ndipo alipoanza kuchanganya vipodozi na manukato ya nguvu yenye harufu mzuri mno.Alipomaliza kujipaka mafuta ayajuayo akafungua kabati lake la nguo na kuanza kuchagua nguo.Ikamchukua zaidi ya dakika kumi mpaka alipokuja kuipata nguo aitakayo.Akaivaa na kutoka.
"Muumy nimependeza?" Dayana akamtupia swali mama yake.
"Unadhani mwangu unaharibu?,yaani we kila nguo unayovaa ni kiboko kabisa"
"Mama nawe una maneno mengi,niambie sasa kama nimependeza au sijapendeza"
"Umependeza bana unataka nisemaje?"
Dayana akamuaga mama yake na kutoka nje,akamkuta mlinzi wake akiwa ndani ya gari tayari kwa safari.Akafunguliwa mlango na gari ikatoka ndani ya ikulu.
Mawazo ya Dayana hayakufikiria kitu chochote zaidi ya kuwaza jinsi atakapofika Solomon hall na kumtazama Ali kiba na kukutana na Mpenzi wake ambaye aliwekeana ahadi tangia siku mbili zilizopita.Akaitoa simu yake yenye thamani kubwa na kutafuta jina la mpenzi wake huyo.
"Hallo dear nipo njiani nakuja muda si mrefu,we uko wapi?" akauliza.
"Mimi nimekwishafika nipo kwenye meza moja mwenyewe tu" sauti mzito kutoka simuni ikasema na kumfanya Dayana atabasamu.
"Poa dakika sifuri nitakuwa hapo baby"
"Okay mwaaah"
"Mwaaaaaah"
Mlinzi huyo hakusita kumtazama binti huyo kupitia kioo chake cha kati.Akatabasamu na kuongeza kasi ya gari.Hatimaye gari ikafunga breki nje ya Hall hilo na mlinzi wa binti huyo akafungua mlango,Dayana akatoka.Sasa mbele akiwa Dayana na nyuma yake mlinzi akiwa bize kumlinda binti huyo kwa uangalizi sana.
Ukumbi ukiwa umefulika watu kufuatiwa kwa ujio wa wasanii wakubwa nchini Tanzania,Dayana akatembea mpaka upande wa wateja maalumu yaani V.I.P,akautana na mpenzi wake akiwa amejaza bia kwenye meza.Wakakumbatiana na kukaa pamoja.Vyuso zao zikaonesha tabasamu ya aina yake.
"Dayana hakuna siku uliyopendeza zaidi kama leo,yaani mtoto unametameta ile mbaya duuuh,mpaka nahisi kupatwa na kigugumizi jinisi ulivyopendeza" Jamaa huyo akazungumza.
"Mmmh mbona nimevaa kawaida sana"
"Kawaida kwako lakini kwangu,uko poa ile mbaya baby" akazungumza kwa msisitizo.Akafungua pochi yake na kutoa noti tano za elfu kumi kumi.
"Unahitaji pongezi ya hali ya juu" Jamaa akasema na kumbandika Dayana noti hizo juu ya paji lake la uso.Dayana akatabasamu na kisha akatoa mkoba wake,akachomoa fedha kiasi cha laki moja.
"Unajua baby hakuna siku uliyofunga vizuri tai kama leo,unahitaji pongezi ya hali ya juu"Dayana akayasema hayo na kumbandika mpenzi wake laki moja kwenye paji la uso.Jamaa huyo macho yakaanza kumtoka na kubaki akimtazama tu.
"Bosco mbona umeyatoa macho namna hiyo?" akauliza Dayana baada ya kuona Mpenzi wake Bosco anakodoa macho namna ile.
"Aaah we umuoni Ali kiba yule kwenye jukwaa" Bosco akasema hayo na kumfanya Dayana agwuka haraka,akakutana na sura ya kijina mcheshi ambaye ameitawala stage ipasavyo.Dayana akainuka haraka na kuanza kusogea lilipo jukwaa lakini mlinzi wake akamuwahi kumshika mkono na kumrudisha.Hisia na mapenzi yakaanza kupita kwenye chemba ya moyo wake huku akitamani sana kucheza nae pale stejini.
"Unataka kwenda wapi,humuoni yule bodigadi wake pale pembeni?" Mlinzi akazungumza na kumfanya Dayana amtazame kwa hasira.
"Wewe inakuhusu,hivi kazi yako huijui?" Dayana akazungumza kwa jazba,akamtazama Bosco naye bado alikuwa pembeni anamtazama.Bosco akainuka na kumsogelea Dayana.
"Basi mpenzi usipaniki,ni mambo ya kawaida tu haya,hivi fikiria baba yako akikuona unacheza kwenye jukwaa namna ile unadhani atakuchukulia hatua gani,isitoshe utamuweka matatani huyu mlinzi wako pamoja na mama yako pia"Bosco akazungumza kwa hisia na kumfanya Dayana anyamaze kimya.
*****
Kazi ngumu anazozifanya Aidan,zinamfanya aendelee kuimalika kimwili ila kiasi cha pesa kinamfanya avunjike moyo kabisa.Magunia mazito ya viazi anayonyanyua na kulinganisha na pesa anayopata,bado hazikizi kabisa mahitaji yake.
Asubuhi na mapema Aidan huamuka na kutembea kwa miguu hadi Kariakoo.Huko hupambana na mizigo mizito toka kwenye malori yaletayo mizigo hiyo kwa wahindi.Aidan kama kawaida yake,huungana na wenzake na kuanza kazi huku wakikimbilia kila lori linaloingia kwa siku hiyo.
Mpaka jioni inaingia na kujipapasa mifukoni anakutana na shilingi elfu tatu na mia nne pekee.Hakukata tamaa,akaamua kuingia kwenye daladala ziendazo manzese,akashuka kituo cha msikitini na kuanza kutembea mpaka barafu huko kilipo chumba chake.
"Eeeh we unaenda wapi miguu kama bakora ya kifimbo cheza,nipatie hela yangu kabla sijafunga chumba babuuuu,unaishi hapa unadhani kwa shangazi yako?" Aidan akakutana na maneno ya mama mwenye nyumba,akakumbuka kuwa mwezi umeisha na mwenye nyumba amekuja kufuata pesa yake.
"Shikamooo"
"Shika mwenyewe,nataka hela yangu tena usinitibue umenipata hapo eeeh"
"Sawa mama laki...."
"Ishia hapo hapo ushaanza maneno yako mengi eeeh,haya elfu thelasini nipatie haraka sada hivi" maneno hayo yakaanza kumuumiza sana kichwa Aidan,hakuwa na kitu chochote cha kuuza ili apate japo ya kumpooza.Mama yupo akaongea maneno mengi na mwisho wake akachukua funguo na kufunga mlango wa chumba hicho cha Aidan.
"Ukipata mshiko wangu utaniambia kwa leo onja usingizi wa kulala nje" Mama huyo akasema hayo na kuondoka zake.Aidan akamtazama bila kumaliza,akajikuta anajiegemea ukuta na kuanza kuteremka nao mpaka chini akitumia mgongo wake.Akachomoa simu yake na kujaribu kuiwasha.Akaenda kwenye namba ya mpenzi wake Rayana,akaipiga na kuiweka sikioni.
"Mambo"
"Poa mpenzi niamabie uko wapi?"
"Yaani acha tu,nimerudi hapa nyumbani,mama mwenye nyumba kanifungia chumba changu,mwezi umeisha anadai hela yake" Aidan akajieleza.
"Anakudau shilingi ngapi?"
"Elfu thelathini"
"Unasemaje?,mbona hela kubwa namna hiyo"
"Ndio thamani ya chumba baby"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mmmh haya subiri nicheki uwezekano" Rayana akasema hayo na kukata simu.Aidan akatoka na kuanza kutembea kuelekea barabarani.
Akaketi juu ya tairi huku akiendelea kuitazama anga ambayo inaanza kuingiwa na giza.
"Aidan unafanya nini hapa muda huu?" Sauti ya kike ikamshtua toka kwenye mawazo mazito na kumfanya amtazame mwanamke huyo.
"Aaah nipunga upepo tu dada"
"Aidan utakuja kuumbuka mjini hapa,unapunfa upepo muda huu haha unanichekesha sana,wenzako wanapunga ufukweni wewe kwwnye hili pira la gari mmh makubwa haya" mwanamke huyo akazungumza kwa nyodo.
"Lakini Mama Grace si...." Kabla hajamalizia akakatishwa na maneno mengine ya mama Grace.
"Au bado unasimamia msimamo wako wa kunikataa,utakuja kufa,ona jinsi nilivyojazia,yule kenge maji wako anakupa nini?" Mama Grace akazungumza huku akimgeukia Aidan na kumuonesha sehemu ya nyuma.Aidan hakuwa na la kujibu zaidi ya kumtazama tu Mama Grace.
"Twende nyumbani basi eeeh"Mama Grace akasema huku akimuinua Aidan.
"Sitaki Mama Grace naomba uniache"
"Mmmh basi chukua hii twende" Mama Grace akachomia noti tano za elfu kumi na kumpatia Aidan.Akamtazama Mama Grace na taratibu akawa anasukumwa na nafsi achukue pesa ile 'Chukua sasa unasubiri nini wakati unashida kibao?' Sauti toka nafsini ikamkoleza Aidan na kujikuta akiipokea pesa hiyo bila kutarajia.
Akalainika na kupanda kwenye gari la Mama Grace.Mama Grace ni mke halali wa Mr Bon anayefanya kasi katika kutengo cha mawasiliano,leo amefanikiwa kumtia mikononi kijana aliyekuwa anamkataa siku zote,hakuamini kabisa kama kweli kampata.Akaiwahsa gari yake na kuelekea njia ya kwenda mazense.Akapinda kona ya Madoto kisha akawa akanyoosha kuelekea Mabibo.Siku hiyo akapania sana kumtumua Aidan atoe hamu aliyokuwa anaikosa sana kutoka kwa mume wake huyo.
"Sasa tunaenda wapi huku?"Aidan akahoji lakini hakupata jibu,bado Mama Grace alikuwa bize kwenye msukani wa gari.
Akafunga breki katika jengo moja lenye ghorofa moja na kuingua ndani.Mama grace akalipia chumba na wote wakazama ndani.
Ile wanafika tu,Mama Grace akamsukumia Aidan na yeye akaja juu yake.Ndani ya dakika tatu wote wakaja kushtuka wakiwa watupu kabisa.
*****
"Eeeeh sasa humu ndani mtaniambia pesa yangu mmeiweka wapi,shilingi elfu Arobaini yangu mmeiweka wapi" mama wa Rayana anawaka kufuatia na kutoonekana kwa pesa yake.
"Sasa mimi mama ninaingia chumbani kwenu mbona mnanipakazia namna hiyo?" Mdogo wa Rayana akawaka baada ya kumuona mama yake anahisia za kumdhania yeye.
"Sasa unadhani nani mtu ambaye haeleweki humu ndani kama sio wewe,sasa pesa yangu mimi utarudisha" mama Rayana akaongea kwa hasira,akatoka akimuacha kijana wake asijue cha kufanya.
Baada ya kusikia mpenzi wake Aidan amefungiwa chumba chake,Rayana akaingia tena chumbani kwa mama yake mzazi na kuiba kiasi cha shilingi elfu arobaini.
"Mama yuko wapi?" Rayana akauliza na kunfanya mdogo wake kuondoka huku akimuacha katika mshangao mkubwa.Akaingia chumbani kwake na kujifungia.
*****
"Naomba niache,please Bosco niache" Dayana akagoma huku akijaribu kujitoa mikononi mwa Bosco ambaye bado amemng'ang'ania kisawasawa.Hakujua kapatwa na kipi mpaka akafikia hatua hiyo ya kutaka kuondoka.
"Umepatwa na nini baby,mbona sikuelewi?" Bosco akalalama lakini bado Dayana akabaki na msimamo ule ule.Dayana akavuta nguo zake na kuzivaa haraka,akatoka kwa haraka na kumuacha Bosco kitandani.Akamkuta mlinzi wake akiwa amelala ndani ya gari lake.Akamshtua na kuondoka katika eneo lile la nyumba ya wageni.
"Twende Msasani kwa rafiki zangu" Dayana akazungumza,mlinzi huyo hakuwa na kipingamizi,akapachika gia na safari ya Msasani ikaanza.Ndani ya muda mchache gari hiyo ikafika nje ya nyumba kubwa na ya kisasa,Dayana akafunguliwa mlango na kuliekea geti kubwa jeusi.Baada ya dakika kadhaa akatokea mlinzi na kumfunguliwa,akaelekezwa kitu fulani na kuelejea mlango wa sebukeni,baada ya kugonga mlango,akatokea msichana wa makamo na kufungua mlango,wakakumbatiana na kuingia ndani huku mlinzi wake akifuata nyuma.
Wakaingia ndani,huko wakakutana na wasichana wengine walivalia nguo fupi zilizowaacha maungo yao dhahiri kabisa.Wote wakajikuta wanakumbatiana kwa furaha na kuketi kwenye sofa.
"Shoga mama yupo?" Dayana akauliza huku akitazama huku na kule.
"Mmh kaenda job mwaya"
"Ahaa maana nataka kuongea mambo hapa ya kikubwa,asije akasikia Mama kikawaka hapa" Dayana akazungumza na stori zikaanza hapo.
"Shosti zangu,yaani leo Bosco kaniboaje,yaani siku zote angalau kidogo lakini leo kaniudhi kupita kiasi" Dayana akaanza kuongea na kuwafanya wenzake waache wanachokifanya na kumsiliza "Yaani leo kanishikashika,alafu akanichafua kimoja tu,likajilaza huko hati kimechoka,mbaya zaidi akaniacha na hamu na mzuka zaidi,Loooh yaani shosti sina hamu,kanitia nusksi tu siku ya leo" Dayana akazungumza na kukaa kimya kwa sekunde chache kisha akasema "hivi mtu kama huyu nimfanyaje?" akanyamaza akisubiria maoni ya rafiki zake.
"Mtu kama huyo ni kamlaza chalii na kusaka mwingine,maana tatizo hilo lipo kwa wanaume wengi tu,hasa hawa wanaojifanya kuwa na pesa zao" ni oni la mmoja wa rafiki zake.
"Bibie mchane ukweli tu anaweza kukujazia uchafu tu kunako..."
"Ndio maana mimi nachukua wanaume wa uswazi,hawa wala burger hawana kitu kabisa"
Maoni hayo yakaanza kufanya kazi kichwani mwa Dayana,ubongo wake ukaanza kukubaliana na kile kitu kinachozungumza na rafiki zake.
"Kwa mfano mimi Yesterday,nilijuta kuingia chumbani kwa huyo mkaka,yaani alinipa mavitu mpaka nikahisi kuna waka moto kwa chini,halafu nikimuambia nimechoka anasema yeye bado hajamaliza round...."
Maneno hayo yakampelekea moja kwa moja Dayana akubaliane na rafiki zake kuwa aachane na Bosco na aingie uswahilini kwani wanaamini kuwa ndiko kunakopatikana wanaume wa shoka wa kuwatosheleza.
"Kwahiyo mabest tunaenda lini uswahili?" Dayana akauliza.
"Labda uswazi gani,maana kuna manzese,kuna Kigogo,tandale.."
"Bi shosti unaijua mitaa wewe haha"
"Mi naona twendeni kesho asubuhi maana leo muda umekwenda" mmoja akashauri.Wakakubalina na mada hiyo ikawekwa pembeni.
Kama ilivyopangwa,kesho yake wakakutana pamoja na kuamua kuchukua gari mbili,moja ikiwa ya Dayana binti wa Raisi na nyingine ni ya Salmaya,mtoto wa Waziri mmoja katika wizara ya juu.Wakaingia na sasa wakaanza kutembea uswazi kutafuta wanaume.Ni kitu cha ajabu sana kwa wasichana kuwatafuta wanaume kama jamii ya kitanzania,lakini kwa mabinti hawa hawakuona tabu kuingia mtaani na kutafuta wapenzi huku wakitumia pesa pamoja na nguvu waliokuwa nayo kicheo,watoto wa viongozi wakubwa hapa nchini.Wakaamua kuanza na Tandale huku wakizunguka na gari zao,huku sehemu zingine wakitumia miguu yao kuzunguka.
******
Aidan siku hiyo akapanda gari toka sokoni kariakoo na kuanza safari ya kurudi nyumbani,mara baada ya kuhisi kuumwa na mgongo.Akajikunyata kwenye siti na kurudi nyumani.Ndipo akashuka kituo cha Msikitini,akaanza kutembea njia ya kwenda barafu sehemu ambayo chumba chake kilipo.
"Wee mkaka samahani kidogo.." Sauti nyororo toka kwenye gari ikamshtua na hapo ndipo alipoinua sura yake na kumtazama nani anayemuita.Haikuwa rahisi kwake kuweka kuaminu kama kweli ni yeye anayeitwa au nani,akajionesha kidole na kuuliza "Mimi?"
"Yaah ni wewe"
Aidan akanyakua guu la kushoto na kulisogekea gari hilo.
"Mwaya unang'oka nae huyu leo,tazama alivyo na kifua kizuri,yaaani hapo kazi kwako tu" Salmaya akamchombeza Dayana naye akachombezeka,lakini moyo ukaanza kumdunda,ataanzaje kumuambia neno 'NAKUPENDA'...
Aidan akafika mlangon na kumsalimia Salmaya ambaye alimwita.
"Naam!" Aidan akaitika
"Samahani kaka habari yako"
"Salama tu"
"Unaweza kutuonesha studio ya Mazuu ilipo,tumesikia ipo huku" Salmaya akajikanyaga huku anamtazama Aidan kwa umakini,akawa anamsanifu taratibu na kubaini kuwa Aidan ana kifua kipana,ndefu zilizokaa vizuri kidevuni kwake,akabaini kuwa kwa namna moja ama nyingine lazima awe na 'Six pack'.Akaelekeza macho yake chini na kuikuta zipu ya Aidan imevura kwa mbele,hapo akajua kabisa kuwa Aidan lazima atakuwa na mzigo mkubwa sirini.
"Samahani kama hutojari naomba upande utupeleke huko" Salmaya akasema na safari hii akaregeza sauti na kuwa nyororo mno.Aidan akatazama huku na huko na kujiridhisha hakuna watu ambao wanamtazama,akapanda na gari ikaondoka.Ndani ya gari Aidan akakutana na sura nyingi za wasichana warembo wenye mvuto wa aina yake,simu zao walizoshik,zikawaonesha wazi kuwa hao ni watoto wa tabaka la juu kabisa,hata kutoa simu yake hakupenda,kwani aliona wazi kufanya hivyo ni sawa na kujiumbua kwa warembo.Salmaya akamfinya Dayana na kumkonyeza jicho moja,ishara zikasomana kwa wawili hawa na kufanya Dayana atazame pembeni kwa aibu.Wakati wote alikuwa anamtazama Aidan kwa macho ya kuiba,akakitazama kifua na lipsi za Aidan,hapo mapigo ya moyo yakawa yanamuenda mbio zaidi ya mara ya kwanza,akahisi msisimko fulani ndani ya mwili wake pale tu amtazamapo Aidan.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapo hapo kwenye geti jeusi"Aidan akaongea kwa sauti huku akionesha geti lililoandika MAZUU RECORD,gari hiyo ikasimama na vioo vikafunguliwa.
"Mi dada zangu wacha niwaache hapa mgongo unaniuma sana" Aidan akasema na kutaka kufungua mlango,ila kabla hajafanya hivyo,akarudishwa na sauti ya Salmaya.
"Sorry! wewe unaishi wapi?"
"Ni hapo tu mbele sio mbele" akazungumza Aidan huku akiachia tabasamu,hakujua lile tabasamu linamchoma sana Dayana.
"Okay subiri kidogo"
Salmaya akachukua bussines Card ya Dayana na kumpatia Aidan.
"Utatutafuta kwa namba hiyo kesho mchana sawa!"
"Sawa" Aidan akachukua na kupiga hatua ndefu kuelekea nyumban kwake.Huku nyuma akaawacha Dayana na wenzake wanamkodolea macho ya matamanio.
"Haha shosti nawe unakaa kimya tu,si tumekuonesha au humtaki?" Msichana anayeitwa Angel akamuuliza Dayana.
"Nooo! I so like him yaan nikimtazama nakuwa kama nimepigwa na shock fulani hivi,kwa kweli he is so handsome...I love him" Dayana akasema yake ya moyoni.Hisia za mapenzi zikaanza kuota mizizi kwa kijana huyo bila kutarajia.
"Kumbe uswazi kuna wanaume wazuri namna hii,mmh so amaizing" Dayana akaendelea kusifu jinsi alivyokaribishwa mtaa wa Mburahati.
****
Rayana,msichana anayempenda sana Aidan,sasa yupo chumbani kwa Aidan.Huwa ana tabia ya kufanya kile anachotaka mpenzi wake ili mradi tu asimsikie mpenzi wake akipata shida.Japokuwa nyumbani kwao hawana kitu lakini anajitoa sadaka na kuiba pesa ya mama yake ili amfurahishe Aidan.
"Baby hebu nishike huku kidogo" Rayana akasema huku akijisogeza vizuri kwa Aidan.Aidan hakutaka kusubiri kabisa kuambiwa amshike wapu,tayari alikwishajua wapi Rayana huwa anapenda kushikwa kila siku,akamtomasa hipsi zake na mhemo wa Rayana ukasikika vizuri masikioni mwa Aidan.
"Ndio mpenzi nakupendea bureew mie,maana sio kwa kunipapasa uko"
"Aaaah mbona kawaida tu,ila nawe kiboko,sijawahi kuona kama wewe unavyobilinga mayoyo" Aidan akasema na wote wakajijuta wanacheka,wakatazamana na kukumbatiana.
"Basi baby mi nitakuja baadae naenda kupika kwanza" Rayana akazungumza na kujivuta toka pale kitandani,akavaa nguo zake na kumkisi Aidan shavuni kisha akaondoka zake.
Aidan akainuka na yeye na kujinyoosha,akahisi mgongo wake kutulia tofauti ya jana.Akavaa bukta yake na kuinuka,akawa anaiendea suruali yake ya jana.Akaichukua na kuikung'uta,ndipo ilipoanguka sarafu ya shilingi mia mbili na kadi ya msichana ambaye alikutana nae jana njia ya barafu.
Akaiokota na kukaa tena kitandani,akachomoa simu yake na kuingiza simuni.Simu ilipoanza kuita akaikata na kuiweka pembeni,baada ya sekunde chache simu ikaanza kuita,alipotazama akabaini kuwa ni namba ngeni,akaipokea na kuiweka sikioni.
"Oyaa muhuni wangu inakuaje,leo huki kwa work?" Sauti ya mwanaume ikampata vizuri sikioni.Akashusha pumzi ndefu na taratibu matuta kwenye paji lake la uso yakaanza kujijienga,akapatwa na hasira,fikra zake angelidhani ni sauti nyororo ya msichana aliyekytana nae jana.Aidan akakata simu na kuitupia kitandani huku akiachia misonyo mfululizo.
"Mijitu mingine bana" akajisemea peke yake huku akilaani kitenda cha rafiki yake kumpigia.Wakati anawaza hayo mara simu ikaita tena na hiyo pia ilikuwa namba ngeni,akaipokea na kuiweka sikioni.
"Helloooo!" Akapokewa na sauti kali na nyororo mno.Moyo wake ukapiga na kujikuta anashikwa na kigugumizi na kushindwa kuongea kabisa.Akajibaraguza na kuitikia kwa shida.
"H...a..llooo mimi ni yu..le ki..jana wa..jana wa kwa Mazuu" akajikanyaga na kusema hayo.
"Ooooh my God uko wapi jamani" sauti ya Dayana ikauliza kupitia upande wa pili wa simu.
"Nipo Ki..gogo huku maskani" Aidan akasema.
"Basi fanya uchukue bodaboda uje huku Coco Beach sawa!" Dayana akasema.
"Sawa lakini mi sina hela ta bodaboda,nina mia mbili tu hapa" akasema Aidan kwa sauti ya chini.
"Usijari nitakulipia mimi"
"Sawa"
Aidan akakata simu na kufungua sanduku lake ka nguo,akatoa nguo alizowahi kuzinunua maeneo ya Karume,akavaa haraka na kuimalizia kiatu chake kilichochanika kwa chini na kutoka chumbani humo.Akawnda hadi kwa madereva bodaboda na kumuambie wapi ampeleke.
"Coco beach shiling elfu kumi na tano" dereva huyo akasema.
"We twende bana kwani una wasiwasi gani?" Aidan akaongea na pikipiki ikachomoka na safari hiyo ya kwenda Coco beach ikawa imepamba moto.Wakachukua nyingi mpaka walipofika kwenye beach hiyo,Aidan akachomoa tena simu na kubipu,akakipigiwa na kuelekezwa sehemu alipo.
"Karibu sana mkaka" sauti ya Salmaya ikamkaribisha vizuri Aidan.
"Asante,samahani yule dereva wa bodaboda anasubiria nauli yake pale" Aidan aliposema hivyo Dayana akafungua pochi yake na kutoa kiasi cha shilingi elfu thelasini.
"Asante sana nakuja sasa hivi" Aidan akakimbia na kuwaacha Dayana na wenzake wakimkodolea macho.Baada ya dakika mbili akarudi sehemu ile ile.Dayana akamtazama Salmaya kisha akarudisha macho kwa Aidan,akamtazama kwa jicho la kuiba,akajilamba lips na kuzilowanisha mate.
"Samahani kaka kwa usumbufu"
"Bila samahani" akazungumza Aidan.
"Aaah ok,mimi naitwa Salmaya ni mtoto wa Waziri wa mambo ya ndani,pia huyu anaitwa Angel ni mtoto wa Waziri wa ujenzi na huyu anaitwa Dayana..." Salmaya akakohoa kidogo na kuendelea
"Huyu ni mtoto wa Raisi"
"Raisi Noel Mkwakwacha!" Aidan akashtuka sana na kuinuka eneo lile,akamtazama Dayana kwa macho ya woga.Kuketi sehemu kama ile na mtoto wa raisi ni kama kujitafutia matatizo.
"Sasa unaenda wapi?" Salmaya akauliza na kumfanya Dayana ainuke na kumfuata Aidan ambaye alikwisha piga hatua tatu kutoka eneo hilo.Dayana akamshika mkono na kumrudisha.Akaamua kutoka sehemu hiyo na kwenda pembeni.
"Usiwe na wasiwasi kabisa,hivi umesema unaitwa nani?"
"Aidan"
"Ooh nice name,mimi naitwa Dayana,kwa kweli nimekuwa nikikufuatilia sana,yaani kila nikuona nahisi mwili wangu kusisimkwa, Aidan..."
"Naam"
"Nakupenda sana Aidan,please reserve my heart,nakupenda sana" Dayana akazungumza kwa hisia mno.
"Noo lakini unadhani nikifahamika kwa baba yao si nakufa mimi?,halafi isitoshe nina mchumba wangu namlenda sana,siwezi kumuacha" Aidan akazungumza na kumfanya Dayana amtazame kwa makini sana.
"Noo Aidan,sema unachotaka mimi nitakupa kila utakacho,sema nini nikupe Aidan" Dayana akajikuta anashuka chini na kupiga magoti bila kutarajia.Aidan akawa na wakati mgumu sana.
"Siwezi utaniweka lehani mwenzio,tazama mimi masikini kabisa,sina nyumba sina hata kimoja cha thamani,je unadhani tutaishi vipi,na baba yako akigundua huu mchezo,si atanikatwa kichwa kabisa" Aidan akalalamika lakini Dayana akwa na msimamo uleule.
"Usiseme hivyo,hakuna mapenzi ya tajiri na maskini,yote yapo sawa,isitoshe baba yangu hana ukali wowote Nakupenda tafadhali Aidan" Dayana akazungumza huku machozi yanaanza kumtoka taratibu,kama mtu aliyekuwa karibu katika eneo hilo na kushuhudia tukio la wawili hao,angelidhani wanacheza movie,Aidan aliyesimama amechakaa mno tofauti ya Dayana anayempigia magoti kweli msemo unaosema 'MAPENZI HAYANA MWENYEWE' hakika haujakosewa kabisa,Mapenzi yaache yaitwe Mapenzi.
Picha ya Rayana ikaanza kupita kwenye ubongo wa Aidan kama mkanda wa picha ndani ya kamera,mambo mema ya Rayana yanajichora na kuleta taswira kamili katika kichwa Aidan,mara maswali mengi anajiuliza,maswali mengine hayana kichwa wala miguu na mengine ni ya msingi lakini ufumbuzi wa majibu unamletea shuruba,anaishia kumtazama Dayana na kutikisa kichwa,anajaribu kuvutana na nguvu ya Mapenzi,mapenzi kati ya Rayana na Dayana.
"Chukua hizi naomba ufikiria jinsi gani utaupokea moyo wangu" Dayana akamkabidhi bahasha Aidan na kumtamkia maneno hayo.
Aidan akaipokea na kuanza kupiga hatua za kuondoka huku mara kadha akigeuka nyuma na kuntazama Dayana.
"Aidaniii!" Dayana akaitwa kwa mbali na kumfanya ageuke.
"I LOVE YOU SO MUCH" Dayana akamtupia maneno matamu ila Aidan hakuonesha uso wa tabasamu kabisa.akakunja kona na kuanza kunyoosha kuelekea zilipo bodaboda.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aidan akafaikiwa kufika nyumbani kwake na kujitupa kitandani huku akiwa amechoka mno.Mtiririko wa mawazo ukaanza kuusumbua ubongo wake,kikubwa kinachomuumiza ni juu ya kumchagua mmoja kati ya DAYANA au RAYANA.
"Daaah ila mtoto wa raisi,si kiki hili hapa mjini" akazungumza pekee yake.Akakumbuka alipewa na bahasha,akaamua kuitoa mfukoni na kuifungua,
"Aaaaah jamani si majaribu haya" Aidan akahamaki baada ya kukuta kitita cha pesa kikiambatanishwa.Akajikuta anatokwa na macho hasiamini kama kweli kibunda kile kapewa yeye.Akachukua kikatatasi na kukifungua,hapo ndipo alipokutana na maandishi yaliyosema kwa herufi kubwa.
Maandishi hayo yakasomeka hivi....
'NATAKA KESHO NIKUTOE AIDAN,TAFADHALI NAOMBA UNITAFUTE BILA KUKOSA.....I LOVE YOU AIDAN'
Aidan akaikunja karatasi hiyo na kuitafuna,akachukua bahasha ya na kuchukua elfu hamsini,akatoka nje na baada ya dakika tano akarudi akiwa na mfuko laini.Alinunua chipsi mayai pamoja na kuku wa kukaanga mzima,akachanganya na mishikaki,baada ya hapo akanunua na juisi ya parachichi,akaweka mezani na kutoa simu yake,akaitafuta namba ya Rayana na kumpigia.
"Naam mchumba uko wapi?" Akauliza na upande wa pili wa simu ukajibu "Nipo nyumbani mpenzi wangu"
"Sawa,sasa njoo gheto kuna zawadi yako tamuuuu!" Aidan akasema.
"Aidan nawe una vituko,una zawadi gani ya kunipa wewe? Hahaaha" Rayana akacheka kidogo na kusema "poa dakika sifuri nitakuwa hapo".
Umbali wa kutoka Mburahati kisiwani mpaka kufika mtaa wa barafu,haukuwa umbali mkubwa,ukamchukua Rayana kutembea ndani ya dakika tano tu.Rayana hakuamini alichokiona,meza ya Aidan ilikuwa imechafuka vyakula vya ghali zaidi ya uwezo wake aliouzoea siku zote.
"Mmh wewe umepata wapi pesa hizi?" Rayana akauliza kwa mshangao.
"We kaa kwanza tule nitakuambia" Aidan akasema na Rayana akaketi pembeni ya Aidan na kuanza kula huku wakitumia njia ya kulishana.
****
Kitu kilichomuuma zaidi Bosco ni baada ya Dayana kutopokea simu yake,moyo ukamuuma sana,hata alivyojaribu kumpigia mama yake Dayana,hakupata jibu kamili kabisa.Kuanzia siku hiyo Bosco akawa mtu wa kukesha kwenye baa na kunywa,hakuwa na njia nyingine ya kuweza kuondoka na mawazo yanayomsibu.Dayana ndiye aliyemtumaini katika maisha yake ili aje kuwa mke wake wa ndoa na ndio maana akaama chuo cha nchi za nje na kuja kumalizia Tanzania,hayo yote ni mapenzi tu aliokuwa nayo kwa Dayana.
Ni siku ya Jumamosi,watu wengi siku hiyo walirudi makazini kwao na kuanza kuisherehekea wikiendi yao sehemu mbalimbali,wapo waliothubutu kwenda Bar,wapo aliokwenda Ufukweni kubalizi,wapo waliobakia majumbani mwao ili mradi kila mmoja aonekane yupo bize katika kujifurahisha na familia zao ndani ya wikiendi.
Bisco kama kawaida yake,akawachukua rafiki zake pamoja na mlinzi wake mmoja na kuingia ndani ya gari aina ya Toyota Mark II,wakawa wanaelekea MLIMANI CITY,huko kulikuwa na tamasha kubwa ambalo liliwakutanisha wasanii mbalimbali.Wakafika sehemu husika na kupaki gari yao,wakashuka na kuingia ndani.Moja kwa moja Bosco akafika hadi kaunta na kuagiza pombe.Baadhi ya wasichana ambao walivalia nguo fupi,wakawa wanajipita karibu sana na Bosco,lakini bado Bosco hakuwa na mpango nao,ndio kwanza akaongeza chupi nyingine.
Baada ya kunywa bia tatu,akaamua kwenda kwenye meza maalumu(VIP),akaagiza bia zingine na kuanza kujumuika na marafiki zake.
Siku hiyohiyo ndio ilikuwa ahadi kati ya Dayana na Aidan,wakapanga wakutane katika tamasha hilo ili wapate wasaa wa kuzungumza.Dayana ndiye mwalikaji,akachukuliwa na mlinzi wake na kuwapitia wakina Salmaya,wakaingia ndani ya gari kisha wakasonga kwenda Mlimani City.Walipofika wakachukua meza na kuagiza vinywaji huku wakimtengea kiti Aidan ambaye bado hajaja katika eneo hilo.Wakawa wanakunywa bia zao taratibu juku wakisindikizwa na wimbo laini wenye hisia ya aina yake.Ikapita nusu saa kabla ya Aidan kuonekana,wakati wanaendelea kunywa mara simu ya Dayana ilpoita,akaitoa na kukuta namba ya Aidan ambayo aliisevu kwa jina la MY HEARTNESS,akaipokea na kuiweka sikioni.
"Hallo my Aidan uko wapi,mi nakurusubiri muda wote huu,please nakuomba uje haraka" Dayana akazungumza kwa hisia,ni wazi kabisa kuwa Dayana amekolezwa na Aidan japokuwa ni ghafla sana na hata mwenyewe hajajua kitu cha namna gani atokee kupenda kiasi kile,tena anayempenda ni fukara kabisa asiye na mbele wala nyuma katika maisha.
'Lakini Mapenzi hayana tajiri wala maskini,mapenzi ni maono ya mtu na mtu,ni maridhiano....yes ni maridhiano...i love Aidan' akajisemea kimoyomoyo huku akimimina chupa ya bia.
"Best mbona unahappy sana vipi tena,Aidan anakukosha nini!" Angel akadakia na wote wakacheka.Ikapita kama dakika tano na ndipo kwa mbali wakamuona Aidan anatazama huku na huko.Dayana akainuka na kumfuta,akarudi naye na kuketi kwenye meza moja.Muda wote Aidan alikuwa mtu wa kushangaa tu na kimya kingi.Hakuwa huru kabisa kuwa katika eneo lile,hofu yake kubwa ni juu ya kuwa karibu na binti huyo.Aidan akawa mdogo kama dawa ya Piritoni,alipotazama pembeni yake akakutana na sura ya mlinzi wa Dayana akiwa amemkazia jicho,hapo ndio woga ukaongezeka mara dufu.
"Samahani dada zangu nahitaji kuondoka" baada ya kimya akaamua kufunguka na kudai kuondoka.
"Mmmh nawe Aidan mbona haraka namna hiyo?" Salmaya akadakia.
"Yaani huku sikuwezi kabisa,hivi watanionaje mimi hawa watu?" Aidan akazungumza kwa sauti ya chini.
"Usijari kabisa tunaondoka sasa hivi Aidan" Dayana akasema kisha akanyanyua glasi ya bia na kuiweka mdomoni,akavuta fundo moja na kuweka glasi chini kisha akasema "naomba tukacheze Aidan please"
"Ha...pa..na siwezi kucheza,natama mi nilivyovaa,harafu nikushike wewe ,si nitakuwa najimaanisha mimi?" Aidan akasema huku analivuta shati lake lililo kubwa.
"Noo usiseme hivyo Aidan nakupenda,please nataka kucheza na wewe tafadhali" Dayana akatamka maneno hayo kwa hisia kali,akainuka na kumshika mkono Aidan,taratibu akaanza kumuinua,Aidan akamtazama mlinzi lakini bado alikuwa katika siriazi ya aina yake.Hatimaye Aidan akavutika na kujitosa katika ukumbi wa kucheza.Jukwaani alipanda msanii wa kike maarufu anayeitwa LINAH na wimbo wake wa Lonely ambao ulikuwa ukipuga kwa upole na kuwaburudisha watazamaji na wachezaji.Kila mmoja wakati huo alikuwa na mtu wake huku taa za rangi zikichukua nafasi yake katika kuupamba ukumbi huo.Aidan na Dayana wakaanza kucheza japokuwa Aidan aliogopa kumshika ila mara kadhaa alilazimishwa na Dayana kumshika sehemu anayotaka.
"Aidan naomba unishike kiuno jamani,kila ukinishika huwa najawa na msisimko wa ajabu,nishike tucheze dear..." Dayana akanena kwa hisia huku akiuvuta mkono wa Aidan na kuuweka kiunoni.
'Mmmh majaribu haya,yaani ukisikia mtoto wa Kigogo nauawa leo na raisi basi leo' Aidan akajisemea huku akicheza taratibu ili kumridhisha Dayana.
"Nikuulize kitu Aidan?" Dayana kasema na kumfanya Aidan alidhie.
"Unanipenda kweli au?" Swali hilo likatamkwa na Dayana huku akimshika kidevu kwa kiganja chake laini mithili ya mtoto mchanga.
"Mmh unasemaje?"
"Unanipenda?"
"Kivipi yaani"
"Aah jamani kwani tulizungumza nini jana kule ufukweni?"
"Ahaa nimekumbuka,yaani ina maana unamaanisha kweli unanipenda?" Akauliza Aidan.
"Yaap i declared to love you,naomba unielewe,hebu jiulize nimekataa wangapi mpaka nimekuona wewe Aidan,laiti kama ningelimpenda mtu mwingine,nisingethubutu kukuona hata machoni mwangu,tazama nimetoroka nyumbani kwa ajiri yako,unataka kama kupigwa nipigwe bure bila hata kuonja joto lako Aidan?...nitakuwa nimefanya nini sasa..." Dayana akazungumza kwa hisia kali mno.Maneno hayo yakaanza kuutawala ubongo wa Aidan taratibu na kujikuta akimtazama tu Dayana huku akitabasamu.
" Dayana nakupenda pia ila naogopa sana juu ya baba yako kama akijua,si atabomoa mtaa wetu kweli?" Aidan akauliza swali lililomchekeshwa Dayana,akacheka kwa sauti kisha akasema.
"Hawezi fanya hivyo Aidan,hebu nipe mdomo wako" Dayana akazungumza na Aidan akapeleka midomi yake na kukutanusha na ya Dayana,wakawa wanazungushana ndimi taratibu huku wakiendelea kucheza.
Sauti ya kucheki cha Dayana,kikamshtua sana Bosco hatua tatu kutoka alipo.Aliitambua vyema sauti ya kicheko,kilio na hata kukohozi cha Dayana,kipenzi chake ambacho kilikuwa kinamliwaza kila siku.Ni zamani sana tangia asikue sauti yake,akaacha kucheza na msichana mmoja kisha akaanza kutafuta wapi ilipo sauti ya Dayana.Kichwani pombe zilikuwa zimemjaa mno lakini hakika hakuacha kusahau sauti ya mpenzi wake hiyo.Alipotazama huku na huko akasikia tena kucheko na safari hii akakutana na sura ya Dayana ikiwa na jamaa ambaye hamfahamu,tena katika mchezo wa kuchezeana ndimi zao.Bosco hakuamini mara ya kwanza,akadhani kama anaota,akapikicha macho yake na kukitikisa kuchwa,akatazama tena lakini bado picha ya Dayana ikawa inajichora kwenye macho yake.
Hasira zikaanza kumoanda taratibu na hapo ndipo alipobaini kuwa alikuwa na bastola yake kiunoni,akaitazama na kuiweka sawa na kuanza kupiga hatua ndefu kuelekea pale alipo Dayana na Aidan.Alipofika hakuwa na haja ya kuuliza,akamshika Aidan shati na kulikunja kisawasawa,akamuangusha chini na kuanza kumtupia ngumi kadhaa za usoni.
"Noo Bosco,unampigia nini mkaka wa watu,kwani si nilikuambia sikupendi mbona unakua hivyo..."Dayana akaanza kupiga kelele lakini Bosco hakujari hayo.Watu wakaanza kujaa na kuwaachanisha Bosco na Aidan,haikuwa rahisi kabisa kwa wawili hao kuachana kwani Bosco alikuwa na nguvu za ajabu kwa muda hao japokuwa alilewa sana.Mlinzi wa Dayana akamshika mkono Dayana na kumvutia mpaka nje,akamfungia ndani ya gari na kuiwasha.
"Sitaki sitakiiiii unanipeleka wapi....nishushe Jimmy,nakuambia nishushe nirudi" Dayana akapiga kelele kwa wingi huku akilia machozi lakini mlinzi huyo hakutilia maanani kilio cha Dayana,japokuwa anakumbana na ngumi pamoja a vibao vya nguvu kutoka kwa Dayana lakini hakujari hata kidogo.
"Nitahakikisha unafukuzwa kazi nakwambia Jimmy...geuza gari nimesemaaaa!" Dayana akafoka kwa hasira,lakini wahwnga wanasema kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.
Nyuma mzozo ukawa mkubwa,Mpaka dakika hiyo Aidan alikwishaloa damu kutokana na kupigwa chupa na rafiki wa Bosco,tamasha lite likawa vurugu kabisa.Aidan akabahatika kuona mpenyo,akachomoka kwa kasi na kumsukuma mlinzi wa mlangoni aliyejaribu kumzuia,akaanguka pembeni na Aidan akatoka mpaka nje,akapanda taski haraka na kueleza wapi apelekwe.Ni jambo la kushangaza baada ya Aidan kumuona Bosco akiwa na bastola mkononi akikimbia na kuanguka kutokana na pombe alizopakia kuchwani,akaanza kulikimbiza gari hilo na baada ya kuona linamuacha kwa umbali mkubwa,akaenda sehemu ambayo wanapaki pikipiki,akamuambia dereva aifuke gari hiyo haraka iwezekanavyo.Watu wengi waliokuwa kwenye lile tamasha wakaachwa katika mshangao mkubwa kwani ni ghafla sana kwa tukio kama lile kutokea.Askari waliokuwa wanasimamia ulinzi wakapakia kwenye gari zao na wao wakaanza kuunga ule msafara usio rasmi huku wakila kiapo kuwa endapo watawakamata,watalipa pesa zote zilizogharamikiwa katika tamasha lile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ongeza mwendo kaka,vipi?" Mwendo wa dereva wa taksi hiyo aliyopanda Aidan akaimizwa vikali na kumfanya aongeze mwendo kasi wa gari.Mpaka wanafika Ubungo ndipo pikipiki moja ikawapita kwa kasi mbele.Hapo Aidan ndipo alipoiona sura ya jamaa aliyemsurubu akuwa amekamata bastola,hofu ikamtanda na sasa haja ndogo taratibu ikawa inabisha hodi kwenye kufuri la Aidan...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment