Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MUUAJI MWEUSI (THE BLACK KILLER) - 5









    Simulizi : Muuaji Mweusi (The Black Killer)

    Sehemu Ya Tano (5)





    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Godfrey na Jonson wanafanikiwa kufika katika kisiwa kidogo kwa kutumia meli ya kijeshi inayosafiri ndani ya maji aina ya Nyambizi (submarine), na kisha kuingia ndani ya kisiwa ,kisiwa ambacho yalikuwa maficho ya Siri ya Paul bila kugundulika na mtu yeyote. "Tunatakiwa tuue kimya kimya, tukitumia bunduki tutawashitua, na bila shaka kazi itakua ngumu zaidi ",Jonson aliongea huku akitumia mikono yake kunyonga baadhi ya walinzi katika ngome ya Paul, na kisha kusonga mbele lakini bila kutegemea walijikuta wakizunguka eneo lote la kisiwa bila kugundua chochote zaidi ya kukutana na magaidi wachache wa jeshi la Paul, na kisha kuwaua. "Nasikia muungurumo wa mashine mbalimbali pamoja na magari chini ya ardhi, bila shaka kambi yao iko chini ya ardhi ",Godfrey aliongea na Jonson, huku wakiitafuta njia ya kuingia ndani ya mahandaki kwa ajili ya kumkamata Paul Agustino. "Hawa washenzi wananifatilia sana, leo ndo mwisho wao ",Paul aliongea huku akiliongoza jeshi lake kutoka nje haraka sana kwa ajili ya kupambana na askari ambao tayali wamekwishavamia eneo lao.



    "Piga mpuuzi huyooo, muue kabisa ",Godfrey aliongea, baada ya Paul kukutana na mateke mawili mfululizo na kumfanya kuweweseka baada ya kutoa kichwa chake nje ya ardhi, kipigo kizito akichopigwa na Jonson. "Kila mmoja apambane kwa ajili ya kujinusuru yeye mwenyewe, pamoja na kambi kwa ujumla ",Paul alisikika akitoa amri huku vijana wake wakiwashambulia askari wawili bila mafanikio, kwani waliuawa kwa wingi bila huruma na kumfanya Paul kutafakari namna ya kutoroka eneo lile haraka sana kwani dalili ya kushindwa ilionekana wazi wazi.



    "Kula naye sahani moja mpuuzi huyo, mkimbize asikuache ",Godfrey alimsihi Jonson kumfatilia Paul, baada ya kutimua mbio kuelekea mahali helikopta ilipokua imepaki huku yeye akiendelea kukata vichwa vya askari wa Paul, ambao walionekana kuwa na mbinu duni za kupambana bila kutumia siraha.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Usi…niue, usinika…mate, naomba uch…ukue madini haya na kisha uniruhusu nitoroke ",Paul aliongea kwa maumivu makali baada ya kupigwa risasi za miguuni na Jonson, alipoonekana kukimbia sana na kutaka kutokomea hali iliyomfanya Jonson kutumia bastora yake kumtandika risasi, ili asiweze kutoroka. "Chu…kua, utakua bilion…ea mkubwa wewe usiwe mjinga, unafanya kazi kubwa lakini unalipwa pesa ya mchicha hah…aaha usichezee utajiri kijana",Paul aliendelea kumsisitiza Jonson kukubali rushwa ile,huku akimkejeli kwa maneno makali na mazito sana.



    "Haraka sana potea eneo hili na uende mbali sana ",Jonson alimruhusu Paul kuondoka huku akipokea madini ya almasi pamoja na dhahabu yaliyokuwa ndani ya kimfuko kidogo na kisha kuyaficha. Huku Godfrey akiwa anakuja anakimbia haraka sana ili kumsaidia Jonson kumkamata Paul,lakin hakuamini alichokiona.



    Paul alitembea kwa kujivuta haraka sana na kujitupa ndani ya helikopta, baada ya kupigwa risasi mguuni huku maumivu makali akiyasikia na kisha kuipaisha ndege kutoweka eneo lile. "Yalaa ……nakufaa ,msaada jamani ",Jonson alipiga kelele za uchungu baada ya kujichoma kisu, njia ambayo aliitumia kumdanganya Godfrey asiweze kugundua chochote kuhusu kukubali rushwa na kushindwa kumkamata jambazi katili aliyeua maelfu ya watu.



    "Pole sana jikaze, usichomoe kisu kwanza mpaka madaktari wa huduma ya kwanza wafike",Godfrey alimweleza Jonson baada ya kufika eneo lile na kushuhudia kisu kikiwa tumboni mwake ,huku Paul akitokomea na ndege eneo lile,na kuamini kuwa Paul ndiye aliyehusika kumchoma kisu bwana Jonson,askari kutoka Afrika kusini.



    Kutokana na Paul kuugulia maumivu,anajikuta akishindwa kuongoza ndege vizuri na kuamua kuitupa baharini,ili kuokoa maisha yake."Haya maboya ya kuogelea yatanisaidia,nisipofanya hivi ndege hii italipuka na kuniangamiza kwani imeshaanza kupoteza uelekeo",Paul aliendelea kuzungumza huku akiishusha helikopta chini tayali kwa ajili ya kuitupia baharini .

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    …………………………………



    Ugonjwa wa kansa unaanza kuibuka usoni kwa jambazi Paul,kansa ambayo inasababishwa na upasuaji alioufanya mara mbili mfululizo kuibadilisha sura yake.Vipele vidogo vidogo vinatokea usoni kwake ,huku ngozi ya uso wake ikibadilika na kuwa nyekundu sana ……



    Baada ya Paul kuitupa ndani ya maji ndege ya kijeshi alipokuwa akitoroka,kwani alishindwa kuiongoza vema kutokana na maumivu ya miguu baada ya kupigwa risasi.Maisha yake yanazidi kuwa hatarini, kwani Samaki mkubwa aina ya papa, akiwa mwenye njaa kali anakutana uso kwa uso na Paul akijitahidi kuogelea bila mafanikio. “Oooh ……aim dead! Aim not able to run away “(ooh……nimekufa!  Sina uwezo wa kukimbia)  ,Paul alizungumza kwa huzuni akiwa amekata tamaa ya kupona kutoka mikononi mwa samaki yule, samaki ambaye alikuwa akija kwa kasi kubwa uelekeo ambao Paul alikuwepo ili kumlalua na kujipatia chakula.



    Lakini bila kutegemea, Paul alishangaa kuona papa yule akishambuliwa kwa mishale pamoja na siraha nyingi za kijadi, na kumfanya kugeuka kutazama watu walioweza kufanya hivyo bila mafanikio, kwani nguvu zilikua zimeshamuishia kabisa na kujikuta akipoteza fahamu. “Haraka shukeni kwenye meli mkamkomboe, mkichelewa atazama na kupoteza maisha “,kundi kubwa la wavuvi ambao haikujulikana wametokea wapi, waliamrishwa na bosi wao kujitupa ndani ya maji na kisha kumuokoa Paul,



    aliyeonekana kabisa angeweza kupoteza maisha asipopata msaada, na kisha kuanza safari ya kuelekea bara akapatiwe matibabu haraka sana ili kuyaokoa maisha yake.



    Kundi la wavuvi wa Kitanzania waliomuokoa Paul, wanafika pwani ya Bahari ya Hindi na kuamua kutoa taarifa  kituo cha polisi, na kisha kujipatia mamilioni ya pesa kutoka kwa raisi wa Tanzania, kwani Paul aliweza kutafutwa muda mrefu na serikali bila mafanikio. Lakini kipindi yote hayo yanatokea, wavuvi wale hawakuweza kuamini kama waliyemuokoa na kumripoti kituo cha polisi ndiye jambazi aliyekuwa akitafutwa duniani kote.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ………………………………



    “Samahani Godfrey na serikali Tanzania, pamoja na serikali yangu ya Afrika kusini, nilipokea madini mengi sana kutoka kwa Paul na kumuacha akitoroka huku mimi nikijichoma kisu, nisiweze kugundulika “,Jonson alizungumza kwa huzuni sana huku machozi yakimtoka,akiwa kitandani akijuta kwa kujichoma kisu, kwani kiliathiri ini lake na hivyo angeweza kupoteza maisha muda wowote. “Usilie ndugu yangu, yote ni mipango ya Mungu “,Godfrey alizungumza na kumfuta machozi Jonson, huku akipokea madini yale tayali kwa ajili ya kwenda kuikabidhi serikali, madini ambayo yaliweza kuuzwa na kuwalipa fidia wahanga wa mlipuko ulioua maelfu ya raia.



    ………………………………



    Mahakama ya hakimu mkazi kisutu inafurika maelfu ya watu wakishuhudia hukumu ya jambazi sugu Paul ikitolewa, watu wakiwa na hasira kali wanamtukana Paul huku wengine wakimpiga na viatu vyao, alipokuwa akiingia mahakamani. “Asipohukumiwa kifo, tutamuua wenyewe kwa mikono yetu, “raia mmoja aliongea kwa hasira na kumpiga Paul kwa kiatu chake kichwani,na kusababisha damu nyingi kumvuja kwani ngozi yake ilikuwa laini sana sababu ya maradhi ya kansa aliyonayo.



    “Baba kwanini ulikuwa muuaji kiasi hiki, nikikua nitahakikisha nakuwa askari mwema, nipambane na waovu kama wewe na kulipa wema kwa mabaya yote uliyowatendea walimwengu ” ,mtoto mdogo wa Paul na Jacline, anazungumza kwa huzuni akiwa mahakamani akishuhudia hukumu ya baba yake ikitolewa, baada ya kuelezwa kila kitu na Godfrey japo alikuwa na umri wa miaka saba tu.



    “Mahakama inatoa hukumu ya kunyongwa mpaka kifo kwa Paul Agustino, na iwe fundisho kwa wengine “,jaji alisikika akitoa hukumu kwa Paul, ambaye alikuwa amenyongonyea sana kwa wakati ule kutokana na kansa iliyoiharibu vibaya sura yake kwa vidonda ,lakini kwa upande wa wananchi, walishangilia kwa furaha baada ya kusikia hukumu ikitolewa.



    “Tha…nk you Go…d, i can die now (asa…nte mun…gu, ninaweza kufa sasa) Jonson akiwa hospitalini amelala kitandani akishuhudia hukumu ya Paul ikitolewa na kurushwa katika televisheni, anatabasamu baada ya kufurahishwa na hukumu ile, huku roho yake ikiuacha mwili na kupoteza maisha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Mwanangu nitakukumbuka sana, ishi vizuri na walimwengu na usiwe kama mimi baba yako “,Paul akiwa amemkumbatia mwanaye, analia kwa uchungu na kumpati wosia kabla ya kwenda kunyongwa mpaka kifo. “Usjali baba yangu, nakuahidi sitakuwa kama wewe “,mtoto wa Paul alimwitikia baba yake kwa uchungu huku akiishika sura ya baba yake, iliyokuwa imeharibika vibaya sana.



    *MWISHO ***


0 comments:

Post a Comment

Blog