Simulizi : Peniela (2)
Sehemu Ya Nne (4)
Sura ya John ikabadilika ghafla baada ya kuwaona watu wawili wakiwa wameongozana na Peniela wakiingia ndani
“ Hebu rudisha nyuma niwaone vzuri watu hao walioongozana na Peniela” akasema John.Josh akarudisha nyuma
“ Ok simamisha” akasema John na kuyaelekeza macho katika sura ya Mathew.
“ Sura hii ni kama ninaikumbuka.Hii si sura ngeni kwangu.Nimewahi kuiona wapi? Akawaza
“ Kumbu kumhu zangu ziko sawa kabisa sura hii nimewahi kuiona sehemu .Lazima nikumbuke nimewahi kuiona wapi? Akafumba macho na kujaribu kumbuka niwapi amewahi kuiona sura ile lakini kumbukumbu hazikuja
“ yawezelana nikawa nimeonana naye kwa miaka mingi iliyopita lakini sura hii ninaikumbuka kabisa na ninaifahamu.Nitarejesha kumbu kumbu hadi nimfahamu mtu huyu ni nani.” Akawaza John
“ Karibu tena nyumbani Eli.Hapa ni sehemu ambayo tunaweza kuamini ni salama zaidi kuliko kule ulikokuwa” Mathew akasema akimkaribisha nyumbani jaji Elibariki.
“ Ahsante sana Mathew.Niliamini kule ningekuwa salama na hakuna yeyote ambaye angeweza kuhisi kwamba niko kule lakini sifahamu nini kimetokea hadi nikafahamika.Hata hivyo nashukuru mmekuwa karibu name na mmenisaida kunitoa kule.” Akasema jaji Elibariki
“ Siku zote hapa ni nyumbani kwako na ni sehemu salama.Hapa tuna uhakika kwamba tutakulinda kwa gharama zozote zile hata kama ni kwa kuyatoa maisha yetu kama alivyofanya Noah.This is our job and that’s what we do” akasema Mathew.Kauli ile ikamkumbusha Elibariki kuhusu Noah,akaumia sana
“ Kila ninapomkumbuka Noah ninasikia uchungu mkubwa.Ninalikumbuka tukio lile Lilikuwa ni tukio la kutisha sana.Risasi zilivuma kama vile tuonavyo katika flamu lakini hii haikuwa filamu bali ni tukio halisi.” akasema jaji Elibariki.Kimya kikatawala mle sebuleni halafuMathew akasema
“Pole sana Elibariki.Tunashukuru umetoka salama katika ajali ile.Ninaamini huu ni mpango wa Mungu kukuacha hai.Kwa hiyo basi kwa vile wamekukosa sasa kinachofuata ni zamu yao.Tutawatafuta wale wote waliofanya tukio hili na tutawapata.Mimi na Anitha hatutalala usingizi hadi tuhakikishe kwamba tumewapata wale wote waliofanya shambulio lile na kumuua Noah.Tumeumizwa sana kwa mauaji yale ya kikatili .Hatusemi kwamba tunakwenda kulipiza kisasi bali tunataka waovu wapatikane na walipie uovu wao.Lazima tuwajue ni akina nani na nini lilikuwa lengo lao la kutaka kukuua.Ili kuwapata watu hawa tunahitaji sana msaada wako na ndiyo maana nikakuhakikishia kwamba tutakulinda kwa gharama zozote zile.Tutahakikisha unaendelea kuwa salama kwa hiyo basi kabla ya yote tungependa kusikia na kulifahamu kwa upana wake tukio lile lilivyotokea na kama kuna yeyote uliyemuona au unahisi anaweza akahusika na tukio lile.” Akasema Mathew.Jaji Elbariki akatazama juu kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“ Kama utakumbuka nilikupigia simu na kukwambia kwamba kuna jambo ambalo ninahitaji kukueleza”
“ Ndiyo ninakumbuka Eli.” Akajibu Mathew
“ Jambo lenyewe lilianza katika ile taarifa ile ya kifo cha Dr Flora mke wa rais uliyonipatia” akasema jaji Elibariki akanyamaza kidogo halafu akaendelea tena
“ Niliiwasilisha taarifa ile kwa familia ya rais na tulimkabidhi rais mkononi na akaahidi kuifanyia kazi.Skuwa na wasiwasi hata kidogo na taarifa ile na niliamini itafanyiwa kazi.Jioni ya siku ile ambayo Dr Flora aliagwa katika viwanja vya ukombozi nilikuwa nimekaa na majaji wenzangu waliokuja kunipa pole kwa msiba wa mama mkwe,nikapigiwa simu na mke wangu na kunitaka nikaonane naye ndani.Nilikwenda kuonana naye na kumbe aliniita nikahudhurie kikao cha familia.Dr Joshua alifika katika kile chumba cha maongezi na ilionekana wazi hakufurahishwa na uwepo wangu pale lakini sikulijali hilo kwani nilikwisha zizoea dharau za familia ile.Kilichonistua ni baada ya kumsikia Dr Joshua akisema kwamba kikao kile ni kwa ajili ya kuisoma taarifa ya madaktari bingwa waliyoitoa baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora.Nilimuuliza Dr Joshua uchunguzi ule ni uchunguzi gani tena wakati nilikwisha leta taarifa za kilichomuua Dr Flora? Nilimchokoza nilipouliza vile na Dr Joshua akaanza kuniporomoshea maneno ya kashfa na dharau.Aliikosoa taarifa ile niliyompelekea na kuiita ni taarifa ya kihuni na ya kuungaunga.”
“ What ?!!..Aliikataaa taarifa ile tuliyoihangaikia usiku kucha? Akauliza Mathew
“ Ndiyo.Aliikataa kabisa na kusema kwamba ni ya kihuni na imejaa uongo mkubwa “
“taarifa iliyotoka kwa hao madaktari bingwa ilieleza nini? Akauliza Mathew
“ Taarifa hiyo ya madaktari bingwa ilisema kwamba Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu na hakukuonekana dalili zozote za sumu katika mwili wake.”
“ Unasema ?! Mathew akaendelea kushangaa
“ Taarifa ya madaktari bingwa ilionyesha kwamba Dr Flora alikufa kutokana na shinikizo la damu na hakukuonekana kuwapo kwa chembe chembe zozote za sumu katika mwili wake.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ This cant be..Taarifa hiyo si ya kweli.Ninawaamini madaktari wale waliofanya uchunguzi ule.Ni madaktari bingwa na walitumia muda mwingi kuutafuta ukweli.Kuna kitu kinafichwa kuhusiana na kifo hiki cha Dr Flora.Kuna kitu kinachoendelea ikulu” akasema Mathew na Dr Joshua akaendelea
“Familia ya rais wote walionekana kuikubali taarifa ile ya madaktari bingwa na hivyo taarifa ile ambayo tuliihangaikia ikatupwa kapuni.Nilikasirika sana na sikutaka tena kuendelea kukaa pale nikaondoka na kuja hapa nikakukosa .Nilipokuwa hapa mke wangu akanipigia simu na kunitaka nikaonane naye kuna masuala muhimu anataka kunieleza.Nilimuaga Noah lakini akaomba tuongozane kwa kuwa alikuwa amechoka kukaa nyumbani peke yake.Kwa kuwa nilikuwa nakwenda mara moja na kurudi nikakubali kuongozana na Noah bila ya kujua kwamba ile ilikuwa ni safari yake ya mwisho.Alisema kwamba alitaka kuufanyia mazoezi mguu wake uliopata jeraha wakati wa kumkomboa mke wa Dr Michael .Nilimuachia gari aendeshe na akaendesha vizuri sana tukafika katika makazi ya rais nikaonana na mke wangu lakini tukashindwa kuelewa.Nilimsisitiza kwamba taarifa ile inayodaiwa ni ya madaktari bingwa haikuwa na ukweli wowote ndani yake na kwamba kuna kitu kinajaribu kufichwa.Pamoja na kujitahidi sana kumuelewesha lakini hakuwa tayari kunielewa nikaachana naye na kuondoka.Nilipokishika tu kitasa cha mlango wa gari langu nikapigiwa simu na mwanamke ambaye sikumfahamu ni nani na akanieleza kwamba nisiingie katika gari langu kuna mpango wa kuniua.Hakunitajia jina lake na wala ni akina nani wanaotaka kuniua na kwa kuwa nilikuwa na hasira nilimpuuza na kuingia garini tukaondoka.Sikuwa na wasiwasi wowote kwamba tunaweza kutokewa na tukio lile.Tulipofika katika taa za kuongozea magari za makutano ya barabara ya Mkwavinyika na Kilimanjaro tulisimama katika foleni tukisubiri kuruhusiwa na ndipo lilipotokea shambulio lile. Ninachokumbuka ni kwamba zilitokea piki piki mbili na ghafla Noah akanirukia na kunigandamiza katika kiti na kilichofuata ni milio ya risasi.Nilimsikia Noah akigugumia kwa maumivu kadiri risasi zilivyokuwa zinaingia katika mwili wake.” Jaji Elibariki akashindwa kuendelea kusimulia akanyamaza .Anitha akashindwa kuendelea kukaa pale sebuleni akainuka na kuelekea chumbani kwake akilia.
“ Tuendelee” akasema Noah.
“Baada ya muda mlango wa gari ukafunguliwa na mwanamke mmoja aliyekuwa ameifunika sura yake akanitoa katika lile gari lililoharibiwa vibaya kwa risasi na kuniingiza katika gari lake tukaondoka kwa kasi eneo lile.Nilikuwa nimechanganyikiwa na sikuelewa alikuwa ananipeleka wapi.Mpaka leo hii simfahamu mwanamke yule ni nani na kwa nini aliniokoa.Tukiwa garini akaniuliza kama kuna sehemu ambayo ninaamini ni salama kwa mimi kwenda kujificha kwa muda na sehemu ya kwanza iliyonijia akilini ni kwa Peniela. Kwa bahati nzuri nimekuwa mwepesi sana wa kuzikariri namba mbali mbali za simu na hivyo nikazikumbuka namba za Peniela na Yule mwanamke akampigia na kumuelekeza sehemu atakayotukuta.Peniela akaja akanichukua na kunipeleka kwake.Nikiwa kule kwa Peniela niliwasiliana na wewe na kukufahamisha kwamba niko salama.Hivyo ndivyo namna tukio zima lilivyotokea “ akasema jaji Elibariki.Kimya kikatawala pale sebuleni .Anitha akarejea
“ samahani jamani nilishindwa kujizuia kulia kwa maelezo yale ya Elibariki” akasema Anitha
“ Its ok Anitha usijali” akasema Mathew na kumgeukia Elibariki
“ Elibariki pole sana .Kama nilivyosema awali uko hai sasa kwa uwezo wa Mungu tu na ana sababu zake za kwanini uko hai mpaka leo hii ” akasema Mathew
“ Kuna vitu ambavyo vimejitokeza katika maelezo yako ambavyo vimetuwashia mwangaza na kutuelekeza njia ya kupita ili kuwabaini waliofanya tukio hili.” Akasema Mathew
“kwanza ni hiyo ripoti inayodaiwa ni kutoka kwa madaktari bingwa,pili ni simu uliyopigiwa na mwanamke usiyemfahamu akikuonya kuhusiana na mpango wa kukuua na tatu ni mwanamke aliyekuokoa.Hivi ni vitu vitatu ambavyo vinaweza vikatufikisha mahala tunakopataka yaani kuwapata waliofanya shambulio lile .Sina shaka yoyote na ukweli wa taarifa ile niliyokupatia ambayo ninaamini ndiyo ya kweli kuhusiana na kilichomuua Dr Flora. Watu waliomuua Dr Flora toka mwanzo walifahamu kwamba kuna uwezekano wa kilichosababisha kifo cha Dr Flora kufahamika kwa hiyo wakajiandaa mapema.Kitu cha kwanza walidhibiti uchunguzi usifanyike kwani endapo uchunguzi wowote ule ungefanyika basi ingebainika sababu ya kifo chake na ndiyo maana taarifa za sisi kufanya uchunguzi zilipowafikia ziliwastua sana na kutuma kikosi cha wanajeshi waje watukamate.Hii inaonyesha wazi kwamba kwa gharama zozote zile kilichomuua Dr Flora kitaendelea kuwa siri.Tulipofanikiwa kuipata taarifa ilena ukaifikisha mikononi mwa rais ninaamini walistuka na wakaja na taarifa mpya wanayodai imetolewa na madaktari bingwa.Unaona mahalali walipojikoroga ? Mwanzo hawakutaka uchunguzi ufanyike lakini baadae wanakuja na taarifa ya uchunguzi wa madaktari bingwa.Hii inaonyesha wazi namna walivyochanganywa na taarifa ile ya kwetu.Ili tuwe na uhakika mkubwa na ushahidi mzito i tunatakiwa tuipate hiyo ripoti na tuifanyie uchunguzi ili kubaini ukweli wake.Nguvu kubwa inatumika kuuficha ukweli wa kifo cha Dr Flora ninaamini lazima kuna sababu kubwa nyuma yake ambayo tunatakiwa kuifahamu. Pili tunatakiwa tumfahamu mwanamke aliyekupigia simu ni nani.Huyu ni muhimu sana kwetu kwani ndiye anayewafahamu watu waliotaka kukuua.Huyu ni muhimu mno kumjua.Tatu ni mwanamkealiyekutoa eneo la tukio na kukukabidhi kwa Peniela.Tunataka kumfahamu ni Nani na kwa nini alikutoa pale katika eneo la tukio? Akasema Mathew
“ Mathew uko sahihi kabisa ingawa kuna jambo ambalo umelisema ambalo linaweza likawa na ugumu kidogo kutekelezeka . Ni kuhusu kuipata ripoti hiyo ya madaktari bingwa .Taarifa hiyo anayo rais na sina hakika kama anaweza akitoa kwa mtu mwingine yeyote.” Akasema Mathew
“ Mke wako ni mtoto wa rais kwa hiyo tutamtumia katika kuipata taarifa hiyo.Ninaamini hawezi kukataa kukusaidia ” Akasema Mathew
“ Sina hakika kama mke wangu anaweza akakubaliana nami kwani nimekwisha kwaruzana naye kuhusiana na jambo hili la kuhusiana na ripoti hizi ” akasema Elibariki
“ She’s your wife and you know how to make her understand you.Tumia kila ainaya ushawishi hadi akuelewe.Ni muhimu sana tukaipata ripoti hiyo .Anitha atakupatia simu ambayo utaitumia kuwasiliana na mkeo.Kitu cha pili tunatakiwa tuifanyie uchunguzi namba ile aliyoitumia yule mwanamke kukupigia na kukutaarifu kuhusiana na mpango ule wa kukuua.Anitha ni mtaalamu sana katika sehemu hiyo na atafanikiwa kumfahamu huyo mtu ni nani kisha tutamfuatilia.Tukisha mpata tutafahamu kama ndiye yule ambaye alikutoa eneo la tuko au ni watu wawili tofauti.” Akasema Mathew
“ Tukiachana na hayo” akaendelea Mathew
“ Kuna mambo kadhaa ambao tumeyagundua kuhusiana na kazi ile uliyotupatia ya kuchunguza kuhusu kifo cha Edson na nani alimuua.”
“Mmempata muuajiwa Edson tayari ? Akauliza Elibariki kwa mshangao
“Ndiyo tayari tunafahamu Edson aliuawa na nani ” akasema
“ Ulikuwa sahihi kumuachia huru Peniela kwani si yeye aliyemuua Edson.”
“ Ouh Ahsante Mungu.” Jaji Elibariki akainua mikono juu na kumshukuru Mungu
“ Kumbe nilikuwa sahihi kumuachia Peniela.Kulikuwa na kila ushahidi uliotosha kabisa kumtia hatiani lakini nafsi yangu ilikataa kabisa kwamba Peniela hakufanya kitendo kile .” akasema Jaji Elibariki
“ Nyie majaji ni watu ambao Mungu anawaongoza ili mtoe hukumu ya haki na ndiyo maana ukagundua kwamba Peniela hakuwa na kosa.” Akasema Mathew
“Uko sahihi kabisa Mathew.Kesi ile ni moja kati ya kesi ngumu kuwahi kuitolewa maamuzi.Nilimuomba sana Mungu anisaidie niweze kutenda haki.Ni nani waliomuua Edson? Akauliza jaji Elibariki
“ Kabla ya kifo chake Edson alikuwa amejiunga na matandao wa watu watatu,yaani yeye ,mzee Matiku na na mzee Mustapha.Kwa pamoja walikuwa na biashara ambayo endapo ingefanikiwa ingewaingizia mabilioni ya fedha.Kuna nyaraka zilizokuwa zinatakiwa kuibwa Ikulu na ili kuzipata nyaraka hizo iliwalazimu Mustapha na Matiku kumshirikisha Edson ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ikulu.Edson alifanikiwa kuziiba nyaraka hizo ikulu na kumpatia mzee Matiku.Kabla hawajaziuza ,kwa tamaa ya kupata fedha nyingi,Mzee Mustapha na Edson wakamzunguka mzee matiku na kuziiba zile nyaraka kwa kumtumia msichana aliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mzee matiku na nyaraka hizo akakabidhiwa mzee Mustapha.Matiku alipogundua kwamba ni Edson na Mustapha ndio waliofanya wizi ule wa nyaraka kwa lengo la kugawana pesa nyingi wenyewe, alikasirika sana na kuamua kuvujisha siri ile kwa viongozi wa Edson na baada ya wiki moja toka igundulike kwamba ni Edson ndiye aliyeziiba nyaraka zile ikulu akauawa na kesi ya mauaji hayo ikamuangukia Peniela.”
“ Oh my God ! akasema Elibariki.Alistushwa sana na taarifsa zile
“ Kwa hiyo Edson aliuawa na ikulu kutokana na wizi wa hizo nyaraka ambazo tunazo hapa nitakuonyesha.”akainuka Mathew na kuelekea chumbani kwake akafungua kabati analohifadhia nyaraka za siri akatoa ile bahasha iliyokuwa na zile karatasi zilizoibwa ikulu.
“ karatasi zenyewe ni hizi hapa”akasema Mathew na kumkabidhi Elibariki zile karatasi akazitazama akashindwa kuzielewa.
“ Hiki ni kitu gani ? Karatasi hizi ni za nini? Akauliza Elibariki akiendelea kuziangalia karatasi zile bila kuzielewa
“ Hizi ni fomula za kisayansi na sisi sote hapa hatuelewi nini kilichoandikwa humu.” akasema Mathew
“ Hizi ndizo karatasi alizoziiba Edson na ndizo zilizotoa uhai wake ? Akauliza jaji Elibariki
“ Ndiyo.Ni hizi karatasi,hata sisi tulishangaa sana tulipozipata .Hatua ya kwanza tumeimaliza na tayari tunafahamu ni kwa nini Edson aliuawa na sasa tunaingia katika hatua ya pili.Tunataka kulichimba suala hili kwa undani zaidi.Tunataka kulichimba suala hili hadi mzizi wake.Tunataka kufahamu karatasi hizi zina umuhimu gani na kwa nini walitaka kuziuza kwa mabilioni ya fedha.Mtu aliyekuwa akitaka kuzinunua karatasi hizi tumemfahamu , ni mtu tajiri sana anaitwa Habib soud anatokea nchi za kiarabu.” Mara Mathew akastuliwa na simu yake iliyoitwa.Alikuwa ni Eva.
“ hallow Eva” akasema Mathew
“ Mathew..!! akasema Eva huku akilia
“ Eva kuna nini ? Akauliza Mathew
“ Sabina ..Am…amefariki dunia”
Mathew akabaki kimya kwa dakika nzima ,halafu akasema
“ Pole sana Eva.Pole sana.” Akasema Mathew
“ Damu ya Sabina iko mikononi mwako.Wewe ndiye uliyemuua .I hate you Mathew !..akasema Eva na kukata simu.Mathew akasikitika sana na kumgeukia Anitha
“ Sabina is gone “ akasema Mathew.Anitha akastuka na kushika kichwa.
“ Sabina ni nani? Akauliza jaji Elibariki
“ Ni msichana ambaye alikuwa na hizi karatasi” akasema Mathew.
“ Mungu atampokea ameteseka sana.” Akasema Anitha kwa uchungu
“ yah.” Akajibu Mathew na kimya kikapita Anitha akasema
“ Yule jamaa tuliyemuweka mle chumbani una mpango naye gani?
“ hatuna kazi naye tena.”
“ Are we going to free him? Akauliza Anitha
“ Hapana hatuwezi kumuachia.Huyu ni jambazi sugu na yeye na wenzake wamekwisha fanya makosa mengi kwa hiyo tutamuweka humu ndani na baada ya kumaliza kazi zetu tutamkabidhi kwa vyombo vya usalama” akasema Mathew.
“ Ok tuendelee “
“ Kitu cha kwanza ambacho tunatakiwa kukifahamu kwa haraKa ni kwamba karatasi hizi ni za nini na kwa nini zina thamani kubwa namna hii ya mabilioni ya shilingi? Tunatakiwa tumpate mtu wa kutoka ndani ya ikulu ambaye anaweza akatufafanulia kuhusiana na umuhimu wa karatasi hizi na kwa kuzifanya ziwe na thamani ya mabilioni ya shilingi.Hapa ninamaanisha kwamba tukifanikiwa kumpata mheshimiwa rais inaweza ikawa ni vizuri zaidi kwani yeye anaweza akawa na ufahamu mkubwa zaidi wa kuhusiana na karatasi hizi.Kwa kuwa unaukaribu na rais inaweza ikawa ni rahisi kutuunganisha naye lakini kwa namna ulivyoniambia rais alivyolichukulia suala la ile taarifa uliyompelekea ya kifo cha dr Flora nimeanza kuingiwa na shaka kama anaweza akatusikiliza.Hata hivyo tutatafuta njia mbadala ya kufahamu karatasi hizi ni za nini.” Akasema Mathew. Elibariki alihisi kuchanganyikiwa hakujua aseme nini.
“ Mathew kwa kweli nimekosa neno la kusema.Kwanza ninapaswa niwashukuru sana kwa namna mlivyopambana hadi mkafanikiwa kumpata muuaji wa Edson.Nimestushwa sana na taarifa uliyonipa.Sikuwahi kutegemea hata siku moja kama kifo cha Edson kinaweza kutokea katika mazingira haya.Ahsnateni kwa kuufahamu ukweli na msijali ndugu zangu malipo yenu yako pale pale.Kila kitu tulichosainiana kitakuwa vile vile.”Akasema Elibariki
“ Elibariki huu si wakati wa kuwaza kuhusu malipo.Suala hili ni la kwetu wote na tunalifanya kwa moyo mmoja bila kuhitaji malipo ya aina yoyote..”akasema Mathew
“ Ahsanteni sana.Mimi nawaahidi kila aina ya ushirikiano hadi tulifikishe suala hili mwisho wake.Mambo uliyonieleza yamenifumbua macho sana na kuna kitu nimekigundua kuhusiana na kifo hiki cha Edson.Sijawahi kumueleza mtu yeyote jambo hili ni kwamba kilichonisukuma ili nifanye uchunguzi wa kifo cha Edson ni kutokana na shinikizo nililokuwa nalipata toka kwa rais la kutaka nimfunge Peniela gerezani” akasema jaji Elibariki.Mathew na Anitha wakabaki wanatazamana.
“ Kabla ya kuingia katika mahusiano na Peniela ,Edson aliwahi kuwa na mahusiano na mtoto wa rais aitwaye Anna ambaye walikorofishana baada ya Anna kugundua usaliti aliofanyiwa na Edson.Pamoja na kutengana lakini waliendelea kukutana na kulikuwa na kila dalili kwamba wangeweza kurudiana.Kifo cha Edson kilimuumiza sana Anna ambaye alikuwa na mategemeo makubwa ya kurudiana na Edson.Kwa hiyo basi kifo cha Edson kiliigusa pia familia ya rais.Pamoja na kwamba familia ya rais iliguswa na kifo kile kwani walimfahamu Edson na kumpenda ,lakini kuna kitu ambacho mimi binafsi kilinishangaza sana.Ni shinikizo nililokuwa nikilipata toka kwa rais la kunitaka nimhukumu Peniela kifungo.Rais anafahamu fika kwamba hapaswi kuingilia mahakama kwani ni mhimili unaojitegemea lakini yeye hakulijali hilo na akatoa shinikizo kwamba lazima Peniela akutwe na hatia na kufungwa .Kigezo alichokuwa akikitumia ni kwamba Peniela amemuumiza sana mwanae Anna kwa kumuua mpenzi wake wa kwa hiyo anastahili adhabu kali ya kifungo gerezani.Nilijiuliza sana sababu za rais kutaka kuingilia mahakama nikakosa jibu.Kwa kuwa niliridhika kwamba Peniela hakutenda lile kosa sikulijali shinikizo lake na nikamuachia huru.Niliendelea kupokea lawama nyingi toka kwa familia ya rais na zaidi sana rais mwenyewe ambaye alinitolea maneno ya kejeli .Kutokana na tabia hii aliyoionyesha rais katika kesi ya Peniela na nguvu kubwa iliyotumika katika kuhakikisha Peniela anafungwa gerezani nililazimika kutaka kuchunguza kwa undani kuhusiana na kifo cha Edson.Sijawahi kumweleza mtu yeyote kuhusiana na jambo hili.”akasema jaji Elibariki.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Elibariki maelezo yako yamenipa picha ambayo sikuwahi kuifikiria hata siku moja.Unadhani rais anaweza akahusika katika kifo cha Edson na ndiyo sababu akawa akitoa shinikizo kwamba Peniela afungwe? Akauliza Mathew
“ Siwezi kusema moja kwa moja kwamba rais anahusika kwa sababu bado sina ushahidi lakini kwa namna alivyokuwa akishinikiza Peniela afungwe na kwa maelezo mliyoyapata kwamba Edson aliiba nyaraka ikulu ninashawishika kuamini kwamba Dr Joshua atakuwa analifahamu jambo hili na kuna uwezekano naye akawa alishirki katika kuamuru Edson auawe.” Akasema Elibariki
“ Hata mimi nashawishika kuamini hivyo.Kwa rais kuvuka mipaka yake na kuingilia maamuzi ya Mahakama lazima kuna sababu nzito iliyompelekea akafanya hivyo na zaidi sana ni katika kulinda maslahi Fulani aidha ya kwake au ya washirika wake.Endapo rais atakuwa anahusika katika jambo hili basi nyaraka hizi tulizonazo zitakuwa na umuhimu mkubwa sana na ndiyo maana wale wote waliozishika wamepoteza maisha “ akasema Mathew
“ Mathew kuna jambo lingine ambalo nimekuwa nikilifikiria sana.Kwa mujibu wa mke wangu ni kwamba usiku uliotangulia siku ya kifo chake alipigiwa simu na mama yake na kumtaka waonane siku itakayofuta kuna jambo la muhimu sana ambalo alitaka kuwaeleza yeye na mdogo wake.Mchana wa siku iliyofuata Dr Flora akafariki dunia na hakufanikiwa kuonana na wanae na kuwaeleza alichokuwa amekusudia kuwaeleza.Baada ya Dr Flora kufariki ghafla kuna nguvu kubwa ambayo imeonekana ikitumika ili kuzuia sababu ya kifo chake isifahamike.Usiku ule mkiwa hospitali mkiendelea na zoezi la kuufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora,Anna mtoto wa rais alimsikia katibu wa rais Dr Kigomba akiongea na simu na kutoa maelekezo kwamba mkamatwe haraka sana.Anna alishanmgazwa na kauli ile na alimtaarifu mke wangu kuhusiana na jambo lile naye akanipigia na ndipo nilipowataarifu .Flaviana alimtaarifu Dr Joshua kuhusu kuwa na shaka na Dr Kigomba na rais akaahidi kulifanyia uchunguzi jambo hilo lakini nilistuka siku ile jioni alipodiriki kusimama na kumtetea Dr Kigomba kwamba hahusiki katika jambo hili .Mambo haya aliyoyafanya rais yamenifanya niwe na hisia kwamba yawezekana hata rais akawa ni sehemu ya watu waliomuua Dr Flora.” Akasema jaji Elibariki.Mathew akamtazama kwa makini na kusema
“ Una maanisha rais anaweza akawa amehusika katika kifo cha mke wake? Akauliza Anitha
“ Siwezi kusema moja kwa moja kwamba amehusika lakini ninalazimika kuwa na hisia hizo kutokana na mambo yaliyotokea.Hainiingii akilini eti katibu wa rais akatoa amri kwamba mwili wa mke wa rais usifanyiwe uchunguzi halafu rais Akakaa kimya .Haiwezekani watu wa karibu na rais wakafanya vitendo kama hivi bila ya yeye kufahamu” akasema jaji Elibariki
“ Hata mimi ninaweza nikakubaliana na Elibariki.Inawezekana kabisa rais akawa anahusika katika kifo cha mkewe.Kama Dr Flora aliwapigia simu wanae na kuwaeleza kwamba kuna jambo anataka kuwaeleza na akafariki ghafla kabla ya kuonana nao ninahisi kuna jambo kubwa la siri alitaka kuwaeleza wanae lakini wakamuwahi kabla hajatimiza lengo lake.Hatuwezi kukataa ukweli kwamba kuna kitu kinaendelea pale ikulu na lazima tukijue.Kama mtakumbuka niliwaeleza awali kwamba awamu ya pili ya uchunguzi wetu itahamia ikulu.Tunataka kufahamu kinachoendelea hivi sasa ndani ya lile jumba jeupe.Tunakwenda kumchunguza rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Hii haitakuwa kazi rahisi hata kidogo na ni jambo la hatari kubwa lakini lazima tulifanye ili tuweze kufahamu kinachoendelea pale ni kitugani.Kama tukigundua kwamba rais anahusika katika kifo cha Edson pamoja kifo cha mke wake,basi shughuli tutakayokuwa nayo ni nzito sana.” akasema Mathew
Wote wakabaki kimya ,Mathew akawatazama halafu akaendelea
“ Jamani kabla hatujaendelea mbele napenda niwatahadharishe kwamba tunaingia katika awamu ngumu sana na katika awamu hii chochote kinaweza kikatokea kwa maana hiyo basi umakini mkubwa sana unahitajika.Kitu cha kwanza tunachotakiwa kukifanya ni kuanza kufanya uchunguzi kama Dr Joshau anahusika katika kifo cha mke wake .Sisi tayari tunafahamu kwamba mke wa rais aliuawa kwa sumu lakini rais na timu yake wamekuja na ripoti yao na wanasema kwamba Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu.Tunachotakiwa hapa ni tuipate ripoti hiyo ya madaktari bingwa na tutaifanyia uchunguzi ili kubaini ukweli wake .Tutawafuata madaktari ambao majina yao yatakuwa yameorodheshwa katika taarifa hiyo na tutaufahamu ukweli. Ili kuipata ripoti hiyo mke wako anaweza akatusaidia sana ” akasema Mathew.Elibariki akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Mimi na mke wangu tulikwaruzana kuhusiana na ripoti hiyo na sina hakika kama anaweza akatoa ushirikiano wowote kwangu” akasema Elibariki
“ Eli,huu ni wakati wa kuweka tofauti zenu zote pembeni .Be nice to her,make her understand you” akasema Mathew
“ Mathew yuko sahihi Eli,hata kama mna tofauti zenu lakini yule ni mke wako_Ongea naye vizuri atakusikiliza.Jishushe kwake na utaona atakuelewa na atafanya vile ulivyomuagiza” akasema Anitha
“ sawa nitajaribu lakini sina hakika kama atakubali” akasema jaji Elibariki
“ Lazima atakubali tu.Kama hata kubali basi tutatafuta njia ya kumfanya akubali.” akasema Mathew.Anitha akatoka pale sebuleni na baada ya dakika tatu akarejea akiwa na simu akampatia Elibariki ambaye aliandika namba za simu za Flaviana na kupiga.Simu ikaanza kuita
Simu iliita mara ya kwanza bila kupokelewa,ikaita mara ya pili na safari hii ikapokelewa
“Hallow” ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili ambayo Elibariki aliitambua ilikuwa ni ya Flaviana mke wake
“ hallow Flaviana” akasema Elibariki
“ Elibariki?!!..Flaviana akasema kwa mshangao
“ Flaviana naomba usilitaje jina langu wala kuonyesha mshangao wowote kama uko karibu na watu.” akasema jaji Elibariki
“ Usijali niko mwenyewe chumbani.Ouh Ahsante Mungu.Nimefurahi sana kuisikia tena sauti yako mume wangu.Uko salama? Uko wapi? Nimelia usiku na mchana nikimuomba Mungu akunusuru na hatari yoyote ile” akasema Flaviana na akasikika akilia kwa kwikwi
“ Flavana nyamaza kulia mke wangu ,mimi ni mzima kabisa na ninaendelea vizuri.Nilitoka salama katika shambulio lile,nilipatwa na majeraha madogo madogo tu lakini kwa ujumla niko salama na usihofu chochote mke wangu” akasema jaji Elibariki
“ Elibarikini nashindwa kujizuia kulia kwa kujua uko hai,toka siku ile ulipopatwa na tukio lile chakula hakipiti ninalia usiku na mchana ili uwe salama.Uko wapi mume wangu?akauliza Flaviana
“ kwa sasa niko sehemu salama nimejificha.Sitaki kujitokeza kwani roho yangu inatafutwa kwa gharama kubwa kwa hiyo nitakuwa mafichoni kwa muda .”
“ Elibariki Tutawapata waliofanya tukio lile.Baba ameahidi kufanya kila linalowezekana ili waweze kujulikana . Tafadhali naomba usiogope ,ulinzi uko wa kutosha .Eli siwezi kuishi bila wewe tafadhali naomba ujitokeze urudi nyumbani tuendelee na maisha yetu.Kwa siku hizi chache nimeiona thamani yako kwangu,nimeuona umuhimu wako.imejiona namna nilivyo mtupu bila wewe.Tafadhali Eli kama kuna mambo nilikukosea naomba unisamehe na tuanze upya maisha.I promise I’ll be a good wife to you.Sintokudharau tena kama zamani.Nitakuheshimu na kufanya chochote utakachoniamuru.Ninakupenda sana Eli “ akasema Flavana huku akilia.Maneno yale yakamgusa sana Elibariki.Mathew akamfanyia ishara kwamba aende moja kwa moja katika pointi ya msingi
“ Flaviana nashukuru kwa meneno yako mazuri na kwa kuniombea,ninadhani kwamba kwa sasa utakubaliana nay ale maneno niliyokwambia kwamba hali si nzuri hata kidogo .Pamoja na hatari inayonikabili nakuahidi nitarudi nyumbani lakini kabla ya kurudi kuna jambo nataka unisaidie kwa kila namna unvyoweza.Flaviana wewe ni mke wangu na kwa kipindi hiki ninahitaji msaada wako sana kuliko hata wakati mwingine wowote.”akasema Elibariki
“ Elibariki niko tayari kufanya chochote kwa ajili yako.Tafadhali niambie unahitaji nuikufanyie nini ?akauliza Flaviana
“ Ninahitaji kuipata ile ripoti ya madaktari bingwa ya kuhusiana na kifo cha mama.Nina kazi nayo kubwa sana” akasema jaji Elibariki.Flaviana akakaa kimya kidogo kisha akasema
“ Ripoti ile anayo baba na sina hakika kama anaweza akanipatia mimi au mtu yeyote yule.” Akasema Flaviana
“ Flaviana do something my love.Fanya kila unavyoweza ili niweze kuipata ripoti hiyo” akasema Elibariki.Flaviana akakaa tena kimya kidogo halfu akauliza
“ Unaitaka lini hiyo ripot?
“ Haraka iwezekanavyo na kama ukiweza kuipata usiku huu itakuwa vizuri zaidi” akasema Elibariki
“ Ok ngoja niangalie namna ya kufanya kama nikifanikiwa kuipata nitakutaarifu.”
“ Nashukuru sana Flaviana , nitaarifu mara moja endapo ukifanikiwa na nitakufahamisha ni wapi tukutane ili unipatie.”akasema Elibariki na kukata simu.Mathew akatabasamu na kusema
“ You did great.Your wife loves you so much” akasema Mathew.Elibariki akatabasamu
“ I don’t know” akajibu Elibariki
“ Anyway tuachane na hayo.Wakati tunamsubiri Flaviana apige simu ,mpatie Anitha laini yako ya simu na tuanze kuifanyia kazi ile namba ya yule mwanamke aliyekupigia na kukupa onyo kuhusiana na kuwepo kwa shambulio.” Akasema Mathew na jaji Elibariki akamkabidhi Anitha simu yake na wote wakaelekea katika chumba ambacho wenyewe wanakiita chumba cha kazi.
Flaviana hakuwa na habari kwamba maongezi yote aliyoongea na mume wake Elibariki yalikuwa yakisika katika kifaa Fulani kilichokuwa ndani ya gari moja jeusi lililokuwa maeneo ya ikulu ambalo hutumiwa na watu wa usalama.Flaviana hakuwahi kugundua kama simu yake imeunganishwa na kifaa hicho na kwamba kila atakachoongea simuni basi kitasikika kwa watu wale kupitia kile kifaa cha elektroniki kilichounganishwa na simu yake kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.Mara tu Flaviana alipokata simu bila kupoteza hata sekunde moja jamaa moja aliyekuwa amekaa katika kiti cha kushoto ndani ya lile gari akawageukia wenzake.
“ Jamani nadhani mmesikia kilichoongelewa hapa.Nini ushauri wenu,tumufahamishe Dr Kigomba?
“ Mimi nadhani tufuate maelekezo tuliyopewa.Tumtaarifu Dr Kigomba kuhusiana na taarifa hii.Alitukabidhi kazi hii kwa hiyo lazima tuifanye kama alivyotuelekeza.Mnaijua hatari yake endapo akigundua kwamba tumemficha kuhusu jambo hili” akasema jamaa aliyekuwa katika usukani
“ Hata mimini nashauri tumtaarifu tu Kigomba.” Akasema jamaa mwingne aliyekuwa amekaa katika kiti cha nyuma.Yule kiongozi wao akakaa kimya akafikiri kwa muda halafu akasema
“ Ok sawa ngoja tumtaarifu “ akachukua simu yake akampigia Dr Kigomba akamtaarifu kuhusu kunaswa kwa maongezi kati ya Elibariki na Flaviana.Kigomba akastuka sana na kuomba atumiwe maongezi yale akayasikia na kisha akamtumia Dr Joshua ambaye naye aliyasikia halafu akampigia simu
“ Dr Kigomba tumuache Flaviana afanye hivyo alivyoagizwa na mume wake.Nitampatia ile taarifa ili ampelekee mume wake.Andaa vijana mahiri wa kuweza kumfuatilia na baada ya kumkabidhi Elibariki taarifa hiyo vijana waanze kumfuatilia Elibariki na kupafhamu mahala alikojificha halafu ndipo achukuliwe na kumzimisha kimya kimya na maiti yake itupwe mbali sana ikiwezekana iharibiwe kiasi cha kutoweza kutambulika.Sitaki Elibariki aonekane tena. Kigomba hii ni fursa nyingine nzuri tumeipata na tunatakiwa tuitumie kikamilifu.Tukishindwa na hapa basi tutakuwa hatarini sana kwa sababu huyu jamaa anaonekana kutokukata tama kupambana na sisi.Anaonekana bado anaendelea kutufuatilia na ndiyo maana anataka kuipata taarifa ile.Sijui anaitaka kwa madhumuni gani lakini mwisho wake umewadia.Tafadhali Kigomba naomba kwa kila namna itakavyowezekana zoezi hili lisishindikane na tuiondoe hatari hii mbele yetu” Akasisitiza Dr Joshua
“ Nakuahidi Dr Joshau safari hii Elibariki hawezi kuponyoka.Hawezi kusalimika.Dakika alizobaki nazo ni chache sana.Nitashughulikia jambo hili mimi mwenyewe na nitakuwepo eneo la tukio ili kuhakikisha kwamba hakuna kosa lolote linalofanyika” akasema Dr Kigomba.
“ Moyo wangu utatulia na kuwa na amani pale tu nitakaposikia kwamba huyu jamaa ameondoka duniani.Ananinyima amani sana huyu jamaa ana sumu kali kuzidi ya nyoka na ni hatari mno kwetu.Sijui kwa nini Flaviana alikubali kuolewa na mtu mjinga kama Elibariki. Lakini pamoja na hayo ninaamini mwisho wake umefika .Huyu ni kijana mdogo sana na hawezi kushindana na mimi ambaye nchi yote iko chini yangu.Hawezi mtummoja akazuia mipango yangu.Lazima nimuonyeshe kwamba mimi ni rais na nina nguvu” akawaza DrJoshua na kuinuka kitandani akaenda kabatini akaichukua ile bahahsa iliyokuwa na ripoti ile ya uongo kuhusiana na kifo cha mke wake halafu akazitoa karatasi zile akaziangalia na kuzirudisha tena katika bahasha.
“ Sifahamu kwa nini anaitaka ripoti hii.Kuna kitu gani anataka kufanya ? Ama kweli sijawahi kukutanana mtu ambaye ameniumiza kichwa kama Elibariki lakini safari hii hataweza kuponyoka tena.”akawaza Dr Joshua halafu akachukua baadhi ya vito vya Dr Flora kama vile herein ,bangili na mikufu akavoweka katika boksi dogo akamuita mmoja wa walinzi wake na kumpa maelekezo avipeleke vitu vile kwa Flaviana pamoja na ile bahasha yenye taarifa ya kutunga.Baada ya mlinzi yule kuondoka Dr Joshua akachukua simu na kumpigia Flaviana
“ hallow baba.Imekuwa vizuri umenipigia kwani nilikuwa na mpango wa kukupigia sasa hivi.” Akasema Flaviana baada ya kupokea simu
“ Nimeona nisilale bila kujua maendeleo yako.Una tatizo lolote Flaviana?akauliza Dr Joshua
“ Ndiyo baba.Unaweza kunipatia ile ripoti ya kifo cha mama ? Ninataka kuipitia unajua Captain Amos alitusomea kwa ujumle wake.”Akasema Flaviana
“ Ina maana bado haijakufikia? Akashangaa Dr Joshua
“ Haijanifikia? Kwani umenitumia? FLaviana naye akashangaa
“ Ndiyo nimekutumia kitambo kidogo.Kuna vito kadhaa vya mama yako kama mikufu,heleni na vingine vidogo vidogo nimemtuma mlinzi wangu akuletee uvitunze kama kumbu kumbu ya mama yako nikiviona vinanipa uchungu sana.Nimempa pamoja na ile ripoti akuletee ili uihifadhi” akasema Dr Joshua
“ Ouh ahsante sana baba.” Akasema Flaviana kwa furaha
“ Usijali Flaviana .Kuna jambo lingine ninataka kukuomba pia,naomba umsaidie sana mdogo wako Anna ili aweze kuizoea hii hali.Kifo cha mama yake kimempa huzuni kubwa sana.Tafadhali naomba uwe naye karibu kwa sababu najua wewe ni mwanamke jasiri na umekutana na mambo mengi sana.Kitu kingine ambacho kimenifanya nikupigie simu usiku huu ni kukutaarifu kwamba bado juhudi za kumtafuta Elibariki zinaendelea kwa kasi na kwa mujibu wa taarifa niliyoipata toka kwa jeshi la polisi ni kwamba kuna matumaini ya kumpata Elibariki .Usijali Flaviana ninafanya kila juhudi ili Elibariki aweze kupatikana na ninakuahidi atapatikana tu” akasema Dr Joshua.
“ Nitashukuru sana baba .Nitafurahi sana Elibariki akipatikana akiwa mzima.Naomba uwe ukinitaarifu pindi upatapo taarifa zozote za kuhusiana na Elibariki” Akasema Flaviana na kukata simu
“ Dah ! baba ni kama alikuwa katika mawazo yangu kuhusiana na ripoti hii.Nilikuwa najiuliza sana namna ya kuweza kuipata lakini imekuwa ni kama vile kayasoma mawazo yangu.Lakini Elibariki anaitakia nini taarifa hii,anataka kufanya jambo gani ? Akajiuliza Flaviana
“ Lakini ni akina nani wanaotaka kumuua na kwa nini ? Kwa sasa nimeanza kuamini maneno yake kwamba kuna jambo linaloendelea hapa.Nimeanza kuingiwa na hofu kwamba huenda ni kweli kifo cha mama kina mkono wa mtu.Elibariki alikuwa anasisitiza sana kuhusiana na jambo hili lakini nilimpuuza lakini sasa kuna kitu nimeanza kukiona kwamba huenda alikuwa sahihi.Elibariki aliniahidikwamba lazima siku moja ukweli utafahamika na ninadhani ndiyo sababu ameitaka taarifa hii. Ngoja nitakapoonana naye usiku wa leoo nitamuomba aniweke wazi.Ninamfahamu Elibariki huwa akilikazania jambo Fulani ni lazima ahakikishe limefika mwisho.Ninamuonea huruma sana mume wangu na ninatamani sana kusikia kwamba watu waliotaka kumuua wote wamekamatwa.Huko aliko sijui yuko wapi,sijui nani anamuhudumia.Nataka awe huru na arejee nyumbani ili maisha yetu yaendelee” akawaza Flaviana huku akilengwa na machozi
******
Anitha alikuwa kimya akiendelea kucheza na komyuta yake akijaribu kutafuta namba ile ya simu iliyotumika kumpigia Elibariki na kumpatia tahadhari kuhusianana mpango wa kumuua iikuwa ni ya nani.Mathew na Elibariki wote walikuwa kimya kabisa wakisubiri amalize kazi yake.Baada ya muda wa zaidi ya dakika thelathini, Anitha akawageukia
“ Pamoja na ujuzi wangu wa kompyuta nimeshindwa kuitambua namba hii ni ya nani.Namba hii ya simu imewekwa katika mfumo ambao ni vigumu kuweza kuifuatilia na kujua mmiliki wake .Ni utaalamu wa hali ya juu sana ambao umetumika hapa.” Akasema Anitha
“ Hii inatuonyesha kwamba mtu huyu anayetumia namba hii ya simu ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na makini katika kazi hizi na ndiyo maana hataki kuacha nyuma kitucchochote kinachoweza kumfanya akatambulika.Mtu anayefanya mambo yake katika hali ya usiri namna hii siku zote huwa ni mtu hatari sana.Tutegemee safari hii kukutana na mtu hatari sana lakini muhimu kwetu.Hakuna njia nyingine yoyote tunayoweza kufanya ili kumpata mtu huyu? Akauliza Mathew
“ kwa hapa sina tena namna ninayoweza kufanya ili kumfahamu mtu huyu ni nani labda niombe msaada kwa wenzangu wenye ujuzi zaidi yangu.” Akasema Anitha
“ kama wewe umeshindwa nadhani itachukua muda mrefu kwa mtu mwingine kuweza kulitatua jambo hili.Anyway tutatafuta namna nyingine ya kufanya ili kuweza kumfah…………” Kabla hajamaliza sentensi yake simu iliyokuwa mezani ambayo Elibariki aliitumia kumpigia mke wake ikaita. Ni namba za simu za Flaviana mke wa Elibariki
“ Mke wako anapiga” akasema Anitha na kumpatia Elibariki ile simu
“ Bonyeza kitufe cha sauti kubwa ili wote tusikie atakachokiongea” akasema Mathew
“ Hallow Flaviana” akasema Elibariki
“ Eli,tayari nimepata ile taarifa”
“ Ouh ahsante sana Flaviana.Umeipataje mapema hivi? Akauliza jaji Elibariki
“ Imekuwa ni kama bahati,mara tu uliponipigia simu nilikuwa nafikiria namna nitakavyoweza kuipata taarifa ile lakini kumbe baba naye tayari alikwisha mtuma mlinzi wake aniletee pamoja na vitu vingine vya mama.Kwa hiyo taarifa ninayo hapa na ninaomba sasa nielekeze mahala tutakapokutana ili nikupatie” akasema Flaviana
“Sawa Flaviana naomba unipe dakika mbili halafu nitakupigia na kukuelekeza ni wapi tukutane” akasema Elibariki na kukata simu akamgeukia Mathew
“ Imekuwa bahati sana kwa Flaviana kuipata taarifa ile mapema zaidi ya nilivyotegemea.Sasa ni sehemu ya kukutana.Tunakutana wapi? Akauliza jaji Elibariki
“ Kabla ya hapo kuna jambo ambalo nimelisikia na limenipa shaka kidogo” akasema Mathew
“ Jambo gani Mathew? Akauliza Elibariki
“Ni kuhusu rais kumpatia Flaviana taarifa hiyo ghafla namna hii.Ukumbuke kwamba rais alikuwa na taarifa hii toka majuzi na katika kipindi chote hicho hakumkabidhi Flavina taarifa hiyo na hakutaka mtu yeyote yule awe nayo .Najiuliza imetokea nini hadi usiku huu ampatie Flaviana taarifa hiyo tena muda mfupi tu baada ya Elibariki kumpigia simu na kumuomba afanye juu chini kuipata taarifa hiyo? Hebu jaribuni kuliona jambo hili kwa jicho la tatu ,hakuna kitu hapa? Akauliza Mathew.
“ Mhh ! hata mimi nimeanza kuhisi kitu”akasema Anitha
“ Ukijiuliza ni kwa nini rais ampatie Flaviana taarifa ile tena usiku huu unagundua kwamba hapa kuna kitu na si bure.”
“ Ahsante Anitha kwa kunielewa nilichokuwa nakimaanisha.Ukichunguza kwa undani hapa lazima utagundua kuna kitu Fulani na si bure.Rais hakuwa tayari kumpa Flaviana wala mtu yeyote yule taarifa ile na ndiyo maana akaifungia chumbani kwake.Kitendo chake cha kupatia Flaviana taarifa ile tena usiku huu na muda mfupi tu baada ya Elibariki kumpigia simu kinatia shaka na kwa kuwa mimi ni mzoefu sana katika mambo haya kuna kitu nimekihisi” akasema Mathew
“ Kuna kitu gani umekihisi Mathew? Akauliza jaji Elibariki.
“ Elibariki this is a trap.Hapa kuna mtego.Najua huwezi kuniamini lakini mimi ni mzoefu katika haya mambo na ninafahamu namna yanavyokwenda.Ninaamini kabisa kwamba huu ni mtego .Baada ya kunusurika katika ajali ile watu wale ambao hawalali wakikutafuta waliamini kabisa kwamba uko hai na waliamini kwamba mtu wa kwanza ambaye utawasiliana naye na kumjulisha kwamba uko mzima ni mke wako kwa hiyo ninahisi kuna kitu wamekiweka katika simu ya mke wako ili kuweza kunasa maongezi yote ambayo atayaongea kupitia simu yake.Ninajua Elibariki utashangaa kwa hiki ninachokuambia lakini mimi ni mzoefu katika mambo haya na niyafahamu vizuri sana .Ninachokueleza hapa nina uhakika nacho.Mpigie simu mkeo na mwambie kwamba atafute simu nyingine ndipo uweze kumpa maelekezo ya wapi pa kukutana.Usimpe maelekezo kwa kutumia simu yake’ akasema Mathew
“ Mathew ninakuamini sana.Una akili ya ajabu.Sikuwahi kuwaza kama kitu kama hiki kinaweza kufanyika” akasema Elibariki na kumpigia simu Flaviana
“ Hallow Flaviana uko karibu na Anna ? akauliza Elibariki
“ Hapana yuko chumbani kwake”
“ Naomba ukachukue simu yake na unipigie kwa kutumia simu yake” akasema jaji Elibariki
“ kwani kuna nini kinaendelea Elibariki ? Simu yangu ina tatizo gani? Hunisikii vizuri? Akauliza Flaviana
“ Naomba ufanye hivyo Flaviana.Naomba uchukue simu ya Anna ndipo nikupe maelekezo” akasema jaji Elibariki
“ Elibariki mbona unaniogopesha? Akasema Flaviana
“ Usiogope Flaviana naomba ufanye hivyo “ akasema Elibariki na kukata simu.Mathew akampa maelekezo namna ya kufanya.
Baada ya dakika mbili Flaviana akapiga simu kwa kutumia simu ya mdogo wake
“ Hallow Elibariki sasa ninatumia simu ya Anna ” akasema Flaviana
“Sawa Flaviana,naomba tukutane pale Simbona hoteli.Mbele kidogo ya hoteli ile kuna kituo cha mabasi na pale utakuta kuna gari moja aina ya Toyota carina lenye rangi ya bluu .Utafungua mlango wa nyuma na kuingia” akasema jaji Elibarikihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Sawa Eli,nitaanza safari muda si mrefu” akasema Flaviana na kukata simu.
“ Elibariki,pamoja na mkeo kubadilisha simu yake lakini bado hatari haijaisha.Macho ya wale wanaokutafuta bado yataelekezwa kwako kwa hiyo basi nina hakika kabisa kwamba lazima atafuatiliwa hivyo lazima tuchukue tahadhari kubwa.Ili tuamini maneno niliyoyasema basi lazima tuweke mtego.Kuna mtu mmoja ambaye tunamshikilia hapa ndani tutamtumia kubaini endapo kuna mtego na kama mkeo anafuatiliwa ama vipi.Yeye atakuwa pale hotelini akiwa na ile gari aina ya Toyota carina na mkeo atakapoingia ndani ya ile gari ataiondoa na kuelekea moja kwa moja katika viwanja vya ukombozi na kama kuna mtu yeyote ambaye atakuwa akimfuatilia mkeo basi tutafahamu na kumdhibiti.Kama hakuna mtu yeyote ambaye atakuwa akimfuatilia basi atatukabidhi hiyo ripoti na tutamrejesha pale Simbona hoteli alikoacha gari lake na ataondoka zake.Lakini endapo tutagundua kwamba kuna watu wanaomfuatilia basi itatulazimu kuingia katika mapambano nao kuwafahamu ni akina nani na wametumwa na nani” Akasema Mathew.jaji Elibariki akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi
“ Mathew are you sure my wife will be safe? Akauliza
“ Elobariki naomba nikuweke wazi kwamba hili si suala jepesi na ni jambo la hatari kubwa ,na chochote lazima kitokee lakini ninakuhakikishia kwamba tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha kwamba mkeo anakuwa salama. “ Akasema mathew
“ Ahsante sana Mathew.Ninakuamini kwa kila utakachokisema.” Akasema Elibariki na Mathew akatoka mle chumbani akaelekea katika kile chumba alichokuwamo yule jamaa wanayemshikilia akamuamsha
“ hallow amka !! akasema Mathew kwa ukali
“ Brother una mpango gani na mimi? Utaniweka hapa hadi lini?Ulichokuwa unakitaka nimekwisha kueleza lakini mbona huniachii? Akauliza yule jamaa
“ Kuna kazi moja ambayo nataka unifanyie na endapo ukifanya vizuri basi nitakuacha uende zako”akasema Mathew
“ Ni kazi gani hiyo brother? Niambie niko tayari”
“ Unaweza kuendesha gari? Akauliza Mathew
“Ndiyo ninaweza kuendesha.”akajibu yule jamaa
“ Good” akasema Mathew na kisha akamuelekeza yule jamaa namna mpango mzima utakavyokuwa.
“ Tutakuwa nyuma yako na endapo ukijaribu kwenda kinyume na nilivyokwambia basi sahau kabisa suala la kuachiwa huru na nitakufanyia kitu kibaya sana .Tena naomba nikuweke wazi kwamba sijakufanyia vile nilivyokuwa nimepanga kukufanyia kwa sababu ulinieleza ukweli na nikaamua kukusamehe.Vinginevyo ningekufanyia kitu kibaya sana kutokana na mambo mliyomfanyia Sabina na kwa taarifa yako Sabina amekwisha fariki dunia.Kwahiyo basi nakusisitiza kwamba unatakiwa ufanye kile tu nilichokuelekeza.Kinyume na hapo basi utakuwa unajiweka wewe mwenyewe hatarini” akasema Mathew
“ Usihofu kitu kaka.Nitafanya kama unavyotaka.Ninataka niwe huru ,ninahitaji kuendelea kuishi kwa hiyo siwezi kufanya jambo lolote la kipuuzi.Kitu kingine kaka nakuomba usinikabidhi kwa vyombo vya dola.Nikifikishwa kule nitafungwa kifungo kirefu gerezani kwani tayari rekodi zangu ziko kule .” akasema yule jamaa
“ Diwezi kukuahidi chochote kwa sasa hadi hapo nitakapohakikisha kwamba umefanya kile ambacho nimekuagiza ukifanye” .akasema Mathew halafu akatoka katika kile chumba akaenda katika gereji yake ya magari na kulitoa gari moja aina ya Toyota carina.Ni gari ambalo bado hajalisajili toka alinunue na huliweka ndani kwa ajili ya kulitumia kwa nyakati kama hizi.Alifunga namba bandia katika gari lile na kulijaribu akahakisha liko sawa akarejea ndani
“ jamani kila kitu kinakwenda vizuri.Sasa ni muda wa kujiandaa kwa ajili ya kuelekea huko.Akasema Mathew na kuwachukua Elibariki na Anitha hadi katika chumba ambacho huhifadhi silaha .Akafungua kabati na kutoa fulana nne zisizopenya risasi akawapatia Elibariki na Anitha na moja ikawa kwa ajili ya yule jamaa mwingine watakayemtumia
“ Eli,unaweza kutumia silaha ? Akauliza Mathew
“ Ndiyo ninaweza Mathew , nimewahi kupitia mafunzo katika jeshi la kujenga taifa kwa hiyo ninafahamu kutumia silaha ingawa sijawahi kuingia katika mapambano.” Akasema jaji Elibariki.Mathew akampatia bastora.
“ Ihifadhi hiyo silaha pengine tunaweza kuihitaji” akasema Mathew halafu akaelekea katika chumba alimo Yule jamaa na kumpatia fula moja isiyopenya risasi .
Walipokuwa tayari wakaingia katika gari na kuanza safari wakitanguliwa na Yule jamaa akiwa katika Toyota Carina
“ Anna jiandae kuna sehemu tunakwenda” Flaviana akamwambia mdogo wake Anna
“ usiku huu? Anna akashangaa
“ Ndiyo kuna sehemu nataka kwenda usiku huu” akasema Flaviana
“Kuna jambo gani la muhimu kiasi cha kutoweza kusubiri hadi asubuhi ? Akauliza Anna ambaye alionekana wazi kwamba hakuwa tayari kuondoka usiku ule.Flaviana akamsogelea na kwa sauti ndogo akasema
“ Elibariki kanipigia simu usiku huu”
“ What ?! Elibariki? Yuko wapi ? Anna akajikuta akiuliza maswali mfululizo
“ Hata mimi sifahamu yuko wapi lakini amenihakikishiwa kwamba yuko sehemu salama” akasema Flaviana
“ Ouh Thank you Lord” akasema Anna
“Umekwishamfahamisha baba kama umeongea na Elibariki? Hata yeye atafurahi sana kusikia kwamba Elibariki yuko mzima .Atafanya mpango wa kwenda kumchukua mahala aliko” akasema Anna
“ Baba nimeongea naye lakini sijamfahamisha chochote kuhusiana na jambo hili na ninaomba usimweleze chochote.Elibariki hataki mtu mwingine yeyote afahamu kuhusiana na jambo hili kwa ajili ya usalama wake .Baada ya Elibariki kunusurika kuuawa sasa nimeanza kuamini yale maneno yake aliyokuwa akisisitiza kwamba kuna kitu kibaya kinachoendelea .” akasema Flaviana
“ Hata mimi shambulio lile limenipa wasi wasi sana .Ninaweza kukubaliana nawe kuhusu jambo hili kwamba kuna kitu kinaendelea chini kwa chini.Unadhani nani anaweza kuwa amefanya shambulio lile?
“ Ni vigumu kufahamu ni nani lakini ninachoweza kuhisi kwa haraka haraka kuna kitu kinachoendela hapa na kama ukikumbuka kuna kitu mama alitaka kutuambia lakini hakuweza kwani alifariki ghafla mchana wa siku ile ambayo alitutaka tuonane naye .Ninahisi kuna jambo kubwa ambalo alitaka kutueleza na kuna hisia zinakuja kwamba huenda jambo hilo alilotaka kutuambia ndilo lillomgharimu uhai wake.Mama alifariki ghafla sana na wewe mwenyewe ulishuhudia sintofahamu iliyokuwepo kuhusiana na sababu ya kifo chake. Elibariki alituambia kwamba wamegundua mama alifariki kwa kuchomwa sindano ya sumu lakini taarifa ile ya madaktari bingwa ambayo baba anaiamini inasema kwamba mama hakufariki kwa sumu.Ukichunguza kwa undani sana masuala haya utagundua kwamba kuna kitu hapa si bure nadhani ndiyo sababu Elibariki hakati tamaa katika jambo hili.Mara ya mwisho nilipooongea naye aliniahidi kwamba hatalala usingizi hadi ukwe liwa jambohili ujulikane na ninahisi hiki ndichokilichotaka kumtoa uhai.Amenitaka nikaonane naye usiku huu kuna jambo anataka kuniambia na nijitahidi niipate ile taarifa ya madaktari bingwa.” Akasema Flaviana
“ Anaitaka ile taarifa? Anataka kuifanyia nini? Akauliza Anna
“ Sifahamu anaitaka kwa ajili gani lakini amesisitiza sana kwamba anaihitaji usiku huu.”
Anna akafikiri kidogo na kusema
“ taarifa yenyewe utaipata vipi wakati anayo baba? Sina hakika kama baba anaweza akakubali Elibariki aipate taarifa ile.”
“ tayari ninayo.Baba amenipatia usiku huu” akasema Flaviana
Anna ambaye tayari alikuwa kitandani akaamka na kujiandaa kisha wakaongozana hadi katika gari la Flaviana wakaondoka.
“ Flaviana unadhani Elibariki alikuwa sahihi kwamba mama aliuawa kwa sumu? Akauliza Anna
“ Siwezi kuwa na uhakika huo Anna lakini ukiangalia namna mambo yalivyotokea unaweza ukakubaliana na jambo hilo kwamba kifo cha mama hakikuwa cha kawaida.Nimekuwa nikilitafakari sana jambo hili .Hebu angalia mama alifariki ghafla na halafu ikatolewa taarifa kwamba usifanyike uchunguzi wowote wa kuhusiana na kifo chake .Hili jambo linashangaza sana kwa sababu haiingii akilini eti mwli wa mke wa rais usifanyiwe uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake cha ghafla.Hii ni sababu iliyonifanya nimuombe Elibariki anisaidie kufanya uchunguzi ili tuweze kubaini kile kilichosababisha kifo cha mama. Katika uchunguzi uliofanyw ana watu wa Elibariki waligundua kwamba mama alichomwa sindano yenye sumu lakini baadae ikaja tena taarifa nyingine ikisema kwamba mama alikufa kwa shinikizo la damu na hakukuwa na dalili zozote za kuwepo kwa sumu katika mwili wake.Jambo hili linanipa mashaka sana na ninalazimika kuamini kwamba huenda kifo cha mama ni kweli kina mkonowa mtu na kikubwa zaidi kinachonifanya niamini hivyo ni baada ya Elibariki kunusurika kuuawa..Ninajiuliza sana kwa nini Elibariki atake kuuawa sasa hivi? Ni kitu cha kawaida majaji kuwa na maadui wengi na ndiyo sababu wamekuwa wakipatiwa ulinzi lakini kwa niniwatake kumuua sasa hivi? Ukijiuliza swali hili utagundua kwamba lazima kuna kitu kinachohusiana na kifo cha mama.Ninamfahamu Elibariki vizuri akilifuatilia jambo kwa nguvu namna hii lazima kuna sababu maalum.” Akasema Flaviana
“Hata mimi nimekuwa na mawazo kama yako na kilichonifanya niwe na mawazo hayo ni kuhusiana na shambulio la Elibariki.Kitu kingine kinachonipa maswali mengi ni kwamba kwa nini baba amekuwa kimya sana kuhusiana na masuala haya? Kwa masikio yangu nilimsikia Dr Kigomba akitoa amri kwamba watu waliokuwa wakifanya uchunguzi kubaini kilichomuua mama wakamatwe na kudhibitiwa lakini tulipomueleza baba kuhusiana na suala hili amekuwa mzito sana kutuamini na badala yake akadiriki kusema kwamba Dr Kigomba hahusiki kwa namna yoyote ile na suala lolote kuhusiana na kifo cha mama.”akasema Anna
“ Anna unahisi kwamba baba anaweza akawa anafahamu kinachoendelea ? Akauliza Flaviana
“ Siwezi kusema kwamba anahusika moja kwa moja lakini kwa namna alivyolishughulikia jambo hili inanipa mashaka kidogo kuaminikwambahawezi kufahamu kinachoendelea .Inaonekana wazi kabisa kwamba hakulipa ule uzito unaostahili.Aliyefariki ni mke wake na alipaswa kulipa uzito mkubwa sana sana suala hili lakini naona imekuwa tofauti kabisa.Haonekanikujali.haonekani kuumizwana kifocha mama.” Akasema Anna
“ Anna unaweza ukawa sahihi katika hili.Hata mimi japokuwa nilikuwa upande wake kuhusiana na ile taarifa ya madaktari bingwa lakini nilishangazwa zaidi na namna alivyolichukulia suala hili kwa wepesi na kukubali kirahisi maelezo ya Dr Kigomba.Halafu kuna jambo lingine ambalo kwangu mimi naliona kama si la kawaida ,Elibarikiamekuwa akihudhuria katika kila kikao tunachokifanya cha kifamilia.yeye ni sehemu ya familia yetu na ndiyo sababu siku ile nilimuita aje katika kikao kile ili kwa pamoja tuisikie taarifa ya uchunguzi wa kifo cha mama toka kwa madaktari bingwa.Kitu cha kushangaza baba hakuonyesha kufurahi kumuona Elibariki katika kikao kile na ndiyo maana akamtolea maneno yale makali.Kama utakumbuka baada ya kikao aliniita nje na akanifokea sana kwa nini nimemuita Elibariki katika kikao kile .Inaonyesha wazi kwamba hakutaka Elibariki afahamu chochote kuhusiana na taarifa ile.Swali kubwa la kujiuliza hapa ni kwamba kwa nini baba hakutaka Elibariki afahamu chochote kuhusiana na taarifa ile ya kifo cha mama? Binafsi yangu naona kama jambo hili linahitaji kufanyiwa uchunguzi ” akasema Flaviana
“ Tutalichunguzaze Flaviana? Akauliza Anna
“ Hata mimi sielewi lakini kuna haja ya kufanya uchunguzi.Ngoja tukionana na Elibariki usiku huu nitaongea naye kuhusu jambo hili.Yeye anaweza kuwa naushaurimzuri zaidi ” Akasema Flaviana
Waliendelea na safari yao hadi walipofika Simbona hoteli mahala alipoelekezwanaElibariki wakutane ,akapunguza mwendo na kusimamisha gari katika kituo cha basi.Kulikuwa na taksichache eneo lile
“ Hapa ndipo mlipangamkutane?akauliza Anna
“ Ndiyo ! tulipanga tukutane hapa” akasema Flaviana huku akiangaza macho kulitafuta lile gari aliloelekezwa na mara akaliona
“ Anna nitashuka na kuingia katika lile gari la bluu pale mbele.Mle ndimo alimo Elibariki.Utanisubiri hapa hapa,sintakawia sana” akasema Flaviana na kufungua mlango akashuka garini na kuelekea moja kw amoja katika lile gari la bluu akataka kuufungua mlango na kuingia akasita akenda kugonga katika kioo cha dereva.Kioo kikashushwa halafu mtu yule aliyekuwamo ndani ya ile gari akamuamuru afungue mlango wa nyuma na aingie ndaniya gari.Huku akiwa na uoga mwingi,Flaviana akafungua mlango wa nyuma akaingia.Elibariki hakuwamo ndani ya gari
“ Elibariki yuko wapi? Akauliza Flaviana
“ Funga mlango” akaamuru yule jamaa.
“ Wewe ni nani? Elibariki yuko wapi? Akauliza Flaviana kwa wasiw asi
“ Fuata maelekezo uliyopewa.Hukuambiwa uniulize maswali ,kazi yangu ni kukupelekea mahala aliko mtu wako.Kama uko tayari hatuna muda wa kupoteza funga mlango wa gari na nikupeleke huko unakotaka,kama hauko tayari shuka” akasema yule jamaa kwa sautiya ukali.Flaviana akafikiri kidogo halafu akaufunga mlango japokuwa mwili ulikuwa unamtetemeka.Gari likawashwa na kuondoka pale kituoni
******
Ni usiku ulionekena kuwa mgumu sana kwa Dr Joshua.Pamoja na uchovu aliokuwa nao baada ya kufanyishwa kazi nzito na Peniela usiku ule lakini hakuwa na dalilizozote za kupata usingizi.Bado suala la Elibariki liliendelea kukisumbua sana kichwa chake. Alikuwa ameketi sofani chumbani kwake akiwa nasimu yake pembani akisubiri kuwasiliana na Dr Kigomba kuhusiana na zoezi lialoendelea la kumfuatilia Flaviana ili kufahamu mahala alikojificha jaji Elibariki.
“ Toka nimeingia madarakani sijawahi kuwekwa katika wakati mgumu namna hii na mtu yeyote yule zaidi ya Elibariki.Nilikosea sana kumuacha hai mpaka leo .Kama ningejua mapema kwamba Elibariki ana sumu kali zaidi ya nyoka ningek…………….” Alikatishwa mawazoyake na muito wa simu.Haraka haraka akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow Kigomba.Mambo yanakwendaje huko?
“ mambo yanakwenda vizuri,hadimuda huu hakuna tulichokigundua bado.Flaviana ameshuka katika gari lake na ameingia katika gari lingine na likaondoka.Nahisi humo ndimo alimo Elibariki.Tunaendelea kulifuatilia na nitakufahamisha kila kitu baada ya muda mfupi” akasema dr Kigomba
“ Kigomba tafadhali jitahidi kwa kila uwezavyo ili jambo hili limalizike.Sitaki kusikia kosa lolote.Hii ni nafasi ya dhahabu tumeipata na tuitumie vizuri” akasema Dr Joshua
“ usihofu mzee.Mimi mwenyewe nimeamua kuingia kazini na vijana leo ili kuhakikisha kwamba hakuna kosa litakalofanyika.Nitakutaarifu tena baadae kidogo kinachoendela” akasema Dr Kigomba na kukata simu
“ Nina hakika safari hii Elibariki hataweza kuponyoka. “akawaza Dr Joshua baada ya kumaliza kuongea na Dr Kigomba.Akamimina whysky katika glasi na kunywa funda kubwa. Mara akastuliwa na mlio wa simu.Zilikuwa ni namba ngeni kabisa katika simu yake na akajiuliza mtu yule ni nani na amezipata wapi namba zake? .Alisita kidogo kuipokea ile simu.Ikaita kwa mara ya kwanza hakuipokea,ikaita kwa mara ya pili akaamua kuipokea
“ hallow “ akasema
“ hallow Dr Joshua” ikasema sauti ya upande wa pili.Dr Joshua akaitambua sauti ile
“ hallow Deus ! akasema Dr Joshua huku uso wake ukiwa na tabasamu
“ hahaha nilidhani hautaweza kuitambua sauti yangu” akasema Deus
“ Siwezi hata siku moja kuisahau sauti yako mtu ambaye uliniachia kijitii.Poel sana nilisikia kwamba ulikuwa unasumbuliwa na miguu na nimepanga kuja kukuona kwa siku za hivi karibuni.Vipi hali yako kwa sasa?
“ Kwa sasa hali yangu inaendelea vizuri sana.Tayari nimekwisha pata tiba naninaendelea vizuri.Nilianguka na kustua mguu wakati nikiwa shambani kufuatilia maendeleo ya mifugo yangu.”
“ usijali Mr Presidnet nitakuja kukutembelea siku za hivi karibuni.Unajua kuna mambo mengiya kujifunza toka kwako kwa kuwa na mimi ninakaribia kumaliza muda wangu wa uongozi kwa hiyo natakiwa kujifunza toka kwenu mlionitangulia namna ya kuishi maisha ya kawaida baada ya kumaliza kuitumikia nchi” akasema Dr Joshua
“ Karibu sana Dr Joshua muda wowote ukiwa na nafasi” akasema Deus ambaye ni rais mstaafu na ndiye aliyemkabidhi ofisi Dr Joshua.Kimya kifupi kikapita halafu Dr Joshua akasema
“ Deus umenistua kidogo kwa simu yako ya usiku huu.” Akasema Dr Joshua
“ usiogope Dr Joshua,nimekupigia muda huu kwanza kukupa pole nyingi sana kwa kifo cha mkeo Dr Flora.Ninamfahamu vizuri Dr \Flora alikuwa na mahusiano mazuri sana na mke wangu kwa hiyo hata sisi tumeondokewa na rafiki muhimu sana wa familia yetu.Sikuweza kufika kwenye msiba lakini mke wangu alikuwepo na aliniwakilisha” akasema Deus
“ Deus nashukuru sana na ninamshukuru Mungu kwa kila jambo.Yeye ndiye mwenye kupanga kila itu kitokee.Ni vigumu sana kuikabili hali hii lakini ninajitahidi” akasema Dr Joshua.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Deus akasema
“ jambo la pili ambalo nimekupigia simu usiku huu ni kutaka tuongee kuhusiana na Package E21.” Akasema Deus na kumstua sana Dr Joshua.Alihisi kama kuna kitu kizito kimempiga kichwani.Kwa sekunde kadhaa akawa ni kama mtu aliyepigwa na butwaa.
“Dr Joshua !!..akaita Deus
“ Hal..hallow deus” akasema Dr Joshua lakini kwa mbali sauti yake ilionekana kutetemeka.
“ Joshua mbona umestuka namna hiyo?akauliza Deus
“ Deus kwa nini unataka tuongelee jambo hilo? Kwa nini leo? Akauliza Dr Joshua
“ Is it safe? Bado iko salama? Akauliza Deus
Dr Joshua akavuta pumzi defu na kuuliza
“ Deus niambie kwa nini unauliza kuhusu jambo hili?
“ Usiogope Joshua,nahitaji tu kujua kama Package E21 iko salama” akasema Deus
“ Kwani kuna tatizo gani Deus ? Akauliza Dr Joshua.
“ Ninataka tu kufahamu kama bado ipo na iko salama” akasema Deus.Dr Joshua akakaa kimya kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Deus naomba unieleze kwa nini umenipgia simu? Unataka nini?Ninakufahamu vizurilazima kuna sababu iliyokufanya ukanipigia simu “ Akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua kuna ubaya gani kujua kama package iko salama? Mimi nilikabidhiwa na nikaitunza kwa miaka yangu yote kumi halafu nikakukabidhi wewe nikiaminikwamba itaendelea kuwa salama kwa hiyo ni jukumu langu kufahamu kama bado iko salama” akasema Deus na maneno yale yakaonekana kumchukiza Dr Joshua
“ Deus ninakuheshimu mno na ninataka nikueleze jambo moja,wakati wa uongozi wako hakuna aliyekuwa akikuingilia katika kila ulichokifanya.Kwa sasa umekwisha maliza uongozi wako na una pumzika kwa hiyo naomba uendelee kupumzika.Masuala ya Package E21 hayakuhusu tena.Hili ni jukumu langu kwa hiyo naomba usiingilie kazi zangu” akasemaDr Joshua
“ Dr Joshua,siwezi kuacha kufuatilia kuhusu kitumuhimu kama hiki.Wakati wa uongozi wangu niliilinda kama mboniya jicho langu tofauti na wewe unavyotaka kufanya” akasema deus na kumstua sana Dr Joshua.Uso wake ukakunja ndita.
“ Umesema nini Deus? Akauliza Dr Joshau kwa ukali
“ Joshua ninafahamu kila kitu unachotaka kukifanya”
“ Mbona sikuelewi unamaanisha nini? Akauliza Dr Joshua
“ Joshua ninafahamu kuhusu biashara unayotaka kuifanya “
“Biashara gani?
“ Usijifanye haufahamu Joshua.Usisahahu kwamba hata mimi nilikuwa katika nafasi kama yako na ninauwezo wa kufahamu kila kinachoendelea katika uongozi wako.I have lots of connections Joshua” akasema Deus.Dr Joshua akahisi joto kali na kijasho kikaanza kumchuruzika.Alihisi kusikia kizungu zungu.
“ Joshua are you there? Akauliza Deus baada ua Dr Joshua kuwa kimya
“ Unasemaje Deus?
“ Joshua ninarudiaa tena kukukumbusha kwamba ninaifahamu biashara unayoifanya na ninafahamu unataka kuwauzia akina nani.”akasema Deus
“ Kwa hiyo baada ya kugundua hivyo ni kitu gani unakihitaji? Akauliza Dr Joshua kwa ukali
“ I want you to stop that business as soon as possible.” Akasema Deus kwa ukali
“ Dr Joshua sikuwahi kufikiria kwamba mtu kama wewe unaweza ukafanya kitu hatari kama hiki kwa taifa.Nilikukabidhi package ile nikiamini kwamba utaitunza na kuilinda kama mboniya jicho lako lakini umeingiwa na tamaa ya fedha na unataka kuhatarisha usalama wa taifa.Joshua please don’t do it.Usifanye kabisa jambo hatari kama hilo.Usiitoe ile package mahala ilipo.Pale iko sehemu salama na itaendelea kukaa pale kwa miaka yote.Ni kwa sababu ya unyeti wake ndiyo maana inahifadhiwa ikulu sehemu ambayo anayefahamu ilipo ni rais wa nchi pekee kwa hiyo Joshua narudia tena kukusisitiza kwamba usifanye hicho kitu unachotaka kukifanya.” Akasema Deus kwa ukali
“ who are you Deus to give me orders? Wewe huna mamlaka yoyote kwa sasa ya kuniamuru mimi jambo lolote!!akafoka Dr Joshua
“ Joshua naomba usisahau kwamba I’m a president too..”akasema Deus
“ Ex president. !! akasema kwa ukali Dr Joshua.
“ hauko tena katika uongozi kwa hiyo kwa sasa huna nguvu yoyote ya kuweza kuniamuru chochote” akaendelea kusema kwa ukali Dr Joshua
“ Kitu gani kinakufanya uwe na uhakika huo kwamba siwezi kukuamuru kitu? Umesahau kwamba mimi ndiye niliyekuteua na kukupigania hadi ukashika nafasi hiyo? Kama nilikuwa na nguvu ya kukuweka hapo ulipo ,unadhani sintakuwa na nguvu ya kukuondoa hapo ulipo ? Akauliza Deus
“ Usinitishe huna lolote Deus.I am a president of United republic of Tanzania and you are just a normal citizen so don’t you ever try to interfere anything in my administration ! Wananchi ndio walioniweka hapa na wala si wewe kwa hiyo usinitshe na huwezi kunifanya chochote na tena ninakuonya kwamba usithubutu tena kunipigia simu na kunitolea vitisho. Mimi ni rais na nina uhuru wa kufanya jambo lolote .Package hii haihusiani na raia yeyote wan nchi hii na kuiuza sijavunja sheria wala katiba ya nchi” akasema Dr Joshua kwa ukali huku jasho likimtiririka.
“ Joshua unapata kila kitu unachokihitaji katika maisha yako,na ukimaliza muda wako wa kulitumikia taifa utaishi kwa raha mustarehe na kwa heshima nyingi.Umekwisha fanya mambo mengi mazuri katika nchi hii na watanzania wataendelea kukukumbuka kwa miaka mingi ijayo kwa mambo uliyowafanyia.Tafadhali usiingiwe na tamaa na ukaharibu yale mazuri yote uliyoyafanya kwa sababu tu ya hayo mabilioni ya fedha unayotarajia kuvuna baada ya kuiuza Package E21.” Akasema Deus
“ Deus naomba usitafute ugomvi kati yangu na wewe kwa sababu unaelewa kwamba huwezi kunishinda hata kidogo.” Akasema Dr Joshua
“ Joshua hii ninakupa amri nasi ombi.Nikisikia kwamba unaendelea na biashara hii unayotaka kuifanya basi jiandae kuondoka katika hicho kiti.Siko tayari kuona ukihatarisha usalama wa nchi yetu kwa tamaa zako.Siko tayari kuona maisha ya mamilioni ya watu yakiwa hatarini kwa tamaa zako.Nitakudhibiti kabla hujafanya unavyotaka kufanya and I will take you down Joshua.Kwa heri kwa sasa” akasema Deus na kukata simu.Zilipita kama dakika mbili Dr Joshua bado alikuwa amesimama akiwa na simu yake mkononi.
“ Huyu shetani katokea wapi tena? Aggghhh!!.. kabla hili halijaisha linaibuka hili.” Akajiuliza Dr Joshua na kumimina mvinyo katika glasi akaugugumia wote .
“ Deus amefahamuje kuhusu mpango huu? Akaendelea kujiuliza akamimina tena mvinyo katika glasi
“ Tunaojua kuhusu siri hii ni watu watatu ,mimi,Kigomba na Amos ,ni nani basi kati yetu ambaye atakuwa amempa taarifa Deus? Lazima ni mmoja kati yetu .Nina ni kati ya Kigomba na Amos? Akajiuliza
“ Akili yangu inanituma kwa Amos.Imani inaanza kunitoka kwake.Nahisi ni yeye ambaye anaweza kuwa akitoa habari zetu.Dr Kigomba sina shida naye ni mtu ambaye nimekwisha fanya naye mambo mengi makubwa na ya hatari na hakuna hata siku moja nimewahi kusikia jambo lolote nililofanya naye limevuja.Baada ya kumshirikisha captain Amos mambo ndiyo yameanza kwenda kombo.Nitamfanyia uchunguzi wa kina Amos na kuzifahamu nyendo zake.Nitaweka vijana wa kumfuatilia katika kila jambo analolifanya na ukweli utajulikana tu.Nikifahamu kwamba ni yeye ndiye anayetoa habari zetu basi sintakuwa na huruma naye,nitamzimisha kimya kimya “ akawaza Dr Joshua
“ Deus Amasile Mkozumi ..” akatamka Dr Joshua kwa sauti ndogo
“ Deus ni mtu ninayemuheshimu sana .Ni mtu ambaye wakati wa uongozi wake alifanya mamabo mengi makubwa kwa nchi hii na heshima yake ni kubwa sana .Kwa msaada wake nilifanikiwa kukipata kiti hiki cha urais.Pamoja na mambo yote aliyonifanyia lakini kwa hiki anachotaka kukifanya amepotea njia.Nitaweka kila kitu pembeni na nitapambana naye.Ninamfahamu vizuri Deus ni mtu ambaye akisema jambo hulitimiza.Kama ameahidi kunitoa katika kiti hiki basi atafanya hivyo.Ni mtu ambaye bado ana ushawishi mkubwa sana na anaweza akawashawishi wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na rais na wakaniondoa madarakani.Ni mtu ambaye sipaswi kumpuuza hata kidogo.Nguvu yake katika siasa bado ni kubwa .Kwa maneno aliyoongea japokuwa nilikuwa nikibishana naye lakini yameniogopesha sana.Natakiwa kuchukua hatua haraka sana na kumaliza Deus kabla hajanimaliza.Mimi ni rais wa nchi na nina kila nyenzo ya kuweza kummaliza Deus na wale wote anaoshirikiana nao.Baada ya Elibariki nimepata adui wa pili.Lazima niwamalize wote haraka sana.Nimekaribia mwisho kabisa wa biashara hii kwa hiyo lazima nihakikishe kwamba ninawaondoa wote haraka iwezekanavyo.” Akawaza Dr Joshua na kuchukua simu yake akabonyeza namba Fulani halafu akaiweka simu sikioni
“ General Adam,tafadhali naomba nikuone hapa ikulu usiku huu.” Akasema Dr Joshua na kukata simu
“ I will destroy you Deus,I must destroy you!!! Akasema Dr Joshua kwa hasira na kunywa mvinyo kwa fujo.
Elibariki alikuwa wa kwanza kulitambua gari la Flaviana mara tu lilipowasili Simbona hoteli na kwenda kusimama katika kituo cha mabasi kama alivyokuwa amemuelekeza.
“ Ile pale gari ya Flaviana” akasema jaji Elibariki akiwalekeza akina Mathew.Toka katika sehemu waliyokuwa wameegesha gari lao waliweza kushuhudia kila kitu kilichokuwa kinatokea.
“ Are you sure? Akauliza Mathew
“ yes i’m sure.Ninalifahamu gari la mke wangu “ akajibu Elibariki
Gari la Flaviana likasimama katika kituo cha daladala na baada ya kama dakika mbili hivi mlango wa gari Flaviana ukafunguliwa akashuka mwanamke mmoja ambaye Elibariki akamtambua pia
“That’s my wife Flaviana’ akasema Mathew
“ She’s pretty.” Akasema Anitha na kumfanya Elibariki atabasamu.Mua huo huo zikawasili gari mbili na kuegesha si mbali sana na gari la Flaviana
Kisha shuka garini Flaviana akaelekea moja kwa moja katika gari la bluu aliloelekezwa akagonga katika kio cha upande wa dereva akazungumza na mtu aliyekuwamo ndani.
“ What is she doing? Akauliza Mathew .
Mara Flaviana akafungua mlango wa gari na kuingia ndani na baada ya muda kidogo gari lile likaondoka .
Dakika moja na sekunde kadhaa baada ya gari alilopanda Flaviana kuondoka pale kituoni ,gari mbili zilizokuwa zimeegeshwa karibu na gari la Flaviana nazo zikaondoka.
“ Mmeona zile gari mbili zilizoondoka mara tu baada ya gari alimo Flaviana kuondoka? Ninahisi lazima watakuwa wamemfuatilia Flaviana.Flaviana ni mtu ambaye anamulikiwa sana na watu wanokutafuta Elibariki na ndiyo maana nikaamua kuweka mtego kama ule ili kuhakiki kama kuna mtu atakuwa akimfuatilia Flaviana.Gari zile mbili zimenipa mashaka sana .Twendeni tuzifuatilie ili tujue kama ni kweli Flaviana anafuatiliwa.” Akasema Mathew
“ Mathew,itakuwaje iwapo ni kweli mke wangu anafuatiliwa? Maisha yake yako hatarini” akasema jaji Elibariki kwa uoga
“ Usiogope Elibariki.Tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuweza kumlinda mke wako” akasema Mathew na kuwasha gari wakaanza safari kumfuatilia Flaviana
*******
General Adam aliwasili katika makazi ya rais kuitika wito wa Dr Joshua aliyemtaka afike mara moja usiku ule.Dr Joshua akiwa chumbani kwakealitaarifiwa kuhusu kuwasili kwa generali Adam na kisha akaenda kuonana naye
“ General Adam,karibu sana” akasema Dr Joshua huku akipeana mikono na gererali Adam
“ Nashukuru sana mheshimiwa rais .” akasema Adam na kisha Dr Joshua akamuongoza katika chumba chake cha maongezi ya faragha
“ Mheshimiwa rais ,kwanza pole sana kwa msiba uliokupata wa kufiwa na mkeo.” Akaanzisha mazungumzo Generali Adam
“ Ahsante sana Adam, nimekwisha poa .Yote hii ni mipango ya Mungu.Yeye ndiye mwenye kupanga kila jambo” akasema Dr Joshua halafu Akaka kimya kidogo na kusema
“ General Adam nafahamu nimechukua muda wako wa mapumziko na kukuita hapa usiku huu.Samahani sana kwa hilo” akasema Dr Jsohua
“ Usijali kuhusu hilo mheshimiwa rais.Sisi ni watumishi na muda wote tuko kazini” akasema Generali Adam
“ Nashukuru sana kusikia hivyo General Adam” akasema Dr Joshua halafu akakaa kimya kidogo akavuta pumzi ndefu na kusema
“ General Adam mimi na wewe tumekuwa ni marafiki wakubwa toka tukiwa jeshini na hata baada ya kushika nyadhifa tumekuwa karibu sana na kila pale ninapokuwa na tatizo kubwa hujawahi kushindwa kunisaidia.” Akasema Dr Joshua
“ Ni kweli Dr Joshua.Hata siku moja siwezi kushindwa kukusaidia Dr Joshua .Hata wewe umekwisha nisaidia katika mambo mengi sana.Wewe ni zaidi ya rafiki ” akasema Adam
“ Ahsante sana kwa maneno hayo General Adam .Kama nilivyotangulia kusema ,nimekuita hapa nina tatizo ambalo ninahitaji sana msaada wako .”
“ Usihofu chochote Dr Joshua kama kuna tatizo lolote nitaarifu na kama liko ndani ya uwezo wangu basi nitakusaidia na kama litakuwa nje ya uwezo wangu basi tutaangalia namna ya kulitatua tatizo hilo” akasema Adam
“ Ahsante sana Adam.Naomba pia kile tutakachokiongea hapa kiwe ni siri kubwa kati yako na mimi na asifahamu mtu mwingine yeyote yule na ndiyo maana nikakuita kwa siri usiku huu”
“ Dr Joshua nadhani unaniamni na ndiyo maana ukaniita hapa kwa hiyo usihofu chochote,siri yako itakuwa salama na hakuna yeyote atakayejua” akasema Adam
Dr Joshau akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Adam Kazi ya urais ni kazi ambayo watu wengi wanaililia na kufanya kila wawezalo ili waipate lakini ukweli hii ni kazi ngumu sana na yenye changamoto nyingi.Kiti hiki cha urais ni kiti cha moto na huwezi kuamini hayo hadi ukipata nafasi ya kukalia kiti hiki.Unapokalia kiti hiki cha urais unajiona tofauti na raia wengine wa kawaida,unajiona uko juu yao na unaweza ukafanya jambo lolote na hilo ndilo huwafanya viongozi wengi wakapotea njia na kufanya mambo yale ambayo yanaweza yakaenda kinyume na maadili au ya uvunjifu wa sheria za nchi.Hakuna kiongozi ambaye anakalia kiti hiki na akamaliza muda wake wa uongozi akiwa hajafanya hata kosa moja.” akasema Dr Joshua na kukaa kimya kidogo
“ Ukikalia kiti hiki cha urais “ akaendelea
“Unakuwa na marafiki wengi lakini unajenga pia na maadui wengi.Hata mimi nina maadui lakini kuna adui mmoja ambaye ni mwenye nguvu na ametishia kiti changu.Hata mimi ninamuogopa kutokana na nguvu aliyonayo katika chama na ni mtu ambaye alichangia sana kwa mimi kukikalia kiti hiki.Kuna jambo nimelifanya ambalo huyu mtu ana maslahi nalo na tayari ametishia kuniondoa katika kiti hiki.Hilo la kuniondoa katika madaraka kwa kuwashawishi wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na mimi silijali sana kwani muda niliobaki nao katika uongozi ni mfupi lakini mtu huyu ataendelea kuniandama hata nitakapomaliza uongozi wangu kwa kuwa jambo ninalotaka kulifanya lina maslahi kwake.Anataka nisilifanye jambo hilo lakini siwezi kuacha kulifanya jambo hilo kwa sababu litanihakikishia kuishi maisha mazuri sana baada ya kumaliza uongozi wangu.Kazi ya uraisi kwa nchi kama hizi za kwetu ni kazi ambayo ina heshima kubwa lakini isiyokuwa na maslahi makubwa.Nimelitumikia taifa kwa miaka kumi lakini nitakapomaliza nitarejea katika maisha yale yale ya kawaida sana .Japokuwa nitakuwa nikitunzwa na serikali bado maisha yangu hayatakuwa mazuri jinsi ninavyotaka kwa hiyo lazima kabla ya kumaliza kipindi changu cha uongozi basi nijipange ili niishi maisha mazuri baada ya kustaafu.”akanyamaza kidogo na kuendela
“ Lazima nichukue hatua za haraka sana dhidi ya mtu huyo ambaye ninamtaja kama adui yangu namba moja kwa sasa.Njia pekee ya kujihakikishia usalama wangu ni kwa kumuondoa huyo adui yangu toka katika uso wa dunia.Bila kufanya hivyo sintakuwa na amani na maisha yangu na nina hakika ataendelea kuniandama kila uchao” akasema Dr Joshua
“ Pole sana Dr Joshua.Nafasi kama hizi za uongozi lazima ukutane na changamoto nyingi sana.Ni nani huyo adui yako na unapendekeza tumshughulikiaje? akauliza Generali Adam
“ Ndiyo maana nilikwambia kwamba mazungumzo yetu ni ya siri na asifahamu mtu mwingine yeyete kwa sababu mtu huyo ninayemzungumzia ni mtu mkubwa sana hapa nchini na aliwahi kuwa rais wa nchi kwa hiyo jambo kama hili ni siri kubwa sana.” akasemaDr Joshua
“ usihofu kitu mzee.Si mara ya kwanza mimi na wewe kufanya kazi kubwa na za hatari na haijawahi kusikia hata siku moja kwamba kuna siri imevuja.Mimi ni mwaminifu sana kwako mheshimiwa rais.Jisikie huru kunieleza chochote “ akasema Generali Adam
“ Good.Mtu huyo ninayemsema hapa ni rais mstaafu Deus Mliswati” akasema Dr Joshua.Kimya kikubwa kikatanda mle ndani wakabaki wakitazamana.Generali Adam alistushwa mno na taarifa ile.
“ Adam najua umestuka sana kusikia jina la Deus.N i jina kubwa na hakuna mtu asiyemfahamu mtu huyu katika nchi hii.Mimi mwenyewe ni mtu ambaye ninamuheshimu sana Deus na nina deni kubwa kwake kwa mambo makubwa aliyonifanyia.Lakini katika siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.Deus leo hii amegeuka kuwa adui yangu na nisipofanya juhudi za makusudi na za haraka kujilinda basi ataniondoa kwani amekwisha dhamiria kufanya hivyo kwa hiyo lazima nijihami mapema.lazima nimuwahi.Nataka tumuue Deus haraka iwezekanavyo” akasema Dr Joshua.Adam akakuna kichwa chake na kuinama akafikiri kidogo na kusema.
“ dr Joshua hili si jambo jepesi hata kidogo.Yule ni rais mstaafu na kummaliza kama unavyotaka ni jambo gumu kidogo.Una hakika una nia ya dhati ya kutaka kumuua Deus? Hakuna namna mnayoweza kumaliza tofauti zenu? Akauliza general adam
“ Adam hakuna namna yoyote ya kufanya zaidi ya kumuua.Deus is my enemy na nisipomuwahi yeye basi ataniwahi mimi.Siko tayari Deus aniteketeze wakati nina kila sababu ya kuweza kummaliza.Hii ni vita na inanibidi nitumie kila aina ya silaha na mbinu ili kummaliza kwa hiyo sitaki kushindwa nataka nishinde hii vita na kitu pekee kitakachonihakikishia ushdini ni kwa kumuua Deus.Nimekuita hapa kama rafiki na mtu wangu wa karibu unisaidiekatika hili.Hili ni jambo zito, na lenye usiri mkubwa kwa hiyo nahitaji kumshirikisha mtu ambaye ninamuamini na wewe ni mtu ambaye ninakuamini sana ”akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua siku zote nimekuwa mtiifu kwako na nitaendelea kuwa mtiifu lakini kuhusu suala hili ninaomba ulifikirie tena upya kwani linaweza kuwa na athari kubwa kwako na kwetu pia .Deus ni rais mstaafu kwa hiyo kitendo cha kumuua kinaweza kusababisha uchunguzi wa kina ukafanywa na inaweza ikajulikana kama umehusika katika kifo hicho na utakabiliwa na matatizo makubwa sana” akasema Generali Adam
“ Adam tafadhali usiogope.Mimi ni rais wa nchi na nina uwezo mkubwa wa kuzuia huo uchunguzi usifanyike.” Akasema Dr Joshua.Generali Adam aliinama chini alionekana kuzama katika mawazo .
“ Unawaza nini general? Akauliza Dr Joshua
“ nI kuhusiana na jambo hili.Sijawahi kushiriki katika jambo kubwa kama hili hususani la kutaka kumuua rais mstaafu.Hili ni jambo zito kwa hiyo lazima nifikirie kwa makini kabla ya kutoa jibu kama ninaweza kulifanya ama la” akasema Deus
“ Nafahamu hii ni kazi ngumu lakini ina ujira mnono.Mkuu wa majeshi Generali Gosbert maziga anastaafu mwezi ujao na nitakuteua wewe kuwa mkuu wa majeshi.” Akasema Dr Joshua na Generali Adam akainuka kichwa
“ Dr Joshua is this a joke? Akauliza Adam
“ Kwa nini nikufanyie masihara Adam.Nitakuchagua wewe kuwa mkuu mpya wa majeshi.Mimi ndiye mwenye uwezo huo kwa hiyo nakuomba tafadhali nifanyie hiyo kazi na utaona matunda yake.Kabla sijamaliza uongozi wangu nitakuacha katika nafasi kubwa na ya juu kabisa katika jeshi.Hivi ndivyo huwa ninafanya kwa wale watu wangu wote wa karibu ambao hunifanyai kazi zangu na kunifurahisha,huwaweka juu katika nafasi za juu sana” akasema Dr Joshua na kumfanya Adam atabasamu
“ Dr Joshua nimekosa neno la kusema kwa furaha niliyonayo .Usiwe na wasi wasi ninakuahidi kwamba nitaifanya kazi yako.Lakini nitahitaji muda kidogo wa kama siku mbili hivi nitulize akili nitafakari ni kwa namna gani tunaweza kuutekeleza mpango huu mku………………” Adam akanyamaza baada ya simu ya Dr Joshua kuita na sura ya Dr Joshua ikabadilika kidogo baada ya kuliona jina la mpigaji
“ Give me one minute Adam.Its an important call” akasema Dr Joshua na kutoka mle ndani ya kile chumba
“ Hallow Kigomba” akasema Dr Joshau baada ya kupokea simu
“ Dr Jos..Joshu.Jos…..” Kigomba alikuwa anatetemeka na kushindwa kuongea.Hali ile ikamstua sana Dr Joshua
“ Kigomba what happened? Akauliza Dr Joshua kwa wasi wasi mwingi
“ Joshua….jos..” Bado Dr Kigomba alishindwa kuongea.Alikuwa akihema kwa kasi
“ Kigomba niambie nini kimetokea.Naomba utulie tafadhali na unieleze nini kimetokea? Akauliza Dr Joshua .
“ Dr Joshua kuna matatizo makubwa yametokea.” Akasema Kigomba
“ Matatizo makubwa ?!!..Nini kimetokea Kigomba? Dr Joshua akauliza huku mapigo ya moyo yakibadilika na kuanza kwenda kwa kasi kubwa
“ Mwanao Flaviana..!! akasema Kigomba
“ Flaviana amefanya nini?
“ Flaviana amepigwa risasi”
Dr Joshua alikisikia kichwa chake kama kikigongwa na nyundo kubwa.Alishindwa aseme nini.Mwili ulimtetemeka.Ilikuwa ni taarifa iliyomstua sana.Baada ya kama dakika moja akakohoa kidogo na kusema
“ Kigomba tell me it’s a joke” akasema Dr Joshua
“ Its not a joke Joshua.Ni kweli kabisa Flaviana amepigwa risasi na hivi sasa tuko njiani tunamkimbiza hospitali ya taifa” akasema Dr Kigomba
“ Imetokeaje Kigomba? Imekuwaje akapigwa risasi? Akauliza Dr Joshua
“ Dr Joshua sina muda wa kukuelezea kwa sasa.Ninachokuomba amka na uanze safari ya kuelekea hospitali mara moja.” Akasema Dr Kigomba
“ Kigomba naomba uniambie ukweli.Is she dead ? akauliza Dr Joshua
“ No ! but she’s in critical condition.Kuna vijana wetu kama watatu au zaidi wamefariki dunia.”akasema Dr Kigomba.Dr Joshua akashika kichwa .Alichanganyikiwa.
“ Ok Kigomba I’m on my way there” akasema Dr Joshua na kuingia katika chumba alimo genereli Adam.
“ Adam tutaendelea na maongezi siku nyingine.Kuna tatizo kubwa limetokea.Binti yangu amepigwa risasi ”
“ Is she ok? Akauliza genereli Adam
“ I don’t know.Fanyia kazi hayo mambo tuliyoongea” akasema Dr Joshua
“ Sawa mzee ,nitayafanyia kazi na nitakujulisha kila kitu.Pole sana mheshimiwa rais” akasema Generali Adam.Dr Joshua akatoka kwa kasi mle chumbani na kuwataarifu walinzi wake kwamba wajiandae wanaelekea hospitali,akaingia chumbani kwake kujiandaa
“ Imekuwaje Flaviana akapigwa risasi? Akajiuliza Dr Joshua.Mwili bado ulikuwa unamtetemeka.
“ Ouh Mungu wangu naomba umponye mwanangu huyu.Ninampenda sana binti yangu na siko tayari afariki” akasema Dr Joshua kwa sauti ndogo halafu akatoka na kuingia kuingia garini safari ya kuelekea hospitali ikaanza.
“ Majanga yanazidi kuniandama. Hata wiki mbili hazijapita toka amefariki flora leo hii tena Flaviana naye yuko katika hatari ya kunitoka.Lakini hizi zote ni changamoto za biashara ile ya ile package.Pamoja na yote yaliyotokea na yatakayoendelea kutokea lakini lazima niifaney biashara hii”akawaza Dr Joshua akiwa garini kuelekea hospitali
“ Lakini imetokeaje hadi Flaviana akapigwa risasi ? Kigomba ana kazi kubwa ya kunielezea kuhusiana na jambo hili lilivyotokea na kusababisha mwanangu apigwe risasi.Ouh halafu nimeondoka bila ya kumtaarifu Anna kuhusiana na kilichotokea” akawaza Dr Joshua na akachukua simu yake na kumpigia Anna
“ Hallow Anna uko wapi?” akauliza Dr Joshua baada ya Anna kupokea simu.Anna akasita kidogo kujibu hakutaka baba yake afahamu mahala alipo
“ Anna uko wapi? Akauliza tena Dr Joshua
“ Nimetoka kidogo baba ”
“Uko wapi? Umetoka umekwenda wapi? Akauliza Dr Joshua
“ Nimetoka na Flaviana?!
“ Umetoka na Flaviana?!! Dr Joshua akazidi kushangaa
“Ndiyo baba ,Flaviana aliniomba nimsindikize mahala Fulani kuna mtu anakwenda kuonana naye usiku huu.”
“ Anna tafadhali naomba unieleze ukweli uko wapi? Sikuulizi kwa lengo baya”
“ Baba ni kweli nimemsindikiza Flaviana .”
“ Anna mbona unazidi kunichanganya.Uko na Flaviana muda huu?
“ Hapana siko naye kuna sehemu amekwenda na mimi niko garini ninamsubiri”
“ Anna tafadhali naomba usiondoke hapo ulipo.Nielekeze mahala ulipo ilinitume walinzi wajewakuchukue mara moja”
“ kwani kuna jambo gani baba?Mbona unaniogopesha?
“ Tafadhali niambie Anna uko wapi?
Anna akafikiri kwa sekunde chache na kusema
“ Niko hapa Simbona hoteli ninamsubiri Flaviana” akasema Anna
“ Ok Anna naomba usitoke hapo ulipo na kama uko garini usishuke hadi utakapowaona walinzi nitakaowatuma” akasema Dr Joshua akakata simu na kuwapigia walinzi ili wamfuate Anna pale alipo.Aliogopa kumweleza ukweli Anna akiogopa kumstua
“ kigomba amenieleza tu kuhusiana na Flaviana lakini hajanipa taarifa za Elibariki kama walifanikiwa kumpata au hawakufanikiwa ? Kama hawakufanikiwa kumpata na safari hii basi tutakuwa na wakati mgumu sana.Lakini kwa nini inakuwa vigumu kumpata mtu kama huyu? Hapana imetosha sasa na siwezi kumvumilia.Nitaitumia nguvu yangu kama rais na Elibarii atapatikana ndani ya kipindi kifupi.Nitatumia mtandao mpana wa jeshi la polisi kumtafuta na nitampata.” Akawaza Dr Joshua huku msafara ake ukienda kwa kasi isyo ya kawaida na hatimaye wakawasili hospitali na kupokelewa na dakari mkuu wa hospitali kuu ya taifa akiwa sambamba na Dr Kigomba ambaye alikuwa ameloana damu
“ Daktari mwanangu anaendeleaje? Akauliza Dr Joshua
“ Hali yake haikuwa nzuri wakati tumempokea na kwa sasa ameingizwa katika chumba cha upasuaji na timu ya madaktari wanaendelea kumuhudumia ili kuokoa maisha yake ” akasema daktari mkuu wakati wakiwa njiani kuelekea katika jengo la upasuaji.Dr Joshua aliomba aruhusiwe kuingia katika chumba cha upasuaji ashuhudie kilichokuwa kinaendelea.Akavalishwa mavazi maalum ya kuingilia katika chumba kile na kuingia akiongozana na daktari mkuu.Kazi ya kuokoa uhai wa Flaviana ilikuwa inaendelea na madaktari walikuwa katika heka heka kubwa.
“ Ee Mungu nafahamu mimi si mkamilfu mbele zako na nimekukosea mambo mengi sana makubwa lakini naomba usiniadhibu kwa kunichukulia binti yangu ninayempenda sana.bado ninamuhitaji sana” Dr Joshua akaomba kimya kimya.Machozi yalimlenga kwa kumuona mwanae akiwa kitandani hajitambui akisaidiwa kupumua kwa mashine.Hakutaka kuendelea kukaa mle ndani akatoka .
“ Dr Marcelo naomba mjitahidi kwa kila namna muwezavyo kuokoa uhai wa mwanangu.Sitaki kumpoteza Flaviana “ akasema Dr Joshua
“ mzee tunafanaya kila linalowezekana ili kuokoa uhai wa mwanao.Wewe mwenyewe umeshuhudia namna madaktari wanavyojitahidi na nina hakika watafanikiwa.Tumuombe Mungu atusadie katika jambo hili” akasema Dr Marcelo.
“ nashukuru sana Dr Marcelo.Nina hakika Mungu atasikia kilo changu na kumnusuru mwanangu” akasema Dr Joshua
“ Mzee unaweza tu kwenda kupumzika na sisi tutaendelea kuifanya kazi hii usiku huu na kama kutakuwa na lolote tutakufahamisha” akashauri Dr Marcelo
“ No Marcelo.Nitakesha hapa kufuatilia hatima ya mwanangu.” Akasema Dr Joshua ikamlazimu Dr Marcelo ampeleke sehemu ya mapumziko wakati wakisubiri Flaviana atolewe katika chumba cha upasuaji.Dr Kigomba naye aliambatana naye
“Dr Kigomba naomba unieleze nini hasa kimetokea? Akauliza Dr Joshua wakiwa wamepumzika wakisubiri upasuaji wa Flavina umalizikie.Midomo ya Dr Kigomba ilikuwa mizito kufunguka
“Kigomba tell me what happened? Akauliza Dr Joshua huku akimtazama Dr Kigomba kwa macho makali
“ Dr Joshua nashindwa hata sehemu ya kuanzia kukueleza namna ilivyokuwa” akasema Dr Kigomba
“ Tell me everything !! akasema r Joshua.Kabla Kigomba hajasema chochote akatokea Anna akiwa ameongozana na walinzi.Alikuwa na wasiwasi mwingi sana
“ Baba kuna nini?akauliza anna.Dr Joshua akamshika mkono na kumketisha kitini.
“ Anna dada yako alikupeleka wapi usiku huu ? Akauliza Dr Joshua
“ Aliniomba nimsindikize sehemu Fulani kuna mtu alikuwa anakwenda kuonana naye?
“ hakukwambia ni nani aliyekuwa anakwenda kuonana naye?
“ Hapana hakuniambia kwani kuna nini?akauliza Anna
“ Ulimuona mtu huyo aliyekwena kuonana naye? Akauliza Dr Joshua
“ Hapana sikufanikiwa kuonana naye kwani aliniacha mimi katika gari na yeye akaenda kuonana na mtu huyo” akajibu Anna
“ Alionana naye wapi?
Anna akasita kidogo halafu akasema
“ Mimi aliniacha katika gari na kuniomba nimsubiri akaingia katika gari Fulani la rangi ya bluu na likaondoka.Sijui alielekea wapi na ikanilazimu kuendelea kumsubiri hadi pale uliponipigia simu na kuniomba nisishuke garini.Kuna nini baba? Akauliza Anna
“ Anna dada yako Flaviana amepatwa na matatizo huko alikokwenda”
“ Matatizo?! Anna akastuka sana
“ Ndiyo amepatwa na matatizo “
“ Matatizo gani baba? Is she ok? Akauliza Anna huku sura yake ikishindwa kuuficha mstuko alioupata
“ Dada yako ameshambuliwa na watu wasiojulikana na hali yake si nzuri ,hivi sasa madaktari wanashughulika kuokoa maisha yake kwa hiyo tunatakiw……………….” kabla Dr Joshua hajamaliza Anna akaanguka na kupoteza fahamu.Haraka haraka walinzi wakamuinua na kumpeleka sehemu husika kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza
“Nilitegemea jambo kama hili lingeweza kutokea na ndiyo maana sikutaka kumweleza chochote Anna akiwa garini kwani ningehatarisha maisha yake” akawaza Dr Joshua na baada ya sekunde kadhaa akamgeukia Dr Kigomba
“ Kigomba I need to know what happened ? Akasema Dr Joshua
Bado dr Kigomba alikuwa akitetetemeka alishindwa kusema kitu kilichotokea.
“Kigomba,mwanangu Flaviana yuko ndani ya chumba cha upasuaji hivi sasa akipigania uhai wake,naomba tafadhali unieleze nini kimesababisha akapigwa risasi ? Wewe ndiye niliyekukabidhi jukumu zima la kusimamia shughuli ile and you’ve failed me again” akasema Dr Joshua kwa ukali.Dr KIgomba akarekebisha koo lake na kusema
“ Tulimfuatilia Flaviana bila ya yeye kutambua hadi tulipofika Simbona hoteli.Pale alishuka katika gari lakena kuingia katika gari lingine dogo la bluu na kisha gari lile likaondoka pale hotelini.Tuliamini ndani ya gari lilendimo alimo Elibariki hivyo tukaendelea kumfuatilia.Tulilifuata gari lile hadi katika viwanja vya ukombozi.Tuliingiwa na shaka kidogo kuhusu dhumuni lake la kwenda pale.Tulijificha kwa takribani dakika kumi hivi tukisubirikuona kama kuna mtu atashuka lakini hakuna aliyeshuka,tukahisi i labda huenda kukawa na jambo linaendelea pale ndani ya gari.Kwa kuwa muda ulizidi kwenda ilinibidiki kuwatuma vijana wawili waende wakachungulie kilichokuwa kinaendelea mle ndani ya gari .Ghafla tukasikia mlio wa risasi mara tu vijana wale walipolikaribia gari na kijana wetu mmoja kati ya wale wawili akaanguka chini.Tulistushwa sana na kitendo kile ambacho hatukuwa tumekitegemea .Kijana wetu mwingine aliyebaki akapatwa na mstuko na kuanza kupiga risasi hovyo ili kujiokoa.Ghafla naye akapigwa risasi akaanguka chini .Ilitulazimu na sisi kuanza kufyatua risasi mfululizo ili kuwachanganya watu waliokuwapo pale uwanjani ambao hatukujua idadi yao.Nadhani milio ile ya risasi ilimstua Flaviana hivyo akafungua mlango wa gari na kushuka akaanza kukimbia na mara mtu mmoja ambaye tunaamini ni mmoja wa watu wa Elibariki alitoka mafichoni na kuanza kumkimbilia akimuita jina lake .Tulidhani mtu yule ni Elibariki na ndipo vijana wetu walipoanza kumrushia risasi .Mtu yule hakuwa Elibariki kwani alionekana ni mtu mahiri sana katika mapambano na namnaya kujikinga na shambulizi.Risasi zilimpata Flaviana akaanguka chini.Toka ndani ya lilegari akatoka tena mtu mwingineambaye tuliamini ni Elibariki na tukammiminia risasi akaanguka na kufariki pale pale .Risasi zikakoma na tulipokwenda kumuangalia mtu Yule hakuwa Elibariki. Kwa hiyo hatukufanikiwa kumpata Elibariki. Baada ya hapo tukapiga simu polisi na kumchukua Flaviana tukamkimbiza hospitali.Hivyo ndivyo ilivyotokea Dr Joshua.Hakuna aliyetegemea kama kungekuwa na shambulio kama lile.Inaonekana watu wale walifahamu kwamba lazima tutamfuatilia Flaviana na ndiyo maana wakatuwekea ule mtego.Dr Joshua hali hii inazidi kuwa mbaya.Elibariki ni mtu ambaye inabidi tumsake kwa kila namna kabla hajasababisha madhara makubwa kwetu.”akasema Dr Kigomba Dr Joshua akabaki kimya alikosa neno la kusema
“He escaped again” akasema Dr Joshua kwa kwa masikitiko.
“yes he did escape again” akasema Dr Kigomba huku akitazama chini
“ Dr Kigomba we have to clear this mess.Najua polisi lazima watafanya uchunguzi wao kuhusiana na tukio hili na wanaweza wakaingia ndani zaidi na wakagundua kwamba tunahusika nalo kwa hiyo tunatakiwa kufuta nyayo haraka sana.Mzigo wote tutamtupia jaji Elibariki.Tutaliweka jambo hili namna hii. Kwamba Flaviana amekuwa na mahusiano na mwanaume mwingine nje ya ndoa yake na hivyo kupelekea jaji Elibariki na huyo mwanaume kukwaruzana na Elibariki kuhisi kwamba mwanaume huyo ambaye amekuwa na mahusiano na mke wake ndiye aliyepanga shambulio lile lililomtokea na kwa hiyo akaamua kulipiza kisasi kwa mke wake.Akampigia simu na kumuomba wakutane mahali fulani usiku ule.Tutasema kwamba alimpeleka katika viwanja vya ukombozi kwa lengo la kumuua na Flaviana alipohisi hatari alinitumia ujumbe na nikatuma walinzi pamoja na wewe haraka sana eneo la tukio na ndipo lilipotokea shambulio lile.Tukifanya hvyo tuamuangushia mzigo wote Elibariki na atatafutwa katika kila kona ya nchi kwa kitendo hiki na atapatikana tu.Unaonaje kuhusu mpango huu?” akasema Dr Joshua “Ni mpango mzuri sana Dr Joshua.Hii ni njia bora sana ya kumpata jaji Elibariki.” Akasema Dr Kigomba.
“ Naomba umtafute mkuu wa kanda maalum ya Dar es salaam,nahitaji kuongea naye kumpa maelekezo ” akasema Dr Joshua na bila kupoteza wakati Dr Kigomba akampigia simu kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam na kumfahamisha kwamba rais anahitaji kuonana naye
“ hallow mheshimwia rais” akasema kamanda wa polisi wa kanda maalum
“ kamanda,kuna tatizo limetokea na ninadhani tayari umekwisha taarifiwa” akasema Dr Joshua
“ Ndiyo mzee.Nimekwisha taarifiwa kuhusiana natukio hilo na niko njiani kuelekea huko sasa hivi.Nimeambiwa kwamba kulikuwa na mapambano ya risasi kati ya watu wa usalama wa taifa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi,na watu wapatao wanne wamekutwa wamekufa na mwanao Flaviana amejeruhiwa kwa risasi” akasema kamanda wa polisi
“ Ndiyo kamishna .Kwa hivi sasa niko hapa hospitali kuu ya taifa na hali ya mwanangu si nzuri.Madaktari wanaendelea na jitihada za kuokoa uhai wake”
“ Pola sana mheshimwia rais .Tutajitahidi kwa kila tuwezavyo ili tuweze kumpata mtu au kikundi cha watu waliofanya jambohili.”akasema kamanda wa polisi
“ Kamishna ,hakuna haja ya kusumbuka sana kwani tayari tumemfahamu mtu aliyefanya shambulio hilo”
“ Mmekwisha mfahamu? akauliza kamanda wa polisi
“ ndiyo kamishna,huwezi amini mtu aliyefanya hivi ni mume wake ,ni jaji Elibariki”
“ jaji Elibariki?! Kamishna akashangaa
“ Ndiyo kamishna.Ni yeye ndiye aliyefanya jambo hili”
“ Mheshimiwa rais ninapata ugumu kidogo kuhusu jambo hili.Imekuwaje jaji Elibariki afanye shambulio kama hili kwa mke wake?Kwa nini atake kumuua mke wake?
“ Ni hivi kamishna,ndoa ya Flaviana na mumewe kwa siku za hivi karibuni imekuwa katika mgogoro mkubwa.Wamekuwa wakituhumiana kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwa kutoka nje ya ndoa.Elibariki alikuwa akikwaruzana sana na mtu ambaye anahisi kwamba ndiye anayeiharibu ndoa yake.Mtu huyo ambaye hatujamfahamu bado inasemakana kwamba ndiye aliyeratibu shambulio lile ambalo Elibariki alinusurika.Baada ya kunusurka jaji Elibariki alitaka kulipiza kisasi na kwa kuanzia alitaka kumuua mkewake na ndiyo maana usiku huu alimpigia simu na kumtaka waonane sehemu Fulani na kisha akamchukua na kumpeleka katika viwanja vya ukombozi . Flaviana alihisi hatari na akanitumia ujumbe ikanilazimu kutuma vijana wa usalama pamoja na katibu wangu Dr Kigomba.Walipofika likatokea shambulio la kustukiza toka katika kundi la Elibariki vijana niliowatuma walianza kupambana ili kumuokoa Flaviana lakini inaonekana Elibariki na kundi lake walikuwa wamejipanga kwa silaha kali na vijana wangu wakazidiwa nguvu na watatu kati yao wakapoteza maisha na Flaviana akajeruhiwa kwa risasi.Elibariki na kundi lake wamefanikwa kukimbia .Ninaomba kamishna kuanzia usiku huu Elibariki aanaze kusakwa katika kila kona ya jiji na hakikisha amepatikana.” Akasema Dr Joshua
“ Sawa mzee nimekuelewa.Ahsante kwa taarifa hizo ambazo zitatusaidia sana katika uchunguzi wetu.Tutaanza msako mkali wa kumtafuta Elibariki kuanzia usiku huu.Na kuna taarifa nimeipokea hivi sasa inasema kwamba mmoja wa watu waliouawa katika tukio hilo ni jambazi sugu ambalo limekuwa likitafutwa sana na polisi kwa wizi wa magari na wizi wa kutumia silaha.Nikiunganisha taarifa hii na maelezo yako tunapata picha kwamba yawezekana Elibariki alimkodisha jambazi huyu ili kumfanyia kazi yake ya kumuua Flaviana”
“ umeona nilichokuwa nakwambaia Kamishna? Elibariki ni mtu hatari sana na tunatakiwa tumpate haraka sana” akasema Dr Joshua
“ Mzee nakuhakikishia kwamba tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu na Elibariki atapatikana ndani ya muda mfupi”
“Nashukuru sana Kamishna.Naomba taarifa za mara kwa mara kuhusiana na uchunguzi huu”akasema Dr Joshua na kukata simu na kumgeukia Dr Kigomba
“ Kwa mujibu wa kamishna ni kwamba kuna mtu mmoja amekutwa aneo la tuko amekufa ni jambazi sugu ambaye amekuwa akitafutwa siku nyingi na jeshi la polisi.Hii inadhihirisha wazi kwamba Elibariki anashirikiana na mtandao wa majambazi hatari.Elibariki si mtu wa kuachiwa akatamba,lazima adhibitiwe haraka sana” akasema Dr Joshua
“ Nnakubaliana nawe kwa sababu mapigano yale yalikuwa makali sana na ilionekana kabisa kwamba watu wale walikuwa ni wajuzi sana wa kutumia silaha” akasema Dr Kigomba
“ Nimesahau kukuuliza,ile taarifa aliyokuwa nayo Flaviana mmefanikiwa kuondoka nayo ?akauliza Dr Joshua
“ Hapana Dr Joshua taarifa ile hatukufanikiwa kuichukua .Kutokana na mvurugano uliokuwepo sikukumbuka hata kuchukua taarifa ile.”
“ Ouh mungu wangu ! kama Elibariki akiipata taarifa ile tumekwisha” akasema Dr Joshua
“ Usiwe na hofu mzee,hata kama akiichukua hakuna sehemu ambayo atapita nayo.Kwa sasa Elbariki ni kama mkimbizi na akionekana sehemu yoyote ile atakamatwa kwa hiyo usipate shida kwa Elbariki kuipata ripoti ile”akasema Dr Kigomba
*******
Anitha na Mathew walimsadia jaji Elibariki kushuka garini na kumuingiza ndani.Hakuwa na nguvu za kutembea.Hakuwa amejeruhiwa sehemu yoyote ile lakini tukio lililotoka usiku ule lilimmaliza nguvu kabisa.
“ Ahsanteni sana ndugu zangu” akasema Jaji Elibariki baada ya kuketishwa sofani.
“Mathew ahsante sana bila wewe leo tungekufa.Umepambana sana kutuokoa. Uliponiambia kwamba unahisi Flaviana atakuwa akichuguzwa nilidhani ni kama unatania vile lakini baada ya kushuhudia kilichotokea sasa ninakuamini.Una akili ya ajabu sana” akasema jaji Elibarki kwa sauti dhaifu.Anitha aliyekuwa ameketi sofani naye alionekana amechoka sana na hakutaka kusema chochote.Mathew akavua ile fulana isiyopenya risasi akaitupa pembeni naye akaketi sofani akainamisha kichwa.Alikuwa katika mawazo mengi sana.Picha ya tukio zima ndiyo iliyokuwa imetawala kichwa chake.Alikuwa anakumbuka namna tukio lile lilivyotokea
Waliliacha gari katika zahanati iliyokuwa karibu na viwanja vya ukombozi wakatembea kwamiguu wakipita njia fupi na kuwahi kufika kabla ya gari alimo Flaviana kuwasili.Eneo la uwanja ule lilikuwa na mwangaza hafifu uliotokana na taa za nyumba jirani.Walijibanza katika sehemu inayotumika kama jukwaa na baada ya dakika nne mwanga wa gari ukaonekana.Lilikuwa ni gari alimo Flaviana
“ Mathew hakuna tena muda wa kupoteza,ngoja nikachukue ile ripoti”akasema jaji Elibariki huku akitaka kuinuka
“ Ngoja kwanza Elibariki ,hatuwezi kwenda hadi tuhakikishe kuko salama”akasema Mathew na kisha wakaendelea kujibanza wakisubiri
‘Mathew yawezekana wale jamaa tuliohisi walikuwa wanamfuatilia Flaviana watakuwa wamekata tamaa na wakaamua kurudi,mbona hawatokei tena? akauliza Elibariki
“ Elibariki naomba uwe na subira kidogo.” Akasema Mathew na baada ya kama dakika kumi hivi watu wawili wakaonekana wakiliendea gari lile.Jaji Elibariki akaogopa
“ watu wale ni akina nani ?akauliza jaji elibariki.Mahala walipokuwa wamejibanza hapakuwa mbali na gari alimo Flaviana kwa hiyo kwa kutumia mwangaza ule wa taa za jirani waliweza kuwaona vizuri watu wale
“ Subiri kwanza tutafahamu ni akina nani.Yawezekana wakawa ni miongoni mwa wale ambao wanamfuatilia Flaviana” akasema Mathew
watu wale walifika katika gari lile na kuchomoa bastora wakaanza kugonga dirisha upande wa dereva wakitaka wafunguliwe mlango
“Mathew do something,watu wale watamdhuru mke wangu” akasema Elibarii kwa uoga.
“ subiri kwanza Elibariki.hatuwezi kuwavamia haraka haraka namna hiyo” akasema Mathew
Ghafla ukasikika mlio wa risasi na mtu mmoja katika ile gari akaanguka chini.Bastora aliyokuwa ameishika jaji Elibariki ilikuwa inatoa moshi.Ni yeye ndiye aliyeachia risasi ile.Baada ya mlio ule wa risasi ikaanza kusikika milio ya risasi toka katika kila upande wa uwanja zikielekea kule iliko gari alimo Flaviana.Mlango wa nyuma wa gari ukafunguliwa na Flaviana akatoka
“ Anitha cover me ! “ akasema Mathew na kutoka kwa kasi kumfuata Flaviana aliyekuwa akikimbia huku milio ya risasi ikisikika.
“ Flaviana get down !!..akapiga kelele Mathew akimtaka Flaviana aache kukimbia na alale chini kwani mivumo ya risasi iliongezeka.Ghafla Flaviana akaanguka huku akitoka ukulele alikuwa amepigwa risasi.Mathew akajirusha na kutua karibu na mahala alipoangukia Flaviana.Hatua chache toka mahala alipoanguka Flaviana kulikuwa na bahasha Mathew akainyakua bahasha ile na kuanza kukimbia nayo.
“ twendni tuondoke,hapafai mahala hapa” akasema Mathew
“ Flaviana tunamuacha?akauliza jaji Elibariki
“ Amepigwa risasi” akasema Mathew
“Mathew hapana siwezi kuondoka na kumuacha Flaviana.Lazima tuondoke naye”
“ Elibariki hatuna muda wa kupoteza hapa watu tunaopambana nao wana silaha kali na hatujui wako wangapi.They’re going tokill us.Lets get out of here !! akasema Mathew na kisha wakaanza kukimbia kuondoka.
“Mathew !! akaita Elibariki na kumtoa Mathew katika kumbukumbu ile akageuka na kumtazama
“ Mathew una hakika mke wangu atakuwa salama? Akauliza Elibariki
“ I don’t know Elibariki..” akajibu Mathew
“ Yote haya ni makosa yangu.Kama ningekusikiliza yasingetoeka haya.Nilifanya makosa kuanza kuachia ile risasi ambayo ndiyo imesababisha mke wangu akapigwa risasi.Ouh Flaviana ..!! akasema jaji Elibariki.Alionekana kuchanganyikiwa
“ Sina hakika kama Flaviana atakuwa hai kwani nilikuwa karibu naye na nikasikia namna alivyokuwa akihangaika kuvuta hewa lakini siwezi kumwambia Elibariki kwani nitazidi kumchanganya.Alifanya kosa kubwa kuachia ile risasi,alitakiwa asubiri maelekezo yangu” akawaza Mathew na kisha akaikumbuka ile bahasha ambayo alikuwa nayo Flaviana akaenda garini kuichukua
“ Pamoja na yote yaliyotokea lakini tumefanikiwa kuipata hii taarifa tuliyokuwa tukiitafuta .taarifa ya madaktari bingwa kuhusianana kifo cha Dr Flora.” Akasema Mathew
“ Mathew nahitaji kufahamu Flaviana anaendeleaje.Please help me” Akasema jaji Elibariki
“ Elibariki hilo ni jambo ambalo haliwezekani kwa sasa.Tunachotakiwa ni kufumba machona kuomba.Anything can happen “ akasema Mathew
“ Mimi na Flaviana tumepitia mambo mengi na ndoa yetu imekumbwa na migogoro mingi lakini sitaki apoteze maisha.Bado anayo nafasi katika maisha yangu.Please Lord save her” akasema jaji Elibariki na michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake
“ Elibariki nadhani unahitaji mapumziko .Kesho asubuhi tutafahamu kinachoendelea” akasema Mathew .Jaji Elibariki hakusema kitu akajitahidi kusimama na kisha aketembea kuelekea katika chumba chake.
“ Anitha hata wewe pia unahitaji mapumziko ,siku imekuwa ndefu sana,mambo mengi yametokea usiku huu ,tupumzikena tujiandae kwa ajili ya siku ya kesho,ila kitu kimoja ambacho sikutaka kukwambia mbele ya Elibariki ni kwamba sina hakika kama mkewake atakuwa salama.Nilimsogelea karibu ilikuchukua ile bahasha nikasikia namna alivyokuwa akihangaika kuvuta hewa.Tusubiri hadi siku ya kesho tutapata taarifa nini kimetokea ,kama ni mzima ama amefariki “
“ maskini Elibariki.Namonea huruma sana.Amepatwa na majanga mengi mfululizo “akasema Anitha
“Kesho tutaanza kuifanya kazi taarifa ile ya madaktari kubaini ukweli wake.Vile vile nitawasiliana na rafiki zangu wa huko nje ili waweze kunisiadia kutambua kilichomo ndani ya zile karatasi zilizoibwa ikulu” akasema Mathew na kila mmoja akaenda chumbani kupumzika.
Saa kumi alfajiri madaktari katika hospitali kuu ya taifa walikamilisha upasuaji waliokuwa wakimfanyia Flaviana ili kuondoa risasi na kujaribu kuokoa maisha yake.Bado Dr Joshua alikuwepo pale hospitali akisubiri kutaarifiwa kuhusiana na hali ya mwanae.Flaviana alitolewa katika chumba cha upasuaji na kupelekwa katika chumba cha uangalizi maalum.Dr Joshua akataarifiwa kuhusu kumalizika kwa upasuaji ule halafu wakaongozana na Dr Marcelo kuelekea ofisini kwake.
“ Mheshimiwa rais upasuaji umemalizika na wamefanikiwa kuziondoa risasi tatu alizokuwa amepigwa Flaviana.Risasi moja ilimpata pajani,nyingine mbili zilimpata kifuani lakini hazikufika katika moyo .Hata hivyo madaktari wamejitahidi sana kuzuia kuendelea kuvuja kwa damu .Madaktari wamefanya kila waliloweza kulifanya kuokoa uhai wa Flaviana na kwa sasa kila kitu tukiweke katika mikono ya mwenyezi Mungu yeye ndiye mwamuzi wa kila jambo lakini bado tunaendelea kumuangalia kwa karibu sana” akasema Dr Marcelo
“Dr Marcelo sina neno la kusema kutosha kuwashukuru nini nyote kwa msaada huu mkubwa mlionisaidia.Utanifikishia shukrani zangu kwa madaktari wote waliopambana kuokoa uhai wa mwanangu.Pamoja na hayo kuna jambo nimekuwa nikilifikiria.”
“ jambo gani Mheshimiwa rais?
“ Ninafikiria kumuhamisha Flaviana na kumpeleka nje ya nchi.Unanishauri vipi kuhusu hilo?
“ Wazo lako sibaya mheshimiwa rais lakini hata hapa tunao uwezo wa kumuangalia mwanao.Kwa hali yake ya sasa sina hakika kama anafaa kusafirishwa .Nakushauri mheshimiwa rais muache hapa hapa ili aendelee kupewa uangalizi .Tunao madaktari wenye ujuzi wa kutosha ”
Dr Joshua akafikiri kidogo a kusema
“ Sawa Dr Marcelo ninakubaliana na ushauri wako .Tumuache hapa hapa nchini kwa siku kadhaa halafu kama hakutakuwa na mabadiliko nitampeleka nje ya nchi kwenye hospitali kubwa na bora zaidi “ akasema Dr Joshua na kuagana na Dr Marcelo akaingia garini akiwa na Dr Kigomba
“ Kigomba nilikuwa nafikiria kumpeleka Flaviana nje ya nchi lakini Dr Marcelo amenishauri kwamba haitafaa kwa sasa ,ngoja tusubiri kidogo na kama hali yake haitakuwa na mabadiliko basi tutampeleka nje ya nchi.Kwa hiyo anza kulifanyia jambo hili maandalizi”akasema Dr Joshua
“ Sawa Dr Joshua.Nitalifanyia kazi jambo hilo .” Akasema Dr Kigomba ambaye alionekana mchovu sana
“ Kitu kingine ambacho nataka nikuweke wazi ni kwamba pamoja na yote yaliyotokea na yatakayotokea biashara ile lazima ifanyike.Hakuna cha kuweza kutuzuia kuifanya biashara ile.Leo hii ninakwenda kuzungumza na wale jamaa ili waanze kuandaa fedha na kuzihamishia katika zile akaunti za nje.Tukisha hakikisha kwamba pesa imeingia katika akaunti zile tutawakabidhi mzigo wao ili tuachane kabisa na jambo hili na tuangalie mambo mengine kwani tayari biashara hii imeanza kuingiwa na vikwazo vingi.Vizingiti vimekuwa vingi mno na maadui wanaongezeka kila uchao.Hatutakiwi kuendelea kulivuta sana jambo hili ” akasema Dr Joshua
“ Uko sahihi Dr Joshua biashara hii lazima tuifanye haraka sana . Kila siku linaibuka jambo jipya.Tukivuta sana muda tutajikuta siku moja tunashindwa kabisa kuifanikisha kwa hiyo wakati ni sasa kama unavyoshauri”akasema r KIgomba
“ Kitu kingine ambacho nataka usisahau ,naomba uendelee kumchunguza Peniela.Ukumbuke lisemwalo lipo .Nataka tuwe na uhakika kwamba Peniela hana mahusiano yoyote na Elibariki.kama atakuwa na mahusino naye basi itakuwa rahisi sana kwetu kumpata Elibariki.Mtu aliyetoa taarifa za kunonekana kwa Elibariki nyumbani kwa Peniela ni mtu mwenye uhakika na hatupaswi kuzipuuza taarifa hizo.Tunatakiwa tuzifanyie kazi.” Akasema Dr Joshua
“ usijali mzee,leo hii hii ninaanza kulifanyia kazi hilo jambo.”akasema Dr Kigomba aliyeonekana kujawa na usingizi .Walifika katika makazi ya rais na kwa kuwa alikuwa amechoka sana akaingia chumbani kwake kujipumzisha.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
Kumepambazuka na siku mpya imeanza.Taifa limeamshwa tena na habari nyingine mpya ya shambulio lililopelekea vifo vya watu wanne pamoja na Flaviana mtoto wa rais kujeruhiwa kwa risasi.Magazeti mengi yaliandika kuhusiana na tukio lile .Wengine walilihusisha tuko lile na ujambazi baada ya mtu mmoja miongoni mwa wale waliofariki kugundulika kwamba ni jambazi sugu.
Peniela aliamka asubuhi na mapema kama kawaida yake na kuanza kujiandaa kwa ajili ya mizunguko ya siku.Siku hii alikuwa ameipanga kwa ajili ya kushughulikia suala la kupata hospitali ambayo John Mwaulaya atafanyiwa upasuaji.Baada ya kuoga akachukua simu na kumpigia Dr Joshua ili kumsisitiza na kumkumbusha kuhusu suala lile
“ Hallow Peniela” akasema Dr Joshua kwa uchoovu.Bado alikuwa na usingizi mwingi
“ Dr Joshua bado umelala? Sauti yako inaonyesha ni ya uchovu sana” akasema Peniela
“ Bado nimelala Peniela.Nimechoka sana”
“ Pole sana Dr Joshua.Siku nyingine sintakuchosha namna hii.” Akasema Peniela
“ Hapana peniela hukunichosha bali nimekesha hospitali”
“ Hospitali? ! Peniela akashangaa
“Ndiyo Peniela.Ina maana hujasikia kilichotokea? akauliza Dr Joshua
“hapana Dr Joshua sijasikia chochote,.nini kimetokea?
“ Mwanangu Flaviana amepigwa risasi jana usiku .”
“ What ?! peniela akastuka
“ Flaviana amepigwa risasi jana usiku na hali yake si nzuri.Nimekesha hospitali na nimerudi asubuhi hii ndiyo maana unaona ninaongea kichovu hivi” akasema Dr Joshua
“ Ouh my God ! Pole sana Dr Joshua.Pole sana.Anaendeleaje kwa sasa?
“ Ahsante sana Peniela.Kwa sasa hali yake si nzuri hata kidogo japokuwa amefanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi lakini bado hali yake si nzuri.Bado yuko katika uangalizi maalum.”
“dah ! Pole sana jamani.Nani lakini aliyefanya jambo hili? Akauliza Peniela
“ Ni mtu ambaye huwezi kumdhania kabisa”
‘ Mmekwisha mfahamu? Akauliza Penny
“ Ndiyo tumemfahamu na kwa sasa jeshi la polisi linamsaka kila kona ya nchi.Ni mumewe jaji Elibariki”
“ Elibariki ?!!..Peniela akastuka sana
“ Ndiyo .Ni Elibariki aliyefanya shambulio hilo” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua mna hakika kwamba ni Elibariki ndiye aliyefanya shambulio hilo?
“ Tuna kila ushahidi wa jambo hilo na kwa sasa vyombo vyote vya dola vinamsaka na tuna imani haitafika jioni ya leo kabla hajatiwa nguvuni.”
“ Mhh ! nimestuka sana kusikia kwamba Elibariki ndiye aliyefanya kitendo hicho.Japokuwa simfahamu vyema lakini anaonekana ni mtu mpole na ambaye huwezi kumdhania kama anaweza kufanya kitendo kama hicho.Pole sana dr Joshua”
“ Ahsante sana Peniela nimekwisha poa.”
“ Natamani ningekuwa karibu yako nikufariji katika wakati huu mgumu ulio nao”akasema Peniela
“ Ahsante sana Peniela kwa kunijali.Ndiyo maana nikakupa ilenyumba.Kama ungekuwa pale ingekuwa rahisi kwangu mimi kuja na kulala pale lakini hutaki kuishi pale sijui kwa nini”
“usijali Dr Joshua kuna mambo nayaweka sawa halafu nitahamia katika ile nyumba.Hata mimi sipendi kukaa mbali na wewe” akasema Peniela
“ Nitafurahi sana Peniela kama nitakuwa na uwezo wa kukupata kila pale ninapokuhitaji.Unajua hizi kazi zetu zinahitaji faraja kubwa kwa hiyo kila pale ninapokuwa nimechoka ninahitaji mtu wa kuniliwaza na katika dunia hii yote nimekuchagua wewe peke yako na ndiyo maana niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako Peniela”
“ Ahsante sana Dr Joshua umekuwa unanijali sana na umedhihirisha unanipenda kweli.Nakuahidi hata mimi nitakupenda daima.”
“ Nafurahi kuisikia ahadi hiyo Peniela.”
Kikapita kimya kifupi Peniela akauliza
“ Dr Joshua najua kwamba uko katika matatizo laini naomba kukuuliza vipi kuhusu lile suala la hospitali? Umelifanyia kazi tayari?
“ ouh samahani sana Peniela.Sikuwa nimelifanyia kazi kutokana na mambo yaliyotokea lakini naomba unipe kama dakika kumi hivi nizungumze na daktari mkuu wa ile hospitali yetu halafu nitakufahamisha.Samahani sana kwa kuchelewa kulifanyia kazi suala hili” akasema dr Joshua
“ Usijali dr Joshua” akajibu Peniela na kukata simu na kuitupa kitandani huku akionekana kuwa na mawazo mengi
“ hapana si kweli kabisa.Elibariki hawezi akafanya jambo kama hilo la kutaka kumuua mke wake.Nina hakika hiki ni kitu kimepangwa na Dr Joshua na wenzake ili waweze kumkamata kirahisi Elibariki.I wont let that happen.I must save him,.” Akachukua simu yake na kuzitafuta namba za simu za Mathew akampigia.
“ hallow Mathew habariza asubuhi? Akauliza Peniela
“ habari za asubuhi nzuri ,unaendelaje?
“Ninaendelea vizuri sana.Ninaweza kuongea na elibariki?
“ Ok subir naomba unipe kama dakika mbili nimpelekee simu”
“ Ahsante sana Mathew.” Akajibu Peniela na kukata simu
“ dr Joshua ni mtu mwenye roho ya kishetani sana na kuanzia sasa inanibidi niwe naye makini mno.Kama ameweza kumuua mke wake basi kwake kuutoa uhai wa mtu ni kitu kidogo sana.Kwa nini anamtesa Elibariki kiasi hiki? Akawaza Peniela na simu anayotumia k uwasiliana na rais ikaita
“hallo dr Joshua” akasema Peniela
“ Peniela tayari nimekwisha wasiliana na daktari mkuu wa pale anaitwa Dr Henry sibowa.Ukifika onana naye tayari nimekwisha mueleza kila kitu “
“ nashukuru sana dr Joshua.Narudia tena kukupa pole kwa matatizo makubwa yaliyokupata .Niko pamoja nawe katika wakati huu mgumu”
“ Nashukuru sana Peniela.Nitakufahamisha baadae nini kinaendelea” akasema Dr Joshua na kukata simu
“ Kuna ule msemo unaosema kwamba kila jambo hutokea kwa sababu maalum.Inawezekana hata tukio hili la kushambuliwa Flaviana limet okea kwa sababau maalum.Sifurahii jambo hili lakini yawezekana ikawa ni mipango ya Mungu ili niweze kuwa na Elibariki.Ninampenda Elibariki na ikitokea kama mke wake akafariki basi nafasi yangu kwake ni kubwa sana.Ni mwanaume ambaye ninataka kuanza naye maisha mapya baada ya kuondoka Team SC41.” Akawaza Peniela na kuchukua tena simu akampigia Mathew
“ hallow Peniela” ikajibu sauti ya upande wa pili ambayo aliitambua ilikuwa ya Elibariki
“ Elibariki my love,uko salama? Unaendelea vizuri? Akauliza Peniela
“ Ninaendelea vizuri Peniela.Vipi wewe unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri sana japokuwa kuna matatizo yametokea jana usiku”
“ tayari ninazo taarifa za kilichotokea jana” akasema Peniela
“ Unazo taarifa za kilichotokea jana?
“ Ndiyo tayari ninazo na ninakupa pole sana kwa mkeo kushambuliwa.”
“ Ahsante sana Peniela.Mke wangu alishambuliwa na sifahamu hadi hivi sasa hali yake inaendelaje? Akauliza Elibariki
“ yuko hospitali na hali yake si nzuri.alfanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi jana usiku nab ado yuko katika uangalizi maalum”
“ Thank you Lord.” Akasema Elibariki
‘ Elibariki did you shoot her? Akauliza peniela
“ Peniela!! Jaji elibariki akashangaa
“ Swali gani hilo unaniuliza ? I think You know me better that anyone,do you think I can shoot my wife? Akauliza jaji Elibariki
“ tell me its not true and I’ll believe you” akasema Peniela
“ Ahsante kwa kuniamini.Siwezi kufanya jambo kama hilo.Kilichotokea ni kwamba nilimpigia simu Flaviana jana usiku na kuomba kuonana naye.Kuna kitu Fulani nilikua nakihitaji toka kwake.Sikujua kama kuna watu walikuwa wanamfuatilia ambao nahisi walifahamu kwamba anakuja kuonana na mimi na ndipo lilipotokea shambulio lile na Flaviana akapigwa risasi.Ni kweli mimi na Flaviana kwa siku za hivi karibuni tumekuwa na tofauti kubwa lakini katu siwezi kuinua silaha na kumpiga risasi.Yule ni mkewangu nasiwezi kumfanyia jambo kama hilo” akasema Elibariki
“ Pole sana Elibariki.Nadhani hizi ni njama za wale wanaoitafuta roho yako usiku na mchana.Naomba Elibariki kwa sasa utulie tu ndani na usionekane kabisa huku nje kwa sababu taarifa zilizosambaa na ambazo zimelifikia jeshi la polisi ni kwamba wewe ndiye uliyepanga shambulio lile na hivi sasa jeshi la polisi liko katika msako mkali kukutafuta kwa hiyo hali si nzuri huku nje”
“ Kwa hiyo kibao kimenigeukia mimi? Elibariki akashangaa
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ndiyo Elibariki.kwa sasa wewe ndiye unayesakwa ukituhumiwa kuhusika na shambulio lile”
“ Ahsante sana kwa taarifa hiyo Peniela.Nitazingatia ushauri wako” akasema jaji Elibariki
“ Elibariki ninahitaji sana kukuona.Najua uko katika wakati mgumu na unahitaji sana faraja.When will I see you? Akauliza Peniela
“ Peniela kwa sasa itakuwa ngumu kidogo kuniona lakini nakuahidi kwamba baada ya mambo kutulia nitatafuta nafasi mimi na wewe tutaonana.Peniela pamoja na matatizo yote yaliyotokea lakini bado uko moyoni mwangu bado umeitawala akili yangu kwa hiyo usijali,tuzidi kuombeana uzima na siku moja tutaonana” akasema jaji Elibariki
“ nashukuru sana Elibariki.Nakupenda sana na tafadhali kuwa mwangalifu.Nitakuwa nikiwasiliana nawe mara kwa mara kujua hali yako” akasema peniela na kukata simu
“ Afadhali sasa ninasikia faraja baada ya kuongea na Elibariki.Ninamuonea huruma sana kwa mambo yanayomkuta.Nitajitahid kufanya kila linalowezekana ili kumsaidia.Kwa sasa ngoja nishughulikie kwanza suala la John .Halafu nimekumbuka kitu,kwa mujibu wa Amos nikwamba leo ndiyo siku ambayo atanikutanisha na Dr Kigomba .Natakiwa nijiandae.” Akawaza Peniela
“ Nasikitika sana kwa kugeuka kuwa chombo cha kuwastarehesha watu lakini mambo haya yote yatakwisha muda si mrefu sana .Tuko katika hatua za mwishoni kabisa kuikamilisha operesheni yetu na nitaanza maisha mapya .Nataka nianze maisha yangu mapya nikiwa na mwanaume ambaye ninampenda kwa moyo wangu wote Elibariki” akaendelea kuwaza Peniela huku akijiandaa kuelekea hospitali
*******
Hali ya John mwaulaya iliendelea kuimarika siku hadi siku na kwa asubuhi hii ya leo aliamka akiwa na nguvu za kutosha kiasi kwamba aliweza hata kuinua mguu na kukanyaga chini
“ Hizi ni dalili njema sana kwa afya yangu kuboreka namna hii.sitaki kufa mapema kwa sababu kuna mambo mengi bado natakiwa kuyafanya kwa Peniela.Lazima kabla ya kufa nihakikishe kwamba maisha yake yanakuwa ya kawaida tena.Hilo ndilo jambo kubwa ambalo ninaweza kulifanya ili kuyajenga tena maisha yake kwa sababu ni mimi ndiye niliyeyaharibu.Pen……….” John akakatishwa mawazo yake na Josh aliyeingia mle chumbani
“ karibu Josh” akasema John
“ mzee nimekuja kukutaarifu kwamba ninakwenda kuifanya ile kazi uliyoniagiza jana nikaifanye leo ya kumteka Jason yule wakili wa Peniela “ akasema Josh
“ Ouh Good.Kumbe unakumbu kumbu sana .Hakikisha unampata leo na atueleze ni alifahamuje kama Elibariki yuko pale kwa Peniela na kwa nini aliamua kuripoti polisi .?.Kitendo kile kingehatarisha usalama wa Peniela na hata wa kwetu sote.Lazima tuifahamu sababu ya yeye kufanya vile “akasema John
“ Usijali mzee nitampata leo na atatueleza kila kitu” akasema Josh ,kijana ambaye kwa hulka yake si muongeaji sana.Josh akageuka na kuanza kupiga hatua kutoka mle ndani na alipofika mlangoni John akamuita akageuka
“ Josh please make him talk” akasema John na Josh akaitika kwa kichwa kuonyesha kukubaliana na John.
“ Josh ni kijana mtiifu sana na anajua kuifanya kazi yake vyema.Huyu naye nitahakikisha ninamuacha sehemu nzuri pia naye awe na maisha mazuri.” Akawaza John
“ lakini huyu Jason aligundua vipi kama Elibariki yuko pale kwa Peniela? Ninahitaji sana kujua.Ninahisi Josh ataifanya kazi yake vyema na tutafahamu kila kitu.Nimemkumbuka Peniela ngoja niwasiliane naye asubuhi hii nijue maendeleo yake” akawaza John halafu akabonyeza kitufe cheusi chini ya kitanda chake akaingia kijana mmoja mwenye taaluma ya udaktari na ambaye ndiye amekuwa akimuhudumia John kwa muda mrefu .John akamuomba ampatie simu na akampigia Peniela
“ Hallow baba” akasema Peniela
“ Hallow Peniela unaendeleaje? Akauliza John
“ Ninaendela vizuri sana baba .Vipi wewe hali yako?
“ hali yangu nzuri na kila siku ninazidi kupata nguvu’
‘ Nafutahi kusikia hivyo.Kwa hivi sasa ninaelekea hospitali kuonana na daktari kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ule upasuaji” akasema Penny
“ Ouh Peniela nakushukuru sana kwa namna unavyonishughulikia.”
“ usijali john,lazima nihakikishe kwamba unapona na unarejea katika hali yako”
“ ahsante sana ,vipi Elibariki anaendeleaje? umefanikiwa kuwasiliana naye?
“ Nimewasliana naye asubuhi hii na hali yake ni nzuri lakini bado yuko katika matatizo makubwa
“Matatizo gani tena?akauliza John
Peniela akamsimulia kila kitu,John akasikitika sana.
“ Penny ninachoweza kukushauri kwa sasa usiwaze sana kuhusu Elibariki nina uhakika mahala aliko yuko salama na nitaangalia baadae namna ya kumsaidia.”
“ Ahsante sana baba,nitashukuru kwa sababu ninampenda Elibariki na yuko katika wakati mgumu sana.Kuna jambo nimekuwa nikilifikiria”
“ jambo gani penny?
“ Wewe una mtandao mkubwa wa watu unaofahamisha nao,kwa nini basi tusimuhamishe Elibariki na kumpeleka nje ya nchi? Nadhani ni jambo ambalo tunatakiwa tulifanye” akasema Peniela
“ Hilo si wazo baya.Naomba uniachie suala hilo nilifanyie kazi halafu nitakupa majibu kama tunaweza tukamuondoa Elibariki hapa nchini”
“Nitashukuru sana baba kama utanisaidia kwa hilo” akasema Peniela na kukata simu
“ Kwa Peniela siwezi kusema hapana.Lazima nimsaidie kumuondoa Elibariki hapa nchini.Uwezo huo ninao ” akawaza John
*******
Jaji Elibariki baada ya kumaliza kuongea na Peniela simuni akatoka na kumfuata Mathew jikoni ambako alikuwa akiandaa mlo wa asubuhi
“ Karibu Elibariki.Anasemaje Peniela? Akauliza Mathew
“ Kuna jambo ameniambia limenistua kidgo”
“ Amekwambia nini?
“ Amesema kwamba taarifa zimesambaa kwamba mimi ndiye niliyefanya shambulio lile la jana nikishirikiana na mtandao wa majambazi na kuua watu wanne pamoja na kumjeruhi Flaviana kwa risasi.Kwahiyo kwa hivi sasa jeshi la polisi linanisaka katika kila kona ya nchi hii.I have no where to run.Mathew nimeogopa sana.Maisha yangu yatakuwaje? Unadhani jeshi la polisi watashindwa kufuatilia na kugundua kwamba niko hapa? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akatabasamu kidogo na kuendelea na kazi zake
“ Relax Eli..Relax..”
“ Mathew this is a serios matter.!!..jeshi lapolisi kwa sasa nguvu yao yote wameielekeza kwangu.Ninatafutwa kila kona.Unadhani nitaweza kuwa na amani tena? Akauliza Elibariki.Mathew hakujibu kitu akaendelea na kazi zake
“ Mathew can you stop what you are doing and to me?
"Nimekwishakusikia Elibariki.Ninakuelewa na ndiyo maana nikakwambia kwamba relax.Ngoja kwanza tupate kifungua kinywa halafu tuanze kupanga kazi za leo”
“ Mathew ,kifungua kinywa ni muhimu kuliko maisha yangu? Look,I’m sorry about yesterday.najua labda umekasirika kwa kitendo nilichokifanya jana kwa kuachia ile risasi na kuhatarisha uhai wetu lakini wewe ndiye tumaini langu.Tafadhalinaomba unisikilize” akasema Elibariki
“ Elibariki ,this is a war and we have to fight back kwa hiyo lazima tujipange vizuri mapambano yetu.Hili ni suala dogo sana na muda si mrefu litafika mwisho kwa hiyo usihofu” akasema Mathew na kuendelea kuandaa kifungua kinywa .Jaji Elibarii akarejea chumbani kwake alikuwa amekasirika sana kwa namna Mathew alivyolichukulia suala lile
“ Sijui Flaviana ana hali gani huko aliko,nitamani sana kufahamu anaendeleaje lakini siwezi.Maisha yangu yamebadilika na ninaishi kama mfungwa” akawaza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dakika ishirini baadae wote wakajumuika pamoja katika mlo wa asubuhi na baada ya hapo wakangia katika chumba cha kazi.
“ Ok Elibariki sasa tunaweza kuongea ” akasema Mathew
“ Mathew ni kama vile nilivyokwambia kwamba tayari taarifa zimesambaa kila kona ya nchi kwamba ni mimi nidye niliyepanga shambulio la jana na kwa hivi sasa jeshi la polisi linanisaka katika kila kona ya nchi.”
“Elibariki nadhani nguvu ya watu hawa wanaokutafuta umeiona na kwa sasa wameamua hata kulitumia jeshi la polisi kukutafuta .Wewe ni mtu hatari sana kwao na kuendelea kwako kuwa hai unawanyima usingizi.Kitu tunachotakiwa kukifanya ni kupambana nao.Tutaanza kwanza kuifanyia kazi taarifa ile ya kuhusiana na kifo cha Dr Flora .katika taarifa hii kumeorodheshwa majina ya madaktari waliofanya uchunguzi huo.Tutalipitia jina moja moja na tuhakiki kama ni kweli walishiriki katika uchunguzi huo na tutapata jibu .Mimi na Anitha tutaifanya kazi hii leo na mpaka jioni ya leo tutakuwa na majibu kuhusiana na taarifa hii kama ni ya kweli ama vipi na baada ya hapo tutajua nini kitafuata.” Akasema Mathew
“ Kuhusu zile karatasi zilizoibwa ikulu ambazo tumeshindwa kuzielewa nimemtumia rafiki yangu mmoja yuko katka chuo kikuu kimoja cha sayansi nchini Israel na baadae ninategemea kupata majibu kuhusiana na nini kilichoandikwa ndani ya karatasi zile kiasi cha kuzifanya ziwe na thamani kubwa kiasi kile.Mpaka jioni ya leo tutakuwa na majibu yote na tutajua nini kitafuata.Kwa hiyo usihofu Elbariki tutapambana nao.” Akasema Mathew
“ Ahsanteni sana Mathew na Anitha.Ninawaomba mtakapokuwa katika mizunguko yenu msisahau kutafuta habari kamili kuhusu maendeleo ya mke wangu.”
“ Tutajitahidi Elibariki lakini kwa wakati huu lazima tujiandae kwa lolote lile litakalotokea” akasema Mathew
Josh kijana ambaye kwa haiba yake anaonekana ni kijana mpole sana,aliwasili katika jengo zilimo ofisi za kampuni ya uwakili ya Jason.Alichukua takribani dakika mbili hivi kablaya kushuka akiangalia hali ya usalama ilivyo eneo lile na kama kulikuwa na kamera zozote za ulinzi zilizofungwa .Aliporidhika kwamba eneo lilikuwa salama akafungua mkoba wake akatoa uturi mzuri na kujipulizia akajiangalia na kuhakikisha yuko katika muonekano mzuri akashuka garini.Kwa yeyote ambaye angemuona Josh asubuhi hii lazima angedhani ni kijana anayefanya kazi nzuri na yenye maslahi mazuri kwa namna alivyovaa na hata namna anavyotembea kwa kujiamini.Aliingia ndani ya ofisi zile na kupokelewa na mwanadada mmoja aliyevaa mavazi yaliyomkaa vyema.
“ habari yako kaka” akasema yule mwanadada
“ habari nzuri dada yangu ,habari za hapa?
“karibu sana.Nikusaidie nini?
“ Ninahitaji kuonana na wakili Jason”
“ Una miadi naye siku ya leo?
“ Hapana sina miadi naye lakini nina tatizo ambalo ninahitaji kuonana naye”
“ sawa kaka lakini Jason ana matatizo binafsi na leo ni siku ya nne Jason hajafika hapa kwa hiyo kama una tatizo la kisheria na unahitaji msaada unaweza ukashughulikiwa na mawakili wengine walioko hapa ambao nao wamebobea pia katika masuala ya kisheria” akashauri yule mwanadada.Josh akafikiri kidogo na kusema
“ Lini Jason atarudi ofisini kwake? Ninahitaji kumuona yeye tu”
“ Hatuna uhakika kwa kweli lini atarudi na wala hajatuambia chochote.Unaweza ukatuachia mawasiliano yako ili atakaporejea basi tukutaarifu kama shida yako inamuhitaji yeye pekee” akasema yule dada.Josh akafikiri na kusema
“ Basi isiwe taabu nitakuwa nikija mara kwa mara kumtafuta na siku moja ninaweza kumbahatisha” akasema Josh na kugeuka akaanza kuondoka.Alipofika mlangoni akageuka na kurejea tena kwa yule dada
“ samahani dada unaweza ukanielekeza nyumbani kwake ili nikaonane naye? Akasema Josh na yule dada bila kuwa na wasi wasi wowote akamuelekeza Josh nyumbani kwa Jason.
Ilimchukua Josh zaidi ya saa moja kufika nyumbani kwa Jason.Akashuka garini na kubonyeza kengele ya getini .Baada ya dakika mbili mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na kijana mmoja aliyekuwa amevalia nadhifu kabisa na ilionekana kama vile alikuwa akihitaji kutoka
“ habari yako kaka” akasema Josh
“ habari nzuri sana,karibu”
“ Ahsante sana.Ninaitwa josh ,nimeelekezwa kwamba hapa ni nyumbani kwa wakili Jason”
“ Ndiyo mimi.karibu sana” akasema Jason
“ Ahsante sana Jason.Nimefika ofisini kwako nilikuwa na shida ya kiofisi nikaambiwa kwamba una siku kama nne hivi hujaonekana pale kazini.Niliambiwa kama nina shida ninaweza kumpata wakili mwingine lakini shida yangu mimi ilikuwa ni wewe tu.Sina imani kabisa na wakili mwingine zaidi yako” akasema Josh na kumfanya Jason atabasamu
“ karibu ndani Josh” akasema Jason na Josh akaingia ndani akakaribishwa katika sebule kubwa.
‘ Jason samahani kama nimekatisha shughuli zako naona ulikuwa katika mkao wa kutoka lakini kama hutajali ninaomba unisikilize japo kwa dakika tano tu”
“ usijali Josh.Una tatizo gani?
“ Ninafanya kazi katika kampuni moja ya madini ambayo ina migodi yake mitatu katika mkoa wa geita lakini ofisi yake kuu iko hapa Dar es salaam.Kampuni yangu imekuwa na mgogoro na serikali kuhusiana na baadhi ya vipengele Fulani viliyomo katika mkataba wa uchimbai wa madini.kwa sasa tunafikiria kuifikisha serikali mahakamani kwa kosa la kukiuka mkataba.li tuweze kushinda kesi hii tunahitaji wakili ambaye ni mahiri na ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja kama ulivyo wewe.Kesi uliyoisimamia ikamalizika hivi karibuni ya yule msichana ,imetudhihirishia kwamba wewe ni wakili ambaye utatufaa sana katika kesi hii.Kwa hiyo Jason nimekuja kukuomba uwe wakili wetu katika kesi hii na kama hutajali basi tuongozane hadi ofisini kwetu kwani wakurugenzi wetu wanakusubiri kwa hamu ili uweze kuelezwa kwa kina kuhusiana na jambo hili.Je uko tayari kwa kazi hii Jason? Kumbuka ni kazi yenye maslahi manono sana” akasema Josh.Jason akamtazama Josh kwa makini na kusema
‘ Nadhani nikishauona mkataba huo na vipengele ambavyo vina utata ninaweza nikasema jambo lakini siwezi kutoa tamko lolote kabla ya kuupitia mkataba huo.” Akasema Jason
“ Ok vizuri Jason.kama hutajali tunaweza kuongozana asubuhi hii hadi ofisini kwetu na ukaupitia mkataba huo kwa umakini mkubwa” akasema Josh
“ Ok sawa tunaweza kuongozana” akasema Jason halafu wakatoka kila mmoja akaingia katika gari lake wakaondoka Jason akilifuata gari la Josh
Moja kwa moja walielekea hadi nyumbani kwa john Mwaulaya.Geti likafunguliwa wakaingia ndani
“ Jason karibu sana hapa ni nyumbani kwa mkurugenzi wetu mkuu na ndipo mikataba yote muhimu huwa inahifadhiwa.Tukitoka hapa tutaelekea ofisini ” akasema josh na kumshangaza kidogo Jason kwani hakutegemea kama wangekuja hapa nyumbani kwa mtu badala ya ofisini kama walivyokuwa wamekubaliana.waliingia sebuleni Josh akamuomba Jason aketi sofani na amsubiri kwa dakika moja ili akamtaarifu mkurugenzi wake kwamba wamefika.Baada ya dakika mbili Josh akarejea na kumuomba Jason amfuate ,wakapanda ghorofani.Josh akaufungua mlango mmoja akaingia na kumkaribisha Jason.katika chumbakile kulikuwa na meza na viti viwili.Josh akamuomba Jason aketi kitini wakati wakimsubiri mkurugenzi wake.Mara tu Jason alpoketi kikatokea kitu ambacho hakukitarajia.Josh alichomoa bastora na kumuelekezea.Jason akabaki akishangaa
“ Josh..Wh..what’s going on? Akauliza Jason huku akitetemeka
“ Give me your phone and everything” akasema Josh na kwa haraka Jason akatoa simu yake na kila kitu akaviweka mezani Josh akavichukua.
“ Josh kuna nini? Kwa.n…” Jason maneno yakashindwa kutoka.
“ Jason naomba unisikilize kwa makini sana.Nimekuleta hapa kuna mambo ninayotaka kuyafahamu toka kwako.Kama hutanieleza ukweli hutatoka humu ndani salama.” Akasema Josh huku ile sura yake ya upole ikiwa imebadilika na sasa alikuwa ana sura ya kikatili ya kiuaji.Jason akazidi kutetemeka.Ilikuwa ni m ara yake ya kwanza kuelekezewa bastora.
“ Josh..tafa.fadhali naomba uniambie ..unataka nini? Nitakueleza kila kitu unachokihitaji lakini tafadhali naomba usinidhuru” akaomba Jason.
“ Nitarejea baada ya dakika mbili.” Akasema Josh na kutoka akaufunga ule mlango na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha John mwaulaya
“ Mzee tayari ile kazi nimeikamilisha.Jason nimempata kwa wepesi sana na yuko hapa ndani katika chumba cha mahojiano”
“ Good ! Josh wewe nikijana hodari sana.Ahsante sana.Umeshaanza kumuhoji?
“ Hapana mzee bado sijaanza kumuhoji”
“Please make him talk” akasema John mwaulaya.Josh akaiwasha luninga moja kubwa kati ya luninga zatu kubwa zilizokuwa ukutani na John akaweza kuona kila kinachoendelea katika chumba kile cha mahojiano.Jason alikuwa amekaa kitini akitetemeka kwa uoga
“ He’s scared.Atatueleza kila kitu” akasemaJosh na kisha akatoka na kueleka chumbani kwake akabadili nguo na kuchukua baadhi ya vitu ambavyo huvitumia katika kumtesa mtu wakati wa mahojiano halafu akaingia tena katika chumba alimo Jason ambaye alipomuona tu akatetemeka sana na kuema
“ josh ..josh ..Please don’t hurt me..Nitakueleza kila kitu unachokihitaji” akasema Jason.Josh hakujibu kitu akavipanga vifaa vile vya kutesea mezani na kuzidi kumuogopesha Jason
“ Jason mimi si mtu mkatili kama unavyodhani na hata sura yangu haionyeshi kama mimi ni mkatili lakini huwa ninalazimishwa kuwa katili pale ambapo mtu ninayemuhoji akanidanganya au akashindwa kutoa ushrikiano kwa hiyo naomba usinilazimsihe niwe mkatili.Ninaoma unieleze ukweli wa kila nitakachokuuliza” akasema Josh
“ Nitakueleza ukweli wa kila kitu Josh ila tafadhali naomba usinitese”akasema Jason.Josh akamtazama na kusema
“ Unamfahamu jaji Elibariki?
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘ Ndiyo ninamfahamu.Nilimfahamu wakati wa kesi ya Peniela kwani yeye ndiye aliyekuwa akiisikiliza kesi ile.Baada ya kesi kukamilika tukawa marafiki”
“ Good.”akasema Josh halafu akamtazam tena jason kwa makini na kumuuliza
“ jaji Elibariki alinusurika kuuawa na watu wasiojulikana hivi majuzi na mpaka sasa hajulikani alipo,unafahamu mahala aliko?
Jason akakaa kimya ,akashindwa kujibu
“ Jason unafahamu mahala aliko jaji elibariki hivi sasa? Akauliza tena Josh
“ hapana sifahamu mahala aliko” akajibu Jason
“ Unataka kunilazimisha nianze kukutesa mapema Jason.Naomba usinidanganye tena.Jana kuna taarifa imeripotiwa polisi kwamba jaji Elibariki yuko kwa Peniela na wewe ndiye uliyeipeleka taarifa hiyo polisi,kwa nini ulifanya hivyo na ulifahamuje kama jaji Elibariki yuko kwa peniela?
Swali lile likamtoa jasho Jason.
“ Sikuwa nikifahamu mahala Elibariki alipo hadi nilipozipata taarifa hizo jana jioni kwa Mathew nilipokuwa nyumbani kwake baada ya kutoka kumzika Noah kijana aliyeuawa katika shambulio lile alilonusurika Elibariki.Mathew ndiye aliyenitaarifu kwamba Elibariki yuko kwa peniela.Nilikasirika sana kusikia kwamba Elibariki yuko kwa Peniela na nilitaka kumuondoa pale na ndiyo sababu nikaenda kutoa taarifa hizi polisi.” Akasema Jason
“ Huyu mathew ni nani? Alijuaje kama Elibariki yuko kwa Peniela? Akaulizia Josh na Jason akasita kidogo kujibu
“ Jason naomba tafadhali usinilzimishe niwe mkali.Nijibu huyu Mathew ni nani?
“ Nilimfahamu mathew kupitia Elibariki kwani ni marafiki wakubwa na Elibariki ndiye aliyenipigia simu Mathew kumfahamisha kwamba yuko kwa Peniela.”
“ Mathew anafanya kazi gani? Akauliza Josh
“ hapanasifahamu kazi yake kwani nimekutanishwa naye na jaji Elibariki kwa hiyo sifahamu kazi yake lakini kwa mujibu wa Elibariki Mathew aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi miaka ya nyuma kidogo na akaacha baada ya familia yake kuteketea kwa moto ”
John mwaulaya aliyekuwa akifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea kupitia Luninga akastuka sana kwa kauli ile ya Jason na kubonyeza kitufe cheusi kilichokuwa chini ya kitanda chake na daktari wake akatokea mara moja.
“ Martin Mpigie simu Josh” akasema John na bila kuchelewa martin akachukua simu na kumpigia Josh
“ hallow Martin” akasema Josh
“ Josh mzee anataka kuongea nawe “ akasema martin na kumpatia simu John.
“ Hallo mzee” akasema Josh
“ Josh muonyeshe huyo jamaa zile picha za jana za wale watu wawili tulizozinasa katika kamera nyumbani kwa Peniela .Muulize kama Yule mwanaume ndiye Mathew ” akasema John na Josh akatoka mle chumbani akaenda kuchukua simu yake na kumuonyesha Jason picha ya Mathew na Anitha iliyochukuliwa katika kamera nyumbani kwa Peniela.Jason akastuka sana baada ya kuona picha zile.
“ Watu hawa ni akina nani? Wana mahusiano gani na Peniela? Kwa nini wanataka kufahamu kuhusu Mathew? Akawaza Jason
“ Unawafahamu watu hawa wawili? Akauliza Josh
“ Ndiyo. huyu mwanaume ni Mathew na huyu mwanamke anaitwa Anitha rafiki yake” akasema Jason. John Mwaulaya akatokwa na jasho.Kuna kitu alikikumbuka.
“ Ndiyo maana baada ya kuona sura ile kumbu kumhu zilikuja kama nimewahi kuiona mahala ile sura.? Sasa nimemkumbuka vizuri.Aliposema kuhusiana na familia yake kuteketea kwa moto ndipo nimekumbuka nimekumbuka kuhusu lile tukio la moto lililotokea kipindi kile.Mathew alinusurika kipindi kile katika shambulio tulipowashambulia kikosi cha makachero waliokuwa wakitaka kumkamata mwanamama gaidi aliyeingia nchini.Ni yeye pekee aliyenusurika katika shambulio lile na haikuishia pale bali tuliiteketeza na familia yake yote ili tuweze kumkamata kirahisi lakini alitoweka na sikuwahi kupata taarifa zake tena hadi leo hii nilipomuona kwa Peniela.Amenistua sana kwani huyu ni mu hatari sana japokuwa sina hakika kama anafahamu ni team SC41 ndio waliofanya shambulio lile baya na kuwaua wenzake wote.Japokuwa ni miaka imepita lakini bado Mathew anaendelea kuwa ni mtu hatari sana kwetu na hatakiwi kabisa kukaa karibu na Peniela wala kuzoeana naye.Lazima tahadhari za haraka zichukuliwe ili kumuweka Penny mbali watu hawa waliomzunguka.Ninahisi labda Mathew anataka kumchunguza Peniela na anamtumia Elibariki katika kumchunguza Penny.Hapana lazima tufanye jambo haraka sana” akawaza John na kubonyeza kile kitufe cheusi cha kengele ya kuita wasaidizi wake na Martin akaingia mara moja mle ndani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Martin mpigie simu Josh,ninahitaji kumuona haraka sana “ akasema John na Martin akampigia simu Josh akamtaarifu kwamba John anahitaji kumuona haraka.Kutokana na mwito ule wa haraka Josh akatoka mbio katika kile chumba akaelekea chumbani kwa John.Kosa alilolifanya Josh ni kuacha kila ktu pale mezani ikiwamo simu yake .
“ Lazima nitafute msaada wa haraka sana,vinginevyo ninaweza kuuawa.Watu hawa wanaonekana wana mahusiano na Peniela na inaonekana wanafuatilia kila kitu kinachoendelea pale kwa Peniela na ndiyo maana wameweza kuzipata picha za Mathew na Anitha kupitia kamera walizozitega pale kwa Peniela.Ni Peniela pekee anayeweza kuniokoa toka kwa watu hawa kwani nina hakika anawafahamu.Kwa bahati nzuri ninazifahamu namba zake kwa kichwa.” Akawaza Jason na kwa haraka akachukua simu ya Josh iliyokuwa mezani akaandika namba za Peniela na kupiga simu ikaanza kuita
“ c’mon Peniela pick up the phone..!! akaomba Jason na mara simu ikapokelewa
“ hallo Josh” akasema Peniela na kumstua Jason
“ Kumbe Peniela anazifahamu hadi namba za simu za Josh.Kumbe hawa ni watu wake.Peniela ninani hasa? Akawaza Jason
“ Hallow Josh” akaita tena peniela
“ peniela,its me Jason.”
“ Jason?!!! Peniela akapatwa na mshangao mkubwa sana.
“ Ndiyo Penny.”
“ Imekuaje uko na simu ya Josh?! Akaulzia Peniela
“ Peniela please help me.Nimetekwa na huyu anayeitwa Josh “
“ what? Akauliza Peniela kwa mshangao
“ Peniela tafadhali naomba unisaidie nimetekwa na kuletwa katika hili jumba ,ninaulizwa maswali mengi kuhusiana na Mathew na Elbariki.Sina hakika kama nitatoka salama ndani ya jumba hili.Josh ametoka kidogo amesahau simu yake nimepata mwanya wa kukupiga.Please help me Peniela.” Akasema Jason .wakati akiongea na Peniela Jason hakuwa na habari kwamba alikuwa akionekana kupitia luninga kubwa iliyokuwamo chumbani kwa Joh mwaulaya.
“ Josh what have you done? Unawezaje kusahau simu? Ona anachokifanya Jason” akasema John.Josh akatupia jicho luningani na kumuona Jason akiongea na simu
“ ouh my God !! akasema Josh na kutoka mbio akarejea kule chumbani alikomuacha Jason.aliufungua mlango na kuingia ndani kwa kasi,akamvamia Jason na kuanza kumshushia kipigo kikali.Alikasirishwa sana kwa kitendo cha Jason kuchukua simu yake na kumpigia Peniela.Jason alilala sakafuni damu nyingi ikimvuja kutokana na kipigo kile kikali.Josh akachukua kila kilichokuwa mezani akatoka akiwa amefura kwa hasira.Mara simu yake ikaita.Alikuwa ni Peniela.Josh akasita kupokea.Simu ikaendelea kuita ikamlazimu aipokee
“ hallo Josh hebu niambie Jason umempeleka wapi? Akauliza Peniela kwa ukali
“ Peniela there is an explanation” akasema Josh
“ Explanation ? Sitaki maelezo yoyote nataka uniambie kwa nini umemteka Jason? Kwa nini unamtesa Jason” Akauliza peniela kwa ukali
“ I’m just following orders Peniela” akasema josh
“ orders from who? john? Tafadhali naomba mpe simu john niongee naye.!! Akaamuru penny
“ Penn….” Josh akataka kusema kitu lakini Penny akamzuia
“ Nimesema mpe simu John” akasema Peniela.Josh akakimbia hadi chumbani kwa John na kumpatia simu
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment