Search This Blog

Tuesday 20 December 2022

THE KING MAKERS - 1

 


http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/the-king-makers.html

IMEANDIKWA NA THE BOLD

************************************************************************

Simulizi : The King Makers 

Sehemu Ya Kwanza (1)



THE KING MAKERS

SEHEMU YA KWANZA


Kampuni ya Samsung inakadiriwa kuchangia 17% ya GDP ya nchi ya Korea ya Kusini, na pia inachangia 20% ya mauzo yote ya nje (exports) za nchi ya Korea Kusini.


Wanaijeria kumi matajiri zaidi wakiongozwa na Aliko Dangote wanakadiriwa kuchangia takribani 12.5% ya pato la Taifa la Nigeria, ambapo Dangote pekee na makampuni yake anakadiriwa kuchangia zaidi ya 7.4% ya GDP ya Nigeria.


Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) inakadiriwa kuchangia karibia 3.5% ya pato la Taifa la Tanzania.


Je, umewahi kujiuliza watu wa dizaini hii (Samsung, Dangote, Mo Dewji n.k.) wanaushawishi kiasi gani katika kuamua nani aongoze nchi na namna gani nchi iongozwe.??



SEOUL, KOREA YA KUSINI

Mwaka huu kunatarajiwa kuanza kwa kesi kubwa inayotabiriwa kuwa itateka ulimwengu na hata kupewa hadhi ya Kesi Ya Karne (Trial Of The Century).


Kesi hii itamuhusisha moja ya watu muhimu zaidi nchini humo, mtu ambaye anaelezwa kuwa na nguvu zaidi na ushawishi hata kumshinda Rais wa nchi hiyo na jarida la Forbes linamuorodhesha kama yuko nafasi ya 35 katika orodha ya watu wenye ushawishi zaidi duniani.. Kesi hii itamuhusu Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Samsung, Bw. Jay Y. Lee ambaye ni mtoto wa Lee Kun-hee mwenyekiti na mmiliki wa Makampuni ya Samsung.


Kesi hii inakuja wakati ambapo Jay Y. Lee anaandaliwa kurithishwa Uenyekiti wa Samsung kutokana na afya ya baba yake kuzorota tangu mwaka 2014 alipopata mshtuko wa moyo.


Kwa sasa inakadiriwa na wachambuzi wengi wa masuala ya uchumi kwamba thamani ya Samsung imefanikiwa kuipita thamani ya mpinzani wake mkubwa kampuni ya Apple kutoka nchini Marekani. Hata 'market share' ya kampuni ya Samsung inakadiriwa kuwa ni kubwa kuishinda ile ya Apple.


Kesi hii inatishia kutokea kwa anguko kubwa la kampuni ya Samsung kutoka kwenye "utukufu" wake na hata kuleta mtikisiko kwenye uchumi wa Korea ya Kusini.


Hakuna jambo jipya sana alilolifanya Lee mpaka kupelekea kushtakiwa kitu ambacho kilikuwa kinaonekana kuwa hakiwezekani, kwani familia ya Lee ni moja ya familia ambazo ni "untouchable" ndani ya Korea ya Kusini.

Lakini ubaya alioufanya katika suala la safari hii ni kutishia maslahi ya kibiashara ya kampuni za Marekani zilizowekeza ndani ya Samsung.


Kesi hii na skandali hii inaelekea kuwa skandali ya kusisimua zaidi kuwahi kutokea mashariki mwa Asia na itachukua miaka mingi sana kutokea tena skandali yenye kumuhusu moja ya watu 'wazito' zaidi duniani.


SS2.jpg

Jay Y. Lee CEO wa Samsung Electronics na Makamu Mwenyekiti wa Samsung |Group akiwa amekamatwa wiki mbili zilizopita


Kiini cha kesi yake kinahusishwa na uhusika wake kwenye skendali iliyopelekea Bunge la Korea Kusini kumuondoa madarakani Rais wa Korea mwanamama Park Geun-hye, mwaka Jana mwezi Desemba tarehe 9.


Uamuzi huo wa Bunge umethibitishwa Jana tarehe 10 March, 2017 na mahakama Kuu ya Korea Kusini, na hivyo kumuondoa rasmi madarakani mama Park Geun-hye.


Skandali hii inathibitisha tuhuma za siku nyingi zinazoelekezwa kwa kampuni ya Samsung kuifanya nchi ya Korea ya Kusini kama mali yao binafsi, kwa kuiweka serikali nzima mikononi mwao na kuhakikisha hakuibuki makampuni mengine yatakayoweza kushindana nao kibiashara.


Sasa ili nchi ya Korea kujisafisha taswira yake katika kwenye ulimwengu wamekubali kum-sacrifice rais wa nchi.. Sasa je, wataenda mbali zaidi na kui-sacrifice kampuni ya Samsung na Viongozi wao??


Na je nini hasa kimetokea mpaka kusababisha mkwamo huu na mtikisiko katika nchi ya Korea na Asia Mashariki kwa ujumla??


Hii mada ni moja ya mada zilizo complex zaidi na yahitaji kutuliza kichwa hasa kuielewa kwa undani wake, na kuona uhuondo wake na labda na sisi kujifunza kitu.. Kwa hiyo nitajitahidi kuenda hatua kwa hatua.. Taratibu.!!


Now, let's start from the begging..


Mwaka 2014 baada ya Mwenyekiti wa Samsung Bw. Lee Geun-hye kupata mshtuko wa moyo na afya yake kuanza kuzorota, yakaanza maandalizi ndani ya Samsung ili kuweza kumrithisha Uenyekiti mtoto wake mkubwa wa Kiume Jay Y. Lee (au Lew Jae-yong kwa kikorea).


Kipindi hiki Jay Lee alikuwa ni Chief Operating Officer wa Samsung Electronics, na kabla ya hapo alikiuwa ni Vice President wa Idara ya Strategic Planning ndani ya Samsung tangu mwaka 1991.


Hivyo basi ili kutengeneza mazingira mazuri ya kumrithisha Uenyekiti, kwanza akapewa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Samsung.

Hatua ya pili ndio ilianzisha utata wote mpaka kupelekea kuondolewa kwa rais wa nchi madarakani na hatimaye juzi kukamatwa kwa Jay Y. Lee mwenyewe.

Hatua hii ilihusisha kuunganisha ya kampuni mbili, yaani Kuunganisha kampuni ya Samsung C&T na kuunganisha na kampuni ya Cheil Industries, kampuni zote hizi zinamilikiwa na Samsung.


Ili kufanikisha hii 'merger' ndipo ambapo Jay Y. Lee na Samsung wakaanza kumtumia Rais Park kuwasaidia kutumia mamlaka yake kama rais kuhakikisha muunganiko huu wa kampuni hizi mbili unatokea.


Hapa ndipo giza lilipoanza kutanda na 'bundi' kutia kwenye kampuni ya Samsung na nchi ya Korea.!!


Kwanza kabisa, swali la kujiuliza… iweje wamiliki wa kampuni watafute msaada wa Rais ili kusaidia kuunganisha kampuni zao wenyewe??


Ili kujibu swali hili na kuelewa chanzo cha skandali hii ili tuweze kwenda vizuri, inatupasa kwenda kwenye shina kabisa la mfumo complex wa kibiashara wa makampuni makubwa ya nchini Korea.


Chaebol

Nchini Korea Kusini kuna mfumo wa uenselshaji makamupi makubwa ambao wenyewe wanauita Chaebol. Kwa tafsiri rahisi ya Chaebol tunaweza kuifananisha na "Conglomerate" kwa kingereza.


Yaani inakiwa ni mkusanyiko wa makampuni mengi ambayo yanakuwa chini ya umiliki wa kamupini moja, tofauti tu na nchi nyingine ni kwamba Chaebol inakuwa chini ya umiliki wa familia ambayo ndiyo inakuwa inatoa Mwenyekiti wa Makampuni hayo.


Mfano wa Chaebol kutoka Korea Kusini, ni kampuni kama Samsung, Hyundai, LG, Doosan na GS Group.


Sasa licha ya kusema kwamba kampuni hizi "Chaebol" zinakuwa zinamilikiwa na familia, ajabu ni kwamba unaweza kukuta familia hiyo labda inamiliki hata 1% pekee ya hisa za Kampuni lakini kunakiwa na mfumo 'very complex' unaowawezesha familia hii kuwa na 'absolute power' ya kuendesha kampuni na kurithishana.


Mfano kwenye Chaebol ya Samsung, Familia ya Lee wanamiliki hisa chini ya 4% ya Samsung yote, lakini wao ndio "wamiliki" wa Samsung, na wanarithishana kampuni na uongozi wa juu kuanzia Babu mtu, Baba na sasa hivi anataka kurithishwa mtoto Jay Y. Lee.



    0 comments:

    Post a Comment

    Blog