Simulizi : Siri: Jasusi/Gaidi
Sehemu Ya Tatu (3)
Mathew akiwa katika gari la jeshi la Marekani alikata kona ya kuelekea katika ubalozi wa Marekani. “I must do this ! akawaza Katika geti la kuingilia ubalozini hapo kulikuwa na ulinzi wa wanajeshi wa Marekani.Gari lile alilokuwa analiendesha Mathew likasimamishwa na Mathew akawahi kuwaeleza kuwa ndani ya gari ana watoto ambao wamewaokoa katikati ya mapigano na akatumwa kuwakimbiza pale ubalozini kupata hifadhi ya muda kabla ya kupelekwa katika kambi maalum hapo kesho.Hakuna aliyetia shaka yoyote kuhusu gari lile wote walijua Mathew ni mwenzao.Geti likafunguliwa na gari likaingia ndani. Mchana wa siku ile Mathew na akina Assad walitumia muda mrefu kujadili suala lile na kumpa Mathew maelekezo yote juu ya utekelezaji wa jambo lile.Mathew akaenda kuegesha gari mahala alikoelekezwa na kuwashusha wale watoto akawapeleka katika mahema yaliyokuwa yamewekwa nje ya ubalozi kwa ajili ya baadhi ya raia wa Marekani na wa nchi nyingine waliokwama Dar es salaam.Baada ya kuwakabidhi watoto wale Mathew akaelekea getini akaomba kutoka akaeleza kuna watoto anawafuata ambao amewaona wakiwa njiani hawana msaada.Alielekezwa achukue gari lakini akadai kwamba hana haja ya gari anakwenda kwa miguu kwa sababu si mbali na pale ubalozini.Wanajeshi waliokuwa wanalinda getini hawakuwa na wasi wasi naye kwani waliamini kwa asilimia mia moja ni mwenzao hivyo wakamuacha akatoka.Akiwa na bunduki yake mkononi alikimbia akifuata barabara.Katika jengo moja la mgahawa ambao ulikuwa umefungwa kuliegeshwa gari jeupe.Mathew alipolikaribia taa zikawashwa na kuzimwa ikiwa ni ishara akaliendea mlango ukafunguliwa akaingia ndani ambamo alimkuta Assad Ismail akiwa na watu wengine wanne. “Nimekamilisha kazi” akasema Mathew “Hakuna tatizo lolote? Hawakutia shaka?akauliza Assad “Hakuna tatizo lolote.Waliamini mimi ni mwenzao” akajibu Mathew “Safi sana” akasema Assad na kumpatia Mathew kifaa Fulani akakiwasha kikaanza kuanzika namba haraka haraka na kufikia sifuri. “Bonyeza kitufe hicho chekundu ili kazi yako iwe imekamilika” akasema Assad na Mathew bila kupepesa macho akabonyeza kile kitufe na mlipuko mkubwa ukatokea na hadi mahala pale walipokuwa wakahisi mtikisiko kutokana na bomu lile lililolipuka kuwa zito.Assad akampa Mathew mkono “Hongera Abu Zalawi umekamilisha kazi yako” akasema na kisha gari likawashwa wakaondoka.Walipishana na magari ya jeshi na zimamoto yakielekea mahala ulikotokea mlipuko.Assad alikuwa anaelekeza njia za kupita na kisha wakafika katika jengo la hoteli ambayo ilikuwa katika hatua za mwisho za ujenzi.Geti la hoteli ile kubwa likafunguliwa gari la akina Assad likaingia ndani na kuelekea moja kwa moja mahala ilikokuwa imeegeshwa helkopta ya jeshi la Marekani. “Abu Zalawi kazi yako hapa Tanzania imekamilika na sasa unaelekea Nairobi Kenya.Utaondoka na helkopta hii hadi nchini Kenya na mambo yataendelea kama nilivyokupa maelekezo.Tafadhali usiende kinyume na maelekezo niliyokupa” akasema Assad “Ahsante Assad kwa ushirikiano na msaada mkubwa ulionisaidia katika kukamilisha kazi yangu” akasema Mathew na kumpa mkono Assad wakaagana akaingia katika helkopta mlango ukafungwa na helkopta ikawashwa.Assad alisimama pembeni ya gari lake hadi helkopta ile ilipopaa na kuondoka.
Helkopta maalum ya operesheni za usiku ya makomando wa SNSA iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ya kutokutoa sauti,ilifika usawa wa nyumba ile walimokuwamo watu wa IS.Bado sehemu kubwa ya jiji la Dar es salaam ilikuwa gizani. Makomando nane waliokuwa wamevaa miwani ya kuwawezesha kuona gizani wakashuka kwa miavuli huku kila mmoja akitua katika sehemu aliyoelekezwa kwani walikwisha fanya mazoezi mchana wa siku ile.Walinzi waliokuwa zamu usiku ule wakilinda nyumba ile hawakuweza kuwaona makomando wakishuka kutokana na giza na hii iliwasaidia makomando wale waliokuwa na miwani ya kuonea gizani kuwaona na kuwamaliza kwa bunduki zao nzito zilizofungwa viwambo vya kuzuia sauti.Makomando wote walitua salama na hakukuwa na mtu hata mmoja aliyekuwa nje ya ile nyumba alibaki hai.Walimiliki eneo lote la nje la ile nyumba.Baada ya kujipanga vizuri makomando wanne wakaenda katika mlango wa mbele wa kuingilia katika ile nyumba na mmoja akachungulia ndani akawaona watu wanne wakiwa sebuleni wakizungumza.Hawakuwa na habari kama wenzao waliokuwa nje wamekwisha uawa wote.Komando Yule akawapa ishara wenzake kwamba kuna watu wanne kisha wenzake wakasogelea mlango,kiongozi wao akakinyonga kitasa cha mlango ukafunguka wakajitoma ndani.Wale jamaa waliokuwa wamekaa katika zuria walipigwa na butwaa wakakosa la kufanya baada ya kujikuta wamezingirwa na wanajeshi wenye silaha nzito.Mmoja wa wale jamaa akageuka haraka ili aweze kuchukua bastora yake lakini mkono wake haukufika katika bastora kwani kichwa chake kilifumuliwa kwa risasi toka katika bunduki nzito ya mmoja wa makomando. “Yuko wapi Marwan Hossam? Akauliza kiongozi wa makomando.Wale jamaa hawakujibu kitu. “Nawauliza tena yuko wapi Marwan? Bado wale jamaa waliendelea kuwa kimya.Akaamuru wafungwe pingu.Wakati komando mmoja akijiandaa kuwafunga pingu mmoja wa wale magaidi akainuka na kupiga ukelele huku akitaka kumvaa mmoja wa makomando lakini hakufanikiwa kitendo alichokusudia baada ya kunyeshewa mvua ya risasi na mara mlango mmoja ukafunguliwa. “Omar kuna nin.....” akauliza jamaa aliyekuwa kifua wazi na kaptura akionekana kutoka kulala “Omar ! akaita Yule jamaa huku akielekea sebuleni “Yarkud ! Yarkud ! akasema mmoja wa wale magaidi kwa lugha ya kiarabu akimtaka Yule jamaa akimbie.Yule jamaa akageuka na kutoka mbio akipita jikoni akaufungua mlango wa nyuma ili aweze kutoka lakini akapigwa teke zito akaanguka chini na kabla hajafanya chochote akajikuta amezungukwa na makomando wanne wakamuinua na kumfunga pingu.Walipommulika wakagundua kwamba Yule alikuwa ni Marwan Hossam. “Tumempata Marwan ! SNSA ofisi kuu wakajulishwa “SNSA tumempata Marwan” akasema Yule komando “Hakikisheni mnawachukua wote mtakaowakuta hapo” akaelekeza Ruby.Marwan alipelekwa sebuleni akaunganishwa na wale wenzake wawili.Nyumba ile ikapekuliwa hakukuwa na mtu mwingine na kiongozi wa wale makomando akaelekeza makomando wake wakavamie yale majengo mengine mawili.Makomando wawili wakabaki wakiwalinda wale magaidi na wengine wakaenda kuvamia katika yale majengo mawili.Watu waliokuwa ndani ya majengo yale mawili walikuwa wamejilaza wakipumzika hawakuwa na habari kama wangevamiwa.Walistukia wakiwa wamezingirwa na makomando na hawakupata nafasi ya kujitetea.Wote wakajikuta wakitiwa nguvuni.Upekuzi ukafanyika katika nyumba zile mbili na ikagundulika kwamba kulitengenezwa bomu kwani kulikutwa na baadhi ya vifaa vya kutengenezea mabomu.Chumba cha Marwan Hossam kikapekuliwa na vitu kadhaa vikachukuliwa ikiwemo simu yake ya mkononi. Baada ya kukamilisha kazi waliyotumwa walitoa taarifa ofisi kuu SNSA na helkopta ile waliyokwenda nayo ikashuka chini na kamba ikashushwa.Marwan akafungwa ile kamba maalum kisha akiwa ameshikwa na komando mmoja kamba ile ikapanda taratibu na Marwan akaingizwa katika helkopta ikaondoka.Makomando wengine walibaki wakiwalinda wale magaidi wapatao tisa.
Helkopta ya SNSA ilitua katika sehemu yake ikitokea katika operesheni maalum ya makomando waliovamia nyumba ya magaidi wa IS.Mlango wa helkopta ukafunguliwa akashuka komando mmoja kisha akamshusha Marwan Hossam.Gosu Gosu akasogea na kumchukua Marwan akaelekea ndani na helkopta ile ikaondoka kwenda kuwachukua watu wengine.Gosu Gosu akamchukua Marwan na kumpeleka katika chumba maalum cha mahojiano kilichopo mita kadhaa chini ya jengo lile akamfungia katika chumba chenye baridi kali kisha akamfuata Ruby aliyekuwa katika ofisi yake “Ruby tayari tumempata Marwan hakuna haja ya kuendelea kusubiri .Tukaanze kumuhoji mara moja ili ikiwezekana usiku huu huu tumpate pia Assad kwani hana taarifa kama wenzake wamevamiwa.Tukichelewa hadi kesho atagundua kilichotokea na atajificha itakuwa kazi ngumu kwetu kumpata” akasema Gosu Gosu kisha Ruby akaelekeza Marwan atolewe katika chumba kile cha baridi apelekwe katika chumba cha mahojiano halafu wakashuka chini “Nina muda mrefu sijawahoji watu kama hawa,ana bahati mbaya sna Marwan ameingia katika anga zangu.Leo atanena lugha zote anazozifahamu” akawaza Gosu Gosu wakiwa ndani ya lifti wakishuka chini. MPENZI MSOMAJI MATHEW AMELIPUA UBALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA IKIWA NI MWANZO WA MISHENI NZITO YA KUELEKEA IRAN,JE MISHENI YAKE ITAFANIKIWA? GOSU GOSU NA RUBY WAMEANZA KUUSAKA MTANDAO WA CHANZO CHA VURUGU TANZANIA JE WATAFANIKIWA KUWAPATA WOTE WANAOHUSIKA? NAWAL ATAFANIKIWA MISHENI YAKE YA KUZUIA KIRUSI KISISAMBAE TANZANIA? USIKOSE SEHEMU IJAYO..
“Gosu Gosu na Ruby waliingia katika chumba maalum cha mahojiano ambacho ndani yake kulikuwa na meza mbili,viti vitano na baadhi ya vifaa vingine vya kuwezesha mahojiano kufanyika.Baada ya dakika chache mlango ukafunguliwa Marwan akaingizwa ndani ya kile chumba.Aliwekwa katika kiti na kufungwa pingu.Alikuwa anatetemeka mwili kwani alitolewa katika chumba chenye baridi kali.Gosu Gosu akamtazama kwa hasira “Relax.Take a deep breath ! akasema Gosu Gosu lakini Marwan alimtazama Gosu Gosu kwa jicho la chuki. “Hata ukinitazama kwa hasira tutaelewana tu ! akasema Gosu Gosu “Jina lako nani?akauliza Gosu Gosu.Marwan akamtazama na huku akitetemeka akasema “la ‘astatie al’iijabat lak alkalaba ! akajibu Marwan kwa lugha ya kiarabu akimaanisha kwamba hawezi kuwajibu mbwa.Ruby na Gosu Gosu wakatazamana “Ninapokuuiza swali nataka ujibu aidha kwa Kiswahili au kiingereza .Umenisikia? ! akauliza Gosu Gosu huku akimtazama Marwan kwa macho yake makali yaliyoonyesha ukatili mkubwa “Nataka utuambie jina lako nani? Akauliza tena Gosu Gosu “turid miny ‘an ajyb? Aismaahu li ‘an ‘atahadath ‘iilaa sahib alkilab ty ! akasema Marwan akimaanisha “Mnataka niwajibu?Nataka nizungumze na mwenye mbwa ! Gosu Gosu akageuka na kumtazama Ruby “Ruby huyu jamaa anaonekana ana kiburi sana nami ninawapenda watu wenye viburi kama huyu.Naomba dakika tatu nimuonyeshe hapa yuko sehemu gani” akasema Gosu Gosu “Go ahead ! akasema Ruby na Gosu Gosu akainuka akaenda katika kabati akalifungua na kuchukua kopo dogo la gesi akaliwasha na kumsogelea Marwan. “madha tuhawil ‘an tfel? Akauliza Marwan akimaanisha “Nini unataka kukifanya? “Sifahamu lugha hiyo unayoizungumza lakini tutaelewana tu.Muda si mrefu tutazungumza lugha moja ! akasema Gosu Gosu na kumtandika Marwan kofi zito lililomfanya aweweseke .Kabla hajakaa sawa akakigandamiza kichwa chake juu ya meza halafu akaanza kulichoma sikio la Marwan “Aaaagghhh !! Marwan akapiga ukelele mkubwa . “Gosu Gosu stop ! akasema Ruby na Gosu Gosu akazima ile gesi.Kwa hasira Marwan akagongesha paji lake la uso katika ile meza na damu ikaanza kumtoka sehemu ya juu ya jicho iliyokuwa imechanika.Gosu Gosu akamnasa kofi halafu akamuinua kichwa “Nataka uzungumze aidha Kiswahili au kiingereza.Ukileta kiburi nitakukata masikio yako.Umenisikia? akauliza Gosu Gosu halafu akamsindikiza na kofi zito “Hawa si watu wa kucheka nao Ruby.Ni watu makatili sana wasio na ubinadamu hata kidogo hivyo ukitaka kupata taarifa kutoka kwao nawe lazima ujitoe ubinadamu uwe kama wao” Gosu Gosu akamwambia Ruby Marwan bado aliendelea kugugumia kwa maumivu yale makali ya kuchomwa sikio la upande wa kulia. “Tunaanza upya.Nataka utuambie jina lako nani?akauliza Gosu Gosu.Marwan hakujibu kitu aliendelea kutoa mguno wa maumivu “Nakuuliza kwa mara nyingine jina lako nani?akauliza Gosu Gosu akiwa amekasirika.Marwan hakujibu kitu.Kwa hasira Gosu Gosu akasimama na kuwasha lile kopo la gesi. “Mimi sipendi kuchezewa na watu kama ninyi ! akasema na kuanza kumuendea Marwan “Hapana ! Hapana ! Usinichome t….” akasema Marwan na Gosu Gosu akasimama “Kumbe unafahamu Kiswahili ng’ombe wewe ! akasema Gosu Gosu na kumtandika Marwan kofi halafu akarejea kukaa “Naomba unitazame machoni” akasema Gosu Gosu lakini Marwan alikuwa ameinamisha kichwa.Gosu Gosu akaipiga meza kwa nguvu “Inua kichwa nitazame usoni ! akasema kwa ukali na Marwan akamtazama “Mimi ni mkatili sana na ukinifanyia mchezo nitakufanyia ukatili ambao hujawahi kuushuhudia katika maisha yako.Nataka unieleze ukweli wa kila nitakacho kuuliza.Umenielewa? akauliza Gosu Gosu na Marwan akaitika kwa kutikisa kichwa “Nataka utufahamishe jina lako tafadhali ! akasema Gosu Gosu “Marwan” akajibu “Marwani nani?akauliza Gosu Gosu “Marwan Hossam ! “Marwan wewe ni mtanzania? “Hapana ninatokea Mombasa Kenya” akajibu “Hapa Tanzania umekuja kufanya nini?akauliza Gosu Gosu,Marwan akabaki kimya “Nakuuliza hapa Tanzania umekuja kufanya nini? Ukimya wa Marwan ukazidi kumchafua Gosu Gosu.Akainuka na kwenda kufungua kabati la vifaa akachukua nyundo akarejea mezani akamnasa kofi Marwan halafu kwa nguvu akaweka kiganja cha mkono juu ya meza akainua nyundo na kuishusha katika vidole Marwan akapiga ukelele kwa maumivu makali aliyoyapata. “Nimekwambia sitaki mchezo.Jibu kwa ufasaha kila ninachokuuliza ! akasema Gosu Gosu huku Marwan akirusha rusha kiganja cha mkono kwa maumivu “Mhh ! Kwa pigo hili la Gosu Gosu vidole vya huyu jamaa viko salama kweli? Ruby akajiuliza “Nini umekuja kukifanya hapa Tanzania? Akauliza Gosu Gosu “Nilikuja kuwatembelea ndugu zangu machafuko yalipotokea nikajikuta nimekwama hapa hapa” akasema Marwan “Mahala tulipoachukua wewe na wenzako kuna nyumba moja na majengo mawili yenye muundo wa bohari.Mnajishughulisha na nini mahala pale? Akauliza Gosu Gosu “Hakuna kitu tunachokifanya zaidi ya makazi” akajibu Marwan “Mko wangapi jumla yenu?akauliza Gosu Gosu “Juma tuko….” Marwan akasita “Nataka ujibu ama sivyo nitaendelea kukuharibu kiungo kimoja kimoja ! akasema Gosu Gosu “Tuko kumi na sita jumla yetu” “Una uhakika kinachofanyika pale ni makazi na hakuna kitu kingine? Akauliza Gosu Gosu “Tuko wengi ndiyo maana wengine wanaishi katika zile nyumba mbili za kuhifadhi mizigo” akasema Marwan Gosu Gosu akafunua faili lililokuwa mezani akachukua picha moja na kuiweka mbele ya Marwan “Unamfahamu huyu mtu pichani? akauliza Gous Gosu Marwan akaitazama ile picha na kusema “Hapana simfahamu” “Una uhakika humfahamu huyu mtu?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo simfahamu” akasema Marwan Gosu Gosu akachukua tena picha ya Mathew akamuonyesha “Huyu naye unamfahamu ?akauliza Gosu Gosu.Marwan akaitazama ile picha ya Mathew na kusema “Hapana simfahamu huyu mtu” “Una uhakika hujawahi kumuona huyu mtu? Akauliza Gosu Gosu “Sijawahi kumuona huyu mtu na simfahamu” akajibu Marwan.Gosu Gosu akaendelea kumtazama kwa hasira “Marwan nakuuliza kwa mara nyingine tena hawa watu niliokuonyesha picha zao unawafahamu? Akauliza Gosu Gosu “Siwafahamu” akajibu Marwan. “Mara ya mwisho.Unawafahamu hawa watu? ‘Hapana siwafahamu” akajibu Marwan. “Ruby huyu mtu ana kiburi.Nataka nimpeleke chumba cha pili.Hatuwezi kuendelea kumbembeleza wakati anafahamu kila kitu” akasema Gosu Gosu “Endelea Gosu Gosu.Fanya kila kinachowezekana hadi afunguke ! akasema Ruby. Gosu Gosu akamfungua Marwan pingu alizokuwa amefungwa akamkunja suruali na kumtoa ndani ya kile chumba akampeleka katika chumba kingine maarufu kama chumba cha pili akaufungua mlango na kumuingiza Marwan.Hiki kilikuwa ni chumba cha kutesea.Ndani ya chumba hiki kulikuwa na meza kadhaa na mitambo mbali mbali maalum kwa ajili ya kutesea.Kwa nguvu Gosu Gosu akamuinua Marwan na kumrushia juu ya meza halafu akamfunga mikono na miguu kwa mikanda maalum iliyokuwa pembeni ya meza ile.Ruby alikuwa pembeni kimya akishuhudia kile alichokuwa anakifanya Gosu Gosu “Marwan nilikutahadharisha awali kwamba mimi ni mtu mbaya sana hasa ninapokutana na watu wenye viburi na wakaidi kama wewe.Nimekuonyesha picha mbili nikakuuliza kama unawafahamu watu wale pichani ukakana kuwafahamu.Umeniudhi sana” akasema Gosu Gosu na kulichukua lile faili lenye picha kutoka kwa Ruby,akaichuka picha ya Mathew akamuoyesha Marwan “Huyu anaitwa Abu Zalawi ametokea Saudi Arabia.Nataka uniambie amekuja kufanya nini hapa Tanzania? Kwa nini akafikia mahala mnapoishi? Akauliza Gosu Gosu ` “Simfahamu na hajawahi kuishi pale tunapoishi” “Marwan nitakuharibu naomba unieleze ukweli.Abu Zalawi amekuja kufanya nini hapa Tanzania? “Simfahamu huyu mtu na sijawahi kumuona” akasema Marwa.Mara simu ya Ruby ikaita akatazama mpigaji na kumtaka Gosu Gosu aendelee,yeye akatoka nje ya kile chumba kwa ajili ya kuipokea ile simu “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby ninakuhitaji hapa ikulu haraka sana.Unaweza kuja mara moja? “Mheshimiwa Rais usiku huu tuko katika operesheni muhimu sana hivyo sintaweza kufika ila nitajitahidi kesho nifike” “Kuna nini kinaendelea hapo SNSA?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kuna jambo tunalifuatilia na tutakapokuwa tayari nitakueleza” “C’mon Ruby I need to know now ! Sina muda wa kusubiri.Niambie tafadhali nini kinachoendelea? “Mheshimiwa Rais ninaomba unipe muda kidogo niweze kulishughulikia suala hili na nitakapokuja kwako niwe na taarifa zenye uhakika mkubwa.Naomba nisikupe taarifa nusu nusu” akasema Ruby “Sawa Ruby nataka mpaka kesho jioni uwe na kitu cha kunieleza.Umenielewa?” “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” “Umekwishapata taarifa kwamba ubalozi wa Marekani hapa Tanzania umelipuliwa? “Ubalozi wa Marekani umelipuliwa?! Ruby akashangaa “Ndiyo.Tukio hilo limetokea usiku huu” akasema Dr Fabian na Ruby akabaki kimya “Ruby ! akaita Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nimestushwa sana na taarifa hizi. Kuna taarifa zozote zinazoonyesha nani wanahusika katika shambulio hilo? Ruby akauliza “Bado hakuna taarifa yoyote iliyotolewa hadi sasa kwani juhudi za uokozi zinaendelea.Tukio hili linazidi kufanya hali ya amani kuwa tete.Ninaziona kila dalili za vurugu kuhama kutoka katika machafuko ya kidini na kuhamia katika ugaidi.Hiki kilichotokea usiku huu katika ubal;ozi wa Marekani naamini ni tukio la kigaidi na halihusiani na vurugu za kidini zilizotokea ila uchunguzi unaendelea na watakapokamilisha watatujulisha” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kuna kila dalili kwamba magaidi wameanza kujipenyeza na kutumia hali hii inayoendelea hapa nchini kwa sasa kufanya mambo yao ya kigaidi kama tukio hilo la kulipua ubalozi wa Marekani.Mimi na idara yangu bado tunaendelea kutafura mzizi wa vurugu zilizotokea.Napenda nikupe uhakika mheshimiwa Rais kwamba tunaelekea pazuri na nitakapokuja kukuona kesho nitakuwa na taarifa kutosha kuhusu mahala tulipofikia hadi sasa kujua chanzo cha vurugu” akasema Ruby “Nimekuelewa Ruby.Naomba muendelee na uchunguzi wenu ii tulifahamu kwa undani zaidi suala hili” akasema Dr Fabian “Tutafanya hivyo mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kukata simu “Duh ! nani kalipua ubalozi wa Marekani? Akajiuliza Ruby “Tutajua hapo baadae kwa sasa ngoja tuendelee na zoezi letu la kuwahoji hawa magaidi” akawaza Ruby na kupiga hatua kurejea katika chumba ambacho alimuacha Marwan akiendelea kuhojiwa na Gosu Gosu.Mlinzi akamfungulia mlango akaingia ndani.Alipatwa na mstuko mkubwa kwa kile alichokishuhudia mle ndani.Sakafu ilitapakaa damu.Marwan Hossam hakuwa akitazamika.Uso wake wote ulikuwa umechafuka damu.Alikuwa anakoroma sauti yake haikuweza kutoka tena kwa maumvu aliyoyapata.Mezani kulikuwa na sikio limekatwa huku Gosu Gosu akiwa na kisu kikali akijiandaa kukata sikio lingine “Gosu Gosu ! akasema Ruby “What have you done?! Akauliza Ruby na kumnyang’anya Gosu Gosu kile kisu. “Ruby hawa si watu wa kuonea huruma.Hawa magaidi ni wanyama kabisa na wagumu mno kufunguka ! akasema Gosu Gosu aliyekuwa amechafuka damu “Gosu Gosu hapana.Hatupaswi kufanya hivi.Watu hawa wanazo taarifa muhimu sana na tunatakiwa kuwahoji na kuhakikisha wanafunguka na kutueleza kile wanachokifahamu.Tazama ulivyomfanya huyu jamaa.Hiki unachotaka kukifanya si utesaji bali ni uuaji.Amepoteza damu nyingi sana huyu jamaa na anaweza akapoteza maisha na huyu ndiye tunayemtegemea aweze kutupa taarifa za mahala alipo Assad ! akasema Ruby akionekana kutokufurahia kile alichokifanya Gosu Gosu.Haraka haraka akapiga simu kitengo cha afya wakafika haraka na kumchukua Marwan wakamkimbiza katika zahanati yao kwa matibabu “Gosu Gosu umekosea sana ! Huyu jamaa ni mtu muhimu ambaye tunamtegemea atuelekeze mahala alipo Assad.Kwa hiki ulichokifanya itatuchukua muda kufahamu mahala alipo Assad ! akasema Ruby “Ruby watu hawa ni wakatili,hawaogopi kufa na ndiyo maana wanaweza kubeba mabomu na kujilipua.Hawa si watu wa kuwahoji huku ukiwachekea.Unapowahoji watu kama hawa inakulazimu kujitoa ubinadamu na kuwa mkatili kama wao ! akasema Gosu Gosu halafu wakatazama kwa sekunde kadhaa “Ruby nakushauri usiwepo katika chumba hiki wakati ninawahoji hawa jamaa kwani mimi siogopi kumchomoa mtu moyo wake na kuuweka mezani nikaukata kata kwa kisu.Lazima tutumie nguvu vinginevyo hatutapata taarifa zozote kutoka kwa hawa jamaa” akasema Gosu Gosu huku akinawa mikono kisha wakatoka ndani ya kile chumba. “Rais alinipigia simu.Amenipa taarifa kwamba ubalozi wa Marekani umelipuliwa usiku huu” akasema Ruby “Ubalozi wa Marekani umelipuliwa? “Ndiyo” akajibu Ruby “Hawa lazima ni magaidi wa IS.Hawa jamaa tunaowashikilia lazima wanafahamu jambo hili.Ruby tuendelee kuwahoji mmoja mmoja nina uhakika atatokea mmoja ambaye atasema kila kitu” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu unanipa mashaka sana kwa namna unavyomuhoji Marwan.Kitendo ulichomfanyia sijakipenda.Najua una hasira na magaidi lakini tunatakiwa kufuata kanuni zetu namna ya kuhoji watu tunaowashikilia na kanuni zetu hazielekezi matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa kuwahoji watuhumiwa” akasema Ruby “Ruby please don’t be so soft on them ! Hakuna kuwac………..” “I’m not soft ! akasema Ruby kwa sauti kali “Gosu Gosu tafadhali niahidi kile ulichokifanya kwa Marwan hakitajirudia tena kama unataka nikuruhusu endelee kuwahoji hawa jamaa” akasema Ruby “Ruby siwezi kukudanganya kwamba nitawahoji hawa jamaa kwa lugha laini.Mimi siwezi.Kama huridhiki kwa namna nilivyomuhoji Marwan ninakuruhusu utafute mtu mwingine” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu please ! akasema Ruby “Ruby naomba niwe mkweli kwako,siwezi kuwahoji hawa jamaa kwa kutumia njia nyepesi kwani ni sawa na kuwatekenya wauaji wakubwa hawa ! Lazima nitumie nguvu ! Kama hutaridhika na aina yangu ya kuwahoji hawa magaidi tafuta mtu mwingine wa kuendelea kuwahoji hawa jamaa ! akasema GosuGosu na milango ya lifti ikafunguka.Walipotoka tu katika lifti simu ya Ruby ikaita alikuwa ni katibu wake muhtasi ambaye alimjulisha kwamba wanamuhitaji haraka katika chumba cha operesheni.Ruby na Gosu Gosu wakaelekea haraka huko. “Kuna nini?akauliza Ruby baada ya kuingia ndani ya chumba kile na kuwakuta viongozi wa idara mbali mbali ndani ya SNSA wakitazama video katika runinga “Kuna video imetumwa mtandaoni muda si mrefu” akasema Latifah na kubonyeza kitanza mbali video ile ikaanza upya.Mtu mmoja akaonekana akiwa amejifunga kitambaa kichwani akiwa nyuma ya kitambaa cheusi chenye maandishi ya kiarabu ambayo ni bendera ya kundi la IS.Mtu Yule alijitambulisha kwa jina la Abd Al ziz Atwah mmoja kati ya viongozi wa IS na katika maelezo yake alidai kwamba IS ndio wnaohusika katika kulipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam usiku ule.Wakati akina Ruby wakiendelea kuitazama video ile akaingia mkuu wa kikosi cha makomando “Mkurugenzi tumeikamilisha kazi uliyotutuma.Kwa ujumla haikuwa kazi ngumu na hatukupata upinzani wowote kwani wale jamaa hawakuwa wametegemea kama wangevamiwa.Tumeua walinzi wanne waliokuwa nje wakilinda eneo lao na tumewachukua watu wengine kumi na mbili wakiwa hai akiwemo na Marwan.Tumepekua nyumba yao tumekuta silaha nyingi na baada ya kuzichunguza tumegundua ni silaha zinazotumiwa na jeshi la Marekani.Vile vile katika moja ya nyumba zao tulikuta masalia ya baadhi ya vifaa vya kutengenezea bomu na tunaamini bomu hilo tayari limekwisha tengenezwa na yawezekana limekwenda kutumiwa sehemu Fulani” akasema mkuu Yule wa makomando wa SNSA “Ahsanteni sana kwa kazi nzuri.Tunaendelea kuwahoji hawa watu mliowakuta mle ndani ili tufahamu mambo mengi wanayoyafanya.Usiku huu kumefanyika shambulio la bomu katika ubalozi wa Marekani na video Ambayo tunaitazama hivi sasa ni ya kiongozi mmoja wa IS ambaye amekiri kwamba wao ndio wanaohusika katika kulipua ubalozi ule wa Marekani hivyo tunataka kuwahoji hawa jamaa na kujiridhisha je bomu hilo ambalo limetumika kulipua ubalozi wa Marekani ni wao wamelitengeneza? Vile vile tunatakiwa tufanye uchunguzi kuhusiana na silaha ambazo unadai ni za jeshi la Marekani tujue wamezipataje? Tunaendelea na zoezi hilo na ninaamini tutapata taarifa tunazozihitaji” akasema Ruby na kutoa maelekezo kadhaa halafu yeye na Gosu Gosu wakaenda ofisini kwake “Gosu Gosu sina hakika kama nawe unafikiri ninavyofikiria mimi” akasema Ruby “Nini unakifikiria Ruby? “Mathew alituambia kwamba amekuja nchini kwa misheni maalum na akatuambia kwamba tusivamie nyumba ile aliyokuwa akiishi na magaidi hadi baadae usiku wa leo.Unahisi nini alikimaanisha kwa hiyo kauli yake? Hudhani alichokimaanisha kina mahusiano na hiki kilichotokea yaani kulipuliwa kwa ubalozi wa http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Marekani? akauliza Ruby “Ruby uko sahihi.Hata mimi nimejaribu kuunganisha picha na picha kubwa ninayoipata ni kwamba kuna uwezekano mkubwa Mathew akawa anahusika katika tukio hili la kulipua ubalozi wa Marekani.Nadhani ndiyo maana alikataa tusivamie ile nyumba jana usiku kwani alijua tukivamia kila kitu kuhusu mipango yao kitaharibika” akasema Gosu Gosu “Ooh Mathew ! Kwa nini lakini amefika hapa alipofika?Kwa nini akashirikiana na magaidi?akasema Ruby kwa masikitiko “Ruby kumbuka alichokisema Mathew kwamba tusistuke kwa kile tutakachokisikia kwani yuko katika misheni maalum” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu utanisamehe kwa hili nitakalolisema lakini naona kama taratibu ninaanza kutokumwamini Mathew.Amekuwa mtu wa tofauti na Mathew yule ninayemfahamu mimi” akasema Ruby “Ruby sikiliza.Mathew kwa vyovyote itakavyokuwa anahitaji sana msaada wetu na ndiyo maana akatuandaa kwa sababu alijua tutakapofahamu kuhusu kinachoendelea tutavunjika moyo sana.Mimi bado nina imani kubwa naye.Hata pale dunia nzima itakapogeuka na kumuona Mathew ni mtu asiyefaa mimi bado nitaendelea kusimama naye na nitaendelea kumuamini.Nakushauri nawe pia usikate tamaa kuhusu Mathew.Bila yeye tusingefanikiwa kuwapata hata hawa akina Marwan” akasema Gosu Gosu na Ruby akafikiri kidogo kisha akasema “Nadhani tukaendelee kuwahoji wengine lakini safari hii nitapeleka mtu mwingine wa kuhoji.Gosu Gosu wewe una hasira sana na sitaki kilichotokea kwa Marwan kitokee kwa watu wengine kwani tutashindwa kupata taarifa muhimu tunazozihitaji sana.Utanisamehe kwa hilo Papii” akasema Ruby “Fine” akasema Gosu Gosu kisha Ruy akampigia simu jamaa mwingine anaitwa Chris akamtaka afike ofisini kwake akampa maelekezo ya taarifa wanazozihitaji kutoka kwa wale magaidi waliokamatwa kisha wote wakaelekea chini mahala kulikokuwa na chumba cha mahojiano na Chris akaanza kuwahoji wale magaidi WASHINGTON DC – MAREKANI Rais William Washington wa Marekani alijitokeza mbele ya waandishi wa habari waliofika katika viwanja vya ikulu ya Marekani. “Habari za mchana ndugu waandishi wa habari.Kama nyote mlivyosikia saa chache zilizopita ubalozi wetu jijini Dar es salaam Tanzania umeshambuliwa kwa bomu na kuharibiwa vibaya.Watu wengi waliokuwepo katika ubalozi huo wakiwemo wamarekani na raia wa mataifa mengine ambao walikuwa wanapatiwa hifadhi ubalozini hapo kufuatia vurugu za kidini zinazoendelea nchini Tanzania wanahofiwa kupoteza maisha. Kundi la kigaidi la IS tayari limekiri kuhusika na shambulio hilo “Ndugu waandishi wa habari,kupitia kwenu nataka nitoe pole kwa wamarekani walipoteza wapendwa wao katika shambulio hilo lakini nataka niwaahidi kwamba hatutakaa kimya.Tumechokozwa na tutajibu vikali.Tutawasaka magaidi wa IS kokote waliko duniani na kuhakikisha tunalifutilia mbali kundi hili hatari kwa sasa ulimwenguni.Hizi ni salamu ninatuma kwa IS na makundi mengine ya kigaidi duniani kwamba siku zao zinahesabika.Hawana sehemu ya kukimbilia kujificha kwani hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe hadi tutakapoakikisha gaidi wa mwisho amepatikana.Nawaomba wamarekani waendelee na shughuli zao za kila siku bila hofu yoyote.Ahsanteni sana” Rais William akamaliza hotuba yake fupi na hakukuwa na maswali akarejea ndani na moja kwa moja akaelekea ofisini kwake.Kabla hajafanya chochote akampigia simu Rais wa Tanzania Dr Fabian Kelelo “Mheshimiwa Rais habari yako” akasema Rais Willaim baada ya Dr Fabian kupokea simu “Habari si nzuri mheshimiwa Rais.Nadhani umekwisha pata taarifa za magaidi kushambulia ubalozi wa Marekani hapa Dar es salaam” “Tayari nimepata taarifa hizo.Poleni sana kwa hiki kilichotokea” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” “Dr Fabian nimekupigia kukujulisha kwamba nimezipokea kwa mstuko taarifa za shambulio la bomu katika ubalozi wetu na ninaahidi kwamba tutawasaka magaidi hao kokote waliko na kuwapata wote.Hatutalala hadi pale gaidi wa mwisho atakapopatikana.Kwa ajili hiyo basi nitatuma vikosi zaidi vya wanajeshi nchini Tanzania kuwasaka magaidi hawa.Naamini hakutakuwa na tatizo katika suala hilo mheshimiwa Rais” akasema Rais William “Hakuna tatizo mheshimiwa Rais.Vikosi hivyo vitakavyokuja vitashirikiana na vikosi vyetu katika kuhakikisha tunawasaka na kuwatia nguvuni magaidi wote” akasema Dr Fabian Mazungumzo kati ya Dr Fabian na William Washington yaliendelea na zaidi sana yalilenga katika mashirikiano ya kijeshi kuwasaka magaidi waliolipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam na kutuliza vurugu zilizokuwa zinaendelea. Wakati Rais William Washington akizungumza na Rais wa Tanzania Dr,makamu wake Mark Piller alitembelewa na David Walker mkuu wa idara ile ndogo ndani ya CIA inayojishughulisha na mahusiano na makundi ya kigaidi. “Karibu sana David” akasema Mark “Ahsante sana Mark”akajibu David ambaye kiumri ni mkubwa kuliko Mark Piller “Hongera sana David.Nimepata taarifa za kilichotokea Dar es salaam nimefurahi sana.Mipango yetu inakwenda vizuri kama tunavyotaka” akasema Mark Piller “Pongezi kwetu sote Mark kwa maendeleo haya mazuri.Hivi sasa dunia nzima inafahamu kuwa ni IS walioshambulia ubalozi wetu jijini Dar es salaam.Tumeanza vyema na nina uhakika mkubwa kwamba safari hii tutapenya hadi zile sehemu za siri za Iran kwani mpango huu wa kumtumia Abu Zalawi ni mpango mkubwa sana” akasema David “Ni kweli David mpango huu nina uhakika mkubwa utafanikiwa kwani Yule jamaa ni mmoja wa magadi ambaye ameonyesha uwezo mkubwa sana tofauti na magaidi tunaowafahamu ambao wanachojua ni kulipua mabomu na kuua watu” “Tukiachana na hilo kuna jambo ambalo limenileta hapa.Ni kuhusiana na ule mpango wetu wa kusambaza kirusi nchini Tanzania” akasema David “Kuna nini katika mpango huo? “Tayari mtu wa kupeleka kirusi hicho Tanzania amepatikana na tayari amekwisha wasili hapa Marekani” “Safi sana” akasema Mark “Hata hivyo kuna tatizo limejitokeza” “Tatizo gani? “Nilikuwa na mazungumzo na wanasayansi wetu wanaotutengenezea hicho kirusi.Maendeleo ni mazuri.Tulipowataka watutengenezee kirusi maalum cha maangamizi tayari walikuwa na aina ya kirusi kilicho na sifa ka kile tunachokihitaji kinaitwa March26.Kirusi hicho kinasambaa kwa njia ya hewa na kinapoingia mwilini mwa binadamu humchukua saa ishirini na nne kuanza kupata dalili za mwanzo ambazo ni homa na mafua makali sana na baada ya muda mgonjwa huanza kukohoa na kutokwa na damu puani.Mgonjwa hufariki ndani ya saa 48 toka apate dalili za mwanzo za maambukizi ya virusi hivyo hatari” akasema David “Hicho ndicho hasa kirusi tunachokihitaji sisi” akasema Mark Piller “Ni kweli ni kirusi ambacho tunakihitaji mno lakini kuna tatizo ambalo limemjitokeza” “Nini kimejitokeza David? Akauliza Mark Piller “Wanasayansi wale bado hawajafanikiwa kupata kinga ya kirusi hicho” akasema David “Hawajapata kinga? Akauliza Mark Piller “Ndiyo bado hawajapata kinga zoezi ambalo wanaendelea nalo hivi sasa.Hilondilo tatizo lililopo Mark” akasema David Walker.Mark Piller akajiegemeza kitini na kuvuta pumzi ndefu. “Kweli hili ni tatizo.Tunahitaji kirusi ambacho tayari kina kinga yake ili tuweze kuwakinga watu wetu.Tunao wanajeshi wetu kule Afrika mashariki na vile vile lazima tujihadhari endapo kirusi hicho kitavuka mipaka ya Tanzania na kusambaa hadi Marekani” akasema Mark Piller na kuzama mawazoni halafu akauliza “Wanasayansi hao wamesema itawachukua muda gani kuweza kupata kinga hiyo?akauliza Mark “Hawana uhakika itachukua muda gani.Yawezekana ikawa ni wiki,miezi au hata mwaka lakini ni zoezi wanaloendelea nalo usiku na mchana” akasema David Walker “Pamoja na jitihada hizo wanazoendelea nazo lakini tunahitaji kirusi chenye kinga.Hatutaki kuweka hatarini maisha ya watu wetu huko Afrika mashariki” akasema Mark Piller na ukimya ukapita “Mark kuna jambo ambalo wanasayansi wamelishauri” “Wameshauri kitu gani? Akauliza Mark Piller “Walichonieleza ni kwamba kuandaa kirusi kingine cha aina tunayoihitaji itachukua muda mrefu na sisi hatuna muda mrefu wa kusubiri.Mpango wetu unahitaji kirusi kwa haraka zaidi na kirusi ambacho wanasayansi wetu wanacho ni hicho ambacho bado hakina kinga yake” “Nini unataka kukisema David?akaliza Mark Piller “Ninataka kushauri kwamba tukitumie kirusi hicho..” “Hapana David ! akasema Mark “Hatuwezi kwa namna yoyote ile kutumia kirusi hicho” akasema Mark “Nisikilize Mark” akasema David “Wanasayansi hao wameshauri kwamba tunaweza kukitumia kirusi hicho na kikasambazwa nchini Tanzania labla hata kinga yake haijapatikana.Kuna namna ambayo wanajeshi na raia wengine wanaweza wakakingwa kwa vifaa maalum” akasema David “Ni vipi kama kirusi hicho kitavuka mipaka ya Tanzania na kusambaa katika nchi nyingine za jirani,baadae Afrika nzima na kisha dunia nzima?Wasiwasi wangu ni pale ambapo kirusi kitasambaa wakati kinga yake bado haijapatikana” “Uwezekano wa virusi hivyo kufika Marekani ni mdogo sana kwani kutafanyika udhibiti mkubwa.Angalia kuna virusi vya ugonjwa wa Ebola ambao ni mbaya sana lakini havijafika bado Marekani nina uhakika mkubwa kwamba hata kama tukipeleka kirusi hicho Afrika hakitaweza kufika Marekani” “Nakubali inaweza kuchukua muda mrefu kwa kirusi hicho kufika Marekani lakini ukumbuke tuna wanajeshi wetu kule Tanzania ambao kuna uwezekano mkubwa sana wakaweza kupata maambukizi ya virusi hivi na ndiyo maana nilitaka tuwakinge kwanza watu wetu ndipo kirusi hicho kisambazwe lakini tukisambaza kirusi bila kuwakinga tutakuwa tumewazika watu wetu wenyewe.Kama watu wetu wataathirika basi kuna uwezekano mkubwa dhumuni la operesheni hii likashindwa kufanikiwa kwani tunataka kuendelea kuchota madini na mafuta” “Usiwe na hofu Mark.Watu wetu kule Tanzania watapewa suti maalum za kuvaa kujikinga na maambukizi hayo na wataendelea na shughuli zao kama kawaida” akasema David “Pamoja na vifaa hivyo David lakini tunawaweka watu wetu katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ! akasema Mark Piller “Mark hii ni kama vita tunapigania uchumi wa nchi yetu hivyo basi kama wakitokea wanajeshi wetu kadhaa wakapoteza maisha nchini Tanzania,watakuwa ni mashujaa waliokufa wakilipigania taifa lao.Hatuwezi kuogopa kupoteza watu kumi au ishirini kwa maslahi mapana ya nchi yetu.Lazima tufanye maamuzi magumu sana ya kusambaza kirusi hivyo hivyo hata kama hakina kinga ila tuchukue tahadhari za kuwasaidia watu wetu kule wasipate maambukizi na wakati huo huo wanasayansi wetu watakuwa wanaendelea kutafuta kinga dhidi ya kirusi hicho.Kwa kuwa wanajeshi na watu wetu wanarejea nyumbani kila mara tutatenga sehemu maalum kwa ajili yao ambako watakaa kwa muda kabla hawajakutana na watu wengine watachunguzwa kama wameambukizwa virusi hivyo na kama wakithibitika hawana maambukizi basi wataruhusiwa kwenda kuonana na familia zao lakini naamini ndani ya kipindi kifupi wanasayansi wetu watafanikiwa kupata kinga dhidi ya kirusi hicho” akasema David Walker “David umenipa wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi kuhusu hili jambo ambalo linaweza kuwa hatari sana kwa mustakabali wa dunia” akasema Mark “Mark usiwe na hofu.Kirusi hiki hakitaweza kufika Marekani kwani udhibiti wa virusi kusambaa utakuwa mkubwa.Jambo lingine la faida kwetu ni kwamba pale wanasayansi wetu watakapofanikiwa kuipata kinga hiyo itatuingizia mabilioni ya dola kama nchi kwani dunia nzima watanunua kinga hiyo kwa hofu ya kile watakachokuwa wamekiona kimetokea Tanzania.Nakushauri Mark tufanye maamuzi haya magumu ya kusambaza kirusi hicho Tanzania ili mipango yetu iendelee.Hili ni dirisha ambalo hatupaswi kuliacha likafungwa” akasema David na Mark akakuna kichwa “Taarifa kutoka Tanzania si nzuri.Tulitegemea baada ya mauaji ya kiongozi mkuu wa waislamu Tanzania zingeibuka vurugu kubwa lakini imekuwa tofauti.Hakuna vurugu na viongozi wa dini na serikali wanajitahidi sana kuzuia vurugu hizo zisiendelee.Kuna kila dalili amani inaanza kurejea Tanzania na kwa sasa wanajitahidi kutafuta chanzo cha vurugu zilizopelekea kushambuliana wao kwa wao na wakigundua kwamba wamefarakanishwa basi mipango yetu yote itakuwa imekwama kwani watajiunga tena na kuwa wamoja na ikifikia hatua hiyo hakuna kitakachoweza kuwafarakanisha.Hii ni nafasi ambayo lazima tuitumie kikamilifu.Wakati wakijaribu kutafuta amani tukasambaze kirusi .Tutaanza kusambaza sehemu zile ambazo tumezilenga.Kwenye machimbo ya madini kama Tanzanite,dhahabu nk.Ugonjwa ukianza kusambaa sehemu hizo tutapeleka watu wetu kwa lengo la kutoa msaada na hiyo ndiyo fursa yetu ya kuchukua madini kiasi chochote tukitakacho na wakati huohuo mafuta yataendelea kumiminika katika hifadhi yetu” akasema David Piller “David ninakuelewa sana lakini kuna sauti ninaisikia ndani mwangu inanionya tusifanye hicho unachonishauri tukifanye”akasema Mark Piller “Mark sauti hiyo ni uoga.Usiiruhusu ikatawala ndani mwako.Huu ni wakati wa kuzikataa sauti zote unazozisikia na kujielekeza katika suala moja tu la faida zitakazopatikana kwa nchi yetu pale tutakaposambaza kirusi hiki” akasema David Walker na Mark akanyamaza akitafakari “Mark ninasubiri jibu lako ili maandalizi yaendelee.Wengine wote wamekubali ni wewe pekee tunayekusubiri” akasema David “David siwezi kusema hapana kama ninyi nyote mmelikubali jambo hili.Mipango iendelee lakini lazima wanasayansi hao wapewe muda maalum wa kuhakikisha wamepata kinga ya kirusi hicho vinginevyo tutakuwa tumeiweka dunia katika hatari kubwa.Vile vie watu wetu kule Tanzania lazima tuwakinge” akasema Mark Piler “Hayo yote yatatekelezwa Mark.Nakuhakikishia maamuzi haya tuliyoyafanya ni sahihi na yana maslahi makubwa sana kwa nchi yetu” akasema David Walker na kuagana na makamu wa Rais akaondoka “Siamini kama hiki tunachokwenda kukifanya ni kitu sahihi.Kusambaza kirusi bila kinga yake ni hatari sana.Ni vipi kama kirusi hicho kitasambaa sehemu mbali mbali duniani na kusababisha maangamizi makubwa? Ni vipi kama kitasambaa na kufika Marekani? Ilipaswa tuwakinge kwanza watu wetu kabla ya kukisambaza kirusi hicho” akawaza Mark “Lakini kwa upande wa pili wazo la David ni zuri.Tunahitaji kusambaza kirusi haraka ili mipango yetu iendelee japo tulipaswa kuwa na kinga kwanza ndipo tusambaze kirusi .Mimi peke yangu siwezi kuwa na nguvu ya kuzuia maamuzi ya wenzangu” Mark Piller alijawa na mawazo mengi sana baada ya David kuondoka DAR ES SALAAM – TANZANIA Hadi kunapambazuka ni matukio machache tu ya vurugu yalikuwa yameripotiwa jijini Dar es salaam.Asubuhi hii jiji la Dar lilionekana kuwa shwari licha ya hofu kubwa kuendelea kutanda kufuatia kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani usiku wa kuamkia siku hii.Tukio hilo ndilo lililotawala vyombo vyote vya habari asubuhi.Maduka machache yalifunguliwa katika baadhi ya mitaa ili watu waweze kujipatia mahitaji muhimu na ulinzi uliimarishwa sana katika mitaa mingi magari ya doria yaliendelea kuzunguka kuhakikisha hali inaendelea kuwa shwari. Katika ofisi za SNSA kazi kubwa iliyofanyika usiku kucha ilikuwa ni kuwahoji magaidi waliokamatwa ili kufahamu mahala alipo Assad Ismal.Hadi jua lilipoanza kuchomoza hakuna gaidi hata mmoja miongoni mwa wale magaidi wote waliokamatwa aliyekubali kusema mahala alipo Assad. “Ruby tumekesha usiku mzima tukiwahoji hawa jamaa lakini hakuna walichokisema.Nilikutahadhar isha mapema kwamba hawa watu ni wagumu mno kufunguka na wako tayari hata kufa kuliko kutoa siri.Kwa namna walivyokuwa wanahojiwa ni kama walikuwa wanapapaswa tu ndiyo maana wameendelewa kuwa na kiburi.Ruby niruhusu niwahoji hawa watu.Nakuhakikishia lazima mmoja wao atafunguka” akasema Gosu Gosu wakiwa ofisini kwa Ruby “Gosu Gosu hapana.Ulichokifanya jana kwa Marwan hakikunifurahisha.Japo kuwa ni watu makatili lakini lazima tuwe na ubinadamu,tusiwatendee ukatili kama ule uliomfanyia Marwan.Kama nisingeingia mle ndani ulikuwa tayari kuendelea kukata viungo vyake halafu nini kingefuata?Marwan angepoteza maisha na tungekosa kila kitu.Utanisamehe GosuGosu lakini sintakuruhusu uwatese hawa jamaa kwani una hasira za karibu sana na huogopi kuua” akasema Ruby “Ruby hawa jamaa hawana ubinadamu hata kidogo na hawastahili huruma.Tazama walichokifanya katika nchi yetu.Ni hawa ambao wametumiwa kuchochea vurugu na watanzania wakaanza kushambuliana na kuuana.Hawa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuifikisha nchi yetu hapa ilipofik…...” “Gosu Gosu nimekwisha sema hautawahoji hawa jamaa and that’s final ! akasema Ruby akionekana kuchoka.Gosu Gosu akamtazama halafu akatikisa kichwa “Nakuhakikishia Ruby kwamba kwa staili hii hatutaweza kupata kitu chochote kutoka kwa hawa jamaa.Umesahau namna Mathew anavyowahoji watu wa namna hii? Akauliza Gosu Gosu “Mathew hayuko hapa na hatuwezi kuiga ufanyaji kazi wake.Watu hawa tutakwenda nao taratibu na nina uhakika mkubwa lazima watafunguka.Zipo njia nyingi tu za kuwafungua watu wa namna hii lakini si kwa kuwakata viungo vyao kama ulivyofanya jana.Jiandae unakwenda Kilimanjaro kumpokea Nawal” “Mimi? Nakumbuka ulisema wewe ndiye utakayekwenda huko” “Nimebadili mipango utakwenda wewe badala yangu na mimi nitabaki hapa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri” akasema Ruby na kutazamana na Gosu Gosu “Ruby kwa nini niko hapa? Kwa nini uliniomba niwe msaidizi wako?Ulinileta hapa niwe mlinzi wako au tusaidiane katika kazi? Akauliza Gosu Gosu “Gosu Gosu najua hili halijakupendeza lakini naomba uvumilie.Naamini hadi jioni ya leo tutakuwa tumepata kitu Fulani kutoka kwa hawa jamaa” akasema Ruby “Kama isingekuwa ni Mathew ameniomba niendelee kuwepo hapa nihakikishe unakuwa salama ningeondoka hapa dakika hii hii ! akawaza Gosu Gosu.Ruby akataka kusema kitu lakini simu yake ikaita “Rais anapiga” akasema Ruby na kuipokea ile simu “Mheshimiwa Rais shikamoo” akasema Ruby “Ruby uko wapi? Akauliza Dr Fabian “Niko ofisini mheshimiwa Rais” “Tazama runinga sasa hivi halafu tutazungumza” akasema Dr Fabian na haraka haraka Ruby akawasha runinga na kukuta kuna habari mpasuko iliyokuwa inaendelea.Katika habari ile kulikuwa na picha ya Mathew Mulumbi na maandishi yaliyopita chini yaliandikwa Gaidi aliyelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam akamatwa Nairobi Kenya.Ruby alihisi nguvu zinamuisha akataka kuanguka Gosu Gosu akawahi kumdaka akamketisha kitini. “Ruby relax ! Take a deep breath ! akasema Gosu Gosu na Ruby akavuta pumzi ndefu mara tatu. “Gosu Gosu nimechoka.Najuta kwa nini nilikuja Tanzania ! Najuta kwa nini nilimfahamu Mathew Mulumbi ! akasema Ruby “Shhhhh ! akasema GosuGosu “Gosu Gosu nitakwenda wapi mimi? Mathew ndiye mwanaume ninayempenda kuliko wote duniani kwa nini akafanya hivi? “Usiseme chochote na wala usijilaumu Ruby.Mathew alikwisha tuandaa kwa jambo hili” “Mwongo mkubwa Yule ! akasema kwa ukali Ruby huku akilia. “Ruby usiseme hivyo tafadhali.Mathew si mwongo.Alijua tutastuka sana na kuumia ndiyo maana akaja kwetu kutuandaa na alitusisitiza kwamba tusistuke tutakaposikia kitu kibaya kuhusu yeye.Kile alichokuwa anakisema ni hiki” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu ni misheni gani hii aliyonayo Mathew hadi akaamua kujiingiza katika ugaidi? Mathew ni jasusi na ..” akasema Ruby na simu yake ikaita alikuwa ni Dr Fabian Kelelo Rais wa Tanzania.Ruby akafuta machozi na kuipokea “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby tafadhali niambie nini kinaendelea? “Mheshimiwa Rais hata mimi sielewi chochote.Wote hapa tumebaki midomo wazi hatuamini hiki tunachokiona” “Mathew Mulumbi ! akasema Dr Fabian naye akiwa haamini “Toka mwanzo sikuwahi kumkubali Yule jamaa.Kumbe nilikuwa sahihi kabisa kutokumwamini na hiki alichokifanya naamini wote walionipibnga watakubaliana nami kwamba nilikuwa sahihi kutomkubali Mathew.Inaniuma kwa sababu tulimuacha akazifahamu baadho ya siri zetu za nchi mtu ambaye ni gaidi ! Imeniumiza sana Ruby “ akasema Dr Fabian kwa masikitiko “Mheshimiwa Rais sijui niseme nini lakini hata mimi binafsi bado siamini.Ninamfahamu Mathew Mulumbi,nimeshirikiana naye katika misheni kadhaa lakini hata siku moja sikuwahi kuota kama angeweza kubadilika na kuingia katika ugaidi.Nimepatwa na mstuko mkubwa sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby,wewe na Gosu Gosu ni watu wake wa karibu sana.Je mlifahamu uwepo wake hapa nchini? Akauiliza Dr Fabian “Hapana mheshimia Rais.Hatukujua kuhusu uwepo wake hapa nchini na wala hatukuhisi kama anaweza akahusika na shambulio lile hadi baada ya taarifa ya kukamatwa kwake kutangazwa” akajibu Ruby “Dah ! ninazidi kuchanganyikiwa kwa mambo haya yanayoendelea hapa nchini kwetu.Naomba tafadhali leo jioni tukutane tujadiliane na unipe taarifa za mahala mlikofikia katika uchunguzi wenu” akasema Dr Fabian “Nitakuja mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Dr Fabian akakata simu “Gosu Gosu nimechanganyikiwa sijui nianzie wapi,sijui nifanye nini” akasema Ruby “Ruby naomba unisikilize” akasema Gosu Gosu na Ruby akainua kichwa akamtazama “Mathew alijua haya yote yatatokea na alijua kwamba dunia nzima itamgeuka lakini akatutaka sisi wawili tusimame naye.Tutafanya kosa kubwa sana kama na sisi tutashindwa kumuamini Mathew.Binafsi naamini yuko katika misheni kubwa kama alivyosema yeye mwenyewe.Hata siku moja Mathew hawezi kuwa gaidi.Lazima ameingia katika mitandao hiyo ya kigaidi kwa lengo maalum.Mtu yeyote anayemfahamau vyema Mathew Mulumbi hataamini akisikia eti amekuwa gaidi.Hebu jiulize kwa nini akajenga mahusiano na Habiba Jawad ambaye anajulikana kwa kufadhili ugaidi duniani? Hapa lazima kuna kitu hatukifahamu.Tuwe na subira na tutafahamu mambo mengi lakini kubwa tumuamini” akasema Gosu Gosu na Ruby akavuta pumzi ndefu “Ruby mambo ndiyo kwanza yameanza.Mathew alitufumbua kwamba hiki kinachoendelea hapa nchini kina pande mbili ndani na nje ya nchi na akaweka wazi kwamba yeye atawashughulikia wale watu wa nje na sisi akatutaka tuwashughulikie wale watu wa ndani. Mathew ameanza sehemu yake na sisi tunatakiwa kuendelea na sehemu yetu”akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu sitaki nikudanganye lakini hili alilolifanya Mathew limevuka mpaka.Mathew si mwenzetu tena na hapaswi kuaminiwa kwa lolote.He’s a liar and a traitor ! akasema Ruby “Is that what you think? Akauliza Gosu Gosu “Gosu Gosu jiandae unaelekea Kilimanjaro kumpokea Nawal.Leave me alone for now ! akasema Ruby na Gosu Gosu akatoka “Kwa nini Mathew ameamua kubadilika namna hii? Ni mtu ambaye amekwisha fanya mambo makubwa kabisa hapa nchini lakini leo hii ameamua kujiunga na magaidi.Natamani hata nigeuke upepo nipotee kabisa nisionekane ! akawaza Ruby
Helkopta ya jeshi la Marekani iliyombeba Mathew Mulumbi ikitokea jijini Nairobi,ilitua katika kambi ya jeshi la wanamaji wa Marekani iliyoko Mombasa Kenya.Mathew alishushwa katika helkopta akiwa amefunikwa mfuko kichwani na mikono yake ikiwa imefungwa pingu.Akiwa ameongozana na makachero wa shirika la ujasusi la Marekani waliomkamata wakati akijaribu kutafuta usafiri wa kumpeleka Mogadishu Somalia,aliingizwa katika boti maalum na safari ya kilometa 1750 kueleka jiji la Victoria nchini Seychelles ikaanza.Ndani ya boti ile kulikuwa na watu wapatao sita. “Mambo yameanza.Naamini mpaka sasa tayari taarifa zimekwisha sambaa duniani kwamba nimekamatwa kwa kulipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam.Nilifanya vizuri kuwapa tahadhari mapema akina Gosu Gosu wasistuke watakapopata taarifa hizi kwani ni moja ya misheni zangu.Naamini watayazingatia yale niliyowaelekeza” akawaza Mathew huku boti ile yenye mwendokasi wa kilometa 250 kwa saa ikichana mawimbi kwa kasi kubwa.
Ndege ya shiria la ndege la Ethiopia ikitokea Riyadh Saudi Arabia kupitia Adis Ababa ilitua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.Tayari ilikwisha timu sa kumi na moja na nusu za jioni.Gosu Gosu akiwa na watu wawili wa SNSA kanda ya Kaskazini tayari walikwisha wasili uwanjani kwa ajili ya kumpokea Nawal.Gosu Gosu ambaye alikuwa amevaa suti nyeusi siku hii aliitoa mfukoni picha ya Nawal akaitazama na kuirudisha mfukoni. “ Anaonekana mrembo sana huyu mwanamke japo anajihusisha na ugaidi” akawaza Gosu Gosu huku akitabasamu “Sitakiwi kwa namna yoyote ile kuruhusu akili yangu ikavutiwa na wanawake hasa hawa warembo.Nimekwisha umwa na nyoka na sasa kila nikiguswa na juani ninastuka.Nilichungulia kaburi kwa kujiingiza katika mahusiano na Melanie na toka wakati ule nimewaogopa sana wanawake ! akawaza Gosu Gosu wakiwa katika sehemu ya kusubiria abiria wanaowasili. Abiria walishuka na kuelekea katika jengo la kisasa la kupokelea abiria kwa ajili ya kukamilisha taratibu mbali mbali na walihudumiwa haraka haraka na kuanza kuelekea sehemu ya kutokea abiria wanaowasili. Macho ya Gosu Gosu yaliyoangaza kama tai yalimuona Yule waliyekuwa wanamsubiri ambaye ni Nawal.Alikuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu na nywele zake ndefu nyeusi alizibana kwa nyuma huku macho yake akiyafunika kwa miwani myeusi.Ili kujiridhisha Gosu Gosu akaingiza mkono katika mfuko wa koti na kutoa picha akaitazama “That’s her” akawaza Gosu Gosu kisha akaanza kumsogelea. “Nawal ! akaita baada ya kukaribia.Nawal akageuka na kumtazama Gosu Gosu ambaye alimpa ishara ya kichwa na Nawal akaielewa akamfuata wakasalimiana “Karibu sana Tanzania.Naitwa Papi Gosu Gosu.Nimetumw ana Ruby kukupokea” akasema Gosu Gosu “Jna lako gumu sana.Gasu Gasu ! “Gosu Gosu” Gosu Gosu akamsahihisha “Usijali utazoea tu” akasema Gosu Gosu na kumsaidia Nawal kukokota mabegi yake hadi kwenye gari kisha wakaondoka pale uwanjani “Tunaelekea wapi? Akauliza Nawal “Tunaelekea Arusha” akasema Gosu Gosu “Ruby yuko wapi?akauliza Nawal “Ruby yuko Dar es salaam na amenituma mimi nije kukupokea badala yake” akajibu Gosu Gosu na Nawal akayaelekeza macho yake nje “Dah ! mtoto huyu si mchezo.Amependelewa uzuri lakini kasoro yake ni hiyo moja tu mama yake ni mfadhili wa magaidi naamini hata huyu kilichomleta huku Tanzania ni kuhusiana na mambo hayo ya kigaidi” akawaza Gosu Gosu akimtazama Nawal kwa kuibia. “Mara ya kwanza kufika Tanzania?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo.Ni mara ya kwanza ninafika Tanzania lakini mara ya pili ninafika bara la Afrika” “Ouh kumbe umekwisha tembelea bara la Afrika” “Ndiyo nilikwenda kwenye matembezi nchini Misri” “Karibu sana Tanzania” “Ahsante nashukuru” akasema Nawal “Nimeshangaa kidogo hali ninayoishuhudia huku ni tofauti na ile tunayoiona katika vyombo vya habari vya nje.Tunashuhudia vurugu kubwa sana maiti za watu zimezagaa barabarani,majumba yanachomwa nk” akasema Nawal “Siku zote vyombo vya habari vya nje vina lengo moja tu la kupotosha taswira halisi ya bara la Afrika na yanapotokea machafuko kama haya yaliyotokea nchini mwetu basi huripoti tofauti na hali halisi ilivyo kwa malengo yao wanayoyajua lakini sikatai vurugu zipo ila kwa hapa Tanzania kuna baadhi ya mikoa ambayo vurugu hizo zilikuwa kubwa sana kama vile mikoa ya Dar es salaam na Tanga.Mikoa mingine kama huku Kaskazini na kwingineko vurugu zilitokea kidogo lakini vyombo vya ulinzi vikawahi kudhibiti na hali imeendelea kuwa shwari.Mikoa ambayo mpaka sasa naweza kusema hali si shwari ni Dar es salaam na Tanga kidogo na mkoa wa Pwani.Miji hiyo miwili naweza kusema ilikuwa imesimama kutokana na machafuko makubwa yaliyotokea.Kwa sasa kidogo hali imeanza kutulia japo bado yapo makundi ya watu wenye silaha ambao wanazunguka mitaani kuendeleza vurugu lakini kwa kiasi kikubwa hali ya sasa si kama vile ilivyokuwa mwanzo.Wakati naondoka Dar es salaam leo asubuhi nilishuhudia baadhi ya maduka yamefunguliwa na watu kujipatia mahitaji na nimepata taarifa kuna masoko mawili matatu yalifunguliwa leo japo bado watu wana hofu kubwa kuonekana katika mikusanyiko ya watu.Kwa ujumla naweza kusema hali imeanza kutulia.Watanzania si watu wa kupenda vurugu na ndiyo maana vurugu hizi zitamalizika muda si mrefu sana na maisha kurejea kawaida” akasema Gosu Gosu “Poleni sana.Ni mara ya kwanza Tanzania inakumbwa na machafuko makubwa kiasi hiki” akasema Naal “Ni kweli watanzania wamezoea amani na siku zote tumekuwa tukiishi kama ndugu kila mtu anajiuliza nini hasa kimetokea hadi tukajikuta hapa tulipofika kuanza kushambuliana na kuuana sisi kwa sisi kwa sababu ya dini? “Serikali yenu inasema nini kuhusu jambo hili? Waasisi wa vurugu hizi tayari wamekamatwa? “Kwa sasa serikali bado inaendelea na jitihada za kutuliza vurugu,kudhibiti makundi ya watu wenye silaha ambao wamekuwa wakiendesha mashambulio mbali mbali na hata kuua viongozi wa dini kwa mfano ni juzi tu wamemuua Mufti wa Tanzania.Jana usiku ubalozi wa Marekani umelipuliwa na kundi la kigaidi la IS.Matukio kama haya yanazidi kuleta hofu lakini serikali inaendelea kujitahidi kudhibiti matukio kama haya yasiendelee kutokea.Baada ya kurejesha hali kuwa ya amani ndipo wataanza kulifanyia uchunguzi jambo hili kulifahamu kiundani na kuwabaini watu waliosabaisha tukafika hapa” akasema Gosu Gosu na ukimya ukatawala garini “Nimetaja kundi la IS amenyamaza kimya.Huyu lazima ni mmoja wao na lazima atakuwa amekuja kwa mipango ya kundi hilo.Imekuwa bahati mbaya kwake ameangukia katika mikono yangu na lazima atasema kila kilichomleta hapa Tanzania. Mama yake ni gaidi lazima huyu naye ni gaidi ! akawaza Gosu Gosu huku akiendelea kumtazama Nawal kwa jicho la wizi. “Hata hivyo ni mrembo na anaonekana kujiamini sana” akawaza Gosu Gosu. Nawal hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote aliyaelekeza macho yake nje na mara kadha alikuwa anatabasamu “Mbona unatabasamu Nawal? Akauliza Gosu Gosu ” “Ninatabasamu kwa uzuri wa mkoa huu.Ukijani kila sehemu,mito mingi inabubujisha maji,majengo mazuri kila mahali nimeupenda sana mkoa huu” akasema Nawal “Bado haujashuhudia uzuri wake.Ukiacha haya unayoyaona njiani lakini kuna mbuga za wanyama katika mkoa huu kama vile Manyara,Arusha na Tarangire vile vile kuna bonde la Ngorongoro,kuna mlima Meru na mambo mengine mengi ya kuvutia” akasema Gosu Gosu “Unaonekana ni mkoa uliobarikiwa kuwa na vivutio vingi.Nitakapomaliza shughuli yangu iliyonileta hapa Tanzania nitakuja kutembelea Arusha kuona vivutio hivyo ulivyonitajia” akasema Nawal “Una siku ngapi za kukaa hapa Tanzania?akauliza Gosu Gosu “Hapa nina siku tisini” “Ouh ni muda mrefu sana huo.Kama ni mpenzi wa kwenda katika vivutio vya kitalii basi utatembelea vivtio vyote vilivyopo hapa nchini kwetu” “Unaweza ukanitajia tafadhali vivutio vingine vilivyopo hapa Tanzania? Akauliza Nawal “Hapa ndipo mtu mzima unaweza kuumbuka.Watanzania tuna vivutio vingi katika nchi yetu lakini hatuvijui.Kwa bahati nzuri nilipokuwa naumwa nilikuwa natazama ile chaneli ya utalii ya taifa na nikabahatika kuvifahamu baadhi ya vivutio vya utalii.Ngoja nimshushie huyu gaidi wana pesa za kuharibu hawa” akawaza Gosu Gosu “Ukicha vivutio nilivyokueleza vinavyopatikana hapa Arusha,vivutio vingine ni mlima Kilimanjaro,mbuga za Serengeti,Mikumi,Ruaha,Buri gi n.k” akanyamaza kidogo akikumbuka “Vile vile kuna Saadan,Gombe,Mahare, na vivutio vingine vingi” akasema Gosu Gosu “Nashukuru kwa ufafanuzi huo.Muda ukiruhusu nitatembelea vivutio hivyo vyote bila kuacha hata kimoja” “Karibu sana” akasema Gosu Gosu na tayari walikwisha ingia katika jiji la Arusha ambako maisha yaliendelea kama kawaida na hakukuwa na dalili zozote za vurugu ila ulinzi ulikuwa mkali sana. “Hili ndilo jiji la Arusha” akasema Gosu Gosu lakini Nawal hakumjibu kitu aliyaelekeza macho yake nje. Walikwenda hadi katika ofisi za SNSA zilizoko eneo la Njiro.Gosu Gosu akaagana na wafanyakazi wa SNSA walioko Arusha kisha akamuongoza Nawal wakaelekea katika helkopta tayari kwa safari ya kuelekea Dar es salaam “Tunaelekea Dar es salaam” Gosu Gosu akamwambia Nawal Baada ya dakika chache helkopta ikapaa na kuondoka Arusha “Ni gharama kiasi gani imetumika kukodisha helkopta hii?Nataka nijue nizirejeshe,sitaki kuwaingiza gharama” akasema Nawal “Usijali Nawal” akasema Gosu Gosu.
Inakaribia saa mbili za usiku helkopta ya idara ya SNSA ilipotua katika ofisi kuu za SNSA Dar es salaam. “Tumefika Dar es salaam karibu sana” Gosu Gosu akamwambia Nawal baada ya helkopta kutua “Hapa ni wapi?akauliza Nawal akionekana kuwa na wasi wasi baada ya kuwaona watu kadhaa wakiwa na bunduki wakizunguka kulinda jengo lile.Gosu Gosu hakumjibu kitu akampigia simu Ruby akamjulisha kwamba tayari wamekwisha rejea,Ruby akatoka haraka akawafuata. “Hallo Nawal karibu sana Tanzania.Naitwa Ruby” akasema Ruby “Nimefurahi kuonana nawe Ruby” akajibu Nawal wakapeana mikono kisha Ruby akamuomba Gosu Gosu waongee pembeni “Tuna kikao na Rais usiku huu hivyo huyu Nawal tutamuacha hapa akilindwa ili tukazungumze kwanza na mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Hapana Ruby.Huyu mtu ametoka kwa mfadhili wa magaidi duniani.Ni mtu hatari huyu kumuacha peke yake.Kitendo cha kumpokea mtu kama huyu ni cha hatari sana kwetu hivyo nashauri wewe nenda ikulu kazungumze na Rais mimi nitampeleka Nawal nyumbani kwangu.Nitamchunga hadi pale utakapomaliza kikao na Rais halafu utanikuta nyumbani ninakusubiri.” akasema Gosu Gosu “Umemueleza chochote kuhusu sisi na shughuli zetu? Ruby akauliza “Hapana sijamueleza chochote ingawa amekwisha anza kuwa na wasi wasi baada ya kuona watu wenye silaha wakizunguka zunguka humu ndani” “Sawa Gosu Gosu.Hakikisha unamchunga.Nitakapomaliza kikao na Rais nitakuja nyumbani kwako” akasema Ruby “Kuna chochote mmekipata kutoka kwa wale magaidi?akauliza Gosu Gosu “Hapana hatujapata kitu chochote mpaka sasa.Wameendelea kuwa wagumu kufungunguka lakini naamini watafunguka tu” akasema Ruby.Gosu Gosu akataka kusema kitu lakini Ruby akamuwahi “Not now Gosu Gosu.Tutazungumza baadae” akasema Ruby kisha akamfuata Nawal “Nawal karibu sana Dar es salaam,karibu sana Tanzania” “Ahsante Ruby” “Gosu Gosu atakupeleka mahala ukapumzike mimi nitakuja kukuona baadae kidogo” akasema Ruby na kuagana na Nawal.Mabegi ya Nawal yakapakiwa katika gari la Gosu Gosu ambalo lilitanguliwa na gari la walinzi wa SNSA wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Gosu Gosu. “Ruby anafanya kazi gani?Pale tulipomkuta ni wapi?akauliza Nawal “Ruby ni mfanya biashara na mimi ni mfanyakazi wake.Pale alipo ni moja ya ofisi zake” akadanganya Gosu Gosu “Nimeona watu wana silaha kali za kivita wakilinda eneo lile” akasema Nawal “Kuna watu wamepewa hifadhi pale kufuatia vurugu hivyo wanalindwa na vikosi vya ulinzi ndiyo maana umeona kuna watu wana silaha.Wale walio katika gari la mbele yetu ni askari wanatusindikiza kuhakikisha tunafika salama nyumbani” akaendelea kudanganya Gosu Gosu na Nawal akawa kimya Jiji la Dar es salaam usiku huu lilikuwa kimya.Karibu maeneo yote waliyopita akina Gosu Gosu yalikuwa tulivu hakukuwa na vurugu kama zile zilizokuwepo siku kadhaa nyuma.Walifika nyumbani kwa Gosu Gosu ambako tayari walinzi wake walikwisha pewa taarifa na Lucy aliyepigiwa simu na Gosu Gosu akimtaarifu kwamba anakwenda na mgeni.Gosu Gosu akaagana na wale walinzi waliowasindikiza kisha wakaingia ndani.Kulikuwa giza Gosu Gosu akaelekeza jenereta liwashwe mara moja “Nawal karibu sana.Hapa ni katika makazi yangu na katika muda wote ambao utakuwa hapa Tanzania utaishi hapa” akasema Gosu Gosu “Ruby anaishi wapi? Nawal akauliza “Anaishi mbali na hapa.Atakuja baadae baada ya kumaliza kazi zake.Kwa sasa nenda kaoge kisha upate chakula na umsubiri Ruby” akasema Gosu Gosu na kumpeleka Nawal katika chumba cha wageni. “Ruby tayari tumefika salama” Gosu Gosu akamjulisha Ruby “Sawa Gosu Gosu endelea kumchunga.Ninakaribia kufika Ikulu.Kama nilivyokwambia nikitoka huku nitakuja.Kuna chochote amekuuliza?akauliza Ruby “Aliuliza unafanya kazi gani na pale ulikuwa wapi nikamwambia wewe ni mfanya biashara na pale ulikuwa katika ofisi yako” akasema Gosu Gosu na kumweleza Ruby kila kitu walichozungumza na Nawal Nawal alikikagua kile chumba alichopewa ili kujiridhisha usalama wake halafu akaufunga mlango na funguo akazima taa akatoa kifaa fulani kidogo akakiwasha kwa lengo la kuangalia kama kuna kamera au kifaa chochote cha siri kimetegwa ndani ya kile chumba lakini hakubaini kamera au kifaa chochote.Akawasha taa na kuingia bafuni kuoga. “Nimefurahi kufika Tanzania nchi anakotoka Mathew Mulumbi.Nimependa zaidi Arusha kuna hali ya hewa safi sana na hata madhari yake ni ya kuvutia mno.Ningetamani kama ningeweza kuonana na Mathew Mulumbi.Nitamuuliza Ruby kama anaweza akafahamu mahala alipo Mathew ili nionane naye nimfahamishe kile nilichokuja kukifanya hapa Tanzania.Lazima nihakikishe kwa namna yoyote ile mpango wa kusambaza kirusi hapa Tanzania haufanikiwi.Mathew ni mtu wangu wa karibu sana na lazima nimsaidie kuiweka nchi yake salama” akawaza Nawal akiendelea kuoga
“Ruby karibu sana” akasema Dr Fabian baada ya Ruby kuwasili ikulu “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akajibu Ruby “Gosu Gosu yuko wapi? “Gosu Gosu nimempangia kazi nyingine ndiyo maana nimekuja peke yangu” “Watu wako wote pale SNSA wako salama? Akauliza Dr Fabian “Tunashukuru wote wako salama kabisa” “Nafurahi kusikia hivyo” akasema Dr Fabian na ukimya mfupi ukapita “Nilitaka tukutane ili unipe ripoti ya kile ambacho mmekuwa mnaendelea kukichunguza ndani ya SNSA lakini kabla ya yote nataka kufahamu kuhusu Mathew Mulumbi.Huyu ni mtu wako wa karibu.Je ulifahamu kuhusu uwepo wake hapa Tanzania? Nilikuuliza swali hili asubuhi kwenye simu lakini nataka kukuuliza ana kwa ana”akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kuna jambo ambalo sikutaka kulizungumza simuni lakini kwa kuwa tumeonana ana kwa ana nitakueleza ila nitaomba libaki kwako na asifahamu mtu mwingine yeyote” “Nieleze tafadhali” akasema Dr Fabian akionekana kuwa na shauku ya kutakakufahamu jambo hilo “Ni kweli Mathew Mulumbi alikuwepo hapa nchini” akasema Ruby na ukimya ukapita “Ni kweli alikuwepo hapa nchini ndiyo maana akalipua ubalozi wa Marekani lakini je wewe ulifahamu kama yuko hapa nchini? Hilo ndilo swali langu” akasema Dr Fabian “Ndiyo mheshimiwa Rais.Alinitafuta na tukaonana” akajibu Ruby na Rais akamkazia macho “Kuna chochote alikwambia kuhusiana na hiki alichokifanya? “Hapana mheshimiwa Rais hakunieleza kuhusiana na hiki alichokifanya.Hata mimi nilistuka sana baada ya kusikia kwamba ndiye aliyelipua ubalozi wa Marekani hapa Dar es salaam” “Nimesikitishwa sana Ruby kwa hiki alichokifanya Mathew.Nimejiuliza maswali mengi kwa nini aamue kujiunga na kundi la kigaidi?Hata hivyo sishangai sana kwani toka nilipopata taarifa zake na hata nilipoonana naye ana kwa ana sikuwahi kumuamini.Kibaya zaidi amebadili hadi jina anaitwa sijui jina gani lile” “Abu Zalawi” http://deusdeditmahunda.blogspot.com/akasema Ruby “Ndiyo.Anajiita hivyo.Nani amemroga Yule jamaa hadi akafanya maamuzi haya mabaya ya kujiunga na IS? Akauliza Dr Fabian “Tena imekuwa vyema amebadili jina na uraia wake na hajulikani kama ni raia wa Tanzania kwani angetutia aibu kubwa endapo angejulikana ni raia wa Tanzania.Nimemchukia sana Yule jamaa na ninaomba afungwe hata maisha huko gerezani au auawe kabisa ! akasema kwa ukali Dr Fabian na Ruby akaonekana kuchukizwa na kauli ile ya Dr Fabian “Samahani Ruby hili suala la Mathew limenikasirisha sana hadi nikasahau kama tuna mazungumzo muhimu.Ulisema kuna jambo la muhimu unataka kunieleza” “Ndiyo mheshimiwa Rais lakini linahusiana na huyo Mathew” “Jambo gani hilo? “Alipofika hapa nchini alinitafuta na lengo kubwa la kunitafuta kwake ni kunipa taarifa muhimu” akasema Ruby na kumtazama Rais aliyekuwa akimsikiliza huku sura yake ameikunja kwa hasira “Mathew alinipa taarifa za watu waliomuua mufti wa Tanzania na akanielekeza mahala wanakoishi” “Aliwafahamu watu waliomuua mufti wa Tanzania! DR Fabian akashangaa “Ndiyo mheshimiwa Rais anawajua na alinielekeza mahala wanakoishi” “Ulimuamini hicho alichokwambia? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninamuamini na tuliifanyia kazi taarifa yake” “Ruby usiniambie baada ya haya yote aliyoyafanya bado unamuamini Yule jamaa ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais.Ni kweli Mathew anashirikiana na kundi la kigaidi la IS na katika mazungumzo yetu alikiri hilo lakini aliniambia ana sababu maalum ya kushirikiana na kundi hilo la IS.” “And you believe him?akauliza Dr Fabian kwa ukali “Yes I do Mr President ! akajibu Ruby kwa sauti ya juu kidogo “Ruby siamini kama haya maneno yanatoka katika kinywa chako.Unawezaje kumuamini Yule jamaa wakati ni gaidi?Zaidi ya watu sabini wameuawa na idadi inaweza kuongezeka.Unawezaje kumuamini huyu muuaji mkubwa? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninamfahamu Mathew Mulumbi na nimelazimika kuamini kile alichoniambia.Alinipa taarifa muhimu kwamba IS wako hapa nchini na ndiyo wanaendesha mashambulio mbali mbali ya kuua viongozi wa dini na kuchochea vurugu.Alituelekeza mahala wanakoishi magaidi hao na tukafanya operesheni ya kuvamia makazi yao kwa kuwatumia makomando tukafanikiwa kuwakamata.Katika upekuzi wa makazi yao tuligundua vitu kadhaa ikiwemo mabaki ya vifaa vya kutengenezea bomu.Tunahisi yawezekana bomu lililotumika kulipua ubalozi wa Marekani lilitengenezwa hapo” akasema Rub na kumtazama Dr Fabian halafu akaendelea “Tuliwakamata watu wote waliokutwa hapo na tunaendelea kuwahoji.Kuna mtu ambaye Mathew alituelekeza tumtafute anaitwa Assad Ismail ambaye ni kiongozi wao.Tukimpata huyo tutafahamu mengi kuhusiana na hizi vurugu zinazoendelea.Mheshimiwa Rais hiki kinachoendelea hivi sasa kina sababu zake na ningeomba utupe muda zaidi wa kuendelea kulichunguza jambo hili nina uhakika siku si nyingi tukafanikiwa kujua kiini cha hizi vurugu.Kama tukifanikiwa kumpata huyo Assad Ismal tutamuhoji kujua nani aliyemtuma afanye mauaji ya viongozi wa dini na kuchochea vurugu ? Mheshimiwa Rais tunaelekea kuzuri katika uchunguzi wetu” akasema Ruby “Ruby umeniweka njia panda sijui nishike lipi.Nashangaa kwa Mathew ambaye amejiunga na magaidi kuwapa taarifa ambazo zitawaweka wenzake katika hatari.Hili haliingii akilini hata kidogo.Iweje awauze wenzake? Akauliza Dr Fabian “Ni kwa sababu Mathew si gaidi” akajibu Ruby “Huo ni iongo Ruby.Kama asingekuwa gaidi asingefanya shambulio lile baya na kuua watu.Hakuna sababu yoyote ya kumtetea mtu huyu ni gaidi na muuaji!! Akasea Dr Fabian “Mheshimiwa Rais, ni kweli Mathew anashirikiana na magaidi lakini ni kwa sababu ya misheni maalum ya siri” “Alikueleza ni operesheni ipi hiyo ya siri? Dr Fabian akauliza “Hakunieleza lakini …” “Hakuna lakini Ruby.Kama hakukueleza basi ni mwongo.Mathew Mulumbi amekuwa mnyama na ………” “Mheshimiwa Rais nakubali umuite Mathew majina yote mabaya kwa hili alilolifanya lakini ningeomba unisikilize mimi ambaye ninamfahamu Mathew vizuri kuliko wewe ! akasema Ruby kwa sauti ya juu kidogo halafu wakatazama kwa muda Ruby akaendelea “Ninamuamini Mathew na ninaamini hiki alichokifanya ni kwa sababu maalum.Hata siku moja Mathew hawezi akashirikiana na magaidi kama hana sababu ya kufanya hivyo.Tukiweka pembeni hilo,ni yeye ambaye ametupa mwanga kuhusiana na hiki kinachoendelea hapa nchini.Tulikuwa tumekwama hatujui tuanzie wapi lakini ni yeye ambaye ametusaidia na sasa ninaweza kusema tuna sehemu ya kuanzia kufahamu chanzo cha vurugu zilizotokea hapa nchini” akasema Ruby.Dr Fabian akamtazama kwa muda na kusema “He lied to you ! akasema Dr Fabian kwa ukali “Amekudanganya nawe ukakubali.Anacheza na akili zenu Yule jamaa na hakuna chochote cha maana.Kama kweli watu hao aliowaelekeza ni magaidi kuna chochote mmekwisha kipata hadi sasa kutoka kwao? “Bado tunaendelea kuwahoji mheshimiwa Rais lakini taarifa aliyotupa Mathew ni ya kweli kabisa na haina mashaka hata kidogo.Mheshimiwa Rais nakuomba uweke akiba ya maneno kwa sasa kwani baadae jambo hili litakapokuwa limefika mwisho usijilaumu kwa maneno yako”akasema Ruby “Usinifundishe nini cha kuzungumza Ruby.Ni aibu sana kwa mtu mkubwa kama wewe kuchezewa akili yako na mtu kama huyu asiye na hata chembe ya utu ! “Mheshimiwa Rais naomba uniamini na uamini kazi inayofanywa na idara yangu.Nakuhakikishia tutaupata mzizi wa hizi vurugu.Tayari tumekwishapata mwanga” akasema Ruby na Dr Fabian akacheka kidogo “Mwanga ulioonyeshwa na gaidi? Katu hiyo si taarifa ya kuamini na sina hakika kama kweli hao mliowakamata ni magaidi” akasema DrFabian “Mheshimiwa Rais uliniamini na kunipa idara ya SNSA niiongoze.Sintaweza kufanya kazi yangu kikamilifu kama hautaniamini.Mheshimiwa Rais kama hauna tena imani nami kwamba kwa kushirikiana na wenzangu tunaweza kulishughulikia suala hili la vurugu zilizotokea, naomba uteue mtu mwingine ambaye unadhani anaweza akaongoza vyema idara ya SNSA kama unavyotaka.Mimi niko tayarikuacha kazi muda huu huu ! akasema Ruby akionekana kukasirika “Ruby huu si wakati wa kufikiria mambo kama hayo.Taifa liko kwenye wakati mgumu mno.Sitaki kusikia tena ukizungumza au hata kufikiria kitu kama hicho cha kuacha kazi.Ninakuamini ndiyo maana nilikutoa Uingereza nikakuleta hapa kufanya kazi hii” “Kama ni hivyo mheshimiwa Rais naomba utuamini mimi na wenzangu.Nakuhakikishia mheshimiwa Rais si muda mrefu kutoka sasa kuna mambo mengi yatajulikana kuhusiana na hiki kinachoendelea.Naomba uniamini na utupe nafasi” akasema Ruby na baadaya muda Dr Fabian akauliza “Ukiacha hao jamaa mliowakamata mkidai ni magaidi kuna mpango gani mwingine mnao wa kutuwezesha kufahamu chanzo cha hizi vurugu?Wale watu mnaowatafuta mnaohisi wana mahusiano na hizi vurugu mmefikia wapi kujua mahala walipo? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais mpango tunaoendelea nao ni kuwahoji wale magaidi tuliowakamata ili tupate taarifa za mahala alipo Assad Ismail ambaye anaweza akatupa maelezo ya kutosha kuhusiana na hizi vurugu kwani ni wao wanaoendesha mauaji ya viongozi wa dini” “Mathew Mulumbi again” akasema Dr Fabian kwa sauti ndogo “Ruby nenda kaendelee na mipango yenu sintawaingilia.Kama kuna chochote mtakipata ambacho unadhani ninapaswa kukifahamu utanijulisha” akasema Dr Fabian “Nashukuru mheshimiwa Rais nitafanya hivyo” akajibu Ruby huku akinyanyuka akaagana na Rais akaondoka “Sina imani tena na SNSA.Hakuna chochote tunachoweza kukipata kutoka kwao kama tayari wanaongozwa na akili ya Mathew Mulumbi.Ningeweza kumtoa Ruby na kumuweka mtu mwingine lakini nilimtoa Uingereza aje aongoze idara hii na amepitia mambo mengi mazito hadi kufika hapa ngoja nimpe muda nione muelekeo wake.Ameniudhi mno leo kwa namna alivyomtetea Mathew Mulumbi eti kitendo alichokifaya cha kulipua ubalozi wa Marekani ni moja ya operesheni zake.Stupid ! akawaza Dr Fabian akiwa na hasira VICTORIA – SEYCHELLES Boti aliyopanda Mathew Mulumbi iliwasili katika pwani ya jiji la Victoria nchini Sheli Sheli.Bado Mathew alikuwa amevishwa mfuko kichwani hivyo hakufahamu walikuwa wapi.Alishushwa kutoka katika ile boti na kuingizwa garini milango ikafungwa magari yakaondoka.Baada ya mwendo wa takribani dakika ishirini gari alilopanda Mathew likapunguza mwendo halafu likasimama.Milango ikafunguliwa akashushwa ndani ya gari akaingizwa katika nyumba,akahisi kama vile wanashuka ngazi kuelekea chini.Akasikia mlango ukifunguliwa akaingizwa ndani ya chumba halafu mlango ukafungwa na watu wote wakatoka kukawa kimya.Chumba kilikuwa na giza nene. Zilipita dakika kama kumi hivi mlango ukafunguliwa tena,taa ikawashwa halafu Mathew akavuliwa ule mfuko kichwani.Mtu mmoja akamsogelea Mathew akachuchumaa na kumfungua pingu za miguu na mikono akamtaka Mathew amfuate wakaingia katika chumba kimoja ambamo waliwakuta watu wanne wakipata chakula. “Karibu Abu Zalawi” akasema Yule jamaa aliyekwenda kumfungua na Mathew akaketi kitini na kujumuika na wale jamaa katika chakula,alihisi njaa kali.Hakuwa ameweka chochote tumboni toka asubuhi.Walikula kimya kimya bila mazungumzo na baada ya kumaliza kula mazungumzo yakaanza “Abu Zalawi pole sana kwa safari ndefu” “Ahsante nashukuru” akajibu Mathew “Naitwa Jeffrey,wenzangu ni Richard,William,Brian,na Christopher” akasema Jefrey akiwatambulisha wenzake kwa Mathew “Tumepewa maelekezo maalum na viongozi wetu ya kuhakikisha misheni yako inakamilika lakini hapo hapo jambo hili lisionekane kama ni tukio la kutengenezwa ndiyo maana utaona ilitumika nguvu kidogo wakati wa kukukamata ili tukio lionekane ni halisi” akasema Jeffrey na kunyamaza kidogo “Muda mfupi ujao tutakufanyia mahojiano ambayo yatafuatiliwa moja kwa moja na makao yetu makuu Langley.Baada ya mahojiano hayo tutakupeleka katika chumba cha mateso ili kukutesa ufunguke na hapo utatusamehe kwani tutatumia nguvu ili ionekane ni jambo la kweli.Tutafanya namna ili upoteze fahamu halafu tutakupeleka katika chumba walimo wale wanasayansi wa Iran na utaanza kujenga ukaribu nao” akasema Jeffrey na kumuelekeza Mathew namna mahojiano yao yatakavyokuwa maswali atakayoulizwa na majibu anayotakiwa kuyatoa.Baada ya mazungumzo yale Mathew Mulumbi akarejeshwa katika kile chumba na kufungwa pingu akavishwa mfuko kichwani. Zilipita dakika kadhaa taa yeye mwanga mkali ikawaka mle ndani halafu mlango ukafunguliwa wakaingia watu wanne mle ndani.Mathew akainuliwa na kutolewa akapelekwa katika chumba kingine akafungwa mikono katika pingu za mezani halafu ikawashwa taa yenye mwangaza mkali na ule mfuko aliofunikwa kichwani ukatolewa.Ndani ya chumba kulikuwa na watu wapatao nane wakiwamo wale ambao alikula nao chakula muda mfupi uliopita.Kulikuwa pia na kamera imeelekezwa upande wake.Mbele yake alikaa Jeffrey akivuta sigara. “Unafahamu hapa uko wapi?akauliza Jeffrey “Nitafahamu vipi wakati mmenifunika na mfuko kichwani muda wote? akajibu Mathew “Usijali uatafahamu tu.Hapa ni moja ya sehemu wanakoletwa watu kama wewe kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano.Naomba nikuweke wazi kwamba hapa ni mahala panapoogopwa mno na mtu yeyote aliyewahi kupita mahala hapa ukimwambia kwamba unataka kumrejesha hapa ataongea kila lugha anayoifahamu ili asiweze kuletwa hapa.Taarifa nyingine ya mahala hapa ni kwamba wote waliowahi kuletwa hapa wote walifunguka na kutoa ushirikiano.Nikupe mifano ya watu waliowahi kupita hapa.Hasan Izz Al Din,Abdelkarim Hussein Al Nasser,Jaber Elbaneh,Ali Saed Bin Ali El Hoorie, na wengine wengi.Hawa wote ni magaidi wakubwa na walihusika katika matukio mbali mbali ya kigaidi na kuua wamarekani.Wote walipofika hapa walifunguka na kutaja mtandao wao wote.Wapo vile vile ambao walifikishwa hapa na hawakutoka hai na wapo ambao kwa miaka mingi wameendelea kushikiliwa sehemu hii kwa kushindwa kutoa ushirikiano.Hakuna yeyote kati ya watu wako anayeweza kukusaidia ukiwa hapa hivyo ni jukumu lako kujisaidia wewe mwenyewe” akasema Jeffrey na kuwasha sigara nyingine. “Anza kwa kututajia jina lako na umetokea wapi” akasema Jeffrey.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema “Naitwa Abu Zalawi,raia wa Saudi Arabia” akasema Mathew na kunyamaza akawatazama wale watu mle ndani “Abu Zalawi unafahamu ni kwa nini uko hapa? Akauliza Jeffrey lakini kabla Mathew hajajibu akaingia mtu mwingine akamnong’oneza Jeffrey kitu sikioni “Jibu Abu Zalawi unafahamu kwa nini uko hapa?Jeffrey akauliza “Nimelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam” akajibu Mathew “Abu Zalawi nataka utufahamishe umewahi kushiriki katika matukio mangapi ya kigaidi kabla ya hili la Dar es salaam? Akauliza Jeffrey “Mengi” akajibu Mathew “Unaweza kuyataja?Jeffrey akauliza “Nilimuua mkuu wa Mossad Afrika Mashariki,nimeshirikiana na kundi la wanamgambo la Ammar Nazar Brigades kufanya mashambulio kadhaa ndani ya Israel” akajibu Mathew bila woga “Sababu gani ilikupelekea ukalipua ubalozi wetu Dar es salaam? Akauliza Jeffrey.Sura ya Mathew ikabadilika na akaonyesha hasira “Ni kwa sababu ya dhuluma na ukandamizaji kunakofanywa na Marekani kwa nchi za kiislamu.Marekani ina chuki dhidi ya uislamu na ndiyo maana kila uchao imekuwa ikizikandamiza nchi za kiislamu na waislamu.Mfano ni nchi ya Iran imekuwa inawekewa vikwazo chungu nzima na Marekani na kama haitoshi bado wana mpango wa kuishambulia kijeshi.Hiki nilichokifanya ni kuionya Marekani kwamba waislamu tutasimama imara kutetea dini yetu dhidi ya ukandamizwaji wowote ule ! Hiki kilichotokea Tanzania kitaendelea sehemu nyingine mbali mbali duniani hadi pale nchi yenu itakapoacha unyanyasaji kwa waislamu na nchi zao ! akasema Mathew kwa ukali.Huku akitabasamu Jeffrey akasema “Abu Zalawi umejinadi kwamba ulichokifanya ni kwa ajili ya kupigania haki za wasilamu wanaonyanyaswa na Marekani lakini Marekani hainyanyasi waislamu na jambo lingine ni kwamba Uislamu hauamini katika ugaidi.Katika shambulio lile umeua pia waislamu.Hivyo ndivyo kitabu kitukufu kinaelekeza kuua watu wasio na hatia yoyote hata waislamu wenzako? Akauliza Jeffrey “Vyovyote mjuavyo ninyi lakini fahamuni mapambano haya yataendelea sehemu mbali mbali duniani ! akasema Mathew “Abu Zalawi shambulio lile ulilolifanya limeua watu zaidi ya sabini na miongoni mwao ni wanawake na watoto wapo waislamu wenzako pia waliokuwa wamepewa hifadhi katika ubalozi wetu wakiamini ni sehemu salama na hii inaonyesha wazi kwamba hatuchukii uislamu na waislam.Damu ya watu hao wote inakulilia wewe.Wengi wa watu uliowaua ni waafrika wenzako na huwezi kujua yeawezekana katika mkusanyiko ule wapo pia ndugu zako.Nafsi yako haikusuti kwa hiki ulichokifanya? Akauliza Jeffrey na Mathew akawakumbuka wale watoto aliowakuta ndani ya gari lililobebab bomu “Masikini wale watoto bado wadogo sana sijui kama walisalimika” akawaza “Abu Zalawi ukimya huo unaonyesha wazi kwamba hata wewe nafsi yako inakusuta kwa hiki ulichokifanya.Hata nikiitazama sura yako haionyeshi ukatili na hii inanipa picha kwamba umefanya kitendo hiki bila ridhaa yako.Nataka utuambie nani waliokutuma ukafanye shambulio lile?Nani viongozi wako? Abu Zalawi tunataka kuzuia mashambulio ya kigaidi yasiendelee kutokea na kuua watu wasio na hatia na wewe nayo nafasi kubwa kabisa ya kusaidia hilo liwezekane.Tuambie nani waliokutuma ukafanye shambulio lile? Akauliza Jeffrey.Mathew akawatazama kisha akasema “Tayari nimetimiza kazi yangu niliyotakiwa kuifanya hapa duniani hivyo sioni sababu ya kuendelea kupoteza muda wenu kunihoji kutafuta taarifa ambazo hamtaweza kuzipata. Nipelekeni huko mnakowapeleka mashujaa kama mimi mkanitese mtakavyo na hata ikiwezakana nichomeni sindano ya sumu nife kabisa siogopi chochote na niko tayari kufa hata sasa kwani naamini kwa nilichokifanya ninangojewa kwa hamu peponi ! akasema Mathew.Jeffrey akamtazama na kusema “Abu Zalawi katika matamshi yako uliitaja nchi ya Iran kwamba inaonewa na Marekani.Kuna nchi nyingi za kiislamu kwa nini ukachagua kuitaja Iran? Kwa nini isiwe Iraq,Syria au nchi yoyote nyingine?akauliza Jeffrey “Iran ni mfano wa nchi inayochukiwa na kukandamizwa na Marekani lakini zipo nyingi” akajibu Mathew “Ulitumwa na serikali ya Iran kufanya shambulio lile? akauliza Jeffrey “Mnapoteza muda wenu bure hapa na kunichelewesha kuiona pepo.Niueni haraka kwani hamtaweza kupata kitu chochote kutoka kwangu” akasema Mathew “Nilikuelekeza hapo awali kwamba ukiingia mahala hapa utake usitake lazima utafunguka lakini wewe naona bado hujapafahamu vizuri mahala hapa.Nitakuchukua na kukutembeza mahala hapa upafahamu vizuri halafu tutakuja tena kuzungumza baadae” akasema Jeffrey na kuelekeza Mathew afunguliwa pingu “Twende tukatembee rafiki yangu.Usiwe na hofu” akasema Jeffery kisha akatoka mle ndani akiwa na Mathew Walitembea katika vyumba kadhaa vya jumba lile huku Jeffrey akimpa Mathew maelezo na mara wakaingia katika chumba kimoja kikubwa chenye vifaa kama chumba cha mazoezi. “Abu Zalawi hapa tutafanya mazoezi kidogo lakini hautafanya na mimi” akasema Jeffrey na kugonga ukuta mlango miwili ikafunguka wakatokea watu sita.Ilikuwa ni mijitu ya miraba minne na yenye sura za kuogofya “Hawa ndio utakaofanya nao mazoezi” akasema Jeffrey na kuwageukia wale jamaa “Nimewaleteeni mgeni anahitaji mazoezi kidogo ili achangamke” akasema Jeffrey na kumsukuma Mathew akaangukia katika mikono ya mmoja wa wale jamaa akamdaka na kumuinua juu juu kisha akamrusha kwa mwenzake akamdaka na kumtandika ngumi nzito ambayo ilimfanya Mathew aone nyota akapepesuka na kupigwa teke akajikuta katika mikono ya mwingine ambaye alimtandika ngumi akanguka chini.Akainuliwa na mwingine akamtandika ngumi Mathew akaenda chini.Alikuwa anapigwa kwa zamu.Ndani ya muda mfupi hakuwa akitazamaika. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ruby aliwasili nyumbani kwa Gosu Gosu akitokea ikulu alikokuwa na mazungumzo na Rais.Alipokewa na Gosu Gosu wakaelekea katika chumba cha mapumziko “Mgeni yuko wapi? Akauliza Ruby “Yuko chumbani kwake anapumzika” “Umezungumza naye chochote? “Hapana Ruby sijazungumza naye chochote.Uliniambia nisimuulize chochote hadi utakapofika wewe mwenyewe” akasema Gosu Gosu “Good.Umekuwa naye toka Arusha unaweza ukamuelezeaje? Akauliza Ruby “Hatukuwa na mazungumzo mengi lakini kwa haraka haraka anaonekana ni mjanja na mwenye kuchukua tahadhari na vile vile hapendi kuchunguzwa .Nadhani utakapozungumza naye tutafahamu mambo mengi kuhusu yeye.Vipi uko utokako? “Huko mambo hayakwenda vizuri na Rais.Mazungumzo yalitawaliwa na mtu mmoja tu Mathew Mulumbi.Rais alikuwa mbogo akitoa matamshi makali kumuhusu Mathew.Nilijaribu kumdokeza Rais kwa kifupi kuhusu kile tunachoendelea nacho hivi sasa ndani ya SNSA nikamdokeza kwamba mafanikio haya yote hadi tukafanikiwa kuwafahamu na kuwapata magaidi wanaoendesha matukio ya mauaji hapa nchini ni kwa sababu ya Mathew Mulumbi lakini hatukuelewana pale nilipomwambia kwamba Mathew yuko katika misheni maalum na kile alichokifanya ni mojawapo ya misheni hiyo.Kwa ujumla maongezi yetu hayakwenda vizuri kufuatia suala hili la Mathew.Rais ametoa maneno mengi ya dharau kwetu ilifika wakati nilitaka kuachana na kazi hii” akasema Ruby “Usijali Ruby.Haya yote Mathew aliyafahamu ndiyo maana akatutahadharisha mapema.Sisi tunaoelewa kinachoendelea tuendelee kusimama naye.Tuendelee kupambana kuhakikisha nchi inakuwa shwari na tunawafahamu wale wote waliochochea vurugu hizi” akasema Gosu Gosu “Twende tuka zungumze na Nawal” akasema Ruby na Gosu Gosu akamuongoza wakaenda katika chumba alimo Nawal akagonga na Nawal akafungua mlango akawakaribisha ndani.Nawal alimtazama Ruby kwa jicho ambalo Ruby alilielewa.Nawal alikuwa anamtaka Gosu Gosu atoke mle ndani. “Usihofu Nawal tunaweza kuendelea Gosu Gosu akiwepo” akaema Ruby “Karibu Tanzania.Pole kwa safari “ “Ahsante.Poleni na nyie kwa yanayoendelea hapa Tanzania” “Tunashukuru Mungu mpaka sasa tu wazima” akasema Ruby na ukimya mfupi ukapita kisha akasema “Nawal nadhani ni wakati sasa wa kuzungumza kuhusiana na kile kilichokuleta hapa Tanzania.Mama yako Habiba Jawad aliponipigia simu aliniomba nikusaidie kufika Dar es salaam na vile vile katika kile kilichokuleta hapa Tanzania.Tayari nimekusaidia umeweza kufika salama Dar es salaam na sasa ninataka kufahamu kuhusu kile ambacho umekuja kukifanya hapa Tanzania” akasema Ruby “Kwanza kabisa nawashukuruni sana Ruby na Gasu Gasu” “Gosu Gosu” akasema Ruby na kumrekebisha Nawal “Jina gumu linanisumbua kutamka hata hivyo ninawashukuruni sana kwa kuniwezesha kufika salama Dar es salaam.Kama ningekuwa mwenyewe ingeniwia ugumu kuingia Dar es salaam haraka na kwa urahisi namna hii.Ahsanteni na ningeomba nipewe gharama zilizotumika kunifuata kule Arusha ili nizirejeshe” akasema Nawal “Usijali Nawal.Wewe ni mgeni wetu hivyo lazima tuhakikishe tunakuhudumia kwa kila kitu kama mama yako alivyompokea na kumtunza Mathew Mulumbi” akasema Ruby “Anaendeleaje Mathew Mulumbi?akauliza Nawal “Mathew hatujui kwa sasa anaendeleaje.Kwani si mko wote Saudi Arabia? Ruby akauliza “Mathew yuko hapa Tanzania.Hamjaonana bado? Akauliza Nawal .Ruby na Gosu Gosu wakatazamana “Ina maana hajui Mathew alichokuja kukifanya hapa Tanzania? Gosu Gosu na nawal wakaongea kwa Kiswahili na Nawal hakuelewa chochote kwani hakuifahamu lugha ya Kiswahili. “Twende naye taratibu tutafahamu kila kitu” akajibu Ruby “Ndugu zangu kitu kikubwa cha kwanza ambacho nataka mnisaidie ni kuonana na Mathew Mulumbi.Tafadhali sana nisaidieni kwa hilo” akasema Nawal “Nawal utatusamehe kwani kwa sasa hatufahamu mahala aliko Mathew Mulumbi” akasema Nawal “Mathew yuko hapa Dar es salaam.Hamjaonana naye?Mnafahamu makazi yake yalipo? Akauliza Nawal “Nawal tafadhali usitake kutuchanganya akili zetu.Ina maana huna taarifa za alichokifanya Mathew? Akauliza Gosu Gosu huku akimtazama Nawal kwa macho makali “Gosu Gosu.! Taratibu” akasema Ruby “Ruby ni kweli ninahitaji mno kuonana na Mathew Mulumbi kabla ya mambo yote.Kama bado hamjaonana naye Mathew yuko hapa Tanzania.Nipelekeni katika makazi yake yawezekana akawa huko” akasema Nawal “Nawal hapa tulipo ndipo makazi ya Mathew Mulumbi ila anayeishi hapa kwa sasa ni Gosu Gosu na sisi tote hapa ni kama nyumbani kwetu kwani Mathew ni mtu wetu wa karibu sana”akasema Ruby “Ina maana Mathew hajawasiliana nanyi alipokuja hapaTanzania? Akauliza Nawal “Hapana hajawasiliana nasi na hatukujua kama Mathew yuko hapa Dar es salaam” “Mathew aliiandika namba yako katika kitabu chake cha kumbu kumbu na kwa kuwa ni namba yako pekee iliyoandikwa humo tuliamini wewe ni mtu wake wa muhimu sana ndiyo maana tutakutafuta tukijua kwamba unaweza ukanielekeza mahala alipo Mathew” akasemaNawal “Nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha anaitwa Najma ambaye ni mke wa Abu Zalawi ambaye baadae niligundua ndiye Mathew Mulumbi akaniambia kwamba Mathew alikuwa ananitafuta simuni.Nimeshangaa unaponiambia kwamba Mathew alikuwepo hapa Tanzania” “Ni kweli Ruby.Mathew Mulumbi amekuja Tanzania” “Amekuja kufanya nini?Kwa nini amekuja kwa siri?Hapa ni nyumbani kwake kwa nini hajakanyaga kama amefika Tanzania? Ruby akauliza “Sifahamu amekuja kufanya nini lakini najua amekuja Tanzania” “Kwa nini unasisitiza sana kutaka kuonana na Mathew Mulumbi? Akauliza Gosu Gosu “Kuna taarifa muhimu nataka kumpatia” “Taarifa ipi? “Ni kuhusu mke wake Najma.Alijiua kwa kujipiga risasi baada ya Mathew kuondoka na hafahamu chochote juu ya jambo hilo” “Nini kilisababisha Najma akajiua?Ruby akauliza “Inadaiwa ni wivu.Alihisi labda Mathew ana mwanamke mwingine na ndiyo maana Mathew alipoondoka tu Najma akabaki akajiua” akasema Nawal “Anafahamika kama Abu Zalawi.Wewe umefahamuje anaitwa Mathew Mulumbi? akauliza Gosu Gosu “Niliambiwa hivyo na mama kwamba jina halisi la Abu Zalawi ni Mathew Mulumbi na anatokea Tanzania ambako hawalifahamu jina la Abu Zalawi”akajibu Nawal “Hapa naona tunacheza mchezo wa kitoto.Tunapoteza muda bila sababu ya msingi” akasema Gosu Gosu kwa hasira na kuinuka “Gosu Gosu nini unataka kukifanya?akauliza Ruby “Ruby hatuwezi kuendelea na mchezo huu wa kipuuzi.Huyu mwanamke asitufanye sisi wajinga” akasema Gosu Gosu “Sikiliza Nawal Mathew Mulumbi amelipua ubalozi wa Marekani hapa Dar es salaam usiku wa kuamkia leo na asubuhi ya leo amekamatwa jijini Nairobi na makachero wa CIA akitafua usafiri wa kumtoa nchini Kenya ili akimbilie Somalia na mpaka sasa hatujui mahala alipo.Nataka utuambie ukweli hukufahamu alichokuja kukifanya Mathew huku Tanzania?akauliza Gosu Gosu “Naomba mniamini ndugu zangu sifahamu chochote kuhusu jambo hilo.Ni Mathew kweli aliyefanya hicho kitu au ni mtu aliyefanana naye? Mathew katu hawezi kufanya kitu kama hicho” akasema Nawal na Gosu Gosu akamtazama kwa hasira halafu akasema “Nawal nitazame vizuri” akasema Gosu Gosu na Nawal akamtazama bila hofu. “Gosu Gosu anataka kufanya nini?akawaza Ruby “Nimeishi msituni katika mapigano makali toka nikiwa na umri chini ya miaka kumi.Kabla sijawa na maisha haya unionayo sasa nilichokuwa nakifahamu ni bunduki ,risasi na kuua tu.Muziki wangu ni milio ya risasi na mabomu.Kwangu mimi kutoa roho ya mtu ni kama kunywa maji.Usinione hivi mimi ni mkatili mno na usijaribu kuingia katika anga zangu utajuta na kumlaumu mama yako kwa nini alikuleta duniani” akasema Gosu Gosu na kunyamaza kidogo “Nimeanza na utangulizi huo ili ufahamu umekutana na watu wa namna gani.Mimi na mwenzangu Ruby tunafahamu kila kitu kuhusu ninyi.Mama yako Habiba Jawad ni mfadhili mkubwa wa ugaidi duniani.Ndiye anayekifadhili kikundi cha IS na makundi mengine mbalimbali.Tulifahamu hiki alichokuja kukifanya Mathew hapa Tanzania.Tulionana naye akatueleza alichokuja kukifanya.Tunataka kufahamu wewe nini kimekuleta hapa Tanzania?Kuna shambulio lingine la kigaidi mnapanga kulifanya Tanzania?Tueleze tafadhali muda wa michezo umeisha ! akasema Gosu Gosu.Nawal akavuta pumzi ndefu “Sikiliza Nawal” akasema Ruby “Kwanza kuna kitu ambacho wewe na hata mama yako Habiba Jawad yawezekana hamkifahamu kuhusu Mathew.Amejiunga nanyi na anafanya mambo ya kigaidi lakini Mathew si gaidi ni jasusi.Pili ni kuhusu sisi.Mimi na huyu mwenzangu Gosu Gosu ni wakurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi ijulikanyo kama SNSA.Jukumu letu ni kuhakikisha nchi inakuwa salama.Tunafahamu wewe umetoka katika familia ya kigaidi na umekuja hapa Tanzania kwa malengo hayo ya kufanya ugaidi.Nawal kwa ufupi tu nataka ufahamu kwamba umeingia katika mkono wa serikali na tutakuchukua kwa ajili ya mahojiano hivyo nakushauri tueleze kile kilichokuleta hapa Tanzania.Huna sababu ya kutuficha kitu kwani tunafahamu kila kitu kuhusu Habiba Jawad.Tuanzie hapo Nawal nini umekuja kukifanya hapa Tanzania? Akauliza Ruby.Nawal akatabasamu.Gosu Gosu akaonekana kukasirishwa na kitendo kile cha Nawal kutabasamu alipoulizwa swali,akasimama “Tunachokifanya hapa ni mzaha?akauliza Gosu Gosu Ruby akawahi kumshika mikono kwani tayari mkono wa kulia ulianza kuinuka “Jizuie GosuGosu ! akasema Ruby ‘Msinielewe vibaya ndugu zangu.Nimetabasamu baada ya kugundua kwamba nimefika mahala nilipopahitaji mno” akasema Nawal.Ruby na Gosu Gosu wakatazamana “Hatujakuelewa Nawal unamaanisha nini unaposema umefika mahala ulipopahitaji? Akauliza Ruby “Chloe Bennet.Ndilo jina langu halisi” akasema Nawal na kuwasimulia akina Ruby historia yake hadi alivyofikia kuolewa na Ammar Nazar. “Oh my God ! Ama kweli dunia hii imejaa siri.Kumbe huyu mwanamke naye ni jasusi dah ! Gosu Gosu akashangaa “Nikiwa kwa Ammar Nazari ndipo nilipokutana na Mathew ambaye kwa wakati huo alikuwa anatumiwa na Mossad kwa lengo la kumsaka Habiba Jawad akifahamika kama Abu Zalawi.Nilijenga naye mazoea na baada ya kufahamiana vizuri nikamfahamisha kuwa mimi pia ni jasusi na nilikuwa pale katika misheni maalum” akasema Nawal na kuwasimulia akina Ruby kuhusiana na safari ya Mathew hadi alipofika pale kwa Ammar Nazari na kujiunga na kikundi kile cha wanamgambo.Ruby alilengwa na machozi baada ya kuelezwa mambo aliyoyapitia Mathew “Sikujua kama Mathew ameteseka namna hii” akawaza Ruby “Israel walifahamu maficho ya Ammar wakayashambulia lakini kwa bahati nzuri mimi na Mathew tulifanikiwa kutoroka na hapo ndipo tulipoanza kumsaka Habiba Jawad.Haikuwa kazi rahisi kumfikia Habiba” akasema Nawal na kuwasimulia akina Ruby safari ngumu waliyopitia hadi kumfikia Habiba Jawad. “Baada ya kufika kwa Habiba misheni ya kumuua ikabadilika na tukajikuta tukiungana naye.Mimi niliolewa na mwanae anaitwa Abu Dahir na Mathew akamuoa mtoto mwingine wa Habiba anaitwa Najma ambaye ndiye alikupigia simu kukuuliza kama unamfahamu Abu Zalawi” akasema Nawal “Kitu gani kiliwapelekea mkabadili misheni mliyokuwa nayo ya kumuua Habiba wakati mkifahamu fika ni mfadhili mkuu wa ugaidi? Akauliza Gosu Gosu “Tulipofika kwa Habiba kwanza tayari alikuwa anatufahamu sisi ni akina nani.Kupitia vyanzo vyake aliweza kufahamu sisi ni majasusi na lengo letu lilikuwa ni kumuua.Alitueleza bila kutuficha kwamba tulikuwa pale kwa ajili ya kumuua na akatutaka tusiendelee na mipango yetu kwani ana malengo mazuri na sisi na ndipo misheni ilipobadilika tukajikuta tukiingia katika familia yake.Kwa ufupi tu Habiba Jawad ni tofauti na watu wanavyomfikiria.Baada ya kuwa naye karibu tumepata bahati ya kumfahamu vizuri na yawezekana msinielewe lakini ni mtu wa tofauti na wengi wamjuavyo” akasema Nawal na sura ya Gosu Gosu ikaonekana kubadilika “Mtu wa tofauti?Anafadhili makundi ya kigaidi na kuua watu halafu unatuambia ni mtu wa tofauti? Habiba ni muuaji mkubwa kwani bila yeye makundi haya ya kigaidi yasingeendelea kuwepo na kustawi ! akasema Gosu Gosu “Usemayo ni kweli Gosu Gosu lakini nina sababu ya kusema kwamba Habiba ni mtu wa tofauti na wengi mnavyomdhania.Niwape mfano mdogo.Miezi kadhaa iliyopita mtu mmoja aliyefahamika kama James Kasai akishirikiana na kundi la IS walifanya mauaji makubwa hapa Tanzania ambapo wake kadhaa za marais waliuawa.Ni Habiba Jawad aliyemuwezesha Mathew kumpata na kumuua James Kasai.Mnalifahamu hilo? Akauliza Nawal.Gosu Gosu na Ruby wakatazamana. “Naamini hamkuwa mkilifahamu hilo.Huo ni mfano mdogo tu kuhusu Habiba Jawad.Bila yeye Mathew asingeweza kufanikisha kumpata James Kasai” akasema Nawal “Sasa nimepata picha kamili.Wakati wa operesheni ile ya kumsaka James Kasai,Mathew alikuwa anazungumza na mtu simuni kila usiku na kila walipomaliza mazungumzo yao alikuwa anakuja na taarifa mpya.Kumbe alikuwa anazungumza na Habiba Jawad.Nadhani ndiyo maana alinikataza nisimfuatilie ili nsigundue kama alikuwa na mashirikiano na Habiba Jawad” akawaza Ruby “Habiba Jawad” Nawal akaendelea “Anatumika tu kufadhili makundi ya kigaidi lakini wapo wahusika wakuu wa ufadhili huo nyuma yake” akasema Nawal na kuwapa maelezo marefu akina Ruby kuhusiana na idara ile ndogo ndani ya CIA ambayo ni maalum kwa mashirikiano na makundi ya kigaidi lakini akina Ruby hawakuonekana kushangaa sana “Usiku wa kuamkia jana tulionana na Mathew na akatueleza kuhusiana na hiyo idara na mahusiano yake na hiki kinachoendelea hapa nchini kwa sasa na akatusaidia pia kutuelekeza mahala walipo magaidi wa IS ambao wanatumiwa kuchochea vurugu ambao tumewakamata tunaendelea kuwahoji.Katika mazungumzo yetu alikwepa sana kutueleza kuhusiana na kile alichokuja kukifanya hapa Tanzania ambacho ni kulipua ubalozi wa Marekani hadi leo asubuhi ilipotangazwa kwamba amekamatwa jijini Nairobi akituhumiwa kuwa ndiye aliyelipua ubalozi ule. Nataka kufahamu ni misheni gani aliyonayo Mathew hadi akalipua ubalozi ule wa Marekani? Akauliza Ruby Nawal akawaeleza kwa kina kuhusiana na misheni ambayo Mathew anaendelea nayo iliyompelekea alipue ubalozi wa Marekani.Gosu Gosu na Ruby wakabaki vinywa wazi. “Oh Mungu wangu ! Kwa nini Habiba akamuhusisha Mathew katika jambo hili? Hii ni misheni ya hatari sana na lengo lake ni ili Mathew auawe kwani uwezekano wa kumaliza salama misheni hii ni mdogo” akasema Ruby “Nakubaliana nawe Ruby kwamba misheni hii ni ngumu na ya hatari kubwa sana yawezekana ni misheni ngumu kuliko zote alizowahi kupitia Mathew na Habiba analifahamu hilo lakini ilikuwa lazima Mathew aifanye” akasema Nawal na kuwaeleza akina Ruby umuhimu wa misheni ile anayokwenda kuifanya Mathew. “Naamini mmeona umuhimu wa Mathew kushiriki katika misheni hii” akasema Nawal na Ruby akatikisa kichwa “Japo ni misheni ya muhimu sana hasa kwa nchi yetu na dunia kwa ujumla lakini ni misheni ya kifo” akasema Ruby “Jukumu letu ni kumuombea ili aweze kumaliza misheni hiyo akiwa salama kabisa” akasema Nawal “Nawal umesema wewe ni jasusi wa CIA.Unaweza kuwasiliana na wenzako na kufahamu mahala alipo Mathew hivi sasa? Nataka kujua kama bado yuko Nairobi ili tufanye mipango ya kumuokoa kwani misheni hii ni mbaya mno na tunaweza kumpoteza” akasema Gosu Gosu “Nikurekebishe Gosu Gosu kwa sasa siko tena CIA.Nilipoamua kuolewa na Abu Dahir ulikuwa ni mwisho wangu na CIA na mpaka sasa hawajui niko wapi hivyo sina mawasiliano na watu wa CIA.Jambo lingine hata kama ningekuwa bado CIA nisingeweza kufahamu mahala alipo Mathew kwa kuwa ni misheni ya siri kubwa.Tatu hata kama tungefahamu mahala alipo hatuwezi kwenda kumuokoa Mathew kwani yeye mwenyewe ametaka kuifanya misheni hii kwa kuelewa umuhimu wake.Nawashauri ndugu zangu kitu kikubwa kwa sasa ni kuendelea kumuombea tu Mathew ili akamilishe misheni hii akiwa salama.Binafsi nina uhakika kwamba atamaliza na atakuwa salama.Nawaomba na ninyi muwe na uhakika huo.Msiwe wepesi kuamini kwamba Mathew ni gaidi.Ameingizwa katika ugaidi kwa malengo maalum lakini ukweli utabaki pale pale kwamba Mathew ni jasusi na hata siku moja hawezi kuwa gaidi.Tumeelewana katika hilo?akauliza Nawal “Hata yeye mwenyewe alitueleza hivyo kwamba tusiamini kile tutakachokisikia juu yake.Tunamfahamu Mathew,tumekuwa naye muda mrefu na tunamuamini”akasema Ruby “Vizuri.Huo ni upande mmoja wa Mathew Mulumbi ambaye anaendelea na misheni yake” akasema Nawal na kunyamaza kidogo “Watu hawa ambao wanaichezea dunia watakavyo bado wana uchu na rasilimali za Afrika.Ndugu zangu mimi ni mmarekani lakini nina damu ya Afrika.Baba yangu asili yake ni Libya hivyo japokuwa nimechanganya damu lakini mimi bado ni mwenzenu mimi ni mtoto wa Afrika na dhumuni la kuja hapa ni kuwasaidia ndugu zangu” akasema Nawal.Ruby na Gosu Gosu wakatazamana wakatabasamu “Karibu Afrika Ruby bara lililojaa utajiri lakini likiongoza kwa umasikini mkubwa kwa sababu ya kunyonywa na hayo mataifa makubwa.Madini yanasombwa tunabaki na mashimo makubwa,rasilimali za misitu zinavunwa na utajiri mwingine mwingi unachukukuliwa na sisi tunachoambulia ni misaada kidogo,mikopo yenye masharti magumu na silaha ambazo tunazimia kuuana wenyewe kwa wenyewe.Libya nchi alikotoka baba yako amani imetoweka.Kumekuwa na mapigano kila uchwao.Kinachoendelea Libya kiko sehemu nyingi ya Afrika.Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na mingi ya migogoro hiyo inasababishwa na wanasiasa wanaogombea madaraka.Viongozi hawataki kung’oka madarakani na mambo mengine mengi.Hiyo ndiyo Afrika.Lakini mengi ya haya niliyokueleza ukichunguza chanzo chake ni mataifa makubwa” akasema Gosu Gosu “Uko sahihi Gosu Gosu. Mataifa makubwa yamekuwa ni chanzo cha migogoro mingi inayoendelea barani Afrika.Nchi za kiafrika hazikupaswa kuwa na umasikini mkubwa kama uliopo sasa” akasema Nawal na Gosu Gosu akaingilia kati “Tazama nchi kama jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ni nchi yenye utajiri mkubwa wa madini na rasilimali nyingine lakini imekuwa ni nchi masikini kutokana na migogoro isiyokwisha.Kila uchao makundi ya waasi yanaibuka.Ukijiuliza yanatokea wapi? Wanatoa wapi silaha ? Utapata jibu kwamba kuna nguvu kubwa kutoka nje ya Afrika” akasema Gosu Gosu “Mfano mwingine ni haya machafuko yaliyotokea hapa Tanzania na Uganda.Yametengenezwa kwa kusudi maalum.Wakati ninyi mkigombana wao wanapata nafasi ya kujipenyeza na kuchukua kile wanachokihitaji na sasa wanayabeba mafuta ya Uganda mapipa kwa mapipa bila kujali damu ya watu inayoendelea kumwagika.Huu ni ukatili mkubwa na aibu kwa nchi kubwa kama Marekani na ndiyo maana niko hapa” akasema Nawal na kunyamaza kidogo “Baada ya mpango wao wa kupata mafuta kufanikiwa sasa wamenogewa na wanataka kwenda mbali zaidi ya mafuta.Wanataka kuingia katika rasilimali nyingine kama vile madini na mazao ya misitu.Ili kulifanikisha hilo lazima vikosi vya Marekani vilivyopo hapa Tanzania viendelee kuwepo kwa muda mrefu na ikiwezekana viongezwe zaidi hivyo basi wameamua kuja na mpango mwingine na safari hii wanataka kuja kusambaza kirusi hatari kitakacholeta maangamizi makubwa” akasema Nawal “Kirusi?! Akauliza Ruby kwa mshangao “Ndiyo wanataka kusambaza kirusi hatari ambacho kiko kwenye maandalizi hivi sasa”Nawal akawaeleza kwa kina kuhusiana na mkakati ule wa kusambaza kirusi nchini Tanzania halafu akainuka akaenda katika sanduku lake akalifungua na kutoa faili dogo akatoa picha akampatia Ruby “Anaitwa Sattar Sayf Al Din” Akasema Nawal.Ruby akazitazama picha zile halafu akampa Gosu Gosu naye akazitazama “Ni nani huyu mtu?akauliza Gosu Gosu “Huyu anatokea kundi la IS na ndiye anayekuja kusambaza kirusi hicho hapa Tanzania.Hivi sasa tayari yuko Marekani akiandaliwa kwa kazi hiyo” akasema Nawal. “Hiyo ndiyo misheni iliyonileta hapa Tanzania.Nimekuja kuhakikisha kwamba mpango huo haufanikiwi na Tanzani ainaendelea kuwa sehemu salama.Kwa mara nyingine tena ni Habiba Jawad ambaye amenituma nije kutekeleza mpango huu kwa siri.Nadhani sasa mtaweza kuona ni kwa nini hata Mathew aliamua kushirikiana na huyu mama.Hayakuwa maamuzi rahisi kuamua kushirikiana mtu ambaye kwa muda mrefu tumekuwa tukiamini ni mfadhili mkuu wa ugaidi duniani”` “Kwa nini Habiba anauma na kupuliza? Akauliza Gosu Gosu “Nimekwisha waambia sababu ya Habiba kufanya hivi anavyofanya ni kwamba anataka kukimaliza kikundi kile kidogo ndani ya CIA ambao wanasababisha haya yote kutokea.Watu hao wasio na huruma hata chembe ndio ambao Mathew Mulmbi amechagua kupita njia ngumu yenye mateso makali ili kuwafikia na kuwamaliza.Kwa hili nathubutu kumuita Habiba Jawad ni shujaa kwani angeweza kuacha wakaendelea na mipango yao na watuhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ wengi wakapoteza maisha lakini amekataa kuendelea kuwa mtumwa wa hawa watu,hataki tena kuendelea kufadhili mauaji ya watu wasio na hatia na ndiyo maana anatutumia mimi na Mathew Mulumbi.Ndugu zangu ninataka tushirikiane katika hili.Peke yangu sintaweza” akasema Nawal.Ruby akamgeukia Gosu Gosu “Gosu Gosu unasemaje?Unamuamini huyu mtu? akauliza Ruby kwa Kiswahili “Ruby nadhani tungejadiliana kwanza pembeni kabla ya kumpa jibu” akasema Gosu Gosu wakamtaka radhi Nawal wakatoka mle ndani wakaenda kusimama katika varanda. “Umemsikiliza vyema maelezo yake.Umemuamini?akauliza Ruby “Kwa maelezo aliyoyatoa kuna kitu kinaniambia nimuamini japo lazima tuwe na tahadhari sana tunaposhirikiana na watu kama hawa ambao wametoka katika mzizi wa ugaidi” akasema GosuGosu “Nini ushauri wako?Tushirikiane naye au?akauliza Ruby.Walijadiliana kwa muda wa dakika kama tano hivi kisha wakakubaliana kushirikiana na Nawal halafu wakarejea ndani “Nawal tumekubaliana kushirikiana nawe.Kama nilivyokueleza awali kwamba sisi ni viongozi wa idara inayoshughulika kwa siri na usalama wa ndani wa nchi.Tunazo rasilimali za kutosha kutuwezesha kutekeleza hicho ulichokuja kukifanya.Tunataka kujua je huyu mtu anayeleta kirusi anakuja lini?Anafikia wapi? Tukifahamu hayo itakuwa rahisi kwetu kufanya maandalizi” akasema Ruby “Kwa sasa bado sina taarifa zozote lakini nategemea kupata taarifa kutoka kwa Habiba Jawad.Yeye anafuatilia kila kinachoendelea kuhusiana na mpango huo wa kukisambaza kirusi.Kitu cha kanza ninachohitaji ni kupata mawasiliano ili niwasiliane na Habiba Jawad” akasema Nawal “Mawasiliano utapata.Lakini tungetaka kufahamu kuhusu huyo mtu anayekuja kusambaza kirusi anakuja kwa kutumia njia gani?Atakuja lini? Akauliza Ruby “Kama nilivyosema kwamba ninategemea kupata taarifa zote kutoka kwa Habiba Jawad.Hatua ya kwanza ilikuwa ni mimi kufika Dar es salaam halafu nitawasiliana naye na atanipa maelekezo.Nisaidieni niweze kuwasiliana naye na kama tayari anazo taarifa atanijulisha” akasema Nawal.Ruby akampa Nawal simu yake ili awasiliane na Habiba Jawad.Nawal akafungua sanduku lake akatoa kijitabu kidogo akaandika namba za Habiba katika simu akapiga simu ikaanza kuita baada ya muda ikapokelewa “Hallo”akasema Habiba “Mama Habiba ni mimi Nawal” “Ouh Nawal.Nimefurahi kusikia sauti yako.Tayari umefika Tanzania? Akauliza Habiba “Ndiyo mama.Tayari nimekwisha fika Tanzania na tayari nimefika Dar es salaam na tayari nimeonana na Ruby”akasema Nawal “Nafurahi kusikia hivyo Nawal.Hautaweza kuonana na Mathew kwani tayari amekwisha anza misheni yake.Jana usiku alilipua ubalozi wa Marekani na leo amekamatwa jijini Nairobi hivyo kwa sasa mpango ule wa kumpeleka Iran unaendelea”akasema Habiba “Tayari nimekwisha zipata taarifa hizo mama.Imekuwa bahati nzuri kwangu kwani Ruby ni mkurugenzi wa SNSA idara ya usalama wa ndani ya nchi hivyo tutasaidiana katika hilo zoezi” “Ouh kweli ! Habiba akashanga “Ndiyo mama” “Vizuri sana .Basi saidianeni kuhakikisha kwamba mnaokoa raia wa Tanzania na dunia kwa ujumla kwani kirusi hicho endapo kikisambazwa basi kinaweza kuvuka mipaka ya Tanzania na kusambaa hadi sehemu nyingine za dunia” “Sisi hapa tuko tayari.Kuna taarifa zozote umezipata tayari kuhusiana na Sattar Sayf Al Din?akauliza Nawal “Taarifa nilizo zipata ni kuwa kirusi kinachotarajiwa kuja kusambazwa Tanzania kiko tayari lakini tatizo lililopo ni kwamba wanasayansi bado hawaja pata kinga yake.Mpango ulikuwa kabla ya kusambaza kirusi hicho lazima iwe imepatikana kinga yake ili kuwakinga wanajeshi wa Marekani walioko Tanzania na vile vile kuwakinga wamarekani endapo kirusi hicho kitavuka mipaka ya Tanzania” “Kwa hiyo wameahirisha?akauliza Nawal “Hapana hawajaahirisha.Mpango uko pale pale.Kwa mujibu wa taarifa nilizozipata ni kwamba kwa sasa vurugu zinaonekana kupungua na hii imewapa hofu hivyo wameamua kukisambaza kirusi hicho hivyo hivyo bila kinga yake kuwa tayari” akasema Habiba “Dah ! akasema Nawal “Nawal kwa namna yoyote ile hakikisha kirusi hiki hakisambai Tanzania au katika ardhi ya Afrika.Watu wengi watakufa kwani hakina kinga bado” “Nakuhakikishia mama kwamba kirusi hicho hakitasambazwa hapa Tanzania.Mipango yao ikoje? Sattar Sayf Al Din anakuja lini Tanzania? Akauliza Nawal “Bado sijajua anakuja lini lakini kwa taarifa nilizozipata ni kwamba atakapofika Tanzania Sattar atapokelewa na mtu anaitwa Assad Ismail.Huyu anaishi Mombasa Kenya lakini nimetaarifiwa kwamba kwa sasa yuko hapo Tanzania na ndiye atakayemsaidia Sattar katika zoezi hilo la kusambaza hicho kirusi.Ili kuweza kumpata Sattar lazima umpate kwanza Assad”akasema Habiba “Umesema anaitwa Assad Ismail?akauliza Nawal “Ndiyo Assad Ismail” akajibu Habiba na Nawal akamgeukia Ruby “Andika katika karatasi Assad Ismail” akasema Nawal “Huyu Assad nitampata vipi hapa Dar es salaam?Anaishi wapi?akauliza Nawal “Bado sijapata taarifa kamili za mahala alipo lakini hadi kufikia kesho mchana nitakuwa nimejua wapi unaweza ukampata” “Mama ahsante kwa taarifa hizi nitazifanyia kazi kwa kushirikiana na wenzangu niliowakuta hapa” akasema Nawal “Sawa Nawal.Naomba uwe makini sana unapolishghulikia jambo hili kwani ni mpango wa siri wa taifa kubwa hivyo lazima watakuwa wamechukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha mpango wao huo haukutani na vikwazo vya aina yoyote.Nawal katika misheni hii hakuna kitu kushindwa umenielewa? Akasema Habiba “Nimekuelewa mama” akasema Nawal na kuagana na Habiba.Nawal akawaeleza kile alichoelezwa na Habiba “Huyu Assad Ismail Mathew alikwisha tupa taarifa zake na tayari tumeanza kumsaka.Huyu ndiye ambaye amekuwa mchochezi mkuu wa vurugu zinazoendelea.Kwa kushirikiana na wenzake wamekuwa wakiendesha mauaji ya viongozi wa dini kwa lengo la kuwafarakanisha waumini wa dini kushambuliana.Tayari tunao watu wanaoshirikiana na Assad unaendelewa kuwahoji”akasema Ruby “Mmekwisha pata taarifa zozote za mahala alipo Assad?akauliza Nawal “Hapana.Tumewahoji watu wale na mpaka sasa bado hatujapata chochote.Wamekuwa wagumu sana kusema chochote.Kuna mtu anaitwa Marwan ambaye Mathew alituelekeza kwamba ndiye anafahamu mahala alipo Assad.Tayari tumempata.Tumemfanyia mahojiano lakini bado hajafunguka” akasema Ruby nawal akashusha pumzi na kusema “Nimeishi na magaidi kwa miaka kadhaa ninawafahamu vyema.Naweza kusema kwamba tayari wameharibiwa akili zao na wako tayari kufa muda wowote.Kupata taarifa kwa hawa watu si jambo la mchezo inahitaji kutumika nguvu kubwa.Kuwahoji magaidi si sawa na kuwahoji wahalifu wengine wa kawaida.Magaidi ni watu wanyama sana na unapowahoji unapaswa nawe uwe kama wao nadhani mmenielewa ndugu zangu ” akasema Nawal na Gosu Gosu akamtazama Ruby “Ruby nafahamu mimi si mtanzania na wala si mtu wa idara yenu lakini ni mwenzenu.Nina ombi moja kwako”akasema Nawal “Omba Nawal” “Ninataka kumuhoji huyo Marwan ambaye Mathew alielekeza kwamba ndiye anayefahamu mahala alipo Assad” akasema Nawal sura ya Ruby ikaonyesha kutokukubaliana na wazo la Nawal “Nawal yuko sawa.Nilikwambia jambo hili toka awali Ruby.Watu hawa wanapaswa kuhojiwa tofauti na watu wengine.Tupe nafasi mimi na Nawal tuwahoji tena wale jamaa.Nina uhakika kuna kitu tutakipata kutoka kwao” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu sipendi namna ulivyomfanyia Marwan.Si…..” “Ruby hii ni vita.Kila mbinu lazima itumike kupata taarifa.Tafadhali kwa mara ya kwanza Ruby fumba macho kuwa na moyo wa jiwe.Ruhusu nguvu itumike kuwahoji hawa magaidi ili tuweze kumpata Assad ambaye lazima tumpate kwa gharama yoyote” akasema Gosu Gosu. “Gosu Gosu kanuni za idara haziruhusu matumizi ya nguvu katika kuwahoji watu.Ulichokifanya ni kinyume na kanuni zetu.Lazima tufuate maelekezo yaliyotolewa katika kufanya mahojiano na kupata taarifa kutoka kwa watu tunaowahoji” “C’mon Ruby.Huu si wakati wa kufuata hizo kanuni ambazo hazitoi matokeo.Tazama kwa kufuata kanuni hizo hizo mpaka leo hii hakuna tulichokipata kutoka kwa wale magaidi ! akasema Gosu Gosu kwa sauti ya juu kidogo “Gosu Gosu mimi ndiye kiongozi wa idara na ndiye mwenye maamzi ya mwisho hivyo siwezi kuruhusu matumizi ya nguvu kubwa kama ulivyofanya kwa Marwan.Sikufurahi hata kidogo kwa kile ulichokifanya ! Ruby naye akajibu kwa sauti ya juu “Kuna nini ndugu zangu?akauliza Nawal baada ya kuona Gosu Gosu na Ruby wakibishana kwa kutumia kiswahili “Hakuna tatizo” akajibu Gosu Gosu “Kama hakuna tatizo nadhani mmenielewa ombi langu la kutaka niwahoji hawa jamaa mliowakamata kwa maelekezo ya Mathew.Si kazi nyepesi kupata taarifa kutoka kwa magaidi kama nilivyowaeleza na wakati mwingine inalazimu kutumia nguvu kubwa”akasema Nawal “Hapo ndipo kuna tatizo Nawal.Idara yangu hairuhusu matumizi makubwa ya nguvu katika kuwahoji watu tunaowashikilia”akasema Ruby na Nawal akamtazama kwa macho ya mshangao “Ruby ni kweli hapo kuna tatizo.Tazama” akasema Nawal “Mimi si mtanzania lakini nimekuja hapa kuwasaidia watanzania na janga kubwa linalowakabili.Katika kulitimiza jukumu langu hilo sintahitaji vikwazo vya aina yoyote ile.Kirusi hicho kikisambaa hapa Tanzania halitakuwa janga la kwenu pekee bali la kidunia hivyo nalazimika kutumia kila njia kuhakikisha kwamba mpango huo wa kusambaza kirusi haufanikiwi.Naomba tushirikiane Ruby.Nafahamu kila idara ina kanuni zake lakini huu si wakati wa kufuata hizo kanuni.Haya ni mapambano ya kufa na kupona.Lazima tuwe na kanuni zetu wenyewe aidha gaidi atoe siri au afe ! akasema Nawal na kwa mbali Gosu Gosu akatabasamu “Nimempenda Nawal.Huyu ndiye anayenifaa kufanya naye kazi ! akawaza Gosu Gosu “Ruby kuna tatizo lolote katika suala hilo? Akauliza Nawal “Hakuna tatizo lakini itabidi tutafute sehemu nyingine kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano hao jamaa.Hatuwezi kutumia ofisi za SNSA kwa jambo hilo” “Hakuna tatizo.Tunazo nyumba tatu kwa ajili ya kazi hiyo hapa Dar es salaam tutatumia moja wapo” akasema Gosu Gosu Kwa shingo upande Ruby akiongozana na Nawal na Gosu Gosu wakaondoka kuelekea ofisi kuu ya SNSA VICTORIA – SHELI SHELI Mathew alianguka chini na kupoteza fahamu kufuatia kipigo kikali alichopewa.Hakuwa anatazamika usoni, alikuwa amechafuka damu.Yote haya yaliyokuwa yanaendelea yalikuwa yakifuatiliwa na viongozi wa CIA nchini Marekani.Baada ya kupoteza fahamu maelekezo yakatolewa kwamba wampumzishe hadi baadae.Mathew akaburuzwa na kutolewa ndani ya kile chumba akashushwa chini zaidi na lango la chumba kimoja likafunguliwa na Mathew akarushiwa ndani ya kile chumba akiwa bado hajitambui kisha lango likafungwa.Ndani ya kile chumba kulikuwa na watu sita.Watu wale walionekana wachovu na waliokata tamaa.Walikuwa na ndevu nyingi na nguo chafu.Watu wale sita kila mmoja alikuwa amelala juu ya godoro dogo na chumba kilikuwa na mwangaza hafifu.Pembeni ya kile chumba kulikuwa na mlango wa choo na bafu.Kulikuwa na meza ya chakula iliyokuwa na viti sita.Pembeni ya chumba kulikuwa na meza ya kusomea yenye viti viwili na juu yake kulikuwa na vitabu vitatu vya quran. Baada ya Mathew kutupwa mle ndani wote waliinuka kutoka katika magodoro yao wakamkazia macho.Hawakumfahamu ni nani.Mmoja wa wale jamaa akainuka na kwenda kumgeuza akamtazama na kutikisa kichwa wa masikitiko kutokana na hali aliyokuwa nayo.Uso wake ulikuwa umevimba na kuchafuka damu “Hawa watu ni wanyama sana” akasema huku akimvua Mathew shati alilokuwa amevaa wale wengine nao wakainuka wakamfuata “Ni mzima? Akauliza mwingine “Hana fahamu amepigwa mno” “Ni nani huyu mtu?Amefanya nini? Kwa nini aje aunganishwe nasi? Mwingine akauliza “Tumsaidie aweze kuzinduka halafu atatueleza” Haraka haraka wakaanza jitihada za kumsaidia Mathew aweze kurejewa na fahamu. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ruby akiwa na Gosu Gosu na Nawal waliwasili katika makao makuu ya SNSA wakashuka garini na kuelekea ofisini kwa Ruby ambaye aliwataka Gosu Gosu na Nawal wabaki mle ofisini yeye akaelekea katika idara ya afya kutazama maendeleo ya Marwan. “Idara kubwa sana hii na nyeti kwa nchi.Haipaswi kuwa na kiongozi mwoga anayeogopa kufanya maamuzi magumu” akasema Nawal baada ya Ruby kutoka mle ofisini “Usijali Nawal.Tutapata tu kile tunachokitafuta” akajibu Gosu Gosu “Sifahamu lugha yenu mnayozungumza lakini wakati mkizungumza niliona kama vile Ruby anaonyesha wasi wasi” akasema Nawal “Ruby anajaribu kuzingatia kanuni lakini kwa hatua hii tuliyofika kanuni hazina nafasi.Nakubaliana na ushauri wako kwamba tuwe na kanuni zetu wenyewe gaidi aidha aseme ukweli au ateseke hadi kufa” akasema Gosu Gosu “Uliniambia kwamba ulikuwa mwanajeshi? Akauliza Nawal “Ndiyo.Nilikuwa mwanajeshi wa kikundi kimoja cha waasi waliokuwa wakipigana vita na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Nimekaa msituni toka nikiwa mdogo kabisa nikipigana vita” “Ouh kumbe asili yako ni jamhuri ya kidemokrasia ya Congo? “Ndiyo.Lakini kwa sasa ni raia wa Tanzania” akajibu Gosu Gosu na mlango ukafunguliwa akaingia Ruby “Marwan anaendelea vizuri.Nimekwisha elekeza apakiwe katika gari maalum yeye na wenzake wawili kisha tutawapeleka katika moja ya nyumba zetu kwa ajili ya mahojiano” akasema Ruby “Ahsante sana Ruby kwa kukubali kufanya maamuzi haya magumu” akasema Nawal.Gosu Gosu akatoka mle ofisini na kwenda kukusanya vifaa kwa ajili ya kuwasaidia katika mahojiano yao na kuvipakia garini.Marwan na wengine wawili wakaingizwa katika gari kisha wakaondoka . “Gosu Gosu anafurahi kwa kumpata mwenzake ambaye anaonekana anapenda matumizi ya nguvu katika kutafuta taarifa.Sifurahi hiki wanachokwenda kukifanya kwani ni kinyume na kanuni zetu na hata haki za binadamu.Si kila wakati njia ya mateso inakuwa na manufaa.Watu kama hawa kuna njia za kuwahoji kwani tayari wamekwisha haribiwa kisaikolojia hivyo inabidi kuanza kwanza kuwarejesha katika maisha ya kawaida ndipo hapo unaweza ukapata kile unachokihitaji kutoka kwao.Sina hakika kama nguvu itafanikisa kupata chochote” akawaza Ruby wakiwa garini. Iliwachukua dakika hamsini na mbili kuwasili katika nyumba ambayo wangeitumia kuwahoji wale magaidi.Nyumba ilikuwa giza na walinzi walikuwa wamejificha kwa ndani.Ruby akawapigia simu akawajulisha kuwa tayari wamefika na geti likafunguliwa.Marwan na wale magaidi wenzake wakaingiza katika chumba wakiwa wamefungwa vitambaa usoni na mikono yao ikiwa imefungwa pingu.Ruby akaelekeza jenereta liwashwe na maandalizi yakaanza.Nawal na Gosu Gosu wakafanya maandalizi ndani ya chumba watakachokitumia kuwahoji wale magaidi na walipokuwa tayari magaidi wote watatu wakaletwa ndani ya kile chumba wakafunguliwa vitambaa walivyokuwa wamefungwa usoni . “Hello Marwan ! akasema Gosu Gosu baada ya kukutanisha macho na Marwan ambaye alionyesha hofu kubwa “Tumekutana tena siku ya leo.Tutaendelea pale tulipoishia siku ile” akasema Gosu Gosu na kumuinua Marwan akampeleka katika kiti.Ruby hakuwemo ndani ya kile chumba alikuwa anafuatilia kinachoendelea akiwa katika chumba kingine “Huyu ndiye Marwan” Gosu Gosu akamwambia Nawal “Asalaam alaikum Marwan” Nawal akamsalimu Marwan ambaye sura yake ilionyesha hasira kubwa baada ya kusalimiwa na Nawal “Hata kama usipojibu lakini tutaelewana tu” akasema Nawal kwa lugha ya kiarabu.Marwan kwa dharau kubwa akamtemea mate.Gosu Gosu aliyekuwa karibu akainua mkono wake na kumnasa Marwan kofi zito “Taratibu Gosu Gosu.Hizi dharau ni za muda tu zitakwisha” akasema Nawal,Gosu Gosu akamuinua Marwan akamketisha kitini “Marwan,naomba nianze kwa kujitambulisha kwako.Naitwa Nawal.Nimekuwa katika kundi la Ammar Nazari brigades kama mke wa Ammar Nazari naamini umewahi kumsikia.Leo hii niko hapa Tanzania kuzungumza nawe.Kuna kitu kimoja tu ambacho nakitaka kutoka kwako.Wapi alipo Assad Ismail? Akauliza Nawal kwa lugha ya kiarabu.Marwan akamtazama kwa hasira na kusema “Shetani wa kike wewe.Kwa nini umetusaliti kiasi hicho na kuungana na hawa viroboto wasio na thamani yoyote? Nakuhakikishia utajutia hiki ulichokifanya ! akasema Marwan kwa hasira naye akitumia lugha ya kiarabu “Marwan ninarudia tena,ninataka kufahamu mahala alipo Assad Ismail”akasema Nawal “Fanya chochote ukitakacho lakini siwezi kukueleza chochote msaliti mkubwa wewe ! akafoka Marwan “Gosu Gosu tuanze kazi hadi atakapokuwa tayari kusema ! akasema Nawal.Gosu Gosu akamuinua Marwan kutoka kwenye kiti akampandisha katika kitanda akamfunga vizuri kwa mikanda mikononi na miguuni “Hakuna mateso yoyote mtakayonitesa yatakayonipelekea nikafungua mdomo wangu na kuwapa kile mkitakacho ! akasema Marwan “Usimjali Gosu Gosu atasema tu ! akasema Nawal kisha Gosu Gosu kwa nguvu akaupanua mdomo wa Marwan na Nawal akaingiza mpira halafu akafungulia maji na tumbo la Marwan likaanza kujaa maji.Baada ya muda akafunga maji na kuuchomoa ule mpira.Marwan alikuwa anaweweseka “Wapi alipo Assad?akauliza Nawal lakini Marwan hakujibu.Nawal akampa ishara Gosu Gosu ambaye aliuinua mguu wake wa kulia akaushusha katika tumbo la Marwan ambaye aliyatapika yale maji yaliyokuwa tumboni. “Tunaanza upya hadi utakaposema mahala alipo Assad ! akasema Nawal na zoezi lile likaendelea Mara nne tumbo la Marwan lilijazwa maji na kutapishwa lakini hakusema chochote. “Sijawahi ona mijitu migumu kama hii ! akasema Gosu Gosu “Usichoke Gosu Gosu atasema tu” akasema Nawal kisha akaelekeza Marwan atolewe pale kitandani wakamfunga katika chuma maalum kilichotengenezwa mfano wa goli la mpira wa miguu.Marwan alining’inizwa akiwa mtupu .Alikuwa amechoka mwili wake haukuwa na nguvu “Marwan kabla hatujaendelea na zoezi la pili nataka utueleze mahala alipo Assad ! akasema Nawal lakini Marwan hakufumbua mdomo wake kusema chochote.Gosu Gosu akapanga vipande vya mbao chini ya miguu ya Marwan akamwagia mafuta “Mara ya mwisho Marwan.Wapi alipo Assad?akauliza Nawal lakini Marwan aliendelea kutoa matamshi kwa lugha ya kiarabu.Nawal akampa ishara Gosu Gosu akawasha kiberiti na kutupia katika zile mbao moto ukalipuka na kufikia miguu ya Marwan ambaye alishindwa kuvumilia akaanza kupiga kelele kubwa kwa maumivu makali aliyoyapata baada ya moto kuanza kuunguza miguu yake. “Assad yuko wapi?akauliza Nawal lakini Marwan hakujibu aliendelea kulia “Gosu Gosu akalegeza mnyororo na Marwan akashuka chini akiukaribia zaidi moto ambao uliendelea kuwa mkali.Kilio kikazidi “Nitasema alipo Assad ! Mmoja wa wale magaidi waliokuwamo ndani ya kile chumba akasema baada ya kuona mateso yale makali aliyopewa Marwan.Gosu Gosu akageuka na kumtazama kwa hasira “Tafadhali msiendelee kumtesa Marwan nitawaeleza kila kitu kuhusiana na mahala alipo Assad ! akasema Yule jamaa na Gosu Gosu akapunguza ule moto.Bado Marwan aliendelea kupiga kelele za maumivu na sauti ilielekea kumkauka “Haya tueleze haraka alipo Assad ama nitakupandisha wewe kukuchoma na moto ule ! akafoka Gosu Gosu “Nitawaeleza jamani naomba msiendelee kumtesa Marwan namna hii ! akasema Yule jamaa ambaye alionekana kuwa na umri mdogo tofauti na wenzake “Unaitwa nani? Gosu Gosu akamuuliza “Naitwa Jabir Hafidh” akasema Yule jamaa “Jabir una miaka mingapi?akauliza GosuGosu “Nina miaka ishirini na mbili” “Ana miaka ishirini na mbili” GosuGosu akamwambia Nawal kwani hakuelewa lugha ya Kiswahili “Kijana mdogo sana kwa nini akaingia katika makundi haya ya kigaidi” akasema Nawal “Jabir tueleze alipo Assad na ninakuonya kama ukitudanganya basi mateso utakayoyapata ni makubwa kuliko haya ya Marwan ! akasema Gosu Gosu “Nitawaeleza ukweli” akasema Jabir “Mimi si mwenyeji wa Dar es salaam lakini kuna sehemu inaitwa Sarara.Pale kuna hoteli moja ambayo bado haijafunguliwa hapo ndipo anapoishi Assad” “Umewahi kufika mahala hapo?akauliza GosuGosu “Ndiyo nimewahi kufika hapo nikiwa na Marwan kuna vitu tulikwenda kuchukua kwa Assad” akajibu Jabir.Gosu Gosu akamweleza Nawal kile alichoambiwa na Jabir “Unamuamini?akauliza Nawal “Anaonekana anasema ukweli” akajibu Gosu Gosu “Sawa mshushe huyo gaidi” akasema Nawal.Gosu Gosu akazima ule moto halafu akamshusha Marwan.Mlango ukafunguliwa akaingia Ruby moja kwa moja akaenda kumtazama Marwan “Ameungua vibaya mno miguu yake” akasema Ruby huku Marwan akiendelea kugugumia kwa maumivu makali “Hakuna dawa yoyote ya kumpunguzia huyu mtu maumivu makali?akauliza Nawal “Hatuna dawa yoyote kwa hapa hadi makao makuu ndiko kuna kitengo cha tiba” akasema Ruby “Kwa hapa tumemaliza.Tayari tumepata kile tulichokuwa tunakihitaji.Turejee makao makuu tumuwahishe huyu jamaa akapate matibabu” akasema Gosu Gosu.Ruby akawaita walinzi wa nyumba ile wakambeba Marwan na kumuingiza garini wakaondoka kurejea makao makuu.Safari ilikuwa ya kimya kimya “Japo tumefahamu alipo Assad lakini hiki kilichofanyika ni ukatili mkubwa sana.Sijawahi kushuhudia mateso ya namna hii yaani mtu anachomwa taratibu anaungua kama nyama.Dah ! akawaza Ruby “Hawa jamaa wamekutana wote wakatili.Gosu Gosu namfahamu ni mkatili sana lakini sikutegemea na huyu mwanamke naye awe na ukatili kama wa Gosu Gosu.Nadhani ndiyo maana yeye na Mathew walielewana sana kwani hata Mathew naye aina yake ya kufanya kazi ni hivi hivi kutumia mateso makali.Yawezekana labda mambo haya ninayaona mageni kwangu kwa sababu mimi si jasusi lakini kwa hawa waliosomea kazi hii kwao wanayaona ni mambo ya kawaida sana.Naanza kufikiria labda na mimi yanipasa kusomea mambo haya kwani nimeingia kuongoza idara hii nikiwa sina ujuzi mkubwa wa mambo haya ya kijasusi.Baada ya suala hili la vurugu kumalizika nitaangalia kama nitaweza kwenda kusomea masuala haya ya ujasusi na kuwa mjuzi kama huyu Nawal” akawaza Ruby Walifika katika ofisi zao na kwa haraka Marwan akashushwa akakimbizwa upande wa afya ili kuanza kupatiwa matibabu kwani hali yake ilikuwa mbaya.Hakuweza kuongea zaidi ya kukoroma.Wale magaidi wengine wakaenda kufungiwa katika vyumba maalum vya kuhifadhia watuhumiwa.Ruby,Gosu Gosu na Nawal wakaelekea katika ofisi ya Ruby ambaye alikaa katika kiti chake akainamisha kichwa “Ruby samahani kwa kile ulichokishuhudia mle ndani lakini ilibidi kutumia njia ile ya mateso ili kuwafungua hawa jamaa.Mambo kama yale ni ya kawaida sana katika shughuli hizi.Wakai mwingine inabidi kujitoa ubinadamu ili kupata taarofa za muhimu.Utatusamehe kama tuliku…...” “Hakuna tatizo.Kitu kikubwa ni kuwa tumepata taarifa za muhimu tulizozihitaji sana.Nini kinafuata baada ya kupata taarifa hizi?Tunavamia hoteli hiyo alipo Assad?akauliza Ruby “Hapana.Hatuwezi kuvamia hoteli hiyo hadi pale tutakapojiridhisha ni kweli Assad anaishi hapo.Hawa watu si wa kuwaamini asilimia mia moja” akasema Nawal “Sawa.Kwa sasa ni usiku hivyo zoezi la kufuatilia nyumba ile kujua kama Assad yuko mle ndani litaanza asubuhi.Tunazo drone kubwa ambazo huzitumia kufuatilia mambo mbali mbali hapa Dar es salaam tutaelekeza moja katika nyuma ile na kuchunguza kila kinachoendelea lakini ushauri wangu kama huyo jamaa anayekuja kusambaza kirusi anamtegemea Assad kumsaidia kusambaza kirusi hicho basi hatuna sababu ya kumkamata Assad.Tuendelee kumfuatilia Assad kimya kimya na pale tukihakikisha tayari amekwisha onana na Sattar basi utakuwa ni wakati wetu wa kuwatia nguvuni wote wawili na kuchukua kirusi hicho” akasema “Hilo ni wazo zuri sana Ruby.Tutafanya hivyo lakini nina ushauri.Hili suala la virusi liwe ni siri yetu sisi watu watatu.Wasifahamu watu wengine ili kuzuia kutokea taharuki” akasema Nawal “Ushauri mzuri.Gosu Gosu mpeleke Nawal nyumbani akapumzike.Amesafiri kilometa nyingi na anahitaji kupumzika.Kesho asubuhi tunakutana hapa kuendelea na kazi” akasema Ruby “Vipi kuhusu wewe? Akauliza Gosu Gosu “Usihofu kuhusu mimi .Nikimaliza kazi zangu nitakwenda kupumzika pia” akasema Ruby akaagana na Nawal ambaye aliondoka na Gosu Gosu
“Ruby anaishi wapi?Nawal akauliza baada ya kufika katika makazi ya Gosu Gosu “Kwa sasa wote tumepiga kambi pale ofisi kuu za SNSA ka sababu ya usalam wetu” akasema Gosu Gosu “Nahisi njaa kuna chochote cha kula humu?akauliza Nawal.Gosu Gosu akaenda jikoni akaangalia katika friji akakuta kuna kuku wawili akamuamsha Lucy awaandalie chakula “Hapana mwambie Lucy akapumzike nitaandaa mimi” akasema Nawal na Lucy akaenda kulala Nawal akaingia jikoni akaanza kuandaa chakula akisaidiana na Gosu Gosu “Mke wako yuko wapi?akauliza Nawal “Bado sijaoa” “Unasubiri nini Gosu Gosu? Akauliza Nawal “Ni kutokana na aina ya maisha niliyoishi.Naweza kusema kwamba nimekulia msituni katikati ya mapigano makali.Nimelelewa na kundi la waasi na kufundishwa ukatili.Baadae niliondoka msituni na kuja Tanzania kutafuta maisha na ndipo nilipofanikiwa kukutana na Mathew Mulumbi ambaye aliyabadili maisha yangu na kuwa hivi nilivyo.Lakini pamoja na maisha yangu kubadilika na kuwa mazuri hivi sasa lakini bado najiona kama siwezi tena kuishi maisha yale ya kawaida kama wenzangu.Bado nahisi kuwa na furaha kufanya kazi kama hizi za kupigana ,kutumia silaha na kutesa watu” akasema Gosu Gosu “Kwa upande Fulani naweza kukubalioana nawe Gosu Gosu kwani ukiwa katika kazi hizi ni mara chache sana utakuwa na furaha endapo utakuwa na familia.Kwanza familia yako watakukosa sana muda mwingi utakuwa kazini,pili ni hatari.Familia yako inaweza kulengwa na watu wabaya kwa hiyo nadhani ni vyema ukaishi mwenyewe kuliko kuwa na familia.Tazama maisha ya Mathew Mulumbi yalivyo kwa sasa” akasema Nawal “Vipi kuhusu wewe hufikirii kuolewa tena? Gosu Gosu akauliza “Unataka kunioa?akauliza Nawal na wote wakacheka “Nani anaweza kukataa kumuoa mtoto mzuri kama wewe? Akasema Gosu Gosu wakaangua tena kicheko “Sina mpango wa kuolewa tena.Nimekwisha olewa mara mbili na watu ambao sikuwatarajia kabisa,Ammar Nazari na Abu Dahir.Labda atokee mtu ambaye ataufanya moyo wangu usimame na hata akitokea mwanaume huyo sina sifa za kuwa mke” akasema Nawal “Mungu ameumba wanawake ili waolewe na wanaume hivyo kila binadamu mwanamke tayari ana sifa ya kuwa mke” akasema Gosu Gosu “Mwanamke anaolewa ili azae watoto na kuijaza dunia ndiyo sifa kuu ya mke lakini mimi sina uwezo wa kuzaa mtoto hivyo tayari nimepoteza sifa ya kuwa mke.Ni nani anaweza akakubali kuoa mwanamke ambaye hatamzalia watoto? Kwa dunia ya sasa inahitaji mwanaume mwenye moyo wa malaika ndiyo maana sihitaji kuolewa tena” akasema Nawal “Una uhakika kwamba huna uwezo wa kuzaa?akauliza Gosu Gosu na Nawal akamsimulia kisa chote kilichosababisha apoteze uwezo wake wa kupata ujauzito. “Pole sana Nawal.Ulifanya haya yote kwa ajili ya nchi yako uipendayo lakini kwa bahati mbaya watu hawajui ni madhira gani wanayokutana nayo watu walioyatoa maisha yao kuhakikisha wanakuwa salama.Ni kama anayopitia Mathew Mulumbi kwa sasa” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu tuachane na hayo mambo kwa sasa chakula tayari twende tukale tujiandae kwa ajili ya siku ya kesho.” akasema Nawal wakaelekea mezani.Gosu Gosu akamvutia kiti Nawal akaketi na kumshukuru “Mimi ni mmoja wao mwenye roho ya kimalaika”akasema Gosu Gosu na wote wakacheka “Gosu Gosu huwezi kuwa na sifa hiyo.Macho yako yanaonyesha una kiu ya damu ! akasema Nawal na kuangua kicheko kikubwa “Niwapo kazini ni kweli ninakuwa mkatili sana lakini katika maisha ya kawaida mimi ni mtu mpole sana” akasema Gosu Gosu huku wakiendelea kula “Nawal mimi nawe tuna vitu vingi tunafanana.Sisi ni kama ndege wa rangi moja.Tunaweza kuruka pamoja” akasema Gosu Gosu “Una maanisha nini Gosu Gosu? “Nina maanisha kama tukiamua kuwa pamoja tunaweza kuwa na maisha mazuri kwa kuwa tunaendana sana” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu bado hunifahamu vyema mimi ni mtu wa namna gani” “Sitakiwi kufahamu kila kitu lakini kwa haya machache niliyoyafahamu naamini kabisa kwamba mimi nawe tunaweza kuwa na furaha sana endapo tutaamua kuwa pamoja” akasema GosuGosu “Umeniona leo tu na unataka tuwe na mahusiano ! akasema Nawal huku akicheka “Kwani inahitaji muda gani mtu kujiridhisha kuwa Fulani anakufaa? Akauliza Gosu Gosu “Gosu Gosu hicho unachohisi unacho kuhusu mimi ni tamaa tu za mwili na si kitu kingine.Ungeniambia kwamba umenitamani ningekuelewa” akasema Nawal huku akicheka “Kuna kitu nakihisi ndani mwangu toka nilipokuona sasa sijui ni tamaa kama unavyosema au ni hisia za kweli juu yako” akasema GosuGosu “Hizo ni tamaa tu Gosu Gosu na hiyo huwatokea wanaume wengi hasa wanapokutana na wanawake wenye maumbo mazuri kama mimi.Kwa bahati nzuri ninajifahamu ni mzuri na ninatamanisha” akasema Nawal huku akicheka “Hata hivyo kuna ubaya wowote kutamani?akauliza Gosu Gosu “Si vibaya kutamani lakini inaumiza pale ambapo waweza kutamani kitu halafu usikipate” akasema Nawal “Sababu zipi zinaweza kupeleka nisipate kile nikitamanicho? “Gosu Gosu tuko kazini.Mambo hayo yana wakati wake.Tumalize kwanza kuondoa hii hatari inayoikabili dunia kwa sasa halafu tunaweza kuzungumza” akasema Nawal wakaendelea kupata chakula “Baada ya kuchungulia kaburi kwa sababu ya Melanie naona kama vile ninaanza kuvutwa na sumaku ya uzuri wa huyu Nawal.Lakini huyu ni tofauti sana na Melanie.Huyu nina uhakika kabisa tunaweza kuendana.Ngoja niende naye taratibu.Sitakiwi kuwa na papara nitaharibu mambo” akawaza Gosu Gosu VICTORIA – SHELI SHELI Mathew alirejewa na fahamu akajaribu kufumbua macho lakini jicho moja halikuweza kufunguka lilikuwa limevimba kufuatia kipigo kikali alichopewa.Alisikia watu wakizungumza lugha ya kiarabu akakohoa kidogo ili kuwapa ishara watu wale kwamba tayari amekwisha zinduka.Haraka haraka akasaidiwa kunyanyuka akakalishwa katika gorodo akapewa maji ya kunywa. “Ahsante” akasema Mathew kwa taabu akitumia kiingereza.Mdomo wa chini ulikuwa umevimba vibaya “Wale jamaa walitaka kuniua nini manake wamenipiga kupitiliza” akawaza Mathew “Pole sana” akasema mmoja wa wale jamaa kwa lugha ya kiarabu “Unaweza kuzungumza kiarabu?akauliza Yule jamaa na Mathew akatikisa kichwa kukubali wale jamaa wakatazamana halafu wakatabasamu “Tuambie wewe ni nani umetokea wapi na kwa nini hawa jamaa wamekutesa namna hii? Akauliza Yule jamaa “Naitwa Abu Zalawi.Ninatokea kundi la wanamgambo la Ammar Nazari Brigades lililokuwa likiongozwa na Ammar Nazar ambaye aliuawa na vikosi vya Israel.Usiku wa kuamkia leo nimelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam Tanzania na asubuhi ya leo nilikamatwa jijini Nairobi wakati nikitafuta usafiri wa kuelekea Mogadishu.Ninyi ni akina nani na kwa nini mko hapa?akauliza Mathew “Umelipua ubalozi wa Marekani?akauliza Yule jamaa “Ndiyo.Nimelipua ubalozi wa Marekani” akajibu Mathew “Hongera sana.Wewe ni shujaa ! wakasema wale jamaa huku kila mmoja akiinuka na kumpa mkono wa pongezi “Ninyi ni akina nani? Mathew akauliza “Mimi naitwa Yasser Wazir” akasema Yule jamaa aliyeonekana mkubwa kuliko wote “Wenzangu ni Abdul Razzaq Zafar,Tayeb Burhan,Shams Fayez,Sajid Hassim na wa mwisho Yule pale ni Muharrem Idris.Sisi wote tunatokea Iran” “Mnatokea Iran? Mathew akauliza “Ndiyo” akajibu Tayeb “Mmefanya nini kwa Marekani hadi mkaletwa hapa? Akauliza Mathew “Hatujafanya chochote kwa Marekani .Sisi ni wanasayansi tulitekwa tukitokea nchini Urusi na tumekuja kutupwa hapa tukisubiri siku yetu ya kufa.Toka tumeletwa hapa hatujawahi kuona mwangaza wa jua na wala hatujui kitu gani kinaendelea huko duniani.Hatujui huu ni mwaka gani hatujui kama ni usiku au ni mchana.Tunapewa mlo mmoja kwa siku na hatujui ni mlo wa asubuhi au wa mchana.Ni mateso makubwa tunayapata” “Poleni sana.Huu ni ukatili mkubwa uliovuka mipaka.Kwani hapa ni wapi? Mathew akauliza “Hakuna ajuaye hapa tuko wapi.Mateso haya makubwa yote tumemuachia Mungu ndiye atakayetulipia.Wewe Abu Zalawi kwa nini umelipua ubalozi huo wa Marekani? Akauliza Abdul Razzaq “Ni kwa sababu ya dhuluma zinazofanywa na taifa hilo hasa kwa nchi za kiislamu.Ndugu zangu,jamaa zangu wameuawa na majeshi ya Marekani hivyo nina hasira nao sana ndiyo maana nililipua ubalozi wao na kama wasingenikamata basi ningeendelea kulipua balozi nyingine za Marekani katika nchi mbali mbali” “Abu Zalawi wewe ni shujaa kwa hiki ulichokifanya.Marekani imekuwa ikizikandamiza mno nchi za kiarabu na hasa Iran.Hatujui hali ikoje kwa sasa lakini hadi tulipokamatwa Iran ilikuwa imewekewa vikwazo vingi vya kiuchumi huku ikizuiwa kuuza mafuta yake kwa lengo la kuizorotesha kiuchumi.Pamoja na vikwazo hivyo vya kiuchumi bado Marekani na washirika wake walikuwa wana mipango ya kuishambulia kijeshi.Ni nchi ya Urusi ambayo ilikuwa mshirika wa Iran na ambayo iliisaidia Iran kujenga vinu vya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha nishati na hata sisi tulitekwa tulipotoka nchini Urusi katika mafunzo ya namna ya kuendesha vinu hivyo vya nyuklia kuzalisha nishati ya umeme” akasema Yasser. “Karibu ndugu yetu Abu Zalawi katika maisha haya tukisubiri siku ya kuchukuliwa na Mungu wetu.Kitu tunachowashukuru wametupatia Quran tukufu,tunasoma na kumtafakari Mungu tukimuomba atupokee pale tutakapoaga dunia”akasema Shams Fayez “ Abu Zalawi nadhani utumie muda huu kupumzika.Tutakuwa na muda mwingi wa mazungumzo kwani tumetupwa katika hili shimo na hatujui kama iko siku tutatoka salama humu.Pumzika” akasema Yasser na kumtaka Mathew alale katika kitanda chake. DAR ES SALAAM – TANZANIA Mshale wa saa ulionyesha saa kumi na mbili za asubuhi,Gosu Gosu na Nawal tayari walikwisha fika makao makuu ya SNSA.Moja kwa moja wakaelekea katika ofisi ya Ruby na kumkuta akiwa amekiegemeza kichwa katika kiti amesinzia.Taratibu Gosu Gosu akamuamsha “Ouh tayari mmefika” akasema Ruby huku akifikicha macho “Ruby hupaswi kuendelea namna hii.Unapaswa kupumzika” “Usijali Gosu Gosu I’m fine” akasema Ruby na kusalimiana na Nawal kisha akaomba wamsubiri akaoge Ilimchukua dakika kumi na tano Ruby kurejea “Sasa tunaweza kuendelea” akasema Ruby na kuwataka wafanyakazi ambao tayari walikuwa kazini zamu ya usiku na wale walioingia asubuhi wakusanyike sehemu ya kupeana taarifa muhimu za kazi.Kama ulivyo utaratibu aliouanzisha kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi hutanguliwa na maombi ambayo yalifanywa kwa dini ya kikristu na kiislamu halafu kikao kikaendelea “Habari za asubuhi ndugu zangu.Tunamshukuru Mungu kwa kutukutanisha tena siku hii ya leo.Kama mtakumbuka juzi tuliendesha zoezi la kuwakamata magaidi ambao tunaamini ndio waliohusika na mauaji ya viongozi kadhaa wa dini na kuchochea vurugu za kidini hapa nchini.Tumewafanyia mahojiano na tumefanikiwa kupata mahala anapoishi Assad Ismail ambaye ndiye kiongozi wa magaidi hao.Tumeambiwa ni eneo la Sarara katika hoteli moja ambayo bado haijafunguliwa.Hatuwezi kuvamia hoteli hiyo hadi kwanza tujiridhishe kama kweli Assad yuko hapo hivyo basi leo tutafanya zoezi la kuchunguza hoteli hiyo.Asubuhi hii timu ya watu wachache watamchukua gaidi mmoja ambaye atakwenda kuwaonyesha ilipo hiyo hoteli.Wakati wakielekea huko sisi tutaendelea kuwafuatilia kwa kutumia drone yetu hadi watakapofika hapo katika hoteli.Baada ya kuipata hiyo hoteli litaendelea zoezi la kuchunguza kila anayeingia na kutoka humo ndani ya hoteli kwa lengo la kumpata Assad Ismail.Hiyo ndiyo kazi ya kipaumbele kwa siku ya leo”akasema Ruby na kuwataka wafanyakazi wakaendelee na kazi yeye na Gosu Gosu wakaondoka kurejea ofisini . “Gosu Gosu utaongoza timu itakayompeleka Jabir kutuonyesha hoteli aliko Assad” akasema Ruby Ndani ya muda mfupi timu ya makomando wanne ilikuwa tayari wakaongozana na Gosu Gosu na Nawal bila kumsahau Jabir ambaye ndiye aliyekuwa anapafahamu mahala hapo wakaondoka huku SNSA wakiwafuatilia kwa kutumia drone Jabir aliwaongoza akina Gosu Gosu hadi katika hoteli ambako anaishi Assad. “SNSA jengo lililo mbele yetu ndilo hotel anakoishi Assad” akasema Gosu Gosu wakiwa wamesimamisha gari mita kadhaa kutoka mahala lilipo jengo lile refu lililopata ghorofa nane. “Tumekupata Gosu Gosu sasa mrudi huku ofisini.Tunaendelea kufuatilia kwa kutumia drone” akasema Ruby na Gosu Gosu akatoa maelekezo kwa dereva wa lile gari kugeuza na safari ya kurejea SNSA ikaanza. VICTORIA – SHELI SHELI Mlango wa chumba walimokuwamo akina Mathew ukafunguliwa wakaingia watu sita wanne wakiwa na silaha.Walimchukua Mathew wakamfunga pingu na kumvisha mfuko kichwani wakaondoka naye.Bado jicho lake moja lilikuwa limevimba na halifunguki vizuri.Akaingizwa katika chumba cha mahojiano akaketishwa kitini na mikono yake ikafungwa katika pingu za mezani kisha akatolewa ule mfuko kichwani akajikuta akitazama uso kwa uso na Jeffrey na wenzakehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Richard,William,Brian a Christopher. “Karibu tena Abu Zalawi.Naamini baada ya kupata makaribisho siku ya jana leo utakuwa tayari kuzungumza nasi” akasema Jeffrey.Mathew hakujibu kitu. “Abu Zalawi unaendelea pale tulipoishia jana.Tunataka kufahamu watu unaoshirikiana nao ambao walikutuma ukalipue ubalozi wetu jijini Dar es salaam” akasema Jeffrey na kushika karatasi ili aweze kuandika majina “Abu tunataka majina ya watu unaoshirikiana nao” akasema tena Jeffrey “Mnajisumbua bure.Siwezi kuwaeleza chochote.Niuen tafadhali niko tayari” akasema Mathew “Abu Zalawi hatuko hapa kufanya mzaha tafadhali ! akasema Jeffrey “Hata mimi sifanyi mzaha.Nataka mniue kwa nini mnanichelewesha?akauliza Mathew “Abu Zalawi unaonekana bado hujapafahamu vizuri mahala hapa” akasema Jeffrey na kubonyeza kitufe pembeni ya meza yake na baada ya sekunde kadhaa mlango wa kile chumba ukafunguliwa wakaingia jamaa wanne miongoni mwa wale waliomtesa jana Jeffrey akawataka waondoke na Mathew wakaendelee kumtesa Mathew akaingizwa tena katika chumba cha mateso akavuliwa nguo na kubakiwa na nguo ya ndani akafungwa katika mti halafu akaanza kuchapwa kwa kutumia fimbo ambazo zilimsababisha atokwe na damu nyingi.Yakachukuliwa maji Fulani katika kopo dogo akamwagiwa mwilini na kutoa ukelele mkubwa kwa maumivu makali.Alihisi kama mwili wake unawaka moto baada ya kumwagiwa maji yale. “Nataka majina ! akasema Jeffrey “Niueni wapuuzi ninyi ! akasema Mathew akaendelea kuteswa hadi alipopoteza fahamu akachukuliwa na kurejeshwa tena katika kile chumba walimo wale mateka wa Iran.Yasser Wazir na wenzake wakaanza tena zoezi la kumsaidia Mathew kuzinduka. DAR ES SALAAM – TANZANIA Katika makao makuu ya SNSA kilichokuwa kinaendelea ni kufuatilia hoteli anamoishi Assad.Hadi ilipotimu saa tisa za alasiri bado hakukuwa na mtu yeyote aliyeonekana kuingia au kutoka ndani ya jengo lile “Ninaanza kupatwa na wasi wasi kama kweli jengo hili ndimo anamoishi Assad” akasema Ruby “Usikate tamaa Ruby.Tuendelee kusubiri hadi jioni kama hakuna chochote tutakachokuwa tumekipata basi tutatuma timu kwenda kuingia ndani ya ile nyumba” akasema Gosu Gosu “Imani imeanza kunitoka kama kweli Assad anaishi ndani ya jengo hili.Naanza kuhisi Jabir amecheza na akili zetu” akasema Ruby “Nilimtazama Jabir machoni.Aliogopa kupewa mateso aliyoona akipewa Marwan ndiyo maana akaamua kusema ukweli.Naamini kabisa ndani ya jengo hili ndimo anamoishi Assad”akasema Gosu Gosu “Tuendelee kuvuta subira na ikifika saa kumi na mbili jioni hakuna mtu aliyeingia au kutoka basi tutatuma kikosi usiku wa leo kwenda kuchunguzandani ya jengo lile kujua nini kinachoendelea na kama Assad anaishi pale” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu anza kuandaa timu ya makomando kwa ajili ya kuvamia hii nyumba na kujiridhisha kama kweli Assad anaishi hapa.Nina mashaka kama tumepewa taarifa ya kweli.Kama kweli Assad angekuwa anaishi humu ndani ungekwisha muona kwani tumeanza kufuatilia hii nyumba kuanzia asubuhi na hatujaona mtu yeyote akiingia au kutoka ! akasema Ruby akionekana kukata tamaa ya kuendelea kufuatilia ile hoteli VICTORIA – SHELI SHELI Chumba cha akina Mathew kilifunguliwa na Mathew akachukuliwa.Hali ya Mathew haikuwa nzuri.Kila sehemu ya mwili wake ilikuwa imevimba. Tayari kiza kilikwisha ingia Mathew akaingiza katika chumba kimoja kilichokuwa na vifaa kadhaa vya matibabu haraka haraka akapokewa na watu watatu waliokuwa wamevaa makoti meupe akalazwa kitandani akaanza kuhudumiwa.Aliongezewa damu na kupewa dawa za kumsaidia kutuliza maumivu aliyokuwa anayapata kutokana na mateso aliyoteswa Baada ya saa mbili hali ya Mathew ilibadilika na mara akaingia Jeffrey. “Habari yako Abu Zalawi.Unajisikiaje? “Mwili umechoka hauna nguvu! Akasema Mathew kwa sauti dhaifu “Pole sana” akasema Jeffrey na kuwataka wale mdaktari watoke nje kwa muda akavuta kiti akaketi karibu na Mathew “Abu kama nilivyokueleza awali kwamba mateso haya yote unayoyapitia ni ili kuonyesha uhalisia.Tunafuatiliwa na viongozi wetu kila tunachokifanya hapa hivyo tunapaswa kuwaonyesha kitu halisi.Umeanza vizuri ninaomba endelea kuvumilia.Safari ya kuwahamisha wewe na wale wanasayansi wa Iran inaandaliwa na itakapokuwa tayari utajulishwa namna utakavyofanya kuwatorosha ili uweze kuingia Iran” akasema Jeffrey Mathew aligangwa majeraha yake halafu akapewa chakula kisha akarudishwa katika chumba chao “Pole sana Abu Zalawi” Mathew akapewa pole “Ahsanteni sana” “Hata sisi walitutesa hivi hivi wanavyokutesa wewe wakitaka tuwaeleze tulitoka Urusi kufanya nini lakini tulikuwa na msimamo mmoja na hatukuwahi kuwaeleza kitu chochote.Walipochoka kututesa wakaamua kuja kututupa humu na hwasumbuki na sisi tena.Nadhani wanatutesa kisaikolojia .Ninachokuomba Abu Zalawi vumilia mateso yote na usiwaeleze chochote” akasema Yasser “Kikubwa wanachokitaka kutoka kwangu ni kupata majina ya watu ninaoshirikiana nao.Mimi nimekwisha kula kiapo cha kutokutoa siri hivyo niko tayari kufa kuliko kuwaeleza chochote kuhusiana na mtandao wangu” akasema Mathew “Safi sana Abu Zalawi.Wewe ni shujaa wa kweli.Usifumbue mdomo wako kuwaeleza chochote watu hawa waonevu wakubwa ! akasema Sajid Hassim DAR ES SALAAM – TANZANIA Tayari imetimu saa moja za jioni lakini bado hakuonekana mtu yeyote akiingia au kutoka ndani ya ile nyumba ambayo SNSA walielezwa kwamba ndimo anamoishi Assad Ismail.Kikosi cha makomando kilikuwa tayari kimejiandaa wakisubiri kupewa ruhusa ya kuondoka kwenda kuingia ndani ya nyumba ile. “Kutwa nzima ya leo tumeshinda humu ofisini tukifuatilia nyumba hii lakini hakuna chochote tulichokipata.Nina wasiwasi na taarifa tuliyopewa” akasema Ruby wakiwa ofisini kwake pamoja na Gosu Gosu na Nawal wakijadiliana kuhusiana na operesheni ile “Ruby umekuwa na wasiwasi tangu mchana lakini nimekuhakikishia kwamba alichokisema Jabir ni kitu cha kweli”akasema Gosu Gosu “Nenda kamchukue Jabir mlete tena hapa atuhakikishie kama kweli Assad anaishi katika nyumba hii ! akasema Ruby na Gosu Gosu akatoka haraka akaenda kumchukua Jabir akamleta katika ofisi ya Ruby akaketishwa kitini “Jabir ulitueleza kwamba Assad anaishi katika nyumba hii lakini tumefuatilia kuanzia asubuhi mpaka giza limeingia hakuna mtu yeyote aliyeingia wala kutoka ndani ya hii nyumba.Nikisema ulitudanganya nitakosea? Akauliza Ruby “Sijawadanganya.Hapo ndipo anapoishi Assad na nilikwenda nikiwa na Marwan” akajibu Jabir “Jabir nitaaamuru urejeshwe tena katika mateso yale makali kama uliyomshuhudia Marwan akiteswa.Nataka unieleze ukweli” “Tafadhali naomba msinipeleke kule kwenye mateso.Nilichowaeleza ni kitu cha kweli kabisa siwezi kuwadanganya” akasema Jabir “Ruby huyu jamaa anasema kweli ! akasema Nawal.Ruby akamuelekeza Gosu Gosu kumrejesha Jabir “Roho yangu inasita sana kutuma kikosi kuvamia nyumba hii” akasema Ruby “Ruby nafahamu wasiwasi wako kwamba yawezekana Assad haishi katika hii nyumba lakini nakutoa wasiwasi kwamba Assad anaishi hapa.Yule kijana hajatudanganya” akasema Nawal kisha wakatoka wakaenda kuzungumza na makomando walio tayari kwenda katika nyumba ile.Kikosi cha ardhini kikiwa na makomando nane kikatangulia na gari huku kikosi cha helkopta kikisubiri kikosi cha ardhini wafike.
Makomando waliokuwa na gari walikaribia kufika katika jengo wanalokwenda kulivamia na kuwajulisha SNSA kisha kikosi cha helkopta kikitumia helkopta maalum inayotumika katika operesheni za usiku ambayo imetengenezwa kwa teknolojia ya kutokutoa sauti,kiliondoka kuelekea eneo la tukio. Sehemu kubwa ya jiji la Dar es salaam bado iliendelea kuwa gizani.Kwa siku ya pili jiji liliendelea kuwa tulivu.Hakukuwa na zile vurugu zilizokuwepo siku kadhaa zilizopita.Taratibu maisha yalianza kurejea katika baadhi ya sehemu na biashara ndogo ndogo zikifunguliwa huku amri ya kutotembea hovyo kuanzia saa moja za jioni ikiendelea.Magari ya doria ya vikosi vya jeshi na polisi yaliendelea kuzunguka katika mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es salaam kuimarisha ulinzi. Helkopta ya makomando wa SNSA ilikaribia kufika katika jengo lile na wakawajulisha wale waliokuwa katika gari ambao walianza kusogea karibu zaidi na jengo lile.Helkopta ilifika juu ya jengo lile na makomando sita wakashuka kwa kutumia kamba na helkopta ikaondoka.Wakiwa wamevaa miwani maalum ya kuwawezesha kuona katika giza makomando wale waliokuwa katika gari wakashuka na kuelekea katika geti ambalo lilikuwa limefugwa kwa kutumia mnyororo na kufuli kwa nje.Toka mchana tayari walikwisha chunguza kila kitu na kujiandaa.Mkasi mkubwa ukaletwa kufuli likakatwa wakaingia ndani.Wale wengine waliopitia juu nao wakavunja mlango wa pande wa juu na kuingia ndani. Mlango mkubwa wa kuingilia ndani ulikuwa umefungwa.Haraka haraka wakabandika utepe Fulani katika mlango uliounganishwa kwa waya na kifaa fuani ambacho kiliwashwa na baada ya muda mlango ule ukalipuliwa .Kiongozi wa kikosi kile cha chini akatoa maelekezo na kisha wakaanza kukagua sehemu ya chini.Mara ghafla mmoja wa wale makomando akasimama na kuwataka wenzake wasimame. “Kuna nini?akauliza kiongozi wao na wote wakawa kimya wakasikia sauti ya kitu kama saa kutoka karibu na pale walipokuwa wamesimama .Wakaanza kufuatilia sauti ile hadi katika jokofu wakalifungua na ndani yake wakakuta bomu likiwa na kifaa mfano wa saa kikihesabu. Kiongozi wa makomando wale akawataka watu wake wasogee mbali kidogo. “SNSA kuna tatizo limejitokeza”kiongozi wa kikosi kile akatoa taarifa kwa SNSA “Tatizo gani limetokea?akauliza Ruby “Tumegundua uwepo wa bomu katika jokofu ambalo tayari limekwisha anza kuhesabu.Nadhani bomu hili lilikuwa limeunganishwa na mlango mkubwa ili ukifunguliwa tu basi bomu linaanza kuhesabu kabla ya kuipuka.Tuna dakika kumi na tatu tu kabla ya bomu kulipuka” akasema Yule mkuu wa kikosi cha makomando “Eneo hilo tayari ni hatarishi ondokeni hapo haraka sana” akasema Ruby “Hapana mkuu hatuwezi kuondoka kabla hatujaikamilisha kazi tuliyokuja kuifanya.Tunazo dakika za kutosha tunaweza kulitegua hili bomu na tukaendelea na uchunguzi wetu”akasema Yule kiongozi wa makomando na kutaka aitwe mtaalamu wa mabomu ambaye alibaki pale makao makuu anaitwa Cyril. Haraka haraka Cyril aliyekuwa katika kambi yao nje ya ofisi za SNSA akaitwa na kiongozi Yule wa makomando akatuma picha za bomu lile Cyril akalitazama na kusema “Hili ni bomu la kutengenezwa kienyeji.Mabomu ya namna hii ni magumu sana kuyategua ukikosea kidogo unaua watu wote”akasema Cyril “Unaweza kulitegua au huwezi?Kama huwezi kuwa muwazi niwaondoe watu wangu haraka sana mahala walipo ! akasema Ruby “Ninaweza” “Dakika nane zimebaki ! akasema Ruby “Naomba dakika mbili” akasema Cyril na kuitazama picha ile ya bomu halafu akaanza kuwasiliana na Yule kiongozi wa makomando akimpa maelekezo. “Cyril imebaki dakika moja ! akasema Ruby “Sekunde hamsini na tatu ! akasema Ruby kwani maelekezo yote aliyoyatoa Cyril hayakuzaa matunda Cyril akamuelekeza Godwin kiongozi wa makomando kukata waya Fulani na kama bomu litaendelea kuhesabu basi hakutakuwa na namna nyingine zaidi ya kukimbia .Kila mtu aliweka mikono kichwani kusikiliza kile kitakachotokea “SNSA bomu limezima.Narudia tena bomu limezima.Ahsante SNSA.Sasa tunaendelea na upekuzi” akasema Godwin .Watu wa SNSA wakashangilia kwa furaha. Upekuzi ulifanyika kwa saa mbili lakini hawakuweza kupata mtu au kitu chochote ndani ya nyumba ile cha kumuhusu Assad. “Tayari alifahamu wenzake wametekwa na alijua lazima watateswa ili waeleze mahala alipo ndiyo maana akaondoka na kutega bomu mahala pale akijua lazima watakwenda pale kumtafuta” akasema Nawal wakiwa katika ofisi ya Ruby baada ya kupokea taarifa ya makomando kumkosa Assad “Nawal yuko sahihi.” akasema Gosu Gosu “Tumekwama tena.Tusaidiane mawazo namna tunavyoweza kumpata Assad ! akasema Ruby “Nahitaji kuzungumza na Habiba Jawad nimuulize kama kuna taarifa yoyote ameipata” akasema Nawal na kupewa simu akampigia Habiba “Mama Habiba habari za huko? Akauliza Nawal “Huku naendelea vizuri.Vipi wewe uko salama huko Dar es salaam?akauliza Habiba “Niko salama mama usihofu.Nimekupigia kujua kama kuna taarifa mpya umeipata lakini vile vile nataka kukufahamisha kwamba bado hatujampata Assad.Tumewakamata watu wake wakatuonyesha maficho yake tulipomfuata tumekuta kahama na hatujui amejificha wapi,tunaendelea kumsaka” akasema Nawal “Nawal kumpata Assad ni lazima.Fanyeni kila muwezalo kuhakikisha anapatikana kwani taarifa niliyoipata ni kwamba tayari Sattar amekwisha ondoka Marekani saa mbili za asubuhi kwa saa za Marekani kuelekea Tanzania akiwa na kirusi hicho na mtu anayemtegemea kumpa msaada ni Assad hivyo mkimpata Assad mtakuwa na uhakika mkubwa wa kumpata Sattar na kirusi” akasema Habiba “Sattar ameondoka Marekani na ndege gani? Akauliza Nawal “Sifahamu ni ndege gani amepanda kwani nimepata taarifa ya jumla kwamba tayari amekwisha ondoka Marekani na yuko angani hivi sasa akielekea Tanzania.Fanyeni kila juhudi kuhakikisha mnampata Assad kabla Sattar hajakanyaga ardhi ya Tanzania” akasema Habiba “Ahsante sana mama kwa taarifa hiyo.Una taarifa zozote kuhusu Mathew Mulumbi? “Hapana sina taarifa zozote hadi sasa kumuhusu Mathew” akasema Habiba “Mama nakushukuru.Nitakujulisha tena pale tutakapokuwa tumefanikiwa kumpata Assad” akasema Nawal na kuagana na Habiba akawageukia akina Ruby “Kwa mujibu wa Habiba Jawad,tayari Sattar amekwisha ondoka Marekani akiwa na kirusi na yuko angani hivi sasa anakuja Tanzania.Tunahitaji kumtafuta Assad kwa namna yoyote ile na kujua mahala alipo kwani ni yeye ambaye anategemewa kumsaidia Sattar katika kukisambaza kirusi hicho” akasema Nawal “Kuna kitu nimekumbuka ambacho kinaweza kutusaidia sana kumpata Assad” akasema Gosu Gosu “Umekumbuka nini Gosu Gosu?akauliza Ruby “Mathew alipokuja kuonana nasi na kutueleza kuhusiana na mambo yanayofanywa na IS hapa nchini alitoa angalizo kwamba tuwe makini tunapomfuatilia Assad na watu wake kwani wanapata msaada mkubwa kutoka kwa vikosi vya Marekani.Alikwenda mbali zaidi akasema kwamba kila siku Assad anapokwenda katika nyumba ile walimokuwa wakiishi akina Marwan husindikizwa na gari la doria la vikosi vya Marekani hivyo naamini lazima watakuwa wanafahamu mahala alipo Assad hivi sasa” akasema Gosu Gosu na Ruby akajipiga kichwani “Ni kweli Mathew alitoa angalizo hilo.Kwa nini nikasahau maelekezo haya? Hivi sasa tungekuwa mbali sana katika kumsaka Assad.Ahsante Gosu Gosu kwa kukumbuka” akasema Ruby “Kwa sasa baada ya kupata picha kuwa Assad anasaidiwa na vikosi vya Marekani nini kinafuata? Ruby akauliza “Kuna kitu kimoja ninakifikiria” akasema Nawal “Marekani lazima wachukue tahadhari kubwa katika kukisafirisha kirusi hicho na kuhakikisha kinafika salama Tanzania hivyo naamimi lazima Sattar atakuwa anakuja na ndege maalum ambayo haitaweza kutua sehemu yoyote ile zaidi ya hapa Dar es salaam.Na hapa Dar e salaam atakuwa anasubiriwa na Assad ambaye tayari tumefahamu anasaidiwa na vilkosi vya Marekani vilivyopo hapa nchini.Kitu ambacho tunapaswa kujua je vikosi vya Marekani vinatumia kiwanja gani cha ndege hapa Dar es salaam? Naamini lazima ndege zao zinaingia na kutoka kila siku hivyo tukifahamu ni uwanja gani wa ndege wanautumia tutakuwa tumempata Sattar” akasema Nawal “Nawal yuko sahihi.Kwani hapa Dar es salaam kuna viwanja vingapi vya ndege? akauliza Gosu Gosu “Kiwanja kikubwa ni cha Julius Nyerere ambacho toka zilipoanza vurugu kilifungwa” akasema Ruby “Kama hakuna kiwanja kingine basi lazima ndege za jeshi la Marekani zinatua katika uwanja huo ambao sasa uko chini ya vikosi vya jeshi na nina uhakika hata ndege hiyo inayomleta Sattar na kirusi lazima itatua katika uwanja huo” akasema Nawal.Ruby akabofya kompyuta yake haraka haraka halafu akasema “Kutoka Washington hadi Dar es salaam ni mwendo wa kama saa ishirini.Hivi sasa ni saa tano na dakika ishirini na saba ambayo ni sawa na saa tisa za alasiri Washington hivyo kama ndege hiyo imeondoka Marekani saa mbili asubuhi ya leo tunategemea itafika hapa Tanzania kuanzia saa sita za mchana kesho.Kama wote tunakubaliana basi macho yetu tuyaelekeze uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kujua kila kinachoendelea pale” akasema Ruby “Uwanja wa ndege unalindwa na vikosi vya jeshi,tutawezaje kupenyeza watu wetu ndani ya uwanja kujua kinachoendelea?akauliza Nawal “Litakuwa ni zoezi la kimya kimya.Jambo zuri ni kwamba taasisi zote za serikali mifumo yao imeunganishwa na SNSA kwa siri hivyo tunaweza kuingia katika mfumo wa taasisi yoyote ya serikali muda wowote.Kuna kamera zaidi ya mia tatu katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere tutatumia kamera hizo kufuatila kila kinachoendelea pale uwanjani vile vile tutatumia pia na drone zetu kufuatilia” akasema Ruby na kuanza kucheza na kompyuta yake kama vile ana vidole nane katika kila mkono.Baada ya muda mfupi tayari alikwisha ingia katika mfumo wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na kamera zikaanza kuonekana.Ruby akamtaka Gosu Gosu kuwakusanya wafanyakazi wote katika sehemu ya kukutania pale kunapokuwa na jambo la muhimu la kuwaeleza “Habari za saa hizi ndugu zangu” akasema Ruby “Kutwa nzima ya leo tulikuwa na zoezi la kufuatilia maficho ya Assad Ismail.Tunashukuru Mungu kwamba watu wetu wote wamerejea salama katika zoezi hilo la hatari.Assad alifahamu kuwa lazima tutamfuata pale ndiyo maana yeye na watu wake wakatega lile bomu ambalo halikuleta madhara kwa watu wetu.Bado suala la Assad liko mezani na ni kipaumbele kikubwa.Tunaendelea kumsaka kwa kila namna tuwezavyo na lazima tumpate” akasema Ruby na kubonyeza kitanza mbali na katika runiga kubwa ikaonekana picha ya Sattar “Anaitwa Sattar Sayf Al Din. Anatoka kundi la kigaidi la IS na anakuja Tanzania” “Anakuja kufanya nini Tanzania?mmoja wa wafanyakazi akauliza “Bado hatufahamu anakuja kufanya nini lakini huyu ana mahusiano na Assad Ismail hivyo basi huyu ndiye atakayetuongoza kujua mahala alipo Assad.Sattar anatokea Marekani kwa ndege maalum na tunahisi anaweza akatua katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere.Mtu huyu ni hatari sana na nitawaeleza hapo baadae kwa nini ni mtu hatari.Kwa hiyo kuanzia sasa tunajielekeza katika uwanja wa ndege wa kimatafa wa Julius Nyerere ambako tunahisi ndiko Sattar atashukia.Kuanzia sasa tufuatilie kamera zote na kujua kila kinachoendelea pale uwanjani.Tufahamu kama kuna ndege zozote zinatua pale na zinatokea wapi na zimekuja kufanya nini kwani uwanja umefungwa na uko chini ya uangalizi wa vikosi vya jeshi.Tunategemea kuanzia kesho mchana Sattar anaweza akatua hapa nchini hivyo basi tuyaelekeze macho yetu uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Hayo ndiyo niliyonayo kwa sasa”akasema Ruby na kuondoka na Gosu Gosu “Gosu Gosu mchukue Nawal mkapumzike hadi asubuhi.Mimi nitaendelea kusimamia shughuli zote za hapa” akasema Ruby Gosu Gosu na Nawal wakaondoka kuelekea katika makazi ya Gosu Gosu kupumzika VICTORIA – SHELI SHELI Saa nane za usiku mlango wa chumba walimo akina Mathew ukafunguliwa wakaingia walinzi wanne.Tayari akina Mathew alikuwa wamepitiwa na usingizi.Mathew akaamshwa na kutolewa mle ndani akapelekwa katika chumba Fulani ambako alimkuta Jeffrey. “Abu Zalawi tumekuondoa usingizini lakini ni kwa jambo la muhimu” akasema Jeffrey “Tumepewa maelekezo kwamba wewe na wale wanasayansi kesho mtapelekwa Marekani kwa ndege maalum” akasema Jeffrey na kumpa Mathew maelekezo ya namna mpango utakavyokuwa “Abu Zalawi sisi tumemaliza kwa upande wetu ahsante sana kwa ushirikiano wako .Nakutakia kila la heri katika jukumu zito ulilopewa” akasema Jeffrey “Nashukuru sana Jeffrey na ninawaahidi kwamba nitafanya kila niwezalo kuhakikisha ninafanikisha kupata kile nilichotumwa nikafanye nchini Iran” akasema Mathew na kuagana na Jeffrey akarejeshwa tena katika kile chumba chao “Hawa jamaa walikuwa wanataka nini? akauliza Yasser baada ya Mathew kurejea “Bado wanaendelea kunihoji wakidhani labda nimebadili msimamo wangu.Wameniambia nitafakari hadi kesho kabla sijakutana na mateso ambayo sijawahi kuyaona” akadanganya Mathew “Abu Zalawi chochote unachokifahamu usiwaeleze hawa jamaa.Hata ukiwaeleza chochote hawatakuacha salama.Usifanye nao makubaliano yoyote makatili hawa” akasema Yasser “Niko tayari kufa lakini si kuwaeleza chochote Marekani.Msihofu ndugu zangu hawawezi kupata chochote kutoka kwangu” akasema Mathew wakampongeza kisha kila mmoja akaenda kulala katika godoro lake “Mpaka hapa nilipofika nimefanya vizuri.Hawa jamaa tayari wameniamini na hicho ndicho hasa kitu kikubwa kwani hawa ndio watakaonisaidia niaminiwe na mamlaka za Iran.Ninaingia katika sehemu ngumu sana ya misheni hii.Namuomba Mungu anisimamie” akawaza Mathew
Saa mbili za asubuhi mlango wa chumba ulifunguliwa akina Mathew wakaamriwa kusimama halafu kila mmoja akafungwa pingu na kuvishwa mfuko kichwani kisha wakatolewa ndani ya kile chumba “Mnakwenda kutuua?akauliza Yasser lakini hakuna aliyemjibu “Tungeomba mtupatie nafasi ya dakika chache tusali kabla ya kuuawa” akasema Sajid Hassim Waliingizwa katika gari mlango ukafungwa wakaondoka.Ndani ya lile gari ambalo hawakulijua ni la aina gani kulikuwa na watu wanne wenye silaha wakiwalinda. Baada ya dakika kadhaa gari lile likasimama mlango wa nyuma ukafunguliwa wakashushwa halafu taratibu walianza kupandishwa ngazi na kuingia katika ndege.Kila mmoja akakalishwa katika kiti chake na kufungwa pingu miguu na mikono zilizounganishwa na mnyororo mrefu.Dakika chache baadae ndege ikapaa na ilipokaa sawa angani mifuko waliyofunikiwa kichwani ikatolewa.Ndani ya ndege kulikuwa na walinzi wanne waliokuwa na silaha. Ndege iliendelea kupasua anga huku akina Mathew wakikirimiwa kwa vinywaji na vitafunwa “Kazi inaanzia hapa” akawaza Mathew na kumuita mmoja wa walinzi akamwambia anahitaji akajisaidie.Mlinzi Yule akafungua mahala minyororo ile ilipofungwa kisha akampeleka Mathew chooni.Akamfungulia mlango Mathe akaingia kisha mlinzi Yule akasimama kwa nje akimsubiri.Mathew akapapasa mahala alipoelekezwa akakuta kuna funguo ya kufungulia zile pingu.Haraka haraka akafungua pingu za mikono halafu akafungua za miguu akawa huru.Akasimama pembeni ya mlango Zilipita dakika tano Yule mlinzi akagonga mlango na kumuuliza Mathew kama amekwisha maliza kujisaidia.Mara akasikia sauti ya muanguko wa kitu akafungua mlango haraka haraka kuchungulia lakini kitendo cha kuchungulia akajikuta akipigwa kichwa kizito halafu akadakwa na kuvutwa ndani.Mathew akamuongeza kichwa kingine na ngumu za mfululizo Yule mlinzi akaanguka chini “Sihitaji kumchunguza kama bado ana fahamu.Ninaiamini mikono yangu,haijawahi kukosea” akawaza Mathew akamsachi Yule jamaa na kuchukua bunduki yake pamoja na bastora akavaa fulana ya kujikinga na risasi aliyokuwa ameivaa Yule mlinzi.Akamfunga Yule mlinzi kwa pingu halafu akafungua mlango taratibu akachungulia nje hakukuwa na mtu maeneo yale ya karibu akatoka na kuanza kutembea kwa kunyata.Alijitokeza katika chumba walimokuwamo wale wanasayansi ambao wote walipatwa na mstuko mkubwa baada ya kumuona Mathew akiwa na bunduki na bastora.Haraka haraka akamfuata Yasser akamfungua pingu za mikono na miguu akawa huru akampa bunduki halafu akamfungua Muharrem Idris na kumtaka aendelee kuwafungua wenzake.Mathew akanyata kuelekea katika chumba ambacho walinzi wale walikuwa wamekaa wakizungumza huku wakipata kinywaji.Hawakuwa na wasiwasi wowote wakiamini mwenzao alikuwa katika chumba cha wafungwa akiendelea na zamu ya ulinzi.Mathew akachungulia katika kioo akawaona namna walivyokaa halafu taratibu akakishika kitasa akakinyonga kikafunguka na kwa kasi ya umeme akajitoma ndani ya kile chumba cha walinzi.Walipatwa na mstuko mkubwa “Wote simameni taratibu huku kila mmoja mikono yake ikiwa juu !! Mathew akaamuru.Taratibu walinzi wale wakaanza kuinuka taratibu na ghafla mlinzi mmoja akashusha mkono akataka kuchomoa bastora yake lakini kabla hajaifikia risasi zikasikika na Yule mlinzi akaanguka chini.Nyuma ya Mathew alikuwa amesimama Yasser akiwa na bunduki inayofuka moshi.Ndiye aliyemmaliza Yule mlinzi Walinzi wale wakachukuliwa wote na kufungwa pingu . “Tunatakiwa kuidhibiti ndege na kuibadili uelekeo wake ! akasema Mathew “Abu Zalawi kuna jambo ambalo hatukuwa tumekueleza.Sisi wote hapa ni wanajeshi na miongoni mwetu Abdul Razaq ni rubani wa ndege hivyo hakuna kitu cha kusubiri twende haraka tukawadhibiti wale marubani ! akasema Yasser kisha wakatoka katika chumba kile wakaanza kunyata kuelekea katika chumba cha marubani.Mlango wa chumba cha marubani ulikuwa umefungwa kwa ndani.Bila kupoteza muda Yasser akamimina risasi katika kitasa na kukisambaratisha Mathew akaurukia teke mlango ukafunguka wakaingia ndani ya chumba kile cha marubani .Mathew akawataka wasimame na watoke katika viti vyao marubani wale wakatii kisha Abdu Razaq na Tayeb Burhan wakashika hatamu na kuanza kuiongoza ndege .Kitu cha kwanza walichokifanya ni kuzima kifaa kinachowezesha ndege kuonekana na kufuatiliwa katika rada. “Abdu badili uelekeo wa ndege tunakwenda nyumbani ! akasema Yasser kwa furaha kubwa. “Mafuta yaliyopo yanaweza kutufikisha Iran?Mathew akauliza “Ndiyo.Mafuta yanatosha kutufikisha nyumbani.Ahsante Abu Zalawi” akajibu Abdu Razaq “Vipi kuhusu mimi?Nitakubaliwa kuingia Iran kutokana na historia yangu ya ugaidi?akauliza Mathew “Abu Zalawi wewe ni shujaa na unastahili sifa kubwa.Ni wewe uliyesababisha haya yote yakawezekana.Ni wewe uliyesababisha leo hii tunarejea tena nyumbani.Utapokelewa kwa mikono miwili Abu Zalawi usihofu” akasema Yasser na kumkumbatia Mathew kwa furaha kubwa kisha akaungana na wenzake kuimba kwa furaha wimbo wa taifa la Iran. MPENDWA MSOMAJI,TAYARI MATHEW MULUMBI ANAELEKEA NCHINI IRAN JE ATAFANIKIWA KUINGIA SALAMA NCHINI HUMO ? SATTAR YUKO ANGANI ANAELEKEA DAR ES SALAAM JE RUBY NA WENZAKE WATAFANIKIWA KUMPATA NA KUZUIA KIRUSI KISISAMBAE? MPENDWA MSOMAJI USIKOSE SEHEMU IJAYO.
Tangu kulipopambazuka,tayari SNSA walianza kufuatilia kilichokuwa kinaendelea katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Hii ni baada ya kuhisi kuwa Sattar Sayf Al Din ambaye anatumwa Tanzania kusambaza virusi angeweza kushukia katika uwanja huo.Tayari walikwisha jiunga na mfumo wa ulinzi wa uwanjani hapo na walikuwa wanafuatilia kamera zote kufahamu kilichokuwa kinaendelea.Uwanja wa Julius Nyerere bado ulikuendelea kufungwa na ulikuwa chini ya uangalizi wa vikosi vya jeshi la Tanzania. Asubuhi hii jiji la Dar es salaam lilikuwa shwari na hakukuripotiwa matukio yoyote ya vurugu.Maduka na masoko yalianza kufunguliwa ili kuwawezesha wananchi kujipatia mahitaji muhimu,wananchi wengine waliokuwa wamekimbilia katika makambi maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kuwahifadhi watu waliokimbia mapigano,walianza kurejea katika majumba yao kufanya usafi na kuhifadhi mali zao.Taratibu hali ya maisha katika jiji la Dar es salaam ilianza kurejea kuwa ya kawaida lakini bado doria za vikosi vya ulinzi na usalama ziliendelea katika mitaa mbali mbali ya jiji ili kuhakikisha hakuna vurugu zozote zinazoendelea kutokea. Saa moja na dakika kumi na saba,Gosu Gosu na Nawal waliwasili ofisi kuu SNSA na moja kwa moja wakaelekea ofisini kwa Ruby na kumkuta akiendelea na kazi “Tayari kazi imekwisha anza.Tumeanza kufuatilia kila kinachoendelea uwanjani hapo toka saa kumi na mbili za asubuhi na mpaka sasa hakuna chochote tulichokipata.Zimetua helkopta mbili za jeshi na ndege moja ya jeshi la Tanzania.Tunaendelea kufuatilia kwani kama nilivyosema jana kuna uwezekano mkubwa Sattar Sayf Al Din akaingia hapa nchini kuanzia saa sita za mchana wa leo” akasema Ruby “Nina mashaka kidogo.Ni vipi kama Sattar atatumia ndege ya kawaida ya abiria na akaenda kutua katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro au hata Nairobi halafu akaja Dar es salaam kwa gari ? Akauliza Gosu Gosu “Hilo haliwezekani” akasema Nawal “Kirusi hicho ni hatari sana na hawawezi kutumia ndege ya abiria kusafirishia.Lazima watatumia ndege maalum kuhakikisha kinafika kikiwa salama hivyo kwa vyovyote vile lazima watatumia uwanja huu wa Julius Nyerere” akasema Nawal “Tuendelee kufuatilia na kama hatutapata chochote tutatafuta namna nyingine ya kuweza kumpata Sattar lakini kwa siku ya leo kwa namna yoyote ile lazima tuhakikishe tumekipata kirusi hicho” akasema Ruby wakaendelea kufuatilia kamera zile za uwanja wa ndege wa Julius Nyerere katika runinga kubwa wakiwa ofisini kwa Ruby “Nawal unaonaje ukimpigia simu Habiba Jawad ukamuuliza kama amepata taarifa zozote za kuhusu Sattar Sayf Al Din pamoja na Mathew? Akauliza Ruby na kumpatia Nawal simu akampigia Habiba Jawad “Mama Habiba”akasema Nawal baada ya Habiba kupokea simu “Nawal unaendeleaje? Akauliza Habiba “Niko salama kabisa mama.Kwa ujumla jiji la Dar es salaam liko salama.Hakuna matukio ya vurugu japo hakuna uhakika kama vurugu zimekwisha au vipi lakini hadi sasa jiji ni salama kabisa.Kuna taarifa yoyote mpya huko?Nawal akauliza “Kwa sasa bado sijapata taarifa yoyote mpya.Bado taarifa niliyonayo ni ile ile kwamba Sattar Sayf Al Din amekwisha ondoka Marekani akielekea Tanzania.Kuna mipango yoyote mnayo ya kujua mahala atakapofikia huyu mtu? Akauliza Habiba “Ndiyo mama.Kwa sasa tunaendelea kufuatilia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hapa Dar es salaam ambako tuna uhakika ndiko atatua.Tunategemea kuanzia saa sita mchana wa leo awe amewasili hapa Dar es salaam kutokana na muda alioondoka Marekani.Nitakujulisha kile tutakachokipata” akasema Nawal “Nawal narudia tena kukusisitiza kwamba kwa namna yoyote ile lazima muhakikishe Sattar anakamatwa kirusi hakisambazwi nchini Tanzania.Umenielewa Nawal? “Nimekuelewa mama,tunafanya kila tuwezalo.Kuna taarifa zooze umepata kuhusu Mathew Mulumbi? Nawal akauliza “Hapana.Bado sijapata taarifa zozote.Msihofu kuhusu Mathew atakuwa salama japo atakumbana na magumu mengi lakini ninao uhakika mkubwa atayashinda yote na atamaliza misheni yake.Tuendelee kumuombea ili awe salama.Kwa sasa jielekezeni zaidi katika kirusi hicho na mimi kila nikipata taarifa yoyote ambayo naamini inaweza kuwa na msaada kwenu nitawajulisha haraka sana” akasema Habiba “Mama wewe unafahamiana na viongozi wote wakuu wa IS.Kwa nini usiwasiliane nao wakueleze mahala alipo Assad ili iturahishishie kumpata Sattar Sayf Al Din endapo hatatumia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere?akauliza Nawal “Mimi ni mfadhili wao tu na si sehemu yao ya uongozi hivyo kuna mambo mengine ambayo hawawezi kuniambia.Hata hivyo nitajitahidi kutafuta taarifa za namna ya kuweza kumpata huyo Assad na nikifanikiwa nitawajulisha” akasema Habiba na kuagana na Nawal “Kama mlivyosikia hakuna jipya kutoka kwa Habiba.Tuendelee na mipango yetu tuliyoipanga” akasema Nawal WASHINGTON DC – MAREKANI Taarifa za kupotea kwa ndege iliyowabeba Mathew Mulumbi mtuhumiwa wa Ugaidi aliyelipua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,pamoja na raia sita wa Iran waliokuwa wanashikiliwa Mateka na Marekani kwa muda mrefu,zilipokelewa kwa mstuko nchini Marekani.Haraka haraka juhudi za kuitafuta ndege hiyo zikaanza.Kitu cha kwanza walichokihisi ni kwamba yawezekana ndege hiyo imeanguka katika bahari ya Hindi. Taarifa hiyo ya kupotea kwa ndege,zikamfikia Rais William Washington wa Marekani ambaye bila kupoteza muda akampigia simu makamu wake Mark Piller “Mheshimiwa Rais” akasema Mark Piller baada ya kupokea simu “Mark nimejulishwa kuhusu kupotea kwa ndege yetu iliyokuwa inamleta mtuhumiwa wa shambulio la ugaidi katika ubalozi wetu jijini Dar es salaam.Kuna chochote unaweza ukaniambia kuhusiana na tukio hilo? Akauliza Rais William “Ndiyo mheshimiwa Rais. Ndege hiyo haijapotea bali kwa sasa imebadili uelekeo na kuelekea chini Iran. Hii ni katika ule mpango niliokueleza kwamba tunataka kumtumia Abu Zalawi kuingia nchini Iran.Usihofu mheshimiwa Rais kila kitu kimepangwa kwa umakini mkubwa sana” akasema Mark Piller “Mark una uhakika hiki mnachokifanya kitafanikiwa? akauliza Rais William “Naomba uniamini mheshimiwa Rais.Mpango huu utafanikiwa na utakuwa na manufaa makubwa sana kwetu.Usiwe na hofu mheshimiwa Rais tuko makini sanana tumejipanga vizuri” akajibu Mark “Mark jitahidini sana kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba jambo hili haligeuki na kuwa mzigo kwetu.Endapo huyo gaidi mnayemtumia akigundulika mtakuwa mmeivua nguo nchi yetu” “Usiwe na shaka mheshimiwa Rais.Tunaamini Abu Zalawi ataifanya vyema kazi anayotumwa kwenda kuifanya kule Iran” akajibu Mark Piller “Vipi kuhusu kile kirusi? Tayari kimefika Tanzania? Akauliza Rais William “Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Sattar Sayf Al Din anakaribia kufika Tanzania na atakapofika tutajulishwa na watu wetu kule.Kila kitu kitakwenda sawa mheshimiwa Rais” “Mark narudia tena kutoa angalizo kwamba kila hatua za tahadhari lazima zichukuliwe kuwalinda watu wetu kule Tanzania.Sitaki kupoteza hata raia mmoja wa Marekani katika suala hili” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais naendelea kukusisitiza kwamba hutakiwi kuonyesha kama unafahamu chochote kuhusiana na haya mambo niliyokueleza.Yote unayoyafahamu endelea kuyafanya siri kubwa ambayo hata mke wako asiifahamu”akasema Mark Piller “Nitafanya hivyo Mark” akajibu Rais William na kuagana na Mark Piller ambaye naye alimpigia simu David Walker kiongozi wa kikundi kile ambacho kimejipa jina la The great 20 au kwa kifupi G20. “David nimetoka kuzungumza na Rais muda mfupi uliopita kuhusiana na kupotea kwa ndege yetu” “Anasemaje Rais? Akauliza David “Hafahamu chochote.Yeye na wenzake wanachoamini ni kwamba yawezekana ndege imeangukia baharini” “Safi sana.Mark mpango unakwenda vizuri sana na hivi tuzungumzavyo tayari ndege hiyo inaelekea Iran.Tunafuatilia na tunaendelea kukujulisha kila kitakachojiri” akasema David Walker na kuagana na Mark kwani alikuwa na safari ya kuelekea kwa Jason Washington mkurugenzi wa CIA.Hakupoteza muda akatoka kuelekea katika gari lake akaondoka kuelekea nyumbani kwa mkurugenzi wa CIA.Tayari mida hiyo ilikaribia saa kumi za usiku kwa saa za Marekani. David alifika nyumbani kwa Jason Washington akakaribishwa ndani na walinzi wa Jason.Alipelekwa moja kwa moja katika ofisi ya Jason akaingia na kumkuta akizungumza na mtu simuni.Jason akamfanyia ishara aketi na asubiri amalize mazungumzo na Yule mtu simuni.Baada ya dakika moja Jason akaagana na Yule aliyekuwa akizungumza naye simuni akamgeukia David “Karibu David” akasema Jason “Jason nikuonapo katika sura hiyo najua kuna jambo haliko sawa” akasema David “Ni kweli David.Jana kijana wangu alichukua gari la mama yake bila ruhusa akaenda nalo katika sherehe ya kuzaliwa mmoja wa marafiki zake na wakati wakirudi amegonga gari lingine” akasema Jason “Ameumia? David akauliza “Hapana hajaumia” akajibu Jason “Usijali Jason hayo ni mambo ya kawaida kwa vijana wetu yatakwisha tu.Kitu kikubwa hajaumia katika ajali hiyo” akasema David Walker “Tuachane na hayo David.Twende moja kwa moja katika kile kilichokuleta hapa alfajiri hii” akasema Jason “Jason kuna jambo limenileta hapa tulijadili mimi na wewe ambalo ni la muhimu sana katika ule mpango wetu unaoendelea” “Ndiyo David.Jambo gani hilo? Kwanza kabla ya yote nataka niwape hongera sana kwa namna mlivyo ratibu mpango huu kiasi cha kutotiliwa shaka hata kidogo kama ni mpango uliotengenezwa.Hivi sasa tayari utafutaji wa ndege hiyo iliyopotea umeanza na wote wanaamini yawezekana ikawa imepata hitilafu ikaanguka na kuzama katika bahari ya Hindi.Una jambo gani muhimu la kuongezea katika mpango huu David? Akauliza Jason “Mpango kama unavyoona unakwenda vizuri sana na tuna uhakika mkubwa kwamba Abu Zalawi ataingia nchini Iran.Hata hivyo kuna jambo ninalifikiria la muhimu sana ambalo hatukulitilia maanani hapo kabla” “Ndiyo nakusikiliza David” akasema Jason “Uhakika wa Abu Zalawi kuingia nchini Iran ni mkubwa.Hatukutegeneza mpango wowote wa kumsaidia Abu Zalawi akiwa nchini Iran.Akiwa kule kuna mambo ambayo atayahitaji kama vile mawasiliano,usafiri nk hivyo lazima awepo mtu wa kumsaidia kuyapata haya kwa siri bila mtu huyo kujulikana” akasema David “Hilo ni wazo zuri sana David lakini hatuna watu wetu kule Tehran.Endapo tungekuwa na watu wetu kule ingekuwa rahisi kumpa Abu Zalawi msaada muda wowote atakaouhitaji”akasema Jason “Ni kweli sisi hatuna watu wetu Tehran lakini tunao wenzetu wa Mossad.Wao wana majasusi wao nchini Iran.Tunaweza kuzungumza nao ili majasusi hao waweze kumsaidia Abu Zalawi.Abu ni mgeni wa jiji la Tehran na kama angeweza kumpata mwenyeji ambaye angemsaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo ingemrahisishia sana shughuli yake.Unaonaje wazo hilo la kuwaomba msaada Mossad? akauliza David.Jason akainamisha kichwa akafikiri kidogo halafu akasema “Ninakubaliana na wazo lako David lakini sina uhakika kama Mossad wanaweza kukubali kutusaidia katika operesheni hii.Kuna msuguano ulitokea hapa kati kati baina yetu hivyo basi mahusiano yetu na Mossad si mazuri kwa sasa” akasema Jason “Jason kwa namna yoyote ile lazima tumsaidie Abu Zalawi kule Iran.Hatuna majasusi wetu Iran na hatuwezi kuingiza majasusi wetu kule lakini Israel ambao ni washirika wetu wakubwa wana majasusi wao Iran ambao tunaweza kuwatumia kumpa msaada Abu Zalawi ili aweze kukamilisha jukumu tulilomtuma kule” akasema David “David kuna jambo lilitokea na kuzorotesha mahusiano yetu na Mossad.Kuna wakati walihitaji kufahamu mahala alipo Ammar Nazari na wakaomba msaaada kwetu lakini sikuwa tayari kuwasaidia kuwapa taarifa za mahala alipo Ammar Nazari kwa kuwa tulikuwa na mtu wetu katika kundi hilo aliyekuw akatika operesheni maalum.Baada ya kuwakatalia kuwapa taarifa za mahala alipo Ammar,Mossad walifanya jitihada zao wenyewe na kufanikiwa kufahamu mahala anapojificha Ammar na wakamuua kwa bomu.Toka wakati huo mahusiano yetu nao si mazuri” akasema Jason “Pamoja na mashirikiano kutokuwa mazuri lakini si vibaya kama tukiwajaribu.Endapo watakataa kutusaidia tutaangalia washirika wetu wengine.Tunao washirika kadhaa wanaoweza kutusaidia lakini tunapenda kufanya kazi na Mossad kwa kuwa majasusi wake wana umahiri mkubwa sana.Jaribu kuwasiliana na mkurugenzi wa Mossad ili tuone kama wanaweza kutusaidia” akashauri David.Kwa kufuata ushauri wa David,Jason akachukua simu na kumpigia Moshe Levine mkurugenzi wa Mossad “Jason habari za siku?akauliza Moshe Levine mkurugenzi wa Mossad baada ya kupokea simu “Huku tunaendelea vyema kabisa”akajibu Jason “Nafuarhi kusikia hivyo.Poleni kwa shambulio la Dar es salaam” akasema Moshe “Ahsante Moshe.Samahani kwa kupiga muda huu lakini nimekupigia kukuomba msaada wako.Nafahamu hatuna mashirikiano mazuri kwa siku za hivi karibuni lakini CIA na Mossad tumekuwa marafiki na kushirikiana kwa muda mrefu hivyo nashauri tusahau yale yaliyopita na tuanze tena mashirikiano mapya baina yetu” akasema Jason “Nini unahitaji Jason? Akauliza Moshe “Nafahamu unao watu wako jijini Tehran” “Ndiyo ninao watu watu wangu Tehran” akasema Jason “Nahitaji msaada wako Moshe.Kuna operesheni kubwa sana tunaiendesha kule Tehran.Kuna mtu wetu tumemtuma huko katika misheni ya muhimu sana.Ninahitaji watu wako kule Tehran wamsaidie huyo mtu wetu aweze kufanikisha misheni yake” akasema Jason “Jason unaweza ukanifafanulia ni operesheni gani inaendelea huko Iran? Akauliza Moshe na Jason akamueleza Moshe kuhusiana na misheni ile wanayotaka kuifanya nchini Iran. “Jason kwanza nashukuru kwa kuniamini na kunieleza kuhusiana na mpango wenu unaoendelea nchini Iran.Mossad tuna watu wetu Tehran na hakuna tatizo katika kumsaidia huyo mtu wenu kufanikisha misheni mliyomtuma kwani misheni hiyo ni muhimu pia kwa taifa la Israel kwani tumekuwa tukipokea vitisho vingi kutoka Iran.Hata hivyo kuna tatizo”akasema Moshe “Tatizo gani Moshe? akauliza Jason “Sina hakika kama huyu mtu mnayemtumia katika operesheni hiyo Abu Zalawi mnamfahamu vyema” akasema Moshe.Jason akamtazama David “Kuna nini kuhusu Abu Zalawi? Akauliza Jason “Huyu mtu mnamfahamu vyema? “Moshe unaonyesha wasi wasi mkubwa.Unamfahamu Abu Zalawi? Akauliza Jason “Ndiyo Jason.Ninamfahamu Abu Zalawi kiundani ndiyo maana ninasema kuna tatizo” akajibu Moshe na Jason akashusha pumzi “Kabla sijawaeleza chochote, ilikuaje mkachagua kumtuma Abu Zalawi kazi hii nyeti? Akauliza Moshe “Tulihitaji mtu ambaye ni Gaidi kwa ajili ya kazi hii na tulipompata Abu Zalawi ilitulazimu kwanza kujiridhisha kama anafaa tukampa mtihani akaufaulu vizuri ndipo tulipomtuma kwenda Iran.Kuna tatizo gani kuhusu huyu mtu?akauliza Jason “Nina wasiwasi mnamtumia mtu ambaye hamumfahamu vyema na ndiyo maana nasema lipo tatizo.Abu Zalawi si gaidi kama mlivyojulishwa”akasema Moshe Levine “Si gaidi? Ki vipi Moshe? Akauliza Jason akionekana kustuka kidogo “Jina lake halisi ni Mathew Mulumbi.Ni jasusi anatokea Tanzania” akasema Moshe na nusura simu imponyoke Jason kwa mstuko alioupata “Sijakuelewa Moshe unachokizungumza” akasema Jason “Huyu mtu mnayemfahamu kama Abu Zalawi jina lake halisi ni Mathew Mulumbi na ni jasusi anayetokea Tanzania” akasema Moshe Levine na kumsimulia Jason kila kitu kuhusu Mathew Mulumbi toka alivyovamia ubalozi wa Israel jijini Nairobi na kumtorosha Edger kaka na hadi walivyofanikiwa kumkamata na kumfunga kwa miaka mitatu nchini Israel.Jason akahisi kuanza kuloa jasho.Moshe akaendelea “Kwa muda mrefu tumekuwa tukimtafuta mfadhili mkuu wa vikundi vya wanamgambo wanaopambana na Israel ambaye anafahamika kama Habiba Jawad.Mathew naye alikuwa katika mpango huo akatushawishi tuungane naye katika kumsaka Habiba na ndipo tulipokuja na mpango wa kumuunganisha Mathew na Ammar Nazari kiongozi wa kundi la Ammar Nazari Brigades aliyekuwa anashikiliwa gerezani na ambaye kundi lake lilikuwa linafadhiliwa na Habiba.Hapo ndipo jina la Abu Zalawi lilipoanza.Hili ni jina ambalo tulimpa alitumie kwa ajili ya kujenga ukaribu na Ammar Nazari na vile vile tukamuweka katika mtandao wetu kama mtu tunayemtafuta.Mathew alifanikiwa kumtorosha Abu Zalawi gerezani na kujiunga naye na baada ya hapo hatukuwahi kupata mrejesho wowote kutoka kwake hadi tulipofanikiwa kumuua Ammar.Mathew aliibuka tena na tayari alikwisha onana na Habiba Jawad ambaye alimtuma kuja Israel kumchukua mwanae Edger Kaka tuliyekuwa tunamshikilia.Tulimkabidhi mwili wa Edger Kaka akapotea na hatukupata tena mrejesho kutoka kwake hadi tulipopata taarifa kuwa amehusika katika shambulio la bomu katika ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam.Yawezekana hayo yote hamkuwa mkiyafahamu kuhusu huyu jamaa mnayemtumia katika hiyo misheni yenu muhimu sana” akasema Moshe.Jason akavuta pumzi ndefu kisha akasema “Moshe umetufumbua macho.Ni kweli hatukuwa na taarifa zozote za kuhusiana na huyu mtu.Tunachokifahamu sisi ni kwamba anaitwa Abu Zalawi raia wa Saudi Arabia.Nimestuka kusikia kwamba jina lake ni Mathew Mulumbi na ni raia wa Tanzania.Moshe ahsante sana kwa taarifa hii ambayo imenichanganya sana.Ninaomba nikupigie baadae kidogo” akasema Jason na kukata simu akatazamana na David “David nini hiki kinachoendelea? akauliza Jason na kumpa David maelezo yote aliyopewa na Moshe Levine mkurugenzi wa Mossad. “Kweli hii ni taarifa ya kustusha mno.Hakuna mtu yeyote aliyefahamu kitu kama hiki.Tumeletewa huyu mtu na Habiba ambaye tunamuamini na tumeshirikiana naye kwa muda na akatupa taarifa zake kuwa ni gaidi na anaitwa Abu Zalawi.Tunamuamini Habiba Jawad hivyo hakuna aliyekuwa na wasiwasi hata kidogo kuhusiana na mtu aliyetuletea” akasema David Walker ukapita ukimya mfupi halafu Jason akasema “Habiba ametuchezea mchezo mbaya sana ! akasema Jason kwa hasira “Ni jambo la kustusha mno” “Baada ya kulifahamu jambo hili nini tunafanya David? akauliza Jason “Imekuwa bahati mbaya sana tumelifahamu jambo hili katikati ya misheni na wakati ambao tayari Abu anaelekea Iran na hatuna namna tena ya kuweza kumzuia asiendelee na misheni hii.Jason kwa sasa sina hakika kama kuna kitu tunachoweza kukifanya.Tumuache tu aendelee na misheni yetu tena kama ni jasusi itakuwa vizuri zaidi kwani atafanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana” akasema David Walker “David,mtu huyu kama alivyosema Moshe tumekosea sana kumpa misheni kubwa kama hii.Tulipaswa kumchimba Abu Zalawi mapema na kumfahamu kiundani kabla ya kumtuma kazi.Tulikosea mno” akasema Jason “Ni kweli Jason.Nikiri tulikosea sana kutokufanya uchunguzi wa kina kuhusu Abu Zalawi kabla ya kumkabidhi misheni hii lakini hii ilisababishwa na imani kubwa tuliyo nayo kwa Habiba Jawad.Tuliamini mtu aliyetuletea hana tatizo lolote kwani amekuwa akitusaidia kupata watu kwa ajili ya shughuli mbali mbali na hakujawahi kutokea tatizo lolote hadi sasa.Ushauri wangu tumuache Abu Zalawi aendelee na misheni hii kwani tayari amekwisha piga hatua kubwa” akasema David Walker “Hapana David hatuwezi kumuacha akaendelea na misheni hii na wala misheni yenyewe haipaswi kuendelea.Tunasimamisha kila kitu ! akasema Jason na kumfanya David apatwe na mshangao “Jason wewe ni mkuu wangu na ndiye mwenye maamuzi ya mwisho kuhusiana na misheni zote tunazozifanya lakini katika hili siwezi kukubaliana nawe hata kidogo.Tumekwisha tumia gharama kubwa sana kwa ajili ya kuandaa operesheni hii na tayari tumefika nusu yake hatuwezi kuishia hapa.Lazima tuendelee hadi pale tutakapotimiza lengo letu.Kumbuka damu za watu zimemwagika kwa sababu ya misheni hii,hatuwezi kuishia hapa! Tumekaribia sana kufika pale ambapo tumekuwa tunapatafuta kwa miaka mingi” akasema David “David nakubaliana nawe kwamba imetugharimu fedha na damu kuandaa misheni hii lakini hatuwezi kuendelea nayo tena.Madhara yake ni makubwa sana kama ikiendelea ukilinganisha na gharama ambazo tumetumia.Huyu jamaa ambaye tayari tumefahamu anaitwa Mathew Mulumbi ni mtanzania.Hamuoni hatari iliyopo kuendelea kumtumia? Ni vipi kama tayari anafahamu mambo tuliyoyafanya kule Tanzania? Sikuwepo wakati mkizungumza naye lakini nataka nifahamu kutoka kwako kwani ni wewe uliyeongoza mahojiano naye kuna chochote mlimwambia kuhusiana na kile tulichokifanya Tanzania? Akauliza Jason na David akaanza kukumbuka. “Eneo la Afrika Mashariki hivi sasa liko katika machafuko makubwa sana ya kidini.Kinachoendelea kule ni moja ya mipango yetu na kwa kuwatumia IS tumeweza kufanikisha kuibuka kwa machafuko makubwa sana ya kidini ambayo yamepelekea Marekani kupeleka vikosi vyake.Hapa unaweza ukaona ni namna gani Marekani inafaidika kutokana na makundi ya kigaidi.Tumewatumia IS kutengeneza vurugu zile na sasa Marekani inafaidika kwa mafuta mengi kutoka Uganda.Meli za Marekani zimepanga foleni zinapishana kujaza mafuta ,akiba yetu ya mafuta inaongezeka.Hii yote ni kazi ya timu hii unayoiona humu ndani na ni mfano wa mafanikio makubwa ambayo yanapatikana kwa kuwatumia magaidi” Sura ya David walker ikabadilika baada ya kumbu kumbu hii kumjia. “Kuna kitu umekikumbuka David?akauliza Jason “Ndiyo Jason.Kuna kitu nimekikumbuka.Katika mazungumzo yetu tulimueleza Abu Zalawi kila kitu tunachokifanya bila kumficha tukiamini yeye ni gaidi na ni raia wa Saudi Arabia.Hatukujua kama ni jasusi tena raia wa Tanzania.Tulifanya kosa” akasema David na ukimya ukapita “Mlimweleza chochote kuhusiana na mpango wa kusambaza kirusi Tanzania? Akauliza Jason “Hapana mpango huo umekuja baada ya yeye kuondoka Marekani.Hafahamu chochote kuhusu mpango huo lakini anachokifahamu ni kuwa,sisi tukiwatumia magaidi wa IS tumechochea vurugu za kidini zilizotokea Tanzania kwa lengo la kujipatia mafuta.Nilikuwa mjinga sana kumweleza jambo hili ! akasema David kwa masikitiko “David nadhani sasa umeona wewe mwenyewe kwa nini ninasema misheni hii lazima isimamishwe haraka sana bila kujali utekelezaji wake umefika hatua gani.Abu Zalawi au Mathew Mulumbi kama anavyojulikana hapaswi kuendelea na misheni hii.Tayari anafahamu kuwa ni sisi tulio nyuma ya machafuko yale yaliyotokea Tanzania lakini bado akakubali kufanya kazi tuliyomtuma akaifanye hudhani kuna kitu huyu jamaa anapanga kukifanya? Kwa mujibu wa Moshe huyu ni mmoja wa majasusi hatari kabisa na kwa miaka mitatu alikuwa katika mateso makali na hakuwahi kufungua mdomo wake kusema chochote.Japokuwa amekubali kuifanya kazi yetu kama vile hakuna chochote kilichotokea lakini hatuwezi kujua moyoni mwake nini anakiwaza.Tumefanya kosa kubwa sana David” akasema Jason “Yote haya ameyataka Habiba Jawad.Yeye ndiye aliyemleta huyu mtu na akatuaminisha kwamba ni mtu sahihi anayeweza kuifanya operesheni hiyo kwa ukamilifu.Kwa nini akamchagua Abu Zalawi? Hapo ndipo tunapaswa kuanzia” akasema David “Unadhani Habiba Jawad alimfahamu Abu Zalawi ni nani lakini bado makusidi kabisa akaa mua kumleta kwetu tumtumie? Akauliza Jason “Ninahisi hivyo.Alimleta kwetu mtu ambaye naamini alimfahamu fika ni nani na ninahisi alifanya hivyo kwa sababu maalum ambayo hatuijui” “Tumeshirikiana na Habiba Jawa kwa muda mrefu toka mume wake alipofariki na tumemuwezesha kuwa na utajiri mkubwa mno,unadhani anaweza kuwa na mpango wowote wa siri dhidi yetu? Akauliza Jason “Tutamfanyia uchunguzi kulifahamu hilo lakini kwa sasa ni kutafakari kuhusu hatua za haraka za kuchukua kuhusiana na misheni hii na huyu jamaa Abu Zalawi” akasema David “Kama nilivyosema awali kwamba kwa namna yoyote ile Abu Zalawi hapaswi kuendelea na misheni hii nyeti”akasema Jason “Hivi sasa naamini Abu atakuwa njiani akielekea Iran.Ndege aliyomo imepotea haionekani na hatuna namna ya kuweza kumpata hadi atakapokuwa ameingia Iran,ndiyo maana nilishauri kwamba aendelee na misheni yake kama kawaida na kama tukif……..” “David huyu mtu hapaswi kuendelea na misheni yetu yoyote.Huyu mtu ni bomu na siku moja atatulipukia.Tayari anafahamu sisi ndiyo sababu ya mamia ya watu kupoteza maisha Tanzania na yawezekana miongoni mwa waliofariki ni ndugu zake,unadhani akisikia tena kitakachotokea Tanzania baada ya kirusi kusambazwa nini atatufanya? Ni wazi anaweza akageuka na kuwa adui yetu mkubwa.Huyu mtu tayari amekuwa mzigo kwetu na kitu pekee ambacho tunapaswa kukifanya kwa sasa ni kutafuta namna ya kumuua kabla hajaanza kufanya chochote nchini Iran” akasema Jason “Tuliwaomba msaada Mossad ili majasusi wao walioko nchini Iran wamsaidie Abu Zalawi tunaweza kubadili badala ya kumsaidia mpango uwe ni kumuua” akasema David “Nadhani itatulazimu kufanya hivyo.Japo nakubali tumefika hatua nzuri lakini mtu tuliyemtumia si mtu sahihi na hatuwezi kuendelea naye.Tunapaswa kummaliza haraka sana kisha tutaanza kujipanga tena upya namna nyingine.Vile vile tumchunguze Habiba Jawad tujue kama alimfahamu Abu Zalawi ni nani lakini bado akamleta kwetu ili tumtumie.Tuchunguze mahusiano yao.Habiba anapaswa ahojiwe kwa kina kuhusiana na huyu jamaa” akasema Jason halafu akachukua simu na kumpigia Moshe Levine mkurugenzi wa Mossad “Moshe nimekupigia tena kuomba msaada wako.Kwanza ninakushukuru kwa kutufumbua macho kuhusu Abu Zalawi.Hatukuwa tukimfahamu ni nani huyu mtu na baada ya kumfahamu tumeamua kukatisha misheni tuliyomtuma akaifanye Iran” akasema Jason Washington “Ni maamuzi mazuri mmeyafanya Jason,kwani huyu jamaa si mtu sahihi kwa misheni hii na hata sisi mpaka leo hii tunajilaumu mno kwa kuamua kushirikiana naye.Ameturejesha nyuma mno katika jitihada zetu za kumsaka Habiba Jawad.Tulidiriki hata kumuachia Ammar Nazari ambaye ni mtu hatari sana kwa Israel tukitegemea kupata matokeo lakini hatujapata chochote mpaka sasa.Huyu mtu anatakiwa aondolewe haraka iwezekanavyo ! akasema Moshe Levine “Ndiyo maana nimekupigia Moshe ili kukuomba tushirikiane tuweze kuumuondoa Abu Zalawi haraka sana kabla hajafanya chochote nchini Iran” akasema Jason “Nina watu wangu jijini Tehran ambao wakatekelea mpango huo wa kumuua Abu Zalawi lakini kuna kitu tutakihitaji kutoka kwenu CIA” akasema Moshe Levine “Nini unakihitaji Moshe? Akauliza Jason “Ninataka kupata taarifa za mahala alipo Habiba Jawad”akasema Moshe “Habiba Jawad? Akauliza Jason kwa mshangao “Ndiyo.Tutahitaji kujua mahala alipo” akajibu Moshe “Hatuna taarifa zozote za kumuhusu Habiba Jawad” akasema Jason “Jason nimewaambia hivyo kwa sababu nafahamu mnazo taarifa za kumuhusu Habiba Jawad.Tunafahamu Abu Zalawi amekutana na Habiba Jawad na kama mmeweza kukutana na Abu Zalawi mkamtuma katika misheni yenu lazima mnafahamu alipo Habiba Jawad.Tunamuhitaji sana Habiba Jawad hivyo tupeni taarifa za mahala alipo na sisi tuwatumie watu wetu kumuondoa Abu Zalawi” akasema Moshe Levine. “Moshe nitakupigia baadae kidogo tuzungumze kuhusu suala hili” akasema Jason Washington na kukata simu akapiga meza kwa hasira “Aaaaghh !! akasema kwa hasira “Mossad wanataka tuwape taarifa za Habiba Jawad ndipo watusaidie kumuonda Abu Zalawi! Akasema Jason “Wamefahamuje kama tunafahamu alipo Habiba Jawad?akauliza David “Ni kwa sababu ya Abu Zalawi.Wanafahamu amekuwa akishirikiana na Habiba Jawad hivyo basi kitendo cha sisi kumtumia katika misheni yetu kinawafanya waamini kwamba tunafahamu mahala alipo Habiba Jawad.David jambo hili linazidi kuwa kubwa” akasema Jason “Jason kwa namna yoyote ile hatuwezi kuwapa Mossad taarifa za Habiba Jawad.Hawapaswi kufahamu kama tumekuwa tukishirikiana naye.Hii ni siri yetu kubwa ambayo hata Rais wetu haijui hivyo hatuwezi kuianika kwa mtu mwingine yeyote hasa hasa Mossad” akasema David “Lakini tunahitaji kumuondoa Abu Zalawi haraka sana na ni Mossad pekee wanaoweza kutusaidia katika hilo kwani tayari wanao majasusi wao jijini Tehran.David tukubali Mossad wametubana katika kona.Tunahitaji kuzungumza nao vizuri katika jambo hili.Tukichelewa tunaweza kumkosa Abu Zalawi kwani tayari tumekiwsha mtengenezea mazingira mazuri ya kuweza kupokelewa bila tatizo nchini Iran na anaweza akageuka kuwa mwiba kwetu na kutuchoma.Hatupaswi kumpa nafasi lazima tuhakikishe anauawa haraka sana ikiwezekana kabla hajakanyaga ardhi ya Iran.Sidhani kama kuna haja ya kubishana na Mossad.Hakuna sababu ya kumficha Habiba Jawad kwani ni yeye ndiye aliyesababisha haya yote yakatokea” akasema Jason “Habiba ni mtu anayefahamu mambo yetu mengi kwani tumeanza kushirikiana naye kwa muda mrefu.Ni mtu ambaye hatuwezi kumtoa kirahisi kwa Mossad.Lakini kwa kuwa na sisi tunahitaji msaada wao basi tunaweza kufanya kitu kimoja.Tukubaliane nao kwamba wamuue Abu Zalawi na sisi tumuue Habiba Jawad.Tunao uwezo wa kumpata Habiba na kumuua hivyo tufanye kazi hiyo sisi wenyewe ili wasije wakagundua mashirikiano yetu na Habiba” akasema David. “Hilo ni wazo zuri David” akasema Jason kwa sauti ndogo kisha ukimya ukapita “Lakini kwa nini tumuue Habiba Jawad? Amekuwa nasi kwa muda mrefu na ametusaidia mambo mengi.Je hatumuhitaji tena? Akauliza David “Habiba Jawad ndiye aliyetufikisha hapa tulipofika.Ametufanya tukaingia katika misheni ambayo ni sawa na kujifunga kitanzi shingoni sisi wenyewe baada ya kumleta kwetu Abu Zalawi ambaye si gaidi bali ni jasusi.Naamini hakufanya hivi kwa bahati mbaya nahisi kuna jambo wanalipanga kati yake na Abu Zalawi hivyo lazima tuwaondoe wote mara moja ili tuendelee kuwa salama.Nakuhakikishia David bila kuwaondoa watu hawa wawili hatutakuwa salama.Usihofu kuhusu utajiri tuliomuwezesha Habiba,tutatafuta mtu mwingine wa kumuwezesha na akatufanyia kazi nzuri kuliko hata Habiba” akasema Jason lakini David alionekana kuzama katika lindi la mawazo. “Jason nadhani suala hili lifike kwanza kwa G20 ili yafanyike maamuzi.Hili jambo ni kubwa mno hatuwezi kufanya maamuzi sisi wawili pekee wakati tunao wenzetu wengine.Ikiwezekana kura inaweza kupigwa kuamua jambo hili.Nitawakusanya ndani ya muda mfupi asubuhi ya leo kisha nitaliwasilisha kwao jambo hili watalitafakari na kulifanyia maamuzi na pengine wanaweza wakawa na mawazo mengine mazuri zaidi” akasema David “Sawa David nenda kakutane na wajumbe hao mzungumze na jibu lipatikane haraka sana ili tujue namna ya kulishughulikia jambo hili”akasema Jason na David akaondoka kwenda kufanya maandalizi ya kukutana na wajumbe wa kikundi chao cha G20 kwa ajili ya kulijadili suala lile nyeti lililojitokeza DAR ES SALAAM – TANZANIA Bado macho ya SNSA yalielekezwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakiendelea kufuatilia kila kinachoendelea pale uwanjani.Ilipofika saa sita na dakika saba yakasikika maongezi kati ya rubani wa ndege na waongoza ndege wa uwanja wa Julius Nyerere.Ilikuwa ni ndege ya jeshi la Marekani ikiomba kutua katika uwanja huo ikiwa imeleta mahitaji mbalimbali kwa ajili ya vikosi vya jeshi la Marekani vilivyoko Tanzania. Dakika chache baadae ndege ya jeshi la Marekani ikatua. “Yawezekana ndege iliyoleta kirusi ni hii kwani imefika kwa muda ule ule ambao tulitarajia ndege iliyombeba Sattar ingewasili” akasema Gosu Gosu “Tuendelee kufuatilia tutajua kama ni hii” akasema Ruby akionekana kuwa na wasiwasi Dakika chache toka kuwasili kwa ndege ile ukawasili msafara wa magari ya vikosi vya jeshi la Marekani vilivyopo Tanzania na kazi ya upakuzi wa mizigo katika ndege ile ikaanza. “Inaonekana ni mizigo ya kawaida inayohusiana na wanajeshi” akasema Gosu Gosu “Tuendelee kuchunguza” akasema Ruby wakati mizigo ikipakuliwa kutoka ndegeni na kuingizwa katika magari “Hakuna dalili zozote za kuwepo Sattar au kirusi katika ndege hii ya mizigo” akasema Gosu Gosu lakini hakuna aliyemjibu watu wote waliyaelekeza macho yao katika kamera wakifuatilia kile kilichokuwa kinaendelea pale uwanjani.Mizigo iliyokuwa katika ndege ile ilimalizika na magari yakajipanga kwa ajili ya kuondoka.Kiongozi wa msafara ule akatoa maelekezo na magari yakaanza kuondoka. “Hakuna kirusi katika ndege hii.Hawa watu wametuc………….” Akasema Gosu Gosu na Nawal akamkatisha “Subiri kwanza Gosu Gosu.Kuna magari manne yamebaki uwanjani.Mnadhani kwa nini yamebaki? Akauliza Nawal “Ni kwa sababu bado kuna kitu wanakisubiri.Yawezekana wanamsubiri Sattar Sayf Al Din” akasema Nawal “Nawal yuko sahihi.Hawa jamaa wanaonekana kuna kitu wanakisubiri.Tuendelee kuwafuatilia tujue kile wanachokisubiri” akasema Ruby “Lakini mbona hakuna dalili zozote za kuwepo Assad Ismail hapa uwanjani?Tulielezwa kwamba yeye ndiye atampokea Sattar Sayf Al Din” akasema Gosu Gosu “Relax Gosu Gosu” akasema Ruby Magari manne ya vikosi vya jeshi la Marekani yaliendelea kubaki pale uwanjani na kwa namna walivyokaa walionekana kuna kitu wanakisubiri. Dakika ishirini baadae yakasikika mazungumzo kati ya waongoza ndege wa uwanja wa Julius Nyerere na Rubani aliyekuwa akiomba kutua katika uwanja huo wa ndege “Hii lazima itakuwa yenyewe ! akasema Nawal Dakika chache baadae ndege ikatua na magari yale ya jeshi la Marekani yaliyokuwa yamebaki yakisubiri yakaanza kuijongelea ndege ile. “Hii si ndege ya jeshi la Marekani.Hii ni ndege inayotumiwa na CIA kupeleka maafisa wake sehemu mbali mbali duniani”akasema Nawal baada ya ndege ile kutua. “Hii inatupa uhakika kwamba ndege hii yawezekana ndiyo imeleta kirusi”akasema Ruby Magari yale yalisogelea ndege ile ambayo mlango wake ulifunguliwa na baadhi ya maafisa wa jeshi wakaingia ndani.Baada ya muda wakatoka wakiwa wameongozana na mtu mmoja aliyebeba masanduku mawili.Wote mle ndani sura zao zikaonyesha mabadiliko baada ya kumshuhudia Yule mtu aliyekuwa amebeba masanduku mawili akiwa ameongozana na maafisa wa jeshi la Marekani kuwa ni Sattar Sayf Al Din “Hatimaye kirusi kimefika Tanzania” akasema Nawal Sattar Sayf Al Din aliongozwa hadi katika mojawapo ya magari yale na kuondoka pale uwanjani. “Nini kinafuata baada ya kujiridhisha kuwa Sattar ameingia nchini na muda wowote wanaweza wakasambaza kirusi?akauliza Gosu Gosu “Huyu Sattar Sayf Al Din ni mtu ambaye lazima watamchunga sana kwani amebeba kitu hatari mno hivyo basi nina uhakika watampeleka katika sehemu maalum watamlinda hadi watakapomkabidhi kwa Assad Ismail kwa ajili ya kuanza kazi ya usambazaji wa kirusi” akasema Nawal “Sattar yuko katika mikono ya vikosi vya Marekani na yawezekana akapelekwa katika kambi yao akahifadhiwa huko na itatuwia ugumu kwetu kuweza kumpata.Lazima tuje na mpango kabambe wa kutuwezesha kuingia katika kambi ya jeshi la Marekani na hatimaye kumfikia Sattar na kuchukua kirusi” akasema Ruby “Nina wazo” akasema Nawal “Ninyi mna mawasiliano ya karibu na Rais wa Tanzania? Akauliza Nawal “Ndiyo tuna ukaribu mkubwa na Rais” akajibu Ruby “Vizuri.Basi italazimu kumshirikisha Rais katika jambo hili” akasema Nawal “Hapana hatuwezi kumshirikisha Rais katika hatua hii.Ni mapema mno.Tutamjulisha Rais baada ya kukipata kirusi” akasema Ruby “Ruby nisikilizeni” akasema Nawal “Tayari tuna uhakika kwamba Sattar Sayf Al Din ameingia hapa nchini na tumemuona akiwa na masanduku mawili ambayo tunaamini kirusi kimo ndani yake.Ili tuweze kujua nyendo zote za Sattar na mipango yake yote ya kukisambaza kirusi hicho ikiwa ni pamoja na kujua mahala alipo Assad Ismail lazima kuingia katika vikosi vya Marekani .Kwa ninyi itakuwa vigumu kwa sababu si wamarekani lakini mimi ni mmarekani hivyo inaweza kuwa rahisi kwangu.Tufanye hivi,tuonane na Rais na aelezwe kila kitu kuhusiana na kirusi hicho na kitu ambacho tutamtaka akifanye ni kumuita kamanda wa vikosi vya Marekani vilivyoko hapa nchini na atanikabidhi mimi kwake akidai kwamba nimeokolewa na vikosi vya Tanzania kutoka katika mikono ya watekaji.Nitajitambulisha kama mpiga picha wa kujitegemea niliyekuja kutembea Tanzania na nikajikuta nimekwama katikati ya machafuko nikatekwa hadi nilipookolewa na vikosi vya jeshi la Tanzania nikapelekwa Dar es salaam.Nikisha kabidhiwa kwao naamini watanipeleka katika kambi yao ambako nitaanza kufanya uchunguzi kuhusiana na mahala alipo Sattar na kujua mipango yote ya kuhusiana na usambazaji wa kirusi huku nikiendelea kuwasiliana nanyi” akasema Nawal “Nawal huo ni mpango wa hatari sana” akasema Ruby “Ni kweli ni mpango wa hatari sana lakini lazima tuufanye kwani ndio pekee utakaotuwezesha kukifuatilia kirusi na kuzuia mpango wa kukisambaza” akasema Nawal “Gosu Gosu una ushauri gani?Ruby akauliza “Mimi naona wazo la Nawal ni zuri tulifanyie kazi ili aweze kuingia katika kambi ya vikosi vya Marekani kumfuatilia Sattar,lakini nina hofu endapo Rais akifahamu kuwa Marekani wako nyuma ya haya yote yanayoendelea hapa nchini anaweza akapandwa na hasira na kuvitaka vikosi vya Marekani vindoke haraka sana na hivyo tukashindwa kukamilisha operesheni yetu” akasema Gosu Gosu “Anachokisema Gosu Gosu ni kitu cha kweli.Tunapaswa kuwa makini sana tunapoamua kumueleza Rais kuhusu jambo hili.Nashauri tumuombe Rais akukutanishe na mkuu wa vikosi vya Marekani hapa nchini bila kumueleza chochote kuhusiana na operesheni wanayoiendesha Marekani hapa nchini hadi hapo tutakapokuwa tumepata taarifa za kutosha” akasema Ruby wakajadiliana kwa muda wakakubaliana halafu Ruby akampigia simu Dr Fabian Kelelo akamuomba waonane kwa ajili ya suala muhimu na Dr Fabian akamtaka aende ikulu. Kutoka ofisi kuu za SNSA hadi ikulu si mbali hivyo iliwachukua dakika kama kumi kufika ikulu “Ruby karibu sana.Mnaendeleaje huko katika idara yenu?akauliza Dr Fabian baada ya akina Ruby kuwasili “Tunaendelea vyema mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kunyamaza kidogo halafu akasema “Mheshimiwa Rais huyu anaitwa Chloe Bennet anatokea Marekani” akasema Ruby na Nawal akasimama akaenda kumpa mkono Rais “Karibu sana Tanzania Chloe” akasema Dr Fabian “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Nawal “Mheshimiwa Rais Chloe yuko hapa kwa jambo mahsusi.Kuna misheni muhimu anasaidiana nasi” akasema Ruby “Naweza kufahamu ni misheni gani inayoendelea kati yenu na Chloe? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninaomba nisikwambie kwa sasa hadi hapo tutakapokuwa tumeikamilisha misheni hiyo” “Ruby hapo ndipo huwa unaniudhi.Kila mara ninapokuuliza kinachoendelea SNSA jibu lako limekuwa hilo hilo moja kwamba huwezi kunieleza kwa sasa hadi hapo baadae?Kwa nini hutaki kuniweka wazi mambo gani yanayoendelea SNSA? Kuna ugumu gani kunieleza kile mnachokifuatilia? Don’t you trust me? Akauliza Dr Fabian kwa sauti ya ukali kidogo “Ninakuamini mheshimiwa Rais” akajibu Ruby “Kama unaniamini kwa nini unasita kunieleza ukweli wa kile kinachoendelea SNSA?Kwa nini unafanya siri?akaendelea kuuliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninakuomba unipe muda kidogo tu halafu nitakuja kwako na kukueleza kila kitu.Ni mambo mazito kidogo.Kwa mchana huu nimekuja kwako kuomba msaada” akasema Ruby.Dr Fabian akachukua kitambaa akafuta jasho usoni halafu akasema “Ruby naomba nikuweke wazi kwamba sijapendezwa na tabia hii ya kunificha mambo yanayoendelea katika idara yako.Usisahau kwamba mimi ndiye mkuu wa SNSA hivyo napaswa kufahamu kila kinachoendelea katika idara hiyo.Nini unataka nikusaidie?akauliza Dr Fabian “Ninahitaji huyu mwenzangu haa Chloe aunganishwe na vikosi vya jeshi la Marekani vilivyoko hapa nchini.kuna misheni ya muhimu sana tunataka kuifanya”akasema Ruby “Ruby unanipa wakati mgumu sana.Hutaki kunieleza chochote kinachoendelea na wakati huo huo unataka nimuunganishe mwenzako na vikosi vya Marekani vilivyoko hapa nchini.Kuna nini mnataka kukichunguza? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais naomba uniwie radhi tena katika jambo hilo” akasema Ruby na Rais akagonga meza kwa hasira “Ruby nimechoka nawe.Ninawezaje kukusaidia bila kujua kile mnachotaka kukifanya kwa vikosi vya Marekani vilivyoko hapa nchini.Unachotaka nikifanye kinaweza kuharibu mahusiano mazuri yaliyopo baina yetu na Marekani.Tunauheshimu sana mchango wao mkubwa walioutoa.Mara tu vurugu zilipoibuka ni Marekani waliotuma vikosi vyao kwa haraka sana kuja nchini kushirikiana na vikosi vyetu.Unaponitaka nishirikiane nanyi kuweka pandikizi katika vikosi vya Marekani lazima unipe sababu ya msingi ya kufanya hivyo na kama utaendelea na majibu yako ya kunieleza baadae sintakuwa na msaada kwako.Nitakuachia ufanye kazi zako wewe mwenyewe ! akafoka Dr Fabian “Ruby kuna nini?akauliza Nawal ambaye hakufahamu kile walichokuwa wakikizungumza Dr Fabian na Ruby. “Rais anahitaji kufahamu dhumuni la kutaka uingie katika vikosi vya Marekani” akasema Ruby “Hakuna namna Ruby mueleze ukweli” akasema Nawal.Ruby akafungua mkoba wake akatoa faili akalifunua na kutoa picha moja akampatia Rais “Anaitwa Sattar Sayf Al Din.Huyu anatokea kundi la kigaidi la IS na yuko hapa nchini” akasema Nawal na kufungua picha za video akamuonyesha Rais namna Sattar alivyokuwa akishuka katika ndege “Sijakuelewa Ruby.Umesema huyu mtu anatokea kundi la IS lakini hapa ninamuona akishuka katika ndege akiwa ameongozana na maafisa kutoka jeshi la Marekani.Sielewi kinachoendelea hapa ! akasema Dr Fabian “Ndiyo maana nikakuomba mheshimiwa Rais nipe muda kwani jambo hili ni kubwa na yawezekana nikikueleza leo hii usinielewe” akasema Ruby “Make me understand ! akasema kwa ukali Dr Fabian halafu ukapita ukimya mfupi “I’m sorry Ruby nimeshindwa kujizuia kukasirika lakini ninahitaji sana kujua kile kinachoendelea hivi sasa.Kama huyu mtu ni gaidi kwa nini yuko na vikosi vya Marekani? Amekamatwa? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais mtu huyu kama nilivyokueleza ni gaidi na amekuja hapa nchini kwa ajili ya kutekeleza shambulio la kigaidi.Mheshimiwa Rais masanduku mawili uliyomuona ameyabeba wakati akishuka ndegeni yana kirusi ambacho amekuja kukisambaza hapa nchini” “Kirusi? ! DrFabian akastuka “Ndiyo mheshimiwa Rais” “Kirusi cha aina gani hicho? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais naomba na mimi nizungumze kidogo.Kama Ruby alivyonitambulisha kwako ninaitwa Chloe Bennet ninatokea shirika la ujasusi la Marekani CIA.Tulipata taarifa za kuwepo kwa shambulio la kirusi hapa nchini Tanzania ambalo linategemewa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha IS.Mtu ambaye umeonyeshwa na Ruby muda mfupi uliopita ni kweli amekuja hapa nchini kwa ajili ya kutekeleza shambulio hilo.Kwa ufupi tu ni kwamba kirusi hicho ambacho kinatazamiwa kusambazwa ni kirusi hatari cha maangamizi makubwa na kinachoua ndani ya muda mfupi na husambaa kwa njia ya hewa.Mheshimiwa Rais mimi na wenzangu akina Ruby tunataka kuzuia shambulio hilo lisitokee lakini kwa bahati mbaya mtu ambaye amekuja kufanya shambulio hilo anapata hifadhi katika kambi ya vikosi vya jeshi la Marekani ndiyo maana tumekuja kwako kuomba msaada wako ninataka uniunganishe na kamanda mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko hapa nchini ili niweze kuingia katika kambi hiyo kufanya uchunguzi huku nikiwasiliana na wenzangu na kujua mipango yote inayopangwa kuhusiana na usambazaji wa kirusi hicho” akasema Nawal “Mnazidi kunichanganya.Nataka kujua nani hasa anayetaka kusambaza kirusi hicho?Ni gaidi huyu mliyenionyesha au ni wanajeshi wa Marekani? Akauliza Dr Fabian “Kirusi kimepangwa kusambazwa na Sattar ambaye ni gaidi kutoka kundi la kigaidi la IS lakini anapata msaada kutoka kwa vikosi vya Marekani vilivyoko hapa nchini na ndiyo maana umeona katika video tulizochukua kutoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Sattar akipokewa na maafisa kutoka vikosi vya jeshi la Marekani walioko hapa nchini” akajibu Nawal “Nini hasa sababu ya kutaka kusambaza virusi hivyo?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais suala hili ni pana sana na ndiyo maana ninaendelea kusisitiza nipe muda nitakuja kwako na maelezo kamili ya kila kinachoendelea hapa nchini lakini kwa leo ninataka unisaidie hicho tulichokuomba.Ninataka kumpandikiza Chloe katika kambi ya vikosi vya Marekani ili aweze kuchunguza na kujua mahala alipo Sattar na kirusi alichokuja nacho” akasema Ruby “Ruby ninashindwa nifan…..” akasema Dr Fabian lakini Ruby akamkatisha “Mheshimiwa Rais ninaomba uniamini katika hili.Najua kuna mambo mengi bado uko gizani na nitakuja hapa kwako kukueleza kila kitu lakini naomba kama hujawahi kuniamini basi niamini katika hili.Nchi iko katika hatari kubwa na ndiyo maana mimi na wenzangu tumeamua kufanya jambo hili la hatari kubwa kwa ajili ya kuiepusha nchi na hatari iliyopo.Tunakuomba sana msaada wako mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Nini unataka nikifanye?akauliza Dr Fabian baada ya kutafakari kwa muda,Ruby akamuelekeza namna walivyoupanga mpango ule na kitu gani anatakiwa kufanya Dr Fabian. Baada ya kupewa maelekezo ya kile anachotakiwa kukifanya bila kupoteza muda Dr Fabian akachukua simu akampigia simu waziri wa ulinzi na kumpa maelekezo kwamba anamuhitaji mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko nchini Tanzania haraka sana pale ikulu ana mazungumzo naye. DAKIKA ISHIRINI BAADAE Helkopta ya jeshi la Marekani iliyombeba Jeneral William Marshall mkuu wa vikosi vya jeshi la Marekani vilivyoko nchini Tanzania,ilitua katika viwanja vya ikulu jijini Dare s salaam.Hii ni kufuatia ombi la Rais la kutaka kuonana na mkuu huyo. Jenerali William akashuka katika helkopta akapokewa na walinzi wa Rais wakamuongoza kuelekea ndani kwa ajili ya kukutana na Rais.Akiwa amevaa sare za jeshi la Marekani alikaribishwa sebuleni na baada ya dakika kadhaa rais Dr Fabian akajitokeza akiwa ameongozana na Nawal.William akasimama na kutoa salamu ya kijeshi kwa Rais kisha Rais akampa mkono na kumkaribisha. “Ahsante sana kwa kufika kwa haraka Jenerali William baada ya kupokea wito wangu” akasema Dr Fabian “Nimeelekezwa na waziri wa ulinzi wa Tanzania ambaye tunawasiliana mara kwa mara kwamba unanihitaji mara moja hivyo nikalazimika kuacha kila nilichokuwa nakifanya nije nikusikilize mheshimiwa Rais” akasema Jenerali William “Karibu sana Jenerali William.Kwanza kabisa ninataka kujua maendeleo ya vikosi vya Marekani hapa nchini.Mnaendeleaje na majukumu yenu? “Tunaendelea vizuri sana mheshimiwa Rais tukishirikiana na vikosi vya Tanzania na kwa kiasi kikubwa ninaweza kusema kwamba tumefanikiwa kudhibiti vurugu.Kwa sasa tunaendelea na doria za ardhini na angani kuhakikisha hakuna tena makundi yoyote yanayoleta uvunjifu wa amani” akasema William “Tunawashukuru sana William kwa kazi kubwa mliyoifanya ya kuhakikisha amani inarejea nchini.Hata hivyo kuna jambo lingine nimekuitia hapa mchana huu” akasema DrFabian na kumgeukia Nawal “Anaitwa Chloe Bennet ni raia wa Marekani ambaye anajishughulisha na upigaji wa picha na wakati machafuko yalipoanza alikuwa katika mbuga ya Serengeti akipiga picha na akajikuta akinasa kati kati ya mapigano.Alitekwa na kundi la vijana akashikiliwa yeye na wenzake wanne raia wa Kenya hadi jana walipokombolewa na vikosi vya jeshi na kuletwa hapa Dar es salaam.Nimekuita ili nimkabidhi kwako uhakikishe usalama wake kwa wakati huu ambapo hakuna ubalozi.Nilitaka kumsafirisha kurejea Marekani lakini Chloe akaniomba aendelee kubaki Tanzania kwani anategemea kuendelea na zoezi lake la upigaji wa picha pale vurugu zitakapokuwa zimemalizika.Ninamkabidhi kwako uhakikishe anakuwa salama na pale vurugu zitakapokuwa zimemalizika basi ataendelea na kazi zake” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninakushukuru sana kwa msaada mkubwa uliomsaidia huyu mwenzetu nakuahidi atakuwa salama katika usimamizi wangu hadi pale vurugu zitakapokoma kabisa” akasema William “Chloe nakutakia mapumziko mema na pale utakapokuwa tayari kwenda kuendelea na shughuli zako za upigaji picha njoo uniage tafadhali na ninakuhakikishia kwamba vifaa vyako vyote vilivyopotea nitavigharamia utapata vipya” akasema Dr Fabian Nawal akasimama akamfuata “Nakushukuru sana mheshimiwa Rais kwa msaada mkubwa ulionipatia.Ninakuhakikishia kwamba nitakapokuwa tayari kwenda kuendelea na shughuli zangu nitakuja kukuaga” akasema Nawal akimshukuru Rais halafu akaenda kusalimiana na William Rais akawaaga wakaondoka kuelekea katika helkopta ya jeshi la Marekani wakaingia helkopta ikapaa na kuondoka maeneo ya ikulu.Dr Fabian akamfuata Ruby aliyekuwa katika sebule nyingine “Tayari nimetekeleza ulivyoniomba na mwenzako amekwisha ondoka na mkuu wa vikosi vya Marekani vilivyoko hapa Tanzania.Ruby mna uhakika na hiki mnachotaka kukifanya?Akauliza Dr Fabian “Ninakushukuru sana mheshimiwa Rais kwa kutusaidia jambo hili.Hii ni njia pekee ya kutuwezesha kuingia katika kambi ya jeshi la Marekani na kumfuatilia Sattar na kuzuia mpango wa kusambaza kirusi hapa Tanzania” akasema Ruby “Ruby nataka kufahamu kwa kina kuhusiana na hiki kirusi.Mna hakika kweli kuna kirusi kinataka kusambazwa hapa nchini? Akauliza Dr Fabian “Kirusi kipo kweli mheshimiwa Rais na tunaendelea kukifuatilia ili kuzuia mpango wa kukisambaza” akajibu Ruby “Ruby hili si jambo la kufanyia mchezo.Kama una uhakika kuna kirusi hatari ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa hapa nchini tunatakiwa kuanza kujiandaa ili pale mpango wenu wa kuzuia kisisambazwe ukishindwa kufanikiwa tuwe na uhakika wa kuwakinga watu wetu” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kwa sasa suala hili litabaki siri yetu na hatakiwi mtu mwingine yeyote kufahamu kwani inaweza kuzuka taharuki kubwa na kuvuruga uchunguzi wetu.Ninakuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha kirusi hicho hakisambazwi hapa Tanzania” akasema Ruby “Ruby ninataka kufahamu je vikosi vya Marekani vinahusika katika jambo hili? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kama nilivyokueleza awali kwamba hili ni jambo pana lakini nitakuja kukueleza kila kitu.Naomba nipe muda ninakuahidi nitakuja nikiwa na maelezo ya kutosha kuhusiana na jambo hili” akasema Ruby lakini Dr Fabian akaonekana bado ana wasiwasi mwingi.Baada ya ukimya mfupi akasema “Ruby umenitaka nikuamini katika suala hili na mimi ninalazimika kufanya hivyo lakini tambua ya kwamba maisha ya watanzania yako mikononi mwako hivyo kwa namna yoyote ile mpango huo wa kusambaza kirusi katika ardhi yetu haupaswi kufanikiwa.Umenielewa Ruby?akauliza Dr Fabian “Nimekuelewa mheshimiwa Rais”akajibu Ruby huku Dr Fabian akimtazama kwa wasiwasi “Ruby please swear to me that you won’t let them win ! akasema Dr Fabian.Ruby akavuta pumzi ndefu na kusema “Mr President I swear I wont let them win ! akasema Ruby “Ahsante sana kwa kunihakikishia hilo Ruby.Narudia tena kukusisitiza kwamba maisha ya watanzania yapo mikononi mwako.Kama kuna msaada wowote utauhitaji muda wowote hata kama ni vikosi vya jeshi nitaarifu na mimi nitakusaidia” “Ahsante sana mheshimiwa Rais nitafanya hivyo” akasema Ruby kisha akaagana na Dr Fabian akaondoka kurejea katika ofisi zao
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment