Search This Blog

Friday 18 November 2022

MZIMU UMERUDI TENA KULIPIZA KISASI - 2

 






Simulizi : Mzimu Umerudi Tena Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Pili (2)




Kokoleza hakuwa na pingamizi alikwenda kuomba hifadhi ya baiskel yake katika kilinge kimoja cha fundi piki piki hapo karibu baada ya kukubaliwa alirudi na kuja kupanda difenta hiyo ya polisi na kuondoka nao!



" Tembeza! Tembeza kijana inatakiwa ndani ya dakika 20 tuwe tumewasili, aliongea mkuu wa kitu akimuhimiza kijana Mohamed kwenda na mda, wakati huo kijana anachenji gia na gari kuzidi kwenda kwa kasi ya ajabu...



Ni ndani ya dakika kumi na saba brek kali ilipigwa katika eneo la tukio sambamba na tairi kusota kwenye lami, moshi wenye kutoa harufu kali ya mpira kuungua ilisikika eneo hilo.. Hahaha! Ni MOHAMED MADUO Na timu nzima ya Askari kutoka katika kituo cha Polisi migori tayari walishatinga katika eneo la tukio,



Basi bila kupoteza mda askari wote walitelemka katika gari yao na haraka wakaanza kulizunguka eneo hili, walimkuta kijana Abdala akiwa amejiinamia huku machozi yakimwagika kama mtoto mdogo, hakika kifo cha dreva wake kilimuuma sana, Kokoleza alianza kazi ya kuchukua picha kwa kufuata kanununi kutoka jeshi la polisi.

,,

Kwingineko, Dickson na kikosi chake baada ya kushuhudia tukio lile la kutisha waliondoka usiku huo huo kwa kukwepa Aibu ya kuwa waliona wakashindwa kudhibiti hivyo walichokifanya ni kutoroka usiku huo huo na kutokomea kusikojulikana...!!



Dili zima lipo hivi, ukweli ni kwamba Dickson na kikasi chake waliogopa kupambana na majambazi wale kwa kuhofia huenda wapo wengi na wengine wamefichama machakani kuona nani mwingine anakuja?? Hivyo walichokifanya ni kutulia pale pale chini walipokuwa awali mpaka pale wale majambazi walipofanikisha Adhma yao na kuondoka, wale polisi baada ya kuhakikisha wameondoka kabisa usiku huo nao wakatoka pale kwa mwendo wa kunyata mpaka eneo la tukio. walimkuta kijana Abdalah akiwa kazimia, upande wa pili maiti, gari imepekuliwa vya kutosha mpaka na yale makanda ambayo huwa yanatumika kufungia maturubai pale roli linapokuwa na mzigo nayo pia walifungua na kuondoka nayo.. Wale polisi walishauriana pale na kuona ni bora waondoke tu kama ni kuachishwa kazi wacha iwe ivyo kuliko kupambana na mashetani kama hao, vijana walipanda gari yao kisha haoo! Wakasepa ikiwa ni mida ya saa sita za usiku mda ambao hata Kijana Abdalah alikuwa hajazinduka bado..

,,

Naam! Hivyo ndivyo ilivyokuwa.. Na sasa twende moja kwa moja mpaka pale tulipoishia katika sehemu ya kumi na tano..

,,

Habari ya tukio lile la ajari mbaya kutokea katika makona ya milima ya Nyang'oro ilikuwa imesambaa takribani mikoa yote kwani mchana huo yale mabasi ya kwenda mikoani yalikuwa yakipita hapo na baadhi ya abiria kuchukua picha kisha kutupia mitandaoni. Hivyo habari ikawa imeenea karibia nchi nzima!!



Kituo kimoja cha runinga kikainasa habari hiyo kupitia mtandao wa Facebook lakini habari hiyo ikawa haijakamilika na kituo hicho kikaanza taratibu za kuwatafuta waandishi wa habari kutoka iringa vijijini, mwaandishi na pia mpiga picha bwana kokoreza photo ni mpiga picha na mwaandishi maarufu sana katika kata ya Ismani hivyo midia iyo ikaona ni vyema kumsaka kokoreza photo kwa njia ya simu ili kama amefika katika eneo la ajari aweze kutoa maelezo kamili jinsi kulivyo huko na ikiwezekana awatumie na picha ili wao wawe wa kwanza kuitangaza rasmi habari hiyo.



Tukirudi huku katika eneo la tukio ikiwa ndiyo inakamilika saa moja asubuhi, kokoreza akishirikiana na jeshi la polisi walikuwa na kazi ya kukusanya habari pia polisi walikuwa wakiendelea na uchunguzi.. Mara simu ya kokoreza ilipata kupigwa. Kokoreza alipoitoa na kuisawiri juu ya kioo aligundua ni simu kutoka kituo kimoja cha terevisheni na moja kwa moja akatambua shida yao



Kokoreza alipoke simu hiyo na kuwasikiliza watu hao wanasemaje?? Makisio yake yalikuwa sahihi watu hao walikuwa wanataka maelezo kamili na yenye udhibisho wa kutokea kwa ajali mbaya huko mkoani Iringa, lakini licha ya hilo kokoreza aliweza kuwaarifu kuwa usiku huo huo kuna uvamizi ulifanyika pia eneo hilo hilo na mtu mmoja kauawa na mmoja yuko hoi, na wahusika waliweza kukimbia usiku huo huo na mpaka sasa jeshi la polisi kutoka kituo cha polisi migori lipo katika uchunguzi kuhakikisha wahalifu wanatiwa mbaroni...



Ilikuwa ni habari nzito sana na sasa kilichofuata ni kampuni hiyo kuirusha moja kwa moja katika chanel mbali mbali asubuhi iyo na habari ikasambaa nchi nzima, na hiyo ndiyo habari iliyomchanganya zaidi kamanda wa kituo cha polisi cha isimani aliekuwa songea kwa uchunguzi wa ajali hiyo hiyo,

************************

SONGEA.... Wale vijana pamoja na bosi wao walifika na kuwasalimia polisi hao kisha wakavuta viti na kuketi..



Ili kwenda na mda hakukuwa na mjadala tena alichokifanya bosi huyo ni kuwasha laptop na kuingia moja kwa moja kwenye faili lililo na vidio ya tukio zima jinsi ajali ilivyotokea tokea, aliwakabidhi polisi hao ili kuitizama vidio hiyo kwa uhuru zaidi.



Kama jinsi ajali ilivyotokea ndivyo hivyo vidio ilivyonesha, ilionekana mwendeshaji wa gari ndogo alikuwa mwendo kwenye eneo ambalo hairuhusiwi hata kwenda na spidi 30, kufika kwenye kona ndo hivyo tena mwendeshaji huyo ambae ni Saida alijikuta gari ikimwelemea na kuzua baraa!!



Kwa jinsi ile vidio ilivyozidi kusogea mbele ndivyo hivyo pia uso wa kamanda yule wa polisi ulivyozidi kukunjamana hii ilionesha dhahiri mkuu alikuwa akikasirika tena saana..



Hatimae mkanda ukafika tamati, wale polisi wakamrudishia bosi huyo laptop yake kisha akasema vijana hao hawakuwa na kosa lolote hivyo kwaanzia sasa itabidi waende wakaichukue gari hiyo waendelee na safari. Na kesi ikahamia kwa saida...



" Yaani huyu mpuuzi katupoteze mda wetu kumbe yeye ndiyo bangi??? '' mkuu wa kituo aliongea kwa ghadhabu sana huku akianza kuinuka kitini, lakini bosi huyo akamwahi.

" Subili mkuu usiwe na hasira hebu jaribu kukaa nae ujue sababu ya kuendesha gari kwa kasi namna hiyo ni nini??? " yule bosi aliongea..

" hapana hao watu si wasikivu kabisa yaani. ''

" ni kweli lakini fanya vile nakwambia ''

" sawa nitamhoji iwapo maelezo yake hayatojitosheleza nitamuweka nyuma ya nondo mimi.... ''



Mkuu huyo alifoka vibaya mno..



" Sasa wakuu wangu ngoja nitawapa gari ya private mtakayorudi nayo mkoani Iringa pamoja na madreva wangu kwaajili ya kwenda kuichukua simi hiyo.. ''

" Ahaa!! Sawa naaa tutaondoka mda gani?? ''

" Kwaanzia hivi sasa gari ipo tayari kwa safari ''

" Sawa basi vijana jiandaeni tuondoke ''



Bakari na moses waliinuka na kutokomea katika vyumba vyao huku wakiwa na fulaha kuu isiyoelezeka!!. Baada ya dakika kadhb walitoka huku wakiwa wamepiga pamba kali baraa..



Basi wote kwa pamoja walitoka mpaka nje huku wakiwa wameongozana na wapelelezi hawa kutoka Iringa..., walikuta gari moja kali sana aina ya LAND ROVER Ikiwa imepaki karibu na mlngoni ikiwasubili.. Lakini kabla hawajapanda yule mkuu wa kituo aliitwa tena chemba na bosi hivyo ilimlazimu awaache Charles, Bakari na Moses wapande yeye aongee kwanza na bosi.. Akapiga hatua za haraka mpaka kwa bosi huyo...



" Ndiyo boss... ''

" Aa samahani mkuu hivi huyo aliepatwa na ajali ni wa jinsia gani?? ''

" ni mwanamke ''

" na yupo wapi kwa sasa hivi?? ''

" Hospitalini IPAMBA ''

" Anaweza kupona kweli?? ''

" Uwezekano wa kupona upo japo mi sina taarifa yoyote tangu jana hiyo alipokimbizwa huko ''



Yule bosi akatikisa kichwa kwa masikitiko makubwa kisha akaingiza mkono mfukona na kutoa waleti ambapo alitoa Shilingi laki tatu na kumpatia kamanda huyo...



" Hakikisha unazifikisha hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya msaada kutoka kwangu hakika nimeguswa sana japo inaonesha ana makosa kwa kuvunja sheria za barabara lakini nahisi kuna jambo nyuma ya pazia, cha msingi wewe fanya kama nilivyokuagiza naanini utapata jibu... '' yule bosi aliongea kisha wakaagana pale na polisi huyo na moja kwa moja akawahi kwenye gari na kupanda kisha haooo....!! Safari ya mkoani Iringa ikaiva ikiwa ni saa nne kasoro asbuhi...

*************************

" Wewe ni mume wake na mama mmoja alieletwa hapa na AMBULACE Ya selikari jana baada ya kupata ajali ya gari '' DK Lous aliongea huku akiwa kamkazia macho Patrick ambae mda wote huo alikuwa kaganda kama gogo!!

" Ndiyo '' Patrick alijibu....

" Sasa kwanini tunakupigia simu unaleta jeuri?? ''



... Kimya .......



" Ndugu naongea na wewe hapo husiki??? ''

" Nisamehe kaka ''

" Yaani unathamini gari kuliko utu wa mtu?? ''

" Ni hasira tu broo ''

" Haya rudi kwa mkeo sasa hivi na ukileta jeuri unakaa ndani umenielewa??? '' Patrick alishikwa na kigugumizi akashindwa kujibu..



" Umenielewa wewe??? '' Lous aliongea kwa ghadhabu huku akichimba mkwara wa kuvua koti lake la udaktari ili amwoneshe kazi huyo jamaa... Patrick kuona hivyo akaogopa na kurudi wodini haraka wakati huo Lous anaingia chumba kingine...http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Patrick alimkuta Saida akiwa kakaa kitako kitandani huku akiwa amejiinamia na matone ya machozi yakidondoka kwenye cement, Mwanamama huyo alikuwa akilia kwa uchungu mkubwa mnoo hasa akifikiria walikotoka ni mbali na wamepita njia mbaya mpaka kufikia mafanikio halafu leo hii inatokea Patrick kamtenga gafla na kumuona takataka?? Daaah!! Alilia Saida mpaka huruma...!!



Patrick kwa Jeuri baada ya kufika mule wodini hakuwa na mpango na saida tena zaidi ya kuka kaando tena mbali na kutoa simu yake walau amtext Ashura pasipo kujua kuwa yule nae ni matatizo tupu ana mtu ampendae na kwa Patrick yupo kimaslahi tu!... Patrick alituma ujumbe mfupi uliosomeka hivi..,



...... MAMBO MPENZI WANGU SHUUU! UPO WAPI?? JAMANI NIMEKUMISI,, RUDI YAMEISHA ...........



Baada ya kuhakikisha ujumbe umetumwa kasoro tu ripoti kurudi kama imepokelewa au laa!! Patrick aliinua tena kichwa chake na kumtizama Saida ambae mda wote alikuwa katika majonzi makubwa.. Alimwangalia kwa dharau kisha akasema...



" Wewe lia uwezavyo ila hakikisha VX Yangu niliyoiagiza kutoka tokyo japan inapona vinginevyo utaishi maisha ya mateso mpaka kufa kwako mwanaharamu wee!! ''



Maneno haya yalisikika kwa ufasaha kabisa katika ngoma za masikio ya Saida na kumsababishia kitu kama moto kulipuka tumboni mwake.. Mara mlango wa wodi hiyo ukafunguliwa na kuingia vijana watatu wakiwa wamevalia sale za polisi....





Baada ya yule Askari kupewa maelekezo yote alirudi wodini na kumchukua mwenzie kisha wakaondoka, Baada ya sekunde kadhaa Dk Lous aliingia wodini hapo, alimkuta Saida akiwa katika kilio cha ajabu! Mpaka daktari mwenyewe alishtuka na kuzani upasuaji wake umefeli nini??



Ismani Iringa

March 3, 2019

Saa 08:52 PM.



SONGA NAYO.......

Maneno haya yalisikika kwa ufasaha kabisa katika ngoma za masikio ya Saida na kumsababishia kitu kama moto kulipuka tumboni mwake.. Mara mlango wa wodi hiyo ukafunguliwa na kuingia vijana watatu wakiwa wamevalia sale za polisi....



Ismani Iringa

February 27, 2019

Saa 08:52 PM.



SONGA NAYO...

Kabla hatujaendelea mbele zaidi hebu turudi nyuma kidogo tujue polisi hao walitoka wapi na wamekuja hapo kwa lengo gani??



Ni hivi baada ya wale polis wapelelezi yaani Charles na mkuu wake kuanza safari ya kurudi iringa mkuu huyo wa kituo cha polisi Ismani alipata wazo akiwa njiani, na bila kupoteza mda akatoa simu yake na kuingia sehemu ya majina (contact) na kuanza kupekua pekua mpaka akaipata namba aliyokuwa akihitaji na bila kupoteza mda akabofya kitufe cha kijani... Punde tu simu ilianza kuita, nae akajiweka sawa kwa kujikoholesha kidogo kulainisha koo!



... Ngrrr!! Ngrrr!! Ngrrr!! Ngrrr! " Haow ''!



Sauti nzito yenye kibesi ilisikika upande wa pili. Nae bila kupoteza mda akapokea...



" Ndiyo mkuu habari ya mda huu! ''

" njema za kwako huko? ''



" salama mkuu.. Aisee ''

" ndiyo... ''



" mimi hivi sasa ninapoongea hivi nipo mkoani songea, kuna ajali jana ilitokea makona ya nyangoro huko sasa nilikuwa katika ufuatiliaji, kubaini chanzo... ''



" ndiyo nakupataa.. Na iyo ajali nimeisikia ''



" Sawa sawa sasa mkuu nilikuwa nakuomba jambo moja hapo ''



" nakusikiliza.... ''



" kuna mgonjwa jana alikimbizwa hospitali ya ipamba ambae ni huyo aliepatwa na ajali, na yupo mikononi mwa serikali mpaka sasa kwani bado hatujawapata ndugu wala mume wake, sasa tangu akimbizwe jana katika hospital ya ipamba sijapata taarifa zake mpaka sasa hivi... ''



" kivipi?? Kwani waliompeleka ni kina nani?? ''



" tulichukua AMBULACE Kutoka kituo cha afya ismani na huyo dreva sijampata hewani nilipojaribu kumpigia.. ''



" Kwani alimpeleka akiwa peke yake??? ''



" ndiyo kwani vijana wangu wote walikuwa wamegawanyika makazini.. ''



" Ook na ulitaka nikusaidiaje labda?? ''



" Nilikuwa naomba unitumie vijana hata wawili waende kuchukua taarifa kule ili niweze kupata taarifa za mgonjwa huyo.. ''



" basi hakuna shaka ''



" Asante kazi njema mkuu ''

" kazi njema pia.. ''



Yalikuwa ni maongezi kati ya mkuu wa kituo cha polisi Isman na mkuu wa kituo cha polisi Iringa mjini,



Na bila kupoteza mda mkuu huyo wa kituo alitoka ofini kwake na akaelekea moja kwa moja katika ukumbi ambao vijana wake ambao hawajaingia mtaani kufanya ulinzi wapo kule wanafanya fanya mazoezi, alipofika pale alichagua vijana watatu na kuwaita chemba..



" Nisikilizeni kwa makini ''

" ndiyo tunakusikiliza mkuu ''



" mnatakiwa kwenda ipamba mara moja kuna mgonjwa yupo kule na inatakiwa mkachukue taarifa zake na mnipe taarifa hizo upesi mmenielewa?? ''

" Tumekupata ila hatujakuelewa ''



" yaani mgonjwa huyo katoka ismani jana, taarifa zinasema kwamba alipata ajari mbaya ya gari, inasadikika waliokwenda kumpa msaada ni polisi kutoka kituo cha isman na ndiyo walimpakia katika AMBULACE Na kukimbizwa hospitalini.. Tupo pamoja mpaka hapo?? ''



" ndiyo.. Ndiyo ''



" Sasa mkuuwa kituo hicho cha polisi kanipigia mda siyo mrfu na kuniomba niwatume nyinyi muende kuchukua taarifa zote za mgonjwa huyo ili tumjuze, yeye na vijana wake wamekosa mda kwani vijana wote wapo makazini na yeye yupo songea kaenda kwa uchunguzi kuhusu ajari hiyo.. Hapo nadhani mmenipata?? ''



" Bila shaka tumekupata kwa uzuri kabisa mkuu.. ''

" Mnakwenda kwa kazi gani huko??.... ''

" tunakwenda kuchukua taarifa za mgonjwa aliyefikishwa hospitalini hapo kwa kupatwa na ajari ya gari na AMBULACE Ya kituo cha afya Ismani ''



" Safii mnapewa saa moja ya kukamilisha kazi hiyo ''

" shaka ondoa ''



Basi wakampiga saruti mkuu wao na kisha kuondoka na kutokomea kwenye vyumba kwaajili ya kujiandaa.. Haikuchukua mda vijana walikuwa wamekamilika kikazi, walitoka na kuikulupua difenta moja hapo kisha haooo!!



Kutoka iringa mjini mpaka ipamba siyo mbali ni mwendo wa gari ni nusu saa hivyo baada ya nusu saa vijana hao wa jeshi la polisi walikuwa wameshatia timu katika hospital iyo yenye hadhi kubwa sana mkoani iringa.. Na kama inavyojulikana polisi ni watu wanaoheshimika na kuogopwa sana katika jamii, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa vijana hao baada ya kufika hospitalini hapo waligawana mmoja akabaki na gari nje na wawili wakatinga ndani, hakukuwa na usumbufu wowote kutoka kwa madaktari kama ilivyo kwa raia wa kawaida ambapo bila kutoa hongo mambo hayatokwenda sawia.



Wao baada ya kuingia hapo ndani walimvamia tu nesi mmoja alieonekana kukatiza sehemu moja kwenda sehemu nyingine wakamsimamisha...



" samahani dada ''

" bila samahani ''

" tumetumwa kutoka center iringa mjini ''

" nawasikiliza... ''

" kuna mgonjwa kaletwa jana na Ambulace kutoka ismani kwa kupatwa na ajari ya gari yupo wapi?? ''

" ahaa! Yule mwanamama?? ''

" bila shaka ''

" yupo wodi namba 35 ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" ipo wapi iyo wodi?? ''

" mnakwenda na hii kordo kuna milango imepangana na kuandikwa namba na nyie tembeeni kwa kufuata kordo hii mpaka mfikie mlango namba 35 ''

" Asante waweza endelea na kazi zako ''



Basi wakaachana pale kisha yule nesi akaendelea na mizunguko yake wakati huo wale vijana tayari wameshaikamata kordo hiyo na wanakwenda na namba kwa kasi kweli kweli, mpaka walipofikia mlango wenye namba 35 hata hawakuulizana wala kugonga bali waliusukuma kwa kushtukiza na kujaa ndani gafla!!



Patrick alishikwa na mshtuko wa ajabu baada ya kuona polisi wameingia gafla chumbani hapo, hisia zake moja kwa moja zikamwambia kuwa ni wale askari waliomtaka afike haraka hospitalini hapo wakati aliokuwa nyumbani asubuhi.. Aisee Patrick alihisi haja ndogo kubisha hodi!



Patrick aliendelea kujikaza ili asishtukiwe na askari kama alikuwa na wasi wasi,



Wale askari wao walikuwa hawajatoka nje ya agizo lao hivyo moja kwa moja walimnyokea Saida aliekuwa kakaa kitako kitandani huku machozi mengi yakimwagika, yote hayo ni kutokana na Patrick.



Polisi hao walijaribu kumumhoji lakini hakuweza kuwaambia chochote zaidi ya kuzidi kulia tena kwa kwikwi, Wakaona kuliko kupoteza mda, mwanaume atoe maelezo kwani kitendo cha Patrick kuwapo pale kilidhihilisha asilimia mia kuwa ndiye mume wa mwanamama huyo...



Mtihani...!!



Askari mmoja alimgeukia Patrick na kumuuliza..

" Samahani broo huyu ni nani yako?? '' Hilo swali ni kama lilimshtukiza Patrick na kumtoa kwa gafla katika dimbwi la mawazo hali iliyopelekea ashikwe na kigugumizi kikali na kushindwa kujibu chochote...



" Wewee!! ''

" Aa..a.. E.. Ee?! ''

" huyu mgonjwa ni mkeo?? ''

" ndiyo afande ''

" ok hebu tupe maelezo kuhusu hali yake kwa sasa iko vipi?? Kapatwa na matibabu?? Na anaendeleaje?? Maana sisi tumeshindwa kupata maelezo yake kwani ni kama hivi analia tu, hebu tusaidiea haraka ''



Haya sasa mtihani mwingine huo hapo kwa Patrick ameombwa kupewa maelezo kuhusu mkewe kama katibiwa na anaendeleaje?? Jamaa kabaki anang'aa macho tu haelewi moja wala mbili, kwani kama unakumbuka tangu kafika wodini hapo kafika kwa ukali na kumfokea fokea mkewe tu!



Wale vijana wa jeshi la polisi baada ya kuona mwanaume huyo hajibu chochote wakadhani labda kachanganyikiwa na hali ya mkewe hivyo ndiyo maana anashikwa na kigugumizi pindi aulizwapo swali..



Na ili kuokoa mda wakaamua kuachana nae,, walijadiliana haraka kujua watatumia njia gani kukamilisha kazi yao?? Mawazo yao yakaangukia kwa madaktari waliamini hao ndiyo watakaowapa maelezo kamili, basi bila kupoteza mda kijana mmoja akatoka hapo wodini kwenda kumchukua angalau hata daktari mmoja na askari aliesalia akajongea taratibu kwenye moja ya kiti kilichokuwa hapo wodini na kuketi,



Ikawa ni kama bahati vile yule askari alietoka kwenda kuwatafuta madaktari, ile anatoka tu mlangoni anakutana na DK Lous akitoka chumba kimoja kwenda kingine...



Akamsimamisha...!



" Samahani daktari ''

" Bila samahani ''



" ok sisi ni vijana wa jeshi la polisi kutoka iringa center, tumetumwa na mkuu wetu kuja hapa kumwona mgonja alieletwa hapa jana na AMBULACE Kutoka ismani, kwa kupata ajali ya gari.. ''



" ok ni kweli tulimpokea jana na yupo wodi namba 35 nadhani tayari mmeoneshewa ''

" Ni kweli ila tumeambiwa tuje kuchukua taarifa zake lakini shida ni kwamba mtu huyo inaonekana hali yake siyo nzuri hajaweza kusema chochote ''

" Kwani hakuna mumewe huko nadani?? ''

" yule mwanaume yupo lakini nae hana chochote cha kutueleza na tumeona tunazidi kupoteza mda tu... "



Dk lous aliyafikiria yale maneno mara kadhaa akagundua kuna tatizo kati Patrick na mkewe, hivyo alichokifanya ni kumweleza tu yule askari kuwa mgonjwa huyo alishafanyiwa oparesheni na hali yake inakwenda kuwa salama..



Baada ya yule Askari kupewa maelekezo yote alirudi wodini na kumchukua mwenzie kisha wakaondoka, Baada ya sekunde kadhaa Dk Lous aliingia wodini hapo, alimkuta Saida akiwa katika kilio cha ajabu! Mpaka daktari mwenyewe alishtuka na kuzani upasuaji wake umefeli nini??





Dk Lous aliketi mule wodini kisha akamtizama Saida ambae kwa mda huo alikuwa katika majonzi ya kutisha, macho yalikuwa mekundu kama mtu alieingiwa na pili pili, mashavu yake yalikuwa yameloa machozi yaliyokuwa yakimtoka kwa wingi na kuweka michili kwa nyonyo zake hatimae kushuka mpaka kwenye sement, Lous pia akamgeukia Patrick ambapo mda huo alikutana na sura ambayo hata haikuitarajia! Patrick alikuwa amefura usoni kwa hasira kali zidi ya Saida hali iliyopelekea macho kuwa mekundu mithili ya mvuta bangi sambasamba na mikunjo mingi kati kati ya paji lake la uso!



Dk Lous akamuuliza....



" Ndugu kwanini unakuwa hivyo?? ''

" mfyuuu! Kwanza mniambie mulichoniitia hapa sasa hivi..!! ''

" kwahiyo kuja kumuona mkeo ni mwiko kwako?? Au unamwombea afe?? ''

" kwanza alikuwa anakwenda wapi?? Anajua hasara aliyonitia??.. Eti we mwanamke ulikuwa unakwenda wapi?? ''



Saida alikosa cha kujibu akabaki akilia tu..



" Unasikia dokta.. ''

" ndiyo.. ''

" huyu mwanamke alikuwa na mtu wake ( mchepuko ) na alikuwa amepanga kutoroka ila baada ya kupata ajali mwanaume kakimbia. ''



Patrick aliongea kwa kujiamini, huku akimwacha Dk Lous na Saida katika taharuki kubwa!



" Patrick '' Saida aliita kwa upole,,

" Ee ''

" lini nikakufanyia hayo unayoyasema?? Ujue utabeba dhambi wewe?? ''

" usinitibue..!! Sasa ulikuwa unakwenda wapi?? ''

" Kwani wewe pia ulikuwa unakwenda wapi?? ''



Saida baadala ya kujibu swali nae aliuliza swali, safari hii mshangao ulioambatana na taharuki kubwa vikahamia kwa Patrick..



" Kivipi?? '' Patrick aliuliza kwa mshangao..!!

" Wewe jana mbona gari yako ilikuwa mwendo sana ulikuwa unakwenda wapi?? ''



Patrick akakosa cha kujibu kwa wakati huo, huku mawazo lukuki yakipita katika ubongo wake, na akaanza kuwaza iwapo Mkewe anajua kuwa alikuwa bondeni huko hata Ishu yake ya kutaka kuwasababishia polisi ajali itavuja na kumletea baraa!



" Mimi ni mume wako sawa?? Nina makukumu kibao ya kufanya umenielewa?? Kwani nina kazi ngapi?? Nina miradi mingapi?? Na yote hayo nayafanya kwa maslahi yetu leo hii unaanza kunichunguza chunguza?? Unaanza kunifata fata?? Mfyuuu... ''



Patrick alikuja juu na kwa kauli ambayo ilimwacha kila mmoja kinywa wazi mle wodini, na baada ya hapo akatoka kwa hasira na kwenda mpaka nje akachukua gari yake na kuondoka kwa kasi ya ajabu mpaka watu wote waliokuwa nje ya Hospital iyo kumshangaa..



Haya sasa majungu yakabaki kwa Saida daah! Mpaka huruma nguvu zilimwishia pale kitandani na kuanza kurudi kinyuma nyume mpaka akalala chali kitandani huku machozi mengi yakimtoka kwa kasi machoni na kuweka michili kupitia masikioni mpaka kwenye godolo...

************************

Kwingineko anaonekana mkuu wa kituo cha polisi Isman akipokea simu..



" Ndiyo sajent Johnson.. ''

" za kutoka jana mkuu ''

" njema sijui nyie huko ''

" kuna tatzo mkuu ''

" toa maelezo ''



Basi Johnson alieleza mkasa mzima kwanzia walipokoswa kufa kwa ajali ambapo kama dreva wao asingekuwa makini, pia alieleza maajabu waliyoshuhudia usiku na hatimae kuweza kutoroka eneo hilo..



" Unaniangusha John ''

" Hapana mkuu eneo lenye siyo rafiki hata kidogo pili ni giza, tatu hatujui wapo wangapi na wanatembeaje?? Nne wana silaha nzito nzito, ni pagumu hapo mkuu ''

" Na mpo wapi kwa sasa hivi?? ''

" Nyang'oro hapa ''

" na kuna mtu yoyote anajua uwepo wenu kule zaidi yetu?? ''

" hapana maana hapa kwa wenzetu tulifika usiku kijiji kikiwa kimepoa kabisa ''



" Sasa unasikia John?? ''

" ndiyo nakupata mkuu ''

" Hii habari imezagaa sana mpaka kwenye vyombo vyo vya habari sasa ili huu msala usituguse fanyeni kama hamkuwapo kule sawa?? ''

" Asante, na asant kwa kutulinda ''

" Sawa nasi tupo njiani tunakuja na wamiliki wa roli hilo waje kulichukua maana taarifa zinaonesha hawana hatia yoyote ''

" Sawa mkuu ''



* Simu zilikata wakati huo ile gari ndogo waliyoipanda mkuu huyo na vijana kadhaa aliokuwa nao katika safari hiyo ikiwa inatia timu Ipogoro sehemu ambayo kuna mgawanyiko wa barabara kati ya inayoingia Iringa mjini na ile ya kwenda Dar Es Saalam. Taratibu Cruiser iyo ikaacha ikaicha barabara kuu na kuikamata barabara Iingiayo Iringa mjini. Wakati huo mkuu mawazo mawili yakicheza kichwani la kwanza ni apitie Ipamba kwenda kumuona mgonjwa?? Au aende kwanza mpaka Ismani? Akiwa kati kati ya mawazo haya mara simu yake inapata kupigwa! Haraka akaitoa na kugundua mpigaji ni mkuu wa kituo cha Polisi Iringa mjini. Akaipokea...



" Ndiyo mkuu... ''

" taraarifa zimefika ''

" sawa ''

" zinasema kuwa mgonjwa kafanyiwa oparesheni jana hiyo hiyo na uwezekano wa kupona ni asilimia mia moja ''

" Sawa, na je? Kuna ndugu yake yoyote kafika huko?? ''

" ndiyo mume wake yupo kule ''

" Ahaa.. Asante kwa msaada wako nami naingia hapo mjini hivi punde ''

" Sawa kamanda ''



Simu pia zilikata wakati huo mkuu huyo akilini mwake akighairi kwenda ipamba na kujisemea kimoyo moyo, .. Mumewe si kaenda?? Kwahiyo hizi pesa nazo nizipeleke?? Aaa haina haja... Tayari polisi huyo kazipigia hesabu zile laki tatu! Hahaha duuuh!!

***********************

AJALINI... Baada ya wale polisi kutoka kituo cha Polisi migori kukusanya taarifa zote na kukamilisha uchunguzi wao waliamua kuwasiliana na kampuni ya HILL LIMITED Na kuwapa taarifa kuwa gari yao moja ilitekwa njiani na dreva wao kauawa hivyo watakiwa kufika Irimga haraka sana iwezekanavyo, Mabosi hao kutoka TUNDUMA Tayari taarifa hiyo walikuwa nayo kwani kama unakumbuka Tayari kuna kampuni ya habari tayari walishawasiliana na kokoleza photo na tayari habari hiyo ilikuwa imesambaa katika vituo vingi vya terevisheni na hata mabosi hao walishaipata hivyo hawakushtuka sana zaidi ya kuwapa jibu kuwa kuna watu wangetumwa pamoja na AMBULACE Kutoka huko tunduma kwaajili ya kum'beba marehemu dreva huyo, naa baada ya mawasiliana hayo polisi hao walibaki pale ili kuendeleza ulinzi mpaka pale wamiliki hao wa gari hiyo waje kuichukua, halafu wasubili mmiliki wa gari hii ndogo ambayo mpaka hapo hawajui ni ya nani??..

************************

Patrick baada ya kutoka kwa mwendo wake wa ajabu pale hospitalini alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake wakati huo akili yake ikiwa kwenye prado yake aliyoitelekeza jana polini huko baada ya kuhofia kukamatwa na polisi kwa kosa la kuendesha gari kwa kasi kwenye maeneo yenye kona kali na kunusurika kusababisha ajali mbaya sana.



Baada ya kufika nyumbani kwake alienda moja kwa moja mpaka uwani na kupaki gari yake kisha akaenda moja kwa moja mpaka chumbani kwake na kubadili nguo na kuvaa nguo nyepesi maana suti na mda huo vilikuwa haviendani kabisa kutokana na jua kuwaka na kusabisha joto kali baraa. Baada ya kukamilisha zoezi hilo akatoka haraka bila kupoteza mda, akawahi barabarani kwaajili ya kupanda daladala..



Kutoka nyumbani kwa Patrick mpaka barabara kuu iendayo Dodoma hakukuwa mbali hivyo alitumia dakika kadhaa tu kufika, na ikawa kama bahati anafika tu daladala ya kwenda CHAPUYA Hii hapa. Mzee mzima akajitosa ndani na safari kuiva,



Alipokuwa ndani ya daladala Patrick alijaribu kumpigia Ashura lakini simu ya mwanadada huyo haikuwa ikipatikana Patrick alianza kuchanganyikiwasana mda huo akiwaza mchumba wake huyo atakuwa kaenda wapi?? Jibu hakulipata ila akajiambia kuwa akishachukua gari yake atakuja kusimama nyang'oro na atamtafuta mpaka ampate..



Baada ya dakika 35 Daladala hiyo iliwasili mahali Patrick alipotakiwa kushukia nae bila hiana aliomba wamshushe hapo, Daladala ilisimama hapo na Patrick kulipa nauli kisha akatelemka daladala ikaondoka.. Patrick akiwa hapo barabarani alijinyosha nyosha kwanza kujiweka sawa, kisha kwa hatua za haraka akaenda mpaka pale alipokuwa amepaki gari jana!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kituko...!!!



Gari haikuwapo!! Patrick alitumbua macho kwa taharuki kubwa huku akishindwa kuamini kile kilichotokea.......





Patrick presha ilianza kupanda na kushaka kwa kasi huku mapigo ya moyo vikibadili gia na kuanza kwenda kwa kasi ya kutisha!! Alishindwa kuamini kile alichokuwa akikishuhudia kwa mda huo alihisi huenda yupo katika ndoto moja ya kutisha sana ambayo ngumu hata kusimulika..!



Taratibu akainamisha kichwa chini kuona hata alama ya matairi yalikoelekea sasa cha ajabu hata matairi hakuna.. Alaaa! Hii gari imepoteaje?? Alijiuliza Patrick huku akikuna kichwa chake!!



Ooooh..!!!



Kumbe gari haikuwa imepotea wala nini? Bali yeye ndiyo alikuwa amepotea! Sehemu alipoicha ilikuwa ni mbele kidogo yeye akashukia nyuma kidogo kabla ya sehemu yenyewe. Maana ake alishukia sehemu waliyotokea na Ashura na siyo sehemu walipoingilia na gari..



Kasheshe...!!!



Sasa wakati Patrick akiwa anahaha huku akibadili mpaka stairi za kisimama mara akona weupe weupe ukionekana kwenye miti kwa magharibi kidogo na alipotizama kwa makini alibaini ni ile gari yake.. Oooh!! Gari yangu upo?? Asante sana maana nilianza kuhisi kama dunia inawaka moto.. Hahahaha...!!! .. Patrick aliwaza hivyo na kuachia kicheko cha nguvu huku akianza kupiga hatua kuelekea huko...



Alifika mpaka hapo na kuizunguka na kukuta ipo salama, akafungua mlango na kuingia ndani na bila kupoteza akachomeka ufunguo na kuiwasha na kuanza kuirudisha kinyume nyume akitafuta baransi ya kuigeuza!!



Alifika mpaka sehemu iliyokuwa na uweupe usio na mti wala kisiki, hapo ndipo alipoigeuza kwa kasi na kukanyaga mafuta na kwenda kwa kasi mpaka ikaikaribia lamai kisha akafunga brek ya nguvu huku akitiza pande zote mbili na alipogundua hakuna gari mwanaume akajitosa kwenye mkanda wa mchina na kama ilivyo kawaida yake kwenda sipidi 100 kwake ni mfano tu!!

************************

Upande mwingine anaonekana Ashura akiagana na mpenzi wake Daniel Masubwa! Pande la kijana waanagana baada ya kustarehe vya kutosha!



" Sasa Dani wacha mimi nikuache niwahi mjini ''

" Sawa mke wangu ila tatizo lako unanisusa sana.. ''

" Usijali ni majukumu tu mume wangu ila nikiwa napata nafasi kama hivi nakuja ''

" Nashukuru sana Aisha ''

" Asante sana wacha sasa nikuache niwahi usafiri ''

" Sawa sawa ''



Ashura aliondoka hapo huku kichwani akiwaza kitu juu ya mwanaume Patrick, na ili ujue kuwa huyu mwanadada ni mtu m'baya sana kwa Patrick kabadili jina kwa mwanaume huyo wakati anajulikana kwa jina la Aisha lakini cha ajabu kwa Patrick kajiita Ashura..



Hahaha Yajayo yanafurahisha.!!



Ashura alitinga mpaka standi ya nyang'oro huku tayari akiwa kaweka line zake na zile za siri kazitoa na kuzificha. Baada ya kufika sehemu ya kupandia magari yaendayo Iringa mjini alitoa simu yake na kuingia sehemu ya majina

(contact) na kuanza kupekua pekua ila kabla hajapiga alisikia king'ora cha polisi kutoka upande wa mashariki haraka akaachana na simu akainua kichwa chake na kutizama huko..



Aiseee timbwili..!!!



Ilionekana difenta ya polisi ikija kwa kasi sana huku zikiwa zimeongozana na gari ndogo nyeupe aina ya Land cruiser, Ashura uwoga ukamshika maana anakumbuka vyema kisanga cha jana hapo alianza kupiga mahesabu ya kujificha kwenye mpishano wa watu! Sasa wakati akigeuka kujipoteza kwenye mpishano watu. Gafla macho yake yakainasa Prado nyeupe ikitokea upande wa magharibi kuja huku..



Na anaitambua vyema gari hiyo kuwa ni ya Patrick roho ikapiga paah! Maana wanakuja kukutana na polisi bila Patrick kujua, Ashura akabaki kaganda huku akisahau na mapango wake wa kufichama..



Mpaka gari la polisi linapita hapo hakuwa na habari yeye macho yalikuwa kwa Patrick,



Patrick nae alikuja kushtuka ameshaingia sehemu ambayo hairuhusiwi hata gari kusimama na mbele anawaona Polisi, lakini kwa kuwa aliamini hawatoweza kumjua basi alijikausha na kupishana nao japo yeye jasho lilikuwa likimtiririka mwili mzima..



Polisi hao hawakuwa na mpango wowote bali walikuja kuwakabidhi kina Bakari gari yao kisha wao wapitilize mpaka kunako eneo la ajari wakaangalie utaratibu wa kuitoa gari ile kule ili isogee huku ili wenye nayo waje kuichukulia huku.



Patrick baada ya kupishana na gari zile mbele alimwona Ashura wake aisee moyo ulilipuka kwa fulaha ya ajabu! Na bila kuchelewesha akamwashia mataa na kuyazima akiimanisha ajiandae kupanda kwenye gari..

Ashura nae alijiweka sawa na kuweka sawa mkoba wake! Punde gari ikasimama hapo na mwanada huyo akatinga ndani, kisha kwa mbwembwe Patrick akachomoka na tano hapo! Hakika kila mtu akabaki kinywa wazi..



" Pole mpenzi '' Ashura alianza..

" Asante daah! Jana umenifanyia nini tena jamani?? ''

" lakini si unajua kuwa mama ni mgonjwa?? ''

" ndiyo sasa imekuwaje?? ''

" mdogo wangu aliniarifu kuwa mama anakua inabidi niwepo ''

" sasa hata kunipa taarifa mwenzio?? ''

" samahani niliona hauko sawa ndo nikaamua nisikusumbue halafu kwa bahati mbaya simu ikakata chaji. ''



Kutokana mwanadada huyo kumchombeza kwa maneno matamu Patrick hakika alijiona anapendwa sana na mtoto huyo na pia alijiona ni mwenye bahati sana kumiliki mtoto kisu kama huyo bila kujua siri iliyopo nyuma ya pazia ambayo inaweza kuwa ni bomu la nyuklia kwake...



Gari hiyo ilikuwa imeshatimga maeneo ya nduli kiwanja cha ndege Patrick alikuwa anadesha gari kwa kasi sana kuwahi mjini ili wakale bata na mrembo huyo bila hata kufikiria hali ya mkewe..



Saa tano na dakika arobaini walikuwa kihesa, Bila kufikiria Patrick akaamua moja kwa moja kumpeleka Ashura nyumbani kwake kwani anajua mkewe yupo hospitalini na hali ni mbaya sana hawezi kuja leo.



****************************

Bwana Emmanuel mlinzi wa geti la Patrick akiwa katulia zake kibandani kwake huku mkononi akiwa na Gazeti la majira majira, kumbuka mda huo ilishakuwa mchana hivyo ile habari ya uvamizi na ajali vilikuwa vimesambaa magazetini takribani nchi nzima hivyo Emanuel nae pia alikuwa akisoma habari ile ile kuhusu ajali vilivoambatana na uvamizi huko makonani, Emanuel akiwa anaendelea kupekua pekua habari ile mara alitaharuki zaidi baada ya kuona gari anayoifahamu kabisa.



** Naota au?? '' Emanuel alijiuliza huku akizi kulikodelea macho lile gari ambalo ukweli ni kwamba ilikuwa gari ya Saida..



Emmanuel alipohakikisha kuwa macho na fikra zake zilikuwa sahihi haraka alitoa simu yake na lengo lake ni kumtafuta Patrick. Alitoa na haraka akaingia sehemu ya majina na kuanza kupekua haraka haraka huku mikono ikitetemeka, mpaka akafanikiwa kuifikia ila kabla hajapiga Honi ikapigwa nje ya geti, Emanuel akatupia jicho kwenye kidirisha chake na kugundua ni bosi wake. Haraka akatoka huku akiwa na gazeti lile mkononi akafungua geti na taratibu Patrick akawa anaingia na gari yake kaliii...



Emanuel hakutaka kulaza damu akamsimamisha na bila ajizi Patrick akakanyanga brek ya mkwara mpaka prado ikanesa!!



" Bosi..! bosi ona..!! ''



Emanuel aliongea huku akimwonesha Patrick lile gazeti ilihali jasho likimwagika mwili mzima, Patrick alilitizama lile gazeti kisha bila kuonesha mshtuko wowote akamwambia aendelee na kazi,, Emanuel alimshangaa mara mbili mbili. Na katika kumtizama Patrick kwa mshangao pia alishtuka na kutaharuki zaidi baada ya kuona upande wa kushoto kakaa mwanadada kisu hatari...!!



Patrick taratibu akaanza kuiondoa gari yake pale huku akimwacha mlinzi akiwa kaduwaa pale!



Emanuel taratibu akafunga geti na kurudi zake kibandani kwake huku mawazo yakipishana kichwani na kushindwa kujua ashike lipi??, alijilaza kwenye kitanda chake huku akitafakari Patrick kaanza lini uchafu huu?? Au ndiyo sababu ya kukosekana kwa amani humu ndani?? Patrick aliwaza pasipo kupata jibu sahihi..



Akaamua achukue simu yake na kumtafuta Saida, Lakini hata hivyo aliambulia patupu baada ya simu hiyo kutokuwa hewani



** Atakuwa mzima kweli huyu mama?? Mbona hata simu yake haipatikani?? Daaah!! '



Patrick aliwaza hayo huku akizidi kukosa Amani kabisa.. Wakati huo Patrick na Ashura wameshapaki gari yao uwani na sasa wanapiga hatua za taraatiiibu kabisa kuelekea ndani ya jumba hilo kubwa kabisa la kifalme....





Waliingia mpaka ndani huku wakimwacha mlinzi wa geti bwana Emanuel akiwa kadakwa na bumbuazi siyo la kawaida kwa maana hakuwahi kutegemea hata siku moja kama bosi wake huyo Patrick mtu na heshima zake atakuja kufanya mambo ya ajabu kama hayo..



" baby.. ''

" niambie Ashuu wangu.. ''

" una nyumba nzuri?? ''



Waliongea huku wakiketi sofani katika sebule kubwa iliyopambwa kwa fenicha za bei ghali sana..



" sasa mtu kama mimi nitaishije nyumba ya kishamba?? ''

" hahahaha.. Patrick bwana?? Huishiwi na vituko we mwanaume??? ''

" pesa inaniambia nisiishiwe na vituko ''

" nijengee na mimi basi maana nyie ndo wanaume wa kuoa siyo vicheche wa mtaani huko ''

" hahahaaa! Sawa lakini mpenzi?? ''

" sema mpenzi ''

" unajua toka tuwe wapenzi sijawahi pata penzi lako ''

" mmmmh! Kwahiyo?? ''

" kwahiyo nini tena jamani?? ''

" watakaje sasa? ''

" m..mm nanihii.. Nanii bwaa aaa!! Mbona unajifanya huelewi wewe??...''

" nanihii??? Ndiyo kitu gani hicho?? ''



Ashura akawa anajifanya kama haelewi vile,, Patrick akamzima na swali hilo hapo... !!



" kwani we ni Bikra?? ''



Kimya!!



" nakuuliza Ashuu! ''

" Aaam hapana ''

" Sasa mbona unanizunguka?? ''

" eneo lenyewe siyo sahihi hili ''

" siyo sahihi nyumbani kwangu?? ''



Patrick alijibu hivyo huku akimvaa Ashura ambae hakuwa na hili wala lile.. Heee! Alipaniki huyo!



" we mwanume hivi akili zako zimekukaa sawa kweli?? U..uu..un..taka..tuu..ufanye ndani kwa mkeo??? ''

" sina mke humu ndani usihofu.. Sikiliza kwanza nitakuzawadia Bughat mpyaa iwapo utanimegea tunda lako leo.. ''

" mmmmh! Patrick?? ''

" Nitakujengea nyumba mpyaa uachane na vyumba vya kupanga vyenye kila aina ya kero, unoko, buguzana na mengineyo ''



Mpaka hapo Ashura hakuwa na la kuongea tena zaidi ya kutulia tuliii...!! Akisikilizia jinsi mikono ya Patrick inavyotalii kwa kasi mwilini mwake...

***********************

Tukirudi hospitalini.. Hali ya Saida ilirudi kuwa mbaya kwa mara nyingine tena baada ya kulia kwa mda mrefu hatimae nyuzi alizokuwa ameshonewa zilifumuka tena kutokana na kilio cha kwikwi alichokuwa akilia pale wodini, damu nyingi ilianza kumtoka tena. madaktari walijazana tena kwa mara ya pili pale wodini ili kujaribu kuyanusuru maisha ya mwanamama huyo ambayo kwa mara nyingine tena yalikuwa hatarini..



" Wakubwa imekuwaje tena??? ''



Daktari mmoja aliuliza baada ya kukuta hali ya Saida imekuwa mbaya gafla wakati aliondoka na kumwacha akiwa katika hali iliyokuwa inaleta matumaini ya kupona, na hakujua kilichojiri nyuma...



" Ebwana mumewe kaja hapa akiwa kapaniki kishenzi.. ''

" kapaniki?? Kwanini?? ''

" Anasema kuwa mkewe alikuwa katika harakati za kutoroka na mchepuko wake ila kwa bahati mbaya wakapata ajali nziani,, jamaa kala kona baada ya kuona huyu kaumia na gari kufa.. ''

" daaaah!! Wanawake hawa shida sana! Kwahiyo inakuwaje?? ''

" Hapa cha msingi ni kumtibia tu! Kwa maana kaletwa na serikali hivyo inatulazimu tumtibu akipata nafuu aruhusiwe ''



Yalikuwa ni maongezi daktari na Lous daktari nguli kutoka OCEAN ROAD Dar es salaam ambae ndiye alijazwa uogo huo na bwana Patrick saa chache zilizopita



Saida alikuwa akiyasikia mazungumzo hayo kwa uzuri kabisa hakika maumivu aliyoyasikia moyoni mwake ilikuwa ni zaidi ya mara mia ya kidonda alichokuwa akishughulikiwa pale wodini, Saida alikata tamaa ya kuishi duniani na alitambua fika Patrick siyo Patrick yule aliekuwa akimfahamu, siyo Patrick yule walietafuta wote mali kwa udi na uvumba mpaka ikafikia wakati mwingine kutenda zambi ili tu waweze kupata kile walichokuwa wamekikusudia... Saida alikumbuka miaka kadhaa iliyopita...

***

KUMBUKUMBU...* Saida anakumbuka,, ilikuwa ni mwaka 2003 Anakumbuka siku hiyo ilikuwa ni siku ya gulio pale mtaani kwao, na ilikuwa ni kawaida sana kwake kutembele gulio hilo hasa nyakati za jioni alikuwa akipenda sana kuburudika na wenzake kwani mpaka hapo alikuwa hajaolewa bado na miaka 20, sasa siku hiyo baada ya kutinga gulioni hata kabla ya matembezi, kuna kijana walikutana nae uso kwa uso! Yule kijana alikuwa akifahamika kwa jina la Patrick, akamkingia kifua kwa lengo la kumsimamisha..

" Pati bwana nini wewe?? ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" simama basi tuongee mawili matatu''

" Hebu wacha ujinga tuonge manini?? Si uje nyumbani?? ''

" sikia Saidaa! Najua unaelewa kile nakusimamishia na hunitaki kwa kudhani ndiyo wale wale.. Lakini tambua kuwa siyo hivyo.. Vile nakwambiaga siku zote ndicho nilichokipanga moyoni.. Mimi ni maskini lakini tukiungana na wewe hakika tutafika mbali nakuahidi. Saida nakupa mda fikiria kwa kina sana mi sijakupenda kwa ajili ya anasa nimekupenda ili tukajenge famili...



YALIKUWA NI MAMENO MATAMU MITHILI YA ASALI KUTOKA KWA KIJANA HUYO AMBAPO KILA MSICHANA MWENYE MALENGO NA MAISHA YAKE NI LAZIMA ADATE..



Baada ya kijana huyo Patrick kuongea hayo alimwacha Saida akiwa kainamisha kichwa chini yeye akaondoka zake, hakika yale maneno yalimwingia sana Saida aliona huyo ndiyo mwanaume wa kumuoa kwa sababu na yeye alikuwa na malengo na maisha yake hakutaka wahuni wasio na kichwa wala miguu kumgusa..



BAADA YA MWEZI MMO MWAKA HUO...



Saida baade alipokuja kukutana na Patrick alikiri ya kwamba amemkubalia ombi lake ila tu! Autunze moyo wake mpaka dakika ya mwisho kwa maana kajikabidhi kwake kwa moyo mmoja.. Patrick aliruka juu kwa nguvu huku akishangilia na kumwagia ahadi kibao.. Na hazikupita hata wiki kadhaa wanandoa hao waliweza kuoana na kwenda kuanza maisha mapya....



Wanandoa hawa waliishi kwa raha mustalehe japo maisha ya Patrick yalikuwa ya kimasikini kuliko hata kawaida lakini Saida alimpenda hivyo, walichokipa basi hicho ndicho walikula pamoja, na siku walipokosa basi walilala..

MIEZI MITANO BAADAE...

Saida alibeba ujauzito kwa mara yake ya kwanza, wote kwa pamoja walifurahi kuona ndoto zao za kujenga familia zinakwenda kutimia japo walikuwa na maisha ya ufukara lakini waliamini ridhiki yao ipo njiani na siku moja nao watakuja kuwa kama wengine. Kikubwa ni kuendelea kushikiriana katika kulisukuma gurudumu la maisha.. Lakini wahenga walisema ng'ombe wa maskini hazai..



Mimba ilipofikia mda wa miezi nane Saida alishikwa na ugonjwa wa ajabu ambapo juhudi zote za Patrick kumwokoa mkewe huyo ziliambulia patupu ujauzito wa Saida uliweza kutoka...



Saida aliweza kupona baada ya ujauzito wake kutoka lakini tatizo hilo liliongeza hali kuzidi kuwa duni sana kwani akiba yote waliyokuwa wamejiwekea iliweza kutumika katika matibabu.. Hivyo basi walikuwa wakiishi kwa kutegemea vibarua vya kutwa ambapo Patrick alikuwa akienda vijiweni kubeba mizigo, Saida yeye alikuwa akielekea mtaani kutembeza matembele kisha jioni wanakutana na kula kile kilichopatikana.. Na maisha yakasonga..



Sasa siku moja Saida aliwahi kumaliza mboga yake na kuwahi kurudi nyumbani mapema sana.. Basi bila kupoteza mda alianza harakati za jikoni ili mumewe akirudi tu! Akute tayari.. Wakati ndiyo pishi limechanganya mara akasikia hodi, haraka akatoka na kukuta ni mumewe Patrick, alimlaki na kumpokea kile alichokuwa kakibeba..



Siku hiyo Patrick alionekana kuwa na jambo moyoni kwa maana alikuwa tofauti na siku zote, Saida alitambua hilo akamuuliza...



" Patrick mume wangu ''

" Ndiyo Saida mke wangu? ''

" Hauko sawa leo kulikoni?? ''

" mmmh! Nina jambo sijui utanielewa?? ''

" uko huru kuwa na amani Mume wangu ''

" Ni jambo moja tuu! Nahitaji tubadili maisha yetu mke wangu ''

" una maana gani mume wangu?? ''

" ni jambo gumu kidogo mke wangu naa sijui kama utanielewa?? ''

" ni jambo gani hilo mume wangu?? ''



" Rafiki yangu mmoja kanishauri ya kwamba huenda nyota yetu ya mafanikio kuna mtu kaikamata ''



Mnyo wa Saida ukalia paaaah!! Akajua tayari mambo ya matambiko yanahusika hapo na ni kitu ambacho hakipendi katika maisha yake yote...



" Yaani mume wangu unataka kujihusisha na uchawi??? ''

" siyo uchawi tunakwenda kurudisha nyota yetu na mambo yanakaa sawa ''

" mmmmh! ''

" usigune mke wangu tizama tunavyoaibika hapa mtaani?? We unapendezwa na hali hii?? Usiwaze sana kesho tunakwenda sumbawanga na tukirudi huko mwenyewe utaona... ''



Saida hakuwa na la kuongea kwani mumewe keshapanga na hawezi kum'bishia.. Basi siku hiyo baada ya chakula walikwenda kulala huku Saida akiwa na mawazo mengi sana kichwani kuhusu uamuzi wa mumewe..



Asubuhi na mapema walijiandaa na kisha kuianza safari ambapo kwa usafiri wa kipindi hicho ilichukua siku tatu kuwasili Sumbawanga mji wa wachawi....



Asubuhi na mapema walijiandaa na kisha kuianza safari ambapo kwa usafiri wa kipindi hicho ilichukua siku tatu kuwasili Sumbawanga mji wa wachawi....



Ismani Iringa

March 21, 2019

Saa 08:35 PM.



.....Kumbuku ya Saida inaendelea......



Waliwasili Sumbawanga ikiwa ni siku ya tatu toka waondoke Iringa hii ilitokana na ubovu wa miundombinu kwa kipindi hicho na kibaya zaidi waliwasiri usiku wa manane teenaa walishukia mstuni na siyo mjini, ni kwa maelezo ya huyo rafiki yake Patrick alivyomweleza kuwa ni razima asiingie sumbawanga mjini kwani mganga huyo anaishi porini..



Saida na mumewe baada ya kushuka garini waliachwa mahali pale na kulikuwa na hali ya hewa ya mvu kabisa kwani kulikuwa na mawingu mazito yaliyokuwa yakiashiria muda wowote ni mvua tu! Kwani maradi yalikuwa yakimulika usipime!



Patrick alitoa kijikaratasi kidogo pamoja na tochi wakati huo Saida akimtizama tu, akwasha tochi na kuikunjurua ile karatasi ndani yake kulikuwa kuna ramani ambayo moja kwa moja ingewafikisha kwa mganga huyo. Patrick aliipitia kwa umakini wa hali ya juu na baada ya kuielewa mahali inapowaelekeza kupita waliongozana.



Hakika ilikuwa ni safari moja ya kutisha sana na kuwahi kutokea maishani mwa mwanamama huyo kwani walipita maeneo ambayo siyo kabisa yaani mabonde makubwa! Giza totoro, harufu kali ya uozo, ndege wa kutisha kama bundi hulia yaani unaambiwa ilikuwa kasheshe...



Baada ya safari ya takribani lisaa lizima waliweza kuwasiri katika makazi ambaya dalili zote zilionesha ni kwa mganga maana kijumba hicho kilikuwa kati kati ya msitu mnene..



Mara! Radi kubwa ikaunguruma sambamba na kuachia mwanga mkali ambao uliweza kusababisa eneo lote lile kuwa kwa mda huo.. Macho ya Saida na Patrick yalikutana na kundi kubwa la fisi waliokuwa wamekizunguka kijibanda hicho..



Oooohoo!! Wakadakwa na uoga Saida alimkimbilia mumewe na kumkumbatia kwa nguvu wakati huo huo Patrick akifanya jitihada za kuwasha tochi yake.. Na kabla hajafanikiwa kuiwasha tochi hiyo sauti nzito ya kiume yenye kukoroma ikasikika ikisema....



" Twaileee!! Twaileee!! Twailee!!.. Nimewaona nimewaona!! Musiogope... !!, ''



Wote wawili mtu na mkewe wakabaki kimya huku kila mmoja akiwa na alama za viulizo kichwani kwake...



Punde tu! Mlango ulisikika ukifunguliwa na Mganga akatoka huku akiwa na kitu kama fuvu la binadamu ambalo lilikuwa likiwaka moto wenye kutoa mwanga mkali usiozimika mwanga huo uliwafanya Saida na mumewe kuweza kuona eneo lote la pale nje ila cha kustaajabisha ni kwamba fisi wale waliowaona mwanzo hawakuwapo tena!!



Walitahamaki.....!!



Yule mganga aliwakaribisha ndani, na bila kupoteza mda alianza kuwashughulikia tatzo lao ambapo inadaiwa ya kwamba alishatabiri ujio wao tangu masaa mawili yaliyopita pindi tu walipoikanyaga ardhi ya sumbawanga..



Patrick na Saida walitazamana usoni maana hawakutegemea kile alichokuwa akikizungumza mganga huyo, na ili kuwathibitishia hilo? Aliwaambia mpaka na gari waliyokuja nayo ingali wakati wanaondoka iringa hawakumwaga mtu yoyote..



Mganga aliendelea kusema kuwa shida iliyowapeleka pale ilikuwa ni kutafta nyota ya mali ambayo wanahisi huenda nyota yao imechukuliwa na wachawi, mganga huyo alimeza mate kisha akaendelea kusema kuwa katika wanandoa hao wawili ni mmoja tuu! Ndiye mwenye nyota ya mali...



Maneno yale yaliwashtua mnoo Saida na mumewe, walibaki kutizamana tu! Wasipate hata neno la kuongea..



Mganga alikaa kimya kidogo kisha akaendelea.. Kwa kusema kuwa mtu mwenye nyota ya mali ni mkewe Patrick ambae ni Saida!!.. Wote wakapigwa na butwaa..! Kwa kusikia vile mpaka Patrick uvumilivu ukamshinda akataka kuuliza kitu ila mganga huyo akamwahi..



" Huruhusiwi kuongea chochote bali nisikilize...''



Mganga huyo akasema Ili wao kuondokana na umaskini, dhiki pamoja na shida zote ni lazima Saida ajisaidie haja ndogo katika kibuyu atakachopewa na mkojo huo utanenewa maneno machache na kwa kuchanganywa na dawa fulani na hapo ndiyo utakuwa ni mwisho wa wao kuwa maskini...



SHARTI..

" mkeo hatokuja kuzaa tenaa na ndiyo sharti pekee mimi huwa sitozi kafara, jadiliana na mkeo mkishakuwa tayari tumalize kazi na muondoke kabla ya jua kuchomoza.. ''



Mganga huyo aliwapa nafasi kwa kuondoka pale ili wajadiliane.. Uchungu mkubwa ukamkuba Saida alijua kabisa ndoa yake ipo matatani kwa kutozaa ni lazima Patrick akipata mali atataka mtoto itakuwaje?? Saida alili huku akimweleza mumewe,, lakini Patrick alimhakikishia kuwa asingemwacha mpaka kifo kije kuwatenganisha!!



Kutokana na wanawake mda mwingine kuwa na huruma Saida hakuwa na budi kukitoa sadaka kizazi chake kwa mganga huyo alikubali shart hilo kwa moyo mmoja! Na mganga aliporudi walimaliza kazi na kisha kupewa dawa nyingine kidogo ambayo waliambiwa watakwenda kuipulizia kwenye nyumba yao ili kuilinda nyota yao isije kuibiwa na wachawi, na mganga huyo aliwahidi kuwa wangefika iringa wakiwa na begi lenye pesa nyingi sana japo hakufafanua kuwa wangezipataje??



Basi waliagana na mganga mda huo ikiwa ni saa kumi na moja kasorobo alfajiri, Saida na mumewe wakaongozana tena kwa mara ya pili katika njia ile ile ambapo licha ya kukaribia kukucha lakini bado kulikuwa na giza nene na la kutisha katika pori hilo..



Walifanikiwa kufika mpaka barabarani, ila kwa mda huo hakuna gari yoyote iliyotoke hali iliyowalazimu kuweka kambi pembezoni mwa barabara hiyo kungoja mabasi ya asubuhi yatokayo sumbawanga kwenda Iringa. Mipango mingi ya kimaisha alianza kuipanga kichwani Patrick hasa kumiliki hoteli kubwa ya kifahari itakayokuwa tishio Iringa nzima pia awe na magari ya kifahari ya kutembelea na vitu vingine kibao...



" Patrick gari iyo inakuja.. ''



Sauti hiyo ya Saida mkewe ikamtoa Patrick katika dimbwi kubwa la mawazo aliyokuwa nayo kuhusu maendeleo..



Naam! Ilikuwa imeshatimu saa kumi na mbili kamili, kuna basi lilikuwa linakuja haraka wakasimama na kulipiga mkono, basi likasimama na wote kwa pamoja wakazama ndani na basi kuondoka. Safari ikaiva kuelekea iringa huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana..



Baada ya mwendo wa takribani masaa matatu na walikuwa wamefikia sehemu moja ambayo ilionekana kuwa na kijilima hivyo basi lilikuwa taratibu. Mara gafla! Ikatokea Scania mbele ikiwa mwendo huku ikiwa imepoteza mwelekeo kabisaa!!



Baraaa!!



Dreva wa basi akasimamisha basi lake kila mmoja alianza kusali maana hiyo ilikuwa ni baraa kabisa bila ubishi, dreva wa scania ile alipofika karibu alijaribu kulikwepa basi hilo lakini juhudi zake hazikuzaa matunda kwani alifanikiwa kulikwepa kwa mbele ila contena likawavaa huku' basi lilitupwa hukoo! Huku likiachana na paa!!



Ajabu..!!



Patrick na mkewe hawakuweza kufa wala kuumia katika ajari hiyo. watu wengi walipoteza maisha na wengi kuumia lakini Patrick na mkewe hawakupata hata jeraha,



Cha kwanza Patrick akauwahi mfuko wake kuona kama dawa yake ipo?? Alipoingiza mkono mfukoni aliikuta akafulahi sana! Na hakutaka kuendelea kupoteza mda hapo cha msingi ni kuangalia ustaarabu wa kuondoka maana kama ni msaada basi kikosi cha MSALABA MWEKUNDU ndiyo watakuja kuhusika.. Patrick akamsaidia mkewe na wote wakatoka ndani ya gari hilo ambalo lilikuwa limebondoka baraa. Wakatoka mpaka nje..



Zari la mentali..!!



Baada ya kufanikiwa kutoka waliona pia ile scania ikiwa imeanguka mbele kidogo na mahali walipo, wakiwa bado wanashanga sahangaa mara wakaona begi kubwa jeusi likiwa limeanguka kando ya bara bara! Karibu na basi hilo! Patrick alipata shaukuu ya kutaka kujua begi hilo lina nini ndani?? Akapiga hatua za haraka mpaka pale na kuliokota. Na kwa jinsi alivyo na papara mara akavuta zipu chwaaa! Ebwana eee!! Alichokikuta hata yeye hakuamini macho yake, zilikuwa ni pesa nyingi sana zilizofungwa katika vibunda vibunda,, Patrick alifunga haraka kisha akatizama huku na huko hakuona mtu yoyote aliezinduka wote walikuwa bado wamekata moto..



Alimwita mkewe kwa ishara kisha wakaondoka eneo hilo kabla wasamalia wema hawajaja kutoa msaada, walitembea umbali mrefu sana huku wakiwa wameambaza barabara Patrick akiwa na begi mgongoni mpaka pale walipokuja kupata gari nyingine ambayo iliwafikisha moja kwa moja mkoani Iringa.. Pesa hizo ndiyo hizo ambazo mganga aliwahidi watafika na pesa nyingi sana iringa na hakufafanua wangezitoa wapi??



--- KUMBU KUMBU YA SAIDA INAISHIA HAPO ----



Saida aligutuka kutoka katika dimbwi lile kubwa la mawazo liliokuwa limemtoa kifikra kalibia dakika 30, na alipokuja kushtuka kutoka katika dimbwi lile kuwa la mawazo alikuta madaktari wakiwa wameshamtibia mpaka wametawanyika! Yeye aliona tu! Akiwa amefungiwa mitambo yenye kusambaza joto katika eneo la tumbo lake alipofanyiwa upasuaji,, huzuni kubwa sana ilitawala moyoni mwake na hakuwa akiamini kabisa kwa mateso yale yooote waliyoyapitia leo hii Patrick anakuja kumuona takataka daaah!!





Saida aliendelea kuungulia na mawazo mengi Sana pale kitandani, hakujua ni njia gani atumie kumthibiti Patrick.. maana hata Kama atasema afunge Safari mpaka sumbawanga ili akaharibu mipango yote itakuwa ni kazi bure tuu..!!



Kwa maana Kwanza hata yeye Hana uhakika Kama mganga huyo bado yupo hai au alikufa?? Licha ya Hilo pia eneo lenyewe analoishi linatisha..!! Yataka mwanaume kweli kweli hivi hivi huwezi kwenda..!! Asa Saida ndiyo atakwenda???



Ni Jambo gumu....



Dakika kadhaa nesi mmoja aliingia wodini hapo na kumkuta Saida akiwa katika majonzi makuwa mno!! Yule nesi alimtizama kwa sekunde kazaa Kisha akamsogelea mwanamama huyu...



" Pole Mama angu.. ''



Saida hakuweza kujibu chochote aliishia kumtizama tuu nesi huyu ambae kiumri alionekana ni mtu ambae umri wake siyo zaidi ya miaka ishirini yaani bado msichana kabisa..



Yule nesi licha ya kutojibiwa lakini pia hakukata tamaa aliendelea kumfariji mwanamama huyo huku akiendelea kum'dadisi na maswali kadhaa..



" Samahani mama ''

" Bila samahani ''

" Mbona tangu uletwe hapa siku mbili zilizopita sijaona ndugu yeyote kuja kukujulia Hali??.. ''

" Mwanangu wanasema kua uyaone mwenzio nimeyaona.. ''

" Una maana gani mama?? ''

" Sipo tayari kulizungumzia Hilo tadhari..''

" Lakini mama huenda nikawa hata na msaada wa ushauri wowote kwako..''

" Ndiyo najua Hilo ila tafadhari Sana sipo tayari kulizungumza...''



Nesi akabaki kimya na kukaa njia panda hakujua ni sababu ipi inamuweka mwanamama huyu katika Hali hii??



' au mumewe alikufa katika ajali hiyo?? Jee?? Hana ndugu?? Mmmh!! ''



Yule nesi aliishia kujiuliza mswali ambayo kwake hayakuwa na majibu Hali iliyopelekea aachie mguno tuu!!



Mara gafla mlango wa hapo wodini ukasukumwa na daktari Lous akaingia huku akiwa katika mavazi ya Safari. Inaonekana alikuwa anata kuianza Safari ya Dar es salaam.



Baada ya kuingia mle wodini alikaa kwenye moja ya viti vilivyomo mle ndani ambacho kilikuwa karibu na kitanda.



Yule doctor alimtizama Saida usoni.. Kisha akalitizama jeraha lake Kisha akatikisa kichwa....



" Pole Sana dada angu na hii ndiyo mitihani ya Maisha..''

" A..ah..s..an..tee''



" Labda Nikusihi kitukimoja tuu!! Jaribu kukaa mbali na mumeo...''

" Atiii uu...um..ema..je?? Dokta?? ''



Saida alikuja juu..



" Iyo ni kwa faida ya uhai wako kaa mbali na mumeo atakuua dada angu.. ''

" Hapana doctor mume wangu tumetoka nae mbali Sasa iweje Leo niwe mbali nae?? ''

" Lakini unakumbuka asubuhi kazemaje hapa?? ''



Swali Hilo likaweka kimya Saida na wakati huo tukio Zima la yaliyotokea asubuhi likianza kujirudia rudia kwa Kasi kichwani mwa mwanamke huyo. Saida hakuwa na la kuongea mpaka hapo maana akikumbuka ni kweli asubuhi Patrick alimshikia bastora...



" Pole Sana mama hii ndiyo dunia ya Leo,,''

" Asante lakini sijakuelewa Doctor ''



" Ninaposema hivyo Nina maana ya kwamba wewe Sasa hivi ni mgonjwa.. halafu mumeo Ana hasira na wewe hivi huoni Kama utaendelea kukaa nae karibu utakufa na mawazo?? Au hata mwenyewe akakuua?? ''



Saida alivuta pumzi ndefu na kuishusha Kisha akasema....



" Asante daktari kwa ushauri wako nitaufanyia kazi..''



" Asante pia kwa kunielewa.. na pia si vibaya nikajitambulisha kwako yawezekana bado hujanijua.. ''



Daktari Lous alizungumza hivyo kisha kimya kidogo kitawala, pumzi ndefu akaivta na kuishusha.. Kisha akaanza kujitambulisha....



" Naitwa Docta Lous natokea Ocean loard Dar es salaam, nimekuja hapa siku mbili zilizopita kuja kumsalimia binti yangu mmoja afanyaye kazi katika Hospital hii, ukweli siku na saa niliyofikia hapa ilikuwa ni wakati m'baya sana kwako kwani tulikutana na madaktari wakikupeleka mochwari...!! ''



" Nini?? ''



Saida aliuliza kwa taharuki kubwa huku akiwa kamkazia macho daktari huyo.. Daktari huyo alivuta pumzi na kuishusha kisha akaendelea..



" Ndiyo hali yako ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba vipimo katika hospital hii pamoja na madaktari walishindwa kubaini kama bado mzima, kwani vipimo vyao vilishindwa kubaini kama moyo wako bado unadunda kwani mapigo yake yalikuwa chini mno ''



Saida macho yalizidi kumtoka pima asiamini kwamba alianza kupelekwa mochwari ingali yupo hai.. Lous pia aliendelea kumsimuli..



" Roho iliniuma sana na pia roho huwa inaniuma sana kuona kina mama wanapitia nyakati ngumu kama hizi,, hivyo sikutaka kuamini kama kweli mwanamama huyo aliekuwa kalazwa juu ya kitanda ambae ni wewe kama kweli umekufa na umefunikwa shuka jeupe tayari kuingizwa mochwari kuwa mekufa ''



Saida mwili mzima ulimsisimka kwa uoga mkubwa ila akazidi kumsikiliza kwa makini daktari huyo..



" Ila tunashukuru baada ya kukutilia shaka na kuamuru urudishwe wodini kisha nikakufanyia vipimo kwa kutumia vifaa vyangu na kugundua bado upo hai japo roho yako ipo katika hatua za mwisho kuachana na mwili tuliingia kwenye pilika pilika kwa kushirikiana na madaktari wa hospital hii hatimae niliweza kukufanyia upasuaji na kutoa damu iliyokuwa imevujia tumboni kwako ''



Aliongea daktari huyo maneno yaliyomwacha Saida katika lindi kubwa la taharuki huku maswali mengi yasiyokuwa na majibu yakikiandama kichwa chake...



" Doocta nashukuru sana kwa msaada wako ''



Hatimae Saida alitokwa na sauti hiyo huku machozi nayo yakianza kumiminika kama maji katika macho yake na kulowanisha mashavu ya mama huyo..



" Mimi sipaswi kushukuriwa bali dada yangu. muumba wetu ndiyo anastahili kushukuriwa kwani yeye ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho... ''



" Hata wewe pia nisipokupa shukran yako nitakuwa sijakutendea haki daktari.. ''



" Asante sana dada Nani?? ''

" Saida.. ''

" Asante sana dada Saida mungu akubaliki na kukuponya ''

" Nashukuru sana kaka ''



Baada ya mazungumzo hayo Dk Lous aliinua mkono wa kushoto na kutizama saa yake na kubaini mda wa kuondoka hapo umetimia hivyo hana tena mda wa kuendelea kukaa pale. Aliagana na Saida kisha akaondoka na kumuacha Saida katika lindi kubwa la mawazo...

************************

Kwingineko, Wanaonekana Patrick na Ashura wakijifuta jasho huku wakikaa sawa kwenye sofa baada ya mtanange mkali wa kukata na shoka!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ni wazi kabisa Patrick alikuwa amemsaliti mkewe kwa mara ya kwanza.



" Uko vizuri Ashuu khaaa!! Sijawahi kuwa na mwanamke mtundu kama wewe ''

" Hehehe!! Wanaume ndiyo mnavyosemaga siku zote na kwa kila utakaekutana nae ''

" sasa mimi ndiyo nakwambiaa sijawahi na kwa maana hiyo sifikirii kukuacha ''

" mmmmh!! Patrick lakini kumbuka una mke wewe? ''

" nina mke nimtoe wapi?? Saa hizi zaidi yako?? ''

" Patrick...!! Unafikiri mkeo simjui?? Kwanza yupo wapi?? ''



Ashura alimuuliza Patrick huku akiwa kamkazia macho ili apate ukweli mkewe huyo yupo wapi?? Alikufa katika ajali?? Au yupo ndani?? ukumbuke hapo wapo sebleni kwenye masofa



Patrick alitafakari kwa mda jibu la kumpa kisha akamwambia..



" huyo mjinga yupo IPAMBA Na hali yake ni mbaya na anaweza kufa mda wowote ''



Patrick aliongea pasipo na wasi wasi wowote wala mshtuko au masikitiko. Yaani anaongea kana kwamba anamzungumzia adui yake ambae alihusika na kifo cha baba yake, kumbe anamzungumzia mkewe wa ndoa kabisaa ambae ndiye aliemfikisha hapo alipo..



Hakika hata Ashura mwenyewe hakupendezewa na majibu hayo, alishia kumtizama Patrick pasipo kutokwa na neno lolote,



" Ashura mi nipo tayari kukuoa.. Nimetoke kukupenda sana na nakuahidi nitakupa chochote utakacho ili mradi wewe mwenyewe uridhie tu,, tafadhari sana usije kuumiza moyo wangu kwa jibu ambalo litakuwa nje na matarajio yangu...''



Patrick aliongea hivyo pasi na aibu yoyote,, Ashura aliishia kumtizama kwa jicho la bashasha. Sijui jicho hilo lilikuwa na maana gani??



" Kuhusu kuolewa na hapana kwani tayari una mke ''

" tafadhari Ashura nishakwambia sina mke kwa sasa humu ndani ''

" Mmmh! Hata hivyo naomba mda zaidi niweze kufikiria hili swala ''

" Upo huru na nina imani hutouumiza mtima wangu ''



Ashura alivuta pumzi ndeefu na kuishusha, moyoni alifurahi sana kwani alijua mpango wake sasa unakwenda kukamilika ataishi maisha ya kifahari ambayo alikuwa akiyatamani siku zote..



Kimya cha mda mfupi kilitawala mle sebleni.. Mara simu ya Patrick ikaita haraka akaitoa na kuisawiri juu ya kioo, Alishtuka baada ya kugundua mpigaji ni kamanda wa polisi kituo cha Ismani mapigo ya moyo yalianza kumwendea kwa kasi sana Patrick alipatwa na wasi wasi kwani hajui mkuu huyo wa poli ana shida gani na yeye??



Kabla ya kupokea alimtizama Ashura kwa jicho la chini chini na kugundua kuwa na kashtushwa na simu hiyo kwani usoni alionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana..



Taratibu Patrick akagusa kitufe cha kijani na kuipeleka simu hiyo sikioni....





Kabla ya kupokea alimtizama Ashura kwa jicho la chini chini na kugundua kuwa na kashtushwa na simu hiyo kwani usoni alionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana..



Taratibu Patrick akagusa kitufe cha kijani na kuipeleka simu hiyo sikioni....



29, March 2019



SONGA NAYO.........



Sasa kabla hatujaendelea hebu kwanza tupate kujua simu hii iliyopigwa na mkuu wa kituo cha polisi Ismani inahusu nini??



Mpango mzima huo hapo...!



Mkuu wa kituo baada ya kuikabidhi scania iliyokuwa imewekwa chini ya ulinzi kwa vijana hao aliotoka nao Songea na kuondoka, nae kichwani aliwaza kuhusu ile gari ndogo iliyopo kule polini. Ilitakiwa ikachukuliwe iletwe kituoni ili mwenye nayo aje kuichukulia kule kituoni,



Basi pale pale akajadiliana na kijana wake wa kazi bwana Charles kisha wakakubaliana kukodi boda boda itakayowakimbiza mpaka kule makonani..



" Oya boda boda...!! '' Charles aliita..

" Naam mkuu '' kijana mmoja aliitikia..

" Uje na boda yako hapa ''



Huyo kijana hakukawia aliwasili hapo huku akiwa na pikipiki kali aina ya BOXER BM 150..



" Tunataka utukimbize kibaoni vipi utatuchaji ngapi?? ''

" Aa'aa kwa nyie mabrother wangu mnichangie mafuta tu! ''



Bila hata kupoteza mda Charles alimwita muuza Petrol mmoja hapo akaja na kidumu chenye ujazo wa lita moja, akamiminia ndani ya tank la pikipiki hiyo, Charles akalipia mafuta hayo kisha taraatiiibu wakaanza kuiacha Nyang'oro..



Baada ya mwendo kama wa dakika arobaini.. Gafla wakakutana na gari ndogo ikiwa imefungwa kitambaa chekundu kuashiria kibendera cha hatari kadharika Hazard zikiwa zimewashwa!



Hali hiyo ilimpelekea dreva boda boda huyo kupunguza mwendo na kuchepuka kabisa maana kama ilivyo sheria ya barabara ukiona kingora, kibendera, Hazard au gari ikiwa imewasha Endiketa zote jua usalama ni mdogo yakupasa kupita kwa tahadhari..



Baada ya kijana aliekuwa amewachukua polisi hao kupaki pembeni ili kupisha msafara huo, polisi hao pia walishuka ili kushuhudia vizuri ni msafara wa nini huo??



Hazikupita dakika nyingi baada ya gari hiyo ndogo kupita, ilifuatia gari nyingine kubwa aina ya Scania/semitera roli hilo likuwa limfungwa kitambaa cheupe mbele kilichoandikwa kwa maandishi mekundu yaliyosomeka...



( WIDE ROAD )



Na nyuma kwenye tera lake ilikuwa imepakiwa mashine moja kubwa sana ya kuchimbia visima vya maji..



Polisi hao akiwemo dreva boda boda wao waliendelea kuosha macho kwa kutizama msafara huo.. Mara Charles katika kutizama tizama macho yake yakakutana na gari ndogo nyeusi iliyochakaa sana kwa kubonyea bonyea..



Charles kumbukumbu zikampeleka makonani ambako siku moja iliyopita alishuhudia ajari mbaya ya gari ya aina hiyo,'



' Ile gari si hii? Au?? '



Charles alijiuliza pasipo kupata jibu sahihi, akaona ni bora amshirikishe mkuu wake kwani yeye alionekana kuwa na mawazo mengine hivyo Charles alijua wazi bado hajaona na Scania hiyo inazidi kupita...



" Mkuu..! Mkuu...! ''

" Ndiyo Charles ''

" Tizama kule ''



Charles alimwambia mkuu wake huku akimwonesha kunako Scania hiyo.. Mkuu huyo haraka akayaelekeza macho yake huko wakati huo Roli ndiyo lipo hatua za mwisho kupita pita,, Kamanda huyo alishtuka baada ya kuiona VX Ambayo ndiyo ile iliyopata ajali kule porini siku moja iliyopita...



" Hii gari si ndiyo ile??? ''

" Bila sh.......... ''



Kabla Charles hajamalizia sentesi yake alikatizwa na mlio wa king'ora uliokuwa ukisikika nyuma ukija. Haraka macho yao wakayaelekeza huko na kukutana na Difenta ile iliyokwenda kule mda mfupi uliopita..



" Jamaa si hawa?? '' Charles alizungumza huku akimtizama mkuu wake usoni,,

" Yaah! Nafikiri wamepata msaada huko ''



Taratibu ile difenta ilianza kupunguza mwendo huku ikisogelea saiti walipokuwa wenzao..



" Kijana unaweza kwenda ''



Mkuu huyo alimruhusu kijana mwendesha boda boda yeye aende kwani wao wanapanda gari, Na bila kupoteza mda yule kijana alipanda pikipiki yake na kuondoka huku nao Kamanda na kijana wake wakipanda difenta na safari ya kituoni ikaiva..



" Eehe tupe signal ''

" Tumepewa msaada na hawa jamaa ''

" mmepakia kwa kutumia nini?? ''

" iyo mashine pia ina Winch ''

" Ahaa! Wao wanaelekea wapi?? ''

" hao wanakwenda msumbiji wanatokea moshi ''

" sawa sawa ''



Yalikuwa ni maongezi kati ya mkuu na moja kati ya vijana wake ambae alikuwa ni sajent katika kikosi hicho kidogo..



Hatimae wanafika Ismani ambapo wamiliki wa roli hilo waliwashushia gari lao na wao kuendelea na safari,, polisi hao nao pia wakalifunga gari hilo nyuma ya difenta na kulikokota mpaka kituoni..



***

" Sasa hapa kilichobaki ni kumtafuta mmiliki wa gari hii na kazi yetu inakuwa imeisha ''



Alizungumza kamanda wa kituo hicho huku akilizunguka gari hilo kutizama Plate number zake ili aweze kuziripoti katika vituo mbali mbali vya polisi na magereji ili kabla mama huyo hajaruhusiwa mumewe aje kulichukua gari hilo,, polisi alifanya hivyo kwani mpaka hapo alikuwa hajamtambua mume wa mwanamama huyo ni nani?? Na anaishi wapi??



Baada ya kuziona na kuhakiki Plate number zile alitoa simu yake na kuingia sehemu ya NOTES Kisha akaziandika namba hizo..



Baada ya hapo alianza kuzipiga hatua za taratibu kuelekea chumba cha mawasiliano, wakati huo wazo la kwanza alilonalo kichwani ni kumpigia kamanda wa jeshi la polisi, kituo cha poli Iringa mjini.



Alifika katika chumba hicho na kuketi katika kiti kikubwa cha kuzunguka kilichomo humo ndani, akachukua mkonga wa simu ya mezani na kuipeleka sikioni wakati huo vidole vya mkono uliosalia vikiwa na kazi ya kubofya bofya simu kubwa iliyokuwa hapo mezani..



****

" ndiyo kapten ''

Ilisikika sauti upande wa pili..

" Habari za mda huu mkuu ''

" Salama kamanda karibu ''

" Aisee nina tatizo kidogo naomba msaada wako ''

" karibu kapten ''

" Asante, swala lenyewe ni hili,, kuna ajali mbaya sana imetokea juzi huko milimani nadhani taarifa unayo mkuu ''



" ndiyo iyo taarifa ninayo ''



" sasa hiyo gari tumeikokota mpaka kituoni hapa na inahitajika mwenye nayo aje kuichukua sasa tatizo linakuja wapi?? Hatumjui huyo mtu ''



" kwani mwanamke aliepatwa na ajari hamkuweza kumdadisi?? ''



" Alikuwa katika hali mbaya sana kwani alikuwa kazimia kabisa, na hatukuweza kupata maelezo yoyote ili kujua ni wapi anatokea? Na mume wake anaitwa nani?? Na huyo mumewe ndiyo tunaemhuitaji...''



" Sasa hapo ulitaka nikusaidie vipi kapten?? ''



" Wazo langu ni kutuma plate number kwa vituo vyote vya polisi nyanda za juu kusini ili nao wazisambaze katika magereji mbali mbali pamoja na vikosi vya usalama barabarani. Nina imani kwa njia hiyo tutaweza kum'baini mtu huyo.. ''



" Sawa je?? Unaweza kunitumia hizo plate number?? ''

" ndiyo mkuu ''

" fanya hivyo ''



Simu ikakata na Mkuu huyo akaiandika Plate number iyo katika sehemu ya ujumbe mfupi kupitia simu yake ya mkononi kisha akamtumia, mda mchache simu yake ikarudisha ripoti kuwa ujumbe umepokelewa!



Mkuu huyu wa kituo akatulia kusubili majibu huku akiwa na shaukuu kubwa ya kumpata mume wa mwanamama huyo ili gari iondolewe haraka kituoni hapo kwa maana kuna Ishu nyingine nyeti ya vijana wake kukimbia majambazi huko makonani na kupelekea kifo cha mtu mmoja hivyo kuendelea kuwapo kwa gari hiyo hapo kituoni huenda ishu iyo ikaanza kuvuja ni vema iondolewe na jarada hilo lifutwe!



Mara simu ya mezani inapatwa kupigwa kwa mara nyingine tena, haraka mkuu huyo akaipoke na kuipeleka sikioni..



" ndiyo mkuu ''

" Nimepata taarifa kutoka gereji moja iliyopo kihesa kuwa gari hiyo wanaifahamu ni mali ya Patrick mango Tajiri mkubwa hapa Iringa ''



" Patrick mango??? ''



Aliuliza kwa taharuki kana kwamba alishtushwa sana na hakutegemea..



" Hapana huyo mtu namjua aisee ''

" basi ndiyo huyo ''

" sawa, nashukuru kwa ushirikiano wako wacha nimtafute ''

" Sawa sawa kazi njema ''

" kazi njema pia mkuu ''



Simu ikakata wakati huo kamanda huyo akatoa simu yake ya mkononi na kuanza kulitafuta jina la Patrick huku kichwani akiwa kapanga njama fulani.. Alilitafuta jina hilo mwishowe akalipata na bila kupoteza mda akapiga,, simu ilianza kuita...

*** *********************

Patrick alipokea simu hiyo na kuanza kuipeleka sikioni huku akiwa katawaliwa na wasiwasi tele.!



" halow!! mkuu ''

" Ndiyo uko wapi Patrick?? '' Hilo swali likamweka matatani kidogo Patrick kwani hakujua ajibu nini?? Na wakati huo hajui anaulizwa kwa sababu ipi?? Jambo lililopelekea apatwe na kigugumizi na kushindwa kujibu chochote..



" naongea na wewe ndugu Patrick upo wapi??? ''

" Nipo njombe '' Patrick alidanganya jibu huku na mapigo ya moyo yakibadili gia na kuanza kumwendea mbiyo baraa!



" Unahitajika kituoni Ismani haraka iwezekanavyo ''



Moyo wa Patrick ukapiga paaaah!! Alianza kuhisi haja ndogo ikianza kusumbua kwani mawazo yake moja kwa moja yakampeleka kwenye tukio kubwa alilolifanya la kutaka kuua Askari kwa kuendesha bila kufata taratibu za barabara.....





" Kuna tatizo gani mkuu?? '' Patrick aliuliza kwa tahamaki huku kijasho chembamba kikichukua nafasi yake..



" Hakuna mda wa kuelezea hayo ila inatolewa amri kuwa unahitajika uripoti kituoni Isman ndani ya masaa matatu!! ''



Alipokwisha kusema hayo kamanda huyo na kabla Patrick hajajibu chochote simu ikakatwa!



Patrick akabaki njia panda, simu ikiwa sikioni, mdomo wazi, meno nje, asijue cha kufanya!



" Nini tena?? '' Ashura aliuliza huku akiwa na mashaka mengi sana..

" Nahitajika kituoni Ismani..''

" kituoni??? Kuna nini tena?? ''

" sijajua ila ngoja niwahi nikawasikilize ''

" lakini unakumbuka ya jana?? ''

" sijui ila sizani kama nimetambulika?? Sina uhakika na hilo huenda ni maswala mengine tofauti tu!! '' Patrick alijipa imani japo hata yeye ana mashaka na hilo..



" Sasa mi utaniacha wapi?? ''

" Baki hapa nitakukuta ''

" akuuuu...!! Patrick acha utani mkeo aweza kuja hapa nitafanyaje??? ''

" We kaa utulie haji huyo mjinga ''



Patrick alim'bembeleza Ashura huku akimshika mkono na kuinuka nae pale chini, kisha kwa hatua za taratiiiibu akawa anamkokota na kumpeleka katika chumba flani ambacho kilikuwa na hadhi kubwa sana yaani hata Saida mwenyewe hakuwa akikitumia, ndani kulikuwa na huduma zote! Mwanzoni Ashura alikuwa akisita kwenda lakini kadiri alivyozidi kumkokota mwishowe alikubali na kujikuta akiingizwa katika chumba ambacho hata hakuwahi kutegemea kukikanyaga kutokana na jinsi kilivyokarabatiwa kwa bei ghali.. Maana kila atakogeukia anakutana vitu vya thamani kubwa, kwanza kulikuwa na Tv kubwa ambayo hata hakuelewa na nchi ngapi?? Pia chini kulikuwa kumepigwa marumaru ya pesa nyingi sana marumaru ambayo mtu akiwa anatembea juu chini inamuonesha kana kwamba anatembea juu ya kioo!, halafu akigeukia upande wa pili anakutana na friji kubwa lenye vinywaji vya kila aina!..



Khaaa!!



Akiwa bado katika tahamaki kubwa huku akiwa anaangaza angaza huku na kule, macho yake yalikwenda kugonga katika masofa ya bei kali sana yaliyokuwa yamekaa kwa mpangilio mzuri katika upande mmoja wa chumba hicho yakiwa yamesanifiwa barabara kabisa na meza nzuri na ghali ya kioo kati kati...



" Utakuwa ukiishi hapa.. ''



Sauti hiyo ilipenya kwa uzuri kabisa kunako ngoma za masikio ya Ashura na kumfanya ashtuke katika lindi lile kubwa la maswali kuhusu chumba hicho,, kwanza ni Kama Ashura hakusikia vizuri. Ilibidi kuuliza tena!



" Unaongea na mimi Patrick?? ''

" Ndiyo naongea na wewe Ashura ''

" umesemaje?? ''

" utakuwa ukiishi ndani ya hiki chumba.. ''



Hapo sasa Ashura alisikia kwa uzuri kabisa ilihali akashindwa kujibu chochote huku mdomo wake ukitawaliwa na kigugumizi kikali kisicho na mfano, hakuwa akiyaamini masikio yake na pia hakuwa akiamini uwepo wake pale, alihisi huenda yupo katika ndoto moja tamu sana asiyotaka ikatike..



" Umenielewa?? ''

" A'aa...e..ee?! ''

" Haaa! Kwani imekuwaje tena Ashura?? ''

" Am.. Hapana nipo sawa ''

" Basi hiki ndiyo chumba chako, kina huduma za kila kitu, umeme, maji, choo, jiko, bafu kila kitu. Bafu na choo yapo mlango ule pale, na jiko lipo upande ule pale. Sawa?? ''

" ndiyo ''

" sawa wacha niwahi halafu nitawahi kurudi ''

" Sawa Patrick ila nina wasiwasi mimi? ''

" Wa nini tena?? ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Hivi mkeo akirudi gafla nitamwambia nini mimi?? ''

" Hana mamlaka ya kukufanya chochote nakuhakikishia hilo ''

" Patrick??? ''

" Licha ya hilo pia haji leo huyo ''



Alipokwisha kusema hayo Patrick aliondoka humo ndani na kumwacha Ashura akishangaa shangaa mithili ya mbuzi alieachwa ugenini..


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog