Simulizi : The King Makers
Sehemu Ya Nne (4)
Tuchukulie kwa mfano kuna baba mwenye watoto wawili, James na Michael.
James anafanya biashara ya kuuza magari, na amefanikiwa kuwa na Yard yake ya magari ambayo ina magari ya kila aina.
Papl hapo, Michael anafanya biashara ya kuuza baiskeli, na ana duka lake la kuuza baisikeli.
Unaweza kuona kwamba James ana biashara yenye thamani kubwa kuliko Michael.
Sasa itokee siku moja, baba yao awaambie kuwa wanapaswa kuunganisha biashara zao.
Unaweza kuona kwamba muunganiko huu wa kibiashara utakuwa na faida kwa Michael anayeuza baisikeli kwani sasa pia atakuwa anamiliki biashara ya magari, lakini kwa upande wa pili muunganikl huu utakuwa na hasara kubwa kwa James ambaye kwa sasa biashara yake ya magari inakuwa sio yake peke yake, pia anakuwa anaimiliki na Michael.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika merger ya Samsung C&T na Cheil Industries.
Muunganiko huu ulikuwa na hasara kwa wanahisa wa Samsung C&T lakini ulikiwa na faida kwa wana hisa wa Cheil Industries hasa hasa Lee Family.
Sasa,
Kama nilivyoeleza kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii, moja wapo ya wanahisa wakubwa wa Samsung C&T alikuwa ni Bilionea wa Kimarekanj Paul Elliot Singer, mmiliki wa kampuni ya uwekezaji ya Elliott’s Associates, huyu alikuwa na hisa 7.1%.
Kitokana na hii merger ya Cheil na SS C&T kuwa na hasara kwa wana hisa wa SS C&T, Paul Singer akaanzisha kampeni kali ya kupinga azma hii ya kutaka kuziunganisha kampuni hizi.
Pia akapinga vikali utaratibu wa Lee Family kujilimbikizia nguvu na ushawishi ndani ya Samsung Group pasipo kuzingatia hasara wanayopata wana hisa wengine.
Familia ya Lee nayo ikaanzisha kampeni kali ya kumchafua Paul Singer kwenye vyombo vya habari vya Korea wakidai kuwa alikuwa ni mnyonyaji wa magharibi aliyejipenyeza ili kuja kuvuruga desturi za biashara za Korea.
Kwa hiyo kukawa na mchuano huo mkali.
Upande mmoja ukiwa ni wanahisa wa SS C&T wakiongozwa na Paul Singer wakipinga kuunganishwa kampuni hizi na upande mwingine Lee Family wakitumia vyombo vya habari kushawishi wanahisa wakubali kupitisha mpango huo.
Ikapangwa tarehe ya mkutano wa wana hisa wote ili kupiga kura kukataa au kukubali kuunganishwa kwa kampuni hizo.
Tarehe hii ilikuwa ni July 10, 2015 na watu wengi walitegemea wanahisa kukataa kampuni hizi kuunganishwa.
Ili mpango huu wa hii merger iweze kupita ilikuwa inahitajika kukubaliwa kwa si chini ya kura 66.7%.
Baada ya kikao kirefu kilichokuwa na mabishano makali, mwishoni zilipokuja kupigwa kura na matokeo kutangazwa ilionyesha kuwa 69.5% ya wana hisa walikubali kampuni hizo ziungane.
Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana, lakini kura ndio zilikuwa zimeshapigwa.. Na Lee family hawakutaka kupoteza muda, wakaziunganisha kampuni hizi mbili na kuwa moja (Samsung C&T ikamezwa ndani ya Cheil Industries, kwa hiyo kwa sasa kuna Cheil Industries pekee yake).
Lakini mwaka Jana, ndipo wafukunyuzi wa mambo wakabaini kuwa Rais Park Geun-hye alihusika kwa kiwango kikubwa kuisaidia familia ya Lee kufanikisha mpango huu wa kuunganisha kampuni hizi.. Kitendo hiki ndicho kilichochangia kuibuliwa kwa skendali iliyosabibishwa mwanamama huyu kuondolewa na bunge kwenye kiti cha Urais..
==========
SEHEMU YA TATU
Katika sehemu ya pili ya mfululizo wa makala hizi, nilionyesha namna ambavyo iliibuka sintofahamu kati ya Samsung Group na wana hisa wake kutokana na mpango wa kuziunganisha (merger) kampuni za Samsung C&T na Cheil Industries.
Katika sintofahamu hiyo, wanahisa wa Samsung C&T walikuwa hawakubaliani na kuunganishwa kampuni yao na kampuni ya Cheil Industries, lakini mpango huo ulikuwa unashinikizwa na Lee family kwa kuwa ulikuwa unawapa nguvu zaidi ya kudhibiti umiliki wa kampuni ya Samsung.
Mwishoni nikaeleza kwamba ulipoitishwa mkutano wa wanahisa.. Majibu yakarudi kwamba mpango huo umepita kwa kura 69.5% kitu ambacho kiliwashangaza wengi.
0 comments:
Post a Comment