Search This Blog

Friday 18 November 2022

MPANGO WA SIRI - 4

 






Simulizi : Mpango Wa Siri
Sehemu Ya Nne (4)




Walifika kituo cha polisi mida ya saa kumi alfajiri. Walimuwahisha Inspekta Nyange hospitalini. Hadi hapo hakuna aliyekuwa anajua kama yule mgonjwa aliye mahututi ni inspekta Nyange. Alikuwa hatamaniki. Alikuwa hatazamiki !



Usiku uleule Lee alipelekwa katika chumba cha mahojiano. Daniel hakukaa. Hakutaka Kumsikiliza Lee muda ule .



Usiku uleule alirudi Kisiwani. Aliomba kila atakachoongea Lee kirikodiwe. Yeye alirudi kazini!



Wale watu thelathini waliotumwa kwenda Masoko kwenda kumtafuta Daniel walipotezwa maboya.

Sasa waliamua kugawana kazi. Kundi la kwanza walipewa jukumu la kupita kwenye nyumba za kulala wageni zote.

Kundi lengine walikuwa na jukumu la kupita kwenye mabaa yote.

Kundi lengine walitumwa waende nyumbani kwake Daniel, lengine lilikuwa linatembea mitaani na kundi la mwisho walizuia barabara ya kutoka nje ya mji.Wenyewe walihisi saa moja litatosha kumkamata Daniel. Mpango ulipangwa na Kishoka na wanachama wote waliingia kazini. Kumsaka Daniel!



Kumbe Daniel Mwaseba alirejea tena kwenye ngome ya Lee. Baada ya kutafutatafuta akakutana na Kompyuta sebuleni kwa Lee. Akajua habari zote atazipata humo. Akaiwasha.

Kompyuta nzima ilikuwa na mafaili matatu tu. Alilifungua la kwanza. Lilikuwa Limehifadhiwa kwa jina Mchezo Mchafu.

Akaanza kulisoma.



“Mchezo Mchafu ni mauaji ya kikatili anayouliwa mtu asiyehusika anayetaka kukaribia kujua habari za Mpango wa Siri. Mauaji haya hufanywa kwa kukatakata mwili wa mtu huyo na kuutoa utumbo wake”



Akalifungua faili la pili. Lenye kichwa cha habari “Watu wa kukaa nao mbali katika mpango huu”.Alilifungua nalo, likafunguka bila shida. Alikuta majina ya watu watatu,picha zao na maelezo yao binafsi. Jina la kwanza lilikuwa ni jina lake, Daniel Mwaseba, jina la pili lilikuwa la Inspekta Nyange na jina la tatu lilikuwa la Mzee Mirambo.



Sasa akasogeza kimshale cha kompyuta kwenye lile faili la tatu. Alihisi faili lile ndio lilikuwa kila kitu katika mpango huu. Lilihifadhiwa kwa jina la Mpango wa Siri. Nywele zilikuwa zinamcheza na damu kumsisimka, hakujua atakutana na mpango gani ?.Alivyobofya faili halikufunguka, lilitaka namba ya siri. Faili lile liliwekewea namba ya siri. Daniel Mwaseba alitumia mbinu zake zote hakufanikiwa kulifungua faili lile. Mpango wa siri ulimgomea Daniel!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wale watu wa Lee walioenda kumtafuta Daniel waliambulia patupu . Hawakumuona nyumba ya kulala wageni.Hawakumuona barabarani. Hawakumuona nyumbani kwake.Daniel aliwaumiza sana vichwa. Sasa walikutana kwa ajiri ya kikao kifupi, kabla ya kurudi Kilwa Kisiwani kumuelezea Lee kuhusu kushindwa kwao kumpata Daniel.



“Daniel hatujamwona, mimi nashauri twende Kisiwani tu tukamueleze Bosi, hatuna jinsi. Uzuri ni kwamba hatujamuona kabisa. Kama tungemuona halafu akatutoroka ingekuwa tatizo” Kishoka aliwaambia wale wenzie. Lilikuwa kundi la watu thelathini lenye hasira, hasira dhidi ya Daniel Mwaseba!



Walifika ufukweni wakapakia kwenye boti safari kurudi Kilwa Kisiwani ilianza. Wakiwa hawajui kama wanayemtafuta yupo huko Kisiwani. Na wanayemfata huko hakuwepo Kisiwani. Ambaye ndiye Bosi wao alikuwa ndani ya chumba cha mahojiano kituo cha Polisi.



Kule ndani Daniel Mwaseba alishindwa kabisa kufungua faili lile lenye Mpango wa Siri. Mara ya tatu sasa alijaribu kufungua faili lile bila mafanikio. Kulikuwa na ubunifu wa ziada uliotumiwa katika kuweka namba ya siri ya faili lile. Ubunifu ambao ulimshinda Daniel.

Hakuweza kulifungua!



***



Huko Dar es salaam katika ofisi moja kubwa kulikuwa na taharuki kubwa ! Kompyuta tatu ndani ya ofisi hiyo zilikuwa zinapiga kelele za tahadhari. Kelele hizo ziliashiria hali ya hatari katika moja ya kompyuta tano zilizohifadhiwa faili lenye Mpango wa Siri. Kompyuta tatu zenye faili lenye mpango huo hatari zilikuwa ndani ya ofisi hiyo. Kompyuta moja ilikuwa kwa Mkurugenzi wa mpango huo, huku kompyuta ya tano ikiwa Kilwa Kisiwani kwa mtekelezaji wa mpango huo ndani ya Kilwa.



John Masaga alikuwa ndio mkuu ndani ya ofisi ile ya siri. Iliyokuwepo ndani ya nyumba moja huko Tegeta. Ilikuwa ofisi yenye wafanyakazi saba. Sita walikuwa wanaume huku mmoja alikuwa mwanamke. Ilikuwa ndio ofisi kitovu katika mpango huu. Waliopachika jina la Mpango wa Siri !



Kompyuta zote tano ziliwekewa programu maalumu ya kutambua hali ya hatari endapo kompyuta hizo zitachezewa na mtu asiye sahihi. Ni mwanadada Devotha ndiye aliyeingiza programu hiyo. Zilikuwa ni namba za siri ambazo ukikosea kuingiza mara tatu kompyuta zote zinapeana taarifa na kutoa ukelele wa tahadhari.



Kwa kasi Devotha akakimbilia moja ya kompyuta pale ofisini na kuangalia kwenye kioo. Aligundua kitu. Kompyuta iliyopo Kilwa ndio ilituma taarifa ile. Inamaana katika kompyuta hiyo kulikuwa na mtu asiye sahihi akijaribu kufungua faili lenye Mpango wa siri.



Devotha alichukua simu na kumpigia Lee. Hakuwa anapatikana!. Akajaribu kumpigia Edgar. Hakuwa anapatikana! Akampigia Edina nae majibu yalikuwa yaleyale. Watu watatu walioaminiwa katika mpango ule hawakuwa wanapatikana !



Kosa alilolifanya Lee ni kutowaeleza mapema mabosi zake vikwazo alivyokutana navyo. Hasa madhara ya Daniel ambao ofisi ile walikuwa wanayatambua vizuri sana. Lee aliamini kupitia programu aliyoibuni mwenyewe na kuipa jina la Mchezo Mchafu angeweza kumtia mikononi mwake Daniel. Alijidanganya!Sasa yupo yeye mikononi huku akiacha taharuki kubwa kwa mabosi wake.



Devotha akampigia Mkurugenzi wa mpango ule ili kumueleza hali ya hatari iliopo huko Kilwa.



“Halo Bosi”Devotha aliita.



“Nambie Devotha” Alijibiwa kwa sauti nene ya Mkurugenzi.



“Kuna mambo hayako sawa”Alimuarifu.



“Wapi?”Bosi aliuliza.



“Kilwa bosi”Devotha alijibu.



“Nakuja sasa hivi”Simu ilikatwa.



****



Ndani ya kituo cha Polisi kulikuwa na vichekesho. Kulikuwa mahojiano kati ya askari polisi na bubu. Lee hakujibu chochote alichoulizwa. Hata jina lake hakuwatajia Polisi. Aliamua kuwa bubu kabisa.

Nusu sasa Lee hajasema kitu.



”Mwacheni akija afande Daniel atasema tu”.Askari mmoja aliwaambia askari wenzake.

Akiwa pale ndani, kwenye ofisi Daniel alikuwa ameshindwa kabisa kufungua faili lile. Alishajaribu zaidi ya mara kumi bila mafanikio. Sasa aliamua kurudi kituo cha Polisi. Aliamini Lee atasema kila kitu juu ya mpango ule. Akiwa kafika mlangoni aligeuka nyuma. Kwenye runinga moja iliyopo ndani ya jengo lile ilimstua. Aliona kundi laa watu likija katika nyumba ile. Kengele ya hatari iligonga kichwani mwake. Daniel sasa hakujiandaa na mapambano, alikuja kufanya uchunguzi tu kisha arudi kituo cha Polisi kumalizizana na Lee. Wakati kundi lile kubwa la watu likipita malango wa mbele kuingia ndani. Daniel alikuwa juu ya ukuta kwa nyuma akiruka kwa ufundi mkubwa na kuangukia nyuma ya nyumba ile. Kwa mara nyingine Daniel aliwakwepa kina mzee Kishoka.

Walipoingia ndani walikuta majanga makubwa. Nyumba mzima ilikuwa inanuka damu. Walipigwa na butwaa. Kambi yao ilikuwa nyang’anyang’a. Hakukuwa hata na harufu ya uhai. Hawakuamini kabisa macho yao. Wakawa wanachambua kila maiti ili kuona kama kulikuwa na maiti ya Lee. Hawakuiona!



Ghafla simu ya Kishoka iliita. Alikuwa amepigiwa na Mkurugenzi wa kundi lao. Moyo ulimripuka! Hakutegemea kupigiwa simu na mtu mkubwa kama yule, tena akiwa katika hali ya hatari kama ile. Aliipokea.

“Halo Mkurugenzi” Kishoka aliita kwa sauti yenye kitetemezi.



“Vipi hali ya usalama huko” Mkurugenzi aliulizia kitu kilichofanya ampigie simu Kishoka.



“Bosi hali ya usalama si nzuri. Sisi tulitoka tulienda kumtafuta mtu mmoja aliyevamia kambi yetu.Tumerudi sasahivi tumekuta hali ya usalama siyo mzuri.

Kambi mzima wameuliwa !”



“Vipi na Lee nae wamemuua”Mkurugenzi aliuliza kwa fadhaha.



“Hatujafanikiwa kuiona maiti ya Lee, nahisi itakuwa wamemteka. Kishoka alijibu.



“Namtuma Devotha sasa hivi. Mpeni ushirikiano unaohitajika” Mkurugenzi alisema simuni.



“Haina shida bosi”Kishoka alijibu.



Muda uleule ilitafutwa ndege ya kukodi kumsafirisha Devotha kwenda Kilwa kuweka mambo sawa. Dakika 45 zilitosha kumsafirisha Devotha hewani na kumfikisha Kilwa. Ndege ile ilitua moja kwa moja Kisiwani. Devotha alishangazwa na maafa yaliyoachwa na Daniel na kundi lake.



“Mbona sijaziona maiti ya Edgar na Edina”Devotha alimuuliza Kishoka baada ya kuziangalia maiti zote.



“Edgar aliuliwa juzi, na Edna alipotea katika mazingira ya kutatanisha”Kishoka alijibu kwa unyenyekevu mkubwa.



“Kwanini hamkutoa taarifa?”Devotha aliuliza.



“Mimi nilifikiri Bosi Lee amewaambia. Kishoka alijitetea.



“Ni nani anaewasumbua sana kati ya askari wote?”Devotha aliuliza.



“Daniel Mwaseba ! ”Watu wote thelathini walijibu kwa pamoja. Ama hakika Daniel alikuwa mwiba mkali sana kwao.



“Daniel Mwaseba?”Devotha aling’aka kwa sauti kubwa.



“Ndio”Safari hii alijibiwa na mzee Kishoka peke yake.



“Daniel Mwaseba amekuja huku. Sasa shughuli itakuwa pevu!”Devotha alisema kwa sauti kali ya kike.

“Ni nani anayewasumbua sana kati ya askari wote?” Devotha aliuliza.



“Daniel Mwaseba ! ” Watu wote thelathini walijibu kwa pamoja. Ama hakika Daniel alikuwa mwiba mkali sana kwao.



“Daniel Mwaseba?” Devotha aling’aka kwa sauti kubwa.



“Ndio” Safari hii alijibiwa na mzee Kishoka peke yake.



“Daniel Mwaseba amekuja huku. Sasa shughuli itakuwa pevu!” Devotha alisema kwa sauti kali ya kike.



Devotha alikuwa anamfahamu vizuri sana Daniel Mwaseba. Alikuwa nae pamoja kwenye mafunzo ya Upolisi kule Moshi. Alikuwa rafiki yake kipenzi. Kabla ya Devina kuasi jeshi la Polisi na kutumikia genge hili la kihuni. Devotha ndiye alikuwa mpinzani mkubwa wa Daniel Mwaseba kule kambini. Katika mazoezi ya kulenga shabaha, mapigano ya ana kwa ana walikuwa wanachuana hasa. Kuja kwa Daniel Mwaseba katika mkasa huu kulimstua sana Devotha. Lakini kwa sasa Devotha hakuwa anamuogopa sana Daniel. Yeye alikuwa ameiva sasa. Baada ya kuasi jeshi la polisi na kujiunga na kundi hili haramu alipelekwa kozi mbalimbali za kimapigano. Alishaenda Urusi kufundishwa mbinu za kijasusi, alishaenda China na Japan kujifunza fani za kung fu na Judo. Devotha sasa alikuwa ameiva. Devotha sasa alikuwa nusu komandoo! Hakumuhofia kabisa Daniel, lakini alikuwa anafikiria siku atakayokutana na Daniel ana kwa ana. Rafiki yake kipenzi ambaye sasa atakuwa ni adui yake, bila shaka adui yake namba moja. Yeye akiutetea mpango wa siri usivuje. Daniel Mwaseba akiwa katika upande wa kutaka mpango huu wa siri uvuje na kuharibika kabisa!



Devotha aliingia ndani sasa kuangalia kompyuta yao. Kompyuta ambaye yeye ndiye aliweka namba za siri katika faili lenye Mpango wa Siri. Alilikuta lipo salama faili lile. Akajua Daniel hakufanikiwa kulifungua faili lile. Sasa Devotha ndio alikuwa mkuu wa kampeni, kampeni iliyopewa jina, Muue Daniel Muokoe Lee, kwa kifupi MDML!

Sasa walijipanga upya.

Watu thelathini walikuwa wengi sana kwa Devotha. Alikuwa na imani kubwa kuwa watafanikiwa katika MDML.



Shughuli ilianza sasa!



Daniel sasa alikuwa anaingia kituo cha Polisi akiwa na hasira kali. Pale kaunta akasimuliwa habari za Lee kujigeuza bubu. Kutotaka kuongea chochote. Pia alipewa habari zilizomstua sana. Kuwa yule mateka waliomuokoa kwa Lee Alikuwa ni Inspekta Nyange. Sasa hasira za Daniel Mwaseba zilipanda maradufu. Ukijumlisha na hasira ya kushindwa kufungua faili lile lililoandikwa Mpango wa siri. Daniel Mwaseba alitoka nje. Akaelekea hospitali kwenda kumuuona Inspekta Nyange.

Alikuta Inspekta Nyange yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi chini ya uangalizi maalumu. Daktari hakumruhusu kabisa Daniel kwenda kumwangallia Inspekta Nyange. Hali ya Inspekta Nyange haikuwa mzuri. Nia ya Daniel kwenda kumuona Inspekta ni kutaka kwenda kumuuliza Inspekta Nyange kuwa Lee alimpa mateso gani. Alikuwa anataka kwenda kurudisha kwa Lee mateso yote aliyompa Inspekta Nyange.



“Itakuwa alifanywa nini daktari” Aliamua kumuuliza daktari angalau apate hata cha kuanzia atakaporudi Polisi.



“Wamempasua vibaya macho, halafu waamempiga mwili mzima,wamemuumiza sana” Daktari alijibu.



“Sawa daktari” Daniel aliitikia na kurudi kituoni.



Wakati anafika kituoni aliona gari moja aina ya Range rover likitoka kwa kasi pale kituoni kwa kasi. Daniel machale yalimcheza. Akaitilia shaka sana gari ile. Akaenda moja kwa moja kituoni bastola mkononi. Aliyoyakuta yalimuacha mdomo wazi. Alikuta kaunta imejaa damu mithili ya machinjio ya Ng’ombe. Miili ya askari watatu imelala pale chini ikiwa haina uhai. Alipoenda katika chumba alichokuwa Lee, hakuwepo. Katika kiti alichokaa Lee alikuta karatasi. Aliichukua na kuifungua, akaanza kuisoma. Akakutana na maneno manne tu ya Kiswahili yakiwa yameandikwa kwa herufi kubwa



“RAFIKI YAKO KIPENZI NIMEKUJA”.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ingawa karatasi iliandikwa kwa Kiswahili lakini hakuelewa kabisa maana ya maneno yale. Akampigia simu OCD na kumueleza kilichofanywa na wauaji wale hatari. Daniel alitoka nje bila kujua anaelekea wapi ?

Daniel sasa alikuwa kama amechanganyikiwa. Alijuta kwanini aliliacha hai lile kundi la waharifu aliowaona wakati wanakuja. Kuwadharau kwangu kumeniponza. Tangu kuanza kwa Mchezo huu Daniel alifanya kosa la kwanza. Kosa lililomgharimu sana. Kosa lililomfanya akose taarifa muhimu toka kwa Lee. Alikuwa anawaza huku anatembea. Alipostuka alijikuta yupo mtaa wa National. Mtaa aliokuwa anakaa mpenzi wake aliyekuwa anaitwa Davina . Akaona bora aende kwa Davina akapumzike ili ajipange vizuri kupambana na genge la Lee.



Alifika kwa Davina. Alipiga hodi lakini kulikuwa kimya. Alisukuma mlango ukakubali. Daniel alikuwa sebuleni sasa.Hali aliyoikuta pale sebuleni ilimtisha, kulikuwa shaghalabagala. Akajua kuna jambo. Akaanza kuita kwa sauti kubwa.



Kulikuwa kimya..



Akaelekea chumbani kwa Davina huku bastola imetangulia mbele kiwiliwili kinafuata. Hakukuwa na mtu. Akawa anaelekea bafuni, alistuka sana. Aliukuta mwili wa Davina umelala katika beseni kubwa la kuogea mule bafuni. Maji yote ndani ya beseni yalikuwa mekundu, damu!

Davina alikuwa amechomwa kisu cha tumbo!

Daniel aliusogelea mwili wa Davina. Alimkuta mpenzi wake Davina ndo anaagana na dunia, anakata roho. Maneno ya mwisho aliyoongea Davina yalipenya vizuri katika masikio ya Daniel



“Ra-fi-ki- yako m-pe-nzi ka-ni-u-a!”.



Daniel akajua sasa anapambana na mtu anayemjua vizuri, ndio maana akajiita rafiki. Akaiona hatari waliyokuwa wanakabiliwa nao watu wake wa karibu



‘Nikiwa mzembe nitawapoteza wote’ Alijisemea.



Mle ndani sasa akaona sio sehemu salama tena. Akawa anatoka kwa mwendo wa haraka sasa. Alipofika sebuleni alimuona mtu kakaa kwenye kochi akivuta sigara. Hakujua mtu yule kaingia ndani saa ngapi…..

Alikuwa amevaa suruali nyeusi, shati jeusi, viatu vyeusi na kofia aina ya kapelo nyeusi. Alikuwa anavuta sigara na kuachia moshi mzito angani. Daniel hakustuka, alijua kustuka ni kuonesha udhaifu kwa mtu yule. Akiwa makini na Bastola yake alisogea hadi sebuleni.



“Habari yako Mr Daniel”Mtu yule alisalimia kwa majigambo.



“Nzuri Mr Kishoka”Daniel alitoa jibu lililomstua sana mtu yule. Hakuwa anategemea kama Daniel anamfamu.

Daniel hakuwa mzembe kiasi hiko. Yaani atafutane na watu ilihali hawajui. Kule ofisini aliona picha za wakuu wa operesheni ile na majina yao.Walikuwa watu watatu. Wawili hakuona haja ya kuyashika majina yao. Walikuwa wameelekea mbele ya haki. Tena aliwaua yeye mwenyewe kwa mkono wake. Jina la huyu aliye hai alilishika .Alijua atakutana nae tu.

Na sasa walikuwa sebuleni kwa Davina, marehemu Davina.



Daniel alikuwa uso kwa uso na Kishoka!!!

Daniel hakuwa mzembe kiasi hiko. Yaani atafutane na watu ilihali hawajui. Kule ofisini aliona picha za wakuu wa operesheni ile na majina yao. Walikuwa watu watatu. Wawili hakuona haja ya kuyashika majina yao. Walikuwa wameelekea mbele ya haki. Tena aliwaua yeye mwenyewe kwa mkono wake.Jina la huyu aliye hai alilishika. Alijua atakutana nae tu.

Na sasa walikuwa sebuleni kwa Davina, marehemu Davina.



“Mimi ni mtu mwema, nimeleta salamu toka kwa rafiki yako kipenzi, anakushauri acha kufatilia mchezo huu kama unapenda kuishi. Yeye anakupenda sana, angeshakuuwa zamani kama angetaka, amekuacha unapumua hadi sasa kutokana na urafiki wenu. Hili siyo ombi ni ushauri kwa sababu anapenda uendelee kuivuta hewa hii” Kishoka alisema kwa kujiamini sana. Daniel akajua kwa kujiamini kule pale siyo mahali salama kwake, halafu hajui adui yuko wapi na kajipangaje.



“Anaitwa nani huyo rafiki yangu kipenzi?” Daniel aliuliza.



“Kwasasa hana haja ya kujitambulisha. Ila amesema ukiendelea kumfuatafuata, utamjua, na siku utakayomjua ndio itakuwa siku yako ya kufa !” Alimwambia hivyo huku akimuonesha ishara ya mkono shingoni akiwa na maana watamchinja.



Kama walileta mikwara basi hapa walikosea. Daniel hakuwa mtu wa kuogopa mikwara. Alipenda mikwara akaoa hatari. Maneno ya Kishoka yalimtia ari akiamini kuwa amewakaribia sana wauaji!



“Mimi naenda Daniel, hilo ni onyo la kwanza na la mwisho” Mzee Kishoka alinyanyuka na kutoka nje.

Daniel hakujibu.

Alibaki amekaa kwenye kochi akitafakari. Kwa mara ya pili wamemzidi ujanja. Wamemchukua Lee, wamemuua Davina. Akajua kuna mtu mpya wamemuongeza katika kundi lao. Mtu makini zaidi tofauti na waliokuwa mwanzo, na huyo mtu labda ndiye rafiki yake. Ni nani???



Daniel aliondoka ndani ya nyumba ile. Hakuwa na mpango kabisa na Kishoka. Alijua kumfatilia kishoka ni kujianika mbele ya wauaji. Alijua hata wao walijua baada ya mkwara ule atamfatilia Kishoka. Walichanga karata zao vibaya. Daniel hakuwa mtu wa aina hiyo. Daniel sasa alitembea kwa makini zaidi. Alijua kwa vyovyote kuna mtu atakuwa anamfatilia.

Huku akijua anafuatwa Daniel alienda moja kwa moja Baa. Akaagiza mchemsho na soda aina ya Fanta. Wakati anakunywa macho yake yaliangaza haraka kwa wateja wote wa Baa ile. Kuna wateja wawili aliwatilia shaka. Hawakuwa wateja kweli. Walikuwa wanafatilia mienendo ya mtu. Na bila shaka mtu huyo ni yeye. Akawa anakula mchemsho huku anatabasamu. Kumjua adui ni nusu ya kuwashinda. Aliamini vijana wale kazi yao imekwisha.

Daniel alinyanyuka kwenye kiti akajifanya kwenda maliwatoni. Kwa jicho la pembeni alimuona mmoja wa watu wale aliowatilia mashaka nae akinyanyuka, akamfata. Alipofika maliwatoni kulikuwa na milango miwili ya choo,wa kike na wa kiume. Daniel akaingia choo cha kike. Yule mtu alipofika pale hakujua Daniel ameingia wapi. Lakini bila shaka aliamini kaingia choo cha kiume. Alifungua mlango wa choo cha kiume akiwa kashika Bastola mkononi. Akiwa anakaribia kuingia mule chooni alistukia akipapaswa begani. Aligeuka kwa pupa alisalimiana na karate kali ya shingo, hapohapo alienda kumsalimia marehemu Edgar. Kabla Daniel hajaamua nini cha kufanya simu ya yule jamaa ilianza kuita. Akaitoa mfukoni, Niga jina lilisomeka kwenye kioo. Daniel aliiacha iite hadi ikakata. Alijua itakuwa yule mtu aliyemwacha kule Baa. Akaichukua ile simu akaandika meseji



”nishamdhibiti Niga njoo choo cha kiume” Daniel Aliutuma huo ujumbe.



“Poa jembe” Majibu yalirudi.



Daniel akajua ameshamnasa ndege wake, alikaa tayari kwa kumchinja.



Niga aliingia chooni huku akipiga mluzi. Alikuja kwa kujiamini akijua Daniel amedhibitiwa. Alipofika chooni aligonga. Daniel ndiye aliyemfungulia. Kwa kasi ya haraka alishikwa shingo na kuvutwa ndani ya choo. Kilikuwa kitendo asichokitegemea, Aliogopa sana. Alipigwa ngumi moja ya uso iliyomfanya aone nyotanyota. Alimpiga ngumi nyingine ya shavu, jamaa uzalendo ukamshinda akaanza kupiga kelele.



"mamaaa nakufaaaaa !



Daniel nusura acheke. Anautaka ugaidi wakati hajagaidika. Watu kwenye Baa wakawa wanaelekea chooni sasa. Walipofungua mlango walikutana na kitambulisho, kitambulisho cha Polisi toka kwa Daniel Mwaseba!

Wote walianza kurudi nyuma, Daniel akamfunga pingu Mtuhumiwa wake na kwenda nae kituoni.



***



Hali ya hewa ya Kilwa sasa iliharibika. Kuteswa kwa Inspekta Nyange, kuuwawa kwa maaskari watatu tena kituoni na kutoroshwa kwa Mtuhumiwa ilikuwa habari mbaya kwa Jeshi la Polisi Tanzania nzima. Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi (RPC) Mohamedi Banji alihamia Kilwa ili kusaidia kuhakikisha wanawatia mbaroni wauaji hao.



Daniel alipofika kituoni na mtuhumiwa yule na baada ya kuwajulisha kuwa yuko katika mtandao wa Lee yule jamaa alijuta. Aligombaniwa kama mpira wa kona. Alichapika sana kabla ya kupelekwa katika chumba cha mahojiano kusubiri kuhojiwa. Jamaa alitapakaa damu mwili mzima !

Safari hii hawakutaka kuchelewa Daniel Mwaseba akaingia kwenye chumba cha mahojiano kumuhoji Mtuhumiwa. Jamaa alikuwa mlaini kama mlenda. Sijui hata kwa nini aliingia kwenye kundi hatari kama lile.



“Jina ? ”Daniel alianza



‘Erick Bamia”Jamaa alijibu



“Kabila ?”Aliendelea Daniel.



“Mnyakyusa”



“Hili kundi ulilopo linaitwaje” Daniel alikuwa analijua ila alitaka kujua kama atadanganya.



“Ocafona”Erick alijibu.



“kauli mbiu ?”



“We live together and will die together”Alijibu kwa kirefu.



“Kiongozi wenu nani ?”



“Alikuwa Lee, sahivi kuna mdada simjui jina lake”Erick alijibu hadi asivyoulizwa.



“Kwasasa wenzio wako wapi ?”Daniel aliendelea kudadisi.



“Mjaka Guest House” Alimwaga mchele Erick.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sisi tunaenda sahivi ole wako tusiwakute”Daniel alimtia mkwara.



“Na uhakika wapo” Erick aliwahakikishia.



Erick alifichua siri bila kibano. Alikuwa mlaini kama jina lake, Erick Bamia.



Askari ishirini wakiwa na silaha walipanda kwenye gari yao kwenda kuivamia nyumba ya kulala wageni ya Mjaka. Walipofika pale ilikuwa vita, kati ya askari na wahalifu. Ndani ya nusu saa wahalifu wote walikuwa wamelala chini. Huku askari saba wakiwa majeruhi. Katika maiti zote hakukuwa na maiti ya Kishoka. Hakukuwa na maiti ya Lee, Hakukuwa na maiti ya dada kama jamaa alivyosema. Askari wakajua kazi bado. Waliichambua ile nyumba ya kulala wageni kama karanga. Hawakuisikia hata harufu ya watu wale watatu.

Walipotea mithili ya moshi.



Wakati askari wanavamia nyumba ile ya kulala wageni Kishoka, Devotha na Lee hawakuwa pale. Walikuwa wamempeleka Lee kwenye zahanati moja ya vichochoroni ili kuiangalia afya ya Lee. Kumbe na bahati ilikuwa upande wao walinusurika kwenye mdomo wa mamba. Wakiwa wanarudi walikuta na Polisi ndio wanatoka. Walinusurika namna hiyo. Sasa wakaona kambi mbovu. Devotha alimpigia simu mkurugenzi awatumie ndege ili waende Dar es salaam. Hali ilishakuwa mbaya sasa. Devotha aliamua waondoke wakajipange upya.



Baada ya saa moja ndege ilitua kinyemela kwenye msitu wa Ngome. Kishoka, Devotha na Lee walikuwa washafika Ngome muda mrefu. Wakapanda ndege na kuelekea Dar es salaam. Huku Mpango wao wa siri wakiuweka kiporo. Ndege ilivyokuwa angani walipumua sasa. Wote walikiri Daniel Mwaseba alikuwa kiboko!!!!!!!!



Baada ya dakika 45 walitua Mabwepande na kuelekea Tegeta kwa kutumia gari yao iliyokuwa inawasubiri. Walimkuta John Masaga amefura kwa hasira.Hakuwa anategemea kama kuna siku Devotha atamkimbia adui. Devotha amesomeshwa kwa hela nyingi na kampuni ili aisaidie kuhakikisha mpango huu unakamilika.Eti leo amewakimbia maadui.Ilimkasirisha sana Masaga. Aligoma sana John Masaga siku ile. Laiti angeijua shughuli ya Daniel Mwaseba.............



***



Kilwa Masoko msako wa kuwasaka Kishoka, Devotha na Lee uliendelea. Zikapita wiki, mwezi, miezi mitatu sasa hawakuwaona kabisa watu wale. Polisi wakahisi ule mpango ulikufa. Sasa walisahau kabisa kama kulitokea mauaji ya kutisha kama yale, Polisi wote walisahau Kisanga kile, lakini siyo Daniel Mwaseba. Hakusahau hata dakika moja.Atasahau vipi wakati harakati za mpango ule uliondoka na roho ya Mpenzi wake Davina. Uliondoka na roho ya Mzee Mirambo. Uliondoka na roho za raia wasio na hatia. Hakusahau kabisa. Na zaidi kutofanikiwa kujuwa nini kilikuwepo ndani ya mpango ule kulifanya umgande katika ubongo wake muda wote. Alimkumbuka Kishoka na mikwara yake. Alimkumbuka aliyejiita rafiki wa Daniel. Daniel alikuwa na hamu sana kumjua alikuwa ni nani ?.







Ilikuwa siku ya Jumamosi tulivu Daniel yupo Baa ya Makondeko akipata mchemsho kama ilivyo kawaida yake. Alimaliza Makongoro yote na ndizi zilizokuwepo kwenye bakuli lake. Sasa alinyanyua bakuli lile ili aunywe mchuzi wote uliobaki ndani ya bakuli. Bakuli halikufika mdomoni, liliishia njiani. Daniel alimuona mtu aliyemfananisha. Hapana alikuwa mwenyewe Devotha Nyang’oro. Rafiki yake kipenzi kipindi wanajifunza mafunzo ya upolisi kule Moshi. Akiwa bado kalishikilia bakuli lake, alikumbuka jinsi Devotha akivyompenda yeye. Lakini yeye hakuwa tayari kulisaliti penzi la mpenzi wake aliyemuacha nyumbani, Davina Shija.



Devotha alikaa katika viti vya pembeni peke yake. Bila shaka alikuwa anamsubiri mtu. Maana meza ile ilikuwa na viti viwili tu. Kimoja alikalia Devotha kingine kilibaki wazi. Sasa Daniel aliamua kunywa mchuzi wake, lakini haukufika mdomoni tena, alimuona mgeni wa Devotha. Daniel alistuka sana. Alikuwa anamjua vizuri sana mtu yule. Alikuwa Kishoka.

Sasa Daniel aliachana na habari za mchuzi, akaliweka bakuli juu ya meza. Akawa makini na meza ile ya kina Devotha.



Baada ya masaa mawili Devotha na Kishoka wakanyanyuka. Baada ya kumlipa mhudumu wakawa wanaondoka. Walikuwa wanatembea kwa miguu huku wameshikana mikono kama mtu na mpenzi wake. Kwa jicho la mtu wa kawaida angedhani watu wale wawili walikuwa wapenzi. Lakini si kwa jicho la Daniel, Daniel hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe, tembea yao tu ilimjulisha watu wale wako kazini, kazi gani hiyo?



Daniel alikuwa anawafuata kwa nyumanyuma. Huku anawafata akapiga simu Polisi. Akaomba Polisi watano kwa kazi maalumu.

Safari ya Devotha na Kishoka ikaishia Mikumi Guest, wakaingia ndani. Askari aliowaagiza Daniel walikuwa wamevaa nguo za kiraia. Watatu aliwaweka mlango wa mbele wa ‘Guest ‘ile na wawili mlango wa nyuma. Aliwaagiza wakiwaona wametoka tu watu wale wawili wampigie simu. Hakuwaambia wale ni akina nani?.Ila aliwatahadharisha atakayefanya kosa tu ajue amekufa. Aliwaambia wale ni watu wabaya sana. Daniel alirudi nyumbani kwake akiwa na mawazo mengi sana.

Daniel alikuwa na taarifa za Devotha kuacha kazi ya Upolisi. Alisikitika sana siku aliyosikia kwani alikuwa anaujua vizuri uwezo wa Devotha. Kuacha kwake kazi ya Upolisi lilikuwa ni pengo kubwa sana Kwa Jeshi la Polisi. Daniel alilala siku hiyo akiwa mwingi wa mawazo.



Saa kumi na moja asubuhi simu ya Daniel iliita. Kuangalia namba ni moja ya wale askari aliowapa kazi ya kuwalinda wakina Devotha. Moyo ukampiga!

Akajua shughuli imeanza.



”Mkuu windo letu linatoka wakiwa na mabegi inaonesha wanasafiri” Sauti ya kunong’ona kwenye simu ilisikika.



”wafatilieni” Nae alinong'ona.



Askari wale walikuwa makini. Walifata bila kujulikana.

Devotha na Kishoka walikuwa wanaenda stendi ya mabasi yaendayo Dar es salaam.Ili warudi Dae es salaam. Safari hii walikuja kama watu wa kawaida ili kupeleleza hali ilivyo baada ya sakata lile lililotokea miezi mitatu iliyopita. Waliamua kuja katika sura ya mtu na mpenzi wake, na kufikia katika nyumba ya kulala wageni ya kawaida na kupanda mabasi ya umma. Hii iliwasaidia kujichanganya na raia wa kawaida na kupata taarifa nyingi walizozihitaji. Bahati mbaya iliwapata siku moja kabla ya kuondoka walipoonwa na jicho la Daniel Mwaseba.



Baada ya kupata taarifa kuwa Kishoka na Devotha wanaoondoka. Daniel alivaa harakaharaka. Alivaa suruali aina ya jeans nyeusi na fulana nyeupe. Chini alivaa viatu vyeusi. Na bastola yake mkononi alienda kazini. Wakati Devotha na mwenzie wakipanda basi la Swahili kuelekea Dar es salaam. Daniel alikuwa amepanda basi la Mashaallah. Aliamua kuwafata kila hatua watakayopiga hadi ategue kitendawili cha Mpango wa Siri.

Basi zote ziliwasili Mbagala saa tatu asubuhi. Zilipishana dakika kumi tu kufika pale stendi. Ilitangulia Mashaallah ikafatiwa na Swahili. Kutangulia kwa Mashaallah ilikuwa faida kwa Daniel. Alibana katika kona moja pale stendi akilisubiri windo lake. Dakika kumi baadae aliwaona Devotha na Kishoka wakishuka ndani ya gari. Aliwaona wakielekea kwenye gari moja nyeusi. Daniel aliikumbuka gari ile. Ilikuwa ni Range Rover aliyoiona inaoondoka kwa kasi siku ile kituoni wakati yeye anatoka kumwangalia Inspekta Nyange. Range Rover iliyohusika katika mauaji ya askari watatu na kutoroshwa kwa Lee. Bila shaka ilihusika na katika kifo cha Mpenzi wake Davina. Daniel alijumuisha ili kuongeza hasira juu ya watu wale.



“Fuata gari ile hakikisha hawatambui kama wanafuatwa” Daniel alimuelekeza dereva teksi baada ya kuingia kwenye gari yake. Akiwa ndani ya teksi kumbukumbu nyingi zilipita kichwani mwake. Sasa alikumbuka ule ujumbe ulioachwa juu ya kiti baada ya Lee kutoroshwa. Alikumbuka ujumbe alioambiwa na Davina wakati anakata roho. Alikumbuka ujumbe alioletewa na Kishoka. Akajua kuwa kumbe waliposema rafiki yako kipenzi walimaanisha Devotha.



Dereva teksi alikuwa mtoto wa mjini hasa, aliifata ile teksi bila kustukiwa. Kina Devotha hawakuwa makini kabisa. Walijiamini wako peke yao hawakuwa wanatilia wasiwasi kabisa magari ya nyuma. Msafara ulikuwa unaelekea ofisini kwao Tegeta.

Kutokana na foleni walichelewa kidogo kufika Tegeta. Daniel Mwaseba aliendelea kuifuata gari waliyopanda kina Devotha. Daniel akiwa amekaa kwenye siti za nyuma za abiria alikuwa makini sana. Alihakikisha hafanyi kosa hata moja. Aliujua uwezo wa akili alionao Devotha.



Msafara ule sasa ulifika Tegeta. Uliishia kwenye nyumba moja yenye geti nyekundu. Kwa mwonekano wa nje tu wa nyumba ileDaniel alikiri ile nyumba ilikuwa ya tajiri. Ilikuwa nyumba nzuri yenye hadhi ya kuitwa nyumba ya kisasa. Daniel alilimlipa dereva teksi ujira wake. Ile teksi ilivyotokomea yeye alienda kwa muuza mahindi mmoja aliyekuwa anauza mahindi ya kuchoma pale barabarani.



“Mahindi bei gani kaka ?” Daniel aliulizia bei ya mahindi.



“Shilingi mia tatu kaka” Muuza mahindi alijibu.



“Nipe moja” Daniel alisema huku akitoa noti ya shilingi elfu mbili.



“Sawa” Muuza mahindi alijibu.



“Kaka naomba nikuulize kitu” Daniel alichokoza.



“Niulize kaka” Muuza mahindi alikaa tayari kumsikiliza.



“Hivi una muda gani tangu uanze kuuza mahindi hapa ? ”



“Mwaka wa tatu huu”



“Hivi unamjua mmiliki wa nyumba ile ? ” Daniel aliuliza huku akiionesha kwa kidole nyumba waliyoingia wakina Devotha.



“Hapana kaka. Sina muda wa kufatilia mambo ya watu, yangu mwenyewe yananishinda” Daniel alijibiwa kijeuri.



“Samahani kaka kama nimekosea kukuuliza”Aliomba msamaha.

“Bila samahani”Muuza mahindi alijibu kwa mkato.



Daniel aliondoka kichwa chini. Daniel alipofika umbali kidogo kutoka pale kwa muuza mahindi. Muuza mahindi alitoa simu yake na kupiga namba fulani, baada ya kupokelewa akaanza kuongea.

Daniel aliondoka kichwa chini. Daniel alipofika umbali kidogo kutoka pale kwa muuza mahindi. Muuza mahindi alitoa simu yake na kupiga namba fulani, baada ya kupokelewa akaanza kuongea.



“Halo Bosi”



“Kuna mtu wa kutilia shaka...”



“Aliiulizia mmiliki wa ofisi”



“Sawa bosi”



“Haina shida”



Kama Daniel alidhani anaongea na muuza mahindi basi alikosea sana. Muuza mahindi yule alikuwa mmoja wa walinzi wa ofisi ile. Na sasa alimpigia simu John Masaga kumuelezea juu ya shaka yake na Daniel. Na sasa aliambiwa amfuatilie wakati Bosi akiwapigia watu wa kuja kumaliza kazi. Kwa kificho kikubwa muuza mahindi alikuwa anamfatilia kwa nyuma Daniel Mwaseba.



Muuza mahindi alikosea sana. Daniel Mwaseba huwa hafuatwi kwa nyuma.

Baada ya kuondoka tu kwa muuza mahindi Daniel alijua atafuatwa. Majibu ya mchoma mahindi yalimjulisha kuna kitu cha siri anaficha. Kwahiyo Daniel aliondoka akijua ataanza kufuatwa na wakina Kishoka. Hakutegemea kama mfataji atakuwa ni yuleyule mchoma mahindi.



Daniel alikuwa anatafuta hoteli ili ale. Alihisi tumbo lake lipo tupu. Aliipata hoteli ndogo maeneo yale yale ya Tegeta. Akaingia ndani na kutulia kitini.



“Habari yako kaka”Alisalimiwa na sauti tamu ya Mhudumu wa kike.



“Salama dada, nataka wali nyama”Daniel aliagiza bila kuulizwa .



“Sawa, karibu sana” Yule dada alijibu na kuondoka.



Baada ya dakika mbili wali nyama uliletwa na dada yuleyule.



“Karibu kaka” Mhudumu alimkaribisha kistaarabu na kuondoka.



Daniel alianza kukishambulia chakula kwa fujo. Ndani ya dakika tano, wali kwa nyama ulikuwa umetulia kwenye tumbo la Daniel. Alimwita yule Mhudumu wa kike kwa ishara ya mkono.

Dada alikuja haraka.



“Naomba maji makubwa”



“Ya lita moja?”



“ndio”



“Nakuletea”



Maji ya lita moja yaliletwa. Daniel aliweka ile chupa mkononi na kuanza kuyamiminia tumboni maji yale. Wakati anayamalizia maji yale aliona kitu. Alimuona muuza mahindi nyuma ya gari moja akiwasiliana na simu. Daniel akacheka kimoyomoyo.

Sasa alijua mchoma mahindi alikuwa shushushu wa wale jamaa. Damu ikamchemka. Hamu ya kupambana ikampanda. Alijifanya kama hajamuona. Baada ya kumaliza yale maji yule muhudumu alikuja. Akamlipa hela zake.



“Nimependa huduma yako” Daniel alimwambia yule Mhudumu.



“Ahsante kaka, karibu sana” Mhudumu alijibu huku akichekacheka.



“Tunaweza kuonana sehemu tofauti na hapa kwa maongezi” Daniel alirusha ndoano yake.



“Hamna tatizo kaka, wewe tu” Mhudumu alijibu kwa sauti ya kideko.



Wakabadilishana namba za simu, na Daniel alielekea maliwatoni.



Maliwato ya hoteli ile yalikuwa uwani. Alipofika hakuwa na haja ya kwenda maliwatoni. Alikuta kuna ukuta mkubwa lakini haukumpa shida kuupanda. Alishuka chini. Alitokea kwenye vichochoro vya nyuma vya hoteli ile na kutokomea. Alimuacha mchoma mahindi akichoma mahindi pale nje.



Daniel sasa alitokea mtaa wa pili, alikuwa na furaha kwa kuwa alishapapata pa kuanzia. Alipanga kesho asubuhi akaanze kwa mchoma mahindi. Kwa kuwa alijua mchoma mahindi alijua hajamuona kwa hiyo kesho yake ataendelea na mtego wake kama kawaida. Daniel sasa alikuwa anatafuta hoteli ya kupumzika ili aanze kazi kesho asubuhi.



Wakati Daniel akitafuta hoteli ya kupumzika na kujipanga. Matatizo makubwa yalimkuta mchoma mahindi. Kumpigia kwake simu Bosi John Masaga kuwa kuna mtu anamtilia shaka halafu sasa anasema eti amempotea. Haikumuingia akilini Masaga hata kidogo. Baada ya kupigiwa simu ile Masaga aliwatuma Kishoka na Devotha kwenda kuucheza mchezo huo. Mchezo waupendao. Hawakumkuta mtu zaidi ya mchoma mahindi akiwa amejibanza nyuma ya gari moja ya mteja aliyekuwa ndani ya hoteli ile. Wema wa mchoma mahindi ulimponza, sasa alionekana mzembe kuliko mtu yeyote yule hapa duniani.



Daniel aliipata hoteli iliyomvutia. Hoteli ya Double view iliyopo Sinza ndio ilichaguliwa na moyo wake. Akapata chumba namba 38 na kujitoma ndani yake. Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye kila kitu ndani yake. Daniel alijitupa kwenye sofa moja ndani ya chumba kile. Alikaa huku akifikiria kazi iliyopo mbele yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alijikuta amesinzia pale kwenye sofa. Alikurupuka saa mbili usiku. Njaa ilikuwa inamuuma. Alipiga simu iliyokuwepo mule chumbani na kuagiza chakula. Baada ya dakika kumi mhudumu alileta chakula alichokiagiza, ugali kwa mboga za majani.

Alikifakamia chakula chote.



Mara simu yake ikaita, alikuwa ni yule dada mhudumu wa hoteli kule Tegeta. Daniel hakuwa na mpango naye muda huo. Akamwambia amepata dharura kidogo yupo nje ya mji, atamtafuta akirudi. Hakuwa nafasi ya kuwa na mwanamke kwa muda ule, hakuwa na hisia kabisa. Akili yake ilikuwa inawaza kazi tu.



”Nikimhitaji nitamuita” Alisema huku akiisafisha bastola yake kwa kitambaa. Baada ya kusafisha akaangalia risasi akazikuta zipo za kutosha. Akaifunga. Akaibusu mara tatu na kuiweka juu ya kitanda. Akaenda bafuni kuoga, halafu akatoka nje ya hoteli kuangalia mandhari ya jiji baada ya kuvaa na kuiweka bastola yake kiunoni.



Hoteli ya Double view ilikuwa na sehemu ya mgahawa pia. Watu wakipata chakula na vinywaji. Safari ya Daniel ilikomea hapo. Alichagua meza moja ambayo haikuwa na mtu pembeni. Alipokaa tu Mhudumu akaja, akamuagiza bia aina ya safari. Mhudumu alipoileta bia na kuifungua Daniel akawa anainywa taratibu.

Daniel alikuwa askari.

Tena askari mpelelezi makini sana, kwa sasa alikuwa anashika chati katika ya orodha ya wapelelezi Tanzania. Daniel alikuwa mpelelezi namba moja. Daniel alikuwa mpelelezi asiye na mipaka. Alikuwa na uwezo wa kwenda mkoa wowote Tanzania na kufanya kazi bila kuulizwa na mtu yeyote. Zaidi ya askari wengine kumpa msaada kila alipouhitaji. Ndio maana kuondoka kwake kwa ghafla Kilwa hakuna aliyehoji. Wakuu wake walijua Daniel yuko kazini, na walikuwa wanasubiri majibu tu ya kazi yake.



Ndani ya mgahawa alimokuwemo alikuwa kazini pia. Hadi bia yake inafika nusu alikuwa ashawasoma watu wote waliokuwa mle Baa. Daniel alikuwa na kipawa hiko. Siyo kwa kufundishwa, Daniel alizaliwa na karama ya uanasaikolojia ya wahalifu. Ndani ya ile Baa aliona iko safi. Watu wote ndani ya ile Baa walikuja kustarehe. Hawakuwa na mambo mengine.

Baada ya kumaliza bia yake Daniel alirudi chumbani kwake. Alipoingia tu ndani alistuka. Aligundua kuna mtu aliingia chumbani kwake na kupekua. Mtu gani?

Hakumjua.

Kitu gani akitafuta? Hakukijua.

Lakini Daniel alimsifu mtafutaji. Alikuwa makini sana katika utafutaji wake. Bila kuwa makini ni ngumu sana kutambua kama chumba kile kilifukuliwa....Lakini si kwa Daniel, aligundua baada ya kutazama kwa jicho moja tu...



Baada ya kumaliza bia yake Daniel alirudi chumbani kwake. Alipoingia tu ndani alistuka. Aligundua kuna mtu aliingia chumbani kwake. Na kupekua. Mtu gani? Hakumjua. Kitu gani akitafuta? Hakukijua. Lakini Daniel alimsifu mtafutaji. Alikuwa makini sana katika utafutaji wake. Bila kuwa makini ni ngumu sana kutambua kama chumba kile kilifukuliwa. Daniel akaona pale siyo sehemu salama. Akafunga chumba akarudi Mgahawani. Akawa anawaza aende wapi ?. Ilikuwa inakaribia saa nne usiku. Daniel akarudia tena zoezi lake la kuwachunguza watu wote pale Hotelini.

Ndipo akamgundua...



Yule dada aliyemuhudumia mchana kule Tegeta alikuwemo mle mgahawani.

Ndio ni yeye!

E bwana wee!!!



Sasa Daniel alielewa kwanini waliyajua maficho yake. Itakuwa ile simu iliyopigwa na yule Mhudumu ndio imewaelekeza maficho yake. Akajua watu hawa wanacheza dili na mitandao ya simu. Ni hao ndio waliolekeza simu yake inaongea kutoka wapi?. Sasa hakutaka kukimbia. Alidhamiria kuianza kazi usiku ule. Alitulia kwenye kiti. Mhudumu alifika. Aliagizia Safari nyingine. Ilifunguliwa lakini hakuinywa, alikuwa anaitazama tu huku akichanga karata zake vizuri. Baada ya dakika kumi Daniel akanyanyuka, akajifanya kama anaenda ndani tena chumbani kwake. Macho sita yalikuwa makini yakimfatilia yeye. Yakifatilia kwa umakini nyendo za Daniel. Macho manne yalikuwa katika mshangao mkubwa hawakutegemea kuwa mtu aliyewafata na kuulizia ofisi yao kuwa ni Daniel Mwaseba! Macho hayo yalikuwa ya Kishoka na Devotha na macho ya Hasna, yule Mhudumu wa hoteli hayakuwa na wasiwasi wowote. Kwakuwa alikuwa hamfahamu vizuri mtu wanayemfatilia.



Mchana ule alipomtoroka muuza mahindi na kumuachia matatizo makubwa Adrian. Devotha alifanya kazi ya ziada. Wakati Masaga akiwa anamgomea Adrian ambaye alikuwa mmoja wa walinzi wa ofisi ile akiyejifanya mchoma mahindi, Devotha alifikiria nje ya boksi. Alirudi kule hotelini na kumuulizia yule dada aliyemuhudumia mtu wakiyemtafuta. Kwa ushawishi wa hela yule Mhudumu alianika kila kitu. Alisema hadi kama wamebadilishana namba za simu. Ilikuwa ni hatua kubwa kwa Devotha. Alimuachia shilingi laki moja na kumwambia atarudi tena. Yule Mhudumu alijiona amekula bingo bila kujua anafanikisha mpango wa siri.



Mida ya saa mbili Devotha alirudi kwenye hoteli ile. Akamwambia yule Mhudumu ampigie simu huyo mtu. Simu ilipigwa na Daniel bila kujua akapokea. Baada ya maongezi mafupi Devotha alimpigia rafiki yake anayefanya kazi kwenye kampuni ya simu ile aliyoitumia yule dada Mhudumu. Devotha akapata taarifa juu ya mnara uliotumika katika kupokelewa simu ile. Alivyotajiwa mnara akawa anafikiria hoteli nzuri iliyopo eneo lile. Hakufikiria kabisa kama mtu huyo atakuwa atakaa kwenye nyumba ya mtu. Alipata jibu Double view hoteli..Zilikuwa hisia tu za Devotha. Wakajipanga na Kishoka na kumchukua yule dada Mhudumu ili awasaidie katika utambuzi. Walipofika pale Mgahawani walimweka yule dada hadharani huku wao wakiwa wamejificha katika kona moja. Alipotokea Daniel kwa mara ya kwanza yule dada aliwakonyeza akina Kishoka. Wakapeana majukumu. Devotha akatafute chumba alichofikia Daniel na Kishoka asubiri pale bila ya kumpa Daniel mwaya wowote wa kufanya mambo yake.

Devotha aliingia hotelini. Hakupata shida kukijua chumba alichofikia Daniel. Penye udhia penyeza rupia. Alimpa Mhudumu pesa, bila kufikiria Mhudumu alimuelekeza Devotha chumba alichofikia Daniel. Yeye alidhani anamuelekeza Changudoa tu bila kujua Mhudumu yule wa mapokezi alikuwa anashiriki katika Mpango wa Siri.



Devotha alienda hadi kwenye mlango namba 38. Chumba cha Daniel Mwaseba. Alifungua kwa kutumia funguo Malaya. Hakupata shida. Funguo ya tatu tu kujaribu mlango ulifunguka. Devotha alikuwa makini sana. Alipekua vitu kwa makini sana. Hakukuta kitu cha ajabu. Alitoka huku akihakikisha anaacha kila kitu kama alivyokikuta.



Daniel sasa alijifanya anaenda upande wa uwani wa hoteli ile. Kumuona Yule Mhudumu ilikuwa ishara mbaya kwake. Akaelewa sasa, kina Devotha itakuwa wapo eneo lilelile. Alipofika uwani alisimama. Alitoa bastola akiwa tayari kwa lolote. Kulikuwa kimya, hakuna aliyemfata. Akaingia maliwatoni. Akatoka baada ya muda mfupi. Aliyeingia maliwatoni ni Daniel, aliyetoka alikuwa mtu mwengine kabisa. Alikuwa kizee wa miaka 60. Daniel alivaa sura ya bandia. Alienda moja kwa moja Mgahawani, akakaa kiti kingine tofauti na pale alipokaa mwanzo. Daniel alikuwa amewazidi akili sasa. Hakutambulika kabisa. Baadae kidogo alimuona mtu anatoka kule uwani, alikuwa Kishoka. Kumbe alimfata. Alimuona Kishoka akiongea na simu, alimuangalia na yule Mhudumu nae alikuwa anaongea na simu. Walikuwa wanawasiliana. Sasa maadui wawili walikuwa katika rada zake. Akawa anasubiri kama kuna maadui walewale au kuna wa ziada.

Kishoka sasa alionekana kutaharuki. Hakuelewa kabisa ameachwa vipi na Daniel.

Alikiri kimoyomoyo.



”Daniel hakuwa binadamu wa kawaida. Alikuwa ni shetani!”



Devotha na ushujaa wake wote alianza kutetemeka. Kichwani kwake alielewa kitu. Ukiona adui kapotea ghafla ujue kakuona. Alishangaa sana Daniel kawaona vipi?. Pale walipojificha hata shetani mwenyewe alikuwa hawaoni, sembuse Daniel? Daniel alitulia pale alipokaa, akapiga jicho kwenye kona moja alimuona mtu aliyemfahamu. Alikuwa rafiki yake kipenzi Devotha!!!.

Sasa akajipanga kuucheza mchezo...

Akanyanyuka pale alipokaa kwa mwendo wa Kizee. Alikuwa anaelekea kule aliposimama Kishoka. Aliamua kuanza na Kishoka.



”Naomba unipeleke Maliwatoni mjukuu wangu” Kwa sauti ya kizee Daniel alimuomba Kishoka msaada wa kumpeleka Maliwatoni. Kishoka akaingia mkenge. Akawa anamsindikiza Daniel Maliwatoni. Walinyoosha korido ndefu kuelekea uwani. Huku Kishoka kamshika mkono mzee yule. Kwenye korido walipishana na watu wachache wakiwa wawiliwawili. Mwanamke na mwanamme. Wakafika uwani, Daniel alikuwa anahesabu kimoyomoyo, moja, mbili, ile tatu, kilimtoka kichwa kikali kilichompata Kishoka kwenye sikio. Kishoka alikuwa anasikia mivumo tu sikioni kwake. Kishoka hajakaa sawa alipigwa ngumi iliyotua barabara katika mbavu zake. Kishoka hakuwa amejipanga kabisa. Hakutegemea kabisa kama mzee yule atamfanyia mambo yale, wema wake ulimponza. Kizee kikageuka mbogo sasa. Alitumia vizuri kuduwaa kwa Kishoka. Alimpiga teke kali la tumbo lililompeleka hadi chini, kwa haraka Daniel alitoa kisu kiunoni na kumchoma nacho wenye usawa wa moyo. Huo ndio ulikuwa mwisho wa Kishoka katika sura ya dunia. Alitema mapovu ya damu huku akitukana tusi zito la nguoni. Kishoka mwanaharamu alikufa huku anatukana...

Akambeba Kishoka akaenda kumuhifadhi chumba namba 38. Chumba chake. Bahati ilikuwa yake koridoni hakukuwa na watu .Akamuhifadhi chumbani akamfungia. Daniel akiwa na sura na mwendo wa Kizee alielekea tena Mgahawani. Akakaa palepale alipokaa mwanzo na taswira yake ya kizee. Akapiga jicho pale alipokuwa Devotha hakumwona. Akapiga jicho pale alipokaa Mhudumu hakuwepo. Akajua kimenuka sasa.



”Tulia Daniel” Alijionya mwenyewe. Alijisikiliza. Alitulia palepale. Kwa macho yake mawili aliwaona Devotha na yule dada Mhudumu wamekaa katika meza moja ya pembeni mule Mgahawani.



Daniel alinyanyuka kwa mwendo wa Kizee kwenda kwenye ile meza. Wale wadada wawili walistuka kumuuona mzee yule anaenda mezani kwao. Hawakuwa wanatarajia mgeni zaidi ya Kishoka. Devotha alikuwa makini zaidi. Yule mzee alivuta kiti akakaa huku akisema



”Naitwa Daniel Mwaseba” Daniel alisema kwa sauti ya upole.



Moyo wa Devotha uliruka kichurachura katika kifua chake. Hakutegemea Daniel atakuja kwa mtindo ule. Hawakujibu wale madada walikaa kimya kila mmoja akifikiria lake kichwani.



Shubaamitiii...



Daniel alinyanyuka kwa mwendo wa Kizee kwenda kwenye ile meza. Wale wadada wawili walistuka kumuuona mzee yule anaenda mezani kwao. Hawakuwa wanatarajia mgeni zaidi ya Kishoka. Devotha alikuwa makini zaidi. Yule mzee alivuta kiti akakaa huku akisema



”Naitwa Daniel Mwaseba” Moyo wa Devotha uliruka kichurachura katika kifua chake. Hakutegemea Daniel atakuja kwa mtindo ule. Hawakujibu wale madada walikaa kimya kila mmoja akifikiria lake.



****



Katika nyumba moja iliyopo Mbezi beach kulikuwa na kikao. Kilikuwa kikao kilichoitishwa kwa dharura. Kikao kiliwahusisha watu watano wenye vyeo vikubwa Serikalini. Kikao kiliongozwa na Mheshimiwa Haridi Buto aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Alikuwepo Mheshimiwa Zaidi Njame waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mheshimiwa Dr Wahabu Nyamzungu aliyekuwa waziri ujenzi, Mheshimiwa Albert Mahiwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi kanda ya Dar es salaam na mwanamke pekee katika kikao kile Mheshimiwa Dr Kazija Juma waziri wa afya na ustawi wa jamii.



Kilikuwa ni kikao cha viongozi wanaoheshimika sana nchini. Viongozi wenye mvuto wa kisiasa. Viongozi walioheshimika kuanzia kwa wananchi hadi Raisi wa nchi. Viongozi wanne kati ya hao walikuwa wabunge kutoka mkoa wa lindi. Mheshimiwa Haridi Buto alikuwa mbunge wa jimbo la Kilwa kusini. Mheshimiwa Zaidi Njame alikuwa mbunge jimbo la Liwale. Mheshimiwa Dr Wahabu Nyamzungu alikuwa mbunge wa jimbo la Lindi mjini na Mheshimiwa Dr Kazija Juma alikuwa mbunge wa jimbo la Nachingwea. Huku kamanda Mahiwa aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi kanda ya Dar es salaam aligombea ubunge jimbo la Mchinga lakini alikosa. Viongozi wote watano walikuwa wazawa wa mkoa wa Lindi.



Kikao kilianza kwa Mheshimiwa Haridi Buto kufungua kikao.



“Ndugu wajumbe tumeitana hapa kuzungumzia maendeleo ya Mpango wetu wa kuuokoa Mkoa wa Lindi toka katika unyonyaaji unaofanywa na Serikali. Mpango ulianza vizuri lakini sasa naona umeanza kusuasua, nchi wahisani wanataka ripoti kwanini mpango huu haujatekelezwa hadi sasa. Wametoa hela zao nyingi sana katika hatua ile ya awali. Na sasa kabla hawajatoa pesa awamu nyingine wanataka ripoti juu ya pesa walizotoa awali.” Mheshimiwa Buto alielezea Ajenda kuu ya kikao kile.



“Hata mimi nashanga maana mambo yameenda ndivyo sivyo, tabidi tumuite Mkurugenzi mtendaji wa mpango huu atwambie Mpango wetu umefikia wapi hadi sasa?” Dr Kazija Juma alitoa ushauri.



Wana kikao wote walikubaliana na ushauri wa Dr Kazija. Mkurugenzi mtendaji wa Mpango huu haramu aliitwa.

Alipoingia alisimama kuwasikiliza wakuu hawa. Mheshimiwa Buto alianza kuongea.



”Karibu sana Ndugu Andrew Chikoka. Wana kikao wanataka taarifa ya mdomo kuhusu utekelezaji wa awali wa mpango huu. Watakaporidhika na maelezo yako ya mdomo utaenda kuandika ripoti yako kwa maandishi tayari kwa kuituma kwa Mkuu ili aiidhinishe itumwe kwa nchi wahisani”



“Ahsanteni sana waheshimiwa. Utekelezaji wa mpango wetu wa siri ulianza vizuri sana. Tulifikia hatua nzuri kule kwenye kambi yetu iliyopo Kilwa. Tulishapata sehemu ya kuhifadhi silaha zetu zote zitakapotumiwa katika awamu ya pili ya mpango huu. Lakini lilitokea tatizo. Kuna watu walianza kupeleleza kazi tukizozifanya kule Kilwa. Tulifanikiwa kuwanyamazisha baadhi ila kuna mmoja alitusumbua sana. Alisababisha ile kambi ishindwe kufanya kazi kabisa. Alifanikiwa kuwauwa vijana wetu shupavu wawili. Walibaki wawili tu ambao na ilibidi warejee Dar es salaam kuja kujipanga upya” Ndugu Chikoka aliwaeleza jopo la wanakamati wale maendeleo ya Mpango ule.



“Kuja kujipanga upya?” Dr Kazija alidakia. ”Hivi unajua tuna miezi mingapi ya kutekeleza mpangu huu? na wakati mnajipanga mnajua jinsi Wananchi wanavyoteseka kule. Serikali inawabagua, haiwajengei shule, hawana zahanati, hawana barabara mzuri, wana matatizo ya maji, wana shida ya umeme. Halafu wewe unatuletea sera za kujipanga upya?” Dr Kazija aliongea kwa jazba sana. Utafikiri kweli alikuwa na uchungu na wananchi.

Dr Nyamzungu akachangia kwa sauti yake ya utulivu.



”Tuna mwaka mmoja tu wa kukamilisha mpango huu. Ni miezi mitatu sasa lakini hatujapiga hatua kabisa. Mpango ulikuwa utekelezwe kwa awamu nne. Awamu ya kwanza ni kuhakikisha tunatengeneza msingi wa mpango huu. Msingi imara kabisa. Awamu ya pili ni kuhakikisha zinaingizwa silaha. Awamu ya pili ya mpango huu inategemea sana uimara wa utekelezi wa awamu ya kwanza. Awamu ya tatu ni kusambaza chuki kwa wananchi waichukie serikali yao kama waitavyo Wahisani. Ila mimi siiti kusambaza chuki, ni awamu ya kuwaeleza wananchi ubaya wa Serikali yao. Mkoa wa Lindi shule chache, maji matatizo, umeme hamna wa uhakika, hata huduma za afya za kusuasua. Lazima tuwaeleze wananchi madhara ya kuing’ang’ania serikali hii na umuhimu wa kujitenga. Na mwisho ni kutekeleza sasa mapinduzi yenyewe ambayo yatauacha mkoa wa Lindi ukiwa huru. Sasa tuna miezi mitatu tangu tuanze mpango huu. Hatujapiga hatua yoyote. Tutawapa ripoti gani Wahisani Chikoka wakati pesa zao nyingi zishateketea?”



“Suala siyo imebaki miezi mingapi kutekeleza mpango huu. Suala la msingi ni kutatua vikwazo vinavyotukabili ili tuendelee ma Mpango huu. Tukitatua tatizo hata wiki inatosha kutengeneza base kule Kilwa” Andrew Chikoka Mkurugenzi wa mpango huu alifafanua.



“Kwani kikwazo kikubwa hasa ni nini?” Mheshimiwa Buto alimuuliza Chikoka.



“Ni Daniel Mwaseba!!” Chikoka alijibu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Hahaha mimi nilidhani tatizo litakuwa fedha au zana.Tatizo ni kidaniel nani sijui. Kamanda Mahiwa kwanini mnashindwa kumdhibiti mtu wenu. Unashindwa kumtuma kazi nje ya nchi ili atuache si tufanye mambo yetu” Dr Kazija alisema kwa nyodo za kike.



“Humjua Daniel Mwaseba mama, Daniel hayupo chini ya Polisi, jeshi wala Usalama wa Taifa. Daniel yupo chini ya Ikulu. Ana uwezo wa kwenda mahali popote atakapo bila kuulizwa ndani ya nchi. Ana uwezo wa kuingilia jambo lolote kupeleleza bila kuagizwa na mtu yeyote” kamanda Mahiwa alimfafanulia Dr Kazija.



“Kwani Daniel ana uwezo gani wa ziada. Si tumteke au tutume watu wakamkate kichwa tu, mipango ya maana inakwama kwa ajili ya Daniel” Mheshimiwa Njame nae alichangia.



“Uwezo wa Daniel ni wa ajabu sana. Historia yake inaonesha alipata mafunzo yake ya Upolisi Moshi tu. Haioneeshi kama alienda kujiendeleza nje ya Nchi wala nini? Lakini Daniel ana akili na mjanja sana. Huwezi kumkamata Daniel kama Kuku. Huwezi kumchinja Daniel kama Ngamia. Sna mbinu za kijasusi za hali ya juu sijui hata kazitolea wapi?”Kamanda Mahiwa akawapa wasifu mfupi wa Daniel.



Kikao sasa kikawa kinamjadili Daniel badala ya mpango wao. Wakapanga kukutana tena wiki ijayo kuendelea na kikao kile. Mpango kazi ulikuwa ni kumuua Daniel ndani ya siku tatu.



Mwenyekiti aliahirisha kikao.



Wakati kikao hiki kinaendelea kikao kingine kilikuwa kinafanyika katika nyumba moja mitaa ya Mikocheni. Hiki kilikuwa kikao cha watu watano pia. Wazungu wanne ndio walikuwa wamiliki wa kampuni ya Ocafona, na mtu wa tano alikuwa mweusi ambaye ndiye alikuwa mkuu wa Mpango huu hapa nchini. Hawa ndio walikuwa wanajua undani hasa cha Mpango huu, wale Mawaziri walikuwa vibaraka tu kufanikisha mipango wasiyoijua.



Wazungu hawa wenye asili ya Ujerumani walikuja kufatilia maendeleo ya Mpango wao. Wazungu hawa wanne ndio waasisi wa mpango huu wakishirikiana na huyo mtu mweusi aliyekuwepo kwenye kikao. Lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha mkoa wa Lindi unajitenga toka Serikali ya Jamhuri wa Tanzania. Walifanya tafiti na kugundua mkoa wa Lindi una rasilimali nyingi sana. Hivyo walitaka kuwatenganisha na serikali ya Tanzania. Lindi iongozwe na vibaraka wao ili wao wanufaiki na rasilimali YA gesi na mafuta.



Wazungu wale ni kati ya wazungu wenye tamaa sana. Walitoka kwenye familia moja huko katika jiji la Kaiserslautern, nchin Ujerumani. Majina yao ni Dickson Lambart, Allen Lambart, John Lambart na Alex Lambart, kwa jina moja wakijiita OCAFONA wakiwa na maana ya One Camp Four Names. Yule mtu mweusi ndiye alikuwa anawapa ripoti wazungu hawa ya utekelezaji wa mpango wao.



***



Kule Double view, Mgahawani kulikuwa na taharuki. Kizee kujitambulisha kwa jina la Daniel Mwaseba kuliwastua sana. Daniel hakuwa na habari na yule dada dhaifu, Mhudumu. Macho na akili yake ilikuwa kwa Devotha. Alikuwa anaijua vizuri sana shughuli ya Devotha.



“Habari my Devo, rafiki yangu kipenzi...” Daniel alimsalimia Devotha kwa jina alilopenda kumwita.

Devotha hakujibu.



“Mambo dada, naona tuna bahati ya kukutana leo”Daniel alimsalimia yule dada.



“Mimi? Sikumbuki tulikutana wapi leo we mzee” Dada hakumfahamu bado Daniel.



“Inawezekana hujakutana na sura hii. Vipi hata sauti hii hujaongea nayo leo? ”Daniel aliongea huku akizidisha umakini kwa Devotha. Hakutaka kufanya hata kosa dogo.



“Sikumbuki mzee” Dada alikuwa ameachwa njia panda.



“Ngoja nikukumbushe. Ulimuhudumia mteja mmoja leo mchana Tegeta, mkabadilishana namba za simu, mida ya saa mbili usiku ukampigia, Mteja huyo anaitwa Daniel Mwaseba, ndio mimi” Baada ya maelezo haya sura ya dada iliingia na aibu na uwoga.



“Devotha kipenzi, unapenda kufa kifo cha aina gani? Swali hili ndio lililonileta hapa kwenye kikao chenu” Devotha hakujibu, alikuwa makini kufikiria mbinu ya kujiokoa.



“Usijaribu kufanya ujanja wowote Devotha, kosa kidogo litakugeuza kuwa tenga. Utaenda kuzimu mwili wako ukiwa na na matobo ya risasi zaidi ya mia. Hapa tulipo kuna bunduki zaidi ya mia za askari zimekuelekea wewe” Daniel alimtisha Devotha, na Devotha alitishika kidogo. Akawa anaangaza Mgahawa mzima kuangalia kama kauli ile ina ukweli.



Devotha kapatikana!! Kule watu wakubwa wapanga mikakati yao huku Daniel akionekana mwiba mkali kwao...inaitwa MPANGO wa SIRI...



Je unaihitaji yote simulizi hii ili kumuunga mkono mwandishi??? Mfate WhatsApp 0674 395733 kwa shilingi 2000 tu utapata simulizi hii hadi Tumuunge mkono mwandishi kwa kununua kazi yake, kama huna subiri kesho hapahapa Mpango wa Siri, itaendelea na itaendelea hadi mwisho...



“Usijaribu kufanya ujanja wowote Devotha, kosa kidogo litakugeuza kuwa tenga. Utaenda kuzimu mwili wako ukiwa na na matobo ya risasi zaidi ya mia. Hapa tulipo kuna bunduki zaidi ya mia za askari zimekuelekea wewe” Daniel alimtisha Devotha, na Devotha alitishika kidogo. Akawa anaangaza Mgahawa mzima kuangalia kama kauli ile ina ukweli.



“Kama hutaki kufa naomba unambie chochote unachokifahamu kuhusu Mpango wa siri” Daniel alizidi kumbana Devotha.



“Siufahamu” Devotha alijibu kwa kifupi huku akibinua mdomo.



“Nafahamu mpango wa siri unasimuliwa sehemu ya siri, twende chumbani ukanisimulie” Daniel alitoa wazo lililokubaliwa na Devotha, Devotha alihisi huko chumbani ndio sehemu pekee ya kwenda kujaribu kujiokoa.

Walinyanyuka na yule dada Mhudumu kuelekea chumbani, Mgahawa mzima uligeuza macho kwa watu hawa watatu. Ilikuwa ni kama kizee kaopoa machangudoa wawili.



Walifika chumbani, Daniel akawa anafunga mlango kwa ndani, alipogeuka aliposimama Devotha alikutana na mdomo wa bastola. Hakuelewa Devotha aliitoa muda gani ile bastola.

Daniel hakuogopa.

Alitembea bila wasiwasi hadi kwenye runinga ya mle ndani. Bastola akiwa ameelekezewa kisogoni kwake. Akawasha runinga kwa sauti kubwa. Yule Mhudumu alikuwa hajiwezi kwa uwoga, anatetemeka. Alikuwa hajawahi kuiona Bastola zaidi za kwenye runinga.

Wakati Daniel anageuka kutoka kuwasha runinga alifanya kitu. Alirusha teke la nguvu kwa haraka lililoupata mkono wa Devotha ulioshika Bastola. Bastola iliserereka hadi uvunguni mwa kitanda.

Sasa marafiki walibaki mikono mitupu wakitweta...



Yule dada alikuwa amekaa sakafuni hajiwezi. Miguu ilishindwa kustahamili uzito wa mwili.



“Kabla hujanambia kuhusu Mpango wa siri unataka tupashe miili yetu?” Daniel aliongea kwa sauti mzito.



“Mwenzio kalala uvunguni, na wewe unapenda kwenda kuungana nae?” Devotha akajua kuwa Kishoka kashauwawa na Daniel Mwaseba !



Daniel alijibiwa maswali yake. Devotha alijibu maswali ya Daniel kwa ngumi kali ya mkono wa kushoto iliyotua sawia katika utosi wa Daniel. Daniel aliyumba, kichwa kikawa kinamuuma. Devotha alirusha teke kwa mguu wa kulia lililokuwa linaelekea palepale kwenye utosi. Daniel aliliona, akainama kidogo likapita. Devotha sasa aligeuka mbogo, alikuwa amefura kwa hasira. Alirusha teke la kulia sasa lililokuwa linaelekea katikati ya nyonga ya Daniel, Daniel alishaliona kabla, alirudi nyuma kidogo, likapita.



“Kumbe Devotha ulienda Urusi” Daniel alimuuliza Devotha, aina ya mapigo akiyopiga Devotha Daniel alikuwa anayajua vizuri. Na yalikuwa yanatolewa nchi ya Urusi pekee.



Yule Mhudumu alikuwa anapiga kelele pale chini. Daniel akaona atawaharibia shughuli. Alimsogelea pale alipokaa, akampiga pigo dogo kwa kutumia mkono wa kushoto kwenye shingo, pigo lile lilikuwa linaitwa ‘lala salama’ Ukipigwa unalala kwa muda usiopungua masaa matatu. Huwa wanalijulia watu wachache sana duniani, na daima hupigwa kwa mkono wa kushoto. Mhudumu alilala, kelele zikapungua.

Sasa walibaki macho miamba miwili.



”Sipendi kupigana na wewe My Devo, napenda tuongee tu” Daniel aliongea maneno hayo huku akirusha ngumi iliyompata Devotha kwenye mwamba wa pua. Devotha hakusikilizia makali ya ngumi ile, nae alirusha teke lililozuiwa kwa mkono na Daniel. Daniel alirusha ngumi iliyokuwa inaenda chini ya kidevu, ngumi ile mara nyingi huwa inarudi na meno mawili au matatu, Devotha aliiona ngumi ile, aliyumba kidogo na kurudi kwa kasi. Devotha alirudi na kichwa kimoja cha hatari kilichotua palepale kwenye utosi wa Daniel. Utosi wa Daniel ukaanza kupwita kwa maumivu. Devotha alirusha ngumi nyengine iliyokuwa inaenda sehemu ileile. Akiwa kwenye maumivu makali Daniel aliamua kujibu mapigo. Alijua akijilegeza kidogo anakufa .Devotha alikuwa anapiga mapigo ya kumuuwa kabisa!



Alikuwa na silaha kiunoni lakini hakutaka kuitumia. Daniel kumuua Devotha kwa risasi aliona ni udhaifu. Sasa alidhamiria, alidhamiria kumuua Devotha!

Alirusha ngumi kali iliyotua katika mbavu za Devotha. Devotha alitoa mguno kuashiria ngumi ile ilimuinga barabara. Devotha akapeleka mkono kupapasa mbavu zake, lilikuwa ni kosa! Ngumi mbili zilitua usoni kwake, zote zilitua kwenye mdomo, akaanza kutoa damu mdomoni. Devotha alipangusa damu kwa mkono wake. Teke la Daniel lilisafirishwa kuelekea katika shingo ya Devotha. Lilitua sawia kwani Devotha alikuwa anajishughurisha kuifuta ile damu. Devotha alitua chini kama mzigo.



“Niambie Mpango wa siri ni nini Devo?” Daniel aliuliza.



Devotha alifyonya mfyonyo mkali!

Akiashiria hasemi kitu, Daniel alimpiga kifuti cha nguvu palepele kwenye mdomo wake. Devotha alitoa ukelele mkali. Daniel hakutaka kumpa nafasi Devotha. Alimpiga kareti kali ya shingo. Kareti hii mara nyingi huwapeleka watu kuzimu. Lakini siyo kwa Devotha, Devotha alikuwa sugu hasa. Karate ile ilimfanya Devotha asimame huku anayumba. Alirusha ngumi dhaifu iliyompta Daniel begani. Devotha alikuwa amechoka sasa. Daniel alipiga karate mbili za shingo za harakaharaka palepale alipopiga ile karate ya kwanza. Devotha aliweza kuvumilia karate ile yakwanza lakini siyo hizi. Alikuwa anaanguka chini huku roho yake ikielekea kuzimu. Huo ndio ulikuwa mwisho wa Devotha...



Daniel akapiga simu kituo cha Polisi Mabatini,waje kuzitoa zile maiti mbili na yule dada Mhudumu wampeleke hospitali. Daniel akahama hoteli ile akiwa katika umbo lake la kizee.



****



John Masaga alichanganyikiwa sana ofisini. Hadi saa nne asubuhi Devotha na Kishoka hawakuwa wamewasili ofisini. Wenyewe walipanga wakutane saa kumi na mbili asubuhi ili wapange namna ya kumkamata huyo mtu anayewafatilia. Kumbe Devotha na Kishoka walienda kuucheza mchezo ule hoteli ya Double view bila kumshirikisha Bosi wao. Nia yao watakapokutana asubuhi wamshangaze Masaga kwa taarifa ya kifo ya huyo mtu aliyewafatilia. Mipango si matumizi, Daniel aliwauwa wote!



Sasa ofisini alikuwepo Lee, Masaga na wafanyakazi wengine sita. Ambao hawakuwa na uwezo mkubwa wa kupambana kama Devotha na Kishoka. Sasa kiliitishwa kikao kidogo na Masaga kutokana na kutoonekana kwa kina Kishoka na namba zao za simu kutopatikana. Hakikuwa kikao chenye manufaa. Wote hawakujua Devotha na Kishoka wamepatwa na nini ?.



Wakati wao wakiwa kwenye kikao ambacho hawakuwa na majibu yao mtu aliyekuwa na majibu ya maswali yao alikuwa mita chache nje ya ofisi yao. Daniel Mwaseba alikaa ndani ya Baa moja iliyokuwa inatazamana na ofisi ile. Alikuwa makini sana na nyumba ile. Akiwa pale Baa alimuona mchoma mahindi akiendelea na biashara zake. Daniel akacheka kimoyomoyo.

Mara simu yake ikawa inaita. Alikuwa ni Inspekta Nyange.



“Halo,vipi Danny” Inspekta Nyange aliita.



“Safi, niambie inspekta” Daniel alijibu.

“Uko wapi ndugu ? ” Inspekta aliuliza



“Tegeta Inspekta, kuna kazi nafanya”



“Nakuja sasa hivi, nipo Mwenge” Inspekta alimwambia



“Nipo kazini lakini Inspekta, uko vizuri?” Daniel alisaili.



“Vizuri zaidi ya sana” Inspekta alijibu kwa majigambo.



“Sawa nakusubiri”



Simu ikakatwa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Daniel akajua sasa mchezo utanoga. Nusu saa ilitosha, Inspekta aliwasili Tegeta kwa pikipiki. Baada ya Daniel kumuelekeza mahali alipo walionana. Inspekta Nyange alikuwa ameharibika sana. Alikuwa na sura tofauti na aliyokuwa nayo mwanzo. Alikuwa na matundu mabaya machoni .Ama kwa hakika Lee alimfanyia kitu kibaya sana Inspekta. Bila juhudi za madaktari wa India Inspekta asingeona tena.



Sasa Inspekta karudi kazini na mtu aliyemsababishia mateso makali bado yupo hai. Wakiwa pale Baa Daniel alimsimulia kwa kifupi hatua aliyoifikia. Inspekta alifurahishwa sana na taarifa kuwa Lee yupo hai.



”Lazima nihakikishe nalipiza kisasi kwa yote aliyonifanya mbwa yule” Inspekta Nyange aliongea akimaanisha.



Wasichikijua ni kwamba, kumbe mchoma mahindi alikuwa amewaona...



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog