Simulizi : Muuaji Mweusi (The Black Killer)
Sehemu Ya Tatu (3)
Camera mbalimbali zilizoko kila kona ya barabara katika nchi ya Marekani, zinakaguliwa na askari na kisha kugundua sehemu ambayo Paul Agustino aliweza kuelekea. Jeshi kubwa la nchi ya Marekani likiongozwa na vijana watatu wa Kiafrika, wanajikuta wakiingia katika msitu wa Amazon kumtafuta Paul, baada ya kuikuta pikipiki aliyoitumia kutoroka ikiwa imetelekezwa barabarani. “Huyu mshenzi nikimkamata nitahakikisha na mkata kata vipande vipande, hawezi kuisumbua dunia kiasi hiki “,Godfrey alizungumza kwa hasira sana huku akitumia panga lake kukata matawi ya vichaka, ili kutengeneza njia ya kupita na kuingia ndani kabisa ya msitu. “Nina hasira naye sana, huu ni mwezi wa sita niko mbali na familia yangu nikiteseka kumtafuta mpuuzi huyu, lazima atalipia tu siku nikimkamata, nina hasira naye sana “Jonson aliongea pia kwa hasira maneno ambayo yaliyodhibitisha kuwa alichoshwa na kazi nzito ya kumtafuta bwana Paul Agustino.
Kwa upande wake Jacline aliumia sana kila aliposikia maneno yaliyohusu adhabu kari atakayopatiwa Paul, mara baada ya kutiwa mikononi. “Nakupenda sana, lakini nitahakikisha nakuua kwa mikono yangu mwenyewe kutokana na mauaji ya kikatiri unayoyafanya kila kukicha ……na sitajali kuhusu kiumbe kilichoko tumboni mwangu kukosa baba “,Jacline aliongea kwa uchungu mkubwa na kwa sauti ya chini, huku machozi yakimtoka. Jacline alizidi kusonga mbele msituni na askari wenzake, bila kumwambia mtu yeyote siri aliyonayo baada ya kugundua kuwa na ujauzito wa bwana Paul Agustino, jambazi sugu lililoitikisa dunia kutokana na habari zake kusambaa duniani kote.
…………………………………
“Mimi naitwa daktari Benezeth Christopher kutoka Tanzania, ndege yetu ilipata ajari miaka hamsini iliyopita tukiwa tunaelekea visiwa vya Haiti kwa ajili ya kutibu wahanga wa vita. Ndege yetu ilikuwa na jumla ya abiria kumi, nane walifariki dunia huku wawili tukitoka salama mimi nikiwa kama daktari mkuu pamoja na nesi wangu. Kutokana na msitu huu kuwa na wanyama wakali, tulishindwa kutoka ndani ya msitu na kujikuta tukianzisha makazi katikati ya msitu huu na kuishi kama mke na mme ” Daktari yule alimuelezea Paul, historia ya maisha yake huku Paul akiwa makini kuisikiliza kwani ilimvutia sana. “Vipi kuhusu historia yako kijana wangu, inaonekana wewe ni askari kutokana na jinsi nilivyokuona ukipambana na joka lile kubwa, na pia inaonekana una siri nzito moyoni mwako kwani muda mwingi nakuona ukiwa na mawazo…niambie tu siri hiyo nitakusaidia “Mzee yule aliyeonekana kuwa na busara nyingi huku uso wake ukionekana kuwa ni mtu mwenye huruma sana alimuulza Paul yaliyomsibu, na kumwomba amwambie ili aweze kumsaidia.
Paul Agustino bila kutegemea anajikuta anamwamini mzee yule, na kumwelezea kila kitu kuhusu historia na siri nzito ya maisha yake, “Nisaidie mzee, sina msaada mwingine zaidi yako ……sasa hivi nimebadilika sio mtu yule wa zamani “,Paul aliongea maneno kwa hisia kali huku machozi yakimtoka, hali iliyomfanya mzee yule akubali kumsaidia.
“Nitaibadilisha sura yako kwa mara nyingine, lakini usithubutu kunifanyia chochote kama ulivyomfanyia dokta Benny, mimi hutoniweza, mimi ni mtu hatari sana zaidi ya unavyofikiria “,mzee yule alimweleza Paul maneno ya kukubali kumsaidia, huku akimuonya asithubutu kumuua kwani asingeweza kufaulu kama alivyofanya kwa dokta Benny.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mara nyingine upasuaji wa kubadilisha sura ya Paul unafanikiwa, kwa kutumia vifaa vya kidaktari ambavyo havikuharibika baada ya ndege kudondoka. Kutokana na ujuzi wa mzee yule kuwa ni wa zamani sana, huku akitumia vifaa vya kizamani vya kufanyia upasuaji, Paul Agustino alionekana kuwa na sura ya kizee baada ya kufanyiwa upasuaji ule. “Bila shaka, sitoweza gundulika ……nakushukuru sana mzee wangu “,Paul aliongea kwa furaha sana na kumshukuru mzee yule, huku moyoni akiwaza kumuua na kisha kutoroka eneo lile.
Kundi la simba wakali wa msitu wa Amazon, wanalivamia kundi la askari kwa ajili ya kujipatia kitoweo, “,Help me, please help me……”,(Nisaidie tafadhali nisaidieni) mmoja wa askari wa kimarekani alipiga kelele kuomba msaada baada ya simba mkubwa kumkamata mguu na kuanza kutokomea naye porini huku likimburuza.”,Pyuuu,pyuuu……pyuuu”,,,Paaaah ……paaah……papaaah”, milio ya bunduki za kivita za kila aina zilisikika,askari wa Kimarekani ambao walikuwa wakiongozwa na Waafrika watatu wakijalibu kumshambulia simba yule bila mafanikio.Ghafla kila askari alianza kujitetea kuokoa maisha yake kwani simba wengi walikuja kwa pamoja na kuvamia,hali iliyowafanya askari wengi kupoteza maisha na wengine kukimbia porini bila uelekeo maalumu.”Help me,help… me”(nisaidieni nisa…idi…eni) sauti ya askari mmoja ilisikika ikiomba msaada huku ikiwa inapungua kadri muda ulivyozidi kwenda,joka kubwa ambalo haijulikani mahali lilipotokea lilimmeza askari yule na kuanza kumtafuna hali iliyopelekea askari wengi kutupa siraha zao na kukimbia na kuwaacha Waafrika watatu majasiri wakimpiga risasi nyoka yule na baadaye kufanikiwa kumuua.
…………………………………
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bomu lililotegwa na Paul Agustino kisiri katika nyumba ya mbao inayomilikiwa na daktari Benezeth,daktari aliyeibadirisha sura ya Paul kwa mara nyingine tena linalipuka na kuua familia nzima ya dokta huyo.”Hahaah…Sijawahi kushindwa na chochote,mimi ndio komando Paul…” Paul alicheka huku akiongea maneno ya kujisifu baada ya kuhakikisha hakuna mtu yeyote aliyekuwa amesalimika katika familia ya dokta Benezeth Christopher,na hatimaye alijihakikishia kurudi Tanzania kwani hakuna mtu yeyote ataweza kumfahamu.
“Pesa zangu zote,zililowa wakati napambana na nyoka mtoni zikiwa ndani ya begi,sitoweza kuishi huku Marekani …inabidi nirudi Tanzania ” ,Paul aliongea huku akivaa miwani pamoja na suti yake nyeusi ,suti iliyomfanya kupewa jina la “THE BLACK KILLER ” (muuaji mweusi) kutokana na kupendelea kuivaa kila anapofanya mauaji na kisha kuanza kuitafuta njia ya kutoka msituni .
…………………………….…
Godfrey, Jonson pamoja na Jacline wanaponea chupuchupu mikononi mwa wanyama wakali wa msitu wa Amazon, huku askari wote wa Kimarekani wakipoteza maisha na wengine kukimbia. “Mmeusikia mlipuko huo wa bomu, twendeni tukashuhudie kilichotokea……tunaweza fahamu chochote “,Jonson aliwaeleza wenzake huku kila mmoja akijiweka tayali kwa mapambano muda wowote, kutokana na wanyama wakali kuwanyemelea kwa ajili ya kujipatia kitoweo.
Godfrey na wenzake wanaelekea sehemu mlipuko wa bomu ulipotokea, na ghafla wanakutana na mzee aliyekuwa amevalia nguo pamoja na miwani ya Paul Agustino na kuwafanya wajulize maswali mengi, Lakini kwa upande wa Paul hakuonesha kushituka sana baada ya kuonana nao lakini alitumia lugha ya kingereza kujitetea ili asiweze kugundulika hasa pale ambapo angetumia Kiswahili.
“My name is mr Joseph, I came into this forest to conduct some research but suddenly the wild animals attacked me ……so i used bomb to kill them “(Jina langu naitwa mr Joseph, nilikuja ndani ya msitu huu kufanya utafiti … lakini ghafla nilivamiwa na wanyama wakali …kwahyo nilitumia bomu kuwaua) Paul alijitetea kwa kujiamini sana, hali iliyowafanya wakina Godfrey kushusha siraha zao walizokuwa wamemuwekea kichwani Paul na kisha kumruhusu kuendelea na safari yake.
“OK, but you have to leave from this forest, it is very dangerous ” ,(sawa, lakini unatakiwa kuondoka ndani ya msitu huu, ni hatari sana) Jacline alimjibu Paul na kisha wakaanza kuelekea sehemu bomu lilipotokea kushuhudia, huku Paul yeye akitokomea na kupotea haraka sana baada ya kuruhusiwa kuondoka. Jacline hakuweza kumtambua mzee yule kuwa ndiye Paul mwanaume pekee aliyempenda na kumpa penzi, bila kutambua kuwa aliweza kumpatia penzi muuaji bwana Paul Agustino.
“Mungu wangu, hawa wanyama aliowaua ndio hizi maiti za watu? Na hii mashine ya upasuaji imefikaje hapa? ……Mmmh yule tuliyekutana naye atakua ndiye Paul mwenyewe kabadilishwa sura kwa mara nyingine tena, siunaona mashine hiyo ya upasuaji na pia si unaona kitambulisho chake hichi hapa kakisahau ” ,Jacline msichana ambaye aliweza kuzitambua mashine za upasuaji kutokana na kupitia kozi mbalimbali za afya akiwa jeshini, aliongea huku akizitazama mashine hizo zikiwa zimeharibika kutokana na mlipuko uliokuwa umetokea …aliendelea kuwaeleza wenzake huku akionyesha kitambulisho cha Paul alichokiokota chini.
Paul anabahatisha mtumbwi uliokuwa umepaki ufukweni mwa mto Amazon, mto uliopita katikati ya msitu na kisha kuutumia mtumbwi huo kutoka ndani ya msitu huo, huku akifurahi na kujiona mshindi dhidi ya Godfrey na wenzake waliotumwa kumkamata.
Bwana Sarehe Athuman aliyewahi kuwa waziri wa ulinzi kabla ya kuvuliwa cheo hicho kutokana na tuhuma nzito ya kuhusika na mauaji kumtafuna na kuwekwa rumande, anakutwa akiwa amekufa ndani ya gereza la Segerea jijini Dar es salaam huku povu zito likitoka mdomoni mwake. Kulingana na ripoti za madaktari, walingundua kifo cha bwana Sarehe kilisababishwa na sumu kali iliyokuwa imewekwa katika chakula chake, maisha yake yalishindwa kuokolewa kwani sumu hiyo kali huua muda mfupi tu baada ya kuingia katika mfumo wa damu. “Sumu hii inaonekana imeathiri tumbo lake, kwani utumbo wake unaonekana kukatika katika kutokana na kemikali hiyo baada ya kuila ikiwa imechanganyikana na chakula alichokula “,dokta alisikika akitoa ripoti ya uchunguzi, kuhusu chanzo cha kifo cha mr Sarehe, kilichotokea katika mazingira ya kutatanisha.
“Hapa sasa, nitaishi kwa uhuru hapa Tanzania …pesa ndo kila kitu bwana …ningezubaa yule mshenzi angenitaja tu baadae “,mfanyabiashara tajiri sana Tanzania anayejihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya pamoja na madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee, bwana Benedict Mathayo, anazungumza maneno ya kujisifu baada ya kutoa rushwa kwa walinzi wa magereza na kukubali kumuwekea sumu Mr Sarehe kwenye chakula chake, na kisha kumsababishia mauti. Bwana Sarehe alishirikina na Benedict pamoja na Paul Agustino kutega bomu katika sherehe ya uhuru wa Tanzania ili kumuua raisi, na kisha waweze kuipindua nchi. Benedict aliamua kumuua kwa sumu mr Sarehe, ili asiweze kumtaja kuwa na yeye alikuwa ni muhusika wa mauaji yale ya maelfu ya watu na viongozi wakubwa yaliyoyokea baada ya mlipuko wa bomu katika uwanja wa taifa, huku raisi akibaki mlemavu wa miguu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
…………………………………
Paul baada ya kupiga makasia kwa muda mrefu katika mto Amazon, anajikuta akitokea nchi nyingine kabisa tofauti na Marekani. “Mmmmh ni nchi gani nzuri kiasi hiki “,Paul alizungumza mwenyewe huku akishangaa ufukwe mzuri wa nchi ngeni aliyoifikia baada ya kupiga makasia kwa wiki nzima ndani ya maji katika mto Amazon. “Welcome Mexico”(karibu Mexico) msichana mrembo aliyekuwa akivua samaki ufukweni mwa mto Amazon alimkaribisha ugenini bwana Paul baada ya kumuona akishangaa sana mazingira ya nchi ya Mexico, msichana yule alionekana kulindwa na walinzi wengi wenye siraha nzito kama bunduki pamoja na siraha za jadi, ishara iliyomfanya Paul kuwa makini na msichana yule kwani aliamini atakuwa ni malkia wa eneo lile. “Thank you my sister, “(asante sana dada yangu) Paul alimjibu msichana yule, na ghafla alidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na njaa kali aliyokuwa nayo kwa muda wa wiki nzima. Baada ya Paul kuzimia, msichana yule mrembo aliwaamrisha walinzi wake kumpatia msaada Paul na kisha kumpeleka katika kambi yao waliyokuwa wakiishi.
Jacline na wenzake wakiwa katika hali ya uchovu sana, wanajikuta wakitokea katika ufukwe wa mto Amazon na kuona nyayo za miguu za Paul Agustino. “Bila shaka mtu huyu kaelekea nchi ya Mexico, siunaona nyayo zake za miguu alizopita ……na mto huu bila kukosea unapita nchi hiyo”,Godfrey aliongea huku akitazama nyayo za miguu zilizoachwa na Paul. “Tupumzikeni hapa, kisha tutaendelea na safari kesho …mimi nimechoka “,Jacline alitoa wazo lililoungwa mkono na kila mmoja kutokana na uchovu mkubwa waliokuwa nao.
…………………………………
“Who are you ??”,(wewe ni nani), Paul alimuulza msichana mrembo baada ya kuzinduka na kisha kupewa chakula na kukibugia kama kichaa, “Aim the queen of this land “,(mimi ni malikia wa eneo hili) mrembo yule aliyekuwa amevalia mavazi ya asili huku akizungukwa na walinzi, alimjibu Paul na kisha kuketi vizuri kwa ajili ya mazungumzo. “Who are you ??( wewe ni nani?) ,malikia yule alimuulza Paul swali, na kwa kujiamini sana Paul aliweza kumdanganya malikia yule bila uongo wake kugundulika. “Aim from Tanzania, our plane got an accident when I was flying back home from Dubai …all passengers died but only my self who is still alive……please can you help me to go back home”,(ninatokea Tanzania, ndege yetu ilipata ajari wakati natoka Dubai kurudi nyumbani Tanzania ……abiria wote walikufa lakini mimi peke yangu ndio bado ninaishi ……tafadhali unaweza kunisaidia nirudi nyumbani) Paul alimweleza malikia yule kwa hisia na uchungu mkubwa, hali iliyomfanya malikia yule kuwa na huruma na kutaka kumsaidia Paul kurudi Tanzania.
“I will help you by giving you gords, you will sell them and get transport fee …”,(nitakusaidia kwa kukupatia dhahabu, utaziuza na utapata nauli) Malikia yule alimweleza Paul namna atakavyomsaidia, huku Paul mawazo yake yakihama kabisa na kufikiria namna ya kuua jeshi la malikia yule na kisha kutokomea na dhahabu zote zilizomilikiwa na jamii ile.
Safari inakua ngumu sana katika mto wa Amazon, Godfrey na wenzake wanajikuta katika wakati mgumu baada ya upepo mkali kuvuma na kusababisha mawimbi makubwa kuupiga na kuusambalatisha mtumbwi waliokuwa wameupanda..”Vuta pumzi… jitahidi, ukikata tamaa utasombwa na maji „” Godfrey alimtia moyo Jacline aliyekuwa anaonekana kuzidiwa na mawimbi, hali ambayo ingepelekea Jacline kuzama kama angeishiwa pumzi kabisa na kushindwa kuogelea.Japokuwa wote walikua hodari sana katika kuogelea, lakini walijikuta wakizidiwa na nguvu ya mawimbi huku kila mmoja akitafuta njia ya kuokoa maisha yake.
Paul Agustino jambazi la kimataifa, anafanikiwa kuwazidi nguvu askari wa malikia wa eneo lile la kisiwa kilicho katika nchi ya Mexico, baada ya mapambano makali kutokea na kisha askari wengi wa malikia kupoteza maisha huku Paul akitoroka na dhahabu nyingi zilizokuwa zikimilikiwa na jamii ile. “Siku sote mimi ni mshindi, Hahaha “,Paul aliongea kwa sauti huku akicheka kwa furaha na kuwafanya watu waliokuwa karibu naye kumshangaa, kwani walimuona kama kichaa kutokana na yeye kuongea peke yake.
“Give me ten billions, “,(Nipatieni bilioni kumi), Paul alitaja kiasi cha pesa alichokitaka, baada ya kwenda kuuza dhahabu alizoziiba katika sehemu ya kuuzia vito vya thamani iliyopo katika jiji la Mexiko„kutokana na dhahabu alizokuwa nazo kuwa na thamani kubwa zaidi ya pesa aliyoitaja, alilipwa pesa hiyo haraka sana na kisha aliweza kutoweka eneo lile. Bila kupoteza muda, Paul alielekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mexiko, tayali kwa ajili ya kusafili kurudi Tanzania siku iliyofuata.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Malikia wa eneo la kisiwa kilichoko Ufukweni katika nchi ya Mexiko, anawakuta vijana watatu ufukweni wakiwa wamepoteza fahamu ,akiwa ameenda kuvua samaki kama kawaida yake. Kutokana na hasira aliyokuwa nayo, baada ya kuibiwa dhahabu zake huku vijana wake wengi wakijeruhiwa na wengine kupoteza maisha, hakuwa na huruma na kina Godfrey bali aliwakamata na kisha kuwafunga katika gereza lake. Huruma na uaminifu wa malikia yule kwa vijana wale watatu, unazidi kupotea baada ya kugundua walikuwa na siraha pamoja na baadhi ya nyaraka za kijeshi zilizokuwa zimelowa maji baada ya kuwakagua katika mifuko yao.
“What do you want in this land, are you spies? “,(mnataka nini katika ardhi hii, nynyi ni wapelelezi?) Malikia yule aliuliza swali kwa hasira, huku jeshi lake likiwa limewanyoshea siraha wakina Jonson, Godfrey pamoja na Jacline. “,We are soldiers from Tanzania, we are here looking for the killer, who killed thousands of people in our country “,(sisi ni askari kutoka Tanzania, tuko hapa kwa ajili ya kumtafuta muuaji aliyeua maelfu ya watu katika nchi yetu) Godfrey alijibu swali la malikia yule, jibu ambalo lilimfanya malikia yule kukumbuka mauaji aliyoyafanya Paul katika ardhi yake na kuamini kweli alikuwa ni jambazi. “There is an old man from Tanzania, has killed my people and has disappeared with my gords …”,(kuna mzee kutokea Tanzania, kaua watu wangu na kutoweka na dhahabu zangu) malikia yule aliongea huku akiamini kuwa mtu aliyehusika na wizi wa dhahabu zake, ndo yule aliyekuwa akitafutwa kwa tuhuma za mauaji. “,Where do you think ,he has gone? “(Unafikilia kaenda wapi?) Jonson alimuulza malikia yule, huku askari wa malikia wakiwafungua kamba na kuwatoa katika gereza lao baada ya kujiaminisha kuwa sio watu wabaya. “,He told me, he want to go back Tanzania …”,(aliniambia, anataka kurudi Tanzania) malikia yule aliongea huku akiamuru chakula kizuri kuletwa, kwa ajili ya Godfrey na wenzake.
Jua kali liliwaka huku moshi wa viwanda mbalimbali vikilipamba anga la jiji la Dar es salaam, ndege kubwa aina ya Boeing 777,Ndege ambayo Paul alipenda kuitumia katika safari zake, iliikanyaga ardhi ya Tanzania. “Nafurahi kurudi nyumbani, ni miaka miwili tu lakini nchi imeendelea sana “,Paul aliongea huku akishangaa uwanja mzuri wa ndege wa mwalimu Nyerere ukiwa unapendeza sana baada ya kufanyiwa marekebisho. Paul bila kupoteza muda anachukua taksi na kisha kuelekea katika hoteli ya kitarii ya sea cliff, hoteli ambayo aliiona nzuri kwake bila kujali gharama kubwa za mahali pale.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
godfrey na wenzake wanafanya mawasiliano na serikali ya Tanzania, baada ya kufika katika jiji la Mexiko lililopo katika nchi ya Mexiko wakitokea katika kisiwa kilichoko ufukweni mwa nchi hiyo, kisiwa kilichotawaliwa na malikia aliyekuwa na huruma sana na kujizolea sifa kedekede katika nchi ya Mexiko kutokana na kuwasaidia watu mbalimbali. “,Tayali nimeshampatia taarifa waziri wa ulinzi wa Tanzania, pamoja na raisi kuhusu kurudi kwa Paul nchini Tanzania akiwa na sura bandia “,Paul aliongea huku akifurahia na wenzake kurudi Tanzania siku iliyofuata.
Siri ya Jacline ya kuwa na ujauzito inafichuka, huku muhusika akiwa hajulikani. “,Twambie muhusika ni nani?, “sisi ni rafiki zako, na pia ni askari wenzako, Jonson aliongea huku akilishangaa tumbo la Jacline lililokuwa limeanza kuwa kubwa. “,Mimi niliziona dalili zako za ujauzito muda mrefu, lakini nilishindwa kukuuliza kutokana na majukumu kutubana “,Godfrey pia alisikika akiongea huku akipanga vitu kwenye begi, kwa ajili ya safari ya kurudi Tanzania. “,Mtafahamu kila kitu muda ukifika, huu sio muda sahihi kuzungumzia swala hilo “,Jacline alijibu maswali aliyokuwa ameulizwa,huku akionekana kukelwa sana na maswali aliyoulizwa.
Tetesi za Paul kurudi nchini Tanzania zinasambaa kila mahali katika jiji la Dar es salaam, huku barabara mbalimbali za mikoani zikifungwa na kisha kila gari lililoingia na kutoka katika jiji hilo liliweza kukaguliwa kwa umakini sana. “Hii ni taarifa ya habari kutoka ITV, jambazi Paul Agustino yasemekana karudi nchini Tanzania huku akiwa na sura nyingine kabisa baada ya kuibadilisha…na muonekano wake uko kama unavyoonekana katika picha “,mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV, alitangaza habari iliyogusa hisia za wengi huku akiwasihi wananchi kutoa taarifa polisi mara watakapomuona popote pale. “Mungu wangu kumbe tunafuga jambazi, siku fahamu kama yule babu aliyekuja hapa jana ndio Paul Agustino …jambazi sugu “,meneja wa hoteli ya sea cleaf aliongea huku akibonyeza simu yake ya mezani kwa ajili ya kuwapigia polisi.
“Duuh tayali mambo yalishahalibika……”,Paul aliongea baada ya kushtushwa na taarifa ya habari aliyoisikia, huku akijiandaa kwa ajili ya kutoweka haraka sana eneo lile. “Huyu mpuuzi bila Shaka analengo baya na mimi, kwanini kaja Tanzania bila kunipatia taarifa “,mfanyabiashara Benedict alilalamika baada ya kusikia taarifa ya habari, kuhusu ujio wa Paul katika nchi ya Tanzania na kumfanya kuutilia hofu ujio huo.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Godfrey na wenzake wanafika nchini Tanzania na bila kupumzika wanajikuta katika jukumu zito la kwenda kumkamata Paul, baada ya kupokea simu kwa siri kutoka katika hoteli ya kitalii ya Sea cleaf. “,Chukueni kila siraha mnayoona itawasaidia, lakini pia hakikisheni barabara zote za jiji la Dar es salaam zinafungwa na kukagua kila gari linalopita kwa umakini mkubwa “, raisi wa Tanzania alitoa amri kwa majeshi yake ya ulinzi, huku akiwapa majukumu askari watatu wakiongozwa na Godfrey kuhakikisha Paul asiweze kutoroka kwa mala nyingine tena.
Muda si mrefu Paul akiwa ndani ya chumba chake akitafakali namna ya kutoroka, ghafla alisikia sauti ya helikopta za kijeshi zikiizunguka hoteli na kumfanya kufanya maamuzi magumu. “,Duuh kumbe askari wameshaizunguka hoteli, nisipokuwa mjanja hapa nitakamatwa “, Paul aliongea maneno hayo baada ya kuchungulia dirishani, na kuona askari wengi wenye siraha nzito wakiwa wameizunguka hoteli. “Tayali nimeshapata njia ya kutoroka, sijawahi shindwa hata siku moja “,Paul alipata wazo namna ya kutoroka, baada ya kutafakari kwa muda mrefu. Haraka bila kupoteza muda alichukua bastora yake, pamoja na kisu chake na kisha kuanza kupanda juu kabisa ya hoteli.
“Pyuuu ……pyuuu ……pyuu “,Paul alimpiga risasi tatu askari aliyekuwa akija bila kuwa makini, na kisha kumvua nguo zake na kuzivaa yeye ,nguo zile zilimrahishia kutoroka kwani alifanana na askari wa jeshi la polisi. Paul kwa umakini mkubwa alitembea huku akiwa anaua askari kimya kimya na kisha kuifikia helikopta iliyokuwa imepaki juu kabisa ghorofa ya mwisho ikishusha askari polisi wengine kwa ajili ya kuongeza nguvu.
“Adui yuko juu, pandeni ngazi haraka sana ……tukamkamte”,Godfrey aliongea huku akiwa anapandisha ngazi kuelekea juu, akiwa ameongozana na Jonson, Jacline pamoja na askari wengine.
“Mikono juu hapo ulipo, ukijitikisa nasambalatisha ubongo wako …”,Paul aliongea huku akimnyoshea siraha rubani wa ndege ya kijeshi, baada ya kuwamaliza askari wengine. “,Nakuomba ondoa ndege hii, unipeleke sehemu ninayokuelekeza “,Paul aliendelea kuongea, huku dereva wa ndege akitii amri aliyopewa na kuipaisha ndege kutoka eneo lile.
Askari wanafika juu ya ghorofa na kushuhudia helikopta ikipaa kutoka eneo lile, huku maiti za askari zaidi ya mia moja zikiwa zimezagaa eneo lile. Pyuuuh …pyuuu…paah ……paah,, askari wakiongozwa na Godfrey, waliishambulia ndege iliyombeba Paul bila mafanikio, na kushuhudia Paul akifanikiwa kutoroka kwa mala nyingine tena.
…………………………………
Jacline anashindwa kuendelea na oparesheni kabambe ya kumtafuta Paul kutokana na ujauzito wake kuzidi kukua, hali ya afya yake inakua mbaya sana kutokana na kazi ngumu aliyokuwa akiifanya bila kujali ujauzito wake alionao. “Mgonjwa inatakiwa aongezewe damu, bila hivyo atapoteza maisha baada ya masaa ishirini na nne yajayo ” ,daktari wa hospitali ya taifa ya muhimbili alizungumza na Jonson pamoja na Godfrey, akiwaelezea juu ya hali mbaya ya Jacline aliyonayo ,akiwa amefikishwa hospitalini muda mfupi tu baada ya kutoka kumkamata Paul bila mafanikio.
Kutokana na hali mbaya ya Jacline , mtu wa kumtolea damu yenye kuendana na grupu lake anakosekana miongoni mwa Jonson na Godfrey ,bila kutegemea anatokea mtu asiyetegemewa kabisa anajitolea damu na kuyaokoa maisha ya Jacline. “Tafadhali dokta, unaweza kutwambia mtu aliyeyaokoa maisha ya ndugu yetu “,Jonson aliomba kuambiwa mtu aliyemuongezea damu Jacline, lakini dokta aligoma katu katu kumweleza .”Muhusika kakataa kutajwa jina lake, na wala kuiweka wazi sura yake …hivyo basi maadili ya kidaktari hayaniruhusu kufanya hivyo kama muhusika alinikataza “,Dokta alizungumza huku akishikilia msimamo wake, wa kutomtaja mtu aliyeyaokoa maisha ya Jacline.
Paul baada ya kufanikiwa kutoroka, akiwa ndani ya ndege anamuua rubani kwa kumpiga na bastora kichwani bila huruma na kuusambaratisha ubongo wake. “Nenda kaliwe na samaki nyau wewe”,Paul aliitusi maiti ya rubani yule na kisha kuitupa ndani ya maji katika bahari ya Hindi. Kwa mbali sana Paul alikiona kisiwa kidogo kabla ya kufika Zanzibar, na kuamua kuishusha ndege ili aweze kuificha eneo lile. “Bila shaka naweza kuificha helikopta hii katika kisiwa hiki, nirudi Dar es salaam haraka sana nikamuue Benedict, mtu pekee ambaye anafahamu siri zangu nyingi sana baada ya hapo nitarudi kuichukua ndege hii na kutokomea “.Paul aliongea huku akiishusha ndege katikati ya msitu katika kisiwa kidogo kilichopo bahari ya Hindi, na kisha kuifunika na magome ya maiti ili isiweze kuonekana.
Paul akiwa katika kisiwa ambacho hakikuwa mbali sana na Dar es salaam, alisubili jua lizame ili iwe rahisi yeye kuingia jijini bila kufahamika. “Waaooh ……kweli nina bahati spidi boti hii ni ya nani?”,Paul aliongea huku akiishangaa spidi boti iliyokuwa imechakaa sana,kutokana na kutotumika kwa muda mrefu, ikiwa imetelekezwa katika kisiwa kile kidogo. Paul alitumia ujuzi wake kuirekebisha mpaka ikawaka, na kisha kuondoka nayo kuelekea Dar es salaam. “Hapa dakika ishirini tu, nitakua mjini nimeshafika tayali “,Paul aliongea huku akiongeza spidi ya boti ile, ili kukamilisha lengo lake kabla hapajakucha na kisha kurudi katika kisiwa kile.
Paul baada ya kufika Dar es salaam, akiwa amevalia koti kubwa lililofunika mwili wake wote, pamoja na kofia iliyouziba uso wake usionekane anashtushwa na taarifa mbaya zilizoenea mjini juu ya afya ya Jacline, msichana aliyetokea kumpenda sana. Huruma pamoja na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Jacline, yanamsukuma kwenda hospitalini kujitolea damu ili kuokoa maisha yake, kama damu yake itakuwa grupu moja na damu ya Jacline.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hongera babu, baada ya kukupima tumegundua damu yako inafaa sana kwa ajili ya kuokoa maisha ya mgonjwa “,daktari aliongea huku akidhania Paul alikuwa ni mzee, kutokana na sura yake kukunjamana huku baadhi ya mnvi zikionekana sehemu ya nyuma ya kichwa kwani Paul alivaa kofia na kuivuta kwa mbele ili kufunika uso wake asiweze kutambulika. “Asante kwa kuokoa maisha ya mgonjwa, lakini jina lako ni nani “,daktari aliongea huku akifunga madirisha na kushusha pazia baada ya Paul kumaliza kujitolea damu, kwani giza lilikuwa tayali limeshakua nene na ilikuwa yapata saa tano usiku. “Sitoweza kutaja jina langu, na wala kukuonesha sura yangu ……lakini msichana huyu akiamka muoneshe kipande hiki kidogo cha ua “, Paul aliongea huku akimkabidhi dokta ua na kisha kutokomea..
…………………………………
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment