Simulizi : Siri: Jasusi/Gaidi
Sehemu Ya Nne (4)
Helkopta iliyowabeba akina Nawal ilitua katika kambi ya jeshi ya vikosi vya Marekani iliyopo kandoni mwa bahari.Kulikuwa na kambi mbili za vikosi vya Marekani jijini Dar es salaam,kambi moja kubwa ikiwa katika uwanja wa Uhuru ambako ndiko vifaa vyote vilikuwa vinahifadhiwa na kambi nyingine ilikuwa ufukweni mwa bahari ya Hindi. Jenerali William alianza kushuka katika helkopta halafu akafuatiwa na Nawal wakaongozana kuelekea katika kontena lenye rangi nyeupe ambalo lilikuwa linatumiwa kama ofisi ya Jenerali William.Ndani ya kontena lile kulikuwa na ubaridi wa kutosha kutokana na kiyoyozi. “Chloe karibu sana.Hii ni ofisi yangu” akasema Jenerali William na kumkaribisha Nawal katika chumba cha kupumzikia. “Pole sana Chloe kwa masahibu yote yaliyokukuta” “Ahsante sana Jeneral nimekwisha poa” akajibu Nawal na mara wakaingia watu wawili na Jenerali William akamtambulisha Nawal kwao halafu akamuomba aendelee kupumzika kwani alikuwa na mazungumzo na watu wale walioingia mle ofisini.Jenerali William alitoka na wale wanajeshi wawili Nawal naye akasimama na kutoka ndani ya kile chumba akachungulia nje akamuona Jenerali William na wale jamaa wakielekea sehemu nyingine.Haraka haraka akarejea katika kile chumba cha mapumziko na kuchukua simu aliyopewa SNSA akampigia Ruby “Nawal ! akasema Ruby baada ya kupokea simu “Ruby tayari nimekwisha ingia katika kambi yao iliyoko ufukweni mwa bahari.Kwa sasa niko katika ofisi ya Jenerali Wiliam Marshall” akasema Nawal “Safi sana Nawal.Una nafasi ya kufanya chochote kwa muda huu? “Jeneral William ametoka na sifahamu atachukua muda gani kurejea,ninataka kutega kamera” “Sawa Nawal.Hakikisha unatega kamera na kifaa cha kunasa sauti katika ofisi hiyo ili tuweze kunasa mazungumzo na kufuatilia kila kinachoendelea hapo ofisini” akasema Ruby “Ninataka nijitahidi nitumie nafasi hii ndogo niweze kutekeleza hilo” akasema Nawal na kukata simu akafungua begi lake dogo la mgongoni alilokuwa nalo akatoa vifaa fulani ambavyo ni kamera ya siri na kifaa kingine cha kunasa maongezi.Akaenda tena kuchungulia katika dirisha kama kuna mtu anaelekea upande ule lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa anaelekea pande zile.Haraka haraka akaelekea katika mlango uliokuwa umefungwa akausogelea akiwa amevaa glovu mkononi akakiminya kitasa mlango ukafunguka akaingia ndani ya ofisi.Mezani kulikuwa na kibao Gen.William Marshall. “Hii ndiyo ofisi yake” akawaza Nawal kisha akatega kifaa cha kunasa mazungumzo chini ya meza,halafu akatega na kamera ya siri katika kabati la vitabu.Wakati akiendelea na kutega kamera ile ya siri mara akasikia vishindo vya mtu haraka haraka akaenda kujificha chini ya meza.Mlango wa ofisi ya Jenerali Willium ukagongwa Nawal mwili ukamtetemeka.Mtu aliyegonga mlango akakiminya kitasa na kuufungua mlango akachungulia ndani halafu akaufunga mlango ule akaondoka zake.Haraka haraka Nawal akamalizia kutega kamera ile ya siri halafu akatoka kwa tahadhari kubwa akarejea mahala ambako aliachwa apumzike.Akachukua simu na kumpigia simu Ruby akamjulisha kwamba tayari amekwisha tega kamera na kile kifaa cha kunasa maongezi.Tayari Ruby alikwisha anza kupata picha za kamera kutoka katika ile kamera aliyoitega Nawal. Dakika tano toka Nawal atoke katika ofisi ya Jenerali William akasikia vishindo vya hatua za mtu na akajitokeza Jenerali William “Samahani Chloe kwa kukuacha peke yako” akasema Jenerali William na kuketi sofani “Bila samahani Jenerali William” akasema Nawal “Mimi ndiye mkuu wa vikosi vyote vya Marekani vilivyopo hapa Tanzania hivyo ninakuwa na mambo mengi ya kushughulikia” akasema Jenerali William “Kwa kuwa hapa kambini ni sehemu yenye shughuli nyingi,utapelekwa katika nyumba ninakoishi mimi na utaishi nasi hapo hadi pale mambo yatakapotulia.Ubalozi wetu hapa Dar es salaam umelipuliwa hivyo sina sehemu nyingine ya kukupeleka zaidi ya mahala ninapoishi.Usihofu ni sehemu salama sana” akasema Jenerali William “Ninashukuru sana Jenerali William kwa msaada huu mkubwa” akasema Nawal na Jeneral William akasimama “Pale kambini utapatiwa kila utakachokihitaji.Mimi nitakuja jioni baada ya kumaliza shughuli zangu na tutapata wasaa wa kuzungumza zaidi” akasema Jenerali William akamuaga Nawal akaondoka. Dakika chache baada ya Jenerali William kuondoka akaingia mwanajeshi mmoja akajitamblisha kwa Nawal kwamba ametumwa na Jenerali William kumpeleka mahala anakoishi.Nawal akavaa begi lake la mgongoni kisha akaongozana na Yule mwanajeshi hadi katika gari la jeshi akaingia wakaondoka kuelekea anakoishi Jenerali William
Nawal alifikishwa katika makazi ya maofisa wa vikosi vya Marekani waliokuwa wakiishi katika mojawapo ya nyumba za wageni muhimu wa serikali.Alipokewa na wahudumu ambao ni wanajeshi pia na tayari taarifa zake walikwisha zipata hivyo basi wakamuhudumia kwa chakula halafu akaenda kupumzika.Ilikuwa ni nyumba ya kifahari sana.Nawal akasimama dirishani akatazama nje kulikuwa na ulinzi mkali karibu kila kona ya jumba lile kulikuwa na mlinzi mwenye silaha,juu ya paa vile vile kulikuwa na wanajeshi wakilinda na katika geti la kuingilia ndani ya nyumba ile kulikuwa na ulinzi mkali na kila gari lililoingia lilikaguliwa kama limebeba mlipuko “Jumba la kifahari sana hili na lenye ulinzi mkali mno hata hivyo ulinzi huu hauwezi kunizuia kutekeleza jukumu langu.Lazima tukimbizane na muda na kuhakikisha tunafahamu mahala kilipo kirusi.Mpaka mapambazuko ya kesho lazima tayari tuwe na kirusi mkononi” akawaza Nawal halafu akachukua simu na kumpigia Ruby akamjulisha kuwa tayari amefika katika makazi ya maofisa wa jeshi la Marekani. “Tumekuwa tunafuatilia ile kamera uliyoifunga katika ofisi ya Jenerali William lakini toka wakati ule hajarejea katika ofisi yake.Tunaendelea kumfuatilia na kama kuna kitu chochote tutakipata nitakujulisha mara moja.Hakikisha unachunguza kila kinachoendelea katika nyumba hiyo na kama ikiwezekana tega kamera na kifaa cha kunasa maongezi ili tujue William anawasiliana na nani na wanaongea nini.Nina uhakika mkubwa lazima anafahamu kinachoendelea kuhusiana na kirusi alichokileta Sattar” “Sawa nitajitahidi kufanya hivyo Ruby” akasema Nawal “Kumbuka kuwa makini sana kwani wakikugundua hao jamaa lazima watakuua” Ruby akasisitiza “Ninalifahamu hilo Ruby na mpaka hapa bado hakuna tatizo lolote” akasema Nawal “Kwa kutumia simu yako tayari tumefahamu mahala ulipo hivyo tunarusha drone yetu mahala hapo ili kuichunguza zaidi na kujua kila kinachoendelea kwa nje” akasema Ruby na kuagana na Nawal. TEHRAN - IRAN Zimekwisha pita saa tisa toka Mathew Mulumbi na wenzake sita walipoiteka ndege iliyokuwa inawapeleka nchini Marekani.Ndani ya ndege ilikuwa ni furaha tupu.Raia wale wa Iran waliimba na kucheza kwa furaha wakifurahia kurejea nyumbani baada ya miaka kadhaa ya kuishi katika mateso makubwa.Ilikuwa ni kama muujiza kwao pale ndege ilipobadili uelekeo na kuelekea nchini Iran.Hawakutegemea kama jambo hili lingewezekana siku moja waweze kurejea nyumbani. Wakati ndege ikiendelea kupasua anga kuelekea nchini Iran,Mathew akachukua zamu ya kuwalinda mateka wao waliokuwa wamefungwa pingu zile ambazo Mathew na wenzake walikuwa wamefungwa. “Mnatupeleka wapi?akauliza mmoja wa mateka ambaye ni rubani wa ndege “Mnakwenda nchini Iran ambako mtakabidhiwa kwa mamlaka husika na yawezekana hamtaweza kuziona tena familia zenu” akasema Mathew huku akiichezea bastora yake.Mmoja wa wale marubani akainamisha kichwa na kumwaga machozi “Tafadhali msitupeleke Iran watatuua.Uhasama wa Iran na Marekani ni mkubwa na watu wale ni makatili wanaweza kubwa watatukata vichwa ! akasema mmoja wa walinzi wale “Taifa lenu ndiyo taifa katili kabisa duniani kuliko yote.Hawa raia wa Iran ambao bado hawaamini kama wanarejea tena nyumbani kwao walikamatwa na kufungwa bila kuwa na hatia.Wameteswa sana na kilichokuwa kinafuata ni kupelekwa Marekani kuuawa.Huu ni ukatili uliopitiliza.Machafuko yanayoendelea eneo la Afrika Mashariki hivi sasa ni nchi yenu ndiyo imeyaratibu kwa lengo la kujipatia mafuta kutoka Uganda.Wakati damu ya watu ikimwagika kila uchao,tani na tani za mafuta zinamiminika Marekani.Huu ni zaidi ya ukatili.Marekani na wamarekani wanastahili adhabu kali ! akasema Mathew kwa ukali “Wewe ni gaidi na umelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam unadhani kwa hiki ulichokifanya utakuwa salama? Akauliza mmoja wa walinzi akimtazama Mathew kwa hasira “Nakuhakikishia hautakuwa salama.Marekani haijawahi kushindwa na gaidi yeyote.Utasakwa kwa maisha yako yote hadi tuhakikishe umekamatwa na kupata adhabu unayostahili kwa unyama ulioufanya ! akasema yulemlinzi lakini Mathew hakumjibu kitu Ndege ilikaribia kuingia katika anga la Iran na Abdu Razaq aliyekuwa anaiongoza ndege ile akawaita wenzake na kuwajulisha kuwa wanakaribia kuingia katika anga la Iran.Abdu Razaq akabonyeza kifaa ambacho walikizima pale walipobadili uelekeo wa ndege ambacho kingewawezesha kuwasiliana na waongoza ndege na vile vile kuonekana katika rada za Iran. Ndege iliingia katika anga la Iran na kuanza kuonekana katika rada za Iran. Abdu Razaq akajitambulisha kuwa wao ni raia wa Iran lakini walikuwa na ndege ya Marekani.Halikuwa jambo jepesi kuwaamini na ndani ya muda mfupi wakajikuta wamezingirwa na ndege nane na kivita za Iran zikiwasindikiza kuelekea katika uwanja wa ndege wa kijeshi jijini Tehran. Kwa kufuata maelekezo waliyopewa na waongoza ndege Abdu Razaq aliiongoza ndege hadi katika uwanja wa kijeshi uliopo nje kidogo ya jiji la Tehran huku ikiendelea kusindikizwa na ndege za kivita za Iran.Mara tu ndege ile iliposimama ilizingirwa na wanajeshi wenye silaha.Abdu Razaq na wenzake wakakumbatiana kwa furaha baada ya ndege kusimama.Walikuwa nyumbani.Wote kwa pamoja wakamshukuru Mathew kwa ujasiri wake uliosababisha wao wakawa huru tena. Mlango wa ndege ukafunguliwa na Yasser Wazir akawa ni mtu wa kwanza kushuka ndegeni.Akashuka ngazi haraka haraka na kukanyaga ardhi akainama akasujudu.Wenzake nao wakashuka na kufanya kama alivyofanya Yasser.Uwanjani pale alikuwepo Meja Jenerali Farhad Karvan mkuu wa majeshi wa Iran ambaye alifika kuwapokea raia wale wa Iran ambao waliaminika tayari wamekwisha uawa.Ulikuwa ni mshangao kwa wote waliokuwepo pale uwanjani baada ya kuwaona tena wenzao wakishuka ndegeni wote wakiwa hai japo walikuwa wamedhoofika sana.Meja Jenerali Farhad akawakaribisha tena nyumbani Wakati salamu zikiendelea katika mlango wa ndege akajitokeza Mathew Mulumbi na kuwafanya watu wote wageuke kumtazama. “Na Yule ni nani?akauliza Meja Jenerali Farhad Karvan “Yule ni mtu muhimu sana.Anaitwa Abu Zalawi ndiye ametuwezesha tukanyage tena katika ardhi ya nyumbani” akasema Yasser Wazir “Huyu mbona kama……” akasema Meja Jenerali Farhad baada ya kumtazama Mathew kwa makini lakini Yasser akamkatisha “Anaitwa Abu Zalawi ndiye aliyelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam.Huyu ndiye aliyepambana na kuhakikisha tunafanikiwa kuidhibiti ndege na kuibadili uelekeo kuja nyumbani.Naweza kusema kwamba bila yeye tusingefanikiwa kukanyaga tena ardhi ya nyumbani tulikuwa tunaelekea kuuawa.Ndani ya ndege kuna walinzi tumewashikilia mateka ambao wote ni raia wa Marekani ” akasema Yasser. Meja Jenerali Farhad akatoa maelekezo Mathew Mulumbi akachukuliwa akaingizwa katika gari na kuondolewa haraka pale uwanjani.Farhad akiwa ameongozana na Yasser wakaingia ndegeni na kuwashuhudia wale mateka waliokuwa wamefungwa pingu.Akatoa maelekezo na mateka wale wakafunguliwa pingu kisha wakashushwa ndegeni na kuingizwa katika gari la jeshi na kupelekewa mahala alikoelekeza.Yasser na wenzake nao pia wakaingizwa katika gari maalum na kupelekwa kwanza katika hospitali ya jeshi kwa ajili ya kuchuguzwa afya zao kabla ya kuruhusiwa kukutana na familia zao.Hakuna aliyejua mahala alikopelekwa Mathew Mulumbi japo Meja Jenerali Farhad aliwahakikishia kwamba amepelekwa sehemu salama WASHINGTON DC – MAREKANI Kitendo cha Abdu Razaq kuwasha tena kifaa kilichowawezesha kuwasiliana na waongoza ndege wa Iran na vile vile kuiwezesha ndege kuanza kuonekana katika rada kiliwawezesha mamlaka za Marekani waliokuwa wakiitafuta ndege hiyo kuiona na kufuatilia uelekeo wake na wakagundua ilikuwa inaelekea nchini Iran Taarifa hiyo ya ndege iliyopotea kuonekana ikielekea nchini Iran iliwafikia G20 wakiwa katika kikao cha kujadili mapendekezo ya mkuu wa CIA Jason Washington ya kutaka Abu Zalawi auawe baada ya kujulikana kuwa si gaidi bali ni jasusi akitokea Tanzania na si Saudi Arabia kama walivyoelezwa na Habiba Jawad.Kikao kilikuwa kizito na kilichukua muda mrefu kutokana na wengi wa wajumbe kutokukubaliana na wazo la kutaka kumuua Mathew Mulumbi kabla hajamaliza kazi aliyotumwa kuifanya. David Walker aliyepigiwa simu na Jason Washington kumjulisha kwamba ndege tayari imeingia katika anga la Iran,aliwapa wenzake taarifa zile. “Hizi si taarifa za kustusha wala kushangaza kwani tulitegemea jambo hilo kutokea kutokana na mipango mizuri tuliyokuwa tumeiweka. Suala mezani bado ni kuhusiana na Abu Zalawi ambaye limetolewa pendekezo la kuuawa baada ya kujulikana kuwa si gaidi kama tulivyoaminishwa na Habiba Jawad.Tunatakiwa kupata muafaka katika jambo hili haraka” akasema David Walker “Binafsi baada ya kuwasikiliza kwa muda mrefu sijaona bado sababu ya msingi ya kutaka kumuua Abu Zalawi hata kama tumegundua si gaidi.Mpaka hatua hii hajaonyesha dalili zozote mbaya na amevumilia mateso makali kwa ajili ya kuitekeleza misheni hii aliyopewa.Nashauri tumuache aendelee na misheni yake kwani mahala alipofika ni muhimu sana.Pale atakapokuwa amekamilisha misheni yake ndipo tumuue lakini kwa sasa tutafanya kosa kubwa kumuua” akasema Willie Simmons ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu wa kikao kile.Wajumbe wengine wakaonekana kumuunga mkono “Kuna tatizo hapa ambalo wengi hamtaki kuliona.Huyu Abu Zalawi au Mathew Mulumbi ambaye tumemtuma akatekeleze kazi yetu nchini Iran anatokea Tanzania na tayari anafahamu kuwa ni sisi tunaohusika na vurugu zile za kidini zilizotokea nchini Tanzania kwa lengo la kuchukua mafuta kutoka nchini Uganda.Kama mtakumbuka wakati tunamueleza kuhusu sisi tulimueleza sehemu mbali mbali ambazo tumetengeneza machafuko na mojawapo ikiwa ni Tanzania.Kwa namna yoyote ile huyu mtu lazima atakuwa na hasira na sisi.Hatuwezi kujua moyoni mwake anawaza nini lakini Abu Zalawi ni mtu hatari sana kuendelea kumtumia kwa sasa katika misheni zetu” akasema David walker “Amefikaje kwa Habiba Jawad hadi wakajenga mashirikiano ya karibu? Yawezekana akawa amebadilika kutoka kuwa jasusi hadi kuwa gaidi hivyo hatakuwa na madhara yoyote kwetu hata kama akifahamu siri zetu” akasema Eric Wood. “Niliwaeleza awali kwa kirefu namna Mossad walivyombadili Mathew Mulumbi kutoka kwenye ujasusi hadi kuwa gaidi Abu Zalawi na lengo kubwa likiwa ni kumuua Habiba Jawad ambaye hadi leo hii Mossad hawajui kama tunashirikiana naye.Swali la kujiuliza hapa ni je kama aliandaliwa kwa ajili ya kumuua Habiba Jawad kwa nini baada ya kuonana naye hakufanya hivyo na badala yake akaanza kushirikiana naye? Kuna nini kati ya Abu Zalawi na Habiba Jawad hadi akaamua kumleta kwetu mtu huyu ili tumtumie? Tukiangalia mtiririko huo wote tunaona ni namna gani misheni yetu ilivyoingia dosari.Hata kama tukikubaliana kwamba tumuache amalizie misheni tuliyomtuma tutakuwa tunajidanganya tu kwani hatujui kuna nini kati yake na Habiba Jawad? Upo uwezekano mkubwa huyu jamaa akabadilika na kuwa mwiba kwetu ndiyo maana lazima tumuwahi kumuua kabla hajafanya chochote nchini Iran” David Walker akaendelea kuwashawishi wenzake wakubali mpango wa kumuua Mathew Mulumbi “Vipi kuhusu Mossad ambao wanataka tuwape taarifa za mahala alipo Habiba Jawad? Akauliza Michael Torres. “Hatutaweza kuwapa taarifa za mahala alipo Habiba Jawad badala yake Habiba tutamuua sisi wenyewe baada ya kumuhoji kujua kuhusu Mathew Mulumbi.Ni yeye ambaye ametufikisha hapa tulipofika hivyo si mtu ambaye tunaweza kumuanini na kuendelea kushirikiana naye tena.Lazima tumuue lakini tutafanya hivyo pale tu ambako Mossad watafanikiwa kumuua Mathew Mulumbi” akasema David Walker. Baada ya mjadala mzito hatimaye wakafikia makubaliano ya kumuua haraka Mathew Mulumbi kwa kuwatumia majasusi wa Mossad walioko nchini Iran.Baada ya kumaliza kikao kile David Walker akaondoka kwenda kuonana na mkurugenzi mkuu wa CIA Jason Washington “Dah ! siamini kama misheni ambayo tumetumia gharama kubwa ya fedha na damu kumwagika imeishia sehemu nzuri kiasi hiki.Tayari Abu Zalawi amekwisha ingia nchini Iran kwa ajili ya kuianza kazi tuliyomtuma.Itatuchukua muda mrefu kuandaa tena operesheni nyingine na kufikia hatua kubwa kama hii ya kupandikiza mtu nchini Iran.Tulifanya makosa sisi wenyewe hatukuwa makini toka mwanzo na zoezi hili hadi tukajikuta tukimtumia mtu ambaye si sahihi.Imeniuma sana kwani hivi sasa Abu Zalawi tayari amekwisha ingia nchini Iran.Kuna wakati ninasikia sauti ambayo inakataa tusifanye hiki tunachotaka lakini ninaisikia tena sauti nyingine ikinionya kuwa Abu Zalawi ni mtu hatari sana kwetu ambaye anapaswa kudhibitiwa haraka sana.Ngoja tukubali kushindwa na tujipange vizuri zaidi ili misheni ijayo iwe na mafanikio makubwa” akaendelea kuwaza David.
“Imekuwa vyema umefika kwa wakati David kwani tunakwenda kuonana na makamu wa Rais amenitaka nifike ofisini kwake” akasema Jason Washington mkurugenzi mkuu wa CIA baada ya David Walker kufika ofisini kwake. Bila kupoteza muda wakaingia katika gari la Jason na kuondoka kwenda kuonana na Mark Piller makamu wa Rais “Nini kimejiri huko katika kikao? Akauliza Jason na David akamweleza kila kitu walichokubaliana katika kikao “Vizuri sana.Nilimdokeza Mark Piller kuhusiana na mpango wetu wa kumuondoa Abu Zalawi.Mark amestushwa sana na jambo hili ndiyo maana amenitaka nikaonanye naye kwani tusingeweza kuzungumza kwa kirefu katika simu.Haamini kile nilichomweleza kuhusu Abu Zalawi” akasema Jason Washington “Suala hili la Abu Zalawi linaumiza vichwa sana.Kila mtuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ anashangaa kuhusu jambo hili limetokeaje? “Hatuna wa kumlaumu katika hili David.Tumekosea sisi wenyewe na lazima tuchukue hatua za haraka sana kuhakikisha jambo hili halitakuwa na madhara kwetu.Kama tungechukua tahadhari mapema haya yote yasingetoke ana misheni ingeendelea kama kawaida” akasema Jason “Kuna kitu nimekuwa najiuliza vipi kuhusu wale jamaa wanasayansi tuliokuwa tunawashikilia kwa muda mrefu? Tunakubali tumewapoteza?akauliza David na Jason akatikisa kichwa akisikitika “Watu wale japo hawajatupa taarifa tulizokuwa tunazihitaji lakini ni watu wa muhimu sana kwa Iran.Katika hili tumewapa Iran ushindi mwepesi lakini lazima tuhakikishe nao pia wanauawa pamoja na Abu Zalawi.” akasema Jason Walifika katika ofisi ya makamu wa Rais ambaye alikuwa anawasubiri na bila kupoteza muda wakaingia katika chumba cha maongezi ya faragha na kikao kikaanza. “Jason nimevuruga ratiba yangu ya siku ya leo ili niweze kuzungumza nanyi.Nataka kufahamu kwa kina kuhusiana na hiki kinachoendelea” akasema makamu wa Rais Mark Piller Jason akamuelezea Mark Piller kila kitu hadi walipogundua kuhusu Abu Zalawi kuwa si gaidi bali ni jasusi pamoja na maamuzi waliyoyachukua ya kumuua “Jason jambo hili limetokeaje? Kwa nini haukufanyika uchunguzi wa kina kuhusiana na huyu mtu Abu Zalawi hadi tumefika hapa tulpofika? Akauliza Mark Piller “Katika hili Mark hatuna wa kumlaumu mtu bali tunapaswa kujilaumu sisi wenyewe.Tulifanya uzembe wa kutokufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na Abu Zalawi” akasema Jason “Lakini yote haya ameyasababisha Habiba Jawad ambaye tulimuamini kwa asilimia mia moja na hivyo tukamuamini yule mtu aliyetuletea.Hata mara moja hajawahi kutuangusha na katika kila operesheni tuliyomshirikisha hakujawahi kutokea matatizo.Hii ni mara ya kwanza Habiba anatufanyia kitu cha namna hii” akasema David Walker “Mnadhani Habiba alikuwa na lengo lake binafsi la kumleta kwetu Abu Zalawi?akaliza Mark Piller “Hatuna uhakika bado ndiyo maana tunataka kulifanyia uchunguzi suala hilo lakini wakati uchunguzi huo ukiendelea tunataka kumuondoa kwanza Abu Zalawi pamoja na wale wanasayansi tuliokuwa tunawashikilia” akasema Jason.Baada ya tafakari ya muda mfupi Mark akauliza “Kutakuwa na athari gani kama tukimuacha Abu Zalawi akaendelea na misheni lakini tukimfuatilia kwa ukaribu mkubwa kujua kila anachokifanya kwa kuwatumia hao majasusi wa Mossad ambao mnataka kuwatumia kumuua?akauliza Mark Piller na Jason akampa maelezo aliyopewa na Moshe Levine mkuu wa Mossad kuhusu Abu Zalawi na Mark akazidi kuchoka. “Mark hatuna namna lazima tumuondoe Abu Zalawi haraka sana ili kujihakikishia usalama wetu.Endapo tukishindwa kumuondoa Abu haraka itatugharimu baadae” akasema Jason.Waliendelea na majadiliano kwa muda halafu Mark Piller akasema “Jason na David nimekubalianba na mapendekezo yenu juu ya suala hili lakini nina ushauri.Hatuwezi kumuua Habiba Jawad nchini kwao Saudi Arabia.Habiba Jawad ana ukaribu mkubwa na mfalme wa Saudi Arabia ambaye ni mshirika mkubwa wa Marekani hivyo lazima tujihadhari tusivuruge mahusiano mazuri kati yetu na serikali ya Saudi Arabia.Habiba aitwe Marekani na akifika huku ndipo atakapouawa” akashauri Mark Piller “Ushauri mzuri tutauzingatia” akasema Jason “Angalizo.Habiba asiuawe kama Mossad hawajamuua Abu Zalawi.Pale ambapo Abu Zalawi atakuwa ameuawa ndipo Habiba auawe kwani tunaweza kumuua Habiba halafu Mossad wakashindwa kumuua Abu Zalawi.Kama kuna jambo wawili hawa wanalipanga lazima tuwaondoe wote wawili akiondolewa mmoja na mwingine akabaki hatutakuwa tumefanya kitu” akasisitiza Mark Piller.Baada ya majadiliano Jason na David wakaondoka .Mark Piller hakupoteza muda akainua simu na kumpigia Rais William Washington “Mheshimiwa Rais nahitaji kukuona sasa hivi” akasema Mark “Njoo ofisini” akajibu Rais William na Mark Piller akatoka ofisini kwake kuelekea ofisini kwa Rais. “Mark mpango wenu unakwenda vizuri.Nimefurahishwa na taarifa nilizozipata kwamba ndege ile iliyopotea imeonekana ikielekea nchini Iran” akasema Rais William baada ya Mark kufika ofisini kwake “Mheshimiwa Rais ni kweli mpango umekwenda vizuri sana na hivi tuzungumzavyo tayari mtu wetu amekwisha kanyaga ardhi ya Iran” akasema Mark Piller “Vipi mna mawasiliano naye baada ya kuwasili Iran? Akauliza Rais William “Mheshimiwa Rais mpango wetu wa kwanza ulikuwa ni kumuingiza Abu Zalawi nchini Iran na mpango huo umefanikiwa vizuri lakini kuna tatizo limejitokeza” akasema Mark Piller na sura ya Rais William aikabadilika “Kumetokea tatizo gani tena” akauliza William “Baada ya Abu Zalawi kufika salama Iran tulihitaji kumpa msaada na kwa vile hatuna wetu wetu kule Iran ilitulazimu kuomba msaada kutoka kwa wenzetu wa Mossad ambao wana majasusi wao Iran na hapo ndipo lilipoibuka jambo ambalo hatukuwa tukilifahamu” akasema Mark Piler na kumueleza Rais William kila kitu walichokifahamu kutoka kwa Mossad kuhusiana na Abu Zalawi.Zilikuwa ni taarifa zilizomstua sana William “Mark kwa nini haya yote yametokea?Kwa nini hamkuchukua tahadhari mapema kuhakikisha mnamfahamu vyema mtu ambaye mnataka kumtumia katika misheni kubwa kama hii? Akauliza William “Mheshimiwa Rais katika hilo tunakiri tulikosea na ndiyo maana tunataka kuchukua hatua za haraka za kurekebisha kwa kumuondoa Abu Zalawi haraka sana kabla hajaendelea na misheni aliyotumwa nchini Iran” “Kumuua Abu Zalawi ni suluhisho la jambo hili?akauliza William akionekana kukasirika “Mheshimiwa Rais huyu mtu ni hatari kwetu kama tukiendelea kumuacha hai.Tayari anafahamu kila kitu kuhusu sisi na baya zaidi anafahamu ni sisi tulio nyuma ya kile kilichotokea Tanzania na Afrika mashariki na anafahamu kwa nini tulifanya vile….” “Pamoja na kufahamu ! akasema kwa ukali Rais William na kumkatisha Mark Piller “Pamoja na kufahamu hayo yote lakini bado Abu Zalawi au vyovyote vile anavyofahamika amekubali kuifanya kazi aliyotumwa na kwa sasa tayari amefika nchini Iran.Anafahamu kabisa kwamba kazi aliyotumwa kuifanya Iran ni kazi ya hatari kubwa na kama akijulikana kuwa ni pandikizi la Marekani anaweza akauawa muda wowote ule lakini bado yuko tayari kufanya.Kumuua Abu Zalawi ni kosa kubwaMark ! akasema Rais William “Mheshimiwa Rais pamoja na Abu Zalawi kukubali kuifanya kazi aliyotumwa aifanye lakini hakuna anayejua moyoni mwake nini anakiwaza,hatujui ana mipango gani dhidi yetu.Kwa taarifa tuliyoipata kutoka kwa Mossad ni kwamba Abu Zalawi ameyatoa maisha yake katika kupambana na ugaidi hasa kundi la IS linaloendelea kuotesha mizizi katika eneo la Afrika Mashariki.Abu Zalawi ni bilionea na ana familia inaishi Paris Ufaransa lakini ameacha hivyo vyote akajielekeza katika kupamba na na magaidi.Jaribu kupata picha mtu kama huyu anakuja kugundua kwamba tunashirikiana na magaidi wa IS na kibaya zaidi kuchochea machafuko katika nchi anakotoka na kusababisha vifo vya watu na sisi tukiendelea kubeba tani na tani za mafuta unadhani mtu kama huyu atafanya nini?Lazima atakuwa na chuki kubwa sana dhidi yetu na hatujui nini anakifikiria lakini ni wazi jambo hili hataweza kulivumilia” akasema Mark Piller “Mark nimekuelewa lakini maamuzi ya kumuua mtu kama huyu si sahihi.Mtu kama huyu bado anaweza akawa upande wetu.Tunaweza kuzungumza naye na kumfanya atuelewe na hata kama alikuwa na kitu moyoni mwake tukakiondoa.Sisi ni taifa kubwa na hatuwezi kukubali kushindwa kirahisi namna hii.Hebu fikiria Mark,nini kingine mtakifanya kitakachowawezesha kupandikiza mtu nchini Iran? Kwa kuwatumia wale mateka wa Iran imekuwa rahisi kwetu kuweza kupenyeza mtu ndani ya Iran na kama mkiharibu msheni hii itachukua miaka mingi kuweza kufanikisha jambo kama hili na pengine lisiwezekane tena.Kwa kuwa tayari Abu Zalawi amekwisha ingia Iran,itafutwe namna ya kuzungumza naye na kumuweka sawa aendelee na jukumu lake badala ya kufikiria kumuua” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais…..” Mark Piller akataka kusema kitu lakini Rais William akamzuia “Mark sitaki kuendelea na mjadala huu.Hatuwezi kuipa Iran ushindi kirahisi namna hii lazima kwa namna yoyote ile misheni hii iendelee.Iran ni taifa tishio kwa Marekani kwa sasa na lazima tufahamu uwezo wake wa silaha hivyo lazima misheni iendelee.Abu Zalawi hapaswi kuuawa ! akasema kwa sauti ya msisitizo kisha wakabaki wanatazamana “Mheshimiwa Rais sidhani kama unaiona hatari iliyoko mbele yetu kama tukiendelea kumtumia huyu Abu Zalawi ! akasema Mark “Mark sijali chochote, ninachohitaji ni Abu Zalawi aendelee na misheni aliyotumwa nchini Iran.Endapo Abu akiuawa na misheni ikashindwa kuendelea ninaapa nitakifuta hiki kikundi chenu kwani hakitakuwa na maana tena.Sijali kama nitauawa ama nini kitatokea lakini lazima nikifute ! akasema Rais William “Mheshimiwa Rais nilipokuja kukueleza kuhusiana na kikundi hiki na mambo yake nilikupa angalizo kwamba unatakiwa usiri mkubwa kwani Rais wa nchi hapaswi kufahamu chochote kuhusu uwepo wa kikundi hiki.Utayaweka maisha yetu sote katika hatari kubwa.Nakuomba mheshimiwa Rais usifikirie kufanya hicho hicho unachotaka kukifanya” akasema Mark Piller “Mark mimi siogopi chochote na ninakuhakikishia kwamba nitafanya hivyo na wamarekani watajua kuwa nchi yao inashirikiana na magaidi” “Mheshimiwa Rais ! akasema Mark “Mark fanya ninavyokuelekeza.Ukitaka kundi lenu liendelee kuwepo.Nataka Abu zalawi aendelee na misheni yake nchini Iran.Sitaki auawe.Fanya kila linalowezekana kuhakikisha misheni yake inafanikiwa.Tunaihitaji sana misheni hii ama sivyo Iran itaendelea kutoa vitisho vya kusishambulia Marekani! Siwezi kuzivumilia kauli chafu za vitisho zinazotolewa na Rais wa Iran dhidi ya Marekani ! akasema Rais William “Mheshimiwa Rais kufanya hicho unachotaka nikifanye ni usaliti mkubwa kwa wenzangu na…..” “Mark kumbuka kwamba sisi ndio tunao ongoza nchi hii na dhamana ya usalama wa watu wetu tumeibeba sisi na kwa sasa watu wetu wana hofu kufuatia vitisho vya Iran kuwa anao uwezo wa kuishambulia na kuiharibu Marekani hivyo basi lazima tufanye kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunaiweka nchi yetu salama pamoja na watu wake ndiyo maana ninasema kwamba tunaihitaji sana misheni hii kwa ajili ya kufahamu wezo wa silaha za Iran na baada ya hapo tutaichakaza vibaya sana.Ikitokea Iran imeshambulia Marekani watakaobeba mzigo wa lawama ni sisi na si hao ambao unaogopa kuwasaliti.Mark fanya kila linalowezekana hata kama ni kwa kuwasaliti wenzako hakikisha Abu Zalawi anakuwa salama na anaendelea na misheni yake nchini Iran.Vuruga mpango wa kumuua ! akasema Rais William na Mark Piller akainamisha kichwa akitafakari “Umenielewa Mark Piller?akauliza Rais William “Nimekuelewa mheshimiwa Rais.Nitafanya kama ulivyoelekeza lakini naomba ufahamu kwamba ni jambo la hatari kubwa” “Usihofu kuhusu hilo Mark.Kama kuna hatari yoyote unaihisi nijulishe na mimi nitakulinda.Tunayafanya haya kwa maslahi ya nchi yetu” akasema Rais William na Mark Piller akaondoka akarejea ofisini kwake na kujiegemeza kitini “Hili jambo linaendelea kubadilika kila wakati.Rais anataka niwasaliti wenzangu na kuvuruga mipango ya kumuua Abu Zalawi ! akawaza Mark “Lakini ukilitazama jambo hili kwa kina zaidi,Rais yuko sahihi.Hatupaswi kumuua Abu Zalawi badala yake tunapaswa kufanya kila liwezekanalo kumuweka upande wetu.Kwa hiyo kwa mara ya kwanza nitalazimika kuwasaliti wenzangu na kuvuruga mpango wa kumuua Abu Zalawi.Kuna mtu mmoja tu ambaye ninatakiwa kuzungumza naye” akawaza na kufungua mkoba wake akatoa simu iliyokuwa na namba kumi na mbili tu ambazo ni namba za watu muhimu akaelekeza kidole chake katika namba ya sita ambayo ilikuwa ni namba ya Habiba Jawad akampigia baada ya sekunde kadhaa simu ikapokelewa. “Mark Piller ! akasema Habiba Jawad akionekana kushangaa “Habiba Jawad unaendeleaje? Akasema Mark “Ninaendelea vizuri Mark.Nimeshangaa kidogo leo umenipigia simu.Sikutegemea kabisa kupata simu yako” akasema Habiba Jawad “Habiba nimelazimika kukupigia simu kuna mambo ya muhimu sana ya kuzungumza mimi nawe na ninakuomba tafadhali yale tutakayoyazungumza hapa yawe ni baina yetu sisi wawili.Mtu mwingine yeyote kutoka G20 hatakiwi kufahamu kama nimekupigia simu.Umenielewa Habiba?akauliza Mark Piller “Nimekuelewa Mark.Nini unataka kuzungumza nami?akauliza Habiba “Kwanza kabisa ninataka kukupa taarifa kuwa mpango wetu umekwenda vizuri na hivi tuzungumzavyo tayari Abu Zalawi amekwisha ingia nchini Iran” akasema Mark Piller “Hizo ni taarifa njema sana.Nimefurahi kusikia matokeo mazuri ya mpango huu.Ninakuhakikishia Mark kuwa kama tayari Abu amefanikiwa kuingia nchini Iran lazima atafanikisha kila kitu alichotumwa kukifanya.Kitu cha msingi kwa sasa ni kujitahidi kutafuta namna ya kuwasiliana naye na kujua maendeleo yake” akasema Habiba “Tayari tumelifanya hilo Habiba ila kuna tatizo limejitokeza” “Tatizo gani Mark?akauliza Habiba “Baada ya kuhakikisha Abu Zalawi ameingia Iran ilitulazimu kuomba msaada kutoka kwa wenzetu wa Mossad ambao wana watu wao kule Iran kwa ajili ya kumpa msaada na hapo ndipo tulipofahamu kila kitu kuhusu Abu Zalawi” akasema Mark na kumueleza Habiba kila kitu walichokigundua kuhusu Abu Zalawi.Kupitia spika za simu Habiba Jawad akasikika akivuta pumzi ndefu “Habiba unaweza ukazungumza chochote kuhusiana na jambo hili?akauliza Mark “Sina cha kuzungumza Mark lakini kila kitu mlichoelezwa kuhusu Abu Zalawi ni cha kweli” akasema Habiba na Mark Piller akahisi mwili unamtetemeka “Kwa nini Habiba kama ulifahamu kuwa Abu Zalawi ni jasusi tena anatokea Tanzania ukamleta kwetu tukampa misheni kubwa kama hii? Akauliza Mark Piller “Kwa sababu Abu Zalawi ndiye pekee anayeweza kuifanya kazi hii.Hakuna gaidi ambaye ana uwezo wa kuingia Iran na kufanya jambo la hatari la kuichunguza Iran zaidi ya Abu Zalawi.Mark hii si misheni ya kigaidi hii ni misheni ya kijasusi na mtu niliyewaletea ndiye anayefaa” akasema Habiba Jawad “Habiba sisi tulihitaji gaidi lakini wewe ukatuletea jasusi tena anatokea Tanzania nchi ambayo kwa kushirikiana na magaidi wa IS tumechochea machafuko ya kidini na kusababisha waumini kushambuliana na damu nyingi kumwagika na kama haitoshi bado tunaendelea na mpango wa kusambaza kirusi hatari kwa lengo la kuendelea kuchota utajiri mkubwa ulioko Afrika Mashariki.Kwa nini ukatufanyia hivi? Akauliza Mark “Mark kama nilivyokueleza kwamba huyu ndiye mtu pekee anayefaa kwa misheni hii” akajibu Habiba “Habiba japokuwa una uhakika kuwa mtu huyu ndiye anayefaa lakini tayari ana kasoro.Hatujui ni kitu gani anakiwaza baada ya kugundua kwamba sisi tuko nyuma ya kile kinachoendelea Afrika Mashariki.Hii ni kasoro kubwa na tayari imetia doa misheni nzima” akasema Mark “Mark nataka nikuhakikishie kwamba Abu Zalawi hana tatizo lolote na msiwe na wasiwasi wowote naye.Anakwenda kutekeleza kile alichotumwa kukifanya Iran na uwezo wa kufanya hivyo anao.Abu Zalawi japo ni jasusi lakini nimembadilisha na anafanya kazi kwangu.Nimembadili kutoka Jasusi kuwa Gaidi.Ni mimi pekee anayenisikiliza kila ninachomuelekeza kukifanya kwani nimemfanya kuwa mwanangu,amemuoa mwanangu Najma hivyo Abu Zalawi ni sehemu ya familia yangu” akasema Habiba “Habiba kama nilivyokueleza kuwa tayari misheni imeingia dosari.Baada ya kugundua kuwa Abu Zalawi si Yule uliyetuaminisha kuwa ni gaidi bali ni jasusi tena anatokea Tanzania,kuna maamuzi yamefanyika” akasema Mark Piller na kunyamaza kidogo “Mmefanya maamuzi gani Mark?akauliza Habiba “Tumekubaliana kumuua Abu Zalawi na misheni itakuwa imeishiahapo” akasema Mark na ukimya ukapita “Mark Piller hilo ni kosa kubwa sana ambalo mtalijutia kwani hamtapata tena nafasi nyingine ya kumuingiza mtu wa kuwafanyia ujasusi nchini Iran.Hii ni nafasi pekee mmeipata na mkishindwa kuitumia vyema ni juu yenu” akasema Habiba “Habiba misheni tayari imevurugika na aliyeivuruga misheni hii ni wewe kwa kutuletea mtu ambaye hakuwa sahihi kwa misheni hii.Tulikuamini sana Habiba na ndiyo maana hatukuwa na wasi wasi wowote na Abu Zalawi lakini baada ya kumfahamu vyema Abu Zalawi umevunja uaminifu na maamuzi yaliyopitishwa ni wewe kuuawa pia” akasema Mark Piller na ukimya ukawala. “Mark ! akaita Habiba Jawad “Unasemaje Habiba? “Mnakwenda kufanya kosa kubwa sana kwa hiyo mipango yenu mliyoipanga” akasema Habiba “Ninafahamu Habiba” “Kwa nini ukanipigia kunijulisha kuhusu mipango yenu?akauliza Habiba “Nimekupigia kwa sababu baada ya kutafakari kwa kina nimegundua kwamba tutafanya kosa kubwa.Tunaihitaji mno misheni hii ifanikiwe hivyo nimekupigia kuomba msaada wako” akasema Mark na ukimya ukatawala tena.Habiba Jawad akavuta pumzi na kusema “Nini unahitaji tena kutoka kwangu Mark wakati tayari mmekwisha panga mipango ya kuniua? Akauliza Habiba “Nimeamua kuwasaliti wenzangu na kukueleza ukweli kuhusu mipango yetu,kwanza ili uchukue tahadhari na kujificha na pili ni kutafuta namna ya kumfikishia Abu Zalawi taarifa za kumtaka achukue tahadhari kwani kuna watu wanaotaka kumuua.Nataka Abu aendelee na misheni hii hadi atakapoikamilisha” akasema Mark Piller “Mark nimekuwa mtumwa wenu kwa miaka mingi,nimewafanyia kazi nyingi kwa manufaa ya nchi yenu lakini hata baada ya kuwafanyia hayo yote ninachoambulia ni kutaka kuuawa.Mmenisikitisha sana Mark” “Habiba ndiyo maana nimekupa siri hii ili uweze kuchukua tahadhari na ikiwezekana uondoke Saudi Arabia ukajifiche mahala” akasema Mark “Siwezi kukimbia Mark.Siwezi kukimbia.Kama mnataka kuniua njooni mtanikuta hapa ninawasubiri lakini fahamuni ya kwamba damu yangu haitawaacha salama ! akasema Habiba Jawad “Habiba tafadhali naomba tusilifanye jambo hili liwe gumu.Wewe mwenyewe unafahamu namna misheni hii ilivyo muhimu.Wengine wote hawalioni hilo lakini mimi ninafahamu umuhimu wake.Habiba tafadhali nakuhitaji sana.Naomba tushirikiane kuhakikisha misheni hii inaendelea na inafanikiwa.Naomba tafuta namna ya kumlinda Abu Zalawi dhidi ya wale wote watakaotumwa kumuua na aendelee na kazi aliyotumwa kuifanya.Habiba nakuahidi nitakulinda dhidi ya mipango yoyote mibaya inayopangwa juu yako” akasema Mark Piller “Mark….. ! “Habiba tafadhali ! Sisi nawe tumetoka mbali sana na umetusaidia mambo mengi naomba mashirikiano yetu yaendelee kama kawaida na ninakuahidi kukulinda hata kama ni kwenda kinyume na wenzangu wote niko tayari kufanya hivyo.Tafadhali Habiba” akasema Mark “Mark nimekuelewa lakini nataka kufahamu jambo moja.Nataka kufahamu namna mlivyopanga mipango ya kutuua mimi na Abu Zalawi” akasema Habiba na Mark akamueleza mipango yote namna ilivyopangwa ya kuwaua yeye na Mathew “Mark Piller unadhani nini kitakutokea pale wenzako watakapobaini kuwa umewasaliti?akauliza Habiba “Ninafahamu nitakuwa matatizoni lakini niko tayari kukabiliana na chochote kitakachonitokea.Misheni hii ni muhimu mno kwa nchi yangu na kwa namna yoyote ile lazima ifanikiwe” akasema Mark Piller “Sawa Mark nimekuelewa.Nitashirikiana nawe kuhakikisha misheni hii inafanikiwa.Nitajitahidi kuhakikisha Abu Zalawi anapata taarifa mapema kabla ya watu wa Mossad hawajamfikia.Ninachotaka ukifanye ni kuendelea kunipa taarifa za mipango yenu yote mnayoipanga ili na mimi nitafute namna ya kumsaidia Abu Zalawi” akasema Habiba “Nitakujulisha kila kitu Habiba Jawad lakini nakuomba nawe uchukue tahadhari kuanzia sasa.Pale utakapoitwa uje Marekani toa kisingizio kwamba hautaweza kwa sasa kuna mambo ya msingi unayashughulikia na mimi nitaongeza nguvu.Ongeza ulinzi na mtu yeyote asiyefahamika asikaribishwe katika makazi yako” akasemaMark Piller “Nakushukuru Mark.Mimi nitahakikisha Abu Zalawi anakuwa salama na anaendelea na mipango yake yote kama alivyotumwa nchini Iran” akasema Habiba wakaendelea na mazungumzo kidogo wakapeana mikakati namna watakavyokuwa wakiwasiliana kwa siri kisha wakaagana. “Nilijua tu lazima watagundua kuhusu Mathew lakini sikutegemea iwe mapema namna hii.Nilifahamu watakapogundua kuhusu Mathew mzigo wote wa lawama nitaubeba mimi na nilikwisha jiandaa kwa jambo hilo.Kwa sasa baada ya kuifahamu mipango yao natakiwa kuhakikisha Mathew anakuwa salama ili aweze kuikamilisha misheni yake” akawaza Habiba Jawad na kuchukua simu nyingine akazitafuta namba Fulani na kupiga kisha simu ikapokelewa “Habiba” akasema mtu aliyepokea simu upande wa pili “Vahid unaendeleaje?akauliza Habiba Jawad “Siwezi kusema naendelea vizuri Habiba.Bado kifo cha mwanangu Najma kinaniumiza mno.Ninajuta kwa nini nilimruhusu aje Riyadh.Kama ningeendelea kukaa naye hapa Tehran yasingemkuta haya yaliyomkuta.Kwa ujumla bado siko sawa na itanichukua muda mrefu kulizoea jambo hili” akasema Vahid Ghorbani baba mzazi wa Najma.Vahid na Habiba waliwahi kuwa na mahusiano na wakamzaa Najma lakini hawakufunga ndoa na kila mmoja akaendelea na maisha yake. “Vahid suala hili linatuumiza sote.Huwezi kujua niko katika hali gani kwa sasa baada ya kuwapoteza wanangu wawili ndani ya kipindi kifupi.Ni wakati mgumu sana huu kwetu sote hivyo tusaidiane kufarijiana badala ya kulaumiana” akasema Habiba “Sikulaumu Habiba nafahamu ulivyompenda Najma.Tuachane na hayo vipi maendeleo yako? “Kama nilivyokwambia Vahdi kwamba siko sawa.Nimewapoteza watoto wawili ndani ya kipindi kifupi ni suala zito kulibeba lakini ninajitahidi.Hata hivyo sijakupigia simu kwa suala hilo.Vahdi kuna jambo nataka unisaidie” “Sema chochote Habiba.Unataka nikusaidie nini?akauliza Vahid “Kuna wanasayansi sita wa Iran waliokuwa wamepotea lakini leo hii wamerejea nyumbani”akasema Habiba “Nimepata taarifa hizo kwamba wale watu wetu waliokuwa wamepotea wamerejea nyumbani leo hii lakini haijatolewa taarifa rasmi kwamba walikuwa wapi muda huu wote” akasema Vahid “Aliyewakomboa watu hao na kuwarejesha nyumbani anaitwa Abu Zalawi” “Abu Zalawi?! Vahdi akauliza http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Ndiyo.Anaitwa Abu Zalawi” “Ni mtu wa wapi huyo Abu Zalawi? “Ni Raia wa Saudi Arabia” “Hatujafahamishwa jambo hilo.Nini unataka nikusaidie Habiba? Akauliza Vahid “Ninataka ufanye kila lililo ndani ya uwezo wako uweze kuonana na huyu Abu Zalawi” “Nionane na Abu Zalawi? Vahid akauliza “Ndiyo.Kuna ujumbe wa muhimu sana ambao nataka umfikishie”akasema Habiba “Habiba sifahamu alipo huyo Abu Zalawi na wala sijui ni jinsi gani nitaweza kumpata” akasema Vahid “Vahid unatakiwa ufanye kila linalowezekana kuhakikisha unampata Abu Zalawi” “Habiba sidhani kama mimi ni mtu sahihi wa kukusaidia kwenye jambo hilo” akasema Vahid “Vahid ni muhimu sana ukaonana na Abu Zalawi.Huyo ndiye mume wa Najma” “Mume wa Najma?! Vahidi akastuka “Ndiyo ni mume wa Najma” “Najma alikuwa na mume?Kwa nini hujawahi kuniambia jambo hili? “Najma mwenyewe ndiye aliyetaka iwe siri na tusikujulishe.Kama unavyofahamu kuwa Najma hakuwahi kuwa na mpenzi lakini alipokutana na Abu Zalawi akajikuta akimpenda na kufunga naye ndoa ya kimya kimya na alitoa maelekezo ya kutokufahamisha jambo hili.Alitaka yeye mwenyewe akujulishe pale atakapokuwa tayari lakini kwa bahati mbaya hakuwahi kufanya hivyo mauti yakamkuta” akasema Habiba “Habiba ulikosea sana kukubali kunificha kuhusu Najma kuolewa wakati mimi ndiye baba yake mzazi.Hukunitendea haki katika hili”akasema Vahid “Nakubali Vahid kwamba nilikosea lakini nilifanya hivyo kuheshimu matakwa ya mtoto.Alitaka akueleze jambo hili yeye mwenyewe muda utakapofika.Tusameheane katika hilo” “Nilipokuja msibani kwa nini huku nijlisha kuwa Najma alikuwa na mume hadi leo hii? “Nilikuwa nimechanganyikiwa Vahid ndiyo maana sikukueleza chochote.Tafadhali naomba sana unisamehe kwa hilo” akajibu Habiba.Baada ya muda Vahid akauliza “Unataka kumfikishia ujumbe gani huyo Abu Zalawi?akauliza Vahid “Nataka uonane naye ana kwa ana na umpe simu nizungumze naye” “Habiba umenipa mtihani mgumu sana.Kwanza ni nani huyo Abu Zalawi?Kwa nini yuko hapa? Akauliza Vahid “Vahid naomba unisaidie hilo ninalokuomba ni muhimu sana” “Habiba niko tayari kukusaidia lakini lazima nifahamu huyu mtu ni nani na kwa nini yuko hapa Iran? “Abu Zalawi anataka kuuawa na Mossad hivyo nataka niongee naye nimpe angalizo awe makini” akasema Habiba “Anataka kuuawa na Mossad?akauliza Vahid “Ndiyo.Kuna majasusi wanatumwa kuja Tehran kwa lengo la kumuua.Anatakiwa aipate haraka sana taarifa hiyo”akasema Habiba “Kwani huyu Abu Zalawi ni nani hadi Mossad watake kumuua? Akauliza Vahid “Vahid nitakueleza kila kitu hapo baadae kuhusiana na Abu Zalawi lakini kwanza naomba unisaidie kufanya kila uwezalo uonane naye na umpatie simu nizungumze naye.Unaweza ukanisadia kwa hilo? Akauliza Habiba “Sawa Habiba.Nitajitahidi kumtafuta huyo Abu Zalawi” “Jitahidi Vahid wewe ni mfanya biashara mkubwa nchini Iran unafahamiana na watu wengi hata viongozi wa serikali naamini haitakuwa kazi ngumu kwako kufahamu mahala alipo Abu Zalawi” akasema Habiba Jawad na kuagana na Vahid. ****************** Baada ya kutoka kuzungumza na makamu wa Rais,Jason na David walirejea katika ofisi ya Jason ambaye bila kupoteza muda akampigia simu Moshe Levine mkurugenzi wa Mossad “Jason Washington” akasema Moshe baada ya kupokea simu “Habari za muda huu Moshe.Nimekupigia kufuatia mazungumzo yetu ya awali” akasema Jason “Ndiyo Jason.Umefikia wapi kuhusiana na yale tuliyoyazungumza?akauliza Moshe Levine “Kama nilivyokueleza asubuhi kwamba tunataka kumuua Abu Zalawi.Bado mpango huo unaendelea na kama nilivyokudokeza tunataka kuwatumia watu wako wa Mossad walioko nchini Iran” akasema Jason “Jason nina watu wangu Tehran ambao wanaweza wakaifanya hiyo kazi muda wowote watakapopewa maelekezo lakini nilitoa masharti asubuhi ya kama mkitaka tuwasaidie kumuua Abu Zalawi basi na nyinyi mtupe taarifa za mahala alipo Habiba Jawad.Mmefikia wapi katika suala hilo?akauliza Moshe Levine “Tumejadiliana na tumekubaliana jambo moja.Habiba Jawad tutamuua sisi wenyewe pale ambapo nanyi mtakuwa mmemuua Abu Zalawi” “Jason hatukukubaliana hivyo.Ninataka mtupe taarifa za mahala alipo Habiba Jawad na tutamkamata sisi wenyewe.Hatutaki kumuua kuna mambo mengi tunahitaji kuyafahamu kuhusiana na mtandao wake kabla ya kumuua hivyo tupeni taarifa za mahala alipo sisi tutamkamata hatuhitaji msaada wa kumuua” akasema Moshe Levine “Moshe sisi tuko tayari kutoa aina yoyote ya ushirikiano kwenu.Kama hamtaki kumuua Habiba hatuna tatizo na hilo.Sisi tutamkamata Habiba na tutamkabidhi kwenu lakini lazima kwanza tuhakikishe Abu Zalawi ameuawa ndipo tutawakabidhi Habiba Jawad.Tunakubaliana katika hilo?akauliza Jason “Jason tunamtaka Habiba Jawad kwanza ndipo tuwafanyie kazi yenu ! Kuna ugumu gani wa kutupa taarifa za mahala alipo Habiba ? akauliza Moshe Levine “Moshe sisi na ninyi ni washirika wakubwa tena wa miaka mingi tunapaswa kuaminiana.Tuna sababu za msingi kwa nini hatuwezi kuwapa taarifa za mahala alipo Habiba Jawad.Naomba uniamini Moshe kwamba tutamkabidhi kwenu Habiba Jawad pale tutakapokuwa na uhakika kwamba Abu Zalawi ameuawa.Hivi tuzungumzavyo tayari timu inaandaliwa kwa ajili ya kwenda kumkamata Habiba Jawad.Tutamuhifadhi hadi pale ambapo mtakuwa mmekamilisha zoezi la kumuua Abu Zalawi” “Jason kutakuwa na ugumu katika jambo hilo.Tupeni Habiba Jawad na sisi tumuue Abu Zalawi” “Moshe nakuhakikishia kwamba hata dakika hii mkimtaka Habiba Jawad mtampata lakini hatuwezi kumkabidhi Habiba kwenu wakati bado hamjatekeleza kazi yetu.Muondoeni Abu Zalawi kwanza ili mumpate Habiba “Tufanye hivi.Tudhihirishieni kwanza kama kweli mnaye Habiba Jawad na tutaelekeza apelekwe katika ubalozi wenu Jerusalem na baada ya kumuua Abu Zalawi mtamkabidhi kwetu.Tunakubaliana katika hilo” “Hakuna tatizo katika hilo.Tutafanya hivyo” “Vizuri.Nashukuru kama tumekubaliana hivyo Jason basi na sisi tunaanza mara moja mpango wa kumuua Abu Zalawi.Tutaendelea kufahamishana kila hatua tunayopiga” akasema Moshe Levine wakaagana “Mambo yanazidi kuwa magumu David” Jason akamwambia David na kumuelezea kila kitu walichozungmza na Moshe Levine “Nini maamuzi yako katika jambo hili? akauliza David Walker “Hatuna ujanja lazima tumkamate Habiba Jawad na kumuandaa kwa ajili ya kuwakabidhi Mossad pale watakapokuwa wamemuua Abu Zalawi” “Jason huo ni mpango wa hatari sana.Ni vipi kama wakimchunguza na kugundua kuwa tumekuwa tunashirikiana naye?akauliza David “Tutamuweka Habiba Jawad katika ubalozi wetu jijini Jerusalem na baada ya wao kumuua Abu Zalawi sisi pia tutamuua Habiba Jawad na kuwakabidhi maiti yake.Hatuwezi kuwakabidhi Habiba akiwa mzima” akasema Jason wakaendelea kujadiliana kuhusiana na mpango ule halafu Jason akainua simu na kumjulisha Mark Piller kuhusu mazungumzo yake na Moshe Levine pamoja na mpango waliouandaa. Mark Piller baada ya kumaliza maongezi na Jason akampigia simu Habiba Jawad “Mark karibu tena” akasema Habiba “Habiba nimerejea tena kama nilivyokueleza awali kwamba nitakuwa ninakupa taarifa mipango yote inayopangwa dhidi yako” akasema Mark na kumueleza Habiba kuhusiana na mpango ule wa kutuma kikosi kwenda kumteka na kumpeleka katika ubalozi wa Marekani jijini Jerusalem tayari kwa kukabidhiwa kwa Mossad pale watakapokuwa wamefanikisha mpango wa kumuua Abu Zalawi. “Ahsante sana Mark Piller kwa angalizo hilo.Tayari nimekwisha anza taratibu za kumtafuta Abu Zalawi na kujua mahala alipo ili niweze kumuonya kuhusiana na mpango wa kumuua.Nategemea kabla ya watu hao wa CIA waliotumwa kuja kunikamata hawajafika hapa tayari nitakuwa nimekwisha mpata Abu Zalawi” akasema Habiba DAR ES SALAAM – TANZANIA Kiza tayari kilikwishatanda katika jiji la Dar es salaam,Nawal alitoka chumbani kwake na kwenda kukaa sehemu ya kupumzikia iliyo mbele ya nyumba ile wanakoishi viongozi wa vikosi vya jeshi la Marekani vilivyopo Dar es salaam.Taa zilikuwa zinawaka katika nyumba hii kwani walikuwa wanatumia jenereta .Ulinzi pia ulikuwa mkali karibu kila pembe ya nyumba hii kulikuwa na walinzi.Akiwa amejipumzisha mbele ya nyumba muhudumu akamfuata na kumuuliza kama angependa kutumia kinywaji chochote na Nawal akamuagiza amtengenezee kahawa “Nilipowasiliana na Ruby saa kumi na mbili jioni,bado Jenerali William hakuwa amerejea ofisini kwake na hadi giza limeingia hatujui mahala alipo Sattar.Kwa namna yoyote ile lazima usiku wa leo tujue mahala kilipo kirusi.Nitamvamia Jenerali William usiku wa leo chumbani kwake na lazima ataeleza alipo Sattar na kirusi.Kitu kikubwa ninachohitaji kufahamu ni watu wangapi wanaoishi ndani ya nyumba hii ili nijue namna ninavyoweza kukabiliana nao na kama nikiona sintaweza basi nitaomba msaada kutoka SNSA.Nitakaa hapa hapa hadi jenerali William atakaporejea” akawaza Nawal na kutolewa mawazoni baada ya kahawa yake kuletwa. “Ahsante sana.Jina lako nani nimelisahau” akauliza Nawal “Naitwa Brenda” “Ouh Brenda .Naitwa Chloe” akasema Nawal na kumtaka Yule muhudumu kukaa kwa ajili ya mazungumzo lakini Brenda akamjulisha kwamba watazungumza pale atakapokuwa amekamilisha majukumu yake “Huyu Brenda anaweza akanipa taarifa za kutosha kuhusu mahala hapa.Ngoja nimsubiri amalize majukumu yake” akawaza Nawal akiendelea kunywa kahawa yake taratibu Akiwa ameyaelekeza macho yake katika geti mara akawaona wanajeshi waliokuwa wakilinda geti wakiwa katika heka heka akakaza macho zaidi ili kujua kinachoendelea.Geti likafunguliwa na gari nne zikaingia mle ndani.Tatu zikiwa ni gari za doria za jeshi la Marekani na moja ikiwa ni aina ya Prado.Kutoka katika mojawapo ya gari akashuka Jenerali William na na makamanda wengine wawili na kutoka katika ile Prado wakashuka watu wanne ambao hawakuwa wanajeshi.Nawal alihisi mapigo ya moyo wake yakibadilika na kwenda haraka haraka baada ya kuziona sura za wale jamaa walioshuka katika Prado “Sattar ! Assad ! akasema kwa sauti ndogo ya mshangao Jenerali William akiwa ameongozana na wale jamaa wengine wanne na wanajeshi wawili wakaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya ile nyumba. “Chloe ! akasema Jenerali William baada ya kumkuta Nawal amekaa nje “Jenerali William” akasema Nawal na kusimama “Habari za toka mchana?Umeshinda salama? Akauliza Jenerali William “Niko salama kabisa Jenerali William.Nimepata huduma nzuri” “Nafurahi kusikia hivyo Chloe.Hawa ni wenzangu Meja Greg na Meja Thomas” akasema Jenerali William na kufanya utambulisho. “Huyu ni mmarekani mwenzetu ambaye alikuwa hapa Tanzania katika shughuli zake za upigaji picha lakini alijikuta amenasa katika machafuko na jana amekombolewa na vikosi vya jeshi la Tanzania akaletwa Dar es salaam na leo mchana Rais akanikabidhi.Chloe ataishi na sisi hapa hadi pale hali ya amani itakapokuwa nzuri” akasema Jenerali William na kumtaka Nawal waingie ndani.Miguu ya Nawal ilikuwa inagongana kwa kile alichokuwa amekishuhudia.Katika wale watu walioongozana na Jenerali William aliwashuhudia kwa macho watu wawili waliokuwa wanawatafuta kwa jasho na damu.Assad Ismail na Sattar Sayf Al Din “Siamini ninachokiona huu ni kama muujiza mkubwa.Watu wote hawa wawili Assad na Satter wote tunawatafuta kwa kila namna.Hadi mwili wangu unatetemeka sikuwa nimelitegemea kabisa jambo hili.Lakini mbona hawana yale masanduku ya kirusi?Wamekipeleka wapi? Au tayari wamekwisha anza kukisambaza?akajiuliza Nawal “Usiku wa leo lazima kila kirusi kipatikane.Wamejileta wenyewe kwenye mdomo wa Mamba na hawatatoka salama” akawaza Nawal Jenerali William akamuelezea Brenda kumpeleka Nawal katika chumba maalum cha mapumziko wakati yeye akiendelea na mazungumzo na wageni wake.Nawal hakwenda katika chumba cha mapumziko bali alielekea moja kwa moja chumbani kwake na kitu cha kwanza alichokifanya ni kuishika simu akampigia Ruby “Hallo Ruby ! akasema Nawal “Nawal kuna nini?Mbona unahema haraka haraka namna hiyo?Kuna tatizo? akauliza Ruby “Ruby wako hapa ! akasema Nawal “Akina nani Nawal?akauliza Ruby “Assad na Sattar wote wako hapa.Wamekuja na Jenerali William” akasema Nawal “Nawal una uhakika ni wenyewe? “Nimewashuhudia mimi mwenyewe kwa macho yangu.Wamefika muda si mrefu wakiwa wameongozana na Jenerali William” “Yale masanduku mawili aliyoshuka nayo Sattar ndegeni ambayo tunaamini yana kirusi yameletwa hapo?akauliza Ruby “Hapana Ruby kirusi hakipo hapa.Yawezekana kuna mahala kimehifadhiwa au yawezekana tayari kimekwisha pelekwa kusambazwa” akasema Nawal “Hapana bado hakijasambazwa kwani mtu pekee aliyeletwa kuja kusambaza kirusi hicho ni Sattar Sayf Al Din.Kama hayuko nacho hapo basi lazima kirusi hicho kimehifadhiwa sehemu Fulani wakisubiri muda ufike wakisambaze.Nawal usiku huu wa leo lazima tuhakikishe tunakipata kirusi hicho.Ni kufa na kupona leo lazima nyumba hiyo ivamiwe tuwachuku watu hao wote waliomo katika hiyo nyumba na watatuonyesha mahala kilipo kirusi.Nawal endelea kufuatilia watu hao kama wataondoka au watalala hapo wakati tunaandaa kikosi kwa ajili ya kuvamia nyumba hiyo.Kuanzia mchana wa leo tumekuwa tukiichunguza nyumba hiyo na kuona namna walivyojipanga kiulinzi.Makomando wetu wako tayari na muda utakapowadia watavamia nyumba hiyo.Nawal tunakutegemea sana uweze kuwasaidia timu ya makomando watakapofika hapo” akasema Ruby “Tayari nimekwisha yasoma mazingira ya hapa na ulinzi ulivyo hivyo hakuna tatizo nitasaidiana na timu itakayofika hapa” akasema Nawal na kumpa Ruby maelekezo kadhaa Mara tu alipomaliza kuzunguma na Nawal Ruby akampigia Gosu Gosu akamtaka afike ofisini kwake mara moja akamueleza kuhusiana na kile alichoelezwa na Nawal “Ruby mpaka hapo naamini tayari tumekwisha kipata kirusi.Usiku huu lazima tuwapate hawa magaidi wote pamoja na kirusi.Nitaongozana na makomando wetu watakaokwenda kuvamia nyumba hiyo” akasema Gosu Gosu “Hapana Gosu Gosu.Tuwaache makomando waende.Wewe utakuwa na kazi ya kuwahoji akina Assad kufahamu mahala kilipo kirusi pale watakapokuwa wameletwa hapa” akasema Ruby “Ruby kwa nini hutaki nishiriki katika misheni siku hizi? Kila ninapotaka kushiriki katika misheni unanizuia.You don’t trust me?akauliza Gosu Gosu “Si hivyo Gosu Gosu.Sitaki kuyaweka hatarini maisha yako wakati tayari tunacho kikosi kinachoweza kupambana .Kumbuka huko wanakoenda kunalindwa na wanajeshi wa Marekani ambao wana mafunzo ya hali ya juu hivyo itakuwa ni nusu vita.Naamini kikosi chetu cha makomando kina uwezo mkubwa sana wa kuweza kufanikisha misheni hii.Kama nilivyokuahidi kwamba wewe utafanya kazi ya kuwahoji akina assad watakapoletwa hapa” akasema Ruby “Ruby imekuaje ukabadili mawazo leo na unataka niwahoji magaidi?akauliza Gosu Gosu “Kwa namna yoyote ile tunahitaji kukipata kirusi hivyo basi kila aina ya mbinu lazima itumike wakati wa kuwahoji magaidi hao ili waweze kufunguka kirusi kiko wapi” “Sawa Ruby nitaifanya kazi hiyo” akasema Gosu Gosu kisha wakatoka kwenda kuanza maandalizi kwa ajili ya misheni ile
Kikosi cha makomando tisa wa SNSA kilikaribia kufika katika nyumba anakoishi mkuu wa vikosi vya wanajeshi wa Marekani walioko Tanzania.Wakati kikosi hicho kikiikaribia nyumba hiyo wenzao waliokuwa katika helkopta maalum wanayoitumia katika operesheni mbali mbali za usiku tayari walikwisha fika usawa wa ile nyumba na walikuwa wanasubiri kupewa taarifa kuwa kila kitu tayari ili helkopta iweze kushuka chini na kushusha kikosi cha makomando ambacho kitadhibiti eneo la juu la nyumba ile. Nawal ambaye alikuwa ndani ya ile nyumba akapewa taarifa kuhusu vikosi vile kuikaribia nyumba ile.Bado Jenerali William na akina Assad walikuwa wanaendelea na mazungumzo katika sebule ya chini. Nawal akatoka chumbani kwake taratibu akaenda jikoni ambako hakukuwa na mtu.Ni sauti za maongezi ya akina William ndizo zilisikika.Nawal akiwa na vifaa vyake katika begi akakata waya unaopeleka umeme katika jiko kubwa la kupikia halafu akafanya utundu wa kuunganisha nyaya na shoti kubwa ya umeme ikatokea iliyosababisha umeme kukatika ghafla jumba lote likawa giza.Haraka haraka akarejea chumbani kwake na kuwajulisha akina Ruby kwamba tayari umeme umekatika. Baada ya kupewa taarifa ya umeme kukatika,helkopta ya makomando ambayo inatumia teknolojia ya hali ya juu ambayo haina mlio ikaanza kushuka taratibu na ilipofika usawa Fulani makomando wakaanza kushuka kwa kutumia miavuli.Tayari walikuwa wanafahamu upande ule wa juu kulikuwa na wadunguaji sita.Kutokana na giza wadunguaji wale hawakuweza kuwaona makomando wa SNSA walipokuwa wakishuka na hawakuwa na wazo lolote la kuvamiwa.Waliendelea kuzungumza wakati wakisubiri umeme uwake. Makomando wa SNSA wote walikuwa wamevaa miwani ya kuwawezesha kuona sehemu za giza na waliweza kuwaona vizuri namna wadunguaji wale waliokuwa juu ya ile nyumba walivyokaa na baada ya kupewa amri risasi kama mvua zilitoka katika bunduki zao zilizofungwa viwambo vya kuzuia sauti.Kufumba na kufumbua wadunguaji wote walikuwa chini.Makomando wa SNSA wakatua taratibu na kulidhibiti eneo la juu la nyumba ile na kila mmoja akachukua nafasi yake.Baada ya kulidhibiti eneo la juu kazi iliyoifuata ni kuwasafishia njia kikosi cha chini ambao walikuwa mita chache kutoka katika jumba lile.Kwa msaada wa miwani ile waliyokuwa wameivaa ya kuona kwenye giza makomando waliokuwa wametawanyika katika sehemu ya juu ya ile nyumba wakajipanga tayari kwa ajili ya kuanza kuwaondoa wanajeshi waliokuwa wakilinda upande wa chini. Ndani ya nyumba bado zoezi la kufuatilia chanzo cha hitilafu iliyopelekea umeme kukatika liliendelea.Wanajeshi walikuwa wanapita chumba kimoja kimoja kuchunguza.Nawal akafungua mlango wa chumba chake akatoka na kuanza kushuka chini akakutana na wanajeshi wale waliokuwa wanafuatilia kujua chanzo cha hitilafu ile ya umeme.Wanajeshi wale wakamtaka radhi kwa hitilafu ile kutokea wakamuahidi kuwa ndani ya muda mfupi umeme utarejea. Nawal akapita sebuleni ambako Jenerali William na akina Assad walikuwa wanaendelea na maongezi.Walikuwa wanatumia taa maalum inayotumia betri “Chloe” akaita Jenerali William baaada ya kumuona Nawal akipita pale sebueleni “Kumetokea hitilafu ya umeme hapa ndani lakini tatizo hilo linashughulikiwa na muda si mrefu umeme utarejea” akasema Jenerali William “Nimeshindwa kukaa ndani kuna joto kali sana ngoja nipunge upepo hapo nje hadi umeme utakaporejea” akasema Nawal na kutoka nje akaenda kujibanza sehemu na kutuma ujumbe kwa Ruby akimjulisha kuwa Assad na Sattar bado wapo mle ndani akawahimiza kufanya hima kwani tayari wamekwisha anza kufuatilia kujua hitilafu ile ya umeme imetokea wapi. Mara tu baada ya Ruby kupokea ujumbe ule kutoka kwa Nawal,akampa taarifa mkuu makomando waliokuwa upande wa juu.Tayari kila komando alikuwa amelenga mwanajeshi na amri ikatolewa ya kuwafagia.Mvua ya risasi kutoka katika bunduki zilizofungwa viwambo vya sauti ikaanza kunyesha na baada ya sekunde kadhaa wanajeshi wote walikuwa wakilinda sehemu ya chini ya nyumba ile walikuwa chini.Bila kukawia kikosi cha makomando waliokuwa nje kikafika kwa haraka na kuvuka geti kisha wakachukua nafasi ili kuhakikisha hakuna hatari yoyote.Nawal akapewa maelekezo kwamba aende akaungane na kikosi kile cha makomando akawafuata na kujitambulisha kwao akawajulisha kuwa watu wanaowatafuta wapo sehemu ya chini ya nyumba ile.Makomando wale wakajipanga vyema na kuanza kusogelea mlango mkubwa wa kuingilia ndani huku wale waliokuwa upande wa juu wa nyumba ile wakishuka chini Wakati wakiendelea na maongezi Jenerali William akastushwa na mlio wa kitu akawataka akina Assad wanyamaze kimya “Kuna nini Jenerali?akauliza Assad na Jenerali William akamfanyia ishara ya kukaa kimya.Zilipita sekunde kadhaa Jenerali William akaupeleka mkono wake wa kulia kifuani kwake akabonyeza kidude katika redio yake ya mawasiliano na kuita “Charles ! Charles ! Unanisoma? Hakupata jibu lolote “Alpha ! Alpha unanisoma?akaita tena lakini hakujibiwa.Akasimama na kutoa bastora yake “Kuna kitu hakiko sawa hapa ! akasema akionekana kuwa na wasiwasi “Kuna nin……..” Assad akataka kuuliza lakini sauti kali ikawaamuru wasimame kama walivyo.Walivamiwa na watu waliokuwa wamefunika nyuso zao.Kwa kasi ya aina yake Assad akataka kuinyakua bastora yake iliyokuwa mezani lakini kabla mkono wake haujaifikia akapigwa risasi ya bega akaanguka chini.. “Wekeni silaha zenu chini taratibu” Sauti ikawaamuru Jenerali William na Sattar.Taratibu Jenerali William akaiweka bastora yake chini,Sattar naye akachomoa bastora yake na kuiweka chini wakainua mikono juu.Haraka haraka wakafungwa pingu na kupandishwa sehemu ya juu ya nyumba ile.Assad akapewa huduma ya haraka ya kuzuia damu kuvuja kwa wingi kisha naye akafungwa pingu na kupandishwa juu ambako tayari helkopta ilikuwa imetua akaingizwa katika helkopta pamoja na akina Sattar.Upekuzi uliendelea ndani ya nyumba ile na baada ya muda wanawake wawili waliokuwa wahudumu wakatolewa na kuingizwa katika helkopta kisha ikapaa na kuondoka. Ruby na makomando wengine wakaingia katika magari yao mawili na kuondoka eneo lile. “Hii ni moja ya operesheni tamu sana ambayo nimewahi kushiriki.Wanajeshi wale hawakujua kama wanaweza kuvamiwa hivyo hawakuwa wamejiandaa.Sifahamu Marekani watatoa tamko gani kesho asubuhi pale watakapokuta miili ya wanajeshi wao wakiwa wameuawa.Lakini haya yote ni malipo ya udhalimu wao.Usiku wa leo hakuna kulala hadi kirusi kipatikane.Haijalishi damu kiasi gani itamwagika lakini lazima kirusi kipatikane” akawaza Nawal akiwa garini wakielekea makao makuu ya SNSA.
Helikopta ilitua ofisi kuu za SNSA ,mtu wa kwanza kushushwa alikuwa Assad aliyekuwa amepigwa risasi ya bega akakimbizwa katika kitengo cha afya ili kupatiwa matibabu.Wakashushwa Jenerali William na Sattar wakiwa wamefungwa pingu na kufunikwa na mifuko vichwani Gosu Gosu akaelekeza wapelekwe katika chumba cha chini ya ardhi.Mwisho wakashushwa wale wahudumu wawili wakapelekwa katika chumba kingine “Ahsanteni sana kwa kazi nzuri” akasema Ruby baada ya kupewa taarifa ya namna operesheni ile ilivyokwenda “Makomando wameimaliza kazi yao sasa mpira umekuja kwetu” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu leo nakuachia uhuru fanya kila uwezalo kuwafungua hawa watu.Kipaumbele cha kwanza ni kujua mahala kilipo kirusi na baada ya hapo tutaendelea kuwahoji mambo mengine yanayohusiana na machafuko yaliyotokea lakini angalizo Gosu Gosu jitahidi kudhibiti hasira” akasema Ruby “Usihofu Ruby kabla ya mapambazuko lazima tuwe tumekipata kirusi” akasema Gosu Gosu na kumsubiri Nawal ili kazi ya kuwahoji watu wale waliokamatwa ianze mara moja. TEHRAN – IRAN Saa nne za usiku kwa saa za Iran,waziri wa ulinzi wa Iran brigedi Jenerali Ahsan Javad aliwasili katika makazi ya bilionea Vahid Ghorbani.Alipokewa na Vahid mwenyewe na kumkaribisha ndani.Vahid ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa na wanaoheshimika sana nchini Iran. “Karibu sana Ahsan” akasema Vahid “Nashukuru Vahid na samahani kwa kuchelewa kuja.Nilikuwa na mambo mengi sana siku ya leo” akasema Brigedia Jenerali Ahsan. “Usijali Ahsan.Ninafahamu majukumu yako mengi” akasema Vahid na baada ya maongezi mafupi ya utangulizi Ahsan akasema “Vahid nimepita kwako mara moja kukusikilza kama ulivyoniomba.Nikitoka hapa kuna sehemu ninaelekea hivyo sintachukua muda mrefu hapa kwako” akasema Ahsan “Ahsan nimekuita hapa ninahitaji msaada wako” “Unahitaji nikusaidie nini Vahid? “Kuna raia wetu waliokuwa wamepotea wamerejea leo” akasema Vahid “Ndiyo wamerejea leo.Umekuwa ni kama mujiza kwetu kwani tayari tulikwisha hisi wameuawa.Hatukuwa na tegemeo la kuwaona tena wakiwa hai.Tumefurahi sana kuwaona tena ndugu zetu wale” akasema Ahsan “Kuna mtu mmoja alikuwa ameongozana nao ambaye si raia wa Iran anaitwa Abu Zal…….” akasema Vahidi lakini Ahsan akamkatisha “Abu Zalawi.Kwa taarifa tuliyoipata ni raia wa Saudi Arabia na anajishughulisha na ugaidi.Abu Zalawi ndiye aliyelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam siku chache zilizopita” akasema Ahsan na kumstua sana Vahid “Ni gaidi?! Vahid akauliza kwa mshangao “Ndiyo ni gaidi ! “Hii inashangaza”akasema Vahid “Ni jambo linalomshangaza kila mtu lakini tutawafanyia mahojiano na kujua nini hasa kimetokea hadi watu wetu wakajikuta wakiwa na huyu gaidi” akasema “Nini mipango yenu kuhusiana na huyu mtu?Hamuoni kama anaweza kuongeza matatizo na Marekani endapo wakifahamu kuwa mtu aliyelipua ubalozi wake yuko hapa nchini kwetu? Akauliza Vahid “Kwa sasa ni mapema sana kusema chochote kuhusu huyu mtu hadi pale tutakapowahoji watu wetu na kufahamu kwa undani nini hasa kilichotokea na imekuaje wakajikuta wakiwa na huyu gaidi.Baada ya hapo tutafanya maamuzi” akasema Ahsan na ukimya mfupi ukapita “Mbona umeuliza kuhusu huyu jamaa? Akauliza Ahsan “Ahsan kuna jambo nataka kuliomba.Yawezekana ni jambo kubwa na hukulitegemea lakini nakuomba unisaidie” “Sema unachohitaji Vahdi nitakusaidia,wewe ni zaidi ya rafiki” akasema Ahsan “Ninataka kuonana na Abu Zalawi” akasema Vahid na mstuko mkubwa ukaonekana usoni kwa Ahsan “Unataka kuonana na Abu Zalawi? Akauliza Ahsan akiwa bado anashangaa.Hakutegemea kama Vahid angeweza kumuomba kitu kama kile “Ndiyo Ahsan ninataka kuonana na Abu Zalawi” Ahsan akavuta pumzi ndefu na kuuliza “Vahid mimi nawe tumefahamiana muda mrefu sana toka tukiwa vijana wadogo masomoni na tumeendelea kuwa marafiki wakubwa hata sasa.Nini sababu ya kutaka kuonana na huyu mtu? Naomba unieleze bila kunificha tafadhali” akasema Ahsan “Nilikueleza kuhusiana na kifo cha mwanangu Najma” “Ndiyo ulinieleza” “Kuna jambo ambalo sikuwa nikilifahamu kuhusiana na Najma ambalo nimelifahamu leo hii” akasema Vahid na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Najma alikuwa ameolewa lakini alifanya siri hakutaka nifahamu” “Alikuwa ameolewa? “Ndiyo lakini kwa siri na hakutaka nifahamu.Kwa mujibu wa mama yake alitaka kunipa taarifa hizo yeye mwenyewe lakini hakufanya hivyo hadi mauti yalipomkuta.Kwa bahati mbaya aliyekuwa mume wake ni Abu Zalawi” “Abu Zalawi?! Ahsan akazidi kushangaa “Ndiyo.Nimeambiwa kwamba ndiye aliyekuwa mume wa Najma” “Najma ametoka wapi na huyu gaidi? Binti yako alikuwa ni msomi mzuri na mwenye sura ya kimalaika inawezekanaje hadi akajikuta akiingia katika mahusiano na huyu jamaa?akauliza Ahsan “Ahsan hata mimi sifahamu nini kilitokea lakini nilichoelezwa ni hicho kwamba aliolewa na Abu Zalawi” akasema Vahid “Vahid yawezekana si Abu Zalawi huyu gaidi.Yawezekana kuna Abu Zalawi mwingine” akasema Ahsan “Ahsan ninaomba msaada wako niweze kuonana na huyu Abu Zalawi na kuzungumza naye japo kwa dakika tano tu ili niweze kupata uhakika kama kweli ni yeye aliyemuoa mwanangu Najma” akasema Vahid “Sawa nitakusaidia Vahid.Nilikueleza kuwa nikitoka hapa ninaelekea sehemu Fulani.Ninakwenda kuwatembelea mashujaa wetu waliorejea leo kujua maendeleo yao na kwa kuwa umeniomba basi baada ya kutoka hapo hospitali tutaelekea mahala alikopelekwa Abu Zalawi ukaonane naye” akasema Ahsan.Hakukuwa na muda wa kupoteza wakaingia katika gari la Ahsan na kuondoka kuelekea hospitali.
Saa tano za usiku waziri wa ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahsan Javad aliwasili katika hospitali ya jeshi walikopelekwa Yasser Wazir na wenzake baada ya kurejea nyumbani wakitokea mahala kusikojulikana.Mpaka muda huu hawakuwa wamehojiwa chochote kuhusiana na mahala walikokuwa kwa muda wote waliokuwa wamepotea.Brigedia Jenerali Ahsan Javad hakuwa peke yake alikuwa ameongozana na Sassan Mahmoud anayeongoza wizara ya ujasusi ya Iran MOIS na vile vile alikuwa na Vahid Ghorbani mfanyabiasha mkubwa nchini Iran na rafiki yake wa karibu. Waliwatembelea na kukagua maendeleo ya akina Yasser na kujiridhisha kuwa wanapatiwa huduma ya afya ya hali ya juu.Baada ya hapo wakaondoka kuelekea mahala alikopelekwa Abu Zalawi.Baada ya mwendo wa dakika kadhaa wakafika katika nyumba moja kubwa yenye ulinzi mkali inayotumiwa na MOIS kwa shughuli zake na kubwa zaidi ikiwa ni kuhifadhi watu mbali mbali wanaohojiwa na idara hiyo. Geti la nyumba likafunguliwa magari yakaingia,milango ikafunguliwa haraka haraka na msimamizi mkuu wa nyumba ile akatoka kuja kuwapokea wageni akawakaribisha ndani “Anaendeleaje mgeni wetu? Akauliza Sassan Mahmoud mkuu wa MOIS “Anaendelea vizuri.Kabla ya kumleta hapa tulimpeleka kwanza katika hospitali yetu akaangaliwa afya yake na kupatiwa matibabu ndipo tukamleta hapa.Anaendelea vizuri” akasema Yule msimamizi wa ile nyumba kisha Ahsan akamtaka Sassan wazungumze pembeni.Baada ya mazungumzo yaliyochukua dakika zipatazo tano Sassan akamtaka Yule msimamizi wa ile nyumba kuzima kamera zote kwa muda halafu akamtaka awapeleke katika chumba alimowekwa Abu Zalawi.Mlango wa chumba ukafunguliwa wakaingia ndani na kumkuta Mathew akiwa amejilaza kitandani akiwa amefungwa bandeji sehemu mbali mbali za mwili wake zilizokuwa na vidonda.Mathew hakuwa na wasiwasi hata chembe akainua kichwa chake akawatazama watu wale waliokuwa wanamtazama kwa woga “Abu Zalawi unaendeleaje?akauliza Ahsan “Ninaendelea vizuri” akajibu Mathew “Karibu sana Iran.Mimi naitwa Brigedia Jenerali Ahsan Javad waziri wa ulinzi wa Iran.Nimekuja kukutazama kujua maendeleo yako” “Ahsante mheshimiwa waziri ninaendelea vyema” “Sawa Abu ninashukuru kama unaendelea vyema.Mimi nawe tutakuta tena pale afya yako itakapokuwa imekaa vizuri.Kwa sasa endelea kupumzika na ninakuhakikishia uko salama hivyo siwe na hofu yoyote” akasema Ahsan “Nashukuru sana mheshimiwa waziri” akasema Mathew “Kabla sijaondoka kuna mtu ambaye anahitaji kuonana nawe” akasema Ahsan na Vahid akaitwa mle chumbani.Watu wote wakatoka na kuufunga mlango akabaki Mathew na Vahid. “Karibu” akasema Mathew akimshangaa Vahid namna alivyokuwa akimtazama “Abu Zalawi” akasema Vahid kwa sauti ndogo “Ndiyo ni mimi karibu.Wewe ni nani? Akauliza Mathew ambaye aliinuka na kukaa kitandani “Naitwa Vahid Ghorbani” “Karibu Ghorbani.Nikusaidie nini? Akauliza Mathew.Vahid akatoa simu na kuzitafuta namba za Habiba akapiga “Kabla sijazungumza nawe chochote kuna mtu ambaye unatakiwa uzungumze naye simuni” akasema Vahid na kumpatia Mathew ile simu “Hallow” ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili sauti ambayo haikuwa ngeni masikioni mwa Mathew “Hallow” akasema Mathew “Mathew Mulumbi.Nimefurahi tena kuisikia sauti yako.Unazungumza na Habiba” akasema Habiba Jawad akitumia lugha ya kiswahili “Mama Habiba.! Akasema Mathew naye akishangaa “Mathew sina muda mwingi wa kuzungumza nawe.Kuna jambo ambalo nataka nikufahamishe” akasema Habiba “Nakusikiliza mama” “G2o tayari wamefahamu kila kitu kuhusu wewe kuwa si gaidi bali ni jasusi” akasema Habiba na Mathew akastuka sana “wamefahamuje?akauliza Mathew “Wamepata taarifa zote kutoka Mossad” “Bastard ! akasema Mathew kwa hasira “Usihofu Mathew japokuwa wamefahamu kila kitu kuhusu wewe lakini kila kitu kinaendelea kama kawaida.Misheni yako inaendelea kama kawaida kwani tayari ndani ya G20 wamekwisha gawanyika.” akasema Habiba na kumueleza Mathew kila kitu kinachoendelea “Kwa hiyo Mathew nimekupigia kukupa tahadhari kuhusiana na mpango huu wa kukuua kwa kuwatumia majasusi wa Mossad” akasema Habiba “Mama nakushukuru sana kwa kunipa tahadhari kuhusiana na mpango huo wa kuniua.Ninakuahidi sintaishia njiani nitahakikisha ninalimaliza hili kundi la G20” “Nakutakia kila la heri Mathew.Kila nitakapokuwa nikipata taarifa zozote nitajitahidi nikufikishie lakini ukiona kimya kwa muda wa wiki moja kuanzia sasa ujue tayari nimekwisha kufa” “Mama Habiba tafadhali endel……….” “Kwa heri Mathew.Kuwa makini” akasema Habiba na kukata simu. “Tayari umeupata ujumbe wako? Akauliza Vahid “Ndiyo nimeupata ninashukuru sana” akasema Mathew na kumrejeshea Vahid simu yake “Abu Zalawi nimepewa muda mfupi wa kuzungumza nawe.Naamini mimi hunifahamu na hujawahi kuniona” “Ni kweli sikufahamu” akasema Mathew “Mimi ni…………..” akasema Vahid na kusita “Karibu Iran Abu Zalawi” akasema Vahid na kugonga mlango ukafunguliwa Mathew akabaki anashangaa “Alitaka kunieleza nini huyu jamaa halafu akasita?akajiuliza Mathew na kuinuka akaketi kitandani. “Kazi imekuwa kubwa zaidi ya nilivyodhani.Kama hawa jamaa tayari wamekwisha nifahamu mimi ni nani na wanataka kuniua natakiwa kutumia akili kubwa ili waweze kuniamini tena.Kwa namna yoyote ile lazima nirejee tena Marekani kumaliza kazi niliyoianza.Siwezi kuishia njiani lazima nifike mwisho na kukifutilia mbali kikundi cha G20.Namshukuru Habiba kwa kunipa taarifa za mpango wao wa kutaka kuniua.Nina wasiwasi sana kama wakati nitakapomaliza misheni yangu Habiba ataendelea kuwa hai kwani hawa jamaa tayari wanadai amewasaliti.Naomba Mungu amsaidie huyu mama awe hai na ashuhudie kwa macho yake namna kundi la G20 linavyosambaratishwa” akawaza Mathew “Kama wanataka kuniua mimi na kusitisha ile misheni waliyonituma,ninapata picha kwamba hata wale jamaa niliowaokoa watakuwa mashakani.Naamini nao pia watakuwa katika mpango wa kuuawa ili isijulikane kama walikuwa wametekwa na Marekani.Lazima niwasadie kwani wale ndio kinga yangu” akawaza Mathew Baada ya kutoka katika chumba cha Mathew,Vahid alipelekwa katika gari ambako Brigedia Jenerali Ahsan alikuwa anamsubiri,kisha wakaondoka “Nimeshindwa kumwambia Abu Zalawi kuwa mimi ndiye baba yake Najma.Nimejikuta nikimuonea huruma ghafla Yule kijana baada ya kumuona namna mwili wake ulivyo na vidonda vingi.Kwa nini kijana Yule akaamua kujiingiza katika masuala ya ugaidi.Kwa nini Mossad wanataka kumuua?Ninahitaji kupata tena wasaa mwingine nizungumze naye kwa kirefu zaidi” akawaza Vahid wakiwa garini baada ya kuondoka mahala alikopelekwa Mathew Wakati Ahsan na Vahid wakiondoka katika nyumba alikopelekwa Mathew,katika moja ya mtaa jijini Tehran watu watatu walikuwa wamekaa juu ya nyumba Fulani wakizungumza.Wawili miongoni mwa watu hao walikuwa majasusi kutoka Mossad walioko jijini Tehran “Nawaahidi hadi kufika kesho mchana tayari nitakuwa nimepata taarifa za mahala alipo Abu Zalawi pamoja na wale raia wengine waliokuwa wamepotea” akasema Zana Behnam ambaye anafanya kazi katika wizara ya ujasusi na usalama wa taifa ya Iran. “Tunashukuru Zana.Tunaamini hautatuangusha” akasema Avner jasusi kutoka Mossad “Siwezi kuwaangusha.Mimi nanyi tumekwisha shirikiana katika mambo mengi” akasema Zana.Avner akatoa bahasha kutoka katika mfuko wa koti na kumpatia Zana “Hiki ni nusu ya kiasi cha fedha ulichokihitaji kwa ajili ya kazi hii.Pale utakapokuwa umekamilisha jukumu lako basi utamaliziwa kiasi kilichobaki” akasema Avner na bila kuhesabu Zana akaiweka bahasha mfukoni wakaagana DAR ES SALAAM – TANZANIA “Nawal hongera sana umefanya kazi nzuri” akasema Ruby baada ya Nawal kuwasili na gari la makomando “Ahsante Ruby lakini tutapata muda wa kuzungumza na kupongezana hapo baadae kwa sasa tunatakiwa kuitumia vyema kila dakika tuliyonayo kabla ya mapambazuko ili kufahamu mahala kilipo kirusi na kukichukua kwani ikifika asubuhi itagundulika kile tulichokifanya na yawezekana tusikipate tena kirusi hicho hivyo kufa au kupona lazima usiku huu kirusi kipatikane.Tunao watu wanaofahamu mahala kirusi kilipo hivyo hakuna kuwaonea huruma lazima tutumie kila mbinu hadi waonyeshe walipokificha kirusi hicho” akasema Nawal na mkuu wa kikosi cha makomando akatokea na kumkabidhi Ruby vazi Fulani “Hili ni moja ya vazi tumelikuta katika nyumba ile baada ya kufanya upekuzi.Yapo mengine kumi na sita na vazi hili ni maalum kwa ajili ya kujikinga na hewa ya sumu au maambukizi ya virusi”akasema “Washenzi hawa walikwisha jiandaa kujikinga na virusi wakati sisi tukiteketea” akasema Ruby “Mtu wa kwanza kumuhoji ambaye anafahamu kilipo kirusi ni Jenerali William.Huyu nitamuhoji mimi mwenyewe” akasema Gosu Gosu kisha maandalizi kwa ajili ya kuanza kumuhoji Jenerali William yakaanza.Maandalizi yalipokamilika Jenerali William akaingizwa katika chumba maalum kwa ajili ya mahojiano.Gosu Gosu Ruby na Nawal walimtazama katika kioo kikubwa wakiwa katika chumba kingine .Gosu Gosu akavuta pumzi ndefu na kutoka ndani ya kile chumba akaingia katka chumba cha mahojiano akavuta kiti na kuketi “Habari yako Jenerali William” akasema Gosu Gosu lakini Jenerali William hakujibu kitu akamtazama Gosu Gosu kwa macho ya dharau “Naitwa Papi G0su Gosu,ni mwanajeshi.Kwa miaka zaidi ya ishrini nimeishi msituni nikipigana vita hivyo nataka tuzungumze kama wanajeshi” akasema Gosu Gosu na Jenerali William akacheka kidogo “Nini maana ya mchezo huu mlioufanya?akauliza Janerali William “Huu ni mchezo wa kijinga sana mmeufanya.Sisi tuko hapa kwa ajili ya kuwasaidia kutafuta amani katika nchi yenu halafu ninyi mnatufanyia hivi ! Ninawahakikishia kwamba hiki mlichokifanya kitakuwa na athari kubwa sana kwenu.Hamtabaki salama hata kidogo ! akasema Jenerali William “Huna hata aibu ya kusema mmekuja kutusaidia ! Akasema Gosu Gosu akionekana kuanza kupandwa na hasira “Ndiyo tumekuja kukusaidieni kutafuta amani baada ya kuanza kuuana wenyewe kwa wenyewe lakini malipo yake ndiyo haya.Mnafanya jambo bay asana kuteka na kuua walinda amani ! akafoka Jenerali William “Jenerali William sisi si watoto wadogo wa kushindwa kutambua mambo.Karibu vurugu nyingi zinazotokea barani Afrika nchi zilizoendelea zina mkono wake.Mnatengeneza machafuko kwa malengo mnayoyajua wenyewe halafu mnaleta vikosi vyenu mkijidai mnakuja kutusaidia kutafuta amani kumbe mna ajenda zenu za siri.Tunafahamu kila kitu mnachokifanya Afrika na sasa mwisho wenu umefika ! akasema Gosu Gosu “Sisi hatuna sababu yoyote ya kuleta machafuko kwa bara masikioni kama hili.Sisi ni taifa kubwa lenye uchumi mkubwa kuliko yote duniani.Ni taifa lenye nguvu kubwa kijeshi kuliko yote duniani kwa nini tusumbuke na watu masikini kama waafrika? Hizo ni dhana potofu mnazojenga kwamba vikosi vya Marekani au nchi nyingine kubwa vikija kulinda amani Afrika vinakuwa na ajenda zao za siri wakati si kweli.Sisi ni taifa linaloheshimu haki za binadamu na hatuko tayari kuona haki za binadamu zikivunjwa na watu kuuawa ndiyo maana tuko mstari wa mbele katika kuhakikisha tunapeleka vikosi vyetu haraka sana sehemu yoyote ile ambako kuna kuwa na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.Tazama hivi majuzi vurugu zilizotokea hapa nchini kwenu mkaanza kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya dini hivyo kwa sababu ya dini,tumeleta vikosi vyetu kuja kuwasaidia kutafuta amani ! “Mwongo mkubwa wewe ! akasema Gosu Gosu kwa ukali huku akigonga meza “Nilikwambia tunafahamu kila kitu mlichokifanya na mipango yenu yote tunaifahamu hivyo usijaribu kunidanganya.Unadhani hatujui mnachokifanya kule Tanga? Tunafahamu namna mnavyopora tani na tani za mafuta ya kutoka Uganda.Tunafahamu machafuko haya yote yaliyotokea mmeyatengeneza ninyi kwa ajili ya kujipatia mafuta.Tunafahamu kila kitu Jenerali na msituone tuko kimya mkajua kuwa hatufahamu chochote ! akasema Gosu Gosu kwa ukali “Hiki ni kichekesho wewe kijana.Marekani haina haja ya kuja kuchukua mafuta huku Afrika.Tuna akiba kubwa ya mafuta na tunaendelea kutengeneza mafuta ya kutosha kutoka katika mimea na tumewekeza sana katika teknolojia rahisi ya kutengeneza magari na mitambo isiyotumia mafuta mengi hivyo basi hatuna haja na mafuta machafu kutoka Uganda ! akasema Jenerali William kwa dharau “Gosu Gosu kompyuta yetu inatuonyesha William amepatwa na mstuko mkubwa ulipomtajia suala hilo la kuchukua mafuta kule Tanga.Endelea kukazia hapo hapo ! Ruby akamjulisha Gosu Gosu kupitia kifaa alichokuwa amekivaa sikioni. “Tunafahamu kila kitu Jenerali William kuhusiana na mipango yenu yote mnayoipanga na magaidi wa IS.Bado muda kidogo tu dunia yote itafahamu kila kitu ambacho kinafanywa na taifa lako kwa siri.Itakuwa ni aibu kubwa kwa taifa kubwa kama Marekani pale tutakapoitangazia dunia namna inavyozinyonya nchi masikini ! akasema Gosu Gosu na Jenerali William akaonekana kupandwa na hasira “Huo ni upumbavu mkubwa ! akahamaki Jenerali William “Marekani haiwezi kushirikiana na magaidi wa IS au kikundi chochote cha kigaidi.Tumekuwa mstari wa mbele katika kupambana ugaidi duniani na katu hatuwezi kushirikiana nao.Hiki unachokitamka ni kitu cha kijinga sana ! akasema kwa ukali Jenerali William huku akijaribu kuitikisa mikono yake lakini ilikuwa imefungwa barabara kwa pingu zilizo katika kiti kile maalum. Gosu Gosu akalifungua faili akatoa picha ya Assad Ismail “Unamfahamu huyu? Akauliza Gosu Gosu “Wewe kijana una upungufu wa akili,maswali gani hayo unaniuliza? “Jenerali William hapa hauna nguvu ya kufanya chochote,tafadhali jibu kile unachoulizwa kwa ufasaha” akasema Gosu Gosu “Kwa nini mmenileta hapa ninyi watu wenye akili finyu? Akafoka Jenerali William “Sisi tuna akili finyu? Leo utafahamu watu wenye akili finyu ni watu wa aina gani ! akasema Gosu Gosu “Unamfahamu huyu mtu pichani? Gosu Gosu akauliza “Simfahamu mtu huyu ! akajibu Jenerali William “Hujawahi kumuona sehemu yoyote? Akauliza Gosu Gosu “Nimekwambia sijawahi kumuona na simfahamu ! akajibu Jenerali William “Kama humfahamu ninakufahamisha kuwa huyu anaitwa Assad Ismail ni kiongozi wa kundi la kigaidi la IS ambaye ndiye mnayemtumia katika kuchochea vurugu za kidini hapa nchini.Yeye na kundi lake ndio wanaofanya mauaji ya viongozi wa dini na kushambulia nyumba za ibada ili kujenga chuki miongoni mwa waumini na kusababisha washambuliane na kuuana” akasema Gosu Gosu na sura ya Jenerali William ikabadilika.Gosu Gosu hakumjali akatoa picha nyingine “Nafahamu hata nikikuuliza huyu ni nani utakana kumfahamu lakini huyu anaitwa Sattar Sayf Al Din.Naye vile vile ni mfuasi wa IS” akasema Gosu Gosu.Jenerali William alikosa maneno ya kuongea akabaki anaikodolea macho picha ile.Gosu Gosu akatoa picha nyingine akaiweka mezani. “Picha hii ni ya mchana wa leo.Hapa ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam ambapo Sattar aliwasili akitumia ndege aina ya Gulfstream G650ER na ndege hii hutumiwa na shirika la ujasusi la Marekani CIA” akasema Gosu Gosu na kumtazama Jenerali William ambaye macho yake aliyaelekeza katika ile picha mezani.Gosu Gosu akatoa picha nyingine “Hapa Sattar akishuka ndegeni akiwa ameongozana na wanajeshi wa Marekani.Ukiitazama picha hii Sattar ana masanduku mawili.Tunafahamu masanduku haya mawili yana kirusi ndani yake ambacho Sattar amekuja kukisambaza hapa Tanzania” “Sielewi unachokizungumza wewe kijana ! akafoka Jenerali William “Utanielewa tu Jenerali William” akasema Gosu Gosu “Marekani baada ya kufanikiwa katika mpango wake wa kuchukua mafuta ya Uganda kupitia bandari ya Tanga wana hofu kwamba amani itarejea muda si mrefu na vikosi vya Marekani havitahitajika tena kuwepo hapa Tanzania hivyo zoezi la uchukuaji wa mafuta litakoma.Mmetafuta namna ya kuviwezesha vikosi vyenu kuendelea kuwepo hapa nchini kwa muda mrefu zaidi na mmekuja na mpango wa kusambaza kirusi hatari cha maangamizi hapa Tanzania ili muweze kuongeza vikosi zaidi.Jenerali William sisi tuna akili finyu kama ulivyosema lakini tunafahamu kila kitu kuhusiana na mipango yenu na ninakuhakikishia kwamba mipango yenu haitaweza kufanikiwa” akasema Gosu Gosu “Huu ni upuuzi uliopitiliza ! akafoka Jenerali William “Jenerali William kuna kitu kimoja tu ambacho ninataka kufahamu kutoka kwako ambacho ndicho kitakachokutoa salama humu ndani.Nataka kujua kirusi hiki alichokuja nacho Sattar kiko wapi? Akauliza Gosu Gosu na kumtazama Jenerali William “Gosu Gosu usimuulize tena swali lingine muache kwanza atafakari njoo huku” Ruby akamwambia Gosu Gosu ambaye aliinuka “Ninakuacha utafakari baada ya muda nitarejea tuendelee na mazungumzo yetu.Nakupa angalizo Jenerali William mimi ni mtu mbaya mno na usiombe uingie katika anga zangu ! Nitarejea baada ya muda mfupi ! akasema Gosu Gosu na kuchukua faili lake akatoka ndani ya kile chumba akaingia katika chmba walichokuwamo akina Ruby “Umemuanza vizuri na kompyuta yetu hapa inatuonyesha kwamba amepatwa na mstuko mkubwa.Hakutegemea kama tungefahamu mipango yao ya siri.Pamoja na hayo kuna jambo lingine ambalo tumelipata.Tumeifahamu familia yake.Ana watoto wawili wa kike ambao majina yao ni Cynthia na Lisa.Vile vile ana mke anaitwa Deborah” akasema Ruby na kumpatia Gosu Gosu picha za familia ya Jenerali William “Hii familia yake ni silaha ya mwisho ambayo tutaitumia katika kumfanya Jenerali William afunguke endapo njia nyingine za kumfungua zitashindikana.Kabla ya kurejea kumuhoji Jenerali William tutamuhoji kwanza Sattar na zoezi hili mtalifanya wewe na Nawal.Wakati mkiendelea kumuhoji Sattar tutaendelea kumtesa Jenerali William kwa kufungua muziki mkubwa” akasema Ruby na bila kupoteza muda Nawal na Gosu Gosu wakaenda katika chumba kingine cha mahojiano alimo Sattar.Nawal akavuta kiti akaketi Gosu Gosu akasimama pembeni “Sattar Sayf Al Din ndilo jina lako? Akauliza Nawal lakini Sattar hakujibu kitu.Gosu Gosu ambaye mikono yake ilikuwa myepesi akakishika kichwa cha Sattar na kukigongesha katika meza mara mbili “Ukiulizwa kitu unajibu haraka ! akafoka Gosu Gosu “Nakuuliza tena jina lako ni Sattar Seyf Al Din? Akauliza Nawal “Ndiyo.Naitwa Sattar Sayf Al Din” “Umetokea nchi gani? “Mimi ni raia wa Syria” “Umeingia Tanzania ukitokea Syria?akauliza Nawal “Hapana nimetokea Marekani” “Umekuja kufanya nini Tanzania? Akauliza Nawal na Sattar akawa kimya “Nakuuliza Sattar Tanzania umekuja kufanya nini? akauliza tena Nawal lakini Sattar hakujibu “Nawal hatuna muda wa kupoteza na hawa watu ! akasema Gosu Gosu na kwenda katika meza iliyokuwa na vifaa mbali mbali akachukua vifaa kadhaa na kumfuata Sattar.Nawal naye akasimama na kumsogelea Sattar “Sattar nakuuliza kwa mara ya mwisho umekuja kutafuta nini Tanzania? Akauliza Nawal lakini Sattar aliendelea kuwa kimya.Gosu Gosu hakumkawiza akamnasa kofi zito lililomfanya Sattar aone nyota nyota halafu Nawal akakikamata kichwa chake akakigandamiza katika kiti Gosu Gosu akaupanua mdomo na kuingiza kifaa mdomoni na kulishika jino moja akaling’oa kwa nguvu damu zikaaza kumwagika huku Sattar akipiga makelele kwa maumivu makali aliyoyapata. “Leo tutaelewana ! akasema Gosu Gosu “Sattar nakuuliza umekuja kufanya nini Tanzania? Nataka ujibu ama sivyo mateso haya yataendelea na tutakuondoa kiungo kimoja kimoja ! akasema Nawal lakini Sattar aliendelea kupiga kelele.Nawal akamfanyia ishara Gosu Gosu wakamkamata tena na kuondoa jino lingine Sattar akapoteza fahamu. “Ruby tunaomba watu wa afya waje haraka humu ndani wamuhudumie huyu mtu atakapozinduka zoezi litaendelea.Wakati tunamsubiri tunarejea kwa Jenerali William” akasema Gosu Gosu kisha wakatoka ndani ya kile chumba wakaelekea katika chumba alimo Jenerali William.Mara tu Gosu Gosu alipoingia mle ndani muziki ukazimwa.Macho ya Jenerali William yalikuwa yanatoa machozi “Kwa nini mnanifanyia hivi?Nawaambia mmekosea sana kunifanyia haya” akasema Jenerali William “Huu ni mwanzo tu Jenerali William bado mengi yanakuja.Marekani mlikuwa mkiwakamata watuhumiwa wa ugaidi na kuwapeleka katika gereza la Guantanamo kuwatesa na leo umefika katika Guantanamo ya Afrika.Utakutana na mateso kama mliyokuwa mkiwatesa wale magaidi hadi pale utakapofunguka na kusema ukweli” akasema Gosu Gosu “Nani amewatuma mnifanyie haya? Hiki unachokifanya wewe kijana kitakuwa na athari kubwa sana kwa nchi yako ! akasema Jenerali William “William tunaanzia pale tulipoishia katika awamu ya kwanza.Ninataka kufahamu kirusi alichokuja nacho Sattar Sayf Al Din kiko wapi? Akauliza Gosu Gosu “Wewe kijana nimekwisha kwambia una akili pungufu.Sifahamu una maanisha nini unapozungumzia kirusi ! akafoka Jenerali William “Sattar Al Din ambaye hadi usiku huu ulikuwa naye katika makazi yako ameleta hapa nchini kirusi kwa lengo la kukisambaza.Nataka kufahamu kilipo kirusi hicho” akasema Gosu Gosu “Sifahamu chochote kuhusiana na kirusi hicho unachokizungumzia” akasema Jenerali William “Jenerali nitazame vizuri nimechafuka damu.Nimetoka kumuhoji Sattar Sayf Al Din ambaye ameleta kirusi hapa nchini na amekiri kukukabidhi wewe kirusi hicho.Nataka uniambie kilipo kirusi hicho” akasema Gosu Gosu “Sikuelewi unachokiongea wewe kijana.Tafadhali naomba mnifungue haraka sana kabla ya vikosi vya Marekani havijavamia mahala hapa ! akafoka Jenerali William “Hakuna kikosi chochote kitakachothubutu kufika mahala hapa na hawatafahamu kamwe kama uko hapa hivyo juhudi za kutoka hapa ni zako wewe mwenyewe.Ninakuhakikishia William kirusi tutakipata na tutakwenda kukisambaza Marekani” akasema Gosu Gosu na kufungua faili lake akatoa picha ya mke wa Jenerali William akaiweka mezani “Mkeo Deborah” akasema Gosu Gosu na kutoa picha za watoto wa William akaziweka mezani “Hiyo ni familia yako ambayo nina uhakika unaipenda kuliko kitu chochote.Utajisikiaje pale utakaposikia kuwa wameathiriwa na kirusi hiki ambacho mmekileta mkisambaze hapa Tanzania? Watoto hawa wadogo watapoteza maisha na watakufa kifo chenye mateso makali.Hebu fikiria mwanamke mrembo kama huyu Debor…………….” Akasema Gosu Gosu lakini Jenerali William akatoa ukelele wa hasira “Aaagghhhh !! akapiga kelele Jenerali William huku akijitikisa katika kiti akijaribu kutaka kuking’oa lakini kilikuwa kiti imara “Ninasema waacheni familia yangu katika hili ! akafoka Jenerali William “Ninarudia tena kukuhakikishia Jenerali William kwamba tutakipata kirusi na baada ya kukipata tutakirejesha Marekani ambako tutakisambaza na tunaanzia katika familia yako na ukumbuke kwamba kirusi hiki hakina tiba wala kinga.Lakini usihofu nitakupa simu utazungumza nao na kuwaaga pale watakapokuwa wameanza kuumwa” akasema Gosu Gosu “Nitakuua ! Nitakuua mkiigusa familia yangu ! akafoka Jenerali William “Huwezi kufanya chochote Jenerali William.Kitu pekee ambacho kinaweza kukusaidia ni kutuonyesha mahala kilipo kirusi hicho ili kujiokoa wewe na familia yako ! akasema Gosu Gosu na Jenerali William akabaki kimya “Jenerali William hakuna faida yoyote kuendelea kuficha kirusi hicho.Tuonyeshe mahala kilipo tutakichukua na kukihifadhi sehemu salama.Hakuna atakayefahamu kuhusu mpango huo na nchi zetu zitaendelea kuwa salama” akasema Gosu Gosu “Sifahamu chochote kuhusu hicho kirusi unachokizungumzia.Wewe ni mwanajeshi wa aina gani ambaye unashindwa kunielewa?Nitazame macho yangu kama ninakudanganya ! akafoka Jenerali William “Gosu Gosu,Sattar amezinduka” Ruby akamfahamisha Gosu Gosu “Ninakuja baada ya muda mfupi na safari hii utanielewa mimi ni mwanajeshi wa namna gani ! akasema Gosu Gosu na kutoka akaingia katika chumba walimo akina Rubyhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Gosu Gosu inakuaje unashindwa kutumia nguvu kumfungua huyu jamaa?Muda unatukimbia na tunatakiwa hadi mapambazuko tuwe tumekwisha kipata kirusi” akasema Nawal “Huyu mtu ni mwanajeshi na si kazi nyepesi kumfungua mwanajeshi lakini nawaahidi nitakaporejea tena anakwenda kueleza ukweli” akasema Gosu Gosu halafu akaongozana na Nawal wakaelekea katika chumba alimo Sattar.Tayari alikwisha rejewa na fahamu na alikuwa amefungwa katika kiti.Baada ya kuingia wale watu wa kitengo cha afya wakatoka wakawaachia uwanja akina Gosu Gosu. “Sattar tumerejea tena. Nakuhakikishia leo utapoteza fahamu hata mara kumi hadi utakapoamua kufunguka na kutueleza ukweli.Tumekuondoa meno mawili tutaendelea kuyaondoa moja baada ya lingine na kama bado utakuwa kimya tutaendelea na viungo vingine.Ili mambo haya yasiendelee tueleze kweli tafadhali ! akasema Nawal.Sattar mdomo wake ulikuwa umevimba na bado alionekana kuwa katika maumivu makali.Gosu Gosu akaenda kuchukua vifaa vile vya kung’olea meno akaviweka mezani.Nawal akachukua picha moja akaiweka mezani “Unaweza ukamtambua huyu mtu pichani? Akauliza Nawal.Sattar akaitazama picha ile na kwa taabu akatamka “Huyu ni mimi ! akajibu kwa kiarabu “Safi.Ahsante kwa kuamua kutoa ushirikiano.Picha hii ilipigwa mchana wa leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere pale ulipowasili.Sattar tunafahamu katika masanduku haya mawili ulibeba kirusi ambacho umetumwa kuja kukisambaza hapa Tanzania.Nataka kufahamu kirusi hicho kiko wapi?akauliza Nawal,Sattar hakujibu akabaki kimya “Sattar nahitaji majibu ama sivyo zoezi litaanza upya ! akasema Nawal lakini bado Sattar hakufumbua mdomo wake.Nawal akasimama na Gosu Gosu akashika tena vile vifaa vyake “Mara ya mwisho nakuuliza kirusi kiko wapi? Akauliza Nawal lakini Sattar bado alikuwa kimya.Gosu Gosu akamnasa makofi mawili mazito halafu kichwa chake kikagandamizwa katika kiti na jino la tatu likang’olewa.Sauti ya Sattar ilielekea kukauka kutokana na kulia kwa maumivu aliyoyapata. “Kirusi kiko wapi Kirusi? Akauliza Nawal. “Nawal huyu bado maumivu hayajamkolea ! akasema Gosu Gosu na kushika tena vile vifaa vyake lakini Sattar akatamka kitu Nawal akamtaka Gosu Gosu asubiri “Unasemaje Sattar? Akauliza Nawal “Nitawaeleza ! akasema Sattar.Gosu Gosu akachukua pamba akamimina dawa Fulani na kumuwekea Sattar pale mahala alipong’oa jino na baada ya sekunde kadhaa damu ikaacha kutoka lakini bado Sattar aliendelea kuhisi maumivu makali mno. “Kiko wapi kirusi? Akauliza Nawal “Nili…aaaghh !akagugumia kwa maumivu “Niliwakabidhi wamarekani wakihifadhi hadi kesho” akasema Sattar kwa taabu. “Unafahamu mahala kirusi hicho kilipohifadhiwa? Akauliza Nawal “Sifahamu ! akajibu Sattar “Sattar eleza ukweli ama sivyo tutaendelea kukung’oa jino moja baada ya lingine ! akafoka Nawal “Nawaeleza ukweli sifahamu wamekiweka wapi ! akasema Sattar “Anasemaje huyu? Akauliza Gosu Gosu ambaye hakuelewa kile alichokisema Nawal kwa kuwa hafahamu lugha ya kiarabu Nawal akamwambia Gosu Gosu alichokisema Sattar “Anaonekana anasema ukweli.Endelea naye taratibu aeleze mambo yote mimi ngoja nikaendelee na Jenerali William” akasema Gosu Gosu na kutoka akarejea katika chumba alichokuwamo Jenerali William “Jenerali William hii nimekuja ni mara ya mwisho nataka unieleze mahala kirusi kilikofichwa ! “Nenda kuzimu Bazazi wewe ! akafoka Jenerali William na kumpandisha hasira Gosu Gosu akamsogelea na kumtandika ngumi mbili za usoni na mdomo wa Jenerali William ukajaa damu “Unanipiga !! akasema Jenerali William kwa ukali “Muda wa mchezo umepita William sasa ni kazi moja tu.Aidha uonyeshe kilipo kirusi au nikuharibu haribu na kukuachia ulemavu wa kudumu ! akasema Gosu Gosu na Jenerali William akamtemea mate yenye damu “Kamwe huwezi kunitisha nyani wewe ! akasema Jenerali William na Gopsu Gosu hakumjibu kitu akaanza kumvurumishia makonde mazito.Ndani ya sekunde chache uso mweupe wa Jenerali William ukabadilika na kuwa mwekundu,ulichafuka kwa damu. “Mimi ni muuaji lakini wewe sintakuua ninataka nikutese ili uwe mfano.Nitakukata ulimi wako hautaweza kuzungumza tena,nitakuondoa vidole vyako vya mikono na miguu na hautaweza kuandika wala kumsimulia mtu kilichokupata.Utateseka na utakufa taratibu.Kwa mara ya mwisho wapi kilipo kirusi? Akauliza Gosu Gosu lakini Jenerali William hakujibu kitu. Gosu Gosu akatoka na kwenda kumchukua Sattar aliyekuwa anahojiwa na Nawal akaingia naye katika chumba alimo Jenerali William ambaye alistuka baada ya kuiona sura ya Sattar ilivyobadilika. “Gosu Gosu anataka kufanya nini? Ruby akauliza kwa wasi wasi “Subiri tuone anachotaka kukifanya” akajibu Nawal “Japo ulikana kutomfahamu lakini huyu ni Sattar Sayf al Din ambaye amekiri kuleta kirusi hapa Tanzania na kuwakabidhi ninyi mkakihifadhi.Nataka kujua mahala kirusi hicho kilipo ! akasema Gosu Gosu lakini bado Jenerali William aliendelea kubaki kimya Ghafla Gosu Gosu kafanya kitu ambacho hakuna aliyekuwa amekitegemea.Alichomoa bastora yake kwa kasi ya ajabu na kumtandika risasi Sattar katika paji la uso akaanguka sakafuni na kufariki .Jenerali William akaingiwa na woga mkubwa “Nini umefanya hiki wewe katili? Akauliza Jenerali William sauti yake ikitetemeka “Tumefika mwisho William.Hatutaki mchezo tena.Huyu ndiye aliyetumwa kuja kusambaza kirusi hapa Tanzania.Nimemuua na hakuna tena mtu wa kukisambaza kirusi hicho.Huyu ndiye aliyekuwa na maelekezo yote ya namna ya kufanya.Una sekunde thelathini za kuamua aidha kuonyesha kilipo kirusi hicho au kumfuata huyu shetani mwenzako ! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu what have you done ?! Ruby akauliza na kutaka kutoka ndani ya kile chumba ili aweze kumfuata Gosu Gosu katika chumba cha mahojiano lakini Nawal akamzuia “Subiri kidogo Ruby.Kuna kitu nimekiona ! akasema Nawal “Umeona nini? “Subiri kidogo” akasema Nawal akiwa ameyaelekeza macho yake akimtazama Jenerali William “Mara ya mwisho William wapi kilipo Kirusi? Akauliza Gosu Gosu lakini Jenerali William akabaki akimtazama.Alionekana kuchanganyikiwa.Gosu Gosu akamnyooshea bastora “Sekunde thelathini zimekwisha.Kwa heri William” akasema Gosu Gosu na William akafumba macho.Gosu Gosu akaachia risasi mbili zilizopita pembeni ya kichwa cha William Sekunde kadhaa zikapita William akafumbua macho.Alikuwa anatokwa na jasho usoni huku akihema haraka haraka “Nimetaka kukuonyesha kwamba ninao uwezo wa kukutoa roho yako muda wowote William.Nimepitisha risasi pembeni makusudi kabisa lakini safari ijayo sintakosa.Nitaingiza risasi kati kati ya kichwa chako.Tuokoe muda nataka unieleze kilipo kirusi ! akasema Gosu Gosu na Jenerali William akafumba macho “William uko tayari kufa kwa ajili ya kulinda kirusi? Hujui kamba kirusi hicho kinaweza kuvuka mipaka na kusambaa hadi nchini kwenu Marekani na hata familia yako inaweza kuathirika? Usiwe mjinga kiasi hicho William.Hawa waliokutuma ufanye hivi ni kwa maslahi yao.Tusaidiane kuokoa watu wetu wasije wakaangamia.Yawezekana labda hujaelezwa kwa undani kuhusiana na kirusi hicho.Labda nikueleweshe William kwamba kirusi hicho ambacho hakina tiba wala kinga kinasambaa kwa njia ya hewa na endapo kikiachiwa hapa Tanzania hakuna namna ya kukizuia kisivuke mipaka ya Tanzania na kusambaa katika nchi jirani hatimaye bara zima la Afrika na mwisho dunia nzima.Hata Marekani lazima kitafika.Utajisikiaje pale ndugu zako watakapoanza kuangamizwa na kirusi ambacho umesaidia kukisambaza? Akauliza Gosu Gosu na kumtazama Jenerali William “Ninakupa nafasi nyingine William ya kuweza kuiokoa dunia dhidi ya maangamizi makubwa yatakayotokea endapo kirusi hicho kitasambazwa.Nakubali endapo kirusi hicho kitasambaa mtafanikiwa kutimiza lengo lenu kwani mtaleta watu wenu wengi tu kwa lengo la kuja kutoa msaada kumbe mna ajenda ya siri nyuma yake.Mtachukua mali nyingi lakini damu za wale watakaokuwa wamefariki kutokana na kirusi hicho hazitawaacha salama.Zitawaandama usiku na mchana.William sitaki kuzungumza mambo mengi nataka ukatuonyeshe mahala kilipo kirusi ! akasema Gosu Gosu.Jenerali William akainamisha kichwa akafikiri kwa muda halafu akainua kichwa na kusema “Nini mtakifanya endapo nitawaonyesha mahala kilipo kirusi hicho? Mtakwenda kukisambaza Marekani kama ulivyoniambia? Akauliza Jenerali William “Sisi si wakatili kama ninyi.Hatutaweza kukisambaza hicho kirusi tutakihifadhi sehemu salama ambako hakitakuwa tishio kwa binadamu” akasema Gosu Gosu Jenerali Wiliam akafikiri kwa muda halafu akasema “Endapo nitawaonyesha mahala kilipo kirusi hicho kuna mambo mawili ninataka tukubaliane” akasema Jenerali William “Nini unakitaka Jenerali William? Akauliza Gosu Gosu “Kwanza kabisa mtaniacha huru na pili suala hili litabaki kati yetu na hakuna atakayefahamu kama kulikuwa na mpango wowote wa kusambaza kirusi hapa Tanzania.Nataka tulimalize suala hili kimya kimya mchukue kirusi mkakihifadhi sehemu salama na suala hili lifike mwisho.Mko tayari kwa hilo? Akauliza Jenerali William na Gosu Gosu akacheka kidogo “Gosu Gosu mkubalie hicho anachokitaka” Ruby akampa maelekezo Gosu Gosu “Nini ?! Gosu Gosu akashangaa “Ninahitaji kujadiliana na wenzangu kuhusiana na suala hili.Nitarejea ndani ya muda mfupi” akasema Gosu Gosu na kutoka mle ndani akawafuata akina Ruby “Ruby are you out of your mind ?! akauliza Gosu Gosu kwa ukali “Gosu Gosu hatuna namna ya kufanya zaidi ya kukubaliana na ombi lake ili tuweze kukipata kirusi hicho.Tusiharibu mambo Gosu Gosu nenda mle ndani mwambie tunakubaliana na matakwa yake na atuonyeshe kilipo kirusi” “Then we let him go? Akauliza Gosu Gosu “Ruby hawa watu ni wanyama sana.Mambo waliyoyafanya katika ardhi yetu si ya kibinadamu.Watanzania wenzetu wengi wamepoteza maisha kwa sababu ya watu hawa.Hatuwezi kumuacha akaenda hivi hivi” akasema Gosu Gosu “Anachokisema Gosu Gosu kina msingi.Hatuwezi kuwaacha watu hawa wakaendelea kuifanya kile wakitakacho lazima wafundishwe adabu ! akasema Nawal “Nini mnashauri kifanyike ili tukipate kirusi hicho? Akauliza Ruby “Tumkubalie ombi lake ili atuonyeshe kilipo kirusi.Tukisha kipata kirusi hicho hatutamuacha salama ! Marekani lazima waondoke hapa nchini kwa nguvu ! akasema Gosu Gosu “Una maanisha tumuue Jenerali Wiliam? Ruby akauliza “Hakuna haja ya kumuonea huruma.Huyu amekuwa akishirikiana na hata kuwalinda watu wa IS wanaochochea vurugu za kidini hapa nchini na kusababisha vifo vya watu wengi.Lazima tupeleke vilio pia Marekani kama wao walivyosababisha vilio hapa nchini” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu tusipoteze muda nenda kazungumze naye na atuonyeshe kilipo kirusi na baada ya kukipata tutajua nini cha kufanya” akasema Ruby na Gosu Gosu akarejea katika chumba cha mahojiano alimo Jenerali William.Sakafu ya chumba kile ilikuwa imetapakaa damu na Sattar Sayf Al Din alikuwa amelalia dimbwi la damu. “Tumeyakubali yale unayoyataka lakini tutatekeleza pale tutakapokuwa tumekipata kirusi.Hivyo bila kupoteza muda tuonyeshe mahala kilipo kirusi hicho” akasema Gosu Gosu “Nitawapeleka mimi mwenyewe mahala hapo” “Wewe utabaki hapa na sisi tutakwenda wenyewe kukichukua kirusi hicho na tutakapokihakiki kwamba ni chenyewe ndipo tutakapokuachia uende zako lakini kabla ya kukitia kirusi hicho mikononi mwetu hautabandua mguu wako ndani ya chumba hiki ! akasema Gosu Gosu “Kirusi hicho kiko mahala ambako ninyi hamuwezi kuingia,kama kweli mnakitaka niko tayari kwenda kuwakabidhi” “Mahala pekee ambako hatuwezi kuingia ni mbinguni anakoishi muumba wetu lakini kwa hapa duniani sehemu yoyote sisi tunaingia.Unadhani ni Marekani pekee ambao mna jeshi au makachero wenye uwezo mkubwa? Hata sisi tunao uwezo mkubwa sana wa kufanya yale mnayoyafanya ninyi na hata zaidi hivyo tuelekeze mahala kirusi kilipo na sisi tutakwenda kukichukua” akasema Gosu Gosu kwa kujiamini “Kwa nini unashindwa kunielewa? Kirusi hakiko baa au shambani kiko sehemu nyeti sana ambako ninyi hamuwezi kufika” akasema Jenerali William “Kiko wapi? Tupe maelekezo na sisi tutakwenda kukichukua tena naomba ufanye hivyo haraka kabla sijabadilika.Nimekwisha kwambia hautabandua mguu wako humu ndani hadi pale tutakapokipata kirusi na kujiridhisha kuwa kweli ni chenyewe ndipo tutakapokuacha uende zako” akasema Gosu Gosu akimtazama William kwa macho makali “Kwa mara ya mwisho wapi kilipo Kirusi? Akauliza Gosu Gosu na kuupeleka mkono wake ilipo bastora “Kirusi kipo katika kambi ndogo ya wanajeshi wa Marekani iliyoko ufukweni” akasema Jenerali William “Kiko sehemu gani ndani ya hiyo kambi? Gosu Gosu akauliza “Kuna kontena ambalo hulitumia kwa ajili ya kuhifadhi miili ya wanajeshi wanapokuwa wamefariki dunia na humo ndimo kilimo kirusi” akasema Jenerali William Gosu Gosu akafungua mlango akatoka na kuingia katika chumba walimo akina Ruby bila kuwasemesha akachukua karatasi na kalamu akarejea katika chumba cha mahojiano na kuviweka mezani. “Nataka uchore ramani ya namna ya kuweza kufika katika hilo kontena lenye kirusi” akasema Gosu Gosu na kumfungua mkono wa kulia. Jenerali William akaunyoosha mkono halafu akaanza kuchora ramani ya kambi ilivyo na namna ya kuweza kufika katika kontena ambalo kumehifadhiwa kirusi. “Ahsante kwa ushirikiano wako.Utaendelea kubaki hapa hapa hadi pale tutakapokipata kirusi” akasema Gosu Gosu “Mnajidanganya bure hamtaweza kufika mahala hapo” akasema Jenerali William “Na wewe maisha yako yatakuwa yameishia humu ndani ! akasema Gosu Gosu na kutoka. “Mambo yameiva ! akasema Gosu Gosu “Tunakwenda kuvamia kambi ya jeshi la Marekani hii si operesheni rahisi hata kidogo” akasema Ruby “Ni operesheni nzito lakini lazima ifanyike usiku huu na lazima ifanikiwe kwa namna yoyote ile ! Akasema Gosu Gosu “Nawal ulifanikiwa kuingia katika kambi hiyo anayoizungumzia William.Nini ulikiona hapo? “Ni kambi ndogo na haina wanajeshi wengi hata vifaa vilivyoko pale ni vichache.Kambi yao kubwa iko katika uwanja wa Uhuru.Tusiogope jamani tunaweza kuvamia kambi hiyo” “Ruby kwa nini tusiombe msaada kutoka kwa Rais atupatie vikosi vya jeshi? Akauliza Gosu Gosu “Operesheni hii ni ya kimya kimya na hawapaswi kujua nani aliyewashambulia.Tukitumia vikosi vya jeshi utakuwa ni mgogoro mwingine tumeuanzisha.Tunao makomando wetu tutawatumia wote na vile vile tunao makachero.Hakuna atakayebaki hapa leo wote wanakwenda kupambana kuhakikisha wanakipata kirusi hicho.Wakusanye watu wote niwajulishe kile tunachokwenda kukifanya usiku huu” akasema Ruby na kabla Gosu Gosu hajatoka Nawal akasema “Nina wazo moja.Katika ile nyumba alikokuwa akiishi huyu Jenerali William kulikuwa na gari la jeshi la Marekani.Ninafikiria kwa nini tusilichukue gari lile na kulitumia katika operesheni hii? Akasema Nawal “Wazo zuri sana Nawal.Gari hilo linaweza kutusaidia kuingia katika hiyo kambi wakidhani sisi ni wenzao halafu tutawapa shambulizi la kushtukiza na watakapostuka wamevamiwa tayari tutakuwa tumekipata kirusi na kuondoka zetu” akasema Gosu Gosu halafu akatoka kwenda kuwakusanya makomando na makachero wengine wote wa SNSA kwa ajili ya kupanga namna ya kwenda kukichukua kirusi katika kambi ndogo ya wanajeshi wa Marekani. Ilichukua saa mbili kufanya maandalizi kwa ajili ya operesheni ile ya kuvamia kambi ya wanajeshi wa Marekani.Baada ya Ruby kujiridhisha kuwa kila kitu kiko vizuri,akatoa ruhusa safari ianze.Msafara wa magari ya makomando na makachero wa SNSA wakiongozwa na gari la jeshi la Marekani ambalo lilikwenda kuchukuliwa mahala alikokuwa akiishi Jenerali William,uliondoka katika makao makuu ya SNSA kuelekea katika kambi ndogo ya jeshi la Marekani.Helkopta maalum kwa ajili ya operesheni za usiku nayo haikubaki nyuma ilipaa angani ikiwa na makomando kuelekea katika kambi hiyo. SAA MOJA BAADAE Ukimya mkubwa ulitawala katika ofisi kuu za SNSA.Ndani ya chumba cha operesheni walikuwemo Ruby,Nawal na wafanyakazi wengine wa SNSA wakifuatilia kwa karibu kile kilichokuwa kinaendelea katika operesheni ya kuvamia kambi ndogo ya jeshi la Marekani kwa ajili ya kuchukua kirusi kilichokuwa kimehifadhiwa hapo.Toka kikosi cha SNSA kilivyofika katika kambi hiyo na kuvamia wakiwa na silaha nzito walikuwa wakiwasiliana na ofisi kuu kuwajulisha kilichokuwa kinaendelea lakini baada ya muda mapambano yakawa makali na kilichobaki kinasikika ni milio ya risasi na sauti za maelekezo ya viongozi.Mapambano yalikuwa makali na hii iliwapa hofu kubwa sana watu waliobaki ofisi kuu za SNSA kuhusu usalama wa wenzao. Baada ya takribani saa moja ikisikika milio ya risasi na mabomu,hatimaye nyuso za akina Ruby zikachanua kwa tabasamu pale walipoisikia sauti ya Gosu Gosu akiwajulisha kuwa wamefanikiwa kukipata kirusi. “SNSA tumemaliza kazi na tumekipata kirusi.Narudia tena tumefanikiwa kukipata kirusi” akasema Gosu Gosu na watu wote waliokuwamo ndani ya chumba kile wakashangilia kwa nguvu. “Mapigano yamemalizika? Akauliza Ruby “Hakuna kilichobaki hapa.Tumeiteketeza kambi yote.Hapa kinachoonekana kwa sasa ni moto unaoendelea kuwaka ! akasema Gosu Gosu “Vipi kuhusu watu wetu wako salama? “Tumepoteza watu saba lakini wote miili yao inarejeshwa hakuna hata mwili mmoja wa watu wetu uliobaki hapa.Tayari vikosi vya ardhini vimekwisha ondoka na sisi tunaondoka sasa hivi na helkopta tutazungumza tukifika huko lakini kitengo cha afya wajiandae kwani watu wengi wameumia wengine vibaya sana” akasema Gosu Gosu “Ahsante Gosu Gosu.Kazi nzuri” akasema Ruby na maandalizi ya kuwapokea wenzao yakaanza mara moja.
Helkopta ya SNSA ilitua katika sehemu yake na mtu wa kwanza kushuka alikuwa ni Papi Gosu Gosu aliyekuwa amebeba masanduku mawili.Alikuwa ameloana damu.Wafanyakazi wa SNSA walikuwa wamejipanga tayari kuwapokea “Hongereni sana kwa kazi hii kubwa” akasema Ruby na kuyapokea yale masanduku mawili kutoka kwa Gosu Gosu “Ahsante sana Ruby.Lilikuwa ni shambulio la muda mfupi lakini kali sana ! akasema Gosu Gosu huku majeruhi wakishushwa kutoka katika ile helkopta na kukimbizwa katika kitengo cha afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu. “Gosu Gosu umeumia sana unatakiwa kwenda kupatiwa huduma kwanza” akasema Ruby na Gosu Gosu akachukuliwa kwenda kupatiwa matibabu. Dakika chache baadae msafara wa magari ukawasili.Majeruhi wakashushwa wakakimbizwa kupatiwa matibabu na miili ya wale waliopoteza maisha ikapelekwa katika chumba maalum kuhifadhiwa.Ruby akawashukuru watu wote kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha kirusi kile kinapatikana. Wakati majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu,Nawal akatumia muda huo kuwasiliana na Habiba Jawad kumjulisha kuwa tayari wamekipata kirusi “Hongera sana Nawal kwa kazi nzuri mliyoifanya wewe na wenzako.Sasa dunia iko salama.Nimefurahi mno kwa mpango huu mbaya wa kusambaza kirusi kushindwa kufanikiwa” akasema Habiba “Kirusi hicho kiko wapi kwa sasa? Akauliza Habiba “Kiko hapa SNSA hii ni idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Utafanyika utaratibu wa kukihifadhi sehemu salama” akasema Nawal “Hongera sana Nawal kwa kazi hii iliyotukuka mliyoifanya” akasema Habiba “Mama wewe ndiye unayestahili hongera kwani bila wewe jambo hili lisngefanikiwa.Vipi kuhusu Mathew Mulumbi una taarifa zake zozote? Akauliza Nawal na Habiba akasita kidogo “Mama una taarifa zozote za Mathew? Akauliza tena Nawal “Ndiyo Nawal.Tayari Mathew yuko Tehran lakini kuna tatizo limejitokeza” akasema Habiba na kumueleza Nawal kile kilichokuwa kimetokea na hatua alizochukua kwa ajili ya kumsaidia Mathew asiuawe. “Mama umenistua sana kwa taarifa hii.Maisha ya Mathew yako hatarini .Yuko peke yake kule Tehran na hawa jamaa wanaweza wakamzidi nguvu wakamuua.Mama nataka niende huko Tehran haraka sana kumsaidia Mathew” akasema Nawal “Unalosema ni jambo la kweli Nawal,Mathew anahitaji sana msaada.Hawa jamaa watafanya kila mbinu kuhakikisha wanamuua hasa watakapopata taarifa kuwa mpango wao wa kusambaza kirusi Tanzania umeshindwa kufanikiwa.Kwa kuwa hapo umekamilisha kazi fanya mpango uweze kuondoka mara moja kuja hapa Riyadh ili tupange namna ya kumsaidia Mathew” “Sawa mama nitafanya mipango ya kuondoka huku haraka na nitakujulisha” akasema Nawal “Kwa mara nyingine tena Nawal hongereni sana kwa kazi nzuri mliyoifanya.Naamini Marekani wakisikia mpango wao umeshindwa kufanikiwa watapasuka vichwa” akasema Habiba na kuagana na Nawal ambaye alirejea katika ofisi ya Ruby na kumkuta Gosu Gosu akiwa tayari amekwisha gangwa jeraha lake la shingoni. “Pole sana Gosu Gosu” akasema Nawal “Ahsante Nawal.Ahsanteni nyote kwa msaada wenu.Ule mpango wako wa kutumia gari lao ulisaidia sana kwani walipoliona hawakuwa na wasi wasi wakajua ni wenzao.Mara tu walipofungua geti watu wetu hawakupoteza muda wakaanza mashambulizi na hapo ndipo shughuli ilipoanzia.Wengi wa wanajeshi waliokuwepo kambini walikuwa wamelala na hawakutegemea kama wangevamiwa na wengine walikuwa wamekwenda doria.Ninakiri wanajeshi wale walikuwa wachache lakini mahiri sana.Baada ya kugundua wamevamiwa kwa haraka sana wakajipanga na tukaanza kushambuliana.Wana mbinu nyingi za kupigana lakini nawasifu makomando wetu nao wameiva barabara kwani waliweza kukabiliana nao na hatimaye tukalifikia lile kontena lenye kirusi tukalifungua na kukichukua na hapo ndipo mapambano yalipozidi kwani tayari watu wetu kadhaa walikuwa wameuawa. Kitu cha kwanza tulichokifanya baada ya kuvamia kambi ile tuliilipua nyumba iliyokuwa na mitambo ya mawasiliano hivyo hawakuweza kuwasiliana na wenzao kuomba msaada.Hata hivyo walijitahidi sana licha ya uchache wao na kama wangefanikiwa kuwajulisha wenzao walioko katika kambi kubwa uwanja wa uhuru sijui kama tungetoka salama.Wale jamaa wako vizuri katika vita” akasema Gosu Gosu “Poleni sana.Japokuwa tumewapoteza wenzetu lakini damu yao haijapotea bure.Wamekufa kishujaa wakilinda nchi yao na wameokoa maisha ya wengi ambao wangepoteza maisha endapo kirusi hicho kingesambazwa” akasema Ruby “Tayari tumekipata kirusi.Nini kinafuata? Tunakihifadhi wapi? Mkumbuke vile vile kuwa tumeiteketeza kambi yao yote na hii haitakuwa taarifa njema kwa Marekani” akasema Gosu Gosu “Ni wakati muafaka wa kumjulisha Rais afahamu kilichotokea na kile kinachoendelea hapa nchini” akasema Ruby “Vipi kuhusu Jenerali William? Akauliza Gosu Gosu “Tulikubaliana tutamuachia huru pale tutakapokuwa tumekipata kirusi na kwa kuwa tumekipata lazima tuheshimu makubaliano yetu na tumuachie huru”akasema Ruby “Ruby niambie humaanishi hicho unachokisema ! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu lazima tuheshimu makubaliano yetu! Akasema Ruby “Ruby hawa watu si wa kuonea huruma hata kidogo.Hawa watu wamesababisha ndugu zetu wengi wakapoteza maisha.Hatuwezi kumsamehe mtu kama huyu.Kama tusingekuwa na taarifa za mpango wao wa kusambaza kirusi hicho kingeanza kusambazwa kesho na hakuna anayejua yawezekana na sisi tungekuwa miongoni mwa wale ambao wangeathiriwa na kirusi hicho.Mamia kama si maelfu ya watu wengepoteza maisha.Huyu ndiye ambaye amekuwa akimlinda Assad Ismail mchochezi mkubwa wa machafuko yaliyopelekea watu wengi kupoteza maisha.Katu mtu kama huyu hatuwezi kumuachia.Hastahili huruma ya aina yoyote kwani yeye hakuona huruma wakati watu wetu wanauana” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu nadhani tutalijadili jambo hili baada ya kuzungumza kwanza na Rais” akasema Ruby na kuchukua simu akampigia Rais Dr Fabian lakini akataarifiwa kuwa simu ya Rais inatumika ikamlazimu kusubiri “Kuna jambo nataka niwataarifu jamani” akasema Nawal “Nimezungumza na Habiba Jawad nikamfahamisha kuwa tayari tumekipata kirusi” akasema Nawal “Ama kweli haya ni maajabu.Ni vigumu kuamini eti Habiba Jawad huyu ambaye tunamfahamu anafadhili makundi ya magaidi ndiye ambaye ameokoa taifa letu lisiingie katika maangamizi makubwa.Bila yeye tusingefahamu chochote kuhusiana na hiki kirusi.Nadhani hata hao wamarekani wenyewe watashangaa tumewezaje kugundua mpango wao uliokuiwa wa siri kubwa. Tunapaswa kumshukuru sana huyu mama” akasema Gosu Gosu “Uko sahihi Gosu Gosu.Habiba Jawad pamoja na mambo anayoyafanya lakini kwa hili anastahili shukran kwani bila yeye maelfu ya watu wangeangamia” akasema Ruby “Kuna jambo lingine amenieleza Habiba la muhimu sana.Amenipa taarifa kwamba tayari Mathew Mulumbi amekwisha ingia Iran” “Oh thank you Lord ! akasema Ruby “Tunamshukuru Mungu kwa kumuwezesha Mathew kuingia salama nchini Iran lakini kuna tatizo limejitokeza.Maisha ya Mathew yako hatarini” “Kivipi Nawal? Akauliza Ruby kwa wasi wasi.Nawal akawapa taarifa ile aliyopewa na Habiba “Bastard ! Gosu Gosu akasema kwa hasira “Japokuwa tayari Habiba amekwisha muonya kuhusiana na mpango wa kutaka kumuua lakini baada ya kutafakari nimeona bado maisha yake yako hatarini.Wale jamaa wanaweza wakamshinda nguvu na kumuua kwani Mathew yuko ugenini na hana msaada wowote.Nimeamua nitakwenda Iran kumsaidia Mathew katika kufanikisha misheni yake” “Unataka kwenda Iran? Akauliza Ruby “Ndiyo.Nitapita kwanza Saudi Arabia kisha nitaelekea Iran.Nimeipenda sana Tanzania na nilitamani kuendelea kukaa hapa lakini kwa hili lililojitokeza lazima niondoke haraka sana kwenda kumsaidia Mathew Mulumbi” akasema Nawal na Ruby akashusha pumzi “Ni wazo zuri sana Nawal.Kwa namna yoyote ile lazima kwenda kumsaidia Mathew ikiwezekana kumuondoa asiendelee na hiyo misheni yake kwani kirusi tayari tumekipata na tutaendelea kuwasaka wote wanaohusika na vurugu hadi tutakapohakikisha wote wametiwa nguvuni.Tatizo ni namna ya kupata usafiri wa haraka wa kukupeleka Saudi Arabia” akasema Gosu Gosu. “Nadhani ……..” Ruby akataka kuzungumza kitu lakini akanyamaza baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni Rais Dr Fabian “Imekuwa vyema Rais amepiga” akasema Ruby na kuipokea simu “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby ulinipigia simu lakini wakati unanipigia nilikuwa nazugumza na mkuu wa jeshi la polisi.Kuna tukio baya limetokea usiku huu.Moja ya kambi za wanajeshi wa Marekani walioko hapa Dar es salaam imevamiwa na watu wasio julikana usiku huu na inasadikiwa wanajeshi wote waliokuwepo kambini wakati wa uvamizi huo wameuawa na kambi yote kuteketezwa vibaya sana kwa mabomu.Matukio haya yanataka kukipasua kichwa changu” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nilikupigia ninaomba kuonana nawe” “Usiku huu ?! akauliza Dr Fabian “Ndiyo mheshimiwa Rais usiku huu.Ni muhimu sana” “Haliwezi kusubiri hadi kesho? “Hapana mheshimiwa Rais ni suala la kuzungumza usiku huu huu” akasema Ruby na Rais akakubali Ruby aende ikulu kuonana naye usiku ule.Aliingia katika gari lake akiongozana na walinzi wake kuelekea ikulu akiwaacha Gosu Gosu na Nawal Mara tu Ruby alipoondoka Gosu Gosu akaenda katika chumba alimo Jenerali William.Ujio wa Gosu Gosu ulimstua Jenerali William “Nimerejea ! akasema Gosu Gosu akimtazama Jenerali William kwa macho yaliyojaa hasira “Tumepoteza watu saba lakini kirusi tumekipata na kambi yote tumeiteketeza.Hakuna mwanajeshi wako hata mmoja aliyekuwapo kambini hapo usiku huu aliyepona wote tumewaua ! akasema Gosu Gosu na Jenerali William akapandwa na hasira “Aaaagghhhh !! akasema kwa hasira Jenerali William huku akijaribu kujitikisa katika kiti alichokuwa amefungwa. “Hakuna unachoweza kukifanya William ! Huu ni mwisho wako ! akasema Gosu Gosu “Tuliweka makubaliano na nimetimiza upande wangu.Sasa ni upande wenu nataka mniachie huru niende zangu kama tulivyokuwa tumekubaliana ! akasema Jenerali William “Siyo rahisi namna hiyo kama unavyodhani William.Itakuchukua miaka kutoka humu na ikiwezekana hautaweza tena kutoka” akasema Gosu Gosu “Tulikubaliana !! akafoka Jenerali William “Sikiliza Jenerali William.Ninyi ni watu makatili msio na hata chembe ya huruma.Mmesababisha mamia ya watanzania wameuana kwa kujenga chuki baina yao.Kana kwamba damu mliyoimwaga haitoshi bado mkataka tena kusambaza kirusi ambacho kingesababisha maangamizi makubwa.Mungu analipenda taifa hili na mpango wenu umeshindwa kufanikiwa.Hatuwezi kukuachia kirahisi namna hiyo Jenerali William.Kwa sasa endelea kupumzika tutazungumza vizuri hapo baadae hizi ni salamu tu nimekufikishia” akasema Gosu Gosu na kutoka
Ruby aliwasili ikulu na kumkuta Dr Fabian akimsubiri. “Karibu Ruby” akasema Dr Fabian huku akimimina kinywaji katika glasi mbili akampatia moja Ruby. “Ruby wewe ni mtu ambaye sikufichi jambo.Nataka nikuweke wazi kwamba sifikirii tena kuwania urais kwa kipindi cha pili pale kipindi changu cha kwanza kitakapomalizika.Hii si kazi nyepesi hata kidogo kuna nyakati ninajuta kwa nini niliingia katika siasa” akasema Dr Fabian “Dr Fabian hayo ni masuala yako binafsi ambayo sisi wengine hatustahili kuyafahamu lakini kwa sasa kwa kuwa bado umekalia kiti cha urais basi jielekeze katika kuwatumikia watanzania.Simama imara kuhakikisha nchi inakuwa salama na maisha ya watanzania yanarejea kuwa ya kawaida” akasema Ruby “Ninachokupenda Ruby ni namna unavyoweza kunieleza ukweli.Wengine hawawezi kunitamkia maneno kama haya uliyonitamkia.Ahsante kwa kuwa mkweli kwangu na nitayaheshimu mawazo yako” akasema Dr Fabian na kunywa funda la kinywaji “Nimepigiwa simu usiku huu na mkuu wa jeshi la polisi akinijulisha kuwa kambi ndogo ya wanajeshi wa Marekani iliyoko kando mwa bahari imevamiwa na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito na kuiteketeza kabisa pamoja na kuua wanajeshi wote waliokutwa hapo kambini.Taarifa hiyo imenichanganya sana kichwa changu ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais tuliweke kwanza hilo pembeni tutalizungumza baadae lakini nimekuja kukupa taarifa ya kile ambacho SNSA tumekuwa tunakichunguza tukianzia kwanza na vurugu zile kubwa zilizopelekea umwagaji mkubwa wa damu” akasema Ruby na kunyamaza kidogo “Toka vurugu zilipoanza tulianza kuchunguza chanzo chake tukijaribu kuziunganisha na vurugu zilizoanzia nchini Uganda lakini napenda nikiri kwako kwamba tulifika mahala tukakutana na giza nene mbele yetu.Hatukuwa na mwangaza ,tulikata tamaa.Mara akatokea Mathew Mulumbi ambaye ndiye aliyekuja kutufumbua macho na kutupa mwangaza” akasema Ruby na kunyamaza baada ya sura ya Dr Fabian kubadilika aliposikia jina la Mathew Mulumbi likitajwa “Mheshimiwa Rais najua jina la Mathew linakuchefua lakini naomba uvumilie kwani litajitokeza mara nyingi katika mazungumzo haya” akasema Ruby “Endelea usijali” akasema Dr Fabian “Mathew alikutana nasi, mimi na Gosu Gosu na akatufahamisha kwamba amekuja nchini kwa misheni maalum ila hakutueleza ni misheni gani.Alichotueleza ni kwamba vurugu zile zilizotokea nchini na kupelekea waumini wa dini kushambuliana na kuuana zina nguvu kubwa kutoka nje ya nchi” akasema Ruby na kumueleza Dr Fabian kila kitu alichoelezwa na Mathew na sura ya Dr Fabian ikabadilika kwa mshangao mkubwa alioupata.Ruby hakumjali akaendelea “Tulifuata maelekezo ya Mathew na kuwakamata wale magaidi wote isipokuwa Assad Ismail ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wao.Wakati tukiendelea kumsaka Assad tukampokea mgeni anatokea Saudi Arabia ambaye ni Yule Chloe niliyekuja naye hapa jana nikakuomba utusaidiekumuunganisha na mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko hapa nchini.Yule ni Jasusi aliyekuwa anafanya kazi na shirika la ujasusi la CIA ambaye alikutana na Mathew huko Palestina katika kikundi kimoja cha wanamgambo wanaopambana na serikali ya Israel ambako Mathew alikuwa amejiunga nao akiwa katika misheni maalum” akanyamaza Ruby baada ya Dr Fabian kumfanyia ishara anyamaze “Ruby mambo unayonieleza ni mazito sana lakini naona kama vile unanieleza juu juu.Ninataka unieleze kwa kina.Umesema huyu Chloe ni jasusi ambaye alikutana na Mathew huko Palestina katika kikundi cha wanamgambo.Mathew alikuwa anafanya nini katika kikundi hicho cha wanamgambo? Ninataka kufahamu tafadhali” akasema Dr Fabian http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Ili ulifahamu jambo hili kwa undani zaidi nitakuanzia mbali kidogo” akasema Ruby na kuanza kumueleza Dr Fabian namna Mathew alivyopotea wakati wa operesheni ya kubadilishana mateka kati yao na magaidi wa IS.Ruby alimueleza Dr Fabian kila kitu toka Mathew alipokamatwa na watu wa Mossad na kufungwa kwa miaka mitatu akiteswa na hadi alipojiunga na kundi la Ammar Nazari Brigades.Historia hii yote alielezwa na Nawal Ruby akaendelea kumpa Rais maelezo ya kuhusiana na safari ya Mathew hadi alipokutana na Habiba Jawad “Baada ya kufika kwa Habiba Jawad misheni ikabadilika na mipango ya kumuua haikuendelea tena badala yake akajiunga naye na kuwa sehemu ya familia kwa kumuoa mtoto wa Habiba” “Dah ! Yaani akathubutu kumuoa mtoto wa mtu anayefadhili ugaidi duniani ! akasema Dr Fabian kwa mshangao “Wote tulistuka tulipopata taarifa hizi lakini mstuko wetu ni kwa sababu hatukuwa tukimfahamu vyema Habiba Jawad ni nani.Mathew alipata bahati ya kumfahamu haraka ndiyo maana akajiunga naye.Nikukumbushe tu mheshimiwa Rais kwamba katika sakata lile la Melanie David na James Kasai wakishirikiana na magaidi wa IS,ni Habiba Jawad ambaye alimuwezesha Mathew Mulumbi kulimaliza lile jambo kwa kumpa taarifa muhimu kuhusu James Kasai na mipango yao yote” akasema Ruby “Are you sure? Akauliza Dr Fabian “100% Mr President” akajibu Ruby “Inashangaza sana.Kwa nini akafanya hivyo wakati yeye ndiye aliyekuwa akiwafadhili magaidi wale? “Baada ya kukamilisha misheni ile Mathew Mulumbi alirejea Saudi Arabia ambako tayari alikwisha kuwa raia na alijulikana kama Abu Zalawi na safari hii ndipo alipogundua siri kubwa aliyokuwa nayo Habiba Jawad” akasema Ruby na kumueleza Dr Fabian kuhusiana na kikundi kinachojulikana kama G20 kilicho ndani ya shirika la ujasusi la Marekani CIA ambacho ndicho kinamtumia Habiba Jawad katika kufadhili makundi ya kigaidi.Mshangao alioupata Dr Fabian ulikuwa mkubwa “Ruby hiki unachokisema ni kitu kizito mno.Naomba uongee vitu ambavyo una uhakika navyo.Marekani kamwe haiwezi kushirikiana na magaidi wakati ni nchi inayoongoza katika kupiga vita ugaidi duniani.Inawezekanaje wakaihadaa dunia kuwa wao ni vinara katika kupambana na ugaidi halafu wakageuka upande wa pili na kushirikiana nao? Ruby naomba uwe makini mno na jambo hili” akasema Dr Fabian “Usihofu mheshimiwa Rais,nina uhakika na hiki ninachokueleza” akasema Ruby “Kikundi hicho cha G20” Ruby akaendelea “Kimekuwa kikishirikiana na makundi mbali mbali ya kigaidi katika mipango mbali mbali duniani yenye maslahi kwa nchi ya Marekani.Vurugu za kidini zilizotokea katika nchi za Afrika ya Mashariki zikianzia Uganda na kusambaa katika nchi nyingine Tanzania na kidogo nchini Kenya ni moja ya mikakati ya kikundi hicho” “What ?! akauliza Dr Fabian “Narudia tena mheshimiwa Rais kwamba vurugu hizi ambazo zimetokea Afrika Mashariki na kusababisha waumini wa dini kushambuliana hazikuibuka hivi hivi tu bali ni mipango ya kundi hili la G20 wakiwatumia magaidi wa IS katika kuchochea vurugu hizo” “That’s not true ! akasema Dr Fabian na kusimama “It is true Mr President ! akasema Ruby “Wapi umeyatoa mambo haya Ruby? Kwa Mathew Mulumbi? Akauliza “Mheshimiwa Rais haijalishi taarifa hizi tumezipata wapi lakini ni taarifa za kweli kabisa na ninaomba uniamini” akasema Ruby “Hata mwendawazimu hawezi akakuamini Ruby kwa taarifa hiyo.Nimekwisha kutahadharisha kwamba taarifa hizi unazopewa na vyanzo vyako si taarifa sahihi na zina lengo la kuleta mgongano baina ya nchi zetu na Marekani.Nchi ya Marekani ni marafiki zetu wa muda mrefu na wamekuwa wakitusaidia sana na hata machafuko haya yalipotokea ni wao waliotuma majeshi yao haraka kuja kutusaidia hakuna nchi nyingine iliyofanya hivyo” “Nalifahamu hilo mheshimiwa Rais lakini naomba utulie nimalizie kile ambacho ninataka kukueleza” akasema Ruby na Dr Fabian akaketi.Ruby akamueleza kwa kirefu kile walichokigundua kutokana na vurugu zile za kidini zilizopelekea mamia ya watu kupoteza maisha.Dr Fabian akabaki mdomo wazi “Kwa hiyo mheshimiwa Rais vurugu hizi zote zilizotokea malengo yake ni kujipatia mafuta ya Uganda na ukitazama kwa makini utaamini kile ninachokwambia.Vurugu zilianzia Uganda na zikafika hadi hapa nchini na kwa hapa nchini vurugu zilianzia jijini Tanga.Kwa nini iwe Tanga na si Kilimanjaro? Jibu ni jepesi tu ni kwa sababu ili waweze kuyapata mafuta ya Uganda walilazimika kuudhibiti mji wa Tanga kwani bomba la mafuta linatoka Uganda na kuishia Tanga na mara tu vurugu zilipoanza Marekani ikatuma vikosi vyake haraka sana kwa lengo la kusaidia kurejesha amani.Hivi sasa meli za Marekani zinapanga foleni zikijaza mafuta jijini Tanga” akasema Ruby na ukimya mfupi ukatanda mle ndani “Ruby unachokizugumza kinaweza kuwa kweli.Sasa nimeanza kukuelewa” akasema Dr Fabian “Baada ya mpango wao wa kuchukua mafuta kufanikiwa,walihitaji kufanya kitu ambacho kitavifanya vikosi vya Marekani viwe na sababu ya kuendelea kuwepo hapa nchini kwa muda mrefu zaidi na ndipo walipokuja na mpango wa kusambaza kirusi hatari cha maangamizi” akasema Ruby na kumueleza Rais kuhusiana na mpango ule wa kusambaza kirusi hapa Tanzania.Dr Fabian akalazimika kufuta jasho usoni.Ruby akatoa faili katika mkoba wake akalifungua na kutoa picha akampatia Rais “Anaitwa Sattar Seyf Al Din.Huyu ndiye aliyetumwa kuja nchini kusambaza kirusi hicho” akasema Ruby na kutoa picha nyingine “Hapa ni wakati akishuka ndegeni katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akiwa ameambatana na wanajeshi wa Marekani.Haya masanduku mawili ndimo kilimo kirusi”akasema Ruby.Dr Fabian akazitazama picha zile kisha akasema “Hebu subiri kidogo Ruby.Ninyi mlifahamuje kama kuna mpango huo wa kusambazwa kwa kirusi hapa Tanzania na hadi mkafahamu mtu anayetumwa kuja kuifanya kazi hiyo? Akauliza Dr Fabian “Chloe alitumwa kuja kutupa taarifa hiyo na Habiba Jawad.Kikundi hicho cha G20 walimtaka Habiba awatafutie mtu kutoka IS ambaye watamtumia katika mpango huo wa kusambaza kirusi hapa Tanzania na akamtafuta Sattar halafu akamtuma Chloe kutuletea taarifa” Akasema Ruby na kuendelea kumsimulia Dr Fabian kilichoendelea baada ya Sattar kuwasili nchini na hadi walivyotumia mbinu ya kumkutanisha Nawal na Jenerali William “Tunashukuru Chloe alipokewa vyema na Jenerali William na akampeleka katika makazi yake na saa mbili za usiku akatupa taarifa kwamba Jenerali William amefika katika makazi hayo akiwa ameongozana na Assad Ismali tuliekuwa tukimtafuta kwa udi na uvumba na vile vile alikuwa ameongozana na Sattar Sayf Al Din.Baada ya kupewa taarifa hiyo tukaanza kujiandaa na kutuma kikosi caha makomando wetu wakavamia nyumba hiyo na kuwakamata Jenerali Wiliam,Sattar na Assad lakini kirusi kilikosekana.Tuliwafanyia mahojiano na Jenerali Wiliam akatuonyesha mahala kirusi hicho kilipohifadhiwa ambako ni katika kambi yao ndogo iliyoko ufukweni mwa bahari.Hatukuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kujipanga na kwenda kuivamia kambi hiyo” “Wait..! ni ninyi mliovamia kambi ya wamarekani? Akauliza DrFabian kwa mshangao “Ndiyo mhshimiwa Rais ni sisi.Tumepoteza watu saba na wengine wamejeruhiwa lakini tumefanikiwa kukipata kirusi ambacho kilitazamiwa kuanza kusambazwa siku ya kesho.Kwa sasa kirusi kimehifadhiwa SNSA na nchi iko salama” akasema Ruby na ukimya ukatawala mle ndani.Baada ya muda Dr Fabian akasema “Nimekosa maneno ya kusema Ruby ! Sijui nitawashukuru vipi kwa jambo hili kubwa mlilolifanya la kuiokoa nchi yetu kutoka katika janga kubwa.Watu hawa ni wanyama wakubwa sikutegemea kabisa kama wanaweza wakatufanyia kitu kama hiki.Watu hawa ambao tunawaheshimu kama rafiki zetu kumbe wana sura mbili ! akasema Dr Fabian kwa hasira “Kwa nini Habiba Jawad anafanya haya kwa nchi yetu? Akauliza Dr Fabian “Ni kwa sababu amechoka kufanya hiki anachokifanya na kwa sasa anashirikiana na Mathew kuweza kukiondoa kikundi hicho cha G20 ambacho amekuwa akifanya kazi kwa niaba yao” akasema Ruby “Hapo ndipo mnaponichanganya.Mathew Mulumbi anashikiliwa na Marekani kwa kulipua ubalozi wake hapa Dar es salaam.Atafanikiwa vipi kukiondoa kikundi hicho wakati ana tuhuma za ugaidi? Akauliza Dr Fabian “Ule ulikuwa ni mpango maalum uliopangwa na hao G20” akasema Ruby “Unataka kuniambia kwamba wamelipua ubalozi wao wenyewe? Akauliza Dr Fabian “Ndiyo mheshimiwa Rais.Mpango huo uko hivi.Hivi sasa Marekani na Iran hazina maelewano mazuri na zimekuwa zikitoleana kauli za vitisho vya kushambuliana.Marekani wana hofu kwamba yawezekana kweli Iran akawa anamiliki silaha kali kama inavyojitapa hivyo basi wakaamua kuja na mpango maalum wa kuweza kufahamu kuhusu silaha za Iran” akasema Ruby na kumweleza Dr Fabian mpango wote wa G20 kumuingiza Mathew nchini Iran kuchunguza silaha za Iran “Hivi sasa Mathew yuko nchini Iran tayari kabisa kuanza kazi yake aliyotumwa” akasema Ruby “Ruby kila unavyozidi kunieleza ninazidi kuchoka.Mambo haya ni makubwa mno.Mathew Mulumbi ameingia katika misheni ya hatari sana” “Ni misheni ya hatari mno na kama akifanikiwa kuimaliza salama basi itakuwa na mafanikio makubwa kwani lazima atakiondoa kikundi cha G20” “Sikufahamu chochote kilichokuwa kinaendelea kuhusu Mathew ndiyo maana nikatamka maneno mengi mabaya na…” “Usijilaumu mheshimiwa Rais hukufahamu chochote kilichokuwa kinaendelea ndiyo maana nilikushauri kuwa usizungumze maneno mabaya kwani utafika wakati ambao utajilaumu kwa maneno yako” akasema Ruby na ukimya ukatanda “Kwa hiyo mheshimiwa Rais hiyo kazi tuliyokuwa tunaifanya ambayo kila uliponiuliza nilikuomba unipe muda zaidi ni hiyo niliyokuleza na hapo ndipo tulipofika” akasema Ruby “Ruby narudia tena sioni maneno mazuri ya kuwashukuruni kwa jambo hili kubwa mlilolifanya kwa taifa letu na dunia nzima kwa ujumla kwani endapo kirusi hicho kingesambazwa hapa Tanzani lazima kingesambaa sehemu nyingine duniani” “Mheshimiwa Rais pamoja na mafanikio haya makubwa tuliyoyapata lakini bado tuna kazi kubwa mbele yetu.Bado tunatakiwa kuufahamu mtandao wote ambao umeshiriki katika kuchochea vurugu zilizotokea hapa nchini na kuwakabidhi jeshi la polisi kwa hatua zaidi za kisheria.Tunaye Assad ambaye tunaamini atatueleza kila kitu kuhusu watu anaoshirikiana nao.Jambo lingine tunacho kirusi hatari ambacho tunatakiwa kutafuta namna ya kukihifadhi na jambo la mwisho tumeua wanajeshi wa Marekani walioko hapa nchini na kwa hilo tumetengeneza mgogoro na Marekani.Tunahitaji msaada wako katika hili kuihakikishia serikali ya Marekani kwamba kilichofanyika ni shambulio la kigaidi” “Hapana Ruby ! Hatuwezi kuwaogopa.Ni wao walioanza na sisi tunamaliza.Kuanzia kesho nitawaondoa wanajeshi wote wa Marekani hapa nchini na nitawaeleza ukweli watanzania na dunia wafahamu ni kitu gani ambacho Marekani imekuwa inakifanya.Hili si suala la kufumbia macho ! akasema kwa ukali Dr Fabian “Mheshimiwa Rais wakati wa kuwatangazia watanzania na dunia juu ya jambo hili bado.Ukifanya hivyo utavuruga misheni ya Mathew kule Iran.Tuvute subira kidogo ili Mathew amalizie misheni yake na kisha akakimalize kile kikundi cha G20 na hapo ndipo tutaitangazia dunia mambo yote waliyokuwa wanayafanya na hadi wakati huo tutakuwa tumekamilisha uchunguzi wetu kuwafahamu watu walioshiriki katika kuchochea machafuko”Ruby akamshauri Rais ambaye aliinama akafikiri halafu akasema “Wazo zuri Ruby lakini hatuwezi kuendelea kuwaruhusu Marekani waendelee kuchukua tani na tani za mafuta ya Uganda.Lazima tuwaondoe bila ya vurugu.Kuna njia nyepesi ya kuweza kuwaondoa hapa Afrika Mashariki.Watu hawa wamekuja kwa ajili ya mafuta hivyo basi pale watakapoyakosa mafuta hawatakuwa tena na ulazima wa kuwepo hapa.Tutalipua bomba la mafuta linalotoka Uganda na hiyo itapelekea mafuta kutokushuka tena Tanga.Wakikosa mafuta wataondoka zao” akasema Dr Fabian. “Hilo ni wazo zuri pia mheshimiwa Rais.Tutajifanya hatujui chochote kuhusiana na mipango yao na hii itasaidia kumpa Mathew nafasi ya kuweza kukamilisha misheni yake” akasema Ruby Majadiliano yaliendelea kwa zaidi ya saa moja wakakubaliana mambo kadhaa ya kufanya halafu Ruby akasema “Mheshimiwa Rais kuna suala lingine ambalo ninahitaji msaada wako” “Sema Ruby nini unahitaji? “Mathew Mulumbi yuko katika hatari kubwa ya kuuawa” akasema Ruby na kumueleza Dr Fabian kuhusiana na mipango ya kumuua Mathew. “Endapo wakifanikiwa mipango yao basi mpango wa kukisambaratisha kikundi cha G20 hautafanikiwa kwani mpango huo unamuhiaji mno Mathew.Kwa namna yoyote ile lazima tumsaidie ili aweze kuwa salama na afanikishe misheni yake” akasema Ruby “Kama waliomtuma hawataki aendelee na misheni waliyomtuma na wanataka kumuua kuna ulazima gani wa kumsaidia afanikishe misheni aliyotumwa na hao jamaa? Kitu cha msingi ni kumsaidia atoke Iran na kurejea nyumbani”Akasema Dr Fabian “Kuna umuhimu mkubwa wa Mathew kuendelea na misheni yake na atakapoikamilisha itakuwa ni tiketi kwake ya kuingia tena Marekani na hapo ndipo atakapopata nafasi ya kukimaliza kikundi cha G20.Bila kukamilisha misheni aliyotumwa hataweza kurejea Marekani na G20 wataendelea kuwa tishio duniani” akasema Ruby “Namna gani unataka kumsaidia? Una mawasiliano naye? Unafahamu mahala alipo?Akauliza Dr Fabian “Sina mawasiliano naye lakini Habiba Jawad tayari amekwisha wasiliana naye na kumjulisha kuhusiana na hatari inayomkabili.Pamoja na kupewa taarifa za hatari hiyo lakini Mathew yuko ugenini na hana msaada wowote wale jamaa wanaweza wakamzidi nguvu na kumuua.Ikitokea bahati mbaya Mathew akauawa hizi juhudi zote tulizofanya zitakuwa bure na hawa jamaa wanaweza wakajipanga na kurejea kivingine.Baada ya kujadiliana tumekubaliana kwamba Chloe atakwenda Tehran kumsaidia Mathew.Yeye itakuwa rahisi kuingia nchini Iran kwa kuwa ana uraia wa Saudi Arabia.Vile vile Habiba Jawad anafahamiana na watu wanaoweza kumsaidia Chloe kuingia kwa urahisi nchini Iran” “Kama mna uhakika kwamba Chloe anaweza kuwa na msaada mkubwa kwa Mathew basi aende mara moja” akasema Dr Fabian “Kuna jambo limetukwamisha.Namna atakavyoweza kuondoka hapa kwa haraka kuelekea Riyadh” akasema Ruby na Dr Fabian akainamisha kichwa na kusema “Hakuna tatizo la usafiri.Kwa jambo muhimu kama hili nitatoa hata ndege ya Rais impeleke haraka huko Riyadh.Lini anataka kuondoka? “Hata sasa hivi akipata usafiri” akajibu Ruby “Nitatoa maelekezo ndege yangu iandaliwe ili aweze kuondoka kesho asubuhi” akasema Dr Fabian “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby Tayari imekwisha timu saa kumi za alfajiri,Ruby akaagana na Rais akaondoka kurejea ofisi za SNSA. Baada ya Ruby kuondoka Dr Fabian akamimina mvinyo katika glasi akagugumia wote “Mpaka sasa mwili unanisisimka kwa mambo aliyonieleza Ruby.Marekani wamekuwa ni rafiki zetu kwa muda mrefu na wamekuwa wakitupa misaada mingi ya kimaendeleo na vile vile ni wachangiaji wa bajeti yetu ya serikali lakini kumbe ni chui mwenye ngozi ya Kondoo.Imeniumiza sana kwa kitendo hiki walichotufanyia.Huu ni uonevu na ukandamizaji uliovuka mipaka.Kama vijana wangu wasingesimama imara na kupambana kuhakikisha mipango yao haifanikiwi,wangeweza kusambaza kirusi hatari na mamia ya watanzania wangeangamia.Huu ni unyama uliovuka kiwango! Akawaza Dr Fabian akiwa ameikunja sura yake kwa hasira akanywa funda lingine la kinywaji “Sasa ninaanza kupata picha kumekuwa na magonjwa mbali mbali yanaibuka zama hizi bila kujua yametokea wapi na mengine mpaka leo hii hayana tiba,yawezekana virusi vinavyoeneza magonjwa haya vinatengenezwa na kuja kusambazwa huku kisha tunatumia gharama kubwa kununua dawa.Dah ! Matukio haya yamenifundisha jambo kubwa sana.Ili kuepukana na haya yote nchi zetu zinapaswa kuachana kabisa na utegemezi wa mataifa makubwa.Nchi zetu za Afrika zinapaswa kuanza kujitegemea zenyewe bila kusubiri wafadhili.Kama tukiendelea kutegemea mataifa makubwa waje watuletee maendeleo matokeo yake ni kama haya yaliyotupata ! akaendelea kuwaza Dr Fabian halafu akawasha simu yake aliyokuwa ameizima ili azungumze na Ruby akatoa maelekezo ndege yake iandaliwe kwa ajili ya safari ya nje ya nchi asubuhi
Ruby alirejea SNSA.Ulinzi ulikuwa umeimarishwa sana. “Vipi maendeleo ya hapa? Akauliza Ruby “Hapa kila kitu kinaendelea vizuri.Vipi huko utokako? Akauliza Gosu Gosu na Ruby akawaeleza kila kitu kilichojiri ikulu. “Ahsante sana Ruby kwa msaada huu mkubwa wa kupatikana usafiri kwenda Riyadh.Inapendeza kama Rais mwenyewe amekubali kutoa ndege yake kwa ajili ya kunifikisha haraka Riyadh.Hii ina maanisha kwamba Tanzania inanituma kwenda kumsaidia mtoto wao ambaye ni Mathew Mulumbi na ninawaahidi kwamba nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba ninamsaidia Mathew na misheni yake inakamilika.Mathew atarejea nyumbani akiwa mzima kabisa” akasema Nawal “Inakaribia saa kumi na moja za Alfajiri,nendeni mkapumzike kwa muda mfupi kwani si muda mrefu kutapambazuka” akasema Ruby.GoSu Gosu akamchukua Nawal wakaingia garini huku wakisindikizwa na walinzi kuelekea nyumbani kwa Gosu Gosu kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuanza safari kuelekea Riyadh. “Gosu Gosu tukifika nyumbani hakuna maongezi mengi.Nataka tutumie muda mfupi uliobaki kuagana kwani yawezekana nisirejee tena Tanzania.Ninafahamu unachokitaka kwangu toka nimefika” akasema Nawal wakiwa ndani ya gari na kumfanya Gosu Gosu asisimkwe mwili kisha akatabasamu. Mara tu baada ya kufika nyumbani, Gosu Gosu hakutaka kusubiri.Bila kujali maumivu aliyokuwa nayo kutokana na majeraha aliyoyapata,akambeba Nawal na kupanda naye ngazi hadi chumbani kwake ambako hakukuwa na muda wa kupoteza mpambano ukaanza mara moja.Gosu Gosu aliumiliki uwanja vilivyo.
“Gosu Gosu ! Amka kumekucha tayari” akasema Nawal ambaye naye alistuliwa na mlio wa simu ya Gosu Gosu iliyokuwa ikiita mfululizo.Gosu Gosu akakurupuka kutoka usingizini na kuichukua simu yake.Mpigaji alikuwa ni Ruby “Ruby habari za asubuhi ! akasema Gosu Gosu kwa sauti ya uchovu “Nzuri Gosu Gosu,tayari nimekwisha anza kupatwa na wasiwasi.Si kawaida yako kuchelewa kupokea simu namna hii” akasema Nawal “Ni uchovu wa jana.Mambo yanakwendaje?Uko salama? Akauliza “Huku shwari kabisa kila kitu kinakwenda vizuri” “Nawal anaendeleaje? “Anaendelea vizuri.Ni yeye aliyeniamsha nilikuwa nimepitiwa na usingizi” “GosuGosu ulikuwa umelala na Nawal? Akauliza Ruby na kumstua Gosu Gosu “Oh no ! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu nimetaarifiwa na Rais kwamba ndege iko tayari .Mwambie Nawal ajiandae kwa ajili ya safari.Ninakuja hapo kuwapitia tuelekee uwanja wa ndege” akasema Ruby na kukata simu “Sikutaka Ruby afahamu kama nimelala na Nawal,hata hivyo hakuna kilichoharibika” akawaza Gosu Gosu na kumfuata Nawal chumbani kwake na kumkuta akitoka kuoga. “Ruby anasemaje? Akauliza Nawal “Ndege iko tayari anatupitia muda si mrefu tuelekee uwanja wa ndege” akasema Gosu Gosu na kumkumbatia Nawal “Tafadhali fanya kila uwezalo urejee Tanzania pindi mtakapokuwa mmekamilisha misheni yenu huko Iran”akasema Gosu Gosu “Nimekwisha kuahidi Gosu Gosu kwamba nitarejea Tanzania.Nimeipenda sana nchi hii” akasema Nawal na kuliachia taulo likaanguka chini “Mama yangu ! akawaza Gosu Gosu baada ya kuushuhudia mwili mwororo wa Nawal “Kama isingekuwa Ruby anakuja ningeanzisha kipute kingine hapa hapa.Lakini ngoja tujiandae kwa safari” akawaza Gosu Gosu “Mbona unanitazama kwa tamaa namna hiyo kama Fisi mwenye njaa? Usijali nitarejea Dar es salaam kwa ajili yako” akasema Nawal na kumfuata Gosu Gosu akambusu na kumtaka akajiandae. “I’m not handsome like Mathew and others lakini nina bahati ya kukutana na kupendwa na warembo wenye uzuri wa kimalaika” akawaza Gosu Gosu akielekea chumbani kwake kujiandaa. Dakika kumi na tano baadae Ruby akawasili na hakukuwa na muda wa kupoteza wakaingia garini wakaondoka kuelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Asubuhi hii hali ya jiji la Dar ilikuwa shwari na sehemu nyingi za jiji watu tayari walianza kuendelea na maisha yao ya kawaida licha ya kuwa na hofu bado kuwa machafuko yanaweza kuanza tena.Vikosi vya jeshi na polisi viliimarisha doria katika mitaa mbali mbali Walifika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ambako Ruby alikutana na wasaidizi wa Rais ambao tayari walikwisha fika uwanjani pale mapema wakawaongoza kuelekea ndani ya uwanja hadi katika ndege ya Rais.Kabla hawajaingia ndegeni Ruby akamuita pembeni Nawal “Nawal ukifanikiwa kuonana na Mathew mpe barua hii”akasema Ruby huku akilengwa na machozi “Nitafikisha ujumbe wako usijali” akasema Nawal na kumkumbatia Ruby na Gosu Gosu halafu akapanda ndegeni.Mlango ukafungwa na taratibu ndege ikaondoka baada ya dakika chache ikapaa kuelekea Riyadh “Tumuombee Nawal afike salama na amsaidie Mathew.Sisi huku bado tunaendelea na mchaka mchaka wetu ! akasema Ruby wakaingia garini na kuondoka kurejea SNSA. MPENZI MSOMAJI - MPANGO WA KUMUUA MATHEW MULUMBI UTAFANIKIWA? - NAWAL ATAFANIKIWA KUINGIA NCHINI IRAN KUMUOKOA MATHEW ? - NINI KITAENDELEA NCHINI TANZANIA BAADA YA WANAJESHI WA MAREKANI KUUAWA NA SNSA? MAJIBU YA MASWALI HAYA NA MENGINE MENGI USIKOSE SEHEMU IJAYO YA SIMULIZI HII. TUNAPOKARIBIA KUFIKA MWISHO WA SIMULIZI HII NDEFU YA SIRI,JIANDAE KWA BALAA LINGINE LA MATHEW MULUMBI KATIKA HADITHI MPYA SCANDAL(KASHFA)
TEHRAN – IRAN Mlango wa chumba ulifunguliwa,Mathew Mulumbi akageuza kichwa taratibu kutazama mtu aliyeingie mle chumbani. “Asalaam alaykum Abu Zalawi” akasalimu yule jamaa aliyeingia mle ndani. “Wa alykum salaam” akajibu Mathew.Yule jamaa akamsogelea karibu “Naitwa Yasser Wajid” akasema “Nafurahi kukufahamu Yasser” akajibu Mathew na kuinuka kitandani akakaa “Vipi maendeleo yako? Akauliza Yasser “Ninaendelea vizuri japo nina maumivu mwili mzima” akajibu Mathew “Pole Abu Zalawi umeumizwa sana.Amka ujiandae nimetaarifiwa kwamba daktari atafika hapa muda si mrefu kwa ajili ya kutazama maendeleo yako” akasema Yasser “Ahsante Yasser” akajibu Mathew na Yasser akaanza kupiga hatua kutoka “Yasser samahani” akasema Mathew na Yasser akageuka “Kuna jamaa Yule mfupi jana alikuwa amevaa suti ya rangi ya kijivu anaitwa nani? Akauliza Mathew “Anaitwa Faqir Jahid” akajibu Yasser “Jana nilimuona akitoa maelekezo kadhaa hapa ndani.Ana cheo gani? Akauliza Mathew “Yule ndiye msimamizi mkuu wa nyumba hii na nyumba nyingine zote kama hizi ambazo ziko chini ya MOIS” “MOIS ni nini?akauliza Mathew “MOIS ni wizara ya intelijensia ya Iran” akajibu Yasser “Faqir atakuja hapa leo? Akauliza Mathew “Ndiyo anakuja na daktari” akajibu Yasser na kutoka akamuacha Mathew akijiandaa. “Kila ninapovuta pumzi ninawaza wale jamaa wa G20.Nilichokiona nyumbani Tanzania kimenisikitisha sana.Baba wa taifa letu alijenga msingi imara kwa watanzania kutokubaguana kwa namna yoyote ile kwa misingi ya dini wala makabila lakini wamekuja hawa jamaa na kupandikiza chuki kubwa za kidini na wakafanikiwa kuwagombanisha watanzania.Ni kitu ambacho kimewashangaza dunia nzima.Wamesababisha damu ya watanzania ikamwagika na wengine kwenda kuishi katika makambi.Watanzania hawakuwahi kufikiri kama siku moja wangeweza kwenda kuishi katika makambi kama wakimbizi tena ndani ya ardhi yao wenyewe.Huu ni ukatili mkubwa sana” akawaza Mathew na kuuma meno kwa hasira alizokuwa nazo “Nitawalipia watanzania.Hawa jamaa hawawezi kumwaga damu nyingi ya watanzania halafu wakabaki salama.Lazima dunia ifahamu nani aliyepeleka watanzania kupigana na kuuana wenyewe kwa wenyewe.Lazima kila kitu kiwekwe wazi ili dunia ifahamu ni namna gani haya mataifa makubwa yanavyonyanyasa mataifa madogo.Dunia lazima ifahamu namna mataifa haya makubwa yanavyopora rasilimali kutoka katika mataifa yanayojitahidi kupiga hatua za maendeleo hususan mataifa ya bara la Afrika” akawaza Mathew na kutoka bafuni akakaa kitandani “Natakiwa kuanza kutafuta namna ya kutoka mahala hapa na kuanza kuifanya kazi iliyonileta.Kitu cha kwanza ni kujenga mtandao hapa Iran na ili niweze kujenga mtandao huo lazima nifanye kitu ambacho kitanifanya niaminike na hiyo itanirahisishia kuweza kukamilisha mipango yangu” akawaza Mathew na mlango ukafunguliwa alikuwa ni Yasser ambaye alimtaka Mathew akapate kifungua kinywa. Wakati Mathew akiendelea kupata kifungua kinywa, akaingia Faqir Jahid akiwa ameongozana na jamaa mmoja aliyebeba mkoba moja kwa moja Mathew akahisi Yule ndiye daktari aliyeambiwa anakuja kujua maendeleo yake. Faqir akamsalimu Mathew halafu akamtambulisha kwa Yule daktari.Mathew akaacha kupata kifungua kinywa akaongozana na Yule daktari kwenda katika chumba akagangwa majeraha yake na kupewa dawa za kuendelea kutumia.Baada ya daktari kumaliza kumganga Mathew,Faqir akampa taarifa kwamba amemletea pia mavazi ya kubadilisha kwani nguo alizokuwa nazo Mathew zilikuwa chafu na zilichafuka kwa damu “Ahsante sana Faqir” akasema Mathew “Umefahamuje jina langu? Akauliza Faqir na Mathew akatabasamu kidogo. “Ninapenda kuwafahamu watu kwa majina yao ndiyo maana nikauliza na kufahamu jina lako” akasema Mathew “Vipi maendeleo yako kwa sasa?Faqir akauliza “Ninaendelea vyema japo mwili una maumivu bado kutokana na hivi vidonda nilivyonavyo” “Pole sana.Endelea kupumzika hadi hapo utakapokuwa umepona majeraha yako ndipo maelekezo yatatolewa” akasema Faqir “Vipi kuhusu Yasser Wazir na wenzake wanaendeleaje? Mathew akauliza “Wanaendelea vyema.Wako hospitali wakitazamwa afya zao ambazo zimezorota sana” akasema Faqir na kunyamaza kidogo kama anafikiria namna ya kumuuliza kitu Mathew “Abu Zalawi taarifa ya awali waliyoitoa akina Yasser ni kwamba wewe ndiye uliyewasaidia wakaweza kurejea tena nyumbani.Ni kweli? Akauliza Faqir Mathew akameza mate halafu akajibu “Ni kweli kabisa.Nilipambana kuhakikisha wanarejea nyumbani” “Hongera sana Abu Zalawi.Wewe ni shujaa” akasema Faqir na ukimya mfupi ukapita “Hapa uko salama na kila unachohitaji utakipata usiwe na hofu yoyote.Serikali na raia wote wa Iran wanakushukuru sana kwa hili ulilolifanya kwani tulikwisha amini wale watu wetu wameuawa” akasema Faqir na kumueleza Mathew kwamba yeye anaondoka kwenda kuendelea na majukumu yake mengine “Faqir samahani kuna jambo ninataka kuzungumza nawe” akasema Mathew “Nini unahitaji Abu Zalawi? Akauliza Faqir “Jana usiku alikuja hapa Brigedia Jenerali Ahsan Javad waziri wa ulinzi wa Iran akiwa ameambatana na watu wengine wawili.Kuna Yule jamaa mnene aliyekuwa amevaa kanzu nimesahau jina lake” “Anaitwa Vahid Ghorbani.Ni mmoja wa matajiri wakubwa hapa Iran.Anamiliki viwanda mbali mbali na vile vile ana visima vya mafuta.Ni mmoja wa watu wanaoheshimika sana” akasema Faqir “Ninahitaji kuzungumza naye.Unaweza kunisaidia kumfikishia ujumbe kuwa ninataka kuonana naye? Akauliza Mathew na Faqir akatabasamu “Abu Zalawi kumfikia Vahid si jambo rahisi kwa mtu kama mimi.Sina mahusiano naye yoyote na hata namba zake za simu sina.Yule ni rafiki mkubwa wa waziri wa ulinzi” akasema Faqir “Ninahitaji sana kuzungumza naye jambo la muhimu.Tafadhali nisaidie kumfikishia ujumbe kuwa ninamuhitaji kuonana naye naamini atakuja kuniona.Au kama ukiweza nipeleke nyumbani kwake tafadhali nikaonane naye mimi mwenyewe” akasema Mathew “Abu Zalawi wewe huruhusiwi kutoka ndani ya nyumba hii kwa sasa.Hayo ndiyo maelekezo yaliyotolewa na Sassan” “Sassan ni nani? Akauliza Mathew “Sassan Mahmoud alikuja jana usiku na waziri wa ulinzi.Ni waziri wa wizara ya intelijensia na usalama wa taifa” “Kama siruhusiwi kutoka humu ndani naomba unisaidie kufikisha ujumbe kwa Vahid kuwa ninataka kuonana naye.Ni muhimu sana” akasema Mathew “Kwani kuna jambo gani la muhimu Abu Zalawi hadi utake kuonana na mtu mkubwa kama huyu Vahid? Unaweza ukanieleza tafadhali? Akauliza Faqir “Natamani sana ningekwambia Faqir lakini siwezi.Nisaidie tafadhali nionane na Vahid” akasema Mathew “Abu Zalawi ninataka sana kukusaidia lakini uwezo wangu wa kumfikia Vahid ni mdogo.Subiri labda akija Sassan utamuomba anaweza akakusaidia” “Atakuja leo huyo Sassan? Akauliza Mathew “Sina hakika kama atakuja leo hii.Sifahamu ratiba zake” akajibu Faqir “Faqir sikiliza.Ninahitaji sana kuonana na Vahid.Kuna jambo nataka anisaidie na yeye pekee ndiye anayeweza kunisaidia.Labda nikugusie kuwa wale jamaa niliowakomboa akina Yasser Wazir wako katika hatari bado” “Wako katika hatari? Akauliza Faqir “Ndiyo wako katika hatari kubwa ya kuuawa” akasema Mathew na kumstua Faqir “Nani anataka kuwaua? Akauliza Faqir “Siwezi nikakueleza kwa sasa lakini watu wale wako katika hatari kubwa na bila kupata msaada wa haraka wanaweza wakauawa hapa hapa katika ardhi ya nyumbani kwao” “Abu Zalawi umefahamuje kama kuna watu wanataka kuwaua? Akauliza Faqir “Faqir ninachokwambia ni kitu cha kweli kabisa.Endapo wakiuawa nitawaeleza wakubwa zako kwamba nilikutaarifu juu ya jambo hili na ukanipuuza” akasema Mathew “Kama hicho unachokizungumza ni kitu cha kweli basi taarifa hizi nitazifikisha kwa taasisi husika ili waongeze ulinzi mahala walipo wale jamaa” akasema Faqir “Hapana hatupaswi kufanya hivyo.Tafadhali naomba umtafute Vahid aje hapa nizungumze naye.Lengo ni kuwasaidia hawa raia wenu ambao walikuwa wamepotea kwa miaka mingi waweze kuwa salama” akasema Mathew “Abu Zalawi naomba hiki unachokisema kiwe ni kitu cha kweli vinginevyo …..” “Usihofu Faqir.Ninachokueleza ni kitu cha kweli kabisa” “Sawa ngoja nitafute namna ya kumpata Vahid na kumfikishia ujumbe huu na kama atakubali basi nitakujulisha” akasema Faqir na kutoka “Ninahitaji kuwasiliana na Habiba na mtu pekee ambaye ninaweza kutumia simu yake kuwasiliana naye ni Vahid.Naamini akipata ujumbe wangu kwamba ninamuhitaji lazima atafika hapa mara moja.Imekuwa vizuri kwa Habiba kutengeneza mtandao wake sehemu mbali mbali” akawaza Mathew Faqir baada ya kutoka chumbani kwa Mathew akaingia garini na kuondoka. “Anachokisema Abu Zalawi ni kitu cha kweli? Amefahamuje kama kuna mpango wa kuwaua wale jamaa waliorejea jana? Hana simu wala kifaa chochote cha mawasiliano amepata wapi taarifa hizi? Akajiuliza Faqir “Lakini ni vipi kama jambo hili likawa kweli na watu wetu wakauawa? Mambo mengine si ya kupuuza.Ngoja nifikishe ujumbe kwa Vahid kama Abu alivyoomba” akawaza Faqir
Faqir aliwasili katika makazi ya Vahid Ghorbani.Bado Vahid alikuwepo nyumbani kwake.Faqir akakaribishwa ndani ambako Vahid alikuwa katika chumba cha chakula akipata kifungua kinywa. “Karibu tupate kifungua kinywa” akasema Vahid na Faqir akajumuika mezani.Baada ya kumaliza kupata mlo ule wa asubuhi wakaelekea sebuleni kuzungumza “Karibu sana kijana.Tumewahi kuonana? Akauliza Vahid “Hapana mzee naamini hunifahamu ila mimi nakufahamu.Naitwa Faqir Jahid ni mfanyakazi wa MOIS idara ya nyumba za siri.Jana usiku ulifika katika mojawapo ya nyumba za siri za MOIS ukiwa na waziri wa ulinzi na waziri wa intellijensia na usalama wa Taifa” akasema Faqir na Vahid akastuka kidogo “Kuna mtu mmoja anaitwa Abu Zalawi amenituma kwako anahitaji kuonana nawe” akasema Faqir Jahid na Vahid akavuta pumzi ndefu na kutazama juu “Abu Zalawi ! akasema Vahid kwa sauti ndogo na kuinamisha kichwa akionekana kutafakari jambo “Abu Zalawi anataka kitu gani? Sitaki ukaribu naye.Watu wanaweza wakaanza kuhisi na mimi nina mashirikiano na magaidi kama nitaendelea kuonana naye mara kwa mara.Nitamweleza Habiba Jawad asinitume tena kwa Yule jamaa.Sitaki kuharibu jina na sifa yangu nzuri kwa watu kunihisi nina shirikiana na hawa magaidi” akawaza Vahid “Mzee Vahid nipeleke jibu gani kwa Abu Zalawi? Akauliza Faqir “Nitakwenda kuonana naye lakini siwezi kwenda pale peke yangu lazima niwe na mwenyeji” “Usihofu mzee mimi nipo kama utahitaji kwenda kuonana naye nitakupeleka” akasema Faqir “Nisubiri kidogo” akasema Vahid na kuelekea chumbani kwake akachukua simu na kumpigia Habiba Jawad “Habari za asubuhi Vahid” akasema Habiba “Habiba nimepokea ujumbe kutoka kwa Abu Zalawi kwamba anahitaji kuonana nami asubuhi hii” akasema Vahid “Ana tatizo lolote? Habiba akauliza “Hajasema chochote kama ana tatizo ama vipi yeye ametuma ujumbe nikamuone” “Vahid naomba ukaonane naye tafadhali.Nafahamu ni usumbufu mkubwa unaupata lakini naomba ukaonane naye kwani asingeweza kuomba kuonana nawe kama hana jambo la muhimu” akasema Habiba “Nitakwenda kuonana naye lakini nitaomba uzungumze naye na umwambie mimi ni nani ili aniheshimu.Mtu mwenye heshima kubwa kama mimi sitakiwi kuitwa itwa na g………..” akasema Vahid na kusita “Hutaki kuitwa na gaidi.Nadhani ndivyo ulitaka kusema” “Samahani Habiba kama nitakukera lakini nilipata taarifa kuwa Abu Zalawi ni gaidi na ndiye aliyelipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.Nilisikitika mno kwa mtu kama huyu kumuoa mwanangu Najma.Ninamsaidia kwa sababu yako Habiba vinginevyo nisingethubutu hata kuzungumza naye.Habiba wewe mwenyewe unanifahamu vizuri sipendi sana magaidi na ndiyo maana hata mimi nawe tulishindwa kufunga ndoa baada ya kugundua kwamba unafadhili makundi ya kigaidi” akasema Vahid “Vahid bado hufahamu chochote kuhusu mimi wala Abu Zalawi.Naomba ukamsikilize na kama kuna tatizo lolote naomba umsaidie” akasema Habiba akionekana kutokufurahishwa na maneno aliyoyasema Vahid “Sawa Habiba ninakwenda huko nitakujulisha nini kimejiri nitakapotoka lakini naomba hii iwe ni mara ya mwisho.Sitaki watu waanze kuhisi kuwa nina mashirikiano na magaidi” akasema Vahid na kukata simu “Habiba ni mwanamke niliyempenda mno hadi nikazaa naye mtoto lakini nilipogundua kuwa ana fadhili makundi ya kigaidi nikaachana naye.Nawachukia mno magaidi lakini ngoja tu niende nikaonane na Abu Zalawi nijue ana tatizo gani” akawaza Vahid na kutoka akaongozana na Faqir wakaelekea katika nyumba aliko Mathew.
“Abu Zalawi habari za leo” akasema Vahid baada ya kufika mahala aliko Mathew Mulumbi “Ahsante kwa kuja Vahid na samahani sana kwa usumbufu” akasema Mathew “Usijali Abu Zalawi.Niambie kitu gani umeniitia hapa? Akauliza Vahid akionekana kuwa na haraka “Vahid kubwa ambalo nimekuitia hapa ninataka kuzungumza na Habiba Jawad” akasema Mathew “Hilo tu? Akauliza Vahid “Ndiyo Vahid ni muhimu sana” akasema Mathew na Vahid akachukua simu akazitafuta namba za Habiba Jawad akapiga halafu akampa Mathew simu ambaye alimtaka Vahid atoke nje ili aweze kuzungumza na Habiba “Hallow Vahid” akasema Habiba Jawad baada ya kupokea simu “Ni mimi Abu Zalawi” akasema Mathew “Mathew habari yako” “Nzuri mama.Vipi wewe unaendeleaje? “Ninaendelea vizuri.Kuna nini Mathew hadi ukataka kuonana na Vahid? “Nilihitaji kuzungumza nawe ndiyo maana nikamtumia ujumbe Vahid nionane naye” akasemaMathew “Vahid hajafurahishwa na amekuja kuonana nawe kwa sababu yangu.Kuna nini unataka kuniambia? “Ninakaribia kuianza kazi niliyotumwa kuja kuifanya lakini ili niweze kuikamilsha kazi hiyo napaswa kujenga kwanza mtandao na ili nipate mtandao natakiwa kufanya kitu kitakachowafanya waniamini” “Unataka kufanya nini Mathew? Akauliza Habiba “Ninataka kuwaanika majasusi wa Mossad walioko hapa Iran.Serikali ya Iran inafahamu kuwa kuna majasusi wa Israel hapa Iran lakini haiwafahamu ni akina nani na wako wapi.Nitakapowafumbua macho majasusi hao ni akina nani na wako wapi nitakuwa nimewasaidia kitu kikubwa sana hivyo nahitaji msaada wako katika hilo.Tafuta namna unavyoweza kufanya ili kuipata orodha ya majasusi wa Israel walioko hapa Iran.Nikifanikiwa kuipata orodha hiyo itanisaidia kunikutanisha na viongozi wa hapa na hapo ndipo nitakapoanza kazi yangu” akasema Mathew “Mathew hilo ni wazo zuri sana tatizo ni namna ya kuweza kuipata orodha hiyo ya majasusi wa Israel walioko Iran” akasema Habiba “Mama Habiba wewe una mtandao mkubwa hata ndani ya mashirika haya ya kijasusi hivyo fanya kila linalowezekana niweze kuipata hiyo orodha ya majasusi wa Mossad ikiwezekana leo hii hii” akasema Mathew “Sawa nitajitahidi niweze kuipata na nitakapofanikiwa nitakujulisha” akasema Habiba “Nashukuru sana mama.Naomba uliwekee uzito jambo hilo.Vipi kuhusu wale jamaa kule Marekani? Kuna taarifa zozote umezipata kutoka kwao? Akauliza Mathew “Mpaka sasa bado sijapata taarifa zozote kutoka kwao.Usijali kila nitakachokipata nitakujulisha”akasema Habiba Jawad na ukimya mdogo ukapita halafu Habiba akasema “Mathew kuna jambo lingine ninataka kukufahamisha” akasema Habiba na kunyamaza kidogo “Hivi tuzungumzavyo Nawal yuko angani anarejea Riyadh akitokea Tanzania” “Nawal alikwenda Tanzania? Akauliza Mathew “Ndiyo Mathew.Nawal alikwenda Tanzania kutekeleza misheni muhimu niliyomtuma.G20 walikuwa na mpango wa kusambaza kirusi hatari nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha kuwepo Afrika Mashariki kwa muda mrefu zaidi ili waendelee na uporaji wa rasilimali.Baada ya kuufahamu mpango huo nikamtuma Nawal kwenda kuuharibu .Nawal akishirikiana na Ruby na timu yake wamefanikiwa kuzima jaribio hilo la kusambaza kirusi hatari nchini Tanzania na nchi iko salama” akasema Habiba “Nawal amekutana na Ruby? Akauliza Mathew “Ndiyo.Amekutana na Ruby na wameshirikiana katika misheni hiyo” akasema Habiba “Ahsante sana mama Habiba kwa msaada huu mkubwa.Naamini bila wewe kuwa na taarifa hizo hivi sasa nchi ya Tanzania ingekwisha ingia katika janga lingine kubwa la watu kupoteza maisha.Mama ninazidi kuwa na hasira na hawa watu na ninaapa lazima nihakikishe ninarudi tena Marekani kuwamaliza.Hawawezi kutufanyia mambo mabaya kama haya na wakabaki salama” akasema Mathew akiwa amejaa hasira “Mathew kuna jambo lingine nataka kukufahamisha.Nawal anakuja Tehran” “Anakuja huku?! Mathew akashangaa “Ndiyo anakuja Tehran kukusaidia” akajibu Habiba “Hapana mama.Nawal hapaswi kabisa kuja huku.Hii ni misheni ya hatari mno mama.Nawal hapaswi kabisa kufika hapa! Akasema Mathew “Mathew hili si ombi.Nawal anakuja Tehran kukusaidia.Mathew misheni hii ni hatari sana na wewe uko peke yako.Lazima uwe na mtu anayeweza kukusaidia.Usihofu hatavuruga misheni yako bali anakuja ili kukupa msaada pale itakapohitajika” akasema Habiba “Mama sidhani kama hilo ni wazo zuri kwa sasa” akasema Mathew “Mathew kama nilivyokwambia kwamba hili si suala la kujadili.Nimekwisha fanya maamuzi Nawal anakuja Tehran.Mathew hii ni misheni kubwa na lazima utahitaji msaada” akasema Habiba na kuagana na Mathew “Kila uchao hasira dhidi ya watu hawa wanaojiita G20 zinaongezeka.Ninatafakari adhabu mbali mbali wanazostahili watu hawa bado sijapata jibu lakini kitu nitakachowafanyia kitabaki katika historia ya Marekani.Sikujua kama walikuwa na mpango mwingine wa kwenda kusambaza virusi nchini Tanzania kwa lengo la kuendeleza uporaji wa rasilimali zetu.Kule Tanzania tunasema za mwizi arobaini.Hawa jamaa wamefikisha siku ya 39 arobaini yao iko kwenye kona.Laiti kama wangefahamu wangeanza kujiandaa kutoka sasa kwani tufani inayowakaribia ni kubwa” akawaza Mathew “Naamini Nawal atakuwa amekiacha kirusi hicho Tanzania.Ninatamani kirusi hicho kingerejeshwa Marekani ili kikawaangamize wao wenyewe lakini hatupaswi kufanya hivyo kwani hatutakuwa na tofauti na wao.Wamarekani hawafahamu kile kinachoendelea nchini mwao na hawana habari kama kuna kikundi kinajiita G20 ambacho kinafanya mambo ya kikatili kabisa sehemu mbali mbali duniani hasa barani Afrika kwa lengo la kupora rasilimali kama vile mafuta na madini.Bara la Afrika limekuwa likigubikwa na migogoro ya mara kwa mara.Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanaibuka kila mara katika nchi za Afrika na ukiichunguza mingi ya migogoro hiyo ina mkono wake kutoka nchi hizi kubwa ambazo zinafaidika kwa kuchochea migogoro hiyo.Wanapata soko la kuuza silaha,wanapora mali nk.Kwa bahati mbaya sana kuna waafrika wenzetu ambao kwa tamaa za mali wamejikuta wakishirikiana na mabeberu hawa katika kuwasaliti wenzao na hata kuchochea mifarakano.Natamani niitangazie dunia hata sasa kile kinachoendelea lakini ngoja nivute subira nimalize misheni yangu hapa Iran ili niweze kupata kibali cha kuingia tena Marekani kukimaliza kikundi cha G20” akawaza Mathew na kukumbuka kuwa alikuwa na simu ya Vahid.Akaufungua mlango na kumfuata Vahid sebuleni alikokuwa amekaa akizungumza na Faqir “Nashukuru sana mzee kwa msaada huu mkubwa” akasema Mathew Vahid akaipokea simu ile na kusimama akamtaka Mathew wasogee pembeni wazungumze “Kijana naamini tayari umemaliza shida yako” “Ndiyo mzee.Nilihitaji sana kuzungumza na Habiba jambo la muhimu” “Hii ni mara yangu ya mwisho kufika hapa.Kama ukihitaji kuzungumza tena na Habiba tafuta namna nyingine ya kuwasiliana naye lakini si kunitumia ujumbe nyumbani kwangu.Sina mashirikiano yoyote na magaidi mimi ! akasema kwa ukali Vahid na kuanza kuondoka akimuacha Mathew amesimama akimtazama. “Sipaswi kukasirika.Napaswa kuvumilia.Ninamshukuru hata hivyo kwa msaada alionisaidia kuzungumza na Habiba mara mbili.Kwa sasa ngoja niendelee kusubiri majibu kutoka kwa Habiba” akawaza Mathew na kurejea chumbani kwake. WASHINGTON DC – MAREKANI Imetimu saa nane za usiku,bado kikao kizito kiliendelea katika ikulu ya Marekani kati ya Rais William Washington na wakuu wa vyombo vya ulinzi vya Marekani.Kikao hicho kilitokana na taarifa ya kustusha waliyoipata kutoka Tanzania kwamba kambi ndogo ya vikosi vya Marekani vilivyoko nchini Tanzania ilivamiwa na watu wasiojulikana ikashambuliwa na kuteketezwa kabisa huku wanajeshi wote waliokuwepo kambini usiku h uo wakiuawa. Wakati kikao kikiendelea,walikuwa wakipokea taarifa mbali mbali kutoka kwa makamanda walioko Tanzania vile vile waliweza kuonyeshwa moja kwa moja picha za kambi yao namna ilivyoharibiwa vibaya sana na wavamizi.Taarifa nyingine iliyowastua ni kwamba kuwa nyumba aliyokuwa akiishi mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko Tanzania Jenerali William nayo pia ilivamiwa na watu wasiojulikana,wanajeshi kadhaa wakauawa na Jenerali William haikufahamika mahala alipo.Jumla ya wanajeshi waliouawa katika matukio hayo mawili walikuwa thelathini na moja. Saa kumi usiku kwa saa za Marekani ndipo kikoa kilipomalizika.Baada ya kikao kumalizika Rais William hakwenda kulala alikuwa na kikao kingine muhimu na makamu wa Rais.Moja kwa moja wakaenda katika chumba cha mazungumzo ya faragha.Bado Mark Piller alikuwa anazungumza na mtu simuni.Baada ya muda akalazimika kumuomba radhi mtu yule aliyekuwa akizugumza naye simuni na kukata simu. “Mark nimechanganyikiwa na hiki kilichotokea ! akaanzisha mazungumzo Rais William Washington “Mheshimiwa Rais kweli hili ni jambo la kustusha mno lakini tunapaswa tuwe watulivu wakati tunasubiri kupata taarifa rasmi nini kimetokea na nani waliofanya shambulio hilo” akasema Mark Piller na ukimya ukapita. “Mark” akaita Rais William na Mark Piller akainua kichwa akamtazama “Tumetazama namna kambi ilivyoharibiwa vibaya na wanajeshi wetu walivyouawa kikatili.Kwa haraka haraka picha gani inakujia kuhusu waliofanya tukio lile? Akauliza Rais William “Kwa haraka haraka picha ninayoipata ni kwamba wavamizi walifanya shambulio la kustukiza.Inaonekana wanajeshi wetu hawakuwa wakifahamu kama watashambuliwa.Picha nyingine ninayoipata wavamizi walikuwa wamejihami kwa silaha nzito sana na ndiyo maana wakaweza kuwaua wanajeshi wetu” akasema Mark Piller “Tutajadili kwa kina sana jambo hili lakini swali ambalo linatakiwa kutawala vichwa vyetu muda huu ni nani waliofanya shambulio lile na kwa nini?Unadhani ni…ah ! ninazidi kuchanganyikiwa Mark” akasema Rais William na kugonga meza kwa hasira “Halafu mbona hakuna maiti hata moja ya watu waliovamia? Je hakuna hata mmoja aliyeuawa? Akauliza William “Mheshimiwa Rais tukio hili lina utata mkubwa.Ukizitazama picha za sehemu ya tukio ninahisi wanaoweza kufanya shambulio kama hili ni watu wenye uwezo mkubwa na mbinu za hali ya juu za mapigano.Raia wa kawaida hawana mafunzo ya hali ya juu namna hii ya kuweza kusambaratisha kambi na kuua wanajeshi wetu wote wenye uwezo mkubwa katika mapigano” “Nini unamaanisha Mark? “Yawezekana ..”Mark akasita “Nini Mark? Kama kuna kitu unakihisi kiweke wazi ! akasema Rais William “Ninajaribu kujenga picha mbali mbali kichwani kwangu lakini ninashindwa kuziunganisha.Tusubiri tupate taarifa kutoka kwa wanajeshi wetu walioko huko Tanzania ambao wanaendelea na uchunguzi watatupa picha nzuri zaidi” akasema Mark “Mark tuliweke kwanza pembeni suala hilo nimetaka tuje hapa tuzungumze kuhusiana na ule mpango wenu wa kusambaza kirusi” akasema Rais William na Mark akavuta pumzi ndefu “Mheshimiwa Rais,muda mwingi wa kikao nilikuwa nazungumza na simu nikiwasiliana na wenzagu ili tufahamu kinachoendelea.Taarifa si nzuri hata kidogo” akasema Mark na sura ya Rais William ikaonesha mstuko “Kuna nini kimetokea? Akauliza “Kwa taarifa nilizopewa na wenzangu wanaoendelea kufuatilia suala hili ni kwamba mtu tuliyemtuma kwenda kusambaza kirusi alifika salama Dar es salaam na alikabidhiwa kwa Jenerali William ambaye ndiye atakayeratibu zoezi zima la usambazaji akisaidiana na Assad Ismail kutoka IS.Taarifa ya kuvamiwa kwa nyumba anamoishi Jenerali William na wanajeshi waliokuwa wakilinda nyumba hiyo kuuawa na Jenerali William kutoweka kinaleta wasiwasi mkubwa sana kuhusu ule mpango wetu wa kusambaza kirusi” akasema Mark Piller na ukimya ukatawala tena “Huyo mtu wenu wa IS anapatikana simuni? Akauliza Rais William “Hapatikani” akajibu Mark Piller “Mark kuna wazo linanijia japo sijui kama lina msingi wowote.Hudhani kama watu wa IS wanaweza kuwa wamehusika katika shambulio hili? Akauliza Rais William “IS? Akauliza Mark Piller “Ndiyo.Hudhani kama wanaweza kuwa wamehusika katika jambo hili? “IS hawawezi kuhusika kabisa katika shambulio hili kwa sababu tunashirikiana nao na tunawalipa pesa nyingi sana vile vile tunawawezesha kwa silaha na mambo mengine kadhaa” akasema Mark Piller “Nimejiwa na wazo hilo kwa sababu yawezekana labda IS wakawa wanakihitaji hicho kirusi na wakaamua kufanya shambulio hilo ili wakichukue na kukitumia katika mambo wanayoyajua wenyewe” akasema Rais William “Hilo unalosema mheshimiwa Rais linawezekana lakini hawa jamaa tumekuwa tunashirikiana nao kwa muda mrefu.Hawawezi kutufanyia hivi” akasema Mark Piller “Kama si wao basi nani aliyefanya shambulio lile? Akauliza Rais William “Mheshimiwa Rais kwa sasa tunahangaika kujua mahala alipo Jenerali William.Yeye ndiye anayefahamu mahala kilipo kirusi na akipatikana basi tutafahamu kila kitu” akasema Mark Piller “Mark hebu nisaidie mawazo nini tufanye? Mimi nimechanganyikiwa hapa” akasema William “Rais wa Tanzania umekwisha zungumza naye? Akauliza Mark Piller “Hapana bado sijazungumza naye” “Zungumza na Rais wa Tanzania yawezekana akawa na taarifa ambazo sisi hatuna kuhusiana na shambulio hili.Naamini vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania navyo vinalichunguza jambo hili na yawezekana tayari wamepata fununu Fulani kuhusu nani waliofanya shambulio hilo” akasema Mark na simu yake nyingine ambayohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ huiweka katika mfuko wa koti ikaita akaitoa mfukoni akatazama mpigaji alikuwa ni Habiba Jawad.Rais William akamtazama kwa macho ya udadisi “Ni Habiba Jawad” Mark akamwambia Rais kisha akaipokea ile simu “Hallow Habiba” “Mark habari za usiku huu.Samahani kwa kukuamsha kama ulikuwa umelala” akasema Habiba “Hapana sijalala.Usiku mzima wa leo umekuwa ni wa vikao mfululizo.Naamini umepata taarifa za kile kilichotokea nchini Tanzania.Kambi yetu imeteketezwa na wanajeshi wengi wameuawa.Ni shambulio baya kabisa” akasema Mark Piller “Tayari nimekwisha zipata taarifa hizo.Poleni sana kwa tukio hilo baya.Tayari mmekwisha fahamu nani waliofanya shambulio hilo? Akauliza Habiba “Mpaka sasa haijafahamika nani waliofanya tukio hilo.Habiba tukio hili limeathiri pia ule mpango wetu wa kusambaza kirusi” akasema Mark Piller na kunyamaza kidogo “Sattar Sayf Al Din alifika Tanzania na alipokewa na mkuu wa vikosi vya Marekani anaitwa Jenerali William ambaye ndiye tuliyemkabidhi jukumu la kumsaidia Sattar katika mpango wa kusambaza kirusi hicho.Nyumba anayoishi Jenerali William nayo pia imevamiwa na watu wasiojulikana walinzi wake wameuawa na yeye mwenyewe ametoweka hajulikani mahala alipo.Yeye ndiye mwenye taarifa zote kuhusiana na kirusi.Tumekwama na tunaendelea kusubiri kama Jenerali William atapatikana ili tujue kuhusiana na kirusi kama kiko salama” akasema Mark Piller “Vipi kuhusu Assad Ismail naye pia hapatikani simuni? Yeye pia alikuwa anategemewa kumsaidia Sattar katika usambazaji wa kirusi hicho” “Assad naye hapatikani simuni.Hili jambo linatuchanganya sana Habiba” “Kama wote hawapatikani yawezekana wako sehemu salama wamejificha na watajitokeza baada ya muda kupita.Au tayari wako katika usambazaji wa kirusi” akasema Habiba “Hapana Habiba hilo haliwezekani.Jenerali William ndiye mkuu wa vikosi vya Marekani kama angekuwa amejificha sehemu hadi muda huu ambao inakaribia saa tano za asubuhi nchini Tanzania angekuwa amekwisha jitokeza lakini hadi sasa hajulikani alipo.Hii inaongeza wasiwasi zaidi na kikubwa tunachotaka kukifahamu ni kama kirusi kiko salama.Mtu pekee ambaye anazo taarifa zote za kuhusiana na kirusi hicho ni Jenerali William” akasema Mark Piller “Mmejiridhisha katika miili iliyopatikana hakuna mwili wa Jenerali William au Sattar au Assad? Akauliza Habiba “Hakuna mwili wa Jenerali William wala hao wengine.Kukosekana kwa miili hiyo katika orodha ya waliouawa inatupa picha kwamba yawezekana wakawa hai.Swali ni je wako wapi? Akauliza Mark Piller “Kama miili yao haijapatikana miongoni mwa wale waliopoteza maisha basi kuna uwezekano mkubwa wakawa hai.Ninaamini watakuwa amejificha sehemu Fulani na baada ya muda watajitokeza au yawezekana tayari usambazaji wa kirusi umeanza” akasema Habiba “Tuliweke hilo pembeni Habiba tunaendelea kulifuatilia.Nini sababu ya kunipigia simu? Akauliza Mark Piller “Nimekupigia simu kuhusiana na ile misheni anayoendelea nayo Abu Zalawi kule Tehran” akasema Habiba “Nini kinaendelea huko? Kuna taarifa yoyote nzuri? Akauliza Mark “Nimewasiliana na Abu Zalawi nikampa taarifa kuhusiana na ule mpango wake wa kumuua.Kuna kitu ameniomba nimsaidie” “Safi sana Habiba.Ahsante kwa kumfikishia taarifa hiyo kwa haraka.Amekuomba umsaidie nini? Akauliza Mark Piller “Abu Zalawi anataka kuanza kuifanya kazi yake kwa kujenga mtandao nchini Iran.Kuna kitu anakihitaji ambacho kitamsaidia katka mpango huo” akasema Habiba “Sema Habiba,Abu Zalawi anahitaji kitu gani? Akauliza Mark Piller “Anahitaji orodha ya majasusi wa Mossad walioko nchini Iran” akasema Habiba “Anahitaji orodha ya majasusi wa Mossad?! Mark Piller akashangaa “Ndiyo Mark.Anaihitaji orodha hiyo ya majasusi wote wa Mossad haraka” akasema Habiba na Mark Piller akavuta pumzi ndefu “Hilo ni jambo lisilowezekana Habiba.Hatuwezi kuipata orodha hiyo ya majasusi wa Mossad.Hata kama tungeweza kuipata orodha hiyo hatuwezi kuitoa kwa mtu yeyote kwa sababu kwa kufanya hivyo tutakuwa tumehatarisha usalama wa majasusi hao kwani watajulikana na wanaweza kuuawa” akasema Mark Piller “Mark kwa namna yoyote ile lazima orodha hiyo ipatikane.Abu Zalawi anaihitaji mno ili kuweza kujenga mtandao.Hii ni misheni kubwa na lazima kufanya kila linalowezekana ili ifanikiwe.Abu Zalawi anahitaji kujenga mahusiano na viongozi wa Iran na orodha hiyo ndiyo itakayomfanya aaminiwe na awe na mahusiano mazuri na viongozi.Mark ninakuomba fanya kila uwezalo kuhakikisha orodha hiyo inapatikana tena kwa haraka” akasema Habiba “Habiba narudia tena kusema kwamba hilo ni jambo lisilowezekana kabisa.Hakuna namna ninayoweza kuipata orodha hiyo ! akasema Mark Piller “Mark umewasaliti wenzako ili misheni ya Abu Zalawi ikamilike hivyo ni wajibu wako kuhakikisha unafanya kila linalowezekana ili misheni hii ikamilike.Usiogope kuwaanika majasusi wa Mossad kwani kitakachopatikana katika misheni hii ni kikubwa na kina umuhimu pia hata kwa Israel kwani hata wao wamekuwa wakipokea vitisho vya mashambulio kutoka kwa Iran.Mark hii ni nafasi imepatikana hivyo usiiache ikapotea bure.Kila atakachokihitaji Abu Zalawi anatakiwa akipate ! akasema Habiba.Mark Piller akafikiri kidogo na kusema “Habiba siwezi kukuahidi chochote kwa sasa.Naomba unipe muda nilifanyie kazi jambo hili” akasema Mark “Mark suala hili ni la leo hii hii halihitaji kuchukua muda mrefu” “Sawa Habiba,nitakupa majibu baadae kidogo.Naomba unipe muda nione ninavyoweza kufanya” “Sawa Mark ninakutegemea” “Habiba tukiliweka hilo pembeni kuna jambo nataka tuzungumze na yawezekana unaweza ukatusaidia kupata jawabu” “Nini unahitaji Mark? “Tumetazama picha za eneo la tukio limeharibiwa vibaya mno na waliofanya shambulio hilo lazima watakuwa ni watu waliojihami kwa silaha nzito.Tunahisi yawezekana kundi la IS limehusika katika shambulio hili” “IS? Habiba akashangaa “Ndiyo” akajibu Mark “IS wamekuwa wakishirikiana nanyi na wao ndio waliotakiwa kusambaza kirusi.Iweje wabadilike na kufanya shambulio? “Tunahisi labda walikuwa wanakitaka kirusi” akajibu Mark Piller “Hapana Mark.Sina hakika kama IS wanaweza wakafanya jambo kama hilo” “Habiba hatujasema kwamba IS wamefanya hilo shambulio ila tunahisi kwamba yawezekana wakawa wanahusika.Tunataka utusaidie kufanya uchuguzi kujua kama wamehusika na kama wamehusika kirusi kiko wapi? Akasema Mark Piller “Mark nitafanya uchunguzi huo kujua kama kweli wamehusika kwa namna yoyote na shambulio hilo nikipata chochote nitakujulisha” akasema Habiba “Tunashukuru sana Habiba.Tunatakiwa kusaidiana kuhakikisha tunakipata kirusi” akasema Mark Piller na kuagana na Habiba Jawad “Nilikuwa nazungumza na Habiba Jawad.Nimemuomba atusaidie kufanya uchunguzi kufahamu kama IS wanahusika kwa namna yoyote na tukio la Dar es salaam” Mark akamwambia Rais William “Amesemaje ulipomtaka afanye uchunguzi huo? “Amekubali kufanya uchunguzi huo na atanijulisha kile atakachokuwa amekipata.Hata hivyo dhumuni kuu la kunipigia ni kunipa taarifa za maendeleo ya misheni ya Abu Zalawi” akasema Mark Piller na rais William aliyekuwa amegeukia ukutani akageuka haraka “Anaendeleaje Abu Zalawi? Akauliza Rais William “Abu Zalawi tayari yuko Tehran na taarifa ya mpango wa kuuawa imekwisha mfikia” “Vizuri”akasema William “Abu Zalawi anajiandaa kuianza kazi yake lakini kuna kitu anakihitaji ambacho ni kigumu kidogo” “Anataka nini? Akauliza Rais William “Anataka apatiwe orodha ya majasusi wa Mossad walioko nchini Iran” akasema Mark “Anataka orodha hiyo aifanyie nini? Akauliza Rais Wiliam “Anataka awaanike kwa serikali ya Iran” “Kwa nini anataka kufanya hivyo? Hajui kwa kufanya hivyo majasusi hao watakuwa katika hatari kubwa ya kuuawa? Iran na Israel hazina mahusiano mazuri hivyo wakiwagundua majasusi wa Israel walioko nchini Iran watawaua wote.Hilo ni jambo la hatari kabisa Mark” “Ni kweli mheshmiwa Rais, ni jambo la hatari kubwa kwa majasusi hao lakini Abu Zalawi anataka kuitumia orodha hiyo kwa ajili ya kutengeneza mtandao.Kwa kuwapa Iran orodha hiyo ya majasusi wa Israel anaamini kwamba watamuamini na kumuweka karibu zaidi” akasema Mark Piller “Bila orodha hiyo ya majasusi wa Israel hataweza kuendelea na kazi aliyotumwa? Akauliza Rais William “Kwa mujibu wa Habiba Jawad ni kwamba Abu Zalawi anadai orodha hiyo ni muhimu sana aipate tena leo hii hii” akajibu Mark Piller.Rais William akatafakari kidogo halafu akauliza “Wewe una maoni gani Mark juu ya suala hilo? “Tumefanya maamuzi kwamba Abu Zalawi aendelee na misheni yake hivyo lazima tuhakikishe tunamsaidia kwa kila iwezekanavyo ili aweze kufanikisha misheni hiyo muhimu.Hatuna namna mheshimiwa Rais lazima tuhakikishe tumeipata orodha hiyo na kumpatia Abu Zalawi” akasema Mark Piller “Lakini Mark kwa kufanya hivyo tutakuwa tumehalalisha majasusi wa Israel wauawe.Iran hawatawaacha salama” “Mheshimiwa Rais hapa tumebanwa katika kona hatuna namna ya kufanya zaidi ya kumpatia Abu Zalawi hicho anachokitaka.Tayari damu nyingi imekwisha mwagika hadi hapa tulipofika hivyo hakuna tatizo kama tukiwatoa sadaka majasusi hao wachache wa Mossad ili tuweze kufanikisha lengo letu.Endapo misheni hii ikifanikiwa itakuwa na msaada mkubwa pia hata kwa Israel yenyewe ambayo imekuwa ikipokea vitisho vya kushambuliwa na Iran” akasema Mark Piller “Mark hili jambo linanitatiza sana .Kwanza ni namna ya kuweza kupata orodha hiyo na pili hata kama tukifanikiwa kuipata orodha hiyo tukampa Abu Zalawi na majasusi wa Israel wakauawa ni vipi kama Israel ikigundua kwamba sisi ndio tuliotoa orodha hiyo kwa Iran? Hili jambo linaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana kati ya nchi zetu” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais naomba nikutoe hofu kuhusu jambo hili.Kwanza kuhusu kuipata orodha hiyo tunaweza kuipata.Si jambo gumu sana kuipata orodha hiyo.Nikiamua kuipata siwezi kushindwa.Kuhusu wasiwasi kwamba Israel wanaweza wakagundua sisi ndio tuliowaanika majasusi wao kwa Iran hilo haliwezi kutokea kwa sababu Iran hawajui kama tunashirikiana na Abu Zalawi na Israel hawatajua chochote kama sisi ndio tuliowaanika majasusi wao kupitia kwa Abu Zalawi.Nakuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba orodha hiyo itapatikana kwa namna ambayo Mossad hawataweza kugundua chochote” “Una uhakika Mark? “Naomba uniamini mheshimiwa Rais.Jambo hili litafanywa kitaalamu sana na halitakuwa na madhara yoyote kwetu” akasema Mark Piller “Mark kama una uhakika jambo hilo linawezekana na halitakuwa na madhara yoyote kwetu fanya hivyo tafadhali.Tunahitaji mno misheni hii ikamilike na kwa kuwa tumekwisha kubali kufanya kila linalowezekana ili misheni hii ifanikiwe hatuna namna,hakikisha Abu Zalawi anapata kila anachokihitaji ili mradi tuwe na umakini mkubwa sana ili mambo haya yasije yakatuletea tena mgogoro mwingine mkubwa na washirika wetu kama Israel” akasema Rais William “Ahsante sana mheshimiwa Rais.Ninakuahidi hakuna kitakachoharibika.Kila kitu kitakwenda vizuri” akasema Mark Piller na ukimya mfupi ukapita “Mark kuna jambo lingine nataka tushauriane.Tayari imekwisha fahamika kwamba ndege ile ya Marekani ambayo ilidhaniwa imeangukia baharini,imeelekea Iran.Waziri wa mambo ya nje anajiandaa kutoa tamko mapema asubuhi kuitaka Iran irejeshe ndege yetu pamoja na raia wake wote waliokuwamo ikiwamo mtuhumiwa wa ugaidi Abu Zalawi.Unaonaje mpango huo? Hautaweza kuvuruga misheni ya Abu Zalawi? Akauliza Rais William “Hapana mheshimiwa Rais hautaweza kuvuruga misheni ya Abu Zalawi.Hata Iran wanajua tumekwisha fahamu ndege yetu imeelekea nchini kwao.Tukikaa kimya watakuwa na wasiwasi kwa nini tumekuwa kimya? Muache waziri wetu wa mambo ya nje atoe tamko lake hapo asubuhi tena liwe ni tamko kali kabisa” akasema Mark Piller “Hudhani baada ya tamko hilo,Iran wanaweza wakamfukuza Abu Zalawi au wakamtaka aondoke kimya kimya hivyo misheni yetu ikashindwa kufanikiwa? Akauliza Rais William “Iran hawawezi kwa namna yoyote ile wakamfukuza au kumuondoa Abu Zalawi nchini kwao.Ni mtu muhimu kwao kwanza amewakombia watu wao muhimu ambao naamini walikwisha wasahau na kuamini wameuawa,pili atakuwa na umuhimu mkubwa zaidi kwao pale atakapo wakabidhi orodha ya majasusi wa Israel walioko nchini Iran” akasema Mark Piller “Ahsante kwa ushauri huo Mark lakini lazima nizungumze na Rais wa Tanzania nijue wamefikia wapi katika uchunguzi na vile vile nataka kufahamu kuhusu Jenerali William” akasema Rais William na kuchukua simu yake yenye namba za simu za marais wote wa dunia akazitafuta namba za Rais wa Tanzania akampigia. DAR ES SALAAM – TANZANIA Habari kuu iliyotawala vinywani mwa watu jijini Dar es salaam,Tanzania nzima na dunia kwa ujumla ni shambulio lililofanywa usiku na watu wasiojulikana katika kambi ndogo ya vikosi vya jeshi la Marekani iliyoko kandoni mwa bahari jijini Dar es salaam.Jambo hili lilizusha hofu kubwa miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar ambalo kwa siku mbili hakukuwa na vurugu zozote zilizoripotriwa na taratibu hali ya maisha ilianza kurejea na kuwa ya kawaida.Watu walianza kuondoka katika makambi yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya kuwahifadhi watu waliokuwa wanakimbia mapigano na kurejea katika majumba yao.Baadhi ya masoko na maduka makubwa yalianza kufunguliwa japo yalikuwa chini ya ulinzi mkali. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo akiwa ofisini kwake alimaliza mazungumzo na mkuu wa jeshi la polisi nchini kuhusiana na hali halisi ya usalama ilivyo katika jiji la Dar es salaam na katika miji mingine hasa Tanga. “Nashukuru sana kwa hali ya amani kuimarika kwa kiasi kikubwa.Hii inachangiwa kwanza na watanzania kutokuzoea mambo haya ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na vile vile kitendo cha SNSA kuwakamata magaidi waliokuwa wanachochea vurugu hizi kimechangia sana kwa vurugu kukoma.Ruby na wenzake wamefanya kazi kubwa sana” Akawaza Dr Fabian ambaye alitolewa mawazoni baada ya simu yake kuita.Akaichukua kutazama mpigaji alikuwa ni Rais wa Marekani.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “Kazi imeanza” akasema kwa sauti ndogo na kuipokea simu ile “Hallo mheshimiwa Rais William habari za muda huu? Naamini ni usiku mwingi huko kwenu” “Ni kweli mheshimiwa Rais Dr Fabian,ni usiku mwingi hapa Marekani lakini bado tunaendelea na kazi.Vipi hapo Dar es salaam mnaendeleaje? “Sisi tunaendelea vizuri japo usiku wa kuamkia leo kumetokea tukio baya ambalo naamini tayari umekwisha pata taarifa zake” “Suala hilo ndilo limenifanya nikupigie simu Dr Fabian” akasema William na kunyamaza kidogo “Sikuweza kukupigia simu kwa haraka mara tu baada ya kupata taarifa za tukio hilo kwani tumekuwa na mfululizo wa vikao kujaribu kulitafakari shambulio hilo na kupata taarifa kutoka kwa makamanda wetu walioko hapo Dar es salaam.Tumeonyeshwa picha za tukio tumesikitishwa mno na jambo hili.Kabla sijaendelea zaidi naamini vyombo vyako vya ulinzi na usalama viliingia kazini kuanzia muda lilipotokea shambulio hilo,mmefikia wapi hadi sasa katika kuwafahamu waliofanya shambulio hilo? Akauliza Rais William “Mheshimiwa Rais kwanza kabisa ninapenda kutumia nafasi hii kutoa pole nyingi sana kwako na kwa wananchi wa Marekani kwa hiki kilichotokea na kuwapoteza wanajeshi wengi.Ni tukio baya sana na halivumiliki.Wanajeshi hao walikuwepo hapa nchini kwa ajili ya kulinda amani na hawakustahili haya yaliyowakuta” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo “Mara tu baada ya kupata taarifa za shambulio hilo,vikosi vya jeshi la wananchi wa Tanzania vilivyokuwa doria vilifika eneo la tukio kwa haraka sana lakini tayari wavamizi hao walikwisha ondoka.Shughuli za uokozi kujaribu kutafuta majeruhi zilianza mara moja lakini hawakufanikiwa kumpata yeyote aliye hai.Nilitoa maelekezo usiku huo huo kwamba msako uanze haraka sana kuwatafuta wale waliofanya shambulio hilo na mpaka sasa vyombo vyetu vya uchunguzi vikishirikiana na wataalamu wa jeshi la Marekani walioko hapa wanaendelea na uchunguzi wa jambo hili na watatupa taarifa rasmi pale watakapokuwa wamefanikiwa kugundua chochote.Ni msiba mkubwa sana mheshimiwa Rais” akasema Dr Fabian “Dr Fabian utanisamehe kwa hili nitakalolisema lakini nitalazimika kutuma vyombo vya uchunguzi kutoka Marekani kuja kuwatafuta watu waliofanya shambulio hilo.Tunahitaji kujua kwa haraka sana nani walioshambulia kambi yetu na kuua wanajeshi wetu” akasema Rais William “William hakuna haja ya kutuma wachunguzi kutoka Marekani.Tanzania ina vyombo vya uchunguzi vyenye ujuzi na weledi mkubwa sana nina uhakika mkubwa waliofanya tukio hili watapatikana hata kama haitakuwa mapema kama unavyotaka lakini lazima watapatikana” akasema Dr Fabian “Dr Fabian Marekani tuna vyombo vyenye uwezo mkubwa sana na nina imani ndani ya muda mfupi watakuwa wamegundua nani waliofanya tukio hi…..” “Mheshimiwa Rais William nina imani na vyombo vyangu vya ndani hivyo uchunguzi wa suala hili utafanywa na vyombo vya uchunguzi vya Tanzania na sintaruhusu wachunguzi wowote wa kutoka nje” akasema Dr Fabian “Dr Fabian una historia ya kutoruhusu wachunguzi kutoka nje ya nchi yako pale kunapotokea shambulio baya katika nchi yako likilenga mali au watu wa kutoka mataifa ya kigeni hata kama vyombo vya uchunguzi vya nchi yako havina uwezo wa kutosha kulifanyia uchunguzi jambo hilo.Tulioshambuliwa ni sisi na tunataka kushirkiana na vyombo vyenu katika kuwatafuta waliotufanyia hivi.Ugumu uko wapi? Akauliza Rais William “Rais William kwanza nakuomba ufute kauli yako ya kwamba vyombo vya Tanzania havina uwezo wa kutosha ! akasema kwa ukali Dr Fabian “Huo ni ukweli Dr Fabian kama kweli vyombo vyako vingekuwa na uwezo mkubwa mpaka hivi sasa tayari mngekwisha fahamu nani walioshambulia kambi yetu ! mkuu wa vikosi vya Marekani hapo Tanzania Jenerali William nyumba yake pia imevamiwa, wanajeshi waliokuwa wanamlinda wameuawa na hadi sasa Jenerali William hajulikani alipo na vyombo vyako vimekuwa vikichunguza toka usiku hadi muda huu na bado hamna hata fununu za nani wameshambulia na kuua watu wetu.Huu ni udhaifu mkubwa wa vyombo vyako Dr Fabian..” akasema Rais William “Rais William sintavumilia dharau hizo dhidi ya vyombo vyangu vya uchunguzi.Narudia tena kukuhakikishia kwamba tukio hilo limetokea katika ardhi ya Tanzania na litachunguzwa na vyombo vya Tanzania.Hakuna chombo chochote cha uchunguzi kutoka nje kitakachoruhusiwa kuingilia uchunguzi unaofanywa na vyombo vya Tanzania ! akasema kwa ukali Dr Fabian “Dr Fabian sielewi kwa nini unapata kigugumizi katika jambo hili.Au kuna kitu hutaki kijulikane? Akauliza Rais William “Vyovyote utakavyofikiria William lakini narudia tena kauli yangu kwamba uchunguzi wa shambulio katika kambi ya wanajeshi wa Marekani utafanywa na vyombo vya uchunguzi vya Tanzania pekee.Pale uchunguzi utakapokuwa umekamilika basi tutawapeni taarifa nani waliohusika katika shambulio hilo.Mheshimiwa Rais kama hauna jambo lingine la kuzungumza zaidi ya hili ninaomba nikuache nina kikao muhimu kinanisubiri” akasema DrFabian “Ni hilo tu kwa sasa Dr Fabian nitawasiliana nawe tena baadae saa kumi na mbili kwa saa za Afrika mashariki nifahamu kama mmekwisha wafahamu waliofanya shambulio hilo na kama Jenerali William amepatikana ! akasema Rais William na kukata simu “Mataifa haya makubwa yana dharau sana mataifa kama yetu kwamba hatuwezi chochote katika masuala ya ulinzi na usalama.Ninaamini muda si mrefu sana tutawaumbua na hawataamini macho yao ! akawaza Dr Fabian na kuchukua simu akampigia Ruby “Ruby uko wapi? Niliwataka mje hapa ikulu baada ya kutoka uwanja wa ndege” akasema DrFabian “Tumekaribia mheshimiwa Rais ndani ya dakika chache tutakuwa hapo” akajibu Ruby “Fanyeni haraka nina vikao vingi siku ya leo.Kuna masuala ya msingi nataka kuzungumza nanyi” akasema Dr Fabian “SNSA walifanya kazi nzuri sana kwani mpaka sasa hakuna hata fununu za nani waliofanya shambulio lile kwa mujibu wa mkuu wa jeshi la polisi.Kinachofuata ni kuviondoa vikosi vya Marekani hapa nchini bila wao kujua kama tayari tumefahamu kinachoendelea nyuma ya pazia.Ninajilaumu sana kwa kukubali haraka haraka msaada wao lakini sikujua kama walikuwa na ajenda yao iliyojificha” akaendelea kuwaza Ruby na Gosu Gosu waliwasili ikulu kuonana na Rais.Siku zote Dr Fabian azungumzapo na akina Ruby hupenda kutumia chumba cha mazungumzo ya faragha ili kuzuia mtu mwingine asiweze kusikia mazungumzo yao. “Poleni sana naamini hamjapata muda wa kupumzika kutokana na kazi kubwa mliyokuwa nayo.Msichoke vijana wangu hadi pale tutakapohakikisha tumewaondoa mabeberu hawa nchini kwetu na Afrika Mashariki kwa ujumla” akasema Dr Fabian “Hatujachoka mheshimiwa Rais na hatuwezi kuchoka hadi pale tutakapohakikisha beberu wa mwisho ameondoka katika nchi yetu hivyo tutaendelea kukesha macho kupigania nchi yetu” akajibu Ruby “Mungu anaipenda sana nchi yetu na ndiyo maana ameweza kuwaumbua wabaya wetu na tumeweza kuifahamu mipango yao miovu dhidi yetu.Muda mfupi uliopita nimezungumza na Rais wa Marekani .Alitaka kufahamu kama tayari tumekwisha wapata waliofanya shambulio lile nikamjibu vyombo vya uchunguzi viko kazini vinaendelea kuwatafuta akadai atatuma timu ya wachunguzi kutoka Marekani kuja nchini kuchunguza tukio hilo lakini nilimkatalia nikamwambia kwamba tukio hili litachunguzwa na vyombo vya ndani hakuna mtu kutoka nje ya Tanzania atakayeruhusiwa kuja kuchunguza kitu chochote hapa nchini.Mazungumzo yetu hayakuisha vizuri kwani alitoa dharau kwa vyombo vyetu kwamba havina ujuzi mkubwa lakini pamoja na dharau hizo nimesimamia msimamo wangu kwamba hakuna mchunguzi kutoka nje ya nchi ataingia hapa nchini” “Ahsante sana mheshimiwa Rais kwa maamuzi hayo” akasema Ruby “Nilitamani nimweleze ukweli kwamba tumekwisha fahamu kile wanachotufanyia lakini nikajizuia kutomweleza chochote kwa sasa hadi pale mambo yote yatakapokuwa yamekamilika.Nawapongeza mlifanya kazi nzuri kwani hadi sasa hakuna hata dalili za kuwafahamu nani waliofanya shambulio katika kambi yao.Baada ya tukio la jana nataka kufahamu nini kinafuata? Akauliza Dr Fabian “Tunao watu muhimu tunawashikilia ambao tutaendelea kuwahoji ili kuupata mtandao mzima uliohusika kuchochea vurugu za kidini zilizopelekea vifo vya watu wengi hapa nchini.Tunaye Jenerali William na vile vile tunaye Assad Ismail.Kupitia kwao tutawafahamu watu wote waliokuwa wanashirikiana nao”akajibu Ruby “Nataka kufahamu hatima ya huyu Jenerali William kwani tayari amekwisha julikana ametoweka na wanamtafuta.Mnadhani kuendelea kumshikilia hakutakuwa na madhara yoyote kwetu? “Huyu jamaa tutaendelea kumshikilia na atatusaidia kutoa ushahidi wa kile ambacho alitumwa kuja kukifanya hapa Tanzania na Afrika Mashariki.Ni mtu muhimu sana ambaye hatuwezi kumuachia kwa sasa.Huyu ni mmoja wa watu waliochangia katika machafuko yaliyotokea hapa nchini.Atakiri kila kitu” akasema Ruby “Huyu ni mwanajeshi mna uhakika anaweza akakubali kufunguka na kutoa siri za nchi yake? Akauliza Dr Fabian “Usihofu mheshimiwa Rais atafunguka na kueleza kila kitu.Tutatumia kila mbinu kuhakikisha anafunguka” akajibu Gosu Gosu “Vizuri sana.Hili jambo linatakiwa lifanyike haraka ili tuwafahamu watu ambao wamekuwa wakishirikiana nao hapa nchini,tuwakamatwe haraka kabla hawajatoroshwa ili kuharibu ushahidi” akasema Dr Fabian “Tutafanya hivyo mheshimiwa rais” akasema Ruby “Jambo lingine.Jana tulizungumza kuhusu namna ya kuviondoa vikosi vya Marekani hapa nchini na tulikubaliana kwamba tuwaondoe kimya kimya kwa kukata kile ambacho wamekifuata yaani mafuta.Damu yote hii iliyomwagika ya waganda na watanzania ni kwa sababu ya mafuta hivyo pale watakapoyakosa hawatakuwa na sababu ya kuendelea kuviweka vkosi vyao hapa Tanzania na Uganda wataviondoa mara moja.Tulikubaliana kulipua sehemu ya bomba la mafuta” akasema Dr Fabian na kufungua droo ya kabati akatoa karatasi kubwa akaiweka mezani.Ilikuwa ni ramani ya bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga Tanzania. “Hii ndiyo ramani ya bomba la mafuta kutokea Uganda hadi Tanga.Ninawakabidhi ninyi jukumu hili.Mtaipitia ramani hii na kuchagua sehemu ambapo mtalipua sehemu ya bomba.Kazi hiyo nataka ifanyike usiku wa leo.Sitaki hadi asubuhi ya kesho Marekani waendelee kuchota mafuta kwani baada ya kulipua kipande hicho mafuta yatafungwa na wamarekani hawatapata kitu tena hivyo hawatakuwa na sababu ya kuendelea kuwepo hapa nchini.Nadhani mmenielewa vijana wangu” “Tumekuelewa mheshimiwa Rais na tunakuahidi kazi nzuri” akasema Ruby “Nawashukuru sana.Muda wowote mtakapohitaji msaada wa aina yoyote nijulisheni haraka sana” akasema Dr Fabian kisha wakaagana Ruby na Gosu Gosu wakaondoka. WASHINGTON DC – MAREKANI Saa mbili za asubuhi kwa saa za Marekani John Pasero anayefanya kazi CIA aliwasili katika makazi ya makamu wa Rais Mark Piller.Alishuka garini na kuelekea ndani ambako makamu wa Rais alikuwa anajiandaa kuelekea ofisini kwake.Wakasalimiana halafu John akatoa bahasha na kumpatia makamu wa Rais “Ile kazi yote uliyonituma iko humu” akasema John “Ahsante sana John.Umekwisha ipitia na kuthibitiosha kwamba ni halisi? “Ndiyo nimeipitia na kujiridhisha ni halisi”akasema John “Sitaki kujua namna ulivyoweza kuipata orodha hii lakini naamini imechukuliwa kitaalamu sana kiasi kwamba haitakuwa na matatizo upande wetu” akasema Mark Piller “Usihofu mheshimiwa,jambo hili limefanywa kwa umakini mkubwa sana na hakuwezi kukawa na tatizo lolote kwetu.Tunao mawakala wetu ndani ya Mossad ambao ameweza kufanikisha orodha hii ikapatikana” akasema John “Safi sana John” akasema Mark Piller na kuelekea ndani akatoka na bahasha iliyokuwa na fedha akamkabidhi John wakaagana akaondoka zake.Mark Piller akaenda katika ofisi yake ndogo akaifungua ile bahasha aliyopewa na John ndani yake kulikuwa na diski mweko akaishika mkononi akaitazama “Tunafanya kitu cha hatari sana hiki.Hawa majasusi wakijulikana watakuwa katika hatari kubwa ya kuuawa lakini lazima tufanye hivi kwa maslahi ya nchi yetu” akawaza Mark Piller na kuirejesha ile diski mweko katika bahasha akaiweka katika mfuko wa ndani wa koti halafu akajiandaa kuelekea ofisini. Mark Piller alipowasili ofisini kwake, kitu cha kwanza alichokifanya ni kwenda kuonana na rais William Washington “Mark kuna maendeleo yoyote toka tulipoachana? Akauliza Rais William “Maendeleo ni makubwa mheshimiwa Rais.Nimefanikiwa kuipata ile orodha tuliyoihitaji” akasema Mark na Rais William akashusha pumzi “Safi sana.Lakini imekuwa mapema sana” “Nimemtumia mmoja wa vijana wangu ndani ya CIA kuipata orodha hiyo.CIA tunao mawakala wetu ndani ya Mossad hivyo haikuwa kazi ngumu kuweza kuipata orodha hiyo” akasema Mark Piller na kuitoa ile bahasha akamuonesha Rais William “Kila kitu kiko humu” akasema Mark “Mark hili ni jambo gumu sana lakini lazima tulifanye.Ila bado ninatoa angalizo kwamba kila juhudi lazima ifanyike ili kuhakikisha Israel hawafahamu kama sisi ndio tuliowaanika majasusi wao” akasema Rais William “Narudia tena kukuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba kila kitu kimeandaliwa vizuri na hakutakuwa na tatizo lolote kwa upande wetu” “Sawa Mark.Tulipoachana nilizungumza na Rais wa Tanzania lakini mazungumzo yetu hayakwenda vizuri.Amekataa timu ya wachunguzi wetu kwenda kuchuguza shambulio lile akadai watalichunguza wao nikajikuta nikipandwa na hasira na hatukupata muafaka wowote lakini hadi muda ule hawakuwa wamepata taarifa zozote za nani wameshambulia kambi yetu” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais,hukupaswa kutumia hasira na wala Rais wa Tanzania hapaswi kuona kama vile tunalazimisha watu wetu waende kufanya uchunguzi.Utakapozungumza naye wakati mwingine itabidi ujishushe kidogo umuombe msamaha kama kuna maneno ulimtamkia ambayo si mazuri” “Hapana Mark siwezi katu kujishusha kwa mtu mweusi ! akasema Rais William kwa sauti ya ukali “Mheshimiwa Rais sisi ndio tunaotafuta kitu,hivyo lazima tutumie kila aina ya mbinu.Tumfanye Rais wa Tanzania awe rafiki yetu na tujizuie kutumia kauli za kumshinikiza afanye vile tunavyotaka sisi.Twende naye taratibu” akasema Mark Piller na Rais William hakujibu kitu na mara ujumbe ukaingia katika simu ya Mark akaufungua akausoma “Mheshimiwa Rais nitakujulisha baadae kile kinachoendelea.Kuna mtu ananisubiri ofisini” akasema Mark Piller na kutoka akaelekea ofisini kwake “David Walker” akasema Mark Piller baada ya kuingia ofisini kwake na kumkuta David Walker akimsubiri. “Karibu sana David” akasema Mark Piller “Ahsante sana Mark” akajibu David na Mark akafunga mlango ili aweze kuzungumza na David “Mark nimepita hapa mara moja kukupa mrejesho wa kile kinachoendelea hadi muda huu” akasema David na kunyamaza kidogo “Mpaka sasa bado hatuna taarifa zozote za kuhusiana na kirusi kilipo.Nimekuwa na mawasiliano ya karibu na mkuu wa majeshi na bado taarifa ya mwisho ni ile ile kwamba mwenye taarifa zote za kuhusiana na kirusi ni Jenerali William.Yeye ndiye aliyekabidhiwa kirusi hicho baada ya Sattar kuwasili Dar es salaam.Tumekwamia hapo kwani watu wetu wote hawajulikani walipo.Tumejaribu kuwasiliana na viongozi wa IS nao pia hawajui watu wao akina Assad Ismail wako wapi.Wote wametoweka.Mark tunahitaji sana kujua mahala walipo hawa watu.Tunahitaji kujua kama ni miongoni mwa watu waliofariki au vipi.Nimepita hapa kwako nikiamini labda ninaweza kupata taarifa ya tofauti na ile ya mkuu wa majeshi” akasema David Walker macho yake yakiwa mekundu na hii ni kutokana na kutokulala usiku.Mark Piller akavuta pumzi ndefu na kusema “Ni kweli usiku mzima nilikuwa na rais na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama tukipokea taarifa mbali mbali kutoka Tanzania.Tayari miili yote ya wanajeshi imekwisha tambuliwa lakini hakuna mwili wa Jenerali William,Sattar wala Assad Ismail” akasema Mark Piller “Mungu wangu ! Nini hiki kimetokea? akasema David Walker na kukuna kidevu. “Rais amezungumza na Rais wa Tanzania kwa simu akamuuliza kuhusiana na uchunguzi wa jambo hili lakini mpaka sasa hakuna taarifa yoyote waliyoipata ya nani walioshambulia kambi yetu” akasema Mark Piller “Mark hili suala linaumiza mno vichwa vyetu na hasa suala la kupotea kwa Jenerali William na akina Sattar.Sisi hatutakiwi kupoteza muda kufuatilia nani kashambulia kambi au nani kaua sisi tunachohitaji ni kujua kirusi kiko wapi? Je kiko salama?Mtu pekee wa kutupa majibu ya maswali hayo ni Jenerali William ambaye hajulikani alipo hadi hivi sasa.Nguvu kubwa tuielekeze hapo kujua mahala alipo Jenerali William” akasema David Walker na ukimya mfupi ukapita “Mark itumie nafasi yako kama makamu wa rais kuhakikisha tunafahamu mahala alipo Jenerali William.Bila kumpata huyu mtu misheni yetu itakuwa imeharibika.Kama kuna ulazima wa kutuma hata kikosi maalum kwenda kumsaka shughulikia hilo! Mshinikize Rais aongeze mbinyo kwa serikali ya Tanzania hata kama ikibidi kutumianguvu basi itumike ili kumpata Jenerali William ! Kama tuliweza kumpata na kumuua Osama Bin Laden hatuwezi kushindwa kumpata mtu wetu katika nchi kama Tanzania ! akasema David Walker “David kuna kitu ninakihisi.Ni vipi kama Jenerali William amekwenda na akina Sattar kuanza kazi ya usambazaji wa kirusi? Nimekuwa na hisia hizo kwamba yawezekana hakutaka kupoteza muda akaamua kukisambaza kirusi hicho mara moja kwani ukiangalia wote wametoweka tena kwa wakati mmoja” akasema Mark.David akafikiri kidogo na kusema “Hilo linawezekana lakini nyumba aliyokuwa anaishi tumeambiwa nayo imevamiwa na watu wote kuuawa.Je aliondoka kabla wavamizi hawajafika? Halafu taarifa inasema kwamba anayekosekana si Jenerali William peke yake bali pia kuna wafanyakazi wengine wawili waliokuwa wakihudumu katika nyumba hiyo aliyokuwa akiishi nao pia hawajulikani walipo.Kama amekwenda kusambaza kirusi je amekwenda nao? Kama amekwenda nao ni kwa madhumuni gani? Walikuwa na umuhimu wowote? Halafu jukumu la kusambaza kirusi halikuwa la Jenerali William.Yeye jukumu lake lilikuwa ni kumpokea Sattar na kumkabidhi kwa Assad na kuwasaidia waweze kufanikisha usambazaji.Mark mpaka hapo bado unaamini Jenerali William amekwenda kusambaza kirusi?Akauliza David Walker na Mark Piller akazama mawazoni kwa muda halafu akasema “Sina hakika David” akajibu Mark Piller “Mark kazi kubwa tuliyonayo ni kuhakikisha tunajua mahala alipo Jenerali William.kama nilivyokwambia kwamba unapaswa kuitumia vyema nafasi yako kuhakikisha tunalifahamu hili” akasema David “Nitajitahidi.Vipi kuhusu mpango wa kumteka Habiba Jawad unaendeleaje? Akauliza Mark “Tayari kuna timu imetumwa Riyadh na…” David akatazama saa yake ya mkononi “Naamini hadi muda huu watakuwa tayari wamekwisha fika” “Vizuri sana.Mpango wa kumteka umekaaje? Lazima uwe ni mpango ulioandaliwa kipekee kabisa ili isijulikane kama sisi ndio tuliomteka Habiba.Nilitoa angalizo awali kwamba Habiba ana mahusiano ya karibu na mfalme wa Saudi Arabia ambaye ni mshirika mkubwa wa Marekani” “Tumeuandaa mpango vizuri Mark usihofu.Habiba hafahamu chochote hivi sasa.Nitampigia simu na kumtaka aende sehemu Fulani akakutane na mtu mwenye ujumbe muhimu na akienda huko atatekwa na kupelekwa katika ubalozi wetu jijini Jerusalem.Baada ya kumpeleka Jerusalem tutawaita Mossad na watathibtisha kwamba tunaye Habiba ili waweze kuharakisha zoezi la kumuua Abu Zalawi” “Sawa David.Utanijulisha kile kitakachokuwa kinaendelea katika mipango yote.Mimi nitashughulikia suala la Jenerali William.Halafu kuna suala lingine ambalo nimekuwa nikilifikiria.Je IS hawawezi kuwa wanahusika na shambulio hili? Akauliza Mark Piller “Kwa nini umehisi hivyo Mark? David naye akauliza “Kwa namna shambulio lilivyotokea inaonesha wazi kwamba limefanywa na watu waliokuwa wamejiandaa vilivyo tena kwa silaha nzito.Sina hakika lakini ninahisi yawezekana IS wamehusika katika shambulkio hili na ndiyo maana Assad na watu wake wote wametoweka na hatujui mahala walipo” akasema Mark Piller.David Walker akafikiri kwa muda na kusema “IS wana sababu yoyote ya kufanya hivyo? Wamekuwa ni washirika wetu wa muda mrefu.Tumewawezesha kwa silaha na tunawapa fedha nyingi kupitia Habiba Jawad” akasema David walker “Ni vipi kama nao wanakihitaji kirusi kwa ajili ya mipango yao ya kigaidi au hata kukiuza kwa mataifa mahasimu zetu ? Akauliza Mark Piller na ukimya mfupi ukapita “Hilo ni wazo la msingi Mark.Tusilidharau tulifanyie uchunguzi kwa sababu haiingii akilini watu wote hawa wakatoweka kwa wakati mmoja na hawajulikani walipo.Yawezekana IS wametugeuka wakamteka Jenerali William wakaua wanajeshi wetu,wakavamia pia kambi wakaondoka na kirusi” “Niachie mimi suala hili nitalifanyia kazi.Hadi jioni ya leo tutakuwa na majibu ya kutosha kuhusu suala hili” akasema Mark Piller na kuagana na David Walker . Baada ya David kuondoka,Mark akachukua simu anayoitumia kuwasiliana na Habiba akampigia “Hallo Mark Piller” akasema Habiba “Habiba habari ya muda huu” “Nzuri Mark.Habari za huko kwenu? “Huku bado mambo si mazuri.Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kuhusiana na tukio la Tanzania.Kibaya zaidi hakuna taarifa zozote za kumuhusu Jenerali William au akina Sattar” akasema Mark “Mark tuvute subira tutafahamu walipo.Kama hawapo katika orodha ya watu waliouawa basi wapo sehemu Fulani.Mimi pia ninaendelea na ule uchunguzi kama IS wanahusika katika shambulio hilo nikipata chochote nitakujulisha” akasema Habiba “Jitahidi Habiba ili tulifahamu jambo hili kwani kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo suala hili linavyozidi kuwa gumu.Tuachane na hilo nimekupigia kwa ajili ya mambo mawili.Kwanza ni kukupa taarifa kwamba ile orodha nimeipata” “Umeipata? Habiba akauliza “Ndiyo nimeipata.Nitakutumia muda si mrefu.Jambo la pili ni kuhusiana na ule mpango wa kukuteka” akasema Markna kumuelezea Habiba mpango wote ulivyoandaliwa “Mark nakushukuru sana kwa taarifa hizo.Kuhusu usalama wangu usiwe na hofu nimekwisha jiandaa vya kutosha.Kitu cha msingi nitumie hiyo orodha nianze kuifanyia kazi” akasema Habiba “Nitakutumia muda si mrefu Habiba” akasema Mark Piller na kuagana na Habiba kwa miadi ya kuwasiliana tena baadae kupeana taarifa za kile kinachoendelea. RIYADH – SAUDI ARABIA Saa kumi na mbili za jioni ndege ya Rais wa Tanzania iliyombeba Nawal iliwasili jijini Riyadh katika uwanja wa ndege ambao hutumiwa na Habiba na familia yake.Nawal aliwashukuru marubani wa ndege ile kwa kumfikisha salama Riyadh na kuwatakia safari njema ya kurejea Tanzania.Uwanjani pale alipokewa na wasaidizi wa Habiba akaondoa kuelekea katika makazi ya Habiba Jawad. “Karibu tena Nawal.Nimefurahi mno kuiona tena sura yako.Wewe na Mathew ni watoto pekee nilio baki nao hivyo kukuona tena ni faraja kubwa mno kwangu” akasema Habiba Jawad akimkaribisha Nawal katika makazi yake baada ya kuwasili akitokea Tanzania “Hata mimi nimefurahi sana kuonana nawe tena mama Habiba” akasema Nawal. “Nawal najua umechoka na safari ndefu lakini pamoja na uchovu wa safari nataka ukajiandae kuna kazi ya kufanya usiku huu” akasema Habiba “Usijali mama mimi nipo tayari kwa kazi muda wowote.Niambie ni kazi gani natakiwa kuifanya” akasema Nawal “Nilikueleza kuhusu mpango wa G20 wa kutaka kumua Mathew Mulumbi.Mpango wenyewe tayari umeanza.Ili Israel itume majasusi wake wamuue Mathew wanataka CIA iwathibitishie kwamba niko katika mikono yao na baada ya kumuua Mathew nitakabidhiwa kwao.Tayari majasusi wamekwisha tumwa kuja kuniteka na kunipeleka Israel katika ubalozi wa Marekani ambako nitakaa hapo kabla ya kukabidhiwa kwa Israel lakini CIA mpango wao ni kuniua kabla ya kunikabidhi kwa Mossad” akasema Habiba “Nimepigiwa simu na David Walker jioni hii amenipa maelekezo ya kwenda kukutana na hao majasusi wa CIA waliotumwa kuja kuniteka.Hawafahamu kama tayari ninafahamu mipango yao.Kazi uliyonayo ni kuhakikisha unawamaliza majasusi hao wa CIA” akasema Habiba na kumuelezea Nawal namna mpango utakavyokuwa “Usijali mama utakuwa salama.Hesabu jambo hilo limekwisha malizika” akasema Nawal “Ahsante Nawal.Jambo lingine ni kwamba Mathew alihitaji orodha ya majasusi wa Mossad walioko Iran na tayari nimeipata orodha hiyo nitamtumia ili iweze kumsaidia” akasema Habiba “Anaendeleaje Mathew? Nawal akauliza “Mathew anaendelea vizuri na baada ya kuipata orodha hiyo ndipo atakapoanza rasmi kazi yake.Mambo mengi utayafahamu utakapokutana naye” akasema Habiba na Nawal akaenda kujiandaa.Habiba akaelekea ofisini kwake na kumpigia simu Vahid Ghorbani. “Habari yako Vahid” akasema Habiba baada ya Vahid kupokea simu “Habiba naomba nikuweke wazi mapema kabisa kwamba kama unahitaji msaada kuhusu Abu Zalawi utafute mtu mwingine wa kukusaidia lakini mimi sitaki tena kuwa na ukaribu na Yule gaidi” akasema Vahid “Vahid ninahitaji msaada wako na yawezekana hii ikawa ni mara ya mwisho lakini ni muhimu mno” “Unahitaji nini Habiba? Akauliza Vahid “Kuna kitu nahitaji umfikishie Abu Zalawi” “Habiba utanisamehe sitaki tena kwenda kule.Sitaki kuonekana mara kwa mara ninazungumza na Yule mtu kwani hata mimi ninaweza kuanza kuhisiwa vibaya” “Nalifahamu hilo Vahid lakini naomba unisaidie.Nakuhakikishia kwambahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ hii itakuwa ni mara ya mwisho na hutanisikia nikikuomba tena msaada.Ni jambo la muhimu mno” akasema Habiba.Vahid akafikiri kidogo halafu akauliza “Nini unataka nimpelekee Abu Zalawi? “Kuna faili nitakutumia nataka uliweke katika diski mweko na umfikishie Abu Zalawi leo hii hii” akasema Habiba “Linahusu nini hilo faili? Akauliza Vahid “Vahid utanisaidia au vipi? Akauliza Habiba “Tuma hilo faili nitalifikisha kwa Abu Zalawi ila nakuomba Habiba hii iwe ni mara ya mwisho kunituma kwa Abu Zalawi.Mimi ni mtu mwenye heshima zangu na sitaki kuanza kuhisiwa vibaya kuwa ninashirikiana na magaidi” “Nakuahidi hii itakuwa mara ya mwisho” akajibu Habiba “Sawa tuma hilo faili” akasema Vahid na Habiba akamtumia faili lenye orodha ya majasusi wote wa Mossad walioko nchini Iran. Vahid hakutaka kusumbuka kulifungua faili lile akaliweka katika diski mweko na kumpigia simu Faqir akamueleza kwamba anahitaji kuonana na Abu Zalawi.Fakiri akamuahidi kumfuata pale nyumbani kwake ili aweze kuongozana naye kuelekea katika nyumba aliko Mathew.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment