Search This Blog

Saturday 5 November 2022

DILI LA DOLA BILIONI NNE - 3

 






Simulizi : Dili La Dola Bilioni Nne

Sehemu Ya Tatu (3)





Kenya ilivurugika, kila kona kulikuwa na maandamano yaliyokuwa yakimtaka waziri mkuu wa nchi hiyo, Bwana Osmon Kimeta kuachia ngazi kutokana na skendo nzito ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili dhidi ya msichana mrembo, Jesca Ibrahim.

Kila mtu nchini humo alitaka kumuona waziri huyo akichukuliwa na kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miaka hamsini au zaidi.

Hakupendwa, kila kona alichukiwa kwa sababu ya ukaribu wake na Rais Andrew Kimoni. Wawili hao walikuwa marafiki kwa kipindi kirefu, walipanga mambo mengi, walifichiana siri nyingi mno huku wakiuhujumu uchumi wa nchi hiyo.

Katika kipindi hicho ambacho Kimeta alikuwa na kazi nzito ya kujisafisha ndicho kipindi ambacho Rais Kimoni alimwambia kuwa angemlinda na kusingekuwa na kesi yoyote ile mahakamani.

Viongozi kutoka katika vyama vya upinzani wakamtafuta Jesca, wakamuweka chini na kuanza kuzungumza naye, msichana huyo alikuwa na ushahidi wa picha ambazo alipiga na mwanaume huyo wakati akiwa anambaka, alifanya hivyo kwa kuwa hakuhitaji kufanya mapenzi.

Picha hizo zilikuwa kwenye barua pepe yake, nyingine akazihifadhi kwenye akaunti yake ya WhatsApp ya kulipia aliyokuwa akiitumia, yaani alihakikisha picha hizo zinahifadhiwa sehemu zote za siri ili iwe rahisi kwake kuwa na kumbukumbu ambazo angezitumia mahakamani.

Rais alimkingia kifua Kimeta, aliwaita mahakimu wote kwa siri na kuanza kuzungumza nao, aliwaonya kwamba kesi hiyo haikutakiwa kutoa hukumu kwa haki, kama kweli waliitaka kazi yao na kuendelea kuwa hai basi kwa yeyote ambaye angeisimamia ilikuwa ni lazima ampendelee Kimeta na kuonekana hata hatia yoyote ile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakakubaliana, vitisho ambavyo walipewa viliwaogopesha. Huku nyuma viongozi wa vyama vya siasa waliendelea kumpampu Jesca aendelee kuisimamia kesi yake mpaka hukumu itakapitolewa.

Aliitwa mara nyingi na rais wa nchi hiyo na kumuomba sana akaifute kesi hiyo lakini Jesca hakukubali hata kidogo, tena aliongea kwa kujiamini kwamba ni lazima amfunge Kimeta ili iwe fundisho kwa watu wengine.

“Hii itakuwa fundisho kwa watu wengine,” alisema Jesca huku akionekana kujiamini.

“Ila usije baadaye kujutia uamuzi wako! Nakuahidi kama utafuta kesi, nitakupa shilingi milioni tano!” alisema rais huku akimwangalia msichana huyo.

“Huwa siongeki! Utupu wangu si wa kuuzwa kama malaya wa mitaani,” alisema msichana huyo.

Kila alipoitwa na rais aliongezewa dau lakini majibu yake yalikuwa yaleyale, hakutaka kukubaliana na rais huyo na alisisitiza kwamba ni lazima Kimeta afikishwe mahakamani na kufungwa kifungo kirefu.

Viongozi wa vyama pinzani walimlinda mno Jesca, walijua Rais Kimoni angefanya kila liwezekanalo kumuua msichana huyo, ili siku ya kesi ifike na hukumu itolewe ilikuwa ni lazima alindwe kwa nguvu zote.

Baada ya siku kadhaa kukatika hatimaye kesi ile ikapelekwa mahakamani, wananchi wote walifurahia, kwenye magazeti na mitandao ya kijamii kila mtu alimpongeza msichana huyo, alionekana kuwa shujaa kupita kawaida ambaye hakutaka kupokea pesa kutoka kwa rais, alichokiangalia ni kuangalia heshima ya utu wake.

Hatimaye jaji ambaye alitakiwa kusimamia kesi hiyo akatangazwa, kila mmoja alimjua mwanaume huyo, aliitwa Ibrahim Kifathi, ila alijulikana zaidi kwa jina la Nyoka.

Huyu alikuwa jaji pekee aliyeipendelea sana serikali, hata kuwe na kesi ya aina gani, hata kama serikali au mtumishi wa umma alifanya kosa la wazi, alipokuwa akisimamia, ilikuwa ni lazima mtu huyo ashinde.

Alichukiwa, kila kona alilalamikiwa lakini hakujali, alichokuwa akikiangalia ni maslahi yake tu. Mwanaume huyo ndiye ambaye alitakiw akuisimamia kesi hiyo kitu kilichompa ushindi mkubwa Kimeta.

“Hapana! Tunataka tubadilishiwe jaji!” kila mtu alilalamika lakini hakukuwa na aliyejali.

Siku zikaenda mbele, baada ya wiki moja hatimaye kesi ikaanza kusomwa. Watu walijazana mahakamani, kila mmoja alihitaji kusikia kilichokuwa kikiendelea, kesi ilikuwa inasomwa lakini kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kujua zaidi kile ambacho kingetokea siku chache ambapo kesi hiyo ingeanza rasmi.

Wakati hayo yakiendelea ndiyo kipindi ambacho Robinson na Robert walifika nchini Kenya. Waliposikia kuhusu kesi hiyo, kitu ambacho kilikuja kichwani mwao kilikuwa ni pesa tu. Walifikiria pesa kuliko kitu chochote kile katika maisha yao.

Kwanza wakagongesheana mikono na kuambiana kwamba sasa kazi ilikuwa imekwisha, yaani walitaka kupiga pesa, wakaanza kufuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Wakagundua kwamba kulikuwa na nafasi kubwa ya kupiga pesa. Kwanza kulingana na kesi yenyewe ilikuwa ni lazima kuwe na ushahidi wa picha ambazo msichana huyo alisema kwamba alikuwanazo.

“Kwanzahizo picha zitakuwa zimehifadhiwa kwenye barua pepe ama sehemu nyingine, sasa kama ni hivyo, ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuzipata,” alisema Robinson.

“Haina shida. Kwa hiyo hapo pesa tutapiga kwa nani na nani?” aliuliza Robert.

“Daah! Yaani hapa kuna nafasi kubwa ya kupiga pesa mzee baba! Kwanza tutapiga pesa kwa huyu Jesca! Halafu tutapiga pesa kwa Kimeta, tutapiga pesa kwa rais Kimoni, halafu tutamcheki na huyu jaji anayesimamia, nitaangalia mafaili yake, naye pia tutapiga pesa kwake,” alisema Robinson huku akimwangalia Robert ambaye hakujua ni kwa namna gani wangepiga pesa hizo.

“Sijakuelewa mkuu!”

“Hahaha! Wewe subiri! Unataka tuanze kwa nani kupiga pesa?” aliuliza.

“Kwa jaji!”

“Hapana! Tuanze kwa Jesca. Atupe dola elfu hamsini!”

“Itakuwaje? Halafu inawezekana kweli akatupa? Inaonekana hana hela huyu!”

“Najua yeye hana pesa, ila watu waliokuwa nyuma yake wana pesa. Hawa viongozi wa vyama pinzani wana pesa sana, ngoja tuanze na yeye. Tukimalizana naye, tunaingia kwa Kimeta halafu rais, kisha jaji!” alisema Robinson.

“Basi sawa! Tuanze kazi!”

“Kazi hii inaanza na wewe mwenyewe!”

“Kivipi?”

“Utatakiwa kujifanya kuwa mwandishi wa habari kutoka Tanzania, omba kuonana na msichana huyu kwa ajili ya kumuhoji, kuwa na namba yake ya simu, wakati ukimuhoji, kuwa na laptop yako, fungua WhatsApp Web, halafu mimi nitaiingiza simu yake katika akaunti yake ya WhatsApp,” alisema Robinson.

“Sijakuelewa! Why WhatsApp?”

“Kwa sababu nilisikiliza mazungumzo yao kwa njia ya simu, msichana huyo alizihifadhi picha hizo kwenye akaunti ya WhatsApp, si unajua akaunti hizo watu wanashindwa kuzidukua, sasa mimi nitataka nitumie simu yake kuidukua,” alisema Robinson.

“Mh! Sawa.”

Huo ndiyo mpango uliopangwa, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutengeneza kitambulishi ambacho kingemfanya Robert kuonekana kuwa mwandishi wa habari, haikuishia hapo, ilikuwa ni lazima pia watafute maiki na logo ambayo wangeiweka na kusomeka Mzalendo Tv ambayo ilikuwa moja ya kituo cha habari kikubwa nchini Tanzania.

Kila kitu kikakamilika na hivyo wote wawili kuanza safari ya kuelekea jijini Nairobi ambapo huko ndipo wangeanza kazi ya kumtafuta Jesca na kuzungumza naye. Ila jambo la kwanza kabisa walilotakiwa kulifanya ni kutafuta barua pepe yake, waingie humo na kuzifuta picha hizo kwanza, halafu wadili na zile ziliokuwa kwenye WhatsApp kitu ambacho kwao hawakuona kuwa kigumu kama tu wangetumia WhatsApp Web.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Hakukuwa na muda wa kukaa Mombasa na ndiyo maana Robinson na Robert waliondoka na kuelekea jijini Nairobi. Walikuwa na pesa hivyo walifanya kila liwezekanalo kupata ukumbi mdogo ambao waliifanya kama sehemu yao ambayo wangekuwa wanafanya mahojiano na watu mbalimbali nchini humo.

Walitengeneza logo kubwa ya Wazalendo TV na kuibandika ukutani, walitaka kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanafanikiwa kupata pesa kutoka kwa watu waliopanga kuwafanyia umafia na ndio maana hawakuona hatari kutumia pesa.

Humo, wakaweka kamera ndogo za CCTV zilizokuwa katika kila pembe ya chumba hicho kwa juu, hizo ndizo ambazo zingefanikisha zoezi lao na kuingia kwenye akaunti ya WhatsApp ya Jesca na kuchukua picha kutoka katika mafaili yake yaliyokuwa kwenye akaunti hiyo.

Kamera hizo ziliunganishwa mpaka katika kompyuta ya Robinson huku zikiwa na nguvu kubwa ya kuvuta kiasi cha kumvuta nzi kutoka chini kwa mbali alipokuwa na kumuweka karibu kabisa.

Wakanunua masofa mawili, wakayaweka humo na kupanga kila kitu kuwa cha hadhi kubwa. Mwenye nyumba ambaye aliwapangisha sehemu hiyo alishangaa baada ya kugundua kuwa wale waliopanga hapo walikuwa waandishi na walitaka kufanya kazi kabla ya kuelekea nchini Tanzania.

“Mimi nitakaa katika chumba kingine. Kwenye mahojiano yako, zungumza naye kwa kina halafu mtumie kitu kwenye WhatsApp halafu mwambie akisome, akifungua akaunti yake hiyo kwenye simu, nitaivuta kwa kutumia kompyuta yangu kupitia moja ya kamera katika upande atakaokuwa,” alisema Robinson huku akimwangalia Robert.

“Unajua mimi nashindwa kukuelewa, hivi hayo yatafanikiwa vipi?” aliuliza Robert.

“Hivi ushawahi kuiona WhatsApp ya kulipia? Achana na hii ya bure huku Afrika, ile ya kulipia kabisa, ushawahi kuiona?” aliuliza Robinson.

“Hapana!”

“Hiyo inakuwa na vitu vingi, kuna sehemu ya kuhifadhi mafaili yako, kwa mbele kabisa kuna sehemu ya WhatsApp Web, si lazima ubonyeze vile vitufe vitatu, hivyo ndiyo ambayo tutaitumia kuingia kwenye akaunti yake,” alisema Robinson.

Kwa Robert alishindwa kuelewa, hakuwa mtu wa kompyuta, kwake, kila kitu alichokizungumza Robinson kilionekana kama muujiza fulani.

Baada ya kukamilisha kila kitu, wakaanza kuitafuta namba ya mwenyekiti wa vyama vya upinzani, Bwana Timoth Oyoyo ambapo baada ya kuipata tu wakaanza kuzungumza naye.

Walimwambia kwamba walikuwa waandishi wa habari kutoka nchini Tanzania ambao walifika Kenya kwa lengo la kufanya mahojiano na Jesca kwa kile kilichokuwa kikiendelea.

Oyoyo alishtuka, hakuamini alichokisikia, moyo wake ulikuwa na furaha tele, aliamini kwamba endapo Jesca angefanya mahojiano na waandishi wa habari kutoka nchini Tanzania basi ingekuwa kazi nyepesi kulisambaza suala hilo na kupata nguvu kwa kila kitu ambacho wangetaka kupata hapo baadaye.

Walizungumza na kukubaliana, baada ya hapo Oyoyo akazungumza na Jesca ambaye hakuwa na wasiwsi wowote ule.

“Ila kuna umuhimu na kufanya mahojiano na waandishi kutoka Tanzania?” aliuliza Jesca huku akimwangalia Oyoyo.

“Ndiyo! Tena hii ndiyo nafasi nzuri! Jesca, kama kweli tutafanikiwa katika hili, nakuahidi tutashinda hii kesi kwa asilimia mia moja,” alisema Oyoyo.

Ilikuwa ni vigumu kwa Jesca kukubali, ni kama moyo wake ulikuwa na hofu lakini hakuwa na jinsi, akakubaliana naye na hatimaye kumwambia Robert kwamba walikubali kufanya mahojiano.

Siku hiyohiyo majira ya saa nane mchana, wakaonana ndani ya sehemu hiyo ambayo ilitengenezwa na kuonekana kama kituo kidogo cha waandishi wa habari ambapo walikuwa wakipatumia.

Hapo kulikuwa na kamera za kukodi, ilikuwa ni lazima watengeneze sehemu ambayo ingeonekana kwamba kweli ilikuwa ni ya waandishi wa habari kutokana na vifaa vya humo kuwa na gharama kubwa.

“Naitwa Robert kutoka Mzalendo Tv,” alijitambulisha Robert huku kamera ikiwa mbele yao ambapo kulikuwa na vijana wawili waliowakodisha kwa ajili ya kazi hiyo.

Robert alionyesha tabasamu, alimwangalia Jesca, alikuwa msichana mrembo ambaye hakutakiwa kabisa kupitia kile alichopitia. Akazungumza na Oyoyo na kujitambulisha na kumwambia kwamba lengo kubwa la kufanya mahojiano hayo ni kwa sababu walitaka kuisambaza habari hiyo Afrika nzima.

“Ni jambo zuri sana!” alisema Oyoyo.

Baada ya kukubaliana, Robert na Jesca wakakaa kwenye kochi na kuanza kumuhoji maswali kadhaa. Jesca hakuwa na hofu, aliamini kwamba kweli mwanaume huyo alikuwa mwandishi wa habari, kila alichoulizwa, alijibu pasipo kugundua kwamba upande wa pili kulikuwa na mwanaume aliyekuwa akiifanya kazi yake kikamilifu kupitia kamera zilizowekwa ndani ya chumba kile.

Mahojiano yalikuwa yakiendelea, ndani ya chumba hicho kulikuwa na watu wengi kutoka kwenye vyama vya upinzani, kipindi hicho huyo Jesca alikuwa akilindwa kuliko kitu chochote kile kwani walihisi kwamba ndiye angekuwa ushindi wao mkubwa na kumdhoofisha rais wa nchi hiyo, Bwana Kimoni.

“Nataka nikuulize maswali ya siri sana, ila sitokuuliza kwa mdomo, nitakuuliza kwa WhatsApp, kama utaliona linajibika, naomba unijibu kwa mdomo,” alisema Robert huku akimpa kikaratasi aandike namba yake, Jesca akafanya hivyo.

“Haina shida.”

Hiyo ndiyo nafasi iliyokuwa ikisubiriwa, kule alipokuwa, Robinson akaanza kuivuta simu ya msichana huyo, swali lilipoulizwa kwenye WhatsApp na kuifungua tu, haraka sana Robinson akaivuta, akaingiza program yake ya udukuaji na kuanza kwenda kwenye kipengele cha WhatsApp Web ambapo huko kulikuwa na Barcode alizoziscan kwenye kompyuta yake na hatimaye kukubali na kuingia kwenye akaunti ya msichana huyo.

“Bravo figlio,” (safi kijana) alisema Robinson kwa Lugha ya Kilatin.

Hakutaka kuchelewa, hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake pekee. Kitu alichokifanya ni kuingia kwenye mafaili ndani ya akaunti hiyo, humo akakutana na vitu vingi zikiwemo picha na video kuhusu kile kilichokuwa kimetokea.

Alichokifanya ni kuanza kuzikopi harakaharaka. Alizichukua zote ambazo kwa pamoja zilikuwa na ukubwa wa 1.6GB na alipomaliza tu, akaamua kuzifuta kwenye akaunti ya msichana huyo.

Hakuishia hapo, kwa sababu akaunti hiyo iliunganishwa na barua pepe, akaingia huko, akapekua kwenye mafolder yaliyohifadhiwa na kuanza kuzifuta picha na video fupifupi zilizokuwa humo ambazo zingetumika kama ushahidi kwenye kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili.

Alipohakikisha amemaliza kila kitu, akazifuta moja kwa moja na kupandikiza kirusi ambacho alikuwa na uhakika kusingekuwa na mtu ambaye angekitoa kwenye akaunti hiyo.

“Nimemaliza mzee baba!” aliandika ujumbe mfupi kwenda kwa Robert ambapo baada ya kuupokea tu, alichokifanya ni kumaliza mahojiano harakahara na kuwashukuru wote kwa ushirikiano waliowapa.

“Tunashukuru sana!” alisema mwanaume huyo, watu hao hawakutaka kupoteza muda, wakaondoka zao mahali hapo huku wakiwa na uhakika kwamba habari hiyo ingesambazwa zaidi na uozo wa Kimeta ungejulikana kila sehemu.

***

Jesca alishtuka, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, aliangalia simu yake kwenye Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp kwa lengo la kuangalia kama kulikuwa na zile picha na video alizokuwa ameziweka kwenye faili lake, alipopekua hakuona kitu jambo lililomfanya kushtuka.

Hakuangalia mara moja, aliangalia zaidi ya mara tatu, alifungua huku na kule lakini hakubahatika kuziona. Hilo likamchanganya, alichanganyikiwa, akaingia kwenye barua pepe ambapo huko pia alizihifadhi, alipofungua, akazikosa na mbaya zaidi akakutana na vitu ambavyo hakuvielewa.

Haraka sana akampigia simu Oyoyo na kumwambia kwamba alitaka kuonana naye, kwa jinsi alivyoongea tu mwanaume huyo akajua kabisa kulikuwa na kitu kilichoendelea hvyo haraka sana akaonana naye na kuanza kuzungumza.

Kwa jinsi msichana huyo alivyoongea na machozi kumtoka aliamini kabisa kulikuwa na jambo kubwa na zito. Alipomwambia tu kwamba zile picha na video hazikuwa zikionekana, akahisi mwili wake ukinyong’onyea na kukaa kwenye kochi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unasemaje?” aliuliza mzee Oyoyo.

“Zimefutwa, kuna mtu aliingia kwenye akaunti na kuzifuta,” alisema Jesca.

Oyoyo alimwangalia Jesca, hakuamini alichokuwa akiambiwa, alihisi kama alitaniwa kwani miongoni mwa vitu ambavyo walitakiwa kuwa makini navyo ni hizo picha na video.

Aliambiwa kwamba zilifutwa kwenye simu yake na barua pepe, zilifutwaje? Nani aliingia na kufanya kazi hiyo? Alimuuliza kama simu yake aliwahi kumgawia mtu yeyote yule na kuitumia, alimwambia kwamba hakufanya hivyo, sasa kama simu hiyo haikuchukuliwa na mtu yeyote, ni nani alifanya kazi hiyo?

Hawakutaka kumwambia mtu yeyote yule, ilikuwa ni lazima wajue kilichotokea mpaka vitu hivyo kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Waliendelea na uchunguzi wa kimyakimya kwamba iilikuwa ni lazima mtu huyo agundulike kwani walikuwa na hofu kwamba inawezekana katika hoteli ambayo walimlaza kulikuwa na mtu aliyeingia na kuiiba simu hiyo.

“Jesca! Inawezekana vipi?” aliuliza Oyoyo huku kijasho kikimtoka.

“Hata mimi nashangaa!”

“Hawa watakuwa watu wa serikali! Ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuhakikisha vitu hivyo vinarudishwa,” alisema Oyoyo.

Hicho ndicho walichokifanya, haraka sana wakawasiliana na vijana wao wa IT na kuwaambia kulikuwa na kazi iliyotakiwa kufanyika haraka sana na kama iliwezekana basi waonane kwenye hoteli hiyo.

Ni ndani ya nusu saa tu vijana hao wakafika hotelini hapo, wakachukuliwa na kupelekwa katika chumba hicho na Jesca kuanza kuelezea kilichokuwa kimetokea.

Vijana hao walimsikiliza kwa makini, tatizo walilokutana nalo siku hiyo lilikuwa kubwa, mbaya zaidi hata kuwahi kuitumia WhatsApp ya kulipia hawakuwahi hivyo walivyoambiwa kuhusu mambo hayo walibaki wakishangaa tu.

“Hakuna mtu anayeweza kudukua akaunti ya WhatsApp, labda kuna mtu alichukua simu yako,” alisema kijana mmoja, kila kitu alichombiwa aliona kabisa haikuwezekana hata kidogo.

“Ila hakuna mtu aliyeichukua!”

“Hata mtu aliyekutaka ufungue akaunti yako?”

“Hakuna...sijawah....hebu subiri! Nafikiri ni wale waandishi wa habari!” alisema Jesca.

“Waandishi gani?”

Jesca akaanza kuwaambia kuhusu watu hao, hapo ndiyo Oyoyo akakumbuka kila kitu, naye akahisi kwamba inawezekana waandishi wale wa habari ndiyo waliohusika katika kungia kwenye akaunti ya Jesca na kuzifuta picha hizo.

Haraka sana Oyoyo akachukua simu yake na kupiga nchini Tanzania katika Televisheni ya Wazalendo na kuomba kuzungumza na meneja mkuu. Hilo halikuwa tatizo, simu ikaunganishwa mpaka huko na kuzungumza naye.

Kwanza alimuelezea kila kitu, jinsi walivyokuwa wakipambana lakini mwishi wa siku waandishi kutoka nchini humo waliondoka na kuelekea Kenya ambapo walifanya mahojiano na Jesca, walihisi kulikuwa na kitu walichokifanya.

“Waandishi kutoka kwetu?” aliuliza mwanaume huyo huku akionekana kushangaa.

“Ndiyo!”

“Hapana! Hatukutuma mwandishi yeyote yule,” alisema meneja kwenye simu.

“Hamkutuma mwandishi yeyote?”

“Ndiyo! Hao ni waandishi gani?” aliuliza meneja.

Kwa kusema maneno hayo tu kukampa uhakika Oyoyo kwamba wale wanaume wawili ndiyo waliokuwa wamehusika katika jambo hilo hivyo ilikuwa ni lazima wapambane kuhakikisha wanawapata na kuchukua picha na video zile.

Hawakujua ni kwa jinsi gani wangeweza kuwapata, waliwaambia wenzao kuhusu watu hao na hivyo kuanza kuwatafuta kimyakimya, kwa kile kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni lazima iwe siri kwani kama isingekuwa hivyo, wangekosa kila kitu kwa sababu kama wangeulizwa kuhusu ushahidi wa picha na video hizo, wasingekuwa na lolote la kuionyeshea mahakama.

“Jamani naomba tupambane! Wale vijana ni muhimu sana, si mnawakumbuka?” aliuliza Oyoyo.

“Mimi nawakumbuka sana! Ila wamefanya nini bosi?” aliuliza kijana mmoja, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu zaidi ya Oyoyo na Jesca.

“Wamefanya jambo moja kubwa sana, kwanza tuwatafuteni, tukiwapata nadhani itakuwa fudisho kwa watu wengine,” alisema Oyoyo huku akijitahidi kila kitu kilichoendelea kuwa siri kubwa pasipo watu wengine kufahamu lolote lile.







Mara baada ya kuzipata picha ambazo Oyoyo na watu wake walikuwa wakilingia nazo, Robinson na Robert wakarudi mjini Mombasa na kukaa katika hoteli ya kawaida ambapo huko wakaanza kupanga mipango yao.

Ilikuwa ni lazima wazitumie picha hizo kupata pesa nyingi kutoka kwa watu hao, ilikuwa ni lazima waionyeshe Afrika kwamba wao walikuwa watu hatari, waliopaswa kuogopwa, watu ambao walikuwa na uwezo wa kufanya mambo magumu ambayo yalishindikana kabisa.

Kitu cha kwanza kilikuwa ni kutafuta namba ya Rais Kimoni kwa lengo la kuzungumza naye na kumwambia kuhusu picha hizo.

Haikuwa kazi nyepesi kuipata namba ya mwanaume huyo hivyo walichotakiwa kufanya ni kutafuta namba za watu wengine ambao waliamini kabisa kupitia wao wangeweza kufanikiwa kuipata namba yake.

Hilo halikuwa tatizo, wakapewa namba ya Waziri wa Fedha, Bwana Machali na kuanza kuzungumza naye. Walimwambia kwamba walikuwa na ishu walitaka kuzungumza na rais.

Waziri huyo hakutaka kuwapa, alihisi kabisa kulikuwa na jambo la hatari na hata hivyo halikuwa jambo jepesi kumpa mtu asiyemjua namba ya rais wake, hivyo akawaambia kwamba hakuwa nayo.

“Unajua sisi tuna jambo muhimu sana tunataka kuzungumza naye, hebu mpigie simu, mwambie kijana mwenye zile picha za Kimeta na yule Jesca anataka kuzungumza na wewe,” alisema Robinson kwenye simu.

Machali hakujua Robinson alimaanisha nini lakini hakuwa na jinsi, alipokata simu tu, akampigia Rais Kimoni na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia kama alivyoambiwa kwamba kulikuwa na kijana ambaye alikuwa na picha za rafiki yake, Kimeta ambaye alipiga na msichana Jesca wakati wakiwa hotelini akimbaka.

Rais alivyoambiwa hivyo hakutaka kuchelewa, haraka sana akaomba hiyo namba, akapewa na kumpigia Robinson, alihitaji kuzungumza naye kuhusu jambo hilo kwa kuwa alichokiamini ni kwamba picha hizo zilikuwa kwa Oyoyo na Jesca, sasa ilikuwaje ziwe kwa mtu mwingine?

Akampigia na kuanza kuzungumza naye. Robinson alimwambia ukweli kwamba picha alizichukua kimazingaombwe tu kutoka katika simu ya Jesca ambapo zilikuwa zimefichwa na kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angeziona tofauti na yeye.

“Kwa maana hiyo wao hawana picha hizo ama?” aliuliza rais huku akionekana kuchanganyikiwa kwa furaha.

“Pigia mstari mzee baba! Yaani mimi ndiye mwenye picha hizo na si mwingine,” alijibu Robinson kwa sauti ya kujiamini sana.

Rais hakutaka kuamini, alihitaji kuziona hizo picha, hilo halikuwa na tatizo, Robinson akamtumia picha moja. Rais alipoipata, akashtuka, hakuamini alichokuwa akikiona.

Ni kweli ilikuwa picha ikimuonyesha rafiki yake, Kimeta akimbaka Jesca chumbani. Yeye mwenyewe ndiyo kwanza ilikuwa mara ya kwanza kuziona picha hizo, hakuamini alichokuwa akikiona.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Akampigia simu Robinson na kumwambia kwamba alikuwa tayari kumlipa kiasi chochote cha pesa lakini alihitaji picha hizo zifutwe na zisionekane tena kwenye dunia hii.

“Sawa! Ninahitaji dola milioni mbili, fanya haraka,” alisema Robinson kiasi ambacho kilimshtua mno rais.

“Unasemaje?”

“Nadhani umenisikia, utanipa ama?” aliuliza Robinson.

“Naomba nijifikirie!”

“Dau linaongezeka zaidi kila baada ya saa moja, ukizidi kuchelewa ndivyo ambavyo pesa itaongezeka zaidi,” alisema Robinson.

Ukimya ukasikika kwa sekunde kadhaa, kiasi alichokitaja kilikuwa ni milioni mia mbili kwa shilingi ya Kikenya na bilioni nne kwa shilingi ya Kitanzania.

Kilikuwa ni kikubwa mno lakini ili kumsaidia rafiki yake kuepuka kifungo ilikuwa ni lazima akilipe kiasi hicho cha pesa kwa sababu bila kufanya hivyo basi mtu wake wa karibu afungwe gerezani.

Akazungumza naye na kumwambia kwamba angempigia muda si mrefu kwani alihitaji kujifikiria zaidi kuhusu malipo hayo.

Mtu ambaye alikuja kichwani mwake alikuwa ni jaji, Ibrahim Kifathi ambaye ndiye aliyechaguliwa kuisimamia kesi hiyo mpaka siku ya hukumu. Akampigia simu na kumwambia kuhusu kilichokuwa kikiendelea, kulikuwa na watu waliokuwa na picha za ushahidi, kama lingekuwa jambo jema basi wazinunue ili kesi hiyo washinde pasipo tatizo lolote lile kwa sababu ushahidi ungekuwa umepotea.

Alichokisema Kifathi ni kwamba hawakutakiwa kuzinunua picha hizo kwa sababu yeye mwenyewe tayari aliseti mipango yake ili kuonekane hakuna kesi yoyote ile hivyo piga ua ilikuwa ni lazima huyo kimoni ashinde kesi hiyo.

“Kwa hiyo nisinunue hizo picha?” aliuliza rais.

“Wala usinunue! Kimeta anashinda kesi bila tatizo,” alisema Kifathi kwenye simu.

Hiyo ikaonekana kuwa nafuu kwa rais, hakutakiwa kununua picha hizo kwa kuwa alihakikishiwa kwamba kesi wangeshinda hata kama picha zilikuwepo. Hakutaka kumwambia Robinson, akaamua kumpotezea kwa kuwa aliamini jaji Kifathi alikuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote lile.

***

Kitendo cha rais kumpigia simu Robinson lilikuwa kosa kubwa, simu ilipokatwa, alichokifanya Robinson ni kuanza kuidukua simu hiyo ili aanze kufuatilia kila simu iliyokuwa ikiingia na kutoka, siyo hiyo tu bali hata meseji ambazo zilikuwa zikiingia na kutoka.

Hilo alifanikiwa pasipo rais wala usalama wa taifa wa Kenya kuligundua. Mpaka kipindi ambacho Rais Kimoni anampigia simu Kifathi na kuanza kuzungumza naye, Robinson na Robert walikuwa wakisikia mazungumzo yao, alikasirika kwa kuwa aliamini kwamba ni kweli Kifathi alikuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote lile.

“Tumefeli,” alisema Robert huku akionekana kukata tamaa, mazungumzo aliyokuwa ameyasikia, yalimvunja nguvu.

“Sijawahi kufeli tangu nizaliwe, na sitoweza kufeli! Hapa bado tutafanikiwa na kupata kiasi hicho ch pesa,” alisema Robinson.

Kitu ambacho kilikuja kichwani mwake ni kuhusu huyo Jaji Kifathi, alichokiamini ni kwamba kulikuwa na mambo mengi ambayo majaji walikuwa wakiyafanya ili kuwanyanyasa watu fulani mahakamani na hata kutoa hukumu ambazo hazikuwa sawa.

Aliamini hilo kwa sababu ndiyo ilikuwa hulka ya baadhi ya majaji barani Afrika. Alitaka kuzijua siri hizo na kwa sababu aliipata namba ya Kifathi, aliamini kuwa iliunganishwa na akaunti yake ya barua pepe hivyo alihitaji kuingia huko.

Kwa uwezo wake mkubwa wa kudukua, akafanikiwa kuingia kwenye barua pepe ya Kifathi na kuanza kuangalia zile zilizokuwa zimeingia na kutoka. Humo hakukutana na yoyote mbaya, zilikuwa ni zile za kawaida.

Hakutaka kuishia hapo, alichokigundua ni kwamba hakukuwa na mtu aliyeiacha barua pepe mbaya sehemu ya wazi, kama kulikuwa na mchezo aliucheza na kushirikishwa humo, ilikuwa ni lazima aifute.

Alichokifanya ni kwenda kwenye sehemu ya kufutwa barua pepe, huko alikutana na baadhi, hakuridhika, kwa kutumia programu yake ya Undelete email, aliyoiweka kwenye kompyuta zake, akaanza kuzitafuta zile barua pepe zote ambazo zilikuwa zimefutwa kabisa na hazikuwepo, ilikuwa ni sawa na kurestore vitu ambavyo vilipotea.

Hapohapo barua pepe nyingi zikaanza kujirudisha huku nyingine zikiwa na picha nyingi. Alizirudisha barua pepe zaidi ya mia moja na kuanza kuzipitia.

Huko ndipo alipokutana na vitu alivyokuwa akivitaka mno, aliweza kuziona barua pepe ambazo mwanaume huyo aliwasiliana na watu wengi waliokuwa na kesi mbalimbali na kuambiwa kwamba angepewa kiasi kikubwa cha pesa kama tu angewasaidia kushinda kesi zao.

Mwanaume wa kwanza ambaye aliwasiliana naye aliitwa Brown Williams. Huyo alikuwa mwekezaji kutoka nchini Uongereza ambaye alifika Kenya mwaka 1990 na kuwekeza katika kilimo cha kahawa.

Alipofika hapo, kutokana na matendo yake ya udhalilishaji wa wanawake waliokuwa wakimfanyia kazi ikiwemo kuwabaka na kuwapiga, akafikishwa mahakamani na jaji ambaye alisimamia kesi hiyo alikuwa Kifathi.

Baada ya kuona kwamba angeshindwa kesi hiyo na kufungwa miaka mingi, akawasiliana na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu lile lililokuwa likiendelea.

Kwanza akamwambia angemlipa dola milioni moja na nusu kama tu angemsaidia kushinda kesi hiyo.

Walizungumza mengi kwenye barua pepe na huyo Kifathi kumwambia awamalize mashahidi wote watatu ili kusiwe na kesi yoyote na barua pepe ambayo ilifuata kutoka kwa Brown ilimwambia Kifathi kwamba tayari mashahidi waliuawa na hivyo kushinda kesi iliyomalizika mwaka 2011.

Ukiachana na hiyo pia kulikuwa na mambo mengine mengi. Robinson mwenyewe alipokuwa akiyaona, alishindwa kuamini kama kweli yule Kifathi alikuwa mtu muovu kiasi hicho.

Alizichukua zote hizo, alikuwa na ushahidi wa barua pepe na hivyo kupanga kumtafuta Kifathi ili amwambie kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea.

“Kumbe kuna watu waovu sana. Aisee yule mzee ukimwangalia unaweza kupiga magoti akuongoze sala ya toba, kumbe mshenzi tu,” alisema Robert.

“Hii ndiyo dunia! Ngoja nimtafute,” alisema Robinson na hapohapo kumpigia simu Kifathi.

Simu haikuita kwa muda mrefu, ikapokelewa na kuanza kuzungumza naye. Alijitambulisha kwa jina la The Ghost ambaye alikuwa akijua mambo mengi kwenye dunia hii ambayo yalijificha, hata yale yaliyokuwa chini ya kapeti aliyafahamu vilivyo kabisa.

“Sijajua unamaanisha nini! Unataka nikusaidie nini wewe The Ghost?” aliuliza Kifathi, kwa jinsi alivyomsikiliza Robinson, aliona kama mwanaume aliyejisifu sana.

“Unamkumbuka Brown Williams?” aliuliza Robinson.

Baada ya kulisikia jina hilo, moyo wa Kifathi ukapiga paa! Hakutarajia kulisikia, lilimshtua kupita kawaida. Robinson akabaki kimya huku akiendelea kumsikilizia mwanaume huyo, alihitaji kusikia kama angezungumza kitu chochote kile.

Alipoona amebaki kimya, akaanza kumwambia kuhusu kilichotokea kati yake na Muingereza hiyo, jinsi alivyopokea rushwa kutoka kwake, alivyomsaidia kushinda kesi yake na kuwamaliza mashahidi watatu ambao waliwekwa kwa ajili ya kesi hiyo.

Hakuishia hapo tu, alimwambia mambo mengi, kesi nyingine ambazo alizisimamia na kujifanya mtuhumiwa kushinda na wakati ushahidi ulionyesha wazi kwamba alishindwa kesi hiyo.

Kwa jinsi alivyokuwa akiambiwa kwa data, Kifathi akabaki akitetemeka, mwili ukaanza kutoa jasho jingi, hakuamini kama siri zake zingejulikana. Hakujua huyo ghost alizijuaje na wakati hata kuwasiliana na Brown alifanya kwa barua pepe tu kwa kuamini mawasiliano ya simu yangeweza kudakwa.

“How do you know all of this?” (umejuaje yote haya?) aliuliza Kifathi swali ambalo alijua wazi kabisa hakutakiwa kuuliza.

“I told you...I am the Ghost...” (nilikwambia...mimi ni mzimu) alisema Robinson na kukata simu.





Kifathi alichanganyikiwa, simu ilikatwa lakini bado alikuwa na hamu ya kuzungumza na mwanaume aliyempigia, hakutaka kupoteza muda, haraka sana akampigia na simu kupokelewa.

Alichanganyikiwa, kijasho chembamba hakikuacha kumtoka, alitetemeka huku akiona kabisa huo ndiyo ulikuwa mwisho wake, yaani kila kitu kilichokuwa kimetokea, kingewekwa wazi, watu wangempuuzia na kumuona mjinga ila kubwa kuliko yote ni kwamba angeshtakiwa na kuhukumiwa kifo kwa kuwa alishiriki kwenye mauaji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alimwambia Robinson kwamba ni kweli alifanya hayo yote yaliyotokea lakini alihitaji amtunzie siri kwani vinginevyo maisha yake yangeharibika na kuonekana kutokuwa na thamani hata kidogo.

Hakuishia hapo tu bali alimwambia kwamba alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile, hata kama angehitaji pesa, kwa mambo aliyokuwa ameyafanya alikuwa tayari kutoa kiasi chochote kile.

Robinson akaanza kucheka kwa dharau, hilo ndilo alilolitaka, akamwambia Kifathi kwamba ishu ile ilikuwa kubwa na hakuwa na mpango wowote ule wa kuchukua pesa kutoka kwake.

Kauli hiyo ikamchanganya zaidi Kifathi, kwenye simu hiyohiyo akaanza kulia kama mtoto mdogo huku akiomba msamaha kwa nguvu kubwa.

Muda wote huo ambao Robinson alikuwa akizungumza na Kifathi, Robert alikuwa pembeni, alikuwa akicheka sana, hakuamini kama kungekuwa na mwanaume aliyekuwa akiogopa kuchafuliwa kama huyo.

“Ninahitaji kiasi cha dola milioni moja kutoka kwako,” alisema Robinson kwenye simu.

Kifathi akashtuka, kiasi alichoombwa kilikuwa kikubwa sana, hakuwa na pesa hiyo, alimwambia Robinson kwamba hakuwa na kiasi hicho cha pesa kwani kilikuwa kikubwa mno.

Alichokisema Robinson ni kwamba kama alishindwa kumpa kiasi hicho basi angetoa siri hizo kwani wakati akifanya mambo yake yote, alichukua pesa kutoka kwa watu hao zaidi ya dola milioni hamsini na nane, sasa ilikuwaje ashindwe kutoa dola milioni moja?

“Kama hauna! Basi sawa. Kwa heri...” alisema Robinson.

“Hapana! Naomba usikate simu, nipo tayari kukupa hizo pesa,” alisema Kifathi huku akitamani hata Robinson awe mbele yake na azungumze naye.

“Hiyo haitoshi! Wewe ndiye unayesimamia kesi ya Kimeta, sasa tunataka kesi hiyo ashindwe kwa kuwa ushahidi wa picha upo. Mwambie rais anunue hizo picha, akishindwa, tutaziweka hadharani na pia na wewe mambo yako yatakuwa hadharani pia,” alisema Robinson.

Hapo ndipo alipogundua kwamba mwanaume huyo inawezekana alikuwa yule aliyezungumza na Rais kimoni. Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alimwambia rais kwamba kesi ile angeshinda bila tatizo lolote lile, alimpa uhakika huo lakini ghafla tu aliambiwa na mtu mwingine kwamba alitakiwa kumshawishi rais huyo anunue picha hizo vinginevyo ushahidi ungewekwa wazi.

Hakujua afanye nini lakini kwa sababu mwanaume huyo alikuwa na maovu yake, hapohapo akampigia simu rais na kumwambia kile kilichotokea.

Rais alishangaa, akagundua kwamba walikuwa wakidili na watu hatari sana, waliokuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote lile. Aliogopa, kama aliambiwa na Kifathi kwamba alitakiwa kununua hizo picha vinginevyo maovu yake yote yangewekwa wazi, hakuwa na jinsi, akakubaliana naye.

Akamwambia Kifathi kwamba ni lazima wapambane kuhakikisha watu hao wanauawa na kitu chepesi alichomwambia Robinson baada ya kumpigia simu ni kumwambia kuhusu malipo ya pesa hizo, yaani azifuate ikulu.

“Unanifanya mimi mtoto sana! Tangu tumewasiliana zimepita saa tatu, na kila saa iliyozidi utalipia dola laki moja,” alisema Robinson.

“Hakuna shida,” alijibu rais kwani alijua kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima afanye kila liwezekanalo kuhakikisha hizo pesa atakazompa Robinson mwisho wa siku zinarudi kwake.

Wakakubaliana malipo kufanyika katika benki, yaani yeye rais azitume kwa namba alizopewa. Kabla ya kufanya hivyo, kitu cha kwanza alichokifanya ni kuwasiliana na uongozi wa benki na kuwaambia kwamba kulikuwa na kiasi ambacho atakiweka kwenye akaunti fulani, kikiingia, hawakutakiwa kukiruhusu kitoke chote mpaka mtu huyo aende benki kwa ajili ya kufanya uhamisho huo, na pindi atakapokuwa huko, awapigie simu polisi na kwenda kumkamata.

“Hakuna tatizo mkuu!”

Hicho ndicho alichokifanya, akawasiliana na Robinson, akamwambia kwamba angemtumia kiasi cha dola milioni tatu na laki tatu, yaani milioni moja ni ya Kifathi, milioni mbili ni zake na laki tatu ni za ile ambazo ziliongezeka kila baada ya saa moja.

Baada ya kuelewana, haraka sana akamtumia kwenye akaunti yake, kwa Robinson pesa ilisoma kwamba iliingia lakini hakujua kama benki hiyo iliizuia pesa hiyo isitoke yote ili akitaka itoke yote basi aende na kuihamisha hukohuko benki.

***

Penzi la Richard lilimchanganya Upendo, hakuamini kama mwisho wa siku angefanikiwa kuwa na mwanaume huyo. Kila kona chuoni hapo alikuwa naye, alimpa pesa na kumpa mapenzi motomoto.

Alimthamini na kumuonyeshea mapenzi ya njiwa, ambayo mwanaume yeyote alitakiwa kuonyeshwa na mpenzi wake.

Kwake, Richard alichukia mno, hakutamani kabisa kuona msichana huyo akimpenda namna ile. Alimchukia lakini kwa kuwa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia, hakuwa na jinsi.

Aliwasiliana na marafiki zake nchini Kenya, walimwambia jinsi walivyofanikiwa kwa kila kitu walichokuwa wakikipanga, walimwambia kwamba mara baada ya kumaliza mipango yote wangeondoka na kuelekea nchi nyingine lakini mwisho wa siku wafanikiwe kwa kile walichokuwa wakikihitaji.

Alifurahi, kiasi ambacho watu hao wangetoa kingekuwa kikubwa sana ambacho kingewapa utajiri mkubwa kabla ya kuondoka na kwenda katika nchi nyingine.

Aliendelea kukaa nchini Tanzania na Upendo, ili msichana huyo aone jinsi alivyokuwa akimpena Richard, kwenye kila sehemu mitandaoni aliweka picha za mwanaume huyo na wakati mwingine akiziposti ili kuwaringia mashoga zake.

Kila msichana aliyeziona picha za Richard alichanganyikiwa, kijana huyo alikuwa mzuri wa sura, watu walizipakua picha hizo na kuziweka kwenye akaunti zao na kumsifia mwanaume huyo kwa jinsi alivyokuwa mzuri.

“Jamani! Ndoto yangu kubwa ni kulala na mwanaume kama huyu. Ana sura nzuri, macho yanaita, angalia mwili wake ulivyojijenga, jamaniiiiii! Natangaza kabisa mwenye mwanaume huyu tutapambana na sisi tunamtaka pia,” aliandika msichana mmoja mrembo mno.

Picha hizo zilichukuliwa na kuwekwa sehemu mbalimbali na hatimaye Richard kupigiwa kura na akaunti nyingi kwamba ndiye mwanaume mzuri kuliko wanaume wote barani Afrika.

Jina lake likaanza kuwa kubwa, kila msichana aliyemuona, alidiriki kusema kwamba kwenye maisha yake yote, japo kwa mara moja alifanikiwa kumuona mwanaume mzuri kama alivyokuwa Richard.

Wanawake hawakuishia hapo, waliposema kwamba walitaka vita walimaanisha na hivyo kuanza kumtafuta Richard. Kumpata haikuwa vigumu, wakafanikiwa na hivyo kuanza kuomba nafasi ya kuzungumza naye au hata kupiga picha.

Kwa Upendo yalikuwa ni maumivu makali, kila alipokaa na Richard, wanawake walimfuata na kutaka kupiga picha pamoja naye. Aliumia lakini hakuwa na jinsi, aliamini kwamba Richard asingeweza kumuacha kwa sababu kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Nitaua mtu!” alisema Upendo.

Aliyasema hayo kama utani lakini moyoni mwake alimaanisha, alikuwa na hasira sana, alikuwa tayari kuchezewa yeye lakini si Richard ambaye kwake alikuwa kama malaika.

Msichana aliyeitwa Manka ambaye alitumia jina la baby_manka kwenye mitandao ya kijamii aliyekuwa na wafuasi zaidi ya laki tisa akaanza kuziweka picha hizo huku akiahidi kiasi cha shilingi milioni moja kwa yeyote ambaye angafanikisha kupatikana kwa namba ya Richard.

Tangazo hilo likawafanya watu wengi kuchangamkia fursa, Manka aliitaka sana namba ya Richard kwa kuwa alikuwa mwanaume aliyempenda kwa moyo wote.

Baada ya siku mbili tu, msichana huyo akaipata namba ya Richard na hivyo kuanza kuwasiliana naye. Hakutaka kujificha, alimwambia ukweli kwamba alimpenda sana na moyoni mwake alikuwa mtu wa thamani mno kuliko yeyote yule.

Richard alikataa lakini Manka hakutaka kukubali, kwake, alikuwa tayari kukosa kila kitu katika maisha yake lakini si kuona akimkosa mwanaume huyo.

Wakati Manka akiendelea kumtongoza Richard, Upendo akaambiwa hila za mwanamke huyo kwamba ilikuwa ni kumuachanisha na Richard ili awe naye.

Kwa Upendo yalikuwa kama matusi, hakutaka kukubali, aliikumbuka gharama aliyoingia mpaka kumpata mwanaume huyo, hivyo kwa moyo mmoja akaridhia amuue huyo manka ili awe na amani moyoni mwake.

Alipanga mipango, hakukuwa na mtu aliyekuwa akijua lolote lile, huko kwenye mitandao Manka alizidi kutamba kwamba angempata Richard ambaye alikuwa usingizi wake pasipo kugundua kama upande wa pili Upendo alikuwa akijipanga kwa ajili ya kummaliza.

Siku ziliendelea kukatika, watu waliendelea kumpongeza Manka na kumwambia aendelee kumfuatilia Richard kwani angeweza kumpata mwanaume huyo na kuanza kuwarusha roho wanawake wengine waliokuwa na majina makubwa nchini Tanzania.

Baada ya wiki moja, maiti ya Manka ikakutwa katika Ufukwe wa Coco, ilikatwakatwa mapanga, ilibakwa na kisha kuchomwa visu mfululizo na kwenda kuitupa katika ufukwe huo huku ikiwa kwenye kiroba.

Watu walioiona, walishtuka, hawakujua maiti ile ilikuwa ni ya nani mpaka pale ambapo polisi waliichukua na kuipeleka hospitali, kusafishwa na kuonyeshwa kwamba alikuwa ni Manka, yule mwanamke aliyekuwa na jina kubwa katika mitandao, mwanamke aliyependwa kwa stori za udaku, kula bata na mambo mengine, ndiye huyo ambaye maiti yake ilikutwa ufukweni. Nani aliyefanya mauaji hayo? Hakukuwa na mtu aliyejua.



Moyo wa Upendo ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kilichokuwa kikiendelea. Kila alipopita kwenye mitandao ya kijamii ni Manka tu ndiye aliyekuwa akitamba. Aliwaambia wafuasi wake kwamba alitaka kutembea na Richard na kwa sababu hata yeye mwenyewe alikuwa mzuri wa sura, hakuona kama mwanaume huyo angekataa kuwa naye.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Upendo alikuwa kwenye wakati mgumu, aliujua uzuri wa mpenzi wake, alikuwa mwanaume wa kipekee aliyekuwa na sura yenye mvuto mkubwa, aliamini kwamba endapo Manka angepambana kwa lengo la kumchukua mwanaume huyo, basi mbali na mkataba waliokuwa wamewekeana ilikuwa ni lazima aachane naye.

Hakutaka kuona hilo likitokea katika maisha yake, alimthamini mwanaume huyo, alimpenda na kumuonyeshea mapenzi ya dhati. Hata siku moja katika maisha yake hakufikiria kumuacha na ndiyo maana alikuwa radhi kufanya jambo lolote lile lakini si kuona Richard akiondoka mikononi mwake.

Kelele za msichana huyo zikawa chukizo masikioni mwake, aliogopa na hivyo alichopanga ni kummaliza tu kwa kuamini kwamba angekuwa na furaha maisha yake yote.

Akawatafuta watu ambao aliwaahidi kuwapa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kazi hiyo. Vijana hao waliokuwa wakikaa Kinondoni hawakuwa na tatizo, kama walipewa kazi na kwa malipo makubwa na mazuri, walikuwa radhi kufanya mauaji hayo lakini si kuziacha pesa hizo.

Kumfahamu Manka hakukuwa na tatizo, alikuwa msichana maarufu, alijulikana kila kona kwa sababu ya ukurasa wake katika Mtandao wa Instagram kuwa na wafuasi wengi, hivyo wakafanya mipango ya kumteka.

Walichokijua ni kwamba Manka alipenda sana kwenda katika Klabu ya Laspinho ambapo huko alikuwa akienda na kampani yake ambapo walicheza muziki, kunywa pombe na hata kufanya mambo mengi yakiwemo ya kutafuta mabwana.

Akawaambia waende huko na walipofika, wakakutana na msichana huyo aliyekuwa na marafiki zake huku akionekana kuwa na furaha mno.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, alikuwa ni malaya wa mitandaoni, aliyaendesha maisha yake kwa kuweka picha alizozipiga studio na kuwavutia wanaume, wengi walimchukua na kufanya naye mapenzi kwa malipo kidogo na kuendelea na mambo yake.

Kijana mmoja miongoni mwa wale watatu waliotumwa, mara baada ya kumuona alipokaa kwenye sofa moja na marafiki zake, akaenda na kukaa hapo, akamuita mhudumu na kuanza kuongea naye.

“Kuna ombe kali ipi hapo?” aliuliza jamaa huyo aliyependa sana kujiita Killer.

“Zote zipo, kali na zile lainiiiiiii...”

“Naomba kali! Nichanganyie,” alisema Killer, akachukua sigara yake na kuanza kuvuta.

Ni ndani ya dakika kadhaa, mezani kulikuwa na chupa saba za pombe kali na za gharama. Manka na wenzake ambao walikuwa pembeni walimshangaa, kwa jinsi alivyokuwa ameagiza pombe nyingi namna ile wakahisi kabisa mwanaume huyo alikuwa na pesa nyingi hivyo wakaanza kujivuta.

“Umependeza...” alisema Manka kwa sauti ya juu kutokana na sauti ya muziki iliyokuwa kubwa humo, alihisi kabisa asingeweza kusikika.

“Ahsante! Unataka kunisaidia?” aliuliza Killer.

“Kama itawezekana! Ila si unaona nina kampani!” alisema Manka.

“Hiyo si tatizo! Subiri,” alisema Killer na kumuita mhudumu.

Pombe zilizowekwa juu ya meza zilikuwa nyingi mno lakini akamwambia mhudumu kwamba alihitaji pombe nyingine. Hilo halikuwa tatizo, haraka sana zikaletwa, akalipia na kuanza kunywa.

Hakuwa mnywaji sana, alikuwa kazini, alijua kabisa kwamba hakuruhusiwa kulewa kwa kuwa alitakiwa kufanya kazi hiyo kwa asilimia mia moja hivyo akaawaachia wanawake hao wanywe kadiri walivyoweza.

Ilipofika majira ya saa tisa usiku, akawaambia kwamba alikuwa akienda kulala na lingekuwa jambo jema kama angeondoka na Manka kwani alitokea kumpenda mno.

“Una hela?” aliuliza Manka kwa sauti ya kilevi.

“Nyingi tu na ndiyo maana nimewanywesha mpaka mnashangaa,” alisema Killer na kumshika kiuno Manka, akamvutia kwake.

Wakanyanyuka na kuanza kuondoka. Manka akawaaga wenzake, aliona amepata buzi kumbe ndiyo alikuwa akienda kufa. Walipofika nje, jamaa akalifuata gari lake, wakaingia na kuondoka mahali hapo.

Manka hakuonekana kuwa na hofu hata kidogo, alichoamini ni kwamba mwanaume huyo alikuwa bwana wake ambaye alijitoa kumgharamia kila kitu kumbe upande wa pili alikuwa muuaji mkubwa.

Wakaondoka! Walipofika maeneo ya Kinondoni, gari likakata kuna ya Manyanya iliyokuwa ikielekea Kinondoni Makaburini, mbele kidogo ikakata kona kulia na kuelekea kwenye njia ya vumbi.

Gari liliendeshwa, Manka alijihisi kuwa salama kabisa, alimuamini mwanaume huyo na alikuwa tayari kufanya lolote lile katika maisha yake lakini si kuona akizikosa pesa ambazo aliamini kwamba mtu huyo alikuwa nazo.

Baada ya dakika kadhaa, gari likasimama nje ya geti moja, kutokana na pombe alizokuwanazo kichwani hakujua alikuwa mahali gani, geti likafunguliwa na gari kuingizwa ndani.

Wanaume wawili wakalifuata gari hilo, wakafungua mlango na kumteremsha Manka kwa mapenzi ya dhati huku wakimuita shemeji na kuelekea naye ndani.

Manka akajisikia huru, kwa sababu alikunywa pombe nyingi, hakuwa na hofu hata kidogo. Akaingizwa mpaka sebuleni, akapitishwa na kuelekea chumbani ambapo akavuliwa nguo zote na kuanza kubakwa mfululizo na wanaume hao watatu.

Hilo ndilo walilolitaka, ilikuwa ni lazima wafanye hivyo kwanza, walizoea kumuona msichana huyo kwenye mitandao ya kijamii, aliringa, alijifanya kuwa na maisha mazuri kwa kupiga picha kwenye majengo ya watu na magari ya kifahari kumbe maisha yake hayakuwa kama yale yaliyoonekana kwenye mitandao.

Kwa sababu alibakwa mfululizo, pombe zilimuisha na kuanza kulia kama mtoto mdogo lakini hakukuwa na mtu aliyemuachia, waliendelea kumbaka zaidi na zaidi.

Walipomaliza, wakaamua kumkatakata na mapanga kisha kumchukua na kumuweka kwenye kiroba na kwenda kumtupa katika Ufukwe wa Coco usiku huohuo na kuondoka zao.

Huo ndiyo ulikuwa mwisho wake, Manka akafa katika kifo kibaya mno, watu walihuzunika, picha zake zilipostiwa kwenye mitandao ya kijamii huku wananchi wakiwasisitiza polisi kufuatilia suala hilo kwa undani kabisa kwani walijua dhahiri kwamba nyuma ya tukio hilo kulikuwa na mtu fulani.

Tetesi zikaanza kusikika kwamba aliuawa na mwanamke mmoja aliyewatuma watu kwa sababu aliibiwa mume wake, mwingine alisema kwamba alifumaniwa, wengine walisema kwamba alitapeli mzigo wa madawa ya kulevya, kwa kipindi hicho hakukuwa na mtu aliyejua undani wa kifo chake, watu wengi walisema kile ambacho walihisi kwamba ilikuwa kweli, hakukuwa na mtu aliyejua kama kilichokuwa kimesababisha kifo chake ni kitendo chake cha kutaka kumchukua Richard kutoka mikononi mwa Upendo.

***

Hakukuwa na kitu ambacho Robinson alikuwanacho makini kama masuala ya pesa, alijua kabisa kulikuwa na mchezo, pesa ziliingia kwenye akaunti aliyokuwa amempa Rais Kimoni lakini alichokishtukia ni kwamba pesa hizo hazikuruhusiwa kutoka.

Ni kweli zilikuwa kwenye akaunti yake lakini alishangaa mno kuona pesa hizo hazichukuliki japokuwa zilikuwa kwenye akaunti hiyo.

Robinson kichwa kilimuuma, alimwambia Robert jinsi kulivyokuwa na mtihani mkubwa kuchukua zile pesa, alimuelezea mambo ambayo hakuyaelewa kwani alizungumza kama mwanaume aliyesoma sana masuala ya IT.

Alitakiwa kupambana! Watu wa benki walikuwa na uwezo mkubwa wa kuingiza codes, kufanya kila kitu walichokiweza lakini kichwa chake kilimwambia hakukuwa na mtu aliyeweza kutengeneza kitu duniani ambacho hakikuwa na uwezekano wa kuvumbuliwa.

Alichezewa mchezo na yeye alichokifanya ni kuingiza codes. Halikuwa jambo jepesi, ili kuingia kwenye database ya benki ilikuwa ni lazima awasiliane na kijana wa IT wa huko na kuzungumza naye, amwambie kuhusu suala lake na hatimaye afanikiwe.

Hiyo ilikuwa kazi ya Robert, yeye ndiye aliyetakiwa kusafiri kuelekea jijini Nairobi kwa ajili ya kuonana na kijana mmoja aliyekuwa akihusika na masuala ya IT ambaye angemwambia kile alichohitaji kukifanya, kama inawezekana amwambie kuhusu codes za kuingia kwenye database ya benki hiyo.

Robert akaenda mpaka Nairobi, ndani ya Benki ya Avatar na kuanza kusubiri na kuangalia mazingira ya humo. Alihitaji kuonana na mmoja wa vijana hao ambao angezungumza nao na kumwambia ukweli kwamba alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni codes za kuingilia kwenye database na angemlipa kiasi kikubwa cha pesa.

Alisubiri kuanzia asubuhi mpaka mchana. Akaona angekaa sana hivyo akaelekea mapokezi na kuomba kuonana na meneja masoko ambaye aliamini kwamba angeweza kumsaidia.

Alipoulizia, hilo halikuwa tatizo, kwa kuwa alisema alikuwa na biashara yake alihitaji sana kuiunganisha na benki hiyo kama walivyokuwa wafanyabiashara wengine, dada yule akampeleka mpaka katika ofisi ya bosi huyo kwa lengo la kuongea naye.

Nyuma ya meza alikaa msichana mrembo aliyeitwa kwa jina la Rachel, alizungumza naye na kumwambia kile alichokuwa akikitaka kwamba kulikuwa na biashara yake ya mtandaoni aliyotaka kuifanya hivyo kama ingewezekana basi ingekuwa ni vizuri kama angeonana na kijana mmoja wa IT kwa lengo la kuzungumza naye.

Kwa jinsi Rachel alivyoonekana, alivyokuwa na nyodo, alimwangalia Robert na kumshusha, alimshangaa, suala kama hilo kwa benki yao hawakuwa wakihusika nalo mpaka mtu alipotakiwa kwenda benki kuu ambapo huko ndipo angeulizwa mambo mengi kuhusu biashara hiyo ya mtandaoni na hivyo kuifanya.

“Hatufanyi jambo kama hilo kwenye benki yetu,” alisema Rachel, si kwamba kweli hawakuwa wakifanya, walifanya ila kwa siri kubwa na hakutakiwa mtu mwingine afahamu.

“Dada! Najua biashara inaweza kufanyika lakini sijajua kwa nini unanikatalia,” alisema Robert.

“Hatufanyi! Naomba unielewe!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Huo ndiyo ulikuwa msimamo wa meneja masoko, Rachel. Hakutaka kumwamini Robert kwa kuwa hakumfahamu, hakujua hasa biashara yake ilikuwa nini.

Robert alimuomba sana lakini msimamo wa Rachel hakubadilika hivyo akaondoka, alipofika nje akampigia simu Robert na kumwambia kilichotokea.

“Unahisi hiyo biashara inafanyika ila hajataka tu kukwambia?” aliuliza Robinson kwenye simu.

“Ndiyo! Nahisi wanaifanya ila kwa siri!”

“Umesema aliyekuwa huko ni msichana?”

“Ndiyo! Tena mzuri, demu wa Kikuyu! Jamani yule demu mkaliiiiiiii...” alisema Robert.

“Basi sawa. Dawa yake ipo. Mpigie simu Richard mwambie aje Kenya haraka sana, hii kazi inabidi ifanyike,” alisema Robinson.











ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog