Simulizi : Siri: Jasusi/Gaidi
Sehemu Ya Pili (2)
Timu ya watu wa SNSA walioko jijini Tanga iliwasili kaika nyumba ambayo kumbu kumbu zinaonyesha ndiko alipokuwa Denis Sambale mara ya mwisho alipotumia simu yake kwa mawasiliano.Walipofika mahala walipoelekezwa walipatwa na mshangao baada ya kukuta nyumba hiyo ikiwa imeteketea kwa moto na kubaki gofu.Kila kilichokuwamo ndani ya nyumba hiyo kiliteketea Kwa mujibu wa uchunguzi wa SNSA,ilibainika kwamba mtu wa mwisho Denis kuwasiliana naye alikuwa ni Augustin Kawala ambaye naye simu yake haikuwa inapatikana.Timu ya watu wa SNSA walielekea mahala alipokuwapo Augustin mara ya mwisho alipotumia simu yake.Nyumba ilikuwa na geti lililofungwa kufuli kwa nje kuashiria kwamba hakukuwa na mtu ndani.Wakavunja kufuli na kuingia ndani ya nyumba ile.Mara tu walipouvunja mlango wa sebuleni walikutana na harufu kali ya uozo.Kwa tahadhari kubwa wakafuatilia harufu ile ilikotoka na kukuta katika chumba kimoja mwanamke mmoja akiwa amelala kitandani akiwa tayari ameanza kuharibika.Kifuani alikuwa amechomwa na kisu kikubwa.Ilionekana kulikuwa na ugomvi kabla ya mwanamke Yule kuuawa kwani vitu vilitawanyika hovyo mle chumbani.Kwa tahadhari kubwa kiongozi wa timu ile ya SNSA akabandika karatasi Fulani katika mpini wa kisu na kuibandua kisha akaimulika kwa tochi na zikaonekana alama za vidole zilizokuwa katika mpini ule wa kisu. Katika uchunguzi wao walikuta kuna picha kadhaa zikimuonyesha mtu aliyevaa mavazi ya kichungaji zikiwa zimebandika ukutani na katika picha nyingine alionekana mwanamke Yule aliyeuawa akiwa na Yule mchungaji ilikuwa ni siku ya harusi yao.Walikusanya kila walichoona kingeweza kuwafaa kisha wakaondoka kurejea katika ofisi yao.Karatasi ile iliyokuwa na alama za vidole kutoka katika ule mpini wa kisu alichochomwa Yule mwanamke waliyemkuta katika nyumba ya Augustin Kawala ikaingizwa katika kompyuta na alama zile zikatumwa ofisi kuu ya SNSA Dar es salaam.
Katika chumba cha mipango ofisi kuu ya SNSA Dar es salaam,Ruby akiwa na Gosu Gosu msaidizi wake pamoja na viongozi kadhaa wa idara mbali mbali zilizomo ndani ya SNSA walikutana kufuatia ripoti waliyoipata kutoka kwa watu wao walioko Tanga. “Muda mfupi uliopita nimepokea taarifa kutoka Tanga.Tuliwaelekeza watu wetu kule kumfuatilia Denis Sambale lakini walipofika katika nyumba ambayo tunaamini ni makazi yake walikuta nyumba hiyo ikiwa imeteketea kwa moto” akasema Ruby na kuwaonyesha picha katika runinga kubwa za namna nyumba ile ilivyoteketea na kubaki gofu “Denis Sambale mara ya mwisho aliwasiliana na Augustin Kawala,watu wetu wakamfuata huyo Augustin ambaye naye simu yake haipatikani na walipofika katika nyumba ambayo alikuwepo alipowasiliana na Denis watu wetu wamekuta nyumba ikiwa imefungwa wakavunja mlango wakaingia ndani na hiki ndicho walichokikuta” akasema Ruby na kuwaonyesha picha za Yule mwanamke aliyekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani “Watu wetu walichukua alama za vidole kutoka katika mpini wa kisu alichochomwa mwanamke huyo .Watu wa idara ya alama wamezifanyia kazi alama hizo na haya ndiyo majibu waliyoyapata.Katika alama zilizokutwa kwenye hicho kisu kuna alama za vidole za mtu huyu hapa” akasema na kubonyeza kitanza mbali na picha ikajitokeza “Augustin Kawala.Huyu ni mchungaji anayemiliki kanisa la ngome ya ushindi.Katika alama hizo pia zimekutwa alama za mtu huyu hapa” akasema na katika runinga ikatokea picha ya mwanamke “Anaitwa Paulina Kawala.Huyu ni mke wa Augustin Kawala.Katika picha zilizotumwa na watu wetu wa Tanga ipo picha inayoonyesha Augustin na Paulina siku ya harusi yao.Kufuatia kukutwa kwa alama za vidole za Augustin katika mpini wa kisu alichochomwa Paulina inaonyesha wazi kwamba huyu jamaa anahusika katika mauaji ya mke wake.Hii ndiyo hali iliyokutwa chumbani” akasema Ruby na kuonyesha picha za namna vitu vilivyovurugika chumbani. “Inaonekana kulikuwa na ugomvi chumbani na kisha Paulina akachomwa kisu.Mtu wa kwanza ambaye tunamuhisi kuhusika na mauaji hayo ni Augustin Kawala.Hatujui mahala alipo na simu yake imezimwa.Kuna kitu kimoja ambacho naamini mmekigundua katika zoezi hili tulilolifanya leo.Tukianza kwa Karim,ametoweka na hatujui yuko wapi.Mtu wa mwisho kuwasiliana naye ni Denis Sambale akiwa jijini Tanga.Huyu naye hajulikani alipo na nyumba yake imeteketea kwa moto.Denis naye mtu wa mwisho kuwasiliana naye ni Augustin Kawala huyu naye ametoweka hatujui alipo ila tunaamini huyu alimuua mkewe na akakimbia.Wote hawa mawasiliano yao ya mwisho yamefanywa siku ambayo machafuko yalianza jijini Tanga na wote simu zao hazipatikani.Binafsi nalazimika kuamini huu ni mtandao ambao una malengo Fulani na ninahisi unahusika kwa namna moja au nyingine na haya machafuko” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Nilipewa orodha ya watu ambao waliwasiliana na Karim wiki moja kabla ya machafuko kuanza.Katika orodha hiyo kuna mwanasiasa mmoja wa Uganda anaitwa Joshua Lulangwa.Nitazungumza na Rais ili aombe msaada kwa mamlaka za Uganda kuweza kupata taarifa za kuhusiana na huyu mtu.Wakati tukisubiri msaada huo kutoka kwa wenzetu wa Uganda sisi tutaendelea kuwafuatilia watu wote walioko katika orodha hii ya watu ambao Karim aliwasiliana nao na tutamfahamu kila mmoja wao na kuchunguza kama ana mahusiano yoyote na vurugu hizi.Hakuna kufumba jicho hadi pale tutakapopata chanzo cha vurugu hizi ambazo binafsi ninahisi wanasiasa wanaweza kuhusika” akasema Ruby.Tayari ni saa kumi na mbili kasoro za jioni akampigia simu Rais akamjulisha kwamba atakwenda kuonana naye jioni ile WASHINGTON DC – MAREKANI Inakaribia saa saba za mchana wakati ndege iliyowabeba Habiba Jawad na Mathew Mulumbi ilipowasili katika anga la jiji la Washington DC.Ni safari iliyowachukua takribani saa kumi na nne kutoka Riyadh. “Mathew imekuwa ni safari ndefu sana na tunakaribia kutua lakini kuna kitu kimoja nataka kukufahamisha kabla ndege haijagusa ardhi” akasema Habiba “Nakusikiliza mama” “Sikupaswa kukwambia lakini wewe ni kijana wangu hivyo lazima nikwambie ili ujiandae.Hawa watu hawakuamini” “Akina nani? akauliza Mathew “Hawa tunaokwenda kuonana nao”akajibu Habiba “Wana haki ya kuwa na wasi wasi nami kwani hawanifahamu na ni mara ya kwanza tunakutana mimi na wao hivyo hali kama hiyo lazima itokee”akasema Mathew “Sikiliza Mathew.Tutakaposhuka watakuchukua na kwenda kukupima.Show them who you are ! “Watanipimaje?akauliza Mathew “Sifahamu lakini lazima upimwe hivyo waonyeshe wewe ni nani.waonyeshe uwezo wako wote ! akasema Habiba lakini Mathew hakuonekana kumuelewa “Mama nashindwa kukuelewa” “Mathew sina muda wa kukufafanulia.Sikiliza kile ninachokwambia na ujiandae kwani sikupaswa hata kukueleza chochote kuhusiana na suala hili.Hakikisha hawagundui kuwa umejiandaa” akasema Habiba “Mama ni ak…………….” Akataka kusema kitu Mathew lakini Habiba akamzuia “Mathew sihitaji maswali.Tunakaribia kutua jiandae” akasema Habiba Ndege ilitua katika uwanja wa kijeshi wa Bollling Airface Base. “Mathew good lucky” akasema Habiba na kuinuka Mathew akachukua sanduku lake akamfuata Habiba wakaanza kutoka nje.Habiba Jawad alikuwa wa kwanza kushuka ndegeni huku Mathew akimfuaa nyuma yake. Kulikuwa na watu watano wakiwa katika mavazi ya suti na wengine wanne walikuwa katika mavazi ya kijeshi.Wanajeshi wawili wakamsogelea Mathew na kumtaka asubiri .Habiba Jawad aliyekuwa ameogozana na watu wanne akageuka akamtazama Mathew kisha akaingia katika mojawapo ya magari manne yaliyokuwepo pale uwanjani na magari mawili yakaondoka yakabaki mawili.Baada ya Habiba Jawad kuondoka Mathew akaelekezwa kushuka ndegeni akaongozana na wale wanajeshi wanne ambao wawili kati yao walikuwa na silaha wakaelekea katika gari.Mlango wa pembeni wa gari lile ukafunguliwa na Mathew akatakiwa kuingia kisha magari yakaondoka bila Mathew kuelezwa chochote “Mnaweza mkanieleza tunakoelekea? Akauliza Mathew lakini hakuna aliyemjibu Walikatisha mitaa kadhaa ya jijila Washington halafu wakaingia katika nyumba moja ambayo kuta zake zote zilikuwa zimeeneza majani ambayo huota kufuata ukuta.Nyuma yote ilikuwa ya kijani kufuatia rangi ya majani yale isipokuwa bati ambalo lilikuwa jekundu.Mathew akatakiwa kushuka garini akaongozwa na wanajeshi wale wanne kuingia ndani.Mlangoni kulikuwa na jamaa mmoja aliyekuwa ameva suti nzuri ya rangi ya bluu akafungua mlango na wanajeshi wawili wakatangulia ndani Mathew akafuata nyuma yao kisha wanajeshi wale wawili wakafuata nyuma ya Mathew pamoja na jamaa wengine watano. “Hapa ni wapi? Yule mama niliyekuja naye ndegeni yuko wapi?akauliza Mathew akionyesha wasiwasi “Tulia na fuata kile utakachoelekezwa” akasema jamaa mmoja halafu akaenda chumbani na kurejea na nguo akamtaka Mathew avue mavazi yake na avae nguo zile alizomletea. “Ninapelekwa wapi?akauliza Mathew “Nimekwambia fanya kile nilichokuelekeza.Vua mavazi yako na uvae mavazi haya” Mathew akashika nguo zile akazikunjua akazitazama “Sikiliza Mathew.Tutakaposhuka watakuchukua na kwenda kukupima.Show them who you are ! Mathew akayakumbuka maneno aliyoambiwa na Habiba Jawad,akazitupa chini zile nguo. “Sivai mavazi hayo hadi mtakaponieleza wapi mnataka kunipeleka ! akasema Mathew na wale jamaa wakatazamana “Tafadhali ndugu vaa mavazi hayo uliyopewa,usijitafutie matatizo”Mathew akaelekezwa “Nimesema sivai mavazi yenu hadi mtakaponieleza wapi mnanipeleka ! akasema Mathew “Hii ni mara ya mwisho nakuomba ndugu vua hayo mavazi uliyovaa na vaa mavazi haya uliyoelekezwa kuvaa ! akafoka mmoja wa wale jamaa aliyekuwa amevaa suti ya kijivu “Hivi ndivyo mnavyowatendea wageni wanaokuja kutembelea nchi yenu?Kwa nini mmenileta hapa?Nimefanya kosa gani? Kuna sheria ya Marekani nimevunja? Akauliza Mathew kwa ukali na wale jamaa hawakumjibu “Hamtaki kunijibu? Akauliza tena Mathew “Kama hamna jibu la kunipa naomba tafadhali mniache niende zangu kabla ubalozi wangu haujaanza kunitafuta ! akasema Mathew na jamaa aliyevaa suti ya kijivu akawapa ishara wale wanajeshi “Hebu mkaribisheni Marekani ! akasema Yule jamaa na wanajeshi wawili ambao walikuwa wamejaza mikono yao wakamsogelea Mathew.Mmoja wa wale wanajeshi akamtandika kichwa Mathew akaenda chini akahisi nyota kwa kichwa kile kizito. “Waonyeshe wewe ni nani.Waonyeshe uwezo wako wote ! Mathew akayakumbuka tena maneno ya Habiba Jawad akiwa ameanguka chini Akiwa pale chini mmoja wa wale wanajeshi akainua mguu wake kwa lengo la kumkanyaga lakini tayari Mathew alikwisha kiona kitendo kile akaukwepa mguu wa Yule mwanajeshi ambao ulipiga ardhi kwa kishindo na Mathew akajigeuza na kumkata mtama Yule mwanajeshi akaanguka mzima mzima sakafuni na kutoa kishindo.Kwa kutumia miguu yake akaibinua meza ndogo iliyokuwa karibu yake akaidaka na kisha akasimama kwa kasi na kumpiga nayo mmoja wa wale wanajeshi ikampeleka chini.Jicho la Mathew lililogeuka kama kinyonga lilimuona mwanajeshi mmoja akimjia nyuma yake akageuka na kumtandika teke zito la uso halafu akapanda juu ya sofa na kumrukia mwanajeshi wa nne mateke mawili mfululizo kifuani akaanguka chini.Yule mwanajeshi aliyepigwa na meza ndogo tayari alikwisha inuka na mkononi alikuwa ameshika ubao uliotoka katika ile meza aliyopigwa nayo na kwa nguvu akaurusha ubao ule kumuelekea Mathew lakini tayari alikwisha uona ule ubao akaukwepa ukampiga jamaa aliyekuwa amesimama akishuhudia wanajeshi wao wakitembezewa kipigo kikali.Baada ya kumkosa na ule ubao Yule mwanajeshi ambaye tayari alikwisha pandwa na hasira akaruka mzima mzima kutaka kumvamia Mathew mahala alipokuwa amejibanza lakini Mathew alikuwa mwepesi zaidi yake akaruka juu na kumuwahi Yule jamaa akiwa juu na kumtandika teke zito la kifua na kumfanya Yule jamaa aanguke kama furushi.Mathew akajigeuza na kutua nyuma ya Yule jamaa aliyepigwa na ubao ambaye alikuwa amepiga magoti damu ikimtoka mdomoni akamkaba kabali kwa mkono wake wa kushoto halafu akaiokota bastora ya Yule jamaa iliyoanguka pembeni akamuwekea kichwani. “Wote inue mikono juu ! Mathew akawaamuru wale jamaa waliovaa suti ambao wote walikuwa wameshika bastora zao wakimuelekezea. “Namaanisha ninachokisema wote inueni mikono juu ! akasema Mathew kwa ukali lakini wale jamaa bao waliendelea kumuelekezea bastora “Nitahesabu hadi tatu kama hamtatii nitamtandika mwenzenu risasi..Moja ! Mathew akaanza kuhesabu “Mbili ! akaendelea “Fanyeni anachowaelekeza ! akasema Yule jama aaliyekabwa kabali ambaye alikuwa anapata taabu kuvuta pumzi. “Wekeni silaha zenu chini na muinue mikono juu ! akaamuru Mathew na taratibu wale jamaa wakaziweka chini bastora zao na kuinua mikono juu kama walivyokuwa wameelekezwa “Wewe inuka ! Mathew akamuelekezea bastora mmoja wa wanajeshi akamtaka ainuke akaziokote zile bastora na kumsogezea karibu.Yule mwanajeshi akafanya alivyoelekezwa akaziokota bastora na kumsogezea Mathew halafu akamtaka kuchukua pingu kutoka katika suti zao na kuwafunga mikono.Mwisho akamtaka Yule mwanajeshi ajifunge pingu yeye mwenyewe.Wanajeshi wengine watatu hali zao hazikuwa nzuri wawili walikuwa wamepoteza fahamu na mmoja alikuwa anatoka damu mdomoni.Mathew alipohakikisha wote wamefungwa pingu akampiga Yule jamaa pigo kichwani akaanguka na kupoteza fahamu akachukua bastora mbili akazifutika kiunoni halafu akatoka mle ndani akaufungua mlango wa mojawapo ya gari akaingia ndani akaliwasha. “Ninaelekea wapi?akajiuliza “Nitajua pa kuelekea ngoja kwanza niondoke mahala hapa” akawaza Mathew na kugeuza shingo akatazama nyuma ili kugeuza gari lakini akasikia muunguruo wa helkopta iliyofikan a kusimama juu ya ile nyumba.Mara akasikia mivumo ya risasi na gari ikabonyea chini matairi yote yalipigwa risasi. “Bastard ! akafoka Mathew huku akiupiga usukani kwa hasira na kutokea upande wa pili ikatokea tena helkopta ya pili ambayo kama ile ya kwanza mlangoni alikuwepo jamaa aliyekuwa na bunduki kubwa.Wakati Mathew akitafakari geti likafunguliwa na gari mbili zikaingia.Mathew akaelekeza macho ukutani na kuwaona watu wanne wenye bunduki wakiwa wamezielekeza kwake.Wale jamaa walioingia na magari wakashuka na mmoja wao akatumia kipaaza sauti kumtaka Mathew ashuke garini. “Sina ujanja,siwezi kutoka salama mahala hapa.Wako wengi na wamejizatiti kwa silaha” akawaza Mathew na kufungua mlango wa gari.Bunduki zote zikaelekezwa katika lie gari.Akatoa mguu akaushusha chini taratibu,akatoa na mwingine halafu akatoa mkono wa kwanza akauonyesha ukiwa mtupu akatoa na mkono wa pili akauonyesha ukiwa mtupu halafu akashuka garini na kuinua mikono juu.Haraka haraka na kwa tahadhali watu wanne wakamsogelea na kuanza kumpeua hakuwa na bastora zote aliziacha garini,akafungwa mikono kwa pingu na kufunikwa mfuko kichwani akaingizwa garini na kuondoka eneo lile.
Gari lilisimama mlango ukafunguliwa na Mathew akashushwa.Watu wale walifanya mambo yao kimya kimya bila maongezi hivyo hakujua kulikuwa na watu wangapi eneo lile lililokuwa na ukimya mkubwa.Aliingizwa katika jumba lililokuwa na ubaridi mwingi.Mlango wa mojawapo ya chumba katika jumba lile ukafunguliwa na Mathew akaingizwa ndani ya chumba hicho akaketishwa kitini halafu akafunguliwa pingu alizokuwa amefungwa mikononi akafungwa katika pingu nyingine zenye mnyororo zilizounganishwa na chuma kilichokuwa juu ya meza akaachwa hapo na watu wale wakaondoka. “Nini wanataka kukihakiki kwangu hawa jamaa ambao Habiba amesema wananifanyia majaribio? Ngoja nifuate maelekezo ya Habiba kwamba niwaonyeshe mimi ni nani” akawaza Mathew Ndani ya chumba kimoja kizuri katika jengo moja lililokuwa kati kati ya jiji la Washington watu tisa walikuwa wameyaelekza macho yao katika runinga kubwa wakifuatilia kile kilichokuwa kinaonekana pale runingani.Katika runinga ile alionekana Mathew Mulumbi akiwa ndani ya chumba alimofungwa akiwa na mfuko kichwani Mathew aliinamisha kichwa upande mmoja na alionekana kama vile anauma kitu kwa meno yake.Baada ya dakika tatu akainamisha kichwa mezani na kusogeza kiganja cha mkono karibu na mdomo akachukua kitu ambacho hakikuweza kuonekana vizuri halafu akaanza kuchokonoa pingu ya mkono wa kushoto ikafunguka akavua ule mfuko aliofunikwa kichwani halafu akaifungua na ile ya mkono wa kulia akawa huru. “Habiba huyu jamaa ni Gaidi au ni jasusi?akauliza Edward Murphy “Huyu ni gaidi” akajibu Habiba “Anafanya mambo ya kushangaza ambayo magaidi wengi hawawezi kuyafanya.Umemtoa wapi huyu?akauliza Robin Ross.Kabla Habiba hajajibu Mathew akaelekea mlangoni wote wakayaelekeza macho runingani kutazama anachotaka kukifanya.Mathew akauchunguza ule mlango akagundua ni mlango unaofunguliwa kwa kutumia kadi ya kielektroniki.Akavua kiatu chake cha mguu wa kulia akang’oa kisigino halafu akang’oa kipande cha chuma kisha akatoa bisibisi ndogo na vitu vingine vidogo vidogo.Wote mle ndani ya chumba wakabaki wanashangaa Mathew akafungua sehemu ya kupitisha kadi ya kielektroiki ya kufungulia ule mlango.Kulikuwa na nyaya kadhaa katika kiboksi kile akazichunguza halafu akakunjua kisu kidogo sana ambacho alikitoa katika kisigino cha kiatu akakata nyaya kadhaa akazichuna na kuunganisha na mara mlango ukafunguka “Yawezekana wakawa wananitazama muda huu ninachokifanya.Hizi ni salamu zao” akawaza Mathew halafu akatoka ndani ya kile chumba akafuata varanda hadi alipokuta mlango uliokuwa umefungwa kwa nje.Pembeni yake kulikuwa na chumba ambacho mlango wake ulikuwa wazi.Akaingia ndani ya kile chumba mara mlango wa kile chumba ukajifunga halafu akasikia hatua za mtu akisogelea ule mlango wa kile chumba alimo akajiandaa kukabiliana na yeyote atakayeingia mle na mara akaona moshi ukipenya chini ya mlango.Taratibu akaanza kuhisi macho yanapoteza nguvu ya kuona akaanguka chini na kupoteza fahamu
Mathew alirejewa na fahamu na kujikuta akiwa amelazwa kitandani.Ndani ya chumba kile kizuri kulikuwa na akina dada wawili warembo wakiwa wameketi katika sofa lililokuwamo mle chumbani.Taratibu akajiinua na kukaa wale akina dada wenye tabasamu murua wakamsogelea na kuketi kitandani mmoja wao akamsugua sugua mgongoni “Pole sana.Unajisikiaje sasa? Kuna sehemu yoyote inauma?akauliza Yule mwanadada kwa sauti nyororo “Kichwa kinaniuma sana” akajibu Mathew na Yule mwanadada akampa vidonge viwili akameza. “Naitwa Sophia mwenzangu anaitwa Emily.Wewe jina lako nani? Akauliza Sophia aliyeonekana mzungumzaji sana “Abu Zalawi” “Abu Zalawi karibu sana Washington DC.Pole kwa yote yaliyotokea na sasa nakuomba uingie bafuni ukaoge halafu tuondoke” “Mnanipeleka wapi? “Sikiliza Abu Zalawi tumepewa maelekezo utakapozinduka tukupeleke sehemu hivyo tusipoteze muda oga vaa mavazi pendeza” akasema Sophia na Mathew akaingia bafuni akaoga kisha akatoka na kukuta kuna suti nzuri nyeusi kitandani pamoja na viatu vizuri vyeusi akavaa.Hakuwa na haja ya kujitazama katika kioo kwani suti ile ilimkaa vyema.Akagonga mlango Sophia na Emily wakaingia. “Mbona hujavaa tai?akauliza Sophia “Sipendelei kuvaa tai” “Sogea hapa karibu” akasema Sophia na kumfungia Mathew tai kisha akampa mfuko ili auvae kichwani.Sura ya Mathew ikabadilika “Najua hupendi Abu Zalawi lakini lazima uvae.Hizi ndizo taratibu” akasema Sophia “Tafadhali vaa Abu Zalawi” akasisitiza Sophia na Mathew akauvaa mfuko ule wakamuongoza kutoka ndani ya ile nyumba hadi katika gari wakaondoka Baada ya mwendo wa dakika zaidi ya thelathini hatimaye gari ikasimama na milango ikafunguliwa Mathew akashushwa na akahisi kuna mikono mizito ya mwanaume ikimkamata mkono wake na kumuongoza kuelekea ndani.Waliingia katika lifti kisha wakashuka na kutembea kidogo akasikia mlango ukifunguliwa wakaingia ndani ya chumba na Mathew akaenda kuketishwa kitini halafu akatolewa ule mfuko kichwani.Ndani ya chumba kile kikubwa na kizuri kulikuwa na meza kubwa ya duara na watu wasiopungua kumi na tano walikuwa wameizunguka meza ile na mmoja wao alikuwa ni Habiba Jawad.Mathew akashusha pumzi baada ya kumuona Habiba “Abu Zalawi napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha sana Washington DC” akasema mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la David Walker. “Ahsante” akajibu Mathew. “Kuna mambo yametokea ambayo yamekushangaza.Ulichukuliwa uwanja wa ndege na kupelekwa mahala usipopafahamu na hukujua kwa nini.Kilichotokea ni utaratibu wetu wa kuwapokea wageni wanaofika kwa mara ya kwanza na vile vile tulikupitisha katika mtihani mdogo kupima uwezo wako.Kila mtu ambaye huwa na ana mahusiano na sisi hupimwa uwezo wake katika mambo mbali mbali.Wengine huwapeleka gerezani au katika nyumba za mateso kuwapima namna wanavyoweza kukabiliana na hali ngumu.Kwako pia ilipangwa iwe hivyo lakini kwa umahiri uliouonyesha nina furaha kukujulisha kwamba umefaulu jaribio kwa alama za juu sana.Mambo uliyotuonyesha hatukuwa tena na ulazima wa kuendelea na zoezi la kukupima.Karibu sana Washington DC” akasema David Walker na Mathew akainamisha kichwa kushukuru “Namshukuru sana Habiba kwa kunijulisha mapema kile walichokipanga hawa jamaa” akawaza Mathew “Abu Zalawi kabla ya yote napenda nimpe nafasi Habiba Jawad afanye utambulisho kisha atoe maelezo machache.Karibu Habiba Jawad” akasema David Walker na Habiba jawad akasimama “Ahsante David” akasema Habiba na kumtazama Mathew “Kwanza kabisa Abu nataka uwafahamu watu walioko humu ndani kwa majina yao.Tukianzia na mwenyekiti pale anaitwa David Walker yeye tayari amekwisha jitambulisha.Anayefuata mkono wake wa kulia ni Richard Smith,anafuata John Hill,anafuata David Carter,Robert Baker,James Campbell,Michael Torres,Donald Cooper,Brian Watson.Tukirudi kwa upande wake wa kushoto tunaanza na Jason Brooks,Eric Wood,Jeffery Jenkins,Carl Henderson,Terry Hughes,Willie Simmons ,Wayne Sullivan,Edward Murphy na Robin Ross”Habiba akanyamaza “Baada ya kuwatambua watu hawa walioko mbele yako sasa nageukia upande wa pili.Aliyeko mbele yenu anaitwa Abu Zalawi.Huyu asili yake ni nchini Misri lakini kwa sasa ni raia wa Saudi Arabia.Anatokea katika kundi la Ammar Nazari brigades ambalo nimekuwa nikilifadhili pia.Kutokana na umahiri wake ninamtumia kama msaidizi wangu na leo hii nimekuja kumtambulisha kwenu rasmi mumfahamu na kumkabidhi majukumu.Ninamuamini Abu Zalawi.Ni mtu ambaye ni mtiifu kwangu na amenisaidia mambo mengi.Naamini nanyi pia mtamuamini kama mnavyoniamini mimi.Mlichokiona leo hii ni sehemu ndogo tu ya uwezo mkubwa alionao Abu Zalawi.Ni mtu sahihi kwa kazi ambayo mnataka kumtuma.Sina mashaka naye hata kidogo” akasema Habiba akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Abu Zalawi naamini unajiuliza kwamba http://deusdeditmahunda.blogspot.com/hawa walioko mbele yako ambao nimewatambulisha kwako ni akina nani?kwa nini tumekuja hapa?Sikukueleza chochote kuhusiana na safari yetu hii lakini leo ni wakati muafaka wa kuufahamu ukweli” akanyamaza halafu akaendelea “Unanifahamu kama mfadhili mkubwa wa makundi mbali mbali ya kigaidi hasa kundi la IS.Naamini umekuwa unajiuliza na si wewe peke bali watu wengi nahata wale ambao ninawafadhili kwamba ninafaidika na nini ninapofadhili ugaidi?Hakuna chochote ambacho ninakipata kutoka kwa magaidi lakini nimekuwa nikitoa mabilioni ya fedha kwa makundi mbali mbali na kufadhili operesheni zao mbali mbali za kigaidi.Ukweli ambao wewe na wengine wote hamuufahamu ni kwamba timu hii unayoiona ndani ya chumba hiki ndiyo inayofanikisha kila kitu.Mimi ninafanya kazi kwa niaba ya timu hii.Wao ndio walioniwezesha kiuchumi na kuwa tajiri mkubwa na utajiri huo ndio ninaoutumia kufadhili makundi ya kigaidi” akasema Habiba na kumtazama Mathew. “Nadhani umestuka sana kusikia kwamba Marekani wanafadhili kundi la IS na makundi mengine ya kigaidi.Kuna chochote unataka kukisema? Akauliza Habiba huku akitabasamu.Mathew akakohoa kidogo halafu akasema “Nimestuka sana.Sikuwahi kufikiri kitu kama hiki.Sikuwahi kufikiri hata siku moja kama Marekani wanaweza wakafadhili makundi ya kigaidi.IS wamekuwa wakifanya mashambulio mbali mbali duniani na kupelekea vifo vya watu wengi na Marekani imekuwa ikitangaza vita dhidi ya kundi hili na tumeona hatua ambazo imekuwa ikizichukua katika kulikabili kundi hili.Napata kigugumizi kidogo kulielewa hili jambo.Inawezekanaje IS wakafadhiliwa na Marekani ambao wamekuwa wakipanga mikakati mizito na kutumia fedha nyingi kugharamia operesheni ya kulimaliza kundi hili la IS.Au ni kundi lipi la IS linalozungumzwa hapa? Akauliza Mathew akijifanya kustuka na kutokujua chochote. “David Walker karibu” akasema Habiba na kukaa akamuachia nafasi David Walker ambaye alitaka kutoa maelezo kumuelewesha Mathew “Unalolisema Abu Zalawi ni kweli kabisa kwamba Marekani tumekuwa tukitenga bajeti kubwa kila mwaka kwa ajili ya operesheni za kupambana na ugaidi sehemu mbali mbali duniani na hii inaifanya Marekani kuwa kinara wa kupinga ugaidi duniani.Pamoja na kuwa kinara katika vita hiyo dhidi ya ugaidi duniani lakini kuna upande wa pili wa ambao watu wengi hawaufahamu ni kwamba licha ya kuendesha vita dhidi ya ugaidi lakini Marekani tunawatumia magaidi hao hao katika mipango mbali mbali yenye maslahi mazito kwa Marekani.Hilo ni jambo ambalo hata wamarekani wenyewe hawalifahamu na si wamarekani pekee hata Rais wa Marekani halifahamu.Ni jambo linalofanywa kwa siri kubwa na timu hii unayoiona humu ndani ndio tunaoshughulika na jambo hilo.Hiki ni kitengo maalum cha siri ndani ya idara ya ujasusi CIA ambacho ni maalum kabisa kwa ajili ya kushughulika na masuala haya ya mashirikiano na makundi ya kigaidi.Ni kitengo nyeti na cha siri mno kiasi kwamba hata wafanyakazi ndani ya CIA hawafahamu uwepo wake hivyo basi kwa mtu kama wewe kufahamu jambo hili ni kwamba umeaminiwa mno na tumekuamini kwa kuwa umeletwa na Habiba Jawad ambaye ni mwenzetu na ambaye ndiye anayefanya kazi kwa niaba yetu.Sisi hatuwafahamu viongozi wa makundi ya kigaidi na wao hawatufahamu sisi lakini wanamfahamu Habiba Jawad hivyo basi tunakuamini kama alivyokuamini Habiba na ndiyo maana umeifahamu siri hii na kuanzia leo hii wewe ni mmoja wetu japo baada ya kumaliza mazungumzo yetu utalishwa kiapo.Sasa tugeukie ni namna gani tunayatumia makundi haya ya kigaidi na ni namna gani tunafaidika nayo? akasema David Walker. “Marekani ni taifa kubwa kiuchumi duniani.Kama nchi tunahitaji malighafi kwa ajili ya kuendesha viwanda vyetu na kuufanya uchumi wetu uzidi kupaa.Malighafi kubwa ambayo tunaihitaji ni mafuta ambayo kwa kiasi kikubwa dunia nzima inategemea mafuta kutoka nchi za Mashariki ya kati.Kwa bahati mbaya Marekani na nchi azalishaji wakubwa wa mafuta duniani hatuna mahusiano mazuri.Ukiangalia nchi ambayo inatajwa kuwa na mafuta mengi zaidi duniani ni nchi ya Venezuela.Unafahamu mahusiano ya Marekani na Venezuela si mazuri.Nchi nyingine ambazo zina akiba kubwa ya mafuta ni Saudi Arabia hawa ni washirika wetu.Nchi ya tatu ni Canada,ya nne ni Iran.Hawa hatuna maelewano mazuri nao hata kidogo.Zipo pia nchi kama Iraq,Kuwait,UAE,Urusi na Libya.Kama nilivyosema kwamba nchi nyingi wazalishaji wa mafuta ziko Mashariki ya kati na nyingi kati ya hizo hazina maelewano mazuri na Marekani na hii ni kutokana na kuwaunga mkono Israel.Kuna chuki kati ya Marekani na nchi za kiarabu japo si zote kwani zipo nchi za kiarabu ambazo ni washirika wetu.Ili tuweze kupata mafuta tunawatumia makundi ya kigaidi katika kuanzisha vita na sisi tunapata nafasi ya kupeleka vikosi vyetu kwa kigezo cha kuwasaka magaidi na kisha huchukua mafuta na kuongeza akiba yetu.Tumekwisha fanya hivyo katika nchi kadhaa sina sababu ya kueleza hapa Habiba atakueleza kila kitu kwa hiyo sababu ya kwanza ya kuwatumia magaidi ni ili kuifanya Marekani kupeleka vikosi vyake katika nchi husika kwa ajili ya kuchukua mafuta.Naomba nisiendelee zaidi kwa kuwa utaendelea kufahamu taratibu kila kitu kuhusiana na sisi” akanyamaza akanywa maji halafu akasema “Abu Zalawi baada ya kukufahamisha kwa ufupi kuhusu sisi ni akina nani na majukumu yetu sasa tunaingia katika kile ambacho kimetukutanisha hapa sisi na wewe” David akanyamaza tena halafu akaendelea. “Tulimuomba Habiba atutafutie mtu mahiri kutoka katika makundi ya kigaidi kwa ajili ya kazi maalum.Baada ya kufanya uchunguzi wake Habiba amekuleta wewe ambaye ndiye anayeona unafaa kwa ajili ya kazi hiyo na tunaamini Habiba hajakosea kwani ameleta hasa mtu yule ambaye tunamuhitaji.Umetuonyesha uwezo wako tumeridhika na sasa ni wakati wa kukufahamisha kazi gani ambayo tunataka ukaifanye” akanyamaza tena kisha akasema “Kwa muda mrefu sasa nchi za Iran na Marekani zimekuwa katika mgogoro mkubwa ambao unahusiana na masuala ya silaha.Iran ikisaidiwa na baadhi ya nchi kubwa imejenga vinu vya nyuklia na inadai kuwa ni kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme lakini tunaamini mpango wa Iran ni kutengeneza kombora la nyuklia.Huu umekuwa ni mzozo wa miaka mingi na umepelekea nchi ya Iran kuwekewa vikwazo mbali mbali vya kiuchumi.Ni kutokana na mzozo huo ililazimika kuwekeana mkataba kati ya Iran na nchi za ulala na Marekani wa kutokuendelea na urutubishaji wa madini ya Urani.Marekani ilijitoa katika mkataba huo na Iran imetishia kuendelea na urutubishaji wa madini ya urani.Miaka kadhaa iliyopita tuliwateka wanasayansi wa Iran waliotoka Urusi kupatiwa mafunzo ya utengenezaji wa bomu la nyuklia.Kukamatwa kwa wanasayansi hao ni kihibitisho tosha namna Iran ilivyojiandaa kutengeneza kombora la nyuklia” akanyamaza kidogo kisha akaendelea “Kwa siku za hivi karibuni mzozo huu umechukua sura mpya kwa kila nchi kutishia kuishambulia nyingine.Rais wa Marekani alitishia kuisambaratisha Iran na Iran imetishia kwanza kuwashambulia washirika wa Marekani katika eneo la Mashariki ya kati na vile vile imetishia kuishambulia hadi Marekani.Iran imetoa vitisho kwamba kama Marekani itathubutu kuishambulia basi itakutana na kipigo ambacho haijawahi kupigwa.Kauli kama hizi hatuwezi kuzipuuza na kuna taarifa za chini chini kwamba Iran ina mfumo wa kisasa wa makombora ya masafa marefu.Kwa muda mrefu sasa Marekani imekuwa ikijaribu kufanya uchunguzi kujua kuhusu silaha za Iran bila mafanikio na hii ndiyo inayoifanya Marekani kusita kuishambulia Iran kijeshi kwa kuhofia kwamba yawezekana ikawa inamiliki hizo silaha inayodai kuwa nazo na tunaweza kuwaweka katika hatari kubwa washirika wetu walio karibu na Iran.Kwa ajili hiyo basi tumeamua kukutumia wewe katika suala hili” David akanyamaza akamtazama Mathew “Tunataka kukutuma uende Iran kufanya kazi mbili kubwa.Kwanza ni kufanya uchunguzi kuhusiana na silaha za nchi hiyo na kazi ya pili ni kuharibu kinu kikubwa cha kurutubisha madini ya Urani” akanyamaza tena na kumtazama Mathew ambaye alikuwa kimya akimsikiliza “Kwa nini mimi?akauliza Mathew “Kwa nini wewe? David naye akauliza kisha akanyamaza kidogo “Ni kwa sababu mbinu ya kutumia majasusi kuichunguza Iran imeshindwa kuzaa matunda na hadi leo hii hatujaweza kupata taarifa zozote za kuhusiana na silaha za nchi hiyo hivyo tunataka kubadili mbinu na tunataka kukupeleka wewe ambaye utapokelewa kama gaidi na shujaa bila kujua kuwa uko pale kwa kazi maalum.Iran utaingia vipi?Huu hapa mkakati wa kukuwezesha kuingiza Iran” akasema David huku watu wote mle ndani wakiwa wamemkazia macho Mathew “Eneo la Afrika Mashariki hivi sasa liko katika machafuko makubwa sana ya kidini.Kinachoendelea kule ni moja ya mipango yetu na kwa kuwatumia IS tumeweza kufanikisha kuibuka kwa machafuko makubwa sana ya kidini ambayo yamepelekea Marekani kupeleka vikosi vyake.Hapa unaweza ukaona ni namna gani Marekani inafaidika kutokana na makundi ya kigaidi.Tumewatumia IS kutengeneza vurugu zile na sasa Marekani inafaidika kwa mafuta mengi kutoka Uganda.Meli za Marekani zimepanga foleni zinapishana kujaza mafuta ,akiba yetu ya mafuta inaongezeka.Hii yote ni kazi ya timu hii unayoiona humu ndani na ni mfano wa mafanikio makubwa ambayo yanapatikana kwa kuwatumia magaidi” akasema David huku akitabasamu na kumlazimu Mathew kutabasamu pia “Kumbe hawa mabazazi ndio waliotengeneza vurugu zile Afrika Mashariki kwa ajili ya kujipatia mafuta ! Hawana huruma hata kidogo mashetani hawa.Natamani niwasambaratishe wote hapa hapa.Yaani ndugu zangu wanakufa Afrika Mashariki wao wanatabasamu kana kwamba si chochote ! Ahsante Habiba kwa kunileta hapa nimeweza kujua chanzo cha vurugu zile za nyumbani.Wamekosea sana kunieleza ukweli ! akawaza Mathew “Safari ya kwenda Iran itaanzia Afrika Mashariki” akasema David “Tutakutuma uende Afrika mashariki nchini Tanzania kule unakwenda kulipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam” “Kulipua ubalozi wa Marekani? Akauliza Mathew akionekana kushangaa “Ndiyo unakwenda kulipua ubalozi wa Marekani” “Mnalipua ubalozi wenu wenyewe? Akauliza Mathew “Ndiyo unakwenda kulipua ubalozi wa Marekani uliopo jjini Dar es salaam.Baada ya kulipua ubalozi huo IS watajitokeza na kudai kwamba wamehusika katika tukio hilo na tutalazimika kuongeza vikosi zaidi Afrika Mashariki kwa dhumuni la kuwasaka IS.Baada ya shambulio hilo tutaanza kukusaka kisha tutakukamata na kuitangazia dunia nzima kuwa tumemkamata mtu aliyelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam.Tukisha kukamata tutakupeleka mahala ambako wamehifadhiwa wanasayansi wa Iran waliotekwa wakitokea Urusi katika mafunzo ya kutengeneza bomu la nyuklia.Utakaa na wanasayansi hao na baada ya muda utasukwa mpango wa kutoroka na utawatorosha wanasayansi hao wa Iran.Kitendo hicho kitapelekea nchi ya Iran wakupokee na kukuamini kwanza watakuona shujaa kwa kulipua ubalozi wa Marekani na pili kwa kuwatorosha wanasayansi wao ambao hakuna anayefahamu hadi leo hii wako wapi.Utaomba kupatiwa hifadhi nchini Iran na hawatakuwa na sababu yoyote ya kukunyima hifadhi na hapo ndipo utakapoanza kuifanya kazi iliyokupeleka huko” David akanyamaza akamtazama Mathew “Si jambo jepesi ndiyo maana tulimuhitaji mtu maalum na wewe ndiye haswa unayefaa kwa kazi hii.Usihofu tutakuwezesha kwa kila kitu hadi utakapofanikiwa kuingia nchini Iran hivyo usiwe na wasi wasi” akasema David zikapita sekunde kadhaa David akasema “Abu Zalawi nimejitahidi sana kukupa maelezo marefu ambayo naamini umenielewa.Kuna swali lolote unataka kuuliza? “Hapana sina swali nimewaelewa vyema” akajibu Mathew “Vizuri sana” akasema David “Tumejitahidi vya kutosha kukueleza kuhusu sisi na kile tunachokihitaji kwako sasa ni zamu yetu kusikia kutoka kwako.Je unakubali kuifanya kazi hii? Mathew hakujibu alikaa kimya kwa muda na wote mle chumbani wakamkazia macho.Akainamisha kichwa akafikiri kwa muda na kusema “Kwanza kabisa nataka nimshukuru sana Habiba Jawad kwa kunitoa mahala nilipokuwa na kuniamini niwe msaidizi wake.Sikutegemea kama siku moja ningeweza kufika sehemu ya juu kama hii.Sikitegemea kama siku moja ningeweza kukutana na timu ya watu wenye nguvu kubwa duniani” akasema Mathew na wale watu mle ndani wakatabasamu “Sikuwahi kufikiri kama siku moja ningeweza kuaminiwa na kupewa jukumu kubwa kama hili nililopewa.Sina sababu yoyote ya kusema hapana.Mmenipa heshima kubwa sana ya kunituma nikafanye kazi ya taifa kubwa duniani.Ninawaahidi kwamba nimekubali na nitafanya kila mlichoniagiza nikifanye.Ninawaomba msiwe na hofu ninajiamini ninao uwezo wa kutekeleza hiki mnachonituma nikafanye” akasema Mathew na makofi yakapigwa DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa moja na dakika ishirini za jioni iliwakuta Ruby na Gosu Gosu tayari wamekwisha fika ikulu kuzungumza na Rais.Iliwalazimu kusubiri kwa saa mbili zaidi ndipo walipoonana na Rais “Karibuni sana jamani.Mtaniwia radhi kwa kipindi hiki mambo ni mengi mno hivyo msione kama vile nimewaweka pembeni” akasema Dr Fabian “Usijali mheshimiwa rais tunalielewa hilo” akajibu Ruby “Nashukuruni sana mmefika” akasema Dr Fabian na kuwachukua akina Ruby wakaelekea katika chumba cha mazungumzo “Kwanza kabisa napenda niwashukuru mno kwa wazo zuri mlilonipa jana.Nimeona matokeo yake.Jioni hii nimepokea simu kutoka kwa Mufti wa Tanzania akaniomba tukutane tuzungumze na akashauri kama ikiwezekana tukutanishwe viongozi wote wa kuu wa dini tukae meza moja tuzungumze tuone namna tutakavyoweza kutoka katika janga hili linalotukabili hivi sasa.Nimekubali wazo lake na tayari nimewaelekeza wasaidizi wangu wanisaidie kuwatafuta viongozi wengine wa dini upande wa wakristu ili tuandae mkutano wa pamoja tuzungumze.Masuala haya yanayohusiana na imani za dini hayawezi kumalizwa na vikosi vya jeshi bali kwa mazungumzo na viongozi wa dini ambao wanayo nguvu ya kuwashawishi waumini wao kuacha vurugu.Nashukurusana kwani ni wazo lenu ndiyo limezaa haya mazungumzo.Nimepokea pia taarifa kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi ameniambia kwamba kwa siku ya leo vurugu zimepungua tofauti na siku ya jana.Wote wanaamini hotuba ile imesaidia sana kwa vurugu kupungua.Hapo pia ninaelekeza shukrani zangu kwenu kwani sikuwa na wazo lile la kuhutubia taifa” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais hata sisi tunashukuru sana kama wazo lile limezaa matunda.Tuna imani kikao hicho cha viongozi wakuu wa dini mbali mbali kitakuwa na matunda mazuri” akasema Ruby “Naamini hivyo.Tunaweza kufikia muafaka mzuri.Vipi kwa upande wenu kuna chochote mmekipata? “Mheshimiwa Rais tumeanza kulifanyia kazi lile suala la kumchunguza Karim Abdallah.Tumefika nyumbani kwake lakini tumemkosa na inaonekaana aliondoka haraka haraka yeye na familia yake.Katika uchunguzi wetu tulipata orodha ya watu kadhaa ambao aliwasiliana nao na mtu wa mwisho kuwasiliana naye alikuwa jijini Tanga.Tuliwatumia watu wetu wa kule Tanga kumfuatilia huyo mtu lakini walikuta nyumba yake ikiwa imeteketea kwa moto.Tulimchunguza tena huyo jamaa na kumfuatilia mtu ambaye aliwasiliana naye mara ya mwisho ambaye naye alikuwa hapo hapo Tanga na watu wetu walipoingia katika hiyo nyumba walikuta kuna maiti ya mwanamke amechomwa kisu kifuani” akasema Ruby na kumuonyesha Rais picha za Yule mwanamke “Huu ni unyama mkubwa sana” akasema Dr Fabian “Watu wetu walichukua alama za vidole katika mpini wa kisu wakazituma kwetu kwa ajili ya kuzifanyia kazi na tukamfahamu mtu aliyefanya kitendo kile ni mumewe ambaye ni mchungaji anaitwa Augustin Kawala.Huyu naye hajulikani mahala alipo.Ukifuatilia kuanzia kwa Karim hadi kwa huyu Augustin wana mambo yanayofanana,wote wamewasiliana ndani ya siku moja na simu zao zimezimwa siku moja halafu wote hawapatikani tena na hawajulikani wako wapi.Hii inatufanya tuamini yawezekana wakawa kitu kimoja” “Dah ! akasema Dr Fabian “Hatukuishia hapo.Baada ya kuwakosa hao watu tuliokuwa tunawatafuta tuliendelea kumchunguza Karim na tukafuatilia mawasiliano yake ya wiki moja kabla ya vurugu kuanza na tukagundua kwamba amewasiliana mara ishirini na tatu na mtu mmoja anaitwa Joshua Lulangwa ambaye ni mwanasiasa wa chama cha upinzani nchini Uganda.Mheshimiwa Rais hapo ndipo tulipofikia na kukwama.Tunataka kumchunguza huyu mwanasiasa Joshua Lulangwa tufahamu mahusiano yake na Karim Abdallah.Wamewasiliana mara nyingi zaidi ndani ya wiki moja kabla ya vurugu kuanza.Tumekuja hapa kuomba msaada wako ili uweze kuzungumza na rais wa mpito wa Uganda Jenerali Paul Mukasa kumuomba atusaidie tuweze kupata taarifa za Joshua Lulangwa” akasema Ruby “Ruby kwanza kabisa nataka niwapongeze kwa namna mnavyojituma katika kutafuta mzizi wa jambo hili.Mimi nitawasiliana na Jenerali Paul kumuomba atusaidie kupata taarifa za huyo mtu ambaye amekuwa na mawasiliano na Karim Abdallah.Ninaamini hadi kufika kesho jioni tutakuwa tumepata taarifa zake” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” “Kuna lingine la kuzungumza?Nina kikao kingine muda si mrefu” akasema Dr Fabian “Ni hilo tu mheshimiwa rais lililotuleta hapa kwako jioni ya leo” “Basi nawashukuruni.Endeleeni na jitihada za kuhakikisha tunaupata mzizi wa jambo hili.Kama kuna chochote mnakihitaji nijulisheni mara moja” akasema Dr Fabian na kuagana na akina Ruby. Baada ya akina Ruby kuondoka Dr Fabian akaelekea chumbani kwake na kuketi sofani akashusha pumzi.Akachukua simu na kuzitafuta namba za simu za Jenerali Paul Mukasa akampigia “Dr Fabian” akasema Jenerali Mukasa “Jenerali Mukasa.Habari za huko? “Huku bado hali si shwari.Vurugu zinaendelea kupamba moto kila uchao.Kadiri siku zinavyozidi kwenda upepo wa vurugu hizi unabadilika na sasa kunaanza kuibuka makundi yenye silaha ambayo yanashambuliana na vikosi vya jeshi.Tunaendelea kuvichunguza vikundi hivi vinatoka wapi na silaha vinatoa wapi.Machafuko haya yanabadilika kutoka katika machafuko ya kidini na sasa yanaelekea kwenye uasi.Hivi vikundi vilivyoibuka vinazidi kuifanya hali ya amani kuwa tete zaidi kwani vina silaha nzito” akasema Jenerali Paul Mukasa “Hilo limeanza kujitokeza hata huku Tanzania.Kumeibuka makundi ambayo siyo ya kidini yanavunja nyumba,maduka makubwa na kupora.Wanaharibu na kuchoma majengo ya serikali na wana silaha.Nimeelekeza tuwachunguze makundi hayo tujue yametokeaje na nini hasa malengo yake.Jana nimeelekeza mawasiliano ya simu yarejeshwe hapa Tanzania na nikalihutubia taifa nikawataka watu watafakari na kuachana na vurugu hizi zinazoendelea.Nimefurahi kumekuwa na maendeleo mazuri kwani taarifa niliyoipata jioni hii ni kwamba machafuko yameanza kupungua na kesho nitakuwa na kikao na viongozi wa dini halafu tutajadili kuhusiana na vurugu hizi” “Mheshimiwa Rais hizo ni dalili nzuri za kuelekea katika suluhu ya vurugu hizi” akasema Jenerali Mukasa “Jenerali Mukasa nimekupigia kuna jambo ninataka tulijadili kidogo.Unahisi nini hasa chanzo cha vurugu hizi ambazo zimeanzia Uganda na kusambaa hadi Tanzania na Kenya? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,kwa kweli hata mimi nashindwa kuelewa namna vurugu hizi zilivyoanza.Zilianza kiajabu ajabu sana na kushika kasi kama moto wa petrol.Mpaka sasa tumeelekeza nguvu katika kuzimaliza na hatujajikita bado kujua chanzo chake” akasema Jenerali Paul Mukasa “Ipo timu hapa Tanzania ambayo nimeipa kazi ya kuchunguza chanzo cha vurugu hizi kwa upande wa Tanzania.Katika uchunguzi wao wa awali wamebaini kuna mtu mmoja ni mwanasiasa ambaye wakati kukiwa na vugu vugu la machafuko hapa Tanzania aliandika ujumbe katika ukurasa wake wa twitter akiwataka waumini wa dini ya kiislamu wakawashambulie watu wa dini nyingine.Tunahisi huyu anaweza akawa anahusiana kwa namna Fulani na machafuko haya.Tunahisi vile vile kwamba machafuko haya yana chembe chembe za kisiasa ndani yake.Tumechunguza watu kadhaa ambao wana mahusiano na huyo mwanasisasa lakini wote wametoweka na simu zao hazipatikani http://deusdeditmahunda.blogspot.com/tena.Inaonekana huu ni mtandao mmoja.Katika uchunguzi wao wamegundua kwamba Karim alikuwa na mawasiliano na mwanasiasa mmoja wa Uganda anaitwa Joshua Lulangwa.Karim na Joshua wamewasiliana mara nyingi zaidi katika wiki moja kabla ya machafuko kuanza.Tunataka kumchunguza Joshua kufahamu mahusiano yake na Karim na kisha tujue kama wana mahusiano yoyote na vurugu hizi zinazoendelea.Tunaomba msaada wako kupata taarifa za huyu mtu” akasema Dr Fabian “Hakuna tatizo mheshimiwa Rais nitawaelekeza watu wangu wafanye uchunguzi kuhusiana na huyo mtu kisha nitakujulisha” “Nashukuru sana Jenerali Mukasa” akajibu Dr Fabian na kukata simu “Naanza kukubaliana na Ruby kwamba yawezekana machafuko haya yana chembe chembe za kisiasa ndani yake.Lazima tuhakikishe kwa gharama zozote wale wote waliosababisha machafuko haya wanapatikana ” akaendelea kuwaza Dr Fabian WASHINGTON DC – MAREKANI “Mama Habiba siamini kwa hiki ulichonifanyia.Hii ndiyo misheni kubwa uliyoniambia kwamba unaniandalia? Akauliza Mathew Mulumbi baada ya kupewa dakika chache kuagana na Habiba kabla ya kwenda kujiandaa kutekeleza jukumu kubwa alilopewa. “Ndiyo Mathew” akajibu Habiba Jawad “Siamini mama kama umekuja kuniuza kwa hawa jamaa ambao sasa wananituma nikafanye kazi zao za hatari.Kwa nini umenifanyia hivi mama Habiba? Akauliza Mathew “Mathew sikiliza hatuna muda mrefu wa kuongea.Nimekuleta hapa kwa makusudi kabisa.Kama kweli una nia ya dhati ya kumaliza ugaidi duniani basi hii ndiyo nafasi pekee unayopaswa kuitumia.Hiki kitengo ndicho kinachoongoza makundi karibu mengi ya kigaidi duniani hivyo umefika sehemu unakotakiwa ufike.Finish them.Fanya wanachokutuma ufanye wachunguze vizuri halafu mwisho wa siku wamalize.Kikundi hiki ni hatari sana kwa mustakabali wa dunia.Hakikisha ……” akasema Habiba na kugeuka baada ya kusikia hatua za mtu akiwafuata ambaye alitumwa kumchukua Mathew.Habiba akamtaka mtu Yule kusubiri dakika mbili “Mathew hakikisha unafanikisha malengo yako.Ifanye dunia ikukumbuke kwa vizazi na vizazi.Maliza kundi la kigaidi la IS na makundi mengine.Kisafishe kikundi hiki kidogo cha watu hawa ambacho ndicho kinachohatarisha amani ya dunia.Hii ni misheni kubwa na ya hatari.Lolote linaweza kutokea katika misheni hii mimi ninakuombea uimalize salama na kila pale nitakapokuwa na uwezo wa kukusaidia nitafanya hivyo.Jambo la mwisho baada ya kumaliza misheni hii kama utakuwa salama tafadhali usirejee tena Riyadh.Nenda nyumbani kaendelee na maisha yako.Kaungane tena na familia yako kwani lengo lako litakuwa limetimia kuhusu kupambana na ugaidi.Kuhusu Najma usiwe na hofu nitazungumza naye na ataelewa.Narudia tena usirejee Saudi Arabia kwani hadi wakati huo sintakuwepo tena.Ule utajiri wako wote niliokupa utaendelea kuwa wako na fedha zote zitawekwa katika ile akaunti yako utakapomaliza misheni hii utatulia na familia yako na kufurahia utajiri huo.” akasema Habiba Jawad ambaye machozi yalikuwa yanamtiririka “Mathew hii naamini itakuwa ni mara ya mwisho kwa mimi na wewe kuonana hapa duniani.Kwa sasa nina amani na ninaamini hata nikifa leo nimeacha chuma ambacho hakishiki kutu ambacho kitamaliza ugaidi.Nakutakia kila la heri” akasema Habiba na kumkumbatia Mathew halafu akaanza kuondoka huku Mathew naye akiwa amesimama akimtazama. “Ahsante Habiba Jawad kwa kunifikisha hapa.Umefanya jambo kubwa sana kunifikisha hatua hii na sintakuangusha” akawaza Mathew akiwa bado amesimama akimtazama Habiba akiingia katika lifti na mlango ukajifunga Mathew aliongozana na Yule mtu aliyetumwa kumchukua hadi katika gari wakaondoka.Ilikuwa ni safari ya kimya kimya na Mathew hakujua alikokuwa anapelekwa. Safari yao iliishia katika nyumba moja ambayo geti lake lilikuwa wazi wakaingia ndani.Yule jamaa akashuka garini na kumtaka Mathew ashuke kisha wakaingia ndani ya ile nyumba ambako walimkuta jamaa mmoja mnene aliyekuwa sebuleni akitazama runinga.Alikuwa kifua wazi na alikuwa amevaa kaptura ya rangi za jeshi.Akawakaribisha na Yule jamaa aliyemleta Mathew katika nyumba ile akatoka nje akawaacha Mathew na yule jamaa “Jina lako nani? Akauliza Yule jamaa akiwa ameyaelekeza macho yake katika mecho ya mpira wa kikapu iliyokuwa inaendelea runingani “Abu Zalawi” Mathew akajibu “Naitwa Peter Tylor.Karibu” akasema Peter huku akiinua kikombe cha kahawa na kunywa “Ahsante” akajibu Mathew.Peter akanywa kahawa halafu akaweka kikombe mezani akazima runinga na kumtazama Mathew “Umewahi kuishi Afrika? Akauliza Peter Tylor “Ndiyo nimewahi kuishi Nairobi Kenya na Cairo” akajibu Mathew “Vizuri.Unakwenda tena Afrika lakini safari hii unakwenda Tanzania.Utaondoka hapa na ndege ya jesi kuelekea Tanzania.Utakapofika Dar es salaam utafikia katika kambi ya wanajeshi wa Marekani na atakuja mtu Fulani anaitwa Assad Ismail kukuchukua.Huyu tayari ana maelekezo yote ya kuhusu wewe na ndiye atakayekusaidia kufanikisha kazi uliyotumwa kuifanya hapo Dar es salaam.” akasema Peter Tylor na kumchukua Mathew katika chumba kimoja akaanza kumpa maelekezo ya kazi ambayo anatakiwa kwenda kuifanya Dar es salaam.Baada ya kupewa maelekezo yote Mathew na Yule jamaa wakaingia garini na kuondoka kuelekea katika uwanja wa ndege wa kijeshi ambako kulikuwa na ndege inamsubiri. “Safari njema” akasema Peter na Mathew akaingia katika ndege ile ya jeshi ambayo haikuchukua muda ikapaa kuelekea Tanzania. “Habiba amenifikisha mahala ambako sikutegemea kufika.Nimegundua siri kubwa sana ambayo dunia haiijui.Nimekutana na kikundi cha watu wachache wenye nguvu ambao wanaamua kitu gani wafanye katika nchi gani hapa duniani.Machafuko yanayoendea Afrika mashariki kumbe ni mipango ya Marekani kutaka kuchukua mafuta ya Uganda.Hawajali mamia ya watu wanaouana kila uchao wao wanachokitazama ni maslahi yao tu.Hawa ni watu wakatili sana ! akawaza “Namshukuru sana Habiba Jawad kwa kunifikisha hapa.Aliponiambia kwamba kuna mambo mengi ambayo siyafahamu bado alikuwa sahihi.Kuna mambo sikuwa nikiyafahamu na mojwapo ni hili la idara maalum ndani ya shirika la ujasusi la marekani CIA kushirikiana na makundi ya kigaidi kwa ajili ya maslahi ya Marekani” akawaza Mathew “Ninakwenda kufanya kazi ya kigaidi.Kutoka ujasusi hadi ugaidi ! akaendelea kuwaza Mathew akiwa ameinamisha kichwa “Nitafanya wanavyotaka lakini hawataamini kwa kile nitakachowafanyia.Ile idara ndogo katika CIA lazima niifuilie mbali,lazima dunia ifahamu kile ambacho watu hawa wanakifanya.Katika hili natakiwa kuwa mvumilivu.Natakiwa kwanza kujenga imani kwao ili waniamini na ndipo nitakapoweza kutekeleza mipango yangu.Lakini nasikitika sana pale dunia nzima watakapojua mimi ni gaidi na nimelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam.Ruby ataumia sana akisikia jambo kama hili.Wenzangu akina Gosu Gosu na Austin hawataamini macho yao pale watakaposikia kwamba mimi ndiye niliyelipua ubalozi wa Marekani.Watoto wangu watapatwa na mstuko mkubwa baada ya picha zangu kutolewa kwamba ndiye niliyelipua ubalozi wa Marekani na nitatajwa kama gaidi.Jina langu litachafuka.Watu wanaonifahamu hawataamini kama kweli nimegeuka kutoka jasusi hadi gaidi.Lakini baada ya kuchafuka kwa kujulikana kama gaidi mwisho wa mchezo huu dunia nzima itanisifu kwa kile nitakachokifanya.Halafu ! akawaza Mathew na kuinua kichwa baada ya mmoja wa wanajeshi waliokuwamo mle ndegeni kumgusa na kumpatia chupa ya bia. “Ahsante” akasema Mathew na kunywa funda moja “Marekani hawajui kama mimi ni mtanzania.Hawajui kama mimi ni jasusi na jina langu ni Mathew Mulumbi na si Abu Zalawi kama walivyoambiwa na Habiba Jawad.Baada ya picha zangu kusambaa duniani kwamba mimi ndiye niliyelipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam lazima siri itafichuka kwamba mimi ni mtanzania na nitakuwa nimejiweka katika matatizo mimi na hata Habiba pia ambaye amewahakikishia wamarekani kuwa mimi ni raia wa Saudi Arabia.Lakini hii haiwezi kunizuia kuendelea na mipango yangu.Dunia itatikisika.Kila chombo cha habari duniani lazima kitaniongelea mimi” akaendelea kuwaza Mathew huku ndege ikiendelea kupasua anga kuelekea Tanzania RIYADH – SAUDI ARABIA Saa nane za mchana Habiba Jawad aliwasili jijini Riyad Saudi Arabia akitokea Washington DC Marekani.Katika uwanja wa ndege alipokewa na mwanae Najma ambaye alistushwa kwa Habiba kurejea peke yake bila ya Mathew Mulumbi. “Mbona umerejea peke yako mama,Abu yuko wapi?akauliza Najma “Tutazungumza tukifika nyumbani Najma” akasema Habiba na safari ikaendelea kimya kimya Waliwasili nyumbani kwa Habiba na Najma hakutaka kupoteza muda akamtaka mama yake wazungumze. “Mama nafahamu umechoka sana kwa safari ndefu.Takribani saa kumi na nne umekuwa angani ukisafiri lakini naomba tafadhali unipe dakika chache tuzungumze.Nina jambo ambalo haliwezi kusubiri na nilitamani nikufuate huko huko Marekani tulizungumze” akasema Najma na Habiba akamtazama mwanae akagundua kweli kuna kitu kinamsumbua “Kitu gani kinakusumbua Najma?Ni kuhusu kutokurudi na Abu Zalawi?akauliza Habiba “Hilo ni moja wapo lakini kuna lingine kubwa zaidi ya hilo” akajibu Najma “Nieleze tafadhali” “Kabla sijakueleza chochote mama nataka unihakikishie kwamba utanieleza ukweli mtupu kwa kile nitakachokuuliza” akasema Najma.Habiba akamtazama halafu akasema “Nini kinakusumbua Najma? Niambie kile kinachokusumbua na mimi nitakujibu” akasema Habiba “Mama nataka unieleze kila kitu kuhusiana na Abu Zalawi” “Abu Zalawi ni mume wako,wewe ndiye uko naye karibu zaidi na ni wewe unayetakiwa kumfahamu vyema.Hukupaswa kuniuliza mimi kuhusu Abu Zalawi kwani tayari umekuwa naye kwa muda wa miezi kadhaa hivi sasa.Unapaswa tayari uwe unamfahamu vyema” akasema Najma “Mama nakuomba tafadhali unieleze ukweli kuhusiana na Abu Zalawi.Ni nani huyu mtu? Umemfahamuje? Akauliza Najma “Najma nini hasa kinachokufanya uniulize mimi habari za Abu Zalawi? “Mama nakuomba sana unisaidie kunieleza kuhusiana na huyu mtu nahitaji sana kumfahamu.Wewe ndiye unayemfahamu vyema kuliko mimi.Naomba tafadhali unieleze kila kitu unachokifahamu kuhusu Abu Zalawi” akasema Najma “Najma unanishangaza.Kuna nini kati yako na Abu Zalawi? Kuna mgogoro wowote kati yenu? Niambie tafadhali kama kuna tatizo lolote” akasema Habiba “Mama ngoja nikuweke wazi ili upate picha halisi ya mzigo ninaoubeba.Ulinitaka niolewe na Abu Zalawi ambaye ulidai ni mwanaume ambaye ananifaa.Nilitokea kumpenda Abu Zalawi kabla hata sijamtia machoni kufuatia maelezo yako na nilipomuona kwa macho nilimpenda na nikakubali kuolewa naye na ninakiri kwako mama kwamba ninampenda sana Abu Zalawi lakini kuna mambo yamejitokeza ambayo yamenifanya nitake kumfahamu vyema huyu mtu ni nani?” “Nini kimetokea Najma? Akauliza Habiba “Kabla ya safari ya kwenda Marekani ulizungumza na Abu Zalawi na aliporejea chumbani alionekana kama vile amechanganyikiwa.Sifahamu ni kitu gani ulimweleza lakini hakuwa Yule niliyemzoea.Alichukua kitabu hiki hapa akakifungua akatafuta namba za simu ambazo zina jina la Ruby akapiga zaidi ya mara tatu lakini simu ya huyo mtu haikuwa ikipatikana.Wakati akiendelea kumtafuta huyo Ruby nilikichukua kitabu hiki na kuzikuta namba hizo za Ruby.Nilimuuliza Ruby ni nani akastuka sana na kuninyang’anya kile kitabu.Mama mimi nina wivu sana na ndiyo maana sikutaka kujiingiza katika masuala ya mapenzi kwa kuhofia kuumizwa. Mlipokwenda Marekani nilipiga zile namba za Ruby alizopiga Abu Zalawi akapokea mwanamke ambaye yuko Tanzania lakini aligoma kunitajia jina lake.Nilimuuliza kama anamfahamu Abu Zalawi akakana kumfahamu,alikana kuwa na rafiki au mtu anayemfahamu mwenye jina la Abu Zalawi.Baadae akanipigia simu akanitaka nimtumie picha ya Abu Zalawi na hapo ndipo kilipotokea kizaa zaa” Najma akanyamaza kidogo halafu akasema “Kwa muda wa miezi mitatu tumekuwa tukizunguka sehemu mbali mbali duniani tukifanya utalii.Katika safari yetu hiyo tulipiga picha nyingi sana lakini kitu cha ajabu ni kwamba nilipozitafuta picha tulizopiga mimi na Abu katika safari yetu sikupata hata picha moja.Nilihifadhi picha nyingi katika kompyuta yangu nyingine zilikuwepo katika kamera na hata katika simu yangu lakini huko kote hakukuwa na picha hata moja.Hiki kitu kimenishangaza sana mama namna picha zilivyotoweka.Hakuna mtu yeyote aliyeingia chumbani kwetu zaidi yetu sisi hivyo naamini aliyefuta picha hizo lazima atakuwa Abu Zalawi.Nimejiuliza maswali mengi kwa nini akafuta picha zetu?Nimeshindwa kupata jibu ndiyo maana nataka unieleze kuhusiana na huyu mtu ni wa aina gani? Tafadhali mama” akasema Najma na Habiba akavuta pumzi ndefu “Mambo yamekwisha haribika.Tayari Najma amekwisha hisi kitu kuhusu Abu zalawi.Nadhani ni wakati wake wa kuufahamu ukweli” akawaza Habiba “Najma kuna jambo ambalo nataka nikueleze kuhusu Abu Zalawi.Kwanza kabisa ni kwamba Abu Zalawi hatarejea tena.Ameondoka” akasema Habiba na sura ya Najma ikabadilika “Unasemaje mama ?! akauliza Najma “Najma Abu Zalawi hatarejea tena.Ameondoka” “Mama sijakuelewa” “Najma kuna mambo mengi ambayo huyafahamu kuhusu mimi” akasema Habiba na kumtazama Najma ambaye alionekana kuchanganyikiwa “Maisha yangu yamejaa siri nyingi ambazo nyingine nitakueleza lakini nyingine nitakwenda nazo kaburini.Nina sababu yangu ya kufanya hivyo” akasema Habiba na kunyamaza tena akamtazama Najma “Siri ya kwanza ni kuhusu huu utajiri wangu.Utajiri wangu huu ambao ninautumia katika kufadhili makundi mbali mbali ya kigaidi niliurithi kwa baba yake Abu Dahir lakini naye utajiri huu hakuupata hivi hivi.Leo nitakupa siri ya huu utajiri wangu” akasema Habiba na kunyamaza akamtazama Najma “Asili ya utajiri wangu huu ni Marekani.Wao ndio waliomuwezesha baba yake Abu Dahir na alipofariki mimi ndiye niliyerithi utajiri huo.Kwa nini Marekani walimpa utajiri huu mkubwa? Akauliza Habiba lakini Najma hakujibu kitu chochote “Ndani ya shirika la ujasusi la Marekani CIA kuna kitengo ambacho kinajishughulisha na mashirikiano na makundi ya magaidi.Kitengo hiki ndicho kilichotuwezesha kuwa na utajiri huu mkubwa na lengo kuu la kutupa utajiri huu ni kwa ajili ya kuyafadhili makundi ya kigaidi katika operesheni zao mbali mbali zenye maslahi kwa Marekani hivyo basi kwa muda huu wote nimekuwa nikifanya kazi na Marekani.Ufadhili huu ambao tumekuwa tukiwapa makundi ya magaidi ni maelekezo ya Marekani” Sura ya Najma ilibadilika alifungua mdomo wake akataka kusema kitu lakini maneno hayakutoka “Nimekustua Najma.Lakini umefika wakati wa wewe kufahamu kila kitu.Nimeamua kukushirikisha siri chache kuhusu mimi” akasema Habiba “Nimefanya kazi na Marekani kwa muda mrefu na sasa nimechoka.Sitaki kuendelea tena kuwa mfadhili wa makundi ya kigaidi ndiyo maana nikamleta Abu Zalawi ili aweze kulimaliza jambo hili.Kuna mambo ambayo huyafahamu kuhusu Abu Zalawi na leo nitakufahamisha”Habiba akanyamaza kidogo halafu akasema “Abu Zalawi jina lake halisi anaitwa Mathew Mulumbi ni mtanzania” “Mungu wangu ! akasema Najma.Habiba akaendelea “Abu Zalawi si gaidi kama nilivyokufahamisha awali bali ni jasusi” “Jasusi ? ! Najma akashangaa “Ndiyo ni jasusi.Najma kuna mengi ambayo ningetaka kukueleza lakini nitazungumza nawe siku nyingine hayo machache yanatosha kwa leo.Kubwa ambalo nataka ulifahamu ni kwamba Abu Zalawi au Mathew alikuwa hapa kwa ajili ya kazi maalum na sasa wakati wake umefika wa kwenda kutekeleza majukumu yake na kazi hiyo anayokwenda kuifanya ni kwa ajili ya usalama wenu wewe na kaka yako.Abu ndie mkombozi wenu kwani akifanikiwa katika misheni hiyo itakuwa ni salama yenu lakini akishindwa maisha yetu yatakuwa shakani.Abu Zalawi hatarudi tena” “Unamaanisha nini mama? “Misheni anayokwenda kuifanya ni misheni ya hatari kubwa sana na uhakika wa kurudi salama katika misheni hiyo ni mdogo” akasema Habiba “Mama kwa nini ukanifanyia hivi? Kwa nini ukanitaka niolewe na Abu Zalawi wakati ukijua ni mtu wa namna gani?Kwa nini ukaniacha nikazama mapenzini na Abu Zalawi halafu unamuondoa? Akauliza Najma “Nilikuwa na sababu zangu kukutaka uolewe na Abu Zalawi.Bila kuolewa naye asingekubali kukaa nasi hapa kwa ajili ya misheni ambayo nimemtuma akaifanye.Amekaa nasi hapa hadi ulipofika muda wake wa kuondoka kwa sababu yako”akasema Habiba “Mama wewe ni shetani.Una roho ya kishetani ! Huna ubinadamu hata kidogo.Mama wewe ni mkatil………….” Akasema Najma na Habiba akamnasa kofi “Haya yote niliyoyafaya ni kwa sababu yenu.Nafanya kila hatua kuwalindeni ili muwe salama vinginevyo ninyi nyote hivi sasa mngekwishauawa.Kuanzia sasa anza kuzoea hali hii.Abu Zalawi ana mke wake na watoto hawezi kurudi tena.Kumpoteza Abu si mwisho wa mais…”akasema Habiba na Najma akatoka mbio huku akilia. “Nimemuumiza sana Najma.Sikutaka aufahamu ukweli hu lakini kwa hatua aliyokuwa ameifikia ni lazima aufahamu ukweli.Itamchukua muda mrefu kukubaliana na ukweli h….” Habiba akastuka baada ya mmoja wa walinzi wake kuingia mle ndani akikimbia “Kuna nini ?akauliza Habiba kwa wasi wasi. “Mama umesikika mlio wa risasi katika nyumba ya Abu Zalawi ! akasema Yule mlinzi na Habiba akatoka mbio akiongozana na Yule mlinzi na kukuta walinzi wengine tayari wamekwisha fika katika nyumba ile ya Mathew.Habiba akiwa na wale walinzi wakaenda chumbani kwa Najma walinzi wakavunja mlango akaingia ndani.Najma alikuwa amelala katika dimbwi la damu.Hakuwa na uhai tena.Alijipiga risasi ya kichwa.Habiba akaanguka na kupoteza fahamu. MPENZI MSOMAJI USIKOSE SEHEMU IJAYO……
DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa tisa za alasiri televisheni ya taifa ilikatisha kipindi kilichokuwa kinaendelea na kujiunga na matangazo ya moja kwa moja kutoka ikulu jijini Dar es salaam ambako Rais wa jamhuri ya muungamo wa Tanzania alitarajia kutoa hotuba kwa watanzania.Kama ilivyokuwa siku iliyotangulia,simu janja zote ambazo zilikuwa zimewashwa muda huo ziliunganishwa na matangazo yale ya moja kwa moja kutoka ikulu kwa lengo la kumuwezesha kila mwananchi kusikiliza ujumbe ambao Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alitaka kuwapa watanzania.Tayari wanahabari walikwisha weka sawa kamera zao na aliyekuwa akisubiriwa ni Rais Mlango ulifunguliwa na Rais Dr Fabian Kelelo akajitokeza akiwa ameambatana na Mufti wa Tanzania Sheikh Seleman Majid.Muongozaji wa shughuli ile alitoa maelezo machche na kumkaribisha Rais aweze kuzungumza na watanzania.Rais alianza kwa kuwatania kidogo waandhishi wa habari kisha akaendelea “Ndugu watanzania wenzangu awali ya yote ninamrejeshea utukufu Mungu wetu aliye juu kwa kutukutanisha tena siku hii.Poleni sana wale wote ambao mmeendelea kuwapoteza wapendwa wenu kufuatia vurugu zinazoendelea na wale wote ambao mnauguza majeraha nawatakiwa uponaji wa haraka. Ndugu watanzania,jana nilizungumza nanyi kwa kirefu na kuwasisitiza umuhimu wa kutunza amani yetu.Ninashukuru sana kwa wengi kunielewa na taarifa niliyoipata ni kwamba vurugu zimepungua na hii ni dalili njema kwamba tunaelekea kuzuri.Bado naendelea kuwasihi ndugu watanzania tuachane na vurugu hizi ambazo hazina maslahi kwetu na hata kwa dini zetu.Tunachokivuna katika machafuko haya ni hasara badala ya faida.Ndugu zetu wengi wamepoteza maisha,wengine hawajulikani walipo,wengine wamepata ulemavu wa kudumu na wengine wanaendelea kuuguza majeraha hospitali.Wengi wetu tumepoteza mali,nyumba zimechomwa moto,majengo ya serikali yamechomwa na kuharibiwa,miundo mbinu imeharibiwa,biashara zimefungwa nk.Ndugu zangu kwa ujumla tunachovuna katika machafuko haya ni hasara kubwa na tuna kazi kubwa ya kuijenga nchi yetu baada ya machafuko haya kumalizika” Rais akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Jana baada ya kumaliza kutoa hotuba yangu,nilipigiwa simu na Mufti wa Tanzania akaniomba tuonane leo tuzungumze.Leo kuanzia asubuhi nilikuwa na kikao kirefu naye na kubwa tulilolijadili ni kuhusiana na vurugu hizi zinazoendelea nchini namna tutakavyoweza kuzmaliza.Imekuwa ni desturi yetu kukaa mezani kila pale inapojitokeza mikwaruzano baina ya dini zetu na mara zote katika mazungumzo ya pamoja tumekuwa tukimaliza tofauti na amani ikamalaki. Tumezungumza mambo mengi katika kikao hicho kirefu na tumekubaliana kuwa na kikao kikubwa kitakachowahusisha viongozi wakuu wa dini zote hapa nchini ili tutafute muafaka.Naahidi kikao hicho kitafanyika mapema sana ili tukae meza moja serikali na viongozi wa dini tujikwamue hapa tulipokwama na maisha yarejee kama kawaida.Kwa kuwa mambo mengi nilizungumza jana leo naomba nimpe nafasi Mufti ana neno la kuzungumza na watanzania.” akasema Dr Fabian na kumkaribisha mufti wa Tanzania Sheikh Seleman Majid ambaye alianza kwa dua kisha akaendelea “Ndugu zangu,awali ya yote nami nataka nianze kwa kuwapa pole nyingi wale wote ambao wamepoteza ndugu zao hadi sasa katika machafuko haya yanayoendelea hapa nchini kwetu na wale wote waliopata majeraha mbali mbali nawaombea wapate nafuu ya haraka. Ndugu zangu watanzania kwa siku kadhaa sasa nchi yetu imekumbwa na machafuko makubwa kabisa kuwahi kutokea hapa nchini.Machafuko haya yalianzia katika nchi ya jirani na yakaenea kama moto wa nyika hadi kufika hapa Tanzania.Ndugu zangu dunia inashangaa nini kimetokea Tanzania?Katika historia ya nchi yetu hakujawahi kutokea machafuko kama haya yanayoendelea ya waumini wa dini kushambuliana.Mheshimiwa rais alieleza kwa kirefu jana namna ambavyo watanzania tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo mkubwa licha ya tofauti zetu za kidini.Tumeishi kindugu tukishirikiana katika mambo mbali mbali sherehe,misiba n.k. Hatujawahi kubaguana hata siku moja kwa imani zetu.Nini kimetufikisha hapa? Swali hili ameliuliza Rais jana wakati anatoa hotuba yake na kwa swali hilo ndiyo lilinifanya nitake kuonana na mheshimiwa Rais ili kwa pamoja tutafute majawabu ya nini kimetufikisha hapa. Tumekuwa na kikao kirefu na tumezungumza kwa upana kuhusu jambo hili.Tumekubaliana kwamba tuwe na kikao kikubwa cha viongozi wakuu wote wa dini ili kwa pamoja tuweze kuzungumza na kutafuta muafaka lakini wakati kikao hicho kikiandaliwa tumekubaliana kwamba sisi viongozi wa dini tuwahamasishe waumini wetu watulie na waache vurugu.Suala hili ni pana zaidi ya tunavyodhani hivyo basi tunataka kuipa serikali nafasi iweze kulishughulikia hili jambo na kupata chanzo chake.Tunapoendelea kushambuliana na kuuana tunaifanya serikali ishindwe kulishughulikia suala hili hivyo Rais ametuomba kila kiongozi wa dini ajitahidi kuhakikisha anawahamasisha waumini wake watulie waache vurugu ili serikali ishughulikie kutafuta chanzo cha jambo hili. Ndugu zangu kufuatia maelekezo hayo ya Rais,niko hapa kuzungumza na ndugu zangu wa upande wa waislamu kuwasihi wasiendelee kushiriki katika vurugu.Uislamu ni dini ya amani na hata tunaposalimiana tunasema Assalam alaikum maana yake amani iwe nawe. Dini ya Uislamu ina mitazamo inayofanana na dini nyingine kuhusu suala hili la amani na usalama.Katika mtazamo wa Uislamu usalama una maana ya amani na utulivu katika jamii. Neno amani kwa ujumla limezungumziwa katika karibu aya 140 za Qur'ani ambacho ni kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.Usalama na amani vina mfungamano na Mwenyezi Mungu Muumba. Mwenyezi Muumba mwenyewe amejitaja kuwa ni "Assalam" kwa maana ya amani na Mwenye amani na salama na kwa msingi huo kila usalama na amani ni mwangwi wa dhati yake tukufu. Dhati ya mwanadamu pia daima huwa katika hali ya kustawi na kufanya harakati za kuelekea kwenye amani na utulivu kamili ambao haupatikani ila kwa amani na usalama , yaani dhati ya Mwenyezi Mungu Muumba.Aya ya 208 ya Suratul Baqara inasema: Enyi Mlioamini! Ingieni katika usalama nyote. Wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliyewazi. Vilevile aya ya 61 ya Suratul Anfal inasema: Na (wapinzani wako) wakielekea kwenye amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. Neno "Islam" pia linatokana na msingi wa neno "Silm", na kwa hakika lina maana ya kumfuata Mwenyezi Mungu ambaye Yeye mwenyewe ndiye amani na usalama mutlaki na utulivu kamili. Neno jingine ni "sulh" ambalo lina maana na amani, maelewano na uhusiano mwema baina ya wanadamu. Uislamu umetumia neno hilo ukitaka kuwepo upendo, kuheshimiana, kujiepusha na uchokozi na uhasama na kuchupa mipaka ya wanadamu wengine. Ili kuweza kupatikana amani na uadilifu, Uislamu umeweka safari yenye awamu tatu tofauti. Kwanza ni usalama na amani ya ndani ya nafsi. Katika awamu hii watu wote wa jamii wanatakiwa kutakasa nafsi zao na kuzipamba kwa taqwa na uchamungu.Katika awamu hii, muumini anapaswa kukomesha mpambano na vita liyopo baina ya matamanio na matakwa yake ya kinafsi na yale ya kiroho, na kufikia amani na usalama wa ndani ya nafsi ili pande hizo mbili za kinafsi na kiroho ziishi pamoja kwa amani na kumsaidia mwanadamu kufikia kilele cha ukamilifu. Ni baada ya hapa ndipo mwanadamu anapokuwa tayari kwa ajili ya harakati ya kijamii na wanadamu wenzake kuelekea kwenye malengo aali na ya juu zaidi. Aya ya 103 ya Suratu Aal Imran inasema: “Na shikamaneni na Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote kwa pamoja, wala msifarikiane” Kwa msingi huo amani ya ndani ya nafsi ndiyo msingi wa ukamilifu wa kimaadili na kiroho kwa ajili ya kuwa na taathira kubwa zaidi katika jamii ya Kiislamu. Awamu ya pili ya amani na usalama katika Uislamu ni amani na usalama wa jamii. Baada ya kuwa tayari kinafsi kwa kuitakasa na kuisafisha, mwanadamu huwa ametengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya muungano mpana zaidi wa kijamii na wanadamu wenzake. Hapa ndipo inapokuja amri ya Mwenyezi Mungu inayowataka Waislamu kuwa na umoja na kujenga udugu. Sehemu moja ya aya ya kwanza ya Suratul Anfal inasema: “Basi mcheni Mwenyezi Mungu na msuluhishe mambo baina yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni waumini.” Kwa utaratibu huo Waislamu hutoka katika minyororo ya ubinafsi, ubaguzi, dhulma na sifa nyingine mbaya na kuwa watu wema na wenye faida kwa jamii. Awamu ya tatu ya amani na usalama inahusiana na usalama na amani kwa wasio Waislamu. Miongoni mwa misingi na kanuni zinazotawala jamii ya Kiislamu ni kuishi kwa amani na usalama na wasio Waislamu. Kinyume na fikra na dhana za wanafikra wengi wasio Waislamu na propaganda chafu za nchi za Magharibi, Uislamu ni dini ya amani na kuishi kwa usalama na wasio Waislamu. Hii ni pamoja na kwamba, huwezi kupata hata aya moja ya Qur'ani inayowalazimisha watu kukubali dini hiyo kwa vita na mabavu. Vita katika Uislamu vina sura ya kujihami na kujilinda mbele ya mashambulizi yanayolenga jamii ya Waislamu au watu wengine wanaodhulumiwa au kwa ajili ya kuzuia uchokozi na hujuma za adui. Suala la kuishi kwa amani na usalama na wasio Waislamu limesisitizwa sana katika aya za Qur'ani tukufu na hadithi, sira na mwenendo wa Mtume na Aali zake watoharifu. Suala hili pia limejengeka juu ya nguzo ya utukufu wa kiumbe mwanadamu. Katika mtazamo wa Uislamu wanadamu wasio Waislamu wana heshima na utukufu wa kidhati na kimaumbile kutokana na kushirikiana kwao na Waislamu katika maumbile na ubinadamu japo wanatofautiana katika dini na imani. Uhakika huu unathibitishwa na sira, mwenendo na maisha ya Mtume Muhammad (saw). Mfano wa wazi wa mwenendo huo wa amani na suluhu na wasio Waislamu ni Mapatano ya Ungwana yaliyofikiwa baina ya Mtume (saw) na washirikina wa Makka kabla ya kutangazwa dini ya Uislamu, Mapatano ya Hudaibiyya, mwenendo wa Mtume Muhammad (saw) na jinsi alivyokuwa akiamiliana na tawala na wafalme wa maeneo mbalimbali kama Iran na Roma na kutumia njia ya kutuma barua kwa watawala na wafalme wa zama hizo baada ya kuunda dola la Kiislamu mjini Madina. Kwa mfano tu Mtume (saw) alisema katika amri aliyompa Amru bin Hazm wakati alipomtuma Yemen kwamba: Kila Myahudi au Mkristo atakayekubali Uislamu na kudhihirisha Uislamu halisi atakuwa mmoja kati ya waumini, atakuwa na haki sawa na za Waislamu na kushirikiana nao katika vipindi vyote vya shida na raha. Na kila mtu atakayeamua kubakia katika dini yake ya Uyahudi au Unaswara kamwe hatalazimishwa kuacha dini yake, kwa sababu ujumbe wa dini na risala za Mitume wote wa Mwenyezi Mungu ni kuleta amani, uadilifu, kueneza masuala ya kiroho,kumkamilisha mwanadamu na kumfikisah kwenye saada na ufanisi", mwisho wa kunukuu. Kwa msingi huo, katika mtazamo wa Uislamu suala la usalama na kuishi kwa amani na wanadamu wengine wenye itikadi na imani tofauti, ni jambo lenye thamani na umuhimu mkubwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, ni katika mazingira ya amani na usalama ndipo wanadamu wanapoweza kuelekea kwenye ukamilifu wa kimaada na kiroho, bali hata kuweza kumjua na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Hivyo suala la kujenga na kuimarisha amani na usalama na vilevile juhudi za kulingania amani na usalama wa kimataifa na kuishi pamoja kwa amani wanadamu wote kwa msingi wa Tauhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu, uadilifu na usafi wa nafsi bila ya kujali dini, rangi, na tofauti zao nyingine ndio lengo la mwisho la Uislamu na wafuasi halisi wa dini hiyo. Ni wazi kuwa, kufuata mafundisho ya dini hiyo kunaweza kuwa suluhisho la kumwondoa mwanadamu katika kinamasi cha vita, mapigano na migogoro ya dunia ya sasa. Ndugu zangu waislamu nimejaribu kutoa ufafanuzi mrefu kidogo kuhusu uislamu na amani.Dini zote hapa duniani zinahubiri amani.Hata akija kiongozi wa dini ya kikristu ataeleza namna biblia takatifu inavyosisitiza amani.Ninawataka ndugu waislamu na wasio waislamu mnaonisikiliza hivi sasa kokote mliko wekeni silaha zenu chini na turejee kuishi kwahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/amanai kama ilivyokuwa hapo kabla.Tuiachie serikali ilifanyie uchunguzi jambo hili tujue nani katufikisha hapa? Nani waliotufarakanisha hadi ndugu tukaanza kuuana? Nawasihi tuweke mbele maslahi ya nchi yetu.Tuna nchi moja tu na tazameni kilichotupata baada ya kuvuruga amani.Tumekosa hata sehemu ya kukimbilia kwani sisi kwa miaka mingi tumekuwa ni kimbilio la wale wote ambao amani imepotea katika nchi zao. Mufti alimaliza hotuba yake kwa kuendelea kuwasisitiza waumini wa dini ya kiislamu na wa dini nyingine kuachana na vurugu ili amani irejee.Baada ya kumaliza kutoa hotuba Mufti na Dr Fabian wakaenda kupata chakula cha mchana pamoja. WASHINGTON DC – MAREKANI Saa tano za asubuhi, Mark Piller makamu wa Rais wa Marekani aliwasili katika nyumba kubwa aliyokuwa akiishi jenerali Akiki Rwamirama.Lilikuwa ni jumba kubwa la kifahari lililokuwa na viwanja vya michezo mbali mbali kama vile mpira wa kikapu,mpira wa wavu na tenisi.Kulikuwa na miti mingi kulizunguka jumba hilo na kulifanya kuwa na utulivu mkubwa,ni sauti za ndege mbali mbali ndizo zilisikika. Jenerali Akiki hakuwa na taarifa kama Mark Piller angekwenda kumtembelea.Alikuwa ndani ya sebule kubwa akitazama runinga akifuatilia taarifa za habari za vyombo mbali mbali vya habari duniani na kubwa alilokuwa analifuatilia ni taarifa za kuhusiana na kile kilichokuwa kinaendelea Afrika mashariki hususan nchini Uganda. Mlango mkubwa wa sebuleni ukagongwa na mmoja wa walinzi wake akaenda kuufungua akakutana na walinzi wa makamu wa Rais.Nje tayari msafara wa makamu wa Rais ulikwisha wasili na alikwisha shuka akipiga hatua kuelekea ndani.Jenerali Akiki alipojulishwa kuwa ni makamu wa Rais amefika akainuka haraka na kwenda kumpokea “Mheshimiwa Rais habari yako” akasema Mark Piller “Mark niite Akiki inatosha.Hayo mambo ya Rais yamekwisha pita.Mimi si Rais tena wa Uganda” akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki sisi tunaendelea kukutambua kama Rais halali wa Uganda hivyo tutaendelea kukupa heshima yako ya Rais” akasema Mark “Nashukuru sana Mark.Karibu” “Ahsante jenerali Akiki.Tunaweza kutembea tafadhali” akasema Mark na Jenerali Akiki akamuongoza wakaelekea katika uwanja wa gofu. “Jenerali Akiki vipi maisha yako yanakwendaje hapa?Unayafurahia?akauliza Mark Piller “Maisha yanakwenda vizuri sana mheshimiwa makamu wa Rais. Ninayafurahia maisha.Tayari akili yangu imekwisha anza kuzoea maisha haya.Kwa ujumla hakuna tatizo lolote.Ninashukuru sana kwa namna mnavyonihudumia.Ninapata kila ninachokihitaji”akasema Jenerali Akiki “Ninafurahi kusikia hivyo mheshimiwa Rais.Ninakuahidi utaishi maisha mazuri kama uko peponi.Utapata kila unachokihitaji na utayasahau maisha yako yaliyopita” akasema Mark Piller “Ahsante Mark.Sikutegemea kama baada ya kuondolewa madarakani ningekuwa na maisha mazuri kama haya.Washenzi wale wametaifisha mali zangu zote na bila ninyi ningekuwa masikini wa kutupwa” akasema Jenerali Akiki “Niliwahi kukwambia Jenerali Akiki kwamba yanapofanyika mapinduzi rais aliyepinduliwa mara nyingi lengo huwa ni kumuua lakini kama akinusurika akakimbia basi mali zake zote ndani na nje ya nchi hutaifishwa na serikali iliyochukua madaraka.Lakini hilo lisikuumize kichwa kwa sasa wewe ni tajiri na utakuwa na mali mara mbili zaidi ya zile ulizokuwa nazo ulipokuwa madarakani.Hata kama ukitaka familia basi unao uwezo wa kuanzisha familia tena kubwa.Kila kitu kinawezekana mheshimiwa Akiki”akasema Mark Piller “Mambo yanaendeleaje Afrika Mashariki ?akauliza Jenerali Akiki “Mambo yanakwenda vizuri mheshimiwa Akiki.Meli zetu kubwa za mafuta zimepanga foleni katika bandari ya Tanga zikipakia mafuta.Kwa ujumla kila kitu kinakwenda vyema” “Safi sana.Nataka ikiwezekana mchukue mafuta yote yaliyopo Uganda muyalete huku kwa watu ambao wana shukrani na utu.Nimeijenga Uganda lakini shukrani zake ni hizi.Mark kama upo uwezekano wa kuongeza zaidi uchukuaji wa mafuta fanyeni hivyo tafadhali”akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki hilo ndilo lililonileta hapa kwako.Jana nilikuwa na mazungumzo marefu na Rais kuhusiana na mpango huu unaoendelea.Katika mazungumzo yetu tumekubaliana kwamba tutanue zaidi operesheni hii.Unajua Afrika Mashariki ni tajiri sana.Tunataka tusiishie kwenye mafuta peke tunataka twende mbali zaidi tuingie hadi katika rasilimali nyingine kama vile madini.Nchi kama Tanzania imebarikiwa madini ya kila aina.Nchi kama jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nayo vile vile ina madini ya thamani.Tanzania kwa mfano ina madini ya dhahabu,almasi,na mengine mengi bila kusahau madini ya Tanzanite ambayo hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani zaidi ya Tanzania pekee.Tunataka operesheni yetu sambamba na mafuta iende pia katika maeneo hayo niliyoyataja.Nimekuja hapa kwako kupata ushauri unadhani nini tufanye kutanua operesheni hii Afrika mashariki? Akauliza Mark Piller “Mheshimiwa makamu wa Rais tena imekuwa vizuri umefika.Muda mfupi kabla hujafika hapa nilikuwa natazama kile kinachoendelea Afrika mashariki.Leo kuna jambo limetokea nchini Tanzania” “Kumetokea nini Tanzania ?akauliza Mark Piller “Rais wa Tanzania amekutana na Sheikh mkuu wa Tanzania na wamekuwa na kikao kirefu wakizungumzia vurugu zinazoendelea.Kikao hicho kinaonekana kuwa na mwelekeo mzuri wa kumaliza vurugu hizo zinazoendelea.Nimezisikiliza hotuba aliyoitoa Mufti na kwa kiasi kikubwa inaweza kuwashawishi waumini kuachana na vurugu zinazoendelea.Kwa kawaida waumini wa dini ni watiifu mno kwa viongozi wao hivyo kama wameambiwa na kiongozi wao waache vurugu basi watafanya hivyo.Watanzania ni wepesi sana wa kumaliza mambo kwa amani na kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa leo,tayari vurugu zimeanza kupungua nchini Tanzania na hii inatokana na hotuba ya jana ya Rais Dr Fabian” akanyamaza akamtazama Mark Piller “Mpango huu uliojadiliana na Rais wako ni mpango mzuri sana na wenye manufaa kwa Marekani lakini ili mpango huo ufanikiwe tunaihitaji mno Tanzania.Vurugu lazima ziendelee nchini Tanzania ili majeshi ya Marekani yaendelee kukaa nchini humo na kama ikiwezekana basi wanajeshi waongezezwe zaidi.Tanzania haitakiwi ipate amani kwani ikiwa shwari hakutakuwa na ulazima wa vikosi vya Marekani kuendelea kuwepo na hivyo hatutaweza tena kuendelea na uchukuaji wa mafuta na rasilimali nyingine” akasema Jenerali Akiki “Nini unashauri kifanyike Jenerali Akiki? Tunategemea sana ushauri wako kwa kuwa wewe unalifahamu vyema eneo la Afrika mashariki.Ushauri wowote utakaoutoa tutauzingatia” akasema Mark Piller “Kunatakiwa kufanyike kitu cha haraka sana kuhakikisha hali inaendelea kuwa tete nchini Tanzania ili vikosi vya Marekani viendelee kukaa huko kwa muda mrefu zaidi na kama ikiwezekana viongezwe vikosi vingine” akasema Jenerali Akiki “Nini basi unashauri kifanyike kwa haraka?Mimi na mheshimiwa Rais tulifikiria kuanzisha kikundi cha waasi ambacho tutakiwezesha kwa silaha na zana nyingine za kijeshi ambacho kitaendesha mapigano na serikali za Afrika mashariki ili tupate nafasi ya kuongeza wanajeshi zaidi katika eneo la Afrika Mashariki.Unaonaje kuhusu mpango huo?akauliza Mark Piller “Huo ni mpango mzuri lakini si muafaka kwa sasa.Kuanzisha kikundi cha waasi ni mpango wa muda mrefu.Si jambo jepesi kuanzisha uasi hasa katika nchi kama Tanzania.Kwa nchi ya jamhuri ya kidemo krasia ya Congo kule hakuna shida kwani wamekwisha zoea mambo kama hayo lakini kwa sasa tunalenga zaidi Tanzania hivyo wazo la kuanzisha kikundi hicho cha uasi tuliweke pembeni tutalishughulikia taratibu”akasema Jenerali Akiki “Vipi kuhusu kuwatumia IS kufanya mashambulio mbali mbali ya kigaidi na kuua watu?akauliza Mark Piller “Hilo nalo ni wazo zuri lakini bado si mpango mzuri tunaouhitaji kwa sasa.Tunatakiwa kufanya kitu cha haraka” “Nini basi unashauri kifanyike kwa haraka jenerali Akiki?akauliza Mark Piller na Jenerali akiki akainamisha kichwa akafikiri kisha akasema “Hapa Marekani mnao wanasayansi wa hali ya juu.Nataka muwatumie wataalamu hao kutengeneza kirusi ambacho kitakuwa ni hatari na ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa kitakachokwenda kusambazwa nchini Tanzania” “Kirusi? Akauliza Mark Piller “Ndiyo Mark.Mnatakiwa kutengeneza kirusi ambacho kinaweza kuwa hatari zaidi na kwenda kukisambaza nchini Tanzania ambacho kitasambaa kwa haraka zaidi na kusababisha vifo vya watu wengi.Baada ya hali kuwa mbaya Marekani itaongeza wanajeshi Tanzania kwa lengo la kwenda kutoa msaada wa kibinadamu.Faida za mpango huu ni kwamba vikosi vya Marekani vitaongezwa na kukaa kwa muda mrefu Afrika mashariki na kuendelea kuchukua mafuta na rasilimali nyingine kama madini” akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki wazo lako ni zuri lakini linaonekana ni la hatari kubwa.Wasi wasi wangu ni vipi kama kirusi hicho kitaweza kuvuka katika mipaka ya Tanzania na kusambaa sehemu mbali mbali duniani na hatimaye kikafika hadi Marekani? Tunaweza kuwa tumetengeneza silaha ambayo inakuja kutuua sisi wenyewe.Wanajeshi wetu walioko Tanzania wanaweza wakaambukizwa ugonjwa huo wakafa au wakaja kusambaza virusi hivyo huku Marekani” “Mark Piller hiyo ndiyo njia pekee na ya haraka ambayo mnaweza mkaitumia ili vikosi vya Marekani viendelee kukaa Afrika Mashariki na hasa Tanzania.Wanasayansi wenu watakapotengeneza kirusi hicho hatari watatengeneza pia na kinga yake na wanajeshi watakaokuwa Tanzania na wale watakaopelekwa huko watapata kinga hiyo hivyo wao hawatadhurika na hicho kirusi” akasema Jenerali Akiki.Mark Piller alishindwa ajibu nini wakabaki wamesimama wakitazama farasi kila mmoja akiwaza lake. “Unalionaje wazo hilo Mark?akauliza Jenerali Akiki “Jenerali Akiki ninashindwa kukupa jibu la haraka haraka kwani mpango huu ni mkubwa na wa hatari sana” “Nini hofu yako Mark?akauliza Jenerali Akiki “Hofu yangu ni kwamba tunaweza kutengeneza kirusi hicho hatari halafu kikageuka na kuwa kisu cha kutuangamiza sisi wenyewe.Kitu kama kirusi kinaweza kusambaa kwa haraka sana na kufika hadi Marekani kitu ambacho hatutaki kitokee na ndiyo maana umeona Marekani hatupigani vita nyumbani tunamfuata adui huko huko aliko.Tunataka raia wetu wawe salama siku zote ndiyo maana ninahofu kwamba tunaweza kutengeneza kirusi na kikasambaa na kufika hadi Marekani na kuua watu wetu” akasema Mark Piller “Hakuna haja ya kuwa na hofu Mark.Nimesema wanasayansi watengeneze kirusi na kinga yake na kila juhudi lazima zifanyike kuhakikisha kwamba kirusi hicho hakivuki nje ya mipaka ya Tanzania.Mzilenge nchi za Tanzania,Uganda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Tena mkitaka kufanikiwa zaidi tengenezeni kirusi ambacho kitasambaa kwa njia ya hewa ili kiweze kusambaa kwa haraka zaidi.Nakuhakikishia Mark kwamba hii ndiyo njia pekee nyepesi ya kuweza kuongeza vikosi Afrika mashariki na kuendelea kuchota rasilimali.Njia nyingine kama makundi ya waasi hizo zitakuja baadae” akasema Jenerali akiki “Jenerali Akiki naomba nilichukue suala hili na kwenda kujadiliana na wenzangu tuone namna tutakavyoweza kulitekeleza lakini ni suala zuri na ahsante sana kwa wazo hili zuri” akasema Mark Pilller “Mark muda unakwenda kwa kasi na taratibu amani imeanza kurejea Tanzania na kama Tanzania ikiwa na amani basi hata Uganda nako kutakuwa na amani.Hampaswi kuacha jambo hili likatokea .Wakati wakiendelea na mikutano yao ya kutafuta amani wanatakiwa wapigwe tena pigo lingine kabla majeraha yao hayajapona” akasema Jenerali Akiki “Ahsante sana jenerali Akiki tutalizingatia hilo.Ninakwenda kuzungumza na wenzangu halafu nitakupa mrejesho nini tumekubaliana. RIYADH – SAUDI ARABIA Kiza kimeanza kutanda katika anga la jiji la Riyadh.Katika makazi ya Habiba Jawad idadi ya watu waliofika kuhudhuria msiba wa mwanae Najma aliyezikwa mchana wa siku hiyo baada ya kujiua kwa kujipiga risasi ilikuwa kubwa.Ulikuwa ni msiba mkubwa kwa Habiba Jawad ambaye huyu alikuwa ni mtoto wake wa pili kufariki baada ya Edger Kaka. Wakati watu wakiendelea na maombolezo Habiba Jawad aliyekuwa katika mojawapo ya nyumba zilizopo katika makazi yake akiwa na akina mama waliofika kumfariji, simu yake ikaita akaitoa haraka haraka kutazama mpigaji kisha akaikata ile simu.Taratibu akainuka na kuaga anakwenda maliwato.Hakutaka mtu yeote amsindikize.Alitoka ndani ya ile nyumba akafuata ujia kuelekea katika nyumba yake na moja kwa moja akaenda katika ofisi yake akawasha runinga kubwa na akaonekana David Walker. “Habari yako Habiba” akasema David Walker “Nzuri David habari yako” “Habiba unaonekana hauko sawa leo.Kuna tatizo lolote?akauliza David “Nina msiba David.Mwanangu amefariki jana na leo tumemzika” “Pole sana Habiba.Hukutujulisha kama una msiba” “Usijali David.Nini kinaendelea huko? Akauliza Habiba “Habiba kuna jambo ambalo limejitokeza na tunahitaji msaada wako” “Sema David nini mnahitaji?akauliza Habiba “Tumekuwa tunafuatilia kwa karibu sana kile kinachoendelea Tanzania na siku ya leo Rais wa Tanzania amekutana na kiongozi wa dini na kubwa walilolizungumza ni kuhusiana na vurugu zinazoendelea katika ukanda huo wa Afrika mashariki.Mazungumzo hayo ya leo kati ya rais na kiongozi huyo yanaonekana kwa na mwelekeo wa kumaliza vurugu zile za kidini zinazoendelea Afrika Mashariki.Endapo vuruguzile zitamalizika basi hakutakuwa na ulazima wa vikosi vyetu kuendelea kuwepo Afrika mashariki na lengo letu ni kuendelea kukaa hapo kwa muda mrefu na hata kuongeza wanajeshi zaidi.Kwa hiyo tumeamua kufanya kitu cha haraka ambacho kitatuwezesha kupeleka vikosi zaidi vya jeshi na kukaa Afrika mashariki kwa muda mrefu zaidi” akasema David Walker “Mmekuja na mpango gani? Habiba akauliza “Tunataka kutengeneza kirusi ambacho kitafanya maangamizi makubwa ambacho kitakuwa hatari kuzidi kirusi cha Ebola.Tutakwenda kukisambaza kirusi hicho Tanzania na baada ya hali kuwa mbaya tutatuma vikosi zaidi vya jeshi kwenda huko kwa lengo la kutoa msaada lakini papo hapo operesheni zetu zikiendelea kama kawaida” “David hili la kusambaza kirusi huoni kama ni jambo la hatari?Ni vipi kama kirusi hicho kitavuka mipaka na kusambaa sehemu nyingine duniani?Mnao wanajeshi wenu kule ni vipi kama wakipata virusi hivyo? Akauliza Habiba “Hilo tayari tumekwisha lijadili kwa kirefu sana.Mwanasayansi anayeandaa kirusi hicho tumempa maelekezo ya kuhakikisha kwamba atakapokamilisha kutengeneza kirusi hicho aandae na kinga yake kwa ajili ya wanajeshi wetu na tahadhari endapo kirusi hicho kitavuka mipaka ya Afrika Mashariki na kuenea sehemu nyingine duniani.Hilo halina tatizo kabisa Habiba” “Nini natakiwa kufanya kwa upande wangu?akauliza Habiba ambaye hakuonekana kutaka maongezi marefu “Kwa upande wako tunataka utusaidie kupata mtu ambaye atapeleka kirusi hicho Tanzania.Tunataka mtu kutoka kundi la IS”akasema David “David kwa nini lazima awe ni mtu kutoka IS?akauliza Habiba “Habiba hili ni shambulio la kibaolojia hivyo basi mtu huyo hapaswi kuwa mmarekani.Tunataka kumtuma mtu wa kundi la IS ili hata kama akigundulika basi ijulikane kuwa ni kundi la IS ndio waliofanya shambulio hilo.Nataka ufanye makubaliano na kundi la IS wape fedha za kutosha waweze kutupatia huyo mtu ambaye anatakiwa hapa Marekani haraka sana ili aanze kuandaliwa.Mtu huyo atawekewa kwanza kinga ya kumkinga dhidi ya kirusi hicho halafu atapandikizwa kirusi hicho ambacho atakwenda kukisambaza Tanzania” akasema David Walker “Lini huyo mtu anahitajika?akauliza Habiba “Tunamuhitaji haraka iwezekanavyo.Tunataka kabla ya amani haijarejea Tanzania basi tuwapige na hicho kirusi.Hatutaki kuwapa nafasi ya kupumua.Namuhitaji huyo mtu haraka sana.Fanya kila uwezalo mtu huyo aweze kupatikana haraka sana” akasema David “Sawa David nitajitahidi” “Ahsante sana Habiba na pole sana kwa tatizo hili kubwa.Kuna chochote tunaweza kusaidia? “Ahsante David.Tutawasiliana pale nitakapokuwa nimempata huyo mtu” akasema Habiba na kuzima ile runinga “Mauaji yanayoendelea hivi sasa nchini Tanzania bado hayatoshi na wanataka kusambaza tena virusi na kuendelea kuua watu.Yote hii ni kwa sababu ya kutaka kuchukua rasilimali ambazo Mungu amewajalia watu wa Afrika Mashariki.Lazima nitafute namna ya kufanya ili niweze kuzuia mpango huu usifanikiwe.Ningeweza kumpigia simu Mathew Mulumbi lakini sifahamu mahala alipo hivi sasa.Hata hivyo lazima nifanye kitu.Huu lazima uwe ni mwisho wa hiki kikundi chenye kufanya maangamizi makubwa duniani” akawaza Habiba na kuwasiliana na mtu mmoja kutoka kundi la IS akampa maelekezo kama alivyokuwa ameelekezwa na David na mtu Yule akamtaka Habiba ampe muda alishughulikie lile suala kisha atamjulisha.Alimtajia kiasi cha fedha ambacho angetakiwa kukitoa kwa ajili ya suala lile.Baada ya kulimaliza hilo suala Habiba akarejea katika nyumba waliko akina mama waliokuja kuungana naye katika msiba. Saa tatu za usiku wakawasili Abu Dahir na mke wake Nawal.Kama ilivyokuwa kwa Mathew na Najma nao pia walikuwa mapumzikoni.Habiba Jawad aliwapa wanae wote mapumziko ya miezi minne.Abu Dahir na Nawal hawakuweza kuwahi mazishi ya Najma kutokana na kutopata taarifa kwa haraka.Baada ya kuwasili Abu Dahir alikwenda kuungana na waombolezaji wengine waliofika pale nyumbani kuwafariji.Nawal yeye alikwenda kuungana na akina mama waliokuwa wanamfariji Habiba. Saa tano za usiku tayari watu wengi walikwisha ondoka.Ni watu wachache tu waliokuwa wamebaki na ndipo Abu Dahir alipoweza kupata nafasi ya kuzungumza na mama yake ili aweze kumueleza kile kilichotokea hadi kupelekea Najma kujiua kwa kujipiga risasi.Habiba Jawad akawataka Abu Dahir na Nawal waelekee nyumbani kwake akawakaribisha katika sebule yake “Mama utatusamehe sana kwa kushindwa kuwahi mazishi ya Najma.Tuliipata taarifa kwa kuchelewa na tulijitahidi sana kwa kila namna ili tuweze kuwahi leo lakini ilishindikana ” akasema Abu Dahir “Usijali Abu.Nilifahamu hamtaweza kuwahi mazishi” akasema Habiba “Mama nini hasa kilichotokea? Kwa nini Najma alijiua?Abu Zalawi yuko wapi?akauliza Abu Dahir akionekana kuwa na shauku sana ya kutaka kufahamu kila kitu kuhusiana na tukio lile. “Poleni sana vijana wangu kwa hiki kilichotokea.Mpaka sasa bado siamini kama kweli Najma binti yangu wa pekee amekwenda na hatutamuona tena.Najma ameondoka na afya na uzuri wake.Imeniumiza sana” akasema Habiba Jawad “Nini hasa kimetokea mama hadi kupelekea Najma kuchukua maamuzi haya magumu namna hii? Akauliza Abu Dahir “Ni hadithi ndefu Abu lakini lazima nikiri kwamba mimi ndiye niliyesababisha kifo chake” “Wewe ndiye uliyesabisha kifo chake? Kivipi mama? Abu Dahir akauliza “Sikumuua kwa mkono wangu lakini kuna maneno nilimueleza na hayo ndiyo yaliyopelekea akachukua maamuzi yale ya kujiua” “Ulimweleza nini mama? Akauliza Nawal na Habiba akamtazama Abu Dahir kisha akasema “Nilimueleza ukweli” “Ukweli? Abu Dahir akashangaa “Ndiyo Abu.Dada yako nilimueleza ukweli” “Sijakuelewa mama.Ukweli upi uliomueleza hadi akaamua kujipiga risasi? Abu Dahir akauliza “Kuna mambo mengi ambayo wewe na ndugu zako hamkuwa mkiyafahamu hasa kuhusu mimi na kile kinachoendelea katika maisha yangu.Nadhani ni wakati wa kuweka mambo wazi ili wewe pia ufahamu” akasema Habiba na Nawal akasimama “Nawal unakwenda wapi? Habiba akauliza “Ninadhani mazungumzo haya yanawahusu zaidi ninyi” akasema Nawal “Hapana Nawal kaa.Wewe pia ni mwanafamilia na ni sehemu ya haya ninayotaka kuyazungumza.Umefika wakati wa kila kitu kuwekwa mahala peupe” akasema Habiba “Huyu mama anataka kufanya nini tena?Mbona muelekeo wake siuelewi?akajiuliza Nawal “Mama kabla hujaendelea nataka kufahamu yuko wapi Abu Zalawi? Abu Dahir akauliza “Abu Zalawi hayupo na hajui kama mke wake Najma amefariki dunia” “Hajui kuhusu kifo cha Najma? Akauliza Nawal “Ndiyo hajui chochote kuhusu kifo cha Najma” “Mama nashindwa kuelewa.Hawa walikwenda mapumzikoni kama tulivyofanya sisi.Nini kili…..” “Niliwarudisha mimi” akasema Habiba na kumkatisha Abu Dahir “Nilimuhitaji Abu Zalawi hivyo nikawasiliana nao na kuwataka warudi nyumbani mara moja.Baada ya kurejea mimi na Abu Zalawi tulifanya safari ya kwenda Marekani na Abu Zalawi alibaki huko” “Alibaki huko? Nawal akauliza “Ndiyo.Alibaki huko na ninapenda kuwajulisha kwamba AbuZalawi hatarejea tena hapa kwetu.Amekwisha ondoka katika maisha yetu” “Mama sijakuelewa.Nini kinaendelea hapa? Mama naomba tafadhali unieleze kila kitu.Naona kuna mambo mengi yamejificha hapa”Akasema Abu Dahir “Abu kama unavyofahamu kwamba baba yako alikuwa mstari wa mbele sana katika kupigania haki na aliuawa akiwa katika mapambano ya kudai haki za wapalestina.Baada ya kifo chake nilivaa viatu vyake na kuendelea na harakati za kudai haki.Nimekuwa nikitoa msaada wa kifedha kwa vikundi mbali mbali vinavyoendesha harakati za kudai haki za wapalestina kutoka kwa taifa la Israel.Si vikundi vya kipalestina tu ambavyo vimekuwa vikipokea msaada kutoka kwangu katika kufanikisha harakati mbali mbali za kudai haki bali nimekuwa nikifadhili makundi mengine kama vile IS kufanikisha mipango yao mbali mbali.Kundi la IS linajulikana kama kundi hatari zaidi la kigaidi kwa sasa duniani na kitendo cha kulifadhili kimenifanya niwindwe na mashirika mbali mbali ya kijasusi na hasa Mossad.Pamoja na kuwindwa huko na Mossad lakini hadi leo hii hawajawahi kunikamata.Umeshawahi kujiuliza swali kwa nini? Akauliza Habiba na Abu Dahir akatikisa kichwa kwamba hajaui. “Kuna siri imejificha hapa kwa nini sijawahi kukamatwa licha ya kutajwa kuwa mfadhili mkubwa wa makundi ya ugaidi duniani” Habiba akanyamaza na kuwatazama Abu Dahir na Nawal “Siri ambayo hamuifahamu ni kwamba ninafanya ufadhili huu kwa makundi ya magaidi kwa niaba ya Marekani” “Marekani ? Abu Dahir akashangaa “Ndiyo Abu.Mimi ni wakala wao.” “Marekani wanafadhili ugaidi? Abu akazidi kushangaa “Ni vigumu kuamini Abu lakini huo ndio ukweli” “Marekani imekuwa ikiendesha vita dhidi ya ugaidi duniani na tumekuwa tukiona namna inavyopata mafanikio makubwa katika vita dhidi hiyo.Iweje kwa upande wa pili wawe na ushirika na magaidi? Akauliza Abu “Hiyo ni siri kubwa Abu Dahir.Ni siri ambayo hata Rais wa Marekani haifahamu” akasema Habiba na kunyamaza kidogo “Ndani ya shirika la ujasusi la Marekani CIA kuna kitengo maalum ambacho kinashughulika na jambo hilo.Ni kitengo cha siri sana na hata waliomo ndani ya CIA hawakifahamu” Habiba akanyamza baada ya Nawal kuonyesha mshangao “Kitengo hiki kazi yake kubwa ni kushughulikia mahusiano na makundi ya kigaidi kwa maslahi ya Marekani.Baba yako ndiye aliyekuwa akitumiwa katika kufadhili ugaidi na aliuawa baada ya kwenda kinyume na matakwa ya Marekani.Baada ya kuuawa nilivaa viatu vyake na kuendelea na kile alichokuwa anakifanya” “Siamini hayo unayonieleza mama.Kwa muda huu wote mmekuwa mkifanya kazi kwa niaba ya Marekani? “Ndiyo Abu.Tumekuwa tukifanya kazi kwa niaba ya Marekani.Alianza baba yako na mimi nimefuata na utajiri huu wote tulionao umetokana na hicho tunachokifanya.Wameniwezes ha utajiri mkubwa niweze kuutumia kufadhili ugaidi kwa niaba yao.Hawataki kujulikana” “Kwa nini ukakubali mama kubeba jukumu hili kubwa mabegani mwako?Kwa nini ukakubali kuchafua jina lako kwa kuwa mfadhili wa ugaidi duniani wakati kumbe wafadhili wakuu wa ugaidi wapo? Akauliza Abu Dahir “Ilikuwa ni lazima nifanye hivyo Abu.Hii imekuwa ni siri yangu kubwa sana na sikupanga kuwaeleza lakini imebidi mfahamu kila kitu” akasema Habiba “Kwa nini umeamua kutueleza mama? Akauliza Nawal “Kwa sababu ni wakati muafaka kwa ninyi kufahamu kile kinachoendelea” akajibu Habiba “Kama nilivyokueleza Abu kwamba baba yako ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifanya kazi hii na mimi niliendelea pale alipoishia yeye.Nimeifanya kazi hii kwa muda mrefu kwa maslahi ya marekani na sasa umefika wakati ambao sitaki kuendelea tena na hiki ninachokifanya kwani hakipendezi machoni pa Mungu.Nimekwisha kuwa mzee sasa na ninahitaji kujiweka karibu na Mungu wetu na sitaki tena kuendelea kukatili roho za watu wasio na hatia.Katika makubaliano yetu na kikundi hiki ni kwamba nitaifanya kazi hii ya kufadhili ugaidi kwa niaba yao hadi pale nitakapovuta pumzi yangu ya mwisho na ndiyo maana wameniwezesha kuwa na utajiri mkubwa sana.Kitendo chochote cha kutaka kujiondoa katika jambo hili ni kuhatarisha usalama wangu na wa familia yangu.Hivi tuzungumzavyo ninyi wanangu wote mnafuatiliwa na muda wowote ambao nikijaribu kwenda kinyume na matakwa yao watawaondoa ndiyo maana nimekuwa kimya sijawahi kuwaeleza kuhusu jambo hili.Nataka muwe salama” akasema Habiba “Unataka tuwe salama? Akauliza Abu Dahir kwa ukali “Abu chunga ulimi wako unapozungumza nami ! akafoka Habiba akionekana kutopendezwa na namna mwanae alivyouliza kwa ukali “Mama ingekuwa vyema ungeendelea kubaki na siri hii na ukafa nayo.Kuamua kutueleza ukweli ni kuhatarisha zaidi maisha yetu.Tazama umemueleza ukweli Najma na akaamua kujiua” akasema Abu Dahir “Abu imenilazimu niwaeleze ukweli ili hata ikitokea nikiondoka leo mjue ni kitu gani kilikuwa kinaendelea katika maisha yangu” akasema Habiba na kunyamaza akamtazama Abu “Ili niweze kujiondoa katika jambo hili ilinilazimu kuja na mpango maalum na hapo ndipo nilipoamua kuwaleta hapa Abu Zalawi na Nawal” akasema Habiba na kunyamaza.Nawal alionyesha wasi wasi mwingi “Abu Dahir,kuna jambo ambalo hujalifahamu bado” akasema Habiba “Mama una siri nyingi umetuficha.Tafadhali kama umeamua kueleza ukweli tueleze kila kitu” akasema Abu Dahir “Ni kuhusu Abu Zalawi na Nawal” akasema habiba “Mama” akaita Nawal “Nawal muache mama aseme anachotaka kukisema” akasema Abu Dahir “Nawal usiwe na hofu.Nataka kila kitu kiwe wazi leo” akasema Habiba “Endelea mama.Kuna nini kuhusiana na hawa watu wawili? Akauliza Abu Dahir “Abu Zalawi na Najma nimewatoa katika lililokuwa kundi la Ammar Nazari brigades.Wawili hawa ni majasusi na walikuwa katika misheni maalum na siyo magaidi.Niliamua kuwachukua na kushirikiana nao kwa ajili ya kw……….” “Mama sijakuelewa.Umesema Nawal na Abu Zalawi ni majasusi na si magaidi?Nawal si alikuwa mke wa Ammar Nazari? Akauliza Abu Dahir na kabla Habiba hajajibu Nawal akasimama “Ni kweli Abu Dahir hiki anachokisema mama yako” Akasema Nawal na kutazama na Abu “Siamini masikio yangu ! akasema Abu Dahir “Mama yako ameamua kuweka kila kitu wazi hivyo hakuna haja ya kuficha chochote.Ni kweli mimi na Abu Zalawi ni majasusi na tulikuwa katika kundi la Ammar Nazari Brigades kwa misheni maalum.Mimi ni jasusi toka CIA Marekani na mwenzangu Abu Zalawi anatokea Mossad.Jina lake halisi ni Mathew Mulumbi na si Abu Zalawi kama anavyojulikana.Katika kundi la Ammari Nazari Brigades mimi nilikuwa na kazi ya kumsaka gaidi mmoja ambaye ana undugu na Ammar Nazari ambaye aliwahi kufanya mauaji makubwa Marekani na kukimbia hivyo niliuganishwa na Ammar na nikawa mke wake.Abu Zalawi yeye alitokea Mossad na alikuwa na misheni maalum aliyotumwa kuitekeleza ambayo ni kumuua Habiba Jawad.Mossad wanafahamu kwamba Habiba amekuwa akifadhili makundi mbali mbali ya wanamgambo wa kipalestina ambao wamekuwa wakiendesha mashambulio mbali mbali ndani ya Israel hivyo wanamtafuta sana Habiba na wakamtumia Abu Zalawi ili kuungana na Ammari Nazari na kutengeneza njia ya kufika kwa Habiba Jawad.Baada ya Ammar Nazari kuuawa na vikosi vya Israel mimi na Abu tuliondoka na kuanza harakati za kumsaka Habiba Jawad lakini tulipofika hapa misheni ikabadilika.Ile mipango ya kumuua Habiba Jawad ikatoweka na badala yake tukajikuta tukiungana na Habiba Jawad katika mipango yake na kuwa wanafamilia” akasema Nawal na Abu Dahir akaonekana kuchanganyikiwa. “Abu Zahir anachokisema mama yako ni………..” akasema Nawal na Abu akamnyamazisha “Nyamaza ! akasema Abu Dahir kwa sauti kali “Wewe na huyu mwanamke wote mko sawa.Wote mama yenu mmoja.Wote ni mashetani waongo wakubwa.Nawal nilikupenda sana na nikawa tayari kufanya chochote kwa ajili yako.Kwa nini nawe ukashiriki uongo huu mkubwa wa mama? Na wewe mama kwa nini ukanishawishi nimuoe Nawal wakati ukifahamu kwamba ni jasusi? Kwa nini hukunieleza ukweli? Akafoka Abu aliyekuwa amepandwa na hasira “Nilikuwa na sababu maalum za kutaka umuoe Nawal” “Ulikuwa unachunguza maisha yetu mimi na Najma ndiyo maana ukatutaka tuwe na mahusiano na hawa majasusi ? Abu akauliza “Hapana sijawahi kuwachunguza.Nilitaka kuwalinda” “Mama wewe una roho ya kishetani kabisa ndiyo maana hujawahi kusikitika hata siku moja kwa watu wanaouawa na magaidi ambao unawafadhili.Najuta kuzaliwa nawe Habiba ! akasema kwa ukali Abu Dahir na Nawal aliyekuwa karibu yake akamnasa kofi “Iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho kumtusi mama yako.Pamoja na yote anayoyafanya na aliyoyafanya huyu bado ni mama yako na ataendelea kuwa mama yako daima.Huyu ndiye aliyekubeba tumboni mwake miezi tisa na akakulea hadi umefika hapa ulipofika.Nakuonya tena ukithubutu kumtusi mama yako mbele yangu nitakufundisha adabu.Hapa unaponiona mimi sina uwezo wa kuzaa mtoto.Nimekwisha ondolewa kizazi.Unajua ni uchungu gani ninaupata kwa kukosa mtoto?Usirudie tena kumtusi mama yako ! akasema Nawal kwa ukali huku akilengwa na machozi.Abu Dahir akamtazama Nawal kwa macho ya mshangao. “Huna kizazi?! Akauliza akiwa ameshika shavuni mahala aliponaswa kofi “Ndiyo sina kizazi na siwezi kupata mtoto ! akajibu Nawal bila hofu “Nawal toka tumefunga ndoa tumekuwa katika jitihada mbali mbali za kutafuta mtoto na umekuwa unanihakikishia kwamba tutapata mtoto hivi karibuni ! Oh Mungu wangu ! akasema Abu kwa masikitiko “Ulikuwa ni uongo.Sina uwezo wa kubeba mimba ! akasema Nawal. Ghafla Abu Dahir akainua taa ya mezani iliyokuwa katika meza ndogo pembeni na pale alipokuwa amekaa na kumpiga nayo Nawal ikapasuka.Abu Dahir akachukua birika na kumrushia Nawal akalikwepa.Abu alionekana kama vile amepatwa na kichaa “Ninyi wanawake leo mtanitambua mimi ni nani ! akafoka Abu huku akirusha vitu kumpiga navyo Nawal “Abu acha ujinga huu tafadhali ! akafoka Habiba “Wewe mama ndiye uliyeyataka haya yote.Una roho mbaya sana! Akafoka Abu na kuinua chungu cha maua kilichokuwa dirishani kwa lengo la kumpiga nacho mama yake lakini Nawal alikwisha isoma dhamira yake akajiinua pale chini alipokuwa akaruka na kukipiga teke chugu kile kikaanguka na kuvunjika.Nawal ambaye hasira zilikwisha mpanda akamrukia Abu mateke mawili mfululizo yaliyomrusha Abu hadi ukutani akajigonga kwa kishindo na kuanguka chini halafu akamfuata Habiba “Mama uko sawa?Hajakuumiza huyu?akauliza Nawal “Nimeumia kidogo.Ahsante kwa kuniokoa” akasema Habiba na Nawal akageuka kumtazama Abu Dahir ambaye alikuwa amelala pale chini akionekana kutokuwa na fahamu.Haraka haraka akamfuata na kujaribu kumtikisa huku akimuita jina lake lakini hakuitika.Akageuka kumtazama Habiba Jawad ambaye naye alionyesha hofu baada ya kuiona sura ya Nawal,akainuka na kumfuata akamtazama Abu Dahir ambaye hakuwa na fahamu.Bila kupoteza muda Habiba akampigia simu daktari wake anayeishi pembeni ya nyumba yake ambaye alifika mara moja akampima Abu kisha akasema “Anatakiwa akimbizwe hospitali haraka sana ! Habiba akainuka akachukua simu na kuwapigia wasaidizi wake ambao walifika haraka haraka na kumchukua Abu Dahir wakamuingiza garini wakamkimbiza hospitali.Habiba na Nawal nao wakaingia garini wakaelekea hospitali. “Mama ni vipi kama nimempiga Abu sehemu mbaya? Akauliza Nawal akionekana kuwa na hofu “Usijilaumu Nawal.Ulifanya ulichopaswa kukifanya.Kama usingefanya vile Abu angenipiga na kile chungu na pengine ningeweza hata kupoteza maisha.Kwa sasa tumuombee ili aweze kuwa salama.Sitaki kupoteza tena mtoto mwingine.Nimekwisha poteza watoto wawili tayari na nimebaki na huyu mmoja” akasema Habiba na kufuta machozi “Lakini mama kwa nini uliamua kufanya hivi ulivyofanya?Kwa nini uliamua kuwaeleza ukweli wanao?akauliza Nawal “Ilikuwa lazima wafahamu Nawal.Sikutaka kuendelea kuwaficha kwani endapo ningefariki dunia bila kuwaeleza ukweli yawezekana nao wangeendelea kufanya kile ambacho mimi na baba yao tumekuwa tunakifanya.Sitaki watoto wangu waendelee kufadhili ugaidi,sitaki waendelee kumwaga damu za watu kama nilivyofanya mimi” akasema Habiba “Ulifanya kitu kizuri kuwaeleza ukweli lakini kwa bahati mbaya mambo hayakwenda kama ulivyokuwa umekusudia” akasema Nawal.Habiba akafuta machozi na kusema “Nadhani Mungu ananiadhibu kwa mambo niliyoyafanya.Nimefanya mambo mengi maovu.Damu nyingi imemwagika kwa sababu yangu na haya ndiyo mapigo ninayoyapata.Naomba Mungu asimchukue Abu Dahir kwani ni mtoto pekee niliyebaki naye” akasema Habiba na kuchukua simu akampigia mmoja wa madaktari katika hospitali alikoelekeza apelekwe Abu Dahir akamjulisha kuwa mwanae amepatwa na matatizo na anapelekwa pale hospitali akaomba ashughulikiwe haraka Abu Dahir alifikishwa hospitali ambako tayari wauguzi walikuwa wamejiandaa wakimsubiri,akashushwa haraka haraka katika gari na kuweka katika kitanda kikakimbizwa ndani katika chumba cha wagonjwa mahututi ambako alianza kupatiwa matibabu.Dakika chache baada ya Abu Dahir kuingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi,Habiba Jawad na Nawal wakawasili.Habiba alifahamika pale hospitali akapokewa na kupelekwa sehemu ya kusubiri madaktari watakapomaliza kumuhudumia mgonjwa wake. Baada ya dakika saba mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi ukafunguliwa na daktari akatoka.Habiba akasimama na kumfuata daktari akamtaka waelekee ofisini kwake “Kijana wangu anaendeleaje daktari?akauliza Habiba akionekana kuwa na hofu “Mama Habiba tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu lakini tumeshindwa kuokoa maisha ya mwanao.Uchunguzi wa awali unaonyesha ana jeraha kichwani.Nini hasa kilimtokea? Amepata ajali? Akauliza Daktari na Habiba Jawad akashindwa kumjibu.Yeye na Nawal wakakumbatiana wakilia. “Ahsante Mungu kwa kila jambo.Wewe ndiye mwenye kutoa na kutwaa kwa muda uutakao.Hatuwezi kupingana na maamuzi yako japo tungependa tuendelee kuwa pamoja na Abu Dahir lakini nakushukuru kwa muda ambao umempa hapa duniani.Naomba utupe nguvu ya kulihimili jambo hili” akasema Habiba machozi yakimwagika Habiba Jawad na Nawal wakapelekwa katika chumba ulikokuwa mwili wa Abu Dahir “Saa chache zilizopita tulikuwa wote ndegeni tukirejea Riyadh kuhudhuria msiba wa dada yako,sikuhisi kama ulikuwa unayafuata mauti yako.Abu Dahir mimi ndiye nimesababisha kifo chako nitalia machozi gani kwa hili nililolifanya? Najua ulikuwa unanipenda sana lakini umekufa ukiwa na hasira nami baada ya kuufahamu ukweli kuhusu maisha ya mama yako na kuhusu mimi.Najuta kwa nini sikukueleza ukweli kuhusu mimi kuwa ni jasusi wa CIA.Najuta kwa nini sikukueleza ukweli kama sina uwezo wa kukupatia mtoto kwani ni jambo hili ndilo lililokupa hasira zaidi.Nisamehe Abu Dahir huko uliko.Nisamehe ! akalia Nawal akiwa amesimama pembeni ya mwili wa Abu Dahir.Wote wawili Habiba na Nawal machozi yalikuwa yanawabubujika.Walitumia dakika kumi ndani ya kile chumba kisha wakatoka na kuondoka kurejea nyumbani “Mama nimemuua mume wangu.Nimemuua mwanao pekee aliyesalia” akasema Nawal wakiwa garini huku akimwaga machozi.Habiba akageuza shingo akamtazama Nawal na kumuinamisha kifuani kwake akamkumbatia “Nawal narudia kukusisitiza kwamba haya yote yanayotokea ni mipango ya Mungu na hupaswi kujilaumu kwa hili lililotokea.Ilikuwa iwe hivyo.Abu Dahir aliandikiwa afe kifo cha namna ile hivyo hakuna namna ambayo ungeweza kukwepa.Lakini tambua kwamba haya yote yanayoendelea hivi sasa ni matokeo ya maisha niliyoishi mimi.Ni mapigo yatokanayo na matendo yangu.Nimetesa watu wengi sana.Machozi ya akina mama waliopoteza watoto wao katika mashambulio yaliyofanywa na makundi ya kigaidi ambayo ninayafadhili hayajaniacha salama.Machozi ya watoto ambao wamebaki yatima baada ya kuwapoteza wazazi wao katika mashambulo ya kigaidi niliyoyafadhili haya ndiyo malipo yake.Nimepoteza watoto wangu wote niliowazaa na sasa nimebaki mwenyewe.Pamoja na mapigo haya lakini Mungu hajaninyima kila kitu.Amewachukua watoto wangu lakini ameniletea watoto wengine ambao ni wewe na Mathew” akasema Habiba na Nawal akainua kichwa chake “Mama umeongea kuhusu Mathew.Nataka kufahamu mahala alipo.Sijamuona katika msiba wa Najma” akauliza Nawal “Mathew ameondoka hatarejea tena kama nilivyowaambia na hilo ni moja kati ya mambo yaliyopelekea Najma akachukua maamuzi ya kujiua” akasema Habiba “Mathew amekwenda wapi? Amekufa? “Hapana hajafa.Nawal tutazungumza baadae lakini kwa sasa tujielekeze katika msiba wa Abu na tutakapomaliza tutazungumza” akasema Habiba DAR ES SALAAM – TANZANIA Ndege ya jeshi aliyopanda Mathew iliwasili jijini Dar es salaam.Kutoka angani ni sehemu chache tu za jiji la Dar es salaam ambazo zilionekana kuwa na umeme.Sehemu kubwa ya jiji la Dar ilikuwa gizani kutokana na miundo mbinu ya umeme kuharibiwa katika machafuko yaliyokuwa yanaendelea. “Nimezoea kuliona jiji la Dar es salaam kutokea angani likiwaka taa kila sehemu lakini leo hii jiji limetanda giza kila sehemu.Kwa tamaa ya mali ambazo Mungu ametujalia ziwepo katika nchi zetu,mabepari wametufikisha hapa.Ni mara ya kwanza Tanzania tumefikishwa hatua hii ya kuchinjana wenyewe kwa wenyewe.Ninaapa kwa gharama zozote zile lazima kikundi hiki cha hawa watu waliotufikisha hapa kwa tamaa za mali yetu nikifutilie mbali na dunia lazima ifahamu kile ambacho mataifa makubwa yanafanya katika nchi ndogo.Huu ni unyama uliopitiliza.Ni unyonyaji usio na mfano.Naamini haya ni maongozi ya Mungu hadi akanifikisha katika kundi hili ambalo limeigeuza nchi yetu uwanja wa mauaji.Tayari nimefahamu kuwa ni Marekani ndio waliotengeneza machafuko haya kwa manufaa yao.Hawako peke yao lazima kuna watu wa hapa nchini au katika nchi za Afrika mashariki ambao wanashirikiana nao katika kuanzisha na kuchochea vurugu hizi.Hawa ndio wanaotakiwa kusakwa kwa haraka sana na kujulikana ni akina nani na kama tukifanikiwa kuwapata hawa basi tutakuwa tunaweza kusaidia kumaliza vurugu hizi.Kuna nguvu mbili hapa ambazo zimeifikisha Tanzania hapa tulipofika.Ipo nguvu ya ndani na nguvu ya nje.Inabidi kuanza na nguvu ya ndani kisha nitaendelea na wale wa nje.Naapa hakuna aliyeifikisha Tanzania hapa atabaki salama”akawaza Mathew na kumkumbuka Ruby “Nilijaribu kumpigia simu Ruby lakini hakupatikana.Nina wasi wasi sana na usalama wake.Gosu Gosu naye sijui anaendeleaje.Nawahitaji sana hawa watu kama watakuwa wazima katika kuhakikisha tunaiokoa nchi yetu kutoka katika machafuko.Ninachoelewa hawa jamaa kwa vile wamekwisha ingia Afrika Mashariki lazima wataotesha mizizi na kuhakikisha kwamba wanaendelea kuchota utajiri wetu.Naomba niwakute wote wako salama” akawaza Mathew na kutaarifiwa kwamba ndege inakaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ambao toka vurugu zilipoanza ulikuwa umefungwa na ukilindwa na wanajeshi . Ndege ile ya jeshi la Marekani ikiwa na vifaa mbali mbali vya wanajeshi wa Marekani waliokuwa nchini Tanzania ikatua salama.Mizigo ikapakuliwa na kuingizwa katika magari kisha wanajeshi waliokuja na ndege ile wakaingia katika magari maalum ya jeshi la Marekani na msafara ukaondoka kuelekea katika kambi yao Mathew Mulumbi akiwa ni mmoja wao “Hawa jamaa hawajui kama hapa nimefika nyumbani.Watakapogundua kwamba mimi ni mtanzania tayari watakuwa wamechelewa sana lakini kwa sasa ngoja niendelee kujifanya mimi ni mgeni wa hapa Tanzania ili niendelee kuusoma mtandao wao” akawaza Mathew na kuona namna alivyokuwa anachungwa.Ndani ya gari alilokuwa amepanda kulikuwa na wanajeshi wanne wenye silaha na gari lile liliwekwa kati kati ya msafara. “Nadhani wameelekezwa wanichunge ndiyo maana wameniweka katikati.Hawapaswi kuwa na hofu nitafanya walivyonieleza lakini watajuta sana na kumlaumu Habiba Jawad kwa kuwakutanisha na mimi.Safari hii ninataka nifanye kitu ambacho kitakuwa cha kihistoria.Tumeonewa vya kutosha na sasa ni wakati wa kuwaonyesha haya mataifa makubwa kwamba hata sisi tunao uwezo na tumechoshwa na mambo wanayotufanyia” akawaza Mathew akiyaelekeza macho yake nje “Dar es salaam haikuwa hivi.Hili ni jiji lililokuwa linakesha lakini muda huu barabara tupu hakuna watu mitaani.Sipati picha namna maisha yalivyo magumu hivi sasa.Maduka yamefungwa,upatikanaji wa chakula na mahitaji muhimu imekuwa ni shida lakini baadhi ya watu wachache wao wanaishi maisha mazuri na kupata kila wanachokihitaji wakisahau kwamba kuna mamilioni ya watu wanaoteseka huku Tanzania na Afrika mashariki kwa sababu yao.Tunatakiwa kupambana kuhakikisha tunairejesha nchi yetu ilivyokuwa na ili kumaliza vurugu hizi ni lazima kuuchimbua mzizi wenyewe ambao ni kikundi kile kidogo ndani ya CIA” akawaza Mathew huku wakiendelea kukata mitaa ya jiji la Dar es salaam ambayo kwa usiku huu ilikuwa kimya.Mioto ya matairi na moshi mzito vilionekana katika baadhi ya barabara na hata majengo yanayoungua moto pia yalikuwepo.Katika baadhi ya barabara walikuta zimefungwa kwa mawe makubwa “Hali ilivyo Dar es salaam utadhani kuna filamu inatengenezwa kumbe ni hali halisi .Inasikitisha sana ! Narudia tena kuahidi kwamba wale wote waliotufikisha hapa hakuna atakayebaki salama.Tanzania hatukupaswa kufikishwa hapa.Lakini hili ni funzo kwa watanzania ili wawe macho kulinda amani yao.Wamekuwa wakihubiriwa kwa miaka mingi kwamba siku amani hii ikipotea watajuta.Wamejaribu kuchezea amani na wameona madhara yake.Hakuna sehemu ya kukimbilia imelazimu wayakimbie makazi yao na kujificha katika makambi.Kwa haya wanayokutana nayo naamini hata akija tena mtu mwingine siku nyingine kutaka kuwarubuni kuchezea amani yao hawatajaribu tena” Mathew akatolewa mawazoni baada ya msafara wao kukutana na kundi kubwa la vijana waliokuwa wamebeba mienge na silaha huku wakiimba.Ikalazimu wanajeshi wa Marekani kutumia risasi za moto kuwatawanya kwani baadhi yao walikuwa na silaha na walianza kushambulia magari katika ule msafara.Baada ya kundi lile la vijana kutawanyika magari yakaongeza mwendo na moja kwa moja wakaelekea katika uwanja wa uhuru ambako ndiko kulikuwa na kambi kubwa ya wanajeshi wa Marekani na vifaa vyao vyote vilikuwa vinahifadhiwa huko.Kambi nyingine ilikuwa ufukweni mwa bahari ya Hindi. Mathew alishushwa garini na kukabidhiwa kwa mmoja wa viongozi wa kambi ile ambaye alimpeleka hadi katika hema. “Karibu Tanzania.Jina lako nani? Akauliza Yule jamaa “Abu Zalawi” akajibu Mathew kikakamavu “Abu Zalawi nimeelekezwa na viongozi wangu kwamba nikupokee na kisha nitakukabidhi kwa mtu ambaye atakuja hapa kukuchukua.Umewahi kufika Tanzania kabla? Akauliza “Hapana sijawahi” akajibu Mathew “Hali ni mbaya sana hasa hapa Dar es salaam na jiji la Tanga pia.Nadhani umejionea hali halisi huko mitaani wakati mkija hapa” “Ndiyo mkuu.Tumekutana na kundi kubwa la vijana wakiwa na silaha na kushambulia msafara wetu” “Basi hiyo ndiyo hali tunayokutana nayo kila siku katika kujaribu kurejesha hali ya amani tukishirikiana na vikosi vya ulinzi vya Tanzania” “Endelea kupumzika na atakapofika mwenyeji wako nitakufahamisha” akasema Yule mwanajeshi na kutoka nje ya lile hema akamuacha Mathew peke yake. “Naamini huyo mtu anayekuja kunichukua ni mmoja kati ya watu wa IS na atakuwa anatumiwa na CIA katika kuratibu na kuchochea hizi vurugu zinazoendelea.Imekuwa vyema wamenielekeza sehemu husika kwani huyo jamaa ndiye wa kuanza naye” akawaza Mathew
Mathew alitikiswa bega na kustuka,alikuwa amepitiwa na usingizi.Saa yake ya mkononi ilionyesha ni saa tisa za usiku. “Abu Zalawi muda wa kuondoka, mwenyeji wako tayari amefika” akasema Yule mwanajeshi aliyempokea Mathew kisha akamuongoza wakaenda hadi nje ya uwanja ambako kulikuwa na magari matatu.Katika gari la kati kati kulikuwa na watu wanne wenye silaha wakiwa wamesimama wamelizunguka.Mmoja wa wale jamaa akamfungulia Mathew mlango akaingia ndani ambako alimkuta jamaa mmoja “Abu Zalawi” akasema Yule jamaa “Assad Ismail? Akauliza Mathew “Farhad Seif” akasema Yule jamaa na Mathew akaonyesha wasiwasi “Yuko wapi Assad Ismail? Akauliza “Usihofu tafadhali.Karibu Dar es salaam” akasema Yule jamaa na gari likawashwa msafara ule wa magari ukaondoka katika uwanja wa uhuru ukitanguliwa na gari la jeshi la Marekani ambalo lilikuwa na mwanajeshi akiwa amejitokeza nje akiwa na bunduki kubwa tayari kukabiliana na makundi yoyote ya vurugu. “Vipi safari yako? Akauliza Farhad “Ilikuwa nzuri” akajibu Mathew na safari ikaendelea kimya kimya. Walikatisha mitaa mbalimbali ya jiji huku wakikutana na magari ya doria ya polisi na jeshi hadi walipofika katika kituo cha basi cha Botha.Mahala hapa panaitwa jina hilo kutokana na awali mzungu mmoja kutoka Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina moja tu la Botha kuishi eneo hilo na kujenga shule ya awali kwa watoto wadogo pamoja na kutoa huduma ya maji bure kwa wananchi waliokuwa wanamzunguka hivyo akawa maarufu. Magari yalisimama na Farhad akashuka akaenda kuzungumza na wale wanajeshi wa Marekani akaagana nao wakageuza gari wakaondoka.Farhad na wenzake nao wakaendelea na safari yao “Mbona wale wanajeshi wamerudi? Huko tuendako ni salama?akauliza Mathew “Una hofu yoyote? Akauliza Farhad “Wakati tukielekea katika kambi ya wanajeshi tumekutana na makundi makubwa ya vijana wakiwa na silaha kwa bahati nzuri wanajeshi walikuwa na silaha kali wakawatawanya” akasema Mathew “Usihofu Abu Zalawi uko salama.Hili ni eneo letu” akasema Farhad na safari ikaendelea kimya kimya huku eneo hili la kwa Botha likiwa kimya sana.Geti jeusi lilifunguliwa na gari zile zikaingia.Ndani kulikuwa na nyumba iliyopakwa rangi ya bluu halafu kukawa na majengo mawili yaliyoonekana kama mabohari.Mathew akaelekezwa kushuka garini kisha akamfuata Farhad wakaelekea ndani ya ile nyumba.Kulikuwa na mlinzi mlangoni akawafungulia mlango wakaingia ndani.Sebuleni kulikuwa na watu wawili wamekaa chini katika zuria wakizungumza. “Karibuni sana” akasema mmoja wa wale jamaa kwa lugha ya kiarabu.Mathew na Farhad wakaketi “Pole na safari ndefu” akasema Yule jamaa aliyewakaribisha “Ahsante sana nashukuru” akajibu Mathew “Naitwa Marwan Hossam” akasema Yule jamaa “Yuko wapi Assad Ismail?akauliza Mathew “Usiwe na hofu utaonana na Assad kutakapopambazuka lakini kwa sasa unatakiwa upumzike kwa safari hii ndefu” akasema Marwan na kuinuka akampeleka Mathew katika mojawapo ya chumba akamtaka apumzike. “Hii nyumba ndimo wanamoishi magaidi wa IS ambao jukumu lao kubwa ni kuendelea kuchochea machafuko.Mpaka sasa wanaamini mimi ni gaidi mwenzao na kesho nitaonana na huyo Marwan mkubwa wao naamini atanieleza mengi” akawaza Mathew huku akikikagua kile chumba “Wakati nikiendelea kuwasoma hawa jamaa natakiwa kutafuta namna nitakavyoweza kuwasiliana na akina Gosu Gosu ili niweze kuwapa taarifa za jambo hili linaloendelea.Sina hakika kama wanafahamu chanzo cha vurugu hizi.Haya yote lazima yafanyike kesho” akawaza Mathew na kujilaza kitandani “Mathew hakikisha unafanikisha malengo yako.Ifanye dunia ikukumbuke kwa vizazi na vizazi.Maliza kundi la kigaidi la IS na makundi mengine.Kisafishe kikundi hiki kidogo cha watu hawa ambacho ndicho kinachohatarisha amani ya dunia.Hii ni misheni kubwa na ya hatari.Lolote linaweza kutokea katika misheni hii mimi ninakuombea uimalize salama na kila pale nitakapokuwa na uwezo wa kukusaidia nitafanya hivyo.Jambo la mwisho baada ya kumaliza misheni hii kama utakuwa salama tafadhali usirejee tena Riyadh.Nenda nyumbani kaendelee na maisha yako.Kaungane tena na familia yako kwani lengo lako litakuwa limetimia kuhusu kupambana na ugaidi.Kuhusu Najma usiwe na hofu nitazungumza naye na ataelewa.Narudia tena usirejee Saudi Arabia kwani hadi wakati huo sintakuwepo tena” Mathew akiwa amejilaza kitandani akayakumbuka maneno ya Habiba Jawad “Habiba hana uhakika kama nitamaliza salama operesheni hii ndiyo maana akaniambia kwamba ile ilikuwa ni mara yetu ya mwisho kuonana.Habiba amekuwa akiniambia kwamba atakufa hivi karibuni lakini hakuwahi kunieleza nini hasa kinachomsumbua ingawa ukimtazama huwezi kugundua chochote kama afya yake ina matatizo.Ninamuomba Mungu aniwezeshe niikamilishe salama operesheni hii na lazima nirejee Riyadh kumuona Najma na pili kujua maendeleo ya Habiba na kama atakuwa amefariki basi nitapenda kuliona kaburi lake kwani mama Yule anastahili pongezi kwa mambo ambayo amenifanyia.Yeye ndiye aliyenifikisha hapa nilipofika hadi nikafahamu mambo mengi na mengine makubwa kabisa ambayo wengi duniani hawayajui” akawaza Mathew halafu akazima taa na kusimama mlangoni akatega sikio kama kuna mtu yeyote yuko mlangoni alipohakikisha kuko shwari akaenda dirishani na kulichunguza kama ni dirisha analoweza kupita lakini ilikuwa ni dirisha imara ambalo halikuwa na uwazi kwa mtu kupita. “Ngoja nipumzishe kichwa na kesho nitajua nini cha kufanya” akawaza Mathew na kupanda kitandani
Kumepambazuka na kijua tayari kimeanza kuchomoza.Asubuhi hii Tanzania iliamshwa na taarifa mbaya za kifo cha Mufti wa Tanzania ambaye aliuawa usiku yeye na familia yake baada ya nyumba yake kushambuliwa kwa mabomu.Ilikuwa ni taarifa iliyostua wengi na kuleta hofu kubwa. Kitasa cha mlango wa chumba cha Mathew kikaminywa kwa nguvu lakini alikuwa amefunga mlango kwa ndani.Mtu aliyeminya kile kitasa akagonga mlango kwa nguvu na Mathew akainuka na kwenda kufungua.Alikuwa ni Marwan “Habari yako Abu Zalawi?akauliza Marwan “Habari nzuri Marwan” “Amka kumekucha.Jiandae kwa ajili ya kuianza siku” akasema Marwan na kumuelekeza Mathew bafu akaenda kuoga halafu akakaribishwa sebuleni kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.Mle sebuleni kulikuwa na watu zaidi ya kumi wote wakipata kifungua kinywa.Mathew akawasalimu kisha naye akaketi na kupata chai.Baada ya kupata kifungua kinywa wale watu karibu wote wakatoka na kwenda katika zile nyumba mbili zilizojengwa kwa mfano wa bohari Mathew akabaki na Marwan “Yuko wapi Assad ?Mathew akauliza “Usihofu Abu Zalawi utaonana naye.Atafika hapa muda si mrefu” “Haishi hapa? “Hapana yeye haishi hapa” http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Nimeona kuna watu wengi hapa,shughuli gani inafanyika katika nyumba hii?akauliza Mathew “Abu Zalawi unaonekana unataka kufahamu mambo mengi kwa wakati mmoja.Jielekeze katika kile kilichokuleta hapa na kama kuna swali lolote unataka kuuliza utamuuliza Assad atakapofika” akasema Marwan na kutoka akamuacha Mathew peke yake mle sebuleni.Mathew akasimama na kuchungulia nje akaanza kuyasoma mazingira ya mahala pale “Inaonekana hii ni sehemu ambako wanapanga mikakati yao ya kigaidi.Katika yale majengo mawili mfano wa bohari kuna nini? Ngoja nimsubiri Assad anaweza akanieleza kila kitu kuhusiana na mahala hapa” akawaza Mathew na kuendelea kuangaza angaza macho. Geti lilifunguliwa na gari la jeshi la Marekani likaingia huku nyuma yake kukiwa na gari lingine lenye rangi nyeusi.Kutoka katika lile gari jeusi wakashuka watu wawili na mmoja wao akaufungua mlango wa kati kati na jamaa mmoja aliyevaa kanzu ya kijivu na koti jeusi akashuka.Kichwani hakuwa amevaa kofia na kichwa chake hakikuwa na nywele hata moja.Macho yake aliyafunika kwa miwani myeusi.Mkononi alikuwa ameshika sigara akivuta.Akaagana na wanajeshi wale wa Marekani wakaondoka.Jamaa Yule aliyeshuka garini akasalimiana na Marwan wakazunguma kwa dakika chache halafu wakaelekea katika zile nyumba mbili mfano wa bohari.Mathew alikuwa dirishani akiwatazama. Baada ya dakika kumi wakatoka katika zile nyumba na kuingia sebuleni,Mathew akasimama “Abu Zalawi ! akasema Yule jamaa aliyeongozana na Marwan huku akimpa mkono Mathew wakasalimiana “Nasikia umekuwa unaniulizia sana ukitaka kuniona.Ndiye mimi Assad Ismail.Karibu sana Tanzania” akasema Assad “Nashukuru sana Assad” akajibu Mathew “Hii sura yako si ngeni.Umewahi kutembelea nchi yoyote ya Afrika Mashariki?akauliza Assad “Ndiyo niliwahi kwenda Kenya.Nilikwenda kumuua mkurugenzi wa Mossad katika ukanda wa Afrika Mashariki” “Ndiyo maana nilipokuona tu nikahisi kama nimewahi kukuona sehemu Fulani.Umewahi kufika Tanzania? “Hapana ni mara ya kwanza ninafika Tanzania” Mathew akajibu “Karibu sana Abu Zalawi.Nimefurahi kukutana nawe.Nimeelezwa kwamba Habiba Jawad ndiye aliyekupendekeza uje huku” akasema Assad huku akiendelea kuvuta sigara “Ndiyo ni Habiba ambaye alinipeleka Marekani na kunikutanisha na CIA ambao wamenituma huku” “Vizuri sana.Vipi maendeleo ya Habiba? “Habiba anaendelea vizuri sana” “Nafurahi kusikia hivyo.Hebu nipe historia yako kwa ufupi namna ulivyokutana na Habiba hadi akakuamini kiasi hiki” akasema Assad “Baada ya kumuua mkuu wa Mossad kanda ya Afrika Mashariki na kati nilikamatwa na Mossad nikafungwa gerezani kwa miaka mitatu na hapo ndipo nilipokutana na Ammar Nazari kiongozi wa kundi la Ammar Nazari Brigades.Nilifanikiwa kutoroka gerezani nikiwa na Ammar na nikajiunga katika kundi lake.Nikiwa katika kundi hilo nilitekeleza mashambulio kadhaa likiwemo lile la kituo cha mabasi jijini Jeruslaem.Vikosi vya Israel vilishambulia makazi ya Ammar na kufanikiwa kumuua mimi nilitoroka nikiwa na Nawal mke wa Ammar na huyo ndiye aliyenielekeza kwamba tumtafute Habiba Jawad kwa ajili ya kupata hifadhi kwani alikuwa ni rafiki wa Ammar.Tulifanikiwa kuonana na Habiba Jawad akatupa hifadhi na ndipo alipoanza kunishirikisha katika shughuli zake akatokea kuniamini baada ya kuridhiswa na utendaji wangu wa kazi.Hiyo ndiyo historia fupi ya namna nilivyoweza kukutana na Habiba Jawad” akasema Mathew “Abu Zalawi mimi naitwa Assad Ismail.Ninasimamia kundi la IS kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati makazi yangu ni Mombasa.Nimekuja Tanzania kwa ajili ya operesheni maalum.Nadhani ulipokwenda Marekani umefahamishwa kile kinachoendelea hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla” “Ndiyo.Nilielezwa kwa kifupi sana na kuambiwa kwamba nitapata maelezo kamili nitakapofika hapa.Hata maelekezo yote kuhusiana na kazi ninayokuja kuifanya hapa Tanzania nimeambiwa kwamba nitayapata kutoka kwako” akasema Mathew na Assad akaonyesha kushangaa “Hawakukueleza unakuja kufanya nini Tanzania? Akauliza Assad “Wamenieleza kwamba ninakuja kulipua ubalozi wa Marekani lakini kila kitu kuhusiana na misheni hiyo nimeambiwa kwamba nitapata kutoka kwako” akasema Mathew “Nitakueleza kwa kifupi ili uweze kupata picha ya kile kinachoendelea hapa Tanzania.Ni kwamba Marekani wana mipango yao hapa Afrika Mashariki na ili iweze kufanikiwa wamelazimika kututumia sisi kwa malipo ya fedha na silaha.Kumekuwa na upungufu mkubwa wa mafuta duniani kutokana na wazalishaji kupunguza kiwango kwa lengo la kupandisha bei katika soko la dunia.Sababu hiyo ndiyo iliyopelekea Marekani kugeukia Afrika Mashariki ambako kuna rasilimali ya mafuta kutoka Uganda nchi ambayo ina akiba kubwa sana ya mafuta ambayo husafirishwa kwa bomba kutoka Hoima hadi jijini Tanga hapa Tanzania.Ili kuweza kuyapata mafuta hayo ililazimu kuliingiza eneo la Afrika Mashariki katika machafuko na machafuko ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka mama moto wa petroli ni machafuko ya kidini.Katika nchi hizi tatu Tanzania,Kenya na Uganda dini kubwa ni mbili wakristu na waislamu hivyo kwa kushirikiana na baadhi ya wanasiasa na baadhi ya viongozi wa dini tuliweza kufanya mauaji ambayo yalileta uhasama mkubwa na waumini wa dini hizo mbili wakaanza kushambuliana wakichomeana nyumba za ibada na hata kuuana.Machafuko hayo yalianza Uganda na kuenea Tanzania na Kenya lakini sana tumelenga nchi za Tanzania na Uganda kwani ili Marekani waweze kupata mafuta ya Uganda lazima watumie bandari ya Tanga hivyo lazima nchi hizi mbili ziingie katika machafuko.Hicho ndicho ambacho tumekuwa tunakifanya hapa Tanzania na ndiyo maana nimeondoka Mombasa kuja hapa Tanzania kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri kwani misheni hii ni ya fedha nyingi sana” akasema Assad “Hongera sana Assad kwa kazi kubwa uliyoifanya.Nchi kama Tanzania ni nchi ngumu sana kwa watu wake kuingia katika machafuko makubwa kama haya yanayoendelea” akasema Mathew “Ni kweli.Haikuwa rahisi.Ililazimu kushirikiana na wanasiasa na baadhi ya viongozi wa dini kutengeneza mtandao wa kuchochea vurugu ndipo tukafanikiwa na kwa mara ya kwanza Tanzania imeingia katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.Hata hivyo watanzania hawajazoea vurugu kwani kulianza kujitokeza dalili za amani kurejea.Rais wa Tanzani alikutana na mufti wa Tanzania wakawa na mazungumzo marefu na baada ya mazungumzo hayo mufti akazungumza na waislamu na kuwataka wasijihusishe na vurugu.Kwa kiasi kikubwa watu wameonekana kumuelewa na vurugu zimeripotiwa kupungua sana kwa usiku wa kuamkia leo.Kwa siku ya leo Rais alipanga kuendelea na mikutano na viongozi wengine wa dini ya kikristu.Kwa kiasi kikubwa juhudi za kutafuta amani zinaonekana kuanza kuzaa madini na kazi yetu ni kuhakikisha kwamba amani haipatikani Tanzania ili vikosi vya Marekani viendelee kukaa Afrika Mashariki kwa muda mrefu zaidi na ili kuvuruga jitihada za kutafuta amani ambazo zimeanza kuonekana usiku wa leo tumemuua mufti wa Tanzania kwa bomu” akasema Assad na Mathew akahisi mwili unamsisimka akajikaza asiweze kuonyesha namna alivyostuka. “Hii haiwezi kujenga taswira kama kuna kikundi cha watu ambacho kinalenga viongozi wa dini?Unadhani waislamu wataamini kwamba ni wakristu ndio waliomuua kiongozi wao? Akauliza Mathew “Usiwe na hofu Abu Zalawi.Tumekwisha jipanga vizuri na kila kitu kitakwenda vizuri.Kwa hili tulilolifanya ni kama kumwagia petrol katika moto ambao umeanza kuzimika na moto ukapata nguvu mpya.Tunao watu wetu ndani ya wakristu na waislamu pia ambao huchochea vurugu hizi.Kwa mfano kwa mauaji haya ya Mufti wapo watu ndani ya uislamu ambao watawachochea waislamu kulipiza kisasi” akasema Assad “Tuachane na hilo nataka kufahamu kuhusiana na kazi yangu niliyokuja kuifanya” akasema Mathew “Ulichokuja kukifanya huku Tanzania kama ulivyoelezwa ni kulipua ubalozi wa Marekani hapa Tanzania.Tayari maandalizi ya bomu litakalotumika yameanza.Litakuwa ni bomu kubwa ambalo litasababisha uharibifu mkubwa sana.Kuna raia wa Marekani ndani ya ubalozi huo pamoja na raia wa nchi nyingine waliojihifadhi hapo wakisubiri vurugu zipungue na wengi watapoteza maisha kufuatia shambulio hilo litaipa sababu Marekani kuongeza vikosi zaidi Tanzania” akasema Assad na kunyamaza baada ya watu wawili kuingia mle ndani wakazungumza na walipotoka Assad akaendelea. “Hawa jamaa waliotoka ni wataalamu wanao unda bomu utakalolitumia kulipua ubalozi huo wa Marekani” akasema Assad “Kwa sasa ubalozi wa Marekani unalindwa na wanajeshi wao walioko hapa nchini.Mpango wa namna utakavyoingia katika ubalozi huo uko namna hii.Kwanza kabisa naomba ufahamu kuwa suala hili linawahusisha pia baadhi ya viongozi wa vikosi vya jeshi vilivyoko hapa Tanzania na kama ulivyoona wewe mwenyewe wamekuwa wakinipa msaada mkubwa.Kutokana na ushirikiano huo tutatumia gari la jeshi la Marekani kuweka bomu kisha utavaa sare za jeshi hilo na kuonekana kama mwenzao.Wanajeshi watakaokuwa na gari hilo watadai kwamba walitekwa na gari lao kuporwa” Assad akanyamaza “Wanajeshi watakaokuwa wakilinda ubalozi huo wakiliona gari la jeshi la Marekani hawatakuwa na wasi wasi na wataamini ni mwenzao.Watakuruhusu kuingia ndani kisha utakwenda kuliegesha gari hio mahala utakapoelekezwa.Ndani ya gari hilo utakuwa umebeba watoto ambao utadai kuwa umewaokota njiani wakiwa hawana msaada.Ukisha egesha gari mahala utakapoelekezwa utashuka na kuondoka hapo ubalozini ukidai kwamba unawafuata watoto uliowaona wako katika hatari.Endapo watakuzuia unaruhusiwa kutumia silaha kuwamaliza walinzi hao.Ukisha toka ubalozini hapo utaelekezwa mahala ambako utakuta gari linakusubiri na hapo ndipo utakapolipua bomu na usiku huo huo utaondoka kuelekea nchini Kenya na siku itakayofuata utakamatwa na makachero wa CIA na baada ya hapo sisi tutakuwa tumekamilisha jukumu letu kwa upande wako na tutaendelea na jukumu letu la kuchochea machafuko” akasema Assad “Nimekuelewa Assad.Ahsante kwa mpango huu mzuri.Lini jambo hili litafanyika?Mathew akauliza “Kwa sasa tunaendelea na utengenezaji wa bomu ambalo tutalitumia.Naamini hadi usiku wa leo litakuwa limekamilika kwani kuna vifaa vichache ambavyo tulikuwa tunavisubiri na tayari tumevipata hivyo basi naamini hadi usiku wa leo wataalamu wetu wanaounda bomu hilo watakuwa wamekamilisha kazi.Kesho jioni tukio hilo litafanyika” akasema Assad “Kuna muda mrefu hadi kesho jioni.Hakuna chochote ninachoweza kusaidia kufanya?akauliza Mathew “Pumzika Abu kwani una safari ndefu sana.Una siku mbili tu leo na kesho za kupumzika kwani baada ya hapo utakabiliwa na kipindi kigumu sana” akasema Assad “Nalifahamu hilo Assad lakini mimi ni mtu wa kazi.Sijazoea kukaa bila kuwa na kazi yoyote.Nielekeze kama kuna kazi yoyote ninaweza kusaidia” akasema Mathew “Abu Zalawi usihofu.Kila kitu hapa kinakwenda vizuri wewe tutakuomba upumzike hadi hiyo kesho jioni utakapoianza safari yako.Una kazi ngumu mno inakukabli mbele yako hivyo tumia muda huu kupumzika.Ninaomba nikakutambulishe kwa watu wangu wakufahamu kwani wengine wanakuona hapa lakini hawakuelewi wewe ni nani” akasema Assad na kumchukua Mathew wakaenda katika moja ya nyumba iliyojengwa kama bohari.Ndani ya nyumba ile kulikuwa na nafasi kubwa na kati kati ya nyumba ile kulikuwa na meza kubwa iliyokuwa imezungukwa na watu zaidi ya kumi.Shughuli ya uundaji wa bomu ilikuwa inaendelea.Assad akawaomba wamsikilize kwa dakika chache “Awali ya yote napenda kwanza niwashukuru kwa kazi nzuri iliyofanyika usiku wa leo ya kumuondoa Mufti wa Tanzania.Baada ya kutekeleza shambulio lile naamini sasa zile vurugu ambazo zilikuwa na mwelekeo wa kumalizika zitaanza upya.Jambo la pili ambalo nataka kuwajulisheni ni kwamba jana tumepokea mgeni hapa katika kambi yetu.Nadhani tayari nyote mmekwisha muona anaitwa Abu Zalawi.Anatokea Saudi Arabia.Alikuwa katika kundi la Ammar Nazari Brigades.Amekuja hapa kwa kazi maalum ambayo ni kulitumia bomu hilo mnaloliandaa.Nimeona nimtambulishe kwenu ili mfahamu kwamba kazi hiyo inatakiwa imalizike kwa haraka ili kesho Abu Zalawi aifanye kazi iliyomleta hapa” akasema Assad na kumtaka Abu Zalawi kwenda kupumzika wakati shughuli ya uundaji wa bomu ikiendelea.Mathew akatoka na kuanza kuzunguka zunguka katika nyumba ile akiyasoma mazingira yalivyo
Inakaribia dakika arobaini sasa,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo akizungumza na Ruby kwa simu.Taarifa ya mauaji ya Mufti wa Tanzania ilimstua sana.Baada ya kumaliza kuzungumza na Rais simuni,Ruby akamgeukia Gosu Gosu “Rais amechanganyikiwa kwa mauaji haya ya Mufti ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kutafuta amani.Mauaji haya yameleta wasi wasi mkubwa sana wa kuongezeka kwa vurugu.Tuliamini muda si mrefu hali itakuwa shwari lakini kwa mauaji haya kuna uwezekano wa vurugu kuanza upya” akasema Ruby “Swali la kujiuliza je ni watu wa imani nyingine ndio waliotekeleza mauaji hayo ya Mufti?Binafsi siamini kama ni watu wa imani ya kikritu ndio waliofanya mauaji haya” akasema Gosu Gosu “Nakubaliana nawe Gosu Gosu mauaji haya ya Mufti wa Tanzania hayaonekani kama yana mlengo wa kidini bali yanaonekana ni kutaka kuchochea zaidi vurugu ili waislamu waamini kuwa ni upande mwingine ndio waliotekeleza mauaji hayo na hapo waumini wa dini hizo wataendelea kushambuliana.Mauaji haya yametokea wakati kukiwa na kila dalili za machafuko kutulia.Rais alikuwa na program ya kuendelea kukutana na viongozi wakuu wa dini na alianza na mufti wakakutana wakazungumza na Mufti akawasihi waislamu asiendelee na vurugu zile.Leo hii Rais alikuwa na mipango ya kukutana na viongozi wengine wa dini katika mwendelezo ule wa kutafuta amani lakini kwa hiki kilichotokea sina hakika kama mazungumzo hayo yataendelea tena kwani viongozi wakuu wa dini wataogopa kuzungumza na Rais kwa hofu ya kuuawa kama ilivyomtokea Mufti wa Tanzania.Hali inazidi kuwa tete” akasema Ruby “Tunahitaji kuongeza juhudi za kuutafuta mzizi wa vurugu hizi.Tukifanikiwa kuupata mzizi wake tutafahamu mengi.Tulimuomba Rais atusadie kupata taarifa za Joshua Lulangwa wa Uganda.Kuna chochote amekueleza?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo.Amesema kwamba taarifa alizopewa kutoka Uganda ni kuwa Joshua Lulangwa ametoweka na hajulikani alipo.Wanasema mara ya mwisho kuonekana nchini Uganda ni siku ambayo machafuko yalianza jijini Kampala.Baada ya hapo hajaonekana tena na wala hajulikani alipo na toka wakati huo simu yake imezimwa” akasema Ruby “Yale yale tuliyoyakuta kwa Karim na wenzake.Ruby ninahisi huu ni mtandao mmoja.Wote wana sifa zinazofanana.Wote simu zao zimezimwa mara tu machafuko yalipoanza na wote hawajulikani walipo.Swali ambalo bado hatujalipatia majibu ni je wanahusika kwa namna yoyote ile na vurugu hizi zinazoendelea Tanzania na Uganda?akauliza Gosu Gosu “Hapo ndipo tulipokwama Gosu Gosu.Tunatakiwa kutafuta kila namna ya kuweza kujikwamua hapo tulipokwama.Nina uhakika mkubwa sana kwamba kuna kitu hapa ambacho kama tukiweza kukifahamu basi kinaweza kutusaidia sana kujua mzizi wa vurugu hizi zinazoendelea”akasema Ruby “Hapa ndipo ninapomkumbuka Mathew” akasema Gosu Gosu “Me too.I miss him so much ! akasema Ruby na kuinamisha kichwa akazama mawazoni “Mimi ni mwanajeshi nimefundishwa kupigana na kuua,sina utaalamu mkubwa katika mambo ya kipelelezi.Ninachofahamu mimi ni kushika silaha na kupambana.Wewe ni mchawi wa kompyuta na hujabobea sana katika mambo haya ya kiuchunguzi ndiyo maana kuna mambo tunashindwa kuyapatia majibu kama hili linaloendelea sasa” akasema Gosu Gosu “Uko sahihi Gosu Gosu.Mimi utaalamu wangu ni katika msauala ya kompyuta na mawasiliano.Masuala ya kipelelezi sijabobea huko japo nimefanya kazi katika taasisi za kipelelezi lakini nikiwa kama mtaalamu wa kompyuta.Lazima nikiri kwamba idara hii ya SNSA japo imekua ikifanya kazi zake vizuri na kwa mafanikio makubwa lakini hakuna mpelelezi mwenye kiwango cha juu ambaye anaweza akakaribiana na Mathew Mulumbi” akasema Ruby “Ruby hakuna ubishi kwamba tunahitaji sana msaada kwa hapa tulipofika na msaada pekee ambao tunauhitaji kuupata hivi sasa ni Mathew Mulumbi” akasema Gosu Gosu na ukimya ukapita halafu Gosu Gosu akasema “Ruby tunafahamu mahala alipo Mathew na unazo namba za simu za mtu ambaye anaweza akatusaidia kutuunganisha naye.Mpigie muombe atuunganishe na Mathew tuzungumze naye tumueleze hali halisi ilivyo kwa sasa hapa nchini.Ruby nina uhakika mkubwa Mathew akifahamu kile kinachoendelea hapa nchini hivi sasa lazima atakuja” akasema Gosu Gosu na Ruby akafikiri kidogo na kusema “Gosu Gosu unachokisema ni cha kweli.Ngoja nimpigie Yule mwanamke aliyenipigia akajitambulisha kuwa ni mke wake” akasema Ruby na kuchukua simu yake akazitafuta namba za Najma akapiga lakini simu yake haikupatikana.Akapiga mara ya pili jibu likawa lile lile simu ya Najma haikuwa ikipatikana “Simu yake haipatikani.Nitajaribu tena baadae” akasema Ruby “Tumekwama tena” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu hatupaswi kushindwa.Machafuko yanakwenda kuanza upya na inaonekana wazi kwamba upo mtandao ambao unachochea machafuko hayo.Lazima kwa namna yoyote ile tuufahamu mtandao huo.Kwa sasa tuendelee kufuatilia hali ya vurugu inavyondelea jijini Dar es salaam huku tukiendelea kuchimbua zaidi kuhusu hawa jamaa waliotoweka.Nina uhakika tunaweza kupata kitu Fulani” akasema Ruby RIYADH – SAUDI ARABIA Msafara wa watu waliokwenda makaburini kumzika Abu Dahir ulirejea katika makazi ya Habiba Jawad.Ilikuwa ni simanzi kubwa na watu wengi walifika kumpa pole Habiba kwa kuwapoteza watoto wawili ndani ya muda mfupi.Kifo cha Abu Dahir kiliwasikitisha wengi. Saa moja za jioni Habiba Jawad akaomba akina mama waliokuwa wanamsaidia kumpeleka katika nyumba yake kwani mwili wake haukuwa na nguvu hivyo alihitaji kutegemezwa.Akasaidiwa kunyanyuka kisha akategemezwa kuelekea katika nyumba yake.Aliomba aachwe katika sebule ya chini kabisa halafu akaomba aitiwe Nawal mjane wa Abu Dahir ambaye aliletwa kisha akawataka wale akina mama wawaache wapumzike.Habiba akamtaka Nawal amsaidie wakaingia katika lifti kwani hakuwa na nguvu za kupanda ngazi.Waliingia katika sebule maalum ya Habiba akamuomba mtumishi wake amtengenezee kahawa ambayo ililetwa ndani ya muda mfupi.Habiba akanywa kidogo na kumtazama Nawal aliyekuwa ameinamisha kichwa huku machozi yakiendelea kumtoka “Pole sana Nawal najua umeumia kwa kifo cha Abu Dahir” akasema Habiba.Nawal akafuta machozi halafu akasema “Mama mimi ndiye ninayepaswa kukupa pole.Unapitia kipindi kigumu sana mama yangu.Umewapoteza watoto wawili ndani ya kipindi kifupi.Hakuna ajuaye ni maumivu kiasi gani unayoyapitia hivi sasa na mimi ni mmoja wa waliochangia kukusababishia maumivu haya makubwa.Nisamehe sana mama sikukusudia kumuua Abu Dahir.Imetokea bahati mbaya tu” akasema Nawal “Nawal nimekwisha kwambia na ninarudia tena kukwambia kwamba katu usihisi hatia katika jambo hili.Halikuwa kusudio lako na ulikuwa unaniokoa mimi.Kama usingekipiga kile chungu kingenipata na yawezekana mimi ndie ambaye ningepoteza maisha badala yake.Siwezi kukulaumu badala yake ninapaswa kukushukuru.Haya yanayonitokea ni adhabu kufuatia mambo mabaya niliyoyafanya.Watu wengi wamekufa kwa sababu yangu.Ninamini Mungu ananiadhibu na ninastahili adhabu hii.Nawal hakuna chochote kizuri nilichokipata kwa haya yote niliyoyafanya zaidi ya kuchuma dhambi.Awali waliponifuata wakaniambia wanataka kunitumia kufadhili makundi ya wanamgambo walinidanganya kwamba ni kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa kifo cha mume wangu ambaye niliamini aliuawa na vikosi vya Israel kumbe aliuawa na Marekani.Pamoja na kumwaga damu ya watu wengi lakini mume wangu hajarudi na sijapata amani niliyotegemea kuipata kwa kulipiza kisasi.Baadae nilikuja kugundua kwamba ni Marekani ndio waliomuua mume wangu na toka hapo nikawa na hasira sana nao na nikaanza kutafuta namna ya kulipiza kisasi hadi mlipojitokeza ninyi” akasema Habiba na kunyamaza “Mama kuna kitu nataka kukwambia” akasema Nawal “Sema usohofu Nawal” “Baada ya haya yote yaliyotokea sidhani kama nitakuwa na amani kama nitaendelea kuishi hapa.Nimetafakari sana nimeamua kurejea nyumbani Marekani” akasema Nawal na Habiba aliendelea kukaa kimya akitafakari halafu akasema “Nawal hapa ni nyumbani kwako.Wewe na Mathew ni watoto ambao nimebaki nao hivyo huna sababu ya kurejea nyumbani” akasema Habiba “Mama Habiba nafahamu namna unavyotupenda mimi na Mathew Mulumbi lakini utanisamehe kwa maamuzi haya.Naomba uniruhusu niende nyumbani” akasema Nawal “Nawal bado ninakuhitaji sana” akasema Habiba “Nafahamu mama lakini naomba uniruhusu niende nyumbani.Sintakuwa na amani hapa.Niache nikatulize akili na pale nitakapokuwa sawa nitarejea” akasema Nawal “Nawal najua uko katika wakati mgumu kufuatia kifo cha Abu Dahir lakini nakuhitaji kwa ajili ya misheni muhimu sana” akasema Habiba “Misheni ipi mama?akauliza Nawal “Halafu hujanieleza alipo Mathew.Yuko salama?akauliza tena Nawal “Nilitaka kukueleza kuhusu Mathew lakini likatokea lile tatizo na kila kitu kikavurugika” akasema Habiba na kunyamaza kidogo “Mathew yuko katika misheni kubwa hivi sasa” “Misheni ipi mama,unaweza ukanieleza? “Nilikueleza kwamba Marekani ndio waliomuua mume wangu wa pili ambaye ni baba yake Abu Dahir.Baada ya kulifahamu hilo niliumia sana na nikaanza mipango ya kukisambaratisha kikundi kidogo ndani ya CIA ambacho kimekuwa kinashirikiana na makundi mbali mbali ya kigaidi.Niliwarejesha akina Mathew waliokuwa katika kisiwa cha Fiji kwani nilimuhitaji Mathew kwa ajili ya operesheni hiyo muhimu” “Ni operesheni ipi hiyo mama? Nawal akauliza “Nadhani tayari umekwisha sikia kwamba Rais wa Uganda alipinduliwa na jeshi” “Ndiyo nilisikia taarifa hizo tukiwa jijini Cairo kutazama mapiramidi” akasema Nawal “Basi mpango ule ulisukwa na hiki kikundi kidogo ndani ya CIA kinachojihusisha na mashirikiano na makundi ya kigaidi.Mpango huu ni kuiwezesha Marekani kupata mafuta ya kutoka nchini Uganda na ili waweze kufikia lengo lao ililazimu kuchochea vurugu za kidini na ndiyo chanzo cha machafuko makubwa yanayoendelea Afrika mashariki hivi sasa.Wanawatumia kundi la IS katika kuchochea machafuko hayo.Watu wanaendelea kuuana huku Marekani wakifurahia neema ya mafuta.Huu ni unyama mkubwa” akasema Habiba “Mathew Mulumbi ameenda huko ndiyo maana hakuonekana katika msiba wa Najma? Akauliza Nawal “Mathew Mulumbi yuko Afrika Mashariki lakini katika misheni tofauti” “Ni misheni gani imempeleka Mathew huko?akauliza Nawal “Marekani na Iran ziko katika mgogoro mkubwa hivi sasa na marais wa nchi hizo mbili wamekuwa wakitupiana maneno mazito ya vitisho.Katika mwendelezo huo wa kutoleana vitisho Rais wa Iran ametishia kuanza kuwashambulia washirika wa Marekani na baada ya hapo ataishambulia Marekani na kuiharibu kabisa.Hilo limewatisha wamarekani na kuwafanya wasimamishe kwanza mipango yao ya kuishambulia kijeshi Iran kwa hofu kwamba yawezekana Iran ikawa inamiliki silaha kama kama inavyojitapa.Ukweli ni kwamba mpaka sasa Marekani bado hawana taarifa za uhakika kuhusiana na silaha ambazo Iran inazimiliki hivyo wameamua kumtumia Mathew Mulumbi katika misheni maalum” “Wanamtumia Mathew Mulumbi? Nawal akashangaa “Ndiyo Nawal.Nilitaarifiwa na kiongozi wa idara hiyo ndogo ndani ya CIA na kunitaka nimtafutie gaidi ambaye anafahamu mbinu za kijasusi kwa ajili ya kumtuma Iran kutekeleza kazi maalum.Kwa kuwa tayari nilikwisha kuwa na mipango ya kuimaliza idara hiyo niliamua kumpelekea Mathew Mulumbi.Wamempokea wakampima wakamuamini kuwa anafaa na tayari amekwisha tumwa kwenda kuanza kutekeleza misheni hiyo ambayo inaanzia nchini Tanzania” akasema Habiba “Mama hii ni misheni ya hatari sana umemuingiza Mathew.Atawezaje kuingia nchini Iran?Nawal akauliza “Mipango imeandalia na ndiyo maana amekwenda nchini Tanzania.Kule anakwenda kulipua ubalozi wa Marekani kisha atakamatwa na dunia nzima itajua kwamba Marekani imemkamata gaidi ambaye amelipua ubalozi wake jijini Dar es salaam.Baada ya kumkamata watamuunganisha na wanasayansi wa Iran ambao walitekwa na Marekani na baadae utatengenezwa mpango ili Mathew aweze kutoroka na wanasayansi hao wa Iran na hiyo itakuwa ni tiketi yake ya kuingia Iran.Kwa hicho alichokifanya kuwakomboa wanasayansi wa Iran atapokelewa kama shujaa na hapo ndipo atakapoanza kuifanya kazi aliyotumwa” “Mungu wangu ! akasema Nawal “Ni misheni ya hatari sana hii mama na sina hakika kama Mathew anaweza akafanikiwa.Kwanza jina lake litachafuka na dunia nzima watamjua kuwa yeye ni gaidi na muuaji.Vipi kuhusu ndugu na familia yake?Unadhani wataumia kiasi gani?Vipi kuhusu nchi yake unadhani watamuamini tena baada ya taarifa kusambaa kwamba ni gaidi na amelipua ubalozi wa Marekani? Mama umeyafanya maisha ya Mathew yawe magumu sana na hata kama akikamilisha misheni hii maisha yake hayatakuwa sawa tena na wewe utakuwa umechangia kwa kiasi kikubwa kuyaharibu” akasema Nawal “Nawal nafahamu hiki alichokwenda kukifanya Mathew ni kitu cha hatari sana lakini ni lazima aende katika misheni hii ili aweze kumaliza ugaidi duniani.Nimempeleka makusudi ili aweze kufahamu ni nani wanaofadhili makundi mbali mbali ya ugaidi duniani hivyo anatakiwa kuwa karibu nao awasome na kisha awamalize.Dunia nzima haijui kama mzizi wa ugaidi uko katika nchi inayopinga ugaidi kwa nguvu zote.Hili hata wamarekani wenyewe hawalifahamu kama mzizi huu uko ndani ya nchi yao.Hawajui kama vita ambayo imekuwa ikiendeshwa na nchi yao na kupata ushindi ni kama hadaa kwao na kwa dunia.Watashangaa kujua kwamba mashambulio mbali mbali ambayo yamekuwa yakifanywa na magaidi katika nchi mbali mbali duniani.Ni jukumu la Mathew Mulumbi kuhakikisha kwamba dunia inafahamu kila kitu kuhusiana na hiki kinachofanywa na Marekani kupitia idara hii ndogo ndani ya CIA na ili aweze kuimaliza idara hii ndogo lazima ashirikiane nao afahamu mambo yao na akusanye ushahidi wa kutosha kisha awamalize na dunia ijue kila kitu” akasema Habiba “Nafahamu ni misheni ya hatari sana lakini ni lazima Mathew aifanye na kama akiikamilisha salama itakuwa na faida kubwa kwa dunia.Ninamuamini Mathew na kuna sauti ndani mwangu inayoniambia kwamba Mathew ataitekeleza misheni hiyo kama alivyotumwa.Mathew atakuwa salama.Nimejiuliza zaidi ya mara elfu moja kama nimefanya kitu sahihi kumpeleka Mathew Mulumbi katika misheni hii? Jibu nililolipata ni kwamba nimefanya kitu sahihi.Mathew Mulumbi ni mtu sahihi.Ni kweli jina lake litachafuka baada ya kukamatwa kwa kulipua ubalozi wa Marekani jijini Dar es salaam lakini mwisho wa misheni hii jina lake litaandikwa kwa dhahabu.Dunia nzima itamuheshimu kwa kile atakachokifanya.Nawal umefika wakati wa kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi lakini ni nchi hizi kubwa ambazo zinafanya dunia isiwe sehemu salama kwa kuchochea machafuko hasa katika nchi za kiafrika na zile ambazo zimebarikiwa utajiri mkubwa” akasema Habiba “Mama lazima na mimi uniunganishe na misheni hii.Mathew hawezi kuifanya peke yake.Anahitaji mtu wa kumsaidia.Tafadhali mama” akasema Nawal “Hapana Nawal.Wewe una misheni nyingine ambayo unakwenda kuitekeleza ambayo nayo ni ya muhimu sana” akasema Habiba “Misheni ipi hiyo mama?akauliza Nawal “Meli za Marekani zimepanga foleni jijini Tanga Tanzania zikipakia mafuta yatokayo nchini Uganda.Kumekuwa na dalili za kupatikana kwa amani nchini Tanzania na hii itaathiri kwa kiasi kikubwa uchukuaji wa mafuta kwani amani ikipatikana, Tanzania haitahitaji tena msaada wa vikosi vya Marekani na zoezi la uchukuaji wa mafuta litakoma.Marekani wanahitaji vikosi vyao kuendelea kuwepo nchini Tanzania na Uganda ili waendelee kuchukua mafuta hivyo basi wamekuja na mpango mwingine ambao utawafanya waongeze vikosi zaidi nchini Tanzania” Habiba akanyamaza “Hivi sasa wanasayansi wa Marekani wanatengeneza kirusi hatari ambacho kitapelekwa kusambazwa nchini Tanzania.Kirusi hicho ambacho bado hakijajulikana jina lake kinatarajiwa kusababisha maangamizi makubwa na kupelekea Marekani kuongeza wanajeshi zaidi nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa msaada hivyo vikosi vya Marekani kuendelea kukaa muda mrefu Afrika Mashariki.Nataka ukavuruge misheni hiyo” akasema Habiba “Hiyo ni misheni ya hatari sana mama lakini niko tayari kuifanya kwa ajili ya kuzuia njama ovu za Marekani.Siamini kama nchi yangu imefikia hatua hii ya kutojali utu kwa ajili tu ya kujipatia mafuta.Huu ni ukatili mkubwa sana” akasema Nawal “Wanaofanya hivi ni kundi la watu wachache sana na hata Rais wa Marekani hafahamu chochote kwani ni kundi linaloendeshwa kwa siri kubwa sana na Rais hapaswi kufahamu” akasema Habiba “Hata kama ni kundi dogo lakini linaiwakilisha Marekani na endapo ikijulikana dunia haitaelewa kama ni kundi la watu wachache bali watakachofahamu kuwa ni Marekani.Nielekeze mama ni namna gani nitaweza kuzuia mpango huu usifanikiwe? Akauliza Nawal “Wanataka kutumia mtu kutoka mtandao wa IS kwenda kusambaza kirusi hicho nchini Tanzania.Kesho mtu huyo atakuja hapa kwa ajili ya safari ya kuelekea Marekani kuandaliwa kwa zoezi hilo la kwenda kusambaza kirusi Tanzania.Itakulazimu kwenda nchini Tanzania” akasema Habiba na kumtazama Nawal “Kuna machafuko makubwa na hadi sasa kiwanja cha ndege kimefungwa lakini ni lazima uende kwani bila kuzuia mpango huo usifanikiwe kirusi hicho kinaweza kuwa hatari sana kwa dunia” “Mimi niko tayari kwenda huko Tanzania mama siogopi machafuko.Nataka nikaonane na Mathew” akasema Nawal “Misheni yako ni tofauti na ya Mathew na hutatakiwa kuonana na Mathew kwani unaweza ukavuruga misheni yake” “Nani basi atakuwa mwenyeji wangu Tanzania?Sijawahi fika huko na kama ningeweza kuonana na Mathew ambaye yuko huko Tanzania angenisaidia sana” “Kumpata Mathew ni ngumu kwa sasa lakini kuna mtu ambaye Mathew ana ukaribu naye yuko Tanzania.Tutawasiliana naye ili awe mwenyeji wako.Naamini tukimwambia kwamba wewe ni mtu wa karibu na Mathew lazima atakubali kukupokea” akasema Habiba “Itakuwa vizuri kama akikubali” “Ni mtu muhimu kwa Mathew hivyo lazima atakubali.Kesho huyo mtu ambaye atakwenda kusambaza kirusi hicho Tanzania atafika hapa kabla ya kuelekea Marekani.Baada ya kumfahamu mtu huyo ni nani,utaondoka kuelekea Tanzania na nitaendelea kuwasiliana nawe kukupa taarifa za kila kinachoendelea kuhusianana mpango huo” akasema Habiba na ukimya mfupi ukapita “Nawal hii ni misheni muhimu sana na haitakiwi kushindwa kwani ukishindwa kuzuia kirusi hicho kusambazwa basi kinaweza kuvuka mipaka ya Tanzania na kuwa janga la dunia.Najua ni jukumu zito lakini ni lazima kwa namna yoyote ile ulitimize” akasema Habiba “Mama usiogope nitalitimiza na kuhakikisha mpango huo haufanikiwi.Nifanyie maandalizi na kila kitu kitakapokuwa tayari nijulishe” akasema Nawal. DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa mbili za usiku jijini Dar es salaam Mathew na wenzake walimaliza kupata chakula cha usiku kisha haraka haraka masanduku ya silaha yakapakiwa katika magari halafu kila mmoja akashika bunduki yake na kuingia garini.Mathew akatakiwa kwenda chumbani kwake kupumzika.Hakutaka kuwauliza wanakwenda wapi lakini ni wazi kwa namna walivyojiandaa walikuwa wanakwenda kufanya shambulio sehemu Fulani.Geti likafunguliwa magari yale yakatoka halafu jenereta likazimwa na kukawa giza.Ndani ya bohari dogo ambako shughuli ya uundwaji wa bomu ilikuwa inaendelea walikuwa wanatumia jenereta dogo lisilotoa sauti Mathew aliingia chumbani kwake akaubamiza mlango ili walinzi wasikie kwamba tayari yuko chumbani “Lazima nitoke hapa usiku huu nikawasake akina Ruby nijue kama wako salama au vipi” akawaza Mathew na taratibu akaufungua mlango na kunyata kuelekea katika mlango wa jikoni ambao haukuwa umefungwa,akausukuma na kuingia ndani ya jiko akatulia kusikiliza kama kuna mtu yeyote,kulikuwa na ukimya mkubwa.Jikoni kulikuwa na mlango wa kutokea nje akakiminya kitasa taratibu mlango ukafunguka akatoka nje na kujibanza ukutani kusikiliza lakini hakusikia sauti yoyote zaidi ya sautio za wadudu.Mchana wa siku ile aliutumia vyema kuyasoma mazingira ya mahala pale hivyo alikwisha fahamu ni wapi atapita.Kutoka pale jikoni akatembea kwa tahadhari hadi katika magari mawili mabovu yaliyokuwa yameegeshwa karibu na ukuta,pembeni ya magari yale kulikuwa na lundo la matofari yamepangwa,akapanda matofari yale na kuushika ukuta.Alijilaza juu ya ukuta na alipohakikisha kuko salama akajirusha nje bila kuoa ukelele. “Sasa nielekee nyumbani kwangu.Kutoka hapa hadi nyumbani kwangu kuna umbali kidogo lakini nitajitahidi kukimbia na kutumia njia za mkato.Sina silaha yoyote lakini Mungu atanifikisha salama” akawaza Mathew huku akifuata uchochoro uliompeleka hadi barabarani.Mtaa wote ulikuwa kimya kabisa na giza.Ni sauti za mbwa wakibweka ndizo zilisikika.Bila upoteza muda Mathew akaanza kukimbia akielekea katika barabara kubwa “Mimi si mgeni wa maeneo haya hivyo siwezi kupata taabu wakati wa kurudi” akawaza Mathew akiendelea kukimbia hadi alipoikuta barabara kuu akaanza kuifuata.Mpaka wakati huo hakuwa amekutana na mtu hata mmoja “Bado mapema sana lakini jiji la Dar es salaam ni tupu,liko kimya wakati jiji hili limezoeleka ni jiji la kukesha.Lazima hili jambo limalizike haraka sana” akawaza Mathew akiendelea kukimbia. Alikimbia kwa dakika hamsini na mara kwa mbali akashuhudia moto mkubwa na kusikia makelele ya watu.Akaendelea kukimbia kwa tahadhari kubwa hadi alipokaribia eneo lile akakutana na kundi la watu wakifurahia baada ya kulichoma gari.Wengine walikuwa na bunduki.Mathew akaungana nao lakini ghafla zikaanza kusikika risasi za moto na kundi lile likatawanyika. “Twendeni huku ! akapiga ukelele jamaa mmoja aliyekuwa na bastora mkononi,Mathew na watu wengine wanne wakaanza kumfuata “Risasi zile zimetokea wapi?akauliza Mathew wakati wakikimbia “Wanajeshi wamefika ! akajibu Yule jamaa mwenye bastora huku akihema kwa kasi Walikatisha vichochoro kadhaa na mara mmoja wao akajikwaa katika jiwe akaanguka na kuanza kupiga makelele ya kuvunjika mguu.Mathew akawataka wasubiri,akamuinua Yule jamaa akamuweka begani akaanza kukimbia naye.Baada ya muda wakajikuta katika njia ya kuelekea bonde la mto Msanzi.Bado Mathew aliendelea kumbeba Yule jamaa mabegani hadi walipofika katika lundo la mchanga wakapumzika.Mathew akamuweka chini Yule jamaa na wote wakaanza kumtazama.Alikuwa amevunjika mguu na vile vile alichomwa na kipande cha chupa tumboni.Hali yake haikuwa nzuri kwani alipoteza damu nyingi “Tunamsaidiaje huyu?akauliza Mathew “Tunasubiri wenzetu waje tujipange tuone namna ya kumsaidia huyu mwenzetu”akasema mmoja wa wale jamaa. “Hapana hatuwezi kusubiri hadi wenzetu wafike tutampoteza huyu jamaa” akasema Mathew “Unashauri nini?Mwingine akauliza “Tumpelekeni hospitali” “Hospitali?! Huoni hali ilivyokuwa mbaya huko mtaani? “Mnataka tumuache huyu mwenzetu afie hapa?Mathew akauliza kwa ukali “Hii si sawa hata kidogo.Hatuwezi kumuacha mwenzetu afe wakati tunao uwezo wa kumsaidia.Lazima tumpeleke hospitali” akasema Mathew “Hospitali gani tumpeleke?Karibu hospitali zote zimejaa majeruhi” “Tujaribu hospitali yoyote ile lakini hatuwezi kumuacha mwenzetu hapa.Kama ninyi hamtaki mimi nitampeleka mwenyewe ! akasema Mathew kisha akamuinua Yule jamaa akaanza kuondoka naye.Wale jamaa wakashauriana halafu wakaamua kuambatana na Mathew wakasaidiana kumbeba Yule jamaa kupandisha kilima hadi walipofika barabarani.Mathew akamuweka begani Yule jamaa na kuanza kutembea haraka haraka wakiwahi hospitali.Wakati wakitembea Mathew akakiona kituo cha mafuta kandoni mwa barabara “Hiki ni kituo cha mafuta?akauliza huku akimulika kwa tochi ya mmoja wa wale jamaa aliokuwa nao “Ndiyo ni kituo cha mafuta,kwa nini umeuliza”akauliza mmoja wao “Kuna gari zimeegeshwa pale.Tunahitaji gari kwani hatuwezi kuokoa maisha ya mwenzetu kama tukiendelea kutembea kwa miguu” “Hatuwezi kupata gari hapa.Watu wameweka hapa magari yao kisha wakakimbia na funguo zao” akasema Yule jamaa “Kuna yeyote ana kisu hapa?:akauliza Mathew na mmoja wao akampa kisu kidogo “Wewe mwenye bastora nifuate” akasema Mathew kisha kwa tahadhari wakaelekea katika kituo kile cha mafuta na kunyata hadi katika magari yaliyokuwa yameegeshwa pale kituoni.Mathew akachagua gari moja lenye rangi nyeusi akakipiga teke kioo cha upande wa dereva kikavunjika akaingiza mkono ndani na kuufungua mlango.Akamtaka Yule jamaa amulike tochi ya simu ndani ya gari,na kwa kutumia kisu akang’oa sehemu ya funguo kisha akakata nyaya na kuzichuna akazigusanisha na mara gari likawaka.Yule jamaa aliyekuwa naye hakuamini macho yake.Mathew akaliondoa gari wakampakia yule mgonjwa na safari ya kuelekea hospitali ikaanza. “Umefanyaje hadi gari likawaka?akauliza Yule jamaa aliyekuwa na bastora “Nina utaalamu kidogo na magari”akajibu Mathew na kupunguza mwendo wa gari baada ya kukuta mawe makubwa barabarani.Wakashuka na kwenda kuyatoa mawe yale na safari ikaendelea.Walipita barabara kadhaa hadi walipofika katika hospitali ya Mtodora ambako kulikuwa na ulinzi mkali sana.Mathew akawajulisha walinzi kwamba kulikuwa na majeruhi garini na walipomuona haraka haraka wakafungua geti na akina Mathew wakaingia ndani.Haraka haraka majeruhi Yule akachukuliwa na kwenda kuanza kupatiwa huduma. “Nini kinafuata?Mathew akawauliza wale jamaa “Kwa sasa ni kufuatilia kujua kama wenzetu wako salama na tujue tunakutana wapi” akajibu mmoja wa wale jamaa huku akitoa simu akawasiliana na watu kadhaa akawajulisha kwamba wao wako katika hospitali ya Mtodora kuna mwenzao wamempeleka pale ameumia.Alipomaliza kuzungumza Mathew akamfuata na kumuomba simu yake awasiliane na mtu Fulani na alipompa Mathew akaziandika namba za simu za Ruby “Nina bahati ubongo wangu una uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu kwani ninazikumbuka namba za simu za Ruby” akawaza Mathew na kupiga simu ikaanza kuita bila kupokelewa.Akapiga tena “C’mon Ruby pick up ! akawaza Mathew na safari hii simu ikapokelewa. “Hallow ! ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Mathew aliitambua ni sauti ya Ruby. “Hallow Ruby ! akasema Mathew “Nazungumza na nani?Ruby akauliza “Ni mimi Mathew Mulumbi.Uko salama Ruby? “Mathew?! Ruby akashangaa “Ruby tuokoe muda.It’s me Mathew.Uko wapi tafadhali? “Mathew?!! Ruby akauliza tena “Sikiliza Ruby nahitaji kuonana nawe usiku huu.Ni muhimu sana” akasema Mathew “Wewe ni Mathew yupi?Mathew Mulumbi ninayemfahamu hayupo Tanzania” “C’mon Ruby It’s me Mathew.Ni mimi mpenzi wako.Niko hapa Tanzania” akasema Mathew na sekunde kadhaa za ukimya zikapita kisha Ruby akauliza “Uko sehemu gani Mathew? “Niko hapa hospitali ya Mtodora” akajibu Mathew “Sawa ninatuma watu waje hapo kukuchukua” akajibu Ruby na kukata simu.
Ruby alihisi mwili wote unamtetemeka baada ya kuzungumza na Mathew simuni. “Huyu niliyeongea naye ni Mathew kweli?Lakini sauti ni yake .Kama kweli ni yeye amekuja lini Tanzania?Mathew mbona ana maajabu namna hii?Alinipigia simu Najma kutoka Saudi Arabia lakini leo hii Mathew yuko hapa amewezaje kuingia nchini? Akawaza Ruby akiwa amejishika kiuno. “Nilidhani ninamfahamu Mathew vizuri kumbe bado sana.Itanichukua muda mrefu kidogo kumfahamu huyu ni mtu wa namna gani” akawaza Ruby na kuchukua simu akampigia Gosu Gosu akamtaka aende mara moja ofisini kwake.Gosu Gosu ambaye alikuwa amekwenda katika chumba chake kupumzika akafika mara moja ofisini kwa Ruby “Kuna nini Ruby?akauliza Gosu Gosu “Gosu Gosu nimetoka kuzungumza na Mathew muda mfupi uliopita” “Umezungumza na Mathew? Akauliza “Ndiyo nimezungumza naye.Yuko hapa Dar es salaam” “Mathew yuko Dar es salaam?! Gosu Gosu naye akashangaa “Ndiyo.Mathew yuko hapa http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Dar es salaam.Nimezungumza naye akiwa katika hospitali ya Mtodora” “Is he okay? Akauliza Gosu Gosu “I don’t know.Hajasema chochote kuhusu anafanya nini hapo hospitali ila amesema kwamba anataka kuonana nami usiku huu ni muhimu sana” akasema Ruby “Ruby una uhakika mtu uliyezungumza naye simuni ni Mathew Mulumbi? Gosu Gosu akauliza “Naifahamu sauti yake.Sina shaka ni yeye.Lakini swali ni je amefikaje hapa nchini? Ameingiaje? Ni juzi tu nimepigiwa simu na Yule mwanamke Najma kutoka Saudi Arabia akisema kwamba Mathew alikuwa ananitafuta halafu leo hii yuko hapa nchini.Haya ni maajabu Gosu Gosu” “Si maajabu Ruby.Ni kweli kabisa.Huyo ndiye Mathew Mulumbi ambaye haishiwi maajabu” “Una uhakika ni yeye? akauliza Ruby “Nina uhakika Ruby.Ninakwenda huko Mtodora kumchukua” akasema Gosu Gosu “Hapana huwezi kwenda peke yako.Utaongozana na kikosi cha makomando wetu kwenda huko hospitali” akasema Ruby na kumuita ofisini kwake kiongozi wa kikosi kile cha makomando ambaye alifika haraka akamtaka achukue makomando0 wanne waongozane na Gosu Gosu kuelekea hospitali ya Mtodora kumchukua Mathew Mulumbi. Haraka haraka waliingia katika gari lao maalum lisilopenya risasi wakaondoka kuelekea hospitali ya Mtodora
Gosu Gosu na timu ya makomando waliwasili katika hospitali ya Mtodora kisha wakamjulisha Ruby kuwa tayari wamewasili na Ruby akapiga namba ile ya simu ambayo aliitumia Mathew kuwasiliana naye.Simu ikapokelewa na sauti nyingine “Samahani kaka kuna mtu mmoja ametumia simu hii kuwasiliana nami si muda mrefu sana.Uko naye karibu?Ninaweza kuzungumza naye?akauliza Ruby akiwa na wasiwasi “Sawa niko naye hapa karibu” akasema Yule jamaa na kumfuata Mathew akampatia simu “Kuna mtu anataka kuzungumza nawe” akasema Yule jamaa na kumpa simu Mathew “Hallo” akasema Mathew “Mathew kuna watu nimewatuma hapo hospitali waje kukuchukua wakiongozwa na Gosu Gosu,tayari wamekwisha fika wako getini” akasema Ruby “Ahsante Ruby” akasema Mathew na kukata simu akamfuata Yule jamaa “Mimi ninaondoka.Hakikisheni mwenzenu amepata nafuu ndipo muondoke hapa hospitali” akasema Mathew ambaye alikuwa amechafuka damu “Unakwenda wapi? Ni hatari sana huko mitaani” akasema yule jamaa ambaye hadi muda huo hawakuwa wamefahamishana majina yao “Usijali nitakuwa salama” akasema Mathew na kuanza kupiga hatua kuondoka halafu akageuka “By the way gari lile mtalirejesha mahala tulipolichukua.Kingine nawashauri baada ya mwenzenu kupata nafuu rudini nyumbani msiendelee kushiriki katika vurugu hizi ambazo hazina manufaa yoyote kwenu” akasema Mathew na kuondoka zake akaenda getini na mara akasikia akiitwa “Mathew” Mathew aliitambua sauti ile akasimama kutazama ilitoka wapi na mara akamuona mtu mmoja akiwa ameinua mkono akimuelekeza mahala alipo akamfuata “Gosu Gosu ! akasema Mathew kwa furaha wakakumbatiana “Mathew siamini kama nimekuona tena kaka yangu ! akasema Gosu Gosu “Mimi ndiye siamini kama nimefanikiwa kuonana tena Gosu Gosu ukiwa katika hali hii.Vipi maendeleo yako? “Ni kama unavyoniona.Ninaendelea vyema kabisa” akasema Gosu Gosu “Vipi kuhusu Ruby?Naye anaendeleaje? “Naye vile vile anaendelea vyema kabisa” akasema Gosu Gosu na kumuongoza Mathew kuelekea katika gari ambalo kulikuwa na watu watatu wanne wamesimama nje wakiwa na bunduki .Gosu Gosu akawajulisha watu wale kwamba mtu waliyemfuata pale hospitalini ni Yule aliyeongozana naye.Mathew akawasalimu wale makomando kisha wakaingia garini na safari ya kuelekea makao makuu ya SNSA ikaanza. “Tunaelekea wapi?Ruby yuko wapi?akauliza Mathew “Tunaelekea SNSA pale ndipo tumeweka kambi kwa sasa kufuatia vurugu hizi zinazoendelea” akasema Gosu Gosu “Nawe pia uko SNSA? Akauliza Mathew “Ndiyo niko SNSA Ruby aliniomba niwe msaidizi wake.Nilikubali ili kuhakikisha anakuwa salama muda wote kwani kazi anayoifanya ni ya hatari kubwa” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana Gosu Gosu kwa kuhakikisha Ruby anakuwa salama.Vipi kuhusu Lucy naye yuko salama? “Lucy yuko salama kabisa ninakwenda kila siku kujua maendeleo yake.Kwa bahati mbaya pale katika kambi yetu wanaoruhusiwa ni wafanyakazi tu wa SNSA vinginevyo ningemchukua pale ili awe salama zaidi” akasema Gosu Gosu Walifika ofisi kuu ya SNSA salama.Hawakupata matatizo yoyote njiani.Mathew aliongozana na Gosu Gosu wakaingia ndani na moja kwa moja wakaelekea katika ofisi ya Ruby ambaye hakujua kama tayari wamerejea.Alikuwa amejiegemeza katika kiti akionekana kuwa katika mawazo mengi.Gosu Gosu ndiye aliyemstua baada ya kugonga mlango na kufungua akaingia ndani huku Mathew akimfuata kwa nyuma.Ruby alipomuona Mathew akainuka na kumkumbatia kwa nguvu. “Mathew my love ! akasema Ruby “Habari Ruby” akasema Mathew “Siamini kama kweli leo hii niko nawe tena.Huu ni kama muujiza kwangu” akasema Ruby “Huu si muujiza Ruby.Ni kweli niko hapa” akasema Mathew lakini Ruby bado alisimama akiendelea kumshangaa “Ruby nimefurahi kuwaona wewe na Gosu Gosu mko salama lakini sina muda mrefu sana wa kukaa hapa” akasema Mathew “Mathew tafadhali kabla hujatueleza chochote nihakikishie kama uko salama” “Niko salama kabisa.Hizi damu nilimsaidia mtu aliyeumia nikamfikisha hospitali lakini mimi niko salama kabisa msihofu” akasema Mathew na kuketi kitini “Nashukuruni ndugu zangu nimefanikiwa kuwaoneni tena mkiwa salama.Nilikuwa nahofia sana usalama wenu kwani ninyi ni watu wangu wa pekee kabisa” akasema Mathew “Tuko salama Mathew.Tumeweka kambi hapa katika ofisi yetu na wafanyakazi wetu wote wanaishi hapa” akasema Ruby “Ruby nina muda mchache sana wa kuwepo nanyi hapa hivyo nataka nijielekeze moja kwa moja katika yale ya msingi.Nina mambo machache ya kuwaeleza moja ni kwamba nimeingia hapa nchini jana usiku.Nimekuja nchini kwa operesheni maalum.Pili ni kuhusiana na hizi vurugu zinazoendelea hapa nchini hivi sasa.Nataka kujua kuna chochote mnakifahamu hadi sasa kuhusiana na vurugu hizi? Mmekwisha zifanyia uchunguzi?akauliza Mathew “Ndiyo.Tumeanza kuzifanyia uchunguzi tayari ili kuupata mzizi wake” akasema Ruby na kumuelezea Mathew namna walivyofanya uchunguzi na mahala walipofikia katika uchunguzi wao “Kwa hapo mlipofika ilikuwa lazima mkwame kwa sababu suala hili lina nguvu kubwa kutoka nje ya nchi” akasema Mathew “Ndani ya idara ya ujasusi ya Marekani CIA kuna idara ndogo ambayo inajishughulisha na mahusiano na makundi mbali mbali ya kigaidi duniani.Wanayatumia makundi hayo ya kigaidi kwa ajili ya manufaa ya Marekani.Wamekuwa wakilitumia sana kundi la IS katika eneo la Mashariki ya kati.Wanalitumia kundi hili kuanzisha mashambulio sehemu Fulani kisha hupeleka vikosi vyao kwa kigezo cha kuwasaka magaidi kumbe wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake na mara nyingi hufanya hivyo kwa nchi zile ambazo zinakuwa na utajiri wa kitu Fulani” Mathew akanyamaza akamtazama Ruby ambaye alikuwa anafuta machozi “Machafuko haya yanayoendelea hapa nchini na Uganda ni mpango wa Marekani” “Mpango wa Marekani?Ruby akashangaa “Ndiyo Ruby” “Marekani wamekitumia kikundi cha kigaidi cha IS kuchochea vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa na lengo kubwa la kufanya hivyo ni ili wapate nafasi ya kuleta vikosi vyao hapa Tanzania na kuchukua mafuta kutoka Uganda.Hivi tuzungumzavyo meli kubwa za mafuta za Marekani zmepanga foleni katika bandari ya Tanga zikipakia mafuta kutoka Uganda” “Jesus Christ ! akasema Gosu Gosu “Mathew nakubaliana nawe na ahsante kwa kutufumbua macho kwani bila wewe ingetuchukua miaka kuweza kuligundua hili.Vurugu hizi zilianzia nchini Uganda kwa kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu kuuawa kisha likatokea shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika kanisa ambalo lilisababisha vifo vya watu wengi.Baada ya hapo wakristu wakaanzisha vurugu kwa kuchoma nyumba za ibada za waislamu na kisha wakaanza kushambuliana.Kwa hapa Tanzania vurugu hizi zilianzia jijini Tanga ambako nako kulifanyika mashambulio katika makanisa na misikiti mashambulo yaliyowalenga viongozi wa dini na kupelekea waumini wa dini hizi mbili kuanza kushambuliana na machafuko yakaenea hadi jijini Dar es salaam.Ukitazama miji ambayo imekuwa na machafukoi makubwa kwa hapa Tanzania ni Dar es salaam na Tanga na baada ya maelezo haya ya Mathew sasa picha imeonekana kwamba vurugu hizi ziko kimkakati zaidi.Huwezi kuchukua mafuta ya Uganda bila kudhibiti bandari ya Tanga na ndicho walichokifanya” akasema Ruby “Lakini IS hawako peke yao.Kuna watu wa ndani ya nchi ambao wanashirikiana nao katika jambo hili na yawezekana miongoni mwao ni hao ambao tayari mmeanza kuwafanyia uchunguzi na hawajulikani mahala walipo.Suala hili halitaweza kumalizika hadi pale litakapochimbwa hadi mzizi wake.Tumekwisha fahamu nani walio nyuma ya hizi vurugu lakini lazima vile vile kujua wanaochochea vurugu hizi hapa nchini ni akina nani na baada ya kuwabaini basi wawekwe wazi dunia iwajue na hii ndiyo itawafumbua macho wananchi kwamba walishawishiwa kuingia katika zile vurugu bila kujua” akasema Mathew “Toka mwanzo niliamini kwamba hili suala linaweza kuwa na mkono kutoka nje ya nchi na sasa tumeufahamu ukweli” akasema Gosu Gosu “Rais alikutana na kufanya mazungumzo na mufti wa Tanzania halafu mufti akatoa hotuba yake akiwahusia waislamu kuachana na vurugu zile lakini usiku wa kuamkia leo aliawa” akasema Mathew “Mauaji haya ya mufti yamekwamisha juhudi za kutafuta amani kwani viongozi wengine wa dini ambao walihitaji kuzungumza na Rais wameingiwa na woga” akasema Ruby “IS ndio waliomuua mufti ili kuchochea vurugu hizi kwa maelekezo ya Marekani.Ilionekana vurugu zinaanza kupungua na Marekani wanahitaji vikosi vyao kuendelea kukaa Afrika mashariki kwa muda mrefu zaidi hivyo walipanga mauaji yale ya mufti wakiwatumia IS ili kuwachochea waislamu na wakristu waendelee kushambuliana” “Tumejiuliza sana kuhusu mauaji yale ya mufti tukakosa jibu.Tunashukuru Mathew kwa kutufumbua macho” “Nimekuja hapa kuwapeni taarifa hizi ili ziwasaidie katika uchunguzi wa suala hili. akasema Mathew “Mathew we need you ! akasema Ruby “I know. I know”akasema Mathew na kumtazama Ruby “Ruby I’m very sorry sintaweza kushirikiana nanyi katika suala hili.Nina misheni nyingine kubwa zaidi ambayo imenileta hapa Tanzania ila nitakachoweza kuwasaidia ni kuwapa taarifa muhimu ninazozifahamu na ninyi mtaendelea.SNSA ni idara kubwa naamini mtaweza kulifanikisha suala hili” akasema Mathew “Mathew we real need you.Tumekwama na hatutaweza kulitatua jambo hili bila wewe” akasema Ruby “Jambo hili lina pande mbili.Kuna upande wa ndani na upande wa nje.Ninyi mtashughulika na upande wa ndani mimi nitashughulikia upande wa nje.Upande wa ndani kuna kundi la IS na kuna watu ambao wanawasaidia IS kufanikisha lengo lao la kuchochea vurugu.Hapa mnatakiwa kuwatafuta watu hao ni akina nani pamoja na kulimaliza kundi la IS hapa Tanzania.Kuwakamata watu wa ndani wanaoshirikiana na IS kuchochea vurugu hizi bado haitakuwa imesaidia kumaliza tatizo kwani nguvu ya nje ni kubwa zaidi na wanaweza wakafanya lolote ili mradi kuendeleza machafuko ili waendelee kuchota rasilimali.Mimi nitashughulika na nguvu hii ya nje.Mambo haya yote yanafanywa na kikundi kidogo cha watu ambao wao wanadai Marekani iko katika mikono yao na wanaiendesha watakavyo.Kikundi hicho kidogo ndicho kinachoisumbua dunia hivi sasa na kusababisha machafuko kila sehemu.Kila ukifungua taarifa za habari hukosi kukuta kuna taarifa za tukio la kigaidi sehemu Fulani na mengi ya matukio haya yanafanikishwa na kikundi hiki.Umefika wakati wa kukimaliza kikundi hiki na kupunguza kama si kumaliza kabisa ugaidi duniani kwa sababu vikundi vingi vya ugaidi vinategemea ufadhili kutoka kwa kikundi hiki kidogo.Ninaomba mniamini ndugu zangu kwamba ninakwenda kukimaliza kikundi hiki.Ni misheni ngumu na ya hatari sana lakini lazima niikamilishe.Wamemwaga damu ya ndugu zetu na siwezi kukubali damu ya mtanzania ikapotea bure lazima ilipwe hivyo nawataka muhakikishe mnawashughulikia watu wa ndani wakati mimi nikishughulika na watu wa nje.Kwa pamoja tutalifanikisha hili jambo” akasema Mathew “Mathew ni asubuhi ya leo mimi na msaidizi wangu Gosu Gosu tulipokwama hatujui nini tufanye tulianza kukujadili kwamba laiti ungekuwepo ungetusaidia kutuondoa katika mkwamo huu kwani sisi hatuna ujuzi mkubwa katika masuala haya kama wewe.Nilimpigia Najma ili niweze kuzungumza nawe lakini simu yake haikuwa ikipatikana” akasema Ruby na sura ya Mathew ikabadilika baada ya kusikia jina la Najma likitajwa “Umesema Najma? Akauliza Mathew “Ndiyo” “Najma yupi ulimpigia kutaka kuzungumza nami? “Najma mke wako.Huna mke anaitwa Najma?akauliza Ruby na Mathew akavuta pumzi ndefu wakatazamana “Kuna kitu unataka kukisema Mathew? Ruby akauliza “Umefahamuje kuhusu Najma?Ulikuwa unanifuatilia? Mathew akauliza “Ndiyo maana uliniambia nisikufuatilie ili nisifahamu kama umebadili jina lako na unaitwa Abu Zalawi raia wa Saudi Arabia na pia umemuoa Najma? Akauliza Ruby “Ulinifuatilia ukayafahamu haya?Kwa nini ukapuuza maelekezo yangu Ruby?akauliza Mathew akimtazama Ruby kwa macho makali. “Sikukufuatilia Mathew.Ninaheshimu makubaliano yetu.Nilipigiwa simu na Najma mwenyewe akajitambulisha kwangu kama mke wako na kwamba ulikuwa unanitafuta simuni hukunipata.Alinipigia kuuliza kama ninakufahamu lakini alikutaja kwa jina la Abu Zalawi na si Mathew Mulumbi.Nilimweleza sikufahamu na wala sina rafiki anaitwa kwa jina hilo.Baadae nilimpigia na kumtaka anitumie picha za huyo Abu akadai kwamba hana picha.Nilipatwa na wasi wasi labda Uingereza wameanza kunitafuta ikanilazimu kuingia mtandaoni kutafuta ndipo nikakupata” akasema Ruby akamtazama Mathew.Macho yake yalilengwa machozi.Mathew akavuta pumzi ndefu kisha akasema “Ni kweli.Yote aliyokwambia Najma ni kweli kabisa lakini hapa si mahali pake tutayazungumza hayo siku nyingine.Nataka tujielekeze katika jukumu lililo mbele yetu” akasema Mathew na Ruby akafuta machozi “Mathew naomba utuamini kwamba tumekwama na tunahitaji sana msaada wako.Tafadhali endelea na misheni yako baada ya kuhakikisha kwamba tumelimaliza hili suala na nchi iko salama.Nisingekuomba haya kama tungekuwa na uwezo huo” akasema Ruby “Ruby siwezi.Misheni ninayokwenda kuitekeleza ni kubwa na yenye manufaa kwa dunia nzima.Ninakwenda katika misheni ya hatari kuliko misheni zote nilizowahi kushiriki” “Mathew ni misheni ipi hiyo unayokwenda kuifanya ambayo ni muhimu kuliko kuisaidia nchi yako?akauliza Ruby “Ninakwenda kukiondoa kikundi hiki kidogo ambacho kimekuwa kikishirikiana na magaidi na kuharibu amani ya dunia” “Mathew ..! akasema Ruby lakini Mathew akamkatisha “Don’t say anything Ruby.Tayari ninafahamu kile unachotaka kukisema.Kikundi hiki ndicho mzizi wa haya machafuko yanayoendelea hapa nchini hivyo misheni hii pia ni mwendelezo wa kuisaidia nchi yetu na dunia” akasema Mathew na ukimya ukapita “Kuna mambo ambayo mtayasikia kuhusu mimi lakini nawaomba mtakapoyasikia msiyaamini hata kidogo.Niko katika misheni nzito na hayo yatakayotokea na kunihusisha mimi ni sehemu ya misheni hiyo.Utakuwa ni mshangao kwa wengi lakini ninyi nawaomba msishangae kuweni na imani na mimi.Baada ya kuikamilisha misheni hiyo nitarejea nyumbani”akasema Mathew na kuwatazama akina Ruby ambao kila mmoja alibaki na maswali kichwani “Tuachane na suala hilo.Kuna mtu anaitwa Assad Ismail.Huyu anaongoza kundi la IS katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.Makazi yake ni Mombasa Kenya lakini kwa sasa yuko hapa nchini na ndiye anayesimamia jukumu la IS la kuchochea vurugu.Yeye na watu wake ndio waliomuua mufti jana na wao ndio waliofanya na wanaoendelea kufanya mauaji ya viongozi wadini ili kuchochea vurugu.Mnatakiwa kumpata huyu Assad kwani atawasaidia sana kufahamu mambo mengi kuhusiana na watu wanaoshirikiana nao hapa nchini na mnaweza mkafahamu vile vile kuhusiana na wale ambao mnahisi wanahusika katika machafuko haya lakini wamepotea na hawajulikani walipo.Sifahamu Assad anaishi wapi hapa Dar es salaam lakini kuna mtu ambaye anaweza akawaongoza kujua mahala alipo Assad.Mtu huyo anaitwa Marwan Hossam.Huyu anaishi kwa Botha nyumba namba 604.Hii ni nyumba wanamoishi magaidi wa IS na mipango yao yote ya mashambulio hupangwa katika nyumba hii.Mkivamia nyumba hii mtapata mambo mengi yanayoweza kuwasaidia kufahamu mambo mengi kuhusiana na hili suala” akasema Mathew “Mathew tunashukuru sana kwa taarifa hii.Nashauri kwa nini tusiende kuvamia nyumba hiyo usiku huu tukiwa pamoja nawe kabla hujaendelea na misheni yako? Akauliza Gosu Gosu “Kwa leo haiwezekani Gosu Gosu.Jambo hili mtalifanya usiku wa kesho baada ya mimi kuondoka.Mimi ninamaliza misheni yangu kesho usiku na kuondoka na ninyi mtaenda kuvamia nyumba hiyo na kumkamata Marwan Hossam ambaye atawapeleka mahala alipo Assad” “Kwa nini leo haiwezekani Mathew?Tunao makomando wetu ambao watatusaidia kuvamia nyumba hiyo”Ruby naye akasisitiza. “Haiwezekani kwa sababu ninaishi ndani ya nyumba hiyo” akasema Mathew na mstuko uliowapata Ruby na Gosu Gosu ulikuwa mkubwa. “Unashirikiana nao?akauliza Ruby akionyesha sura ya wasi wasi “Ni sehemu ya misheni yangu ndiyo maana nikatangulia kuwaomba kwamba msistuke kwa mtakachokisikia kuhusu mimi hapo baadae” akasema Mathew “Kitu gani umekuja kukifanya Mathew? Umewezaje kuingia hapa nchini? Akauliza Ruby “Ruby natamani sana niwaeleze lakini sitakiwi kufanya hivyo.Ninawaomba mniamini ndugu zangu.Naamini utafika wakati ambao nyote mtashikwa na butwaa lakini naomba ninyi wawili muendelee kuwa na imani nami.Yote mtakayosikia ni sehemu ya misheni yangu kubwa” akasema Mathew “Mathew unatuogopesha sana kwa haya maneno yako.Nini kinakwenda kutokea?akauliza Gosu Gosu “Usihofu Gosu Gosu utasikia tu.Nawaombeni ndugu zangu kwa sasa tuliweke pembeni hilo na tujielekeze katika hiki kinachoendelea hapa nyumbani.Suala hili ni kubwa na ninawaomba muwe na umakini mkubwa sana mnapolishughulikia.Magaidi hawa wa IS wana silaha nzito na wanapata msaada kutoka kwa vikosi vya Marekani.Kwa mfano Assad anapotoka mahala anakoishi kwenda katika nyumba hiyo ambayo ni kambi ya magaidi husindikizwa na gari la doria la vikosi vya Marekani.Hali ni mbaya huko mtaani na kwa hili walilolifanya la kumuua Mufti litaongeza zaidi machafuko haya.Usiku huu wameondoka tena na silaha nzito naamini kuna mahali wamekwenda kufanya shambulio” akasema Mathew “Mathew nakushukuru sana kwa kuja.Kwa mara nyingine tena umedhihirisha ni namna gani ulivyo na umuhimu mkubwa kwa nchi hii.Hatukuwa tukifahamu chochote kuhusu haya yanayoendelea.Tulifika mahala tukakwama na hatujua wapi kwa kutokea lakini umetokea wewe na kutumulikia mwanga sasa tumepata sehemu ya kuanzia.Naamini misheni hiyo uliyonayo ni muhimu sana kwani hujawahi hata mara moja kukataa kufanya misheni kwa ajili ya nchi yako.Tumekuelewa Mathew na tunakutakia kila la heri katika hiyo misheni yako ambayo kama ulivyotuhakikishia ni kwamba itakuwa na manufaa makubwa sana kwa nchi na dunia nzima.Sisi tutaendelea kusimama nawe na kukuombea uweze kumaliza salama operesheni hiyo.Muda wowote utakapohitaji msaada wetu sisi tupo tayari kukusaidia” akasema Ruby “Ruby ninashukuru kwa kunielewa.Muda wowote nitakapohitaji msaada wenu nitawasiliana nanyi haraka sana” akasema Mathew na ukimya ukapita “Ruby na Gosu Gosu ninashukuru tena kwa kuonana nanyi ndugu zangu na kuhakikisha mko salama.Nilikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na usalama wenu lakini kwa sasa nina amani na hata huko nitakapokuwa nitakuwa na amani kwamba ndugu zangu wako salama.Naomba sasa mniruhusu niondoke lakini naomba mnipatie mavazi nibadilishe” akasema Mathew na Gosu Gosu akaenda kumletea mavazi ya kubadilisha kwani nguzo zile alizokuwa amevaa zilikuwa zimechafuka damu. “Mathew sijui niseme nini.Sijui ni………” akasema Ruby baada ya Gosu Gosu kuondoka “Don’t say anything.Pray for me.I promise I’ll come back” akasema Mathew “Mathew nina wasi wasi sana kuhusu usalama wako” “Usihofu Ruby.Nitakuwa salama na nitarejea.Narudia tena kuwaomba hakikisheni kwa namna yoyote ile mnawapata hawa watu niliowapa taarifa zao ili nchi iwe na amani.Tanzania haikupaswa kuwa namna hii.Mambo kama haya tulikuwa tunayaona katika nchi nyingine lakini sasa yamefika kwetu.Hali ni mbaya sana huko mitaani.Nakuhakikishia Ruby kwa hiki walichokifanya kumwaga damu za watanzania namna hii huku wao wakiendelea kushangilia neema ya mafuta kutoka Uganda hawatabaki salama.Nitahakikisha kikundi hiki kidogo cha hawa watu ninakifutilia mbali.Ni misheni ndefu na ya hatari lakini nitakufa nikijaribu.Bila kukiondoa kikundi hiki dunia haitakuwa mahala salama” akasema Mathew “Mathew sijui kwa nini ninahisi baridi kila unapotamka kuhusiana na misheni hiyo ya hatari ambayo umeshindwa kutueleza ni misheni gani.Kama ingekuwa ni kwa ridhaa yangu ningekuzuia usiende huko lakini siwezi.Oh Mathew ! akasema Ruby na kuinamisha kichwa machozi yalikuwa yanamtoka “Ruby huu si wakati wa kumwaga machozi.Damu za watanzania wenzetu zinamwagika hivyo hatupaswi kumwaga machozi tunatakiwa kupambana kuhakikisha tunarejesha maisha kuwa ya kawaida” akasema Mathew na Gosu Gosu akaingia.Mathew akavua zile nguo zilizochafuka damu na kuvaa nguo alizopewa na Gosu Gosu.Ruby akasimama na kumkumbatia Mathew “Mathew please be safe my love” akasema Ruby “I will” akajibu Mathew na kumuachia Ruby wakaongozana kutoka nje wakaelekea katika gari lile la makomando Mathew hakugeuka nyuma kumtazama Ruby akaingia garini na gari likaondoka,Ruby akarejea ofisini kwake akajifungia akilia.
Mathew aliwataka akina Gosu Gosu wamuache karibu na mtaa ilipo nyumba ile ya magaidi . “Gosu Gosu tafadhali hakikisha Ruby anakuwa salama.Hakikisheni pia amani inarejea hapa nchini tayari nimekwisha wapa mwanga sehemu ya kuanzia” akasema Mathew “Mathew ninakushukuru sana kwa taarifa hizi ulizotupa.Nakuahidi hakuna atakayesalia.Tutawasaka wote hadi mtu wa mwisho” akasema Gosu Gosu “Ahsante Gosu Gosu.Mbaki salama” akasema Mathew kisha akaanza kukimbia kuelekea katika mtaa alikofikia.Kulikuwa na ukimya mkubwa.Alifika katika nyumba yao akazunguka upande wa nyuma akapanda ukuta na kurukia ndani bila kutoa ukelele.Hakukuwa na mtu yeyote mahala pale akatembea kwa tahadhari kuelekea katika mlango wa nyuma akaufungua na kuingia jikoni kisha akaelekea moja kwa moja chumbani kwake.Ilipata saa kumi kasoro za alfajiri.Mathew akajilaza kitandani. “Ahsante Mungu kwa kunirejesha salama bila hawa watu kujua” akasema kwa sauti ndogo. “Nimefurahi kuwakuta Ruby na GosuGosu wakiwa salama.Hiki ndicho kitu ambacho nilikuwa naomba sana kuwakuta watu hawa wako salama.Ninashukuru vile vile kwa Gosu Gosu kuungana na Ruby na hii inanipa uhakika mkubwa kwamba Ruby atakuwa salama.Hata hivyo kuna kitu ambacho sikukitegemea kabisa.Najma kumpigia simu Ruby na kujitambulisha kuwa yeye ni mke wangu.Nilistuka sana.Sikutegemea kabisa kitu kama hiki kutokea.Sikutaka Ruby afahamu chochote kuhusu maisha yangu kule Saudi Arabia.Nimejaribu kumtuliza lakini ameumia.Kwa nini Najma alimpigia simu Ruby? Akajiuliza Mathew na kukumbuka kitu. “Nakumbuka siku ile tuliporejea kutoka Fiji na Habiba akanieleza kuhusu machafuko yanayoendelea hapa Tanzania nilitaka kumpigia simu Ruby kujua kama yuko salama lakini simu yake haipatikani nakumbuka Najma alikiona kitabu kile nilichokuwa nimeandika namba za simu na akaiona namba ya simu ya Ruby akaniuliza Ruby ni nani? Nadhani kuanzia pale alianza kuwa na mashaka na nilipoondoka akaamua kumpigia simu Ruby akitaka kumfahamu kama ni mpenzi wangu.Hata hivyo tumefikia mwisho kwani Habiba alinitaka nisirejee tena Saudi Arabia.Kama misheni hii ikimalizika na nikabahatika kuwa mzima nitarejea Tanzania na kumuoa Ruby” akawaza Mathew na kuvuta pumzi ndefu “Kuna nyakati ninaingiwa na hofu kubwa kuhusiana na misheni hii ninayokwenda kuifanya.Ni misheni ya hatari sana na itagharimu damu ya watu wengi” akawaza “Lakini sipaswi kuogopa.Bila kuifanikisha hii misheni nchi zetu zitaendelea kuwa uwanja wa vita.Machafuko yataendelea huku mabepari hawa wakiendelea kuchota mai zetu na kunufaisha nchi zao.Lazima nijitoe mhanga kuhakikisha hili haliendelei.” akawaza Mathew na kijiusingizi kikaanza kumpitia akalala.
Saa kumi na mbili za asubuhi ilimkuta Ruby akiwa bado ofisini kwake.Hakupata usingizi hivyo aliendelea kufanya kazi usiku.Wafanyakazi walipoanza kuingia ofisini asubuhi walimkuta akiwa ofisini akiendelea na kazi.Saa mbili za asubuhi akawakusanya wote kwa ajili ya kuwapa taarifa muhimu. “Habarini za asubuhi ndugu zangu.Naamini nyote mnaendelea vyema” Ruby akawasalimu wafanyakazi wa SNSA “Usiku wa kuamkia jana watu wasiojulikana walimuua Mufti wa Tanzania ikiwa ni katika muendelezo wa mauaji ya viongozi wa dini ambayo ndiyo chanzo cha vurugu hizi zinazoendelea.Kutwa nzima ya jana tulikuwa katika kutafuta nani waliomuua kiongozi huyo wa dini bila mafanikio lakini usiku wa jana tulipata taarifa kutoka katika chanzo chenye uhakika kwamba mauaji haya yanayoendelea yanafanywa na kikundi cha kigaidi cha IS” akasema na kunyamaza akawatazama wafanyakazi “Vurugu hizi zote ambazo zinaendelea nchini hivi sasa IS ndio waliozichochea.Walifanya mauaji ya kule Tanga ambayo ndicho kilikuwa chanzo cha vurugu kwa hapa Tanzania.Walihamia Dar es salaam na kuendelea na zoezi lile lile la kuua viongozi wa dini kwa ajili ya kuchochea vurugu baina ya waumini wa dini za kikristu na kiislamu.Juzi mufti wa Tanzania alikutana na Rais wakazungumza faragha na baadae wakazungumza na watanzania akawaomba waislamu wasiendelee na vurugu lakini usiku wa siku hiyo akauawa kwa bomu yeye na familia yake.Kwa nini Mufti aliuawa? Akauliza Ruby “Hotuba aliyoitoa Mufti kuwataka watanzania wasiendelee kushambuliana na kuuana ilionekana kuwa na mapokeo mazuri kwani vurugu zilipungua kwa kiasi kikubwa baada ya hotuba ile na hii iliwapa hofu wale wanaotaka vurugu kuendelea ndiyo maana wakamuua” Ruby akanyamaza “Haikuishia hapo katika mauajiya Mufti.Usiku wa kuamkia leo nyumba ya imevamiwa na watu wenye silaha kwa lengo la kufanya shambulio lakini walikutana na upinzani mkali kutoka kwa askari polisi waliokuwa hapo wakilinda kwani serikali imeweka ulinzi mkali katika nyumba zote za watawa,shule za dini,makanisa na misikiti.Wavamizi hao waliokuwa na silaha nzito walishindwa kutekeleza lengo lao baada ya kuzidiwa nguvu na kukimbia huku wakitelekeza silaha zao.Waliofanya shambulio hilo tunaamini ni kikundi cha IS ambao lengo lao ni kuchochea vurugu.Wamemuua kiongozi wa waislamu ili ionekane ni wakristu wamefanya hivyo na wakataka tena kuua watawa wa kikristu ili ionekane kwamba waislamu wamefanya mauaji hayo ili kulipiza kisasi kwa kiongozi wao kuuawa na lengo kubwa ili waumini wa dini hizi mbili waendelee kushambuliana” akanyamaza Ruby na kushika kitanza mbali akabonyeza na picha kubwa ikatokea katika runinga “Anaitwa Assad Ismail.Huyu ni kiongozi wa IS katika eneo la Afrika Mashariki na kati na makazi yake ni Mombasa Kenya ila kwa sasa yuko hapa nchini kwa ajili ya misheni ya kuchochea vurugu.Assad yuko hapa Dar es salaam lakini hatujui ni sehemu gani na huyu ndiye ambaye anaongoza kikosi cha magaidi wanaoua viongozi wa dini na kuchochea machafuko zaidi” akabonyeza tena kitanza mbali ikatokea picha nyingine “Anaitwa Marwan Hossam.Huyu anaishi hapa Dar es salaam eneo la kwa Botha nyumba namba 604.Huyu ndiye anayefahamu mahala anakoishi Assad hapa Dar es salaam.Kwa taarifa tulizo nazo ni kwamba nyumba hii ndimo ambao IS wamekuwa wakipanga mipango yao yote ya mauaji” akasema Ruby akatulia kidogo “IS hawako peke yao.Kuna watu wanashirikiana nao katika kuchochea vurugu hizi.Watu hao lazima wapo hapa nchini.Kama mtakumbuka tumekuwa na zoezi la kuwafuatilia watu kadhaa ambao tunahisi wana mahusiano na vurugu hizi zinazoendelea lakini tumegundua wote wametoweka na hawajulikani walipo.Tunaamini upo mtandao ambao unashirikiana na magaidi hawa katika kuanzisha vurugu.Swali ambalo tunatakiwa kujiuliza ni je IS wanafanya haya yote kwa faida ya nani?Je kuna nchi au kikundi cha watu kimewatuma wafanye haya? Hayo ndiyo maswali ambayo tunatakiwa kuyatafutia majibu.Usiku wa leo tunakwenda kuvamia nyumba hiyo wanamoishi magaidi wa IS na kumchukua Marwan Hossam ambaye atatusaidia kujua mahala alipo Assad.Tukifanikiwa kumpata Assad tutajua kuhusu mtandao wa watu wanaoshirikiana nao katika kuchochea vurgu hizi wale wa ndani na nje ya nchi” akasema Ruby “Mchana wa siku ya leo tutaelekeza drone yetu katika nyumba hiyo wanamoishi hao magaidi kufuatilia kila kinachofanyika hapo ndani huku makomando wetu wakijipanga namna ya kuingia ndani na kuwachukua magaidi hao.Mmoja wa madereva wetu atapeleka gari hadi mbele ya nyumba hiyo ili tuwe na uhakika wa nyumba tunayoilenga.Mchana kutwa wa leo tutaanza kufuatilia kila kinachoendelea ndani ya nyumba hiyo na usiku wa leo kikosi cha makomando wetu kitavamia hapo.Tutachukua kila atakayekuwepo mahala hapo na kuja kuwafanyia mahojiano lakini mlengwa mkuu katika misheni hiyo ni Marwan Hossam ambaye atatuongoza kujua mahala alipo Assad Ismail” akasema Ruby na kutaka maandalizi yaanze mara moja kisha akaelekea ofisini kwake. Baada ya dakika kumi akaingia Gosu Gosu “Tayari dereva amekwisha ondoka na moja ya gari kuu kuu ambalo limewekewa mkanda maalum kwa juu ili kutuwezesha kumfuatilia.Baada ya kupata picha za nyumba hiyo wanamoishi magaidi makomando wataanza maandalizi ya namna wakatavyoweza kuingia humo ndani” akasema Gosu Gosu “Good” akajibu Ruby “Ruby kwa nini hujawaeleza ukweli kwamba ni Marekani ndio wako nyuma ya haya yote yanayoendelea hapa nchini?akauliza Gosu Gosu “Hapana hawapaswi kufahamu jambo hilo.Litabaki kati yetu kwa sasa.Nina hofu yawezekana jambo hili likivuja linaweza kuvurga kila kitu na tukashindwa kuwapata watu wanaojihusisha na machafuko hayo” akasema Ruby “Ruby macho yako mazito sana.Hujalala usiku wa kuamkia leo.Unahitaji kwenda kupumzika kidogo” akasema Gosu Gosu “Hapana Gosu Gsou siwezi kwenda kulala.Tuna kazi nyingi za kufanya kuhakikisha tunaupata mtandao wote wa watu wanaochochea vurugu hizi.IS wanaendelea kufanya mauaji hivyo lazima tuhakikishe kwamba tunawapata wote na kufahamu watu wanaoshirikiana nao” akasema Ruby “Tutawapata Ruby usihofu.Mathew amekwisha tupa mwanga na kuanzia hapa tunajua wapi tuelekee” akasema Gosu Gosu “Nilidhani ninamfahamu vizuri Mathew Mulumbi kumbe nilikuwa najidanganya.Bado simfahamu vizuri ni mtu wa aina gani.Mambo yake yananishangaza sana.Ni misheni gani aliyonayo ambayo inamfanya ashirikiane na hawa magaidi? Kitu gani kitatokea ambacho anasema tusikiamini tutakapokisikia?akauliza Ruby “Lazima itakuwa ni misheni kubwa sana lakini tusubiri tutajua” akasema Gosu Gosu RIYADH – SAUDI ARABIA Bado watu waliendelea kufika katika makazi ya Habiba Jawad kumpa pole kufuatia vifo vya mfululizo vya watoto wake wawili Najma na Abu Dahir.Saa tatu za asubuhi gari moja lilifika katika makazi yale ya Habiba na watu watano wakashuka.Walipokewa na Sayid Omar ambaye alikuwa anawapokea wageni mbali mbali wanaofika pale nyumbani akawapeleka katika nyumba Fulani akawakaribisha sebuleni nzuri halafu akamfuata Habiba Jawad akamjulisha kuwa wageni wamefika.Habiba akiwa ameongozana na Nawal wakaelekea katika nyumba walikopelekwa wale wageni. “Yule mtu kutoka IS ameletwa” Habiba akamwambia Nawal. Waliingia katika nyumba ile wakasalimiana na watu wale wakampa pole nyingi Habiba kwa msiba mzito uliompata.Baada ya hapo yakaanza maongezi kuhusiana na Yule mtu ambaye Habiba alimuhitaji kutoka IS kwa ajili ya kwenda kutumika katika zoezi la kusambaza kirusi nchini Tanzania.Aliitwa Sattar Sayf Al Din. Habiba na wale jamaa walikuwa na mazungumzo marefu yaliyochukua saa mbili kisha wakafikia makubaliano na wale jamaa wakamuaga Habiba wakaondoka ila Sattar akabaki.Baada ya wale jamaa kuondoka Habiba akamtaka Nawal kumpiga picha Sattar ili aweze kuzitma Marekani wamfahamu kwani alitarajia kuondoka jioni ya siku ile na ndege kuelekea Marekani.Baada ya kuzipata picha zile akamkabidhi Sattari kwa Sayid Omar ili ampeleke katika mojawapo ya nymba za wageni akapumzike wakati safari yake ya kwenda Marekani ikiandaliwa. “Tayari tumemfahamu mtu ambaye atatumiwa na Marekani kusambaza virusi nchini Tanzania” akasema Habiba “Ndiyo mama” akasema Najma “Kinachofuata ni wewe kwenda kumsubiri nchini Tanzania” akasema Habiba “Hakuna tatizo mama mimi niko tayari kwenda huko Tanzania” “Vizuri.Nitawasiliana na Yule mtu ambaye Najma aliwasiliana naye anaitwa Ruby ili nimuombe akupokee kwani ni mara yako ya kwanza kufika Tanzania” akasema Habiba “Nitajuaje kama Sattar amewasili Dar es salaam? Naamini safari yake ya Tanzania itakuwa ya kimya kimya sana” Akauliza Nawal “Nitawasiliana na watu wa IS ili wanipe mawasiliano ya mtu wa IS aliyeko Dar es salaam.Ninaamini yeye atakuwa na mawasiliano na Marekani na lazima atafahamu kuhusu Sattar na jibu nitakalolipata nitakujulisha.Utakapofika huko jitahidi upate mawasiliano”akasema Habiba “Nitajitahidi mama.Lakini ni vipi kama huyo mtu wa IS aliyeko Tanzania akakosa taarifa za Sattar?akauliza Nawal “Sattar lazima awe na mtu wa kumsaidia akiwa nchini Tanzania na mtu pekee ambaye anaweza akatumiwa ni aliye katika mtandao wa IS.Usihofu nitafanya kila niwezalo kupata taarifa za kuhusiana na Sattar” akasema Habiba “Sattar anaondoka leo kwenda Marekani na hatujui ni lini ataondoka Marekani kwenda Tanzania hivyo wewe utaondoka Kesho hadi Nairobi Kenya.Uwanja wa ndege wa Nairobi Kenya haujafungwa unaendelea kupokea ndege na kutoka pale utatafuta usafiri wa kukuingiza nchini Tanzania.Nitazungumza na Ruby nijue kama anaweza akakusaidia ukaweza kuingia Tanzania.Endapo hatakuwa na uwezo wa kukusaidia nitatafuta namna ya kuweza kukuingiza nchini Tanzania siwezi kushindwa” akasema Habiba halafu akaenda kuchukua kitabu ambacho Mathew alikuwa ameandika namba za simu akapekua na kuupata ukurasa ambao ulikuwa na namba za simu za Ruby,akaziandika katika simu yake na kupiga. “Simu inaita” akasema Habiba DAR ES SALAAM – TANZANIA Ruby alihisi uchovu mwingi akakiegemeza kichwa chake kitini.Mara simu yake ikaanza kuita akanyoosha mkono akaichukua na kutazama mpigaji zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake. “Hizi ni namba za simu za Saudi Arabia.Huyu lazima atakuwa ni Najma.Ngoja nimsikie anachotaka kunieleza” akawaza Ruby na kupokea ile simu “Hallow” akasema “Hallow,naongea na Ruby?akauliza mwanamama wa upande wa pili.Sauti ile haikuwa ya Najma.Ruby akastuka kidogo “Nani anaongea?akauliza Ruby “Naitwa Habiba Jawad,ninapiga simu kutoka Saudi Arabia” “Habiba Jawad?Ruby akauliza “Ndiyo.Nazungumza na Ruby?akauliza Habiba na Ruby akawa kimya.Alistuka sana “Hallow” akaita Habiba “Hallow umesema wewe ni nani?Ruby akauliza “Naitwa Habiba Jawad ninapiga simu kutoka Saudi Arabia.Wewe ni Ruby?akauliza Habiba “Ndiyo naitwa Ruby.Umenifahamuje?Umetoa wapi namba zangu?akauliza Ruby “Unamfahamu Mathew Mulumbi?akauliza Habiba na kuendelea kumstua zaidi Ruby “Ruby ! akaita Habiba “Nimekuuliza unamfahamu Mathew Mulumbi?akauliza Habiba “Umemfahamuje Mathew Mulumbi? “Mathew ni kijana wangu amemuoa binti yangu Najma ambaye alikupigia simu hivi majuzi” akasema Habiba na Ruby akahisi baridi ikimpenya “Ruby sikiliza mwanangu.Ninamfahamu Mathew Mulumbi na anaishi hapa kwangu na binti yangu Najma.Ni mimi niliyemtoa katika taabu na mateso aliyokuwa nayo na kuanza maisha mapya hivyo namchukulia kama mwanangu.Nimepata namba zako kutoka katika kitabu chake maalum” akasema Habiba “Unahitaji nini Habiba?akauliza Ruby huku sauti yake ikionekana kutetema “Nina shida naomba msaada wako” “Msaada gani unauhitaji? “Kuna binti yangu anakuja Tanzania.Ni mara yake ya kwanza hivyo nakuomba ukubali kumpokea na kumsaidia”akasema Habiba “Binti yako anakuja Tanzania?Najma? Ruby akauliza “Hapana si Najma.Anaitwa Nawal” akasema Habiba na Ruby akavuta pumzi ndefu. “Ruby ! akaita Habiba “Anakuja kufanya nini Tanzania? Akauliza Ruby “Kuna kazi anakuja kuifanya.Nakuomba umpokee tafadhali na umsaidie.Kwa kuwa uwanja wa ndege wa Dar es slaam umefungwa atalazimika kupita nchini Kenya atashukia jijini Nairobi na kutokea pale atatumia magari ya kawaida kuingia Tanzania kupitia mpaka wa Namanga akielekea Dar es salaam” akasema Habiba “Hakuna haja ya kwenda kushukia jijini Nairobi.Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro umekwisha funguliwa kwa sasa na unaendelea kutoa huduma.Ndege zote ambazo zilipaswa zitue katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam sasa zinakwenda kutua uwanja wa Kilimanjaro.Mikoa ya Kaskazini hakuna vurugu kubwa kama ukanda huu wa pwani hivyo nashauri kama anakuja ashukie Kilimanjaro na mimi nitakwenda kumpokea hapo” “Ahsante sana Ruby.Nitalifanyia kazi hiyo ili aweze kushukia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.Nategemea aondoke kesho asubuhi na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia” “Mimi niko Dar es salaam lakini nitafanya utaratibu wa kuhakikisha huyo mwanao anafika Dar es salaam” “Nashukuru sana Ruby .Ni namna gani nitaweza kukutumia fedha za kufanikisha jambo hilo?Sitaki uingie gharama kwa kutumia fedha zako.Kama kuna namna yoyote naweza kukutumia fedha nielekeze tafadhali” akasema Habiba “Usijali mama.Huna haja ya kutuma fedha.Kwa kuwa umemsaidia Mathew basi nami nitamsaidia mwanao.Unaweza ukaniambia anakuja kufanya nini Tanzania wakati huu wa machafuko?akauliza Ruby “Kuna jambo muhimu sana linamleta hapo Tanzania.Tafadhali naomba umsaidie” akasema Habiba “Nitamsaidia usijali” “Sawa.Nitakutumia picha zake ili umfahamu” akasema Habiba na kuagana na Ruby “Haya ni mambo gani yanaendelea? Mathew anashirikiana na Habiba Jawad? Ruby akajiuliza.Alishangaa sana “Nini kimetokea hadi Mathew akaamua kujiunga na Habiba Jawad?Huyu mama ndiye anayefadhili makundi ya kigaidi duniani. Dah ! ni vigumu kuamini ! akawaza Ruby “Ninahisi mwili unakosa nguvu kwa kulifahamu hili.Mathew anafahamu kabisa Habiba Jawad ni nani lakini ameamua kushirikiana naye na kama haitoshi amemuoa hadi mwanae Najma.Nini kimemtokea Mathew Mulumbi hadi akaamua kushirikiana na magaidi? Ndiyo maana alinionya nisimfuatilie kwa kuogopa ningeweza kugundua anashirikiana na Habiba Jawad mfadhili mkubwa wa ugaidi duniani.Kadiri ninavyoendelea kumfahamu Mathew ninazidi kugundua mambo mengine ambayo yananitisha na kunifanya nimuogope.Mathew ninayemuona sasa si Mathew Yule ambaye nilimfahmau miaka kadhaa iliyopita ambaye nilitokea kumpenda kupita ninavyojipenda mwenyewe.Nadhani ninachokipata mimi ndicho alichokipata Peniela na akaamua waachane.Ninaanza kuona maamuzi ya Peniela kuachana na Mathew yalikuwa sahihi.Ninampenda sana Mathew kwa moyo wangu wote lakini sina hakika kama nina kifua cha kuvumilia haya yanayomzunguka” akawaza Ruby na kutazama juu “Kama tayari ameanzisha mashirikiano na Habiba Jawad ni wazi ameamua kushirikiana na kundi la IS na hapa nchini anadai amekuja kwa ajili ya misheni maalum.Lazima alichokuja kukifanya kinahusiana na kundi la IS.Nini amekuja kukifanya? Huyo Nawal naye anakuja kufanya nini?Naamini huyu Nawal naye kuna kitu anakuja kukifanya hapa Tanzania ambacho kinahusiana na IS” akaendelea kuwaza. “Hapana siwezi kumuacha Mathew akapotea namna hii.Lazima nimsaidie japo hatapenda lakini lazima nifanye kitu kumsaidia kwani akiendelea kushirikiana na mtandao huu wa kigaidi maisha yake yatakuwa mashakani.Siwezi kukubali Mathew awe gaidi.Kwa kuwa tayari amekwisha tuelekeza nyumba walimo magaidi wa IS nitaelekeza vikosi kuvamia nyumba hiyo na kuwachukua magaidi wote akiwamo Mathew.Atashikiliwa kwa muda ili kumuhoji kujua ni kitu gani kimemsababisha akabadilika kutoka Jasusi hadi Gaidi.Siwezi kuvumilia lazima haraka sana makomando wetu wakavamie nyumba hiyo” akawaza na kuchukua simu akampigia Gosu Gosu akamtaka aende ofisini kwake mara moja “Kuna nini Ruby? Akauliza Gosu Gosu “Gosu Gosu ninazidi kuchanganywa na huyu Mathew” “Kuna nini tena kuhusu Mathew?akauliza Gosu Gosu na Ruby akavuta pumzi ndefu “Nimepokea simu muda si mrefu kutoka Saudi Arabia” “Kutoka kwa Najma?akauliza Gosu Gosu “Unamkumbuka Habiba Jawad?akauliza Ruby “Habiba Jawad Yule mfadhili wa ugaidi?Ninamkumbuka” akajibu Gosu Gosu “Huyo ndiye aliyenipigia simu” “Habiba Jawad amekupigia simu?! Gosu Gosu akashangaa “Ndiyo amenipigia simu” “Amepataje mawasiliano yako? “Ni mambo ya ajabu sana Gosu Gosu” “Niambie Ruby.Habiba Jawad amepataje namba zako?Alikupigia kwa dhumuni gani? Akauliza Gosu Gosu “Habiba Jawad ni mama yake Najma ambaye ameolewa na Mathew” akasema Ruby na mstuko ukaonekana usoni kwa Gosu Gos “Najma ni mtoto wa Habiba Jawad? “Ndiyo.Habiba amenihakikishia kwamba Mathew anaishi kwake na amemuoa mwanae Najma” “Haya ni maajabu.Inawezekanaje Mathew akajiunga na Habiba ambaye anafadhili ugaidi?akauliza Gosu Gosu “Nimejiuliza swali hilo sijapata jibu.Mathew anafahamu fika kwamba Habiba ni mfadhili wa ugaidi lakini amekubali kujiunga naye.Gosu Gosu,Mathew huyu wa sasa si Yule tuliyemfahamu.Hata siku moja Mathew Mulumbi hawezi akajiunga na magaidi ! akasema Ruby “Yawezekana hii ni sababu kwa nini alikwambia usimfuatilie atakapoondoka” akasema Gosu Gosu “Exactly.Alijua nitafahamu kuwa anashirikiana na Habiba Jawad” “Mungu wangu ! Mathew kwa nini amefanya maamuzi haya ya kushirikiana na magaidi wa IS? “Hata mimi najiuliza swali hilo sijapata jibu” akasema Ruby “Habiba alitaka nini alipokupigia simu? “Amenieleza kuwa mwanae anaitwa Nawal anakuja Tanzania akaniomba nimsaidie aweze kuingia salama” “Mwanae anakuja Tanzania? Anakuja kufanya nini wakati huu wa machafuko? “Hajanieleza anakuja kufanya nini ila amesema kuna jambo muhimu linalomleta hapa Tanzania. Akaniomba nimsaidie aweze kufika Dar es salaam.Naamini kinachomleta hapa ni mojawapo ya shughuli za IS kama ilivyo kwa Mathew” “Anakuja lini? “Kesho.Nitakwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro” “Haya mambo yanachanganya sana” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu huyu Mathew si Yule tumjuaye.Huyu ni Mathew tofauti kabisa.Hata siku moja Mathew Mulumbi hawezi kushirikiana na magaidi hivyo nimefanya maamuzi ya kutuma makomando wetu wakavamie nyumba ile mchana huu na wawachukue wote watakaowakuta akiwemo Mathew .Tutamshikilia sehemu salama kwa mahojiano ili atueleze kwa nini amefanya maamuzi haya ya kushirikiana na magaidi?akasema Ruby.Gosu Gosu akafikiri kwa muda kisha akasema “Hapana Ruby hatuwezi kufanya hivyo” “Kwa nini Gosu Gosu?Mathew amebadilika na hatuwezi kumuacha akaendelea namna hii.Anashirikiana na magaidi na hata sasa kuna kitu wanapanga kukifanya hapa Dar es salaam siku ya leo ndiyo maana alituzuia tusivame ile nyumba hadi usiku wa leo.Kwa hiki anachokifanya Mathew maisha yake tayari yapo hatarini na kama mtu wetu wa karibu ni jukumu letu kuhakikisha tunamsaidia.Yawezekana haoni hatari iliyoko mbele yake au anashirikiana nao kwa shinikizo.Tunatakiwa tufahamu kila kitu” akasema Ruby “Ruby sikubaliani na wazo lako kwa sababu Mathew ni mtu anayejua nini anakifanya.Kama ameingia katika mashirikiano na magaidi basi ni kwa sababu maalum.Si mara moja Mathew ameingia katika sehemu za hatari kwa ajili ya kufanikisha misheni muhimu.Naamini hata huku aliko sasa hajaenda kwa bahati mbaya,ana sababu maalum na kama unakumbuka jana amezungumza nasi na akatutahadharisha kwamba tutakachokisikia kuhusu yeye tusikiamini.Sasa nimeelewa kwa nini alitupa taarifa ile mapema kwani alijua tungeweza kufahamu mambo kama haya kuhusu yeye kushirikiana na magaidi.Alituandaa tusistuke tutakapogundua hilo na alitupa maelekezo vile vile kwamba tusifanye chochote hadi usiku wa leo.Hii ina maana kwamba kuna misheni inaendelea na kama angekuwa hana nia njema asingefanya jitihada za kututafuta na kutupa taarifa muhimu.Ni yeye ambaye ametupa mwanga kuhusiana na vurugu hizi zinazoendelea na sasa tuna sehemu ya kuanzia.Hatua zozote za kwenda kinyume na maelekezo ya Mathew kinaweza kupelekea kwanza tukavuruga misheni ya Mathew na vile vile tunaweza kujikuta tumevuruga kila kitu kuhusu misheni yetu” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu ! “Hapana Ruby hatutafanya chochote tutafuata maelekezo ya Mathew.Ninamuamini Mathew sana na kama wewe umeanza kupoteza imani kwake mimi bado namuamini na nitaendelea kufuata maelekezo yake” akasema Gosu Gosu “Papii,Mathew huyu si Yule ambaye tunamfahamu.Hata siku moja Mathew Mulumbi tunayemfahamu hawezi akakubali kushirikiana na magaidi” akasema Ruby “Ruby hakuna sababu yoyote ya kuvamia yumba wanayoishi Mathew na watu wa IS mchana huu.Operesheni itaendelea usiku kama tulivyopanga.Kitu kingine ambacho ninakiona cha msingi tumsubiri huyo mtoto wa Habiba Jawad anayekuja kesho anaweza akatueleza mambo mengi zaidi.Hatupaswi kwenda haraka haraka tutavuruga kila kitu.Kumbuka tulikuwa tumekwama na hatukujua sehemu ya kuanzia lakini ni Mathew aliyekuja kutukwamua.Nakuomba Ruby tuwe na uvumilivu katika hili.Mathew anajua kwamba watu wake wa karibu lazima watafahamu kuwa anashirikiana na magaidi na wataumia hivyo alitutaka tusitetereke.Naomba tubaki hivyo” akasema Gosu Gosu na Ruby akabaki akimtazama
Licha ya kutokea kwa mauaji ya kiongozi mkuu wa waislamu Tanzania lakini jiji la Dar es salaam na viunga vyake halikuwa na vurugu ambazo zilitegemewa kutokea.Maelfu ya waumini wa dini ya kiislamu walihudhuria mazishi ya kiongozi wao yaliyofanyika mchana wa siku hiyo.Ulinzi ulikuwa mkali sana wakati wa mazishi hayo na viongozi waliokuwepo walitumia muda mwingi kuwaomba waumini wasilipize kisasi kwani kitendo hicho kingeongeza vurugu zaidi na damu nyingi ingeendelea kumwagika.Walitumia muda mwingi zaidi kuhubiri uwepo wa amani kama njia ya kumuenzi kiongozi Yule aliyeuawa ambaye alipenda kuona amani inapatikana nchini. Kiza kilianza kutanda angani bado jiji la Dar es salaam halikuwa na vurugu kama zilizokuwepo siku chache zilizopita.Saa moja na nusu geti la nyumba alimo Mathew Mulumbi na watu wa IS lilifunguliwa na gari mbili zikaingia mojawapo likiwa ni gari la jeshi la Marekani.Kutoka katika gari lililokuwa mbele akashuka Assad Ismail na kusalimiana na Marwan.Wanajeshi wawili wakashuka kutoka katika lile gari la jeshi wakaongozana na Assad kuelekea ndani. Mlango wa chumba cha Mathew Mulumbi ukagongwa akaenda kuufungua akakutana na Marwan ambaye alimtaka ajiandae kwani muda umefika.Mathew akatoka katika kile chumba akaelekea sebuleni akasalimiana na Assad kisha wakaongozana kuelekea katika bohari lililokuwa likitumika kuunda bomu.Tayari bomu lilikuwa limekamilika.Assad akalikagua kisha akawapongeza wataalamu waliounda bomu lile halafu akaelekeza lipelekwe katika gari la jeshi.Ndani ya lile gari la jeshi kulikuwa na watoto wadogo sita wenye umri wa miaka mitano hadi nane.Gari lile likafunguliwa sehemu ya nyuma na bomu lile kubwa likawekwa vizuri.Wakati wataalamu wale wakiendelea na kuliweka bomu katika gari Assad akamchukua Mathew wakarejea ndani.Mmoja wa wale wanajeshi akavua mavazi yake ya kijeshi na kumpa Mathew akavaa. “Abu Zalawi sasa uko tayari kwa kazi uliyokuja kuifanya.Tumezungumza mengi mchana wa leo kuhusiana na kazi hii na nina imani hakutakuwa na usumbufu wowote.Vyovyote itakavyokuwa hakikisha bomu hilo linalipuka.Umenielewa Abu? Akauliza Assad “Nimekuelewa Assad” “Sawa.Basi kila kitu ni kama tulivyopanga.Nakutakia kila la heri” akasema Assad.Mathew akatoka mle ndani akiwa ameongozana na wale wanajeshi hadi katika gari lile akapewa maelekezo kadhaa na wale wanajeshi halafu akaingia garini akaliwasha na kuondoka “Nawaonea huruma sana watoto hawa wadogo.Laiti ningekuwa na uwezo wa kuwasaidia ningefanya hivyo lakini hawa ndio watakaoniwezsha kuingia katika ubalozi wa Marekani.Inauma sana lakini hakuna namna” akawaza Mathew akiendelea na safari ya kuelekea katika ubalozi wa Marekani.
Wakati Mathew Mulumbi akiwa njiani kuelekea ubalozi wa Marekani,katika makao makuu ya SNSA kikosi cha makomando kilikuwa kinajiandaa kwa ajili ya kwenda kuvamia nyumba wanamoishi watu wa IS waliyoelekezwa na Mathew.Mchana kutwa walikuwa wameelekeza drone kubwa inayotumiwa na SNSA katika nyumba hiyo http://deusdeditmahunda.blogspot.com/wakifuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumbe ile na kupanga mikakati namna watakavyoweza kuingia ndani. Ndani ya jengo la SNSA kulikuwa na heka heka nyingi wakiwa wamejielekeza katika kuhakikisha operesheni ile inafanikiwa. “Tusikilizane ndugu zangu” akasema Ruby aliyetoka kuagana na makomando waliopanda helkopta kuelekea katika misheni yao. “Toka asubuhi ya leo tulikuwa na zoezi la kuchunguza nyumba ambayo wanaishi watu wa IS na watu wale tunaowalenga Marwan na Assad tumewaona katika nyumba hiyo.Muda umefika na makomando wetu tayari wameondoka kuelekea huko.Ni jukumu letu kuhakikisha tunawasaidia kwa kila namna tuwezavyo_Operesheni hii ni muhimu mno na kwa namna yoyote lazima iende kama ilivyopangwa hivyo kila mmoja ahakikishe kwa upande wake anafanya kila kinachotakiwa kuhakikisha makomando wetu wanafanikiwa” akasema Ruby na kutaka kazi ziendelee.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment