Search This Blog

Saturday 5 November 2022

KARATA YA BARADHULI - 2

 








Simulizi : Karata Ya Baradhuli

Sehemu Ya Pili (2)





ALIMWELEZA. Na hakumficha kitu. Alianzia mbali, akimzungumzia marehemu Malick, akimjenga kuwa alikuwa mtu wa watu, akionyesha upendo kwa kila mtu bila ya kubagua hali ya mtu kimaisha. Pia alikuwa akitoa sana misaada kwa watu na vikundi mbalimbali.



“Hata mimi ni yatima,” aliendelea. “Mzee amenilea, akanisomesha na kunipa ajira na majukumu makubwa ndani ya milki yake kiasi cha baadhi ya watu kuhisi kuwa ama nimemloga au ni mwanae wa kuzaa.



“Lakin kuhusu mkewe…” kufikia hapo akasita na kuwa kama ambaye hajazungumza lolote muda mfupi uliopita.



“Enhe, mkewe?”



“Kwa kweli hakuwa …au tuseme sio mtu mzuri,” sauti ya Karim ilipooza. “Sio mtu, ni mnyama! Hakuwa akimjali marehemu mzee, alikuwa akiujali utajiri aliokuwa nao. Na siku ambayo mzee aliaga dunia, alimwambia bayana kuhusu wewe; kwamba ndiye utakayerithi mali. Mmh!”



Kufika hapo akashusha pumzi ndefu na kupunguza mwendo. Kisha akaendelea, “Kwa kweli mwanamke yule alibadilika! Akabwata maneno machafu! Kama mimi na dokta tusingekuwepo, kwa vyovyote vile angemdhuru…”



Alizungumza kwa kirefu, na alizunguma yote aliyojua kuwa alipaswa kumsimulia Ablah.



Woga ukamrudia Ablah. Akasema, “Karim, kwa ujumla una mzigo wa kipekee na tena ni mzigo mkubwa. Ninaamini kuwa una ujasiri wa aina yake ambao si rahisi kwa mtu mwingine kuwa nao. Nakushukuru kwa kuwa na baba yangu kwa kipindi chote cha uhai wake. Bila wewe mali yote ingepukutika.



“Lakini Karim, nahofia usalama wangu! Nahisi huenda huyo mwanamke ataniua!”



“Hapana, hawezi kukuua! Ondoa hofu kuhusu hilo.”



“Ataniua, Karim!”



“Hawezi! Wewe niamini mimi, Ablah! Niko nawe bega kwa bega. Siwezi kukutupa! Siwezi kuuacha wasia wa marehemu tajiri wangu. Ondoa hofu, Ablah!”



“Lakini Karim,” Ablah alisema na kusita.



“Ndiyo, sista.”



“Unadhani naweza kumiliki mali hiyo bila ya kuwa na mwenzangu?”



“Mwenzako?”



“Ndiyo, Karim,” Ablah alijibu kwa unyonge. “Napaswa kuwa na mume atakayenisaidia kuitunza mali hiyo. Siwezi kuilinda peke yangu, Karim!”



Ukimya ulitanda. Karim alishindwa kutamka chochote.

Ablah akaongeza, “Karim, sijui kama utanielewa. Kwa kweli natamka hili kutoka moyoni; shukrani pekee niwezayo kukupa, na msaada mkubwa unaoweza kunipa maishani mwangu ni mimi na wewe kufunga ndoa.”



Karim alishtuka. Akaguna. Akahisi nguvu zikimomonyoka mikononi kiasi cha kushindwa kuudhibiti vizuri usukani. Gari likayumba kidogo. Haraka akairejesha akili na kupangua gia. Kisha akaegesha pembeni. Akainamia usukani bila ua kutamka chochote.



Ablah alishangaa. Akamgusa bega na kumuuliza, “Karim, kwani vipi?”



Akili ya Karim ilirudi nyuma, akayakumbuka maneno ambayo Mzee Malick alimwambia kabla hajafariki dunia. Alisema, KWA KUWA WEWE NA ABLAH MTABAKI MKIWA YATIMA, KWA NINI NISIWAOZE? ABLAH AWE MKEO BADALA YA KUCHUKULIWA NA JITU NISILOLIJUA. NITAFARIJIKA SANA KAMA NITAKUWA NIKIJUA KUWA NITAKUFA HUKU NIKIMWACHA MWANANGU AKIWA NA MCHUMBA WA MAANA AU KAOLEWA NA KIJANA WANGU NIMPENDAYE.



Maneno hayo yalielea kuchwani mwake muda huo ambao Salma katamka maneno hayo mazito. Akaunyanyua uso na kumtazama Ablah. Macho yao yakagongana.



“Maneno yako ni mazito sana, Ablah,” hatimaye alisema. “Marehemu mzee aliniambia maneno hayo kabla hajafariki. Lakini sikumkubalia. Najiona kuwa nitakuwa na hatia kama tutafikia hatua hiyo unayosema. Najiona kuwa mimi na wewe ni kaka na dada. Sikupingi, Ablah. Ngoja tufike nyumbani. Hayo tutayazungumza tu.”



*****







*****

ASUBUHI hii, ikiwa ni baada ya matanga kuanuliwa jana yake, Sharifa aliamka saa 1 na kuingia bafuni kuoga. Kisha alivaa vazi laini ambalo lilionyesha maungo yake ya ndani kwa uwazi.



Lakini hakutoka chumbani akiwa na vazi hilo pekee, alivaa kanga juu yake. Hakutaka macho yasiyohusika yalishuhudie umbo lake la ndani, umbo ambao aliamini kuwa lina mvuto mkali mbele ya mwanamume yeyote mkamilifu. Alihitaji macho ya mtu mmoja tu ndiyo yalifaidi umbo hilo. Mmoja tu!



Bado jumba zima lilikuwa kimya, ashirio kuwa wakazi wengine bado wamelala. Aliifurahia hali hiyo. Akafungua mlango na kutokeza koridoni. Alikuwa hana hata kandambili miguuni, alitembea kwa kunyata hadi kwenye mlango wa chumba cha Karim. Akagonga mara mbili



Kimya!



Akagonga tena, mara mbili, safari hii kwa nguvu zaidi.



Kimya!



Akashangaa. Haikuwa kawaida kwa Karim kulala hadi muda huo. Huwa ni mtu wa kuamka kabla ya saa 12: 30 asubuhi na kufanya shughuli hizi na zile zilizomhusu. Leo hadi saa hizi bado kalala!



Mara akakumbuka simu. Akarudi chumbani kwake na kutwaa simu yake, na bila ya kutoka humo akaamua kumpigia Karim. Lakini tofauti na matarajio yake akaambulia jibu: Samahani, simu ya mteja uliyopiga haipatikani.



Akasonya kwa hasira na kuitupa simu kitandani. Kwa nini Karim azime simu? Na kwa nini awe amelala hadi saa hizi? Maswali hayo yalimjia akilini na kujikuta akiwa njia panda.

Mara akakurupuka na kutoka tena chumbani humo.



Moja kwa moja hadi kwenye chumba alichotumia daktari Suleyman. Akagonga mlango kwa nguvu. Muda mfupi baadaye akasikia mtu akihema kwa nguvu na kupiga mwayo huko chumbnani.



Akaharakisha kugonga tena, safari hii akifuatisha na wito wa sauti ya juu: “Dokta! Dokta! Please..!”



Mlango ukafunguliwa. Daktari Suleyman akasimama mbele yake. Sharifa, akionekana kukosa utulivu moyoni, akamuuliza, “Mbona hivi?”



“Hivi, ki-vipi?” daktari naye akamtupia swali.



“Mbona mambo hayaeleweki?”



“Mambo gani?”



“Nyumba imepooza! Kama ni msiba, tu’shamaliza, na jana tumeanua matanga. Lakini sioni dalili yoyote ya uhai humu ndani. Ina maana hata usafi haufanyiki?”



Daktari aliachia tabasamu dhaifu kisha, kama asiyejali, akasema, “Nadhani hayo unayoniambia hayanihusu. Au kuna tatizo jingine?”



“Lipo. Karim hajaamka?”



“Kwa nini?”



“Yuko wapi? Hii huwa siyo kawaida yake!”



Kwa mapozi daktari alitikisa kichwa akiashiria kuafiki. “Ni kweli siyo kawaida yake. Umemgongea?”



“Sana tu! Na hata simu yake haipatikani! Why?”



Kwa muda mfupi ukimya ukapita, wakitazamana. Kisha Suleyman akauvunja ukimya huo.



“Hayupo,” alisema kwa utulivu.



“Hayupo?! Kaenda wapi?”



“Sijui, lakini hayupo!”



Sharifa alimkazia macho Suleyman na kujiwa na wazo la haraka, wazo aliloamini kuwa ni ukweli halisi. Karim kamfuata mrithi!



Ndiyo, aliamini hivyo. Na hakutaka kulificha hilo wazo au imani yake. Lakini aliamua kuwa mpole ili aithibitishe imani yake. Kwa mbali akaachia lile tabasamu lake huku akiendelea kumtazama Suleyman sawia.



Kisha: “Sikia, dokta. Hakuna haja ya kuficha. Sema tu kama kaenda kumfuata mtoto.”



“Nd’o maana’ake.”





Kiti kama radi kikapita machoni mwa Sharifa pyuu! Akahisi kizunguzungu, lakini akajitahidi kustahimili. Masikio yakavuma vuuu!



Mtoto! Mrithi



Hakuyaamini masikio yake. Tabasamu likaendelea kuchanua huku akiwa hana hata hata chembe ya furaha moyoni mwake. Lakini kwa kuwa alijaaliwa moyo wa kipekee, moyo usiojali wala kuhofia chochote, moyo usiokuwa na walao chembe ya huruma, uthibitisho huu ulimteteresha kwa sekunde tatu tu na kurejewa na hali yake ya kawaida.



“Atarudi lini?”



“Siwezi kujua.”



Ilitosha. Dakika chache baadaye, Sharifa alikuwa akimgongea mlango kaka yake, Abdul, ambaye naye bado alikuwa amelala.



“We Abdul!” kwa hasira alimwita.



Abdul alishtuka ma kukurupuka kitandani. Akafungua mlango na kumpisha Sharifa aliyengia kama anayefukuzwa.

“Bwege kakifuata kijibwa chao!” yalimtoka Sharifa huku kasimama, mikono kiunoni, akimtazama Abdul kwa macho makali.



“Una hakika?”



“Ndiyo. Dokta kanithibitishia!”



“Kaenda lini?”





“Itakuwa leo alfajiri,” mara baada ya Sharifa kusema hivyo, akaenda dirishani kuchungulia. Kisha, akamgeukia tena Abdul. “Si unaona! Ile Range Rover haipo! Atakuwa kaitumia kwenda Arusha!”



“Achana nae, Abdul alisema akionekana kutojali. “Cha muhimu, akimleta usionyeshe kumchukia. Mchangamkie na kuwa naye karibu. Uwe fala kwa muda. Jipendekeze na kuonyesha upendo kwake.”



“Hilo sio la kunifundisha.”



*****



KARIM na Ablah walifika kwenye jumba la kifahari la marehemu Malick saa 10 jioni. Karim akaliegesha gari na kuteremka. Kisha akamfungulia Ablah mlango kama heshima kuu.



“Tumefika,” lilikuwa ni neno pekee alilosema Karim.



Ablah aliteremka huku akishangaa. Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika katika jumba hili la marehemu baba yake. Kwa sekunde kadhaa alisimama na kulistaajabia.



“Ablah,” Karim alimzindua. “Twende. Twende ndani. Utapazoea taratibu.”



Ablah alikaribishwa na baadhi ya wafanyakazi wa jumba na miradi ya marehemu Malick. Kisha Karim akampeleka kwenye kaburi la baba yake, ambako kutokana na jinsi lilivyotengenezwa, Ablah alimwona kwa usahihi. Ndiyo, aliuona uso wa marehemu baba yake ulivyotulia kama vile bado yungali hai. Machozi yakamtoka, akisikitika kwa kuwa na bahati mbaya ya kuwa ni mtoto ambaye hakuwahi kucheka na baba yake kama wototo wengine.



Hali hiyo ilimfanya Karim aamue kumwondoa hapo huku akisema, “Yamepita, Ablah. Huyo ndiye mzazi wetu. Sote tulimpenda lakini mola alimpenda zaidi. Hatuna budi kutambua kuwa sote njia yetu ni hiyohiyo.”



Wakaingia ndani kimyakimya ambako Ablah alionyeshwa chumba maalum cha malazi ambacho kilikuwa ghorofani. Kisha akatembezwa hapa na pale kabla ya kutambulishwa rasmi kwa wafanyakazi wengine wa hapo sanjari na Sharifa na Abdul.



Ablah akawa ameanza maisha mapya, maisha ya jijini Dar, kwenye jumba la marehemu baba yake, akiwa anatambua kuwa amekuja kwa minajili ya kurithi mali. Hakuwa na shida yoyote, na isitoshe Sharifa alimkaribisha kwa namna iliyomwondolea upweke. Akamchangamkia Ablah na kuonyesha ukarimu wote. Kwa siku tatu mfululizo chakula hakikupita kinywani mwa Sharifa bila ya Ablah kuwa pamoja naye.



Wiku moja ilipokatika walikuwa wamezoeana kwa kiasi kikubwa hata ikafikia Ablah kuanza kujihoji kuhusu taarifa aliyopewa na Karim juu ya tabia ya Sharifa. Ni taarifa za ukweli au Karim ana chuki binafsi?



Walifikia hatua ya kwenda pamoja saluni mitaa ya katikati ya jiji wakitumia gari aina ya Mercedes Benz jeusi, ambalo Karim alimkabidhi Ablah tangu walipofika. Ilmradi kila alikokwenda Sharifa, hakutaka kumwacha Ablah. Na Ablah alifanya hivyohivyo.

Ni katika kuzoeana huko ndipo siku moja, wakiwa peke yao, katika mgahawa wa Steers katikati ya jiji wakinywa juisi, Sharifa alipofungua ukurasa mpya wa maongezi.









“Hivi, Ablah, una mchumba?”



Lilikuwa ni swali lililomshtua Ablah. Akachukua sekunde kadhaa akilitafakari. Kwa nini anaulizwa hivyo? Ni majuzi tu kaja, na hata kuzoena na huyu ‘mama’ yake hawajazoeana sana kiasi cha kuanza kuzungumza au kuulizana maswali ya ndani zaidi yahusuyo historia ya maisha ya mtu au malengo ya baadaye. Kama ana mchumba au hana inamhusu nini?



Maswali ya aina hii, akilini mwa Ablah aliyachukulia kama maswali ya wambeya wa uswahilini, wale ambao hawana kazi ya kufanya zaidi ya kuchunguza nani anafanya nini, anafanya kazi gani, ana watoto wangapi, ana uwezo gani kifedha, ndani mwake ana samani za aina gani na kadhalika na kadhalika.



Hizo ndizo tabia za wambeya, na ndiyo maswali yao huku macho yao yakitaka kuona kila kinachotokea mtaani! Na huyu ‘mama’ yuko hivyo? Ablah alijiuliza.



Hata hivyo, hakutaka Sharifa agundue kuwa kashangazwa na swali lake. Akachanua tabasamu la kirafiki na kujibu, “Sina. Kwa kweli nipo-nipo tu, mama.”



Sharifa naye akaachia tabasamu zito na kuuliza, “Hujampata au huhitaji kwa sasa?”



“Aah…nadhani bado mapema sana. Najua nitampata tu. Hilo s’o tatizo.”



“Lakini…” Sharifa alisema na kusita. Akawaza ujumbe anaotarajia kuufikisha kwa Ablah utapokewa kwa namna gani.



Ablah aliusoma uso wa Sharifa na kuhisi jambo zaidi ya jambo. Alimwona kama mwenye shaka. Akambana, “Vipi, mbona unasita?”



“Aaa…kwa kweli nilikuwa nina pendekezo,” hatimaye Sharifa alisema.



“Pendekezo gani?”



“Ni vizuri kama kaka yangu angekuoa. Sidhani kama itakuwa vizuri ukoo ukisambaratika. Kaka yangu ametokea kukupenda sana Ablah. Kama mtaoana, nadhani italeta picha nzuri sana.”



Ablah akashangaa. Akaguna na kusema, “Ni jambo la ajabu sana.”



“Ajabu gani, Ablah?”



Ablah alitulia kidogo. Akanywa juisi yake kisha akasema, “Wewe ni mama yangu. Iweje kaka yako, ambaye mimi namwita ‘mjomba’ ndiye anioe? Inakuja kweli hiyo?”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Achana na sera hizo, Ablah…” Sharifa aliitetea hoja yake. “Kumbuka kuwa mimi nilikuwa mke wa marehemu baba yako. Kwa bahati mbaya hatukujaaliwa kupata mtoto. Kwa hali hiyo, mimi nitabaki kuwa mama yako kiivyo tu. Lakini nataka ukoo usisambaratike. Hakutakuwa na ubaya kama Abdul atakuoa. Isitoshe, yeye ni mzoefu wa kusimamia miradi. Kwa hilo atakusaidia sana. Amesomea uchumi…”



Aliongea mengi akimpigia debe kaka yake, Abdul. Hata hivyo, Ablah alikuwa makini, na akahisi mara kwa mara sauti ikimnong’oneza: ‘Jihadhari. Yakumbuke maneno ya Karim na usiyapuuze.’



Alichofanya ni kumwambia Sharifa kuwa suala hilo halina pingamizi lakini halihitaji haraka isiyo ya lazima.



“Ok, lakini haya tuliyozungumza yabaki kwetu, usimwambie mtu yeyote; sawa shosti?” Sharifa alimwambia.



“Usihofu. Hakuna wa kumwambia. Kwanza nani wa kumwambia suala la kuolewa kwangu zaidi ya bibi na babu yangu niliowaacha Arusha?”



Sharifa alimtazama Ablah kwa namna ya kuridhika na jibu lake. Akanyanyuka na kutoka huku akimwambia, “Natarajia baada ya siku chache utakuwa wifi yangu kamili.”



“Mungu akipenda.”



“Atapenda tu.”





*****



“NITAKUUA… Kama hutaki, nitakuua!” mtu huyu mwenye mwili mkubwa alimsimamia Ablah huku akiwa uchi kama alivyozaliwa, kisu kirefu chenye makali ya kutisha kikiwa mkononi.



Ndiyo kwanza Ablah alikuwa anatoka bafuni huku kajifunga taulo pekee mwilini. Bafu hili lilikuwa halimshinikizi kutoka chumbani mwake. Lilikuwa humohumo.



Aliduwaa na kubaki akitetemeka. Akajiuliza huyu mtu kaingiaje humu ndani? Chumba chake kilikuwa ghorofani na kwa yeyote ambaye angehitaji kuingia, hususan muda huo, ingempasa kubonyeza kengele mlangoni. Kengele hiyo ingelia kwa usahihi, na hata yeye huko bafuni angesikia. Na hii ni saa 5 usiku! Kapita wapi mtu huyu?



“Lazima nikuue! Huwezi kurithi mali ambayo hata hujui ilivyotafutwa! Nitakuua! Na nitakuua sasa hivi, tena hapahapa!”



Macho ya mtu huyu yalizidi kuwaka, akimtazama Ablah kwa namna zote za kuua! Rangi ya ngozi yake nyeusi ilizidi kumfanya atishe maradufu! Mkono uliokakamaa, uliokishika kisu kilichomeremeta, ilikuwa ni taswira nyingine ya kuogofya.



Isitoshe, kisu hicho kilikuwa kimetapakaa damu mbichi! Mtu huyo wa ajabu alionekana kama vile muda mfupi uliopita kaua mtu na sasa, humu chumbani alikuwa katika mwendelezo tu wa kazi aliyokwishaianza. Ukishadiriki kuing’oa roho ya binadamu wa kwanza kwa dhamira na ujasiri mkubwa, hutashindwa kuzing’oa roho kumi nyingine huku ukicheka. Itakuwa ni kazi nyepesi kuliko ilivyo!



Huyu mtu alionekana kuwa kazi ya kuua, kwake ni miongoni mwa burudani zilizoukonga moyo wake.



“Utakufa!” kwa mara nyingine alifoka, safari hii akianza kumsogelea taratibu Ablah. “Nitakuua! Na hakuna atakayejua!”



Alizidi kumsogelea, kisha akaunyayua mkono wenye kisu na kuuelekeza kifuani kwa Ablah.



Macho yalimtoka Ablah! Hofu ikamtawala. Akanyanyua mikono juu akitaka kupiga mayowe lakini sauti haikutoka. Mara akalishuhudia lile jisu likimshukia kifuani.



*****

KARIM alishtuka usingizini na kutupia macho simu yake iliyokuwa kwenye meza ndogo chumbani mwake, ikiita. Akaitazama huku akifikicha macho kwa vidole. Mara akayahamishia macho ukutani kulikokuwa na saa.



Akashangaa. Ilikuwa ni saa 8 usiku! Akaiacha saa hiyo na kuirudia simu yake. Bado ilikuwa ikiita! Akaitupa shuka kando na kujitoa kitandani haraka. Hakukumbuka ni lini kwa mara ya mwisho alipigiwa simu muda huo.



Simu ambayo alipigiwa huku akiwa ameshalala, ilitoka kwa tajiri wake, Malick, enzi za uhai wake, ambayo alimpigia saa 5 usiku. Na ilikuwa ni mwaka mzima uliopita! Na ilikuwa ni siku moja tu.



Siku hiyo mzee Malick alikumbwa na maumivu makali ya mgongo na ilimpasa kwenda hospitali. Hivyo hakuwa na budi kumwamsha kijans ampendaye , Karim. Ndipo alipompigia simu hiyo iliyomshtua Karim.





Haikuwahi kutokea tena akapigwa simu zaidi ya saa 2 usiku, kama yeye pia alivyokuwa na mazoea ya kutompigia simu mtu yeyote kuanzia saa 2 usiku na kuendelea.



Hii simu iliyopigwa majira haya ilimweka katika wakati mgumu. Usiku wa manane! Huku mapigo ya moyo yakiwa yameongeza kasi aliinyakua simu huyo na kuitupia macho kwenye skrini. Mshangao na mshtuko vikazidi kumtawala!





Jina la ABLAH lilionekana kwenye skrini hiyo!



Saa 8 usiku! Kuna nini? Amepatwa na nini? Ame…Ame…maswali mengi yalimiminika kichwani mwake na hakuna hata moja aliloweza kulipatia jibu. Akabaki ameikodolea macho simu hiyo hadi ikakatika. Mara ikaanza kuita tena! Sasa Karim akazinduka. Akabonyeza kitufe cha kupokelea na kuitega simu sikioni haraka.



“Karim!” sauti yenye taswira ya hofu na mfadhaiko ikapenya sikioni mwake papohapo.



“Ablah!”



“Karim, njoo! Njoo haraka!”



“Kuna nini Ablah?”



“Njoo! Njoo haraka Karim!”



Karim hakusubiri wala kufikiri zaidi. Alitwaa shati na kulivaa haraka. Hakuvaa suruali; bukta ilitosha. Akatoka mkuku. Chumba cha Ablah kilikuwa ghorofani, ilhali cha Karim kilikuwa chini sanjari na vyumba vya Sharifa, Abdul, Daktari Suleyman na watumishi wawili wa usafi.



Chumba cha malazi cha Ablah kilikuwa ni maalum kwa wageni maalum wa mzee Malick. Kilikuwa hakitumiwi na mtu yeyote mwingine mathalani mgeni asiye maalum. Ni heshima ya Ablah iliyomfanya Karim amkabidhi chumba hicho.



Zaidi ya chumba hicho cha malazi huko ghorofani, pia kulikuwa na ukumbi pekee, ukumbi wenye zulia la thamani na masofa ya kuvutia. Ndani ya ukumbi huo ndiko kulikokuwa na sehemu ya kupumzikia na kuliwaza kutokana na upepo murua kutoka baharini.



Enzi za uhai wa Mzee Malick, kabla maradhi hayajaanza kumsulubu, alipendelea kuketi huko ukumbini na mkewe Sharifa, wakigida pombe huku wakizungumza na kuchezeana kimahaba. Na kwa kuwa haikuwa rahisi kwa yeyote kuja huko ukumbini bila ya ruksa yao, walijisikia huru kustarehe kwa namna yoyote mithili ya walio chumbani peke yao.



Ili mtu yeyote aweze kufika kwenye ukumbi huo, hakuwa na budi kupita ndani ya chumba hiki cha wageni maalum, na hivyo ilikuwa dhahiri kuwa kwa kipindi hiki ambacho Ablah ndiye aliyekuwa akimiliki eneo hilo la juu, alikuwa peke yake, vinginevyo mtu wa pili aingie kwa ruksa yake.



Kwamba, kuna uwezekano wa mtu kuingia kwa hila huko chumbani kwa Ablah, ni jambo ambalo halikumwingia akilini Karim. Hivyo, wakati akitoka chumbani mwake hima, hakuwa akijua wala kukisia ni jambo gani lililomsibu mtoto pekee wa marehemu tajiri Malick Sikonge.



Muda mfupi baadaye, baada ya kuzikwea ngazi mbili-mbili za kuelekea huko ghorofani, alijikuta mbele ya mlango wa chumba cha Ablah. Papohapo akabonyeza kengele.



*****

ILIKUWA ni ndoto, lakini haikuwa ndoto ya kawaida. Kwa Ablah, ndoto hii ilikuwa ni zaidi ya ndoto. Tangu azaliwe hakuwa na kumbukumbu ya kuota ndoto kama hii. Akabaki akitweta. Mara akasikia kengele ikiita. Akili yake ikamwambia kuwa kwa vyovyote mtu huyo hatakuwa mwingine zaidi ya Karim ambaye amempigia simu muda mfupi uliopita. Akakurupuka kwenda kufungua mlango.



Alikuwa ni Karim.



“Vipi, Ablah?” Karim alimUuliza huku akiingia chumbani humo hima na kuangaza macho huku na kule.



“Nimeota ndoto mbaya Karim!”



“Ndoto?”



“Ndiyo, ni ndoto lakini siyo ndoto ya kawaida.”



Alilazimika kumsimulia Karim kuhusu ndoto hiyo na kudai kuwa hana imani na usalama wake katika nyumba hiyo. Na akaongeza, “Siwezi kulala peke yangu, Karim. Siwezi!”



Ilimwia vigumu Karim kumwacha peke yake Ablah. Na, ni usiku huo ndipo Ablah alipomwambia Karim kuhusu maongezi kati yake na Sharifa mchana uliopita kule katika mgahawa wa Steers.



“Anataka kaka yake ndiye anioe!”



“Yaani Abdul?” Karim alishangaa.



“Nd’o maana’ake.”



“Ana lake jambo! Kama nilivyokwambia, ni mwanamke hatari! Anataka uolewe na Abdul ili baadaye mali yote iwe chini yao. Unapaswa kuwa mwangalifu sana kwa hilo.”



“Kwa hiyo nitafanya nini, Karim?”



Badala ya kumjibu, Karim naye akamuuliza, “Kwani ulimpa jibu gani?”



“Nimemwacha njia panda. Sijamwambia kuwa nimekubali au sitaki. Nimemwambia tu kuwa tutaangalia.”



“Good! Cha muhimu ni kujitahidi kuwa makini, usimfanye akashtuka kuwa hukubaliani naye.”



“Nimekuelewa. Sifanyi kosa, lakini usiniache mbali Karim. Nina wasiwasi na usalama wangu. Ndoto ya leo imenitisha, na sijui inamaanisha nini!”



“Usihofu, Ablah. Tuko pamoja. Ingawa siamini sana mambo ya ndoto, lakini hii ya kwako huenda inaashiria jambo fulani. Tutakuwa pamoja muda wote.”



*****



NI hapo Sharifa alipoona kuwa alipaswa kuzungumza vizuri na kaka yake. Vinginevyo huenda wakakorofishana na kujikuta wakishindwa kufikia malengo yao.



Akamweleza mbinu ya awali aliyoitumia, ya kumtaka Ablah awe wifi yake. “Lakini hajanipa jibu halisi, alihitimisha.



“Lakini unamwonaje? Anaelekea-elekea?” Abdul alimuuliza.



“Siwezi kujua. Lakini sidhani kama tunahitaji hiyari yake. Kama unavyojua, yule bwege nd’o kamfuata na kumleta. Kwa vyovyote atakuwa kishamjaza maneno!”



“Kwa hiyo unataka kun’ambia nini?”



“Nina wazo moja,” Sharifa aliishusha zaidi sauti yake. “Tumuue yule kidampa!”



Abdul alishtuka, akamkazia macho dada yake.



“Ndiyo, tumuue!” Sharifa alisisitiza. “Tukishamwondoa njia itakuwa nyeupe. Huyo kijibwa wa mzee Malick utamuoa apende, asipende! Na ukishamweka ndani tayari mali tunaimiliki. Umeona eeh?”



“Nimekusoma, sista,” Abdul alisema kwa utulivu. “Hata hivyo nadhani si vizuri kumuua huyo bwege. Tukimuua tutakuwa tumeharibu dili zima.”



“Ki-vipi?”



“Tambua kuwa Karim anatambulika kwa watu wengi kuwa ni mtu aliyekuwa karibu sana na yule bwege mumeo. Na kila mtu au tuseme baadhi ya watu humu mjengoni wanajua kuwa wewe ulikuwa mkorofi sana kwa bwana’ako. Huenda pia wameshaambiwa juu ya kauli ya huyo babu yako kukirithisha kijibwa chake mali yote badala ya wewe mke wa ndoa. Upo hapo?”



“Nakusoma,” Sharifa alijibu.



“Hivi unadhani ule mzozo wa siku ile ambao bwana’ako alikufa haujayafikia masikio ya wanafiki wengine?”



“Siwezi kujua.”



“Ndivyo ilivyo! Wengi wanajua! Na hilo linaweza kusababisha ushtukiwe mapema sana kama kutatokea madhara yatakayowagusa hao wawili.



“Na bado kuna daktari. Yeye pia anaweza kuwa shahidi mzuri wa kukukandamiza kwa askari. Na hapo ndipo utakapojikuta mahakamani ivi-ivi!”



“Ni kweli,” Sharifa aliafiki. “Kwa hiyo tufanye nini?”



“La kufanya ni kunipa mkwanja nisepe,” Abdul alijibu, macho yake mekundu yakimtazama Sharifa kwa makini. Akaongeza, “ Kwani huna fungu lolote la maana uliloachiwa na yule bwege wako kabla hajakata kamba?”



“Aliniandikia cheki ya pesa kidogo.”



“Kama ngapi?”



“Fifty.”



“Fifty…una maana…”



“Milioni hamsini!”



“S’o mbaya sana. Nifanyie kumi basi niondoke zangu.”



“Nini?” Sharifa alimshangaa. “Abdul mbona unaleta vichekesho? Una maana milioni kumi?!”



“Nd’o maana’ake. Sa’ kumbe unafikiriaje? Wewe kwa akili yako unataka kunikatia ngapi?”



Ukimya ukatawala kwa muda. Kisha Abdul akaendelea, “We’ nipe hizo ning’oke hapa kwa muda kama tulivyokubaliana majuzi. Niende zangu uswazi, nikajichimbie huko huku tukiwasiliana kwa ajili ya kumaliza mchezo.”



Ukimya mwingine ukapita, Sharifa akionekana kutafakari jambo. Abdul akaamua kuendelea, “Ninapokwambia kuwa unijaze mshiko nikakae uswazi, ujue kuwa ni huko ndiko nitakakosuka mpango mzima kuhusu huyo demu. Sina ulazima wa kumwoa. Pesa kwanza! Kuoa naweza kuwa namwoa siku moja-moja. Na hata hivyo kwani pumzi yake ina manufaa gani kwetu mbele ya mamilioni ya pesa?”



“Pumzi yake haina manufaa yoyote!” Sharifa alitamka kwa sauti inayotisha, macho yake meupe yakielea-elea kama shetani. “Hatukuwa tunamjua! Tumemwonea hapahapa! Hatuna nasaba naye, kwa nini kichwa chake kisiwe halali yetu?”



“Hapo umeonekana ni mwanamke wa shoka, sista,” Abdul alisema huku akitwaa sigara na kuiwasha. “Nimekukubali. Kwa hiyo kinachoendelea?”



“Nakupa milioni tano. Zitatosha kwa kuanzia katika mpango mzima.”



“Sista jiwe!”



*****

ABDUL aliondoka siku ya pili jioni, akiwa na begi lake la nguo tu. Aliondoka kistaarabu, akiwaaga Karim na mtoto wa marehemu mzee Malick, Ablah kwa namna ya moyo mkunjufu na kudai kuwa anakwenda nyumbani alikozaliwa, mkoani Morogoro.







“Mungu akipenda tutaonana tu…nitakuwa nakuja mara kwa mara huku Dar kwa shughuli za kibiashara,” aliongopa.



Kwa Ablah ilikuwa ni habari njema. Alikumbuka kuwa Sharifa alikuwa akimpigia debe huyu Abdul eti amuoe. Sasa akaona atapumua, suala hilo litapotezwa kisayansi.



Wakati Abdul akiingia ndani ya gari dogo, Honda Civic lililotumiwa na Sharifa siku zote tangu aolewe, akilini mwake alijua kuwa katika kipindi atakachokuwa nje ya jengo hilo, atasuka vya kusukika na baada ya siku chache mambo yatakuwa mazuri. Utajiri aliuona ukinukia mbele yake.



Gari liliondoka taratibu, usukani ukiwa umeshikwa na Sharifa. Walinzi walipofungua geti na gari kutokomea, hatimaye Sharifa akamuuliza Abdul, “Una mpango wa kukaa wapi?”



“Twende Kinondoni tu,” Abdul alijibu. “Hakuna haja ya kwenda mbali sista. Nitajichimbia Kinondoni, Biafra. Najua pale huwa kuna wazee wa kazi. Nitazoza nao tufanye kweli. Au vipi?”



“Poa,” Sharifa alijibu huku akiwa makini barabarani, gari likiwa katika mwendo mkali.

Dakika ishirini baadaye, Sharifa alikanyaga breki nje ya nyumba ya wageni iitwayo Madina eneo la Biafra. Abdul aliichagua gesti hiyo kwa kuwa alishawahi kulala hapo mara tatu na mwanamke mmoja changudoa aliyemwopoa maeneo ya Leader’s Club nyakati za usiku.



Ilikuwa ni gesti isiyokuwa maarufu sana lakini ikiwa katika viwango vya juu; kiyoyozi, televisheni na usafi wa hali juu katika sehemu zote.



Baada ya kuegesha gari wote waliteremka na kwenda mapokezi ambako walikamilisha taratibu zote na kisha wote wakaingia chumbani.



Sharifa akajitupa sofani na kuangaza huku na kule akionekana kuridhishwa na ubora wa chumba hicho. Abdul yeye kwanza aliwasha kiyoyozi kisha akaketi kwenye kitanda kikubwa kilichotandikwa shuka safi nyeupe. Mara akaingiza mkono mfukoni na kutwaa sigara. Akaiwasha na kuvuta mikupuo miwili huku akizungusha macho chumbani humo.



“Unapaonaje hapa?” hatimaye Abdul alimuuliza dada yake.



“Pako poa sana,” Sharifa alijibu huku akiendelea kuangaza macho chumbani humo. “Pametulia sana lakini usijitanue kwa sana na kila mbwa akajua kuwa uko hapa.”



“Yeah, hata wash’kaji zangu ninaotaka kusuka nao dili sitaki wajue kuwa niko humu. Siku hizi hakuna kuamini mtu.”



Ukimya ukapita kidogo kisha Sharifa akamuuliza, “Unatarajia kufanyaje ili tufanikishe dili?”



Abdul hakuwa na haraka ya kujibu. Alivuta tena mkupuo mkubwa wa sigara yake kisha akasema, “Kuna wash’kaji zangu wawili nitaongea nao, tumteke huyo pakashume aliyetoka Arusha kisha tumshinikize huyo kijakazi wao, chokoraa aliyeokotwa na bwege wako aliyekufa na kumfanya kama msimamizi wa kila kitu, atupe pesa ya kueleweka vinginevyo, tumchinjilie mbali chotara wao.”



“Ni wazo zuri, lakini umakini unatakiwa,” Sharifa alisema. “Kwanza hao watu wako hawapaswi kujua ni kiwango gani tunachotaka kuchukua kwa hawa mbwa koko. Wakijua itakuwa ishu; nao watapandisha dau. Pili, tuhakikishe kuwa tunapata pesa inayoeleweka. Siyo chini ya milioni mia mia tano.”



******

SIKU iliyofuata baada ya Abdul kuhamia hapo Madina Guest House, aliamka mapema, akaagiza supu ambayo baada ya kuifakamia alitoka. Moja kwa moja hadi Kawe Mzimuni. Japo alikuwa na simu nzuri, ya kisasa hata hivyo alilazimika kukodi teksi hadi huko Kawe akiwa anamfuata rafiki yake wa siku nyingi, Jitu Mpendachuma kwa kuwa hakuwa na namna yoyote ya kuwasiliana naye kabla; hakuwa na namba yake ya simu.



Alipofika nyumbani kwa Jitu, akamshukuru Mungu kwani alikuta ndiyo kwanza mtu mwenyewe ameamka. Alikuwa nje akisafisha meno.



Teksi iliposimama na Abdul kuteremka, Jitu aliduwaa. Akamtazama Abdul huku povu likiwa mdomoni na akasita kuendelea kufanya kile alichokuwa akikifanya.



“Jitu!” Abdul alibwata kwa sauti ya kilevi.



“Abdul!” Jitu naye akabwata kwa mshangao, sauti yake pia ikiwa na kijimkwaruzo cha mbali ilhali macho yakiwa yanaonyesha kuwa hajapata usingizi wa kutosha usiku.



“Karibu….dah….siamini…” Jitu aliendelea kushangaa na sasa harakaharaka akasafisha kinywa na kusukutua kwa maji kisha akamkaribisha ndani Abdul.



“Nadhani ujio wako una jambo, msh’kaji wangu maana’ake si kawaida yako,” Jitu alisema wakati wameketi chumbani kwenye sofa kubwa.



Jitu alikuwa amepanga chumba kikubwa na akakisheheneza samani za kisasa. Namna alivyoweza kufanikisha maisha yake yawe mazuri ni wachache sana waliojua, mmojawao akiwa huyu Abdul.



Zilimchukua dakika takriban kumi Abdul kumsimulia Jitu kuhusu kiini cha kumleta hapo asubuhi hiyo. Akamwambia kuwa baada ya Mzee Malick kufariki kuna watu wajanja wamejiingiza kwenye kugawana mali ilhali dada yake Sharifa ndiye mwenye haki zaidi.



“Huo ni uonevu, msh’kaji,” mwishoni Abdul alifafanua. “Sista ndiye aliyekuwa mke wa ndoa, lakini leo eti amenyimwa kila kitu na badala yake wanataka kumpa huyo kikaragosi waliyemwokota sijui huko Arusha….inakuingia akilini kweli?”



“Ni u…(Jitu akatamka tusi zito) haiwezekani. Kwa hiyo unaniambiaje?”



“Nataka watutambue msh’kaji wangu,” Abdul alisema kwa kusisitiza. “Lazima watupe umateumate wa kueleweka, mwanangu.”



“Kama kiasi gani?”



“Kitu kama hamsini hivi.”



“Milioni hamsini?”



“Nd’o maana’ake. Tupate pesa hizo tujue cha kufanya.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwa hiyo inakuwaje?”



Abdul aliwasha tena sigara nyingine kisha akasema, “Nataka atekwe yule kijibwa aliyeletwa kutwaa urithi.”



Ni hapo ndipo mjadala ulipoibuka. Wakazungumza kwa kirefu na kufikia mwafaka kuwa Jitu na mwenzake, Damian wamteke Ablah ndani ya wiki moja kuanzia siku hiyo.



“Hapo sasa tuzungumzie umateumate,” Jitu alimwambia. “Umejiandaa vipi?”



“Sema wewe.”



“Fanya emu tatu.”



“Kwani mko wangapi?”



“Wawili tu. Mimi na msh’kaji wangu mmoja, humjui.”



“Ok, tufanye mbili.”



“Nina sababu yangu ya kukwambia andaa tatu tufanye kazi,” Jitu alisisitiza. “Unazungumzia ishu nzito Abdul, s’o mchezo. Kama vipi achana nayo.”



Abdul alifikiri kidogo kisha akasema, “Nipe muda nishughulikie suala hilo. Baada ya nusu saa tuwasiliane.”



“Nipe namba yako,” Jitu alimwambia.



Abdul akampa namba za mitandao miwili ya simu.



*****



ABDUL alimpigia simu dada yake na kumweleza kuhusu maongezi kati yake na Jitu. Sharifa akamuuliza, “Kwa nini hukumpa hizo milioni mbili? Si una pesa hapo?”



Abdul alicheka kisha akasema, “Sista hii ni pesa ya kunilinda siyo ya kazi. Hayo mamilioni yote bado nataka nichomoe hapa kwenye vijisenti hivi!”









“Ok, wanasema wataifanya kazi hiyo lini?”



“Ndani ya wiki moja tu.”



“Kwa hiyo tuwape pesa bila ya kujua kwamba kazi itafanyika kwa ufanisi?”



“Hatuwapi zote. Tunatoa advansi.”



“Ngapi?”



Ukimya ukapita kidogo kisha Abdul akajibu, “Tufanye moja unusu.”



Ukimya ukapita tena kisha Sharifa akaibuka, “Ok, tuonane jioni. Nitakuja saa kumi.”



Jioni, kitu kama saa 12 Sharifa alikuwa akiegesha gari nje ya gesti ya Madina. Muda mfupi baadaye alikuwa na Abdul chumbani.



Alimkuta Abdul akiwa ameketi sofani, chupa ya whisky ikiwa mezani, sigara mkononi, akiendelea kuiliwaza akili yake.



“N’ambie,” Sharifa alimwambia.



“Nd’o kama nilivyokwambia. Wash’kaji wanataka mshiko wafanye kazi.”



“Unawaamini vipi hao watu wako?”



“Sista ni wewe nd’o unapaswa kuniamini mimi, kwa sababu ni mimi ndiye niliyeingia mkataba na hao wash’kaji. Kuhusu mimi kuwaamini au kutowaamini, hilo lisikutie mchecheto. Siwezi kuzungumzia ishu nzito kama hiyo na watu nisiowajua.”



Sharifa alionekana kuwaza. Alikuwa na shaka kuhusu kufanya mpango mzito unaoweza kugharimu maisha ya mtu, na je kama ikitokea kutoelewana katikati ya mpango huo? Je, mambo yakiharibika na yeye akabainika kuwa ndiye aliyeusuka, atanusurika na kifungo?



Kwa kiasi fulani woga ulimwingia, lakini bado hakuwa radhi kuliachia suala hilo. Kitu fulani kilimwonya kuwa baada ya muda si mrefu atatimuliwa ndani ya nyumba hiyo ya marehemu Malick Sikonge. Na kitendo cha kukabidhiwa zile pesa, shilingi milioni 50 ilikuwa ni kama kupewa mafao ya kustaafu kazi. Ni kama alipewa ‘mkono wa kwa heri.’



Ni wazo hilo lililomrejeshea ile roho yake ya kutohofia chochote. Akayakumbuka maneno ya huyu kaka yake kuwa hii ndiyo karata yake ya mwisho, aicheze kwa umakini.



Akamtazama Abdul kwa jicho kali kisha akasema, “Sikia Abdul. Ongea nao leo hii, uwaambie tunawapa advansi, milioni moja na nusu. Lakini wakati huohuo wakwambie wanatarajia kufanyaje mpango wao na lini watakuwa wamekamilisha kazi. Na lazima uwatie mkwara kuwa wasijaribu kuingia mitini na pesa yetu.”







“Kwa hilo us’konde, sista,” Abdul alisema kwa kujiamini. “Nitalisimamaia vizuri tu suala hili. Usihofu. Kwa hiyo inakuwaje? Lini mzigo huo unanipa?”



“Kesho asubuhi nitakuja. Tufanye sasa nne hivi.”



“Poa.”



*****

SAA mbili usiku Jitu alikuwa ndani ya kijibaa kidogo eneo la Kawe Mzimuni ikiwa ni ni mitaa miwili tu kutoka kwake. Kando yake alikuwepo mwanamke aliyekuwa amekolewa na kilevi lakini akionekana kutopoteza mhimili wake. Aliposimama na kuelekea maliwatoni, hakuyumba. Alitembea kikakamavu. Na hata alipozungumza hakuwa na sauti iliyoonesha kuwa kazidiwa na kinywaji.



Aliitwa Maimuna. Alizaliwa Kinondoni Shamba na akakulia Kinondoni Shamba hadi sasa alipotimiza umri wa miaka 24. Elimu, kwake ilikuwa ni kero fulani isiyovumilika. Alipomaliza darasa la saba hakukubaliana na wazazi wake walipotaka kumpeleka katika shule ya sekondari ya kulipia. Alikataa katakata!



Alitaka kuwa huru ajifanyie mambo yake na kujipatia pesa za haraka. Hivyo alianza kwenda kando ya Barabara ya Tunisia jirani na viwanja vya Leaders Club usiku ambako alijinadi kwa wanaume waliofika katika maeneo hayo wakifuata machangudoa.



Umbo lake zuri na sura yake ya ujana zaidi, vilikuwa vivutio mbele ya wakware walikuwa wakizuru eneo hilo usiku.





Miezi sita ya awali ilipokamilika akawa ameyazoea maisha hayo. Kumchojolea mlevi, anukaye mdomo au mtu anukaye jasho, sasa ilikuwa ni sehemu ya maisha yake ya kawaida.



Alizoea!



Siku moja alijiwa na mteja mpya kabisa tofauti na wale waliokuwa wakiibika na kutokomea kila baada ya siku tatu, nne, wiki au mwezi.



Huyu alikuja na teksi na kuegesha kwenye kundi la wanawake watatu waliokuwa kando ya barabara hiyo. Wote wakaikimbilia teksi hiyo. Mteja akawatazama jinsi walivyojinadi kwa maneno haya na yale, lakini yeye akavutiwa sana na huyu Maimuna. Akaondoka naye.



Aliyoyapata kwa Maimuna usiku huo yalimfanya kesho yake amfuate tena. Hatimaye akawa amemfanya kama mke. Kila anapojisikia anampigia simu, Maimuna anamfuata.



Wakawa wanakutana popote na siku ambazo mifuko ya Jitu huwa imenona, walikuwa wakienda kwenye kumbi za starehe ambako walikunywa na kula kabla ya kwenda nyumbani kwa Jitu ambako waliumaliza usiku wakiitotesha jasho miili yao.



Pamoja na ujanja wake wote, Jitu alijikuta akikwama kwa Maimuna. Ndiyo, Maimuna alijua mengi, alijua yote na alikuwa tayari kuyafanya yote wakati wowote.



Usiku huu alikuwa amemwita Maimuna baada ya kugundua kuwa kuna suala la kutengeneza pesa kutoka kwa Abdul, hivyo akiba aliyokuwa nayo hakuona kuwa inaweza kuleta madhara kama ataitumia na huyu mwanamke wa shoka, mwanamke mtundu kupindukia. Ndiyo, aliamua usiku huu aukonge tena moyo na kuupa zoezi mwili wake pale kitanda kitakapowalaki.



Tayari alikuwa na bia tatu kichwani, ilhali Maimuna alikuwa na mbili. Hawakuwa na dalili ya kuondoka, ndiyo kwanza vichwa vilikuwa vimeanza kuchangamka hivyo, walitaka kuendelea na kuendelea.



Kwenye kona hii waliyokaa, hakukuwa na mwangaza mkali bali kivuli kizito kilichotengeneza kijigiza walichokihitaji. Hawakuwa na majirani. Meza nyingine tatu zilizokuwa jirani nao hazikuwa na wateja. Ni hapo ndipo Maimuna alipoamua kukosa adabu, akawa akimpapasa Jitu hapa na pale kwa uhuru, vituko ambavyo kwa Jitu ilikuwa ni burudani aliyoihitaji.



Vidole laini vilitambaa kifuani kwa Jitu, vikashuka hadi tumboni, mara vikagota kwenye lisani ya suruali ambako vilihangaika kidogo kabla ya kufanikiwa kupenya ndani zaidi na kuendelea kufanya kile kilichostahili kufanywa.



Vinywa vikakutana. Ndimi zikapambana, kila mmoja akaifaidi ladha ya mate ya mwenzake. Pumzi zikawapanda na kuwashuka huku sasa Maimuna naye akitanua miguu na kuuruhusu mkono wa Jitu upenye katikati ya mipaja ile mikubwa na kugota pale alipopakusudia…mwanamume ‘akasachi mtandao.’



Mara simu ya Jitu ikaita. Jitu akaitoa na kuitazama kwenye kioo. Jina la Abdul lilikuwa likielea. Papohapo Jitu akabonyeza kitufe na kuitega sikioni.



“Mheshimiwa.”



“Uko wapi mkuu?” Abdul aliuliza simuni.

“Kawe. N’ambie.”



“Nataka tuonane.”



“Vipi, kimejibu? Uko poa?”



“Yeah. Nataka tuzungumze.”



“Uko wapi?”



“Kinondoni.”



“Kama uko njema, basi njoo pale Salamander Pub, Mwenge tuzungumze. Unapajua.”



“Mimi nikose kupajua Salamander? We’ vipi msh’kaji wangu? Kwa hiyo baada ya muda gani?”



“Fanya ndani ya nusu saa tuwe pale.”



“Poa.”







Simu hii iliivuruga ratiba ya Jitu. Papohapo akanywa bia kwa kasi kisha akaitua chupa mezani na kumgeukiaMaimuna. “Nina dharura baby, “ alimwambia.



“Hee…yamekuwa hayo tena?”



“Usijali. Inanilazimu kutii wito huu ili baadaye tufurahie maisha” Jitu alisema na kumbusu shavuni.



“Kwa hiyo inakuwaje?”



Jitu aliingiza mkono mfukoni na kuchomoa noti mbili za shilingi elfu kumi kumi na kumpatia. “Endelea kupata. Sidhani kama nitachelewa. Kwani una haraka ya kwenda viwanja?”



“Kama huna mpango na mimi leo nitakwenda.”



Jitu alifikiri kidogo kasha akasema, “Nipe nusu saa hivi, nitakupigia simu tuzungumze. Kwa muda huo nitakuwa nimeshajua kama itakuwa ngumu kurudi au vipi.”



“Poa.”

Dakika tano baadaye, Jitu alikuwa kwenye bodaboda iliyokwenda kasi wakielekea Mwenge. Na alipofika Salamander Pub akamkuta Abdul kama kawaida yake; sigara mkononi, glasi ya kinywaji ikiwa mezani.

“Yap, nambie,” ilikuwa ni kauli ya kwanza kutoka kinywani mwa Jitu mara tu alipovuta kiti na kuketi.



“Taratibu,” Abdul alisema kwa majivuno, huku akipuliza moshi angani.

“Unatumia kinywaji gani?”



Jitu alimkumbuka Maimuna papohapo. Akawaza kama ataanza kunywa bia tena hapo, kwa vyovyote muda utakwenda zaidi na hapo atalazimika kumruhusu Maimuna aende kwenye mawindo yake ya wanaume.



Hata hivyo alitambua kuwa suala alilokuja kulizungumzia hapo ni nyeti na lenye manufaa kwake kwa mapato. Hivyo, hakujali kuhusu Maimuna. Kipi bora,viuno vya Maimuna au pesa?



Akajikuta akipata jibu la PESA KWANZA. Ndiyo, pesa zilipaswa kuchukua hatamundipo mapenzi yatafuata. Lakini alimhitaji sana Maimuna kwa leo. Mambo yake makubwa kitandani! Anajua kila kitu na yuko tayari kufanya kila kitu. Siyo mwanadamu wa kawaida japo machoni mwa watu alionekana ni mwanadamu wa kawaida mwenye umbo la kawaida na sura ya kawaida akizungumza na watu wengine kama kawaida.



Akaamua kuwa hadi dakika zile alizomwahidi Maimuna zitakapotimu, atajua ni kipi cha kumwambia. Kama ataondoka hapo na dau basi lazima ambembeleze na kumwahidi dau zaidi.



Mhudumu alikuwa kando yao. Jitu akamwambia, “Tusker baridi.”



Mhudumu alipoondoka, Jitu akamgeukia Abdul.“Enhe, nambie.”



“Uko tayari kikazi?”



“Yeah, mkwanja kama upo. Naingia kazini.”



“Ok, tukubaliane advansi.”



“Tenga milioni mbili tupeane majukumu.”



Jitu alisema na kusita baada ya kumwona mhudumu akiwa kando yao na chupa ya bia. Chupa ilipofunguliwa na mhudumu huyo kuondoka, Jitu akamalizia, “Umenisoma mkuu?”



“Usikonde. Kuna moja u nusu kama advansi.”



‘Unazo hapa?”



“No keshosaa 4 tuonane nikupe. Lakini nataka uhakikisho, mtaifanya kazi hii lini? Na unanithibitishia vipi kuwa hakutatokea kushindwa? Na mkifeli itakuwaje?”





Jitu aliipeleka chupa ya bia kinywani, akanywa mafunda mazito ya bia kisha akaitua mezani. Akaachia tabasamu la dhihaka. “Nadhani hiyo ni dharau sasa Abdul. Unakuwa kama hunijui!”



“No! Jitu lazima tuwe tunaangalia pande zote. Suala la kujuana ni jingine.”



“Mi nadhani ukubali kuwa hakuna kitakachoshindikana. Kama una wasiwasi sana basi ishu ife,” Jitu alisema huku kakunja uso.



“Ishu haiwezi kufa, Jitu.”



“Ok, zungumza kama mwamaume. Ili kesho niamini kuwa dili linaendelea, n’katie kitu kidogo cha kueleweka kwanza, halafu kesho muda huo unaosema tuonane.”



“Kama ngapi?”



“Laki mbili za kuumalizia usiku. Kuna mtu wangu nimemwacha huko nikaja kukusikiliza. Hatuna haja ya kukaa sana.”



Abdul alifungua pochi na kutoa shilingi 150,000. Akampatia huku akisema, “Zikulinde.”



Jitu alizipokea na kuzihesabu haraka haraka kisha akauliza, “Kwa hiyo inakuwaje?”



“Nikishakuwa poa nitakupigia. Lakini sidhani kama itazidi saa 5 mchana.”



“Ok, sasa hapo kuna jambo linalobidi ujipange nalo.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

‘Lipi tena?”



“Ukishakuwa kamili na unataka tukutane, hakikisha unakuja na namba yake ya simu, ratiba yake ya kila siku, kama unawajua marafiki zake pia niambie. Unaweza kuipata picha yake?”



“Dah…inakuwa ngumu sidhani labda nimwambie mtu ampige picha fasta kwas imu.”



‘Yeah kama simu ni ya ukweli unaweza kupata picha yake nzuri sana.”



“Poa, tutacheki kesho.”



Jitu aliondoka hapo akiwa na kiburi. Pesa alizopewa na Abdul na mkakati waliouweka ulionyesha kuwa kesho kutakuwa na pesa nyingine, kulimfanya ajisikie mzito kimfuko na kimwili. Akajiona yu mwanamume kati ya wanaume. Hakuchelewa, akaivaa bodaboda na kuondoka.

Njiani akapiga simu kwa Maimuna na kumtaka amsubiri palepale alipomwacha.



“Uko vizuri?”



“Si unanijua. Leo hakuna kwenda viwanja baby.”



Maimuna akacheka kimbea na kudakia,”Haya bwana wee…utashindwa mwenyewe.”



“Si ni kama kweli nitashindwa.”



“Tutaona.”







********

SHILINGI 150, 000 kibindoni, kwa Jitu aliona kuwa mambo yanamwendea vizuri. Akacheka kimoyomoyo wakati pikipiki aliyopanda ilipokuwa ikiegeshwa pale alipomwacha Maimuna.



Kama ana pesa za ziada muda huo na ana miadi ya kupata pesa zaidi za kutakata kesho, kwa nini asiyafurahie maisha? Huu usiku ulikuwa mzuri kwake.



Akamkuta Maimuna akiwa palepale alipomwacha na sasa alikuwa amekwishaongeza bia mbili.



“Baby…” Jitu alimvaa na kumbusu shavuni.



“Bwana nini?” Maimuna akasema kidekodeko.



“Nimerudi…n’ambie baby.”



“Nikwambie nini?” Maimuna aliendeleza kudeka. “Wewe tu. Ushndwe mwenyewe.”



Pamoja na kuendelea kufaidi vinywaji, hata hivyo Jitu alikuwa makini akihakikisha hapotezi kumbukumbu ya aliyokwishayafanya na aliyopanga kuyatekeleza.



Akaitwaa simu na kubofya kidogo kisha akaitega sikioni.

Ikapokelewa na Kevin.



“Uko wapi mkuu?” Jitu alimuuliza.



“Kama kawaida, niko na shemeji yako. Vipi, kinaeleweka?”



“Kiasi fulani. Nimeshaonana na yule bwege mwenye kazi yake.”



“Enhe?”



“Kasema kesho analeta advansi.”



“Ngapi?”



“Moja unusu.”



“Na anataka kazi ikamilike lini?”



“Hatujakubaliana kuhusu hilo. Akishatoa advansi nd’o tutazungumza.”



“Kwa hiyo?”



Kesho asubuhi nitakuatana nae na nd’o nitajua kinachoendelea.”



“Poa.”



********



USIKU huo Sharifa alipata usingizi wa mang’amung’amu. Hakuamini kuwa mpango wake unaweza kufanikiwa kama walivyojipanga. Alijiuliza kuhusu hao watu wanaotarajiwa kutumika katika mpango huo. Hawawezi kutoa siri?



Wasiwasi huo ulimfanya ajikute akiambua usingizi alfajiri na kushtuka mapema saa 1. Akaingia bafuni kuoga kisha akaketi mezani ambako alikuta tayari wafanyakazi walikuwa wamekwishaweka stafutahi kwa ajili ya yeyote atakayewahi kuamka.



Akajihudumia kiasi chake na baada ya kutosheka alirudi chumbani mwake ambako alichukua muda kuchagua nguo ya kuvaa. Hakutaka kuvaa nguo yoyote ya kifahari. Aliamua kutinga fulana nyeupe na suruali ya jeans iliyomkamata vilivyo maungoni mwake.



Akaitwaa miwani ya jua ambayo haikuyaficha sana macho yake, akaiweka machoni kisha akasimama mbele ya kioo kikubwa kilichokuwa humo chumbani mwake. Akatabasamu kwa kujiona kuwa amekuwa ni mwanamke mzuri mbele ya kijana yeyote wa kiume pale atakapopita mitaani, na ataonekana kuwa ni mwanamke wa kawaida anayeishi maisha ya kawaida ila tu pesa hazimpigi chenga.



Hakuwa na haraka ya kuondoka. Akaketi katika sofa lililokuwa humo chumbani mwake na kuwasha televisheni. Akawa akiangalia stesheni moja iliyokuwa ikipiga muziki mfululizo.



Dakika ya kwanza akawa amezama katika wimbo uliokuwa hewani. Dakika ya pili mawazo hayakuwa hapo kwenye televisheni tena.



Miadi kati yake na kaka yake, Abdul ilimuumiza kichwa. Alijua kuwa ilimpasa kuwahi kuchukua pesa benki kisha aende kumkabidhi Abdul. Lakini alisita kumpa kaka yake pesa bila ya kuwa na hakika kuwa zitawafikia walengwa kwa kiwango halisi. Alimfahamu vizuri Abdul, kuwa ni mpenda pesa kuliko pesa zinavyompenda.



Hatamzidi ujanja? Akajikuta akicheka peke yake na kuamua kuwa bega kwa bega na Abdul hata wakati wa kukabidhi hizo pesa kwa walengwa. Japo hakupenda kuionyesha sura yake kwa hao watu watakaopewa tenda ya kufanya kazi nzito, hata hivyo sasa aliamua kuwa liwalo na liwe; atakutana nao na uso kwa uso awafahamu.



Wakati akijiandaa kuondoka, mara simu yake ikaita. Akaishika na kuitazama. Jina la Abdul lilikuwa likielea kwenye skrini. Akabonyeza kitufe na kuitega sikioni. “N’ambie,” likamtoka kwa mapozi.



“Jana nimefikia mwafaka na msh’kaji. Leo atakuja saa nne au tano ili tumalizane,” Jitu alisema simuni.



“Tukutane wapi? Au hapohapo maskani kwako?”





“Unaweza kuja hapahapa maskani lakini sitaki wale watu wajue kuwa niko hapa. Si nilikwishakwambia!”



Ukimya mfupi ukapita kisha Sharifa akawa hewani tena. “Sikia Abdul. Sema tukutane wapi, na tuwe pamoja wakati wa kupeana majukumu na hao jamaa zako.”



Abdul akajibu, “Kuna ki-pub fulani cha kish’kaji pale ‘Kwa Manyanya, kinaitwa Wasela Camp, mbele kidogo ya kituo cha cha daldala Kinondoni A. kama unakwenda town. Ukikata Mtaa wa Wibu, kulia utakiona. Ki-pub hicho huwa kinapiga kazii saa ishirini na nne. Njoo hapo. Mida hii huwa hakuna wateja. Njoo pale na mimi nitamwambia msh’kaji yule tukutane pale. Yeye anapajua.”



“Ok.”



Sharifa alikata simu na kunyanyuka. Akatwaa pochi lake kubwa na kufungua. Akapekua na kuiona kadi ya benki. Lakini akajua kuwa hiyo kadi isingemsaidia kutoa kiasi kikubwa cha pesa zaidi ya shilingi milioni moja.



Hivyo aliondoka akitambua kuwa atalazimikka kwenda kuchukua pesa dirishani.



Saa 3 alikuwa ndani ya gari akielekea Kinondoni katika benki moja aliyokuwa na akaunti hapo. Saa 4 alikuwa ameshatoka hapo benki na shilingi milioni 3 ndani ya lile pochi lake. Sasa akawa anakwenda kwa Abdul. Akiwa njiani alimpigia simu na kumtaarifu kuwa yuko kamili. Abdul naye akampigia simu Jitu na kumtaka ahakikishe anatimiza miadi kwa kujali muda.



*******

SHARIFA aliingia Wasela Camp saa 4.30 asubuhi. Alipoegesha gari hakutoka. Akapiga simu kwanza kwa Abdul na ilipopokewa, akamwahi, “Umo ndani?”



“Yeah. Kama umeshatia tim njoo. Niko peke yangu. Msh’kaji yuko njiani.”



Sharifa alivaa miwani ya jua usoni na kuteremka. Hakupenda kila mtu ajue kuwa ni yeye na zaidi hakupenda kutambulika kuwa kaja hapo.



Akaingia ndani ya kijibaa hicho na kukumbana na ubaridi mkali uliotokana na kiyoyozi kilichogandishwa ukutani.

Alimkuta Abdul tayari akiwa na glasi yenye toti kadhaa za whisky na kama kawaida sigara ikiteketea mdomoni.



Sharifa alipoketi mara mhudumu akamjia. “Soda. Fanta orange.”



Mhudumu alipoondoka Sharifa akamrudia Abdul. “Umeshaanza mapema hivi, jioni utaiona kweli?”



Abdul akacheka. “Hata nilipokuwa majuu nilikuwa naanza mida kama hii na wakati mwingine kabla ya muda huu.”



Mara simu ya Abdul ikaita. Akaitwaa na kuitega sikioni. Akasikiliza kidogo kisha akasema, “Tupo ndani, ingia.”



Dakika iliyofuata, pandikizi la mwanamume, akiwa amevaa shati la miraba na suruali ya jeans aliingia humo ndani na moja kwa moja akawafuata Abdul na dada yake mezani.



Sharifa hakuhitaji kujiuliza mara mbili kuwa huyu mtu ni wa aina gani. Tembea yake na mwili wake vilitosha kuonesha kuwa ni mkakamavu. Isitoshe haya macho yake yalikuwa yakimweka katika daraja la pekee, daraja la watu amabao huwa wako tayari kufanya lolote, wakati wowote na dhidi ya mtu yeyote kama itakuwa ni kwa masilahi yake.



Huyo ndiye Jitu, ambaye Abdul alimtegemea na katika kufanya kazi itakayowapatia mamilioni ya pesa kabla ya kuachana na familia ya Ablah na Karim.



Sharifa alishusha pumzi ndefu na kuamini kuwa Jitu amempata mtu wa kazi.



Na hata alipotabasamu wakati akipeana mikono na Abdul na Sharifa, tabasamu lake lilizidi kumdhihirishia kuwa huyu sio mtu wa masihara. Hata kiganja chake kikubwa kilipomshika mkono, Sharifa alihisi kashikwa na mkono wa chuma.



Kama Abdul, Jitu naye alipoketi aliagiza kinywaji kikali; toti tatu na alipokwishapiga funda dogo, alimwambia Sharifa, “Samahani sista, akili yangu huwa haifanyi kazi mpaka nishtue kwa fegi.”



“Usijali. Vuta tu.”



Dakika tano baadaye ndipo Abdul alipokata mzizi wa fitina.

“Jitu,” alisema. “Huyu ndiye sista wangu. Tuko pamoja kwa ile ishu.”



Jitu alitikisa kichwa akiashiria kukubali. Kisha akasema, “Nimekusoma. Kwa hiyo inakuwaje?”



“Tuko hapa kamili.”



“Kikazi zaidi!” Jitu alikazia.

“Nd’o maanake!”



“Ok, bado nataka msaada wenu.”



“Kama?”



“Nataka kujua ukaribu mlionao,” Jitu alisema huku akimkazia macho Sharifa. “Nina maana yule mdada huwa kuna wakati mnatembea wote au mnajua ratiba zake za kila siku?”



Sharifa alikunja uso kidogo kisha akajibu, “Huwa sio mtu wa kutembea-tembea. Lakini mimi huwa ninakwenda naye mara chache ‘beach’ au kule mjini kama Steers kunywa juisi na kupiga stori.”



“Unaweza kwenda naye tena huko leo au kesho?” Jitu aliuliza tena.



“Inategemeana kama nikimsuka akakubali.”



“Poa. Ninapenda tumkute nje ya mazingira ya home kwenu. Kwa hiyo, kama unaweza niachie mkwanja wetu, halafu fanya mkakati umtoe kidogo. Mtoto wa mjini kama wewe huwezi kushindwa kumdanganya mtoto wa shamba aliyetoka hukou Umasaini. Mpige maneno kuwa unataka mwende hata kule Mlimani City kucheki bidhaa f’lani halafu unitonye. Tutakuja fasta kukamilisha kazi. Umenisoma?”



Sharifa alikunja uso kidogo kisha akamgeukia kaka yake na kuwa kama anamwambia yeye. “Itawezekana lakini sina uhakika kuhusu ratiba yake ya leo. Anaweza kunitolea nje na kunipa ratiba ya siku nyingine.”



“Siyo mbaya,” Jitu alisema huku akitwaa glasi na kunywa toti zote za kinywaji chake kisha akaitua glasi mezani. Akakunja uso na kuvuta mkupuo mkubwa wa sigar na akaendelea, “Mambo mazuri hayataki haraka. Tujiwekee malengo kuwa ndani ya siku tatu uwe umeshamtoa kule ngomeni na kuingia naye mitaani kisha unani-call. Kumteka mkiwa nje ya nyumbani ni bora zaidi kuliko kuja huko kwenu Masaki.”



Walizungumza na kuzungumza, wakapanga ya kupangika hatimaye mkoba ulifunguliwa, Jitu akakabidhiwa shilingi milioni moja na nusu na kukubaliana kuwa awe tayari muda wowote kuanzia siku hiyo jioni hadi kesho yake jioni kwa kazi iliyomfanya akabidhiwe kitita hicho.



“Labda mimi nisiwe Sharifa,” sauti ya majigambo na kiburi cha kilo mia moja sanjari na macho ya kujiamini kupita kiasi vilitoa taswira ya dhamira ya utekelezaji wa kazi iliyo mbele yao.





******



USIKU huu, saa tatu kasoro dakika kadhaa, Sharifa alikuwa sebuleni na Karim naAblah wakitazama televisheni huku wakinywa juisi. Maongezi yalishamiri, wakizungumzia siasa, kuhusu migogoro inavyovisakama vyama mbalimbali sekeseke la Katiba mpya. Ablah na Karim walionekana kuzungumzia sana mada hiyo tofauti na Sharifa ambaye yeye kwake siasa ulikuwa ni mchezo mchafu usiostahili kuchezwa na wala hakuelewa ni kwa nini kuna siasa duniani.



Karim alikuwa akikitetea chama tawala, akidai kuwa migogoro yake humalizwa kidiplomasia zaidi na mambo huwa shwari haraka tofauti na vyama vingine. Pia alitetea sera ya chama hicho tawala kuhusu Katiba inayopendekezwa.



Ablah hakukubaliana naye, yeye alikitetea chama fulani cha upinzani. Alikuwa akidai kuwa chama tawala kimehodhi rasilimali za umma na kujitwalia viwanja vingi na kujenga majengo mengi yanayogeuzwa vitegauchumi ilhali ni fedha za wananchi walalahoi ndizo zilizotumika. Kuhusu Katiba inayopendekezwa, yeye alidai hajui chochote hivyo katiba yoyote itakayopitishwa kwake ni sawa tu.



Labda hoja hiyo ingeendelea zaidi kama Sharifa asingeikatiza.

“Ablah, kesho una ratiba gani?” alimuuliza.



Ablah alisita kidogo kisha akasema, “Kesho sijajipanga. Kwani vipi?”



Sharifa aliinua uso na kutazama darini kisha akakunja uso kimadaha-madaha. “Nilitaka kesho unisindikize Mlimani City kwenye shoping.”



“Saa ngapi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Jioni. Kitu kama saa kumi hivi.”



“Shoping jioni? Kwa nini isiwe asubuhi?”



Sharifa alifikiri kidogo kisha akajibu, “Asubuhi kuna ishu f’lani nitakuwa naishughulikia. Mizunguko ya asubuhi ni mingi. Jioni nd’o nina nafasi.”



Ablah alifikiri kidogo kisha akajibu, “Poa. Hakuna tabu mama.”



“Ok, mi’ nakwenda kupumzika. Leo najisikia uchovu sana,” Sharifa alisema huku akinyanyuka sofani na kuelekea chumbani, akiwaacha Ablah na Karim ambao sasa waliiua hoja ya siasa na badala yake Karim akaweka kanda moja ya filamu ya mikasa ya mapenzi.



Kwa kuwa wote walikuwa wapenzi wa filamu, walijikuta wakiitazama kanda hiyo ya Kimarekani hadi picha ilipofika mwisho ikiwa ni baada ya saa moja na nusu tangu walipobaki peke yao. Hatimaye kila mmoja alikwenda chumbani kwake kulala.



*****

SI kweli kwamba Sharifa alikuwa na usingizi au uchovu, bali alihitaji kupata muda zaidi wa kupanga mpango wake kikamilifu na Jitu na Abdul. Alipaswa kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda vizuri ili kuepuka hatari inayoweza kumkuta endapo mpango huo utaharibika na siri kuvuja.



Hivyo, alipoingia chumbani, kitu cha kwanza kufanya ilikuwa ni kushughulika na simu yake, akipekua jina la kaka yake, Abdul. Hatimaye alipolipata alipiga. Muda mfupi baadaye akasikia simu ikipokewa katika sehemu iliyosheheni kelele.



‘Yuko baa…’ Sharifa alisema huku kakunja uso. Hatimaye akaisikia sauti yenye mkoromo wa wastani, “Haloo.”



“Abdul… uko baa?”



“Sista, vipi kwani?”



“Nakuuliza uko baa unalewa? Mbona kelele sana?”



“Usijali, subiri dakika mbili, nitakupigia.”



Simu ikakatwa.



Baada ya muda mfupi simu ikapigwa tena, safari hii Sharifa alipoipokea alisikia utulivu mkubwa.



“N’ambie sista.” Alikuwa Abdul.



“Hivi wewe bado unaendekeza ulevi tu wakati unaona sasa tumeingia kwenye mfumo mpya wa maisha?” Sharifa alifoka simuni ingawa kwa huko chumbani kwake isingekuwa rahisi kwa mtu wa nje kumsikia.



“Huuoni uzito wa jukumu lililo mbele yetu? Kwa nini hukui? Unakuwa kama kinda kila siku! Hubadiliki!”



“Sista, mbona unakuwa mkali?” Abdul aliuliza kwa upole, sauti yake ya kilevi ikidhihirika hata masikioni mwa Sharifa. “Kwani kuna kipi nimeharibu? Hapa nina mzinga wangu wa pili tu wa Konyagi. Na nikimaliza hapa nasepa zangu maskani. Niko tu freshi mbona…sista wala usiingie mchecheto kuhusu ile ishu. Vipi kuna jipya?”



Sharifa alisonya kisha akasema, “Sikia. Kama kweli uko fresh, wasiliana na yule bwege, mwambie anipigie tuongee sasa hivi, ili kama inawezekana kesho akamilishe kazi. Umenisoma?”



“Hakuna noma sista,”Abdul alijibu kwa kunyenyekea japo mkoromo wa kilevi ukiwa palepale.



******



“TULIA…huuwezi muziki wangu wewe…ngoja nikupe kitu halisi…nataka usiwafuate machangu wengine….hapa umefika…” mwanamke huyu aliyekuwa na Jitu alisema kwa namna ya kujiamini.



Jitu alikuwa akihemea juu-juu, akawa akimwachia mwanamke huyu ajitume kwa namna alivyoona inafaa. Maimuna naye katika kuhakikisha anadhihirisha kuwa yu mtaalamu zaidi katika fani, alitumia ujuzi na wepesi wake wa viungo kufanya kile kilichomtoa macho pima Jitu.



Kitu kilichomfanya Jitu awe akimfuata huyu mwanamke kila alipokuwa na hamu ya kufanya mapenzi ni hivi vimbwanga vyake. Alikuwa tayari kumridhisha mwanamume kwa namna yoyote aitakayo. Hakujali kufanya chochote kwa kutumia sehemu yoyote ya mwili wake. Na kwa usiku huu, akiwa amekabidhiwa shilingi laki moja, aliamua kuifanya kila kitu katika kumpagawisha Jitu.



“Maimuna…” kuna wakati Jitu aliita.



Maimuna hakuitika.



“Mai…Mai…utaniua baby…” mwanamume alibwabwaja.



Ilikuwa ni kama kumtia hamasa Maimuna. Mwili wake teketeke ulikuwa ukijikunja na kujikunjua kwa ufundi wa aina yake, akihakikisha anailipia laki iliyoingia mkobani mwake muda mfupi uliopita —







Aliondoka alfajiri, akimwacha Jitu hoi. Hata hivyo, kisaikolojia Jitu alikuwa vizuri; hakuwa na wasiwasi, milioni moja na ushei zilimtia kiburi.



Saa mbili kasoro ndipo Jitu alijitoa kitandani, akiwa amezinduka baada ya kuuchapa usingizi kwa mara nyingine baada ya Maimuna kuondoka.



Akafikicha macho na kuitwaa simu iliyokuwa kando yake katika kitanda hicho kipana. Akakuta ‘missed call’ tatu. Hakuweza kusikia wakati simu zilipopigwa kwa kuwa alikuwa ameondoa mlio. Haikuwa kawaida yake kufanya hivyo bali alfajiri ya siku hii alifanya hivyo kwa ajili ya kupata wasaa na utulivu wa kusinzia baada ya mshikemshike uliopita usiku.



Akakuta kumbe aliyekuwa akimpigia mara nyingi alikuwa ni Kelvin, rafikiye ambaye jana alimwambia kuhusu mpango wa kujipatia shilingi milioni tatu. Mwingine aliyempigia alikuwa ni Abdul. Na wote hao walimpigia katika kipindi alichoamini kuwa alikuwa amedhibitiwa na Maimuna.



Akafikiri aanze kumpigia nani? Baada ya muda mfupi akaamua kumpigia Kelvin.



“Vipi mkuu?” Kelvin alipokea haraka.



“Poa. Mambo vipi?”



“Nakusikiliza wewe,” Kelvin alijibu na kuongeza, “ile ishu imefikia wapi?”



“Iko pazuri. Kama unaweza njoo tuzungumze.”



“Nije kuzungumza?”



“Nd’o maanake. Usiwe na akili-mbuzi. Kwani unafikiri naweza kukwambia nikutoe huko bushi kwako Kunduchi na kuja hapa kupiga ndumu? We vipi?”



“Ok, nakuja.”



*******



KELVIN alikuwa akiishi Kunduchi. Hakuwa na nyumba huko bali aliamua kuikimbia Mabibo baada ya kuwatapeli marafiki zake wawili waliotaka kukodi baa moja wafanye biashara baada ya kufanya uporaji mkubwa wa madini huko Mirerani.



Ili ajihakikishie usalama, na akitambua fika kuwa hao marafiki zake siyo wenyeji wa Jiji la Dar, ndipo alipoamua kukimbilia huku Kunduchi ambako akiwa na shilingi milioni kumi na nane aliamua kutafuta nyumba ya kawaida yenye vyumba vitatu ambavyo alipanga kwa mkataba wa miaka miwili.



Hata hivyo, hakuwa mbumbumbu wa kujisahau kwa kujiona bado ana mamilioni ya shilingi aendelee kutanua, bali alitumia akili yake kutafuta makazi bora, ambayo yatampa hadhi mbele ya jamii iliyomzunguka ingawa kati yao hakutakuwa na yeyote atakayejua anaishi kwa mfumo gani wa maisha.



Aliyejua kuwa kaja huku ni Jitu peke yake, ambaye japo hakushiriki katika mpango wa kupora madini huko Mirerani, wala kushiriki kuwatapeli wale rafikize Kelvin, hata hivyo alikuwa ni rafiki yake mkubwa aliyemtegemea sana katika mipango mikubwa ya pesa.



Hivyo, alichofanya baada ya kuwatapeli wale wash’kaji zake ni kumtafuta Jitu na kumkatia pesa kidogo, shilingi laki tatu huku akidai kuwa amecheza kamari ya matokeo ya mechi za soka za Ulaya na kujipatia shilingi milioni tatu.



Jitu alimwamini na alikuwa na ulazima wa kumwamini kwa kuwa nguvu ya kulazimisha kuupata ukweli hakuwa nayo. Maisha yakaendelea. Wiki tatu baadaye wakampata mtu mmoja ambaye alikuwa akihangaika kutafuta nyumba ya kupanga ili afungue saluni itakayojihusisha na masuala ya masaji. Mtu huyo aliyetoka Kongo alikuwa amejiandaa na pesa za kutosha na alitaka nyumba hiyo kubwa iwe na vyumba visivyopungua vitano na iwe eneo la ama Oysterbay, Kinondoni ‘A’, Kinondoni ‘B’, Makumbusho au Msasani eneo la Namanga.



Kelvin akitumia uwezo wake wa kuzungmza lugha za Kiingereza na Kifaransa, alimlaghai mtu huyo kuwa kulikuwa na nyumba bora iliyostahili kwa huduma hiyo. Ndipo walipompeleka kwa dalali mmoja na kumtaarifu kuhusu suala hilo.



Dalali huyo naye hakulemaa, akijua fika kuwa anacheza mchezo mchafu, alimpeleka Mkongo huyo eneo la Sinza Madukani ambako kulikuwa na nyumba iliyokuwa ikipangishwa. Mwenye nyumba hiyo hakuwepo, lakini walikuwepo watoto wake ambao walimfahamu dalali huyo.



Alichofanya dalali huyo ni kumwonyesha eneo la sebule ya nyumba hiyo wakati wakiwa wameketi kwenye masofa na akawa anadai kuwa mwenye nyumba yuko Nairobi kikazi ila yeye, dalali ndiye kaachiwa majukumu yote na kwamba pesa akabidhiwe Kelvin ambaye ni mdogo wa mwenye nyumba.

Mkongo akiwa hajui kuwa anaingizwa mjini, alikubali kutoa robo tatu ya malipo yaliyohitajika, shilingi milioni kumi na tano.



Makubaliano hayo yaliwafanya waondoke, wakaenda benki ambako Mkongo alichukua pesa na kuwakabidhi kwa maandishi.

Huo ukawa mwisho wa kukutana. Dalali na Kelvin wakabadili laini za simu, Mkongo hakuwapata tena simuni, wala hakuwaona tena. Maisha yakaendelea. Maisha ya mjini.



Ndipo Kelvin alipokwenda Mirerani na kupata pesa ambazo alikuja kuwadhulumu wenzake hapo Mabibo.



Hili suala la mpango wake na Jitu alihitaji kupata uhakika kama litakuwepo kweli au ndiyo limesharibika. Na ndipo alipopiga simu mara nyingi bila kumpata. Lakini kwa wito huu aliopewa na Jitu akaamua kujiandaa haraka na kwenda. Nusu saa baadaye alikuwa na Jitu, chumbani mwa Jitu.



“Advansi imetolewa,” Jitu alimwambia.



“Ngapi?”



“Moja u nusu.”



Kelvin alikunja uso kidogo. “Sijakuelewa ujue.”



Jitu alinyanyuka kitandani na kuketi. “Wamesema wanatoa milioni tatu. Kwa hiyo wametanguliza milioni moja na laki tano. Umenisoma?”



“Duh!” Kelvin alishangaa. “Yaani wanataka tuwafanyie kazi ya kigaidi kwa vihela mbuzi hivyo! Kwa nini umekubaliana nao?”



“Wamesimamia hapo,” Jitu alisema. “Hata hivyo, inaonekana kuwa kazi hiyo siyo kubwa sana. Ni kiasi cha kumteka mtu wao na kukaa naye kwa saa zisizozidi ishirini na nne na kisha tunaachana nae. Wao watakuwa wameshaelewana kivyao.”

Kelvin alitikisa kichwa. “Bado hii siyo dili, msh’kaji wangu,” alisema. “Mkwanja mbuzi huo Jitu. Lakini tusiache ila nina wazo moja.”



“Wazo gani?”



“Wasitufanye mabwege. Pale wanataka kutengeneza mamilioni ya pesa. Vipi watoe mkwanja mdogo hivyo?”



“Zungumza wazo lako Kelvin, usigeuke mwanasiasa.”



Kelvin alikunja uso kidogo kisha akasema, “Lazima watuongeze mkwanja. Tumtaiti huyo mtu wao halafu kabla ya wao kufanya chochote tuwashinikize waongeze pesa.”



Jitu alifikiri kidogo na kuuona ukweli wa maneno ya Kelvin. Aliwaza, ni kwa nini Abdul na dada yake wawe tayari kufanya jambo zito kiasi hicho kama si kutaka kujipatia mamilioni mengi ya pesa au kumuua Ablah na kutwaa mali zote za marehemu?



Wakati Mzee Malick alipofariki dunia, takriban Dar nzima ilijua. Ilikuwa ni habari kubwa. Vyombo mbalimbali vya habari vilijua. Na siku Abdul alipomtaka kufanya kazi hii iliyo mbele yake, ndipo alipobaini kuwa ni suala linalohusu mali za Malick Sikonge.



Kama Malick alikuwa tajiri kiasi kile, iweje suala la kumteka mwanaye lilipiwe milioni tatu tu? Na hawa Abdul na dada yake wajipatie utajiri wote!



“Nimekuelewa,” hatimaye alisema kwa utulivu, ndita zikiwa zimejiunda kwenye paji lake.



“Umeonaee,” Kelvin alidakia. “Lakini twende nao sawa mpaka mwisho.”



“Poa, na nimekuta missed call ya Abdul. Sijui kapiga saa ngapi, au labda mipombe bado inamchanganya. Ngoja nim-call.”



Jitu akampigia Abdul na kusikilizia. Muda mfupi baadaye sauti yenye mkoromo ikapenya sikioni mwake. “Jitu vipi mambo?”



“Poa. Nimeona ulinipigia. Vipi kuna mpya?”



“Yeah…jana nilikupigia sijui ulikuwa umelala…sista alisema umpigie ili ikibidi leo kazi uifanyike.”



“Leo?” Jitu aliuliza kama ambaye hajaelewa.



“Yeah. Leo.”



“Ok nipe namba yake.”



Dakika chache baadaye Jitu na Sharifa walikuwa wameongea kwa kina kuhusu mpango wa kufanya kazi siku hiyo. Hata hivyo mwafaka ulikuwa haujapatikana. Ndipo Jitu akasema, “Sikia sista, ukiwa na uhakika kuwa utakwenda Mlimani City, nambie ili tujipange. Sawa?”



Ukimya ukapita kidogo kasha Sharifa akasema, “Nipe dakika kumi nitakupa uhakika. Inabidi niwasiliane na mlengwa na kumshawishi, maanake ana ratiba zake. Nitakupigia baada muda huo.”



*******

ASUBUHI hii, Karim alikuwa ndani ya ofisi ambayo marehemu mzee Malick alikuwa akiitumia kwa shughuli zake. Alifungua saraka hii na ile, akapekua jalada hili na lile na hatimaye akifungua saraka ambayo ilimshtua. Ndani ya saraka hiyo hakukuwa na kitu kingine zaidi ya bastola.

Aliguna akashangaa. Tangua aanze kuishi hapo hakuwahi kujua kuwa Mzee Malick alikuwa silaha hiyo. Na hata hivyo hakuona kama ni kosa kwa mzee huyo kuimiliki.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





KWA mzee Malick, na utajiri aliomiliki, ilikuwa ni haki kuwa na silaha ya kumlinda. Malick aliamini hivyo.



Akaitoa silaha hiyo na kuiweka mezani. Kisha akaifungua na kukuta ndani kuna risasi tatu. Akaifunga na kuirejesha kwenye saraka huku akijiuliza ni kwa nini Mzee Malick hakuwahi kumdokeza kuwa ana silaha hiyo? Au hakuwa akimwamni?

Hata hivyo hakujali. Akaendelea kufanya shughuli nyingine kwenye kompyuta kisha akampigia simu Ablah. Alitaka wakutane na aanze kumwonesha miliki halisi ya marehemu baba yake na jinsi ya kuiendesha miradi iliyopo.



Simu ya Ablah ilikuwa ikitumika. Karim akatulia kidogo kisha akapiga tena; bado ikamjibu kuwa inatumika. Akaamua kuendelea na kazi zake nyingine.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog