Search This Blog

Friday 18 November 2022

MPANGO WA SIRI - 1

 






IMEANDIKWA NA : HALFANI SUDY



*********************************************************************************



Simulizi : Mpango Wa Siri
Sehemu Ya Kwanza (1)


 Ilikuwa ni siku iliyoisha vizuri ndani ya Mji mdogo wa Kitalii Kilwa Masoko. Hakukuwa na taarifa yoyote kubwa ya kihalifu katika vitabu vya jeshi la Polisi ndani ya Kilwa Masoko. Ni mwaka wa tano sasa mfululizo Mji huu ulitulia. Askari walikuwa wamepumzika, habari za mauaji walikuwa wanazisikia mikoa mingine tu. Kwao kulikuwa shwari.

Ndani ya jumba moja ndani ya Mji wa Masoko kulikuwa na mtu mmoja amelala usingizi mzito. Lakini alistuka ghafla kutoka usingizini. Moyo wake uliruka sarakasi ndani ya kifua chake. Alistuka sana. Kupigiwa simu saa 9 za usiku iliashiria hali si shwari. Inspekta Nyange akaangalia kioo cha simu yake tena, namba iliyompigia ilikuwa katika mfumo wa ‘private number’, hali ya wasiwasi ikazidi kumuandama



"Halooo" Aliyepiga simu aliuliza.

“Habari” Inspekta Nyange alisema kwa sauti iliyotoka usingizini.

“Kuna mauaji!” Sauti kavu ya mpiga simu ilisema.

“Wapi?” Inspekta Nyange aliuliza kwa wahka.

“Mtaa wa Lumumba,nyumba namba tano!” Sauti ya kwenye simu ilisema tena bila wasiwasi.

“Wewe ni nani?” inspekta Nyange aliuliza huku akikaa vizuri kitandani.

“Msamaria mwema” Jamaa alisema bila woga.



Inspekta Nyange hakupata hata nafasi ya kuitikia wala kusaili zaidi. Simu ya mtu yule aliyejiita msamaria mwema ilikatika, au tunaweza sema ilikatwa !



Bila kufikiria mara mbili, Inspekta Nyange alivaa nguo zake za Polisi na kuchukua silaha yake, bastola, alitoka chumbani kwake hadi ukumbini, akatoa simu yake ya kiganjani na kupiga .

“Halo ”

“Halo Inspekta ”

“Tukutane mtaa wa Lumumba nyumba namba tano kuna mauaji!, njoo na askari wenzio wanne ”

“Sawa mkuu ”

Alipofika karibu na mtaa wa Lumumba alipokewa na vilio. Vilio vya maombelezo. Ilikuwa yapata saa kumi alfajiri wakati Inspekta Nyange anawasili eneo la tukio, lakini wingi wa watu wa eneo lile ulimshangaza sana, kulikuwa na umati mkubwa wa watu,wakilia!

Wakilia kwa uchungu mkubwa sana!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Inspekta Nyange alienda moja kwa moja katika nyumba namba tano. Nyumba aliyoelekezwa na Msamaria mwema aliyetumia ‘private number’.

Umati wa watu ulikuwa umejaa, lakini baada ya kumuona Inspekta Nyange amevaa sare za jeshi la Polisi walimpisha. Alifika ukumbini na kusalimia aliowakuta hapo, baada ya salamu aliulizia mwenyeji wa nyumba ile.

"Wenye nyumba wote wameuwawa! " Mama mmoja alijibu.

“wewe ni nani ?”

“Jirani ”

“Balozi wa Mtaa huu yuko wapi?”

“Mimi hapa ” Mzee mwengine aliyekuwa pembeni alijibu.

“Twendeni ”

Mama huyo aliyekuwa jirani, pamoja na Balozi ndio waliomuongoza Inspekta Nyange hadi katika miili ya marehemu, maiti zilikuwa zimefunikwa na shuka nyeupe zilizokuwa zimelowa damu !

Zilikuwa maiti za watu watatu, mwanaume mmoja, mwanamke na mtoto mdogo wa kiume.



Inspekta Nyange alianza kufunua shuka ya maiti wa kiume.

Ilikuwa hatari!

Kwa mtu wa kawaida asingeweza kuiangalia maiti ile, ila Inspekta Nyange hakuwa mtu wa kawaida. Maiti ilikutana na muuaji mkatili anayeijua vyema kazi yake. Utumbo wa Mwanamme yule ulikuwa nje ya tumbo lake, sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa vibaya na kuwekwa kifuani kwake. Hakuwa na macho, bali kulikuwa na matundu mawili katika sehemu yanapokaa macho.

Maiti ilitobolewa macho na kutolewa!

Yule mama hakuweza kuvumilia. Alitapika vibaya huku akilia.

Inspekta Nyange aliifunua maiti ya pili. Ilikuwa maiti ya mwanamke. Maiti hii ilitisha kuliko maiti ile ya kwanza. Maiti iliachwa na uwazi tumboni, haikuwa na utumbo, haikuwa na macho, haikuwa na maziwa. Ilikuwa na vidonda vikubwa katika mapaja yake. Alipofungua maiti ya mtoto alishangaa, mtoto hakuwa na alama yoyote katika mwili wake, bila shaka itakuwa alikuwa amenyongwa kwa mikono!

Baada ya muda mfupi Polisi wa kituo cha Polisi Masoko waliwasili na gari lao. Baada ya kufanya uchunguzi wao wa awali wakabeba maiti na kuzipeleka katika hospitali ya wilaya Kinyonga kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Inspekta Nyange alibaki kwa ajili ya mahojiano. Aliwahoji yule mama pamoja na Balozi na watu wengine wawili watatu.

Lakini hawakuwa wanajua lolote.

Inspekta Nyange alichanganyikiwa sana. Akaanza kuikagua nyumba yote ile. Nyumba ya Mzee Mirambo. Alitajiwa jina la mwenye nyumba na yule Mama jirani . Aliyejitambulisha kwa jina la Mama Juma.

Nyumba ya Mzee Mirambo ilikuwa nyumba yenye vyumba vitatu vya kulala. Ilikuwa na sebule moja kubwa. Jiko na choo cha ndani cha kisasa. Ilikuwa nyumba nzuri sana, bora na ya kisasa.

Katika vyumba vya awali viwili walivyopita hawakupata lolote la maana. Lakini walipofika jikoni walikutana na jambo la kustusha sana. Kulikuwa na harufu. Harufu ambayo haijawahi kupenya kwenye pua za inspekta Nyange, Balozi wala Mama Juma tangu wazaliwe.

Katika jiko la umeme mule jikoni kulikuwa na sufuria iliyofunikwa kwa sahani ya bati. Ndani ya sufuria hiyo ndiyo kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kinatoa harufu ile ya ajabu!

Kwa uangalifu mkubwa Inspekta Nyange alifunua ile sahani ya bati kwa kutumia kitambaa. Harufu sasa ilisambaa zaidi mule jikoni. Sasa ikaanza kusambaa hadi watu walioko ukumbini waliipata.

Inspekta Nyange alichungulia ndani ya sufuria ile ajue kuna nini. Macho yalimtoka pima! Ndani ya sufuria kulikuwa na utumbo wa binadamu, maziwa pamoja na macho. Vilikuwa vinachemshwa. Bila shaka yalikuwa macho, maziwa na utumbo wa yule mama maiti!

Hali ilikuwa ya kutia hofu sana !. Inspekta Nyange alikuwa mzoefu wa matukio ya kutisha kama yale lakini hili lilimtisha sana!

Mama Juma alishindwa kustahamili. Miguu yake ilisaliti mwili wake, miguu ilishindwa kustahamili uzito wa mwili wa Mama yule. Alianguka chini mithili ya mzigo. Alikuwa amezimia !

Inspekta Nyange alitoka nje kwa mwendo wa haraka na kuita vijana wanne. Waliokuja kusaidia kumtoa nje mama Kessy akiwa hajitambui wakishirikiana na Balozi.

Inspekta Nyange aliendelea kuikagua nyumba ile, alienda jikoni ambako hakukuta kitu chochote cha maana, kumsaidia katika upelelezi wake.

Akatoka na kuelekea stoo ya nyumba ile. Huko nako hakuona la maana zaidi ya magunia machache ya mkaa na maboksi matupu. Wakati anatoka nje ya stoo ile akaona kipande cha karatasi chini. Akakiokota. Ilikuwa ni karatasi nyeupe iliyoandikwa kwa wino mwekundu!

Inspekta Nyange aliiangalia kwa makini, akagundua kitu. Karatasi ile haikuandikwa kwa wino wa kalamu. Iliandikwa kwa wino wa damu. Bila shaka Damu ya binadamu!

Umakini wa Inspekta Nyange uliongezeka maradufu. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka kwa mbali. Mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi. Alikuwa nahamu, hamu ya kujua kilichoandikwa katika kikaratasi kile.

Akaanza kukisoma. Karatasi ile iliandikwa maneno mawili tu.

'Mpango wa siri'



Umakini wa Inspekta Nyange uliongezeka maradufu. Kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka kwa mbali. Mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi. Alikuwa nahamu, hamu ya kujua kilichoandikwa katika kikaratasi kile.

Akaanza kukisoma. Karatasi ile iliandikwa maneno mawili tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



'Mpango wa Siri''



Hayo ni maneno pekee yaliyoandikwa katika karatasi ile kwa kutumia damu.

Inspekta Nyange alitabasamu kidogo. Halikuwa tabasamu halisi. Lilikuwa tabasamu la hasira. Hasira ya kuwakamata wauaji.



Alitoka stoo na kuelekea bafuni. Hakukuta chochote cha ajabu. Alitoka nje ya nyumba ile kupitia sebuleni. Aliwaaga waombolezaji aliowakuta pale. Akatoka nje.



Pale nje aliwaona wakina mama wakimpepea mama Juma. Aliyeanza kuzinduka na kuonekana kupata ahueni sasa.



*****

Inspekta Nyange alienda moja kwa moja kituo cha Polisi. Aliingia ofisini kwake bila kusalimia mtu pale kaunta. Alikuwa na mawazo sana. Hakika Inspekta Nyange alichanganyikiwa mno.



“Sitaki mgeni yeyote ” Alisema kwa sauti ya amri kumwambia katibu muhtasi wake.



“Sawa afande” Katibu Muhtasi wake alijibu.



Inspekta Nyange alijifungia mlango kwa ndani. Alikaa kwenye kiti akiwa kaiinamia meza. Aliwaza sasa mlolongo wa matukio kuanzia tangu alipopigiwa alfajiri ile simu alfajiri .



"Hii ni dharau" alijikuta amesema kwa sauti. Kwa asilimia zote alihisi aliyempigia ile simu alfajiri bila shaka atakuwa anahusika moja kwa moja katika kadhia hili.



"kwanini atumie 'private number' kama yeye ni Msamaria Mwema ?, alijiuliza mwenyewe.



Inspekta Nyange aliona dharau kubwa sana kupigiwa simu na muuaji. Na kuachiwa ujumbe wa vitisho pia.



“Eti Mpango wa siri! “Nitawasafisha tu!”

Akanyanyuka kwenye kiti.Akasogelea friji ndogo iliyopo ofisini kwake.Akafungua.Akatoa maji safi ya kunywa.Akapiga funda refu.Akarudi kwenye kiti. Akatulia.

Akavuta mkonga wa simu ya mezani ya pale ofisini.Akabonyeza namba fulani za simu ya upande wa pili ikaanza kuita na kupokelewa.

“Habari afande”

“Safi afande”

“Upo wapi?”

“Ndio naingia ofisini afande”

“Nakuhitaji sasa hivi ofisini kwangu”

“Sawa afande”



Baada ya dakika tano afande Edwin aliwasili. Aligonga mlango. Inspekta Nyange alinyanyuka kitini na kwenda kufungua. Baada ya salamu na saluti Inspekta Nyange alimuelezea Edwin kuhusu mauaji yale ya kikatili. Na kumkabidhi aishughulikie kesi ile.

Edwin alikuwa kijana anayeaminiwa zaidi katika kituo kile cha Polisi cha Masoko. Alikuwa kijana mkakamavu na jasiri. Aliyefudhu kwa kiwango cha juu katika fani za mapigano ya judo na karate alizosomea nchini China. Alikuwa kaiva hasa !



Inspekta Nyange kumkabidhi kesi ile ngumu ya mauaji afande Edwin alijiona ameutua mzigo mzito kichwani mwake .



" kuwa makini lakini Edwin maana hatujui adui ni nani?, na amejipanga vipi?"



“Sawa Mkuu”.



Baada ya Edwin kuondoka inspekta Nyange nae alitoka ofisini. Akiwa na matumaini tele, alijiona kama nusu ya kazi ya kuwakamata wauaji ameimaliza. Hakujua, Hakujua!



Usiku wa manane simu ya Inspekta Nyange iliita. Inspekta Nyange alikurupuka toka usingizini. Kuangalia namba inayompigia ilikuwa katika mfumo wa ‘private number’ tena. Moyo wake uliruka katika kifua chake. Inspekta Nyange aliichukua simu huku akitetemeka. Alikuwa anategemea kupokea taarifa mbaya kutoka katika simu hiyo. Kilichomtetemesha zaidi ni swali alilokuwa akijiuliza



"ni nani kauliwa safari hii?. Na kwa mtindo gani?"



"Haloo"



“Haloo”



“Kuna mauaji nyumba namba arobaini na tano mtaa wa Mkumilu”

Simu ikakatwa!



Inspekta Nyange alichanganyikiwa hasa kupokea taarifa ile. Alikuwa anaijua vizuri nyumba iliyokuwa inazungumziwa. Ni yeye ndiye aliyemtafutia nyumba Mpangaji wa nyumba hiyo, ilikuwa ni namba ya nyumba anayoishi afande Edwin!



Inspekta Nyange aliamka. Leo hakuvaa sare za Polisi. Alivaa suruali ya kitambaa nyeusi na shati jeupe. Chini alivaa viatu vyeusi vilivyochongoka, maarufu kama mkuki moyoni. Hakusahau Bastola.Wakati anatoka alikumbuka kuangalia saa yake ya ukutani, sebuleni kwake. Ilikuwa saa kumi alfajiri. Muda uleule aliopigiwa simu ya mauaji ya jana.



Alipanda pikipiki lake. Safari Mkumilu. Akiwa juu ya piki piki inspekta Nyange aliwaza mengi. Alifikiri kwanini anawahofia wahalifu kiasi cha kutetemeka.Ilhali yeye ndio mwenye dhamana ya kuwatia mkononi wahalifu hao. Sasa alivaa moyo wa kijasiri wa kupambana na wahalifu.Kuumaliza Mchezo mchafu unaoendelea !

Inspekta Nyange aliwaza ni nani atakuwa wamemuua safari hii?.Haikumuuungia akilini kabisa kuwa wauaji wale wamemuua Afande Edwin. Alikuwa anauamini sana uwezo wa Edwin katika mapambano ya ana kwa ana lakini alisahau kitu kimoja. Hakuwa anafahamu hata chembe uwezo wa upande wa pili. Upande wa wauaji!



Kutoka mtaa wa Faya anaokaa Inspekta Nyange mpaka mtaa wa Mkumilu anaokaa Afande Edwin ni mwendo usiozidi dakika kumi kwa pikipiki. Safari hii Inspekta Nyange hakuwapigia Polisi kituoni kuwataarifu juu ya taarifa ile ya mauaji. Lakini alipofika aliwakuta Polisi wake wameshafika tayari.Kulikuwa na watu wachache nje ya nyumba ya afande Edwin.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alimvuta kijana mmoja pembeni na kumuuliza

“kimetokea nini?.Kwakuwa Inspekta Nyange Alikuwa amevaa kiraia kijana yule hakujua kama anaongea na polisi.

"Kuna Njagu kapoteza ndani humo" Yule kijana alijibu kwa lugha ya mtaani.

Taarifa ile ilimstua sana Inspekta Nyange. Hakutegemea taarifa ya kuuwawa kwa Afande Edwin.Sasa akaelewa kidogo juu ya uwezo na ubora walionao wauaji.Ikabidi aingie ndani kwenda kuhakikisha. Ni kweli afande Edwin aliuuwawa?.

Alifika ukumbini.Alikuta watu sita wapo pale ukumbini.Inspekta Nyange aliwatambua watu wawili kati ya wale sita.Afande Mwita aliyekuwa katika sare safi za askari Polisi. Na Evelyne, Mchumba wa afande Edwin.

Inspekta Nyange aliwasalimia wote kwa pamoja.Wakaitikia.Evelyne au Eva kama afande Edwin alivyozoea kumwita Alikuwa amevimba sura. Bila shaka kwa kulia muda mrefu .

Inspekta Nyange alitambulishwa wale watu wanne waliobaki.Kulikuwa na Mzee mmoja, mwenyekiti wa mtaa. Nduguye Edwin wa kiume. Na vijana wawili ndugu wa Eva.



Baada ya utambulisho Inspekta Nyange aliingia chumbani ambako kulikuwepo mwili wa marehemu. Mle chumbani aliwakuta mapolisi wanne. Wote wakampigia saluti.Hakujishughulisha kuzijibu saluti zao.Chini sakafuni kulikuwa na mwili wa mtu uliofunikwa kwa kanga. Kanga ilikuwa imelowa damu.

"Funua"akaamrisha. Afande mmoja akafunua ili Inspekta Nyange auone mwili wa marehemu. Ilikuwa ni kasheshe! Haukuwa mwili wa Afande Edwin bali yalikuwa mabaki ya vipande vya mwili wa Afande Edwin. Kila kiungo kilitenganishwa toka kwa uliokuwa mwili wa Afande Edwin.Mguu kwake, kichwa kwake, kiuno kwake! kila kitu kwake!

Inspekta Nyange hakuamini macho yake.Kuuliwa kwa afande Edwin kulimtambulisha Inspekta Nyange ubora wa wauaji.Kumuua mtu aliyefudhu kimapigano kwa kiwango cha juu kama Edwin kulihitaji mtu hatari, hatari kuliko hatari yenyewe!

Kuuliwa kinyama kwa Afande Edwin pia kulimjulisha mambo mawili Inspekta Nyange. Moja, wauaji walipata taarifa kwamba jukumu la kuwatafuta wauaji wa Mzee Mirambo na familia yake amepewa Edwin. Au itakuwa Edwin alipiga hatua katika kuwakamata au kukaribia kuwakamata wauaji hao.

Nadharia ya kwanza hakuipa nguvu sana,nani wa kutoa siri ilhali jukumu la Edwin kuwasaka wauaji alilitoa yeye tena wakiwa wawili tu.

Nadharia ya pili ilimuingia akilini kidogo Inspekta Nyange. Itakuwa Edwin alipiga hatua kuwakaribia wauaji.Ni hatua gani hiyo?. Akaanza kuitafuta ndani ya Nyumba ya Edwin.

Alizunguka Nyumba mzima ya Edwin, hakuambulia kitu.Akarudi katika chumba cha Edwin. Mwili wa Edwin sasa ilikuwa umeshatolewa.Kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.

Akafungua kabati la nguo la Edwin.Akakutana na nguo chache za Edwin, na nguo za kike. Bila shaka zilikuwa za mchumba wake Edwin.

Inspekta Nyange akatafuta kila alipopafikiria. Kwenye droo zote. Alipanda darini, alichungulia uvunguni hakupata kitu.Wakati anatoka nje,akakiona kikaratasi cheupe chini Sebuleni, aliinama na kukiokota. Alikisoma. Kilikuwa kimeandikwa maneno yaliyomstua sana



Inspekta Nyange akatafuta kila alipopafikiria. Kwenye droo zote. Alipanda darini, alichungulia uvunguni hakupata kitu.Wakati anatoka nje,akakiona kikaratasi cheupe chini Sebuleni, aliinama na kukiokota. Alikisoma.

Alikiangalia kwa makini. Wino mwekundu wa damu iliyokuwa imeganda. Kudhihirisha walimuua zamani Afande Edwin.Akakichukua kile kikaratasi .

Baada ya kuwahoji wafiwa wote.Hakuambulia kitu. Hawakuwa wanajua kitu.Wote walikuja eneo la tukio wakati Edwin kashauwawa.

Inspekta Nyange akiwa ametopea kwenye dimbwi la mawazo simu yake ikaita.OCD Kilwa, ndio jina lililosomeka katika kioo cha simu yake. Akaipokea.



"Haloo”

“Uko wapi Inspekta ?”

“Nyumbani kwa Afande Edwin”

“Njoo ofisini kwangu haraka”

“Sawa mkuu”

Inspekta Nyange alikuwa anaitwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilwa. Akiwa na mavazi yake ya kiraia, alienda kuitikia wito. Baada ya dakika kumi na tano alifika ofisini kwa Bosi wake.

" Habari afande”

“Mzuri Mkuu”

“Najua unazo taarifa za Mauaji yanayoendelea ”

“Ninazo afande ”

“Umechukua hatua gani hadi sasa Inspekta ?”

“Nilimkabidhi Edwin jukumu la kuwakamata Wauaji,naye wamemuua” OCD hakuonekana kustuka, bila shaka itakuwa alishasikia habari za mauaji ya Edwin.

“Sasa nataka nikupe mtu wa kusaidiana nae ili kuhakikisha munawakamata wauaji wote ”

“Sawa Mkuu ” Inspekta Nyange aliitikia huku akisubiri kuambiwa askari atakayepewa kushirikiana nae.

“Utafanya kazi ni yule askari mpya. Anaitwa Daniel ”

"Sawa afande"

Inspekta Nyange aliitikia huku akiwa na taswira kichwani mwake.Taswira ya kuuona utumbo wa Daniel saa kumi alfajiri, huku mwili wake ukiwa umekatwa katwa vipande.Aliamini lazima Daniel atauwawa!

“Kama Edwin aliyefudhu kimapigano ya karate na judo kwa kiwango cha juu tena nchini China walimkatakata vipande mithili ya viazi dume. Sasa huyu Daniel. Polisi wa kawaida toka CCP Moshi si watamsagasaga kabisa!” Inspekta Nyange alikuwa anawaza.

Daniel Mwaseba akaitwa.

‘Habari Daniel”

“Safi afande”

“Kuna haya mauaji ya kinyama yanayoendelea hapa Mjini.Tumepokea ombi lako la kutaka kuwasaka wauaji hao ”

“Ndio afande ”Daniel alijibu huku anatabasamu.

“Ombi lako limekubaliwa, utakuwa sambamba na Inspekta Nyange katika operesheni hiyo ”.

“Sawa afande ”. Daniel aliitikia.

Daniel na Inspekta Nyange walishikana mikono kama ishara ya umoja katika harakati za kuwafichua wauaji hao hatari.

Muda wa jioni Daniel alikuwa anarudi nyumbani kwake kupumzika.Gari yake ndogo aina ya Starlet ilikuwa imechochea moto. Kumbe nyuma yake kulikuwa na gari nyeusi aina ya Noah ikimfatilia kwa siri. Ndani ya Noah hiyo kulikuwa na watu waliokuwa wakimfatilia tangu asubuhi, alipopewa jukumu la kufatilia kesi ile na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilwa.Walimvizia pale Polisi bila mafanikio. Na sasa walikuwa wanamfata!

Ndani ya Noah ile nyeusi kulikuwa na watu watatu hatari, kulikuwa na mwanadada Edina Reuben, ambaye ndiye alikuwa nyuma ya usukani wa Noah ile nyeusi. Edina alikuwa dereva hodari sana. Alikuwa ana uwezo wa kuliendesha gari kwa mwendo autakao. Bila kutetereka, bila kuyumba.Bila kuyumbishwa. Alikuwa dereva makini wa kike!

Pembeni yake alikaa kijana mmoja mrefu. Wenyewe walikuwa wanamwita 'tall wa ajabu'. Ni kweli alikuwa mrefu sana.Alikuwa mrefu mithili ya Hasheem Thabiti.Pia Edgar alikuwa muuaji katili anayetegemewa katika kundi hili.

Nyuma ya kiti cha dereva. Alikaa mzee mmoja. Kitaswira alikuwa mzee. Ndio!Ni mzee hasa. Lakini kwa vitendo alikuwa kijana.Mzee mkata chipsi. Huyu ndiye Mzee akiyetumika katika kukatakata maiti za watu. Historia yake zamani alikuwa anafanya kazi katika bucha moja la Ng'ombe huko Mwanza. Taaluma yake ya kukatakata nyama ya Ng'ombe sasa aliihamishia kukatakata binadamu wenzie. Alikuwa anaitwa Mzee Kishoka.

Wakati gari likilofuata likiwa na watu watatu hatari. Gari likilofuatwa lilikuwa na mtu mmoja. Kijana mdogo lakini makini sana. Kiumri Alikuwa na miaka 25 tu. Kijana ambaye baada ya kumaliza kidato cha sita shule ya Sekondari Sangu iliyopo mkoani Mbeya. Alijiunga na jeshi la Polisi. Kuwa Askari Polisi Ilikuwa ni ndoto yake tangu akiwa mtoto. Kwa maana hiyo leo hii alikuwa anaishi katika ndoto zake. Ndoto za kukomesha uhalifu na uonevu nchini. Aliipenda sana kazi hii ya Polisi, na zaidi alipenda kushiriki katika mikasa ya hatari kama hii. Kuingia katika hatari yoyote ili kuiokoa nchi yake ndio kitu akichokipenda zaidi katika maisha yake. Alikuwa tayari kuingia katika hatari yoyote ili kutetea raia wema. Hata kazi ya kushiriki katika mkasa huu aliiomba mwenyewe kwa OCD, kwa madhumuni maalumu. Akakubaliwa. Na sasa yupo kazini.

Gari ya Daniel ilikuwa katika mwendo wa kawaida.Wakati ile gari ya kina Kishoka ikiwa nyuma ya gari ya Daniel.Waliachia magari matatu kati yao na gari na gari la Daniel.Ili wasitambulike kama wanaifatilia .Gari lao likawa la nne kutoka gari ya Daniel.

Kuacha magari matatu kati walidhani hawatatambulika na Daniel.Lakini Daniel hakuwa mtu wa aina hiyo.Aligundua kuwa atafatwa kabla hajatoka ofisini kwake. Aliiona ile Noah nyeusi imepaki muda mrefu karibu na kituo cha Polisi.Alilitilia shaka. Alijaribu kuchunguza sura za watu waliopo katika gari lile.Hakufanikiwa kuwaona.Vioo vya Noah ile viliwekwa karatasi ngumu nyeusi ‘Tinted’ Akawa na subira. Akajisemea,

"Utafika muda muafaka wa kuwafahamu" na sasa ndio wanamfata wenyewe!

Daniel Mwaseba alikuwa anaelekea nyumbani kwake. Mtaa wa Kariakoo.Lakini baada ya kuona anafuatwa na gari ile akagairi.Sasa akanyoosha,akawa anaifuata njia ya kwenda jijini Dar es salaam.

Alipofika mtaa wa Magereza Daniel akaongeza mwendo. Edina naye akaongeza mwendo.Sasa walikuwa wanakimbizana bila kificho. Ilibaki gari moja tu kati yao. Nalo Edna akalipita kwa kasi !



Daniel Mwaseba alikuwa anaelekea nyumbani kwake. Mtaa wa Kariakoo. Lakini baada ya kuona anafuatwa na gari ile akagairi. Sasa akanyoosha,akawa anaifuata njia ya kwenda jijini Dar es salaam.



Alipofika mtaa wa Magereza Daniel akaongeza mwendo. Edina naye akaongeza mwendo. Sasa walikuwa wanakimbizana bila kificho. Ilibaki gari moja tu kati yao. Nalo Edna akalipita kwa kasi !

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kama Edina alidhani kuwa yeye alikuwa hodari wa kukimbiza gari kuliko mtu yeyote duniani basi alijidanganya sana. Daniel alikuwa kiboko yake. Alilikimbiza hasa gari. Akawaacha umbali mrefu kidogo wakina Edina.

Alipofika njia panda ya kwenda Dar es salaam na Kivinje, Daniel alikata kona ya upande wa kulia. Alielekea Kilwa Kivinje. Wakati kina Mzee Kishoka wanafika Singino. Daniel alikuwa ameshasimamisha gari stendi kwa Bi Adha, Kilwa Kivinje. Akaingia kwenye duka moja la nguo akijifanya kuchagua nguo, huku akiwa makini na kila hatua inayoendelea nje ya duka lile.



Mara akaiona ile Noah nyeusi imesimama pale Stendi. Daniel akawa makini zaidi akitarajia labda atashuka angalau mtu mmoja kutoka katika ile Noah.



'Subira siku zote yavuta heri'



Aliona mlango wa mbele wa ile Noah ukifunguliwa.

Kwa macho yake Daniel alimshuhudia mtoto wa kike akishuka kwa madaha katika gari ile. Hakuwa na sura ya uhalifu kabisa. Hakuwa na mwendo wa kihalifu. Hakuwa na muonekano wa kuendesha gari kwa fujo kama ikivyoendeshwa muda mfupi gari ile.

Edina alivyoshuka. Akamuita kijana mmoja na kumuuliza.



“Habari yako kaka”



“Nzuri dada”



“Naomba kukuliza kaka”



“Ndio, nakusikiliza”



“Mwenye gari ile yuko wapi?”



Edina alisema huku akilionesha kwa kidole gari ya Daniel.



“Hata sifahamu dada,sikuwa makini nae wakati anashuka”



“Ahsante kaka”



Daniel Mwaseba aliyaangalia yote kwa umakini mkubwa. Aliipapasa bastola yake iliyokuwa kiunoni. Ilikuwa inamsubiri yeye tu kwa matumizi. Ilikaa tayari kwa lolote!

Edina akamuendea mtu wa pili. Alikuwa mwanamke muuza samaki wa kukaanga aliowaweka kwenye beseni lake kubwa pale stendi. Baada ya kumuuliza Edina alipewa jibu kama la mwanzo. Muuza samaki pia hakuwa anajua Daniel ameelekea wapi?



Kule dukani Daniel alikuwa makini sana. Jicho moja akiwa anamwangalia Edina. Jicho la pili analiangalia lile gari. Akaona mlango wa nyuma unafunguliwa. Akashuka mzee Kishoka.



Sasa Kishoka na Edina walikuwa wanaongea nje ya ile gari. Bila shaka wakipeana majukumu ya kumtafuta Daniel. Wakati Edina akielekea uelekeo wa hospital kumtafuta. Mzee Kishoka nae alielekea uelekeo wa pwani.Ndani ya gari walimuacha Edgar Bituro'Tall wa ajabu' , Kulilinda lile gari.

Walichokuwa hawakifahamu kwamba wanayemtafuta ni Daniel Mwaseba. Wangemjua vizuri Daniel ni nani, labda wangebadili mbinu zao. Daniel alikuwa ni sumu. Sumu hatari sana!



Baada ya nusu saa Edina Na Mzee Kishoka walirudi, hawakufanikiwa kumuona Daniel. Waliambulia patupu huko walikokwendwa.

Wakaingia ndani ya gari yao. Sasa waliamua kughairisha msako ili warudi walipotoka, Masoko. Wakajipange upya.

Walipoingia ndani ya gari, walimomuacha Edgar. Hawakumkuta Edgar! Bali waliukuta mwili wa Edgar ! Walimkuta Edgar ndani ya gari akiwa kaegemea siti ya gari. Hana kovu lolote, wala alama yoyote. Lakini hakuwa na roho !

Kwa mtu asiye mzoefu wa maiti angedhani Edgar amelala usingizi. Lakini siyo kwa watu wachezao na maiti kila siku kama hawa. Kuingia tu ndani ya gari waligundua Edgar ameuwawa.

Tena ameuwawa kimyakimya!

Ilikuwa taharuki ndani ya gari. Hakuna aliyemsemesha mwenzie ndani ya dakika tano. Walikuwa wauaji makatili sana. Ila kifo cha Edgar kiliwaogofya sana! Walikuwa wanaujua uwezo wa Edgar kimapambano. Kuuwawa kimya kimya vile hakikuwa kitu walichokitarajia kabisa .



Baada ya dakika tano Mzee Kishoka alitoa kauli.



“Sasa Edina tunafanyaje ?”



“Mimi hata sielewi Kishoka ”



“Itabidi tumpigie simu bosi kumueleza ”



“Kumpigia simu kabla ya kumkamata adui?”



“Ndio, tumueleze tuu ”

“Sawa” Edina alikubali kwa uwoga.



Tangu walipoanza hili jukumu la siri. Leo ndio walipata kikwazo. Toka kwa mtu wasiomtegemea. Mtu waliomdharau kabisa.

Mzee Kishoka alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia Bosi wao. Kumpa taarifa ile mbaya kabisa.



"Halo Bosi"



“Nambie Kishoka”



“Kuna tatizo Bosi”



“Tatizo gani tena?”



“Edgar ameuwawa?”



“Ameuwawa!”



“Ndio Bosi”



“Aliyemuua naye bado anapumua? ”



“Ndio Bosi, hatujampata bado”



“Hakikisheni halioni jua likizama !”



“Sawa bosi”



“Na muniletee kipande cha utumbo wake! ”



Simu ikakatwa!



“Itabidi tuendelee kumtafuta” Mzee Kishoka aliongea huku akitoka nje.



“Sawa”



Baada ya Kishoka kushuka na Edina naye alikuwa anajiandaa kushuka ndani ya gari. Ndipo alisikia sauti iliyomstusha sana.

"Usihangaike kwenda kunitafuta nje, nipo humu humu ndani ya gari"



Mwili wa Edina uliingiwa na ubaridi. Sauti ya Daniel kwa Edina haikuwa sauti ya kawaida, ilikuwa sauti iliyofanana na kifo.

Edina aligeuka nyuma akiwa na hofu!. Akakutana na sura iliyokuwa ikitabasamu, alikuwa ni Daniel Mwaseba!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Baada ya Kishoka kushuka na Edina naye alikuwa anajiandaa kushuka ndani ya gari. Ndipo alisikia sauti iliyomstusha sana.



"Usihangaike kwenda kunitafuta nje,nipo humu humu ndani ya gari"



Mwili wa Edina uliingiwa na ubaridi. Sauti ya Daniel kwa Edina haikuwa sauti ya kawaida, ilikuwa sauti iliyofanana na kifo.

Edina aligeuka nyuma akiwa na hofu!. Akakutana na sura iliyokuwa ikitabasamu, alikuwa ni Daniel Mwaseba!



"Naitwa Daniel Mwaseba" Alijitambulisha kwa kejeri.



Edina hakuwa na hali wala kauli. Pigo moja la judo ya shingo lilimlaza Edina usingizi mnono kwenye kiti chake...

Noah nyeusi sasa ilimilikiwa na mikono mingine, ilikuwa inarudishwa Kilwa Masoko. Ikiwa na dereva mpya na abiria wawili waliolala usingizi tofauti. Mmoja usingizi wa muda na mwingine usingizi wa milele.



Daniel alipofika maeneo ya Mpara. Kilometa chache kufika mji wa Masoko aliona kitu kilichomstua. Yalipangwa magogo barabarani.



" Hatari" alijisemea kimoyomoyo.



Kama walioweka magogo walidhani Daniel ni dereva wa kitoto. Walikosea sana. Daniel alikuwa ni mtundu sana kwenye uendeshaji wa gari.



Gari likiwa mwendokasi uleule. Lakini Daniel alifunga breki ya ghafla! Alianza kulirudisha gari nyuma, na kuzungusha usukani kwa haraka. Gari liligeuka lilipokuwa linatoka. Kwa kasi ya ajabu Daniel alilikimbiza gari kurudi alikotoka.



Kwa kutumia kioo cha pembeni aliziona pikipiki nne, zikimfata kwa kasi vilevile.

Daniel aliongeza mwendo wa ile Noah. Akashika usukani kwa mkono wa kulia. Mkono wa kushoto aliutumia kujipapasa mifukoni. Akiitafuta simu yake ya kiganjani. Hakuiona!

Akakumbuka, simu aliiacha kwenye gari yake aliyoiacha Kivinje. Akaangalia katika siti ya upande wa kushoto ilipo maiti ya Edgar. Akapekua katika mfuko wake wa suruali aliyovaa, akaipata simu. Akaichukua kwa mkono wa kushoto na kuandika namba alizokuwa amezihifadhi kichwani. Akaweka simu sikioni. Akisikiliza kama itaita.



***



Ilikuwa mida ya saa kumi na mbili ya jioni. Ilimkuta Inspekta Nyange akiwa katika Baa ya Makondeko, akipata bia mbili tatu. Kupoteza mawazo.

Kupewa Daniel kushirikiana nae kwenye mkasa wa kutisha kama huu kulimpa mawazo mengi sana. Hakumwamini kabisa Daniel.



"Mtoto katoka depo juzi leo umpe kesi ngumu ya kupeleleza kama hii, watampasua tumbo mithili ya ng'onda"Alijisemea kimoyomoyo.



Juu ya meza aliyokaa kulikuwa na chupa tano tupu za bia ya safari, zilizokuwa zimeshamiminwa katika tumbo la Inspekta Nyange. Sasa alikuwa anamalizia bia yake ya sita huku akiangazaangaza huku na kule. Labda atampata msichana wa kuondoka nae miongoni mwa wateja waliojaa katika Baa ile maarufu Kilwa.

Alidhamiria kuufurahisha mwili wake, kabla ya kupokea simu ya ‘Private number’ usiku, ikimuarifu juu ya kifo cha Daniel. Alikuwa na uhakika Daniel lazima atauwawa usiku!

Hakufanikiwa kupata msichana wa kuondoka nae. Wengi wao walikuwa na watu wao. Na wachache waliokuwa peke yao hawakumridhisha.

Alimwita Mhudumu na kulipa bili akiyodaiwa, baada ya kulipa bili yake akasimama.Tayari kwa kuondoka. Ndipo

simu yake iliita. Alikaa vizuri kitini.Kuangalia ampigiae kwenye kioo cha simu yake, alistuka sana. Alikuwa ni ‘private number’!

Akaipokea.



“Inspekta ”



“Haloo”



“Ni Daniel Mwaseba”



“Eti!”



“Hatuna muda wa kuongea sana, naomba utume vijana wakaichukue gari yangu ipo stendi Kivinje, funguo upo chini ya kiti cha abiria. Wailete hapo kituoni. Nikija tutaongea kwa kirefu”



Inspekta Nyange pombe zilimtoka. Alijiuliza imekuwaje Daniel atumie simu ya private number?!

Na kwasasa yuko wapi mpaka awaagize watu wakachukue gari yake Kivinje?! Hakupata jibu, wa kumpa jibu alikuwa ameshakata simu.



Akachukua simu yake ili ampigie Daniel. Akakumbuka alitumia ‘private number’. Alitafuta namba nyingine katika simu yake, aliipata, sasa alipiga namba halisi ya Daniel, lakini haikupokelewa. Aipokee nani wakati simu ilikuwa ndani ya gari Kilwa Kivinje, na Daniel alikuwa anaingia Nangurukuru sasa.



Daniel alikuwa mtu wa ajabu sana. Pamoja na kuwa katika hali ya hatari kama ile lakini alimpigia simu Inspekta Nyange. Na aliongea nae kama yupo sehemu salama kabisa. Kumbe Daniel alikuwa katika hatari kubwa. Pikipiki nne zikimfata nyuma. Ndani ya gari alilokuwemo kulikuwa na maiti moja. Na kiumbe hai mmoja, aliyemuacha aendelee kupumua kwa shida kwa malengo maalumu.

Pamoja na kushangaa, lakini Inspekta Nyange alitekeleza alichoambiwa na Daniel. Alituma vijana wawili kwenda Kivinje. Kulichukua gari la kijana hatari Daniel Mwaseba.





***



Katika nyumba moja kubwa, iliyozungushiwa ukuta kwa kutumia matofali, huku ukilindwa na walinzi wengi walioimara. Hali ndani ya nyumba hii ilikuwa tofauti siku ya leo .



Ndani ya nyumba hii siku zote kwao ilikuwa sikukuu kasoro leo tu. Walikuwa wanajua kutumia pesa kwa sababu walikuwa nazo za kutosha. Walikuwa wanalewa watakavyo kwa sababu walikuwa na pombe za kutosha, kreti kwa makreti. Walikuwa wanachezea wanawake watakavyo. Ndio, walikuwa na pesa mpaka pa mwisho, watakosaje mwanamke wanayemtaka mbele ya pesa?



Nyumba hii ilikuwa katika Kisiwa cha kihistoria. Ndimo mipango ya Mpango wa siri ilimopangwa, na ndimo wachezaji wa Mpango wa siri walikuwa wanaishi. Ilikuwa ndani ya kisiwa ,Kilwa Kisiwani.



Kutokana na ustaarabu wa watu wa Kilwa Kisiwani, hakukuwa na mtu aliyetilia shaka uwepo wa nyumba ile kubwa Kisiwani kwao. Waliichukulia ni nyumba ya kawaida, na kweli kwa nje ilikuwa ni nyumba ya kawaida. Lakini ndani ya Nyumba ile walikuwa wanakaa watu hatari sana, wauaji wazoefu na makatili kupitiliza!



Ndani ya chumba kimoja ndani ya nyumba ile kulikuwa na kikao cha siri. Kilikuwa kikao cha watu sita hatari. Waliokuwa wanamsikiliza kwa makini mtu mmoja. Aliyeonekana kuchanganyikiwa.



"Kishoka hebu tueleze kilichotokea huko".

Mtu wakiyemuita Bosi alimtaka Kishoka awaelezee kilichotokea, katika operesheni ndogo waliyotumwa ya kumuua Askari aliyekabidhiwa jukumu la kufatilia kifo cha mzee waliyemuuwa .



Kishoka aliwaelezea kila kitu. Tangu walivyoanza kumfatilia Askari yule, mpaka walipoikuta maiti ya Edgar Bituro ndani ya gari. Aliwaelezea jinsi walivyogawana njia kumtafuta kama ambavyo yeye Bosi alivyowaagiza. Na jinsi alivyoiona gari yao ikimpita kwa kasi akiwa hospitali ya Kinyonga, na kuhisi kwa vyovyote gari yao itakuwa mikononi mwa adui, kwa kuwa hawakukubaliana na Edina amuache Kivinje, ndipo akaamua kuwapigia simu Bosi ili waweke mtego Mpara.



Kazi ya kwenda kulichukua gari la Daniel walipewa Askari wawili. Afande Mathew Emmanuel na Afande Hamza Mkata. Walifika Kilwa Kivinje na kulikuta gari la Daniel palepale walipoelekezwa na Inspekta Nyange.

Hamza akafunua kiti cha abiria na kuukuta funguo wa gari lile.

Baada ya afande Mathew kukaa siti ya abiria, afande Hamza alikaa katika siti ya dereva na kupiga stata ili kuiondosha gari.

Ndio ilikuwa stata yake ya mwisho kupiga katika maisha yake...

Vipande vya gari ya Daniel vilielea hewani. Moshi mzito ulitanda mawinguni. Ukifatiwa na moto mkali. Kumbe gari la Daniel lilikuwa limetegwa Bomu! Haukuonekana mwili wa Hamza wala Mathew. Wote waliteketea kwa moto, waliyeyuka katika sura ya dunia mithili ya saruji!



Taarifa za vifo za askari wawili aliowatuma wakachukue gari ya Daniel, zilimfikia Inspekta Nyange akiwa amejipumzisha sebuleni kwake. Akiwa makini akiangalia runinga yake, filamu nzuri ya Likanchinda ilimteka hasa. Filamu iliyochezwa na magwiji wa filamu Kilwa, Kilwa Sanaa Group.

Simu yake ya mkononi iliita. Alikuwa afande Janeth wa kituo cha Polisi Kivinje. Alimtaarifu Inspekta Nyange habari ya kuteketea kwa gari la Daniel. Na kuyeyuka kwa askari wawili ambao afande Janeth hakuwajua. Ni watu waliokuwa karibu na gari hilo wakati tukio linatokea ndio walimuambiahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

kuwa waliingia askari wawili kabla ya gari hilo halijaripuka.

Afande Janeth hakuwa anawafahamu askari hao. Ila Inspekta Nyange aliwajua vizuri. Ni yeye ndiye aliyewatuma, Hamza na Mathew. Taarifa hii ilimuhuzunisha sana Inspekta Nyange. Aliona ni dharau kwa jeshi la Polisi.Askari watatu kufariki ndani ya juma moja. Ni dharau isiyovumilika. Alikumbuka pia vifo vya kinyama vya raia wema. Vilimuhuzunisha sana. Sasa Inspekta Nyange aliamua kuingia kazini. Kupambana na wauaji yeye mwenyewe!



***



ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog