Search This Blog

Tuesday, 20 December 2022

THE KING MAKERS - 5

  


http://pseudepigraphas.blogspot.com/2020/06/the-king-makers.html


Simulizi : The King Makers 

Sehemu Ya Tano (5)




Niliahidi kueleza uhusika wa Rais Park Guen-hye katika kufanikisha mchakato wa kuunganisha kampuni hivi na kuipa nguvu na ushawishi zaidi Lee Family ndani ya kampuni ya Samsung.


SKANDALI YA CHOI SOON-SIL

Rais Park Geun-hye ni mtoto wa Rais wa zamani wa Korea aliyeitwa Park Chung-hee aliyetawala miaka ya 1970s.


Katika kipindi hiki lilitokea tukio la mauaji ya kupangwa (assassination) ya Mke wa Rais (mama yake Rais Park).


Katika kipin hiki ndipo ambapo Park alifahamiana na mwanamama aliyeitwa Choi Soon-sil.

Huyu alikuwa ni mtoto wa muhudumu wa kiroho (shamakh) aliyeitwa Choi Tae-min ambaye alikuwa kiongozi wa huduma ya kiroho ya Yongsae-gyo (Church of Eterne Life) na mara moja akaanza kuwa na ushawishi mkubwa kwa Park na hatimaye kuwa ‘mentor’ wake.


Kwa hiyo urafiki kati ya Park na binti wa mentor wake (Choi Soon-sil) ukakua kutoka kipindi hicho mpaka alipokuja kuwa Rais mwaka 2013.


Mara tu baada ya Park kuukwaa Urais, huyu rafiki yake Choi Soon-sil ambaye kama nilivyoeleza kuwa alikuwa ni binti wa mentor wake, akaanza kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya serikali ya rais Park japokuwa hakuwa na cheo chochote rasmi.

Yeye ndiye alikuwa na ushauri wa mwisho kwa Rais Park. Yeye ndiye alikuwa mwenye sauti na amri kwa rais park kuhusu masuala yote ya kisera.

Choi Soon-sil akatumia ushawishi wake huo kufanya mambo mengine ya kipuuzi kabisa..


Kwafano alikuwa na binti yake aliyeitwa Chung Yoo-ora ambaye alipomaliza elimu ya sekondari hakuwa na alama zenye kutosheleza kupata udahili wa kujiunga na Chuo Kikuu, alichokifanya Choi Soon-sil akaamuru chuo kikuu cha Ewha Women University kishushe chini sifa zao za udahili ili binti yake aweze kupata admission.


Choi hakuishia hapo tu, kwa kushirikiana na Rais Park, wakaanzisha mashirika ya misaada (Foundations) matatu kwa ajili ya kujipatia fedha kutoka kwa matajiri wa Kikorea.

Mashirika hayo yalikuwa ni, Bu-il Foundation ambalo lilihusika na elimu, pia kulikuwa na Mir Foundation ambayo ilihusika na masuala ya utamaduni, pamoja na K-Sports Foundation ambayo ilihusika na michezo.


Turejee kwenye ‘merger’ ya Samsung..

Baada ya kutoka sintofahamu kati ya wanahisa wa Samsung C&T na Familia ya Lee, ndipo hapa rafiki wa Rais Park, mwanama Choi Soon-sil akafanya mawasiliano na familia ya Lee na kuwa eleza kuwa rais ana uwezo wa kuwasaidia kwenye hilo.

Wakafanya makubaliano ya siri ni namna gani Rais atasaidia na familia ya Lee wakaweka ahadi yao ni namna gani “watamshukuru” rais akisaidia kufanikisha hilo.


Niwafahamishe kwamba katika kipindi hiki 11% ya hisa za kampuni ya Samsung C&T zinamilikiwa na shirika la serikali la mafao NPS (National Pensions Services). Asilimia hizo za hisa zinawapa NPS 27% ya kura za maamuzi (voting shares).

Kwa hiyo alichokifanya Rais Park ni kumuamuru waziri wa Afya ambaye ndiye wizara yake ndio inasimamia shirika hilo, kumuagiza Mkurugenzi wa NPS ahakikishe kuwa siku ya mkutano wa upigaji kura Tarehe 10 July, ahakikishe anapiga kura kuunga mkono kampuni hiyo kuunganishwa na Cheil Industries.


Kwahiyo asilimia hizi za kura za NPS, ukiunganisha na kura zinazotokana na hisa za familia ya Lee wenyewe zikaleta kama 55% ya kura na ukijumlisha na kura za marafiki zao wachache wenye hisa Samsung C&T ndipo zikaleta 69.5% ya kura za NDIYO kukubali kampuni kuunganishwa.


Kwa hiyo hivi ndivyo ambavyo mpango huu ulifanikishwa na kuhakikisha Familia ya Lee inaendelea kufanya ushawishi wake ndani ya Samsung Group unakuwa thabiti zaidi lakini wakati huo huo wanahisa wao wakapata hasara kubwa.


Licha ya mpango huu kufanikiwa mwaka juzi 2015, wafukunyuzi wa mambo wakaendelea kudadisi ni nini kilimfanya rais Park kuingilia kati kuwasaidia Familia ya Lee kuunganisha kampuni za Samsung C&T na Cheil Industries..


Baada ya ufukunyuku na upekuzi wa muda mrefu, ikaja kubainika kwamba.. Familia ya Lee ilimuhonga Rais Park kiasi cha fedha za kikorea Won Bilioni 77.4 (zaidi ya dola milioni 60 za Marekani) kupitia mashirika yake ya Mir Foundation na K-Sports Foundation.

Baada ya taarifa hizi kuwekwa hadharani, ndizo zikawa chanzo cha kuibuka kwa kashfa maarufu ya “The Choi Soon-sil Scandal” ambayo ilikuja kuwa chanzo cha maandamano ya wananchi nchi nzima kupinga utawala wa Rais Park Guen-hye.


Baada ya maandamano kupamba moto na umaarufu wa Rais Park kudorora kwa wananchi, hatimaye Tarehe 9 December 2016, bunge likapiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Park.


Juzi Tarehe 10 March, Mahakama ya katiba ikahalalisha uamuzi huo wa bunge na kumuondoa rasmi madarakani rais Park Guen-hye na nafasi yake kukaimiwa na Waziri Mkuu wake.


Pia wiki iliyopita waendesha mashitaka wa Korea walifungua mashtaka dhidi ya Jay Y. Lee mtoto mkubwa wa kiume wa Mwenyekiti wa Samsung ambaye kwa sasa ni CEO wa Samsung Electronics na Makamu mwenyekiti wa Samsung Group na siku chache zijazo anatarajiwa kupokea mikoba ya baba yale na kuwa mwenyekiti wa Samsung.

Waendesha mashitaka wa Korea walifanikiwa kupata kibali cha kumkamata Jay Y. Lee, na wamemkamata na kumfungulia mashitaka ya rushwa na kwa sasa kesi iko inaendelea mahakamani na ina ‘joto’ la hali ya juu.


Kesi hii imekuwa ni ya kwanza na ya aina yake kufunguliwa dhidi ya mwanafamilia kutoka familia za “Chaebols”, na hii inaakisi kuchoshwa kwa wananchi dhidi ya kiburi na utamaduni wa familia hizi kuiweka nchi ya Korea kiganjani mwao na kufanya kama watakavyo..

Hakuna anayejua.. Labda huko mbeleni, mfumo huu wa Chaebols unaweza kupigwa marufuku kabisa nchini Korea.


Leo nimehitimisha, awamu ya kwanza wa mfululizo wa makala hizi.. Lakini kama nilivyoahidi mwanzoni mwa makala kwamba.. Nitaangazia kila pembe ya dunia kuchambua namna wafanya biashara wanavyoshawishi mifumo ya uongozi wa nchi na ufanyaji maamuzi ya serikali.


MWISHO



    0 comments:

    Post a Comment

    Blog