Search This Blog

Friday 18 November 2022

MZIMU UMERUDI TENA KULIPIZA KISASI - 1

 






IMEANDIKWA NA : ANDREA STEPHANO



*********************************************************************************



Simulizi : Mzimu Umerudi Tena Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Kwanza (1)


 Katika Eneo moja la makazi liitwalo kihesa likiopo ndani ya mkoa wa Iringa, ndani eneo hili kulikuwa na familia moja ijulikanayo kama familia ya bwana patrick ni kijana wa makamo kidogo ni kijana mwenye miaka 32 Bwana patrick alikuwa na wake wawili mke wa kwanza anajulikana kwa jina la Saida huyu ndiyo mke alieanza nae maisha tangu bwana patrick akiwa maskini mpaka leo hii anamiliki magari, majumba, mahoteli na mali zingine kibao, zote hizo kachuma akiwa na mkewe wa kitambo sana ajulikanae kwa jina la Saida!



Ni miaka mitatu sasa imepita tangu bwana patrick awe tajiri sasa amekuwa ni mtu wa kusindikizwa na mitutu kila mahali aendako. Iwe chooni, chumbani yaani mahali popote alipo patrick kuna njema kadhaa zilizovalia suti huku viunoni mwao wakiwa na miguu ya bata

(bastola)



Na leo ni Asubuhi na mapema bwana patrick anaamshwa na kengere ya alam bwana patrick anaamka na kuingia bafuni kwaajili ya kuoga huku kama kawaida yake kukiwa na ulinzi mkali pembeni yake, haraka alioga na kuludi mezani alikuta mkewe saida akiwa amemuandalia chai kwa vitumbua patrick alikunywa chai kisha akaagana na mkewe na kumwambia kuwa alikuwa akielekea katika hotel yake ya PATRICK HOTEL na angeludi saa saba mchana!



Saida hakuwa na pingamizi lolote kwani hiyo ni kawaida! Alimtengeneza tai mumewe kisha akamkisi na kumtakia safari njema!!



Gari moja kali ya kitajiri sana aina ya prado taratibu inaondoshwa pale huku nyuma ikifuatiwa na toyota hilux yenye walinzi wake patrick!



Baada ya msafara huu kuondoka mlinzi wa geti alifunga geti na kurudi kibandani kwake wakati huo saida akiwa sebleni akizisindikiza gari hizo kwa macho kupitia dirishani mpaka zinapoteleaa...!! Taratiibu saida machozi yalianza kumlenga lenga hatimae aliangua kilio ambacho hatujui ni cha nini???

**********************

Tukija huku kwa bwana patrick, ni kwamba baada ya kutoka nyumbani kwake alinyoosha mpaka katika nyumba yake moja maarufu sana ambayo ni maarufu kwa wapangaji matajiri alifika pale na kupaki gari yake nje ya geti huku na msafara wake ukiwa na nyuma kuhakikisha bosi wao anakuwa salama! ' Mmoja wa hawa walinzi wa patrick alishuka garini na kwenda moja kwa moja mpaka mlangoni, akabofya kitufe cha kengere kisha akasimama hapo getini akisubili geti lifunguliwe huku umakini ukichukua nafasi yake!



Dakika tano mbele geti lilifunguliwa huku akitoka mwanadada mmoja makini sana ambae kwa kumtizama tu huenda ukahisi ni jini kwa jinsi alivyobalikiwa kuwa mzuri wa sura! Umbo na shepu kiujumla alikuwa ni mwanadada ambae kwa umri wake siyo chini ya miaka 23-25 Mwanadada huyu baada ya kufungua geti alitoka kwa mwendo wa madaha huku kila umbo likisapoti kila hatua apigayo! Taraatibu bwana patrick alifungua mlango wa gari yake na kushuka chini... Mwanadada huyu ajulikanae kwa jina la Ashula alikwenda kujaa kifuani mwa patrick.......

**********************

" Saida mbona unalia dada yangu?? '

" ha.. Ham...mmm...na... ''

" tafadhari naomba uniambie huenda nikawa msaada dada angu..

" Imanwel naomba uniache sipo sawa kwa sasa hivi ''

" lakini hujaniambia nini tatizo dada ujue unapokuwa huna fulaha hata mimi nitakosa amani niwapo kazini??

" tafadhari nitakwambia niwapo sawa ''

" daah! Sawa dada sasa chai yangu vipi mbona mpaka sasa hivi saa mbili hii??

" Ahaa ok uende pale jikoni utaikuta pamoja na chapati pale juu ya kabati.. ''

" sawa , asante ''



Yalikuwa ni maongezi kati ya mlinzi wa geti la Patrick na Saida mke wa patrick mlinzi huyu aliamua kwenda ndani kumuangalia mke wa patrick kwani leo hajamletea chai tangu bosi wake atoke asubuhi mpaka sasa hivi inaelekea saa mbili asubuhi mke wa bosi wake huyo hajatoka ndani kumletea chai, hivyo patrick aliamua kufuata mwenyewe ndani kwani kashindwa kuvumilia kwa jinsi baridi ilivyojaa tumboni... Lakini kitu kisicho cha kawaida anakutana na kilio sebleni mke wa patrick akiwa kajiinamia mezani analia kilio kisicho cha kawaida huku machozi yakichururuzika kutoka mezani kudondoka chini. Bwana emanuel mlinzi wa geti alipigwa na butwaa baada ya kukutana hali ile! Haraka hisia zake zikamtuma kuwa saida amepatwa na msiba! Alijisogeza mpaka pale na kujaribu kumdadisi lakini majibu aliyoyapata hata hakuridhishwa nayo. Emanuel aliamua kumuacha bosi wake huyo na kufuata maelekezo yake akingia mpaka jikoni. Kweli aliikuta chai japo tayari ilishapoa kwa kukaa mda mrefu kwenye kikombe, hii ni baada ya saida kuiandaa kwaajili ya mlinzi huyo halafu hakuipeleka....



Emanuel aliibeba chai hiyo hivyo hivyo huku ikiwa imepoa kwani hakuwa na jimsi tena akachukua na vitafunio kisha kwa hatua za kivivu akaanza kutoka nje huku akiwa na mawazo mengi mno kichwani kwake kuhusi bosi wake saida kapatwa na nini????? Mara nyini mlinzi huyu wa geti alihisi huenda bosi wake huyo wa kike kapatwa na msiba.. Emanueli alijiwekea asilimia mia kuwa saida kapatwa na msiba!! Je?? Ni kweli saida kapatwa na msiba??

*********************





Bwana Emanuel mlinzi wa geti la tajiri patrick alijongea taratiibu mpaka katika kijibanda chake cha mlinzi wa geti na kuweka mazaga zaga yake chini kisha akaweka mikono yake mashavuni akiwaza ni jambo gani linalomsumbua mke wa bosi wake?? Emmanuel ni mtu wa dini sana na ni mtu mwenye huruma kupita maelezo hivyo kitendo cha Saida kuwa katika majonzi kilimpa mawazo mengi sana mlinzi huyo wa geti ambae yeye alihisi huenda amepatwa na msiba...

***********************

Tukija huku ndani hali ilikuwa ni tete kabisaaa unaambwiwa kilio alichokuwa analia mwanamama huyu unaweza kusema kapatwa na msiba wa mwanae wa pekee!!



Hii hali imeanza kujitokeza humu ndani takribani wiki moja iliyopita, bwana patrick amekuwa ni mwanaume wa ajabu ajabu sana, katika siku za nyuma walikuwa wakisafiri pamoja na mke wake huyu Saida katika gari moja pindi wanapokwenda kutembelea miradi yao mbali mbali.



Lakini hali hii imebadilika gafla patrick kawa mkali kila akirudi kutoka safari mara kadhaa anarudi akiwa amelewa na mkewe kuchezea kipigo kila anapojaribu kumlaki..



Hali hii ilimuumiza sana saida. katika siku za mwanzo alijua huenda ikawa ni hasira za stress za mawazo kwa mumewe. huyo lakini alipojaribu kumchunguza mwenendo alijua wazi kabisa kuna kitu nyuma ya pazia. Siku moja Bwana Patrck aliudi jioni akiwa amelewa chakarii kiasi kwamba hata gari ilikuwa ikimshinda kuendesha kwani alilazimika kumkodi mtu amrudishe nyumbani, hali hii ilimuumiza sana Saida kwani alijua laiti kama mumewe asingemkataa kutembea pamoja yeye ndiye angemuendesha pindi hajiwezi...



Baada ya yule jamaa aliemleta mumewe kupewa chake na kusepa saida alimwendea mumewe wakati huo yupo chumbani anavua suti zake..

" patrick mume wangu??? ''

" nini wewe?? ''

" lakini kwanini umekuwa hivyo?? ''

" Ebu fata yako ''

" lakini.......

" Nimekwambia fata yako we mwanamke mbona hujielewi??? ''

" Patrick huo ujasili umetoa wapi wewe jamani??? ''

" ebu nitokee hapa kwanza hujui tu! Kila neno unalolitamka nahisi kama mdomo wako unatoa funza!! yaani matapishi yananijia mpaka kooni.. ''

" patrick...!!!! ''

" Toookaa!! Na ukiendelea kujibizana na mimi utachezea vitasa sasa hivi oooohoo!!! ''



Kiukweli maneno yale yalikuwa ni kama kaa la moto kati kati ya kidonda kibichi, mapigo ya moyo wa saida yalianza kwenda mbio kiasi kwamba alihisi kama moyo unataka kuchomokea mdomoni. Tumbo lilikuwa likimvuruga kama mtu aliekunywa mafuta ya kondoo. Machozi ya uchungu yalianza kumwagika saida kwa kasi kweli kweli..



Hata hivyo hakutaka kubishana nae kwani alijua nini kitafuata. Alichokifanya ni kuchukua suti za patrick na kuzikunja vizurii kisha akaziweka kwenye begi. Wakati huo patrick alikuwa amekwenda bafuni kuoga. Saida alichokifanya ni kupanda kitandani na kuvuta shuka lake na kulala...



Usiku huo ulikuwa ni usiku wa majonzi kwa saida. Mawazo mengi yalikuwa yakipita kichwani kwake. Mpaka inatimia saa kumi na moja alfajiri alikuwa macho naweza kusema kwa usiku huo saida hakupata hata lepe la usingizi....



Asubuhi ya siku hiyo ndiyo siku hiyo kama unakumbuka katika sehemu ya kwanza ya simulizi hii patrick aliaga kuwa anakwenda kuangalia moja kati ya miladi yake hivyo saida alimwandalia nguo zake kisha akaondoka na baada ya patrick kuondoka tunashuhudia mkewe Saida akimsindikiza kwa macho mpaka anapotele kishaa akaangua kilio kisicho na mfano kilio ambacho mlinzi wa geti bwana Emanuel alihisi huenda ni msiba umempata mwanamama huyo?? Jambo ambalo halikuwa la kweli...

,,

NAAM HUO NDIYO MKASA MZIMA UNAOMLIZA MWANAMAMA SAIDA.

,,

Mawazo mengi sanaana yaliyompata mlinzi wa geti bwana Emanuel yalipelekea kusahau hata kunywa chai hiyo ambayo baada ya kuifuata na kumkuta mwaandaaji akiwa katika hali ya majonzi hata yeye hamu ya chai hakuwa nayo tena kwani alifika kibandani kwake na kuiweka chini kisha akajiinamia na kushika mashavu yake jambo lililopelekea akili kuhama kabisa na kusahau kama alikuwa na chai hapo.. Na baade kuja kushtua chai imeshapoa kama maji...

*******************

" Baby!! ''

" mmmh!! ''

" mimi leo nataka unipeleke mtera ''

" ukafanye nini uko tena?? ''

" aaa! Baby mi nataka kwenda kula samaki jamani.. ''

" khaaa!! Baby nae kwani mjini hapa si zimejaa tu?? ''

" mimi leo nataka kufurahi kuona sehemu zinakovuliwa.. ''

" sawa usiwaze wangu tutaenda kesho.. ''

" babyyy!!! Jamani mi nataka leo kwani kesho hiyo unayosema wewe mimi nasafiri kuelekea nyang'oro mama ni mgonjwa ''

" aahaa! tena ndiyo itakuwa vizuri zaidi tunampitia hapo kisha tunapitiliza.. ''

" sikia baby siku nzuri ni leo kwani leo yupo hospitalini Ipamba na na kesho analudi hivyo ni lazima niwahi na nikashinde kule hivyo sitokuwa na mda tena.....



Ilikuwa ni katika hotel moja maarufu sana ijulikanayo kama PATRICK HOTEL mwanadada ajulikanae kwa jina la Ashura toto la kishua toto la mjini toto lililomchanganya patrck mpaka kufikia kumsau mkewe wa ndoa ndiye aliekuwa akimpanga patrick hotelini hapo.. Baada ya Huyo mwanadada huyo kum'bembeleza kwa mda mrefu sana hatimae Patrick alikubali siku hiyo wakalie starehe katika bwawa la mtera lililopo mpakani kati ya IRINGA Na DODOMA.

*********************

Tukija huku nyumbani sasa!! Ni shiiida aseee... Saida nae aliacha kulia na kujiandaa haraka haraka kisha akachukua ufungungo wa gari yake na kutoka nje.. Kichwani alipania kumfuatilia mumewe kwa siri ili kubaini kisa na mkasa.....



Baada ya kulia kwa mda mreefu sana mpaka macho kuwa mekundu Saida alipata wazo jipya kichwani ambalo yeye kwa upande wake aliamini huenda likawa utatuzi katika ndani ya ndo yake ambayo imeingia dosari na kumsababishia matatizo makubwa sana. Saida hakutaka kulaza damu haraka akainuka na kuingia bafuni na kuoga chap chap, na kurudi ndani, dakika tano zilimtosha mwanamama huyu kujiandaa, akachukua mkoba wake mdogo na kuweka simu yake ndani pamoja na kiasi kidogo cha pesa ambacho aliamini kingemsaidia kwa mchana wa siku hiyo kwani hakuwa na tegemeo la kurudi nyumbani mchana.



Baada ya kujiridhisha na maandalizi hayo taratibu alijongea kabatini na kuchukua funguo za gari yake kisha akatoka mpaka sebleni..

"... Nimesahau nini?? " saida alijiuliza huku akiwa bado kasimama sebleni.

" ...ahaa ok " haraka akarudi ndani kana kwamba kuna kitu kasahau..



Kwa hatua za haraka akajongea mpaka chumbani. Moja kwa moja mpaka kabatini akafungua na kutoa bastola yake na kuikagua kama ina risasi ndani ndani alipojiridhisha akatoka na kufunga mlango na kwenda moja kwa moja mpaka eneo la maegesho ya magari akatoa gari moja makini sana aina ya VX Mayai na kusogea nayo mpaka getini....



" pi..piiiiiiiiiiip!!!!! ''



Sauti kali ya honi ya gari ilipenya vyema kabisa katika ngoma za masikio ya mlinzi wa geti hilo bwana Emanuel jambo lililomtoa katika dimbwi kubwa la mawazo. Haraka akainua kichwa na kuchungulia katika kijidirisha kidogo kilicho katika kijibanda hicho ambacho humwezesha mlinzi huyo kumwona aliyepo getini kabla ya kwenda kufungua...



Mlinzi alishtuka kuona gari ya mke wa bosi wake.. " anakwenda wapi huyu sasa hivi??? '' mlinzi alijiuliza pasipo kupata jibu...http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



" pi.. Piiiiiiiiiiiph!!!! '' honi ililudia tena...

" nakuja nakuja dada angu.. ''

" wahi wahi ''



Mlinzi akatoka mbio mbio ila kabla ya kwenda kufungua alimwendea kwanza mke wa bosi wake huyo...

" samhani dada angu unakwenda wapi kwani??? ''

" Emanuel lini nawe umeanza maswali kama hayo?? ''

" samhani kama nimekukwaza ila naona leo hauko sawa ndiyo maana nikauliza.. ''

" Ebu fungua geti huko!! ''



Saida aliongea kwa hasira kidogo huku akipandisha kioo cha gari. Mlinzi kuona hivyo hakuwa na jipya zaidi ya kufungua geti ili kuepuka longo longo maana huyu mwanamke leo hajatulia kabisaaa.. Taratibu saida akakanyaga mafuta na gari kuanza kuondoka eneo hilo huku emanuel akimsindikiza kwa jicho flani lenye mashaka



Mwendo aliotoka nao saida ulitosha kabisa kumdhibitishia Emanuel kuwa mwanamama huyu hakuwa sawa kabisa kiakili.. Hivyo alianza kumuombea asije akapatwa na ajali maana siyo kwa spidi hiyo. Baada ya kuona saida amepotelea Emanuel alifunga geti lake kisha akarudi kwenye kijibanda chake na kutulia tuli.

************************

Huku mjini mambo yalikuwa yamepamba moto Mwanadada Ashura alikuwa amefanikiwa kumpanga Patrick na tayari walikuwa wamekubaliana kwenda kushinda bwawani mtera siku hiyo. Kwa upande wa Ashura ilikuwa ni fulaha tele kwani hakuwa amewahi kukanyaga bwawani huko tangu azaliwe hivyo leo itakuwa mara yake ya kwanza..



Basi kwa pamoja walitoka hapo PATRICK HOTEL Na kuelekea benk ili patrick akatoe pesa itakayowasaidiakatika safari, kutoka hapo walipo mpaka benk hapakuwa mbali hivyo haikuwapa shida kufika walifanikiwa kufika benk patrick akatoa kiasi cha shilingi milioni mbili za kitanzani kisha akazichimbia mfukoni, wakatoka hapo taratibu wakapitia katika pab moja na patrick kupata moja moto ili kuzimua akili. huku Ashura akipata pepsi bariidi. Baada ya kutosheka wakatoka na kuingia garini na safari kuanza...!! Lakini kabla hawajaenda patrick akakumbuka kitu....

" ebu tupitie sheli nijaze mafuta maana hii barabara haina sheli tukitoka hapa mjini sioni sehemu ya kujaza mafuta.. ''

" sawa fanya ivyo.. ''



Basi papo hapo wakakatiza na kuingia sheli na kukutana na kijana mmoja wa kiarabu lakini ni muongeaji mzuri wa kiswahili..

" habari kijana?? ''

" salama karibu boss ''

" ok ebu nijazie lita 30 hapo ''

" sawa ''

" itakuwa ngapi?? ''

" Elfu Sitini tu boss ''

" Changamka basi ''

" sawa sawa boss ''



Baada ya dakika kadhaa ilikuwa tayari bwana patrick alilipa kisha akapanda ndani ya gari na kumkuta Ashura akiwa anachati na Smartphone yake kubwaaa!!

" tayari?? " Ashura aliuliza....

" Ndiyo ''

" Sawa ''

Basi bila kupoteza mda gari iliondolewa hapo kwa mbwembwe nyingi, huku yule dogo wa kiarabu akimtizama jamaa anavyoondoka kwa mkwara mkali mpaka kijana alicheka peke yake.. Patrick aliingia road na kuikamata vyema barabara kuu ya IRINGA to DODOMA Ikichangia na pombe imeanza kupanda kichwani aaaaaa!!!

************************

Masikini Saida baada ya kutoka nyumbani akilini mwake aliwaza mumewe atakuwa katika nyumba yao moja ya kupangisha ambayo ilikuwa katika ukarabati hata hivyo aliambulia patupu!! Kwani baada ya kuwakuta mafundi walimwambia bosi wao huyo mara ya mwisho kwenda hapo ilikuwa ni juzi na alishawalipa na kuwambia yeye ametingwa hivyo mda wa kwenda hapo mara kwa mara hana hivyo akaamua kuwalipa ujira wao na kuwaahidi kuwa angekuja baada ya siku tatu mda ambao angehisi kazi itakuwa imekamilika. Saida kusikia hivyo alichoka kwani mahali pa kumkuta patrick kwa mda huo hakupajua, Akili ikangukia PATRICK HOTEL Hotel yao maarufu..

".. Ebu nikajaribu kuangalia na kule..''

Saida baada ya kupata wazo hilo aliagana na mafundi hao na kuingia kwenye gari lake na kuondoka...



Saida aliipa gari mafuta kisawa sawa kuhakikisha anamwahi Patrick katika hotel hiyo bila kujua mumewe huyo mda huo alikuwa safarini mda huo. Saida alifika Sehemu ambapo ni kivuko na pia ndiyo kutaniko Kati ya barabara kuu iendayo dodoma na njia za uchochoro.. Saida alilazimika kusimama ili kutizama kushoto na kulia kabla ya kuingia barabara kuu..



Sasa akiwa anatizama kushoto Mara aliona gari ambayo bila Shaka ilikuwa ni ya Patrick. Saida Alishtuka na kushusha kioo ili kuona vizuri. Macho hayakudanganya alichokiona ndicho kilichokuwa gari ilikuwa ni ya mumewe na ilikuwa Moto haijawahi tokea..

" Mungu wangu!!! Patrick anakwenda wapi na spidi hi?? ''

Saida alijiuliza maswali mengi bila kupata majibu, alichokifanya ni kupandisha kioo ili mumewe asimuone. Maana Kama atapita na spidi hiyo itakuwa ngumu kugundua Kama gari hiyo ni ya mkewe...



Sekunde kumi..!! Patrick alipita hapo Kama upepo!! Saida nae hakushangaa alitizama pande zote baada ya kuona hakuna gari nae akajitosa barabara kumfukuzia Patrick........





Sekunde kumi patrick alipita hapo kama upepo!! Saida nae bila kupoteza mda alitizama pande zote baada ya kuhakikisha hakuna gari yoyote nae akajitosa barabarani kumfukuzia patrick.



Saida kumkamata patrick lilikuwa ni jambo gumu sana kwani patrick gari ilikuwa imechanganya kwa mda mrefu na hapo alikuwa yupo spidi 200 sasa mpaka saida aje afikishe spidi hiyo itakuwa ni shughuli kumkatamata jamaa na ikichangia tayari alikuwa amepiga moja moto duuh!! Ebu tusikiliziee.....

************************

" baby! ''

" mmh!! ''

" ujue mi leo ndiyo mara yangu ya kwanza kwenda kuliona bwawa la mtera?? ''

" khaaah!! Mwongo wangu!! ''

" hakika sijawahi kuliona nalisikiaga tu!!

" sasa unakwenda kuliona!! "

" nashukuru sana mpenzi nakupendaa!! ''

" asante nakupenda pia Ashuu!! ''

" kweli patrick??? ''

" na ndiyo maana nafanya yote haya kwaajili yako. ''

" nashukuru sana kusikia hivyo. ''

" Usijali wangu ''



Yalikuwa ni maongezi kati ya Patrick na mchepuko wake Huyo ajulikanae kwa jina la Ashura! Wakati huo gari imeikamata tambarale ya nduli yaani unaambiwa huyu mwheu anatembeza gari utazani yupo katika mashindano ya Magari lakini gafla wakapigwa mkono na trafic

( askari wa usalama barabrani ) kitendo kile kilimchukiza sana patrick kwani aliona anacheleweshwa kwenda kula starehe na mtoto wa kishua ajulikanae kwa jina la Ashura!!



Patrick alianza kupangua gia taratiibu hatimae akasimamisha gari yake kisha akateremka na kuwaendea matrafic hao wakati huo Ashura akabaki garini akiwa anakula burudani nene ya muziki kupitia earphone zilizounganishwa na simu ya bei kaliii aliyohongwa na patrick.



" ndiyo mwendo gani huu??? " trafic alimuuliza patrick huku akiwa kakunja uso.

" mnisamehe wakubwa natakiwa kuwahi dodoma mara moja kuna mgonjwa yupo katika hali mbaya.. " patrick alidanganya hivyo..

" hata kama hili siyo eneo la kutembelea spidi hiyo.. ''

" lakini si nimekwambia nina matatizo??? ''

" unasikia wewe?? Mimi matatizo yako siyajui bali nalinda usalama wa barabara na watumiaji wengine sawa?? Paki pale...!! ''

" sikia kaka....... ''

" Usinizingue kibao kileee kinakwambia pita eneo hili na spidi 50 Wewe iweje uje na 200??? ''



Patrick akaona bila kutumia akili ya ziada atakesha pale hivyo alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kutoa waleti yake, kisha akavuta laki tatu na kuwagaia trafic hao ili kuwazima.

" sikieni kaka zangu najua sheria zote za barabara ila nimetenda kosa hili kutokana tatizo kubwa nililonalo, naomba mpokee hiki kiasi cha pesa kama adhabu yangu.. '' Patrick aliongea hivyo huku akiwakabidhi trafic hao kibunda chenye pesa takribani laki tatu!



Mbele ya pesa hakuna sheria tena trafic walizipokea pesa hizo kisha patrick akaluhusiwa.

" basi tunakutakia safari njema ''

" nanyi kazi njema waheshimiwa ''



Baada ya maagano hayo patrick aliludi haraka garini na kuiwasha wakati huo Ashura anaburudika tu na muziki kupitia earphone zilizoziba mazikio yake.

" mmemalizana?? '' Ashura aliuliza....

" Aaa wana njaa tu hao walikuwa wanataka hela. ''

" sasa hawajakupiga hela ndefu?? ''

" Ya kawaida tu ''



Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Patrick na mchepuko wake huyo Ashura, wakati huo gari inasoma namba tatu tayari imeshaanza kupaa!!!

************************

Maskini saida kumbe alikuwa ameshaachwa kilometa nyiingi mnoo japo patrick kasimamishwa takriban dakika tano lakini mpaka anaondoka hapo saida hakuwa amefika bado. Lakini kwa mda huu hakuwa mbali. Trafic baada ya kupokea mkwanja ule walijisahau na kwenda kukaa kando kabisa na barabara na kuanza kupiga stori. Saida nae gari ilikuwa imekubali kisawa sawa trafic wakiwa hawana hili wala lile walishtukia gari ikipita kama kimbunga cha haiti. Unaambiwa kwa spidi aliyopita nayo ilikuwa ni baraa tupu!! Trafic wenyewe walishindwa cha kufanya wakabaki kutizamana tu, wakati huo gari ya saida ishapotea mda mreefu!!. Kutokana na patric kusimama kwanza na gia zote kupanguliwa hii ilipelekea saida kuwaona kwa mbali kwani yeye hakusimamishwa na trafic. Hata hivyo pia ilikuwa ngumu kumkamata patrick kwani tayari gari ilianza kwenda kwa kasi baada ya gia zote kupangwa kama awali na spidi kuludi pale pale.



Hatimae msafara huu wa mwendo kasi ulifika katika makona ya nyang'oro. Hii sehemu ni hatari sana nadhani kwa wale ambao mmewahi kusafiri kati ya iringa dodoma au kutoka mikoa ya kusini kwenda mikoa ya kaskazini mwa tanzania. mnaijua hii sehemu ni sehemu moja mbaya sana kwani ina kona nyingi na kali hatari pia pia kuna majabali ya mawe pamoja na mabonde ya kufa mtu. Kiujumla hili eneo ni hatari kwani barabara imepita mlimani. Sasa msafara ulikuwa umetinga katika maeneo haya.



Saida alikuwa kaachwa tena kwa mara nyingie, na mara ya mwisho Saida kuiona gari ya patrick ni katika kijiji kimoja kijulikanacho kwa jina la kibaoni hiki ndicho cha mwisho ukitoka hapo unaingia makonani na hakuna tena makazi ya watu hii ni pori kwa pori, kona kwa kona, majabali kwa majabali, mabonde kwa mabonde mpaka unamaliza mlima huu wenye urefu wa kilometa takriban 40. Sasa saida kwa mara ya mwisho kuiona gari ya patrick ni katika kijiji hicho cha kibaoni na baada ya hapo gari hiyo ikapotea katika upeo wa macho ya saida, saida alijua moja kwa moja patrick kashuka bondeni je anakwenda wapi?? Dodoma au??? Saida alijiuliza bila kupata jiabu sahihi, na bila kupoteza mda nae akajitosa makaonani. hakutaka kukata tamaa kabisa alitaka mpaka aone mwisho wa safari ya Patrick.



Saida alizidi kuipa gari mafuta pasipo kujua mbele ni hatari yeye hakujali Hilo mawazo yake yalikuwa kwa Patrick tu. Tayari alishaingi mlimani Sasa alianza kukumbana na Kona za ajabu. Na kila anavyozidi kwenda Kona Kali zinazidi kujipanga mbele. Nae hakutaka kupunguzia mwendo kwa kuhofia huenda akachelewa Sana mpango wake kuingia dosari hivyo aliendelea kwenda hivyo kwa mwendo wa Kasi pasi na kujali Kawa inaweza kumletea madharara mbeleni. Na kibaya zaidi ni kwamba siyo mzoefu wa kuendesha mgari katika barabara yenye Kona Kali kama hii huwezi amini gari ilianza kumsumbua mwanamama huyu alijitahidi Sana gafla akukana na Kona Tatu dabo na Kali baraa!! Ya kwanza alifauru, ya pili alibahatishia, eebwana ee!! Ya tatu ikwa kimbembe kwake kwani gari ilitaka kupitikiza haraka akaiwahi na kuirudisha kwa nguvu Jambo lililopelekea gari kupoteza mwekekeo kabisa, kwani ilirudi kwa Kasi na kuhama saiti na kibaya zaidi ni kona.



Saida akiwa bado kashikwa na bumbuazi Mara ikatokea scania ikiwa na doble tela!! Na kibaya zaidi alikuwa katikati ya saiti ya semi Hilo..



Nae dreva wa lori Hilo alijua kabisa kigari hicho kimepoteza mwelekeo hivyo balaa ni mda wowote!! Dreva wa lori alijaribu kulikwepeshea Lori lake saiti ya pili ili kunusuru wasigongane. Hata hivyo ilikuwa ni kazi bure tu kwani gari hii ya Saida ilikuwa spidi hatari, kabla Lile Lori halijaihama saiti hiyo kishindo kikubwa kiliskika nyuma....



Gari Saida ilikwenda moja kwa moja na kujigonga katika tairi za nyuma za gari hili la mizigo. Gari ya Saida ilirushwa huko na kwenda kujigonga kwenye majabali yaliyomo pembezoni mwa barabara hii kitendo kilichopelekea gari ya Saida kubondeka bondeka siyo kawaida.....



Dreva wa scania alijitahidi sana kumkwepa mwanamama huyu ila tatizo ni kwamba gari yenyewe ni ndefu sana, kwa mbele alifanikiwa kumkwepa ila kutokana na mwendo mkali aliokuwa nao Saida ulipelekea aende kuvaa nyuma kunako matairi jambo lililopelekea gari ya saida kurushwa na kwenda kutua katika majabali ya mawe yaliyopo pembezoni mwa barabara hii. Unaambiwa gari ilibondeka siyo kawaida.....



Yote hayo kondo wa roli hili aliyashuhudia moja kwa moja bila chenga kupitia kioo cha pembeni yaani ( site mirror )

" tumeua!! '' kondakta aliongea kwa wasiwasi huku akimtizama dreva usoni...

" ebu ichungulie imeingia uvunguni??? ''



Yule konda akatoa kichwa na kutizama nyuma...

" oya tusepe msala huu ''

" amekufa??? ''

" jibu ni hilo ''

Yule dreva alichanganyikiwa balaa...

" sasa yupo uvunguni ama?? ''

" hapana katua pembeni.. '?



Huyu dreva kusikia hivyo akaiondoa gari haraka na hawakuthubutu kusimama ili kuona mtu huyo yupo katika hali gani?? Wao walichojua ni kwamba mtu huyo hayupo hai kutokana na jinsi gari ilivyo haribiwa.. Njiani walianza kushauriana kuwa nini? Wafanye?? Ili kuepukana na msala huu? Kwani ni rahisi sana kugundulika pale ilipojigonga gari ya Saida na wakigundulika na police itakuwa habari nyingine tena hakutakuwa na maelewano zaidi ya kuwekwa ndani..!! Hii semi ilikuwa ikitoka mwanza kuelekea songea na ilikuwa imebeba magunia ya dagaa.



Baada ya mashauriano ya mda mrefu kati ya konda na dreva wake walifikia uamuzi wa kuitelekeza gari hiyo kabla ya taarifa za ajali hiyo kusambaa na ikagundulika kuwa nao walichangia. Hivyo basi baada ya vijana hao kufika karibu na Nyang'oro walipaki gari hiyo ya mizigo pembezoni mwa barabara na wao kushuka kisha wakaitelekeza hapo na kukimbia. Yaanii kibarua kwao kikawa kimeota nyasi....!!!!!

************************

Mwanaume Patrick yeye alikuwa ni mzoefu sana wa kuendesha gari na barabara hiyo anaijua mwanzo mwisho hivyo kona hizo kwake ilikuwa ni burudani tuu!! Tayari walishaumaliza mlima hatari wa nyang'oro ambao ni tishio kubwa kwa madreva wote wanaotumia barabara hiyo, patrick na mchepuko wake tiari walishatinga MIGORI Inamaana wakitoka hapo basi ni mtera moja hiyo. Basi walipumzika kidogo pale migori na kupata vinywaji ili kuipa nguvu miili kwaajili ya kujiaanda na safari upya..

" Sasa ngoja nifanye mpango tuoge kabisa au?? '' patrick aliongea.

" sawa fanya hivyo. ''



Patrick kusikia hivyo akachangamka mpaka wakapata bafu ambalo ni spesho kwa wasafiri hasa abiria. Baada ya dakika kadhaa walikuwa wameshaoga tayari walitoka na patrick akalipia na taratibu wakaanza kuondoka kuelekea kwenye gari, lakini patrick akaona ngoja kwanza....

" Ashuu tangulia kwenye gari nitakukuta huko ''

" we unaenda wapi tena?? ?? "

" nakuja sasa hivi ''

" sawa ''

Ashura hakuwa na kipingamizi alitangulia zake kwenye gari na kama kawaida yake akaendelea kuburudika na mziki mnene.



Huku nyuma patrick akaenda moja kwa moja mpaka kwenye kiji pub moja hivi. Nahisi aliona kichwa kinaanza kuwa kizito!! Bila kupoteza mda akaagiza CASTLE Mbili na kuanza kuzibwia kwa fujo kweli kweli, wahudumu waliokuwa mule ndani walianza kumchanganya jamaa hasa ikichangia na uvaaji wa wahudumu wa baa duu! Patrick alijiapiza kuwa ipo siku atakakuja kuwazoa wotee!! Aliwaza hivyo huku akiinyonya chupa ya mwisho mfululizo mpaka inaisha! Hakika mpaka wahudumu walishangaa, kwa kuwa patrick alikuwa na mtu anae msubili garini kule hakuwa na mda wa kupoteza hapo zaidi ya kulipa pesa ya bia alizokunywa na kuanza kuondoka...

" kaka mbona hujachukua chenchi?? '' mhudumu aliuliza baada ya kuona patrick katoa hela ya chenchi ila anaanza kuondoka pasipo kuichukua.

" iyo baki nayo tu!! '' patrick aliongea huku akitokomea nje!



Alikwenda mpaka kwenye gari ambapo alimkuta Ashura akiwa kakaa kihasara hasara hukua akiwa kalala fofofo!! Patrick hakushughulika nae alimwacha aendelee kuuchapa usingizi hapo, yeye akavuta mkanda wa gari na kuuvaa akachukua funguo na kuichomeka kisha akawasha gari. Ila kabla hajaiondoa akakumbuka kitu. Haraka akachukua simu yake na kuanza kuitafuta namba ya moja kati ya wafanya kazi wake wa ujenzi maana alikumbuka kuna alimpigia ila hakupokea. Aliiona kisha akapiga na sekunde chache simu ilianza kuita.......

" ngrrr!!! Ngrrr!! Ngrr.... Naam boss!! ''

" kuna mda niliona ukinitafuta vipi?? Nilikuwa nimetingwa kidogo ''

" mke wako mmeonana?? ''

" wapi? Saa ngapi?? ''

" mida kama ya saa mbili hivi alikuwa anakuulizia sana mpaka hapa amepita '' Patrick kusikia hivyo roho ikapiga paah!!

" sasa ameelekea wapi?? ''

" alisema atakwenda kukungalia PATRICK HOTEL Nami nikaona ngoja nikushtue ili kama haupo hapo uende mkutane. ''

" ahaaa asante kwa taarifa ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" sawa boss kazi njema ''

" kazi njema pia ''

" asante ''



Simu zikakatwa kisha mda huo huo patrick akaitafuta namba ya mlinzi wake wa geti bwana Emmanuel, simu iliita mara mbili ikapokelewa.

" boss! ''

" naam kaka upo hapo nyumbani???''

" ndiyo boss wangu ''

" shemeji yako yupo karibu hapo?? ''

" Hapana boss kaondoka tangu mda ule ule ''

" Alaaaa!! Hajakwambia wapi anaelekea?? ''

" hapana boss ila alipokuwa anatoka alionekana kuwa na hasira sana ''

" duuuh!! Sawa atakaporudi nijulishe ''

" hakuna shaka ''



Simu zikakatwa huku patrick akiwa na maswali lukuki kichwani kwake. " huyu mwehu kaenda wapi??? " patrick alijiuliza huku akianza kuitafuta namba ya Saida Haikuwa kazi ngumu aliipata kisha upesi akaitwanga.....

.... NAMBA UNAYOIPIGIA HAIPATIKANI KWA SASA TADHARI JARIBU TENA BAADAE......

Hilo ndiyo jibu alilokutana nalo bwana Patrick alipojaribu kumpigia mkewe Saida..



Patrick akavuta pumzi ndefu na kuishusha huku mapigo ya moyo yakianza kumwendea Kasi baraa! " Daaah!! Kama atabuni akili ya kwenda sumbawanga nimekwisha mie kwani mashart yote anayo yeye mwenyewe.. '' Patrick aliwaza hivyo huku akipiga hesabu ya haraka afanye Nini??? " Hapana ngoja nimwahi huyu mwanamke atakuwa kaondoka kihasira hasira na anakwenda sumbawanga kuharibu kila kitu na jina la Patrick linakwenda kufa!!! Basi bila kupoteza mda Patrick aligeuza gari kwa Kasi ya ajabu kuanza kurudi walikotoka. Lengo lake ni kumwahi Saida iwapo amepanga kwenda kuharibu Siri nyeti ambayo wanaijua wao wenyewe..

*****************************

Tukija huku kwa mwana mama Saida ni kwamba baada ya kupata ajali ile ya kutisha alizima kabisaa!! Haikupita mda mreefu tangu ile scania aliyokumbana nayo kuondoka. Kuna gari ndogo ambayo ndani alikwepo mmama mmoja wa makamo kidogo mwana mama huyu ni mfanya biashara hivyo alikuwa akitokea dodoma kurudi kwao mbeya.



Sasa baada ya kufika eneo Hilo la ajari aliona gari ndogo ikiwa imeharibiwa siyo kawaida, " hee yupo hai kweli??? '' alijiiuliza mwanamke huyo huku akito simu yake ya mfukoni. Kisha akaanza kutafuta namba za simu za police kituo Cha Ismani , haikuwa kazi ngumu alifanikiwa kuiona na bila kupoteza akapiga. Simu ilita Mara mbili ikapokelewa...



" Unaongea na mkuu wa police kituo Cha Ismani karibu..."

" Naitwa Anjerina mwasy natokea dodoma ila njiani nimekutana na Ajali,

" Nini?? "

" Ajali mbaya Sana ''

" Iyo Ajali imehusisha gari gani ''

" Ni vx "

" Sawa tunakuja.. ''



Basi simu zilikatwa huku mwanamama huyu akiteremka kutoka katika gari yake ili aweze kukagua vizuri. Baada ya kushuka alikutana na michirizi mingi ya damu ikitokea ya gari hiyo kwenda chini. Mwanamama huyo aliendelea kukagua kagua Mara akaiona sura ya kike ndani..

" Toobaaa!! Ni mwanamke?? Halafu keshakufa Yule '' alikuwa akiongea peke yake mwanamama huyo huku machozi yakimtoka kwa Kasi baada kugundua aliepatwa na Ajali hiyo ni mwanamke..



Dakika kumi na tano mbele ving'ora vya magari ya police pamoja na gari ya wagonjwa (AMBULANCE) kutoka kutoka katika kituo Cha afya Ismani viliskika vikikaribia eneo Hilo mwanamama huyo alikwenda kupanda katika gari yake na kukaa kimyaa!!. Mara gari ya kwanza ya polisi iliwasili hapo huku ikiwa spidi baraa ikifuatiwa na AMBULANCE ya wagonjwa kutoka kituo Cha afya Ismani. Baada ya dreva alikuwa akiiedesha gari hii ya police iliyokuwa mbele kuona ameshafika katika eneo la ajari aliwasha taa za tahadhari kuwaarifu wakioka nyuma kuwa wameshafika...



Bila kupoteza mda police walisimamisha magari yao na kuweka vibao vya tahadhari kila upande wakati huo wengine wakiwa wanashughulika kutoa mwili wa Saida ambao ulikuwa katika hali mbaya!...



Dakika tano ziliwatosha kuhakikisha mwasilika huyu wa Ajali ameshatolewa katika gari yake..

' ebwana eeee!! Huangalii Mara mbili kwa jinsi Saida alivyokuwa amechakaa! Yaani ilikuwa ni baraa na haijabainika Kama ni mzima au amekufa, police walisaidiana kum'beba na kumpakia katika gari ya wagonjwa Kisha gari hiyo ikawashwa tayari kwa kuondoka...

" Mfikishe Ipamba haraka!! ''

" Sawa mkuu ''



Mkuu wa polisi alimwagiza dreva wa AMBULANCE hiyo kumfikisha mgonjwa huyo katika hospital ya Ipamba kwani mgonjwa yupo katika hali mbaya kiasi kwamba hata polisi wameshindwa kutambua Kama ni mzima au kafa?? Dreva alikubaliana na mkuu wa polisi na bila kupoteza mda gari ikaondolewa kwa Kasi hapo Kama upepo........



Saida alikuwa katika hali mbaya sana kiasi kwamba hata polisi walishindwa kubaini kama kafa au yu hai?? Hivyo walichoamua ni kwamba majeruhi huyu awahishwe katika hosptali ya ipamba, basi yule dreva wa gari ya Wagonjwa iliyokodiwa kutoka katika kituo cha afya cha Ismani aliambiwa amwahishe ipamba mara moja, bila kupoteza mda AMBULANCE Iliondolewa kwa kasi kama upepo eneo hilo.



Polisi nao walianza kuchunguza eneo la ajali ili kubaini hii ajali imesababishwa na nini?? Hata hivyo ilikuwa ngumu kidogo kwani hakuna brek yoyote iliyopigwa kabla ya gari hiyo kupata ajali..

" hii ajali tumeshindwa kugundua chanzo yaani ili mradi tu tunaona gari iko msingini ila chanzo tumeshindwa kubaini '' kamanda wa polisi kituo cha Ismani aliongea,

" hapana mkuu hii gari inaonekana ilikuwa inashuka bondeni sasa cha msingi tunatakiwa kuwahi ndolela kwenye mzani ili tukapate orodha ya magari yote yaliyopita hapo kuanzia saa tatu zilizopita huenda tukapata infomartion yoyote '' aliongea kijana mmoja wa kikosi hicho cha polisi wazo lililokubalika kwa asilimia mia na kikosi kizima.



Kwa kuwa mtu alikuwa kashatolewa ndani ya gari iliyokuwa imepata ajali polisi hawa hawakushughulika kuanza kuliinua gari hilo kwa mda huo, wao walichokihitaji kwa mda huo ni chanzo cha gari hiyo kupata ajali. Basi askari wote walijazana ndani ya difenda zao na safari kuanza huku wakiwa wapo kasi baraa ili kujaribu kuokoa mda.



Baada ya kutembea takribani mda wa dakika ishirini na sekunde kadhaa waliweza kufika katika eneo la nyang'oro ambapo sasa ndipo ilipotelekezwa scania hiyo.

" oya!! oya!! Ebu simamisha kwanza gari '' aliongea askari mmoja huku akiwa tayari kwa kuruka. Dreva alisimamisha kisha askari wote kushuka na kulizingira gari hili huku wakiwa makini kulikagua kila kona!



" wanangu gari iliyomsabishia huyu mama ajali hii hapa '' aliongea polisi mmoja na polisi Wote wakakusanyikia mahali alipokuwa kasimama polisi huyo.

************************

Patrick tayari alishaukamata mlima wa nyang'oro wenye kona kali baraa lakini hakuwa akijali hilo mwanaume alikuwa akilala nayo baraa! Ashura yeye bwana alikuwa akiuchapa usingizi pasipokujua kuwa safari yao imeingia dosari, sasa kibaya zaidi ni kwamba hakuwa amefunga mkanda na gari iko moto siyo mchezo kitendo kilichopelekea kujigonga kwenye vioo afikapo konani. Hali ilianza kuwa tete kwani kila dakika walizi kuingia kwenye kona kali kiasi kwamba mzee mzima patrick akilala nayo Ashura huhama mpaka siti na kwenda kumlalia jamaa! Na akiigeuzia upande wa pili Ashura huhama kwa mara nyingine na kwenda kujigonga kwenye vioo jambo lililopelekea kuzinduka usingizini. Alikutana na kivumbi cha mwaka halafu hakujua kama wapo wapi??

" patrick mbona mwendo mkali ivyo?? Kwani bado mbali sana?? ''

" kuna dharura imetokea mjini hivyo nahitajika mara moja '' patrick alijibu hivyo huku akibadili gia na gari kuzidi kwenda kwa kasi ya ajabu, Ashura alibaki mdomo wazi asijue aongee nini? Na gari iko mafuta kweli. Ashura alichokifanya ni kuvuta mkanda wa siti yake na kuuvaa kwa usalama wake maana si kwa mwendo huu ni shiida..

************************

Mdau ukisikia neno AMBULACE Ujue ni muunganiko wa vitu viwili hatari sanaa! Kwanza madreva wa gari hizi wanakuwaga ni shiida halafu na gari zenyewe zinakuwaga siyo za mchezo mchezo. Sasa AMBULACE Ya kituo cha afya Ismani ni Rand rover zile za kijapan unaambiwa ni shiida aiseee!! Ni ndani ya dakika 35 Tayari gari hii ya wagonjwa ilikuwa imetinga katika hospital moja maarufu sana hapa mkoani iringa ali maarufu kama " IPAMBA '' madaktari na manesi baada ya kusikia king'ora nje ya hospital wakajua moja kwa moja kuna mtu yupo katika hali mbaya ya kukumbwa na mauti, hivyo kila mhudumu aliacha kile alikuwa anakifanya kwa mda huo na kukimbili nje kuona kupo vipi?? Kitanda cha matairi kilitolewa na kusukumwa mpaka karibu na gari hiyo. Saida alitolewa! Aisee unaambiwa kwa hali aliyokuwa nayo madaktari walianza kukataa tamaa.



" Sasa mnatuletea mtu keshakufa wa kazi gani??? '' daktari mmoja alimuuliza yule dreva wa AMBULACE Iliyomleta Saida.

" Samahani daktari mimi nimeagizwa na mkuu wa kituo cha polisi Ismani nimlete huyo mtu '' dreva nae alijitetea.

" Ebu mpelekeni chumba cha upasuaji haraka sana '' daktari huyo aliamuru hivyo baada ya kujua kuwa mtu huyo yupo chini ya serikal,



Saida alipelekwa moja kwa moja katika chumba cha upasuaji huku pilika pilika zikianza, kitu cha kwanza ilikuwa ni kukagua mapigo ya moyo kama yanasikika au?? Daktari mmoja nguli sana alikuja na kifaa chake cha kusikilizia mapigo ya moyo ili aweze kubaini iwapo mtu huyo ni mzimaa?? Au apelekwe mochwari?! Taratibu akaweka kifaa chake kifuani mwa Saida upande wa kushoto kisha akaanza kusikiliza kwa umakini daktari huyo alisikilizia zaidi ya dakika tano pasipo kutoa majibu yoyote hali iliyozua wasi wasi mkubwa kwa baadhi ya mdaktari waliokuwa hapo.

************************

Huku nyang'oro tayari polisi walishalipata gari ambalo wao wanamini kuwa ndiyo lilimsababishia saida ajali ile mbaya na ya kutisha! Basi msako mkali wa kuwasaka dreva na konda wake waje kujibia na kutoa maelezo jinsi ajali hiyo ilivyotokea, msako ulikuwa ni mkali saana, unaambiwa ilikuwa ni nyumba kwa nyumba! Chumba kwa chumba! Kitanda kwa kitanda! Lakini msako huo haukuwa na maana yoyote wala faida yoyote kwani waendeshaji wa gari hilo walishatembea kitambo sana. Walishalitambua hilo na wakayeya kabla ishu haijabuma....



Polisi walikuwa wameweka msako maki sana wakijua kuwa waendeshaji wa gari hilo huenda wapo katika migahawa ya hapo nyang'oro hivyo msako mkali uliendele huku gari hilo likiwa chini ya ulinzi mkali, Baada ya msako wa mda mrefu na bila mafanikio waliamua kurudi ilipo scania hiyo ili kukaa pamoja kujua nini wafanye???

" nani ana wazo?? '' mkuu wao aliuliza.

" hapa kamanda nadhani tupekuea gari huenda tukapata hata docment zozote ambazo huenda zikawa na picha za dreva huyo. Wazo hilo liliungwa mkono kwa asilimia zote, basi bila kupoteza mda wakaingia ndani ya gari na kuanza kulikagua kila kona kwaanzia chini ya siti na sehemu zote walizohisi huenda wakaona karatasi yoyote lakini waliambulia patupu! Kwani watu hao waliondoka na kila kitu walicha funguo za gari tu! Askari walikata tamaa..



" Oya! Oya! Tusihangaike saana kumbe hii gari imefungwa camera ya CCTV Mbele. Hapa cha msingi ni kumtafuta bosi wa gari hili atupatie laptop iliyounganishwa na camera hii tutapata kuona kila kitu! "

Aliongea polisi mmoja huku akiitizama camera ile iliyofungwa kwa ustadi wa hali ya juu mbele ya kioo. Askari wote walifurahi kuona uchunguzi wao unakwenda kuzaa matunda.

************************

Patrick huku akiwa moto kama ilivyo kawaida yake na safari hii alionekana kuchafukwa siyo kawaida! Kwani mwendo aliokuwa nao ni mara dufu ya ule unaotumika katika mashindano ya magari. Ashura alishindwa kuvumilia kabisa mwendo ule, tumbo lilianza kuvuruga vibaya mnoo na hatimae alianza kutapika hovyo... Gafla bin vuuuh!! Wanafika katika eneo alipopatia ajali Saida..!! Patrick alipunguza mwendo aone ni nini tena?? Sasa kutizama vizuri haaaaaa!!!!!



Gafla!! Bin vuuuh! Patrick anafika katika eneo ambalo saida alipatia ajali, taratibu patrick alianza kupunguza mwendo ili kuona ni nini kimetokea hapo?? Sasa kutuzama vizuri haaaaaa!!



Patrick hakuamini macho yake alihisi huenda yupo katika ndoto moja ya kutisha saana! Siyo kwa vile saida kapata ajali au kafa au nini?? Kilichomuuma patrick kwa mda huo ni gari hiyo aliyoinunua kwa bei ghari halafu cha kushangaza hata mwezi haijamaliza Saida kiasi kwamba hata kutengeneza sidhani kama itawezekana!! Patrick alijawa na hasira ya gafla gafla na moyo kuanza kumwendea kasi huku akihisi kama moyo ukitaka kusimama! Pumzi zilianza kukata kata jambo lililopelekea patrick kuanza kupumua kwa nguvu huku pumzi zake zikitoa vijimlio flani hivi..



Wakati yote hayo yakitendeka Ashura mtoto wa kishua toto lililomzuzua kijana patrick. yeye alikuwa kaduwaa tu! Asijue afanya nini???

Patrick alivua mkanda wake kisha akateremka garini na kusogea mpaka sehemu gari hiyo ilipo.. Kisha akaitizama kwa mda wa dakika tatu huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga lenga....



" Weweee!! Saidaaa!! Upo wapi?? We malaya umeua gari yangu!! Ulikuwa unakwenda wapi we mwanamke??? Nauliza upo wapi???? ''



Patrick alianza kupayuka peke yake kama mwenda wazimu mwanaume gari imemuuma kweli kweli,, baada ya kuona hakuna chochote moja kwa moja akatambua kuwa Saida katolewa hapo. Nae akarudi mpaka gari na kuwasha na kuingiza gia kisha huyoo akachomoka hapo kama mzimu!!

************************

Uamuzi ambao polisi walikuwa wameafiki mpaka hapo ilikuwa ni kumtafuta bosi wa roli hili la mizigo ili waweze kupatiwa laptop iliyounganishwa na camera hii ndogo iliyofungwa mbele ya kioo ambayo kazi yake ni kurekodi safari nzima. Polisi waliamini ya kwamba uchunguzi wao unakwenda kukamilika na huenda ikawa rahisi hata kumkamata dreva wa roli hilo kwani ni lazima bosi wake akawa na pasport za dreva huyo hivyo ni lazima atawapatia.....

" kijana wazo lako zuri tunatakiwa kulifanyika kazi haraka iwezekanavyo.. ''

" Asante mkuu ''

Yalikuwa ni maongezi kati ya mkuu wa kituo cha polisi pamoja na mmoja kati ya vijana wake. Basi mkuu huyo akatoa simu yake kubwa ya mkonga kisha akaipiga na kuiweka sikioni.. Hatimae ilianza kuita na baada ya sekunde kadhaa ilipokelewa...

" haloo mkuu ''

" wapi sajent?? ''

" tupo mtera bwawani ''

" mnafanya nini huko?? ''

" tulipata simu ya dharura kuwa kuna uvuvi haramu umefanyika.''

" vipi mmewatia mbaroni wahusika??

" ndiyo tupo nao hapa ''

" kazi nzuri vijana wangu basi hakikisheni mnawaleta huku pamoja na samaki hao. ''

" sawa sawa ''

" ni tenga ngapi?? ''

" ni tenga thelathini mkuu ''

" duuuh!! Waleteni haraka sana ''

" nimekupata mkuu ''



Simu zikakatwa huku mkuu huyu akiwageukia vijana wake hao alionao hapo.

" Hili ni tatizo kubwa vijana wengi wapo mtera je? tufanyaje?? '' mkuu huyu wa polisi aliuliza huku akitafakari na kusubili mchango kutoka kwa vijana wake. Kijana yule yule akapata wazo tena!!



" mkuu mi naona tujigawe tu sisi wenyewe na inatakiwa wanaokwenda kumuona bosi huyo wasiwe wengi sana mi nafikiri wawili tu! Wanatosha, halafu hapa kwenye gari hata wakibaki wanne itakuwa powa, ili tuliobaki tuwahi eneo la ajari tukangalie utaratibu wa kuiinua gari ile ili ivutwe iende kituoni.''



Yaani unaambiwa mkuu mwenyewe alibaki akikuna kichwa kwa jinsi kijana wake alivyoongea point!.

" wazo zuri sana kijana wangu sasa bila kupoteza mda tugawane hapa chapchap! Dick wewe utalinda gari hapa ukiwa na wenzio watatu, Johnson pamoja na wenzio nende kule ilikotokea ajali na hakikisheni hamuitoi pale mpaka tutakaporudi ama kuwapigia simu. Tumeelewana?? ''

" ndiyo mkuu ''

" Basi charles utaondoka nami mpaka kituoni ili tukajiandae kwaajili ya safari ya kuelekea songea ambako inasadikika bosi wa semi hii anapatikana! ''

" tumekupata vizuri kabisa mkuu ''

" sawa tutawanyike ''



Basi kama kawaida ya jeshi au polisi wao ni watu wa chap chap!! Hivyo fasta wale ambao walipangiwa kurudi mahali gari la saida walipanda gari na kuwasha king'ora kisha haooo!!!!



Mkuu wa kituo pamoja na askari mmoja anaejulikana kwa jina la charles wao walikodi boda boda kwaajili ya kuwahi kituoni ili wakaanze kujiandaa na safari ya kuelekea songea!



Dickson au Dick. Akiwa pamoja na wenzake watatu wao walipangiwa kulinda scania hii isije kuondoka hapa mpaka ajulikane mwenye nayo pamoja na dreva wake na pia wajue chanzo kizima cha ajali ile, basi vijana hawa walianza kulizunguka zunguka gari hili kuimarisha ulinzi.

************************

" docta tupe majibu ''

" inaonesha ameshafariki huyu ''

" nini?? ''

" nimesikiliza kwa makini sana ila sijasikia mapigo ya moyo ''

" jamani mama wa watu!! ''

" Angalieni utaratibu wa kumwingiza mochwali ''

" sawa docta ''



Yalikuwa ni mazungumzo ya madaktari katika wodi aliyokuwa amelazwa Saida. Vipimo vya daktari huyu bingwa ambae ndiyo tegemezi katika hospital hii vinasema Saida hana uhai tena!!,, Basi hakukuwa na jinsi tena mwili wa Saida ulianza kuandaliwa kwaajili ya kuingizwa mochwali,, kitanda cha matairi kinachotumika kutembezea wagonjwa kilianza kutoka taratiibu katika wodi aliyokuwemo Saida. huku Juu kikiwa na mwili uliofunikwa shuka jeupee! Hakuwa mwingine bali alikuwa ni mwanamama Saida. sasa alikuwa akitolewa wodi ya wagonjwa kupelekwa mochwali.



Kwa upande wa pili nje ya Hospital hii kubwa kuna gari moja kali sana ya kifahari ilipaki mbele ya geti la hospital hii, mlango ulifunguliwa akashukaa mwanaume ambae umri wake ni mtu wa makamo kidogo yaani siyo mzee na kwenye ujana ameshatoka, mtu huyu alikuwa gmepiga suti ya bei mbaya, kiatu cha pesa, pia machoni alikuwa amevalia miwani ya tin-ted, mwanaume huyu alishuka garini kisha akavuta kijibegi chake kidogo na kukitia begani akafunga mlango wa upande wake kisha akazunguka upande wa pili na kufungua mlango ambapo alitoka mwanamama ambae umri wake siyo chini na wala siyo zaidi ya miaka 30. Baasi taraatiiibu na kwa hatua za mikogo walianza kutembea kulisogelea geti kuu la kuingilia ndani mwa hospitali hii kubwa ijulikanayo kwa jina la

" IPAMBA HOSPITAL'' Baada ya kufika getini walikutana na mlinzi...



" Za sasa hivi?? ''

" njema habari nyinyi?? ''

" njema kabisa ''

" sawa karibu ''

" Asante je?? Naweza kuonana na madaktari wa hii hospital??? '' yule mwanaume alimuuliza mlinzi wa geti huku akiwa kamkazia macho.

" mmmh!! Hapana mpaka wapewe taarifa na kuwaruhusu wenyewe ''

" usigope kijana ukazani sisi ni majabazi ama vibaka?! ''

" onesheni vitambulisho vyenu vya kazi,''

Yule mwanaume alíngiza mkono mfukoni na kutoa kitambulisho chake cha kazi akamkabidhi mlinzi huyo ambae nae alianza kukipitia taratibu,,

" kumbe nawe ni daktari kaka?? '' yule mlinzi aliuliza baada ya kukuta kitambulisho ni cha udaktari.

" ndiyo ''

Basi hakukuwa na pingamizi tena watu hawa wakaruhusiwa moja kwa moja kuzama ndani...!!

***********************

Hapa sasa tunakwenda kukutana na mabosi inabidi tuvae suti katika missio hiii,'' alikuwa ni mkuu wa kituo akimpa ushauri moja kati ya vijana wao..

" sawa mkuu nimekuelewa ''

" basi usikawie ndani twende ''

" sawa sawa ''

Basi waliachana pale kisha kila mtu aliingia chumbani kwake na kuanza kubadili nguo chap chap! Baada ya dakika kadhaa wote walitoka wakiwa wamevaa vizuri baraa kiasi kwamba hata ukikutana nao barabarani huwezi kutambua kama ni polisi.

" Aaa! Charles upo smart?? ''

" kawaida bosi we ndiyo upo juu ''

" ahahaha ebu twende tuwahh usafiri,,

Basi wote kwa pamoja wakatoka kwenda kupata usafiri barabarani, na kutoka hapo kituoni mpaka barabarani siyo mbali hivyo basi haikuwa kazi kwa polisi hawa kufika barabarani...



Kwa bahati nzuri sehemu waliyopanga kwenda kupandia walikuta trafic wapo pale wakiendelea kuimarisha ulinzi pale. Hakukuwa na maongezi marefu ni kwamba baada ya salamu na maelezo machache trafic aliwaelewa, na kuwaihidi kwamba angewasimamishia basi la SUPER FEO Ambalo lingewatumbukiza moja kwa moja mpaka kwenye mji wa wangoni yaani SONGEA! mkuu wa kituo alifulahi mnoo kwani wao walipanga kwamba wangepanda coastel mpaka Iringa mjini ndipo wadake mabasi ya songea,, punde si punde SUPER FEO Hiyoo! Haraka trafic akaipiga mkono basi likasimama kisha yule trafic akaongea na dreva wa basi hilo kisha wale polisi wakapanda na taraatiiibu ngoma ikaanza kuondoka..........



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Punde si punde basi la Kampuni ya SUPER FEO Hiloo! Haraka trafic akalipiga mkono, basi likasimama hapo na haraka trafic akaenda kuongea na dreva, kisha wale polisi wakaingia ndani ya basi hilo na taraatibu ngoma ikaanza kuondoka...



Njiani wale polisi walianza kujadiliana jinsi ya kumpata tajiri wa roli hilo la mizigo..

" Hapa itabidi tukifika songea tumpigie simu au??? '' mkuu wa kituo alimuuliza kijana wake mmoja alie nae hapo aitwae charles.

" hapana tukimpigia simu tutaharibu kwani huenda akatafuta njia ya kuukwepa msala huu. '' charles alikuja na wazo hilo.

" halafu kweli wazo zuri sasa tufanyaje?? ''

" ebu ngoja tufike kwanza songea tutajua nini cha kufanya. ''

" sawa ''



Yalikuwa ni majadiliano kati ya mkuu wa kituo cha polisi na kijana charles moja kati ya vijana hatari sana katika kituo cha polisi isiman. Wakati huo wakiwa mkungugu tayari sasa wanaanza kuitafuta iringa mjini.

************************

Tukija kwa mzee mzima patrick huyu bwana alikuwa amepagawa haswaa unaambiwa mpaka macho yalikuwa mekundu ikichangia na pombe! We acha tu! Kwani mbona hata ashura mwenyewe alitamani kushuka hata polini kwa maana mwendo aliokuwa nao mwanaume huyu ulikuwa wa mauaji kabisa kwani mwendo ulikuwa mkali, halafu hajali saiti yaani akifika konani ni mwendo wa kuhama saiti tuu! Tena mara kadhaa alikuwa akinusulika kupitiliza konani sema ujuzi wake wa mda mrefu wa kuendesha magari ndiyo uliokuwa ukimsaidia. Baada ya kutembea takriban kilomita ishirini kutoka katika ajali ile na kwa sasa alikuwa ameshaziramba kona zote sasa imebaki kona moja kali ambayo ukiimaliza iyo unaingia katika kijiji cha kwanza kiitwacho kibaoni. Mzee mzima patrick alikuwa ameikaribia kona hiyo sasa gafla kikasikika kingo'ora cha gari polisi ya polisi mbele. Patrick hakujali hilo sijui tuseme hajasikia au nini??

" We Patrick kuna king'ora mbele '' Ashura aliongea huku akimtizama patrick kwa macho ya wasiwasi.

" tulia wewe ao wasenge tuu wanaume ni sisi ''

" We patrick wewee!!! ''

" We mwanamke nini ebu funga mdomo wako bwana ''



Yaani ile patrick anamalizia kumjibu Ashura na kabla Ashura hajibu ilitokea difenda ya polisi ikiwa moto baraaa! Na king'ora juuu!!! Halafu kitu imepita kati kati ya barabara na kibaya zaidi wanakunania konani... heeee!!!!

" patrick...!!!! '' Ashura aliita kwa sauti ya juu! Iliyoambatana na uoga ndani yake huku sauti hiyo ikicha mwangi ndani ya gari hii kwani walifunga madrisha yote kwaajili ya kuepuka upepo mkali kuingia kwaana gari ilikuwa mwendo sana.



Kiukweli ni ajali moja mbaya sana inakwenda kutokea maana polisi wapo spidi na hawana wasi wasi wowote kwani wamewasha king'ora kinachoashiria wana dharura hivyo wanatakiwa kukwepwa naamanisha gari yoyote ambayo dreva atasikia king'ora hicho ni lazima akwepe na kusimama kando kwanza ili msafara huo upite. Sasa hapa wamekutana na kichaa! Hahaha!! Ebu tusikilizieee..........



Dreva aliekuwa akiendesha gari ya polisi aligundua kuwa huyu mtu anaekuja na gari mbele yao hayuko sawa kiakili na akileta uzembe wanakwenda kupata ajali moja mbaya na jinsi gari ilivyo mwendo ikichangia na eneo lenyewe ni baya kinoma hivyo hakuna atakaepona! Wakati huo zimebakia meta/hatua kama nne hivi wakutane!! Aaa! Dreva wa difenda ya polisi alikunja usukani kwa nguvu na kuiyumbishia gari yao kushoto aisee kwa jinsi difenta hii ilivyokuwa moto ilikatiza kwa spidi barabara nusura ikagonge machuma ya pembezoni mwa daraja hili. Hata hivyo dreva huyu wa gari ya poli aliiwahi na kuirudisha lakini tayari ilishayafiki machuma hayo kitendo kilichopelekea gari hiyo kujiburuza kiubavu katika machuma hayo baada ya dreva huyo kufanikiwa kuikunja,, pale pale baada ya gari kukaa barabarani Johnson kiongozi wa msafara aliinuka fasta na bunduki yake kwani alikuwa amekaa nyuma na kikosi chake, haraka akaitizama gari ya Patrick katika darubini ya bunduki yake akaiona ndiyo inaanza kupotelea kona, haraka akalitafta tairi la nyuma kwenye tageti yake akaliona lilee gari inaanza kupolea kona!! Haraka akapiga risasi tatu mfululizo hata hivyo hakuna alichokifanya kwani gari ya patrick ilishapotea kwenye shabaha yake kitambo saanaa!! Cheza na mwendawazimu huyu...!!!



Baada ya misuko suko ya kutaka kupata ajali mbaya ya kutisha kutulia gari ya polisi ilisimama na polisi wote kushuka, John kiongozi wa kikosi hicho kidogo alimpa mkono dreva wao na kumpa hongera nyingii....

" kazi nzuri.!! Kazi nzuri saana mkuu.. ''

"asante kiongozi vipi lakini haujafanikiwa kumtwanga huyu bwege?? ''

" Aaa! Nilimkosa pumbavu zake. ''

" Lakini huyu msenge kataka kutuua ''

" Lakini licha ya kutukimbia hapa lakini lazima tumkamate na lazima kwanza atoe sababu za kukimbia na gari namna hii ikiwa ni eneo la hatari hili? ''

" sasa tutamkamataje?? ''

" huyu ngoja kwanza ''



Aliongea Johnson huku akitoa simu yake na haraka akaingia sehemu ya majina na kuanza kupekua haraka haraka kisha akaipata namba anayoitaka na kupiga.. Simu iliita mara kadhaa na kupokolewa....

" Halow?? ''

" Habari mkuu? ''

" Njema vipi kijana?? ''

" aisee kuna tatizo kidogo ''

" lipi ilo kijana?? ''

" kuna prado moja imetaka kutuua halafu imetukimbia tunaomba muizue hapo getini. ''

" wapi?? Ina rangi?? Ebu tupe plate number zake ''

" Kwa bahati mbaya hatujaweza kunaza plate number zake kutokana na valangati tulilokumbana nalo. ''

" na rangi je?? ''

" nyeupee kabisa ''

" sawa hakuna tatizo haitopita hapa ''

" sawa kazi njema mkuu ''

" poleni pia ''

" asante sana mkuu ''



Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Johnson kiongozi wa msafari wa kikosi hiki kidogo kinachoelekea kuimarisha ulinzi kunako ajali, pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani ambapo walikuwa wakizungumzia kuhusu kumkatama Patrick ambae nusura awasababishie mauti. sasa tatizo hawajamjua hiyo ndiyo shida...



Tukija kwa patrick sasa... Patrick nae hakuwa mtoto na wala hakuwa chizi bali kachizika tu! Na mchepuko wake huyo na pili kachukia gari yake kuharibiwa na mwanamke ambae kwa sasa hivi hataki hata kusikia jina lake.

Sasa wakati zile risasi zinapigwa alizisikia vizuri kabisa na akatambua kuwa huko nyuma polisi wamemkosa na risasi kwa sababu ya kutoheshimu kingora chao na kutaka kuwasababishia ajali,, na alitambua kuwa kule mbele aendako atakamatwa hivyo inatakiwa atumie akili ya kuzaliwa, na mda wote huo Ashura yeye alikuwa kimya kwani alikuwa ameshikwa na bumbuazi siyo la nchi hii..!!



Patrick baada ya kuwaza na kuwazua kwa mda mreefu akapata wazo la kuitelekeza gari hiyo polini kwanza halafu yeye aende na daladala mpaka mjini ili ikifika usiku aje kuichukua, baada ya kupata wazo hilo hakutaka tena kuranda randa barabarani alichokifanya ni kuangalia sehemu ambayo gari inaweza kupita na kuiingiza porini alifanikiwa kuiona njia basi haraka akachepuka na kuiingiza prado hiyo ya kifahari machakani...!!!

************************

HOSPITALINI..!!! Wale wageni baada ya kurusiwa na mlinzi walianza kupiga hatua za taraaatibu kuingia ndani ya hospitali hii ya ipamba. Walikutana na foleni nyiingi sana za watu ambao walikuwa wakisubili matibabu pale. Lakini huduma kwa upande wao zilikuwa zimesimama kidogo kutokana na dharura ya mgonjwa aliepatwa na ajali ambapo madaktari wote walikuwa wamekwenda kujaribu kuokoa uhai wa mwanamama Saida, wale wageni waliendelea kwenda ndani zaidi hatimae wakaifikia wodi ambayo alikuwa amelazwa saida!! Wanakutana na msururu mkubwa wa madaktari na manesi wakitoka mle wodini huku nyuma kikifuata kitanda cha kusukuma huku juu akiwemo mtu aliefunikwa shuka jeupee!!

" Babaaa babaa!! '' nesi mmoja baada ya kuwaona wageni hao alipayuka kuita babaa!! babaa!! Huku akiwakimbia kana kwamba ni wazazi wake...

" Huyu vipi??? '' yule mwanaume baadala ya kumhag mwanae yeye aliuliza kuhusu maiti ile.

" amekufa baba ''

" alikuwa anasumbuliwa na nini?? ''

" Alipatwa na ajali huko ismani ''

" lini??? ''

" leo kaletwa hapa siyo mda ''

" ameumia sana?? ''

" Amekatwa katwa sana na vioo ''

" unajua tunavyozungumzia kuumia tunaanzia kichwani na majeraha makubwa makubwa na sehemu mbaya mbaya je?? Ni sehemu mbaya ipi aliyoumia mpaka kumpelekea mauti huyu mtu?? ''



Mwanaume huyo aliuliza huku akikisogelea kitanda hicho na kumfunua majeruhi huyu akaanza kumkagua kwa makini huku akishika sehemu hatari katika mwili wa binadam ambazo mtu akiumia ni rahisi sana kufariki, alianzia kichwani akashuka maeneo ya mbavu mpaka tumboni huku akiwa makini kweli kweli kuona kama moja ya sehemu hizo ina hitilafu.





Yule mwanaume ambae hatujajua kama ni daktari ama vipi? Alikuwa akimkagua Saida sehemu hatari katika mwili wa binadam ambazo akimuia ni rahisi sana kufariki, alianzia kichani akaja mbavuni hatimae tumboni na alikuwa makini sana kubaini iwapo moja kati ya sehemu hizo ina hitlafu.



Baada ya kumsabahi sana alifungua kijibegi chake kidogo alichokivaa bega la kushoto akatoa kifaa cha kusikilizia mapigo ya moyo. Hapo sasa ndipo tunatambua kuwa mtu huyu ni daktari. Taratibu alikavaa masikioni na upande ule mwingi kuugandamiza taratibu kwenye kifua cha mwanamke huyu upande wa moyo na kutulia tulii kama dakika tano hivi huku jopo zima la madaktari wa hospital hiyo wakiwa wamemzunguka kungoja majibu yake.



Baada ya kusikiza kwa mda mreefu sana kiasi kwamba mpaka daktari huyu alitaka kukata tamaa. Lakini gafla kwa mbaali sana aliyasikia mapigo ya moyo wa mwanamama huyu ambayo yalikuwa taratibu sana kana kwamba ndiyo yanaelekea kusimama!!

" mrudisheni ndani..!! Mrudisheni ndani haraka ''

Aliongea docta huyu mgeni huku akivua koti lake la suti na kumkabidhi mkewe na yeye kubaki na shati jeupe la mikono mirefu, kitanda kilirudishwa tena wodini huku yule docta akiwa karibu kabisa na mgonjwa huyo. Baada ya kitanda kupakiwa mahali pake yule docta aliwaagiza kumletea mashine kusaidia mgonjwa alie katika hali mbaya kupumua. Pilika pilika zilianza upya mle ndani madaktari na manesi walianza kupishana na kukimbiza huku na kule kuhakikisha wanamletea kila kitu alichoagiza docta huyu ambae anaonekana ni nguli sana japo haijulikani katokea wapi??. Baada ya dakika kama 10 watu walitulia baada ya kumsogezea daktari huyu kila kifaa alichoagiza, kwanza Saida alifungiwa mashine kubwa ya kumsaidia kuhema baada ya hapo yule daktari akampiga sindano ya ganzi kisha vifaa vya kufanyia upasuaji vikaanza kusogezwa hapo.

************************

Saa tisa na dakika arobaini basi la kampuni ya SUPER FEO Linatinga mjini songea! Wale polisi ambao walikuwa miongoni mwa abiria. ambapo aliokuwa akiwatambua ni dreva pekee, walishuka na moja kwa moja walielekea sehemu moja ambayo wao waliiona inafaa kwa wao kupumzika maana palionekana ni kijibaraza kikubwa kilicho na viti vingi sana tena pako nje wakaona hapo ndiyo pako freshi wakajisogeza pale na kuagiza vinywaji ambapo mkuu wa kituo akiagiza HEINEKEN Ya baridi bila kumsahau kijana mzima bwana charles yeye alivuta sprite ya kopo. Basi walianza kunywa huku masikio wakiwa wameyatega ili kunasa kila lisemwalo na mtu yeyote maana hapo wapo katika upelelezi mmoja kabambe sana kuhakikisha wanampata bosi wa roli lile pasipo yeye kushtuka mapema. Sasa kijana Charles alikuwa makini sana na kila gari iingia na kutoka pale stendi na sijui lengo lake ni nini??



Mkuu wake yeye hakuwa na hili wala lile yeye alikuwa bize na chupa yake akitoa loku. Mara Charles aliona roli moja kubwa aina ya Scania lenye dabo tela likiingia hapo standi ya SONGEA na inavyoonekana hii ngoma inatoka masafa marefu ila kwa kulitizama aligunua rangi ya scania hii kwa upande wa kichwani ni aina moja na lile la kule ismani. haraka akili ikamwambia hilo roli ni kampuni au mmiliki mmoja na lile lililohusika katika ajali kule ismani. Basi akalikazia macho kuhakikisha halimpotei. Roli hili taraatibu lilianza kujisogeza getini mahali wanalipia ushuru. Haraka charles akamshtua mkuu wake maana gari zote zikishafunguliwa getini hazisimami maana ake ile ni sehemu ya kulipia ushuru.

" mkuu ''

" ndiyo kijana ''

" unaiona ile semi?? ''

" ndiyo vipi kwani?? ''

" umehisi baada ya kuiona?? ''

Swali la charles likamfanya mkuu huyu kulitizama kwa makini hili roli kujua kijana wake ana maana gani kumuuliza hivyo?? Baada ya kulitizama kwa makini akili yake ikamrudisha mpaka nyang'oro ambako ile scania inayozaniwa kuhusika katika ajali ya saida ipo. Moja kwa moja akatambua kuwa yamefanana rangi kwa kiasi kikubwa. Basi akamgeukia Charles na kumwambia.

" hii scania nahisi bosi wao ni mmoja na ile tuliyoiweka chini ya ulinzi kule nyang'oro ''

" nami ndo nilikuwa na maana hiyo mkuu ''

" bila shaka tuanze kazi ya kuifutilia hii gari ''



Basi hawakupoteza mda tena zaidi ya kuinuka na kuchukua taxt kisha wakaanza kuifutilia ile scania bila madreva wa roli hilo kujua.

************************

Tukija kwa Yule dreva na konda wake baada ya kulitelekeza semi lile walikodi boda boda ambayo walitaka iwapitishe njia za panya mpaka wakaikamate barabara ya dar es salaam ili kama watafanikiwa kufika huko wapate usafiri wa kuwafikisha dar na waliamini endapo watafika katika barabara hiyo hawatakosa usafiri kwani kuna maroli mengi ya kampuni wanaliyokuwa wanaifanyia kazi yanatoka msumbiji na Africa kusini yakiwa na mizigo kuelekea Dar na mikoa mingine ya kaskazini. hivyo uhakika wa kufika dar kwa siku hiyo ulikuwa mkubwa.



Baada ya safari ndefu kupitia njia ya panya watu hao walifanikiwa kufika Ilula! Kwa wakulima wa nyanya! Kama nilivyowahi kuwambia katika sehemu ya kwanza ya riwaya hii kuwa tutapitia maeneo mengi hapa Iringa ikiwemo kwa wakulima wa nyanya!! Iyo ni ILULA!!.... Tuendelee...



Baada ya kufika ilula konda alipata wazo jipya na kutaka kuliwakilisha kwa dreva wake, kwanza roho ilikuwa ikimuuma sana konda huyu kucha kazi kizembe namna hiyo ikiwa hawajahusika hata kidogo katika ajali hiyo, kwanza aliwaza hivi ni kweli ndo anaanza kumwacha mkewe ambae ni mjamzito akiwa hana msaada wowote kwani tegemo kubwa ilikuwa ni mshahara aliokuwa akilipwa yeye, pili mama yake nae anamtegemea kwani nae hana uwezo Wa kujikimu kimaisha. mumewe ambae ni baba ake konda huyo alifariki mwaka uliopita akiwa hana chochote na kumwacha mwana mama huyo katika hali mbaya kweli kweli, baada ya miezi kadhaa mwanamama huyo alipatwa na baraa jingine baada ya kupata ajali na kuvunjika mkono akiwa anatoka shambani kwake,



Toka hapo akawa hana la jipya zaidi ya kungoja mwanae apokee mshahara wake wa ukonda aje awalishe. Sasa leo kibarua kimeota nyasi bwana...!!



Huyu konda aliwaza na kuwazua. '' ivi ni kweli namwacha mke wangu akiwa mjamzito?? Namwacha mama akiwa kilema?? Nani atawatunza?? Nani atawalisha?? Mke wangu atakuwa katika hali gani kama hatoniona tena?? Hapana haiwezekanii... '' Aliwaza kondakta huyo huku akianza kutafuta njia ya kumshuri dreva wake.. Sasa kwa bahati nzuri ni kwamba baada ya kufika ilula walikuwa wamepatwa na kiu ya maji. kitu kilichowalazimu wapumzike kidogo na kupata maji.



Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee kwa kondakta huyo kujaribu kumshauri dreva wake waache kukimbia bali wajaribu kuongea na bosi wao ajaribu kuwatetea katika kesi hiyo. Kwanza alichokifanya huyu konda ni kuagiza kachumbali ya kutosha!! Huku akitafuta sehemu tulivu ya kukaa, yule boda boda aliyewaleta aliingia katika vijibanda vya ulanzi na kuanza kunywa!!



" Oya kaka bakari '' konda huyo aliita..

" naam moses ''

" ebu njoo hapa chemba kidogo ''

Basi walijivuta na kukaa kona moja tulivu sana huku yule mhudumu aliyepewa kazi ya kuwaandalia kachumbali akileta sinia likiwa limejaa kachumbali saafi. Basi vijana hawa walianza kula huku kijana bakari ambae ni dreva akimsikiliza moses ambae ni konda wake maana yeye ndiyo kamwita chemba..



" Sikia kaka ''

" nakusikia mose ''

" unaonaje tukiahirisha huu mpango tuliouanzisha wa kukimbia?? ''

" halafu iweje?? ''

" mi naona tuwasiliane na bosi ajaribu kututetea katika hili maana hatujahusika kabisa katika hili ''

" ni kweli hatujahusika lakini jee? Unadhani nani atatuelewa?? Siku hizi pesa ndiyo inaiongoza sheria sasa wewe una pesa?? Sheria tunayo ila sheria hii itageuzwa kichwa chini miguu juu iwapo watakuja wenye nazo sijui unanielewa?? '' Bakari aliongea kwa msisitizo huku akimtizama moses usoni ambae nae alionekana ana jambo la kuongea..

" Ni kweli ila kujaribu siyo kushindwa ''

" we ulitaka tujaribu vipi labda?? ''

" Tumpigie bosi halafu tusikie anasemaje akizingua tunasepa ''

" Wazo zuri moses je? Sasa tunaanzaje?? ''

" Mwambie kuna mtu alikuwa spidi sasa kufika konani gari ikamshinda na kuja kutuvaa kwenye saiti yetu kisha tumsikie atasemaje?? ''



Sasa vijana hawa walikuwa wamesahau kuwa ile gari iko na kamera. wangelijua tangu mapema hata wasingekimbia. Basi bakari akatoa simu yake na kutafuta namba ya bosi wao alipoiona haraka akaiweka hewani.. Simu Iliita mara kadhaa ikapokelewa...

" haloow... ''

" shikamoo bosi ''

" marhaba mpo wapi sasa hivi?? '' bosi anauliza akijua gari ipo njiani inakuja....

" Boss safari yetu imeingia dosari kidogo kuna mtu katusababishia matatizo.. ''

" matatizo??? Matatizo gani tena?? ''

" Boss kuna gari ndogo aina ya VX tulikutana nayo katika makona ya nyang'ora sasa mwendeshaji alikuwa yupo spidi kweli na alipofika eneo flani ambalo lina kona kali gari hiyo ikamshinda na kuhamia sait yetu na kuja kutuvaa.

" Nini?? Sasa imekuwaje?? ''

" kwa asilimia 99 Tunaamini mtu huyo hana uhai na hili ni tatizo kubwa sasa utatusaidiaje bosi?? ''

" ok ngojeeni nitawapigia sasa hivi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bosi huyo alikata simu na akili mwake alijua vijana hao wameua na wanataka kukimbia ili kesi iangukie kwake hivyo alichokifanya ni kuwakatia simu kwanza ili aende kuikagua ajali yenyewe jinsi ilivyotokea maana anajua mkanda mzima upo kwenye laptop iliyounganishwa na camera za gari hilo.



" Nashuka hapa '' ilikuwa ni sauti laini na nyororo! Ya kumto nyoka pangoni, hakuwa mwingine bali alikuwa ni Ashura. Patrick alishtuka na kushikwa na kigugumizi kikali kiasi kwamba alishindwa kutokwa na neno lolote! Na wakati huo dreva anaanza kupangua gia na gari inaanza kusimama taraatibu huku Ashura nae akianza kuinuka kitini.



SONGA NAYO:

Patrick hakuweza kusema chochote na Ashura akashuka mpaka nje na kuanza kuondoka taratibu. Lakini gafla konda akamkuda kwa nyuma..

" wee! Dada acha utapeli mbona hujalipa nauli??? ''

" ahaa samahani nilisahu kaka ngoja nitoe.. ''

Ashura alifungua mkoba wake haraka huku mikono ikiwa inatetemeka akatoa noti ya shilingi elfu tano na kumkabidhi kondakta huyo na kabla hata yule konda hajatoa chenchi Ashura ameshapotea! Basi bila hiana yule konda akadandia ile daladala kisha haoo!!



Unajua katika dunia hii ya sasa jali huyo ulie nae awe mumeo au mkeo mjali sana kwani ndiyo atake kuokoa katika shida zote na atakuwa nae katika shida na raha kwa sababu kakubali kuoa/kuolewa nae ni dhahili amekubali kukabiliana nawe katika shida na raha hivyo ebu mjali, mlinde, mpende na mfariji pale anapokuwa na matatizo.



KWANINI NASEMA HIVYO???

Nasema hivyo kwa sababu tumemuona Ashura hapo ameamua kumtelekeza patrick baada ya kuona ameshapataa tatizo na mda wowote anaweza kukamatwa na poli hivyo kaamua kumuacha akamatwe peke yake kwani kwa mda huo hana time nae kwani anampenda tu pale wanapokuwa bar au mahotel makubwa ya kitalii kiufupi ni kwamba kampendea pesa tu..



Hiace hii aliyoipanda Patrick imeikamata barabara kisawa sawa ikichangia na huku hakuna makona gari zinakwenda hatari,, Patrick yeye mda huo alishakuwa ni mtu wa mawazo mengi yaani pombe yote aliyokunywa ilimuishia kwani kichwani mawazo yalikuwa yakipishana balaa, anawaza Saida kaua gari yake ya mamilioni, gari yake nyingine ipo porini kule na hana uhakika kama ataikuta salama kwani wawindaji au wachungaji wakipita hapo na kuikuta huenda hata wakibonda na mawe!. Haya yeye mwenyewe pia hajiamini huenda akakamatwa. Ashura nae kashuka tu na haieleweki kaenda wapi?? yaani ilikuwa ni shida juu ya shida kwa Patrick alijikuta taratibu shati lake la ndani likianza kuloana taratibu na jasho lilokuwa likimwagika kwa kasi mwilini mwake Na akicheki mbele geti lileee! Na kuna ulinzi mkali usipime Patrick aliona na siti ya moto nakwambi....!!!

************************

Gafla saa ya Charles iliwaka mwanga mwekundu kuashiria cctv zipo katika jengo lile na tayari zimeshawanasa....

" mkuu ''

" twende kijanja ''

Waliambizana hivyo polisi hao wapelelezi huku bila kuangaliana yaani kijanja kwani yule mkuu alipoambiwa twende kijanja tayari alishatambua kuwa huko mbele hakupo salama. Sasa polisi huyu alianza kuwaza na kuwazua ni vipi wataweza kuingia humu? Kama camera zipo?? Alikuwa akiwaza mkuu huyu polisi huku wakizidi kuusogolea uzio huo uliojengwa kwa umahiri wa hali ya juu. Charles yeye alikuwa makini mno akitizama huku na huko.

Hatimae wanafika getini sasa, walianza kuangaza kwa makini huku na kule kuona kama kuna kitufe cha kengele lakini hakuna! Walishangaa sasa watu wanaingiaje hapa ikiwa geti limefungwa halafu halina kengele?? Lakini gafla wakiwa wanawaza hayo gafla!! Geti likafunguka kwa kasi ya ajabu... Huku wakifuata wanajeshi waliotoka kwa kasi na kuwazingira polisi hawa...

" nyoosha mikono juu '' aliongea mwanajeshi mmoja huku akiwa kawanyooshea polisi hawa mtutu!. Charles na mkuu wake hawakuwa na neno zaidi ya kutii amri na kunyosha mikono juu, kisha wakatangulizwa ndani ya uzio ambako ndani walikutana na majengo ya kifahari balaa!! Pia licha ya hilo ndani pia kulikuwa na maswiming pol ya kutosha ambapo kulikuwa na watu wengi wakiogelea, ukiachana huko waliendelea kutembeza macho kila upande, kiukweli hili eneo linavutia mnoo! Kulikuwa na gaden nzuri za kuvutia pia eneo lenyewe lilikuwa ni pana lenye nafasi ya kutosha!. Charles na mkuu wake waliendelea kutalii eneo hili ili kwani mpaka hapo katika upelelezi. Hivyo hata kama wamewekwa chini ya ulinzi lakini bado macho yanatembea...

" kaeni hapo '' walioneshwa mahali wakakaa..

" Sheria ya hapa ni kwamba mtu yoyote aingiaye hapa lazima akaguliwe kwahiyo ukaguzi unaanza.. '' Aliongea mwanajeshi mmoja huku akiweka bunduki yake chini tayari kwa kuwakagua watu hawa.

************************

Ilikuwa imetimia saa kumi na moja na nusu sasa, na ni masaa matatu yameshakatika sasa tangu saida afanyiwe oparesheni katika hospital ya IPAMBA. Na mpaka hapo hakuna hata dalili yoyote kuwa mtu huyu atazinduka mida hiyo,, sasa tukiachana saida tuje kwa huyu alietoa msaada ni nani haswa??? Kila docta na nesi alikuwa na shaukuu ya kutaka kumjua mtu huyu, ila mpaka hapo walikuwa hawajamjua bado kwani baada ya kazi ya upasiuaji aliwaamuru kwanza waende wakahudumie watu huko mpaka foleni iishe ndipo waje.. Ili mwenye swali aulize! Mwenye maoni atoe.. Sasa hapo ilikuwa imetimia saa kumi na moja na nusu ni mda ambao watu walikuwa wameshapunguaa sana,, madaktari wote walikusanyika kwenye wodi aliyokuwa amekazwa saida ambako ndipo alipo daktari huyu mgeni na wamekusanyika hapo nadhani kila mtu ana lake moyoni..



Kwanza kabisa daktari yule mgeni alianza kwa kujitambulisha kama ifuatavyo..



" Kwanza niwashukuru sana madaktari wa Hospital hii kwa ushirikiano wenu mkubwa mnaouonesha katika kuwasaidia wagonjwa,, mimi naitwa daktari ruis gama natokea OCEAN ROAD Dar es salaam, nilikuja hapa kumsalimia binti wangu huyo.. '' aliongea huku akiwaonesha madaktari hao mtoto wake huyo ambae kama unakumbuka awali wakati wanafika nilikwambia kuwa kuna nesi alimkimbilia mwanaume huyu pamoja na mkewe kwenda kuwalaki, hao walikuwa ni wazazi wake,,

" tunashukuru sana docta kwa msaada wako mkubwa uliouonesha mbele ya mama huyu hakika baraka nyingi zitakushukia docta ''

" asante sana docta na huu ni wito wangu kuhakikisha namsaidia kila mmoja alie na matatizo. ''

" tunashukuru sana.. ''

" basi munaweza kutawanyika na kuendelea na majukumu yenu.. ''



Basi madaktari hawa pamoja na manesi na wauguzi walitawanyika katika chumba hicho baada ya utambulisho na ujio wa daktari huyo na huku wodini waliachwa madaktari kadhaa akiwemo bwana rous kutoka ocean road. Kiukweli hali ya Saida ilikuwa bado mbaya sana madaktari wote waliokuwemo mle wodini akiwemo bwana rous walikuwa wakipiga dua na kusali sana ili kumuombea uzima mama huyu aliyeko kitandani.

*************************

Kwa mwendo wa pikipiki Bakari na jamaa yake hawakukawia kufika Iringa mjini, basi wakamlipa ujira wake yule boda boda kisha wakaenda kukata tiketi katika basi lingine tena la kampuni ya SUPER FEO Ambalo makonda waliwaambia litaondoka hapo iringa saa mbili na nusu usiku.



Bakari na moses hawakuwa na jinsi japo gari hilo waliona linachelewa sana kuondoka lakini hakukuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na hali halisi kwani hakuna gari jingine zaidi,, masaa nayo hayagandi hatimae saa mbili na dakika ishirini na tano! Dreva mahili kabisa wa makamo ambae kichwani tayari baadhi ya maeneo zimeanza kuonekana nywele nyeupe,, aliiwasha ngoma iyo hapo!! Taratibu ilianza kuunguruma huku kila mmoja akiwa na shaukuu ya kuondoka... Hatimae saa mbili na dakika ishirini na tisa, sekunde ya thelathini na nae, dreva aliingiza gia na kuruhusu ngoma kuanza kuiacha stendi ya mabasi Iringa.

*************************

Huku kwenye ajari, Jonhson na kikosi chake wasi wasi mwingi ukaanza kuwasumbua! Kwani giza ndiyo hilo linazidi kusika hatamu na mpaka hapo hawajaweza kupokeaya simu yoyote kutoka kwa kiongozi wao yani toka wameachana nyang'oro mida ya saa tano asubuhi mpaka mida hiyo ni saa mbili na nusu sasa na kibaya zaidi ni kwamba barabara hii kwa eneo la nyang'oro makonani huwa kuna ujambazi wa kutisha! Magari hutekwa na watu kuuawa na majambazi kisha huwapora mali zao zote!



Hali hii ilianza kumchanganya sajent huyu wa kikosi hicho kidogo, na hata vijana wake nao waliungana nae katika swala zima la uoga kwa maana tayari giza limeingia na hii barabara ina majambazi sugu, tena kwa kuwa ni giza walihisi huenda mda wowote au saa yoyote watashambuliwa..

Vijana walikuwa wakiongozwa na Johnson uoga ulikuwa umewabamba siyo kawaida maana eneo walilopo wanaijua historia yake mara nyingi mali za watu huporwa katika makona hayo na watu kuuawa, hivyo hayo maeneo hayana cha polisi wala mwanajeshi na ubaya ni kwamba giza limeshashika hatamu vilivyo halafu sasa wao wapo barabara na mataa ya magari yapitayo kila mda huwamulika na hicho ni kitu kibaya sana kwao kwani kama majambazi yapo karibu hapo mstuni watawauwa kirahisi kabisa pasipo wao kufanya chochote.



Hivyo bwana sajent mdogo johnson alikuwa akitafakari ni nini wafanye ili kuepukana na baraa hilo??

" hey hebu kusanyikeni mara moja ''

Johnson aliwaita vijana wenzake na bila kupoteza mda wenzake walikusanyika pamoja,



" Sikieni wakuu nimewaita hapa kuwajuza hivi mnatambua kuwa hapa tupo katika hatari kubwa??? ''

" ndiyo tunaelewa mkuu sijui wewe una mpango gani?? ''

" mimi nafikiri tutafute mahali salama tutulie maana hii tawanyika tawanyika ya kulinda skrepa itatuponza ''

" Safi sana sajent john kumbe una akili kaka ''

Walimpongeza kiongozi wao kwa mawazo mazuri aliyoyatoa na bila kupoteza mda wakatoka hapo kwenye lile gari na kujivuta pembeni kidogo ambapo walikutana na mtaro ulikaa vizuri ambao ndani yake kuna mchanga laini ambao hauwezi kuwaumiza, na pia mtaro huu ni mrefu kiasi kwamba hata gari ikipita mwanga wa mataa ya gari hiyo hayawezi kumulika mpaka ndani...



Basi wote kwa pamoja walirundikana ndani ya mtaro huo huku macho yakiwa kule kwenye gari wanayoilinda. Mda huo ilikuwa inasoma saa tatu kamili usiku na hata hali ya hewa ilianza kubadilika na kuanza kupuliza ile baridi ya usiku. Punde si punde mara zilianza kusikika hatu za watu wakiwa wanafuata barabara kuelekea kule iliko gari ya Saida!. Sasa kibaya ni kwamba ni giza nene kwani hata polisi hawa walipojaribu kuinua vichwa vyao kuona ni kina nani hawakuweza kufanikiwa kuwajua zaidi ya kuona vivuli vya watu wakiwa wamevaa makoti tu!! Askari hawa walizidisha umakini ili kuona nini kinakwenda kutokea katika gari hiyo??....

************************

Basi la kampuni maarufu sana mkoani songea ambalo Wale konda na dreva wake walikuwa wanasafiri nalo kuelekea songea tayari lilishaiacha iringa kitambo saana na sasa abiria walianza kuhesabia masaa na inasadikika kuwa songea litaingia saa moja kamili asubuhi ya kesho..., mule ndani bakari na rafiki walianza kupiga story za hapa na pale ili kupoteza mda maana kama ni usingizi haupo kabisa, kwani abiria wengi wameshauchapa usingizi lakini wao bado wapo macho. Basi ili safari yao iende vizuri vijana hao walianza kupiga stori za hapa na pale...



" hivi jamaa angu moze wale watu wazima kweli?? '' bakari ambae ni dreva alimuuliza konda wake aitwae moses hapo wanazungumzia ile ajali.

" Daah! Sina uhakika kwa kweli. '' moses alijibu kwa masikitiko.

" ujue mi sijaona hata. we mwenzangu uliefanikiwa kuchungulia hivi ilikuwaje?? ''

" inavyoonekana mtu yule alienda kujigonga sehemu maana kigari chake kirirushwa pembeni na kubondeka vibaya ''

" Aisee au ndiyo tunajipeleka gerezani?? Maana sielewi!! '' Bakari alikuwa ni mtu mwoga mwoga sana hivyo alivyosikia tena kisanga hicho kwa mara nyingine nywele zilimsisimka kwa uoga na alianza kuziona nondo zilee....

" hapana ushahidi wetu mkubwa ni ile camera ya CCTV Hatutofungwa kaka jiamini '' moses alimjibu jamaa yake huyo. Bakari alivuta pumzi ndefu na kuishusha na mida sasa inasoma saa saba na nusu usiku...

************************

Tuje kwa jamaa yetu patrick.. Ni kwamba mda ule ile daladala ilifika mpaka getini, geti hilo lipo sehemu moja wanaita NDOLELA Nadhani kwa wale wenyeji wa Ismani na wale waliowahi kusafiri kati ya Iringa & Dodoma wanalitambua vyema geti hilo, basi kama ilivyo kawaida dreva alianza kupangua gia za gari hilo kupunguza mwendo ili kama polisi wanataka kufanya ukaguzi wowote iwe rahisi kwa dreva huyo kulisimamisha gari hilo. Hili geti ndugu msomaji huwa linatumika kukamatia samaki waliovuliwa kinyume na sheria huko bwawani mtera. Na ndiyo maana huwa kunakuwa na ukaguzi hapo getini..



Mda wote huo Patrick tumbo lilikuwa moto maana kama atadakwa tu na polisi na ikajulikana kama ni yeye ndiyo alienusurika kuua polisi huko makonani kwa kutembea mwendo kasi mbona ataisoma namba??

" Bwana Agrey hujaona gari yoyote ndogo aina ya PRADO nyeupe ikiwa imepaki sehemu au kui- over take njiani?? " polisi mmoja alimuuliza kijana mmoja aitwae Agrey ambae ni dreva wa daladala hiyo..

" Hapana mkuu '' kijana alijibu...

" una uhakika?? Ebu kumbuka vizuri au umesahau?? ''

" hapana ni kweli sijaipita gari yoyote njiani.. ''

" ok unaweza kwenda ''



Daladala hiyo iliruhusiwa kuondoka na geti likafunguliwa kisha haoo!! Hahaha!! Patrick alivuta pumzi ndeefu na kuishusha huku akijifuta jasho maana pale getini alisihi kama katumbukizwa ndani ya chungu chenye joto kali kwani pumzi zilikuwa zikimwishia na jasho jingi kumwagika mwilini mithili ya mtu alietupwa mtoni.. Chezea polisi...!!!



Daladala hiyo ilikuwa ikienda kwa kasi sana mpaka Hapo walishawasili nduli ambapo Patrick aliomba kushushwa hapo maana ndani ya gari hajiamini kabisa anahisi mda wote atatiwa pingu.. Basi ile haisi ilisimama na Patrick kulipa nauli kisha akashuka na ile dalaladala ikateleza.. Nae hakuendelea kuzubaa hapo alitoa simu yake na kumpigia moja kati ya vijana wa hapo nduli anaefahamiana nae aje kumchukua na boda boda ili ampitishe njia za panya mpaka kihesa yalipo makazi yake.



Yule kijana aliepigiwa simu na Patrick aliwasili hapo na piki piki moja matata sana aina ya KING LION 150, Na bila kupoteza mda Patrick alipanda nyuma. Kijana akauliza....

" Wapi kaka?? ''

" Kihesa nyumbani kwangu si unapajua?? ''

" Ndiyo napajua.. ''

" Nahitaji unifikishe ila kwa njia za mkato sijui utanichaji ngapi?? ''

" Hapoo nitoe buku tano tu kaka ''

" Sawa twende... ''



Pikipiki iliondolewa hapo kwa spidi kali na kuanza kukata mitaa huku kila mtaa ukiwa na walinzi wa sungu sungu! Maana mida yenyewe ilishakuwa usiku hivyo vikosi vya sungu sungu vilikuwa vimezagaa kila mahali kuhakikisha ulinzi wa mitaa.. Huyu kijana alikuwa ni mwenyeji sana wa njia za panya kwani baada ya mwendo kama wa dakika kumi na tano waliwasiri katika mjengo wa bwana patrick uliopo katika eneo la kihesa! Kijana alilipwa ujira wake kisha huyooo! Akayeyaaa!!!

***

Mlinzi we geti la Patrick bwana Emanuel akiwa katulia zake kwenye kijibanda chake cha mlinzi wa geti huku akiwa na mawazo mengi sana kuhusu mabosi wake wote wawili kutoonekana nyumbani mpaka muda huo ambapo imeshakuwa usiku wa manane tangu waondoke asubuhi kiukweli alikuwa hapati jibu kuwa watu hao wamepatwa na nini??....

.. Mara gafla kengele ya kumtaarifu kuwa nje kuna mtu anataka kuingia ikaanza kutoa sauti.....

" ngriiii....!! Ngriiiii...!! Ngriiiii.... !!! '''

Mmmh! Kwanza Emanuel alishtuka sana Na kuogopa nani huyo anaetaka kuingia mida hii?? Kwanza kabla ya kufungua alisogea kwanza kwenye kidirisha kidogo kinachomwezesha kuona nje! Akachungulia kwanza kuona ni nani huyo?? Maana isije kuwa ni uvamizi.. Mwanga wa mataa yaliyofungwa pembezoni mwa uzio wa nyumba ya Bwana Patrick yalimwezesha kumwona na kumtambua mgaongaji ambae ni bosi wake. Haraka akaenda kufungua huku akiwa na mawazo tele kuwa huyu mtu kaacha wapi gari mpaka aje kugonga kengele ikiwa siku zote huwa anapiga honi?? Jibu hakulipata. Akafungua geti na kukutana bosi wake akiwa kakunja ndita siyo kawaida!... Emanuel hakumwelewa...



" Saida yupo wapi??? ''



Patrick aliuliza kwa sauti nzito na ya kukoroma kiasi kwamba mpaka mlinzi mwenye akashikwa na kigugumizi kikali mpaka akashindwa kujibu..



" Nauliza Huyu mwanamke yupo wapi?? Au husikii?? ''

" Si...s...sijui... ''

" Kwani hajarudi??? ''

" Hapana tangu aondoke asubuhi ''

" mfyuuuuuuuu!!!! ''

Patrick aliachia msonyo wa nguvu kisha akamwacha hapo mlinzi wa geti na yeye akatokemea ndani kwake na kwenda kulala...



Emanuel akabaki njia panda kuwa afunge geti?? Au aliache bosi bado anatoka? Maana gari haijaingia, kwa kuwa emanuel haelewi kitu na kaachwa njia panda ilimrazimu asimame pale huku geti likiwa wazi wakati huo mwenzie anauchapa usingizi tu huko...

**************************

Tuje kwaa... ASHURA Huyu mwanadada ni shiida aiseee! Hahaha!! Ni kwamba baada ya kumtelekeza Patrick alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye baa moja ambayo ipo ndani ndani kabisa katika kijiji hiki cha nyang'oro au kwa rugha nyingine tunasema baa hii ipo uswahilini.. Ndani ya baa hii kulikuwa na changanyikeni baraa!! yaani mziki wa nguvu wanaume kwa sana!! ulevi wa kupindukiaa! Unaambiwa watu wanacheza mziki na chupa mikononi huku bia zikimwagika! Wao hawana habari..



Hii sehemu Ashura aliona ipo sahihi sana kwake na kitu cha kwanza alichokifanya ni kubadili LINE kwa kutoa zile ambazo anajua namba zake Patrick anazo, akaweka zingine yaani line ambazo namba zake Patrick hana alifanya hivyo kukwepa usumbufu wa mwanaume huyo... Na baada ya hapo mwadada huyo akajitumbukiza changanyikeni... Wanaume wote waliokuwa mle ndani ya baa wakapiga mayowe...!!

... " Oyooooooooooooo!!!!! ''..........



Sasa turudi nyuma kwanza mpaka kwa kikosi cha Jonhoson kule polini kulikokuwa na balaa kubwa, polisi hawa hawakuthubutu kufanya chochote kwa watu hao wasiowajua bali waliendelea kuwatizama na kungojea nini kitatokea?? Wale watu ambao hawajulikani ni kina nani walikwenda moja kwa moja mpaka kwenye gari ya Saida iliyopata ajali na bila kupoteza mda wakatawanyika na kuizingira gari hiyo.. Vijana hawa wa jeshi la polisi waliendelea kukaa kimya kuona nini kitajiri??



Punde si punde kulionekana mwanga wa mataa ya gari ikija eneo hili, Jonhson na vijana wake wakazidi kulala chini ili wasije onekana hata kofia, gari hilo lilizidi kusogea eneo hilo na hatimae likafika mahali gari ya Saida ilipokuwa imedondoka ila cha ajabu wale watu hawakuonekana!! Polisi walitaharuki...!!

" haaa! Mkuu wale watu wapo wapi?? ''

" shiiii....!! Tulia hata mi sielewi ''

" au mawenge nini?? ''

" hapana kulikuwa na watu wee hukusikia boot zile?? ''

" ndiyo ila mbona hawapo?? ''

" tulia tulia.....!! ''



Johnso alimstopisha kijana wake mmoja ambae alioneka mwehu mwehu sana! Johnson alifanya hivyo kwa maana gari ile iliyokuwa inakuja ilionekana kupunguza mwendo kana kwamba ilikuwa ikisimama.. Ni kweli ilikuwa ni scania kubwa iliyosheheni magunia ya dagaa na tayari walishafika eneo la ajari. Sasa wale watu mle ndani ya gari yaani konda na dreva wake walijawa na roho ya huruma baada ya kuona gari ndogo ikiwa imepata ajari moja mbaya sana. Na akilini mwao walijua gari hiyo itakuwa imepata ajali usiku huo na hakuna alieona hivyo walikusudia kutoa msaada...



Gari hiyo kubwa ya mizigo ilipaki pembeni kidogo, na wakati huo kile kikosi cha polisi wanaona kila kitu.., dreva wa roli hilo alimwamuru konda kushuka wakati huo yeye analizima gari na kuanza kufungua mkanda tayari kwa kushuka, konda alikuwa ameshashuka tena kitambo tu! Na kaanza kukizunguka zunguka kigari hicho kinachoonekana kubondeka bondeka baraaa!!!

.... Kuna alie nusurika kweli???.....

Yule kondakta aliwaza huku akizunguka upande wa pili....

,'' mara gafla!!! Akatwishwa jiwe la maana la kichwa mpaka akenda kuyavaa matairi ya gari hiyo ndogo!! Akiwa bado hajakaa sawa network ziludi, mara matochi yenye kutoa mwanga mkali yaliwashwa kutoka mtaroni kuelekezwa barabarani eneo lote hili kukawa kweupeee!! Dreva alipomcheki konda wake anaona yuko hoi,, damu nyingi zikiwa zinamwagika,, matochi nayo hayoo! Yanazidi kumweka kati na alipotizama kwa makini dreva huyo aliziona bunduki hatari sana aina ya AK47 Zikija kwa upande wake!! Aisee alitaharuki na kutaka kukimbia lakini papo hapo mishindo mitatu dabo ilisikika na yule dreva kwenda chini na gari lao kuwekwa kati,, yote hayo polisi waliyashuhudia kwa macho yao lakini hakuna aliethubutu kufanya chochote....

************************

IPAMBA HOSPITAL..... Ilikuwa yapata saa kumi na moja alfajiri ndani ya wodi aliyokuwa kalazwa mwanamama saida kulionekana msongamano mkubwa wa manesi na madaktari na wengi wao walioneka kuwa na tabasam pana nyusoni mwao, Saida alikuwa amezinduka kutoka katika usingizi wa kifo japo akili ilikuwa haijakaa sawa bado, madaktari hawakutaka kumghasi hivyo walimwacha ili ufahamu umkae sawa hivyo wao waliendelea na story zingine za hapa na pale,



Saa moja kamili asubuhi, Saida alionekana kukaa sawa kikumbukumbu hivyo daktari huyu nguli kutoka OCEAN ROAD Alianza kumuuliza maswali ya kizushi ili kumumpima kisaikolojia...

" dada unaitwa nani??? ''

" Patrick yupo wapi?? ''

Hii inaitwa rugha gongana ndugu msomaji, maana kauliza anaitwa nani yeye anajibu Patrick yupo wapi?? Duuuh! Ama kweli upendo ukizi sana pia ni ugonjwa!, daktari huyu hakukata tamaa aliendelea kumuhoji kiaina huku akimtizama usoni...

" Nisikilize dada ''

" ndiyo nakusikia ''

" unaitwa nani?? ''

" mimiiii aaaa naitwaaa.. Mmmm Saida, '' watu wote waliokwemo wodini walipiga makofi...

" saaafi sana!! Je?? Unatambua wewe ni mkazi wa wapi?? ''

Swali lile lilionekana kuwa ni mtihani kwa saida kwani hakuwa na jibu na hii ilidhilisha wazi kuwa Saida bado hakuwa sawa. matukio mengi ya nyuma alikuwa hajayakumbuka bado,, mda nao ulikuwa unazidi kusonga saa moja na nusu hiyo hapo!, madaktari hawa waliona kuwapata ndugu zake Saida bado kuna mtihani mgumu kwani huyu mwana mama inaonekana kumbukumbukt kurudi katika hali ya kawaida itachukua mda sana hivyo walitakiwa kujiongeza.. Basi wazo walilolipata madaktari hao ni kupekua nguo zake kuona kama simu yake itakuwepo??



Kweli walifanikiwa kuipata ila shida ni kwamba simu hiyo ilikuwa imeharibiwa vibaya mnoo! Kiasi kwamba hata maandishi tu haioneshi. lakini hilo halikuwapa tabu walichokifanya ni kutoa line na kuweka kwenye simu nyingine. Baada ya simu hiyo kuwashwa na mtandao kukaa sawa walianza kupekua majina kuona kama watapata jina lolote ambalo inawezekana akawa ndugu yake, baada ya kupekua kidogo walikutana na jina la maandishi makubwa yakiwa yanasomeka....

........ MY HUSBAND ........

" Mumewe huyo piga '' basi bila kupoteza mda simu ilipigwa na nesi mmoja aliekuwa akitafuta majina baada kupiga akaiweka sikioni.. Sekunde kadhaa simu ilianza kuita....

***********************

Ikiwa ni mida ya saa moja na nusu bwana Patrick akiwa bado anauchapa usingizi nyumbani kwake. mara simu yake inaanza kuita.. Patrick alishtuka usingizini baada ya kusikia simu inaita, kwanza aliachia msonyo wa nguvu kisha kiviivu akanyoosha mkono kuichukua huku akiwa na hasira kali kwa kukatizwa usingizi.



Aliichuku na kuisabahi kwenye kioo huku akiwa na lengo la kumtukana huyo aliempigia asubuhi yote hiyo na kuharibiana stimu za usingizi. Sasa baada ya kuisawili Patrick alibaki kinywa wazi huku mwili mzima ukisisimka! Matukio ya jana yalianza kupita kwa kasi kichwani kwake na hasira kali kuanza kumshika. ni baada ya kuliona jina la Saida juu ya kioo cha simu. Patrick alipokea namna hiyo.......



" we mbwa umerudi kutoka kuzimu?? Nauliza umerudi kutoka kuzimu??? Gari yangu ipo wapi we malaya?? Ipo wapi??? Eeee!!?? Nasema ipo wapi????? ''



Patrick alikuja juu namna hiyo bila kujua kuwa simu ipo na nani?? Na kule hospital madaktari walibaki kutizamana tu! Hawakuwa na jibu lolote zaidi ya kumtizama Saida ambae na taratiibu machozi yalianza kumshuka kwa kasi kweli kweli kwani majibu ya mumewe aliyasikia kwa uzuri kabisa bila chenga.



" Ebu lete iyo simu hapa '' yule daktari mgeni kutoka OCEAN ROAD Aliiomba simu hiyo na wakati huo ilikuwa imeshakata. Alichokifanya mgeni huyu ni kupiga tena, sekunde chache simu hiyo ilipokelewa tena na safari hii kabla patrick hajaongea chochote huyu daktari akamwahi na kusema......

" kwanini unalivumjia heshima jeshi la polisi?? ''

Patrick alishtuka kupita maelezo na kigugumizi kikali kikamshika gafla! Na akakosa cha kujibu kwa mda huo..

" nauliza kwani unalijibu shombo jeshi la polisi?? Au unapingana na sisi?? ''

" Ha...ha...haa...p...an..a ''

" Unahitajika IPAMBA mara moja sijui tumeelewana??? ''

" Ndiyo nipe nusu saa ''

" haraka ''

" sawa mkuu ''



Baada ya simu kukata Patrick alikurupuka kitandani na kukimbia bafuni na kuoga haraka haraka kisha akarudi na kuja kuvaa suti zake kisha haraka akatoka chumbani huo, alipita mpaka sebleni na kukuta meza kavu leo mwaandaji hayupo! Hivyo ilimlazimu kwenda hivyo bila kupata kifungua kinywa. Patrick alitoka mpaka nje na moja kwa moja alikwenda mpaka uwani na kuchukua land cruiser moja kali sana yenye kwenda mwendo wa kasi kama zile za mabunge na bila kupoteza mda aliirudisha nyuma kwa kasi na kuiweka sawa kisha akapiga honi kali sana kumwamsha mlinzi wake wa geti bwana Emanuel ili afungue geti,, Emanuel alikuwa macho na alitoka haraka na kufungua geti kisha jamaa huyoooo!! Akateleza...

*************************

SONGEA... Mkuu wa kituo cha ismani akiwa na kijana wake machachari aitwae charles ni kwamba baada ya kutaitiwa na ulinzi mkali katika eneo lile la geti kali walikwenda kuweka chini ya ulinzi, na bila mda kupotezwa walianza kusachiwa! Kila mmoja, sachi sachi baadae wale wanajeshi waliwakuta na vitambulisho vyao vya kazi,



walianza kuwahoji mda huo ikiwa ni usiku tayari,

" tunatambua kuwa nyinyi ni polisi je? Shida ipi mnayo hapa?? ''

" ni kweli sisi ni polisi kutoka kituo cha polisi kilichopo mkoa wa iringa kata ya ismani.. ''

" sawa je?? Mna shida gani?? ''

" tunahitaji kuonana na bosi wa hii kampuni,, ''

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Yule mwanajeshi alicheka kwa zarau kisha akasema bosi hawezi kuletwa hapa au kuoneshwa mahali yupo bila kujua nyie mna shida gani haswa?? Mnaweza kuwa majambazi walio na vyeti bandia si tutajuaje??.. Yule mwanajeshi aliongea huku ulinzi ukiimarishwa kila upande...



" sikieni nyie kuna gari kubwa ya mizigo ambayo rangi yake kwa kiasi kikubwa imefanana na magari yaliyopo hapa na gari hiyo imewekwa chini ya ulinzi kwa kosa la kusabisha ajali moja mbaya sana hivyo tupo kwenye uchunguzi tunamhitaji bosi wa hii kampuni haraka ili kuokoa mda.. ,''



Mkuu wa poli yule aliongea kwa kufoka mpaka wale wanajeshi kidogo wakaogopa na bila kupoteza mda kuna mmoja alitumwa kwenda kumwarifu bosi wao kuhusu ujio wa polisi hao wapelelezi. Ndani ya dakika tano yule askari alietumwa alirudi na taarifa kuwa bosi ameomba kuonana na polisi hao mapema asubuhi, nadhani bosi kafanya hivyo kwa kujua kina bakari wapo njiani na itakuwa vizuri na wao wawepo...





Sasa kabla hatujasonga mbele zaidi hebu turudi nyuma kwanza mpaka kwa mwanadada Ashura ili tupate kujua nini kilijiri pale PUB Ya uchochoroni???



Ni hivi Ashura baada ya kushuka na kumlipa konda na bila hata kungoja nauli akaondoka kana kwamba alikuwa na haraka sana kiasi cha kusahau mpaka chenchi, basi alizipiga hatua za haraka huku mara kwa mara akigeuka kuona kama ile daradara aliyopanda Patrick imeondoka na Patrick hajashuka?? Alipojiridhisha kuwa ile daladala imeenda na Patrick hajashuka alitasam kidogo kisha akasogea mahali pana mti na kujiegesha pale kisha akatoa simu yake na kuingia sehemu ya majina

(Contact).



Alianza kupekua majina kwenye simu ile haraka haraka mpaka akalifikia jina lililoandikwa MY BEST FRIEND Bila kupoteza mda akapiga ile namba papo hapo ikaanza kuita.....

" Ngrrr!! Ngrrr! Ngrrr! Ngrrr.... Halow...!! '' Sauti ya kijana ilisikika upande wa pili na mtu huyo alionekana yupo changanyikeni kweli maana zilisikika kila aina ya kelele....

" Khaaa! Dani upo wapi wewe?? '' Ashura aliuliza kwa taharuki...

" Tunakulaaa bataaa hukuu ''

Kijana alijibu kilevi kweli kweli...



" mi nimekuja sasa ''

" upo wapii?? ''

" apa stand ya nyangoro ''

" sasaaa bar yetu ya usiku si unaijua?? ''

" ndiyo napafahamu ''

" njoo ndipo nilipo ''

" poa ''



Simu zikakatwa na Ashura akaanza kwenda mdogo mdogo katika bar iyo ambayo ipo pembezoni sana na hii bar ina mtindo wa kupokea wanafunzi wa secondary ambao usiku wanatoroka mageto yao na kwenda kula bata kule, kiufupi ni bar ambayo haitambuliki na wengi iyo ni spesho kwa michepuko wake za watu huwakosi mle usiku sanjali na waume za watu...!!



NAAM...!! ILIVYOKUWA MPAKA ASHURA ANAKWENDA KATIKA BAR HIYO MAANA AKE ALIKUWA NA MWENYEJI WAKE...



Ashura alijiachia mle ndani wakati huo mtoto wa kike hana hata shida line kabadili hata Patrick akimpigia hampati....



" Oyooooooooooooooo!!!! ''



Bar nzima ililipuka kwa makelele ya hali ya juu baada ya wanaume kuona mrembo huyo akijichanganya changanyikeni..



" Wangu huyo wangu huyo!!! " oya oya tuheshimiane basi wako kivipi?? '' Oyaaaa!! Acheni kuzingua tutarushiana chupa za bia humu??? " weweeee!! Nyie mshakuwa wazee watoto kama hao tuachieni vijana.. '' Ku**nina acha umama dogo nani mzee?? Utachezea vitasa?! Oohooo!!..... ''



Unaambiwa pale ndani kwa mda huo palikuwa hapakaliki, kila mtu anamgombea huyo mwanadada rugha za matusi na kejeli ndizo zilizotawala kwa mda huo, lakini fujo hizo zikaja kuzimwa na kijana mmoja mwenye umbo flani wanaume hulipenda sana! Yaani kaenda juu kidogo halafu kajazia misuli na kifua asikwambie mtu! Si mwingine huyo anaitwa DANIEL MASUBWA (DANI)



Alifika pale na kumshika mkono Ashura kisha wakaondoka! Vijana wote mle ndani wakabaki kushangilia, Ashura na Dani wakatokomea moja kwa moja katika chumba kimoja ambacho inasadikika huyo jamaa alikuwa ameki-odi, mle ndani kulikuwa na chupa kadhaa za bia, sinia la nyama choma pamoja na kachumbari iliyotengeneza kwa umahiri wa hali ya juu!



" Karibu wangu jiskie upo kwako '' sauti ya Daniel ilisikika..

" Asante japo mimi sijiskii kula kwa sasa hivi ''

" kwanini jamani mtoto mzuri?? ''

" sijikii njaa ''

" basi piga hii hapa ili tukianza kupelekana mpute mpute hapa usichoke... '' Daniel aliongea huku akimpa Ashura chupa ya Castle, Ashura alipokea kisha akaifungua na kuinyonya kwa kasi mpaka ikafika kati, alipumzika kidogo kisha akaimalizia na kudai nyingine, Daniel alimpatia KILIMANJARO safari hii. nayo pia aliikung'uta kama maji..!! Duuh! Kumbe Ashura ni mnywaji kiasi hiki???



Baada ya hapo wakabebana mpaka kunako kijitanda kilichokuwa pembezoni mwa chumba hicho na kurushina huko.... Kilichojiri...!! Kilichofuata...!! Wote mnajua mechi kali mpaka kucheeeee!!!!

************************

SONGEA...... Mkuu wa kituo cha polisi ismani pamoja na kijana wake waliwekewa ulinzi mkali siku hiyo mpaka kunakucha walikuwa bado wapo kwenye ulinzi, na asubuhi na mapema ikiwa ni mida ya saa kumi na mbili polisi hao walitolewa na kupelekwa moja kwa moja mpaka sehemu moja ambayo ilionekana ni ukumbi mkubwa wa mapumziko au wa kupatia chakula kwani kulikuwa na viti na meza nyingi sana pia pembeni kulikuwa na flat creen TV Ya nguvu na kulikuwa kuna habari inatanganzwa kwenye chanel iliyokuwa ikioneshwa wakati huo. Wapelelezi hao walitega masikio na macho yao vyema ili kuona na kujua nini kinatangazwa!



Habari ilikuwa inasema............

,,

......Mtu mmoja amefariki dunia na mmoja kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo usiku katika eneo la makona ya nyang'oro chanzo cha tukio hilo ni MAJAMBAZI Wenye silaha walivamia roli kubwa la mizigo lililokuwa likitoke mkoani mwanza kwenda tunduma, duru zinasema roli hilo lilisimama katika sehemu moja baada ya kukuta gari ndogo aina ya VX Ikiwa imepata ajali watu hao walikuwa na nia ya kutoa msaada lakini kumbe mahali pale kulikuwa na majambazi ambapo punde tu! Baada ya roli hilo kusimama kondakta alipigwa jiwe la kichwa dreva nae alipojaribu kujitetea alipigwa risasi ya kichwa na kupoteza maisha papo hapo.. Na wale majambazi kupora mali zote na kutoweka nazo......

,,

Ile taarifa iliwaacha vinywa wazi wale polisi hawakujua imetokeaje iyo ingawa vijana wengine wa jeshi la polisi wapo kule?? Au walirudi?? Mkuu alikuwa akijiuliza mara mbilimbili pasipo kupata jibu, hali sasa ilianza kuwa tete kwa askari hawa kwani walianza kujikuta katika maswali mengi yasiyo na majibu, mawazo tele hata hamu ya kazi walikosa tena....



Sasa wakiwa bado kwenye tafakari hiyo mara.. Mtu mmoja mwenye kuvalia suti na akionekana ni mtu wa pesa kidogo kwani mtu huyo alikuwa na urefu wa wastani, pia kitambi alikuwa nacho licha ya hilo pia alikuwa na suti ya gharama kali, mtu huyo ambae mkononi alikuwa na laptop alijongea mpaka karibu na polisi hao kisha kukaa karibu kabisa hapo...



" Habari zenu wakuu?? '' yule mwanaume alisalimia.

" Salama.. Salama za kwako?? " Wote kwa pamoja waliitikia na pia kumrudishia salam...

" za kwangu njema kabisa karibuni..... ''

" asante sana mkuu ''

" Ok ili kwenda na mda nimekuja hapa kuitika wito kutoka kwenu ''



Wale polisi walitizamana baada ya kugundua yule ni mtaita yaani ndiyo bosi wa hii kampuni yenye kumiliki majumba ya kutisha humu ndani na yamezungushiwa uzio wa kufa mtu....!! Magari ndiyo usiseme



" Ahaa kamanda hapo unaitwa nani?' '' Huyo bosi aliludia swali jingine baada ya kuona la mwanzo halijajibiwa mpaka dakika hiyo,, sasa kibaya zaidi ni kwamba hata swali hilo ambalo lilikuwa linahusu mkuu wake Charles pia nalo halijajibiwa, hii ilipelekea yule tajiri kuanza kuingiwa na wasiwasi akizani kuwa huenda wale siyo polisi na kuna mchezo mchafu anachezewa ndani ya kampuni yako na wazo la haraka alilolipata kichwani mwake ni kuweka tahadhari...

************************

IPAMBA HOSPITAL..... Mwanamama Saida alikuwa katika majonzi makubwa sana hasa alipoyafikiria matamshi ya mumewe kupitia simu mda mchache uliopita alijikuta akiangua kilio kisichokuwa na mfano kwani hakuwahi kutegemea hata siku moja kama Patrick angekuja kuanza kumfanyia ukatili wa namna hiyo, kuna mda Saida alianza hata kujutia kuolewa na Patrick hii ni kutokana na anavyoutesa moyo wake kwa mda huo kitu kinachopelekea hata atamani kujiua maana kila akifikiria walikotoka mpaka hapo walipofikia kiukweli wamepita njia nyingi, mbaya na za hatari ili tu! Kufanya maisha yao yawe mazuri ila cha ajabu leo hii anaambiwa kila neno analolitamka yeye anaambiwa na Patrick anahisi maneno yake hutoka na funza!! Wenye harufu kali yaani mpaka matapishi humjuia Haaaaa!!



Kila saida alipoyakumbuka yale maneno alihisi kitu kama msumari wa moto ukipenya kati kati ya moyo wake na kumsababishia maumivu makali yasiyovumilika! Mashavu ya Saida yaliloa machozi yaliyotokana na kilio cha mda mrefu,



Pale chumbani madaktari na manesi wote walikuwa wameondoka na kumwacha Saida akiwa peke yake.. Mara! Mlango wa wodi hiyo ulifunguliwa, Haraka Saida akayaelekeza macho yake huko.. Laa!! Haula!! Hakuamini macho yake baada ya kumuona Patrick akiwa katika sura ya kikali kweli kweli akiingia wodini huo. Saida alihisi mwili mzima kama umepigwa shoti vile....



" Sikia wee! Malaya hebu niambie ulikuwa unakwenda wapi mpaka kuniulia gari yangu??? ''



Patrick aliuliza kwa ghazabu huku akichomoa bastora yake na moja kwa moja kuielekeza kichwani kwa Saida, Na wakati huo Saida kabaki kinywa wazi haelewi nini afanye, wala nani atakuwa msaada wake na wodini wapo wawili tuu! PATAMU HAPO...



Patrick aliuliza kwa ghazabu huku akichomoa bastora yake na moja kwa moja kuielekeza kichwani kwa Saida, Na wakati huo Saida kabaki kinywa wazi haelewi nini afanye, wala nani atakuwa msaada wake na wodini wapo wawili tuu!

******************

Sanjali na yote hayo Saida hakuonesha kushtuka wala kutetemeka bali alibaki kumtumbulia macho Mumewe Patrick ambae hadi mkono ulikuwa unatetemeka kwa hasira kali alizokuwa nazo..



" Niue '' Saida aliongea maneno yaliyozidi kumghazabisha Patrick..

" Ivi we mwanamke mhuni usie na haya una akili wewe??? Nitakupoteza mbwa wewe!! '' Patrick aliongea kwa ghazabu huku akizidi kumsogezea Saida bastora kichwani huku akiwa kaikamata mikono yote..!!



" Tatzo lako hujui kama humu kuna CCTV We thubutu tu! ''

" Eee?? '' Patrick alishtuka na haraka kuficha bastora yake..

" Fyooo! Nini hujaskia au?? '' Saida nae akaja juu,

" Ahaa!! Hakuna shida ''



Patrick alikasirika kwa jibu lile alilopewa na mkewe na hakutaka tena waendelee kujibizana mle ndani akatoka kwa hasira na kuuvuta mlango kwa hasira kisha akatoka na kuuachia ukajibamiza kwa nguvu mpaka watu takribani hospital nzima wakasikia si unajua tena majengo yavyosambazaga sauti??



Hamadi Patrick ndo anaanza kuikamata kordo ile ndefu mara wakakutana uso kwa uso na bwana Rous nae akitokea vyumba vingine, Rous alimtilia shaka Patrick kwa kubamiza vile mlango moja kwa moja akatambua kuwa huenda ndiyo huyo mume wa yule mama, si akamstopisha kwa kumweka mkono kifuani, na Patrick alivyo mwoga akasimama na kutulia tuli kama maji ya mtungi.

************************

Yule mwanaume ambae inasadikika ni bosi wa kampuni hiyo alimgundua kuwa yule kamanda wake Charles alikuwa kwenye dimbwi kubwa la mawazo ila hakujua ni ya nini??



" Samahani wakuu jana nilipewa taarifa kuwa roli linalofanana na maroli ya kampuni yangu limehusika katika ajali huko Iringa katika tarafa ya Ismani, kijiji cha nyangoro, kitongoji cha Kibaoni katika makona ya mlima nyang'oro je?? Ningependa kujua utaratibu ukoje?? ''



Charles alimtizama kamanda wake ambae mda wote huo alikuwa kwenye kigugumizi kikali na sijui ni kwanini?? Charles akaona ajibu yeye tu maana mkuu wake zimehama kabisaa!!



" ni kweli bosi Scania hiyo imewekwa chini ya ulinzi baada ya waendeshaji kuitelekeza na wao kutokomea kusikojulikana! ''

" Ok je?? Nyinyi mmekuja kwa lengo gani labda?? ''

" Aaa tumegundua kuwa gari hiyo imefungwa CCTV camera hivyo tumekuja kuomba laptop iliyounganishwa na camera hiyo ili tuweze kuona ilikuwaje?? ''

" Sawa na kuhusu hilo msiwaze na pia madreva wangu hawakukimbia ila walikwepa kidogo tu na watatua songea asubuhi hii ''



Wakati wanaendelea kuongea hayo mara mkuu wa kituo alionekana akitoa simu na kutaka kupiga ila akazuiliwa!



" Samahani afande hili eneo haturusu watu kuongea na simu tafadhari ''

" Ahaa nimekuelewa ''



Basi yule bosi aliwaambia kuwa atawapa iyo laptop ila mpaka waendeshaji wa gari hiyo wafike, hakuna aliekuwa na pingamizi juu ya hilo, basi yule bosi akatoka zake nje huku akiwaacha wageni hao wakitizamana usoni.



" Mimi unajua sielewi chochote?? '' Mkuu wa kituo alimwambia kijana wake Charles baada ya kuona yule mwanaume ameenda..

" Daah! Mkuu hata mimi nashangaa nahisi kama hii taarifa imechapiwa,... ''

" Hapana hii ni midia kubwa hawawezi kurusha taarifa za uongo huu ni ukweli mtupu, na sijui Dickson kafanya kazi gani huko.. '' Mkuu aliongea kwa masikitiko yaliyochanganyikana na Hasira kali sana,, mara gafla mlango ukasukumwa na vijana wawili wakaingia huku wakiongoza na bosi mwenyewe na si wengine bali ni Bakari na Moses...

************************

UNAJUA MKASA MZIMA UKOJE???

Ni hivi wakati yule kondakta na dreva wake wanashambuliwa na majambazi Dickson na kikosi chake walikuwa wakishuhudia moja kwa moja bila chenga lakini hakuna aliethubutu kufanya chochote kwani wale majambazi walionekana kuwa na siraha hatari na za kisasa zaidi hivyo kifupi tu! Polisi waliwaogopa wahalifu hao!



Mshindo ule uliopiga na bunduki ya majambazi risasi yake ilimpata barabara kabisa dreva huyo katika paji la uso na kufanya kichwa kugawanyika na kutoka vipande vipande,! Hiyo ni AK47 Baba! Ni shiida!,, Wakati huo yule kondakta alikuwa bado kazimia katika matairi ya gari ya Saida, wale majambazi walifanya upesi kuwapekua pekuwa pamoja na kupekua garini na kubeba kila kilichobebeka na kutokomea msituni..



Ilipotimu saa kumi na moja alfajiri yule kondakta aliweza kuzinduka huku akiwa na wenge zito kweli kweli alianza kuchunguza mazingira huku akivuta kumbukumbu mpaka pale fahamu zilipokaa sawa na kukumbuka kila kitu, taratibu alinyanyuka pale chini huku mwili mzima ukiwa unanuka damu kwani pale kichwani walitia ngeo ya maana iliyopelekea shati kuloanishwa na damu sanjali na mwili mzima kunuka damu.



Alinyanyuka huku akipepesuka na kutembea kwa mwendo wa kuyumba yumba mpaka kwenye roli lao alikuta pako kimya mno! Na wakati huo kunaanza kupambazuka, akazunguka upande wa pili kwa dreva wake. Cha kwanza anakutana na matone ya damu chini ya mlango alipopandisha macho juu.. daaah! Hakuamini macho yake baada ya kuona kichwa cha rafiki yake kikiwa kinaning'inia mlangoni huku kikiwa kimechakazwa kweli kweli na mwili umekwema ndani kwani akabla hajadondoka nje mlango wa gari ulijifunga na kumbana dreva huyo hivyo akabaki akining'inia..



Yule kondakta alishikwa na uchungu mkubwa uliopelekea aanze kulia kilio cha kwikwi huku akizunguka upande wa pili kwenda kuchukua simu ya dharura ambayo huwa imehifadhiwa kwenye sehemu maalumu kwenye gari na hii ni spesho kwa shida za zarura kama hizi, yule konda alifanikiwa kuikuta simu hiyo na bila kupoteza mda akaikwapua na kuanza kutafuta namba za Vituo mbali mbali vya polisi maana simu hiyo ya dharura imeunganishwa na vituo vya polisi karibia nchi nzima, sasa kondakta huyo alianza kuisaka na ya kituo cha police ismani ila kwa bahati mbaya hawakupatikana kwani mkuu hakuwepo pale pamoja na vikosi vyake. Kijana huyo hakutaka kukata tamaa akili ikampeleka mpaka Migori pale pia kuna kituo cha polisi, haraka akaanza kuitafuta migori mwishowe akaipata namba ya kituo hicho.. Bila kupoteza mda akapiga,, na kwa upande wa mda ilikuwa inasomeka saa kumi na mbili kamili. Simu ilianza kuita na baada ya mda kidogo ilipokelewa...



" Halow...!! '' sauti nzito ya kibesi ilisikika upande wa pili...

" Ndiyo mkuu habari ya asubuhi ''

" salama karibu unaongea na kamanda wa polisi kituo kidogo migori ''

" Asante na unaongea na Musa Abdalah kutoka kampuni ya HILL LIMITED ''

" Ndiyo tunatambua kuwa namba hii ni ya kampuni ya HILL LIMITED Karibu ''

" Samahani tumevamiwa na majambazi katika makona ya nyang'oro tukiwa njiani kutoka mwanza kuelekea TUNDUMA ''

" Umesemaje?? Hamjaumizwa?? ''

" Mpaka sasa dreva ameshapoteza uhai kwa kupigwa risasi ya kichwa '

" Ooooh!! Shiit tunakuja ''

" Asante ''



Polisi huyo ni mwenyeji sana wa barabara hiyo hivyo hakutaka kupoteza mda wa kuendelea kuhojiana na mhanga huyo zaidi ya kukata simu, mkuu huyo alitoka ofisini mwake mkuku mkuku mpaka nje akawakuta vijana wake wakipiga TIZI Ya asubuhi..



" Oya!! Oyo!! Hebu acheni kwanza kuna tatizo limetokea! ''

" Tatizo gani?? '' mmoja aliuliza...

" Kinahitajika kikosi cha askari 20 Waende haraka iwezekanavyo katika makona ya nyang'oro kuna gari imevamiwa na majambazi hivyo tunahitajika mara moja.. ''

Kamanda huyo aliongea kwa msisitizo wa hali ya juu!!



Vijana wale wale waliokuwa wakifanya zoezi pale ndiyo walijikata watu kama 25 Hivi na kuingia ndani kujiandaa.. Baada ya dakika tatu wote walitoka wakiwa kamili kwa lolote! Dreva wa kuwaendesha aliitwa MOHAMED MADUO Kijana mmoja hatari sana kwenye usukani, na mara nyingi huwa anakodiwa na vikosi vya zima moto kutokana umahiri wake wa kukimbiza gari,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Difenta ilitolewa kutoka katika maegesho na vijana wote wakapanda akiwemo kamanda wao, basi gari ikaanza kuondolewa. Sasa ile wanataka kuunga lami tu mara wakamuona mpiga picha na pia ni mwaandishi wa habari kanda ya ismani bwana KOKOREZA PHOTO Akiwa zake taratibu na kibaiskel chake kidogo aina ya BMX Akitokea maeneo ya bwani kusogea lami, polisi hao wakaona nivema waende nae hivyo difenta ikasimamishwa. Askari mmoja alimwendea mpiga picha huyo na kumweleza kuwa walihitaji kwenda nae sehemu moja ambako kumetokea uvamizi ili aweze kusambaza taarifa hiyo kwa maana huyo jamaa anafanya kazi na midia mbali mbali..


ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog