Search This Blog

Friday 18 November 2022

OKTOBA 15 RAIS ANAENDA KUFA - 1






IMEANDIKWA NA : HASSAN MBONECHE



*********************************************************************************



Simulizi : Oktoba 15 Rais Anaenda Kufa
Sehemu Ya Kwanza (1)


 Sononeko!



Sononeko ni adui miongoni mwa maadui wakubwa katika maisha ya binadamu. Sononeko huondoa furaha, amani ya moyo na huacha mzigo mkubwa wa maumivu akilini. Akili hushindwa kufanya kazi ipasavyo, kama ilivyo kawaida yake na hupelekea maumivu makali. Maumivu yenye kuleta
udhoroteshaji kifikra na madhara mengine pia. Uwepo wa kitu hiki, hata utoaji wa maamuzi nao huwa mbaya, kwani humfanya mtu aondokane na ukawaida na kuingia kwenye lindi la tafakuri juu ya kile kimtatizacho. Endapo ikiwa endelevu siku hadi siku, hugeuka kuwa desturi. Ina maana kwamba huwa mfumo wa maisha.

Sononeko huchangia kupoteza dira ya kimaisha. Kutokana na ufanisi wa utendaji wa mtu hudidimia, kila baada ya muda akumbwapo.



Hali hii ipo kabiru kwa watu wote ulimwenguni. Ila hutofautiana. Wale wenye uwezo haraka sana hutafuta tiba na kuliondoa tatizo. Huenda kwa wataalamu ama hutekeleza kile kinachomtatiza. Kwa kufanya hivi akili hurudi katika hali ya kawaida. Ila kwa wale wasio na uwezo, hugeuka mwiba mkali, ambao huchoma na kuvunjikia mwilini. Ukishavunjikia, hulazimu kutafuta mahali kuketi, ikibidi apate vifaa vya kutolea. Kama vile wembe na pini. Yamkini kwa wakati huo hatokuanavyo, itamlazimu kuvitafuta. Upatikanaji wake ukiwa mgumu, mwiba utaanza kumpatia madhara. Madhara yatayogeuka kuwa sumu kwake. Na sumu hiyo itamuangamiza taratibu, huku dira yake kimaisha itakuwa ndoto tena. Japo zipo baadhi ya ndoto ukiota, hicho ukiotacho hukutokea. ****



Loh!...Maskini!



Mabango mengi yenye jumbe yalipata pamba kuta za majengo mbalimbali na sehemu nyinginezo, yaliyoashiria baadhi ya watu kutoa kero kwa kiongozi wao. Kila kona ya Jiji yalienea, huku jumbe zilizoandikwa zikionekana kuwa kali mno. Yamkini kero hizo walikuwa nazo tangu muda mrefu. Ila muda tu, wa kuzitoa, kwa kipindi cha nyuma walikosa. “TUMEKUCHOKA, NA SERIKALI YAKO PIA TUMEICHOKA, MZEE ACHIA NGAZI HATUITAJI SIASA ZAKO,” Moja miongoni mwa mabango hayo lilisomeka. Wale wenye bango hizo walionekana kuchoshwa na utawala wa kiongozi mkuu wa taifa lao. Ambaye ni Rais. Bila ajizi, mabango yalionekana kutengenezwa na watu wa daraja la chini, wale waishio maisha duni. Hivyo kwa sasa walihitaji kuendelea, baada ya kuona maisha yamewapiga chenga kwa muda mrefu. Kero walizonazo ndizo ziliwafanya waamke kudai haki yao, kutokana na sononeko la muda mrefu walilopata kuwanalo. Ambalo lilizaa sumu na kuanza kuwaangamiza, tena kwa kiasi kikubwa. Wananchi walichoshwa na utendaji wa serikali kwa watu wenye maisha duni. Utendaji wao kwa watu wa namna hii ulipata kuwa kwa kiwango cha chini, hawakuhudumiwa ipasavyo katika huduma mbalimbali wanazohitaji. Walipata huduma zisizo na viwango stahili. Japo kwa wale wenye ubavu kiasi, ina maana wale wenye uwezo kifedha. Matajiri, asilimia kubwa hawakuhathirika sana na utendaji huo, walifurahishwa nao. Hali iliyopelekea kujenga matabaka kati ya wasionacho na walionacho, jambo lililobarikiwa na serikali. Kwa sababu tu, matajiri wanawawezesha kiasi fulani. Ila hawakukosekana baadhi ya matajiri wachukizwao na utendaji wa serikali hiyo. Hasa wale waliokuwa wanakinzana na matakwa nyonyaji yatolewayo.



Ni matajiri wachache walionekana kuwa bega moja na watu walio daraja la chini, wengi waliiogopa serikali, kwa kuhofia kuwekewa vizingiti kwenye biashara zao. Hivyo wakawa sambamba nayo. Hakika! Hii ilikuwa balaa. Wananchi wenye maisha duni hawakuonekana kuwa na thamani, thamani yao pekee ilionekana pindi taifa linaelekea kwenye harakati za uchaguzi. Kipindi hicho walihadawa kwa kila namna, ili tu wafanikishe kuwapatia madaraka wale wachache wanaowania. Baada ya kuwafanikishia kile wanachohitaji na thamani yao huishia hapo. Naam! Hiyo ndiyo Mangaka!

****



Mangaka! Ni nchi iliyo kusini mwa bara la Afrika, lenye ukubwa wa kilomita za mraba laki saba hamsini na tatu elfu kumi na tano, huku ikikadiriwa kuwa na watu milioni ishirini na tano, na mikoa ishirini na nane na wilaya mia moja thelathini na tano. Nchi hii imepakana na nchi zipatazo nne kwa pande tofautitofauti pamoja na bahari ya hindi. Kwa upande wa mashariki imepakana na bahari ya hindi, kusini imepakana na nchi ya Reno, kaskazini nchi ya Gundu na Kabil, wakati magharibi imepakana na nchi ya Hanga. Mji mkuu wake ukiwa ni Lidede. Kwa mara ya kwanza nchi hii ilifahamika baada ya kupata uhuru wake toka kwenye utawala wa mkoloni miaka hamsini na tano iliyopita, baada ya mapigano yaliyopelekea kumwaga damu na hatimaye kufanikiwa. Utawala wao ulianza rasmi Oktoba 15, 1962 kwa kikundi cha kiharakati kilichotambulika kwa jina la MANGAKA MOVEMENT FOR LIBERATION(MML) Kilichoanzishwa na Dkt. Chimpele Mwakatubu kikiwa na wapiganaji ishirini na tano ambao waliweza fanikisha mapigano ya kuondoa utawala wa mkoloni.



Kwa wakati huo kulikuwa na vikundi vyingi vya kiharakati, lakini vyote viliunganisha nguvu zao kwa kikundi cha MML. Hivyo baada ya kupata uhuru waliunda mfumo wa serikali yao, ambayo Rais ndiyo alikuwa kiongozi mkuu wa serikali, kukawa na Mawaziri, ambao walikuwa viongozi wa wizara, Wakuu wa mikoa na wilaya, ambao walikuwa viongozi wa mikoa na wilaya. Serikali hiyo iliongozwa na Dkt. Chimpele Mwakatubu. Ndiyo alikuwa Rais.



Baada ya kuchukua madaraka toka chini ya utawala wa kikoloni, Dkt. Mwakatubu aliandaa harakati mbalimbali za kimaendeleo ambazo zilionekana kwa kiasi kikubwa kufurahisha wanamangaka. Juhudi zake zilionekana, kwani ilifikia wakati walijitegemea kwa baadhi ya bidhaa. Kwani, viwanda vingi vilijengwa, tena vya kila aina ya bidhaa, usafiri ulikuwa wa uhakika na wa kila aina, wa majini, anga na nchi kavu. Tena vyombo vya usafiri hivyo vilikuwa vinamilikiwa na serikali.



Kwa namna moja ama nyingine Dkt. Mwakatubu alihitaji wananchi wake wawe na maisha bora na taifa lipate kuendelea, hivyo alihakikisha anafanya jitihada madhubuti katika hili kwa muda wote ataopata kuwa madarakani, ili akiondoka wananchi wasipate nung'unika.



Kweli!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Miaka ishirini baadaye Dkt. Mwakatubu aliachia ngazi nchi ikaongozwa na mwingine. Ambaye ni Mchungaji Anyeli Kibunda. Huyu naye alikuwa na mikakati yake, ila mingine aliiendeleza ile aliyoiacha Dkt. Mwakatubu, na mingine ile ya Dkt. Mwakatubu aliiua baada ya kuona kwake haitomfaa. Hali ilikuwa namna hii, tawala kadhaa zilipita, na kila tawala ilifanya mambo yake ili iweze kuendeleza taifa. Miaka kadhaa baadaye viliundwa vikundi viwili vingine vya kiharakati, ambavyo waanzilishi wake nao walikuwa wanachama wa kundi tawala kipindi cha awali. Vikundi hivi vilikuwa mahususi kupinga kikundi tawala, baada ya kuona kundi tawala wanafanya mambo mengine sivyo. Vikundi hivyo ni MANGAKA LIBERATION PEOPLE UNITY(MLPU) Na MANGAKA LIBERATION GANG(MALIGA).



MALIGA ndiyo kilikuwa kikundi kikuu cha upinzani, kutokana na kuwa na wanachama wengi, pia nguvu kubwa mtaani. Kundi hili liliongozwa na Kapten Moomoo Mnukia, ambaye alikuwa Afisa wa Jeshi la ukombozi wa wananchi Mangaka (JUWM) Kipindi cha nyuma. Naye alikuwa mmoja miongoni mwa wana MML walioikomboa Mangaka toka kwenye utawala wa mkoloni. Kadri siku zilivyozidi kusonga mbele vikundi hivi vilizidi kukua na kuwa na nguvu maradufu, wananchi nao walitokea kuviamini na kuvipenda pia. Wakati wa chaguzi hawakusita kuwapitia mamlaka waogembea wa kundi hizi, ambao waliamini wanaweza kuwa wakombozi wao kwa kiasi kikubwa. Hali ilikuwa namna hiyo kila uchao.



Pia taifa hili lilitambuliwa kwa mambo mengi katika uso wa Dunia. Kama vile demokrasia, vivutio mbalimbali vya utalii. Mbuga za wanyama, milima mito na vitu vingine kadha wa kadha. Vitu hivi viliipa umaarufu mkubwa, tena umaarufu wa kipekee Duniani kote. Vilevile ilisifika kwa amani na upendo kwa wananchi wake, ijapokuwa kuna matendo mbalimbali ya kiuhalifu hayakwisha fanyika. Wizi, utekaji wa raia na viongozi mbalimbali wenye itikadi kali za kizalendo. Hakika! Ilipata kujijengea jina kila uchao. Hali ya kiuchumi ndani ya taifa haikuwa nzuri kwa upande wa serikali na wananchi wake kiujumla. Serikali ilikuwa na kiasi kikubwa cha deni toka kwa mataifa yaliyoendelea, mabenki ya nje na ndani pamoja na wafanyabiashara wakubwa wa Mangaka, huku wananchi wake ndiyo kuzidi, kwani wengi wao tegemezi lao pekee ni kilimo, tena kilimo cha mkono.



Hivyo hali hii ilipelekea harakati za maendeleo kwenda taratibu, kwani asilimia kubwa pato la ndani lilikuwa halitoshi kwa miradi mikubwa ambayo ilikuwa hitajio kubwa kwa wananchi. Serikali ilitegemea misaada na mikopo kutoka nchi zilizoendelea kufanikisha hili, misaada yenyewe ilikuwa misaada yenye masharti ndani yake, masharti yaliyonyonya na kukandamiza wanyonge. Asilimia kubwa ya wananchi wengi walichoshwa na hili, nao walitaraji siku moja wapate kuwa na maisha yaliyo bora kwa kupata huduma stahiki kwa wakati. Kama vile afya, maji safi na salama, elimu, miundombinu itayowafanya kuwa na uhakika na safari pamoja na vitu vinginevyo. Hakika! Walikuwa na matamanio hayo.



Wale wanaharakati wa kundi pinzani walionekana kuaminika na wananchi, walizalisha chukizo kubwa kwa serikali na hatimaye kuanza kuwanyanyasa, kwa kuwafanyia matendo ambayo ni kinyume na matakwa ya sheria. Thamani yao kama viongozi kwa wananchi serikali ilihitaji kuifuta, tena kwa gharama zozote ili wasipate kusumbuliwa, jambo lililozua mjadala mzito kwa wananchi mtaani. Mambo mengi walitendewa ili kupunguza kasi yao kiutendaji, lakini wananchi hawakuchoka kuwa nao bega kwa bega kwa kuwa walishachoshwa na utendaji wa serikali, hivyo wakawa tayari kwa lolote. ****



Ilikuwa ni Februari 26, 2002 wananchi wengi wakiwa na mabango yao mkononi jijini Naparavi, walitanda barabarani kuzifuata ofisi za kiongozi mkuu wa taifa, Rais. Mohammed Mlunji kumshinikiza ajiuzulu. Wengi wao dhahiri walionekana kuwa na maisha duni, ijapokuwa walichangamana na wachache wenye uwezo ambao hawakuhitaji wala kupenda utawala wa Ndg. Mlunji. Walichanja mbuga huku wakiimba nyimbo mbalimbali ilhali azma yao isikike. Walikuwa ni maelfu ya watu, waliokusanyika toka miji mbalimbali na kwenda jijini Naparavi, kudhihirisha hawako tayari kuendelea kutawaliwa na Ndg. Mohammed Mlunji. Mwendo ulikuwa wa kawaida, na baada ya dakika kadhaa, walifanikiwa kulikaribia jengo la ofisi ya Rais, almaarufu Ikulu, umbali wa mita mia mbili. Wakiwa na hekaheka hizo, mboni zao ziliruhusu, uonwaji wa kitu kwa umakini. Hivyo, walivyoikaribia Ikulu, mboni ziling’amua askari wa jeshi la polisi toka kitengo cha kutuliza vurugu al-maarufu Mangaka Force (MF), wakiwa na zana zao maalumu kwa kutuliza vurugu.



Wananchi hawakujali. Wao walizidi kusonga mbele huku wakirusha mawe na vitu mbalimbali kule waliko askari wa kikosi cha MF. Mara baada ya hali hiyo, kiongozi wa MF, alitoa onyo kwa wananchi, kupitia kipaza sauti, kilichounganishwa kwenye spika kubwakubwa zilizofungwa ndani ya gari zao, lakini wananchi hawakutilia maanani, walipuuzia, na kuzidi kusonga.

“MF shambulia!” Alisikika kiongozi wa MF, baada ya wananchi kuendelea kupinga onyo alilotoa.



Pasi na kukawia askari wa kikosi cha MF walijigawa kukabiliana na waandamanaji.



Vurugu kali iliibuka, kwani askari walitumia zile zana walizonazo kukabiliana nao, ambazo ni virungu, mabomu pamoja na risasi za moto na baridi. Ilikuwa ni piga nikupige, wananchi nao hawakusita kurudisha mapigo kwa kutumia zana asilia za mapambano ambazo ni mawe, mkuki, mshale, manati na mabomu asilia ya kutengeneza. Hali haikuwa ya kawaida karibia jiji lote la Naparavi. Hali ya hewa ilichafuka, kwani moshi mwingi ulitanda angani na ardhini, tena ni moshi wenye sumu ndani yake. Na kila baada ya muda fulani vishindo vya nguvu havikuacha kusikika, ambavyo kama mgonjwa yupo karibu anaweza poteza maisha.

“Tupo tayari kukatisha uhai wetu leo, ili tu huyo kiongozi wenu aondoke madarakani,” walisikika wananchi huku wakiendelea kupambana na askari wa kikosi cha MF walioonekana kutokuwa na huruma hata kidogo.



Pindi vurugu zinaendelea nje karibu na jengo la ofisi ya Rais, kikosi maalumu cha usalama wa taifa kijulikanacho MIA (Mangaka Intelligence Agency) Kilipata kuwemo ndani ya ofisi hiyo hima kabisa kwa ulinzi wa Ndg. Mlunji asipate hudhurika, wakati huo mipango mingine iliendelea. Kikosi chicho ni kikosi ndani ya idara ya usalama wa taifa ambacho ni maalumu kwa ulinzi wa Rais, kikiundwa na watu tisa ambapo mmoja miongoni mwao ni mlinzi wa karibu wa Rais. Ambapo jina maarufu walilopata kutambuliwa ni PSS (Presidential secret service).

“Namba tisa hali ikoje?”

“Usalama ni wa kutosha!”

“Ni vizuri, hakuna kuruhusu mtu yeyote apite, hata kama ni mfanyakazi wa ofisi hii.”

“Nimekupata kiongozi.”

“Namba nane kwako vipi?”

“Pasi na shaka, utulivu umetawala”.

“Okay! Ni vyema. Umakini unahitajika, kiongozi anaondoka, njia ni kwenu.”



Yalikuwa ni maongezi baina ya mkuu wa kikosi cha PSS Zaulyin Mwakibunda na vijana wake, akiwahitaji wawe makini na tayari kwa zoezi lililo mbeleni.

“Kama muonavyo huko nje hali sio shwari, hivyo kiongozi ataondoka nchini kuelekea nchi jirani mpaka pale hali itapotulia. Ninyi ndiyo watu pekee tuwategemeao kwa ulinzi wa kiongozi wa taifa, tunawaomba msituangushe,” alisema Mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa, Kanali mstaafu Faidha Mwembere, pindi akiongea na wanaPSS.

“Hamna shaka mkuu, tutawajibika ipasavyo”.

“Namba moja!”

“Naam! Kiongozi.”

“Tunakuaminia,” alisema Kanali mstaafu. Faidha Mwembere na kuonesha ishara ya saluti.



Pasi na kukawia!



Raisi, Ndg. Mohammed Mlunji aliambatana na wanaPSS na baadhi ya viongozi wa juu wa majeshi kuondoka ndani ya jengo hilo kwa kutumia mlango wa siri wasipate bainika. Haraka sana walikaza miguu, na kuufikia mlango mweusi chakavu. Uliofunikwa na zulia jekundu sakafuni. Zulia liliondolewa, kisha mlango ukafunguliwa. Punde ulivyofunguliwa, waliingia, kwa kutumia ngazi zilizowatambulisha wapo ndani ya bomba kubwa. Hawakusita. Kila aliyetua toka ngazini alifuata uelekeo wa mwenziye aliyoko mbele yake. Walilifuata bomba hilo kule linakoelekea. Mwendo wa dakika kumi walifanikiwa kufika mwisho na kutokeza kwenye fukwe ya bahari ambapo walikuta usafiri wa helkopta ya kijeshi, iliyokuwa inalindwa na watu wa PSS ambao ni namba tisa na nane iko timilifu tayari kwa safari. Ndg. Mlunji aliwashukuru viongozi wote waliomsindikiza kisha taratibu alianza ingia ndani ya helkopta.

“Nitapakumbuka sana nyumbani. Nimeshindwa kung’amua kosa nitendalo kwa wananchi wa taifa langu. Mimi Mohammed Mlunji, leo hii nageuka kuwa mkimbizi…Wapeni salamu wananchi wangu. Waambie, hicho wafanyacho sio kosa lao, ila ipo siku watafahamu ukweli wa mambo,” alisema Rais, Ndg. Mohammed Mlunji kwa sauti iliyojaa kikuku pindi akipanda ndani ya helkopta.





Mara baada ya kupanda, wanaPSS waliopaswa kuondoka naye, nao bila kukawia walipanda kisha safari ilianza. Dakika tano baadaye tayari helkopta ilianza kutafuta anga na kuacha ardhi ya fukwe ya bahari ya hindi. Ilikuwa safari ya watu kumi na nne, wanaPSS tisa, Rais, washauri wake wawili na marubani wawili wa helkopta. Kwa pamoja walionekana kutokuwa na sura yenye furaha kwa kile kiendeleacho ndani ya jiji la Naparavi. Kila mmoja alionekana mwenye tafakuri, kutafakari jambo fulani akilini mwake. Hivyo kuifanya safari hiyo itawaliwe na ukimya. Rais Mlunji ndiyo aliyekatisha ukimya huo, dakika kadhaa baadaye, wakiwa washalifikia anga la nchi paswa waliyohitajika kutua, punde alivyoita.

“Namba moja!”

“Naam! Kiongozi.”

“Nitaaminika kweli?”

Namba moja alisita kwa muda kisha akajibu.

“Nina uhakika huo kiongozi.”



Dakika sita baadaye toka walivyomaliza yale maongezi mafupi, helkopta iliwasili uwanja maalumu ndani ya jengo kubwa la kifahari nchini Msumbiji. Jengo lililonakshiwa kwa rangi nyeupe, na kuwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi, tena likitawaliwa na mandhari nadhifu yenye kuvutia. Juu ya unadhifu uliopo, ukimya ulipata kutamalaki, huku ni sauti tu za ndege waliokuwa wanarukaruka kwenye miti ya maua na magari machache yaingiayo na kutoka ndiyo yalipata kusikika.



Ilikuwa ni Ikulu. Jengo lililoaminika kuwa takatifu la kiserikali, ndipo helkopta ile iliyombeba Rais, Ndg. Mohammed Mlunji na ugeni wake ilipata kutua. Taratibu waliteremka, punde ilivyotulia, kisha kupokelewa na mwenyeji wake, ambaye ni Rais wa nchi hiyo Joyce Atunus Chisano. Baada ya wote kukamilika waliongozana na mwenyeji wao hadi ndani ya jengo, wakasalimiana kwa mara nyingine kisha kuanza kuteta mambo mbalimbali baina ya nchi hizo mbili.

“Karibu sana Msumbiji. Nadhani hii sio mara yako ya kwanza kutembelea taifa langu, jisikie huru mpaka pale utaporidhika na kuona uko tayari kuondoka,” alisema Rais Joyce Chisano.

“Hamna shida kiongozi, nashukuru kwa msaada wako.”

“Amina! Naamini utafurahia maisha ya kwetu.”

“Sahihi.”



Kwa usiri mkubwa Ndg. Mlunji na kikosi chake cha ulinzi kiliendelea kuishi hapo, pasi na watu wa Mangaka kufahamu zaidi ya wale viongozi wakuu wa majeshi na baadhi waliohusika kumsindikiza. Muda wote alionekana mtu aliyekosa furaha na amani ndani ya moyo wake, kwani uso wake uliweza kumtambulisha. Vilevile hakuwa mtu wa kujichanganyachanganya sana katika maongezi na wale walinzi wake wa siri. Alikesha kukaa peke yake, tena akiwa na wingi wa mawazo.

“Nahitaji kuwa huru,” alisema asubuhi moja akiwa na walinzi wake wa siri (PSS) Pindi wakipata kisebeho. Kauli iliyowastaajabisha wanaPSS, kwa kutotambua amaanichasho.



Upande wa pili hali ya Mangaka iliendelea kuwa mbaya, tena mbaya haswa. Utulivu ulikosekana, machafuko yalikithiri karibia miji yote kushinikiza Rais, Ndg. Mlunji apate kujiuzulu tokana na hali ya uchumi jinsi ilivyo. Wananchi wengi walipata poteza maisha yao na kujeruhiwa lakini wengine waliendeleza maandamano ili tu, kile wanachohitaji kitekelezwe. Hawakuthubutu kuruhusu tamaa ya kushindwa iwatawale, walitanguliza ushujaa ijapokuwa mara kwa mara hawakuisha kukutana na matokeo ya kuogofya.

Sio wananchi tu, bali hata askari nao baadhi yao walipoteza maisha ila sio wengi kama ilivyokuwa kwa wananchi.



Hali ilivyozidi kuwa mbaya, jeshi la polisi wakisaidizana na majeshi mengine hususani la akiba (MGAMBO) Walijitahidi kwa kila hali na mali kuitetea serikali, japo wananchi nao kila kukicha walipata kuongezeka baada ya kupeana hamasa. Ilikuwa ni kazi ya usiku kucha, iliyopelekea kupoteza matumaini ya mafanikio kwa upande wa jeshi la polisi, kutokana na maelfu ya watu walivyozidi kuhamasika kuuondoa utawala wa Rais, Ndg. Mohammed Mlunji. Hatimaye baada ya jeshi la polisi kuzidiwa nguvu, jeshi la ukombozi wa wananchi likachukua nafasi huku wakisaidizana na yale yaliyopo awali. Kitendo cha jeshi hili kuchukua nafasi kilirudisha ari kwa yale majeshi, hivyo kupelekea mafanikio upande wao. Kwani silaha za kivita zilipata kutumika pasi na kuwaonea huruma waandamanaji.

“Usicheke nao hao, kwani hawana utu hata uwatendee mema kiasi gani,” ndiyo kauli iliyopata kusikika toka kwa askari na wale wanajeshi wa ukombozi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Siku nne mbeleni baada ya jeshi la ukombozi kuingilia kati vurugu zikapata tulia, huku zikiacha makovu makubwa baada ya mali za wananchi na serikali pia kuharibiwa. Kama vile majengo kubomolewa na kuchomwa moto, kuvunjwa kwa madaraja na kuchimbwa mashimo barabarani. Hakika! Ulikuwa uharibifu mkubwa ulioleta hasara. Kutokana na gharama zilizotakiwa kufanyia ukarabati kwa pande zote zilizoharibiwa. Ilichukua siku kadhaa hali kukaa sawa, wafu kuzikwa na baadhi ya mali za serikali kuanza kukarabatiwa na wale wananchi walioathirika nao kuanza kukarabati mali zao. Ukarabati huo ulifuatana na lawama ndani yake, watu wa serikali wakiwalaumu wananchi kwa kutokuwa wasikivu huku wananchi wakiilaumu serikali na majeshi, sanjari kabisa na taasisi za haki za binadamu kutoka ndani na nje ya Mangaka zililaani kitendo hicho.

****



Maisha ndani ya Msumbiji yaliendelea vizuri kwa Rais, Ndg. Mohammed Mlunji na watu wake, huku wakiendelea kutobainika kuwa wapo ndani ya nchi hiyo katika jiji la Maputo. Kadri siku zilivyozidi kusonga mbele hawakuwa wageni tena wa mazingira, kwa kiasi fulani walianza kuyazoea. Hawakuacha kutoka kwa baadhi ya siku, kwenda kuangalia mazingira nje ya jengo wakitumia magari maalumu toka Ikulu.



Ni April 14, 2002 siku ya jumapili majira ya mchana yapata saa sita, muda mfupi baada ya Rais, Ndg. Mohammed Mlunji na watu wake kutoka kwenye ibada. Alimuita mlinzi wake wa karibu, ambaye ndiyo PSS namba moja ajulikanaye James Kesho, sehemu tulivu wapate kuteta jambo. Ni wao tu ndiyo waliketi karibu, walinzi wengine walikaa umbali kidogo na wao wakisubiri wamalize maongezi yao kisha wajumuike pamoja.

“Bw. James, nakuamini sana ndiyo maana nimeamua nipate kuketi nawe tuelezane kitu muda huu,” alisema Rais, Ndg. Mlunji.

“Pasi na shaka kiongozi ruksa kufanya hivyo.”

“James! Nahitaji msaada wako, kwa hali na mali. Maji yashanikaa shingoni, sina budi kujitetea. Hali ya Mangaka ni mbaya na hamna mtu mwingine wa kuikomboa zaidi yangu, James..,” alisema na kutulia. Takribani sekunde arobaini kisha akaendelea.

“…Nahitaji urudi Mangaka”.

“Itawezekana vipi kiongozi? Na vipi kuhusu ulinzi wako?” Aliuliza James kwa taharuki kubwa.

“Kuhusu ulinzi usiwe na shaka nalo, ninyi mupo wengi, wenzako watachukua jukumu hilo. Naomba unisaidie, kwani nachafuka pasi na sababu yoyote. Nahitaji kuuweka ukweli wazi, lakini sihitaji kuuweka wazi bila kukutana na watu fulani. James nawahitaji watu hao,” aliendelea zaidi kusema Rais, Ndg. Mlunji kwa sauti iliyojaa masikitiko.



Baada ya maongezi ya kina mwanaPSS namba moja. James Kesho, kama anavyotambulika, hakuwa na budi, alikubaliana na ombi la Rais. alipatiwa majina ya wahusika, ambao alitakiwa akutane nao kwa siri pasi na watu wengine kubaini, katika miji tofautitofauti ndani ya Mangaka. Hivyo usiku wa siku hii aliagana na wenziye huku akishindwa kuweka wazi ni kazi gani inayomrudisha, zaidi ya kuwaongopea kuwa kapatiwa likizo ya dharura kutokana na utendaji wake wa kazi kupungua. Alirejesha baadhi ya vifaa vimtambulishavyo kuwa Afisa usalama wa Taifa kwa mkuu wao wa kitengo Zaulyin Mwakibunda, kisha akaanza maandalizi ya safari aliyopaswa kuifanya siku iliyofuata.



Mkuu wa kitengo chao Zaulyin Mwakibunda alijaribu kuhoji sababu ya kitendo hicho, kwa Rais na Mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa lakini hakupatiwa majibu yakutosha zaidi ya lile alilowaambia mwenyewe kuwa utendaji wake wa kazi umedhorota.

“Msamaha wako hauwezi kusaidia, nimeshaamua wacha akapumzike kwa muda na kufanya marekebisho ya pale alipokosea, kisha baada ya siku kadhaa atarejea tena,” ilikuwa kauli ya Rais, Ndg. Mlunji mara baada ya kuhojiwa na mkuu wa PSS.



Alivyojaribu kuhoji kwa mkuu wao wa idara, Kanali mstaafu Faidha Mwembere jibu halikutofautiana na lile alilopatiwa na Mheshimiwa Rais.

“Mkuu kaamua, hivyo hatuna budi kutekeleza. Wacha arudi, kisha baadeye atarejea,” ilisikika kauli ya Kanali mstaafu Faidha mara baada ya kuhojiwa.



Mapema sana asubuhi, siku iliyofuata, punde baada ya kisabeho James alikuwa ndani ya moja ya gari za kifahari za Ikulu safari uwanja wa ndege, tena chini ya ulinzi wa askari wa Msumbiji toka Ikulu. Mwendo wa dakika kadhaa msafara wao uliwasili uwanja wa ndege, James aliteremka na kuagana na wale waliomsindikiza kisha akatafuta uelekeo. Dakika kumi na tano baadaye tayari alikuwa ndani ya ndege ya shirika la Pakistan na muda huohuo ndege ilianza safari. Taratibu ilitembea kwenye njia zake za kurukia na baada ya muda ikaanza kuacha ardhi kulitafuta anga huku abiria waliomo wakiwa tulivu mithili ya maji mtungini. Akiwa ndani ya ndege, baada ya ndege kukaa sawa angani, James alikumbuka maongezi baina yake na Rais, Ndg. Mohammed Mlunji. Hivyo kumfanya afikirie kwa kina maongezi yale na namna alivyokuwa anazungumza kwa masikitiko.

“Ama kweli mzee kakwama!” Alijisemea James kimoyomoyo, baada ya kumaliza kumbukumbu zake. Lakini ghafla alionekana kushtuka, kama kuna kitu kingine alikikumbuka.



Kweli! Mshituko wake ulimaanisha ukumbusho wa jambo fulani, haraka sana aliingiza mkono wake wa kuume katika moja ya mfuko wa mbele wa suruali yake na kutoka na kipande cha karatasi, akakumbuka kikaratasi hicho alipatiwa na Rais pindi wakiendelea na maongezi yao. Pasi na kukawia alianza kukinjua, na kukutana na maandishi kadhaa yenye wino wa bluu, kisha taratibu alianza kuyasoma maandishi hayo.

“Joram Isaac-LUKWIKA, Kasanjara Chomeko- NANDERU na Magreth Okuku- KISIMATULI.”







Punde baada ya kumaliza kusoma alikirejesha mahala husika, pale alipokitoa awali. Muda wote alionekana mtu aliyekosa furaha, kwani ukimya ulikuwa sahemu ya safari yake. Hata abiria aliyeketi jirani naye hakupata kuzungumza naye zaidi ya salamu awali pindi walivyoketi kwenye siti zao. Msaada aliouhitaji kuutoa kwa kiongozi wake Mkuu wa nchi ndiyo ulimfanya awe hivyo, kufikiria ni namna gani atakutana na watu alioelezwa na kwa muda gani atafanikisha zoezi hilo. Masaa kadhaa baadaye ndege ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata jijini Nairobi nchini Kenya, ambapo kulikuwa na mapumziko ya dakika kadhaa huku baadhi ya abiria wakiteremka, kwani ulikuwa mwisho wao wa safari huku wengine wakipanda kuianza.



James ni mmoja miongoni mwa abiria walioteremka, kisha kuunga safari yake na ndege nyingine, ya shirika la Mangaka (Mangaka Airyways) Ambayo ndiyo ilimpeleka moja kwa moja nchini Mangaka. Mnamo saa kumi na nusu jioni ndege hiyo iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dkt. Chimpele Mwakatubu (CMIA) jijini Naparavi. Abiria wote waliteremka. Baada ya hapo walifanya taratibu za kiusalama, walipokamilisha waliendelea na mambo yao. James alivyokamilisha aliondoka. Kwa usafiri wa taksi aliouita mbele baada ya kupiga hatua na kuliacha jengo la kiutawala la uwanja.

“Nifikishe Jalana Lodge!” Alimuamuru dereva taksi.



Dereva alitii kauli yake, kwa kuzidi kukanyaga mafuta ili asipate kukawia kurudi na kuendelea na shughuli afanyazo. Baada ya muda mfupi waliwasili mahala husika, James aliteremka na kufanya malipo, baada ya hapo aliongoza kuelekea mapokezi, kuulizia kama anaweza kupata chumba kwa ajili ya mapumziko ya mwili kwa siku hiyo. Bahati ikalala upande wake, alifanikiwa kupata. Usiku wa siku hii alifanya mapumziko, huku akiendelea kukumbuka jukumu alilonalo mbeleni. Mapema sana siku iliyofuata, punde baada ya kumaliza kustaftahi alikabidhi funguo na kuomba bili ya matumizi yake yote aliyofanya. Alivyokabidhiwa, aliitathmini, kuona viwango vya pesa hitajika kama vinawiana na huduma aliyopata. Alivyoridhika nayo, alilipa, na hatimaye kuondonda.

“Naanza rasmi sasa!” Alisema James kimoyomoyo baada ya kuumaliza uga wa nyumba ile ya kulala wageni.



Mnamo saa tatu na robo asubuhi James alianza rasmi kazi yake ya kuwatafuta wale watu anaohitajika kuonana nao mmoja baada ya mwingine. Alikichukua kile kikaratasi kilicho na majina ya watu husika na kuweka alama ya tiki katika moja ya yale majina na kuirejesha tena mahala alikoichukua awali. Joram Isaac, ndiyo jina aliloiwekea alama ya tiki, kisha kuchanja mbuga kutafuta usafiri utakaompeleka mjini anakoishi Joram. Lukwika!



Moja kwa moja alielekea kituo kikuu cha mabasi, Mkwajuni. Yaelekeayo miji mbalimbali ndani ya Mangaka na nje ya Mangaka. Hakuna mtu yeyote ambaye aliweza kumfahamu kuwa yeye ndiyo yule mlinzi anayeambatana na Rais kila apitapo katika shughuli zake mbalimbali, kwa namna ambavyo alivaa. Miwani yake nyeusi imkingayo dhidi ya mwanga na vitu mbalimbali ilizidisha zaidi kupoteza muonekano wake pamoja na kofia yenye rangi nyeusi kichwani. Alitafuta basi zielekeazo ndani ya mji wa Lukwika, na maeneo mengine ya kusini. Pasi na kukawia alifanikiwa kupata moja wapo. Hakusita! Alipanda ndani ya basi na kutafuta namba ya siti iliyopo kwenye tiketi aliyokabidhiwa akaketi. Dakika nane baadaye mara baada ya James kupanda safari ilianza. Alifanya dua iliyomchukua dakika chache kuimaliza, kisha akajiweka sawa kusikilizia vizuri utamu wa mwendo wa basi aliyoko na safari kwa ujumla.



Muda wote akili yake ilikuwa inawaza namna ya kumpata Joram Isaac, kwani uso wake dhahiri ulionesha kuna jambo limtatizalo, hadi watu walioketi jirani naye waliweza kulibaini hilo. Miongoni mwao hawakusita kumuuliza, ila hakuweza kuwapa ukweli wa kile kilichopo ndani ya akili yake.

“Nipo sawa, wala msiwe na shaka lolote juu yangu,” ndilo jibu pekee ambalo James aliwapatia watu wamuulizao.



Safari iliendelea kuwa nzuri kwa upande wake, kwani hadi anafikia hatua hiyo hakuna mtu yeyote aliyembaini ama kumtilia shaka kuwa yeye ndiyo yule mlinzi wa kiongozi mkuu wa taifa lao, ambapo mara nyingi walimuona runingani, alipendezwa na hali hiyo, hivyo akamuomba Mungu aendelee kuwa upande wake mpaka atapokamilisha kile anachohitaji. Haikuwa safari ndefu sana, masaa matano tu, yalimfikisha ndani ya mji wa Lukwika. Aliteremka ndani ya basi huku akiwa na begi ndogo la mgongoni alilohifadhia baadhi ya vitu, kama vile nguo na vinginevyo. Aliita taksi na kumuomba amfikishe katika moja ya nyumba za kulala wageni mjini hapo.



Dereva taksi alifanya vile alivyoambiwa, dakika chache tu alimfikisha mteja wake eneo husika alilokuwa anahitaji.

“Hapa ndiyo sehemu nzuri na yenye hadhi kwa hapa mjini kwetu. Panaitwa J&I HOTEL, nahisi panakufaa,” alisema dereva taksi, punde baada ya kuegesha gari katika uga wa maegesho wa hoteli hiyo.

“Ahsante sana. Pia nikutakie kazi njema,” alisema James pindi akiteremka ndani ya taksi mara baada ya kukamilisha malipo.



Moja kwa moja alielekea ofisi za mapokezi. Aliulizia chumba na kufanikiwa kupata. Hapo ndipo alipendekeza kuwa makazi rasmi, ambapo angeishi mpaka siku atayofanikiwa kumpata Joram Isaac. Mmoja miongoni mwa watu wanaohitajika kwa udi na uvumba na Rais wao, aliyoko mafichoni. Hakutaka kukawiza. Ili aweze kufanikiwa, aliigawa kazi hiyo katika makundi matatu. Moja; utafutaji wa habari, mbili; uchambuzi wa habari na mwisho; utekelezaji wa habari. Alijiapiza kumsaidia Rais, kufanya kile chenye msaada akiwa kama mlinzi aaminiwaye na serikali na idara nzima ya usalama wa taifa ndani ya Mangaka. Hivyo kitu cha kwanza, alipaswa amfahamu Joram ni nani. Wapi atapata taarifa? Ni mtihani. Lakini kupitia mafunzo aliyonayo, aliamini anaweza kufanikiwa.



Chanzo sahihi cha habari alilazimika kuwanacho. Chenye kumpatia habari makini, na zenye uhakika. Alidadavua sehemu ipi hupendwa na wengi, hasa watu wa zima na vijana, tena kwa mjumuisho wa rika na jinsia zote, ila ilikuwa shida, si kiurahisi hivyo, kwa kuwa hakuweza kukadiria, Joram ana umri gani. Angelikuwa na ufahamu umri wake ungelimsaidia kufahamu hilo. Hivyo aliorodhesha, kupitia kumbukumbu aliyopata miaka kumi na nane nyuma, awapo chuoni kwao. Chuo cha mafunzo. Michezo ipendwayo na wengi. Kisha alitumia hisia, kuchagua mchezo mmoja pekee ambao hupendelewa sana.

“Mpira wa miguu!” Alijikuta anaropoka peke yake, kiasi kwamba mtu apitaye koridoni husikia.



Hivyo alipaswa kufahamu pia, sehemu zipi ndani ya mji huo, ni maarufu kwa burudani hiyo kabambe, ichangamkiwayo sana nchini mwao. Alifanya tafakuri, iliyomchukua dakika kumi kufikia tamati. Na muafaka wa sehemu ipi mahususi kwa hiyo burudani. Majukumu aliyaanza siku iliyofuata. Achilia ile aliyowasili mjini Lukwika. Hapa ilikuwa ni mwendo wa kutumia mafunzo yake kiutendaji zaidi. Japo hakuhitajika kufahamika. Hivyo hata jina alibadili. Akajiita Sadiki Mbwela. Na ndilo alilotumia kujitambulisha pale hotelini. Alianza zunguka mtaani. Kudadisi mazingira yalivyo, na mienendo ya mji na watu wake walivyo. Matembezi hayo, ndiyo alifanyia tathmini, ya maeneo anayohitaji kuyatambua. Ili siku za baadaye asipate usumbufu. Ilimchukua takribani saa nne kuzunguka baadhi ya mitaa, na vijiji vilivyoko nje na mji. Baada ya hapo alirejea hotelini alipofikia. Matembezi hayakuwa ya bure. Kuna mambo aliyavumbua, yaliyomuongezea ufahamu na uhitaji wa kufanya mambo mengine endapo vile alivyopanga vitaenda tofauti.

“Kuishi mtaani na kufungua kituo cha usafishaji viatu,” aliandika katika orodha ya mahitaji. Kwamba endapo mambo hayatokaa sawa, yamlazimu kuhama hoteli na kuanza biashara. Ya ufunguzi wa usafishaji viatu.



Utamu huja mambo yachanganyiapo. Mwanzoni huanza kwa udhia, na manung’uniko na mawazo hasi yenye unyong’onyo. Kadri siku zilivyozidi kusonga mbele, ndivyo naye alizidisha doria yake. Pasi na kukosea, alifuata uhitaji uliopo kwenye orodha. Alianza changamana na watu, wa rika mbalimbali, katika klabu kubwa za usiku. Huku mchana akishinda kwenye vijiwe vya soka. Kwani asilimia kubwa watu washabikiao mpira, hata wasivyofahamiana vyema wana uwezo wa kuonesha hali kama wamefahamiana miaka mingi iliyopita. Kijiwe cha soka alikutana na wazee, vijana na watoto wasikilizaji wenye wito na mpira tangiapo. Katika hali ya kuwateka. Alijitengenezea mazingira ya watu wengi wamfahamu, hivyo alikuwa mchangiaji na mtoa mada mkubwa katika kijiwe aendacho. Alienda vijiwe tofautitofauti. Alizoeleka, alikubalika na kuaminiwa, hivyo endapo mabishano hujitokeza, pasi na kufikia muafaka hutafutwa. Aidha, kwa njia ya simu, kwa watu wachache aliowapatia namba zao, ama husubiriwa hadi atapokuja. Huelezwa kisa kisha naye hueleza kwa ufahamu alionao.

“Kaka!......kaka!...nishakueleza, yule mzee, kocha wa Kili FC hana taaluma yoyote ya mpira, hivyo huwezi,…huwezi kumfananisha na Mkogo anayefundisha timu yetu ya taifa sasa.”

“Taaluma gani aliyonayo yuleee. Katoka mtaani huko, kapandishwa pandishwa tu vyeti, leo hii, anapewa timu ya taifa. Ni unduguundugu tu ndiyo umetumika katika uteuzi ule. Ona watu wengi wanavyolalamika na wasivyomkubali. Kocha wa Kili FC yuko vyema. Yule mzee.”

“Hapana! Hapana! Huwezi nieleza kitu katika hilo. Mkogo kamzidi elimu yule mzee, na mafanikio katika ulimwengu wa mpira ndiyo maana kapatiwa ukocha. Huyo mzee wako hana historia yoyote ya mafanikio.”

“Kwa nionavyo. Hatuwezi fika muafaka. Kama vipi tumsubiri profesa wetu wa haya mambo, Sadiki atufafanulie.”

“Sahihi,…sahihi…maana hata nami siwezi amini kauli zako.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Yalikuwa ni mabishano yaliyowaunganisha vijana wawili, na mashuhuda lukuki wakipimana nguvu kuhusu uhalali wa kocha wa timu yao ya taifa. Walifanya subra, James alipowadia, ambaye wao walimtambua kwa jina la Sadiki Mbwela kundi lote lililopo lilipuka shangwe kumshangilia. Hivyo ndivyo alijitengenezea mazingira ya kukubalika. Hakuna hata mtu yeyote aliyeweza kumtilia chembe ya shaka, kuwa yupo kwa kazi maalumu katika vijiwe akaavyo. Walivyojaribu kudadisi, wapi anaishi walifahamu. J&I Hotel. Ila kwenye kazi iliwapatia wakati mgumu wa kutambua kazi gani aifanyayo. Waliishia kubashiri aidha, anafanya kazi kwa wachina, watengenezao barabara, iunganishayo mji wa Lukwika na Misawaji. Wengine walibashiri kwa kumpatia wadhifa, anafanya kazi ndani ya ofisi kubwa mjini kwao. Alivyowasili alitoa darasa, walivyomuelewa aliomba kuondoka, huku akiomba kijana mmoja kumsindikiza. Hii pia ilikuwa kawaida yake. Muda wa kuondoka kijiwe, huondoka na mtu, kwa kigezo cha kumsindikiza, ila afikapo umbali fulani huanza kutekeleza jukumu. Kumuuliza masawali kadhaa yahusianayo na mtu amtafutaye.



Alitumia watu wengi. Na kila amtumiaye hakuna aliyemfahamu mtafutwa. Hali iliyopelekea kuhisi mengine. Kwamba yumkini tayari kashatangulia mbele ya haki. Ila hakuzipa nafasi sana hisia hizo zitawale. Alivyorudi hoteleni, kwa saa chache atumiazo kuwepo humo, hutumia kuperuzi mtandaoni, lakini mote mambo yalikuwa bilabila. Kwani watu aliokutana nao mtandaoni mwenye jina hilo, ni wale watokao mataifa ya nje. Wazungu! Na kama ni wenye asili ya Afrika, basi ni wale waishio mataifa ya Afrika Magharibi. Hakuna mtu aitwaye Joram Isaac apatikanaye ndani ya taifa la Mangaka. Kuona hivyo. Akahisi, amtafutaye anaweza kuwa ni mzungu. Ama mwafrika, wa mataifa ya Afrika Magharibi. Hivyo yampasa kuachana na wenyeji, awatafute wageni asaili nao. Usiku kabla ya kulala, alihudhuria kumbi mbalimbali za disko. Nako alitumia wasaa kumuulizia. Lakini matokeo yaliwiana.

“Huyu itakuwa si mwenyeji wa taifa letu,” alijisemaza. Wakati huo akiwa tafakurini, kumdadavua Joram.

“Ningelikuwa na picha zao, ingelinisaidia. Lakini hivi. Mambo ni magumu. Na sijui kama nitafanikiwa. Halafu!...” James aliendelea kusema, lakini alishindwa kumalizia kauli yake. Baada ya kuonekana kuna jambo fulani kakumbuka.



Alisogeza kwa ukaribu fikra zake. Zilizomtengenezea kumbukizi ya jambo, ila isivyo bahati akajikuta taratibu akilipoteza baada ya kuchanganya mambo. Alivyokuja zinduka, aanze kufanyia kazi wazo lake tayari lilishayeyuka. Kila alivyojaribu rudisha kwa mara nyingine, ni kitu gani alipanga kufanya, aliambulia patupu. Mwishowe aliishia kusonya tu. Hatimaye siku zilizidi kusonga mbele. Majukumu yaliongezeka uzito. Mtu amtafutaye hakupata hata chembe ya habari yake moja imhusuyo. Miezi kadhaa ilikata. Takribani minne. Dalili za mafanikio hazikuonekana na pesa aliyoiandaa kwa ajili ya malazi kwa muda wote ataopatikana hapo ilianza pungua. Ilibaki kiasi kidogo sana, ambacho asingeweza kumudu gharama za hoteli. Muda huo ndiyo alianza tumia nyongeza ya mahitaji aliyoorodhesha. Kuhama hoteli kisha kufungua ofisi ya kusafisha viatu. Na ndivyo alifanya. Alihama hotelini na kwenda kutafuta chumba mtaani. Umbali mdogo na mji ulipo. Alivyofanikiwa, yakawa makazi mbadala. Na kwa sababu kiwango cha kodi kilikuwa nafuu mno. Aliamini ataweza kuishi hapo hadi mwisho wa uhitaji wake.



Sababu hakuwa na godoro wala kitanda. Alitafuta boksi kubwa, na mifuko akageuza kuwa hivyo vitu. Pia alitafuta eneo. Moja ya genge atumialo kupiga stori, akafungua ofisi yake ya usafishaji viatu. Maisha yakaendelea. Marafiki hakusita kuwanao. Ambao walimsaidia katika baadhi ya mambo. Na kumpa hamasa ya kuendelea kuwepo ndani ya mji huo.

“Vipi hujafanikiwa kumpata tu huyo umtafutaye?” Aliuliza kijana aitwaye, Makambo wakiwa ofisini kwake, akitengeneza viatu.

“Sijafanikiwa. Na sijui nitumie njia ipi nifanikishe kumpata. Maana hata picha yake sina. Hivyo hata sasa hivi nikikutana naye barabarani nitapishana naye tu.”



Hakika! Alichotengeneza kilimsaidia. Umaarufu wa muda mfupi akawa na lundo kubwa la marafiki. Waliomkaramsha kila uchao na kumjaza tabasamu, majukumu asione magumu. Japo hao rafiki hawakutambua kazi nzito aliyonayo mbeleni yenye kutuliza amani ya nchi. Ilikuwa ni jumamosi. Mnamo majira ya saa kumi na moja jioni. Mawingu yametanda kiza, upepo wa wastani uliobeba uashiriao muda wowote wananchi wa mjini Lukwika kuwa na matarajio ya kupata mvua. James (Sadiki) alikuwa kaketi sehemu yake ya biashara. Akijitahidi kuweka sawa mazingira ya ofisi yake, punde alivyomaliza kushughulika kushona kiatu cha mama mmoja afanyae kazi kwenye ile hoteli aliyofikia awali kabla ya kuhama. Baada ya hapo alichukua moja ya kitabu kilichopo kwenye begi lake atumialo kuhifadhia dhana za ushonaji. Sindano, uzi na gundi. ‘MAISHA YA WANA MANGAKA KABLA NA BAADA YA UKOMBOZI’ ndivyo kilisomeka kitabu hicho. Taratibu alipitia kurasa moja baada ya nyingine. Kitabu kielezeacho mienendo ya dola na vyombo vyake. Pasi na sahau maisha ya wananchi wake namna yaliyokuwa hapo nyuma, kipindi cha ukoloni na baada ya kupata uhuru.



Katikati ya kisomo chake. Yule mhudumu wa J&I aliwasili. Alisitisha kusoma, na kufunika kisha kufanya hima kumhudumia amkabidhi mzigo wake. Wakati huo macho ya mama mhudumu, yalizunguka kuangaza huku na kule kuangalia mazingira ya ofisi yalivyopambika. Pindi yeye anafanya hivyo, James naye, macho yake yalikuwa pima, kuangalia umbo la mama huyo lilivyoumbika. Angaza ya mama yule alishuhudia, kile kitabu kilichofunikwa, kwa uzuri, pasi na kizuizi, alishuhudia jina la kitabu na mwandishi wake. Kwa James alishuhudia, tatuu, na kidani kilichovaliwa kifuani chenye nembo ya bawa. Hata mchoro wa tatuu ulikuwa wa picha yenye nembo hiyo, ikipendezeshwa na rangi tatu za nchi yao. Bluu, nyekundu na nyeupe. Jambo fulani alilikumbuka. Lakini kutokana na sheria za kazi yao, hakuonesha wazi mshituko wa kumbukumbu. Watu wengine wasishuhudie, yule mama na baadhi ya watu walioketi jirani. Alisubirishia, mama aondokapo afanyie kazi kumbukizi yake.

“Fundii! Unaonekana kuhitaji kulikomboa taifa letu kwa mara nyingine,” alisema yule mama mhudumu. Akichukua kile kitabu na kusogeza jirani naye. Ashuhudie kwa uzuri zaidi.

“Hawa waliotajwa humu ndiyo wakombozi wa kweli wa taifa letu. Soma, utafurahia kilichoandikwa. Mwandishi kaandika mambo matamu na yenye uhakika.”

“Sahihi. Japo sijafika mwisho, hizi kurasa za mwanzo nilizosoma zimenivutia.”

“Hajakosea kabisa. Utaniambia tu, tukija onana kwa mara nyingine,” alisema mama huyo, akikabidhiwa viatu vyake, kisha kuondoka.



Alivyofika umbali fulani, ambao mtu akiteta jambo hawezi sikia. James alimuita kijana mmoja miongoni mwa wale majirani.

“Unamfahamu yule mama?” Aliuliza james.

“Ndiyo. Yupo pale J&I Hotel. Ila sema huwa haonekaniki sana.”

“Ana wadhfa gani pale hotelini? Na una muda gani toka ulivyoanza mfahamu?”

“Sijajua majukumu yake ni yapi. Na ana muda mrefu sana hapa Lukwika. Takribani miaka sita sasa.”

“Poa. Ahsante kwa kunifahamisha.”

“Haya!”



Kijana aliondoka. Naye kuingiza moja ya mkono wake kwenye suruali aliyovaa na kutoa kitu fulani. Ilikuwa picha ile ya nembo ya bawa. Ama beji. Ambayo ilikuwa sawa na yule mama aliyoivaa. Kasoro ya kwake haikuwa na cheni tu. Ilifanana kwa kila kitu. Rangi na ukubwa wa umbo. Hakuishia hapo. Alifungua vifungo kadhaa vya shati alilovaa. Na kushuhudia tatuu, kama ileile aliyochorwa yule mama. Alipoa ghafla! Upi ukweli kuhusu hivyo vitu alivyonavyo hakufahamu. Wapi kavipatia hakutambua pia. Kwani siku aliyokabidhiwa, alikabidhiwa pindi akiwa hajitambui. Alipoteza fahamu. Hivyo alivyoamka ndipo akakutana navyo. Ni vitu alivyopata katika mazingira tatanishi, kwani vilikuwa havihusiani na idara ya kazi aliyopo. Nini maana? Ulikuwa mtihani ugumu.



Mshawasha wa kwenda kumuuliza yule mama ulijaa. Ila ataanzaje? Kila alivyotafakari hakupata jibu sahihi. Alitumia zaidi ya dakika nne, alipokuja zinduka. Alizunduka na kumbukumbu ya kauli ya Mhe. Rais, Ndg. Mohammed Mlunji.

“Hawa ni wakombozi wa taifa letu. Hivyo wana mengi ya kunifaa. Ambayo kwa jitihada zao za ukombozi, nataka niwapatie heshima siku ya kusherehekea kupata kwa uhuru wa taifa letu. Oktoba 15. Jitahidi, kwa muda mchache ufanikiwe kuonana nao. Tumia taaluma yako, na ujuzi wa ziada, pale uonapo mambo hayaendi vyema. Udororaji ukiuona.”

Aliikumbuka kauli hiyo. Iliyotamkwa na Rais, Ndg. Mlunji pindi akipewa maagizo. Huku akipatiwa kitabu cha ‘Maisha ya wana Mangaka kabla na baada ya ukombozi’

“Hiki kitabu kitakusaidia. Kukuongezea maarifa na kukuondolea uchovu. Ili mambo yabaki mahali pake,” alisema Rais, Ndg. Mlunji.



Kumbukumbu hizi mbili ukujumlisha na kauli ya yule mama, aliamini kuna kitu ndani ya kitabu, chenye uwezo wa kumsaidia kufanikisha oparesheni iliyoko usoni. Chap, alirudi kitabuni kuendelea kusoma. Hakika! Kitabu kilikuwa kizuri. Kilijaa mambo ya kijasusi na maendeleo. Furaha yake ikajikita kwenye ujasusi, mambo yalipo sana idarani kwao. Katika nafasi hiyo, aliwasoma watu watatu walio hodari, walioweza kujikita vilivyo kuhakikisha Mangaka inajikomboa toka kwa mkoloni. Kilienda mbali, kwa kuwaonyesha walivyoingia ngome pinzani na kudukua mambo mengi, yaliyowasaidia wakati wanadai uhuru wao. Kitabu hicho kiliwadadavua vyema, hao watu, ambao ni wanawake, waliotambulika kwa majina ya Aramina, Zanifa na Maua. Naye, hakuishia hapo. Aliendelea kuwafuatilia kila hatua na kunakili majina yao pembeni na baadhi ya mambo waliyokwisha fanya pasi na sahau alama fulani alizokutana nazo, hususani kidani cha bawa, na ile tatuu yenye mchoro wa bawa. Kisha kugundua maana zake pia.

“Kama haya majina niliyopatiwa ni ya mashujaa waliokomboa taifa letu mbona hawajatajwa ndani ya hiki kitabu? Ama Rais kanidanganya?” Alisema James kimoyomoyo. Na kufanya tafakuri kwa muda mfupi, alivyokuja zinduka alitoka na wazo jipya, nini cha kufanya.

“Nitaenda shughulika na hii kesi nifikapo nyumbani. Siwezi fanywa mjinga. Kwa kupewa kazi yenye fumbo namna hii,” alisema kisha kuendelea na kazi yake kama kawaida.





Jioni baada ya kuhitimisha biashara yake, alirejea nyumbani alikopanga. Kichwa kikiwa na lundo tele la mawazo, atafumbuaje fumbo lililopo kwenye shughuli aliyokabidhiwa. Muda mwingine alimlaani hadi kiongozi mkuu wa serikali, Rais kwa kumpatia jukumu hilo likiwa kwenye kificho. Japo muda mwingine alihisi yamkini yupo vipimoni. Ana uwezo kiasi gani. Alivyowasili nyumbani, alianza pitia kurasa kadhaa za kile kitabu, ambazo zilikuwa zinaelezea historia fupi ya wakombozi wanaozungumziwa. Lini wamezaliwa, wapi wamesoma, na nafasi walizotumikia na wapi wanaishi kwa sasa. Mambo aliyokutana nayo yaliendelea kumpatia mshangao. Kwani historia iliyoandikwa, ndiyo historia aliyopatiwa James. Hasa kwa sehemu waishizo. Aramina alielezewa kuishi Lukwika, Zanifa Nanderu na Maua Kisimatuli. Aliwekwa njia panda. Zaidi, katika orodha aliyokabidhiwa, ilionesha kuwa na wanaume wawili na mwanamke mmoja. Huku kwenye kitabu ikionesha wote ni wanawake.

“Yupi ni sahihi? Ama mwandishi kafanya upendeleo? Kuna baadhi ya wakombozi kawaacha kwa maslahi yake? Ila mimi acha tu nimfuate kiongozi wangu. Katika wasaa wa kuwatambua hawa watu sita lazima nitumie masomo yetu,” alisema James huku akitoa vitabu vidogovidogo viwili, na kikubwa kimoja kilichoandikwa kamusi. Kamusi ya namba mchanganyiko na herufi.



Alphabetical security alert na ulingani ndiyo masomo aliyopaswa kuyatumia katika utatuzi wa fumbo hilo. Ni somo lielezealo maana ya herufi mbalimbali na maneno, pia ufananisho wa maneno na namba. Alianza na yale majina ya awali aliyokabidhiwa na Rais, ayatambue, kama ni majina halisia ama yapo katika kificho. Aliyadadavua kwa herufi mojamoja. Alivyofahamu akawa na uhitaji wa kufahamu maana ya neno zima. Lakini isivyo bahati, majina yote hayakuwemo katika kamusi. Akaachana nayo. Kisha kuyafanyia kazi yale aliyokutana nayo kitabuni. Alianza na herufi mojamoja akafuatia neno zima, ila neno zima halikuwepo. Yalikuwa maneno yaliyokatwakatwa. Hivyo ikabidi achukue maana jinsi ilivyo. Katika maneno yaliyokatwa alikutana na neno, Ara = 1, Mina = 6 alivyounganisha akapata 16 alivyoenda angalia maana ya kumi na sita kamusini, aliona inamaanisha THE GUADNER ambao kwa umaarufu, alionao katika kazi, alifahamu kuwa mtu aitwaye The guardner ni ‘mlinzi na mshauri wa karibu wa Rais’ na mara nyingi huwa na alama zile alizozibaini. Nembo ya bawa na kidani cha bawa. Hata alivyoyaangalia majina yaliyofuata pia, yalikuwa na maana hiyohiyo aliyokutana nayo awali. Hivyo watu awatafutao ni walinzi na washauri wa karibu wa Rais. Vipi kuhusu yeye?

“Ina maana hadi mimi ni Guardner? Lakini mbona niko ndani ya PSS,” alijiuliza James na kusita kwa muda kisha akaendelea.

“Yumkini ni sahihi. Ila niliyopo mafunzoni, ndiyo maana nimekosa cheni. Vipi kuhusu yule mama pia? Naye ni Guardner? Inabidi nimfuatilie kiundani. Anaweza akawa yupo miongoni mwa watu niwafuatiliao. Na kama hayupo, basi atanipa mwanga, wa kuwapata hawa.”



Siku iliyofuata alianza mfuatilia kama alivyojiapiza. Kila baada ya muda wa dakika kadhaa, hakuisha kutembelea maeneo jirani na hoteli ya J&I kutazamia wenda anaweza muona. Ilikuwa shughuli ya asubuhi, mchana na usiku, ila hakubahatika fanikiwa katika siku zote alizozuru maeneo hayo, kumuona. Alivyojaribu kuwaulizia baadhi ya wahudumu, nao hawakumpatia ushiriakiano wa aina yoyote.

“Hatuna mhudumu kama huyo, hapa kazini kwetu,” wengi wa wahudumu walijibu. Kauli iliyomtatanisha.

“Jamaa! Una uhakika yule mama niliyekuulizia ile siku ni mhudumu wa hoteli ya J&I?” aliuliza James. Kumuulizia kijana aliyemfahamisha siku mama huyo alivyokuja ofisini kwake kupata huduma.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ndiyo. Vipi?”

“Nimejaribu kumuulizia hapo hotelini, wahudumu wengi wanadai hawamfahamu. Ama kuna hoteli nyingine ya J&I hapa mjini?”

“Hapana! Hoteli ni ileile moja. Hao watakuwa wamekuongopea, ama yawezekana kweli hawamtambui. Mwenyewe si ulimuona akiwa kavaa sare za pale hotelini?”

“Eeh! Ndipo nashangaa. Wahudumu wenziye wanadai hawamfahamu.”

“Kama hautojali, unaweza nishirikisha katika mpango wa kukuhakikishia kuwa yule mama ni mfanyakazi wa ile hoteli.”

James alifikiria kwa dakika chache. Takribani mbili baada ya hapo akatoka na jibu la ombi la kijana huyo. Aitwaye Mashaka. Ambaye ni Dereva taksi.



Kesho yake walianza kazi pamoja. James hakufungua ofisi siku hii. Mapema mno saa kumi usiku, waliamka na kwenda kutega eneo jirani na hoteli ya J&I kutazamia wahudumu, wageni na wafanyakazi wengineo waingiao. Walishuhudia kuanzia mhudumu wa kwanza, hadi wote walivyomalizika, kulivyokucha, hawakumuona mlengwa. Ila hawakukata tamaa. Walijithibitishia nia itimie ndipo waendelee na mipango mingine. Muda wa chai na chakula ulivyowadia waliingia ndani ya gari na kupata. Kwani walikwishapika vitu vyote vitakavyowatosheleza kwa muda wote wataokaa mahali hapo. Mambo yalikuwa magumu. Dalili za kufanikiwa zilikosekana, mawazo mengine yakawakumba. Yamkini wamtafutao kasafiri. Hivyo wajaribu siku zifuatazo. Kiza kilivyoingia, walichoka zaidi. Hamu ya kuondoka iliwapanda, wakaingia garini, Mashaka akaitekenya gari, aina ya Toyota Mark II tayari kwa kuianza safari. Alikanyaga mafuta, kisha wakaanza liacha eneo hilo, huku wakiangaza namna wahudumu walivyokuwa wanakaza kutoka ndani baada ya muda wa kazi kufika tamati. Mwendo wa mita kumi, upande mwingine wa hoteli. Walishuhudia, gari dogo, aina ya Audi A4 ikitoka ndani ya jengo hilo. Eneo la maegesho ya chini. Ghafla! Walishauriana kulifuatilia. Kilichowahimiza, sehemu ya kibao cha namba ya usajili wa gari hiyo, kulikuwa na kibao chenye bendera na ngao ya taifa mbele yake. Namba ambazo, kwao ndiyo mara ya kwanza kuziona.

“Ifuatilie ile gari,” alisema James.



Pasi na chelea! Mashaka aligeuza gari kisha kuanza ifuata nyumanyuma. Aliendesha kawaida, ili wasigundulike kama wana nia mbaya na watu walioko gari ya mbele yao. Ilivyoongeza mwendo nao waliongeza kiasi, hadi sehemu ya mwisho, ambapo walishuhudia gari ikiingia baada ya geti lilipo kufunguliwa na kiungambali. Wao walisimamisha la kwao umbali wa mita kadhaa. Walitulia kwa muda, kisha kuiona ikitoka. Ndani kukiwa na dereva pekee. Waliweza tambua hilo, kwa kuwa vioo havikufungwa na taa za ndani zilikuwa zimewashwa. Walifikia maamuzi ya kulifuatitia kwa mara nyingine, kutambua wapi linaelekea. Na kufanya hivyo. Awamu hii namba ya usajili ilibadilishwa, ilibandikwa nyingine, iliyosomeka DB 97 33 MNG. James aliinakili namba hiyo katika kitabu chake cha kumbukumbu kisha safari ikaiva. Moja kwa moja waliishia jirani na eneo la maegesho la magari na vyombo vingine vya moto vya usafiri vya serikali, mtaa wa Namarupi.



Baadaye waligawana majia. Mmoja alielekea hotelini, kisha mwingine alirejea kule, kwenye nyumba watokako. Ambaye ni James. Alitafuta eneo akaketi. Punde baada ya kupasafisha kinaga ubagha, na kufanya makazi yake, ili ashuhudie alicholenga. Hali ya hewa ikamfanya awe anasinzia sinzia kila baada ya muda fulani, hivyo baadhi ya vitu vilivyokuwa vinaendelea alishindwa kushuhudia. Alivyokuja kuamka alikuwa anaweweseka kwa kuona ashapitwa na mengi, kitendo kilichoambatana na kuangalia saa, aliyovaa mkononi. Ilivyowadia saa nane usiku, alizinduka kupitia muito wa alam aliyotega. Alipikicha macho na kukaa kidete, macho pima langoni. Haikupita muda mrefu. Lango lilifunguliwa. Lililomsukuma macho na akili kuhamishia huko. Sekunde kadhaa baadaye alishuhudia gari dogo, ileile ya jana ikiingia ndani, ikiwa na namba nyingine ya usajili. Iliyosomeka AA MNG katikati ya hizo namba kukiwa na picha ya ngao ya taifa. Alizinakili pia kwenye kitabu chake cha kumbukumbu kisha kujiweka sawa kusubiri lijalo. Hakuna lililopita kwake pasipo kuweka alama, kwani aliamini ndiyo msaada wa siku zijazo, katika safari yake ya mafanikio, kukamilisha kile alichoagizwa.



Nusu saa baadaye aliishuhudia ikitoka. Naye kunyanyuka pale alipoketi, alivyoachwa umbali wa takribani mita themanini, alianza ifuata na kumtaarifu mwenziye awe makini, kwani aliamini moja kwa moja uelekeo utakuwa huko. Mashaka alitii. Kwa kujiweka sawa na kuufanya mwili wake kuwa changamfu. Ang’amue kwa usahihi lolote lipitalo mbele yake na si kwa ubashiri. Mwendo wake ulikuwa mchakamchaka wa wastani, kama mtu afanyaye mazoezi, asibainike na wala hakuruhusu kuikaribia. Kufanya hivyo, aliamini mpango wake utaharibika. Pale ilipomuacha, umbali mrefu, uliomfanya ashindwe kuliona, hasa konani, ndipo aliongeza mwendo ili aweze kuliona, akishafanikiwa hurudi kawaida. Wakati huo pia, gari iliwekwa namba nyingine. Iliyosomeka AA 16AA katikati kama ilivyo ada, kulikuwa na picha ya ngao ya taifa. Hii nayo aliinakili kitabuni. Kisha kumpa fursa ya kuchanganua nini maana ya mabadiliko hayo ya mara kwa mara. Alifanya tafakuri ya kina kuhusu hilo, lakini hakung’amua kitu, kila aliwazalo aliona halihusiani na shughuli iliyoko mbele yake. Ila hakutaka kuyapotezea.



Alivyofika hotelini aliungana na mwenziye. Mashaka! Wakahabarishana kila kilichojiri, kisha kutega kutazamia kama kuna gari nyingine inaweza wasili hotelini hapo na kutumia lango hilo. Walikaa kwa muda mrefu, pasi na mafanikio ya matazamio yao. Hakuna gari iliyowasili kwa muda wote waliokaa. Gari zote zilizowasili zilitumia maegesho ya wazi yaliyoko mbele ya jengo. Baadaye walifanya udadisi, kulikoni? Kwa wahudumu, walinzi na wageni wazoefu watumiao hoteli hiyo. Kwani kipindi James (Sadiki) alifanya makazi yake hapo, hakufahamu mazingira ipasavyo, na wala hakuwahi huliza ama kuona kitendo hicho. Kwa kuwa muda mwingi alikuwa hapatikani. Ni muda wa kulala pekee, ndiyo alitumia muda mwingi kuwepo. Tena sio siku zote. Ni siku chache tu.

“Kwanini gari nyingi zinatumia hayo maegesho ya mbele,” aliuliza James kwa mhudumu mmoja wa kike ambaye alikwishajenga mazoea naye pindi yuko hapo.

“Ndiyo maegesho pekee yaliyopo. Hamna maegesho mengine zaidi ya hayo,” alijibu mhudumu huyo. Jibu lililowapa sintofahamu kina James. Na kumpa msukumo Mashaka wa kutaka kuuliza, ila James akamsitisha.

“Acha!” alisema James akiwa ameziba mdomo wa Mashaka kwa kidole chake cha shahada.



Waliachana na mhudumu huyo na kwenda kumuuliza mwingine. Lakini jibu lilikuwa ni lilelile. Halikubadilika. Nao kufanya wasiridhike na jibu wapatiwalo. Wakazidi hoji watu mbalimbali, ila wale wenye ujuzi wa mambo ya kiusalama wakawafungia kazi. Wawaeleze kwanza sababu ya kuhoji ndipo wawajibu.

“Ninyi kina nani hadi muniulize hivyo? Mna lengo gani?” aliuliza mteja mmoja punde alivyohojiwa. Swali lililowafanya kina James wasite kwa muda kisha kujibu.

“Nasi ni wateja wa hoteli hii, tuna usafiri wetu, lengo tuegeshe egesho la chini kama lipo. Maana tuna muda mrefu wa kukaa hapa hotelini, halafu hatutotumia mara kwa mara usafiri tulionao,” alisema James. Kwa kumuongopea.

“Nendeni kwa meneja wa mapokezi pale, mukaulize. Hawa wahudumu wengine ni wachanga. Hawana muda mrefu kazini.”

“Ahsante!” walisema kwa pamoja na kuondoka.



Sababu James alikwishazoeleka na baadhi ya wahudumu, hakufanya vile alivyoambiwa. Matokeo yake alimuamuru Mashaka waondoke mazingira hayo. Waliondoka mashaka akiwa njiapanda, kulikoni James kafanya hivyo na si vile walivyoelezwa. Alivyojaribu kutaka kuhoji, alikatishwa kwa maneno machache tu yaliyompa moyo kwa muda. Ila baadaye mawazo juu ya tukio hilo yalijirudi.

“Usiwaze sana kijana. Kesho nayo ni siku. Tutarudi tena. Wacha kwa leo tukapumzike kwanza,” alisema James wakiuacha uga wa maegesho wa hoteli hiyo.



Upande wa pili taarifa walizopatiwa ziliwapa ukakasi. Inawezekana vipi wahudumu wasifahamu mazingira ya eneo wafanyialo kazi. Hivyo ikawafanya waingie kwenye tafakuri, kila mmoja na mtazamo wake, halmashauri ya kichwa chake ilivyomuaminisha. Mashaka alihisi, gari waliyokuwa wanaifuatilia ndiyo hutumiwa na Mama wamfuatiliao, wakati huo James, alihisi mchezo mchafu unaoendelea kufanyika ndani ya hoteli hiyo. Unaomhusisha Mama huyo. Kuna muda, kwa pamoja walihisi kile wakishuhudiacho ni mambo ya kimazingara, kauli waliyojipinga nayo wenyewe pale waonapo hawana ufundi wowote kuhusu kitendo hicho. Habari ya Joram Isaac, hapa ilisahaulika. Mama alifungua ukurasa mwingine kwa James. Alimuongezea jukumu, japo haina uhakika kama lilikuwa linahusiana na lile alilopatiwa na Mhe. Rais, Ndg. Mlunji.



Zoezi lilisitishwa saa nne asubuhi. Kwa kisingizio cha James kuwa amechoka. Alirudi nyumbani, na Mashaka naye alirejea kwake baada ya kufanyiwa malipo ya kina ya pesa kwa shughuli aliyofanya. Alivyofika nyumbani hakupumzika. Kama alivyomhaidi Mashaka. Aliendelea na kazi. Awamu hii alizifanyia kazi, zile dondoo alizopata na kunakili kitabuni. Ila kabla ya zoezi kuanza, alishika kitabu chake, kuanza kusoma. Alipitia kurasa kadhaa, katika mada iitwayo UTAMBULISHO WA VIONGOZI NA ZANA ZAO. Mada ielezeayo muundo na vitu watumiavyo sana viongozi wakiwa kwenye majukumu. Alitumia takribani dakika kumi na saba, kuimaliza kusoma mada hiyo. Alivyohitimisha alifunika na kuhamia zoezi lingine mbadala. Alianza kuoanisha yale aliyopata kitabuni na pindi yuko doria za kumsaka yule Mama. Kwa msaada wa kamusi na kitabu cha kumbukumbu ya matukio muhimu yaliyotokea nchini mwao miaka ya nyuma.



Palipo mshinda, alijaribu kufanya mawasiliano na wenziye. Wampatie msaada, lakini isivyo bahati, mawasiliano yake kwenda kwao, na ofisi za idara kwa ujumla yalifungwa. Alihitajika ahangaike mwenyewe, pasi na msaada toka idarani. Jambo lililo ngumu kwa upande wake. Kutokana na ufinyu wa taaluma katika baadhi ya hatua za kiusalama. Japo ndiye mwanaPSS anayeaminiwa zaidi kuliko wote idarani. Siku hii alikesha pia. Majukumu yalimzidi, na yote alilazimika kumaliza siku hiyohiyo, ili aamkapo kesho aamke na kitu kingine. Hata siku iliyofuatia nayo, hakukamilisha. Lilikuwa zoezi gumu, lililoichanganya na kuitafakarisha akili yake kwa kina ipate ufumbuzi. Sababu, herufi hizo zilikuwa za kificho sana. Zilifichwa kwa lugha ya picha. Hivyo alipaswa kuzichambua picha zilivyo ndipo apate maana. Kukesha tena ilimlazimu, hadi afanikiwe kwani hakuhitaji kukatisha.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Usiku wa saa tisa. Ndipo alifanikiwa. Kupata maana halisi ya namba za usajili zilizokuwa zinatumiwa kwenye lile gari. Namba za kiserikali. Idara kongwe iliyopo ndani ya usalama wa taifa. Ambapo maana ndani ya kamusi zilisomeka; AA – Kiongozi wa shughuli za serikali ( Waziri Mkuu) MNG – Kifupi cha utaifa (Mangaka) AA MNG – Waziri Mkuu taifa la Mangaka, AA 16AA – Mlinzi na mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu (Guardner). DB – Kiongozi Mkuu wa walinzi wanawake ndani ya PSS. DB 97 33 MNG – Kiongozi Mkuu wa walinzi wanawake wa tisini na saba Mangaka.

“Pumbavu! Yule mama ni mlinzi na mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu. Lakini kwanini anafanya kazi hotelini?” alijiuliza James kimoyomoyo. Hali iliyompa shauku ya uhitaji wa kuonana naye muda huohuo. Aliyefahamika kwa jina la Mama Tausi.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog