IMEANDIKWA NA : HAKIKA JONATHAN
*********************************************************************************
Simulizi : Muuaji Mweusi (The Black Killer)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Nchi ya Tanzania inakumbwa na janga la kutisha, kila kona ya nchi vilio vya wananchi masikini vikisikika baada ya kupoteza ndugu zao katika mlipuko wa bomu uliotokea siku ya kusherekea sikukuu ya uhuru wa Tanzania.
Vyombo vya usalama nchini Tanzania vikishirikiana bega kwa bega kutambua chanzo na muhusika wa mlipuko huo, huku vijana wengi na baadhi ya wanasiasa wakikamatwa na kutiwa rumande kwani walituhumiwa kuhusika na tukio hilo baada ya kura za maoni kupigwa kubaini wahalifu hao.
“Hii ni taarifa ya habari kutoka “TBC “, hali ya raisi wa Tanzania inaendelea vizuri na sasa karejea kutoka nchini india kwenye matibabu ………raisi wa Tanzania mheshimiwa Samuel Kizito anawapa pole wafiwa wote na majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea huku akiomba radhi kwa vifo na kujeruhiwa kwa baadhi ya viongozi wakubwa wa nchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo ” …Sauti ya mtangazaji wa televisheni ya taifa ilisikika, na kumfanya afande mpelelezi wa Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam bwana Godfrey Manumbu kusitisha shughuli zake na kuwa makini kusikiliza taarifa ile ya habari .
“Angalau tutaanza kupumua japo kazi bado ni ngumu, lakini muhusika wa tukio hili alikusudia nini mpaka kuua maelfu ya watu wasio na hatia??, na kwanini kaamua kutugawa watanzania? Kwa sasa wananchi wanatuchukia sana, kwani wanatuona kama wazembe na hatufatilii kutambua muhusika wa janga hili ni nani………” Afande mpelelezi bwana Godfrey Manumbu aliendelea kujiuliza maswali mengi kichwani yasiyo na majibu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
………………………………
Siku zilizidi kusonga mbele huku nchi mbalimbali zikiilaumu serikali ya Tanzania kwa kutodumisha ulinzi imara siku ya sherehe za uhuru, na kupelekea vifo vya viongozi wa nchi zao. Mlipuko huu uliidhoofisha sana nchi katika nyanja zote za maendeleo, kwani hata urafiki wa Tanzania na nchi nyingi walizoshirikiana kibiashara ulitoweka kabisa.
“Just go to join the police force of Tanzania, we want to know the killer of our honourable president………I trust you my soldiers ” (nendeni muungane na jeshi la polisi la Tanzania ,tunahitaji kufahamu muuaji wa mheshimiwa raisi wetu……nawaamini sana askari wangu “) sauti ya amri ilisikika kutoka kwa mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi ya Afrika kusini, bwana Jacob Nelson akiwatuma vijana wake nchini Tanzania kumtafuta mtuhumiwa huyo aliesababisha kifo cha raisi wao mheshimiwa Jackson Mbeki.
…………………………………
Ndege kubwa aina ya Boeing 777 inayomilikiwa na kampuni kubwa ya usafiri wa anga “Fly emirates ” inagusa ardhi nzuri ya jiji la New York nchini Marekani.Kijana mtanashati Paul Agustino anashuka kwenye ndege akiwa amebeba briefcase yenye mabilioni ya pesa, baada ya kufanikiwa kutega bomu katika sherehe za uhuru nchini Tanzania. “Thanks to God, aim safe now……hahahaha ” (Asante mungu, niko salama sasa ……hahaha).Kijana muuaji na katili akiwa amevaa suti nyeusi pamoja na miwani ya gharama sana iliyomuwezesha kuona kila kitu katika mwili wa yeyote yule aliyekua mbele yake, alizungumza kwa sauti ya chini na kisha kucheka kwa furaha baada ya kufanikiwa kutoroka nchini Tanzania.
Alitembea kwa wasiwasi na umakini mkubwa, huku akikwepa askari waliokuwa wakifanya ukaguzi wa kila raia wa kigeni aliyeingia na kutoka nchini Marekani.Kutokana na taarifa za mauaji yaliyotokea nchini Tanzania kusambaa duniani kote, bwana Paul Agustino alitumia mafunzo yake ya kikomando aliyoyapata nchini Urusi kutoroka bila kugundurika na mtu yeyote katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Newyork internatinal airport.Paul Agustino aliwahi kuwa komando wa jeshi la ulinzi la Tanzania kabla ya kujiingiza katika ugaidi na ujambazi wa kutumia siraha kwasababu ya tamaa ya pesa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hey boy ……take me to Casabranca Hotel as soon as possible …I will pay you well “(Kijana ……nipeleke katika hoteli ya kasabranka haraka iwezekanavyo ……nitakulipa vizuri ” )Paul Agustino akiwa mwenye kuhema sana baada kuruka ukuta wa uzio wa uwanja wa ndege na kukata nyaya zilizopeleka mawasiliano katika cctv Camera ili asijulikane, anajipakia kwenye taxi na kisha kumuomba dereva kumtoa haraka sana mahali pale.
“Whatsup ……nigga “you will give me only fifty dollars “(sawa……niga utanilipa dola hamsini tu) dereva alimjibu Paul Agustino na kisha kuondoa gari kwa kasi sana, hakua na hofu yoyote kwani alizani Paul alikuwa ni “brack American ” (mmarekani mweusi )……hivyo alimchukulia kama raia wengine tu wa Marekani.
Muda si mrefu gari lilitua pembeni ya hotel kubwa ya kitalii ya Kasabranka, huku kijana Paul Agustino akiwa na furaha sana kufika mahali apo baada ya kukubaliana na dokta Benny Hanson wakutane mahali hapo ili kupanga mipango ya kumuwekea Paul sura bandia.
,…………………………………
Nchini Tanzania afya ya raisi mheshimiwa Samuel Kizito ilizidi kuimalika siku hadi siku, huku akitembea kwa kuchechemea baada ya kuwekewa miguu ya bandia. Raisi wa Tanzania Samuel Kizito alinusurika kufa baada ya mlipuko wa bomu kupitia miguu yake na kuisaga kabisa huku mlinzi wake akipoteza maisha kwani alimkumbatia ili kumuokoa raisi,na kuunguzwa mgongoni na kichwani na moto uliotokana na bomu hilo.
“Welcome Tanzania my friends, feel at home “(Karibuni Tanzania rafiki zangu, mjiskie mko nyumbani) afande mpelele zi wa jeshi la polisi bwana Godfrey Manumbu aliwakaribisha kwa furaha askari wawili kutoka Afrika kusini ,waliotumwa kwa ajiri ya kushirikiana na askari wa Tanzania kumsaka muhusika wa mlipuko wa bomu uliotokea na kureta maafa makubwa.
“My name is police inspector Jonson ……nice to meet you “,(jina langu ni mkaguzi wa polisi Jonson ……nafurahi kukutana na wewe), “my name is Jacline ……nice to meet you (Jina langu naitwa jacline……nafurahi kukutana na wewe).…askari wale walijitambulisha majina yao na kisha kupanda defender ya polisi kwa ajili ya kuelekea ikulu.
…………………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dokta Benny Hanson anafanikiwa kuibadirisha sura ya Paul Augustino, shughuli iliyofanyika kwa siri ndani ya chumba cha wageni katika hotel ya Kasabranka.
“Doctor Benny your the best, I have changed alot in such a way that even my woman can not identify me …”(Dokta Benny wewe ni bora zaidi, nimebadilika sana kiasi kwamba hata mwanamke wangu hawezi kunitambua )…..Paul Agustino alizungumza kwa furaha huku akimuhesabia pesa nyingi dokta Benny, kama malipo ya kazi kubwa aliyoifanya.
“Don’t worry young boy …this is my job “(usijali kijana …hii ni kazi yangu) dokta Benny alimjibu Paul huku akihesabu pesa zake kama zilikua zimekamilika.
Upelelezi unaanza huku afande Godfrey Manumbu akiongoza kundi hilo lenye watu watatu. “Twanzie kwa ukaguzi wa cctv camera ……twaeza gundua kajambo “askari wa kike kutoka Afrika kusini aliyeitwa Jacline aliwashauli wenzake huku akijitahidi kuongea kwa kiswahili, “Ndio hilo ni wazo zuri ” Jonson alimjibu Jacline kwa kiswahili kilichonyooka na kumfanya Godfrey kushangaa sana..”Kumbe mnafahamu Kiswahili …naamini itaturahisia kazi “Godfrey aliongea huku akitabasamu,na kuwafanya wote wacheke kwa furaha. “Hahaahaa ……tumekuja mara nyingi sana kwa Afrika Mashariki kwahiyo Kiswahili tunaongea pia, na ni moja ya sababu iliyotufanya tuchaguliwe kuja huku “…Jacline alimjibu Godfrey huku wakikagua baadhi ya cctv camera zilizoko uwanja wa taifa, mahali mlipuko ulipotokea.
“Njooni muone hii camera ,mfumo wake haukuharibiwa na bomu “Godfrey aliwaita wenzake baada ya kuhangaika muda mrefu kukagua camera iliyokuwa bado nzima, kwani camera nyingi ziliweza kuharibiwa na bomu vibaya sana.
“Waooh …this can help us “(waooh ……hii inaweza kutusaidia) Jonson aliongea huku akiitazama na kuikagua vizuri camera ile.
…………………………………
Sura ya Askari aliyewahi kuwa komando wa Tanzania inaonekana ikipandikiza bomu kubwa sana lenye uzito wa kilo tano, bomu hilo lilitegwa huku likiwa limetengenezwa kwa mfano wa mdoli wa kuchezea mtoto. Kutokana na muonekano huo ilikua vigumu mtu yoyote kulitambua bali baadhi ya watoto walionekana wakicheza nalo kutokana na muonekano wake kuwavutia.
“mmmh mbona inaonesha ni komando Paul Agustino, haiwezi kuwa kweli ……siamini macho yangu Paul kashakufa miaka mitano iliyopita kwa ajari ya ndege akiwa anaelekea nchini Canada katika shughuri za kijeshi “……Afande Godfrey alishangaa baada ya cctv camera kuonesha kila kitu ilipounganishwa na kompyuta, huku maelezo ya muhusika na historia yake ikionekana kwenye kompyuta hiyo. “Hapa kutakua kuna siri nzito,, kama muhusika inasemekana kafa na alikua ni askari wa Tanzania ……hapa kuna mkono wa mtu “Jonson aliongea huku akionekana kuchanganywa sana na maneno aliyoyaongea Godfrey.
“We should go to the area where he was buried … we can find something to help us “(tunapaswa kwenda eneo alipozikwa …tunaweza pata kitu cha kutusaidia ) Jacline aliongea maneno yaliyokubaliwa na wenzake na haraka sana walifunga safari kuelekea mahakamani ili kupewa kibali cha kufukua kaburi ambalo ilisemekana komando Paul Agustino aliweza kuzikwa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Aliyezikwa hapa ni mtu feki, kutokana na dokomenti zilizopo …Paul alikua na damu grupu O …lakini vipimo vyangu vinaonyesha kua mtu huyu kabla ya kupoteza maisha, alikuwa na damu grupu AB huku fuvu lake likiwa na tundu la risasi kichwani jambo ambalo linaonesha maiti hii siyo sahihi ” daktari alitoa ripoti baada ya kukamilisha uchunguzi wa maiti iliyokuwa ikisemekana ni ya Paul Agustino.
“Hapa sasa nimeshapata jibu, twendeni uwanja wa ndege tukachunguze camera za watu walioingia nchini na kutoka kabla na baada ya tukio “,Godfrey alizungumza jambo ambalo halikupingwa na mtu yeyote na haraka sana waliondoka katika makaburi ya manispaa ya Kinondoni kuelekea Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
“Mhhh mhusika anaonekana hakua anaishi Tanzania kama inavyoonekana ……aliingia nchini siku mbili kabla ya tukio “Godfrey aliongea huku wakiwa makini na wenzake kufuatilia cctv camera iliyokuwa ikionesha matukio yaliyopita uwanjani hapo.
“What !!………waziri wa ulinzi atakua anahusika kwa namna moja au nyingine kwanini alienda kumpokea uwanja wa ndege ” ,bwana Godfrey aliongea huku wakishuhudia mheshimiwa Sarehe Athuman ambaye ni waziri wa ulinzi wa Tanzania akimpokea mtuhumiwa aliyekuwa akionekana kutokea Canada kutokana na taarifa zilizotolewa na wahudumu wa usafiri wa anga.
“Our cctv camera system was hacked the next day after explosion ……I think the suspected person disappeared on that day “(mfumo wetu wa cctv camera ulihakiwa siku iliyofuata baada ya kutokea mlipuko ……nafikiri mtuhumiwa alitoweka siku hiyo) mhudumu wa kizungu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere aliongea hasa baada ya taarifa za kutoka nchini mtuhumiwa zikiwa hazionekani kwenye kompyuta.
“What you are saying can be right, if not! Still the suspect might be here in Tanzania ……”(unachokisema kinaweza kuwa sahihi, kama siyo sahihi! Mtuhumiwa atakua bado yuko Tanzania) Jacline alizungumza maneno yaliyoungwa mkono na kila mmoja.
“Mi naona waziri wa ulinzi akamatwe ahojiwe, atakuwa anafahamu kila kitu kuhusu mlipuko huu na mahali muhusika alipo. “Jonson alishauri jambo ambalo liliweza kuleta manufaa katika upelelezi na kutambua ukweli kuhusu kifo cha Paul Agustino, mmoja kati ya makomando kumi pekee wa jeshi la Tanzania.
“Kuanzia leo natengua uteuzi wa waziri wa ulinzi mheshimiwa Sarehe Athuman kutokana na tuhuma nzito alizonazo za kuhusika na mauaji yaliyotokea, na akamatwe haraka iwezekanavyo kwa mahojiano………” Raisi alitoa amri iliyoungwa mkono na viongozi mbalimbali wa nchi ya Tanzania huku, wananchi wakipiga kelele za shangwe kufurahia maamuzi hayo ya raisi yaliyokuwa yakirushwa hewani kupitia redio na televisheni zote nchini.
…………………………………
“Yalaaa………mnisamehe jamani …nakufa mimi …Msiniue nitasema kila kitu, Paul Agustino yuko hai na ndio kahusika na shambulio la kigaidi lililotokea kwa ajili ya kumuua raisi ili mimi niweze kuipindua serikali iliyoko madarakani ….na niweze kuwa raisi wa Tanzania ………Paul hakufa kama ilivyokua inafahamika bali tulifanya mpango wa kulidanganya taifa kuhusu kifo chake ili tuweze kumtumia katika shughuri zetu kulingana na uhodari na ushujaa alionao katika masuala ya kivita “,waziri wa ulinzi aliongea kwa maumivu makali baada ya mateso ya siku mbili mfululizo bila kula chakula cha aina yoyote ile, huku akipigwa bila huruma na kundi la askari watatu wakiongozwa na afande Godfrey Manumbu.
“Paaaah ……” mlio wa kitako cha bunduki ulisikika na kufanya kichwa cha bwana Sarehe kuvuja damu, “Sema mpuuzi wewe, mtuhumiwa yuko wapi ……” Jonson aliongea kwa hasira huku akikumbuka kifo cha raisi wao wa Afrika Kusini kilichosababishwa na mlipuko huo huku bwana Sarehe akiwa muhusika namba moja wa tukio hilo ……..”ooooh !!…msiniue tafadhali ……nitasema ukweli mtuhumiwa kakimbilia nchini Marekani katika jiji la Newyork ……” Bwana Sarehe aliongea kwa maumivu makali huku akitoboa siri nzito iliyokuwa imefichika.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Paul Agustino akiwa mwenye kujiamini sana baada ya kubadilisha sura yake, anaponda starehe na wadada katika kasino na hoteli ya Kasabranka bila kujali gharama ya pesa aliyokuwa akitumia. “My girls, just drink ……drink ……I will pay “(wasichana wangu ……kunyweni ……kunyweni nitalipa) bwana Paul aliwaondoa hofu wadada zaidi ya sita waliokuwa wamemzunguka wakiponda naye raha na kunywa vinywaji vya kila aina bila kujali gharama zake. “Thank you nigga “(asante nigga …)walimshukuru bwana Paul na kumwita nigga kutokana na weusi aliokuwa nao huku akiwa amevalia suti nyeusi iliyompendeza vilivyo.
…………………………………
Vijana watatu wazalendo wa nchi zao wanaiacha ardhi ya Tanzania, huku kila mmoja akiwa na mawazo mengi akifikiria jinsi ya kuikabili kazi nzito iliyoko mbele yake. “Bila shaka tutafika Marekani kesho saa sita mchana “,mrembo Jacline mmoja wa askari hodari kutoka Afrika Kusini alikisia muda wa Kufika Marekani na kujalibu kuwajulisha wenzake, ili wawe tayali kwa safari ndefu ndani ya ndege.Kutokana na kuishi Tanzania kwa takribani mwezi sasa,Jacline alikuwa tayali anafahamu kuongea Kiswahili vizuri hali iliyorahisisha mawasiliano baina ya mashujaa watatu waliotumwa na nchi zao kwenda kumtafuta bwana Paul Agustino akiwa hai au amekufa.
…………………………………
Mfanyabiashara wa madawa ya kulevya pamoja na madini ya Tanzanite,bwana Benedict Mathayo anakuwa katika wakati mgumu akifikiria namna ya kujiokoa ili asiweze kukamatwa kwani alishirikiana na waziri wa ulinzi bwana Sarehe Athuman kufanya mipango ya kumuua raisi ili waipindue nchi.”Bwana Sarehe hajanitaja,lakini ninahofu huyu mpuuzi akikamatwa lazima na mimi nitiwe hatiani……” mfanyabiashara muuaji na katili aliyekuwa ameahidiwa uwaziri mkuu na bwana Sarehe watakapofanikiwa kuipindua nchi,aliendelea kutafakari bila kupata jibu lolote namna ya kujiokoa kutoka katika kesi nzito iliyokuwa ikiwakabili mara tu atakapo kamatwa bwana Paul Agustino.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyu mpuuzi kabadili hadi namba ya simu,ngoja nitumie barua pepe (email) nibahatishe kama ujumbe utamfikia……anatakiwa ahame Newyork haraka sana kabla hawa washenzi waliotumwa kumkamata hawajafika……” bwana Benedict alilalamika baada ya kupiga namba ya simu ya mkononi ya bwana Paul Agustino mara kadhaa,bila kupatikana na kuamua kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia barua pepe.
…………………………………
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment