Search This Blog

Thursday 17 November 2022

SIRI : MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA - 4

 






Simulizi : Siri: Maisha Na Kifo Cha Melanie Chuma

Sehemu Ya Nne (4)





Saa moja za jioni zilifika gari mbili na kumchukua Melanie na kuondoka naye.Hakujua alikuwa anapelekwa wapi lakini moyoni alikuwa akiamini yuko salama.Gari zile mbili baada ya mizunguko kadhaa ya jiji la Kampala ambalo Melanie hakuwa akiifahamu vyema hatimaye wakawasili katika jumba moja lililokuwa likiwaka taa nyingi.Hakukuwa na mlinzi yoyote nje na mara tu walipokaribia geti likafunguka wakaingia ndani.Wale jamaa waliokuwa wamevaa suti nyeusi wakashuka mmoja wao akamfungulia Melanie mlango wa gari akashuka.Kutoka ndani ya ile nyumba akatoka jamaa mmoja ambaye alikuwa amevalia suti nzuri ya rangi ya kijivu akampokea Melanie “Karibu sana Melanie akasema Yule jamaa na kumshika Melanie mkono akamsaidia kupanda ngazi kuelekea ndani ya jumba lile zuri.Walipanda ngazi kuelekea ghorofani hadi katika mlango mmoja uliokuwa na walinzi wawili wenye silaha wakafunguliwa mlango wakapita na kulifuata korido ambalo lilikuwa na walinzi kadhaa wenye bunduki.Wakaukuta tena mlango mwingine ukafunguliwa wakaingia na kujikuta ndani ya chumba kikubwa kizuri.James Kasai alikuwa ametulia sofani akivuta sigara huku mbele yake kukiwa na chupa kadhaa za pombe kali. “Melanie Davis” akasema James alipomuona Melanie akasimama wakakumbatana kisha akamuelekeza sehemu ya kukaa “Karibu sana Melanie.Nimefurahi kukuona tena japo umekuja wakati ambao nimekuwa na heka heka nyingi” akasema James “Ahsante James na samahani kwa kuja kwa wakati kama huu” “Usijali Melanie wewe ni mtu muhimu sana kwangu hivyo nimeahirisha kila kitu kwa sababu yako.Kama unavyojua baada ya tukio lile la juzi kule Dar es salaam baadhi ya nchi zimeapa kunisaka hadi wanikamate.Wengine wamediriki kufanya mashambulio katika vijiji vinavyozunguka misitu mikubwa wakiamini nimejificha humo.Nchi ya Uganda kwa sasa imeingia katika mgogoro mkubwa na majirani zake na tayari wamekwisha anza kushambuliana kwa hali hiyo basi nimeamua kuondoa vikosi vyangu kutoka Uganda na tunaelekea jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwenda kuanza rasmi mapambano na serikali ya Congo.Kwa heshima yako nimewaacha vijana wangu wakiendelea na zoezi hilo la kuhama na mimi nimekuja hapa kukutana nawe.Karibu na jisikie nyumbani” “James utanisamehe sana kwa kukuingiza katika matatizo haya makubwa”akasema Melanie “Hapana Melanie.Hujaniingiza katika matatizo yoyote bali haya ndiyo maisha yamgu na tumekwisha yazoea.Nilihitaji sana kufanya tukio kama lile ili kutuma salamu kwa Patrice Eyenga kwamba nipo na ninakuja.Karibu Melanie tufurahie kinywaji” akasema James na kumiminia Melanie kinywaji katika glasi. “Mipango inakwenda vyema kama ulivyokuwa unataka.Kama hali ikiendelea hivi ilivyo sasa basi jumuya ya Afrika Mashariki itabaki historia.Hivi sasa kuna mvurugano mkubwa sana kila nchi ndani ya jumuiya haielewani na nyingine” akasema James Kasai ambaye kama kawaida yake alikuwa amevaa fulana ya kukatwa mikono huku mabega yake yaliyojaa michoro mingi yakiwa wazi.Shingoni alivaa mikufu ya thamani kubwa.Vidole vyake vote vya mikono vilichafuliwa na pete za thamani kubwa sana “Nashukuru kwa mipango inakwenda vyema.Baada ya mpango wetu ule wa kwanza kufanikiwa nimekuja tena kwako kuomba msaada wako” akasema Melanie “Karibu” akasema James “Kama nilivyokueleza simuni jana kwamba mpango wangu unaofuata ni kumuua Rais Patrice Eyenga.Huyu na mwenzake wa Tanzania ndio waliopanga mauaji ya wazazi wangu. Sifahamu nitawezaje kulitekeleza hilo ndiyo maana nimekuja hapa kwako kuomba msaada” akasema Melanie.James akaitupa sigara aliyokuwa anaivuta katika chombo kilichokuwa mezani halafu akachukua sigara nyingine kubwa akaiwasha akavuta.Ulipita ukimya wa dakika tatu kisha akasema “Melanie Davis.Ulichokitamka ni kitu kikubwa sana ambacho sikuwahi kufikiria kama unaweza ukakitamka.Kinazidi uwezo wako” akasema na kuvuta sigara ile kubwa “Pamoja na ukubwa wake lakini nimelipokea wazo lako kwa mikono miwili kwa sababu ni kitu ambacho ninakihitaji sana japo kwa bahati mbaya hata mimi mwenyewe sifahamu nitaweza kumuua vipi Patrice.Lakini kwa kuwa tayari wazo liko mezani lazima tutafute namna ya kuweza kumuondoa Rais Patrice Eyenga.Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akatusaidia ambaye tunakwenda kuonana naye usiku wa leo.Naomba unisubiri hapa nikajiandae kwani mtu tunayekwenda kuonana naye ni mtu mzito” akasema James Kasai na kunyanyuka akaondoka.Baada ya dakika kumi akatoka akiwa amevaa suti nzuri rangi nyeusi iliyomkaa vyema “Wow ! kumbe huyu jamaa akivaa suti anapendeza sana.Ni mara ya kwanza ninamuona akiwa amevaa suti nimezoea kumuona akiwa katika mavazi yake ya kijeshi” akawaza Melanie “Melanie sasa tunaweza kuondoka”akasema James akamshika mkono Melanie wakashuka ngazi hadi nje ambako kulikuwa kumeandaliwa magari yapatayo manne yote aina ya marcedece benz rangi nyeusi wakafunguliwa milango na kuingia katika mojawapo ya gari kisha msafara ule wa magari ukaondoka. “Melanie tunakwenda kuonana na mtu mzito sana hivyo tutamueleza ukweli wote bila kumficha hata kitu kimoja kuhusu wewe” akasema James “Sawa James” akasema Melanie “Vipi maendeleo ya Gosu Gosu?akauliza James “Bado hali yake si nzuri.Tumuombee kwani lolote linaweza kutokea” akasema Melanie na safari ikaendelea.Taratibu walianza kuliacha jiji la Kampala na kufuata barabara iliyokuwa imepandwa miti pembeni.Baada ya mwendo wa dakika ishirini wakazikuta taa kandoni mwa barabara na kwa mbali kidogo ulionekana mji Fulani mdogo.Mara mwendo wa magari ukapungua walikuwa katika kizuizi,kulikuwa na wanajeshi wenye silaha zaidi ya kumi.Magari yote yakakaguliwa halafu yakaruhusiwa kupita.Baada ya dakika tano wakakuta tena kizuizi kingine na mtu aliyekuwa katika gari la mbele kabisa akashuka akazungumza na wale maafisa wa jeshi na hapo magari yakakaguliwa tena kisha yakaruhusiwa kuendelea na safari.Walikwenda kwa mwendo wa dakika kumi wakakutana na kizuizi kingine wakakaguliwa tena na kisha wanajeshi sita wakaingia katika gari na kuyaongoza magari yale wakafuata barabara ya upande wa kushoto.Walikuwa ndani ya kambi ya jeshi.Ulinzi ulikuwa mkali sana ndani ya kambi ile.Melanie aliingiwa na hofu Baada ya mwendo wa dakika kadhaa wakipita katika barabara iliyokuwa kandoni mwa kambi ile wakakuta geti lililokuwa na ulinzi mkali sana.Geti likafunguliwa magari yale yakaingia ndani.James Kasai hakuwa na hata chembe ya wasi wasi.Walielekea katika jumba moja kubwa la rangi nyeupe.Magari yakasimama na milango ya gari walimopanda James na Melanie ikafunguliwa James akamtaka Melanie washuke walikuwa wamefika safari yao.Mtu mmoja aliyevalia nguo za kijeshi aliyechafuka vyeo mabegani akampokea James na kumsalimu Melanie halafu akawaongoza kuingia ndani ya jumba lile zuri.Waliingia katika sebule nzuri na kumkuta mtu mmoja aliyevaa mavazi ya kijeshi akiwa anazungumza na simu akiwa amegeukia dirishani Yule mwanajeshi aliyewapokea akawaelekeza sehemu za kukaa.Melanie alihisi miguu yake inamuisha nguvu baada ya Yule mtu aliyekuwa akizungumza na simu kugeuka na kuwatazama.Alikuwa ni Rais wa Uganda Jenerali Akiki Rwamirama. “Rais wa Uganda !! akashangaa “Karibuni sana.James Kasai karibu”akasema Jenerali Akiki akasalimiana na James huku Melanie akiwa amesimama.Rais Akiki akamgeukia Melanie “Anaitwa Melanie Davis”James akamtambulisha Melanie kwa Rais “Melanie karibu sana.Nimefurahi kukutana nawe” akasema Jenerali Akiki “Melanie huyu ni Rais wa Uganda.Anaitwa Jenerali Akiki Busingye Rwamirama” akasema James Kasai “Karibuni sana.Nadhani kabla ya yote tukapate kwanza chakula kilichokwisha andaliwa.Uliponiambia unakuja na mgeni muhimu kwa mazungumzo niliandaa kabisa chakula kwa ajili yake” akasema Jenerali Akiki kisha akaongozana na akina James kuelekea katika chumba cha chakula akawakaribisha mezani wakapata chakula “Mama yuko wapi?akauliza James Kasai ambaye alionekana kuzungumza na Jenerali Akiki kama mtu wake wa karibu sana “Mama amesafiri amekwenda nje ya nchi kupumzika na familia hadi hapo upepo mbaya unaovuma sasa hivi utakapotulia.Unajua yanapotokea mambo kama haya yanayoendelea hivi sasa familia huwa ya kwanza kulengwa ndiyo maana nimewaondoa kuwapeleka nje kupumzika hadi pale mambo yatakapokuwa shwari basi watarejea.Vipi zoezi linakwendaje? “Zoezi linakwenda vyema na hivi tuzungumzavyo tayari kila kitu kimekwisha hamishwa na usiku wa leo vijana wanafika Congo na kuanza kujenga kambi” “Good” akasema Jenerali Akiki wakaendelea kupata chakula.Walipomaliza kula chakula Jenerali Akiki akawachukua hadi katika sehemu ya mazungumzo “Sasa tunaweza kuendelea na mazungumzo yetu.Melanie Karibu sana.Umekuwa kimya muda mrefu yawezekana ni mazingira yanakuogopesha lakini nakusihi usiogope.Hapa ni sehemu salama kabisa na ndiyo maana unaona niko hapa.Nyumba hii ni maalum kwa ajili ya Rais pale kunapokuwa na kitisho chochote cha usalama.Hali ya kiusalama kwa sasa si nzuri sana ndiyo maana nimeletwa hapa” akasema Jenerali Akiki. “Sina hofu yoyote mheshimiwa Rais baada ya kukuta Amani imetawala na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida” akasema Melanie “Uganda ni shwari tofauti na taarifa za habari za vyombo vya magharibi ambao wamekuwa wakikuza taarifa kwamba eneo zima la Afrika Mashariki halikaliki.Wewe mwenyewe umeshuhudia watu wakiendelea na maisha yao ya kila siku bila hofu yoyote na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa Tanzania.Sikatai kwamba hakuna kitisho cha amani lakini hali si kama wanavyotangaza hawa jamaa.Sisi kama nchi lazima tujihami dhidi ya kitisho chochote kutoka nchi yoyote.Kumekuwa na mfululizo wa majibizano ya risasi na mabomu kuanzia jana usiku katika mpaka wetu na Rwanda.Watu wengi hawaelewi mgogoro wetu na Rwanda haujaanza kwa sababu ya tukio la juzi bali ni wa siku nyingi lakini baada ya tukio la juzi Rwanda wamepata sababu ya kutaka kuanzisha vita nasi.Nimekwisha waonya kwamba nitaichakaza ile nchi.Nimejipa siku chache za kuona mwenendo wao na kama watakuwa bado wanataka kupigana nasi nitaipiga ile nchi vibaya mno.Ni nchi ndogo ambayo haiwezi kuniumiza kichwa changu.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo halikadhalika tumekuwa na mzozo nao wa muda mrefu na wote wanataka kuitumia nafasi hii kupigana nasi.Tanzania hatujawahi kuwa na ugomvi nao ni ndugu zetu.Ni hasira tu za Dr Fabian lakini naamini washauri wake watamshauri vyema.Naamini sisi na Tanzania katu hatutaweza kupigana ndiyo maana utaona Tanzania haijapeleka vikosi vyake vya jeshi katika mpaka wake na Uganda kwa ajili ya vita.Ninaamini hata kile kikosi cha umoja wanachokiunda Tanzania walishawishiwa na hawa marais wa Rwanda na Congo.Kwa ujumla ugomvi wetu mkubwa ni sisi na Rwanda na Congo ndiyo maana nimeamua kuwaita nyumbani mabalozi wangu na kuwafurusha mabalozi wao,sitaki mchezo” akasema Jenerali Akiki. “Tuachane na hayo.James karibu.Nieleze kile kilichotukutanisha hapa usiku wa leo” akasema Jenerali Akiki.James Kasai akarekebisha tai yake na kusema “Mheshimiwa Rais kuna jambo kubwa ambalo limenileta kwako usiku wa leo” akasema na kunyamaza kidogo “Mheshimiwa Rais nadhani unamkumbuka Lucy Muganza” akasema James “Ndiyo ninamfahamu.Lucy Muganza alikuwa ni rafiki wa familia yangu.Yeye na mke wangu walisoma pamoja hivyo walikuwa na ukaribu mkubwa.Kila nilipopata safari ya kwenda Paris Lucy na mumewe walinikaribisha katika makazi yao Paris na Lucy alinipikia chakula yeye mwenyewe kwa mikono yake.Hakutaka chakula changu kipikwe na wapishi wengine.Kwa ujumla naweza kusema Lucy alikuwa ni kama ndugu yetu.Tulishibana sana.Wiki mbili kabla ya kuuawa walikuwa na mazungumzo na mke wangu kuhusiana na kuanzisha kampuni ya kutengeneza taulo za kike hapa Uganda na alimuahidi kwamba anakwenda katika uchaguzi na pale uchaguzi utakapomalizika basi watalijadili suala hilo lakini kwa bahati mbaya alikatishwa maisha yake kikatili” akasema Jenerali Akiki “Japo hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliopatikana kuhusiana na waliomuua Lucy na mumewe lakini tunafahamu mauji yale yalipangwa na Tanzania na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Hakuna kitu cha kuficha Congo na Tanzania walipanga mauaji yale.Tunafahamu kwamba Patrice Eyenga na Dr Fabian Kelelo ndio wahusika wakuu wa mauaji yale” akanyamaza kidogo na kuwasha sigara halafu akaendelea “Nakumbuka tulimaliza mkutano wa kawaida wa jumuiya ya Afrika mashariki na Rais Fabian akachukua uenyekiti na katika mkutano huo tuliikaribisha rasmi jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kama mwanachama mpya.Kikao kilipomalizika Rais Patrice na Dr Fabian walikuwa na mazungumzo marefu ya siri na wiki moja baadae Lucy akauawa nchini Tanzania.Patrice alikuwa na wasiwasi kama angegombea na Lucy lazima angeshindwa uchaguzi ndiyo maana akapanga njama za kumuua.Ni ukweli ulio wazi kwamba kama Lucy angeshiriki katika uchaguzi ule angeshinda kwa namna anavyokubalika nchini Congo.Kama Lucy angeshinda uchaguzi mashirikiano yetu yangekuwa makubwa sana na niliahidi kumpa ushirikiano mkubwa sana katika uongozi wake.Kwa bahati mbaya mambo hayakuwa kama yalivyokusudiwa.Kuna wakati naichukia sana siasa.Kama isingekuwa siasa basi hivi sasa Lucy angekuwa mzima kabisa” akasema Jenerali Akiki na kuvuta sigara “Mheshimiwa Rais” akasema James “Aliyeko mbele yako,Melanie Davis ni binti wa Lucy na Laurent Muganza ambaye jina lake halisi ni Theresia Muganza” akasema James.Nusura sigara aliyoshika Jenerali Akiki imponyoke kwa mstuko alioupata.Akamtazama Melanie kwa mshangao mkubwa “Huyu ndiye Theresa Muganza mtoto wa Lucy? Akauliza Jenerali Akiki “Ndiyo mheshimiwa Rais” akasema James “Hapana si yeye.Nimekuwa karibu na familia ya Muganza ninawafahamu wote ninamfahamu Theresia Muganza na hata picha zao ninazo lakini huyu hafanani kabisa na Theresia ! akasema Jenerali Akiki huku akiendelea kumtazama Melanie.James akamfanyioa ishara Melanie aendelee “Nakumbuka mama alinipigia simu jioni iliyotangulia siku ya kuuawa kwake akaniambia kwamba kesho yake watakuja Dar es salaam kunichukua tunakwenda wote Kinshasa kwa ajili ya sherehe za mama kutambulishwa kama mgombea uchaguzi kupitia chama cha upinzani cha CDP.Nilikataa kwenda Kinshasa nikamweleza mama kwamba wao waende peke yao kwani nilikuwa najiandaa kwa mitihani,lakini alisisitiza kwamba lazima twende wote kama familia.Kesho yake alitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere nikawapokea.Walihitaji kupumzika kidogo Dar es salaam kabla ya kuelekea Kinshasa hivyo tukaondoka uwanja wa ndege kuelekea katika nyumba niliyokuwa ninaishi.Tukiwa njiani ndipo lilipotokea lile shambulio.” Akanyamaza kidogo na kutazama chini.Baada ya muda akaendelea “Baba na mama wote walifariki pale pale kwa risasi na mimi nikapigwa risasi ya kifua nikakimbizwa hospitali nikafanyiwa upasuaji na baadae nikahamishiwa Paris kwa matibabu zaidi. Mazishi ya wazazi wangu niliyashuhudia kupitia runinga.Nilitibiwa kwa siri hadi nilipopata nafuu.Siku moja alikuja kunitembelea Rais wa Ufaransa Michael Weren na ndipo akanieleza kila kitu kuhusiana na chanzo cha kuuawa wazazi wangu” Melanie akanyamaza tena kidogo halafu akamtazama Rais Akiki na kuendelea “Rais Michael Weren alinieleza mambo mengi namna rasilimali za Congo zinavyochotwa na watu wachache.Alinieleza kwamba walihitaji mtu ambaye angeweza kusimamia rasilimali za Congo ziwanufaishe watu wa Congo na ndipo wakamshawishi mama yangu aweze kugombea urais kupitia chama cha CDP na akakubali kwa bahati mbaya hakufikia malengo yake akauawa.Nilielezwa mambo mengi na mwisho Rais Michael akanitaka nivae viatu vya mama yaani niyaendeleze yale ambayo mama alitakiwa kuyakamilisha akimaanisha kuikomboa nchi yangu ya Congo kutoka katika makucha ya wanyonyaji.Nilikuwa na hasira na watu waliomuua mama hivyo nikakubali na ndipo ulipoanza mkakati wa kuniandaa.Jambo la kwanza nililofanyiwa lilikuwa ni kubadili mwonekano wangu.Ililetwa timu ya madaktari bingwa wa upasuaji wa plastiki wakanifanyia upasuaji mwonekano wangu ukabadilika na kuwa hivi ninavyoonekana sasa.Baada ya hapo nikatumwa Afrika Mashariki kwa ajili ya kuja kuendelea na kazi ambayo mama alitakiwa kuifanya yaani kuikomboa Congo kutoka katika makucha ya wanyonyaji” akasema Melanie na Jenerali Akiki akawasha sigara nyingine akavuta “Kwa hiyo mheshimiwa Rais mimi ndiye Theresa Muganza mtoto wa Lucy na Laurent Muganza” akasema Melanie “Nimekuelewa Melanie.Huna haja ya kuelezea zaidi” akasema Jenerali Akiki na kuvuta mkupuo mkubwa wa sigara akapuliza moshi “Lini hawa jamaa watatuacha huru? Miaka mingi wametutawala wametufanyia kila aina ya udhalilishaji tumekuwa watumwa wao,wametuchapa viboko,wamechukua kila aina ya mali waliyotaka lakini bado hata kidogo tulichobaki nacho wanakitaka.Nina hasira sana na haya mataifa ya magharibi” akasema na kupuliza moshi “Sikujua kama Ufaransa ndio waliomshawishi Theresia Muganza kuingia katika siasa kwa maslahi yao huku wakimdanganya kwamba anakwenda kuikomboa Congo.Kwa miaka nenda miaka rudi nchi hizi kubwa wamekuwa wakifadhili makundi ya waasi ambao wamekuwa wakipigana vita isiyokwisha kwa maslahi yao wenyewe.Wote tunalitambua hilo.Hata wakongomani wanalitambua hilo ndiyo maana mimi niliamua kumuunga mkono James Kasai ambaye hakuwa chini ya nchi yoyote ya Ulaya na mapambano yake yalikuwa ni kuikomboa Congo kutoka katika makucha ya mabeberu.Alikuwa akipambana kwa maslahi ya kweli ya wakongomani.Huyu ndiye pekee ambaye anaweza akairejesha Congo katika mikono ya wakongomani na wakafaidika na rasilimali zao lakini wengine wote wanaodai kutaka kuikomboa Congo ni vibaraka wa mataifa makubwa.Mabeberu hao wamemshtaki James katika mahakama ya uhalifu wa kivita na hivi sasa anatafutwa lakini nimeapa kumpigania James hadi mwisho kwani amejitolea kupambana kuikomboa Congo.Kwa nini Lucy alikubali kudanganywa na hawa watu? Akauliza Jenerali Akiki “Kama haitoshi bado wanataka kumtumia tena na mwanae.Melanie hawa watu wamekuingiza katika hatari kubwa sana kwa ajili ya maslahi yao wenyewe ! akafoka Jenerali Akiki “Ninafahamu mheshimiwa Rais” akasema Melanie na Jenerali Akiki akavua kofia akaiweka mezani na kumtazama Melanie kwa macho makali “Mheshimiwa Rais” akasema Melanie “Ninafahamu wanachokitaka hawa watu ambao wamenituma kuja huku.Wanadai kwamba ninachokifanya ni kwa ajili ya kuikomboa Congo wakati kumbe kuna mambo wanayatafuta.Ninafahamu mheshimiwa Rais kwamba wanataka kunitumia kwa maslahi yao na waliponituma nilikubali kwa kuwa nilikuwa tayari na mipango yangu mingine” “Mipango ipi uliyo nayo Melanie?akauliza Jenerali Akiki “Mpango wa kwanza ni kulipiza kisasi kwa wale wote waliohusika katika vifo vya wazazi wangu na ndiyo maana nilimfuata James Kasai anisaidie katika mpango wangu wa kulipiza kisasi.Nilianza kwanza na wake za marais Dr Fabian na Patrice Eyenga” akasema Melanie “Ulifanya vizuri sana Melanie na sikulaumu kwa ulichokifanya.Kitendo walichokifanya wale jamaa ni kibaya sana na hakikubaliki na wanastahili adhabu kali.Ninakuunga mkono kwa ulichokifanya japo kimezua mtafaruku mkubwa lakini jambo kubwa ni kwamba hawa wakatili lazima nao wapate mateso makali” akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais” akasema James “Baada ya kile kilichotokea Dar es salaam,Melanie alinipigia simu akaniambia kwamba anataka kuingia katika awamu ya pili ya mpango wake akaniambia kwamba safari hii anataka kumuua Patrice Eyenga” akanyamaza baada ya sura ya Jenerali Akiki kuonyesha mstuko kidogo “Kumuua Patrice Eyenga?akauliza Jenerali Akiki “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ninataka kumuua Patrice Eyenga na nikitoka hapo nitahamia Tanzania nataka kumuua pia Dr Fabian Kelelo.Hawa ndio waliowaua wazazi wangu na katika mpango wangu lazima nao niwaondoe” akasema Melanie “Aliponieleza jambo hilo” James akaendelea “Nilishindwa kumpa jibu la moja kwa moja nikamtaka aje Kampala tuzungumze kwani hata mimi jambo hili liko juu ya uwezo wangu.Kwa hiyo mheshimiwa Rais tumekuja hapa kwako kwa suala hilo.Melanie anataka Patrice Eyenga auawe” akasema James Kasai na Jenerali Akiki akainuka akaenda dirishani akafunua pazia akachungulia nje halafu akaenda kuegemea meza.Akainamisha kichwa akatafakari kisha akasema “Melanie kwanza kabisa ninashukuru sana kukutana nawe.Nilikuwa najiuliza sana mahala alipo Theresa Muganza na hatimaye umenifikia.Ninashukuru sana James kwa kumleta mwanangu huyu.Kwa ukaribu niliokuwa nao na wazazi wako wewe ni sawa na mwanangu”akasema Jenerali Akiki “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Melanie “Naomba nikuhAkikishie kwamba ninakuunga mkono kwa mpango wako wa kulipiza kisasi kwa wale wote waliofanya unyama mkubwa wa kuwaua wazazi wako.Hata hivyo mpango wa kumuua Patrice Eyenga huu ni mpango mkubwa sana na hauwezi ukatekelezeka kwa haraka kama unavyodhani.Kumuua Rais wa nchi hata kama ni ndogo si mpango mdogo.Ni jambo zito na gumu sana hasa kwa nyakati hizi ambapo ulinzi kwa marais wengi umekuwa mkali mno.Kwa miaka ya zamani ilikuwa rahisi kidogo na ndiyo maana marais wengi waliuawa lakini kwa miaka ya sasa marais ni watu wanaolindwa mno.Nadra sana kusikia Rais wa nchi Fulani ameuawa zama hizi” akasema Jenerali Akiki na kunyamaza kwa muda “Hata hivyo mpango huu wa kumuondoa Patrice Eyenga si mbaya.Ni mpango mzuri kwani huyu naye amekuwa ni kibaraka wa baadhi ya mataifa ya makubwa.Alisaidiwa na Marekani kuingia madarakani na alipoingia tu ikulu akayafukuza makampuni mengine yote makubwa kutoka mataifa ya Ulaya yaliyokuwa yamewekeza katika sekta ya madini na sasa sekta ya madini nchini Cogo inashikwa na makampuni ya kimarekani.Japokuwa hakuna vita nchini Congo kwa sasa lakini bado sehemu kubwa ya mali inazidi kuchotwa na wageni hawa kufuatia mikataba mibovu inayowapa nafasi wawekezaji wa kimarekani kufaidika na rasilimali za Congo kuliko wazawa hivyo bado nchi ya Congo haijampata mtu yule ambaye atakuwa mzalendo wa kweli na atahAkikisha rasilimali zote ambazo Mungu amewapa wakongo zinawanufaisha kuliko kwenda kuyanufaisha mataifa makubwa ya kigeni” akanyamaza tena akafikiri kidogo halafu akasema “Mtu pekee ambaye ninaamini ana uchungu na nchi ya Congo na ambaye anaweza akasimamia rasilimali za Congo ili ziwanufaishe wananchi wa Congo ni James Kasai.Sina mashaka naye hata kidogo kwani ninafahamu harakati zake toka enzi za baba yake ambaye aliuawa na vikosi vya serikali ya Congo” akanyamaza akamtazama Melanie na kusema “Melanie mimi niko tayari kuungana nanyi katika mpango huu endapo tutakubaliana kwamba baada ya mauaji hayo James Kasai ndiye atakayechukua nafasi ya Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” akasema Jenerali Akiki na James Kasai akatabasamu “Mheshimiwa Rais mimi ninachokihitaji ni kuwamaliza wale wote ambao waliwaua wazazi wangu.Hata hivyo kifo cha Patrice Eyenga ni kitu ambacho mataifa ya Ulaya hasa Ufaransa watakifurahia sana kwani kitawapa nafasi ya kuweza kurejea tena nchini Congo” “Usihofu Melanie.Hakuna nchi ambayo itasogeza pua yake Congo.James Kasai akichukua urais wa Congo atawafurusha wawekezaji wote na mali zote za Congo zitamilikiwa na wazawa.Kupitia madini hayo watoto watasoma shule bure,huduma za afya zitaboreka ujenzi wa miundo mbinu utafanyika na mambo mengine mengi” “Mheshimiwa Rais jambo hili ndilo ambalo nimekuwa nikilipigania kwa miaka mingi hivyo nadhani ni wakati sasa umefika wa kuibadili historia ya Congo” akasema James Kasai “Nakubaliana nawe James.Wakati umefika wa kufanya ukombozi wa kweli kwa nchi ya Congo.Mimi nitashirikiana nanyi katika mpango huo hata hivyo tambueni kwamba mpango huu utatugharimu fedha nyingi mno kuutekeleza” akasema Jenerali Akiki “Kuhusu pesa mimi nitagharamia mheshimiwa Rais.Kiasi chochote kitakachohitajika mimi nitatoa” akasema Melanie na Jenerali Akiki akamtazama “Niachieni suala hili nilifanyie kazi halafu nitawaita na kuwapa mrejesho.Nitazungumza kwanza na mkuu wa majeshi wa Congo ambaye nina undugu naye.Nitamdokeza suala hili kisha tutajadiliana namna tutakavyoweza kumuondoa Patrice Eyenga.Hatuwezi kutekeleza mpango huu sisi wenyewe bila kushirikiana na watu wa ndani ya serikali ya Congo” akasema Jenerali Akiki Kikao kilimalizika saa saba za usiku kwa jenerali Akiki kulibeba suala lile na kuwaahidi kuwapa mrejesho siku inayofuata.Melanie na James Kasai wakaondoka katika makazi yale ya Rais yaliyomo ndani ya kambi ya jeshi. DAR ES SALAAM – TANZANIA Nahodha wa meli kubwa ya mizigo alitoa maelekezo na meli ile ikasimama.Ilikaribia sana kufika katika bandari ya Dar es salaam. “Annabel sasa umefika.Hatuwezi kwenda nawe hadi bandarini.Vijana wangu watakupeleka hadi ufukweni kisha baada ya hapo utajua mwenyewe utakavyoendelea”akasema Nahodha wa meli ile ambayo Ruby alisafiri nayo kutokea bandari ya Le havre nchini Ufaransa.Wafanyakazi wengine wote wa meli ile walikusanyika pamoja kwa ajili ya kumuaga Ruby ambaye kwa kwa muda wote wa safari alikuwa ni kama mwenzao.Walimzoea sana kwani alikuwa ni mwanamke pekee melini hivyo walihAkikisha wanamtunza kwa kila namna ili aweze kufika salama Tanzania “Kaka zangu sina neno zuri la kuwashukuru kwa wema wenu mkubwa na ukarimu wa ajabu sana mlionifanyia.Ahsanteni sana kwa kila kitu.Nimefurahi mno kuwa nanyi kwa muda huu wote wa safari hadi kufika hapa.Nimefurahi kuwafahamu na katika maisha yangu sintaweza kuwasahau kamwe.Ninyi nyote mtakuwa ndani ya moyo wangu hadi siku ninaingia kaburini” akasema Ruby na makofi yakapigwa. “Naomba niwashukuru kwa ujumla wenu kwani nikisema nimshukuru mmoja mmoja muda haunitoshi hivyo naombeni mpokee sana shukrani zangu za dhati kabisa.Nitaendelea kuwaombea ili msafiri salama kurejea nyumbani na tutazidi kuwasiliana.Mtakapokuja tena Tanzania aidha mmoja mmoja kwa matembezi au kikazi kama hivi msiache kunitafuta na nitakuwa mwenyeji wenu” akasema Ruby na kuwakumbatia kuwaaga mmoja mmoja halafu akasindikizwa na nahodha hadi katika boti ile ndogo ambayo ilikuwa na watu wanne ikashushwa majini kisha ikawashwa na kuondoka kuelekea ufukweni. Walimfikisha Ruby ufukweni wakaagana na kuondoka akaanza kutembea taratibu.Hakujua alikuwa sehemu gani kwani jiji la Dar es slaam hakulifahamu vyema.Aliiona kwa mbali barabara na magari yakipita akaanza kuelekea huko.Wakati akitembea mara akakutana na vijana waliokuwa wamekaa kikundi jumla yao wakiwa sita.Wote wakatimua mbio walipomuona akacheka kwa namna walivyotimua mbio “Wamestuka kuniona hapa usiku huu.Wanadhani mimi ni mzimu” akawaza Ruby huku akiendelea kupiga hatua.Alikuwa na begi lake la mgongoni na pochi ndogo ambayo alikuwa ameweka fedha na vifaa vingine vidogo vidogo.Suruali yake alikuwa ameikunja hadi magotini akavaa fulana ndefu ambayo iliificha bastora aliyokuwa ameichomeka katika suruali. “Dar es salaam jiji lisilolala.Nikifika barabarani nitajua nielekee wapi” akawaza Ruby huku akiongeza hatua kuelekea barabarani. Hatimaye baada ya kutembea kwa dakika kadhaa akaifikia barabara.Magari yalikuwa mengi barabarani akatembea barabara akiwa hana wasiwasi wowote wa kukutana na vibaka kwani alikuwa na bastora kiunoni.Alivuka barabara na kuingia upande wa pili akatembea hadi katika mtaa mmoja akamkuta mlinzi anayelinda duka akamuuliza mahala anakoweza kupata teksi akamuelekeza na Ruby akafuata maelekezo ya Yule mzee akajikuta ametokea katika klabu moja ya usiku.Kulikuwa na magari mengi yameegeshwa na watu wengine walikuwa wamekaa nje kulikokuwa na sehemu nzuri za kukaa wakipata kinywajihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/.Ruby akamfuata mlinzi mmoja aliyekuwa amevaa sare zenye rangi nyekundu na nyeusi akiwa na rungu akamsalimu na kumuuliza mahala anakoweza kupata taksi.Mlinzi yule akamuelekeza mahala zinakoegeshwa taksi Madereva taksi walimchangamkia sana walipomuona,Ruby akachagua gari moja zuri akamtaka dereva ampeleke katika hoteli nzuri isiyo ya ghali sana lakini yenye usalama wa kutosha. “Umetokea wapi dada?akauliza Yule dereva taksi ambaye alionekana kulifahamu vyema jiji “Hapa hapa Dar”akajibu Ruby kwa ufupi akionekana kutotaka mazungumzo yoyote na yule dereva “Dar es salaam ni kubwa.Sehemu gani ya Dar unatokea? Akauliza Yule dereva na Ruby akakasirika “Stop asking questions.Drive ! akasema Ruby kwa sauti kali kidogo “Samahani dada.Ni kawaida yetu sisi madereva kuwachangamkia wageni” akasema Yule dereva na safari ikaendelea kimya kimya Dereva taksi akafungua droo ya gari na kumpatia Ruby vipeperushi sita vya mahoteli mbali mbali “Huwa tunatembea na vipererushi hivi kwa ajili ya wateja wetu hasa wanaotoka nje ya Dar es salaam au nje ya nchi.Tazama kama kuna hoteli itakayokupendeza kati ya hizo” akasema Yule dereva na Ruby akachukua vile vipeperushi akavipitia “Nipeleke Hotel Marcelino” akasema Ruby Mazungumzo yalikuwa machache sana garini hadi walipofika hoteli Marcellino “Hapa ni sehemu nzuri na salama naamini patakufaa” akasema yule dereva huku akiegesha gari maegesho.Ruby akafungua ule mkoba wake mdogo akampa Yule dereva dola kadhaa za kimarekani kama nauli kwani hakuwa na fedha ya Tanzania.Yule dereva akatoa tabasamu kubwa sana “Sister kama utahitaji dereva mwaminifu anayeifahamu kila sehemu ya jiji usiache kunitafuta” akasema Yule dereva na kumpatia Ruby kadi yake ya biashara.Wakaagana na Ruby akaingia ndani ya hoteli akapokewa vizuri sana na wahudumu wachangamfu na kuchukua chumba kizuri kilichokuwa ghorofa ya sita.Alikodisha chumba kwa muda wa siku mbili na kulipa kwa kutumia dola za kimarekani “Ahsante Mungu umenifikisha salama Tanzania.Haikuwa safari rahisi lakini umenisimamia toka mwanzo hadi sasa.Naamini una kusudi na mimi ndiyo maana ukaniepusha na mitego yote iliyotegwa ili nife.Ee baba nimerudi nyumbani,nimekuja kuitumikia nchi yangu.Nakuomba uniongoze niweze kuitumikia nchi yangu kwa kila uwezo ulionijalia”Ruby akaomba mara tu baada ya kuingia chumbani. “Sasa nimeingia Dar es salaam.Mtu wa kwanza kumtafuta ni Rais Dr Fabian ambaye natakiwa kumjulisha kwamba tayari nimefika.Ningefurahi sana kama kipenzi changu Mathew Mulumbi angekuwepo furaha yangu ingekamilika.Hata hivyo kwa kuwa tayari nimefika salama Dar es salaam nitatafuta ukweli juu ya kifo chake.Lazima nijue alikufaje na kama ikiwezekana kujua alizikwa wapi na kupata masalia yake.Lakini kuna kitu ndani ya nafsi yangu kinakataa kabisa kuamini kuhusu kifo cha Mathew.Kwa vile tayari niko hapa nitaujua ukweli kwa sasa nishughulikie kwanza mawasiliano na Rais” akawaza Ruby na kuingia bafuni kuoga kisha akakaa sofani akaishika kompyuta yake akataka kuiwasha akasita “Ngoja nisiiwashe kwanza wale jamaa kule Uingereza wanaweza wakaiona kwani bado ilikuwa imeunganishwa na mtandao wao.Kuna vitu natakiwa kuvifanya lakini hadi pale nitakapokuwa na kompyuta nyingine pembeni” akawaza Ruby na kuchukua kitabu chake cha kumbu kumbu akazitafuta namba za simu za Rais Dr Fabian akapiga simu mapokezi na kuomba huduma ya simu binafsi.Baada ya dakika chache akapigiwa simu na kujulishwa kwamba anaweza akapiga namba yoyote ya simu anayoitaka.Akampigia Dr Fabian.Simu ikaita na kupokelewa. “Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Ruby aliitambua mara moja ni ya Dr Fabian “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Nazungumza na nani?Dr Fabian akauliza “Unazungumza na Ruby” “Ruby? “Ndiyo.Ruby Rafael Magalla” “Oh my God ! Ruby.Uko wapi? Akauliza Dr Fabian “Tayari nimeingia Dar es salaam usiku huu” “Thank you Lord” akasema Dr Fabian na kushusha pumzi “Uko salama kabisa? “Ndiyo mzee niko salama kabisa” akajibu Ruby “Ruby nashukuru sana umefika salama.Mimi kwa sasa siko Dar es salaam niko Mbeya.Nadhani ulipata taarifa za tukio lililotokea juzi” “Tukio gani mheshimiwa Rais? “Hujapata taarifa za tukio lililotokea juzi? “Hapana mzee.Sikuwa nafuatilia habari zozote nilijiweka nje kabisa ya dunia” “Kuna tukio limetokea hivi majuzi hapo Dar es salaam na watu kadhaa walifariki akiwamo mke wangu.Kesho tutamzika Tukuyu Mbeya kisha nitarejea Dar es salaam.Nitakuja kuzungumza nawe mara nitakaporejea” “Pole sana mheshimiwa Rais” “Ahsante sana.Nataka kufahamu mahala ulipofikia” akasema Dr Fabian na Ruby akamfahamisha hoteli alikofikia chumba na jina analotumia la Annabel. “Dakika chache zijazo watakuja wasaidizi wangu hapo hotelini watakuchukua na kukupeleka sehemu salama.Wewe ni mtu muhimu sana.Jiandae muda si mrefu watakuja kukuchukua” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” “Ahsante sana Ruby kwa kujitahidi hadi umeweza kufika salama.Nilikuwa na wasiwasi mkubwa kama ungeweza kufika salama.Kesho tutazungumza kwa kirefu zaidi nitakaporejea” akasema Dr Fabiana na kuagana na Ruby “Ahsante Mungu kwa kuendelea kuninyooshea mambo yangu.Huyu ndiye hasa niliyetakiwa kuwasiliana naye kabla ya yote na kumfahamisha kwamba niko Dar es salaam.Amesema kuna tukio limetokea hivi majuzi ni tukio gani hilo hadi mke wake akafariki dunia? Nitajua hiyo kesho tutakapoonana.Natamani kuwasilianana Gosu Gosu kumjulisha kwamba niko Dar es salaam lakini ngoja kwanza nisubiri atafahamu hapo baadae nitakapokuwa nimetulia” akawaza Ruby huku akipakia vitu katika begi lake Dakika kumi na tano zilipita toka alipozungumza na Rais mlango wa chumba chake ukagongwa.Akaishika bastora yake halafu akasogea taratibu mlangoni na kuufungua kwa tahadhari kubwa.Kulikuwa na watu wapatao wanne “Annabel?akauliza mmoja wa wale jamaa “Ndiyo” “Tumepewa maagizo na mzee tuje tukuchukue.Mizigo yako iko wapi?akauliza Yule jamaa huku akiingia mle chumbani mwa Ruby “Sina mizigo zaidi ya hili begi dogo”akasema Ruby na mmoja wa wale jamaa akalibeba begi lile wakatoka hadi mapokezi ambako Ruby alirudisha chumba na kuongozana na wale jamaa hadi nje ambako kulikuwa na magari matatu ya rangi nyeusi. Ruby alipelekwa hadi katika nyumba moja nzuri sana na kukaribishwa katika chumba kikubwa na kizuri. “Hapa sasa naweza kulala usingizi mzuri.Sina hofu yoyote”akawaza Ruby akiwa kitandani RIYADH – SAUDI ARABIA Kumepambazua tena jijini Riyadh.Saa mbili za asubuhi tayari Mathew Mulumbi alikwisha wasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mfalme Khalid jijini Riyadh.Alikuwa ameongozana na mkewe Najma ambaye waliagana na Mathew akaenda kukamilisha taratibu halafu akaenda sehemu ya kusubiria ndege.Muda ulipofika waliingia ndegeni na safari ikaanza kuelekea Cairo Misri Ilikuwa ni safari ya saa mbili kutoka Riyadh hadi Cairo Misri.Kutokea pale Mathew alitakiwa kuondoka na ndege ya shirika la ndege la Misri kuelekea Tanzania ambayo ilikuwa inaondoka Cairo saa kumi za jioni. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ni kama vile Ruby alifumba macho na kufumbua akajikuta tayari imekwisha fika asubuhi.Akatoka kitandani na kwenda kufunua pazia akatazama nje.Kulikuwa na madhari ya kuvutia mno.kulikuwa na uwanja mkubwa uliokuwa na nyasi nzuri za kijani.Kulikuwa pia na bwawa kubwa la kuogelea “Hapa ni wapi? Ni hoteli au ni wapi?Mbona pazuri namna hii?Nyumba nzuri,mandhari safi,ulinzi wa kutosha.Namshukuru sana Rais kwa kunileta hapa.Nimelala usingizi mzuri sana leo nikiwa na uhakika niko salama” Ruby akageuka baada ya mlio wa simu kusikika akaenda mezani akaichukua na kupokea “Hallow” akasema “Ruby habari yako”akasema mtu wa upande wa pili na Ruby akaitambua sauti “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Umeamkaje Ruby? “Nimeamka salama kabisa” “Nafurahi kusikia hivyo.Nimekupigia kujua maendeleo yako.Unahudumiwa vizuri? “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ninahudumiwa vyema” “Sawa Ruby endelea kupumzika nitarejea jioni tutaonana.Kama kuna sehemu yoyote unataka kwenda wasaidizi wangu hapo watakupeleka.Kuwa huru jisikie nyumbani” akasema Dr Fabian “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Rais akakata simu “Sasa baada ya kuwa na uhakika kuwa niko salama natakiwa kuanza maandalizi.Mua wote niliokaa ndani ya meli safarini kuja huku nilisahau kabisa kuupendezesha mwi…” akatolewa mawazoni baada ya kengele ya mlango kulia akaenda kuufungua akakutana na mwanamama mmoja mnene. “Shikamoo mama” akasema Ruby “Marahaba mwanangu hujambo? “Sijambo.Karibu mama” “Ahsante.Naitwa mama Adelina.Mimi ndiye muangalizi mkuu wa nyumba hii.Sikuwepo jana usiku ulipofika nilikuwa Mbeya msibani lakini alfajiri ya leo Rais amenirejesha Dar es salaam kwa helkopta ili nije nihAkikishe unapata huduma nzuri.Karibu sana jisikie nyumbani”akasema Yule mama na Ruby akatabasamu “Nashukuru sana mama” akasema Ruby kisha wakazungumza kidogo na mama Adelina akamuacha Ruby ajiandae.Alipojiandaa alikuta gari liko tayari linamsubiri akaondoka kwenda kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali hasa nguo na vipodozi UGANDA Saa kumi na moja za jioni helkopta iliyombeba mkuu wa majeshi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo iliwasili katika kambi ya muda iliyowekwa na vikosi vya Congo katika mpaka wake na Uganda.Wanajeshi hawakuwa na taarifa zozote za mkuu wa majeshi kuwatembelea kule mpakani. Helkopta aina ya UH – 60 Black Hawk ya jeshi la anga la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ilitua katika kambi ya muda.Mlango ukafunguliwa akashuka Jenerali Jean Paul Mutombo mkuu wa majeshi ya Congo.Alipokewa na mkuu wa kikosi kile kilichopiga kambi mpakani kisha akamuongoza hadi katika ofisi ya muda ambako akapewa taarifa fupi ya maendeleo ya kambi toka walipofika. Kisha akazungushwa katika kambi ile akaikagua halafu akazungumza na wanajeshi akawataka wawe tayari muda wowote kupambana na adui yeyote atakayetishia amani na utulivu wa nchi yao. Baada ya kuzungumza na wanajeshi na kuwapa moyo Jenerali Mutombo akaagana na maafisa wa jeshi akaingia katika helkopta,akawapa maelekezo marubani waelekee upande wa Uganda.Marubani wale walitii amri kisha helkopta ikapaa na kuondoka pale kambini.Ndani ya helkopta alikuwepo Jenerali Mutombo,mlinzi wake na marubani wawili.Jenerali Mutombo aliwapa maelekezo marubani wake sehemu ya kuelekea na baada ya dakika arobaini wakawasili katika uwanja mkubwa uliokuwa katikati ya msitu.Pembeni ya uwanja ule kulikuwa na helkopta moja na wanajeshi kadhaa wakiwa wameizunguka kuilinda.Helkopta ya Paul Mutombo ikatua ikatua katika uwanja ule,akashuka na kupokewa na jamaa wawili waliovaa suti nzuri,wakasalimiana kwa furaha wakionekana ni watu wanaofahamiana sana.Jenerali akawataka mlinzi wake na wale marubani wamsubiri akaelekea ndani ya nyumba nzuri ya rangi nyeupe.Aliingia ndani hadi katika sebule nzuri ambako alimkuta Rais wa Uganda Jenerali Akiki.Wakasalimiana kwa furaha kisha akamkaribisha katika chumba kingine kwa ajili ya mazungumzo “Jenerali Mutombo ahsante sana kwa kufika” akasema Jenerali Akiki “Nisingeweza kukataa mwito wako mheshimiwa Rais.Nimetoka kukagua vikosi vilivyoko mpakani ndipo nikaja hapa” akasema Jenerali Mutombo “Vipi maendeleo ya vijana? “Vijana wanaendelea vizuri,wako tayari kukuchakaza” akasema Jenerali Mutombo na wote wakaangua kicheko kikubwa sana “Uganda na Congo hatuwezi kupigana hata siku moja.Najua wengi hasa nchi za magharibi wanasubiri sana jambo hilo litokee lakini nakuhAkikishia katu hatutapigana.Imekuwa ni kawaida yetu kutunishiana misuli ila hatutaweza kupigana” akasema Jenerali Akiki “Ni kweli mheshimiwa Rais kupigana ni kitu ambacho hakiwezi kutokea lakini hata hivyo Yule jamaa James Kasai alifanya jambo baya kabisa kumuua mke wa Rais Patrice ndiyo maana amekasirika na kusogeza majeshi mpakani.Asingefanya vile haya yote yasingetokea” akasema Jenerali Mutombo “Umeongea jambo zuri na hapo ndipo sehemu nzuri ya kuanzia mazungumzo yetu Jenerali Mutombo” akasema Jenerali Akiki na kubonyeza kitufe chini ya meza na sekunde chache mlango ukafunguliwa akaingia mmoja wa walinzi wake na kupiga saluti “Mvinyo tafadhali” akasema Jenerali Akiki na chupa tatu za mvinyo zikaletwa haraka sana akamkaribisha Jenerali Mutombo “Mvinyo safi wa Uganda huu.Siku hizi hatuagizi mvinyo toka nje tunatengeneza mvinyo hapahapa Uganda” akasema Rais Akiki “Ni hatua nzuri.Ni mvinyo safi kabisa” “Sasa tuendelee na mazungumzo yetu” akasema Jenerali Akiki na kunywa funda la mvinyo “Uligusia kuhusu kile alichokifanya James Kasai.Nakubaliana nawe kwamba hakufanya jambo zuri na amesababisha hali ya amani kuchafuka katika eneo lote la Afrika Mashariki hata hivyo kuna jambo fulani ambalo nataka kukufahamisha” akasema Jenerali Akiki na kunyamaza kidogo kisha akaendelea “Unakumbuka miezi michache iliyopita aliuawa Lucy na mumewe Laurent Muganza nchini Tanzania” “Ndiyo nakumbuka mheshimiwa rais” akasema Jenerali Mutombo “Mpaka sasa hakuna ripoti yoyote inayoeleweka kuhusiana na mauaji yale.Serikali ya Tanzania inadaiwa kwamba waliotekeleza mauaji yale walikuwa ni majambazi na wote waliuawa lakini ukweli hauko hivyo.Mauaji yale yalipangwa.Patrice Eyenga na Dr Fabian Kelelo ndio waliopanga mauaji yale na walimuua Lucy kwa hofu ya Patrice kushindwa katika uchaguzi kama angegombea na Lucy ambaye alikuwa anakubalika sana nchini Congo” akasema Jenerali Akiki “Wengi tulihisi hivyo mauaji yale yalikuwa ya kisiasa” akasema Jenerali Mutombo “Ndiyo.Walijitahidi kujipanga vizuri ili Lucy auawe nchini Tanzania na serikali ya Congo isihusishwe katika mauaji yale.Wauaji walipewa maelekezo ya kuiteketeza familia nzima lakini kwa bahati mbaya mtoto wa Lucy aitwaye Theresa Muganza alinusurika” “Tulielezwa hivyo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba hadi sasa hakuna anayejua Theresa yuko wapi na hali yake inaendeleaje.Tuna wasiwasi naye atakuwa ameuawa kimya kimya” akasema Jenerali Mutombo.Rais Akiki akanywa mvinyo kidogo na kusema “Theresa Muganza yuko hai,amerejea Afrika mashariki na amekuja hapa Uganda kuonana nami.Amekuja kulipiza kisasi kwa wale wote walioshiriki katika mauaji ya wazazi wake.Amekuja na nguvu kubwa na kile kilichotokea juzi nchini Tanzania yeye ndiye yuko nyuma yake” “Theresa ndiye aliyefanya tukio lile? Anashirikiana na James Kasai? akauliza Jenerali Mutombo “Theresa Muganza ndiye aliye nyuma ya tukio lile na mengi yatakayofuata.Amekuja kulipiza kisasi kama nilivyokwambia.Ameanza na wake za marais Patrice Eyenga na Dr Fabian na sasa amekuja na mpango mkubwa zaidi” Jenerali Akiki akanyamaza na kumtazama Jenerali Mutombo “Amekuja na mpango upi?akauliza “Anataka kumuua Patrice Eyenga.Nimekuita hapa ili tujadili suala hili” akasema Jenerali Akiki.Mutombo akamtazama kwa muda halafu akashusha pumzi “Tafadhali niambie unachokizungumza hapa ni utani” “Si utani Mutombo ni ukweli mtupu na ninamaanisha.Niko upande wa Theresa na ninataka kumsaidia kumuua Patrice Eyenga.Alifanya ukatili mkubwa sana kumuua Lucy” Ulipita tena muda kidogo halafu Jenerali Mutombo akasema “Hivi sasa Congo hawajui kama nimekuja hapa kukutana nawe ni siri yangu na walinzi wangu.Endapo itajulikana nitaonekana msaliti kwa taifa.Nimekuja hapa kwa kuwa ninakuheshimu sana mheshimiwa.UKiacha mahusiano yetu ya kindugu ,umekuwa mwalimu wangu kijeshi na nimefika hapa nilipofika kwa sababu yako lakini pamoja na hayo sikutegemea kama umeniita hapa kunieleza ujinga kama huu” akasema Jenerali Mutombo huku akisimama “Tafadhali jenerali Mutombo kaa unisikilize kile ninachotaka kukueleza.Nipe dakika kumi tu kisha utaondoka”akasema Jenerali Akiki na Mutombo akaketi.Rais Akiki akachomoa mkebe na kutoa sigara moja kubwa akaiwasha na kuchukua nyingine. “Cigar ?akasema na kumrushia Jenerali Mutombo kisha wote wakavuta sigara kidogo halafu Rais Akiki akasema “Jenerali Mutombo naomba ufahamu kwamba maafisa wengi wa jeshi la Congo wamepita katika jeshi la Uganda na nimewafundisha mimi hivyo ninafahamu kila kinachoendelea ndani ya jeshi lenu.Ninafahamu wewe na maafisa kadhaa mmeandaa mpango wenu wa mapinduzi mnataka kumuondoa Rais Patrice madarakani na sababu kuu ya kutaka kufanya mapinduzi ni kutokana na kuikomesha biashara ya silaha ambayo iliwanufaisha sana wewe na maafisa wengine wa jeshi.Mlikuwa mkiwauzia silaha makundi ya waasi lakini kwa sasa hakuna tena biashara hiyo kwa sababu hakuna uasi.Ninafahamu kuna nchi moja kubwa ambayo inatengeneza silaha na ndiyo inafadhili mpango wenu wa kumuua Patrice Eyenga ili machafuko yatokee na muendelee na biashara ya kuuza silaha.Ni mengi ninayafahamu lakini sitaki kuyasema hapa kwa sababu ya muda.Nikosoe kama ninasema uongo” akasema Jenerali Akiki na Mutombo hakujibu kitu. “Ukimya huo unaonyesha kwamba ninachokisema ni cha kweli” akasema Jenerali Akiki na kuvuta sigara yake kubwa “Jenerali Mutombo nimekuita hapa kukujulisha kwamba ninataka kuungana nanyi katika mpango wenu wa kumuua Patrice Eyenga” akasema Jenerali Akiki na ukimya ukapita huku sigara zikiendelea kutoa moshi “Mheshimiwa Rais ni kweli tunao mpango huo wa mapinduzi lakini wewe kwa nini unataka kujiunga nasi? Akauliza Mutombo “Lucy Muganza alikuwa rafiki yangu na nimekasirishwa sana na kitendo alichokifanya Patrice Eyenga cha kumuua.Yule ni mtu mkatili sana na amekwisha waua watu wengi kimya kimya hasa mahasimu wake kisiasa.Hatuwezi kumuacha huyu mtu aendelee kuua watu kimya kimya.Unadhani akifahamu kuhusu mpango wenu wa mapinduzi mtabaki salama?Hakuna atakayebaki salama nyote mtauawa lakini kama mtashirikiana nami endapo kutatokea chochote basi mtakuwa na sehemu ya kukimbilia.Nitawapa hifadhi nchini Uganda.Paul ni wakati sasa wa kuleta mabadiliko ya kweli nchini Congo.Ni wakati wa wakongomani kunufaika na mali zao.Hilo litawezekana pale tu Rais Patrice Eyenga atakapoondolewa madarakani” akasema Rais Akiki halafu akaiweka sigara yake katika kisahani cha kuwekea majivu “Paul nchi za nje zimekwisha nufaika vya kutosha na nchi ya Congo.Ni wakati wa kusema hapana.Ni wakati wa kuendesha mapambano kwa manufaa ya wakongo.Wakati wa kutangulizwa na mataifa ya nje kumwaga damu ya wakongo umekwisha.Msikubali tena kuwa vibaraka wa mataifa ya kigeni” “Umesema Theresia Muganza amekuja kulipiza kisasi nani wanaompa nguvu ya kuweza kufanya haya yote?akauliza Paul Mutombo “Theresia anaungwa mkono na Ufaransa na ndio waliomuwezesha hadi akafika hapa alipofika”akajibu Jenerali Akiki “Kama anaungwa mkono na Ufaransa kwa nini basi akamtumia James Kasai kutekeleza shambulio lile la Dar es salaam?Akauliza Jenerali Mutombo “Ufaransa hawataki kujulikana kama wanahusika na kile kitakachotokea Congo ndiyo maana wanataka kuwatumia waafrika wenyewe ili hata pale mambo yatakapoharibika wao wasihusishwe na lolote hivyo basi wao wanamuwezesha Theresia kifedha ili aweze kutengeneza mtandao wa kumuwezesha kufanikisha mipango yao.Katika harakati zake za kutafuta namna ya kulipiza kisasi Theresa alijikuta akifika kwa James Kasai na ndiye aliyemsaidia kutekeleza shambulio lile la Dar es salaam” “Mheshimiwa Rais,Theresia anatakiwa akae mbali kabisa na James Kasai.Hana sifa nzuri na anatafutwa kila kona.Kama haitoshi tayari amegeuza kundi lake kuwa la kigaidi.Anashirikiana na magaidi wa IS.Huyu mtu hafai hata kidogo kuungwa mkono na…” “Jeneral Mutombo” akasema Rais Akiki na kumkatisha Mutombo “Katika mpango wa mapinduzi James Kasai naye anapaswa kushiriki” akasema Akiki na Mutombo akamtazama kwa macho makali “Mheshimiwa Rais hilo ni jambo lisilowezekana.James Kasai hawezi kushirikiana nasi!” “Baada ya kumuondoa Patrice Eyenga James Kasai anatakiwa apate nafasi ndani ya serikali mpya itakayoundwa tena nafasi ya juu ya uongozi.Hilo ni jambo moja ambalo lazima tukubaliane”akasema Jenerali Akiki na kumfanya Jenerali Mutombo kuangua kicheko kikubwa halafu akasimama “Ahsante mheshimiwa rais kwa kunipotezea muda wangu.Nahitaji kurejea Congo” akasema Mutombo “Jenerali Mutombo kaa chini tafadhali tuendelee na mazungumzo ! akasema Rais Akiki “Ahsante kwa mvinyo safi mheshimiwa rais” akasema Jenerali Mutombo na kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni “Fikiria kuhusu familia yako Jenerali Mutombo ! akasema Rais Akiki na Jenerali Mutombo akasimama akageuka na kumfuata Akiki “Usijaribu kucheza na familia yangu Jenerali Akiki.Kabla hujafikiria yangu hebu fikiria kwanza familia yako uliyoipeleka mafichoni nje ya nchi ! akasema Jenerali Mutombo na Akiki akatabasamu “Kaa chini tuendelee na maongezi yetu” akasema Akiki na Mutombo akaketi “Tafadhali naomba iwe mwanzo na mwisho kuihusisha familia yangu katika jambo hili.Ukithubutu kuigusa familia yangu na wewe ya kwako hakuna atakayesalimika ! akasma Paul Mutombo “Tusifike huko Jenerali Mutombo.Tuko hapa kujadili jambo lenye maslahi makubwa kwa nchi ya Congo” “Mheshimiwa Rais umenistua uliposema kwamba James Kasai anatakiwa kupatiwa nafasi ndani ya serikali itakayoundwa baada ya mapinduzi kufanyika”akasema Paul “Sikiliza Paul.Ushiriki wa James Kasai katika suala hili ni muhimu sana.Yeye ndiye atakayemuua Rais Patrice Eyenga.Jeshi la Congo halitahusishwa katika lawama yoyote ya kumuua Patrice Eyenga.Mzigo wote ataubeba James Kasai na mara tu itakapotangazwa kwamba Rais Patrice amefariki jeshi litatangaza kushika nchi” akasema Jenerali Akiki “Mpaka hapo kidogo ninakuelewana na mpango huo ni mzuri lakini tatizo liko hapo kwa James Kasai.Japo tunaweza kumtumia katika mpangowetu lakini si mtumzuri kushirikiana naye na hapaswi kupewa nafasi ndani ya serikali kwa sababu ndiye atajulikana na dunia nzima kuwa amemuua Rais Patrice.Tutakuwa ni watu wa ajabu sana kama tutampa madaraka mtu aliyemuua Rais.Mtu huyu tayari anajulikana ni gaidi na kwa namna yoyote ile hapaswi kushika nafasi yoyote ya madaraka” akasema Jenerali Mutombo na kumtazama Rais Akiki “Fikiria wewe mwenyewe mheshimiwa Rais jambo hili.Tutachekwa na hata ndege wa angani kumpa James madaraka yoyote ndani ya serikali mtu ambaye dunia nzima inamjua ni gaidi na amekwisha fanya ukatili mkubwa sana” “Unalolisema Jenerali Mutombo ni jambo la kweli.James Kasai ameharibu sana kushirikiana na magaidi wa IS.Juhudi zote alizozifanya kwa miaka mingi kupambana kwa maslahi ya Congo zimeharibiwa na kitendo chake cha kujiunga na magaidi wa IS.Hata hivyo tunamuhitaji katika mpango huu na kama akishirikiana nasi hatuwezi kumuacha hivi hivi lazima naye afaidike na mapinduzi hayo” akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais nashauri kila mmoja akatafakari zaidi jambo hili na tuwe tena na kikao kingine ambacho kitatupa mwangaza zaidi.Umekuwa ni mwanzo mzuri.Naomba tukutane tena baada ya siku tatu tuendelee na mjadala huu” akasema Jenerali Mutombo “Sawa Jenerali Mutombo nakubaliana nawe Tukutane tena baada ya muda huo.Tafadhali tujitahidi kulitafakari kwa kina suala hili ili tutakapokutana tuweze kuzungumza lugha moja halafu tuanze mchakato rasmi” akasema Jenerali Akiki na kuagana na Jenerali Mutombo akaondoka “Jenerali Mutombo yuko sahihi kuhusu James Kasai.Ni ukweli ulio wazi aliharibu sana harakati zake pale alipojiunga na kikundi cha kigaidi cha IS.Sifa yake ilibadilika kutoka mpambanaji hadi gaidi.Haitawezekana kumpa madaraka ndani ya serikali pale yatakapofanyika mapinduzi.Nitazungumza naye na kumfahamisha kwamba suala la urais halitawezekana tena” akawaza Jenerali Akiki - MELANIE DAVIS AMEANZA MIPANGO YA KUMUUA RAIS PATRICE EYENGA KATIKA HARAKATI ZAKE ZA KULIPA KISASI KWA WALE WALIOUA WAZAZI WAKE JE MPANGO HUU UTAFANIKIWA? - RUBY TAYARI AMEWASILI DAR ES SALAAM SALAMA KWA AJILI YA KUONGOZA IDARA YA SIRI YA USALAMA WA NDANI WA NCHI KAMA ALIVYOOMBWA NA RAIS - MATHEW MULUMBI YUKO NJIANI AKIELEKEA TANZANIA KATIKA MISHENI YA KUMUUA JAMES KASAI JE ATAFANIKIWA? - MPENZI MSOMAJI USIKOSE SEHEMU IJAYO





Kengele ya mlango wa chumba cha Melanie Davis ililia akainuka na kwenda mlangoni akakutana na jamaa wawili waliovalia suti nzuri wakamtaka ajiandae kwani Rais anahitaji kuonana naye usiku ule “Nadhani Jenerali Akiki anataka kunipa mrejesho kuhusiana na lile suala tuliloliwasilisha kwake jana kwani aliahidi kutupa mrejesho leo” akawaza Melanie wakati akijiandaa.Alivaa haraka haraka suti ya rangi ya kijivu akachukua mkoba wake na kuongozana na wale jamaa hadi katika gari wakaondoka “Natamani sana kujua maendeleo ya Gosu Gosu lakini siwezi kumpigia Austin kwani sitaki ajue kama niko Uganda.Sitaki afahamu mambo yangu.Ngoja nikamsikilize kwanza Rais nijue kuna nini anataka unieleza halafu nitajua kama ntarejea nyumbani kesho au nitaendelea kubaki hapa hapa Kampala” akawaza Melanie akiwa garini “Kuna wazo limenijia mchana wa leo na sijui lilitoka wapi lakini ni wazo ambalo naona kama lina msingi.Ninampenda sana Gosu Gosu na nimeumizwa na kitendo cha kupigwa risasi lakini ni vipi kama Gosu Gosu atazinduka na kisha akamueleza Austin kwamba nilikuwa nimemtuma kwenda Paris kuua mtu? Austin lazima atakuwa na wasiwasi nami na wanaweza wakaanza kunichunguza na kama hilo likitokea kuna uwezekano wakanifahamu mimi ni nani.Sitakiwi kuliruhusu hilo litokee lazima niwe mwepesi sana katika kuchukua tahadhari mapema kabla mambo hayajaharibika.Hapa kuna kitu kimoja tu ambacho kinatakiwa kifanyike nacho ni kumuua Gosu Gosu” akawaza Melanie na kufumba macho “Oh my God ! akajikuta ametamka kwa sauti na wale jamaa aliokuwa nao garini nao wakastuka “Madam are you okay?akauliza mmoja wao “I’m okay” akajibu Melanie “Kila ninapowaza na kufikia katika sehemu ya kumuua Gosu Gosu mwili wote unanisisimka.Ni mtu ambaye nilitaka kumtumia kwa kazi mbali mbali za uuaji lakini ndani ya moyo wangu ninajihisi kumpenda pia hasa kwa mambo anayonifanyia na kinachonifurahisha zaidi ni kwamba yuko tayari kufanya kitu chochote kwa ajili yangu kwa sababu ananipenda sana.Nikimuua mwanaume Yule nitaweza kweli kumpata mwingine wa aina yake? Akajiuliza Melanie “Ngoja kwanza niliache jambo hili nijielekeze katika jambo la msingi la kumuua Rais Patrice Eyenga.Kwa namna yoyote ile lazima Patrice auawe.Niliwaahidi wazazi wangu hivyo kwamba wale wote waliowakatili uhai wao lazima nao waondoke duniani hivyo lazima niitimize ahadi hii kwa kutumia njia yoyote ile.Sintawatendea haki wazazi wangu kama nitashindwa kuwaua watu hawa Patrice na mwenzake Dr Fabian wakati uwezo wa kufanya hivyo ninao.Ufaransa na washirika wake wamenipa uwezo mkubwa wa kuweza kulipa kisasi kwa wabaya wangu wote kwa malipo ya kuivuruga Afrika Mashariki na kuwatengenezea njia ya kurejea kuinyonya nchi ya Congo.Kwa hivi sasa wanafurahia sana hiki kinachoendelea Afrika Mashariki laini laiti wangeifahamu mipango yangu katu wasingethubutu kunituma kuja Afrika mashariki.Ngoja niendelee kuwafurahisha huku nikiendelea kutimiza ahadi yangu ya kulipa kisasi na nitakapomaliza hawataamini macho yao kwa kile nitakachowafanyia”akaendelea kuwaza huku gari likienda katika mwendo mkali Waliwasili katika makazi ya rais ndani ya kambi kubwa ya jeshi nje kidogo ya jiji la kampala.Melanie akashuka garini na kukaribishwa ndani “Melanie Davis ! akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais” akasema Melanie na kusalimiana na Rais Akiki “Karibu sana Melanie.Samahani kwa kukusumbua usiku huu” akasema Jenerali Akiki “Bila samahani mheshimiwa Rais.Nimefurahi sana kuja hapa kuonana nawe” “Ahsante Melanie” akasema Jenerali Akiki “Vipi siku yako imekwendaje?akauliza Jenerali Akiki “Siku yangu imekwenda vyema mheshimiwa Rais.Nashukuru ninahudumiwa vizuri ninajiona kama nipo nyumbani” akasema Melanie na Jenerali Akiki akatabasamu “Afrika Mashariki ni ndugu moja.Ukiwa katika nchi yoyote ndani ya jumuiya hii unajihisi uko nyumbani” akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais kwa hiki kinachoendelea sasa hivi ndani ya jumuiya hii hudhani kwamba inakwenda kusambaratika?akauliza Melanie.Jenerali Akiki hakujibu akachukua mkebe uliokuwa mezani akaufungua na kutoa sigara moja kubwa akawasha na kuvuta “Melanie hutajali twende tukakae nje? akauliza “Sawa mheshimiwa Rais” akasema Melanie kisha wakatoka na kwenda kuketi katika kibaraza wakiyatazama kwa mbali kidogo mataa ya kambi ile kubwa ya kijeshi “Usihofu Melani sehemu hii ni salama sana” akasema Jenereali Akiki “Sina hofu mheshimiwa Rais ninapokuwa nawe naamini ulinzi uliopo ni mkubwa” akajibuMelanie “Uliniuliza kuhusu hofu ya kusambaratika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki” akasema Jenerali Akiki “Ndiyo mheshimiwa Rais.Kuna kila dalili kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki inakwenda kusambaratika.Uganda na Rwanda hazielewani,Uganda na Congo hazielewani,Tanzania na Uganda zina mgogoro,unadhani kwa mgogoro huu uliopo jumuiya hii itaendelea kuwa hai? Akauliza Melanie “Ni kweli kuna hatari kubwa kuhusu kusambaratika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki.Yote haya ni matokeo ya mipango ya mabeberu.Wanataka kutugawanya,wanataka kuendelea kututawala na kutunyonya ndiyo maana mambo kama haya yanatokea. Melanie mabeberu hawa wanakutumia katika mipango yao,wanatumia kigezo cha kulipiza kisasi lakini kumbe wana mipango yao.Pale Rais Patrice Eyenga atakapokuwa ameuawa basi utakuwa umewatengenezea njia ya kupita kuelekea Congo ndiyo maana ninataka James Kasai ashike madaraka ya Congo kwani Yule ndiye kiboko yao.Hakuna beberu atapeleka pua yake Congo kama James atakuwa madarakani. ” akasema Jenerali Akiki. “Ninafahamu mheshimiwa Rais kwamba ninatumiwa na mabeberu katika kufanikisha mipango yao lakini sina namna lazima kwanza nihakikishe nimelipa kisasi kwani viongozi hawa walimuua mama yangu kikatili sana” akasema Melanie “Usijilaumu Melanie.Usiwaze kuhusu jumuiya kuvunjika.Wewe unachotakiwa kujielekeza ni katika mpango wako wa kulipa kisasi kwa wale wote walioondoa uhai wa wazazi wako na kukuacha yatima.Hiki kinachotokea sasa ni matokeo ya uovu wao na hakuna wa kukulaumu” akasema Jenerali Akiki na kunyamaza akaendelea kuvuta sigara yake “Melanie narudia tena kukusisitiza kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki ivunjike au isivunjike lakini lazima wale wote waliotoa uhai wa wazazi wako kikatili walipe uovu wao na gharama ya kile walichokifanya ndiyo hii hivyo usirudi nyuma.Songa mbele na mimi niko nyuma yako ninakuunga mkono kwa kila hatua unayochukua hadi pale utakapohakikisha kwamba wote wameuawa.Naamini pale mtu wa mwisho atakapouawa basi kila nchi itakuwa imebaki peke yake hakutakuwa tena na jumuiya.Unanisikia vizuri Melanie?akauliza Jenerali Akiki “Ninakusikia mheshimiwa Rais” “Vizuri.Fahamu hauko tena peke yako katika mpango huu tuko pamoja” akasema Akiki “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” Zilipita dakika mbili za ukimya na Rais Akiki akasema “Jioni ya leo nimetoka kuzungumza na Jenerali Jean Paul Mutombo mkuu wa mejeshi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” akasema Jenerali Akiki na kunyamaza kama kawaida yake ya kuzungumza kwa vituo “Labda kwa kukupa tu taarifa nina undugu na Jenerali Mutombo na vile vile amewahi kupata mafunzo katika jeshi la Uganda hivyo basi ni mwanafunzi wangu na nilipomuita aliitika mara moja akaja japo nchi zetu ziko katika mgogoro hivi sasa” akanyamaza tena kwa muda halafu akasema “Kikubwa nilichomuitia ni kuhusu ule mpango wako wa kumuua Rais Patrice Eyenga.Kama nilivyowaeleza jana kwamba hatutaweza kumuua Patrice Eyenga bila kuwashirikisha watu wa ndani ya nchi yake na watu wa karibu yake ndiyo maana nikaanzakwa kuzungumza na mkuu wa majeshi” akasema Jenerali Akiki na kunyamaza “Kwa nini nimetaka kuzungumza kwanza na mkuu wa majeshi?akauliza Jenerali Akiki “Kuna mpango wa mapinduzi unaandaliwa na viongozi wa juu wa jeshi la Congo.Wanataka kuiangusha serikali ya Patrice Eyenga” “Jeshi linataka kufanya mapinduzi?akauliza Melanie “Ndiyo Melanie.Makamanda wa juu wa jeshi la Congo wana andaa mpango kabambe wa mapinduzi wanataka kumuondoa Rais Patrice madarakani.Machafuko yaliyokuwepo nchini Congo yaliwanufaisha sana makamanda hawa wakuu wa jeshi kwani walikuwa wakifanya bishara ya kuwauzia silaha waasi na kujipatia fedha nyingi na madini kutoka kwao lakini kwa sasa baada ya Patrice Eyenga kumaliza uasi hawana tena chanzo cha mapato hivyo wanataka kumuondoa Patrice madarakani ili kurejesha uasi na waendelee kujipatia fedha.Ninaufahamu mpango huo na nilimuita Jenerali Paul kumtaka tushirikiane naye katika mpango huo wa kumuondoa madarakani Patrice Eyenga.Kikubwa nilichokuwa nakitaka tuelewane naye ni kumuweka James Kasai madarakani baada ya mapinduzi hayo kufanyika lakini mambo yamekuwa magumu kidogo” akasema Jenerali Akiki na sura ya Melanie ikaonyesha hofu “Amekataa kushirikiana nawe?akauliza Melanie “Hapana hajakataa lakini ugumu unakuja kuhusu James Kasai.Hawako tayari kumpa James Kasai madaraka yoyote yale baada ya mapinduzi kufanyika kutokana na sifa yake mbaya.Sababu alizozitoa Paul hata mimi nimezielewa.Kwa ufupi ni kwamba James Kasai ameharibu sana sifa yake baada ya kuanzisha mashirikiano na kikundi cha kigaidi cha IS.Kwa sasa kila mtu anamjua kama Gaidi na si mpiganaji kwa maslahi ya Congo”akanyamaza tena kidogo halafu akaendelea “Melanie italazimu kuendelea na mpango wetu wa kumuua Patrice Eyenga bila ya kumshirikisha James Kasai” akasema Jenerali Akiki “Unamuondoa James Kasai katika mpango huu? Melanie akauliza “Ndiyo.Wakuu wale wa jeshi la Congo hawataki kushirikiana naye katika mpango wa mapinduzi.James Kasai ni mtu ambaye amekwisha fanya mauaji ya watu wengi nchini Congo na hata nchi jirani na kwa sasa anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kutokana na uhalifu mkubwa uliofanywa na kikundi chake cha waasi anachokiongoza.Kama utakumbuka jana nilimuahidi James kwamba nataka awe Rais wa Congo baada ya mapinduzi lakini hilo halitawezekana tena.Itabidi tumuweke James pembeni.Hatafurahi lakini hakuna namna lazima tumuondoe katika mpango huu.Wale wakuu wa jeshi hawako tayari kushirikiana naye katika mpango wowote wa mapinduzi” akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais wewe mwenyewe umekuwa ukisema mara kwa mara kwamba ni James Kasai pekee ambaye anapambana kwa maslahi ya Congo ni wakati wa kulithibitisha hilo kwa kumsaidia aweze kuingia madarakani .Umekiri wewe mwenyewe kwamba ulikubali kumsaidia James Kasai katika harakati zake kwa kuwa uliamini ndiye pekee anayefaa kuiongoza Congo.Tembea katika kauli yako hiyo” akasema Melanie “Melanie nilichokisema kina ukweli.James hakufadhiliwa na nchi yoyote kubwa kutoka nje ya bAra ya Afrika.Mimi ndiye niliyekuwa mfadhili wake mkuu kwa kila kitu kuanzia fedha za kujikimu askari wake hadi silaha lakini lazima niwe muwazi kwamba James Kasai ameharibu sifa yake baada ya kujiunga na kundi la kigaidi la IS.Hata raia wa Congo hawatakuwa tayari kumuunga mkono au kuongozwa na mtu mwenye sifa ya kushirikiana na magaidi” akasema Jenerali Akiki “James hakuwafuata IS bali wao ndio waliomfuata na alikuwa katika shida kubwa ya fedha na silaha ndiyo maana akakubali kushirikiana nao.Alihitaji kujenga jeshi lake liwe imara ili akapambane na jeshi la serikali ya Congo.Haikuwa rahisi kukataa kushirikiana na IS ambao walimuahidi fedha nyingi na silaha za kisasa.Mheshimiwa Rais kwa namna yoyote ile lazima James Kasai ashiriki katika mpango huu wa mapinduzi na kisha aingie nchini Congo kushika madaraka.Hao wakuu wa jeshi la Congo lazima watakuwa wanaandaa mpango huo kwa kushirikiana na nchi za nje ambao ni wazalishaji wakubwa wa silaha hivyo hatutakuwa tumeisaidia Congo badala yae tutakuwa tumerejesha tena matatizo na hicho ndicho Ufaransa wamenituma kuja kukifanya na mimi sitaki kuirejesha Congo katika machafuko baadaya kumuua Patrice Eyenga” akasema Melanie “Melanie utake usitake lazima machafuko yatatokea tu baada ya Patrice kuuawa.Majenerali wale lengo lao kubwa ni kuanzisha machafuko ili wapate sehemu ya kuuzia silaha.Melanie kuna mambo ambayo hatuwezi kuyalazimisha.Ninaomba unielewe” Akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais ninakuelewa sana lakini bado naendelea kusisitiza kwamba hatuwezi kuendelea na mpango huu bila ya kumshirikisha James” akasema Melanie “Melanie shida yako ni Patrice Eyenga auawe.Hata bila ya James Kasai Patrice atauawa” “Mheshimiwa Rais kwa namna yoyote ile lazima James ashirikishwe” akasisitiza Melanie “Kwa nini unasistiza sana ushiriki wa James Kasai?akauliza Jenerali Akiki “Kwa sababu ninamuamini anaweza akafanya vile ninavyotaka.Siwezi kuwaamini jenerali hao wa jeshi ambao yawezekana mpango wao ukashindwa kufanikiwa au wanaweza wakafanya mapinduzi bila kumuua Rais Patrice lakini James Kasai kama atashiriki atahakikisha Patrice anauawa” “Melanie usihofu bado majadiliano na mkuu wa majeshi wa Congo yataendelea hivyo suala hilo la kuhakikisha Patrice Eyenga anauawa litazingatiwa”akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais sifahamu mazungumzo hayo yatachukua muda gani na mimi sina muda mrefu wa kusubiri.Nahitaji jambo hili lifanyike haraka kwani nina mambo mengi ya kukamilisha hivyo nashauri tuendelee na mpango wetu wa kumuua Patrice Eyenga bila kushirikiana na jeshi la nchi hiyo” akasema Melanie na Jenerali Akiki akawasha sigara nyingine. “Melanie una mpango wowote kichwani mwako ambao unadhani tunaweza kuutekeleza bila kulihusisha jeshi la Congo?akauliza Jenerali Akiki. “Ndiyo ninao mpango mheshimiwa Rais” akasema Melanie “Nieleze tafadhali” “Hivi sasa nchi yako na Congo hazina maelewano mazuri.Nataka kuitumia fursa hiyo.Utampigia simu Rais wa Tanzania na kumueleza kwamba unataka kukutana na kufanya mazungumzo naye pamoja na Rais wa Congo mazungumzo yanayolenga kutafuta amani katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na mazungumzo hayo yafanyike nchini Tanzania.Naamini Rais wa Tanzania atakubali jambo hilo na atamualika Rais Patrice kuhudhuria mazungumzo hayo.Kikubwa utakachowaeleza utakaputna nao ni kwamba uko tayari kutoa taarifa za mahala alipo James Kasai.Wakati mazungumzo hayo yakifanyika litapandikizwa bomu ndani ya ndege ya Rais Patrice na atakapoondoka akiwa angani bomu hilo litalipuliwa na utakuwa ndio mwisho wa Patrice Eyenga” akasema Melanie na Jenerali Akiki akamkazia macho huku akipuliza moshi mwingi. “Mpango huo”Melanie akaendelea “Hautawahusisha watu kutoka ndani ya serikali ya Congo lakini naamini majenerali hao wa jeshi ambao wanaandaa mpango wa mapinduzi pindi watakaposikia kwamba Patrice Eyenga ameuawa basi watatangaza jeshi kushika nchi na hiyo ni fursa nyingine kwa James Kasai kuanzisha mapambano na jeshi la serikali na huku wewe ukimuunga mkono na hiyo ndiyo fursa yako kama unataka James Kasai aiongoze Congo” akasema Melanie.Baada ya kutafakari kwa muda Jenerali Akiki akasema “Melanie mpango huo si mbaya.Ni mpango mzuri lakini ni wa hatari kubwa sana na utekelezaji wake unaweza kuwa mgumu mno” akasema Jenerali Akiki “Mheshimiwa Rais mpango huu japo unasema ni mgumu lakini ndio hasa mpango ambao mimi nauona ni rahisi na utakaotusaidia kumuua Patrice Eyenga kwa haraka” “Ugumu ninaouzungumza mimi ni namna ya kuliingiza hilo bomu ndani ya ndege.Kuhusu kuwaita marais hilo halina ugmu ninaweza nikajishusha na nikaomba kukutana nao lakini je hilo bomu litaingizwa vipi ndani ya ndege? Ni vipi kama likagundulika mapema na mpango ukashindwa kufanikiwa?Sote tutakuwa katika hatari kubwa”akasema Jenerali Akiki “Usihofu mheshimiwa Rais.Ninao mtandao mkubwa na nina uhakika suala la kuingiza bomu katika ndege ya Rais halitakuwa tatizo.Ninachohitaji ni wewe kukubali kujishusha na kuitisha kikao na marais hao wa Tanzania na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo”akasema Melanie “Hata kama mpango huo utafanikiwa na Patrice Eyenga akauawa lazima lawama zote zitaiangukia serikali ya Uganda.Lazima dunia nzima itaamini sisi ndio tuliomuua na huo utakuwa ni mgogoro mwingine unaoweza kusababisha hata vita kati ya Congo na Uganda ndiyo maana nilitaka kuwatumia watu wa ndani ya Congo ili hata kama ni vita basi iwe ni baina yao wenyewe sisi tusihusishwe na lolote” akasema Jenerali Akiki “Pamoja na faida zake lakini mpango huo utachukua muda mrefu.Majadiliano hatujui yatachukua muda gani hadi kufikia makubaliano na mimi nataka jambo hili liende haraka haraka kwani bado nina mambo mengi ya kufanya.Naomba mheshimiwa Rais kama kweli una nia ya dhati ya kunisaidia kubaliana na mpango wangu huu nilioupendekeza” akasema Melanie na ukimya ukatawala mahala pale.Baada ya dakika kadhaa za tafakari Jenerali Akiki akasema “Melanie endapo nitakubali kufanya haya yote unayoyataka niyafanye nini yatakuwa malipo yangu? Nataka kujua namna nitakavyofaidika kupitia mpango huo. Wewe utakuwa umelipiza kisasi na utajihisi amani na mimi pia nahitaji kufaidika” akasema Jenerali Akiki “Endapo tukiamua kuukubali mpango wa mapinduzi kwa kushirikiana na jeshi wewe utafaidika na nini?akauliza Melanie “Zipo faida ambazo ningezipata kupitia mpango ule tena kubwa tu” akasema Jenerali Akiki “Wewe unahitaji nini mheshimiwa Rais?Fedha? Kiasi gani?akauliza Melanie na Jenerali Akiki akatabasamu “Sihitaji fedha.Ninazo fedha za kutosha.Nahitaji kitu kingine” “Kitu gani? Melanie akauliza “Wewe” akajibu Jenerali Akiki akiwa na macho makavu.Melanie akatoa kicheko kidogo na kusema “Unanihitaji mimi?! Akauliza Melanie “Ndiyo” “Unanihitaji kivipi mheshimiwa Rais?Melanie akauliza “Melanie wewe si mtoto mdogo wa kushindwa kutambua ninamaanisha nini”akasema Jenerali Akiki.Ukapita ukjimya mfupi Melanie akauliza “Mheshimiwa Rais tafadhali niambie kama humaanishi hicho unachokisema” akasema Melanie “Ninaamisha Melanie.Nakuhitaji wewe.Nakuhitaji uwe mpenzi wangu wa siri” akasema Jenerali Akiki na Melanie akacheka kidogo “Mheshimiwa Rais jana ulisema kwamba ulikuwa na ukaribu mkubwa sana na wazazi wangu hasa mama ambaye alisoma na mke wako na ukatamka kwa ulimi wako kwamba kutokana na ukaribu huo mimi ni kama mwanao kwa nini leo unataka kulala na mwanao? “Sikiliza Melanie wewe tayari ni mtu mzima na mambo ya kupenda unayaelewa vyema.Ni kweli nilikuwa na ukaribu na wazazi wako lakini nimeshindwa kuudhibiti moyo wangu kufukuta toka nilipokuta machoni.Melanie hakuna kitu chochote kibaya kitatokea kama mimi nawe tutakuwa wapenzi wa siri.Nikubalie nikitakacho na ninakuahidi utapata kila unachokitaka” akasema Jenerali Akiki “Nimekutana na kigingi kingine tena.Wanaume hawa wakoje? Wameumbwaje?Mbona wote http://deusdeditmahunda.blogspot.com/wako sawa? Akawaza Melanie “Melanie unasemaje kuhusu hilo nililokuomba?akauliza Jenerali Akiki huku akiwasha sigara nyingine tena “Kwa nini unanifanyia hivi mheshimiwa Rais?akauliza Melanie “Kuna ubaya gani mimi na wewe tukiwa wapenzi wa siri Melanie?Au ukinipa hicho ninachohitaji utapungukiwa nini?Ninachokiomba kutoka kwako ni kidogo sana ukilinganisha na kile ambacho nitakifanya kwa ajili yako.Ninakwenda kuubeba mzigo mzito sana kwa ajili yako.Wewe hautajulikana bali ni mimi ambaye ninaweza kutilia shaka kuhusika na mauaji hayo hivyo sidhani kama kuna haja ya kuwa na majadiliano makubwa zaidi katika suala hili” akasema Jenerali Akiki “Huyu anaweza akanikwamisha mipango yangu kwa kuwa anajua ninamuhitaji sana.Ni kweli namuhitaji sana katika suala hili lakini mzee mzima naye amekwisha waka tamaa na sasa anataka nimpe mwili wangu.Sina namna ngoja nimpe anachokitaka ili mambo yangu yaende lakini ajue kila mwosha huoshwa.Iko siku yake” akawaza Melanie “Mheshimiwa Rais sina namna.Ninakuhitaji sana katika mpango huu.Niambie lini unanihitaji na wapi mimi nitakuja” akasema Melanie na Jenerali Akiki akatoa tabasamu “Tunaanza usiku wa leo” “Leo? “Ndiyo.Hakuna anayejua kesho yake hivyo ninakuhitaji kuanzia usiku wa leo” “Mpaka lini?Lazima kuwe na ukomo hatuwezi kuendelea na mchezo huu.Wewe ni rais wa nchi una mke ambaye ni rafiki wa mama yangu ambaye akijua kama unatembea na mimi ambaye ni sawa na mwanao utaingia katika mgogoro mkubwa wa familia yako” akasema Melanie “Ni kweli mimi ni Rais wa nchi lakini vile vile ni binadamu na nina mahitaji kama wanadamu wengine hivyo mambo yangu mimi na wewe hayahusiani chochote na urais wangu” “Nimekuelewa mheshimiwa Rais lakini usiku wa leo niache niende na kesho nitakuwa mgeni wako.Ninataka nije nikiwa nimejiandaa vyema kimwili na kiakili kwa siku ya leo sikuwa nimejiandaa kwa suala hilo” akasema Melanie “Hakuna tatizo Melanie.Nashukuru kwa kunielewa.Nadhani kesho tutapata wasaa mzuri zaidi wa kujadili kwa kina hili suala letu namna tutakavyoweza kulikamilisha.Ninachokuomba James Kasai asifahamu chochote kuhusiana na haya tuliyoyazungumza leo hadi pale wakati muafaka utakapofika” akasema Jenerali Akiki.Hakukuwa na mazungumzo mengine tena akamsindikiza Melanie hadi katika gari akaondoka.Jenerali akiki akarejea ndani “Melanie Davis ! akawaza huku akiwasha sigara akavuta mikupuo kadhaa huku akiachia tabasamu pana sana “Ningechekwa na dunia kama mtoto Yule angeondoka Uganda bila kumgusa hata kidogo.Ni kweli mama yake alikuwa ni rafiki wa familia yetu lakini nimeshindwa kuvumilia.Japo uzuri wake ni wa kutegenezwa lakini umenichanganya sana” akawaza Jenerali Akiki. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ndege ya shirika la ndege la Misri ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam saa nne za usiku ikitokea jijini Cairo kupitia Nairobi Kenya.Abiria walishuka ndegeni na kuingia katika jengo la uwanja ili kukamilisha taratibu za kuingia nchini.Mathew Mulumbi akiwa miongoni mwa abiria waliokuja na ndege hii alikuwa na hati ya kusafiria inayomuonyesha kuwa ni raia wa Saudi Arabia mwenye jina la Abu Al Zalawi. “Ninarejea nyumbani kama mgeni wakati hii ni nchi yangu ya kuzaliwa lakini imenilazimu nirejee namna hii.Hapa uwanjani wapo watu wengi wanaonifahamu ila naamini kwa mwonekano huu nilio nao sasa hakuna atakayenigundua.Nilifanya jambo zuri kufuga hizi ndevu nyingi.Kwa muonekano huu kila mtu atadhani labda mimi ni kiongozi wa kidini huko nilikotoka” akawaza Mathew akiingia ndani ya jengo la uwanja.Hakuwa akizungumza Kiswahili alizungumza kiingereza akichanganya na kiarabu kidogo.Aliwaona baadhi ya watu kadhaa pale uwanjani aliokuwa akifahamiana nao akajitahidi kuwakwepa asionane nao. Baada ya kukamilisha taratibu na kuruhusiwa kuingia nchini Mathew akaenda katika duka la kubadili fedha za kigeni akabadili fedha alizokuwa nazo na kupata fedha za Tanzania na kutoka nje.Alitamani asujudu na kuibusu ardhi ya Tanzania kwa furaha aliyokuwa nayo. “Natamani niibusu ardhi ya nchi yangu kwani sikuwa nimetegemea kuikanyaga tena katika maisha yangu lakini leo kwa nguvu ya Mungu nimerejea nchini” akawaza akiendelea kukokota torori lenye mabegi yake hadi alipotoka nje.Hakukuwa na mtu yeyote aliyekuja kumpokea hivyo akachukua taksi. “Nikupeleke wapi kaka?akauliza dereva taksi kwa lugha ya kiingereza “Ninaomba unipeleke katika hoteli yoyote nzuri yenye utulivu mkubwa lakini kabla hujanipeleka huko nahitaji kupita katika supermarket yoyote kubwa kuna vitu nahitaji” akasema Mathew na dereva akaondoa gari “Baada ya miaka mitatu hatimaye niko tena ndani ya jiji la Dar.Jiji limebadilika sana.Maendeleo makubwa yamefanyika katika kipindi hiki” akawaza Mathew akiwa amekaa kiti cha nyuma akielekeza macho nje Hatimaye baada ya kuzunguka katika supermarket kadhaa kubwa na kukuta zimefungwa ,wakaipata ambayo ilikuwa wazi.Mathew akashuka garini na kuingia ndani ya duka lile akaelekea katika upande wa vifaa vya elektroniki akachukua mashine ya kunyolea nywele pamoja na vitu vingine kadhaa akaenda kuilipia na kurejea garini safari ikaendelea.Dereva Yule alimfikisha katika hoteli moja nzuri wakaagana huku Yule dereva akimpa kadi yake ya biashara.Mathew akapokewa na wahudumu wachangamfu na kupewa chumba “Ni kama ndoto lakini ni kweli niko Dar es salaam.Kwa anayenifahamu atashangaa sana kuniona hapa hotelini kwani ninafahamika sana hapa Dar es salaam kama mmoja wa watu matajiri.Nimewekeza katika majumba mengi tu lakini kwa mujibu wa Habiba Jawad Peniela ameuza mali zangu zote zilizoko Dar es salaam hivyo siwezi kujua katika mauzo hayo nyumba ipi imeuzwa na ipi imesalimika.Zipo baadhi ya nyumba ambazo Peniela hazifahamu anayezijua ni Gosu Gosu.Mtu wa kwanza kabisa ambaye natakiwa kumtafuta kesho ni Gosu Gosu,nikimpata huyu nitafahamu mengi kutoka kwake” akawaza Mathew na kuingia bafuni akaanza kunyoa ndevu zote alizofuga akajitazama na kutabasamu “Hii ndiyo sura halisi ya Mathew Mulumbi.Nilipotoka kwa Ammar Nazari nilikuwa nimechakaa sana lakini baada ya kuanza kuishi na Najma kidogo najiona nimeanza kunawiri” akawaza huku akipaka dawa katika kidevu chake halafu akajitazama tena katika kioo “Welcome back Mathew Mulumbi” akasema kwa sauti ndogo akaoga kisha akaenda kujilaza kitandani. “Natakiwa kumjulisha Habiba kwamba tayari nimefika salama Dar es salaam” akawaza Mathew.Hakuwa na simu akachukua kompyuta yake akaiunganisha na intaneti.Hoteli ile ilikuwa na huduma ya mtandao wa intaneti.Baada ya kuunganisha akamtafuta Habiba Jawad na kumpigia simu kwa kutumia mtandao wa skype. “Mathew Mulumbi” akasema Habiba baada ya kupokea simu ya Mathew “Mama Habiba” akasema Mathew huku akitabasamu “Naona uso wako una furaha kubwa leo.Umenyoa ndevu umebadilika sana.Umerudi kuwa Mathew Mulumbi na si Abu Zalawi” akasema Habiba huku akitoa kicheko kidogo “Ni kweli mama nina furaha ya kufika nyumbani.Nimekupigia kukujulisha kwamba tayari nimefika Tanzania na hapa nilipo nipo hotelini” “Pole kwa safari Mathew.Nashukuru umefika salama.Kwa sasa endelea kupumzika hadi kesho tutazungumza zaidi.Jitahidi upate simu kwa ajili ya mawasiliano utakapokuwa hapo kwani hatuwezi kuwasiliana kila mara kwa kupitia mtandao” “Ni kweli mama.Kesho nitashughulikia kila kitu na jioni nitakupigia tuzungumze” akasema Mathew na kuagana na Habiba kisha akachukua juisi aliyonunua supermarket akanywa . “Sasa nijipumzishe nijiandae kwa siku ya kesho.Nitakuwa na mizunguko mingi” akawaza na kujilaza kitandani





Sauti za watu waliopita wakizungumza nje ya mlango wa chumba alicholala ndizo zilimstua Mathew kutoka usingizini akafungua macho na chumba kilikuwa na mwanga wa kutosha.Akayaelekeza macho ukutani kulikokuwa na saa kubwa ambayo ilionyesha ni saa mbili na dakika kumi na nane “Usingizi wa nyumbani mtamu sana ndiyo maana nimelala hadi nikapitiliza namna hii.Kawaida yangu huamka saa kumi na mbili za asubuhi” akawaza Mathew kisha akatoka pale kitandani akavaa nguo za mazoezi na kuelekea katika chumba cha mazoezi.Hoteli ile aliyofikia ilikuwa na chumba maalum cha mazoezi.Alifanya mazoezi kuuweka mwili sawa halafu akaenda kuoga kujiandaa kwa ajli ya kuikabili siku.Siku hii alivaa suruali ya jeans rangi nyeusi na fulana ya rangi nyeupe kichwani akavaa kofia ya rangi nyeusi ,macho akayafunka kwa miwani myeusi bila kusahau mkufu wa dahabu kifuani akajitazama katika kioo akaridhika kwa mwonekano ule kisha akaelekea sehemu ya chakula akaagiza kifungua kinywa.Wakati akiendelea kupata kifungua kinywa akapita kijana muuza magazeti Mathew akanunua magazeti matatu akapitia kwa juu juu lakini kubwa ambalo lilitawala magazeti yale ni matukio ya kushambuliana yanayoendelea baina ya Uganda na Rwanda.Alipomaliza kifungua kinywa akaenda kulipa na kumuachia chenji muhudumu kisha akatoka nje akaanza kutembea kwa miguu “Sijui kwa nini nikiwa sina silaha ninajiona mzito sana lakini hata kama itatokea hatari yoyote ninao uwezo wa kukabiliana nayo bila kuwa na silaha” akawaza huku akivuka barabara kuelekea upande wa pili ambako aliona taksi nyingi zimeegeswa.Akakodisha taksi moja akamtaka dereva ampeleke sehemu Fulani “Sehemu ya kwanza ninakoanzia leo ni nyumbani kwangu.Nataka nikamfahamu aliyenunua ni nani na nijue vitu vilivyokuwamo mle ndani vimepelekwa wapi.Kulikuwa na vitu vyangu vingi na vingine vya siri kabisa.Nilijenga nyumba ile kwa ajili yangu na ndiyo maana nikaweka baadhi ya vitu kama sehemu za siri za kuhifadhia silaha n.k.Peniela alikosea sana kuiuza nyumba yangu ile lakini siwezi kumlaumu kwa sababu anajua tayari nimefariki dunia na yeye hana mpango wa kuja tena kuishi Tanzania ndiyo maana akaamua kuiuza.lakini kwa nini Peniela akaamini haraka namna hii kwamba nimefariki dunia?Kitu gani klichomuaminisha haraka hivyo?Kwa nini hakutaka kufanya uchunguzi kujua kama kweli nimekufa? Anyway nisiumize kichwa kwa hilo majibu yote anayo yeye mwenyewe” akawaza Mathew huku gari likiendelea kukata mitaa kuelekea katika nyumba ya Mathew “Natamani sana kumtafuta Ruby na kujua maendeleo yake.Najua nilimuacha katika wakati mgumu sana,nakumbuka ni siku moja tu ilipita toka anieleze kwamba ananipenda na anataka tuwe wapenzi na nilimuahidi kwamba baada ya kumaliza operesheni ile basi tungekwenda mahala sisi wawili pekee kupumzika.Tayari nilikwisha amua kuwa na mahusiano ya siri na Ruby lakini kwa bahati mbaya sikurejea tena Tanzania.Atakuwa aliumia mno.Yuko wapi sasa hi0vi?Anafanya nini?Ameolewa au bado?Yote haya natakiwa kujua.Nitamuuliza Gosu Gosu nikionana naye” akaendelea kuwaza Mathew Hatimaye dereva wa ile taksi aliyopanda alifika katika mtaa ilipo nyumba ya Mathew. “Huu mtaa wangu nimeukumbuka sana.Umejengeka mno sasa hivi.Mimi ndiye muasisi wa mtaa huu.Nilianza kujenga wakati hakuna nyumba hata moja” akawaza huku akitabsamu na gari likienda kwa mwendo wa taratibu.Dereva akakata kushoto kufuata barabara ya zege iliyoelekea nyumbani kwa Mathew.Mapigo ya moyo wake yakaanza kumwenda kasi walipokaribia geti la nyumba yake.Kulikuwa na walinzi wawili wakawasimamisha.Mathew akafungua mlango akashuka akamlipa dereva akaondoka halafu akawafuata walinzi.Hakuwa akiwafahamu walinzi wale akasalimiana nao vizuri kisha wakamuuliza shida yake “Nahitaji kuonana na wahusika wa nyumba hii” akasema Mathew Walinzi wale wakataka kufahamu yeye ni nani na katokea wapi akawajibu kwamba ametokea nje ya nchi na ni ndugu ya wanaoishi pale.Mmoja wa walinzi akaingia ndani na kupiga simu ndani ya nyumba akieleza kwamba kuna mgeni wao ametokea nje ya nchi. “Subiri kidogo kuna mtu anakuja” akasema Yule mlinzi aliyeingia ndani kupiga simu.Baada ya dakika tatu mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na msichana mmoja akajitokeza “Lucy !! akasema Mathew huku akivua miwani na kofia mara kikatokea kitu kilichowashangaza wote.Lucy aligeuka haraka akatimua mbio kurudi ndani huku akipiga kelele wale walinzi wakaanza kumkimbiza.Mathew akavuka geti akaingia ndani.Lucy hakufika mbali akaanguka chini na kupoteza fahamu.Walinzi wale wakaungana na Mathew wakaanza kumpatia huduma ya kwanza “Ana matatizo gani huyu? Mathew akauliza “Tukuulize wewe kwani alipokuona tu ndipo alipoanza kupiga makelele na kukimbia.Wewe ni nani?akauliza mlinzi mmoja “Tusubiri azinduke tutajua tatizo lake” akasema Mathew huku walinzi wale wakionekana kuwa na woga. Baada ya muda Lucy akaamka na mara tu alipomuona Mathew yuko pale sebuleniakaanza tena kupiga kelele na kutaka kukimbia lakini walinzi wakamzuia,Mathew akamuendea “Jamani msimruhusu anisogelee ni mzimu huyo ! akapiga kelele Lucy na wale walinzi wakabaki wanashangaa “Lucy ! akaita Mathew lakini Lucy akapiga kelele kubwa.Mlinzi mmoja akataka kumzuia Mathew asimsogelee Lucy lakini Mathew akamsukuma akasogea pembeni “Lucy !! akaita Mathew na kumshika Lucy mabegani.Alikuwa anatetemeka “Mimi si mzimu.Nitazame vizuri ni mimi Mathew.Ni mimi Yule Yule unayenifahamu” akasema Mathew “Mathew amekwisha fariki miaka mitatu iliyopita ! akasema Lucy huku akitetemeka “Hapana Lucy sikufariki.Mimi ni mzima ila nilikuwa katika matatizo makubwa na taarifa mliyoipata kwamba nimefariki si taarifa ya kweli.Mimi ni mzima kabisa.Mimi si mzimu” akasema Mathew lakini bado Lucy aliendelea kutetemeka “Lucy usiwe na wasiwasi ni mimi Mathew nimerejea” akasema Mathew na mara mmoja wa walinzi akamsogelea Lucy “Lucy unahitaji msaada wa polisi? Akauliza mmoja wa walinzi “Msijali ndugu zangu.Mimi ni mwajiri wake wa zamani na ndiye mmiliki wa nyumba hii.Nilipotea kwa miaka mitatu na taarifa waliyopata ni kwamba nimekufa kumbe niko hai”Mathew akajaribu kujieleza “Ni kwel Lucy hayo anayoyasema huyu jamaa?akauliza mlinzi na Lucy akatingisha kichwa kukubali “Una hakika hatakuwa na madhara tukikuacha naye humu ndani?akauliza mlinzi “Ndugu zangu msiwe na wasiwasi na mimi hata kidogo.Hii ni nyumba yangu na huyu ni mfanyakazi wangu.Hamnifahamu lakini mimi ndiye mwenye nyumba hii” akasema Mathew “Nendeni msiwe na wasi wasi hakuna tatizo” akasema Lucy na walinzi wale wakatoka lakini bado wakiwa na wasiwasi. “Lucy tafadhali nyamaza kulia ni mimi Mathew nimerudi” akasema Mathew baada ya Lucy kuanza tena kulia baada ya walinzi kutoka. “Tafadhali usilie Lucy” akasema Mathew na kutoa kitambaa akamfuta machozi na mara Lucy akamkumbatia kwa nguvu. “Mathew jamani kaka yangu !! akasema Lucy huku akiendelea kumwaga machozi “Imetosha Lucy usiendelee kulia” akasema Mathew “Mathew niache nikulilie kaka yangu hujui ni machungu gani nimeyapata kwa kuamini kwamba umefariki dunia.Nimekulilia usiku na mchana.Nimekuombea sana upumzike kwa amani nikiamni umekufa ndiyo maana nilipokuona nilipatwa na mstuko mkubwa sana.Niache nikulilie kaka Mathew” akasema Lucy. “Nyamaza Lucy.Nimerudi niko mzima wa afya.Hakuna sababu ya kuendelea kumwaga machozi.Ahsante kwa maombi yako ambayo naamini yamenisaidia sana hadi tumekutana tena hapa”akasema Mathew “Nini kilikutokea Mathew?Ulikuwa wapi?Nani waliosambaza taarifa kwamba umekufa? Lucy akauliza huku akifuta machozi “Tutazungumza hayo yote baadae nitawaeleza nilikuwa wapi lakini kwa sasa nataka kufahamu nani wanaishi hapa? “Tunaoishi hapa ni mimi na Gosu Gosu” “Gosu Gosu? “Ndiyo” “Hakuna watu waliouziwa nyumba hii? “Hakuna kaka.Nilisikia kuna mali zako zimeuzwa lakini nyumba hii haikuuzwa.Tunaendelea kuuishi mimi na Gosu Gosu” “Ahsante Mungu” akasema Mathew na kushusha pumzi “Gosu Gosu yuko wapi?akauliza Mathew na Lucy akaanza tena kulia “Imetosha Lucy usilie tena” akasema Mathew “Nieleze tafadhali mahala alipo Gosu Gosu” “Gosu Gosu…” akasema Lucy na kushindwa kuendelea akaendelea kulia “Yuko wapi Gosu Gosu? Mathew akauliza “Yuko hospitali amepigwa risasi juzi” “Amepigwa risasi? “Ndiyo? “Nani kampiga risasi? “Bado haifahamiki nani waliompiga risasi” akasema Lucy na Mathew akavuta pumzi ndefu na kuuliza “Vipi hali yake? “Hali yake ni mbaya anapumua kwa msaada wa mashine” “Oh my God ! akasema Mathew “Yuko hospitali gani?akauliza “Hospitali ya Mtodora” akajibu Lucy na Mathew akasimama “Lucy vile vitu vilivyokuwa chumbani kwangu vimewekwa wapi?akauliza Mathew “Hakuna kitu hata kimoja kilichotolewa chumbani kwako.Chuba chako kilifungwa .Ni mimi tu ambaye huingia na kufanya usafi” “Ahsante sana Lucy naomba ufunguo wa chumbani kwangu” akasema Mathew na Lucy akaenda chumbani kwake akachukua funguo na kumpatia Mathew wakaelekea katika chumba cha Mathew.Akaufungua mlango wakaingia ndani “Kila kitu ni kama nilivyokiacha” akasema Mathew “Nimekuwa nikiingia mara kwa mara kufanya usafi” “Lucy nakushukuru sana.Naomba unipe dakika chache nisubiri hapo nje” akasema Mathew na Lucy akatoka.Mathew akaenda kukaa kitandani “Chumba hiki sikutegemea kukiona tena.Ahsante Mungu kwa kunifikisha leo katika chuba changu.Nawashukuru pia hawa waliokitunza chumba hiki kwa umakini mkubwa.Kila kitu kiko vile vile nilivyokiacha” akawaza Mathew na kufungua chumba chake cha siri ambacho hukitumia kuhifadhi silaha mbali mbali “Silaha zangu zote ziko vile vile”akawaza na kuchukua bastora moja akaijaribu ikiwa haina risasi na kutabasamu kisha akaweka risasi na kuifutika kiunoni “Nani kamshambulia Gosu Gosu na kwa nini? Akajiuliza Mathew “Tayari nimepata pigo la kwanza.Gosu Gosu nilimtegemea sana katika misheni hii hivyo sintaweza kuwa naye.Kama anapumua kwa msaada wa mashine basi hali yake ni mbaya sana.Ninamuombea aweze kupona.Sitaki kumpoteza Yule mwanajeshi.Hata kama nitamkosa katika misheni hii lakini nitamuhitaji huko mbeleni.Kwa sasa ngoja nielekee hospitali alikolazwa nikajue maendeleo yake” akasema Mathew na kutoka akamuomba Lucy funguo za gari.Kulikuwa na gari limeegeshwa mbele ya nyumba aina ya Mercedece benzi alilokuwa analitumia GosuGosu.Mathew akamuaga Lucy kuwa anakwenda hospitali kumtazama Gosu Gosu. “Nimefurahi kwa Peniela kutokuiuza nyumba yangu.Nimefurahi pia kwa namna Gosu Gosu alivyoitunza hadi leo hii.Chumba changu hakijawahi kuguswa kila kitu kiko vile vile.Je Gosu Gosu aliamini siku mojaninaweza kurejea ndiyo maana akakifunga chumba changu na hakutaka kukitumia? akawaza Mathew na kuingia katika kituo cha mafuta akajaza mafuta ya kutosha katika gari na kuelekea hospitali Geti la kuingilia hospotali ya mtodora lilikuwa wazi Mathew akapita na kwenda hadi maegesho akafungua mlango na kushuka akatazama pande zote kuhakiki usalama halafu akaanza kupiga hatua kuelekea katika jengo la mapokezi ambako aliwakuta wahudumu kadhaa akawauliza mahala alipo mgonjwa wake Gosu Gosu,akaelekezwa kwamba yuko katika jengo la wagonjwa mahututi bila kupoteza muda Mathew akaelekea huko.Alipolikaribia jengo hilo akasimama ghafla baada ya kumuona mtu Fulani kwa mbali “Austin ?! akajiuliza Mathew kwa sauti ndogo “Ni yeye kweli au nimemfananisha? Akajiuliza akiendelea kumtazama “Macho yangu bado yana nguvu ya kutosha.Sina shaka na kile ninachokiona.Yule atakuwa ni Austin.He’s alive” akawaza Mathew na kuanza kupiga hatua kumsogelea.Mtu Yule alikuwa ameinamisha kichwa akitazama chini alionekana kuwa na mawazo mengi sana “Hallo brother” akasema Mathew na kumstua Yule mtu ambaye aliinua kichwa wakatazamana.Mathew akavua kofia na miwani. “Mungu wangu !! akasema Austin kwa mstuko mkubwa.Alikuwa ameshika karatasi kadhaa zikamponyoka.Walitazamana kwa muda wa sekunde kadhaa “Hallo Austin ! akasema Mathew “Ma..mamamamath…” Austin alitetemeka mdomo akashindwa kutamka.Akatazama kulia na kushoto kama vile anataka kukimbia “Usiogope Austin ni mimi Mathew Mulumbi” akasema Mathew na kumpa mkono “How’re you?akauliza Mathew.Bado Austin aliendelea kumtazama kwa hofu “Austin usiwe na hofu.Ni mimi Mathew.I’m not a ghost.Nishike mkono tafadhali” akasema Mathew akiwa ameunyoosha mkono wake.Taratibu Austin akauinua mkono wake wa kulia na kuushika mkono wa Mathew akauminya kidogo na kumtazama usoni “This is unbelievable !! akasema kwa sauti ndogo halafu akamkumbatia Mathew kwa nguvu. “Ouh Mathew my brother !! akasema Austin na Mathew akahisi bega lake lilikuwa linaloa machozi “It’s okay Austin.Imetosha.Hatuna sababu ya kumwaga machozi.We cry for the dead but I’m not dead.I’m still alive” akasema Mathew lakini Austin akajikuta amechuchumaa chini akimwaga machozi.Watu waliokuwepo eneo lile wakawatazama wakihisi labda Austin amepata taarifa mbaya kuhusu mgonjwa wake “Austin usilie.Inuka tafadhali” akasema Mathew na kumnyanyua . “Mathew Mulumbi ! akasema Austin na kumkumbatia tena Mathew. “Huu kwangu ni muujiza mkubwa sana ambao sikuwa nimeutarajia kabisa.Mathew !! Bado Austin alikuwa katika mshangao . “Austin tutazungumza mengi lakini kikubwa kilichonileta hapa ni Gosu Gosu.Nataka kujua maendeleo yake” “Hali yake si nzuri.Naamini hadi umefika hapa tayari umekwisha pewa taarifa kwamba hata kupumua ni kwa msaada wa mashine.Mathew tunaweza kumpoteza Gosu Gosu.Anything can happen! akasema Austin akionekana kukata tamaa. “Dah ! hili ni pigo kubwa sana.Nahitaji kumuona. I need to talk to him” akasema Mathew na Austin akazungumza na wauguzi,Mathew akavishwa mavazi maalum na kuingia ndani ya chumba alimolazwa Gosu Gosu.Akamtazama “Please God don’t take him yet.We still need him” Mathew akaomba kimya kimya kisha akavuta kiti akaketi karibu na Gosu Gosu “Papi Gosu Gosu it’s me Mathew Mulumbi.I’m not dead and I’m back home” akasema na kuvuta pumzi ndefu “Kwa mara ya kwanza nilipokuja kukuchukua kutoka kwa Kasu niliamini mimi nawe tunaweza kuwa watu wa karibu sana na ndivyo ilivyokuwa.Sifahamu kwa nini nilikuamini sana na baada ya operesheni ile kumalizika nikakuweka msimamizi wangu wa miradi kazi ambayo uliifanya kwa umakini na uaminifu mkubwa sana.Umekuwa si rafiki bali ndugu yangu.Nikiwa njiani nikirejea nyumbani wewe ndiye mtu wa kwanza ambaye nilitaka kukutana naye lakini kwa bahati mbaya nimekukuta ukiwa katika hali hii.Gosu Gosu wewe ni mwanajeshi usiyeogopa chochote.I know you’re going to fight this.Please fight my brother.I need you so badly so don’t leave me yet.I know you’re listening to me right now so fight for your life.I have a bigger mission and I need you.Utakapoamka nitakueleza nilikuwa wapi na kwa nini ninakuhtaji sana” akasema Mathew na kusimama “Please fight Gosu Gosu and wake up very soon ! akasema Mathew na kutoka “Umeona mwenyewe hali yake ilivyo” akasema Austin “Hali yake inakatisha tamaa sana lakini Gosu Gosu ni mpiganaji nimemwambia apambane aamke naamini amenisikia” akasema Mathew “Hata mimi nimekuwa nikiamini hivyo kwamba ataamka muda si mrefu kutokana na ujasiri wake lakini naona siku zinakwenda hakuna maendeleo yoyote ya kutia moyo.Usiku unapita unakuja mchana unaingia tena usiku lakini bado Gosu Gosu hana dalili zozote za kuamka.Mathew mimi ni jasiri sana lakini katika hili nimeanza kukata tamaa.Tunakwenda kumpoteza Gosu Gosu” akasema Austin “Austin usiruhusu hata siku moja roho ya kukata tamaa ikakuingia.Unatakiwa uwe na imani hata pale ambapo hakuna matumaini.Kuwa na moyo mgumu kama wa jiwe usikubali kushindwa.Kwa hili la Gosu Gosu bado hatuna sababu ya kukata tamaa.Tuendelee kusimama imara karibu yake na atazinduka.Akiwa katika hali ile anaweza akakaa hata mwaka na hatupaswi kukata tamaa.Ni wajibu wetu kumkumbusha kila mara kwamba tuko karibu yake na tunamuhitaji azinduke.Atatusikia na atazinduka.Gosu Gosu is our brother,we love him and we don’t give up on people we love.You understand me Austin ? akasema Mathew “I understand Mathew” akasema Austin.Baada ya muda kidogo Mathew akauliza “Tukio hili limetokeaje?Nani waliompiga risasi Gosu Gosu? “Mpaka sasa haifahamiki nani waliofanya tukio hili.Taarifa za Gosu Gosu kupigwa risasi nilizipata kutoka kwa mchumba wake anaitwa Melanie.Alinipigia simu usiku na kunijulisha kwamba Gosu Gosu yuko hospitali amepigwa risasi ndipo nikaja hapa mara moja na kumkuta akiwa ametoka kufanyiwa upasuaji na alikuwa anaendelea vyema lakini usiku hali yake ikabadilika akalazimika kuwekwa katika mashine ya kumsaidia kupumua” akasema Austin “Gosu Gosu tayari ana mchumba?Yuko wapi? Mathew akauliza “Hata mimi sikuwa nikifahamu alifanya siri.Baada ya tukio hili kutokea ndipo nikamfahamu.Aliniaga juzi kwamba atakuwa na safari lakini hakunieleza anakwenda wapi na toka wakati huo sijamuona tena hapa hospitali wala kupiga simu kuulizia hali ya mchumba wake ikoje” akasema Austin “Kwa maelezo aliyonipa Melanie ni kwamba Gosu Gosu alikuwa anatoka ofisini kwake nyakati za jioni na wakati akijiandaa kuingia katika barabara kuu ikatokea piki piki ikiwa na watu wawili wenye silaha wakaanza kulishambulia gari la Gosu Gosu kwa risasi.Walikuwa na lengo la kumuua kabisa lakini kilichomsaidia akanusurika ni fulana isiyopenya risasi aliyokuwa ameivaa.Ilimsaidia kuzuia risasi nyingi kuingia mwilini.Nimekuwa nikifuatilia kwa jeshi la polisi kama kuna mtuyeyote amekamatwa kuhusiana na suala hili lakini mpaka leo hii hakuna aliyekamatwa ila uchunguzi unaendelea” akasema Austin “Kikubwa kwa sasa ni kumuombea ili apone.Yeye ndiye mwenye majibu yanani waliompiga risasi na yawezekana labda aliwaona kwa macho.” akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita “Nimefurahi kukuona Austin.Vipi maendeleo yako? Akauliza Mathew “Mimi ninaendelea vyema lakini bado niko kwenye mstuko mkubwa.Sikutegemea kabisa kukuona hapa” akasema Austin lakini Mathew “Hata mimi sikutegemea kabisa kama ningekukuta hapa.Sikujua kama ulisalimika usiku ule” akasema Mathew “Nilisalimika Mathew lakini tulipoteza watu wengi sana usiku ule na wote tuliamin………..” akasema Austin lakini Mathew akamkatisha “Austin tuna mengi ya kuzungumza na mazingira haya si rafiki sana.Tutafute sehemu nzuri tutulie tuzungumze” akasema Mathew na haraka haraka Austin akaenda kuzungumza na wauguzi kisha akamfuata Mathew akamtaka waondoke. “Jaribu kumpigia simu huyo mchumba wa Gosu Gosu ninataka kuonana naye” akasema Mathew na Austin akapiga simu lakini simu ya Melanie haikuwa ikipatikana “Hapatikani simuni” akasema Austin “Unafahamu anakoishi? “Hapana sifahamu.Kwa ujumla simfahamu vyema huyo mwanamke.Nimefahamiana naye hapa hapa hospitali na hatujapata nafasi ya kuzungumza kujuana vizuri.Nimeshangaa kwa Gosu Gosu kutonijulisha kuhusu suala hili la kuwa na mchumba wakati masuala yake karibu yote huwa ananijulisha” akasema Austin.Mathew akakata kona kuingia katika hoteli iliyokuwa karibu na hospitali.Wakatafuta sehemu tulivu wakaketi muhudumu akafika na kuagiza vinywaji “Austin najua una maswali mengi unataka kufahamu kuhusu mimi.Nilikuwa wapi na yote yaliyonitokea lakini nakuomba usiniulize chochote kuhusu suala hilo.Kitu cha msingi ni kufahamu tu kwamba niko hai inatosha” akasema Mathew “Ni kweli Mathew kuna mengi ninataka kuyafahamu.Kuanzia usiku ule wa tukio hadi leo hii ulipotokea.Hakuna aliyeamini kama uko hai kufuatia shambulio lile baya” akasema Austin.Mathew akanywa kinywaji chake kidogo kisha akauliza “Did you search for me? Akauliza Mathew.Swali lile lilimfanya Austin abaki kimya “Answer me Austin.Baada ya tukio la usiku ule mlijaribu kunitafuta kujua mahala nilipo?akauliza Mathew “Rais alituma kikosi maalum siku iliyofuta kwenda kukutafuta lakini ni kikosi hicho kilichorejea na majibu kwamba kuna uwezekano mkubwa uliuawa na kuliwa na fisi” akasema Austin “Siulizi kuhusu Rais nauliza kuhusu wewe.Did you search for me? Akauliza Mathew na Austin akabaki kimya “Wewe ndiye uliyeongoza kikosi cha pili ambacho jukumu lake kubwa lilikuwa ni kulinda kikosi cha kwanza ambacho nilikuwa nakiongoza mimi.Baada ya shambulio lile kutokea ukiwa kama kiongozi ulijaribu kunitafuta? Akauliza Mathew na Austin akafikiri kidogo kisha akasema “Baada ya shambulio lile la ghafla kukoma tulianza kukusanya miili ya watu wetu na karibu kikosi chako chote ulichokuwa unakiongoza kiliuawa na miili ikapatikana lakini ni wewe pekee uliyekosekana.Niliwaelekeza watu wangu tuendelee kukutafuta tukagundua pia kwamba watu wa IS nao karibu wote walikuwa wameuawa lakini Edger Kaka hakuwa miongoni mwao.Tuliamini labda umejificha sehemu Fulani karibu na pale lakini wakati tukiendelea kukutafuta taarifa zilimfikia Rais ambaye kwa wakati huo alikuwa kambini akifuatilia kwa karibu tukio lile na akaamuru tuondoke haraka sana eneo lile.Nilimueleza kwamba wewe umekosekana lakini akaamuru niondoe kikosi mhala pale kwani tayari ilikuwa ni hatari kwetu.Kama tungeendelea kukaa pale kukutafuta tungeendelea kuwaweka hatarini hata wale mateka tuliowakomboa hivyo nikaondoa kikosi.Samahani sana Mathew mzigo wote wa lawama nastahili kuubeba mimi” akasema Austin “Hustahili lawama.Ulitimiza amri uliyopewa na mkuu wako.Najua usingekubali kuniacha porini kwani siku zote kiongozi unapopewa kikosi ukiongoze katika misheni Fulani unapaswa kuwarejesa watu wako wote nyumbani wakiwa wazima au wamekufa” “Ahsante Mathew kwa kulitambua hilo lakini ni jambo ambalo limekuwa likinitesa sana moyoni kwamba sikufanya juhudi za kutosha usiku ule kukutafuta” “Austin usibebe lawama ambazo hustahili.Tuachane na hayo vipi kuhusu wale mateka tuliokwenda kuwakomboa walifika nyumbani salama? “Wote walifika nyumbani salama” “Pamoja na yote yaliyotoea lakini kumbe misheni ilifanikiwa.Vipi kuhusu Olivia huwa mnaonana? “Mara chache sana huwa tunaonana.Taarifa za kifo chako zilimumiza mno” akasema Austin “Vipi kuhusu Ruby mnawasiliana?akauliza Mathew “Ruby amekuwa akiwasiliana na Gosu Gosu mara kwa mara na kwa sasa anafanya kazi katika mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza GCHQ” “Anafanya kazi GCHQ? “Ndiyo.Mahusiano yangu naye si mazuri toka wakati ule ulipopotea na ananilaumu mimi kwa kile kilichotokea na kusababisha kile ambacho wengi tuliamini kifo chako.Mara ya mwisho kuwasiliana naye ni miezi kadhaa imepita.Mimi na Gosu Gosu tulihitaji msaada wake katika misheni Fulani muhimu sana” “Misheni ipi?akauliza Mathew “Ilikuwa ni misheni moja muhimu sana kwa nchi na ambayo ilileta kiza zaa kikubwa” akasema Austin “Ilihusu nini hiyo misheni? Mathew akauliza “Tulitakiwa kumuua mwanasiasa mmoja wa kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” akasema Austin “Nini ilikuwa sababu ya kutaka kumuua?Nieleze kwa undani zaidi jambo hilo”akasema Mathew “Mheshimiwa Rais Dr Fabian alipewa taarifa na Rais Patrice Eyenga wa Congo kwamba kuna mwanasiasa mmoja anatumiwa na mataifa ya nje katika mpango wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki.Rais wa sasa wa Congo Patrice Eyenga amefanikiwa kumaliza mchafuko yaliyoitawala nchi hiyo kwa muda mrefu na hilo halijawapendeza nchi kubwa waliokuwa wakifaidika na machafuko hayo ndiyo maana wakataka kumtumia mwanasiasa huyo ili awe daraja la kuwavusha kurejea tena kuendelea kuinyonya Congo.Baada ya kupewa taarifa hiyo Ras Dr Fabian alitupa sisi kazi ya kumuondoa mwanasiasa huyo aliyeitwa Lucy Muganza” “Mwanasiasa huyo alikuwa ni mwanamke?Mathew akauliza “Ndiya alikuwa ni mwanamama bilionea.Nikishirikiana na Gosu Gosu na vijana wengine tulifanikisha misheni hiyo na kumuua Lucy Muganza na mume wake Laurent Muganza.Baada ya mauaji hayo kuna makosa yalifanyika.Tulipomuua Lucy Muganza na mumewe tulitakiwa kwenda mbali zaidi lakini tulijisahau na miili le ikafanyiwa uchunguzi na ikagundulika kwamba risasi zilizotumika katika mauaji hayoni kutoka katika bunduki zinazotumiwa na wadunguaji na taarifa hiyo ikamfikia balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini ambaye aliendelea kuishinikiza serikali kuruhusu wachunguzi wa kutoka umoja wa ulaya kuja chini kuchunguza mauaji yale.Balozi huyo alikuwa na taarifa kwamba bunduki ambazo zilitumika kuwaua Lucy Muganza na mumewe zinamilikiwa na jeshi na hapo ndipo Rais akatutaka tumchunguze balozi huyo tujue anapata wapi taarifa nyeti kama hizo za kuhusiana na silaha za nchi.Ilitulazimu kumuomba msaada Ruby katika kumchunguza balozi huyo na ndipo nilipofahamu kuwa anafanya kazi katika mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza.Tulifanikiwa kugundua kwamba balozi huyo alikuwa na mawasiliano ya karibu na mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi aliyejulikana kama Tamar.Kwa bhati mbaya kabla ya kupiga hatua kubwa kumchunguza balozi huyo aliuawa” Austin akaendelea kumueleza Mathew kwa undani namna misheni ilivyokuwa hadi pale ambapo mambo yalikuja kutulia “Dah ! hongereni sana kwa kazi kubwa mliyoifanya.Nimefurahi kwa namna mlivyoendesha misheni hiyo.Umeniambia kwamba mlimshauri Rais amuite Ruby nyumbani ili awe mkurugenzi wa ile idara ya SNSA” “Ndiyo.Tulimshauri hivyo mheshimiwa Rais na aliahidi kulitekeleza hilo suala lakini mpaka leo hatujapata mrejesho wowote kutoka kwake amefikia wapi katika suala hilo la kumshawishi Ruby aweze kuja hapa nchini” akasema Austin “Ahsante sana kwa kumshauri Rais jambo hilo.Idara ile ni muhimu sana kwa nchi lakini tayari mabeberu wamekwisha pandikiza watu wao.Naamini hata baada ya Tamar kuondoka bado kuna mapandikizi yamebaki kwani hawezi kuwa peke yake lazima wawepo watu aliokuwa anashirikiana nao ambao wataendeleza kufanya kile wanachokitaka mabeberu.Ruby ni chaguo zuri na anafaa sana kuongoza idara kama ile.Kuna ulazima wa kufuatilia kujua Rais amefikia wapi katika suala hilo.Una namba za simu za Ruby?akauliza Mathew “Hapana sina nanba zake.Ni Gosu Gosu ndiye aliyekuwa akiwasiliana naye” “Simu ya Gosu Gosu iko wapi? “Sifahamu mahala ilipo simu hiyo” akajibu Austin. “Unafahamu anakoishi Rais mstaafu Dr Evans?akauliza Mathew “Ndiyo ninafahamu.Anaishi katika nyumba yake mpya” akajibu Austin “Nipeleke huko nahitaji kuonana naye” akasema Mathew huku akisimama wakaondoka kuelekea katika gari la Mathew ambaye alimtaka Austin aendeshe kwa kuwa yeye hakuwa na leseni.Austin akaondoa gari wakaondoka kuelekea katika makazi ya Rais mstaafu Dr Evans.







Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akitokea mkoani Mbeya katika mazishi ya mke wake Millen Kelelo.Kutoka katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dr Fabian alielekeza apelekwe katika nyumba yake aliyokuwa akiishi kabla ya kuwa Rais. Ruby akiwa amepumzika ndani ya chumba chake alistushwa na muungurumo wa magari akainuka kuchungulia nje kupitia dirishani akayaona magari ya msafara wa Rais yakijipanga “Rais amekuja” akasema Ruby na haraka haraka akaelekea katika meza ya vipodozi akaanza kurekebisha uso wake kabla ya kukutana na Rais.Akiwa katika kujiandaa mlango wake ukagongwa.Akajitazama katika kioo halafu akaenda mlangoni akaufungua akakutana na walinzi wawili ambao walimtaka aongozane nao wakaelekea hadi sebuleni ambako alimkuta Rais Dr Fabian akiwa ametulia sofani.Akasimama baada ya Ruby kuingia “Ruby ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais shikamoo” “Marahaba Ruby vipi maendeleo yako? “Ninaendelea vyema mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Rais akamfanyia ishara aketi “Pole sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ahsante Ruby nimekwisha poa.Ni mapito ya mwanadamu na sote njia yetu ni hiyo isipokuwa mwenzetu ametutangulia.Japo nina majonzi lakini nimefurahi kukuona Ruby karibu sana.Jana nilishindwa kurejea kama nilivyokuahidi niliombwa na wazee nibaki kwa ajili ya kukamilisha mambo ya kimila.Naamini umekuwa ukihudumiwa vizuri” akasema Dr Fabian “Usijali mheshimiwa Rais.Nafahamu unapitia kipindi kigumu hivyo hata kama ingenichukua mwezi mzima kukusubiri hakuna tatizo kwa upande wangu kwani hapa niko nyumbani” akasema Ruby “Ruby napenda kwanza kabla ya yote kukupa pole nyingi sana kwa yote uliyopitia katika safari ya kuja hapa.Najua mimi ndiye sababu ya mambo yale yote kutokea kwa kukutaka uache kazi uliyokuwa unaifanya uje nyumbani.Umepitia mambo magumu sana hata kunusurika kifo.Nilipoona jina lako katika orodha ya watu waliofariki katika ile ajali ya ndege nilijilaumu mno kwa kukuomba uje nyumbani lakini nakushukuru kwa namna ulivyopambana kuhakikisha unafika salama Tanzania.Naamini hii yote ni mipango ya Mungu kwani umefika katika kipindi ambacho unahitajika sana” akasema Dr Fabian “Ni kweli mheshimiwa Rais nimepitia mambo magumu hadi kufika hapa.Kazi niliyokuwa naifanya nchini Uingereza iliniwezesha kufahamu mambo mengi sana ya siri hivyo nilipowasilisha maombi ya kuacha kazi walistuka na walifanya kila mbinu kunishawishi nibatilishe mpango wangu huo wa kuacha kazi lakini niliendelea kushikilia msimamo wangu na ndipo walipoamua kupanga mpango ule wa kuniua.Ulikuwa ni mpango wa siri sana na ninamshukuru mmoja wa marafiki zangu ambaye aliweza kunijulisha kile kilichokuwa kimepangwa dhidi yangu na akanisaidia hadi nimefika hapa.Ilikuwa ni safari ndefu na ngumu kwangu lakini namshukuru Mungu nimefika salama nikiwa na afya njema” akasema Ruby “Kwa nini walikuwa na hofu ya wewe kuacha kazi?akauliza Dr Fabian “Edward Snowden wa Marekani amewapa fundisho ndiyo maana walistuka sana na walihisi labda na mimi nina mpango kama ule wa kutoa siri zao.Waliamini nimelipwa pesa nyingi ili niweze kuuza siri ndiyo maana suluhisho pekee walilokuwa nalo ni kuniua.Ninasikitika kwamba maisha ya watu wengi yalipotea kwa sababu yangu” akasema Ruby “Pole sana Ruby.Ninakuahidi kukulinda kwa kila namna dhidi ya hawa jamaa ambao mpaka sasa wanaamini tayari umekwisha fariki” “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” “Mimi ndiye ninayepaswa kukushukuru wewe kwa niaba ya watanzania.Kitendo ulichokifanya ni cha kizalendo.Umeacha kazi uliyokuwa ukiifanya ambayo ilikuwa na maslahi manono na ukakubali kuja kuitumikia nchi yako.Ni uzalendo wa hali ya juu sana” akasema Dr Fabian “Tanzania ni nchi yangu na lazima niitike ndiyo kila pale ninapoitwa kuitumikia.Mheshimiwa Rais niko tayari kwa ajili ya kazi ya kuitumikia nchi yangu” akasema Ruby “Karibu sana Ruby.Kwa kuwa kwa sasa nina ratiba nyingine nitakuomba jioni ya leo ikulu kwa ajili ya chakula kisha tutazungumza kwa kirefu sana kuhusiana na kazi ambayo nimekuita uje kuifanya” akasema Dr Fabian “Nitafika mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Dr Fabian akasimama na kumpa mkono “Ruby kwa mara nyingine tena karibu Tanzania.Karibu nyumbani” akasema Dr Fabian kisha akaagana na Ruby akaondoka. KAMPALA – UGANDA Gari nne aina ya range rover zenye rangi nyeupe zilifika katika nyumba ambayo alifikia Melanie.Ulikuwa ni msafara wa James Kasai ambaye alishuka na kuingia ndani ya jumba lile.Melanie akiwa chumbani kwake akafuatwa na mmoja wa wahudumu akaitwa akatoka kwenda kukutana na James Kasai aliyekuwa sebuleni. “James Karibu sana” akasema Melanie “Nashukuru sana Melanie.Habari za toka juzi?akauliza James Kasai “Ninaendelea vizuri sana sina tatizo lolote.Unapendeza sana ukivaa suti kuliko yale mavazi yako ya kijeshi”akatania Melanie na wote wakaangua kicheko “Nashukuru kusikia hivyoMelanie lakini nimezoea sana kuvaa mavazi yale ya jeshi kwa kuwa muda wote niko katika mapambano.Samahani kwa kutokuja kuonana nawe siku ya jana” “Usijali James ninaelewa.Nimekupigia simu ili tuje tuzungumze kuhusiana na lile suala letu.Umekwisha pata mrejesho wowote kutoka kwa Rais?akauliza Melanie “Hapana sijapata mrejesho wowote bado kutoka kwa Rais.Alituahidi angewasiliana nasi jana lakini hakufanya hivyo.Wewe hujapata chochote kutoka kwake? Akauliza James na Melanie akatoa kicheko kidogo “Hawezi kuwasiliana nami kabla hajakujulisha kwanza wewe.Hata hivyo dhumuni la kukuita hapa kuna jambo nataka tulijadili kuhusiana na ule mpango wetu wa kumuua Patice Eyenga” “Karibu”akasema James “Juzi tulipokwenda kuzungumza na Rais alitueleza kwamba anataka kushirikiana nawatu kutoka ndani ya serikali ya Congo katika mpango wa kumuua rais Patrice Eyenga.Anachotaka kukifanya Rais Akiki si kitu kibaya lakini tatizo la huo mpango wake ni kwamba utachukua muda mrefu kwanza kuwashawishi watu waweze kukubaliana na mpango huo na vile vile upo uwezekano kwamba watu hao ambao anataka kuwashirikisha wakakataa kushirikiana naye.Kama ikitokea watu hao wakakataa kushirikiana naye mpango utakuwa umekwama na siri itakuwa imevuja kwamba Rais Patrice anataka kuuawa.Nimelitafakari sana hilo nikaamua kuja na mpango mpya ambao tutauwasilisha kwa Rais Akiki” akasema Melanie na kunyamaza kidogo “Mpango gani umekuja nao?akauliza James “Kwa hivi sasa Uganda na Congo hazina maelewano mazuri.Hii ni fursa ambayo tunatakiwa kuitumia.Jenerali Akiki atawasiliana na Rais wa Tanzania ambaye ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sasa na atamuomba wakutane pamoja na rais wa Congo ili kutafuta suluhu ya mgogoro unaoendelea hivi sasa na kikao hicho kifanyike jijini Dar es salaam.Wakati kikao hicho kikiendelea tutapandikiza bomu katika ndege ya Rais Patrice na pale atakapokuwa angani akirejea Congo tutailipua ndege yake.Ni mpango ambao hautahitaji mtandao mkubwa kama anaotaka kuutengeneza Rais Akiki na vile vile hautachukua muda mrefu.Unauonaje mpango huo?akauliza Melanie.James akafikiri kidogo na kusema “Ni mpango mzuri japo nao una changamoto yake.Changamoto kubwa ni namna ya kulipandikiza hilo bomu katika ndege ya Rais ambayo inakuwa na ulinzi mkali wakati wote” akasema James “Ndiyo maana nikauita hapa ili tuweze kujadiliana suala hilo.Mimi kwa upande wangu ninaweza kutengeneza mtandao ambao unaweza ukatusaidia kuingiza bomu katika ndege hiyo ya Rais Patrice ”akasema Melanie “Hilo ndio hasa kubwa tunalolihitaji katika huo mpango.Kama unao uwezo wa kutengeneza mtandao unaoweza kutusaidia basi hakuna tatizo tunaweza kuendelea na mpango huu”akasema James “Katika huo mpango tutawahitaji watu wa IS.Baada ya mlipuko kutokea na Patrice kuuawa IS watajitokeza na kudai kwamba wao ndio waliohusika katika shambulio hilo bila kutoa sababu yoyote.Hakuna ambaye atajua umehusika bali mzigo wote wataubeba IS.Baada ya kifo cha Patrice jeshi naamini linaweza kutangaza kuchukua nchi na hapo ndipo machafuko yatakapoanza na wewe utaendelea na mapambano na serikali na safari hii ukiwa na jeshi lenye nguvu na zana za kisasa.”akasema Melanie “Kweli ni mpango mzuri na hata mimi nimeupenda sana hivyo basi tuanze maandalizi.Kwanza tuanze kwa kuzungumza na Rais Akiki.Nitawasiliana naye kumueleza kwamba tunahitaji kuzungumza naye na tukikutana nitajaribu kumshawishi aukubali mpango huu ambao naamini hataweza kuukataa hivyo jambo kubwa ni kuandaa namna bomu hilo litakavyoweza kuingizwa katika ndege ya Rais.Hata hivyo kuna kitu ninakiwaza.Kwa nini bomu hilo lisiingizwe ndegeni jijini Kinshasa? Tunaweza kumchagua rubani mmoja wa ndege ya Rais tukaiteka familia yake na kumlazimisha aliingize sanduku lenye bomu ndani ya ya ndege ya Rais wakati akijiandaa na safari ya kuja Tanzania na Rais Patrice auawe kabla hajafika Dar es salaam.Unaonaje wazo hilo? “Ni wazo zuri pia.Tutayajadili haya yote na Rais Akiki pale tutakapokutana naye.James mimi ninafanya hivi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa wazazi wangu lakini wewe fanya kwa ajili ya harakati zako za kuiomboa Congo.Kama alivyosema Jenerali Akiki kwamba ni wewe pekee ambaye unapambana kwa maslahi mapana ya Congo lakini wengine wote wanapambana kwa maslahi yao na wakubwa wanaowafadhili hivyo hakikisha mapambano yanandelea na siku moja unafanikiwa kuingia hadi Kinshasa” akasema Melanie “Melanie ahsante kwa ushauri huo mzuri.Ni kweli kama alivyosema Rais Akiki kwamba ninapambana kwa ajili ya maslahi ya Congo na ndiyo maana siungwi mkono na taifa lolote la Ulaya bali anayeniunga mkono ni Rais Akiki pekee ambaye anafahamu nia yangu ya dhati ya kuikomboa Congo.Ninakuahidi kwamba mapambano yataendelea hadi pale nitakapohakikisha nimeitawala Congo” akasema James “Kuhusu IS umepanga kushirikiana nao hadi lini? Melanie akauliza “IS nitaendelea kushirikiana nao kwa ajili ya kuniwezesha kijeshi.Kwa sasa ninahitaji kikosi chenye nguvu kubwa hivyo basi nategemea kupata silaha kali na za kisasa kutoka kwao.Mkataba wa mashirikiano yangu nao ni kwa ajili ya kuwasaidia kujenga kambi yao ya mafunzo katikati ya misitu” “Ni vipi kama baadae likawa jeshi kubwa na wao pia wakaanza kupigana na serikali? Akauliza Melanie “Wanachokitaka wao ni sehemu ya kufanyia mafunzo kwa watu wao ambao watawatuma sehemu mbalimbali duniani.Hawana mpango wowote wa kushambulia Congo” akasema James “James nimeuliza swali hilo kwa sababu watakapopata sehemu ya kuweka kambi ya mafunzo wataanza kujiimarisha taratibu na pale watakapokuwa na jeshi kubwa basi wataanzisha mapigano na serikali na kama unavyojua hawa jamaa wakikita mizizi yao sehemu Fulani kuwaondoa huwa vigumu sana” akasema Melanie “Usiwe na hofu Melanie.Nimekwisha kubaliana nao kuwasaidia kupata kile wanachokitaka na mimi niweze kupata kile ninachokitaka.Tuachane na suala hilo una taarifa zozote za Gosu Gosu? “Sijapiga simu nyumbani kuuliza hivyo sijui kinachoendelea kuhusu hali yake” akasema Melanie “Melanie unatakiwa kumjulia hali mpenzi wako.Piga sim…” akasema James na Melanie akamkatisha “Nitawasiliana nao kujua maendeleo yake usihofu” akasema na James akamuaga kwa ahadi ya kumpa mrejesho baadae pale atakapokuwa amezungumza na Jenerali Akiki. DAR ES SALAAM – TANZANIA Gari la akina Mathew lilisimamishwa na askari waliokuwa wakilinda geti la kuingilia nyumbani kwa Rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Evans.Hawakuwa na miadi ya kuonana na Dr Evans hivyo mmoja wa askari akapiga simu ndani ikapokelewa na mtumishi wa ndani akamuomba azungumze na Dr Evans akamjulisha kuwa kuna wageni wake ambao ni Austin January na mwenzake wamefika kuonana naye.Baada ya kuzungumza na simu askari Yule akaelekeza geti lifunguliwe na akina Austin wakaruhusiwa kuingia ndani. “Umewahi kuja huku?akauliza Mathew “Ndiyo nimekuwa nikifika mara kadhaa kumsalimu mzee” akajibu Austin. Waliegesha gari na kushuka.Mmoja wa watumishi wa Dr Evans akaenda kuwapokea na kuwaongoza kuelekea ndani.Austin alitangulia mbele na Mathew akamfuata nyuma.Aliwakaribisha sebuleni akawahudumia vinywaji halafu akaenda kumuita Dr Evans.Baada ya dakika chache Dr Evans akatokea akiwa ameshika gazeti mara gazeti alilolishika likaanguka chini baada ya kukutanisha macho na Mathew Mulumbi. “Jesus Christ ! akasema huku akigeuka na kutazama nyuma kama vile alitaka kukimbia “Shikamoo mzee” akasema Austin “Mar..marahaba Austin ! akaitika Dr Evans huku macho yake akiwa bado ameyaelekeza kwa Mathew. “Shikamoo mzee”akasema Mathew na Dr Evans akamtazama Austin “Is this real?akauliza “It’s real mr President” akajibu Austin. Mara Dr Evans akashika kifuani na kunza kupepesuka akataka kuanguka.Austin akamuwahi akamdaka na kumkalisha sofani “My pills” akasema Dr Evans kwa taabu.Mathew akamuita mtumishi wa Dr Evans na kumtaka aonyeshe zilipo dawa za mzee.Mtumishi Yule akakimbia na kwenda kuleta kichupa kidogo cha dawa akatoa dawa mbili na kumpa Mathew ambaye alimpa Dr Evans akanywa haraka haraka kisha akalazwa sofani. “Mzee amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo na tatizo kama hili limekuwa likimtokea mara kwa mara” akasema Yule mtumishi wake.Mathew akamuelekeza ampigie simu daktari wake. “Mathew utaua watu kwa mstuko.Kila anayekuona anapatwa na mstuko mkubwa.Hakuna anayeamini kama bado uko hai mpaka sasa.Hata mimi nilipatwa na mstuko mkubwa na nilichuchumaa chini kwa kuwa miguu iliniisha nguvu” akasema Austin “Naomba ujio wangu usije ukasababisha maafa” akasema Mathew. Daktari wa Dr Evans alifika akampima na kumkuta anaendelea vizuri. “Hakuna tatizo anaendelea vyema” akasema Daktari na kumpa maelekezo Yule mtumishi kisha akaondoka “Mlinzi wa mzee yuko wapi?Alipaswa kuwa naye hapa” akasema Mathew “Mlinzi wa mzee amepata dharura ndiyo maana leo hayupo” akajibu Yule mtumishi.Dr Evans akainuka sofani na kuketi “Mzee unajisikiaje? Akauliza Austin “Najisikia vizuri” akajibu Dr Evans “Pole sana mzee” akasema Mathew “Mathew ..” akasema Dr Evans na kutaka kunyanyuka lakini Mathew akamtaka aketi.Akaendelea kumtazama kwa macho yaliyojaa hofu. “I can’t believe this.Ni wewe kweli Mathew Mulumbi? Akauliza Dr Evans “Ni mimi mzee.I’m still alive” akajibu Mathew “I’m so sorry Math……” “Usijali mzee.Austin tayari amekwisha nieleza kila kitu kilichotokea” akasema Mathew “Mathew ninatamani hata niyapofue macho yangu nisiweze kukutazama usoni.Ninaona aibu.Ulifanya jambo kubwa sana kwa nchi na kwangu pia.Uliwakomboa watoto waliokuwa wametekwa na magaidi na vile vile ukamkomboa mwanangu aliyekuwa mikononi mwa magaidi lakini kama alivyokueleza Austin usiku ule lilipotokea lile shambulio baya kabisa nilifanya maamuzi magumu ya kumtaka akiondoe kikosi kile na miili yote iliyopatikana.Nilihofia kungekuwa na shambulio lingine na yawezekana tungeweza hata kupoteza kikosi kizima.Nakiri yalikuwa ni maamuzi magumu sana kuyafanya katika kipindi changu chote cha urais.Nilikubali kikosi kiondoke na kumuacha mtu muhimu kabisa kwa taifa.Siku iliyofuata nilituma tena kikosi kingine kwenda eneo la tukio kutafuta kama wangeweza kukupata walau hata mwili wako lakini hawakupata kitu chochote na taarifa waliyoirejesha ni kwamba utakuwa ulifariki dunia na maiti yako kuliwa na fisi kwani walikuta kuna mabaki kadhaa ya maiti zilizoliwa na fisi eneo lilipofanyika lile shambulio.Baada ya kupewa taarifa ile nilituma ujumbe kwa mke wako Peniela jijini Paris Ufaransa kumfahamisha kilichotokea na kumpa pole sana.Hakuna aliyejua kama uko hai Mathew tusamehe sana” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais nafahamu yalikuwa ni maamuzi magumu kabisa uliyafanya na siwezi kukulaumu kwani hata mimi ningekuwa mahala pako ningefanya hivyo hivyo lakini unapotuma watu katika misheni Fulani lazima uhakikishe wote wanarejea nyumbani wawe wazima au wamekufa.Watu wanapotumwa misheni Fulani wanakwenda kupambana kwa ajili ya nchi hivyo lazima hata kama wamefariki wazikwe kishujaa katika ardhi ya nyumbani kwao.Kilichofanyika kwangu kiwe somo wakati mwingine kuwathamini wale wanaotumwa kupambana kwa maslahi ya nchi.Hata hivyo ninataka kujua baada ya taarifa kurudi kwamba nimeliwa na fisi mlichukua hatua zipi?Mlithubutu hata kutengeneza kaburi mkazika hata kiatu changu kuonyesha kunithamini? Akauliza Mathew “Hatukufanya hivyo” akasema Dr Evans “Hukuwa na mawazo hayo kwa kuwa kile ulichokuwa unakihitaji ulikwisha kipata.Mwanao alikombolewa na hukujisumbua tena kuhusu Mathew Mulumbi.Hukutaka hata kutuma timu ya kufanya uchunguzi wa kina kufahamu nini kilitokea.Ulifanya hivyo? “Hatukufanya hivyo” akajibu Dr Evans “Mpaka leo hamjui nini hasa kilitokea usiku ule! Hamjui nani walitushambulia na kwa nini! Hukutaka kusumbuka kwa sababu mwanao alikuwa amepatikana.Katika orodha ya watu waliofariki dunia kwenye ile misheni mlithubutu hata kuliweka jina langu? Akauliza Mathew na wote wakawa kimya “Mheshmiwa Rais ninaipenda sana nchi yangu lakini ninyi viongozi mnakatisha tamaa wazalendo kama mimi ambao wako tayari kumwaga damu yao kwa ajili ya nchi.Licha ya mchango mkubwa nilioutoa kwa nchi yangu lakini bado thamani ninayoipata ni ndogo mno.Hata hivyo siko hapa kuomba nithaminiwe kwani ni Mungu pekee atakayeweza kunilipa lakini ninataka kuwaeleza mtambue makosa mliyoyafanya.Najua hauko katika uongozi hivi sasa lakini unayo sauti na unasikika ukiongea hivyo basi nataka uwashauri walio katika madaraka hivi sasa kuwathamini watu kama mimi,kama Austin watu kama Gosu Gosu ambaye hivi sasa yuko mahututi akipigania maisha yake.Hatuombi litokee kwani Mungu ndiye mpanga yote lakini anaweza akapoteza maisha na akifariki ndiyo anasahaulika kabisa.Nataka uwabadilishe viongozi walio madarakani wawe na uthubutu wa kuthamini mchango wa wale wanaojitolea kwa ajili ya nchi yao.Wapo wanajeshi,askari polisi na wengine kutoka vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama.Mnawajali vipi pindi wakistaafu utumishi au wakiumia wakiwa kazini? Fikisha ujumbe huu kwa wenzako walio madarakani ”akasema Mathew kisha akavua fulana aliyokuwa ameivaa akafungua fulana ya kuzuia risasi aliyokuwa ameivaa ndani na kuwaonyesha Austin na Dr Evans makovu yaliyoko mwilini mwake “Dah ! akasema Austin “Haya ndiyo niliyopitia.Mwili wangu wote umechafuliwa na makovu ya vidonda” akasema Mathew “Pole sana Mathew.Unaweza ukatueleza nini hasa kilichotokea?Ulikuwa wapi? Akauliza Dr Evans “Lengo la kuja hapa si kueleza mahala nilikokuwa na yapi nimepitia.Ukurasa huo umekwisha fungwa lakini nilitaka tu kuwapa somo kwamba mlichokifanya kilikuwa ni kitu kibaya kabisa” akasema Mathew “Mathew ninakosa maneno ya kusema kijana wangu” akasema Dr Evans “Usiseme chochote.Sikuja hapa kwa malumbano au kwa hasira kwa nini mlinicha porini lakini kubwa lililonileta hapa ni kukujulisha kwamba niko hai na sijafa kama mlivyoamini” akasema Mathew na Dr Evans akavuta pumzi ndefu “Mathew hapa nilipo sijitambui kama nina furaha au majonzi lakini kikubwa ambacho ninataka kukwambia kwamba watu kama wewe huzaliwa wachache sana katika dunia ya sasa.Kwa nini ninasema hivyo? Ni kwa sababu kwa sasa nchi yetu iko katika mgogoro mkubwa na kati kati ya mgogoro huo umeibuka kutoka kusikojulikana.Mathew unaongozwa nahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ roho wa Mungu ndani yako ndiyo maana umetokea kwa wakati huu ambao nchi hii inakuhitaji sana” akasema Dr Evans “Sijakuelewa mzee nchi inanihitaji kivipi?Walijua nitarejea?Wanafahamu mahala nilikokuwa?Wanafahamu niliyoyapitia hadi umeniona hapa leo?akauliza Mathew “Hakuna aliyefahamu mahala ulipo,hakuna aliyekuwa anafahamu kama utakuja lakini nchi ilikuhitaji sana mtu kama wewe.Umetokea wakati ambao ni muafaka kabisa.Mathew Mungu amekuleta kwa wakati huu isikie sauti yake na uisaidie nchi” akasema DrEvans “Mzee sijakuelewa nini unakimaanisha” akasema Mathew “Mathew naamini Austin amekwisha kueleza kile ambacho kimetokea hapa nchini siku chache zilizopita kama bado hujasikia katika vyombo vya habari huko ulikokuwa” “Ninafahamu kilichotokea mzee.Ninafuatilia kila siku taarifa za nyumbani kujua kila tukio linalotokea hapa” akasema Mathew “Nashukuru kama unafuatilia habari za nyumbani. Kinachoendelea hivi sasa ni mpango wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Huu ni mpango wa nchi kubwa kutugawanya.Kikubwa wanachokitaka ni kuvuruga umoja wetu kila nchi ikae peke yake ili wapate nafasi nzuri ya kutunyonya.Huu ni mkakati mzito san…..”akasema Dr Evans na Mathew akamkatisha “Mzee ninafahamu kila kitu kinachoendelea hapa nchini na kila kitu kuhusiana na mpango huu wa kuigawanya afrika Mashariki.Ninafahamu nchi inayolengwa zaidi katika mpango huu ni jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Wanataka machafuko yarejee nchini Congo ili wapate nafasi ya kurejea kuchuma mali za nchi hiyo.Ninafahamu kila kitu mzee huna hja ya kuelezea sana” akasema Mathew. “Where have you been Mathew?akajiuliza Dr Evans na ukimya ukatawala pale sebuleni. “Mzee najua nyote mko katika mstuko mkubwa kwa kuniona.Nafahamu mnayo maswali mengi mngependa kuniuliza,mngetaka kujua nilikuwa wapi muda huu wote lakini kitabu kile kilikwisha malizika kwa mimi kutoweka hivyo hakuna tena haja ya kuendelea kuulizana maswali kuhusiana na suala hilo.Kikubwa ambacho mnapaswa mkifahamu ni kwamba niko mzima na nimerejea nyumbani” akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema “Mzee umezungumza maneno fulani kwamba Mungu amenileta kwa wakati huu ambao ni muafaka.Nakubaliana nawe mzee kwa sababu hata mimi sikutegemea kama ningekuwa hapa muda huu nikizungumza nanyi lakini kwa uweza wa Mungu niko tena katika ardhi ya nyumbani.Nimekuja nyumbani kumaliza kile ambacho kinaendelea hivi sasa” akasema Mathew na mstuko mkubwa ukaonekana katika nyuso za Dr Evans na Austin “Huyu ni binadamu kweli au ni mzimu? Alikuwa wapi huyu hadi akaibuka kwa wakati huu?akajiuliza Dr Evans “Bado mpaka sasa inaniwia ugumu kuamini kama kweli huyu ndiye Yule Mathew halisi.Nina wasiwasi tusije kuwa tunachezewa na mzimu hapa” akawaza Austin. “Naona nyuso zenu zimepatwa na mshangao lakini narudia tena kuwahakikishia kwamba nimekuja kumaliza hiki kinachoendelea hivi sasa hapa nchini.Nimekuja kuiokoa jumuiya ya Afrika Mashariki isisambaratike.Nimekuja kummaliza James Kasi na kuung’oa mzizi wa ugaidi hapa Afrika mashariki” akasema Mathew “Mathew unaniogopesha kwa maneno hayo unayoyatamka” akasema Dr Evans “Usiogope mzee.Ulisema mwenyewe kwamba nimekuja kwa wakati muafaka.Ninaweza kusema kwamba Afrika Mashariki imeniita na siwezi kusema hapana.Mimi ni mtoto wa Afrika na Tanzania ambayo iko ndani ya Afrika Mashariki inaponihitaji lazima niitike haraka sana.I’m back guys.I’m the same Mathew Mulumbi.Yawezekana mkaona nimebadilika kidogo lakini mimi ni Yule yule mliyenifahamu” akasema Mathew na kuwatazama akina Austin ambao wote bado walikuwa kimya wakimsikiliza.Dr Evans akasimama “Come here my son.I need to hug you ! akasema Dr Evans na Mathew akainuka akamfuata Dr Evans wakakumbatiana “Karibu tena nyumbani mwana Tanzania.Sasa moyo wangu una amani baada ya kukuona wewe na nimepata faraja kubwa kwa maneno yako kwamba umekujwa kuiokoa Afrika mashariki.Baada ya shambulio lile la kigaidi kutokea na kuuawa kwa wake za marais nilikesha nikitafakari dhumuni la shambulio lile na nikagundua kwamba ule ulikuwa ni mtego na viongozi wetu tayari wamenasa katika mtego huo kwa kuamsha hasira baada ya wake zao kuuawa na kutaka kuanza kushambuliana wao kwa wao.Kila nchi kwa sasa inaweka majeshi yake katika utayari.Hakuna tena nchi inayomuamini mwenzake.Rwanda na Uganda zinashambuliana japo mapambano si makubwa lakini amani baina ya nchi hizo mbili haipo.Kitendo cha nchi mbili ndani ya jumuiya kurushiana risasi ni kiashiria kikubwa kwamba jumuiya hiyo inaelekea ukingoni.Uganda imewarejesha nyumbani mabalozi wake kutoka nchi za Rwanda na Congo na kuwatimua mabalozi wa nchi hizo walioko Uganda.Nilimfuata Rais wetu Dr Fabian na kuzungumza naye nikamuonya kuhusiana na hatua za kijeshi mbazo wanataka kuzichukua dhidi ya Uganda.Wanaandaa kikosi cha jeshi ambacho kitakwenda Uganda kumsaka James Kasai.Uganda imekwisha onya kuhusu kitendo chochote cha kutuma kikosi cha jeshi katika ardhi yake kwamba ni kitendo cha kichokozi na imeapa kujibu kwa nguvu zote uchokozi wowote utakaofanywa na nchi yoyote ya ndani au nje ya jumuiya ya Afrika mashariki.Nilijaribu kumueleza kuhusu hatari ya kusambaratika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki lakini inaonekana Rais ameyapuuza mawazo yangu na kwa taarifa niliyoipata ni kwamba tayari wanajeshi kutoka katika nchi za Rwanda na Congo wamekwisha wasili nchini na maandalizi ya kikosi cha jeshi cha umoja kwa ajili ya kwenda Uganda yanaendelea.Viongozi wetu wametanguliza hasira mbele bila kujali maslahi ya nchi zao na jumuiya.Wameungana pamoja na wanachokitaka ni kulipa kisasi kwa wake zao kuuawa” akasema Dr Evans “Mzee ukilitazama jambo hili utakuta kati kati yake anasimama mtu anaitwa James Kasai.Yeye ndiye aliyesababisha haya yote yakatokea.Kama asingefanya shambulio nchini Tanzania kusingekuwa na hofu iliyoko hivi sasa ya nchi zetu kufikia hatua ya kutaka kushambuliana.Misheni yangu ya kwanza ni kumuondoa James Kasai.Huyu jamaa kama akiondolewa hakuna nchi ambayo itaendelea na mpango wa kuishambulia nyingine.Tanzania,Rwanda na Congo wanajiandaa kufanya operesheni ya kijeshi nchini Uganda kumsaka James.Kama ulivyosema mzee wameingia mtegoni bila wao kujua kwani hawataweza kumpata James Kasai kwa kutumia nguvu za kijeshi hivyo James akiondolewa hakutakuwa tena na ulazima wa kutuma kikosi hicho cha jeshi” akasema Mathew “Jambo la pili ni kwamba James Kasai hayuko peke yake.Anashirikina na kikundi cha igaidi cha IS na kwa pamoja ndio waliotekeleza shambulio lile na kuua wake za marais na mabalozi.Baada ya kummaliza James Kasai itafuata operesheni nyingine ya kuung’oa kabisa mzizi wa IS hapa nchini na Afrika Mashariki.Hizi mbili si operesheni nyepesi nitahitaji sana msaada wenu” akasema Mathew. “Sema chochote unachokihitaji Mathew.Mimi niko tayari kukusaidia” “Nitahitaji kuonana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania .Mimi naye hatufahamiani.Ameingia madarakani wakati sipo hivyo nahitaji mtu wa kuniunganisha naye.Nataka nikamshauri aachane na operesheni za kijeshi anazotaka kuzifanya na mimi nitamuhakikishia kummaliza James Kasai” akasema Mathew “Nitakuunganisha na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Alikwenda Mbeya kwa ajili ya mazishi ya mke wake nitampigia simu baadae kujua kama amerejea Dar es salaam” “Sawa mzee.Suala hili nililokueleza naomba iwe ni siri yako” akasema Mathew “Usihofu Mathew siwezi kumueleza mtu bila ridhaa yako” “Kwa sasa sina mawasiliano yoyote utawasiliana nami kwa kutumia simu ya Austin” akasema Mathew wakaagana na Dr Evans wakaondoka. “Austin kama nilivyowaeleza kwamba nimerudi hapa nchini kwa kusudi maalum.Nina misheni nzito ya kumuondoa James Kasai na ninakutaka uungane nami katika misheni hiyo” akasema Mathew “Mathew unafahamu jibu lake.Katu siwezi kusema hapana.Tulikula kiapo cha kuilinda nchi dhidi ya adui wa ndani na wa nje kwa hiyo kila pale linapotokea jukumu la kuilinda nchi siwezi kusema hapana” akasema Austin “Ahsante sana Austin.Ningefurahi sana kama Gosu Gosu angekuwa mzima ajiunge nasi lakini kwa bahati mbaya haitawezekana.Ruby naye angekuwepo ni mtu muhimu sana.Misheni za sasa zinakwenda sambamba na teknolojia.Tutahitaji kuongeza watu wawili katika timu yetu badala ya Gosu Gosu na Ruby” akasema Mathew “Wapo vijana wawili Tom Denzel na mwingine anaitwa Aidan Kengele.Hawa ni vijana mahiri sana ambao wametoka mafunzoni hivi karibuni.Wana uwezo mkubwa sana”akasema Austin “Utanipa mafaili yenye taarifa zao niyapitie” akasema Mathew na ukimya ukapita halafu Mathew akauliza “Unazo taarifa zozote za mali zangu kuuzwa? “Mali zako kuuzwa?Austin naye akashangaa “Ndiyo.Una taarifa zozote? “Hapana sina taarif zozote za mali zako kuuzwa.Nani kauza?Gosu Gosu?akauliza Austin “Hapana si Gosu Gosu.Mke wangu Peniela” akasema Mathew “Sina taarifa zozote za jambo hilo.Kwa nini kachukua maamuzi hayo? Mbona Gosu Gosu hajanieleza chochote? Tufuatilie tufahamu undani wa suala hili” akashauri Austin “Usijali Austin.Kama kauza siwezi kumlaumu sana kwani yeye kama wengine wote aliamini nimekwisha fariki dunia.Isitoshe sikuja kwa ajili ya hilo.Nimekuja kwa misheni maalum kabisa” akasema Mathew ukapita ukimya kidogo Austin akauliza “Peniela hajakueleza chochote kuhusu jambo hilo?akauliza Austin “Sina mawasiliano naye.Hafahamu kama niko hai” akasema Mathew “Where were you Mathew? Akauliza Austin “Austin let’s focus on our mission” akasema Mathew na kumuelekeza Austn waelekee katika hoteli aliyokuwa amefikia ili akachukue mizigo yake. Mara tu baada ya akina Mathew kuondoka,Dr Evans akampigia simu Rais Dr Fabian “Mheshimiwa Rais” akasema Dr Evans baada ya Dr Fabian kupokea simu “Mzee shikamoo” “Marahaba Dr Fabian.Vipi maendeleo yako? “Tayari nimekwisha rejea Dar es salaam.Nilishindwa kurejea jana.Nashukuru kila kitu kimekwenda vizuri na tumerejea salama” “Dr Fabian najua mambo ni mengi sana lakini nakuomba nipate nafasi ya kuonana nawe jioni ya leo.Kuna jambo la muhimu sana nataka kuzungumza nawe” akasema Dr Fabian “Mzee kwa siku ya leo utanisamehe sana.Ratiba yangu imebana sana.Mambo ni mengi .Kuna mengi ya kuzungumza nawe mzee wangu naomba iwe kesho ili tupate nafasi ya kutosha kuzungumza.Samahani sana mzee” akasema Dr Fabian “Usijali Dr Fabian.Hata kesho tunaweza kuonana” akasema Dr Evans wakaagana na Dr Evans akampigia simu Austin akamjulisha kuwa kikao kitakuwa siku ya kesho





Saa moja za jioni Ruby aliwasili katika makazi ya Rais ikulu Dar es salaama.Mlango wa gari lake ukafunguliwa na mmoja wa walinzi aliokuwa ameongozana nao akashuka na kupokewa na msaidizi wa Rais akamkaribisha ndani akamtaka amsubiri Rais alikuwa anamalizia mazungumzo na watu waliokuja kumpa pole.Dakika arobaini baadae Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo akaingia sebuleni akiwa ameongozana na walinzi wake.Ruby akasimama kwa heshima “Ruby ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Dr Fabian akampa mkono “Karibu sana Ruby” akasema Dr Fabian na kuketi “Samahani kwa kuchelewa.Nilikuwa na kikao na mabalozi waliokuja kunipa pole hivyo nikashindwa kuwaacha peke yao” “Usijali mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby nimefarijika sana kukuona hapa” akasema Dr Fabian na kumtaka Ruby waelekee katika chumba cha chakula ambako kulikuwa kumeandaliwa chakula maalum. “Ruby karibu sana.Nimeandaa hiki chakula kwa heshima yako” akasema Dr Fabian “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kila mmoja akajisaidia chakula alichohitaji “She used to sit there” akasema Dr Fabian akimuonyesha Ruby kiti ambacho mke wake Millen alipenda kukaa wakati wa chakula “Pole sana mheshimiwa Rais”akasema Ruby “Itanichukua muda mrefu kuizoea hali hii ya maisha bila Millen.She was everything to me” akasema Dr Fabian na kuweka kijiko mezani “Mheshimiwa Rais hili ni jaribu kubwa ambalo unapitia hivyo itakulazimu kuwa jasiri sana kulikabili.Najua unaumia moyoni lakini jitahidi kuirejesha akili katika jukumu kubwa la kuongoza watu zaidi ya milioni hamsini ambao wote wanakutazama wewe.Utalia siku utakapomaliza urais lakini kwa sasa bado una kazi kubwa ya kuongoza so focus ! akasema Ruby kwa sauti kavu.Dr Fabian akamtazama halafu akainua kijiko “Ahsante Ruby.Katika wote waliokuja kunipa pole wewe ni wa kwanza kunieleza maneno kama hayo na uko sahihi ninatakiwa kuielekeza akili yangu katika masuala ya msingi ya uongozi wa nchi” akasema Dr Evans “Watoto wako wapi?akauliza Ruby “Wamebaki Mbeya na ndugu wengine kuna ibada itafanyika kesho.Watarejea baada ya wiki moja.Tuliweke hilo pembeni.Pamoja na yote yaliyotokea Ruby nimefurahi sana kukuona.Ujio wako umenifarji sana” akasema Dr Evans na kuendelea kula walipomaliza wakaenda katika chumba cha mapumziko “Ruby naomba nianze kwa kukueleza sababu iliyopelekea kukuita hapa nyumbani” akasema Dr Evans na kuanza kumuelezea Ruby kila kitu toka mauaji ya Lucy Muganza hadi walipogundua kwamba Tamar aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi kushirikiana na balozi wa umoja wa Ulaya aliyeuawa na watu wasiojulikana. “Baada ya Tamar kuuawa ndipo Austin aliponifuata na kunieleza kwamba kuna mtu ambaye anafaa sana na anaweza kuiongoza SNSA na akakupendekeza wewe.Sikuwa nikikufahamu na ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia jina lako” akanyamaza kidogo “Nilipoingia madarakani nilikumbana na changamoto moja ambayo ni kuamini watu wanaonizunguka.Nilipata somo kutoka kwa rais aliyenitangulia Dr Evans ambaye aliyekuwa waziri mkuu wa serikali yake alikuwa ni mfuasi wa mtandao wa kigaidi wa IS.Nilipata taabu kidogo kupata watu nitakaowaamini kwa ajili ya ile misheni ya kumuua Lucy Muganza na ndipo Dr Evans akanitambulisha kwa Austin ambaye alinihakikishia ni mtu ninayeweza kumuamini.Toka wakati huo nimekuwa na imani kubwa kwa Austin ndiyo maana aliponieleza kwamba unafaa kuiongoza idara nyeti kama ya SNSA sikumuhoji mara mbili moja kwa moja nikamtaka anielekeze mahala ulipo.Nashukuru sana kwa kulikubali ombi langu na ukafanya kila jitihada kuhakikisha unafika Tanzania kuifanya kazi hiyo niliyokuomba.Sina neno zuri zaidi la kukushukuru Ruby kwa hiki ulichokifanya”akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais naamini Austin alikueleza historia yangu.Mimi ni mtanzania lakini kwa sasa nina uraia wa Uingereza.Kwa muda mrefu sikuwahi kurejea nyumbani na sikuwa na mpango huo hadi pale nilipokutana na mtu mmoja anaitwa Mathew Mulumbi ambaye ndiye aliyenifundisha kwamba japokuwa nina uraia wa nchi nyingine lakini nina deni kubwa kwa nchi walikotoka wazazi wangu ambako ndiko asili yangu” akasema Ruby “Mathew Mulumbi hili si jina geni katika masikio yangu.Who is he?akauliza Dr Fabian “Mathew Mulumbi aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi.Anatajwa mmoja wa majasusi mahiri kabisa kuwahi kutokea hapa nchini.Ni yeye ndiye aliyenirejesha nyumbani Tanzania na kunishirikisha katika misheni mbali mbali alizokuwa akizifanya.Misheni ya mwisho kushrikiana naye ni miaka mitatu iliyopita ambapo tulishirikiana kuwakomboa mateka waliokuwa wametekwa na kundi la kigaidi la IS” akasema Ruby “Where is he now? “Alifariki katika misheni hiyo.Alikwenda nchini Kenya katika misheni ya kuwakomboa mateka waliokuwa wanashikiliwa na kundi la IS na miongoni mwao alikuwemo mtoto wa Rais Dr Evans.Walifanikiwa kuwakomboa mateka lakini Mathew hakurejea tena nyumbani.Alifia huko” akasema Ruby na kuinamisha kichwa “Dr Evans hajawahi kunieleza chochote kuhusiana na suala hilo” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,Mathew Mulumbi ndiye hasa aliyenifundisha kuipenda nchi nilikotoka na ndiyo maana uliponipigia simu kunitaka nije Tanzania kufanya kazi sikujiuliza maswali bali nilianza mara moja mchakato wa kuondoka kule Uingereza kurejea huku.Haikuwa rahisi kama nilivyokueleza kwamba waliamini nimenunuliwa ili nikatoe siri zao na ndiyo maana wakapanga mpango ule wa kuniua.Kwa bahati nzuri nilijulishwa juu ya mpango ule na kuukwepa.Haikuwa safari rahisi hadi kufika hapa lakini nashukuru Mungu ameniongoza nimefika salama na niko tayari kwa kazi” akasema Ruby “Kweli haya ni maongozi ya Mungu kwani hata mimi sikutegemea kama ungeweza kufika Tanzania salama.Kama nilivyokueleza wakati ninakupigia simu kwamba kazi unayokuja kuifanya ni kuongoza idara nyeti ya usalama wa ndani wa nchi ambayo inafanya kazi zake kwa siri” “Ninaifahamu idara hiyo na majukumu yake” akasema Ruby “Nashukuru kama unaifahamu lakini idara hii ina umuhimu mkubwa sana kwa nchi tofauti na unavyoifahamu ndiyo maana ninahitaji mtu wa kuiongoza ambaye atakuwa ni mzalendo wa kweli ambaye hataitumia idara hii kwa ajili ya manufaa yake kama walivyofanya waliotangulia” akanyamaza kidogo na kusema “Kufuatia Tanzania kuchafuka kimataifa kutokana na kifo cha Lucy Muganza,Millen alinishauri tufanye kitu kwa ajili ya kuirejesha tena sifa ya Tanzania kama kisiwa cha amani na akashauri kuandaa mkutano mkubwa wa wake za marais wa dunia nzima kupitia taasisi yake.Tulitumia gharama kubwa kuandaa mkutano huo muhimu na wiki moja kabla ya mkutano kufanyika balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hapa nchini alimfuata Millen akamueleza kwamba anataka kuwakutanisha wake za marais wa Rwanda na Congo na akamtaka Millen kumsaidia katika mpango huo.Millen alikubali kwa kujua kwamba ni jambo jema na maandalizi ya hafla ya kuwakutanisha wake hao za marais ikaandaliwa na siku ilipofika wakakutana kwa ajili ya hafla hiyo na ndipo mabomu matatu yakalipuka.Mke wangu Millen,wake za marais wa Rwanda na Congo,mabalozi wanaoziwakilisha nchi hizo hapa Tanzania pamojana familia zao na raia wengine wa kutoka nchi hizo waliokuwa wamealikwa walipoteza maisha” “Pole sana mheshimiwa Rais.Nilikuwa melini na sikujua chochote kilichotokea” akasema Ruby “Ninafahamu ndiyo maana nilikwambia nitakuja kukueleza nitakaporejea” akanyamaza kidogo “Baada ya shambulio kutokea alijitokeza mtu mmoja anaitwa James Kasai akadai kuhusika na lile shambulio akisaidiana na kikundi cha kigaidi cha IS” “James Kasai.Who is he?akauliza Ruby “Huyu anaongoza kikundi cha waasi ambacho kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini wa sasa baada ya kufurushwa nchini Congo inaaminika ameenda kuishi nchini Uganda” “Katika maelezo aliyoyatoa alidai nini sababu ya kufanya shambulio hilo? Ruby akauliza “Alidai ni kulipiza kisasi kwa Rais Patrice Eyenga” akasema Dr Fabian na kunyamaza akatazama na Ruby kwa muda halafu akasema “Kwa hvi sasa Tanzania ikiungana na Rwanda na Congo tuko katika maandalizi ya kuandaa kikosi cha jeshi kitakachokwenda nchini Uganda kumsaka James Kasai na kuhakikisha anapatikana akiwa mzima au amekufa.Mazoezi ya kikosi hicho yanaendelea na pale watakapokuwa tayari wataelekea nchini Uganda kumsaka James Kasai” akasema Dr Evans na kunyamaza kwa sekunde chache “Tunaamini balozi Germinus Mapupu hakuwa peke yake lazima kuna watu alioshirikiana nao katika kuandaa hafla ile.Nimewapa jukumu hilo SNSA la kuhakikisha wanachunguza na kujua nani waliokuwa wanashirikiana na balozi Mapupu lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya maana kutoka kwao.Umefika kwa wakati muafaka kabisa ninataka uanze na jambo hili.Ninataka uhakikishe tunafahamu nani walioshirikiana na balozi Mapupu.Tunajua James Kasai ndiye aliyefanya shambulio lakini lazima wapo watu wa hapa nchini ambao walishirikina naye na hao ndio tunaotaka kuwafahamu.Jambo lingine ninataka kufanya mabadiliko makubwa katika idara ile na nitategemea sana ushauri wako.Utakapoanza kazi rasmi utaisoma ile idara na kutoa mapendekezo ni wapi panahitaji mabadiliko na mimi nitafanya bila kusita” akasema Dr Fabian “Nimekuelewa mheshimiwa Rais na ninakuahidi utendaji uliotukuka” akasema Ruby “Ahsante Ruby naamini utaweza kwani wenzako wamekusifia sana na kukupendekeza kuwa unafaa.Tafadhali naomba ukarejeshe heshima ya idara hii ambayo ina umuhimu mkubwa sana.Kwa kuwa umesafiri safari ndefu naamini bado una uchovu hivyo basi ninakupa wiki moja ya mapumziko ili kujiweka tayari kwa kazi.Wiki ijayo nitakutangaza rasmi kama mkurugenzi mpya wa SNSA” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais.Mimi nimezoea kufanya kazi usiku na mchana hivyo hata sasa ukiniambia nikaanze kazi niko tayari” akasema Ruby na Dr Fabian akatabasamu kidogo “Ninapenda sana watu kama wewe Ruby wenye ari ya kazi walio tayari kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya nchi yao lakini ninakupa mapumziko hayo ya wiki moja ili kujiandaa kwa sababu kazi unayokwenda kuifanya si kazi ndogo.Unakwenda kuongoza idara kubwa sana na nyeti kabisa.Nimekwisha toa maelekezo kwa wasaidizi wangu wakuandalie nyumba utakayoishi yenye hadhi yako,utapata pia walinzi wa kukulinda kila uendako na kuhakikisha unakuwa salama.Mambo hayo yote yatakapokamilika utafahamishwa” akasema Dr Evans Waliendelea na mazungumzo na ilipofika saa nne za usiku Ruby akaondoka kurejea katika makazi yake ya muda. KAMPALA – UGANDA Gari tatu ziliwasili katika nyumba alimofikia Melanie.Tayari ilikwisha timu saa mbili za usiku.Rais wa Uganda Jenerali Akiki Rwamirama akashuka na kuelekea ndani akiwa na walinzi wake.Moja kwa moja wakaelekea katika mlango wa chumba cha Melanie mmoja wa walinzi wake akagonga mlango na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa na Melanie akiwa na tabasamu akajitokeza.Jenerali Akiki akawaelekeza walinzi wake wampe nafasi akaingia ndani na kuufunga mlango.Kabla hajaketi Melanie ambaye usiku huu alikuwa amevaa gauni jepesi lililoonyesha kila alichokivaa ndani akamkumbatia na kumbusu “Karibu sana mheshimiwa Rais” akasema Melanie na Jenerali Akiki akatabasamu “Nashukuru sana Melanie” akasema Jenerali Akiki na kuketi sofani,Melanie akamkaribisha kinywaji “Umeshindaje leo Melanie? “Nimeshinda salama kabisa.Pole na mihangaiko ya siku nzima”akasema Melanie huku akimvua koti Jenerali Akiki akalitupa pembeni akachukua glasi ya pombe kali akamnywesha “Melanie mapokezi yako si ya kawaida.Ni miaka mingi sijawahi kupokelewa namna hii” akasema Jenerali Akiki “Mke wako hakupokei namna hii?Melanie akauliza “Hapana.Mambo kama haya amekwisha yasahau kabisa.Yawezekana umri ukawa kigezo.Tumekwisha kuwa watu wazima sasa.Wanawake wana tatizo hilo wakifikia umri Fulani yale manjonjo yote waliyokuwa nayo mwanzo wa ndoa yanatoweka mnabaki mkiishi kwa mazoea” “Usiseme wanawake.Wewe umechukua hatua gani kuboresha penzi lenu?.Mheshimiwa Rais mapenzi hayana umri.Ili muyafurahie hata pale mtakapokuwa mmezeeka lazima kila mmoja aweke juhudi za kuyaboresha”akasema Melanie “Ahsante kwa somo hilo Melanie nitalizingatia” akasema Jenerali Akiki na Melanie akamnywesha tena kinywaji kisha akaanza kufungua vifungo vya shati la Akiki akaanza kukichezea kifua chake. “Mimi ni wako kwa usiku wa leo ninajiweka katika mikono yako” akasema Melanie na kumbusu Jenerali Akiki ambaye tayari mashetani yake yalikwisha amka akashika hatamu.Maandalizi ya mechi yalifanyika kisha wakaingia uwanjani. “Hili jamaa linatumia nguvu kana kwamba hii ni mara yake ya mwisho kufanya mapenzi.Hakuna raha yoyote ninayoipata hapa zaidi ya karaha.Ndiyo maaana ninampenda GosuGosu.Ni mwanaume wa aina yake.Ana nguvu lakini anajua kuzitumia na si kama huyu jamaa.Ngoja nimuache ajiridhishe ninachotaka ni mambo yangu yafanikiwe.Ninaamini baada ya kuonja asali hataacha atataka tena na tena na hapo ndipo nitampeleka kama ng’ombe” akawaza Melanie wakati Jenerali Akiki akiendelea kujishughulisha kwa nguvu Akiki alifika mshindo na kujitupa pembeni akihema kama amekimbia kilometa elfu moja. “Keshamaliza hoi kabisa.Muone kwanza.Yale maguvu yote alikuwa anakimbilia wapi? Akawaza Melanie na kumkumbatia Akiki “Ahsante sana mheshimiwa Rais.Sikutegemea u mjuzi hivi wa haya mambo.Umenipeleka mbio..” akasema Melanie. “Ahsante pia Melanie.Huu umekuwa ni usiku wangu wa kipekee kabisa” akasema Jenerali Akiki huku Melanie akiendelea kumchezea kifua kwa mkono wake. “Melanie nina ombi moja kwako” akasema Jenerali Akiki “Omba chochote mheshimiwa Rais.Unataka nini? “Ninaomba tusiishie hapa.Nataka tuendelee.Nataka tuwe wapenzi kwa siri na mimi nitakufanyia kila kitu unachokitaka.Hata ukitaka nikununulie ndege uwezo ninao lakini tafadhali naomba tuendelee” akasema Jenerali Akiki .Melanie akatabasamu na kumbusu kisha akasema “Una maneno matamu sana mheshimiwa Rais.Mimi sina tatizo na ombi lako ili mradi tu unihakishie kwamba mkeo hatajua” “Usihofu Melanie mke wangu hatatafahamu chochote.Itakuwa ni siri yetu kubwa” akasema Jenerali Akiki “Kama unanihakikishia hivyo mimi sina kipingamizi chochote.Tuendelee na mahusiano ya siri” “Ahsante Melanie.Nakuahidi kukupa kila unachohitaji.Nitakufanyia mambo hadi utashangaa mwenyewe” akasema Jenerali Akiki huku Melanie akifanya juhudi za kuamsha mambo ikulu bila mafanikio “Ikulu kumelala kabisa.Haamki tena” akawaza Melanie akainuka kitandani na kumimina pombe kali katika glasi na kumpa Jenerali Akiki wakakaa kitandani “Leo nimekutana na James Kasai” akasema Melanie “Umekutana naye wapi? “Nilimpigi simu akafika hapa.Nilimueleza kuhusiana na ule mpango wangu niliokueleza jana” “Akasemaje ulipomueleza? “Aliukubali ni mpango mzuri lakini akashauri hadi tukutane nawe kwanza tujadili kwa kina.Tafadhali kubali kukutana nasi pale atakapokupigia simu kukuomba”akasema Melanie “Usijali Melanie kesho tutakutana sisi watatu kulijadili hili suala na tutalijadili lile suala lako.Kwa sasa ushirikiano na wale majenerali wa jeshi hakuna tena” “Nakushukuru sana mheshimiwa Rais kwa namna unavyonijali na kukubali kunisaidia katika mpango wangu huu” akasema Melanie “Melanie nimekwisha kueleza kwamba niko tayari kukufanyia kitu chochote unachokitaka ili mradi kiwe ndani ya uwezo wangu.Nimekwambia hata ukitaka ndege nitakununulia” akasema Jenerali akiki ambaye tayari macho yake yalianza kuwa mazito akionekana kuwa na usingizi DAR ES SALAAM – TANZANIA Ilikuwa siku ndefu kwa Mathew Mulumbi.Saa tatu za usiku alikuwa chumbani kwake amekaa kitandani. “Imekuwa siku ndefu nashukuru imekwenda vizuri na sasa ni wakati wa kuwasiliana na Habiba Jawad”akawaza na kuchukua kompyuta yake akajiunga na matandao wa intaneti kisha akampigia simu Habiba “Habari yako Mathew Mulumbi” akasema Habiba Jawad “Nzuri mama shikamoo” “Marahaba habari za Dar es salaam?akauliza Habiba “Dar es salaam kwema ninaendelea vizuri” “Nafurahi kusikia hivyo” “Vipi maendeleo ya Najma? “Anaendelea vyema.Usimpigie simu sitaki ajue uko wapi” akasema Habiba “Nitafanya hivyo mama” “Vizuri.Tayari umekwisha anza kufanya maandalizi ya operesheni? “Ndiyo mama nimekwisha anza maandalizi” “Vizuri.Ukisha kuwa tayari unijulishe.Jitahidi ndani ya kipindi kifupi uwe umekamilisha maandalizi yote” “Nadhani baada ya kesho kila kitu kitakuwa tayari” “Ukishakuwa tayari nijulishe ili niweze kukupa taarifa za kuhusina na James kasai’ akasema Habiba na kuagana na Mathew. “Baada ya miaka mitatu hatimaye leo ninalala katika kitanda changu” akawaza Mathew wakati akijiandaa kulala.





Saa kumi na mbili za asubuhi ilimkuta Mathew Mulumbi akiwa hospitali ya Mtodora alikoenda kumtazama Gosu Gosu.Pale hospitali alikutana na Austin ambaye alilala pale pale na kumjulisha kwamba hali ya Gosu Gosu bado haikuwa na mabadiliko yoyote.Mathew akaomba kuingia ndani ya chumba kile alimo Gosu Gosu akavishwa mavazi na kuingia akavuta kiti na kumsogelea “Gosu Gosu najua unanisikia.It’s me Mathew Mulumbi again.I’m back and I need you.Please wake up.Fight and wake up.Please don’t force me to switch off this machine.If you want to live my brother please fight and wake up !You hear me?Please fight ! Don’t quit ! akasema Mathew kisha akatoka mle ndani.Tayari Austin alikwisha muita mmoja wa vijana kutoka katika kikosi chake kukaa pale hospitali kuhakikisha Gosu Gosu anakuwa salama.Akamtambulisha kijana Yule kwa Mathew “Austin we need to go.Saa tano leo tuna miadi ya kwenda kuonana na Rais.Tunatakiwa kujiandaa” akasema Mathew wakaelekea katika gari na kuondoka “Umewasiliana na mchumba wa Gosu Gosu?Mathew akauliza wakiwa garini “Bado simu yake haipatikani” “Inanipa taabu kidogo.Ni mwanamke wa aina gani huyo ambaye anaweza akamuacha mchumba wake katika hali ile na kuondoka.Kweli ni mchumba wake? Mathew akauliza “Kwa mujibu wa Lucy ni kwamba Gosu Gosu alikwenda Ufaransa na aliporejea ndipo alipoanza kuonekana na huyo mwanamke.Lucy anadai kwamba mwanamke huyo amekuwa akienda karibu kila siku nyumbani kwa Gosu Gosu lakini hajawahi kulala pale.Wakimaliza mambo yao huondoka zake.Hata Lucy mwenyewe hana taarifa za kutosha kuhusiana na huyo mwanamke”akasema Austin “Unasema Gosu Gosu alikwenda Ufaransa? Mathew akauliza “Ndiyo.Kwa mujibu wa Lucy ni kwamba Gosu Gosu alisafiri ya kwenda Ufaransa na aliporejea akaanza kuonekana na huyo mwanamke” “Alikwenda kufanya nini Ufaransa?Mathew akauliza “Hata mimi sifahamu.Hakuwahi kunieleza chochote kama anasafiri na hata suala la kuwa na mchumba alinificha pia.Nimeyafahamu haya yote baada ya kupigwa risasi.Mathew unahisi labda mwanamke huyo anaweza akahusika na tukio hili?akauliza Austin “Siwezi kusema moja kwa moja kwamba anahusika but something is not right about this woman.How she looks like?akauliza Mathew “She’s pretty.Very pretty” akasema Austin “Austin tunatakiwa kumtafuta huyo mwanamke.Nahitaji kumfanyia mahojiano” akasema Mathew “Tutamuuliza zaidi Lucy kwani yeye ndiye anayemfahamu zaidi.Anaweza akatusaidia kufahamu mahala tunakoweza kumpata huyo mwanamke” akasema Austin na ukimya mfupi ukapita “Gosu Gosu alipokwenda Ufaransa alifanikiwa kuonana na Peniela? Akauliza Mathew “Natamani Gosu Gosu afumbue macho hata sasa.Kuna maswali mengi ambayo anatatakiwa kuyajibu” akasema Mathew “Mathew I’m sorry to say this.Hudhani kama Peniela anapaswa kufahamu kwamba uko hai?akauliza Austin na Mathew akatafakari kwa sekunde chache halafu akasema “Hapana.Hapaswi kufahamu chochote kuhusu mimi.Tayari anafahamu kuwa nimekwisha kufa na itaendelea kubaki hivyo.Wamekwisha kubaliana na ukweli na sitaki kuvuruga maisha yao” akasema Mathew “Vipi kuhusu watoto? “Austin sitaki tuongelee suala hilo.Tuna mambo mengi ya kufanya tujielekeze huko kuliko kujadili kuhusu masuala yangu” akasema Mathew “Sorry” akasema Austin na safari ikaendelea kimya kimya “Mathew alikuwa wapi?Kwa nini hataki kuongelea chochote kuhusiana na mahala alikokuwa?Ameibuka tu kutoka kusikojulikana na hataki kuzungumza chochote.Amekuja moja kwa moja akijielekeza katika misheni ya kutaka kumuua James Kasai.Amekuja akiwa anafahamu kila kitu kilichotokea hapa nchini.Amefahamuje mambo haya? Kurejea kwake kunaibua maswali mengi lakini hataki kuulizwa chochote” akawaza Austin. Walikwenda kwanza nyumbani kwa Austin akajiandaa kisha wakaondoka hadi nyumbani kwa Mathew akajiandaa haraka haraka akajitazama “Mwonekano huu unaruhusu kuingia ikulu” akawaza na kutoka chumbani kwake na kukutana na Lucy mtumishi wake “Lucy naomba kwa dakika chache unieleze kuhusu mchumba wa Gosu Gosu” akasema Mathew “Simfahamu vyema.Gosu Gosu hakuwa na mazoea ya kuleta mwanamke hapa nyumbani hadi hivi majuzi aliporejea kutokea Paris Ufaransa ndipo nilipoanza kumuona na huyo mwaname akamtambulisha kwangu kwamba anaitwa Melanie na amekuwa akija hapa mara kwa mara” “Unaweza kufahamu mahala anakoishi? “Hapana sifahamu hajawahi kunieleza” “Kuna kingine chochote unachoweza kukikumhuka kuhusu huo mwanamke? “Simfahamu kiundani na kila ajapo huwa wanajifungia chumbani kwa Gosu Gosu na hajawahi kulala hapa.Simfahamu vyema” akajibu Lucy “Gosu Gosu alikwambia anakwenda Ufaransa kufanya nini?akauliza Mathew “Aliniambia kwamba anakwenda katika mambo ya kibiashara.Hakunieleza zaidi” akasema Lucy “Ahsante Lucy.Nitakuomba kitu kimoja.Ingia katika chumba cha Gosu Gosu jaribu kutafuta picha ya huyo mwanamke ninataka kumuona” akasema Mathew wakaingia garini na kuondoka kuelekea kwa Rais mstaafu Dr Evans.Wakati safari ikiendelea Mathew alikuwa akiyapitia mafaili mawili aliyopewa na Austin kuhusiana na wale watu wawili ambaoMathew alitaka waongezwe katika timu anayoiandaa kwa ajili ya operesheni ya kumuondoa James KasaiAkayapitia kwa makini halafu akayafunika “Si wabaya.Wameiva.Tunaweza kuwatuia” akasema “Itakuwa ni misheni yao ya kwanza toka wametoka mafunzoni” akasema Austin na safari ikaendelea “Mathew kuna kitu nataka ukifahamu” akasema Austin “Kitu gani Austin?akauliza Mathew na Austin akameza mate kulainisha koo na kusema “Watu wote waliamini kwamba umekufa except me and Gosu Gosu.Hatukuamini hilo jambo na tuliwahi kujadiliana tufanye uchunguzi wetu kuufahamu ukweli ” akasema Austin na Mathew akatabasamu “Kwa nini mliamini sijafariki dunia? Mathew akauliza “Binafsi kuna kitu ndani mwangu kilinifanya niamini hivyo.Hakuna hata usiku mmoja umewahi kupita bila kukukumbuka” akasema ustin “Thank you so much.I appreciate that.You are true brothers” akasema Mathew na safari ikaendelea hadi walipofika nyumbani kwa Rais mstaafu Dr Evans.Walinzi wakawafungulia geti wakaingia ndani na kupokewa na mlinzi wa Dr Evans.Siku hii Dr Evans alikuwa na walinzi watatu.Baada ya muda DrEvans akatokea na kusalimiana na akina Mathew “Hatuna muda vijana tuanze safari”akasema Dr Evans wakaingia katika magari na kuondoka. “Ulipozungumza na Rais kuomba kuonana naye ulimueleza jambo linalotupeleka huko?akauliza Mathew “Hapana sikumueleza chochote” akajibu Dr Evans ambaye alionekana bado anamuogopa Mathew “Taarifa nilizozipata asubuhi ya leo ambazo haijatangazwa ni kwamba usiku wa kuamkia leo ndege za Uganda zimeshambulia vijiji vilivyo karibu na mpaka wao na Rwanda na inasemekana watu kadhaa wameuawa.Bado taarifa rasmi haijatolewa lakini hiyo ni taarifa ya kweli kabisa.Taratibu jumuiya ya Afrika Mashariki inamomonyoka.Kinachoniumiz a ni kwamba wakati wa uongozi wangu niliweka nguvu kubwa sana pamoja na marais wengine kuiimarisha jumuiya hii.Zipo faida nyingi za jumuiya hii ambayo kwa sasa imefikia hatua nzuri na kubwa ya kuwa na sarafu moja kwa hiyo haya yanayoendelea hivi sasa yananisonnesha mno” akasema Dr Evans “Usihofu mzee.Jumuiya haitaweza kusambaratika wakati vijana wa kusimama kuitetea tupo.Ninakuahidi tutasimama imara kuhakikisha kwamba jumuiya inaendelea kuwepo na kustawi.Wale wote waliopandikiza chuki na kuleta chokochoko baina ya wanachama ili wapigane wanakwenda kushindwa vibaya.Si muda mrefu wale makuwadi wa mabepari watakwenda kukiona cha mtema kuni.Siku zao zinahesabika” akasema Mathew na Dr Evans akatabasamu “Mathew hujabadilika.Bado ni Mathew yuleyule mwenye maneno mazito ya kizalendo.Nilifanya kos……” akasema Dr Evans na Mathew akamkatisha “Mzee tumekwisha toka huko.Kitabu kile tumekwisha kifunga na kama kuna makosa yalifanyika yote tumeyafukia sasa tunajielekeza katika mambo mengine ya msingi.By the way how’s your daughter?.akauliza Mathew “She’s fine.Kwa sasa anaishi nchini Afrika kusini amepata kazi huko.Huwa ninakwenda kumtembelea mara kwa mara na haachi kukushukuru kwa ushujaa uliouonyesha siku ulipowakomboa” akasema Dr Evans Mathew na safari ikaendelea Waliwasili ikulu na kupokewa na msaidizi wa Rais wakakaribishwa ndani ambako wakamkuta Dr Fabian akiwasubiri. “Mzee karibu sana” akasema Dr Fabian akipeana mkono na Dr Evans “Ahsante sana mheshimiwa Rais” “Nilidhani uko peke yako kumbe umekuja na ugeni” akasema Dr Fabian huku akisalimiana na Austin “Austin.Sikujua kama unakuja na mzee.Vipi hali ya Gosu Gosu? Sikuweza kukupigia kujua hali yake kutokana na kutingwa sana na mambo mengi ya mazishi ya mke wangu.Utanisamehe usije ukaona kama nimewatupa vijana wangu” akasema Dr Fabian “Usijali mheshimiwa Rais tunaelewa kipindi unachokipitia na sisi tuko pamoja nawe” akasema Austin “Anaendeleaje mwenzako?akauliza Rais “Hali yake bado iko vile vile hakuna mabadiliko” “Poleni sana.Nimekwisha wasiliana na uongozi wa hospitali kufanya kila lililo ndani ya uwezo wao kuokoa maisha yake na mimi nikipata wasaa nitakwenda kumtembelea vile vile nimemuagiza mkuu wa jeshi la polisi kuhakikisha jeshi la polisi linawapata watu waliofanya kitendo hicho” akasema Dr Evans “Tunashukuru sana mheshimiwa Rais’ akasema Austin na kukaa Dr Evans akajikuta akitazamana na Mathew “Karibu sana ndugu” akampa mkono.Hakuwa akimfahamu “Anaitwa Mathew Mulumbi.Aliwahi kufanya kazi katika idara yetu ya ujasusi” Dr Evans akamtambulisha Mathew kwa Rais ambaye alishindwa kuzuia mstuko usionekane katika uso wake “Mathew Mulumbi?!! Akauliza kwa mshangao “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ninaitwa Mathew Mulumbi” akasema Mathew na bado Dr Fabian akaendelea kumtazama kwa woga “Mathew Mulumbi yupi? Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Mathew Mulumbi amefariki dunia.Ni jana tu nilikuwa na Ruby hapa tukizungumza akanieleza kwamba ni Mathew Mulumbi ambaye alimfundisha kupenda nchi alikotoka na akasikitika kwamba huyo Mathew amefariki dunia lakini leo ninaletewa Mathew Mulumbi mbele yangu.Dr Evans what is this?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais umesema ulikuwa na Ruby?akauliza Mathew “Ndiyo nilikuwa naye jana na tulizungumza kuhusu marehemu Mathew Mulumbi” “Oh my God ! Ruby is here?akauliza Mathew kwa furaha Dr Fabian akabaki anashangaa “Dr Evans what’s going on?akauliza DrFabian “Mheshimiwa Rais utanisamehe kwa mkanganyiko huu uliotokea.Tunaweza kuzungumza faragha kidogo?akauliza Dr Evans “Excuse us guys” akasema Dr Fabian akatoka mle sebuleni na Dr Evans “Ahsante Mungu.Ruby amekuja nchini ! akasema Mathew kwa furaha “Austin ahsante sana kwa kumshauri Rais amuite Ruby nyumbani.Ulifanya jambo kubwa na zuri sana.I can’t wait to see her ! akasema Mathew na kumpa Mathew mkono wa pongezi “Haya ni maajabu.Nyote wawili watu muhimu mmefika kwa wakati mmoja” akasema Austin “Hii ni mipango ya Mungu.Ni yeye ambaye ametaka iwe hivi ilivyo.Sasa unaweza ukaamini kwamba kwa namna yoyote ile Afrika Mashariki haitaweza kusambaratika” akasema Mathew Dr Fabian na Dr Evans waliingia katika chumba Fulani ambacho hakikuwa na mtu ndani. “Dr Evans nini hiki kinaendelea?I real don’t understand.Mathew Mulumbi ambaye nilielezwa na Ruby kwamba alifariki dunia ni huyu uliyeongozana naye hapa au kuna mwingine?akauliza Dr Fabian “Dr Fabian kuna Mathew Mulumbi mmoja tu ambaye ni huyu niliyeogozana naye” akasema Dr Evans “Haya ni maajabu.Niliambiwa amefariki sasa ametokea wapi tena?Ni yeye kweli au ni mzimu ule? Akauliza DrFabian “Ni yeye mwenyewe Mathew Mulumbi” akasema Dr Evans.Ukapita ukimya mfupi Dr Fabian akauliza “Kwa nini ikadaiwa amefariki dunia? “Kuna hadithi ndefu hapa nitakueleza lakini ukweli ni kwamba Mathew hakufariki dunia kama tulivyodhani.Mathew ni mzima” “Alikuwa wapi? “Hajasema chochote kuhusu mahala alikokuwa.Ameibuka tu toka kusikojulikana.Dr Fabian mimi nawe tutakuwa na mazungumzo marefu kidogo baadae na nitakueleza kila kitu lakini nakuomba nimekuja na hawa vijana tuna mazungumzo nawe” akasema Dr Evans na Dr Fabiana akaonekana kusita “Tafadhali Dr Fabian tunahitaji kuzungumza na hawa vijana” “Kuna nini? Akauliza Dr Fabian “Kuna jambo kubwa la kujadili.Tafadhali sana” akasema Dr Evans “Mzee naomba liwe ni jambo lenye maslahi kwa sababu dalili ninazoziona si njema” “Niamini mimi Dr Fabian” akasema Dr Evans kisha wakatoka na kurejea mahala walikowaacha Mathew na Austin “Samahani tuliwakimbia kidogo.Tulikuwa na mazungumzo ya faragha.Karibuni sana vijana.Mathew Mulumbi karibu sana.Ni furaha yangu kukutana nawe leo” akasema Dr Fabian. “Hata mimi nafurahi kukutana nawe mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Mzee wangu hapa anasema kwamba kuna mazungumzo muhimu.Naomba tuelekee katika chumba cha maongezi” akasema Dr Fabian na kuwaongoza akina Mathew kuelekea katika chumba cha mazungumzo ya faragha “Karibuni sana vijana wangu.Mtanisamehe kwa mkanganyiko uliotokea awali” akaanzisha maongezi Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nimekuja na hawa vijana wangu kwa ajili ya mazungumzo muhimu yanayohusiana na kile kilichotokea na kinachoendelea hivi sasa katika nchi yetu na Afrika Mashariki kwa ujumla.Nisiwe mzungumzaji mkubwa naomba nimpe nafasi Mathew Mulumbi aendelee” akasema Dr Evans “Karibu Mathew” akasema Dr Fabian na bila kupoteza muda Mathew akasema “Mheshimiwa Rais,kama rais mstaafu Dr Evans alivyokwisha nitambulisha kwako naitwa Mathew Mulumbi,niliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi Tanzania kabla ya kuanza kujishughulisha na biashara lakini hata wakati ninafanya biashara zangu bado niliendelea kushiriki katika misheni mbali mbali kubwa zenye maslahi mapana kwa nchi yetu”akanyamaza kidogo “Sitaki kuongelea tukio la mimi kupotea na kujulikana nimefariki dunia na nisingependa kuulizwa nilikuwa wapi.Ninaomba nijielekeze moja kwa moja katika suala la msingi lililotuleta hapa” akanyamaza tena kidogo “Japokuwa sikuwepo hapa nchini lakini ninafahamu kile kilichotokea na kinachoendelea na baada ya kufika hapa nchini nikapata tena taarifa nyingine ambazo sikuwa nikizifahamu kuhusiana na hiki kinachoendelea hivi sasa.Ambacho sikuwa ninakifahamu ni mauaji ya Lucy Muganza na mumewe” akasema Mathew na kunyamaza huku wote mle ndani wakimsikiliza kwa makini sana “Mheshimiwa Rais kinachoendelea hivi sasa ni mpango mkubwa wa nchi kubwa tajiri kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki nadhani unalifahamu hilo ndiyo maana Lucy Muganza akauwa” akasema Mathew na Dr Fabian akatikisa kichwa kukubaliana naye. “Baada ya kifo cha Lucy Muganza mambo hayakuishia pale.Mpango ule bado uliendelea na hiki kinachoendelea hivi sasa ni muendelezo wa kile alichotakiwa kukifanya Lucy Muganza lakini akawahi kuuawa.Mataifa walioandaa mpango huu wanailenga zaidi jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini hawawezi kuingia nchini Congo bila kuiondoa kwanza nchi hiyo katika jumuiya ya Afrika Mashariki na ili kuiondoa nchi ya Congo katika jumuiya ya Afrika mashariki lazima kwanza kuisambaratisha jumuiya hiyo na kile kilichotokea juzi hapa nchini ni mkakati wa mabeberu kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki na kutengeneza njia kuelekea Congo.Tayari mpango wao huo umeanza kuonyesha matunda kwani umetokea mvurugano mubwa baina ya nchi wanachama na kuna kila dalili kwamba uhai wa jumuiya hii uko mashakani” akanyamaza kidogo na kumtazama Dr Fabian aliyekuwa ameweka mkono shavuni akisikiliza kwa makini sana “Wametumia akili kubwa kumtumia James Kasai kutekeleza shambulio lile na kuamsha hasira kali na sasa kila nchi inataka kuishambulia Uganda kwa kigezo cha kumsaka au kulipiza kisasi kwa James Kasai.Utaniwia radhi mheshimiwa Rais lakini sina lugha nyingine ninayoweza kuitumia kulisema hili lakini mlikurupuka sana kuanza kuchukua hatua za kijeshi.Hamkutakiwa kuishambulia au kupanga mipango ya kuingia Uganda kijeshi kwa ajili ya kumsaka James Kasai.Wewe mheshimiwa Rais ukiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki ulitakiwa kuwa mstahimilivu na kutafuta njia muafaka ya kulimaliza hili suala lakini ulikuwa mstari wa mbele kuwaunganisha Rwanda na Congo kuunda kikosi cha jeshi kwenda nchini Uganda.Naweza kusema kwamba kuna mkono wako katika mvurugano huu unaoendelea hivi sasa katika eneo la Afrika Mashariki” akasema Mathew na kunyamaza baada ya sura ya Dr Fabian kubadilika “Dr Evans nini hasa kimekuleta hapa? Umewaleta vijana hawa waje waanze kunifundisha uongozi? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nadhani ungeendelea kumsikiliza Mathew Mulumbi bado hajamaliza kile anachotaka kukueleza” akasema Dr Evans “Huu ni upotevu mkubwa wa muda wangu ..” akasema Dr Fabian huku akitaka kunyanyuka “Sir,we’re not wasting any of your time” akasema Mathew “Yes you are. Nimekaa nanyi hapa kwa heshima ya huyu mzee wangu lakini kumbe mambo mnayokuja kunieleza ni upuuzi mtupu” “Si upuuzi mheshimiwa Rais” akajibu Mathew naye akasimama “Mathew please sit down” akasema Dr Evans “Ndiyo ni upuuzi mtupu.Unadiriki kunifundisha mimi namna ya kuongoza nchi?! Who are you?Unadiriki kumtetea gaidi muuaji ambaye ameua watu kikatili kabisa.Wewe ni nani kuhoji maamuzi yangu?Mimi ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ninayeogoza watu zaidi ya milioni hamsini ambao natakiwa kuhakikisha usalama wao wewe ni nani wa kuhoji hatua ninazozichukua? Akafoka Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nafahamu umeumizwa na kifo cha mke wako na hata sisi sote tumeumizwa pia likini hatua zile ulizozichukua wewe na wenzako wa Rwanda na Congo kukabiliana na suala hili si hatua sahihi.Narudia kusema tena na utanisamehe kwamba mlikurupuka ! akasema Mathew na Dr Fabian akamtazama kwa hasira “Dr Evans ninakuheshimu sana mzee wangu na nilitegemea una kitu kikubwa unakuja kunieleza lakini kumbe umeniletea huyu mgonjwa wa akili.Narudia tena kukuuliza Mathew Mulumbi wewe ni nani wa kuhoji maamuzi ya Rais? Unadhani katika watu milioni hamsini ninaowaongoza wewe pekee ndiye mwenye akili kubwa kuliko wote? Akauliza Dr Fabian akiwa amewaka hasira “Dr Evans nashukuru kwa kuja kunitembelea.Tumemaliza kuna mambo mengine natakiwa kuyafanya” akasema Dr Fabian na kugeuka kuanza kuelekea mlangoni “Mr President we’re not finished yet. You have to listen to me ! akasema Mathew “Siongei na wagonjwa wa akili mimi ! akafoka Dr Fabian akipiga hatua kuelekea mlangoni “You’re not going to find James Kasai ! akasema Mathew na Dr Evans akageuka “What ?akauliza “Umenisikia vizuri mheshimiwa Rais.Hamtaweza kumpata James Kasai ! Mathew akasisitiza na Dr Fabian akatoa kicheko kidogo “Dr Evans hiki kituko gani umeniletea mzee wangu? Akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais naomba umsikilize Mathew kile anachotaka kukueleza.Ana kitu cha muhimu sana” akasema Dr Evans “Dr Evans nakushangaa sana.Unamuaminije huyu mtu? Ameibuka kutoka kusikojulikana na halafu unamuamini? Ni vipi kama…oh my God ! akasema Dr Fabian “Mr president I know Mathew Mulumbi and I trust him.Nisingeweza kuja naye hapa kama hana kitu cha maana cha kukueleza ! akasema Dr Evans “Please Mr president ! akasema Dr Evans “Kwa heshima ya huyu mzee ambaye ninamuheshimu sana nakupa dakika tatu unieleze hicho unachotaka kukisema lakini ukiendelea na upuuzi wako wa kuhoji maamuzi yangu kikao hiki kitakuwa kimefika mwisho” akasema Dr Fabian “Thank you Mr President” akasema Mathew “Samahani kwa maneno niliyoyatumia awali yawezekana yalikuwa makali lakini ninaendelea kusisitiza kile nilichokisema kwamba hatua za kijeshi dhidi ya Uganda kwa kigezo cha kumsaka James Kasai hazitakuwa na manufaa yoyote badala yake zitakuwa ni kama kuongeza mafuta katika moto” “Mathew unaniudhi mno kwa kauli hiyo ya kwamba maamuzi yetu ya kutumia nguvu za kijeshi hayakuwa maamuzi sahihi.Hatukuwa wajinga tuliofanya maamuzi haya ya kuunda kikosi cha pamoja kwenda Uganda kumsaka James Kasai ! akasema kwa ukali Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninasema kwamba hayakuwa maamuzi sahihi kwa sababu hamtaweza kumpata James Kasai kwa nguvu za kijeshi” “Kwa nini tusimpate? Wewe unafahamu sana kuliko sisi?Mimi ni Rais wa nchi na nina kila taarifa za kila kinachoendelea hapa nchini hivyo hatukukurupuka narudia tena kusema kwamba iwe mvua iwe jua lazima James Kasai apatikane ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ni kweli una kila taarifa ya kila kinachoendelea hapa nchini lakini kwa bahati mbaya wewe na wenzako hamna taarifa sahihi kuhusiana na James Kasai ndiyo maana mkachukua maamuzi yale lakini kama mngekuwa na taarifa sahihi msingeandaa kikosi kwenda Uganda kumsaka” “Wewe unazo hizo taarifa za James” “Hicho ndicho hasa kilichonirejesha nyumbani” akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema “Nimekuja kwa lengo moja tu kummaliza James Kasai na kuiokoa jumuiya yaAfrika mashariki katika hatari ya kusambaratika” akasema Mathew na Dr Fabian akatoa kicheko “Wewe ! akasema Dr Fabian kwa mshangao “Unataka kumuondoa James Kasai? Unajua unachokizungumza Mathew Mulumbi? Akauliza Dr Fabian na kumgeukia Dr Evans “Dr Evans nilikwambia umeniletea mgonjwa wa akili.Hajui anachokizungumza ni kitu gani” “Dr Fabian ninakuheshimu sana na ninakuomba uniheshimu pia.Huyu anayezungumza si mgonjwa wa akili na anajua anachokisema” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais ninamaanisha kile ninachokisema kwamba nimekuja kummaliza James Kasai na kuinusuru jumuiya ya Afrika Mashariki.Ningeweza kumuondoa James kima kimya bila kukueleza chochote kwani ninazo taarifa zote za kuhusiana naye lakini nimekuja kwako kukueleza kuhusiana na kile ninachotaka kukifanya na kukuomba usitishe operesheni zote za kijeshi mlizopanga kuchukua kuhusu kumsaka James Kasai na vile vile uwashauri wenzako wa Rwanda na Congo waondoe majeshi yao katika mipaka ya nchi zao na Uganda” akasema Mathew na Dr Fabian akazama mawazoni kisha akauliza “Taarifa gani unazo kuhusu James Kasai ambazo unadhani sisi hatuna? “Mnachofahamu ni kwamba James Kasai amejificha katika misitu ya Kaskazini mwa Uganda.Siyo Sahihi.James Kasai hayuko huko” “Kama hayuko huko msituni yuko wapi?akauliza Dr Fabian “Siwezi kusema kwa sasa yuko wapi lakini hayuko msituni na mkipeleka kikosi msituni utakuwa ni upotevu wa muda na uchokozi kwa Uganda” “Kama hujui mahala alipo James Kasai unataka kumuondoa vipi? Dr Evans huyu mtu anacheza na akili zetu.Anasema anao uwezo wa kumuondoa James Kasai lakini hajui mahala alipo” “Hata kama ningekwambia usingeniamini.Umetanguliza hasira mbele unataka kulipiza kisasi kwa kifo cha mkeo bila kuzingati maslahi mapana ya nchi na jumuiya ya Afrika mashariki.James Kasai amezidi kujitanua na kwa sasa amejiunga na kundi la kigaidi la IS ambao wanamfadhili kwa fedha na vifaa vya kijeshi na ana nguvu kubwa hivyo mnapofikiria kupambana na James Kasai mfikirie pia kuhusu kupambana na kundi la kigaidi la IS.Mheshimiwa Rais tafadhali nakuomba uniamini hiki ninachokwambia kwamba ninao uwezo wa kumuondoa James Kasai na vile vile kuuondoa mzizi wa kundi la IS ambalo kwa miaka ya karibu limeendelea kujiimarisha katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.Mimi si mwanasiasa na sina maneno matamu ya kukushawishi lakini nilichokueleza hapa ni ukweli mtupu.Ni juu yako kufanya maamuzi aidha kufuata yale niliyokushauri au kuendelea kuibomoa jumuiya ya Afrika mashariki kwa kuendelea na mipango ya kijeshi dhidi ya Uganda” akasema Mathew.Dr Evans akakohoa kidogo na kusema “Mheshimiwa Rais kijana ameweka wazi kila kitu.Ninamfahamu Mathew Mulumbi na ninasimama upande wake.Alichokueleza ni sahihi na maamuzi yote ni juu yako.Mimi kwa ushauri wangu badala ya kuendelea kumpinga na kumuona kama mgonjwa wa akili ungekubali kushirikiana naye kwani anahitaji sana kuungwa mkono kwa kitendo hiki cha kizalendo anachotaka kukifanya.Imekuwa ni kawaida ya Mathew kuyaweka hatarini maisha yake kwa maslahi ya taifa lake hivyo ni mtu anayehitaji kupongezwa na si kubezwa.Lakini kama bado unamuona ni mwendawazimu basi endelea na mipango yako ya kijeshi na wenzako na utauona mwisho wake.Mimi na vijana wangu tunaondoka lakini pale maji yatakapofika shingoni usijaribu kunitafuta au kuwatafuta vijana hawa” akasema Dr Evans na kusimama “Mheshimiwa Rais kabla hatujaondoka nataka kuuliza swali.Nani alitoa wazo la kuundwa kwa kikosi cha umoja kwenda kuivamia Uganda kumsaka James Kasai?akauliza Mathew Dr Fabian akabaki kimya “Lilikuwa ni wazo lako mheshimiwa Rais? Dr Evans naye akauliza “Lilikuwa ni wazo la pamoja” “Nani aliyelileta mezani?akauliza Mathew na Dr Fabian akabaki kimya “Ukimya huo unaonyesha kwamba si wewe uliyebuni wazo hilo la kuundwa kwa kikosi cha jeshi cha pamoja kwa ajili ya kwenda Uganda kumsaka James Kasai.Wazo hilo lilitoka aidha kwa Rais wa Rwanda au Congo.Mheshimiwa Rais utanisamehe kwa mara nyingine tena kwa lugha ninayotumia lakini labda nizungumze kwa kiingereza they’re using you.Rwanda na Congo kila moja kwa muda mrefu imekuwa na mahusiano yasiyo mazuri na nchi ya Uganda na wanataka kutumia nafasi hii kuiadhibu Uganda.Wote wamejificha ndani ya koti lako la inaonekana kwamba ni Tanzania ndiyo inayoongoza kikosi hicho kinachoandaliwa kwenda Uganda.Mheshimiwa Rais tunao uwezo wa kumuondoa James Kasai kimya kimya bila hata kutumia nguvu za kijeshi na kuinusuru jumuiya hii ya Afrika Mashariki kusambaratikia katika mikono yako.Kama ni kulipiza kisasi kwa kile alichokifanya James kumuua mke wako nakuahidi ninaweza kumleta akiwa hai na wewe ukamfanya kile utakacho ili kumaliza hasira yako” akasema Mathew na Dr Fabian akainamisha kichwa kafikiri kwa muda na kusema “Mathew una hakika unao uwezo wa kumuondoa James Kasai? Akauliza Dr Fabian “Ndiyo mheshimiwa Rais.Ninao uwezo wa kumuondoa James Kasai na ndicho ambacho nimekuja kukifanya na nitaendelea na mipango yangu hiyo hata kama hautakubaliana nami kwa sababu kwa mipango yenu hamtaweza kumuondoa James Kasai na ataendelea kuwa mtu hatari kwa eneo hili la Afrika mashariki ” akasema Mathew “What do you need?akauliza Dr Fabian na Dr Evans akaonyesha tabasamu usoni “Kitu cha kwanza ninachokihitaji ni kuwasiliana na marais wenzako wa Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuwataka waondoe vikosi vyao vya jeshi katika mipaka ya nchi zao na Uganda.Tunataka kwanza kuondoa hatari ya kutokea machafuko makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na hilo litawezekana pale ambapo vikosi vya jeshi vitaondolewa mipakani na wewe kama mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki ndiye mwenye uwezo wa kulifanya hilo na si mimi wala Dr Evans” akasema Mathew na Dr Fabian akaguna “Mathew suala hilo si rahisi kama unavyodhani.Mataifa haya mawili wote wamekwisha athirika na James Kasai.Amefanya ukatili mkubwa Congo na hata Rwanda pia na kwa muda refu nchi hizi mbili zimekuwa zikiishinikiza Uganda kumfukuza James katika misitu ya nchi hiyo lakini Uganda imekuwa ikipuuza na kwa sasa wameamua kuchukua hatua.Nafahamu kama ulivyoeleza kuwa nchi hizi zimekuwa na migogoro yao ya muda mrefu lakini kwa sasa wote wamepata chanzo cha kutaka kuishambulia Uganda.Wazo la kuundwa kwa kikosi cha pamoja halikuwa langu bali la Rais wa Rwanda.Kwa upande Fulani ninaanza kukubaliana nawe Mathew kwamba yawezekana tuliharakisha sana kufanya maamuzi yale ya kutumia nguvu za kijeshi kutafuta James Kasai na sasa inaniwia ugumu namna ya kuanza kuwashawishi hawa wenzangu kutokutumia nguzu za kijeshi.Lazima watajitenga nami na kujiunga wao wenyewe wakaendelea na operesheni zao.Kitu cha msingi ambacho kinaweza kunipa hata mimi nguvu ya kuwataka waondoe majeshi yao mpakani ni kama tukifanikiwa kumuua James Kasai .Hawatakuwa tena na sababu nyingine ya kuendelea na mapambano na Uganda hivyo Mathew Mulumbi kama kweli unataka kusaidia katika jambo hili muue James Kasai na mambo yote yatakuwa yametulia” “Ahsante mheshimiwa Rais kwa kuanza kunielewa.Narudia kukuhakikishia tena kwamba uwezo wa kumuua James Kasai ninao na nitamuondoa lakini naomba japo kwa kipindi hiki ambacho nitakuwa nikilishughulikia suala hilo operesheni zozote za kijeshi zisifanyike nchini Uganda ili kutokuharibu mambo” “Ninakupa siku saba Mathew uwe umempata James Kasai na kama ukishindwa ndani ya siku hizo saba basi kikosi cha umoja kitaendelea na kazi yake bila kujali athari zitakazojitokeza kwani hatuwezi kuendelea kumuacha huyu mtu mmoja aendelee kuua watu hovyo wakati uwezo wa kumuondoa tunao.Ninakuruhusu ukafanye operesheni yako ndani ya siku saba uwe tayari umempata James” “Ahsante mheshimiw Rais.Nakuahidi kabla ya siku hizo saba hazijamalizika nitakuwa nimempata James Kasai” “Kitu gani unahitaji nikusaidie?akauliza Dr Fabian “Kitu cha kwanza ninachokihitaji ni kuunda timu ambayo tutaifanya hiyo operesheni.Tayari ninaye Austin.Nilimtegemea Gosu Gosu lakini kwa bahati mbaya amepigwa risasi lakini tayari tumekwisha pata vijana wengine wawili ambao tutasaidiana nao vile vile ninamuhitaji Ruby” “Ruby? Akauliza Dr Fabian “Ndiyo.Ninamuhitaji sana Ruby katika operesheni hii” “Ruby nimemuita hapa nchini kwa ajili ya kazi nyingine kabisa.Operesheni hiyo ni hatari na siwezi kuruhusu akajiunga na timu hiyo na kuhatarisha maisha yake” akasema Dr Fabian “Ninamuhitaji Ruby pamoja na idara anayokuja kuiongoza” akasema Mathew “SNSA? Unaifahamu idara hiyo?akauliza Dr Fabian “Ndiyo ninaifahamu vyema” akasema Mathew “Ruby bado sijamkabidhi rasmi nafasi ya ukurugenzi wa SNSA na nimempa nafasi ya kupumzika kwa wiki moja kabla ya kuanza kazi rasmi” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais hii ni vita na hakuna muda wa kupumzika.Ruby anatakiwa aanze kazi mara moja.Tunaihitaji ile idara ikiwa chini yake.Nakuomba ikiwezekana hata kesho ukamkabdhi ofisi.Ruby ni mchapkazi hachoki hata ukimuita hapa sasa hivi na kumkabidhi ofisi ataanza kazi hivyo hakuna haja ya kumpa mapumziko ya wiki nzima”akasema Mathew “Mathew unanilazimisha kufanya jambo ambalo sikuwa nimelikusudia.Ruby amepitia mambo mazito hadi kufika hapa ndiyo maana nimempa muda wa kupumzisha akili yake” “Mheshimiwa Rais najua unalo tatizo la kuamini watu lakini nakuomba katika hili ujaribu kuniamini” “Mheshimiwa Rais hata mimi nakusisitiza kwamba mtimizie Mathew kila anachokitaka na hutajutia” akasema Dr Evans “Kwa ajili yako Dr Evans nitafanya lakini roho yangu haitaki kabisa” akasema Dr Fabian na Mathew akainuka “Mheshimiwa rais ahsante kwa kulikubali ombi langu.Sina kingine ninachohitaji toka kwako.Ninachoomba kwa sasa ni kuonana na Ruby” akasema Mathew na Dr Evans akamuita mmoja wa wasaidizi wake akamtaka awapeleke akina Mathew katika nyumba yake aliko Ruby.Mathew na Austin wakawaaga Dr Fabian na Dr Evans wakaondoka kuelekea anakoishi Ruby. “Dr Evans nini hiki umenifanyia leo? Sikutegemea kabisa ! akasema Dr Fabian baada ya akina Mathew kuondoka “Fabian leo umefanya kitu kibaya sana.Umeonyesha dharau kubwa kwa Mathew Mulumbi.Sikutegemea kabisa.Taifa linamuhitaji sana Mathew kwa wakati huu na ninaweza kusema kwamba ni Mungu ndiye aliyemleta.Hukupaswa kumtamkia maneno kama yale” akasema Dr Evans “Utanisamehe mzee wangu lakini Yule kijana aliniudhi sana.Kuibuka kutoka kusiko julikana halafu anaanza kuhoji maamuzi yangu.Anataka kunifundisha namna ya kuongoza nchi.Sikupenda jambo lile” “Hakuwa anakufundisha kuongoza bali alikuwa anasema kitu cha kweli.Makosa makubwa yamekwisha fanyika Fabian japokuwa hamtaki kukubali na ulipaswa kushukuru kwani Mathew Mulumbi ndiye ambaye amekuja kurekebisha pale ulipokosea.Hakukosea kusema kwamba mliongozwa na hasira kufanya maamuzi yale ya kuandaa kikosi cha jeshi kumsaka James Kasai.Alitumia lugha kali kidogo ya kukurupuka na mimi ninarudia kusema kwamba mlikurupuka.Fabian kinachoendelea hivi sasa Afrika mashariki kinawafanya mabeberu wafungue chupa za shampeni wakifurahia.Muache Mathew Mulumbi akamuondoe James Kasai.Mpe kila anachokihitaji na utaona matokeo yake” akasema Dr Evans. Walikuwa na mazungumzo marefu kisha Dr Evans akaaga na kuondoka







Mathew na Austin waliwasili katika nyumba ya Rais anakoishi Ruby.Walikaribishwa ndani kisha mmoja wa watumishi akaenda kumjulisha Ruby kwamba kuna wageni wake wamekuja kumtembelea.Ruby hakupoteza muda akatoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni huku akijua wageni wale lazima watakuwa wametumwa na Rais.Alipoingia sebuleni mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni Austin “Austin ! akasema kwa sauti ndogo ya mstuko na kuanza kupiga hatua ndogo mara akapawa na mstuko wa mwaka http://deusdeditmahunda.blogspot.com/baada ya kugonganisha macho na Mathew.Mstuko alioupata ulikuwa mkubwa akataka kuzungumza kitu sauti haikutoka midomo ikamtetemeka. “Hallo Ruby ! akasema Mathew lakini Ruby hakujibu kitu alishindwa kuzungumza “Ruby it’s me Mathew.Please say something ! akasema Mathew “I…I…I.don…I don’t kn………..”akasema Ruby akitetemeka mdomo kisha akajikuta ameangukia mikononi mwa Mathew nakuanza kulia machozi mengi “Nyamaza Ruby” akasema Mathew “Why Mathew ?!! Why ?!! akauliza Ruby huku akiendelea kumwaga machozi “Ruby please.I know this is a surprise to you and you have so many question to ask but right now you and I we need to go somewhere” akasema Mathew na Ruby akainua kichwa akafuta machozi na kumtazama Mathew “Oh my God ! Why Mathew?Kwa nini umenitesa namna hii?akauliza Ruby na kukilaza kichwa chake kifuani kwa Mathew akiendelea kulia “Ruby tutazungumza nitakueleza kila kitu lakini kwa sasa nakuomba ujiandae tuondoke” “Sina haja ya kujiandaa Mathew.Twende kokote unakotaka hivi hivi nilivyo” akasema Ruby kisha wakainuka na kuelekea katika gari wakaondoka.Ndani ya gari bado Ruby aliendelea kumwaga machozi hadi walipofika nyumbani kwa Mathew ambako walishuka kisha akampa Austin maelekezo kadhaa na kumuachia gari akaondokanalo wao wakaingia ndani na kuelekea moja kwa moja hadi chumbani kwa Mathew. “Ruby there is only one thing I need right now ! akasema Mathew na kumkumbatia Ruby akaanza kumbusu.Ruby alisisimka unyayo hadi unyweleni.Hatimaye mwanaume Yule aliyempenda kwa moyo wake wote leo hii ametua tena katika mikono yake.Bado Ruby alijihisi kama yuko ndotoni.Kadiri sekunde zilivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kuona mabadiliko katika mwili wake na kugundua kile ambacho kilikuwa kinaendelea.Akamkumbatia Mathew kwa nguvu na kuanza kumporomoshea mabusu mengi.Mathew akaivua fulana akaitupa na Ruby akastuka baada ya mkono wake laini kukutana na makovu makubwa ya vidonda mgongoni kwa Mathew “Mathew what’s this?akauliza “Utauliza baadae..” akasema Mathew huku akiendelea na zoezi.Ruby alishindwa kuvumilia zaidi akamtaka Mathew kuanzisha mpambano.Filimbi ikapulizwa na mpambano wa kukata na shokaa ukaanza.





“Mathew is this real?Au niko ndotoni?akauliza Ruby akiwa amemkumbatia Mathew baada ya kumaliza mzunguko mmoja “Ruby hii si ndoto.Ni kweli tuko wote” akasema Mathew “Mathew ninashindwa niseme nini ndiyo maana ninabaki tu ninalia” “Usilie Ruby ni mimi Mathew Mulumbi Yule Yule unayemfahamu.Usiwe na wasiwasi wowote” akasema Mathew “Ulikuwa wapi?What happened to you? Nimelia machozi mengi sana kwa ajili yako Mathew lakini leo Mungu amesikia kilio changu na amekuleta tena.Naamini haya ni maongozi ya Mungu kwani nimepitia magumu mengi hadi kufika hapa Tanzania lakini kumbe yale yote niliyokuwa nayapitia ni kwa ajili ya kuja kukutana tena nawe Mathew” akasema Ruby na machozi yakaanza tena kumtoka “Ruby huu si muda wa kulia” “Mathew niache nilie tafadhali nimeteseka sana,nimelia sana baada ya kupata taarifa ya kufariki kwako.Nashindwa hata nikueleze vipi” akasema Ruby “Naelewa Ruby.Hata mimi haukuwahi kubanduka katika mawazo yangu.Ruby kuna mengi ya kuzungumza.Naamini unataka sana kujua nini kilinitokea na nilikuwa wapi.Mimi pia nina hamu sana ya kutaka kufahamu mengi kuhusu wewe katika kipindi hiki chote ambacho sikuwepo lakini hayo ni baadae kwa sasa kuna kitu cha muhimu nataka kukufahamisha” akasema Mathew “Niambie Mathew” akasema Ruby “Kuna misheni nzito imenirudisha hapa nyumbani na ninakuhitaji sana katika misheni hiyo muhimu” akasema Mathew na Ruby akaonyesha mstuko kidogo “Mathew hata baada ya masahibu yote kukutokea bado unaendelea na hizi kazi?akauliza Ruby “Ni misheni muhimu sana kwa nchi Ruby” “Misheni ipi hiyo? Akauliza Ruby “Nadhani Rais amekwisha kufahamisha kuhusiana na kile kilichotokea hapa nchini siku chache zilizopita” “Ndiyo nilikutana na Rais jana ikulu tukawa na mazungumzo marefu kuhusiana na kazi aliyoniita nije kuifanya.Rais ameniita hapa nyumbani kwa ajili ya kuiongoza idara ya siri ya mambo ya ndani ya nchi ile ambayo alikuwa anaiongoza Devotha” akasema Ruby “Ninafahamu.Austin amekwisha nieleza kila kitu na Rais pia ameniambia hivyo” “Umeonana na Rais tayari? “Ndiyo nimeonana na Rais.Nilitoka ikulu kuonana naye ndipo nikakufuata” “Umekuja lini hapa nchini? “Nimekuja juzi usiku” akajibu Mathew “What a coincidence” akasema Ruby “Nadhani utaona namna sote wawili tulivyorejeshwa nyumbani katika muda ulio karibu sawa.Sikujua kama nitakutana nawe huku na wewe hukujua kama utakutana nami.Kukutana huku kuna sababu kubwa.Nchi yetu kwa sasa inapitia kipindi kigumu sana kufuatia shambulio lile lililotokea hivi majuzi na kuua wake watatu wa marais,mabalozi na raia wengine.Sitaki kurudia kwani Rais amekwisha kueleza kila kitu” “Ndiyo amenieleza kila kitu jana.Ni tukio baya kabisa kutokea”akasema Ruby “Aliyefanya tukio lile anaitwa James Kasai ambaye ameshirikiana na kundi la kigaidi la IS na kuleta mvurugano mkubwa katika nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.Hivi sasa nchi hazielewani na nyingine zinashambuliana.Huu ni mpango mkubwa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na nchi kubwa na lengo kuu la kufanya hivyo wanailenga jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Shambulio lile ulikuwa ni mtego kwa nchi za Afrika mashariki na kwa bahati mbaya nchi zetu zimenasa katika mtego huo na hivi sasa amani imeanza kutoweka na jumuiya ya Afrika mashariki iko hatarini kusambaratika na mabeberu wanaelekea kupata ushindi.Misheni iliyonileta ni kumuondoa James Kasai na kuutegua mtego wa mabeberu wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Vile vile nimekuja kuung’oa mzizi wa IS uliopo hapa nchini.Ni misheni kubwa na nzito ndiyo maana ninakuhitaji sana uuungane nami katika misheni hiyo” akasema Mathew “Mathew Mulumbi sijawahi kusema hapana kila pale uliponiita kwa ajili ya misheni yoyote toka tumefahamiana na hata sasa siwezi kusema hapana.Lakini Mathew huyu James Kasai anaongoza kundi kubwa la waasi na wanaishi msituni.How are we going to end him?Rais Dr Fabian na wenzake wa Rwanda na Congo tayari wameandaa kikosi cha jeshi ambacho kitakwenda kumsaka James Kasai msituni na kuhakikisha kinamtia nguvuni” “Huo ndio mtego ambao viongozi wetu hawa walitegewa na wamenasa.Kutuma kikosi cha jeshi Uganda ni kosa kubwa wanataka kulifanya kwani kutaongeza machafuko badala ya kumsaka James.Uganda tayari imekiita kitendo hicho ni uchokozi mkubwa na imeahidi kukisambaratisha hicho kikosi endapo kitakanyaga ardhi yake na huo utakuwa ni mwanzo wa machafuko makubwa sana na hicho ndicho mabeberu wanakihitaji.Ninasema kwamba nguvu za kijeshi hazitafaulu kwa kuwa James Kasai haishi msituni kama inavyodaiwa bali anaishi maisha ya kifahari sehemu Fulani jijini Kampala” “James Kasai haishi msituni? Ruby akashangaa “Ndiyo.James haishi msituni.Kwa muda mrefu serikali ya Uganda imekuwa ikimfadhili James katika mapambano yake dhidi ya serikali ya Congo na wakati dunia nzima wakifahamu James anaishi msituni lakini ukweli ni kwamba James anaishi kifahari jijini Kampala.Watu wengi hata ndani ya Uganda yenyewe hawajui kama James Kasai anaishi kifahari katika ardhi yao” akasema Mathew “Unafahamu anakoishi James ?Ruby akauliza “Nitafahamu muda si mrefu mahala alipo na ndiyo maana nilimfuata Rais leo na kumtaka asitishe mipango yote ya kijeshi ya kumsaka James Kasai kwani nimerejea nyumbani kwa ajili ya kazi hiyo”akasema Mathew “Rais amekubali? “Amenipa siku saba niwe nimefanikiwa kumpata James Kasai au atapeleka kikosi cha jeshi cha umoja ambacho kinaendelea na mazoezi hivi sasa.Tayari nimeandaa timu kwa ajili ya operesheni hiyo.Mimi,Austin vile vile tutawaongeza vijana wawili.Gosu Gosu hatakuwepo kwa kuwa yuko hospitali amepigwa risasi na watu wasiojulikana” akasema Mathew “Gosu Gosu amepigwa risasi?! Ruby akashangaa “Ndiyo.Hali yake si nzuri.Kwa hivi sasa anapumua kwa msaada wa mashine” “Oh jamani” akasema Ruby kwa masikitiko “Nimezungumza na Rais tumekubaliana kwamba kesho ataenda kukukabidhi rasmi ofisi ili kazi ianze mara moja.Tutaihitaji sana ofisi ile kwani ina msaada mkubwa kwetu katika misheni hii.Baada ya kumaliza misheni ya James Kasai tutaingia katika misheni nyingine ya kuung’oa mzizi wa IS hapa nchini” akasema Mathew “Mathew kama nilivyokwambia awali kwamba siwezi kusema hapana.Niko nawe katika misheni hii.Ninakuahidi kufanya kila niwezalo kukusaidia kuweza kufanikisha misheni hii” “Ahsante sana Ruby” akasema Mathew na kuanza tena maandalizi kwa ajili ya kuingia katika mzunguko wa pili. KAMPALA – UGANDA Saa moja za jioni,katika makazi ya Rais wa Uganda yaliyo ndani ya kambi ya jeshi,kulikuwa na kikao kinaendelea kati ya Jenerali Akiki Rwamirama Rais wa Uganda.James Kasai na Melanie Davis “Mheshimiwa Rais jana nilikutana na James.Nilimuita mimi na kubwa nililomuitia ni kujadili kwa kina kuhusiana na ule mpango wetu niliouleta kwenu wa kumuua Rais Patrice Eyenga.Tulipokutana mara ya mwisho ulituahidi kutupa mrejesho baada ya kuzungumza na mkuu wa majeshi wa Congo lakini baada ya kutafakari sana nikaona kuungana na wanajeshi wa Congo kutakuwa na changamoto kubwa ambayo ni kuchelewa kwa mpango wenyewe ambao mimi nataka ufanyike haraka.Baada ya kukutana na James tumekuja na mpango mpya” akanyamaza kidogo na kusema “Utampigia simu Rais wa Tanzania na kumtaka aitishe kikao kati yako na Rais wa Congo kwa ajili ya mazungumzo ya kutafuta muafaka kwa njia ya amani.Naamini Rais Patrice Eyenga lazima atakubali kukutana kwa ajili ya mazungumzo hayo.Atakapokuwa Dar es salaam wakati mazungumzo yakiendelea bomu litawekwa katika ndege yake na atakapoondoka kurejea Kinshasa bomu hilo litalipuliwa na utakuwa ni mwisho wa Patrice atakuwa amebaki mtu mmoja katika orodha yangu Dr Fabian Kelelo” akasema Melanie.Baada ya kutafakari kidogo Jenerali Akiki akasema “Ni mpango mzuri na mimi ninauunga mkono lakini ugumu wa mpango huo ni namna ya kuliingiza bomu katika ndege hiyo ya Rais” akasema Jenerali Akiki “Kwa upande huo hakutakuwa na ugumu wowote.Mimi nitalishughulikia suala hilo.Ninao mtandao mpana jijini Dar es salaam hivyo hakutakuwa na tatizo katika kuingiza bomu hilo ndani ya ndege ya Rais” akasema Melanie “Mimi nina wazo lingine lakini halijaenda mbali na mpango huo wa kumuua Patrice Eyenga.Badala ya kupandikiza bomu ndani ya ndege ya Rais,kwa nini tusiandae shambulio la kujitoa mhanga na kuwamaliza marais hao wote wawili kwa wakati mmoja yaani Rais Patrice Eyenga na Rais Dr Fabian Kelelo? Kwa kuwa tayari unao mtandao mkubwa tunaweza kumuandaa mtu atakayebeba bomu na pale Rais Fabian atakapokuwa anamsindikiza Rais Patrice basi mtu huyo atajilipua na kuwauwa marais hao wote wawili kwa mara moja na orodha yako itakuwa imekamilika utaendelea na maisha yako kama kawaida” akasema James Kasai “Huu nao unaonekana ni mpango mzuri sana James” akasema Melanie “Hata mimi naona huu ni mpango mzuri” akasema Jenerali Akiki “Kama nyote mnakubaliana na mpango huu nitazungumza na watu wa IS ili wanipatie mtaalamu wa kuunda mabomu ya kujitoa mhanga ambaye atakuja Dar es salam kwa ajili ya kutengeneza bomu hilo hivyo basi Melanie unatakiwa ufanye mpango ili niweze kuingia Dar es salaam kwa ajili ya jambo hilo.Unao mtandao mkubwa na nina imani kwa mimi kuingia Dar es salaam hakutakuwa na tatizo” akasema James “Ndiyo ninao mtandao mkubwa na unaweza ukaingia na kutoka Dar es salaam bila matatizo yoyote.Kuna idara inaitwa SNSA.Hii ni idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Mkurugenzi wa idara hii yupo katika mtandao wangu na amewekwa pale makusudi kabisa kwa ajili ya kunisaidia mimi kufanikisha operesheni zangu hivyo basi kwa kumtumia yeye na idara yake utaingia Tanzania na kutoka salama” akasema Melanie Waliendelea na kikao na kukubaliana namna watakavyofanikisha suala lile kisha James akamrejesha Melanie mahala alikofikia na yeye akaondoka kuelekea katika makazi yake.Nusu saa baada ya Melanie kurejea mahala alikofikia,Jenerali Akiki akawasili “Mheshimiwa Rais” akasema Melanie kwa mshangao kidogo hakuwa ametarajia kama Jenerali Akiki angeweza kumfuata usiku ule. “Melanie siwezi kupitisha usiku huu bila kuwa nawe ndiyo maana nimekuja.James hajagundua chochote kama mimi nawe tulionana na tukazungumza? “Hajafahamu chochote” “Vizuri sana.Naomba usihofu kila kitu kitakwenda sawa kabisa .Pale mtakapokuwa mmekamilisha mipango yote kuhusiana na hilo bomu basi mtanijulisha na mimi nifanye yala ya upande wangu yaani kuwaita mezani marais hao wanaotakiwa kuuawa.Nitakuunga mkono Melanie katika kila unachotaka kukifanya.Hata hivyo nina wazo moja kwa nini usiingie katika siasa? Mimi nitakupigania na utafika mbali sana.Unaweza hata kuwa Rais” akasema Jenerali Akiki “Hapana mheshimiwa Rais.Sitaki kuwa mwanasiasa.Nina mipango mingine kabisa” “Mipango ipi? Akauliza Jenerali Akiki “Siwezi kuisema kwa sasa ngoja kwanza nimalize mpango wangu wa kulipiza kisasi halafu nitakwambia nini kinafuata” akajibu Melanie DAR ES SALAAM – TANZANIA Mathew na Ruby walirejea nyumbani kwa Mathew baada ya kutoka hospitali kufuatilia maendeleo ya Gosu Gosu ambaye bado hali yake haikuwa na mabadiliko.Ruby alipitiliza moja kwa moja bafuni kisha Mathew akafungua kasiki akatoa kompyuta yake na kuelekea katika chumba cha ofisi akamtafuta Habiba Jawad mtandaoni na kumpigia “Mathew Mulumbi habari za Dar es salaam? “Huku kwema mama.Mnaendeleaje huko?akauliza Mathew “Huku tuko salama.Vipi wewe maendeleo yako? Mipango yako inakwendaje? “Leo nimekutana na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania nikazungumza naye nikamueleza kuhusu misheni yangu ya kumuondoa James Kasai nikamtaka asitishe operesheni zozote za kijeshi wanazotaka kuzifanya nchini Uganda kumsaka James.Hakuonekana kufurahishwa na ombi langu hilo ila amenipa siku saba niwe nimempata James Kasai ama sivyo wataendelea na operesheni zao za kijeshi kama walivyopanga.Tayari nimeunda timu maalum kwa ajili ya operesheni hiyo na sasa ninasubiri maelekezo yako mama ili kazi ianze mara moja” akasema Mathew “Vizuri sana” akasema Habiba na kunyamaza kidogo “Usiku huu nimepata taarifa kwamba kuna mtu anaitwa Khalid Sultan Khalid.Huyu anatokea nchini Syria.Ni mtaalamu mkubwa sana wa milipuko.Taarifa niliyoipata ni kwamba Khalid anakuja Tanzania.Ameelekezwa na viongozi wa IS kwenda Tanzania na kwa taarifa nilizozipata ni kwamba Khalid anakuja kukutana na James Kasai jijini Dar es salaam” “James Kasai anakuja Dar es salaam? “Ndiyo anakuja kukutana na Khalid.Inaonekana IS kwa kushirikiana na James Kasai wanataka kufanya shambulio lingine kubwa jijini Dar es salaam.Kazi yako ni kuhakikisha mipango hiyo haifanikiwi na uhakikishe unamuua Khalid na James Kasai.Mathew kama kuna shambulio linaandaliwa basi litakuwa ni kubwa sana kwani Khalid hushiriki katika mashambulio makubwa makubwa.Taarifa hiyo nimekupa ni jukumu lako wewe na timu yako kuhakikisha mnafahamu ni kitu gani Khalid na wenzake wanakipanga na kama ni shambulio basi mhakikshe halifanyiki na mwisho kabisa Khalid na James Kasai hawapaswi kutoka hai nchini Tanzania.Umenielewa Mathew? Akauliza Habiba “Nimekuelewa mama.Nitatekeleza kama ulivyoagiza .Lini Khalid anatarajiwa kuingia nchini? Akauliza Mathew “Khalid anatumia hati ya kusafiria ya Saudi Arabia yenye jina Nassor Khalid.Kwa taarifa nilizonazo Khalid ataingia nchini Tanzania kesho kutwa.Nitakupa taarifa zote kuhusiana naye kesho usiku” “Vipi kuhusu James Kasai amekwisha ingia Tanzania? Au anatarajiwa kuingia nchini lini na kwa njia gani?akauliza Mathew “Bado sijajua.Mathew siwezi kujua kila kitu.Ni jukumu lako sasa kutafuta James Kasai ataingiaje nchini Tanzania lakini nitakapofahamu chochote nitakujulisha.Nitakutumi vile vile picha za Khalid Khalid ili uanze kumfuatilia” akasema Habiba “Sawa mama nashukuru sana kwa taarifa hizi ulizonipa.Nitaanza kuzifanyia kazi mara moja” akasema Mathew akaagana na Habiba Jawad akaifunika kompyuta yake “Mambo yameanza kupamba moto.IS na James Kasai wanapanga tena shambulio lingine.Safari hii wameliekeza wapi hilo shambulio? Akajiuliza Mathew. “James Kasai ni mtu mweye roho ya jiwe.Pamoja na kujua kwamba anatafutwa sana na serikali ya Tanzania kufuatia shambulio kubwa alilolifanya siku chache zilizopita lakini bado anataka kuingia nchini na kupanga tena shambulio lingine.Kwa nini anajiamini kiasi hiki? Akajiuliza “James hawezi kuingia hapa nchini kama hakuna watu wanaomsaidia.Lazima anao mtandao wake wa watu ambao wanamuwezesha kuingia nchini na kutoka atakavyo.Hana wasi wasi hata kidogo kama anaweza akakamatwa.Lakini ni nani hao wanaomuwezesha kuingia nchini mtu kama huyu?akajiuliza “Ameungana na kundi la kigaidi la IS.Kwa namna yoyote ile hawa ndio wanaomuwezesha kuingia hapa nchini na kutoka bila wasiwasi.Lazima IS wana mtandao mrefu sana hapa nchini na ndiyo maana Habiba alinitaka nije niung’oe.Nakumbua wakati ule hadi waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alikuwa ni mmoja wa watu wao hii inaonyesha ni namna gani hawa jamaa walivyodhamiria kujijenga katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”akawaza Mathew na kuvuta pumzi ndefu “Mwisho wa James Kasai umewadia.Atakapoingia nchini hatatoka salama” akawaza Mathew na kuifungia kompyuta yake katika droo kisha akarejea chumbani na kumkuta Ruby akiwa amejilaza kitandani. “Are you okay Mathew?akauliza Ruby “Kuna taarifa nimeipata kwamba James Kasai anakuja hapa Dar es salaam” “James anakuja Dar es salaam? Ruby naye akashangaa “Ndiyo anakuja Dar es salaam” “He mus be crazy.Anawezaje kuthubutu kuja Dar es salaam huku akijua kwamba anatafutwa kwa nguvu zote kufuatia shambulio lile alilolifanya?akauliza Ruby “Hata mimi nashangaa anajiamini nini” “Taarifa hiyo uliyopata imetoka katika chanzo kinachoaminika?Ruby akauliza “Ndiyo ni chanzo cha kuaminika sana.Si James Kasai pekee anayekuja Tanzania bali pia kuna mtu anaitwa Khalid Sultan Khalid ambaye ni mtaalamu wa milipuko mikubwa ndani ya kundi la IS naye anakuja Tanzania na anakuja kuonana na James Kasai hapa Dar es salaam.Inaonekana kuna shambulio lingine kubwa linaandaliwa na hawa jamaa ndiyo maana wanakuja kukutana hapa Dar es salaam” akasema Mathew na kukumbuka kitu “Habiba alinituma Dubai kushuhudia IS wakisaini makubaliano ya kumtumia James Kasai kiasi kikubwa cha fedha ambacho kilitoka kwa Habiba ndiyo maana Najma alikuwepo kumuwakilisha.Sikumbuki jina la Yule mwanamke mrembo aliyemuwakilisha James lakini nakumbuka alitokea Tanzania.Sura yake bado haijanitoka kichwani,bado ninamkumbuka. Fedha ambazo IS wanampatia James zinapita Tanzania kwa Yule mwanamke.Nina uhakika mkubwa kama James anakuja Tanzania lazima ataonana naye hivyo tukimpata Yule mwanamke tutakuwa tumempata James Kasai” akawaza Mathew na kutoa tabasamu “Sasa nimepata picha kwa nini Habiba Jawad alinituma Dubai nikashuhudie makubaliano yale kati ya IS na James Kasai.Yule mwanamama ana akili sana” akawaza Mathew na kutoka akaelekea katika ofisi yake akachukua kalamu na karatasi Akakaa mezani na kuanza kuikumbuka sura ya Yule mwanamke ambaye alimuwakilisha James Kasai Dubai huku akiichora katika karatasi. “Namshukuru Mungu aliyenipa pia kipaji kikubwa cha uchoraji’akawaza Mathew wakati akiendelea kuichora sura ya Yule mwanamke.Alipomaliza akaitazama picha ile na kutabasamu. “Alikuwa hivi hivi” akawaza Mathew kisha akatoka na kurejea chumbani “Ruby kuna kazi ambayo nahitaji unisaidie” akasema na kumpa Ruby ile picha aliyoichora “Huyu ni nani? Ruby akauliza “Ninataka unisaidie kumfahamu mwanamke huyu ni nani.Kesho utakapokwenda SNSA kitu cha kwanza ambacho ningetaka ukifanye ni kuingia katika kumbu kumbu zote za usajili hapa Tanzania na umtafute mwanamke huyu.Ni muhimu sana” akasema Mathew “Anahusiana na James Kasai?akauliza Ruby “Nitakueleza hapo kesho tutakapokuwa tumepata taarifa zake ndiyo maana nilimtaka Rais akukabidhi ofisi kesho kwani ukiwa ndani ya SNSA una uwezo wa kupata kila aina ya taarifa tunayohitaji” akasema Mathew





Sa kumi na mbli za asubuhi tayari Mathew alikuwa amefika katika nyumba ya Rais alikofikia Ruby akimrejesha baada ya usiku mzima kuwa naye nyumbani kwake.Waliagana kwa miadi ya kuonana tena baadae kisha moja kwa moja akaelekea hospitali alikolazwa Gosu Gosu.Mara tu alipofika hospitali alikutana na Austin ambaye alikuwa na sura yeye tabasamu kubwa “Austin tabasamu hili la asubuhi nashindwa kulielewa” akasema Mathew “Hali ya Gosu Gosu imebadilika ghafla usiku wa leo na kwa sasa ameondolewa katika ile mashine ya kumsaidia kupumua.Madaktari wanasema mifumo yake yote imeanza kufanya kazi vyema na sasa anapumua kama kawaida” “Ahsante Mungu” akasema Mathew na kugonganisha mikono na Austin kisha akaingia katika chumba alichokuwa amelazwa Gosu Gosu.Hakuwa amerejewa na fahamu bado lakini kwa mujibu wa madaktari hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na walitegemea haingechukua muda mrefu kabla hajarejewa na fahamu zake “Ahsante sana Papi kwa hatua hii nzuri.Umezifanya nyuso zetu zitabasamu asubuhi ya leo.Naamini muda si mrefu utafumbua macho.Natamani sana tuonane uso kwa uso Papii” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Mambo yameanza Gosu Gosu.Mji unakwenda kuwaka moto natamani sana ugekuwepo ndugu yangu lakini usijali ninakuhitaji sana katika misheni nyingine zinazokuja.Endelea kupambana,nataka nitakapokuja tena hapa jioni ya leo nikukute ukiwa tayari umefumbua macho na tuzungumze” akasema Mathew kisha akatoka na kumfuata Austin “Mathew nilikuona jana ukimtamkia Gosu Gosu maneno Fulani kwa hisia kubwa.Naamini amekusikia” akasema Austin “Tumshukuru Mungu kwa maendeleo haya mazuri ya Gosu Gosu” akasema Mathew na kumtaka Austin waelekee garini “Ulifanikisha maelekezo yangu ya jana?akauliza Mathew “Ndiyo Mathew.Jana tulipoachana nilikamilisha kila kitu” akasema na kushuka katika gari la Mathew akaenda katika gari lake akachukua mkoba mdogo na kurejea kwa Mathew “Nilifanikiwa kusajili laini tatu za simu kama ulivyokuwa umeelekeza” akasema Austin na kumpatia Mathew simu tatu “Good.Mimi nitakuwa na moja,wewe pia utakuwa na moja na itakayobaki atatumia Ruby.Mambo yameanza Austin.Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba James Kasai anatarajia kuingia hapa nchini sijafahamu lini na ataingia vipi ” akasema Mathew “James Kasai anakuja Dar es salaam? Austin naye akashangaa “Ndiyo Austin.James Kasai anakuja Dar es salaam.Anakuja kuonana na mtu anaitwa Khalid Sultan Khalid ambaye ni mtaalamu mkubwa wa milipuko kutoka katika kundi la IS.Kuna shambulio lingine wanakuja kulipanga hapa Dar es salaam” akasema Mathew “Nimeshangaa sana kusikia huyu gaidi ana mpango wa kuja Tanzania wakati bado vidonda vya shambulio alilolifanya hivi majuzi havijapona” akasema Mathew “Kwa bahati nzuri atakapokuja hatarejea tena Uganda.Utakuwa ndio mwisho wake na kama ananisikia huko aliko labda aahirishe safari lakini kama akija Tanzania ndipo roho yake itakapoachana na mwili” akasema Mathew “Tatizo ni kufahamu ni namna gani ataingia nchini.Je atakuja kwa ndege,atapita kiwanja gani?Hivi sasa video yake imesambaa kila mahala na kila mtu anamjua ni gaidi atapita wapi?Austin akauliza “James anao mtandao wake katika nchi hizi za Afrika Mashariki ndiyo maana mpaka leo imeshindikana kumkamata anaweza akaingia katika nchi yoyote na kutoka vile atakavyo lakini safari hii kiama chake kimefika hatatoka salama”akasema Mathew na kumtaka Austin akawachukue wale vijana wawili waliopanga kuwa nao katika operesheni ile na kupanga wakutane nyumbani kwake ambako ndiko kutakuwa ofisi kuu





Msafara wa Rais wa jamhuroi ya muungano wa Tanzania uliwasili katika jengo la makao makuu ya idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Hakuwa ametoa taarifa kama atafika pale hivyo kufika kwake ulikuwa ni mshangao kwa kila mtu.Edwin Mbeko mkuu wa idara ile alitoka mara moja ofisini kwake na kwenda kumpokea Rais akamkaribisha ndani.Rais hakuwa peke yake alikuwa ameambatana na Ruby wakaingia ndani na wafanyakazi wote wakaacha kazi zao wakasimama mara Rais alipoingia.Akawasalimu kisha akaongozana na Edwin hadi katika ofisi yake “Karibu sana mheshimiwa Rais” akasema Edwin “Nashukuru sana Edwin.Utanisamehe kwa kuja bila taarifa” “Usijali mheshimiwa Rais hapa ni nyumbani kwako huna haja ya kubisha hodi” akasema Edwin “Edwin sitaki kuchukua muda mrefu sana.Nimekuja kwa jambo moja tu la muhimu” akasema na kumgeukia Ruby “Huyu mwanamama niliyeongozana naye anaitwa Annabel Jones.Nimemteua kuwa mkurugenzi mpya wa idara hii kuanzia leo na wewe utaendelea kuwa msaidizi wake.Atatumia ofisi iliyokuwa ya Tamar kwa muda wakati ofisi yake mpya ikiandaliwa.Ahsante sana kwa kukaimu nafasi hii muda mrefu umefanya kazi nzuri na sasa nimempata mtu ambaye atachukua nafasi ya ukurugenzi.Natagemea utampa ushirikiano mkubwa” akasema Dr Fabian na Edwin akajenga tabasamu “Karibu sana mama Annabel.Mimi ni Edwin Mbeko kama alivyosema mheshimiwa Rais nimekuwa nikikaimu nafasi hii ya ukurugenzi kwa zaidi ya miaka mitatu.Ninamshukuru sana Rais kwa kukuteua na ninakuahidi ushiriano mkubwa kutoka kwangu na kwa wafanyakazi wote” akasema Edwin.Baada ya kumaliza kile kilichompeleka pale Dr Fabian akaondoka zake.Baada ya Rais kuondoka Edwin akawataka wafanyakazi wote wakusanyike katika ukumbi mkubwa kisha akaenda kumtambulisha Ruby kama mkurugenzi mpya wa idara ile.Baada ya utambulisho ule akaenda kumfungulia Ruby ofisi ambayo ataitumia na Ruby akaanza rasmi kazi kama mkurugenzi mkuu wa SNSA. Wakati Ruby akiwa ofisini kwake Edwin akatoka na kwenda sehemu ambako alitoa simu na kumpigia simu Devotha “Edwin habari za Tanzania?akauliza Devotha “Habari za huku ni njema lakini kuna jambo limetokea asubuhi hii nimeona nikujulishe mara moja” “Kumetokea nini?akauliza Devotha “Mheshimiwa Rais ametoka hapa muda si mrefu” “Amekuja kutafuta nini? “Amemleta mkurugenzi mpya wa SNSA” “Mkurugenzi mpya? “Ndiyo Devotha” “Kwa nini amekuacha wewe ambaye umekaimu kwa muda huu wote na akamteua mtu mwingine? “Sifahamu hayo ni maamuzi yake.Nimekupigia kukujulisha kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo nitashindwa kuyatekekeleza kwa kuwa sintakuwa na nguvu niliyokuwa nayo awali” “Usijali kuhusu hilo.Tuko karibu sana kumaliza misheni yetu.Umewasiliana na Melanie? “Ndiyo nimewasiliana naye na amenitaka nifanye maandalizi jioni ya leo niende kumpokea kwani anakuja na James Kasai.Tayari nimekwisha fanya maandalizi yote ndege yetu ndogo iko tayari na baadae leo nitaelekea Bukoba kumpokea”akasema Edwin “Una hakika ujio wa huyo mkurugenzi mpya hautaathiri kitu chochote katika mipango yetu?akauliza Devotha “Hapana haitaathiri kitu chochote.Bado ni mgeni na hafahamu kitu chochote” “Vizuri.Tunakutegemea sana Edwin na hakikisha hakuna kitu kitakachoharibika hata kama amekuja mkurugenzi mpya lakini endapo utaona anakuwa ni kikwazo katika kufanikisha mambo yetu basi hakuna haja ya kumchelewesha tumuondoe mara moja” akasema Devotha “Usiwe na hofu Devotha hakuna kitu kitakachoharibika” akasema Edwin “Muda wowote kama kuna tatizo lolote nijulishe haraka sana” akasema Devotha na kuagana na Edwin.





Austin aliwasili katika makazi ya Mathew akiwa aeongozana na vijana wawili Tom Denzel na na Aidan Kengele.Mathew aliyekuwa akiwasubiri kwa hamu akawakaribisha na kuwapeleka moja kwa moja katika ofisi yake “Karibuni sana Ton na Aida.Mimi naitwa Mathew Mulumbi.Naamini tayari kiongozi wenu Austin amekwisha wajulisha mimi ni nani hivyo naomba tuokoe muda na tuelekee moja kwa moja katika suala la msingi” akasema Mathew kisha akaenda mezani kulikokuwa na makaratasi mengi pamoja na picha akaichukua picha moja akaenda kuibandika katika ubao “Mtu anayeonekana pichani anaitwa James Kasai.Huyu ana umri wa miaka arobaini na nne.Ni mzaliwa wa Kivu Kaskazini na amepata elimu yake ya msingi,sekondari hadi chuo kikuu nchini Congo.Ana shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Kinshasa.Baada ya kumaliza chuo kikuu alijiunga na jeshi.Baba yake pia alikuwa mwanajeshi katika jeshi la serikali mwenye cheo cha Jenerali lakini baadae aliasi na kuanzisha kundi lake ambalo lilianza kupambana na serikali.Jenerali Kasai baba yake James aliuawa na majeshi ya serikali na ndipo James alipochukua uongozi wa kukiongoza kikundi cha waasi kilichoanzishwa na baba yake.Baada ya makundi yote ya waasi kukubali kuweka silaha chini na kumaliza machafuko yaliyodumu kwa miaka mingi,ni James Kasai pekee aliyegoma kuweka silaha chini hivyo akatimuliwa kutoka katika misitu ya Congo na kukimbilia nchini Uganda ambako inadaiwa amekuwa akiishi katika misitu iliyo Kaskazini mwa Uganda.Hivi majuzi James Kasai amefanya shambulio hapa nchini na kuua wake za marais wa Tanzania,Congo na Rwanda.Huyu ndiye mtu ambaye tunamsaka.It’s a capture or kill mission” akasema Mathew akawatazama watu wale waliokuwa wakimsikiliza kwa makini sana kisha akaendelea “James Kasai haishi msituni kama inavyodaiwa bali anaishi jijini Kampala.Kwa muda mrefu amekuwa akifadhiliwa na serikali ya Uganda na kwa miaka ya hvi karibuni hali yake kifedha haikuwa nzuri hivyo alilazimika kuingia makubaliano na kundi la kigaidi la IS ambao wanamfadhili kwa fedha na zana za kijeshi.Kwa nini IS wameingia makubaliano na James Kasai na si mtu mwingine?akauliza Mathew “IS wana mpango wa kujitanua barani Afrika na wamechagua kujikita katika eneo la Afrika Mashariki na kati.Kwa sasa wanataka kupata sehemu ya kuweka kambi yao ya mafunzo ya ugaidi na wamekusudia kuweka kambi hiyo katika misitu ya Kaskazini mwa Congo ndiyo maana wanamuhitaji James Kasai.Wanamuwezesha kwa fedha na zana za kijeshi ili aweze kurejea katika misitu ya Congo na kudhibiti eneo hilo.Wataweka kambi yao ya mafunzo ya kigaidi kati kati ya misitu ambayo itakuwa inadhibitiwa na James Kasai na ambaye ndiye atakayekuwa akiwalinda hivyo basi James Kasai ni mtu hatari sana kwa eneo zima la Afrika mashariki.Endapo IS watafanikiwa kujenga kambi yao ya mafunzo ya kuwandaa magaidi basi eneo zima la Afrika Mashariki na kati halitaweza kukalika litakuwa katika hatari kubwa ya mashambulio ya kigaidi hivyo basi kwa namna yoyote ile lazima James Kasai akamatwe au auawe” “Umesema James Kasai haishi msituni bali anaishi jijini Kampala,unafahamu anapoishi? Iwapo tutalazimika kwenda Kampala Uganda kumfuata James ni vipi endapo serikali ya Uganda watagundua kwamba tunafanya operesheni ndani ya Uganda hivyo tukawa tumeanzisha mgogoro? Akauliza Tom Denzel “Swali zuri Tom.Hatuna haja ya kwenda Kampala kumfuata James kwani anakuja hapa hapa nchini” “James anakuja nchini?akauliza Aidan “Ndiyo anakuja hapa nchini.Anakuja kukutana na huyu mtu” akasema Mathew na kuchukua picha nyingine akaibandika ubaoni “Anaitwa Khalid Sultan Khalid.Huyu ni mtaalamu wa milipuko katika kundi la kigaidi la IS.Kukutana kwao jijini Dar es salaam ni kiashiria kwamba kuna shambulio lingine kubwa wanaliandaa kwani Khalid hushirikishwa pale panapotakiwa kufanyika shambulio kubwa” akasema na kunyamaza kidogo “Naamini mtakuwa mnajiuliza James Kasai anafahamu kabisa kwamba anatafutwa kwa shambulio lile alilolifanya kwa nini haogopi kuja Tanzania?Jibu ni kwa sababu tayari anao mtandao wake hapa Tanzania.Fedha ambazo James anapewa na kundi la IS zinapita hapa Tanzania.Kwa sasa mwenzetu mmoja anaitwa Ruby ambaye ameanza kazi leo katika idara moja nyeti ya serikali anashughulikia kumtambua mtu huyo ambaye ndiye IS wanapitishia kwake pesa kwenda kwa James Kasai.Pale atakapokuwa amepata chochote basi atatujulisha.Tom na Aidan nimeambiwa na kiongozi wenu hii itakuwa ni misheni yenu ya kwanza toka mmemaliza mafunzo.Naomba niwaweke wazi wadogo zangu kwamba hii si misheni rahisi hata kidogo.Ni misheni ngumu na ya hatari kwani watu tunaowatafuta ni hatari pia.Kabla ya misheni kuanza rasmi ninawataka kama kuna yeyote anataka kutoendelea na misheni hii awe wazi ili tutafute mtu mwingine wa kushika nafasi yake.Remember we’re doing this for our country” akasema Mathew na vijana wale wakamuhakikishia kwamba wako tayari kuendelea na misheni ile kisha Mathew akawataka wakaanze kujiandaa kwani muda wowote wanaweza wakahitajika.Tom na Aidan wakaondoka kwa kutumia gari la Austin. Dakika chache baada ya akina Tom kuondoka Mathew akajulishwa na walinzi kwamba kuna mgeni wake getini.Akatazama katika runinga iliyounganishwa na Kamera akaliona gari jeusi aina ya Mercedece benz.Hakujua nani alikuwa ndani ya gari lile akaruhusu liingie kisha akashuka kwenda kumtazama mgeni Yule ni nani.Gari lile lilifika hadi karibu na kibaraza kisha mlango ukafunguliwa akashuka Ruby. “Ruby ! akasema Mathew na kuachia tabasamu.Ruby akamfuata akamkumbatia “Karibu sana.Sikutegemea kama ungekuja mida hii”akasema Mathew “Imenilazimu nije kuna kitu cha muhimu” akasema Ruby kisha Mathew akamuongoza wakaelekea ndani “How’s your first day at work?Mathew akauliza “Kikubwa nilichokifanya baada ya kupewa ofisi ni kujikita katika misheni yetu.Masuala mengine yatafuata baadae.Vipi nyie mnaendeleaje?Vipi Gosu Gosu?akauliza Ruby “Mungu mkubwa kwani hali yake imebadilika usiku na sasa mifumo yake yote ya mwili inafanya kazi vyema amekwisha ondolewa katika mashine ya kumsaidia kupumua” akasema Mathew “Ahsante Mungu.Namuombea apone kwa haraka” akasema Ruby “Tunamuhitaji sana” akasema Mathew na kuufungua mlango wa ofisi ambamo alikuwemo Austin akasalimiana na Ruby “Ruby karibu sana.Muda mfupi uliopita tulikuwa na vijana ambao tutashirikiana nao katika misheni hii nikijaribu kuwapa picha ya misheni itakavyokuwa.Vijana wameelewa na wako tayari kwa misheni.Kwa upande wako kuna taarifa gani?akauliza Mathew “Nilipokabidhiwa ofisi nilianza mara moja kushughulikia ile picha uliyoichora.Sijafanikiwa kumpata mwenye ile picha lakini nimefanikiwa kuipata picha ya mtu mwingine ambaye anafanana mno na hii picha uliyoichora.Mwanzoni niliamini ni mwenyewe lakini baada ya kuichunguza hii picha uliyonipa na hii niliyoipata nimekuta kuna utofauti.Picha hii ambayo nimeipata ni ya mwanamke anaitwa Melanie Chuma ambaye ni mfanya biashara.Hana taarifa nyingi na haionyeshi anaishi wapi wala biashara gani anayoifanya.Picha ya Melanie chuma inamuonyesha akiwa na kidoti chesi chini ya jicho na ana kovu katika kidevu chake.Hizo ni tofauti nilizozipata katika picha hizi mbili lakini sura ni ile ile.Mathew kwa kuwa wewe ndiye unayemfahamu vyema huyo mwanamke jaribu kuitazama vyema picha hii ya Melanie Chuma na uthibitishe kama kweli ni yeye.Yawezekana katika mchoro wako ulisahau kuweka vitu hivyo viwili nilivyovitaja” akasema Ruby na kutoa picha katika mkoba wake akampatia Mathew akaitazama picha ile halafu akafumba macho kama vile kuna kitu anakikumbuka “What’s goig on here.Sura hii ni ile ile ya Yule mwanamke niliyemuona kule Dubai akimuwakilisha James Kasai lakini kama Ruby yuko sahihi kuna utofauti.Ninaikumbuka vyema sana sura ya yule mwanamke na hakuwa na kidoti cheusi kwenye jicho lake wala hakuwa na kovu kidevuni vitu ambavyo huyu Melanie Chuma anavyo.Je wawili hawa ni mapacha? Akawaza Mathew na kustuliwa na Ruby “Mathew ! akaita Ruby “Najaribu kuvuta kumbu kumbu zangu kama nilikosea katika ile picha niliyochora lakini sikukosea.Mwanamke Yule niliyemchora hakuwa na kidoti wala kovu” akasema Mathew “Ni vipi kama alifuta kidoti hicho na hilo kovu kwa kutumia poda wanazopaka akina mama” akasema Austin huku akimtazama Ruby “Make up” akasema Ruby “Exctly.Ni vipi kama atakuwa amefunika alama hizo kwa make up? Austin “Kwa nini afanye hivyo?Kuna sababu yoyote inayoweza kumfanya afunike alama hizo kwa make up?Ruby akauliza “Hata kama angetumia make up kufunika hizo alama alizonazo lazima hili kovu la kidonda lingeonekana kwani linaonekana ni kovu kama la kuungua lakini sikuona kovu lolote usoni kwake.Ngozi yake ilikuwa nyororo kama malaika.Kila kitu unachokiona katika picha hii ni yeye isipokuwa alama hizo mbili.It’s real confusing” akasema Mathew na kuiweka picha ile mezani Austin akaichukua akaitazama na kupatwa na mshangao mkubwa. “Nini Austin?Mbona umestuka?akauliza Mathew “Huyu ndiye mchumba wa Gosu Gosu ! akasema “What? “Huyu ndiye mchumba wa Gosu Gosu.Alijitambulisha kwangu anaitwa Melanie” akasema Austin “Austin are you sure?akauliza Mathew “Ndiyo.Nimekutana naye zaidi ya mara moja ni huyu huyu lakini……” akasema Austin na kusita kidogo “Lakini nini Austin?Mathew akauliza “Nikijaribu kuvuta picha ya sura yake hana hili kovu linaloonekana pichani wala hiki kidoti chini ya jicho.Lakini naye alijitambulisha kwangu kwa jina la Malanie ila hakunitajia jina la ukoo wake lakini kila kitu ni hivi hivi”akasema Gosu Gosu “Austin mtazame vizuri kama kweli huyu ndiye mchumba wa Gosu Gosu” akasema Austin “Mathew sina shaka hata kidogo.Nimekutana naye zaidi ya mara moja hivyo siwezi kumpotea.Ni mwenyewe kabisa isipokuwa hizi alama sijawahi kumuona nazo”akasema Austin “Huyu Melanie Chuma ni nani hasa? Je ni ndugu na huyu mwanamke ambaye niliichora sura yake? Akauliza Mathew “Kuna taarifa chache sana kuhusiana na Melanie Chuma ambazo nimezipata” akasema Ruby na kutoa karatasi akampa Mathew akalisoma kisha akalitupa mezani “Taarifa ni chache sana kama alivyosema Ruby ambazo haziwezi kuwa na msaada wowote kwetu.Kwa nini amekuwa na taarifa chache namna hii? Akauliza Mathew lakini hakuna aliyekuwa na jibu.Baada ya muda Ruby akauliza “Mathew huyu mwanamke uliyemchora sura yake ambaye anafanana na Melanie Chuma umekutana naye wapi? Anaingia vipi katika misheni hii? akauliza Ruby.Mathew akainamisha kichwa akafikiri kidogo na kusema “Nimewaeleza akina Austin kwamba James Kasai baada ya kufurushwa kutoka katika misitu ya Congo hali yake ya kifedha si nzuri na alihitaji kukiimarisha kikosi chake kabla ya kurejea tena msituni kupambana hivyo akaingia makubaliano na kundi la kigaidi la IS na katika makubaliano hayo IS walimuahidi kumpa fedha nyingi pamoja na silaha za kisasa kuimarisha kikosi chake.IS wanataka kumtumia James Kasai kwa ajili ya kupata sehemu ya kuweka kambi yao ya mafunzo ya kigaidi katika misitu ya kaskazini mwa Congo.Huyu mwanamke ambaye nimeichora picha yake na kumtaka Ruby amtafute tumfahami ni nani na yuko wapi ndiye alisaini makubaliano ya fedha kati ya IS na James Kasai na fedha kutoka kwa IS zinapita kwake kabla ya kufika kwa James Kasai.Ninaamini kama tungeweza kumpata huyu mwanamke tungepata mambo mengi kuhusiana na James Kasai lakini sasa naona mambo yamejichanganya.Amejitokeza mwanamke ambaye anafanana kwa kila kitu na huyu muwakilishi wa James Kasai lakini kuna tofauti ndogo” akasema Mathew “Mathew kuna kitu ambacho kinazunguka kichwani kwangu.Unasema huyu mwanamke uliyeichora sura yake ndiye anayepokea fedha kutoka IS kwa niaba ya James Kasai? Akauliza Ruby “Ndiyo” akajibu Mathew “Kwani umemfahamu vipi huyo mwanamke? Ruby akauliza.Mathew akatafakari kidogo halafu akasema “ I was there and I witnessed everything” akasema Mathew.Austin na Ruby wakabaki wanamtazama “I don’t understand Mathew.You witnessed what? Akauliza Ruby “Guys” akasema Mathew na kuvuta pumzi ndefu “Hamtaweza kunielewa kwa sasa.Ukweli ni kwamba nilikuwepo na nkashuhudia kila kitu wakati mwanamke huyu Melanie Chuma akisainiana makubaliano na wawakilishi kutoka kundi la IS ya kupokea fedha kwa niaba ya James Kasai.Tafadhali naomba nisiulizwe maswali ilikuaje nikashuhudia jambo kama hilo” akasema Mathew “So you knew about James Kasai and yet you let him do what he did? Akauliza Ruby “Yes I did ! akajibu Mathew “Why Mathew? That’s not Mathew Mulumbi we all know.Mathew Mulumbi katu hawezi kukubali magaidi wakafanikiwa mipango yao ! akasema Ruby “Ndiyo maana nikasema kwamba hamtaweza kunielewa” akasema Mathew “Make us understand ! akasema Ruby “Let’s not talk about that okay? Akasema Mathew na ukimya ukapita “Mathew mahala tulipofika tumekwama na wewe unazo taarifa ambazo zinaweza kutukwamua.Tafadhali tushirikishe na sisi pia kile unachokifahamu ili tusaidiane mawazo namna ya kuweza kulikabili jambo hili linalozidi kuwa gumu” akasema Austin “I didn’t do anything because I was undercover.Please don’t ask me more okay?akasema Mathew “Austin unasema kwamba mchumba wa Gosu Gosu ambaye alijitambulisha kwako kwa jina la Melanie hana alama hizi alizonazo Melanie Chuma? Mathew akauliza “Ndiyo hana alama hizi alizo nazo Melanie Chuma.Nimekutana naye zaidi ya mara moja na sijawahi kumuona na alama hizi japo sura na kila kitu ni Melanie Chuma” akasema Austin “Mwanamke Yule ambaye nilimuona Dubai akisaini makubaliano na IS naye anafanana kwa kila kitu na Melanie Chuma isipokuwa ni hizo alama.Kwa hiyo yawezekana huyo mchumba wa Gosu Gosu ndiye Yule mwanamke ambaye anashirikiana na James Kasai” akasema Mathew “Kwa maelezo haya uliyoyatoa hata mimi naweza kuamini hivyo” akasema Austin “Kama ikiwa hivyo je kupigwa risasi Gosu Gosu kuna mahusiano yoyote na James Kasai?Kuna kitu alikigundua ndiyo maana wakataka kumuua?Mathew akauliza “Lakini mwanamke Yule alionekana kuguswa sana na kitendo kile cha GosuGosukutaka kuuawa.Ni rahisi kumtambua mtu anayeigiza au anayeumia kutoka moyoni,Melanie alionekana kuumia kutoka moyoni.Anaonekana kumpenda Gosu Gosu” akasema Austin “Gosu Gosu alikutana vipi na huyo mwanamke? Mathew akauliza “Kwa maelezo aliyoyatoa Lucy ambaye anaishi humu ndani na Gosu Gosu anadai kwamba Gosu Gosu alikwenda Ufaransa na aliporejea ndipo alipoanza kuonekana na huyo mwanamke.Swali linalokuja ni kwamba je alikutana nae Ufaransa?Je walikuwa na mahusiano kabla ya hapo? Mwenye majibu ya maswali haya ni Gosu Gosu ambaye bado yuko hospitali na hawezi kutujibu maswali yetu” akasema Austin ukapita mfupi ukapita halafu Mathew akatoka akamuita Lucy mtumishi wa ndani “Lucy samahani kwa kukusumbua.Nilikupa kazi ya kuchunguza katika chumba cha Gosu Gosu kutafuta picha ya mpenzi wake je umeipata?akauliza Mathew “Hapana kaka sijafanikiwa kupata chochote.Hakuna picha yoyote ya Yule mwanamke chumbani kwa Gosu Gosu” “Unaweza ukakumbuka lini ilikuwa mara ya mwisho kwa Yule mwanamke kufika hapa nyumbani? “Alifika hapa nyumbani asubuhi ya siku ile ambayo Gosu Gosu alipigwa risasi.Siku hiyo Gosu Gosu hakwenda kabisa kazini walijifungia chumbani baadae mwanamke huyo akaondoka.Ilipofika jioni Gosu Gosu akaondoka lakini hakuniambia anakwenda wapi hadi baadae nilipopata taarifa za kuwa amepigwa risasi” akasema Lucy “Ahsante Lucy unaweza kwenda” akasema Mathew “Lucy ameweka wazi kwamba siku ya Gosu Gosu kushambuliwa mwanamke huyo alifika hapa asubuhi.Kuna kamera za ulinzi tupitie kumbu kumbu tujue gari alilotumia ili tuanze kulifuatilia” akasema Mathew na kuanza kupitia kumbu kumbu za kamera katika siku ambayo Gosu Gosu alipigwa risasi. Gari moja la kifahari lenye rangi nyekundu lilionekana likiingia katika geti na Mathew akasimamisha picha ile ili waweze kuipata namba ya gari.Ruby akaiandika namba ile kisha akaitoa kompyuta yake katika mkoba na kuanza kazi.Mathew akahamia katika kamera iliyo mbele ya nyumba.Gari lile likaenda hadi mbele ya nyumba ile na kusimama kisha mwanamke mmoja akashuka.Aliinamisha sura yake chini wakati akielekea ndani “Inaonekana alifahamu kuna kamera hapa ndiyo maana akainamisha kichwa ili asiweze kuonekana.She’s very smart ! akasema Mathew “Ruby kuna chochote umekipata kuhusiana na hilo gari?akauliza Mathew na Ruby akaguna kidogo “Kuna tatizo hapa.Namba hii imesajiliwa kwa jina la Stella kasamaki lakini jina hili halipo sehemu yoyote.Namaanisha halijasajiliwa katika taasisi yoyote ile” akasema Ruby “Kwa lugha rahisi tunasema ni jina hewa” akasema Austin “Exactly ! Ni hewa.Halipo” akasema Ruby na wote wakatazamana.Mara simu ya Austin ikaita akaipokea akazungumza na aliyempigia na mara sura yake ikabadilika “Austin kuna nini?akauliza Mathew “Gosu Gosu ! akasema Austin kwa wasi wasi “Kafanya nini Gosu Gosu?akauliza Mathew “Aliyenipigia simu ni kijana ambaye nimemuweka pale hospitali kumlinda Gosu Gosu.Anasema hali ya Gosu Gosu imebadilika ghafla na ameondolewa haraka katika chumba alimokuwa amelazwa muda mfupi uliopita na hana uhakika kama ni mzima” akasema Austin “Nini kimetokea tena?Mbona hali yake tayari ilikwisha kuwa nzuri?akauliza Mathew na wote wakatoka haraka wakaingia katika gari la Mathew wakaondoka kuelekea hospitali.Ukimya mkubwa ulitawala ndani ya gari. “Listen to me guys” akasema Mathew “Chochote kinaweza kutokea kwa Gosu Gosu hivyo nawaomba muwe na moyo mgumu.Kumbukeni tunayo kazi kubwa mbele yetu tujielekeze huko.Bado tunaendelea kumchunguza huyu mwanamke ambaye anashirikiana na Jame Kasai.Kabla ya kupata taarifa ya Gosu Gosu tulikuwa tumepata watu wawili wanaofanana karibu kwa kila kitu isipokuwa alama mbili.Mmoja anaitwa Melanie Chuma ambaye ana alama tofauti na mwenzake ambaye naye jina lake ni Melanie lakini hana alama kama za Melanie Chuma.Kiwango cha kufanana cha watu hawa ni kikubwa sana hivyo kunifanya nihisi yawezekana wakawa ni mapacha lakini huyu Melanie mchumba wa Gosu Gosu nashawishika kuamini kwamba ndiye Yule hasa tunayemtafuta kwani yeye hana alama hizi alizonazo Melanie Chuma.Lakini wapi pa kuanzia kumtafuta?Hapo ndipo tumekwama” akasema Mathew akiwa amekaa kiti cha nyuma na Ruby huku Austin akiwa katika usukani “Mathew kuna kitu ninajiuliza.Ni vipi kama huyu ni mtu mmoja?akauliza Ruby “Una maanisha nini Ruby?Austin akauliza “Ninamaanisha ni vipi kama huyu Melanie mchumba wa Gosu Gosu na Melanie Chuma ni mtu mmoja?Kama alivyosema Mathew kiwango cha kufanana kwao ni kikubwa sana isipokuwa tofauti hizo mbili.Ninawaza yawezekana akawa ni mtu mmoja ambaye anatumia majina tofauti ili kutuchanganya” akasema Ruby “Hilo linawezekana kabisa.Hata mimi ninahisi hivyo yawezekana huyu Melanie ndiye huyu huyu Melanie Chuma.Wamefanana karibu kila kitu na hata majina yao ni Melanie.Yawezekana kama alivyosema Ruby akawa ni mtu mmoja lakini mwenye sura mbili tofauti”akasema Mathew “Gosu Gosu angeweza kuzungumza angeturahisishia sana kulifumbua fumbo hili” akasema Austin “Gosu Gosu is not here.Tunatakiwa kujitahidi sisi wenyewe kuhakikisha tunampata huyu mwanamke” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “I have an idea.Ninaikumbuka tarehe ambayo Yule mwanamke aliwekeana saini na IS makubaliano ya kupokea fedha kwa niaba ya James Kasai.Ingia katika kumbu kumbu za wasafiri waliosafiri kupitia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kati ya tarehe hizi tuone kama tunaweza kupata chochote” akasema Mathew na kumpatia Ruby tarehe ambazo alitaka achunguze wasafiri waliosafiri kupitia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere. “Ninaamini kama alisafiri kutokea Dar es salaam kwenda Dubai basi lazima itakuwa ni katika terehe hizo na lazima alipita katika uwanja huu” akasema Mathew na Ruby akiwa na kompyuta yake akaanza kufanya kile alichoelekezwa na Mathew Austin akiwa katika usukani alijitajidi kupita njia ambazo hazikuwa na msongamano mkubwa wa magari ili wawahi kufika hospitali “Aaaaghhh !! akasema Austin kwa hasira baada ya kusimama katika taa za barabarani “Relax Austin.”akasema Mathew “Tunatakiwa kufika haraka hospitali kujua kilichomtokea Gosu Gosu” akasema Austin “Hatuwezi kubadilisha chochote hata kama tukiwahi kufika.Ruby umepata chochote? “Nisubiri kidogo.Mtandao unasumbua” akasema Ruby.Taa zikawaka na safari ikaendelea.Walipokaribia kufika hospitali Ruby akasema “Tayari nimeipata orodha ya wasafiri waliosafri katika tarehe hizi kupitia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kuelekea nchi mbalimbali.Nataka niipitie orodha hii kujua wale waliosafiri kwenda Dubai” akasema Ruby “Good job Ruby.Keep looking” akasema Mathew wakati wakivuka geti la hospitali na kuelekea katika maegesho.Wote wakashuka na kukimbia kuelekea katika jengo la wagonjwa mahututi na kukutana na Yule jamaa ambaye Austin alimuweka kumlinda Gosu Gosu “Jerry nini kimetokea?akauliza Austin “Hata mimi nashangaa.Mgonjwa alikuwa anaendelea vizuri kabisa na tayari alikwisha fumbua macho.Timu ya madaktari walifika wakampima na kusema anaendelea vizuri wakashauri asisumbuliwe tumuache aendelee kupumzika ili arejewe na fahamu kamili.Baada ya kama nusu saa hivi akaja daktari mmoja akampima na kuchoma sindano katika chupa ya maji aliyotundikiwa halafu akatoka.Dakika chache baada ya kutoka nilisikia king’ora kikilia katika chumba cha mgonjwa nikaingia ndani hakukuwa na muuguzi nikakimbia kwenda kuwatafuta wauguzi wengine wakaja mbio na madaktari na kumkuta mgonjwa akitapa tapa kitandani na mara akatulia wakasema moyo wake umesimama.Wakatumia mashine ya umeme ya kuustua moyo na mapigo ya moyo yakarejea halafu wakamuondoa ndani ya kile chumba na kumuingiza katika chumba hiki na mpaka sasa hawajatoka kunipa majibu yoyote.Nawaona wakikimbia wakiingia na kutoka” akasema Jerry “Ee Mungu tafadhali msaidie Gosu Gosu” akasema Ruby kwa masikitiko “Okay guys let’s not panic.Hatujui kilichomtokea mwenzetu na hatujui kinachoendelea kuhusu hali yake.Tusubiri madaktari watakapomaliza kazi yao ya kuokoa uhai wake watatueleza nini kimetokea na vile vile tuwe tayari kupokea taarifa zozote ziwe nzuri au mbaya kwa sababu kwa hatua hii chochote kinaweza kutokea.Tumshukuru Mungu kwa chochote kitakachotokea” akasema Mathew na kugeuka kutazama watu wakikimbia kuelekea sehemu Fulani “Nini kimetokea kule watu wanakokimbilia?akauliza Mathew na mara mlango ukafunguliwa na madaktari watatu wakatoka wakikimbia nao wakielekea kule ambako watu walikuwa wanakimbilia. “Kuna nini?Mbona wote wanakimbilia huko?akauliza Ruby.Wakati wakijiuliza akatokea muuguzi akitokea upande ule watu waliokuwa wakikimbilia Mathew akamsimamisha na kumuuliza kumetokea nini kule ambako watu wanakimbilia “Kuna mfanyakazi mwenzetu amejirusha ghorofani amefariki dunia” “Nini sababu ya kujirusha? akauliza “Hakuna anayejua” akasema Yule muuguzi aliyeonekana kuwa na haraka. “Wakati tunaendelea kusubiri taarifa ya madaktari Ruby tuendelee na lile zoezi” akasema Mathew na Ruby akaikunjua kompyuta yake akaendelea na kazi .Baada ya dakika tano akamuita Mathew aliyekuwa amesimama mbali kidogo na Austin wakizungumza.Wote wakaja mbio “Kuna kitu nimekipata” akasema Ruby “Nimempata mtu anaitwa Melanie Davis .Huyu aliondoka tarehe hii na ndege ya shirika la ndege la Emirates kuelekea Dubai” “Melanie Davis ! Who is she ?Mathew akauliza na Ruby akaendelea kubofya kompyuta yake halafu akasema “Huyu anatumia hati ya kusafiria ya Ufaransa” akasema Ruby “Ni raia wa Ufaransa?Mathew akauliza “Ili kulijua hilo natakiwa kuingia katika mtandao wa GCHQ na kudukua taarifa za Ufaransa kumtafuta huyu Melanie Davis ili kujua kama ni raia wa Ufaransa”akasema Ruby “Hilo ni jambo la hatari sana Ruby.Hawa jamaa wanaamini tayari umekwisha fariki katika ajali ya ndege itakuwa ni hatari kubwa kwako wakijua kama uko hai bado” akasema Mathew “Mathew usemacho ni kweli.Ninachotaka kufanya ni kitu cha hatari lakini tunahitaji sana kupata taarifa za Melanie Davis hivyo hatuna ujanja lazima nifanye hivyo” “Unadhani hakutakuwa na tatizo kwa upande wako? Mathew akauliza “Nitajaribu kutumia njia ambayo hawataweza kunigundua” akasema Ruby “Sawa fanya hivyo” akasema Mathew na Ruby akaanza kucheza na kompyuta yake huku Mathew na Austin wakishuhudia.Wakati Ruby akiendelea na zoezi lile,madaktari wawili wakatoka akina Mathew wakawafuata.Wakajitambulisha kwamba wao ni ndugu za Gosu Gosu.Daktari mmoja aliyevaa kitambulisho kilichomuonyesha anaitwa Dr Masawe akawataka waelekee sehemu kwa ajili ya mazungumzo.Ruby akakunja kompyuta yake akaongoza na akina Mathew hadi katika chumba maalum kwa ajili ya mikutano.Madaktari wakaongezeka na kufika wanne.Dr Masawe akasema “Vijana wangu tumewaiteni hapa kuwapeni taarifa za kuhusiana na maendeleo ya mgonjwa wenu na kile kilichotokea.Usiku wa kuamkia leo hali yake ilibadilika na kuwa nzuri mifumo yake yote ilianza kufanya kazi vizuri kama kawaida hivyo tukamuondoa katika mashine ya kumsaidia kupumua.Saa tano na dakika ishirini na moja tulijulishwa kwamba mgonjwa amefumbua macho tukaenda kumpima alikuwa anaendelea vyema tukatoa maelekezo aendelee kupumzishwa.Muda mfupi baadae tukaitwa tena kwamba hali ya mgonjwa imebadilika.Tukawahi na kumkuta akiwa ana hali mbaya na tukiwa pale moyo wake ukasimama ikatulazimu kuustua kwa kutumia mashine ya umeme na kwa bahati nzuri ukaanza kufanya kazi tena.Tukamuondoa na kumpeleka katika chumba maalum tukaanza kumchunguza nini kimesababisha hali ile na tumegundua mgonjwa alichomwa sindano ya sumu kali” akasema daktari Yule na akina Mathew wakatazama “Bado hatujajua ni sumu gani ,sampuli ya damu iko maabara hivi sasa ikichunguzwa kujua ni aina gani ya sumu alichomwa.Aliyefanya kitendo hiki ni dhahiri alidhamiria kumuua kwa haraka lakini tunashukuru tuliwahi na tukaokoa maisha yake” “Thank you lord ! akasema Mathew kwa sauti ndogo “Suala hili tayari tumelifikisha katika kitengo cha usalama hapa hospitali wameanza kulifanyia kazi ili tujue nani aliyemchoma mgonjwa sindano yenye sumu.Tutawajulisheni kila hatua itakayochukuliwa” akasema daktari na Mathew akasimama “Daktari kwanza kabisa tunashukuru sana kwa jitihada kubwa ambazo mmekuwa mkizifanya kuokoa maisha ya ndugu yetu.Kuhusiana na tukio la leo tunaye kijana wetu ambaye tulimuweka hapa kwa ajili ya ulinzi wa mgonjwa wetu ambaye ametueleza kwamba muda mfupi baada ya timu ya madaktari kutoka kumpima mgonjwa na kuelekeza apumzike, aliingia dakari mwingine na kuchoma sindano katika chupa ya maji aliyokuwa ametundikiwa mgonjwa na muda mfupi baadae ndipo hali ile ikajitokeza.Kama mtaruhusu tunaweza kumuita akaeleza nini kilitokea” akasema Mathew na daktari akaruhusu kijana Yule aitwe.Austin akatoka haraka akaenda kumchukua Jerry akamleta katika kile chumba.Jerry akaeleza ilivyokuwa na kueleza muonekano wa daktari huyo.Ikalazimu mtu anayeshughulika na masuala ya wafanyakazi wote wa hospitali ile aitwe akafika na kompyuta yake na Jerry akamuelezea muonekano wa huyo daktari aliyemchoma GosuGosu sindano ya sumu “Kuna wafanyakazi mia nne na ishirini katika hospitali hii.Siwezi kuwafahamu wote labda tujaribu kukaa na kupitia mfanyakazi mmoja mmoja ili aweze kumtambua huyo daktari aliyefanya huo uhalifu” akasema Yule meneja “Kuna njia rahisi ya kuweza kumtambua huyo daktari” akasema Mathew na kuomba apewe karatasi na kalamu akaanza kuchora picha ya huyo daktari aliyemchoma sindano Gosu Gosu kwa kufuata maelezo ya Jerry.Baada ya dakika kumi picha ikawa tayari Mathew akamuonyesha Jerry ile picha “Mungu wangu ! akasema Jerry kwa mshangao mubwa.Hakuamini kile alichokiona “Ni huyu huyu ambaye aliingia na kumchoma sindano mgonjwa” akasema Jerry.Mathew akawaonyesha madaktari wale picha ile aliyoichora na wote wakabaki na mshangao mkubwa. “Dr Sebastian Makebu” akasema Dr Masawe. “Huyu ni daktari wetu anayehusika na dawa za usingizi.Kijana una uhakika ni huyu?akauliza DrMasawe “Ni yeye”akajibu Jerry bila woga “Kwa nini Dr Seba akafanya kitendo kama hiki?akauliza Dr Masawe na kupiga simu katika idara ya usalama pale hospitali na kuagiza Dr Sebastian Makebu kutafutwa haraka sana na kukamatwa kama yuko katika maeneo ya pale hospitali “Dr Masawe kuna kitu kingine ninataka kuuliza.Karibu muda wote huwa hapakosekani muuguzi katika chumba kile cha Gosu Gosu.Nini kimetokea leo hadi daktari huyu akaweza kuingia na kufanya kile alichokifanya? Mathew akauliza “Ni kweli.Mgonjwa wenu ni mmoja wa wagonjwa wanaopewa kipaumbele kikubwa sana hapa hospitali kwani Rais alipiga simu na kuagiza kwamba kila juhudi zifanyike kuhakikisha mgonjwa huyu anahudumiwa vizuri na maelekezo yakatolewa kusikosekane muuguzi katika chumba chake na ndivyo inavyokuwa kila siku toka ameletwa hapa.Hata mimi nashangaa leo kumetokea nini kusiwe na muuguzi mle chumbani hadi akaingia huyu kijana na kufanya hiki alichokifanya.Kuna mtu mmoja ambaye tungeweza kumuuliza nini kimetokea hadi chumbani kwa Gosu Gosu kusiwe na muuguzi lakini kwa bahati mbaya wakati tukiendelea kumuhudumia mgonjwa wenu tukapokea taarifa kwamba mkuu wa wauguzi hapa hospitali amejirusha ghorofani na kufariki dunia.Sijui nini kinaendelea hapa” akasema Dr Masawe na simu yake ikaita akaipokea akazungumza halafu akawatazama akina Mathew.Sura yake ilionyesha wazi kuna kitu hakiko sawa “Nimetaarifiwa na idaraya ulinzi kwamba Dr Sebastian tayari amekwisha toka nje ya hospitali.Alipita getini na akasaini kutoka.Nimejulishwa pia kwamba muuguzi ambaye alitakiwa kuwepo katika chumba cha Gosu Gosu amekutwa sasa hivi akiwa amefariki chooni.Sifahamu ni mambo gani yanaendelea hapa hospitali. Vyombo vya dola vitatusaidia katika suala hili lakini ninawahakikishia kwamba Dr Sebastian atapatikana tu.Hawezi kukwepa mkono mrefu wa dola.Ahsanteni sana kwa kutusaidia tumeweza kupata mwanga wa nini kilitokea na nani amefanya.Tukiliweka pembeni suala hilo kwa muda kuna suala lingine muhimu sana ambalo mnatakiwa mlifahamu” akasema Dr Masawe. “Kufuatia sumu kali aliyochomwa Gosu Gosu kuna tatizo kubwa limejitokeza.Ini lake linashindwa kufanya kazi hivyo basi anahitaji kupandikizwa ini haraka iwezekanavyo ama sivyo atapoteza maisha” “Jesus ! akasema Ruby “Najua nimewastua sana vijana wangu lakini huo ndio ukweli.Ili kuokoa maisha ya mwenzenu lazima kumfanyia upasuaji na kumpandikiza ini.Bila kufanya hivyo tutampoteza” akasema Dr Masawe “Daktari unadhani Gosu Gosu ana muda gani wa kuweza kuishi kuanzia sasa?Mathew akauliza “Kwa hali aliyo nayo sasa ninaweza kusema kwamba ana saa arobaini na nane kama asipopandikizwa ini atakufa” akajibu Dr Masawe. “Ni muda mfupi sana huo tutapata wapi ini la kumpandikiza? Tunaweza kupata ini hapa hospitali?akauliza Mathew “Hapa hospitali ni vigumu kwani kuna orodha ndefu ya wagonjwa wanaohitaji kupandikizwa ini lakini idadi ya wanaojitokeza kuchangia ini ni ndogo sana au niseme hakuna kabisa” akasema Dr Masawe. “Unatushauri nini mzee?Mathew akauliza “Anatakiwa mmoja wenu ajitolee kumchangia ini mwenzu.Si lazima awe ni ndugu wa damu mtu yeyote ambaye yuko tayari kujitolea ini kwa ajili ya huyu mwenzenu atapimwa na akionekana ini lake linafaa basi kitachukuliwa kipande na kupandikizwa kwa mgonjwa.Ni upasuaji ambao unaweza kuchukua saa tano au zaidi” “Endapo ini hilo likipatikana upasuaji huo unafanyika hapa hapa hospitali au nadi nje ya nchi?akauliza Mathew “Tunapandikiza hapa hapa hospitali” akajibu Dr Masawe “Vijana kujitolea ini kuokoa maisha si kitu cha hatari kabisa japo wengi wanaogopa.Tunachukua kipande kidogo cha ini safi tunakipandikiza katika ini la mgonjwa.Baada ya miezi mitatu ini litarejea katika hali yake ya kawaida” akasema Dr Masawe.Mathew akawaomba madaktari wale wawape dakika mbili wakajadiliane “Guys kwanza kabisa tunashukuru kwa Gosu Gosu kuwa hai mpaka sasa.Jaribio la kumuua limeshindwa lakini bado yuko kwenye hatari kama asipopata ini.Sisi ndio ndugu zake hivyo inabidi kufanya kila tuwezalo kuokoa maisha yake.Binafsi ninajitolea kupimwa na kama nikikutwa ninaweza kutoa ini basi nitafanya hivyo kuokoa maisha ya Gosu Gosu”akasema Mathew “Hapana Mathew.Wewe hupaswi kuwa kitandani.Wewe ni mtu muhimu sana kwa sasa.Niache mimi nikapimwe na kama ikionekana ninafaa basi nitolewe mimi ini ili wewe na Ruby muendelee na operesheni” akasema Austin “Nadhani Austin yuko sahihi.Mathew hutakiwi kulala kitandani kwa muda huu.Kumbuka una siku saba tu za kuhakikisha unampata James Kasai “ akasema Ruby “Sawa Austin.Nalikubali wazo lako.Wakati vipimo vikiendelea mimi na Ruby tutaendelea na operesheni ambayo kwa sasa inazidi kutanuka kwani tunatakiwa kumpata huyo mtu aliyetaka kumuua Gosu Gosu kwa sumu ambaye nina uhakika mkubwa ametumwa afanye hivyo” akasema Mathew wakarejea ndani ya kile chumba na wakawajulisha madaktari kwamba Austin amejitolea kutoa ini litakalopandikizwa kwa Gosu Gosu. “Dr Masawe nahitaji kufahamu huyu daktari Sebastian anaishi wapi?akauliza Mathew na kuelekezwa kisha wakaondoka pale hospitali na kumuacha Austin akijiandaa kwa ajili ya kupimwa. “Ruby kuna picha inaendelea kujitengeneza kufuatia hiki kilichomtokea Gosu Gosu.Kuna watu wanataka auawe.Naamini kuna kitu anakifahamu ndiyo maana watu hao hawataki apone na wakamtumia huyo Dr Sebastian ili akamchome sindano ya sumu afe.Kifo cha muuguzi mkuu na muuguzi aliyekuwa akimuuguza GosuGosu vinahusiana na hiki kilichomtokea Gosu Gosu.Naamini kabisa kwamba Dr Sebastian alimtumia muuguzi mkuu kumuondoa muuguzi katika chumba kile cha Gosu Gsou ili aweze kupata nafasi ya kwenda kumchoma sindano ile ya sumu na wauguzi wale wawili wameuawa ili kuharibu uchunguzi” akasema Mathew akiwa katika usukani wakielekea nyumbani kwa Dr Sebastian “Kwa vyovyote vile lazima mwanamke huyo ambaye anadai ni mchumba wa Gosu Gosu anahusika na hiki kilichomtokea Gosu Gosu na ndiyo maana ametoweka na hajulikani alipo.Umefanikiwa kupata taarifa za Yule Melanie Davis?akauliza Mathew “Nimekwisha sahau kama nina kazi kubwa ya kufanya.Nimejielekeza katika suala la Gosu Gosu” akasema Ruby na kuikunjua komputa yake akaanza tena kazi. “Melanie Davis na Melanie Chuma ! akawaza Mathew “Hawa ni watu wawili tofauti au ni mtu mmoja? Akajiuliza “Ngoja tuendelee na uchunguzi tutaupata ukweli” akawaza Mathew akiendelea kukanyaga mafuta “Mathew unaweza ukasimamisha gari?Kuna kitu nataka uone” akasema Ruby na Mathew akatafuta sehemu nzuri akasimamisha gari . “Kuna nini Ruby?akauliza Mathew “Nimepata taarifa za Melanie Davis” akasema Ruby na kumpa Mathew kompyuta ili asome “It’s her ! akasema Mathew baada ya kuiona picha ya Melanie Davis “Huyu ndiye Yule mwanamke niliyekuwa ninamzungumzia.Huyu ndiye ambaye nilimshuhudia Dubai akisaini makubaliano ya kupokea fedha kwa niaba ya James Kasai. Hata ukitazama sura yake haina kovu lolote ni kama ile picha niliyoichora” akasema Mathew “Taarifa inaonyesha anaitwa Melanie Davis.Ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” “Melanie Davis ana asili ya Congo ! Mathew akashangaa na kuendelea kusoma ile taarifa na kuimaliza “Taarifa inaonyesha Melanie Davis ana utajiri mkubwa aliorithi kutoka kwa wazazi wake waliofariki katika ajali.Anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea wenye umri mdogo lakini haijaonyesha anamiliki miradi au biashara zipi nchini Ufaransa na hata wazazi wake hawajatajwa kwa majina ili tujue walikuwa wanamiliki miradi ipi.Bado kuna ukakasi kuhusu huyu Melanie Davis”akasema Mathew “Ninajiuliza kama anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea wakubwa nchini Ufaransa amekuja kutafuta nini Tanzania? Akauliza Ruby “Yawezekana amewekeza hapa Tanzania na ndiyo maana IS wanapitisha fedha kwake.Ninadhani hata vyombo vya fedha havijaweza kuwa na mashaka naye kwa vile ni mtu mwenye utajiri mkubwa.Ruby tutaendelea baadae kuwachimba hawa watu wawili Melanie http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Davis na Melanie Chuma.Kwa sasa tuwahi nyumbani kwa Dr Sebastian” akasema Mathew na kuingia barabarani wakaendelea na safari “Melanie Davis ambaye ninaamini ndiye aliyesaini makubaliano ya fedha na IS na ndiye tunayeamini ni mchumba wa Gosu Gosu anatokea Ufaransa.Gosu Gosu naye alikwenda Ufaransa na baada ya kurejea ndipo akaanza kuonekana na huyo mwanamke.Ni vipi mahusiano yao yalianza? Je walikutana Ufaransa? Nini anakifanya huyu mwanamke hapa nchini ? Melanie Chuma amefanana naye kwa kila kitu je wana undugu au imetokea tu wakafanana? Au ni mtu mmoja? Haya yote baadae kwa sasa ngoja tumsake kwanza huyu daktari aliyetaka kumuua Gosu Gosu” akawaza Mathew Walifika katika nyumba anakoishi Dr Sebastian kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa kule hospitali.Ni nyumba ambayo ilikuwa na uzio wa maua na geti la bati.Mathew na Ruby wakashuka garini na kuliendea geti kwa tahadhari kubwa.Akajaribu kulisukuma geti halikuwa limefungwa wakaingia ndani.Taratibu wakaelekea hadi katika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ulikuwa umefungwa.Mathew akazunguka nyuma ya ile nyuma ambako kulikuwa na mlango mwingine akajaribu kuufungua nao ulikuwa umefungwa.Akatoa vifaa Fulani vidogo na kuvichomeka katika kitasa akaufungua mlango wakaingia ndani wakaanza kukagua vyumbani.Katika chumba kikubwa cha kulala wakakuta vitu vimepanguliwa hovyo..Kabati la nguo lilikuwa tupu “Tumechelewa.He’s gone.Inaonekana baada ya kufanya kitendo kile alikuja hapa na kuchukua vitu akaondoka haraka.Unaweza ukajua mara ya mwisho alizungumza na nani?akauliza Mathew wakatoka na kurejea katika gari Ruby akachukua kompyuta yake na kuziingiza namba za Dr Sebastian katika program maalum na baada ya dakika mbili akasema “Aliwasiliana na mtu anaitwa Salome Mtete” akasema Ruby na kuufungua ujumbe huo “Unaweza ukafuatilia na kujua mahala alipo?akauliza Mathew na Ruby akafungua program nyingine akamtafuta huyo mtu aliyewasiliana naye mara ya mwisho akaweza kujua mahala alipo. “Samawati tower” akasema Mathew kisha akaondoa gari wakaondoka. MPENZI MSOMAJI MATHEW MULUMBI TAYARI AMEANZA KAZI ILIYOMLETA TANZANIA USIKOSE SEHEMU IJAYO…





Baada ya kutoka katika geti la hospitali ya Mtodora Dr Sebastian alichukua simu na kumpigia mpenzi wake Salome Mtete “Hallo Darling” akasema Salome baada ya kupokea simu “Salome ninakuja hapo kazini kwako muda si mrefu naomba usitoke nisubiri tafadhali” akasema Dr Sebastian. “Sawa nakusubiri mpenzi” akajibu Salome na Dr Sebastian akakata simu kisha akaizima kabisa. Kutoka hospitali anakofanya kazi hadi nyumbani kwake ilimchukua dakika ishirini na tano.Alipofika nyumbani kwake akashuka garini huku akikimbia na kufungua mlango akaelekea chumbani kwake akachukua sanduku lake kubwa akafungua kabati na kuanza kupakia nguo haraka haraka halafu akafungua ndoo za kabati akachukua nyaraka zake za muhimu.Akaangalia mle chumbani kama kuna kitu cha muhimu amekisahau na aliporidhika kwamba kila kitu kiko sawa akatoka akafunga nyumba yake na kuondoka.Moja kwa moja akaelekea katika jengo la kibiashaa lililojulikana kama Samawati tower anakofanya kazi mchumba wake Salome.Alipofika akaegesha gari na kushuka garini akatembea haraka haraka kuelekea katika katika duka la kuuza vifaa vya electroniki anakofanya kazi Salome ambaye alipomuona akatoka akamfuata. “Seba kuna nini leo?Mbona unaonekana una haraka sana? akauliza Salome wakati wakishuka ngazi kwa haraka kuelekea chini “Nimepata safari ya dharura ya kikazi ndiyo maana unaniona nikiwa na haraka namna hii” akasema Sebastian “Unasafiri kwenda wapi?akauliza Salome lakini Seba hakumjibu akampatia funguo za nyumba yake “Funguo hizi za nyumba yangu utazitunza.Gari pia ninakuachia utaendelea kulitumia hadi pale nitakaporejea” akasema Dr Sebastian “Seba mbona hutaki kunieleza unakwenda wapi?akauliza Salome “Nitakupigia simu nikifika” akasema Sebastian huku akifungua buti ya gari na kutoa sanduku lake akaita taksi halafu akambusu Salome “Baki salama Salome.Nakupenda sana” akasema Dr Sebastian na kuingia katika taksi akaondoka akimuacha Salome akiwa ameduwaa.Hakuwahi kumuona mchumba wake akiwa katika hali ile. “Seba amepatwa na nini?Mbona ghafla namna hii?Halafu mbona anaonekana kuwa na wasiwasi mwingi?akajiuliza Salome wakati taksi aliyopanda mpenzi wake ikitoka katika geti la kuingilia Samawati tower. Dr Sebastin alimuelekeza dereva wa ile taksi aliyopanda ampeleke sehemu Fulani na alipomfikisha mahala hapo akamlipa fedha akashuka halafu akaifuata gari moja nyeusi iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya kibanda cha kuuzia magazeti akaufungua mlango na kuingia kisha lile gari likaondoka.Kulikuwa na mtu mmoja tu mle garini ambaye hakumuuliza chochote Dr Sebastian.Gari lile alilopanda Seba lilikwenda hadi katika nyumba iliyozungushwa ukuta wa rangi nyeupe na juu kukawekwa seng’enge.Akapiga honi geti likafunguliwa wakaingia ndani.Yule dereva akashuka akamfungulia mlango Dr Sebastian na kulishusha sanduku lake.Toka ndani ya ile nyumba wakatoka watu watatu na mmoja wao akiwa ni Edwin Mbeko mkurugenzi msaidizi wa SNSA. “Dr Sebastian karibu sana.Umefika kwa wakati muafaka” akasema Edwin Mbeko huku akiitazama saa yake “Ahsante sana Edwin” akasema Dr Sebastian “Dr Sebastain naiomba simu yako” akasema Edwin na kuichukua simu ya Sebastian akaikanyaga ikasambaratika halafu akamtazama DrSebastian na kusema “Dr Sebastian taarifa niliyoipata kutoka kwa watu wangu ni kwamba yule jamaa yuko hai” akasema Edwin na Dr Sebastina akastuka sana “Yuko hai?akauliza “Ndiyo yuko hai.Madaktari wamefanikiwa kuokoa maisha yake na hii inaashiria kwamba hukuifanya vyema kazi yako” “That’s impossible.Sumu niliyomchoma ni kali sana na inayoua baada ya muda mfupi.Niliichoma sumu ile katika chupa ya maji aliyokuwa ametundikiwa na niliamini ndani ya muda mfupi angepoteza maisha kutokana na ukali wa sumu ile na………” akasema Dr Sebastian na Edwin akamkatisha “Dr Seba makubaliano yetu yalikuwa ni kumuua Yule jamaa Gosu Gosu lakini hukufanya hivyo na Yule jamaa ni mzima.Kibaya zaidi ni kwamba tayari umefahamika kuwa ni wewe uliyetaka kumuua na tayari suala hilo limefika katika vyombo vya uchunguzi.Tumeua watu wawili muuguzi mkuu na muuguzi aliyepangiwa chumba cha Gosu Gosu lakini hakuna manufaa yoyote tuliyoyapata hivyo basi wewe ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba” akasema Edwin Mbeko na kwa kasi ya ajabu akachomoa bastora iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti na kumpiga Dr Sebastian risasi katika paji lake la uso akaanguka katika majani.Hakuwa na uhai tena “Get rid of the body ! Edwin akawaamuru vijana wake wawili halafu akaelekea katika gari lake akaliwasha na kabla ya kuondoka akampigia simu Devotha “Hello Edwin naamini kila kitu kimekwenda vizuri” akasema Devotha baada ya kupokea simu “Madam Devotha mambo hayajaenda vyema.Kuna makosa yamefanyika katika lile zoezi la kumuua Gosu Gosu na kwa taarifa niliyoipata ni kwamba bado yuko hai” akasema Edwin “Nini kimetokea Edwin? Suala lile lilikuwa la muhimu sana kwani Yule jamaa endapo akipona anaweza akawaeleza wenzake mambo anayoyafanya Melanie hivyo kumuweka katika hatari kubwa na Melanie akiingia katika hatari sisi sote tunakuwa hatarini” akasema Devotha “Daktari niliyemtumia alifanya makosa kidogo na kusababisha hayo yakatokea lakini tayari nimekwisha mshughulikia.Nimemuua ili kuondoa matatizo kwani suala hili limekwisha fika katika vyombo vya dola lakini nitalimaliza endapo litataka kuleta shida upande wetu” akasema Edwin “Edwin jitahidi sana kusitokee tena makosa ya aina yoyote ile.We’re so close.Tumekaribia sana kumaliza misheni yetu”akasema Devotha “Nitajitahidi madam Devotha” akasema Edwin “Vipi kuhusu huyo mkurugenzi mpya unamuonaje? Anaweza akawa kikwazo katika mipango yeu?akauliza Devotha “Kama nilivyokwambia asubuhi kwamba huyu bado ni mgeni na hajui mambo mengi hivyo hadi pale atakapoanza kuielewa idara hii atakuta tayari tumekwisha kamilisha kila kitu.Kwa muonekano wake haonyeshi kama atakuwa kikwazo chochote kwetu.Kwa muda huu mfupi toka amefika nimejitahidi kujenga ukaribu naye ili niweze kumsoma vizuri.Hatakuwa na shida usihofu”akasema Edwin “Safi sana edwin.Sikukosea kukuweka hapo.Umekuwa ni msaada mkubwa kwangu na ninakuahidi kwamba hautajutia hiki unachokifanya.Matunda yake ni makubwa sana.Tumebakiza muda mchache tu na utaanza kuyaona matunda.Kwa sasa endelea kufuatilia kwa karibu sana maendeleo ya Gosu Gosu na kutafuta namna nyingine ya kumuua kwani kitendo alichokifanya huyo daktari leo cha kushindwa kumuua tayari kimewasha taa nyekundu na wataanza kuchukua tahadhari kubwa wakimlinda” akasema Devotha “Usijali madam ninafuatilia kwa karibu sana na tutamuondoa Gosu Gosu kabla hajaleta hatari yoyote kwetu” akasema Edwin “Umekwisha wasiliana na Melanie?akauliza Devotha “Melanie nimewasiliana naye asubuhi ya leo na hivi sasa niko njiani ninaelekea kupanda helkopta kuelekea Kagera ambako ninakwenda kuwapokea.Kila kitu kinakwenda vizuri.Kwa kuwa wataingia hapa Tanzania jioni watalala Kagera na kesho nitawaleta Dar es salaam” “Edwin kuwa makini sana kwani unajua namna James Kasai anavyotafutwa kwa nguvu kubwa.Hili ni moja ya jambo gumu ambalo tumewahi kulifanya na sikupenda wazo la Melanie la kutaka James aingie Tanzania kwani endapo akigundulika kila kitu kitakuwa kimekwisha.Serikali za afrika mashariki zimewekeza nguvu kubwa katika kumsaka James” akasema Devotha “Nalifahamu hilo madam Devotha na nimekwisha jiandaa kikamilifu kuhakikisha James anaingia hapa nchini na kutoka bila matatizo yoyote.Hilo lisikupe hofu madam” akasema Edwin “Sawa Edwi naomba tafadhali unijulishe kila hatua,kila kinachoendelea.Na kama kuna tatizo lolote tafadhali nijulishe haraka sana”akasema Devotha na kuagana na Edwin “Sifahamu kwa nini Melanie aliamua kuingia katika mahusiano na Yule jamaa Gosu Gosu wakati akifahamu kwamba ni mtu hatari.Matokeo yake ndiyo haya tunalazimika kuanza tena mipango ya kumuua na kama tusipofanikiwa kumuua Yule jaama anaweza akawa ni mtu hatari sana kwetu.Nitakaporudi toka Kagera nitakaa na vijana wangu tuone namna mpya ya kuweza kumuondoa Gosu Gosu” akawaza Edwin. Aliwasili katika jengo la ofisi zao,akashuka garini na kuelekea katika ofisi yake.Akampigia simu rubani wa helkopta ya idara yao akamtaka ajiandae kwa safari ya kuelekea Kagera.Baada ya dakika ishirini akajulishwa kwamba helkopta iko tayari akachukua baadhi ya vitu vyake vichache muhimu akatoka bila kuaga mtu na kuelekea katika helkopta akaondoka kuelekea Kagera.





Mathew na Ruby waliwasili Samawati Tower.Ni jengo lililokuwa na biashara nyingi hivyo watu walioingia na kutoka walikuwa wengi pia. “Bado yuko hapa hapa” akasema Ruby aliyekuwa akimfuatilia Salome kwa kutumia program maalum katika kompyuta yake “Mpigie simu mtake ashuke tuonane naye” akasema Mathew na Ruby akachukua simu akaziandika namba za Salome akampigia “Hallow” akasema Salome baada ya kupokea simu “Hallow Salome habari yako” akasema Ruby kana kwamba ni mtu anayemfahamu vyema “Nzuri dada habari yako nawe” “Salama kabisa.Samahani Salome yawezekana hunifahamu lakini mimi ninaitwa Dr Prisca ninafanya kazi na Dr Sebastian ndiye aliyenipa namba zako za simu” “Ouh sawa Dr Prisca nikusaidie nini?akauliza Salome “Dr Sebastian amepatwa na safari ya ghafla leo na wakati akiondoka mimi sikuwepo alinipigia simu akanipa namba zako niwasiliane nawe kuna vitu Fulani ninavihitaji na aliniambia nikuone wewe” akasema Ruby “Wewe uko wapi?akauliza Salome “Niko hapa chini katika jengo ulimo.Unaweza ukashuka tafadhali tukaonana mara moja?akauliza Ruby “Sawa ninakuja.Naomba kama dakika tano tu nitakuwa hapo chini” akasema Salome na kukata simu.Wakashuka garini na kwenda kusimama karibu na mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya jengo. “Huyu Salome lazima atakuwa ni mtu wa karibu na Dr Sebastian kwani baada ya kuwasiliana naye akazima simu kabisa.Tukimfuatilia huyu anaweza akatusaidia kujua mahala aliko Dr Sebastian”akasema Mathew “Nimeweka program Fulani katika simu yangu.Nitakapokuwa karibu naye program hiyo itaitafuta simu yake na kujiunganisha nayo kisha tutaanza kumfuatilia na kila pale atakapowasilian na Dr Sebastian tutafahamu” akasema Ruby.Baada ya dakika chache simu ya Ruby ikaita.Alikuwa ni Salome “Hallow dada uko wapi?akauliza Salome. “Niko hapa nimesimama karibu na maua haya ya rangi nyeupe” akasema Ruby “Sawa nimekuona” akasema Salome na kukata simu.Baada ya dakika chache mwanamke mmoja aliyevaa suruali ya jeans rangi ya bluu akajitokeza. “Habari yako dada” akasema Salome “Nzuri Salome.Habari yako? “Karibuni sana” akasema Salome. “Ahsante.Huyu anaitwa Dr Cosmas sote kwa pamoja tunafanya kazi kitengo kimoja na Dr Sebastian.Alinipigia simu na kunieleza kwamba amepatwa na safari ya dharura akanieleza nije nikuone.Amepatwa na dharura gani? Ruby akauliza “Hata mimi hakuniambia amepatwa na dharura gani.Alinipigia simu mchana huu akaniambia kwamba anakuja kuniona.Alifika hapa nikaonana naye akaniambia kwamba amepata safari ya dharura ya kikazi akaniachia gari na funguo ya nyumba yake akapanda taksi na kuondoka” “Alikueleza anakwenda wapi? Akauliza Mathew “Hapana hakunieleza anakwenda wapi.Aliponikabidhi funguo za gari na za nyumba yake akaondoka.Nilidhani nyie wenzake mtakuwa mnajua ni kazi gani ya dharura iliyojitokeza” “Alikuwa amebeba nini?akauliza Mathew “Alikuwa na sanduku kubwa la nguo” “Ni mara yake ya kwanza kuondoka ghafla namna hii au amekwisha wahi fanya hivyo siku za nyuma?Mathew akauliza “Hajawahi kuondoka kama alivyoondoa leo.Imekuwa ghafla mno na alionekana kuwa katika haraka kubwa” akasema Salome na Mathew akamtazama Ruby “Hakuna mzigo mwingine alikuachia?akauliza Ruby “Zaidi ya gari na funguo za nyumba yake hakuna kingine chochote alichoniachia”akajibu Salome “Ahsante Salome.Kama hakukuachia chochote basi tutamsubiri hadi atakaporejea” “Nini mlikuwa mnakihitaji toka kwake? Yawezekana amekiacha nyumbani kwake akasahau kuniambia.Ninaweza kwenda kuwatazamia nyumbani kwake” akasema Salome “Ni vifaa vya kazi.Usijali tutawasiliana naye na kumuuliza mahala alikoviweka.Ahsante Salome tunashukuru kwa muda wako” akasema Ruby wakamuaga Salome na kuelekea katika gari lao. “Do you believe her?akauliza Ruby “Ndiyo.Hafahamu chochote.Alichosema ni cha kweli.Sebastin tayari amekwisha toroka na hatujui amekwenda wapi.Kwa kuwa suala hili tayari liko katika mikono ya polisi kama amekimbilia mikoni lazima atapatikana.These people are very smart.Walikwisha jiandaa kwamba baada tu ya kumuua Gosu Gosu basi Dr Sebastian aondoke haraka sana Dar es salaam” akasema Mathew huku akiliondoa gari “Alichokifanya Dr Sebastian ni kucheza na Yule muuguzi mkuu ambaye naamini ndiye aliyemuondoa Yule muuguzi katika chumba cha Gosu Gosu ndipo Sebastian alipopata nafasi ya kwenda kumchoma ile sindano ya sumu.Kwa bahati nzuri alikuwepo kijana wetu pale hospitali ambaye aliweza kusaidia sana kufikisha taarifa kwa madaktari ambao waliweza kuokoa maisha ya Gosu Gosu.Huu lazima ni mtandao mpana ambao unajua nini wanakifanya”akasema Mathew “Ninachojiuliza kwa nini GosuGosu awe ni hatari kwao hadi watake kumuua? Hii ni mara ya pili wanajaribu kumuua na ninaamini wataendelea kujaribu tena na tena”akasema Ruby “Ni kwa sababu kuna kitu anakifahamu na wanaogopa kwamba akipona anaweza akaweka wazi na wao hawati kijulikane.Naomba Mungu amsaidie Gosu Gosu apone kwani ni mtu anayeweza kutusaidia sana kufahamu kinachoendelea na hasa kuhusu huyu Melanie Davis ambaye tunaamini ndiye Yule anayeshirikiana na James Kasai.Natamani sana kufahamu wawili hawa namna walivyokutana na kuanza mahusiano yao.Nataka kupata taarifa za kutosha kuhusu huyu Melanie Davis ambaye anaendelea kuumiza vichwa vyetu” akasema Mathew “Nini kinafuata?Ruby akauliza “Tunarejea tena hospitali.Wenzetu wanatuhitaji kule” akasema Mathew Baada ya muda Ruby akaita “Mathew” “Unasemaje Ruby?akauliza Mathew “Natambua ulisema hutaki kuulizwa kuhusiana na wapi ulikokuwa na nini hasa kilikutokea lakini inaniwia ugumu sana Mathew.Tafadhali natamani sana kufahamu kilichokutokea.Unaonekana umepitia masahibu makubwa” akasema Ruby na kuinamisha kichwa kwa sekunde kadhaa halafu akasema “Hakuna siku ambayo sikuwahi kudondosha chozi kukulilia Mathew.Ninakupenda Mathew kiasi ambacho siwezi kueleza.Nimefurahi nimekuona tena.Nafsi yangu imetulia lakini nahisi kuna kitu kinaukata moyo wangu taratibu.Natamani sana kujua kinachoendelea Mathew katika maisha yako. Sifahamu nini kitatokea kesho.Utaondoka tena na kuniacha hapa peke yangu?” akasema Ruby na kulengwa machozi.Mathew akaendelea kuendesha gari baada ya muda akasema “Ruby kwa muda huu wote niliopotea sikuwahi kupitisha hata usiku mmoja bila kuileta sura yako kichwani kwangu.Umekuwa ukiishi ndani mwangu” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Kama unakumbuka nilikuahidi kwamba baada ya kurejea kutoka kuwakomboa mateka mimi na wewe tungepata nafasi ya kwenda sehemu tukapumzike.Nilikuwa namaanisha kile nilichokisema lakini kwa bahati mbaya sikuweza kurejea tena nikapotelea huko huko.Hata nikiwa huko nilikokuwa bado umeendelea kuwepo moyoni na katika akili yangu.Wanasema ili kujua thamani ya kitu ni hadi pale utakapokikosa.Nimekukosa kwa miaka mitatu na nimeiona thamani yako kwangu.Sitaki kukukosa tena Ruby kwani nakupenda pia.Lakini……...” akasema Mathew na kutulia kidogo.Ruby akamkazia macho kusikia kile alichotaka kukisema “Uliniuliza kama nitaondoka tena na kukuacha peke yako” akasema Mathew na kunyamaza baada ya dakika moja akasema “Ndiyo nitaondoka baada ya operesheni hii kumalizika lakini nitarejea tena kwa ajili yako.Nafahamu unaumia ukisikia hivyo lakini ni lazima nipotee tena na nitakaporudi itakuwa ni moja kwa moja sintaondoka tena.Ninachokuomba pale nitakapoondoka usilie tena bali uwe mvumilivu ukiendelea kuniombea ili nirejee salama” akasema Mathew na Ruby akakiegemeza kichwa katika kiti. “Mathew neno lako ni amri kwangu.Chochote utakachokisema mimi nitakitii.Nitakusubiri kama ulivyoahidi kwani naamini wewe hutembea katika maneno yako.Ukiahidi kitu lazima ukitimize.Niko tayari kukusubiri hata kama itanigharimu maisha yangu yote kwa sababu wewe ni mwanaume pekee uliyejaa ndani ya moyo wangu”akasema Ruby huku macho yake yakilengwa na machozi.Mathew akamtazama na kutabasamu “C’mon cry baby.Please don’t cry “ akasema Mathew na Rubyakafuta machozi “Jambo lingine nitakapoondoka tafadhali usijaribu kunitafuta nimekwenda wapi.Nafahamu wewe unao uwezo mkubwa wa kucheza na teknolojia na unaweza ukataka kufahamu mahala nilikoenda lakini nakuomba usifanye hivyo.Kuwa na imani nami kwamba nitarejea” akasema Mathew “Sintafanya kitu ambacho umenikataza kukifanya Mathew”akasema Ruby “Good” akasema Mathew na ukimya ukatawala “Natamani sana nijue kile kinachoendelea katika maisha ya Mathew lakini ninashindwa namna ya kumshawishi akanieleza.Hakuna anayefahamu alikuwa wapi.Ameibuka kutoka kusiko julikana na hataki kusema chochote.Ngoja niendelee kuwa mvumilivu kama alivyonitaka yawezekana siku moja akanieleza kile kinachoendelea katika maisha yake” akawaza Ruby “Mungu akinisaidia operesheni hii ikamalizaka salama nitarejea tena kwa Habiba Jawad nikafahamu ni kitu gani alinitaka nirejee nikafanye na nitakapokamilisha lazima nirejee nyumbani kwa ajili ya Ruby” akawaza Mathew Waliwasili hospitali na kumfuata Austin katika chumba ambacho alikuwa amelazwa akiandaliwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji ili kutolewa kipande cha ini cha kumpandikiza Gosu Gosu.Mathew akamsimulia kile walichofanikiwa kukipata walikoenda kumfuatilia Dr Sebastian “Hawa watu lazima watarejea tena kutaka kummaliza Gosu Gosu na hawatakata tamaa mpaka wahakikishe Gosu Gosu amekufa” akasema Austin “Lazima kuna jambo ambalo Gosu Gosu analifahamu kuhusu hawa jamaa na wanaogopa akifumbua macho anaweza akalisema ndiyo maana wanataka kumuua.Ninahisi anaweza kuwa amegundua kitu kuhusu Mel……..” akasema Mathew na kunyamaza baada wauguzi watatu kuingia mle ndani na kuwataka akina Mathew watoke kwani mgonjwa alikuwa anapelekwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.Wakaagana naye na kumuahidi kwamba wataendelea kuwepo pale hospitali kufuatilia kila kinachoendelea.Walikwenda kukaa nje ya wodi ya wagonjwa mahututi alimokuwa amelazwa Gosu Gosu. “Natamani Gosu Gosu aamke sasa na aseme hata maneno mawili tu kutufumbulia fumbo hili”akasema Ruby “Ruby usihofu hatujawahi kushindwa katika operesheni yoyote tuliyowahi kuwa pamoja na hata misheni hii pia tutaimaliza.Niamini” akasema Mathew.Waliendelea kukaa pale nje wakiwa kimya kila mmoja akiwaza lake. Wakiwa pale nje mara akatoka Dr Masawe na alipomuona Mathew akamuita “Sikujua kama uko hapa” akasema Dr Masawe “Vipi maendeleo ya mgonjwa wetu?akauliza Mathew “Mgonjwa maendeleo yake siwezi kusema ni mabaya sana wala mazuri.Ni hamsini kwa hamsini.Bado tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana maendeleo yake.Austin anaendelea kufanyiwa vipimo ili tuone kama anaweza akafaa kumpa mgonjwa ini.Naomba msiwe na wasiwasi tunafanya kila jitihada kuokoa maisha ya Gosu Gosu na endapo ikitokea akapoteza maisha basi ni mapenzi ya Mungu lakini sisi kwa upande wetu tunaweka nguvu kubwa sana katika kuhakikisha mgonjwa anapona.Kuhusu suala la Dr Sebastian tayari liko kwenye vyombo vya dola vinalishughulikia na lazima atapatikana.Alichokifanya ni kitu kib……..” Dr Masawe akanyamaza baada ya mwanamke aliyekuwa akipita mbele yao kujikuta akiangusha mkoba aliokuwa ameushika mkononi kwa mstuko alioupata.Mathew akageuka kumtazama mwanamke Yule naye akastuka “Kisa ! akasema Mathew kwa mshangao akimtazama mwanamke Yule aliyekuwa amesimama karibu yao huku akionekana kuwa katika mstuko mkubwa na mwili ukimtetemeka “Mathew ! Ni wewe kweli au nimekufananisha? Akauliza Yule mwanamama kwa uoga “Hujanifananisha Kisa.Ni mimi Mathew Mulumbi” akasema Mathew “No that’s not true.Mathew is dead.Samahani” akasema Yule mwanamama huku akiinama aokote mkoba wake Mathew akamshika bega. “Kisa ni mimi Mathew Mulumbi.I’m not dead” akasema Mathew.Taratibu na woga mkubwa Yule mwanamama akapiga magoti akakaa chini na kuanza kulia “Kisa tafadhali usipige kelele eneo hili.Inuka tafadhali” akasema Mathew lakini bado Kisa aliendelea kumwaga machozi.Mathew akatumia nguvu akamuinua na kumtoa eneo lile akampeleka katika kiunga kilichokuwa na majani mazuri “Kisa tafadhali naomba unisikilize ! akasema Mathew “Mathew niambie tafadhali kama kweli ni wewe” “Ni mimi usihofu” “Jamani nini hiki knaendelea?! Akasema Kisa na kuinua kichwa akamtazama Mathew “Ni mimi Kisa usiwe na wasi wasi.Inuka tafadhali twende kule mgahawani tukazungumze” akasema Mathew na kumsaidia Kisa kunyanyuka akashika viatu mkononi wakaelekea katika hoteli iliyoko pale hospitali “Ujio wangu huu unaweza ukasababisha mtu kufa kwa mstuko.Karibu watu wote wanajua kwamba nimefariki dunia ndiyo maana kila anayeniona anastuka sana na wengine wakitaka kukimbia wakidhani mimi ni mzimu” akawaza Mathew akitazamana na Kisa aliyekuwa bado akimtazama Mathew kwa woga. “Kisa naomba uvute pumzi ndefu tafadhali” akasema Mathew na Kisa akavuta pumzi ndefu “Pole sana Kisa kwa mstuko ulioupata” “Naomba unihakikishie kama kweli ni wewe Mathew” akasema Kisa “Kisa ni mimi usiogope.Ni mimi Mathew Mulumbi unayemfahamu na si mzimu” akasema Mathew na Kisa akamwaga tena machozi. “Tuliambiwa umefariki dunia” akasema Kisa akiendelea kulia. “Nyamaza Kisa usilie tena.Mimi sijafa niko hai kama unavyoniona” akasema Mathew “Tumelia sana Mathew.Tumekulilia mno jamani kwa nini Mathew?Nini kilitokea?akauliza Kisa na kuanza tena kulia “Kisa imetosha.Usilie tena” akasema Mathew “Niache nilie Mathew.Machozi haya ni furaha ya kukuona tena.Sikutegemea kabisa.Bado naona kama niko njozini” akasema Kisa “Hii si njozi Kisa.Ni kitu cha kweli kabisa.Ni mimi halisi” akasema Mathew “Siamini.Haya ni maajabu makubwa” akasema Kisa akifuta machozi “Sijui hata nianzie wapi Mathew.Nahisi kuchanganyikiwa” “Pole sana Kisa.Vipi maendeleo yako?akauliza Mathew “Ninaendelea vizuri Mathew.Mimi na wote kazini tunaendelea vyema kabisa.Nini kilikutokea Mathew?Ulikuwa wapi?Kwa nini wakakuzushia umefariki dunia? Akauliza Kisa “Kisa naamini una maswali mengi sana unataka kuniuliza lakini hapa si mahala pake.Nitatafuta nafasi tutakutana tutazungumza mengi sana kuhusiana na mimi nini kilinitoea hadi watu wakanizushia nimekufa” akasema Mathew “Ni kweli Mathew.Nilikuwa nimekuja hapa kufuatilia maendeleo ya Gosu Gosu.Toka alipopatwa na matatizo sikuwa nimekuja kumtazama.Nilikuwa na vikao vingi leo lakini kuna kitu kilikuwa kinanisukuma kuja hospitali kumbe ninakuja kukutana na muujiza huu mkubwa.Naamini hata wewe pia uko hapa kwa sababu yake” akasema Kisa “Ndiyo niko hapa kufuatilia hali ya Gosu Gosu.Alikuwa anaendelea vizuri na aliweza kufumbua macho lakini kuna mtu alifika na kumchoma sindano ya sumu kwa lengo la kumuua.Madaktari wamejitahidi sana kuokoa maisha yake na kwa sasa kinachoendelea anahitajika kupandikizwa ini ambalo limeharibika kutokana na sumu hiyo kali” “Mungu wangu !! akasema Kisa “Ndiyo hali inayoendelea sasa” akasema Mathew “Mungu amsaidie aweze kupona” akasema Kisa akiwa ameiweka mikono kifuani “Kwa hali aliyonayo tunahitaji kumuombea sana kwani lolote linaweza kutokea lakini Mungu wetu ni mwema atamsaidia” akasema Mathew “Gosu Gosu jamani nani lakini wanaotaka kumuua?Ni mtu mzuri sana hana tatizo na mtu.Hajawahi kugombana na mtu yeyote.Kazini kila mtu anampenda.Toka ilipokuja taarifa umefariki yeye ndiye ambaye amekuwa akisimamia biashara zote na hakuna aliyetegemea kama angeweza kusimamia kwa ufanisi namna ile lakini amefanya maajabu kila mtu akabaki anashangaa.Makampuni yako yote yamefanya vizuri na kuendelea kustawi hadi tulipostuliwa na taarifa kwamba yameuzwa.Tulistushwa sana na maamuzi yale ya kuamua kuuza mali zako” akasema Kisa “Nani ameuziwa makampuni yangu?akauliza Mathew na Kisa akaonekana kushangaa “Ina maana hufahamu nani aliyenunua makampuni yako? “Hapana sifahamu chochote” “Mathew ni kweli hufahamu chochote kuhusiana na suala hili?akauliza Kisa “Suala hili nimelikuta hapa hapa Dar es salaam.Sifahamu chochote” akasema “Haya mbona maajabu ! akasema Kisa “Tumetambulishwa mwanamke mmoja bilionea anaitwa Melanie Davis kuwa ndiye mmiliki mpya wa makampuni yako.Lakini kuna kampuni kama mbili hivi ambazo ziko bado chini ya Gosu Gosu” akasema Kisa Mathew alistuka baada ya kusikia jina Melanie Davis likitajwa “Umesema Melanie Davis? “Ndiyo unamfahamu? “Hapana simfahamu.Ametokea wapi?Ni mtanzania?Mathew akauliza “Hakuna anayemfahamu vizuri huyo mmiliki mpya lakini inasemwa kwamba ni raia wa Ufaransa ila anazungumza kiswahili vizuri kabisa.Kwa ujumla kama nilivyosema bado hatumfahamu vizuri.Hajajiweka wazi kwetu tumfahamu.Ni Gosu Gosu pekee ambaye yuko naye karibu sana na ndiye anayemfahamu vyema kwani alisafiri kwenda Ufaransa na aliporejea alikuja na huyo mwanamke akatutangazia kwamba ndiye mmiliki mpya” akasema Kisa “Dah ! akasema Mathew “Mpaka leo hatufahamu hata ofisi yake iko wapi kwani kila kitu ameendelea kushughulikia Gosu Gosu kama ilivyokuwa awali” akasema Kisa “Unafahamu anakoishi huyo Melanie Davis?akauliza Mathew “Hakuna anayejua.Kuna mambo yanafumbwa fumbwa sana hapa na ambaye anafahamu kila kitu ni Gosu Gosu pekee.Yeye ndiye anayeweza kuwa na majibu yote kuhusiana na huyo Melanie Davis” “Basi usijali Kisa ninyi endeleeni na kazi kama kawaida nitalifuatilia suala hili kwa undani zaidi kujua nini hasa kilitokea hadi yakafanyika maamuzi haya ya kuuza kampuni zangu.Tuachane na hayo wengine wote hawajambo? “Wote wazima lakini tumempoteza mzee Msimbo na Julitha walipata ajali ya gari mwaka jana” “Poleni sana” “Sipati picha wafanyakazi watakapopata taarifa za kuwa uko hai.Itakuwa ni mshangao mkubwa sana lakini kila mmoja atashangilia.Mathew tulilia sana tulipopata taarifa za kifo chako kwa sababu wewe umetufanya tuishi kama familia moja.Umemfanya kila mtu afanye kazi kwa bidii na kujituma.Umetufanyia mambo mengi makubwa ambayo siwezi kuyaeleza ndiyo maana nasema kwamba taarifa za kuwa upo hai zikiwafikia itakuwa ni shangwe kubwa sana na wengi hawataamini na wengine wanaweza wakapoteza hata fahamu kwa mstuko” akasema Kisa “Kisa kuna kitu kimoja ambacho nataka tukubaliane” “Kitu gani Mathew? “Sitaki upeleke taarifa hizi wamba niko hai.Muda utakapofika mimi mwenyewe nitakuja kuwatembelea lakini kwa sasa sitaki mtu mwingine yeyote afahamu labda kama ikitokea tukakutana kama tulivyokutana mimi nawe” “Kwa nini Mathew hutaki wajue kuwa uko hai? “Nina sababu zangu.Naomba unisaidie kwa hilo” “Lakini wanakuja sana hapa hospitali kumjulia hali Gosu Gosu ipo hatari wakakukuta hapa” “Ikitokea hivyo sawa lakini usiwaeleze chochote.Umenielewa Kisa? “Nimekuelewa Mathew” “Ahsante sana” akasema Mathew “By the way unamfahamu mchumba wa Gosu Gosu? Akauliza Mathew “Mchumba wa Gosu Gosu? Kisa akashangaa kidogo “Ndiyo” “Hapana simfahamu.Gosu Gosu ana mchumba?Anataka kuoa?akauliza Kisa “Ndiyo.Nimeambiwa ana mchumba lakini sijamuona akifika hapa hospitali kujua maendeleo ya mchumba wake” akasema Mathew “Huyo atakuwa si mchumba lazima atakuwa ni mwanamke wa kupotezea wakati.Kama angekuwa kweli ni mchumba wake angekesha hapa hospitali akifuatilia maendeleo ya mchumba wake.Huyo lengo lake lilikuwa ni kumchuna pesa na alipoona Gosu Gosu amepata matatizo haya akaamini hawezi kupona akatokomea zake” akasema Kisa Waliendelea na mazungumzo kidogo halafu Mathew akasema “Kisa imekuwa vizuri nimekutana nawe umenijulisha mambo mengi ambayo sikuwa nikiyafahamu.Kwa kuwa tumekutana mahala hapa kwenye matatizo nakuahidi kutafuta tena nafasi nyingine nzuri tukae tuzungumze.Kuna mengi nataka kuyafahamu kutoka kwako” “Mathew hata mimi nimefurahi mno kwa kuiona sura yako tena.Naamini leo sintapata usingizi nikiwaza juu ya jambo hili” akasema Kisa na Mathew akasimama “Natakiwa kwenda kufuatilia kwa karibu kinachoendelea kuhusu zoezi la kumpandikiza Gosu Gosu ini.Endapo mtu aliyejitolea kumpa ini Gosu Gosu vipimo vitaonyesha kwamba hawaendani basi tutakuja kuomba msaada kwa wafanyakazi kwani Gosu Gosu ana saa 48 tu kwa mujibu wa daktari kama asipopandikizwa ini katika muda huo atakufa” “Mathew endapo itatokea hivyo nijulishe haraka sana na mimi nitazungumza na wafanyakazi.Nitawashawishi wajitokeze kuokoa maisha ya Gosu Gosu.Namba yako ya simu ni ile ile?akauliza Kisa na Mathew akacheka kidogo “Sikuwepo kwa miaka mitatu nimekuta kuna mabadiliko mengi yametokea hivyo nitahitaji kupata laini mpya ya simu.Nipatie namba zako tafadhali” akasema Mathew na Kisa akampatia kadi yake ya biashara kisha wakaondoka kurejea kule wodini ambako walimkuta Ruby “Ruby huyu anaitwa Kisa Mwakalukwa ni mhasibu mkuu wa yaliyokuwa makampuni yangu,amefika hapa kujua maendeleo ya Gosu Gosu na kwa bahati nzuri tukakutana.Kisa huyu ni rafiki yangu anaitwa Ruby” Mathew akafanya utambulisho Ruby na Kisa wakasalimiana wakazungumza kidogo kisha Mathew akamtaka Kisa akaendelee na shughuli zake na endapo kutatokea kitu chochote atamjulisha.Kisa akaaga na kuondoka. “Ruby tutafute sehemu tukakae kuna watu wanakuja kumtazama Gosu Gosu ambao wanaweza kunikuta hapa na yakatokea kama yale ya Kisa” akasema Mathew “Mathew hili suala la wewe kuonekana hai linawastua watu wengi ndiyo maana kila anayekuona anastuka mno.Wewe ni mtu mwenye roho nzuri kwa watu ndiyo maana wengi walikulilia walipopata taarifa za kifo chako na wanapokuja kukuona ukiwa hai wengi wanaamini labda wewe si Mathew halisi ni mzuka” akasema Ruby “Wewe unaamini nini?Mimi ni halisi au mzuka?akauliza Mathew “Mzuka hauwezi kuwa na nguvu kitandani kiasi kile”Akasema Ruby na wote wakacheka. Mathew alimtaka Jerry awajulishe kila kitakachokuwa kinaendelea wakaenda kukaa mbali kidogo na wodi ile ya wagonjwa mahututi “Kuna jambo lingine nimelipata kutoka kwa Kisa” akasema Mathew “Ni kweli mali zangu zimeuzwa na mtu aliyenunua mali hizo ni bilionea Melanie Davis”akasema Mathew “Melanie Davis again?akauliza Ruby kwa mshangao “Ndiyo” “Mhh ! hili jambo mbona linazidi kujichanganya ! akasema Ruby “Nilistuka sana aliponitajia jina hilo lakini sikutaka agundue chochote”akasema Mathew na ukimya ukapita “Kwa mujibu wa Kisa” Mathew akaendelea “Gosu Gosu alisafiri kwenda Ufaransa na aliporejea ndipo alipowatangazia wafanyakazi wote kwamba makampuni yameuzwa na akamtambulisha mmiliki mpya ambaye ni Melanie Davis.Kisa anadai kwamba mpaka sasa hakuna anayemfahamu kiundani Melanie.Hakuna anayejua ametokea wapi anaishi wapi ni Gosu Gosu pekee.Nadhani hiki kilichomtokea Gosu Gosu kutaka kuuawa kina mahusiano na Melanie Davis.Kuna mambo ambayo nadhani Gosu Gosu ameyafahamu kuhusu yeye na ndiyo maana anatakiwa auawe” akasema Mathew na kushika kichwa akawaza kidogo halafu akasema “Kama Gosu Gosu alikwenda Ufaransa na aliporejea ndipo alipoanza kuonekana akiwa na Melanie Davis basi mambo yote ya mauziano yalifanyika huko kwa Peniela na ndiyo maana alimuita Gosu Gosu kwani ndiye aliyekuwa akifahamu biashara zangu nyingi.Naamini Peniela atakuwa akimfahamu vyema huyu Melanie Davis.Oh God ! I didn’t want this to happen.Sikutaka Peniela ajue kama niko hai ! akasema Mathew na kushika kichwa “You want to call her?Ruby akauliza “Gosu Gosu ambaye anaweza kutupa taarifa za Melanie hali yake ndiyo hii.Hawezi kutusaidia chochote kwa sasa.Peniela pekee ndiye anayeweza kutupa taarifa za kumuhusu Melanie Davis kwani ndiye aliyenunua makampuni yangu.Hakuna namna lazima nimpigie simu Peniela nizungumze naye kuhusu suala hili na nimuombe anieleze kwa undani kuhusu Melanie Davis.Lazima atakuwa na taarifa zake za kutosha” akasema Mathew akafikiri kidogo kisha akasema “Twende tuondoke hapa” “Tunaelekea wapi? “Nyumbani” akajibuMathew kisha wakaenda kumuaga Jerry wakaondoka “Tunakwenda kufanya nini nyumbani?Ruby akauliza “Kuna jambo nataka tukalifanye” akajibu Mathew







Walifika nyumbani kwa Mathew ambaye moja kwa moja akaelekea chumbani kwa GosuGosu akaanza kupekua katika kabati na kuipata hati ya kusafiria ya Gosu Gosu akaichukua wakaelekea ofisini “Nataka kujua tarehe ambayo Gosu Gosu alirejea kutoka Paris Ufaransa kisha tujue kama Melanie Davis naye aliingia nchini siku hiyo hiyo” akasema Mathew na kumpa Ruby tarehe ambayo Gosu Gosu alirejea nchini akitokea Paris Ufaransa na Ruby akaanza kuifanyia kazi.Baada ya dakika kadhaa akasema “Gosu Gosu alirejea nchini siku hiyo akitumia ndege ya shirika la ndege la Ufaransa ikipitia Nairobi Kenya.Melanie Davis pia alikuwemo katika ndege hiyo naye akitokea Ufaransa” “Kama wote waliingia nchini siku moja na walikuwa katika ndege moja ina maanisha kwamba walikutana nchini Ufaransa hivyo basi mtu ambaye anaweza akatusaidia kumfahamu Melanie ni Peniela” akasema Mathew na kuinamisha kichwa akavuta pumzi ndefu “Hakuna ujanja lazima nimtafute Peniela” akasema Mathew na kuchukua kitabu ambacho aliandika namba za simu za watu wengi akaitafuta namba ya Peniela “Sina hakika kama atakuwa bado anatumia namba hii ya simu ngoja nijaribishe” akasema Mathew na kuziandika namba zile katika simu yake akapiga simu ikaanza kuita “Simu inaita” akamwambia Ruby.Baada ya muda ikapokelewa “Hallow hapa ni nyumbani kwa Peniela,nikusaidie nini tafadhali?ikauliza sauti ya mwanamke “Ninaomba kuzungumza na Peniela tafadhali” “Nimwambie nani anapiga simu? “Mwambie kuna taarifa muhimu kutoka Tanzania” akasema Mathew “Sawa naomba usubiri kidogo” akasema Yule mwanamama na Mathew akaendelea kusubiri.Baada ya dakika chache akasikia sauti ambayo ilimfanya asite kuitikia “Hallow! Ikasema sauti ambayo aliitambua ilikuwa ya Peniela “Hallow habari yako.Nani mwenzangu?akauliza Peniela “Hallo Penny ! akasema Mathew na ukimya ukatanda “Penny ! akaita Mathew “Wewe ni nani?akauliza Peniela “Umeshindwa kuitambua sauti hii? Mathew akauliza “Niambie tafadhali wewe ni nani ama sivyo nitakata simu .Sipendi kuchezewa ! akasema Peniela kwa ukali “Ni mimi Mathew Mulumbi” akasema Mathew na simu ikakatwa “Amekata simu ! akasema Mathew “Haamini kama kweli ni wewe ndiyo maana amekata simu.Mpigie tena” akasema Ruby na Mathew akapiga tena lakini simu haikupokelea. “Ngoja nijaribu kutumia mtandao wa skype akiniona ataamini” akasema Mathew na kuchukua kompyuta yake akampigia Peniela kwa kutumia mtandao wa Skype.Simu ikaita na kupokelewa.Macho ya Peniela yalijaa machozi “Tafadhali wewe unayetumia sura ya Mathew shindwa ! akasema kwa ukali Peniela “Peniela tafadhali naomba unisikilize ! akasema Mathew “Nimekwambia shindwa ! Rudi huko huko kaburini ulikotoka.Muache Mathew apumzike kwa amani ! akasema Peniela “Peniela mimi si mzimu wala mchawi.Mimi ni Mathew Mulumbi mume wako ! “Mume wangu amekwisha fariki miaka mitatu iliyopita.Tafadhali naomba uniondokee mchawi mkubwa wewe unayediriki kuvaa sura za watu” akasema Peniela “Peniela naomba unisikilize.Nipe dakika chache tu kuna kitu ninataka kuzungumza nawe” akasema Mathew lakini Peniela hakujibu kitu aliendelea kulia “Peniela kwanza nataka ufahamu mimi sijafa.Mimi ni mzima japo iliaminika kwamba nimefariki dunia.Si wewe tu uliyeamini hivyo bali kila mtu alijua kwamba nimekufa.Mimi ni mzima kabisa na ni Mathew Yule yule mume wako unayemfahamu” akasema Mathew “Nitazame vizuri Penny ni mimi Yule Yule nimerudi” akasema Mathew “Haya mbona mauza uza ! akasema Peniela “Si mauza uza Penny ni kweli nimerejea” “Ee Mungu naomba unipe nguvu.Hili jambo limenizidi uwezo wa kulibeba” akasema Peniela na kuinamisha kichwa “Peniela najua nimekustua sana lakini naom…….” Akasema Mathew na Peniela akamkatisha “Whoever you are please I can’t talk right now ! akasema Peniela na kukata simu “Amekata simu.Ndiyo maana sikutaka kuzungumza naye.Nilijua angepatwa na mstuko mkubwa sana” akasema Mathew “Mpigie tena simu.Suala hili ni muhimu zaidi kuliko mstuko wake.Akipokea nenda moja kwa moja kumuuliza kuhusu suala hili la Melanie ambalo ndilo limekusababisha ukampigia simu masuala ya kifamilia huu si wakati wake” akasema Ruby na Mathew akapiga tena simu ikapokelewa “Wewe ndugu nimekwishakwambia niache usinisumbue.Unan……….” “Peniela kuna kitu nataka kujua.Nimekuta mali zangu nyingi hapa Dar es salaam zimeuzwa ninataka kujua je ni wewe uliyefanya jambo hili? Ni wewe uliyeuza? akauliza Mathew na Peniela akaonekana kustuka. “Mali ?akauliza “Ndiyo.Naamini sasa umekwisha anza kuamini kwamba mimi si mzimu bali ni Mathew halisi.Nimekuta mali zangu nyingi zimeuzwa lakini sifahamu nani ameuza na kwa nini.Sina wa kumuuliza kwani Gosu Gosu amepigwa risasi yuko hospitali ndiyo maana nikaona nikupigie nikuulize jambo hili” “Oh mon Dieu” akasema Peniela kwa lugha ya kifaransa akimaanisha oh Mungu wangu kisha akafunika uso kwa kiganja chake cha mkono “Peniela tafadhali nahitaji sana kujua kuhusu jambo hili ! “Hivi ni wewe kweli Mathew?akauliza Peniela “Ni mimi Peniela usihofu” akajibu Mathew “Ni ngumu kuamini” “Peniela tutazungumza mengi hapo baadae lakini naomba kwanza unipe jibu kuhusiana na hicho nilichokuuliza” akasema Mathew na Peniela hakumjibu kitu akakata simu. “Amekata simu” akasema Mathew “Tumekwama” “Kuna kitu kimoja ambacho nalazimika kukifanya” “Kitu gani? “Natakiwa kwenda Paris Ufaransa” “Paris?! Ruby akashangaa “Ndiyo.Natakiwa kwenda Paris Ufaransa haraka sana kuonana na Peniela.Amepatwa na mstuko mkubwa na kama nisipomuwahi anaweza akaharibu mambo kwa kuzungumza na Melanie kwamba niko hai na ninaulizia mali zangu” “Mathew kwa wakati huu haitakuwa rahisi kwani kuna mambo mazito yanayoendelea.Khalid Khalid na James Kasai wanawasili nchini na tunakutegemea sana wewe katika zoezi hili.Ninakushauri usiende Paris bali mpigie simu tena Peniela na umtake aje Tanzania mzungumze na atakueleza kila kitu” akasema Ruby na Mathew akafikiri kisogo na kusema “Ushauri mzuri sana” akasema Mathew na kumpigia tena simu Peniela. “Jamani ninakuomba kakaangu usinisumbue tena kwa kunipigia simu” “Peniela naomba unisikilize.Nakuhitaji uje Tanzania nizungumze nawe.Ningeweza kuja Paris lakini sitaki kuleta mstuko kwa watoto.Nakuomba tafadhali uje Tanzania kama utaweza siku ya kesho nataka sana kuzungumza nawe.One more thing usimweleze mtu yeyote kuhusu mimi hasa watoto.Tafadhali Peniela nakuomba sana uje Tanzania kesho” akasema Mathew na kukata simu “Amesemaje?Ruby akauliza “Sikutaka kumpa nafasi ya kujibu chochote.Ninamfahamu Peniela naamini atakuja”akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita “Ruby tupumzike kidogo kabla ya baadae kurejea tena hospitali kujua kile kinachoendelea huo” akasema Mathew Thanks Quote Reply Report Thanks Reactions:Smart911 Mbududa JF-Expert Member Joined Apr 4, 2017 627  1,000 Oct 4, 2019 Add bookmark #815 SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA SEASON 9 : EPISODE 4 Saa tano za usiku geti la nyumba moja iliyozungukwa na migomba mingi likafunguliwa na gari mbili zikaingia ndani ya jumba lile.Lango la gereji likafunguliwa gari moja ikapitiliza hadi ndani ya gereji “Tumefika mahala tutakapopumzika kwa usiku wa leo kabla ya kueleka Dar es salaam hapo kesho” akasema Edwin Mbeko huku akifungua mkanda na kushuka akwafungulia wageni wake milango wakashuka.Kwa kutumia mlango mdogo uliokuwemo ndani ya gereji wakaingia ndani ya ile nyumba wakaenda sebuileni. “Karibu sana” akasema Edwin “Edwin tunashukuru sana kwa kazi kubwa uliyoifanya” akasema mmoja wa wale wageni wawili “Usijali madam Melanie.Ni jukumu langu kuhakikisha unakuwa salama muda wote” akasema Edwin na kwenda kuleta chupa kadhaa za mvinyo akaziweka mezani akawakaribisha akina Melanie waendelee kunywa Edwin Mbeko alikuwa ametoka kuwapokea Melanie na James Kasai na kuwapeleka katika nyumba moja mjini Bukoba kwa mapumziko ya usiku ule kabla ya kuelekea Dar es salaam siku inayofuata. “Sikuwepo Tanzania kwa siku kadhaa.Mambo yanakwendaje hapa?akauliza Melanie “Mambo yanakwenda vizuri.Hakuna wasiwasi wowote”akajibu Edwin “Juhudi za kumsaka James Kasai zimefikia wapi?akauliza Melanie huku akitoa kicheko kidogo na kumtazama James ambaye naye alitabasamu “Kikosi cha umoja kinaendelea na mazoezi kabla ya kuelekea Uganda muda wowote kitakapoamriwa kufanya hivyo.Kwa idara nyingine mpaka sasa hawajapata kitu chochote” akasema Edwin na James Kasai akatoa kicheko kidogo wakaendelea kunywa pombe .Baada ya muda chakula kikaletwa na kuwekwa mezani wote wakajumuika.





Mshale wa saa ulionyesha ni saa saba za usiku pale mlango wa chumba cha upasuaji ulipofunguliwa na vitanda kutolewa vikisukumwa kuelekea wodini.Upasuaji wa kumpandikiza ini Gosu Gosu ulikuwa umemalizika.Saa mbili za usiku ndipo upasuaji ule uliochukua saa tano ulioanza.Mathew na Ruby walikuwepo hospitali wakisubiri upasuaji ule umalizike na muda mfupi baada ya upasuaji kumalizika Dr Masawe akatoka na kuwaita akina Mathew ofisini kwake akawajulisha kwamba upasuaji ulifanyika kwa mafanikio makubwa akawataka wasiwe na wasiwasi tena. Akina Mathew waliondoka hospitali na kurejea nyumbani kwa Mathew ilipata saa nane za usiku.Wakati Ruby akioga Mathew akaenda ofisini kwake akachukua kompyuta yake na kumpigia Habiba Jawad. “Mathew Mulumbi.Inakaribia saa tisa za usiku sasa lakini bado sijapata usingizi hata kidogo.Nimekuwa na hofu kubwa juu yako kwani umezoea kunipigia simu saa nne au saa tano.Nini kimekutokea leo?Ulikuwa katika hatari yoyote?Habiba akauliza “Samahani mama kwa kukupa wasiwasi lakini sikuwa katika hatari yoyote nilikuwa hospitali” akasema Mathew na kumsimulia Habiba kila kitu kuhusu Gosu Gosu. “Poleni sana.Naamini mgonjwa wenu huyo atapona inshallah” akasema Habiba “Mama nimekupigia kupata taarifa za kuhusiana na ujio wa Khalid Sultan ambaye uliniambia atawasili nchini hapo kesho” akasema Mathew “Umepata chochote kuhusu James Kasai?akauliza Habiba “Bado sijafahamu ataingia vipi nchini lakini kuna mtu ambaye ninamfuatilia na nikifanikiwa kumpata naamini nitakuwa nimempata James Kasai.Ulinituma Dubai kushuhudia yakisainiwa makubaliano ya fedha kati ya IS na James kasai na alikuwepo mwakilishi wa James Kasai ambaye anatokea Tanzania.Huyo mwanadada anaitwa Melanie Davis na ambaye ndiye nimeanza kumtafuta.Naamini nikimpata huyo basi nitakuwa karibu sana kumpata James kasai” akasema Mathew “Una akili sana Mathew.Nilikutuma Dubai kwa kusudi kabisa nikakwambia utulie ujifunze na sasa umeona faida zake.Sikutaka kukueleza chochote kuhusu Melanie Davis nilitaka nikuache nikupime nione utafanya nini lakini kumbe umefanya kile ambacho nilitegemea ukifanye.Melanie Davis ndiye kiungo kati ya James Kasai na IS.Kama James anakuja Tanzania lazima atakutana naye hivyo hakikisha unampata.Kuhusu Khalid Sultan atawasili kesho saa moja za jioni na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia.Picha zake unazo naamini mtajipanga vyema kumfuatilia kujua kilichomleta Tanzania lakini ufunguo wa hili fumbo ni Melanie Davis”akasema Habiba “Mama kuna chochote unakifahamu kuhusu Melanie ambacho unadhani kinaweza kunisaidia kufahamu mahala alipo?Mathew akauliza “Mathew wewe ni mtu mahiri sana katika kazi hii.Hata kama ningekuwa nikifahamu nisingekueleza kwani nataka uumize kichwa ili uweze kugundua mambo mengine mengi.Mimi nitakueleza yale mambo makubwa tu na mengine ni juu yako kuyafanyia kazi.Umenielewa Mathew? “Ndiyo nimekuelewa mama” “Vizuri.Nakutakia kazi njema na kesho nipate mrejesho wa nini kinaendelea.Kumbuka Khalid Khalid na James Kasai hawapaswi kutoka salama nchini Tanzania.Kumbuka vile vie hakuna kuwaua watu hawa wawili kabla kwanza ya kufahamu nini wanakipanga kukifanya” “Nimekuelewa mama” akasema Mathew na kuagana na Habiba Mathew akashusha pumzi “Mambo yameiva.Habiba naye anakiri kwamba Melanie Davis ndiye mwenye ufunguo wa fumbo hili.Wapi alipo huyu mwanamke?Ngoja nitulize kwanza kichwa na kujiandaa kwa siku ya kesho” akawaza Mathew na mara mlango wa ofisi yake ukagongwa.Akaifunika komputa yake haraka haraka na kwenda kuufungua akakutana na Lucy mtumishi wake wa ndani “Karibu Lucy” “Kaka samahani kwa kukusumbua.Ruby ameniambia kwamba nije nikuone huku” akasema Lucy na kunyamaza kidogo “Kuna jambo ninataka kukwambia.Nimepigiwa simu na madam Peniela pale ulipoondoka akaniuliza kama kweli umerejea nikamuhakikishia kweli ni wewe na umerejea.Alikuwa analia sana na akaniambia kwamba nisikueleze chochote.Nimeona nije nikwambie kaka suala hilo” “Ahsante sana Lucy.Umefanya vyema kunieleza” “Sawa kaka.Vipi hali ya Gosu Gosu? “Tayari amekwisha fanyiwa upasuaji wa kupandikizwa ini na kwa mujibu wa madaktari ni kwamba kila kitu kilikwenda vizuri.Usiwe na wasi wasi kama kuna chochote kibaya nitakujulisha” akasema Mathew na kuagana na Lucy “Kama Lucy amemuhakikishia Peniela kweli ni mimi nimerejea basi lazima atakuja Tanzania .Huyu ndiye atakayenipa ukweli wote kuhusiana na Melanie Davis” akawaza Mathew na kutoka akarejea chumbani “Khalid Sultan ataingia nchini kesho saa moja za jioni na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia” Mathew akamwambia Ruby “Hizi taarifa Mathew anazipata wapi? Lazima kuna mtu anawasiliana naye ambaye ndiye anayempa taarifa hizi.Natamani kumchunguza kujua kinachoendelea lakini naogopa akijua nitaharibu kila kitu na mimi sitaki kumkorofisha huyu jamaa” akawaza Ruby “Kuhusu Melanie Davis” Mathew akaendelea “Naamini kesho tutapata kila kitu kuhusu yeye kwani nina uhakika mkubwa Peniela lazima atakuja.Alimpigia simu Lucy kupata uhakika kama kweli ni mimi niliyempigia simu”akasema Mathew “Do you miss her?akauliza Ruby “Not much” akajibu Mathew “Ni mke wko wa ndoa nilidhani ungekuwa na hamu sana ya kutaka kumuona” akasema Ruby “Nina hamu sana ya kutaka kuwaona watoto wangu” “Kwa nini mama yao huna hamu ya kutaka kumuona?akauliza Ruby “Ruby tusiongelee mambo hayo tafadhali” akasema Mathew





Saa kumi na mbili za asubuhi Mathew na Ruby walipofika hospitali tayari Austin alikwisha zinduka kutoka usingizini na alikuwa anaendelea vizuri.Taarifa ya madaktari waliokuwa wanafuatilia hali ya Gosu Gosu toka alipotolewa chumba cha upasuaji ilionyesha alikuwa anaendelea vizuri.Saa moja za asubuhi wakalazimika kuondoka kurejea katika makazi yao ambako Ruby aliacha gari lake kwani alihitajika kwenda ofisini kwake asubuhi hiyo.Baada ya Ruby kuondoka kwenda kujiandaa Mathew naye akajiandaa halafu akaondoka kuelekea uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Alikuwa anamtafuta mtu mmoja aliyeitwa Salim Chongo.Huyu ni rafiki yake wa muda mrefu.Aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi kabla ya kuacha baada ya kupata kazi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere katika idara ya usalama.Aliekekezwa ofisi mpya ya Salim na kuelekea huko.Aligonga mlango wa kioo na mwanadada aliyekuwamo ndani akamkaribisha ndani akaeleza shida yake ya kuonana na Salim akamuombwa asubiri kwani Salim alikuwa katika kikao cha kazi ambacho kilikaribia kumalizika. Ilipita saa moja na dakika ishirini ndipo kikao kilipomalizika na Salim akaingia mle ofisini.Alistuka alipomuona Mathew “Mathew Mulumbi ! akasema Salim kwa mshangao “Salim” akasema Mathew huu akisimama wakakumbatiana. “Umepotelea wapi Mathew?Nina zaidi ya miaka mitatu hatujaonana” “Nilikuwa nje ya nchi ndiyo maana hatujaonana” akasema Mathew na Salim akamkaribisha ofisini kwake “Mathew nimefurahi sana nimekuona leo.Karibu sana” akasema Salim “Salim ninashukuru sana lakini nimekuja nina shida ndugu yangu nahitaji msaada wako” “Shida gani Mathew? “Kuna kumbu kumbu ya kamera nataka kuipitia” akasema Mathew na Salim akatoa kicheko kidogo “Mathew usiniambie mpaka sasa bado hujaacha ile kazi”akasema Salim “Hapana sijaacha.Bado ninaendelea nayo”akajibu Mathew “Mulumbi wewe ni mtu wa ajabu sana.Pamoja na utajiri wote huu ulio nao lakini bado unaendelea kufanya kazi hizi za hatari.Waachie vijana ili ule maisha.Uliyoyafanya yanatosha” akasema Salim. “Kuna yale maandishi mgongoni kwangu uliwahi kuyasoma ukacheka sana unayakumbuka?Mathew akauliza “Kama sijasahau uliandika People sleep peaceably on their bed at night only because rough men stand ready to do violence on their behalf.Nadhani umeandika hivyo” “Exactly.Kazi ile iko damuni na kamwe siwezi kuiacha” akasema Mathew “Nini unahitaji nikusaidie Mathew?akauliza Salim.Mathew akachukua karatasi akaandika tarehe kisha akasema “Ninataka kupitia kumbu kumbu za kamera kwa tarehe hiyo” “Nini hasa unataka kukitazama Mathew?Salim akauliza “Kuna mtu ninamfuatilia ambaye aliingia nchini tarehe hiyo akitokea Ufaransa kwa kutumia ndege ya shirika la ndege la Ufaransa kupitia Nairobi” akasema Mathew na Salim akatazama katika kompyuta yake akasema “Ni kweli tarehe hiyo kulikuwa na ndege ya shirika la ndege la Ufaransa” Salim akamtaka Mathew amfuate wakaingia katika mlango uliokuwemo mle chumbani wakaingia katika chumba chenye kompyuta runinga zaidi ya kumi kisha akaitafuta tarehe ile aliyoiandika Mathew na muda ambao ndege ile ya Ufaransa iliwasili nchini.Mathew akawatambua Gosu Gosu na Melanie ambao ni miongoni mwa abiria waliokuja na ndege ile “Huyu mwanamke ndiye hasa nataka kufuatilia” akasema Mathew Baada ya kukamilisha taratibu akaruhusiwa kuingia nchini Salim akabadili kamera na kuhamia katika kamera ya sehemu ya abiria wanaowasili.Melanie alionekana akiwa na Gosu Gosu halafu mwanamke mmoja akawasogelea akasalimiana na Melanie “Simamisha hapo” akasema Mathew na kumtazama Yule mwanamke ambaye alimpokea Melanie uwanjani.Nataka kupata picha ya huyu mwanadada aliyempokea huyu mgeni” akasema Mathew na Salim akamchapishia ile picha kisha wakaendelea kufuatilia katika kamera.Walihamia kamera nyingine ya kwenye maegesho ya magari na kuwaona wakiingia katika gari.Mathew akachukua namba za gari lile akamshukuru Salimu akamuaga na kuondoka.Baada ya kuingia katika gari lake akampigia simu Ruby “Ruby vipi maendeleo yako?akauliza Mathew “Ninaendelea vizuri na kazi.Vipi kuna habari yoyote mpya?akauliza Ruby “Nimetoka kuonana na rafiki yangu mmoja wa muda mrefu anaitwa Salim anafanya kazi idara ya ulinzi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.Nimepitia kumbu kumbu za kamera za ulinzi zilizoko uwanjani pale siku waliyorudi Gosu Gosu na Melanie Davis.Nimemfuatilia Melanie alipokewa uwanjani na mwanadada mmoja ninakutumia picha yake sasa hivi ili umtafute ni nani” akasema Mathew na kumtumia Ruby ile picha ya Yule mwanamke aliyempokea Ruby uwanja wa ndege.Akawasha gari na kuondoka.Baada ya dakika tano Ruby akampigia simu “Anaitwa Felista Kabasa ni mfanya biashara anaishi mtaa wa Mwakisule nyumba 204” “Ahsante Ruby ninaelekea huko sasa hivi” akasema Mathew Mathew alifika mtaa wa Mwakisule kama alivyoelekezwa na Ruby akaitafuta nyumba 204 akashuka garini na kuelekea getini akabonyeza kengele ya mlangoni baada ya muda mfupi akatokea mama mmoja mnene akamkaribisha Mathew kwa tabasamu “Karibu sana kaka” “Ahsante mama yangu” “Nikusaidie nini?akauliza Yule mama “Ninamtafuta dada mmoja anaitwa Felista Kabasa” akasema Mathew “Felista?akauliza Yule mama “Ndiyo” Mathew akajibu “Hapana haishi hapa huyo dada” akasema Yule mama “Nimeelekezwa anaishi hapa” “Waliokuelekeza au kama ni yeye kakuelekeza amekudanganya kaka yangu.Haishi hapa huyo mtu.Humu ndani ninaishi mimi,mume wangu na watoto wetu wawili na wala hatuna mtoto anayeitwa Felista hata mtumishi wetu wa ndani hana jina hilo” akasema Yule mama “Samahani sana yawezekana nimekosea lakini nimeelekezwa ni nyumba hii” akasema Mathew na kutoa picha akamuonyesha Yule mama “Unamfahamu huyu dada?akauliza Mathew “Hapana simfahamu na wala sijawahi kumuona mtaa huu” akasema Yule mama “Una hakika hujawahi kumuona mtaa huu? akauliza Mathew “Kwanini nikudanganye kaka yangu?Huyu dada sijawahi kumuona mtaa huu.Kaka yangu kuwa makini siku hizi wanawake wamekuwa wadanganyifu sana” akasema Yule mama “Ahsante nakushukuru sana” akasema Mathew na kurejea katika gari lake akaondoka.Akachukua simu na kumpigia Ruby “Ruby nimetoka katika nyumba ile uliyonielekeza kwamba anaishi Felista nimekutana na mtu mwingine kabisa.Felista nimemkosa” akasema Mathew “Lakini taarifa zake zinaonyesha anaishi hapo.Yawezekana labda alikuwa akiishi hapo lakini amehama.Ngoja niendelee kumchimba zaidi kama nitapata taarifa zake” akasema Ruby Baada ya kutoka mtaa wa Mwakisule Mathew akarejea nyumbani kwake na moja kwa moja akamfuata Lucy akamuonyesha ile picha ya Yule mwanadada “Melanie amekuwa akifika mara kwa mara hapa umewahi kumuona akiwa na huyu mwanamke?akauliza Mathew “Huyu ni dereva wake anaitwa Joyce.Amekuwa akija naye hapa kila ajapo.Akiwa chumbani na Gosu Gosu Joyce hubaki sebuleni na mimi ndiye ninaye muhudumia” akasema Lucy “Una hakika jina lake ni Joyce? “Ndiyo.Jina lake ni Joyce na hata Melanie humuita hivyo Joyce” “Amewahi kukueleza mahala anakoishi?akauliza Mathew “Hapana hajawahi kunieleza.Hatujawahi kuzungumzia chochote kuhusu yeye” akasema Lucy “Ahsante sana Lucy” akasema Mathew na kurejea katika gari lake akaondoka halafu akampigia simu Ruby “Ruby nimetoka nyumbani sasa hivi nimeelezwa na Lucy kwamba huyu mwanamke ambaye umepata taarifa zake anaitwa Felista jina lake ni Joyce.Ni dereva wa Melanie” “Joyce?akauliza Ruby kwa mshangao kidogo “Ndiyo.Kwa mujibu wa Lucy hilo ndilo jina lake” akasema Mathew “Mbona taarifa zake hazisemi hivyo?akauliza Ruby “Nimegundua hawa watu wanatumia majina bandia.Mtandao huu wa Melanie ni mkubwa na wamejipanga vyema.Wanajua wanachokifanya.Kwa sasa ninaelekea hospitali kujua maendeleo ya wagonjwa kwani kutokana na kazi tutakayokuwa nayo baadae yawezekana tusiweze tena kupata nafasi ya kwenda kuwaona wagonjwa” akasema Mathew “Nami pia ninakuja hapo hospitali” akasema Ruby





Helkopta ya idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi ikitokea Kagera ilitua katika sehemu ya kutulia ndani ya uwanja wa bohari la idara ambako huhifadhiwa vitu mbali mbali vya idara ya SNSA vile vile kuna karakana ya kutengeneza magari na vifaa mbali mbali vya idara.Edwin Mbeko alikwisha mpa maelekezo dereva wake ampelekee gari lake katika bohari na tayari gari lilikwisha fika.Helkopta ilipotua gari la Edwin Mbeko likaanza kusogea taratibu.Injini ilipozimwa gari la Edwin likasogezwa karibu zaidi na helkopta mlango ukafunguliwa akashuka Edwin Mbeko akafuatiwa na James Kasai na Melanie na wote wakaingia katika gari la Edwin ambaye alimtaka dereva wake aingie katika helkopta wakutane ofisi kuu.Akashika usukani na kuondoka eneo lile. “Karibuni Dar es salaam” akasema Edwin Mbeko.James Kasai hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote Kutoka bohari kuu la SNSA moja kwa moja walielekea nyumbani kwa Melanie. “Karibuni ndani” Melanie akawakaribisha ndani Edwin na James “Ahsante sana Melanie” akasema Edwin Mbeko lakini kabla hajaketi simu yake ikaita. “Hallo” akasema Edwin “Edwin unaongea na Annabel” “Madam Annabel habari yako? “Nzuri.Sijakuona ofisini na hakuna taarifa yoyote.Uko wapi?akauliza Annabel ambaye ni Ruby “Ninakuja madam nilipata dharura nje ya mkoa.Tayari nimerejea na nitafika hapo ofisini muda si mrefu” akasema Edwin “Sawa Edwin” akasema Ruby na kukata simu. “Melanie tayari mmefika salama.Ninahitajika ofisini .Nilikwambia kwamba kuna mkurugenzi mpya ameletwa na Rais ndiye huyo ananihitaji.Nitawasiliana nawe tena baadae kwa ajili ya zoezi la kumpokea Khalid” akasema Edwin “Edwin ahsante sana kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kutufikisha salama Dar es salaam.Nakutegemea sana hapo baadae katika kuhakikisha Khalid anaingia nchini salama bila matatizo yoyote”akasema Melanie “Jambo lingine Melanie suala la Gosu Gosu ni kama nilivyokueleza kwamba jaribio la kumuua hospitali lilishindikana hivyo basi hii ni taa nyekundu kwa watu wake wa karibu na kuwafanya waimarishe ulinzi na vile vile wanaweza wakaanza kuchunguza nani wanaotaka kumuua Gosu Gosu.Wakati tunatafuta namna nyingine ya kumuua Gosu Gosu tafadhali usitumie zile simu zako zote bali tumia simu mpya niliyokupa na wala wala usiende hospitali.Naamini ndani ya siku mbili hizi tayari tutakuwa tumepata mpango mpya wa kumuua.Kama alivyosema Devotha huyu jamaa ana ukaribu na watu hatari ambao wanaweza wakaharibu mipango yetu hivyo kwa sasa jiweke mbali na Gosu Gosu”akasema Edwin na kuondoka .







Ruby aliwasili hospitali na kukutana na Mathew ambaye alimpa taarifa za maendeleo ya Gosu Gosu na Austin. “Mungu mkubwa.Naamini Gosu Gosu atapona tu” akasema Ruby “Umechimba zaidi kupata taarifa za Yule mwanamke niliyekutumioa picha yake Joyce?akauliza Mathew “Ndiyo lakini sijaona taarifa zake nyingine zaidi ya zile nilizokutumia.Nimeshangaa uliponiambia eti anaitwa Joyce” akasema Ruby “Kwa mujibu wa Lucy ni kwamba yule mwanamke anaitwa Joyce na ni dereva wa Melanie.Kama nilivyokueleza simuni hawa watu wanaonekana wanatumia majina bandia.Sasa ninaanza kuamini lile wazo lako kwamba yawezekana kabisa Melanie Davis na Melanie Chuma akawa ni mtu mmoja.Ruby huu ni mtandao mkubwa na una watu makini sana.Wanajua wanachokifanya na ndiyo maana hata fedha za kutoka IS zinapita kwao bila vyombo vya fedha kugundua.Kila aliyemo katika mtandao huu inakuwa vigumu sana kumfuatilia na kumpata” akasema Mathew na kumtazama Ruby “Nadhani kwa sasa tujielekeze zaidi kwa Khalid Sultan ambaye atawasili nchini jioni ya leo kwa ajili ya kukutana na James Kasai.Tukimfuatilia Khalid atatufikisha kwa James lakini kuna tatizo limejitokeza”akasema Mathew “Tatizo gani Mathew?akauliza Ruby “Kuna vijana ambao Austin aliwaandaa kwa ajili ya kutusaidia katika operesheni hii na nilitegemea jioni ya leo kuwa nao katika zoezi la kumfuatilia Khalid lakini wamenipigia simu wakati nikija hospitali na kunieleza kwamba wamepata safari ya kikazi kwenda Morogoro hivyo hawataweza kushiriki katika operesheni yetu hadi pale watakaporejea”Mathew akanyamaza baada ya muda akaendelea “Ninataka tuwashirikishe idara yako katika zoezi hili ili waweze kumfuatilia Khalid toka atakapoingia nchini hadi pale atakapokuwa amefikia.Pale SNSA mna kila kitu kinachohitajika katika zoezi hilo mnao watu na vifaa vya kutosha hivyo itakuwa vyema kama tukiwashirikisha kufuatilia Khalid lakini usiwaeleze kama anakuja nchini kukutana na James Kasai inaweza ikazua taharuki kubwa.Ujio wa James Kasai itabaki ni siri yetu kwa sasa” akasema Mathew. “Ni wazo zuri pia kwani tunao watu wa kutosha wenye mafunzo na ujuzi mkubwa pale SNSA”akasema Ruby “Nataka zoezi zima la kumfuatilia Khalid litakalofanywa na idara yako liunganishwe katika ofisi yangu nami pia nifuatilie lakini asijue mtu yeyote kama ninafuatilia.Can you do that? akasema Mathew “Nitakuwa pamoja nawe wakati wa kufuatilia zoezi hilo.Utanipa maelekezo nini cha kufanya na mimi nitakuwa nikiwasiliana na timu itakayokuwa ikiendelea na zoezi hilo la kumfuatilia Khalid” akasema Ruby na kunyamaza baada ya simu ya Mathew kuita alikuwa ni Lucy “Lucy” akasema Mathew “Kaka Mathew samahani kwa usumbufu.Nimekupigia kukujulisha kwamba mama Peniela yuko hapa nyumbani amefika sasa hivi” akasema Lucy “Peniela amekuja?! Akauliza Mathew akionyesha mshangao kidogo. “Ndiyo amekuja muda si mrefu na amesema nikupigie simu kuwa anakuhitaji hapa nyumbani” akasema Lucy “Sawa Lucy ninakuja hapo nyumbani muda si mrefu” akasema Mathew na kukata simu akashusha pumzi “Mambo yameiva.Peniela amekuja” akasema Mathew “Dah ! akasema Ruby “Natakiwa nikaonane naye.Usiogope hakuna kitakachoharibika.Andaa timu kwa ajili ya zoezi la jioni na unijulishe kila kinachoendelea”akasema Mathew “Kama Peniela atakuwepo haitakuwa vyema mimi kuja nyumbani kwako jioni lakini nitakuunganisha na kila kinachoendelea” akasema Ruby “Ruby lazima uje nyumbani na tutaongoza zoezi kutokea pale.Jambo hili ni muhimu mno” akasema Mathew na kuagana kila mmoja akaingia katika gari lake na kuondoka. “Nilijua tu lazima Peniela atakuja.Nashukuru kwa ujio wake kwani utanisaidia kufahamu mambo mengi kuhusiana na Melanie Davis lakini hata hivyo liko tatizo.Lazima Peniela atataka kufahamu kilichokuwa kimenitokea.Nilikuwa wapi,kwa nini nikatangazwa nimekufa na mambo mengine kadha wa kadha.Nitafuata maelekezo ya Habiba sintamueleza mtu yeyote hata Peniela mahala nilikokuwa” akawaza Mathew akielekea nyumbani kwake OFISI KUU SNSA Ruby alirejea ofisini kwake na muda mchache baadae mlango wa ofisi yake ukagongwa akaingia Edwin Mbeko “Habari yako madam Annabel” akasema Edwin kwa adabu “Edwin ulikuwa wapi?Toka jana hujaonekana hapa ofisini na hakuna taarifa zozote za mahala ulikokuwa” akasema Ruby “Madam kama nilivyokueleza uliponipiga simu kwamba nilikuwa nimekwenda nje ya mkoa kikazi” akasema Edwin “Ninataka kupata orodha ya kila operesheni inayoendelea hivi sasa ndani ya SNSA na kila pale unapohitaji kwenda nje ya mkoa nijulishe tafadhali.Mimi hapa ni mgeni bado kuna mmbo mengi siyafahamu ninakutegemea sana wewe hivyo usipokuwepo inanipa ugumu katika kazi zangu” akasema Ruby “Sawa madam nitakupa orodha ya operesheni zote zinzaoendelea na samahani sana kwa kilichotokea.Hakitajirudia tena” akasema Edwin kwa adabu. “Nataka kuzungumza na wafanyakazi wote ndani ya dakika tano.Kuna zoezi ambalo linatakiwa kupewa uzito mkubwa” akasema Ruby “Sawa madam” akajibu Edwin na kutoka kwenda kuwakujulisha wafanyakazi kwamba mkurugenzi atazungumza nao muda mfupi ujao.Zilipita dakika tano kama alivyokuwa ameahidi Ruby akatoka ofisini kwake akaelekea katika ukumbi mkubwa.Edwin akawataka wafanyakazi wote kuacha kazi zao kumsikiliza mkurugenzi ambaye alianza kwa kuwasalimu halafu akageukia mbele kulikokuwa na runinga kubwa “Nafahamu zipo operesheni mbali mbali ambazo mmekuwa mkiendelea nazo hapa ningependa kuzifahamu zote na tayari nimekwisha muelekeza Edwin aniwekee mezani orodha ya operesheni zote zinazoendelea hivi sasa.Pamoja na kazi nzuri mnazoendelea nazo sasa hivi lakini kuna zoezi moja muhimu sana ambalo nataka wote tujielekeze huko kuanzia sasa” akasema Ruby akageukia runingani akabonyeza kitanza mbali picha kubwa ikatokea. “Anaitwa Khalid Sultan Khalid” akasema Ruby na kunyamaza kidogo “Anatokea Syria.Ni mmoja kati ya watu wa juu kabisa wa kundi la IS ambaye anahusika na milipuko mikubwa.Huyu mtu anakuja nchini Tanzania” Ruby akanyamaza kidogo kisha akaendelea “Ujio wake nchini Tanzania unatufanya tuamini kwamba IS wanapanga tena shambulio lingine kubwa hivyo ni jukumu letu kama idara yenye dhamana ya kuhakikisha nchi inakuwa salama kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha hakuna tena shambulio lingine ambalo litatokea hapa nchini Tanzania” akasema Ruby na kunyamaza tena kidogo. “Leo saa moja za jioni Khalid ataingia nchini na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia akitokea Cairo Misri.Tutamfuatilia kuanzia atakaposhuka katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere hadi atakapofikia.Tunatakiwa kufahamu kila anachokifanya hapa nchini,tumjue kila anayekutana naye.Khalid haji Tanzania kwa mapumziko tunaamini kuna kitu kikubwa kinachomleta hivyo basi zoezi hili ni muhimu mno.Edwin utapanga timu ya watu wetu kuanzia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumfuatilia Khalid kila mahala anakoenda hadi mahala atakapofikia.Naomba niwakumbushe kwamba hii ni operesheni muhimu mno hivyo tuwekeze nguvu kubwa na ujuzi wetu wote katika operesheni hii.Ninyi ni wazoefu katika mambo haya mmekwisha fanya operesheni mbali mbali na kwa mafanikio makubwa hivyo naamini hata katika zoezi hili litafanyika kwa ufanisi mkubwa sana.Mkumbuke pia kwamba IS wametekeleza shambulio lingine baya sana hapa nchini siku chache zilizopita na bado machozi ya walichokifanya hayajakauka hivyo tusiwape nafasi hata ndogo ya kutekeleza tena shambulio lingine katika ardhi yetu ya Tanzania.Ni wakati wa kuung’oa mzizi wa IS hapa nchini na zoezi hilo litaanza usiku wa leo.Khalid atatuongoza kuweza kuwafahamu washirika wake hapa nchini” akasema Ruby na kuwatazama wafanyakazi wale waliokuwa kimya wakimsikiliza “Mkumbuke pia kwamba IS wanashirikiana na James Kasai ambaye nchi zetu zinamsaka kwa udi na uvumba na nina uhakika kwa kumfuatlia Khalid tunaweza pia kupata taarifa za kumuhusu James Kasai.Narudia tena kuwasisitiza ndugu zangu kwa kiasi kikubwa sana usalama wa nchi unatutegemea sisi hivyo tukishindwa sisi tutakuwa tumewapa IS ushindi na nafasi ya kumwaga tena damu ya watanzania.Tusikubali tena damu yoyote ikamwagwa na magaidi hawa.Tupambane kufa na kupona kwa ajili ya nchi yetu.Nadhani mmenielewa.Kuna yeyote mwenye swali kuhusiana na zoezi hili la jioni ya leo? Akauliza Ruby na kuwatazama wafanyakazi waliokuwa kimya wakimsikiliza.Hakuna aliyeuliza swali lolote. “Hakuna swali naamini mmenielewa vizuri.Ahsanteni sana.Sasa tuanze maandalizi” akasema Ruby na kumtaka Edwin waelekee ofisini kwake. “Edwin kama ulivyosikia kwamba mtu huyu anayekuja Tanzania Khalid Sultan Khalid ni mtu hatari sana.Ni mtaalamu wa milipuko mikubwa na IS wamekuwa wakimtumia sana nchini Syria.Ninaamini kwamba ujio wake hapa Tanzania si bure lazima kuna jambo anakuja kulifanya.Lazima IS wanapanga kufanya shambulio lingine hapa nchini.Kama nilivyoeleza kwamba tutaanza kumfuatilia Khalid toka atakaposhuka ndegeni.Nataka upange vijana mahiri kabisa wenye ujuzi na uozefu wa kutosha katika kazi wamfuatilie Khalid.Sitaki lifanyike kosa hata moja” akasema Ruby “Sawa madam Annabel jambo hilo linakwenda kutekelezwa kwa ufanisi wa aina yake.Tunayo timu ya vijana mahiri wenye uwezo mkubwa ambao watafanya zoezi hilo.Hizi ni kazi zetu na tuna uzoefu mkubwa wa kuzitekeleza” “Nitashukuru sana kama zoezi likienda vizuri” akasema Ruby “Madam ninataka kufahamu kama taarifa hii ya ujio wa huyo mtu imetoka katika chanzo cha kuaminika” akasema Edwin.Ruby akamtazama na kusema “Taarifa imetoka katika chanzo kisichokuwa na shaka hata kidogo” “Unaweza kunishirikisha nikajua chanzo cha taarifa hiyo? Akauliza Edwin “Huniamini Edwin?akauliza Ruby huku akitabasamu “Ninakuamini madamAnnabel lakini ninataka tu kuchukua tahadhari kwani tumewahi kupata taarifa kama hizo na tukatumia nguvu kubwa kujiandaa lakini baadae tukagundua kwamba si taarifa za kweli ndiyo maana tumekuwa tunataka kujiridhisha kila pale tunapopata taarifa kama hiyo kujua chanzo chake kama kinaaminika ii tusije jikuta tunatumia muda na rasilimali kwa taarifa ambayo haina ukweli wowote” akasema Edwin “Ni jambo zuri Edwin kujiridhisha kila pale mnapopata taarifa kama hizi lakini kwangu mimi nakuomba usiwe na wasiwasi wowote.Nina uhakika na kile ninachokisema.Naomba ukaanze kufanya maandalizi” akasema Ruby na Edwin akatoka akaelekea sehemu Fulani iliyojificha akachukua simu na kumpigia simu Melanie katika namba ambayo huitumia kwa ajili ya kuwasiliana na watu muhimu tu. “Edwin” akasema Melanie “Melanie kuna jambo limetokea nimeona nikujulishe mapema” “Jambo gani?akauliza Melanie “Tumetoka katika kikao muda mfupi uliopita.Huwezi amini mkurugenzi wetu tayari anafahamu kuhusu ujio wa Khalid” akasema Edwin “That’s not true ! akasema Melanie “Nakwambia ukweli.Hata mimi hapa nilipo mwili unanitetemeka siamini nilichokisikia kutoka kwa mkurugenzi.Sifahamu amepata wapi taarifa hizo” akasema Edwin na Melanie akashusha pumzi “Hizi ni taarifa za kustusha sana Edwin.Ujio wa Khalid ulikuwa ni kitu cha siri kubwa” akasema Melanie “Inashangaza namna mkurugenzi alivyofahamu “ “What are we going to do Edwin?akauliza Melanie “Nadhani njia nzuri ni kutafuta namna ya kumjulisha Khalid abadili uelekeo na asije tena Tanzania” “That’s impossible.Tayari Khalid yuko angani anakuja Tanzania.Hatuwezi kuahirisha safari yake.Kwa nana yoyote ile lazima Khalid aingie nchini.Jukumu zima liko juu yako hivyo fanya kila linalowezekana kuhakikisha Khalid anaingia nchini bila matatizo yoyote” akasema Melanie na Edwin akawa kimya akitafakari “Edwin ! akaita Melanie “Nakusikia Melanie” “Kama nilivyokueleza kwamba fanya kila linalowezekana kuhakikisha Khalid anaingia nchini hata kama tayari taarifa za ujio wake zimekwisha ifikia idara yako.Nini mnakusudia kukifanya kuhusu Khalid?akauliza Melanie “Nimeelekezwa kuweka timu itakayomfuatilia kutoka uwanja wa ndege hadi mahala atakapofikia”akasema Khalid “Imekuwa vizuri umepewa jukumu hilo wewe mwenyewe hivyo basi hakikisha unaivuruga timu hiyo inayomfuatilia Khalid.Umenielewa Edwin?akauliza Melanie “Nimekuelewa Melanie.Niachie jambo hili nitalishughulikia” “Good.Nijulishe tafadhali kila kinachoendelea huko.Edwin kwa namna yoyote hakuna kushindwa katika hili.Ukishindwa tutakuwa tumeshindwa wote kwani mategemeo yetu yote yako kwako” akasema Melanie na kukata simu. “Dah ! Huyu mkurugenzi amenistua sana.Amejuaje kuhusu Khalid?Amekuja jana tu lakini tayari ameanza na nguvu kubwa namna hii.Natakiwa kujitahidi sana katika jambo hili kwani kama wakiwafinikiwa kumfuatilia Khalid wanaweza wakagundua kuhusu James Kasai na wakifika hatua hiyo sote ambao tuko kwenye mtandao tunakwenda kuangamia.Natakiwa kujitahidi mno kuhakikisha kwamba zoezi zima la kumfuatilia Khalid linavurugika” akawaza Edwin na kurejea ndani akaenda moja kwa moja katika meza ya mwanadada mmoja mfupi mwembamba akamtaka amfuate wakaenda katika chumba kimoja kilichokuwa na kompyuta kadhaa na hakukuwa na mtu. “Dina unakumbuka uliwahi kuniomba mkopo wa fedha wiki iliyopita.Bado unahitaji zile fedha?akauliza Edwin “Ndiyo bado ninahitaji sana”akajibu Dina “Ni kwa ajili ya nini? Akauliza Edwin “Ni ada kwa mdogo wangu ambaye amekosa mkopo wa serikali kwenda chuo kikuu.Mimi ndiye ninayemsomesha” “Kiasi gani unahitaji?akauliza “Milioni tano” “Nitakupa hizo fedha.Mara mbili ya hizo unazohitaji.Nitakupa milioni kumi” akasema Edwin na Dina akaruka ruka kwa furaha “Uko tayari sasa hivi nikakupatie hizo fedha?akauliza Edwin “Niko tayari Edwin.Mungu akubariki sana” akasema Dina kwa furaha kubwa.Haraka haraka wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Edwin “Edwin pamoja na furaha nliyonayo kwa kukubali kunikopesha fedha tena kiasi kikubwa kama hicho nina wasi wasi kwamba yawezekana nikashindwa kurejesha kwa wakati”akasema Dina wakiwa garini “Usiwe na wasi wasi Dina.Fedha hizo ninakupa na si mkopo”akasema Edwin na Dina akastuka “Unanipa siyo mkopo?! “Ndiyo” “Ni fedha nyingi sana hizo mtu kupewa bila kutakiwa kurejesha” “Sitaki unirejeshee hata shilingi moja lakini kuna kitu nitahitaji kutoka kwako” “Kitu gani Edwin?akauliza Dina “Si kitu kikubwa ni msaada mdogo tu” “Nieleze tafadhali” “Nitakueleza usijali” akasema Edwin Walifika nyumbani kwake akamkaribisha Dina sebuleni na baada ya dakika chache akarejea akiwa na mfuko wa karatasi uliojaa mabunda ya noti. “Hizi ni milioni kumi” akasema na kumkabidh Dina ambaye alitokwa na machozi ya furaha. “Edwin ninashukuru sana.Naona ni kama muujiza mkubwa.Sikutegemea kabisa”akasema Dina “Dina baada ya kupata kiasi hicho naamini mdogo wako atakwenda shule bila matatizo.Kuna kitu kidogo ninakihitaji kutoka kwako” “Sema Edwin unahitaji kitu gani?akauliza Dina “Jioni ya leo tutakuwa na zoezi la kumfuatilia Khalid Sultan kama alivyosema mkurugenzi.Ninataka unisaidie kuvuruga mfumo wetu kwa dakika mbili tu kisha uurejeshe tena katika hali yake ya kawaida” http://deusdeditmahunda.blogspot.com/akasema Edwin “Sijakuelewa Edwin” akasema Dina “Ni hivi.Tutakuwa na zoezi la kumfuatilia Khalid Sultan jioni ya leo.Wakati zoezi hilo linaendelea mimi nitakupa ishara na utavuruga mfumo wetu wote kwa dakika mbili halafu utaurejesha tena kama kawaida.” Akasema Edwin na Dina akaonekana kushangaa “Are you serious Edwin?Yaani kwa kazi hiyo ya dakika mbili unanipa kiasi chote hiki cha fedha?akauliza Dina “Ndiyo Dina.Nataka unisaidie kwa kazi hiyo pekee” “Usijali nitakufanyia vile utakavyo” “Thank you” akasema Edwin “Lakini ni vipi kama nikigundulika nimevuruga mfumo wetu wakati wa zoezi muhimu? “Mimi ndiye kiongozi wa operesheni hiyo.Hivyo hakuna yeyote atakayekuletea tatizo endapo itagundulika.Lakini wewe ni mtaalamu sana wa mambo haya ya mtandao hivyo ufanye katika namna ambayo hakuna atakayeweza kugundua.Fanya ionekane ni hitilafu za kiufundi au hali ya hewa au chochote unachoweza ili mradi isigundulike ni kitu kimefanyika makusudi” akasema Edwin “Sawa Edwin nitafanya hivyo” “Kumbuka utafanya pale tu nitakapokupa ishara” akasema Edwin kisha wakaondoka kurejea kazini.











ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog