Search This Blog

Friday 18 November 2022

MPANGO WA SIRI - 2

 






Simulizi : Mpango Wa Siri
Sehemu Ya Pili (2)




Daniel Mwaseba sasa alikuwa anaingia Nangurukuru kwa mwendo mkali. Alikata kona ya kushoto. Njia iliyokuwa inaelekea mkoani Lindi. Alikuwa ameziacha mbali kidogo pikipiki nne, zilizokuwa zinamfuata...



Kijiji cha Nangurukuru ni miongoni mwa vijiji Maarufu zaidi kwa biashara wilayani Kilwa. Jiografia ya kijiji hiki Ilikuwa nzuri. Magari yaendao mikoa ya Kusini Ilikuwa ni lazima wapite katika barabara iliyopita katika kijiji hiki. Kupitia barabara hiyo kuu, ilikuza sana biashara na uchumi kwa ujumla katika kijiji hiko.

Nangurukuru Kulikuwa na njia kuu nne. Barabara ya kuelekea jijini Dar es salaam. Barabara ya kuelekea Njinjo. Barabara ya kuelekea mjini Kilwa Masoko, alikokuwa anatoka Daniel. Na barabara ya kuelekea mkoani Lindi ambako sasa Daniel alikuwa anaelekea.



Uwepo wa barabara hizo nne uliwachanganya wauaji wale waendesha pikipiki walipofika Nangurukuru. Hawakujua Daniel kaelekea wapi?.

Wakajaribu kuulizia watu Noah nyeusi imeelekea wapi hawakupata jibu. Kila mtu alikuwa bize na biashara zake. Waache kuuza samaki wao, wawe makini na gari zisiziwahusu ?

Wakaamua kugawana barabara. Pikipiki mbili zilielekea barabara ya Dar es salaam. Ambapo walihisi Daniel itakuwa kaifata barabara hiyo. Pikipiki moja ikaelekea barabara ya Njinjo. Na pikipiki ya nne ilielekea barabara iliyokuwa inaelekea Lindi.



Kikao cha siri, cha watu sita kiliendelea huko Kilwa Kisiwani. Baada ya Kishoka kuelezea jinsi alivyohisi kutekwa kwa Noah yao. Na kuamua kwenda kutega bomu katika gari ya Daniel ili limlipue atakapokuja kulichukua gari hilo.

Sasa ilikuwa zamu ya kumsikiliza mwenyekiti wa kikao hiko. Wenyewe walipenda kumuita Bosi Lee. Alikuwa mtu mwenye maarifa sana. Ujuzi wa kupigana mtindo wowote. Mtu asiyeogopa kifo. Mtu ambaye burudani yake ni kushudia mtu amekufa kwa kutolewa utumbo!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sasa waheshimiwa inabidi tufanye kitu,unaj......" Hakumalizia sentensi yake. Simu yake ya kiganjani iliita........



Upande wa Daniel Mwaseba alikuwa bado anaendesha gari kwa kasi. Sasa alikaribia kijiji cha mavuji.

Alikuwa porini sana. Giza likiwa linaingia kwa kasi. Akasimamisha gari.

Alishuka ndani ya gari, akawa anarudi alikotoka kwa miguu. Alimuacha kwenye gari Edina. Aliamini kwa pigo alilompiga pamoja na kamba alizomfunga hawezi kufanya ujanja wowote. Pigo lile la nguvu akipigwa mwanaume aliyeshiba humhamisha katika dunia kwa masaa kumi na mbili. Sasa je yule msichana mrembo si atalala siku tatu?. Hakujua. Edina hakuwa msichana wa kawaida. Ni mstuko tu ndio uliomfanya apigwe kizembe vile. Edina alikuwa zaidi ya mwanamme aliyeshiba. Kwa nje alionekana mwanamke mrembo, ila alikuwa mwanamke hodari, mwanamke mwenye hila nyingi na katili wa kupitiliza.



Daniel alirudi nyuma kama mita mia tatu toka pale alipoliacha gari lake. Mkono wa kulia ukiwa imara kashika bastola. Mkono wa kushoto kabeba kamba ndefu ya katani. Kamba maalum, kwa kazi maalumu...

Alifika mahali alipopakusudia. Kulikuwa na mti mkubwa aina ya muarobaini pembeni ya barabara. Akaifunga ile kamba. Akaipitisha katikati ya barabara hadi upande wa pili. Ambapo aliishika ncha iliyobaki ya ile kamba. Alikuwa mviziaji akiyewavizia wakimbizaji.

Kwa mbali aliona taa ya pikipiki.



"vibaraka wanakuja" Alijisemea kimoyomoyo.



Giza lilikuwa upande wa Daniel. Mwendesha pikipiki alikosa umakini kidogo. Kwa mwendo wa kasi akawa anaikaribia ile kamba, kamba ngumu ya katani. Kwa nguvu zake zote Daniel aliivuta ile kamba. Ikamvaa yule mtu mwenye pikipiki shingoni. Alirushwa juu!



Daniel alitegemea yule mtu atajibwaga barabarani na kujifia. Haikuwa hivyo. Yule mtu alikuwa mjuaji. Alijiviringisha kulekule hewani kwa mtindo wa sarakasi. Alitua kwenye lami akiwa amesimama. Ile pikipiki yake ikiburizika mbali na pale. Ikiwa haitamaniki!



Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana. Kilimuacha Daniel akiwa katika mshangao mkuu. Hakutegemea kama yule mtu ataweza kuepuka kifo kwa namna ile. Yule mtu alivyotuachini akaigusa shingo yake kwa mkono wa kulia. Alihisi kuna mkwaruzo kidogo. Sasa Alikuwa anaangaza kumtafuta aliyomchezea mchezo ule hakumwona. Kwa tahadhari alisogea hadi eneo la tukio. Aliiona ile kamba iliyotaka kumnyonga.



"Bila ya kulegeza shingo ningekuwa marehemu leo" Aliwaza.



Akiwa upande wa pili wa barabara Daniel alimwona vizuri yule mtu. Alikuwa na uwezo wa kumpiga bastola palepale alipo na kummaliza. Lakini hakufanya hivyo. Alivutiwa na uwezo ulioonyeshwa na yule mtu. Alikuwa na hamu. Hamu ya kupimana nae ubavu!



Haya sasa Daniel anataka kwenda kupambana na jamaa aliyeonesha umahiri mkubwa gizani, je ataweza? Kule nako kuna simu ya siri imepigwa, je itakuwa inahusu nini? Na imetoka kwa nani? Njoo tena kesho hapa Halfani Sudy akusimulie..







Inspekta Nyange aliacha kuangalia ile filamu.



"huu si wakati wa kuangalia filamu, ni wakati wa kupambana”. Alisema polepole. Alienda chumbani kwake akabeba zana ambazo alijua zitamsaidia katika mapambano.



***



Mwenyekiti wa kikao, kule Kilwa Kisiwani alipokea simu yake. Aliyekuwa anampigia ni mkurugenzi wa Mpango wa siri. Alipokea simu huku akitoka nje. Kumsikiliza Mkurugenzi.Baada ya dakika tano alirejea, akiwa amebadilika,

taarifa alizopewa kutoka kwenye simu ziliharibu kabisa mwelekeo wa sakata hili!



Baada ya kuongea na simu ile Bosi Lee alirudi katika kikao chao cha siri na muhimu kwa mafanikio ya mpango wao. Aliwaeleza wajumbe wa kikao kile kila kitu alichoambiwa na Mkurugenzi.



"Mpango wetu unakaribia mwisho. Lakini upo katika hatua hatari sana kwa sasa. Taarifa zetu kuhusu Mpango huu zimenaswa na mpelelezi namba moja Tanzania, Daniel Mwaseba. Alikuja hapa kama Polisi wa kawaida. Kumbe hakuwa Polisi wa kawaida. Amekuja kuusambaratisha Mpango wetu. Anataka kukwamisha mpango wetu. Sasa inabidi tufanye juu chini kuhakisha Daniel Mwaseba anaenda kuzimu. Kama tunahitaji mpango huu tuufanikishe. Na kama tunapenda uhai wetu pia.Daniel ni mtu hatari sana. Tusipokuwa makini tutaumbuka. Bado tunapeleleza Daniel alinasa vipi siri za Mpango huu" Mwenyekiti alimaliza kwa sauti ya upole sana. Haikuwa kawaida yake kuongea kwa sauti namna ile. Ila alikuwa anaijua shughuli ya mpelelezi huyu. Daniel Mwaseba alikuwa na moto.....



***



Kule upande wa fundi Daniel Mwaseba. Kijana mwendesha pikipiki alikuwa makini kumtafuta Daniel pale porini. Kama mzimu Daniel alitokea mbele yake! Wanaume wawili walikuwa wanatazamana sasa...

Giza halikuwazuia kuonana. Wote walikuwa na macho ya ajabu. Walionana vyema gizani. Kwa kasi ya ajabu yule kijana alimfata Daniel. Kwa kasi ileile alipiga Inaitwa 'Tripple kick'. Alimpiga mateke matatu kwa mpigo, miguuni, kiunoni na shingoni. Daniel aliyumba. Hajui ashike wapi. Wakati Daniel akijifikiria, yule kijana alirusha ngumi ya nguvu iliyokuwa inaelekea kwenye mwamba wa pua wa Daniel, Daniel aliiona, akayumba kidogo ngumi ilipita. Alisikia mvumo tu wa hewa wa ngumi ile.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Daniel sasa alijipanga vizuri. Alipiga ngumi safi iliyotua kwenye mbavu za yule kijana, akaguna kidogo. Daniel alirusha teke lililotua sawia katika shingo ya jamaa. Jamaa akakosa mwelekeo sasa, Daniel akalipa. Alimpiga yule jamaa 'Tripple kick' kama aliyopigwa yeye. Jamaa aliunguruma kama Simba. Jamaa hasira zikampanda na umakini ulimpotea. Alirusha ngumu sita mfululizo, tatu kwa mkono wa kulia, na tatu kwa mkono wa kushoto. Hakuna ngumi iliyompata Daniel. Alizipangua zote kiurahisi. Ngumi zile hazikurushwa kiufundi. Daniel aliitumia hiyo nafasi ya kutomakinika kwa jamaa. Alimpiga ngumi mzito chini ya kidevu. Jamaa alirushwa hewani kwa uzito wa ngumi ile. Meno mawili aliyaacha hukohuko hewani. Jamaa alianguka chini kama gunia la viazi. Daniel alimkanyaga kwa nguvu usoni kwa mguu wake wa kushoto, ilikuwa kama anaua nyoka vile. Jamaa alisalimu amri. Roho ilitangulia kuzimu kuusubiri mwili dhalimu wa jamaa yule. Aliaga dunia akiwa anaustajabu uwezo wa Daniel Mwaseba!



Ilichukua kama dakika kumi na tano pambano la wababe hawa. Daniel alirudi kwenye gari ili aendelee na mpango wake. Mpango wa kwenda kumhoji mateka wake wa kike.

Daniel aliamini uwezo wa kamba alizomfunga mwanamke yule kwa umakini. Miguuni na mikononi. Na zaidi aliamini uwezo wa ile judo kali aliyompiga shingoni. Akafungua mlango wa dereva kwa funguo ili aliendeshe gari kwenda porini kumhoji mwanamke yule. Aliamini kwa mateso atakayompa angeutapika tu ukweli. Lakini aliambulia patupu!

Hakukuwepo maiti ya Edgar wala mateka wake wa kike. Wote walitoweka...



***



Kikao cha siri ndani ya jumba kubwa kule Kilwa Kisiwani kilimalizika. Kilimalizika kwa kupeana mpango mkakati na majukumu mazito. Sasa hawakuwa na utani wala simile. Waliamua hivi, watu watano waende katika Nyumba ya Inspekta Nyange kummaliza. Na kuna kundi lingine liliongezwa kwenye msako wa kumtafuta Daniel. Sasa waliamini Daniel ndiye adui yao mkubwa na hatari zaidi.

Lakini wakiwa bado mle ndani waliona kitu cha ajabu. Kupitia kwenye runinga walimwona mtu akinyemelea jumba lao. Ndio Alikuwa ni inspekta Nyange...

Alionekana dhahiri na macho kumi na mbili ya wajumbe wa kikao kile cha siri.



Baada ya kutoka nyumbani kwake. Akiwa na nguvu na ari mpya. Huku akiwa ameapa kuwamaliza wauaji wale, alipokea simu. Simu ya majigambo toka kwa wauaji. Wakimuahidi kumuua sekundi chache zijazo. Inspekta Nyange hakutetemeka. Vitisho vilikuwa moja ya majukumu yake kazini.

Baada ya simu ile kukatwa, Inspekta Nyange alimpigia John Siseme. Rafiki yake wa siku nyingi, alikuwa anafanya kazi katika kampuni ya simu ambayo ile simu ya vitisho ilikuwa inatoka. John Siseme alimueleza kila kitu kuhusu simu ile. Kuwa ilikuwa inatokea mnara wa Kilwa Kisiwani. Inspekta Nyange alienda bandarini, kupanda boti na kuelekea Kilwa Kisiwani.

Ni nyumba mbili tu ndizo ambazo inspekta Nyange alizitilia shaka Kilwa Kisiwani. Ni machale ya kiaskari tu ndiyo yaliyomfanya azitilie shaka nyumba zile. Moja ya nyumba hizo ni hii aliyokuwa anainyemelea. Bila kujua anaonekana waziwazi na kamera. Nyumba ile ilitegwa kamera kila pembe. Zilizokuwa zinaonesha matukio yanayotokea nje ya jengo lile. Kwa bahati mbaya inspekta Nyange hakuwa analijua hilo.



Kikao sasa kilifungwa rasmi. Wakawa wanaangalia runinga. Ikiyomuonesha mnyatiaji. Walishuhudia akiwanyonga walinzi wawili kwa mikono kwa ustadi mkubwa. Na kuuruka ukuta. Wakajua wamevamiwa na Daniel Mwaseba....



Inspekta Nyange aliendelea kunyatia ndani ya uwanja wa jumba lile la ajabu. Uwepo wa walinzi wenye silaha kali uliamwaminisha yupo katika sehemu sahihi. Alizipongeza hisia zake. Alikuwa na faraja moyoni kuelekea kuutibua mchezo huu. Mchezo mchafu!!!

Alikuwa tayari kuua...

Tayari Kuuwawa...



Bosi aliinuka mwenyewe. "Ngoja nikamlete Mwanaharamu" Aling'aka.

Inspekta Nyange sasa alikuwa kwenye uwanja mpana. Akielekea katika mlango wa kuingia katika nyumba ile hatari. Alipofika mlangoni, na mlango ulifunguliwa Inspekta Nyange alikutana uso kwa uso na Bosi...





Bosi aliinuka mwenyewe.

"Ngoja nikamlete Mwanaharamu" Aling'aka.

Inspekta Nyange sasa alikuwa kwenye uwanja mpana. Akielekea katika mlango wa kuingia katika nyumba ile hatari. Alipofika mlangoni, na mlango ulifunguliwa Inspekta Nyange alikutana uso kwa uso na Bosi...



****



Kule porini Ilikuwa shughuli pevu. Daniel aliamini yeye sio wa kutorokwa vile. Alijua kwa vyovyote yule mwanamke atakuwa maeneo yaleyale. Akisubiri Daniel afanye kosa lolote. Ulikuwa mviziano wa watu wenye akili.



Akiwa pembeni porini kidogo Edina alimwona vizuri Daniel. Aliamua kutoka na maiti ya Edgar ili kumchanganya tu Daniel. Aamini Edgar hakufa...

Na sasa alikuwa anamnyatia Daniel kwa nyuma pale mlangoni aliposimama. Akiwa ameshika gongo kubwa la mti. Alimkaribia kabisa. Edina Alikuwa mnyatiaji aliyebobea. Ardhi haikutoa ishara yoyote kuwa inakanyagwa na kiumbe chenye uhai.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Edina alilinyanyua lile gongo kwa mikono yake yote miwili. Akawa analielekeza kwa nguvu zake zote katika kisogo cha Daniel. Aliyekuwa amegeukia ndani ya gari...

Kama ingelikuwa mimi na wewe tusingeweza sikia mnyato wa mwanadada Edina Reuben. Lakini siyo kwa Daniel Mwaseba. Hakuwa na masikio ya binadamu wa kawaida. Hakuwa na hisia za binadamu wa kawaida. Alikuwa na uwezo wa kuhisi hatari yoyote inayomnyemlea karibu yake.



Ujio wa Edina akiwa na gongo kubwa aliuhisi zamani. Kwa kutumia macho yake yenye 'sight mirror' alimwona vizuri sana Edina akija kwa kumnyemelea. Alikuwa na tabasamu, maana kutoroka kwa Edina kulikuwa kunamuogopesha zaidi kuliko hili gongo alilokuwa anakuja nalo.

Kwa kasi ya ajabu Daniel alijivuta pembeni. Lile gongo halikukosa pa kupiga, lilipiga kwa nguvu katika siti ya mbele ya dereva. Edina akaliachia lile rungu. Sasa alikuwa mikono mitupu. Akitazamana na Daniel uso kwa macho...



Daniel alikuwa na uwezo mkubwa wa kupigana Na Edina. Lakini hakutaka. Alijua kwa sasa anatakiwa afanye vitu kwa haraka. Risasi moja ya kichwa ilitosha kutanguliza roho ya Edina kuzimu wakati mwili wake ukisubiri kuliwa na tai pale porini.

Daniel akawasha gari na kurudi Masoko. Kuukabili mchezo mchafu.



"Mwanaume hakimbii matatizo, bali anayakabili"Daniel alijisemea akiwa garini.



****



Inspekta Nyange alikutana uso kwa uso na Bosi Lee. Bosi katili kwa maadui zake. Mnoko kwa wafanyakazi wake. Walikuwa wameelekeziana bastola. Walikuwa hawaongei mithili ya mabubu. Kila mmoja akimsubiri mwenzie afanye kosa dogo limgharimu.

Bahati mbaya ilikuwa kwa inspekta Nyange. Aliingia kwenye ngome iliyojipanga. Yenye walinzi wasiopungua mia.Yeye aliwaua watatu tu akiamini amewamaliza. Kumbe walinzi wengine walipewa taarifa na Bosi wamwache mnyatiaji, waone mwisho wa unyatiaji wake.



Mara, alisikia spana zikilia kwa nyuma yake. Haikuwa nguvu ya spana moja bila shaka kulikuwa na washika spana wengi. Alipogeuka alikutana na kundi la watu lisiopungua hamsini. Walikuwa wamevaa maovaroli ya bluu na spana mkononi kama mafundi magari vile.Kugeuka ndio lilikuwa kosa la mwaka akilolisubiri Bosi Lee alifanye askari yule. Kosa ambalo lilimgharimu Inspekta Nyange.



Bosi Lee alirusha teke kali lililoenda moja kwa moja kwenye mkono wa kulia wa Inspekta Nyange. Mkono ambao ulikuwa umeshika bastola. Uzito wa teke lile ulitosha kudondosha bastola chini. Inspekta Nyange alikuwa mikono mitupu sasa.

Bosi Lee nae aliweka bastola yake chini. Sasa ulikuwa muda muafaka wa kuoneshana uwezo. Wakiwa mbele ya macho ya watu hamsini ambao walikuwa hawana msaada wowote kwa Inspekta Nyange, wenye spana mkononi.Na wengine wakishuhudia kwenye runinga kule ndani.

Inspekta Nyange alikutana uso kwa uso na Lee. Zilianza ngumi.



Bosi Lee alikuwa na hasira sana. Akikumbuka alivyosurubiwa na Mzee Mirambo hasira zilizidi kumpanda. Alikuwa anaruka mithili ya nyani. Inspekta Nyange alipigwa sana. Wakampeleka katika chumba cha mateso kusubiri hukumu. Safari hii walikuwa makini sana. Walimfunga pingu miguuni na mikononi. Na funguo aliichukua mwenyewe Bosi Lee. Hakutaka kosa lolote lifanyike.

Ulikuwa wakati mgumu sana kwa Inspekta Nyange. Aliumizwa vibaya sana na Lee. Kuwekwa chumba kisichokuwa na hewa kuliongeza mateso pia. Laiti angejua kuwa yale hayakuwa mateso. Mateso makuu yalikuwa njiani yanakuja...



Pambano hili liliwakumbusha washika spana pambano lililofanyika siku moja nyuma. Pambano kati ya Bosi Lee na Mzee Mirambo. Walikutana katika uwanja huu. Pamoja na uzee wake lakini Mzee Mirambo alimuumbua sana Bosi Lee.



****



Jana yake yalitokea haya...



Ilikuwa siku ya kuwatembelea wanafunzi wasomao shule ya Msingi Kisiwani. Shule ambayo mtoto wa kiume wa Mzee Mirambo alikuwa anasoma. Mzee Mirambo alikuwa ameongozana na mke wake. Ilikuwa siku ya furaha sana kwa familia hii.



Walikuwa wamempelekea zawadi nyingi sana mtoto wao aliyekuwa anaitwa Nasri.

Walimkabidhi zawadi zake walikula pamoja na kunywa. Wakati wanarudi kwa kutumia boti la abiria ndipo Mzee Mirambo alikutana na mtu wa ajabu ndani ya boti.



Mzee Mirambo alikuwa ni mstaafu. Aliishi maisha yake akiwa mfanyakazi mwaminifu wa Usalama wa Taifa. Alikuwa mzoefu sana na sura za wahalifu. Leo hii alipomuona mtu huyu ndani ya boti alijua amekutana na mhalifu wa kutisha. Alianza kumfatilia kwa siri kwa kutumia macho wakiwa ndani ya boti.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mtu akiyefatiliwa na macho ya Mzee Mirambo alikuwa ni mtu hatari. Muuaji mzoefu mwenye kugundua hatari kabla haijamkaribia. Siku zote husafiri kwa boti zao ila leo hii alipanda boti ya abiria. Alikuwa anaenda kununua mafuta ya kwenye boti zao Kilwa Masoko. Waliishiwa kabisa mafuta.



Ndani ya boti Edgar Bituro hakuwa na wasiwasi wowote kabla. Ila macho yake yalipogongana na mzee mmoja ndani ya boti ile alistuka. Yalikuwa siyo macho ya kawaida.Edgar akawa na tahadhari tangu alivyogongana na macho ya mzee yule.



Sasa Edgar na Mzee Mirambo walikuwa wanaviziana. Kila mmoja akimwangalia mwenzie kwa kuibia kila walipopata wasaa. Dakika tano zilitosha kuwasafirisha abiria wa boti lile kutoka Kisiwani mpaka Kilwa Masoko. Boti lililopakia watu wawili wakioviziana. Mviziaji akiviziwa na mviziaji.



Edgar Bituro alikuwa wa kwanza kushuka kwenye ile boti, huku mzee Mirambo akiwa mtu wa mwisho kushuka katika boti ile. Moja kwa moja Edgar alielekea kwenye Noah nyeusi iliyokuwa imeegesha pale bandarini. Bila shaka ikimsubiri yeye. Mzee Mirambo na mkewe wakapanda kwenye gari yao nao wakitoka pale bandarini.



Mzee Mirambo alikuwa anaifatilia ile Noah nyeusi bila Edgar kujua kama anafatiliwa na mfatiliaji makini. Hata mkewe waliokuwa pamoja ndani ya gari hakujua kama wanamfatilia mtu.



Gari aliyopanda Edgar ilipofika karibu na benki ya NMB Kilwa ilisimama. Alipofika pale Mzee Mirambo nae alisimamisha gari. Hawakushuka ndari ya gari. Mlango wa mbele wa Noah ulifunguliwa. Alishuka msichana mrembo kwa madaha akiwa anaelekea benki, Edina.



Baada ya dakika tano Edgar nae alishuka. Alikuwa anaongea na simu huku akielekea ndani ya benki. Bila shaka alikuwa anaongea na yule mwanadada mrefu aliyetangulia muda mfupi uliopita.



Mzee Mirambo nae alishuka. Uelekeo wake ulikuwa ni kwenye mashine ya ya kutolea pesa ya benki ile. Wakati Edgar na Edina wao walielekea ndani ya benki ile. Mkewe Mzee Mirambo hakuwa anaelewa lolote. Alikuwa anasinzia ndani ya gari yao. Akimsubiri mumewe aliyemuaga anaenda kutoa pesa.



Edina na Edgar sasa walitoka ndani ya benki. Edgar akiwa amebeba bahasha kubwa mbili. Edgar alipoangalia kwenye mashine ya ATM alistuka. Alimuona yule mzee aliyemtilia shaka kule kwenye boti. Kengele za hatari ziligonga katika kichwa chake...



“Sasa kumekucha" Aliropoka kwa nguvu.



"Kuna nini?" Edina alimuuliza.



"Tulia" Alimnyamazisha.Edina alitulia, alijua kuna itakuwa kaona kitu sio cha kawaida.



Wakaingia kwenye gari yao. Edina akiwa dereva, Edgar akiwa amekaa katika siti ya abiria na mzee Kishoka akiwa ametulia katika siti ya nyuma ya dereva. Kwa kutumia vioo vya pembeni Edgar aliliona gari la yule mzee likitoka nalo. Likiwafuata... Sasa Edgar akaamini alichokihisi.Akamsimulia Edina habari za mzee yule.



"Mwache atufuate ana hamu ya kufa"Edina alijibu kwa kifupi baada ya Edgar kumsimulia habari za mzee yule.



Wakaingia kwenye gari yao. Edina akiwa dereva, Edgar akiwa amekaa katika siti ya abiria na mzee Kishoka akiwa ametulia katika siti ya nyuma ya dereva. Kwa kutumia vioo vya pembeni Edgar aliliona gari la yule mzee likitoka nalo. Likiwafuata... Sasa Edgar akaamini alichokihisi. Akamsimulia Edina habari za mzee yule.



"Mwache atufuate ana hamu ya kufa"Edina alijibu kwa kifupi baada ya Edgar kumsimulia habari za mzee yule.

Edina aliongeza kasi kidogo ya gari lao. Nia yake ni kuuona mrejesho wa yule Mzee. walikuwa sahihi, walikuwa wanafuatwa!

Alipoongeza kasi na gari ya nyuma yao iliyokuwa inaendeshwa na Mzee Mirambo nayo iliongezwa kasi maradufu...

Mzee Mirambo naye sasa aliona mchezo umekuwa mtamu.Aliupenda.



"Mke wangu itabidi utangulie nyumbani na gari. Mimi nataka nipitie kwa Mzee Silimu” Mzee Mirambo alimdanganya mkewe. Mzee Silimu Alikuwa rafiki wa siku nyingi wa Mzee Mirambo.



"Sawa mume wangu. Lakini usichelewe kurudi si unajua niko mpweke"Mke wa Mzee Mirambo alijibu. Alikubaliana na uwongo wa mumewe. Akamruhusu.



Gari ya akina Edgar ilifuata njia ya kuelekea sokoni. Njia iliyokuwa inapita katika saluni ya Las Vegas. Saluni maarufu ya kiume Wilayani Kilwa, walikata kona kuelekea sokoni. Hiyo ndio nafasi akiyoihitaji Mzee Mirambo. Alisimamisha gari lake na kushuka harakaharaka. Akimwacha mkewe akitangulia na gari nyumbani.

Yeye alikodi pikipiki. Sasa alikuwa juu ya pikipiki aliyekuwa anaiendesha yeye mwenyewe. Alikubaliana na mwenye pikipiki kuirejesha baada ya masaa matatu. Kutokana na umaarufu wake alipewa pikipiki. Aliliwasha na kufuata windo lake.

Hakuwa na sababu ya msingi kulifuata gari lile. Kwani kutilia shaka sura ya Edgar ndio sababu sahihi ya kulifuata gari lile? Lakini dhamira ndani ya moyo wake ilimwambia'kuna kitu cha siri kwa waliopo ndani ya gari lile'.Mzee Mirambo aliisikiliza dhamira hiyo na kuifuata.



Akiwa juu ya pikipiki Mzee Mirambo aligairi kulifuata lile gari. Alijua kuendelea kulifuata ni kujianika mbele ya wauaji. Sasa aling'oa pikipiki na kurudi walikotoka. Alirudi bandarini kulisubiri windo lake. Alijua kuwa alikuwa anacheza pata potea kwa maana hakuwa na uhakika kama lile gari lingerejea tena bandarini.

Ile Noah nyeusi ililipita nyuma ya maduka ya pale sokoni kwa kasi,likazunguka 'round about' ya Toa Hoja na kuelekea kulia, likipitia kwenye kijiwe maarufu cha Chama kimoja cha siasa. Lengo la msafara huu ni kuthibitisha zaidi juu ya ufatiliwaji wao. Kisha kuchukua hatua. Bila shaka hatua ya kuuwa.... Lakini walipoangalia kwenye 'sight mirror' hawakuliona lile gari. Walibabaika sasa. Hawakujua limewapotea vipi lile gari katika rada zao.

Kwa mbele walikata kulia barabara iliyokuwa inawarejesha Bandarini. Lile gari hawakuliona tena lilikuwa kama limeyeyuka katika macho yao. Wakaanza kudharau hisia zao. Na kuamini yule Mzee huenda alikuwa tu katika mihangaiko yake ya kimaisha.

Sasa walielekea kwenye kituo cha mafuta, ambayo ndio ilikuwa dhamira yao kuu tangu wanatoka Kilwa Kisiwani. Wakanunua mafuta ya kutosha kwa ajili ya boti zao. Wakaanza safari ya kurudi bandarini. Hawakujua kama walikuwa wanasubiriwa na Mzee wao. Mzee Mirambo...

Walipofika bandarini hawakupanda boti za abiria. Walikuwa na madumu mengi ya mafuta. Iliwabidi Wakodi boti iliyowavusha mpaka ng'ambo ya pili. Walijifanya wamesahau kabisa habari za yule Mzee.

Mzee Mirambo alishuhudia kila hatua waliyokuwa wanapiga.

Mzee Mirambo nae aliamua kukodi boti iliyomvusha kumpeleka Kilwa Kisiwani, kulifata windo lake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walipofika Kilwa Kisiwani kina Edgar walipokelewa na vijana kumi waliovaa maovaroli ya bluu. Kila kijana alibeba dumu moja la mafuta. Walielekea kambini kwao. Hakukuwa na gari aina yoyote ndani ya Kisiwa hiki muhimu kwa historia ya Kilwa na Tanzania kwa ujumla. Wenyeji wa Kisiwa kile walitumia zaidi usafiri wa baiskeli.



Mzee Mirambo alilifatilia windo lake kwa umakini mkubwa sana. Uwepo wa magofu na vichaka vichache ulimsaidia katika kuufatilia msafara ule wa watu kumi na mbili.

Wakati Mzee Mirambo akiwawinda akina Edgar, bila kujua na yeye alikuwa anawindwa. Hatua chache nyuma yake alikuwa anafuatwa na Mzee mmoja....

Aliokuwa anawawinda hawakuwa watu wa kawaida. Walikuwa makini katika kila hatua waliyokuwa wanapiga na akili nyingi sana. Pamoja na kutoliona gari la Mzee Mirambo lakini hawakuacha kujilinda.



"Ni kosa kumdharau adui yeyote" Hii ni kanuni namba moja ndani ya kundi hili hatari.

Ingawa Mzee Mirambo aliwashuhudia watu wawili wakishuka katika Noah nyeusi lakini ndani ya gari lile hakukuwa na watu wawili. Katika siti ya nyuma ya dereva kulikuwa na mzee makini ametulia. Hakuwa na papara wala maneno. Na ni yeye aliyeshauri kina Edgar watangulia yeye akiwalinda kwa nyuma. Mpango wa Mzee yule makini ulifanikiwa. Baada ya akina Edgar kukodi boti na kuondoka, alimuona yule Mzee nae akikodi boti. Bila shaka kuwafata akina Edgar. Baada ya dakika moja nae alikodi boti kumfatilia yule Mzee. Na sasa yuko hatua chache nyuma yake vichakani. Mzee huyu akiyemuinda mwindaji alikuwa anajulikana kama Mzee Kishoka....

Akina Edgar walifika getini ndani ya nyumba ile kubwa. Mlinzi aliyekuwa na bunduki mkononi aliwafungulia geti. Mzee Mirambo alimshuhudia mlinzi yule na zaidi alishuhudia bunduki ile mkononi. Akajipongeza kimoyomoyo. Hisia zake mbaya juu ya watu hawa alihisi ziko sahihi. Nyumba kulindwa na bunduki hakikuwa kitu cha kawaida katika kisiwa hiki.



Kule ndani, katika chumba kimoja ndani ya nyumba ile ilishuhudia kila kinachoendelea kuizunguka nyumba ile. Runinga iliyokuwa katika chumba kile ilikuwa inauwezo wa kuonesha mita mia tatu kuizunguka nyumba ile.

Iliwawaonesha akina Edgar wakija na madumu yao ya mafuta. Mtu wa pili alipoonekana kwenye runinga ile mtazamaji wa runinga ile alistuka. Alimwona mtu ambaye hakuwa na kibari cha kuingia katika nyumba ile.

Mtazamaji wa runinga alimpigia simu Kishoka, kwakuwa hakumuona katika msafara ule. Lilikuwa kosa, simu ile ya Bosi Lee kwenda kwa Kishoka ilizua kosa la kiufundi...



Wakati Mzee Mirambo akinyemelea kuelekea katika nyumba ile aliyohisi kuna jambo la siri na la hatari linaloendelea, Kishoka alikuwa mita chache nyuma yake akiwa amejibana katika kichaka kimoja akifuatilia nyendo za Mzee yule. Mara simu ya mkononi ya Kishoka iliita kwa sauti kubwa, alisahau kuiweka simu yake kwenye mtetemo au kimya. Mara nyingi wanapokuwa katika harakati kama hizi huweka simu zao kwenye mtetemo au kimya .Leo hii Kishoka alifanya kosa la kiufundi.



Sauti ile ya mlio wa simu ya Kishoka ilitua vizuri katika sikio la Mzee Mirambo. Naye hakufanya ajizi, kwa haraka alitoa bastola na kuelekeza pale ulipotokea mlio wa simu. Kishoka nae hakutaka kufanya kosa lengine la kiufundi. Kosa si kosa, siku zote kosa kurudia kosa. Badala ya kutoa simu iliyokuwa inaita yeye alitoa bastola iliyokuwa imetulia tuli katika mfuko wa koti lake. Kishoka alitoa bastola na kumuelekezea Mzee Mirambo. Wanaume wawili sasa wakajikuta wameelekezeana bastola...Hatari!!!



Ilikuwa wahi nikuwahi, fyatua nikufyatue, subiri nikusubiri.



Mtazamaji wa runinga kule ndani alimuona yule mtu akiyenyemelea katika himaya yake na kuelekeza kwa nyuma bastola. Hakuwa anamwona mtu aliyeelekezewa bastola. Kwakuwa Kishoka alikuwa nje ya mita mia tatu ambazo ziliwezwa kunaswa na kamera zao.



Kishoka alitoka kichakani akiwa makini. Alijua kosa moja tu linaweza kumpeleka kuzimu. Sasa wote walikuwa ndani ya himaya ya Bosi Lee. Walionekana vizuri kwenye runinga kule ndani. Ulikuwa muelekezano wa bastola ya wazee wawili hatari. Walivimbiana mithili ya majogoo...



Ndani ya dakika tano hakuna aliyemsemesha mwenzie pia hakuna aliyefanya kosa lolote.

Kule ndani bosi Lee alishika mkonga wa simu ya mezani na kumpigia Edgar.



"Kuna mvamizi ndani ya kambi, yuko mlango wa nyuma kule, mwambie Kishoka amlete akiwa hai" Alitoa amri bosi Lee.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kule ndani bosi Lee alishika mkonga wa simu ya mezani na kumpigia Edgar.



"Kuna mvamizi ndani ya kambi, yuko mlango wa nyuma kule, mwambie Kishoka amlete akiwa hai" Alitoa amri bosi Lee.



"Sawa mkuu" Edgar alijibu.



Watu hamsini wakiwa na maovaroli ya bluu. Spana mkononi wakizigonga gonga walizunguka duara kuwazunguka Kishoka na Mirambo. Watu hao walikuwa wafanyakazi wa Ocafona army waliopatikana sehemu mbalimbali za nchi kuja Kilwa kutekeleza Mpango wa Siri.

Duara la wafanyakazi wale ilikuwa hasara kwa Mzee Mirambo na faida kwa Kishoka. Mzee Mirambo alikosa uthabiti na kutetereka. Kishoka akawa anamfata na mzee Mirambo anarudi nyuma. Walijikuta wameingia kambini. Kwa mtindo ule. Kabla Mzee Mirambo hajafikiria cha kufanya mlango wa nyumba kubwa ulifunguliwa na Bosi Lee alitoka.Mzee Mirambo alikuwa anatazamana macho kwa macho na Lee. Kiongozi wa wilaya katika mpango huu haramu na wa siri..



"Shusheni silaha chini, wanaume kamili wanapambana kwa mikono yao" Bosi Lee alitamka maneno haya kwa majigambo makubwa. Silaha ziliwekwa chini. Na pambano kati ya Mzee Kishoka na Mzee Mirambo lilifunguliwa rasmi.

Wakiwa wamezungukwa na watu wasiopungua hamsini wanaume hawa walianza kupigana. Mzee Kishoka alikuwa anamwona dhaifu sana Mzee Mirambo. Edgar na Edina walikuwa wamekaa katika kona moja ya uwanja ule wakishuhudia pambano. Wote walikuwa wanajiamini. Wakiuamini sana uwezo wa Kishoka na kumdharau Mzee Mirambo.



'Don't judge a book by its cover'



Kishoka alimfata Mzee Mirambo kwa mtindo wa sarakasi. Alimkuta Mzee Mirambo yuko imara. Alivyotua tu chini toka sarakasini alikutana ana kwa ana na ngumi ya nguvu iliyotua sawia katika pua yake. Mzee Kishoka alianza kutoka damu puani. Ngumi ile iliharibu ladha ya pambano lile. Kishoka alikosa umakini. Mzee Mirambo alirusha mateke matatu ya kinyumenyume mfululizo. Yote matatu yalitua barabara katika kichwa cha Mzee Kishoka. Wakati Kishoka anatua chini mithili ya gunia la pamba, Mzee Mirambo alikuwa amesimama imara kimya....

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bosi Lee aliona zile ni dharau. Kupigwa kwa mtu aliyemwamini kama Kishoka tena ndani ya himaya yake ilikuwa ni dharau. Baada ya kutoa dozi kwa Kishoka Mzee Mirambo alitulia tuli. Akisubiri amri Itakayofuata toka kwa Lee.

Haikuwa amri. Lee alisogea mwenyewe uwanjani. Kupambana na Mzee yule aliyeonekana kuwa tishio sasa. Uwanja mzima ulikuwa kimya. Watu wote wakiwa na shauku ya kujua hatima ya mpambano huu unaofuata.



****



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog