Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MAPIGO YA MOYO - 2

 












Simulizi : Mapigo Ya Moyo

Sehemu Ya Pili (2)







Jumba kubwa la kifahari, jumba ambalo lilikuwa limezungukwa na ukuta mrefu sana kiasi kwamba nyumba ilikuwa haionekani kutokana na kuzuiliwa na ukuta,lilikuwa kimya sana huku sauti pekee za mbwa ndizo zilikuwa zikichangamsha mji huu.Nyumba hii ilimilikiwa na mfanyabiashara maarufu sana, si mwingine bali mzee Jastin.



"Karibu nyumbani kipenzi changu ",Rose aliongea huku akinikalibisha ndani, nyumba ambayo ilikuwa mala yangu ya pili kuikanyaga, japokuwa siku zote sikuweza kumkuta mzee Jastin, mzee ambaye sijui angenifanya nini kama angenikuta ndani kwake.



"Asante mpenzi!, nimekalibia ",niliongea huku nikiketi na kuangaza kila kona ndani ya jumba lile, jumba ambalo sikuweza kuuzoea uzuri wake, hivyo ilikua ni jambo la kawaida kulishangaa.



"Rose naomba nikuulze kitu! Utanisamehe kama nitakuwa nimekosea kukuulza swali hili ……",niliongea huku nikijiweka tayali kwa ajili ya kumuulza swali Rose, bila kutambua kuwa nilikuwa hatarini kwani mzee Jastin alikuwa njiani akija nyumbani kwake baada ya kutoka kumsindikiza Rodgers.



"Hivi ulikusudia kunigonga na gari! ",ilibidi niulize swali ambalo sikuzote lilizunguka kichwani kwangu, na kila nilipokuwa nikitaka kumuulza swali hili Rose, roho yangu ilisita kwani sikupenda kumchukiza Rose, msichana mrembo ambaye ilinigharimu sana kumpata!



"Sina budi kukwambia ukweli Robert ……! Nilikugonga na gari kwa makusudi ili nikuue kabisaa, awali nilikuwa sikupendi na nilikuchukia sana………lakini kwa msaada wa wananchi walioshuhudia tukio walitaka kunishambulia nilipotaka kutoweka, ikabidi nirudi kukuchukua na kukupeleka hospitali ",Rose aliongea kwa huzuni sana, huku akionekana kujutia kitendo alichonifanyia. Lakini kwa upande wangu mapenzi yalitoweka ghafla! mala tu baada ya kuniambia alitaka kuniua, niliona ilikuwa ni kweli kwani nilimfuatilia muda mrefu sana lakini sikuwa na bahati ya kupendwa, zaidi ya kuambulia mateso tu!



"Kwanini ulitaka kuniua?, nilikukosea nini ?",niliongea huku nikiwa nina hasira, sikutaka kukaa tena mahali pale kwani niliona yote Rose aliyokuwa akinifanyia alikuwa kama anajilazimisha tu kunipenda, na pengine inawezekana alikuwa na lengo baya juu yangu.



"Nilipokuwa chuoni nilimpenda sana Peter ……,lakini Peter alikuwa akiniambia kuwa hawezi kuwa na mimi kwasababu alizani mimi na wewe ni wapenzi,hivyo siku zote nilikuchukia kwani nilikuona wewe ndiye chanzo cha mimi kumkosa Peter"Rose aliongea huku akipiga magoti, lakini sikujali! Niliona kama alikuwa akiniigizia tu.



"Vipi kuhusu Jacob! " ,niliendelea kumswalisha Rose, na bila shaka aliweza kutambua kuwa nilikuwa nimechukia. Sikuwa na hofu, kwani ningeweza kuondoka sehemu yoyote na kuishi kwani nilikuwa nimepatiwa pesa nyingi sana na mheshimiwa raisi.

"Kuhusu Jacob, sikumpenda!, nililazimishwa tu na baba! .Nisamehe Rose lakini sasa hivi nakupenda kwa dhati, umevumilia mengi sana lakini hukusita kunipenda! Ndio maana najutaaa makosa yangu",Rose aliongea mpaka nikaanza kumuonea huruma, kusema ukweli nilimpenda sana msichana huyu. Hivyo kitendo cha kumuona akianza kulia, ikabidi nipunguze hasira na maswali ambayo nilikuwa nazidi kumuuliza Rose.



********************



Vyombo vya habari vinatangaza juu ya kutafutwa kwa muhusika aliyehusika na mauaji ya Jacob, televisheni ziliweza kuonesha picha za muuaji lakini stesheni za radio nazo hazikupitwa na taarifa hii, zilielezea muonekano wa muuaji vizuri sana kiasi kwamba hakuna mtu yoyote ambaye angeshindwa kumtambua muuaji kama angekutana naye uso kwa uso.



Mzee Jastin akiwa amekamatilia uskani wa gari yake, aliona kama gari halikimbii. Kwani alikuwa na haraka sana baada ya kusikia taarifa ya habari kupitia radio yake, alikuwa anawahi nyumbani kwake eneo la Temeke kwa ajili ya kufanya jambo fulani ili kumuokoa Rodgers asiweze kukamatwa mala atakapofika Mombasa.Kwani alitambua kuwa Rodgers kafanikiwa kutoka Dar es salaam salama, kwani kipindi anaondoka na ndege, taarifa ya habari ilikuwa bado haijatangazwa.



"Inatakiwa nimtarifu haraka sana Okumu, aweze kutuma vijana uwanja wa ndege wakampokee, lakini simu imezima chaji!,sina jinsi zaidi ya kuwahi nyumbani ……",Jastin aliongea huku akiikanyaga mafuta gari yake, na kila taa nyekundu zilipowaka muda mwingine hakuweza kusimama kwani aliona kama Rodgers alikuwa muhimu sana kuliko faini atakayolipa kama trafiki wakimtia mikononi.



********************

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Japokuwa taarifa ya habari haikuweza kuwafikia abiria waliokuwa ndani ya ndege, huku simu zao zikiwa zimezimwa. Lakini Rodgers machale yaliweza kumcheza, alihisi jambo baada ya kumuona askari mmoja akikagua abiria mmoja baada ya mwingine. Hivyo ilibidi Rodgers atumie akili za kuzaliwa ili kukwepa kukamatwa na polisi yule aliyekuwa amevalia jezi zake huku picha ya Rodgers akiwa ameishika mkononi, alitazama sura ya abiria na kisha kutazama sura ya Rodgers.Bila shaka! alionekana kuwa na asilimia mia moja kuwa mtuhumiwa aliweza kuwemo ndani ya ndege ile.



Mapenzi ni hisia za ajabu sana, ukimpenda mtu kwa dhati utajikuta ukifanya kila jambo uweze kumpata. Pengine hata kutoa uhai wa binadamu mwenzio ili tu moyo wako uweze kupata furaha. Hilo ndilo jambo pekee ambalo lilimkuta msichana mrembo Rose ,alikuwa kama mtumwa wa mapenzi.



Hakuwa tayali kulala bila kuiona sura ya Peter, mvulana pekee aliyetokea kumpenda siku zote alizokuwa akisoma chuo kikuu cha Sokoine mkoani Morogoro.



Kusema ukweli Peter na Rose waliendana sana ,na wote walikuwa maarufu sana chuoni. Ungeonekana mshamba sana kama ulikuwa unasomea SUA na hukuwa unamfahamu Rose. Vivyo hivyo kwa Peter, wale tu waliopenda kuvaa na kuendana na fasheni chuoni ndio waliokuwa wakimfahamu Peter, kijana pekee aliyeshinda mataji ya ubunifu wa mavazi ya kiume chuoni.



“Naitwa Rose Jastin, bila shaka mwenzangu unaitwa Peter Mathew ……”,yalikuwa ni maneno ambayo Rose  aliweza kuyaongea mwaka mmoja uliopita,mwaka ambao ulikuwa wa mwisho chuoni wa masomo yake.Bila kujali ugumu wa kozi ya Biotechnology aliyokuwa akisoma, hakusita kushiriki mashindano ya urembo chuoni, na siku zote aliibuka mshindi wa taji hilo, na kuvunja rekodi kuwa msichana wa kwanza kubeba taji hilo la  umisi chuoni miaka yote ya masomo yake huku akisoma kozi ngumu.



“Bila shaka ndiye mimi ……”,Peter aliongea huku akijifanya kama ndiyo ilikuwa mala yake ya kwanza kumuona Rose, japokuwa alipokea kadi nyingi pamoja na sms za kimapenzi kutoka kwa msichana huyo, lakini hakumpenda. Yeye aliridhika na maisha ya kiplay boy, maisha ya kuwatumia wanawake kama chombo cha starehe ndio maisha pekee ambayo Peter aliweza kuyachagua. Pesa haikuwa tatizo kwake, kwani baba yake alimiliki hoteli nyingi za kitalii pamoja na mabasi mengi ya abiria yaendayo mikoani. Hivyo basi, akaunti ya Peter ilikuwa na pesa nyingi kumtimizia kila alichokitaka kama kijana.



“In short, sikupendi! mpende sana Robert kwani anakupenda na sio mimi “,ni maneno ambayo mshindi wa kiume katika ubunifu wa mavazi, kijana mtanashati aliyekuwa akipendwa sana na wasichana chuoni aliongea kumjibu Rose kuhusu ombi lake la kuwa wapenzi, ombi ambalo Rose aliahidiwa kupatiwa jibu na Peter katika part hiyo. Siku zote Rose  hakuweza kumtamkia hisia zake Peter uso kwa uso, bali alimtumia kadi za kimapenzi, hakuishia hapo alitafuta namba ya Peter na alipoipata hakusita kuwasilisha hisia zake kwa kijana huyu mtanashati.



“Kwanini lakini hutaki kunipenda, familia zetu zote zina pesa, harafu pia mimi na we ……”Rose alitaka kumalizia sentesi yake, lakini alishangaa sana Peter akiondoka huku akimtamkia kauli ya mwisho ambayo ilimfanya Rose kuumia sana na kuapa kulipiza kisasi, kwa yule aliyesababisha aweze kumkosa mwanaume aliyempenda sana.



“Robert ndiye mtu pekee unayepaswa kumpenda, kafeli mala nyingi sana mitihani yake sababu yako, kaaibika sana sababu ya kukupenda…



Kuanzia leo ukinifuatilia tena nitakuua …”,Peter aliongea huku akiwa ana hasira sana ,hakuwa tayali kuniona nikiendelea kuteseka mimi kama rafiki yake, urafiki ambao ulinifanya na mimi nionekane kama miongoni mwa watu kati ya watu.



Urafiki wetu ulianza mala tu baada ya kumwagiwa kisahani changu cha chipsi siku moja nikiwa katika hoteli iliyoko maeneo ya chuo chetu cha SUA pale main Campus, hakuishia hapo, nilipokea matusi mengi sana kama unavyojua watoto wa kizaramo! wakiamua kukuaibisha, siku hiyo lazima ujute. Aliyenifanyia matendo hayo ya ajabu hakuwa mwingine bali Rose, mala baada ya kuingia hotelini na kunikuta nikiwa nimeketi nikila chipsi zangu. Siku zote alinichukia kwani kwa siku alipokea sms nyingi za kimapenzi kutoka kwangu, sababu pekee iliyomfanya abadili namba yake ya simu kila wakati. Japokuwa alinionya nisimpigie simu wala kumtumia meseji, lakini sikuweza kujali chochote kile!, moyo wangu ulikuwa tayali kupokea maumivu ya kila aina.



“Nimeshakukataza usinipigie simu maskini wewe, huna hadhi ya kuwa na mimi “,ni maneno ambayo Rose aliweza kuyaongea na kisha kunibatiza kwa maji ya Kilimanjaro, chupa ya maji ambayo alikuwa ameishika mikononi mwake.



Rose na kundi lake waliondoka baada ya kuniaibisha, kusema ukweli nilichoka! wenye huruma walinihurumia, lakini maadui zangu hasa wanafunzi wenzangu walionidharau kwa umaskini wangu walinicheka sana baada ya kushuhudia kitendo nilichokuwa nimefanyiwa.



“Pole sana kaka, kula chakula hiki, na niambie mtu gani mubaya kakufanyia hivi “,nikiwa nimeinama nikificha aibu ya kuzomewa, nilishtuka mkono wa mtu ukiwa begani kwangu. Niliinua uso wangu na kushangaa nikikabidhiwa chakula kizuri na mtu ambaye siku zote niliogopa hata kumsalimia ,kwani hakuwa  sawa na mimi. Alikuwa ni mtoto wa tajiri maarufu mkoani Morogoro aliyejulikana kwa jina la Peter, baba yake mzee Mathew alikuwa na pesa nyingi sana hivyo basi sikuwa nina hadhi ya kuwa na urafiki naye. Kwani wazazi wangu walikuwa maskini kiasi kwamba nilivaa nguo moja wiki nzima chuoni mpaka watu walinishangaa .



“Kuanzia leo wewe ni rafiki yangu ,nitahakikisha una mpata binti huyu kama kweli unampenda japo inaonekana hana tabia nzuri kama mke wa kuishi naye “,ni maneno ambayo Peter aliongea baada ya kumsimulia kila kitu,japo Peter alipenda sana wanawake, lakini nilishangaa akitamka jambo moja la muhimu sana ambalo nililipuzia kuwa Rose alikuwa ana tabia mbaya hakufaa kuwekwa ndani kama mke wangu. Ndugu msomaji ,hivyo ndivyo niliweza kumpata Peter kama rafiki mpya chuoni na kuyabadilisha maisha yangu. Shida yangu ilikuwa yake mpaka tukamaliza chuo huku nikiwa ninaheshimika na wanafunzi wenzangu chuoni tofauti na awali. Lakini urafiki wetu ulitoweka ghafla kama jinsi ulivyoanza, kwani Peter baada ya kumaliza chuo alisafiri kwenda nchini Uingereza, na huo ndio ukawa mwisho wangu  mimi na yeye kuwasiliana.



**–****—



“,Sawa Peter asante kwa kunikataa na kuniaibisha, lazima nitalipiza kisasi kwa mtu huyu mpumbavu aliyenifanya nitoe machozi leo hii ” ,Rose aliongea huku akimjibu Peter aliyekuwa akiondoka kwa hasira katika part, part ambayo ilifanyika baada ya mashindano mbalimbali ya sanaa kumalizika katika chuo chetu cha SUA.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Na huo ndio ukawa mwanzo wa visa vikali mimi na Rose, alimwambia baba yake kuhusu mimi mpaka kupelekea wazazi wangu kuuawa. Hakuishia hapo! aliamua kunigonga na gari ili aniue kabisa aliponiona nikivuka barabara kizembe huku nikitembea kwa miguu. Ilikuwa barabara ya Morogoro, karibu na kituo cha mwendokasi cha Ubungo baada ya kufika muda mfupi tu na basi la Abood kutoka kijijini kwetu Mikese mkoani Morogoro, kuja Dar es salaam kutafuta shule ya kufundisha na pia kumtafuta kipenzi changu Rose ambaye nilimfikilia kila muda bila kukoma.



Plani yake ilifeli! alijikuta anashambuliwa na watu waliokuwa eneo lile la mwendokasi mala tu baada ya kutaka kuliondoa gari   .Bila kupenda alijikuta akinifikisha hospitalini, ili kukwepa kichapo kutoka kwa wananchi hawa walioshuhudia ajari ile na kugundua kuwa Rose ndiye aliyekuwa na makosa.



Hakuwa na jinsi kuitafuta plani B ya kulipiza kisasi!, na plani pekee aliyoiona inafaa nikujirahisisha kwangu, na kuniweka karibu yake. Aliona bora kumkosea baba yake aliyekuwa akitaka aolewe na mtoto wa raisi aliyeitwa Jacob ,na kukubali kuolewa na mimi ili tu aweze kuniua kirahisi na kulipiza kisasi kwani nilisababisha aweze kumkosa mtu aliyempenda sana, kijana pekee ambaye alikuwa katika moyo wake ambaye aliitwa Peter.



Kenya;



Hatimaye baada ya saa moja kupita,ndege ndogo ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Air Tanzania ilianza kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mombasa (MOI).Ilikuwa ni safari ya mateso kwa Rodgers kwani alitumia muda mwingi wa safari hiyo akiwa amejificha chooni baada ya kumuona askari mmoja akimtafuta ndani ya ndege. Kusema ukweli alimanusura akamatwe kama asingewahi kumuona askari yule ,na kweli alipona! kwani Rodgers tiketi yake ilikuwa ya mwisho kukatwa, hivyo alikaa mwishoni siti ya nyuma kabisa.Askari alipojaribu kuulza kwani alikuta siti ya mwisho ikiwa wazi, aliambiwa mtu yule kaelekea chooni anasumbuliwa na tumbo la kuhara! Askari kwa vile alikagua asilimia kubwa ya abiria wote na kumkosa adui yake, aliamini hata mgonjwa aliyeelekea chooni atakuwa siye muhusika.



Dar es salaam;



 Hatimaye honi ya gari la mzee Jastin ilitushtua sana mimi na Rose, kwani sikujua mzee Jastin angenifanyia kitendo gani kama angenikuta ndani kwake.



Rose hakuwa tayali kumuona baba yake akiniua, sio kwamba alinipenda! La hasha, alitaka aniue mwenyewe na kulipiza kisasi kwa mikono yake mwenyewe.



“Piiiii! Piiiii ……”mzee Jastin aliyekuwa anapiga honi nje ya geti lake kwa mara ya kwanza, baada ya siku nne kupita alipojaribu kuniua bila mafanikio huku Jacob akifa badala yangu, aliendelea kupiga honi kwa fujo kwani alitaka kuingia ndani haraka sana aweze kufanya mawasiliano na majambazi wenzie walioko Kisauni, Mombasa nchini Kenya.



Dar es salaam;



Nyumbani kwa mzee Jastin kulikuwa na hekaheka, japokuwa nilikuwa sina miguu lakini niliweza kushuka kwenye sofa ambalo nilikuwa nimeketi na kisha kutambaa kuelekea chumbani kwa Juliet. Sekunde chache tu, nilikuwa uvunguni mwa kitanda. Huku nikipumua kwa kasi sana, upumuaji ambao ulikuwa mithili ya mgonjwa mahututi wa Pumu.



Kitendo cha mimi kutoweka sebuleni kwa mwendo wa ajabu, mwendo ambao niliufananisha na spidi ya magari yaendayo mikoani. Ndicho ambacho kilinifanya mimi kupumua kwa kasi, kwani pumzi iliniishia kabisa.



“Leo ni leo, nimepatikana, mzee huyu akibahatika kuiona sura yangu, lazima aniue “,nilizungumza peke yangu bila kujali kama kuna mtu yeyote aliweza kuisikia sauti yangu au laa!. Niliendelea kutambaa na kujivuta polepole kwa mwendo wa taratibu mithili ya kinyonga, na kuketi katikati uvunguni mwa kitanda. Sehemu ambayo mtu yeyote ambaye angechungulia kwa macho ya kawaida asingeniona, kwani giza totoro lilikuwa uvunguni mule, na lazima yeyote ambaye angetaka kuona kilichokuwa uvunguni, lazima atumie vifaa kama tochi bila hivyo asingeweza kuniona.



********

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mzee Jastin alipiga honi ya gari lake kwa muda mrefu sana, lakini hakuna  mtu yeyote aliyeweza kwenda kumfungulia geti. Akiwa na hasira sana, alitoka ndani ya gari na kisha kuisogelea batani moja iliyokuwa ukutani na kisha kuibonyeza. Rose akiwa sebuleni, aliendelea kusimama kama sanamu kwani hakujua nini afanye kwa wakati ule, jambo pekee ambalo lilimfanya apigwe na butwaa. Ujio wa baba yake nyumbani ghafla, na tena bila taarifa ndio sababu iliyomfanya Rose kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kichwani mwake.



“Au kuna mamluki kampatia taarifa baba, kuwa Robert yuko nyumbani !,siko tayali kumuona baba akimuua, moyo wangu sitakuwa nimeutendea haki”,Rose aliongea kwa sauti ya juu bila kujitambua, sauti ambayo hata mimi niliweza kusikia kila kitu alichokiongea nikiwa uvunguni mwa kitanda, ndani ya chumba chake.



“Griiiiiii, griiiiiiiii, griiiii ……” mlio wa kengele ulisikika katika masikio ya Rose, na kumfanya akurupuke kutoka katika mawazo aliyokuwa akiwaza. Bila shaka alitambua hasira ambayo baba yake alikuwa nayo, hasa baada ya kuamua kubonyeza kitufe cha kengele, alipoona honi ya gari haijazaa matunda na geti kufunguliwa.



“Shikamoo baba! “, Rose aliongea kwa upole sana na kumsalimia baba yake, baba ambaye alikuwa na sura iliyokunjamana utazani alikuwa amekula chumvi nyingi kumbe sivyo!, hasira aliyokuwa nayo ndiyo iliyosababisha kukunja sura yake, sura ambayo Rose aliweza kuogopa kumsogelea kwani pengine angeambulia kofi au mateke kwani siku zote baba yake ndicho kitendo alichokuwa akimfanya Rose akiwa amemkosea.



“Hebu fungua geti mwanaharamu wewe! Na utaniambia kilichokufanya unikalishe hapa nje nusu saa nzima bila sababu “,mzee Jastin akiwa na hasira, alitamka maneno ambayo yalimshangaza sana Rose. Hakuamini kama kweli baba yake ndiye aliyeweza kumtamkia maneno makali kiasi kile, tena binti yake pekee wa kumzaa.



“Baba hivi kweli wewe ni baba yangu, unaniita mwanaharamu!!! Kweli baba! Kweliiii “,Rose alijikuta akisahau kama ndani alikuwa amemwacha mtu ambaye hapendwi na baba yake, alisahau kila kitu kuhusu kulipiza kisasi na kuniua, kwani aliniona  kuwa chanzo cha yeye kumkosa Peter. Jambo ambalo lilikuwa kichwani mwake, ni kuhusu mahusiano yake yeye na baba yake mzee Jastin.



“Hivi baba yako wa kukuzaa anaweza kukaa siku tano bila kukupigia simu na hujui kaenda wapi!, baba yako wa kukuzaa anaweza kukuficha ndugu zako! baba yako wa kukuzaa anaweza kukuacha uishi peke yako nyumbani bila hata mlinzi au mfanyakazi wa ndani!,baba yako mzazi anaweza kukupangia kuolewa na mtu anayemtaka yeye ili kuendeleza biashara zake! na pia isitoshe anakuita mwanaharamu kwelii!



“Noo, noo, no! This is not my dady! aim sure hundred percent! But where is my real parents? ” (Hapanaa, hapanaa, hapana! Huyu sio baba yangu !nina uhakika asilimia mia moja !Lakini wako wapi wazazi wangu halisi?)



Rose akiwa ameegemea geti kubwa baada ya kumfungulia baba yake mzee Jastin, alijiuliza maswali mengi na hatimaye kupata jibu lake. Jibu ambalo lilimfanya atokwe na machozi mengi sana, kwani aliamini mzee Jastin hakuwa baba yake mzazi.



********



Mzee Jastin aliingia ndani na kubamiza mlango kwa fujo, aliamini kabisa Rodgers atakuwa tayali amekamtwa na polisi, kwani muda ulikuwa umepita mrefu sana! Hivyo basi ingekuwa vigumu kumtorosha uwanja wa ndege wa Mombasa akiwa salama.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Shitiii! hizi ndizo hasara za kuishi na watoto wa kuokota! Mitoto haina akili kabisaa! And this bastard president, aim sure! Kafanikiwa kumkamata kijana wangu”,jambazi la kutisha nchini Tanzania, mzee aliyetumia kivuli cha biashara kuficha makucha yake. Mzee aliyejulikana kwa jina la Jastin, mmoja wa wafanyabiashara ambao walikuwa na sauti kubwa katika serikali ya Tanzania, aliongea maneno bila kutambua kuwa kuna mtu aliweza kuyasikia. Adui ambaye siku zote aliweza kumchukia, na kujalibu kumuua mala nyingi bila mafanikio ,kijana Robert ndiyo aliyeweza kusikia maneno yake ambayo yalimfanya kujiuliza maswali mengi.



“Rose kasema hataki kumuona baba yake akiniua, anataka autendee haki moyo wake yeye mwenyewe! Kuna nini hapa katikati? “,



“Mzee Jastin anasema Rose kamuokota!!, ndio maana anamfanyia mambo ya ajabu “,nilijiuliza maswali moyoni mwangu, na kuapa kumweleza Rose kila kitu nilichokisikia kama nitafanikiwa kutoka salama uvunguni mwa kitanda nilipokuwa nimejificha.



“Kijana imefika salama Mombasa! ile kijana imafia kabisa, imetoroka polisi yote uwanja kwa ndege bila kukamatwa “,ilikuwa ni sauti ya simu, sauti ambayo bila shaka iliwekwa roud speaker !.Ilikuwa ni sauti ya mtu aliyeonekana kutokuwa mtanzania kutokana na kiswahili chake alichokuwa akiongea, niliposikia neno Mombasa likitajwa! Bila shaka niliamini mtoa taarifa alikuwa raia wa Kenya.



“Waaaoh! Aim happy now! Good work Rodgers ……!”,(waaoh, nina furaha sasa, kazi nzuri Rodgers …” ,)nilisikia sauti ya mzee Jastin, mzee aliyeongea huku akiwa amechomeka simu chaji bila kujali hatari yoyote ambayo ingeweza kumkuta kwa kufanya mawasiliano huku simu ikiwa inachajiwa.Niliamini asilimia mia moja kuwa alikuwa akiongea na mtu aliyemtaja katika maongezi, mtu aliyejulikana kwa jina la Rodgers kumbe sikuwa sahihi.



“Hapa ngoja niende kambini, kwenye kambi yetu ya Mbezi, sasa hivi hapa nyumbani sio salama mimi kuishi “,mzee Jastin alichomoa simu yake chaji, lengo lake la Rodgers kusafiri bila kukamatwa liliweza kutimia, hivyo hakuwa na budi kutoweka nyumbani kwake.Alimpita Rose akiwa kibarazani na mawazo mengi sana, kwani baada ya Rose kuchoka kuegemea geti aliamua kwenda barazani na kupunga upepo huku akitafakali namna ya kuanzia kutambua siri iliyofichika kuhusu ukweli wa maisha yake.



“Wewe mpuuzi usisahau kufunga geti! mimi naondoka zangu “,mzee Jastin kweli alibadirika!,Alikuwa tofauti na zamani alipokuwa akionyesha mapenzi ya kuigiza kwa mwanae Rose, sasa hivi alimuonyesha chuki ya waziwazi kabisa. Mzee huyu aliongea huku akisindikiza mitusi kwa msichana mrembo Rose, na kisha kuondosha gari lake eneo lile na kuacha geti likiwa wazi.



“Yes i have got the way! his computer can aswer me every thing ……” (Ndio nimepata njia!  Kompyuta yake inaweza kunijibu kila kitu),hatimaye Rose aliweza kutabasamu, fikra zake hazikwenda bure! aliamini komyuta ya baba yake iliyomfanya kutambua kazi halisi ya baba yake na lengo la kumlazimisha kuolewa na mtoto wa raisi aliyeitwa Jacob, ingeweza kumpatia majibu pia kuhusu historia ya maisha yake.



Rose alitabasamu kwa mbali huku akifuta machozi yake yaliyokuwa yakimtiririka usoni na kisha kwenda kufunga geti haraka sana, geti ambalo liliachwa wazi na baba yake alipolifungua na kutoweka nyumbani na gari yake. Hakuwa na sababu ya kuchelewa! Lengo lake ilikuwa ni kwenda kuchezea kompyuta ya baba yake, kompyuta ambayo mzee Jastin aliamini Rose alikuwa hafahamu namba zake za siri kuifungua.



********



Raisi wa Tanzania hakuamini taarifa aliyokuwa ameambiwa, aliamini kabisa camera za uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere zilizonesha Rodgers kusafiri usiku ule, na pia aliamini taarifa aliyopewa mwanzoni kabisa na mtoa ticketi za ndege aliyeitwa Juma, kijana aliyemsariti rafiki yake mzee Jastin na kumpatia taarifa raisi kuwa muuaji wa mwanae alikuwa akisafiri kutoweka Tanzania. Baada ya raisi kupokea taarifa kutoka kwa Juma, aliamuru ndege isiweze kuruka mpaka askari wake aliyemwamini sana atakapofika na kusafiri katika ndege hiyo huku akiifanyia ukaguzi na kumsaka mtuhumiwa.



Lakini bila kutegemea! ndege ilifika Mombasa bila Rodgers kukamatwa, askari wa Kenya walipojaribu kukagua camera za uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mombasa (MOI),nao pia walishangaa, sura ya Rodgers haikuonekana kufika uwanjani hapo usiku huo.



Jambo hilo lilimtatiza sana raisi, raisi aliamini Rodgers alikuwa mtu hatari sana na kazi ya ziada ilihitajika na pengine hata kuomba msaada wa askari wapelelezi wa kimataifa. kuja kumtafuta mtuhumiwa huyu aliyeonekana kuwa moto wa kuotea mbali.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unajua sielewi! Uwanja wa ndege anaonekana akipanda ndege, lakini Kenya hajaonekana! Insipekta Chacha amekagua ndege hajamuona! Hapa inatakiwa mtumie akili za kuzaliwa bila hivyo tutakufa sisi kabla yake “,raisi akiwa amekasirika, aliongea maneno ya kuoneshwa kushangazwa sana na taarifa aliyopatiwa na askari wake, tena askari aliokuwa akiwaamini sana katika kazi zao.



Dar es salaam;



 Woga ulitoweka kabisa, tabasamu likaipamba sura yangu kwa mala nyingine tena. Pumzi ndefu ilinitoka kupitia mdomo wangu, tofauti na awali nilipokua nikitumia mdomo wangu kupumua. Kitendo cha mzee Jastin kuondoka nyumbani kwake bila kugundua uwepo wangu mahali pale, ndio jambo pekee ambalo liliweza kunifurahisha. Kusema ukweli nilipona kifo! kifo ambacho kingenikuta kama mzee yule katili angenitia machoni pake.



“Thanks God, aim safe! (Asante Mungu, niko salama) .Hatimaye nilizungumza kizungu, lugha ambayo siku zote niliweza kuiongea kama nikiwa nina furaha. Japokuwa nilikuwa na elimu ya chuo kikuu,elimu ambayo ilinifanya niwe vizuri katika lugha hiyo ya  kimataifa.



“Robert naomba unisaidie kitu!”,msichana mrembo Rose, msichana ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote, japokuwa alikuwa hanipendi kama nilivyokuwa nafikilia.Aliongea kwa upole sana, kichwani mwake alisahau kila kitu kuhusu nia yake mbaya ya kuniua na kulipiza kisasi chake. Jambo pekee ambalo alikuwa akiwaza kwa sasa, ni kujua historia halisi ya maisha yake.



“Nikusaidie kitu gani mpenzi wangu, Harafu baba yako kazungumza kitu kimoja ambacho sijakielewa kwakweli, anasema eti amekuokota!!! lakini naomba usichukie “,nilimweleza Rose bila kutambua kuwa alifahamu kila kitu ambacho baba yake aliweza kukiongea..



“Hilo ndilo jambo mbalo nilitaka unisaidie !pia naomba unisamehe, siku zote nilikuwa nakuongopea kuwa nakupenda lakini nilikuwa nakudanganya tu, nilikuwa nina nia mbaya ya kukuua kabisa kwa sababu nilikuona kama chanzo cha mimi kumkosa Peter, naomba unisamehe kwa yote! lakini mzee Jastin inawezekana mimi sio mwanae wa kumzaa, na kuna siri nzito imejificha ,kwahiyo naomba unisaidie “,moyo wangu ulipasuka mithili ya puto ambalo limejazwa upepo kupita uwezo wake. Sikumwamini tena Rose! nilimuona kama muuaji aliyejivika ngozi ya kondoo.



“Rose nikufanyie nini ujue nakupenda! wazazi wangu walipoteza maisha sababu yako, umenigonga na gari na kunivunja miguu ,isitoshe hujaridhika! bado unajifanya unanipenda ili uniue kirahisi! Inatoshaaa, Rose inatoshaaa! sina budi kukubali kuwa mimi ni mjinga, umenifanya kichaa wa mapenzi “,niliongea maneno mengi kwa huzuni sana,sikuamini kama kweli Rose alikuwa na roho ngumu kiasi kile mpaka kupelekea kutaka kuniua.



Mapigo ya moyo wangu hayakuwa katika hali ya kawaida, yalikimbia mbio ndefu sana kiasi kwamba Rose aliweza kugundua.



“Please Robert! usipaniki, mapenzi ni ya ajabu sana!  nisamehe bure kipenzi changu “,msichana mrembo sana ambaye angemvutia mwanaume yeyote rijali, aliongea na kunisogelea. Kisha alichuchumaa chini na  kunipiga busu katika paji langu la uso.



Kipenda roho hula nyama mbichi! nilijikuta nikimsamehe Rose baada ya kupigwa busu lile, na kujikuta nikiendelea na ujinga wangu kwani tayali roho yangu ilikua imependa kwa dhati. Mapenzi ndiyo yaliyonifanya nivumilie vitendo vyote vibaya ambavyo nilikuwa nimetendewa na Rose, mapenzi ndiyo yaliyomfanya Rose kufanya mipango ya kuniua ili alipize kisasi kwasababu aliniona kama chanzo cha yeye kumkosa Peter. Hivyo kulaumu kusingenisaidia chochote kile! jambo pekee ambalo nilitakiwa kulifanya nikutoa ushirikiano kwa Rose katika kila jambo, na kumuonesha mapenzi ya kila aina ili upendo wake aweze kuhamishia kwangu na wala sio kunichukia.



“Sawa Rose! nimekusamehe, naahidi kukupenda daima hata kama wewe hautakua tayali kunipenda! “,



“Hapana Robert usiseme hivyo! Nimefuta kisasi chote, na niko tayali kukupenda, nisamehe bure mpenzi “,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Naomba unipende, nipende kama mimi ninavyokupenda ,nakupenda sana Rose “,



“,Usjali kabisa Robert, Sasa hivi nisaidie kujua ukweli kuhusu maisha yangu, wazazi wangu halisi wako wapi?, harafu baada ya hapo tukaishi zetu Uingereza, akaunti yangu ina pesa za kutosha, hata wewe pia raisi kakupatia pesa nyingi ambazo hazitaisha leo wala kesho “,Rose aliongea huku akinimwagia mabusu mengi mfululizo, mabusu ambayo yalinifanya nifungue kabisa moyo wangu, na kusahau maumivu ambayo Rose alikuwa ananisababishia kila kukicha.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog