Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MUUAJI MWEUSI (THE BLACK KILLER) - 2

 










Simulizi : Muuaji Mweusi (The Black Killer)

Sehemu Ya Pili (2)







“Waaaooh kumbe nchi ya Donald Trump ni nzuri kiasi hiki……” Jacline aliongea huku akitabasamu baada ya kufika nchini Marekani,na kuanza kushangaa uzuri wa jiji la Newyork.”Ndio ni pazuri sana,na hapa ni mwanzoni tu mwa jiji” Jonson alimjibu Jacline huku wakijiandaa kwa ajiri ya kushuka ndani ya ndege kubwa inayomilikiwa na shirika la ndege la Dubai Airlines.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mbona sioni askari waliokuja kutupokea nimechoka na safari, mimi ni mwenyeji sana wa jiji hili ……na hoteli ya Kasabranka ndo napenda kufikia kila nifikapo Marekani ……kwahyo tunaweza kwenda kupumzika mahali pale kwa siku ya leo kabla ya wenyeji wetu kuja kutuchukua “…Godfrey alishauri jambo na kukubaliwa na askari wenzake kutokana na uchovu wa safari ndefu waliyokuwa nayo.



“Hey Africans, can i help you? “……(hey Waafrika  ninaweza kuwapatia msaada) ,dereva taksi aliyempokea Paul Agustino kwa mara nyingine tena anaona sura ngeni za Kiafrika nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Newyork, na kuomba kuwasaidia.



“Yes ……you can help us”(ndio ……unaweza kutusaidia “) msichana mrembo Jacline mwenye asili ya Kiafrika aliyemvutia kila mwanaume rijali aliyemtazama, alimjibu dereva taksi yule wa Kimarekani huku wakipakia mizigo katika taksi yake “



“Take us to Casabranca hotel, we will pay you well “(tupeleke kasabranka hoteli, tutakulipa vizuri) …Jonson aliongea na kumfanya dereva yule atabasamu sana kwa furaha kwani ,Jonson aliongea maneno yaleyale aliyoyaongea Paul Agustino mara tu alipofika Marekani na kukutana na dereva huyo.



“Why are you loughing …??'”(kwanini unacheka) ,Jonson alimuulza swali dereva yule na kupewa jibu lililowafanya wote kujawa na shauku kubwa ya kumuulza maswali dereva yule.



“There is a certain brack American, told me the same words as yours when he arrived here at the airport …he asked me take him to Casabranca hotel and then he payed me alot of money ……hahaha “(kuna Mmarekani mweusi mmoja aliniambia maneno kama uliyoniambia wewe,baada ya kufika hapa uwanja wa ndege. Aliniomba nimpeleke katika hoteli ya Kasabranka halafu akanilipa pesa nyingi sana……hahaha ” dereva taksi aliongea huku akicheka na kutabasamu kwa furaha, baada ya kuulizwa chanzo cha kicheko chake na Jonson.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Please do you know this person, we will give you alot of money ……”(tafadhali unamfahamu mtu huyu,tutakulipa pesa nyingi sana) Jacline alitoa picha na kumwonyesha dereva, ilikua ni picha ya Paul Agustino akiwa amevalia suti nyeusi kama kawaida yake pamoja na miwani yake huku picha ikiwa imeandikwa “THE BLACK KILLER ” (muuaji mweusi) kwa herufi kubwa, na kumfanya dereva azidi kuogopa zaidi.



“Yes i know him, is the person whom I was telling you about “(ndio namfahamu, huyu ndo mtu yule ambaye nilikuwa nawambia ) dereva taksi aliongea kwa woga sana, huku kina Jacline wakifurahi kwa kupata jibu zuri ambalo litawafanya wakamilishe kazi waliyotumwa kwa muda mfupi zaidi.



Baada ya muda wa takribani masaa mawili, gari dogo aina ya taksi, lilipaki nje ya hoteli kubwa ya kitalii ya Kasabranka. Mziki mnene ulisikika huku biashara za kila aina zikifanyika katika hoteli  ile, “Take your money……and thank you “(chukua pesa yako……na asante) Godfrey alimlipa pesa ya kutosha dereva wa taksi na kisha kumshukuru. “Thank you alot ……Africans”(asante sana …Waafrika)  dereva yule alipokea na kushukuru sana kwani alilipwa pesa nyingi, takriban dola mia mbili sawa na zaidi ya shilingi laki tano za Kitanzania.



Godfrey na wenzake walichukua vyumba vya kulala wageni katika hoteli ya Kasabranka, na kukataa kulala katika nyumba za wageni walizokuwa wameandaliwa na serikali ya Marekani ili tu waweze kupeleleza kwa siri, katika hoteli ya Kasabranka baada ya kukisia kuwepo kwa Paul Agustino katika hoteli hiyo kutokana na taarifa walizopewa na dereva taksi. Bila kutegemea siku zilizidi kukatika, bila kutambua kitu chochote kuhusu Agustino na mahali alipo.



********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Paul Agustino aliendelea kukaa katika hoteli ya Kasabranka akisubilia kuitwa na matajiri waliokuwa wakimtumia kwa kazi mbalimbali, bila kutambua kuwa kuna baadhi ya askari walikuwa wameshawasili katika hoteli hiyo kumkamata.



Ilikua ni jioni nzuri iliyokuwa inaangazwa vema na mbalamwezi, huku upepo mzuri ukivuma na kuipendezesha mandhari ya nje ya hoteli ya Kasabranka. Msichana mrembo Jacline akiwa ameketi nje akipunga upepo, kwa mbali alimuona mwanaume handsome na mtanashati akipita mbele yake. Hisia za mapenzi zilimuingia Jacline, na kujikuta akitamani kumpata mwanaume yule awe mpenzi wake.



“Jina langu naitwa Mr Pius …nafurahi sana kukutana na muafrika mwenzangu kama wewe katika nchi ya ugenini ……” bwana Paul Agustino alijitambilisha kwa jina la uongo mbele ya msichana mrembo Jacline. “Nafurahi pia kukutana na mwanaume mtanashati wa kiafrika nikiwa ugenini ……sijui umejuaje kama nafahamu Kiswahili ” Jacline aliongea kwa tabasamu nzuri zenye hisia za mapenzi ndani yake mbele ya Paul Agustino, aliyejitambulisha kama mr Pius. “Hahaha…Mswahili anajulikana  popote pale”Paul Agustino alicheka huku akifurahi kukutana na msichana mrembo sana Jacline, moyoni aliapa kumpata Jacline kwa gharama yoyote ile awe kama mpenzi wake bila kutambua kuwa Jacline ni mmoja kati ya askari hodari watatu waliotumwa kuja kumkamata.



“Samahi mr Pius, unatokea nchi gani Afrika?? “,Jacline alimuulza bwana Paul Agustino huku akimwita kwa jina la mr Pius, jina ambalo Paul alidanganya tangu alipofika katika hoteli ya Kasabranka kwa mara ya kwanza. “Natokea nchi ya Tanzania, nchi ambayo mrima mrefu barani Afrika ……mrima wa Kilimanjaro unapatikana “,Bwana Paul aliongea na kuisifia nchi ya Tanzania na kumfanya Jacline atabasamu kwani alimuona Paul kama mzarendo wa nchi yake.



Ghafra ujumbe mfupi wa barua pepe uliingia katika simu ya Paul, kutokana na siri nzito iliyokua moyoni mwake hakuweza kumwamini mtu yeyote hivyo aliufungua na kuusoma kwa siri bila Jacline kufahamu chochote. “Samahani mrembo ……ukinihitaji napatikana chumba namba mia moja, ghorofa ya kumi. ……nimechoka sana ngoja nikapumzike ” ,Paul alikatisha mazungumzo na Jacline haraka sana na kisha kuondoka haraka eneo lile na kumwacha Jacline akipigwa na butwaa.. Kutokana na Paul Agustino kubadilisha sura yake, Jacline hakuweza kumuhisi kuwa ndiye bwana Paul Agustino, jambazi katili walilokuwa wakilitafuta bali aliamini kuwa ni mr Pius ambaye alikuwa raia wa Tanzania huku akiwa hatambui kazi yake kwani mazungumzo yao yalisitishwa ghafra bila Jacline kuitambua sababu iliyosababisha Paul kuondoka haraka kiasi kile.



“Nitamtembelea kesho chumbani kwake ……”Jacline aliongea kwa sauti ya chini peke yake huku akielekea chumba namba tano, ghorofa ya kwanza. Jacline na wenzake waliamua kuishi vyumba vya ghorofa ya kwanza ili angalau waweze kuona watu waliokuwa wakiingia na kutoka hotelini hapo, kama wangeweza kubahatisha kuiona sura ya Paul Agustino..

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya Paul kupokea ujumbe mzito kuhusu kukamatwa kwa waziri Sarehe, na kuifahamisha serikali kuhusu kuwepo hai kwa Paul Agustino na wala hakuwa amekufa kama ilivyojulikana, Paul alichanganyikiwa ghafra na kujikuta akielekea chumbani haraka sana ili aweze kuvaa miwani yake iliyomuwezesha kuona kila kitu katika mwili wa yeyote yule aliyekuwa mbele yake. Miwani hii ingemsaidia kugundua watu ambao hawakuwa salama kwake pale hotelini.



“Waziri ni mpuuzi, kwanini aseme kila kitu kuhusu mimi mpaka kuhusu swala la mimi kutorokea huku Newyork ……inatakiwa nianze kuua baadhi ya watu wanao fahamu siri zangu ili kujilinda “Paul aliongea huku akiwa amejilaza kitandani akisoma kwa kurudia rudia ujumbe aliokuwa ametumiwa na bwana Benedict, ujumbe ambao ulimfahamisha juu ya kuwasili jijini Newyork kwa askari waliotumwa kumkamata.



…………………………………



Jacline akiwa mwenye kusumbuliwa na mapenzi,alishindwa kulala kwani alikosa usingizi kabisa akimfikiria Paul Agustino ,kijana aliyejitambulisha kama mr Pius na kuziteka hisia za Jacline.



“Lazima nimpate kwa gharama yoyote ile,kesho kukipambazuka ……jambo la kwanza naamkia chumbani kwake”,Jacline aliendelea kusumbuliwa na hisia za mapenzi na kufikia uamuzi wa kuonana na Paul,asubuhi iliyofuata.



Godfrey na Jonson wakiwa katika hali ya kukata tamaa,wanajikuta wakisumbuliwa na mawazo mengi kwani shughuri ilizidi kuwa ngumu siku hadi siku huku matarajio ya kumkamata Paul yakiwa yametoweka ghafra.”Nimepakumbuka nyumbani ……nakupenda sana Afrika kusini”Jonson aliongea peke yake kwa sauti ya chini huku akiwa anatazama kitambaa chake cha mkononi chenye bendera ya nchi yake.”Usjali ipo siku utarudi ukiwa na medali ya ushindi shingoni mwako,” Godfrey kijana jasiri wa Kitanzania alimtia moyo Jonson baada ya kuyasikia maneno aliyoyatamka.



Ndi…ndii…ndiii…kengele ilipiga fujo na kumshtua kutoka usingizini bwana Paul,akiwa amevalia bukta na singrendi na kufanya kifua chake kuonekana vizuri. Alikwenda kufungua mlango wa chumba chake haraka sana kwani alidhani muhudumu wa hoteli alikuwa amemletea chai kama ilivyo kawaida.



“Waaaooh kumbe ni wewe mrembo,karibu sana”Paul aliongea kwa sauti iliyojaa tamaa ya mapenzi huku akimkumbatia Jacline.”Aaasantee…nte”Jacline alijibu kwa kusita sita huku wakiwa wamekumbatiana na Paul,hali iliyowafanya wote kuzidiwa na tamaa za mwili na kujikuta wakishiriki tendo la ndoa bila kutegemea.



Bila kutegemea Jackine akiwa haamini kilichotokea,alitabasamu na kupuuzia mawazo ya kujuta kukubali kutoa penzi kwa mwanaume asiyemtambua kwa undani zaidi na kuendelea kupumzika katika kifua cha Paul,huku moyo wake ukiwa na furaha kumpata mwanaume aliyetokea kumpenda sana.



“Mhhh siamini macho yangu……hichi kitambilisho cha jeshi cha Paul Agustino kimefikaje hapa…”Jacline aliongea kwa sauti ya chini sana huku akishangaa kitambulisho cha jeshi cha Paul Agustino,mara tu alipoamua kukagua mifuko ya suruali ya Paul ambaye Jacline alimfahamu kwa jina la Pius,wakati Paul akiwa ameenda bafuni kuoga.



Jacline alirudisha kitambulisho kile haraka sana baada ya kusikia mlango wa bafuni ukifunguliwa, huku Paul akitoka na kuhisi hali isiyo ya kawaida kwani Jacline alionekana kutojiamini kama awali huku wasiwasi na woga ukiionekana wazi katika sura yake. “Vipi mpenzi, kuna tatizo lolote “Paul alimuulza Jacline huku akijifuta vizuri mwili wake kwa taulo na kukausha maji yaliyokuwa yakitililika mwilini. “Hapana mpenzi niko sawa,ondoa hofu kabisa “Jacline aliongea kwa sauti nzuri iliyomfanya Paul kupotezea swala lile.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

…………………………………



“Kuna jambo nataka niwafahamishe, kuna kijana nimekutana naye ……inaonekana anafahamiana na Paul Agustino, kijana huyu nilikagua suruali yake alipokuwa ameenda kuoga na bila kutarajia nilikuta kitambulisho cha jeshi cha Paul. ” Jacline aliwafamisha wenzake baada ya kutoka chumbani kwa Paul na kugundua jambo ambalo alishindwa kulihifadhi moyoni, kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Paul kwani hisia za mapenzi zilimsumbua na kumtaka asitoe siri ile kwani angemuweka mahali pabaya Paul ambaye yeye alimfahamu kama mr Pius. “Kijana huyo anaitwa nani?……na umefahamiana naye kivipi ” Jonson alimuulza swali Jacline, huku Godfrey akiwa makini kusikiliza mazungumzo hayo.



“Kijana huyo anaitwa mr Pius, nilikutana naye nje ya hoteli jana baada ya kusikia akiongea Kiswahili, kutokana na kuniambia anatokea Tanzania nilijikuta nikiwa rafiki yake ” Jacline alimjibu Jonson huku akionekana kuchoshwa na maswali mengi aliyokuwa akiulizwa. “Mi nakuomba endelea kuwa karibu naye na uzidi kumchunguza zaidi, lazma atakuwa anafahamu kitu “Godfrey askari aliyekuwa na busara sana katika kila maamuzi aliyoyachukua, alimsihi Jacline aendelee kuwa karibu na Paul, bila kutambua madhara makubwa yatakayotokea mbeleni.



“Mimi pia, naona hilo ndo jambo sahihi nalotakiwa kulifanya ……”Jacline aliongea huku akitabasamu kwa furaha baada ya kuruhusiwa kuwa karibu na Paul, hali iliyowashangaza Jonson na Godfrey kwani hawakufahamu chochote kuhusu furaha hiyo.



…………………………………



Paul Agustino akiwa chumbani kwake anajiandaa na kutafakari namna ya kumuua  Benny Hanson, daktari aliyemfanyia upasuaji na kuibadilisha sura yake. “Nikifanikiwa kumuua Benny, angalau nitaishi kwa amani kwani ndio mtu pekee anayefahamu siri hii ya mimi kubadili sura yangu “Paul aliongea huku akiisafisha bastora yake na kuiondolea mfumo wa sauti na kuwa na uwezo wa kuua bila kutoa mlio (silent). “Hello doctor, aim very sick …just come to help me “(haloo daktari, naumwa sana njoo unisaidie) Paul Agustino alimpigia simu Benny Hanson kwa sauti ya unyonge sana na kujifanya anaumwa ili aweze kufika haraka na kumuua.



Muda si mrefu dokta Benny aliwasili kwani aliyaamini maneno aliyozungumza na Paul kwenye simu, kwani haikuwa kawaida ya Paul kuongea naye kwa sauti ya kinyonge kiasi kile. “Ndiii…ndiiiii ……ndiii…ndiii” mlio wa kengele ulisikika na kumfanya Paul kuikoki bastora yake, kwani kengele hiyo iliashilia dokta Benny alikuwa tayali amewasili. “Aaaaah…. …ah…aah” dokta Benny alilalamika baada ya kupigwa risasi ya ubavuni huku akichomwa na kisu tumboni ……shambulio lililofanywa kwa sekunde kadhaa baada ya kufunguliwa mlango wa chumba cha Paul. “Ndii …ndiii “kengele ilitoa mlio kwa mara nyingine kuashilia ujio wa mgeni katika chumba cha Paul, hali iliyomtia hofu Paul na kumfanya kuchukua maamuzi ya kikomando kwani alikuwa tayali ameshaandaa begi lake dogo lenye kila kitu alilolitumia katika safari.



Jacline aliendelea kugonga mlango huku akihofia Paul ambaye yeye alimtambua kwa jina la mr Pius, atakuwa amepatwa na matatizo kutokana na kelele za maumivu alizokuwa akizisikia chumbani.



Paul Agustino anashuka ghorofani kwa kutumia kamba ndefu aliyoifunga dirishani, akiwa katika mavazi yake ya suti nyeusi anafanikiwa kutokomea katika hoteli ya Kasabranka kishujaa baada ya kumpiga teke raia wa kizungu aliyekuwa amepaki pikipiki yake nje ya hotel akisubili wateja, na kisha kutokomea nayo huku akimuacha mzungu yule akilia kwa maumivu makali aliyoyasikia baada ya kupigwa teke.



Godfrey na Jonson wanafika haraka sana chumba namba mia moja baada ya kutumiwa ujumbe wa hatari na Jacline ,ujumbe huo ulitumwa kwa kutumia saa za kijeshi walizokuwa wamezivalia mikononi kila mmoja wao. “Hatuna budi kuvunja mlango ……”Godfrey aliongea na kisha kupiga teke la nguvu mlango ule na kisha kufunguka ,katika hali ambayo hawakutarijia walishangaa kumwona mzungu raia wa Marekani akiwa amepigwa risasi na kisha kuchomwa kisu huku mtuhumiwa akiwa ametoweka kupitia dirishani kwani kamba aliyoitumia ilikua ikining’inia. “Huyu aliyehusika inaonekana aliwahi kuwa askari “Jacline aliongea huku akishangaa sana kile kilichokuwa kimetokea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Take this file, you will know the one who killed me ……”(shika faili hili, utamfahamu aliyeniua) Mzungu yule alimkabidhi faili Godfrey na kisha kupoteza maisha.



Wote kwa pamoja walilipitia faili lile,huku kila mmoja akishangazwa sana na taarifa zilikuwa latika faili lile,kwani waliishi na Paul bila kumtambua kutokana na sura yake kubadilishwa na dokta Benny ambaye tayali alikuwa marehemu.”Mpuuzi kweli huyu,alinidanganya anaitwa Pius kumbe ni muuaji mkubwa” ,Jacline alilia kwa uchungu huku akijuta kumpatia penzi Paul kabla ya kumfahamu vizuri.



Vyombo vya habari duniani kote vilipambwa na taarifa ya jambazi Paul ,huku picha zikioneshwa katika televisheni na magazeti na donge nono likitolewa kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake.”Popote alipo tutamkamata,akiwa hai au amekufa” vijana watatu waliongea na waandishi wa habari huku wakiwa na hasira sana dhidi ya Paul Agustino.



Paul Agustino anaitelekeza pikipiki yake barabarani, na kutokomea ndani ya msitu wa Amazon. Msitu mkubwa nchini Marekani unaosifika kwa kuwa na wanyama wengi wakali, hakuna binadamu yeyote aliyefanikiwa kutoka salama baada ya kuingia katika msitu huo. Paul akiwa ameshikilia bastora yake pamoja na kisu kikali cha kijeshi mikononi mwake, aliendelea kuingia kabisa katikati ya msitu, bila kuogopa kitu chochote kutokana na ujasiri aliokuwa nao.



Ghafla Paul anajikuta katika wakati mgumu baada ya joka kubwa aina  ya chatu lililokuwa juu ya mti, kumdondokea na kisha kujiviringisha katika mwili wa Paul tayali kwa ajili ya kummeza. “Shenzi wewe, umeingia choo cha kike “,Paul alizungumza maneno ya kejeli kwa joka lile kubwa huku akipambana nalo ili kujikomboa. Bila kutegemea joka lile linamtupa Paul ndani ya maporomoko ya maji ya mto Amazon, mto ambao ulikuwa umejaa mamba wengi sana wenye njaa kali, na kumfanya Paul kuwa katika wakati mgumu kupambana na joka lile kubwa pamoja na mamba waliokuwa wanaonekana kuwa na njaa kali kwa muda mrefu.



“Paaah ……paaah ……paah “milio ya risasi ilisikika pamoja na mishale mingi ,iikitokea katikati ya msitu na kushambulia mamba  pamoja na joka lile kumbwa ambalo lilikuwa tayali limemshinda nguvu Paul na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili. “Pole sana baba, nitakusaidia kukutibu “mzee wa makamo alimpa pole Paul, huku vijana walio onekana kuwa ni watoto wa mzee yule wakimkokota Paul na kumtoa ndani ya maji huku akiwa amejeruhiwa vibaya sana. “Asante sana mzee wangu, ilikuwaje mpaka ukafahamu kuongea lugha ya Kiswahili, na kwanini unaishi ndani ya msitu huu ambao ni hatari sana ……”Paul alimuulza mzee yule swali, huku akionekana kushangazwa sana na mzee yule aliyemsaidia, mzee ambaye alikuwa amevalia ngozi ya mamba pamoja na vijana wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Utafahamu kila kitu, tuondoke eneo hili tuelekea kwenye kambi yetu……eneo hili ni hatari sana kwa wakati huu kwani wanyama wakali wanapenda kuja kunywa maji hapa mtoni, lakini tukifika kambini nitakuelezea kila kitu “,mzee yule alimjibu Paul huku wakiondoka sana eneo lile, lakini kwa upande wa Paul, mawazo mengi yalizidi kumtawala na woga kumtawala kwani alimuona mzee yule hakuwa mtu wa kawaida kutokana na muonekano wake na  njinsi alivyomuokoa kutoka kwa wanyama wakali.



…………………………………





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog