Search This Blog

Tuesday 20 December 2022

JAMBAZI MSOMI NA ALIYEFANIKIWA ZAIDI KATIKA AZMA YAKE - 1

 


http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/jambazi-msomi-na-aliyefanikiwa-zaidi_10.html

IMEANDIKWA NA THE BOLD

************************************************************************

Simulizi : Jambazi Msomi Na Aliyefanikiwa  Zaidi Katika Azma Yake 

Sehemu Ya Kwanza (1)



Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.


Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)


Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'!


Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.


Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu


ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEDI"


Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.


Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha, ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na fedha..



    0 comments:

    Post a Comment

    Blog