Search This Blog

Saturday, 5 November 2022

MAPIGO YA MOYO - 3

 












Simulizi : Mapigo Ya Moyo

Sehemu Ya Tatu (3)





Mombasa _Kenya ;



       Rodgers alikuwa na furaha sana, alijiona mshindi dhidi ya raisi wa Tanzania aliyetuma vijana wake waweze kumkamata bila mafanikio.



Akiwa anaendelea na mazoezi ya karate kama kawaida, lakini kwa wakati huu alifanya mazoezi makali bila kupumzika. Alitambua muda wowote, angeweza kukabiliana na askari wa Kenya au Tanzania ambao walikuwa wanamtafuta kila kona ili aweze kujibu mashtaka ya mauaji aliyokuwa ameyafanya.



“Duuuh! kama wameshindwa kunikamata kwenye ndege, wasitegemee kama watanikamata kirahisi uraiani, tena katika ngome yetu yenye ulinzi makini “,aliongea huku akitabasamu, mala baada ya kukumbuka jinsi alivyojifanya mgonjwa mahututi na kukosa nguvu za kutoka chooni alipokuwa amejificha muda wote ndege ilipokua safarini.



Abiria wote walishuka, lakini muhudumu alishangaa abiria mmoja akiwa haonekani. Alipojaribu kukagua kila sehemu ndani ya ndege hakuweza kuona mtu, lakini alikumbuka mgonjwa aliyekuwa ameelekea chooni tangu ndege ilipoanza safari Dar es salaam. Muhudumu aliamini kutakuwa na tatizo!, haraka haraka alielekea chooni, na kama alivyokuwa akifikilia, alimkuta Rodgers akihema kwa nguvu, huku akiwa hawezi hata kusimama. Bila kupoteza muda, ambulance ilifika na wahudumu wa ndege ile walishirikiana kumnyenyua Rodgers na kumuweka ndani ya gari. Hawakuruhusu mgonjwa kupigwa picha zozote zile, kwani waliogopa kuchafua shirika lao la ndege kwa kutoa huduma mbovu mpaka kupelekea abiria akizidiwa kiasi kile bila kugundulika na kupatiwa huduma ya kwanza.



Wahudumu wale wa ndege hawakujua kuwa Rodgers aliwadanganya, hakuwa anaumwa ugonjwa wowote ule bali aliigiza tu. Ambulance haikuweza hata kukaguliwa na askari, kwani waliamini mgonjwa yule aliyefunikwa mwili mzima mpaka uso wake, hawezi kuwa jambazi waliyekuwa wamepokea taarifa zake za mauaji kutoka Tanzania, mauaji ambayo aliyafanya kwa kumuua mtoto wa raisi aliyeitwa Jacob.



Ndio maana hata cctv camera za uwanja wa ndege wa Mombasa, hazikuweza kuinasa sura ya Rodgers.Jambazi hatari na mzoefu sana, siku zote hakubahatisha bali alijiamini na kufanya kazi zake kwa umakini wa hali ya juu, jambo ambalo lilimfanya apendwe na mabosi wake.



……………………………



Madaktari na manesi ambao walimpokea Rodgers katika hospitali ya Mombasa, walishangaa sana kwani walimfanyia vipimo vya kila aina, lakini hawakuweza kuona ugonjwa wowote. Cha kushangaza, Rodgers alipata nafuu haraka sana na baadaye wakamruhusu kuondoka. Madaktari hawakuwa na haja ya kumuuliza maswali mengi kwani wahudumu wa ndege waliomfikisha hospitalini walitaka jambo lile liweze kuwa siri, hawakutaka kuishushia heshima kampuni yao ya usafiri wa anga ya Air Tanzania.



Waliona bora Rodgers kapona haraka sana na kuondoka, kabla vyombo vya habari havijainasa sura ya Rodgers na kuichafua kampuni hii ya Kitanzania. Rodgers alikua ameibalisha sura yake kwa kujifunga kiremba mithili ya mpemba wa Zanzibar, na kuvaa miwani iliyomfanya awe na mwonekano tofauti kabisa. Hivyo ndivyo Rodgers alivyoepuka kukamatwa na askari waliotumwa kumkamata kwenye uwanja wa ndege wa Mombasa Kenya.



Dar es salaam;

Raisi wa Tanzania hakukubali kushindwa, hakuwa tayali kumkosa Rodgers kirahisi namna ile. Aliamua kutumia pesa kumkamata adui yake kwani aliamini pesa ndiyo kila kitu Japo alifahamu mzee Jastin alihusika na kifo cha mwanae, lakini hakutaka kumkamata moja kwa moja bila kumpata kijana aliyempiga risasi na kumuua mwanae.



"welcome Africa! welcome Tanzania once again! ",(Karibu Afrika !Karibu Tanzania kwa mala nyingine tena) ilikuwa ni sauti ya raisi wa Tanzania, raisi kipenzi cha watu. Aliongea kwa furaha sana baada ya kumpokea mpelelezi wa kimataifa aliyekuwa amempatia fedha nyingi kwa ajili ya kuja Afrika kumtafuta Rodgers.



"Thank you! ,Tanzania ni nyumbani, "ilikuwa ni sauti ya Kendrick, Mtanzania pekee aliyepata bahati ya kufanya kazi katika mashirika makubwa ya kupambana na ugaidi duniani. Akiwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na nane tu, alibahatika kujiunga na jeshi la wananchi wa Tanzania. Juhudi zake katika mazoezi, zilimfanya apendwe sana na wakufunzi wake. Huo ndio ukawa mwanzo wa mafanikio ya Kendrick Mathias, kwani nafasi moja iliweza kutolewa na umoja wa mataifa kwa Tanzania, kutoa mwanafunzi mmoja akajifunze mafunzo zaidi ya kijeshi nchini Marekani, na baada ya mafunzo aweze kutumikia Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Kendrick kutokana na nidhamu pamoja na juhudi katika kujifunza, aliweza kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mafunzo hayo, mafunzo ambayo yaliweza kufanyika nchini Marekani.



Hatimaye Kendrick akawa gumzo! alikuwa mwanafunzi wa kwanza katika masomo yake, aliwashinda zaidi ya vijana wenzake mia moja inshirini na nane kutoka nchi washirika wa umoja wa mataifa.Alikuwa na uwezo wa karate kama vile alikuwa mzaliwa wa China, alifahamu kila kitu kuhusu utengenezaji wa siraha za nyuklia kama vile alikuwa Mkorea Kaskazini na isitoshe alikuwa na uwezo mkubwa katika matumizi ya kompyuta. Mashirika makubwa ya kupambana na ugaidi duniani kama FBI na CIA walimuhitaji Kendrik akafanye nao kazi, lakini Kendrick alikataa, alitaka kurudi Tanzania kulitumikia taifa lake.



Vikundi vya kigaidi havikuwa nyuma! waliposikia sifa za Kendrick zikitajwa na kuwa gumzo duniani kote. Mala baada ya kufaulu katika kiwango cha juu sana, katika mafunzo ya pamoja ya kijeshi yalioendeshwa na umoja wa mataifa(UN).Alqaeda, Alshabaabu na M23 walishindana kumgombania Kendrick, kundi hili lilipotaja pesa hii na kundi lingine likaweza kuongeza dau kwa Kendrick, lakini kijana huyu alikuwa mzarendo na mwenye nidhamu ya hali ya juu. Hakukubali kutumia uwezo wake aliopatiwa na Mungu kuua watu, alikataa pesa nyingi sana alizokuwa amepewa na magaidi hao. Hatimaye akaamua kujiunga na shirika la FBI lililoko nchini Marekani, na akaahidi kuwa tayali kulitumikia taifa lake la Tanzania kwa moyo wote pale litakapomuhitaji.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

…………………………………



Kuwasili kwa Kendrick kukawa gumzo kila kona nchini Tanzania, na Afrika Mashariki kwa ujumla. Wananchi wa Tanzania walichoshwa na mauaji yaliyosikika kila siku katika eneo la Kibiti mkoani Pwani.Walitaka kufahamu muhusika wa mauaji hayo na kisha aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria. Hawakutaka kulisikia neno "WATU WASIOJULIKANA " ,neno ambalo liliwaongezea hasira kila lilipotajwa katika stesheni za radio na televisheni, kila tukio la mauaji lilipofanyika.



"Chuma cha pua kimewasili!, nina uhakika, huyu mtu asiyejulikana aliyemuua mtoto wa raisi atakamatwa baada ya siku mbili tu ……",



"Muuaji mbona anajulikana, anaitwa Rodgers! naskia alama za vidole alizoziacha kwenye bunduki aliyoitumia, ndizo zimefanyiwa uchunguzi na wataalamu, na hatimaye wameweza kumtambua, naskia muuaji kakimbilia Kenya kujificha ",



Yalikuwa ni maongezi kati ya vijana wawili wa kijiweni, vijana ambao walikaa katika eneo moja la kuuzia magazeti na kusoma habari za Kendrik katika magazeti hayo,Kariakoo, Dar es salaam, nchini Tanzania.



…………………………………



Mwili wangu ulichoka, Rose alilala katika magoti yangu, huku mimi nikijikaza kiume na kuendelea kupekua kompyuta ya baba yake.Usiku mzima tangu baba yake aondoke nyumbani pale, mimi na Rose tulikesha tukipekua na kufungua mafaili mbalimbali ya siri katika kompyuta ya mzee Jastin. Hatimaye usingizi ulimchukua Rose kutokana na uchovu, lakini mimi niliendelea kuchezea kompyuta ile ya baba yake bila kupata hata chanzo chochote cha kutusaidia kufahamu ukweli wa maisha ya Rose.



"Rose! Rosee, amka mala moja ",



"Robert nimechoka mpenzi, niache nipumzike ",



"Angalia hili faili! limekataa kufunguka! Kaweka namba ya siri tofauti na jina lako ……",



"Unasema?, mmh Robert hapa kuna kitu ",yalikuwa ni maongezi kati yangu na Rose, lakini Rose alipoamka na kushuhudia faili lile kwa jinsi lilivyokuwa limefichwa lisiweze kuonekana kirahisi, na isitoshe kuwa na neno la siri tofauti na mafaili mengine, aliamini kuna jambo zito liliweza kuhifadhiwa ndani yake.



"THE PAINFUL SECRET "(siri ya maumivu), Rose alisoma kwa sauti kichwa cha habari cha faili lile, na kutufanya tuwe na hamu ya kujua nini ambacho kiliweza kuandikwa ndani yake.



"Jina Rose, ndio neno siri la mafaili yote, kwanini hili hapa kabadilisha! bila shaka alitambua faili hili sipaswi mimi kulifungua ",

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Unaweza kuwa sahihi Rose, lakini mambo yote yaliyokuwa kwenye kompyuta hukupaswa kuyafahamu ndio maana hakuwahi kukuambia neno la siri, neno siri Rose ulitumia kubahatisha tu " ,



"Mpenzi, hapa kuna kitu sio bure! nashauri Robert tufanye kamchezo kakubahatisha namba ya siri kama mwanzoni nilivyofanya ",



"Hiyo ndio njia pekee ya kufanya, naamini tutafanikiwa",tuliongea mimi na Rose huku tukishauriana jambo la kufanya, na bila kupoteza muda tulianza harakati za kutambua namba ya siri ya faili lile katika kompyuta ya baba yake mzee Jastin.



Kenya;

Rodgers akiwa katika kambi yao iliyoko Kisauni, Mombasa, nchini Kenya. Hofu ilimtawala alipopokea taarifa ya Kendrick kufika nchini Tanzania, alimfahamu vizuri Kendrick, kwani waliwahi kushiriki mafunzo ya kijeshi wote kwa pamoja nchini Tanzania kabla Kendrick hajachaguliwa kwenda katika mafunzo ya pamoja ya kijeshi nchini Marekani. Mafunzo ambayo yalijumuisha nchi wanachama wa umoja wa mataifa, huku kila nchi ikitoa mwanafunzi mmoja kuiwakilisha.



Rodgers baada ya kuona mafunzo yakiwa magumu, mafunzo yaliyohitaji vijana wenye nidhamu ya hali ya juu, na isitoshe aliweza kukosa nafasi ya kwenda Marekani. Nafasi ambayo ilichukuliwa na Kendrick, aliamua kutoroka kambini na kuachana kabisa na mafunzo ya kijeshi nchini Tanzania, na kujiunga na kikundi hatari sana kilichohusika na usambazaji wa madawa ya kulevya afrika Mashariki, kilichojulikana kama EADD (East African Drugs Dealers).Chama ambacho kilipigwa vita siku zote na serikali za Afrika Mashariki, lakini walishindwa kukitokomeza kwani baadhi ya vigogo wa serikali hizi walikuwa miongoni mwa wanachama wa shirika hili.



"Huyu jamaa ni hatari sana, kabla hajaenda kusoma Marekani alikuwa akitupiga mazoezini kama watoto, sasa hivi naamini ameiva vya kutosha ",Rodgers aliongea huku akiendelea na mazoezi yake kama kawaida, kwani hata yeye shirika lake lilimpeleka nchi kazaa kama Urusi na China kwenye mafunzo kadhaa ya kivita. Hivyo basi…! alikuwa na ujuzi mwingi na wa kutosha kupambana na Kendrick.



…………………………………



Mzee Jastin hatimaye alikuwa katika barabara ya kuelekea Tanga, huku vijana wake kadhaa wakiongozana naye. Waliamua kuikimbia ngome yao iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam, kwani waliamini muda wowote wangeweza kuvamiwa na jeshi la serikali ambalo lilimsaka Rodgers kila kona. Safari ya mzee Jastin ilianza usiku mala baada ya kutoka nyumbani kwake, na kutuacha mimi na Rose tukijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Alipofika Mbezi alichukua vijana wake, na kisha safari ya kuelekea Mombasa iliweza kuanza kwani aliona ndio sehemu salama ya yeye kujificha.



Asingeweza kutumia ndege! Kwani aliamini safari yake isingekuwa ya siri tena, na lazima safari yake ingeweza kuwekewa vikwazo.



Dar es salaam;

Mapenzi yalinoga,mpaka nikasahau mambo mengi ambayo Rose aliweza kunitendea na kuumiza mtima wangu.Alizidisha utundu katika mapenzi yetu, na kunifanya nianze kumuamini. Nilideka kama mtoto mchanga kila nilipokuwa naye, na kutufanya wote kuwa na furaha wakati wote. Tulipika pamoja, tukala pamoja, tukaoga pamoja na kulala kitanda kimoja kama mke na mume. Kusema ukweli maisha yalibadilika sana, niliamini Mungu aliweza kuona mateso yangu na kuamua kunifuta machozi ambayo yalichuruzika siku zote katika paji la uso wangu.



Zilikua zimepita siku tatu sasa, tangu mzee Jastin alipoikanyaga nyumba yake kwa dakika kadhaa na kisha kutoweka sehemu ambayo tulikuwa hatufahamu, mimi na mpenzi wangu Rose. Tangu atoweke, kazi pekee ambayo tulikuwa tukiifanya ilikuwa ni kuchezea kompyuta yake, kompyuta ambayo aliitumia kuhifadhia siri zake zote. Maneno ya matusi na kejeli aliyomtamkia Rose kabla ya kutoweka nyumbani kwake usiku, ndiyo yaliyotufanya tupekue kompyuta ya mzee Jastin, kutambua historia halisi ya Rose, kwani tuliamini kwa asilimia mia moja kuwa mzee yule hakuwa mwanae wa kumzaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



"Mpenzi njoo uone, faili limefunguka, wahii Rose! ",



"Acha utani Robert!! ",



"Njoo uhakikishe, Mungu wangu nini tena hii !……",



"Heeeh! umeandika namba zipi za siri mpaka faili limefunguka?, "



"Robert, nijibu basi, umeandika namba zipi za siri mpaka faili limefunguka……!" ,



"Mpenzi acha porojo! Angalia picha hizi na kisha soma historia fupi iliyoandikwa " ,



Nilikuwa mpole ghafla, sikuamini nilichokiona baada ya kufanikiwa kufungua faili ambalo lilikuwa limefichwa mbali sana, na kisha kuandikwa kichwa cha habari chenye kuleta maswali mengi kwa kila mtu aliyeweza kulifikia faili lile. Niliamua kumuita mpenzi wangu Rose, msichana mrembo sana niliyempenda kwa dhati. Rose alitoka Maliwatoni, hakufuta hata povu vizuri mwilini mwake, jambo pekee ambalo lilikuwa kichwani mwake na kulipatia uzito ni kuja kutazama siri ambayo ilikuwa imeandikwa ndani ya faili lile.



"The painful secret, (siri ya maumivu), ndio neno la siri la faili ,jina la faili hili ni sawa na neno lake la siri. ",niliongea huku nikishangaa picha ya mtoto mdogo wa kike, mtoto aliyeonekana ombaomba katika eneo la minzani, Mikese Morogoro.



"Huyu ni nani mpenzi? ",Rose aliweza kuniuliza swali, huku machozi yakimtoka. Sio kwamba hakufahamu jibu la swali ambalo aliweza kuniuliza, la hasha! alitaka kujiaminisha kama kweli fikra zake na zangu zilikuwa sahihi.



"Bila shaka huyu msichana mdogo ni wewe Rose! ",nilimjibu mpenzi wangu huku mapigo ya moyo wangu yakipiga kwa kasi sana.Kichwa kilianza kuuma, na nikajikuta napoteza fahamu baada ya kusoma historia fupi iliyokuwa imeandikwa chini ya picha ile.



"Robert! amka usinifanyie hivyo! amka tujue tunaanzia wapi kuwatafuta wazazi wangu ……" ,Rose alipiga kelele huku akilia baada ya mimi kupoteza fahamu, hakufahamu chanzo cha mimi kupoteza fahamu ghafla kiasi kile huku muhusika ambaye ni yeye akiwa katika hali ya kawaida tu.



Hakutambua kuwa msongo wa mawazo ndio ulinifanya niweze kupoteza fahamu, baada ya kusoma maelezo na historia ya Rose iliyokuwa imeandikwa chini ya picha ile..Baada ya kusoma jina Jacline, jina ambalo lilikuwa limeandikwa chini ya picha ya Rose akiwa kama ombaomba katika eneo la minzani, Mikese, Morogoro. Nilikumbuka miaka mingi sana iliyokuwa imepita nyuma, siku ambayo familia yetu ilikuwa na machungu sana, kwani mdogo wangu aliyeitwa Jacline aliweza kupotea.



Familia yetu yote, si baba wala si mama ,wote tulilia kwa huzuni huku tukimlaumu baba kwani yeye ndiye alikuwa chanzo cha Jacline kupotea. Alikuwa mvivu siku zote, alimuacha mama peke yake akipambana na shughuli za shambani kila siku, na mazao yalipouzwa na pesa kupatikana. Baba alimuibia mama pesa na kwenda kunywa pombe, huo ndio ukawa mwanzo wa Jacline kuanza maisha ya kuomba omba.



Kwani yeye kama mdogo wangu wa kunifuata, alipenda elimu kama mimi nilivyokuwa nikipenda kusoma, na siku zote alifuata nyayo zangu. Alipenda kusoma masomo ya ziada ili kuongeza ufaulu shuleni, lakini pesa alizozitegemea baba aliweza kuziiba na kwenda kunywa pombe. Ilibidi atafute nguo zilizochakaa, na kisha kwenda kuomba pesa kwa abiria wa mabasi, katika minzani ya Mikese.Neno sina wazazi, ndio lililowafanya watu wengi waweze kumuonea huruma na kumpatia msaada.



Siku ya kwanza aliomba omba na kupata pesa nyingi sana, zaidi ya elfu arobaini. Pesa ambazo tulizitumia kununulia vifaa vya shuleni, na kununua chakula. Huku kiasi kingine cha pesa kilichobakia, Jacline alikwenda kulipia masomo yake ya tuisheni.



Hatimaye omba omba ikawa kama moja ya kazi za Jacline, kwani kila baada ya kutoka shuleni, baba alimlazimisha kwenda kufanya kazi hiyo ili tuweze kupata pesa ya kununulia chakula, na baba apate pesa ya kunywea pombe.



Siku moja tulishangaa sana, kwani Jacline hakurudi nyumbani. Tulisubili mpaka tukachoka, tulilia tukanyamanza. Hatimaye siku iliweza kupita, baadaye wiki, mwezi na hatimaye mwaka ukaisha bila kufahamu Jacline alipotelea wapi.



Wazazi wangu waliamua kuweka msiba,na hatimaye tukaamua kumsahau kabisa Jacline kwani tuliamini aliweza kupoteza maisha. Hatukutaka kujikumbusha machungu, familia ikaamua kutomzungumzia kabisa Jacline, huku tukichoma moto hata picha zake, pamoja na nguo zake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ndio maana nilishtuka sana baada ya kuona gauni lake alilokuwa amevaa, lakini haikuishia hapo, nilijikuta nazimia kabisa baada ya kuona jina Jacline likiwa limeandikwa chini ya picha ya Rose. Sikuamini kama kweli nilimpenda mdogo wangu kimapenzi,na isitoshe tumefanya tendo la ndoa bila kutambua kama Rose alikuwa mdogo wangu wa kuzaliwa na baba mmoja na mama mmoja. Msongo huo wa mawazo ndio ulinifanya niishiwe nguvu na kupoteza fahamu, kusema ukweli usilo lijua ni kama usiku wa giza, kwani sikujua nini kitamtokea Rose baada ya kumwambia kama mimi ndiye kaka yake wa kuzaliwa naye. Enzi zile nilikuwa dalasa la nne na yeye dalasa la tatu, tulikuwa wakubwa tu lakini sikufahamu kwanini yeye hakuwa na kumbukumbu yoyote ile, siku zote aliniambia alizaliwa Dar es salaam. Kwa upande wangu,nilimfananisha sana Rose na mdogo wangu Jacline kila nilipomtazama, kwani madimpo yake yaliipamba sura yake kila alipotabasamu na hakuishia hapo, alikuwa mzuri sana wa sura kama alivyokuwa mdogo wangu. Sikutambua kuwa niliyemfananisha na mdogo wangu na kumuona kama mke wangu, alikuwa ndiye Jacline ndugu yangu wa kuzaliwa familia moja.



………………………………



Kenya;

Mzee Jastini akiwa ameshawasili Kenya, baada ya kusafiri kwa boti, boti ambayo alipanda na vijana wake katika bandari ya Tanga. Hakutaka kusafiri kwa gari tena na kupitia katika mpaka, kwani askari wa mpakani lazima wangeivujisha siri ya mfanyabiashara huyu maarufu nchini Tanzania kusafiri kwa siri ,tena kwa gari, kwani hadhi yake ni ya kusafiri kwa ndege. Lazima wangeingiwa na wasiwasi juu ya safari yake hiyo.



"Rodgers peleka mzigo huu Uganda! ",



"Sawa bosi!, "ilikuwa ni sauti ya Rodgers ikikubali amli kutoka kwa bosi wake msaidizi mzee Jastin, hakuwa na wasiwasi wa kupeleka mzigo wa madawa ya kulevya nchini Uganda, kwani aliamini hali ilikua shwari bila kufahamu kuwa kijana machachali Kendrick alikuwa kazini kumsaka.





Mheshimiwa raisi hatimaye alitabasamu, alikuwa na matumaini ya kumtia mikonono kijana Rodgers, muhusika wa mauaji ya mwanae. Kwani kwa masaa machache tu ambayo Kendrick alikuwa amefika Tanzania na kuanza upelelezi wake, tayali alikuwa ameshagundua mambo mengi sana kuhusu siri za muuaji.



"Mheshimiwa, unafahamu kundi hili la EADD ?",



"Hapana Kendrick!, silifahamu kundi hili ",



"Mhh Hulifahamu kundi hili linalohusika na usambazaji wa madawa ya kulevya Afrika mashariki? ………



"Ohoo! nimekupata kijana wangu, unazungumzia chama hiki tunachokipiga vita kila siku, "THE EAST AFRICAN GRUGS DEALERS ",



"Ndio mkuu, kwa kifupi ndo kinaitwa ivyo, EADD " ,



"Ahaaa, nilikuwa sijaelewa vizuri! mawazo yangu yalikuwa yanafikilia mbali sana, siunajua majukumu ya kuongoza nchi yalivyo magumu ",



"Nafahamu mkuu!, kwahiyo kwa uchunguzi wa matukio mbalimbali ya kimataifa ambayo yamewahi kutokea, inaonesha Rodgers ni mmoja wa vijana wa kundi hili, na bila shaka kuna wakubwa zake ",



"Huu ndio wakati sahihi, wa kuliteketeza kundi hili,, nakuamini kijana wangu ",yalikuwa ni mazungumzo kati ya Kendrick na mheshimiwa raisi, mazungumzo ambayo yalikuwa yakifanyika ikulu jijini Dar es salaam, baada ya Kendrick kuwasilisha taarifa za maendeleo ya upelelezi wake, ili raisi aweze kutambua hatua aliyoifikia.Jambo ambalo lilimfurahisha sana raisi, na kujikuta akiwa na matumaini makubwa sana ya kulipiza kisasi kwa yeyote yule aliyehusika na mauaji ya mwanae.



…………………………………



Kijana handsome na aliyeweza kumvutia msichana yoyote yule kimapenzi, alisimama katika barabara moja kubwa ya kuelekea jijini Nairobi. Kusema ukweli kijana huyu alipendeza sana, kwani alikuwa amevalia suti nyeupe iliyoonekana kuwa ya gharama kubwa sana, huku chini kiatu cheupe kikiupamba mguu wake. Hakuweza kusahau kofia, vazi ambalo lilifunika upala wake wa asiri usiweze kuonekana. Kutokana na kupendelea kuvaa miwani, hakuweza kuisahau pia. Alivaa miwani mizuri sana, na kila kitu ambacho alikuwa amekivaa kilikuwa na rangi nyeupe, na kumfanya aonekane smart na mtu yeyote yule ambaye aliweza kumtazama. Kijana huyu hakuwa mwingine, bali Rodgers, akiwa ameweka ndevu za bandia na kumfanya awe na mwonekano tofauti kabisa na Rodgers ambaye alikuwa akitafutwa na serikali ya Tanzania. Huku donge nono likitolewa kwa yeyote yule atakayefanikisha kukamatwa kwake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Samahani kaka! sijui wewe aenda wapi ?",ilikuwa ni sauti ya msichana mrembo sana, msichana aliyekuwa amelisogeza gari lake dogo pembeni, usawa ambao Rodgers alikuwa amesimama na kisha kumuuliza swali kwani alimuona akiwa anajaribu kusimamisha magari kadhaa yaliopita barabarani hapo bila mafanikio.



Kijana Rodgers akiwa ameshikilia briefcase lake, briefcase ambalo lilikuwa na unga wa sembe ndani yake kama jinsi vijana wengi wa uswahilini wanavyouita. Alitabasamu kwa furaha, kwani ni masaa mengi yalikuwa yamepita tangu gari linalomilikiwa na kundi lake kumshusha mahali hapo. Gari hilo lisingeweza kuendelea na safari kwani liliogopa kukaguliwa na matrafiki mbalimbali pamoja na polisi waliokuwa wanakagua kila gari ambalo lilikuwa linaelekea Nairobi, likitokea Mombasa.



"Naelekea Nairobi mrembo! bila shaka na wewe unaelekea huko, "Rodgers aliongea huku akitabasamu kumtega msichana yule, aliamini kabisa urahisi wa msichana yule ungemuwezesha kufika Nairobi kwa urahisi bila kugundulika na kisha kutimiza kazi aliyokuwa ametumwa.



"Wewe ni Mtanzania? unaongea kiswahili nzuri sana, hata mimi inaelekea Nairobi, wewe ni kijana mzuri sana huwezi kosa mtu kama mimi ya kukubeba kwa gari yangu ",binti yule mweusi na mrembo wa asiri, raia wa Kenya. Alimuuliza swali kuhusu rafudhi ya Kiswahili aliyokuwa nayo, bila shaka aliamini Rodgers alikuwa ni Mtanzania.

Kwasababu hakuweza kumtambua kuwa ndiye muuaji aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba nchini Tanzania na kukimbilia Mombasa ,Rodgers aliamua kukubali kuwa alikuwa Mtanzania ili kukwepa maswali mengi zaidi kutoka kwa binti yule.



"Ndio mimi ni Mtanzania, naomba pandisha vioo, nipeleke haraka sana Nairobi kuna abiria wangu namuwahishia mzigo huu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nairobi, trafiki yoyote akikusimamisha mlegezee sauti akuache uendelee na safari kwa sababu atatuchelewesha, nikifikisha mzigo nitakulipa pesa nzuri sana ",Rodgers alizungumza na kumlaghai binti yule, binti ambaye hakuwa na kipingamizi chochote kile kwani alikuwa tayali amevutiva na Rodgers kimapenzi.



"Usjali kaka, huna haja ya kunilipa pesa, siwezi jua! pengine waweza kuwa my husband badaye ",msichana yule alimjibu Rodgers kimasihara, kauli ambayo pengine mtu yeyote angefikilia ilikuwa na utani ndani yake. Kumbe haikuwa kweli hata kidogo!, binti yule wa Kijaruo alimaanisha kile alichokuwa amekiongea.



Dar es salaam

Hatimaye niliweza kupata fahamu, nilijaribu kuchunguza mazingira niliyokuwa na kuyatambua vizuri sana. Bila shaka yoyote ile niliamini nilikuwa hosptalini kutokana na pilikapilika za manesi wodini.



"Nimefikaje hapa Rose! " ,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Usjali mpenzi pumzika kwanza, mimi ndio nilikuleta hapa asubuhi baada ya kupoteza fahamu " ,nilimuuliza swali Rose, kwani alikuwa ameketi pembeni yangu kitandani. Lakini jibu lake lilinifanya nikumbuke kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Hakupaswa kuniita mpenzi wake, hivyo basi! nilikuwa na kazi kubwa ya kumueleza kwa urefu zaidi aweze kunielewa kuwa mimi ni kaka yake wa damu, tulizaliwa na baba mmoja pamoja na mama mmoja.



"Pumzika, harafu tuombe ruhusa ya kurudi nyumbani, kisha unielezee jambo ambalo limekufanya ushituke na kupoteza fahamu " ,Rose aliongea kwa ujasiri, hakutambua maumivu makubwa yasiyotibika atakayoyapata baada ya kufahamu ukweli na chanzo cha mimi kupoteza fahamu. Nilibaki tu nimejilaza nikimtazama, huku nikifikilia namna nitakavyoanza kumsimulia ukweli juu ya maisha yetu mpaka aweze kunielewa.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog