Search This Blog

Saturday 5 November 2022

JUDITH...JUDITH - 1

 






IMEANDIKWA NA : INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)



*********************************************************************************



Simulizi : Judith....Judith

Sehemu Ya Kwanza (1)



**** **** **** ****



PUUU! Mlango mkubwa wa nyumba ya mzee Ndayishimiye ulitikisika kwa kishindo. Kisha ukimya ukarejea. Mzee Ndayishimiye ambaye wakati huo alikuwa mezani na familia yake wakipata mlo wa usiku, walishtuka na kubaki wameduwaa.



Kwa kipindi cha wiki tatu mfululizo, matukio ya kutisha na kusikitisha yalishamiri jijini Kigali nchini Rwanda. Watu wengi waliuawa kwa kuvunjwa shingo, kupondwa na nyundo vichwani, kuchomwa moto na hata kwa risasi.



Yalikuwa ni mauaji yaliyoitikisa nchi nzima ya Rwanda, ukanda wa Maziwa Makuu, nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Afrika na hata dunia nzima. Mauaji hayo ya kimbari yalisababishwa na tatizo sugu la ukabila lililokuwa likiitawala ‘meli’ ya Rwanda.



Mtutsi alijiona kuwa yeye ni yeye ndani ya Rwanda. Nani mwingine anayetaka kuwa na sauti? Mhutu naye hakuwa amelala. Yeye pia aliamini kuwa ni yeye ndiye mwenye haki na raia halali wa Rwanda, kwamba Mtutsi ni mkimbizi tu!



Ni kutokuelewana huko ndiko kulikozua mzozo na hatimaye mapigano yaliyosababisha uadui mkubwa baina ya makabila hayo mawili makubwa nchini humo.



Usiku huu, saa 2.30, ndiyo kwanza Mzee Ndayishimiye alikuwa amerejea huku akitweta kwa woga. Hakuwa katika hali ya kawaida. Amani ilikosekana moyoni mwake. Tangu alipoingia humo ndani kwake, alitaka kumweleza mkewe hayo aliyoyashuhudia huko alikotoka lakini alijikuta akisita. Aliona kuwa ni mapema mno kulizungumzia hilo.



Fikra zake zilikuwa umbali wa nusu kilometa ambako alishuhudia rafikiye mpenzi, mzee Shomvi Niyonzima akiuawa kikatili pamoja na familia yake. Mzee Shomvi aliuawa kwa kufungiwa ndani ya nyumba kisha nyumba hiyo kuchomwa moto. Lilikuwa ni tukio lililomtisha na kumsikitisha sana mzee Ndayishimiye!



Alishuhudia nyumba hiyo ikiteketea huku sauti za vilio vya mkewe Shomvi na wanae waliokuwa ndani humo zikisikika! Vilio hivyo hivyo awali vilisikika kwa nguvu lakini hatimaye vilipungua taratibu na kuzidi kutia simanzi kwa kuwa moto ule ulizidi kuwaka na paa likatumbukia ndani, hali iliyotoa taswira ya kuwa hakuna kiumbe yeyote atakayenusurika.



Ilimuuma mzee Ndayishimiye!



Hali ya hewa ilikuwa imechafuka! Mzee Ndayishimiye naye sasa akakiona kifo kikimchungulia. Akajenga imani ya zahama hiyo kufika nyumbani kwake! Kwa mfadhaiko mkubwa kichwani mwake, akatembea kwa hatua ndefu hadi kwake ambako aliwakuta wanafamilia wake wakiwa ndiyo kwanza wakijiandaa kupata mlo wa usiku.



Bila ya kuwaambia chochote alijiunga nao mezani. Lakini mwonekano wake ulimshangaza mkewe ambaye hakusita kumuuliza, “Baba Judi vipi, za huko ulikotoka?”



Mzee Ndayishimiye hakujibu, badala yake alitwaa tonge la ugali na kutowelea kwenye mboga kisha akalipeleka kinywani. Wala hakumtazama hata mkewe, hali iliyozidi kuwashangaza mama Judi na Judith ambaye ndiye aliyekuwa mtoto mwenye uwezo wa kupambanua mambo.



“Baba!” Judith alimwita baada ya kumwona akiduwaa na tonge la pili mkononi bila ya kulipeleka kinywani.



Ndiyo, Mzee Ndayishimiye hakuwa timamu. Sasa alitoa macho pima, akawatazama mkewe na watoto wake kwa zamu huku kijasho chembamba kikimtoka kwenye paji la uso.



“Baba kwani kuna nini?” Judith alimuuliza kwa msisitizo, naye sasa akiacha kula na kumtazama kwa makini.



Mama Judith alipeleka mnofu wa nyama kinywani huku akimtazama mumewe kwa jicho kali na la udadisi. Akamgeukia mwanaye, Judith kisha akayarejesha tena kwa mumewe ambako alimkuta akimtazama Judith bila ya kupepesa, jicho nyanya!



“Wamewamaliza!” hatimaye mzee Ndayishimiye alisema kwa sauti ya chini, nzito na iliyojaa fadhaa.



Mara Judith akayarudisha macho kwa baba yake. Akamtazama bila ya kutamka chochote. Walipokutanisha macho, mzee Ndayishimiye akaamua kumgeukia mkewe ambaye naye bado alikuwa akimtazama.



“Nini?” mkewe alimuuliza, sauti yake ikionyesha dhahiri jinsi alivyoipokea kauli ya mzee huyo kwa mshangao.

Kabla mzee Ndeayishimiye hajajibu, ndipo mlango wao ukalia puu! Ukatikisika kwa nguvu! Akili na macho ya wote yakahamia hapo mlangoni. Wakaduwaa! Macho yamewatoka pima! Kisha ukimya ukarejea!



Kisha tena, puu! kwa mara nyingine mlango ukagongwa na kutikisika zaidi. Pigo la tatu liliulazamisha mlango ufunguke! Wanaume wanne wenye silaha wakaivaa sebule hiyo.



Ndiyo, walikuwa ni wanaume wenye nyuso zilizotangaza shari, mavazi yao ya kijeshi yakiwa ni ishara kuwa wako kazini.

Mzee Ndayishimiye na familia yake wakaendelea kuwa katika hali ileile, wameduwaa, na zaidi, kila mmoja alikuwa katahayari!



Wale wanaume wakawasogelea wanafamilia hao bila ya kutamka chochote. Kisha wakatulia. Wakatazamana. Mara mmoja wao akainua bunduki na kumlenga mzee Ndayishimiye kifuani. Ilikuwa ni kama vile mchezo fulani wa kuigiza. Askari huyo alitulia kwa sekunde chache na kumgeukia mwanzake ambaye alionekana kama kiongozi wa msafara. Wakatikisa vichwa kwa pamoja kama ishara ya kukubaliana.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mara mlipuko mkubwa ukaitawala sebule hiyo. Risasi mbili zikazama kifuani mwa mzee Ndayishimiye. Akakata roho huku akishangaa vilevile, macho kayakaodoa, akiwatazama watu hao ilhali hawaoni!



Mchezo haukuishia hapo! Ukahamia kwa wanafamilia wengine. Alianzwa Martha, binti wa pili kuzaliwa, ambaye alikuwa akikimbilia kwenye miaka 18. Huyo alilishwa risasi ya kichwa!

John, Abel na Ndiyokubwayo ambao walikuwa na umri wa kati ya miaka saba na kumi, wao kabla hata hawajajua ni kipi kilichotokea, risasi kadhaa zikazama miilini mwao.



“Mungu wangu wee!” mke wa mzee Ndayishimiye aliomboleza, na kilikuwa ni kilio chake cha mwisho; mmoja wa wanaume wale hakumchelewesha, alimmiminia risasi mbili usoni, risasi zilizokifumua kisogo na kuumwaga ubongo nje huku mwenyewe akiuangukia mwili wa mumewe taratibu.



Aliyebaki hai ni Judith, ambaye kwa wakati huo aliduwaa, huenda hata akili yake haikuwa na uwezo wa kufikiri chochote. Aliyakodoa macho akiwatazama wageni hao ilhali hawaoni! Tonge la ugali alilokuwa amelishika kabla ya uvamizi huo lilibaki limetulia mkononi vilevile!



“Simama!” mmoja wa wale watu alimwamuru.



Alisikia, hakuelewa. Kwa jumla alikuwa ameathirika kisaikolojia kwa kiwango kikubwa. Alikuwa nusu mfu! Kilichofuata siyo amri tena bali kono la mtoa amri lilimshika kwenye ukosi wa blauzi na kumnyanyua kimsobemsobe, akaburutwa akipelekwa nje.



Ikawa ni kama tamthilia fulani isiyopendeza akilini mwa Judith.



********



JUDITH alikuwa ni binti ambaye tayari alitosha kuyavuta macho ya mwanamume yeyote mpenda wanawake wazuri. Kifua chake kidogo, kilichoyabeba matiti yenye ukubwa wastani yaliyovutia, kilikuwa kivutio machoni mwa wengi. Mapaja makubwa, na miguu minene iliyomeremeta, pia zilikuwa ni taswira kuwa muumba aliikamilisha kazi yake kwa upendo na labda hisia za wanadamu wengine zikawa ni kwamba ameifanya kazi yake kwa upendeleo.



Isitoshe, kichwa chake ambacho hakikustahili kuitwa kidogo au kikubwa kilifunikwa na nywele nyingi nyeusi tii, nywele zilizomwagika hadi mabegani na kuuongeza mvuto ambao wengi wa mabinti wa rika lake hawakuwa nao.



Macho yake yaliyorembuka muda wote kama yabembelezayo, pua ndefu na mdomo mdogo ulioyahifadhi meno meupe yaliyopangika vizuri, ni miongoni mwa vigezo vilivyompandisha katika chati ya juu kiasi cha kuwapagawisha wanaume wengi, Wahutu kwa Watutsi.



Makella ni mmoja wa wanaume waliomtazama Judith kwa ‘macho mia.’ Akiwa ni mzaliwa wa mchanganyiko wa makabila hayo mawili makubwa nchini Rwanda, Makella alijisikia kumpenda na zaidi kumtamani Judith. Naye, kama wanaume wengine waliomtamani na kumhitaji Judith, hakumwachia hivihivi; alimtamkia maneno mawili, matatu lakini akaambulia majibu yasiyomridhisha, na zaidi yalikuwa ni majibu ya kumkatisha tamaa:



“Shaa…hivi unaniona-aje?”



“Sina muda wa kupendana na mtu…”



“Nina malengo yangu ya maisha kwanza kwa miaka mitatu hivi mbele…”



“Sijui nina ugonjwa gani…sijui kupenda ni nini…labda mpaka nikaombewe kanisani…” na kadhalika na kadhalika.



Ndiyo, yalikuwa ni majibu ya kumkatisha tamaa, lakini hakuwa mtu wa kukata tamaa wala kukubali kushindwa. Alijali kuwa mtu mwenye uvumilivu, asiye na papara, akiamini kuwa ipo siku atafanikiwa. Mama yake Makella alikuwa ni wa uzao wa Kitutsi na baba, Mhutu. Lakini hadi Makella anafikisha umri wa kuijua historia ya wazazi wake, wenyewe walikwishafariki kitambo kutokana na uhasama na mapigano hayohayo ya kikabila.



Makella akatunzwa na baba yake mdogo hadi alipofikia hatua ya kuwa jasiri asiyeogopa chochote wala kumwogopa yeyote. Aliweza kuua kwa risasi, kisu, panga hata kwa mikono!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





Katika mfumo huo wa maisha, kikafikia kipindi ambacho alimsahau Judith kwa muda, Judith ambaye ni mwanamke pekee aliyetokea kumwingia moyoni tangu siku alipomtia machoni kwa mara ya kwanza, siku ambayo timu ya taifa ya soka ya Rwanda (Amavubi) ilipocheza na timu ya taifa moja la ukanda wa Afrika ya Magharibi katika Uwanja wa Amahoro.



Ni mchana huo wa maafa, siku ambayo ilianza kwa sekeseke la risasi kurindima huku na kule, visu kuchomwa kwa hawa na wale, mapanga na kila aina ya silaha kutua miilini mwa raia wengi, ndipo kumbukumbu kuhusu Judith ilipomjia Makella.



Kumbukumbu hiyo ilimjia wakati yeye na wenzake wamebakiza mitaa mitatu tu kabla ya ule alikoishi Judith, huku hiyo mitaa waliyokwishaipitia wakiwa wameziacha maiti lukuki za Kitutsi, maiti ambazo Makella na wenzake walichekelea pale walipoua kwa kutumia risasi, kunyonga kwa mikono yao hata kwa kuchoma visu.



Ilikuwa ni burudani kubwa kwao kushuhudia mtu akianguka chini na kukata roho kwa maumivu japo baadhi ya hao wanauawa wakiomba waachwe hai, wakitumia sauti za kusihi na macho ya kubembeleza.



Makella na wenzake walifikia katika nyumba ya mzee Ndayishimiye saa 2 usiku, dhamira yao ikiwa ni ileile, kukifutilia mbali kizazi cha Kitutsi katika ardhi ya Rwanda. Wakiwa mbele ya nyumba ya mzee Ndayishimiye, walitulia, wakatazamana.



Dakika iliyofuata ndipo wakachukua hatua na kufanikiwa kuingia ndani ambako walijikuta kwenye varanda kubwa iliyosheheni sofa chakavu na mikeka. Eneo hilo lilitoa taswira ya kuwa ni sehemu isiyo rasmi kwa wageni, zaidi palitumiwa na watoto au hata watu wazima wa familia hiyo kwa kujipumzisha nyakati za mchana.



Mbele kulikuwa na mlango mwingine. Na huo pia haukuwa umefungwa lakini pazia nene lililojaa hapo liliwafanya Makella na wenzake wasiweze kuona ndani zaidi.



“Ni humo,” hatimaye aliwaambia wenzake huku akitangulia kuelekea huko ndani.



Kama awali, wenzake walimfuata.



**********



MZEE Ndayishimiye na familia yake walikuwa ni Watutsi. Na zoezi la Makella na wenzake lililenga kuwateketeza Watutsi pekee! Lakini Makella na kundi hilo walipoifikia hii nyumba aliwahadharisha wenzake akiwaambia, “Humu kuna mwanamke wangu…ninataka kumwoa! Huyo msimguse!”



“Ni Mtutsi?!” mmoja wa watu waliomzunguka alimuuliza kwa mshangao.



“Ndiyo, ni Mtutsi!” Makella alijibu kwa msisitizo, lakini sauti yake ikiwa ya chini.



Kauli yake iliwafanya wenzake wote wamkodolee macho ya mshangao, wakionekana kutoamini wakisikiacho.



“Unataka kuoa Mtutsi?!” mwingine alimdaka.



“Hivyo hivyo!” Makella aliwaka. “Hata kama sitamuoa, lakini ni afadhali hata…” akaiacha sentensi hiyo ikielea.



Wenzake wakakosa nguvu ya kuendeleza maswali au udadisi. Muda haukuwaruhusu. Wote wakafuatana na kuingia kwa kishindo, bunduki zilizokamatwa na wawili zikiwa zimewatangulia.



Wenyeji wao walikuwa mezani wakipata mlo wa usiku. Ilikuwa ni sebule yenye mvuto, sebule ambayo kwa mgeni yeyote, wa hadhi yoyote lazima atajisikia burudani pindi atakapokaribishwa.



Kulisheheni samani aghali na zenye kuvutia. Seti mbili za sofa zilikuwa zimeichukua robo tatu ya chumba hicho huku kabati kubwa la vyombo vya kauri na televisheni kubwa ya kisasa, iliyokuwa kwenye kijimeza chake maalumu vikiongeza ubora wa sebule hiyo. Pia kulikuwa na vijistuli kadhaa hapa na pale vilivyowekwa kwa mpangilio mzuri na kuzidi kukifaharisha chumba hicho.



Kule alikokaa mzee Ndayishimiye na familia yake kulikuwa na meza kubwa na viti maalum likiwa ni eneo maalum kwa maakuli. Kwa jumla ilikuwa ni sebule iliyostahili kuitwa ‘sebule bora.”

Makella na wenzake waliwakodolea macho yenye kila dalili ya kuua! Hawakuwa kama binadamu wa kawaida, simama yao na tazama yao ilitosha kuonyesha kuwa wako tayari kwa lolote na kwa yeyote



“Ni yule pale! Msimguse!” Makella alisema kwa msisitizo huku akimnyooshea kidole mmoja wa wanafamilia hao, Judith.

Na ilikuwa kama alivyoamuru. Ni Judith pekee aliyebaki hai. Ndipo Makella alipomwamuru Judith kusimama, amri ambayo Judith hakuwa na budi kuitii, na ndipo pia akashikwa mkono na kuburutwa akipelekwa nje. Huko pia alikokotwa kama mzoga, akitembea kwa tabu kutokana na kuishiwa nguvu mwilini.



Angezipata wapi nguvu ilhali muda mfupi uliopita ameshuhudia wazazi na ndugu zake wakiuawa?



Kwa jumla hakuwa timamu kiakili. Athari za kisaikolojia ziliutawala ubongo wake. Tukio la muda mfupi uliopita lilikuwa ni kama ndoto isiyopendeza akilini mwake.



**********



WALIPOFIKA mbali kidogo, Makella aliwaambia wenzake, “Tangulieni…ninataka kuongea kidogo na Judi.”



Wenzake walimtazama kidogo na kutii maneno yake. Wakatangulia mbele, yeye akabaki na Judith nyuma wakitembea taratibu.



Kisha Makella akamshika mkono Judith na kumtomasa kidogo kiganjani. Kisha akasema, “Sikia Judi, mtoto mzuri, tambua kuwa uhai wako una maana kubwa sana kwangu, uhai wako ni zaidi ya mimi ninavyojali kuwa hai! Niko tayari kufa kuliko kushuhudia wewe ukiuawa. Naomba uniamini. Wewe haukupaswa kuuawa ingawa katika operesheni ya leo tulipaswa kumuua kila Mtutsi tutakayemtia machoni. Lakini kwa amri yangu wewe umebaki!”



Kufikia hapo alitulia kidogo na kumtazama Judith kwa makini akitarajia pongezi, jambo ambalo Judith hakulifanya. Zaidi, aliuinamisha uso wake kwa majonzi, machozi yakambubujika.



Makella alimgusa begani na kusema, “Pole sana Judi. Usilie. Tulia mpenzi. Umepona kwa sababu naujali sana uhai wako. Naujali uhai wako kwa kuwa nakupenda kwa dhati. Mapenzi yangu kwako ni mapenzi kutoka moyoni.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walikuwa wamekwishavuka nyumba zaidi ya nne kutoka kwao Judith na kwa ratiba yao ilikuwa sasa askari hao wasitishe zoezi lao. Hivyo walikuwa wakirudi kambini.



Wakati huo Judith alianza kurejewa na utulivu kichwani. Akawa amepungukiwa na woga kwa kiasi kikubwa, badala yake hasira ndizo zikamjaa moyoni kwa kiwango kisichokadirika. Isitoshe chuki dhidi ya Makella ilikuwa ikimtawala kwa kiasi kikubwa. Akahisi kitu kama kaa la moto likimkwama kooni!



Alijua kuwa ilimpasa sasa kupiga moyo konde na kuwa makini, akitambua fika kuwa chochote atakachokifanya kinyume na mapenzi ya Makella kinaweza kuyagharimu maisha yake. Huyu Makella amekuwa akimfuata kwa muda mrefu. Na haya maneno yake anayomwambia hayakuwa kipimo sahihi kuwa ana mapenzi ya dhati, hapana. Kwa hilo Judith hakutaka kujidanganya.

Kama amekwishadiriki kuua watu kama vile kuua panya au mende na hata amediriki pia kuwaua wazazi wake na wadogo zake, mbele yake, ni kipi kitamfanya asite kummaliza yeye kama atagundua kuwa bado hapendwi? Makella ni mtu mwenye moyo wa binadamu au mnyama?



Akilini mwake alimchukulia Makella kama binadamu mwenye akili ya mnyama japo alikuwa na viungo vya kawaida, akizungumza kama binadamu wa kawaida na akivaa kama binadamu wa kawaida Hivyo, jambo moja aliamua kuliwekea nadhiri; kuwa tayari kuilinda heshima yake hata kama itabidi kuyagharimu maisha yake.



“Unasikia mpenzi?” Makella aliendelea. “Wewe haustahili kufa! Wewe ni malkia wangu na ni malaika wangu! Judi! Utakuwa mke wangu! Tutaishi maisha mazuri katika nyumba yenye hadhi, nyumba nitakayokabidhiwa na serikali baada ya kufanya kazi hii kwa ufanisi. Haya nd’o matunda ya kuwa mwanajeshi!



“Utakuwa mke wa askari mwenye cheo cha juu. Hutasumbuka kwa kufanya kazi za ndani zitakazouchosha mwili wako…hapana…kutakuwa na watumishi wanne watakaokuwa wakifanya kazi za ndani na nje. Kazi yako kubwa ni kukaa na kucheki muvi, ukinywa bia au soda kwa raha zako, basi! Jioni tunatoka na kwenda kupata nyama choma mahali huku tukishushia bia, eti?”



Judith hakujibu. Hakuwa na akili ya kujibu chochote. Kwa ujumla hakuwa timamu kiakili kwa wakati huo.







“Mpenzi, utakuwa na gari!” Makella aliendelea. “Kwa ufupi utaishi kama uko paradiso, ukiwa ni mke wa mwanajeshi, na mwanajeshi mwenyewe ni mwenye madaraka makubwa jeshini na ana pesa! Nani kama wewe?”



Yote hayo yalipenya masikioni mwa Judith kwa utulivu mkubwa. Eneo hilo lilikuwa tulivu na askari wengine walikuwa wametangulia mbele kwa kiasi cha hatua kama hamsini hivi, hivyo kila alichokisema Makella kilipenya masikioni mwa Judith kwa usahihi mkubwa.



Judith alimsikia lakini hakumwelewa, na hakuwa ni mtu wa kuelewa chochote kutoka kwa Makella wakati huo. Baba, mama na wadogo zake wameuawa kikatili na hawa watu waliomteka! Halafu eti huyu mmojawao anamliwaza kwa maneno laini na kumwahidi maisha bora!



Ni maisha gani bora atakayopata chini ya himaya ya huyu mtu ambaye moyo wake hautofautiani na ule wa Mjerumani fashisti Adolph Hitler aliyedhamiria kukiteketeza kizazi cha Waisraeli katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia? Katika vita vile Hitler aliwaua Waisraeli zaidi ya milioni 6, huyu Makella na wenzake katika haka kanchi kadogo sana, tayari wameshaua maelfu ya watu kwa muda mfupi tu! Ni kwa nini wasifananishwe na Hitler?



Eti Makella anamrai kwa maneno matamu! Akilini mwa Judith hiyo ilikuwa ni ndoto nyingine, ndoto isiyopendeza, ndoto mbaya zaidi iliyomtabiria kifo kibaya, zaidi ya vifo vilivyowakuta wazazi wake na wadogo zake.



Wakati huo walikuwa wamesimama, mkono mmoja wa Makella ukiwa begani kwa Judith na mwingine ukimtomasa matiti.



“Na leo hutalala kambini,” Makella aliendelea. “Tutakwenda Kiyovu Hotel. Mrembo kama wewe haustahili kulala sehemu duni na kulala na watu wengine wasiokuwa na mpango. Eti mpenzi?”



Kama ambavyo awali hakujibu, safari hii pia Judith alibaki kimya. Lakini pamoja na hayo kwa mbali alihisi ujasiri ukimwingia. Na alitambua kuwa umakini ulipaswa kupewa kipaumbele vinginevyo maisha yake pia yatakatishwa na mtu huyo kama mzaha!



Akakumbuka kuwa mara kadhaa, siku kadha wa kadha zilizopita, Makella alimtongoza lakini hakumkubalia ombi lake. Sababu? Hakumvutia! Ile sura yake yenye makovu na kichwa ambacho ni kama kilifinyangwa na msanii mchanga, kikiwa hakitofautiani na mchoro wa msanii maarufu wa katuni, msanii achoraye picha za kutisha au kuchekesha, vilikuwa ni vigezo vya awali vilivyomshusha hadhi na kumfanya Judih asimfikirie kwa namna yoyote.



Mhutu! Kabila hilo nalo, kwa Judith lilikuwa ni kabila lisilokubalika wala kuthaminika nafsini mwake, ni kabila lisilostahili kuwepo duniani! Ni kabila ambalo ni hatari zaidi ya hatari yenyewe! ‘Nimvulie nguo Mhutu! Tena Mhutu mwenyewe anayetisha zaidi ya kifo!’ alijisemea kimoyomoyo kwa kujiapiza.



Ndiyo, hakuwa radhi kuwa na uhusiano wowote na Makella, iwe ni kwa mapenzi ya muda mfupi au hata ya muda mrefu. Lakini usiku huo yuko naye. Wako wawili tu! Tena mbali na kwao Judith! Ni Makella huyuhuyu ambaye tangu mchana hadi usiku huo tayari alishatoa roho za watu ambao hata idadi yao yeye mwenyewe haikumbuki! Roho za Watutsi! Baba, mama na wadogo zake Judith wakiwa miongoni mwao.



Afanye nini?



Ujasiri ulihitajika katika kuulinda msimamo wake na ilihitajika hekima katika kuchukua uamuzi wowote atakaoona unafaa kwa kuilinda hadhi yake na kuulinda uhai wake.



“Hakuna tatizo,” ni jibu lililomtoka baada ya kuzitafakari kwa kina kauli za Makella. Na alijibu hivyo huku akijua kuwa ilimpasa kutumia akili katika kufanya lolote lile la kumtoa katika mikono ya jahili huyo.



Kwamba ni kipi atakachokifanya katika kujinusuru, hilo lilikuwa ni suala la kutekelezwa kwa umakini wa hali ya juu. Hakupaswa kuwa na papara, hakutaka kumfanya Makella agundue mapema kuwa kuna jambo tofauti na matarajio yake.



Lilikuwa ni jibu lililomfariji na kumsisimua Makella kwa kiwango kikubwa. Papohapo akamvuta Judith na kumkumbatia, kisha akambusu kwenye paji la uso wake huku mikono yake iliyokosa uvumilivu ikitalii hapa na pale katika mwili wake mwororo uliovutia.



Hata hivyo, miongoni mwa mambo ambayo Judith hakuyapenda na yalikuwa ni kero zaidi ya kero, ni kitendo cha kukumbatiwa-kumbatiwa, kupapaswa, kutomaswa, kupigwa busu au kufanywa vyovyote vile kwa namna ya kimahaba na mtu, mwanamume asiye mpenzi wake wa dhati.



Makella alikuwa ni mmoja wa watu hao, na alimkera! Lakini afanye nini? Hakuwa na budi kufuata ule usemi wa “mtaka cha uvunguni sharti ainame.”



“Ok, twen’zetu,” Makella alimwambia Judith huku akimshika mkono na kuanza kutembea tena. Dakika tano baadaye walikuwa Kiyovu Hotel, wakiwa wamesimama kaunta, na kwa sauti ambayo haikutofautiana na amri, Makella alimwambia mhudumu wa kike aliyekuwa mbele yao: “Chumba tafadhali.”



“Single au double?”



“Single.”



“Kipo.”



Dakika chache zilizofuata zilikuwa za kukamilisha taratibu za upangaji, kisha mhudumu akawapeleka chumbani.



**********



KILIKUWA ni chumba kilichostahili kuitwa chumba cha daraja la kwanza. Kitanda kikubwa, zulia zito sakafuni, jokofu lililosheheni vinywaji na televisheni ndogo iliyoegeshwa ukutani katika kijisanduku cha aina yake zilikuwa ni samani zilizotosha kukifanya chumba hicho kuwa maridadi. Isitoshe, simu kwa ajili ya kuwasiliana na utawala wa hoteli ilikuwa juu ya kimeza kidogo kilichokuwa kando ya sofa mbili.



Mpangaji hahitaji kuhangaika kuuliza wapi bafu na choo vilipo. Ni kiasi cha mtu kujua kusoma, ama Kiingereza, Kiswahili, Kinyarwanda au Kifaransa. Milango miwili yenye maandishi ya lugha hizo, yenye maelekezo kuhusu matumizi ya vyumba hivyo ilikuwa kulia mwa chumba hicho.



“Karibu..karibu mpenzi,” Makella alimwambia Judith huku akimtazama kwa namna iliyoashiria hitaji kamili la starehe ya mapenzi.



Ilikuwa ni tazama ambayo Judith hakuhitaji mtu wa kumfafanulia kuwa tayari Makella yuko mbali na yu taabani, uroho wa fisi ukiwa umekwishamtawala. Lakini hakuhofu. Aliyaepuka macho hayo huku moyoni akisema, 'tutaona.' Akalifuata sofa moja na kuketi kwa kujiachia kihasarahasara, nusu kaketi, nusu kalala.



Makella alimtazama kidogo kisha akaurudisha mlango na kumfuata pale sofani. “ Nakupenda Judith,” alinong’ona huku akimpapasa katika paja la kulia.



Kwa Judith, upapaswaji huo haukumletea msisimko wowote. Zaidi, alihisi kupapaswa na popobawa, kiumbe wa ajabu ambaye miaka kadhaa iliyopita aliviteka vyombo mbalimbali vya habari hususan yale magazeti pendwa akidaiwa kuwa alikuwa na tabia ya kuwaingilia wanaume na wanawake kimiujiza usiku wakiwa wamelala, taarifa ambazo mpaka leo hazijapata uthibitisho wowote.



Hakuwa radhi kuuachia mwili wake utumiwe na mtu huyu ambaye hakumtofautisha na shetani, achilia mbali huyo popobawa. Alimwogopa, na zaidi alimchukia. Haikumwingia akilini asilani kumwachia Makella apenye katikati ya miguu yake na kustarehe. Hapana, hakuwa tayari kwa hilo, labda maiti yake ndiyo inajisiwe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Hivyo, wakati Makella akimpapasa huku akimtazama kwa matamanio makubwa, yeye alikuwa mbali kifikra, akipanga namna ya kujiokoa.



Alishakichunguza chumba hicho kwa makini. Kumtoroka Makella kwa kupitia dirishani lilikuwa ni jambo lisilowezekana. Dirisha kubwa lililokuwa kaskazini mwa chumba hicho, lilisheheni nyavu imara na nondo madhubuti, hivyo isingekuwa rahisi kufanya chochote katika kujiokoa. Akatupa macho juu ya meza ndogo iliyokuwa katikati ya chumba hicho.



Akauona ufunguo.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog