Simulizi : Muuaji Mweusi (The Black Killer)
Sehemu Ya Nne (4)
Baada ya dokta kugoma kuwambia Godfrey na Jonson kuhusu mtu aliyemuongezea damu Jacline, na kisha kuokoa maisha yake …bila kutegemea Jacline anapata fahamu na kuanza kujishangaa kwani hakutambua kafikaje hospitalini. “Nimefikaje hapa hospitalini, vipi muuaji kakamatwa “,Jacline aliongea huku akishangaa mazingira yale ya hospitali, na kisha kuwauliza kina Jonson kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa baada ya kuwaona. “,Usijali kuwa na amani, utafahamu kila kitu “,daktari aliongea na kisha kumsimulia Jacline kila kitu baada ya kuwaomba wakina Jonson kutoka nje kwa muda, lakini Jacline alianza kulia kwa uchungu huku akiushika ujauzito wake baada ya kugundua kuwa mwanaume katili na muuaji, aliyempenda sana bila kumtambua kaweza kuokoa maisha yake baada ya kuoneshwa na daktari ua, ua ambalo lilichumwa eneo ambalo Jacline na Paul Agustino walipokutana kwa mara ya kwanza nje ya hoteli ya Kasabranka nchini Marekani.
Walinzi wakiwa wamelizunguka jengo zuri la kifahari eneo la Masaki wakiwa na siraha zao, wanajikuta katika usingizi mzito baada ya Paul kuwapulizia dawa ya usingizi kimya kimya.Baada ya kuhakikisha hakuna mlinzi hata mmoja alikuwa macho kwa wakati ule, aliingia chumbani kwa mfanyabiashara Benedict na kumkuta akifanya ufuska na kijana mmoja mwenye tabia za kike (shoga),kwa hasira Paul alimuua kijana yule kwa kumpiga risasi nyingi sana. “Pyuuu, pyuuu, pyuuu, pyuuu……”,milio ya risasi ilisikika na kumtoboa toboa punga yule sehemu mbalimbali za mwili. “Shenzi kabisa wewe, hiyo adhabu ndiyo inayowafaa wanaume wote wenye tabia kama wewe. ” Paul alimlaani mwanaume yule baada ya kumuua, na kisha kumnyoshea bastora kichwani mfanyabiashara maarufu na mtu mzima sana ambaye huwezi kutegemea kama anaweza kufanya upuuzi ule wa mapenzi ya jinsia moja.
“Sasa hii ni zamu yako, wewe ulimuua mr Sarehe ili kujilinda, na mimi nakuua wewe ili nijilinde nisikamatwe ” ,Paul aliongea kwa sauti isiyokuwa na utani kwa yale aliyokuwa akiongea, bila kupoteza muda alimpiga risasi kichwani mr Benedict na kisha kutoweka eneo lile kabla ya Polisi kufika kutokana na milio ya risasi kusikika mtaani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jacline akiwa hospitalini anajikuta akijifungua mtoto wa kiume, kwani miezi tisa ilikuwa tayali imetimia. “,Nimejifungua salama, lakini naamini mtoto wangu atatengwa kama akigundulika ni mtoto wa jambazi Paul ” ,askari wa kike Jackine aliongea moyoni mwake, huku akimtazama mtoto wake aliyekuwa ametokea kufanana sana na sura halisi ya Paul Agustino kabla hajafanyiwa upasuaji.
Bila kutegemea Paul anajikuta mikononi mwa Polisi, kwani mr Benedict alituma ujumbe haraka sana Polisi kwa siri kuhusu kutaka kuuawa na Paul Agustino, hivyo Polisi waliweza kuweka kamera za ulinzi na kuziunganisha makao makuu ya jeshi la Polisi Hivyo baada ya Paul kuvamia nyumba ya Benedict, askari waliweza kumwona kupitia kamera zile zilizokuwa zimefungwa katika nyumba ya Benedict. “Utatukoma mpuuzi wewe, tumekutafuta sana, “Godfrey aliongea huku akimpiga teke zito Paul, teke lililomfanya kugaagaa kwani mikono yake ilikua imefungwa pingu hivyo hakuweza kujitetea. “Yaaala………aa”,Kelele za maumivu zilisikika kutoka kwa Paul, baada ya kukatwa kidole kimoja cha mguuni na Jonson bila huruma ,kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya kumpania kwa muda mrefu.
Habari za kukamatwa kwa Paul zinakua gumzo nchini Tanzania ,huku watu wengi wakitamani kuiona sura yake uso kwa uso bila kuambiwa na mtu yeyote. Vyombo vya habari hasa magazeti yalipambwa na habari iliyohusu kukamatwa kwa Paul, na kuwavutia wasomaji wengi. “Huyu jambazi anyongwe tu, kaua watu wengi sana,”mmoja wa wananchi alisikika akiongea huku akitazama magazeti yaliyokuwa yakitembezwa na kuuzwa na machinga. “Mwenye pesa sio mwenzako, utashangaa kusikia jamaa katoroka au kaachiwa huru “,raia mwingine alisikika akimjibu mwenzake, na kisha kuondoka eneo lile.
Jacline anamtazama Paul kwa huruma akiwa mahabusu, akisubili siku yake ya hukumu huku damu nyingi na madonda yakiutapakaa mwili wake.”Pole sana Paul, nimejifungua mtoto wa kiume ……mtoto ambaye ni damu yako lakini mwanangu hatabahatika kuiona sura ya baba yake kutokana na wewe kunyongwa kwa dhambi ulizozifanya”,Jacline aliongea huku akiwa ameshikilia vyuma vya gereza la Segerea, akiitazama sura ya Paul iliyoonekana kutafakali mambo mengi sana kwa wakati ule.
“Kama nikifa naomba umtunze sana mwanangu, na hakikisha hawi mtu mbaya kama baba yake na wala usije kumwambia lolote kuhusu baba yake “,Paul alizungumza maneno yalimchoma sana Jacline, na kuifanya sura yake kulowa machozi kwa huzuni. Lakini kutokana na mapenzi makubwa Jacline aliyekuwa nayo, anajikuta akiweka uaskari pembeni na kusahau maovu yote Paul aliyoyafanya na kumsaidia kutoroka mahabusu.
“Naskia kuna mfuniko wa chemba ya taka humo ndani ,unaopeleka maji taka baharini ,tumia njia hiyo kuondoka mahali hapa na kisha ondoka Dar es salaam haraka sana “,Jacline alimpatia siri Paul iliyomuwezesha kutoroka eneo lile.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya ukimya ikiwa imetawala eneo lote la gereza la Segerea, huku wafungwa wengi pamoja na askari waliokuwa lindo, wakiwa wanakoloma kutokana na uchovu. Paul anafanikiwa kufungua mfuniko alioelekezwa na Jacline, baada ya kuhangaika kwa muda mrefu. Bila kupoteza muda aliingia ndani ya shimo lile na kisha kusombwa na maji taka yaliyokuwa yakipita kwa kasi, na kisha kwenda kumtupia baharini.
Taarifa za Paul kutoroka gerezani zinatangazwa,baada ya kuamka na kukuta akiwa hayumo mahabusu asubuhi, huku askari wengi waliokuwa zamu wakiachishwa kazi kwa uzembe mkubwa walioufanya. “Naamini Jacline kahusika na kutoroka kwake, hakuna mtu yeyote aliyeifahamu njia hii zaidi yake na nilimuona akiongea naye jana “,Jonson aliongea huku akionekana kukasirishwa na tukio lile. “Kaamua kuweka mapenzi mbele, mi nilijua tu kuwa hili litatokea ” ,Godfrey aliongea huku akitoa amri ya Jacline kukamatwa haraka sana, kujibu tuhuma za kuhusika na utorokaji wa Paul mahabusu.
“Hahahaa, we kichaa unanuka sana hebu toka hapa “,mvuvi mmoja alicheka sana huku akiziba pua yake kutokana na harufu mbaya ya Paul, baada ya kumwona akiwa amechakaa tope la maji taka.Bila kutegemea alijikuta akipigwa mateke mawili mfululizo, na kuugulia maumivu makubwa. “Chunga mdomo wako, sura zingine siyo za kuchezewa “,Paul aliongea na kumpatia onyo kali mvuvi yule, na kisha kuondoka eneo lile.
Wananchi wenye hasira kali wanamtupia Jacline mawe, huku wengine wakitumia viatu vyao kumuadhibu Jacline kutokana na siri nzito aliyoifichua baada ya kupewa mateso makali bila huruma. “Nastahili mateso haya, mwanangu nikifa naomba usiwe mbaya kama baba yako”,Jacline aliongea na kulia kwa uchungu, baada ya kukubali kuhusika na kumtorosha Paul, huku akikubali kuzaa naye mtoto hali iliyowafanya wananchi kukasirika na swala lile.
“Mungu wangu, nini hiki tena “,askari mmoja alishangazwa baada ya kumkuta Jacline mahabusu akiwa amepoteza maisha, baada ya kujiua kwa kutumia kisu. “Jacline, rudi rafiki yangu rudi………umechukua maamuzi magumu, rudi twende nchini kwetu sitaki kurudi peke yangu “,Jonson aliongea huku akilia kwa uchungu, baada ya kushuhudia maiti ya Jacline huku damu mbichi zikimtoka tumboni mwake.
Kifo cha Jacline kinakuwa gumzo sana nchini Tanzania, huku taratibu za kumuaga kijeshi zikifanyika katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, kwa ajili ya kuisafirisha maiti nchini kwao Afrika ya Kusini. Jonson kwa huzuni alimuaga mwenzake, huku akiapa kulipiza kisasi kwa kuhakikisha Paul anawajibishwa kwani yeye ndiye alikuwa chanzo cha matatizo yote yaliyotokea huku akimtazama mtoto mchanga wa Jacline aliyekabidhiwa na serikali kuishi naye na kumlea.
Paul akiwa na huzuni na kukosa cha kufanya baada ya kufika katika kisiwa kidogo, mahali alipoificha helikopta na ghafla kupokea ujumbe kuhusu kifo cha Jacline kupitia redio ya kijeshi iliyokuwa ndani ya ndege ile baada ya kuiwasha. “Ni nani atakuwa amepewa jukumu la kumlea mwanangu?,” Paul aliongea huku akiwa na mawazo mengi juu ya kifo cha Jacline, huku akifikilia mahali mwanaye atakuwepo, ili akamchukue kwa siri na kisha kumlea mwenyewe.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ghafla Paul anajikuta akitekwa na kundi kubwa la magaidi, bila shaka alifikilia ni maharamia kutoka Somaria kutokana na mavazi yao pamoja na siraha walizokuwa nazo, lakini alishangazwa baada ya kukutanisha macho uso kwa uso, na kiongozi wa kundi lile la kigaidi. “Paul kijana wangu, sura yako umeibadilisha lakini huwezi nidanganya mtu kama mimi ninayekufahamu vizuri, ukishavaa miwani yako tu tayali nakufahamu kwani ni miwani pekee duniani ” ,Waziri Sarehe aliyesemekana amekufa kwa sumu, sumu iliyowekwa na Benedict kwenye chakula chake alipowapatia rushwa askari magereza aliongea huku akimtazama Paul kwa furaha sana. “Ndiyo nafahamu, miwani hii tulimnyanganya mtoto wa malikia wa Uingereza baada ya kumvamia na kuwapiga walinzi wake na kutokomea nayo alipokuja Tanzania kuupanda mlima Kilimanjaro, Lakini imekuaje mpaka ukawa hai wakati niliskia ulikufa kwa sumu “,Paul aliongea huku akimtazama aliyekuwa waziri wa ulinzi Sarehe Athuman, aliyeonekana kumiliki kundi kubwa la kigaidi kwa ajili ya kujalibu kuipindua nchi ya Tanzania kwa mara nyingine tena. “Siwezi kuuawa kirahisi na mtoto mdogo kama yule, nilimpatia pesa daktari na kutoa ripoti ya uongo na kutengeneza maiti yangu feki iliyobadilishiwa sura na kufanana na mimi ” ,Sarehe aliongea huku akifurahi kukutana na Paul kwa mara nyingine tena, kwani alimuamini sana katika shuguli zake.
“Nakuomba tuungane kwa mara nyingine tena, tutimize malengo yetu “mzee Sarehe aliongea huku akiamrisha jeshi lake kushusha siraha zao, kwani walikuwa bado wamemteka Paul na kumnyoshea siraha zao kichwani kwake ili atakapo leta fujo wasambaratishe kichwa chake. Lakini kwa wakati wote ambao Sarehe aliyazungumza hayo, Paul alikua amesimama akiwa amepigwa na butwaa akimtazama waziri yule kwani hakuamini alichokuwa anakiona mbele ya macho yake kuwa mzee Sarehe alikuwa bado hai.
“Inabidi nimkubalie, lakini nitamuua muda wowote haraka sana na mimi niwe kiongozi wa kundi hili …mzee huyu ni msaliti hawezi kutunza siri, mambo yakiwa mabaya anataja taja tu ilimradi awe huru ” Paul alizungumza maneno yake ambayo aliyatambua yeye mwenyewe, huku akitikisa kichwa kuonesha ishara ya kukubaliana na ombi la waziri muasi bwana Sarehe Athuman.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda siyo mrefu, kundi dogo la kigaidi linalongozwa na Mzee Sarehe, waliongozana na Paul mpaka kwenye kambi yao iliyokuwa ndani ya mahandaki makubwa katika kisiwa ambacho Paul alienda kujificha. “Hapa ndipo mafichoni kwetu, ulipofika mara ya kwanza na helikopta tulikusikia kutokana na mtikisiko, ikabidi tutoke ndani ya mahandaki yetu kwani tulifikili tumevamiwa na askari wa Tanzania, bila kutegemea tulikuta ndege imefichwa kwa majani huku muhusika katoweka, ikabidi tuwe tunafanya dolia kila siku katika eneo lile ili tumtambue mtu aliyeweza kuficha helikopta katika himaya yetu “,mzee Sarehe aliongea maelezo marefu sana, huku akimkalibisha Paul ndani ya mapango waliyoyatumia kwa ajili ya kujificha dhidi ya maadui. “Duuu, Asante sana mkuu ,naamini kila kitu kitakwenda sawa ” Paul aliongea huku akiwaza na kuwazua namna ya kumuua Sarehe ili yeye ndo awe kiongozi mkuu wa himaya ile.
Siku moja Paul akiwa anafanya mazoezi peke yake nje ya mahandaki yao, katikati ya msitu ulioko ndani ya kisiwa kidogo kilichopo katika bahari ya Hindi.Ghafla Paul alikutanisha macho uso kwa uso na joka kubwa aina ya “black mamba “(koboko), likiwa limeinua kichwa juu na kisha kusimama tayali kwa ajili ya kumlukia na kumshambulia Paul. “Hapa nijifanye sijaliona, kutokana na njaa zake ,likinilukia tu nitalikata kichwa haraka sana “,Paul aliwaza kichwani haraka sana kama umeme, na kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha nyoka yule baada ya nyoka kuluka hewani kwa ajili ya kumuangamiza .”Hapa tayali, Sarehe hana jipya mbele yangu mimi ndo muuaji mweusi kama navyofahamika ,mimi Siyo Benedict sitoshindwa kumuua”,Paul aliongea huku akikamua sumu ya nyoka yule na kuiweka katika kichupa kidogo cha maji ya kunywa, huku akifurahi sana kwani aliamini mzee Sarehe hatoweza kuepuka kifo, kwani sumu ya nyoka huyo aina ya koboko ndo sumu kali sana kuliko nyoka wote ulimwenguni na huua kabla ya masaa ishirini na nne baada ya kuingia katika mfumo wa damu.
“Kuanzia leo mimi ndiyo kiongozi wenu ,”Paul alitoa amri mbele ya kundi kubwa la jeshi la mzee Sarehe, baada ya kuwatandika na kuwajeruhi vibaya huku wengine wakipoteza maisha, baada ya kutaka kumpinga na kulipiza kisasi walipongundua Paul kahusika na mauaji ya mkuu wao mzee Sarehe, kwa kutumia sumu ya nyoka iliyowekwa ndani ya maji ya kunywa na kisha kumpatia mzee Sarehe. “Ndiyo mkuu “,sauti kubwa yenye unyonge, hasira na chuki ilisikika ikitamka maneno ya kukubaliana na uongozi mpya wa bwana Paul Agustino.
"Samani mkuu, tumeweza kupata mawasiliano ya ndege yetu iliyotekwa na Paul, kompyuta inaonesha ndege yetu iko katika kisiwa kidogo ndani ya bahari ya Hindi, bila shaka mtuhumiwa atakuwepo mahali hapo " ,mmoja wa askari katika kitengo cha mawasiliano, alitoa ripoti yake ya uchunguzi kwa kiongozi wao bwana Godfrey. "Inatakiwa tuvamie eneo hilo kwa siri, haitakiwi umwambie mtu yeyote, tutatangulia wawili tu mimi na Jonson, lakini nyie mtakuja baadaye " ,Godfrey alimjibu askari yule aliyempatia taarifa hiyo, huku akijiandaa kwa ajili ya kuelekea katika kisiwa hicho haraka sana.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa upande wake Paul, ngome yake iliendelea kuwa tajiri, kwani walizivamia meli za abiria na mizigo katika eneo lote la bahari ya Hindi, na kupora mali mbalimbali pamoja na vito vya thamani na kisha kuua abiria waliokuwa ndani ya meli hizo. Bila kutambulika, waliweza kuendelea na shughuli zao za kikatili huku wakitumia rushwa kama moja ya siraha za kujilinda. "Meli yetu moja ya mizigo imetekwa na maharamia baharini, wameiba kila kitu na kisha kuua watu wote waliokuwa ndani ya meli hiyo ", kiongozi mmoja wa ngazi za juu katika serikali ya Kenya, alisikika akitoa taarifa mbaya kuhusu upotevu wa nyara za serikali zilizoibiwa huku wahusika wakitokomea bila kufanikiwa kukamatwa, na kuomba askari wake kuweka ulinzi imara ili kupambana na maharamia wanaoteka meli zao.
…………………………………
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment