Search This Blog

Thursday 17 November 2022

SIRI : MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA - 5

 





    Simulizi : Siri: Maisha Na Kifo Cha Melanie Chuma

    Sehemu Ya Tano (5)





    Mathew aliwasili nyumbani kwake “Mungu naomba unisaidie” akawaza na kushuka garini akaelekea ndani akakutana na Lucy mlangoni “Karibu kaka” “Ahsante Lucy.Yuko wapi Peniela? “Yuko katika chumba cha mapumziko anakusubiri huko” akasema Lucy “Nashukuru sana Lucy” akasema Mathew na kupanda ngazi kuelekea katika chumba cha mapumziko kilichopo ghorofani.Kupitia mlango mkubwa wa kioo akamuona Peniela akiwa amesimama dirishani akitazama nje.Akaufungua mlango taratibu na kuingia ndani.Peniela aliposikia mlango ukifunguliwa akageuka wakagonganisha macho.Kila mmoja alisimama mahala pale akimtazama mwenzake kwa dakika mbili na taratibu michirizi ya machozi ikaonekana mashavuni mwa Peniela “Hallo Penny” akasema Mathew “Hallow Mathew” akasema na kuchukua kitambaa akafuta machozi “Karibu sana.Pole na safari” akasema Mathew na kumtaka Peniela aketi. “Ahsante sana kwa kuja Peniela.Nimefurahi kukuona tena” akasema Mathew “Mathew I’m sorry nimeshindwa nifanye nini baada ya kuiona sura yako.Nimeshindwa nikukumbatie niangue kilio au nifanye nini” akasema Peniela “Nafahamu Peniela uko katika mstuko bado na itachukua muda kuamini kama kweli ni mimi lakini naomba nikuthibitishie kwamba ni mimi Yule Yule unayenifahamu” akasema Mathew “Kwa nini Mathew umetutesa kiasi hiki?Unajua ni mateso gani mimi na watoto tumeyapitia ? akauliza Peniela “Ninafahamu Peniela na sipati neno zuri la kuwaomba samahani kwa wakati mgumu mliopitia lakini hata wewe mwenyewe unafahamu nising…..” “Hapana hufahamu kitu chochote Mathew ! akasema Peniela kwa ukali na kumkatisha Mathew “Hufahamu chochote kuhusu mateso ambayo mimi na watoto tumeyapitia.Ungejua kama tutateseka usingetengeneza kifo chako! “Penny sikufanya hivyo na siwezi kufanya hivyo hata siku moja.Unajua ni namna gani ninakupenda wewe na watoto hivyo nisingeweza kufanya kitu ambacho kingewaumiza” “Mathew ninajuta kukupenda mtu kama wewe.Ningejua kama nitaishi maisha kama haya nikiwa nawe katu nisingekubali kuolewa nawe! “Usiseme hivyo Peniela” “Ni lazima niseme ili ufahamu.Ninajuta kuishi na mtu kama wewe.Unadiriki hata kutunga kifo chako na hufikirii familia yako itateseka kiasi gani.Kitu gani umekikosa Mathew.Nimekupa utajiri mkubwa maisha ya kifahari lakini bado unarudia kazi zako hizi zisizo na maana yoyote.Unapata nini kutoka katika kazi hizi zinazokufanya uipe familia yako mateso makubwa?Maneno yale ya Peniela yakaonekana kumchoma sana Mathew “Peniela una haki ya kunitukana mimi matusi ya kila namna unayoyafahamu lakini katu usithubutu kuitukana na kuidharau kazi yangu.Ni kazi hii hii ambayo leo unaidharau ndiyo kazi ambayo imekufanya leo hii ukajulikana dunia nzima.Isingekuwa kwa kazi hii usingekuwa Peniela huyu wa leo hivyo nakuonya usithubutu kudharau kazi yangu ! “Lazima niseme ! Kazi hiyo imekuingizia nini hadi sasa? Toka umeanza kuifanya kazi hii hakuna manufaa yoyote uliyowahi kuyapata zaidi ya hasara.Umeipoteza hadi familia yako ya kwanza kwa sababu ya kazi hii lakini bado hujajifunza na sas…………..” “Peniela stop !! akasema Mathew kwa hasira “You want to hit me?Go ahead hit me I’m not scared of you ! akatamba Peniela “Sifahamu nani kakuloga Mathew hadi unaacha hivi vyote nilivyokupa na kurejea katika kazi kama hizo zisizo na mshahara wowote.I didn’t know you are such a stupid…..” Peniela hakumaliza kile alichotaka kuisema akajikuta ameanguka sakafuni baada ya kulambwa kofi zito.Akagala gala pale chini na kuinuka akavua kiatu chake akaipiga meza ya kioo ikavunjika akachukua kipande cha kioo akakirusha lakini Mathew akawa hodari akakikwepa halafu akamfuata tena na kumnasa kofi lingine zito Peniela akajikuta amekaa sofani.Damu zilianza kumtoka mdomoni. “Nimekuonya dhidi ya dharau na kejeli zako kwa kazi yangu.Nitukane utakavyo lakini si kutukana na kudharau hiki ninachokifaya.Do you know what I’m going through right now?Nina majukumu mazito ya kuisadia nchi hivyo sintavumilia kejeli za mtu kama wewe.Sintajali wewe ni mke wangu au nani lakini utakaponikosea heshima katika kazi yangu lazima nikufunze adabu ! Hii ni mara ya kwanza ninakupiga toka nimekuoa na nimekupiga kutokana na dharau ulizozionyesha.Ulipaswa kunionea huruma badala ya kuanza kunikejeli.Unadai umenipa utajiri ?Mimi ndiye niliyekupa huo utajiri ambao leo hii unakupa kiburi! Akafoka Mathew “Everything came from blood.You have nothing you stupid ! akafoka Peniela huku akilia “Fine.Kwangu mimi utajiri wa mali si kitu na sihangaiki nao.Ninahangaika kwa ajili ya nchi yangu na watu wake wakae kwa amani na wala sihitaji mtu anilipe kwa kazi hiyo bali ni Mungu mwenyewe ndiye atakayenilipa kwa njia anazojua yeye mwenyewe hivyo tafadhali usinitusi kuhusu mali hizi ambazo ninaweza kuzitafuta na kupata kushinda hata hizo ulizonazo.Nimekuta umeuza mali zote na sijakulaumu kwa sababu sihangaiki na mali” “Kama uhangaiki na mali kwa nini ukanipigia simu? “Nilitaka kupata uhakika kama ni wewe uliyeuza” “Ni mimi nimeuza jasho langu.Siwezi kuacha mali zangu kwa mtu asiye na shukrani hata chembe! “Ni wewe ambaye umekosa shukrani kwangu kwani kama nisingesimama imara mimi haya yote usingekuwa nayo” “Huna uimara wowote Mathew.Ungekuwa imara usingetengeneza kifo chako na kuiacha familia yako katika mateso makubwa” “I didn’t fake my death but …..” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Hukuonekana kuumizwa na kifo changu hata kidogo ndiyo maana hukusumbuka kutafuta ukweli hukusumbuka hata kutafuta kaburi langu liliko” “Ninajutia hata machozi niliyoyamwaga kwa ajili yako.Hustahili machozi yanguMathew ! Wewe ni mtu mnyama sana ! “Ninalifahamu hilo.Sikustahili machozi yako kwa sababu tayari ulikwisha nitoa ndani ya moyo wako.Nafahamu mapenzi kati yetu yalikwisha zamani ni mimi ambaye niliendelea kubembeleza na ulipopata taarifa za kifo changu ulishukuru” akasema Mathew na kuvuta pumzi ndefu “Ninafahamu kuhusu mapenzi yako na Nahum kijana wa kutoka Israel.I saw you and I was hurt”akasema Mathew na Peniela akabaki kimya akimtazama Mathew “Ulifanya haraka sana kuamua kuwa na mwanaume mwingine wakati hujaupata ukweli halisi kuhusu kifo changu” “Ouh kumbe ulikuwa unanifuatilia ! Stupid. ! akasema Peniela na kufuta damu kwa kitambaa “Imekuwa vizuri kama ulikuwa unanifuatilia na umegundua kwamba nilikuwa na mwanaume mwingine anayejitambua kuliko wewe ! “Nahum alikuwa anakuchezea tu Peniela.Alikuwa ni jasusi wa Israel na alikuwa kazini! akasema Mathew na Peniela akawa kimya.Baada ya muda akasema “Sijali kama alikuwa ananichezea ama vipi lakini alikuwa anajielewa kuliko wewe.Sitaki mjadala mrefu na wewe.Nimesafiri usiku kucha kuja hapa Tanzania kwa ajili ya kitu kimoja tu” akasema Peniela na kunyamaza akamtazama Mathew “Nimekuja kulimaliza hili” akasema tena na kufuta machozi “Mathew nilitegemea kuwa mwanamke mwenye furaha kubwa katika maisha yangu lakini imekuwa kinyume chake nimekuwa ni mwanamke mwenye mateso makubwa kuliko furaha.Nyakati nilizowahi kuwa na furaha toka nimekuwa nawe ni chache sana.Nimejitahidi kuvumilia nikitegemea labda siku moja mambo yatabadilika lakini hakuna dalili zozote za mabadiliko na ninaendelea kuumia na wewe mwenzangu huonekani kujali furaha yangu na wanangu.Umesema nisidharau kazi yako na siwezi kufanya hivyo lakini kwa kauli hiyo umedhihirisha wazi kwamba umechagua kazi kuliko mimi na watoto.Hauoni tena thamani yetu ndiyo maana umekuwa ukiendelea na maisha yako huku sisi tukimwaga machozi kila siku kukulilia na kukuombea.Sitaki kuendelea na maisha haya Mathew na Mungu atanisamehe kwa maamuzi haya niliyoyachukua” akasema Peniela na kuinuka akaenda kuchukua mkoba wake akaufungua na kutopa bahasha ya khaki akampatia Mathew akaifungua na kukuta ni nyaraka za mahakama za kutengua ndoa.Mathew akaziweka karatasi zile na kumtazama Peniela kwa hasira “Utanisamehe Mathew hayo ndiyo maamuzi niliyoyachukua na sintabadili tena maamuzi yangu.Nataka niwe na furaha katika maisha yangu na furaha hiyo siwezi kuipata nikiwa nawe hivyo nimeamua kuachana nawe ili kila mmoja aendelee na maisha yake kwa amani.Wewe utaendelea na kazi yako ambayo ni ya muhimu kuliko sisi na mimi nitaendelea na maisha yangu na kama Mungu akinijalia basi nitampata Yule ambaye atanipa furaha ya maisha ninayoihitaji” akasema Peniela na Mathew akazichukua tena zile karatasi akazisoma kisha akamtazama Peniela “Are you sure you want to do this?akauliza Mathew “I’m sure 100%” akajibu Peniela “Please sign the papers Mathew.Hakuna namna unayoweza ukanishawishi nikabadili maamuzi yangu.It’s over please accept it.Kuhusu mali usiwe na wasiwasi nitakugawia robo ya mali zangu zote” akasema Peniela.Mathew akatafakari akavuta pumzi ndefu na kusema “Arlight let’s end this.Lakini…” akasema Mathew na kumtazama Peniela “Naomba ufahamu kwamba ninapo weka saini makaratasi haya ninaufunga mlango ambao hautafunguliwa tena.Lifahamu hilo na ninaomba uwe na uhakika na hiki unachotaka kukifanya” “Saini karatasi Mathew.I don’t care if there is a door or window between us.Ninachokihitaji ni kuachana nawe rasmi.Siwezi kuishi na mtu ambaye anakufa na kufufuka.Hujui lini atakufa kifo cha kweli.Siwezi kuendelea kuteseka kiasi hiki.Labda Mungu atakujalia utampata Yule ambaye atakuelewa na atakuwa tayari kuishi nawe lakini mimi nimeshindwa kukuelewa na siko tayari kuendelea kuishi nawe” akasema Peniela.Mathew akazitazama tena zile karatasi kwa makini “Kama alivyotamka yeye mwenyewe kwamba it’s over.Hakuna namna ninavyoweza kumshawishi akabadili maamuzi yake na mimi siwezi nikaacha kazi hii muhimu kwa nchi nikamfuata mwanamke.Kwangu nchi kwanza na mengine baadae kwa hiyo niko tayari kuitoa sadaka ndoa yangu.Ngoja nimuache aende kwani sintaweza kumpa furaha anayoihitaji katika maisha yake.Nitakuwa mchoyo kama nitaendelea kung’ang’ania kuwa naye” akawaza Mathew “Peniela naomba unisikilize” akasema Mathew “Nimekuelewa kile unachokitaka na nitakutimizia.Sitaki kuwa mchoyo nataka ukaitafute furaha ya maisha unayoihitaji lakini kabla ya kuweka saini karatasi hizi kuna mambo ambayo nataka tukubaliane” akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema “Kwanza kabisa ni kuhusu watoto.Ninaomba sana jambo hili liwe ni letu peke yetu na watoto wasifahamu chochote.Wataendelea kufahamu kuwa nimefariki dunia hadi hapo baadae mambo yangu yatakapotulia nitawatafuta na kuwaeleza ukweli.Jambo la pili ni kuhusu mali” akanyamaza tena kidogo “Sihitaji chochote kutoka katika mali zako Peniela.Kama uliamua kunitengea fungu langu ligawanye mafungu manne na kila mtoto wangu apate fungu lake.Jambo la tatu kuna msaada ninauhitaji kutoka kwako” “Kama umekataa mali nilizokupa unataka nikusaidie nini tena? akauliza Peniela. “Ninahitaji taarifa” “Taarifa zipi unahitaji?akauliza Peniela “Nataka kumfahamu Yule mtu uliyemuuzia mali za hapa Dar es salaam Melanie Davis” akasema Mathew na uso wa Peniela ukaonyesha mshangao “Melanie Davis?! Kwa nini unataka kumfahamu? “Ninahitaji kupata taarifa zake.Wewe ndiye unayemfahamu vyema hivyo basi nakuomba unipe taarifa zake” akasema Mathew “Unataka kumfanya nini Melanie? Tafadhali naomba usimguse mimi ndiye niliyemuuzia mali zangu na zilizobaki nikampa Gosu Gosu.Sikujua kama utafufuka tena” akasema Peniela “Peniela narudia tena kukukumbusha kwamba sihitaji mali.Ninao uwezo wa kuishi maisha ya aina yoyote ile hivyo mali si kipaumbele kwangu.Huyu Melanie sihitaji kumsumbua kwa chochote kuhusu mali alizonunua kwani amenunua kihalali kabisa” “Kwa nini sasa unataka taarifa zake? “Utanipa taarifa zake au haunipi?Mathew akauliza “Utanifanya nini kama nisipokupa taarifa zake? “Sintasaini karatasi hizi na wewe utaendelea kuwa mke wangu hadi kifo kitutenganishe” akasema Mathew na kuweka kalamu chini. “Simfahamu Melanie Davis vizuri.Niliwatangazia watu wangu wa karibu hasa wafanya bishara kuhusu mpango wangu wa kuuza mali zilizoko Tanzania na kuwataka wanisaide kutafuta mnunuzi.Walikuja wanunuzi wengi lakini akajitokeza Melanie ambaye alikuja na bei nzuri na kuwazidi wale wote waliokuja mwanzo hivyo basi nikamuuzia kila kitu” “Melanie anatajwa kuwa mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Ufaransa utajiri ambao alirithi kutoka kwa wazazi wake.Wewe umekuwa miongoni mwa mabilionea wa Ufaransa je umewahi kumsikia Melanie Davis hapo kabla?akauliza Mathew.Melanie akafikiri na kusema “Hapana sikufahamu Melanie kabla” “Umewahi kuwasikia wazazi wake?akauliza Mathew “Hata wazazi wake sina kumbu kumbu kama nimewahi kuwasikia.Taarifa hizi zote umezipata wapi?akauliza Peniela “Ukiacha haya makampuni uliyomuuzia hapa Tanzania unazifahamu biashara zake nyingine? Akauliza Mathew “Hapana sizifahamu” “Ikawaje ukamuuzia kampuni zako mtu ambaye humfahamu vyema?akauliza Mathew “Nilihitaji mnunuzi na alipojitokeza sikutaka kumchunguza mara mbili nikamuuzia” akajibu Peniela “Unafahamu yalipo makazi yake jijini Paris? Mathew akauliza “Mathew sihitaji maswali yako tena.Kama unahitaji kumfahamu mtafute wewe mwenyewe ukamuhoji ! akasema Peniela kwa ukali “Peniela I real need your help.Muda mfupi ujao nitakapoweka saini yangu katika hizi karatasi utakuwa ni mwisho wetu na mlango utafungwa.Only God knows when we’ll meet again hivyo basi huu ni msaada wangu wa mwisho ninakuomba unisaidie.Ni muhimu sana kwangu na ….” Akasema Mathew na Peniela akamkatisha “Melanie ana umuhimu gani kwako? Kwa nini unatafuta taarifa zake unamchunguza? Akauliza Peniela “Peniela nisingependa kukueleza chochote kwa sa…” “Kama hutanieleza sababu za kutafuta taarifa za Melanie sintakueleza chochote ninachokifahamu” akasema Peniela. “Arlight unataka kufahamu? Ni kwamba mtu uliyemuuzia makampuni yako hapa Tanzania Melanie Davis ana mahusiano na kikundi cha kigaidi cha IS na vile vile ana mashirikiano na James Kasai kiongozi wa kundi la waasi ambaye hivi karibuni alifanya shambulio hapa nchini ambalo liliua wake za marais wa Tanzania,Congo na Rwanda.IS wamekuwa wakimtumia Melanie kupitishia fedha kwenda kwa James Kasai.Umemuuzia mali mtu hatari kabisa kwa usalama wa nchi yetu” akasema Mathew na Peniela akabaki mdomo wazi na mara simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Dr Masawe. “Samahani nataka kuipokea hii simu” akasema Mathew na kuipokea ile simu “Dr Masawe” akasema Mathew “Mathew nimekupigia kukupa taarifa kwamba tumepokea taarifa muda mfupi uliopita kutoka polisi kwamba mwili wa Dr Sebastian umeokotwa ufukweni akiwa amekufa.Polisi wanasema alipigwa risasi ya kichwa” “Sebastian ameuawa! Mathew akashangaa “Ndiyo Mathew ameuawa” “Dr Masawe suala hili ni kubwa.Nitafika hapo hospitali tutazugumza kwa kirefu zaidi.Nashukuru sana kwa taarifa” akasema Mathew na kukata simu akamtazama Peniela. “Unafahamu kama Melanie na Gosu Gosu wana mahusiano ya kimapenzi?akauliza Mathew “Ndiyo ninafahamu.Ni mimi ndiye niliyewaunganisha.Nilimuita Gosu Gosu Ufaransa kwa ajili ya kufanya mauziano na Melanie na walipokutana wakapendana wakawa wapenzi” akasema Peniela “Tunahisi kwamba Gosu Gosu kuna kitu alikigundua kuhusu Melanie ndiyo maana wakataka kumuua.Alipigwa risasi nyingi ili afariki lakini siku yake haikuwa imefika akanusurika na jana likafanyika tena jaribio lingine la kutaka kumuua.Daktari mmoja alitumika kumchoma sindano ya sumu Gosu Gosu kwa bahati mbaya jaribio hilo la kumuua halikufanikiwa lakini imelazimu Gosu Gosu kufanyiwa upasuaji wa kupandikizwa ini jana usiku kwani ini lake liliharibiwa kabisa na sumu.Melanie ni mwanamke hatari kabisa hata wewe ujihadhari naye sana kwani mtandao wake ni mkubwa” akasema Mathew “Kwa hiyo hivi sasa unaendesha zoezi la kumsaka Melanie Davis?akauliza Peniela “Ndiyo.Ninamsaka Melanie Davis na ndiyo maana ninahitaji sana msaada wako” “Mathew unamtafuta Melanie kwa sababu anashirikiana na magaidi wa IS au kwa sababu amenunua mali zako? Peniela akauliza “Kwa mara nyingine tena Peniela nakukumbusha kwamba mimi sihitaji mali.Hizi zote ni mali zako na mimi nilikuwa msimamizi wake tu hivyo sina kinyongo chochote na Melanie kununua mali zangu.Nilikuwa naendelea na operesheni yangu ya kuwasaka magaidi na ndipo Melanie Davis alipojitokeza na nikaanza kumfuatilia na kugundua ndiye aliyenunua mali zangu. Sikuwa na sehemu nyingine ya kuweza kupata taarifa zake ila kwako ndiyo maana nikakupigia” akasema Mathew “Nilichokueleza ndicho kitu niachokifahamu kuhusu Melanie labda nitakusaidia kufanya uchunguzi na nikipata taarifa zozote za kumuhusu yeye nitakujulisha” akasema Peniela “Nitashukuru sana” akasema Mathew “Maswali yamekwisha can you sign now?akauliza Peniela Mathew akaishika kalamu na kumtazama Peniela kisha akaanza kusaini zile karatasi.Alipomaliza akazirudisha ndani ya bahasha na kumkabidhi Peniela “Ahsante Mathew na samahani sana kwa maamuzi haya ” akasema Peniela. “Usijali Peniela.Ninakupongeza kwa maamuzi haya magumu ambayo umeyafanya.Unahitaji furaha katika maisha yako na mimi si mtu sahihi ninayeweza kukupa hiyo furaha.Maisha yangu hayataweza kubadilika kamwe kwani nililetwa duniani kwa ajili ya kazi hii na nitandelea nayo hadi siku ya kufa kwangu.Ninakushukuru sana kwa kunivumilia kwa muda mrefu na samahani vile vile kwa kuwasababishia maumivu makubwa lakini halikuwa kusudi langu kuwaumiza.Ninachokuomba wakuze watoto katika maadili mazuri wawe na bidii katika masomo,wamjue Mungu wafundishe kusaidia watu wenye uhitaji kwa kuwa wao wamezaliwa katika utajiri mkubwa.Wasaidie kuhakikisha wanatimiza ndoto zao lakini kamwe,narudia tena kamwe usiruhusu mtoto wangu yeyote akafanya kazi kama ninayoifanya mimi.Sitaki waje kuishi maisha kama ninayoishi mimi.Sitaki wayapitie yale ninayoyapitia.Waweke mbali kabisa na dunia hii ninayoishi mimi.Nadhani umenielewa Peniela” akasema Mathew na Peniela akafuta machozi “Nimekuelewa Mathew na mimi pia ninakuomba samahani sana kila pale nilipokukosea.Najua sikuwa mkamilifu nimekukwaza mara nyingi,tuliwahi kutengana na mimi nilikuwa chanzo,nimewahi kuwa na mahusiano na wanaume kadhaa ulifahamu lakini ulinivumilia.Nisamehe sana kwa yote” akasema Peniela “Hakuna mwanadamu mkamilifu.Sote tuna mapungufu yetu na mimi niliyafahamu mapungufu yako nikayakubali na kuyabeba.Nategemea Yule atakayekuja baada yangu naye atakuwa mvumilivu kama mimi.Ninakutakia kila la heri Peniela”akasema Mathew na kusimama “Mathew kabla hatujapeana kwa heri ya kuonana kuna kitu nataka kukifahamu.Ulizungumza kuhusu Nahum.Umemfahamuje?Ulifa hamuje kama mimi na yeye tulikuwa na mahusiano?akauliza Peniela na Mathew akaketi “Haitakuwa na umuhimu wowote tena kwako kwa sasa lakini kwa umeuliza nitakueleza ukweli wa kile kilichotokea” akasema Mathew na kumsimulia kuanzia Olivia Themba alivyotekwa na SNSA,sakata la Edger Kaka na hadi operesheni ile ya kuwakomboa mateka waliotekwa na IS na hadi alivyopigwa risasi na kutekwa.Mashavu ya Peniela yaliloa machozi “Nilipofumbua macho nilijikuta katika chumba chenye kiza na baadae nikagundua nilikuwa nchini Israel. Nilianza kupatiwa mateso makali na nimeteswa kwa muda wa miaka mitatu” akasema Mathew na kuvua fulana akamuonyesha Peniela makovu ya vidonda vilivyotokana na mateso aliyoyapata.Peniela akafumba macho hakutaka kutazama.Mwili wa Mathew ulijaa makovu ya vidonda. “Haya ndiyo niliyoyapitia huko Israel kwa miaka mitatu.Sikumbuki ni mara ngapi nilipoteza fahamu wakati nikiteswa lakini ni mara nyingi.Pamoja na mateso hayo makali lakini sikuwahi kufungua mdomo wangu kusema chochote na ndipo walipoamua kuitumia familia yangu kunilazimisha niongee.Wakamtuma Nahum Yatom aje Ufaransa aanzishe mahusiano nawe na lengo lake likafanikiwa.Nahum alikuwa ni jasusi kutoka shirika la ujasusi la Israel Mossad.Hakuwa na malengo yoyote nawe bali alikuwa kazini.Zilifungwa kamera chumbani kwako na Mossad walikuwa wanafuatilia kila mlichokuwa mnakifanya na Nahum.Nilionyeshwa mkiwa chumbani mkifanya mapenzi na Nahum nikaumia sana na Mossad walikuwa wakihitaji niumie ili niweze kuzungumza na kwa maumivu niliyokuwa nayo nikajikuta nikianza kuzungumza” akasema Mathew “It was true then ….” Akasema Peniela akifuta machozi “Nini Peniela? “Kabla ya kuuawa Nahum aliniambia uko hai nikutafute lakini nikapuuza maneno yake” “Alikwambia hivyo?akauliza Mathew “Ndiyo aliniambia hivyo” akajibu Peniela “Nani alimuua Nahum?Mathew akauiza “Hadi leo hii haijulikani nani waliomuua” “Lazima atakuwa ameuawa na Mossad” akasema Mathew “Mathew I’m sorry sikuyafahamu hayo yote uliyoyapitia” akasema Peniela “Usijali Penny yamekwisha pita ila nakuomba usimueleze mtu yeyote haya niliyokueleza” “Sintamueleza mtu yeyote Yule” akasema Peniela “Naamini sasa utakuwa huru Peniela jitahidi uwe na furaha katika maisha yako.Usiwaze chochote kuhusu mimi.Maamuzi haya uliyoyafanya ni maamuzi sahihi kwa wakati sahihi” akasema Mathew na Peniela akaendelea kulia. “Mathew please I need a hug” akasema Peniela na Mathew akainuka akaenda kumkumbatia. “Mathew I’m very sorry ! akasema Peniela akilia na kumwaga machozi katika bega la Mathew “Peniela unahitaji kuwa jasiri wala usisikitike kwa maamuzi haya uliyoyachukua” akasema Mathew na kumuachia Peniela. “Unarejea leo Paris?Mathew akauliza “Nimekuja na ndege yangu ninaondoka leo hii kurejea Paris.Kabla sijaondoka naomba unipeleke nikamuone Gosu Gosu” akasema Peniela na Mathew akamuogoza hadi katika gari lake wakaondoka kuelekea hospitali kumtazama Gosu Gosu. “Watoto wanaendeleaje?akauliza Mathew “Kwa sasa wametulia wanaendelea vizuri na masomo na maisha yao kwa ujumla lakini kwa miaka miwili hapo nyuma walikuwa wameathiriwa sana na kifo chako” “Ndiyo maana sitaki wafahamu chochote kuhusu mimi kuwa hai kwa sasa hadi hapo baadae.Nakuomba tena usiwaeleze chochote kuhusu mimi” akasema Mathew “Sintawaeleza chochote kwani watachanganyikiwa zaidi” “Peniela …” akaita Mathew “Unasemaje Mathew? “Naomba ufahamu hayakuwa mategemeo yangu maisha yetu yawe namna hii.Sikutegemea kama siku moja tungemaliza mahusiano yetu namna h……” akasema Mathew na Peniela akamkatisha “Mathew tumekwisha yamaliza hayo kitu cha msingi ni kutazama yale ya mbele yetu.Muda wowote ukihitaji kitu chochote tafadhali usisite kuniambia.Namba yangu ya simu ni ile ile”akasema Peniela “Am I doing the right thing?akajiuliza Peniela na kumtazama Mathew kwa jicho la wizi “Namuonea huruma sana Mathew kwa mambo anayoyapitia.Mwili wake umeumizwa vibaya sana hadi nilisisimkwa mwili nilipoyaona makovu yale katika mwili wake.Sikuufahamu ukweli na nikadhani alitengeneza kifo chake kumbe alikuwa katika mateso.Nimechanganyikiwa.N ifanyaje wakati tayari amekwisha saini hizi karatasi?Nilimtamkia maneno mabaya sana yaliyomuudhi hadi akaamua kunipiga kitu ambacho hajawahi kukifanya toka tumekuwa wapenzi.I was so stupid.Nilikurupuka sana kufanya maamuzi kama haya kwa mtu kama huyu ambaye amekwisha fanya mambo mengi sana kwa ajili yangu.Amesimama nami katika nyakati ngumu ambazo hakuna aliyewezaa,amenivumilia kwa mengi,huyu ni mwanaume wa kipekee kabisa na ninaumia kwa hiki nilichokifanya lakini maamuzi haya ni kwa faida yetu sote.Mathew amechagua kuendelea na kazi yake ya ujasusi” akaendelea kuwaza Peniela. Walifika katika hospitali kuu ya Mtodora alikolazwa Gosu Gosu.Mathew akafanya mpango na Peniela akaruhusiwa kuingia kwenda kumuona Gosu Gosu akamwaga machozi alipomuona akiwa amelala kitandani hana fahamu.Baada ya kutoka kumuona Gous Gosu Mathew akampeleka katika chumba alimolazwa Austin akamtambulisha kwa Peniela. “Huyu ndiye aliyejitolea sehemu ya ini alilopandikizwa GosuGosu” akasema Austin na Peniela akamshukuru kwa kile alichokifanya.Baada ya zoezi hilo kukamilika Peniela hakuwa na kitu cha ziada ulikuwa ni wakati wake wa kuondoka kurejea Paris.Mathew akamsindikiza uwanja wa ndege “Nimeumizwa sana na hali ya Gosu Gosu.Nakuahidi nitakwenda kutafuta taarifa za kuhusu Melanie Davis na nitakujulisha” akasema Peniela wakiwa garini “Ahsante sana” akasema Mathew Hakukuwa na mazungumzo mengi garini hadi walipofika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Mathew akashuka na kumfungulia Peniela mlango “Penny this is it.” Akasema Mathew “Mathew thank you for everything” akasema Peniela wakakumbatiana na kwa mara ya mwisho Mathew akambusu Peniela “Please go and don’t look back” akasema Mathew na Peniela akaelekea ndani ya jengo la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere huku machozi yakimdondoka. Mathew hakuondoka pale uwanjani hadi alipoiona ndege ya Peniela yenye maandishi makubwa Penny air ubavuni, ikipaa na kuondoka. “Kwa heri Peniela”akasema Mathew na kuingia katika gari lake akaondoka. “Naona kama ndoto lakini ni kweli nimeachana na Peniela.Nimetoka naye mbali,tumepitia mengi na hatimaye safari yetu imehitimishwa rasmi leo.Inaniumiza kuacha na mtu ambaye niliahidi kuishi naye hadi kifo lakini ahadi hiyo imeshindwa kutimia” akawaza Mathew Kutoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akarejea nyumbani kwake akaenda moja kwa moja chumbani kwake na kuchukua albamu lenye picha mbali mbali alizowahi kupiga na Peniela na familia yake. “Tumewahi kuwa na nyakati nyingi nzuri lakini kwa sasa sina hakika kama ninaweza tena kumfanya Peniela awe na furaha.Siwezi kumlaumu kwa maamuzi aliyoyachukua.Natakiwa kusonga mbele na maisha yangu” akawaza Mathew na kumpigia simu Ruby akamjulisha kilichotokea kati yake na Peniela na Ruby akamuahidi kwamba atamfuata nyumbani kwake. Ndege ya Peniela ilipokaa sawa angani akachukua simu yake ya intaneti akampigia mtu Fulani na simu ikapokelewa “Peterson ni mimi Peniela.Ninapozungumza nawe hivi sasa niko Afrika.Niliondoka jana jioni lakini kwa sasa niko angani narejea Paris”akasema Peniela “Peniela pole kwa safari ndefu” akasema Yule jamaa aliyekuwa akizungumza na Peniela simuni “Nashukuru Peterson.Nimekupigia simu kuna kazi muhimu nataka unisaidie kuifanya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Kuna mtu mmoja anaitwa Melanie Davis.Huyu anatajwa kuwa mmoja wa mabilionea wa jiji la Paris.Nataka umfanyie uchunguzi wa kina na kesho asubuhi uniletee ripoti nyumbani” akasema Peniela “Peniela nini hasa unachotaka tukichunguze kwa huyo Melanie Davis? Akauliza Peterson “Kila kitu kuhusu maisha yake.Ametokea wapi,wazazi wake,anakoishi hapa Paris,anafanya biashara gani na ziko wapi,akaunti zake za benki,marafiki zake ni akina nani wanafanya nini n.k.Nataka kujua kila kitu mnachoweza kukipata kuhusu Melanie”akasema Peniela “Sawa mama Peniela.Hiyo ni kazi ndogo sana kwetu.Kesho saa kumi na mbili za asubuhi nitakugongea mlango kukupa ripoti” akasema Peterson na kuagana na Peniela “Ngoja niwatumie hawa wapelelezi wa kujitegemea kumchunguza Melanie.Mathew amenistua sana kuniambia kwamba anashirikiana na magaidi wa IS.Lakini Melanie ni mwanamke mwenye uzuri wa kipekee kabisa kwa nini anashirikiana na magaidi wa IS?Kinachoniumiza zaidi ni kwamba anajificha nyuma ya biashara nilizomuuzia kutekeleza mambo yake.Mathew aliniambia kwamba amekuwa akipokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka IS.Yawezekana ni fedha hizo hizo ndizo ambazo alizitumia kununulia kampuni nilizomuuzia.Imeniuma sana na ninajiona mjinga.Niliona aibu kubwa mbele ya Mathew aliponiuliza sababu ya kuuza mali zetu kwa mtu anayeshirikiana na magaidi.” akawaza Peniela na sura ya Mathew ikamjia akaanza kutiririkwa machozi “Mathew amepitia mateso makubwa sana kwani mwili wake wote umejaa makovu ya vidonda vilivyotokana na mateso makali aliyokuwa akiteswa.Kwa nini lakini Mathew ameamua kuchagua kuendelea kufanya kazi hii na kuacha maisha mazuri aliyokuwa akiishi?akajiuliza Peniela “Mathew amenifanya niwachukie magaidi na watu wanaowasaidia kama akina Melanie kwani ndio waliomfanya Mathew ashindwe kutulia na kutumia muda wake mwingi akihangaika kupambana nao hadi kufikia hatua hii ya kutengana” akawaza Peniela







    Ruby alifika nyumbani kwa Mathew saa kumi na mbili na nusu za jioni “Samahani Mathew nimechelewa sana nilikuwa nafuatilia maandalizi ya zoezi la jioni ya leo.Kila kitu kimekwisha andaliwa” akasema Ruby wakaelekea katika ofisi ya Mathew na Ruby akajiunga na ofisi yao na picha kutoka katika kamera mbali mbali katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere zikaanza kuonekana. “Tayari vijana wamejipanga vizuri.Wapo walioko ndani kabisa ya uwanja na katika sehemu mbali mbali za uwanja na Khalid atafuatiliwa toka atakaposhuka uwanjani hadi atakapoingia ndani ya gari na watu wetu wengine wamejipanga sehemu mbali mbali.Kwa ujumla maandalizi yote yamekamilika” akasema Ruby Saa moja na dakika tano za jioni ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Lango la ndege likafunguliwa abiria wakaanza kushuka.Edwin Mbeko ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza operesheni ile kutoka ofisi kuu ya SNSA akawataka watu wake wakae makini.Hatimaye Yule aliyekuwa akisubiriwa akatokeza katika mlango wa ndege.Alikuwa amevaa suti ya rangi ya bluu “Khalid Sultan anashuka ndegeni.Narudia Khalid Sultan anashuka ndegeni” mmoja wa watu wa SNSA aliyekuwa ndani ya uwanja akawajulisha ofisi kuu “Tumekupata namba 3.Endelea kumfuatilia.Namba 5 jiandae Khalid anaelekea upande wako” akaelekeza Edwin Mbeko. Khalid Sultan aliingia ndani ya jengo la uwanja wa ndege kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuingia nchini.Baada ya kukamilisha taratibu Khalid akaruhusiwa kuingia Tanzania. “Khalid tayari ameruhusiwa kuinga nchini anaelekea sehemu ya abiria wanaowasili” akasema jamaa mwingine aliyekuwamo ndani ya jengo la uwanja. Kamera za ndani ya sehemu ya abiria wanaowasili ilimuonyesha Khalid akiingia kisha akapokewa na vijana wawili wadogo waliokuwa wameshika bango lenye jina la KSK.Wakasalimiana na kumsaidia kuyabeba masanduku yake kuelekea katika maegesho. “Khalid anatoka nje ya uwanja anaelekea eneo la maegesho ya magari” akaripoti jamaa mwingine “Endeleeni kumfuatilia” akaelekeza Edwin “Kwa nini Khalid amepokewa na vijana wale wadogo?Nilitegemea angepokewa na watu wazima” akasema Ruby kwa mshangao lakini Mathew hakumjibu kitu Vijana wale wawili walimuongoza Khalid hadi katika gari moja aina ya Prado rangi nyeupe wakaingia na kuondoka pale uwanjani. “Khalid anaondoka hapa uwanjani” jamaa aliyekuwa nje eneo la maegesho ya magari akaripoti “Namba nane na timu yako kazi kwenu anzeni kumfuatilia.Mtu huyu ni makini sana hivyo mjitahidi kuweka umbali kati yenu ili asijue kama anafuatiliwa.Mtamfuatilia kwa msaada wa Satelaiti” akaelekeza Edwin Wakati zoezi la kumfuatilia Khalid likianza Ruby alikuwa anashughulikia kuzitambua picha za wale vijana wawili waliompokea Khalid uwanja wa ndege na baada ya muda akaguna. “Vijana wale ni wadogo na inaonekana hawajafikia umri wa kusajiliwa katika sehemu mbali mbali za usajili kwa ajili ya kupata vitambulisho vya taifa leseni nk.” Akasema Ruby.Bado Mathew hakumjibu kitu alikuwa kimya kabisa Katika runinga mchoro mwekundu na wakijani iliendelea kuonekana ikijongea.Mchoro mwekundu ukiwa ni wa gari alilopanda Khalid na mchoro wa kijani ukiwa ni wa gari la SNSA linalomfuatilia Khalid. “Mmelikaribia sana gari la Khalid tafadhali acheni umbali kidogo” Edwin Mbeko akatoa maelekezo. Gari lile alilopanda Khalid lilipita barabara kadhaa na halafu likafika katika mzunguko wa chama.Ghalfa mawasiliano yakakatika. “Nini kimetokea?Mathew akamuuliza Ruby “Sifahamu.Mawasiliano yamekata ghafla” akasema Ruby na kuchukua simu yake akampigia Edwin “Edwin kompyuta yangu imekata mawasiliano ghafla.Kuna tatizo lolote huko?akauliza Ruby “Madam Annabel kuna tatizo limetokea si kwako tu bali hata huku.Kuna matatizo katika satelaiti tunayotumia na timu imeanza kulishughulikia hilo tatizo” akasema Edwin “Kuna tatizo limetokea katika satelaiti na wanalishughulikia” Ruby akamwambia Mathew ambaye alipiga meza kwa hasira “Usikasirike Mathew.Wanashughulikia suala hili na muda si mrefu litakuwa tayari” akasema Ruby “Ofisi kuu kuna tatizo gani?Mawasiliano yamekatika ghafla hatulioni tena gari la Khalid” akasema kiongozi wa timu iliyokuwa ikimfuatilia Khalid. “Kuna tatizo limetokea lakini linashughulikiwa na muda si mrefu mawasiliano yatarejea tena” akasema Edwin Baada ya dakika mbili mawasiliano yakarejea lakini mduara uliokuwa ukionekana ni mmoja tu wa kijani ambao ni gari la SNSA, gari alilopanda Khalid halikuwa likionekana “We’ve lost him ! Tumempoteza Khalid.How could they let this happen?! Mathew akafoka “I don’t know Mathew” akajibu Ruby kwa uoga kisha akampigia simu Edwin hakupokea.Akampigia tena simu mtu mwingine akapokea na kumjulisha kwamba Edwin alikuwa na timu ya ufundi wakijaribu kujua nini kilitokea “Ruby do something ! akasema Mathew “Nadhani natakiwa niende ofisini nikajue nini hasa kilitokea” “Hata kama ukienda bado haitasaidia kitu.Khalid tumekwisha mpoteza.Dakika mbili ni nyingi sana kwa gari.Hatutaweza kumpata mida hii.Kwa nini tatizo hili limejitokeza sasa wakati wa zoezi muhimu kama hili? Akauliza Mathew “Mathew matatizo kama haya ya kukatika mawasiliano hutokea mara nyingi” akasema Ruby “Nafahamu Ruby lakini..oh my God ! akasema Mathew na kushika kiuno “Jaribu kufuatilia zile namba za gari alilopanda Khalid” akasema Mathew na Ruby akacheza na kompyuata yake baada ya muda akasema “Namba zile ni bandia hazipo hazijulikani katka mfumo wa usajili wa namba za magari” akasema Ruby “Dah ! Mathew akasema na kukaa juu ya meza.Akafikiri halafu akasema “Ruby nisikilize” “Hili suala lililotokea halikutokea kwa bahati mbaya.Huu ni mchezo umechezwa” “Mathew tusifike huko kwanza.Hii yaweza kuwa ni hitilafu ya kiufundi imetokea.Tusubiri timu ya ufundi ifanye uchunguzi wake na tutagundua nini hasa kilitokea” akasema Ruby “Ruby nafahamu hitilafu kama hizi huwa zinatokea lakini hiki kilichotokea usiku huu na tukampoteza Khalid si bahati mbaya.Hiki ni kitu kilichopangwa” akasema Mathew “Nani anaweza akafanya kitu kama hiki?akauliza Ruby “Hebu jiulize kwa nini wametumwa watoto wadogo kwenda kumpokea Khalid? Ni kwa sababu walifahamu kuwa Khalid anafuatiliwa na mtu ambaye angeenda kumpokea angechunguzwa yeye ni nani ndiyo maana wakawatumia wale watoto kwenda kumpokea ambao hatuwezi kuwatambua.Khalid ni mtu mkubwa na hawezi kupokewa na wale watoto wadogo.Kama haitoshi namba za gari lile alilopanda Khalid ni za bandia na waliweka namba hizo bandia ili tusiweze kumtambua mmiliki wa gari hilo.Walijua tunamfuatilia na ndiyo maana wakajiandaa namna hii.Huu ni mtandao mkubwa Ruby una watu makini na wanajua wanachokifanya.Walifahamu tunamfuatilia Khalid ndiyo maana mawasiliano yakakatika na hilo lilifanyika ili kulipoteza gari la Khalid kwani mawasiliano yaliporejea gari lile halikuonekana tena.Tunachotakiwa kujiuliza ni je wamefahamuje kama tunamfuatilia Khalid? Wamefahamuje mipango yetu? Wamewezaje kukata mawasiliano kati ya ofisi kuu na timu iliyokuwa inamfuatlia Khalid? Akauliza Mathew na baada ya kufikiri kidogo Ruby akasema “Nadhani tuanze kulitafutia majibu hili swali la mwisho ulilouliza kwamba mawasiliano yamekatikaje? Akasema Ruby “Kwa ninavyofahamu mimi mfumo wa mawasiliano wa idara kama hii umejengwa katika mfumo ambao si rahisi kwa mtu wa nje kuuingilia na kufanya chochote anachokitaka.Imetumika teknolojia ya hali ya juu sana” “Unataka kuniambia kwamba mtu wa nje hawezi kuingia katika mfumo na kukata mawasiliano kati ya ofisi kuu na watu walioko nje ya ofisi? Akauliza Mathew “Hapana haiwezekani.Ili kukata mawasiliano kati ya ofisi kuu na watu walioko nje ya ofisi lazima kwanza mfumo ukutambue hapa ninamaana ya kwamba lazima uwe ndani ya mfumo wetu ndipo unaweza ukafanya kitu kama hiki kilichofanyika” akasema Ruby “Kwa maana hiyo kama mawasiliano yalikatwa makusudi mtu aliyefanya hivyo lazima atakuwa anatoka ndani ya SNSA” akasema Mathew “Ndiyo” akasema Ruby “Mathew nina….” Akasema Ruby na kunyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni Edwin “Edwin ! akasema Ruby “Madam Annabel samahani nilishindwa kupokea simu yako uliponipigia.Nilikuwa na timu ya wataalamu tukifuatilia kujua nini hasa kilichotokea na kusababisha mawasiliano kukatika.Kwa mujibu wa wataalamu wetu ni kwamba lilikuwa ni tatizo la kawaida ambalo linaweza kutokea kufuatia hali mbaya ya hewa na hakukuwa na makosa yoyote ya kibinadamu” akasema Edwin “Sawa Edwin hakikisha jambo kama hili halitokei tena siku nyingine hasa tunapokuwa katika operesheni kubwa kama hizi.Mmefikia wapi katika kumsaka Khalid?Kuna mafanikio yoyote? “Mpaka sasa hakuna madam na hatujui mahala alikoelekea kwa sababu mahala pale ambako mawasiliano yalikatikia pana njia nne hivyo hatujui njia ipi gari lile lilielekea.Tunaendelea na uchunguzi madam kujua mahala alikoelekea.Ninaamini tutalipata tu lile gari” akajibu Edwin “Edwin hakikisha ndani ya muda mfupi tunfahamu mahala aliko Khalid” “Usijali madam tunaendelea na zoezi hilo” akajibu Edwin na Ruby akakata simu akamueleza Mathew kile alichoambiwa na Edwin. “Ruby ninaamini mno utaalamu wako katika masuala haya ya kompyuta na mawasiliano kuliko mtu mwingine yeyote na ndiyo maana hata kule Uingereza ulikokuwa unafanya kazi hawakutaka kukuacha uende.Sina hakika kama ndani ya idara ya SNSA kuna mtu mwenye utaalamu mkubwa wa kompyuta kama ulio nao wewe.Nataka ulifanyie uchunguzi suala hili ili tujue kama kweli ni tatizo la kukatika kwa mawasiliano kama inavyodaiwa?akasema Mathew “Ushauri wako ni mzuri Mathew.Itanilazimu sasa nielekee ofisini na uchunguzi huo nikaufanyie nikiwa pale ndipo nitakapoweza kujua nini hasa kimetokea.Ninakuomba twende wote” akasema Ruby “Mimi si mfanyakazi wa SNSA hivyo nikionekana pale haitaleta picha nzuri kwako utaonekana unaleta ndani ya idara watu wasiohusika” akasema Mathew. “Mimi ndiye mkuu wa idara hivyo usiwe na wasiwasi wowote”akasema Ruby.Hawakupoteza muda wakaingia katika gari la Ruby wakaondoka kuelekea ofisi kuu ya SNSA.



    Baada ya mawasiliano kukatika kati ya ofisi kuu ya SNSA na timu iliyokuwa ikimfuatilia Khalid Sultan,jamaa aliyekuwa katika usukani wa gari lile alilopanda Khalid ambaye aliweka kifaa Fulani sikioni kwa ajili ya mawasiliano akaelekezwa kuendelea na mpango kama ulivyokuwa umepangwa.Dereva Yule akaelekea katika barabara ya Arusha halafu akakata kulia akaingia mtaa wa Mtepa akaingia katika shule moja ya watoto wadogo.Khalid na watu wengine wawili wakashuka na kuingia katika gari lingine lenye rangi nyeusi,likatoka ndani ya ile shule na kuelekea Kisulo Car wash Khalid na watu wale wawili wakashuka na kuingia katika gari ambalo kulikuwa na dereva mwanamke ambaye aliliondoa lile gari mahala pale.Safari ilikuwa ya kimya kimya hadi walipofika katika makazi ya Melanie Davis geti likafunguka gari likaingia ndani.Khalid na wale jamaa wawili wakashuka garini wakapokewa na Melanie Davis akawakaribisha ndani. “Khalid karibu sana Tanzania,karibu sana Dar es salaam.Utatusamehe kwa mzunguko mrefu hii ni kwa sababu za kiusalama”akasema Melanie “Ninawapongezeni kwa tahadhari kubwa mlizozichukua.Ninyi ni watu makini sana nimefurahishwa na umahiri wenu katika kuhakikisha ninakuwa salama” akasema Khalid wakitumia lugha ya kiingereza “Khalid kwa kuwa umefika salama nadhani ningekupeleka chumbani kwako ukaoge kisha tupate chakula halafu mazungumzo yataanza” “James Kasai amekwisha fika?akauliza Khalid “James Kasai amekwisha wasili yuko chumbani kwake akipumzika.Utaonana naye baadae” akasema Melanie na kumpeleka Khalid katika chumba alichoandaliwa kisha akarejea sebuleni walikokuwa wale watu wawili waliokuja na Khalid. “Madam sisi tumemaliza kazi yetu tuliyopewa ambayo ilikuwa ni kuhakikisha mgeni anafika hapa salama na sasa tunaweza kuondoka”akasema mmoja wa wale jamaa. “Ahsanteni sana kwa kumfikisha mgeni salama.”akasema Melanie na kumtaka Joyce dereva wake awapeleke wale wageni. Baada ya Khalid kuoga akaelekea sebuleni ambako alikutana na James Kasai.Wakasalimiana kwa furaha “Nimefurahi sana kukutana nawe James”akasema Khalid “Mimi pia” akasema James Melanie akawapeleka katika chumba cha chakula wakapata chakula cha usiku pamoja.Wakati wakipata chakula Edwin Mbeko akawasili na kujumuika na akina Melanie mezani kwa chakula.





    Ruby na Mathew waliwasili ofisi kuu ya SNSA wakashuka garini na kuelekea moja kwa moja katika ofisi ya Ruby ambako Mathew alikaribishwa kisha Ruby akatoka na kumfuata Edwin ofisini kwake. “Karibu madam” akasema Edwin “Edwin nataka kufahamu mahala mlikofikia hadi sasa katika kumtafuta Khalid” akasema Ruby “Madam mpaka sasa bado hatujafanikiwa na mimi ninajiandaa kwenda kuungana na timu ya nje kuendelea na zoezi la kumsaka Khalid.Hatutalala leo hadi tuhakikishe Khalid amepatikana” “Nataka nipate taarifa ya wataalamu wetu kuhusiana na namna tukio lile la kukatika mawasiliano lilivyotokea” akasema Ruby “Madam awali tulidhani labda kuna mkono wa mtu katika tukio lile lakini baada ya wataalamu wetu kufanya uchunguzi wao wanasema kwamba ni hali mbaya ya hewa ndiyo iliyopelekea tukio lile kutokea” akasema Edwin “Sawa Edwin.Namtaka mkuu wa idara ya ufundi ofisini kwangu mara moja” akasema Ruby na kuelekea katika ukumbi mkubwa ambako kazi zilikuwa zinaendelea. “Naomba mnisikilize tafadhali” akasema Ruby na watu wote wakaacha shughuli zao na kumgeukia Ruby. “Asubuhi niliwaeleza kuhusiana na ujio wa Khalid Sultan Khalid na namna gani mtu huyo alivyo hatari kwa nchi yetu.Niliwaeleza kwamba mtu huyu anatoka IS na ni mtaalamu wa milipuko mikubwa na niliweka wazi hofu yangu kwamba kuna uwezekano mkubwa IS wanaandaa tena shambulio lingine kubwa hapa nchini ndiyo maana Khalid amekuja nchini.Pamoja na kujipanga vizuri sana kumfuatilia Khalid lakini teknolojia imetuangusha na tumejikuta tukimpoteza Khalid bila kutarajia na sasa tuna kazi nyingine kubwa ya kumsaka Khalid na kujua mahala alipo.Lazima tufanye kila tuwezalo kuhakikisha tunampata Khalid.Uwezo huo tunao kwani tunao uwezo wa kuona asilimia tisini ya kamera zote za usalama zilizoko barabarani,tunao uwezo wa kudukua mitandao yote ya simu hapa nchini hivyo hatuna sababu yoyote ya kutufanya tushindwe kufahamu mahala alipo Khalid.Tumieni kila tulichonacho katika idara yetu kuhakikisha Khalid anapatikana.Edwin anakwenda kuungana na timu ya nje kuendelea na zoezi la kutafuta mahala aliko Khalid na sisi tulioko hapa tuendelee pia na zoezi hilo.Tunakesha hapa usiku wa leo hakuna mtu atakayeondoka kwenda nyumbani hadi tuhakikishe Khalid anapatikana” akasema Ruby kisha akaelekea ofisini kwake.Mara tu alipoingia ofisini Fidelis mkuu wa idara ya ufundi akaingia Ruby akamchukua wakaelekea katika chumba kidogo cha mazungumzo kilichokuwa pembeni ya ofisi ile ya Ruby. “Fidelis wewe ndiye mkuu wa idara ya ufundi nataka uniambie nini hasa kilichotokea na kusababisha mawasiliano yakakatika hadi tukampoteza mtu muhimu kabisa?akauliza Ruby na Fideli akaanza kumuelezea kile alichokigundua katika uchunguzi wake.Wakati wakiendelea na mazungumzo akaingia Edwin na kumkuta Mathew akiwa ameketi sofani akamsalimu halafu akafungua mlango wa kioo wa chumba walichokuwamo Ruby na Fidelis wakizungumza. “Madam ninaondoka ninakwenda kuonana na vijana kuendelea na lile zoezi” akasema Edwin “Sawa Edwin .Nataka mawasiliano ya mara kwa mara tafadhali”akasema Ruby na Edwin akatoka. Baada ya takribani dakika ishirini za mazungumzo Fidelis akatoa ofisini kwa Ruby. “Watu wa idara hii hawajanifahamu vyema mimi ni nani”Ruby akamwambia Mathew baada ya kutoka kuzungumza na Fidelis “Huyu jamaa aliyetoka hapa muda mfupi uliopita anaitwa Fidelis ni mkuu wa idara ya ufundi.Baada ya tukio lile kutokea huyu jamaa na timu yake ndio waliochunguza kujua kilichotokea.Nilimuita hapa ili anieleze kwa kina nini hasa kilichotokea lakini maelezo anayonipa hayaingii akilini ni kama vile anampa maelezo mtu ambaye hana ujuzi wowote wa kompyuta.Kwa bahati nzuri hapa idarani hakuna anayejua uwezo wangu katika mambo haya ya teknolojia ya kompyuta” akasema Ruby “It’s time to show them who you real are.Mimi bado naamini kabisa kwamba kuna kitu hapa katika lile tukio” akasema Mathew “Mathew ninataka kulishughulikia suala hili na nitakuomba univumilie hadi pale nitakapomaliza kazi yangu” “Usijali Ruby endelea na kazi yako.Tunahitaji sana kuufahamu ukweli” akasema Mathew “Thank you my love” akasema Ruby huku akitabasamu kisha akaanza kazi katika kompyuta yake.





    Baada ya kupata chakula Melanie akawaongoza akina Khalid katika chumba cha mazungumzo. “Khalid na James Kasai karibuni sana Tanzania karibuni sana Dar es salaam” akasema Melanie “Melanie ninashukuru sana kwa mapokezi mazuri sana hadi mkanifikisha hapa.Nilisema pale awali na ninarudia tena kwamba ninyi ni mahiri sana katika mipango yenu.Mnastahili pongezi kubwa.Ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania na sikutegemea kukutana na watu wenye ujuzi mkubwa namna hii kama ninyi.Kingine ambacho kilinipa mawazo mengi sana ni kama James Kasai angeweza kuingia hapa nchini kufuatia kutafutwa sana na nchi za Afrika mashariki kutokana na lile shambulio la hivi majuzi.Nilipoambiwa kwamba tayari yuko hapa nchini sikuamini hadi pale nilipomtia machoni.Ninajisikia fahari kufanya kazi na watu kama ninyi.Kama mmeweza kufanikisha kumuingiza James Kasai nchini Tanzania licha ya ulinzi mkali ulioko mipakani na kila sehemu basi mnaweza kufanya kitu chochote hapa nchini” akasema Khalid “Ahsante sana kwa pongezi Khalid.Tunao uwezo wa kufanya chochote hapa nchini lakini haya yote yanawezekana kwa sababu ya huyu mtu hapa” akasema Melanie na kumshika bega Edwin “Anaitwa Edwin Mbeko.Huyu ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi.Yeye ndiye anayechukua nafasi kubwa katika haya yote yanayoendelea hivi sasa.Hata katika mipango yetu yote tutakayoipanga huyu ndiye hasa ambaye ataitekeleza” akasema Melanie “Hongera sana Edwin.Kazi yako tumeiona.Ni kazi nzuri sana” akasema Khalid. “Nadhani sasa tuendelee na mazungumzo” akasema Melanie “Nmeelekezwa nije Tanzania na wakuu wangu kwamba kuna kazi ya kufanya lakini sijui ni kazi gani kwa hiyo ninyi ndio mnaotakiwa mnipe taarifa ni kitu gani hasa nimekuja kukifanya huku Tanzania” akasema Khalid na Melanie akampa ishara James Kasai aendelee. “Jambo kubwa ambalo limetukutanisha hapa ni kujadiliana kuhusu mpango wa kuwaua marais wa Tanzania na Congo kwa bomu la kujitoa mhanga” akasema James Wakati mazungumzo ya kuhusu mpango wa kuwaua marais Dar Fabian Kelelo na Patrice Eyenga yakiendelea nyumbani kwa Melanie Davis, katika ofisi kuu ya SNSA Ruby aliendelea na zoezi la kujaribu kutafuta chanzo cha mawasiliano kukatika ghafla na kupelekea Khalid kupotea.Dakika arobaini zimekwisha pita toka alipoanza zoezi hilo.Mathew Mulumbi badi alikuwa ofisini kwa Ruby akisubiri zoezi lile limalizike.Mawazo yake yalikuwa mbali sana.Kichwa chake kilijaa mawazo ya namna walivyoachana na Peniela.Alikumbuka historia yao walikotoka mambo waliyopitia na hadi walivyoachana. “Mambo yanayokuja kichwani kwangu kuhusu mimi na Peniela ni kama ninatazama filamu lakini hii si filamu bali ni kitu cha kweli kabisa.Ni maisha halisi ambayo mimi na Peniela tumeyaishi.Tulikuwa na mipango mingi sana ya siku za usoni lakini yote hatawezekana tena” akawazaMathew “Sasa niko huru wa kuwa na mwanamke mwingine na kama nikiambiwa nichague basi Ruby anafaa sana kuchukua nafasi ya Peniela lakini je ni vipi kama yatamkuta kama yale ya Peniela je ataweza kuvumilia au nitakuwa ninamuumiza huyu binti malaika?Kila ninapomtazama Ruby ninapata mawazo mengi sana.Najua ananipenda na mimi pia ninampenda lakini…....” “Mathew ulikuwa sahihi”akasema Ruby na kumtoa Mathew mawazoni akasimama “Unasemaje Ruby?akauliza “Ulikuwa sahihi.Mawasiliano kukatika hakukusababishwa na hali ya hewa kama inavyodaiwa bali ni kitendo kilichofanywa na mtu kwa makusudi” “Oh my God ! Unaweza ukafahamu nani aliyefanya hivyo?akauliza Mathew.Ruby akaendelea kubonyeza kompyuta yake na baada ya dakika tatu akasema “Tatizo hilo lilitokea katika stesheni 5” akasema Ruby na kufungua faili Fulani “Stesheni 5 ni ya mtu anaitwa Edina Mkwena” “Ruby are you sure? Mathew akauliza “I’m sure”akasema Ruby “Jambo hili lilifanywa kitaalamu sana lakini kwa bahati mbaya hawakujua kama mimi ni mtaalamu zaidi yao.Hawafahamu kama nimeanza kucheza na kompyuta toka nikiwa na miaka minne na kwa maisha yangu yote ndicho kitu ambacho nimekuwa ninakifanya.Nilifanya vyema kutojitambulisha kwao uwezo wangu na sasa tumeanza kupata picha ya namna mambo yanavyokwenda katika idara hii” akasema Ruby “Nilijua tu kwamba lazima jambo lile limefanyika kwa makusudi kabisa hasa ukiangalia mahala ambako mawasiliano yalikatikia kwenye mzunguko wenye barabara nne na baada ya mawasiliano kurejea hatujui gari lile lilifuata barabara ipi.Mpaka hapa tayari tumeanza kupata mwanga kwamba kuna mtu ndani ya idara hii anahusika katika lile tukio.Yawezekana huyu amepandikizwa maalum kwa ajili ya kufuatilia kila kinachoendelea ndani ya hii idara na kuwapa taarifa hao waliomtuma.Yuko hapa kwa malengo maalum na inawezekana huyo ndiye aliyewapa taarifa kwamba Khalid anafuatiliwa na wakapanga wafanye vile walivyofanya.Hawa watu kama nilivyokwambia kwamba ni watu makini sana na wanajua wanachokifanya.Wameotesha mizizi yao karibu kila sehemu muhimu ya serikali” akasema Mathew “What are we going to do? Akauliza Ruby “Tayari tumepata chanzo hivyo hatupaswi kwenda naye haraka.Tunachotakiwa kufanya ni kumchunguza kwa siri sana kila anachokifanya.Tufuatilie mawasiliano yake tujue anaowasiliana nao na wanawasiliana nini,tufunge kamera za siri nyumbani kwake na kufuatiliakila kinachoendelea hapo kwake.Huyu ndiye atakayetuongoza kuelekea mahala walipo waliomtuma.Anza kwa kujenga naye urafiki.Muweke karibu yako ili iwe rahisi kumfuatilia” akasema Mathew na Ruby akainua simu akapiga stesheni 5 ambayo ni ofisi ya Edina lakini simu ikaita bila kupokelewa.Akapiga tena simu ikaita haikupokelewa. “Hapokei simu” akasema Ruby na kumpigia mtu mwingine akamtaka akamuangalie Edina ofisini kwake.Baada ya dakika mbili simu ikaita Ruby akaipokea akajulishwa kwamba Edina hakuwepo ofisini kwake.Ruby akampigia simu mtu mwingine akamuita ofisini kwake akamtaka akamtafute Edina “Nina wasiwasi kama atakuwepo bado mahala hapa” akasema Mathew “Nilitoa maelekezo asiondoke mtu yeyote leo kwenda nyumbani hadi tuhakikishe tumempata Khalid hivyo lazima atakuwepo hapa hapa ndani” akasema Ruby. “Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo ni kwamba Khalid anakuja nchini kuonana na James Kasai.Nashawishika kuamini kwamba mtandao huu ambao umemleta nchini Khalid ndio ambao unamleta na James Kasai hapa Dar es salaam.Huyu Edina ni muhimu sana kwetu kwa sasa kutusaidia kuufahamu mtandao huu” akasema Mathew “Kwa nini tusimkamate tukamuweka ndani na kumfanyia mahojiano ya kina akateswa na akaeleza kila kitu anachokifahamu kuhusiana na mtandao wao na watu waliomtuma?akauliza Ruby “Tungeweza kufanya hivyo lakini tutawastua na kuwapeleka mafichoni.Tumfuatilie taratibu na kwa karibu sana tutafika hadi kwa watu waliomtuma” akasema Mathew Wakati wakiendelea na mazungumzo mlango wa ofisi ya Ruby ukafunguliwa akaingia Yule jamaa ambaye alitumwa kwenda kumtafuta Edina. “Madam nimezunguka kila kona Edina hayupo” akasema Yule jamaa “Una hakika hayumo humu ndani?Ruby akauliza “Hayupo.Nimetafuta kila sehemu hayupo” akajibu Yule jamaa na kutoka. “Hayuko hapa.Tayari amekwisha ondoka” akasema Mathew “Ameondokaje?akauliza Ruby na kuinua simu akapiga geti kuu akawauliza kama Edina amepita pale getini usiku ule na kwenda nje akajibiwa kwamba hajapita pale kwani kila anayetoka lazima apitishe kadi yake ya ufunguo katika mashine iliyoko getini. “Hata geti kuu wanasema hawajamuona akitoka” akasema Ruby “Kuna mageti mangapi hapa ya kuingia na kutoka? “Geti lililopo ni moja tu na ambalo kila mfanyakazi lazima apite ili ajulikane kama hayupo au yupo ndani.Kama hajaonekana getini basi lazima atakuwa yuko humu humu ndani’ “Kama yuko humu ndani yuko wapi?akauliza Mathew “Hapo ndipo ninapokosa majibu.Naomba unipe dakika mbili” akasema Ruby na kushuka hadi katika ukumbi ule mkubwa “Samahani jamani naomba tusikilizane” akasema Ruby na watu wote wakaacha kazi wakamgeukia kumsikiliza “Kuna mwenzetu mmoja ambaye haonekani humu ndani na taarifa ya geti kuu inaonyesha kwamba hajatoka anaitwa Edina.Kuna yeyote anaweza akasaidia kujua mahala alipo?Kuna yeyote ambaye amemuona sehemu yoyote humu ndani?akauliza Ruby ‘Tafadhali kama kuna yeyote amemuoa au anajua mahala alipo anieleze ninamuhtaji sana kuna kazi ya muhimu nahitaji kumpatia sasa hivi” akasema Ruby na watu wakaanza kuulizana lakini hakuna aliyefahamu mahala alipo. “Kuna yeyote anayefahamu nyumbani kwake?akauliza Ruby na watu zaidi ya watano wakanyoosha mikono “Naomba mmoja wenu anielekeze nyumbani kwake.Namuhitaji sana” akasema Ruby na dada mmoja akamuelekeza mahala anakoishi Ruby “Ahsanteni sana.Endeleeni na kazi zenu.Kumbukeni kabla ya mapambazuko lazima tuwe tumempata Khalid Sultan” akasema Ruby na kurejea ofisini kwake. “Mathew uko sahihi.Huyu Edina hayuko humu ndani.Tayari amekwisha ondoka lakini sifahamu ameondokaje” akasema Ruby “Yawezekana amekwenda mahala na atarejea tena”akasema Mathew “Nimeelekezwa mahala anakoishi.Twende tumfuate nyumbani kwake yawezekana tukapata kitu muhimu cha kuweza kutusadia kumfahamu vyema huyu mtu” akasema Ruby wakaondoka kuelekea katika gari lake SAA MOJA ILIYOPITA Ofisi kuu ya SNSA ilikuwa katika heka heka kubwa kila idara ndani ya ofisi hiyo wakijaribu kutafuta sababu ya mawasiliano kukatika ghafla na kukwamisha zoezi la kumfuatilia Khalid Sultan Khalid.Wakati watu wanaohusika na masuala ya ufundi wakijitahidi kurejesha mawasiliano,Edwin akaingia katika chumba kilichojulikana kama chumba cha seva ambamo kulikuwa na kompyuta nyingi kubwa.Hakuna aliyemjali kila mmoja alikuwa anashughulika akamfuata Edina aliyekuwa amesimama akiangalia kile kilichokuwa kinaendelea akamshika mkono na kumpa kijikaratasi.Edina akatoka mle ndani akaenda maliwato akakikunjua kile kikaratasi na kukisoma “Baada ya mawasiliano kurejea nataka nikupeleke nyumbani ukahifadhi fedha zako wakiziona hapa wataanza kuulizana ulikozitoa.Jitahidi utokapo asikuone mtu nenda hadi katika gari langu fungua mlango jifiche kiti cha nyuma halafu utanitumia ujumbe nitakupeleka nyumbani ukahifadhi mzigo wako na kukurudisha” ndivyo ulivyosomeka ule ujumbe Mawasilinao yalirejea na kazi zikaendelea kama kawaida na baada ya muda mkurugenzi akawasili na kuzungumza na wafanyakazi na kisha likaanza zoezi la kumsaka Khalid Sultan.Wakati zoezi likindelea Edina akachukua bahasha yake iliyokuwa na fedha akatoka kama vile anaelekea maliwato na kuelekea moja kwa moja katika maegesho ya magari ya wakuu wa idara,analifahamu gari la Edwin akafanya kama alivyoelekezwa akaingia katika kiti cha nyuma halafu akamtumia ujumbe Edwin kumjulisha kwamba tayari amekwisha ingia garini.Edwin akamuaga Ruby kisha akatoka akaingia garini na kutoka.Baada ya kutoka katika geti kuu Edina aliyekuwa amejificha kiti cha nyuma akaibuka na kukaa “Ahsante sana Edwin kwa msaada huu mkubwa” akasema Edina “Usijali Dina” akasema Edwin ambaye alionekana kutohitaji maongezi akafungua mziki kwa sauti ya juu Walifika nyumbani kwa Edina wakashuka garini,Edna akamkaribisha ndani “Edwin karibu ndani kutana na mdogo wangu anaitwa Stella.Huyu ndiye anayesoma chuo kikuu na ile fedha ni kwa ajili yake” akasema Edina.Edwin na Stella wakasalimiana.Dina akamuandalia Edwin juisi ya matunda kisha akaelekea chumbani kuhifadhi zile fedha “Nimefurahi kuonana nawe Stella.Dada yako amekuwa anatueleza sana sifa zako na bidii yako kubwa katika masomo” akasema Edwin “Nashukuru sana” akasema Stella. “Stella naomba maji ya kunywa tafadhali” akasema Edwin na Stella akainuka kwenda kumchukulia Edwin maji ya kunywa katika friji mara Edwin akaingiza mkono katika mfuko wa koti na kutoa bastora iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti na mara tu Stella alipogeuka akaizinga bastora na kuachia risasi iliyompata Stella kati kati ya paji la uso akaanguka.Sauti ya glasi kuvunjika ikamstua Edina aliyekuwa chumbani. “Stella ! akaita Edina lakini hakujibiwa akafungua mlango wa chumba akatoka ili kuangalia kuna nini akakutana na risasi mbili zilizompata katikati ya paji la uso akaanguka chini.Edwin akawaongeza tena risasi ili kuhakikisha hakuna anayebaki hai kisha akaingia ndani ya chumba alimotoka Edina akavaa glovu mikononi akafungua kabati kubwa la nguo akafungua droo ndogo akazikuta fedha ambazo Edina alikuwa amezihifadhi akazichukua na kutoka “I’m sorry Dina” akasema Edwin na kuchukua simu za Edina na mdogo wake akachukua ufunguo akafunga mlango kwa nje akaondoka. “Sasa nielekee kwa Melanie” akawaza Edwin





    Mathew na Ruby waliwasili katika nyumba anayoishi Edina.Waliegesha gari mbele ya nyumba ile ambayo haikuwa na uzio wakaelekea mlangoni.Taa ya nje ilikuwa inawaka Mathew akagonga mlango lakini hakujibiwa.Akagonga tena lakini hakujibiwa. “Inawezekana hayupo nyumbani’ akasema Ruby “Kama hayupo itakuwa vizuri kwetu,tuingie ndani pengine tunaweza kupata kitu cha kutusaidia” akasema Mathew na kuchukua vifaa vyake ambavyo humuwezesha kufungua kitasa au kufuli la aina yoyote ile kisha akaufungua ule mlango wa nyumba ya Edina. “Jesus Christ ! akasema Mathew kwa mstuko na kwa haraka akatoa bastora yake “Kuna nini Mathew?akauliza Ruby naye akaingia ndani “Edina ?!! akasema Ruby kwa mstuko.Mathew akaingia kwa tahadhari katika vyumba vyote lakini hakukuwa na mtu yeyote akarejea sebuleni akaigeuza miili ile ya Edina na mdogo wake “Wameuawa usiku huu” akasema kisha wakaingia chumbani wakaanza kukagua kama wangeweza kupata kitu chochote cha kuwasaidia lakini hawakupata chochote wakatoka na kuondoka “Hawa watu ni wakatili wakubwa sana.Baada ya kumtumia Edina wameamua kumuua kwani waliohofia labda angeweza kugundulika.Ni watu wenye kuchukua tahadhari kubwa kila wakati.Ruby unapaswa uwe makini sana kwani watu hawa wana mtandao mkubwa na hata idara yako tayari wameotesha mizizi yao.Naamini Edina hayuko peke yale lazima kuna watu ambao bado wapo ndani ya idara” “Mathew nimejikuta nikiingiwa na woga wa ghafla” “Usiogope Ruby niko nyuma yako hakuna yeyote ambaye atathubutu kucheza na maisha yako” akasema Mathew. “Tunaelekea wapi hivi sasa? Akauliza Ruby “Turejee SNSA.Nahitaji kumuhoji Yule mkuu wa idara ya ufundi” “Unadhani kuna kitu anakifahamu?akauliza Ruby “Naamini hivyo.Kuna kitu anakifahamu kuhusu jambo hili” akasema Mathew “Itanilazimu kutumia madaraka yangu ili ukamuhoji Fidelis kwani wewe si mfanyakazi wa SNSA lakini ni vipi endapo hatakuwa anafahamu chochote? Akauliza Ruby “SNSA iko chini ya Rais na anafahamu hiki tunachokifanya hivyo hakuna yeyote atakayekuuliza kitu chochote.Umepewa madaraka hivyo lazima uyatumie.Usijali kuvunja taratibu katika kutafuta taarifa za muhimu” akasema Mathew “Ruby umepewa idara nyeti sana uiongoze hivyo jifunze kufanya maamuzi magumu pale inapohitajika.Nina uhakika mkubwa kwamba huyu jamaa Fidelis kuna kitu anakifahamu kuhusu hiki kilichotokea.Ruby idara yako imeingiliwa na kirusi kibaya sana.Una kazi kubwa ya kukiondoa kirusi hicho.Inaonekana tayari mabeberu hawa wamekwisha otesha mizizi katika idara yako na wanaitumia katika kufanikisha mipango yao na hii inakuweka katika hatari kubwa sana lakini usihofu nitakulinda” akasema Mathew “Kwa hiki kilichotokea leo ninaamini hicho ukisemacho.Idara hii ilianzishwa kwa ajili ya usalama wa ndani wa nchi lakini naweza sema kwamba bado haijafanya kazi yake ile inayotakiwa.Imekuwa ikitumiwa katika kufanikisha mipango mbali mbali miovu dhidi ya nchi yetu na mkosi ulianzia kwa Devotha.Kama utakumbuka huyu alikuwa ni wakala wa Mossad hapa nchini na ikaendelea hivyo hadi kwa aliyefuata aliitwa Tamar.Kuna kazi kubwa ya kuisafisha idara hii ili ifanye kazi iliyokususdiwa”akasema Ruby “Umemtaja Devotha umenikumbusha mbali sana.Yuko wapi Yule mwanamke?akauliza Mathew “Sifahamu yuko wapi labda wale walioko hapa nchini Gosu Gosu na Austin wanaweza wakafahamu mahala alipo.Sitaki kabisa kufahamu chochote kuhusu Yule mwanamke ninamchukia sana alitaka kuniua pasi na kosa” akasema Ruby na ukimya ukapita “Najaribu kujiuliza Edina ametokaje pale ofisini wakati kuna geti moja tu? Nani kamuua? Akasema Ruby “Usiumize sana kichwa Ruby niachie jambo hilo tutapata majibu yake” akasema Mathew “Tumekuwa na mambo mengi sana hata nimesahau kuuliza kuhusu Peniela.Nini kilitokea?Alikueleza chochote kuhusu Melanie Davis? Halafu mbona kaondoka haraka namna hiyo?Nilitegemea angelala hapa Dar es salaam kwa mume wake” akasema Ruby “Peniela alikuja kwa jambo moja tu” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Alikuja kuhitimisha ndoa yetu.Mimi naye basi tena” “Mmeachana?! Ruby akashangaa “Ndiyo” akajibu Mathew na kumsimulia Ruby kila kitu kilichotokea kati yake na Peniela “Mathew I’m so sorry.I don’t know what to say” akasema Ruby “Usijali Ruby haya ni mapito katika maisha” “Sikutegemea kama mambo yangekuwa namna hii.Lakini Peniela amechukua maamuzi ya haraka sana” akasema Ruby “Simlaumu Peniela kwa maamuzi aliyoyachukua kwani yote haya nimeyataka mimi mwenyewe.Nilichagua kazi badala ya familia.Nimewaumiza sana ana haki ya kuendelea na maisha yake bila mimi.Anahitaji mtu ambaye atampa furaha katika maisha yake jambo ambalo mimi nimeshindwa.Haya ndiyo maisha yangu na lazima niyakubali” akasema Mathew “Kikubwa ambacho ninashukuru ameahidi kunisaidia kutafuta taarifa za Melanie Davis.Kama akilifanikisha hilo atakuwa ametusaidia jambo kubwa sana” akasema Mathew “Mathew you are mine now.Hakuna yeyote au chochote cha kunitenganisha nawe.Mimi ndiye hasa ninayestahili kuwa nawe.Mimi ndiye Yule ambaye niliumbwa kwa ajli yako.Ninakupenda zaidi ya ninavyojipenda mwenyewe.Ahsante Peniela kwa maamuzi haya uliyoyachukua ambayo yameniachia mimi uwanja wa kutawala.Sasa mpira uko kwangu na katu siwezi kushindwa kufunga” akawaza Ruby Walifika ofisi kuu ya SNSA wakaelekea ofisini kwa Ruby ambaye bila kuchelewa akapiga simu idara ya usalama ndani ya SNSA akawataka wamchukue Fidelis wampeleke katika chumba cha mahojiano namba 2 halafu akaelekeza kamera zote katika chumba hicho cha mahojiano namba mbili zizimwe.Baada ya dakika chache akataarifiwa kwamba Fidelis tayari amepelekwa katika chumba cha mahojiano “Mathew mtu unayemuhitaji tayari amekwisha pelekwa katika chumba cha mahojiano” akasema Ruby na kumuongoza Mathew hadi katika chumba alimowekwa Fidelis.Mlinzi aliyekuwa mlangoni akaufungua mlango Ruby na Mathew wakaingia. Ruby akachomoa nyaya zote zilizounganishwa na kamera kwa tahadhari kwani hakuwaamini wafanyakazi wa idara ile. “Mathew he’s all yours” akasema Ruby.Mathew akavuta kiti na kuketi. “Madam what’s going on? Who is this guy? akauliza Fidelis “My name is Mathew Mulumbi.Nitakuuliza maswali naomba unijibu kwa usahihi” akasema Mathew “Huwezi ukaniuliza chochote.Wewe si mfanyakazi wa hapa na siwezi kukujibu chochote.Madam nini kinaendelea hapa?Kwa nini umenileta hapa?akauliza Fidelis na kutaka kunyanyuka. “Sit down ! akasema Mathew kwa ukali “I’m not going to sit down.Wewe ni nani wa kunipa amri…aaaagghhhh !!!.” Fidelis hakumaliza sentensi yake akajikuta chini baada ya kupigwa kofi zito.Mathew akamfuata pale chini alipoanguka na kumtaka ainuke aketi kitini.Bila ubishi Fidelis akainuka na kuinua kiti ambacho nacho kilikuwa kimeanguka akaketi “Jina lako nani?akauliza Mathew “Fidelis Makweba” “Unashughulika na nini hapa SNSA?akauliza Mathew “Mimi ni mkuuwa idara ya ufundi ambayo kazi yetu ni kuhakikisha mifumo yetu yote inakuwa salama muda wote na kompyuta zote zinakuwa katika hali nzuri” akajibu Fidelis. “Usiku wa leo wakati wa zoezi la kumfuatilia Khalid likiendelea mawasiliano yalikatika kati ya ofisi kuu na watu wetu waliokuwa barabarani.Nini kilisababisha hali ile kutokea?akauliza Mathew na Fidelis akaanza kuelezea kiufundi tatizo lililotokea “Hata mkurugenzi aliniita akaniuliza nikamueleza kila kitu kuhusiana na hiki kilichotokea” akasema Fidelis na Mathew akamgeukia Ruby “Fidelis maelezo uliyonipa hayana ukweli wowote”akasema Ruby na Fidelis akaonyesha mstuko mkubwa.Ruby akaanza kumpa maelezo kuhusiana na kile kilichotokea.Matone ya jasho yakaonekana usoni kwa Fidelis “Wewe kama fundi mkuu lazima ufahamu kitu hiki” akasema Ruby na kuhitimisha maelezo yake “Umesikia alichokisema mkurugenzi wako.Unakubaliana na maelezo yake?akauliza Mathew na Fidelis akawa kimya.Alijaribu kufungua midomo ikabaki inamcheza “Ukimya wako ni jibu kwamba alichokisema mkurugenzi wako ni kitu cha kweli kabisa” akasema Mathew na kumtazama Fidelis “Khalid Sultan Khalid ni mtu hatari sana ambaye amekuja nchini kwa lengo la kupanga shambulio kubwa.Idara yenu imefahamu kuhusu ujio wake na kuweka mikakati ya kumfuatilia kujua alichokuja kukifanya hapa nchini vile vile kuwafahamu washirika wake.IS wana mzizi wao hapa nchini na sasa wanataka kusambaa katika bara zima la Afrika.Operesheni ile ya kumfuatilia Khalid ingetuwezesha kuwafahamu washirika wake na mtandao mzima wa IS hapa nchini lakini kwa makusudi kabisa umeshiriki katika kukwamisha zoezi lile la kumfuatilia Khalid na sasa hatujui yuko wapi wala washirika wake ni akina nani.Kwa hiki ulichokifanya umeiweka nchi katika hatari kubwa na unajua adhabu wanayopewa watu kama wewe ambao wanahatarisha usalama wa nchi.Fidelis ninataka nikusaidie kukuondoa katika kitanzi hiki ulichojivisha lakini hadi pale utakaponieleza ukweli wote.Kwa nini ulisema uongo kuhusu tukio lile?Kwa nini ulimdanganya mkurugezi wako? Tuanzie hapo” akasema Mathew.Fidelis hakujibu kitu alibaki kimya “Fidelis muda unakwenda naomba tafadhali unijibu maswali niliyokuuliza” akasema Mathew Fidelis hakujibu kitu “Fidelis nafahamu hauko peke yako katika jambo hili.Nani wengine ulishirikiana nao?akauliza Mathew lakini bado Fidelis aliendelea kuwa kimya “Fidelis unapokaa kimya unazidi kupoteza nafasi ya kusaidiawa” akasema Mathew “Labda ngoja nikufahamishe kitu Fidelis.Tatizo hili lilianzia stesheni 5 ambayo ni ya Edina.Naamini jambo hii ulilifahamu vizuri lakini ukakubali kupindisha ukweli.Kwa taarifa yako ni kwamba baada ya kugundua kwamba ni Edina ambaye alifanya kitendo kile nilianza kumtafuta bila mafanikio nikaamua kumfuata nyumbani kwake nimekuta ameuawa”akasema Ruby na sura ya Fidelis ikaonyesha mstuko mkubwa “Watu waliomtumia Edina wamemuua kikatili.wewe unayo nafasi nzuri ya kusaidiwa yasikukute kama yaliyomkuta Edina lakini tutakusaidia tu pale ambapo utatueleza ukweli nani alikutuma useme uongo kuhusiana na tukio lile?akauliza Mathew na Fidelis alionyesha uoga mkubwa “Fidelis hii ni nafasi pekee ya kukuokoa umeipata na kama ukishindwa kuitumia basi tutakukabidhi kwa vyombo vya dola ufunguliwe mashtaka ya kuhatarisha usalama wa taifa.Naomba ufunguke tafadhali” akasema Mathew lakini Fideli bado alikuwa kimya “Fidelis una watoto?akauliza Mathew na swali lile likaonekana kumstua Fidelis na akaikumbuka sauti ya Edwin masikioni “Endapo ukithubutu kufunguka na kusema ukweli kuhusiana na tukio hili hutaiona tena familia yako ! Fidelis aliyakumbuka maneno haya aliyoambiwa na Edwin akahisi baridi “Fedha alizonipa Edwin zimeniponza natamani niwaeleze ukweli hawa watu lakini nahofia familia yangu kwani Edwin alinionya nisithubutu kusema ukweli kuhusu jambo lile kwani ama sivyo nitaikosa familia yangu. Natakiwa kuendelea na msimamo wangu wa kutokusema chochote.Mambo tayari yameshaharibika” akawaza Fidelis “Fidelis ninaanza kuchoshwa na tabia yako ya kujifanya bubu.Hii ni mara ya mwisho ninakuuliza nani waliokutuma useme uongo kuhusu kukatika kwa mawasiliano katika zoezi muhimu? akauliza Mathew bado Fidelis alikuwa kimya “Hujanifahamu vyema kijana, mimi huwa sipendi mzaha ninapokuwa kazini” akasema Mathew na kunyanyuka akamfuata Fidelis akamuinua akampeleka katika nguzo akachukua kamba akamfunga mikono nyuma ya nguzo na miguu akaikaza barabara kwa kamba. “Kwa kuwa umekataa kufunguka kwa njia ya amani sasa tunaingia katika njia ya pili ya kutumia nguvu.Kabla sijaanza zoezi langu ninakupa nafasi ya mwisho ya kunieleza ukweli” akasema Mathew.Fidelis alikuwa anatetemeka mwili lakini hakusema chochote.Bado aliendelea na msimamo wake wa kukaa kimya.Mathew akachukua kopo dogo la gesi akaliwasha kisha akaanza kuunguza vidole vya mikono “Aaaaaaghhhh !! Fidelis akapiga ukulele mkubwa “Nani alikutuma?akauliza Mathew lakini Fideli hakujibu kitu aliendelea kulia huku akihisi maumivu makali.Mathew akamchoma tena na gesi lakini bado Fidelis aliendelea kugugumia maumivu makali bila kusema chochote ”This isn’t working” akasema Mathew na kuchukua mashine ndogo ya umeme. “Fidelis mimi ni mtu mbaya sana kama ukinifanyia mchezo.Unaonekana kunichezea na mimi sitaki mchezo” akasema Mathew na kuiwasha mashine ile akamchoma Fidelis kwa umeme akaanza kutetemeka Mathew akaizima “Uko tayari kuzungumza? akauliza Mathew lakinihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Fidelis aliendelea kuwa kimya “Huyu bazazi anacheza na mimi” akawaza Mathew na kuitupa ile mashine ya umeme “C’mon Fidelis tell me the truth !! akasema Mathew.Fidelis hakufumbua mdomo wake kutamka chochote.Mathew akazidi kukasirika akaanza kumporomoshea Fidelis magumi mazito sehemu mbali mbali za mwili wake.Ndani ya muda mfupi uso wa Fidelis haukuwa ukitazamika ulikuwa umeloa damu.Ruby akamfuata na kumzuia Mathew asiendelee kumpiga “Mathew imetosha.Umekwisha muumiza sana.Bado tunamuhitaji atupe taarifa muhimu” akasema Ruby.Bado Mathew aliendelea kumtazama Fidelis kwa hasira. “Fidelis ! Fidelis ! akaita Ruby lakini Fidelis hakuitika alikuwa anamwagika damu mdomoni na alionekana hana fahamu.Haraka haraka Ruby akafungua mlango na kumtaka Yule mlinzi aliyekuwa mlangoni akawaite watu wa afya haraka sana. “Mathew ulitaka kumuua kabisa huyu mtu” akasema Ruby “Bado nina hasira naye.Hawajui nimepitia mambo gani hadi kufanikiwa kuipata taarifa ile muhimu ya Khalid lakini kwa fedha chache wanazopewa wanadiriki kuvuruga misheni yetu na kuhatarisha usalama wa nchi.Watu kama hawa si wa kuwavumilia hata kidogo ! akafoka Mathew Mlango ulifunguliwa na watu wanne wakaingia wakiwa na machela.Wakamfungua Fidelis wakampakia katika machela na kuondoka naye. “Mathew nafahamu una hasira sana na watu hawa lakini nakuomba jitahidi kujizuia kutumia nguvu kupitiliza kwani ugeweza kumuua Fidelis na ungeniweka mimi katika matatizo” akasema Ruby “I’m sorry.Ni kweli nilikuwa na hasira naye sana.Huyu jamaa anafahamu kila kitu lakini anaogopa kusema.Yuko tayari kuvumilia mateso makali kwa ajili ya kuwaficha watu hao waliomtuma” akasema Mathew “Baada ya kushindwa kupata taarifa kutoka kwa Fidelis nini kinaendelea?akauliza Ruby “Tayari tunaye mtu ambaye anahusika katika mpango ule wa kuvuruga zoezi la kumfuatilia Khalid.Fidelis anafahamu nani aliyemtuma lakini anamficha.Kwa sasa yeye ndiye pekee anayeweza kutueleza ukweli.Tumsubiri atakapozinduka tutaendelea naye lazima atueleze kila kitu anachokifahamu” akasema Mathew





    Mishale ya saa ilizidi kuyoyoma na nyumbani kwa Melanie Davis bado kikao kiliendelea.Melanie na James Kasai walimueleza Khalid Sultan Khalid mpango wao wa kuwaua marais wawili kwa kutumia bomu.Khalid baada ya kuyasikia mawazo yao aliyakubali na kukubaliana na pendekezo lao kwamba bomu litakalotumiwa kuwaua marais hao wawili liwe la kujitoa mhanga.Alieleza aina ya bomu linalohitajika,namna atakavyolitengeneza na madhara yakayoweza kuletwa na hilo bomu.Baada ya watu wote kuzungumza juu ya nafasi zao katika mpango ule ikafuata zamu ya Edwin Mbeko.Huyu ndiye ambaye alitegemewa kumaliza mchezo wote .Mpango ule wote ulimtegemea yeye ili ukamilike “Katika kuukamilisha mpango huu nitafanya hivi.Nitahitaji mtu kwa ajili ya kujitoa mhanga.Mtu huyo ataingizwa uwanja wa ndege akiwa amevaa mavazi ya askari wa kutuliza ghasia.Mara nyingi askari hawa huvaa fulana nene za kujikinga na risasi lakini huyu wa kwetu fulana yake haitakuwa kwa ajili ya kujikinga na risasi bali litakuwa ni bomu.Hakuna ambaye atamtilia shaka mtu huyo kuwa si askari hivyo atajitahidi kuwasogelea marais na akiwakaribia umbali Fulani atajilipua” akasema Edwin na kufafanua namna atakavyomuingiza ndani ya uwanja mtu huyo atakayevaa mavazi ya askari polisi na kubeba bomu.Kila mmoja akatoa mawazo yake kuhusiana na wazo lile la Edwin na baada ya majadiliano wakafikia makubaliano.Khalid aliahidi kumleta haraka sana nchini mtu ambaye angeweza kubeba bomu hilo na kujitoa mhanga.Baada ya kufikia makubaliano Edwin Mbeko akaondoka kurejea ofisi kuu ya SNSA. Mara tu alipoingia ndani ya ofisi zao akakutana na hali isiyo ya kawaida. “Kuna nini hapa?Mbona watu wako namna hii?akauliza Edwin na kuelezwa kile kilichomtokea Fidelis.Edwin akahisi miguu ikimtetemeka kwa mstuko alioupata.Hakutegemea kama Fidelis angeweza kugundulika.Akaelekea ofsini kwake na kukaa juu ya meza “Huyu mwanamke amegunduaje kama Fidelis anafahamu kilichotokea?Kama ameweza kugundua mawasiliano yalikatwa makusudi basi lazima atakuwa amefahamu nani aliyefanya hicho kitendo.Nilifanya jambo zuri sana kumuua Edina.Kwa sasa natakiwa kumuondoa Fidelis pia halafu nianze kushughulika na huyu mwanamke kwani nisipomshughulikia mapema anaweza akaharibu mipango yetu yote” akawaza Edwin na kuelekea sehemu ya afya alikokuwa amelazwa Fidelis.Tayari alikwisha pata fahamu na Edwin alipoingia akamtambua mara moja “Fidelis ! akasema Edwin “Edwin ! akasema Fidelis kwa sauti dhaifu. “Nini kimetokea Fidelis?akauliza Edwin “Annabel anafahamu..aagh ! akasema huku akigugumia kwa maumivu “Anafa…fahamu kila kitu” akasema Fidelis “Umemueleza chochote? Akauliza Edwin na Fidelis akatingisha kichwa kukataa “Vizuri sana.Nimekwisha ita gari la wagonjwa linakuja tunakupeleka hospitali kuu ya Mtodora ukapate matibabu makubwa” akasema Edwin kisha akafungua mlango akachungulia nje kama kuna mtu halafu akarejea ndani akachukua mto akamgandamiza Fidelis kwa nguvu pale kitandani.Fidelis alianza kuhangaika kutafuta hewa lakini tayari mwili wake ulikwisha kuwa dhaifu hivyo hakuweza kushindana na Edwin.Baada ya muda Fidelis akatulia Edwin akatoa ule mto na kumtazama tayari Fidelis hakuwa na uhai. “I’m sorry Fidelis” akasema Edwin na kuweka kitanda vizuri halafu akafungua mlango na kutoka mbio akiita madaktari ambao walifika kwa haraka sana kuangalia kuna nini.Haraka haraka wakampima lakini tayari Fidelis alikwisha fariki.Edwin akionekana kuwa na hasira akaelekea katika ukumbi ambako kazi zilikuwa zinaendelea. “Naombeni mnisikilize ndugu zangu ! akasema Edwin na watu wote wakamgeukia. “Kuna taarifa mbaya nimewaleteeni.Mwenzetu,ndu gu yetu Fidelis amefariki dunia muda mfupi uliopita ! Sura zote zikaonyesha mstuko mkubwa kwa taarifa ile “Nimejulishwa kwamba mkurugenzi wetu mpya akiwa na mtu ambaye ameambatana naye ambaye si mfanyakazi wa idara yetu walimuita Fidelis katika chumba cha mahojiano na kisha wakamlazimisha aseme tukio lile la kukatika kwa mawasiliano lilifanywa makusudi.Fidelis alikataa na ndipo alipoanza kupigwa.Huu ni unyama mkubwa amefanyiwa Fidelis.Mkurugezi amevunja kanuni za idara kwanza kwa kumuingiza ofisini mtu ambaye si mfanyakazi wa idara hii ya siri ya serikali lakini pili mtu huyo ambaye hatumfahamu ni nani amesababisha kifo cha mwenzetu.Hatuwezi kulikubali jambo hili.Mkurugenzi huyu ana siku ya pili katika ofisi na tayari ameanza kuleta humu ndani watu wasiohusika nina mashaka naye sana kama anaweza akaongoza idara hii nyeti kabisa kwa nchi.Ndugu zangu nchi kwa sasa inatutegemea sana sisi hivyo hatuwezi kuongozwa na mtu kama huyu katika wakati huu.Kanuni zetu ziko wazi kwamba wafanyakazi wa idara wanao uwezo wa kumuondoa katika ofisi kwa muda wa siku saba mkuu wa idara endapo ataonekana kushindwa kumudu majukumu yake vyema au kuvunja kanuni na taratibu za idara au kuwa kikwazo katika kufanikisha mambo muhimu kwa usalama wa nchi.Katika siku saba hizo suala la kuondolewa ofisini mkuu wa idara litafikishwa kwa Rais kujadiliwa na kisha kutolewa maamuzi.Nyote mnazo kanuni na mnazifahamu hivyo basi kwa kitendo alichokifanya mkurugenzi leo amevunja kanuni na kukwamisha zoezi la kumtafuta Khalid Sultan kwani Fidelis ni mmoja wa watu ambao tunawategemea sana hapa katika idara.Hata lilipotokea lile tatizo la kukatika kwa mawasiliano yeye ndiye aliyeshughulika na timu yake na wakafanikiwa kurejesha tena mawasiliano.Ninawaomba mniunge mkono tumuondoe mkurugenzi katika nafasi yake mara moja ili zoezi la kumtafuta Khalid liendelee usiku huu” akasema Edwin na watu wote wakaonekana kukubaliana naye. “Ahsanteni sana kwa kuniunga mkono.Sasa ninakwenda kumuondoa mkurugenzi ili asiendelee kutuvuruga” akasema Edwin na kuelekea katika ofisi ya Ruby Ruby akiwa katika ofisi yake na Mathew alijulishwa na daktari mkuu wa idara kwamba Fidelis amefariki dunia.Ilikuwa ni taarifa iliyomstua sana Ruby na kumfanya aweke mezani mkono wa simu “Kuna nini Ruby mbona umestuka sana? “Nimetaarifiwa na daktari mkuu kwamba Fidelis amefariki dunia” “That’s not true ! “Ni kweli Mathew.Fidelis amefariki dunia” akasema Ruby “Imetokeaje?Nini kimesababisha kifo chake?akauliza Mathew na kabla Ruby hajajibu mlango ukafunguliwa akaingia Edwin Mbeko akiwa ameongozana na watu wanne wenye silaha “Edwin umerejea.Mambo yamekwendaje huko?Kuna mafanikio yoyote?akauliza Ruby “Madam Annabel sijaja hapa kwa ajili ya jambo hilo” akasema Edwin na Ruby akaonekana kukasirika “Nini kimekuleta hapa basi? “Madam naamini umepata taarifa za kifo cha ghafla cha Fidelis mmoja wa wataalamu wetu mahiri kabisa ambaye amekuwa na mchango mkubwa mno katika kufanikisha shughuli zetu mbali mbali” “Ndiyo nimejulishwa” “Nimejulishwa kwamba kifo cha Fidelis kimesababishwa na kipigo ambacho wewe na huyu mtu wako mmempiga” akasema “Edwin hukuwepo ofisini wakati jambo hilo linatokea hivyo basi unatakiwa utulie uulize na ueleweshwe nini kimetokea?akasema Ruby “Madam sina muda wa kuuliza wakati kila kitu kiko wazi nimekuja hapa kwa jambo moja tu.Kwa niaba ya wafanyakazi wengine wa idara hii nimetumwa kukujulisha kwamba kwa kitendo hiki ulichokifanya leo umevunja kanuni kwanza kwa kumuingiza ndani ya ofisi hii nyeti mtu ambaye si mfanyakazi wa idara.Hilo ni moja ya jambo lisiloruhusiwa kabisa kwani ofisi hii ina siri nyingi za nchi.Pili kwa kusababisha kifo cha mfanyakazi wa idara.Kwa mujibu wa kanuni zetu wafanyakazi wanayo madaraka ya kumuondoa mkurugenzi katika ofisi yake kwa siku saba hivyo kwa kutumia kanuni zetu kwa niaba ya wafanyakazi wote ninakuondoa katika nafasi yako na suala lako linapelekwa kwa Rais kwa ajili ya maamuzi.Kuanzia sasa kabidhi kila kitu cha idara na hutakiwi kuonekana hapa katika idara kwa muda wa siku saba na utarejea hapa pale Rais atakapokwambia hivyo” akasema Edwin na Ruby akacheka kidogo “You can’t be serious Edwin” “I’m very serious madam” akasema Edwin “Aliyeniweka katika nafasi hii ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wewe huna mamlaka yoyote ya kuniondoa mimi katika nafasi yangu ! akasema Ruby “Ni kweli madam sina uwezo huo lakini kanuni ambazo zimetiwa saini na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndizo zinazokuondoa” “No I won’t leave ! akasema Ruby kwa ukali “Madam tafadhali usisababishe nguvu ikatumika kwani kanuni zinaelekeza nguvu inaweza ikatumika vile vile kukuondoa.Tafadhali kabidhi kila kifaa cha idara sasa hivi” akasema Edwin “Just do it ! Mathew akamwambia Ruby “No I can’t ! akasema Ruby “Wape kila kitu chao tuondoke hapa kwa amani” akasema Mathew na Ruby akatoa kadi yake ya ufunguo bastora na vifaa vingine akaviweka mezani “Ahsante sana madam Annabel” akasema Edwin huku akikusanya vifaa vile.Ruby akaichukua kompyuta yake na kuiweka katika mkoba. “Madam kopyuta hiyo huwezi ukaichukua hadi ikaguliwe tujiridhishe kama haina siri za idara” akasema Edwin “Nimekuwa hapa siku mbili tu sina siri zozote za idara” akasema Ruby kwa ukali “Huo ni utaratibu madam” akasema Edwin “Ruby pakia kompyuta yako na vifaa vyako vingine tuondoke ! akasema Mathew “And you,who are you? Akauliza Edwin huku akimtazama Mathew kwa hasira “Mimi ni mtu ambaye hupaswi kumfahamu ! akajibu Mathew “Usijibu kwa dharau ndugu ninao uwezo wa kuamrisha ukawekwa ndani sasa hivi.Wewe si mfanyakazi wa hapa na huruhusiwi kuwepo katika ofisi hii ! akafoka Edwin “Bwana mdogo usinijaribu.Sipendi kujaribiwa ! akasema Mathew kwa ukali huku akimsogelea Edwin “Okay guys tusilifanye suala hili likawa kubwa.Edwin the office is yours now.Please make sure you find Khalid Sultan” akasema Ruby “Yes madam we will find him” akajibu Edwin “Thank you for everything.I hope we’ll meet again soon” akasema Ruby na kumshika Mathew mkono wakatoka.Hakumuaga mfanyakazi yoyote wa idara ile wakaelekea hadi katika gari lake wakaingia na kuondoka. “Mathew mimi sijaelewa hiki kilichotokea ! Bila wewe kunilazimisha nikubali kamwe sikuwa tayari kutoka mle ofisini.Nimepewa ofisi na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania nawezaje kuondolewa kienyeji namna hii na mtu asiye na hadhi yoyote?akauliza Ruby akiwa amekasirika. “Ruby ni kweli umepewa ofisi na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania lakini idara hii ya SNSA tayari imekwisha ota mzizi mkubwa wa mabeberu na umeondolewa makusudi kabisa kwani tayari umeanza kuonekana kikwazo kwao.Zoezi la kumfuatilia Khalid limekwamishwa makusudi kabisa na aliyefanya kitendo kile ameuawa.Pili ni kifo cha Fidelis.Nina mashaka sana kama kipigo kile nilichompiga ndicho kimesababisha kifo chake” “Unadhani Fideli ameuawa?akauliza Ruby “Ndiyo.Yeye pia aliufahamu ukweli kuhusiana na kukatika kwa mawasiliano wakati wa lile zoezi la kumfuatiliaKhalid na kama ilivyokuwa kwa Edina naye pia ilibidi aondolewe haraka.Nina uhakika mkubwa ameuawa.Ninayafahamu haya mambo” akasema Mathew “Wameamua kutumia kanuni ili kukuondoa na mipango yao iendelee.Nilikwisha liona hilo na ndiyo maana nikakutaka ukabidhi kila kitu chao na tuondoke kwani bila kufanya hivyo yangeweza kuibuka mambo mengine makubwa zaidi.SNSA ya sasa si ile ambayo ilianzishwa kwa malengo ya kulinda usalama wa nchi.Imekuwa ni sehemu ya kuhatarisha usalama wa nchi na hilo limedhihirika usiku wa leo.Zoezi muhimu sana la kumfuatilia Khalid limeshindwa kufanikiwa.Edina na Fidelis hawako peke yao ndani ya SNSA lazima upo mtandao mkubwa” “Sasa tutafanye nini Mathew? Rais atanielewaje akisikia hiki kilichotokea? “Rais anakuamini sana lakini kwa misheni hii tutaiendesha sisi wenyewe bila kutegemea SNSA.Tutamsaka Khalid na kuhakikisha tunampata vile vile James Kasai.Nina uhakika mkubwa tutawapata naomba uniamini” “Mathew ninakuamini sana lakini hapa tulipo tumekwama.Tutawezaje kujikwamua kutoka katika mkwamo huu?akauliza Ruby “Ahsante kwa kuniamini.Endelea kuniamini na tutalimaliza suala hili” akasema Mathew Mara tu baada ya Mathew na Ruby kuondoka,Edwin akampigia simu Dr Fabian Kelelo akamjulisha kile kilichotokea na hatua walizozichukua kuhusu Ruby lakini hakumueleza kitu chochote kuhusu Khalid. “Edwin kwa nini ukachukua maamuzi kama hayo bila kunishirikisha kwanza mimi?akauliza kwa ukali Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nililazimika kufanya vile kwa sababu tayari wafanyakazi walikwisha goma kuendelea kufanya kazi na madam Annabel.Hata kanuni zinaeleza hivyo mheshimiwa rais” akasema Edwin na Dr Fabian akashusha pumzi “Sawa niachie suala hili nitalishughulikia kama kanuni zinavyoelekeza” akasema Dr Fabian na kukata simu akampigia Ruby “Rais anapiga simu” Ruby akamwambia Mathew “Tayari amekwisha elezwa kila kitu na Edwin” akasema Mathew na kumtaka Ruby apokee ile simu “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby nimepokea simu kutoka kwa Edwin muda mfupi uliopta amenipa maelezo ambayo yamenistua sana.Nini hasa kimetokea? “Mheshimiwa Rais kwa sasa siwezi kukueleza chochote naomba unipe muda ili nikutane nawe tuzungumze kuhusiana na suala hili” “Alichokisema Edwin kwamba umesababisha kifo cha mfanyakazi wa SNSA ukishirikiana na mtu ambaye si mfanyakazi wa idara ni kweli? “Ni kweli mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Kwa nini Ruby?Kwa nini ukafanya hivyo?Alichokifanya Edwin ni kitu sahihi kabisa.Ulivunja kanuni na wakalazimika kukuondoa kwani wafanyakazi wote hawakuwa tayari kuendelea kufanya kazi nawe.Hata hivyo niachie suala hili nitalishughulikia.Kanuni zinasema ni siku saba utakaa nje ya ofisi na baada ya hapo utarejea kazini” “Sawa mheshimiwa Rais nitasubiri kwa siku hizo saba” “Ni nani uliyekuwa naye ofisini ambaye anatajwa kushiriki kumuua mfanyakazi? “Ni Mathew Mulumbi mheshimiwa Rais? “Mathew Mulumbi !! Dr Fabian akashangaa “Ndiyo mheshimiwa Rais nilikuwa na Mathew” “Huyu mtu ametokea wapi na kuja kuleta matatizo makubwa namna hii?Kila sehemu alipo huyu jamaa ni matatizo matupu ! I’m sorry to say this but I don’t like that guy ! akasema Dr Fabian kwa ukali na ukapita ukimya kisha akasema “Nenda kapumzike Ruby tutazungumza zaidi kesho.Nitahitaji nisikie pia upande wako kujua nini hasa kilitokea”akasema Dr Fabian na kuagana na Ruby Mathew na Ruby walifika nyumbani tayari ilikwisha kuwa usiku mwingi.Wakati Ruby akiwa bafuni anaoga Mathew akaenda ofisini kwake akafungua kasiki akatoa kompyuta yake na kumpigia simu Habiba Jawad “Mathew habari yako.Unaonekana umechoka sana leo” akasema Habia “Ni kweli mama siku imekuwa ndefu sana na mambo yaliyojitokeza ni mengi pia” “Naamini umefanikiwa kumuona Khalid na kumfuatilia” akasema Habiba “Kuna tatizo limejitokeza mama wakati wa kumfuatilia Khalid” akasema Mathew na kumsimulia Habiba kilichotokea “Mathew usalama wa nchi yako uko hatarini hivi sasa.IS wanapanga kufanya shambulio kubwa lakini bado sijajua ni shambulio gani na wapi lakini fahamu kuna shambulio kubwa linaandaliwa.Misheni hiyo niliyokutuma ni mtihani kwako kwani ukifaulu basi utakuwa umefuzu kwenda kufanya misheni nyingine kubwa zaidi.Endapo utashindwa na IS wakishirikiana na James Kasai wakafanikiwa kutekeleza shambulio lao utanipa mashaka kama utaweza misheni nyingine kubwa inayokusubiri.Hawa jamaa wana mtandao mkubwa sana usimuamini mtu yeyoe kuanzia sasa.Fanya wewe mwenyewe kila kitu.Umenielewa Mathew? “Nimekuelewa mama” “Vizuri.Nategemea kesho utakaponipigia simu uwe na majibu mazuri ya kunipa.Ninataka uonyeshe umahiri wako na usitegemee mimi kukupa kila taarifa” “Nimekuelewa mama” akasema Mathew na kuagana na Habiba “Habiba Jawad yuko sahihi.Nimetetereka sana.Natakiwa kurudi kuwa Mathew Mulumbi wa kipindi kile.Mambo yaliyotokea leo hayakupaswa kutokea.Nilipaswa hadi muda huu niwe tayari na taarifa za mahala alipoKhalid na kama James Kasai amekwisha ingia nchini lakini mpaka sasa sina taarifa zozote .Sifahamu alipo Khalid wala James”akawaza Mathew na kugonga meza “Kuanzia kesho jiji hili halitakalika.Mathew Mulumbi will be back.Siwezi kuchezewa na magaidi kiasi hiki” akawaza Mathew na kurejea chumbani kupumzika









    Saa kumi na mbili za asubuhi simu ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo iliita akaunyoosha mkono na kuichukua akatazama mpigaji sura ikabadilika “Jenerali Akiki ! akasema kwa sauti ndogo akiwa amekunja ndita “Anataka nini huyu jamaa asubuhi yote hii?Huyu ni mtu ambaye sitaki kabisa hata kuisikia sauti yake ! akawaza Dr Fabian akiitazama simu ile ikiita na kukatika ikaanza kuita tena “Ngoja nimsikilize anachotaka kuniambia.Akiniletea dharau zake leo hii hii nitapelekea majeshi Uganda nikamchakaze vibaya sana ! akawaza Dr Fabian na kuipokea simu ile ya Jenerali Akiki. “Mheshimiwa Akiki habari za asubuhi” akasema Dr Fabian “Dr Fabian samahani sana kwa simu hii ya asubuhi ambayo hukuwa umeitarajia” “Ni kweli sikutarajia kabisa kupokea simu yako.Unasemaje Jenerali Akiki? “Dr Fabian nimekupigia tuzungumze kidogo mambo ya msingi.Nafahamu hasira ulizo nazo juu yangu na ndiyo maana hata mara ya mwisho tulipozungumza simuni mazungumzo yetu hayakuisha vizuri.Dr Fabian Uganda na Tanzania hatupaswi kufikia hatua hii tuliyofika.Sisi si majirani tu bali ni ndugu.Uganda tunapolia wa kwanza kusikia kilio chetu ni Tanzania na Tanzania inapolia wa kwanza kusikia kilio chao ni Uganda.Mheshimiwa rais naomba hiki kilichotokea siku chache zilizopita kisivuruge mahusiano mazuri ya kindugu kati ya nchi zetu hizi mbili” “Jenerali Akiki sina imani kama hayo unayoyasema yanatoka moyoni.Kama ungetambua Tanzania na Uganda ni ndugu usingethubutu kumuacha James Kasai akaishi Uganda ! Yote haya yanatokea kwa sababu serikali yako inamuhifadhi James Kasai na sasa anajulikana kama gaidi James Kasai ! akasema Dr Fabian kwa sauti ya ukali “Mheshimiwa Rais ni suala hilo ambalo limenifanya nikupigie simu asubuhi hii” “Nini unataka kuniambia?akauliza Dr Fabian “Ninataka suala hili limalizike hivyo nataka tuwe na kikao cha pamoja kati yako na Rais wa jamhuri ya kidemokerasia ya Congo bwana Patrice Eyenga mapema sana ikiwezekana hata kesho .Nataka tukae tuzungumze na tumalize suala hili kindugu.Katika kikao hicho tutazungumza mengi na kubwa ni kuhusu James Kasai” akasema Jenerali Akiki “Jenerali Akiki kwa muda mrefu umekuwa ukipigiwa kelele sana na nchi za Rwanda na Congo kuhusu James Kasai lakini wewe na serikali yako mmekuwa mkikana kabisa James kuwepo nchini Uganda na matokeo yake ndiyo haya yaliyotokea hivi majuzi.Unasema unataka kukaa nasi tuzungumze kitu gani kipya unataka kutueleza ambacho hujawahi kutueleza? Akauliza Dr Fabian “Dr Fabian ninataka tulimalize hili suala ili kuepusha nchi zetu kuingia katika machafuko ambayo wanayoathiriwa nayo ni raia wetu” “ Jeneral Akiki kitu pekee ambacho tunakihitaji kwa sasa na ambacho kinaweza kutuleta mezani kwa mazungumzo ni kujua mahala alipo James Kasai” akasema Dr Fabian “Hicho ndicho kikubwa ambacho ninataka kuzunguza nanyi.Najua James ndiye aliyechafua amani ya Afrika Mashariki na ninataka kumaliza sintofahamu hii.Naomba uandae kikao hicho cha siri baina yetu ili tuzungumze kama ndugu” akasema Jenerali Akiki “Umeelekeza kwamba unataka kuzungumza na mimi na Patrice Eyenga,vipi kuhusu Rwanda?Nao pia ni waathirika wa James Kasai” akasema Dr Fabian “Suala la Uganda na Rwanda halijatokana na James Kasai mheshimiwa Rais.Kuna matatizo yetu ya muda mrefu na sitaki kukaa meza moja na Rwanda” “Jenerali Akiki nitawasiliana na rais Patrice na kumshawishi akubali tukae na tuzungumze lakini naomba tafadhali mazugumzo hayo yawe na tija” “Nakuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba sintawapotezea muda wenu nina nia ya dhati ya kulimaliza suala hili.Ninaomba sana iwe mapema zaidi hata kesho kama ikiwezekana”akasema Jenerali Akiki “Sawa nitawasiliana na Rais Patrice halafu tutaona kama tukutane kesho au siku nyingine.Nitakujulisha”akase ma Dr Fabian “Nashukuru sana mheshimiwa Rais.Nategemea sana jibu lako” akasema Jenerali Akiki. Mara tu alipomaliza kuzungumza na Dr Fabian,jenerali Akiki akampigia simu Melanie Davis “Mheshimiwa rais” akasema Melanie “Melani habari yako mpenzi wangu” “Nzuri kabisa mheshimiwa Rais.Nimekuwa nakuwaza sana usiku wa leo.Tayari nimeanza kukumbuka Uganda” akasema Melanie na wote wakacheka “Melanie hata mimi nitafurahi sana kama nitakuona tena Uganda.Nategemea utapanga tena safari hivi karibuni” akasema Rais Akiki “Usihofu mheshmiwa Rais.Nitakuja Uganda tena na tena” akasema Melanie “Melanie nimekupigia kukujulia hali lakini vile vile kukujulisha kwamba nimetoka kuzungumza na Rais Dr Fabian nimemtaka aandae kikao cha pamoja na Rais Patrice Eyenga” “Amekubali?!akauliza Melanie “Ndiyo amekubali.Nimetaka kikao hicho kiwe kesho lakini amesema atanipa jibu baadae baada ya kuwasiliana kwanza na Rais Patrice na kila mmoja kuangalia ratiba yake.Natumai kwa upande wenu mnaendelea kujiandaa vizuri” “Ndiyo mzee kwa upande wetu hakuna tatizo,tunasubiri upande wako” “Msiwe na wasiwasi kila kitu kitakwenda vizuri kama kilivyopangwa ninachowasisitiza ni umakini mkubwa kwani hii ni misheni kubwa.Endapo mtakosea hata kidogo tu basi misheni hii itashindwa kufanikiwa na sisi sote tutakuwa katika matatizo hivyo kumbukeni hakuna kufanya kosa hata dogo.Kila kitu kipangwe kwa umakini mkubwa sana” akasema Jenerali Akiki na kuagana na Melanie. PARIS – UFARANSA Kengele ya mlangoni kwa Peniela ikalia akainuka akafikicha macho kisha akachukua kitanza mbali akabonyeza kitufe na mtu aliyekuwa mlangoni akaonekana katika runinga iliyokuwa ukutani “Maggie unasemaje?akauliza Peniela kwa sauti ya uchovu “Kuna mgeni wako amefika anasema ana miadi nawe anaitwa Peterson” “Sawa ninakuja sasa hivi” akasema Peniela akainuka akavaa vizuri kisha akatoka akaelekea sebuleni “Peterson” akasema Peniela “Peniela samahani sana kwa kukusumbua lakini nilikuahidi saa kumi na mbili za asubuhi nitafika hapa” “Karibu sana Peterson.Uliifanya ile kazi niliyokutuma? “Ndiyo madam.Nimeifanya”akasema Peterson na kufungua mkoba wake akatoa bahasha akampatia Peniela akaifungua akatoa makaratasi yaliyokuwamo ndani. “Ni ripoti ndefu hii nitapata muda baadae wa kuipitia naomba unieleze kwa mdomo kile ambacho mmekigundua kuhusu Melanie Davis” akasema Peniela “Tulichokigundua ni kwamba Melanie Davis ni rais wa Ufaransa lakini hakuna taarifa zake za kueleweka.Watu wanaotajwa kuwa ni wazazi wake na kwamba walifariki dunia hakuna taarifa zozote za kuwahusu,hakuna mahala wamewahi kusajiliwa kama wafanya biashara na hawajulikani walikuwa wanaishi wapi.Melanie Davis hana makazi hapa Paris wala hakuna biashara yoyote iliyosajiliwa kwa jina lake hapa Ufaransa.Akaunti yake ya benki ina shilingi trilioni tano ambazo hatujui zimetokana na biashara gani.Kwa sasa Melanie anaishi Tanzania ambako amewekeza katika biashara.Ulielekeza tuchunguze pia na watu wake wa karibu tumegundua kwamba Melanie Davis hana marafiki hapa Paris ila ana mtu mmoja tu ambaye ndiye amekuwa akiwasiliana naye mara kwa mara anayeitwa Devotha Adolph.Tumemchunguza huyo Devotha Adolph tukagundua kwamba huyu Devotha amewahi kuwa wakala wa Mossad” “Amewahi kuwa wakala wa Mossad? “Ndiyo.Alikuwa wakala wa Mossad toka akiwa nchini Marekani na hata alipohamia Tanzania bado aliendelea kuwa wakala wa Mossad” “Bado anaendelea hadi sasa na kazi hiyo ya uwakala?akauliza Peniela “Hapana kwa sasa si wakala wa Mossad tena.Ukisoma katika ripoti inaonyesha anaishi kifahari sana hapa Paris anatumia magari ya kifahari ana walinzi wanaomlinda lakini hajulikani anafanya kazi gani ila tumegundua ana ukaribu mkubwa sana na Rais wa Ufaransa ambaye wanawasiliana karibu kila siku” “Wana mahusiano gani? “Uchunguzi unanyesha ukaribu wao ni wa masuala mengine na si mapenzi na tunahisi labda ukaribu huo na Rais ndio unaomfanya aishi maisha ya kifahari” akasema Peterson “Huyu Devotha ameingia lini Ufaransa? “Miaka mitatu iliyopita” akajibu Peterson na Peniela akazama mawazoni hakafu akasema. “Peterson nakushukuru sana kwa kazi hii kubwa mliyoifanya ndani ya kipindi kifupi.Hata hivyo kuna kazi nataka ifanyike leo.Huyu Devotha ninamfahamu na nitahitaji kumfanyia mahojiano leo.Nitampigia simu na kumtaka aje hapa nyumbani kwangu leo hii kwa mazungumzo na atakapotoka Hapa nataka atekwe apelekwe sehemu mnayotumia kwa mahojiano halafu mtanijulisha” akasema Peniela. “Sawa madam Peniela.Ahsante kwa kutupa kazi kwani hatukuwa na kazi ya kufanya leo.Utanijulisha mara tu atakapokuwa amefika ili zoezi lifanyike haraka”akasema Peterson DAR ES SALAAM – TANZANIA Mathew na Ruby waliwasili hospitali kuwajulia hali Austin na Gosu Gosu.Siku hii ilianza kwa tabasamu kwani taarifa waliyoipata kutoka kwa daktari ni kwamba tayari Gosu Gosu alikwisha fumbua macho na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.Hii ilikuwa ni taarifa njema sana kwa akina Mathew.Asubuhi ile hawakuruhusiwa kuingia kumuona ili kumpa nafasi ya kuendelea kupumzika zaidi wakaelekea katika chumba alikolazwa Austin ambaye naye alikuwa anaendelea vizuri.Austin alifurahi sana kusikia kuhusu maendeleo mazuri ya Gosu Gosu. Baada ya kutoka kumtazama Austin Mathew na Ruby wakaelekea katika nyumba Fulani. “Hii ni moja ya nyumba zangu ambazo Peniela haifahamu hivyo nina uhakika haijauzwa.Anayeifahamu ni Gosu Gosu peke yake.Nafikiria kumuhamisha Gosu Gopsu kutoka hospitali na kumleta hapa kwa ajili ya usalama.Pale hospitali hayuko salama hata kidogo” Mathew akamwambia Ruby “Ni wazo zuri lakini itategemea na madaktari kama watakubali mgonjwa ahame” akasema Ruby “Watake wasitake lazima Gosu Gosu ahame.Nitaigeuza nyumba hii hospitali kwa ajili ya Gosu Gosu.Kuendelea kuwepo pale hospitali kwa sasa wakati hali yake imenza kuimarika ni kuendelea kuhatarisha maisha yake.Watu wanaotaka kumuua lazima watajaribu tena na tena hadi pale watakapofanikisha lengo lao” akasema Mathew na kushuka garini akaelekea katika geti ambako kulikuwa na kisanduku kidogo cheupe chenye vitufe viwili vya rangi ya kijani na nyekundu.Akaweka dole gumba katika kitufe cha kijani na mwanga ukatokea halafu zikatokea namba akatabasamu na kubonyeza namba Fulani kisha geti likaanza kufunguka wakaingia ndani. “Nyumba nzuri lakini inaonekana ina muda mrefu haijakaliwa na mtu yeyote”akasema Ruby “Ni kweli ina muda mrefu haijakaliwa na mtu.Niliijenga nyumba hii kwa ajili ya kuipangisha lakini baadae niliamua kuifanya kuwa ya mapumziko binafsi.Kila nilipohitaji kupumzisha akili yangu huja hapa.Nashukuru Gosu Gosu kwa kuendelea kuifanyia usafi na kuiboresha.Naamini hata kama nikifa leo bado watakuwepo watu watakaonienzi na mmoja wao ni Gosu Gosu.Japokuwa iliaminika nimekufa lakini bado vile vitu ambavyo vilinihusu sana amekuwa akivitunza kama vile aliamini siku moja nitarejea” akasema Mathew na kufungua sehemu akatoa funguo akafungua mlango wa sebuleni wakaingia ndani.Wakazungukia nyumba yote wakaikagua ili kuwa vizuri. “Nitamleta Lucy kufanya usafi wakati maandalizi mengine ya kuigeuza nyumba hii hospitali kwa ajili ya Gosu Gosu yakiendelea” akasema Mathew kisha wakaondoka kurejea hospitali ambako Mathew alitaka kuzungumza na madaktari kuhusu suala la kumuhamisha Gosu Gosu. PARIS – UFARANSA Ni saa tatu za asubuhi jijini Paris gari moja lenye rangi nyeusi liliwasili katika makazi ya bilionea Peniela.Mlango wa mbele ukafunguliwa akashuka jamaa mmoja aliyevaa suti nzuri nyeusi akatazama kila upande kuhakiki usalama halafu akaufungua mlango wa nyuma na mwanadada mmoja akashuka akaelekea katika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ambako alipokewa na mwanadada aliyevalia sketi nyeusi na shati jepesi jeupe akamuongoza kuelekea ndani ya jumba kubwa la Peniela akamkaribisha sebuleni.Baada ya dakika chache akatokea Peniela akiwa amevaa suruali nyeupe,shati jekundu lililokatwa mikono na kofia nyeupe ya mduara. “Devotha ! akasema Peniela na kukumbatiana na Devotha “Karibu sana Devotha”akasema Peniela “Nashukuru sana Peniela kwa kunikaribisha tena katika makazi yako.Nilifurahi sana uliponipigia simu na kunitaka nifike hapa kwako.Nilikuwa natafuta sana nafasi ya kuja kuonana nawe kuzungumza masuala Fulani muhimu nadhani hii ni fursa nzuri.Ningependa kwanza kusikia kile ulichoniitia kabla sijakueleza ya kwangu” akasema Devotha “Ahsante sana” akasema Peniela “Kikubwa nilichokuitia hapa ni masuala ya biashara.Nilitaka kuzungumza na Melanie lakini nikaona nizungumze kwanza nawe.Kama unavyofahamu mimi ni mfanya biashara mkubwa.Nina makampuni mengi na biashara nyingi.Nilimuuzia Melanie baadhi ya bisahara zangu zilizokoTanzania lakini bado ninazo biashara nyingine barani Afrika.Nina kampuni ziko Afrika Kusini,Misri ,Zimbabwe n.k.Ninataka kuyauza makampuni hayo yote.Sitaki kuendelea na uwekezaji wowote barani Afrika.I’m done with Africa.Ninataka kumpa Melanie nafasi ya kwanza katika wale ninaofikiria kuwauzia biashara zangu lakini kabla ya kufanya hivyo ninataka kufahamu uwezo wake wa kifedha je unadhani anaweza akamudu gharama za kununua makampuni hayo? Wewe ni mtu wake wa karibu unamfahamu vyema.Naomba uniweke wazi kama anaweza akamudu basi nizungumze naye” akasema Peniela na Devotha akatasamu. “Melanie ni tajiri sana sidhani kama anaweza akashindwa kununua makampuni hayo.Ana fedha za kutosha ndiyo maana hata ulipomtajia bei ya makampuni yale ya Dar es salaam hakusita wala hakuomba kupunguziwa.Uwezo anao wa kununua makampuni zaidi kama utapenda kumuuzia” akasema Devotha “Nimefurahi sana kusikia hivyo.Ninataka kuyaacha makampuni hayo kwa mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kuyaendeleza sitaki nimuuzie mtu makampuni halafu nisikie baada ya mwaka mmoja kumebaki magofu” “Nakuhakikishia Peniela ,Melanie anao uwezo mkubwa wa kununua makampunio hayo” akasema Devotha na Peniela akapokea simu akazungumza kwa muda kisha wakaendelea na maongezi “Ukiacha biashara zile nilizomuuzia Melanie kule Tanzania,ni biashara zipi nyingine anamiliki?akauliza Peniela na swali lile likaonekana kumbabaisha kidogo Devotha “Melanie utajiri wake ni wa kurithi.Wazazi wake walikuwa matajiri wakubwa sana na walipofariki katika ajali ya gari Melanie akaendeleza utajiri wa wazazi wake” akasema Devotha “Wazazi wake walimiliki biashara zipi hapa Ufaransa?akauliza Melanie “Sifahamu sana mambo ya Melanie.Nimekutana naye hapa hapa Ufaransa tukawa marafiki hivyo mambo mengi kuhusiana na biashara zake siyajui bado”Devotha akaonekana kukwepa kuzungumzia kuhusu biashara za Melanie “Peniela kwa nini unataka kuuza mali zako zote Afrika?akauliza Devotha “Kama nilivyosema I’m done with Afrika.Sitaki tena kuwekeza kule”akasema Peniela “Ni kwa sababu ya kifo cha mumeo? “Ndiyo.Hiyo ni sababu kubwa iliyonifanya niichukie Afrika na ndiyo maana nataka kuuza kila kitu sitaki kurejea tena kule”akasema Peniela.Waliendelea na maongezi mengine na baada ya muda Peniela akasema “Devotha ulisema kuna kitu ulitaka kunieleza tukionana ni kitu gani hicho? Devotha akavuta pumzi ndefu na kusema “Nina mpango wa kuwania urais wa Tanzania” akasema Devotha na Peniela akastuka “Unataka kuwania urais? “Ndiyo.Ninataka kuingia katika mbio za kuwania urais wa Tanzania” “Umenistua.Hadi kupata nafasi ya kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania urais si jambo dogo” “Ni kweli hicho unachokisema Peniela lakini ninao mtandao ambao ndio unaonitengenezea mambo hivyo ninahitaji sana pale muda utakapofika ninyi watanzania wenzangu mniunge mkono ili niweze kufanikisha ndoto yangu hiyo” “Dah ! hongera sana kwa kuwa na ndoto kubwa namna hiyo.Uongozi wa nchi si jambo dogo Devotha inahitaji uzoefu mkubwa” “Ninao uzoefu wa kutosha.Ninayafahamu majukumu ya Rais na ndiyo maana ninaamni nitaweza” “Umewahi kufanya kazi kulu? “Nilikuwa mkurugenzi wa SNSA.Secret National security Agency.Hii ni idara nyeti sana ambayo inashughulika na usalama wa ndani ya nchi na kwa kuwa kiongozi wa idara hii ambayo iko chini ya Rais ikulu kulikuwa ni kama nyumbani.Hapo ndipo nilipopata nafasi ya kufahamu mambo mengi kuhusiana na kazi ya urais na ndiyo maana nikasema kwamba ninaweza kuongoza nchi” akasema Devotha Mara tu Devotha alipotamka SNSA Peniela akastuka “Mathew alitamka hii idara wakati ananieleza kile kilichomtokea hadi akapotea.Kumbe huyu amewahi kufanya kazi katika idara hiyo.Vile vile Mathew aliniambia kwamba alitekwa na watu wa Mossad wakati wa operesheni ya kubadilishana mateka kati yao na magaidi wa IS lakini mpaka leo hii hata yeye hajui Mossad walifahamuje kuhusu mabadilishano yale.Sasa nimepata picha.Huyu alikuwa mkurugenzi wa SNSA na vile vile akawa ni wakala wa Mossad.Kama anamfahamu Mathew basi huyu ndiye atakuwa alimuuza Mathew kwa Mossad.Nitafahamu kila kitu leo mimi na yeye.”akawaza Peniela “Kwa nini uliacha kazi hiyo ya ukurugenzi katika idara ya SNSA?akauliza Peniela “Niliacha kazi ili nianze mchakato wa urais” “Kwani hapa Ufaransa umekaa kwa muda gani? “Nina miaka mitatu sasa” akajibu Devotha “Devotha mimi nimefurahi sana kusikia una ndoto kubwa namna hiyo.Nitakuunga mkono lakini pale utakapokuwa umechaguliwa na chama chako kugombea.Gharama zote za kampeni ni juu yangu mimi.Nitatoa ndege,helkopta na magari kwa ajili ya kukusaidia katika kampeni zako” akasema Peniela “Peniela ninakushukuru mno kwa kunielewa na kuahidi kunisaidia.Sijui nikushukuruje” “Usijali.Ni lazima nikuunge mkono mwanamke mwenzangu” akasema Peniela akazungumza kidogo na simu halafu akasema “Samahani Devotha unajua ninapokea simu nyingi za biashara hivyo univumilie” “Ninaelewa Peniela usijali” “Ulisema uliongoza idara ya SNSA ulimfahamu mume wangu Mathew Mulumbi?Huyo naye alikuwa anashughulika na masuala hayo hayo ya usalama”akauliza Peniela na Devotha akaoyesha mstuko kidogo “Mathew Mulumbi?! Akauliza Devotha “Ndiyo aliwahi kufanya kazi na idara yenu? “Hapana hajawahi kufanya kazi na idara yetu” akajibu Devotha.Waliendelea na mazugumzo halafu Peniela akamtaka radhi Devotha akaelekea chumbani kwake akachukua simu na kumpigia Peterson Lebrave mkurugenzi wa kampuni ya wapelelezi wa kujitegemea “Madam Peniela” akasema Peterson “Peterson mtu Yule tayari ninaye hapa ndani vijana wako tayari wamejipanga?akauliza Penila “Vijana wangu wako tayari.Atakapotoka hapo kwako utanijulisha” akasema Peterson kisha Peniela akarejea sebuleni alikomuacha Devotha wakaendelea na maongezi kuhusu mambo mbali mbali ya maisha na kubwa likiwa ni suala la Devotha kuwania urais.Dakika arobaini baada ya Peniela kuzungumza na Peterson simuni Peniela akamuomba radhi Devotha kwamba anahitajika ofisini.Wakaagana kwa miadi ya kukutana tena kwa mazungumzo zaidi.Peniela akamsindikiza Devotha hadi katika gari lake wakaagana akaondoka.Peniela akamtumia ujumbe Peterson kumjulisha kwamba Devotha anatoka getini. Eneo la makazi ya Peniela lilizungukwa na miti mingi na kutoka katika makazi hayo hadi kukuta barabara kuu ni umbali wa kilometa moja na nusu ukipita katika msitu.Walipokaribia daraja katika mto unaopita katika msitu ule wakayakuta magari mawili yameegeshwa.Dereva wa gari la Devotha akapunguza mwendo.Alipotazama katika kioo cha pembeni akaona kuna gari nyingine mbili zinakuja nyuma yao pamoja na piki piki mbili. “Kuna nini kinaendelea pale darajani?akauliza mlinzi wa Devotha aliyekuwa amekaa kiti cha mbele “Nashangaa kwa nini zile gari mbili zimeegeshwa pale darajani” akajibu dereva.Waliyakaribia yale magari mawili yaliyokuwa yameegeshwa darajani na kusimama dereva akapiga honi na mara pikipiki mbili zilizokuwa zikija nyuma yao zikafika na wale jamaa wawili wakachomoa silaha na kuanza kumiminia risasi dereva na mlinzi wa Devotha wote wakafa pale pale.Devotha alikuwa anatetemeka mwili kwa woga.Haraka sana watu wengine sita wakashuka kutoka katika magari mlango gari la Devotha ukafunguliwa akashushwa na kufunikwa mfuko kichwani akaingizwa katika mojawapo ya gari lililokuwa limeegeshwa darajani kisha likaondoka kwa kasi.Maiti za dereva na mlinzi wa Devotha zikaingizwa katika gari lingine na kuondolewa pale kisha usafi ukafanyika eneo lile kuhakikisha kwamba hakuna hata kioo kitakachoonekana.Mkoba wa Devotha ukachukuliwa simu yake ikazimwa,gari lake likapekuliwa kisha likasukumwa likaangukia mtoni.Baada ya kuhakikisha kila kitu kimekwenda vizuri wale jamaa wakaondoka zao





    Peniela akiwa nyumbani kwake akajulishwa kwamba kila kitu kimekwenda vizuri na akaelekezwa mahala alikopelekwa Devotha “Ni wakati wa kwenda kutafuta majibu.Yule mwanamke anamfahamu vyema Melanie na leo atanieleza Melanie ni nani hasa? Nilimuahidi Mathew kumtafutia majibu kuhusu Melanie na sasa ninakwenda kuupata ukweli” akawaza Peniela na kuvua mavazi aliyokuwa amevaa akavaa suruali ya jeans na fulana vyote rangi yeusi akavaa na kofia nyeusi akaondoka bila dereva wala mlinzi akaelekea mahala alikoelekezwa na Peterson kwamba ndiko anakoshikiliwa Devotha. “Kabla ya kukutana na Mathew Mulumbi niliwahi kufanya kazi na Team SC41.Ni kazi ya hatari sana nilikuwa naifanya lakini ni Mathew ndiye aliyeniondoa katika maisha yale na nikawa hivi nilivyo leo.Kila nikiyakumbuka maneno yale niliyomtakia jana roho yangu inaumia mno.Sikupaswa kumtamkia maneno kama yale.Sijui nitafanya nini kuyafuta maneno yale katika akili yake.Lakini kwa nini niliaamua kuchukua maamuzi kama yale?Je yalikuwa ni maamuzi sahihi?Toka ndani kabisa mwa moyo wangu ninampenda sana Mathew na hatatokea mwanaume ambaye nitampenda kama yeye” akawaza Peniela Peniela alifika mahala alikopelekwa Devotha.Ilikuwa ni katika bohari moja kuu kuu lililoonekana kutelekezwa.Aliingiza gari ndani ya bohari lile akashuka na kupokewa na Peterson “Ahsante sana Peterson kwa kuifanikisha kazi hii kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa” akasema Peniela wakati wakielekea katika ofisi ya Peterson “Madam Peniela kama nilivyokueleza kwamba vijana wangu hawakuwa na kazi ya kufanya leo ndiyo maana wakaifanya kazi ile kwa haraka sana” akasema Peterson wakaelekea katika ofisi yake akamweleza Peniela namna zoezi la kumteka Devotha lilivyofanyika na kila hatua waliyochukua kuhakikisha wanaondoa kila ambacho kingeweza kuleta matatizo endapo uchunguzi wa kutoweka kwa Devotha ungefanyika.Peniela akafurahi na kuahidi kuwalipa mara mbili ya kiasi walichokuwa wamehitaji. “Huyu mtu unataka tumfanye nini?akauliza Peterson “Huyu nataka mniachie mimi mwenyewe nitashuhulika naye.Kuna taarifa muhimu sana nazihitaji kutoka kwake” akasema Peniela na kupelekwa katika chumba kilichokuwa na kioo kikubwa akamtazama Devotha akiwa ndani ya chumba kingine amefungwa katika kiti. “Hatujampa mateso yoyote tulikuwa tunakusubiri kwanza ufike” akasema Peterson “Ahsante Peterson nifungulieni mlango nizungumze naye” akasema Peniela na kufunguliwa mlango akaingizwa ndani ya kile chumba alimo Devotha. “Hallo Devotha ! akasema Peniela huku akitabasamu akavuta kiti akaketi akatoa kofia na miwani.Mstuko alioupata Devotha ulikuwa mkubwa.Alihisi yuko njozini na si kitu cha kweli anachokishuhudia “No ! This is not true ! akasema Devotha “It’s true Devotha.Unachokiona si njozi ni kitu cha kweli kabisa.Aliyeko mbele yako ni mimi Peniela” akasema Peniela na Devotha akamtazama kwa hasira “Wewe ndiye uliyenifanyia hivi?! Akauliza kwa ukali “Ndiyo Devotha ni mimi! “Kwa nini Penielea?Nimekukosea nini hadi unifanyie hivi?akauliza Devotha “Devotha nimekuleta hapa kwa mahojiano na ninakuomba unijibu kwa ufasaha maswali nitakayokuuliza na endapo utaleta mzaha au kiburi this will be the end of the road for you” akasema Peniela “Don’t threaten me Peniela.Hunifahamu mimi ni nani na huna uwezo wa kuniamuru chochote.Kwa taarifa yako mambo kama haya nimeyapitia ninafahamu kila kitu na huwezi ukanitishia kunitesa.Peniela nakushauri usitake kungia katika matatizo makubwa.Mimi si mtu wa kutaka kuingia naye katika matatizo.Nakushauri tulia na maisha yako mazuri haya mengne yaache kabisa! akasema Devotha “Devotha ninakufahamu vizuri wewe ni nani.Ninaifahamu historia yako umetoka wapi na hadi umefika hapa na ninakuhakikishia kwamba bado hujawahi kupitia mateso.Bado hujawahi kuaona mateso na leo utayashuhudia labda ukubali kutoa ushirikiano ndipo utajiokoa lakini kama ukiwa kiburi basi utazungumza lugha zote unazozifahamu leo ! akasema Peniela “Peniela nani wanataka kukuingiza katika matatizo haya makubwa?akauliza Devotha “Devotha ninataka unieleze kuhusu Melanie Davis.Nimegundua kwamba anashrikiana na kikundi cha kigaidi cha IS na wewe kama mtu wake wa karibu lazima jambo hili unalifahamu vizuri.Nataka unieleze ukweli Melanie Davis ni nani ? Akauliza Peniela “You go to hell shetani wa kike wewe ! akasema Devotha kwa ukali “Huwezi ukaniweka hapa na kunihoji maswali.Wewe ni mtu mdogo sana wa kunihoji mimi ! akaendelea kufoka “Devotha nimekuuliza swali naomba unijibu.Melanie Davis ni nani?Peniela akauliza “Siulizwi maswali na panya mchafu kama wewe ! akasema Devotha. “Devotha nimekuuliza Melanie Davis ni nani?akauliza Peniela “We kahaba siwezi kukujibu swali lako lolote.Please go to hell ! akasema Devotha “Sawa Devotha tutaona mimi na wewe nani atakayetangulia kwenda huko unakosema niende ! akasema Peniela na kubonyeza kitufe na Peterson akaingia “Naomba niandaliwe vifaa ! akasema Peniela na Peterson akafungua kabati la chuma akatoa vifaa mbalimbali akaviweka mezani “Unahitaji msaada wowote Peniela? Akauliza Peterson “Huyu nitashughulika naye mimi mwenyewe.Ninahitaji watu wawili kwa ajili ya kumshika.Nataka nimuonyeshe kweli mimi ni shetani wa kike ! akasema Peniela.Peterson akawaita jamaa wawili wakaingia mle ndani Peniela akaenda mezani akachukua mkasi wa kukatia vitu vigumu “Devotha hii ni mara ya mwisho nitakuuliza.Melanie Davis ni nani? Akauliza Peniela “Peniela narudia kukuonya kwamba usiendelee na mchezo huu utajuta sana baadae” akasema Devotha na Peniela akawaelekeza wale jamaa wawili waliojazia miili wamkamate Devotha wamfunge katika kitanda cha chuma kilichokuwamo mle ndani.Devotha akanyanyuliwa na kufungwa katika kitanda kile “Melanie Davis ni nani?akauliza Peniela Devotha akamtemea mate usoni.Peniela akakishika kiganja cha mkono mmoja wa Peniela uliokuwa na vidole vitatu na kwa kutumia mkasi akakikata kidole cha mwisho “Aaaaaaaaghhh !! Devotha akatoa ukelele “Melanie Davis ni nani?akauliza Peniela “Nitakuua Peniela ! akasema kwa hasira Devotha .Peniela akakishika kidole kingine na kukikata Devotha akaendelea kupiga kelele. “Who is Melanie Davis?akauliza Peniela.Devotha aliendelea kupiga kelele kubwa kwa maumivu makali aliyoyapata. “Devotha nilikutahadharisha toka awali kwamba huu unaweza ukawa ni mwisho wako kama hautakuwa makini na ninarudia tena kukutahadharisha kwamba endapo hautakuwa makini huu utakuwa mwisho wako.Sina utani na Mungu atanisamehe kwani nitakufanyia kitu kibaya sana ! akasema Peniela kwa ukali lakini bado Devotha alikuwa anatetemeka na kulia kwa maumivu makali.Peterson akamsogelea Peniela akamnong’oneza kitu halafu akafungua droo na kutoa chupa yenye dawa ya chumvi chumvi akaenda kupaka mahala Peniela alipokata vidole.Devotha alitoa kelele kubwa akijaribu kujitoa katika kamba zile lakini alifungwa barabara.Aliweweseka akizungumza maneno kama mwenda wazimu. “Ulisema huogopi mateso na huu ni mwanzo Devotha.Nitakuharibu haribu leo.Naomba tafadhali unieleze Melanie Davis ni nani? Akauliza Peniela lakini Devotha hakujibu kitu aliendelea kulia huku akiweweseka kwa maumivu makali. “Devotha nitamaliza vidole vyote vya mikono na utabaki huna hata kidole kimoja.Malengo yako ya kuwa Rais yanakwenda kupotea .Tafadhali nijibu ili tuyamalize haya mambo ! akasema Peniela ambaye alikuwa na hasira kama Mbogo.Devotha aliendelea kulia Peniela akaushika tena mkasi akakimalizia kidole kilichokuwa kimebakia.Devotha aliendelea kupiga kelele kubwa hadi sauti ikaanza kukwama. “Devotha nimemaliza kiganja cha kwanza ninahamia kiganja cha pili.Nimekwambia leo nitakufanyia ukatili ambao haujawahi kuushuhudia” akasema Peniela na kukishika kidole cha mwisho cha mkono mwingine akakikata. “Peniela please !! Niko chini ya miguu yako tafadhali usiendelee kunitesa nama hii.Nimekukosea nini hadi unifanyie hivi?akauliza Devotha akiwa katika maumivu makali “Melanie Davis ni nani?akauliza Peniela “Nitakwambia Peniela tafadhali usiendelee kunitesa namna hii ! akasema Devotha “Nataka unieleze kila kitu kuhusu Melanie Davis! Akasema Peniela “Melanie Davis…. “Ndiyo nataka unieleze ni nani?Ana mipango gani nchini Tanzania? Akauliza Peniela.Devotha akavuta pumzi ndefu kisha akasema “Melanie ..aaahg…..ni mfanya biashara….Aaagh Peniela umeniharibu kwa nini lakini? Akaendelea kulia “Melanie anashirikiana na magaidi wa IS wana mipango gani nchini Tanzania?akauliza Peniela Devotha hakujibu akaendelea kugugumia kwa maumivu “Devotha naomba jibu haraka sana kabla sijaendelea kukuharibu ! akasema Peniela “Nitakueleza ukweli Peniela” akasema Devotha na kuvuta pumzi ndefu mara tatu halafu akasema “Melanie nimekutana naye…aaaghh ! akanyamaza na kufumba macho kwa maumivu makali halafu akaendelea “Nimekutana naye hapa Paris na tukawa marafiki.Akanieleza anataka kuwekeza Afrika nikamshauri akawekeze Tanzania na ndipo nilipoambatana naye kuja kwako kutaka kununua makampuni yako.Simfahamu kwa undani na wala sifahamu kama anashirikiana na magaidi ! akasema Devotha “Devotha unanidanganya ! akasema Peniela na kukibana kidole kwa mkasi “Peniela usinikate kidole tafadhali ninachokueleza ni kitu cha kweli kabisa.Simfahamu vizuri Melanie ! akalia Devotha. “Peniela nionee huruma unaniumiza bure sifahamu chochote kuhusu mambo anayoyafanya Melanie.Nilimsaidia kumleta kwako na sifahamu mambo yake mengine ! akaendelea kuomba Devotha “Unafanya kazi gani hapa Paris? Akauliza Peniela,Devotha akawa kimya “Unaishi maisha ya kifahari hapa Ufaransa unafanya kazi gani?akauliza tena Peniela na kukibana kidole “Usikate Peniela nitakwambia.Nina gharamiwa na Rais wa Ufaransa.Ninamshauri kuhusu masuala ya Afrika” akasema Devotha “Ulinieleza kwamba uliwahi kufanya kazi SNSA nikakuuliza kama unamfahamu Mathew Mulumbi ukakana kutomfahamu.Nakuuliza tena kwa mara nyingine tena unamfahamuMathew Mulumbi? Akauliza Peniela “Devotha nakuuliza kwa mara ya mwisho unamfahamu Mathew Mulumbi? Akauliza Peniela na kuendelea kukibana kidole “Peniela utaniua jamani usinikate tena vidole vyangu.Nitaishi vipi mimi?akalia Devotha “Nitakuua kweli kama hautanieleza ukweli”akasema Peniela “Ninamfahamu Mathew Mulumbi” “Mathew alishirikiana na idara uliyokuwa unaiongoza kuwakomboa mateka waliotekwa na IS lakini alitekwa na Mossad na hajulikani alipo.Nataka unieleze ukweli nani aliyewapa taarifa Mossad kuhusu operesheni ile aliyokwenda kuifanya Mathew? Akauliza Peniela “Sifahamu chochote Penielahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/akasema Devotha “Devotha nafahamu wewe ulikuwa wakala wa Mossad.Niambie ukweli kama ni wewe uliyewapa taarifa za Mathew Mulumbi na wakamteka?akauliza Peniela Devotha alishindwa kujibu.Peniela akakibana kidole na kukikata kikaruka.Devotha akalia kwa uchungu lakini sauti ilikwama kutoka “Devotha niambie ukweli ama sivyo huu utakuwa ni mwisho wako ! akasema Peniela kwa hasira lakini Devotha hakujibu alifumba macho akigugumia kwa maumivu huku akizungumza maneno yasiyoeleweka. Peniela akatupa ule mkasi akaenda kuchukua shoka dogo na kuwataka wale jamaa waufungue mkono mmoja wa Devotha na kuuweka katika meza “Devotha ni wazi wew e ndiye uliyemuuza Mathew kwa Mossad.Ninakusamehe kwa hilo lakini nataka unieleze nini mipango ya Melanie Davis na IS nchini Tanzania ! akasema Peniela Devotha bado aliendelea kumwaga machozi.Peniela akainua shoka juu kwa ajili ya kukata kiganja cha mkono Devotha akapiga kelele akimtaka asimkate “Nitakueleza Peniela.Nitakueleza kila kitu tafadhali usinikate mkono” akasema Devotah “Nieleze haraka sana mipango ya Melanie na IS ! akafoka Peniela “Sifahamu mpango wowote wa Melanie na IS ! akasema Devotha na bila kuuliza mara ya pili Peniela akainua shoka juu na kulishusha kwa nguvu katika kiganja cha mkono kikaruka chini.Devotha alishindwa kupiga kelele kwani sauti haikutoka tena “Devotha kinachofuata nitaukata mkono mzima.Leo nitakuondoa kiungo kimoja kimoja kama hautanieleza ukweli.Nataka uniambie mipango ya Melanie na IS ! akasema Peniela Devotha aliendelea kukoroma sauti haikuwa inatoka.Peniela akakasirika na kuukata mkono katika bega “Devotha nieleze ukweli! Akasema Peniela.Peterson akamsogelea akamnong’oneza sikioni “Peniela huyu hataweza kusema chochote tena.Kiwango cha mateso alichokipata ni kikubwa sana! Kwa hatua hii aliyofikia kuna kitu kimoja tu cha kufanya ni kumuua”Akasema Peterson “Devotha nina hasira sana nawe kwani umeyavuruga maisha yangu. Kitendo chako cha kumuuza Mathew kwa Mossad kimesababisha hadi sasa maisha yangu yakose furaha kwani siwezi tena kuwa na mtu niliyempenda katika maisha yangu! Mathew ameteswa na kumizwa mno na kwa ajili yako leo nitamlipia kisasi ! akasema Peniela huku akimtazama Devotha kwa hasira “Naomba u…u.uuusi….niue ! akaomba Devotha macho lakini Peniela aliyekuwa na hasira kama Mbogo akalishusha kwa nguvu shoka likatua katika goti na kuutenganisha mguu. “Hii ni kwa ajili ya Mathew na mateso yote aliyoyapitia kwa sababu ya tamaa zako ! akasema kwa hasira na kuukata mguu wa pili. “Nilikwambia nitakufanyia unyama mkubwa sana leo ! akasema Peniela na kumtazama Devotha “Kwa heri Devotha ! akasema Peniela na kushusha shoka kwa nguvu katika shingo ya Devotha na kuhitimisha safari yake ya maisha hapa duniani.Peniela akaenda katika chumba kilichokuwa na tanuru kubwa kwa ajili ya kuchomea miili akavua zile nguo zilizokuwa zimetapakaa damu akavaa nguo nyingine alizokuwa amekwenda nazo halafu akarejea ndani ya kile chumba Peterson akampa karatasi “Hii ni orodha ya namba za simu ambazo Devotha amekuwa akiwasiliana nazo mara kwa mara” akasema Peterson.Peniela akaipitia ile orodhana kukuta kuna namba nne kutoka Tanzania ambazo Devotha alikuwa anawasiliana nazo. “Ahsante Peterson” akasema peniela na kuchukua simu yake akampigia Mathew kwa njia ya video “Hallow Peniela” akasema Mathew baada ya kupokea simu “Mathew kabla ya kukueleza chochote kuna kitu nataka ukitazame” akasema Peniela na kuisogeza kamera ya simu karibu na mwili uliokatwa katwa wa Devotha “Unaweza ukaitambua sura hii” akauliza Peniela “Oh my God that’s Devotha ! akasema Mathew kwa mshangao “I killed this devil ! “You what ?! Mathew akauliza “Nimemuua.Huyu ndiye aliyekuuza kwa Mossad.Alikuwa wakala wa Mossad wakati ule na ndiye aliyewapa taarifa zako wakakuteka” “Jesus ! akasema Mathew “Huyu ndiye mshirika mkubwa wa Melanie Davis.Mathew hawa watu watakuwa na mipango mikubwa sana kwani Devotha amekuwa tayari kufa kuliko kueleza kile ambacho MelanieDavis anapanga kukifanya” “Melanie na Devotha wanafahamiana? “Ndiyo wanafahamiana na Devotha ndiye aliyemleta kwangu Melanie” akasema Peniela “Sijapata kitu chochote cha maana kutoka kwake kuhusu Melanie lakini nimepata namba nne ambazo amekuwa akiwasiliana nazo mara kwa mara nchini Tanzania.Mtazifuatilia kuwafahamu watu ambao amekuwa akiwasiliana nao.” akasema Peniela “Peniela sijui nikushukuruje kwa hiki ulichokifanya” “Mathew hawa ndo waliosababisha mimi nawe tukatengana hivyo nina hasira nao sana.Nimefanya hivi kwa ajili yako.Tafadhali hakikisha unampata Melanie Davis.Nimetumia wapelekezi wa kujitegemea kutafuta taarifa za Melanie lakini walichokipata kinashangaza.Hakuna biashara zozote zilizosajiliwa kwa jina lake hapa Ufaransa,hajulikani mahala anakoishi hapa Paris,hakuna taarifa zozote za kueleweka kuhusu wazazi wake lakini akaunti yake ina kiasi kikubwa cha fedha karibu trilioni tano.Ninaweza kusema kwamba huyu Melanie Davis amevaa uhusika bandia kwani taarifa zake zote zilizopo zinaonekana ni za kutengenezwa kwa madhumuni Fulani na ninahisi hata wakubwa wa serikalini hapa Ufaransa wanalifahamu hilo jambo kwani Devotha ambaye nimemuua ana ukarbu mkubwa sana na Rais wa Ufaransa ambaye tunahisi ndiye anayemfanya aishi maisha ya kifahari hapa Paris.Hicho ndicho nilichoweza kukipata Mathew” akasema Peniela “Peniela nimekosa neno zuri la kukushukuru kwa hiki ulichokifanya” akasema Mathew “Usinishukuru Mathew.Ni wajibu wangu kukusaidia.Kama kuna kitu chochote kingine ambacho unataka nikusaidie usisite kuwasiliana nami.Mwisho kabisa Mathew I’m very sorry for what I said yesterday.Sikupaswa kukutamkia maneno kama yale.Ni wewe uliyenifikisha hapa nilipo leo.Nisamehe sana zilikuwa ni hasira tu” akasema Peniela “Usihofu Peniela yale yamekwisha pita” akasema Mathew na kuagana na Peniela DAR ES SALAAM – TANZANIA Mathew Mulumbi akavuta pumzi ndefu baada kumaliza kuzungumza na Peniela.Kwa sekunde kadhaa alifumba macho yake halafu akayafumbua akamgeukia Devotha aliyekuwa pembeni yake.Walikuwa wameegesha gari pembeni ya barabara wakati Mathew akizungumza na Peniela “Hatimaye shetani amepatikana na kuuawa ! akasema Mathew na ujumbe ukaingia katika simu yake ukitoka kwa Peniela.Alikuwa amemtumia namba za simu za watu walioko Tanzania ambao wamekuwa wakiwasiliana na Devotha pamoja na picha za mwili wa Devotha baada ya kuuawa.Mathew akamuonyesha Ruby picha alizotumiwa na Peniela.Ruby alijikuta akibubujikwa machozi “Nimeshindwa kuvumilia Mathew kwa furaha niliyonayo kwa huyu mwanamke kuuawa.Nilichungulia kaburi kwa sababu yake.Siku nyingine ukiwasiliana na Peniela naomba umpe shukrani zangu kwa hiki alichokifanya kumuua Devotha” akasema Ruby huku akifuta machozi “Kwa mujibu wa Peniela huyu ndiye aliyewapa Mossad taarifa za operesheni ile na wakaniteka.Nashukuru Peniela amenilipia kisasi kwa mateso niliyoyapitia” “Hukuwahi kuniambia kama ulitekwa na Mossad lakini Peniela ulimweleza ! akasema Ruby “Muda utafika nitakueleza kila kitu.Lakini huyu mwanamke ndiye chanzo cha mateso yote niliyoyapata. Anastahili kufa kifo cha namna hii” akasema Mathew “Peniela ametuma namba hizi za watu ambao wamekuwa wakiwasiliana na Devotha,tuanze kuzifuatilia kuwafahamu wenye namba hizi.” akasema Mathew kisha Ruby akaichukua kompyuta yake akaweka sawa program zake na kuanza kupiga zile namba.Namba tatu hazikuwa zinapatikana na alipoingiza namba ya nne kwa ajili ya kupiga akastuka kwani alikuwa nayo ile namba tikana. “Edwin Mbeko ! akasema Ruby “Edwin Mbeko?Mathew naye akauliza “Ndiyo hii ni namba yake” akasema Ruby “Sasa picha imeanza kujitengeneza Ruby.Hebu tazama huu mtiririko.Devotha ambaye ni mtu wa karibu na Melanie amekuwa na mawasiliano na Edwin Mbeko wa SNSA.Jana tumempoteza Khalid Sultan kwa kitendo kilichofanywa kwa makusudi na watu ndani ya SNSA aliko Edwin.Kwa Edwin kuwa na mawasiliano na Devotha ambaye ni mtu wa karibu na Melanie nalazimika kuamini kwamba lazima Edwin atakuwa katika mtandao wa akina Melanie na ndiye anayewezesha mambo ya yote ya matandao huo kufanikiwa” akasema Mathew “Mathew hapa nilipo ninahisi mwili wote unanitetemeka kwa woga.Sikutegemea kabisa kama Edwin angeweza kuwepo katika mtandao huu” akasema Ruby na Mathew akamtaka awashe gari “Tunaelekea wapi? “Tunakwenda nyumbani nikachukue silaha kisha tunamfuata Edwin ofisini kwake SNSA” “Hawataturuhusu kuingia pale kwani mimi si mkurugenzi kwa sasa hadi suala langu litakapotatuliwa” “Ndiyo maana ninakwenda kuchukua silaha zitakazotuwezesha kungia pale SNSA” “Mathew huo ni mpango wa hatari kubwa.Ofisi ile ina ulinzi mkali na si rahisi kuivamia” akasema Ruby “Tutaingia pale ndani na lazima tumpate Edwin.Usihofu Ruby uko na Mathew Mulumbi the unstoppable! akasema Mathew “Mathew naomba nikushauri mpenzi wangu.Kwa mchana huu tulikuwa na mpango wa kumshughulikia Gosu Gosu.Tumuhamishe Gosu Gosu na kuhakikisha anakuwa sehemu salama halafu usiku wa leo ndipo tukavamie SNSA na kumchukua Edwin.Naamini mpaka muda huo hatakuwa anafahamu kama Devotha ameuawa na wala hatakuwa akijua kama tumefahamu ana mawasiliano na Devotha” akashauri Ruby.Mathew akafikiri kisha akasema “Ushauri mzuri.Tumuhamishe kwanza Gosu Gosu na kumpeleka sehemu salama halafu nitamonyesha Yule Edwin na mtandao wake mimi ni nani” akasema Mathew MPENZI MSOMAJI TUNAPOKARIBIA KUMALIZA SIMULIZI HII YA MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA KAA TAYARI KWA AJILI YA SEHEMU YA TATU NA YA MWISHO YA SIMULIZI YA SIRI ITAKAYOJULIKANA KAMA JASUSI/GAIDI. TUKUTANE SEHEMU IJAYO



    Geti la nyumba anayoishi Melanie Davis lilifunguliwa na gari la Edwin Mbeko likaingia.Akashuka garini na kufungua buti akatoa maboksi matano watumishi wa ndani wa Melanie wakatoka na kumsaidia kubeba maboksi yale wakayaingiza ndani. Mtumishi akamuongoza Edwin kwenda bustanini walikokuwa wamekaa Melanie.James Kasai na Khalid Khalid. “ Nimefurahi sana kuwaoneni tena mkifurahia hali ya hewa safi ya Dar es salaam” akasema Edwin baada ya kusalimiana na akina Melanie “Dar es salaam ni jiji zuri.Nitakuja tena kutembea siku nyingine.Nitakapokuja wakati mwingine Melanie naomba unitafutie mtoto mzuri wa kitanzania wa kustarehe naye.Nimepapenda sana Tanzania” akasema James Kasai huku akivuta sigara na mezani kukiwa na chupa kubwa ya pombe kali akinywa taratibu. “Umekuja na vifaa vyote nilivyoelekeza?akauliza Khalid “Ndiyo nimefanikiwa kupata kila kitu” akajibu Edwin “Edwin ninafurahi sana kufanya kazi nawe.Nimependa namna ulivyo makini katika kazi yako natumai huko siku za usoni tutashirikiana katika kazi nyingi zaidi za hapa Tanzania” akasema Khalid “Usijali Khalid mashirikiano haya yataendelea” akasema Edwin “Kwa kuwa kila kitu tayari mimi ninakwenda kuanza kutengeneza bomu” akasema Khalid na wote wakainuka wakaelekea ndani.Maboksi yale aliyokuja nayo Edwin yakaingizwa katika chumba maalum ambacho kiliandaliwa kwa ajili ya kutengenezea bomu vifaa vikatolewa katika maboksi,Khalid akavikagua kama vimetimia na bila kupoteza muda kazi ikaanza. Wakati Khalid akianza kutengeneza bomu Edwin akamuomba Melanie watoke wakazungumze nje. “Melanie kuna kitu kimetokea jana usiku sikukujulisha nilitaka nikifanyie kazi kwanza ndipo nikujulishe” akasema Edwin. “Nini kimetokea Edwin? Akauliza Melanie macho yake yakionyesha wasiwasi. “Jana usiku baada ya kutoka huku nilirejea tena ofisini nikakuta kuna kitu kimetokea.Mkurugenzi wetu mpya alifahamu kwamba kuna mchezo ulifanyika wakati wa zoezi la kumfuatilia Khalid” “Amegundua?akauliza Melanie “Ndiyo amegundua” “Amegundua vip?akauliza Melanie “Kuna watu ndani ya idara ambao niliwatumia katika kuvuruga zoezi lile kwa kuwapa fedha kidogo.Baada ya zoezi kumalizika nilimuondoa mmoja na kwenda kumuua kwa ajili ya usalama wetu Yule mwingine nilitegemea baada ya kutoka huku ndipo ningeenda kummaliza lakini niliporejea ofisini nikakutana na taarifa kwamba mkurugenzi akishirikiana na mtu mwingine ambaye si mfanyakazi wa idara yetu walimpeleka huyo jamaa katika chumba cha mahojiano wakamuhoji kisha wakaanza kumtesa hadi akapoteza fahamu.Nilipofika nilimkuta akiwa tayari amepata fahamu nikamuuliza nini sababu ya kuteswa vile akanieleza kwamba tayari Annabel anafahamu kuhusu kile kilichofanyika na alimtesa ili amueleze ukweli..” “Alimueleza chochote ?akauliza Melanie kwa wasi wasi “Hapana hakumueleza chochote” akajibu Edwin “Ahsante.Tayari nilikwisha anza kuwa na wasi wasi kwamba mpango wetu umeingia kirusi” akasema Melanie “Nilikuwa nimempa onyo kwamba akithubutu kusema chochote ataikosa familia yake ndiyo maana hakusema chochote kwa ajili ya familia yake.Hata hivyo nililazimika kumuua pale pale katika chumba alichokuwa amelazwa” “Ulifanya jambo zuri sana.Vipi kuhusu huyo mkurugenzi?Naye pia anatakiwa ashughulikiwe haraka sana kwani kuna kitu amekwisha anza kukihisi.Huyu ni hatari mno kwetu” akasema Melanie “Tayari nilikwisha anza kumshughulikia.Jana hiyo hiyo nililazimika kutumia kanuni zetu kumuondoa katika nafasi yake ya ukurugenzi.Pale idarani tunazo kanuni ambazo zinatuwezesha wafanyakazi kumuondoa kiongozi na niliwashawishi wenzangu tukazitumia kanuni hizo kumuondoa Annabel katika nafasi yake.Atakaa nje ya ofisi kwa muda wa siku saba.Nilifanya hivi kwa lengo la kumuweka nje ya ofisi ili tuendelee na mipango yetu.Kwa sasa hakuna wasi wasi na kila kitu kitaendelea kama kawida” akasema Edwin “Ahsante Edwin kwa hicho ulichokifanya hata hivyo bado haitoshi.Huyu mwanamke kama amefanikiwa kugundua jambo hilo hatakaa kimya lazima ataendelea kuchunguza hadi aufahamu ukweli.Kwanza amefahamuje jambo hilo?Au watu uliowatumia hawakuwa makini na wakasababisha akagundua walichokifanya?akauliza Melanie “Niliowatumia ni watu makini sana na wanajua wanachokifanya.Niliyemtumia kuvuruga mawasiliano anaitwa Dina ndiye ambaye tunamtegemea sana katika masuala yote ya satelaiti.Kwa ujumla wote hawa wawili niliowatumia wametekeleza nilivyowaambia hata mimi nashindwa kuelewa imetokeaje hadi Annabel akagundua kuhusu mchezo ule.Nitaendelea kuchunguza kujua namna alivyofahamu” akasema Edwin “Sawa Edwin lakini huyu mwanamke ni kama fisi.Tayari amenusa harufu ya nyama na ataendelea kuifuatilia kujua mahala alipo .Huyu Annabel tayari amekwisha hisi kuna kitu kinaendelea na hata kama akiwa nje ya ofisi ataendelea kufuatilia hadi aufahamu ukweli. Huyu ni mdudu ambaye anatakiwa kufinyangwa haraka .Nataka auawe haraka sana kabla hajaleta madhara” akasema Melanie “Huo ndio mpango wangu lakini kwanza nilitaka nimuondoe ofisini ili atupe nafasi ya kutekeleza mipango yetu na baada ya kutoka ofisini sasa ninaanza kuandaa mpango wa kumuua kumuondoa kabisa ili kuwa na uhakika kwamba hakuna kiumbe yeyote ambaye anaweza kuwa hatari kwetu”akasema Edwin “Vipi kuhusu Gosu Gosu ? Kuna taarifa zozote umepata kutoka hospitali?akauliza Melanie “Gosu Gosu sijapata bado taarifa zake zozote” “Kill him today ! akasema Melanie “Nataka hadi jua litakapochwea Gosu Gosu awe tayari ameuawa.Kwa namna yoyote ile hakikisha siku ya leo haipiti bila Gosu Gosu kuuawa.Yule ni mtu hatari sana kwani mipango yangu mingi anaifahamu na kwa mujibu wa Devotha,Gosu Gosu ana ukaribu na watu ambao wanaweza kuwa hatari kwetu.Endapo akifumbua macho anaweza akawaeleza watu hao kuhusu mimi na mambo yakaharibika.Make sure you kill him today.Sitaki kuwe na uchafu wowote njiani tunamopita” akasema Melanie “Usijali Melanie nitakapotoka hapa ninakwenda kushughulikia suala hilo.Devotha umewasiliana naye leo?akauliza Edwin “Nilijaribu kumtafuta lakini hapatikani simuni.Nitamtafuta tena baadae” akasema Melanie “Jenerali Akiki alinipigia simu asubuhi akanijulisha kwamba alizungumza na Dr Fabian kuhusu kuandaa mkutano na amekubali” “That’s good” akasema Edwin huku akitabasamu “Lini wanakutana kwa mazungumzo?akauliza Edwin “Jenerali Akiki alitaka iwe kesho lakini Dr Fabian ameahidi kumjulisha hapo baadae baada ya kuwasiliana kwanza na Rais Patrice Eyenga” “Kama Dr Fabian amekubali basi hata Patrice hawezi kukataa na kama Jenerali Akiki ametaka kikao kifanyike kesho basi kitafanyika hiyo kesho.Hii ni fursa ambayo wanaitafuta sana kukaa meza moja na Jenerali Akiki kuzungumza na hawataweza kuipuuzia hata kidogo.Melanie ninakusifu sana kwa uwezo mkubwa ulio nao hadi ukaweza kumshawishi Jenerali Akiki akakubaliana nawe” “Kila penye nia pana njia Edwin.Ninataka kulipiza kisasi na lazima nifanye kila linalowezekana kuhakikisha mipango yangu inakamilika” “Khalid amekwisha fanya mawasiliano na mtu aliyeahidi kumleta kwa ajili ya kutekeleza shambulio la kujitoa mhanga?akauliza Edwin “Ndiyo.Tayari amekwisha fanya mawasiliano na hivi tuzungumzavyo tayari mtu huyo amekwisha anza safari.Ni mtu kutoka katika kundi la Alshabaab la nchini Somalia ambaye makazi yake ni nchini Kenya.Tayari amekwisha vuka mpaka wa Namanga hivi sasa anaelekea Arusha.Kesho asubuhi tutampokea hapa Dar es salaam” akasema Melanie “Huyu anatakiwa kufika Dar es salaam leo hii hii ili tuwe na uhakika mkubwa kwamba tunaye mtu wa kutekeleza shambulio hilo.Hivi sasa bomu linatengenezwa na alitakiwa awepo hapa tayari kwa kazi hiyo.Khalid anatakiwa kuwasiliana na huyo mtu na kumtaka akifika Arusha asiendelee tena na safari.Mimi nitaruka na helkopta kwenda kumchukua.Kila kitu lazima kikamilike leo hii hii” akasema Edwin “Hilo ni wazo zuri sana Edwin” akasema Melanie wakaelekea ndani ambako Khalid alikuwa anaendelea na maandalizi ya kuunda bomu. Wakamueleza mapendekezo ya Edwin akakubaliana nayo kisha kwa kutumia simu ya Melanie akawasiliana na huyo mtu aliyekuwa njiani akielekea Dar es salaam kwenda kutekeleza shambulio la kujitoa mhanga akampa maelekezo ya kutoendelea na safari atakapofika Arusha na asubiri maelekezo mengine “Kwa kuwa limejitokeza suala hili la huyu mtu nalazimika kuahirisha baadhi ya mambo ili nielekee Arusha kumchukua kisha nirejee mapema Dar es salaam kuendelea na masuala mengine” akasema Edwin “Sawa Edwin lakini hakikisha unapoondoka umeacha watu watakaolishughulikia suala la Gosu Gosu pamoja na mkurugenzi wako Annabel” akasema Melanie “Sawa Melanie nitatoa maelekezo kwa vijana wafanye uchunguzi namna tukavyoweza kumuua Gosu Gosu.Lazima kwanza tufanye uchunguzi kwa kuwa naamini umakini utakuwa mkubwa sana baada ya jaribio lile la kwanza la kumuua kushindwa kufanikiwa.Vijana wataniletea mapendekezo ya namna tutakavyoweza kutekeleza mpango huo wa kumuua Gosu Gosu halafu tutajipanga kwa usiku wa leo tuweze kumuonda.Kuhusu Annabel nitalazimika kumfanyia uchunguzi kwa kuwa mpaka sasa sifahamu mahala anakoishi.Kwa Rais kumpa nafasi kama ile ya ukurugenzi wa idara nyeti lazima amejiridhisha kuwa ana sifa.Lazima atakuwa ni mtu mwenye mafunzo ya ujasusi na anafahamu mbinu nyingi hivyo kumuua inahitaji umakini mkubwa.Nitalishughulikia suala lake nitakaporejea kutoka Arusha.Msiwe na wasiwasi wowote kila kitu kitakwenda vizuri.” akasema Edwin kisha akaagana na Melanie akaondoka “Melanie yuko sahihi kbaisa.Annabel anastahili kuuawa lakini kuuawa kwake kunapaswa kufanywa kiutaalamu mno.Nitalishughulikia hili baada ya kurejea kutoka Arusha” akawaza Edwin akiwa garini baada ya kuondoka nyumbani kwa Melanie PARIS – UFARANSA Mlinzi aliyesimama katika mlano wa ofisi ya Rais wa Ufaransa aliufungua mlango watu wawili wakaingia na Rais Michael Weren akasimama akawakaribisha watu wale wakasalimiana kisha akawaelekeza waketi sofani. “Nilitegemea Devotha awe amekwisha fika hapa hadi mida hii lakini bado hajafika naomba dakika chache tumsubiri kwani yeye ni muhimu sana katika mazungumzo haya” akasema Michael Weren na kwenda mezani kwake akachukua simu akampigia Devotha lakini simu yake haikuwa inapatikana “Simu ya Devotha haipatikani nadhani tuendelee na mazungumzo atakuta tukiendelea” akasema Michael Weren “Mheshimiwa Rais kubwa ambalo limetuleta hapa ni kutaka kupata mrejesho kuhusiana na ule mpango wetu wa Afrika.Nini kinaendelea hadi hivi sasa?akauliza mmoja wa wale jamaa aliyekuwa na suti ya rangi ya kijivu “Kwa ujumla mpango wetu unakwenda vizuri sana mpaka sasa.Kama mnavyosikia katika vyombo vya habari ni kwamba hali ya kiusalama katika eneo la Afrika mashariki ni tete.Kumetokea mvurugano mkubwa sana na jumuiya kwa sasa iko hatarini kuvunjika.Rwanda na Uganda zinashambuliana mpakani.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nayo imepeleka vikosi vyake katika mpaka wake na Uganda.Nchi tatu za Tanzania,Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo zinaandaa kikosi cha pamoja kwa ajili ya kuvamia nchini Uganda kumsaka James Kasai ambaye alitekeleza shambulio lililopelekea mvurugano huu ukatokea.Tayari Uganda imetoa onyo kwamba endapo kikosi hicho kitathubutu kutia mguu wake nchini Uganda basi itatumia nguvu kubwa kukisambaza.Haya yoteni matokeo ya mipango yetu na hakuna ubishi kwamba jumuia ya Afrika mashariki inakwenda kusambaratika” akasema Michale Weren “Tunafuatilia sana hali ya mambo inavyokwenda Afrika mashariki na zipo dalili kwamba jumuiya hiyo inaweza ikasambaratika na sisi tukapata njia ya kupita kuelekea Congo lakini kuna jambo ambalo linaleta ukakasi kidogo njia iliyotumika katika kusababisha hali hii ikatokea.James Kasai anayeongoza kikundi cha waasi pamoja na kikundi cha kigaidi cha IS walishirikishwa katika mpango huu.Hii imetia doa mpango wetu.Hatukupanga kuwatumia magaidi au James Kasai ambaye amekwisha ua mamia ya watu na anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kutokana na mauaji aliyoyafanya.Mtu kama James Kasai au kikundi cha IS kufahamu mipango yetu ni hatari kubwa sana kwetu” akasema Yule mzee “Hata mimi nilipoelezwa mara ya kwanza kwamba James Kasai na kikundi cha kigaidi cha IS wameshirikishwa katika mpango huu nilistuka na kutaka mpango huo wa kuwatumia watu hao usitishwe mara moja lakini nikapewa ufafanuzi na faida za kuwatumia James na IS nikaona ni mpango mzuri nikatoa maelekezo kwamba waendelee kushirikiana nao” akasema Michael “Unaweza ukatueleza mheshimiwa Rais faida za kuwatumia hawa magaidi na James Kasai? “Faida kubwa ni kwamba mpango huu hautajulikana kama sisi tunahusika utaonekana ni mpango wa IS na James Kasai.Mpaka sasa nchi za Afrika mashariki zinamsaka James kwa udi na uvumba na hii inatupa sisi nafasi ya kuendelea na mipango yetu bila ya kutambulika”akasema Rais Michael na kuwaeleza kuhusiana na mpango unaoendelea wa kuwaua marais wa Tanzania na Congo kuwafafanulia faida zake “Kama mpango huo utafanikiwa basi itakuwa ni chanzo cha vita kati ya majeshi ya serikali ya Congo na kikundi cha James Kasai na vikundi vingine pia vitaibuka nchi ya Congo itarejea kuwa kama ilivyokuwa zamani.Patrice Eyenga amekuwa ni kikwazo kikubwa kwetu lakini kama jumuiya ya Afrika mashariki ikisambaratika na tukafanikiwa kumuua Patrice Eyenga basi njia itakuwa nyeupe ya kuingia Congo”akasema Michael “Ni mpango mzuri sana huo lakini nina mapendekezo kwamba huyu mtu ambaye ametumwa kwenda kufanikisha mpango huu auawe mara tu atakapokamilisha mpango huo.Mtu huyo kuendelea kuwa hai ni hatari sana kwetu.Ni vipi kama siku moja James Kasai akakamatwa na kumtaja kuwa anashirikiana naye? Itakua ni aibu kubwa kwetu hivyo napendekeza mara tu atakapokuwa amemaliza kazi yake auawe mara moja na sisi tuendelee na mipango mingine” akatoa ushauri mmoja wa wale jamaa “Ushauri wako ni mzuri na nitauzingatia.Ni kweli huyu mtu akiendelea kuwepo hai itakuwa ni hatari kubwa kwetu.Wazo la kumuua ni zuri” akasema Rais Michael Weren na baada ya mazungumzo ya takribani saa mbili akaagana na wageni wake wakaondoka.Mara tu wageni wake walipoondoka Rais Michael akachukua tena simu na kumpigia Devotha lakini bado simu yake haikupatikana “Devotha uko wapi? Ninahitaji sana kujua taarifa za kinachoendelea Tanzania” akawaza Michael na kuketi katika kiti chake akaweka miguu juu ya meza “Kwa nini Melanie akaanzisha mashirikiano na magaidi wa IS? Naamini lazima atakuwa amewaeleza kuhusiana na mipango yetu na hiki ni kitu kibaya sana.Jambo hili si la kuchukulia kirahisi kwani magaidi hawa wanaweza wakatugeuka siku za usoni na kutuchafua.Nadhani pendekezo la kumuua Melanie ni zuri.Mara tu atakapomaliza mpango wa kuwaua marais wa Tanzania na Congo lazima naye auawe.Nitajadiliana na Devotha kwa kina suala hili” akawaza Michael. TANZANIA Saa kumi bna mbili za jioni helkopta ya idara ya SNSA ilitua katika bohari kuu la idara hiyo.Edwin Mbeko alikuwa ametoka jijini Arusha kumchukua mtu ambaye angetekeleza shambulio la kujitoa mhanga lililolenga kuwaua marais Dr Fabian na Patrice Eyenga.Tayari gari lake lilikwisha fika mahala pale akashuka katika helkopta pamoja na mtu wake aliyekwenda kumchukua Arusha wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Melanie Davis. “Abdi karibu sana Dar es salaam” akasema Edwin lakini Abdi hakujibu kitu alikuwa ameelekeza macho yake nje akitazama pilika pilika za jioni za wakazi wa jiji la Dar es salaam. Safari iliendelea kimya kimya hadi walipowasili nyumbani kwa Melanie akafunguliwa geti na kuingia ndani.Melanie aliwapokea na kuwakaribisha sebuleni ambako James Kasai alikuwa ametulia sofani akiwa na chupa kubwa ya mvinyo. “Karibu sana Abdi.Huyu ni James Kasai naamini umewahbi kusikia taarifa zake” Melanie akafanya utambulisho na Abdi alionekana kustuka kidogo kumfahamu James Kasai. Melanie akamchukua na kumpeleka katika chumba alichoandaliwa ili apumzike kabla ya mazungumzo hapo baadae. “Mambo yanakwendaje hapa?akauliza Edwin “Mambo yanakwenda vizuri.Khalid anaendelea na uundaji wa bomu na kwa maelezo yake anaelekea katika hatua za mwisho kulikamlisha”akajibu Melanie “Vizuri sana.Mpaka hapa tuna uhakika kwamba bomu linaelekea kukamilika na mtu wa kulilipua tunaye.Umepata mrejesho wowote kutoka kwa Jenerali Akiki?Edwin akauliza “Ndiyo.Amenipigia simu akanijulisha kwamba marais Dr Fabian na Patrice Eyenga wamekubali kukutana naye kesho jijini Dar es salaam.Mipango yetu yote inakwenda vizuri” “Safi sana.Nitarejea hapa baadae natakiwa kurejea ofisini nikashughulikie suala la Gosu Gosu kwani niliwachia kazi vijana wachunguze namna tutakavyoweza kumuua.Kabla ya mapambazuko ya lazima Gosu Gosu awe ameuawa.Devotha umewasiliana naye? Akauliza Edwin “Hapana hajanipigia simu.Mara nyingi yeye hunitafuta kutaka kujua kila kinachoendelea huku lakini nashangaa mpaka muda huu hajanitafuta na siyo kawaida yake” akasema Melanie “Sawa nitamtafuta nimjulishe kile kinachoendelea” akasema Edwin akaagana na Melanie akaingia garini na kabla ya kuondoka akachukua simu akazitafuta namba za Devotha akampigia lakini simu yake haikupatikana. “Where are you Devotha?Kwa nini leo hupatikani?akajiuliza Edwin akawasha gari na kuondoka “Kila kitu kimekamilika kwa ajili ya tukio la kesho.Dr Fabian kama angejua kwamba kesho atakufa angeanza kutubu kuanzia sasa kumuomba Mumgu amsamehe makosa yake kwani sku ya kesho hataimaliza atakuwa amekufa.Nina hasira naye sana Yule jamaa ameniweka kukaimu nafasi kwa miaka mitatu halafu anakuja kumpa ukurugenzi mtu mwingine kabisa na kuniacha mimi ambaye nimefanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa miaka mitatu.Baada ya kufariki mimi nitaendelea kuwa mkurugenzi kwani Annabel hatarejea tena.Hakuna wa kumrejesha” akawaza na kutabasamu “Usiku huu nitamuondoa Gosu Gosu na baada ya hapo nitaanza kumsaka Annabel.Lazima naye afe.Kama alivyosema Melanie kwamba Annabel ni mdudu anayetakiwa kufinyangwa haraka sana kabla hajaleta madhara makubwa” Edwin aliendelea kuwaza mambo mengi hadi alipofika katika jengo la makao makuu ya SNSA akashuka garini na kuelekea ofisini kwake ambako alipewa taarifa kuhusiana na maandalizi ya mazishi ya Fidelis na vile vile akajulishwa kuhusu kifo cha Edina .Edwin akaonyesha masikitiko makubwa kwa taarifa ile mbaya.Hakupoteza muda akaenda kuzungumza na wafanyakazi “Ndugu zangu habari za muda huu.Awali ya yote ninapenda kuwashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa mliouonyesha jana hadi tukafanikiwa kumuondoa Annabel ambaye alionekana kushindwa kumudu vyema majukumu yake na hata kupelekea kifo cha mwenzetu Fideli.Tayari suala lake liko kwa Rais analishughulikia na tunasubiri maamuzi yake.Nimetaarifiwa pia kwamba maandalizi ya mazishi ya Fidelis yanaendelea vizuri na kwa mujibu wa wanafamilia atazikwa kesho kutwa na sisi tutashiriki kikamilifu. Tukiachana na taarifa hizo za Fidelis,nimepewa tena taarifa nyingine mbaya za kuhuzunisha kwamba mwenzetu,kipenzi chetu,mdogo wetu dada yetu Edina amefariki dunia.Nimestushwa sana na taarifa hizo.Taarifa zinadai amepigwa risasi yeye na mdogo wake.Huu ni ukatili mkubwa sana amefanyiwa huyu mwenzetu.Japokuwa tayari jeshi la polisi linaendela na uchunguzi wa suala hili sisi pia tunapaswa kufanya uchunguzi kujua nani hasa aliyemuua Edina? Binafsi ninaunganisha kifo cha Edina na kifo cha Fidelis.Nina uhakika vina muunganiko na aliyesababisha kifo cha Fidelis ndiye aliyemuua Edina.Tutaandaa timu ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu jambo hili.Hili ni pigo lingine kubwa tunalipata ndani ya kindi kifupi hta hivyo hatupaswi kukata tamaa.Tutaendelea na jukumu letu la ulinzi wa nchi na wale wote wenye lengo la kutukwamisha hawatafanikiwa”Edwin akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Jambo la tatu ninalotaka kuwajulisheni ni kwamba ninaliondoa rasmi mezani suala la Khalid Sultan Khalid lililoletwa na Annabel.Mpaka sasa hatuna ushahidi wowote wa kutosha kuhusiana na huyu mtu ambaye tuliagizwa kumfuatilia.Annabel akipaswa kutupa uthibitsho usio na shaka kuhusiana na uhatari wa huyu mtu kwa nchi yetu.Hatutaendelea tena kupoteza muda kumtafuta Khalid ambaye hatuna uhakika kama ni gaidi hadi hapo Annabel kama atabahatika kurejea atupe uthibitisho kwamba kweli mtu huyu ni gaidi kutoka IS hivyo kuanzia sasa hakuna mtu yeyote kuendelea na suala lile nimeliondoa rasmi” akasema Edwin na kutoa maelekezo kadhaa akarejea ofisini kwake ambako vijana wawili ambao aliwatuma kufanya uchunguzi hospitali kutafuta namna ya kumuua Gosu Gosu wakamfuata “Victor naamini kazi niliyowatuma mmeikamilisha” akasema Edwin “Mkuu ile kazi haijakamilika kw…….. “Kwa nini haijakamilika wakati niliwaambia kwamba ni kazi ya muhimu? Akauliza Edwin kwa ukali “Mkuu kuna jambo limejitokeza ndiyo maana tulishindwa kuikamilisha kazi uliyotutuma” akasema Victor “Nini kimetokea?akauliza Edwin “Gosu Gosu hayupo hospitali amehamishwa” “Amehamishwa?! Edwin akashangaa “Ndiyo mkuu amehamishwa.Hayupo pale hospitali” Edwin akavuta pumzi ndefu na kuwatazama vijana wake akauliza “Amehamishiwa wapi?akauliza “Hatujui mkuu” Edwin akagonga meza kwa hasira “Kwa nini msijue amehamishiwa wapi? “Mkuu hilo jambo limefanywa kwa siri kubwa na hata wafanyakazi wa hospitali hawajui mahala alikohamishiwa Gosu Gosu.Kwa mujibu wa watu tuliowahoji ni kwamba lilifika gari la wagonjwa ambalo si la hospitali ile na Gosu Gosu akatolewa katika wodi akaingiwa garini likaondoka bila taarifa kwamba linaelekea wapi lakini tulipata maelezo kwamba kabla ya kuondolewa hospitali daktari anayejulikana kama Dr Masawe alikuwa na mazungumzo na watu Fulani wawili ofisini kwake halafu baada ya muda likafika hilo gari Gosu Gosu akahamishwa na huyo daktari na wengine wawili pamoja na wauguzi wawili waliondoka na gari lingine na tunadhani walilifuata lile gari lililombeba Gosu Gosu.Tumefuatilia hospitali mbali mbali kubwa lakini hajapelekwa huko” akasema Victor na Edwin akashika kichwa . “Walifahamu Gosu Gosu yuko hatarini kuuawa ndiyo maana wameamua kumtoa pale hospitali na kumpeleka mafichoni.Wamempeleka wapi? Akajiuliza Edwin “Mkuu kutokana na uchunguzi wetu inaonekana huyo Dr Masawe kuna kitu anakifahamu kuhusu kuhamishwa kwa Gosu Gosu na kama tukimpata tunaweza kufahamu alikopelekwa mgonjwa.Tulikwenda mbali zaidi na kufahamu hadi mahala anakoishi huyo Dr Masawe lakini hatukuweza kufanya chochote tukisubiri maelekezo yako”akasema Victor “Good.Kazi nzuri sana mmeifanya.Kama tayari mmefanikiwa kufahamu mahala anakosihi Dr Masawe itakuwa rahisi sana kwetu kufahamu mahala alipo Gosu Gosu” akasema Edwin na kuwaelekeza wale vijana kwenda kujiandaa “Kwa namna yoyote ile lazima Gosu Gosu apatikane na auawe.Lile tayari ni bomu na linaweza kulipuka muda wowote hivyo lazima tulitegue haraka sana.Melanie alifanya kosa kubwa kuanzisha mahusiano na mtu kama Yule na sasa inatugharimu kuanza kumuwinda” akawaza Edwin na kumuita dereva wake ambaye alifika mara moja “Jackson kuna kazi ambayo nataka nikupe ikaisimamie na kuhakikisha inakamilika” akasema Edwin na kumuelekeza Jackson kuhusiana na zoezi lile la kumuua Gosu Gosu na akamtaka ahakikishe anaipata familia nzima ya Dr Masawe.Baada ya maelekezo yale Jackson na vijana wengine watatu wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Dr Masawe.





    Tangu alipotolewa hospitali na kuletwa katika nyumba ambayo Mathew aliiandaa,hali ya Gosu Gosu bado iliendelea kuwa mbaya.Alipoteza fahamu wakati wa zoezi la kumuhamisha kumtoa hospitali na hadi giza linangia hakuwa amerejewa na fahamu. “Mathew lengo lako la kumtoa Gosu Gosu kule hospitali na kumleta hapa ni zuri sana kwa ajili ya usalama wake lakini kwa hali hii aliyonayo nasikitika kusema kwamba tutalazimika kumrejesha tena hospitali akafanyiwe uchunguzi zaidi.Hapa hatuna vifaa vya kuweza kumfanyia uchunguzi kufahamu nini hasa tatizo lake” Dr Masawe akamueleza Mathew. “Dr Masawe naomba unieleze ukweli kuhusu Gosu Gosu.Is he going to make it?akauliza Mathew “I don’t know Mathew.Hali ya Gosu Gosu inatuchanganya sana ndiyo maana ninashauri tumrejeshe tena hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.Kwa hali yake ilivyokuwa hakupaswa kuhamishwa kuletwa hapa.Kama ni usalama wake tutatumia walinzi au tutaomba msaada wa jeshi la polisi kumlinda isitoshe ana mahusiano na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania tukimueleza hali halisi anaweza akatupa msaada.Kuendelea kumuweka hapa Gosu Gosu ni kuhatarisha maisha yake” akasema Dr Masawe.Mathew akainamisha kichwa akazama mawazoni. “Mathew umejitahidi sana kuhakikisha mwenzako anakuwa salama lakini kwa hapa ilipofika hakuna namna lazima arudi hospitali” akaendelea kusisitiza Dr Masawe. “Ahsante kwa ushauri wako Dr Masawe lakini hapana.Gosu Gosu ataendelea kukaa hapa hapa.Hatarejea tena hospitali.Endeleeni kumuhudumia hapa hapa na kama ni kupoteza maisha apoteze maisha akiwa hapa ndani kwa amri ya Mungu na si binadamu mwingine kuitoa roho yake” akasema Mathew “Mathew mimi ni daktari na ninashauri Gosu Gosu arejeshwe hospitali ili tuweze kuokao maisha yake.Tafadhali sana” akasema Dr Masawe “Dr Masawe nimeigeuza nyumba hii hospitali kwa ajili ya Gosu Gosu.Nimenunua kila kifaa ulichokiorodhesha kwa ajili ya kumsaidia Gosu Gosu akiwa hapa hivyo ataendelea kupatiwa matibabu hapa hapa na hatakwenda tena sehemu yoyote.Endeleeni kumuhudumia kwa kila uwezo mlio nao na kama akipoteza maisha itakuwa ni amri ya Mungu.Hakuna tena mjadala katika hilo Dr Masawe ! akasema Mathew “Mathew nafahamu umetumia gharama kubwa sana kununua mashine na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumsaidia Gosu Gosu lakini bado ushauri wangu uko pale pale kwamba tunatakiwa kumrejesha hospitali.Yawezekana waliokuwa wanataka kumuua wamekwisha fika hospitali na kugundua amehamishwa na hawajui mahala alipo hivyo wataachana na zoezi hilo” “You don’t know anything Dr Masawe” akasema Mathew na kutoka sebuleni akaenda katika chumba alimokuwa amelazwa Gosu Gosu akawakuta madaktari wengine wawili na wauguzi wakiwa wamesimama wanamtazama Gosu Gosu.Akamsogelea karibu “Gosu Gosu nimefanya maamuzi magumu kukuhamisha kutoka hospitali kukuleta hapa ambako naamini ni sehemu salama.Siogopi kutumia hadi shilingi ya mwisho kuhakikisha unakuwa salama.I hope you are going to wake up soon brother ” akawaza Mathew huku akimtazama GosuGosu halafu akatoka mle chumbani akaenda katika chumba alimolazwa Austin ambaye naye alihamishwa hospitali na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri akamueleza kile kinachoendelea “It’s a taugh call Mathew but it’s the right one.Mathew ahsante sana kwa maamuzi haya uliyoyafanya ya kuhakikisha tunakuwa salama kwa kutuleta hapa.Pale hospitali chochote kingeweza kutokea.Hawa watu lazima wangefanya kila juhudi kuhakikisha tunauawa.Mathew wewe ni kaka yet…….” Austin akanyamaza baada ya Ruby kuingia mle ndani kwa kasi na kuwastua sana “Kuna nini Ruby?akauliza Mathew “Dr Masawe” akasema Ruby “Kafanya nini?Mathew akauliza “Wakati tunaendelea na maongezi amepigiwa simu na mtu halafua kafungua kitu kama video katika simu yake na sura yake ikabadilika ghafla kisha akanitaka nikamfungulie geti kuna mahala anaelekea.Ameondoka kwa kasi ya ajabu” akasema Melanie “What’s going on?Hajakueleza chochote?akauliza Mathew “Hapana hajaniuliza chochote” akajibu Ruby.Mathew akajaribu kumpigia lakini hakupokea simu. “Hapokei simu yawezekana amepata taarifa mbaya za mgonjwa na anamuwahi” akasema Mathew “Kwa mstuko alioupata baada ya kutazama ile video katika simu yake pokea ile simu na kwa namna alivyoondoka sina hakika kama anamuwahi mgonjwa.Halafu hata kama angekuwa anamuwahi mgonjwa lazima angetueleza lakini ameondoka kimya kimya bila kusema chochote.Something is not right” akasema Ruby “Usihofu Ruby kama kuna kitu kibaya Dr Masawe atatueleza” akasema Mathew huku akitazama saa yake “Austin sisi tunaondoka.Usiku wa leo tunavamia ofisi za SNSA.Ninahitaji kumpata Edwin Mbeko usiku wa leo.Madaktari wako hapa na wauguzi wanaendelea kumtazama Gosu Gosu.Natamani tungekuwepo na sisi pamoja nanyi lakini tuna kazi nyingine kubwa ya kufanya.Ni kazi ngumu na ya hatari kutokana na ulinzi mkali uliopo SNSA lakini nakuahidi tutarejea salama” akasema Mathew “Ninaelewa Mathew.Ninawatakia kila la heri.Hakikisheni mnampata huyo Edwin” akasema Austin.Mathew akachomoa bastora na kumpa. “Kama likitokea tatizo lolote kabla hatujarejea please save yourself and Gosu Gosu too” akasema Mathew kisha wakatoka na kwenda kuwaaga wale madaktari wanaomuhudumia Gosu Gosu na kuwakuta wakijadiliana kuhusiana na namna Dr Masawe alivyoondoka.Mathew akawaaga kwamba wanaondoka na watarejea baadae wakaingia garini na kuondoka. “Mathew I’m scared.Tunaondoka wakati hali ya Gosu Gosu ni mbaya”akasema Ruby “Tunahitaji kuwa majasiri sana wakati huu.Kama hali ya Gosu Gosu ingekuwa inaruhusu kusafirishwa kwenda nje ya nchi tungefanya hivyo lakini kwa hali yake hatuwezi kumsafirisha na kule hospitali hatuwezi kumrejesha tena kwa sababu za kiusalama.Kilichobaki hapa ni kumkabidhi Mungu suala hili yeye ndiye mwamuzi wa yote akiamua kumchukua Gosu Gosu sisi hatupaswi kulalamika.Naamini Mungu anaona mawazo yetu na anasikia maombi yetu hivyo atamponya Gosu Gosu” akasema Mathew



    “Ruby hii ni misheni ya hatari sana hivyo hatutaongozana wote.Nitakwenda peke yangu wewe utabaki hapa ukiniongoza” akasema Mathew wakiwa katika ofisi ya nyumbani kwake “Sawa Mathew nitajiunga na SNSA nitakuongoza hadi kufika katika ofisi ya Edwin.Hata kama hatakuwepo ofisini lakini unaweza ukafanikiwa kupata kitu ambacho kinaweza kutusaidia kufahamu kwa kina mahusiano yake na Devotha na vile vile tujue kama ana mahusiano na Melanie Davis” akasema Ruby “Kitu cha kwanza ninachokitaka baada ya kuvuka geti kuu ni kuzima umeme.Kukiwa giza nitaweza kuingia kwa urahisi zaidi ndani” “Kuna chumba maalum ambacho kina kila kitu kinachohusiana na umeme wa jengo lile na ndani ya chumba hicho kuna jenereta la dharura pindi umeme ukikatika.Unapoingia katika maegesho ya viongozi mkono wako wa kulia utaiona nyumba ina madirisha makubwa na nyumba hiyo ndiyo ina jenereta na vifaa vyote vya umeme wa jengo” akasema Ruby huku akiendelea kubofya kompyuta yake “I’m in” akasema Ruby kisha ramani ya jengo la makao makuu ya SNSA ikaonekana katika kompyuta yake akaihamishia katika runinga kubwa ukutani “Hii ndiyo ramani ya jengo la makao makuu ya SNSA.Ile nyumba ninayokwambia ilimo jenereta ya umeme haiko katika ramani hii kwa sababu haina muda mrefu toka imejengwa.Utakapozima umeme utaelekea katika maegesho ya viongozi na utatumia mlango huu wa maegesho ya viongozi kuingia ndani ya jengo. Umeme unapokatika jenereta huwaka baada ya dakika moja lakini nitabadilisha katika mfumo ili liwake baada ya dakika tatu.Nitafanya hivi ili uweze kutumia muda huo kuufungua mlango wa kuingilia ndani kupitia maegesho ambao hufunguliwa kwa kadi maalum lakini wewe utatumia vifaa vyako kuufungua mlango huo . Ukishaingia ndani ya jengo hilo umeme utawaka na utapita njia hii hapa ambayo ni njia ya dharura ya kupita viongozi endapo kutatokea dharura yoyote aidha ya moto au kitu chochote cha hatari.Utakutana na mlango ambao namba zake za kufungulia ni KW23T860.Ukifungua huo mlango itaonekana katika mfumo wao hivyo ukiufungua na kuingia ndani utabonyeza namba TTY79 na itajulikana ni mmoja wa watu wa idara ya SNSA.Utaelekea hadi ghorofa ya tano ambako ndiko ziliko ofisi zetu.Nitakuunganisha na kompyuta hii ili niwe nakuona na kukupa maelekezo njia ya kupita kuelekea katika ofisi ya Edwin” akasema Ruby. Mathew akatoka na kuelekea katika chumba chake ambacho kulikuwa na silaha na vifaa vingine mbali mbali akaanza kujiandaa.Alipokuwa tayari akarejea ofisini alikomuacha Ruby. “Mathew umevaa kikomando hasa” akasema Ruby “Ni kutokana na ulinzi uliopo mahala hapo ninakoelekea ndiyo maana nimejiandaa kiasi hiki”akasema Mathew na kuweka mezani kifaa Fulani kama boksi akakifungua na kukiwasha halafu akachukua kidude kidogo na kukiweka sikioni “Huu ni mtambo mdogo kwa ajili ya mawasiliano.Kuna dishi kubwa la satelaiti liko nje ya nyumba ambalo ni maalum kwa ajili ya kifaa hiki ambacho ndicho tutatumia kwa mawasiliano.” akasema Mathew na kufanya majaribio na kifaa kile kilifanya kazi vizuri “Mathew hakikisha unafanikiwa kumpata Edwin.Ni mtu ambaye tunamuhitaji sana”akasema Ruby “Usijali Ruby nitatumia kila uwezo nilio nao kuhakikisha Edwin anapatikana usiku huu” akasema Mathew wakakumbatiana “Mathew please be safe ! akasema Ruby na Mathew akachukua begi lake akalivaa mgongoni akaelekea katika gari na kuondoka.





    “Ee Mungu naomba usimame na familia yangu ili hao waliowateka wasiwafanyie kitu chochote kibaya” Dr Godwin Masawe alimuomba Mungu. Alipokuwa nyumbani kwa Mathew akizungumza na Ruby alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akamtaka atazame video atakayomtumia na alipoitazama video aliyotumiwa aliwaona mke na watoto wake wakiwa wamefungwa mikono huku wamepigishwa magoti na watu wawili waliofunika nyuso zao wakiwa na bunduki wakiwalinda.Mtu Yule aliyempigia simu alimtaka awashe gari na aondoke mahala alipo aende nyumbani kwake na asithubutu kuwajulisha polisi au mtu yeyote kuhusu tukio lile.Hii ndiyo sababu iliyomfanya Dr Masawe kuondoka kimya kimya nyumbani kwa Mathew bila kuaga mtu yeyote. “Nani hawa walioteka familia yangu? Nini wanakitaka hadi wakafanya hivi?akajiuliza maswali mengi Dr Masawe alifika nyumbani kwake akapiga honi lakini hakuna aliyetoka kumfungulia geti akalazimka kushuka garini akaenda taratibu na kulisukuma geti halikuwa limefungwa akaingiza gari ndani.Akashuka kwa tahadhari na kuingia ndani akamuita mke wake lakini hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu mle ndani.Ni sauti ya runinga ndiyo iliyosikika sebuleni.Akaizima na kisha akaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine lakini hakukuwa na mtu yeyote mle ndani.Dr Masawe akachanganyikiwa. “Hawa watu wanataka nini kwangu?Wamewapeleka wapi familia yangu? Akajuliza akiwa amesimama ameegemea mlango wa chumba chake cha kulala “Natamani niwajulishe polisi lakini naogopa wale jamaa wanaweza wakaidhuru familia yangu kwani walinionya nisithubutu kuwaambia chochote polisi” akawaza na kuelekea chumbani kwake akafungua kasiki lake akaanza kuhesabu fedha zilizopo. “Nahisi hawa jamaa wanahitaji fedha ndiyo maana wakateka familia yangu.Hapa nina jumla ya shilingi milioni thelathini na saba na kama wakihitaji zaidi nitajitahidi kukopa sehemu yoyote kwa ajili ya kuikomboa familia yangu” akawaza Dr Masawe na mara simu yake ikaita.Akatazama mpigaji akahisi mwili unamtetemeka kwani zilikuwa ni namba za Yule jamaa mtekaji “Hallow” akasema kwa woga “Dr masawe kuna mtu anakuja hapo nyumbani kwako kukuchukua. Ndani ya dakika tano mtu huyo atakuwa amefika. Ninapokata simu hii zima simu yako tafadhali.” akasema Yule jamaa “Nini unakitak…..” akasema Dr Masawe lakini Yule mtekaji alikata simu.Kijasho kilimtoka Dr Masawe usoni.Akaizima simu yake kama alivyoelekezwa akaelekea sebuleni.Baada ya dakika tano kama alivyokuwa ameelekezwa mlango wa sebuleni ukagongwa “Nahisi huyo ndiye mtu aliyetumwa kuja kunichukua” akawaza na kutoka akakutana na mtu mmoja aliyevaa suti nyeusi na mkononi akiwa na bastora .Dr Masawe akatetemeka “Funga nyumba yako ! akaelekeza Yule jamaa na Dr Masawe akafunga nyumba Yule jamaa akamtaka amfuate wakatoka nje ya geti ambako Yule jamaa alikuwa ameegesha gari lake.Akamfungulia mlango Dr Masawe akaingia garini halafu akamfunga kitambaa usoni na safari ikaanza Dr Masawe hakujua mahala anakopelekwa.Baada ya mzunguko wa dakika kadhaa gari lile likasimama na mlango ukafunguliwa Dr Masawe akashushwa garini akashikwa mkono akaongozwa kuelekea ndani ya jengo kisha wakaingia katika lifti baada ya muda milango ya lifti ikafunguka wakatoka wakatembea kwa muda mfupi mlango wa chumba ukafunguliwa Dr Masawe akaingizwa ndani akakalishwa katika kiti akafungwa mikono kwa pingu zilizokuwa katika meza halafu mlango ukafungwa akabaki peke yake “Ee Mungu naomba unisaidie mimi na familia yangu tuwe salama.Watu hawa hawaonekani kuwa watu wazuri na wana lengo baya nasi” akaomba Dr Masawe Zilipita dakika kadhaa mlango ukafunguliwa tena na watu wakaingia ndani ya kile chumba Dr Masawe akavuliwa kitambaa usoni .Mle ndani ya chumba kulikuwa na watu wanne mmoja ndiye aliyekuwa amekaa kitini wengine wamesimama. “Hallow Dr Masawe pole sana kwa mstuko ulioupata.Mimi naitwa Edwin Mbeko ni mkurugenzi wa idara ya SNSA yaani idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi” akasema Yule jamaa aliyekuwa amekaa kitini.DrMasawe hakuweza kujibu chochote alikuwa anatetemeka “Relax Dr Masawe.Take a deep breath” akasema Edwin kisha akaamuru Dr Masawe afunguliwe zile pingu mikononi. “Usiogope Dr Masawe uko hapa kwa jambo dogo tu kisha utaondoka na familia yako” akasema Edwin “Familia yangu wako wapi? Akauliza Dr Masawe “Usihofu Dr Masawe.Familia yako iko salama ! akasema Edwin akachukua kitanza mbali akakielekeza katika ukuta wa kioo akakibonyeza na rangi ya kioo ikabadilika na upande wa pili familia ya Dr Masawe wakaonekana wakiwa wamekaa sofani.Mke wake akiwa amewakumbatia watoto wake.Yule jamaa akabonyeza tena kitanza mbali na rangi ya kioo ikabadilika na kuzuia watu waliokuwa upande wa pili kuonekana. “Ahsante Mungu familia yangu wako salama” Dr Masawe akashukuru kimya kimya “Tayari umewaona familia yako wote wako salama na muda mfupi ujao utaondoka nao” akasema Edwin “Nini mnakitaka kutoka kwangu?akauliza Dr Masawe “Kuna kitu kidogo sana Dr Masawe ninachokihitaji kutoka kwako.Ni taarifa ndogo tu na ukinipatia hiyo basi familia yako watakuwa salama na utaondoka nao sasa hivi” akasema Edwin “Niambieni tafadhali mnachokihitaji niwapatie kama ni fedha niko tayari kuwapa kiasi chochote kile mnachokihitaji ili mradi msiidhuru familia yangu” akaomba Dr Masawe. “Kuna mgonjwa mmoja anaitwa Papi Gosu Gosu alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mtodora akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.Mgonjwa huyo amehamishwa leo kutoka hospitalini hapo na kupelekwa kusikojulikana.Ninachokihaji kutoka kwako ni kunieleza mahala aliko Gosu Gosu.Ukijibu hilo ninakuhakikishia wewe na familia yako mtaondoka hapa salama” Edwin akanyamaza na kumtazama Dr Masawe “Wapi alipo Gosu Gosu?akauliza Edwin “Hili ni jaribu kubwa sana.Yawezekana hawa jamaa ndio wanaotaka kumuua Gosu Gosu” akawaza Dr Masawe “Dr Masawe wapi alipo Gosu Gosu?Nieleze tafadhali ili tuokoe muda na uondoke hapa na familia yako” “Sifahamu mahala aliko huyo mgonjwa” akajibu Dr Masawe na Edwin akamtazama halafu akatabasamu “Una uhakika Dr Masawe hufahamu mahala alipo Gosu Gosu?akauliza Edwin “Ni kweli sifahamu mahala alipo Gosu Gosu.Kama ningejua mahala alipo ningewaeleza” akajibu Dr Masawe “Dr Masawe tunafahamu Gosu Gosu amehamishwa leo kutoka hospitali ya Mtodora na wewe ukiwa na madaktari wengine wawili na wauguzi wawili mliongozana naye kwenda mahala alikohamishiwa ili kuendelea kumpatia matibabu.Nataka unieleze mahala alikopelekwa Gosu Gosu.Yule mtu ni hatari sana kwa usalama wa nchi” “Sifahamu alikohamishiwa Gosu Gosu na wala sikuongozana na waliomuhamisha” akasema Dr Masawe “Dr Masawe ninakuheshimu sana mzee wangu na sitaki kukufanyia jambo lolote baya.Ninakuuliza kwa upole kabisa wapi alipo Gosu Gosu?Nieleze tafadhali uondoke haraka na familia yako” “Sifahamu kwa kweli alipo huyo Gosu Gosu” akajibu Dr Masawe.Edwin akamtazama kisha akawasha sigara akavuta na kupuliza moshi halafu akasema “Kwa nini unaficha mahala alipo Gosu Gosu.Ana umuhimu gani kwako? “Simfichi ila sifahamu mahala alipo.Mnataka kumuua amewakosea nini? Akauliza Dr Masawe na kwa kasi ya umeme Edwin akainuka na kumlamba kofi zito Dr Masawe “Huna ruhusa ya kuuliza swali lolote hapa.Nimekuuliza swali jibu haraka sana na si kuniuliza swali.Nakuuliza kwa mara ya mwisho wapi alipo Gosu Gosu? Ukishindwa kunijibu nitaanza kuitesa familia yako huku ukishuhudia ! akasema kwa ukali Edwin ambaye sura yake ilikuwa imebadilika na kuonyesha ukatili mkubwa “Wapi alipo Gosu Gosu?akauliza lakini Dr Masawe hakujibu kitu.Edwin akasimama “Dr Masawe hujanifahamu vyema mimi ni nani.Sasa umenilazimisha nifanye kitu ambacho sikuwa nimetarajia kukifanya ! akasema na kuelekeza kitanza mbali katika kioo akabonyeza na familia ya Dr Masawe ikaonekana. “Binti yako ana umri wa miaka mingapi? Akauliza “Tafadhali naomba msiwaguse familia yangu ! Kama ni kunitesa niteseni mimi ! akasema Dr Masawe na kulambwa tena kofi zito “Niambie binti yako ana miaka mingapi? Akauliza “Ana miaka kumi na mbili” “Sawa.Leo hii tunampatia mchumba hapa na kwa mara ya kwanza ataingiliwa kimwili huku ukishuhudia” akasema Edwin na Dr Masawe akasimama “Nasema msimguse binti yangu tafadh…” hakumaliza sentensi yake akapigwa ngumi iliyompeleka chini.Damu zilianza kumtoka mdomoni.Akainuliwa akatolewa mle ndani na kuingizwa katika chumba walichokuwamo familia yake ambao waliangua kilio walipomuona baba yao.Edwin akawanyamazisha halafu akamfuata binti wa Dr Masawe “Binti unaitwa nani?akauliza Edwin “Naitwa Paulina” akajibu Yule binti huku akitetemeka.Edwin akamshika mkono na kumtaka ainuke akampeleka katika kiti akamtaka aketi “DrMasawe hii ni mara ya mwisho ninakuuliza wapi alipo Gosu Gosu? “Tafadhalini jamani naomba binti yangu mumuache kwani hahusiki kwa namna yoyote na suala hili.Nitawasaidia kutafuta taarifa za mahala aliko huyo mtu mnayemtafuta lakini nawaomba msimguse binti yangu ! akasema Dr Masawe “Dr Masawe wapi alipo Gosu Gosu? Akauliza Edwin “Naombeni mniamini vijana wagu sifahamu mahala alipo Gosu Gosu.Kama ningefahamu ningewaeleza lakini sijui chochote ! akasema Dr Masawe “Unatulazimisha tufanye ukatili ambao hatukuwa tumetegemea kuufanya ! akasema Edwin na kuwapa ishara watu wake.Jamaa wawili waliojazia miili yao wakamshika Paulina binti wa Dr Masawe na kumpandisha juu ya meza.Alikuwa analia. “Dr Masawe fursa ya mwisho wapi alipo Gosu Gosu? “Naombeni jamani muacheni binti yangu hana mahusiano yoyote na suala hili.Ninawaahidi nitawasaidia kutafuta mahala alipo Gosu Gosu ! akasema Masawe aliyekuwa amefungwa pingu mikononi “Mume wangu kama unafahamu hicho wanachokuuliza wajibu tafadhali ili kumuepusha binti yetu na ukatili ambao anakwenda kufanyiwa na hawa watu! akasema mke wa Dr Masawe huku akitokwa na machozi “Sifahamu mke wangu mahala alipo huyo mtu wanayemtaka.Kama ningejua mahala alipo ningewaeleza ! akasema Dr Masawe.Edwin akawaelekeza watu wake kuendelea na zoezi.Kwa kutumia nguvu Paulina akavuliwa gauni alilokuwa amevaa akabaki mtupu.Alikuwa anapiga kelele kubwa.Dr Masawe na mke wake walikuwa wamedhibitiwa na watu wenye silaha ili wasiweze kufanya chochote.Mmoja wa wale jamaa waliojazia miili yao akavua suruali yake bila aibu na kuutoa uume wake uliosimama. “Nitawaeleza ! Nitawaeleza ! Nitawaeleza ! akasema Dr Masawe “Unasemaje Dr Masawe ? akauliza Edwin “Nitawaeleza mahala alipo Gosu Gosu.Tafadhali naombeni msimfanye chochote binti yangu” akasema Dr Masawe na Edwin akaelekeza wale jamaa wamuache Paulina kisha Dr Masawe akatolewa ndani ya kile chumba akarejeshwa katika chumba alichokuwamo awali.





    Mathew Mulumbi alikaribia kufika katika geti kuu la kuingilia ofisi za SNSA. “Ruby tayari ninalitazama geti kuu la SNSA” Mathew akamwambia Ruby “Good.Ninakuona na tayari nimekwisha cheza na kamera zote zilizoelekezwa eneo la geti kuu.You have two minutes to finish the main gate” akasema Ruby “Thank you Ruby” akajibu Mathew na kupunguza mwendo baada ya kukutana na kibao kilichomuelekeza afanye hivyo.Alipolikaribia geti kuu akakutana na kibao kingine kilichomtaka asimame kwa ajili ya ukaguzi.Jamaa mmoja aliyevaa sare za ulinzi za rangi nyeusi akasogelea kioo Mathew akakishusha “Habari yako ndugu” akasalimu Yule mlinzi “Nzuri ndugu yangu” “Nikusaidie nini? “Mimi ni mgeni wa Edwin Mbeko yuko ndani? Akauliza Mathew “Mathew kuna walinzi wengine watatu wako hapo getini” Ruby akamwambia Mathew kupitia kile kifaa alichokiweka sikioni Yule mlinzi akamtaka Mathew asubiri kidogo ili akawasiliane na Edwin Mbeko alipogeuka tu mkono wa Mathew ulikuwa mwepesi ukanyanyuka kwa kasi ya aina yake na kwa kutumia bastora yenye kiwambo cha sauti akamlenga Yule jamaa risasi akaanguka chini kisha kama nyani akashuka kutoka ndani ya gari lile na kuelekea katika nyumba ya walinzi na kama alivyoelekezwa na Ruby kulikuwa na walinzi watatu.Mathew alicheza na bastora yake kama vile ana mikono minne na ndani ya sekunde chache wale walinzi wote wakawa sakafuni wakivuja damu “I’m sorry guys wakubwa wenu ambao wanashirikiana na magaidi wamesababisha mkafikwa na masahibu haya” akasema Mathew huku akiwavuta walinzi wale na kuwaingiza katika chumba kidogo cha mapumziko “Mathew you have 10 seconds to get out of there ! Ruby akamuelekeza Mathew ambaye aliingia katika gari lake na kutoka mahala alipo Ruby akalifungua geti na Mathew akapita.Moja kwa moja akaelekea sehemu ya maegesho ya viongozi wa idara.Kabla hajashuka garini akalitazama eneo lile kama lina mlinzi yeyote halafu akawasiliana na Ruby “Tayari niko eneo la maegesho ninataka kutoka garini” “Sawa Mathew unaweza kutoka.Hakuna hatari yoyote eneo hilo” akasema Ruby na Mathew akafungua mlango wa gari akashuka akachukua begi lake akalivaa mgongoni bila kusahau kofia yake ngumu ambayo ilifungwa miwani ya kumuwezesha kuona sehemu yenye giza.Moja kwa moja akaelekea katika jengo ambalo ndimo mna vifaa vyote vya umeme pamoja na jenereta la dharura pale umeme unapokatika.Akalizunguka kwa nyuma jengo lile halafu akatoa mkasi mgumu akakata kipande cha wavu akapenya na kuingia ndani.Akaelekea moja kwa moja katika sehemu ya kukatia umeme akachukua kifaa Fulani kutoka katika begi lake akakiweka katika sanduku kubwa la umeme na baada ya sekunde chache kukatokea cheche kubwa na jengo zima umeme ukakatika kisha akatoka kwa kasi kupitia mahala alikoingilia akaelekea upande ule wa maegesho ya magari akachomoa vifaa kutoka mfukoni na kuuchokonoa mlango ukafunguka akaingia ndani.Kulikuwa na giza lakini aliweza kuona kutokana na ile miwani ya kuonea usiku. “I’m in”Mathew akamwambia Ruby “Good.Sekunde ishirini na nne umeme utawaka hivyo elekea njia ya kushoto kwako yenye kibao emergency exit.” Akaelekeza Ruby na Mathew akaanza kupanda ngazi taratibu na kwa tahadhari kubwa.Alisikia kwa mbali watu wakizungumza kutokea nje Ndani ya chumba alichokuwa anahojiwa Dr Masawe mahojiano yalisimama baada ya umeme kukatika na umeme uliporejea Edwin akatoa simu yake akapiga kwa fundi mkuu “Masoud kuna nini kimetokea hadi umeme ukakatika na kuchelewa kuwaka? “Mkuu imetokea hitilafu katika boksi kubwa na kutulazimu kuchepua umeme katika njia nyingine hadi hapo tutakapofahamu chanzo cha hitilafu iliyojitokeza” “Nakuhitaji ofisini kwangu haraka sana unieleze kwa kina kilichotokea kwani jengo hili halipaswi kukosa umeme zaidi ya dakika mbili kutokana na unyeti wake lakini imechukua zaidi ya dakika tano umeme kurejea” akasema Edwin na kuwaelekeza vijana wake waendelee kumchunga Dr Masawe ili akafahamu kilichokuwa kimetokea na kusababisha hitilafu ile Mathew aliufikia mlango alioelekezwa na Ruby akabonyeza namba huku akielekezwa na Ruby lakini zikagoma “Yawezekana wamebadili namba ! akasema Ruby “Ruby find me another way ! akasema Mathew “Nipe sekunde chache Mathew nione kitu cha kufanya” akasema Ruby na kushusha pumzi akaanza kubofya kompyuta yake haraka haraka na mara simu yake ikaita alikuwa ni Rais “Oh no ! kwa nini anapiga wakati huu?akasema Ruby kisha akaichukua ile simu na kutoka nje ya kile chumba akaipokea “Hallo mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby uko wapi ninahitaji kuzungumza nawe usiku wa leo kuhusiana na kile kilichotokea jana kule SNSA.Nielekeze mahala ulipo tafadhali ili nitume watu wangu waje kukuchukua” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais utanisamehe kwani kwa usiku huu haitawezekana.Naomba kama itawezekana tuonane kesho” “Kesho haitakuwa rahisi kwa upande wangu kwani nitakuwa na kikao muhimu sana na marais wenzangu.Naomba tafadhali tuzungumze usiku huu ili niweze kulimaliza hili swala nahitaji urejee haraka sana SNSA kabla ya hizo siku saba” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kwa usiku huu haitawezekana kwa sababu ninamsaidia Mathew Mulumbi kufanikisha misheni ya muhimu sana” akasema Ruby “Misheni ipi? Naomba unieleze tafadhali.Nataka kufahamu anachokifanya Mathew” akasema http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Dr Fabian “Kuna uchunguzi anakwenda kuufanya ndani ya SNSA na mimi ndiye ninayemsaidia ili aweze kufanikisha hilo jambo” “Umesema Mathew anakwenda kufanya uchunguzi SNSA? “Ndiyo mheshimiwa Rais”akajibu Ruby “Anakwenda kuchunguza nini?akauliza Dr Fabian “Kwa sasa naomba nisikueleze mheshimiwa Rais lakini pale uchunguzi utakapokamilika tutakujulisha” akasema Ruby “Ruby you have to tell me everything.SNSA ni ofisi iliyo chini yangu natakiwa kujua kila kinachoendelea pale.Nataka kufahamu kitu gani anachokwenda kukichunguza Mathew?Mle kuna siri nyingi za usalama wa nchi ambazo mtu kama Mathew ambaye si mfanyakazi hapaswi kuzifahamu.Ruby nini kinaendelea?Mara ya kwanza umemuingiza ndani ya SNSA na akashiriki katika tukio la kusababisha kifo cha mmoja wa wafanyakazi na leo anarejea tena kufanya uchunguzi ..! “Mheshimiwa Rais tafadhali naomba umuamini Mathew.Kuna jambo kubwa linaendelea hapa nchini hivi sasa na pale tukikamilisha uchunguzi tutakujulisha” “So you are with him ! “Yes Mr President.I’m with him” akajibu Ruby na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “Ruby ninakuamini sana na ndiyo maana nikakuomba uje uongoze idara nyeti kama ile lakini kwa mambo haya unayoyafanya unanipa wasiwasi wa kuendelea kukuamini.Mathew Mulumbi si mtu wa kumuamini hata kidogo.Hakuna anayejua alikuwa wapi na kwa nini ametokea katika wakati huu.Huyu ni mtu wa kuogopwa sana na kwa namna yoyote ile hukupaswa kumsaidia kuingia ndani ya ofisi nyeti kama SNSA! “Mheshimiwa Rais nitazungumza nawe kesho.Sorry ! akasema Ruby na kukata simu akakimbilia ndani akavaa spika za masikioni na kumuita Mathew “Mathew unanisoma?akauliza Ruby “Ulikuwa wapi Ruby?! Tayari nimekwisha anza kuingiwa na wasi wasi labda kuna kitu kimekutokea” akasema Mathew “I’m sorry” akasema Ruby na kuendelea kubonyeza kompyuta yake kwa kasi kubwa “Umefikia wapi kunitafutia njia nyingine? “I’m changing the codes.Ndani ya sekunde chache nitakupa namba mpya za kufungulia huo mlango” akasema Ruby “Fanya haraka Ruby ! akasema Mathew Mara tu baada ya Ruby kukata simu Dr Fabian akampigia Edwin Mbeko “Mheshimiwa Rais ! akasema Edwin “Edwin uko wapi?akauliza Dr Faban “Niko ofisini mheshimiwa Rais” “Kila kitu kiko sawa hapo ofisini? “Ndiyo mheshimiwa Rais kila kitu kiko sawa kabisa” “Are you sure? “Ndiyo mheshimiwa Rais kila kitu kiko sawa kabisa ukiacha yale matukio mawili ya kuwapoteza wafanyakazi wetu ambayo nimekwisha kufahamisha lakini hakuna tena tatizo lingine lolote” akasema Edwin “Hakuna tukio lolote limetokea hapo ofisini ambalo si la kawaida usiku huu?akauliza Dr Fabian ‘Kilichotokea muda mfupi uliopita ni umeme kukatika na niko hapa na mhandisi wetu wa umeme akinieleza namna tukio lilivyotokea” “Oh my God ! akasema Dr Fabian “Kuna nini mheshimiwa Rais?akauliza Edwin “Edwin kuna mtu tayari yuko ndani ya jengo lenu.Amesaidiwa kuuingia ndani na mtu aliyeko nje anayelifahamu vizuri jengo hilo na mifumo yake.Sifahamu mtu huyo anakuja kutafuta nini lakini nahisi kuna siri anazitafuta.Tafadhali zima kabisa kila kitu ili mtu huyo asifanikiwe lengo lake na hakikisha anatiwa mikononi na ahojiwe kitu anachokuja kukifanya hapo SNSA” akasema Dr Fabian na Edwin akaonyesha mstuko mkubwa “Edwin umenisikia? “Nimekusikia mheshimiwa Rais” akasema Edwin na Rais akakata simu.Edwin akatoka mbio na kuelekea ghorofa ya tatu ambako kulikuwa na watu wakiendelea na kazi akawataka wazime kila kitu kwa haraka pamoja na kufunga milango yote ya usalama. Ruby aliyaelekeza macho katika kompyuta yake ambayo iliendelea kuzunguka ikionyesha asilimia themanini na nane ili namba mpya alizoziweka ziweze kutambuliwa na mfumo wa SNSA na Mathew aweze kuufungua mlango.Ilipofika asilimia tisini na saba mara mawasiliano yakakatika ghafla.Ruby akapiga meza kwa hasira akaendelea kubonyeza kompyuta yake haraka haraka lakini hakuweza kujiunganisha na mfumo wa SNSA “Bastard ! akasema kwa hasira kisha akavaa spika zake za masikioni “Mathew we have a problem” akasema “Nini kimetokea tena Ruby?akauliza Mathew “Mawasiliano yamekatika ghafla inaonekana wamezima kila kitu.I can’t access anything ! akasema Ruby “They know I’m here ! akasema Mathew “Mathew please get out of there ! akasema Ruby “Hapana Ruby siwezi kurudi.Lazima nimpate Edwin Mbeko.Ninayo ile ramani ya jengo zima uliyonitumia katika simu yangu.I have to do it on my own.Usiendelee kuwasiliana nami kwani wanaweza wakafuatilia mawimbi na wakagundua mahala ulipo ukawa katika hatari.Thank you Ruby let me do this on my own” akasema Mathew na kuchomoa kifaa kile alichokuwa amekivaa sikioni akakikanyaga kanyaga na kukata kabisa mawasiliano na Ruby “Wamegunduaje kama niko hapa? Nitafahamu baadae kwa sasa natakiwa kuhakikisha ninafika katika ofisi ya Edwin Mbeko kwa namna yoyote ile” akawaza Mathew na kutoa bomu dogo katika begi lake akaenda kuliweka katika kitasa cha mlango halafu akarudi nyuma hatua tano na kulilenga bomu lile kwa kutumia bastora yake yenye kiwambo cha sauti ukatokea mlipuko na mlango ukasambaratika.Akajibanza katika kona kusikilizia kama kuna mtu yeyote atajitokeza lakini hakukuwa na mtu yeyote akaanza kupanda ngazi haraka haraka kwa tahadhari kubwa. Milango yote ya kuingia na kutoka ndani ya jengo la SNSA ilikuwa imezingirwa na walinzi wenye silaha ili kuzuia Mathew asiweze kutoka nje na kutoroka. Wafanyakazi wote wakakusanywa katika chumba kilichotengenezwa maalum kwa nyakati kama hizi kama kutatoea hatari yoyote ya kushambuliwa.Ni chumba kilichotengenewa maalum ambacho kina milango isiyopenya risasi na kina uwezo wa kuwakinga wafanyakazi dhidi ya shambulio lolote la kibaolojia. Edwin Mbeko akiwa ameongozana na walinzi wawili wakainga katika chumba kile ambacho wafanyakazi wote walikuwa wamekusanywa.Mara tu alipoingia wafanyakazi wakataka kufahamishwa kile kinachoendelea “Poleni sana ndugu zangu kwa mstuko mlioupata.Halijawahi kutokea tukio kama hili hapa katika idara yetu.Kilichotokea ni kwamba nimepokea taarifa muda mfupi uliopita kwamba ndani ya jengo letu kuna mtu amevamia na lengo lake ni kutafuta siri za usalama wa nchi.Baada ya kupata taarifa hiyo ya kustusha hatua ya kwanza ilikuwa ni kuzima kila kitu ili lengo la mtu au watu hao lisifanikiwe.Kama mnavyofahamu humu ndani kuna siri nyingi kuhusiana na usalama wa nchi hivyo basi hatuwezi kuwapa nafasi watu hao ya kufanikisha mipango yao.Ninachowaomba kwa sasa tuendelee kutulia humu ndani wakati suala hili linashughulikiwa.Tayari kikosi cha makomando wa idara yetu kiko njiani kutoka katika kambi yao wanakuja hapa kwa ajili ya kuhakikisha mtu au watu hao wanadhibitiwa haraka sana” akasema Edwin na simu yake ikaita akaipokea akazungumza na aliyempigia halafu akasema “Nimetaarifiwa kwamba walinzi wote waliokuwa geti kuu usikuhuu wameuawa na hao watu ndipo wakapata nafasi ya kupita kuingia ndani ya jengo.Milango yote kwa sasa imefungwa na kuna ulinzi hivyo hawawezi kutoka nje.Ninawahakikishia kwamba tutawapata wote” akasema Edwin “Mkuu inawezekanaje mtu au watu hao wakaweza kuvamia ofisi zetu bila kujulikana?Kuna kamera kila mahala na kila mtu au gari linalokaribia eneo hili linaonekana na kukaguliwa imezekanaje mtu au watu hao wakaweza kufika hadi geti kuu bila kujulikana? Mmoja wa wafanyakazi akauliza “Tutalifanyia uchunguzi suala hilo kujua namna mtu huyo alivyoweza kufika hadi geti kuu akaua walinzi na kuingia ndani bila kunaswa na kamera zetu.Tuna mfumo wa kisasa mno na hata mimi ninashangaa kwa nini kamera zetu zimeshindwa kunasa tukio hilo .Tutafanya uchunguzi na kuufahamu ukweli na wote walioshiriki katika suala hili watajulikana na kuchukuliwa hatua kali lakini kwa muda huu kipaumbele kikubwa ni kuhakisha mvamizi au wavamizi hao wanakamatwa” akasema Edwin “Mkuu taarifa hii ya kuwapo kwa mvamizi umeipata wapi? Mtu huyo aliyekupa taarifa hii amejuaje kama kuna mtu kavamia jengo letu wakati sisi tuliopo ndani hatufahamu chochote?akauliza mfanyakazi mwingine. “Si jambo zuri kuweka wazi chanzo cha taarifa lakini katika hili napenda kuweka wazi kuwa taarifa hii nimeipata kutoka wa mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ofisi hii iko chini yake” akasema Edwin na wote wakabaki na mshangao minong’ono ikaanza kusikika “Mingong’ono hiyo ni ya kujiuliza Rais amefahamuje kama kuna mtu katuvamia kabla yetu sisi? Hata mimi sifahamu Rais amejuaje lakini baada ya kumtia nguvuni huyo mvamizi wetu nitazungumza na Rais naamini atanipa taarifa kamili ya namna alivyoweza kupata taarifa za huyo mtu” akasema Edwin na ujumbe ukaingia katika simu yake akausoma halafu akasema “Ndugu zangu nimetaarifiwa kwamba kikosi cha makomando wetu kinakaribia kufika.Ninakwenda kuwapokea .Kila kitakachoendelea mtajulishwa” akasema Edwin na kutoka mle ndani akawakuta watu wanne nje ya kile chumba wakimsubiri “Mkuu kumegundulika uwazi mkubwa katika nyumba ya jenereta tunaamini huyo mvamizi alikata wavu na kuingia ndani kisha akakata umeme.Vile vile tumekuta gari katika maegesho ya wakuu wa idara na tunahisi ni gari lake” akasema mmoja wa wale jamaa. “Kama gari lake limeonekana upande huo yawezekana ameingia ndani kupitia njia ya dharura ya vongozi wa idara ambayo watu wengi hata walio ndani ya idara hawaifahamu.Huyu mtu anaonekana kulifahamu sana jengo hili ama kuna mtu ambaye anashirikiana naye” akasema Edwin na mlio wa helkopta ukasikika “Makomando wamefika nahitaji kuwapokea” akasema Edwin kisha akaongozana na walinzi wawili wakaelekea ghorofani kwa ajili ya kuwapokea makomando hao ambao hutumiwa na SNSA katika operesheni kubwa na za hatari kwa usalama wa nchi. “Ni nani huyu mtu aliyethubutu kuvamia ofisi zetu.Kitu gani anakitafuta?Halafu anaonekana kulifahamu vyema jengo hili je kuna watu wa humu ndani ya idara anashirikiana nao? Akajiuliza Edwin huku wakipanda ngazi haraka haraka kuelekea juu ya jengo. Helkopta iliyowaleta makomando ilisimama juu ya jengo la SNSA makomando wakaanza kushuka kwa kutumia kamba.Jumla ya makomando nane waliojihami vilivyo wakashuka kiongozi wao akasalimiana na Edwin kisha wakaelekea katika ofisi na Edwin akawaeleza kile kilichotokea na kupelekea kuwaita pale.Akawafahamisha kwamba wanahisi mvamizi huyo anaweza kuwa amejificha katika njia ya dharura Makomando waligawanyika katika vikosi viwili vya watu wanne kikosi kimoja kikashuka chini katika mlango wa kuingilia wakuu wa idara ambako ndiko gari la Mathew lilikoonekana kikosi cha pili kikaenda ghorofa ya tano ambako ndiko njia ile ilikuwa inaelekea zilipo ofisi za wakuu wa idara.Kikosi cha makomando wanne walioshuka chini wakiwa na mbwa mkubwa kiliingia katika njia ile ya dharura na kuanza kupanda juu kwa tahadhari kubwa.Walikuta mlango mkubwa ukiwa umefumuliwa kwa bomu wakawasiliana na wenzao wakawajulisha kisha wakaendelea kupandisha taratibu huku mbwa mkubwa wa kijeshi waliyekuwa naye akiwaongoza kuelekea katika mlango mmoja uliokuwa umefungwa.Kulionekana mchirizi wa damu chini ya mlango.Mbwa Yule akawaongoza kuelekea katika mlango ule ulikotokea mchirizi ule wa damu.Kiongozi wa kile kikosi akawataka wasimame kisha akatangulia mbele taratibu akiwa katika tahadhari kubwa.Ghafla mbwa akaruka juu na mkanda ukamponyoka yule jamaa aliyekuwa amemshika akakimbia mbio akaurukia mlango ambao haukuwa umefungwa na mara tu mlango ule ulipofunguliwa kukatokea kishindo kidogo na wale makomando wakalala chini.Ndani ya sekunde chache eneo lote likajaa moshi mzito na wale makomando wakaanza kuhisi kuishiwa nguvu na kushindwa kupumua.Wakati wakihangaika kuvuta pumzi Mathew Mulumbi akajitokeza akiwa amevaa maski usoni ya kumkinga dhidi ya hewa chafu. Mkono wake wa kulia alikuwa ameshika bunduki ndogo na mkono wa kushoto alikuwa na kopo.Alibonyeza lile kopo na kupulizia hewa eneo lile moshi ukatoweka na hewa safi ikapatikana akavua maski yake na akaweza kuwaona vizuri wale makomando waliokuwa wakihangaika kutafuta hewa huku wakiwa hawana nguvu.Haraka haraka akazikusanya bunduki zao na kuziweka sehemu moja halafu akachukua pingu za plastiki akawafunga kisha akatoa kitu Fulani katika begi lake akaanza kuwapulizia puani na baada ya muda mfupi wakaanza kujihisi vizuri na ndipo walipojikuta wakitazamana na mtu aliyekuwa amewaelekezea bunduki. “Poleni sana ndugu zangu” akasema Mathew “Aaaaghh ! akatoa ukelele kiongozi wa kikosi kile akitaka kukata pingu zile za plastiki walizokuwa wamefungwa “Please don’t do that or I’ll shoot you ! akasema Mathew kwa sauti isiyo na masihara Yule komandoo akamtazama kwa dharau na kutunisha misuli akitaka kukata ile pingu mara risasi mbili zikapita pembeni ya kichwa chake na kupiga ukuta. “Next time nitakifumua kichwa chako kama utaendelea kuwa mkaidi ! akasema Mathew na Yule jamaa akawa mpole.Mathew akawatazama kwa muda halafu akasema “Listen to me brothers ! akanyamaza na kuwatazama tena wale jamaa “Mimi ndiye mnayenitafuta.Naitwa Mathew Mulumbi ni…” “Mathew Mulumbi ?! Kiongozi wa kile kikosi akastuka “Ndiyo mimi ni Mathew Mulumbi” “Unafanya nini hapa Mathew?akauliza Yule jamaa “Unanifahamu? Mathew akauliza “Nimezisikia sana habari zako.Ninaye ndugu yangu anafanya kazi katika idara ya ujasusi ndiye ambaye amenieleza mambo yako mengi.Sikujua kama ni wewe ambaye tumekuja kukutafuta” akasema Yule jamaa huku wenzake wakimshangaa. “Huyu anaitwa Mathew Mulumbi amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi Tanzania na mambo aliyoyafanya ni makubwa sana.Ni mmoja kati ya manguli wa ujasusi hapa nchini” Yule kiongozi wa makomando akawafahamisha wenzake “Aliyosema mwenzenu ni kweli kabisa” Mathew akaongeza “Kwa nini umevamia jengo hili na kuua watu?Hujui kwamba hilo ni kosa? Tumeambiwa kwamba umeua walinzi wa geti kuu huo tayari ni uhalifu ! akasema mwingine “Ni kweli niliwaua wale walinzi geti kuu ili nipate nafasi ya kuingia humu ndani kwani bila kufanya vile nisingeweza kuingia humu.Hata ninyi ningeweza kuwamaliza lakini sikufanya hivyo kwa kuwa ninyi ni wenzangu na mnaweza mkanielewa nikiwaeleza kile kilichonileta hapa”akasema Mathew “Nini kimekuleta hapa? Unatafuta siri za serikali? akauliza komando mwingine “Sijaja hapa kuiba siri za serikali na siwezi kufanya hivyo.Niko hapa kwa sababu nyingine ya usalama wa nchi”akasema Mathew “Usalama wa nchi ndio uvamie ofisi ya serikali na kuua watu? “Labda niwaeleze kwa ufupi tu pengine mnaweza mkanielewa.Si muda mrefu sana IS walifanya shambulio hapa Dar es salaam ambalo liliua wake za marais na mpaka sasa watu waliohusika katika shambulio hilo hawajakamatwa.Nilipata taarifa kutoka katika vyanzo vyangu vya habari kwamba kuna mtu anaitwa Khalid Sultan Khalid kutoka katika kundi la kigaidi al IS anakuja hapa nchini.Huyu ni mtu anayejishughulisha na milipuko mikubwa.Mkurugenzi mpya wa idara hii anaitwa Annabel ni rafiki yangu na nilimuomba tuitumie idara yake kumfuatilia Khalid na kufahamu kile alichokuja kukifanya hapa Tanzania pamoja na washirika wake.Zoezi lilifanyika vizuri lakini katikati ya zoezi hilo mawasiliano yakakatika na timu iliyokuwa ikimfuatilia Khalid ikashindwa kufanya kazi yake na Khalid akapotea hadi sasa hatujui mahala alipo.Baada ya kufanya uchunguzi tukagundua kwamba mawasiliano hayo yalikatwa kwa makusudi na mfanyakazi anaitwa Edina .Tulimfuatilia huyo Edina na kukuta ameuawa nyumbani kwake.Baada ya Edina kuuawa tukalazimika kumuhoji mhandisi mkuu ambaye alisema uongo kwamba mawasiliano yale yalikatika kutokana na hali ya hewa.Ilitumika nguvu kidogo kumuhoji kwani aligoma kusema chochote na alipelekwa katika chumba cha matibabu baada ya kupoteza fahamu.Baadae tukaambiwa amefariki dunia na kitu cha kushangaza ni kwamba mkurugenzi huyo mpya ambaye aligundua kuhusiana na sababu ya kukatika kwa mawasiliano yale akaondolewa katika nafasi yake kwa kutumia kanuni za idara na aliyeongoza zoezi hilo ni Edwin Mbeko.Huo ni upande mmoja.Upande wa pili kuna mtu anaitwa Melanie Davis huyu anaishi hapa nchini na anashirikiana na James Kasai ambaye kwa kushirikiana na IS walitekeleza shambulio lile lililoua wake za marais.Huyu Melanie mpaka sasa tunamsaka na hatujafanikiwa kumpata lakini kuna mtu wa karibu na Melanie ambaye anaishi Ufaransa na baada ya kumchunguza huyo mtu tukagundua ana mawasiliano ya karibu na Edwin Mbeko na hiyo ndiyo sababu niko hapa.I’m here for EdwinMbeko.Nimekuja kumchunguza kwani ninahisi anaweza kuwa na mahusiano na Melanie Davis ambaye anashirikiana na magaidi wa IS.Nina uhakika hata tukio lile la kumpoteza Khalid Sultan Khalid anahusika.Hivyo ndugu zangu nadhani kwa hayo machache mmenielewa” akasema Mathew “Kama unamtafuta Edwin kwa nini ukamfuata hapa?Kwa usingemtafuta sehemu nyingine nje ya hapa? “Edwin Mbeko anatumia ofisi hii kama mwavuli wa kufichia mambo yake na ndiyo maana nimekuja hapa kufanya uchunguzi katika ofisi yake.Ndugu zangu nisingeweza kuja sehemu hii ya hatari kama nisingekuwa na sababu ya msingi niliyowaeleza.Kuna hatari kubwa ya kufanyika kwa shambulio lingine kubwa hapa nchini hivyo kila juhudi lazima zifanyike kuhakikisha tunalizuia hilo lisitokee”akasema Mathew “Kwa nini usiwasilishe suala hili katika vyombo husika vilishughulikie? “Nisingeshindwa kufanya hivyo lakini hawa jamaa wana mizizi mirefu hadi katika taasisi za serikali kama hii.Ninawaomba ndugu zangu mnisaidie ili niweze kufanikisha jukumu lililonileta hapa.Kama msiponisaidia nikafanikisha kile kilichonileta hapa hamtakuwa mnatekeleza wajibu wenu wa ulinzi wa nchi na nina uhakika mtaona aibu pale mtakaposikia magaidi wametekeleza shambulio lingine hapa nchini” akasema Mathew kisha akachukua kisu na kukata zile pingu za plastiki halafu akawarejeshea silaha zao. “The choice is yours.Take me down or save the country ! akasema Mathew.Kiongozi wa kikosi kile akawatazama wenzake halafu akauliza “What do you want?akamuuliza Mathew “Nataka nifike katika ofisi ya Edwin.I need your help” akasema Mathew “Kama nisingekuwa nimesikia habari zako nisingekuamini lakini nimesikia mambo makubwa uliyoyafanya kwa ajili ya nchi hii na ninakuamini.Mimi na wenzangu tutakusaidia kufanikisha kile kilichokuleta hapa japokuwa ni hatari kwetu lakini ni jambo sahihi kulifanya kwa ajili ya ulinzi wa nchi” “Ahsanteni sana ndugu zangu” akasema Mathew “Kwa sasa wafanyakazi wote walioko ndani ya jengo hili wamekusanywa ndani ya chumba maalum na kila kitu kimezimwa.Milango yote ya kuingiana kutoka imewekwa walinzi hivyo si rahisi kwa wewe kuweza kufika huko unakotaka kwenda.Sisi tumekuja jumla nane na tumegawanyika makundi mawili.Kundi moja ni sisi tuliokuja huku chini na kundi la pili liko juu.Tutakachokifanya utavaa mavazi ya mmoja wetu ili uonekane kama mwenzetu kisha utaongozana na mmoja wetu kuelekea katika ofisi ya Edwin na wakati huo sisi tutaendelea kuwepo huku tutawaeleza wenzetu kwamba tunaendelea kukutafuta.Naomba ndani ya dakika kumi uwe umemaliza kazi yako katika ofisi hiyo kwani walioko juu wanaweza wakaingiwa na wasiwasi tumechukua muda mrefu huku chini” akasema Yule mkuu wa ile timu “Ahsante sana nashukuru kwa msaada wenu.You are doing the right thing for the country” akasema Mathew huku akianza kuvua mavazi yake na kubadilishana mavazi na mmoja wa makomando wale kisha akaongozana na komando mwingine wakashuka ili kwenda kupita katika mlango mkubwa. Katika sehemu ya juu ya njia ile ya dharura,makomando wanne wakiwa na Edwin Mbeko na walinzi wengine wawili waliendelea kusubiri taarifa kutoka kwa wenzao waliokuwa wamepita chini. “Hakuna njia nyingine ambayo huyo mvamizi anaweza akapita na kutokomea zake?akauliza mkuu wa kikosi kile. “Hakuna sehemu anayoweza kutoka.Ukiacha mlango huu hapa juu,upo mlango mwingine ghorofa ya pili ambao hufunguliwa kwa namba maalum ambazo walizo nazo ni viongozi pekee hakuna tena mlango mwingine zaidi ya hii miwili” akajibu Edwin “C2 nini kinaendelea huko chini?Mmechukua muda mrefu mko kimya.Tujulisheni kinachoendelea ova ! akasema Yule mkuu akiwasiliana na kikosi kilichokwenda chini akajulishwa kwamba wanaendelea na upekuzi wa kina Mathew akiwa katika mavazi waliyovaa wale makomando akiwa ameongozana na komando mwingine wakaelekea upande wa ofisi za wakuu wa idara.Anaifahamu ofisi ya Edwin Mbeko akausogelea mlango haukuwa umefungwa kwani Edwin alitoka kwa haraka na kusahau kufunga ofisi yake.Mathew akamtaka Yule komando kumsubiri nje akausukuma mlango akaingia ndani moja kwa moja akaelekea katika meza ya Edwin.Makaratasi mengi yalikuwepo mezani na hakujua aanzie wapi mara akauona mkoba wa kompyuta ukiwa pembeni akaushika kwa umakini huku mkononi akiwa amevaa glovu akaufungua na kutoa kompyuta ndogo na makaratasi kadhaa akayapitia na kustuka baada ya kuiona karatasi moja ikiwa imeandikwa kwa mkono ikiwa na orodha ya vitu mbali mbali “Hivi ni vifaa vya kutengeneza mlipuko.Ahsante Mungu” akawaza Mathew kisha akapiga picha karatasi zile kwa kutumia simu yake “Ningeondoka na kompyuta ya Edwin lakini akiikosa atajua nimefika ofisini kwake.Ngoja nimpigie Ruby anipe maelekezo kuhus…………”akawaza Mathew na kutolewa mawazoni na Yule komando aliyekuwa nje ya mlango aliyemjulisha kwamba anasikia vishindo vya watu wanakuja.Haraka haraka Mathew akarudisha kila kitu katika mkoba namna kilivyokuwa akatoka wakaondoka eneo lile wakarejea kule walikowaacha wenzao. “Umefanikiwa kupata kile ulichokuwa unakitafuta?akauliza kiongozi wa ile timu ya chini “Nimepata kitu kidogo lakini naamini kitakuwa na msaada mkubwa.Please help me get out of here” akasema Mathew “Kila kitu kimezimwa sasa hivi hakuna kamera yoyote inayofanya kazi.Utatokea upande wa magharibi kwani geti kuu kuna walinzi.Utapanda ukuta utaruka nje kisha utawasiliana na wenzako watakufuata” “Ninashukuru sana ndugu zangu kwa msaada huu mkubwa mlionisaidia.Mungu atawajalia kwa hili mlilolifanya kwa nchi yenu” akasema Mathew kisha akavaa mavazi yake akaongozana na makomando wawili wakatoka mle ndani.Kulikuwa na walinzi katika mlango wa kutokea nje lakini hawakuwauliza chochote.Mathew na wale makomando wakaelekea upande wa magharibi na Mathew akapanda ukuta akaruka nje wale makomando wakarejea ndani kisha wakawajulisha wenzao kwamba wametafuta kila sehemu Mathew hakuwepo. “Haiwezekani ! akasema Edwin kwa hasira “Mtu huyo alikuwemo humu ndani.Ametoka vipi? “Yawezekana aliwahi kutoka kabla hatujafika” akajibu mkuu wa kile kikosi cha makomando na Edwin akawataka waiingie wote kwa mara nyingine kupekua ili kujiridhisha kwamba kweli hakukuwa na mtu.Baada ya kupekua kona zote hakuonekana mvamizi yeyote.Edwin akaelekeza makomando wale kupekua sehemu nyingine zote za jengo lakini Mathew hakuonekana .





    Ruby akiwa katika ofisi ya Mathew alihisi kuchanganyikiwa.Alikuwa akiingia na kutoka ndani ya ofisi ile huku akizungumza mwenyewe “What am I going to do to save Mathew?akajiuliza “Ee Mungu naomba umsaidie Mathew aweze kutoka salama ndani ya lile jengo.Maisha yake yako hatarini.Endapo akikamatwa mambo yote yataharibika” akaomba Ruby na kukaa juu ya meza akiwaza “Ngoja nipigie simu Austin yawezekana akawa na msaada japo anaumwa” akawaza Ruby na kumpigia simu mmoja wa madaktari anayewauguza Austin na Gosu Gosu na kumuomba azungumze na Austin “Hallow Ruby ! Sauti ya Austin ikasikika baada ya muda mfupi. “Austin samahani kwa usumbufu najua una umwa lakini sina mwingine ninayeweza kumkimbilia kuomba msaada” akasema Ruby “Kuna nini Ruby?akauliza Austin na Ruby akamueleza kile kilichotokea “We need to save Mathew.Please help me” akasema Ruby “Ruby please relax ! Nipe dakika tano nipige simu niombe msaada wa vijana wangu waende wakamkomboe Mathew” akasema Autin “Thank you Austin” akasema Ruby Dakika mbili toka awasiliane na Austin simu yake ikaita akaitoa mfukoni haraka haraka na kustuka baada ya kukuta mpigaji ni Mathew hakupoteza hata sekunde akaipokea “Mathew are you okay?akauliza Ruby “Niko salama Ruby.Tayari nimetoka ndani ya jengo” “Ouh thank you Lord.Umewezaje kutoka? “Ruby tutazungumza baadae lakini kwa sasa nahitaji msaada.Nataka uje unichukue hapa mahala nilipo.Gari langu nimeliacha SNSA” akasema Mathew na kumuelekeza Ruby mahala alipokuwa.Ruby akakimbia nje akaingia garini na kuondoka kwa kasi.Mara tu alipotoka getini akampigia simu Austin na kumjulisha kwamba tayari amewasiliana na Mathew amekwisha toka ndani ya lile jengo la SNSA.



    Upekuzi katika jengo la SNSA ulikamilika bila ya kumpata mvamizi aliyetajwa kuvamia jengo lile.Kikosi cha makomando wa SNSA kilichokuja kupambana na wavamizi kikaondoka kurejea katika kambi yao.Edwin Mbeko akaamuru shughuli ziendelee kama kawaida huku ulinzi ukiimarishwa kila kona ya jengo lile. “Rais hawezi akanidanganya lazima mvamizi alikuwemo humu ndani.Amewezaje kutoka ndani wakati milango yote ilikuwa na walinzi?Inanishangaza sana.Au yawezekana wakati Rais ananipa taarifa tayari huyo mvamizi alikwisha toka.Nitazungumza na Rais na kumfahamisha kila kitu,kwa sasa ni wakati wa kulimaliza lile suala la Gosu Gosu kisha nitakuja kuendelea na hili suala la huyu mvamizi” akawaza Edwin na kuelekea katika chumba alichokuwamo Dr Masawe “Dr Masawe nimerejea tena.Safari hii sitaki mzaha nataka unieleze mahala alikopelekwa Gosu Gosu .Nakuhakikishia ukinieleza ukweli utaondoka salama na familia yako” akasema Edwin “Nitakueleza ukweli lakini naomba familia yangu wasiguswe” akasema Dr Masawe “Nimekwisha kwambia kwamba utakaponieleza ukweli familia yako itakuwa salama na utaondoka nao” akasema Edwin na Dr Masawe akavuta pumzi ndefu halafu akamueleza Edwin mahala alipo Gosu Gosu. “Ahsante kwa kunieleza ukweli lakini utaondoka hapa na familia yako baada ya kujiridhisha kwamba ulichoniambia ni cha kweli” akasema Edwin na kutoka akarejea ofisini kwake akawaita vijana wake wanne wakiongozwa na dereva wake Jackson akawapa maelekezo ya kwenda mahala aliko Gosu Gosu kumuua. “Hakikisheni hakuna mtu mnayemuacha hai mahala hapo ! akasisitiza Edwin na wale vijana wakaondoka kisha akampigia simu Rais “Edwin mmempata Mathew Mulumbi? Akauliza Dr Fabian “Mathew Mulumbi ni nani mheshimiwa Rais?akauliza Edwin “Ndiye aliyevamia hapo” “Mheshimiwa Rais hatujafanikiwa kumpata huyo mtu” “Hamjampata?! Dr Fabian akashangaa “Ndiyo mheshimiwa Rais hatujampata” “That’s impossible” “Kweli mheshimiwa Rais” “Amewezaje kutoka humo ndani bila kukamatwa? “Mheshimiw Rais mara tu uliponipa taarifa ile kila kitu hapa kilisimama na tukaanza msako haraka sana na pia makomando wa idara yetu walifika wakaendelea na zoezi la kumtafuta bila mafanikio” “This man is not a real human.He’s a ghost ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa rais huyu Mathew Mulumbi ni nani?Edwin akauliza “I don’t know much about him.Inasemekana alifariki miaka mitatu iliyopita lakini ameibuka hivi karibuni kutoka mahala kusikojulikana na ameanza kuleta matatizo.Sina hakika kama ni binadamu wa kawaida.Hakuna chochote ambacho amechukua hapo? “Hakuna mheshimiwa Rais tuliwahi kuzima kila kitu isipokuwa ameua walinzi wetu watatu waliokuwa geti kuu” “Dah ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais huyuo mtu ni nani tuweze kumfuatilia?akauliza Edwin “Nitakutafuta baadae Edwin lakini kwa sasa hakikisheni ulinzi unaimarishwa sana hapo katika idara” akasema Dr Fabian na kukata simu “Mathew Mulumbi ni nani?akajiuliza Edwin baada ya Rais kukata simu “Rais amefahamuje kama kuna mtu amevamia idara yetu? Akaendelea kujiuliza Edwin “Ngoja nimsubiri yawezekana akanieleza baadae alikopata taarifa za mtu huyo kuvamia idara yetu.Kwa sasa ngoja nijielekeze zaidi katika mipango yetu” akawaza Edwin na kuchukua simu akamtafuta Devotha lakini bado simu yake haikupatikana “Devotha amekwenda wapi?Kwa nini hapatikani simuni ? Yeye ndiye kiongozi wa mipango yote hatakiwi kukosekana simuni lakini tumekuwa tunamtafuta toka asubuhi hapatikani na hajatoa maelezo yoyote ya mahala alipo.Anatupa wakati mgumu wa kufanikisha m ipango yetu” akawaza Edwin







    Mathew alitoka mafichoni baada ya Ruby kuwasili mahala alikokuwa amejficha akaingia garini na Ruby akaliondoa kwa kasi “Thank you Ruby” akasema Mathew “Mimi ndiye ninayepaswa kumshukuru Mungu kwa kukuwezesha kutoka salama ndani ya lile jengo.Niliogopa sana nikalazimika kumpigia simu Austin kumuomba msaada na muda mfupi baadae ukapiga simu” akasema Ruby “Ahsante sana Ruby kwa kufanya kila jitihada za kuniokoa.Walifahamuje kama nimeingia mle ndani? Akauliza Mathew “Hata mimi bado ninajiuliza wamefahamuje” akasema Ruby na mara akakumbuka kitu “Rais alinipigia simu akanitaka niende ikulu usiku huu tukazungumze kuhusiana na lile suala langu la kuondolewa SNSA nikamwambia haitawezekana kwani tuko katika operesheni muhimu.Akaniuliza ni operesheni gani inaendelea nikamueleza kwamba umekwenda SNSA kuna jambo unakwenda kulichunguza.Rais hakuonekana kufurahi” akasema Ruby “Ulimueleza Rais kuhusu operesheni hii?akauliza Mathew “Nilimueleza kwamba kuna jambo unakwenda kulichunguza SNSA lakini sikumueleza unachokwenda kukifanya pale” “Basi ni yeye aliyewapa taarifa SNSA ! akasema Mathew kwa hasira “Hukupaswa kumueleza chochote.Ameharibu sana misheni yetu.Mida hii tulipaswa kuwa na Edwin Mbeko tunamuhoji lakini tumeshindwa kwa sababu yake.From now on hakuna kupokea simu yake yoyote hadi hapo tutakapomaliza operesheni yetu.Forget about SNSA ! akasema Mathew kwa ukali “Kwa nini lakini afanye hivi?Kwa nini awaeleze SNSA huku akijua kwamba kwa kufanya hivyo anavuruga misheni yako? Akauliza Ruby “Rais haniamini hata kidogo.Toka nilipokwenda kuonana naye kumueleza suala la James Kasai hakuonekana kuniamini” akasema Mathew “Uliwezeje kutoka mle ndani? Ruby akauliza na Mathew akamueleza kila kitu kilichotokea hadi alivyofankiwa kutoka nje ya jengo lile. “Ahsante Mungu kwa kumtoa salama huyu mwanaume ninayempenda kuliko wote ndani ya hatari kubwa” akawaza Ruby “Katika mkoba wa Edwin nimekuta kuna kompyuta lakini sikuweza kuifungua badala yake nikabandika kadi ndogo chini ya kompyuta ambayo itatuwezesha kumfuatilia.Vile vile katika mkoba huo nimekuta makaratasi kadhaa na nilipoyapitia kwa haraka haraka nilikuta kuna karatasi moja limeandikwa kwa kalamu ya wino ina orodha ya vitu mbali mbali na nilipoipitia haraka haraka nikagundua katika orodha hiyo kuna vitu vinavyotumika katika kutengeneza mlipuko.Nimezipiga picha karatasi zote ili tuweze kuzifanyia uchunguzi” akasema Mathew “Good Job Mathew.Ilikuwa ni kazi ya hatari sana lakini kwa hiki kdogo ulichokipata ni mafanikio makubwa kwetu”akasema Ruby “Sikufanikiwa kumpata Edwin usiku wa leo lakini tayari amekwisha ingia katika rada zetu na saa zake zinahesabika.Hana muda mrefu kabla ya kutua katika mikono yetu” akasema Mathew alipomtazama Ruby michiziri ya machozi ikaonekana machoni pake. “Ruby let me drive” akasema Mathew na Ruby akasimamisha gari pembeni ya barabara Mathew akashika usukani. “Nini kinakutoa machozi Ruby?akauliza Mathew “Najiuliza kama hao makomando wangekataa kukusaidia ungekuwa wapi mida hii? Kinachoniumiza zaidi ni mimi ndiye ambaye ningekuwa nimesababaisha misheni ile kuharibika kwa kumueleza rais” akasema Ruby na kuinamisha kichwa “Ningeweza kuwaua makomando wale lakini niliwaacha hai kwa kujua lazima wangenisaidia.Endapo wangekataa kushirikiana nami nisingekuwa na kitu kingine cha kuwafanya zaidi ya kuwaua.Mimi ninapokuwa katika kazi yangu huwa sina huruma hata kdogo.Kikwazo chochote kinachokuja mbele yangu lazima nikiondoe ili niweze kufanikisha misheni yangu.Bahati yao walikubali kushirikiana nami.Niliwaweka katika hatari lakini walifanya kitu sahihi kwa ajili ya nchi yao.Kuhusu Rais usijilaumu kwani hukujua kama angewezakufanya kitu kama kile.Kuanzia sasa kata kabisa mawasiliano naye.Amekwisha onyesha si mtu tunayeweza kumuamini” akasema Mathew Safari iliendelea wakielekea katika nyumba waliko akina Gosu Gosu.Mita kadhaa kabla ya kuifikia nyumba waliyokuwamo akina Gosu Gosu likaonekana gari nje ya geti.Mathew akapunguza mwendo wa gari. “Kuna gari pale nje ya geti.Dr Masawe amerudi na kushindwa kuingia ndani?akauliza Mathew “Kama angekuwa amerudi na kushindwa kuingia ndani lazima angekupigia simu halafu ile si gari ya Dr Masawe” akasema Ruby.Mathew akasimamisha gari “Something is not right.Nimepata wasiwasi kuhusiana na gari lile.Tushuke hapa hapa tutembee kwa miguu” akasema Mathew kisha akavua koti alilokuwa amevaa akampatia Ruby bastora moja kisha wakashuka na kuanza kutembea kwa miguu kuliendea geti la ile nyumba.Walilikaribia lile gari na kulichunguza hakukuwa na mtu yeyote ndani yake. “Wenye hili gari wako wapi? Akauliza Ruby Mathew akauparamia ukuta na kuchungulia ndani akastuka baada ya kumuona mtu mmoja akiwa na bunduki amesimama mlangoni huku akivuta sigara akarudi chini bila kutoa ukelele. “Ruby they’re here ! akasema Mathew “Akina nani? Akauliza Ruby “Wale watu wanaotaka kumuua Gosu Gosu” akasema Mathew “Wamefahamuje kama amehamishiwa hapa? Akauliza Ruby “Let’s find out.Follow me” akasema Mathew wakazunguka nyuma ya nyumba Mathew akapanda ukuta na kurukia ndani bila kishindo.Bastora ikiwa mkononi akanyata kuelekea upande wa mbele ya nyumba kwenye mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni.Yule jamaa mwenye bunduki bado aliendelea kuzunguka zunguka pale mlangoni.Mathew akautikisa mti wa maua na Yule jamaa akastuka akageuka kutazama kuna nini hakuona kitu,akaanza kutembea kwa tahadhari kuelekea ulipo ule mti ili kujiridhisha kama kweli hakuna kitu Mathew akajiweka tayari.Mara tu Yule jamaa alipokaribia ule mti Mathew akaruka kama kima akamvamia Yule jamaa na kumpiga kichwa kizito kilichompeleka chini akapoteza fahamu.Mathew akachukua pingu ya plastiki akamfunga mikono na kujaza tambara mdomoni kisha akamtupa pembeni sehemu yenye mwanga hafifu akaenda mlangoni akachungulia ndani kupitia dirisha lililokuwa pembeni ya mlango lakini hakukuwa na mtu yeyote sebuleni akakiminya kitasa cha mlango akaufungua taratibu sana akaingia sebuleni akanyata hadi katika korido akachungulia na kumuona mtu mmoja akiwa amesimama nje ya chumba alimolazwa Gosu Gosu akiwa na bunduki.Mathew akaenda katika runinga akaongeza sauti.Yule jamaa aliposikia sauti imeongezeka akaanza kupiga hatua kuelekea sebuleni kutazama nani ameongeza sauti ya runinga.Mathew akajiweka tayari na Yule jamaa alipojitokeza akakutana na ngumi nzito iliyompeleka ukutani,kabla hajakaa sawa akavutwa na kupigwa kichwa kizito akaanguka chini.Mathew hakutaka kumtazama tena kwani kwa kichwa kile tayari hakuwa na fahamu.Mathew akapiga hatua ndefu za tahadhari kuelekea katika chumba cha Gosu Gosu.Mlango haukuwa umefungwa akachungulia ndani akawaona madaktari na wauguzi waliokuwa wanamuhudumia Gosu Gosu wakiwa wamepigishwa magoti chini huku jamaa wawili wakiwaelekezea bunduki “Natoa nafasi ya mwisho.Nataka mniambie nani aliyewatuma mumtoe huyu mgonjwa hospitali? Akauliza mmoja wa wale jamaa kwa ukali.Mmoja wa wauguzi alikuwa analia na kuwaomba wale jamaa wawasamehe “Nitahesabu hadi tatu kama hamtanieleza nitawapiga wote risasi ! akasema Yule jamaa mwenye macho ya kikatili akaanza kuhesabu kuanzia tatu.Kabla hajamaliza kuitamka moja Mathew akaizinga bastora yake na kumpiga risasi Yule jamaa katika kiganja cha mkono bunduki ikaanguka chini.Yule mwenzake aliyekuwa naye alistuka baada ya kumuona mwenzake ametoa mguno baada ya risasi kumpiga kiganja cha mkono.Kabla hajajua risasi ile ilikotoka tayari Mathew alikwisha ingia me chumbani akamtandika tee zito la mbavu Yule jamaa aliyempiga risasi ya mkono akaenda kujibamiza ukutani halafu akamuelekezea bastora Yule jamaa mwingine mwenye bunduki “Weka silaha yako chini taratibu ! akasema Mathew kwa ukali akimuelekezea Yule jamaa bastora.Taratibu Yule jamaa akaiweka chini bunduki yake.Mathew akampa mmoja wa wale madaktari pingu ya plastiki na kumtaka amfunge Yule jamaa mikono kwa nyuma halafu akawataka wamsaidie Yule jamaa aliyepigwa risasi kiganja cha mkono kuzuia damu kuendelea kumwagika “Kuna yeyote ameumizwa?akauliza Mathew “Hakuna aliyeumizwa wote tuko salama.Umetokea kwa wakati muafaka kabisa kwani ungechelewa kidogo sote tungeuawa.Ahsante sana Mathew kwa kutuokoa bado siamini kama tumenusurika kifo ! akasema mmoja wa wale madaktari huku akilia. “Wagonjwa wote wanaendeleaje? “Wote wanaendelea vizuri.Hawa watu ni akina nani?akauliza daktari mwingine “Hata mimi siwafahamu lakini muda si mrefu tutawafahamu wote” akasema Mathew kisha akawaelekeza madaktari wawakusanye wale jamaa waliopoteza fahamu wawaweke sebuleni akampigia simu Ruby na kumtaka aingie ndani kwani hatari imekwisha na wale jamaa wamedhibitiwa.Yule jamaa aliyepigwa kiganja cha mkono akapatiwa matibabu halafu naye akafungwa mikono kwa waya na wote wakachukuliwa wakapelekwa sebuleni wakaungana na wenzao wawili ambao hawakuwa na fahamu. Ruby alikwenda kuchukua gari mahali walikoliacha akafungua geti akaingia ndani.Aliposhuka garini akaingia sebuleni na kupatwa na mstuko mkubwa alipowaona wale jamaa waliokuwa wamedhibitiwa na Mathew “You ?! akasema Ruby akimshangaa mmoja wa wale jamaa ambaye naye alistuka mno alipomuona Ruby akiingia mle ndani “Unawafahamu?akauliza Mathew “Ndiyo.Huyu mmoja ninamfahamu anafanya kazi SNSA ni dereva wa Edwin Mbeko” “Dereva wa Edwin?! Akauliza Mathew naye akishangaa na kuwatazama wale jamaa kwa hasira “Ahsante sana Ruby kwa kunijulisha wanakotoka watu hawa” “Watu wote humu wako salama? Akauliza Ruby “Wote wako salama.Niliwahi kabla hawajawaumiza” akasema Mathew kisha akawageukia wale jamaa “Wakati tunawasubiri wenzenu wazinduke nataka mfahamu kwamba hapa mlipoingia ni katika tanuru la moto.Uhakika wa kutoka hai hapa ni mdogo sana labda kama mtakuwa tayari kunieleza ukweli lakini endapo mtakuwa kiburi huu ndio mwisho wenu ! akasema Mathew na kuwatazama kwa hasira kisha akamnyooshea bastora Yule jamaa aliyetambuliwa na Ruby “Jina lako nani? Akaulia Mathew Yule jamaa akawa kimya “Nakuuliza jina lako nani? Akauliza tena “Tafadhali sema ukweli ukijifanya kiburi utapata taabu sana ! Ruby akamweleza Yule jamaa “Jina lako nani?akauliza Mathew Yule jamaa bado akawa kimya na kuzidi kumpandisha Mathew hasira.Akamfuata Yule jamaa mwingine aliyepigwa risasi ya kiganja cha mkono akamuinua kisha akachukua kisu na kuzichana chana nguzo zake akabaki mtupu halafu akamgeukia Yule dereva wa Edwin “Jina lako nani?akauliza Mathew Yule dereva bado akawa kimya.Mathew akageuka kwa kasi na ghafla Yule jamaa aliyepigwa risasi ya kiganja akatoa ukelele mkubwa wa maumivu makali.Alikuwa amekatwa uume wake.Aligalagala chini kwenye damu.Mathew hakumjali akamfuata Yule dereva na kumchana chana nguo zake kwa kisu naye akabaki mtupu “Umeona kilichomtokea mwenzako.Nakuuliza kwa mara ya mwisho jina lako nani? Akauliza Mathew “Naitwa Jackson Kandala” akasema Yule jamaa huku akitetemeka kwa woga. “Nani kawatuma hapa? “Tumetumwa na mkuu wetu” “Mkuu wenu nani? “Edwin Mbeko ! akasema Jackson halafu Mathew akamgeukia Ruby akamtaka awaite madaktari waje wamshughulikie Yule jamaa aliyekatwa uume wake.Madaktari wakafika na kumchukua Yule jamaa wakampeleka katika chumba kitupu wakaanza kumuhudumia ili kuzuia damu kuendelea kumwagika “Umeona kilichomtokea mwenzako nawe pia kitakutokea kama hiki endapo utaendelea kuwa kiburi.Nataka unieleze ukweli Edwin Mbeko amekutuma nini hapa?akauliza Mathew Jackson akawa kimya.Mathew akaushika uume wa Yule jamaa na kuuvuta akainua mkono wenye kisu juu “Usinikate tafadhali nitakueleza! akasema Jackson “Edwin amekutuma nini? “Ametutuma kuja http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kumuua mgonjwa ambaye amehamishwa kutoka hospitali na kuletwa hapa anaitwa Gosu Gosu” “Amewaeleza sababu za kutaka kumuua Gosu Gosu? “Hapana hajatueleza chochote.Katutuma tuje hapa kufanya kazi moja tu ya kuwaua watu wote tutakaowakuta humu ndani” akasema Jackson “Amefahamuje kama Gosu Gosu yuko hapa?akauliza Mathew Jackson akasita kujibu “Jackson nitakuharibu sasa hivi kama Yule mwenzako naomba unijibu tafadhali ! akasema Mathew.Jackson akaingiwa hofu baada ya kuona macho ya Mathew yaliyoonyesha alikuwa tayari kumfanyia ukatili mkubwa. “Anamshikilia daktari mmoja anaitwa Dr Masawe na familia yake na ndiye aliyemuelekeza mahala alipohamishiwa Gosu Gosu” “Edwin anamshikilia Dr Masawe? “Ndiyo.Aliiteka kwanza familia yake kisha akampigia simu na kumpa maelekezo na huyo daktari ndiye aliyemuelekeza Edwin mahala alipo GosuGosu” akasema Jackson.Mathew na Ruby wakatazamana. “Dr Masawe yuko wapi hivi sasa?akauliza Mathew “Yuko SNSA yeye na familia yake.Edwin atamuachia pale tu Gosu Gosu atakapokuwa ameuawa.” akajibu Jackson.Mathew akamtaka Jackson avae suruali yake wakaenda nje sehemu ya kupumzikia kulikokuwa na sofa nzuri akamtaka achukue simu yake “Mpigie simu Edwin mwambie kwamba tayari mmeimaliza kazi aliyowatuma.Gosu Gosu na wote mliowakuta hapa mmewaua” akasema Mathew.Jackson akazitafuta namba za simu za Edwin akampigia huku akiguswa na mdomo wa bastora kichwani. “Jackson” akasema Edwin baada ya kupokea simu “Edwin kazi tumeimaliza.Gosu Gosu tumemuua pamoja na wote tuliowakuta humu ndani.Tumeua madaktari wawili,wauguzi wawili na wagonjwa wawili Gosu Gosu na mwenzake” “Good job Jackson.Mmenifurahisha sana.Kabla ya kuwaua mliwahoji madaktari wakasema nani aliyewatuma kumuhamisha Gosu Gosu?akauliza Edwin “Tuliwahoji lakini hawafahamu chochote tukawaua”akajibu Jackson “Ahsante Jackson.Rejesheni silaha kisha mkapumzike” akasema Edwin “Ahsante sana mkuu” akajibu Jackson.Mathew akaichukua simu ile na kuizima kabisa. “Umefanya vizuri Jackson.Bado kuna mambo ambayo nataka kuendelea kukuuliza kuhusu Edwin Mbeko”akasema Mathew “Wewe umekuwa ni dereva wa Edwin Mbeko.Unaweza ukaniambia sehemu ulikompeleka kwa siku mbili jana na leo?Wapi ulimpeleka nje ya ofisi?akauliza Mathew “Kwa wiki nzima sijampeleka Edwin sehemu yoyote.Amekuwa akiendesha gari lake yeye mwenyewe” “Jackson mimi ni mtu mbaya sana pale mtu anaponidanganya au kunionyesha kiburi.Umeona nilichomfanyia Yule mwenzako.Nimetoa uanaume wake na hata wewe ninaweza kukufanyia vile vile nilivyomfanya mwenzako.Yawezekana jua la kesho msilione tena kama mtaendelea kunifanyia kiburi.Nieleze ukweli uokoe maisha yako na wenzako ! akasema Mathew “Nitakueleza ukweli kaka naomba uniamini” “Nieleze haraka ! akasema Mathew “Nimekwambia ukweli kwamba kwa wiki nzima sijamuendesha Edwin amekuwa akiendesha gari lake yeye mwenyewe lakini alinituma mara mbili nimpelekee gari lake katika bohari kuu la idara” “Yeye alikuwa wapi hadi akakutuma umpelekee gari lake huko katika bohari? akauliza Mathew “Mara ya kwanza alikuwa safarini Kagera akanipigia simu na kunielekeza nimpeleke gari lake bohari.Aliposhuka katika helkopta akaingia ndani ya gari na kuondoka na wageni wake” “Alikuwa na wageni? “Ndiyo alikuwa na wageni” “Uliwaona wageni hao? “Ndiyo alikuwa na wageni wawili mwanaume na mwanamke” akasema Jackson Mathew akamgeukia Ruby “Ulikuwa mkuu wa Edwin.Alikujulisha kuhusu safari hiyo ya Kagera? “Hakunijulisha chochote kama anasafiri.Nakumbuka kuna siku nilimtafuta nikamkosa na kesho yake akaniambia kwamba alikuwa safari nje ya mkoa nadhani ndiyo safari hiyo aliyokwenda Kagera”akajibu Ruby “Jackson mara ya pili alipokuelekeza umpelekee gari katika bohari ilikuwa lini?akauliza Mathew “Ni leo jioni.Alikwenda Arusha na akanitaka nimpelekee gari bohari.Alikuja na mgeni mmoja mwanaume akaingia garini na kuondoka”akajibu Jackson “Wageni ambao alikuja nao mara ya kwanza unaweza ukawafahamu ukiwaona? Mathew akauliza “Ilikuwa jioni na kiza kilianza kuingia walipotua hivyo siwezi kuzikumbuka vyema sura zao.Mwanamke aliingia haraka haraka ndani ya gari sikumuona vizuri lakini Yule mwanaume ninaweza kumkumbuka alikuwa mrefu alivaa suti ya bluu na kofia ya mduara kichwani.Alivaa miwani mikubwa kuficha macho yake na kidevu chake chote kilijaa ndevu Maelezo yale yakamstua Mathew.Akamtaka Ruby akalete picha ya James Kasai.Ruby akaenda katika gari na kurejea na kompyuta yake akaifungua picha ya James Kasai “Jackson tazama vizuri picha hii” akasema Mathew na Jackson akayaelekeza macho yake katika ile picha ya James Kasai “Mtu huyo uliyemuona akishuka katika helkopta na Edwin anafanana na huyu katika picha?akauliza Mathew na Edwin akaikazia macho picha ile na kusema “Huyu jamaa pichani anafanana na Yule niliyemuona lakini kidogo sana hasa maeneo ya kidevuni” akasema Jackson.Ruby akaichukua kompyuta yake na kuuliza “Uliyemuona alikuwa amevaa kofia ya namna gani? Jackson akamuelekeza kofia aliyokuwa amevaa Yule jamaa na Ruby akacheza na kompyuta yake akaivisha kofia ile picha ya James Kasai. “Miwani ya namna gani alikuwa amevaa?akauliza James,Jackson akamuelekeza kila kitu alichokuwa amekivaa Yule mtu na Ruby akakiweka katika ile picha halafu akamuonyesha Jackson akabaki anashangaa “Yule mtu alikuwa hivi hivi isipokuwa ndevu zake zimekuwa nyingi kidogo tofaui na hizi katika hii picha” akasema Jackson.Mathew akamtazama kwa makini na kuuliza “Jackson are you sure? “Yes I’m sure” akajibu Jackson “Jackson ahsante sana kwa maelezo haya uliyotupa.Twende ndani” akasema Mathew na kumchukua Jackson akampeleka katika chumba kitupu akamfunga mikono kwa pingu za plastiki halafu akaenda kuwachukua na wale jamaa wengine wawili ambao bado hawakuwa wamezinduka akawapekua na kuchukua simu zao kisha akawapeleka katika chumba kidogo cha stoo akawafungia humo kisha akamfuata Ruby “Ruby sina shaka na maelezo ya Jackson kwamba mtu huyo ambaye aliongozana na Edwin Mbeko katika helkopta kutoka Kagera ni James Kasai” akasema Mathew “Ninataka sana kumuamini Jackson lakini ninasita” akasema Ruby “He’s telling the truth ! akasema Mathew “Edwin Mbeko alikwenda Kagera na helkopta ya idara ya SNSA na akaenda kumchukua James Kasai.Tulifahamu James anakuja nchini lakini hatukujua ataingia vipi.Kila sehemu kulikuwa na picha yake na hakukuwa na sehemu ambayo angeweza kupita bila kujulikana.Ilihitajika mtandao mkubwa wenye nguvu kuweza kumuingiza James Kasai hapa nchini na SNSA ndio waliotumika.James Kasai alivuka mpaka akaingia Kagera Edwin Mbeko akaruka na helkopta hadi Kagera akaenda kumchukua James Kasai na kumleta hapa Dare s salaam.Mpaka hapa tuna uhakika mkubwa kwamba Edwin Mbeko,Devotha na Melanie Davis ni kitu kimoja na Edwin Mbeko kwa kutumia idara ya SNSA hufanikisha mipango ya mtandao huu.Mfano mzuri ni namna zoezi la kumfuatilia Khalid Sultan lilivyoshindwa kufanikiwa na jambo hilo lilifanywa ndani ya SNSA. Edwin Mbeko alifahamu jambo hili na ndiye aliyefanikisha huo mpango.Kama haitoshi akamuua pia Yule mwanadada Edina ambaye uligundua kwamba ndiye aliyekata mawasiliano.Naamini Edina alifanya vile kwa maelekezo ya Edwin ndiyo maana akamuua.Hata Yule jamaa tuliyemuhoji Fidelis naamini aliuawa ili kuendelea kuficha siri.Edwin Mbeko ni shetani wa mguu mmoja ! akasema Mathew kwa hasira “Dr Fabian alifahamu hiki kinachoendelea katika idara ya SNSA ndiyo maana akanitaka nije kuiongoza? Akauliza Ruby “Inaumiza sana kwa idara nyeti ya serikali kutumika katika kufanikisha mipango miovu ya magaidi” “Dah ! akasema Mathew “Baada ya kufahamu kuhusu Edwin Mbeko nini kinafuata? Ruby akauliza “Kwanza Edwin hatakiwi kujua kama tumekwisha mgundua lakini tuendelee kumfuatilia kwa karibu sana na ndiye ambaye atatuongoza mahala alipo James Kasai.Alipo James ndipo alipo Melanie Davis na ndipo alipo Khalid.Edwin ni mtu muhimu sana kwa sasa” akasema Mathew “Kwa nini tusimjulishe Rais kuhusu Edwin itakuwa rahisi kumkamata kumuhoji na kisha kujua mahala alipo James Kasai?akauliza Ruby “Rais hatakiwi kufahamu chochote kuhusu suala hili kwa sasa.Edwin akikamatwa tutashindwa kuwapata akina James na watu wengine wanaohusiana na mtandao wao hivyo tutamfuatilia kwa siri sana na tutafahamu kila kitu” akasema Mathew na kukumbuka kitu “Katika zile karatasi nilizozipata katika mkoba wake kuna orodha ya vifaa vya kutengenezea mlipuko.Khalid Sultan ni mtaalamu wa milipuko na ambaye zoezi la kumfuatilia lilivurugwa na SNSA.Nashawishika kuamini kwamba Khalid akishirikiana na washirika wake ambao ni akina Melanie na James Kasai wanatengeneza mlipuko na wanapanga kufanya shambulio lingine hapa nchini.Ili tufahamu lini na wapi shambulio hilo litafanyika lazima tuendelee kumfuatilia Edwin Mbeko kwa karibu sana” akasema Mathew “Mathew I’m so scared.Kwa nini tusimjulishe Rais jambo hili mapema ili hatua zianze kuchukuliwa? Tukichelewa hawa jamaa wanaweza wakatekeleza shambulio lao na watu wengi wakapoteza maisha lakini tukimjulisha angali mapema vyombo vyote vya usalama vitaanza kuchukua tahadhari” “Hatuwezi kumjulisha Rais kwa sasa kuhusiana na suala hili kwani jamaa wakifahamu tayari wamegundulika wanaweza wakajificha na tukashindwa kuufahamu mtandao wao wote.Tunachopaswa kukifanya ni kuhakikisha tunawatafuta watu hawa na tufahamu kama wanatengeneza bomu na wapi wamepanga kulitumia hilo bomu.Taarifa ikianza kusambaa sasa hivi itavuruga kila kitu.Hawa jamaa wana mtandao mrefu na wamejipachika katika idara mbali mbali za serikali na wanaweza wakapata taarifa haraka kama wanatafutwa” akasema Mathew na kumtazama Ruby akamshika bega “Ruby we can do this.We’re going to end them and save our country.Have faith in me” akasema Mathew “I believe you Mathew” “Thank you” akasema Mathew “Niliweka kadi nyuma ya kompyuta ya Edwin.Activate that card now.Tunatakiwa kuanza kumfuatilia kujua anakoelekea” akasema Mathew na kumpa Ruby namba za ile kadi aliyoiweka nyuma ya kompyuta ya Edwin na Ruby akaanza kucheza na kompyuta yake.Baada ya dakika mbili akasema “Kadi tayari inafanya kazi na mpaka sasa inaonekana kompyuta iko katika jengo la SNSA.Edwin Mbeko bado yuko pale”akasema Ruby “Good.Tutaanza kumfuatilia bila yeye kufahamu na kujua kila sehemu anakoelekea na tutafahamu mengi kuhusu mtandao wao.Lakini hata hivyo nina swali najiuliza.Ni vipi kama ataiacha kompyuta yake ofisini? Kama ikiwa hivyo hatutakuwa tumefanya chochote. EdwinMbeko ndiye pekee ambaye tunategemea atuongoze katika kuifanikisha misheni hii hivyo lazima tumchunguze kwa kutumia kila mbinu.” akasema Mathew “Mathew umesema kitu kizuri.Anaweza akaiacha kompyuta yake ofisini na sisi tukaendelea kudhani kwamba yuko ofisini kumbe hayupo” “Kuna kitu nakifikiria.Yule dereva wake anaweza akawa na msaada kwetu.Tunaweza tukamtumia” akasema Mathew “Unataka kumtumia Yule jamaa?akauliza Ruby “Ndiyo nataka kuzungumza naye ili aweze kushirikiana nasi” “Nadhani hilo si wazo zuri Mathew.Yule jamaa ni mtiifu kwa Edwin na anaweza akamueleza kila kitu kuhusu sisi” akasema Ruby “Yule jamaa ndiye anayemfahamu zaidi Edwin kuliko sisi na vile vile Edwin anamuamini sana hivyo tukiweza kumtumia anaweza akawa na msaada mkubwa sana kwetu.Let’s try talk to him” akasema Mathew na kwenda kumchukua Jackson “Jackson nimekuleta tena hapa tunataka kuzungumza nawe.Kuwa huru usiogope.Sisi siyo watu wabaya hadi pale tunapolazimishwa kuwa hivyo.Nataka tuzungumze kirafiki sisi na wewe” akasema Mathew na kumtazama Jackson “Una watoto wangapi Jackson? “Nina watoto wawili” “Wanasoma? “Ndiyo wanasoma” “Good.Mimi pia ni baba nina watoto wanne.Nadhani unafahamu majukumu ya baba ni kuhakikisha anailinda familia yake dhidi ya hatari yoyote ile na siku zote baba atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha familia yake wanakuwa salama.Nasema uongo?akauliza Mathew “Ni kweli kabisa”akajibu Jackson “Vizuri sana.Kama ilivyo kwa baba kuhakikisha familia inakuwa salama ndivyo ilivyo serikali ambayo ina jukumu la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa salama ndiyo maana kuna majeshi na idara mbalimbali za ulinzi yote hii ni katika kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na salama.Serikali ilianzisha idara ya SNSA kwa lengo la kupanua zaidi wigo wa ulinzi na usalama wa nchi.Kwa bahati mbaya idara hii nyeti na muhimu sana kwa nchi imeyumba na haitekelezi tena majukumu yake.Mabeberu tayari wamekwisha otesha mizizi yao katika idara hii na sasa wanaitumia kwa malengo yao.SNSA haifanyitena kazi ya kulinda nchi bali imekuwa ni hatari kwa nchi” akasema Mathew na kunyamaza akaichukua komputa ya Ruby akafungua sehemu ya kuhifadhi picha akaifungua picha ya Melanie Davis akamuonyesha Jackson “Huyu mwanamke anaitwa Melanie Davis.Ni mshirika wa James Kasai ambaye alitekeleza shambulio la hivi majuzi na kuua wake za marais.James Kasai ana mashirikiano na kikundi cha kigaidi cha IS na anapokea fedha na silaha kutoka kwa kikundi cha IS ambazo zinapita katika mikono ya huyu mwanamke ambaye ni tajiri hivyo moja kwa moja mwanamke huyu ana mashirikiano na IS.James Kasai na IS wanapanga kufanya shambulio lingine hapa nchini na kwa bahati mbaya idara ya SNSA inatumika katika kufanikisha mipango hiyo.Bosi wako Edwin Mbeko anashirikiana na mtandao huu hatari na anaitumia idara anayoiongoza kufanikisha mipango ya mtandao huu” akasema Mathew na Jackson ambaye alionyesha kustuka kidogo akasema “Hii picha ya huyu mwanamke uliyenionyesha amefanana na Yule mwanamke niliyemuona siku ile jioni Edwin aliporejea kutoka Kagera” akasema Jackson “Una hakika ulimuona mwanamke kama huyu?akauliza Mathew “Ninakumbuka alifanana na huyu japo alikuwa amevaa miwani lakini anafanana sana na huyu” “Kama una hakika mwanamke uliyemuona anafanana na huyu hakuna shaka mwanamke huyo ni Melanie Davis na hii inazidi kuonyesha ukaribu wa Edwin Mbeko na mtandao huu.Yule mwanaume uliyemuona jioni ile ni James Kasai ambaye kwa sasa anashirikiana na kundi la kigaidi la IS.Baada ya James kuingia nchini tulipata taarifa nyingine kwamba kuna mtu anaitwa Khalid Sultan Khalid anatokea kundi la IS anakuja hapa nchini.Huyu ni mtaalamu wa milipuko.Tuliomba idara ya SNSA isaidie katika kumfuatilia Khalid atakapoingia hapa nchini na ikaandaliwa timu maalum ikaanza kumfuatilia lakini wakati zoezi la kumfuatilia likiendelea mawasiliano kati ya timu hiyo na ofisi kuu yakakatika na tukampoteza Khalid na hadi sasa hatujui mahala alipo.Baada ya kufanya uchunguzi tukagundua kwamba mawasiliano yalikatwa makusudi na mmoja wa wafanyakazi ndani ya SNSA anaitwa Edina na tulipomfuatilia tukakuta ameuawa kwa kupigwa risasi” Akasema Mathew na kunyamaza akamtazama Jackson “Jackson nimekupa maelezo haya marefu kidogo kwa lengo la kukupa picha ya kile kinachoendelea hapa nchini na katika idara ya SNSA.Edwin Mbeko mkuu wa idara yenu anashirikiana na magaidi ambao wanapanga kufanya shambulio lingine kubwa hapa nchini.Mimi na wenzangu tunapambana katika kuhakikisha tunazuia shambulio hilo lisitokee pamoja na kuwatia nguvuni wahusika wote wa mtandao wa kigaidi hapa nchini.Tukishindwa kuzuia shambulio hilo damu nyingine itamwagika na utakuwa ni ushindi kwa magaidi.Hatupaswi kuwaacha wakafanikisha mipango yao miovu.Hakuna anayejua shambulio hilo limepangwa kufanywa wapi na lini.Yawezekana ikawa ni kanisani,shuleni au sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu na huwezi ukajua yawezekana mwanao akawepo eneo la shambulio na akapoteza maisha.Kama si mwanao basi ni mtoto wa mtu mwingine ambaye ni sawa na mwanao.Hatupaswi kuacha hilo likatokea na uwezo wa kuwadhibiti watu hao waovu tunao na ndiyo maana tunakuomba ushirikiane nasi katika harakati zetu za kuwazuia watu hawa wabaya kwa nchi yetu.Hatukulazimishi kwani ni misheni ya hatari sana lakini sisi sote unaotuona hapa tumeyatoa maisha yetu kwa ajili ya nchi na hatuogopi kufa.Ukiwa kama mwajiriwa wa idara ya SNSA ambayo malengo yake ni kuhakikisha nchi inakuwa salama hivyo kushiriki katika misheni hii ni moja ya wajibu wako.Baada ya haya niliyokueleza nini maamuzi yako?akauliza Mathew “Kaka samahani naomba niwafahamu ninyi ni akina nani? Akauliza Jackson “Mimi naitwa Mathew Mulumbi na mwenzanu anaitwa Ruby.Sisi hatufanyi kazi katika idara yoyote ya serikali lakini tumeyatoa maisha yetu kwa ajili ya kuisaidia nchi kupambana na wale wote wanaohatarisha usalama wa nchi” akasema Mathew “Kaka Mathew naomba nikiri kwamba sijawahi kupata mstuko mkubwa kama nilioupata leo kwa maneno uliyonieleza.Sikujua kama kuna hatari kubwa kiasi hiki hapa nchini.Nimekuwa SNSA toka wakati wa Tamar na sasa Edwin na nimekuwa dereva wake kwa miaka mitatu lakini sikuwahi hata mara moja kufahamu siri zake kama ni mtu mbaya namna hii.Aliponielekeza nipeleke gari lake bohari kuu nilijua kuna jambo linaendelea lakini kwa kuwa nilikuwa mtiifu kwake sikuweza kuhoji chochote kumbe ni mtu mkatili asiye na huruma hata chembe.Umeniambia silazimishwi kujiunga nanyi lakini kwa hiari yangu mwenyewe nataka kujiunga nanyi kuwadhibiti hawa watu wasifanikishe mipango yao” akasema Jackson “Tutakuamini vipi kama una nia ya dhati ya kujiunga nasi na si kugeuka msaliti?akauliza Ruby “Kaka hapa amenipa maelezo marefu kidogo na nimeyaelewa ndiyo maana kwa hiari yangu mwenyewe ninataka kushirikiana nanyi.Kuhusu kuniamini hilo litakuwa ni juu yenu lakini mimi niko tayari kushirikiana nanyi katika jambo hili.Nipeni kazi yoyote nitaifanya.Nini mnataka niwasaidie?akauliza Jackson “Nataka usiku huu uchukue silaha zenu zote mlizokuja nazo na uzirejeshe ofisini kwenu ili wasiwe na wasiwasi kuhusu ninyi wakikuuliza kuhusu wenzako waeleze kwamba wamekwenda makwao kupumzika.Kesho asubuhi utawahi kazini na Edwin atakapofika utaweka kifaa tutakachokupa chini ya gari lake na kazi yako itakuwa imekwisha.Endapo itajitokeza tena kazi nyingine basi tutawasiliana lakini utaendelea kuchunguza nyendo za Edwin hapo ofisini na tutakuwa tunakupa maelekezo nini cha kufanya.Unaweza ukalifanya hilo?akauliza Mathgew “Ndiyo ninaweza kulifanya hilo” “Good” akasema Mathew “Vipi kuhusu wenzangu? Nao mtawaachia? “Hapana tutaendelea kuwashikilia hadi pale tutakapokuwa tumekamilisha misheni yetu na wahusika wote kutiwa nguvuni ndipo tutawaachia.Yule mmoja mgonjwa ataendelea kuhudumiwa hapa hapa na madaktari”akasema Mathew na kumtazama Jackson “Jackson niangalie vizuri usoni mimi huwa ni mtu mbaya mno pale ambapo utajaribu kutuchezea na kugeuka msaliti.Ninaapa nitakusaka na nitakuua kwa mateso makali sana.Umenielewa Jackson? Mathew akauliza “Nimekuelewa kaka.Ninaelewa ninachotakiwa kufanya na sintajaribu kuwasaliti kwani hii ni kwa faida ya nchi yetu.Nitafuata maelekezo yako” akasema Jackson “Good” akasema Mathew na kwenda ndani akamletea Jackson nguo za kuvaa halafu akamtaka akachukue silaha za wenzake akapewa kifaa ambacho alielekezwa kukiweka chini ya gari la Edwin wakaagana akaondoka. “Mathew do you trust that guy?Ruby akauliza “Yes I do.Ruby hatuna namna lazima tumuamini.Atafanya kama tulivyomuelekeza.Kama akifanya tofauti tutatafuta namna nyingine lakini kwa sasa tuendelee kumuamini” akasema Mathew “What’s next? Akauliza Ruby “Umekuwa ni usiku mrefu wenye hatari nyingi na mafanikio pia.Kwa sasa tupumzike hadi kesho asubuhi” akasema Mathew wakaenda kuwatazama madaktari wakawatoa hofu kuhusu usalama wao





    Saa kumi na mbili za asubuhi ilimkuta Edwin Mbeko amekwisha wasili nyumbani kwa Melanie Davis. “Karibu sana Edwin.Habari za huko utokako? “Habari ni njema lakini jana kuna tukio lilitokea katika idara yetu kuna mtu alivamia kwa lengo la kuiba siri za usalama wa nchi”akasema Edwin na kumsimulia Melanie kila kitu kilichotokea usiku “Poleni sana kwa tukio hilo.Unahisi huyo mtu kitu gani alikuwa anakitafuta hapo katika ofisi zenu? “Hakuna anayejua lakini itakuwa ni siri za usalama wa nchi.Nitazungumza na Rais baadae leo ili anieleze kwa kina kuhusiana na huyo mtu ni nani na namna alivyoweza kupata taarifa za ofisi zetu kuvamiwa.Kwa maelezo ya Rais anaonekana kumfahamu huyo mtu kwani alimtaja kwa jina lake la Mathew Mulumbi na akadai kwamba huyo mtu alikuwa amefariki na ameibuka hivi karibuni kutoka kusikojulikana.Asubuhi ya leo ninakwenda kuonana na Rais amenitaka niende nadhani ni kwa ajili ya kuzungumza suala hilo hilo” akasema Edwin “Edwin umesema huyo mtu aliyejaribu kuvamia ofisi zenu anaitwa Mathew Mulumbi?akauliza Melania “Ndiyo.Unamfahamu? “Hapana simfahamu lakini nimewahi kulisikia jina hilo.Si jina geni kwangu” akasema Melanie na kukumbuka kitu “Devotha ! akasema na kuchukua simu yake akajaribu kumtafuta Devotha lakini hakupatikana “Kwa nini Devotha hapatikani toka jana? Nakumbuka ni yeye aliyewahi kunitamkia hilo jina.Ndiyo nakumbuka hivyo Devotha amewahi kulitamka hilo jina.Tukimpata yeye anaweza akatupa maelezo kuhusiana na huyo Mathew Mulumbi ni nani” akasema Melanie “Tuachane na hilo suala Melanie tutapata majibu yake baadae tuzungumze kuhusu mipango yetu.Mambo yanakwendaje hapa? Edwin akauliza “Mambo yanakwenda vizuri.Usiku kucha Khalid ameendelea na kazi ya kuunda bomu na ilipofika saa kumi za alfajiri amemaliza kazi na sasa bomu liko tayari” akasema Melanie na kutabasamu “Edwin leo ni siku kubwa sana kwetu.Ni siku ya kuandika historia katika nchi hii.Ni mara ya kwanza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anakwenda kuuawa.Binafsi nina furaha kubwa kwani ninakwenda kulipiza kisasi kwa watu wawili ambao kwa pamoja walishirikiana katika kuwaua wazazi wangu kikatili.Mimi mwenyewe nilinusurika kifo kwa namna ya ajabu lakini malengo yao yalikuwa ni kuua familia nzima.Kama wao walivyotaka kuimaliza familia yangu yote ndivyo itakavyokuwa kwao.Nilianza na wake zao leo ni zamu yao na baadae watafuata watoto wao.Nitahakikisha ninazisafisha kabisa familia hizi mbili na kusibaki hata na kumbu kumbu yao.Ahsante sana Edwin kwa kunisaidia hadi tumefikia hatua hii.Tusingeweza kufika hatua hii kama si kwa msaada wako.Nakuahidi baada ya tukio la leo utaishi maisha mazuri kama uko peponi.Yale yote tuliyokuahidi utayapata kweli na hata zaidi” akasema Melanie “Melanie mimi nakushukuru sana kwa kuwa msikivu na kufuata maelekezo japokuwa mwanzo kulikuwa na kutoelewana kati yetu lakini yale yamekwisha pita.Nashukuru kwa mipango kwenda vizuri.Ninakwenda ikulu asubuhi hii na nitapata ratiba kamili.Nitakapotoka huko nitakuja hapa na sare za jeshi la polisi ambazo ndizo mtu wetu atakayejitoa mhanga atavaa ili aweze kuingiaa ndani ya uwanja wa ndege.Ninao watu wangu ndani ya jeshi la polisi hivyo hakutakuwa na wasiwasi wowote wa jambo hili kufanikiwa” akasema Edwin “Edwin tafadhali hakikisha hakuna kitu chochote kitakachoingilia na kuharibu siku ya leo.Huu ni mpango mkubwa sana ambao kwa namna yoyote ile lazima ufanikiwe” akasisitiza Melanie “Melanie nakuhakikishia kwamba kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.Hakuna kitakachoweza kuvuruga mipango yetu.Andaa shampeni nzuri kwa ajili ya kujipongeza jioni ya leo wakati nchi nzima wanalia” akasema Edwin na kuagana na Melanie alikuwa anakwenda kujiandaa kwenda ikulu kuonana na Rais. “Mathew Mulumbi ! akawaza Melanie baada ya Edwin kuondoka “Hili si jina geni kulisikia.Devotha aliwahi kulitamka siku moja na sikumbuki alikuwa anazungumza kuhusu nini” akawaza Melanie “Hili jina la Mathew Mulumbi halina mahusiano na Gosu Gosu au Penielea?akajiuliza “Nakumbuka kama Devotha alilitaja jina hili wakati tukizungumza kuhusu aidha Peniela au GosuGosu” akawaza Melanie na kuchukua simu tena akampigia Devotha lakini simu yake haikupatikana. “Where are you Devotha?Kuanzia jana haupatikani simuni umekwenda wapi?Kwa nini hujatupa taarifa? Akajiuliza Melanie “Nimepata wazo ngoja nimpigie simu Peniela nimuulize kama anaweza kumfahamu huyu Mathew Mulumbi.Sifahamu kwa nini nimestuka baada ya kulisikia jina hili” akawaza Melanie na kufungua katika kitabu chake cha kumbukumbu akaziandika namna za simu za Peniela katika simu yake akampigia “Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili “Hallow Peniela” akasema Melanie “Nani mwenzangu?akauliza Peniela “Ni mimi Melanie Davis” “Oh Melanie habari za Dar es salaam? “Nzuri kabisa Peniela.Habari za Paris? “Huku kwema pia.Ni mara ya kanza tunawasiliana toka umefika Dar es salaam” “Ndiyo Peniela hatujawasiliana tangu nimeondoka Paris” “Melanie nina hamu sana ya kuzungumza nawe mambo mengi lakini naomba nikupigie baada ya dakika kumi na tano kuna mgeni muhimu niko naye tuna mazungumzo ya kibiashara.Usiende mbali tafadhali” akasema Peniela “Ahsante Peniela samahani kwa usumbufu” “Hakuna usumbufu wowote Melanie hata mimi nimefurahi sana kwa kunipigia.Nitakupigia ili tuzungumze mambo mengi.Kuna makampuni mengine ambayo nataka kuyauza.Nisubiri kwa dakika ishirini” akasema Peniela “Sawa Peniela ukiwa tayari nipigie simu” akasema Melanie na kukata simu “Shetani jike wewe leo umejileta mwenyewe .Umekwisha ! akasema Peniela baada ya kukata simu na bila kupoteza muda akampigia simu Peterson ambaye anamiliki kampuni ya wapelelezi wa kujitegema. “Peniela habari za asubuhi” akasema Peterson “Peterson habari ni nzuri.Samahani kwa usumbufu wa asubuhi hii” “Usijali Peniela tayari niko kazini” “Kuna simu nataka kuifuatilia nchini Tanzania na kujua mtu huyo yuko sehemu gani.Nakuhitaji hapa mara moja uje na vifaa vyako kwa ajili ya kuifuatilia simu hiyo” akasema Peniela “Sawa Peniela ninakuja hapo nyumbani kwako” “Hautaweza kuwahi kwa muda ninaoutaka.Ninatuma helkopta ije ikuchukue” akasema Peniela na kumuelekeza Peterson sehemu ya kwenda kupanda helkopta itakayompeleka nyumbani kwa Peniela.





    Peterson alishuka katika helkopta iliyokwenda kumchukua akiwa na sanduku jeusi na kuelekea katika jumba la Peniela. “Karibu sana Peterson” akasema Peniela wakaelekea katika ofisi yake ya nyumbani “Kama nilivyokueleza simuni kuna mtu nataka kumfuatilia kujua mahala alipo nchini Tanzania” “Hiyo ni kazi ndogoPeniela” akasema Peterson huku akifungua sanduku lake akatoa kompyuta ndogo na kuweka sawa program zake akaweka kifaa kingine mezani na kumtaka Peniela ampigie simu mtu anayemfuatilia “Jitahidi kumuweka kwa muda mrefu katika laini ya simu” akaelekeza Peterson na Peniela akampigia simu Melanie “Hallo Peniela” akasema Melanie “Melanie samahani kwa kukukatisha wakati ule” “Usijali Peniela.Ahsante kwa kupiga” “Sasa niko huru unaweza ukanieleza kile ulichotaka kunieleza” “Umewasiliana na Devotha kuanzia jana?akauliza Melanie “Devotha?! Peniela akauliza “Ndiyo.Umewasiliana naye ? “Hapana sijawasiliana naye.Kuna nini? “Nimejaribu kumtafuta kuanzia jana na hapatikani simuni” “Nitajaribu kumtafuta nikimpata nitamjulisha kuwa unamtafuta” “Ahsante sana Peniela.Jambo lingine kuna kitu nataka kuuliza” “Uliza Melanie usihofu” “Kuna mtu anaitwa Mathew Mulumbi unamfahamu? “Mathew Mulumbi? “Ndiyo unamfahamu? “Hapana simfahamu huyo mtu.Ni nani ?akauliza Peniela “Hata mimi simfahamu lakini nimewahi kulisikia mahali hilo jina likitamkwa ndiyo maana nikaona nikuulize kama unamfahamu” “Hapana simfahamu huyo mtu lakini kama unamuhitaji sana ninaweza kukusaidia kumtafuta.Ni mfanya biashara? Akauliza Peniela “Hata mimi sifahamu Peniela kuhusu huyo mtu.Simfahamu na sina taarifa zake” “Sasa imekuaje ukamuulizia wakati humfahamu? Akauliza Peniela “Nimesikia watu wakizungumza kama alifariki na ameonekana hai.Niliposikia jina hilo nikakumbuka nimewahi kulisikia mahali lakini sikumbuki wapi ndiyo maana nikakuuliza” “Jaribu kumuuliza Gosu Gosu yeye anaweza kuwa na taarifa nyingi za watu mbali mbali hapo Dar es salaam” “Gosu Gosu am…….” Akasema Melanie na kusita “Amefanya nini Gosu Gosu? Akauliza Peniela “Alivamiwa na majambazi akapigwa risasi” “Mungu wangu ! Peniela akaonyesha mstuko kama vile hafahamu chochote “Vipi hali yake?akauliza “Hali yake si nzuri nitaendelea kukujulisha maendeleo yake” akasema Melanie Peterson akamfanyia ishara Peniela kwamba tayari amekamilisha zoezi “Melanie taarifa hizi za Gosu Gosu zimenistua sana.Naomba endelea kufuatilia kwa karibu hali yake utanijulisha.Nitakuwa na safari ya Tanzania wiki ijayo tutazungumza masuala ya biashara kuna makampuni yangu mengine nataka kuyauza.Tutazungumza nitakapokuja” akasema Peniela “Sawa Peniela.Nitafurahi sana kuonana nawe tena.Utakapokuja tafadhali usiondoke bila kuonana nami” akasema Melanie na Peniela akakata simu “Umepata mahala alipo huyu niliyekuwa nazungumza naye simuni?akauliza Peniela “Ndiyo tayari nimepata mahala alipo nchini Tanzania” akasema Peterson na kumuonyesha Peniela ramani katika kompyuta yake “Yuko katika jiji la Dar es salaam mahala hapa kwenye mduara mwekundu” akasema Peterson “Ahsante sana Peterson.Naomba unitumie picha hiyo katika simu yangu” akasema Peniela kisha akaagana na Peterson akapanda helkopta kurudishwa mahala alikochukuliwa.Mara tu Peterson alipoondoka Peniela akampigia simu Mathew Mulumbi. “Peniela” akasema Mathew “Mathew habari za Dar es salaam? “Huku kwema.Unaendeleaje na watoto? “Sisi tuko vizuri.Mathew uko katika nafasi nzuri tuzungumze? “Ndiyo Peniela” “Ninakutumia ramani katika simu yako sasa hivi.Ukitazama katika mduara mwekundu ni mahala alipo Melanie Davis” akasema Peniela na kumueleza Mathew kila kitu kilichotokea hadi akafahamu mahala alipo Melanie “Peniela nakushukuru mno.Sipati maneno mazuri ya kueleza shukrani zangu kwa haya uliyonifanyia” akasema Mathew “Mathew ni mimi ambaye nina deni kubwa kwako la kulipa kwa mambo uliyonifanyia hivyo kila pale utakapohitaji msaada wangu usisite kunijulisha” akasema Peniela na kuagana na Mathew “Sikutegemea kama Peniela anaweza akawa na msaada mkubwa namna hii” akawaza Mathew na kuifungua picha aliyotumiwa na Peniela ilikuwa ni ramani ya jiji la Dar es salaam. “Melanie Davis ! Hatimaye umeingia katika mikono yangu ! akasema Mathew huku akiuma meno kwa hasira.Akamfuata Ruby chumbani alikokuwa anaoga akafunga maji “Kuna nini Mathew? “Ruby tumepata mahala alipo Melanie Davis”akasema Mathew na kumueleza namna Peniela alivyoweza kugundua mahala alipo Melanie. “Siku njema huonekana asubuhi.Itakuwa siku ndefu na ngumu sana”akasema Ruby “Kweli ni siku ngumu sana.Leo ni sisi au wao.Mbio zao zimefika ukingoni” “Nini tunakifanya baada ya kujua mahala alipo Melanie Davis?Ruby akauliza “Kwanza ni kuchunguza na kujiridhisha kama kweli Melanie Davis anaishi mahala hapo.Tukisha kuwa na uhakika kwamba Melanie Davis Yuko ndani ya nyumba hiyo tutaingia katika hatua ya pili lakini kwanza lazima tujiridhishe.We’re going there.Tutaweka kambi karibu na nyumba hiyo na kufuatilia kila kinachoendelea ndani ya nyumba hiyo.Ninayo kamera ya siri yenye muundo wa ndege ambayo tutairusha ndani ya nyumba na itatupa picha ya kila kinachoendelea humo ndani.Si rahisi kugundulika kama ni kamera kwani inafanana sana na ndege wa kawaida anayeruka angani” akasema Mathew “SNSA wana drone kubwa ambazo hurushwa angani kila asubuhi na kuzunguka sehemu mbali mbali za jiji na huwasaidia kupata picha mbali mbali.I can hack one drone”akasema Ruby “We’re done with SNSA.Wanaweza wakagundua kwamba tunatumia drone yao na wakavuruga misheni yetu.Hatuhitaji drone ya SNSA.Ninayo pia kamera nyingine ndogo ambayo tutaitumia.Ni aina mpya ya kamera za kijasusi ambayo inafanana sana na nyuki.Kamera hii inaweza ikaingia hadi ndani ya nyumba na kutupa picha nzuri” akasema Mathew “Kwa kamera hizo mbili hatuna haja ya kutumia drone ya SNSA” akasema Ruby huku akifuta maji na kutoka bafuni





    “Jackson jiandae nataka unipeleke ikulu ninakwenda kuonana na Rais” Edwin Mbeko akamwambia Jackson dereva wake mara tu alipowasili katika ofisi za SNSA akitokea nyumbani kwa Melanie Davis. Jackson akaenda katika gari la Edwin akaanza kulifuta vumbi.Akatazama pande zote hakukuwa na mtu katika maegesho yale ya viongozi akachukua kile kifaa alichopewa na Mathew akakibandika chini ya gari halafu akampigia simu Mathew “Kaka tayari nimekibandika kile kifaa katika gari la Edwin” akasema Jackson “Good job Jack.Nini kinaendelea hapo SNSA kwa sasa? “Edwin anataka nimpeleke ikulu asubuhi hii” “Sawa Jack endelea kutujulisha kila mahala anakoelekea na sisi tutaendelea kufuatilia kupitia hicho kifaa ulichokiweka katika gari lake” akasema Mathew na kukata simu “Jackson tayari ameweka kile kifaa katika gari la Edwin” Mathew akamwambia Ruby wakati wakijiandaa kuondoka nyumbani kwao kwenda kwa Melanie.Ruby aliyekuwa pembeni ya Mathew akiwa na kompyuta yake akakiona kile kifaa alichokiweka Jackson “Tayari nimekiona.Sikutegemea kama angeweza kufanya tulivyomuelekeza” “Unatakiwa kujifunza kuwaamini watu.Nitakufundisha namna ya kumtambua mtu ambaye anasema ukweli” akasema Mathew na ujumbe ukaingia katika simu yake akausoma ulitoka kwa Dr Masawe “Please stop calling me.I’m done with you ! “Dr Masawe hatarejea tena.Kitendo cha jana kutekwa na Edwin tayari kimempa uoga mkubwa kuendelea kushirikiana nasi.Hakuna tatizo tutaendelea kuwatumia wale madaktari waliobaki ambao wamekubali kuendelea kumuhudumia Gosu Gosu.Nitawalipa mara mbili zaidi ya tulivyokubaliana” akasema Mathew



    Edwin Mbeko aliwasili ikulu alikoitwa na Rais. “Edwin karibu sana.Nashukuru umefika kwa wakati” akaanzisha maongezi Dr Fabian “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” “Nimetaka uje asubuhi hii tuzungumze kwa sababu nina ratiba ndefu siku ya leo.Nina ugeni wa marais wa Uganda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Tutakuwa na kikao muhimu sana hivyo mazungumzo yetu yatakuwa mafupi sana” akasema Dr Fabian “Edwin nimekuta hapa kuja kukujulisha rasmi kwamba kuanzia sasa wewe utakuwa ndiye mkurugenzi mkuu wa SNSA.Umekaimu nafasi hii kwa miaka mitatu na umefanya kazi nzuri sana hivyo kwa mamlaka yangu nimekuteua kuwa mkurugenzi mkuu na msaidizi wako nitamteua hapo baadae” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais umenistua sana.Sikutegemea kabisa ama ungeweza kuniteua kushika nafasi hiyo” akasema Edwin “Unastahili nafasi hiyo” akasema Dr Fabian “Nashukuru mno mheshimiwa Rais kwa kuniona ninafaa” “Unafaa Edwin.Umekuwa katika nafasi ya ukaimu kwa miaka mitatu na hakujawahi kutokea tatizo lolote.Nilifanya makosa makubwa kuamua kumleta mtu ambaye haijui vyema idara ile na tazama mambo yaliyotokea.Ndani ya siku mbili tu ambazo Annabel amekuwa katika nafasi ya ukurugenzi yametokea mambo ya ajabu sana.Ameingiza watu wasio watumishi wa idara.Vimetokea vifo vya wafanyakazi wawili n.k.Kama angeendelea kwa mwezi mzima sifahamu nini kingetokea hivyo sitaki tena kumuona katika idara ile.Ulifanya vizuri sana kutumia kanuni kumuondoa katika nafasi yake.” “Mheshimiwa Rais ninashukuru sana kwa uteuzi huu na ninakuahidi kufanya kazi iliyotukuka kabisa”akasema Edwin “Edwin nataka ukafanye kazi .Nataka nchi iwe salama” akasema Dr Fabian “Usiwe na hofu mheshmiwa Rais.Idara yetu hailali watu wanafanya kazi saa ishirini na nne kuhakikisha nchi inakuwa salama” “Good.Kubwa nililokuitia hapa ni hilo la kukupa hiyo taarifa nzuri” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa rais kwa mara nyingine ninashukuru sana na ninakuahidi kazi nzuri.Hata hivyo nina swali dogo kama utaniruhusu kuuliza”akasema Edwin na Dr Fabian akaitazama saa yake kisha akasema “Uliza” “Ni kuhusiana na tukio la jana usiku.Uliniambia mtu ambaye alivamia ofisi zetu anaitwa Mathew Mulumbi.Ni nani huyo mtu? “Mathew Mulumbi hata mimi simfahamu vyema lakini wanaomfahamu wanadai aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi kabla ya kuanza kujishughulisha na biashara zake binafsi.Licha ya kuacha kazi katika idara ya ujasusi lakini inadaiwa Mathew ameendelea kufanya kazi za ujasusi kwa kujitegemea na inasemekana miaka mitatu iliyopita alishiriki katika misheni ya kuwakomboa mateka waliotekwa na kundi la IS na mmoja wa mateka hao akiwa ni mtoto wa Rais aliyemaliza muda wake kwa bahati mbaya katika misheni hiyo inadaiwa alifariki dunia lakini kwa mshangao mkubwa Mathew ameibuka wiki hii kutoka kusikojulikana.Mambo anayoyaongea na kuyafanya yanatia shaka sana kama kweli ni binadamu wa kawaida au ni mzimu unatuchezea.Kwa mfano jana aliwezaje kutoka ndani ya jengo lile bila kuonekana? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais hata sisi tumejiuliza alitokaje ndani ya jengo lile bila kuonekana?Lakini mheshimiwa Rais bado kuna kitu kimoja nataka kukifahamu kama itakupendeza “ “Sema Edwin usiogope” “Nataka kufahamu chanzo cha taarifa ile ya Mathew kuingia ndani ya jengo letu” akasema Edwin “Ni Annabel” “Annabel?Edwin akashangaa “Ndiyo.Yeye ndiye aliyeniambia kwamba anamsaidia Mathew kuingia ndani ya ofisi zenu na ndipo nikakupigia.Hiyo ni moja ya sababu kubwa iliyonifanya nikamuondoa katika nafasi ile ya ukurugenzi” “Mheshimiwa Rais Annabel alikueleza Mathew alikuja kutafuta nini katika ofisi zetu?akauliza Edwin “Hakunieleza sababu za kumsaidia Mathew kuingia SNSA” “Mheshimiwa rais utaniwia radhi lakini kwa hiki alichokifanya Annabel na Mathew wamekwisha ingia kwenye orodha ya watu hatari kwa usalama wa nchi.Annabel japo amekuwa mkurugenzi wa SNSA kwa siku mbili lakini ameyafahamu mambo mengi ya idara,tayari amezifahamu siri nyingi za usalama wa nchi na kama amemsaidia Mathew kuingia ndani ya ofisi zetu ni wazi kuna siri wanazitafuta na watajaribu kila njia hadi wafanikiwe lengo lao” akasema Edwin “Unalolisema Edwin ni la kweli kabisa.Tayari Annabel amekwisha onekana kuwa hatari hivyo tunatakiwa kuanza kummulika na kujua mwenendo wake.Nitakuita tena kesho tutalizungumza hili kwa kirefu zaidi” akasema Dr Fabian huku akinyanyuka kitini “Kwa heri mheshimiwa rais,jivinjari ikulu mara ya mwisho kwani kabla ya machweo leo tayari utakuwa umerejea kwa muumba wako” akawaza Edwin wakati akiagana na Rais







    Mathew na Ruby waliegesha gari lao mita chache kutoka geti la kuingilia jumba la Melanie Davis.Ni mtaa wanaoishi matajiri wakubwa hivyo kulikuwa na ukimya mkubwa.Kulikuwa na magari mawili yameegeshwa kandoni mwa barabara hivyo gari la akina Mathew likawa la tatu. “Kwa mujibu wa ramani yetu,Melanie Davis alizungumza na Peniela akiwa katika nyumba ile pale” akasema Ruby huku akiitazama ramani yake “Tunarusha kwanza kamera ya ndege ichunguze ndani ya nyumba ile kuna nini halafu tutarusha ile kamera ndogo ya nyuki” Akasema Mathew na kufungua boksi lililokuwa na ndege wa bandia aliyefungwa kamera.Kwa kumtazama kwa haraka haraka isingekuwa rahisi kujua kama ndege ile ni bandia kwani alionekana kama ndege halisi mwenye rangi za kuvutia.Mathew akatazama pande zote kama kuna watu wanaowatilia shaka halafu akaiwasha kamera ile akafungua dirisha na kumrusha Yule ndege huku Ruby akiwa na kifaa cha kumuongozea.Ndege Yule alipaa na kutua juu ya paa la nyumba ya Melanie na eneo lote la nyumba ile likaanza kuonekana.Hakukuwa na mtu yeyote nje.Kulikuwa na bustani nzuri ilyopandwa maua mazuri na eneo kubwa la nje lilipandwa majani mazuri ya kijani.Ruby akaizungusha kamera ile upande wa nyuma ya nyumba na mwanamke mmoja akaonekana akifanya usafi.Ruby akachukua picha ya mwanamke Yule akaiingiza katika programu na kumtafuta lakini hakuweza kupatikana “Mwanamke Yule hayupo katika mfumo wowote wa serikali” akasema Ruby “Tumekuja sehemu husika.Hii ni kazi ya mtandao wa akina Melanie.Watu wao wengi hawajulikani katika mifumo ya serikali” akasema Mathew.Ruby akampeleka ndege Yule juu ya ukuta akaielekeza kamera katika mlango mkuu wa kuingilia ndani ili waweze kushuhudia kila anayeingia na kutoka kupitia mlango ule mkubwa “Time to send in our second camera” akasema Mathew na kufungua sanduku lingine dogo akatoa kiboksi kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na kamera ndogo yenye muundo sawa na nyuki. “Teknolojia imekua sana zama hizi hadi vitu kama hivi vinatengenezwa.This is wonderfull” akasema Ruby “Hizi ni kamera za hali ya juu za kijasusi ambazo zinatumiwa na mataifa makubwa” akasema Mathew na kuiwasha ile kamera ndogo “Sweet bee go inside and do a nice job” akasema Mathew akamrusha Yule nyuki nje Ruby akaanza kumuongoza kuelekea ndani huku wakipata picha nzuri “This is amazing.Sikutegemea kama nyuki Yule anaweza akarusha picha nzuri namna hii” akasema Ruby na kumuongoza nyuki Yule hadi katika mlango mkubwa wa mbele akitafuta nafasi ya kumuingiza ndani lakini hakukuwa na upenyo wowote.Akamzungusha nyuma ya nyumba ambako nako tayari mlango ulikuwa umefungwa. “Betri ya huyu nyuki inaweza kudumu kwa muda gani? Ruby akauliza “Saa tatu hadi nne.Tutaendelea kusubiri hadi pale mlango utakapofunguliwa” akasema Mathew





    Baada ya kutoka ikulu Edwin Mbeko alimuelekeza Jakson ampeleke katika nyumba za maafisa wa polisi Mikunguni. “Jackson ahsante kwa kazi nzuri mliyofanya jana usiku” akasema Edwin “Usijali mkuu.Muda wowote utakaponituma kazi yoyote nitahakikisha inafanyika kikamilifu” “Nafurahi kusikia hivyo.Ninakuahidi kukuweka sehemu nzuri sana kwani kwa sasa mimi ndiye mkurugenzi.Rais ameniteua leo niwe mkurugenzi wa SNSA” akasema Edwin “Hongera sana mkuu.Unafaa kuongoza idara ile.Rais hajakosea kukupa nafasi hiyo” “Ahsante sana Jack” akasema Edwin “Vipi kuhusu Yule mama tuliyetambulishwa kuwa ndiye mkurugenzi?Atarudi tena SNSA?akauliza Jackson “Yule habari yake imekwisha.Hatarejea tena SNSA.Ni mwanamke hatari sana yule na ndiye aliyesaidiana na Yule jaama aliyeingia katika ofisi zetu jana usiku.Ni hatari kabisa kwa usalama wa nchi” akasema Edwin “Nini walikuwa wanakitafuta katika ofisi zetu jana? Akauliza Jackson “Wanatafuta siri za usalama wa nchi.Kuna mtu anaitwa Mathew Mulumbi nimeambiwa ndiye ambaye alivamia ofisi zetu.Tukimpata huyo atatueleza alichokuwa anakitafuta katika ofisi zetu” akasema Edwin “Mathew Mulumbi ni nani? Akauliza Jackson “Hata mimi simfahamu lakini nimeambiwa aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na baadae akapotea sasa amerudi tena na haijulikani ametoka wapi.Ni mtu hatari sana kwa usalama wa nchi” akasema Edwin na simu yake ikaita akaipokea “Hallo Melanie” akasema Edwin “Edwin bado uko ikulu? Huku kila kitu tayari na ni wewe tunayekusubiri hivi sasa” akasema Melanie “Tayari nimekwisha toka ikulu hivi sasa ninakwenda kuchukua zile sare halafu nitakuja hapo muda si mrefu” akasema Edwin na kukata simu halafu akamtaka Jackson kuongeza mwendo zaidi ili wawahi kufika mahala wanakoelekea Walifika katika nyumba za maofisa wa polisi Mikunguni Edwin akamuelekeza Jackson kuegesha gari nje ya nyumba Fulani ya mmoja wa maofisa wa polisi halafu akashuka na kugonga kengele ya geti na ndani ya muda mfupi mlango mdogo wa geti ukafunguliwa akaingia ndani. Mara tu Edwin alipoingia ndani ya ile nyumba Jackson akatoka nje ya gari akampigia simu Mathew “Jackson nini kinaendelea kwa upande wako?Mathew akauliza baada ya kupokea simu “Kaka nimekupigia simu kukujulisha kuwa tayari tumetoka ikulu na Edwin amenielekeza nimlete hapa Mikunguni katika nyumba za maafisa wa polisi hivi sasa ameingia katika mojawapo ya nyumba hizi.Kuna mambo mawili yametokea kwanza Rais amemteua kuwa mkurugenzi mkuu wa SNSA pili tukiwa garini alipigiwa simu na mtu anaitwa Melanie.Nadhani atakuwa ni Yule Melanie uliyenionyesha picha yake jana unayemtafuta.Sikusikia upande wa Melanie alichokizungumza lakini kwa upande wa Edwin nilimsikia akisema kwamba tayari ametoka ikulu na sasa anakwenda kuchukua zile sare kisha atamfuata.Kwa sasa ameingia ndani ya nyumba yenye kibao Block D 39” “Ahsante sana Jackson kwa kazi nzuri endelea kumfuatilia na kutujulisha kila kinachoendelea” akasema Mathew na kukata simu “Edwin amepewa ukurugenzi wa SNSA na Rais” Mathew akamwambia Ruby “Hakuna tatizo.Anamuamni ndiyo maana amempa nafasi hiyo lakini bado hajui kama Edwin ni nyoka wa vichwa viwili.Siku akilijua hilo tayari atakuwa amechelewa sana” akasema Ruby “Ukiacha hilo Jackson anasema wakiwa garini Edwin alipigiwa simu na Melanie na katika mazungumzo yao Edwin akamwammbia Melanie kwamba anafuatilia sare” “Sare?Ruby akauliza “Ndiyo amesema anafuatilia sare na sasa yuko Mikunguni ambako wanakaa maafisa wa polisi.Kuna kitu hapa kinajitokeza.Je huko mikunguni ndiko amefuatilia hizo sare?Je ni sare zipi hizo? Akauliza Mathew na mara katika kioo cha mashine ya kuongozea ile kamera ya ndege ukaonekana mlango mkubwa wa mbele ya nyumba ukifunguliwa.Mtu mmoja aliyevaa fulana ya kukatwa mikono akiwa na sigara mkononi akatoka. “James Kasai ! akasema Mathew Haraka haraka Ruby akacheza na kompyuta yake akaichukua picha ya yule mtu aliyetoka ndani ya ile nyumba akaiingiza katika programu ya utambuzi na majibu yakaja kwamba kwa asilimia mia moja Yule ni James Kasai “Oh my God it’s him ! akasema Ruby James Kasai akiwa na sigara yake alikwenda kuketi katika bustani mahala kulikokuwa na viti vzuri vya kupumzika.Baada ya muda mlango ukafunguliwa akatoka Yule mwanamke ambaye walishindwa kumtambua awali akiwa amebeba sinia lenye chupa kubwa ya mvinyo na glasi akamuwekea James mezani na kummiminia kidogo katika glasi.James akavuta sigara akapuliza moshi mwingi halafu akainua glasi ya mvinyo akanywa akaendelea kuvuta sigara yake. “Enjoy life for the last time bastard ! akasema Mathew akimtazama James kwa hasira.Mlango ukafunguliwa akatoka mwanamke ambaye hakukuwa na haja ya kutumia programu ya utambuzi kumtambua.Wote walimtambua haraka haraka alikuwa ni Melanie Davis “That’s Melanie Davis.Yule ndiye shetani wa kike anayetusumbua ambaye tumekuwa tukimsaka bila mafanikio” akasema Ruby “Kwa nini mwanamke mzuri namna hii akavaa roho ya kishetani anaua watu bila ya huruma?akauliza Mathew “Nani alikwambia shetani ana sura mbaya?Kumbuka shetani aliwahi kuwa malaika kabla ya kufukuzwa kwa hiyo usishangae ukiona mwanamke mzuri kama huyu ana roho ya kishetani” akasema Ruby “Your days are over Melanie.Leo ni wewe au sisi ! akasema Mathew akiendelea kumtazama Melanie akitembea kwa kuringa kuelekea mahala alipokuwa James Kasai ambaye aliinuka akavuta kiti Melanie akaketi halafu akammiminia kinywaji katika glasi “What a gentleman ! akasema Ruby huku akitabasamu.Mathew akageuka akamtazama na wote wakajikuta wakitabasamu Melanie na James waliendelea na mazungumzo. “Natamani nisikie kile wanachokizungumza.Tunawez a kumsogeza Yule nyuki karibu kusikia maongezi yao” akasema Mathew na Ruby akairusha kamera ile hadi karibu na mahala walipokuwa akina Melanie akaishusha katika majani halafu nyuki Yule akaanza taratibu kutembea katika majani hadi chini ya meza na sauti za maongezi ya Melanie na James Kasai zikaanza kusikika “Nimependa sana Dar es salaam ! akasema James Kasai “Usijali utakuja na kuondoka Dar es salaam kila pale utakapohitaji.Unaweza ukaja kila mwisho wa wiki ukastarehe kisha ukaondoka kurejea Uganda.Uwezo huo upo kwani tunaweza kufaya chochote ndani ya nchi hii”akasema Melanie “Ningefurahi sana kama ingekuwa hivyo.Naipenda Tanzania na ninaishambulia kwa kuwa imebidi iwe hivyo lakini sikuwahi kuwa na mpango wa kushambulia” akasema James “Hata mimi ninaipenda Tanzania.Nimeishi na kusoma hapa,watu wake ni wakarimu,watanzania hawana ugomvi na mtu yeyote.Kwa ujumla Tanzania ni nchi nzuri wabaya ni viongozi wake ! Lakini baada ya leo mambo yatatulia” akasema Melanie na mmoja watumishi wake akamfuata akamjulisha kwamba anahitajika ndani. “Melanie anadai ameishi na kusoma hapa.Ni nani huyu mwanamke?Mbona inaonyesha ametokea Ufaransa? Akauliza Ruby “Kuna jambo kubwa liko nyuma ya huyu mwanamke na leo lazima tulifahamu.Melanie Davis ni zaidi ya tunavyomdhania.Halafu katika maongezi yao kuna kitu amekiongea Melanie amesema baada ya leo mambo yatatulia.Kauli hii inaashiria kuna kitu kinakwenda kutokea leo.What are they planning today?akauliza Mathew na simu yake ikaita alikuwa ni Jackson “Jackson nipe habari” akasema Mathew “Edwin ametoka katika ile nyumba alimoingia akiwa na sanduku dogo.Hakutaka niongozane naye tena amenipa shilingi laki moja nitafute usafiri nirejee ofisini”akasema Jackson “Ahsante sana Jack kwa taarifa.Usiondoke maeneo hayo.Fanya utafiti kujua nyumba hiyo ni afisa gani wa polisi anaishi na mwenye cheo gani halafu nijulishe mara moja” akasema Mathew “Sawa kaka” akasema Jackson na kukata simu “Edwin amekwisha ondoka katika ile nyumba alimoingia.Hajataka kuongozana na Jack bali amempa shilingi laki moja atafute usafiri mwingine.Ametoka akiwa na sanduku dogo mfuatilie tujue anaelekea wapi” akasema Mathew na Ruby akaigeukia kompyuta yake akaanza kukifuatilia kile kifaa kilichowekwa katika gari la Edwin. “Kama utakumbuka Jack alisema wakati wanaelekea Mikunguni Edwin alizungumza na Melanie simuni na akamjulisha kwamba anafuatilia sare.Kwa taarifa ya sasa hivi Jack anadai kwamba Edwin alitoka ndani ya hiyo nyumba alimoingia akiwa na sanduku dogo.Je humo alimoingia ambamo ni kwa afisa wa polisi ndimo alimokwenda kuchukua hizo sare? Je ni sare zipi hizo? Akauliza Mathew “Mathew ukiunganisha hilo la sare na yale maneno ya Melanie kwamba “baada ya leo” unapata picha kwamba kuna kitu kinaandaliwa leo na hawa watu”akasema Ruby “Bado kuna mtu mmoja hatujathibtisha kama yuko ndani ya nyumba hii Khalid Sultan Khalid.Je yumo humu ndani au yuko sehemu nyingine? Lakini taarifa zilionyesha kwamba anakuja Tanzania kuonana na James Kasai hivyo basi kama James yuko humu ndani kuna uwezekano mkubwa Khalid akawa mle ndani.Tuendelee kuvuta subira tutajua kila kitu” akasema Mathew





    Edwin Mbeko alipotoka Mikunguni akaelekea moja kwa moja nyumbani kwa Melanie Davis.Mathew na Ruby waliendelea kumfuatilia bila yeye kufahamu na kugundua alikuwa anaelekea maeneo yale.Alipofika katika geti la nyumba ya Melanie gari lake likasimama kwa sekunde kadhaa halafu geti likafunguliwa akaingia ndani.Kamera mbili za akina Mathew zilizokuwa mle ndani zote zikaelekezwa katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni.Gari likasimama mlango ukafunguliwa akashuka Edwin Mbeko akafungua mlango wa nyuma akachukua sanduku dogo kisha akaingia ndani haraka haraka “Sanduku lile dogo ndilo alilotoka nalo kule Mikunguni kwa mujibu wa Jackson.Natamani nikaingie mle ndani nishuhudie kile kinachoendelea lakini tutaharibu mambo” akasema Mathew “Tuwe wavumilivu na tutajua tu kila kinachoendelea mle ndani” akasema Ruby Edwin alipoingia mle ndani akasalimiana na James Kasai na Melanie “Kwema huko utokako?akauliza Melanie “Kwema kabisa.Kuna habari nzuri.Rais ameniteua kuwa mkurugenzi wa idara ya SNSA” “Wow ! hongera sana” “Ahsante.Kwa sasa tuna nguvu kubwa na tunaweza kufanya kila tutakalo” “Imekuwa vyema amekukabidhi cheo kwa mara ya mwisho” “Marais wa Uganda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tayari wamewasili na hivi sasa kikao kinaendelea ikulu Dar es salaam” akasema Edwin “Jenerali Akiki alinipigia simu wakati anaondoka Kampala kuja Dar es salaam” akasema Melanie “Melanie hii ni siku yetu kubwa sana na kizuri ni kwamba mipango yetu yote inakwenda vizuri.Inapendeza sana kama kila mnachokipanga kinakwenda vyema” akasema Edwin na kufungua sanduku alilokuja nalo na kutoa sare za jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia.Wakazikagua halafu wakaelekea katika chumba alimokuwamo Khalid Sultan.Akasalimiana na Edwin halafu akamuonyesha bomu alilolitengeneza ambalo lilifanana na fulana za kuzuia risasi wavaazo jeshi la polisi. “Bomu ambalo niliitwa kulitengeneza ni hili hapa limekamilika na kazi imebaki upande wenu kulilipua.Hili ni bomu kubwa na madhara yake ni makubwa pia.Nina hakika wale wote waliolengwa kuuawa na bomu hili hawatasalimika.Nimetengenez a pia bomu lingine la akiba kwa ajili ya siku nyingine” akasema Khalid halafu akaenda kumchukua Abdi kijana wa miaka ishirini na nane kutoka katika kundi la Alshabaab . “eabdi kl shay’ jahiz wahan alwaqt alan lildhahb” (Abdi kila kitu kimekamilika na muda wa kuingia kazini umewadia) Khalid akamwambia Abdi akitumia lugha ya kiarabu. “ana mustaeidum” (niko tayari” akajibu Abdi “eabdi eayilatuk satatrik hayatan fakhiratan libaqiat hayatihim bsbb ma tafealuh alyawm (Abdi familia yako itaishi maisha ya kifahari kwa maisha yao yote kwa sababu ya hiki unachokwenda kukifanya leo” akasema Khalid “amiyn ! akasema Abdi halafu akavua mavazi aliyokuwa amevaa akaanza kuvaa mavazi yale ya askari yaliyoletwa na Edwin.Alionekana kama askari halisi wa kikosi cha kutuliza ghasia kwa mavazi yale.Taratibu Khalid akaichukua fulana ile ambayo ni bomu akamvisha akaifunga vizuri. Khalid akazungumza na Abdi kwa lugha ya kiarabu halafu akawageukia akina Melanie “Kila kitu tayari Abdi amekwisha pewa maelekezo nini cha kufanya hivyo msiwe na wasi wasi wowote.Kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa” akasema Khalid Hakukuwa na kupoteza muda Edwin akaagana na akina Melanie kisha akamchukua Abdi wakaelekea nje Mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni ukafunguliwa na Ruby akamstua Mathew “Mlango umefunguliwa” akasema na mara akaonekana Edwin Mbeko na nyumayake akaonekana askari wa kikosi cha kutuliza ghasia. “What’s going on in there?akauliza Mathew “Sijaweza kuipata sura ya Yule askari kwani ametoka haraka haraka sana na kuingia garini”akasema Ruby “Edwin alipozungumza na Melanie alimwambia anakwenda kufuatilia sare na alipotoka katika nyumba ya mmoja wa afisa wa polisi alikuwa na sanduku ambalo alikuja nalo hapa akaingia nalo ndani.Naamini sare alizokuwa anafuatilia ni sare za jeshi la polisi ambazo amevaa Yule jamaa na hii inatoa picha kwamba Yule jamaa yawezekana si askari.Yawezekana wamemvisha sare zile ili aonekane kama askari na wamtumie katika mipango yao.Ningeweza kumfuatilia kujua wanakoelekea lakini kwa kuwa kuna kifaa katika gari la Edwin tutafahamu anaelekea wapi.Ndani ya nyumba hii kuna watu muhimu sana ambao hatupaswi kuwapoteza” akasema Mathew Wakati Mathew na Ruby wakiendelea kufuatilia kile kinachoendelea ndani ya nyumba ya Melanie Jackson akapiga simu. “Kuna taarifa gani Jackson?Mathew akauliza “Uliniambia nifuatilie ni afisa gani anakaa katika ile nyumba alimoingia Edwin” “Ndiyo.Umekwisha fahamu ni afisa gani? “Anaitwa Inspekta Fanuel Mwabukusi au kwa jina lingine anaitwa afande mwarabu” “Ahsante sana Jackson usiondoke maeneo hayo hadi nitakapokwambia” akasema Mathew Katika nyumba ya Melanie bado milango iliendelea kufungwa. “Ruby hatuwezi kuendelea kusubiri namna hii wakati tayari tumekwisha pata uhakika kwamba ndani ya nyumba ile yupo James Kasai na Melanie Davis.We have to do something ! akasema Mathew “Unataka kufanya nini Mathew? “I want to get in there and……….” “Hapana Mathew sikushauri ufanye hivyo.Kuna mambo mengi tutashindwa kuyafahamu kama tukiwavamia sasa hivi.Tujipe muda kidogo”akasema Ruby “Ruby hujui ni namna gani ninaumia kuwaona wale watu walivyo huru wakiendelea na mipango yao mle ndani” “Muda utafika Mathew.Vuta subira kidogo” akasema Ruby “Kuna mtu mmoja tu ambaye bado hatuna uhakika naye mahala alipo Khalid Sultan.Kama ningekuwa na uhakika yuko mle ndani nisingekuwa na muda wa kusubiri” akasema Mathew “Subira yavuta heri.Tuendelee kusubiri tunaweza kugundua mambo mengine mengi zaidi” akasema Ruby na ile kamera ndogo ya nyuki ikaonyesha kuanza kuisha chaji ikalazimu Ruby kuirudisha “Kamrea hii imetusaidia sana Mathew” akasema Ruby “Teknolojia imerahisisha sana kazi za ujasusi siku hizi.Kama isingekuwa teknolojia ingetuchukua muda kufahamu kama James Kasai na Melanie wako mle ndani” akasema Mathew





    Edwin Mbeko alipoondoka kwa Melanie alielekea moja kwa moja Mikunguni.Jackson akiwa katika kibanda cha kuuza juisi kilichotazamana na nyumba ya afande mwarabu aliiona gari ya Edwin ikikata kona kuelekea katika geti la nyumba ile.Akapiga honi na geti likafunguliwa gari likaingia ndani geti likafungwa.Jackson akasogea hadi katika geti akatafuta upenyo na kuchungulia ndani akamuona Edwin akiwa amesimama na askari mmoja wa kikosi cha kutuliza ghasia pamoja na askari mwingine aliyevaa mavazi ya kiofisa akiwa na fimbo mkononi.Walizungumza kwa dakika kama tano halafu Edwin akaingia peke yake ndani ya gari yule askari akabaki.Geti likafunguliwa gari la Edwin likatoka na kuondoka.Simu ya Jackson ikaita alikuwa ni Edwin Mbeko “Hallo mkuu” akasema Jackson “Jackson umekwisha fika ofisini?akauliza Edwin “Ninakaribia kufika mkuu” “Fanya hivi.Nataka hapo hapo ulipofika ugeuze.Nataka nikukute katika bohari ili nikuachie gari langu nitakuwa na safari” “Sawa mkuu ninaelekea huko sasa hivi” akasema Jackson halafu akampigia simu Mathew “Jackson tumeona hapa Edwin amerejea tena mikunguni” akasema Mathew “Ndiyo mkuu amerejea katika nyumba ile ile ya afande mwarabu” “Alipoondoka hapa kwa Melanie alikuwa na mtu aliyevaa sare za jeshi la polisi” “Nimemuona huyo mtu alikuwa amesimama naye wakizungumza na afande mwenye mavazi ya kiofisa ambaye naamini ni afande Mwarabu.Kwa sasa Edwin ameondoka lakini yuko peke yake garini Yule askari amemuacha hapa kwa Mwarabu.Amenipigia simu na kunitaka niende katika bohari ili anikute kule aniachie gari anadai anataka kusafiri” akasema Jackson “Anataka kusafiri?! “Ndiyo.Ameniambia hivyo” akajibu Jackson “Jackson naomba unisubiri hapo mahala ulipo.Ninakuja sasa hivi nataka twende wote huko katika bohari” akasema Mathew “Sawa mkuu nakusubiri” akajibu Jackson na Mathew akakata simu “Mathew unataka kufanya nini?akauliza Ruby “Sikiliza Ruby.Edwin anataka kusafiri.Ninahisi safari hii ni nje ya mkoa hivyo lazima kuna kitu.I have to stop him.Ninakwenda huko katika bohari pamoja na Jackson na kumdhibiti Edwin asiweze kuondoka.Wewe utaendelea kukaa hapa hapa ukiendelea kufuatilia kwa karibu kila kinachoendelea na utanijulisha.Usiogope you’ll be safe.Kama kutatokea hatari yoyote kuna silaha iko humu utatumia.Nikimaliza huko nitarejea hapa mara moja”akasema Mathew “Sawa Mathew mimi nitaendelea kufuatilia kila kinachoendelea hapa na kukujulisha” akasema Ruby.Mathew akashuka ndani ya gari na kuanza kutembea haraka haraka kuelekea barabara kuu kwa ajili ya kuchukua piki piki akamuelekeza Jackson sehemu ya kukutana.





    Mathew alimchukua Jackson mahala alipomuelekeza wakutane kisha wakaelekea nyumbani kwake. “Jackson karibu sana hapa ni nyumbani kwangu” “Hapa ni kwako?akauliza Jackson “Ndiyo.Mbona umeshangaa? “Una nyumba nzuri mno.Unaonekana una maisha mazuri kwa nini unafanya kazi hizi za hatari?akauliza Jackson “Tutazungumza hayo baadae lakini kwa sasa nataka kufahamu ulinzi ulivyo katika bohari” “Kuna walinzi wanne getini.Wawili wana silaha mmoja ana mbwa na mmoja kwa ajili ya mawasiliano.Kuna walinzi wengine sita wenye silaha kuzunguka ukuta wa bohari.Ndani huwa kuna wafanyakazi kumi na mbili.Kwa kawaida ni wafanyakzi wa bohari pekee ambao huruhusiwa kuingia.Wewe si mfanyakazi wa bohari hivyo hautaweza kuingia”akasema Jackson “Nitaingia katika buti ya gari” “Ikiwa hivyo utaweza kuingia mle ndani” akasema Jackson. “Jackson kabla ya kuondoka hapa naomba nikuonye kwamba hiki tunachokwenda kukifanya huko ni kitu cha hatari sana hivyo endapo hauko tayari kwenda unaweza ukaniambia na mimi nitakuelewa” akasema Mathew “Kaka mimi nimejitolea kwa ajili ya nchi yangu hivyo siogopi hata kama nikifa nitakuwa nimekufa nikilinda usalama wa taifa langu” akasema Jackson “Good ! akasema Mathew kisha akaenda chumbani kwake akaongeza silaha katika begi lake dogo akachagua gari ambalo lingeweza kuwafaa kwa shughuli ile akaingia katika buti na safari ikaanza







    Edwin Mbeko alirejea kwa Melanie Davis baada ya kutoka Mikunguni “Kila kitu kimekamilika na hivi tuongeavyo tayari Abdi anapelekwa uwanja wa ndege kutimiza jukumu lake” “Huyo mtu anayempeleka Abdi uwanja wa ndege unamuamini?akauliza Melanie “Ninamuamini .Ni mtu wangu wa karibu na licha ya hayo amechukua tayari milioni mia moja hivyo kila kitu kitakwenda vizuri.Msiwe na wasi wasi wowote kila kitu kimekaa vizuri” akasema Edwin “Edwin umenifurahisha sana kwa namna unavyofanya kazi zako.Ahsante sana kwa kuukamilisha mpango huu” akasema James Kasai “James Kasai hata mimi ninafurahi kukutana na kufanya nawe kazi” akasema Edwin “Nilimwambia Melanie kwamba nitapenda kuja tena Dar es salaam kwa mapumziko ya hata wiki moja na amenihakikishia nisihofu.Ninakubaliana na Melanie kwamba nisihofu kuhusu kuja Tanzania kwani nina hakika wa kuja na kuondoka salama kwa sababu yako.Hongera sana Edwin” akasema James Kasai na kumpa mkono Edwin kumpongeza “Nashukuru sana James na ninakuahidi kwamba kwa muda wowote ambao utahitaji kuja nchini Tanzania unakaribishwa na ninakuhakikishia utakuwa salama” akasema Edwin “Ndugu zangu ninawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mkubwa.Tutaendelea kuwasiliana”akasema James Kasai huku akiwapa mikono Melanie na Khalid halafu akaagana na watumishi wawili wa Melanie kisha wakatoka nje kuelekea garini. Melanie na James wakakumbatiana wakaagana.James akafunguliwa mlango akaingia garini Edwin akaliondoa taratibu huku Melanie akipunga mkono kisha akarejea ndani.







    Mathew Mulumbi akiwa ndani ya buti ya gari akielekea bohari kuu la SNSA simu yake ikaita alikuwa ni Ruby “Hallo Ruby ! akasema Mathew “Mathew uko wapi mbona unapatikana kwa mbali sana? “Niko ndani ya buti ya gari ninaelekea bohari kuu SNSA.Vipi maendeleo huko?Kuna chochote umekipata?akauliza Mathew “Edwin Mbeko ameondoka hapa muda mfupi uliopita akiwa na James Kasai.Inaonekana James Kasai anaondoka nchini”akasema Ruby “Kama vile nilivyohisi.Thank you Ruby.Watanikuta kule katika bohari” “Mathew kuwa makini sana na hawa jamaa” akasema Ruby “Usihofu Ruby.Endelea kufuatilia kila kinachoendelea hapo katika hiyo nyumba” akasema Mathew na kukata simu. Taratibu Jackson alianza kupunguza mwendo wa gari alipokaribia kufika geti kuu la bohari ambako mmoja wa walinzi aliwasha taa yenye maandishi yanayomtaka asimame.Taratibu akapunguza mwendo wa gari na kusimama walinzi wakaanza kulisogelea gari.Akiwa ndani ya buti ya gari Mathew alikuwa amejiweka tayari endapo kungetokea tatizo lolote.Jackson akashusha kioo cha gari na walinzi wakajikuta wakiangua kicheko baada ya kumuona.Hawakulikagua tena gari bali yakaanza maongezi mafupi “Samahani mkuu hatukujua kama ni wewe.Unabadili magari sana siku hizi” akasema mmoja wa wale walinzi kisha geti likafunguliwa Jackson akaingia ndani ya bohari.Moja kwa moja akaenda kuegesha gari katika maegesho ya magari.Kulikuwa na magari manne ya wafanyakazi lake likawa la tano.Akafungua mlango akashuka na kuangaza angaza kama kuna mlinzi karibu na eneo lile lakini hakuona mlinzi yeyote akaenda nyuma ya gari na kugonga buti mara mbili.Mathew Mulumbi taratibu akafungua buti na kuchungulia nje “Kuko shwari kaka hakuna mlinzi yeyote mahala hapa” akasema Edwin huku macho yake yakigeuka kama kinyonga kutazama kila upande.Haraka haraka Mathew akatoka ndani ya buti ya gari na kuingia katika kiti cha nyuma. “Eneo liko kimya sana hili” akasema Mathew “Ile pale ni karakana ya kutengenezea magari mabovu ya idara ingawa kwa sasa haitumiki tena kwani magari yote hupelekwa katika gereji binafsi.Lile pale ndilo jengo la bohari.Ndani mle kuna vitu mbalimbali vya idara” Jackson akamuelekeza Mathew “Silaha pia mnahifadhi mle? “Hapana silaha hazihifadhiwi hapa.Hifadhi ya silaha iko kule wanakoishi kikosi cha makomando wa SNSA” akajibu Jackson na mara ukasikika mlio wa helkopta “Hiyo ndiyo helkopta ya idara ambayo ataondoka nayo Edwin” akasema Jackson na wote wakaishuhudia helkopta ile ikitua katika sehemu yake maalum. “Sogeza gari karibu” akasema Mathew na Jackson akawasha gari akalisogeza taratibu karibu na helkopta kama alivyoelekezwa na Mathew.Injini ya helkopta ikazimwa “Nataka ukamtoe Rubani ndani ya helkopta umpeleke ndani ya jengo.Can you do that?akauliza Mathew na Jackson akashuka garini akafungua mlango mkubwa wa helkopta. “Desmond ! akasema Jackson akisalimiana na Yule rubani “Jack mambo vipi.Naona umewahi sana” “Nimefika hapa dakika chache zilizopita.Safari ya wapi? “Tunaelekea Kagera” akajibu Yule rubani “Safari ndefu sana.Twende ndani tukapate vitafunwa kabla bosi hajafika.Yuko mbali hataweza kufika sasa hivi” akasema Jackson “Wazo zuri Jack.Ninahitaji pia kujisaidia” akasema Yule rubani na kushuka ndani ya helkopta “Gari zuri sana hili”akasema Desmond baada ya kuliona gari lile alilokuwa anaendesha Jackson “Usafiri wangu mpya huu.Twende ndani utakuja kulijaribu ukirejea kutoka Kagera.Nitakuachia wiki nzima ulitumie” akasema Jackson na kumuondoa Desmond aliyekuwa ameshika kitasa cha mlango akitaka kufungua kuangalia gari lile kwa ndani. Mara tu walipoondoka Mathew Mulumbi akashuka kutoka ndani ya gari akaufungua mlango wa helkopta akaingia ndani akafungua begi lake akatoa bomu na kulitega ndani ya helkopta halafu akatoka na kuingia ndani ya gari.Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana. Kwa mbali aliwaona Jackson na Desmond wakirejea.Desmond akafungua mlango wa mbele akaenda kuketi katika kiti chake akiwa ameshika mfuko uliokuwa na vitafunwa mbalimbali walivyovitoa ndani.Jackson akaliondoa gari na kulirejesha sehemu ya maegesho Zilipita dakika thelathini na nane gari la Edwin Mbeko likawasili kwa kasi na kwenda kusimama mbali kidogo na helkopta. “Edwin tayari amewasili.Nini kinaendelea?akauliza Jackson. “Subiri kwanza washuke garini” akasema Mathew. Rubani wa helkopta akashuka na kwenda katika gari la Edwin akafungua mlango Edwin akashuka.Akazunguka upande wa pili akafungua mlango akashuka James Kasai wakaanza kutembea kuelekea ilipo helkopta. “It’s show time” akasema Mathew na kukibonyeza kidude alichokuwa amekishika mkononi na mara ukatokea mlipuko mkubwa helkopta ikalipuka.Edwin,James Kasai na Desmond wote wakaanguka chini.Kama mshale Mathew na Jackson wakachomoka kutoka katika lile gari kuwafuata akina Edwin.James Kasai ndiye aliyekuwa wa kwanza kuinuka kutoka mahala pale walipoangukia akamfuata Edwin Mbeko aliyekuwa ameanguka na kumsaidia kuinuka.Mara Edwin akachomoa bastora baada ya kuiona sura ya Mathew Mulumbi akikimbia kuelekea mahala walipo “Run ! Edwin akamwambia James Kasai kisha akaanza kuachia risasi kuelekea upande wa Mathew mara kiganja cha mkono wake kikapigwa risasi bastora ikaanguka. “Aaaaggghhh ! Edwin akatoa mguno na mara akapigwa tena risasi nyingine ya paja.James Kasai aliinuka na kuanza kukimbia huku akigeuka nyuma na kuachia risasi lakini Mathew aliendelea kumkimbiza. “Leo ni mimi au wewe shetani wewe ! akasema Mathew na kuongeza mbio kumfukuza James aliyekuwa anaelekea yalipo magari mabovu.James aligeuka akaachia risasi Mathew akajibanza katika mnazi James alipogeuka ili aendelee kukimbia Mathew akaachia risasi mfululizo na James akaanguka chini.Alipigwa risasi kiunoni.Licha ya kupigwa risasi bado James aligeuka na kuanza kuachia risasi hovyo na moja ya risasi ikamchubua Mathew shingoni akajibanza nyuma ya mti uliokuwa karibu. “Shetani Yule angeweza kuniua ! akawaza http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mathew huku akiendelea kusikia mivumo ya risasi kutoka kwa James Kasai. “Siwezi kumuacha huyu muuaji akatoroka” akawaza Mathew na kugeuka haraka akaanza kuachia risasi mfululizo.James Kasai aliyekuwa anajivuta kuelekea katika mojawapo ya gari akapigwa risasi nyingine katika mguu wa kushoto na katika bega la kushoto akalala sakafuni.Huku akigugumia kwa maumivu James akageuka akiwa ameishika bastora yake akamuona Mathew akimfuata akaizinga bastora ili kuachia risasi lakini bastora yake haikuwa na kitu.Risasi zilikwisha malizika. “Aaaaghh ! akasema Mathew kwa hasira huku akimimina risasi katika bunduki yake na kifua cha James hakikutazamika tena.Bunduki ile ya Mathew ilikwisha risasi akaitupa akachukua bastora akamtazama kwa hasira James ambaye tayari alikwisha fariki. “Edwin weka bastora yako chini.It’s over ! sauti kali ikamuamuru Edwin aliyekuwa anagugumia kwa maumivu ya kupigwa risasi.Edwin alipatwa na mstuko mkubwa akabaki anashangaa asiamini macho yake alipomuona Jackson akiwa na bastora inayofuka moshi. “Jack ?!! akasema Edwin kwa mshangao “It’s over Edwin ! akasema Jackson ambaye alifanya kosa kubwa kugeuka kutazama walinzi waliokuwa wakikimbia kuelekea eneo lile.Edwin akaitumia nafasi ile akaiokota bastora yake kwa mkono wa kushoto akamlenga Jackson na kuachia risasi zilizompata Jack akaanguka chini. Walinzi waliokuwa na vizimia moto walifika na kuanza kuuzima moto ule. “Kuna jambazi amekimbilia kule karakana.Hakikisheni mnampata ! akaelekeza Edwin kisha Desmond akamtaka mmoja wa walinzi amsaidie wakamnyanyua Edwin kumpeleka katika bohari. Baadhi ya walinzi waliokuwa na silaha wakaanza kuelekea eneo lile la karakana kulikokuwa na magari mabovu kwa ajili ya kumsaka jambazi waliyeelekezwa na Edwin. “Hatimaye nimefanikisha kile nilichokuja kukifanya.Nilikuja Tanzania kukuua na nimefanikiwa kukuua ! akasema Mathew huku akimtazama James Kasai aliyekuwa amechafuliwa kwa risasi.Mara akasikia sauti ya mbwa akibweka. “Wananitafuta ! akawaza kisha akazama ndani ya uvungu wa gari na kutokea upande wa pili akajibanza katika moja wapo ya gari.Walinzi wale walioongozwa na mbwa mkubwa wakaukuta mwili wa James Kasai.Mmoja wa walinzi akachukua redio ya mawasiliano na kuibonyeza akawataarifu wenzake “Jambazi mmoja ameuawa huku katika karakana ya magari” akasema Yule jamaa akidhani James Kasai ndiye jambazi waliyetumwa wamtafute.Ghafla Mathew Mulumbi akajitokeza akiwa na bastora mbili na kuanza kunyesha mvua ya risasi walinzi wale wakaanguka chini wote.Mbwa Yule mkubwa akatoka mbio na kutaka kumrukia lakini Mathew alikwisha muona na kumpa konde zito la mkono wa kuliwa mbwa akaanguka chini hakuinuka tena “Zamu ya Edwin Mbeko” akasema Mathew na kutoka eneo lile la karakana akawaona baadhi ya walinzi na wafanyakazi wakiendelea na zoezi la kuzima moto. “Lazima nimpate Edwin” akawaza Mathew kisha akachukua bomu la kurusha kwa mkono akang’oa kifuniko na kulirusha mbali kidogo na ule moto uliokuwa unawaka likalipuka na kuzua taharuki kubwa watu wakaacha kuzima moto wakaanza kukimbia kunusuru maisha yao.Mathew akaitumia fursa ile akatoka mbio kuelekea mahala moto ulipokuwa unawaka akastuka baada ya kumuona Jackson akiwa amelala chini “Oh no ! akasema Mathew kwa mstuko na kumfuata Jackson akamtingisha “Jack ! Jack ! akaita Mathew na Jack akafumbua macho “Edwin alinipiga risasi akadhani ameniua nami nikalazimika kujifanya nimekufa.Ahsante kwa hii fulana ya kuzuia risasi imeokoa maisha yangu” akasema Jackson “Yuko wapi Edwin? “Ameingia ndani ya jengo” akasema Jackson Mathew akamshika mkono akamnyanyua “James Kasai tayari nimemuua.Tunamfuata Edwin” akasema Mathew wakaanza kukimbia kuelekea katika jengo la bohari alikoenda Edwin Desmond alikwenda katika stoo ya vifaa vya afya akachukua bandeji na kumfunga Edwin jeraha lake la risasi katika kiganga cha mkono ili kuzuia damu kuendelea kuvuja. “Desmond I need to get out of here before that nataka uende ukamtafute Yule jamaa niliyekuwa naye garini.Chukua walinzi muelekee katika karakana ndiko alikoelekea.Hakikisha unampata” akasema Edwin na kumpa Jackson bastora “Mkuu kwa nini nisichukue gari nikakuondoa kwanza wewe haraka ili ukapate matibabu?Eneo hili limekwisha kuwa hatarishi na yawezekana wale jamaa wakaja na kukukuta humu wakakumaliza” akasema Desmond “Desmond siwezi kuondoka hapa bila Yule mtu niliyekuja naye ! Go find him ! akasema Edwin.Desmond na Yule mlinzi walitoka Edwin akachukua simu yake akampigia Melanie “Edwin ! akasema Melanie “Melanie tumevamiwa ! akasema Edwin “Mmevamiwa?! Melanie akastuka “Ndiyo.Tumevamiwa na watu siwafahamu.Helkopta yetu imelipuliwa na bomu” “Mungu wangu.Are you okay?akauliza Melanie kwa sauti iliyojaa wasi wasi “Nimepigwa risasi lakini James amekimbia nimetuma watu wakamtafute” “Edwin get out of there now ! “Melanie siwezi kuondoka nikamuacha James Kasai.Lazima nimpate ndipo tuondoke hapa.Melanie sikiliza kama kuna kitu chochote kitanitokea basi usihofu kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.Tayari Yule kijana wetu aliyebeba bomu yuko uwanjani akiwasubiri marais wafike” akasema Edwin “Edwin tafadhali jitahidi uweze kuondoka hapo mara moja” akasema Melanie “Nitaondoka Melanie.Nimewatuma watu wakamchukue James kisha tutaondoka.Nitakujulisha kinachoendelea” akasema Edwin na kukata simu “Taratibu wekeni silaha zenu chini na kisha muinue mikono” Sauti kali ikawaamuru Desmond na Yule jamaa aliyekuwa naye mara tu walipojitokeza katika mlango wa kuingilia katika bohari.Taratibu wakaweka silaha chini. “Yuko wapi Edwin Mbeko?akauliza Mathew .Desmond akamtazama Jackson kwa hasira “Sikujua kama u msaliti kiasi hiki Yuda wewe ! akasema kwa ukali “Shut up ! akafoka Mathew “Yuko wapi Edwin?akauliza Mathew “Hatufahamu alip……” Kabla Desmonda hajamaliza sentensi yake tayari Mathew aliizinga bastora na kumchapa risasi Desmond akabaki Yule mlinzi “Yuko wapi Edwin?akauliza Mathew “Yuko ndani ! akajibu Yule mlinzi kwa woga na Mathew akamtaka ampeleke mahala alipo Edwin Mbeko. “Desmond ! akaita Edwin Mbeko aliposikia hatua za watu wakielekea mahala alipo “Desmond is that you? Akauliza tena Edwin na Mathew akampiga Yule mlinzi pigo moja kichwani akaanguka chini akaanza kunyata akifuata sauti ile ilikotokea.Akausukuma mlango wa moja wapo ya chumba na Edwin Mbeko akakutwa akiwa amekaa chini.Wakatazamana kwa sekunde kadhaa. “Ni wewe uliyeshirikiana na Annabel kumuua Fidelis na mmeshirikiana tena kuvamia bohari yetu na kufanya uharibifu mkubwa.Umekosea sana kwa hiki ulichokifanya”akasema Edwin Mbeko “Naamini umeniona lakini hunifahamu .Naitwa Mathew Mulumbi” “Mathew Mulumbi?! Edwin akashangaa “Wewe ndiye uliyevamia ofisi zetu ! “Ni mimi niliyevamia ofisi zenu na nilikuja kukutafuta wewe ! Sikukupata siku ile lakini leo nimekupata.Edwin nafahamu yote unayoyafanya.Nafahamu umekuwa unashirikiana na Melanie Davis.Ninafahamu kila kitu unachokifanya kushirikiana na magaidi na sitaki kuyasema hapa.Kwa taarifa yako James Kasai amekwisha fariki dunia.Nimemuua kwa mkono wangu.Fahamu vile vile kwamba hivi tunavyoongea kuna watu wako nje ya nyumba ya Melanie Davis na muda wowote atatiwa nguvuni na mtandao wenu wote utasambaratika.Naweza kukusaidia Edwin na kukuacha hai lakini ni pale utakapoamua kunieleza ukweli” “Unajidanganya wewe marehemu.Hakuna chochote utakachoweza kukipata.Wewe na hao waliokutuma mmejidanganya” akasema Edwin.Simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Ruby “Mathew nimemuona Khalid.Yuko ndani ya nyumba hii” akasema Ruby “Ruby are you sure? “Ndiyo Mathew.Nimemuona.Ametoka muda si mrefu nje.Yuko na Melanie wamekaa katika sehemu ya kupumzikia bustanini wakijadiliana jambo” “Ahsante Ruby.Nitafika hapo muda si mrefu” akasema Mathew na kukata simu “Tayari tunafahamu mahala alipo Khalid Sultan Khalid na muda si mrefu kutoka sasa naye atauawa.Nitakuacha hai kama utanieleza ni kitu gani mmepanga kukifanya hapa Dar es salaam leo?akauliza Mathew “Go to hell ! akasema Edwin “Mara ya mwisho Edwin nakuuliza nini mmepanga kukifanya leo hii?Nijibu na ninakuahidi sintakuua” “Unadhani ninaogopa kufa? Najua nitakufa lakini mmeshachelewa sana.Hakuna chochote mtakachoweza kukifanya kwa sasa.Hadi jioni ya leo tayari mtakuwa mmepata salamu” akasema Edwin “Mara ya mwisho Edwin nakuuliza nini mmepanga kukifanya leo?Wapi mmepanga kushambulia?akauliza Mathew na Edwin akacheka “Wewe na wapumbavu wenzako nimewaambia tayari mmechelewa sana.Subirini mtapata majibu! Akasema Edwin Mathew akapandwa hasira akaanza kummiminia Edwin risasi na kumuua akaichukua simu yake haikuwa na laini.Pembeni yake kulionekana vipande vya laini ya simu iliyoharibiwa “Bazazi huyu ameharibu laini yake ya simu ! akasema Mathew. “Jackson tuondoke haraka eneo hili” akasema Mathew wakatoka kwa haraka.Hakukuwa tena na watu eneo lilikuwa tupu watu wote walikimbia kuokoa maisha yao.Jackson aliingia katika gari lao Mathew akamuelekeza kulisogeza katika karakana wakasaidiana kuubeba mwili wa James Kasai wakauweka katika buti ya gari kisha wakaondoka.Katika geti kuu la kuingilia bohari waliwakuta baadhi ya walinzi na wafanyakazi wakiwa wamekusanyika Mathew akatoa bomu la kutupa kwa mkono akang’oa kifuniko na kulirusha likalipuka na watu wote wakalala chini halafu wakainuka na kuanza kukimbia.Mathew akashuka akafungua geti wakaondoka. “Kilichotokea pale ndani ni kama filamu lakini ni kitu cha kweli.Huyu jamaa ni mtu hatari sana.Sikujua kama ana uwezo mkubwa namna hii wa kupambana.Sikutegemea kama tungeweza kutoka hai.Nashukuru alinipa fulana ya kuzuia risasi kwani bila ile hivi sasa ningekuwa marehemu” akawaza Jackson





    Melanie alichanganyikiwa baada ya kupigiwa simu na Edwin akamjulisha kwamba wamevamiwa na watu wasiojulikana.Mara tu Edwin alipokata simu Melanie akamfuata Khalid chumbani kwake akamtaka watoke nje wakazungumze wakaenda kuketi nje bustanini “Melanie kuna nini?Mbona unaonekana una wasiwasi mwingi?akauliza Khalid “Kuna jambo limetokea Khalid” “Jambo gani Melanie?akauliza Khalid “Nimepigiwa simu na Edwin ameniambia wamevamiwa na watu wasiojulikana” “Wamevamiwa? “Ndiyo” “Imekuaje wakavamiwa? Ni tukio la ujambazi? akauliza Khalid “Hajanieleza vizuri kwa undani” “Wako salama yeye na James Kasai?akauliza Khalid “Helkopta yao imelipuliwa,Edwin amepigwa risasi na James amekimbia.Nimechanganyikiw a Khalid sina hakika kama watatoka salama” “Melanie tunatakiwa kutafuta namna ya kuwasaidia wenzetu kabla mambo hayajawa mabaya.Kwanza kama James Kasai amekimbia ni mbaya zaidi kwani anafahamika,picha zake ziko kila mahali hawezi kufika mbali atajulikana.Edwin naye amepigwa risasi na Yule ndiye pekee tuliyekuwa tunamtegemea aweze kumuondoa James Kasai hapa nchini.Kama helkopta imelipuliwa basi utakuwa ni mlipuko mkubwa na lazima litakuwa ni bomu hivyo basi watu wa karibuna eneo hilo watakuwa wameusikia mlipuko huo na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama.Polisi wakifika hapo wanaweza wakampata James Kasai na kila kitu kikaharibika.Tunatakiwa kuwaondoa haraka sana eneo la tukio Edwin na James Kasai kabla polisi hawajafika” akasema Khalid “Hilo unalosema ni la kweli Khalid lakini namna gani tutaweza kuwaondoa James Kasai na Edwin mahala hapo?Mimi sina kikosi na mtu pekee niliyekuwa namtegemea ni Edwin ambaye naye amepigwa risasi”akasema Melanie “Usihofu.Sisi tunao vijana wetu hapa Dar es salaam.Ninaomba simu yako nataka kuwasiliana na mtu Fulani ili anipatie vijana wa kwenda kuwakomboa James na Edwin” akasema Khalid na Melanie akampa simu yake.Khalid akaenda ndani na baada ya muda akarejea akiwa na kitabu kidogo akakifungua akaipata namba ya simu ya mtu aliyetaka kumpigia akapiga.Akazungumza kiarabu na mtu Yule kwa takribani dakika tano halafu akampa simu Melanie akamtaka amuelekeze Yule mtu pale mahala walipo Melanie akamuelekeza Yule mtu kisha akampatia simu Khalid ambaye aliendelea kuzungumza tena na Yule jamaa halafu akakata simu “Huyu niliyezungumza naye ni mkuu wa kundi la IS hapa nchini na ukanda wote wa Afrka Mashariki anaitwa Sayid Al Noor.Nilitakiwa kuonana naye jioni ya leo baada ya shambulio kutokea lakini kwa hili lililojitokeza nimelazimika kumuomba msaada na vijana watakuja hapa muda si mrefu ili kupata maelekezo ya mahala walipo Edwin na James Kasai.Kitu cha msingi kabla vijana hao hawajafika tunatakiwa kufahamu mahala walipo akina Edwin” akasema Khalid “Sifahamu mahala walipo.Alisema wanakwenda katika bohari kuu na sifahamu bohari hilo liko wapi.Ngoja nimpigie simu nimuombe anielekeze” akasema Melanie na kupiga namba za simu za Edwin lakini simu yake haikupatikana.Akajaribu tena lakini bado simu haikupatikana. “Simu yake haipatikani tena.Nitawasiliana na nani anisaidie?Simfahamu mtu mwingine yeyote wa idara yake” akawaza Melanie na mara akapata wazo “Devotha ! Ngoja nimtafute” akawaza na kuzitafuta namba za simu za Devotha akampigia lakini simu ya Devotha haikuwa ikipatikana. “Mungu wangu nini hiki kinaendelea? Mbona kila ninayempigia kumuomba msaada hakuna anayepatikana?Devotha naye yuko wapi?Kwa nini hapatikani kuanzia jana?Joyce naye hayupo najuta kwa nini nilimkubalia aondoke asubuhi ya leo kwenda Kigoma.Ngoja nimjaribu pengine anaweza kuwa na msaada” akawaza Melanie akampigia simu Joyce dereva wake lakini naye simu yake haikupatikana “Aliyesema siku ya kufa nyani miti huteleza hakukosea.Timu ya kwenda kuwaokoa akina Edwin inakuja na sijui mahala Edwin alipo.Nimepata wazo ngoja nimjaribu Peniela yawezekana akawa amepata taarifa za alipo Devotha.Yule ndiye msuka mipango yote kwa nini ametoweka ghafla wakati kama huu?Hakupaswa kuondoka bila kutujulisha kwani yeye ndiye tunayemtegemea sana kwa kila kitu” akawaza Melanie na kumpigia Peniela simu ikaita akashusha pumzi “Afadhali huyu simu yake inaita” akawaza Melanie na mara simu ikapokelewa “Hallo Melanie” akasema Peniela “Peniela samahani kwa usumbufu” “Bila samahani Melanie.Nikusaidie nini? “Nataka kujua kama ulifanikiwa kumpata Devotha” “Hapana sikufanikiwa kumpata” “Mungu wangu ! akasema Melanie “Kwani vipi Melanie?Una shida naye sana? “Ndiyo Peniela nina shida naye kubwa sana” akasema Melanie “Sikiliza Melanie kama Devotha hayupo hata mimi ninaweza kukusaidia.Kama kuna kitu kimekwama niambie nina mtandao mkubwa tu hapo Tanzania na mashariki kwa ujumla” akasema Peniela “Kuna rafiki yangu amevamiwa na majambazi.Amenipigia simu muda si mrefu akaniambia kwamba amevamiwa na amepigwa risasi.Ninataka kufahamu mahala alipo ili nitume watu wakamsaidie.Devotha anafahamiana na watu wa mitandao ya simu ambao wanaweza wakafahamu huyo rafiki yangu alikuwa wapi aliponipigia simu. Hilo ndilo kubwa ninalolihitaji” “Usiwe na wasiwasi Melanie.Hata kama Devotha hayupo nitakusaidia.Ninao mtandao mkubwa tu hapo Tanzania.Nielekeze mahala ulipo kuna mtu ambaye ni mtaalamu wa hayo mambo ya mtandao.Nitamuelekeza afike kwako haraka sana akusaidie” akasema Peniela na Melanie akamuelekeza mahala alipo “Usihofu Melanie.Ninamuelekeza huyo mtu wangu anakuja hapo sasa hivi atakusaidia kujua mahala alipo mtu wako” akasema Melanie “Nashukuru sana Peniela” “Usijali Melanie.Muda wowote ukiwa na tatizo nijulishe nitakusaidia” akasema Peniela na kukata simu “Umejileta wewe mwenyewe katika mdomo wa Mamba na mimi kazi yangu ni kukutafuna.Pole sana Melanie kwani mbio zako zimefika ukingoni” akasema Peniela na kumpigia simu Mathew “Peniela ! akasema Mathew “Mathew nimepigiwa simu na Melanie muda mfupi uliopita anamtafuta Devotha nikamuomba anieleze shida yake nimsaidie akaniambia kwamba anamtafuta rafiki yake ambaye ametekwa na watu wasiojulikana na anataka atume watu wakamsaidie lakini hafahamu mahala huyo rafiki yake alipo.Anachohitaji ni mtu wa kumsaidia kujua rafiki yake alipiga simu akiwa wapi? Nimemwambia kwamba ninamtumia mtu ambaye ana uwezo huo wa kumsaidia na kujua mahala alipo huyo rafiki yake.Mathew hii nafasi imepatikana ya kummaliza Melanie.Utakwenda nyumbani kwake na utajifanya wewe ndiye huyo mtu ambaye unataka kumsaidia kujua mahala alipo rafiki yake”akasema Peniela “Peniela sijui nikushukuruje kwa msaada huu mkubwa ulionisaidia.Sikutegemea kab….” “Mathew tusipoteze muda.Melanie anakusubiri sasa hivi.Ukifika mwambie umetumwa na Peniela” akasema Peniela “Ahsante Peniela” akasema Mathew na kukata simu na kumpigia simu Ruby “Ruby nimepigiwa simu na Peniela muda si mrefu ameniambia kwamba Melanie amempigia simu akamuomba amsaidie kupata mtu ambaye atamsaidia kujua rafiki yake aliyetekwa yuko wapi ili atume watu wakamsaidie.Nadhani Edwin Mbeko alimpigia simu akamjulisha kilichotokea. Peniela amemwambia kwamba anamtuma mtu nyumbani kwake muda si mrefu ili aweze kumsaidia” “Mathew this is our chance to finish Khalid Sultan” akasema Ruby “Ondoka hapo ili tukutane tuweze kujipanga namna ya kuingia mle ndani” akasema Mathew na kumueleza Ruby sehemu ya kukutana.” akasema Mathew na kukata simu akamuelekeza Jackson aongeze mwendo wa gari.







    Mazungumzo kati ya marais watatu yalimalizika ikulu Dar es salaam na marais wale ambao kwa siku chache zilizopita hawakuwa wakitazamana usoni kufuatia shambulio lililofanywa na James Kasai nchini Tanzani ambaye anatajwa kufadhiliwa na serikali ya Uganda.Katika kikao hicho ambacho mazungumzo yake yalikuwa ya kirafiki sana Jenerali Akiki Rwamirama Rais wa Uganda aliahidi kutoa ushirikiano katika zoezi la kumsaka James Kasai. Kikao kilimalizika kwa mafanikio makubwa sana na marais wote wakashikana mikono kupongezana kwa mafanikio yale makubwa “Tulichokifanya leo ni kitu cha kihistoria na kitaingia katika vitabu vya historia.Tumeonyesha mfano kwa mataifa mengine kwamba tunaweza kuzungumza na kumaliza tofauti zetu sisi wenyewe.Tumewaabisha wale waliodhani labda Afrika Mashariki itasambaratika .Ahsante sana Jenerali Akiki kwa kujisusha kwa ajili ya maslahi ya Afrika Mashariki” akasema Dr Fabian Jenerali Akiki ndiye aliyekuwa wa kwanza kuondoka kurejea Uganda na kuwaacha Rais Patrice Eyenga na Dr Fabian ambao walikuwa na mazungumzo mengine ya faragha.Waziri wa mambo ya nje wa nchi ndiye aliyemsindikiza Rais Akiki uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.





    Mathew akiwa na Ruby ndani ya gari waliwasili nyumbani kwa Melanie.Mathew aliyekuwa katika usukani akapiga honi mara tatu halafu geti likafunguka “Are you ready Ruby?akauliza Mathew “I’m ready” akajibu Ruby kisha gari likaingia ndani taratibu geti likajifunga.Mathew akapeleka gari hadi katika baraza.Mwanamke mmoja akaenda katika kioo cha dirisha akagonga.Ruby akafungua mlango akashuka .Yule mwanamke akampekua kama ana silaha “Huyu nani ndani ya gari?akauliza Yule mwanamke “Huyu ni dereva wangu” akasema Ruby na Yule mwanamke akamtaka Mathew atoe gari pale karibu na mlango mkuu wa kuingilia sebuleni. “Hakuna haja.Ninachukua muda mfupi sana hapa kisha naondoka” akasema Ruby akionekana kuwa na haraka.Yule mwanadada akamuongoza Ruby kuingia sebuleni akakutana na Melanie “Karibu sana dada” akasema Melanie “Melanie Davis?akauliza Ruby “Ndiyo.Umetumwa na Peniela? “Ndiyo nimetumwa na Peniela”akasema Ruby “Karibu sana” “Ahsante.Wapi tunafanyia kazi yetu?akauliza Ruby “Hapa hapa sebuleni hakuna tatizo” akajibu Melanie na Ruby akaitoa kompyuta katika mkoba akaanza kazi yake.Ruby alicheza na kompyuta haraka haraka kama vile ana vidole sita kila mkono na hakuna aliyejua kitu alichokuwa anakifanya.Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuunganisha kamera ya siri katika kompyuta yake na kompyuta ndogo iliyokuwamo ndani ya gari ili kumuwezesha Mathew kuona kile kinachoendelea mle ndani.Alipokamilisha hilo akaomba namba za simu za mtu ambaye anamtafuta kisha akaziingiza katika program yake na kuanza kutafuta mahala alipo Yule mtu. Kupitia ile kompyuta ndogo aliyounganishwa na Ruby,Mathew aliweza kuona namna watu walivyokaa mle ndani.Ruby alikuwa mezani halafu kukawa na wanawake wawili wakiwa nyuma ya Melanie.Mathew akaziweka sawa bastora zake halafu akafungua mlango taratibu na kwa tahadhari akashuka akatembea kuelekea katika mlango mkubwa wa sebuleni.Akakishika kitasa cha mlango akakinyonga na kufungua mlango kisha kama kima akajitoma ndani. Kabla hajafanya chochote mmoja wa wale wanawake akamsukuma Melanie akaanguka chini kisha mwingine akachomoa bastora na kuanza kumimina risasi kuelekea kule alikokuwa Mathew ambaye aliruka na kujificha nyuma ya kabati kubwa la vitabu.Yule mwanamke mwingine aliyemuangusha chini Melanie akamuinua na kumuongoza kukimbia pale sebuleni huku Yule mwanamke mwingine akiendelea kuachia risasi kumzuia Mathew asiweze kujitokeza.Risasi zilimalizika katika bastora ya kwanza na kwa haraka akachukua bastora ya pili na Mathew akautumia mwanya huo akajitokeza na kuanza kuachia risasi.Yule mwanamke akainua stuli akairusha Mathew akayumba kuikwepa na Yule mwanamke akapata upenyo akainuka na kuanza kukimbia kufuata varanda ambalo Melanie na Yule mwanamke mwingine walipita.Macho ya Mathew yalikwisha mng’aza akarukia katika sofa kisha akarukia juu ya meza na kuanza kuvurumisha risasi Yule mwanadada akaingia katika mojawapo ya chumba Mathew akanyata taratibu hadi katika mlango wa chumba kile akaupiga teke ukafunguka akaingia ndani na kwa kasi ya ajabu mkono wake uliokuwa na bastora ukapigwa teke bastora ikaanguka chini akapigwa teke lingine la mbavu akaanguka chini na Yule mwanadada akamuelekezea bastora.Mara ghafla akatoa mguno na kuanguka.Ruby alisimama mlangoni akiwa na bastora aliyokuwa ameificha katika sanduku dogo aliloingia nalo mle ndani “Thank you Ruby uko salama?akauliza Mathew “Niko salama Mathew.” akaelekeza Ruby “Ruby unatakiwa uende nje niachie mimi nipambane na hawa watu humu ndani.Mpigie simuJackson aje ndani” akasema Mathew “Mathew siwezi kukuacha peke yako humu ndani” akasema Ruby “Ruby nisikilize.Hii sehemu ya hatari nenda nje ! akafoka Mathew na Ruby hakutaka kubishana na Mathew akachukua kompyuta yake akatoka kwa tahadhari hadi katika gari akaliwasha na kutoka hadi getini akashuka akajaribu kulifungua geti halikufunguka akatoa bastora na kumimina risasi sehemu ambayo inapokea taarifa kutoka kompyuta iliyo ndani akakisambaratisha kiboksi kile halafu akafungua geti na kutoka nje. Baada ya Ruby kutoka Mathew akaanza kufuata lile varanda kwa tahadhari akiingia katika chumba kimoja kimoja na mara akapigiwa simu na Ruby “Kuna gari mbili zimefika katika geti.Geti halitaweza kufunguka kwa kompyuta kwani nimeliharibu” akasema Ruby Gari zile mbili zikaanza kupiga honi ili geti lifunguliwe.Mathew akasikia mlio wa simu sebuleni akaufuata mlio ule na kuiokota simu iliyokuwa ikiita na mara ujumbe ukaingia akausoma. “Vijana tayari wamefika mahala mlipoelekeza.Wapokeeni na muwaelekeze mahala alipo huyo mtu wakamfuatilie haraka” ukasomeka ule ujumbe. Mathew akatoka mle ndani na kutembea kwa tahadhari kubwa kuelekea getini alipolikaribia akatoa mabomu mawili ya kutupa kwa mkono akang’oa vifuniko na kuyarusha nje ya geti yaliko magari ya wale jamaa na milipuko kutokea. Baada ya kuokolewa sebuleni Melanie Davis na Yule msaidizi wake walikimbilia ghorofa ya pili kilipo chumba cha Melanie “Mfuate Khalid haraka chumbani kwake mwambie tumevamiwa ! akaelekeza Melanie na kuingia chumbani kwake.Akajipekua kutafuta simu yake lakini hakuwa nayo “Mungu wangu nimeangusha simu ! akasema Melanie kwa mstuko. “Kitu gani Peniela amenifanyia? Hawa watu aliowatuma ni akina nani?akajiuliza Melanie na kuhisi kuchanganyikiwa.Akafungua dirisha akachungulia nje kama anaweza akaruka akaogopa na kulifunga.Akatazama saa yake na kuvuta pumzi ndefu “It’s over ! hawa watu wanaonekana tayari wamekwisha tufahamu.Naamini ndio hawa hawa waliomvamia Edwin na sasa wamekuja kwangu.It’s over” akawaza kisha haraka haraka akaenda mezani akaikunjua kompyuta yake akaanza kujirekodi. Kupitia kamera zilizo nje ya chumba chake Melanie alimuona Khalid akielekea katika mlango wa chumba chake akiwa ameongozana na Yule mwanamke aliyetumwa kwenda kumjulisha kwamba wamevamiwa.Haraka haraka Melanie akabonyeza sehemu Fulani na mlango wake ukajifunga.Khalid alianza kugonga mlango kisha kwa hasira akampiga risasi Yule mwanamke akaanguka chini.Akaendelea kugonga mlango kwa nguvu akimtaka Melanie afungue na alipoona hafungui akaanza kumimina risasi katika mlango lakini mlango ule haukuwa ukipenya risasi Baada ya kurusha yale mabomu nje ya geti,Mathew akakimbia kuelekea ndani na alipofika mlangoni akasikia mlio wa risasi ukitokea ndani ya ile nyumba.Akaanza kutembea kwa tahadhari akifuata ngazi kuelekea ghorofa ya kwanza akasikia tena milio ya risasi mfululizo katika ghorofa ya juu yake.Akapanda kwa tahadhari kubwa.Mara tu Mathew alipojitokeza katika ghorofa ya pili akakoswa na risasi ikamlazimu kushuka chini kidogo.Akachukua kioo kidogo akakiinua juu na kumuona mtu mmoja akiwa na bastora amesimama katika mlango huku mtu mwingine akiwa ameanguka chini amepigwa risasi.Mathew alipoinua kichwa tu ikasikika milio ya risasi akajificha tena halafu akaambaa na mbao ya ngazi taratibu kisha akaruka na kutokeza katika varanda akaachia risasi na kumpiga Yule jamaa risasi katika bega la kushoto akaanguka chini akaanza kumsogelea “Khalid ! akasema Mathew baada ya kumgundua mtu Yule alikuwa ni Khalid Sultan Khalid. “Usinisogelee nina bomu ! akasema Khalid na kumuonyesha Mathew kilipuzi alichokuwa nacho mkononi.Khalid alikuwa amevaa fulana ya mabomu.Jicho la Mathew liliona kama la kinyonga.Aliweza kukiona kidole gumba kikibonyeza kile kilipuzi akageuka na kuruka hatua tatu kubwa na mara ukasikika mlipuko.Khalid akajilipua.Mathew akajikuta amerushwa na kujigonga ukutani.Baada ya sekunde kadhaa akajiinua mahala alipoangukia.Alikuwa amepasuka juu ya jicho.Varanda lilijaa moshi.Akatoa kopo Fulani katika begi lake alilovaa mgongoni akapuliza hewa iliyokuwamo ili kuondoa ule moshi. Bomu lile alilolipua Khalid liliusambaratisha mlango wa chumba cha Melanie na sehemu ya chuma ya mlango ule uliosambaratika ilimpiga Melanie kichwani akaanguka chini na kupoteza fahamu. Moshi ulipungua kufuatia hewa ile aliyoipuliza Mathew na akaweza kumuona Khalid akiwa amesambaratishwa na bomu.Mlango wa chumba cha Melanie uling’oka,Mathew akapuliza ile hewa toka ndani ya kopo na moshi ukatoka mle chumbani akauona mwili wa mwanamke ukiwa umelala sakafuni akamuendea haraka haraka akamgeuza alikuwa ni Melanie Davis ambaye hakuwa na fahamu. “I need you Melanie ! akasema Mathew na kumchunguza kama amekufa akagundua hakuwa amekufa bali alipoteza fahamu kwani bado mapigo ya moyo yalikuwepo.Haraka haraka akatoa simu na kumpigia simu Ruby “Mathew are you okay? Tumesikia mlipuko mkubwa na moshi ukatoka humo ndani.Nimeogopa”akasema Ruby “I’m okay Ruby.Nini kinaendelea huko nje? Akauliza Mathew “Huku nje kuna taharuki kubwa kufuatia milipuko ile ya mabomu” “Jackson yuko karibu? “Niko hapa kaka” Jackson akajibu akitokea nje ya kile chumba kile alimo Mathew “Niliamua kuingia ndani kuhakikisha kama uko salama baada ya mlipuko kutokea” akasema Jackson “Niko salama Jackson” akasema Mathew “Ruby tayari nimemuona Jackson” “Mathew nasikia ving’ora vya polisi wanaelekea eneo hili”akasema Ruby “Tayari wamekwisha pata taarifa za milipuko ile ya mabomu” akasema Mathew na kuiokota kompyuta iliyoanguka chini.Programu ya kurekodi ilikuwa inaendelea.Mathew akaisimamisha na kuanza kupitia kile ambacho Melanie alikuwa anakirekodi.Akasikiliza kile alichokisema Melanie “Mungu wangu ! akasema Mathew kwa mstuko baada ya kumaliza kusikiliza maelezo yale ya Melanie “President ! akasema na kumtaka Jackson ambebe Melanie wakatoka na kuanza kushuka chini Magari mawili ya polisi yaliyojaa askari yakawasili katika jumba la Melanie na askari wakashuka haraka haraka wakalizingira jumba lile na kuzungusha utepe wa njano kuzuia watu kukaribia mahala pale halafu wengine wakaelekezwa kujiandaa kwa ajili ya kuingia ndani.Geti likasukumwa na kikosi cha askari kumi wakaingia ndani na mara katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni wakajitokeza Mathew na Jackson aliyekuwa amembeba Melanie wakaamriwa kusimama mahala walipo. “SNSA” akasema Mathew huku askari wakiwasogelea kwa tahadhari “SNSA tafadhali ! akasema tena Mathew askari wale walipowakaribia zaidi “Tunatoka idara ya SNSA ! akasema Mathew “SNSA ni kitu gani ? akauliza kiongozi wa kikosi kile cha askari “Secret national security agency” akasema Mathew na Yule kiongozi wa kikosi akachukua kile kitambulisho cha Jackson akakisoma na kumrudishia “Sijawahi kusikia kitu kama hicho.Ninyi nyote mko chini ya ulinzi kama mmetoka idara ya nini mtajitambulisha huko mbele ya safari” akasema Yule kamanda “Afande SNSA ni idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Sisi tunafanya kazi kama mnayoifanya ninyi lakini sisi tunafanya kwa siri.Unapoendelea kutuweka hapa afande unatufanya tushindwe kutimiza wajibu wetu” akasema Mathew “Hata sisi tuko kazini ndugu yangu tusifundishane kazi” akasema Yule kamanda “Afande kuna shambulio limepangwa kufanyika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere walengwa ni marais wa Tanzania na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Kuna bomu liko tayari uwanja wa ndege na tukichelewa marais hao watauawa ! akasema Mathew “Wapekueni haraka watu hawa kisha muwafunge pingu tunakwenda nao kituoni watajieleza huko mbele ya safari ! akasema kwa ukali Yule kamanda.Mathew na Jackson wakapekuliwa silaha zao zikachukuliwa na Yule kamanda akaomba kukiona kitambulisho cha Jackson.Akakisoma halafu akamtazama Mathew “Nini kimetokea hapa? Akauliza “Magaidi wa IS walikuwa wanaitumia nyumba hii kwa ajili ya kuandaa mpango wao wa kuwaua marais wa Tanzania na Congo” “Nitaamini vipi kama kweli idara hii ipo na…..” “Afande naomba twende ndani tukazungumze” akasema Mathew na Yule kamanda akaongozana na Mathew hadi ghorofa ya pili “Huyu ambaye mwili wake umesambaratika anaitwa Khalid Sultan Khalid anatoka kikundi cha IS.Ni mtaalamu wa milipuko na alikuja hapa Tanzania kutengeneza bomu ambalo litatumika kuwaua marais wetu na kila kitu kimefanyika ndani ya nyumba hii.Idara yetu imekuwa ikiwafuatailia hawa watu kwa muda sasa na leo tumewatia nguvuni.Afande tunavyozidi kukaa hapa maisha ya rais wetu yako mashakani kwani tayari bomu limekwisha ingizwa uwanja wa ndege.Ni jukumu letu sisi tukisaidiana na ninyi kuweza kulizuia hilo lisitokee” “Bomu hilo unalosema limeingiaje ndani ya uwanja wa ndege?akauliza Yule kamanda “Kuna askari mmoja mwenye cheo cha mkaguzi wa polisi ndiye amesaidia bomu hilo kuingizwa ndani ya uwanja wa ndege”akasema Mathew na Yule kamanda akaonyesha mshangao “Ngoja nipige simu kuwajulisha viongozi walioko uwanja wa ndege kulitafuta hilo bomu” akasema Mathew “Hiyo si njia nzuri na hawataweza kulipata kwani aliyelibeba bomu hilo amevaa sare za askari polisi na endapo akifahamu kuwa amegundulika anaweza akakimbia tukashindwa kumpata” “Nini unashauri tufanye? “Nahitaji kuzungumza na Rais kumuomba asiende uwanja wa ndege sasa hivi ili tuweze kumsaka huyo mtu aliye na bomu na kumtia nguvuni” akasema Mathew “Unataka kuwasiliana na Rais? “Ndiyo.Nina mawasiliano naye” akasema Mathew na kufunguliwa pingu akampigia simu Ruby akamueleza kuhusiana na mpango ule wa kumuua Rais na kumtaka ampige simu Rais amzuie asiende uwanja wa ndege hadi hapo Yule jamaa mwenye bomu atakapokamatwa.Ruby akampigia simu rais lakini simu hakupatikana. “Simu ya rais haipatikani.Tunahitaji kuwahi uwanja wa ndege kabla hajafika.Kutoka hapa hadi uwanja wa ndege si umbali mrefu.Chukua vijana wachache tutumie gari la polisi kuwahi uwanja wa ndege.” akasema Mathew wakatoka kwa haraka kwa ajili ya kuelekea uwanja wa ndege. Mathew akawaelekeza Jackson na Ruby kumkimbiza Melanie hospitali kisha yeye akaingia katika gari la polisi ambalo liliondoka kwa kasi kuelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere. Gari lile la polisi lilikwenda kwa mwendo mkali sana huku likipiga king’ora kuomba kuachiwa njia na baada ya dakika kumi na saba wakawasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Kamanda Yule aliyejitambulisha kwa Mathew anaitwa Afande Titus akashuka garini na kupiga simu halafu akamtaka Mathew amfuate wakaelekea katika ofisi Fulani ambako waliwakuta makamanda watatu.Afande Titus akamtambulisha Mathew kwa makamanda wale wakataka kufahamu kuhusiana na taarifa ile ya uwepo wa bomu pale uwanjani lililolenga kuwaua marais.Mathew akawaeleza namna bomu lile lilivyoingizwa uwanjani wote wakabaki wanashangaa.Mathew akawaelekeza namna watakavyoweza kumpata Yule askari mwenye bomu wakakubaliana kisha akaongozana na afande Titus wakaingia ndani ya uwanja.Titus alikuwa na kitabu na kuanza kumfuata askari mmoja mmoja akimuuliza namba yake akaiandika katika kitabu.Karibu na jukwaa ambalo husimama marais kwa ajili ya nyimbo za taifa walisimama askari wawili.Mathew na afande Titus wakamfuata askari wa kwanza wakamuhoji namba zake na walipomfuata askari wa pili akababaika “Askari taja namba zako tafadhali ! akasema afande Titus lakini Yule askari hakuweza kutamka chochote.Mathew taratibu akaupeleka mkono akaishika bastora yake “Askari taja namba yako tafadhali ! akafoka afande Titus na katika redio ya mawasiliano akasikika mtu aliyeko uwanja wa ndege akiwajulisha askari wachukue nafasi kwani msafara wa marais umekwisha wasili pale uwanjani. “Askari !! akafoka afande Titus “Husikii ninachokuuliza? Taja haraka sana namba yako tafadhali ! akafoka afande Titus. Jicho la Mathew liliuona mkono wa Yule askari ulikokuwa unapelekwa akaruka na kumsukuma afande Titus akaanguka chini kisha akaupiga teke mkono wa Yule jamaa akaaguka chini. “Titus kimbiaaa !! akapiga kelele Mathew na Titus akainuka akaanza kukimbia.Yule jamaa aligeuka na kukishika kidude chekundu.Kabla hajakishusha kidole gumba katika kile kilipuzi Mathew akawahi kumrukia na kumtandika kichwa kizito usoni na Yule jamaa akaachia kile kilipuzi.Mathew akakikamata kidole gumba akakivunja,akamtandika ngumi mbili mfululizo usoni.Yule jamaa akaukunja mguu wa kulia akampiga Mathew kichwani kwa kutumia goti na kumsukuma Mathew pembeni.Akainuka na kukishika kilipuzi kwa mkono wake wa kushoto Mathew akamkata mtama akaanguka ksha akaushika mkono wa kushoto akauvunja.Yule jamaa akalia kwa maumivu.Akaukamata pia mkono wa kulia akauvunja Yule gaidi akaendelea kupiga kelele za maumivu. Taharuki kubwa ilitanda pale uwanja wa ndege wa Julius Nyerere baada ya taarifa kusambaa kwamba kulikuwa na bomu.Watu waliokuwa ndani ya uwanja kwa ajili ya kuwaaga marais waliondolewa haraka.Marais waliondolewa haraka sana pale uwanja wa ndege na kurejeshwa ikulu. Baada ya kumdhibiti Yule gaidi Mathew akamvua ile fulana yenye bomu akaiweka pembeni akasimama na kutoa ishara kwamba askari wasogee.Wataalamu wa mabomu kutoka jeshi la polisi wakaondoka na lile bomu. Baada ya kuikamilisha kazi yake Mathew akawaachia maafisha wa usalama waendelee na kazi yao kwa ahadi ya kwenda kituoni kutoa maelezo ya kina kuhusiana na suala lile.Mathew akampigia simu Ruby na kutaka kufahamu mahala walipo kisha akaomba kupelekwa hospitali ya Mtodora alikopelekwa Melanie.Gari la polisi lilimpeleka hadi hospitali ya Mtodora ambako aliwakuta Ruby na Jackson.Ruby alimkumbatia Mathew kwa nguvu huku akibubujikwa na machozi “We did it Mathew ! We did it ! akasema Ruby huku akimwaga machozi “We saved our president ! akasema Mathew halafu akamfuata Jackson “Jackson Ahsante sana.Tusingeweza kufika hapa bila msaada wako.Umeingia katika historia ya nchi hii kwa kufanya kitu cha kizalendo” akasema Mathew akakumbatiana na Jackson “Madaktari wanasemaje kuhusu Melanie? “Wanaendelea kumuhudumia.Bado hajapata fahamu mpaka sasa” akasema Ruby “Tutarejea hapa hospitali lakini kwa sasa wasiliana tena na Rais tukaonane naye.Anapaswa kufahamu kila kilichotokea” akasema Mathew na Ruby akampigia simu rais na simu yake ikapokelewa “Unasemaje Ruby? “Mheshimiwa Rais pole sana kwa kilichotokea leo” “Ahsante” “Mheshimiwa Rais tunahitaji kukuona” “Haitakuwa rahisi kuonana nanyi kwa sasa kutokana na itifaki za kiusalama hasa pale kunapotokea kitisho cha usalama kama kilichotokea leo” “Mheshimwia rais ni muhimu sana tukaonana nawe.Kuna mengi ambayo unapaswa kuyafahamu.Kwa ufupi tu sisi ndio tuliofanikisha kila kitu kilichotokea leo.Ni mambo mazito ambayo unapaswa kutusikiliza” akasema Ruby ukapita ukimya kidogo na Dr Fabian akakubali kuonana nao. Wote watatu wakaingia katika lile gari alilokuwa anaendesha Jackson ambalo lilikuwa na mwili wa James Kasai katika buti ya gari wakaondoka kuelekea ikulu.Njiani bado Ruby aliendelea kutiririkwa na machozi. “Ruby nini kinakuliza? “Nimetazama rekodi ile ya Melanie imenisikitisha sana.Kumbe ni binti mdogo tu lakini amegeuka akawa mkatili kiasi hiki.Nimejikuta nikimuonea huruma” akasema Ruby “Hakuna kumuonea huruma mtu ambaye anashirikiakana na magaidi.Alichokipata anastahili na ana bahati ameingia katika mikono yangu akiwa hana fahamu nilikuwa na hasira naye sana ! akasema Mathew akaichukua kompyuta ile ya Melanie na kuanza tena kusikiliza ile rekodi . “Afrika Mashariki iko salama.Njama za mabeberu zimeshindwa kufanikiwa.Mungu anaendelea kusimama na Tanzania” akasema Mathew “Kwangu mimi naona ni muujiza kumuua James Kasai ambaye ameleta hofu kubwa Afrika mashariki” akasema Ruby kwa hisia kali na kumwaga tena machozi





    Akina Mathew waliwasili ikulu ambako walinzi wake uliongezeka maradufu.Walipokewa na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mikutano midogo cha Rais “Ni mara yangu ya kwanza kufika ikulu” akasema Jackson “Utaendelea kufika hapa mara kwa mara.Huu ni mwanzo tu” akasema Mathew Dakika chache baadae mlango ukafunguliwa wakaingia walinzi wa Rais halafu akaingia Rais Dr Fabian Kelelo.Mathew na wenzake wakasimama na Rais akawataka waketi.Akawatazama kwa muda halafu akasema “Nimechelewa kufika hapa kuzungumza nanyi nilikuwa katika simu na mkuu wa jeshi la polisi nchini akinijulisha kuhusiana na matukio yaliyotokea leo jijini Dar es alaam.Nimeambiwa kwamba helkopta ya idara ya SNSA imelipuliwa leo katika bohari la idara hiyo na kumefanyika mauaji ya watu huko.Nikaambiwa tena kuna milipuko ya mabomu imetokea katika nyumba moja kwenye kijiji cha mabilionea na huko watu kadhaa wameuawa na kwa taarifa ambayo mkuu wa jeshi la polisi nchini ameipata ni kwamba mlikutwa eneo hilo na mkajieleza kuwa mnatoka SNSA na mkaeleza kuwa kuna mtu ana bomu katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na amelenga kutuua mimi na Rais Patrice Eyenga.Amenieleza kile kilichotokea uwanja wa ndege namna ulivyoweza kumdhibiti Yule gaidi.Nataka mnieleze kwa kina kila kitu kilichotokea” akasema Dr Fabian na Mathew akamueleza kila kitu namna walivyoendesha operesheni yao hadi walivyoikamilisha.Mashavu ya Dr Fabian yalionekana na michirizi ya machozi wakati Mathew akiendelea kumsimulia.Akatoa kitambaa akafuta machozi akashinda kujizuia kulia kwa kwikwi “Let him cry ! Mathew akawaambia wenzake.Dr Fabian alilia kwa takribani dakika tatu halafu akafuta machozi akavaa miwani yake “Mtanisamehe nimeshindwa kujizuia kumwaga machozi” akasema Dr Fabian “Mathew Mulumbi wewe ni halisi au ni mzimu kama wengi wanavyohisi?akauliza Dr Fabian “Mimi ni halisi mheshimiwa Rais” akajibu Mathew “Nashindwa niseme nini.Nilikudharau sana Mathew Mulumbi.Sikujua kama leo hii wewe niliyekudharau ndiye ambaye umeniokoa.Kama si wewe basi hivi sasa mimi na mwenzangu Patrice tungekwisha fariki dunia” “Ni Mungu anayepaswa kushukuriwa kwanza kwani hakutaka kukuchukua siku ya leo kwani kama ingekuwa ni kwa mipango yake hata mimi nisingeweza kukuokoa lakini vile vile kuna watu wengine nyuma yangu ambao kwa pamoja tumeshirikiana katika operesheni hii kwa niaba yao ninasema ninapokea ahsante sana” akasema Mathew na Dr Fabian akavua tena miwani akafuta machozi “Mtanisamehe vijana wangu kwa hali hii nashindwa kujizuia” “Mheshimiwa rais nadhani ungeitazama rekodi ile ya Melanie” akasema Mathew na kumsogezea Dr Fabian kompyuta ya Melanie akamchezea ile rekodi ya Melanie “Nafahamika kama Melanie Davis au Melanie Chuma lakini hilo si jina langu halisi.Jina langu halisi ni Theresia Muganza mtoto wa Laurent na Lucy Muganza kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambao waliuawa nchini Tanzania.Nilikuwa ninasoma hapa Tanzania na niliipenda sana nchi hii lakini mambo yalibadilika pale walipouawa wazazi wangu, mauaji ya kikatili sana ambayo chanzo chake ni sababu za kisiasa.Mama yangu alikuwa bilionea na hakuwahi kufikiri hata mara moja kuingia katika siasa hadi pale aliposhawishiwa na serikali ya Ufaransa agombee urais kwa manufaa yao.Rais Patrice Eyenga alipoingia madarakani alikata mirija yote ya mabeberu waliokuwa wakinyonya rasilimali za Congo na hilo halikuwapendeza mabeberu hivyo wakaanza kutafuta namna watakavyoweza kurudi tena kufaidika na rasilimali za nchi ya Congo wakamshawishi mama yangu awanie urais.Waliamini atashinda uchaguzi hivyo wakampa kazi nyingine ya kuhakikisha anaisambaratisha jumuiya ya afrika mashariki .Kwa bahati mbaya aligundulika mapema akauawa na mimi nikanusurika Nilipelekwa Ufaransa kwa matibabu na Mungu akanijalia nikapona ndipo nilipoelezwa ukweli wa kile kilichotokea kuhusu mauaji ya mama yangu.Nilipandikizwa hasira ambazo zilizaa chuki kubwa dhidi ya nchi za Tanzania Congo na Afrika mashariki kwa ujumla nikaulizwa kama niko tayari kuvaa viatu vya mama yangu nikakubali nikafanyiwa upasuaji bandia kubadili mwonekano wangu halafu nikatumwa kuja Tanzania kwa lengo la kulipiza kisasi lakini kubwa likiwa ni kuivuruga jumuiya ya afrika Mashariki.Nilibadilishwa jina nikapewa jina la Melanie Davis.Hapa Tanzania nilikutana na mtu anaiwa Edwin Mbeko ambaye ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi SNSA ambaye huyu aliwekwa maalum kwa ajili ya kuhakikisha mipango yangu yote inafanikiwa.Nilipewa jina lingine la Melanie Chuma ili wakati mwingne nijulikane kama mtanzania.Nilinunua makampuni hapa Tanzania na fedha nilipewa na serikali ya Ufaransa ambao ndio wananifadhili.Niliingia hapa nchini kama mwekezaji na mpango wangu wa kwanza ulikuwa ni kuwaua wake za marais wa Tanzania na Congo.Nilikutana na balozi wa Congo hapa nchini nikamshawishi aandae chakula maalum na kuwakaribisha wake za marais wa Congo na Rwanda na lakini kukawa na ugumu wa kumpata mke wa Rais wa Rwanda na ndipo alipomtumia mke wa Rais wa Tanzania ili kumleta mezani mke wa rais wa Rwanda.Niliandaa mpango ule nikishirikiana na James Kasai ambaye nilikwenda kuonana naye Uganda. Baada ya shambulio lile lililowaua wake za marais nikaelekezwa tena kuandaa shambulio lingine ambalo linalenga kumuua Rais Patrice Eyenga.Nilimfuata James Kasai nikaongea naye suala hili naye akanipeleka kwa Rais wa Uganda Jenerali Akiki ambaye alikubali kushirikiana nasi katika mpango huo na alitaka baada ya Patrice kuuawa James Kasai achukue nchi.Akiki alinieleza kwamba Majenerali wa jeshi la Congo walikuwa wanandaa mpango wa mapinduzi hivyo akamuita mkuu wa majeshi wa Congo akazungumza naye lakini wakashindwa kuelewana kuhusu James Kasai kushirikishwa katika serikali baada ya mapinduzi ndipo tulipoamua kuendelea na mpango wa kumuua James Kasai bila kushirikiana na wakuu wa jeshi la Congo.Tulipanga Jenerali Akiki aombe kukutana jijini Dar es salaam na marais wa Tanzania na Congo azungumze nao kuhusu kutafuta muafaka wa amani kufuatia mashambulizi yale yaliyofanywa na James Kasai jijini Dar es salaam.James aliwasiliana na IS wakamtuma mtu anaitwa Khalid Khalid ambaye ni mtaalamu wa mabomu kuja kuandaa bomu ambalo litaweza kuwaua marais wa Tanzania na Congo.Edwin Mbeko kwa kutumia idara ya SNSA aliweza kufanikiwa kuingia nchini kwa James Kasai pamoja na Khalid Khalid.Rais Akiki alimpigia simu Rais wa Tanzania akamtaka aandae mkutano naye akakubali bila kujua ni mtego.Kwa kumtumia Edwin Mbeko pia tuliweza kumuingiza nchini mtu ambaye angejitoa mhanga na kuwaua marais. Leo hii kumefanyika kikao hicho cha marais watatu na ninaamini muda si mrefu kutoka sasa AfrikaMashariki itaingia katika msiba mkubwa wa kuondokewa na marais wawili kwa wakati mmoja.Shambulio la bomu litakalotokea muda mfupi ujao na kuwaua marais wa Tanzania na Congo tumeliandaa sisi. Nimeamua kueleza ukweli huu kwani nyumba yangu kwa sasa imezingirwa na watu ambao naamini ni wapelelezi hivyo sintatoka hai ndani ya chumba hiki.Baada ya kumaliza hii rekodi nitajimaliza mwenyewe kwa risasi,siko tayari kukamatwa.Katika dakika hizi ambazo nyumba yangu imezingirwa na wapelelezi ninakiona kifo changu na ninaumia sana kwa mateso na maumivu niliyowasababishia watu ambao niliwaua ndugu zao, nimejikuta nikijutia kile nilichokifanya.Mimi ni msichana mdogo bado lakini nimeingia katika historia ya watu makatili wakubwa si kwa kupenda bali ni kwa sababu ya maslahi ya mabeberu.Ninajilaumu kwa kukubali kutumika.Nilikubali kuwa kibaraka wao na kuua waafrika wenzangu.Nimeyasema haya ili waafrika wenzangu wajifunze kwani si mimi peke yangu ninayetumiwa na mataifa makubwa ya nje.Wapo watu wengi katika taasisi za serikali na hasa viongozi wa siasa.Hawa wamekuwa wakitumiwa sana na serikali za mabeberu katika kuleta migongano ndani ya nchi zao.Machafuko mengi yanatokea katika nchi zetu za afrika chanzo chake ni wanasiasa ambao ukiwachunguza wanatumiwa na mabeberu kutuvuruga ili mabeberu hao waweze kupata mwanya wa kuingia katika nchi zetu na kuchota rasilimali.Wanafanya haya kwa malipo ya fedha ambazo zinawawezesha kuishi maisha ya kifahari kama niliyoishi mimi na kusahau kwamba nchi zetu zinaendelea kuwa masikini na kunyonywa kila uchao.Niliingia katika mtego wao nikanasa na katika dakika zangu za mwisho nimegundua kosa nililolifanya.Kama nisingekubali kutumiwa na mabeberu ningekuwa na maisha marefu na ndoto zangu nyingi zingetimia lakini nimekatisha ndoto zangu katika umri huu mdogo.Huu ni mfano kwa wale wote wenye kufanya mambo kama niliyoyafanya mimi kuwa mwisho wenu ni mbaya na yawezekana mwisho wenu ukawa mbaya kuliko wa kwangu.Usaliti kwa nchi yako ni dhambi kubwa.Ninat………………” Rekodi haikuendelea tena kukasikika kishindo na kukawa giza.Ni pale ambapo Khalid alijilipua na kipande cha mlango kikampiga Melanie kichwani “Nimekosa maneno ya kusema ! akasema Dr Fabian “Nani mwingine ambaye ameiona rekodi hii? Akauliza Dr Fabian “Hakuna mwingine zaidi yetu sisi” akajibu Mathew “Good.Rekodi hii inapaswa kufanyiwa kazi haraka sana na vyombo husika……….”akasema Dr Fabian na Mathew akamkatisha “Mheshimiwa rais sisi tumekamilisha jukumu letu la kuilinda nchi na hatua zinazofuata tunaiachia serikali.Kwa mfano kuna mtandao wa IS hapa nchini ambao unapaswa kufumuliwa nk.Kama hutajali mheshimiwa Rais ninaomba tukakukabidhi mwili wa James Kasai ili uthibitishe kwamba kweli ameuawa”akasema Mathew kisha Dr Fabian akaelekeza Rais Patrice Eyenga aitwe ili kwa pamoja wakashuhudie mwili wa James Kasai. Akina Mathew wakiongozana na marais wale wawili wakaelekea katika gari la Mathew buti likafunguliwa na mwili wa James Kasai ukaonekana.Dr Fabian na Patrice wakathibitisha kuwa ni yeye,akaelekeza liitwe gari la kubebea wagonjwa ili mwili ule ukahifadhiwe hospitali.Wakarejea ndani katika chumba cha mikutano midogo “Vijana wangu sijui nizungumze nini kwa hiki mlichokifanya.Ni kitu kikubwa sana ambacho vizazi na vizazi vinapaswa kuusoma ujasiri wenu.Hiki mlichokifanya kinapaswa kuingia katika historia ya nchi ili mkumbukwe na watoto wa watoto wenu kwamba waliwahi kutokea vijana Fulani ambao walionyesa uzalendo wa ajabu kwa nchi hii.Mathew umepambana na gaidi aliyekuwa na bomu.Ni vipi kama gaidi Yule angeweza kulipua bomu lile wakati ukimdhibiti?Hukulijali hilo lakini ulichokuwa unahitaji ni kuokoa maisha yangu.Sina neno la kusema.Sijui ni tuzo gani upewe itakayolingana na hiki ulichokifanya.Nitalihutubia taifa usiku wa leo na ningependa watanzania wafahamu kitu kikubwa mlichokifanya leo” akasema Dr Fabiana na kuwatazama akina Mathew “Mheshimiwa Rais tulichokifanya ndicho tulichoapa kukifanya.Tuliapa kuilinda nchi dhidi ya adui wa ndani na wa nje na leo tumetimiza wajibu wetu.Kwa niaba ya wenzangu tunaomba jambo hili libaki kama lilivyo na tusitambulishwe kwamba sisi ndio tuliomuua James Kasai na kuzima shambulio la kigaidi.Wewe ukitushukuru basi tunaamini watanzania wote wametushukuru hivyo basi hatutapenda kutangazwa” akasema Mathew Kikao kiliendelea hadi ilipotimu saa kumi na mbili za jioni ndipo Rais Patrice Eyenga akaondoka nchini kurejea nchini kwake jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Mwili wa James Kasai ukachukuliwa na kupelekwa hospitali kuu ya Mtodora kuhifadhiwa Mathew na wenzake wakaagana na Rais wakaondoka wakaelekea hospitali ya Mtodora kujua maendeleo ya Melanie.Walijulishwa na madaktari kwamba ubongo wa Melanie umekufa hivyo hataweza kuamka tena. Kutoka hospitali ya Mtodora wakaelekea katika nyumba walikolazwa Austin na Gosu Gosu.Hali ya Gosu Gosu iliendelea vizuri na aliweza kufumbua macho lakini wakati walipofika akina Mathew alikuwa amelala na hawakutaka kumuamsha.Walimsimulia Austin kilichotokea “Nasikitika nimekosa mengi” akasema Austin na wote wakacheka “Usijali Austin hata uwepo wako hapa hospitalini ni jambo kubwa sana kwani umeokoa maisha ya GosuGosu” akasema Mathew kisha wakamuaga Austin na kurejea nyumbani kwao.Ruby akayaganga majeraha yote aliyoyapata Mathew kisha wakapata chakula halafu wakaelekea sebuleni kutazama hotuba ya Rais “Ndugu watanzania wenzangu,napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uhai na kuendelea kusimama na nchi yetu Ndugu watanzania wenzangu siku,chache zilizopita nilisimama hapa nikiwapa taarifa za tukio baya kabisa kutokea hapa nchini ambapo watu wasio na ubinadamu wenye roho za kishetani walivamia nchi yetu na kutekeleza shambulio baya kabisa ambalo lilikatisha kikatili maisha ya wapendwa wetu. Niliposimama hapa niliwaahidi kwamba mimi na serikali yangu hatutakaa kimya kwa yeyote aliyeshiriki katika shambulio lile baya.Niliahidi kwamba tutawasaka kokote duniani wale wote waliomwaga damu ya watanzania. Shambulio lile baya kabisa lilifanywa kwa ushirikiano wa James Kasai kiongozi wa kundi la waasi ambaye anashirikiana na kundi la kigaidi la IS.James Kasai alifurushwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kugoma kushiriki katika mpango wa amani na akakimbilia nchini Uganda ambako amekuwa akiishi na kukijenga kikundi chake akifadhiliwa na serikali ya Uganda. Wakati dunia nzima ikiamini James Kasai anaishi msituni nchini Uganda lakini James Kasai amekuwa akiishi katika jiji la Kampala maisha ya kifahari sana na hili hata wananchi wengi wa Uganda hawalifahamu. Kwa kushirikiana na nchi za Rwanda na Congo tuliahidi kumsaka James Kasai kokote aliko duniani na kuhakikisha tunamtia nguvuni.Wakati mipango na mikakati yetu ikiendelea , James Kasai kwa kushirikiana na mtandao wake aliweza kuingia hapa nchini.Vijana wetu wazalendo kwa nchi yao waliokula kiapo cha kuifia nchi yao walizipata taarifa hizo za James Kasai kuja Tanzania wakamfuatilia. Ndugu watanzania wenzangu ninasimama hapa kuwajulisha kwamba James Kasai Yule muuaji aliyemwaga damu ya watanzania bila hatia ameuawa leo mchana na vijana wetu wazalendo.Si yeye peke yake bali pia washirika wake wa karibu pia wameuawa na wengine hivi sasa wanatafutwa. Ndugu watanzania vijana hawa wazalendo ambao wamefanikisha,kumuua katili huyu na genge lake wameokoa jumuiya ya Afrika mashariki kusambaratika.Ndugu zangu jambo hili ni pana zaidi ya tunavyolifikiri.Ipo nguvu kubwa kutoka mataifa makubwa ambayo inataka kutusambaratisha na kuvuruga umoja wetu lakini Mungu ameendelea kusimama na nchi yetu pamoja na jumuiya ya Afrika mashariki.Tumekwisha zifahamu nchi hizo,tumekwisha wafahamu viongozi wa nchi hizo ambao wanapanga mipango ya kutuvuruga na tutaendelea kuchukua hatua mbali mbali lakini naomba mfahamu kwamba tuko katika vita mbaya ya kiuchumi na katika vita hii tunapambana na mataifa makubwa yenye nguvu kutushinda sisi.Wanawatumia watu wetu wenyewe kutugawa na kutuvuruga .Wapo viongozi ndani ya serikali,wapo wanasiasa wapo viongozi wa dini ambao wanatumiwa na mataifa makubwa ya nje katika vita hii.Ninawaomba ndugu zangu watanzania tuipende nchi yetu.Kuisaliti nchi yako kwa fedha kidogo kutoka kwa mabeberu ni dhambi kubwa na mwisho wake ni mbaya. “Mathew my love kuna jambo nataka kuuliza” akasema Ruby wakati wakiendelea kutazama hotuba ya Rais “Uliza mpenzi” akasema Mathew “Hatimaye misheni imekwisha,James Kasai ameuawa,washirika wake pia wameuawa na wengine wa mtandao wa IS wanaendelea kutafutwa na vyombo vya usalama.Baada ya kazi hii ngumu nini kinafuata? Akauliza Ruby “Kama nilivyokueleza awali kwamba nitaondoka baada ya kukamilisha misheni hii lakini nitarejea tena kwa ajili yako.Narudia tena kukukumbusha kwamba nitakapoondoka usijaribu kunitafuta kuwa mvumilivu nitarudi” akasema Mathew BAADA YA SIKU 3 Afya ya Gosu Gosu iliimarika sana na sasa aliweza hata kuinuka na kukaa mwenyewe kitandani.Ni siku ya tatu toka alipouawa James Kasai. Saa nne za asubuhi gari la wagonjwa liliwasili katika hospitali kuu ya Mtodora kitanda cha wagonjwa kikashushwa garini na kusukumwa kuelekea katika wodi alikolazwa Melanie Davis.Pembeni yake walikuwepo Mathew na Ruby Melanie aliwekewa mashine ya kumsaidia kupumua.Gosu Gosu alipomuona sura yake ikabadilika.Mathew akawaomba watu wote watoke mle ndani akabaki Gosu Gosu akimtazama Melanie “Sikujua kumbe u shetani uliyevaa mwili wa binadamu Melanie.Nilikupenda kwa moyo wangu wote nikiamini wewe ni mwanamke ambaye umeumbwa kwa ajili yangu.Nilikuwa tayari kufanya kila ulichokitaka na kwa sababu yako nilichungulia kaburi.Ninashukuru nimekuona ukiwa katika hali hii kwani ungekuwa mzima ningekuua kifo kibaya sana” akasema Gosu Gosu kwa sauti ya chini halafu Mathew akaingia “Gosu Gosu muda umefika.Kamilisha zoezi ukapumzike” akasema Mathew na Gosu Gosu akasogezwa kitufe ili azime mashine ile ya kumsaidia Melanie kupumua. “Kwa heri Melanie” akawaza Gosu Gosu na kubonyeza kitufe kile akazima mashine ya kupumua na ukawa mwisho wa Melanie Davis.





    Ni Ruby pekee aliyefahamu kuhusu kuondoka kwa Mathew Mulumbi kwani ndiye aliyemsindikiza uwanja wa ndege akapanda ndege kuelekea Cairo Misri. “Nimemaliza misheni ya kwanza.James Kasai ameuawa na Afrika mashariki iko salama.Njama za mabeberu zimeshindwa.Ninamshukuru sana Habiba Jawad ambaye ameniwezesha kwa kiasi kikubwa kufanikisha misheni hii muhimu sana kwa nchi yangu.Ninakwenda tena katika misheni nyingine ambayo kwa mujibu wa Habiba Jawad ni kubwa kuliko hii niliyoimaliza.Mungu ataendelea kusimama nami” akawaza Mathew akiwa ndegeni

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TAMATI



    MWISHO WA SIMULIZI YA MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA.

    USIKOSE SEHEMU YA TATU NA YA MWISHO YA SIMULIZI YA SIRI IITWAYO JASUSI/GAIDI.

0 comments:

Post a Comment

Blog