Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MAPIGO YA MOYO - 5

 











    Simulizi : Mapigo Ya Moyo

    Sehemu Ya Tano (5)







    “What!this man is drug dealer, and also guns’ seller (nini! Mtu huyu ni muuzaji wa madawa ya kulevya, na pia ni muuzaji wa siraha) hatimaye saa ya Kendrick iliweza kugundua siraha za kivita, japo hakufahamu mahali ambapo ziliweza kuhifadhiwa. Alijikuta akipigwa na butwaa pale neno la kizungu “drugs ” ,lilipoonekana katika kioo cha saa yake. Hakuamini kama kweli eneo lile ambalo alikuwepo lilikuwa na punje za madawa ya kulevya. Punje ambazo ziligunduliwa na saa yake, baada ya kudondoka wakati zikisafirishwa katika magari. Siku zote saa yake haikuweza kumdanganya, aliamua kutoka haraka sana eneo hili, akajipange kwa ajili ya kuvamia kasri hili na kufanya upelelezi zaidi.



    Hatimaye jibu la swali lake liliweza kupatikana, alitambua ni kwanini Rodgers alionekana akitoka na kuingia katika jengo hili la Makamu wa raisi kama alivyo ambiwa na Yusto. Ilibidi Kendrick kuvua miwani yake na kisha kutoweka ndani ya jengo hili.



    …………………………………



    Hatimaye mawasiliano katika kompyuta za kina John Owino yaliweza kurudi, hawakuamini kwani Kendrick alikuwa haonekani katika kompyuta zao.



    “Mzee Jastin nenda juu kaangalie nini kinaendelea, chukua vijana wawili wa kukulinda na kisha leta ripoti “,John Owino alimpatia maelekezo rafiki yake, na haraka sana mzee Jastini aliweza kutii amli ya bosi wake, kwani haraka sana safari ya kutoka nje ya handaki kwa kutumia usafiri wa gari iliweza kuanza. Gari lilipanda juu na kutoka nje ya handaki kwa kutumia njia zilizotengenezwa kwa mduara, kadri gari ilivyopanda na kuizunguka barabara ndivyo ilivyolisogelea lango la kutokea ndani ya handaki.



    Tanzania;



          Hatimaye nilijikaza kiume,nikaamua kumsimulia mheshimiwa raisi kila kitu ambacho kiliweza kutokea. Historia yangu ilikuwa kali na yenye kuumiza sana, kiasi kwamba hata raisi aliweza kutoa machozi.



    “Msijilaumu sana kwa jambo hili ambalo limetokea, mungu alikuwa na makusudi yake ya nyie kupendana kwanza, na kisha kufahamiana kwa undani zaidi “,raisi aliongea huku machozi yakimtoka na kudodonka mithili ya mnvua ambayo ilitaka kukatika baada ya kunyesha kwa muda mrefu. Historia kuhusu siri iliyokuwa imejificha, siri ambayo aliweza kusimuliwa na mimi iliweza kumchoma na kumuumiza sana. Lakini yote yalikuwa ni mapenzi ya Mungu, hatukuwa na budi kukubaliana na aibu hii.



    “Kuanzia sasa! naahidi mzee Jastini atatafutwa popote pale na kisha kufikishwa katika vyombo vya sheria “,kwa kujiamini, raisi alitoa kauli ya kishujaa na yenye kuwa na ukweli ndani yake. Tulimwamini sana na ndio maana tulimwelezea siri hii, aweze kumfikisha mzee huyu katika vyombo vya sheria.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kenya



    Gari aina ya Defender  liliweza kufika katika lango la kutokea ndani ya handaki,mlinzi aliyekuwa juu aliweza kuliona katika kompyuta yake,na haraka sana kwenda kulifungulia.Batani kubwa iliweza kubonyezwa na mlinzi huyu, na kisha geti kubwa ambalo liliwekewa cement kwa juu kufunguka, na kisha mzee Jastini kutoka na gari lake. Lilikua limebakia geti moja, geti ambalo lilikuwa katika nyumba ya John Owino, geti ambalo lilitengenezwa katika parking ya magari. Mtu yeyote asingetambua kuwa katika parking hiyo ya magari kulikuwa na lango la kuingilia ndani ya handaki, kama asingeambiwa.



    “Tusitoe gari, tuliache hapa hapa …… ,huyu jamaa ni hatari akituona tunatoka na gari anaweza kuhisi jambo “,mzee Jastini aliwaambia vijana wake wawili, na kisha kuliacha gari lao parking. Kwa umakini mkubwa vijana wale walitoa siraha zao, na kisha kuchungulia nje ya nyumba ya bosi wao John Owino. Waliona ukimya ukiwa umetawala na Kendrick hakuwepo mahali pale, hivyo basi!  hawakuwa na haja ya kukamatilia siraha zao, ilibidi wazirudishe katika mifuko yao ya suruali.



    “Bosi nje hakuna hatari yoyote, twende tukaulize nini kimetokea “,vijana wawili ambao walikuwa tegemeo sana katika kundi la John Owino walimweleza jambo bosi wao msaidizi mzee Jastini, na kisha kutoka nje kwani hawakuona hatari yoyote ile.



    “Samahani, kuna nini kimetokea! “,mzee Jastini aliwauliza askari wa jeshi la polisi ambao walikuwa zamu kulinda katika geti kuu katika nyumba ya John Owino. Siku zote walimfahamu mzee Jastini kama ndugu yake Makamu wa raisi, na vijana ambao mzee Jastini alitoka nao waliwafahamu kama watoto wa John Owino, akiwemo Rodgers ambaye alikwenda nchini Uganda kupeleka madawa ya kulevya.



    Siku zote hawakutambua kuwa ndani ya jengo la John Owino kulikuwa na biashara haramu ambazo zilikuwa zikiendelea,kwani hawakuruhusiwa kukagua gari lolote kubwa au dogo ambalo lilikuwa likiingia ndani ya jengo hili. Wao walitazama nembo ya gari, pamoja na kitambulisho cha dereva wake.Kama vyote vilionyesha nembo ya John Owino pamoja na sahihi yake,gari liliweza kuruhusiwa kupita.



    Hawakutambua kuwa magari ambayo yaliingia na kutoka katika jengo la makamu wa raisi, mala nyingi yalibeba watoto wadogo wa kike pamoja na madawa ya kulevya  Baadhi ya watoto walisafirishwa barani Ulaya na Asia kwenda kuuzwa na wengine  walifanyiwa upasuaji na kupakiwa madawa ya kulevya.



    “Kuna mpelelezi wa kimataifa kafika hapa na kumuulizia kaka yako, bila shaka anataka kumchafua, kachunguza mazingira ya humu ndani  ,lakini ghafla ameondoka bila hata kuaga “,askari yule alizungumza na mzee Jastini, huku akipekua simu yake aweze kuwasiliana kwani mtandao uliweza kurudi baada Kendrick kuondoka.



    Machale yalimcheza mzee Jastini, alihisi lazima kuna kitu ambacho Kendrick alikigundua na kusababisha atoweke haraka sana katika ngome yao. Ilibidi warudi haraka ndani ya handaki, na kumfahamisha bosi wao John Owino, kuhusu taarifa hii.



    Uganda;



            Safari ilikuwa ndefu sana, lakini bila vikwazo vyovyote vile waliweza kufika mpakani mwa Kenya na Uganda salama. Rodgers na George kibira hawakutambua kuwa tayali Kendrick aliweza kutambua kuwa, katika jengo la bosi wao  na makamu wa raisi wa Kenya John Owino, kulikua na biashara haramu inafanyika.



    Tabasamu zuri lilionekana katika nyuso ya Rodgers, hakuamini kama George Kibira aliheshimika kiasi hiki, kwani geti kuu la kuingilia nchini Uganda lilifunguliwa haraka sana pale askari wa mpakani walipoiona sura ya George Kibira ndani ya gari, huku wakimpigia saluti kama ishara ya heshima. Rodgers alimuona John Owino kama mtu mjanja sana,kwani alitafuta watu wakubwa na kufanya nao kazi, ndio maana kundi lake lilikua kubwa siku hadi siku.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Barabara kubwa ya kuelekea Kampala ilionekana kuwa na magari mengi, lakini dereva ambaye aliwaendesha Rodgers pamoja na George Kibira aliendelea kukanyaga mafuta, na kuuacha mpaka wa Kenya na Uganda. Alitaka kufika Kampala mapema sana kabla giza halijaingia, kama alivyokuwa amepatiwa maelekezo na bosi wake, kanali George Kibira, mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Uganda.



    Tanzania ;



           Baada ya kuondoka ikulu, mimi na dada yangu Rose. Hatimaye raisi alianza harakati za kuwasiliana na Kendrick, alitaka kumpatia kazi nyingine tena ya kumtafuta mzee Jastini kwani hakutambua kuwa  sehemu ambayo mzee Jastini alikuwepo, ndiyo sehemu ambayo Kendrick aliweza kufika na kuifanyia upelelezi.



    “Haloo! Kendrick, umefikia wapi! “,



    “Kazi inaendelea vizuri, Rodgers anaonekana kushirikiana na kiongozi wa Kenya John Owino, katika jengo la makamu wa raisi nimegundua madawa ya kulevya, pamoja na siraha. Na inasemekana, Rodgers anafika mara kwa mara kwa kiongozi huyu John Owino! “,Kendrick alizungumza na kumpatia taarifa raisi wa Tanzania  ,taarifa hii ilimchanganya na kumshitua sana raisi kiasi kwamba akasitisha zoezi la kumpatia kazi nyingine Kendrick ya kumtafuta mzee Jastini. Aliona ugumu wa kazi kwa Kendrick, kwani kiongozi John Owino aliaminika sana na wananchi pamoja na serikali kwa ujumla. Hivyo basi! Ushahidi wa uhakika ulihitajika kwa ajili ya kumtia hatiani kiongozi huyu wa Kikenya.



    “Sawa kijana wangu, endelea na kazi, tafuta ushahidi tuwaweke hatiani Rodgers pamoja na John Owino, nazani wanatambua vizuri kuhusu EADD! ukimaliza kazi hii, nitakupatia kazi nyingine ya kumtafuta mtu mwingine anayejulikana kwa jina la mzee Jastini “



    “Sawa mheshimiwa “,Kendrick akiwa amejipumzisha katika kitanda kizuri, baada ya kazi nzito aliyoifanya Kisauni kumpeleleza John Owino. Uzuri wa hoteli ya Mombasa picnic, ulimfanya akili yake kutulia na kujipanga kwa hatua nyingine ya upelelezi.



    Dar es salaam;



    Jengo la mzee Jastini tuliliona chungu, furaha ilitoweka kabisa katika maisha yetu. Muda mwingi tulioneana aibu mimi na dada yangu, pale macho yetu yalipokutana uso kwa uso. Aibu ilizitawala nyuso zetu, muda mwingi nilifikilia kuhama Tanzania nikaishi mbali sana  kwani kama pesa nilikuwa tayali ninayo ya kutosha. Mawazo ya Rose yalikuwa sawa na ya kwangu, aliniona kama mtu ninayemuongezea machungu kila nilipokaa karibu yake. Kwani aliponiona, alikumbuka machungu na machozi yaliweza kumtoka.Muda mwingine alimlaumu Mungu,kwa kutukutanisha mimi na yeye huku tukiwa tayali tumeishi kama wapenzi mpaka kupeana ujauzito.



    Muda mwingine alitamani kujiua,lakini kiumbe ambacho kilikuwa tumboni hakikuwa na makosa,kilipaswa kuishi japo kilizaliwa na wazazi ambao walikuwa ndugu wa damu moja bila kujitambua.Aibu ilitutawala ,tulikosa pa kuficha nyuso zetu japo hatukukusudia.



    Sikutambua kuwa roho ya kujiua ilimtawala sana dada yangu Rose,japo mala kadhaa aliniambia kuhusu jambo hilo lakini sikuamini kama kweli angeweza kuyatoa maisha yake kwa kukwepa aibu.Tena aibu kubwa ya kuzaa na kaka yake wa tumbo moja.



    “SAMAHANI KAKA NIMEAMUA KUJIUA,AIBU IMENISHINDA NGUVU,MOYO UNANISUTA,SIWEZI KUZAA NA KAKA YANGU,MTOTO ATATUITAJE,MUNGU NISAMEHE” yalikuwa ni maneno mazito ambayo yaliweza kuandikwa katika kipande cha karatasi.Sikuamini kama kweli dada yangu Rose aliweza kujiua kwa kunywa sumu ya panya,nililia kwa uchungu sana lakini jambo tayali lilikuwa limeshatokea.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuamini kama kweli Rose aliweza kuniacha,alikuwa ndiyo ndugu yangu pekee wa damu aliyekuwa amebakia.



    Nililia kwa huzuni sana baada ya kuingia katika chumba chake,kwani tangu asubuhi tulipotoka ikulu kwa raisi,sikufahamu Rose alielekea wapi baada ya kufika nyumbani.Nilisubili sana lakini hakurejea,giza hatimaye likaingia bila Rose kuonekana.



    Ikabidi nimtafute kila chumba  katika jengo kubwa la mzee Jastini,lakini nilishangaa kila chumba ambacho niliingia sikuweza kumwona.Bafuni hakuwepo,chooni hakuwepo,jikoni tena hakuwepo,hatimaye mapigo yangu ya moyo yalidunda mithili ya kitenisi cha kuchezea watoto.Niliamini kwa asilimia mia moja kuwa dada yangu alikuwa hatarini,lakini ghafla nilikumbuka chumba kimoja ambacho sikuweza kuingia,na haraka sana niliweza kuelekea huko.



    Sikuamini nilichoweza kukishuhudia! Povu jeupe lilimtoka mdomoni dada yangu pekee kipenzi,dada ambaye awali niliishi naye kama mpenzi wangu na kumkabidhi moyo wangu bila kutambua kuwa alikuwa ndiye mdogo wangu kipenzi aliyepotea miaka mingi iliyopita.



    Uvimbe wa tumbo lake,tumbo la ujauzito ambao nilimpatia ndio aibu ambayo ilimuumiza sana na kumfanya kujiua kwa sumu ya panya.Kwani niliona pakti ya sumu ,pakti ambayo iliweza kuchorwa mchoro wa panya juu yake na kuamini kuwa ndiyo sumu iliyohusika kumtoa uhai dada yangu Rose.Kwa hasira nilichana chana mpaka cheki za benki ambazo alikuwa ameziandika na kuziweka juu ya karatasi aliyoniandikia,alitaka nikachukue pesa zake zote benki na kuyaendesha maisha yangu.



    Hasira ilinitawala,huzuni ikaipamba sura yangu.Pesa hazikuwa na thamani tena ,kuliko ndugu pekee aliyekuwa amebakia na kutoweka ghafla.Kutokana na kifo cha ghafla kilichonigusa kwa hali ya juu,mapigo yangu ya moyo yaliongezeka na kunifanya nipoteze fahamu mahali pale.



    …………………………………



    Mombasa



            Kendrick alijipumzisha ,huku kichwani akichora ramani ya kuingia katika jengo la John Owino usiku  wa manane wa saa tisa usiku. Tayali raisi wa Tanzania alimuahidi kufika Mombasa usiku huu kwa ndege ya raisi, mala tu atakapotoka kwa mzee Jastini kuchukua kompyuta yenye ushahidi wa mzee huyu ili maadui wasije kuichukua kabla Kendrick hajaanza hata kumtafuta mzee huyu. Hakutambua kuwa mzee Jastini alishirikiana na John Owino na alikuwa katika jengo lake lililoko Mombasa, jengo ambalo Kendrick alijipanga kwenda kulivamia.



    ………………………………

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dar es salaam



           Ukimya wa jengo la mzee Jastini unamtia hofu muheshimiwa raisi, ni baada ya kututembelea mimi na Rose usiku ambao asubuhi yake tulikwenda ikulu na kumpatia siri juu ya maisha yetu, pamoja na mzee Jastini. Kiza kiliweza kutawala ndani ya jengo kwani taa hazikuwa zimewashwa, kiasi kwamba askari walitangulia kulikagua jengo zima la mzee Jastini.



    Raisi alihuzunika kwa mala nyingine, hakuamini kama miili ya watu wawili ilikuwa katika chumba alichokuwa ameonyeshwa na askari wake. Aliamini sote tuliweza kujiua, kwani sumu ya panya ilionekana juu ya kitanda ambacho mwili wa marehemu dada yangu Rose ulikuwepo.



    “Haraka sana mnyenyueni kijana wangu Robert, muwahisheni hospitalini, mwili wa binti huyu muupeleke mochwari na uhifadhiwe vizuri “,raisi aliongea baada ya kuhisi mapigo yangu ya moyo kwa mbali sana, aliamini nilipatwa na mshituko kutokana na kifo cha Rose, kwani karatasi ambayo Rose aliweza kuniandikia, nilikuwa nimeishika katika mkono wangu wa kushoto.



    Safari ya kuelekea Mombasa raisi aliweza kuiahirisha, alitaka tuongozane naye mala tu nitakapopata fahamu.Baada ya Kufikishwa katika hospitali ya manispaa ya Temeke, hospitali ambayo ilikuwa karibu na nyumba ya mzee Jastini, nyumba ambayo mimi na Rose tulikuwa tukiishi. Raisi aliketi pembeni ya kitanda changu, akisoma siri mbalimbali katika kompyuta ya mzee Jastini.Hakupata shida yoyote ile, kwani tayali tulikuwa tumezitoa namba zote za siri tayali kwa ajili ya kumkabidhi raisi atakapokuja kuichukua kompyuta kwa ajili ya ushahidi. Raisi hakulala,aliendelea kusoma mambo mbalimbali katika kompyuta ya mzee Jastini, huku askari wengi wakidumisha ulinzi katik wodi ambayo niliweza kulazwa.



    Mombasa



        .    Jeshi la John Owino lilikaa tayali, muda wote siraha zilikua mikononi mwao. Taarifa ya hofu ambayo mzee Jastini aliweza kuwafikishia ndani ya handaki, waliweza kuiamini kwa asilimia mia moja. Waliamini muda wowote hasa usiku, Kendrick angeweza kuivamia ngome yao.



    Hawakulala usiku huu, macho yao yalikodoa katika kompyuta zao, kompyuta ambazo ziliunganishwa na Kamera ambazo zilizunguka jengo lote la John Owino.Hivyo basi! adui yoyote ambaye angeisogelea kambi yao lazima wangemuona kupitia kompyuta zao.



    Kendrick aliamka mida ya saa nane usiku, alijiandaa kwa mapambano makali, ili aweze kulivamia jengo la John Owino. Lengo kuu la kulivamia jengo hili la makamu wa raisi wa Kenya, ni kutafuta ushahidi uliokamilika kuwatia hatiani Rodgers pamoja na John Owino.



    Aliamini mpaka saa moja asubuhi, tayali misheni yake ingekuwa imekamilika. Taarifa alikuwa tayali ameshazituma katika serikali zote za Kenya na Tanzania, kufika haraka sana katika jengo la John Owino, pale atakapobonyeza saa yake, saa ambayo aliiunganisha mawasiliano na vyombo vyote vya ulinzi vya serikali zote mbili. Hivyo basi!  Serikali zote mbili zilikaa tayali kusubili taarifa kupitia saa ya Kendrick, saa ambayo ingewapatia taarifa na kufika katika jengo la John Owino kukamata wahusika wa kuuza siraha pamoja na madawa ya kulevya, kama ambavyo Kendrick aliweza kuripoti taarifa ya mwanzoni ambayo ilikuwa haijadhibitishwa.



    Mombasa;



     Kendrick aliweza kukamilika kila idara, aliamini angeweza kukamilisha misheni yake ndani ya masaa matatu. Kwa wakati huu hakupanda bodaboda kama awali, bali alikodi pikipiki kubwa aina ya Baja, na kuendesha mwenyewe. Aliangalia saa  yake, kwa upande wa wakati ilikua yapata saa nane na nusu usiku. Hatimaye alitoweka katika eneo la hoteli ya kitarii iliyojulikana kwa jina la picnic hotel, huku mgongoni akiwa amebeba kibegi kidogo ambacho kilikuwa na vifaa vya kijeshi ndani yake, kama kamba ya kuvukia vikwazo pamoja na mabomu.



    Aliendesha pikipiki kama mwendawazimu, kwani barabara ya kuelekea mtaa wa Kisauni kutokea katika hoteli ambayo aliweza kukodi chumba, haikuwa na magari mengi wakati wa usiku.



    Ndani ya nusu saa tu, Kendrick aliweza kupaki pikipiki yake, umbali wa mita mia tano, kutoka sehemu ambapo jengo la mzee John Owino lilikuwepo.



    Aliweza kugundua kuwa kamera ambazo zilizunguka jengo la John Owino, zingeweza kufanya aweze kugundulika kirahisi na kuharibu misheni yake. Hivyo basi, alibonyeza batani na kuruhusu mionzi mikali ya miwani yake kabla hata hajalisogelea jengo la John Owino. Miwani yake ingemsaidia kukata mawasiliano ya Kompyuta ambazo ziliunganishwa na kamera ambazo zilifungwa kuzunguka ngome ya John Owino.



    Kwa mwendo wa kunyata alisogelea ukuta wa kasri hili kubwa la John Owino, alitabasamu baada ya kukuta askari wote wa getini wakiwa wamelala fofofo.



    Haraka sana alifungua begi lake na kisha kutoa kamba yake ndefu, na kuirusha juu ya ukuta, aliivuta kuhakikisha kama kweli iliweza kunasa vizuri asiweze kuanguka.



    “Dakika tano zinatosha kufika ndani “, Kendrick aliongea huku akianza kupanda ukuta mrefu sana wa kasri la John Owino, alipanda kwa umakini wa hali ya juu asiweze kunaswa na nyaya za umeme ambazo zilizungushwa juu ya ukuta, kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.



    Hatimaye alifika juu kabisa ya ukuta, na kisha kudumbukia ndani. Alinyata na kujibana kwenye maua, na kisha kuanza kupiga mahesabu namna ya kuingia ndani kabisa na kufanya upelelezi. Kwa umbali  kama wa mita mia moja aliweza kuliona jengo la parking, na kuona kama njia pekee ya kumuwezesha kuingia katika nyumba ya mwanasiasa huyu wa chama cha upinzani nchini Kenya.



    Hakuamini alichokiona baada ya kuingia katika jengo la parking ya magari, alikuta mlinzi akiwa amelala huku kukiwa na kompyuta mbele yake. Kimya kimya alimpiga na bastora mlinzi yule, na kisha kuisogelea kompyuta yake na kuanza kuitazama. Hakuamini kama chini ya jengo kulikuwa na handaki kubwa sana. Haraka sana aliweza kubonyeza batani baada ya kusoma maelekezo katika kompyuta ya mlinzi yule aliyemuua. Alistaajabu sana! lango kubwa liliweza kufunguka, na kuanza kuhesabu muda wa dakika kumi, liweze kujifunga. Haraka sana aliingia ndani ya handaki, na kisha lango la handaki liliweza kujifunga.



    Risasi kama mvua zilianza kumiminika katika mwili wake baada ya mlango wa handaki kujifunga, kumbe jeshi la John Owino pamoja mzee Jastini waliweza kujiandaa kwa ajili ya kushambulia kiumbe chochote ambacho kingeingia ndani ya handaki. Ni baada ya mawasiliano ya kompyuta zao kupotea ghafla, na kushindwa kuona chochote ambacho kilikuwa kikiendelea nje ya handaki, ndipo walipogundua kuwa Kendrick aliweza kurudi tena, kwani mawasilino yalikata ghafla kama awali, hawakuwa na budi kukoki bunduki zao, na kujiandaa kumshambulia adui yao atakapoingia katika handaki lao.



    Bila kutegemea Kendrick aliweza kushambuliwa, lakini vazi la kijeshi alilolivaa, lilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi (bullet proof),hivyo risasi hazikufanikiwa kumzuru. Ilibidi ajibanze katika ukuta, na kuificha sura yake isiweze kuonekana.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pandeni magari, safari ya kuelekea juu ianze kwenda kumshambulia ” ,amli ilitoka kutoka kwa John Owino, lakini Kendrick aliona ndio muda sahihi wa kushambulia kundi hili la EADD.



    Alitupa mabomu mawili ya machozi, mabomu ambayo yaliwafanya askari wa John Owino kushindwa kuona vizuri, na machozi kuanza kuwatoka. Kusema ukweli walipoteana! Haraka sana aliteremka chini kwa kutumia kamba yake na kisha kuanza kuwashambulia askari wa EADD kwa risasi na ndani ya dakika tano alikuwa tayali amemaliza wote, isipokuwa watu wawili ambao walionekana kuvalia suti nzuri na za bei kali sana. Aliamini kuwa, hawa ndio walikuwa viongozi wakuu wa kundi hili, na kweli ilikuwa hivyo, mzee Jastini na John Owino ndio walikuwa viongozi wakuu wa kundi hili..



    Aliwakamata na kisha kuwafunga na kamba miguuni na mikononi, mpaka muda huu walikuwa bado hawajamtambua vizuri adui yao kwa sura, kwani macho yao yalikuwa bado yamefumba na kutoa machozi kutokana na mabomu ambayo Kendrick aliwatupia.



    Kwa upande wa Kendrick moshi wa mabomu yale haukuweza kumuathiri hata kidogo, miwani aliyoivaa ilikuwa na uwezo mkubwa sana, na kuyalinda macho yake yasiweze kuathiriwa na moshi wa mabomu.



    Baada ya kuhakikisha alikuwa tayali ameteketeza askari wote wa John Owino, alianza kuzungukia majengo mbalimbali yaliomo ndani ya handaki kumtafuta Rodgers, lakini alishangaa kukutana na kundi kubwa la watoto wa kike wakiwa wamefungwa kama mateka katika majengo haya,huku wengine wakiwa wamefanyiwa upasuaji na kupakiwa madawa ya kulevya tumboni.Kwa msaada wa miwani yake,aliweza kushuhudia kila jambo ambo lilifanyika katika miili ya watoto hawa.



    “diiii! diiii! diiiii!”,Kendrick aliamua Kubonyeza saa yake, na alamu iliweza kupiga kelele. Alamu hii iliashiria misheni kukamilika, na kutaarifu jeshi la Kenya pamoja na vyombo vya habari kufika katika jengo la John Owino.



    “Niambie Rodgers yuko wapi, sema! Nitakuua “,



    “Yuko njiani na kanali George Kibira wanapeleka madawa ya kulevya jijini Kampala nchini Uganda! “,makamu wa raisi John Owino aliamua kuwa mpole, aliamini mtu aliyewavamia hakuwa wa kawaida na muda wowote angewaua kama wasingefuata alichokitaka. Aliamua kusema ukweli, kukwepa kifo japo hukumu ya kunyongwa ingeweza kumkuta kama angefikishwa mahakamani.



    …………………………



    Nilikiwa nimeongozana na raisi baada ya kupata fahamu usiku wa manane, na haraka sana tulianza safari ya ndege kuelekea kisauni Mombasa, nchini Kenya.



    SAA MOJA BAADAYE;



            Baada ya kufika kisauni,Mombasa ,Kendrick alikuwa tayali amewakamata watuhumiwa. Tulishangazwa na umati mkubwa wa raia pamoja na askari, nje ya jengo la John Owino. Japo tulikuwa tayali tumeshapokea taarifa kutoka kwa Kendrick, baada ya kufanikiwa kukamilisha upelelezi wake.



    Wananchi walilia sana baada ya kushuhudia watoto wadogo ambao walikuwa wametekwa, huku wengine wakiwa hawaamini kama makamu wa raisi ambaye walimpenda sana, ndiye aliyekuwa muhusika mkuu na kiongozi wa kundi la EADD.



    Asubuhi hii ilikuwa ya tofuti sana, vyombo vyote vya habari vilipambwa na taarifa hizi zilizomuhusu John Owino pamoja na mzee Jastini. Kwa upande wa muheshimiwa raisi alifurahi sana, baada ya kushuhudia mzee Jastini akiwa miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa.



    “Hongera sana kijana, mtu uliyemkamata pamoja na John Owino, ndiye ambaye nilitaka ukamtafute baada ya kukamilisha kazi hii, hongera sana “,raisi aliongea huku akitabasamu,kiasi kwamba hata mimi niliweza kufurahi na kupata faraja, kwani niliamini tayali Mungu aliweza kumlipa mzee Jastini kwa mabaya yote aliyonitendea.



    ………………………………



     Baada ya safari ndefu ya siku moja na masaa kadhaa, hatimaye George Kibira na msafara wake waliweza kufika jijini Kampala. Alishangaa sana baada ya kukuta jeshi la Uganda likiwa na siraha nzito, tayali kwa ajili ya kulishambulia gari lake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipojaribu kufokea askari wake! Alipokea kipigo yeye pamoja na Rodgers, kwa sasa hakuwa mkuu wa majeshi tena kwani Kendrick alikuwa tayali ameshatoa taarifa na kumripoti serikalini. Briefcase la Rodgers lilipokaguliwa na kukuta madawa ya kulevya, ndipo hasira kwa askari wa Uganda ilipoongezeka maradufu na kuwashushia kipigo kitakatifu, kanali George Kibira pamoja na Rodgers, na baadaye kupandishwa katika karandinga tayali kwa ajiri ya kupelekwa rumande.



    **MWISHO ***


0 comments:

Post a Comment

Blog