Search This Blog

Friday, 18 November 2022

SIRI : JASUSI/GAIDI - 1

 






IMEANDIKWA NA : PATRICK CK



*********************************************************************************



Simulizi : Siri: Jasusi/Gaidi

Sehemu Ya Kwanza (1)



SIRI PART 3 JASUSI/GAIDI

SEASON 1 SEASON 2 SEASON 3 SEASON 4 SEASON 5 SEASON 6 SEASON 7 SEASON 8 SEASON 9 SEASON 10



KAMPALA – UGANDA Barabara iliyolekea katika kanisa la utukufu wa Mungu ilifurika mamia ya waumini waliokuwa wakielekea katika kanisa hilo kubwa jijini Kampala kuhudhuria ibada ya Jumapili.Ni saa tatu za asubuhi lakini tayari kanisa lilikaribia kujaa huku mamia ya watu bado wakiendelea kujongea kanisani hapo.Kania la Utukufu wa Mungu ni moja ya kanisa lililojizolea umaarufu mkubwa sana katika jiji la Kampala na Uganda kwa ujumla kutokana na miujiza mikubwa inayotendeka kanisani hapo chini ya mtumishi wa Mungu nabii Yeremia Aganda.Watu wenye matatizo mbali mbali wamekuwa wakiombewa na kufanikiwa kutatua matatizo yao kama vile magonjwa,kupata watoto,kazi n.k. Saa nne za asubuhi ibada kuu ya jumapili ilianza ikiongozwa na nabii mkuu Yeremia Aganda,akisaidiana na wachungaji wasaidizi wake.Ulifika wakati wa kusifu na wimbo uliopigwa na bendi maalum ya kanisa uliwafanya karibu watu wote mle kanisani kusimama na kushangilia kwa shangwe wakimsifu Mungu.Wakati wimbo ule wa sifa ukiendelea huku watu wakicheza kwa furaha,mlipuko mkubwa wa bomu ukatokea na jengo la kanisa likatetemeka,sekunde mbili baadae ukatokea mlipuko mwingine.Sekunde nne milipuko mingine miwili mikubwa zaidi ikasikika na kulitetemesha kanisa. Watu waliokuwa nje ya kanisa wakifuatilia ibada walianza kukimbia hovyo kuokoa maisha yao mara ghafla yakatokea magari mawili, sehemu za juu za magari yale zikafunguliwa wakajitokeza watu waliofunika nyuso zao wakiwa na bunduki kubwa kisha wakaanza kumimina risasi hovyo kwa watu wale waliokuwa wakikimbia kunusuru maisha yao.Eneo la kanisa liligeuka kama uwanja wa vita kwa namna watu walivyokuwa wakianguka kutokana na risasi zilizotoka kwenye bunduki nzito za wale jamaa waliokuwa katika magari.Tukio lile la kuwashambulia watu kwa risasi lilidumu kwa takribani dakika tano kisha magari yale yakaondoka kwa kasi na kuacha idadi kubwa ya watu wakiwa wameanguka chini na wengi wao wakiwa wamefariki dunia







Saa moja za jioni Jenerali Paul Mukasa Rais wa mpito wa Uganda alijtokeza katika televisheni ya taifa akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa jeshi kwa lengo la kulihutubia taifa “Ndugu zangu Waganda, leo Saa nne za asubuhi wakati ibada ikiendelea katika kanisa la Utukufu wa Mungu,mabomu manne yalilipuka kanisani hapo na kusababisha vifo vya watu wengi waliokuwa ndani ya kanisa hilo wakiadhimisha ibada ya jumapili.Muda mfupi baada ya mabomu hayo kulipuka ndani ya kanisa,walijitokeza watu wengine wakiwa ndani ya magari mawili na kuanza kuwamiminia risasi waumini waliokuwa wakikimbia kuokoa maisha yao na kuua watu wengi.Taarifa niliyoipata muda mfupi kabla ya kuja hapa kuzungumza nanyi, jumla ya watu mia mbili ishirini wamepoteza maisha yao siku ya leo na wengine mia nne wamejeruhiwa wengine vibaya sana.Ninavishukuru vikosi vyetu vya ulinzi na uokozi vilivyofika haraka sana eneo la tukio na kufanya kazi kubwa ya uokozi na kuwakimbiza majeruhi haraka sana hospitali. Ndugu zangu,uchunguzi wa haraka uliofanywa unaonyesha kwamba kilichotokea leo ni shambulio la kujitoa mhanga.Bado hatujafahamu watu waliofanya tukio hili ni akina nani na wametoka wapi.Uchunguzi wa kina unaendelea na tutawajulisha matokeo ya uchunguzi huo pale utakapokuwa umekamilika. Walichokifanya hawa watu wenye roho za kishetani,hakikubalili na hakivumiliki.Ni kinyume cha ubinadamu na ninawaahidi ndugu zangu waganda tutawasaka kokote waliko watu hawa na kuwashikisha adabu.Hakuna aliyeshiriki katika mauaji haya ya kinyama atabaki salama.Tutahakikisha wote wanatiwa nguvuni.Hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe.Hatutamuogopa mtu,kikundi au taifa.Yeyote aliyeshiriki katika jambo hili la kikatili atakutana na mkono wetu.Ninacho waomba ndugu zangu waganda muwe watulivu katika wakati huu,vyombo vya uchunguzi viko kazini vikiendelea na uchunguzi wa kina wa jambo hili ili kuwabaini mashetani hawa ni akina nani.Lengo la watu hawa ni kuvuruga umoja wetu hivyo nawaomba ndugu zangu mshikamane.Tuendelee na shughuli zetu kama kawaida na pale kutakapokuwa na jambo lolote la kuwajulisha tutafanya hivyo mara moja. Kwa wale wote waliopoteza ndugu zao katika shambulio la leo, tunawapa pole sana.Serikali iko pamoja nanyi katika wakati huu mgumu mnaoupitia na tunawaahidi kwamba serikali itagharamia mazishi ya ndugu zetu wote waliopoteza maisha yao.Maandalizi yanaendelea na pale yatakapokamilika mtajulishwa Kwa mara nyingine narudia tena kuwapeni poleni sana waganda wote Mungu ibariki Uganda Ahsanteni kwa kunisikiliza Hii ilikuwa ni hotuba fupi ya Rais wa mpito wa Uganda Jenerali Paul Mukasa kwa wananchi wa Uganda Mara tu alipomaliza kutoa hotuba yake kwa taifa,Jenerali Paul Mukasa akapewa taarifa kwamba wakati akihutubia umetokea mlipuko mwingine wa bomu katika nyumba ya watawa waliokuwa waliokuwa wamekusanyika katika kanisa lao dogo wa ajili ya ibada ya usiku.Jenerali Paul Mukasa akazidi kuchanganyikiwa.Damu iliendelea kumwagika katika jiji la Kampala.



Jumatatu asubuhi,Jiji la Kampala lilikuwa katika simanzi kubwa kufuatia mashambulizi makubwa yaliyofanyika siku iliyopita.Karibu kila kona ya jiji la Kampala kulikuwa na vilio.Tukio la kuuawa kwa watawa arobaini waliokuwa katika ibada ya usiku liliendelea kuwapa hofu kubwa wakazi wa jiji la Kampala.Bado haikujulikana ni nani aliyekuwa anafanya mauaji yale makubwa bila huruma na kwa nini. Wakati wakazi wa jiji la Kampala wakiwa katika simanzi na hofu kubwa kufuatia mashambulio yale ya mabomu,basi lililobeba wanafunzi wa shule ya msingi inayomilikiwa na kanisa lilipuliwa na bomu wakati likipeleka wanafunzi shuleni.Zaidi ya wanafunzi arobaini walipoteza maisha katika shambulio hilo.Damu iliendelea kumwagika katika jiji la Kampala. Muda mfupi baada ya gari la wanafunzi kulipuliwa kwa bomu,katika mitandao ya kijamii ilianza kusambaa video ikimuonyesha mtu mmoja aliyeficha sura yake akiwafahamisha wananchi wa Uganda kwamba matukio yale ya mashambulio ya mabomu yaliyotokea ni kulipiza kisasi kwa mauaji ya kiongozi wao wa dini aliyeuawa.Mtu Yule aliendelea kutoa vitisho kwamba mashambulio yale yaliyotokea ni mwanzo tu na wataendelea kufanya mashambulio kila siku wakilipiza kisasi. Wakati video ile ikiendelea kusambaa na kuzidisha hofu kwa wakazi wa jiji la Kampala,katika redio inayojulikana kama Utukufu Redio,inayomilikiwa na kanisa la utukufu wa Mungu aliwasili askofu Nobert Odongo anayesimamia redio hiyo.Sura yake ilionyesha hasira kali.Alielekea moja kwa moja katika chumba cha matangazo na kuamuru muziki wa maombolezo uliokuwa unapigwa usimamishwe akavaa spika za masikioni na kuanza kutangaza. “Ndugu wakristu wenzangu bila kujali dhehebu unakotoka,wale wote mnanisikiiza muda huu ambao mmeumizwa na unyama unaoendelea hapa nchini kwetu,nimekuja hapa kuzungumza nanyi na ninaomba mnisikilize kwa makini sana.Acha shughuli zako zote na sikiliza ujumbe huu kwa makini. Kama mnavyofahamu, jana kumefanyika shambulio la bomu katika kanisa letu la Utukufu wa Mungu.Tumepoteza watu wengi katika shambulio la jana na miongoni mwao wako watumishi wa Mungu waliokuwa wakihudumu katika ibada ya jana akiwemo mkuu wa kanisa letu,Nabii mkuu Yeremia Aganda ambaye ameumia vibaya sana.Katika mwendelezo wa mauaji hayo, jana usiku limefanyika shambulio lingine katika kanisa nyumba ya watawa waliokuwa wamekusanyika kwa ibada ya jioni.Watu hawa wasio na hata chembe ya huruma hawakuishia hapo wameendelea na umwagaji wa damu ambapo asubuhi ya leo watoto wetu waliokuwa wakienda shuleni wameuawa kikatili kabisa baada ya basi lao kushambuliwa kwa bomu.Huu ni ukatili mkubwa uliovuka kiwango cha ukatili kwa binadamu. Ndugu zangu mashambulio haya yote yaliyotokea yamelenga watu wa imani moja tu,wakristu.Hii ni chuki ya wazi kabisa inayojidhihirisha dhidi yetu.Waliofanya mauaji haya wanafahamika ni akina nani na wanajitapa kuendelea kufanya mashambulio zaidi na zaidi dhidi yetu.Wanafahamika ni akina nani,wako wapi lakini serikali yetu imeshindwa kuchukua hatua za dhati za kuwadhiti wasiendelee na kumwaga damu yetu.Kwa kuwa serikali ya kijeshi imeshindwa kutulinda dhidi ya hawa wanaotuwinda watumalize basi umefika wakati wa sisi wenyewe kuchukua hatua za kuanza kujilinda na kupambana nao.Hatuwezi kuendelea kuuawa huku tukiona,lazima tuchukue hatua za haraka sana kujilinda.Ndugu zangu waumini wa kanisa la utukufu wa Mungu na wakristu wa madhehebu yote kokote mliko nawaomba inukeni twendeni tukapambane na wale wanaotaka kutumaliza.Kokote ulipo unaponisikiliza acha kila unachokifanya hivi sasa.Kama uko nyumbani funga nyumba yako,kama uko katika biashara funga biashara yako elekea katika kanisa la utukufu wa Mungu tutakusanyika pale ambapo damu ya wenzetu imemwagika.Ukisikia tangazo hili mjulishe na mwenzako.Mshike mkono mwenzako muongoze muelekee kanisa la utukufu wa Mungu” Yalikuwa ni maneno kutoka kwa askofu Nobert Odongo akiwataka watu wa dini ya kikristu kukusanyika katika kanisa la utukufu wa Mungu ambako jana yake kulitokea milipuko ya mabomu na kuua watu wengi waliokuwa katika ibada. Baada ya maneno yale, askofu Nobert akatoka katika chumba cha matangazo akaelekea katika gari lake lakini kabla hajaingia garini simu yake ikaita akatazama mpigaji alikuwa ni Joshua Lulangwa mwenyekiti wa chama cha siasa cha ukombozi wa Uganda. “Nilikuwa nakusikiliza askofu.Umefanya vizuri sana.Naamini tayari watu wameanza kuelekea mahala ulipowaelekeza wakutane.Tayari silaha zimeanza kupakiwa katika magari tayari kupelekwa sehemu ya kukutania.Askofu kumbuka mara tu vurugu zitakapoanza ondoka haraka sana,helkpota iko tayari inatusubiri tuondoke” akasema Joshua “Nimekuelewa Joshua.Tutakutana muda huo” akasema askofu Nobert “Kila la heri” akasema Joshua na kukata simu.Askofu Nobert akaingia katika gari na kuondoka kuelekea nyumbani kwake Tamko lile la askofu Nobert lilisambaa kwa kasi kubwa kwani redio utukufu ni moja kati ya redio yenye wasikilizaji wengi sana jijini Kampala.Kama alivyoelekeza askofu Nobert,watu walianza kuhamasishana kuelekea katika kanisa la utukufu walikoelekezwa wakutane.Makundi ya vijana na waumini wa dini ya kikristu walielekea huko kwa haraka na ndani ya saa moja tayari uwanja mkubwa wa mpira ulio karibu na kanisa ulijaa watu na wengine wengi waliendelea kuelekea hapo.Utepe wa njano kuzuia watu kuingia kanisani ulizungushwa kanisa zima ili kuipa timu ya wachunguzi nafasi ya kufanya kazi yao. Askofu Nobert aliwasili kanisani akapokewa na wachungaji akapanda juu ya meza akashika kipaaza sauti na kuongoza nyimbo kadhaa halafu akasema “Ninawashukuru sana ndugu zangu kwa kuitika wito kwa haraka.Pamoja na kufiwa,pamoja na huzuni kubwa mliyonayo lakini mmeitika wito na kufika kwa haraka sana.Kama mlivyosikia katika maelezo niliyoyatoa redioni……” kabla hajaendelea magari matatu ya jeshi yalifika na watu wote wakageuka kuyatazama. “Msiogope ndugu zangu.Kuweni majasiri.Hao waliofika hapa hawatatutafanya chochote.Hao ni wale walioshindwa kutulinda na kuacha tukiuawa kama wadudu.Hata kama wamekuja na bunduki na silaha za maangamizi lakini kuweni majasiri.Daudi alipambana na Goliath aliyekuwa amejihami kwa silaha hali yeye akiwa na mawe tu na akashinda.Ninawahakikishia hata ninyi msitishwe na magari yao,msitishwe na silaha zao tunao uwezo wa kuwashinda kama Daudi alivyomshinda Goliath ! akasema askofu Nobert na kuwapandisha hasira waumini wake “Nataka hapo mlipo kila mmoja ainame aokote kilichopo chini yake.Kama kuna jiwe okota,kama kuna tofali okota na kwa pamoja tuwaelekee wale wanajeshi tuwaondoe eneo hili.Nikihesabu mpaka tatu tunaanza kuwashambulia bila kukoma ! akasema Nobert na waumini wake wakaitika kwa nguvu kisha akahesabu hadi tatu na mvua ya mawe ikaanza.Waumini hawakuogopa walianza kuvurumisha mawe kwa wanajeshi wale na kuvunja vioo vya magari yao na kuwalazimu wanajeshi wale kuondoka haraka eneo lile. “Tumeshinda ! Tumeshinda ! Tumeshinda ! akapaaza sauti askofu Nobert huku waumini wake ambao waliendelea kumiminika kwa wingi wakishangilia “Bwana aliye hai ametushindia.Kama tumeweza kuwashinda wale watu waliokuwa na silaha nzito hatuwezi kushindwa kwa hawa wanaotuua ! akasema na waumini wakashangilia kwa nguvu “Ndugu zangu katika yale magari matatu pale kuna silaha.Kila mmoja atapita pale achukue kile kinachomfaa iwe panga,kisu,nyundo au chochote atakachoona.Tunawafahamu wanaotuua na tunawafuata huko huko waliko.Tutabomoa nyumba zao za kuabudia na kuwaondoa kabisa katika jiji hili.Tumeelewana? akauliza na waumini wale wakaitika kwa nguvu kisha wakaanza kuelekea yalipo magari matatu aina ya fuso na kila mmoja akapewa silaha aliyoihitaji.Kulikuwa na zana mbali mbali kama visu,mapanga,mashoka.Silaha zile hazikutosha kwani watu walikuwa wengi sana na askofu Nobert akawataka waumini wake waelekee ulipo msikiti ambao haukuwa mbali na pale kanisani.Akiwa na shoka begani aliwaongoza waumini wake wakatembea kwa haraka wakaelekea katika msikiti ule na kuanza kuubomoa halafu wakauchoma moto.Askofu Nobert akawaelekeza waumini wake kuelekea katika msikiti mwingine. Taarifa za kile kilichofanywa na waumini wa kanisa la utukufu wa Mungu,zilisambaa kwa kasi na kuwafanya waumini wa dini ya kiislamu nao kuanza kujipanga kwa ajili ya kupambana na kundi hilo kubwa la waumini wa kanisa la utukufu waliokuwa wanavamia kuharibu na kuchoma misikiti. Hadi jua lilipoanza kuzama,jiji la Kampala lilikuwa tayari katika machafuko makubwa yakihusisha makundi ya waumini wa dini za kikristu na kiislamu.Watu kadhaa tayari walikwisha poteza maisha kufuatia vurugu hizo.Jeshi la Uganda liliingia mtaani kujaribu kuzima vurugu hizo za wafuasi wa dini lakini tayari vurugu hizo zilikwisha kuwa kubwa na kusambaa katika sehemu mbali mbali za jiji la Kampala.





Usiku kucha mapigano yaliendelea kati ya waumini wa dini wakishambuliana na kwa upande wa pili wakishambuliana na vikosi vya jeshi vilivyokuwa vikijaribu kutuliza vurugu hizo. Kijua kilianza kuchomoza huku hali ikizidi kuwa tete katika jiji la Kampala.Vurugu ziliripotiwa kuendelea katika sehemu mbali mbali za jiji hilo na kwa asubuhi hii si Kampala pekee bali vurugu zilianza kuripotiwa katika miji mingine mikubwa.Vikosi vya jeshi vikisaidiana na vikosi vingine vya ulinzi vilisambaa mitaani lakini makundi ya watu waliokuwa na silaha mbali mbali za jadi na za moto yaliendelea kuleta upinzani mkubwa sana kwa vikosi hivyo na kulazimisha vikosi hivyo vya jeshi kutumia silaha za moto. Saa mbili za asubuhi iliripotiwa kundi kubwa la watu kuvamia kituo cha polisi wakaua askari na kuiba silaha ambazo walizitumia katika mapambano yake na vikosi vya jeshi.Hadi ilipotimu saa nne za asubuhi iliripotiwa wanajeshi ishirini na saba walikuwa wamepoteza maisha.Kumi na nne walifariki baada ya gari lao kushambuliwa kwa bomu wakati wakielekea katika viunga vya jiji la Kampala, wengine kumi na tatu waliuawa wakati wakikabiliana na watu waliokuwa na silaha za moto.Vifo vya wanajeshi wale vilipelekea kutolewa kwa amri ya kutumia nguvu zaidi ili kudhibiti vurugu zile amri ambayo iliwafanya wanajeshi kumpiga risasi kila aliyejaribu kuwashambulia. Katika mji wa Jinja nako vile vile kuliripotiwa kuvamiwa kwa ghala la silaha na silaha nyingi kuibwa.Kadiri muda ulivyozidi kusonga ndivyo machafuko yalivyozidi kuwa makubwa.Wakati waumini wa dini wakiendelea kushambuliana wakiuana na kuchomeana nyumba za ibada,liliibuka kundi lingine la watu waliokuwa na silaha za moto ambao walikuwa wanavamia kupora na kuchoma majengo hasa ya serikali.Hawa walikuwa wakitembea na bendera ya Uganda huku wakiimba kutoutambua utawala wa kijeshi.Taratibu kundi hili la tatu nalo lilianza kuungwa mkono na watu wengi Saa sita za mchana ubalozi wa Marekani jijini Kampala ulivamiwa na kundi kubwa la watu wenye silaha hivyo kuwalazimu wanajeshi waliokuwa wakilinda jengo la ubalozi huo kutumia risasi za moto kutaka kuwatawanya watu hao lakini watu wale walikuwa wengi huku wakirusha mabomu ya kurusha kwa mkono ndani ya ubalozi na kuwalazimu wanajeshi wale kuomba msaada kutoka kwa jeshi la Uganda.Wakati wakisubiri msaada wa jeshi kundi lile la watu walifanikiwa kuvunja geti na kuingia ndani ya jengo na kuua kila waliyemkuta kisha wakalichoma jengo la ubalozi huo.Vikosi vya jeshi la Uganda vilipofika vilikuta jengo la ubalozi huo likianza kuungua.Magari ya zimamoto yalifika haraka sana na kuuzima moto ule ulioanza kusambaa katika ghorofa ya kwanza.Jumla ya maiti kumi na nne zilitolewa katika jengo lile. TANGA – TANZANIA Katika moja ya bandari bubu jijini Tanga,jahazi lilitia nanga,watu sita wakashuka haraka haraka wakiwa na mabegi makubwa migongoni mwao wakaingia katika gari lililokuwa linawasubiri wakaondoka.Hakukuwa na mazungumzo ndani ya lile gari wakaenda moja kwa moja katika nyumba Fulani “Karibuni sana ndugu zangu”akasema jamaa mmoja mwembamba aliyekuwa na ndevu nyingi “Ahsante sana” akajibu jamaa mwingine ambaye alionekana kiongozi wa wale jamaa waliokuja na jahazi. “Mambo yanakwendaje hapa? akauliza “Kila kitu tayari kimekamilika.Wawili watatumia piki piki kwenda katika shule ya Mt Bernadetha,wengine tutatumia gari” akasema Yule jamaa mwenyeji na kuweka mezani ramani ya jiji la Tanga wakaelekezana halafu wakaingia katika chumba kimoja wapo wakayafungua mabegi yao wakaanza kuunganisha silaha walizokuwa wamebeba katika mabegi yao.Kila mmoja alipohakikisha silaha yake iko tayari wakaelekea katika gari moja lililoandaliwa kwa ajili ya shughuli wanayotaka kuifanya.Watu watano wakaingia ndani ya gari lile zuri aina ya Rav 4 lenye rangi nyeusi wengine wawili wakapanda piki piki kisha wakaondoka. Nabii Jonathan Mbegela wa kanisa la Calvary Chapel alikua ofisini kwake akiendelea kusikiliza watu mbali mbali wenye matatizo na kufanya maombi maalum ya mtu mmoja mmoja mara ikasikika milio ya risasi nje ya ofisi yake.Akamuacha Yule mtu aliyekuwa akimuhudumia akafungua mlango akatoka nje kuchungulia kuna nini. Alipofungua tu mlango akapigwa risasi ya kichwa akaanguka chini.Risasi zilirindima kanisani pale na takribani watu arobaini na mbili waliofika pale kwa ajili ya huduma ya maombi wakauawa.Risasi zilirindima kanisani pale kwa takribani dakika kumi na wale jamaa walipomaliza kile walichokuja kukifanya wakaingia katika gari lao na kuondoka kwa kasi kubwa.Gari tatu zilizojaa askari polisi zilifika haraka sana baada ya kupata taarifa ya tukio lile lakini tayari wavamizi wale walikwishatoweka. Wakati vilio vikitanda katika kanisa la Calvary Chapel,katika shule ya msingi ya Mt.Bernadetha kengele ya dharura iligonga na wanafunzi wakaanza kutoka madarasani wakikimbilia sehemu ya kukuanyikia.Waalimu walistuka na kutoka kuchungulia nani aliyegonga kengele ile na ndipo wakagundua aliyegonga kengele hakuwa mtumishi wa ile shule.Mara ghafla kutoka katika mti wa maua akatokeza jamaa mmoja akiwa na bunduki na kuanza kumwaga risasi.Yule jamaa aliyegonga kengele naye akatoa bunduki kutoka katika begi lake la mgongoni naye akaanza kuvurumisha risasi.Wanafunzi walianza kuanguka kama kumbi kumbi.Mvua ya risasi ilidumu kwa dakika tano halafu watu wale wakaweka bunduki zao katika mabegi ya mgongoni na kuondoka wakitumia piki piki nyeusi . Baada ya kufanya mauaji yale watu wale wakarejea katika ile nyumba walimofikia.Nusu saa baadae likafika gari moja zuri lililokuwa na vioo vyeusi akashuka jamaa mmoja aliyevalia suruali ya jeans na kufunika kichwa chake kwa kofia. “Hongereni sana kwa kazi nzuri mliyoifanya.Imekuwa ni kazi yenye mafanikio makubwa.Watanzania hawajazoea kuyaona mambo kama haya yaliyotokea leo na nchi imetikisika.Tumeanza vizuri lakini bado tuna kazi kubwa ya kufanya.Si kazi nyepesi kuwafarakanisha watanzania kwa kutumia dini lakini tutajitahidi.Tumeanza na kanisa,jioni ya leo tunahamia katika msikiti.Mpaka sasa wakristu wanaamini waislamu ndio waliofanya shambulio katika kanisa na kuua waumini.Tayari tumepanda mbegu ya chuki.Jioni ya leo tutavamia nyumba ya shehe mkuu wa mkoa wa kumuua.Hii itaongeza mafuta kwenye moto.Waislamu wataamini ni wakristo wamefanya mauaji hayo na watajipanga kulipiza kisasi na machafuko yataanzia hapo.Tayari kuna watu wamekwisha andaliwa kwa ajili ya kuhamasisha suala hilo” akasema Yule jamaa kisha akwaaga na kuondoka. ************ Taarifa kubwa ambayo ilitawala vyombo vya habari duniani ni machafuko yanayoendelea nchini Uganda.Hali iliendelea kuwa tete na tayari machafuko yalisambaa katika miji yote mikubwa ya nchi hiyo huku vifo vingi vikiendelea kuripotiwa.Hali ikiwa hivyo nchini Uganda,nchini Tanzania nako mambo hayakuwa shwari hata kidogo.Jijini Tanga yalifanyika mauaji katika kanisa kubwa la Calvary Chapel ambapo kiongozi wa kanisa hilo Nabii Jonathan Mbegela pamoja na waumini wake thelathini na mbili waliuawa na watu waliokuwa na silaha.Shule ya msingi ya Mt.Bernadetha nayo ilishambuliwa na watu wenye silaha na takribani wanafunzi ishirini na tatu walipoteza maisha katika shambulio hilo.Wakazi wa jiji la Tanga na watanzania kwa ujumla waliingiwa na hofu kubwa ya kutokea yale yaliyokuwa yanaendelea nchini Uganda.Ili kudhibiti machafuko yoyote yasitokee serikali ilimwaga polisi wa kutosha katika jiji la Tanga.Nyumba zote za ibada ziliwekewa ulinzi kwa hofu ya makundi ya waumini kuvamia kwa lengo la kulipiza kisasi. Pamoja na ulinzi mkali uliowekwa katika nyumba zote za ibada ndani ya jiji la Tanga lakini asubuhi wakazi wa jiji hili waliamshwa na taarifa ya kustusha mno.Sheikh mkuu wa mkoa wa Tanga na familia yake waliuawa usiku kwa kupigwa risasi.Baada ya mauaji hayo kufanyika iliachwa barua mezani ambayo ilieleza kwamba wamefanya mauaji yale kulipiza kisasi kufuatia mauaji yaliyofanywa katika kanisa la Calvary Chapel na katika shule ya msingi ya Mt.Bernadetha.Mauaji yale yalizua taharuki kubwa miongoni mwa waumini wa dini ya kiislamu.Shughuli zilisimama katika jiji la Tanga watu wakihofia ualama wao.Mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania aliwasili jijini Tanga kwa helkopta akafika katika nyumba ya Sheikh mkuu wa mkoa aliyeuawa kwa kupigwa rissi na familia yake yote halafu akaelekea katika kanisa la Calvary Chapel na katika shule ambako waliuawa wanafunzi.Baada ya kutembelea sehemu hizo zote mkuu huyo wa jeshi la polisi akawa na kikao cha ndani na makamanda wa polisi kikao kilichochukua saa tatu kisha akakutana na waandishi wa habari na kwa kupitia kwao akawataka watanzania wawe watulivu kwani jeshi la polisi lilikuwa kazini kuwasaka watu au kikundi cha watu wanaoendesha mauaji yale. Nusu saa baada ya mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania kutoa tamko,mmoja wa wanasiasa vijana kabisa ambaye anatokea mkoa wa Tanga akaandika katika ukurasa wake wa mtandao wa twitter “Hii haikubaliki na haivumiliki.Kiongozi wetu hawezi kuuawa kinyama namna hii halafu tunaambiwa tusubiri uchunguzi ufanyike wakati wauaji wanafahamika. Wametuchokoza na hatuwezi kukaa kimya lazima tujibu.Twendeni sisi wenyewe tukawatafute wale wenye nia ovu dhidi yetu” Mwanasiasa Yule kijana hakuishia hapo tu,aliwatumia jumbe mashehe wa mkoa wa Tanga ambazo ziliendelea kuwahamasisha wawashawishi waumini wao kuanzisha vurugu dhidi ya wale ambao wanadaiwa kumuua kiongozi wao. Saa nane za mchana jiji la Tanga lilijikuta katika machafuko makubwa,waumini wa dini wakishambuliana huku wakipambana na vikosi vya polisi.Kadiri muda ulivyozidi kwenda ndivyo vurugu zilivyozidi kushika kasi na ilipofika saa kumi na mbili za jioni maiti za watu zilionekana katika mitaa mbali mbali ya jiji la Tanga.Saa moja za jioni ikaripotiwa vurugu kubwa kuibuka jijini Dar es laam na watu kushambuliana.





Machafuko ya kidini yaliyoanzia jijini Kampala Uganda yalisambaa katika nchi za Tanzania na Kenya pia.Waumini wa dini waliendelea kushambuliana na kuuana wao kwa wao hivyo kupelekea vikosi vya ulinzi kutumia nguvu kubwa kuwatawanya na kupelekea vifo vya watu wengi kutokea.Machafuko haya yalishika kasi kutoka katika miji mikubwa na kuingia katika miji midogo midogo.IIi kudhibiti watu kutumiana jumbe za kueneza chuki mitandao yote ya simu ililazimwa ili watu wasiwasiliane lakini bado haikusaidia vurugu ziliendelea. WASHINGTON DC - MAREKANI Rais William Washington alijitokeza mbele ya waandishi wa habari katika ikulu ya Marekani kabla ya kupanda helkopta ya Marine one kuelekea katika uwanja wa ndege wa jeshi kupanda ndege “Wamarekani wenzangu,wengi wenu mnafuatilia taarifa za habari za vyombo mbali mbali vya habari duniani na mnaona kile kinachoendelea Afrika mashariki.Watu wanauana na kuchinjana kwa ajili ya imani.Hii si sawa hata kidogo.Binadamu wote ni sawa na Mungu tunayemuabudu ni mmoja hivyo hatupaswi kuuawa kwa sababu ya dini.Machafuko haya yaliyoanzia jijini Kampala Uganda tayari yamesambaa eneo kubwa la Afrika Mashariki na damu inaendelea kumwagika.Ukitazama maiti zilivyozagaa mitaani inasikitisha sana. Mwaka 1994 dunia ilishuhudia mauaji makubwa kuwahi kutokea katika historia ya dunia pale yalipofanyika mauaji ya kimbali nchini Rwanda.Dunia nzima ilishuhudia mauaji yale yakifanyika lakini hakuna walichokifanya zaidi ya kuacha watu wakiuana.Mauaji yale makubwa yalianza hivi hivi kama yalivyoanza machafuko ya Uganda kwa kupanda mbegu za chuki na watu wakaanza kuuana hovyo.Hatutaki tena historia ile ya Rwanda ijirudie hivyo basi serikali ya Marekani itatuma wanajeshi wake kwenda Afrika mashariki kurejesha amani na kuhakikisha yale ya mwaka 1994 hayatokei tena.Kuna tetesi ya kikundi cha kigaidi cha IS kushiriki katika machafuko hayo hivyo basi wanajeshi watakaokwenda Afrika mashariki watakuwa na kazi mbili moja ni kudhibiti machafuko yanayoendelea.Jukumu la pili ni kukabiliana na kikundi cha IS ambacho kimejipenyeza katika machafuko hayo na kufanya hali ya amani katika eneo la Afrika Mashariki kuzidi kuwa tete. Wamarekani wenzangu,katika machafuko hayo makubwa kuwahi kutokea katiuka ukanda wa Afrika mashariki,ubalozi wetu jijini Kampala umechomwa moto na makundi ya watu wenye hasira na tumepoteza wamarekani wenzetu kumi na nne.Kikosi cha wanajeshi wetu wanaokwenda Afrika Mashariki watakuwa na jukumu pia la kuwaondoa raia wa kigeni waliokwama kufuatia machafuko hayo. Mungu ibariki Marekani William Washington Rais wa Marekani alimaliza kutoa hotuba yake fupi kwa wamarekani halafu akaongozwa na walinzi wake kuelekea katika helkopta iliyokuwa inamsubiri. SIKU NNE BAADAE - TANZANIA Siku mbili toka Rais wa Marekani atoe tamko la kutuma wanajeshi wa Marekani katika eneo la Afrika Mashariki kwa ajili ya kuzuia mauaji yaliyokuwa yanaendelea kufuatia vurugu za kidini,Meli kubwa mbili za jeshi la Marekani zilitia nanga katika bandari ya Tanga zikitokea katika kambi kubwa ya jeshi la Marekani iliyoko Djibout.Meli hizo zilisheheni vifaa mbali mbali ambavyo wanajeshi wa Marekani wangevitumia katika jukumu lao la ulinzi wa amani.Meli nyingine mbili zilitia nanga katika bandari ya Dar es salaam nazo zikiwa zimesheheni vifaa mbali mbali vya kijeshi na shughuli ya kuandaa kambi kwa ajili ya wanajeshi wa Marekani ikaendelea katika miji ya Dare s salaam na Tanga.Meli nyingine kubwa mbili nazo ziliwasili katika bandari ya Dar es salaam zikiwa na vifaa ambavyo vingetumika na wanajeshi watakaokwenda nchini Uganda Maandalizi ya kambi yalipokamilika ndege tatu za jeshi la Marekani zilitua katika uwanja wa ndege wa Tanga zikiwa zimesheheni wanajeshi waliotumwa nchini kulinda amani.Vikosi vingine vya wanajeshi vilipelekwa katika majiji ya Dar es salaam na Kampala ambako vurugu zilipamba moto. MIEZI MITATU ILIYOPITA KAMPALA – UGANDA Jumatano asubuhi mvua kubwa iliyoambatana na radi iliyoanza kunyesha saa tisa za usiku bado iliendelea kunyesha na haikuwa na dalili za kukatika hivyo kuwatatiza watu wengi waliohitaji kuwahi katika shughuli zao mbali mbali za kila siku.Pamoja na ukubwa wa mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha lakini habari kubwa iliyosambaa jijini Kampala na nchi nzima ya Uganda ni mauaji ya spika http://deusdeditmahunda.blogspot.com/wa bunge la Uganda profesa Joseph Muganda ambaye aliuawa yeye pamoja na familia yake yote.Ilikuwa ni taarifa iliyowastua watu wengi asubuhi hiyo. Rais wa Uganda Jenereali Akiki Rwamirama aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa twitter kusikitishwa kwake na mauaji yale ya spika wa bunge na kuyaita ni mauaji ya kinyama na akaahidi kwamba wale wote waliohusika katika mauaji yale watasakwa kila kona ya nchi na kuhakikisha wanapatikana. Wakati mvua ile kubwa ikiendelea kunyesha gari moja liliwasili katika makazi ya Rais wa Uganda mlango wa mbele ukafunguliwa akashuka haraka haraka mtu mmoja aliyekuwa na mwavuli akaukunjua na kuufungua mlango wa kati kati jamaa moja mwembamba aliyevalia nadhifu akashuka akasindikizwa kuingia ndani ya jengo lile la makazi ya Rais “Karibu sana Nzeza” akasema Jenerali Akiki baada ya kusalimiana na mgeni wake. “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Yule jamaa ambaye Rais alimuita kwa jina moja tu Nzeza. “Ahsante sana Nzeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya usiku wa leo.Nimefurahi sana” akasema Jenerali Akiki. “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akajibu Nzeza “Hakukuwa na tatizo lolote katika utekelezaji wa kazi ile?akauliza Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais hakukuwa na tatizo lolote.Kazi yetu tumeikamilisha vizuri kama ulivyotuelekeza na tumefanikiwa kuipata ile rekodi” akasema Nzeza na kuingiza mkono katika koti lake akatoa kifuko kidogo cha nailoni ambacho ndani yake kulikuwa na diski mweko akasimama kwa adabu na kumpatia Rais Akiki.Halafu akatoa tena bahasha ndogo ya khaki na kumpatia Rais “Katika hii bahasha kuna orodha ya watu ambao Spika alikuwa anawasiliana nao mara kwa mara utaipitia kisha utatupa maelekezo nini kifanyike” “Ahsante sana Nzeza.Nifikishie shukrani zangu kwa vijana na kila kitu kitakuwa kama nilivyowaahidi” akasema Jenerali Akiki “Usihofu mzee tuko macho tunafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea na yeyote ambaye ataonekana kuwa hatari kwako tutamuondoa” akasema Nzeza akaagana na Rais akaondoka.Jenerali Akiki akavuta pumzi ndefu akajiegemeza kitini na kuzama mawazoni “Profesa Joseph alikuwa ni rafiki yangu sana lakini sifahamu kitu gani kilichombadilisha hadi akawa adui yangu.Alikosea sana kutaka kuniondoa madarakani na hii haitaishia kwa Profesa Joseph pekee bali itaendelea kwa yeyote ambaye ataendeleza hiki alichotaka kukifanya spika.Hakuna anayefahamu ni magumu gani niliyopitia hadi kukalia kiti hiki cha urais.Anayetaka kuniondoa madarakani asubiri kwanza hadi pale muda wangu utakapomalizika vinginevyo nitaendelea kuwakata pumzi za uhai kila uchao ! akawaza Rais Akiki akainuka na kuelekea chumbani kwake





Jenerali Akiki aliingia ofisini kwake akaelekeza asiruhusiwe kuingia mtu yeyote hadi pale atakaporuhusu.Akajifungia ofisini akatoa ile diski mweko aliyopewa na Nzeza akaichomeka katika kompyuta yake ikajitokeza video ya Melanie Davis akahisi mwili wote ukimsisimka. “Melanie !! akajikuta akitamka kwa mstuko alioupata “Imekuaje profesa Joseph akawa na rekodi ya Melanie? Akajiuliza na kuanza kusikiliza rekodi ile huku akihisi mwili kumtetemeka “Mwanamke huyu ni shetani kabisa ! akawaza Jenerali Akiki alipomaliza kuitazama rekodi ile,akairejea tena kwa mara ya pili na ya tatu.Akatoa kitambaa akafuta jasho. “Siamini macho yangu.Huyu kweli ni Melanie Yule ninayemfahamu mimi au ni Melanie wa kutengenezwa? Akajiuliza na kuendelea kufuta jasho “Lakini huyu ni Melanie yule Yule ninayemfahamu.Kwa nini akafanya hivi? Sikutegemea kabisa kama siku moja angeweza kufanya kitu cha kijinga namna hii ! akawaza Jenerali Akiki “Baada ya shambulio lile lililowaua wake za marais nikaelekezwa tena kuandaa shambulio lingine ambalo linalenga kumuua Rais Patrice Eyenga.Nilimfuata James Kasai nikaongea naye suala hili naye akanipeleka kwa Rais wa Uganda Jenerali Akiki ambaye alikubali kushirikiana nasi katika mpango huo na alitaka baada ya Patrice kuuawa James Kasai achukue nchi.Akiki alinieleza kwamba Majenerali wa jeshi la Congo walikuwa wanandaa mpango wa mapinduzi hivyo akamuita mkuu wa majeshi wa Congo akazungumza naye lakini wakashindwa kuelewana kuhusu James Kasai kushirikishwa katika serikali baada ya mapinduzi ndipo tulipoamua kuendelea na mpango wa kumuua James Kasai bila kushirikiana na wakuu wa jeshi la Congo.Tulipanga Jenerali Akiki aombe kukutana jijini Dar es salaam na marais wa Tanzania na Congo azungumze nao kuhusu kutafuta muafaka wa amani kufuatia mashambulizi yale yaliyofanywa na James Kasai jijini Dar es salaam” Kipande hiki Jenerali Akiki alikirudia kukitazama zaidi ya mara tano. “Yule binti amenivua nguo zote.Kitu gani kilimfanya aamue kusema ukweli? Ninajuta kwa nini nilimfahamu Melanie.Ameniletea matatizo makubwa sana.Haya yote aliyataka James Kasai kwani ndiye aliyemleta Melanie kwangu.Sikuwa nikimfahamu huyu shetani” akawaza Jenerali Akiki huku sura yake ikiwa imejikunja kwa hasira “Ndiyo maana Spika alikuwa anajiamini sana kwa kuwa alijua anao ushahidi mkubwa kama huu.Melanie ameweka wazi kila kitu,hajaniacha na nguo hata moja.Kwa rekodi hii ikisambaa ka wananchi sijui nini kitatokea.Lakini je hakuna mbunge yeyote aliyeiona? Kama wapo wabunge ambao wamekwisha iona nikiwabaini nao poa lazima wataondoka kama profesa Profesa Joseph.” Akawaza Jenerali Akiki “Lakini rekodi hii Spika ameitoa wapi?Ninapata picha kwamba mpango wa kuniondoa madarakani lazima ni mpango wa serikali ya Tanzania.Naamini wao ndio waliompa Spika wa Bunge ile rekodi naye akataka kulitumia bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani nami kuniondoa katika madaraka.Huyu lazima ni Dr Fabian anataka kulipiza kisasi.Dah ! siamini kama mambo haya yamefika hapa lakini kikwazo cha kwanza nimekiondoa ambacho n I Spika wa bunge.Aliyafanya maisha yanguyawe magumu sana ndani ya siku mbili zilizopita” akawaza Jenerali Akiki na kuvuta kumbu kumbu kilichotokea siku mbili zilizopita KAMPALA - SIKU 2 ZILIZOPITA Inakaribia saa kumi na mbili za jioni mvua za rasha rasha ziliendelea kunyesha katika jiji la Kampala.Ikulu Rais wa Uganda Jenerali Akiki Rwamirama alipata ugeni ambao hakuutarajia.Mgeni aliyefika jioni hiyo kumtembelea alikuwa ni Spika wa bunge la Uganda. “Mheshimiwa Spika karibu sana” akasema Jenerali Akiki “Ahsante sana mheshimiwa Rais.Samahani kwa kukuvamia jioni hii na kuvuruga ratiba zako lakini sintachukua muda mrefu” akasema Profesa Joseph Muganda spika wa bunge la Uganda “Usijali mheshimiwa spika.Hapa ni nyumbani unaweza kuja muda wowote utakao” akasema Jenerali Akiki “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema spika na ukimya mfupi ukapita kisha akasema “Mheshimiwa Rais kuna jambo muhimu limenileta hapa kwako ambalo ni kuhusiana na kile kilichotokea katika eneo letu la Afrika Mashariki wiki kadhaa zilizopita” akasema Spika na kumstua kidogo Jenerali Akiki “Mambo mengi yalitokea hapa Afrika Mashariki katika kipindi hicho.Kitu gani hasa unataka kukizungumzia?akauliza Jenerali Akiki “Yote yaliyotokea” akajibu Spika.Jenerali Akiki akachukua mkebe akatoa sigara akaiwasha na kuvuta akapuliza moshi na kusema “Karibu” “Mheshimiwa Rais mengi yametokea katika jumuiya yetu katika kipindi cha wiki chache zilizopita na yote unayafahamu.Mauaji ya kinyama yamefanyika na hata jumuiya ya Afrika Mashariki iliponea chupu chupu kusambaratika.Tuyaweke yote pembeni lakini nataka kuzungmzia mambo mawili tu.Kwanza mpango wa mauaji ya marais wa Tanzania na Congo na pili ni James Kasai” Spika akanyamaza baada ya Jenerali Akiki kuonyesha mstuko mkubwa.Nusura sigara aliyoishika mkononi imponyoke. “Mheshimiwa Rais ninaoushahidi usio na chembe ya mashaka kwamba ulishiriki katika mpango wa kutaka kuwaua marais wa Tanzania na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” akasema Spika na Jenerali Akiki akaangua kicheko “Huo ni upuuzi mkubwa sana.Mimi nitawezaje kushiriki katika njama za kuwaua marais wenzangu? Huo ni uzushi na upuuzi mkubwa mheshimiwa Spika ! akasema Jenerali Akiki akionekana kuanza kupandisha jazba. “Mheshimiwa Rais kama nilivyokwambia kwamba ninao ushahidi usio na hata chembe ya mashaka kwamba ulishiriki katika mpango huo wa kuwaua marais hao wawil……” Spika akanyamaza baada ya Jenerali Akiki kusimama kwa hasira “Mheshimiwa Spika sijawahi kushiriki katika jambo hilo na kama kuna watu wamekuletea taarifa kuwa nimeshiriki katika njama hizo za mapinduzi ni wazushi,waongo na wanastahili adhabu kali.Profesa Joseph wewe ni msomi mkubwa hupaswi kusikiliza uongo kama huo ambao unatungwa na wapinzani wangu kisiasa.Tunakaribia uchaguzi,lazima vitu kama hivi vijitokeze ili wanichafue.Naapa lazima niwapate wale wote wanaotaka kunipaka matope ! akasema Jenerali Akiki huku akigonga meza kwa hasira “Hakuna anayekupaka matope mheshimiwa Rais kwa sababu ni kweli umeshiriki na ushahidi ninao.Kataa mbele yangu kama humfahamu Melanie Davis? Akauliza Spika na midomo ya Jenerali Akiki ikatetemeka “Melanie nani? akauliza “Melanie Davis.Humfahamu? “Simfahamu.Ni mara ya kwanza ninamsikia mtu huyo.Ni nani?akauliza Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais mdomo wako unakana kumfahamu Melanie lakini macho yako yanakubali.Ulishirikiana na Melanie Davis na James Kasai katika mpango huo wa mapinduzi.Taarifa zote ninazo.Uliomba kukutana na marais wa Tanzania na Congo kwa lengo la kukamilisha mpango wa mauaji yao kwa bahati nzuri mpango huo haukufanikiwa”akasema spika “Mheshimiwa Spika siwezi kuvumilia uzushi kama huo.Mimi ni Rais wa Uganda nitawezaje kushiriki katika mpango wa kuwaua marais wenzangu? Jenerali Akiki akahamaki “Usihamaki mheshimiwa Rais wakati unafahamu fika kwamba haya yote ninayoyasema hapa ni kweli tupu” “Hakuna ukweli wowote Spika.Huo ni uzushi na uongo mkubwa ! akafoka Jenerali Akiki “Tukiachana na hilo suala la kushiriki katika mpango wa mapinduzi kuna suala lingine la James Kasai.Huyu ni mtu ambaye alifanya ukatili mkubwa kwa kuua mamia ya watu nchini Congo na baada ya kufurushwa ulimpa hifadhi Uganda.James amekuwa mshirika wako wa karibu sana na tayari imebainika wewe ndiye uliyekuwa ukimsaidia kijeshi katika mapambano yake dhidi ya serikali ya Congo.Kibaya zaidi ulimpa hifadhi hapa Kampala akaishi maisha ya kifahari huku dunia nzima ikijua James yuko msituni.Kwa nini mheshimiwa Rais ukafanya hivi? Akauliza Spika na Jenerali Akiki akaendelea kuvuta sigara yake kwa fujo sura akiwa ameikunja “Mheshimiwa Rais haya yote niliyokueleza ni ya kweli kabisa na ushahidi wa kutosha ninao kwamba umehusika katika kupanga njama za mauaji ya marais wa Tanzania na Congo na vile vile umekuwa mshirika wa James Kasai” akasema Spika na ukimya ukatawala mle ndani.Baada ya muda Jenerali Akiki akasema “Nini unakitaka Spika? Kwa nini umekuja kunieleza haya mambo? “Kuna kitu kimoja tu ambacho ninakitaka.Jiuzulu” akasema Spika na Jenerali Akiki akaitupa sigara katika chombo cha majivu akasimama “Spika siwezi kufanya kitu kama hicho.Mimi nijiuzulu ?!! akasema Jenerali Akiki na kutoa kicheko kidogo “Hiki ni kichekesho.Siwezi kujiuzulu kwa kuwa sihusiki na hizo tuhuma zilizopikwa na wapinzani wangu wa kisiasa.Kamwe siwezi.Narudia tena siwezi !! akasema kwa ukali huku akigonga meza kwa nguvu “Mheshimiwa Rais nimekufuata mimi mwenyewe kukutaka uachie ngazi kwa heshima.Toa sababu yoyote ile ambayo wananchi wataikubali uondoke madarakani kwa heshima na suala hili litakuwa limezikwa rasmi.Heshima yako itaendelea kuwepo na maisha yako yataendelea kuwa mazuri hakuna atakayefahamu haya mambo” akasema Spika.Jenerali Akiki akamtazama kwa macho makali na kusema “Ninarudia tena siwezi ! Nielewe spika siwezi kuachia ngazi kwa mambo ya kijinga kama hayo.Nilichaguliwa na wananchi wa Uganda niwaongoze hivyo nitaendelea kuwatumikia hadi pale muda wangu utakapokwisha.Umenielewa Spika?akauliza Jenerali Akiki kwa sauti ya ukali “Mheshimiwa Rais kama ukikaidi hiki ninachokwambia kuna mambo mawili yatafanyika.Aidha uondolewe na bunge au na wanananchi.Nitawasilisha ushahidi nilionao bungeni,wabunge watajadiliana na kupiga kura ya kutokuwa na imani nawe na yawezekana chama chako kikakunusuru katika kura hiyo lakini wananchi hawataweza kukuacha ukaendelea kukalia kiti cha urais.Mimi binafsi nitahamasisha maandamano makubwa ya wananchi ambayo hayajawahi kushuhudiwa hapa nchini wakishinikiza uachie madaraka.Kwa nini tufike huko mheshimiwa Rais?Kwa nini tukuondoe kwa fedheha? Fanya vile ninavyokushauri na utaendelea kubaki na heshima yako” akasema Spika “Joseph wewe si mgeni kwangu unanifahamu mimi ni nani.Sipendi kuyumbishwa na mtu yeyote.Ninakuonya Joseph achana na hili jambo.Kama kuna watu wamekutuma waeleze kwamba suala hili haliwezekani.! Akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais huu si wakati wa kunitolea vitisho.Mimi nawe tunafahamiana vyema ndiyo maana nimekufuata kiungwana kukutaka uachie ngazi kwa heshima.Usitake suala hili likafika kwa wananchi itakuwa ni aibu kubwa kwako ! akasema Spika “Spika ninarudia tena kukuonya kwamba achana na hili jambo litakuingiza katika matatizo makubwa.Kitu gani umekikosa Spika? Unataka urais? “Sihitaji urais na wala sihitaji kitu chchote kutoka kwako nimeridhika na kile nilichonacho.Umenionya niachane na hili jambo na mimi ninakuonya kwamba usithubutu kufanya kitu chochote cha kijinga.Naamini wewe una nguvu kubwa unaweza ukaninyamazisha mimi lakini hautaweza kuwanyamazisha wananchi.Ukiniondoa mimi ataibuka mwingine ataendeleza pale nilipoachia mimi na hakuna kuchoka hadi pale utakapoachia ngazi.Tunataka kuongozwa na Rais mwadilifu asiye na hata chembe ya doa sifa ambayo wewe huna mheshimiwa Rais” akasema Spika.Jenerali Akiki akaendelea kumtazama kwa macho makali “Mheshimiwa Rais nakushukuru kwa kunisikiliza.Mimi ninaondoka lakini nataka hadi kufika kesho saa kumi na mbili za jioni ujitokeze katika televisheni ya taifa na utangaze kuachia ngazi.Kama ukipuuza muda huo niliokupa basi usije kunilaumu.Kwa heri mheshimiwa Rais” akasema spika na kuondoka huku Jenerali Akiki akimtazama kwa hasira Jenerali Akiki akatabasamu baada ya kumbu kumbu ile kumjia “Nilimuonya profesa Joseph aachane na suala hili litamletea matatizo hakutaka kusikia.Nitaendelea kuwashughulikia wale wote ambao watavaa viatu vyake na kutaka kuliendeleza hili suala.Hakuna atakayeniondoa madarakani.Nitatawala hadi pale muda wangu utakapomalizika” akainuka na kwenda dirishani akachungulia nje “Nimewaogopa sana wanawake hasa wale wenye uzuri wa kimalaika.Melanie alinichanganya kwa uzuri wake hadi kujikuta nikifanya mambo ya kijinga ambayo sikupaswa kuyafanya kama Rais wa nchi.Kwa sababu ya tamaa zangu nimewasababishia vifo wale majenerali wa jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambao walikuwa wanapanga kufanya mapinduzi ambao Melanie amewataja katika rekodi hii kwamba walikuwa wanaandaa mpango wa mapinduzi.Majenerali saba waliokuwa wanaandaa mpango wa mapinduzi akiwemo mkuu wa majeshi waliuawa wiki iliyopita kwa nyakati tofauti.Mpaka leo haijulikani nani aliwaua wakuu wale wa jeshi lakini baada ya kutazama rekodi ile ya Melanie tayari nimepata jibu kuwa wameuawa na serikali yao.Naamini tayari Rais Patrice Eyenga amekwisha itazama rekodi ile na ndiyo maana akaamua kuchukua hatua za haraka za kuzima mpango wa mapinduzi kwa kuwaua kimya kimya wale waliotaka kumpindua.Nitaendelea kumlaumu sana James Kasai kwa kumleta kwangu Melanie Davis ambaye amenisabaishia haya yote” akawaza na kurejea mezani akaishika karatasi moja akaipitia kwa makini “Katika hii orodha ya watu ambao wamewasiliana na Spika wa bunge toka juzi naamini lazima yupo mmoja wao ambaye anafahamu kuhusiana na rekodi hii ya Melanie.Natakiwa kufanya uchunguzi wa kina kumfuatilia mmoja baada ya mwingine kujua ni yupi ambaye anafahamu kuhusu rekodi hii.Nitawaondoa wote bila kujali ni akina nani.Damu lazima imwagike kama ninataka kujilinda nibaki madara……....” Ghafla Jenerali Akiki akastuka baada ya milio ya risasi kuanza kusikika.Haraka haraka akainuka kwa lengo la kwenda kuchungulia dirishani kujua milio ile ya risasi ilisikika wapi lakini kabla hajalifikia dirisha mlango wa ofisi yake ukapiga teke ukafunguka wakaingia walinzi wake wanne wakamshika na kuanza kutoka naye nje “Kuna nini?akauliza Jenerali Akiki lakini hakujibiwa “Rekodi ! akasema Jenerali Akiki lakini walinzi wale hawakumsikia alichokisema waliendelea kukimbia naye huku milio ya risasi na mabomu vikisikika nje ya jengo la ikulu “Kuna nini kimetokea?akauliza Jenerali Akiki lakini hakujibiwa Walinzi wake walimpeleka Rais Akiki katika njia ya siri ambayo ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kumuondoa Rais ikulu pale kunapotokea hatari. “Weka namba za siri mkuu lango lifunguke” akasema mmoja wa wale walinzi na Rais akaelekeza jicho lake katika mojawapo ya kioo na baada ya sekunde chache lango likajifungua wakaingia katika njia ile ya siri ambako kulikuwa na gari maalum ambalo halipenyi risasi.Wakaingia katika gari lile na kufuata barabara iliyokuwa chini ya jengo la ikulu na walipofika kilometa kadhaa gari likasimama wakashuka na Jenerali Akiki akatamka neno la siri lango likajifungua wakapanda ngazi na kutokea katika bustani moja nzuri.Mlango wa nyumba iliyokuwepo mahala pale ukafunguliwa na ndani yake kulikuwa na magari manne ya kifahari ambayo ni maalum kwa ajili ya kumuokoa Rais.Bila kupoteza muda wakaingia katika gari ambalo funguo yake ilikuwa chini ya zuria upande wa dereva na kuondoka eneo lile “Nini kimetokea? Kwa nini hamtaki kunieleza kumetokea nini? akauliza Jenerali Akiki huku akihema kwa kasi “Ikulu imevamiwa mheshimiwa Rais ! akajibu mmoja wa walinzi “Ikulu imevamiwa? Nani kavamia? “Vikosi vya jeshi” Jenerali Akiki akavuta pumzi ndefu na kujiegemeza kitini “Nimepinduliwa ! akawaza.Baada ya dakika mbili akauliza “Mnanipeleka wapi? “Mheshimiwa Rais tunaelekea uwanja wa ndege ili uweze kuondoka nchini haraka iwezekanavyo” “Familia yangu iko wapi? Akauliza Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais hatujui mahala walipo lakini jukumu letu la kwanza ni kuhakikisha unakuwa salama ndipo tuanze kuitafuta familia yako.Usihofu mheshimiwa Rais watakuwa salama” Mmoja wa walinzi wale akapigiwa simu akaipokea na alipomaliza kuzungumza sura yake ilibadilika “Kuna nini?akauliza Jenerali Akiki “Nimetaarifiwa kwamba vimefika vikosi vya jeshi sasa hivi na kuuzingira uwanja wa ndege hakuna ndege inayoruhusiwa kuruka au kutua.Ndege ya Rais pia imezingirwa na wanajeshi ! “Mungu wangu ! akasema Jenerali Akiki na kushika kichwa “Tunaelekea wapi?akauliza mmoja wa walinzi “Naomba simu” akasema Jenerali Akiki akapewa simu akazungumza na balozi wa Marekani nchini Uganda akamueleza kilichotokea na kumuomba hifadhi katika ubalozi huo akakubaliwa “Twendeni ubalozi wa Marekani” akaelekeza Jenerali Akiki ************* Televisheni na redio ya taifa ya Uganda vilikatisha matangazo ghafla.Jenerali Paul Mukasa akajitokeza na kulihutubia taifa. “Ndugu zangu wananchi wa Uganda habari za mchana.Ninaitwa Jenerali Paul Mukasa mkuu wa majeshi wa Uganda.Nimejitokeza mbele yenu mchana huu kuwapeni taarifa kwamba Rais Jenerali Akiki Busingye Rwamirama amepinduliwa na jeshi limeshika uongozi wa nchi.Mimi na wenzangu tumeamua kumuondoa madarakani Rais Akiki kutokana na kupoteza sifa za kiuongozi kama mtakavyoelezwa hapo baadae. Ninawahakikishia ndugu wananchi kwamba mapinduzi haya yamemalizika na damu kidogo imemwagika kwa wale askari wachache watiifu kwa Jenerali Akiki na nchi iko salama kabisa.Ninawataka wananchi wote muendelee na shughuli zenu bila wasiwasi.Shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida chini ya uongozi wa jeshi hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika na Rais mpya kupatikana.Tunaahidi kufanyika uchaguzi mkuu ndani ya miezi sita kutokea sasa lakini hadi hapo utakapofanyika uchaguzi huo mimi Jenerali Paul Mukasa nitashika nafasi ya Rais Ninarudia tena kuwahakikishia wananchi wa Uganda kwamba nchi iko salama na ninawaomba asitokee mtu yeyote akathubutu kutaka kuleta vurugu za aina yoyote ile kwani jeshi liko imara na litakabiliana na yeyote ambaye atadiriki kuleta aina yoyote ya vurugu.Kuanzia sasa hadi wiki mbili ninatangaza amri ya kutotembea hovyo kuanzia saa mbili za usiku.Marufuku mikusanyiko isiyo na kibali cha jeshi au maandamano ya aina yoyote. Katika kipindi hiki ambacho jeshi limeshika madaraka tutakuwa wawazi na wa kweli.Mtafahamu kila kinachoendelea katika serikali ya Uganda,mtafahamishwa kila senti moja ya serikali ilivyotumika.Ule mtandao wote wa kifisadi wa Rais Akiki tutaufyeka na mali zote walizoiiba zilizoko ndani na nje ya nchi zitarejeshwa katika mikono ya serikali Narudia tena kuwaomba utulivu na tuendelee na shughuli zetu za kujiingizia kipato kama kawaida. Mungu ibariki Uganda Ahsanteni kwa kunisikiliza Jenerali Paul Mukasa alimaliza kutoa hotuba yake fupi kwa taifa kuhusiana na mapinduzi yale yaliyofanywa na jeshi la Uganda na kujtangaza yeye kuwa Rais wa mpito wa Uganda hadi pale utakapofanyika uchaguzi mkuu ndani ya miezi sita DAR ES SALAAM – TANZANIA Akiwa ofisini kwake Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo alistuka baada ya simu yake kuita na jina la mpigaji likajitokeza katika kioo cha simu.Akakunja sura kwa hasira “Dr Natukukunda ! akasema Dr Fabian akiitazama simu ile ikiita halafu akaipokea “Hallow Dr Natukunda” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais samahani sana nimekupigia kuomba msaada wako” “Unahitaji msaada gani nikusaidie?akauliza Dr Fabian “Jeshi limepindua nchi.Mume wangu sifahamu alipo,mimi na watoto tumefanikiwa kutoroshwa na walinzi na hivi sasa ninakaribia kufika mpakani ninakuja Tanzania.Mheshimiwa Rais ninakuomba msaada wako tupate hifadhi ya muda nchini Tanzania wakati tukitafuta namna ya kuweza kuondoka Afrika Mashariki” akasema Dr Natukunda Rwamirama mke wa Jenerali Akiki.Ukapita ukimya mfupi. “Mheshimiwa Rais nakuomba tafadhali tuko kwenye hatari kubwa na hatuna sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya Tanzania ! akaendelea kuomba Dr Natukunda “Mko wangapi?akauliza Dr Fabian “Niko na watoto wangu wawili msaidizi na walinzi watatu” “Sawa nitatoa maelekezo kwa vyombo husika viweze kuwasaidia mtakapofika mpakani” akasema Dr Fabian “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akajibu Dr Natukunda na kukata simu “Mmejipeleka wenyewe katika mdomo wa Mamba mwenye njaa.Bado nina hasira kubwa na Jenerali Akiki.Kama isingekuwa kwa msaada wa Mathew na wenzake hivi sasa ningekwisha poteza maisha kwani Akiki na wale magaidi walikuwa tayari wamekamilisha mipango yote ya kutuua mimi na Patrice Eyenga.Akuanzae mmalize.Alinianza na mimi ninammaliza.Nimeanza na yeye kuondoka madarakani na sasa naelekea kwa familia yake.Nataka huko aliko apate machungu,aumie kama ninavyoumia mimi kwa kifo cha mke wangu Millen.Yeye ndiye aliyemfadhili James Kasai ambaye ndiye aliyemuua mke wangu” akawaza Dr Fabian na kumpigia simu waziri wa mambo ya ndani ya nchi akampa maelekezo ili Dr Natukunda na wote alioongozana nao waruhusiwe kuingia nchini na kupewa hifadhi. “Sasa ni zamu yako Jenerali Akiki.Kokote uliko salamu zangu utazipata.Utakufa taratibu sana kwa mateso utakayoyapata” akaendelea kuwaza Dr Fabian MAKAO MAKUU – IDARA YA SIRI YA USALAMA WA NDANI WA NCHI (SNSA) Idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi, kazi ziliendelea kama kawaida kwa sasa ikiwa chini ya uongozi mpya wa mwanamama Ruby au Annabel jina ambalo amekuwa akilitumia toka alipofika Tanzania akitokea Uingereza. Baada ya Edwin Mbeko kuuawa rais alimkabidhi Ruby idara hii nyeti aiongoze na toka alipoanza kuiongoza idara hii mabadiliko mengi makubwa yamekwisha fanyika na ufanisi ulikuwa mkubwa kufuatia mabadiliko makubwahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ yaliyofanywa katika idara hii. Akiwa katika ofisi yake akiendelea na kazi simu yake ikaita alikuwa ni Rais Dr Fabian “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby baada ya kupokea simu “Ruby habari za leo? “Nzuri kabisa mheshimiwa Rais” “Tayari umepata taarifa za kilichotokea Uganda? Akauliza Dr Fabian “Ndiyo mheshimiwa rais tayari tumepata taarifa za mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika leo hii” “Yule shetani ameondolewa madarakani na jeshi na mpaka sasa hajulikani mahala alipo.Ninashukuru kwa kuwa amepata alichokistahili” akasema Dr Fabian huku aitoa kicheko kidogo “Mheshimiwa Rais unahusika kwa namna yoyote na haya mapinduzi? Akauliza Ruby “Kwa nini umeuliza Ruby? “Nataka nifahamu kama unahusika kwa namna yoyote na haya mapinduzi kwani yametokea ndani ya kipindi kifupi sana toka kushindwa kwa jaribio la kutaka kuwaua wewe na Rais Patrice Eyenga na hakuna sababu kubwa ya maana iliyotolewa na jeshi kwa nini wamefanya mapinduzi yale” akasema Ruby “Ruby yule jamaa alistahili hiki alichokipata tena hata zaidi ya hapa.Alitakiwa akamatwe na kupewa mateso makali sana.Kuhusu mimi kuhusika na mapinduzi hayo hapana sijahusika kwa namna yoyote ile” akasema Dr Fabian “Sawa mheshimiwa Rais.Sisi tunaendelea na majukumu yetu vyema na hakuna tatizo lolote” akasema Ruby “Ruby ninakuhitaji hapa ikulu sasa hivi nina mazungumzo muhimu nawe” akasema Dr Fabian “Sawa mheshimiwa Rais ninakuja hapo sasa hivi” akajibu Ruby na Rais akakata simu. Ruby akachukua kompyuta yake akafunga ofisi na kuelekea maegesho akamuelekeza dereva wake waelekee ikulu. “Dr Fabian ameonekana kufurahishwa sana na mapinduzi yaliyotokea leo nchini Uganda.Ninapata mashaka kidogo kuamini hana mkono wake katika mapinduzi haya.Wasi wasi wangu ni kwamba yawezekana uchunguzi ukafanyika na ikagundulika kwamba Tanzania ina mkono wake katika mapinduzi yale basi nchi itachafuka sana.Kwa kuwa amekiri yeye mwenyewe kwamba hahusiki kwa lolote katika mapinduzi hayo basi vizuri.Hata kama kukitokea na umwagaji damu, Tanzania hatutalaumiwa.Kwa upande Fulani hata mimi nimefurahi kwa Jenerali Akiki kuondolewa madarakani.Alikosea sana kushirikiana na magaidi kutaka kuwaua marais wenzake” akawaza Ruby akiwa njiani kuelekea ikulu Kutoka ofisi kuu za SNSA hadi ikulu si mbali hivyo alitumia dakika kumi na tano kufika ikulu.Walinzi wake wawili wakawahi kushuka garini mmoja akamfungulia mlango akashuka na kuelekea ndani ya jengo la ikulu kuonana na Rais “Karibu sana Ruby” akasema Dr Fabian baada ya Ruby kuwasili “Nashukuru mheshimiwa Rais” “Shughuli zinakwendaje hapo SNSA? “Kila kitu kinakwenda vyema hakuna tatizo lolote” “Nafurahi kusikia hivyo.Ruby kuna mambo mawili nimekuitia hapa.Kwanza ni kuhusu suala la msaidizi wako.Nina mafaili ya watu kadhaa ambao ninafikiria kumteua mmoja wao kuwa msaidizi wako.Idara nyeti kama hii lazima uwe na mtu wa kukusaidia.Nina majina ya watu nane ambao nimeletewa na wasaidizi wangu na wote hao ni watu wenye ujuzi na uzoefu mkubwa katika masuala ya usalama.Ninaendelea kuyapitia mafaili yao na nikimaliza nitakushirikisha nawe pia katika kuamua ni nani anafaa kuwa msaidizi wako” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nimekwisha liweka wazi suala hili toka awali kwamba mtu pekee ambaye nataka awe msaidizi wangu ni Papi Gosu Gosu sitaki mtu mwingine” akasema Ruby.Rais akamtazama na kuuliza “Kwa nini Papi Gosu Gosu na si mwingine? “Nimeshiriki naye katika operesheni kadhaa ninamfahamu vizuri na zaidi ya yote ninamuamini sana.Ninataka mtu ambaye atashika nafasi yangu pale nisipokuwepo awe ni mtu ninayemuamini na chaguo langu ni GosuGosu hivyo mheshimiwa Rais usipoteze muda kupitia hayo mafaili ya watu wengine” akasema Ruby “Lakini huyu jamaa kwa maelezo niliyoyapata kutoka kwa Austin si mtanzania wa kuzaliwa” “Mheshimiwa Rais usisahau kuwa hata mimi nina uraia wa Uingereza japo asili yangu ni Tanzania” akasema Ruby na Dr Fabiana akaguna kidogo “Vipi kuhusu afya yake? Akauliza “Anaendelea vizuri.Ninawasiliana naye kila siku na kwenda nyumbani kwake kujua maendeleo yake.Anaendelea vizuri na hata madaktari wanaomuhudumia wamenihakikishia hilo” “Kazi hizi hazihitaji mtu mwenye tatizo lolote la kiafy….” “Mheshimiwa Rais Gosu Gosu yuko vizuri naomba uniamini mimi.Hata kama leo na kesho nisipokuwepo yeye anafaa sana kuongoza idara kubwa kama hii” akasema Ruby “Sawa Ruby nitalifikiria hilo suala” “Ahsante mheshimiwa Rais” “Umemtaja Gosu Gosu nimemkumbuka Mathew Mulumbi.Mnawasiliana? “Hapana.Baada ya kumaliza operesheni ile alitoweka na hakuna anayejua alikwenda wapi wala hakuna mwenye mawasiliano naye” “Yule ni mtu wa ajabu sana.Sikumfahamu hapo kabla na hata nilipoelezwa kuhusu yeye sikuamini hadi pale alipoonyesha maajabu makubwa kwa kumuua James Kasai mtu ambaye tulikuwa tumeandaaa kikosi cha kwenda kumsaka.Kingine ambacho mpake leo hii kinausisimua mwili ni jinsi alivyoweza kupambana na mtu mwenye bomu.Ninajiuliza ni vipi kama Yule mtu angeamua kujilipua? Sina cha kusema kuhusu Mathew.Ningepata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu zaidi ningemuomba abaki hapa nchini ningempa kazi nzuri sana katika masuala ya usalama.Anafaa sana” akasema Dr Fabian “Mathew anajitosheleza kwa kila kitu katika maisha yake na hahitaji ajira serikalini” akasema Ruby “Tuachane na hayo ya Mathew Mulumbi.Nilikwambia nimekuita hapa kwa masuala mawili” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo halafu akasema “Nimepigiwa simu na Dr Natukunda Rwamirama mke wa Rais wa Uganda aliyepinduliwa.Amefanikiwa kutoroka na familia yake.Alinipigia simu akiomba hifadhi nchini Tanzania” “Umemkubalia ombi lake? “Ndiyo nimekubali ombi lake na tayari nimemuelekeza waziri wa mambo ya ndani ya nchi ahakikishe mama huyu na wote alioongozana nao wanaingia nchini na kupatiwa hifadhi” akasema Dr Fabian “Vizuri sana.Umeonyesha uungwana mkubwa sana licha ya mambo ya ajabu aliyotaka kuyafanya mume wake” akasema Ruby.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu kisha akasema “Ruby kuna jambo nataka ulifahamu ambalo yawezekana hautalipenda” “Jambo gani mheshimiwa Rais? “Nina sababu maalum ya kukubali mke wa Jenerali Akiki apewe hifadhi Tanzania” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo “Mke wangu Millen aliuawa na James Kasai ambaye alikuwa anafadhiliwa na Jenerali Akiki.Kama haitoshi Jenerali Akiki akashirikiana na James Kasai na magaidi wa IS kuandaa mpango wa kuniua.Sikufichi Ruby bado nina jeraha bichi la kuondokewa na mke wangu.Kila usiku ninapoitazama picha yake kidonda nilichokipata nahisi kinavuja damu.Nina hasira na Jenerali Akiki na ninataka maumivu haya niyapatao naye ayapate” akasema Dr Fabian “Unataka kufanya nini mheshimiwa Rais? Akauliza Ruby huku sura yake ikionyesha wasi wasi.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu na kusema “Nataka kuiteketeza familia yote ya Jenerali Akiki watakapokuwa hapa Tanzania” Ruby alipatwa na mstuko akasimama “Mheshimiwa Rais hapana ! Aliyeshiriki katika mpango wa kutaka kukuua ni Jenerali Akiki na si familia yake.Hawahusiki na chochote hivyo hakuna sababu ya kuwaumiza ! akasema Ruby “Nalifahamu hilo Ruby lakini ninataka kumuumiza Jenerali Akiki kama mimi ninavyoumia ! akasema Dr Fabian “Mr President no ! Hatuwezi kuua familia ambayo si hatari kwa usalama wa nchi ! “Ruby hili si ombi.Nimekwisha dhamiria hivyo na jambo hili lazima lifanyike.Familia yote watauawa watakapokuwa hapa nchini.Nataka uandae watu mahiri katika idara yako watakaotekeleza jambo hilo kwa siri” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais utanisamehe kama nitakosa nidhamu lakini idara ninayoiongoza inajishughulisha na kulinda usalama wa ndani wa nchi na si idara ya kutumika katika mauaji binafsi.Familia hii ambayo unataka iuawe si hatari kwa usalama wa ndani wa nchi wanakuja hapa nchini kwa ajili ya kupata hifadhi hivyo mimi kama mkuu wa idara hiyo siwezi kuandaa timu ya kushiriki katika mauaji hayo ambayo hayana tija kwa usalama wa nchi” akasema Ruby na Dr Fabian akamtazama kwa macho makali “Ruby mimi ndiye mkuu wa idara hii unayoiongoza na ndiye mwenye uamuzi wa mwisho katika kila jambo hivyo kama kiongozi wako ninakuamuru nataka uandae timu itakayotekeleza jambo hilo na hakuna mjadala katika hilo suala ! akasema Dr Fabian kwa sauti kali kidogo “Nafahamu mheshimiwa Rais kwamba idara ya SNSA iko chini yako lakini umeniteua mimi niwe mkurugenzi wake na kwa mamlaka uliyonipa ninao uwezo wa kukataa kufanya jambo lolote ambalo halitakuwa na maslahi kwa usalama wa nchi.Mauaji ya famili ya Jenerali Akiki ni ya kulipiza kisasi na si kwa sababu za kiusalama” akasema Ruby na Dr Fabian akasimama “Ruby nakuonya chunga sana kauli yako unapozungumza nami.Huzungumzi na mchumba wako,hapa unazungumza na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo kuwa na adabu ! akafoka Dr Fabian “Ninakuagiza na hili si ombi bali ni amri.Nataka uandae timu ya watu mahiri kwa ajili ya kuimaliza familia ya jenerali Akiki.Narudia tena kwamba hili si ombi ni amri nenda kaitekeleze ! akasema Dr Fabian kwa sauti kali “Mheshimiwa Rais ulinitoa Uingereza ili nije kuongoza idara ya usalama wa ndani ya nchi.Hukunileta hapa kuja kufanya mauaji kwa kufurahisha nafsi yako.Kama kuna ulazima wa kuua basi ni kwa sababu za usalama wa nchi lakini sioni hatari ya familia hii kwa usalama wa nchi yetu.Narudia tena mheshimiwa Rais utanisamehe kwa haya maneno yangu lakini huo ndio msimamo wangu na endapo utaendelea kusisitiza suala hilo ni bora ukaniondoa katika nafasi hii ya ukurugenzi kisha ukaendelea na mipango yako ya kuua watu wasio na hatia ! akasema Ruby na Dr Fabian akamtazama kwa hasira “Ruby nakushangaa sana.Unafahamu fika alichonifanyia Jenerali Akiki na..” “Ninafahamu mheshimiwa Rais lakini familia hii hawahusiki na chochote alichokifanya Akiki hivyo hawastahili hicho unachotaka kuwafanyia.Nakushauri mheshimiwa Rais sitisha huo mpango wako.Mambo yamekwisha tulia hivi sasa,James Kasai aliyekuwa tishio hayupo tena,mtandao wa IS hapa nchini umeng’olewa,SNSA imesafishwa na inafanya kazi vizuri, na nchi iko salama.Nakushauri mheshimiwa Rais achana na hilo suala linaweza kuibua matatizo mengine kwa wakati huu ambapo mambo yametulia” akasema Ruby.Dr Fabian akafikiri halafu akasema “Sawa Ruby nimekuelewa.Ahsante kwa ushauri wako” “Nashukuru mheshimiwa rais kwa kunielewa” “Niliyokuitia ni hayo mawili hivyo tumemaliza mazungumzo yetu.Kuna lolote lingine ambalo unataka kuniambia?akauliza Dr Fabian “Hakuna mheshimiwa Rais” akajibu Ruby wakaagana akaondoka “Sikujua kama Ruby ni mwanamke mwenye msimamo mkali namna hii.Lakini alichokisema ni cha kweli.Idara yake inasimamia usalama wa ndani wa nchi na familia ya Jenerali Akiki haina hatari yoyote kwa usalama wa nchi.Hata hivyo,nafsi yangu inakataa kabisa kuwaacha salama.Nataka nimuumize Akiki.Nimeanza kwa kumuondoa madarakani na ninataka kumuongezea mateso kwa kuimaliza familia yake pia.Ninataka aishi maisha magumu yenye mateso makali.Nimekwisha muelekeza Jenerali Mukasa kuhakikisha wanataifisha mali zake zote zilizoko ndani na nje ya nchi,kuzuia akaunti zake zote za benki ili Jenerali Akiki aishi maisha ya taabu.Ningeweza kupanga mpango wa kumuua lakini nataka afe taratibu kwa mateso” akawaza Dr Fabian na kuchukua simu akampigia mtu Fulani akamtaka afike ofisini kwake mara moja. Baada ya kutoka ikulu Ruby akaelekea nyumbani kwa Gosu Gosu kumjulia hali. “Karibu sana Ruby” akasema Gosu Gosu aliyekuwa amekaa pembeni ya bwawa la kuogelea akisoma kitabu cha hadithi “Ahsante Gosu Gosu.Sikujua kama nawe u msomaji wa vitabu” akasema Ruby “Ni kweli sikuwa msomaji wa vitabu lakini nimeanza kuvutiwa na huyu mwandishi Patrick Ck ninasoma kitabu chake hapa” akasema Gosu Gosu na kufunika kitabu alichokuwa anakisoma. “Habari za huko utokako?akauliza “Huko kwema.Vipi maendeleo yako? “Ninaendelea vizuri.Nimetoka hospitali wamenipima na kuniambia ninaendelea vizuri” “Nafurahi kusikia hivyo” “Usihofu Ruby muda si mrefu nitakuwa tayari kuanza majukumu yangu”akasema Gosu Gosu “Nimetoka ikulu kuonana na Rais nimemkumbusha tena kwamba ni wewe ndiye ninayekuhitaji kuwa msaidizi wangu ndiyo maana ninakuombea umalize mapumziko uliyopewa ili uje kunisaidia katika majukumu yangu” akasema Ruby na Gosu Gosu akatabasamu “Ruby ahsante sana kwa kunichagua niwe msaidizi wako.Ninakuahidi pale tu mapumziko yangu yatakapomalizikana madaktari kuniruhusu kuendelea na kazi basi nitaanza kazi haraka sana katika idara yako” akasema Gosu Gosu “Umesikia kilichotokea Uganda leo? “Amenipigia simu Austin akanijulisha kwamba Rais wa Uganda amepinduliwa na jeshi” “Ni kweli amepinduliwa na jeshi na mpaka sasa hajulikani mahala alipo ila familia yake wameomba hifadhi nchini Tanzania” “Rais amekubali kuwapa hifadhi Tanzania? “Ndiyo amekubali kuwapa hifadhi lakini nina hofu” “Hofu ya nini Ruby? “Kuhusu usalama wao” “Rais hakupaswa kuwapa hifadhi.Jenerali Akiki ni mtu mbaya sana !” akasema Gosu Gosu. “Lakini familia yake haihusiani na yale aliyoyafanya Akiki ndiyo maana Rais ameamua kuwapa hifadhi” akasema Ruby wakaendelea na mazungumzo mengine jhalafu Ruby akaondoka akarejea ofisini kwake KAMPALA - UGANDA Magari ya jeshi yaliendelea kumwaga wanajeshi katika mitaa ya jiji la Kampala kufanya doria kuhakikisha jiji linakuwa salama.Japo shughuli ziliendelea kama kawaida lakini watu walikuwa na hofu kubwa kwamba yangeweza kutokea machafuko. Katika ubalozi wa Marekani jijini Kampala alikokimbilia Jenerali Akiki,ulinzi uliimarishwa.Kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani kilifika haraka sana katika ubalozi huo kikitokea katika kambi ya wanajeshi wa Marekani waliokuwa katika program ya mafunzo maalum kwa wanajeshi wa jeshi la Uganda na kujiandaa kukabiliana na hatari yoyote ambayo ingeweza kutokea ubalozini hapo. Saa tatu toka yafanyike mapinduzi na Jenerali Akiki kukimbilia katika ubalozi wa Marekani,helkopta mbili za jeshi la Marekani kutoka katika kambo yake iliyoko nchini Kenya ziliwasili na kutua katika ubalozi wa Marekani nchini Uganda.Bila kupoteza muda Balozi wa Marekani nchini Uganda akiwa na familia yake akaingia katika mojawapo ya helkopta ikaondoka halafu Jenerali Akiki akaingizwa katika helkopta nyingine akaondoka kuelekea nchini Kenya. “Ahsante Mungu kwa kunisaidia nimeweza kutoka salama Uganda.Waliofanya mapinduzi walikuwa na lengo la kuniua.Lakini imewezekanaje yakapangwa mapinduzi bila ya watu wangu wa usalama kufahamu? Naamini katika mpango huu wa mapinduzilazima walifahamu lakini wakakaa kimya.Kwa sasa kinachoniumiza kichwa ni familia yangu.Je wamefanikiwa kutoka salama au wanashikiliwa na jeshi? Akajiuliza Jenerali Akiki akiwa ndani ya helkopta wakielekea nchini Kenya “Watanzania wana methali isemayo kikulacho ki nguoni mwako.Leo nimeamini methali hii ni ya kweli kabisa.Sikutegemea kama Paul Mukasa angeweza kunipindua.Sasa nimeamini Paul na Profesa Joseph walikuwa kitu kimoja.Sikuelewa profesa Joseph aliposema kwamba hata kama nikimuondoa yeye ataibuka mwingine kuendeleza pale alipoishia sasa nimefahamu mtu aliyekuwa anamzungumzia ni Paul Mukasa ambaye nimemlea,nimemfundisha nimempandisha cheo hadi akawa mkuu wa majeshi lakini leo hii kwa kufuata ushauri wa wabaya wangu ameamua kunisaliti akanipindua.Kweli katika hii dunia hupaswi kumuamini mtu yeyote.Wa kuaminiwa ni Mungu pekee.Nilimuamini Melanie mwisho wa siku akanivua nguo na kuanika mipango yetu,nilimuamni Mukasa nikamuweka katika nafasi ya juu kabisa lakini malipo yake ni kunipindua tena kama walinzi wangu wasingewahi kuniokoa ningeweza hata kuuawa.Ngoja nikatulize kwanza akili niitafute familia yangu na baada ya kuwapata ninaahidi Uganda haitakalika.Paul Mukasa atajuta kile alichokifanya ! akawaza Jenerali Akiki Iliwachukua saa moja na dakika arobaini kuwasili nchini Kenya wakaelekea moja kwa moja katika kambi ya kijeshi ya Marekani iliyokuwa nje ya jiji la Mombasa.Dakika chache baada ya kuwasili katika kambi hiyo ya kijeshi ya vikosi vya Marekani vilivyoko nchini Kenya katika operesheni ya kulisambaratisha kundi la kigaidi la Alshabaab,Jenerali Akiki akapelekwa katika chumba cha mikutano ya moja kwa moja kwa njia ya video ambako alikutana na mkuu wa kambi ile. “Jenerali Akiki karibu sana katika kambi yetu.Naitwa Kanali Robert Darby mkuu wa kambi hii ya wanajeshi wa Marekani hapa Mombasa.Pole sana kwa kilichotokea” “Ahsante sana Kanali Robert.Ninashukuru mno kwa kunitoa Uganda na kunileta hapa” akasema Jenerali Akiki “Kabla ya yote kuna mtu anataka kuzungumza nawe” akasema Kanali Robert,akabonyeza kitanza mbali na katika runinga akaonekana Rais wa Marekani William Washington “Mheshimiwa Rais, Jenerali Akiki yuko tayari kwa mazungumzo”akasema Kanali Robert “Jenerali Akiki” akasema Rais William Washington “Mheshimiwa Rais ! akasema Jenerali Akiki “Pole sana Jenerali Akiki kwa yaliyotokea leo.Sijafurahishwa na huu mfululizo wa mapinduzi unaoendelea katika nchi za Afrika.Kilichotokea leo ni kama ugonjwa ambao umeenea kwa kasi barani Afrika.Kumekuwa na mapinduzi katika nchi mbali mbali na wakati mwingine kupelekea umwagikaji mkubwa wa damu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Ninakuhakikishia mimi na serikali yangu hatukubaliani na hiki kilichofanywa na jeshi na hatuiungi mkono serikali hiyo inayoongozwa na jeshi.Bado tunaendelea kukutambua wewe kama Rais halali wa Uganda”akasema Rais William “Nashukuru sana mheshimiwa Rais kwa maneno hayo” “Nini mipango yako baada ya haya yote kutokea?akauliza Rais William “Kwa sasa baada ya kuwa niko sehemu salama ninataka kuitafuta familia yangu ambao mpaka sasa sifahamu mahala walipo.Sijui kama wako hai au wanashikiliwa na jeshi” akasema Jenerali Akiki “Usihofu Jenerali Akiki.Nitawaelekeza maafisa wa ubalozi wetu nchini Uganda wafuatilie kujua mahala iliko familia yako kisha watachukuliwa na kuletwa hapo Mombasa kisha tutajua nini cha kufanya.Kwa sasa endelea kupumzika hapo wakati taratibu nyingine zikiwekwa sawa” “Nashukuru sana mheshimiwa Rais kwa msaada huu mkubwa ambao sikuwa nimeutarajia” akasema Jenerali Akiki na Rais William akazima runinga yake “Rais William yuko sahihi.Afrika huu ugonjwa wa mapinduzi tayari umeota mizizi.Ngoja kwanza niipate familia yangu halafu nitajipanga namna ya kuwafundisha adabu wasaliti hawa.Ninaapa Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla hakutakalika.Wamekosea sana kunipindua







Wakati bado tukio la mapinduzi ya kijeshi nchini Uganda yaliyomuondoa madarakani Rais Jenerali Akiki Rwamirama halijapoa,Afrika Mashariki iliamshwa na taarifa nyingine za kustusha na kuhuzunisha.Familia ya Jenerali Akiki ambayo iliomba kupatiwa hifadhi nchini Tanzania ilifariki yote katika ajali ya gari. Saa moja na dakika ishirini na mbili za asubuhi baada ya kumaliza mazoezi ya asubuhi Ruby alirejea chumbani kwake kwa ajili ya kuoga ili ajiweke tayari kuikabili siku,alipotazama simu yake akakuta amepigiwa na watu kadhaa wa idara yake pamoja na Gosu Gosu “Kuna nini asubuhi yote hii wanaanza kunitafuta? Akajiuliza na kuamua kumpigia kwanza Gosu Gosu “Hallo Gosu Gosu.Vipi hali yako?akauliza Ruby “Ninaendelea vyema.Vipi wewe uko salama? “Salama kabisa” “Nilikupigia simu ikaita bila kupokelewa nikapata wasiwasi” akasema Gosu Gosu “Nilikuwa mazoezini.Is everything okay?akauliza Ruby “Jana tulipokuwa tunazungumza kuhusiana na mapinduzi ya kijeshi nchini Uganda ulinieleza kwamba familia ya Rais aliyepinduliwa iliomba hifadhi nchini Tanzania” “Ndiyo waliomba hifadhi nchini Tanzania na rais akamuelekeza waziri wa mambo ya ndani ya nchi ahakikishe familia hiyo inapewa hifadhi” “Ulionyesha wasi wasi kuhusiana na usalama wao wakiwa hapa nchini.You knew something was going to happen to them? Akauliza Gosu Gosu “Kwani vipi Gosu Gosu mbona maswali mengi?akauliza Ruby “Taarifa ambazo zimepatikana asubuhi hii ni kwamba familia yote wamefariki katika ajali ya gari alfajiri ya leo wakati wakija Dar es salaam” “Ajali ya gari?! akauliza Ruby kwa mshangao “Ndiyo Ruby.Taarifa zinadai kwamba gari walilokuwa wamepanda liligongana na lori kubwa la mizigo na watu wote waliokuwa katika gari hilo dogo wamepoteza maisha” “Jesus Christ ! akasema Ruby kwa mstuko.Akabaki ameduwaa kwa muda hadi pale Gosu Gosu alipomstua “Ruby ! “Gosu Gosu taarifa hizi ni za kweli? Akauliza “Ni taarifa za kweli kabisa.Ni taarifa ambayo imesambaa sana katika mitandao ya kijamii na hata katika taarifa ya habari ya asubuhi leo wametangaza” “Dah ! akasema Ruby na kufikiri kidogo halafu akasema “Gosu Gosu ahsante kwa kunipa taarifa hizi.Nitawasiliana nawe tena baadae” akasema Ruby na kukata simu “Aaaaggghh !! akasema kwa hasira baada ya kumaliza mazungumzo na Gosu Gosu “Hii si ajali ya kawaida.He killed them ! akasema kwa uchungu “Tulikubaliana akanihakikishia kwamba hatawaua tena kumbe alikuwa ananidanganya ili kuniridhisha.Ameniudhi mno Dr Fabian.Sikutegemea kama angeweza kufanya kitu kama hiki cha kukatili uhai wa watu wasio na hatia yoyote ! akawaza Ruby na kuchukua simu akampigia Dr Fabian lakini hakupokea simu. “Kwa nini viongozi hawa wanakuwa wakatili kiasi hiki? Amepata faida gani baada ya kuwaua familia ile?Mke wake amerejea baada ya kuua familia ya Jenerali Akiki?Badala yake amechuma dhambi bure kwani watu wale hawakuwa na tatizo lolote naye.Hawakuwa na hatari yoyote kwa nchi” akawaza Ruby akiwa amekaa kitandani “Nitawezaje kufanya kazi na mtu kama huyu ambaye anatumia madaraka yake kuua kila amtakaye?Hapana hatuwezi kwenda namna hii.Vifo vya familia ya Akiki vimeniumiza sana” akawaza Ruby na kumpigia tena simu Dr Fabian lakini haikupokelewa. “Hata kama hapokei simu nitamfuata huko huko na kumueleza ukweli” akawaza Ruby akiwa amefura hasira MOMBASA – KENYA Saa tatu za asubuhi balozi wa Marekani nchini Uganda ambaye amehamishiwa nchini Kenya kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Jenerali Akiki,aliwasili katika kambi ya wanajeshi wa Marekani alikokuwa amehifadhiwa Jenerali Akiki.Akiongozana na Kanali Robert Darby wakaelekea moja kwa moja katika chumba alimolala Jenerali Akiki “Habari za asubuhi mheshimiwa Rais” akasema balozi “Karibuni.Kuna taarifa zozote kuhusu familia yangu?Mmekwisha fahamu mahala walipo? Akauliza Jenerali Akiki akionekana kuwa na wasiwasi “Mheshimiwa Rais,tumepokea taarifa asubuhi hii kutoka kwa watu wetu waliotumwa kufuatilia mahala ilipo familia yako” akasema balozi “Familia yangu iko salama?akauliza Akiki “Mheshimiwa Rais kwa taarifa tulizonazo ni kwamba baada ya mapinduzi kutokea familia yako waliokolewa na walinzi na wakaelekea nchini Tanzania ambako waliomba kupewa hifadhi……” “Subiri kwanza.Unasema familia yangu waliomba hifadhi Tanzania? Akauliza Jenerali Akiki “Ndiyo,waliomba hifadhi nchini Tanzania na wakakubaliwa” “Mungu wangu ! akasema Jenerali Akiki akionyesha wasiwasi mkubwa. “Wako salama?akauliza baada ya ukimya wa sekunde kadhaa “Mheshimiwa Rais taarifa zilizopatikana asubuhi ya leo kutoka Tanzania zinasema familia yako yote wamefariki katika ajali ya gari wakati wakielekea Dar es salaam usiku wa kuamkia leo” Jenerali Akiki aliyekuwa amesimama akahisi miguu inamuisha nguvu taratibu akaanza kwenda chini Kanali Robert akamdaka na kumketisha sofani. “Ee Mungu baba kwa nini umeniadhibu namna hii? Ungenipa adhabu nyingine yoyote lakini si kunichukulia familia yangu.Wanangu walikuwa kila kitu katika maisha yangu ! akasema kwa uchungu Jenerali Akiki akiwa amefunika uso wake kwa viganja vya mikono.Kanali Robert na balozi wakatoka wakamuacha Jenerali Akiki peke akiendelea kububujikwa na machozi “Dr Fabian ! akasema kwa hasira “Naamini hii ni mipango ya Dr Fabian kulipiza kisasi kwangu.Hata mpango huu wa mapinduzi ni yeye aliyeshirikiana na jeshi kuuandaa na hakuridhika kunitoa madarakani akaamua kuimaliza na familia yangu pia.Ameniumiza sana.Nitawaliliaje familia yangu? Akaendelea kuwaza Jenerali Akiki akiendelea kububujikwa machozi “Ninaapa kama nitaendelea kuwa hai nitalipiza kisasi kibaya sana kwa Uganda na Tanzania.Nchihizi mbili nitahakikisha hazikaliki ! akawaza WASHINGTON DC – MAREKANI Katika chumba kimoja ndani ya ikulu ya Marekani watu wanne walikutana kwa ajili kikao cha dharura.Aliyeitisha kikao hicho ni Mark Piller makamu wa rais wa Marekani. “Ahsanteni sana kwa kufika katika kikao hiki cha dharura na nimewaiteni hapa kwa sababu ninyi ni watu ninaowaamini.Tumekuwa tunashirikiana katika mipango mbali mbali yenye maslahi kwa Marekani” akafungua kikao makamu wa Rais “Kama mlivyosikia kile kilichotokea nchini Uganda.Jeshi limempindua Rais wa nchi hiyo Jenerali akiki Rwamirama na jenerali Paul Mukasa aliyekuwa mkuu wa majeshi amejitangaza kuwa Rais wa Uganda.Mahusiano kati ya Uganda na Marekani kwa siku za hivi karibuni yameboreka hasa baada ya kumpeleka balozi mpya ambaye amefanya kazi kubwa ya kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili.Baada ya mapinduzi hayo kutokea Jenerali Akiki aliomba hifadhi katika ubalozi wetu jijini Kampala.Kutokana na hali tete ya usalama ilitulazimu kumuhamisha na kumpeleka katika kambi yetu ya kijeshi iliyoko Mombasa Kenya ambako yuko hadi sasa na yuko salama”akasema Mark Piller “Huu mchezo wa kupindua serikali umeanza kuota mizizi katika bara la afrika hivi sasa.Ndani ya miezi sita tayari serikali zaidi ya tano zimekwisha pinduliwa” akasema mmoja wa wale watu walioshiriki kikao kile “Katika kila mapinduzi unayoyaona yanatokea barani Afrika lazima kuna mkono wa mataifa ya nje hasa mataifa makubwa” akasema Mark Piller “Haya mapinduzi ya Uganda kuna taifa lolote linahisiwa limehusika? “Ni mapema bado kusema chochote hadi pale uchunguzi utakapofanyika” akajibu Mark Piller “Tumemuhifadhi Rais huyo wa Uganda katika kambi yetu nini mipango yake au mipango yetu? Akauliza mshiriki mwingine wa kikao kile “Ndiyo maana nimewaita hapa ili tujadiliane kuhusu suala hili.Mapinduzi haya yanaweza kuwa na faida kwetu. Jenerali Akiki anaweza kuwa muhimu kwetu” “Faida zipi tunaweza kuzipata kutokana na mapinduzi haya? Akauliza mmoja wa washiriki wa kile kikao “Mafuta” akasema Mark Piller na kuwatazama wenzake halafu akaendelea “Kwa taarifa zilizopatikana,Uganda ina akiba kubwa sana ya mafuta kuliko nchi zote kusini mwa jangwa la Sahara.Utafiti unaonyesha kuwa inaweza kuongoza kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta barani Afrika.Tunaweza kuitumia fursa hii kujipatia akiba ya mafuta kutoka Uganda.Kwa sasa kumekuwa na uhaba mkubwa wa mafuta duniani baada ya nchi wazalishaji wakubwa wa mafuta kuzalisha kwa kiasi kidogo tofauti na mahitaji ya dunia ili kupandisha bei.Tunahitaji mafuta hivyo hatuwezi kutegemea mafuta ya nchi za Mashariki ya kati wakati zipo nchi zina akiba kubwa ya mafuta na tunaweza kuyapata bila gharama kubwa na mojawapo ikiwa Uganda”akasema Mark Piller “Hilo ni wazo zuri sana mheshimiwa makamu wa Rais.Bei ya mafuta katika soko la dunia imepanda mno na kama nchi ya Uganda ina akiba kubwa ya mafuta litakuwa jambo zuri lakini ni namna gani tutaweza kuyapata hayo mafuta? “Wazo langu ni kumleta Jenerali Akiki hapa Marekani kisha nitazungumza naye na kumshawishi kumpatia makazi hapa Marekani na huo utakuwa ni mwanzo wa kuelekea katika mpango wa kuelekea katika mafuta.Kama tunakubaliana na mpango huu basi nataka tufanye maandalizi ili Jenerali Akiki aweze kuletwa kwa siri hapa Marekani” akasema Mark Piller na mazungumzo yakaendelea kisha wote wakafikia makubaliano juu ya suala lile BAADA YA SAA MBILI MOMBASA KENYA Zilipita saa mbili toka Jenerali Akiki alipopewa taarifa za vifo vya familia yake.Kanali Robert na balozi wa Marekani nchini Uganda wakarejea tena katika chumba kile cha Jenerali Akiki “Pole sana Jenerali Akiki” akasema balozi “Kuna taarifa nyingine mmezipata kuhusu familia yangu? “Taarifa tulizozipata ni kwamba utaratibu unafanyika hivi sasa nchini Tanzania kwa kushirikiana na balozi wa Uganda nchini Tanzania ili miili ya marehemu iweze kurejeshwa Uganda kwa mazishi.Tutaendelea kukujulisha kila kinachoendelea” akasema balozi “Ouh jamani ! akasema Jenerali akiki na kuinamisha kichwa “Jenerali Akiki hiki ni kipindi kigumu sana kwako lakini unapaswa kuwa jasiri.Wewe ni mwanajeshi ukianguka hupaswi kulala hapo,inuka na usonge mbele.Mapambano yanaendelea na ili uweze kupambana unahitajika uwe jasiri sana” akasema Kanali Robert “Sijawahi kuumia namna hii katika maisha yangu ! “Pamoja na yote haya Jenerali Akiki hupaswi kukata tamaa.Kama alivyosema Kanali Robert kwamba mapambano bado yanaendelea,inuka kamata silaha songa mbele” akasema balozi “Nipambane na nani kwa nini?Nimekata tamaa kabisa sioni hata sababu ya kuendelea kupambana.Nilipambana kumuondoa dikteta nchini Uganda ambaye aliiipeleka nchi shimoni,nimeirudisha nchi katika ramani ya dunia na haya ndiyo malipo yake.Imetosha.Sitaki tena mapambano sitaki kitu chochote.Ninachokihitaji hivi sasa ni kufa nikaungane na familia yangu ! akasema kwa uchungu Jenerali Akiki huku machozi yakiendelea kumtoka “Jenerali Akiki maneno kama hayo hayapaswio kutamkwa na mwanajeshi kama wewe.Umepitia mambo mengi hadi kufika hapa ulipofika na hujawahi kushindwa na mafanikio yote uliyoyapata ni kwa sababu ya kutokata tamaa.Unalopitia sasa hivi ni kubwa lakini hupaswi katu kukata tamaa.Mungu ana sababu zake kwa nini amekuacha hai.Ungeweza kuuawa katika mapinduzi yale lakini walinzi wako walikuokoa na hivi sasa uko katika mikono salama.Hii yote ni mipango ya Mungu” “Mungu yupi ? akauliza Jenerali Akiki “Sidhani kama yupo huyo Mungu kwani asingekubali familia yangu yote iteketee ! akasema Jenerali Akiki kwa hasira “Jenerali Akiki,nimepewa maelekezo na makamu wa Rais wa Marekani kwamba tukuondoe hapa na kukupeleka nchini Marekani.Atakuwa na mazungumzo nawe marefu hivyo jiandae ndani ya nusu saa kutoka sasa utaondoka na ndege ya jeshi kuelekea Marekani” akasema Balozi na Jenerali Akiki hakujibu kitu.Balozi na Kanali Robert wakatoka wakimuacha Jenerali Akiki katika tafakari nzito. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ruby aliwasili ikulu kwa ajili ya kuonana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Ni kawaida yake kufika hapa kila asubuhi ili kumpa Rais muhtasari wa kile kinachoendelea ndani ya idara ya SNSA.Asubuhi hii hakuwa na faili lolote alilobeba zaidi ya mkoba wake mdogo. Akiwa ndani ya ofisi yake,Dr Fabian alisikia mabishano nje ya ofisi yake na mara mlango ukafunguliwa akaingia Ruby akiwa ameongozana na katibu muhtasi wa Rais. “Mzee nimempa maelekezo lakini amenipuuz…..” “It’s ok Sauda” akasema Dr Fabian na Sauda akatoka akamuacha Ruby katika ofisi ya Rais “Karibu uketi” akasema Dr Fabian huku akiendelea na shughuli zake “What’s the meaning of this?akauliza Ruby na Dr Fabian akalifunika faili alilokuwa analipitia “Unamaanisha nini Ruby?akauliza Dr Fabian “Hupokei simu yangu, halafu umetoa maelekezo hakuna mtu kuingia ofisini kwako leo.Nini maana yake? Unanizuia hata mimi? akauliza Ruby “Ruby eleza kilichokuleta uondoke ukaendelee na shughuli zako.Leo si siku nzuri kwangu ! akasema Dr Fabian.Ruby akamtazama halafu akasema “Hatimaye umefanikisha lengo lako” “Lengo gani Ruby? “You killed them” “Akina nani? “Familia ya Jenerali Akiki ! “Taarifa niliyoipokea ni kwamba wamefariki katika ajali ya gari na hakuna mtu aliyewaua.Sihusiki na chochote katika vifo hivyo” akasema Dr Fabian na Ruby akaendelea kumtazama kwa macho makali “Nini umekipata baada ya kuiteketeza familia ambayo haikuwa na hatari yoyote kwa nchi? Umepata amani ya moyo? Mkeo Millen amerejea? Akauliza Ruby kwa sauti kali na Dr Fabian akanyanyuka kwa hasira “Ruby chunga sana ulimi wako.Hapa unazungumza na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si hawara yako hivyo kuwa na heshima. Wewe ni nani wa kuja kunipandishia sauti? Umeanza kupoteza heshima Ruby kuwa muangalifu sana ! akafoka Dr Fabian “I’m sorry Mr President ! akasema Ruby “One more thing,usirudie tena kulitamka jina la mke wangu kama unataja boga ! akafoka Dr Fabian huku akimnyooshea Ruby kidole. “Samahani mheshimiwa Rais sintarudia tena”akasema Ruby “Na iwe hivyo.Heshimu ofisi hii na usije tena ukaanza kunifokea ! akasema Dr Fabian wakatazamana kwa muda akaketi “Sit ! akasema Dr Fabian na Ruby akaketi “Nina ratiba ndefu siku ya leo.Tuzungumze masuala ya kazi na si masuala hayo mengine yasiyohusiana na kazi yako” “Mheshimiwa Rais,kilichonileta hapa kwako ni suala hilo la familia ya Jenerali Akiki” “Hilo suala nimekwisha lifunga.Sitaki mjadala wa suala hilo uendelee.Umenisikia Ruby? “Nimekusikia mheshimiwa Rais” akajibu Ruby “Good.kama hakuna lingine nenda kaendelee na shughuli zako kama ukiwa na jambo muhimu tutawasiliana.Suala la hiyo ajali linashughulikiwa na jeshi la polisi wao ndio watakaotoa taarifa nini hasa kilichosababisha ajali hiyo” akasema Jenerali Akiki na Ruby akasimama akachukua mkoba wake akaanza kupiga hatua kuelekea mlangoni.Kabla hajakishika kitasa cha mlango akasimama akafikiri kidogo halafu akageuka akaudi mezani “Kuna kitu umesahau Ruby?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kunyamaza akamtazama Dr Fabian “Nini unataka kusema Ruby?akauliza Dr Fabian.Ruby akameza mate na kusema “Mheshimiwa Rais utanisamehe kwa hiki ninachokisema lakini ni lazima nikiseme.Nina uhakika mkubwa ajali ile imetengenezwa ili kuiondoa familia ile.Lakini fahamu kwamba umefanya kosa kubwa na hiki ulichokifanya iko siku athari zake utaziona” akasema Ruby kisha wakaangaliana kwa sekunde kadhaa halafu Dr Fabian akauliza “Umemaliza? “Ndiyo mheshimiwa Rais” “Good.Go back to work” akasema Dr Fabian na Ruby akageuka akaondoka “Huyu mwanamke itanilazimu niwe naye makini sana.Anaonekana si mtu ambaye anaweza akanisikiliza kwa kila ninachomuamuru kukifanya.Hapendi kupindisha mambo.Nisipokuwa makini naye iko siku anaweza akaniingiza katika matatizo” akawaza Dr Fabian huku akichezea kalamu yake “Edwin Mbeko alikuwa mtiifu sana alifanya kila nilichomuelekeza lakini kwa huyu japo anafanya kazi yake vizuri ila nitapata wakati mgumu sana kumtumia katika mambo yangu binafsi.Lakini watu kama hawa dawa yao ni ndogo tu.Nitaanza kumuweka karibu yangu.Yawezekana labda mimi naye hatujazoeana sana ndiyo maana anakuwa mzito kutekeleza majukumu yangu.Huyu hataweza kunisumbua dawa yake ni ndogo tu” akawaza Dr Fabian huku akitabasamu Ruby alipotoka kuonana na Rais hakurejea tena ofisini kwake akafululiza moja kwa moja kwa Gosu Gosu “Ahsante sana Ruby kwa kuja kunitembelea.Ninapata faraja kubwa kwa namna mnavyonijali” akasema Gosu Gosu “Usijali Gosu Gosu.Sisi tayari ni ndugu moja hivyo lazima kufuatilia maendeleo yako kwa karibu sana” akasema Ruby “Is something wrong Ruby?akauliza Gosu Gosu “Nothing wrong Gosu Gosu” “Hapana Ruby.Sura yako inaonyesha wazi kuna kitu kinakusumbua.Niambie kuna tatizo gani linakusumbua? Akauliza Gosu Gosu “He killed them ! akasema Ruby kwa hasira “Nani unamzungumzia? “Rais Dr Fabian ! akasema Ruby “Kafanya nini Rais? “Naamini ndiye aliyeelekeza familia ya Jenerali Akiki wauawe” “Kwa nini unasema hivyo Ruby? “Alinipa maelekezo kutuma timu ya kuwaua lakini nilikataa.Idara yetu inashughulika na usalama wa nchi na familia ile hawakuwa na hatari yoyote kwa nchi ! akasema Ruby na kuinamisha kichwa kwa sekunde chache halafu akasema “Imeniumiza sana.Kulikuwa na watoto wadogo ambao hawafahamu hata mambo anayoyafanya baba yao.Kwa nini wauawe bila kosa? Hii si sawa hata kidogo” akasema Ruby “Uko sahihi Ruby.Kama familia hiyo hawakuwa na hatari yoyote kwa nchi hakukuwa na sababu ya kuuawa” akasema Gosu Gosu “Hicho ndicho kinachoniumiza zaidi ! akasema Ruby “Lakini isikuumize sana kwani idara yako haijahusika katika suala hili.Imekuwa vizuri umemuweka wazi na ameufahamu msimamo wako lakini ………..” Akasema Gosu Gosu na kunyamaza kidogo “Lakini nini? “Kwa hiki ulichokifanya cha kukataa kuifanya kazi yake kinavuruga mahusiano mazuri mliyo nayo na inaweza ikakupa ugumu kufanya kazi zako.Idara hii ya usalama wa ndani inatumiwa sana na marais katika kufanikisha baadhi ya masuala yao binafsi.Viongozi wote wa SNSA waliopita walikuwa watiifu kwa marais na walitekeleza kila walicho watakiwa wafanye” “Mimi ni tofauti na hao waliopita ! akasema Ruby “Ruby naamini Rais hajafurahishwa na hiki ulichokifanya kukataa kushiriki mauaji ya familia ya Jenerali Akiki.Nina wasi wasi sana kama mazingira ya kufanya kazi yako yatakuwa rafiki.Rais anaweza akakuona wewe kama kikwazo katika kufanikisha mambo yake hivyo akafikiria hata kukuondoa” akasema Gosu Gosu “Unalosema ni kweli lakini sina hakika kama Dr Fabian anaweza akafikia hatua hiyo” akasema Ruby “Ushauri wangu mdogo,achana na hiyo kazi tufanye biashara.Yale makampuni yote ambayo Melanie aliyanunua kwa Peniela yamerudishwa kwa Mathew na yanahitaji usimamizi.Achana na hiyo kazi ambayo tayari imeanza kuleta mtafaruku.Naamini atakuja tena na suala lingine atakuelekeza ulifanye na ukikataa utakuwa adui yake.Kwa nini ifike huko? Angali bado mapema achana na hiyo kazi na tujikite kwenye biashara” akasema Gosu Gosu,Ruby akatabasamu “Ni mapema mno kuogopa.Nina muda mfupi ndani ya SNSA hivyo sipaswi kuogopa.Ngoja nijipe muda zaidi na kama kukionekana kuna hatari yoyote kwa mimi kuendelea kufanya kazi SNSA basi nitafuata ushauri wako” akasema Ruby “Sawa Ruby uamuzi ni wako lakini kuwa makini sana” akasema Gosu Gosu wakaendelea na mazungumzo mengine kisha Ruby akaondoka kuelekea ofisini kwake









Imetimu saa mbili za usiku Ruby akiwa amejipumzisha nyumbani kwake gari nne nyeusi zilifika katika geti la nyumba yake.Akiwa sebuleni kwake aliona taa ya kijani ikiwaka katika kisanduku kilichokuwa ukutani pembeni ya runinga iliyounganishwa na kamera za usalama zilizofungwa kuzunguka nyumba yake.Taa ile ya kijani huwaka pale geti kubwa linapofunguliwa.Alistuka na haraka haraka akachukua kitanza mbali akabonyeza kamera ya getini akaziona gari nne zikiingia “Nani hawa? Mbona sina ratiba ya kuonana na mtu yeyote usiku huu?Kwa nini walinzi wameruhusu watu kuingia bila kunijulisha? Akajiuliza Ruby.Aliogopa.Haraka haraka akacheza na kompyuta yake na kuifunga milango yote kwa ndani halafu akaendelea kuwafuatilia watu wale kujua ni akina nani.Gari mbili za mbele wakashuka watu waliovalia suti nadhifu na kulizunguka gari la tatu.Macho yao hayakutulia waliangaza kila kona kisha wawili kati ya wale jamaa wakaelekea katika mlango mkubwa wakagonga.Ruby akawachunguza kwa makini kwa kutumia kamera ya mlangoni “Akina nani hawa?Mbona siwafahamu?Wanataka nini?akajiuliza Ruby wale jamaa wakiendelea kugonga mlango.Akachukua simu na kuwapigia walinzi wake getini kuuliza kwa nini wameruhusu watu kuingia bila ruhusa yake na akajibiwa kwamba wamelazimka kufungua kwani ni msafara wa Rais.Haraka haraka Ruby akaenda mlango akafungua.Wale jamaa wawili wakaingia ndani wakakagua sebuleni halafu mmoja wao akausogeza mkono ake aliovaa saa karibu na mdomoni wake akasema “Clear ! Haikupita hata dakika moja mlango ukafunguliwa wakaingia watu wanne kisha akafuata Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo “Hello Ruby” akasema Dr Fabian akitabasamu “Mheshimiwa Rais ! akasema Ruby na Rais akawataka wale walinzi wake watoke nje “Umenistua sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby “I’m sorry Ruby.Sikutaka kukueleza kama ninakuja kwako nilitaka nikustukize”akasema Dr Fabian “Karibu sana.Utapenda kunywa nini? Akauliza Ruby “Chochote utakachoniandalia nitashukuru” Ruby akaenda katika kabati ambalo huhifadhi vinywaji vikali akachukua chupa mbili na kuziweka mezani,akammiminia Rais kinywaji katika glasi na yeye akajimiminia “Karibu” “Ahsante Ruby” “Ungeniambia kama utakuja ili nikuandalie hata chakula kidogo” akasema Ruby “Usijali Ruby.Nilitaka nikustukize nione namna unavyoishi hapa.Are you alone? “Ndiyo niko peke yangu” akajibu Ruby “Kwa nini unaishi mwenyewe?Huna mtu wa kuishi naye? “Nina mfanyakazi wa ndani ambaye kuanzia jana amepata dharura amekwenda kumuuguza mama yake mgonjwa,vile vile nina walinzi na kama haitoshi nina mbwa anaitwa Bravo nilipewa na Mathew ninampenda sana” akasema Ruby “Wewe na Mathew mnaonekana mna ukaribu mkubwa” “Ni kweli mheshimiwa Rais nina ukaribu na Mathew Mulumbi” “Vizuri sana.Lakini unahitaji kuwa na mwenzi sasa.Utaishi namna hii hadi lini? Akauliza Dr Fabian na Ruby akatoa kicheko kidogo “Mambo hayo mheshimiwa Rais hayataki haraka.Muda utakapofika basi nitakuwa naye lakini kwa sasa nimejielekeza katika kazi yangu” “Kwa hiyo huna mchumba? Akauliza Dr Fabian na Ruby akacheka tena kidogo “Mchumba ninaye ila yuko nje ya nchi” “Hongera.Ana bahati sana huyo aliyekupata.Siku akija nchini umlete kwangu nimfahamu” “Usijali mheshimiwa Rais nitamleta” akasema Ruby na ukimya mfupi ukapita “Ruby nimekuja hapa bila taarifa kuna suala ambalo limenileta usiku huu” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Ulipokuja ofisini kwangu asubuhi ya leo hatukuwa na mazungumzo mazuri.Nilikutolea maneno ambayo si ya kiungwana.Nafahamu nilikukera hivyo nimekuja kukuomba msamaha.Siku ya leo haikuwa siku nzuri kwangu ndiyo maana nilikuwa katika hali ile.Nakuhakikishia it won’t happen again” akasema Dr Fabian na Ruby akatabasamu “Mheshimiwa Rais mambo kama yale ni ya kawaida kutokea katika sehemu za kazi hivyo sikushangaa kwa vile nimekwisha yazoea.Nimefanya kazi katika ofisi ambayo inaweza kumpa mtu shinikizo la damu lakini nilimudu vyema na ndiyo maana hawakutaka niondoke hivyo suala lile lilimalizika pale pale.Mimi pia ninaomba samahani sana kwa tabia yangu asubuhi ile.Nilikosa heshima kwako mkuu wa nchi,sikupaswa kuzungumza nawe namna ile.Nami pia naomba unisamehe mheshimiwa Rais hata kama nitakuwa na jambo limenikaba kooni nitajitahidi kutafuta namna nzuri ya kuliwasilisha” akasema Ruby “Nimekusamehe Ruby” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Dr Fabian akanyanyua glasi yake “Friends again? Ruby akatabasamu na kusema “Friends” kisha wakagonganisha glasi zao. “Mheshimiwa Rais ninataka kuuliza na ninaomba uwe mkweli na muwazi kwangu” “Usijali Ruby uliza” “You did it? Akauliza Ruby na Dr Fabian akawa kimya kwa muda halafu akatingisha kichwa kukubali “Yes I did it” akasema na kunyamaza kidogo “Naomba niwe muwazi kwako Ruby.Ajali ile ilikuwa ya kutengeneza kwa lengo la kuwamaliza familia ya Akiki.Nina hasira kubwa na Jenerali Akiki kwa kitu alichotaka kunifanyia na niliapa kumfanyia kitu kibaya sana na hasira hizo ndizo ambazo zimenipelekea kuimaliza familia yake namna ile.Dr Natukunda alikuwa ni rafiki wa mke wangu na sikutegemea kama siku moja ningeweza kumfanyia ukatili huu lakini ni mume wake ndiye aliyenifanya niwe na roho ya ukatili hata nikalazimika kuimaliza familia ile yote.Ninataka nimuumize Akiki.Kama si kwa jitihada zenu ninyi kuweza kung’amua mipango aliyokuwa nayo Jenerali Akiki, hivi sasa tayari ningekwisha kuwa marehemu ndiyo maana wewe na wenzako akina Mathew mnayo nafasi kubwa ndani ya moyo wangu kwani mlipambana kuokoa maisha yangu.Jasiri Mathew Mulumbi aliweza kupambana na mtu mwenye bomu ambalo lililengwa kuniua.Mimi na Jenerali Akiki tulikuwa marafiki na tulikuza mashirikiano kati ya Uganda na Tanzania.Kila ninapofirikia kwa nini Akiki ajiunge katika mpango wa kuniua ninajikuta ninapatwa na hasira kali.Hukupendezwa na kile nilichokifanya kwa familia ya Jenerali Akiki I’m so sorry lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya,roho ya kisasi ilikwisha niingia” akasema Dr Fabian na kunyamaza akanywa funda moja kisha akasema “Kuna jambo lingine ambalo nataka nikufahamishe leo ambalo ni la siri kubwa.Tumeufungua ukurasa mpya hivyo sitaki kukuficha jambo” akasema Dr Fabian akanywa tena funda lingine akasema “Mapinduzi yaliyofanyika jana nchini Uganda yaliyomuondoa madarakani Jenerali Akiki mimi pia nimeshiriki katika kuyapanga” Ruby aliyekuwa ameshika glasi akiipeleka mdomoni akajikuta akiishusha haraka mezani kwa mshangao alioupata. “Nimekustua,samahani kwa hilo lakini nimelazimika kukueleza ukweli.Kuna kitu kimoja ambacho unapaswa ukifahamu kuhusu mimi.Nina tatizo la kuamini watu ndiyo maana jambo kama hili nimelifanya mwenyewe kwa siri na wewe ni mtu wa kwanza unalifahamu kwa hapa nchini.Nimechagua kukuamini na kukushirikisha katika mambo yangu nyeti” akasema Dr Fabiana akanyamaza akamtazama Ruby “Dah ! akasema Ruby “Kama nilivyokueleza awali kwamba chuki niliyokuwa nayo dhidi ya Jenerali Akiki ni kubwa sana hivyo nilidhamiria kumuumiza,kumfanya awe na maisha magumu.Niliwasiliana na spika wa bunge la Uganda nikamtaka aje Tanzania kimya kimya nikazungumza naye kwa kirefu kuhusiana na mambo yote anayoyafanya Rais Akiki naye alishangaa sana.Hakufahamu kama James Kasai alikuwa anaishi jijini Kampala.Nilimpatia rekodi ile ya Melanie Davis tukakubaliana aitumie kumtaka Akiki aachie ngazi kwa hiari yake na kama akigoma basi bunge litumike kumuondoa.Tulitengeneza mtandao mkubwa na kumshirikisha pia mkuu wa majeshi wa Uganda ili endapo mpango wa kwanza wa kumtaka aachie ngazi au kuondolewa na bunge kushindwa kufanikiwa basi jeshi lifanye mapinduzi.Kwa bahati mbaya katika mchakato huo spika wa bunge la Uganda aliuawa yeye na familia yake na ndipo jeshi lilipochukua nchi” akasema Dr Fabian na kuchukua glasi akanywa funda moja kubwa “Say something Ruby ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais sijui niseme nini.Nakushukuru kwa kunieleza ukweli” akasema Ruby “Baada ya kuufahamu ukweli nini maoni yako?Ni wewe pekee ambaye una uthubutu wa kusimama na kunieleza ukweli.Usiogope nieleze ukweli” “Sina maoni yoyote mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Dr Fabian akanywa kinyaji kidogo halafu akasema “Asubuhi wakati unaondoka ofisini ukiwa umekasirika ulinieleza kwamba kwa hiki nilichokifanya nitasababisha matatizo makubwa.Ulimaanisha nini? “Zilikuwa ni hasira tu mheshimiwa Rais lakini sikumaanisha chochote.By the way yuko wapi Jenerali Akiki kwa sasa? “Hajulikani alipo.Alifanikiwa kutoroka mara tu wanajeshi walipovamia ikulu.Naamini hata huko aliko salamu zangu atazipata.Mali zake zote zitataifishwa na serikali atabaki hohehahe.Atapata mateso makali na atakufa taratibu” “Kuna uwezekano amejificha nchini Uganda?akauliza Ruby “Bado haijulikani lakini jeshi linandelea na uchunguzi kumtafuta mahala alipo” akasema Dr Fabian na ukimya ukapita “Mheshimiwa Rais mimi bado si mtaalamu sana wa mambo ya kiusalama lakini ushauri wangu ni kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunafahamu mahala alipo Jenerali Akiki na kummaliza.Kama ataendelea kuwa hai nina uhakika mkubwa atajipanga kulipiza kisasi” “Jeshi la Uganda linaendelea na msako na watanijulisha kila watakachokipata halafu tutaangalia nini cha kufanya.Kwa kuwa ameondoka madarakani Akiki hana nguvu tena na hawezi kupanga njama zozote.Mali zake zote ziko nchini Uganda na zote zimetaifishwa na jeshi hivyo basi hana nguvu yoyote ya kuweza kupanga shambulio la aina yoyote ile” Ruby na Dr Fabian walikuwa na mazungumzo marefu hadi ilipotimu saa tatu za usiku ndipo Rais alipoondoka kurejea ikulu WASHINGTON DC – MAREKANI Jenerali Akiki alifikishwa Marekani na kupelekwa katika nyumba aliyoandaliwa jijini Washington DC.Ilkuwa ni nyumba nzuri kubwa na yenye ulinzi wa kutosha. “Maisha yana maajabu sana.Yanaweza kubadilika ndani ya sekunde moja tu.Jana nilikuwa Rais,jeshi lote likiwa chini yangu,nilikuwa na ulinzi mkali na kauli yangu ilikuwa ya mwisho lakini leo tazama mahala nilipo.Niko ugenini,sina kitu chochote ninalishwa na kuvishwa,sina msafara tena,sina timu ya walinzi na zaidi ya yote sina familia” akawaza na kuinamisha kichwa chake kwa mawazo “Kila ninapoikumbuka familia yangu ninapatwa na uchungu mkubwa mno.Naamini kabisa kwamba ajali iliyowaua ni mpango wa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Dr Fabian.Anataka kulipiza kisasi baada ya kugundua kwamba nilishiriki katika kupanga mauaji dhidi yake na Patrice Eyenga.Hata mimi kupinduliwa naamini ana mkono wake kwani Spika wa bunge asingeweza kuipata rekodi ile ya Melanie.Lazima aliipata kutoka Tanzania na mtu ambaye naamini aliyempa rekodi ile ni Rais Dr Fabian” akavuta pumzi ndefu alihisi kizungu zungu akajilaza kitandani “Yote haya ameyasababisha James Kasai.Yeye ndiye aliyemleta Melanie kwangu nikamtamani na kujikuta nikikubali kufanya kila alichotaka nikifanye.Yule mwanamke nahisi alikuwa shetani kwani sikujielewa nilikuwa nakubali tu kutekeleza kila alichonielekeza.Ni aibu kwa Rais kama mimi kuanguka penzini na binti mwenye umri sawa na mwanangu.Ni aibu kubwa hii” akawaza na kuinuka “Natamani hata nijipige vibao kwa ujinga nilioufanya.Kwa tamaa zangu nimekosa kila kitu.Nimemkosa Melanie,nimeikosa familia yangu na hata urais wangu nimeupoteza.Hivi sasa ninaishi kama mkimbizi” akaendelea kuwaza huku akibubujikwa na machozi “Nilikuwa nikisikia tu marais wakipinduliwa sikujua kama http://deusdeditmahunda.blogspot.com/huwa wanapata taabu za namna hii.Mbaya zaidi nilishiriki katika mpango wa kumpindua Rais Patrice Eyenga lakini mpango haukufanikiwa na kibao kimenigeukia mimi,jeshi likanipindua.Nimejifunza mengi kupitia haya yaliyonikuta.Kuna muda ninaichukia siasa natamani ningebaki jeshini lakini tamaa za madaraka zikanipeleka kufanya mapinduzi nikamuondoa Rais madarakani na nilichokifanya ndicho kimenitokea mimi” akaendelea kuwaza Jenerali Akiki “Kuna sauti ninaisikia ndani mwangu ikiniambia niachane na siasa nianze maisha mapya.Nina mali nyingi nimezichuma ninaweza kuishi maisha mazuri tu bila matatizo lakini papo hapo kuna sauti nyingine ninaisikia inaniambia nisikubali lazima nilipize kisasi kwa hawa watu walionifanyia ubaya.Lakini hata kama nikiamua kujipanga kulipa kisasi ni kwa ajili ya nani? Akajiuliza “Ngoja niachane kwanza na haya mawazo kwa sasa.Pale akili yangu itakapokuwa imetulia nitajua nini cha kufanya lakini kwa sasa siwezi kufanya maamuzi yenye kufaa” akawaza na kujilaza kitandani Saa mbili za usiku kwa saa za Marekani watu sita wakaingia ndani ya nyumba alimokuamo Jenerali Akiki aliyekuwa amejikunyata sebuleni akitazama runinga.Watu wale hawakumsemesha kitu wakafanya ukaguzi katika nyumba nzima halafu akaingia Mark Piller makamu wa rais wa Marekani.Huyu ni mmoja wa mwanasiasa kijana sana na anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Marekani.Jenerali Akiki akasimama “Mheshimiwa makamu wa rais ! akasema Jenerali Akiki.Hakutegemea kama Mark Piller angekwenda kumtembelea usiku ule. “Jenerali Akiki” akasema Mark wakasalimiana “Karibu sana mheshimiwa makamu wa Rais.Sikutegemea kukuona hapa mida hii” akasema Jenerali Akiki “Nimekuja mida hii kwa kuwa nisingeweza kuja mchana kwanza kutokana na kazi nyingi na pili ni kuhusu uwepo wako hapa Marekani” William akanyamaza kidogo halafu akasema “Naomba ufahamu Jenerali Akiki kwamba uwepo wako hapa Marekani tumeufanya siri.Wanaofahamu uko hapa ni watu wachache sana.Sababu kubwa ya kufanya jambo hili kuwa siri hatutaki dunia ifahamu kuwa uko hapa Marekani hivyo usishangae kwa masharti ya kutowasiliana na mtu yeyote.Kwa ujumla naomba usihofu kitu hapa uko salama kabisa,ulinzi ni mkali” “Nashukuru sana mheshimiwa makamu wa Rais” akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki pole sana kwa yote yaliyokutokea na kubwa zaidi tukio la kuipoteza familia yako” akasema Mark “Ahsante mheshimiwa makamu wa Rais.Ninajaribu kuifanya akili yangu ikubali kwamba suala hili ni la kawaida lakini inakuwa ngumu.Kuondokewa na familia nzima kwa wakati mmoja si kitu rahisi hata kidogo.Itanichukua muda kulizoea jambo hili na kuliona la kawaida” “Pole sana Jenerali Akiki.Maisha yetu ya kila siku yamejawa na mitihani mingi na huu uliokupata ni mojawapo ya mtihani wa maisha ambao inakubidi uushinde.Kwa namna yoyote ile Jenerali Akiki lazima ushinde mtihani huu” akasema Mark “Ninajitahidi sana mheshimiwa makamu wa rais ,ninajiahidi lakini ni ngumu.Itanichukua muda kulizoea jambo hili.Hata kama ingekuwa ni wewe ungekuwa katika hali yangu ungeona ugumu wa haya ninayoyaptia.Jana tu nilikuwa Rais wa nchi nikitembea na msafara mkubwa,nikitoa amri na kuheshimiwa na kila mtu lakini leo hi tazama mahala nilipo.Hili pekee linatosha kabisa kukupa ugonjwa wa moyo lakini kama haitoshi famili yangu pia wameuawa.Haya ni mateso yasiyovumilika hata kidogo lakini nitajitahidi” akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki moja ya kile kilichonileta hapa kwako usiku huu ni kukuhakikishia kwamba serikali ya Marekani bado inasimama nawe.Hatuitambui serikali ya kijeshi na kesho Rais atatoa tamko la kutoitambua serikali hiyo.Marekani ni taifa kubwa na tukitoa tamko mataifa karibu yote makubwa yataungana nasi kuupinga utawala huo wa kijeshi.Tutautaka utawala huo wa kijeshi kurejesha madaraka kwa serikali waliyoipindua haraka sana ama sivyo watakabiliana na vikwazo vikubwa vya kiuchumi.Tutazishawishi nchi kubwa ambazo ni wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Uganda wapunguze au kuacha kabisa kununua mafuta ya Uganda na kuufanya uchumi wa nchi hiyo kuporomoka kwa kasi.Tutaweka vikwazo vya kila aina kushinikiza serikali hiyo ya kijeshi kurejesha madaraka kwa serikali iliyopinduliwa.Naomba usife moyo Jenerali Akiki sisi tunakutambua wewe bado ni Rais wa Uganda na tutasimama nawe hadi tuhakikishe unarejea madarakani” akasema Mark Piller “Ahsante sana mheshimiwa makamu wa rais.Nimekosa neno la kushukuru kwa maneno haya mazito ambayo yamenifariji sana” “Usijali Jenerali Akiki.Karibu sana Marekani jisikie nyumbani” “Mungu akubariki wewe na serikali yako kwa msaada huu mkubwa” akasema Jenerali Akikiakiwa ameikunja mikono yake kifuani akishukuru “Jenerali Paul Mukasa ! akasema Mark na kunyamaza kidogo akamtazama Akiki “Huyu alikuwa mkuu wa majeshi.Lazima ni mtu uliyemuamini sana.Imekuaje akaamua kukugeuka?akauliza Rais William.Jenerali Akiki akavuta pumzi ndefu na kusema “Paul Mukasa alikuwa mwanafunzi wangu jeshini.Nilimpenda alikuwa kijana mtiifu na mkakamavu.Katika kila hatua niliyokuwa ninapanda jeshini sikumuacha nyuma niliendelea kumpigania ili naye aweze kupanda cheo.Nilipofanya mapinduzi mtu pekee ambaye niliamini angeweza kufaa kuwa mkuu wa majeshi ni Paul na bila kupoteza muda nikamteua akawa mkuu wa majeshi.Tumefanya kazi kwa mashirikiano makubwa na sikuwahi hata kuota kama siku moja Paul angeweza kufanya kitu kama hiki alichokifanya.Nilistuka mno nilipoambiwa kwamba Paul amejitangaza ndiye Rais wa Uganda baada ya mapinduzi” akasema Jenerali Akiki na kunyamaza akainamisha kichwa “Unadhani nini kimesababisha akafanya hiki alichokifanya?akauliza Mark Piller “Suala hili lazima lina mkono kutoka nje ya Uganda.Paul peke yake asingeweza kufanya hiki alichokifanya.Alikuwa mtiifu mno kwangu” “Unasema kuna mkono wa mataifa ya nje?Ni taifa gani unahisi limehusika katika mpango huu wa mapinduzi?akauliza Mark Piller.Jenerali Akiki akafikiri kidogo na kusema “Tanzania” “Tanzania?! “Ndiyo” akajibu Jenerali Akiki “Tanzania na Uganda ni nchi marafiki wakubwa.Iweje Tanzania ishiriki katika kuipindua serikali ya Uganda?akauliza Rais William na Jenerali Akiki akawa kimya “Jenerali Akiki unadhani kwa nini Tanzania ikashiriki katika kuipindua serikali ya Uganda? Kama unafahamu chochote nieleze tafadhali” akasema Mark Piller “Nitakueleza ukweli Mark Piller lakini naomba kile nitakachokuambia kisivuke nje ya kuta za nyumba hii” “Niamini tafadhali” akasema Mark Piller “Kulikuwa na mpango wa mapinduzi kuiondoa madarakani serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na mimi nilishiriki katika mpango huo” “Mlitaka kuipindua serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo?Mark Piller akauliza “Ndiyo.Nilishiriki katika mpango huo wa kumuondoa madarakani Rais Patrice Eyenga” “Kwa nini mlitaka kumuondoa madarakani Rais Patrice Eyenga? Akauliza Mark Piller “Mheshimiwa makamu wa Rais naamini unajua kwamba vita iliyokuwa inaendelea katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ilikuwa na manufaa makubwa kwa nchi tajiri” “Hilo nalifahamu.Nchi nyingi tajiri zimefaidika sana kwa vita iliyokuwa inaendelea nchini Congo” akasema Mark Piller “Uganda pia ilifaidika katika mapigano yale kwani sisi tulikuwa tunamfadhili James Kasai.Alipoingia madarakani Rais Patrice Eyenga alimaliza machafuko yaliyodumu kwa miaka mingi na kukata ile mirija yote iliyokuwa inazifaidisha nchi mbalimbali.Majenerali wa jeshi la Congo hawakufurahishwa na kile alichokifanya Patrice Eyenga kwani walikuwa wakifadikika kutokana na mapigano yale hivyo waliandaa mpango wa mapinduzi kumuondoa madarakani Patrice Eyenga.Hilo lilikuwa kundi la kwanza lakini kulikuwa na kundi la pili ambalo liliandaa mpango wa mapinduzi ambalo ndilo nilishirikiana nalo” akasema Jenerali Akiki na kumueleza Mark Piller kila kitu kuhusiana na mpango ule wa Melanie Davis wa kuwaua marais Patrice Eyenga na Dr Fabian Kelelo. “Hivyo ndivyo ilivyokuwa mheshimiwa makamu wa Rais” akasema Jenerali Akiki “Nilisikia kuhusu mpango ule wa kuwaua marais wa Tanzania na Congo kwa bomu la kujitoa mhanga lakini sikujua kama wewe nawe ulishiriki katika mpango ule.Ahsante kwa kunieleza ukweli” akasema Mark Piller na ukimya ukapita. “Jenerali Akiki sahau hayo yote yaliyotokea na hapa umekuja kuufungua ukurasa mpya.Kabla sijakueleza chochote nataka kukuhakisha kwamba mimi binafsi niko tayari kukusaidia lakini nataka kujua tutaanzia wapi kukusaidia.Nataka kusikia mipango yako.Je unataka kurudi tena Uganda? Bado unataka kukalia kiti cha Urais? Nieleze mipango yako tafadhali” akasema Mark Piller “Mheshimiwa makamu wa Rais kwa kweli mpaka sasa sifahamu nini hasa ninakihitaji.Akili yangu naona kama imefika mwisho wa kufikiri” akasema Jenerali Akiki “Akiki wewe ni mwanajeshi usiruhusu akili yako ikashindwa kujua hatima yako.Katika maisha kuna kuanguka lakini ukianguka simama haraka endelea mbele.Nawe pia umeanguka hivyo unapaswa kusimama na kusonga mbele.Hukufika hapa ulipofika kwa bahati mbaya.Ulipambana ukafika hapa ulipofika hivyo usikubali kirahisi watu hawa wakaharibu kila kitu ulichokipigania kwa muda mrefu.Umeijenga Uganda usiwape nafasi watu hawa ya kuiharibu Uganda na kuvuruga yale yote uliyoyajenga.Unapaswa kupambana” “Mheshimiwa makamu wa Rais sitaki tena kupambana.Nataka nibadili maisha yangu” “Maisha ya namna gani unataka kuishi Jenerali Akiki? “Sitaki tena kurejea Uganda.Nataka nipate sehemu niishi maisha yaliyotulia yenye amani.Ninafahamu mnao uwezo wa kunirejesha madarakani lakini sitaki tena urais.Nimeponea tundu la sindano sitaki tena kurejea Uganda.” “Nimekuelewa jenerali Akiki na mimi nakuahidi kukusaidia kwa hilo lakini naomba ufahamu kwamba hautakuwa na maisha yenye furaha na amani unayoyataka kama wale watu ambao wamekuondoa madarakani wataendelea kusalia madarakani.Kokote yanakofanyika mapinduzi kuna mambo mawili tu ambayo humtokea Rais anayepinduliwa.Kuuawa au kufungwa gerezani na mali zake zote hutaifishwa awe amezipata kihalali au kifisadi.Akibahatika kukimbia Rais huyu hugeuka mkimbizi na wakati mwingine anaweza akaishi ugenini kwa maisha yake yote yaliyobaki.Paul Mukasa na wenzake wataendelea kukusaka kujua mahala ulipo.Hii inakufanya uwe katika hatari kubwa lakini nakutoa hofu kwamba hapa Marekani utakuwa salama.Utapewa uraia wa Marekani na utaishi maisha mazuri yenye hadhi yako” “Nashukuru sana makamu wa Rais” “Jenerali Akiki kama umechagua kutorejea tena Uganda hayo ni maamuzi yako na tunayaheshimu,hata hivyo kuna jambo ambalo lazima tulifanye.Wasaliti wale waliokupindua hatuwezi kuwaacha hivi hivi lazima tuwafunze adabu” akasema Mark “Nini unakitaka mheshimiwa makamu wa Rais?akauliza Jenerali Akiki “Nataka Uganda isitawalike.Nataka wananchi wa Uganda wauchukie utawala wa kijeshi na wapaaze sauti kuukataa utawala huo na kutaka kurejeshwa kwa serikali ya kiraia.Mambo yatakapokuwa magumu wanajeshi watalazimika kurejesha madaraka kwa serikali ya kiraia.Unaonaje wazo hilo? Akauliza Mark Piller “Ni mpango mzuri sioni tatizo lake” akasema Jenerali Akiki “Ahsante kwa kukubali.Kinachotakiwa ni kuzusha vurugu kubwa nchini Uganda zitakazolilazimisha jeshi kutumia nguvu na kupelekea umwagikaji mkubwa wa damu na hii itajenga chuki kubwa kati ya utawala wa kijeshi na wananchi.Jumuiya ya kimataifa haitakaa kimya itapaaza sauti kuutaka utawala wa kijeshi kuondoka na kuachia madaraka kwa serikali ya kiraia.Jenerali Akiki nataka unisaidie mawazo ni namna gani tunaweza kuchafua hali ya amani nchini Uganda ili tuweze kuidhoofisha serikali ya kijeshi iliyokuondoa madarakani?akauliza Mark Piller.Jenerali Akiki alichukua muda kidogo akatafakari na kusema “Kikubwa inachotegemea serikali kwa sasa ni mafuta ambayo yanaipatia Uganda fedha nyingi sana.Tunaweza kuwadhoofisha kwa kuondoa chanzo hiki kikubwa cha mapato.Kuna bomba la mafuta ambalo linatoka Uganda kwenda Tanga Tanzania.Bomba hili likilipuliwa nchi itakosa mapato na watashindwa kuendesha serikali.Nashauri tuwadhibiti katika mafuta mheshimiwa makamu wa rais” akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki tukilipua bomba la mafuta linalokwenda Tanzania bado hatutakuwa tumefanya kitu.Ninachotaka mimi ni kuleta machafuko nchini Uganda ambayo yatapelekea vurugu kati ya jeshi na wananchi.Nataka damu imwagike” akasema Mark Piller.Jenerali Akiki akamtazama Mark kwa muda halafu akasema “Mark Piller nimekueleza ukweli wangu wote kwa nini nimepinduliwa.Nataka nawe unieleze ukweli.Kwa nini unataka itokee vurugu Uganda? Ni kweli vurugu hizo unazozizungumzia ni kwa ajili ya kuidhoofisha serikali ya kijeshi au ni kwa maslahi yenu? Akauliza Jenerali Akiki “Jenerali Akiki usizungumze kuhusu ninyi bali sema ni kwa maslahi yetu.Wewe tayari ni mmoja wetu na kwa kuwa u mmoja wetu nitakueleza ukweli” Mark Piller akanyamaza kidogo halafu akasema “Nchi ya Uganda ina mafuta mengi mno kuliko nchi nyingine yoyote Afrika.Akiba ya mafuta ya Uganda iliyogunduliwa ni kubwa sana kuzidi hata zile nchi zinazofahamika kwa uzalishaji mkubwa wa mafuta.Unaonaje kama tukichukua kiasi kidogo cha mafuta ya Uganda na kuongeza katika akiba yetu ya mafuta? Akauliza Mark Piller.Jenerali Akiki akafikiri kidogo kisha akasema “Mheshimiwa makamu wa Rais sasa nimepata picha nzima kuhusiana na haya mazungumzo yetu.Kila kitu tulichokizungumza hapa msingi wake ni mafuta ya Uganda” “Ndiyo Jenerali Akiki” akajibu Mark Piller na ukimya ukapita “Usiogope Jenerali Akiki,tayari wewe ni mwenzetu na kiasi kidogo cha mafuta tutakachokichukua na kuongeza katika akiba yetu ni kwa ajili ya ndugu zako wamarekani.Ukiwa kama mtu mwenye mchango mkubwa katika jambo hili utanufaika sana.Utaishi maisha ya kifahari sana hapa Marekani yenye hadhi yako.Umefanya kazi kubwa sana katika nchi yako,umeiweka Uganda ikaonekana katika ramani ya dunia lakini hakuna thamani yoyote unayopewa,hata mali zako zimechukuliwa na lengo lao ni ili uishi maisha magumu ya taabu.Hustahili kutendewa hivyo.Hapa Marekani tunakuthamini na utaishi mazuri yaliyojaa amani na furaha.Hutatamani tena kurejea Afrika” akasema Mark “Mheshimiwa makamu wa Rais hilo unalotaka nilifanye ni usaliti mkubwa kwa nchi yangu na bara la afrika.Huo ni unyonyaji mkubwa” akasema Jenerali Akiki na maneno yale Mark Piller hakuonekana kuyapenda “Jenerali Akiki,kauli kama hizo zilizungumzwa miaka mingi na viongozi wazalendo kwa bara la Afrika mfano Rais wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere na wengineo ambao walikuwa na uchungu wa kweli na bara la Afrika lakini kwa wewe hupaswi kutamka maneno kama hayo.Hauna sifa hiyo ya uzalendo kwa nchi au bara lako.Umemfadhili James Kasai kiongozi wa waasi ambaye aliua watu wengi.Kiongozi mwenye uzalendo kwa bara lake hawezi akafanya kitu kama hicho.Ulishiriki katika mpango wa mauaji ya maraisi wenzako,kiongozi mzalendo huwezi ukafanya jambo kama hilo.Jenerali Akiki hivi sasa hauna kitu chochote,hauna mahala pa kwenda na hakuna nchi wanayoweza kukupokea.Serikali ya marekani imekupokea kwa mikono miwili na kukupa makazi ya kama haitoshi utapata mara mbili ya kile ulichokipoteza baada ya mapinduzi.Ni juu yako ukubali au ukatae.Ukikubali utakuwa raia wa Marekani na kufaidika lakini endapo utakataa basi hatutakuwa na namna nyingine zaidi ya kukuruhusu ukatafute hifadhi nchi nyingine au tutakurejesha Uganda.Chaguo ni lako jenerali Akiki.Labda nikuweke wazi kwamba Marekani inapokea watu wale ambao watakuwa na manufaa kwa nchi.Kama nawe unataka kuwa raia wa Marekani lazima uwe na faida kwa nchi hii” akasema Mark Piller na kumtazama Jenerali Akiki “Nini unakitaka Jenerali Akiki? Unataka kuwa raia wa Marekani au unataka kurejea Afrika?akauliza Mark Piller “Sitaki kurejea Afrika.Nitaishi hapa Marekani” “Kama unakubali kuishi hapa Marekani huna budi kukubaliana na haya niliyokueleza” akasema Mark Piller “Kama mpango ni kuchukua mafuta basi vurugu ndani ya Uganda pekee hazitasaida kufanikisha mpango huo.Bomba la mafuta linaanzia Uganda na kwenda katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.Ili mpango huo ufanikiwe lazima eneo lote la Afrika Mashariki liingie katika machafuko ndipo itawezekana kuchukua mafuta hayo katika bandari ya Tanga” akasema Jenerali Akiki “Hapo sasa tunazungumza.Ni vipi basi tunaweza kuliweka eneo la Afrika Mashariki katika machafuko ili tuweze kufanikiwa kudhibiti mafuta? Akauliza Mark Piller “Kuna njia moja tu ambayo inaweza ikatumika kuleta machafuko makubwa katika eneo zima la Afrika Mashariki” akasema Jenerali Akiki “Nakusikiliza Jenerali Akiki.Ni jambo gani hilo? Akauliza Mark Piller “Ni kwa kutumia dini” “Dini? “Ndiyo.Tukitumia dini inaweza ikaleta machafuko makubwa si Uganda peke yake bali eneo lote la afrika Mashariki” “Hebu nifafanulie namna dini inavyoweza ikaleta machafuko Uganda na Afrika mashariki” akasema Mark Piller “Kiongozi mkuu wa waislamu nchini Uganda atauawa na watu wasiojulikana.Baada ya mauaji hayo,tutazungumza na kikundi cha kigaidi cha IS ambao watafanya mashambulio ya mabomu katika makanisa na mashule yanayomilikiwa na dini ya kikristu.IS wataeleza kwamba mashambulio hayo ni ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya kiongozi mkuu wa waislamu nchini Uganda” akasema Jenerali Akiki “Subiri kidogo Jenerali umesema kuhusu kushirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS? Akauliza Mark Piller “Ndiyo mheshimiwa makamu wa Rais ! “Hilo haliwezekani.Marekani katu haiwezi kushirikiana na magaidi kwa namna yoyote ile.Magaidi ni maadui zetu na tunawasaka kwa udi na uvumba kila mahala walipo na kamwe,narudia tena kamwe hatuwezi kushirikiana nao katika jambo lolote” “Kama mnahitaji mafuta ya Uganda basi mashirikiano na IS ni kitu cha lazima.Si IS pekee bali kikundi chochote cha kigaidi iwe Alshabaab au Boko Haram” akasema Jenerali Akiki “Hebu nieleze namna unavyotaka kuwatumia IS katika suala hili” “Kama nilivyo tangulia kusema kwamba kikundi ha IS kitashambulia makanisa na shule za taasisi za kidini na kusababisha vifo vingi.Tutamtafuta mtu ambaye atatumika kuchochea na kuwapandisha hasira wakristu ili wakalipize kisasi kwa waislamu na hapo tutakuwa tumepanda mbegu ya chuki kwa waumini wa dini hizi mbili.Machafuko ya kidini yakianza ni kama moto wa petroli,jeshi halitaweza kuyazuia.Yatasambaa nchi zote za Afrika mashariki”akasema Jenerali Akiki “Lakini uislamu haukubaliani na matendo ya kigaidi.Watakanusha kwamba waliofanya mashambulio hayo katika makanisa na misikiti hawauwakilishi uislamu” akasema Mark Piller “Ni kweli. Lakini maelezo watakayoyatoa baada ya mashambulio hayo hawatajitaja kuwa ni kundila IS bali watasema ni kikundi cha waislamu” “Hilo ni wazo zuri pia.Ni vipi kama akristu hawatachukuah atua zozote baada ya mashambulio hayo kutokea katika nyumba zao za ibada?akauliza Mark “Hapa kuna watu ambao lazima tuwatumie ili kuamsha hasira kwa waumini wa dini ya kikristu na kuchochea machafuko.Kuna mwanasiasa mmoja anaongoza chama cha upinzani ambaye tutazungumza naye na yeye ndiye atakayewapanga viongozi wa dini watakaowachochea waumini wao kuanzisha mashambulizi dhidi ya watu wa dini nyingine.Hawa nao lazima muwape hifadhi hapa Marekani.Baada ya machafuko wataondoka Uganda na kuja huku kimya kimya huku wakiacha moto ukiendelea kuwaka Uganda” “Hilo halina tatizo.Lazima wataangaliwa kwa namna ya kipekee kabisa” akasema Mark Piller “Machafuko haya yatakuwa makubwa yatasambaa katika miji mingine ya Uganda na hatimaye nchi nzima.Uganda ikiingia katika machafuko,tutahamia Tanga Tanzania.Ili kuweza kuchukua mafuta lazima jiji la Tanga liingie katika machafuko pia.Nina uhakika mkubwa sana kama tukitumia dini kuwagombanisha wakristu na waislamu basi machafuko yatakuwa makubwa na damu itamwagika.Machafuko yatakapokuwa makubwa mtakuwa mmepata kigezo cha kupeleka majeshi yenu Afrika Mashariki kwa lengo la kulinda amani na mtafanikiwa kuchukua kila mkitakacho lakini ili mpate sababu ya kutosha ya kupeleka wanajeshi Afrika Mashariki kuna jambo lazima lifanyike ambalo sina hakika kama mtakubaliana nalo” “Jambo gani Jenerali Akiki? Akauliza Mark Piller “Ubalozi wa Marekani ulioko Kampala inabidi ulipuliwe” “Kulipua ubalozi wa Marekani?! Mark Piller akashagaa “Ndiyo Mark.Lazima iwepo sababu ya kupeleka wanajeshi Uganda na Afrika mashariki hivyo ili kuongeza uzito lazima ubalozi wa Marekani Kampala ulipuliwe na raia wa Marekani kuuawa” akasema Jenerali Akiki.Mark Piller akafikiri kidogo halafu akasema “Sawa nitaunda timu maalum ya kulishughulikia suala hilo” “Mtu ambaye atahamasisha machafuko kutokea anaitwa Joshua Lulangwa.Huyu ni mwanasiasa anayeongoza chama cha upinzani kijulikanacho kama chama cha ukombozi wa Uganda.Huyu ndiye atakayewaandaa viongozi wa dini ambao watahamasisha wafuasi wao kushambuliana.Ataandaa kiongozi mmoja mwenye ushawishi upande wa wakristu na mwingine upande wa waislamu.Narudia tena hawa watakaochochoa machafuko mnatakiwa muwape hifadhi Marekani.” akasema Jenerali Akiki “Hilo halina tatizo Jenerali Akiki tutalitekeleza” akasema Mark Piller. KISIWA CHA VITI LEVU – FIJI Baada ya matembezi marefu katika msitu mnene Mathew Mulumbi na Najma walirejea kupumzika katika hoteli walikofikia.Mara tu walipofika mapokezi Mathew akajulishwa na muhudumu wa mapokezi kwamba wakati wamekwenda kutembea msituni kuna mtu alifika kumtafuta.Mathew alistushwa kidogo na taarifa ile hakujua nani aliyekuwa anamtafuta.Hakufahamiana na mtu yeyote katika kile kisiwa kwani walikuwa na siku tatu tu toka wamefika katika kisiwa kile kwa mapumziko. “Hakutaja jina lake huyo mtu aliyekuja kunitafuta? akauliza Mathew “Hapana hakutaja jina lake ila alisema atarejea tena baadae” akasema Yule muhudumu kisha Mathew akaelekea chumbani kwake “Abu kuna nini alikuwa anakwambia Yule mwanadada wa mapokezi?akauliza Najma ambaye alimuacha Mathew akizungumza na muhudumu wa mapokezi akaelekea chumbani. “Alikuwa ananipa taarifa kwamba kuna mtu alikuja kunitafuta” akasema Mathew “Nani huyo aliyekuja kukutafuta? Hakutaja jina lake? Kuna mtu unafahamiana naye hapa? “Hakutaja jina lake.Nashangaa kwa kuwa hakuna mtu anayetufahamu huku ugenini.Tutamfahamu mtu huyo kwani aliahidi kurudi tena baadae” akasema Mathew kisha wakaoga na kwenda kupata chakula cha mchana. Kwa muda wa miezi mitatu Mathew na mpenzi wake Najma wamekuwa katika mapumziko wakizunguka sehemu mbali mbali duniani kutalii.Baada ya kurejea kutoka Dar es salaam ambako alifanikiwa kumuua james Kasai na Khalid Sultan Khalid,Habiba Jawad kwa kufurahishwa na kazi aliyoifanya Mathew alimtaka yeye na Najma wakazunguke sehemu mbali mbali duniani kwa muda wa miezi minne ili kuweka akili sawa kabla ya kuingia katika misheni nyingine.Kwa kipindi cha miezi mitatu Mathew na Najma wamekuwa wakizunguka sehemu mbali mbali duniani wakifanya utalii.Walifika sehemu nyingi maarufu kwa utalii duniani na siku tatu zilizopita walifika katika kisiwa cha Fiji wakiendelea na mapumziko yao.Kwa muda huo wa miezi mitatu Mathew Mulumbi alijitahidi kujiweka mbali na runinga au simu.Hakutaka kutazama au kusikia kitu ambacho kingeweza kuharibu mapumziko yao. Baada ya kupata chakula walirejea chumbani kwao kupumzika kabla ya jioni ya siku ile kwenda katika matembezi ya miguu ufukweni. Saa moja za jioni walirejea hotelini ndipo walipokutana na Yule mtu aliyekuwa akiwatafuta.Ni mmoja kati ya walinzi wa Habiba Jawad wakamkaribisha katika chumba chao kikubwa “Tulijiuliza sana tulipoambiwa kuna mtu amekuja kutuulizia kwani hatuna mtu tunayefahamiana naye hapa Fiji” akasema Mathew “Hata mimi nilijua mtastuka na sikutaka kutaja jina langu makusudi ili kuwastua” akasema Malik na wote wakaangua kicheko.Chakula kikaletwa wakala na maongezi rasmi yakaanza “Abu Zalawi nimetumwa na mama Habiba anawahitaji mrejee nyumbani.Amenituma niwaombe samahani kwa kukatisha mapumziko yenu” akasema Malik “Kuna tatizo ganinyumbani?akauliza Najma “Hakuna tatizo lolote lakini amenituma hivyo” akasema Malik “Kama hakuna tatizo kwa nini mama anatusumbua katika mapumziko yetu?akauliza Najma “Hajatusumbua kwani tumekuwa na mapumziko marefu sana.Kwa miezi mitatu tumekuwa angani na majini tukistarehe.Ni wakati wa kurejea nyumbani” akasema Mathew “Tunaondoka usiku huu.Ndege iko tayari uwanja wa ndege wa Nadi kwa ajili ya kuelekea Saudi Arabia”akasema Malik.Hakukuwa na muda wa kupoteza Mathew na Najma wakaanza kujiandaa kwa ajili ya kurejea Saudi Arabia japo Najma hakuonekana kufurahia kuondoka mapema kisiwani Fiji.





Saa saba za mchana siku iliyofuata ndege ya akina Mathew iliwasili Riyadh Saudi Arabia.Ilikuwa ni furaha kwa kila mmoja wao kuwaona tena Mathew na Najma.Baada ya kuoga walikwenda kujumuika katika chakula cha mchana pamoja na Habiba Jawad kisha wakaenda kupumzika kutokana na uchovu wa safari kwani walitembea angani kwa takribani saa kumi na sita kutoka kisiwa cha Fiji hadi Riyadh Saa moja za jioni walikutana nyumbani kwa Habiba kwa chakula cha jioni alichokiandaa kwa ajili yao.Walizungumza mengi kuhusiana na miezi mitatu ya kuzunguka sehemu mbali mbali duniani.Baada ya kumaliza kula chakula Habiba akamuomba Najma akapumzike na amuache Mathew alikuwa na mazungumzo naye.Habiba akamchukua Mathew wakaelekea katika chumba chake maalum kwa mazungumzo “Mathew mtanisamehe sana kwa kukatisha mapumziko yenu” akaanzisha maongezi Habiba “Usijali mama tumepumzika vya kutosha sana.Vipi maendeleo yako? Akauliza Mathew “Hilo ni mojawapo ya mambo yaliyopelekea nikawarudisha nyumbani” akasema Habiba na kunyamaza kidogo “Mathew kama nilivyokueleza wakati ule nilipokutuma Dar es salaam kwamba sina muda mrefu sana wa kuishi na sasa ninazidi kuelekea ukingoni” akasema Habiba “Mama unaniogopesha ukisema hivyo.Unaonekana una afya njema kabisa.Huonekani kama ni mtu ambaye unahesabu siku” akasema Mathew na Habiba akacheka kidogo “Sitaki kukuogopesha Mathew Mulumbi lakini ninaelekea ukingoni.Sina muda mwingi sana kutoka sasa” “Nini kinakusumbua mama? “Tuyaweke hayo pembeni kwa muda lakini narudia tena kukusisitiza kwamba hii ni siri kubwa na nimechagua wewe uifahamu kwa kuwa ninakuamini” akasema Habiba “Ahsante sana mama kwa kuniamini na kunishirikisha katika jambo hili kubwa.Ninakuahidi kwamba sintamweleza mtu mwingine yeyote” akasema Mathew “Nafurahi kusikia hivyo” akasema Habiba na kunyamaza kwa sekunde chache halafu akasema “Mkiwa mapumzikoni kuna mambo yametokea ambayo naamini hujayasikia bado” akasema Habiba “Ni kweli mama nikiwa mapumzikoni sikutaka kutazama runinga au kuwasiliana kwa simu.Sikutaka kuvuruga mapumziko yetu” akasema Mathew “Kuna mambo yametokea Afrika mashariki.Rais wa Uganda Jenerali Akiki Rwamirama alipinduliwa na jeshi” “Jenerali Akiki amepinduliwa?! Mathew akashangaa “Ndiyo amepinduliwa na jeshi” “Anastahili kupinduliwa.Hafai kuongoza nchi”akasema Mathew “Inakaribia miezi mitatu toka jeshi la Uganda lilipofanya mapinduzi hayo na hali ilikuwa shwari kabisa lakini siku chache zilizopita yameibuka machafuko makubwa sana yaliyoanzia Uganda na kusambaa katika nchi nyingine za Tanzania na Kenya.Kumekuwa na umwagaji mkubwa wa damu na inahofiwa yanaweza tena kutokea mauaji mengine kama yale yaliyotokea Rwanda mwaka 1994” akasema Habiba. “Nini kimesababisha machafuko hayo? Yameibuka makundi ya waasi? Mathew akauliza “Haya ni machafuko ya kidini.Waumini wa dini za kikristu na kiislamu wanashambuliana na kuuana” akasema Habiba “Machafuko ya dini yamefika hadi Tanzania? Akauliza Mathew “Ndiyo.Machafuko hayo yamefika hadi Tanzania” “Hilo haliwezekani kwa Tanzania.Kwa miaka mingi waumini wa dini tofauti tumeishi kama ndugu.Ukifika Tanzania hutajua dini ya mtu kwani wote tu ndugu moja.Nini kimetokea leo hadi ndugu wafarakane na kuanza kuuana? Akauliza Mathew “Jambo hili lilianza kama mzaha.Aliuawa kiongozi mmoja wa dini na upande ambao kiongozi wao aliuawa walianza kulipiza kisasi kwa wenzao na hadi sasa machafuko hayo yamekuwa makubwa na vyombo vya usalama vimeshindwa kuyadhibiti.Kuna kila dalili kwamba machafuko haya ya kidini yanaweza kuenea katika sehemu nyingine za bara la Afrika na kama yasipodhibitiwa mapema yanaweza yakasambaa dunia nzima.Tayari Marekani imekwisha peleka vikosi vya jeshi Afrika Mashariki katika jitihada za kujaribu kuzuia machafuko hayo yasiendelee kusambaa” akasema Habiba “Mama Habiba bado sijapata picha nini sababu ya machafuko hayo? Kwa ninavyowafahamu watanzania ni vigumu mno kuingia katika vita ya kidini.Tumeishi kwa miaka mingi kama ndugu moja na kila pale kunapotokea mivutano ya kidini humalizwa kwa mazungumzo kati ya viongozi wa dini.Nini kimetokea leo wakaacha utamaduni ule wa kukaa meza moja wakazungumza na kuanza kushambuliana? Akajiuliza Mathew “Mathew kinachoendelea http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Afrika mashariki ni zaidi ya mapigano ya kidini.Yalianza mapigano ya makundi ya waumini wa dini na sasa yameibuka tena makundi mengine ya makabila,makundi ya kisiasa n.k.Suala hili limezidi kuwa pana zaidi kila uchao” “Serikali za Afrika Mashariki zimefanya juhudi gani katika kumaliza vurugu hizo?akauliza Mathew “Mathew machafuko ya kidini ni mabaya sana na kila siku yanaongezeka ukubwa na nguvu yake kama kimbunga.Majeshi yamelazimika kutumia nguvu kubwa na kilichotokea ni watu wengi kuuawa.Kwa ujumla hali ni mbaya sana Afrika Mashariki” akasema Habiba “Ruby,Gosu Gosu,Austin.Wako salama kweli?akajiuliza Mathew “Tuliweke na hilo pembeni nilitaka tu ufahamu kinachoendelea nyumbani.Kubwa zaidi nililokuitia hapa ni kwamba kesho alfajiri tunasafiri mimi na wewe tunakwenda Marekani” “Marekani?! Mathew akashangaa “Ndiyo.Mbona umeshangaa? “Nini tunakwenda kufanya huko? Akauliza Mathew “Tunakwenda kuonana na wakuu wa IS” “Wakuu wa IS wako Marekani? Akauliza Mathew na Habiba akatabasamu “Mathew niliwahi kukwambia kwamba kuna mengi bado huyafahamu unatakiwa ujifunze.Nitakueleza kidogo.” Akasema Habiba na kunyamaza kidogo halafu akasema “Kundi la IS lilianzishwa na Marekani kama chombo cha kuwasaidia kuvamia nchi za kiarabu zenye utajiri wa mafuta na vile vile kuidhibiti nchi ya Iran isiweze kuwa taifa lenye nguvu zaidi katika eneo la Mashariki ya kati.Usishangae kusikia kwamba kundi la IS limeanzishwa na Marekani.Yawezekana hufahamu lakini Mwaka 197o shirika la ujasusi la marekani CIA lilikitumia kikundi cha Muslim Brotherhood cha Misri katika kuzuia Urusi isieneze sera zake katika nchi za kiarabu.Marekani pia waliunga mkono kundi la Sarekat dhidi ya Surkano nchini Indonesia,vile vile waliunga mkono kikundi cha Jamaat e Islami dhidi ya Zulfiqar Ali Bhutto nchini Pakistan.Hii ni historia fupi nimekupa utambue kwamba Marekani wamekuwa wakivisaidia vikundi vinavyojihusiana na ugaidi pale inapolazimika kwa ajili ya maslahi yao.Tukiweka pembeni makundi hayo niliyokutajia tuje katika kundi la IS.Hili kundi ni zao la Marekani kama nilivyokueleza ambao wanatumia kundi hili kuvamia nchi maadui wa Marekani katika eneo la Mashariki ya kati,kulitumia kama kigezo cha kuvamia kijeshi nchi hasa zile zenye utajiri mkubwa wa mafuta na ndani ya Marekani wanatumia kundi hili kama tishio kwa usalama wa nchi hivyo kuhalalisha udukuajiwa taarifa za wananchi kwa kigezo cha usalama. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifahamika kama mfadhili mkuu wa kundi la IS na makundi mengine ya kigaidi lakini ukweli ni kwamba mimi ni chombo tu kinachotumika katika ufadhili huo bali wafadhili wakuu ni Marekani.Umewahi kujiuliza kwa nini sikamatwi japo ninafadhili ugaidi? Ni kwa sababu mimi ninatumika tu kama chombo.Mume wangu alikuwa anafanya hivyo na alipofariki nilibeba mimi jukumu hilo.Wanaofahamu suala hili hata ndani ya Marekani ni watu wachache sana.Ninakwenda nawe kesho Marekani nataka ukajifunze kwani wewe ndiye utakayechukua mikoba baada yangu.Tutakaporejea safari hiyo nitakupa maelekezo nini kinafuata.Nadhani umenielewa Mathew.Ninakupa maelezo mafupi mafupi kukupa nafasi ya kujifunza.Jiandae kwa mambo makubwa yanayokuja huko mbeleni” akasema Habiba Jawad. Habiba alihitaji kupumzika hivyo hakutaka maongezi zaidi akamtaka Mathew naye akapumzike na kujiandaa kwa safari yao ya alfajiri. Mathew alirejea chumbani kwake lakini kichwa chake kilikuwa kimevurugika kabisa “Nina wasi wasi mkubwa na usalama wa Ruby kufuatia machafuko hayo makubwa yanayoendelea Afrika Mashariki.Ninatamani kumpigia simu lakini sitaki ajue mahala nilipo” akawaza Mathew “Abu kuna nini?Mbona sura yako imerudi tofauti na ulivyoondoka?Mama amekwambia nini?akauliza Najma “Kesho tuna safari.Ninasikitika kukuacha peke yako” Mathew akadanganya “Ouh mpenzi wangu kumbe ni hilo tu.Usipate taabu kwani mtarejea na utanikuta hapa ninakusubiri.Mama kakwambia mnakwenda wapi? “Tunakwenda Marekani.Safari ya kibiashara” “Mama anakuamini sana Abu Zalawi” akasema Najma na Mathew akachukua kitabu katika kabati lake akaitafuta namba ya simu ya Ruby akapiga lakini simu haikupatikana “Hii inazidi kunipa wasi wasi kama Ruby ni mzima.Natamani niondoke hata sasa hivi niende Tanzania kujua kama yuko salama.Ruby ninampenda kwa moyo wangu wote na nilimuahidi kurudi nyumbani kwa ajili yak…..” “Abu,huyu Ruby ni nani? Akauliza Najma.Mathew aliyekuwa ameelekeza macho ukutani akageuka na kustuka baada ya kumkuta Najma akiwa na kile kitabu chake ambacho ameandika mawasiliano ya watu mbali mbali “Ruby ni Rafiki yangu” akasema Mathew na kuchukua kile kitabu akakifungia kabatini. MPENZI MSOMAJI MAMBO YAMEANZA..USIACHE KUENDELEA NA SIMULIZI HII KATIKA SEHEMU YA PILI







DAR ES SALAAM – TANZANIA Mataifa mbali mbali duniani yaliendelea kutoa wito kwa makundi ya kidini yanayopigana kuacha mara moja na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuzuia umwagikaji mkubwa wa damu unaoendelea katika eneo la Afrika Mashariki .Vikosi vya majeshi ya ulinzi vya nchi za Afrika mashariki vikisaidiana na vikosi vya jeshi la Marekani viliendelea na juhudi za kudhibiti mapigano yale makubwa lakini pamoja na juhudi zao bado hali iliendelea kuwa mbaya.Mapigano yaliendelea kushika kasi kila uchao.Majengo mengi ya ibada na yale ya serikali pamoja na magari vilichomwa moto na makundi ya watu wanaopigana. Nchini Tanzania mawasiliano ya simu na inteneti vilizimwa ili kuzuia watu kuwasiliana na kuhamasishana kushiriki katika vurugu.Ni taasisi muhimu tu za serikali ndizo zilizoendelea kuwa na mawasiliano.Licha ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya simu,bado vurugu ziliendelea na kuilazimu serikali kuongeza ulinzi zaidi katika sehemu muhimu kama vile mahospitali,mitambo ya kuzalisha umeme,mitambo ya kusukuma na kusambaza maji,mabenki na vituo vya polisi ambako makundi ya watu walikuwa wakivamia na kupora silaha ambazo walizitumia katika mapigano. Saa tano na dakika kumi za usiku,Rais Dr Fabian alimaliza kikao na wakuu wa vyombo vya usalama kikao kilichoanza saa kumi na mbili za jioni.Kwa muda wa siku nzima Dr Fabian amekuwa akifanya kikao baada ya kingine katika kujaribu kutafuta suluhu ya machafuko yale.Baada ya kumaliza kikao na wakuu wale wa vyombo vya ulinzi na usalama akawa na mazungumo ya faragha na mkuu wa majeshi kwa takribani dakika arobaini na walipomaliza akataarifiwa kwamba wakuu wa idara ya SNSA walikuwa wanamsubiri kwa ajili ya kuzungumza naye.Rais akaelekeza wapelekwe nyumbani kwake ataenda kukutana nao huko kwani bado alikuwa na mazungumzo ya faragha na mkuu wa idara ya usalama wa taifa. Saa saba kasoro dakika tisa Rais akaingia sebuleni kwake ambako aliwakuta Ruby na Gosu Gosu wakimsubiri. “Samahani sana vijana wangu kwa kusubiri muda mrefu” akasema Dr Fabian “Usijali mheshimiwa Rais,tunaelewa uzito wa majukumu uliyonayo” akasema Ruby “Sikuwajumuisha katika kikao cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuwa idara yenu ni ya siri na kazi zake zinafanywa kwa usiri mkubwa hivyo msijisikie kutengwa” akasema Dr Fabian huku akilegeza tai yake “Tunaelewa mheshimiwa Rais” akajibu Ruby “Kama hamtajali naomba tukapate chakula kwani hivi mnionavyo sijala chakula toka nilipokunywa chai asubuhi” akasema Dr Fabian na kuongozana na akina Ruby katika chumba cha chakula. “Vijana wangu urais ni mgumu sana.Nawashangaa wale wanaong’ang’ania madarakani.Sijamaliza hata kipindi changu kimoja cha urais lakini tayari nimeanza kufikiria kutowania kuteuliwa tena kipindi cha pili.Urais ni mzigo mzito.Tazama hivi sasa nchi imeingia katika machafuko na watu wote wananitazama mimi.Nimeubeba mzigo mzito mabegani mwangu kana kwamba mimi ndiye niliyeanzisha hizi vurugu.Toka asubuhi sijapata hata nafasi ya kupumzika ni kikao baada ya kikao” akasema Dr Fabian “Pole sana mheshimiwa Rais.Ni kweli umebeba mzigo mzito sana” akasema Ruby “Tuachane na hayo.Mnaendeleaje upande wenu? Akauliza Dr Fabian “Tunashukuru Mungu tuko salama na tunashukuru pia miundo mbinu yetu pia iko salama.Jengo letu kuwa karibu na ikulu imesaidia sana kwa machafuko kutofika huku” akasema Ruby “Wafanyakazi wenu wote wako salama? Akauliza Rais “Ndiyo mheshmiwa Rais wote wako salama.Tumeweka kambi pale pale katika jengo letu na sote tuko hapo hadi pale hali ya amani itakapokuwa nzuri” akasema Ruby na ukimya mfupi ukapita “Jioni ya leo nimezungumza na Rais wa Marekani akanitaka tusitumie nguvu kubwa katika kutawanya makundi ya wanaopigana.Anadai idadi ya watu wanaouawa na vikosi vya ulinzi imekuwa kubwa hivyo kuchochea machafuko zaidi.Si yeye tu bali hata umoja wa ulaya umetaka hivyo” akasema Dr Fabian na kunyamaza akaendelea kula halafu akasema “Nawashangaa sana hawa viongozi wanaodai tusitumie nguvu kubwa.Yawezekana hawajawahi kukutana na machafuko kama haya ya kidini katika nchi zao ndiyo maana inakuwa rahisi kudai isitumike nguvu.Watu wanavamia majengo ya serikali,wanachoma majengo ya ibada,wanapora,wanaharibu magari,wanachoma makazi ya watu,wanaharibu miundo mbinu halafu tusitume nguvu kuwazuia?? Akauliza kwa ukali “Huu ni upuuzi mkubwa sana.Lazima tutumie nguvu kuzuia machafuko haya yasiendelee.Wanauawa watu wasio na hatia.Wanawake na watoto ndio wanaopata taabu kubwa katika machafuko haya.Tanzania tumezoea kupokea wakimbizi kutoka nchi nyingine lakini na sisi yametukuta,hatuna kwa kukimbilia.Tumeichezea amani yetu na sasa tunayaona madhara yake ! Naapa kuendelea kutumia nguvu kubwa kuhakikisha haya makundi yanayochafua amani yetu yanafutiliwa mbali ! akasema Dr Fabian na kuweka kijiko chini hakuwa tena na hamu ya kula chakula.Alizama katika mawazo “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Suala hili linanikosesha amani kabisa.Malizeni kula twende katika mazungumzo” akasema Dr Fabian.Ruby na Gosu Gosu walimaliza kula Dr Fabian akawachukua wakaenda katika chumba cha mapumziko “Ni saa tisa sasa mapambazuko yanakaribia.Toka mapambazuko ya jana sijafumba jicho na ninawataka ninyi wasaidizi wangu nanyi pia msifumbe macho yenu hadi pale tutakapohakikisha balaa hili limepita” akasema Dr Fabian halafu ukapita ukimya “Vijana wangu nimefurahi kuwaoneni tena mkiwa salama.Nataka kufahamu kile kinachoendelea ndani ya SNSA kwani toka zilipoanza vurugu sijapata wasaa wa kukaa nanyi tukazungumza yale yanayoendelea katika idara yenu.Vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuanzia jeshi polisi,jeshi la wananchi,zimamoto na vingine vyote mnavyovifahamu wamejielekeza katika kudhibiti vurugu lakini mpaka sasa hakujakuwa na mafanikio yoyote vurugu bado zimeshika kasi” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais idara yetu kama ilivyo jina lake haijihusishi sana na masuala ya udhibiti wa vurugu kwani hiyo ni kazi ya jeshi la polisi lakini katika suala hili sisi tumejikita zaidi katika kufahamu chanzo cha hizi vurugu ni nini au ni nani? Japo vurugu hizi zinatufanya tushindwe kufanikisha jukumu letu ipasavyo lakini kuna mambo kadhaa tumeyabaini.Katika uchunguzi wetu wa awali tumebaini kwamba vurugu hizi zinaweza kuwa ni zaidi ya tunavyofikiri.Yawezekana ikawa ni zaidi ya chuki za kidini” “Kwa nini unasema hivyo?Kuna kitu mmekigundua? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,kuna chembe chembe za siasa ndani ya vurugu hizi” akasema Ruby halafu akanyamaza kidogo “Muda mfupi baada ya mkuu wa jeshi la polisi kutoa tamko akiwa jijini Tanga kuwataka watu waendelee kuwa wavumilivu na kwamba serikali inayafanyia uchunguzi matukio yale ya mauaji ya viongozi wa dini yaliyokuwa yanaendelea jijini Tanga,katika ukurasa wake wa twitter Karim Abdallah ambaye anaongoza chama cha siasa cha TPD aliandika ujumbe akiwahimiza waumini wa dini ya kiislamu jijini Tanga kwenda kuwatafuta wale ambao anadai walimuua Sheikh mkuu wa mkoa wa Tanga.Ujumbe huo wa kichochezi haukukaa sana akaufuta lakini tayari watu wengi walikwisha usoma kwani Karim ana watu wengi wanaomfuatilia katika mitandao ya kijamii.Kwa mwanasiasa kama huyu kuandika ujumbe kama ule ambao una mlengo wa uchochezi inatupa wasiwasi na kutufanya tulione suala hili kama lina chembe chembe za siasa ndani yake.Ukichunguza katika vurugu hizi utaona kuna makundi yameibuka ambayo yanalenga katika kuharibu miundo mbinu muhimu vile vile kuvamia na kuharibu majengo ya taasisi za serikali”akasema Ruby na Dr Fabian akapandwa na hasira “Namfahamu Yule kijana ni mwanasiasa mchonganishi na amekuwa akiandika mara kadhaa jumbe za uongo na uchonganishi kati ya wananchi na serikali. Ruby kuna picha nimeanza kuipata kufuatia maelezo yako.Sikuwahi kuusoma huo ujumbe wa twitter aliouandika lakini naamini kabisa lazima Karim atakuwa na mahusiano na vurugu hizi.Kijana mshenzi sana Yule ! akasema kwa ukali Dr Fabian “Aliufuta ujumbe huo ndani ya muda mfupi tu lakini wengi tayari walikwisha usoma” akasema Ruby “Mmekwisha anza kumfanyia uchunguzi huyu jamaa??akauliza Dr Fabian akionekana kuwa na hasira kali “Mheshimiwa Rais kuna ugumu kidogo katika kulitekeleza hilo.Kwanza tumeshindwa kufuatilia mawasiliano yake yote kwani hakuna mawasiliano ya simu wala intaneti.Pili ni ugumu wa kumfuatilia nyendo zake kwani huko mitaani kumetapakaa vurugu na magari yanachomwa.Barabara nyingi zina vizuizi vya kuzuia magari hivyo tumepata ugumu katika kuifanya kazi yetu” akasema Ruby “Mngenieleza mapema ili niangalie namna ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yenu” akasema Dr Fabian “Ndiyo maana tuko hapa mheshimiwa Rais kuleta maombi yetu kwako” “Nini mnakihitaji Ruby?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kwa hivi sasa hakuna mawasiliano ya simu hapa nchini isipokuwa kwa ofisi nyeti za serikali.Pamoja na kuzima mawasiliano ya simu kwa lengo la kuzuia watu kuhamasishana kushiriki katika vurugu,lakini bado haijasaidia sana kwani bado vurugu zinaendelea.Tunashauri mawasiliano ya simu yarejeshwe kama kawaida” akasema Ruby na Dr Fabian akaonyesha mstuko kidogo “Turejeshe tena mawasiliano ya simu? Hali itakuwa mbaya zaidi kwani watu wanatumia simu kuwasiliana na kuhamasishana kushiriki katika vurugu na hili ndilo lilipelekea tukaamua kuzima mawasiliano yote ya simu na intaneti na hii itaendelea hivi hivi hadi pale vurugu zitakapokoma kwani tukirejesha mawasiliano tutaendelea kuongeza chuki na vurugu zitapamba moto ! Akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais pamoja na nia njema ya jambo hilo lakini kuna athari zake vile vile.Siku hizi watu wanategemea sana simu zao katika shughuli mbali mbali hivyo mkiwanyima fursa ya kutumia simu zao ni kuwafanya maisha yao yawe magumu zaidi hata hivyo sababu kubwa ambayo tunashauri mawasiliano ya simu yarejeshwe kama kawaida ni ili kuwafanya watu waone maisha yamerejea kawaida wataamini kwamba hali ya amani imeanza kuboreka.Jambo lingine ni kwamba mamilioni ya watanzania sasa wanamiliki simu janja.Tutazitumia simu hizo kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu umuhimu wa amani na kuepuka kushiriki katika vurugu zinazoendelea hivi sasa.Mheshimiwa Rais utalihutubia taifa na ili ujumbe wako uweze kuwafikia watu wengi zaidi na kwa haraka tutatumia teknolojia ili hotuba yako iweze kutazamwa na watu wote wenye simu janja zao kwa mara moja”akasema Ruby “Inawezekana? akauliza Dr Fabian “Ndiyo mheshimiwa Rais inawezekana.Simu janja zote ambazo zitakuwa zimewashwa muda huo zitapokea hotuba yako moja kwa moja bila mmiliki kujiunga sehemu yoyote.Kwa mfano waweza kuwa unawasiliana na mtu Fulani au unafanya chochote katika simu basi kila kitu kitasimama kwa muda na mtumiaji ataunganishwa moja kwa moja na hotuba ya Rais.Pale hotuba itakapokuwa imemalizika basi mawasiliano yao yataendelea kama kawaida na ujumbe utakuwa umewafikia karibu nusu ya nchi na hii inaweza ikasaidia sana kuwafanya watu wakatafakari kuhusu hizi vurugu na inaweza ikasaidia zikapungua kama si kumalizika kabisa” akasema Ruby “Hilo ni wazo zuri Ruby.Sikuwa nimelifikiria kabisa” akasema Dr Fabian “Hilo linawezekana mheshimiwa Rais na itatusaidia hata sisi kupata nafasi nzuri ya kumfuatilia Karim kujua mienendo yake na kufahamu mahala alipona tutamchukua ili atueleze alichomaanisha katika ule ujumbe wake wa uchochezi” akasema Ruby “Nimekuelewa Ruby na ahsante sana kwa wazo hili nitalifanyia kazi.Hilo jambo litatekelezwa kesho.” akasema Dr Fabian “Baada ya hotuba yako hiyo unaweza ukawatafuta viongozi wa dini mkakaa meza moja kulijadili suala hili na mnaweza kujikuta mmepata muafaka kwani chanzo cha vurugu zote ni masuala ya kiimani” akasema Ruby “Kuhusu hilo la kukutana na viongozi wa dini nilikuwa nafikiria kuwakamata viongozi wote wakuu wa dini na kuwafungia sehemu moja niwaache wazungumze hadi muafaka upatikane.Tukifaulu kudhibiti makundi ya dini tutakuwa tumelimaliza suala hili kwani hayo makundi mengine ya waporaji yanajikinga na mwavuli wa machafuko ya kidini” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais sidhani kama hiyo ni njia nzuri kwa sasa.Kuwakamata viongozi hao wa dini kwa sasa itakuwa ni kuongeza mafuta kwenye moto kwani chanzo cha vurugu hizo ni kuuawa kwa viongozi wa kidini hivyo viongozi wengine wakikamatwa hata kama ni kwa nia njema basi vurugu hizi zitaongezeka mara mbili” akasema Ruby “Ruby hawa viongozi wanaweza wakawa na mchango mkubwa sana katika kutafuta suluhu ya vurugu hizi.Umekuwa ni utamaduni wetu kukaa mezani kuzungumza kila pale kunapokuwa na tofauti zozote za kiimani naamini hata sasa kama wakikaa pamoja basi wanaweza wakazungumza wanaweza wakafikia makubaliano na wakazungumza na waumini wao kuwasihi waache vurugu” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,nasema haitakuwa rahisi kwa viongozi hao wa dini kuwa na maelewano hasa ukiangalia chanzo cha vurugu hizi.Ukiangalia namna vurugu hizi zilivyoanza hapa kwetu Tanzania ,aliuawa kiongozi mmoja wa kanisa na waumini wake kadhaa,usiku wa siku hiyo hiyo akauawa sheikh mkuu wa mkoa wa Tanga na hii ilipeleka kila upande kulaumu watu wa imani nyingine kuhusika katika mauaji yale ya viongozi na vurugu zikaanzia hapo.Mbegu mbaya ya chuki tayari imekwisha pandwa miongoni mwa waumini na viongozi wao wa dini,kila upande ukiwachukia wengine.Hata ukiwaweka pamoja kila upande utalaumu upande mwingine kwamba ndio chanzo cha vurugu.Njia pekee ya kulitatua suala hili ni kutafuta chanzo cha vurugu ni nini au ni nani? Tunatakiwa kufahamu nani waliomuua yule kiongozi wa kanisa na waliomuua Sheikh mkuu wa Tanga? Tukifanikiwa kuwafahamu watu hao basi tunaweza kupata mwanga wa vurugu hizi na hata ukiwakutanisha viongozi wa dini na ukawaeleza kuhusiana na hiki tunachokifanya wanaweza wakaelewa” akasema Ruby “Papo hapo tusisahau kwamba vurugu hizi zilianza Uganda na kuenea Tanzania hadi Kenya.Tukitaka kupata kiini cha vurugu hizi tuanze kuchunguza namna zilivyoanza nchini Uganda.Huu ni kama ugonjwa ambao umeibuka Uganda ukaingia Tanzania na Kenya na kama hakutakuwa na tiba ya haraka basi ugonjwa huu unaweza ukasambaa Afrika nzima” akasema Gosu Gosu “Uko sahihi Gosu Gosu.Hali hii lazima idhibitiwe kwa gharama zozote.Hatuwezi kuacha hali hii ikaendelea.Nchi imesimama kutokana na vurugu hizi ambazo ni kubwa hadi kushindwa kudhibitiwa na vikosi vyetu vya ulinzi.Wamekuja wanajeshi wa Marekani lakini bado hawatoshi.Vurugu ni kubwa” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa rais kwa nini Marekani imetuma wanajeshi wake Afrika mashariki? Uliomba msaada kwao? akauliza Ruby “Sikuomba msaada wowote kutoka Marekani.Rais wa Marekani alilazimika kutuma wanajeshi kwa ajili ya kusaidia kuimarisha hali ya amani vile vile kulinda raia wa Marekani na wa nchi nyingine za kigeni waliokwama Afrika mashariki vile vile kulinda balozi zake.Kama mnavyojua ubalozi wa Marekani nchini Uganda ulichomwa moto na watu katika vurugu hizi zinazoendelea hivyo wamechukua tahadhari katika balozi zao nyingine za Dar es salaam na Nairobi.Vile vile wanatusaidia katika ulinzi wa miundo mbinu muhimu kama vile bandari.Wameleta meli za kijeshi katika bandari za Dar es salaam na Tanga ambazo zinasaidia katika ulinzi wa bandari hizo.Huu ni msaada mkubwa wametupa” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,kubwa lililotuleta kwako ni hilo tulilokueleza kwamba mawasiliano ya simu yarejee kama kawaida ili kutuwezesha kufanya shughuli zetu kwa wepesi zaidi” akasema Ruby “Hilo litafanyiwa kazi kesho msihofu lakini hakikisheni huyu kijana Karim anapatikana tena ikiwezekana achukuliwe ahifadhiwe katika moja ya nyumba zetu ateswe sana hadi aeleze alimaanisha nini kuhusiana na ujumbe huo wa kichochezi aliouandika katika ukurasa wake wa twitter.Nataka huu uwe ni mwisho wa Karim ! akafoka DrFabian “Tunalifanyia kazi hilo mheshimiwa Rais na tutafahamu kila kitu” akasema Ruby na kumtazama Gosu Gosu “Mheshimiwa Rais umechoka sana naomba tukuache upumzike hata kidogo kwani inakaribia saa kumi na moja za alfajiri sasa” akasema Ruby “Nitawezaje kulala wakati wananchi wangu hawajalala wanakesha kwa hofu na wengine wakiishi katika makambi kama wakimbizi ndani ya nchi yao kwa hofu ya usalama wao?Nitalala pale ambapo vurugu zitakoma.Kwa hivi sasa ninakwenda kuzungumza na Rais wa China katika simu.Nawashukuruni sana kwa mawazo mazuri mliyonipa.Nadhani hata wasaidizi wangu nao pia wamechanganyikiwa na haya yanayoendelea ndiyo maana hakuna hata mmoja wao aliyenipa ushauri kama huu mlionipa ninyi.Nendeni mkaendelee na kazi muhakikishe watu wenu wote wanakuwa salama na vile vile muhakikishe mnawapata walioanzisha vurugu hizi” akasema Dr Fabian akaagana na akina Ruby wakaondoka kurejea katika jengo la ofisi yao ambalo halikuwa mbali na Ikulu.Toka vurugu zilipoanza,karibu wafanyakazi wote wa SNSA waliweka kambi hapo katika jengo la ofisi yao kwa ajili ya usalama wao. “Gosu Gosu tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha tunapata kiini cha vurugu hizi.Naamini hazikuibuka hivi hivi lazima wapo waliozianzisha.Ni akina nani na nini lengo lao? Hayo ndiyo maswali ambayo tunahitaji kuyatafutia majawabu” akasema Ruby “Nyakati kama hizi ndipo humkumbuka sana Mathew Mulumbi.Naamini huko aliko anaona kile kinachoendelea hapa nchini.I miss him so much” akasema Gosu Gosu. “Are you scared Papii?akauliza Ruby “I’m not scared.Mimi ni mwanajeshi toka nikiwa mdogo nimeishi katikati ya mapigano makubwa hivyo sijawahi ogopa hata mara moja na sintoogopa kamwe” akasema Gosu Gosu “Good.Mathew hayupo na jukumu hili ni letu.Tutamshirikisha pia Austin pale itakapolazimu.Tuna kazi kubwa ya kuhakikisha tunauchimba mzizi wa machafuko haya” akasema Ruby na ukimya mfupi ukapita halafu Gosu Gosu akasema “Ruby kuna kitu nataka kuuliza naomba tafadhali uwe mkweli” akasema Gosu Gosu “Siku zote nimekuwa mkweli kwako.Uliza nitakujibu” “Ni kuhusu Mathew.Wewe ndiye ulikuwa mtu wa mwisho kuonana naye.Unafahamu mahala alipo? akauliza Gosu Gosu.Ruby hakujibu akaendelea kuendesha gari.Usiku huu hakuwa na dereva yeye ndiye aliyeshika usukani. “Nijibu Ruby.Unafahamu mahala alipo? “Kwa nini unahitaji kujua Gosu Gosu? “Mathew ni kaka yangu,ni mtu wangu wa karibu.Nilipofumbua macho na kumuona sikuamini macho yangu kama kweli ni yeye.Nilidhani labda ni mzimu ninauona.Kumbe siku zote hisia zangu kwamba hakuwa amefariki ni za kweli.Kwa bahati mbaya nilipata muda mfupi sana wa kuwa naye kisha akatoweka tena na sijafahamu alikuwa wapi,nini kilimtokea na amekwenda wapi.Nahitaji kufahamu kama kuna chochote alikwambia” akasema Gosu Gosu.Zikapita dakika mbili Ruby akasema “Alinieleza kwa ufupi sana kuhusiana na mambo aliyoyapitia.Aliniambia kwamba alitekwa na Mossad na amepitia mateso mengi sana.Ukimtazama mgongo wake wote umejaa makovu mengi ukionyesha namna alivyopitia mateso makali.Alikuwa makini sana katika kueleza mahala alipokuwa.Kuhusu mahala alipo sasa sifahamu na alinitaka atakapoondoka nisimtafute ila aliweka ahadi kwamba atarejea tena”akasema Ruby “Hakukueleza anakwenda wapi? Akauliza Gosu Gosu “Hapana hakunieleza na alinitaka nisijaribu kumtafuta lakini…….” Akasema Ruby na kunyamaza kidogo “Kuna nini Ruby? “Kuna kitu nilikigundua” akasema Ruby na kunyamaza tena. “Katika kipindi chote alichorejea nilikuwa naye na niligundua kuna mtu alikuwa anawasiliana naye na kumpa taarifa mbali mbali kuhusiana na operesheni ile iliyomalizika ya kumuua James Kasai” “Alikuwa akiwasiliana na mtu? akauliza Gosu Gosu. “Ndiyo kuna mtu alikuwa anawasiliana naye” “Hukufanya uchunguzi kujua alikuwa anawasiliana nani?akauliza Gosu Gosu “Hapana sikuchunguza.Mathew hapendi kuchunguzwa.Mtu huyo alikuwa anawasiliana naye usiku tu na alikuwa anawasiliana naye akiwa amejifungia ofisini kwake hii ina maana kwamba hakutaka mimi au mtu yeyote kufahamu kuhusu mawasiliano yao na mimi sikutaka kuchunguza.Kila alipotoka kuwasiliana na mtu huyo alikuwa anakuja na taarifa mpya.Mathew ana siri kubwa sana anatembea nayo.Tufuate vile alivyoelekeza na muda utakapofika atarejea na atatuweka wazi nini kinaendelea katika maisha yake.Sisi ni ndugu zake na hataweza kutuficha kitu” akasema Ruby “Sawa Ruby nimekuelewa.Ahsante sana kwa kuwa muwazi” akasema Gosu Gosu “Naamini umeridhika kwa haya niliyokueleza.Tunalifunga suala la Mathew hadi pale tutakaposikia chochote kutoka kwake kwa sasa tujielekeze katika kuuchimba mzizi wa hizi vurugu zinazoendelea” akasema Ruby. Walifika katika jengo la ofisi yao kuu.Ni watu wachache tu waliokuwa ofisini alfajiri hiyo wengi walikuwa katika mahema yaliyotengenezwa kwa ajili yao pembeni ya jengo la ofisi. “Gosu Gosu tutumie muda huu mfupi uliosalia kabla ya mapambazuko tupumzike kwani tutakuwa na ratiba ndefu sana siku ya leo” akasema Ruby na kila mmoja akaelekea katika sehemu yake ya kulala WASHINGTON DC – MAREKANI Ni saa tatu za usiku jijni Washington DC Marekani.Katika ikulu ya Marekani Rais William Washington na makamu wake Mark Piller walimaliza kutazama hotuba ya Rais Armen Hijazi wa Iran.Ni hotuba iliyosubiriwa kwa hamu duniani,wengi wakitaka kusikia msimamo wa Iran kuhusiana na matamshi ya rais wa Marekani William Washington kwamba atalifuta taifa la Iran.Katika hotuba yake hiyo ya kumjibu William Washington,Rais Armen Hijazi aliionya vikali Marekani kutothubutu kwa namna yoyote ile kuvamia ardhi ya Iran kwani watakachokipata kitaingia katika historia ya dunia.Kama haitoshi Rais Armen alimtaka Rais wa Marekani kufuta kauli yake kwamba atalifuta taifa la Iran kwani kauli yake hiyo ingeweza kumrudia yeye na taifa lake.Ilikuwa ni moja ya hotuba iliyoleta hofu kubwa kwa Marekani na dunia wakihofia kuzuka kwa vita kubwa kwani Rais Armen aliweka wazi kwamba nchi yake iko tayari kwa vita na Marekani na alisistiza kwamba wataishambulia Marekani pamoja na washirika wake watakaoisaidia na alitishia kwamba baada ya vita hiyo Marekani haitakuwa sawa tena na itachukua zaidi ya miaka hamsini kuijenga tena Marekani.Katika kumalizia hotuba yake Rais Armen aliweka wazi mipango ya Iran ya kuendelea na urutubishaji wa madini ya Urani. “Huu ni upuuzi mkubwa sana ! akafoka Rais William baada ya hotuba ile kumalizika “Siwezi kuvumilia upuuzi kama huu.Armen hawezi kututamkia maneno kama haya sisi ! akaendelea kufoka William. “Mheshimiwa Rais haya maneno yote aliyoyazungumza Armen ni upuuzi na ni maneno ya mtu aliyeshindwa.Iran haina uwezo wowote wa kuipiga Marekani”akasema Mark Piller “Siwezi kuvumilia ujinga wa namna hii.Marekani ni taifa kubwa na hatuwezi kukubali taifa kama Iran kututolea vitisho vya namna hii.Ninaapa lazima niishikishe adabu Iran ! akaendelea kufoka William ambaye ni mwepesi sana wa kupandwa na hasira “Mheshimiwa Rais hiki alichokisema Armen kisikukoseshe amani.Hakuna anachoweza kufanya kwetu.Haya matamshi yake aliyoyatoa leo dhidi yetu hayatabadili mipango yetu dhidi ya taifa hilo lakini nashauri mheshimiwa Rais huyu mtu tumuendee taratibu” akasema Mark Piller “Kiburi alichokionyesha Armen hakiwezi kuvumilika.Ameongea kwa kujitapa kabisa kwamba nchi yake itaendelea na urutubishaji wa madini ya Urani.Hatuwezi kuiacha Iran ikaendelea na zoezi hili la urutubishaji wa madini ya Urani.Lazima tuchukue hatua kali sana dhidi ya taifa hilo ! akaendelea kufoka William Washington “Mheshimiwa Rais suala hili si jepesi na tunahitaji umakini mkubwa sana katika kulishughulikia.Armen ni Rais mjanja sana.Ametoa matamshi yale akitegemea kwamba Marekani lazima itahamaki na kuanza haraka kuchukua hatua.Lazima tuwe makini naye sana.Tumuonyeshe Arman kwamba sisi ni taifa kubwa na hatukurupuki”akaksema Mark Piller “Mark hatuna muda wa kumbembeleza huyu mtu.Uvumilivu wangu umefika ukomo.Kinachofuata ni kumtandika vikali,kuharibu vinu vyake vya nyuklia na kumuondoa madarakani rais Armen ! akasema William “Mheshimiwa Rais,ni mapema sana kufikia hatua hiyo” akasema Mark lakini William aliyekuwa amewaka hasira akamgeukia akamtazama kwa macho makali na kusema “Unataka huyu mtu aendelee kutoa vitsho kwa Marekani? Unadhani ni hofu ya namnagani wameipata watu wetu kufuatia matamshi yake ya kuivuruga Marekani? Katu hatuwezi kuwaacha wananchi wetu waendelee kuishi kwa hofu ya vitisho vya Iran.Hawatatuelewa tutakaposhindwa kuchukua hatua zozote za kuwalinda.Msuguano huu na Iran umechukua muda mrefu na sasa umefika wakati wa kuumaliza.Niamini Mark ninakwenda kulimaliza suala hili .Siwezi kuipa nafasi Iran ya kuendelea kuruubisha madini ya Uran.Iran ikifanikiwa kutengeneza bomu la nyuklia hatutaweza kumdhibii tena na eneo lote la Mashariki ya kati litaingia katika hofu kubwa.Lazima tuwahi angali mapema na njia pekee ni kuitandika kijeshi” akasema William “Mheshimiwa Rais msuguano huu wa Marekani na Iran umechukua muda mrefu kwa sababu mpaka sasa hatufahamu Iran anamiliki silaha za namna gani.Mpaka sasa hatufahamu kwa nini Iran inakuwa na kiburi cha kutunishiana misuli ya kijeshi na Marekani.Hakuna taifa katika zama hizi ambalo limewahi kutamka kuishambulia Marekani zaidi ya Iran.Lazima kuna kitu kinaipa kiburi Iran cha kuwa tayari kuingia vitani na Marekani hata kesho.Nimekuwa katika shirika la ujasusi CIA kwa muda mrefu na tumekuwa tukihangaika kujua Iran ina silaha gani kali lakini mpaka leo hatujafanikiwa kujua Iran anamiliki silaha gani.Iran wamekuwa wakidai kwamba wana makombora ya masafa marefu na wametishia kushambulia nchi zote washirika wa Marekani katika Mashariki ya kati ikiwemo Israel.Mpaka sasa hatuna uhakika kama hiki wanachokisema ni cha kweli ndiyo maana nasema kwamba hatuwezi kukurupka katika suala hili.Tunao uwezo wa kumtandika Iran lakini ni vipi kama madai yake ya umiiki wa silaha kali ni ya kweli.Vile vile tukiivamia Iran kijeshi tutakuwa tumeanzisha mgogoro mwingine kwani Iran na Urusi wana urafiki mkubwa na wamekuwa wakisaidiana kijeshi.Hatutapigana vita na Iran pekee bali tutakuwa vitani na Urusi pia.Usisahau vile vile kwamba hivi karibuni Rais wa Iran alifanya ziara nchini China na mahusiano ya Iran na China yameanza kuboreka hivyo nchi hizi lazima zitamuunga mkono Iran kama tutaishambulia kijeshi.Tazama namna Iran na Urusi walivyoshirikiana kuiunga mkono serikali ya Syria hadi kuiwezesha kukomboa asilimia zaidi ya tisini ya maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na waasi ambao tulikuwa tunawaunga mkono.Suala hili ni pana sana mheshimiwa Rais na inahitaji busara kubwa na mikakati mizito katika kulishughulikia” akasema Mark Piller “Mark kauli yako ni uoga.Siogopi kuipeleka nchi vitani ili kuisambaratisha Iran.Marekani si taifa la kutolewa vitisho na taifa dogo na dhaifu kama Iran ! “Mheshimiwa Rais ninazungumza kama kachero mbobezi.Kabla ya kufanya maamuzi yoyote tunahitaji kwanza kujiridhisha kuhusu uwezo wa Iran kijeshi na aina ya silaha ilizonazo.Tunahitaji kujiridhisha kuhusu madai hayo ya Iran kuwa na makombora ya masafa marefu.Tunahitaji kujiridhisha kuhusu uwezo wake wa kutengeneza bomu la nyuklia.Tunahit………” “Mark Piller ! akasema Rais William na kumkatisha Mark “Umefanya kazi CIA karibu nusu ya umri wako na kwa muda huo wote mmekuwa mkihangaika kupata taarifa kuhusu mfumo wa makombora na silaha za Iran bila mafanikio.Itapita miaka mingapi ili tuweze kupata taarifa hizo za silaha za Iran? Kama marais waliopita walivumilia mimi sina uvumilivu huo.Nataka nilimalize suala hili.Iran awe na makombora makubwa au madogo lazima atandikwe ! akaendelea kusisitiza William “Mheshimiwa Rais kuna jambo muhimu naomba nikueleze” akasema Mark Piller “Mark tunazungumzia suala la Iran na tutakapomaliza ndipo utanieleza hilo unalotaka kunieleza.Nataka mimi na wewe tufike muafaka kwanza kuhusu suala hili la Iran kabla sijaomba ridhaa ya bunge ! “Mheshimiwa Rais ninachotaka kukwambia ni kuhusiana na suala hilo hilo la Iran” akasema Mark na Rais William aliyekuwa amesimama akaketi “Nini unataka kunieleza? “Nimekuwa nikiandaa mpango wa siri wa namna tutakavyoweza kulishughulikia suala hili la Iran” akasema Mark “Unaandaa mpango wa siri ? Akauliza William akionekana kushangaa “Ndiyo mheshimiwa Rais.Sikuwahi kukwambia suala hilo kwani maandalizi yake hayakuwa yamekamilika lakini kwa hapa tulipofika inabidi nikueleze ukweli ili mimi nawe tuwe katika ukurasa mmoja.” “Nakusikiliza Mark” akasema William “Kabla ya kukueleza kuhusu mpango huo kuna jambo ambalo nataka ulifahamu ambalo naamini hulijui ila halitakufurahisha” “Nini unataka kunieleza Mark? Akauliza William.Ukapita ukimya mfupi Mark akitafakari namna ya kuanza kumweleza Rais kisha akasema “Kwa muda mrefu Marekani tumekuwa tunashirikiana na makundi kadhaa ya kigaidi katika mipango mbali mbali yenye maslahi kwa Marekani.Tumefanya hivyo katika nchi mbali mbali kama vile..” Mark akanyamaza baada ya Rais William kuhamaki “Kushirikiana na makundi ya kigaidi?akauliza William kwa mshangao “Ndiyo mheshimiwa Rais” akajibu Mark “Marekani haiwezi kushirikiana na magaidi hata siku moja.Tumekuwa vinara katika kupiga vita ugaidi duniani.Ni kwa juhudi hizo za kupamba na ugaidi tulifanikiwa kumuua Osama bin Laden kiongozi mkuu wa Alqaeda kundi la kigaidi lililokuwa hatari duniani.Tumeendelea pia kuvisambaratisha vikundi mbali mbali vya kigaidi sehemu mbali mbali duniani.Nashangaa unaponiambia kwamba Marekani tunashirikiana na magaidi ! “Mheshimiwa Rais, ni kweli tunashirikiana na makundi ya kigaidi lakini hili ni suala la ndani mno na la siri kubwa.Hata marais waliopo madarakani huwa hawafahamishwi jambo hili na hawapaswi kulifahamu.Kwa ufupi tu ni kwamba kuna kitengo maalum cha siri ndani ya CIA ambacho kinashughulikia mahusiano na mashirikiano na makundi ya kigaidi kwa maslahi ya Marekani.Kwa muda mrefu sasa Marekani tumekuwa tukivifadhili kwa pesa na silaha vikundi mbali mbali vya kigaidi ambavyo vimekuwa vikitekeleza mashambulio ya kigaidi sehemu mbali mbali duniani kwa maslahi ya Marekani” “Mungu wangu ! akasema William akimtazama Mark Piller kwa macho ya woga “Mheshimiwa Rais kama nilivyokueleza kwamba jambo hili ni la siri kubwa.Labda kwa kukupa mfano ni kwamba tumekuwa tukifadhili operesheni mbali mbali za kundi la kigaidi la IS sehemu mbali mbali duniani na moja kati ya operesheni ambazo tumetumia kundi la IS ni katika machafuko yanayoendelea Afrika Mashariki hivi sasa” akasema Mark na Rais William akasimama “Machafuko ya Afrika mashariki yameratibiwa na Marekani kwa kuwatumia IS?! Rais William akashangaa “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ni mipango ya Marekani” akasema Mark na Rais William akasimama akamtazama Mark kwa mshangao mkubwa “Mark naomba uniambie hiki unachonieleza si cha kweli” akasema William “Mheshimiwa Rais ninachokueleza ni ukweli mtupu na jambo hili lina maslahi makubwa kwa Marekani” akasema Mark “Mark watu wanakufa kama kuku Afrika Mashariki hadi tumelazimika kutuma vikosi vyetu kwenda kusaidia kurejesha amani.Dunia inashuhudia machafuko makubwa kabisa ya kidini kuwahi kutokea halafu unaniambia kwamba ni kwa maslahi ya Marekan…...” “Mheshimiwa Rais ! akasema Mark na kumkatisha Rais William. “Kinachoendelea hivi sasa Afrika Mashariki kina maslahi makubwa kwa Marekani.Tazama bei ya mafuta ilivyopanda katika soko la dunia baada ya nchi wazalishaji wa mafuta kuweka mgomo baridi na kuzalisha kiwango kidogo cha mafuta kuliko mahitaji ya dunia.Hii imepelekea akiba yetu ya mafuta kuanza kupungua na wakati huo huo tuna migogoro na nchi nyingi ambazo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani.Hatuna mahusiano mazuri na Venezuela,Mashirikiano yetu na Saudi Arabia yametetereka pia,Iran ambao nao ni wazalishaji wakubwa wa mafuta ni maadui zetu,Iraq pia hatupati mafuta ya kutosha kwani serikali iliyoko madarakani hivi sasa haitaki mashirikiano na Marekani.Nchi nyingine kama Urusi ambayo unafahamu mahusiano yetu nao.Nchi kamaLibya ambao wanashika nafasi ya tisa kwa akiba kubwa ya mafuta nako kumechafuka.Kwa ujumla mahusiano yetu na nchi wazalishaji wa mafuta duniani si mazuri na mafuta yetu hapa nchini hayatutoshi hivyo kwa namna yoyote ile tunahitaji kuongeza akiba yetu ya mafuta na Afrika Mashariki kuna kiasi kikubwa cha mafuta.Nchi ya Uganda inakadiriwa kuwa na mafuta mengi zaidi kuliko nchi zote katika bara la Afrika hivyo mipango yetu kuhakikisha tunapata mafuta kutoka Uganda” akasema Mark Piller “Mafuta? ! akauliza William kwa hasira “Mafuta yana thamani kuliko uhai wa watu ? Sikutegemea kabisa kama Mark unaweza ukashiriki katika jambo hili ovu ! akasikitika Rais William “Mheshimiwa Rais mafuta ni uchumi.Kuna mgomo baridi kwa wazalishaji wa mafuta duniani.Hizi ni njama za wapinzani wetu dhidi ya uchumi wetu.Lazima tutumie kila njia kupata mafuta ndiyo maana tumeyafuata Afrika Mashariki.Mheshimiwa Rais yawezekana haya tunayoyafanya yasionekana sawa lakini ni kwa ajili ya nchi yetu.Marekani lazima iendelee kuwa taifa kubwa lenye uchumi mkubwa kuzidi yote duniani hivyo kila aina ya mbinu lazima itumike katika kuhakikisha hilo linatimia” akasema Mark “Siamini kama ni wewe kweli Mark unayezungumza haya” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais,haya yote yanafanyika kwa maslahi ya Marek…….” “Hata kama ni kwa maslahi ya Marekani hatukupaswa kusababisha machafuko yale yanayoendelea Afrika mashariki.Ule ni unyama uliovuka mipaka ya ubinadamu.Maiti za watu zimesambaa mitaani huku sisi tukifaidika kwa mafuta ambayo Mungu amewajalia wenzetu.Hili haliwezekani na siwezi kulifumbia macho.Lazima nichukue hatua kalisana kwako na kwa wenzako wote mlioshirikiana kuandaa unyama wa namna hii Afrika Mashariki na kwingineko duniani ambako mmekwisha fanya !! akafoka William “Mheshimiwa Rais usithubutu kufanya chochote kuhusiana na jambo hili.Hukupaswa kulifahamu suala hili lakini kwa kuwa u mtu wangu wa karibu nimeamua kukueleza kile kinachoendelea lakini kwa kwaida Rais hapaswi kabisa kufahamu chochote kuhusiana na mambo haya nyeti mno kwa nchi” akasema Mark “Mark huwezi ukanipangia nini cha kufanya.Mimi ni Rais wa Marekani na nitafanya kila niwezalo kuhakikisha ninakisambaratisha kikundi hicho cha wauaji ndani ya CIA.Siwezi kukubali wakaendelea na haya wanayoyafanya ! “Mheshimiwa Rais narudia tena kukuonya usithubutu kufanya chochote.Utaendelea kuufunga mdomo wako kama vile hufahamu chochote kinachoendelea ! “Mtanifanya nini wewe na wenzako? Akauliza Rais William “Utauawa ! akasema Mark na ukimya ukapita.William Washington alionyesha woga kwa kauli ile ya makamu wake Mark Piller “Mheshimiwa Rais nakushauri fuata kile ninachokuelekeza.Ukienda kinyume chake basi sote maisha yetu yatakuwa hatarini” “Kwa nini umenieleza jambo hili Mark wakati ukifahamu kuwa sipaswi kujua chochote? Akauliza Rais William “Ni kwa sababu kuna mpango mkubwa unaoendelea kuhusu Iran ambao nataka uufahamu ili usiendelee na mipango yako ya kuivamia kijeshi Iran hadi mpango huo utakapokuwa umekamilika” “Mpango gani Mark?akauliza Rais William akionekana kuanza kupunguza hasira alizokuwa nazo “Nitakurejesha kwanza Afrika Mashariki.Mapinduzi yale yaliyofanywa na jeshi la Uganda yaliyomuondoa madarakani Rais Jenerali Akiki Rwamirama tuliyapanga sisi tukishirikiana na Rais wa Tanzania” “Tanzania pia walishiriki katika mapinduzi yale?! Akauliza Rais William “Kutokana na mashirikiano yetu na IS tuliweza kupata taarifa kuhusiana na mpango ulioshindwa kufanikiwa wa kuwaua marais wa Tanzania na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa bomu la kujitoa muhanga.Katika mpango huo Jenerali Akiki pia alishiriki.Baada ya kupata taarifa hizo nilimtuma mjumbe maalum kwa Rais wa Tanzania akazungumza naye kuhusu kumuondoa madarakani Rais Akiki kwani tuliamini lazima atakuwa na hasira naye na ndipo ukaandaliwa mpango wa mapinduzi” akasema Mark “Rais wa Tanzania naye alikubali yatokee haya yanaoendelea katika nchi yake? Ni rais wa namna gani huyu ambaye anakubali kuona raia wake wakiuana namna ile? Akauliza Rais William kwa ukali “Mpango wetu na Tanzania ulikuwa ni kumuondoa Jenerali Akiki madarakani na kuuweka utawala mpya.Baada ya mpango huo kukamilika ndipo tuliandaa haya machafuko yanayoendelea hivi sasa.Tulipanga kuanzisha vurugu nchini Uganda ili kuilazimisha serikali mpya ya kijeshi kutumia nguvu kubwa kuzima vurugu hizo na kusababisha umwagikaji mkubwa wa damu hali ambayo ingepelekea kujengwa kwa chuki kubwa kati ya serikali na wananchi.Vurugu hizo zingekuwa kubwa na hivyo kuilazimisha Marekani kupeleka vikosi vyake Uganda na hapo ndipo tungepata nafasi ya kudhibiti visima vya mafuta na kuchukua kiasi cha mafuta tunachokihitaji.Ili kulifanikisha hilo tulihitaji msaada wa Jenerali Akiki.Haikuwa rahis kumfanya jenerali Akiki akubali kushirikiana nasi hadi tulipotengeneza ajali ambayo iliripotiwa kwamba familia nzima ya Jenerali Akiki waliokuwa wanaelekea Dar es salaam walikoomba hifadhi baada ya kupinduliwa na jeshi walifariki” “Subiri kidogo Mark.Umesema mlitengeneza ajali ambayo ilisadikisha watu kuwa familia yote ya Akiki walifariki katika ajali hiyo.Nini unakimaanisha? akauliza William “Mheshimiwa Rais,familia ya Jenerali Akiki iko salama na hawakufariki katika ile ajali kama ilivyodaiwa.Ajali ile ulikuwa ni mchezo ili kumpa hasira jenerali Akiki na kumfanya akubaliane na mpango wetu kwa nia ya kulipiza kisasi kwa wale walioua familia yake” akasema Mark Piller na Willim akaendelea kumtazama kwa macho ya mshangao “Mark siamini kama haya maneno yanatoka katika kinywa chako.Iko wapi familia ya Akiki hivi sasa? Miili ile iliyosafirishwa katika majeneza kwenda Uganda ni miili ya nani? Akauliza Rais William “Mheshimiwa Rais familia ya Akiki kwa sasa iko sehemu salama katika nchi Fulani wakiishi kwa amani wakiwa chini ya uangalizi wa CIA.Wako salama kabisa wanatunzwa vizuri na wanapata kila wanachokihitaji.Katika yale masanduku kulikuwa na miili lakini haikuwa ya familia ya Akiki.Mheshimiwa Rais jambo hili limefanywa kitaalamu sana kiasi cha kutoweza kufahamika hadi leo hii ninapokueleza” “Dah ! akasema Rais William halafu akainamisha kichwa akafikiri kwa muda kisha akamtazama Mark Piller na kusema “Mark ninajaribu kuiaminisha akili yangu kwamba ni wewe ninaye kufahamu ndiye unanieleza haya au ni Mark mwingine” “Ni mimi mheshimiwa Rais.Najua haya niliyokueleza yamekustua sana lakini naomba usistuke kwani yote ni mipango kwa ajili ya nchi yetu” akasema Mark na kunyamaza kidogo “Baada ya kumleta Akiki hapa Marekani nilizungumza naye akakubali kushirikiana nasi kuanzisha vurugu Uganda na akashauri njia pekee ya kuweza kuleta machafuko nchini Uganda ni kwa kutumia dini.Alishauri kama tukiweza kuwafarakanisha waumini wa dini ya kikristu na kiislamu lazima machafuko makubwa yatatokea.Akiki alikwenda mbali zaidi akashauri kwamba kama tunataka kuchukua mafuta basi machafuko ya Uganda pekee hayataweza kutusaidia bali tunahitaji kueneza machafuko hayo hadi nchini Tanzania kwani bomba la mafuta linatoka Uganda hadi Tanga nchini Tanzania ambako ndiko meli zetu zingeweza kupakia mafuta.Tuliuchukua ushauri huo na kuanzia hapo tuliwahitaji IS ili waweze kuanzisha choko choko za kidini nchini Uganda na Tanzania.Vile vile kwa msaada wa Akiki tuliweza kuwapata mwanasiasa mmoja wa Uganda na mwingine wa Tanzania ambao wangeweza kuchochea vurugu hizo katika nchi zao na wanasiasa hao pamoja na wale viongozi wa dini kwa sasa wako hapa Marekani.Tulikubaliana baada ya vurugu hizo kuanza watakuwa wameimaliza kazi yao na watakuja kuishi Marekani.IS walifanya mauaji ya viongozi wa dini na kusababisha hasira na chuki kubwa miongoni mwa waumini wa dini hizo na Yule mwanasiasa wa Uganda akawachochea viongozi wa dini ya kikristu kuanzisha mashambulizi dhidi ya nyumba za ibada za waislamu na hapo ndipo machafuko yalipoanzia.Vurugu zilipoenea Uganda tulihamia pia Tanga Tanzania ambako nako vurugu zikaenea na kusambaa katika sehemu mbali mbali za Tanzania.Mheshimiwa Rais hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi tukafanikiwa kupeleka vikosi vyetu Afrika Mashariki na sasa meli zetu zimepanga foleni katika bandari ya Tanga nchini Tanzania zinapakia mafuta na hifadhi yetu ya mafuta inaongezeka.Hatuna tena sababu ya kusumbuka na mafuta ya kutoka Mashariki ya kati.Hadi vurug hizi zitakjapomalizika tutakuwa na akiba kubwa sana ya mafuta.Pima mwenyewe mheshimiwa Rais je hiki kilichofanyika kina maslahi kwa nchi yetu au hakina? Akauliza Mark Piller na Rais Wiliam akavuta pumzi ndefu “Mark mlichokifanya kweli kina maslahi makubwa kwa nchi yetu kwani tunahitaji sana mafuta lakini tatizo ni njia mliyotumia.Tumemwaga damu za watu kwa ajili ya kujipatia mafuta.Machoni pa Mungu hii si sawa hata kidogo” akasema William “Nakubali mheshimiwa Rais lakini tumekuwa tukifanya hivi kila mara na hakukuwa na namna nyingine ya kufanya kuweza kujipatia mafuta zaidi ya kutumia njia hii” akasema Mark Piller “Kwa nini mkaniweka kando kuhusiana nahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ masuala haya?Kama si wewe kuamua kunieleza leo hii nisingefahamu chochote kuhusu kile kinachoendelea.Niliposhauriw a tupeleke vikosi vyetu Afrika mashariki niliamini ni kwa nia njema ya kuzuia mauji kuendelea kumbe ni mpango umetengenzwa ili tukachukue mafuta” “Mheshimiwa Rais kama nilivyokueleza awali kwamba mambo haya yanafanywa kwa siri kubwa sana na Rais wa nchi hatakiwi kabisa kufahamu kitu chochote na hata mimi kukueleza nimevunja kanuni zetu kwani iwapo nitagundulika nitauawa hivyo ni jukumu lako kuufunga mdomo wako ili mimi na wewe tuendelee kuwa salama” akasema Mark Piller na ukimya ukatawala. “Mheshimiwa Rais ! akasema Mark Piller na Rais William aliyekuwa ameinamisha kichwa akainua kichwa akamtazama “Katika mpango huu unaoendelea Afrika Mashariki kuna mpango mwingine umezaliwa ndani yake ambao nao una manufaa makubwa sana ambao unahusiana na Iran” “Una mpango gani kuhusu Iran?akauliza William “Nilikueleza awali kwamba kwa muda mrefu tumekuwa tukiichunguza Iran kufahamu silaha zake bila mafanikio.Nimekuja na mpango mpya ambao unaweza ukatusaidia kufahamu kuhusu silaha za Iran na vile vile kulipua kinu kikubwa ambacho Iran inakitegemea katika kurutubisha madini ya Urani” akasema Mark Piller na ile mikunjo katika sura ya Rais William Washington ikatoweka “Nieleze kuhusu mpango huo.Nini umekibuni? Akauliza Rais William “Kuna mtu ambaye tumekuwa tukimtumia katika mipango yote ya kufadhili vikundi vya kigaidi ambavyo tuna mashirikiano navyo.Mtu huyo ni mwanamama anaitwa Habiba Jawad.Huyu ni raia wa Saudi Arabia.Mume wake ndiye tuliyekuwa tukimtumia katika kazi hiyo lakini baadae alionyesha mabadiliko na tukalazimika kumuua.Baada ya kuuawa mkewe akarithi utajiri wote na akaendelea kuifanya ile kazi aliyokuwa anaifanya mumewe yaani kufadhili makundi ya kigaidi.Tulimuwezesha kimtaji na utajiri wake ni mkubwa sana.Ni mmoja kati ya mabilionea wa Saudi Arabia na mwanamama mwenye heshima kubwa.Toka alipochukua jukumu hili amelifanya kwa ufanisi mkubwa.Mpaka sasa yeye ndiye anayetambulika kama mfadhili mkuu wa kundi la IS na makundi mengine madogo madogo ya kipalestina yanayopigana na serikali ya Israel.Ni kwa sababu yake hadi leo dunia haifahamu kama Marekani ndio wafadhili wakuu wa kundi la IS na itabaki hivyo.Hata ndani ya IS ni watu wachache tu wanaolifahamu hilo” “Sifahamu hayo yote unayonieleza Mark”akasema Rais William “Hupaswi kuyafahamu mheshimiwa Rais.Si wewe tu bali rais yeyote wa Marekani hapaswi kuyafahamu haya”akasema Mark Piller “Mheshimiwa Rais,Habiba Jawad anakuja Marekani.Ananiletea mtu mmoja ambaye amekubuhu katika masuala ya ugaidi.Mtu huyo tutamtuma Iran” “Sijakuelewa Mark.Tutamtumaje gaidi kwenda Iran?Tunamtuma akafanye nini? “Gaidi huyo ambaye Habiba anakuja naye ndiye atakayekwenda Iran kuchunguza kuhusu silaha za Iran na mfumo wake wa makombora na vile vile kuharibu kinu kikubwa ambacho Iran inakitegemea katika urutubishaji wa madini ya Urani” akasema Mark na Rais William akajikuta akitoa kicheko “Sikupaswa kucheka lakini Mark umenifanya nicheke.Kwa nini umtume gaidi Iran badala ya majasusi wetu? Magaidi hawana mafunzo yoyote wao wanachofahamu ni kuua tu.Mpango huo ni wa chini sana kufanywa na taifa kubwa kama la Marekani lenye maelfu ya majasusi wenye ujuzi wa hali ya juu mno.Tuna shirika kubwa la ujasusi kuliko yote duniani.Tuwatumie hao kuliko kumtuma gaidi akafanye kazi kwa niaba yetu.Huu ni mpango wa aibu” akasema Rais William “Mheshimiwa Rais,nimekuwa ndani ya CIA kwa muda mrefu.Hakuna kitu ambacho kinaumiza vichwa vya watu wa CIA kama suala la Iran na Korea Kaskazini.Pamoja na kuwa na majasusi wa kiwango cha juu mno bado mpaka leo hatujafanikiwa kufahamu kuhusu mfumo wa makombora wa Iran au silaha inazomiliki.Na hili ndilo ambalo limeleta ugumu mpaka leo tunasita kuitandika Iran kijeshi kwani hatuna uhakika yawezakana akawa kweli anamiliki silaha za maangamizi makubwa kama wanavyodai.Kwa kuwa majasusi wetu wameshindwa tunataka kujaribu njia ya pili ambayo ni kumtumia gaidi” akasema Mark Piller “Hiki ni kichekesho Mark.Gaidi anawezaje akaingia Iran na kufanya uchunguzi kuhusu silaha zake? “Mpango uko hivi mheshimiwa Rais” akasema Mark Piller na kunyamaza akanywa maji kulainisha koo. “Gaidi huyo tutampeleka Afrika Mashariki ambako atalipua ubalozi wetu jijini Dar es salaam” “Kulipua ubalozi wa Marekani ?! William akahamaki “Ndiyo mheshimiwa Rais” “Hilo ni jambo lisilowezekana kabisa.Hatuwezi kumtuma mtu akalipue ubalozi wetu na kuua watu wetu ! akasema kwa ukali Rais William “Tayari tumekwisha fanya hivyo jijini Kampala mheshimiwa Rais.Ubalozi wetu kule ulivamiwa na kuchmwa moto ule ulikuwa ni mpango maalum umepangwa ili kuwafanya wamarekani wakubaliane na hatua ya kupeleka vikosi vyetu Uganda” akasema Mark Piller “Mungu wangu ! akasema William akimtazama Mark Piller kana kwamba ni mara ya kwanza anakutana naye “Mheshimiwa Rais” akaendelea Mark “Tutaulipua ubalozi wetu jijini Dar es salaam kisha tutamkamata huyo gaidi na kumpeleka mafichoni” akasema Mark na kunyamaza kidogo “Miaka sita iliyopita ndege ya shirika la ndege la Qatar ikitokea Moscow Urusi kuelekea Tehran ikiwa na abiria mia moja ishirini na saba ndani yake ililazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Almaty nchini Kazakhstan kufuatia hitilafu iliyojitokeza katika mojawapo ya injini zake.Baada ya kutua abiria wote walishushwa ndegeni na kupelekwa hospitali kwa uchunguzi wa afya zao kufuatia wengi wa abiria kupatwa na mstuko mkubwa kutokana na tukio lile.Mheshimiwa Rais sisi ndio tuliotengeneza tukio lile hadi ndege ikatua nchini Kazakhstan.Tulikuwa na sababu maalum” akasema Mark na kunyamaza kidogo halafu akaendelea. “Miongoni mwa abiria wa ndege ile,walikuwemo wanasayansi sita wa Iran wakitokea nchini Urusi ambako walikwenda kupatiwa mafunzo ya siri namna ya kutengeneza bomu la nyuklia.Tulizipata taarifa hizo na kutengeneza mpango ule kisha tutakafanikiwa kuwapata wanasayansi hao ambao tunaendelea kuwashikilia hadi sasa tukiendelea kuwahoji japo hawajasema chochote” “Wako wapi hao wanasayansi? ‘Tunaendelea kuwashikilia katika mojawapo ya nyumba salama za CIA” akajibu Mark “Gaidi tunayekusudia kumtuma kulipua ubalozi wetu Dar es salaam atakamatwa baada ya kutekeleza shambulio hilo.Kisha kamatwa atakwenda kuunganishwa na wanasayansi hao mahala walikofichwa na kujenga ukaribu nao.Baada ya kuzoeana nao atasuka mpango wa kuwatorosha wanasayansi hao na wakifanikiwa kutoroka wataelekea moja kwa moja nchini Iran.Serikali ya Iran itakuwa na kila sababu za kumuamini huyo gaidi kwani kwa wakati huo dunia nzima itakuwa ikifahamu kitu alichokifanya yaani kulipua ubalozi wa Marekani na Iran watampokea kama shujaa.Akiingia Iran ndipo atakapoanza kuifanya kazi yetu tuliyomtuma” akasema Mark Piller na ukimya ukatawala mle ndani halafu Rais William akasema “Mark huo unaonekana ni mpango mzuri sana lakini tatizo ni huyo jamaa ambaye unataka kumtumia katika mpango huo.Hana mafunzo ya kijasusi na hawezi kutekeleza vyema kazi aliyotumwa na nina wasi wasi anaweza akagundulika kuwa ametumwa na Marekani na akauawa hivyo tukakosa kila kitu”Rais William akaonyesha wasiwasi mkubwa “Hata kama akigundulika kwamba ametumwa na Marekani tutakana tuhuma hizo na dunia itatuelewa kwanza mtu huyo si raia wa Marekani na kwa wakati huo atakuwa anajulikana kama gaidi ambaye anatafutwa na Marekani kwa kulipua ubalozi wake jijini Dar es salaam na vile vile atakuwa anatafutwa kwa kutoroka kutoka katika mahala alipokuwa anashikiliwa.Kwa sababu hizo mbili tutakuwa tumejitoa katika jambo hilo lakini kwa namna mpango ulivyo uhakika wa mtu huyo kugundulika ni mdogo sana” “Yawezekana mkawa mmejipanga vizuri kabisa lakini tatizo ni uwezo wa huyo gaidi kutekeleza mpango mkubwa kama huu.Jambo kama hili linahitaji jasusi mbobezi.Tunao wengi sana majasusi wa namna hiyo ambao tunaweza kuwatumia katika mpango huo.Kwa nini tusitafute mmoja wao tukamtumia badala ya huyo gaidi? Sijaukataa mpango huu lakini sikubaliani na mtu mnayetaka kumtumia.Ni mpango mzuri sana na kama ungeniambia kwamba anayekwenda kuutekeleza ni jasusi nguli wa Marekani basi ningekubaliana nawe kwa asilimia mia moja lakini kwa gaidi kwenda kutekeleza mpango huo nashindwa kukubaliana nawe Mark” “Mheshimiwa Rais,hatutaki kumtumia raia wa Marekani katika jambo hili.Mtu huyo ambaye Habiba anakuja naye ni raia wa Saudi Arabia ambao hawana maelewano mazuri na Iran.Endapo misheni itashindwa kufanikiwa na mtu huyo akakamatwa basi mzozo utakuwa ni kati ya Iran na Saudi Arabia sisi hatutahusika.Kwa mujibu wa Habiba Jawad mtu huyo anayemleta ni mtu mahiri na sahihi kwa kazi hiyo.Atakapokuja hapa tutampima na kuona uwezo wake lakini sina wasiwasi naye hata kidogo.Ninamuamini Habiba Jawad.Nina uhakika mkubwa mtu anayemleta atakwenda kuitekeleza vyema kazi tutakayomtuma akaifanye Iran” “Mark nina wasi wasi sana kuhusu jambo hili unalotaka kulifanya.Sijui kwa nini ninakuwa na wasiwasi mkubwa namna hii” akasema Rais William “Naomba uniamini mheshimiwa Rais.Nina uhakika mkubwa sana na hiki ninachokwenda kukifanya.Tumekuwa tukifanya mambo kama haya sehemu mbali mbali na tukafanikiwa.Mheshimiwa Rais katika haya yanayoendeleaAfrika Mashariki tutaua ndege wawili kwa jiwe moja.Tunaongeza akiba ya mafuta na vile vile kwa mara ya kwanza tutafanikiwa kujua aina ya silaha ilizo nazo Iran.Haya ni mafanikio makubwa sana mheshimiwa Rais” akasema Mark Piller “Mark katika suala la mafuta japo mmetumia njia ambayo si ya kibinadamu lakini nataka niwapongeze.Tunahitaji sana mafuta na nchi za Mashariki ya kati ambazo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani ziko katika mgomo baridi wa kuzalisha mafuta kwa lengo la kutukomoa sisi kutokana na sera zetu za kuiunga mkono Israel.Wamesahau kwamba Marekani wana uwezo wa kupata mafuta kutoka sehemu yoyote ile wanayoitaka.Kwa sasa mafuta kutoka Afrika yanaendelea kumiminika katika hifadhi zetu za mafuta.Hongereni sana Mark.Japo niliwekwa pembeni katika jambo hili lakini lazima niwapongeze.” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Mark Piller “Kuna kitu nataka kukiongeza hapo.Eneo hili la ukanda wa Afrika Mashariki ni tajiri sana.Lina utajiri mkubwa wa madini mbali mbali ambayo tunayahitaji mno.Kwa mfano nchini Tanzania pekee yanapatikana madini ya thamani kubwa yanaitwa Tanzanite ambayo hayapatikani sehemu nyingine yoyote duniani zaidi ya Tanzania,yapo pia madini mengine kama dhahabu,almasi,na zaidi sana madini ya Urani.Ukienda Uganda kuna mafuta,ukienda jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuna madini mengi pia ya thamani kubwa.Kwa ujumla eneo hili lote limejaa madini.Kwa kuwa tayari tumekwisha ingia Afrika Mashariki ni jukumu letu kuhakikisha tunajiimarisha na tunakwenda mbali zaidi ya mafuta.Wekeni mikakati ya kuhakikisha tunaongeza vikosi zaidi Afrika Mashariki na tunakwenda mbali zaidi kwa kupeleka vikosi vyetu sehemu zile zenye utajiri lakini jambo hili lifanyike kwa ustadi na umakini mkubwa kama mlivyofanya katika haya machafuko.Nataka hadi tutakapoondoa vikosi vyetu Afrika mashariki tuwe tumefaidika na akiba kubwa ya mafuta na madini mengine ya thamani”akasema Rais William “Mheshimiwa Rais ninashukuru kwa kuanza kuelewa kile tunachokifanya kwa ajili ya nchi yetu.Ili tuendelee kujiimarisha na kukaa muda mrefu zaidi Afrika Mashariki inatulazimu kutafuta namna ya kuongeza machafuko katika ukanda huo wa Afrika Mashariki.Nitakaa na wenzagu tuone namna ya kufanya lakini kuna kitu ninakifikiria ambacho kinaweza kutupa sababu ya kuongeza vikosi vyetu na tukaendelea kuchota Rasilimali” akasema Mark Piller “Nini unakifikiria kuhusiana na hilo wazo langu? Akauliza William “Kutoka katika machafuko haya yanayoendelea Afrika Mashariki ninafikiria kuanzisha kikundi cha uasi ambacho tutakipa nguvu na kukifadhili silaha kali ambacho kitasambaa katika nchi za Tanzania na Uganda.Hatuna shida sana na nchi ya Kenya.Shida yetu ni Tanzania,Uganda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nchi ambazo zina utajiri mkubwa.Kikundi hicho ambacho kitasambaa katika nchi hizo tatu kitawezeshwa silaha nzito na kuendelea kulifanya eneo la Afrika mashari liwe ni eneo hatari na sisi tutaongeza vikosi vyetu Afrika Mashariki kulinda amani.Nitazungumza na Jenerali Akiki kuhusiana na suala hili na tutaona nini tukifanye lakini nakuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba haya maelekezo yako yatafanyiwa kazi.Ninachokuomba niamini na kila kinachoendelea nitakujulisha lakini nakuomba haya niliyokwambia iwe ni siri yako asifahamu mtu mwingine yeyote mambo haya.Narudia kukupa angalizo mheshimiwa Rais kwamba endapo haya niliyokwambia yatavuja utakuwa ni mwisho wetu.Hii ni moja kati ya siri kubwa sana ya nchi ya Marekani” akasema Mark Piller Mazungumzo yao yalidumu kwa saa tatu kisha wakaagana na Mark Piller akaondoka zake. DAR ES SALAAM – TANZANIA MAKAO MAKUU YA SNSA Saa mbili za asubuhi wafanyakazi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi wakiwa katika ofisi yao kuu wakiendelea na majukumu yao katika ukumbi mkubwa waliyaelekeza macho yao katika runinga kubwa mbili wakifuatilia picha kutoka katika drone kubwa zilizokuwa zinazunguka angani juu ya jiji la Dar es salaam kufuatilia hali inavyokwenda.Mitaa mingi hata ile ambayo ilizoeleka kuwa na msongamano mkubwa wa watu ilikuwa mitupu.Makundi ya watu yakijiandaa kwa ajili ya kuendelea na mapambano yalionekana katika sehemu mbali mbali za jiji.Vikosi vya ulinzi viliendelea kufanya doria katika baadhi ya mitaa lakini barabara nyingi zilikuwa zimefungwa kwa kuwekwa mawe makubwa na kuchomwa matairi.Katika baadhi ya picha yalionekana majengo yakiungua moto.Maiti za watu zilionekana pia katika baadhi ya mitaa. Wakati wafanyakazi wale wakiendelea kufuatilia picha zile,katibu muhtasi wa Ruby akamfuata na kumjulisha kwamba Rais anataka kuzungumza naye katika simu.Haraka haraka Ruby akaenda ofisini kwake na kuinua mkono wa simu “Mheshimiwa Rais shikamoo” akasema Ruby “Marahaba Ruby vipi mnaendeleaje?akauliza Rais Dr Fabian “Tunaendelea vizuri mheshimiwa Rais.Tunafuatilia picha za drone kuona namna hali ilivyo katika mitaa mbali mbai ya jiji lakini hali bado ni tete.Barabara nyingi zimefungwa,majengo yanaungua moto makundi ya watu wanaendelea kujiandaa kuingia mitaani katika vurugu.Huduma hazipatikani na maisha yanazidi kuwa magumu” akasema Ruby “Nimepokea taarifa asubuhi hii kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi kwamba bado hali ni tete huko mitaani.Hata hivyo nimekupigia kukujulisha kwamba ndani ya dakika kumi zijazo mawasiliano ya simu yatarejeshwa kama ulivyokuwa umeshauri na baadae nitalihutubia taifa ili tuone kama inaweza ikasaidia kupunguza vurugu hata kwa kiasi kidogo” akasema Dr Fabian “Ahsante sana mheshimiwa rais kwa kulifanya kazi suala hili.Nina uhakika linaweza kuwa na matokeo mazuri na watu wakakuelewa” akasema Ruby “Ruby kubwa ambalo limenifanya nitake mawasiliano ya simu yarejeshwe ni ili kuwawezesha kumfuatilia Karim.Mliniambia kwamba kukosekana kwa mawasiliano kumewafanya mkashindwa kumfuatilia Yule jamaa.Mawasiliano yatarejea muda si mrefu nataka mumfuatilie Karimu na kuhakikisha mnafahamu kila kitu kuhusu yeye na jioni ya leo nipewe taarifa kama tayari mmemkamata au vipi” akasema Dr Fabian “Mheshimwia Rais tutalifanyia kazi suala hilo na jioni ya leo nitakujulisha kile ambacho tutakuwa tumekipata katika uchunguzi wetu kuhusiana na Karim Abdallah” akasema Ruby na kuagana na Rais kisha akakaa katika kompyuta yake kwa dakika tano akafanya kazi fulani halafu akarejea katika ule ukumbi mkubwa ambako wafanyakazi wa SNSA walikuwa wanaendelea kufuatilia picha za Drone kujua hali ilivyo katika mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es salaam. “Naomba tusikilizane jamani” akasema Ruby na watu wote wakawa makini kumsikiliza “Toka machafuko haya yalipoanza mawasiliano ya simu yalikatwa kwa lengo la kuzuia watu kutumia simu kuhamasishana kuhusu vurugu.Pamoja na kukata mawasiliano ya simu lakini bado haijasaidia kupunguza vurugu” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Muda mfupi uliopita nimetoka kuzungumza na mheshimiwa Rais na amenieleza kwamba ndani ya dakika chache zijazo mawasiliano ya simu yatarejeshwa” akanyamaza baada ya watu kushangilia “Jana usiku tulikuwa na mazungumzo na Rais tukamuomba aruhusu mawasiliano ya simu yarejeshwe na amekubali ombi letu hivyo ndani ya muda mfupi mawasiliano ya simu yatarejea.Kubwa ambalo lilinifanya nimuombe Rais aruhusu mawasiliano ni kwa ajili ya kumchunguza huyu mtu” akasema Ruby na kubonyeza kitanza mbali na picha ya Karim Abdallah ikaonekana runingani “Anaitwa Karim Abdallah.Ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha TPD.Kwa nini ameonekana katika runinga yetu? Huyu jamaa kabla machafuko hayajaanza aliandika ujumbe wa uchochezi katika ukurasa wake wa twitter akiwataka waislamu wa mkoa wa Tanga waungane wakawatafute wale waliomuua Sheikh mkuu wa mkoa huo aliyeuawa na watu wasiojulikana.Ujumbe huo japo aliufuta haraka lakini tayari ulikwisha somwa na watu wengi.Tunajiuliza nini sababu ya kuandika ujumbe kama ule? Kuna wasiwasi machafuko haya yanayoendelea yakawa na chembe chembe za kisiasa ndani yake hivyo nataka mawasiliano yatakaporejea tuanze kumfukua huyu jamaa kufahamu kila taarifa zake.Tunahitaji kujua mahala alipo,kufahamu nani anawasiliana nao na wanawasiliana nini,marafiki zake ni akina nani.Kwa ujumla nataka tufahamu kila kitu kumuhusu huyu jamaa.Sasa kila mmoja aende mahala pake na tuanze kazi mara moja” akasema Ruby kisha akaelekea ofisini kwake akaichukua simu yake akaiwasha tayari mawasiliano yalikwisha rejea. “Ahsante Mungu.Sasa kazi inaanza”akasema Ruby RIYADH – SAUDI ARABIA Toka Mathew alipoondoka na Habiba kuelekea Marekani,Najma hakutoka ndani.Alikuwa amejifungia chumbani kwake akiwa na mawazo mengi sana.Pembeni yake kulikuwa na simu ya Mathew pamoja na kitabu cheusi.Aliishika simu ile na kuitazama halafu akairusha pembeni “Huyu Ruby ambaye Abu ameandika namba zake za simu katika kitabu chake cha kumbu kumbu ni nani?Kwa nini nilipomuuliza Ruby ni nani alibadilika na haraka haraka akaninyang’anya kile kitabu? Akawaza Najma. “Katika simu yake amepiga namba za Ruby zaidi ya mara tatu lakini kwa bahati mbaya simu hiyo haikuwa ikipatikana.Tatizo langu nina wivu mbaya mno na hii ndiyo sababu kubwa iliyonifanya nikawa sitaki kuingia katika masuala ya mahusiano.Ninampenda sana Abu Zalawi na sitaki awe na mwanamke mwingine zaidi yangu” akaendelea kuwaza Najma “Najilaumu sana kwa kuingia katika mahusiano na Abu Zalawi bila kuifahamu historia yake ametoka wapi na maisha yake yalikuwaje huko alikotoka.Je alikuwa na mke au na familia?Hata yeye mwenyewe hajawahi kunieleza chochote kuhusiana na historia yake” Najma akainuka kitandani na kukaa “Lakini kwa nini niteseke wakati namba za simu za huyo Ruby ninazo? Kwa nini nisimpigie kuufahamu ukweli?Yawezekana akawa ni rafiki yake au ni mtu ambaye waliwahi kuifanya kazi wote.Nimepata wivu kwa sababu Abu hajawahi kuonyesha kumafuta simuni mwanamke kama alivyofanya kwa Ruby jana” Najma akaendelea kutafakari “Hapana siwezi kuendelea kuumia.Ngoja nimpigie simu huyu Ruby nimfahamu vizuri na nifahamu ana mahusiano gani na Abu” akawaza Najma na kubonyeza namba zile za Ruby akapiga simu ikaanza kuita akahisi kama mwili unamtetemeka. “Simu yake inaita” akawaza huku akihisi woga kwa mbali “Hallow ! ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili wa simu na Najma akasita kujibu “Hallow ! ikaita tena sauti ile “Hallow ! akasema Najma kwa lugha ya kiingereza “Habari yako?akauliza Yule mwanamke upande wa pili “Nzuri habari yako? “Nzuri.Nazungumza na nani kutokea wapi? “Naitwa Najma niko Riyadh Saudi Arabia” “Riyadh ! Yule mwanamke akaonyesha mshangao “Ndiyo.Wewe uko wapi?akauliza Najma na Yule mwanamke akasita kidogo “Hallow ! Najma akaita “Najma umenifahamuje?Umepata wapi namba zangu za simu? “Unamfahamu Abu Zalawi? Akauliza Najma “Abu Zalawi?yule mwanamke akashangaa “Ndiyo unamfahamu? Najma akauliza “Hapana simfahamu.Ni nani huyo mtu? “Ni mume wangu lakini ana namba zako katika kitabu chake cha kumbukumbu za mawasiliano na jana alikupigia simu mara tatu lakini simu yako haikuwa ikipatikana” akasema Najma “Utanisamehe dada yangu lakini simfahamu mtu mwenye jina hilo na wala sijawahi kuwa na rafiki mwenye jina hilo la Abu Zalawi.Ni mara ya kwanza ninalisikia” “Abu ameandika namba zako za simu katika kitabu chake na alikupigia alionekana ana jambo la muhimu sana anataka kukueleza.Kwani wewe si Ruby?akauliza Najma na mwanamke wa upande wa pili akasita “Hallow? Najma akaita “Nakuuliza kwani wewe si Ruby?Najma akauliza tena “Naweza kuzungumza na huyo Abu Zalawi ” akauliza Yule mwanamke “Abu Zalawi amesafiri Alfajiri ya leo.Naomba tafadhali kama akikupigia tena simu usimwambie chochote kuhusu mimi kukupigia simu.Ahsante sana nimefurahi kuzungumza nawe japo umekataa kunitajia jina lako” akasema Najma na kukata simu akashusha pumzi na kutazama namba zile halafu akaigiza namba za mwanzo katika kompyuta yake ili kujua namba zile ni za nchi gani na majibu yakaja kuwa ni Tanzania. “Tanzania ! akasema Najma na kuvuta pumzi ndefu “Niliona kwa macho yangu mawili katika kitabu chake ameandika jina Ruby.Iweje huyu mwanamke niliyempigia ambaye japo amekataa kunitajia jina lake lakini naamini ni Ruby akane kumfahamu Abu? Akajiuliza Najma “Au Abu ana jina lingine anatumia tofauti na Abu Zalawi?Amefahamiana vipi na uyu mwanamke wa Tanzania?” akawaza Najma “Ninahitaji kumfahamu Abu Zalawi kiundani na mtu pekee ambaye anaweza akanieleza kila kitu kuhusiana na huyu mtu ni mama.Atakaporejea katika hiyo safari waliyokwenda nitamtaka anieleze ukweli kuhusiana na Abu Zalawi kwani kuna mambo yameanza kunipa mashaka sana kuhusiana na huyu mtu.Mama amefahamiana vipi na Abu?Kuna kitu gani wanakipanga? Nitafahamu kila kitu watakaporejea” akawaza Najma DAR ES SALAAM – TANZANIA Ruby aliendelea kuishikilia simu yake baada ya kuzungumza na Najma. “Abu Zalawi ! akajiuliza “Ni nani huyo mtu? Sijawahi kuwa na rafiki yeyote mwenye jina hilo la Abu Zalawi wala sina rafiki yeyote Saudi Arabia sasa huyu mtu amenifahamuje hadi ana namba zangu tena ninazotumia hapa Tanzania ? Sijawahi kumpa namba za simu ninazotumia Tanzania mtu wangu yeyote wa nje ya nchi,huyu Abu Zalawi amezpata wapi?” akajiuliza Ruby “Au labda Uingereza wamekwisha gundua kwamba sikufariki katika ile ajali ya ndege na sasa wanaanza kunichunguza ili wapate uhakika kama ni mimi? Akaendelea kujiuliza “Kwa nini nisimpigie simu Najma na kumtaka anitumie picha ya huyo Abu Zalawi nimuone kama ninamfahamu? Nadhani hilo litakuwa jambo jema” akawaza na kuchukua simu akampigia Najma kwa kutumia zile namba alizompigia. “Hallow” akasema Najma baada ya kupokea “Najma samahani sana kwa usumbufu,Unaweza ukanitumia picha ya Abu Zalawi nimuone kama ni mtu ninayemfahamu?akauliza Ruby “Sawa ninakutumia muda si mrefu” akasema Najma na kupekua simu ya Mathew lakini hakukuwa na picha hata moja ya Mathew.Akapekua katika simu yake lakini hakukuwa na hata picha moja ya Mathew akachanganyikiwa “Haya mbona ni maajabu makubwa.Picha zote zimekwenda wapi? Tumepiga picha nyingi sana tukiwa katika mapumziko.Ni maelfu ya picha lakini hakuna hata picha moja na sielewi zimekwenda wapi” akawaza na kuchukua kamera yake ambayo nayo pia alikuwa anaitumia wakati wakiwa mapumzikoni lakini hakukuwa na picha hata moja. “Mungu wangu haya mbona maajabu? Akasema kwa mshangao na kuchukua kompyuta yake mpakato na haraka haraka akafungua sehemu ya kuhifadhi picha ambako alikuwa anahifadhi picha kila pale kadi ya kuhifadhia kumbu kumbu ilipojaa lakini akakutana na kioja kwani zile picha zote ambazo walipiga katika mapumziko hazikuwepo. “Jamani haya ni mambo gani yanatokea?Tumepiga maelfu ya picha kwa miezi mitatu na hata jana nilikuwa nazitazama nikichagua zile nzuri kwa ajili ya kuweka kumbu kumbu lakini ajabu leo hii hakuna hata picha moja.Hakuna picha katika simu yangu,ya Abu,katika kamera na hata katika kompyuta.Zimekwenda wapi?Nani amezifuta na kwa nini?akajiuliza na mara simu yake ikaita tena akazitazama zile namba ni Yule mwanadada aliyempigia kutoka Tanzania “Nitamjibuje huyu dada? Ataniona mwongo” akawaza Najma halafu akaipokea ile simu “Najma samahani umeipata picha hiyo ya Abu Zalawi?akauliza “Hapana bado.Nitakutumia baadae kidogo naomba unisubiri” akasema Najma na kukata simu. “Haya ni maajabu ambayo sijawahi kuyashuhudia” akawaza na kuendelea kupekua kompyuta yake kama angeweza kupata picha zile akini hakukuwa na picha yoyote “Humu ndani hakuna mtu mwingine yeyote aliyeingia zaidi yetu mimi na Abu.Kama angekuwa mtu mwingine ameingia ningehisi labda ndiye aliyefuta picha hizo lakini hakuna tulikuwa humu watu wawili pekee.Ningeweza kusema ni kirusi labda kimefuta picha hizo lakini picha zilizofutwa ni zile nilizopiga na Abu pekee nyingine zote zipo” akawaza na kushika kidevuni “Hapa kuna kitu kinaendelea.Picha zile hazijajifuta zenyewe bali zimefutwa kwa sababu maalum na aliyezifuta lazima atakuwa ni Abu.Kwa nini akafanya hivi? Amefuta muda gani hizo picha? Najma akapandwa na hasira “Huyu Abu Zalawi ni nani hasa?Mbona anaanza kunipa mashaka? Nadhani nahitaji kumfahamu kwa undani zaidi ni mtu wa aina gani huyu.Yawezekana ninavyomfahamu sivyo alivyo” akaendelea kuwaza Najma.





Ruby alitoka ofisini kwake akamfuata Gosu Gosu “Nikiiona tu sura yako ikiwa namna hiyo najua kuna kitu hakiko sawa.Kuna habari mbaya?Gosu Gosu akauliza mara tu Ruby alipoingia ofisini kwake “Gosu Gosu kuna kitu kimetokea kinanipa wasi wasi kidogo” akasema “Nini kimetokea Ruby?Nieleze tafadhali” “Nimepigiwa simu muda mfupi uliopita na mwanamke mmoja anaitwa Najma akitokea Saudi Arabia.Anadai kwamba mume wake anaitwa Abu Zalawi ana namba zangu za simu na jana alinipigia mara tatu lakini simu yangu haikuwa ikipatikana.Nilistuka na kumjibu kwamba simfahamu huyo Abu Zalawi na wala sina rafiki mwenye jina hilo.Najma aliendelea kusisitiza kwamba huyo mume wake ameziandika namba hizo katika kitabu chake cha anuani mbali mbali na ameandika jina Ruby.Baadae nikampigia tena nikamuomba anitumie picha ya huyo mume wake nimuone yawezekana nikawa ninamfahamu akaniomba nimpe muda kidogo na nilipompigia tena akadai kwamba hajaziona picha atanitumia baadae.Gosu hii imenistua kidogo.Sina rafiki yeyote Saudi Arabia na kinachonipa hofu zaidi ni kwamba mtu huyo ananifahamu na ana namba zangu hizi ninazotumia hapa Tanzania.Nimeogopa Gosu Gosu ninahisi labda uingereza wakawa wamegundua kwamba sikufariki katika ile ajali ya ndege na wanaanza kunichunguza” akasema Ruby “Ruby nashauri kitu kimoja kifanyike.Tumtafute huyo Abu Zalawi ni nani?Wewe ni mtaalamu sana wa mambo hayo.Yawezekana akawa ni mtu unayemfahamu” akasema Gosu Gosu. “Gosu Gosu umenipa wazo zuri sana.Ngoja nimtafute nimfahamu ni nani huyo Abu Zalawi” akasema Ruby na kutoka katika ofisi ya Gosu Gosu akarejea ofisini kwake na haraka haraka akaingia katika program maalum ya kutafuta watu akaanza kumtafuta Abu Zalawi.Ilichukua dakika tatu program ile kumaliza kutafuta na kutoa majibu.Akafungua taarifa aliyopewa na program yake na kukuta kuna majina zaidi ya mia mbili ya Abu Zalawi. “Watu wengi sana hawa.Ni yupi kati ya hawa ambaye ananifahamu? Halafu mbona karibu wote wanaonekana kuwa na asili ya kiarabu?akajiuliza Ruby kisha akaanza kuwapitia mmoja mmoja akitafuta kuona kama kuna mmoja anaweza akamfahamu katika wale.Ghafla alihisi kama macho yake yamemdanganya.Akafikicha macho ili aone tena kile alichokiona katika kompyuta yake “No ! This is not true ! Haiwezekani ! akasema Ruby kisha akainua simu na kumpigia Gosu Gosu akamtaka aende haraka sana ofisini kwake.Haikuisha dakika moja Gosu Gosu akawa ameingia ofisini kwa Ruby “Kuna nini Ruby? Akauliza Gosu Gosu baada ya kumkuta Ruby amesimama mbali na kompyuta yake.Alionekana kama vile anaiogopa kompyuta ile “Kuna nini Ruby?Mbona uko mbali na kompyta yako? Akauliza Gosu Gosu lakini Ruby hakumjibu “Kumetokea nini Ruby?akauliza Gosu Gosu huku akiisogelea kompyuta ya Ruby,akastuka baada ya kuiona picha ya Mathew. “That’s him ! akasema Ruby “Mathew ? “Ndiyo.Ni yeye aliyekuwa ananitafuta hiyo jana” akasema Ruby huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni “Ruby sijakuelewa” akasema Gosu Gosu “Hujaelewa nini Gosu Gosu?Nilimtafuta Abu Zalawi na yametokea majina zaidi ya mia mbili nikaanza kupitia jina moja baada ya lingine na kumkuta Mathew naye akifahamika kwa jina hilo la Abu Zalawi.Taarifa zinaonyesha kuwa ni raia wa Saudi Arabia” akasema Ruby “Mathew amepata uraia wa Saudi Arabia? Gosu Gosu akauliza “Ndiyo.Ana uraia wa Saudi Arabia na kama haitoshi tayari ana mke ambaye ni Najma Yule aliyenipigia simu akitaka kunifahamu mimi ni nani” akasema Ruby na kuanza kuwaga machozi “Ruby ! Ruby ! akasema Gosu Gosu huku akimtikisa Ruby aliyekuwa ameinamisha kichwa chake akilia “Kwa nini Mathew amenifanyia hivi? Kwa nini hakuniweka wazi kwamba ana mke na familia nyingine huko Saudi Arabia?akasema Ruby “Nisikilize Ruby” “Nimeumia sana Gosu Gosu kwa hiki alichonifanyia Mathew.Ndiyo maana aliniambia kwamba akiondoka nisijaribu kumtafuta kwani alijua nitafahamu kuwa yuko Saudi Arabia na tayari ana mke ! akasema Ruby “Ruby sikiliza.Naomba nikiri kwamba hata mimi mwenyewe nimestuka sana kwa hiki nilichokiona lakini ni mapema sana kusema chochote kuhusu jambo hili.Ninamfahamu Mathew Mulumbi kama ameamua kuchukua uraia wa Saudi Arabia basi ni kwa sababu maalum.Lazima kuna kitu anakifanya kule na ndiyo maana alikutaka usimtafute pindi atakapokuwa ameondoka.Siku zote Mathew amekuwa ni mtu wa kuona mbali mara mbili yetu hivyo naamini kabisa kwamba hayuko huko Saudi Arabia kustarehe lazima kuna kitu anakifanya.Hata huyo mwanamke ambaye yuko naye huyo aliyejitambulisha kuwa mke wake nina uhakika mkubwa ni sehemu ya mipango yake.Nimekuwa naye karibu kwa muda mrefu kidogo na nimebahatika kujua namna anavyoendesha mambo yake.Alikuahidi kwamba atarejea amini hivyo.Mathew Mulumbi hutembea katika maneno yake.Akisema atarudi basi lazima atarudi tu” “Gosu Gosu tafadhali naomba usinifanye niamini haya unayoniambia” akasema Ruby “Naomba uniamini Ruby.Ninamfahamu Mathew vizuri.Anaipenda nchi yake kuliko kitu chochote.Kumbuka alikataa kuchukua uraia wa Ufaransa ili aweze kuishi na familia yake kwa kuwa ana mapenzi makubwa na Tanzania hivyo kuchukua uraia wa Saudi Arabia si kwa kupenda lazima ipo sababu kubwa.Nimeanza kupata picha kuhusiana na kile ulichonieleza kwamba katika ile operesheni ya kumuua James Kasai na yule gaidi wa IS Mathew alikuwa anawasiliana na mtu kila siku usiku na ulihisi mtu huyo aliyekuwa akiwasiliana naye alikuwa akimpa taarifa mbali mbali kuhusiana na operesheni ile.Nadhani Mathew yuko Saudi Arabia kimkakati zaidi.Kama jana alikutafuta awasiliane nawe basi lazima atapiga tena simu.Lazima kuna jambo anataka kuwasiliana nawe na ninahisi yawezekana ikawa ni kuhusiana na hizi vurugu zinazoendelea” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu umeongea kitu cha maana sana.Mathew alipotea kwa miaka mitatu na aliporejea alikuja kwa kazi moja tu ya kummaliza James Kasai.Alikuja akiwa anafahamu kila kitu kilichokuwa kinaendelea hapa Tanzania na alikuja akiwa ana taarifa zote za kuhusiana na James Kasai.Hakuna aliyekuwa anafahamu kama James Kasai anaishi katika jiji la Kampala maisha ya kifahari.Wengi tulikuwa tunaamini kwamba James Kasai anaishi msituni lakini ni Mathew aliyekuja kutufumbua macho kwamba James haishi msituni.Hakuna aliyefahamu kuhusu ujio wa Khalid Sultan lakini jambo hili alilifahamu Mathew.Baada ya kumaliza kile kilichomleta akaondoka zake.Kitendo cha kunitafuta kwa wakati huu wa hizi vurugu yawezekana kuna kitu anataka kunieleza pia.Ahsante sana Gosu Gosu kwa kushusha presha yangu ambayo tayari ilikwisha panda.Nilikuwa nawaza mambo mengine kabisa nikasahau kufikiri mambo ya msingi” akasema Ruby “Imekuwa bahati tumefahamu mahala alipo Mathew lakini kama alivyotaka yeye mwenyewe kwamba asitafutwe hadi pale atakapotutafuta yeye mwenyewe.Kitu cha kujiuliza je huko Saudi Arabia anafanya kitu gani? “Nahisi yuko sehemu ambako anapata taarifa nyingi za mambo mbali mbali yanayoendelea duniani.Gosu Gosu ninahisi tayari Mathew anaweza kuwa na taarifa kuhusiana na hiki kinachoendelea Afrika Mashariki.Nahisi hiki kinachoendelea kina nguvu ya kutoka nje ya nchi”akasema Ruby “Hata mimi nimekuwa nikihisi hivyo hasa ukiliangalia suala hili namna lilivyoanza.Kuna kile kitu kinaitwa gawanya na tawala.Kumbuka mabeberu walishindwa kuigawanya jumuiya ya Afrika mashariki kwa kumtumia Melanie Davis na yawezekana wameamua kutumia njia hii ya machafuko ili wapate nafasi ya kupenda na kuchota rasilimali.Watu hawa ni wajanja sana na wana mbinu nyingi.Watanzania si watu wa kugombana wao kwa wao lakini sasa hivi wamejikuta katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.Lazima kuna nguvu kubwa imetumika hapa si bure” akasema Gosu Gosu Wakati wakiendelea na mazungumzo mlango wa ofisi ya Ruby ukagongwa akaingia katibu muhtasi wake. “Rais atatoa hotuba muda wowote kuanzia sasa” akasema Yule katibu muhtasi wa Ruby na haraka haraka Ruby akachukua kitanza mbali akawasha runinga iliyokuwa ukutani.Kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja kutokea ikulu ambako Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo alikuwa anatarajia kulihutubia taifa.Tayari ndani ya ukumbi ambao angetumia kuhutubia taifa,viongozi mbali mbali walikwisha wasili na aliyekuwa anasubiriwa ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hatimaye mlango ukafunguliwa na Rais Dr Fabian Kelelo akajitokeza akiwa ameongozana na walinzi wake.Kwa kuwa ni yeye tu aliyekuwa akisubiriwa akawataka watu waliokuwa wamesimama waketi na hakupoteza muda akaanza moja moja hotuba yake.Katika simu janja zote ambazo zilikuwa zimewashwa muda huo ziliunganishwa na hotuba ya Rais kama Ruby na Gosu Gosu walivyokuwa wameshauri “Ndugu watanzania ambao kwa muda huu mmepata bahati ya kunisikiliza,awali ya yote ninaanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuweka hai hadi sasa.Ninapenda pia kuchukua nafasi hii kuwapa pole sana wale wote ambao wamepoteza ndugu zao katika vurugu zinazoendelea hivi sasa hapa nchini kwetu.Ninawaombea vile vile majeruhi wote uponaji wa haraka. Ndugu zangu watanzania wenzagu,kabla ya kuanza hotuba yangu naomba niwaeleze kitu kimoja ambacho yawezekana wengi wenu hamkijui.Jina langu naitwa Dr Fabian Jumanne Mkawi Kelelo.Baba yangu Mungu amrehemu aliitwa Jumanne Mkawi Kelelo.Alikuwa mwislamu na alioa wake wawili mama yangu akiwa ni mke mdogo.Mke mkubwa aliitwa Zamaradi alikuwa ni mwislamu na mama yangu aliitwa Veneranda yeye alikuwa mkristu.Kwa mama yangu mimi ni mtoto wa tatu kuzaliwa,nina kaka zangu wawili na ninao pia wadogo zangu wawili.Kaka zangu walioniangulia ni waislamu wakifuata dini ya baba na mimi nilifuata dini ya mama,hata wadogo zangu pia walifuata dini ya mama.Kwa miaka yote hakujawahi kutokea mgogoro wowote ndani mwetu huku kila mmoja akiheshimu dini ya mwenzake.Baba yangu aliheshimu sana dini ya mama halikadhalika mama aliheshimu sana dini ya baba.Sisi watoto pia tuliheshimiana na kupendana na hakuna aliyedharau dini ya mwenzake. Nimeamua kuanza kwa kuwapa mfano huu wa familia nilikotoka lakini naamini zipo familia nyingi za aina hii na wanaishi kwa amani.Lengo langu ni kutaka kuwaonyesha kwamba kwa miaka mingi watanzania tumekuwa tukiishi kama ndugu moja licha ya utofauti wetu wa dini.Wakristu,waislamu na waumini wa dini nyingine tumekuwa tukiheshimiana na kuishi kwa upendo mkubwa.Mara kadhaa kumeibuka watu au vikundi vya watu wa dini moja wakikashifu au kutoa matamshi ya kuudhi waumini wa dini nyingine.Kila pale kulipotokea mikwaruzano yoyote baina ya dini zetu viongozi wa dini walikaa wakazungumza na kuyamaliza na amani ikatamalaki.Nini kimetokea sasa hivi hadi tumefikia hapa tulipofika? Nani katufikisha hapa? Najua kwa sasa ni vigumu kupata majibu ya maswali haya lakini lazima tujiulize maswali haya na tukipata majibu tutajua nini kimetufikisha hapa. Dunia nzima inashangaa nini kimetokea Tanzania? Hii ndiyo nchi ambayo kwa miaka mingi imekuwa ni kioo cha amani.Tanzania imekuwa ni kimbilio la watu kutoka nchi zile ambazo amani imetoweka.Nini kimepelekea kuipoteza amani yetu? Ndugu zangu maswali ni mengi sana ya kujiuliza kwa nini tumefika hapa tulipofika.Tumeipoteza amani yetu ambayo imetunzwa kwa miaka mingi na sasa tunatumia gharama kubwa kuisaka tena amani…. Wakati hotuba ya Rais ikiendelea,katika ofisi ya Ruby akaingia Pamela akiwa na kompyuta mpakato “Pamela kuna kitu umekipata? “Ndiyo mkurugenzi” akasema Pamela na Ruby akapunguza sauti ya runinga wakaenda mezani “Simu ya Karim haipatikani tena imezimwa.Tumejaribu kuiwasha kwa mbali lakini haipatikani na inawezekana tayari amekwisha toa betri” “Bastard ! akasema Gosu Gosu “Lakini tumepata mawasiliano ya Karim ya siku saba kabla ya kuanza kwa machafuko.Tumefahamu pia kwamba mara ya mwisho aliitumia simu yake akiwa katika nyumba hii hapa” akasema Pamela na kumuonyesha Ruby mahala alipokuwepo Karimu mara ya mwisho alipoitumia simu yake “Tumefanikiwa pia kuipata namba ya simu aliyowasiliana nayo mara ya mwisho na namba hiyo imesajiliwa kwa jina la Denis Sambale.Tumemfuatilia huyu mtu ni mfanya biashara anaishi jijini Tanga” akasema Pamela “Good job Pamela”akasema Ruby “Kazi imeanza.Tayari tumepata sehemu ya kuanzia.Itanilazimu kuchukua timu na kuwahi mahala hapo alipokuwa Karim kuanza uchunguzi” akasema Gosu Gosu “Hapana Gosu Gosu.Ni hatari kubwa huko nje.Tutatuma kikosi chetu cha makomando wa idara watakwenda mahala hapo na tutawafuatilia kwa kutumia drone zetu tutajua kila kinachoendelea mahala hapo” “Ruby..” “Gosu Gosu nimekwisha sema hauendi huko mtaani hali si nzuri.Ngoja tutume kikosi chetu cha makomando ambao watavamia nyumba hiyo na kufanya uchunguzi na kama Karim atakuwepo hapo basi ataletwa hapa kwa mahojiano.Naomba tusiwe na mjadala katika hilo” “Sawa Ruby” akasema Gosu Gosu na bila kupoteza muda Ruby akampigia simu mkuu wa kikosi cha makomando cha SNSA ambao walikuwa wamepiga kambi katika makao maku ya SNSA kuimarisha ulinzi akamtaka wakutane katika chumba maalum cha mipango. “Gosu Gosu usinielewe vibaya lakini wewe mwenyewe unaona namna hali ilivyo huko mitaani.Siwezi kukuacha ukaenda huko.Hawa makomando tunaowatuma watafanya kazi nzuri.Wewe ni mtu mkubwa kwa sasa unatakiwa upumzike na uwe ukitoa maelekezo tu.Haya mapambano tunawaachia vijana” akasema Ruby na Gosu Gosu akatabasamu “Nimekuelewa Ruby” akasema Gosu Gosu kisha wakatoka na kuelekea katika chumba cha mipango ambako tayari kikosi cha makomando nane walikuwa wamefika. “Habari za asubuhi ndugu zangu” Ruby akawasalimu kisha akaelekea katika runinga iliyokuwa mbele ya chumba kile. “Kuna kazi ndogo imejitokeza ndugu zangu” akasema Ruby na kubonyza kitanza mbali na katika runinga ikaonekana picha ya Karim Abdallah “Anaitwa Karim Abdallah.Huyu ni mwanasiasa ambaye anaongoza chama cha upinzani.Ni chama kidogo kisicho na uwakilishi bungeni lakini ni chama ambacho kimekuwa kikijihusisha na matukio mbali mbali ya uchochezi.Chama hiki kimekuwa kikitoa matamko mbali mbali yenye nia ya kujenga chuki kwa wananchi dhidi ya serikali.Wakati vugu vugu la machafuko yanayoendelea hivi sasa lilipoanza,Karim aliandika katika ukurasa wake wa twitter ujumbe wa uchochezi na kuufuta haraka.Tunataka kumuhoji kuhusiana na ujumbe ule aliouandika ambao ulikuwa ujumbe wa kujenga chuki baina ya waumini wa dini ya kikristu na kiislamu.Tuna wasiwasi yawezekana machafuko haya yanayoendelea hivi sasa yana chmbe chembe za kisiasa ndani yake” akasema na kubonyeza tena kitanza mbali na picha nyingine ikajitokeza “Tumefuatilia mawasiliano yake lakini simu yake imezimwa lakini mara ya mwisho alitumia simu yake akiwa katika nyumba hii hapa pichani” akasema Ruby na kuwaonesha ila picha “Mnakwenda kuvamia nyumba hii na kama Karimu yuko humo basi achukuliwe na aletwe hapa kwa mahojiano.Yeyote atakayekuwemo ndani ya nyumba hiyo achukuliwe kwani lazima atakuwa akifahamu kuhusu Karim.Jambo la kuzingatia machafuko ni makubwa sana huko nje hivyo basi yeyote atakaye jaribu kuwashambulia mtajibu haraka sana ! akasema Ruby kisha wakauliza maswali kadhaa halafu wakatoka kwenda kujiandaa.Ruby na Gosu Gosu wakaenda kuzungumza na wafanyakazi ambao karibu wengi walikuwa wanaendelea kutazama hotuba ya Rais. “Tusikilizane ndugu zangu” akasema Ruby “Katika uchunguzi wa haraka haraka imegundulika kwamba simu ya Karim Abdallah imezimwa lakini mara ya mwisho aliitumia simu hiyo akiwa katika nyumba hii hapa” akabonyeza kitanza mbali na nyumba ikaonekana runingani. “Katika nyumba hii ndimo Karim alitumia simu yake mara ya mwisho na aliwasiliana na mtu anaitwa Denis Sambale ambaye ni mfanya biashara wa jiji la Tanga.Kikosi chetu cha makomando kinaelekea katika nyumba hiyo hivi sasa kuchunguza na kama wakifanikiwa kumpata Karim ataletwa hapa kwa ajili ya mahojiano.Nataka tujielekeze huko kwa sasa.Drone zetu zielekezwe katika misheni hii ndogo ili tuweze kuhakikisha watu wetu wanakwenda na kurejea wakiwa salama” akasema Ruby na zoezi likaanza mara moja. Makomando nane wakapanda katika helkopta na kuondoka kuelekea katika nyumba wanayokwenda kuichunguza.Tayari drone moja ilikwisha elekezwa katika nyumba ile ambayo makomando walikuwa wanakwenda na hakukuonekana mtu yeyote kwa nje.Milango na madirisha vyote vilikuwa vimefungwa. Ilichukua dakika kumi na mbili kwa helkopta iliyowabeba makomando kufika katika nyumba ile.Hali ilikuwa shwari maeneo yale hakukuwa na makundi ya wananchi waliokuwa wanapambana.Makomando wale walihakikishiwa toka ofisi kuu waliokuwa wanalichunguza eneo lile kwa drone kuwa ni salama na wanaweza kushuka.Hakukuwa na sehemu ya helkpota kuweza kutua hivyo makomando wakaanza kushuka kwa kutumia kamba na waliposhuka wote helkopta ikabaki angani ikiwasubiri wamalize jukumu lao. Haraka haraka mlango wa mbele wa nyumba ukavunjwa wakaingia ndani.Sebuleni hakukuwa na mtu yeyote na nyumba ilikuwa kimya.Walipita katika vyumba vyote lakini hakukuwa na mtu yeyote. “Hakuna mtu yeyote ndani ya hii nyumba,narudia tena hakuna mtu yeyote ndani ya hii nyumba” mkuu wa kikosi kile cha makomando akawajulisha SNSA. “Kuna kitu chochote mmekiona humo ndani kinachoweza kutusaidia? Ruby akauliza “Katika vyumba vya kulala tumekuta makabati yako wazi na hakuna nguo hata moja ndani yake na inaonyesha kwamba waliokuwa wanaishi humu waliondoka haraka haraka” akasema kiongozi Yule na kugeuka baada ya mmoja wa makomando kumfuata na albamu la picha akalifungua akapitia picha kadhaa kisha akasema “SNSA inaonekana hapa ni nyumbani kwa Karim kwani tumekuta kuna albamu la picha zake na familia yake” “Ahsante kamanda kwa kazi nzuri.Mnaweza kurejea ofisini” akasema Ruby “Tumemkosa huyu jamaa.Yuko wapi? Akauliza Ruby “Kitendo cha kuondoka kwake kinazidi kutufanya tuendelee kumchimba zaidi.Baada ya kumkosa Karim zoezi sasa linahamia Tanga kwa Denis Sambale ambaye alipigiwa simu na Karim” akasema Gosu Gosu “Ninakwenda Tanga.Nitaongozana na kikundi cha makomando” akasema Gosu Gosu na Ruby akamtazama akataka kusema kitu “Najua unachotaka kukisema Ruby lakini safari hii ninakwenda Tanga na timu ya makomando kumtafuta Denis Sambale.Usihofu Ruby nitakuwa salama” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu ninasita sana kukuruhusu uende huko lakini ..” “Ruby niruhusu niende nitakuwa salama.Mimi ni mwanajeshi na siwezi kuogopa.Nitaongozana na kikosi cha makomando kwenda Tanga kumfuatilia huyo mtu.Tutashirikiana pia na watu wa ofisi yetu ya Tanga” akasema Gosu Gosu na Ruby akatafakari kwa muda halafu akasema “Gosu Gosu kuna watu wetu wako Tanga.Tutawatuma kwenda kumtafuta huyo mtu aliyewasiliana mara ya mwisho na Karim” akasema Ruby “Tanga ndiko kuna machafuko makubwa zaidi na inahitaji watu wenye uzoefu wa mapigano kama mimi ! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu watu hawa tuliwaamini kwamba wanaweza kazi ndiyo maana tukawakabidhi ofisi.Hawakupewa ofisi bila kukidhi vigezo.Wamepitia mafunzo na wanafahamu nini wanatakiwa kufanya.Hatuwezi kutuma watu kutoka Dar es salaam kwenda Tanga wakati kule kuna timu ya watu wetu.Tutawatumia hao watu wetu kumsaka Denis Sambale” akasema Ruby halafu wakatoka kwenda kuzungumza na wafanyakazi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Kama mlivyoshuhudia makomando wetu wamefika katika nyumba ambayo imegundulika ni makazi ya Karim Abdallah lakini hajapatikana inaonekana yeye na familia yake wametoweka na hakuna ajuaye wameelekea wapi.Baada ya kumkosa Karim sasa tunageukia kwa mtu ambaye aliwasiliana naye mara ya mwisho anaitwa Denis Sambale.Huyu ni mfanya biashara wa jiji la Tanga.Tunaamini yawezekana kuna kitu anakifahamu kuhusiana na mahala alipo Karim.Tuna watu wetu walioko Tanga tutawatumia kumsaka huyu Denis Sambale.Nataka tufahamu mahala alipo huyu mtu na kama simu yake imewashwa tumfuatilie na kuwasiliana na watu wa Tanga ili wamkamate.Tumchimbe na tujue watu anaowasiliana nao ni akina nani.Nataka zoezi hilo likamilike kwa haraka ili tuweze kuwasiliana na watu wa Tanga” akasema Ruby na mara moja kazi ikaanza ya kumchunguza Denis Sambale Thanks Quote Reply Report











ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog