Search This Blog

Friday, 18 November 2022

SIRI : JASUSI/GAIDI - 5

 





    Simulizi : Siri: Jasusi/Gaidi

    Sehemu Ya Tano (5)









    “Faqir ahsante sana kwa msaada huu mkubwa” akasema Vahid akiwa garini na Faqir aliyemfuata nyumbani kwake kama alivyomuahidi “Usijali mzee” akasema Faqir aliyekuwa katika usukani.Vahid akatoa bahasha katika mfuko wa koti na kumpatia Faqir “Hii ni ahsante yangu kwa msaada wako” akasema Vahid “Mzee hakuna haja.Huu ni wajibu wangu kukusaidia” akasema Faqir “Faqir naomba uchukue ahsante hii” akasisitiza Vahid na Faqir akachukua bahasha ile iliyokuwa na fedha. Walifika katika nyumba alimo Mathew http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mulumbi Faqir akaelekeza kamera zote kuzimwa kisha akamuongoza Vahid hadi katika chumba cha Mathew aliyekuwa amejilaza kitandani.Faqir akatoka mle ndani na kuwaacha Vahid na Abu Zalawi. “Abu Zalawi habari yako” “Nzuri mzee Vahid karibu tena” “Ahsante.Nimekuja tena kukuona na hii itakuwa ni mara ya mwisho kuniona hapa” akasema Vahid na kutoa ile diski mweko akamkabidhi Mathew “Habiba Jawad amenituma nikuletee mzigo huu” akasema Vahid.Mathew akaitazama ile diski mweko halafu akasema “Nashukuru sana mzee kwa kunifikishia mzigo huu muhimu.Kama hutojali ninaweza kuzungumza na Habiba Jawad? Akauliza Mathew.Vahid akatoa simu na kumpigia Habiba halafu akampa Mathew ile simu “Hallo Vahid” akasema Habiba “Mama Habiba unaongea na Abu Zalawi” akasema Mathew “Mathew unaendeleaje? “Ninaendelea vizuri mama.Wananitunza vizuri ninapata kila ninachohitaji” “Vizuri sana.Naamini Vahid amekufikishia mzigo” “Nimeupata mama nashukuru sana” “Sawa Mathew nakutakia kila la heri na pale utakapohitaji chochote usisite kunijulisha nitakusaidia kadiri niwezavyo” “Nashukuru sana.Baada ya kuipata orodha hii sasa ninaanza rasmi kazi yangu” “Sawa Mathew.Nawal tayari amekwisha fika hapa akitokea Tanzania na kesho atakuja Tehran.Utaonana naye hiyo kesho” akasema Habiba na kuagana na Mathew ambaye alimrejeshea Vahid simu yake “Nashukuru sana mzee” akasema Mathew na Vahid hakutaka maongezi zaidi akamuaga Mathew na kuondoka. “Habiba amefanya jambo la maana sana kunipatia orodha hii” akawaza Mathew baada ya Vahid kuondoka. ************ Saa mbili kasoro dakika kumi na saba,gari dogo liliwasili katika geti la nyumba alimo Mathew Mulumbi.Kutoka katika lile gari akashuka mtu mmoja aliyevalia nadhifu sare za uhudumu wa hoteli akaenda kugonga geti la nyumba ile na mmoja wa walinzi akafungua mlango mdogo akatoka wakasalimiana na muhudumu Yule wa kike mwenye tabasamu la kuvutia “Nimeagizwa kuleta chakula hapa” akasema Yule muhudumu aliyejitambulisha kwa jina la Munira. “Chakula? Akauliza Yule mlinzi “Ndiyo” akajibu Munira “Nani amekutuma ulete chakula hapa? Akauliza Yule mlinzi “Yametolewa maelekezo na kiongozi mmoja wa serikali katika hoteli yetu kuwa chakula kiletwe hapa” akasema Munira “Kiko wapi hicho chakula? Akauliza Yule mlinzi na Munira akaenda katika gari akafungua mlango na maboksi ya chakula yakaonekana. “Subiri kidogo” akasema Yule mlinzi na kurejea ndani akawafuata wenzake waliokuwa sebuleni wakicheza karata akawaeleza kuhusu chakula kile kilicholetwa.Wote wakabaki wanashangaa na kujiuliza nani ametuma chakula kile.Baada ya kujadiliana kwa muda wakakubaliana wachukue chakula kile wakiamini labda kimetumwa na mmoja wa wakubwa zao.Mchezo wa Karata ukaishia pale wakatoka kwenda kuchukua chakula kile kilicholetwa.Munira hakuruhusiwa kuingia ndani akaagana nao na kuondoka.Maboksi yale ya chakula yakapelekwa sebuleni na kufunguliwa.Wote wakapatwa na mshangao mkubwa kwa vyakula walivyovikuta ndani ya makosi yale.Kulikuwa na chakula ghali sana kinachoitwa Saffron na kingine ni Cavier.Walibaki wanashangaa kiongozi gani aliyeweza kuwanunulia chakula ghali namna ile. “Hakuna haja ya kushangaa ndugu zangu.Hii ni neema imetuangukia hivyo tukae mezani tuendelee kula.Sijawahi kuonja hiki chakula Saffron katika maisha yangu leo itakuwa mara ya kwanza” akasema mmoja wa walinzi aliyefahamika kama Mehdi. Maandalizi yakafanyika na wote wakakaa mezani wakaanza kupata chakula huku geti likiwa limefungwa.Hawakuacha hata mlinzi mmojan je.Hakuna aliyekuwa na wasi wowote na usalama wao.Sebuleni kulitawala vicheko vya furaha wote wakikifurahia chakula kile ghali sana “Jamani mbona tunakula peke yetu na kumsahau Abu Zalawi? Akauliza Najib ambaye huusika na mfumo wa kamera wa nyumba ile “Najib anasema kweli.Abu Zalawi ni mtu muhimu sana.Anatakiwa aje kujumuika nasi hapa katika chakula hiki kitamu” akasema Shams aliyekuwa kiongozi wa walinzi usiku ule.Najib akainuka kwenda kumuita Mathew. “Abu Zalawi tunaomba uungane nasi katika chakula” akasema Najib na Mathew ambaye alihisi njaa akainuka wakaelekea sebuleni.Mara tu walipotembea hatua tatu baada ya kutoka chumbani ikasikika sauti ya muanguko wa viti na sahani.Mathew akasimama na kumtaka Najib kusimama. “Subiri kidogo ! akasema Mathew na kutega sikio kusikiliza “Hakuna kitu Abu Zal….” “Shhhh !! akasema Mathew na kumfanyia ishara anyamaze kimya kisha akamtaka amfuate wakaanza kutembea kwa kunyata kuelekea sebuleni .Nyumba ile ilikuwa kubwa na yenye vyumba vingi. Mara tu walipokaribia kufika sebuleni wakasikia sauti kali ikiuliza “Yuko wapi Abu Zalawi ?! “Yuko chumbani kwake ! akajibu mmoja wa wale walinzi.Mwili wa Mathew ukasisimka. “Jina lako nani? Akauliza Mathew “Naitwa Najib” “Sikiliza Najib tumevamiwa.Hawa waliovamia hapa wananitafuta mimi.Una bastola? Au kuna chumba cha silaha humu ndani? “Ninayo bastola lakini iko ofisini kwangu” akajibu Najib “Naihitaji hiyo bastola ili niweze kupambana na hawa jamaa” akasema Mathew kisha kwa kunyata wakarudi nyuma na kuelekea katika ofisi ya Najib “Kuna kamera ngapi za ulinzi katika nyumba hii? Akauliza Mathew akiyaelekeza macho yake katika runinga iliyokuwa inaonesha picha mbali mbali kutoka katika kamera zinazoizunguka ile nyumba. “Kuna kamera kumi na sita” akajibu Najib “Nataka kamera ya sebuleni nijue wavamizi wako wangapi” akasema Mathew na Najib akabofya kamera ya sebuleni na kile kilichokuwa kinaendelea sebuleni kikaonekana.Walinzi wawili walikuwa wamelala chini wakivunja damu ni wazi walikuwa wameuawa.Wavamizi hawakuweza kuonekana sura zao walikuwa wamezifunika kwa kofia maalum za kuziba uso na kuacha macho pekee. Jumla yao walikuwa saba mle ndani.Nje walionekana wawili wakiwa katika kibaraza wakiwa na bunduki Najib alifungua droo ya meza yake ambamo kulikuwa na bastola mbili akampatia Mathew moja naye akabakiwa na moja.Mathew akaihakikisha ina risasi za kutosha kisha wakatoka ndani ya kile chumba Najib akaanza kumuelekeza Mathew njia ya kuelekea sebuleni kwani nyumba ile ilikuwa na zaidi ya korido moja.Mara wakasikia hatua za watu wakielekea upande ule waliopo wakajibanza pembeni ya kabati tupu.Baada ya muda mfupi wakapita wavamizi wawili wakiwa wamemtanguliza mbele mmoja wa walinzi. “Hawa jamaa lazima wanaelekea katika chumba changu” akasema Mathew na kutoka mahala walipokuwa wamejibanza akaanza kunyata kuwafuata wale jamaa ambao kama alivyokuwa amehisi kweli walikwenda hadi katika chumba cha Mathew.Mlinzi akakinyonga kitasa na kuufungua mlango.Mmoja wa wale jamaa akamrukia mlinzi teke zito akaangukia ndani ya kile chumba kisha kwa kasi ya upepo jamaa wale wakajitoma ndani.Chumba kilikuwa kitupu.Mathew hakuwemo. “Abu Zalawi hayupo katika hiki chumba.Narudia tumemkosa Abu Zalawi” akasema mmoja wa wale wavamizi aliyekuwa ameweka sikioni kifaa cha kumuwezesha kuwasiliana na wenzake. “Tuonyeshe haraka wapi alipo Abu Zalawi? Akauliza mmoja wa wavamizi wale huku akimuelekezea Yule mlinzi bastola kichwani akitishia kumuua “Chumba chake ni hiki.Alikuwemo humu ndani na sijui amekwenda wapi! Akajibu Yule mlinzi huku akitetemeka kwa woga. “Kwa mara ya mwisho nakuuliza kiko wapi chumba cha Abu Z…………..” Hakumaliza sentensi yake kwani mlango ulipigwa teke zito ukafunguka na mtu mmoja akajiviringisha hewani na kutua mle chumbani.Wakati akitua aliwaona wale jamaa namna walivyokuwa wamesimama na wakati wakijiuliza nini kimetokea Mathew akazunguka mateke mawili mfululizo na wale jamaa wawili wote wakajikuta chini.Mmoja wa wale majasusi akainuka haraka lakini macho ya Mathew yalikuwa makali kama macho ya tai yalikwisha muona Yule jamaa.Kwa kasi ya ajabu akaruka juu na kwa kutumia mguu wake wa kulia akamtandika Yule jamaa teke kali katika mkono wake uliokuwa umeshika bastola,akiwa bado hewani mguu wake wa kushoto ambao huutumia mara chache katika mapigano kutokana na umuhimu wake ukatua katika shingo ya Yule jamaa ambaye alijibamiza ukutani kwa kishindo na kuanguka chini.Mathew akatua chini na kugeuka haraka sana akamuona Yule jamaa mwingine akiwa ameizinga bastola akimuelekezea lakini ukasikika mlio wa risasi na Yule jamaa akaanguka chini.Mlangoni alikuwa amesimama Najib akiwa na bastola.Ndiye aliyempiga risasi yule jamaa. “Ahsante Najib” akasema Mathew na kuiokota bastola ya yule jamaa aliyempiga teke,akamfuata akamtazama alikuwa anatokwa na damu mdomoni.Hakuwa na dalili za uhai.Mlinzi Yule aliyekuwa chini hakuamini kile kilichokuwa kimetokea mle ndani.Aliona kama filamu. “Bastola za hawa jamaa zote zimefungwa kiwambo cha kuzuia sauti hivyo basi mlio wa risasi uliosikika lazima utawapa mashaka wenzao na wanaweza wakafika hapa kujua kile kinachoendelea.Tunatakiwa kwenda kuwakomboa wenzetu walioshikiliwa kule sebuleni.Kuna mlango mwingine wa kutokea nje? Mathew akauliza “Ndiyo upo mlango wa nyuma” akajibu Najib kisha wakatoka ndani ya kile chumba kila mmoja akiwa na bastola wakatembea kwa tahadhari kuelekea katika mlango wa kutokea upande wa nyuma wa ile nyumba.Mathew akawataka Najib na Yule mlinzi mwingine wajifiche sehemu na wamuache yeye akapambane na wale wavamizi kwani alikwisha tambua uwezo wao katika mapambano ni mdogo kuliko wa wale wavamizi.Mkononi alikuwa na bastola moja ya wale jamaa waliowaua ndani ya kile chumba. Mbele ya kibaraza kulikuwa na watu wawili wakiwa na bunduki ndogo.Mathew aliyekuwa amejificha sehemu yenye kiza akazidungua taa mbili kubwa zilizokuwa zinamulika sehemu ya mbele ya ile nyumba.Eneo la mbele likawa na mwanga hafifu kutoka katika taa ya barazani.Wale jamaa wawili wakastuka sana kwa kile kilichotokea.Kabla hawajatafakari nini cha kufanya Mathew akaizinga tena bastola na kuachia risasi mbili akiwalenga wale jamaa vichwani.Walipoanguka chini Mathew akatoka mbio kuelekea katika kibaraza na kabla hajakifikia mlango ukafunguliwa wakatoka jamaa wawili.Mathew hakuwakawiza akajitokeza na kuachia risasi zilizompata jamaa mmoja na mwingine akaurukia mlango ili kurejea ndani lakini Mathew alikuwa mwepesi zaidi yake akamuwahi kwa risasi na jamaa akaanguka ndani kwa kishindo kama jiwe huku akivuja damu. Kitendo cha mwenzao kuanguka mle ndani akiwa anavuja damu kiliwastua wavamizi watatu waliokuwa sebuleni wakiwashikilia mateka walinzi wa ile nyumba.Kabla hawajafanya chochote kufumba na kufumbua Mathew Mulumbi akiwa na bastola mkononi akaviringika akitokea nje na kuingia mle sebuleni huku macho yake yakizunguka kama kinyonga na kuwatazama namna wale wavamizi walivyokaa mle sebuleni.Kabla hajatua chini tayari mmoja wa wale wavamizi alikuwa chini akivuja damu baada ya kuchakazwa kwa risasi.Mmoja wa walinzi baada ya kuwaona wale wavamizi wote wameyaelekeza macho yao kwa Mathew akachomoa kisu taratibu na kumrukia mmoja wao akamchoma kisu cha mgongo akachomoa na kumchoma tena halafu akamtandika teke akaanguka chini.Walinzi wote wakasimama na kunyakua silaha zao.Alibakia mvamizi mmoja akaielekeza bastola kichwani na kujipiga risasi akaanguka chini.Mathew akiwa ameongozana na walinzi wale wakatoka nje ya ile nyumba na kuanza kuikagua kama kuna mtu mwingine aliyebakia lakini hakukuwa na mtu yeyote. “Hawa jamaa walikuja bila gari? Akauliza mmoja wa walinzi “Hawakuwa peke yao.Lazima walikuwa na wenzao ambao baada ya kugundua wenzao waliokuwa ndani wamezidiwa nguvu na kuuawa wakakimbia” akasema Mathew Walirejea ndani na kuwatazama wale walinzi wawili waliokuwa wamelala chini wamepigwa risasi,tayari awlikuwa wamekufa.Simanzi kubwa ikatanda.Wakati wakihuzunika Mathew akaanza kuwapekua wale wavamizi kuona kama angepata kitu chochote kutoka kwao lakini hawakuwa na kitu zaidi ya kuvaa vifaa vya mawasiliano. “Hawa ni wale majasusi wa Mossad waliotumwa kuja kuniua.Kazi imeanza” akawaza Mathew na kumuelekeza Shams kutoa taarifa kwa Faqir kumjulisha kile kilichotokea. RIYADH – SAUDI ARABIA Gari la kifahari la Mercedece Benz likiendeshwa na Habiba Jawad liliwasili katika hoteli ambako alielekezwa na David Walker kwenda kukutana na mtu aliyepewa ujumbe muhimu ampelekee.Usiku huu Habiba alikuwa peke yake garini kwani David alimtaka asiongozane na walinzi wake au mtu yeyote anapokwenda kuonana na huyo mtu kwani ni mtu ambaye hataki kuonekana na watu.Habiba hakuwa na wasi wasi hata kidogo,akashuka garini na kuelekea katika sehemu ya chakula akasalimiana na watu kadhaa waliokuwa wanamfahamu aliowakuta pale hotelini halafu akatoka na kuelekea katika lifti.Lengo la Habiba kupita sehemu ya chakula ni kumpa ishara Nawal aliyekuwa katika mojawapo ya meza akipata kinywaji taratibu .Nawal alikaa sehemu ambayo angeweza kumuona kila aingiaye na alimuona Habiba Jawad mara tu alipoingia Habiba Jawad akaelekea katika lifti akapanda na kuelekea ghorofa ya kumi na sita ambako ndiko alielekezwa kukutana na mtu huyo mwenye ujumbe maalum.Alishuka katika lifti na kuelekea katika chumba alichoelekezwa.Wakati akipiga hatua kuelekea katika chumba hicho Nawal alikuwa nyuma yake kwa mbali kidogo akimfuata taratibu.Usiku huu Nawl alivaa mavazi ambayo haingekuwa rahisi kumtambua. Habiba alibonyeza kengele ya mlango wa chumba alichoelekezwa na mlango ukafunguliwa.Wakati mlango ukifunguliwa Nawal alikuwa anapita na kuchungulia ndani akamuona mtu mmoja aliyekuwa amevaa suti ya bluu.Habiba akakaribishwa ndani. “Habiba Jawad karibu” akasema Yule jamaa aliyekuwamo mle chumbani. “Habari yako” akasema Habiba “Nzuri Habiba.Karibu uketi” “Sina muda mrefu hapa.Nimefuata ujumbe wangu” akasema Habiba “Sawa karibu uketi” akasema Yule jamaa.Habiba alikuwa amevaa kifaa cha kunasa mawasiliano ambacho kilimuwezesha Nawal kufuatilia mazungumzo yake na Yule jamaa Habiba akaketi sofani na Yule jamaa akaenda katika meza akafungua sanduku dogo akaanza kutoa makaratasi na kuyaweka pembeni kana kwamba kuna karatasi anazitafuta.Wakati akipekua mle sandukuni akapeleka mkono na kubonyeza kifaa Fulani kidogo halafu akalifunga sanduku na kuchukua makaratasi Fulani akayaweka katika meza ndogo. “Kuna ujumbe nimetumwa nikufikishie.Ni ujumbe muhimu mno na wa siri kubwa ndiyo maana ulipewa maelekezo uje peke yako bila walinzi kwani sitaki kujulikana kama nimeonana nawe” akasema Yule jamaa ambaye hakuwa amejitambulisha jina lake. Wakati akiyapanga yale makaratasi mara mlango ukafunguliwa wakaingia watu wanne na bila kuongea chochote Habiba akakamatwa na kuwekewa kitambaa cheupe puani baada ya muda akapoteza fahamu. Nawal aliyekuwa amejibanza katika kona akiyaelekeza macho kule katika chumba alimoingia Habiba,aliuona mlango wa chumba kinachotazamana na kile alimoingia http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Habiba ukifunguliwa wakatoka watu wanne na kuingia katka chumba alimo Habiba. “Kazi imeanza” akawaza halafu akatoka pale mahala alipokuwa akaanza kuelekea katika chumba walimoingia wale jamaa ambamo ndimo alimo Habiba Jawad.Gauni refu alilokuwa amelivaa akalifungia kiuononi halafu akachomoa bastola yake iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti akausogelea mlango Mle ndani ya chumba wale jamaa wakajiandaa kumbeba Habiba ili kumtoa ndani ya kile chumba.Jamaa mmoja akaufungua mlango kwa lengo la kuchungulia nje kama kuna mtu katika korido.Mara tu alipofungua mlango na kutoa kichwa alikutana na teke zito toka kwa Nawal lililomrejesha ndani akaangukia meza ya kioo ikavunjika.Kwa kasi ya kimbunga Nawal akajitoma ndani.Kilikuwa ni kitu cha ghafla sana ambacho wale jamaa hawakuwa wamekitarajia hivyo Nawal hakupoteza muda akaanza kugawa dozi ya risasi kutoka katika bastola yake.Hakuna aliyekuwa amejiandaa kwa shambulio hivyo Nawal alimiliki mchezo na hakuna aliyepata nafasi ya kuchomoa bastola yake.Ndani ya sekunde chache chumba kilikuwa kimya.Wale jamaa wote walikuwa chini wakivuja damu.Wote walikuwa na matundu ya risasi katika mapaji yao ya uso.Baada ya kumaliza mchezo ule Nawal akachukua chupa Fulani ndogo kutoka mfukoni akaifungua na kumuwekea Habiba puani baada ya muda Habiba akaanza kupiga chafya mfululizo na kuzinduka. “Pole sana mama.Unajisikiaje? akauliza Nawal.Habiba akazungusha macho mle chumbani akawaona wale jamaa waliolala chini wakivuja damu “Ahsante Nawal” akasema Habiba. “Mama tunatakiwa kuondoka mahala hapa haraka sana kwani tayari mauaji yamekwisha fanyika humu” akasema Nawal na kumsaidia Habiba kunyanyuka “Una hakika hakuna aliyesalia? Akauliza Habiba “Nmewamaliza wote hakuna aliyebaki” akajibu Nawal kisha wakatoka ndani ya kile chumba mlimojaa harufu ya damu wakaenda kupanda lifti wakashuka chini.Nawal akaushika usukani wakaondoka mahala pale kurejea nyumbani. Mara tu baada ya kufika nyumbani Habiba akampigia simu Mark Piller akamjulisha kwamba lile zoezi la kumuua limeshindwa kufanikiwa. “Nafurahi kusikia uko salama Habiba.Hata hivyo huu ni mwanzo wa mapambano mapya.G20 wataendelea kukusaka hadi wahakikishe wamekupata ili Mossad waweze kuendelea na mpango wa kumuua Abu Zalawi.Ninashauri uondoke Riyadh kwa muda ukajifiche sehemu Fulani hadi pale mambo yatakapotulia.Niko tayari kukusaidia kwa hilo Habiba.Ninasema hivyo kwa sababu bado tunakuhitaji sana.Wewe ndiye kiungo muhimu kati yetu na Abu Zalawi.Sitaki jambo lolote likupate Habiba ndiyo maana nikaamua kukupa siri zote za mipango ya G20 juu yako” akasema Mark Piller “Mark ninakushukuru sana kwa yote lakini suala la kuondoka na kwenda kujificha halimo kichwani mwangu.Ningeweza kufanya hivyo lakini siwezi kukimbia.Nitaendelea kuwepo hapa hapa Riyadh na mipango yote itakwenda kama kawaida.Usiwe na wasiwasi wowote kuhusu Abu Zalawi atamaliza misheni yake salama hata kama sintakuwepo” akasema Habiba “Habiba bado ushauri wangu unabaki ule ule kwamba uondoke hapo Riyadh uende mahala ukajifiche.Narudia tena ninaweza kukusaidia kwa hilo”akasema Mark Piller “Huna haja yakunisaidia Mark kama ninataka kukimbia na kwenda kujificha ninaweza kufanya hivyo muda wowote bila msaada wako lakini kwa sasa siwezi kukimbia.Mark naomba tujielekeze zaidi katika misheni ya Abu Zalawi tuachane na hili suala la kutoroka.Endelea kufutailia mipango yote ya G20 na unijulishe” akasema Habiba na kuagana na Mark Piller “Siwezi kukimbia na kwenda kujificha kwani kifo tayari kinaniandama.Ninamuona ziraili nyuma yangu hivyo hata nijifiche katika mwamba gani lazima nitakufa tu.Kitu kikubwa ambacho ninajivunia hata kama nikifa leo ni kwamba tayari nimetengeneza bomu litakalokwenda kuwalipua G20 ambalo ni Mathew Mulumbi.Huyu nina uhakika mkubwa sana hata kama nisipokuwepo kwa hatua aliyofikia atakwenda kukisambaratisha kabisa kikundi cha G20 na dunia nzima itafahamu udhalimu unaofanywa na watu hawa” akawaza Habiba Jawad na kumfuata Nawal “Nawal kesho asubuhi utapanda ndege kuelekea Tehran tayari kabisa kwa kumsaidia Mathew Mulumbi” akasema Habiba “Mama nina wasi wasi sana na usalama wako.Hawa jamaa hawataacha kukuandama.Kama utaona inafaa naomba niwepo hapa kwa siku kadhaa kwa ajili ya kuhakikisha unakuwa salama” akasema Nawal “Nawal usihofu kuhusu mimi.Kwa sasa tunapaswa kuelekeza nguvu kubwa kumsaidia Mathew Mulumbi.Misheni yake ni kubwa na yenye manufaa makubwa hivyo kila aina ya msaada tuielekeze kwake.Kesho utakwenda Tehran mimi nitakuwa salama” akasema Habiba TEHRAN – IRAN Faqir Jahid msimamizi mkuu wa nyumba zote za siri zilizo chini ya MOIS alifika kwa haraka sana baada ya kupata taarifa kwamba nyumba ya akina Mathew imevamiwa na watu wasiojulikana. “Poleni sana” Faqir akawapa pole walinzi aliowakuta nje wakilinda.Aliposhuka garini akakimbilia ndani.Kitu cha kwanza alichotaka kufahamu ni kama Abu Zalawi ni mzima “Abu Zalawi ni mzima kabisa tumempeleka kwenye chumba cha mapumziko” akasema Shams na kuanza kumuelezea Faqir namna tukio lile lilivyotokea.Baada ya kupokea maelezo Faqir akaelekea katika chumba alimo Mathew “Pole sana Abu Zalawi kwa hiki kilichotokea.Ahsante pia kwa kuwaokoa walinzi wangu kwani maelezo niliyoyapata kutoka kwao kama si wewe wote wangeuawa” akasema Faqir “Faqir nilikueleza asubuhi kuhusiana na jambo hili nadhani sasa umeniamini” akasema Mathew “Utanisamehe sana Abu Zalawi ni kweli sikuyaamini maneno yako uliponiambia kwamba kuna hatari lakini sasa nimekuamini.Hata hivyo bado najiuliza maswali watu hawa ni akina nani? Wamefahamuje kama uko hapa? Akauliza Faqir “Faqir nina ombi moja kwako na ninataka unisaidie” “Sema Abu nini unahitaji? Akauliza Faqir “Nataka kuzungumza na waziri wa intelijensia wa Iran” “Sassan Mahmoud? Akauliza Faqir “Sifahamu anaitwa nani lakini ninahitaji kuzungumza naye” “Abu Zalawi zipo taratibu za kufuata ka………” akasema Faqir lakini Mathew akamkatisha. “Faqir huu si muda wa kufuata taratibu.Naomba tafadhali unisaidie niweze kuzungumza naye.Kuna mambo ya muhimu sana nataka kumueleza kuhusiana na hiki kilichotokea leo hapa.Bado hatari haijakwisha.Naomba uniunganishe naye nionane naye ana kwa ana usiku huu huu” akasema Mathew na Faqir akaonekana kusita “Faqir ninaomba uniamini.Mimi si mtu mbaya na nina malengo mazuri kwa nchi yenu ndiyo maana niliweza kuweka maisha yangu katika hatari nikawakomboa wale mateka sita nikawarejesha nyumbani.Bado kuna mambo mazito ambayo nataka kuyafikisha kwa waziri muhusika.Nisaidie kwa hilo tafadhali” akasema Mathew na Faqir akaonekana kumuelewa.Akachukua simu na kumpigia waziri Sassan Mahmoud akamfahamisha kuhusiana na tukio lile la uvamizi katika ile nyumba na namna Mathew alivyoendesha mapambano hadi akafanikiwa kuwaokoa wale walinzi na kuwaua wavamizi wote.Ilikuwa ni taarifa iliyomstua sana waziri Sassan “Watu hao ni akina nani na wamefahamuje kama Abu Zalawi amepelekwa katika nyumba hiyo? Akauliza Sassan “Mheshimiwa waziri kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akajibu swali hilo” akasema Faqir “Ni nani huyo mtu? Akauliza Sassan “Abu Zalawi” “Abu Zalawi?! Waziri Sassan akashangaa “Ndiyo mheshimiwa waziri.Anahitaji kuzungumza nawe usiku huu kuna masuala muhimu anadai anataka akueleze”akasema Faqir “Anataka kunieleza kitu gani? “Sifahamu mheshimiwa waziri hajanieleza lakini inaonekana ana jambo la muhimu sana la kukueleza” akasema Faqir “Unamuamini? Akauliza Sassan baada ya kutafakari kwa muda “Mheshimiwa waziri ninadhani ungeonana naye ingekuwa vizuri zaidi.Huyu jamaa anaonekana anafahamu mambo mengi” akasema Faqir “Sawa Faqir fanya utaratibu umlete hapa nyumbani kwangu usiku huu na vile vile maiti zote zipelekwe hospitali hadi pale uchunguzi wa suala hili utakapokamilika” akaelekeza waziri Sassan “Waziri amekubali ukaonane naye usiku huu.Nitakupeleka nyumbani kwake” akasema Faqir na kutoka akaenda kutoa maelekezo halafu akamchukua Mathew wakaondoa kuelekea nyumbani kwa waziri Sassan Mahmoud. DAR ES SALAAM – TANZANIA Helkopta ya SNSA ambayo hutumiwa na makomando wa idara hiyo katika operesheni mbali mbali za usiku ilirejea katika ofisi kuu za SNSA ikatua na makomando wakashuka.Walikuwa wametoka kutekeleza misheni ya kulipua sehemu ya bomba la mafuta ili kuzuia mafuta kwenda bandari ya tanga ambako meli za mafuta za Marekani zilikuwa zinapakia na kuyapeleka Marekani Mkuu wa timu ile ya makomando akamfahamisha Ruby namna kazi ilivyofanyika “Ahsanteni sana kwa kazi hii muhimu” akasema Ruby na kuwataka makomando wale wakapumzike akampigia simu Rais Dr Fabian Kelelo “Mheshimiwa Rais nimekupigia simu kukujulisha zoezi limekamilika na makomando wamerejea salama” akasema Ruby “Kazi nzuri sana Ruby.Tayari taarifa zimekwisha fika kwa mamlaka husika na wanalishughulikia suala hilo kuhakikisha kwamba hakuna madhara makubwa yanayotokea.Tayari mafuta yamekwisha fungwa hivyo hakuna mafuta yanayokwenda Tanga.Nimezungumza na Rais wa Uganda na kumtaka ahakikishe uchimbaji wa mafuta unasimamishwa mara moja.Ruby ninao uhakika mkubwa kwamba mpango huu utakuwa na matokeo mazuri na vikosi vya Marekani vitaondolewa hapa nchini haraka kwani havitakuwa na sababu ya kuendelea kuwepo hapa wakati mipango yao yote imeshindwa kufanikiwa.Kirusi hakijasambazwa na sasa mafuta yamekatwa.Mmepata taarifa zozote kutoka kwa Mathew Mulumbi kuhusiana na misheni yake? Akauliza Dr Fabian “Tumewasiliana na Nawal tayari amefika Ruyadh na kesho ndipo ataanza safari ya kuelekea Tehran kuonana na Mathew.Akifika huko atatujuza kile kinachoendelea” akasema Ruby “Vizuri sana.Naamini kila kitu kitakwenda vizuri.Ruby hakikisheni mnafanya kila linalowezekana kupata taarifa muhimu kutoka kwa hao jamaa mnaowashikilia mkianza na huyo Jenerali William na wale wengine magaidi.Kuna mambo mengi sana tunahitaji kuyajua na kubwa zaidi ni watu wanaoshirikiana nao hapa nchini.Tunatakiwa kufanya usafi mkubwa sana kusafisha hawa wote na asibaki hata mmoja wao.Kitendo cha kushirikiana na hawa mabeberu kuvuruga amani,kuchochea watanzania wauane wenyewe kwa wenyewe ni kitendo kibaya sana na wanastahili adhabu kali ili liwe fundisho kwa wengine ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kazi hiyo tunaianza usiku wa leo kwani kutwa nzima tulikuwa tunashughulikia mpango wa kulipua bomba la mafuta.Kwa kuwa tayari tumeukamilisha sasa tunahamia katika kuwahoji hawa jamaa na ninakuahidi lazima watasema kila kitu” “Sawa Ruby .Kama kuna msaada wowote mtauhitaji msisite kunieleza nami nitawasaidia” akasema Rais Dr Fabian na kuagana na Ruby “Rais anatoa pongezi nyingi kwa mafanikio makubwa na ameelekeza kwa namna yoyote ile lazima tuhakikishe tunapata taarifa muhimu kutoka kwa hawa jamaa.Gosu Gosu uwanja huu ni wako.Sintakuingilia tena naomba utumie kila mbinu kuhakikisha hawa jamaa wanafunguka.Tutaanza na Jenerali William halafu tutaendelea na wengine akina Assad” akasema Ruby “Ahsante Ruby.Nakuhakikishia hawa jamaa watafunguka na watasema kila kitu.Jenerali William alituita sisi ni watu wenye akili finyu hivyo basi nitamuonesha watu wenye akili finyu ni watu wa namna gani” akasema Gosu Gosu na kwenda kufanya maandalizi kwa ajili ya kuanza kumuhoji Jenerali William TEHRAN – IRAN Faqir http://deusdeditmahunda.blogspot.com/aliwasili katika makazi ya Sassan Mahmoud waziri wa intelijensia na usalama wa taifa wa Iran.Japokuwa Faqir ni mmoja wa wafanyakazi wa MOIS lakini gari lake lilikaguliwa na bastola yake ikachukuliwa na walinzi kisha wakaruhusiwa kuingia ndani kuonana na waziri Sassan. “Karibuni sana na poleni kwa yote yaliyotokea” akasema Waziri Sassan baada ya kuwakaribisha akina Mathew sebuleni kwake “Tunashukuru mheshimiwa waziri” “Nataka kujua nini hasa kimetokea? Akauliza Sassan “Abu Zalawi wewe ulikuwepo eneo la tukio unaweza ukaelezea vizuri zaidi nini hasa kilitokea” akasema Faqir “Nikiwa chumbani kwangu nimejipumzisha,lilifika gari likiwa na chakula na muhudumu akawaambia walinzi waliokuwepo kwamba chakula kile kimetumwa na mmoja wa viongozi.Walinzi walikipokea chakula kile na kukusanyika mezani wakaanza kula.Wakati wakila wakakumbuka kwamba nimeshaulika wakamtuma Najib kuja chumbani kwangu kuniita.Ni wakati huo ndipo wavamizi walipovamia.Kile chakula ulikuwa ni mtego wao,walikitanguliza ili waweze kupata nafasi ya kuingia ndani kirahisi.Baada ya kugundua kwamba tumevamiwa ndipo tulipoanza kuchukua hatua kupambana nao hadi tulipofanikisha kuwamaliza kabisa” akasema Mathew “Hongera sana Abu Zalawi na ahsante kwa kuwaokoa watu wetu ambao walinasa katika mtego kwa tamaa ya chakula.Lakini najiuliza watu hawa ni akina nani? Wamefahamuje kama wewe uko pale? Nini dhumuni la kukutafuta? Akauliza Sassan “Mheshimiwa waziri ningeomba tuzungumze faragha kama hutajali” akasema Mathew na Sassan akamuomba radhi Faqir na kumtaka Mathew amfuate wakaenda katika chumba kidogo kilichokuwa na sofa mbili. “Karibu Abu Zalawi.Nini unataka kunieleza? Aliponipigia simu Faqir alisema unataka kuonana nami kuna jambo muhimu unataka kuniambia.Nieleze tafadhali” akasema Sassan “Mheshimiwa waziri ni kweli kuna jambo muhimu sana nataka kukufahamisha.Ni kuhusiana na hiki kilichotokea leo” akasema Mathew na Sassan akawa kimya akisikiliza. “Naamini tayari unafahamu mimi ni nani” akasema Mathew “Ndiyo Abu.Tayari tunazo taarifa zako kwamba unahusika katika kulipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam” “Ni kweli.Nililipua ubalozi wa Marekani na kukamatwa jijini Nairobi wakati nikitafuta usafiri wa kuelekea Mogadishu Somalia.Baada ya kukamatwa nilipelekwa Victoria nchini Sheli Sheli ambako nilipatiwa mateso makali sana halafu nikaunganishwa na akina Yasser Wazir.Baadae nikaja kufahamiana nao wakanieleza kwamba walitekwa na kupelekwa mahala pale.Baada ya siku kadhaa za kuwepo pale Victoria tukapandishwa ndege kuelekea Marekani hapo ndipo nilipoamua kujitoa mhanga kuiteka ndege ile na kuielekeza Iran” akasema Mathew na kumuelezea Sassan namna walivyofanikiwa kuiteka ile ndege “Dah !Abu Zalawi wewe ni shujaa mkubwa.Unastahili pongezi” akasema Sassan “Ahsante sana” akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita “Marekani wanafahamu niko hapa Iran na wananitafuta kwa udi na uvumba” akasema Mathew “Hilo ni kweli.Leo hii waziri wa mambo ya nje wa Marekani ametoa maneno makali sana akiipa Iran saa sabini na mbili tuwe tumekusalimisha wewe pamoja na raia wa Marekani waliokuwamo ndani ya ndege hiyo pamoja na kuiachia ndege ya Marekani.Amedai kwamba Marekani itachukua hatua kali sana dhidi ya Iran endapo tutashindwa kumkabidhi kwao mtuhumiwa wa ugaidi aliyelipua ubalozi wao” akasema Sassan na kutoa kicheko “Hayo ni mambo ya kawaida tumeyazoea.Utoaji wa matamko na vitisho haujaanza leo.Tuendelee” akasema Sassan “Marekani wananisaka wanikamate na watatumia kila mbinu ili kufanikisha mpango huo.Hawana majasusi wao hapa Iran hivyo basi wanashirikia na na Mossad ambao wana majasusi wao ndani ya Iran.Wale waliovamia leo katika nyumba ninakoishi ni majasusi wa Mossad ambao wametumwa na Marekani” akasema Mathew “Wamefahamuje kama uko katika nyumba ile? Ninashangaa kwa kuwa mahala ulipo palifanywa siri kubwa”akauliza Sassan “Mossad tayari wana mtandao wao mkubwa hapa nchini na wamejipenyeza katika sehemu mbali mbali muhimu na wakati mwingine wanashirikiana na wafanyakazi katika idara za serikali” akasema Mathew “Tumejitahidi sana kudhibiti majasusi hasa wa Mossad na CIA kujipenyeza hapa nchini na kuzifanyia ujasusi nchi zao.Tumekuwa tukiwapa adhabu ya kifo kila pale tunapowabaini majasusi hao” akasema Sassan “Mheshimiwa waziri kuna jambo muhimu nataka tuzungumze mimi na wewe.Kuna kitu nitakupatia lakini na mimi kuna kitu nitakihitaji” akasema Mathew na Sassan akacheka kidogo “Nini unakihitaji Abu Zalawi? Akauliza Sassan “Mheshimiwa waziri kama ulivyoshuhudia mwenyewe siko salama.Marekani wananiwinda waniue kwa gharama zozote.Ninaomba hifadhi hapa Iran ambako kwa kiasi Fulani ninajiona niko salama” akasema Mathew na sura ya Sassan ikaonesha mabadiliko kidogo. “Nafahamu mheshimiwa waziri kwamba jambo hilo litakuwa ni kama kuongeza mafuta kwenye moto,litachochea zaidi mgogoro uliopo baina ya Iran na Marekani.Hata hivyo kuna kitu muhimu sana nitakupatia kama gharama za kupewa hifadhi hapa Iran” akasema Mathew “Abu Zalawi imekuwa vyema umefahamu kwamba uwepo wako hapa tayari umekwisha ongeza mzozo.Kama nilivyokueleza awali kwamba tumepewa muda tukusalimishe kwa Marekani ama sivyo tutakiona.Hivyo ni vitisho vya kawaida hatuviogopi.Hata hivyo hatuwezi kukusalimisha kwao kwani wewe ni mtu wetu wa muhimu sana.Umefanya kitu cha kishujaa mno kwa kuwarudisha nyumbani watu wetu muhimu ambao tayari tulikwisha amini wameuawa.Hata kama usingeomba hifadhi sisi tayari tumekwisha kupa hifadhi na hatuwezi kukukabidhi kwao labda wakuue kama walivyojaribu leo.Utaishi hapa kwa amani hata kama ukipenda kwa maisha yako yote yaliyobakia japokuwa ni kwa sharti moja kwamba uachane na mambo ya ugaidi na ujifunze kuwa raia mwema” akasema Sassan “Nashukuru sana mheshimiwa waziri.Ni jambo kubwa mmenifanyia.Nakuahidi mheshimiwa waziri kwamba nitaachana na masuala haya ya ugaidi na kuwa raia mwema” “Kama utakuwa tayari kwa hilo basi karibu Iran Abu Zalawi”akasema Sassan na kumpa mkono Mathew “Ahsante mheshimiwa waziri” akasema Mathew “Ulisema kuna kitu muhimu unataka kunipatia.Ni kitu gani hicho? Akauliza Sassan.Mathew akaingiza mkono mfukoni akatoa diski mweko(flash disc) na kumpatia Sassan “Nini hiki? Akauliza Sassan “Mheshimiwa waziri ndani ya hiyo diski mweko kuna orodha ya majasusi wote wa Mossad walioko hapa Iran” akasema Mathew na sura ya Sassan ikaonesha mshangao mkubwa. “Unasema? akauliza Sassan “Hiyo ni orodha ya majasusi wote wa Mossad walioko hapa Iran” akasema Mathew na Sassan akaitazama ile diski kama vile haamini kile alichoelezwa. “Abu Zalawi hicho unachokisema ni kitu kikubwa sana na kisichowezekana.Kupata orodha ya majasusi wa Mossad si kitu rahisi” akasema Sassan “Nafahamu si kitu rahisi lakini nakuhakikishia kwamba hiyo ni orodha ya majasusi wote wa Mossad walioko hapa Iran” akasema Mathew.Sassan akamtaka Mathew watoke mle katika kile chumba wakaelekea katika ofisi yake.Alibonyeza namba kadhaa katika kifaa kilichokuwa pembeni ya mlango ukafunguka wakaingia ofisini.Akachukua kompyuta ndogo akaiwasha na kuchomeka ile diski halafu akalipakua faili lililokuwemo ndani yake akalifungua na kuanza kulipitia.Mwili ulimsisimka.Akageuka na kumtazama Mathew “Umetoa wapi hiki kitu? Akauliza “Ninao watu wangu ndani ya Mossad ambao wamenisaidia nikaweza kuipata hiyo orodha” akajibu Mathew “Nini hasa sababu ya kuitaka orodha hii? Akauliza Sassan “Kama nilivyoikueleza kwamba Marekani wanawatumia majasusi wa Mossad katika mpango wa kuniua ndiyo maana nikataka nipate orodha ya majasusi wote wa Mossad na mahala walipo kwa ajili ya kujihakikishia usalama wangu nikiwa hapa Iran lakini nimeona halitakuwa jambo jema kukaa na orodha hii nikaamua nije nikukabidhi ili muifanyie kazi na kuwaondoa majasusi wote wa Mossad” akajibu Mathew. Sassan akaipitia tena orodha ile akakuna kichwa “Abu Zalawi siwezi kukuficha mwili wangu umenisisimka.Tunafahamu kuna majasusi wa Israel hapa Iran lakini kuwabaini imekuwa vigumu sana.Sikujua kama wako wengi kiasi hiki.Majasusi zaidi ya thelathini.Nimestuka zaidi kwani wengine ninawafahamu ni wafanyakazi wa idara za usalama hapa Iran na wengine ni marafiki zangu sikujua kama wanaifanyia ujasusi Israel.Majasusi hawa ni wengi na hatua za haraka sana zinapaswa kuchukuliwa.Rais anapaswa kulifahamu jambo hili.Kwa usiku wa leo utapumzika hapa.Nina vyumba vya wageni hivyo karibu jisikie nyumbani” akasema Sassan wakatoka mle ndani na kurejea sebuleni.Sassan akamfahamisha Faqir kwamba Abu Zalawi atalala pale nyumbani kwake kwa usiku ule.Akamuita mtumishi wa ndani na kumuelekeza amuandalie Abu chumba cha wageni kisha yeye na Faqir wakaondoka.Dakika chache baadae mfanyakazi Yule wa ndani akamfuata Mathew na kumjulisha kwamba chumba tayari kimeandaliwa na Mathew akainuka akaenda kupumzika. “Nimeanza vizuri.Jamaa wamenikubali.Mungu anisaidie niweze kukamilisha misheni yangu salama” akawaza Mathew na kujilaza kitandani WASHINGTON DC – MAREKANI Saa kumi za alasiri jijini Washington DC,David Walker aliwasili katika ofisi ya makamu wa Rais Mark Piller ambaye bado alikuwa ofisini. “Mark umenistua kwa wito wako wa haraka.Kuna taarifa yoyote umeipata? Akauliza David Walker “Kuna taarifa imefika kutoka Tanzania”akasema Mark Piller “Jenerali William amepatikana? Akauliza David “Hapana bado hakuna taarifa zozote za kupatikana kwa Jenerali William.Kuna taarifa nyingine kuhusiana na mafuta” “Kuna tatizo lolote? Akauliza David “Hivi sasa ni saa sita inaelekea saa saba za usiku nchini Tanzania.Tumepokea taarifa kwamba bomba la mafuta limelipuliwa usiku huu” “Bomba la mafuta limelipuliwa? Akauliza David.Taarifa ile ilionekana kumstua sana “Ndiyo.Bomba limelipuliwa” “Mungu wangu ! akasema David na kuegemea kiti akashusha pumzi na ukimya wa muda ukapita “Kuna taarifa zozote za kuhusiana na watu waliofanya kitendo hicho? Akauliza David “Hakuna taarifa zozote kutoka serikali ya Tanzania.Taarifa hizi tumezipata kutoka kwa makamanda wetu walioko jijini Tanga Tanzania” “Hii taarifa ni ya kustusha na inazidi kuongeza mkanganyiko katika kile kinachoendelea kutokea Tanzania.Nani waliofanya kitu cha kijinga kama hiki? Akauliza David “David ni kweli hili jambo linastusha na nimekuita hapa ili tuweze kujadiliana kuhusiana na jambo hili.Ni wazi kwa hiki kilichotokea hakuna mafuta yatakayokuwa yanakwenda jijini Tanga hivyo uchukuaji wa mafuta unasimama.Nini kinachoendelea Tanzania? Akauliza Mark “Mark swali hilo ni zuri kwa kuanzia kujiuliza kuhusu kile kinachoendelea Tanzania.Inaonekana mipango yetu imeanza kufeli.Nini kimetokea? Wapi tumekosea? Mbona tulijipanga vizuri sana na mambo yakaenda vizuri nini kimetokea hadi mambo yakaanza kwenda mrama ghafla tu? Akauliza Mark Piller “Matatizo yameanza baada ya kutuma kirusi.Kirusi kilipofika Tanzania ndipo wanajeshi wetu wakashambuliwa na kuuawa huku wale wahusika wakuu waliokuwa na kirusi wakipotea na hawajulikani walipo.Kama haitoshi bomba la mafuta nalo limelipuliwa.Ukiunganisha matukio haya yote yaliyotokea mfululizo unaona kabisa kwamba kuna kitu kinaendelea hapa” akasema David Walker “Unadhani nini kinachoendelea David? “Mark ni wazi matukio haya yote yanayoendelea kutokea nchini Tanzania yana lengo la kukwamisha mipango yetu isifanikiwe.Tazama tukio la kushambuliwa kwa kambi ya wanajeshi wetu limekwenda sambamba na kupotea kwa Jenerali William na wale watu wa IS ambao tumekuwa tunashirikiana nao.Kama hiyo haitoshi tukio la kulipuliwa bomba la mafuta linaashiria kwamba upo mpango unaoendelea wa kuhujumu mipango yetu nchini Tanzania.Kulipua bomba la mafuta hakujafanywa makusudi.Ni mpango wa kuhakikisha kwamba hatuendelei kuchukua mafuta” akasema David.Mark Piller akazama katika tafakari halafu akasema “Kwa mtazamo David unadhani tayari mipango yetu imekwisha fahamika? Akauliza Mark “Hilo liko wazi Mark.Matukio haya mfululizo hayajatokea kwa bahati mbaya.Tazama matukio yote yamelenga Marekani.Hili la kulipuliwa bomba la mafuta ndilo linaashiria kabisa kwamba kuna kitu hakiko sawa” akasema David Walker “Unahisi serikali ya Tanzania inahusika katika matukio haya? Mark akauliza “Sina hakika kama serikali ya Tanzania inahusika katika matukio haya.Tunahitaji kufanya uchunguzi kulibaini hilo” akasema David “Kama si serikali ya Tanzania nani ambaye anafanya mtukio haya ya kutuhujumu? Akauliza Mark Piller “Nina mashaka si serikali ya Tanzania inayohusika na matukio haya kwani kama ingekwisha gundua kuhusu mipango yetu isingeweza kukaa kimya hadi sasa hivi isitoe tamko lolote.Tayari vikosi vya Marekani vingekwisha timuliwa nchini Tanzania na hata mahusiano ya Tanzania na Marekani naamini yangekuwa katika hali mbaya sana” akasema David Walker “Nakubaliana nawe David.Jambo tulilolifanya nchini Tanzania ni kubwa.Damu nyingi imemwagika na serikali ya Tanzania isingeweza kukaa kimya hadi sasa bila kusema chochote kama kweli wangekuwa wamegundua sisi tunahusika na kile kilichotokea Tanzania.Swali tunalopaswa tulitafutie majibu kama si serikali ya Tanzania nani anahusika na matukio haya yanayoendelea nchini Tanzania ambayo ni wazi yanalenga kuvuruga mipango yetu? Akauliza Mark Piller “Abu Zalawi ! akasema David kwa sauti ndogo “Unasema nini David? “Abu Zalawi ndiye anayefahamu mipango yetu na yeye anatokea Tanzania.Nahisi atakuwa anahusika na haya matukio.Lakini…..” David akanyamaza kuna kitu alikumbuka. “Lakini kuna kitu nimekikumbuka.Abu Zalawi alipokwenda Tanzania alikuwa katika udhibiti mkali.Hakuruhusiwa kuonana au kuwasiliana na mtu yeyote na hata alipokabidhiwa kwa Assad alikuwa chini ya ulinzi na walihakikisha hatoki katika mazingira yao hadi alipokwenda kutekeleza kazi aliyotumwa.Hakuweza kuonana wala kuwasiliana na mtu yeyote Tanzania” akasema David na ukimya ukapita halafu akasema “Lakini haya yote yameanza kutokea wakati Abu Zalawi akiwa nchini Iran.Yawezekana baada ya kufika huko amewasiliana watu wake au serikali yake na wakatekeleza mipango hii.Kwa namna yoyote ile lazima anahusika” “Kwani mpango wa kumuua umefikia wapi?Vipi kuhusu Habiba Jawad tayari amekwisha patikana? Akauliza Mark Piller kana kwamba hajui chochote kinachoendelea na David akaonekana kusita kidogo “Kuna nini David? Abu amekwisha uawa? “Nilipokea taarifa kutoka kwa mkurugenzi wetu Jason kwamba…..” akasema David na kusita “Mbona unasita David.Kuna nini? Akauliza Mark Piller.David akakuna kichwa na kusema “Majasusi wa Mossad waliotumwa kumuua Abu Zalawi wote wameuawa” “Wameuawa? Akauliza Mark kwa mshangao “Ndiyo wameuawa wote.Mossad wanaendelea na uchunguzi kujua kilichotokea.Baada ya kupokea taarifa hivyo tumewatafuta wale watu wetu tuliowatuma kwenda kumteka Habiba ii wasitishe mpango huo lakini mawasiliano yao yamepotea na hawapatikani tena.Tunaendelea kuwatafuta lakini ukimya wao hauleti picha nzuri” akasema David Walker “David hao majasusi wa Mossad waliouawa hawawezi kugundulika kama ni watu wa Mossad? Nauliza hivyo kwa sababu wakigundulika kama ni watu wa Mossad huu utakuwa ni mgogoro mpya kati ya Iran na Israel”Akasema Mark Piller “Kwa mujibu wa Jason ni kwamba haitakuwa rahisi kugundulika kwa kuwa watu wote hao ni raia wa Iran hivyo hakuna anayejua kama wanafanya kazi na Mossad” akasema David “Lakini imetokeaje majasusi hao wakauawa? Akauliza Mark “Hakuna anayejua Mark lakini taarifa rasmi ni kwamba Abu Zalawi bado mzima na mipango ya kumteka Habiba Jawad itasitishwa kwa muda hadi pale tutakapowasiliana tena na Mossad kujua kama wana mpango mwingine mbadala wa kumuua Abu Zalawi” akasema David “David mambo yanazidi kutuendea kombo.Kila tunalolifanya linakuwa na mkwamo ndani yake.Hebu nipe ushauri tufanye nini? Akasema Mark “Kwanza ni kuhusu suala la Tanzania. Hatupaswi kuingilia au kusema chochote kuhusiana na hiki kitendo cha kulipua bomba la mafuta ambacho tunajua wazi kimefanywa kwa lengo la kutukosesha mafuta.Kuna jambo moja tu ambalo tunaweza kulifanya katika mkanganyiko huu nalo ni kuwarejesha nyumbani wanajeshi wetu.Tutumie kigezo cha kuvamiwa kwa kambi na wanajeshi wetu kuuawa kuwarejesha wengine wote waliobaki.Rais anatakiwa kutoa tamko kali kwamba tunawaondoa wanajeshi wetu waliokuwa wanasaidia kulinda amani nchini Tanzania baada ya kushambuliwa na kuuawa.Dunia nzima itajua kwamba sababu kuu ya kuondoka Tanzania ni kuuawa kwa wanajeshi wetu.Kwa sasa ni usiku nchini Tanzania hivyo basi hadi kufika kesho asubuhi meli zetu zote zilizokuwa zinasubiri kupakia mafuta katika bandari ya Tanga ziwe zimeondoka zibaki zile za kijeshi zikipakia vifaa vya jeshi.Hiyo ni hatua ya kwanza tunayotakiwa kuichukua na baada ya hapo tutaingia katika uchunguzi kujua nini hasa kimetokea.Nani waliotushambulia? Je serikali ya Tanzania inafahamu kuhusu mipango yetu au haijui chochote? Mwisho kabisa tunatakiwa kujua wapi aliko Jenerali William pamoja na akina Assad” akasema David “Ushauri wako ni mzuri David.Nadhani kuna haja ya kurudi nyuma kwanza na kujipanga tena vizuri baada ya kujua nini kimetokea.Lazima tujue tumekosea wapi.Hata hi….” Akanyamaza Mark baada ya simu ya David Walker kuita.Akaipokea akazungumza kwa muda halafu akamtazama Mark Piller kwa macho ya wasiwasi “Kuna nini David? “Nimezungumza na mkurugenzi Jason.Anasema kwamba amepokea taarifa muda mfupi uliopita kutoka Riyadh kwamba wale watu wetu tuliowatuma kwenda kumteka Habiba Jawad wote wamekutwa wameuawa katika hoteli” “Mungu wangu ! Mark Piller akashangaa. “Mark mambo yanazidi kuwa magumu kwa upande wetu.Kwa nini kila tunachokifanya kinashindwa kufanikiwa? Haijawahi kutokea tukashindwa vibaya namna hii” akasema David “David kama watu wetu wameuawa ni wazi kwamba tayari Habiba amekwisha fahamu kilichokuwa kinakwenda kutokea kwamba ulikuwa ni mpango wa kumteka .Kwani mpango huu mliuandaa vipi? Akauliza Mark na David akamueleza namna walivyokuwa wameuandaa mpango ule wa kumteka Habiba Jawad “David haya mambo si madogo.Tunapaswa kuchunguza kwa makini nini kimetokea.Mimi nitamshauri Rais afanye kama ulivyoshauri lakini nataka kujua kuhusu Abu Zalawi? “Abu Zalawi kwa namna yoyote ile lazima auawe.Ngoja tuwasikilize Mossad wanasemaje kwani tunawategemea wao katika jambo hili lakini Habiba Jawad..….” Akasema David na kunyamza kidogo “Kitendo cha watu wetu kuuawa kinaonyesha wazi kwamba Habiba Jawad amekwisha fahamu kuhusu mpango wetu wa kutaka kumteka na kumuua.Huyu amegeuka kuwa mtu hatari zaidi kuliko hata Abu Zalawi kwani anafahamu mambo yetu mengi.Lazima mpango wa kumuua uanze haraka sana.Kwa kutumia njia yoyote ile lazima tumuue Habiba Jawad ! Nikitoka hapa ninakwenda kukutana na wenzangu tujadiliane kuhusu mpango mpya wa kumuua Habiba Jawad” akasema David Walker. “Sawa David.Tusipoteze muda nenda kakutane na G20 mimi ninakwenda kuzungmza na Rais sasa hivi ili nimpe ushauri huu angali mapema asije akafanya maamuzi mengine yanayoweza kutuletea matatizo” akasema Mark Piller “Angalizo Mark.Kumbuka kwamba Rais hapaswi kufahamu chochote kuhusu mambo haya hivyo unapozungumza naye hakikisha unakuwa makini asigundue kama kuna kitu kilikuwa kinaendelea kule Tanzania” akasema David Walker “Nalifahamu hilo David usihofu” akasema Mark na kuagana na David akaondoka. “Nakubaliana na David kwamba matukio haya yanalenga kuvuruga mipango yetu kule Tanzania.Lakini nani anayefanya haya? Je ni serikali ya Tanzania? Lakini bado nakubaliana na David kwamba kama serikali ya Tanzania ingeyafahamu haya isingeweza kukaa kimya lazima hivi sasa dunia nzima ingefahamu.Lazima kuna kikundi cha watu kinafanya haya mambo ili tushindwe.Hata hivyo kiasi cha mafuta tulichokichukua bado ni kikubwa na kama mipango yetu isingevurugika hivi sasa tungekuwa tunajiandaa kuingia katika madini ambako nako tungekusanya kiasi kikubwa sana cha madini.Ushauri wa David ni mzuri ngoja kwanza turejeshe wanajeshi wetu halafu tujitafakari upya nini kimetokea? Lingine kubwa ambalo bado tunapaswa kulitafutia majibu ni mahala alipo Jenerali William na akina Sattar” akaendelea kuwaza Mark Piller halafu akatoka kwenda kuonana na Rais William “Mark karibu” akasema Rais William baada ya kumaliza kuzungumza na simu “Ahsante mheshimiwa Rais” “Mark naamini kilichokuleta hapa ni taarifa ya kilichotokea Tanzania” “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ni kuhusiana na kulipuliwa kwa bomba la mafuta” “Nimezipokea taarifa hizo tayari kutoka kwa waziri wa ulinzi.Nimestuka kidogo kwa jambo hili kutokea hasa kwa wakati huu” akasema Rais William “Muda mfupi uliopita nilikuwa na David Walker tukilijadili jambo hili na tulijiuliza swali hilo hilo kwa nini iwe sasa? Akasema Mark “Nini maoni yako Mark juu ya jambo hili? Akauliza Rais William “Mheshimiwa Rais ukiyatazama matukio haya yaliyotokea kwa ujumla wake utagundua kuna kitu kinaendelea chini kwa chini ambacho mpango wake ni kuvuruga mipango yetu isiendelee.Matukio haya yalianza pale kirusi kilipofika nchini Tanzania ambapo kambi yetu ikavamiwa na wanajeshi kuuawa.Ambacho kinatufanya tuhisi huu ni mpango wa kuvuruga mipango yetu ni kupotea kwa Jenerali William na akina Satter ambao walifahamu kuhusu mpango ule wa kusambaza kirusi nchini Tanzania.Kabla hilo hilo halijapoa bomba la mafuta limelipuliwa na hatuwezi tena kupata mafuta.Mheshimiwa Rais huoni kama huo ni mpango wa kuvuruga mipango yetu? Aliyelipua bomba la mafuta ni wazi alifahamu kile kilichokuwa kinaendelea kule Tanga na lengo lake ni kutuzuia tusiendelee kuchukua mafuta” akasema Mark Piller na Rais William akavuruga nywele zake kwa hasira “Mark unataka kuniambia kwamba tayari mipango yenu yote imekwisha fahamika? Akauliza Rais William “Mheshimiwa Rais kutokana na namna matukio yalivyotokea mfululizo ni wazi mipango yetu imekwisha fahamika” akasema Mark Piller “Unahisi ni serikali ya Tanzania? Akauliza William “Hapana mheshimiwa Rais kama serikali ya Tanzania ingefahamu mipango hii isingeweza kukaa kimya.Tayari mambo yangekwisha wekwa hadharani lakini mpaka sasa wako kimya na hii inaashiria kwamba hawafahamu chochote.Bado ninaendelea kuhisi kwamba kuna uwezekano mkubwa mambo haya yanafanywa na kundi la IS” akasema Mark Piller “Lakini IS mmekuwa mkishirikiana nao kwa muda mrefu katika mipango mbalimbali” “Ndiyo mheshimiwa tumekuwa tukishirikiana nao kwa muda mrefu lakini wanaweza wakatugeuka na kuvuruga mipango yetu.Ndiyo maana nilimuomba Habiba Jawad atusaidie kuchunguza” akasema Mark Piller “Umemtaja Habiba nimekumbuka kuhusu mipango iliyokuwa inafanywa na kundi lako kumteka.Wamefikia wapi? “Mambo yamekwenda vizuri mheshimiwa Rais.Wale jamaa wote waliotumwa kwenda kumteka wameuawa” “Vizuri sana.Vipi kuhusu Abu Zalawi? Akauliza William “Taarifa niliyoipata ni kwamba majasusi wote wa Mossad waliotumwa kumuua Abu Zalawi wameuawa.Jambo hili limewastusha sana Mossad.Hata hivyo bado G20 wanaendelea na mipango ya kumuua Habiba Jawad kwani tayari amekwishafahamu kuwa anatakiwa kuuawa”akasema Mark “Mark kuna jambo ninalifikiria ila sijui kama lina msingi wowote.Hudhani kama Habiba Jawad yuko nyuma ya matukio haya yanayotokea hivi sasa? Akauliza Rais William “Habiba Jawad tumekuwa naye kwa muda mrefu na tumempa utajiri mkubwa na yeye ametusadia katika mipango mingi.Sina hakika kama anaweza akahusika na mambo haya.Kwa nini umehisi Habiba anaweza kuhusika?akauliza Mark Piller “Kinachonifanya nihisi Habiba akahusika na matukio haya yaliyotokea ni kitendo chake cha kumleta Abu Zalawi akidai ni gaidi wakati si kweli.Huoni kuna kitu hakiko sawa hapa? Japokuwa anatusaidia sana lakini kuna wakati ninapoteza imani na huyu mama.Anaweza kuwa ni muhusika mkuu katika haya yanayoendelea.Yawezekana yeye mwenyewe ameshirikiana na IS na wakafanya hujuma hii kubwa.Pamoja na kushirikiana naye hebu tumchunguze kwa makini huyu Habiba Jawad kuna mambo naamini tunaweza kuyafahamu kutoka kwake” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais mawazo yako ni mazuri lakini bado moyo wangu unakataa kabisa kama Habiba anaweza akatuzunguka kiasi kikubwa namna hii.Tumeshirikiana naye kwa muda mrefu na hakujawahi kutokea matatizo yoyote hata mara moja.Habiba hana sababu zozote za kufanya mambo kama haya” akasema Mark Piller “Mark usimuamini mwanadamu kiasi hicho.Kumbuka hata Kristo alisalitiwa na mmoja wa wafuasi wake hivyo si ajabu kwa Habiba kuwazunguka hata kama mmekuwa naye kwa muda mrefu na mmempa utajiri mkubwa.Usiyapuuze mawazo yangu jaribu kufanya uchunguzi wako kimya kimya” akasema Rais William “Sawa mheshimiwa rais nitafanya hivyo.Tukiliweka pembeni hilo nataka tujielekeze zaidi katika hili la Tanzania.Nini mawazo yako mheshimiwa Rais? Akauliza Mark “Mpaka sasa sijafanya maamuzi yoyote Mark” akajibu William “Mheshimiwa rais nimekuja na wazo nini cha kufanya” “Karibu” “Kama nilivyokueleza awali kwamba mipango yetu inahujumiwa isifanikiwe hivyo basi tunatakiwakuwaondoa wanajeshi wetu Afrika mashariki haraka sana.Hakuna sababu ya wanajeshi wetu kuendelea kuwepo nchini Tanzania au Uganda wakati kitu kikubwa tulichokifuata kule ambacho ni mafuta hakipo tena.Itachukua muda mrefu kufanya marekebisho katika bomba hilo na hadi wakati huo tayari eneo lote la Afrika mashariki litakuwa shwari na wanajeshi wetu hawatahitajika tena” akasema Mark Piller “Mark ule mpango wa kirusi umeishia wapi? Kama kirusi kile kingefanikiwa kusambazwa wanajeshi wetu wangeendelea kuwepo Tanzania tena tungeongeza vikosi na badala ya mafuta tungeanza kusomba madini” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais mpaka sasa hakuna kinachojulikana kuhusiana na mahala kirusi kilipo kwani wale wahusika wakuu wote wamepotea na hawajapatikana bado.Baada ya kuwarejesha wanajeshi wetu nyumbani tutaanza kufuatilia taratibu kujua mahala waliko Jenerali William na akina Sattar lakini kwa sasa ushauri wetu ni kwamba wanajeshi warudi nyumbani.Kigezo kikuu cha kuwarejesha nyumbani wanajeshi wetu ambacho kila mtu anaweza akakielewa ni kutokana na shambulio lililofanywa na wanajeshi wetu kuuawa.Katika maelezo yako utakayoyatoa onyesha kwamba wanajeshi wetu wamekufa kishujaa kwani walikuwa katika kutimiza wajibu wao wa kulinda amani lakini watu wasio na huruma wakawaua hivyo basi hakuna sababu ya kuwaweka wanajeshi mahala ambako hawatakiwi” akasema Mark Piller “Sawa Mark nitafanya hivyo lakini bado kutakuwa na maswali mengi kuhusiana na Jenerali William.Lazima wamarekani watataka kufahamu tumechukua hatua gani kumtafuta? Kibaya zaidi Rais wa Tanzania hataki tutume wachunguzi wetu kwenda kumtafuta” “Nilikueleza mheshimiwa Rais kwamba jishushe kwa Rais wa Tanzania.Watu weusi wanapenda kuonekana wako juu.Rais kama wewe ukijishusha kwake atajiona wa thamani kubwa na atafanya kila utakachomuelekeza” akasema Mark “Mark hilo ni suala gumu sana.Kujishusha kwa mtu mweusi?! “Usihofu mheshimiwa Rais.Hiyo nayo ni mbinu wakati wa mapambano” “Nitaangalia nini cha kufanya lakini kitu kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha wanajeshi wetu wanarejea kwanza nyumbani.Lakini tumefanikiwa kupata mafuta ya kutosha? “Tumepata mnafuta mengi mheshimiwa Rais.Mengi sana” “Sawa Mark nitalishughulikia hilo ili pale miili ya wanajeshi wetu waliouawa inaporejea nyumbani basi iambatane na wanajeshi wengine wote” akasema Rais William TEHRAN – IRAN “Sassan kuna jambo gani la muhimu usiku huu ambalo haliwezi kusubiri hadi kesho? Akauliza Rais Armen Hijazi wa Iran baada ya Sassan Mahmoud kuwasili katika makazi yake. “Mheshimiwa Rais samahani sana kwa usumbufu usiku huu lakini kuna jambo muhimu sana ambalo ninadhani haliwezi kusubiri hadi kesho” akasema Sassan “Haya karibu” akasema Rais Armen Sassan akakohoa kidogo halafu akasema “Mheshimiwa Rais kama unavyofahamu kuwa wale ndugu zetu sita waliokuwa wamepotea wamerejea nyumbani na kwa mujibu wa maelezo yao mtu aliyefanikisha kurejea kwao ni Abu Zalawi ambaye tumekwisha fahamu kuwa ni Gaidi na amehusika katika kulipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.Kwa ruhusa yako ulikubali tumpokee na tumpe hifadhi hapa nchini.Tulifuata maelekezo yako na kumpatia hifadhi.Tulimuweka katika mojawapo ya nyumba zetu za siri.Usiku wa leo nimepigiwa simu na mkuu wa kitengo kinachosimamia nyumba zetu za siri anaitwa Faqir,akanijulisha kwamba kuna jambo limetokea,watu wamevamia nyumba alimo Abu Zalawi na kutaka kumuua.Aliniambia kwamba Abu Zalawi anataka kuniona na nikamuelekeza amlete nyumbani kwangu.Baada ya kufika kwangu walinipa maelezo ya namna tukio lile lilivyotokea” akasema Sassan na kumsimulia Rais Armen namna tukio lile lilivyotokea. “Ni akina nani hao watu na walifahamuje kama Abu Zalawi yuko katika nyumba hiyo? Akauliza Rais Armen “Hilo ni swali ambalo sote tulijiuliza lakini Abu Zalawi akaniomba tuzungumze faragha na ndipo aliponipa siri ya tukio lile.Wale watu waliotaka kumuua ni majasusi wa Mossad” “Mossad? “Ndiyo ni majasusi wa Mossad.Marekani tayari wanafahamu kuwa Abu Zalawi yuko hapa Iran na waziri wao wa mambo ya nje tayari ametoa tamko la kututaka tumsalimishe kwao.Wanajua kwamba hatuwezi kufanya hivyo ndipo wakaja na mpango wa kumuua kwa kuwatumia majasusi wa Mossad ambao wamejitahidi kutafuta hadi wakafahamu mahala alipo na kwa bahati nzuri mpango wao umeshindwa kufanikiwa” akasema Sassan http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Abu Zalawi amefahamuje kama wale watu waliokwenda kutaka kumuua ni majasusi wa Mossad? Akauliza Rais Armen “Abu Zalawi ana watu wake ndani ya Mossad ambao wamekuwa wakimpa taarifa mbali mbali za mpango ya Mossad.Kikubwa zaidi amenipatia hii” akasema Sassan na kumuonyesha Rais Armen diski mweko(flash disc) “Hiki nini? Akauliza Rais Armen “Hiki ni kitu ambacho tumekuwa tunakitafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio.Ni orodha ya majasusi wote wa Israel walioko hapa nchini kwetu” akasema Sassan na Rais Armen akashusha pumzi “Sassan una uhakika hicho alichokupatia ni kitu cha kweli? Akauliza Rais Armen “Nimeipitia orodha hii ni ya kweli.Haina mashaka hata kidogo” akasema Sassan na kuichomeka ile diski mweko katika kompyuta yake aliyekwenda nayo na kuanza kumuonyesha Rais Armen kile kilichokuwa ndani ya ile diski mweko. “Hiki ni kitu muhimu sana kwetu.Nilifahamu kuna majasusi wa Israel hapa Iran lakini sikujua kama wako wengi kiasi hiki.Abu Zalawi ameipataje orodha hii? Akauliza Rais Armen “Kama nilivyokwambia mheshimiwa Rais kwamba Abu ana watu wake ndani ya Mossad ambao wamekuwa wakimpa taarifa muhimu kwani Abu anasakwa pia na Israel.Amewahi kutoroka gerezani nchini Israel na vile vile amehusika katika shambulio la bomu jijini Jerusalem.Abu amekuwa akishirikiana na mojawapo ya kundi la wanamgambo wa kipalestina katika kuendesha mashambulio dhidi ya Israel hivyo kuna watu ndani ya Mossad ambao wanawasaidia kwa kuwapa taarifa muhimu” akasema Sassan “Sassan nataka ukae na wataalamu wako kesho muipitie orodha hiyo kama ni ya kweli.Mkijiridhisha kuwa ni ya kweli basi hili litakuwa ni jambo kubwa sana kwetu” akasema Rais Armen “Ndiyo maana nikaona nije nikuone usiku huu huu kuhusu jambo hili” “Ni jambo kubwa sana hili Sassan kama orodha hiyo itakuwa ya kweli” “Sina mashaka nayo lakini nitafanya kama ulivyoelekeza.Nitakaa na wataalamu wangu na kuipitia kujiridhisha kama ni ya kweli.Hata hivyo mheshimiwa Rais Abu Zalawi ana maombi yake” “Anataka nini? Akauliza Rais Armen “Anaomba apewe hifadhi hapa Iran kwani hana sehemu nyingine ya kwenda kwa sasa na kwa namna anavyofuatiliwa akitoka nje ya hapa atauawa haraka sana” akasema Sassan “Kuhusu hifadhi hilo halina tatizo.Ataishi hapa kwani anaonekan anaweza akawa na msaada kwetu.Sassan namuhitaji Abu Zalawi kesho jioni hapa kwangu.Nitakuwa na mazungumzo naye” akasema Rais Armen “Sawa mheshimiwa Rais nitalifanikisha hilo” akasema Sassan wakaendelea na mazungumzo na walipomaliza Sassan akaondoka kurejea nyumbani kwake.Kitu cha kwanza alichokifanya alipofika nyumbani kwake ni kugonga mlango wa chumba cha wageni alimolala Mathew akaamka “Abu Zalawi samahani kwa kukuamsha.Nimekuja kukupa taarifa kwamba nimezungumza na Rais.Kubwa lilikuwa ni hii orodha uliyonipatia.Rais amelipokea ombi lako la kupewa hifadhi hapa Iran na ameelekeza tukutafutie makazi maalum na vibali vya ukaazi lakini wakati mchakato huo ukifanyika utaendelea kuishi hapa nyumbani kwangu kwa ajili ya usalama wako” akasema Sassan “Nashukuru sana Sassan kwa jambo hili kubwa.Nifikishie pia salamu zangu kwa mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Nitafikisha shukrani hizo” akasema Sassan na kumtazama Mathew “Abu Zalawi” akaita “Naam” akaitika Mathew “Jambo hili tayari limefika ngazi za juu,nataka unihakikishie kwa mara nyingine tena kwamba orodha hii ni ya kweli” akasema Sassan “Nakuhakikishia kwamba hii ni orodha ya kweli kabisa Sassan.Siwezi kuja na kitu kikubwa kama hiki halafu kikawa si cha kweli.Ifanyieni uchunguzi ili mjiridhishe kama ni ya kweli au si kweli.Kama mkigundua si ya kweli niko tayari kupata adhabu yoyote hata kufukuzwa nchini” akasema Mathew kwa kujiamini “Unajiamini sana Abu Zalawi.Ahsante kwa uhakika huo” akasema Sassan na ukimya mdogo ukapita “Sassan kuna jambo nataka kukuomba unisaidie” “Jambo gani Abu Zalawi? “Nataka kuonana na Yasser Wazir hapo kesho kama itawezekana” akasema Mathew “Hilo halitakuwa jambo rahisi.Yasser na wenzake wamehifadhiwa sehemu maalum kwa sasa wakipatiwa matibabu katika mojawapo ya hospitali za jeshi.Bado hajaruhusiwa mtu yeyote kuonana nao.Vuta subira pale watakapokuwa wametoka hospitali utaonana nao” akasema Sassan na kumuaga Mathew DAR ES SALAAM – TANZANIA Simu ya Dr Fabian Kelelo Rais wa Tanzania iliita.Ni saa kumi na moja kasoro dakika kumi na nane lakini Dr Fabian alikuwa macho hakuwa na usingizi hata chembe.Akanyoosha mkono na kuichukua ile simu akatazama mpigaji na kuinuka halafu akashusha pumzi.Alikuwa ni William Washington Rais wa Marekani. “Hallow Rais William” akasema Dr Fabian baada ya kupokea simu “Habari za asubuhi mheshimiwa Rais Dr Fabian.Naamini ni alfajiri kwa saa za huko kwenu”akasema Rais William “Ndiyo mheshimiwa Rais ni alfajiri.Habari za huko kwenu? “Huku bado ni majonzi kufuatia vifo vya wanajeshi wetu.Hata hivyo tuliweke hilo pembeni kwani tayari tumekwisha lizungumza.Kikubwa nilichokupigia simu ni kukujulisha kwamba kufuatia tukio lile la kushambuliwa na kuuawa kwa wanajeshi wetu tumefikia maamuzi ya kuwaondoa wanajeshi wetu wote waliobaki.Mheshimiwa Rais nia yetu ilikuwa nzuri sana kusaidia ndugu zetu na marafiki zetu wa muda mrefu kurejesha amani kufuatia machafuko yaliyotokea nchini kwako na wanajeshi wetu wamefanya kazi nzuri sana na tungependa waendelee kuwepo nchini kwako lakini dosari imetokea pale walipovamiwa wakashambuliwa na kuuawa.Jambo hili limewachukiza mno wamarekani na wanataka wanajeshi wao waliobaki warejee nyumbani mara moja hivyo nimeona nikujulishe angali bado mapema kwamba kuanzia leo wanajeshi wetu wataanza kuondoka kurejea nyumbani.Kama ulivyotuahidi kwamba mnafanya uchunguzi wa shambulio lile naomba mtakapokuwa mmekamilisha uchunguzi wenu mtujulishe mara moja tufahamu nani walioshambulia na kuua wanajeshi wetu.Vile vile bado kuna mwanajeshi wetu mmoja aliyekuwa mkuu wa vikosi vyetu hapo Tanzania Jenerali William mpaka sasa hajulikani alipo.Ningeomba mtusaidie kumtafuta huyo mtu wetu na kama ikiwezekana tunaweza kutuma watu wetu wakashirikiana na idara zenu katika kumtafuta” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais kwanza kabisa niendelee kutoa pole nyingi sana kwa vifo vya wanajeshi wenu na ninakuahidi kwamba idara zetu za uchunguzi zinafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha waliofanya mauaji yale wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria.Kuhusu Jenerali William tutaendelea kumtafuta hadi tuhakikishe anapatikana.Kama nilivyokwambia awali kwamba hatuhitaji msaada kutoka nje idara zetu zina uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi na ninakuhakikishia kwamba tutawapata waliofanya shamulio lile.Kuhusu kuwaondoa wanajeshi wa Marekani walioko hapa nchini sina kipingamizi katika hilo na ninawashukuru sana kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kusaidia kurejesha amani na hadi sasa hivi hali inarejea kwa kasi kuwa ya kawaida.Watu wameanza kuendelea na maisha yao ya kila siku” “Ahsante Dr Fabian.Ni hilo tu nililotaka kukujulisha alfajiri ya leo.Natumai tutaendelea kuwasiliana zaidi” akasema Rais William wakaagana na kukata simu “Mshenzi mkubwa huyu ! akasema Dr Fabian na kuitupa simu pembeni “Mpango wetu umefanikiwa.Walichokuwa wanakihitaji ni mafuta tu na baada ya kuyakosa wameamua kuondoa wanajeshi wao.Namuombea Mathew Mulumbi huko aliko amalize misheni yake haraka ili tuweze kuwaeleza dunia nini kimefanywa na Marekani” akawaza Dr Fabian na kuchukua simu akampigia Ruby “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby samahani kwa kukuamsha” “Hapana sijalala mheshimiwa rais sisi bado tunaendelea na kazi.Tulikuahidi kwamba hatutalala hadi tuhakikishe tumemaliza zoezi” “Poleni na ahsanteni sana kwa kazi hiyo kubwa mnayoifanya.Kuna lolote mmelipata mpaka hivi sasa kutoka kwa wale jamaa mnaowahoji? “Watu wale ni wagumu sana kufunguka hasa huyu jenerali William.Lakini Gosu Gosu anaendelea na zoezi la kuwafungua na nina uhakika watafunguka na kueleza kila kitu” akasema Ruby “Sawa Ruby.Nimekupigia kukujulisha kwamba nimetoka kuzungumza na Rais wa Marekani muda mfupi uliopita.Alinipigia kunijulisha kwamba wameamua kuwaondoa wanajeshi wao kufuatia shambulio katika kambi yao lililopelekea wanajeshi kuuawa.Mpango wetu umekwenda vizuri kama tulivyokuwa tunataka na baada ya kukosa mafuta wenyewe wameamua kuondoka” akasema Dr Fabian na Ruby akacheka kidogo “Wameona hakuna tena sababu ya kuendelea kutumia gharama kuhudumia wanajeshi wao hapa wakati hakuna manufaa yoyote wanayoyapata.Hii inaonyesha kuwa hupeleka wanajeshi wao mahala ambako kuna maslahi kwao.Unapoona mahala kuna wanajeshi wao ujue lazima kwa namna moja au nyingine kuna kitu wanafaidika nacho kwa wanajeshi wao kuwapo mahala hapo lakini sehemu ambazo hakuna faida katu hawatumi wanajeshi ndiyo maana wameamua kuondoka baada ya mafuta kukatika.Wasidhani kwamba mambo yameishia hapa bado hayajakwisha.Yawezekana wanadhani hatujui chochote kuhusiana na mipango yao miovu juu yetu” akasema Ruby “Kuna taarifa zozote kutoka kwa Mathew Mulumbi? “Nimezungumza na Nawal leo saa tisa akaniambia kwamba ataanza safari ya kuelekea Tehran leo saa mbili za asubuhi.Ni safari ya saa tano hadi sita hivi na tunategemea kuanzia saa saba atakuwa amefika Tehran na ndiye atakayetupa taarifa zote za kuhusiana na Mathew Mulumbi” akasema Ruby “Sawa Ruby.Naomba mjitahidi sana kuwabana hao jamaa hadi wafunguke kila kitu” “Tunajitahidi mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kuagana na Rais. Ruby akitoka ofisini kwake na kuelekea katika upande wa afya ambako Jenerali William alipelekwa baada ya kupoteza fahamu akamkuta Gosu Gosu akisubiri ili akaendelee kumuhoji “Vipi maendeleo yake? Ruby akauliza “Tayari amezinduka ila madaktari wameshauri tumpumzishe kidogo kama saa moja ndipo zoezi likaendelee” akasema Gosu Gosu.Jenerali William alikuwa amelala kitandani na mikono imefungwa pingu.Uso wake haukuwa ukitazamika. “Nimezungumza na Rais muda si mrefu” akasema Ruby na kumueleza Gosu Gosu kila kitu alichoelezwa na Rais “Hatimaye wameondoka hawa ambao naweza kuwaita majambazi wa rasilimali zetu.Imetumika akili kubwa kuwaondoa vinginevyo wangeendelea kuchukua mafuta hadi yakauke”akasema Gosu Gosu “Tunaendelea kuishinda hii vita japo bado mapambano yanaendelea lakini hakuna kukata tamaa tutapambana hadi mwisho wake” akasema Ruby “Huyu mwanajeshi wao alituita sisi watu wenye akili finyu na hivi sasa ninamuonyesha watu wenye akili finyu ni watu wa namna gani.Analia kama mtoto mdogo na kuomba msamaha hatarudia tena kutamka maneno yale.Kiburi kimemuisha” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu unadhani anaweza akafunguka hivi karibuni? “Itachukua muda.Huyu ni mwanajeshi mkomavu na kwa mwanajeshi wa aina yake si jambo jepesi kutoa siri lakini tutatumia kila njia hadi tuhakikishe anafunguka na kusema ukweli” akasema Gosu Gosu “Ninataka kumuhoji tena kabla ya kumpumzisha kisha nimuanze Yule gaid Assad” “Sawa Gosu Gosu.Kabla hujaendelea kwa nini usichukue mapumziko mafupi halafu uendelee baadae? “Hakuna muda wa kupumzika Ruby.Hawa jamaa hawakupumzika kuchukua mafuta na mipango yao inafanyika usiku kucha.Hapa ni kazi tu.Wewe nenda kapumzike Ruby mimi hapa umenifikisha nyumbani.Nilipokuwa msituni hatukuwa na muda wa kulala hivyo hadi hawa jamaa watakapofunguka ndipo nitakwenda kupumzika” akasema Gosu Gosu “Sawa Gosu Gosu mimi ngoja nikapumzike kidogo umekuwa ni usiku mrefu sana lakini wenye mafanikio” akasema Ruby na kutoka akaenda kupumzika. TEHRAN – IRAN Nawal aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomein jijini Tehran.Baada ya kukamilisha taratibu zote na kuruhusiwa kuingia nchini Iran, Nawal alipokelewa na mtu aliyekuwapo pale uwanjani akimsubiri akampeleka katika hoteli alikoandaliwa kisha akapelekwa nyumbani kwa Vahid Ghorbani “Nawal karibu sana Tehran” akasema Vahid baada ya Nawal kuwasili katika makazi yake “Ahsante sana” akajibu Nawal “Mara ya kwanza Tahran? Akauliza Vahid “Ndiyo hii ni mara yangu ya kwanza ninafika hapa Tehran” “Karibu sana Tehran.Jisikie nyumbani” akasema Vahid kisha wakaungana wote katika chumba cha chakula kupata chakula cha mchana baada ya hapo Vahid na Nawal wakawa na mazungumzo “Nawal naamini Habiba amekwisha kueleza mengi kuhusu mimi” akasema Vahid “Mama Habiba alinipa maelezo mafupi tu kwamba nitapokelewa uwanja wa ndege lakini hakuniambia nani atanipokea hivyo sifahamu chochote kuhusu wewe” akajibu Nawal “Naitwa Vahid Ghorbani.Mimi na Habiba tuliwahi kuwa katika mahusiano na mimi ndiye baba mzazi wa Najma” akasema Vahid na Nawal akaonyesha mshangao “Wewe ndiye baba mzazi wa Najma? “Ndiyo.Mimi ni baba yake mzazi” “Hata hivyo mmefanana sana.Pole mzee kwa kuondokewa na mwanao” akasema Nawal “Ahsante nashukuru” akajibu Vahid na ukimya mfupi ukapita “Umemuita Habiba mama.Wewe pia ni mwanae? Akauliza Vahid “Mimi nilikuwa mke wa mwanae Abu Dahir” “Ouh kumbe wewe ndiye uliyekuwa mke wa Abu Dahir.Pole sana pia kwa kifo cha mumeo.Habiba amepata pigo kubwa kwa kupoteza watoto wawili ndani ya kipindi kifupi” akasema Vahid “Ni kweli inaumiza mno kupoteza mtu unayempenda” akasema Nawal “Nini hasa dhumuni la kuja Tehran Nawal? Uko hapa kwa mapumziko? Habiba aliniambia nikupokee lakini hakunieleza nini unakuja kufanya hapa Tehran”Akauliza Vahid “Hapana mzee siko hapa kwa ajili ya mapumziko.Niko hapa kuonana na Abu Zalawi” “Abu Zalawi?! Vahid akashangaa “Ndiyo.Habiba aliniambia wewe ndiye utakayenisaidia niweze kuonana naye” akasema Nawal.Vahid akavuta pumzi ndefu “Nilikwisha mueleza Habiba kwamba sitaki kujihusisha tena na suala lolote linalohusiana na Abu Zalawi.Sitaki kuwa na ukaribu wowote na magaidi ! akasema Vahid kwa sauti kali kidogo “Mzee Vahid ninaomba unisaidie niweze kuonana na Abu Zalawi ni muhimu sana” “Wewe naye unahusika na mambo hayo? Akauliza Vahid “Mambo gani mzee? Akauliza Nawal “Ugaidi.Nawe pia unajishughulisha na mambo hayo? “Hapana mzee mimi sijihusishi na hayo mambo ila nina ujumbe muhimu sana kwa Abu Zalawi kutoka kwa Habiba.Nisaidie nionane naye tafadhali.Sina mtu mwingine hapa Iran anayeweza kunisaidia zaidi yako” akasema Nawal na Vahid akakunja sura “Nilimwambia Habiba na ninarudia kukwambia nawe pia kwamba hii itakuwa ni mara ya mwisho mnanihusisha na Abu Zalawi.Nitakusaidia kwa sababu umesafiri umbali mrefu lakini ni marufuku kunihusisha na Abu Zalawi.Sitaki kulisikia tena jina Abu Zalawi katika masikio yangu.Umenielewa Nawal? Akauliza Vahid “Nimekuelewa mzee” akasema Nawal. “Vizuri” akasema Vahid na kuchukua simu yake na kumpigia waziri wa ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahsan Javad ambaye ni rafiki yake mkubwa “Vahid habari yako” akasema Brigedia Jenerali Ahsan Javad “Nzuri sana mheshimiwa waziri.Nimekupigia ninahitaji msaada wako tena” “Nini unahitaji Vahid? Akauliza waziri wa ulinzi. “Ninahitaji kuonana tena na Abu Zalawi” akasema Vahid na Brigedia Jenerali Ahsan Javad akasita “Mheshimiwa waziri” akaita Vahid “Vahid kuna jambo limetokea jana usiku na sina hakika kama umepata taarifa” “Jambo gani mheshimiwa waziri? “Nyumba aliyokuwa anakaa Abu Zalawi ilivamiwa na watu jana usiku wakitaka kumuua” “Abu Zalawi ni mzima? Akauliza Vahid kwa wasi wasi “Usihofu,Abu Zalawi ni mzima.Waliweza kupambana na wavamizi hao na wakawashinda.Kwa sasa Abu Zalawi amehamishwa kutoka katika yale makazi na kupelekwa sehemu nyingine.Nitawasiliana na waziri wa intelijensia mheshimiwa Sassan.Nitawasiliana na Sassan kufahamu mahala alipo kisha nitakufuata hapo kwako” akasema Brigedia Jenerali Ahsan Javad “Ahsante sana waziri” akasema Vahid na kukata simu “Abu Zalawi alivamiwa jana usiku na watu wasiojulikana” Vahid akamwambia Nawal “Abu ni mzima? Akauliza Nawal kwa wasi wasi “Ndiyo ni mzima.Hana tatizo lolote.Wavamizi zote waliuawa.Hata hivyo amehamishwa makazi na kupelekwa katika makazi mengine” akasema Vahid wakaendelea na mazungumzo





    Toka asubuhi Mathew alikuwa amepumzika katika jumba kubwa la Sassan.Ulinzi ulikuwa mkali kuzunguka jumba hili la waziri wa intelijensia na usalama wa taifa wa Iran.Akiwa amepumzika pembeni ya bwawa la kuogelea baada ya chakula cha mchana Mathew akafuatwa na mlinzi na kujulishwa kwamba anahitajika ndani.Mathew akanyanyuka na kuelekea ndani akidhani labda Sassan amerejea.Mara tu alipoingia ndani akapatwa na mstuko baada ya kukutana na watu ambao hakuwatarajia.Waziri wa ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahsan Javad alikuwa ameongozana na Vahid pamoja na Nawal “Karibuni” akasema Mathew.Nawal akainuka na kwenda kumkumbatia “Abu Zalawi nimefurahi kukuona tena” akasema Nawal “Mimi pia Nawal nimefurahi,sikutegemea kukuona hapa” akasema Mathew “Abu Zalawi pole sana kwa tukio la jana usiku” akasema Brigedia Jenerali Ahsan Javad “Ahsante sana mheshimiwa waziri” akasema Mathew “Hawakufanikiwa kukuumiza wale wavamizi? Akauliza Vahid “Hawakufanikiwa.Tuliwaw ahi kabla hawajafanikiwa lengo lao” akasema Mathew “Abu Zalawi tunashukuru kwa kuwa uko mzima na unaendelea vizuri.Kilichotuleta hapa mchana huu ni huyu mgeni wako ambaye amekuja kuonana nawe.Tutamuacha hapa mtazungumza kisha baadae atakuja kuchukuliwa kurejeshwa hotelini kwake”akasema Vahid Brigedia Jenerali Ahsan Javad na Vahid waliondoka na kumuacha Nawal ambaye aliongozana na Mathew kwenda katika bwawa la kuogelea. “Nawal karibu sana Iran.Niliambiwa na Habiba kwamba unakuja Tehran nikadhani ni utani.Nilipokuona nimestuka sana sikutegemea” akasema Mathew “Mathew mimi nawe tumekwisha kuwa kama mapacha.Ulipo nami nipo.Mahala pekee ambako siwezi kukufuata ni mbinguni ambako kila mmoja ataenda kwa wakati wake lakini kwa hapa duniani siwezi kukuacha ukawa sehemu ya hatari lazima niwepo karibu yako ” “Ahsante sana Nawal.Karibu tena kwa mara nyingine” akasema Mathew na muhudumu akafika akawaletea vinywaji “Mahala pazuri sana hapa na unapata huduma nzuri” akasema Nawal “Hapa ni nyumbani kwa waziri wa Intelijensia na usalama wa taifa anaitwa Sassan” akasema Mathew “Inapendeza kama tayari umekwisha tengeneza mtandao” akasema Nawal “Ili kufanikisha misheni yangu lazima nitengeneze mtandao kwanza na ninashukuru Mungu kwamba mipango yangu yote inakwenda vizuri kabisa.Kabla hatujaendelea mbele nataka unipe habari za Tanzania.Ruby na Gosu Gosu wazima? Akauliza Mathew na Nawal akaanza kumsimulia kila kilichotokea nchini Tanzania.Ilikuwa ni simulizi iliyomsisimua sana Mathew “Nawal nimekosa neno la kukushukuru kwa haya uliyoyafanya kwa kushirikiana na akina Ruby.Bila ninyi hivi sasa Tanzania ingekwisha tumbukia katika janga lingine kubwa sana na maelfu ya watu wangepoteza uhai.Ahsante sana Nawal” akasema Mathew “Mathew anayepaswa kushukuriwa katika hili ni Mungu pekee ambaye ametuwezesha sisi kuhakikisha mipango ile miovu haifanikiwi na vile vile tumshukuru pia mama Habiba Jawad.Amewasaliti wenzake ili Tanzania iwe salama” akasema Nawal “Kila ninapomtafakari Habiba ninashindwa nimuweke katika kundi gani.Siamini kama mtu yule ambaye nilikula kiapo cha kumuua amegeuka na kuwa mmoja kati ya watu muhimu mno” akasema Mathew “Sote hatukuwa tukimfahamu vyema Habiba Jawad hapo kabla” akasema Nawal “Vipi maendeleo yake? Akauliza Mathew na Nawal akamueleza kila kitu kuhusiana na kile kilichotokea Riyadh.Mathew aliyekuwa ameinamisha kichwa akitafakari akainua kichwa na kusema “Nawal umefanya kosa kuja Tehran.Unapaswa kurejea Riyadh.Mama Habiba hapaswi kabisa kuwa peke yake.Hapaswi kuwa katika hatari yoyote kwa sasa kwani bado tunamuhitaji mno.Yeye ndiye daraja kati yetu na G20 na mipango yote ya G2o yeye ndiye anayetupatia hivyo hapaswi kwa namna yoyote ile kuwa katika hatari” akasema Mathew “Mathew mama Habiba analifahamu hilo lakini yeye mwenyewe ameweka kipaumbele kikubwa kwako na ndiyo maana akanituma nije hapa kukusaidia na kuhakikisha unakuwa salama” akasema Nawal “Hapana Nawal lazima urejee Riyadh.Hatuwezi kumuacha Habiba peke yake.Yuko katika hatari kubwa” akasema Mathew “Mathew misheni unayoifanya ni kubwa sana na ndiyo maana Habiba ameona maisha yake hayana thamani kama hiki unachokifanya huku na akanitaka nije kukusaidia” “Nalifahamu hilo Nawal lakini lazima tumlinde Habiba na tuhakikishe anakuwa salama.Usihofu kuhusu mimi nitakuwa salama na nitaifanikisha misheni yangu bila matatizo” akasema Mathew “Mathew ! akasema Nawal “Nawal naomba tusiendelee kujadili hilo.Sote tunafahamu umuhimu wa Habiba hivyo lazima tuendelee kumlinda.Habiba akiuawa kuna mengi tutayakosa hivyo basi naomba urudi Riyadh kuhakikisha Habiba anakuwa salama.Endapo nitahitaji msaada sintasita kukuomba uje unisaidie” akasema Mathew wakaendelea na maongezi mengine.





    Saa moja za jioni Sassan Mahmoud akiwa na Mathew waliwasili ikulu kama alivyokuwa ameelekeza Rais Armen Hijazi ambaye alitaka kuonana na Mathew.Walipokewa na wafanyakazi wachangamfu sana na kukaribishwa katika makazi ya Rais wa Iran.Baada ya muda Rais Armen Hijazi akajitokeza na kuwakaribisha.Armen Hijazi alikuwa ni mcheshi tofauti na anavyoonekana katika hotuba zake mbali mbali “Abu Zalawi nimefurahi kukutana nawe.Karibu sana Iran” akasema Rais Armen halafu akamuomba radhi Mathew kuwa ana mazungumzo muhimu na waziri Sassan.Mathew akabaki peke yake pale sebuleni Rais Armen na Sassan wakaenda katika chumba kingine kwa ajili ya mazungumzo. “Sassan nataka kupata mrejesho kuhusu ile orodha.Tayari mmeipitia na kujiridhisha kama ni ya kweli? Akauliza Rais Armen “Ndiyo mheshimiwa rais.Tumeipitia ile orodha na tumejiridhisha ni ya kweli” akajibu Sassan “Vizuri sana.Sasa baada ya kujiridhisha kwamba ni ya kweli nataka hatua za haraka sana zianze kuchukuliwa kwa wale wote walioorodheshwa katika ile orodha.Nataka kazi hiyo ianze usiku huu.Nataka hadi kufika kesho asubuhi majasusi wote wa Israel wawe wametiwa nguvuni na jambo hili lifanyike kimya kimya bila kutumia nguvu yoyote.Wakisha kamatwa wapelekwe mahala wakahojiwe tujue kile ambacho wamekuwa wakikichunguza hapa Iran” akasema Rais Armen halafu wakatoka ndani ya kile chumba wakarejea sebuleni na Sassan hakukaa akamuaga Mathew kwamba anakwenda katika majukumu mengine. “Abu Zalawi ,mheshimiwa Sassan anaondoka kidogo anakwenda kuendelea na majukumu mengine.Kazi yake ilikuwa kukuleta tu hapa.Naomba Kama hutajali tutoke nje kidogo.Mimi hupenda kufanya mazungumzo na wageni wangu nikiwa bustanini” akasema Rais Armen wakatoka mle ndani wakatembea kuelekea katika bustani nzuri ambako kulikuwa na sehemu nzuri kwa ajili ya kupumzika na maongezi. “Abu Zalawi napenda kwanza kuchukua nafasi hii kukukaribisha sana Iran” akaanzisha maongezi Rais Armen “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” “Pili napenda nikupe shukran nyingi sana kwa kitendo cha kishujaa ulichokifanya cha kuwarejesha nyumbani watu wetu ambao tulikwisha hisi wameuawa .Kila mtu hapa Iran anafurahi sana kwa kitu ulichokifanya.Hongera sana” akasema Rais Armen na Mathew akatabasamu “Kabla sijaenda mbali zaidi nataka nikupe pole sana kwa kile kilichotokea jana usiku.Alinifuata waziri Sassan na kunieleza kilichokuwa kimetokea pale mahala ulipokuwa ukiishi.Nikushukuru tena kwa kuongoza mapambano na kuwashinda wale wavamizi.Bila wewe watu wetu wote wangeuawa.Ahsante sana Abu Zalawi” akasema Rais Armen na Mathew akatingisha kichwa kupokea shukran zile “Bado nitaendelea kukushukuru kwa kutupatia orodha ya majasusi wa Israel walioko hapa nchini.Kwa muda mrefu mahusiano yetu na Israel yamekuwa si mazuri .Israel wanatutuhumu kwa kufadhili makundi ya wanamgambo wa Hezbollah,Islamic Jihad na Hamas ambao wamekuwa wakipambana na serikali ya Israel kwa muda mrefu.Tunafahamu kuwa Israel wana majasusi wao hapa Iran lakini ilikuwa ni kazi ngumu kwetu kuwabaini ni akina nani na wako wapi hivyo basi kwa orodha ile uliyotupatia itatusaidia mno katika kuwabaini majasusi hawa na kuchukua hatua kali dhidi yao_Orodha hii hata majasusi wetu wameshindwa kuipata hivyo narudia tena kukupa pongezi nyingi kwa jambo hili kubwa” akasema Rais Armen na kunyamaza kidogo “Waziri Sassan alinieleza kwamba unaomba kupatiwa hifadhi hapa Iran.Usihofu kuhusu hilo kwani tayari nimekwisha toa maelekezo kwamba upatiwe hifadhi hapa Iran na mchakato huo umekwisha anza.Ninaamini hapa utakuwa salama” akasema Rais Armen “Nashukuru sana mheshimiwa Rais kwa kukubali kunipatia hifadhi.Hapa naamini nitakuwa salama zaidi” akasema Mathew na wahudumu wakafika wakawaandalia kahawa.Rais Armen hupenda sana kunywa kahawa nyakati za jioni “Abu Zalawi” akasema Rais Armen baada ya wahudumu kuondoka “Ujio wako hapa Iran umekuwa ni kama vile kuongeza mafuta kwenye moto.Umezidi kuchochea msuguano wetu na Marekani kwani tayari wanafahamu uko hapa na tayari wamekwisha toa tamko kupitia kwa waziri wao wa mambo ya nje kwamba tukusalimishe wewe na wale mateka wengine lakini ninakuhakikishia kwamba hatuwezi kufanya kitu kama hicho.Ninafahamu kitendo ulichowafanyia cha kulipua ubalozi wao nchini Tanzania kitawafanya wakusake usiku na mchana hadi pale watakapohakikisha wamekupata lakini narudia tena kukuhakikishia Abu Zalawi kwamba hatutaweza kamwe kukukabidhi kwa wamarekani.Utaishi hapa ikiwezekana kwa maisha yako yote yaliyobaki kama utapenda na tutakulinda” akasema Rais Armen “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Mzozo wetu na Marekani unazidi kukua siku hadi siku.Kama unavyofahamu kuwa tumewekewa vikwazo vingi vya kiuchumi kwa lengo la kuporomosha uchumi wetu lakini vikwazo hivyo vinawaumiza raia wa Iran ndiyo maana kwao mtu anayefanya jambo baya kwa wamarekani anaonekana shujaa.Raia wamejenga chuki kubwa sana dhidi ya Marekani kutokana na ukandamizaji inaoufanya kwa taifa letu ndiyo maana hawatatuelewa endapo tutakukabidhi kwa Marekani.Abu Zalawi naomba kama hutajali unieleze historia yako ili nikufahamu vyema kwani tayari nimeelezwa mambo kadhaa na wasaidizi wangu lakini nitafurahi zaidi kama nikisikia kutoka kwako wewe mwenyewe” akasema Rais Armen na Mathew akamuelezea historia yake ile ya kutengeneza kama Abu Zalawi “Historia yako inasisimua sana japo ndani yake ina mambo ya kigaidi lakini kwa ukandamizaji unaofanywa na nchi za Marekani na Israel ninathubutu kusema kwamba wanastahili kushambuliwa.Siku za karibuni mzozo wetu umekuwa mkubwa zaidi na tumefikia hadi hatua ya kutishiana kushambuliana.Marekani wamekuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi na washirika wao ambao ni nchi jirani zetu na sisi tumetoa onyo kwamba wakithubutu kurusha hata risasi moja katika ardhi ya Iran basi tutaiharibu Marekani.Tutaichakaza vibaya mno kipigo ambacho hawataamini” akasema Rais Armen “Hapa sasa amenifikisha ninapopahitaji” akawaza Mathew “Marekani” akasema Mathew “Imejiona ni mtawala wa ulimwengu huu na kwamba wanaweza kufanya chochote katika taifa lolote lile wakiamini wao ndio wenye uwezo mkubwa kijeshi kuliko mataifa mengine duniani” akasema Mathew na Rais Armen akacheka kidogo “Wanajidanganya.Nchi nyingi kwa sasa zinapanua teknolojia yao ya silaha hivyo basi wakijidanganya kwamba wao ndio wenye uwezo mkubwa kijeshi watajikuta wakipigwa kipigo kikali sana siku moja” akasema Rais Armen “Mheshimiwa Rais Marekani wamekuwa wanatishia kuishambulia Iran vitisho vilivyoanza muda mrefu.Unadhani kwa nini mpaka leo hii hawajaweza kufanya hivyo? Ni kwa sababu ya vitisho mnavyowapa? “Si vitisho.Tunachokiongea sisi si vitisho ni vitu vya kweli.Nikisema tutaichakaza Marekani ni kitu cha kweli kwani uwezo huo tunao” “Kwa sasa Iran inao uwezo wa kurusha kombola linaloweza kufika Marekani? Akauliza Mathew “Bajeti yetu ya ulinzi haiwezi kulingana na ile ya Marekani lakini uwezo wetu wa kivita umeimarika mno hivi sasa.Tumesomesha watu wetu wengi na sasa wanatusaidia katika kupanua teknolojia yetu ya silaha na kwa taarifa yako hata wale raia wetu uliowakomboa na kuwarejesha nyumbani ni wanasayansi walioko jeshini na walikwenda Urusi kujifunza teknolojia mbali mbali za utengenezajiw a silaha.Tunazo silaha kali sana hivi sasa na tunao uwezo wa kuishambulia Marekani.Tumekuwa tunasaidiana na washirika wetu wa karibu katika kupanua teknolijia yetu ya silaha na hili ndilo limeiogopesha Marekani kutaka kuingia katika vita na sisi na yamebaki maneno tu kwamba watatushambulia” akasema Rais Armen “Mheshimiwa Rais kumekuwa na tuhuma kutoka kwa Marekani kwamba Iran inazo au inakusudia kutengeneza silaha za nyuklia kuna ukweli gani juu ya jambo hili? Akauliza Mathew “Abu Zalawi ungefaa sana kuwa mwandishi wa habari kwa maswali unayouliza lakini kujibu swali lako hizo ni propaganda tu za Marekani na washirika wake hazina ukweli.Bado hatujafikia hatua ya kutengeneza bomu la nyuklia japo tukiamua hatuwezi kushindwa.Abu Zalawi suala hili la sisi na Marekani ni suala pana sana na lenye mambo mengi hivyo hatuwezi kulimaliza kwa usiku huu.Hayo tuliyoyazungumza hayakuwa msingi wa kile nilichokuitia hapa.Kubwa hasa ukiacha shukrani kwako ni kutaka kufahamu namna ulivyoweza kupata orodha ile ya majasusi wa Mossad walioko hapa Iran” akasema Rais Armen “Mheshimiwa rais ninao watu wangu ndani ya Mossad ambao wameniwezesha kuipata orodha ile” “Abu Zalawi kama umeweza kupata orodha kama hii basi unaweza ukafanya mambo mengine makubwa zaidi kwetu.Ninakuona ni mtu mwenye faida kubwa kwetu na kwa kuwa utaishi hapa Iran ninataka kukupatia kazi” akasema Rais Armen “Nipo tayari mheshimiwa Rais kwa kazi yoyote utakayonipatia” “Ninataka utoke kuwa gaidi na kuwa jasusi.Nitakupeleka mafunzoni utafundishwa masuala ya ujasusi na utakapomaliza utafanya kazi katika wizara yetu ya ujasusi ukijielekeza zaidi Israel ambako tayari una watu wako ndani ya Mossad.Utaachana na mambo ya kuua watu kwa ugaidi na badala yake utafanya kazi kubwa zaidi ya kuwalinda watu wa Iran” akasema Rais Armen na ukimya ukatanda “Picha imegeuka tena.Nikikubali kwamba nikafundishwe ujasusi ni mafunzo ya muda mrefu na mimi sina muda wa kuendelea kupoteza hapa Iran.Nikisema hapana wataanza kuwa na mashaka nami.Hapa nimewekwa mtegoni na endapo nikikosea kidogo tu misheni nzima itaharibika” akawaza Mathew “Abu Zalawi usihofu utakuwa salama.Maisha yako yatakuwa mazuri na utayafurahia.Nimefanya maamuzi haya baada ya kuona uwezo mkubwa ulio nao hivyo nimeona unafaa zaidi kuwa jasusi kuliko kuwa gaidi.Hata hivyo sikulazimishi unipe jibu leo.Nakupa muda ukafikirie hadi kesho uwe tayari umefanya maamuzi ili maandalizi yaanze mara moja” akasema Rais Armen.Mathew akazama mawazoni kwa muda halafu akasema “Mheshimiwa Rais kuna jambo nataka nikueleze lakini ninakuomba kile nitakachokueleza kibaki baina yetu.Nataka nikueleze ukweli” “Usihofu Abu Zalawi niambie chochote nitakitunza”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ akasema Rais Armen “Mheshimiwa Rais kama nilivyokwambia kwamba nataka nikueleze ukweli…” akasema Mathew na kusita kidogo “Endelea Abu Zalawi” “Mheshimiwa Rais mimi si gaidi,mimi ni jasusi” akasema Mathew na nusura kikombe cha kahawa alichokishika Rais Armen kimponyoke na kuanguka “Unasema? Akauliza Rais Armen “Mimi si gaidi kama ninavyojulikana sasa bali mimi ni jasusi” “Jasusi ? Mbona sikuelewi Abu Zalawi? “Jina langu ni Mathew Mulumbi na si Abu Zalawi.Mimi mtanzania” akasema Mathew na kuzidi kumchanganya Rais Armen “Bado sikuelewi Abu Zalawi.Hebu jaribu kutafuta namna ya kunifanya nikuelewe hicho unachoniambia” akasema Rais Armen “Nafahamu mheshimiwa Rais haitakuwa rahisi kunielewa lakini nataka nirudie tena kukuhakikishia kwamba mimi ni jasusi na si gaidi kama ninavyojulikana hivi sasa.Jina langu ni Mathew Mulumbi mzaliwa wa Tanzania na nimefanya kazi katika shirika la ujasusi Tanzania kwa muda mrefu hadi nilipoamua kuachana na shirika hilo na kuanza kufanya shughuli zangu binafsi” akasema Mathew na kunyamaza kidogo huku sura ya Rais Armen ikiendelea kuonyesha mshangao mkubwa. “Pamoja na kuacha kazi katika shirika la ujasusi la Tanzania niliendelea bado kushirikishwa katika misheni mbali mbali za kijasusi na hadi misheni ya mwisho ambayo ndiyo imenipelekea mimi kufika hapa nilipofika leo na kufahamika kama Abu Zalawi” Mathew akamsimulia Rais Armen mkasa mzima wa kutekwa kwa Olivia namna alivyoweza kupambana na magaidi wa IS hadi alipotekwa na majasusi wa Mossad na kupelekwa Israel. “Haya mbona maajabu” akawaza Rais Armen akimtazama Mathew kwa jicho la mshangao.Mathew hakumjali akaendelea “Nilifungwa katika gereza nchini Israel kwa miaka mitatu nikipatiwa mateso makali lakini sikuwahi kufumbua mdomo wangu kutamka chochote hadi pale walipoamua kuigusa familia yangu ndipo tulipoingia makubaliano na Mossad ya kumsaka Habiba Jawad ambaye alikuwa mfadhili mkuu wa makundi ya kigaidi ya IS na mengine ya wanamgambo wa kipalestina wanaopigana na serikali ya Israel” akasema Mathew na kumuelezea Rais Armen makubaliano aliyoyafanya na Mossad na namna alivyoweza kujenga urafiki na Ammar Nazari. “Hapo ndipo jina la Abu Zalawi lilipoanza.Taarifa zote za kuhusiana nami kama Abu Zalawi si za kweli bali zimetengenezwa na Mossad kunifanya nikubalike na Ammar Nazari” akasema Mathew na kuendelea kumsimulia namna alivyoweza kutoroka gerezani na Ammar Nazari na kujiunga katika kundi lake la Ammar Nazari brigades.Mathew alimueleza Rais Armen kila kitu alichokifanya akiwa na kundi la Ammar Nazari brigades hadi pale Israel walipoweza kugundua maficho ya Ammar na kumshambulia wakamuua huku yeye na Nawal wakinusurika baada ya kutaarifiwa kuhusu shambulio hilo “Baada ya kunusurika katika shambulio hilo niliendelea na safari ya kumsaka Habiba Jawad” akasema Mathew na kueleza mambo waliyoyaptia hadi walipofanikiwa kukutana na Habiba Jawad. “Baada ya kuonana na Habiba Jawad ile mipango yangu yote niliyokuwa nayo ya kutaka kumuua ikayeyuka” akasema Mathew na kumtazama Rais Armen ambaye bado alikuwa anamtazama kwa macho yaliyojaa mshangao “Najua utaniuliza nini sababu ya kubadili mpango wangu wa kumuua Habiba ambaye alifadhili kundi la kigaidi la IS lililofanya matukio mabaya nchini Tanzania.Jibu ni kwamba nilimuoa mtoto wa Habiba anaitwa Najma.Kumuoa mtoto wa Habiba peke haikuwa sababu ya kunifanya nibadili mtazamo wangu bali kulikuwa na sababu nyingine kubwa.Niligundua kwamba Habiba Jawad ambaye nilikuwa namfikiria kabla ya kukutana naye ni tofauti na Habiba Yule ambaye nilimfahamu baada ya kuonana naye.Alinisaidia nikafahamu mambo mengi” akasema Mathew na kumweleza Rais Armen kuhusiana na namna Habiba alivyomsaidia katika misheni ile ya kupambana na Melanie Chuma. “Baada ya kufanikisha misheni hiyo na Tanzania ikawa salama nilirejea Riyadh na hapo ndipo nilipogundua jambo kubwa na la siri ambalo wengi hawalifahamu” akasema Mathew na kumuelezea Rais Armen kuhusiana na kikundi cha G20. “Abu Zalawi unazidi kunichanganya .Hebu nieleze taratibu nikuelewe.Hicho unachonieleza ni kitu kigeni kabisa kwangu” akasema Armen na Mathew akaanza kumueleza tena kuhusiana na kikundi cha G20. “Kwa hiyo Habiba Jawad alikuwa anafadhili makundi ya kgaidi kwa niaba ya G20” akasema Mathew “Abu haya unayonieleza ni mambo ya kweli au ni hadithi umetunga? Akauliza Rais Armen “Haya yote ninayokueleza ni ya kweli mheshimiwa Rais” akasema Mathew na kumueleza Rais Armen kile kilichotokea nchini Tanzania na namna Marekani walivyofanikiwa kuwachonganisha watanzania kwa kutumia dini na kupelekea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kuibuka huku wao wakichukua mafuta. “Wote tulistushwa na mapigano yale yaliyotokea Tanzania.Tunaifahamu Tanzania ni nchi iliyojaa amani na watu wake wanaishi kwa upendo mkubwa licha ya tofauti zao za dini na rangi lakini kitendo cha kuanza kushambuliana wao kwa wao kiliishangaza dunia.Kumbe hizi zote ni fitina za Marekani kwa ajili ya kuchota mafuta ! akasema Rais Armen kwa hasira “Mambo haya yanaendeshwa kwa siri kubwa hata Rais wa Marekani hatakiwi kufahamu chochote kuhusu uwepo wa G20” akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Habiba alinipeleka Marekani nikakutana na kikundi hiki cha watu hatari kabisa duniani” akasema Mathew na kuelezea yale aliyopitia kabla ya kukutana nao “Waliporidhika na uwezo wangu ndipo nikakutana nao kwa ajili ya kunikabidhi kazi waliyotaka nikaifanye” akasema Mathew na kumuelezea Rais Armen kazi ambayo alitumwa kuifanya.Sura ya Rais Armen libadilika na kujikunja zaidi.Alipandwa na hasira “Hivyo basi nililipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kama nilivyokuwa nimeelekezwa” “Kumbe kulipua ubalozi ulikuwa ni mpango wao wenyewe? “Ndiyo ulikuwa ni mpango wao ili nionekane gaidi na nianze kutafutwa” Mathew akamueleza mpango mzima namna ulivyoandaliwa. “Na wewe kwa nini ulikubali kuingia katika kazi yao na kuchafua jina lako? Tazama sasa dunia nzima wanafahamu wewe ni gaidi. ! akaendelea kusema kwa ukali Armen “Nilikubali kwa kuwa nilikuwa na mpango mahususi na Habiba Jawad” akasema Mathew na kuendelea kueleza namna alivyokamatwa jijini Nairobi hadi alivyopelekwa jijini Victoria nchini Sheli Sheli ambako alikutanishwa na wale raia sita wa Iran waliokuwa wametekwa na kufichwa hapo.Akaeleza namna mpango ulivyoandaliwa wa kuwawezesha kuiteka ndege hadi walivyoingia nchini Iran.Rais Armen alibaki mdomo wazi “Baada ya kufika hapa ndipo wakagundua kwamba mimi ni jasusi na si gaidi kama walivyoelezwa na Habiba na mpango wa kuniua ukaanza wakiwatumia majasusi wa Mossad” “Wewe ulifahamu vipi kuhusu mpango huo wa kukuua? “Ni kupitia Habiba Jawad”akasema Mathew na kumueleza namna Habiba anavyowasiliana na makamu wa Rais Mark Piller na hadi walivyoweza kuipata ile orodha ya majasusi wa Israel “Mheshimiwa Rais utanisamehe kwa maelezo yangu marefu lakini nimelazimika kutumia maelezo hayo marefu ili uweze kunielewa.Kwa hiyo mheshimiwa Rais hapa nilipo nipo katika misheni.Nimevaa joho la ugaidi lakini mimi si gaidi ni jasusi” akasema Mathew.Zilipita dakika tano za ukimya halafu Rais Armen akasema “Abu Zalawi usinione niko kimya namna hii ni kwa sababu nimekosa maneno ya kuongea.Haya uliyonieleza yamenipa baridi ya ghafla na sijui niseme nini.Ni mambo mazito ambayo sikuwa nimetarajia kuyasikia.Lakini kwa nini umeamua kunieleza ukweli? Kwa nini usingeendelea na misheni yako kimya kimya? “Nimeamua kukueleza ukweli kwa sababu ninahitaji msaada wako ili niweze kurejea tena Marekani na kukimaliza kikundi hiki cha G20 ambacho kimesababisha damu nyingi imwagike sehemu mbali mbali duniani na hasa nchini kwangu Tanzania” “Marekani na dunia nzima wanafahamu wewe ni gaidi na unatafutwa kwa kulipua ubalozi wao nchini Tanzania.Huoni kwamba unataka kujiweka katika hatari kubwa sana endapo utataka kurejea Marekani? “Wamarekani hawaufahamu ukweli.Hawajui nini kinachoendelea nchini mwao.Ninataka kwenda kuwaeleza ukweli.Ninataka kuwafumbua macho wafahamu udhalimu unaofanywa na watu wao wenyewe.Hawana habari kama kuna kirusi kilitakiwa kusambazwa nchini Tanzania ambacho kingeweza kusambaa dunia nzima.Nataka nikayaweke haya yote wazi wayafahamu” akasema Mathew “Abu Zalawi hiki unachotaka kukifanya ni kitu cha hatari kubwa.Hawa jamaa hawataweza kukuacha hai” “Nalifahamu hilo mheshimiwa Rais lakini niliweka ahadi lazima nikimalize kikundi hiki ambacho kimetesa watu wengi sana duniani hadi sasa.Lazima nihakikishe nimekiondoa na kuwalipia kisasi watu wote ambao damu zao zimemwagika kwa sababu ya kundi hili hivyo siogopi kufa.Nimepitia magumu mengi hadi kufika hapa na siwezi kuishia njiani lazima nihakikishe nimeimaliza misheni hii.Damu za watu zimemwagika katika misheni hii,maisha ya watu muhimu kama Habiba Jawad yako hatarini kwa sababu ya misheni hii hivyo kwa namna yoyote ile lazima nihakikishe ninaimaliza” akasema Mathew “Abu Zalawi nimekuelewa.Ninaiona ndani mwako dhamira ya dhati ya kukimaliza kikundi hiki hatari na mimi siwezi kukuzuia hasa kwa kuzingatia kwamba umepitia mchakato mgumu sana hadi kufika hapa ulipofika na umekuwa mkweli kwangu.Nini unataka nikusaidie ili uweze kufanikisha misheni yako kwa sabau hata mimi ninatamani sana kikundi hicho kiondoke naamini kimekuwa kinachochea zaidi mgogoro kati yetu na Marekani” “Ninataka kupata picha halisi ya kile kinachoendelea katika vinu vyenu vya nyuklia ili nipate kitu cha kunikutanisha tena na Mark Piller makamu wa rais wa Marekani.Walitaka nilipue kinu hicho lakini siwezi kufanya hivyo wakati tuhuma kwamba kuna utengenezaji wa silaha za nyuklia si za kweli hivyo nitahitaji nipate picha kwa ajili ya kwenda kuwathibitishia kilekinachoendelea katika kinu hicho.Jambo la pili nataka itengenezwe taarifa bandia kuhusu mfumo wa silaha wa Iran ambayo ndani yake kutakuwa na silaha kali ambazo zina uwezo wa kushambulia nchi zote jirani na Iran,makombora ya masafa marafu ambayo yanaweza kuzishambulia manowari za adui hata zikiwa umbali mrefu na katika taarifa hiyo ionekane kuna kazi inaendelea ya kutengeneza kombora ambalo litakuwa na uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na kufika hadi katika jiji la Los angeles.Wamarekani wanaogopa kushambuliwa nyumbani hivyo baada ya kuiona taarifa hiyo wataogopa na kusitisha mpango wa kuishambulia Iran kijeshi.Mpango huo ukifutika dirisha la mazungumzo litafunguliwa ili kutafuta amani na hapo ndipo Iran itasimama kidete kutaka vikwazo vyote vya kiuchumi viondolewe.Mwisho kabisa nitaomba wale mateka wa marekani waachiwe pamoja na ile ndege ili kuondoa msuguano unaoweza kujitokeza.Huo ndio msaada ninaoutaka mheshimiwa Rais” akasema Mathew na zaidi ya dakika tano za ukimya zikapita “Abu Zalawi nimejaribu kuyatafakari maombi yako yana msingi.Wewe ni mtu mwenye akili nyingi sana.Ulipaswa kuzaliwa Iran wewe” akasema Rais Armen na wote wakacheka kidogo “Kwa ujumla ni mpango mzuri hata mimi ninakubaliana nao.Kesho nitatoa maelekezo na utapelekwa katika kinu kikubwa kabisa cha nyuklia ambacho Marekani na washirika wake wamekuwa wakipiga kelele kwamba tunakitumia katika kutengeneza silaha za nyuklia.Utapiga picha uthibitishe kwamba madai yao si ya kweli na wakati huo huo taarifa hiyo ya silaha unayoihitaji itakuwa inaandaliwa” akasema Rais Armen Mazungumzo ya Mathew na Rais Armen yaliendelea hadi ilipofika saa sita za usiku ndipo Mathew aliporejeshwa katika makazi ya waziri Sassan.Mara tu alipofika alichukua simu ya nyumbani kwa Sassan na kupiga hotelini alikofikia Nawal akaomba kuunganishwa na chumba chake “Hallow” ikasema sauti ya Nawal akionekana kutoka katika usingizi “Nawal ni mimi Mathew.Samahani kwa kukuamsha” “Usijali” “Nawali nimekupigia kukujulisha kwamba nimetoka ikulu ya Iran sasa hivi kuzungumza na Rais Armen Hijazi”akasema Mathew na Nawal akastuka “Umetoka ikulu? “Ndiyo nimetoka ikulu.Nimezungumza kwa kirefu sana na Rais Armen na taarifa nzuri ni kwamba misheni yetu inakaribia kufika ukingoni” akasema Mathew na kumueleza Nawal kila kitu walichokizungumza na Rais Armen Hijazi. “Mathew umenitoa machozi.Sikutegemea kama mambo yangekwenda namna hii” akasema Nawal “Hata mimi sikuwa nimetegemea jambo kama hili.Nilipata akili hii hapo hapo wakati ninazungumza na Rais na ninashukuru kwamba ameyakubali mawazo yangu” “Mungu ashukuriwe sana.Mathew mimi kesho ninakwenda Riyadh kama tulivyokuwa tumekubaliana.Nitaondoka saa mbili za asubuhi nadhani hatutapata nafasi ya kuonana” akasema Nawal “Nawal tunakaribia kufika mwisho wa misheni yetu hivyo kuna mambo yatabadilika.Kwanza nitakuhitaji Marekani.Ili kuimaliza misheni hii nahitaji msaada wako kule.Pili ulinieleza kwamba kuna Yule mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko Tanzania anashikiliwa na SNSA .Nataka kuipata rekodi yake akikiri kushiriki katika mipango ya G20.Vile vile wale magaidi nao pia lazima wakiri kuhusika katika mipango ya G20 ya kuchochea vurugu.Vile vile nakihitaji kirusi ambacho kilitakiwa kusambazwa Tanzania” akasema Mathew “Mathew kwa mpango huo,itanilazimu nirejee tena Tanzania ili nikakamilishe hayo mambo.Nimewasiliana na Ruby nilipofika hapa hotelini akaniambia kwamba Jenerali William amekubali kueleza kila kitu.Amepewa mateso makali na Gosu Gosu” akasema Nawal na Mathew akatabasamu “Kama alikuwa anahojiwa na Gosu Gosu lazima afunguke.Basi anatakiwa arekodiwe akikiri kuhusika katika mipango yote ya G20 na vile vile wale magaidi nao wanatakiwa wakiri kuhusika katika mipango ile iliyosababisha machafuko makubwa nchini Tanzania.Unadhani ukifika Riyadh unaweza ukapata ndege ya kuelekea Afrika mashariki hiyo kesho? Akauliza Mathew “Mathew nimepata wazo.Kwa kuwa Rais wa Tanzania yuko upande wetu na yuko tayari kutusaidia kila aina ya msaada kwa nini nisizungumze na Ruby nimuombe azungumze naye ili atoe ndege yake ianze safari kesho alfajiri na mapema kuelekea Riyadh?Ni mwendo wa takribani saa tisa kutoka Dar es salaam hadi Riyadh na mimi nikiondoka hapa Iran saa mbili asubuhi nitafika Riyadh saa saba za mchana hivyo nitazungumza kidogo na Habiba kisha nitaondoka kuelekea Tanzania na kurudi na ndege hiyo hiyo” akasema Nawal “Huo ni mpango mzuri sana Nawal.Fanya hivyo” akasema Mathew na kumpa Nawal maelekezo DAR ES SALAAM – TANZANIA Bado taarifa kuu iliyotawala vyombo vya habari asubuhi hii nchini Tanzania ni kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kufuatia shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana na kuua wanajeshi zaidi ya thelathini.Habari nyingine ilikuwa ni kulipuliwa kwa sehemu ya bomba la mafuta litokalo nchini Uganda. Maisha katika jiji la Dar es salaam kwa kiasi kikubwa yalirejea kuwa ya kawaida japo doria za magari na miguu za askari na wanajeshi bado ziliendelea.Maduka ,masoko na biashara nyingine zilifunguliwa lakini bado wanafunzi hawakuruhusiwa kwenda mashuleni hadi hapo serikali itakapojiridhisha kwamba hakuna kitisho chochote cha kuibuka tena kwa vurugu. Katika ofisi kuu za SNSA kazi ziliendelea kama kawaida.Chini ya ardhi kulikokuwa na vyumba maalum kwa ajili ya mahojiano na watuhumiwa,mkurugenzi msaidizi wa SNSA Papi Gosu Gosu akiwa kifua wazi alikuwa amesimama pembeni akimsubiri mtu aliyekuwa anafunga kamera amalize ili shughuli nyingine ziendelee.Baada ya kumaliza kufunga kamera taa zikawashwa na majaribio yakafanyika halafu Gosu Gosu akaagiza aletwe katika chumba kile Jenerali William. Baada ya dakika chache mlango ukafunguliwa akaingizwwa Jenerali William ambaye hakuweza kutembea alikuwa anavutwa na watu wawili.Mikononi alikuwa amefungwa pingu na uso wake ulikuwa umevimba.Jicho lake moja halikuwa likiona kutokana na kuvimba.Alikuwa kifua wazi na mwili wake wote ulijaa vidonda.Jenerali William alitia huruma sana kumtazama. Aliketishwa kitini hakuwa na nguvu kichwa kikainama.Gosu Gosu akamshika nywele na kukiinua kichwa. “Kama tulivyokubaliana sasa unakwenda kukiri mbele ya kamera yale mambo yote uliyokiri kule ndani ili tuweke kumbu kumbu.Tafadhali angalia kamera na endapo ukijaribu kuleta upuuzi wowote nitakurejesha kule ndani na safari hii nitakuondoa uume wako.Umenisikia?! akauliza Gosu Gosu kwa ukali “Nimekusikia ! akasema Jenerali William kwa sauti dhaifu.Gosu Gosu akaelekeza anyweshwe maji halafu zoezi likaanza mara moja.Jenerali William akaeleza kila kitu alichokifanya na maelekezo yote aliyokuwa anapewa na mwisho akakiri kupokea maelekezo ya kusambaza kirusi nchini Tanzania.Baada ya zoezi kukamilika Gosu Gosu akaelekeza Jenerali William apelekwe akapumzishwe kitengo cha afya akaelekeza aletwe Assad Ismail. Assad akaletwa naye kama ilivyokuwa kwa Jenerali William hakuwa na nguvu za kutembea.Alichafuka damu kana kwamba alikuwa anaogelea katika dimbwi la damu.Hakuwa na sikio la upande wa kushoto na mkono wake wa kulia haukuwa na kidole hata kimoja alikuwa amefungwa bandeji.Mkono wa kushoto aliwekewa kifaa maalum kwani ulikuwa umevunjika.Mdomo ulikuwa umemvimba na kinywani hakuwa na meno kadhaa.Assad hakuwa akitazamika “Nataka dunia ione kwamba Tanzania hatuna mchezo na magaidi au wale wote wanaochezea amani yetu” akawaza Gosu Gosu akimtazama Assad. “Assad umeletwa hapa kwa ajili ya kukiri mbele ya kamera yale yote uliyoyafanya.Ongea kila kitu kama ulivyokiri tukiwa kule ndani” akasema Gosu Gosu na kisha kwa taabu Assad akaanza kueleza kila kitu namna alivyoshiriki katika kuandaa machafuko ya kidini yaliyotokea nchini Tanzania na kupelekea mamia ya watu kufariki dunia. Baada ya kumaliza Assad naye akapelekwa katika sehemu ya afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu “Ruby nimemaliza kazi” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana Gosu Gosu kwa kazi kubwa uliyoifanya.Watu hawa ni wagumu na kama isingekuwa wewe sijui kama wangeweza kufunguka” “Tujipongeze sote kwa kazi kubwa na nzuri tuliyoifanya” “Gosu Gosu sasa ni wakati wako wa kwenda kupumzika mimi ninakwenda kuonana na Rais nimkabidhi majina ya watu wote hapa nchini ambao wametajwa na Assad kwamba walikuwa wanashirikiana nao katika kuratibu na kuchochea vurugu ili ayakabidhi kwa vyombo husika viyafanyie kazi” akasema Ruby na Gosu Gosu akaondoka kurejea nyumbani kwake kupumzika. TEHRAN - BAADA YA SIKU 2 Saa mbili za usiku jijini Tehran,magari matatu yaliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomein.Gari zile zilipita katika geti wanako ingilia viongozi wakuu wa kitaifa na kuelekea karibu na ndege moja.Milango ya gari la mbele ikafunguliwa na watu wanne wakashuka na kutoka katika gari la nyuma watu watatu wakashuka halafu mmoja wao akafungua mlango wa gari la kati kati akashuka Mathew Mulumbi akiwa amevalia nadhifu.Akaagana na wale jamaa kisha akaanza kupiga hatua kuelekea ndegeni mara akasimamishwa na mmoja wa wale jamaa aliyemkimbilia na kumpa simu “Rais anataka kuzungumza nawe” akasema Yule jamaa na Mathew akaichukua ile simu “Mheshimiwa Rais” akasema “Abu Zalawi kabla hujaondoka ninapenda nikutakie kila la heri katika misheni yako.Ninategemea kila kitu kitakwenda vizuri.Kuhusu wale mateka na ndege yao wataondoka kesho” “Nashukuru mheshimiwa Rais” “Mimi ndiye ninapaswa kukushukuru wewe Abu zalawi kwa kitendo chako cha kuamua kuwa muwazi kwangu.Hakikisha kwa namna yoyote unafanikisha misheni hiyo ambayo ina umuhimu pia kwa Iran na endapo utafanikisha misheni yako salama unakaribishwa tena Iran muda wowote” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Kila la heri” akasema Rais Armen na kukata simu Mathew akairejesha simu kisha akaelekea ndegeni na kuondoka kuelekea Riyadh Saudi Arabia. RIYADH – SAUDI ARABIA Saa saba za usiku Mathew aliwasili jijini Riyadh.Nawal alikuwepo uwanjani kumpokea kisha wakaelekea moja kwa moja nyumbani.Habiba Jawad alikumbatiana kwa furaha na Mathew huku machozi yalimdondoka “Mathew sikutegemea kama ningeweza kukuona tena mapema namna hii.Nilitegemea misheni ingechukua muda mrefu na pengine tusingeweza kuonana tena.Karibu nyumbani Mathew” akasema Habiba Baada ya mapokezi yale hakukuwa na muda wa kupumzika usiku ule ule kukawa na kikao muhimu cha kupanga kuhusiana na kile wanachokwenda kukifanya nchini Marekani.Waliweka mikakatio mizito namna misheni ile itakavyokwenda kumalizika nchini Marekani.Nawal akamkabidhi Mathew rekodi za Jenerali William na Sattar wakikiri kuhusika katika kuratibu na kuchochea vurugu nchini Tanzania kwa maelekezo ya G20. “Mama Habiba sijui nikushukuruje kwa mafanikio haya makubwa tuliyoyapata” akasema Mathew “Tunayepaswa kumshukuru ni Mungu wa mbinguni kwa kutusimamia na kutuongoza hadi hapa tulipofika.Yote haya yanafanikiwa kwa maongozi yake.Mathew hakuna kupoteza muda bado unayo safari ndefu.Bado unazo saa kumi na tatu kusafiri angani kwenda kumaliza misheni yako.Tayari nimekwisha mjulisha Mark PIller kwamba misheni yako Iran imekamilika na anakusubiri kwa hamu kubwa.Mathew hakikisha hakuna anayebaki hai.Watu wengi wamepoteza maisha kwa sababu ya kikundi hiki hivyo nao lazima waonje ladha ya kifo ! akasema Habiba “Mama Habiba kwa sasa wakati tunaelekea mwisho wa misheni yetu ni wakati wa wewe kuondoka kwenda mahala kuweka makazi.Rais Armen Hijazi yuko tayari kukupokea na ukaishi kule kwa amani” akasema Mathew “Mathew usihofu kuhusu mimi nitakuwa salama.Nenda kakamilishe misheni yako” akasema Habiba halafu akampatia Diski mweko akamtaka aihifadhi inaweza ikamsaida “Humo ndani nimeweka ushahidi wote wa kuhusiana na mashirikiano yangu na G20.Kuna video mbali mbali ambazo nimekuwa nikiwasiliana nao,kuna kila kitu humo.Nina imani inaweza kuwa na msaada mkubwa kwako” akasema Habiba Mathew akaagana na Habiba akapanda gari kuelekea uwanja wa ndege wa bilionea Habiba Jawad ambako ndege maalum ilikuwa inamsubiri tayari kwa safari ya kuelekea Marekani “Safari njema Mathew.Mimi pia niko nyuma yako kwa saa moja.Tutakutana Washington DC” akasema Nawal wakaagana Mathew akaingia ndegeni na kuondoka. Baada ya kuhakikisha Mathew ameondoka,Nawal akarejea katika makazi ya Habiba ambako alistushwa na kukuta magari ya polisi yakiwasha vimuli muli na vilio vilisikika.Nawal akalazimika kushuka garini akakimbia kuelekea ndani kujua nini kimetokea.Mapigo ya moyo yalimuenda mbio.Katika mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ya Habiba kulikuwa na askari na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia ndani.Nawal akajitambulisha kwamba yeye ni mmoja wa wanafamilia lakini hakuruhusiwa kuingia ndani.Mara akamuona mmoja wa wafanyakazi wa Habiba aliyekuwa amekaa chini akilia akamfuata “Nasra nini kimetokea hapa? Akauliza “Mama Habiba amejiua kwa kujipiga risasi” akasema Nasra.Nawal akahisi nguvu zinamuisha akaanguka chini.Haraka haraka akachukuliwa na kukimbizwa katika gari la wagonjwa lililokuwepo pale ndani kwa ajili ya kupatiwa huduma





    Nawal alirejewa na fahamu na kuanza kuangua kilio baada ya kusikia vilio vya akina mama wengine nje.Akiwa mle ndani akaingia mtumishi wa muda mrefu wa Habiba “Nawal pole sana” “Kwa nini mama Habiba amefanya hivi? Akauliza Nawal huku akilia. “Nimeachana naye usiku huu nikamsindikiza Abu Zalawi uwanja wa ndege kumbe tulikuwa tunaagana! Akasema Nawal akiendelea kumwaga machozi “Inauma sana Nawal.Muda mfupi kabla hajajiua alikuja kunigongea mlango wa chumbani kwangu akanipa bahasha akaniambia nikupatie ukirudi akaenda chumbani kwake na mara tukasikia mlio wa risasi.Walinzi wakakimbilia ndani na kuvunja mlango wakakuta tayari amekufa.Bahasha aliyonipa nikupatie ni hii hapa” akasema Yule mama na kumpatia Nawal ile bahasha akaifungua na kukutana na kipande cha karatasi akakikunjua akakisoma huku machozi yakimdondoka “Nawal najua nimewaumiza sana lakini nawaomba msiumie wanangu.Haya ni maamuzi magumu nimeyafanya ambayo yataumiza wengi lakini imenilazimu kufanya hivi.Nimekuandikia namba za kufungulia kasiki chumbani kwangu utakuta nimewaandalia nyaraka za umiliki wa mali zangu zote wewe na Mathew kwani ndio wanangu pekee waliobaki.Ninawapenda sana mbaki salama” Ndiyo ulivyosomeka ule ujumbe wa Habiba. Nawal alilia machozi mengi sana. “Kwa nini mama Habiba hakusubiri hadi misheni ikamilike ndipo ajiue?Mbona ameniweka katika wakati mgumu sana? Natakiwa kwenda Marekani kuungana na Mathew je niondoke na kuacha msiba? Akajiuliza Nawal http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Kwa namna yoyote ile lazima misheni ikamilike hivyo nitakwenda Marekani.Habiba atazikwa pale misheni yetu itakapokuwa imekamilika.Ametuchagua mimi na Mathew kuwa warithi wake hivyo basi tunao uwezo wa kuzuia mazishi yasifanyike hadi hapo tutakaporejea.Natakiwa kuanza kulishughulikia hili mapema” akawaza Nawal na kuinuka akawasiliana na Sayid Omar mmoja wa watu wa karibu sana na Habiba akamtaka wakutane wazungumze kuhusiana na suala lile.Haikuwa vigumu kwa Sayid Omar kukubaliana na Nawal kwani alifahamu namna Habiba alivyowapenda Nawal na Mathew.Baada ya makubaliano yale Nawal akaondoka kuelekea uwanja wa ndege akitumia ndege binafsi ya Habiba akaondoka kuelekea Marekani kuungana na Mathew WASHINGTON DC – MAREKANI Saa tano kasoro kwa saa za Marekani ,ndege aliyopanda Mathew Mulumbi ilitua katika uwanja wa ndege wa kampuni moja kubwa ya kutengeneza madawa ya mifugo kama malekezo yalivyotolewa na Mark Piler.Tayari walikwisha andaliwa watu wa kumpokea pale uwanjani haraka haraka akaingizwa katika helkopta na kuondoka.Alikuwa amevaa kofia kubwa ya mzunguko na kuyaficha macho yake kwa miwani myeusi.Kidevuni aliweka ndevu bandia hivyo haikuwa rahisi kumtambua kwa haraka. “Naomba Mungu kusitokee tatizo lolote nikajulikana kabla ya kuonana na Mark Piller” akawaza Mathew Helkopta ile ilikwenda kutua katika jumba moja kubwa Mathew akashushwa na kuingizwa ndani.Kulikuwa na walinzi wachache wakiwa wamevalia suti zao nadhifu pamoja na vifaa vya mawasiliano masikioni mwao.Moja kwa moja Mathew akapelekwa katika chumba kimoja kikubwa “Utakaa humu hadi hapo baadae yatakapotolewa maelekezo mengine.Hakuna kutoka ndani ya chumba hiki na kama kuna kitu chochote unakihitaji basi utabonyeza hapa kisha atakukuja mtu kukusikiliza” akasema Yule mlinzi na kumuelekeza Mathew sehemu ya kubonyeza kama akihitaji kitu chochote.Ndani ya chumba kile kuliwekwa kila kitu.Kulikuwa na friji kubwa lililosheheni vinywaji na vyakula vya kila aina,kulikuwa na sehemu ya jiko dogo kama angependa kupika,kwa ujumla kila kitu muhimu kilichohitajika kilikuwemo.Mathew akaenda katika friji akalifungua na kuchukua kinywaji baridi akanywa kisha akaenda kujilaza kitandani. “Naamini macho ya dunia yataelekezwa Marekani siku ya leo kwa kile kinachokwenda kutokea.Naomba Mungu anisaidie” akawaza Mathew Kama walivyokuwa wamepanga,saa mbili baada ya Mathew kuwasili,ndege ya Habiba Jawad iliyombeba Nawal ilitua katika uwanja mdogo wa ndege ulio pembeni ya makazi ya bilionea mmoja anayeishi nje kidogo ya jiji la Washington DC. Derrick Jones mmoja wa marafiki wa karibu sana wa Nawal aliyewahi kufanya naye kazi katika shirika la ujasusi la Marekani CIA alikuwepo katika uwanja huo kumpokea Nawal.Wakakumbatiana kwa furaha kubwa “Chloe ! akasema Derrick wakiwa wamekumbatiana kwa nguvu.Derrick alilifahamu jina la Chloe.Hakulifahamu jina la Nawal “Derrick ! akasema Nawal “Huu ni kama muujiza.Sikujua kama nitakuona tena.Karibu tena nyumbani Chloe” akasema Derrick “Ahsante Derrick” akasema Nawal kisha wakaingia katika gari na kuondoka “Uliponiambia kwamba unakuja sikuamini.Nilidhani labda ni mtu anaigiza sauti yako” akasema Derrick wakiwa garini “Ni mimi Derrick.Mambo yanakwenda je hapa? “Kila kitu kinakwenda vizuri.Maisha yanakwenda vizuri .Nini kilikutokea Chloe? Sote tuliamini tayari umekwisha poteza maisha katika misheni uliyotumwa mashariki ya kati” akasema Derrick “Derrick tuna mengi ya kuzungumza lakini kuna jambo la muhimu lililonileta na ninahitaji sana msaada wako” “Jambo gani Chloe? Akauliza Derrick “Tutazungumza tukifika nyumbani” akasema Nawal na safari ikaendelea kimya kimya “Chloe ungependa kwanza kupita nyumbani kwako? Akauliza “Hapana.Nataka twende nyumbani kwako.Kuna tatizo lolote? “Hakuna tatizo.Mimi bado niko peke yangu.Sijapata bado mwanamke ambaye ninaweza kumpenda kama wewe Nawal” akasema Derrick “Acha mambo hayo Derrick yamekwisha pita muda mrefu sana” akasema Nawal “Huwezi amini Chloe kwamba pamoja na kwamba umepita muda mrefu lakini bado wewe ndiye mwanamke wa pekee ambaye ninataka kuwa naye katika maisha yangu.Najua kwa wakati ule ilikuwa vigumu……………..” akasema Derrick Nawal akamkatisha “Derrick sitaki tuzungumzie masuala hayo.Nimekuja kwako ninahitaji msaada unisaidie hivyo sitaki hadithi zozote za mapenzi” akasema Nawal “Nimekuelewa Chloe.Samahani” akasema Derrick na safari ikaendelea kimya kimya hadi walipofika katika makazi ya Derrick “Nyumba hii ni yako? Akauliza Nawal “Ndiyo ni nyumba yangu” “Hongera.Maisha yako yamebadilika sana siku hizi” “Samahani sikuwa nimekueleza kwamba nimekwisha acha kazi CIA kwa sasa ni mlinzi binafsi wa bilionea ambaye ndege iliyokuleta imetua katika uwanja wake.Ninalipwa mshahara mzuri na maisha yanakwenda vizuri.Karibu ndani Chloe” akasema Derrick kisha wakaingia ndani. “Jisikie nyumbani.Hapa ni nyumbani kwako pia” akasema Derrick “Ahsante Derrick” akasema Nawal na kwenda katika friji akajihudumia kinywaji.Derrick haraka haraka akaenda jikoni kufanya maandalizi ya chakula.Nawal akiwa sofani alikuwa anatazama kifaa mithili ya simu ambacho kilikuwa na ramani na sehemu katika hiyo ramani ikiwaka taa ya kijani hapo ndipo alipo Mathew Mulumbi ambaye alikuwa amevaa saa maalum iliyounganishwa na kifaa kile na kumuwezesha Nawal kujua mahala alipo. Derrick akaweka mezani chakula wakala na baada ya kula wakaenda sebuleni “Chloe ni muda sasa wa kunieleza kitu ulichokuja kukifanya hapa DC” akasema Derrick “Derrick sote tumefanya kazi CIA lakini kuna mambo hatukuyafahamu.Kuna siri kubwa ambayo ni watu wachache tu wanaifahamu hata rais wa nchi haijui” “Kuna nini Chloe? Akauliza Derrick kwa wasi wasi kidogo “Kuna idara ndogo ndani ya CIA ambayo ni ya siri kubwa inaitwa G20’ “G20? “Ndiyo inaitwa hivyo kwa kuwa ina watu ishirini ndani yake na ndiyo maana wakaamua kujiita G20.Idara hii kazi yake kubwa ni kushirikiana na makundi ya kigaidi katika kufanikisha mipango yenye maslahi ya Marekani sehemu mbali mbali duniani” akasema Nawal na kumuelezea kwa kina Derrick kile kinachofanywa na G20. “Haya ni maajabu Chloe.Ndani ya CIA kuna kitu kama hicho? Akauliza Derrick “Ndiyo maana nikakwambia hiki ni kitu cha siri sana na wamarekani hawajui chochote kinachoendelea” “Dah ! akasema Derrick na kutingisha kichwa kwa masikitiko Nawal akaendelea kumueleza kuhusu kile kilichofanywa nchini Tanzania na G20 na Derrick akaonekana kupandwa na hasira “Kile tulichokishuhudia kinatokea Tanzania ni mipango ya nchi yetu? Akauliza Derrick “Ni mipango ya hiki kikundi kidogo.Wamarekani hawajui chochote” akasema Nawal “Hii haikubaliki hata kidogo.Yaani kusababisha machafuko na damu kumwagika kwa sababu ya kupata mafuta? Huu ni wizi na hakuna mmarekani atakayekubali kitu kama hiki” Nawal akaendelea kumueleza Derrick kuhusiana na ule mpango wa kusambaza kirusi nchini Tanzania mpango ambao umeshindwa kufanikiwa.Akayafungua masanduku mawili yaliyokuwa na kirusi ndani yake akamuonyesha Derrick akatetemeka. “Endapo kirusi hiki kingeweza kusambazwa nchini Tanzania kuna uwezekano mkubwa kingesambaa dunia nzima kwani hakina kinga na kingeweza kufika hata Marekani na kutuangamiza sisi wenyewe.Derrick nadhani umeuona unyama unaofanywa na hiki kikundi kidogo kinachodai kinafanya haya yote kwa maslahi ya Marekani” akasema Nawal.Bado Derrick alikuwa anatetemeka kwa woga “Derrick nimekuja kukimaliza kikundi hiki” akasema Nawal “Chloe ni namna gani utaweza kupambana na watu hawa ambao wanaonekana wana nguvu kubwa ya kufanya chochote ndani na nje ya nchi? Akauliza Derrick Nawal akamueleza Derrick namna mpango ulivyoandaliwa. “Nataka kujua Derrick kama uko nami katika jambo hili.Nahitaji sana msaada wako” akasema Nawal Bila kupepesa macho Derrick akasema “Nawal jibu unalifahamu.Siwezi kukuacha peke yako katika jambo kubwa kama hili.Tutakuwa pamoja” akasema Derrick kisha wakaanza maandalizi





    Saa mbili za usiku,Mathew akachukuliwa na gari maalum na kupelekwa katika nyumba Fulani ambako alikaribishwa sebuleni.Baada ya nusu saa Mathew wakachukuliwa na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa na meza na viti viwili.Kilionekana ni maalum kwa ajili ya mazungumzo.Zilipita tena dakika tano mlango ukafunguliwa na walinzi wakaingia halafu akafuata makamu wa Rais Mark Piller ambaye aliwataka walinzi wake wawape nafasi ya kuzungumza.Baada ya walinzi kutoka,Mathew na Mark wakatazama kwa muda halafu Mark akasema “Abu Zalawi karibu tena Marekani.Nimefurahi kukuona tena ukiwa mzima”akasma Mark Piller “Ahsante”akajibu Mathew “Pole pia kwa yote uliyokumbana nayo hadi kufika Iran.Najua ni mambo mengi tuyaweke pembeni na tujielekeze katika kile kitu cha msingi ambacho ni misheni yako nchini Iran” akasema Mark Piller na Mathew akavuta pumzi ndefu “Nilielezwa kila kitu na Habiba kuhusiana na mipango ya kuniua.Nakushukuru kwa kumjulisha Habiba mipango ya G20 na kuokoa maisha yangu.Kama si wewe ningekwisha uawa kwani wale jamaa walikuwa wamejipanga vyema”akasema Mathew na Mark akatabasamu “Ni kweli Abu kulikuwa na mipango ya kukuua baada ya kugundua kwamba wewe si gaidi bali ni jasusi.Sikutaka uuawe wakati umekwisha fika nusu ya misheni yako hivyo nikawasaliti wenzangu ili wewe uwe hai na umalizie misheni yako” akasema Mark Piller “Nashukuru sana” akasema Mathew “Abu Zalawi kitu nilichokifanya ni kitu kibaya sana na endapo nikijulikana nitauawa hivyo basi mara tu utakaponikabidhi taarifa ya kile ulichokipata nchini Iran utaondoka kimya kimya hapa Marekani na kwenda sehemu yoyote unakotaka ukaanze maisha mapya.Nitakupatia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kukuwezesha kuishi maisha mapya sehemu ya mbali kabisa” akasema Mark Piller.Mathew akafungua mkoba wake akatoa diski mweko akampatia Mark ambaye aliinuka akafungua mlango na kumtaka mmoja wa walinzi wake akamletee kompyuta yake garini.Kompyuta ilipoletwa akaweka ile diski akakuta kuna picha na video mbali mbali “Hiki nini? akauliza “Hicho ni kinu cha nyuklia ambacho nilipewa maelekezo ya kukilipua lakini sikuona sababu ya kukilipua.Video hizo ni kile ambacho kinaendelea ndani ya kinu hicho unaweza kushuhudia wewe mwenyewe” akasema Mathew “Video hizi umezitoa wapi? “Nimezichukua mimi mwenyewe.Nimeingia katika kinu hicho na kupita kila sehemu nikachukua hizo video ili kuwathibitishia kwamba madai ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia katika kinu hicho si ya kweli” akasema Mathew na Mark Piller akabadili sura. Mathew hakumjali akatoa diski mweko nyingine akampatia Mark Piller “Utapitia taratibu na kwa nafasi video hizo.Naomba uitazame na hii pia” akasema Mathew na Mark akaichomeka ile diski nyingine “Hiyo ina taarifa zote za kuhusiana na silaha za Iran” akasema Mathew na Mark akapitia haraka haraka. “Umewezaje kuzipata hizi taarifa? Akauliza Mark huku sauti yake ikionekana kuwa na kitetemeshi “Mlinituma kazi na nimeifanya kazi mliyonituma kama mnavyotaka” akasema Mathew halafu akatoa diski nyingine na kuinuka akaenda katika kompyuta ya makamu wa Rais akaichomoa ile diski na kuiweka nyingine na mara akaonekana mtu mmoja aliyevimba uso wake “Naitwa Jenerali William kutoka jeshi la Marekani ambaye ni mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko nchini Tanzania” Mark Piller akatetemeka na kugeuka akamtazama Mathew “Kitu gani hiki? Akauliza Mark “Endelea kutazama” akasema Mathew na Mark akaendelea kuitazama ile video ambayo Jenerali William alieleza kila kitu alichoelekezwa kukifanya kuanzia kuratibu na kuchochea vurugu hadi mpango wa kusambaza kirusi.Mark Piller midomo ilimtetemeka alitaka kusema kitu akashindwa Mathew akatoa diski ile na kuweka nyingine ambayo ilimuonyesha Assad Ismail akikiri kuhusika katika kuchochea vurugu nchini Tanzania kwa maelekezo ya G20.Alieleza kila kitu “Mark Pil…..” akasema Mathew lakini kwa haraka Mark akaunyoosha mkono wake akataka kubonyeza kitufe kidogo kilichokuwa chini ya meza ambacho kingewapa ishara walinzi wake ili waingie mle ndani mara moja lakini Mathew alikwisha kiona kitendo hicho akamtandika ngumi nzito Mark akaanguka chini pamoja na kiti alichokuwa amekalia. “Hakuna chochote unachoweza kukifanya kwa sasa Mark Piller.Uongozi ninao mimi na utafuata kile nitakachokueleza.Nyanyuka! akasema Mathew na Mark Piller akanyanyuka akatoa kitambaa na kujifuta damu zilizotoka mdomoni “Abu Zalawi unajidanganya kjana,hautaweza kutoka salama ndani ya nyumba hii.Huu ni mwisho wako ! akasema Mark kwa hasira “Sikiliza Mark Piller.Wewe ni makamu wa Rais wa Marekani na una uwezo wa kutoa maelekezo nikauawa lakini kabla hujafanya hivyo naomba unisikilize” akasema Mathew na kutazamana na Mark aliyefura kwa hasira “Siko peke yangu ninayeifahamu siri hii.Nina wenzangu wako hapa Marekani ambao kama hawatapata taarifa zozote kutoka kwangu kwa muda tuliopanga watajua nimeuawa hivyo wataanika mambo yote mnayoyafanya wewe na wenzako kwa wamarekani na dunia nzima ili wafahamu uovu wenu mashetani wakubwa nyie.Kama hiyo haitoshi kirusi ambacho mlitaka kukisambaza nchini Tanzania tayari kiko hapa Marekani na ikitokea nimeuawa basi kitasambazwa hapa Marekani” akasema Mathew.Mark Piller aliyekuwa anahema haraka haraka akasema “Nini unakitaka Abu Zalawi? “Nataka umpigie simu David Walker awakusanye G20 wote mkutane mahala ambako huwa mnakutana kila siku ! “Hilo haliwezekani.Mimi ni makamu wa Rais wa Marekani na siwezi usiku huu kwenda sehemu kama hizo hatarishi ! “Kama umeweza kufika hapa basi unaweza kwenda sehemu yoyote muda wowote” akasema Mathew “Abu Zalawi hapa ni nyumbani kwangu .Nini unakitaka? Tafadhali Abu Zalawi usilifanye jabo hili liwe gumu kwa upande wako.Achana na hiyo mipango yako,mimi ninakupa fursa ya kuyaanza maisha mapya sehemu yoyote duniani na tutakuwezesha kwa kila kitu.Tafadhali sana” akasema Mark Piller “Mark chukua simu mpigie David Walker haraka sana nataka G20 wote wakusanyike ndani ya dakika ishirini kutoka sasa” “Abu Zalawi unajiweka katika matatizo makubwa sana.Naomba kubali fursa niliyokupa uondoke usiku huu na ukayaanze maisha yako.Nimekuandalia masanduku sita yaliyojaa fedha ili ukayaanze maisha mapya.Nakuomba kijana usiiache fursa hii ikakupita” akasema Mark Piller “Mark unapiga simu hupigi? Akauliza Mathew “Utanifanya nini nikisema hapana?Utaniua? akauliza Mark “Nina saa hii mkononi na endapo nikibonyeza kitufe hiki hapa nitawapa ishara wenzangu ambao watatekeleza yale niliyokwambia tutayafanya.Huu si utani MarkPller.Una sekunde tano za kufanya maamuzi” akasema Mathew akiwa ameishika saa yake akahesabu sekunde tano. “Subiri! Akasema Mark Piller “Nini unataka kukifanya Abu Zalawi? Akauliza Mark Piller “Fanya kile nilichokuelekeza Mark! Akafoka Mathew na Mark Piller akapiga simu kwa David Walker akamtaka awakusanye watu wote wa G20 katika ofisi yao ya siri. “Wakati tukiwasubiri wenzako wakusanyike endelea kutazama video hii” akasema Mathew na kumuwekea Mark Piller video ya Habiba Jawad akijieleza na kuzungumzia mambo mbali mbali ambayo amekuwa akiyafanya kwa kushirikiana na G20.Ilikuwa ni video ndefu na kabla hajaimaliza kuitazama akapigiwa simu na David Walker ambaye alimjulisha kwamba tayari wamekwisha kusanyika wanamsubiri.







    Mathew akiwa na makamu wa Rais Mark Piller waliwasili katika nyumba ambayo G20 huitumia kama ofisi yao na mara nyingi hukutana hapo.Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na ukumbi mzuri wa mikutano ambao huutumia kwa vikao vyao. Baada ya kushuka garini Mark akapokewa na David Walker ambaye hakuweza kumtambua Mathew kwa namna alivyokuwa amejibadilisha.Mark alionekana kuwa na haraka sana wakaongozana kuelekea ndani na David akamzuia Mathew kuingia ndani ya ule ukumbi akidhani ni mmoja kati ya walinzi wa makamu wa Rais lakini Mark Piller akamtaka amruhusu aingie ndani “Hapana Mar…………” kabla David hajamaliza sentensi yake akajikuta amepigwa teke akaangukia ndani.Walinzi wa makamu wa Rais wakataka kumdhibiti Mathew lakini Mark Piller akawataka wasifanye hivyo na Mathew akaingia ndani ya ule ukumbi na kufunga mlango.Bado David Walker alikuwa amelala chini.Wenzake wakamuinua na kumkalisha kitini huku akigugumia kwa maumivu makali ya mbavu.Mathew akabonyeza moja ya kitufe katika simu yake ambacho kiliwapa ishara akina Nawal kwamba pale alipo ndipo mahala ambapo kila kitu kitafanyika.Nawal na Derrick wakiwa na kundi la watu ishirini waliowakodisha kwa ajili ya kazi ile hawakuwa mbali kwani walikuwa wanamfuatilia Mathew kupitia kile kifaa alichokuwa nacho Nawal. “Tusikilizane tafadhali.Nataka kila mmoja achukue nafasi yake ! akasema Mathew na sauti ile ikawastua wale watu mle ndani hasa David Walker ambaye licha ya maumivu makali lakini akainua kichwa kumtazama mtu Yule.Mathew akavua kofia na miwani halafu akavua zile ndevu bandia na taharuki iliyotokea ndani ya ukumbi ule haielezeki. “Ni mimi Abu Zalawi naomba msistuke ! akasema Mathew.Bado watu hawakuamini kama walichokuwa wanakiona mbele yao ni kitu cha kweli. “Nafahamu hamkutegemea kuniona tena hapa lakini atakayeweza kuiondoa roho yangu katika hii dunia ni Mungu pekee” akasema Mathew “Tayari mmekwisha nifahamu lakini rasmi nitajitambulisha kwenu kuwa jina langu halisi ni Mathew Mulumbi na si Abu Zalawi na kikubwa zaidi ni kwamba mimi si gaidi bali ni jasusi.Mlinituma nchini Iran lakini nikiwa kule mlituma watu kuniua na mpango huo haukufanikiwa.Mnajua kwa nini? Ni kwa sababu mwenzenu Mark Piller aliwasaliti ! “Abu Zalawi ! akasema Mark kwa ukali “Tulia Mark Piller ! akasema Mathew “Mathew na Rais walitaka misheni iendelee na wakanisaidia hadi nilipomaliza misheni yangu na leo niko hapa mbele yenu kuhitimisha uovu wenu.Kulipa damu ya watanzania na wale wa sehemu nyingine duniani ambao wamepoteza maisha yao kwa sababu ya mipango yenu kwa kushirkiana na makundi ya kigaidi.Leo ni mwisho wenu” akasema Mathew akainuka Donald Cooper na kumnyooshea Mathew bastola “Kama ulishindwa kuuawa nchini Iran kwa sababu ya usaliti wa huyu shetani Mark basi umejileta wewe mwenyewe katika mdomo wa kifo ! akasema Donald na Mathew akacheka kidogo “Weka silaha yako chini Donald.Najua ninyi nyote mna bastola na mnaweza kuniua lakini hebu nipeni dakika kumi tu nizungumze nanyi” akasema Mathew “Donald kaa chini tafadhali ! akasema Mark Piller “Mark ni wewe uliyesababisha haya yote.Kwa nini ukatusaliti wenzako ? Akauliza kwa hasira Donald Mark akawa kimya.Mathew akachukua diski mweko na kuichomeka katika kompyuta iliyounganishwa na projekta na katika runinga kubwa mtu mmoja akaonekana .Baada ya mtu yule kujitambulisha kuwa ni jenerali William wote wakabaki midomo wazi.Waliitazama video ile hadi ilipomalizika kisha akawawekea video ya Assad Ismail na wakati wakiendelea kuitazama saa yake ikatoa mlio mnara tatu akaitazama “Mmefanya mambo mengi maovu sehemu mbali mbali duniani.Mmemwaga damu nyingi…..” akanyamza Mathew baada ya milio ya risasi kusikika nje ya mlango wa kile chumba kisha mlango ukapigwa teke ukafunguka akaingia Nawal akiwa na bunduki inayofuka moshi. “Mathew tumalize mambo haraka haraka imesikika milioya risasi kutoka kwa walinzi wa makamu wa Rais hivyo askari wanaweza wakafika hapa muda wowote ! Nawal akamwambia Mathew.Mara Mathew na Nawal wakarukiwa na Derrick akawaangusha chini na ukasikika mlio wa risasi kutoka katika bastora ya Donald akitaka kumuua Mathew.Derrick akageuka haraka na kummiminia risasi Donald akaanguka na kufariki pale pale. “Ahsante Derrick” akasema Nawal Haraka haraka wakaingia vijana wawili wakiwa na kamera wakaiungansha na kompyuta halafu wakawapa ishara akina Mathew kwamba kila kitu kiko tayari.Mathew akajitokeza mbele ya Kamera na matangazo ya moja kwa moja yakaanza “Habari zenu Marekani.Sura hii si ngeni kwenu.Ninatafutwa kwa tuhuma za kulipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam Tanzania.Mnanifahamu kwa jina la Abu Zalawi lakini hilo si jina langu halisi.JIna langu halisi ni Mathew Mulumbi na ninatokea Tanzania. Ndugu wamarekani ninazungumza nanyi nikiwa hapa Washington DC Marekani na lengo la kuja mbele yenu usiku huu ni kuwaeleza ukweli ambao hamuufahamu” akasema Mathew na kugeuka. “Ndani ya chumba hiki kuna watu wapatao ishirini wakiongozwa na makamu wa rais wa Marekani Mark Piller.Hawa wote ni wafanyakazi wa shirika la ujasusi la Marekani.Ndani ya CIA kuna idara ndogo ya siri yenye watu ishirini inayojulikana kama G20 ambayo majukumu yake ni kushirikiana na magaidi katika kufanikisha mipango mbali mbali yenye maslahi kwa Marekani” akasema Mathew Taarifa za kuwepo kwa video ile ya moja kwa moja ya gaidi Abu Zalawi akizungumza ilisambaa kwa haraka sana na watu wengi wakasimamisha shughuli zao kuitazama.Vituo mbali vya runinga na redio vilikatisha matangazo yao na kuanza kurusha video ile.Runinga kubwa zilizokuwa katika majengo makubwa zote ziliunganishwa na matangazo yale na watu waliokuwa mabararani wakafuatilia kile kilichokuwa kinaendelea. Rais William Washington akiwa amepumzika katika makazi yake ikulu alitaarifiwa kuhusu uwepo wa video ile akataka kuitazama lakini tayari sehemu kubwa imekwisha mpita “Tukio la kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani ni tukio la kupangwa na wamarekani wenyewe kupitia watu hawa waliomo humu ndani ukiwa ni mpango wa kuniwezesha kuingia nchini Iran” akasema Mathew na kueleza kila kitu kuhusiana na mipango ile ya kumpeleka Iran. Rais Wiliam akampigia simu mkuu wa FBI na kumuuliza kuhusu hatua walizozichukua kufuatia matangazo yale ya moja kwa moja ya gaidi Abu Zalawi “Tayari tumekwisha fahamu mahala matangazo hayo yanakotokea na hivi sasa vikosi vinaelekea huko.Tayari helkopta zimekwisha izingira nyumba hiyo na kuzuia jaribio lolote la magaidi hao kutoroka.Vikosi vitakapowasili vitafanya kila linalowezekana kuweza kumuokoa makamu wa rais na watu wengine walioshikiliwa mateka na huyu gaidi Abu Zalawi ! akasema mkuu wa FBI “Izingireni nyumba hiyo lakini kusifanyike jaribio lolote la kutaka kuivamia nyumba hiyo hadi pale Abu Zalawi atakapomaliza kutoa maelezo yake ! Jambo lingine kwa namna yoyote ile Abu Zalawi hapaswi kuuawa.Tumieni mbinu za kumpata akiwa mzima”akaelekeza Rais William “Wamarekani wana haki ya kuufahamu ukweli wa kile kinachoendelea katika nchi yao.Imekuwa vyema amejitokea huyu Abu Zalawi na kuweka wazi kila kitu.Ni uovu mkubwa umefanyika kupitia kundi hili” akawaza Rais William Washington Video ile ya Mathew haikusambaa tu Marekani bali pia vituo vingine vikubwa vya habari navyo vilirusha video hiyo na sehemu mbali mbali duniani wakafuatilia mubashara kile kilichokuwa kinaendelea kule Marekani Taarifa za kuwepo kwa video hiyo zilimfikia Rais wa Tanzania ambaye kwa haraka akatafuta chaneli iliyokuwa inarusha video ile halafu akampigia Ruby na kumtaka aitafute chaneli ile aitazame.Taarifa zilisambaa kwa haraka . Wakati kijua kikichomoza nchini Tanzania watu walikuta matngazo yale yakiendelea na kwa kuwa taarifa zilisambaa kwa kasi kubwa watu wengi waliweza kuifuatilia japo walikuwa wamepitwa na mambo mengi aliyoyazugumza Mathew. Mathew aliendelea kutoa maelezo yake akaletewa sanduku moja lenye kirusi akalifungua na kutoa chupa nyembamba yenye urefu mithili ya bomba la sindano “Humu ndani kuna kirusi ambacho kilitakiwa kikasambazwe nchini Tanzania.Kirusi hiki kimetengenezwa hapa Marekani kwa lengo la kwenda kuwaangamiza watanzania ili watakapoanza kuumwa na kufa kama ndege wamarekani watume watu wao kwa lengo la kwenda kutoa msaada lakini nyuma ya pazia ajenda yao kubwa ni kuchota madini ya Tanzania” akaendelea kueleza Mathew hadi alipomaliza maelezo yake “Baada ya maelezo yangu marefu nataka mpate ushuhuda mwingine wa maovu ya watu hawa” akasema Mathew na kuweka diski mweko katika kompyuta na kupitia projekta watu wakaanza kumshuhudia Jenerali William akikiri kila kitu alichokifanya nchini Tanzania.Baada ya maelezo ya Jenerali William Mathew akaweka tena video ya Assad Ismail akikiri kuhusika katika kuchochea vurugu na mauaji nchini Tanzania. “Ndugu wamarekani naamini kwa maelezo haya marefu tayari mmefahamu kile kinachoendelea katika nchi yenu.Hii ni siri kubwa ambayo msingeweza kuifahamu na leo nimeamua kuweka wazi kila kitu.Kwa mambo waliyoyafanya hawa jamaa walistahili kumalizwa hapa hapa lakini mimi na wenzangu wote si makatili kama wao hivyo nitaviachia vyombo husika vitafanya kazi yake.Lengo langu lilikuwa ni kuwaeleza ukweli.Sasa ninajisalimisha kwa vyombo vya dola.Ahsanteni na usiku mwema” akasema Mathew na kamera ikazimwa Kwa takribani saa tatu,Marekani ilisimama kufuatia Mathew kuviteka vyombo vyote vya habari kwa video yake ile ya moja kwa moja. “Mathew unataka kufanya nini? Mbona mipango yetu haikuwa kuwaacha hai hawa watu? Tulipanga tuwamalize kwani wamekwisha fanya uovu mkubwa.Adhabu yao ni kuuawa ! akasema Nawal kwa ukali “Hapana Nawal.Tukiwaua hawa tutakuwa sawa na wao.Sisi si wauaji Nawal.Kitu kikubwa ni kwamba wamarekani wameufahamu ukweli” “Mathew ! akasema Nawal “Nawal tumemaliza kazi tujisalimishe kwa vyombo vya dola” akasema Mathew “Mathew tumezungukwa na vyombo vya dola.Hatuwezi kutoka humu ndani salama.Tunajulikana kuwa tumemteka makamu wa Rais ! akasema Nawal “Nawal narudia tena kazi imekwisha ! akasema Mathew kwa ukali Nawal akampa maelekezo Derrick ya kuwataka watu wake wote waweke silaha chini na wasalimu amri. Wakati Mathew akijianda kujisalimisha,Rais William akampigia simu mkuu wa FBI akamueleza kwamba anahitaji kuonana na Mathew Mulumbi usiku ule.Vile vile akaelekeza watu wote wa G20 wakamatwe usiku ule ule akiwamo makamu wa Rais Mark Piller. Mathew akafungua geti na kutoka nje akanyoosha mikono juu akasalimu amri na wenzake pia wakafanya hivyo wakafungwa pingu na kuingizwa katika magari.Mathew akachukuliwa katika gari maalum na kupelekwa ikulu kama rais Wiliam alivyoelekeza “Abu Zalawi karibu sana ikulu.Nimelazimika kutoa maelekezo uletwe hapa baada ya kufuatilia maelezo yako uliyoyatoa usiku huu” akasema Rais William baada ya Mathew kufika ikulu “Kwanza nakupongeza kwa ujasiri wako na kupambana hadi hapa ulipofka.Hili si jambo jepesi najua umepitia mengi magumu” “Ndiyo mheshimiwa Rais haikuwa rahisi” akasema Mathew ukapita ukimya halafu Rais akasema “Sikuwa nikifahamu kuhusu hiki kikundi cha G20 hadi hivi karibuni ambapo Mark Piller aliamua kunieleza kuhusu uwepo wake.Ah ! …” akasema Rais William kwa masikitiko. “Mathew sijui hata ninataka kusema nini lakini kuna jambo moja tu ambalo nataka ulifahamu ni kwamba yote uliyoeleza ni ya kweli kabisa.Ni mambo mengi maovu yamefanywa na kikundi hiki na tayari nimeelekeza wote wakamatwe.Usiku huu wa leo ndio mwisho wa hiki kitu kinachoitwa G20.Ahsante sana Abu Zalawi kwa kuuanika ukweli huu kwa wamarekani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika.Abu Zalawi nimeishiwa maneno ya kusema lakini kuna mambo mawili ya muhimu” akasema Rais William na kuvuta pumzi ndefu “Kwanza ninataka kukuhakikishia kwamba hautafunguliwa shtaka lolote hapa Marekani kwani haujahusika katika jambo lolote.Kila kitu kimefanywa na wamarekani wenyewe na hata bomu lile lililolipua ubalozi wetu limetoka Marekani.Tumelipua ubalozi wetu sisi wenywe.Hii ni aibu kubwa.Abu Zalawi uwe na kosa au huna kosa mimi ninakuachia uende zako.Nitatoa ndege ya kukupelekea sehemu yoyote unayotaka kwenda” “Ahsante sana mheshimiwa Rais lakini huwezi ukaniachia mimi peke yangu.Kuna wengine niliokuwa nao ambao wanashikiliwa hivi sasa” “Usijali wote wataachiwa huru” akasema Rais William “Jambo la pili ambalo wewe ni mtu wa kwanza kukwambia ni kwamba kesho nitalihutubia taifa na nitatangaza kuachia ngazi.Nitajiuzulu nafasi yangu kwani na mimi nimeshiriki katika uovu huu mkubwa uliofanyika.Kila mtu anastahili adhabu kwa nafasi yake.Mara tu baada ya kujiuzulu nafasi yangu nitajikabidhi kwa vyombo vya husika kwa ajili ya hatua stahiki kuanza kuchukuliwa.Ninaomba uondoke Marekani wakati bado nikiwa rais kwani baada ya mimi kuondoka na kuja utawala mpya unaweza ukapata ugumu wa kuondoka hapa kwani umegusa maslahi ya watu wengi.Suala hili litabeba watu wengi sana” akasema Rais William “Mwisho kabisa ninakushauri endelea na moyo huo huo wa kizalendo kwa nchi yako.Umeonyesha mfano kwa vijana wa nchi za kiafrika kwa kupigania nchi yako.Mungu akipenda yawezekana siku moja tukaonana tena” akasema Rais Wiliam. Mathew alilengwa na machozi ya furaha kwa maneno yale ya Rais William akamshukuru na kumpatia zile rekodi zote alizokuwa nazo halafu Rais akapiga simu akaelekeza wale watu waliokamatwa pamoja na Mathew waachiwe huru.Mathew akapewa gari maalum na walinzi akaenda kukutana na akina Nawal wakakumbatiana kwa furaha kubwa wakapongezana. “Nawal hatuna muda mrefu wa kuwepo hapa.Tumekwisha imaliza kazi yetu na Rais ametoa muda wa sisi kuondoka haraka iwezekanavyo.Ametoa ndege kwa ajili ya kutusafirisha kwenda sehemu yoyote tuitakayo” akasema Mathew “Mathew hatuhitaji ndege kwani ndege niliyokuja nayo bado iko hapa hapa Marekani tutaitumia hiyo kuondoka nayo” akasema Nawal wakaingia katika magari na kuelekea katika uwanja wa ndege ilikokuwa ndege ya Habiba.Waliagana na Derrick wakamshukuru kwa msaada wake mkubwa halafu wakaingia ndegeni na baada ya muda ndege ikapaa. Baada ya ndege kukaa sawa,Mathew na Nawal wakapongezana “Mathew tumefanya jambo kubwa tunastahili furaha lakini kuna jambo lilitokea ambalo ni la huzuni kubwa” “Jambo gani? “Mama Habiba amefariki dunia” akasema Nawal.Ilimchukua Mathew zaidi ya dakika tano kutamka neno “Nawal tafadhali naomba unieleze ukweli” “Si utani Mathew.Mama Habiba amefariki dunia” akasema Nawal na kumueleza Mathew kila kitu kilichotokea.Mathew akadondosha machozi “Mama Habiba alistahili kushuhudia namna tulivyolimaliza kundi la G20.Naamini aliogopa fedheha baada ya ukweli kujulikana ndiyo maana alirekodi maelezo yale mapema akijua ana mpango wa kujiua” akasema Mathew





    Haijulikani ni muda gani watu walipeana taarifa kwani kulipopambazuka tu watu walianza kumiminika katika ikulu ya Marekani na ilipofika saa mbili za asubuhi maelfu ya watu tayari walikwisha kusanyika nje ya ikulu hiyo na wengi wakiwa na mabango ya kulaani kile ambacho nchi yao imekuwa ikikifanya kupitia kikundi cha G20.Waliwataka viongozi wao wakuu wawajibike Ndani ya ikulu kulikuwa na heka heka kubwa.Toka usiku baada ya video ile ya Mathew Mulumbi kulikuwa na vikao mfululizo. Saa tatu za asubuhi Rais wa Marekani William Washington akajitokeza mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wamekusanyika katika bustani ya ikulu.Yalikuwa ni matangazo ya moja kwa moja kutoka ikulu na watu wengi walisubiri kusikia kauli ya Rais kufuatia kile kilichokuwa kimesemwa na Mathew Mulumbi. “Habari za asubuhi ndugu wamarekani” akaanza hotuba yake “Toka usiku wa jana Marekani haijalala kufuatia maelezo ya kina aliyoyatoa Abu Zalawi ambaye tayari wengi tulikuwa tunamfahamu kama gaidi aliyelipua ubalozi wetu nchini Tanzania Toka alipotoa maelezo yake,kumekuwa na mjadala mkubwa sana watu wakijaribu kuchambua kile kilichoelezwa na Abu Zalawi na wengine wakidiriki kutaka kukanusha au kupindisha ukweli wa kile alichokisema.Nimesimama mbele yenu asubuhi hii kuweka sawa jambo hili” Rais William akanyamaza kidogo akawatazama waandishi wa habari halafu akasema “Yote aliyoeleza Abu Zalawi jana ni ukweli mtupu.Narudia tena kwamba yote aliyoeleza Abu Zalawi jana usiku ni kweli hakuna hata neno moja la uongo alilolitamka hivyo kusifanyike juhudi zozote za kutaka kupindisha ukweli ili kuwasaidia watu waliohusika katika uhalifu huu mkubwa. Ni kweli ndani ya CIA kumekuwa na kitengo cha siri chenye jina G20 ambacho kazi yake kubwa ni kujenga mashirikiano na makundi mbalimbali ya kigaidi.Kikundi hiki kinaendeshwa kwa siri kubwa na wanaofahamu uwepo wake ni watu ishirini tu ndiyo maana wakajiita G20.Hii imekuwa ni siri kubwa na hata rais hatakiwi kufahamu uwepo wa kikundi hiki. Sina hakika kama marais wa Marekani waliopita wanafahamu kitu kama hiki lakini mimi nilipata bahati hivi karibuni ya kuwafahamu uwepo wa kikundi hicho ila sikuweza kufanya chochote kwa kuhofia kuuawa.Nilikuwa mwoga” akanyamaza tena kidogo Nilifahamu uwepo wa kundi hili wakati wakijiandaa na mpango wa kuchochea machafuko nchini Tanzania na katika eneo zima la Afrika Mashariki.Nilifahamishwa mpango huo na mimi nikaushiriki” akanyamaza akameza mate na kwa mbali alilengwa na machozi “Watu wengi wameuawa Afrika Mashariki hasa nchini Uganda na Tanzania kufuatia machafuko ya kidini yaliyotokea ambayo na mimi pia nimeyashiriki kwa lengo la kupata mafuta kutoka nchini Uganda.Nyote mlishuhudia damu nyingi iliyomwagika nchini Tanzania na Uganda lakini wakati mauaji haya yakifanyika na damu ikimwagika sisi tuliendelea kufurahia neema ya mafuta .Meli zetu zilikuwa zimepanga foleni katika bandari ya Tanga nchini Tanzania zikipakia tani na tani za mafuta.Huu ni ukatili mkubwa sana. Kama haitoshi bado kulifanyika mpango wa kwenda kusambaza kirusi nchini Tanzania na mimi pia nilishiriki katika mpango huo lengo kuu likiwa ni kuendelea kuchota rasilimali mbali mbali zilizoko nchini humo na hasa madini.Sitaki kurudia yale aliyoyasema Abu Zalawi lakini nataka nifafanue na nyote msikie kutoka katika kinywa changu kwamba yote yale yana ukweli. Pamoja na hayo yote bado tulimtuma Abu Zalawi nchini Iran na katika mpango huo tukalipua ubalozi wetu jijini Dar es salaam.Abu Zalawi hahusiki chochote katika shambulio lile yeye alitumika kuingiza gari lenye bomu katika ubalozi wetu.Gari lililobeba bomu ni gari la kwetu na hata bomu lililolipua ubalozi wetu ni letu hivyo tumeua watu wetu sisi wenyewe. Ndugu zangu wamarekani kwa hayo niliyoyaeleza na mengine mengi ambayo sijayaeleza ninasimama mbele yenu kukiri kwamba sisi viongozi wenu tumewaangusha.Tumetenda makosa makubwa sana.Jana usiku nilielekeza G20 wote wakiongozwa na makamu wa Rais Mark Piller wakamatwe na mashitaka dhidi yao yaanze mara moja kwani ushahidi wa kutosha wa matendo yao upo. Pamoja na hatua hiyo ya kuwakamata viongozi wote wa G20 lakini zipo pia hatua nyingine ambazo nimezichukua katika suala hili.Kwanza kuna viongozi na watu kadhaa kutoka Afrika Mashariki ambao walishirikiana na G20 katika kuchochea vurugu ambao wamekuja kupatiwa hifadhi nchini Marekani.Mmoja wao ni aliyewahi kuwa Rais wa Uganda Jenerali Akiki Rwamirama aliyepinduliwa na kukimbilia hapa Marekani.Huyu amekuwa ni mmoja wa watu walioasisi kwa kiasi kikubwa mpango huu wa kuchochea vurugu na kupata mafuta.Mbinu zote za machafuko yale yeye ndiye aliyebuni.Wapo vile vile viongozi wengine wa dini na siasa kutoka nchi za Tanzania na Uganda walioshiriki katika machafuko yale kisha wakakimbilia hapa Marekani na kupewa hifadhi wao na familia zao baada ya machafuko kuwa makubwa.Hawa wote watakamatwa na kurejeshwa makwao kujibu mashitaka watakayofunguliwa na nchi zao kwa kushiriki kuchochea vurugu zile.Ni aibu kwa viongozi kutoka bara la Afrika kuwa tayari kuwasaliti watu wao,kusaliti nchi zao na kuungana na mataifa makubwa katika kuchota rasilimali na wao kufaidika kidogo.Nakiri kumekuwa na wizi mkubwa wa rasilimali mbali mbali katika bara la Afrika unaofanywa na mataifa makubwa wakishirikiana na waafrika wenyewe hasa viongozi na hivyo kulifanya bara la Afrika kuendelea kuwa masikini.Nawasihi waafrika wawe na uzalendo na kuzipenda nchi zao na kuzipigania kama alivyofanya Abu Zalawi Jambo la pili,baada ya kukubali kwamba tumefanya uhalifu itatulazimu kulipa fidia kwa nchi zilizoathiriwa.Mafuta yote tuliyochukua kutoka Uganda tutayalipa pamoja tathmini ya fidia zitakazowasilishwa kwetu kutoka kwa nchi husika. Mwisho kabisa kwa kuwa na mimi ni sehemu ya uhalifu huu ninapaswa kuwajibika hivyo ninatangaza kwamba kuanzia sasa nimejiuzulu nafasi yangu ya urais ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.Siwezi kubaki bila kuwajibika hasa kwa haya madhambi makubwa ambayo tumeyafanya. Mungu ibariki Marekani. Rais William Washington akamaliza hotuba yake na kurejea ndani huku nje ya ikulu watu wakiendelea kuongezeka. DAR ES SALAAM – TANZANIA Nchini Tanzania bado gumzo kubwa lilikuwa ni maelezo ya Mathew Mulumbi na hotuba aliyoitoa Rais William Washington akikubaliana na kile alichokisema Mathew.Kuanzia asubuhi ya siku ile kulikuwa na kamata kamata kubwa.Majina yote ya watu ambao walishiriki katika kuchochea vurugu za kidini zilizopelekea mamia ya watu kupoteza maisha ambayo yalitajwa na Assad Ismail yalikabidhiwa kwa jeshi la polisi na msako mkubwa ukafanyika kuwawakamata wote. Hotuba ya Rais William akiwataja baadhi ya watu kutoka Afrika Mashariki hasa Jenerali Akiki Rwamirama aliyewahi kuwa Rais wa Uganda iliwastua watu wengi wa Afrika mashariki.Hawakutegemea kabisa kama Jenerali Akiki angeweza kuhusika katika machafuko yale Saa mbili za usiku kwa saa za Afrika Mashariki Rais wa Tanzania Dr Fabian kelelo akalihutubia taifa.Katika hotuba yake akawatangazia watanzania kwamba hakuna tena vurugu zitakazotokea kwani wachochezi wote wa vurugu zile wamekamatwa na wengine kuuawa.Aliwasisitiza watanzania kuendelea kuishi kwa upendo kama walivyokuwa wakiishi kabla ya kuchonganishwa ili wachukiane.Aliwataka kwa namna yoyote ile wasikubali kuchonganishwa tena na mtu yeyote na kupelekea kupigana wao kwa wao.Ilikuwa ni hotuba ndefu iliyobeba mambo mengi na kubwa likiwa ni amani upendo na kuvumiliana hata pale kunapokuwa na tofauti za kiimani.Mwisho kabisa aliwaahidi watanzania kuzilinda rasilimali za nchi kwa gharama zozote zile na kuwataka watanzania wote kila mmoja awe mlinzi wa rasili mali hizo kwa faida yao na vizazi vijavyo.Kabla hajamaliza hotuba yake Dr Fabian akawamwagia sifa tele Mathew na wenzake ambao walipambana usiku na mchana kuhakikisha kwamba wanaufahamu ukweli. Baada ya kumaliza hotuba yake,simu zikaanza kuingia mfululizo katika simu ya rais lakini hakutaka kupokea simu hata moja kwa wakati ule lakini alipoiona simu ya Ruby akaipokea. “Hallo Ruby” akasema DrFabian “Mheshimiwa Rais nimekupigia kukupongeza kwa hotuba nzuri uliyoitoa” akasema Ruby “Ahante sana Ruby.Utanisamehe sikuweza kuwataja kwa majina lakini nimewashukuru nyote kwa ujumla wenu kwa kazi kubwa mliyoifanya” “Usijali mheshimiwa Rais” “Vipi kuhusu Mathew Mulumbi umewasiliana naye? “Ndiyo nimekuwa nawasiliana naye mara kwa mara leo yuko Riyadh Saudi Arabia.Habiba Jawad amefariki dunia” “Habiba amefariki dunia? “Ndiyo amefarki dunia amejiua kwa kujipiga risasi” “Lini atarejea nyumbani? Akauliza DrFabian “Bado hajaweka wazi lini atarejea nyumbani lakini akiwa tayari atatujulisha” akajibu Ruby “Sawa Ruby.Lazima tumpokee kwa shangwe shujaa wetu kwani amefanya mambo makubwa sana” akasema Dr Fabian na ukimya ukapita “Ruby kama ukipata nafasi usiku wa leo tunaweza kuonana? Akauliza Dr Fabian.Ruby akafikiri kidogo na kusema “Hakuna tatizo nitakuja” akajibu Ruby ambaye alijawa na furaha kubwa siku hii “Kwa sasa baada ya mambo yote kumalizika ni wakati wa kumueleza Ruby ukweli.Ninampenda na ninataka awe mke wangu.Ana kila sifa ya kuwa mke.Yawezekana nikiwa naye ninaweza kufikiria hata kuwania kipindi cha pili cha urais” akawaza Dr Fabian huku akitabasamu RIYADH – SAUDI ARABIA Saa tatu za usiku Mathew na Nawal waliwasili Riyadh wakitokea nchini Marekani.Sayid Omar alikuwepo uwanjani kuwapokea ksha wakaelekea nyumbani.Watu walikuwa wengi na majonzi yalitawala .Baada ya Mathew na Nawal kuwasili nyumbani kwa Habiba vilio vikaanza upya.Nawal alilia mno.Mathew akaenda kuungana na watu waliokuja kuwafariji na wengi wakimpongeza kwa kile alichokifanya.Tayari alikuwa ni mtu maarufu kufuatia kile alichokifanya nchini Marekani ambacho kilitazamwa na karibu dunia nzima Ilipofika saa saba za usiku Mathew akaenda kupumzika katika nyumba yake kujiandaa na siku ya kesho ambapo Habiba angezikwa. “Imekuwa ni kama filamu ambayo imefika mwisho.Nimepitia mengi sana katika sakata hili toka lilipoanza.Nafikiri nahitaji kuyatafakari tena maisha yangu.Ngoja kwanza tumzike mama Habiba halafu nitajua nini kitafuata” akawaza Mathew na kulala DAR ES SALAAM – TANZANIA Ruby aliwasili ikulu saa nne za usiku kama alivyoombwa na Rais Dr Fabian ambaye usiku huu alichangamka sana. “Ruby karibu” akasema Dr Fabian na kumkaribisha katika sebule yake “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akajibu Ruby huku akitabasamu “Ruby kabla ya yote nataka kwanza tufungue shampeni kusherehekea ushindi mkubwa tulioupata” akasema Dr Fabian na kufungua shampeni wakagonganisha glasi Baada ya maongezi kidogo Dr Fabian akasema “Ruby hii imekuwa ni vita ngumu lakini tumeipigana tumeimaliza ahsante kwako na wenzako.Kwa sasa baada ya vita hii kumalizika maisha lazima yaendelee.Nimekuita hapa usiku huu sitaki tuzungumze kuhusu kazi kwani kila tunapokutana imekuwa ni mazungumzo ya kazi.Nataka usiku huu tuzungumze kuhusu maisha.Tusizame katika kazi na kusahau kwamba kuna muda na sisi tunahitaji kuwa na maisha ya kawaida kama wengine” akasema Dr Fabian “Ni kweli mheshimiwa Rais” akajibu Ruby “Nini mipango yako hasa baada ya jambo hili kubwa kumalizika? “Mheshimiwa Rais hiki kilichotokea kimenifundisha mambo mengi .Nimeingia katika kazi hii ya kuongoza idara nyeti kama SNSA bila kuwa na ujuzi mkubwa wa masuala ya ujasusi.Mimi ni mtaalamu wa kompyuta na kinachonisaidia ni uzoefu mdogo nilionao baada ya kuwa karibu na Mathew Mulumbi na nikashiriki naye katika misheni mbali mbali.Kwa hiyo mheshimiwa Rais nimeamua kwenda kusomea masuala ya ujasusi ili niive kabisa” akasema Ruby “Ruby una uhakika unataka kwenda kusomea masuala ya ujasusi? “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ninataka kusomea ujasusi” akajibu Ruby “Ruby naomba niwe muwazi kwako.Binafsi sitaki uendelee na kazi hii ya ujasusi.Nimeshuhudia ni kazi iliyojaa hatari sana na kwa mtoto mzuri kama wewe haikufai.Ninataka kukutafutia nafasi nzuri zaidi kuliko hiyo” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ulinitoa Uingereza nije niifanye kazi hii hivyo nataka nikasome ili niifanye kwa ufanisi” “Hapana Ruby sitaki uende ukasomee masuala haya” akasema Dr Fabian “Kwa nini mheshimiwa rais” “Ruby sisi ni watu wazima hivyo sitaki kuzunguka zunguka kama wafanyavyo vijana.Naomba niwe mkweli kwako.Ninakupenda sana Ruby na lengo langu ni mimi nawe tuwe na mahusiano na ikiwezekana tuishi pamoja” akasema Dr Fabian na Ruby hakustuka akatabasamu “Mheshimiwa Rais ninashukuru kwa kunieleza ukweli.Hili ni jambo ambalo siwezi kulitolea majibu ya haraka.Naomba unipe muda mheshimiwa Rais nitafakari halafu nitakujibu” akasema Ruby “Ruby naomba ujipe muda kisha utanijibu na nitakubaliana na jibu lolote utakalonipatia lakini narudia tena Ruby kwamba ninakupenda na ninakuhitaji mno katika maisha yangu.Baada ya kumpoteza Millen ni wewe ambaye Mungu amekuleta karibu yangu” akasema Dr Fabian “Nimekwisha kuelewa mheshimiwa Rais usihofu” akasema Ruby Walizungumza mambo mengi kuhusiana na maisha yao kisha wakaagana Ruby akaondoka RIYADH – SAUDI ARABIA Mazishi ya Habiba Jawad yalilifanya jiji la Riyadh lizizime.Umati mkubwa mno ulijitokeza kumsindikiza Habiba Jawad katika safari yake ya mwisho. Saa nne za usiku baada ya watu kuondoka Mathew na Nawal waliingia ndani ya chumba cha Habiba Jawad,Nawal akafungua kasiki la Habiba ambako walikuta nyaraka ambazo Habiba aliziandaa zinazoonyesha kwamba utajiri wake wote amewaachia Mathew na Nawal. “Mathew tumeachiwa utajiri mkubwa sana na Habiba.Nini mawazo yako? Akauliza Nawal “Nawal kitu kimoja tu ninachoweza kusema ni kwamba utajiri huu wote ninaukabidhi kwako” “Hapana Mathew.Mama Habiba ametukabidhi sote utajiri huu wote” “Nakubali lakini na mimi ninakukabidhi wewe utajiri huu” “Kwa nini Mathew? “Ninahitaji kupotea.Nahitaji kwenda mahala mbali kabisa ambako nitapata muda wa kutafakari kuhusu maisha yangu na kusahau yale yote niliyoyapitia.Nimepitia mambo mengi sana Nawal” “Vipi kuhusu Ruby? “Ninampenda Ruby lakini sina hakika kama mimi ni mwanaume sahihi kwake.Maisha yangu yamekuwa namna hii na siwezi kumpatia furaha ya maisha anayoihitaji.Yawezekana haya ndiyo maisha niliyopangiwa na Mungu.Utazungumza naye na kumwambia kwamba ninampenda lakini aendelee na maisha yake na asinisubiri” akasema Mathew wakaendelea na mazungumzo yao. BAADA YA MWAKA MMOJA Watuhumiwa wote wa vurugu zilizopelekea umwagikaji mkubwa wa damu Afrika Mashariki walikwisha hukumiwa kuanzia miaka thelathini hadi kifungo cha maisha gerezani.Amani ilitamalaki tena watu wakiendelea kuishi kama ndugu. Baada ya kujiuzulu Rais William Washington,Marekani ilipata Rais mpya ambaye alifanya mazungumzo na Rais wa Iran na baada ya muda mrefu muafaka kati ya mataifa haya mawili ukapatikana na nchi ya Iran ikaondolewa vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa. Baada ya kukosa ufadhili wa fedha,makundi mbali mbali ya kigaidi yalidhoofika na mengine kufa kabisa. Idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi SNSA ilipata mkurugenzi mpya baada ya Ruby na Gosu Gosu kuacha kazi.Gosu Gosu aliendelea kusimamia biashara za Mathew Tukio kubwa kabisa lililotokea baada ya mwaka mmoja ni ndoa ya Dr Fabian Kelelo na Ruby.Ilikuwa ni sherehe kubwa iliyolitikisa jiji la Dar es salaam.Ruby aliamua kufunga ndoa na Dr Fabian baada ya kuhakikishiwa na Nawal kwamba Mathew amempa ruhusu ya kuendelea na maisha yake. Watu wengi walijiuliza mahala alipo shujaa Mathew Mulumbi na wengi wakijiuliza kwa nini hakurejea nyumbani ili wampongeze baada ya jambo kubwa alilolifanya miezi kumi na mbili iliyopita.Mathew alifanya siri kubwa mahali alipo.Hakutaka kujulikana alikwenda wapi kwani alihitaji mapumziko marefu na kujitafakari kuhusu maisha yake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     TAMATI

0 comments:

Post a Comment

Blog