Simulizi : Siri: Maisha Na Kifo Cha Melanie Chuma
Sehemu Ya Tatu (3)
Melanie alifika nyumbani kwake na kupokewa na Edwin Mbeko ambaye alikwisha fika pale nyumbani kwake akimsubiri.Hakuwa peke yake alikuwa na wanawake wawili wamewakaa sebuleni wakitazama runinga. “Melanie Davis karibu sana” akasema Edwin Mbeko “Ahsante sana Edwin”akajibu Melanie “Samahani kwa kuvamia nyumbani kwako lakini nimekutafuta sana simuni kutwa nzima ya leo hakuna simu yako hata moja inapatikana ndiyo maana nikaamua kuwaleta wageni moja kwa moja hapa nyumbani.Wamewasili jioni ya leo”akasema Edwin “Edwin tunaweza kuzungumza kidogo faragha?akasema Malanie na kwenda katika chumba cha mazungumzo ya faragha wakiwaacha wale wasichana wawili sebuleni. “Ulikuwa wapi Melanie?Nimetaarifiwa na walinzi wako kwamba ulikwenda uwanja wa ndege ukapanda ndeg………………” “Edwin ! akasema Melanie na kumkatisha Edwin.Sauti na sura ya Melanie vilionyesha hakuwa anataka masihara “Edwin ninakuheshimu sana lakini kitendo cha kuingia ndani ya nyumba yangu wakati sipo kimeniudhi sana.Unafikiri hapa ni bar au klabu ya disko unakoweza kuingia muda wowote na kutoka utakavyo?akafoka Melanie.Edwin hakuamini kumsikia Melanie akifoka “Ndiyo maana nilitangulia kusema samahani kwani baada ya kukukosa simuni niliamua kuwaleta wale wasichana hapa moja kwa moja baada ya kuwapokea uwanja wa ndege” akasema Edwin “Hukupaswa kuingia humu ndani kama kwako.Hii ni nyumba yangu na mimi ndiye mwenye amri.Kuanzia sasa sitaki uingie ndani ya nyumba hii bila ya ruhusa yangu na nitabadilisha mfumo mzima wa kuingia humu ndani.Lazima uwe na heshima.Unanionaje mimi?akauliza Melanie kwa ukali “Madam Melanie samahani sana.Nimekosea sintarudia tena” akasema Edwin “Na iwe hivyo.Usithubutu tena kurudia jambo kama hili! Akasema Melanie kwa ukali “Nimekuelewa madam” “One more thing” akasema Melanie “Kuanzia sasa na kuendelea sitaki uniulize kuhusu safari zangu.This is my operation and I’m doing it my way.Kama unataka kufanya kazi na mimi utafuata masharti yangu.You understand me? Akauliza Melanie kwa ukali “Nimekuelewa mama” “Good.Tell your team…..” Melanie akanyamaza kidogo “Waambie watu wako wanaonifuatilia kuacha mara moja.I don’t need any back up.Pale nitakapowahitaji nitakujulisha but for now I can manage on my own.You understand me? Akauliza Melanie “Lakini madam Melanie hayo yalikuwa ni maelekezo ya kutoka kwa Devotha” akasema Edwin “Forget about Devotha ! akafoka Melanie “She’s not here ! I repeat this is my operation and I’m I’m gong to do it my way.You,Devotha and everyone will listen to me because I’m your boss.You understand me? “Nimekuelewa madam Melanie” “Good.Una taarifa zozote mpya? “Taarifa mpya leo ni ujio wa hawa wanawake wawili wasaidizi wako” akasema Edwin kisha wakashuka chini sebuleni ambako Melanie akatambulishwa kwa wale wanawake wawili akawakabidhi kwa Joyce yeye akaenda chumbani kwake kupumzika “Toka nilipoyaona makaburi ya wazazi wangu hali yangu imebadilika.Najiona kama ni Melanie mwingine kabisa.Nimekuwa na hasira kwa kila mtu nimeingiwa na roho ya ukatili na siogopi chochote.Ninachokihitaji ni kitu imoja tu kulipa kisasi kwa wale wote waliowaua wazazi wangu kikatili na kwa kuanzia ninaanza na mke wa Patrice Eyenga halafu nitakuja kwa Rais wa Tanzania hadi wote wapate maumivu kama haya niliyonayo mimi” akawaza Melanie RIYADH – SAUDI ARABIA Saa ya ukutani ilionyesha ni saa saba za usiku pale mlango wa chumba alimolazwa Mathew Mulumbi ulipofunguliwa.Tayari alikuwa usingizini lakini alistuka baada ya kusikia mlango ukifunguliwa,akafumbua macho na kustuka baada ya kumuona aliyeingia mle ndani ni mwanamke alipomtazama vizuri alikuwa ni Dr Abiha.Mathew akainuka na kukaa “Dr Abiha ! akasema “shhhhh ! akasema Dr Abiha akimtaka Mathew akae kimya.Akatulia kwa sekunde chache kusikia kama kuna mtu yeyote atajitokeza halafu akamtaka Mathew ainuke.Akatoa mfuko uliokuwa na nguo suruali ya jeans na fulana ya kijivu akavaa kisha akamtaka amfuate.Dr Abiha akafungua mlango taratibu na kuchungulia katika korido kama kuna mtu.Kulikuwa na ukimya mkubwa.Wakatoka na Dr Abiha akaufungua mlango taratibu wakatokea nje wakajibanza katika tanki tupu la maji kwa sekunde kadhaa halafu wakatembea haraka haraka wakaelekea katika geti la Dr Abiha.Akafungua buti ya gari na kumtaka Mathew aingie kisha wakaondoka.Akiwa ndani ya buti Mathew aliingiwa na hofu baada ya gari kusimama na Abiha akaanza kuzungumza na walinzi kisha akasikia sauti ikuamuru geti lifunguliwe na gari la Dr Abiha likatoka.Baada ya mwendo wa kama nusu saa gari lie la Dr Abiha likazima na sekunde chache baadae buti likafunguliwa Dr Abiha akamtaka Mathew ashuke.Akamuongoza kuelekea ndani.Ilikuwa ni nyumba nzuri “Dr Abiha nakushukuru sana kwa kunitoa katika mikono ya wale jamaa” “Usijali Abu Zalawi ninawafahamu wale jamaa ni watu makatili ndiyo maana nikafanya kila niwezalo kukusaidia” “Ulifanikiwa kupata taarifa zozote kuhusuana na Nawal? “Hapana sijapata taarifa zake zozote.Abu Zalawi umemapata nafasi ya kuponyoka kutoka katika mikono ya wale jamaa sahau kuhusu Nawal” akasema Dr Abiha “Dr Abiha ninashukuru sana kwa msaada wote ulionisaidia hadi ukanitoa katika mikono ya wale jamaa lakini siwezi kuondoka Riyadh bila ya Nawal.Nitamsaka kila kona hadi nimpate na kuhakikisha yuko salama.Nilibeba dhamana ya kuhakikisha anakuwa salama” akasema Mathew “Abu Zalawi huyu Nawal ana umuhimu gani kwako hadi uwe tayari kuhatarisha maisha yako kiasi hiki? “Niliweka ahadi ya kuhakikisha anakuwa salama na lazima niitimize” akasema Mathew “Sawa nimekuelewa.Kwa sasa ni usiku mwingi utapumzika na kesho asubuhi tutaanza harakati za kumtafuta Nawal” akasema Dr Abiha na kumpeleka Mathew Mulumbi katika chumba kimoja ndani ya nyumba ile akamtaka alale “Usihofu Abu hapa ni sehemu salama sana.Wale jamaa hawataweza kukufikia wala kujua kama uko hapa” “Vipi kuhusu wewe?Hawatajua kama ndiye uliyenitorosha pale hospitali?akauliza Mathew “Hawatafahamu kama ni mimi ndiye niliyekutorosha.Walinzi wanaolinda geti nilizungumza nao na kuwalipa fedha”akasema Dr Abiha na kumuaga Mathew akatoka “Ahsante Mungu kwa kunisaidia nimeweza kutoka katika mikono ya wale mashetani.Wamenitesa mno.Mikono yangu wameitoboa kwa visu.Siwezi kusahau mateso yale makali waliyonipa” Mathew akaomba kimya kimya “Sasa baada ya kutoka kwa wale jamaa kinachofuata ni kumtafuta Nawal nijue mahala alipo.Naamini Abdel Fattah atakuwa anafahamu mahala alipo Nawal nitamuomba Dr Abiha anisaidie nifike anakoishi Abdel Fattah.Nitavamia makazi yake na nitafanya kitu ambacho hataamini macho yake na nitampata Nawal.Nikisha mpata Nawal nitaendelea na mchakato wangu wa kumtafuta Habiba Jawad.Nimefika katika ardhi alipo Habiba na siwezi kuondoka bila kuhakikisha nimeonana naye” akawaza Mathew na kuanza kukumbuka alikotoka hadi alipofika “Fatma yuko wapi? Yeye ndiye aliyetuleta hapa Riyadh kwa nini amepotea na kutuacha tukihangaika namna hii?Alihangaika sana huko njia hadi kuhakikisha tunafika hapa.Kuna sehemu nyingine tulisimamishwa katika vizuizi akalazimika kutumia fedha na yote haya aliyafanya ili kuhakikisha tunafika Riyadh kuonana na Habiba Jawad.Je naye ametekwa?akajiuliza Mathew “Nitapata jibu kesho.Siogopi kama niko katika nchi ya watu lakini nitauwasha moto hapa Riyadh na hawataamini.Nina hasira nyingi na hawa watu na laiti Abdel Fattah Sarraf angejua kile kinachokwenda kumtokea kuanzia kesho angekimbia.Nina hasira naye sana”akawaza Mathew na kuamua kujilaza kitandani
“Abu Zalawi” Sauti ya Dr Abiha ilipenya katika masikio ya Mathew na kumfanya ahisi kama anaota hadi pale alipotikiswa ndipo alipofumbua macho na kumkuta Dr Abiha akiwa amesimama mbele yake akitabasamu “Habari za asubuhi Abu Zalawi” “Nzuri Dr Abiha” “Vipi maendeleo yako? “Ninaendelea vizuri.Yale maumivu yamepungua” “Vizuri amka ujiandae tuna safari” “Tunaelekea wapi? “Usihofu amka uoge ujiandae” akasema Dr Abiha na kumuonyesha Mathew lilipo bafu akaingia kuoga.Kisha oga akarejea chumbani kwake akakuta kuna suti nzuri ya rangi nyeusi ikiwa kitandani.Mathew akatabasamu na mara mlango wake ukagongwa akaufungua na kukutana na Dr Abiha wakatazama kwa sekunde chache Dr Abia akatabasamu na kusema “Utavaa suti hiyo kitandani” akasema na kuondoka Mathew akaivaa suti ile nzuri ikamtosha vizuri.Akatabasamu baada ya kujitazama katika kioo namna alivyopendeza “Dr Abiha amenikumbusha mbali sana enzi zangu haya ndiyo yalikuwa mambo yangu.Nilikuwa nanyuka suti balaa lakini hivi sasa nimechakaa sina mvuto tena na hata suti hazinipendezi.Hata hivyo pamoja na kuchakazwa na mateso na hali ngumu ninayopitia I’m still handsome” akawaza na kutabasamu. “Abu Zalawi uko tayari?akauliza Dr Abia baada ya kuingia mle ndani bila kubisha hodi “Niko tayari.Wapi tunaelekea?akauliza Mathew “Usiwe na wasiwasi”akasema Dr Abia wakatoka mle chumbani wakaelekea sebuleni ambako aliwakuta watu watano.Mathew akahisi kuna hatari akajiandaa kukabiliana nao “Abu Zalawi hawa jamaa watakupelekea sehemu fulani” akasema Dr Abia na mmoja wa wale jamaa akamshika Mathew mkono na kumuongoza kuelekea nje ambako kulikuwa na magari matatu.Gari mbili ndogo na kati kati ya gari zile mbili kulikuwa na gari moja ambalo hutumika katika kusafirishia chakula au vitu vinavyoharibika haraka.Milango ya nyuma ya gari lile ikafunguliwa akaingizwa ndani.Ndani ya gari lile kulikuwa na viti na kitanda cha kupumzikia.Milango ikafungwa na gari likawashwa na kuondoka. “Wananipleka wapi hawa jamaa?akajiuliza Mathew Ndaniya gari lile kulikuwa na hewa nzuri japokuwa hakukuwa na dirisha hata moja.Mara kadhaa gari lile lilisimama kisha likaendelea na safari.Hatimaye baada ya mwendo mrefu gari lile likasimama na milango ikafunguliwa.Watu wawili wakaingia ndani ya lile gari Mathew akavishwa mfuko kichwani akashushwa garini akaingizwa ndani ya nyumba na mfuko ule ukatolewa kichwani.Alijikuta katika sebule nzuri. “Sebule nzuri sana.Samani zake zinaonyesha ni za gharama kubwa.Nani anaishi hapa?Lazima atakuwa na uwezo mkubwa kifedha kwa sababu vitu ninavyoviona humu si vya kawaida.Huyu mtu lazima ni tajiri mkubwa sana” akawaza Mathew na kuketi sofani.Muhudumu akafika akiwa na sinia akamuandalia Mathew juice na kumkaribisha.Wakati akiendelea kupata juice wakaingia watu watano waliovalia suti wakazunguka mle sebuleni.Hakuna aliyemsemesha kitu chochote Mathew. “Maandalizi yanafanywa,inaonekana kuna mtu anakuja.Sintakubali kuteswa leo na nitakabiliana na yeyote atakayethubutu kunigusa” akawaza Mathew huku akionyesha kutokujali chochote akaendelea kunywa juice.Baada ya dakika tatu toka wale jamaa waingie pale sebuleni akatokea jamaa mmoja aliyevaa kanzu nzuri nyeupe.Alikuwa ameongozana na walinzi wengine wanne. “Abu Zalawi” akasema Yule jamaa huku akitabasamu na kumpa Mathew mkono “Karibu sana” akasema na kuwataka walinzi wote watoke mle ndani na kuwaacha peke yao “Naamini hunifahamu bado.Ninaitwa Sayid Omar.Ni moja wa wafanyabiashara wakubwa hapa Riyadh” akasema Yule jamaa na Mathew akakumbuka mbali wakati akishughulikia suala la Olivia aliwahi kusama barua pepe kati ya Olivia na Sayid Omar. “Huyu ndiye Yule ambaye alishirikiana na Olivia kutengeneza kirusi” akawaza Mathew “Abu Zalawi nakupa pole sana kwa yote yaliyokupata kwanza kuanzia kufungwa gerezani,mateso yote uliyopitia na hadi uliponusurika katika shambulio na vikosi vya Israel.Ninamfahamu Ammar Nazari na niliposikia ametoka gerezani nilifurahi sana.Siku alipotoka gerezani alinipigia simu nikampongeza na akaniambia namna alivyofanikiwa kutoroka gerezani.Kilikuwa ni kitendo cha hatari lakini cha kishujaa.Nilipopata taarifa za kifo chake nilistuka na kuumia sana.Tumempoteza mtu mmoja muhimu katika mapambano ya kudai haki” akasema Sayid Omar.Mathew hakusema chochote aliendelea kumsikiliza “Tulipata taarifa kutoka kwa Fatma kwamba mjane wa Ammar anaitwa Nawal amekwenda kwake akiwa ameongozana na Abu Zalawi na wanahitaji msaada na kubwa walilohitaji ni kuonana na Habiba Jawad.Nilimtaka awaulize sababu kuu ya kutaka kuonana na Habiba na akasema ni Abu anazo taarifa kuhusiana na mtu anayeitwa Edger Kaka.Nilimtuma Fatma aulize mara mbili kuhusu hicho alichoambiwa kwamba wana uhakika wanazo taarifa za kumuhusu Edger Kaka na baada ya kunithibitishia kwamba Abu Zalawi anazo taarifa muhimu za Edger Kaka nilimtaka Fatma afanye taratibu na kuhakikisha anawaleta Riyadh yeye mwenyewe.Japokuwa umekuwa na Ammar kwa muda na hata umefanikiwa kutekeleza shambulio la Jerusalem lakini bado ilitulazimu kujiridhisha kuhusu wewe.Je kweli wewe ni Abu Zalawi? Tulifanya hivyo kwa sababu Habiba Jawad ni mtu anayetafutwa sana na Israel na tulihofu wanaweza wakatumia mbinu ya kumpandikiza mtu katika mtandao wa kigaidi ili aweze kufahamu mahala alipo Habiba.Kuuawa kwa Ammar Nazari kulitupa wasi wasi kwani kwa miaka mingi Israel hawakuwahi kufahamu mahala anapoishi Ammar.Lakini baada ya ujio wako katika kundi la Ammar Nazari brigades Ammar amejulikana mahala alipo na akauawa.Tulitafuta katika mitandao na kuzipata taarifa zako kwamba unatafutwa na Israel lakini tukataka tujiridhishe zaidi.Tulitengeneza taarifa za mtu ambaye tulimfanya ni Abu Zalawi ili wewe uonekane unadanganya.Abdel Fattah alipewa kazi ya kukuhoji na ndipo alipoanza kukutesa.Wewe na mwenzako Nawal mlipatiwa mateso kwa wakati mmoja.Wakati mkiteswa tulikuwa tunafuatilia kila kitu.Pamoja na mateso yale yote hukutetereka na hukulikana jina lako.Kwa mateso yale makali hakuna ambaye angeweza kuvumilia na kama ungekuwa si Abu Zalawi ungeweza kukiri.Japo ulivuka mtihani wa kwanza tulikupeleka hospitali ambako tulimtumia Dr Abiha kuendelea kukuchunguza na kujiridhisha kama kweli wewe ni Abu Zalawi na una nia ya dhati ya kuonana na Habiba jawad.Kama utakumbuka Dr Abiha amekuwa akikuuliza mswali mengi lengo likiwa ni kutaka kukufahamu zaidi.Tumefuatilia maongezi yako yote na Dr Abiha na mwisho tukajiridhisha kwamba kweli wewe ni Abu Zalawi.Baada ya kuridhika nawe ndipo nikaelekeza nikutane nawe.Pole sana kwa yote uliyokutana nayo.Ilikuwa lazima upitie mateso yale ili tujiridhishe.Tunafanya hivi kwa ajili ya kumlinda Habiba Jawad ambaye anatafutwa sana na Israel.Mtu yeyote ambaye anataka kuonana naye hawezi kwenda moja kwa moja lazima kwanza apitie mitihani kama ile na ashinde ndipo anapoweza kupata nafasi ya kuonana na Habiba Jawad.Wewe umefanikiwa kushinda mtihani huo na ndiyo maana uko hapa.Mimi ni mshirika mkubwa wa Habiba Jawad na huwezi kuonana na Habiba jawad bila kupitia kwangu” akasema Sayid Omar na Mathew akalengwa machozi “Kumbe ujasiri wangu wa kuvumilia mateso na kushikilia msimamo kwamba mimi ni Abu Zalawi umenisaidia.Endapo ningekata tamaa mapema ningepoteza kila kitu” akawaza Mathew “Vipi maendeleo yako Abu Zalawi?akauliza Sayid Omar “Ninaendelea vizuri.Dr Abiha amenihudumia vizuri sana” “Abu Zalawi nakuomba uwe na amani na usiwe na hasira na mtu yeyote kwa yale uliyoyapitia.Ilikuwa lazima uyapitie.Wale wote waliokupitisha katika mtihani ule hawana ubaya nawe bali walikuwa wanafuata maelekezo waliyopewa.Tusameheane kwa yote yaliyotokea” akasema Sayid Omar “Mwenyezi Mungu Subhanahu wa ta’ala ametusisitiza tusameheane na siwezi kwenda kinyume na maelekezo yake hivyo nimesamehe yote yaliyonitokea na moyo wangu una amani”akasema Mathew “Ahsante sana Abu Zalawi.Kwa kuwa tayari umeshinda mtihani basi wewe ni mwenzetu na nitakupeleka kuonana na Habiba Jawad uzungumze naye umueleze kile ambacho unatataka kumueleza lakini kuna taratibu ambazo lazima uzipitie” akasema Sayid Omar na kuinuka akawaita walinzi wake na kuwapa maelekezo Mathew akafunikwa mfuko kichwani na kutolewa mle ndani akaingizwa katika helkopta na baada ya dakika chache ikapaa na kuondoka. DAR ES SALAAM – TANZANIA Melanie Davis aliamka mapema sana na kujiandaa kwa ajili ya kuikabili siku.Alipokuwa tayari hakusubri kifungua kinywa kilichokuwa kinaandaliwa na wale watumishi wake wa ndani akamtaka Joyce dereva wake waondoke.Moja kwa moja wakaelekea kwa Gosu Gosu.Hakuwa amemtaarifu kama atakwenda asubuhi ile “Sikukujulisha kama ninakuja nilitaka kuja kufumania” akasema Melanie na wote wakacheka “Karibu sana” akasema Gosu wakaelekea chumbani na kumuacha Joyce sebuleni “GosuGosu nimeshindwa kulala usiku wa leo nikikuwaza ndiyo maana nilipoamka asubuhi ya leo hata kifungua kinywa nimeshindwa kupata nimeharakisha nije nikuone” akasema Melanie huku akiwa amekumbatiana na Gosu Gosu wakipeana mabusu “Melanie hapa ni kwako na unaweza ukaja muda wowote unaotaka.Usihofu kama ninaweza kukusaliti siwezi katu kufanya hivyo.Ninakupenda mno” “Nashukuru sana Gosu Gosu” akasema Melanie “Kuhusu lile suala la jana” akasema Gosu Gosu “Ehee” “I made some phone calls.Nitapata jibu baadae lakini muelekeo wa kufanikiwa kuonana na James Kasai ni mkubwa” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana Gosu Gosu kwa kusimama nami katika hili” “Usijali mpenzi wangu mimi nitasimama nawe katika kila jambo.Kama nilivyokuahidi kwamba nitatangulia mbele na kuwa ngao yako kukulinda na kitu chochote kibaya” akasema Gosu Gosu “Sikufanya kosa kukupenda Gosu Gosu.Wewe ni wa kipekee kabisa kwangu” akasema Melanie “Melanie mpenzi wangu naomba nikuweke wazi.James Kasai si mtu wa mchezo.Ni mtu hatari sana.Nchi za Congo na Uganda wanamfahamu.Kitendo cha kutaka kuonana naye kinatuweka katika hatari kubwa.Hata hivyo ninakuahidi tutakuwa salama.Nitakulinda usijali.Lakini kuna kitu nahitaji kufahamu kama hutajali” akasema Gosu Gosu “Uliza chochote Gosu Gosu nitakujibu” “Nini dhumuni la kutaka kuonana na James Kasai?akauliza Gosu Gosu “Nataka kumuua Rebeca Eyenga mke wa Patrice Eyenga.Nataka kumuumiza Patrice Eyenga” “Kama ni hilo hakuna haja ya kuhatarisha maisha kwenda Uganda kuonana na James Kasai.Ninaweza kuifanya hiyo kazi.I’m a soldier and I can kill for you” akasema Gosu Gosu.Melanie akatabasamu akambusu GosuGosu “My love ninakupenda sana na ninajua unanipenda na unaweza ukaifanya hiyo kazi lakini sitaki nikuingize katika hayo mambo ndiyo maana ninataka kumtumia adui wa Patrice Eyenga kufanya kazi hiyo.Naomba uwe na amani mpenzi wangu” akasema Melanie na kumbusu tena Gosu Gosu “Usiwe na haraka ya kutaka kuua kwa ajili yangu iko siku utafanya mauaji ambayo hata shetani asingeweza kuyafanya.Siku hiyo yaja GosuGosu kaa tayari” akawaza Melanie. Walipata kifungua kinywa kisha wakatoka kwenda kutembelea baadhi ya miradi ambayo Melanie alikuwa ameinunua kutoka kwa Peniela RIYADH – SAUDI RABIA Helkopta aliyopanda Mathew ilitua bila Mathew kuelewa mahala alikopelekwa.Muda wote ilipokuwa angani alikuwa amevalishwa mfuko mweusi kichwani na kuwekewa vifaa maalum masikioni ili asiweze kusikia wala kuona chochote.Mara tu helkopta ailipotua Mathew akashushwa na kukimbizwa ndani bado aliendelea kufunikwa kichwani.Alipandishwa ngazi na kuingizwa katika chumba kimoja chenye ubaridi mzuri uliotokana na kiyoyozi akakalishwa katika sofa.Hakuweza kuona chochote kutokana na ule mfuko aliovishwa kichwani lakini aliweza kuhisi kuna watu mle sebuleni ambao aliamini walikuwa wanamlinda.Baada ya dakika kumi akasikia hatua za mtu akiingia mle chumbani na harufu ya uturi mzuri sana ikajaa mle sebuleni.Mfuko aliovishwa kichwani ukatolewa na Mathew akajikuta akitazamana na Nawal ambaye alikuwa amerembwa vilivyo.Alikuwa amevaa mavazi ya gharama kubwa na vito vya thamani.Mathew akabaki mdomo wazi.Ulikuwa ni mshangao mkubwa kwake. “Nawal ! akasema Mathew kwa mshangao “Hallow Abu Al Zalawi” akasema Nawal “Siamini macho yangu.Nilikuwa na mawazo mengi sana kuhusu wewe.Sikujua umepelekwa wapi na nitakupataje” akasema Mathew “Ahsante kwa kunijali Abu Zalawi lakini mimi niko salama usihofu” akasema Nawal “Nini kilitokea?Ulipelekwa wapi?Umefikaje hapa?akauliza Mathew “Nilipitia hatua ulizopitia wewe.Siku ile ulipochukuliwa kutoka katika ile nyumba tulimofikia mimi pia nilichukuliwa na kupelekwa sehemu ambako niliteswa sana.Nilipitia mateso makali” akasema Nawal huku akilengwa na machozi “Pole sana Nawal” akasema Mathew na Nawal akatabasamu “Ahsante.Yameshapita.B aada ya kuteswa sana nikaingizwa katika helkopta na kuletwa hapa.Niliuliza kuhusu wewew nikahakikishiwa kwamba uko salama na wewe pia utaletwa hapa.Nimefurahi nimekuona tena Abu” akasema Nawal “Pole Nawal.Nilikuwa na wasiwasi mwingi sana kuhusu usalama wako” “Waliniambia umekuwa unaniulizia kila mara na uliahidi kwamba huwezi kuondoka Riyadh bila mimi.Ahsante sana kwa kunijali Abu Zalawi.Pole vile vile kwa yote uliyoyapitia” akasema Nawal “Haikuwa rahisi.Nimepitia mateso mengi lakini nashukuru jana nimeonana na Sayid Omar akanieleza kwamba mateso yale yote niliyopitia ulikuwa ni mchakato wa kunipima kabla sijaonana na Habiba Jawad.Mahala hapa ni wapi? Akauliza Mathew “Hapa ni makazi ya bilionea Abu Dahir” “Abu Dahir ni nani?akauliza Mathew “Ni mfanya biashara tajiri sana na mtoto wa Habiba Jawad” “Sayid aliniambia kwamba ninakuja kuonana na Habiba Jawad je naye anaishi hapa?Mathew akauliza “Sina hakika kama naye anaishi hapa kwani toka nimefika hapa sijafanikiwa kuonana naye.Niliyeonana naye ni mtoto wake Abu Dahir” “Kwa nini tumeletwa hapa?akauliza Mathew “Mathew kuna jambo ambalo unapaswa kulifahamu” Akasema Nawal “Jambo gani Nawal?akauliza Mathew akionekana kuwa na wasiwasi. “Nieleze Nawal kuna tatizo gani? “Abu dahir anataka kunioa” “Abu anataka kukuoa?! Mathew akashangaa “Ndiyo anataka kunioa.Aliponiona alinipenda na akaagiza niletwe hapa.Nimepewa jumba kubwa la kuishi wakati tukisubiri taratibu nyingine zikamilike kabla ya kufunga ndoa”akasema Nawal “Wewe umekubali kuolewa na huyo Abu Dahir?akauliza Mathew “Ndiyo niko tayari kuolewa naye.Kwa sasa sina mume hivyo sioni sababu ya kukataa kuolewa naye” akasema Nawal Mathew alizisoma alama za mwili alizoonyeshwa na Nawal na akazielewa. “Mimi sina kipingamizi chochote katika suala hilo.Kama umempenda Abu Dahir unaweza kuolewa naye hakuna tatizo” akasema Mathew na ukimya ukapita na mwanamke mmoja mnene akaingia mle ndani na kumjulisha Nawal kwamba anahitajika katika chumba cha marembo “Abu Zalawi tutaonana baadae.Nimefurahi kukuona” akasema Nawal na kuondoka akiwa na walinzi na wasichana wawili wasaidizi wake.Mathew akabaki peke yake pale sebuleni “Nimefurahi kuonana tena na Nawal.Nilikuwa naumiza kichwa ningempata wapi kumbe naye alipelekwa kuteswa.Nashukuru kwa hatua hii tuliyofikia kwani tuko karibu sana kuonana na Habiba Jawad.Jambo lingine la kufurahisha ni Nawal kutakiwa kuolewa na Abu Dahir mtoto wa Habiba Jawad.Hili ni fanikio kubwa kwani tutafahamu mambo mengi kuhusiana na ufadhili wa ugaidi duniani.Naomba mipango hii iende kama ilivyopangwa kusitokee mambo yoyote yakavurugika hapo kati kati na kama kila kitu kikienda namna hii basi Habiba Jawad siku zake zinahesabika” akawaza Mathew na mtu mmoja akaingia mle sebuleni akamtaka Mathew amfuate akampeleka katika chumba kimoja kizuri akamtaka apumzike. DAR ES SALAAM – TANZANIA Akiwa ameambatana na Gosu Gosu.Melanie alizungukia baadhi ya makampuni aliyoyanunua kutoka kwa Peniela yaliyo chini ya MAPEN GROUP akajitambulisha na kufahamiana na wafanyakazi.Mzunguko ule uliwapeleka hadi saa kumi za jioni ndipo Melanie aliporejea nyumbani kwake kupumzika. “Makampuni yote yanaendelea vizuri na nimefurahi kukutana na wafanyakazi hata hivyo akili yangu mimi haipo katika biashara.Kikubwa kinachonila akili yangu hivi sasa ni kulipiza kisasi” Simu yake ikaita akaichukua akatazama alikuwa ni Devotha “Hallow Devotha “Melanie habari yako?Habari za Dar es salaam? “Huku kwema ninaendelea vizuri” “Nashukuru kulifahamu hilo.Melanie nimejulishwa na Edwin kwamba umempiga marufuku asikanyage hapo kwako na vile vile umesema hutaki tena timu maalum ya walinzi waliowekwa kukulinda.Hizi ni taarifa za kweli?akauliza Devotha “Ni kweli kabisa Devotha.Nilifanya hivyo” “Kwa nini Melanie?Edwin ndiye ambaye anasimamia kila kitu kukuwezesha wewe uweze kufanikisha mambo yako kwa wepesi.Bila yeye hautaweza kufanikiwa katika kitu chochote.Kuhusu ulinzi kwa nini hutaki tena walinzi?akauliza Devotha “Yule mtu wako hana adabu hata kidogo.Alithubutu kufungua milango na kuingia ndani wakati sipo.Kitendo kile kilinikasirisha sana ndiyo maana nikampiga marufuku asiingie humu ndani kama sipo.Hata yeye mwenyewe alikiri kwamba alifanya kosa na akaomba msamaha.Kuhusu walinzi ni kweli sihitaji walinzi kwa sasa hadi hapo nitakapomjulisha” “Kwa nini Melanie? “I can manage on my own ! “Sikiliza Melanie walinzi wale ni muhimu sana.Kwa namna yoyote ile unahitaji walinzi na wataendelea kukulinda hata kama hutaki” “Devotha nimekwisha sema sitaki ulinzi wowote.Mmekwisha nipa mlinzi mmoja Joyce inatosha sana hao wengine sitaki kuwasikia” “Melanie nini kimekutokea?Kwa nini umebadilika namna hii?akauliza Devotha Melanie akawa kimya “Nisikilize vizuri Melanie.Mimi ndiye mkubwa wako,ndiye kiongozi wako na utafuata kile ninachokuelekeza.Nakuonya usithubutu kwenda nje ya mstari utajuta.Utamsikiliza Edwin ndiye atakayekuwa akikuongoza.Chochote atakachokuelekeza ufanye bila kusita.Umenielewa Melanie?akauliza Devotha kwa ukali “Devotha naomba na mimi unisikilize.Mmenituma kuja huku Tanzania kufanya kazi zenu chafu.Mmenitumia mimi kwa sababu mnajua ninaweza hivyo basi kuanzia sasa mtanisikiliza mimi kile nikitakacho na operesheni hii itafanyika vile nitakavyo mimi.Sitaki kupangiwa au kuamrishwa chochote.Nyote kaeni kimya nisikilizeni mimi.Mmenipa kazi ya kufanya basi niacheni nifanye kazi.Tumeelewana Devotha? Akauliza Melanie “Jambo lingine naomba usithubutu tena kunitisha Devotha” akasema Melanie na kukata simu akaitupa pembeni. “This is my war,this is my revenge and I’m going to do it my way.Hakuna atakayenieleza chochote.Si Devotha wala nani.Wote watakaa kimya waangalie kile nitakachokifanya.Najua maneno niliyomweleza yatamuudhi sana Devotha na hata Rais Michael lakini potelea mbali kwani ni wazazi wangu ndio waliouawa hapa na lazima niwalipie kisasi” akawaza Melanie na kuichukua simu yake nyingine iliyokuwa inaita.Alikuwa ni GosuGosu “Mfalme wangu” akasema Melanie baada ya kuipokea “Melanie mpenzi wangu habari za muda huu? “Nzuri kabisa GosuGosu” “Melanie kuna jambo nataka tuzungumze hapa nyumbani kama hutajali” “Ninakuja hapo kwako Gosu Gosu.Nisubiri tafadhali” akasema Melanie na kukata simu “Ngoja niende kwa Gosu Gosu nikasikie alichoniitia.Lazima kitakuwa ni kitu muhimu sana.Halafu Devotha tayari amenitibua na dawa yangu pekee ninapotibuliwa ni kufanya mapenzi” akawaza Melanie na kumpigia simu Joyce akamtaka ajiandae waondoke
“Gosu Gosu nadhani unafahamu utaratibu wangu kila nikija hapa” akasema Melanie baada ya kufika nyumbani kwa Gosu Gosu.Hakujibiwa kwa maneno bali kwa vitendo.Gosu Gosu ambaye alikuwa na nguvu kama tembo akamuinua Melanie na kumuweka juu ya meza ambayo huitumia kwa ajili ya kusomea akiwa mle chumbani,akamtoa nguo ya ndani na mtanange ukaanzia hapo.Mzunguko mmoja wa haraka haraka ulimalizika kisha wakahamia kitandani kwa ajili ya mzunguko wa pili.Kama kawaida kila wakutanapo wawili hawa ni Melanie ambaye huomba apewe muda wa kupumzika. “Daaah ! Gosu Gosu sijui nikueleze nini lakini ninazidi kukupenda zaidi na zaidi kila uchao.Unanipa raha ya ajabu mno unanifanya niyafurahie maisha.Ahsante sana” akasema Melanie baada ya mzunguko wa pili kumalizika “Nakupenda pia Melanie.Unanipa furaha kubwa katika maisha yangu” akasema Gosu Gosu “Haya nieleze kile ambacho ulitaka kunieleza” akasema Melanie “Ulinipa kazi ya kutafuta namna utakavyoweza kukutana na James Kasai.Sijafanikiwa kuwasiliana naye yeye mwenyewe bali nimefanikiwa kumpata mtu mmoja anaitwa Edie.Huyu ni rafiki na James.Mimi na Edie tunafahamiana tuliwahi kushiriki wote katika vita ya msituni.Kwa sasa yeye anajishughulisha na biashara ya silaha.Nimemueleza nia yangu ya kutaka kukutana na James Kasai na ameahidi kunisaidia” “Good.Umemueleza sababu za kutaka kuonana na James Kasai? “Hapana sijamueleza chochote” akajibu Gosu Gosu “Ni vipi tutaonana na huyo Edie?Melanie akauliza “Kesho tunakwenda Uganda na tutakutana na Edie ambaye atatupeleka kwa James Kasai” “Ahsante sana Gosu Gosu.Nakushukuru kwa kunisaidia” “Usijali Melanie.Niko tayari kufanya chochote kwa ajili yako”akasema Gosu Gosu na Melanie hakutaka kupoteza muda kwa furaha aliyokuwa nayo wakaingia katika mzunguko mwingine wa tatu RIYADH –SAUDI ARABIA Kiza kimekwisha ingia pale mlango wa chumba alimopumzika Mathew ulipogongwa na jamaa mmoja aliyevalia nadhifu akamsalimu,kisha akampatia nguo zilizokuwa katika mfuko akamtaka avae.Mathew akaufungua mfuko ule na kukuta ndani yake kuna kanzu nzuri nyeupe akavaa kisha akatoka na kuongozana na Yule jamaa.Alipelekwa katika ukumbi mkubwa uliokuwa na meza kubwa ya chakula iliyosheheni vyakula vya aina mbali mbali.Wahudumu waliovalia nadhifu walikuwa wamejipanga tayari kuhudumia.Mathew akakaribishwa mezani akishangaa kwa uwingi ule wa chakula. Akiwa amekaa pale mezani mara akatokea http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nawal akiwa ameongozana na wanadada wawili wakasalimiana na wakati wakiendelea kuzungumza likatokea kundi la watu kumi hivi na meza ikazungukwa.Katika watu wale Mathew aliweza kumtambua Sayid Omar.Bila kupoteza muda Sayid Omar akasimama “Ndugu zangu tuliokusanyika hapa,chakula hiki jioni ya leo ni maalum kabisa kwa ajili ya kuwakaribisha ndugu zetu wawili waliotutembelea.Tunaye Abu Zalawi” akasema Sayid huku akitabasamu na kumnyooshea mkono Mathew akasimama huku akitabasamu “Abu Zalawi amekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya kudai haki na kupambana na wale maadui zetu Israel na washirika wake.Akiwa jijini Nairobi aliweza kumuua mkuu wa Mossad Afrika mashariki pamoja ma majasusi wengine wa Mossad.Abu Zalawi alikamatwa akafungwa katika gereza kwa miaka mitatu nchini Israel na huko akakutana na shujaa Ammar Nazari na kwa ushujaa alifanikiwa kuandaa mpango wa kutoroka gerezani na kufanikiwa.Huyu ndiye aliyemtorosha Ammar Nazari gerezani.Baada ya kutoka gerezani alijiunga na Ammar Nazari brigades na mlipuko uliotokea Jerusalem katika kituo cha treni hivi majuzi huyu ndiye aliyetekeleza shambulio lile.Abu Zalawi tuna furaha kuwa nawe hapa.Karibu jisikie nyumbani” akasema Sayid Omar. “Ahsante sana Sayid” akasema Mathew “Tunaye mgeni mwingine pia.Huyu amekuwa nasi hapa kwa siku mbili sasa.Anaitwa Nawal.Huyu alikuwa mke mdogo wa Ammar Nazari hadi pale majeshi ya Israel yalipokatisha uhai wake” akasema Sayid na Nawal akatabasamu “Wageni wetu karibuni sana.Mimi naitwa Sayid Omar ambaye tayari mnanifahamu” akasema Sayid na kufanya utambulisho kwa watu waliokuwepo mezani na mwisho akamtambulisha mtu muhimu “Mwisho kabisa ninamtambulisha kwenu mtu muhimu sana ambaye mmepitia safari ndefu mkimtafuta.Habiba Jawad” akasema Sayid Omar na Habiba akanyoosha mkono huku akitabasamu.Habiba alikuwa na unene wa kadiri na mweupe wa sura.Umri wake japo ulionekana mkubwa lakini bado sura yake ilivutia kutokana na kutunzwa vyema.Usiku huu alivaa gauni zuri la rangi ya kijani na kujitanda ushungi mwepesi wa rangi ya gauni.Masikioni alivaa hereni za gharama kubwa,vidole vyake vilijaa pete za thamani. Baada ya utambulisho ule wakajumuika wote kupata chakula kile kizuri kilichoandaliwa kwa ajili ya wageni wale wawili Mathew na Nawal.Kisha maliza kula Habiba akamuelekeza Sayid awapeleke wageni katika chumba cha mazungumzo kisha naye akaenda kuungana nao “Abu Zalawi na Nawal karibuni sana.Nimefurahi kuwaoneni hapa” akaanzisha mazungumzo Habiba “Hata sisi tumefurahi mama kukutana nawe” akasema Mathew “Poleni kwa yote mliyopitia najua haikuwa rahisi hadi mmefika hapa lakini tunafanya vile ili kujilinda.Mimi na wenzangu tunasakwa sana na serikali ya Israel na washirika wake hivyo lazima tuchukue tahadhari kubwa kwa mtu yeyote anayetaka kuonana nami.Najua Sayid Omar amekwiha kueleza kila kitu lakini nachukua nafasi hii kwa mara nyingine tena kukuthibitishia kwamba hatuna tatizo nawe wala Nawal.Yale yaliyofanyika ni kwa mujibu wa taratbu zetu.Tusameheni na tuufungue ukurasa mpya hivyo amani itawale” akasema Habiba Jawad “Tunashukuru sana mama” akasema Mathew “Mimi ndiye Habiba Jawad ambaye mmekuwa mkinisikia lakini leo hii mko nami ana kwa ana” akasema Habiba huku akitabasamu halafu akamtazama Nawal “Nawal,wewe nenda kapumzike nitakuwa na mazungumzo nawe kesho leo nataka nizungumze kwanza na Abu Zalawi” akasema Habiba na Nawal akatoka ndani ya kile chumba akawaacha Mathew na Habiba “Abu Zalawi naomba tufanye matembezi kidogo.Mimi hupenda kuwatembeza wageni katika himaya yangu” akasema Habiba kisha wakatoka ndani ya kile chumba wakatembea kuelekea katika bustani nzuri. “Vipi hali yako Abu Zalawi”Habiba akauliza “Ninajisikia vyema mama Habiba.Maendeleo yangu ni mazuri.Baada ya kuonana nawe nahisi majeraha yangu yote yamepona” akajibu Mathew kisha wakatembea kimya kimya na kwenda kukaa mahala ambako kumetengenezwa maalum kabisa kwa ajili ya kupumzika.Habiba akamtazama Mathew na kusema “Yapata miaka minne au zaidi kidogo niliwahi kukaa mahala hapa na binti mmoja aliitwa Olivia Themba akitokea Tanzania na leo hii niko nawe tena Mathew Mulumbi kutoka huko huko Tanzania” akasema Habiba huku akitabasamu lakini Mathew alipatwa na mstuko mkubwa sana kusikia Habiba Jawad akilitamka jina lake.Akahisi baridi ya ghafla. Mathew Mulumbi alihisi tumbo likivurugika kwa ndani akamtazama Habiba Jawad kama mtu aliyeona mzimu.Alitamani apae apotee zake lakini haikuwezekana.Habiba hakuwa na wasiwasi alikuwa anatabasamu “Huku ndiko kuruga jivu unakanyaka moto.Natamani nigeuke upepo nipotee lakini sina nguvu hiyo.Kama ningekuwa na ugonjwa wa moyo ningeanguka nakufa hapa hapa kwa mstuko nilioupata.Sikutegemea kabisa kwa habiba kutamka jina langu.Au labda ananifananisha?Ngoja nimjaribu” akawaza Mathew akitazamana na Habiba “Mama umekosea kutamka jina langu.Mimi ni Abu Al Zalawi na si Mathew Mulumbi kama ulivyotamka” akasema Mathew akijilazimisha kutabasamu.Habiba akatabasamu na kusema “Relax son.Usiwe na hofu.Hakuna kilichoharibika” akasema Habiba Jawad kwa sauti yake ya upole.Mathew alibaki anamtazama Habiba kwa hofu.Alikosa neno la kusema “Mathew Mulumbi huna haja ya kuendelea kukana jina lako kama ulivyofanya kwa Abdel Fattah Sarraf wakati anakufanyia mahojiano.Mimi sikufanyii mahojiano kwani ninakufahamu wewe ni nani na kwa nini uko hapa.Taarifa zako zote ninazo.Nina mtandao mrefu sana katika nchi mbali mbali duniani hivyo ninapata taarifa nyingi.Nina watu wangu Tanzania unakotoka,nina watu wangu Israel ndani ya Mossad,nina watu wangu ndani ya CIA na mashirika mengine makubwa ya ujasusi duniani.Ninafahamu mipango yao yote kuhusu mimi.Umewahi kujuliza swali Israel pamoja na ukubwa wa shirika lao la ujasusi lakini mpaka leo hii wameshindwa kunikamata kwa nini? Yamebaki ni maneno tu kwamba tunamsaka Habiba Jawad lakini hawawezi kunifikia.Umejiuliza pia Marekani kwa kupitia shirika lao la ujasusi CIA mpaka leo wameshindwa kuwasaidia Israel kufahamu mahala nilipo kwa nini?Unadhani CIA hawajui nilipo? Wanafahamu mahala nilipo lakini hawawezi kuwapa Israel taarifa zangu.Mimi ndiye Habiba Jawad” akasema Habiba na kutoa kicheko kidogo kisha akamtazama Mathew “Mathew ninakufahamu wewe ni jasusi kutoka Tanzania japo haufanyi tena kazi katika shirika la ujasusi Tanzania lakini umekuwa ukishirikishwa katika operesheni mbali mbali kubwa kubwa.Nafahamu hivi sasa wewe ni mfanyabiashara una mke anaishi Ufaransa anaitwa Peniela na una watoto wanne.Wawili ukiwa umezaa na Peniela na wawili ukiwa umezaa na mwanamke mwingine lakini wote wako Paris.Ukiwa Tanzania uliingia katika mahusiano ya kimapenzi na daktari Olivia Themba ambaye kama nilivyokueleza awali kwamba niliwahi kukaa naye mahala hapa hapa tukazungumza miaka kadhaa iliyopita.Dr Olivia alikuwa ni mpenzi wa Edger Kaka na alitekwa na idara ya serikali ya Tanzania baada ya kubainika ana mawasiliano na watu wa IS na hapo ndipo ulipojitokeza wewe na sitaki kuelezea kile kilichoendelea kwani unafahamu kila kitu lakini mwisho wa sakata lile ni pale ambapo ulitekwa na vikosi vya Israel wakati mkibadilishana mateka.Tanzania mkiwahitaji Olivia na mtoto wa Rais na IS wakimuhitaji Edger Kaka.Mabadilishano hayo ya matea hayakufanikiwa kwani mlivamiwa na wewe ukatekwa pamoja na Edger kaka.Nadhani tayari unafahamu kwamba waliokuvamieni wakati wa mabadilishano yale walikuwa ni vikosi vya Israel lakini je umejiuliza walipataje taarifa za kufanyika kwa mabadilishano yale?Nani aliwapa taarifa hizo? Unataka kumfahamu?akauliza Habiba na Mathew Mulumbi akatikisa kichwa kukubaliana na Habiba “Nitakueleza siku nyingine lakini kukamatwa kwako ulikuwa ni mpango maalum.Ulipelekwa Israel ambako ulifungwa na kupatiwa mateso mengi kwa miaka mitatu na uliyavumilia mateso hayo bila hata kutamka neno lolote na ndipo Mossad walipomtuma mtu wao ambaye alianzisha mahusiano na mkeo Peniela na wakakuonyesha picha wawili hao wakifanya mapenzi,lengo likiwa ni kukuumiza.Walifanikiwa lengo lao kwani ulikubali kushirikiana nao na ndipo mlipoandaa mpango kabambe wa kunitafuta mahala nilipo.Ulijenga mahusiano na Ammar Nazari ukamtorosha gerezani na ukajiunga na kundi lake.Hakujua kama wewe ulikuwa nipandikizi la Israel.Ulijenga uaminifu mkubwa kwa Ammar ili siku moja aweze kukuleta kwangu unipe taarifa za Edger Kaka lakini lengo lako likiwa ni kuniua kama ulivyotumwa na Mossad.Niliwapa maelekezo wakupe mateso kidogo kukupima na kweli umeiva katika ujasusi kwani pamoja na kuteswa kote lakini uliendelea kushikilia wewe ni Abu Zalawi.Wengine wote waliamini kwamba wewe ni Abu Zalawi lakini mimi kwa kuwa tayari ninakufahamu niliwaelekeza wakulete moja kwa moja kwangu hivyo karibu sana jisikie nyumbani.Mimi ndiye Habiba Jawad yule ambaye uliweka kiapo cha kuhakikisha unampata na kumuua” akasema Habiba na kumtazama Mathew aliyekuwa kimya akimsikiliza.Alikuwa mpole kama vile amemwagiwa barafu. “Nawal aliyekuwa mke wa Ammar naye ni pandikizi la CIA.Aliolewa na Ammar lakini alikuwa katika misheni maalum ya kumtafuta gaidi mmoja aliyeitwa Abdul Yasin Al Nasser ambaye anatafutwa na Marekani kwa kuhusika katika matukio kadhaa ya milipuko ya mabomu.Jana Abdul Yasin amekamatwa na makachero wa CIA.Unajua wamemkamata vipi?Ni kwa sababu mimi ndiye niliyetaka akamatwe.Nilimpa Nawal taarifa za mahala alipo Abdul,akawapa watu wake na Abdul Yasin akakamatwa.Hivi sasa tayari amekwisha fikishwa Marekani.Kama nisingeamua Abdul akamatwe asingekamatwa.Nimekueleza haya ili ujue Habiba Jawad ni mtu wa namna gani.Nina nguvu kubwa na si mtu ambaye unaweza ukapanga kuniua kirahisi rahisi namna hiyo” akasema Habiba na kucheka kidogo. “Mathew Mulumbi mtandao wote wa kigadi duniani uko hapa katika kiganja changu ninafahamu kila kitu kuhusu ugaidi duniani kwa sababu wote hawa mimi ndiye mfadhili wao.Wote mimi ndiye mlezi wao.Ninawasaidia kupata silaha,fedha za kugharamia operesheni zao na wakati mwingine hadi fedha za kujikimu.Mezani kwangu kuna maandiko kutoka katika makundi kadhaa yakihitaji ufadhili katika operesheni zao” akanyamaza kwa muda halafu akaendelea. “Edger kaka” akasema Habiba Jawad kwa hisia kali na kunyamaza kwa muda “Jina lake halisi si Edger Kaka.Jina lake halisi anaitwa Seif Jawad” “Seif Jawad?! Mathew akashangaa “Ndiyo.Anaitwa Seif Jawad.Ngoja nikupe historia kidogo Mathew Mulumbi” akasema Habiba na kunyamaza kidogo kwa sekunde chache akasema “Mimi asili yangu ni Somalia lakini nilizaliwa na kukulia nchini Kenya.Baada ya kumaliza shule niliolewa na tajiri mmoja aliitwa Nasser jawad.Alikuwa ni tajiri mkubwa sana pale Kenya.Mimi na Nasser tulipata mtoto mmoja Seif Jawad ambaye ninyi mnamfahamu kama Edger Kaka.Seif alipofikisha umri wa miaka mitano tulimuhamishia nchini Tanzania.Kuhamia kwa Seif Tanzania kulikuwa na sababu maalum.Niliichukia Tanzania na nilitaka kulipiza kisasi kwa kumtumia Seif.Wazazi wangu waliokuwa wakizunguka sehemu mbali mbali Afrika Mashariki wakifanya mihadhara ya kidini waliuawa nchini Tanzania wakidaiwa kwamba walikuwa wanahamasisha ugaidi.Jambo hili liliniumiza sana kwani nawafahamu wazazi wangu hawakuwa magaidi na mihadhara aliyoifanya baba haikuwa na mlengo wowote wa chuki wala kuhimiza ugaidi. Japo serikali ya Tanzania walidai kwamba wazazi wangu waliuawa na majambazi lakini taarifa nilizozipata ulikuwa ni mpango wa viongozi wa Afrika mashariki kuwaua wakidai kwamba walikuwa wanahamasisha watu kujiunga na vikundi vya kigaidi hivyo nilimuingiza Seif Tanzania kwa lengo la kumtumia katika kulipiza kisasi.Toka akiwa mdogo Seif alianza kuandaliwa kuwa mwanasiasa na lengo kuu ni siku moja aweze kushika madaraka makubwa na kuiongoza Tanzania.Nilimkabidhi Seif kwa familia ya watanzania waliomlea na kumbadili jina akaitwa Edger Kaka na kutambuliwa kama mtanzania.Watu hao walikuwa wakiishi nchini Kenya na walikuwa na mtoto wa kiume mwenye umri sawa na Seif lakini alifariki hivyo Seif alitumia jina la huyo mtoto ambaye alikuwa amefariki nchini Kenya.Niliwarejesha watuhao Tanzania na kuendelea kugharamia maisha yao.Baba yake Seif alifariki kwa ugonjwa wa saratani nikaolewa na mwanaume mwingine Abdul Dahir.Huyu nilizaa naye mtoto mmoja anaitwa Abu Dahir.Abdul alikuwa mpalestina na alikuwa tajiri sana.Alitumia utajiri wake kufadhili makundi mbali mbali ya wanamgambo waliokuwa wakipambana na serikali ya Israel wakidai haki ya ardhi yao.Kwa bahati mbaya Abdul naye alifariki dunia kwa kuuawa na vikosi vya Israel.Baada ya kifo cha Abdul nilishika hatamu na kuendeleza kile alichokuwa anakifanya.Niliendelea kufadhili makundi ya wanamgambo na baadae nikaendelea kufuatwa na makundi mengine ya kigaidi sehemu mbali mbali duniani wakiomba msaada nikalazimika kuwasaidia na ndipo nilipojikuta nikiwa mfadhili mkubwa wa ugaidi duniani” akanyamaza na kumtazama Mathew “Nchini Tanzania bado Seif aliendelea kuandaliwa.Aliingia katika siasa kwa kugombea ubunge na akashinda.Baada ya kuingia bungeni Seif au Edger alianza kutengeneza jina kwa kuibua kashfa mbalimbali za ufisadi.Ulifanya uchunguzi wako na unafahamu kila kilichokuwa kinaendelea namna alivyokuwa anapewa taarifa mbalimbali za mafisadi.Mtandao wote unaufahamu” akasema Habiba “Mathew Mulumbi kuna mengi ya kukueleza lakini kwa hayo machache naamini tayari umepata picha kubwa kuhusu mimi na harakati zangu.Narudia tena kukukumbusha kwamba nafahamu kwa nini uko hapa,umetumwa na Israel uje uchunguze na kuwapa taarifa mahala nilipo au ikiwezekana uniue.Nafahamu Ammar Nazari hakuuawa na mabomu ya Israel bali wewe na Nawal mlimuua.Ninazo picha za namna mlivyomuua ambazo Nawal aliwatumia CIA” akasema Habiba na Mathew akazidi kuchoka. “Lakini Mathew usiwe na hofu yoyote.Ninayefahamu kuhusu ninyi wawili kuwa ni majasusi ni mimi peke yangu.Hakuna yeyote kati ya wasaidizi wangu anayefahamu ninyi ni akina nani na sintawaeleza chochote.Mimi ni mama na ninyi ni kama watoto wangu sitaki muuawe.Sitaki mingie katika matatizo.Mateso mliyoyapitia yametosha na hapa mmekuja kupata pumziko.Ninataka kuwasaidia Mathew wewe na mwenzako Nawal.Nataka kuwaondoa katika maisha haya ya mateso makubwa mnayoyapitia na kuwaingiza katika maisha mapya yaliyojaa amani na furaha tele ndiyo maana sijataka mtu wangu yoyote afahamu kuhusu ninyi ni akina nani” akanyamaza tena na kumtazama Mathew “Nawal amepitia mateso makubwa kwa Ammar Nazari na kama angejulikana angeuawa.Wewe vile vile umepitia mateso makali nchini Israel kwa miaka mitatu.Nini mnakipata katika mateso hayo yote mnayoyapitia?Je nchi zenu zinazowatuma mfanye operesheni hizo za hatari zinawapa thamani gani? Kwa mambo uliyoyafanya nchini kwako mtu kama wewe ulitakiwa kupewa tuzo kubwa ya heshima lakini hakuna chochote unachokipata badala yake maisha yako yamekuwa kama ya ndege.Hivi sasa hakuna anayesumbuka kukutafuta wakiamini tayari umefariki dunia.Hii si sawa hata kidogo walipaswa kutumia kila aina ya uwezo kukutafuta na kukurejesha nyumbani.Kikubwa ninachotaka ukifahamu hapa ni kwamba mambo unayoyafanya ni makubwa lakini thamani yako bado ni ndogo mno.Baada ya kupitia hayo yote hatimaye mmefika nyumbani.Hapa ninawajali na kuwathamini.Mlikuwa ni maadui zangu lakini ninataka kuwafanya kuwa watoto na watu wangu wa karibu.Nataka kubadili maisha yenu muishi kwa amani na furaha” akasema Habiba na kuendelea kumtazama Mathew “Nadhani tayari Nawal amekwisha kueleza kwamba mipango inaandaliwa ili aweze kuolewa na mwanangu Abu Dahir.Abu alipomuona Nawal alitokea kumpenda na akaniomba kama anaweza akamuoa mimi sikuwa na kipingamizi chochote na hapo ndipo nilipopata wazo la kuwatoa kuwa maadui zangu na kuwafanya watoto wangu.Kinachoendelea hivi sasa ni taratibu za kidini zikamilike ili Nawal na Abu waweze kuoana.Najua wewe si muislamu lakini unaufahamu uislamu na unazifahamu taratibu za kiislamu zilivyo kwa mwanamke ambaye amefiwa na mumewe kutaka kuolewa tena.Nawal hana tatizo amekubali kuolewa na hii ndiyo sababu umemuona Nawal amebadilika tofauti na ulivyomfahamu alipokuwa kwa Ammar Nazari.Naamini utajiuliza siogopi kwamba Nawal kuolewa na mwanangu Abu Dahir nitakuwa nimejiweka katika hatari zaidi kwamba Nawal atapeleka taarifa zangu CIA? La hasha siogopi chochote na jambo hilo haliwezi katu kutokea.Ninajiamini na kile ninachokifanya” akasema Habiba.Ulipita ukimya mfupi halafu Habiba akaendelea “Baada ya kifo cha Abdul Dahir nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na tajiri mmoja lakini hatukufunga ndoa.Katika mahusiano hayo tulifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike anaitwa Najma.Baba yake ni Raia wa Iran na kwa muda mrefu Najma alikuwa akiishi na baba yake.Kwa sasa ni daktari,amesomea nchini Urusi na ninaishi naye hapa Riyadh.Kwa bahati mbaya hakuweza kujumuika nasi kwa chakula cha usiku lakini utapata nafasi ya kukutana naye.Kama nilivyokueleza Mathew kwamba ninataka kuwafanya wewe na Nawal muwe watoto wangu.Nataka nihitimishe maisha yenu ya shida na mahangaiko mliyoyapitia kwa miaka mingi.Kama ilivyokuwa kwa Nawal nataka nawe Mathew Mulumbi umuoe mwanangu Najma” akasema Habiba na Mathew akahisi kama nyundo imegonga kichwa chake.Habiba akamtazama Mathew na kutabasamu “Nauona mstuko mkubwa katika uso wako baada ya kukueleza umuoe mwanangu Najma.Kitu gani kimekustua Mathew?akauliza Habiba.Mathew akakohoa kidogo na kusema “Mama Habiba nimestuka kwa kuwa hilo jambo ulilolisema haliwezekani.Mimi nina mke na watoto wanne na siwezi tena kuoa mke mwingine” akasema Mathew na Habiba akatoa kicheko kidogo “Hauna mke Mathew Mulumbi,unaye mjane.Peniela si mkeo tena.Huko aliko anaamini tayari umekwisha fariki dunia na ameamua kuendelea na maisha yake.Labda nikupe siri ya kitu ambacho hukifahamu.Mali zako zote zilizoko Dar es salaam tayari zimeuzwa” “Zimeuzwa?Mathew akashangaa “Ndiyo.Peniela ameuza mali zote zilizoko Tanzania.Unadhani kwa nini ameamua kufanya hivyo?Ni kwa sababu anajua hutarudi tena,umekwisha kufa.Maisha yako Tanzania yamekwisha ndiyo maana nataka kukuanzishia maisha mengine hapa.Ningekuwa sina nia nzuri kwako ningeweza kuelekeza uuawe lakini sijafanya hivyo.Sioni sababu yoyote ya kukuangamiza Mathew Mulumbi.Bado unayo nafasi ya kuendelea kufurahia maisha yako.Familia yako wamekwisha kubaliana na ukweli kwamba umeondoka na hautarudi tena hivyo hakuna haja ya kwenda kuwasumbua na kuvuruga maisha waliyonayo sasa.Nakupa nafasi ya kuanza maisha mapya ukiwa na Najma.Ninao utajiri mkubwa sana na utakuwa mmoja wa watoto wangu ambao nitawaingiza katika orodha ya warithi wangu.Mali zako zote ulizopoteza Tanzania utazipata hapa hata mara kumi zaidi” akasema Habiba na Mathew akainamisha kichwa “Mathew najua yote niliyokueleza yamekustua sana.Hukutegemea kama ninafahamu wewe ni Mathew Mulumbi,hukutegemea kama ninafahamu mipango yako yote.Umepatwa na mshangao mkubwa sana kwa uliyoyasikia lakini naamini ni kwa sababu hukuwa ukimfahamu Habiba Jawad ni nani.Habiba Jawad ni zaidi ya mnavyoelezwa katika mashirika yenu ya kijasusi.Habiba Jawad anaelezewa kijuu juu tu kwa sababu hafahamiki lakini kwa wanaomfahamu Habiba wanamuogopa sana.Sitaki kukuogopesha lakini nataka umfahamu Habiba ni nani na ukishamjua utajilaumu sana kwa kupoteza muda wako kumfuatila mtu ambaye hapaswi kufuatiliwa.Tuyaweke hayo pembeni nataka unieleze kuhusu Edger Kaka.Ulisema unafahamu mahala alipo?akauliza Habiba.Mathew akameza mate kuloanisha koo kisha akasema “Ndiyo ninafahamu mahala alipo” akasema Mathew “Nieleze ukweli kuhusu Edger” akasema Habiba “Kwanza kabisa naomba ufahamu kwamba Edger hakuwa anashikiliwa na serikali ya Tanzania bali alikuwa ametekwa na Israel na alikuwa akishikiliwa katika ubalozi wao jijini Nairobi.Mimi ndiye niliyeongoza timu iliyovamia ubalozi huo wa Israel jijini Nairobi na kumchukua Edger Kaka.Alikuwa amefungwa katika chumba chenye giza akipatiwa mateso makali.Edger alikuwa katika hali mbaya alikuwa amekonda na hakuwa na uwezo hata wa kutembea.Baada ya kumuokoa tulimpeleka Dar es salaam ambako ilitulazimu kufanya mabadilishano na IS kwa ajili ya kuwapata mtoto wa Rais pamoja na Olivia Themba ambao walikuwa wanashikiliwa na IS.Niliongoza mabadilishano hayo na katikati ya mabadilishano ndipo tukavamiwa na vikosi vya Israel na mabadilishano hayakufanyika tena.Mimi nikachukuliwa mateka na Edger pia akachukuliwa.Kwa bahati mbaya wakati wa purukushani zile Edger alianguka na kugonga kichwa katika jiwe kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kukimbia.Alipoteza fahamu na toka wakati huo hajawahi kuzinduka tena.Alipofikishwa Israel hali yake ilizidi kuwa mbaya na akalazimika kuwekwa katika mashine ya kumsaidia kuishi lakini kwa taarifa ya daktari ni kwamba ubongo wa Edger umekufa na hakuna uwezekano wa kuzinduka tena.Kwa ufupi ni kwamba Edger amekwisha fariki na kinachomuweka hai hadi sasa ni mashine” akasema Mathew na Habiba akainama akafuta machozi. “Mwanangu nilikuwa na mipango naye mikubwa sana lakini mipango yote haijafanikiwa imeishia njiani.Inaniuma sana” akasema Habiba na kuendelea kufuta machozi. “Mathew nakuomba ukaniletee mwanangu walau niweze kumzika kwa heshima zote.Naamini akiendelea kukaa huko aliko watamfukia kama mzoga kwa chuki walizonazo kwetu.Naomba fanya kila lililo ndani ya uwezo wako uniletee mwili wa mwanangu.Nakuomba sana” akasema Habiba akiendelea kufuta machozi “Sawa mama nitakuletea mwili wa mwanao” akasema Mathew “Utafanyaje kuupata mwili huo?akauliza Habiba “Nitaondoka hapa na kurejea Israel.Nitaonana na wakuu wa Mossad nitawaeleza kwamba nimewasiliana nawe kwa simu na umenitaka nikupelekee mwili wa Edger.Nina uhakika mkubwa watakubaliana nami na watanipa mwili wa Edger” “Mathew ninakutuma nenda kaniletee mwili wa mwanangu lakini ninakuonya usijaribu kufanya jambo lolote la kipuuzi kwani nitajua na utakuwa umefanya jambo baya sana” “Mama usiwe na wasi wasi nami.Nakutaka uniamini na nitamrejesha Edger nyumbani” akasema Mathew “Mathew ahsante.Nini utakihitaji katika zoezi hilo? “Ninahitaji kufikishwa katika mpaka wa Israel na Jordan” “Sawa.Nitakukabidhi kwa Sayid Omar na atashughulikia kila kitu” akasema Habiba na kisha akainuka wakaondoka wakarejea ndani akampigia simu sayid Omar akafika mara moja na kumchukua Mathew wakaenda kupanga mipango ya kwenda kuondoka kuelekea Israel kuchukua mwili wa Edger Kaka MPENZI MSOMAJI TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………
UGANDA Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe nchini Uganda.Miongoni mwa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hii iliyotokea Dar es salaam Tanzania ni Melanie Davis na Gosu Gosu.Kisha kamilisha taratibu za uwanjani hapo waliruhusiwa kuingia nchini Uganda na nje ya wanja walipokewa na mwenyeji wao aliyeitwa Eddie Okello.Huyu alikuwa ni rafiki wa muda mrefu wa Gosu Gosu waliwahi kupigana wote vita ya msituni.Eddie na Gosu Gosu walikumbatiana kwa furaha kubwa baada ya kuonana baada ya muda mrefu “Papii siamini macho yangu ni wewe kweli?akasema Eddie na kumkumbatia tena Gosu Gosu.Ilikuwa ni furaha iliyopitiliza kwa marafiki hawa wa muda mrefu kuonana tena. “Eddie kutana na Melanie Davis ni mchumba wangu” akasema Gosu Gosu na Eddie akabaki mwenye mshangao akiushangaa uzuri wa Melanie. “Hallow Eddie” akasema Melanie baada ya kumuona Eddie amepigwa na butwaa. “Hallow Melanie.karibu sana Uganda” akasema Eddie na kupeana mkono na Melanie kisha akawaongoza hadi katika gari lake wakaingia na kuondoka pale uwanjani “Papii uliponiambia kwamba unakuja Uganda sikuamini ndiyo maana furaha niliyonayo leo haielezeki.Umebadilika sana Papii,si yule niliyekufahamu msituni” akasema Eddie na Gosu Gosu akatabasamu “Sote tuna mabadiliko makubwa baada ya kuachana na mambo yale ya msituni.Kila mmoja ana maisha mapya hivi sasa” akasema Gosu Gosu na kukumbushana mengi kuhusu maisha yao ya msituni.Muda huo wote Melanie alikuwa kimya alikuwa mbali kimawazo. Hatimaye walifika katika jumba moja kubwa Eddie akawakaribisha ndani “Hapa ndipo ninapoishi.Karibuni jisikieni nyumbani” akasema Eddie na kumuita muhudumu akawahuduia wageni vinywaji “Eddie kama nilivyokueleza kwamba hatutakuwa na muda mrefu hapa Uganda tunataka tumalize kilichotuleta hapa leo na kurudi nyumbani hivyo ingekuwa vyema kama ungetupa mwongozo kuhusu safari yetu” akasema Gosu Gosu “Usihofu Gosu Gosu maandalizi yamefanyika na mtaonana na James Kasai lakini naomba ninaweke wazi kwamba si safari nyepesi.Mahala alipo James ni ndani sana msituni hivyo tutakuwa na safari ndefu kidogo.Tutakwenda na helkopta na tutafika sehemu tutachukua gari kuelekea huko msituni anakoishi” akasema Eddie “Hakuna tatizo sisi tuko tayari” akasema Gosu Gosu na hawakupoteza muda wakaingia garini na kuondoka hadi katika jumba moja kubwa lililoonekana kama hoteli.Eddie akashuka garini akaingia ndani ya jumba lile akatumia kama dakika kumi hivi kisha akatoka akiwa ameongozana na mtu mmoja mnene aliyevaa suti nyeusi.Eddie akamtambulisha Yule jamaa kwa akina Melanie kama rafiki yake na ndiye mmiliki wa jumba lile,wakasalimiana kisha Eddie akawataka washuke garini wakatembea katika njia nzuri kuelekea nyuma ya jumba lile ambako kulikuwa na helkopta ya rangi nyeusi.Gosu Gosu na Melanie wakatakiwa kuingia ndani ya helkopta,Eddie akabaki akizungumza na yule rafiki yake halafu naye akaingia katika helkopta wakaondoka.Walituia zaidi ya dakika arobaini angani kisha wakatua ndani ya uwanja mkubwa uliopandwa nyasi nzuri uliokuwa pembeni ya jumba moja la ghorofa.Eddie akawataka akina Gosu Gosu washuke “Kutokea hapa tutaendelea na safari yetu kwa kutumia gari” akasema Eddie na kuwaongoza hadi katika magari mawili yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya safari ile wakaingia katika gari mojawapo na safari ikaanza “Kutokea hapa tutachukua muda gani kufika tuendako? akauliza Gosu Gosu “Itatuchukua muda wa saa tatu hadi nne.Miundo mbinu hasa barabara huko tuendako ni mibovu sana na endapo tutakuta mvua imenyesha basi inaweza kutuchukua hata masa matano hadi sita.Kuna sehemu nyingine itatulazimu kushuka na kutembea kwa miguu.Ni safari ndefu itawalazimu kuvumilia.”akasema Eddie “Hakuna tatizo tunachokihitaji ni kuonana na James” akasema Gosu Gosu Hakukuwa na mazungumzo mengi garini,walipita katika barabara za vumbi zenye mashimo mengi na kuna sehemu ambazo barabara ilikuwa mbaya zaidi na kuwalazimu kushuka wakatembea kwa miguu ndipo wakaendelea na safari.Ulikuwa ni mwendo wa zaidi ya masaa manne.Melanie alichoka sana.Hatimaye baada ya mwendo wa takribani saa tano wakafika sehemu Fulani ambako walikuta kuna kizuizi na watu zaidi ya kumi wakiwa na sare za kijeshi wakawasimamisha na kuwashusha garini.Eddie akazungumza nao na kiongozi wa kikosi kile akafanya mawasiliano kisha akawaamuru waingie katika gari lao na wakaanza kusindikizwa na gari mbili za wanajeshi wale wa kikundi cha James Kasai.Baada ya mwendo wa dakika thelathini wakaukuta mto na hapo ulikuwa mwisho wa kutumia gari kwani hakukuwa na daraja kwa ajili ya kuvusha magari.Walishuka garini na kuanza kuvuka daraja la kamba kuelekea ng’ambo ya pili.Haikuwa rahisi kwa Melanie kuvuka katika daraja lile la kamba ikamlazimu Gosu Gosu kumshika mkono na kumsaidia kuvuka katika daraja lile ambalo Mamba walionekana wakizunguka zunguka.Baada ya kuvuka katika lile daraja wakaanza kutembea kwa miguu kama dakika ishirini.Melanie alichoka mno na wakati mwingine ikamlazimu Gosu Gosu kumbeba. Baada ya kumaliza kuvuka daraja walitembea kilometa chache kisha wakaanza kukutana na mahema ya wanajeshi.Kila mwanajeshi waliyekutana naye alikuwa na sura ya kutisha na amebeba bunduki ya vita.Ilikuwa ni sehemu ya kutisha sana.Hatimaye wakafika katika nyumba ya ghorofa iliyojengwa kwa mbao na miti.Ilikuwa imezungukwa na walinzi kila kona na mizinga kadhaa ya kutungulia ndege ilionekana kuzunguka nyumba ile.Pembeni yake kulikuwa na nyumba nyingine za mbao kama nane hivi.Kambi hii ilikuwa katikati ya msitu mnene.Yule kamanda aliyewapokea katika kizuizi akawaongoza wakaingia katika ile nyumba ya ghorofa akawakaribisha katika sebule ambayo haikuwa na vitu vya thamani akawaacha pale akapanda juu ghorofani “Hapa ndipo anapoishi james Kasai” akasema Eddie “Dah ! nimewaona wale wanajeshi nimekumbuka mbali sana maisha tuliyoishi msituni” akasema Gosu Gosu “Tumetoka mbali sana.Yale si maisha ya kutamani kuyarudia hata kidogo.Ni maisha magumu sana yaliyojaa hatari kila sekunde” akasema Eddie Wakiwa pale sebuleni kila mmoja akiwaza lake mara akatokea Yule mwanajeshi aliyewapokea kizuizini akiwa ameongozana na jamaa mmoja mrefu aliyevaa suruali ya kijeshi na fulana nyeusi iliyokatwa mikono.Mabega yake yote yalikuwa yamechafuliwa na michoro mbali mbali.Kichwani alivaa kofia ya mduara na macho yake aliyafunika kwa miwani myeusi.Nyuma yake alikuwa na watu sita wakiwa na bunduki wakimlinda.Eddie alipomuona akishuka akawataka akina Gosu Gosu wasimame “Karibuni sana wageni wangu.Poleni kwa safari ndefu hadi kufika hapa” akasema Yule jamaa huku akiwapa mikono akina Gosu Gosu halafu akawataka wapande ghorofani ambako kulikuwa na sebule nzuri sana yenye samani za kuvutia. “Wageni wetu tunawashukuru mmefika salama Poleni sana kwa safari ndefu ya kufika hapa.Si safari nyepesi kufika hapa lakini haya ndiyo maisha yetu tumekwishayazoea.Naamini mmechoka kwa safari mtaenda kupumzika na baadae tutakutana kwa mazungumzo” akasema James na mmoja wa makamanda wake akasogea karibu akapiga saluti kali mbele yake. “Wapeleke wageni wakapumzike” akasema James na akina Gosu Gosu wakachukuliwa wakapelekwa katika nyumba moja iliyojengwa kwa mbao lakini ukiwa ndani huwezi amini kama imejengwa kwa mbao kutokana na uzuri wake.Walikaribishwa katika chumba kizuri sana kilichoandaliwa kwa ajili yao.Melanie alikuwa amechoka kupita maelezo.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya safari ngumu kama ile. “Pole sana mpenzi wangu kwa safari hii ndefu” akasema Gosu Gosu wakiwa wamejilaza kitandani baada ya kuoga. “Sijawahi kuchoka kiasi hiki.Ni mara yangu ya kwanza kufanya safari ndefu na ngumu kama hii” akasema Melanie “Pole sana.Hata hivyo lengo letu limetimia na tumefanikiwa kukutana na James Kasai”akasema Gosu Gosu “Yule jamaa hapatikani kirahisi.Kwanza anaishi katika msitu mnene na kufika hapa si kazi nyepesi” “Maisha haya ya msituni ndiyo niliyokuwa nikiishi” akasema Gosu Gosu “Ilikuaje hadi ukaingia msituni na kujiunga na makundi ya waasi?akauliza Melanie “Niliingia msituni angali nikiwa mdogo sana.Nilikuwa na miaka nane nilipotekwa na makundi ya waasi waliovamia kijiji chetu usiku na kuua watu,wakabaka wanawake na kisha wakateka watoto na kutupeleka msituni.Tulikuwa jumla yetu ishirini na nane na tukaanza kutunzwa na waasi.Tulianza kwa kutumwa na wakubwa zetu baadae tukaanza kupewa mazoezi mbali mbali na kufundishwa silaha.Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na tatu tayari nilikuwa na uwezo wa kupigana vita.Mara yangu ya kwanza kuua mtu nilikuwa na miaka kumi na tatu.Baada ya hapo nikawa mpiganaji na mtu katili sana.Sehemu kubwa ya maisha yangu yote nimekuwa nikiishi msituni” akasema Gosu Gosu “Ilikuaje ukatoka msituni na kuja kuishi hapa Tanzania?akauliza Melanie na Gosu Gosu akampa historia yake namna alivyotoka msituni akaja kuishi hapa Tanzania na hadi alipokutana na Mathew Mulumbi ambaye amemfikisha hapa alipofika “Ninatamani sana kumfahamu huyo mtu Mathew Mulumbi.Alikuwa mtu wa aina gani hasa?akauliza Melanie “Mathew alikuwa jasusi ambaye aliifanya kazi yake kwa mafanikio makubwa sana.Nashindwa namna ya kumuelezea ana sifa nyingi.Siku zote atabaki kuwa mtu wa pekee kwangu na kwa nchi pia japo mchango wake hauthaminiwi”akasema Gosu Gosu “Alifariki vipi?akauliza Melanie “Alifariki akiwa katika misheni ya kuwakomboa mateka waliokuwa wametekwa na kundi la IS.Ilikuwa ni misheni ya hatari sana” akasema Gosu Gosu na kisha wakaendelea kupumzika. Saa moja za jioni walitakiwa kujiandaa kwa ajili ya kukutana na James Kasai. “Unajisikiaje hivi sasa mpenzi?Gosu Gosu akamuuliza Melanie “Kwa sasa baada ya kupumzika najisikia vyema” akasema Melanie wakatoka na kwenda kukutana na James Kasai.Eneo lote lilikuwa linawaka taa walikuwa wanatumia umeme unaozalishwa kwa maporomoko ya maji. Walikaribishwa katika sehemu maalum ambako James alikuwa anawasubiri wageni wake “Natumai mmepumzika kidogo.Ni wakati wa kupata chakula kisha tuendelee na mazungumzo”akasema James Kasai na kuwaongoza akina Melanie katika meza iliyokuwa imeandaliwa vyakula mbali mbali wakaketi na kupata chakula kisha wakaenda sehemu ya maongezi “Natumai kwa sasa tuko tayari kwa mazungumzo” akasema James “James tunashukuru sana kwa makaribisho mazuri tuliyoyapata hapa na sasa tuko tayari kwa mazungumzo” akasema Gosu Gosu “Mimi kama nilivyojitambulisha awali ninaitwa James Kasai ndiye kiongozi wa kikundi hiki.Historia yangu si nzuri sana lakini ninapigana kwa ajili ya maslahi ya nchi yangu.Ninataka kuikomboa Kongo kutoka katika makucha ya wanyonyaji” akasema James Kasai na kuinua chupa ya mvinyo iliyokuwa mezani akamimina katika glasi akanywa na kusema “Nilipata taarifa kwamba kuna watu wanataka kuniona kuna jambo muhimu sana wanataka kuzungumza nami.Taarifa hiyo niliipata toka kwa Eddy ambaye nimefahamiana naye kwa miaka mingi na ni mshirika wangu wa karibu sana ndiyo maana nikakubali kuonana nanyi.Eddie alinijulisha kwamba mmoja wa watu wanaohitaji kuonana nami amewahi kupigana vita ya msituni nikafurahi kukutana na mwanajeshi huyo ambaye naamini ni wewe” akasema James Kasai na kumtazama Gosu Gosu “Ni mimi” akasema Gosu Gosu “Kwa nusu ya maisha yangu nimeishi msituni nikipigana vita” akasema Gosu Gosu na kumtajia James majina ya watu ambao walikuwa pamoja katika mapambano yale ya msituni.James Kasai alifurahi sana kumsikia Gosu Gosu akiwataja watu wale. “Nimefurahi sana kukutana nawe Gosu Gosu.Umenikumbusha mbali sana.Tukipata nafasi tutazugumza mengi lakini kwa sasa tujielekeze katika kile kilichotukutanisha hapa” akasema James Kasai “Nimeambatana na mpenzi wangu anaitwa Melanie Davis.Yeye ndiye ambaye ana jambo la kuzungumza nawe”akasema Gosu Gosu “Melanie karibu sana.Nimekutana na Gosu Gosu nikajkuta nikikumbuka mbali sana na kukusahau kabisa.Jisikie nyumbani”akasema James Kasai. “Ahsante nashukuru” akasema Melanie na kumtazama Gosu Gosu akamfanyia ishara Fulani na Gosu Gosu akasimama “Nitawaacha mzungumze nitarejea baadae mkisha maliza” akasema Gosu Gosu na James akamuita mmoja wa walinzi wake akamtaka ampeleke Gosu Gosu katika sehemu ya kupumzika maofisa “Melanie karibu sana.Haya ndiyo makazi yetu tuko kati kati ya msitu”akasema James baada ya Gosu Gosu kuondoka “Nashukuru sana.Japo ni mbali na kufika kwake si kazi nyepesi lakini nimependa mazingira yake ya utulivu na hewa safi” akasema Melanie na James akatabasamu “Melanie umenifahamuje?akauliza James “Mimi nina asili ya Congo nilikuwa naishi Ufaransa lakini kwa sasa nimehamia Tanzania.Nina makampuni kadhaa Tanzania” “Hongera sana.Nafurahi kukufahamu Melanie kumbe wewe ni mtu wa nyumbani kabisa” akasema James na kunywa funda la mvinyo “Nimekuwa nikisoma sana historia ya Congo ndiyo maana nikakufahamu” akasema Melanie “Historia yangu ni mbaya na hadi sasa ninatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita nikajibu mashtaka ninayotuhumiwa nayo.Nimejiuliza pamoja na historia yangu hiyo kuwa mbaya lakini bado umetaka kuonana nami.Kitu gani hasa kilichokufanya upande milima na mabonde kutaka kuonana nami?akauliza James na Melanie akavuta pumzi ndefu akasema “Nina jambo kubwa ambalo nimekuja kuzungumza nawe na ninaamini nimekuja sehemu muafaka kabisa” akasema Melanie “Usihofu Melanie nieleze chochote kama ni siri nitaitunza” akasema James.Baada ya sekunde kadhaa Melanie akasema “Naamini umewahi kumsikia Lucy Muganza” akasema Melanie “Lucy Muganza ninamfahamu.Ni Yule mwanamke tajiri sana ambaye aliuawa yeye na mumewe nchini Tanzania.Alikuwa amechaguliwa na chama kikuu cha upinzani ili agombee urais katika uchaguzi mkuu uliopita” akasema “Wale walikuwa wazazi wangu” “Wazazi wako?! James akashangaa “Ndiyo ni wazazi wangu.Jina langu halisi ni Theresia Muganza.Nilikuwa pamoja na wazazi wangu Dar es salaam siku walipouawa na mimi nilinusurika kwa kupigwa risasi ya kifua.Nilipelekwa hospitali nikapatiwa matibabu ya haraka,baadae serikali ya Ufaransa ikanitaka nihamishiwe Paris kwa matibabu zaidi na nimekuwa Paris kwa muda wote hadi hivi juzi nilipokuja tena Tanzania.Baada ya kupona ilinilazimu kufanyiwa upasuaji wa kubadili mwonekano wangu kwa ajili ya usalama kwani bado ninaamini wale watu ambao walitaka kuiteketeza familia yetu bado wapo na kama wakijua mimi ni Theresia Muganza lazima wataniua.Kwa sasa nina sura mpya na jina jipya la Melanie Davis” akasema Melanie na James akavua kofia akaiweka pembeni “Pole sana Melanie.Umepitia mambo makubwa.Nani lakini waliofanya mauaji yale?Nini malengo yao?akauliza James “Yalikuwa ni mauaji ya kisiasa.Inatajwa kwamba tukio lile lilikuwa na kijambazi na siku ile ile ya tukio waliuawa majambazi kadhaa lakini kuna tarifa zenye kuaminika kwamba halikuwa tukio la kijambazi bali yalikuwa ni mauaji yaliyopangwa na majambazi wale waliangushiwa mzigo.Miili ilipofanyiwa uchunguzi imekutwa na risasi za bunduki kubwa za wadunguaji ambazo majambazi wale hawakuwa nazo na bunduki hizo zinamilikiwa na serikali.Hii inatupa picha ya wazi kwamba mauaji yale yalifanywa na serikali ya Tanzania wakishirikiana na serikali ya Congo”akasema Melanie “Hata mimi niliamini lazima kuna jambo nyuma ya mauaji yale” akasema James “Ipo sababu kwa nini wazazi wangu waliuawa” akasema Melanie na kunyamaza kidogo baada ya muhudumu kuleta sinia lililojaa nyama za kuchoma “Karibu nyama Melanie.Hii ni nyama ya Swala ambayo humuandalia kila mgeni anayetutembelea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Usihofu iko salama.Japo tuko msituni lakini tuko vizuri katika suala la afya.Tunao madaktari wetu ambao hupima kila chakula kabla hakijaliwa.” akasema James .Melanie akachukua finyango chache akaweka katika sahani “Ipo sababu ya wazazi wangu kuuawa” akasema Melanie na kutafuna nyama moja halafu akaendelea “Baada ya kushinda uchaguzi,Rais Patrice Eyenga alikutana na makundi vya waasi waliokuwa wakipigana na serikali ya Congo kwa muda mrefu na wakakubaliana kuweka silaha zao chini na huo ukawa ni mwisho wa mapigano ya Congo amani ikarejea tena.Ni wewe pekee ambaye hukutaka kukubaliana na mkataba ule wa amani” akasema Melanie “Ni kweli kabisa” akasema James na Melanie akaendelea “Patrice alifumua kila alichokikuta kimefanywa na watangulizi wake.Alifukuza wawekezaji wakubwa katika sekta mbali mbali na kutafuta wawekezaji wapya.Lakini baadae ikaja kugundulika kwamba viongozi wa makundi ya waasi walikubaliana kuweka silaha zao chini kwa kupata asilimia kadhaa ya fedha iliyotokana na mauzo ya madini hivyo kufanya kuwe na kundi dogo linalofaidika na rasilimali za nchi.Serikali ya Ufaransa baada ya kuligundua hilo walitafuta njia ya kuweza kuliondoa genge hilo la walafi wanaohujumu rasilimali za nchi wakiongozwa na Patrice Eyenga na ndipo walipoamua kutumia uchaguzi mkuu uliopita ili kumuondoa Patrice na genge lake.Walimchagua mama yangu agombee urais kupitia chama kikuu cha upinzani.Walimchagua mama yangu kwa vile alikuwa ni mtu mwenye jina kubwa nchini Congo na alitegemewa kushinda ndiyo maana akauwa kabla ya chaguzi kufanyika.Serikali za Tanzania na Congo zilishirikiana katika mauaji yale ya wazazi wangu” akanyamaza na kutafuna nyama kisha akaendelea “Nilipatiwa matibabu nchini Ufaransa na baada ya kupona Rais Michael weren alikuja kuzungumza nami akanieleza kila kitu kuhusiana na mauaji yale ya wazazi wangu na akanitaka nivae viatu vya mama niendeleze kile ambacho alikusudia kukifanya yaani kulisafisha genge la walafi wanaomaliza rasilimali za Congo.Haikuwa rahisi mimi kukubali lakini baada ya kutafakari sana nikakubali kuifanya kazi hiyo aliyotakiwa kuifanya mama na ndipo nilipofanyiwa upasuaji wa kubadili mwonekano wangu ili watu wasinitambue kama Theresia Muganza, nikapewa jina jipya Melanie Davis ama bilionea Melanie Davis” akasema Melanie na James akatoa tabasamu kubwa “Nimekuja Afrika Mashariki kwa malengo mawili makubwa.Kwanza ni kuisambaratisha jumuiya ya afrika Mashariki na pili ni kumuondoa madarakani Rais Patrice Eyenga na kuliondoa genge la mafisadi wanaopora mali za nchi.Nimeisoma historia yako na Rais Patrice ndiyo maana nikaamua kukufuata ili tuunganishe nguvu katika mapambano dhidi ya kuung’oa utawala wake” akasema Melanie na James Kasai akatoa pakiti la sigara akawasha moja na kuvuta akapuliza moshi halafu akasema “Kwa muda wote ambao nimekaa msituni hapa sijawahi kupata mgeni muhimu kama wewe Melanie.Ahsante sana kwa kuja na ninakuhakikishia kwamba hujakosea kuja kwangu” “Ahsante sana James kwa kunipokea na ninaamini mimi nawe tutatengeneza timu nzuri sana” akasema Melanie “Baada ya kunieleza kuhusu wewe na historia yako nataka sasa kusikia sababu hasa ya kuja kuniona” akasema James “Kama nilivyokueleza kwamba nimekuja Afrika Mashariki kwa malengo mawili kwanza kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki na pili kumuondoa Rais Patrice Eyenga madarakani” “Ninataka uniambie kuhusu mpango wako namna ulivyojipanga kutekeleza hayo malengo yako mawili.Unao mpango wowote umeuandaa? Akauliza James “Ndiyo ninao mpango ambao ndio ulionileta hapa kwako” akasema Melanie “Nieleze tafadhali” “Mkutano mkubwa wa wake za marais kutoka nchi zote duniani unatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam wiki ijayo.Ninataka kuitumia nafasi hiyo kuwaua wake za marais wa Congo na Rwanda.Kama ujuavyo nchi ya Congo na Rwanda hazina mahusiano mazuri.Halikadhalika nchi ya Congo na Uganda hazina mahusiano mazuri.Nataka Uganda ibebe lawama za kuhusika na mauaji hayo ya wake za marais wa Congo na Rwanda.Baada ya mauaji hayo wewe utajitokeza na kudai kwamba kundi lako ndilo lililotekeleza mauaji hayo.Nchi za Congo na Rwanda zitaipigia kelele Uganda kwa kukuhifadhi wewe na kundi lako na msuguano utaibuka katika jumuiya ya Afrika Mashariki.Hakutakuwa na maelewano baina ya nchi wanachama.Nchi za Rwanda na Congo lazima zitataka kutuma majeshi yao msituni kukutafuta lakini serikali ya Uganda haitakuwa tayari kwa hilo na huo utakuwa ni mwanzo wa mzozo mkubwa sana na taratibu jumuiya ya Afrika Mashariki itaanza kutengeneza ufa na baadae kusambaratika kabisa.Kwa upande wangu nitakuwa nimeua ndege wawili kwa jiwe moja kwanza mpango wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki utakuwa umefanyika na vile vile nitakuwa nimelipiza kisasi kwa Patrice Eyenga kwa alichokifanya kwa familia yangu.Kwa upande wako na kundi lako mtakuwa mmejiongezea nguvu zaidi na baada ya jumuiya ya Afrika Mashariki kusambaratika mtarejea kupambana na serikali ya Congo” akasema Melanie.Kwa muda wote ambao Melanie alikuwa anaelezea mpango wake,James alikuwa anavuta sigara wa fujo huku akimsikiliza.Zilipita dakika mbili za ukimya kisha James akasema “Baba yangu alikuwa jenerali katika jeshi la serikali ya Congo lakini hakuridhika namna mambo yalivyokuwa yakiendeshwa na watawala akaamua kuasi na kuanzisha kikundi chake.Kwa wakati huo nilikuwa mwanajeshi wa kawaida katika jeshi na nikalazimika kuacha jeshi kumfuata baba yangu msituni na kuanza harakati za kuindoa serikali madarakani.Harakati hizo za kuiondoa serikali madarakani zilipelekea wazazi wangu wote wawili kuuawa kwa bomu na majeshi ya serikali na baada ya hapo mimi ndiye niliyeshika usukani na kuvaa viatu vya baba.Niliendeleza mapambano dhidi ya serikali na nilifanikiwa kudhibiti miji miwili yenye utajiri mkubwa wa madini.Kundi langu liliogopwa sana na ilihofiwa siku moja ningeweza kuiondoa serikali madarakani.Baada ya Patrice Eyenga kushinda uchaguzi wa Rais aliwaita makundi yote ya waasi na wakakubaliana kusitisha vita lakini ni mimi pekee na kundi langu ndio tuliosema hapana.Patrice Eyenga alianzisha mashirikiano na nchi ya Marekani ambao walimsaidia kupata zana za kisasa za jeshi na kutuondoa mimi na kundi langu kutoka katika miji tuliyokuwa tunaishikilia tukakimbilia hapa Uganda.Kutokuelewana kati ya Congo na Uganda ni kwa sababu yangu mimi.Serikali ya Congo inailaumu Uganda kunipa hifadhi.Siri ya mimi kupewa hifadhi na Uganda ni kwa sababu nimemuoa mdogo wake na mke wa Rais wa Uganda.Mke wangu na watoto wanaishi nje ya nchi” akanyamaza na kumsisitiza Melanie aendelee kula nyama. “Jeshi la Congo kwa kushirikiana na vikosi vya Marekani waliua wanajeshi wangu wengi hivyo kunirudisha nyuma sana.Kwa muda mrefu tangu nimehamia katika misitu hii nimekuwa na kazi moja kubwa ya kusuka upya jeshi langu.Ninataka kuwa na kikosi kidogo lakini chenye nguvu kubwa katika vita.Kuunda jeshi jipya haijawa kazi nyepesi kwangu.Kama unavyojua nimekuwa ninatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita hivyo siwezi kusafiri kwenda nchi yoyote kutafuta msaada.Ninahitaji silaha na zana nyingine za vita,ninahitaji mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wanajeshi wangu na haya yote yanahitaji fedha.Nilikuwa na akiba kubwa ya madini ambayo nimeitumia katika kujiimarisha.Pamoja na changamoto zote hizo lakini ninaendelea vizuri na kikosi changu kimeendelea kujiimarisha.Ninafanya maandalizi haya yote kwa ajili ya kurejea tena nchini Congo.Ndoto yangu itatimia pale nitakapofanikiwa kuingia ikulu” akasema James na kuwasha sigara nyingine akaanza kuvuta “Ndiyo maana nikachagua kuja kwako James kwani mimi nawe ndoto zetu zinafanana.Sote tunataka kuikomboa Congo.Pamoja na nia zetu zinazofanana za kuikomboa Congo lakini kila mmoja wetu anayo ajenda yake binafsi.Wewe unataka kutawala Congo na mimi ninataka kulipiza kisasi kwa wale wote waliowaua wazazi wangu.Hivyo basi ili kutimiza malengo yetu lazima tusaidiane.Nisaidie kulipiza kisasi na mimi nitakusaidia katika mpango wako wa kuitawala Congo” akasema Melanie na James akamimina mvinyo katika glasi akanywa na kuuliza “Endapo nitakubali kushirikiana nawe na kukusaidia katika mpango wako wa kulipiza kisasi wewe utanisaidia vipi katika mpango wangu? “Ninaungwa mkono na Ufaransa na mataifa mengine makubwa ya Ulaya hivyo basi ninayo nguvu ya kuwashawishi waweze kukuunga mkono katika harakati zao na vile vile kukusaidia vifaa na zana za kivita” akasema Melanie “Melanie mimi nina kanuni moja”akasema James “Sitaki kuwa na taifa lolote nyuma yangu.Mataifa haya yametutumia vya kutosha.Yametukandamiza kwa kiwango kikubwa.Kwa miaka mingi yametutumia kama chanzo cha machafuko katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Tumekuwa tukipigana wenyewe kwa wenyewe lakini nyuma ya mapigano hayo yapo mataifa ambayo yalikuwa yananeemeka.Sitaki tena kuungwa mkono na taifa lolote la kigeni katika harakati zangu.Ninataka nifanye mapinduzi ya kweli ambayo yatawanufaisha watu wa Congo.Nataka niirudishe nchi na rasilimali zake kwa wakongomani.Nikikubali msaada kutoka mataifa hayo unyonyaji hautakwisha.Yapo mataifa ambayo yako tayari kunisaidia lakini kwa masharti kwamba nitakaposhika madaraka nao lazima wafaidike jambo ambalo siko tayari.Hata wewe ninakushauri uwe makini na hao uliowataja kuwa wanakuunga mkono wanakutumia na mwisho watakuacha au kukuua”akanyamaza akanywa mvinyo na kusema “Kwa miezi kadhaa sasa nimekuwa na mazungumzo na watu wa kikundi cha IS” “Islamic State?akauliza Melanie akionekana kushangaa “Ndiyo.Nimekuwa na mazungumzo nao.Kikubwa wanachokitaka ni mashirikiano kati yangu nao” “Kile ni kikundi cha kigaidi.Unawezaje kushirikiana nao?Unataka kubadili harakati zako kuwa za kigaidi?akauliza Melanie “Hapana Melanie sitaki kukigeuza kikundi changu kuwa cha kigaidi.Kwa miaka ya hivi karibuni IS wamekuwa wakijiimarisha sana katika bara la Afrika.Wanataka kujiimarisha zaidi katika eneo la Afrika Mashariki na kati.Wanataka kuungana nami lakini wanachokihiaji ni kupata fursa ya kujificha katika misitu minene ya Congo ambako watajenga kambi za mafunzo kwa ajili ya watu wao.Watanisaidia na kuniwezesha kurejea tena msituni kupambana na serikali ya Congo na kudhibiti eneo kubwa kisha wao wataingia na kuimarisha kambi yao ya mafunzo.Wanapata ugumu kupata sehemu ya kuweka kambi ya mafunzo ndiyo maana wakanifuata na wazo hilo la kutaka tushirikiane.Bado majadiliano yanaendelea lakini sina sababu ya kusema hapana.Ninahitaji kuendeleza operesheni zangu,ninahitaji kupata fedha za kugharamia jeshi langu ninahitaji vifaa na zana za kisasa kwa ajili ya kuanzisha tena vita na serikali ya Congo na IS wanao uwezo wa kunipatia silaha na zana za kivita ninazozihitaji hivyo basi sioni sababu ya kusema hapana kuhusu ombi lao la kuanzisha mashirikiano” akasema James “Pamoja na sababu ulizoeleza James lakini hawa watu ni magaidi na hupaswi kushirikiana nao kwa namna yoyote ile kwani nawe utaonekana kama gaidi na utaanza kusakwa” akasema Melanie “Melanie usiwe na hofu yoyote.Hawa watu wanachohitaji ni kupata sehemu ya kuweka kambi yao ya mafunzo na wao wataniwezesha mimi kuweza kupata kile ninachokihitaji sana yaani fedha na zana za vita.Nakuhakikishia Melanie kwamba watu hawa ninawahitaji sana.Tutawatumia pia katika mashambulio mbali mbali.Kwa mfano ninafikiria kuwatumia katika shambulio hilo unalolipanga la kuwaua wake za marais wa Rwanda na Congo endapo tutakubaliana.Hawana kitu kikubwa wanachokihitaji zaidi ya kupata hifadhi msituni ili waendeshe kambi zao za mafunzo.Watu wao watakaofundishwa katika kambi hizo za mafunzo si kwa ajili ya kushambulia Congo bali watapelekwa katika nchi mbali mbali duniani kutekeleza kazi zao za kigaidi”akasema James Kasai “James nimekuja safari hii ndefu kuomba kushirikiana nawe lakini baada ya kusikia kwamba una mashirikiano na kikundi cha kigaidi cha IS nimeanza kusita kama tunaweza kuendelea na mashirikiano haya” akasema Melanie “Melanie unachokihitaji wewe ni kulipiza kisasi kwa walioua wazazi wako na ndiyo maana uko hapa.Umekuja kuhitaji msaada wangu na mimi niko tayari kukusaidia lakini nimekueleza ukweli kwamba kuna watu ambao niko katika mazungumzo ya mashirikiano na watu hao ni kikundi cha IS.Ni kweli IS ni kikundi cha kigaidi lakini mimi nao tuna sehemu ambazo tutashirikiana.Ninahitaji fedha na silaha na hivi vitu vyote wameahidi kunipatia na kutoka kwangu wanachohitaji ni sehemu ambayo wataweza kuweka kambi yao ya mafunzo.Sioni tatizo kama nikishirikiana nao.Ni fedha na silaha pekee ndicho ninahitaji kutoka kwao” akasema James akapuiza moshi na kusema “Melanie tafadhali usisite wala kuhofia kushirikiana nami.Nina mahitaji makubwa ya fedha kama nilivyokwambia” “Ninao utajri mkubwa na kama unahitaji fedha nitakupatia lakini achana na mpango wa kushirikiana na magaidi” akasema Melanie.James akavuta mkupuo mkubwa na kupuliza moshi mwingi akamtazama Melanie na kusema “Melanie naomba tuelewane jambo moja.Umekuja kwangu ukihitaji msaada hivyo kama unataka nikusaidie utafuata kile ninachokielekeza mimi.Endapo hutaridhika na masharti yangu basi sikulazimishi ushirikiane nami unaweza ukatafuta mwingine wa kushirikiana naye” akasema James na kuwasha tena sigara nyingine alionekana kuanza kukasirika “James bado tuna mengi ambayo tunaweza kushirikiana mimi na w….” akasema Melanie na James akamkatisha “Nataka sana kukusaidia Melanie lakini sitaki uniwekee masharti yoyote.Nimekueleza ukweli kwa kuwa nawe pia umenieleza ukweli wako wote hivyo kama ukiamua kushirikiana nami tambua kwamba lazima ushirikiane pia na IS” akasema James na kumtazama Melanie kwa sekunde kadhaa “Melanie nakupa muda ukalitafakari tena suala hili na pale utakapokuwa tayari utanijulisha maamuzi yako” akasema James.Melanie akaimaisha kichwa akazama mawazoni na James akasimama “Melanie nadhani tumemaliza mazungumzo yetu.Nenda ukalale utafakari na Gosu Go…………” akasema James na kunyamaza akamtazama Melanie “Melanie wewe na Gosu Gosu ni wapenzi?akauliza na Melanie akainua kichwa “Ndiyo sisi ni wapenzi” “Nilikuwa najiuliza kwa nini hujataka kumshirikisha Gosu Gosu katika suala hili?Kwa nini hutaki aifahamu mipango yako? Humuamini?Akauliza James “Gosu Gosu hafahamu chochote kuhusu mimi” “Hafahamu kama wewe ni Theresia Muganza? “Hapana hafahamu chochote na sitaki afahamu” “Kwa nini hutaki kumueleza ukweli kuhusu wewe?Naamini angekuwa na msaada mkubwa sana kwako” akasema James “Siwezi kumueleza ukweli kuhusu mimi na hatakiwi kufahamu chochote” akasema Melanie “Kwa nini Melanie? “Nina sababu zangu binafsi.James tuachane na suala hilo,bado hatujamaliza suala letu” akasema Melanie “Nini unataka kukisema Melanie? Nimekwisha kwambia kwamba nenda katafakari kisha utanijulisha maamuzi utakayoyachukua kama utakuwa tayari kushirikiana nami” akasema James Kasai “James nimekuja umbali huu mrefu kwa ajili ya kutafuta msaada na siwezi kuondoka hapa bila ya kuwa na uhakika kwamba mipango yangu itafanikiwa.Nimekuja kwako kwa kuwa ninakutegemea sana unisaidie” “Melanie niko tayari kukusaidia lakini lazima ufuate kile ninachokitaka mimi na si kunipangia nini cha kufanya.Kama uko tayari kwa hilo tuendelee na mazungumzo”akasema James “James nahitaji msaada wako na samahani kwa kukukwaza.Naomba tushirikiane” “Nataka tukubaliane endapo utahitaji msaada wangu basi utakubaliana na masharti yangu.Uko tayari kwa hilo?akauliza James “Niko tayari” “Vizuri sana.Sasa tunaweza kuendelea kuzungumza” akasema James “Umeniambia mpango wako ni kuwaua wake za marais wa Randa na Congo.Kuna mpango wowote tayari umekwisha uandaa? “Mpango nilioufikiria ni huu.Nitazungumza na balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nchini Tanzania na nitamshawishi aandae chakula cha usiku na kuwakaribisha wake za marais hao katika makazi yake na hapo ndipo watakapouawa wote”akasema Melanie “Ni mpango mzuri.Mshawishi balozi kwamba wewe utagharamia kila kitu katika chakula hicho cha pamoja cha wake za marais wa Rwanda na Congo.Ninao wanajeshi wangu hapa ambao n I wapishi wazuri wana ubora wa kimataifa.Wao ndio wanaotakiwa kuwa wapishi siku hiyo. Watawahi kuingia na silaha zilizofichwa na baadae wakati watu wakianza kula chakula ndipo mauaji yatakapofanyika.Kuna jambo moja ambalo nataka ulifanyie kazi” akasema James “Jambo gani James?akauliza Melanie ‘Nataka utafute namna wapishi hao watakavyoweza kuingia na kutoka Tanzania” “Usihofu hilo ni jambo dogo sana kwangu.Nitalifanyia kazi” akasema Melanie “Basi hakuna tatizo.Mimi nitakusaidia katika suala hilo.Kitu cha msingi ni kuhakikisha unanikiwa kuwakutanisha wanawake hao sehemu moja na vijana wangu watafanya kazi moja tu ya kuwamaliza wote” akasema James “James ahsante kwa kukubali kunisaidia.Huu ni mwanzo mzuri wa mashirikiano yetu makubwa na nina hakika yapo mambo mengi huko mbeleni tutashirikiana”akasema Melanie “Melanie mimi nimekubali kukusaidia katika mipango yako ya kulipiza kisasi lakini na mimi kuna mambo ambayo nitajitaji msaada wako.Kila mmoja lazima afaidike na mwenzake” akasema James “Unahitaji nini James?akauliza Melanie “Nilikueleza awali kwamba bado tunaendelea na majadiliano na kikundi cha IS kuhusu mashirikiano yetu.Yapo mambo kadhaa ambayo tumekwisha kukubaliana lakini lipo suala ambalo mpaka sasa bado hatujaweza kulipatia ufumbuzi nalo ni kuhusu fedha” “Nini kinaleta ugumu?Hawajakubali kiwango unachokihitaji? “Hapana si hivyo bali namna nitakavyokuwa nikipokea fedha kutoka kwao.Kwa ujio wako tayari nimepata ufumbuzi” akasema James “Ufumbuzi upi James? “Wewe ni mfanya biashara unamiliki makampuni makubwa na biashara nyingine kubwa kubwa.Nataka pesa kutoka IS zipitie kwako.Hakuna ambaye anaweza akakutilia shaka kwa kuwa u mfanya biashara mkubwa” “Pesa za magaidi zipitie kwangu?! Melanie akauliza kwa hamaki “Nakukumbusha tena si magaidi bali ni washirika.Kama umekubali kushirikiana nami basi ukubali kushirikiana pia na IS ndiyo maana nilikuuliza kama utakuwa tayari na ukakubali hivyo basi kama kweli una nia ya dhati ya kushirikiana nami sitaki kusikia ukitamka neno ugaidi katika kinywa chako.Tumeelewana Melanie? “Tumeelewana.Samahani” akasema Melanie “Vizuri” akasema James “Ninahitaji fedha kutoka kwa hawa jamaa na wao wako tayari kunipatia hiyo fedha lakini tatizo lilikuwa ni namna ya fedha hizo kunifikia.Kumekuwa na ugumu sana katika usafarishaji wa fedha duniani.Serikali nyingi duniani zimekuwa macho sana katika suala hilo la usafirishaji wa fedha kwa hofu ya ufadhili wa ugaidi.Wewe ukiwa kama mfanya biashara fedha hii itapitia kwako na hakuna ambaye atakuwa na wasiwasi nawe hata kidogo.Utasimama kati yangu na IS na kila kitu kitapitia kwako.Si kazi nyepesi na wala si ngumu kwako” akasema James “Sawa James mimi niko tayari kufanya hivyo na nitakusaidia kwa kila kitu ili mrad tu unihakikishie kwamba kile ninachokihitaji kitatimia” akasema Melanie “Nakuhakikishia kwamba kila unachokihitaji kitatimia.Unataka kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki hilo litatimia,jumuiya hii itasambaratika.Kuna jambo unahitaji lifanyike lakini hutaki kuliweka wazi.Unahitaji machafuko yatokee nchini Congo.Hicho ndicho walio nyuma yako wanakihitaji.Nakuhakikishia machafuko yatatokea kama wanavyotaka.Lakini Melanie naomba nikuweke wazi kitu kimoja” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Hawa watu walio nyuma yako hawana uchungu na nchi yetu.Kwa miaka mingi wamekuwa wakifadhili makundi mbali mbali ya waasi damu nyingi imemwagika lakini si kwa maslahi ya Congo bali kwa maslahi yao.Tani na tani za madini zinatoroshwa kutoka nchini kwetu na yanabaki mashimo.Sitaki tena kumwaga damu ya wakongomani kwa ajili ya hawa jamaa.Nchi yetu inaendelea kuogelea katika umasikini huku nchi zao zikiendelea kutajirika.Nitaenda tena msituni kupigana na serikali ya Congo kwa ajili ya maslahi ya wakongo na si kwa ajili ya nchi tajiri.Melanie mimi nawe tunaweza kuunganisha nguvu na kuwa wakombozi wa nchi yetu ya Congo.Nakushauri achana na hao mabeberu ambao hawana lengo lolote zuri na nchi zetu” akasema James. “James ninachokihitaji mimi ni kukamilisha misheni zangu na sijali kama kuna mabeberu watafaidika ama vipi.Naomba tuendelee na mipango yetu” akasema Melanie “Sawa Melanie mimi nitakaa na watu wangu na nitawaeleza haya tuliyokubaliana na kisha nitakujulisha kila kitu kitakavyokuwa.Wewe nenda kaanze maandalizi ya mpango huo wa mauaji ya wake za marais na utanijulisha kila kinachoendelea” akasema James kisha ukapita ukimya “Melanie nakukumbusha kuwa makini na Gosu Gosu.Ni mtu hatari sana na akifahamu kama wewe ni Theresia Muganza atakasirika kwa kumficha na anaweza akakufanyia kitu kibaya sana.Nimeelezwa sifa zake si mtu mzuri” akasema James “Usihofu James,Gosu Gosu hawezi kuwa na hatari yoyote kwangu” akasema Melanie.Majadiliano yaliendelea hadi ilipofika saa sita za usiku na Gosu Gosu akaitwa kisha James Kasai akawapeleka katika chumba chao cha kulala “Mambo yamekwendaje katika maongezi yenu? akauliza Gosu Gosu “Haikuwa rahisi lakini tumekubaliana mambo kadhaa” akasema Melanie “James amekubali kukusaidia katika mpango wao?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo amekubali kusaidiana nami” akasema Melanie ambaye alionekana mwingi wa mawazo.Hakutaka mazungumzo mengi akamkumbatia Gosu Gosu ambaye alifahamu kile alichokitaka Melanie na kuuanzisha mtanange. “Nimehangaika hadi kumfikisha Melanie sehemu hatari kama hii lakini kwa nini hajataka nishiriki katika mazungumzo yake na James?Kuna kitu gani hakutaka nikifahamu?akajiuliza GosuGosu akiwa amejilaza pembeni baada ya mtanange kumalizika. “Jambo hili limezidi kuwa kubwa.Itanilazimu kushirikiana pia na magaidi wa IS.Sifahamu nini kitatokea endapo Devotha akigundua hiki ninachotaka kukifanya.Lakini potelea mbali ninachokitaka mimi ni mipango yangu ikamilike na wale walowaua wazazi wangu nao pia walipe uovu wao” akawaza Melanie TEL AVIV – ISRAEL Moshe Levine mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Israel Mossad alistuliwa kutoka usingizini na mke wake baada ya simu yake kuita mfululizo. “Nani huyo asubuhi yote hii? akauliza Moshe kwa sauti iliyoonyesha bado alikuwa na usingizi na alihitaji kuendelea kulala.Simu ilikatika na kuanza kuita tena akainuka na kuichukua akatazama mpigaji akastuka kidogo.Alizifahamu zile namba za simu zilizompigia,akaipokea “Hallow Nawal” akasema Moshe “Ni mimi Abu Zalawi na si Nawal” ikasema sauti ya kiume “Mathew Mulumbi ! Moshe akashangaa “Mathew ni wewe? Akauliza bado alikuwa katika mshangao “Ndiyo ni mimi mkurugenzi.Habari za asubuhi” akasema Mathew na Moshe akainuka akatoka mle chumbani “Mathew uko wapi? Uko salama?akauliza “Niko salama mkurugenzi usihofu.Nimefika Jerusalem alfajiri hii.Nahitaji kukuona” akasema Mathew “Nielekeze mahala ulipo tafadhali hapo Jerusalem” akasema Moshe.Mathew akamuelekeza mahala alipo na Moshe akamtaka asubiri kwa dakika chache pale pale alipo. “Katika jiji hili nilimwaga damu ya watu wasio na hatia.Inaniuma sana lakini nilifanya vile kwa lengo la kumfanya Ammar Nazari aniamini na mwishowe nifike kwa Habiba Jawad na baada ya safari ndefu hatimaye nimeonana na Habiba jawad” akawaza Mathew na kuanza kukumbuka mara ya kwanza alipomtia machoni Habiba “Nilijiapiza kumtoa uhai Habiba Jawad nitakapomtia machoni lakini imekuwa tofauti.Mambo hayajakwenda kama nilivyotegemea.Habiba Jawad is no t who we think she is.Wengi wanaomtafuta Habiba hawajawahi kumuona na hawana taarifa zake sahihi.Moto wote niliokuwa nao nikiamini ndani ya muda mfupi nitakuwa nimekamilisha kazi yangu ya kumuua Habiba Jawad umezimika na nimejikuta nikiwa mtumwa ndani ya himaya yake.Mathew Mulumbi kutoka ujasusi hadi ugaidi.Ni vigumu kuamini lakini ni kweli tayari nimeingia katika dunia ya ugaidi” akawaza Mathew na kutazama watu wakiwa katika pilika pilika zao za siku “Lazima nikubali kwamba maisha yangu tayari yamebadilika.Safari yangu haitakuwa nyepesi kama nilivyotegemea,bado nina safari ndefu.Habiba ananifahamu vyema mimi ni nani,anayafahamu maisha yangu na anafahamu kama nimetumwa kumuua lakini haogopi chochote.Sijawahi kukutana na mtu wa aina yake katika maisha yangu ndani ya ujasusi. Amenifanya akili yangu ishindwe kuwaza mengine nimebaki nikimtafakari yeye tu ni mtu wa namna gani.Hata hivyo mimi si mtu wa kukata tamaa.Ninao mlima mrefu wa kupanda lakini misheni yangu kwa namna yoyote ile lazima niikamilishe.Kwa sasa misheni yangu imekuwa kubwa tofauti na nilivyotegemea hivyo hata mbinu zangu lazima zibadilike na ziwe kubwa kulingana na misheni yenyewe” akawaza Mathew huku akiwa makini kuhakikisha usalama wake “Nimeingia katika kitovu cha ugaidi duniani.Habiba Jawad ndiye nguvu ya ugaidi duniani kwani karibu makundi mengi ya kigaidi duniani yanamtegemea yeye ili kujiendesha.Kuna mengi ya kujifunza kuhusu Habiba Jawad,kuna mengi pia ya kujifunza kuhusu ugaidi duniani na ili niweze kulikamilisha hilo kwa namna yoyote ile lazima nifanye maamuzi magumu sana nayo ni kuachana na kila kitu na kujiunga na Habiba Jawad.Kujiunga na Habiba Jawad ina maana kwamba nitakuwa nimejiunga na ugaidi” akaendelea kuwaza “Habiba Jawad angeweza kuelekeza tuuawe haraka sana lakini hakufanya hivyo.Pamoja na kufahamu sisi ni majasusi na mpango wetu ni kwenda kumuua hajamjulisha mtu wake yeyote jambo hilo.Kwa nini amewaficha siri hii na hataki wajue? Watu wake wote wanafahamu mimi na Nawal ni magaidi tuliotoka katika kundi la Ammar Nazari.Kitu gani anakitafuta kwetu? Akawaza Mathew na kukumbuka kitu “Sijapata nafasi nzuri ya kukaa na kuzungumza na Nawal kujua mambo aliyopitia lakini nitajitahidi kutafuta muda nizungumze naye.Kuna mambo yananipa ukakasi kidogo kwani nimemkuta kwa Habiba Jawad tayari amekwisha zoea na amekubali kuolewa na Abu Dahir mtoto wa Habiba.Kuna kitu hakikai vizuri akilini,kwa nini amekubali haraka hivyo kuolewa na huyo Abu? Kuna mambo ambayo nahitaji kuyafahamu vizuri.Halafu dah !!..Mathew akainamisha kichwa chini “Habiba anataka nimuoe mwanae Najma” akawaza Mathew na kuyakumbuka maneno ya Habiba. “Hauna mke Mathew Mulumbi,unaye mjane.Peniela si mkeo tena.Huko aliko anaamini tayari umekwisha fariki dunia na ameamua kuendelea na maisha yake.Labda nikupe siri ya kitu ambacho hukifahamu.Mali zako zote zilizoko Dar es salaam tayari zimeuzwa” “Habiba anafahamu kila kinachoendelea katika maisha yangu.Nilistushwa na taarifa ya Peniela kuuza mali zetu zilizokuwa Dar es salaam” “Unadhani kwa nini ameamua kufanya hivyo?Ni kwa sababu anajua hutarudi tena,umekwisha kufa.Maisha yako Tanzania yamekwisha ndiyo maana nataka kukuanzishia maisha mengine hapa.Ningekuwa sina nia nzuri kwako ningeweza kuelekeza uuawe lakini sijafanya hivyo.Sioni sababu yoyote ya kukuangamiza Mathew Mulumbi.Bado unayo nafasi ya kuendelea kufurahia maisha yako.Familia yako wamekwisha kubaliana na ukweli kwamba umeondoka na hautarudi tena hivyo hakuna haja ya kwenda kuwasumbua na kuvuruga maisha waliyonayo sasa.Nakupa nafasi ya kuanza maisha mapya ukiwa na Najma” Maneno ya Habiba bado yaliendelea kumjia Mathew kichwani “Yawezekana kweli familia yangu wamekwisha kubalianana na matokeo kwamba nimekwisha fariki na sintarejea tena,wameamua kusonga mbele na maisha yao ndiyo maana Peniela ameamua kufanya maamuzi hayo ya kuuza mali kwani hana tena mpango wa kurejea kuishi Tanzania.Habiba amenieleza kwamba maisha yangu Tanzania yamekwisha,anaweza akawa anasema kweli kwa upande mmoja lakini maisha yangu Tanzania bado yapo.Nilizaliwa Tanzania na nitazikwa Tanzania.Haya yote ninayoyapitia ni kwa sababu ya mapenzi makubwa niliyonayo kwa Tanzania.Amenitaka nimuoe mwanae Najma na nianzishe maisha mapya.Huu ni mtihani mgumu sana lakini kama ninataka kukamilisha misheni yangu sina budi kukubaliana na Habiba kumuoa huyo Najma.Sifahamu kitakachotokea huko mbeleni lakini ninachokihitaji mimi ni m…..” Mathew akatolewa mawazoni baada ya gari moja ndogo rangi nyeusi kusimama karibu na aliposimama mlango ukafunguliwa akashuka mtu mmoja akamfuata “Abu Zalawi?akauliza Yule jamaa na Mathew akaitika kwa kichwa.Yule jamaa akamtaka amfuate wakaingia ndani ya lile gari ambamo alikuta kuna watu wengine wawili na kuondoka mahala pale.Hakukuwa na mazungumzo yoyote.Walikwenda hadi katika ofisi za Mossad jijini Jerusalem na kuingia katika helkopta ikapaa na kuondoka. Hakukuwa na mazungumzo yoyote ndani ya helkopta hadi walipofika jijini Tel Aviv.Helkopta ikatua katika makao makuu ya Mossad na Mathew akashushwa.Mara tu aliposhuka akakutana na Moshe Levine akimsubiri. Wakasalimiana kisha akamtaka Mathew waeelekee ofisini kwake. “Mathew karibu sana.Sikuamini uliposema kwamba ni wewe” akasema Moshe,Mathew hakujibu kitu “Mathew Mulumbi sifahamu nianzie wapi lakini kama idara tumepitia kipindi kigumu sana kwa maamuzi tuliyoyafanya ya kumtorosha Ammar Nazari.Tulipata wakati mgumu kwa vile tulichokitegemea hakikufanyika kama tulivyotarajia.Tulikubali kumuacha Ammar Nazari atoroke gerezani kwa kutegemea kwamba tunatengeneza njia ya kuelekea kwa Habiba Jawad.Ulituahidi kutafuta namna ya kutupa mrejesho mara utakapokuwa umefika kwa Ammar Nazari brigades lakini hukutupa taarifa zozote.Tulihitaji sana kupata mrejesho kutoka kwako ili tuweze kuendelea na mipango yetu lakini muda ulipokuwa mrefu bila kupata taarifa zako zozote tulilazimika kuamini yawezekana umeuawa hivyo tukakuondoa katika mipango yetu” akasema Moshe na Mathew akamtazama kwa muda na kusema “Mlifanikiwa kupata mahala alipo Ammar nazari na mkalipua mabomu bila kujali uwepo wangu pale.Kama isingekuwa Nawal ningekwisha fariki dunia” akasema Mathew “Naomba ufahamu kwamba hatukuwa na namna nyingine ya kufanya.Hatukuwa na mawasiliano yako na tulihitaji kumuua Ammar hivyo baada ya kufanikiwa kupata mahala alipo kazi yetu ilikuwa moja tu kumsambaratisha yeye na wafuasi wake.Halikuwa kosa letu kama ungefariki katika mashambulio yale kwa sababu hatukuwa na taarifa zako” akasema Moshe na Mathew akamtazama kwa hasira “Mlifanikiwa kumuua Ammari Nazari katika mashambulio yale?akauliza Mathew “Ndiyo tulimuua Ammar Nazari.” Akasema Moshe na Mathew akacheka kidogo “Pamoja na kufahamu mahala alipo Ammar Nazari lakini msingeweza kumuua.Ammar alikuwa amejiandaaa vilivyo” akasema Mathew “Lakini tulifanikiwa kumuua na hicho ndicho kikubwa tulichokuwa tunakitafuta.Ammari Nazari brigades halipo tena na tuna uhakika wa watu wetu kuwa salama” akasema Moshe “Nilimuua Ammari Nazari kabla hamjaangusha mabomu yenu” akasema Mathew “Ulimuua Ammar? “Ndiyo” akasema Mathew na kuchukua simu ya Nawal akamuonyesha Moshe picha “Hivi ndivyo Ammar Nazari alivyouawa.Mliisambaratisha ngome yake kwa mabomu lakini tayari alikwisha uawa.Mimi na Nawal tulimuua” “Nawal? “Ndiyo.Mlimpigia simu Nawal na kumtaka aondoke mara moja eneo lile kwani mlipanga kulipua mabomu ndipo tulipomuua Ammar kwani angeweza kutoroka” “Ulikuwa na ukaribu na Nawal? “Ndiyo.Nilikuwa na ukaribu naye mkubwa” “Kwa nini usingetumia simu yake kuwasiliana nasi kutujulisha kwamba uko salama? “Nawal alikuwa katika misheni nyingine na hakutaka simu yake itumike katika mawasiliano na Mossad kwa ajili ya usalama wake” akasema Mathew “Pole sana Mathew kwa yaliyotokea lakini yote haya yamesababishwa na ukosefu wa mawasiliano baina yetu.Kama kungekuwa na mawasiliano mazuri baina yetu yote haya yasingetokea.Nashukuru kwamba u mzima” akasema Moshe “Naamini katika mawazo yenu mliamini nimetoroka na kutokomea zangu lakini nisingeweza kufanya hivyo kabla ya kukamilisha misheni yangu ya kumpata Habiba Jawad.Hamkupaswa kuondoa imani kwangu.Mimi si mtu mwenye ndimi mbili.Nikiamini kitu lazima nikitekeleze.Sjawahi kupewa misheni nikaishia njiani hivyo mlikosea sana kupoteza imani kwangu.Habiba Jawad si muhimu kwenu tu bali kwa nchi yangu Tanzania na ulimwengu mzima hivyo sintaweza kuishia njiani katika misheni hii hadi pale nitakapohakikisha Habiba Jawad aidha ameuawa au ametiwa nguvuni” akasema Mathew “Nakubali Mathew tulifanya kosa lakini tulikuwa katika shinikizo kubwa baada ya Ammar Nazari kutekeleza shambulio lile katika kituo cha treni na kuua watu.Utatusamehe sana kwa lililotokea.Mambo kama haya katika kazi zetu hizi huwa yanatokea” akasema Moshe “Ninaelewa Moshe lakini ningefurahi sana kama kungekuwa na kuaminiana baina yetu.Hakuna tunachoweza kukifanya kufanikisha misheni hii kama hakutakuwa na kuaminiana baina yetu” akasema Mathew “Mathew tunakuamini sana.Kama tusingekuwa tunakuamini tusingeweza kukubali wazo lako la kumtoa Ammar Nazari gerezani.Yule alikuwa mtu hatari kwa taifa lakini tulikubali kumtorosha gerezani kwa sababu tulikuamini.Kilichotokea baina yetu ni ukosefu wa mawasiliano.Kama tungekuwa tunawasiliana vizuri basi haya yote yasingetokea.Tuachane na hayo karibu tena.Nataka kujua kila kitu toka ulipoondoka na Ammar” akasema Moshe na Mathew akamuelezea kila kilichotokea.Namna alivyoingia katika kundi la Ammar Nazari na kila kilichoendelea.Katika maelezo aliyoyatoa Mathew hakuweka wazi kama yeye ndiye aliyetekeleza shambulio lile la bomu katika kituo cha treni jijini Jerusalem. “Nilikuwepo katika kikao kile cha kupanga shambulio la Jerusalem lakini nisingeweza kuwajulisha kwani kama shambulio lile lingeshindwa kufanikiwa Ammar na kundi lake wangejiuliza sababu ya kushindwa kufanikiwa na wangeanza uchunguzi” akadanganya Mathew zikapita sekunde kadhaa za ukimya halafu akaendelea “Baada ya kumuua Ammar Nazari mimi na Nawal tuliondoka kuelekea Ramallah ambako tulionana na mwanamama mmoja anaitwa Fatma ambaye alikuwa ni rafiki wa Ammar.Tukiwa pale Nawal ambaye alikuwa na kitabu ambacho Ammar amekuwa akiandika mambo yake muhimu aliwasiliana na mtu mmoja akamueleza kilichotokea na akamtaka atukutanishe na Habiba Jawad.Jamaa huyo alitutaka tuelekee Amman Jordan.Tulifanikiwa kupata hati za kusafiria na kuvuka mpaka hadi Jordan ambako tulipokewa na mtu mmoja akatupeleka katika nyumba Fulani ambayo siikumbuki kwani ilikuwa ni usiku.Alfajiri tulichukuliwa tukiwa tumevishwa mifuko kichwani tukapelekwa sehemu Fulani na huko tulianza kupatiwa mateso” Mathew akamuonyesha Moshe vidonda alivyovipata katika mateso “Pole sana.Nini hasa ilikuwa sababu ya kuteswa?Walitaka nini? “Walitaka kuthibitisha kama kweli mimi ni Abu Al zalawi.Niliteswa sana lakini baadae waliridhika kwamba mimi ni Abu Zalawi” akasema Mathew “Nini kilifuata baada ya hapo? “Tulikutanishwa na mtu aliyejitambulisha kwetu anaitwa Sayid Omar.Kwa mujibu wa maelezo yake ni mtu wa karibu sana na Habiba.Aliniuliza sababu ya kutaka kuonana na Habiba Jawad nikamweleza kwamba ninazo taarifa za mahala alipo Edger Kaka.Kwa kutumia kompyuta yake niliweza kuwasiliana na Habiba Jawad kwa kupitia simu ya mtandaoni tukazungumza”akasema Mathew na Moshe akashusha pumzi wakatazamana “Ulizungumza na habiba Jawad?akauliza Moshe “Ndiyo.Baada ya mateso makali nilifanikiwa kuzungumza na Habiba Jawad” akasema Mathew “Nini mlizungumza? “Nilijitambulisha kwake kama Abu Zalawi kutoka kwa Ammari Nazari brigades na nikamweleza kwamba ninafahamu mahala alipo Edger Kaka.Nilimwambia ukweli kwamba hali yake si nzuri na anaishi kwa kutumia mashine.Habiba alinitaka nithibitishe ninachokisema kwa kumpelekea mwili wa Edger ambaye anaonekana kweli ni mtu muhimu sana kwake” “Hii ni hatua kubwa ambayo sikuwa nimeitegemea.Umezungumza na Habiba Jawad na akakuamini! “Bado hajaniamini kama ninachomweleza ni kitu cha kweli na ndiyo maana akanitaka nilithibitishe ninalolisema kwa kumpelekea mwili wa Edger kaka akiwa mzima au amekufa.Moshe japo sijafanikiwa kuonana ana kwa ana na Habiba Jawad lakini kuzungumza naye tu kwenye simu na kutaka nimpelekee mwili wa Edger Kaka ni hatua kubwa sana.Kwa asilimia hamsini naweza kusema tuko karibu kumfikia Habiba Jawad” akasema Mathew “Nakubali haya ni mafanikio makubwa sana.Toka tumeanza kumsaka Habiba Jawad hatujawahi kufikia hatua hii kubwa.Hongera sana Mathew kwa mafanikio haya” akasema Moshe “Ahsante” “Nawal yuko wapi? “Nawal anashikiliwa hadi pale nitakapoupeleka mwili wa Edger” “Unaweza ukapakumbuka mahala ulikofikia na sehemu mlizokuwa mkipelekwa kwa ajli ya kuteswa?Moshe akauliza “Hapana sikumbuki chochote.Kila mahala nilikokuwa ninapelekwa nilikuwa nimefunikwa mfuko kichwani” “Nataka kujua.Ulimweleza Habiba mwili wa Edger uko sehemu gani? “Nilimweleza kwamba Edger amewekwa kwenye mashine ya kumsaidia kuishi katika hospitali moja hapa Tel Aviv.Walitaka kunipa kikosi lakini nilikataa nikawahakikisha kwamba mahala hapo hapahitaji kikosi.Ninao uwezo wa kuingia na kumchukua Edger Kaka” akasema Mathew “Mathew narejea tena kukupa pole na kukupongeza kwa hatua hii kubwa uliyopiga katika kumtafuta Habiba Jawad.Hatua lilipofika suala hili tunahitaji umakini mkubwa sana.Hatupaswi kufanya makosa hata kidogo.Nitawashirikisha wenzangu suala hili ili tuone namna tutakavyoweza kujipanga kwa jambo hili kubwa.Kwa sasa utakwenda kupumzika baada ya safari ndefu yenye misuko suko mingi”akasema Moshe na kupiga simu akaingia jamaa mmoja akampa maelekezo ya kumpeleka Mathew kupumzika. ****************** Saa tano za asubuhi Mathew akaletewa simu na moja wa walinzi wa nyumba ile alimokuwa amepelekwa kupumzika.Moshe Levine ndiye aliyempigia simu na kumtaka ajiandae kwani anahitajika katika kikao. “Mambo yameiva.Naamini hivi sasa watakuwa tayari wamekwisha jadiliana na kufikia muafaka.Lazima niwasaliti Israel ili kujenga imani kwa Habiba Jawad.Nitakachowafanyia kitawapa hasira lakini kitakuwa na manufaa makubwa kwa siku za usoni si kwa Israel pekee bali kwa dunia nzima” akawaza Mathew huku akijiandaa.Nusu saa baadae lilifika gari na kumchukua kumpeleka katika ofisi kuu za Mossad.Alipelekwa moja kwa moja katika ofisi ya Moshe Levine na kupokewa na katibu muhtasi ambaye alimjulisha mkuu wake kwamba Mathew tayari amefika pale ofisini.Moshe akatoa maelekezo apelekwe katika chumba cha mikutano.Katibu muhtasi wa Moshe akampa maelekezo mlinzi Yule aliyekuwa ameongozana na Mathew ambaye alimpeleka katika chuma kile cha mikutano maalum.Mlango ukafunguliwa Mathew akakaribishwa ndani ya kile chumba.Aliangaza macho haraka haraka kulikuwa na watu nane.Alioweza kuwatambua ni Moshe Levine na Efraim Dagan.Akaelekezwa kiti akaketi. “Mathew karibu sana na ninatuma umepata muda mzuri wa kupumzika” akasema Moshe na Mathew akaitika kwa kichwa “Walioko mbele yako naamini unawafahamu.Si mara yako ya kwanza kukutana nao.Umeshakutana nao katika vikao kadhaa” akasema Moshe na Mathew akaitika kwa kichwa “Kwa muda wa saa kadhaa sasa tumekuwa tukijadiliana kuhusu suala lako ulilonieleza.Tumekuwa na mjadala mpana sana na ninapenda kukujulisha kwamba kila mmoja ndani ya chumba hiki anakupongeza sana kwa ushujaa wako kwanza kwa kumuua Ammar Nazari.Ni jambo kubwa sana umelifanya kwetu.Jambo la pili ni ushujaa wako wa kuvumilia mateso makali na hatimaye umeweza kupiga hatua kubwa katika kumfikia Habiba jawad.Tulikuwa tumepoteza matumaini ya wewe kuwa hai lakini umeibuka ukiwa na jambo kubwa na la muhimu.Nimejitahidi kuwaeleza wenzangu kwa upana kila ulichonieleza na wameelewa” akanyamaza kidogo “Tumekuita hapa ili wewe uweze kutueleza mpango wako namna mlivyokubaliana kuweza kuufikisha mwili wa Edger Kaka kwa Habiba Jawad” akasema Moshe na Mathew akakohoa kidogo kuweka sawa koo lake na kusema “Habiba Jawad alinitaka niupeleke mwili wa Edger Kaka lakini mipango yote tulifanya mimi na Sayid Omar.Huyu ni mtu muhimu sana na wa karibu kwa Habiba.Tulikubaliana kwamba nikiupata mwili wa Edger nijitahidi nifike mpakani mwa Israel na Jordan na nitakuta kuna watu pale wananisubiri kisha baada ya hapo nitawakabidhi mwili wa Edger na wao watajua wapi pa kuelekea.Naamini itakuwa ni safari ya kuelekea kwa Habiba Jawad” akasema Mathew “Ni vipi kama baada ya kuupata mwili wa Edger kaka watakuua na kutokomea zao?akauliza mmoja wa wajumbe wa kikao kile “Hilo lina asilimia hamsini kutokea.Wanaweza wakaniua na mimi niko tayari kwa hilo lakini ushauri wangu mwili wa Edger uwekewe kifaa ambacho kitawawezesha kuufuatilia kwa kutumia satelaiti.Endapo ikitokea nikauawa njiani basi zoezi litaendelea na mwili huo utakakopelekwa ndiko atakuwepo Habiba Jawad” akasema Mathew “Wazo la kuweka kifaa katika mwili wa Edger ni zuri lakini ni vipi kama wakikuua na halafu wakauchunguza mwili huo kama una kifaa chochote na wakagundua kifaa hicho na kukitoa? Tutakuwa tumekosa kila kitu”akauliza Efraim Dagan “Naombeni niwatoe wasiwasi wakuu wangu.Haikuwa rahisi kufika hatua hii hata kuweza kukutana na Sayid Omar na vile vile kuzungumza na Habiba Jawad.Nimepitia mateso makali” akasema Mathew na kusimama akavua shati akawaonyesha viongozi wale vidonda alivyokuwa navyo ambavyo havijapona bado alivyovipata kufuatia mateso aliyoteswa. “Mateso niliyopitia ni makubwa na siwezi kuyaelezea lakini niliendelea kushikilia msimamo wangu kwamba mimi ni Abu Zalawi.Baada ya kunitesa sana wakaridhika kwamba mimi ndiye Abu Zalawi na ndipo waliponikutanisha na Sayid Omar nikazungumza naye na akaniunganisha na Habiba.Tayari wananiamini na kitendo cha kumpeleka Edger Kaka kitawafanya waniamini zaidi.Mlinikabidhi suala hili na ninawaomba muendelee kuniamini kwamba nitafika mahala alipo Habiba jawad” akasema Mathew “Mathew Mulumbi una uhakika kwamba watu hawa wanakuamini na unaweza ukafika alipo Habiba Jawad?akauliza Moshe Levine “Siwezi kusema kwamba nina uhakika asilimia mia moja kwamba nitafanikiwa kufika kwa Habiba jawad kwani sifahamu upande wao nini wanakipanga lakini kitu kimoja ambacho kinanipa matumaini ni kwamba hawa jamaa tayari wananiamini na imani hiyo inaweza ikanifikisha mbali.Tulipoanza misheni hii hakuna aliyetegemea kama ningeweza kufika hapa nilipofika hivyo naomba muendelee kuwa na imani kwangu.Ninawaahidi kwamba nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha ninafahamu mahala alipo Habiba Jawad.Lazima tukubali kucheza kamari,kupata au kukosa.Tukikosa tutajipanga tena upya na hautakuwa mwisho wa kumsaka Habiba Jawad.Mapambano yataendelea na mwisho Habiba atapatikana kama alivyopatikana Osama Bin Laden” akasema Mathew na chumba kile kikawa kimya.Moshe akavua miwani akafuta vioo vyake halafu akavaa tena na kusema “Mathew ameeleza vyema nadhani tufuate ushauri wake.Tuweke kifaa katika mwili wa Edger Kaka ambacho kitatuwezesha kufuatilia na kujua mahala ambako mwili ule utapelekwa.Ninakubaliana na Mathew kwamba watu hawa wamekwisha onyesha kumuamini hasa baada ya kumpitisha katika mateso hivyo suala la kumuua lina asilimia ndogo sana” akasema Moshe Levine “Kuongezea hapo mkurugenzi” akasema Efraim Dagan ambaye toka awali alionyesha kumuamini sana Mathew Mulumbi. “Tuitumie vyema fursa hii ya Mathew kuaminiwa na kundi la Habiba.Kuonana na Sayid Omar ni hatua kubwa hivyo nina hakika kwa imani hiyo waliyonayo kwa Mathew hawana tena sababu ya kumchunguza.Nashauri Mathew naye awekewe kifaa ambacho kinaweza kutusaidia kufuatilia na kujua mahala alipo”akasema Efraim “Mathew unasemaje kuhusu hilo wazo la Efraim? akauliza Moshe “Si wazo baya ingawa wale jamaa wakigundua kwamba nina kifaa mwilini nitakuwa nimeharibu kila kitu lakini niwekeeni kifaa hicho” akasema Mathew “Vizuri.Kwa mujibu wa daktari ni kwamba Edger Kaka amekwisha fariki kitambo sana na kinachomuweka hai mpaka sasa ni mashine hivyo pale mashine zitakapozimwa utakuwa ndiyo mwisho wa Edger Kaka hivyo utakachoondoka nacho ni maiti yake.Mathew utapewa nafasi ya kipekee ya kuzima mashine kuashiria mwisho wa Edger na baada ya hapo mwili wake utaanza kuandaliwa.Kila kitu kikikamilika utaondoka kwa usafiri wa helkopta hadi karibu na mpakani ambako utapewa gari na ukifika mahala mlipokubaliana utawasiliana na watu hao.Sisi hatutaingilia chochote tutakuwa mbali lakini tutakuwa tunakufuatilia kuhakikisha kwanza unakuwa salama na pili tunajua mahala mwili huo unakopelekwa” akasema Moshe “Hakuna tatizo Moshe” akasema Mathew “Kabla hatujahitimisha kikao hiki nataka kuuliza swali.Unahisi Habiba Jawad anaishi nchini Jordan?akauliza mmoja wao “Siwezi kusema moja kwa moja kama anaishi Jordan kwa sababu sijabahatika kukutana naye ana kwa ana.Hiki tunachokwenda kukifanya leo kinaweza kutupa picha ya mahala alipo Habiba Jawad kama yuko nchini Jordan au yuko wapi” akajibu Mathew. Baada ya kikao kile kumalizika,wote waliingia katika magari na kuelekea katika hospitali alikolazwa Edger Kaka. “Mathew kama nilivyokueleza tunakupa heshima ya kuzima mashine hii inayomsaidia Edger kuishi kama ishara ya kuhitimisha safari yake hapa duniani” akasema Moshe na Mathew akaelekezwa sehemu ya kuzima “Ninakuita kwa jina lako halisi Seif Jawad.Ulikuwa na malengo mabaya sana kwa nchi yangu Tanzania lakini kwa nguvu ya mwenyezi Mungu wewe na wenzako hamkuweza kufanikiwa na sasa ninakwenda kuhitimisha safari ya maisha yako hapa duniani.Kabla ya kuzima mashine hii ninakuahidi kwamba kama ninavyomaliza safari yako leo ndivyo nitakavyommaliza mama yako Habiba jawad” Mathew aliyatamka maneno haya kimoyo moyo na kisha akazima mashine ile na baada ya sekunde chache mashine inayoonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo ikabadili mlio na grafu yake ikabadilika pia “Tayari amekwisha kufa” akasema daktari na kila kitu kikazimwa “Safari ya Edger imefika mwisho.Sasa yanaanza maandalizi” akasema Moshe na mwili wa Edger ukachukuliwa na kupelekwa katika chumba maalum kwa ajili ya kuuandaa kwa safari.Mathew naye kama walivyokuwa wamekubaliana aliwekewa kifaa kidogo katika mkono wake wa kushoto ambacho kingewawezesha Mossad kuweza kumfuatilia na kujua mahala alipo Zoezi la maandalizi ya mwili wa Edger Kaka lilikamilika mida ya saa kumi na moja za jioni na Mathew akawa tayari kwa safari. DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa kumi na mbili za jioni ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam ikitokea Uganda.Miongoni mwa waliokuwamo katika ndege hiyo ni Melanie Davis na Papii Gosu Gosu.Joyce Dereva wa Melanie alikuwepo uwanjani kuwasubiri.Waliingia garini na kuelekea nyumbani kwa Gosu Gosu wakaagana na Melanie akaelekea katika makazi yake.Hakuhitaji mazungumzo yoyote alikuwa amechoka mno kwa safari ndefu akaenda kujifungia chumbani kwake.Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuingia katika bafu lake zuri akaoga na kwenda kujilaza kitandani “Safari ilikuwa ndefu na ngumu lakini nashukuru nimefanikiwa kuonana na James Kasai.Mafanikio ya safari yangu ni makubwa japo yamejitokeza mambo mengine ambayo sikuwa nimeyafikiria lakini hakuna kitakachoharibika.Nitafanya kama alivyoelekeza James yaani kushirikiana na magaidi wa IS ambao watakuwa wakipitishia fedha kwangu.Si jambo jepesi kushirikiana na magaidi lakini kwa vile niliweka ahadi ya kufanya kila niwezalo kuhakikisha ninalipa kisasi kwa watu walioua wazazi wangu nitashirikiana nao” akawaza Melanie na simu yake ambayo aliiweka maalum kwa ajili ya watu wake wa muhimu ikaita jina lilionyesha James “James Kasai.Nadhani anataka kujua kama tumekwisha fika salama” akawaza Melanie na kuipokea simu “Hallow James” akasema Melanie “Melanie mmefika salama? Akauliza James “Ndiyo james tumefika salama.Ninashukuru sana kwa mapokezi na huduma nzuri mlizotupa” “Usijali Melanie.Nashukuru kama mmefika salama” “Tuko salama usihofu” “Melanie kuna jambo lingine ambalo nataka kukujulisha.Kesho kutwa utakuwa na safari ya kwenda Dubai” “Dubai? “Ndiyo.Utakwenda kukutana na wajumbe maalum ambao mtajadiliana nao kuhusu masuala yale ya fedha namna zitakavyopita kwako” akasema James “James kwa nini umenistukiza hivyo? Hata mimi nina ratiba zangu” “Sikuwa nimetegemea hata mimi kama ingetokea safari ya ghafla namna hii lakini baada ya kuwajulisha jamaa kuhusiana na makubaliano yetu wameomba wakutane nawe haraka hivyo jiandae kesho kutwa unatakiwa Dubai” akasema James Kasai “Sawa james nitajiandaa kwa hiyo safari” akasema Melanie “Ahsante Melanie.Nitakupa maelekezo yote kuhusiana na safari hiyo kesho”akasema James kasai na kuagana na Melanie akaitupa simu pembeni kitandani “Sitaki ufike wakati nijilaumu kwa maamuzi niliyoyafanya kwa kukubali kujiunga na James Kasai”akawaza Melanie “Kuna nyakati ninakuwa na wasi wasi sana na suala hili la kushirikiana na IS.Kinachonipa hofu ni pale ambapo akina Devotha watagundua.Hawatafurahi kwani nitakuwa nimeenda kinyume na maelekezo na mipango yao.Rais wa Ufaransa Michael Weren ambaye amejitahidi sana kuhakikisha ninafika hapa nilipofika hatafurahi lakini potelea mbali ninataka kuendesha mapambano haya kwa namna ninavyotaka mimi.Mpango wao umelenga zaidi katika maslahi ya nchi zao huku wakilipa umuhimu mdogo sana suala la kuhakikisha wale waliotekeleza mauaji ya wazazi wangu wanalipa uovu wao.Devotha ana ndoto za urais wa Tanzania na ameahidiwa hivyo na umoja wa Ulaya.Rais Michael Weren na wenzake ndoto yao ni kurejesha machafuko nchini Kongo ndiyo maana wanataka Afrika Mashariki isambaratike na machafuko yaanze ili wapate nafasi nzuri ya kuweza kupenya na kuendelea kuchota rasilimali.Mimi si mtoto mdogo ambaye siwezi kushindwa kung’amua malengo yao.Niliwakubalia kufanya kazi yao kwa lengo la kupata nafasi ya kutimiza mpango wangu” akawaza Melanie na sura yake ikabadilika “Kama si wao na tamaa zao za rasilimali za Congo hivi sasa wazazi wangu wangekuwa hai.Walimrubuni mama yangu agombee urais na mwisho wake akauawa.Kama wasingemuingiza katika masuala yao ya siasa mpaka sasa mama angekuwepo.Hakuwa na shida na fedha lakini wao walimrubuni kwa madaraka makubwa na aliyetumwa kufanya hivyo ni Devotha.Anadhani mimi sifahamu kama yeye ndiye aliyetumiwa na serikali ya Ufaransa kumshawishi mama yangu akubali kuwania urais?Yeye na wenzake ninaweka pembeni kwanza nitawashughulikia mwisho.Hakuna aliyeshiriki atakayepona.” akaendelea kuwaza Melanie. ISRAEL Mathew Mulumbi aliwasili mahala alikopanga kukutana na timu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuupokea mwili wa Edger Kaka.Ilikuwa ni katika mpaka wa Israel na Jordan.Alipelekwa na helkopta hadi karibu na mahala hapo kisha akaingia katika gari na kuelekea upande wa Jordan mahala ambako alipanga kukutana na watu wale waliowekwa maalum kwa ajili ya kuupokea mwili wa Edger Kaka Aliwasiliana na mtu aliyeelekezwa awasiliane naye kisha baada ya dakika tano zikatokea gari mbili.Mwili wa Edger kaka ukashushwa kutoka katika gari la Mathew na kuingizwa katika mojawapo ya gari walizokuja nazo wale jamaa kisha wakaondoka. Mara tu walipoanza safari gari lililokuwa na majasusi wa Mossad waliokuwa wakimfuatilia Mathew wakawasiliana na majasusi wenzao waliokuwa upande wa Jordan wakawajulisha kwamba tayari safari imeanza na Mathew yumo katika moja wapo ya magari yale yaliyovuka mpaka.Majasusi wale waliokuwa upande wa Jordan walishika usukani wa kuendelea kumfuatilia Mathew ambaye alikuwa amewekewa kifaa maalum mkononi klichowawezesha kujua mahala alipo Akiwa ndani ya gari Mathew akamtaka Yule jamaa kiongozi wa ile timu iliyokuja kuupokea mwili wa Edger ampe simu yake.Alipopewa akaifungua akatoa laini na kuivunja vunja. “Kwa nini unafanya hivyo?akahamaki Yule jamaa aliyejulikana kwa jina la Bashar “Kwa sababu za kiusalama”akasema Mathew na kuchukua simu aliyokuwa nayo akaikanyaga ikavunjika kisha akatoa laini yake akaivunja vunja na kuvitupa vipande vyote nje.Hakuwa na simu tena.Katika kompyuta za Mossad simu ile aliyokuwa anaitumia Mathew iliyokuwa imeunganishwa ili kufuatilia mawasiliano yote atakayoyafanya ikapotea ghafla “Lazima nihakikishe ninawapoteza Mossad wasijue ninaelekea wapi” akawaza Mathew. Saa nne za usiku waliwasili katika jiji la Amman. “Tunaelekea wapi? Mathew akamuuliza Bashar ambaye bado alikuwa amekasirika kwa kitendo cha Mathew kuivunja simu yake “Hutakiwi kuuliza chochote.Utatufuata sisi tunakoelekea” akasema Mathew na kutaka gari lile lisimame ili wazungumze.Bashar akaamuru gari lisimame wakashuka “Unasemaje?akauliza Bashar kwa ukali “Ninafahamu wewe ni kiongozi na umepewa maelekezo hata hivyo nataka kukuweka wazi kwamba tuko katika hatari kubwa na endapo hamtakuwa tayari kunisikiliza mimi basi hatutaweza kufika huko tunakoelekea” akasema Mathew “Hupaswi kunifundisha kazi yangu ! akasema Bashar kwa hasira na kuanza kuondoka.Mathew akamfuata akamvuta mkono,Bashar akageuka kwa hasira akarusha ngumi na Mathew akaiona akamtandika ngumi nzito iliyompeleka chini.Mathew akamuwahi na kuichukua bastora yake na mara watu waliokuwa katika magari wakashuka na kumuelekezea Mathew bunduki “Sikilizeni ndugu zangu.Mimi ndiye niliyepambana vya kutosha hadi kufanikiwa kuupata mwili huu wa Seif Jawad.Hapa tulipo hatuko salama majasusi wa Mossad wanaendelea kutufuatilia.Endapo hamtafuata maelekezo yangu hatutaweza kufika salama huko tuendako.Mwili huu wa Seif Jawad umewekewa vifaa maalum vya kuwawezesha Mossad kufuatilia na kujua mahala unakopelekwa kwani wanaamini mtu huyu ana ukaribu na Habiba Jawad.Mkipuuza maelekezo yangu mtakuwa mmemuweka mama Habiba na Sayid Omar katika hatari kubwa.Mimi siko tayari kuwaweka watu hawa muhimu katika hatari ya Mossad.Niko tayari mniue hapa hapa endapo hamtakubaliana na ushauri wangu” akasema Mathew na watu wale wakabaki kimya “Ninawahakikishia ndugu zangu hiki ninachowaeleza ni kitu cha kweli na kama hamuamini mimi sintakuwa tayari kuendelea na safari.Niko tayari mniue hapahapa” akasema Mathew na kuitupa bastora ya Bashar chini na kuinua mikono juu “Nipigeni risasi sasa hivi.Siko tayari kuendelea na safari hii kama hamtakuwa tayari kusikiliza kile ninachowaelekeza” akasema Mathew kwa ukali.Wale jamaa wakatazamana kisha Bashar akauliza “Unataka tufanye nini? “Tunahitaji kupata hospitali yenye mashine ya MRI ambayo itatuwezesha kupata picha za ndani ya mwili wa Seif na kujua vifaa hivyo vimewekwa sehemu gani” akasema Mathew na wale jamaa wakajadiliana halafu Bashar akachukua simu ya mmoja wa wale jamaa akataka kupiga Mathew akamzuia “Usipige simu yoyote.Hapa tulipo wanatufuatilia na ukipiga simu yoyote watajua na kumfuatilia huyo mtu unayetaka kumpigia ndiyo maana niliiharibu simu yako kwa vile nilikupigia.Bila kufanya vile wangekutafuta hadi wahakikishe wamekutia mikononi mwao” akasema Mathew “Ndugu zangu tusitafute msaada wowote kutoka nje kwa sasa.Tunatakiwa kupambana sisi wenyewe.Ninyi mnalifahamu vyema jiji hili na mnazifahamu hospitali zote kubwa na nzuri.Nielekezeni hospitali moja mnayodhani kutakuwa na mashine hiyo ya MRI” akasema Mathew.Bashar na wenzake wakajadiliana kwa sekunde chache kisha akasema “Advaclinic.Iko mtaa wa Suleiman Al Hadidi lakini muda huu itakuwa imefungwa.Kwa kawaida hufunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa moja za jioni”akasema Bashar “Sawa tunaelekea huko na mtafuata maelekezo yangu” akasema Mathew wakaingia ndani ya magari na safari ya kuelekea AdvaClinic ikaanza.Wakiwa ndani ya gari kuelekea Adva clinic mvua kubwa ikaanza kunyesha.Bashar akamjulisha Mathew kwamba wamekaribia kufika katika jengo la kliniki.Mathew akaomba apewe bastora,Bashar akampa bastora yake iliyofungwa kiwambo cha sauti.Magari yaliwasha taa kuashiria kuingia Advaclinic “Wanaelekea Advaclinic” mmoja wa majasusi wa Mossad waliokuwa garini wakiwafuatilia akina Mathew,akawajulisha Mossad ofisi kuu Tel Aviv “Wanakwenda kufanya nini hapo hospitali usiku huu? Akauliza Efraim Dagan aliyekuwa katika chumba kikubwa wakiendelea kuwafuatilia akina Mathew “Wamesimamishwa na walinzi getini” Majasusi wale wakaendelea kutoa taarifa “Nataka kujua Advaclinic inahusika kutibu magonjwa gani? Akauliza Efraim na kuwataka watu wake wafuatilie baada ya dakika mbili mwanadada mmoja akasema “Inahusika na huduma ya vipimo mbali mbali kwa njia ya mionzi.MRI,CT Scan,X-ray,Ultra sound na vingine kadhaa” akasema Yule mwanadada na Efraim akashika kichwa. “Kuna kitu hakiko sawa hapa.Sielewi sababu ya kwenda katika kliniki hiyo” akasema Efraim na kuwataka wale majasusi waliokuwa wakiwafuatilia akina Mathew waendelee kuwafuatilia kwa karibu kujua nini wanakwenda kukifanya katika kliniki ile. Geti la kuingilia hospitali lilikuwa limefungwa na walinzi walikuwa ndani kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.Mathew akaichukua bastora yeye kiwambo cha kuzuia sauti akashuka garini na kwenda mlangoni akagonga geti lakini walinzi hawakusikia kutokana mvua ile kubwa.Mathew akajaribu kufungua mlango mdogo wa pembeni haukua umefungwa akaingia ndani na kuwaona walinzi wakiwa wamesimama katika chumba chao pembeni ya geti.Mlinzi mmoja akachukua mwavuli akamfuata. “As salaam Alaikum” akasema Mathew akimsalimu Yule mlinzi “Wa alaikum salaam” akajibu Yule mlinzi “Nikusaidie nini?akauliza “Ninahitaji huduma.Nina mgonjwa ana hali mbaya sana” akasema Mathew “Kwa sasa hakuna huduma yoyote inayotolewa hapa.Kliniki imefungwa.Hufunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa moja za jioni.Nawashauri mumkimbize katika hospitali nyingine ambazo zinafanya kazi kwa saa ishirini na nne” akajibu Yule mlinzi na Mathew akatoa bastora akamuonyeshea Yule mlinzi na kumtaka afungue geti.Mlinzi Yule akatupa mwavuli na kupiga kelele akikimbilia katika nyumba ya walinzi lakini kabla hajaingia ndani ya ile nyumba yao iliyokuwa pembeni ya geti Mathew aliyekuwa mwepesi kama unyoya akaizinga bastora yake na kumtandika risasi mbili akaanguka.Wenzake wawili waliokuwa ndani ya ile nyumba wakatoka kwa haraka lakini walikutana na risasi kutoka katika bastora iliyoshikwa na mkono mwepesi wa Mathew Mulumbi na wote wawili wakaanguka chini.Kwa tahadhari akaenda kutazama ndani ya kile chumba hakukuwa na mlinzi mwingine.Akawasachi wale walinzi na kupata funguo ya geti akaenda kulifungua na kuwataka wenzake waingize gari ndani.Haraka haraka gari zikangizwa ndani. “Geti limefunguliwa na gari zao zinaingia ndani” Majasusi wale waliokuwa wakiwafuata akina Mathew wakatoa taarifa “Nini kimewapeleka hapo kliniki usiku huu? Efraim Dagan akauliza “Mkuu kuna kitu nimekipata kuhusiana na Advaclinic” akasema Bayla Brahm “Umepata nini Bayla?akauliza Efraim “Kliniki hii hufunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa moja za jioni hivyo muda huu hakuna huduma yoyote inayotolewa pale” akasema Bayla “Kama hakuna huduma yoyote inayotolewa muda huu wamekwenda kutafuta nini?akauliza Efraim na kuwataka majasusi wale wafuatilie kile kinachoendelea mle ndani. “Wavuteni hao walinzi muwafiche katika maua” akaelekeza Mathew baada ya kufunga geti.Mlango mkubwa wa kioo wa kingilia mapokezi ulikuwa umefungwa Mathew akapiga teke kioo kikavunjika akapenya akaingia ndani,Bashar naye akamfuata.Ndani ya jengo kulikuwa kimya kabisa.Mathew akatafuta sehemu ya kuwashia taa akaipata na kuiwasha.Watu wengine wote walibaki nje ndani ya magari wakisubiri maelekezo. “Tunahitaji kukipata chumba chenye mashine ya MRI” akasema Mathew na mara Bashar akamuita.Alikuwa amesimama katika ramani iliyoelekeza sehemu mbali mbali za jengo lile “Ghorofa ya tatu ndimo kilimo chumba cha MRI” akasema na Mathew akajiridhisha kwamba kweli ni ghorofa ya tatu kama ramani ilivyoelekeza wakapanda ngazi haraka haraka kuelekea ghorofa ya tatu wakakuta kuna kibao kinachoelekeza kilipo chumba cha MRI.Wakakifuata kibao kile na kukikuta chumba ambacho juu ya mlango kulikuwa na kibao Chumba cha MRI.Mathew akajaribu kukiminya kitasa kuufungua mlango lakini haukufunguka.Akarudi nyuma na kuruka teke zito mlango ukaachia wakaingia ndani.Akatafuta ukutani akapata sehemu ya kuwashia taa na chumba kikawa na mwanga.Kulikuwa na vyumba viwili.Chumba cha kwanza kilikuwa na mashine na chumba cha pili kulikuwa na kompyuta ambayo imeunganishwa na ile mashine na ambayo ndiyo husoma mwili wa mgonjwa.Mathew akamuelekeza Bashar kwenda kuuleta mwili wa Edger Kaka. “Tutafanyaje bila daktari?akauliza Bashar “Usihofu nitafanya mimi.Ninafahamu mambo haya” akasema Mathew na Bashar akataka kusema kitu lakini Mathew akamtaka akaulete mwili wa Edger.Nje bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.Bashar kwa kutumia bastora yenye kiwambo cha sauti akailenga taa kubwa iliyokuwa ikimulika eneo la nje na kukawa na giza kisha akaelekeza magari yale yasogee karibu na mlango mwili wa Edger ukashushwa na kuingizwa ndani. “Joseph kuna chochote unakiona kinachoendelea hapo ndani?Efraim akamuuliza Jasusi Yule ambaye alikuwa katika harakati za kutaka kujua kinachoendelea ndani ya kliniki walimoingia akina Mathew “Nashindwa kuona chochote wamezima taa ya nje na kuna mvua kubwa sana inanyesha huku”akajibu Joseph na Efraim akakasirika akavua spika zile za masikioni alizokuwa amevaa kwa ajili ya mawasiliano akazitupa chini “Katika maisha yangu ya ujasusi nimejifunza mambo mengi sana na niliwahi kufundishwa namna ya kutumia mashine kama hizi lakini ni muda mrefu sana umepita sijawahi kutumia mashine.Mungu nisadie tuweze kufanikisha malengo yetu” akawaza Mathew Bashar na watu wake wakasaidiana kuubeba mwili wa Edger na kuuingiza ndani ya kile chumba cha MRI.Mathew akauandaa mwili ule kwa ajili ya kuuingiza katika mashine ile ambayo alikwisha iwasha.Akampa Bashar maelekezo halafu akaingia katika chumba cha pili na taratibu mwili wa Edger ukaanza kuingia katika mashine ile huku Mathew akiangalia katika kompyuta. “Mossad bado hawajanifahamu vizuri mimi ni nani” akawaza Mathew na kutabasamu baada ya kufanikiwa kukiona kifaa kidogo ambacho kilikuwa kimewekwa kitaalamu sana sehemu ya kifua.Baada ya kuhakikisha ni kifaa kimoja tu kilichokuwa kimewekwa mwilini mwa Edger akatoka na kuingia katika chumba kile ilimo mashine akaomba kupewa kisu na kupasua sehemu ile ambayo alikiona kile kifaa kidogo akakitoa huku wote wakibaki wanashangaa.Akafungua dirisha na kukitupa kifaa kile nje.Mwili wa Edger ukatolewa mle ndani ya chumba Mathew akabaki nyuma na walipotoka watu wote akapasua sehemu ya mkono wake alikowekewa kile kifaa kidogo cha kuwawezesha Mossad kumfuatilia kujua mahala alipo akakitupa kile kifaa nje ya jengo na kuzima kila kitu kisha naye akatoka. “Kwa hapa naweza kusema tuko salama lakini wanafahamu kama tuko hapa hivyo lazima kutafuta namna ya kuwapoteza” akasema Mathew “Tuelekee barabara ya Zaharani.Kuna handaki la Suhaib.Pale ndipo tutakapowapoteza.Gari moja litarejea tulikotoka na lingine litaendelea.Tutakuwa tumewapoteza wale wanaotufuatilia hawatajua wafuatilie gari lipi” akasema Bashar “Huo ni mpango mzuri.Haraka tuondokeni mahala hapa” akasema Mathew na magari yale mawili yakaondoka “Magari yanaondoka hospitali” Joseph akawajulisha Mossad Tel Aviv “Joseph haraka sana wewe na wenzako ingieni hapo ndani.Kompyuta yetu inatuonyesha Mathew Mulumbi yuko hapo ndani ya hospitali pamoja na mwili wa Edger Kaka.Tunataka mkahakikishe kama Mathew ni mzima.Yumo humo ndani na tuna wasiwasi na usalama wake” akaelekeza Efraim.Bila kupoteza muda Joseph na wenzake wakaingia ndani.Hakukuwa na mlinzi yeyote na baada ya kupekua katika kuchunguza wakakuta miili mtatu ya walinzi “Walinzi watatu wameuawa kwa risasi” Joseph akatoa taarifa kisha wakaingia ndani.Walizunguka mle ndani ya hospitali na hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu. “Hakuna dalili zozote za kuwepo mtu humu ndani” akasema Joseph “Tumempoteza Mathew.Tumepoteza kila kitu” akawaza Efraim Dagan. “Tunasubiri maelekezo mkuu” akasema Joseph “Ondokeni sehemu hiyo haraka sana.Tutawasiliana wenzetu wa Jordan kuomba msaada katika suala hili na tutafahamu ukweli”akasema Efraim Kama walivyokuwa wamepanga.Baada ya kufika katika handaki la Suhaib gari moja likageuza kurejea lilikotoka na lingine likaendelea na safari kwa lengo la kuwapoteza wale waliokuwa wakiwafuatilia.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Pembezoni mwa jiji la Amman nchini Jordan kulikuwa na kijiji cha bilionea Rayan Jaber.Huyu alikuwa mmoja wa matajiri wakubwa sana na walioheshimika nchini Jordan.Alimiliki visima vya mafuta katika nchi kadhaa za kiarabu na vile vile kilichomuongezea umaarufu ni kumuoa mpwa wa mfalme wa Jordan.Rayan alikuwa na wake wawili hivyo alijenga kijiji chake ambako aliishi yeye na ukoo wake na baadhi ya watu wachache aliopenda waishi karibu yake.Katika kijiji hicho cha kifahari kulikuwa na huduma zote muhimu. Gari walilokuwamo akina Mathew Mulumbi lilifika katika geti la kuingilia kijiji cha Jaber .Bashar alipewa maelekezo ya kufika hapa na taarifa zao zilikuwepo kwa walinzi hivyo mmoja wa walinzi akaongozana nao kuelekea katika nyumba Fulani akawataka akina Mathew wabaki garini akaenda kugonga mlango na jamaa mmoja akaufungua wakazungumza kwa dakika chache Yule jamaa akaenda kuwasalimu akina Mathew garini halafu akarejea tena ndani na baada ya dakika chache akatoka akiwa na gari aina ya jeep akawataka wamfuate.Walimfuata hadi katika hospitali.Wakazunguka nyuma ya jengo lile la hospitali ambako kulikuwa na jengo zuri kwa ajili ya kuhifadhia maiti.Mwili wa Edger ukashushwa na kuingizwa katika friji ukahifadhiwa hapo.Yule jamaa ambaye hakujitambulisha jina lake akamtaka Mathew aingie katika gari lake akaagana na akina Bashar kisha wakaondoka na Yule jamaa akaendesha gari hadi walipofika katika kasri kubwa lililojengwa kati kati ya kijiji kile cha kifahari.Geti likafunguliwa wakaingia ndani na kwenda kusimamisha gari katika sehemu maalum ya maegesho wakashuka.Walinzi wakafika wakiwa na silaha na mbwa wawili ambao walimkagua Mathew kila sehemu na bastora yake ikachukuliwa.Kisha kaguliwa wakaelekea ndani.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mathew kuingia katika jumba la kifahari namna ile. “Kuna watu ndani ya dunia hii wanaishi kama vile hawataondoka hapa duniani.Maisha ya namna hii ni kufuru.Huu ufahari umepitiliza”akawaza wakati wakipita ndani ya jumba lile wakielekea katka sebule.Katika sehemu mbali mbali walizopita kulikuwa na walinzi wamesimama kwa adabu Waliingia katika sebule kubwa na kukaribishwa na mwanadada mrembo.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mathew kukalia kiti cha dhahabu .Baada ya dakika chache akaingia jamaa mmoja na kuzungumza na Yule jamaa aliyekuwa ameongozana na Mathew.Wote wawili wakamfuata Yule jamaa wakatoka nje na kuelekea katika bwawa la kuogelea.Sakafu ilikuwa imetengenezwa kwa madini yenye kung’aa Katika bwawa kubwa la kuogelea jamaa mmoja alikuwa amekaa katika kiti kizuri.Alikuwa kipande cha mtu na alionekana alikuwa ametoka kuogelea.Walisimama umbali wa hatua kadhaa kisha Yule jamaa aliyekwenda kuwachukua akina Mathew kule sebuleni akamfuata Yule jamaa akamjulisha kwamba wale watu tayari wamekwisha fika Yule jamaa akaelekeza wapelekwe sehemu ya kupumzika.Yule jamaa aliyekuwa na Mathew alionekana ni mwenyeji wa nyumba ile kwani alipoelekezwa akamtaka Mathew waondoke.Walikwenda katika sehemu moja yenye uzuri wa kipekee.Pembeni ya mahala pale walipokuwa wamekaa kulikuwa na banda kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na chui wawili ambao usiku huu walionekana wakizunguka zunguka katika banda lao kubwa. “Wanyama hawa lazima wanatoka Afrika.Nani anaishi hapa?Je hapa ni moja ya makazi ya Habiba Jawad? akajiuliza Mathew na kutamani kumuuliza Yule jamaa kuhusiana na mahala pale walipokuwa lakini Yule jamaa hakuonekana kutaka mazungumzo yoyote. “Nimezunguka sehemu mbali mbali nimefika katika makazi mengi ya matajiri lakini kwa utajiri huu niliouona hapa katika hii nyumba ni kufuru.Ni mara yangu ya kwanza ninakalia kiti cha dhahabu katika maisha yangu.Pesa iliyotumika kununua samani za ile sebule kama zingetolewa msaada kwa nchi za Afrika zingesaidia sana” akatolewa mawazoni baada ya Yule jamaa waliyemkuta akiogelea kuingia mahala pale .Alikuwa amevaa koti refu lenye nakshi za kupendeza.Akaketi kitini na kuwasalimu akina Mathew “As salaam Alaikum” akasema Yule jamaa aliyekuwa ameongozana na walinzi kadhaa ambao walisimama mbali kidogo na alipokuwa amekaa. “Wa alaikum salaam” Mathew na yule jamaa aliyekuwa naye wakajibu “Mkuu nimemleta mgeni na kila kitu kimefanyika kwa mujibu wa maelekezo” akasema Yule jamaa aliyekuwa na Mathew “Ahsante sana Majid” akasema Yule jamaa tajiri na Majid akasimama akamuaga akaondoka. “Abu Zalawi karibu sana katika himaya yangu.Naamini hunifahamu mimi ninaitwa Rayan Jaber.Ni mfanya biashara mkubwa hapa Jordan.Ninamiliki visima vya mafuta katika nchi mbali mbali.Habiba Jawad ni rafiki yangu sana.Urafiki wetu umeanza muda mrefu toka wakati akiwa na mumewe na baada ya kufariki mumewe tumeendelea kuwa marafiki wa karibu sana.Alinieleza kuhusu wewe na ndiye aliyetaka uje ufikie hapa kwangu baada ya kutoka Israel.Pole sana kwa misukosuko yote.Vipi safari yako ilikuaje huko ulikotoka? Akauliza Rayan “Rayan nashukuru sana kwa kunikaribisha hapa katika himaya yako,safari yangu haikuwa rahisi.Haikuwa rahisi kuupata mwili wa Edger kaka kwani ulikuwa umefichwa mahala pa siri na Mossad lakini nashukuru Mungu nimefanikiwa kuupata na nitakwenda kuukabidhi kwa Habiba Jawad” akasema Mathew na Rayan alionyesha mstuko kidogo Mathew alipotamka kuhusu Mossad “Una hakika wale jamaa hawajakufuatilia na kujua umekuja hapa?akauliza Rayan “Hapana hawajui kama niko hapa ndiyo maana nikasema kwamba haikuwa rahisi kuweza kufika hapa.Nimechukua kila aina ya tahadhari” “Vizuri sana.Narudia tena kukupa pole nyingi na kukushukuru pia kwa kufanikiwa kuupata mwili wa Seif. Habiba amekwisha lia machozi mengi sana kwa ajili ya Seif.Mimi kama mtu wake wa karibu huwa hanifichi jambo.Ninafahamu uchungu alioupata kuhusu mwanae huyu na hatimaye amefanikiwa kuupata mwili wake na atauzika kwa heshima.Kwa hili ulilolifanya,umemfanyia Habiba kitu kikubwa sana ambacho hatakisahau katika maisha yake” akasema Rayan akanyamaza kidogo na kusema “Utalala hapa usiku wa leo na kesho tutaongozana kuupeleka mwili wa Seif kwa mama yake” akasema Rayan na kumuita mmoja wa walinzi wake akamuelekeza jambo kisha mlinzi Yule akamtaka Mathew amfuate “Rayan nashukuru sana na usiku mwema” akasema Mathew na kuondoka akamfuata Yule mlinzi.Alipelekwa katika nyumba moja iliyokuwa na chumba cha kulala,sebule kubwa na nzuri na sehemu ya kulia chakula.Ilionekana ni nyumba maalum kwa ajli ya wageni kwani hakukuwa na dalli zozote za kuishi mtu ndani ya nyumba ile.Mathew akaingia ndani ya chumba cha kulala na kuustaajabia uzuri wake.Akatabasamu kwa uzuri wa chumba kile kisha akakaa juu ya kitanda kikubwa. “Dunia hii wapo watu wanaishi kama wako peponi.Hawana mawazo kama siku moja wataondoka katika hii dunia.Tazama chumba hiki cha wageni namna kilivyo kizuri ni vipi katika chumba chake cha kulala? Akajiuliza “Lakini haya mambo hayanihusu kikubwa ambacho natakiwa kujielekeza ni kuhakikisha mwili wa Edger kaka unafika salama kwa Habiba Jawad.Naamini Mossad hivi sasa watakuwa wananitafuta sana baada ya kuwapoteza pale Advaclinic.Wataamini kwamba wale jamaa niliokuwa nao wamegundua kwamba mimi na Edger tumewekewa vifaa mwilini na wakavitoa.Sitaki wafahamu chochote kuhusu Habiba Jawad kwa sasa.Nataka nipate nafasi nzuri ya kumfahamu mwanamama huyu wa aina yake.Tayari nimeanza kuufahamu mtandao wake.Kama huyu jamaa Rayan ana utajiri mkubwa kiasi hiki ni vipi kuhusu Habiba Jawad?Naamini utajiri wake ni mkubwa mno na ndiyo maana haoni hasara kufadhii makundi ya kigaidi” akawaza Mathew na kuingia bafuni kuoga.Alipotoka akajilaza kitandani mara mlango wake ukagongwa.Alikuwa ni jamaa mmoja aliyejitambulisha kama daktari.Akalitibu jeraha la Mathew mkononi pale mahala alipokuwa amewekewa kile kifaa akampima na kila kitu kilikuwa kinakwenda vizuri.Baada ya daktari kuondoka mlinzi akamfuata na kumjulisha kwamba chakula tayari kimeandaliwa akaenda katika chumba cha chakula akala na kurejea chumbani kwake akajilaza kitandani. DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa kumi na moja za alfajiri simu ya Melanie ikaita.Alikuwa amechoka sana akaiacha ikaita na kukatika ikaanza kuita tena. “Nani huyu alfajiri yote?akasema na kuinuka akaichukua simu akatazama mpigaji alikuwa ni Devotha “Asubuhi yote hii anatafuta nini?akajiuliza Melanie na kuipokea ile simu. “Hallow Devotha” akasema Melanie kwa sauti ya uchovu “Melanie habari yako? “Nzuri kabisa.Habari za huko? “Huku kwema.Vipi maendeleo yako? “Ninaendelea vizuri” “Juzi na jana ulikuwa wapi Melanie? Akauliza Devotha na Melanie akawa kimya “Nilikutafuta nilikuwa na jambo la msingi sana la kuzungumza nawe lakini hukuwa ukipatikana simuni.Ulikuwa wapi?akauliza Devotha “Ni kweli nilikuwa sipatikani kuna masuala nilikuwa nayafuatilia” “Melanie nimekwisha kuelekeza kwamba usifanye kitu chochote bila ya Edwin kujua.Yeye ndiye kiongozi wako hapo Dar es salaam.Masuala yote kuhusiana na usalama wako yeye ndiye tumemkabidhi.Ulionekana ukiondoka na sanduku ulikwenda wapi?akauliza Devotha “Devotha nimekwisha kwambia kwamba kuna suala muhimu nilikuwa nalifuatilia” “Ni suala gani hilo? “Usihofu Devotha litakapokamilika nitakujulisha” akasema Melanie “Melanie unafahamu umuhimu wa suala lililokupeleka Tanzania lakini unaonyesha kupuuzia.Suala unalokwenda kulifanya ni zito.Kusambaratisha jumuiya kubwa kama ya Afrika Mashariki si suala dogo ndiyo maana imetuchukua miaka kuliandaa jambo hili na sasa tumeanza utekelezaji wake lakini unaanza kwenda katika mwelekeo usio sahihi.Suala hili huwezi ukalifanya peke yako ndiyo maana tumetengeneza mtandao mpana ambao utakusaidia wewe uweze kutimiza misheni yako.Kwa sasa macho yote yameelekezwa kwako hivyo tafadhali nakuomba ufanye kile ulichoelekezwa kwenda kukifanya.Ukienda kinyume na maelekezo utasababisha mambo kushindwa kufanikiwa hivyo shirikiana na mtandao mkubwa ulioko hapo Tanzania” akasema Devotha “Devotha huna haja ya kunikumbusha majukumu yangu.Ninafahamu kilichonileta hapa na ndicho ninachokifanya.Pamoja na mtandao mliouandaa kwa ajili ya kunisaidia lakini lazima mimi mwenyewe niwe na mipango ambayo itanisaidia katika kutimiza malengo yangu hivyo unaponitafuta katika simu na kuikosa fahamu kwamba niko katika kutimiza majukumu yangu” akasema Devotha “Ninalielewa hilo Melanie lakini naomba sana shirikiana na Edwin.Kila unachotaka kukifanya mshirikishe” “Nitafanya hivyo” “Vipi maandalizi yamefikia wapi? “Ninaendelea kufanya maandalizi na ndani ya siku chache nitakupa mrejesho” akasema Melanie “Jitahidi sana Melanie kukamilisha maandalizi haraka kwani zimebaki siku chache kwa mkutano kufanyika” akasema Devotha.Baada ya mazungumzo kidogo wakaagana na Devotha akakata simu Melanie akairusha simu pembeni na kuendelea kulala. Saa tatu za asubuhi,mlango wa chumba cha Melanie uligongwa akainuka na kwenda kuufungua alikuwa ni Joyce. “Madam nimepigiwa simu na Frimina anasema saa nne na nusu leo utakuwa na kikao muhimu na watu kutoka mamlaka ya mapato.Hivi sasa ni saa tatu na dakika ishirini” akasema Joyce “Mwambie Mina avunje ratiba yangu nzima ya siku ya leo.Ninahitaji kupumzika.Kuhusu hao watu wa mamlaka ya mapato amuelekeze GosuGosu atalishughulikia hilo suala” akasema Melanie “Kila kitu kinakwenda sawa Melanie?akauliza Joyce “Nimechoka sana nahitaji kupumzika” akasema Melanie na Joyce akatoka. “Mwili wote umechoka.Safari ya Uganda ilikuwa ndefu na ngumu.Siku ya leo natakiwa kushughulikia safari ya kesho Dubai.Halafu natakiwa kuonana na balozi Mapupu ili kuanza maandalizi ya mpango wangu” akawaza Melanie na kumpigia simu Joyce ambaye alifika haraka “Joyce kesho nina safari ya kuelekea Dubai.Tafadhali naomba ushughulikie suala hilo na asifahamu mtu mwingine yeyote kama nimekwenda Dubai.Kuwa makini sana hasa na hawa wanawake wawili humu ndani.Usiwaeleze chochote kuhusu safari zangu”akasema Melanie “Sawa Melanie” akasema Joyce na kutoka ndani Melanie akaitafuta namba ya simu ya balozi Mapupu akampigia “Hallo Melanie” akasema balozi Mapupu “Mheshimiwa balozi habari yako? “Nzuri Melanie.Unaendeleaje?Umekwis ha rejea safari yako ya Kinshasa?akauliza balozi Mapupu “Tayari nimekwisha rejea nilibanwa na majukumu ndiyo maana nikashindwa kuwasiliana nawe” “Pole sana na majukumu.Safari yako ilikuwa na mafanikio?akauliza balozi Mapupu “Ndiyo ilikuwa na mafanikio makubwa sana” ‘Ninafurahi kusikia hivyo” akasema balozi Mapupu “Mheshimiwa balozi nahitaji kukutana nawe kwa chakula na mazungumzo kama hutajali” akasema Melanie “Hakuna tatizo Melanie.Unataka tukutane lini na wapi?akauliza balozi Mapupu “Nitakukaribisha nyumbani kwangu leo kama hutajali” “Ahsante sana Melanie lakini nyumbani kwako sipafahamu” “Usijali balozi utanielekeza mahala ulipo nitamtuma dereva wangu atakuja kukuchukua na kukuleta mahala nilipo” akasema Melanie “Sawa tutawasiliana hapo baadae”akasema balozi Mapupu na kukata simu “Uzuri huu nilio nao umekuwa ni kama sumaku ambayo inavuta kila mwanaume ninayemuhitaji.Tayari ninaye GosuGosu,na sasa ni balozi Mapupu.Kumkaribisha nyumbani kwangu ameona ni nafasi ya dhahabu hakuwa ametegemea kabisa bila kujua kwamba taratibu anajipeleka katika mdomo wa Mamba” akawaza Melanie na kuendelea kulala AMMAN – JORDAN Mathew Mulumbi aliwahi kuamka asubuhi na kuoga akajiweka tayari kwa kile kitakachojiri siku hii.Daktari alifika mapema na kulitibu jeraha lake mkononi na ilipofika saa mbili za asubuhi muhudumu akafika akiwa na kanzu nzuri nyeupe Mathew akavaa na kuchukuliwa akapelekwa katika jumba kubwa la Rayan Jaber akakaribishwa katika chumba maalum kwa ajili ya kifungua kinywa.Kulikuwa na meza ya duara ambayo iliwekwa vyakula mbali mbali kwa ajili ya mlo wa asubuhi.Muda mfupi baadae Rayan Jaber akaingia.Siku hii alikuwa amevaa kanzu nyeupe “As salaam Alaikum Abu Zalawi” akasema Rayan. “Wa alaikum salaam” Akajibu Mathew “Vipi maendeleo yako? “Ninaendelea vizuri Rayan.Nashukuru sana kwa kunikaribisha na nimepata huduma nzuri” akasema Mathew “Nimepata heshima kubwa kwa uwepo wako hapa kwangu na mimi nashukuru sana” akasema Rayan huku wakiendelea kupata kifungua kinywa “Mwili wa Seif unaandaliwa hivi sasa kwa ajli ya kusafirishwa.Tukimaliza hapa tutaelekea moja kwa moja uwanja wa ndege tayari kwa safari.Tungeweza kuuandaa hapa kwa kila kitu lakini hatuwezi kufanya hivyo hadi pale Habiba atakapouona mwili wa mwanae ndipo taratibu nyingine za mazishi zitaendelea” akasema Walipomaliza kifungua kinywa Rayan akamchukua Mathew na kumpeleka katika chumba cha mapumziko akamtaka apumzike na atarejea baada ya muda mfupi.Dakika kumi baadae Rayan akarejea na kumtaarifu Mathew kwamba kila kitu tayari na wanaweza kuondoka.Waliingia katika gari la kifahari la Rayan na kuelekea katika uwanja wa ndege uliopo kwenye kijiji cha Rayan.Ndege tatu za bilionea Rayan zilikuwepo pale kiwanjani.Mwili wa Edger ambao uliwekwa katika jeneza maalum ukaingizwa katika mojawapo ya ndege kisha Rayan na Mathew pamoja na walinzi wa Rayan wakaingia ndegeni na baada ya muda mfupi ikapaa na kuondoka. TEL AVIV – ISRAEL Efraim Dagan aliingia katika ofisi ya mkurugenzi mkuu wa Mossad Moshe Levine.Uso wake ulionyesha alikuwa na mzigo wa mawazo.Akaketi katika kiti kilichokuwa mbele ya meza ya Moshe “Efraim kuna taarifa gani mpya? Akauliza Moshe “Tumempotezaje Mathew Mulumbi” Akasema Efraim “Nini kimetokea?Tumempotezaje?aka uliza Moshe “Tulimfikisha Mathew mpakani kama tulivyokuwa tumekubaliana na akakutana na watu wale kama alivyokuwa ameeleza na safari ya kuelekea Amman ikaanza.Majasusi wetu walioko upande wa Jordan walishika usukani na kuendelea kumfuatilia na sisi tukiendelea kumfuatilia kwa kutumia kile kifaa tulichomuwekea mkononi.Baada ya kuingia Amman gari la akina Mathew likaelekea Advaclinic ambayo inajishughulisha na vipimo mbalimbali.Watu wetu walishindwa kuona kilichokuwa kinafanyika kutokana na hiyo mvua kubwa.Baada ya gari za akina Mathew kuondoka waliingia ndani ya hospitali lakini hawakuweza kumpata Mathew wala mwili wa Edger Kaka japo vile vifaa viliendelea kutuonyesha kuwa walikuwa katika maeneo hayo ya hospitali.Ililazimu kuomba msaada kwa wenzetu wa Jordan na asubuhi ya leo nimepata majibu.” Efraim akanyamaza kisha akaendelea “Uchunguzi umefanyika na ndani ya kliniki hiyo hakuna mwili wowote uliopatikana wa Mathew au Edger.Taarifa inasema kwamba waliua walinzi watatu ndipo walipoweza kuingia ndani ya hospitali.Walichokifanya ndani ya hospitali walikwenda hadi katika chumba chenye mashine ya MRI na rekodi zinaonyesha kwamba waliitumia mashine hiyo.Nadhani umekwisha fahamu ni kitu gani walikusudia kukifanya” “Walitaka kuona kama kuna vifaa vyovyote tumeviweka katika mwili wa Edger Kaka na walipogundua wakakiondoa pamoja na kile cha Mathew ndiyo maana tukaendelea kuviona vifaa vile vile pale hospitali.Mathew ametoweka na hatujui mahala alipo” akasema Efraim.Moshe akainamisha kichwa “Kama wameweza kugundua Mathew alikuwa na kifaa mwilini hawatamuacha salama lazima watakwenda kumuua.Tuombe msaada kwa vyombo vya Jordan watusaidie kutupa taarifa kama kuna mtu yeyote ataripotiwa kuuawa. Jambo lingine,siku zote tumekuwa tukiamini kwamba Habiba anaishi Saudi Arabia lakini ukifuatilia taarifa ya Mathew alidai kukutana na Sayid Omar ambaye ni mtu wa karibu sana na Habiba nchini Jordan na nina uhakika hata Habiba alikuwa Jordan alipozungumza naye ndiyo maana nashawishika kuamini kwamba tukiwekeza nguvu nchini Jordan tunaweza kumpata Habiba Jawad au hata kuufahamu mtandao wake.Hatua aliyopiga Mathew ni kubwa sana ametufungulia dirisha ambalo tukilitumia vyema basi tutapiga hatua kubwa” akasema Moshe Levine. “Ulichokisema hata mimi nilikuwa nakiwaza kuna uwezekano mkubwa Habiba Jawad akawa na makazi yake nchini Jordan lakini inabidi suala hilo tulichunguze wenyewe bila kuwashirikisha Jordan kwani Habiba mtandao wake unaweza kuwa mkubwa.Kuhusu Mathew Mulumbi bado nina imani naye.Kuna kitu ndani yangu kinanifanya niendelee kuamini kwamba yawezekana akawa hai.Tusikate tamaa mapema.Hata wakati ule tulikata tamaa lakini amekuja kuibuka na kumbe yeye ndiye aliyemuua Ammar Nazari.Japo mazingira yanaonyesha kuna uwezekano mkubwa wa Mathew akaenda kuuawa lakini tusikate tamaa” akasema Efraim RIYADH – SAUDI ARABIA Ndege waliyopanda akina Mathew ilitua katika uwanja mdogo wa ndege unaomilikiwa na familia ya Habiba Jawad.Rayan akamtangulia Mathew kushuka ndegeni.Nje kulikuwa na watu zaidi ya ishirini na magari saba yote yakiwa na rangi nyeusi.Watu kadhaa wakaingia ndegeni na mwili wa Mathew Mulumbi ukashushwa na kuingizwa katika gari maalum kisha magari yale yakaondoka pale uwanjani.Katika watu wale wote waliowakuta pale uwanjani hakuna hata mtu mmoja ambaye Mathew alimfahamu.Mathew alikuwa mgeni katika jiji la Riyadh hivyo hakujua walikuwa wanaelekea wapi. “Hawa jamaa utajiri wao ni wa kufuru.Wana ndege zao binafsi na wana viwanja vyao vya ndege.Bado nina safari ndefu na ngumu ya kumfahamu vyema Habiba Jawad ni mtu wa aina gani na ninapoendelea kumfahamu Habiba Jawad siwezi kuwaacha watu wake wa karibu.Mmoja ni huu Rayan Jaber.Utajiri wake unatisha.Mambo niliyoyaona nyumbani kwake hatujazoea kuyaona nchini kwetu.Mimi ni tajiri….Oh my God nimejisahau sipaswi kujiita bilionea.Nilikuwa bilionea na ninawafahamu mabilionea wengi nchini kwetu hawana maisha ya kufuru kama ya Rayan.Hadi vikombe vya kunywea chai ni vya dhahabu ! akawaza Mathew na kutazama nje “Kwa hiki nilichokifanya cha kuuleta mwili wa Edger Kaka kitaniweka karibu zaidi na Habiba Jawad.Kingine kitakachoniweka karibu yake zaidi ni pale nitakapokubali kumuoa mwanae Najma kama alivyokuwa amenitaka.Lakini ni vipi kama nitajikuta nikimpenda huyo Najma na kujikuta nikianza maisha mapya huku na kusahau misheni yangu? Ni hiki ndicho anachokitaka Habiba Jawad? Nini hasa malengo yake kwangu na kwa Nawal? Akajiuliza huku msafara ule ukienda kwa kasi Dakika zipatazo ishirini wakawasili katika geti moja kubwa lililokuwa linalindwa na walinzi wanne.Geti lilikuwa limefunguliwa na msafara ule wa magari ukaingia ndani.Kulikuwa na majumba kadhaa makubwa na mengine madogo na yote yakiwa yamepakwa rangi nyeupe.Barabara zote za kuelekea katika majumba yale zilijengwa vizuri kwa lami.Kulipandwa miti ya maua mazuri bila kusahau taa za barabarani.Kilionekana kama kijiji kidogo lakini si kama kile cha Rayan Jaber.Mathew aliyekuwa amepanda gari moja na Rayan wakashuka.Kulikuwa na watu wamejipanga kwa ajili ya kuwapokea.Mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa ni Abu Dahir mtoto wa Habiba “Abu Zalawi ahsante sana kwa kumrejesha nyumbani ndugu yangu” akasema Abu Dahir.Kisha Mathew akasalimiana na Sayid Omar na watu wengine waliopata ishirini.Mwili ukashushwa garini na kubebwa ukapelekwa katika jumba moja kubwa jeupe ukawekwa katika chumba maalum na baada ya muda mfupi Habiba Jawad akaingizwa akiwa ameshikwa na akina mama wawili.Hakuwa na nguvu.Macho yake yalikuwa mekundu.Akasogezwa karibu na jeneza likafunguliwa akamuona mwanae Edger au Seif Jawad.Habiba alimwaga machozi mengi akiwa ameweka mikono yake katika kichwa cha mwanae.Aliporidhika akatoa ruhusa taratibu nyingine za mazishi ziendelee. Mathew na watu wengine waliokuwamo ndani ya jumba lile kubwa wakatoka na kwenda katika sehemu kulikoandaliwa hema kubwa na ambako kulikuwa na watu wasiozidi mia mbili.Sayid Omar aliyekaa pembeni mwa Mathew akamshika mkono na kumtaka amfuate wakaenda sehemu Fulani kwa ajili ya mazungumzo. “Abu Zalawi wakati maandalizi yakiendelea nimeona tuzungumze kidogo.Kwanza kabisa pole sana kwa safari ndefu hadi kuufikisha mwili hapa.Najua haikuwa rahisi” “Ni kweli Sayid.Haikuwa kazi nyepesi” “Nimejulishwa na Bashar kuhusu mlichokifanya pale Amman.Nakupongeza ulikuwa ni ujasiri mkubwa sana.Umefanya kitu kikubwa mno na hata Habiba Jawad amekushukuru mno” akasema Sayid “Habiba tayari anajua kilichotokea Amman?akauliza Mathew “Ndiyo.Utaratibu wetu hapa lazima ajulishwe kila kinachotokea.Tayari anajua na akipata muda wa kuonana nawe baadae atakupa shukrani zake.Ulifahamuje kama mwili wa Edger umewekewa kifaa maalum? Akauliza Sayid Omar “Mossad wanamtafuta sana Habiba Jawad na wanajua Edger Kaka ni mtu wake wa muhimu hivyo kwa namna yoyote ile wasingeweza kumuacha hivi hivi lazima wangemuwekea kifaa maalum.Nimekuwa nikipambana na Mossad kwa muda mrefu hivyo ninawafahamu vyema” akasema Mathew na mara vin’gora vikasikika na msafara wa magari ya kifahari ukaingia “Huyo ni mwana mfalme wa Saudi Arabia amekuja kuungana nasi.Mfalme wa Saudia ni rafiki sana na Habiba hivyo amemtuma mwanae kuja kumuwakilisha.Vile vile mwanamfalme huyu ni rafiki mkubwa wa Abu Dahir.Tutazungumza baadae ngoja nikampokee” akasema Sayid Omar na kwenda kumpokea mwana mfalme,Mathew akarejea kuungana na waombolezaji wengine.Mwana mfalme alipokelewa na Sayid Omar na Abu Dahir na moja kwa moja akapelekwa katika chumba alimokuwamo Habiba Jawad akampa pole na salamu za mfalme kisha akapelekwa sehemu waliko waombolezaji wengine akaungana nao.Wengi wa waliokuwepo katika msiba ule walionekana ni watu wenye uwezo mkubwa kifedha.Walikaa kimakundi wakizungumza wakati wakisubiri mwili wa Edger uandaliwe kwa ajili ya mazishi.Ni Mathew pekee ambaye hakuwa na mtu wa kuzungumza naye alikuwa peke yake.Alionekana tofauti na wengine wote kwanza kwa rangi na hata kwa muonekano.Mabilionea wale hawakujua kama walikuwa wamekaa na mtu hatari sana.Wakati wengine wakiendelea na mazungumzo yao huku wahudumu wakipita na kugawa sahani za vitafunwa mbali mbali Mathew alikuwa mbali sana kimawazo.Aliwaza mambo mengi sana kuhusu mustakabali mzima wa maisha yake. Mwili wa Edger uliandaliwa na kuletwa kwa waombolezaji kwa ajili ya taratibu za ibada.Imamu aliongoza swala na taratibu nyingine kisha mwili ukachukuliwa kupelekwa katika makaburi.Taratibu mwili ukaingizwa kaburini na kuzikwa. “Mwisho wa Edger Kaka ndio mwanzo wa Habiba Jawad.Haijalishi nitatumia miaka mingapi lakini lazima kwa namna yoyote ile Habiba Jawad na mtandao wake wapotee.Yawezekana nikashindwa kutimiza malengo yangu ya kuwaangamiza wafadhili hawa wa ugaidi duniani lakini nitajaribu.Nitakufa nikijaribu” akawaza Mathew wakati kaburi la Edger Kaka likifukiwa. Baada ya shughuli ya mazishi kumalizika waombolezaji wakarejea katika sehemu zao.Mwana mfalme hakukaa sana akawaaga waombolezaji akaondoka zake.Chakula kiliandaliwa waombolezaji wakala na kisha wakaanza kuondoka mmoja mmoja.Abu Dahir akamchukua Mathew na kumpeleka katika nyumba Fulani ndogo “Abu Zalawi natumai tutapata nafasi ya kuzungumza zaidi lakini kwa sasa ninapenda nikushukuru kwa mara nyingine tena kwa kitendo hiki ulichokifanya cha kuuleta nyumbani mwili wa kaka yangu Seif.Tumehangaika kwa muda mrefu sana kumtafuta.Hadi tunampumzisha leo Seif amepitia magumu mengi sana.Kwa ufupi tu ni kwamba Seif alikuwa akiishi nchini Tanzania na alikuwa ni mbunge.Alikuwa na maadui wengi hivyo aliwekewa sumu kwa lengo la kumuua lakini kwa bahati nzuri akapona katika jaribio hilo.Baada ya kupona ikatokea ajali ambayo tulitangaziwa kwamba amefariki dunia lakini baadae tukagundua kwamba yuko hai na tukaanza harakati za kumtafuta.Niliwahi kufika hadi Tanzania kukutana na mwanadada mmoja anaitwa Olivia Themba nikiwa katika harakati za kumtafuta Seif.Mambo mengi yalitokea hadi usiku ule ambao Seif alitakiwa kukabidhiwa kwetu na serikali ya Tanzania lakini akatekwa na majasusi wa Israel.Binafsi japokuwa nina majonzi lakini nina furaha sana ya kumuona kaka yangu japo hatukuweza kuzungumza lakini nimemzika kwa heshima.Ahsante sana Abu Zalawi” akasema Abu Dahir Mathew hakujibu chochote alikuwa kimya kabisa “Ninakushukuru vile vile kwa kumuokoa Nawal kutoka katika mashambulio ya Israel.Nadhani umekwishadokezwa kwamba ninataka kumuoa Nawal” akasema Abu Dahir “Ndiyo.Mama Habiba amekwisha nijulisha suala hilo” akasema Mathew “Kuna tatizo lolote?akauliza Abu Dahir “Hakuna tatizo lolote.Nawal alikuwa ni mke wa kiongozi wangu Ammar Nazari na mimi sina tatizo lolote kwa wewe kumuoa kwani kwa sasa hana mume” “Nashukuru sana Abu Zalawi.Tutaendelea kufahamiana zaidi kwani kwa mujibu wa taarifa aliyonipa mama ni kwamba utaendelea kukaa nasi hapa.Karibu sana na jisikie nyumbani”akasema Abu Dahiri na kuagana na Mathew baada ya kupigiwa simu.Mathew naye akatoka na kurejea mahala walikokuwepo waombolezaji wengine akaungana nao. DAR ES SALAAM – TANZANIA Mlio Fulani ulisikika chumbani kwa Melanie Davis,akayaelekeza macho yake katika runinga iliyokuwa ukutani ambayo iliunganishwa na kamera zilizokuwa getini na kuliona gari la Joyce likivuka geti.Joyce alikuwa ametumwa kwenda kumchukua balozi Germinus Mapupu ambaye Melanie alikuwa amemualika kwa chakula cha jioni.Melanie akajitazama na kutabasamu “Sihitaji kujifanyia maandalizi makubwa kwani bila hata kujiremba mimi ni mzuri na balozi Mapupu tayari alikwisha onyesha kuchanganyikiwa mara ya kwanza tu aliponiona.Wanaume Mungu aliwapa udhaifu mkubwa kwa mwanamke” akawaza huku akikoleza rangi ya mdomo. Mlango ukagongwa akaingia Joyce. “Tayari mheshimiwa balozi amekwisha fika” akasema Joyce “Ahsante Joyce.Mpeleke katika sebule yangu nitakuja hapo muda si mrefu.Msimuhudumie chochote kwanza hadi nitakapofika mwenyewe” akasema Melanie Balozi Mapupu alipelekwa katika sebule maalum ya Melanie.Baada ya dakika chache Melanie akaingia pale sebuleni.Usiku huu alikuwa amevaa sketi fupi nyeusi alivaa pia fulana ya rangi nyeupe ambayo ilimpwaya iliyokuwa na shingo pana na kuonyesha kifua chake kizuri. “Mr Mapupu” akasema Melanie kwa sauti yake laini na kumfuata balozi Mapupu ambaye alisimama na kumkumbatia “Karibu sana mheshimiwa balozi.Nimefurahi sana kunitembelea hapa kwangu” akasema Melanie.Balozi Mapupu mapigo ya moyo yalimbadilika baada ya kukumbatiwa na kimwana Yule. “Ahsante sana Melanie kwa kunikaribisha nyumbani kwako.Siwezi kuelezea furaha yangu” akasema balozi Mapupu “Mheshimiwa balozi unatumia kinywaji gani usiku wa leo? Akauliza Melanie “Nitakuomba unichagulie kinywaji chochote nitatumia.Kwako siwezi kusema hapana kwa chochote utakachonikirimu” akasema balozi Mapupu na Melanie akaachia tabasamu pana sana akainuka na kutoka baada ya dakika chache akarejea akiwa na sinia lililokuwa na chupa kadhaa za mvinyo. “Mr Mapupu naomba usiku huu uchague kinywaji tutakachokitumia” akasema Melanie na balozi Mapupu huku akitabasamu akachagua chupa moja Melanie akamimina katika glasi mbili na kumkaribisha “Kwa ajili ya urafiki wetu” akasema Melanie huku akiinua glasi wakagonganisha na kila mmoja akanywa funda moja “Balozi naomba kwa mara nyingine tena nikushukuru kwa kukubali mwaliko wangu.Nafahamu una shughuli nyingi lakini umeacha shughuli zako zote umekuja kuungana nami hapa.Ahsante sana” akasema Melanie “Melanie ningewezaje kukataa mwaliko kutoka kwa mtu muhimu kama wewe? U mtu muhimu sana kwa nchi yetu ya Congo.Binafsi ninajihisi fahari kubwa kuwepo hapa pamoja nawe usiku huu” akasema balozi Mapupu “Vipi kuhusu safari yako ilikuwa na mafanikio?akauliza balozi Mapupu na Melanie akamueleza kwa upana kuhusu lengo lake la kuwekeza nchini Congo.Balozi Mapupu alifurahi sana kwa maelezo hayo aliyoyatoa Melanie.Baada ya mazungumzo Melanie akamkaribisha balozi Mapupu kwa chakula kizuri kilichoandaliwa.Baada ya chakula kile wakaelekea katika chumba cha mapumziko “Melanie ninashukuru sana kwa chakula kizuri sana”akasema balozi Mapupu “Ahsante balozi” akasema Melanie kisha akainuka na kwenda kuketi karibu na balozi “Usihofu balozi hapa tuko peke yetu hakuna mtu atakayefika hapa” “Mumeo yuko wapi Melanie?akauliza balozi Mapupu “Mume? Akauliza Melanie na kutoa kicheko. “Sina mume” “Huna mume? Balozi Mapupu akashangaa “Ndiyo sina mume.Ni ajabu kukosa mume?akauliza “Si ajabu lakini kwa mrembo kama wewe kwa nini ukose mume? “Nimeamua nikae hivi kwanza hadi hapo baadae” akasema Melanie huku akitabasamu “Lakini mara moja moja nimekuwa nikitoka na wanaume mbali mbali lakini sitaki ule urafiki wa kudumu” akasema Melanie na balozi Mapupu akawa kimya ‘Balozi Mapupu kuna jambo nataka kulileta kwako kama utaona inafaa” “Omba Melanie chochote” “Si ombi bali ni pendekezo” “Nitalipokea kwa mikono miwili” akasema balozi Mapupu “Mkutano mkubwa wa wake za marais unatarajiwa kufanyika hapa Tanzania wiki ijayo.Nchi ya Congo na Rwanda kwa sasa hazina mahusiano mazuri.Kama Tanzania wameweza kuandaa mkutano huu mkubwa na kuwakaribisha wake za maraisi kutoka duniani kote kwa nini wewe na balozi mwenzako wa Rwanda msiitumie fursa hii kuwaweka karibu wake za marais wa Rwanda na Congo? Mnaweza kuandaa chakula cha jioni mkawaalika wote wakakutana na kuzungumza.Huo utakuwa ni mwanzo mzuri wa kuleta amani katika nchi zao.Kama akina mama hawa wakielewana na kuzungumza lugha moja basi watakwenda kuzungumza na waume zao na mambo yatakaa sawa”akasema Melanie “Melanie una akili sana.Hilo ni wazo zuri mno na sikuwa nimelifikiria kabisa.Ahsante kwa kunipa wazo kama hilo ambalo kama likifanikiwa ni kweli linaweza kuwa chanzo cha amani kwa nchi zetu hizi mbili.Ni kweli nchi ya Congo na Rwanda kwa sasa hazina mahusiano mazuri.Maraisi hawa wawili wamekuwa katika vita ya maneno nadhani mkutano huu unaweza ukawa ni chachu ya kuondoa vita ya maneno ya marais hawa wawili.Jambo hilo linawezekana.Kumpata Rebeca Eyenga mke wa Rais wa Congo si kazi ngumu na nina uhakika lazima atakubali mwaliko wangu lakini kazi itakuwa katika kumpata mke wa Rais wa Rwanda.Kama unavyofahamu msuguano uliopo umepelekea hata sisi mabalozi ambao tunaziwakilisha nchi zetu hapa tusiwe na mahusiano mazuri.Mimi na mwenzangu wa Rwanda hatuna maelewano mazuri” akasema balozi Mapupu “Nalifahamu hilo ndiyo maana nikashauri kwamba mkutano huu utumike katika kuleta amani.Wewe na mwenzako wa Rwanda mtaanzisha maelewano,wake za marais wataelewana na kitakachozaliwa hapo ni marais wa Rwanda na Congo kuelewana.Mimi nitagharamia kuandaa chakula hicho kwa kila kitu wewe kazi yako itakuwa ni kutafuta namna ya kuwakutanisha wake hawa za marais” akasema Melanie “Ahsante sana Melanie kwa kulileta wazo hili na hata kujitolea kugharamia jambo hili kubwa.Ubalozi wangu hautakuwa na maana kama nitashindwa kuitumia nafasi hii kusaidia kuleta amani katika nchi zetu.Ninakuahidi nitafanya kila kitu kwa ajili ya kuhakikisha ninawaleta mezani wanawake hawa.Hata hivyo kuna wazo nimelipata” akasema balozi Mapupu na kunyamaza kidogo “Umepata wazo gani mheshimiwa balozi?akauliza Melanie kwa sauti laini na kuupeleka mkono wake katika tai ya balozi Mapupu “Ili jambo hili lifanikiwe anahitajika mtu wa tatu ambaye anaweza akawaleta wanawake hawa katika meza moja na kuwaunganisha” “Unadhani nani anayeweza kuifanya kazi hiyo ya kuwaweka wanawake hawa mezani na wakazungumza? Akauliza Melanie “Millen Kelelo mke wa Rais wa Tanzania.Yeye ndiye muandaaji wa mkutano na ndiye anayeweza kuwaalika wanawake hawa kwa pamoja na wakajikuta sehemu moja.Hawataweza kukataa mwaliko wake”akasema balozi Mapupu “Hilo ni wazo zuri sana mheshimiwa balozi” “Melanie mambo ya mheshimiwa ni pale tunapokuwa kazini lakini nje ya hapo niite Mr Mapupu inatosha” “Mr Mapupu hilo ni wazo zuri sana kumshirikisha mke wa Rais wa Tanzania.Pamoja na kumshirikisha huko lakini iwe ni katika kuwaleta mezani wanawake hao tu.Hatuwezi kumbebesha mzigo wa kuandaa chakula hicho kwani amekwisha tumia fedha nyingi kuandaa mkutano mkubwa” akasema Melanie “Usijali kuhusu hilo Melanie.Sisi tutaandaa kila kitu” “Maandalizi yaanze mara moja.Kutana na bi Millen uzungumze naye kuhusu nia yako hiyo na nina uhakika hawezi kukataa na baada ya hapo utatafuta ni sehemu gani ambako unadhani panaweza pakafaa kwa kufanyia jambo hilo pamoja na gharama nyingine zote.Mimi nitagharamia kila kitu,nitawaleta wapishi wa kimataifa wenye uwezo wa kupika kila aina ya chakula,tutaandaa pia burudani kadhaa ili kunogesha usiku huo.Utakuwa ni usiku wa aina yake na mambo makubwa lazima yafanyike usiku huo.Naipenda sana nchi yangu na ninapenda kuiona ikiwa na amani bila mikwaruzano na majirani zake hivyo ni jukumu letu mimi na wewe kuhakikisha kwamba tunalifanikisha jambo hili na baada ya hapo hakuna ajuaye pengine mimi nawe tunaweza kupata nafasi nzuri zaidi ya kujipongeza kwa kazi kubwa tuliyoifanya” akasema Melanie huku akiuchukua mkono wa Mr Mapupu akaushika na kuuweka katika paja lake. “Melanie tutafanikiwa.Kesho asubuhi kazi yangu ya kwanza ni kwenda katika ofisi ya mke wa Rais na kuzungumza naye juu ya jambo hili na halafu nitakujulisha majibu yake.Nina uhakika hawezi kukataa jambo jema kama hili.Nakuhakikishia Melanie hata kama mke wa Rais wa Tanzania hatatuunga mkono katika jambo hilo mimi binafsi nitafanya kila njia ili wanawake hawa waweze kukaa meza moja” “Nitashukuru sana balozi kama utalifanikisha hilo na kama nilivyokuahidi kwamba baada ya kufanikisha jambo hilo mimi nawe tutapata nafasi nzuri ya kupongezana” akasema Melanie “Tunaweza kuanza kupongezana kwani jambo hili hesabu limekwisha na limefanikiwa” akasema balozi Mapupu na Melanie akatabasamu “Kwa leo haitawezekana mheshimiwa balozi.Vuta subira hadi hapo tutakapofanikisha jambo hili kubwa” “Kuna mtu yeyote anakuja hapa kwako usiku huu? “Hakuna yeyote anayekuja” “Kwa nini basi tusipongezane kwa kuanzisha urafiki huu mkubwa? Niruhusu mimi nikupongeze kwa kunipa wazo zuri kabisa ambalo hata mimi sikuwa nalo” akasema balozi Mapupu “Usijali Mr Mapupu.Tutapata wasaa mzuri zaidi wa kupongezana baada ya kumaliza shughuli hiyo muhimu.Isitoshe kwa siku ya leo sitaki kuchoka kwani kesho nina safari ya Dubai” “Unakwenda Dubai? “Ndiyo.Ninakwenda kuhudhuria kikao cha biashara” “Utatumia siku ngapi huko? “Siku mbili nitakuwa nimerejea nyumbani” “Utakaporudi uwasiliane nami ili nikupe mrejesho” “Nitafanya hivyo balozi”akasema Melanie “Hata hivyo kuna kitu nataka kukuomba Mr Mapupu” “Omba chochote Melanie” “Sitaki kujulikana kama nimejitolea kugharamia jambo hili.Naomba uhusika wangu uwe wa siri.Nitagharamia kila kitu lakini nataka ionekane wewe ndiye uliyegharamia kwa fedha zako” akasema Melanie “Kwa nini hutaki kutambulika kama sehemu ya mafanikio makubwa yatakayopatikana? ‘Sipendi sana kujulikana na isitoshe nataka sifa zote zije kwako Mr Mapupu” akasema Melanie “Basi usihofu.Nitalizingatia ombi lako.Hakuna atakayejua kama wewe ndiye uliyefanikisha kila kitu” Waliendelea na mazungumzo hadi ilipofika saa tano za usiku balozi Mapupu akaondoka.. “Ameongozeka Millen Kelelo.Balozi yuko sahihi kumtumia Millen kuwakutanisha wanawake hao wawili.Naamini Millen akiwaalika katika chakula usiku huo hakuna anayeweza kukataa.Kama Millen atahudhuria sherehe hiyo lazima naye awe miongoni mwa watakaouawa.Yatakuwa ni mauaji makubwa yatakayoibua mzozo mkubwa ndanio ya jumuiya ya Afrika Mashariki.Taratibu itaanza kumeguka.Marais Fabian Kelelo na Patrice Eyenga watapata uchungu usioelezeka.Machozi yangu ninayomwaga kila siku kuwalilia wazazi wangu yataondoka na wengi” akawaza Melanie RIYADH – SAUDI ARABIA Karibu watu wote waliohuduhuria mazishi ya Edger Kaka walikwisha ondoka na waliobaki ni familia ya Habiba Jawad.Sayid Omar ambaye alikuwa na pilika pilika sana siku hii akamfuata Mathew aliyekuwa amekaa na watu wengine wakicheza karata akamtaka amfuate “Samahani sana Abu Zalawi usione kama tumekuacha peke yako ni kutokana na heka heka nyingi siku ya leo.Kama unavyoona wageni wanakuja na kuondoka na mimi ndiye ninayewapokea wote” “Usijali Sayid Omar ninaelewa.Pole sana kwa jukumu hilo gumu” akasema Mathew “Habiba anataka kuzungumza nawe.Hakuweza kupata nafasi ya kuzungumza nawe mchana kutokana na kutingwa sana” akasema Sayid Omar na kumpeleka Mathew katika nyumba alimo Habiba Jawad.Alikuwa katika chumba kimoja cha ukubwa wa wastani akiwa na akina mama wengine watano waliokuwa wakimsaidia.Sayid Omar na Mathew walipoingia Habiba akawataka wale akina mama waliokuwa naye watoke anataka kufanya mazungumzo “Karibu sana Abu Zalawi” akasema Habiba Jawad “Ahsante mama.Pole sana” akasema Mathew na kupiga magoti akamsalimu Habiba kwa adabu. “Sayid waambie watuandalie bustanini.Mimi hupenda sana kufanya mazungumzo bustanini” akaelekeza Habiba na Sayid akatoka “Sikupata muda wa kuzungumza nawe kutokana na wageni wengi waliokuwa wakija na kuondoka.Uliowaona leo ni watu wachache tu waliofahamu na wengine sijui wamefahamu vipi,suala hili niliwaeleza watu wachache sana nashangaa taarifa zilivyosambaa lakini nawashukuru wote waliofika kwa mapenzi mema na kunisaidia kumhifadhi mwanangu kwa heshima zote.Mfalme wa Saudi Arabia alitaka kuja mwenyewe lakini nilimwambia anaweza akatuma mwakilishi akamtuma mwanae.Mfalme wa Jordan naye ananilaumu sana kwa kutomjulisha jambo hili.Kwa ufupi ….” Habiba akanyamaza baada ya mtu mmoja kuingia mle ndani akamjulisha kwamba tayari bustanini kumeandaliwa. “Abu twende tukakae bustanini tuzungumze mimi hupenda sana kuzungumzia bustanini” akasema Habiba wakatoka na kuelekea bustanini kulikokuwa na sehemu maalum ambayo Habiba hupenda kupumzika kila jioni. “Mathew Mulumbi” akasema Habiba “Naam mama” akaitika Mathew “Nitakuita kwa jina lako pale tukapokuwa wawili tu tena sehemu kama hii ambako hakuna ambaye anasikiliza maongezi yetu.Ukiacha Nawal ni mimi pekee ambaye ninafahamu wewe ni nani.Tukiwa katika maisha ya kawaida utaendelea na jina lako la Abu Zalawi na ndilo utakalotumia katika maisha yako yote utakayoishi hapa” akasema Habiba na ukimya ukapita “Mathew kwanza kabisa napenda nikushukuru sana kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kuniletea mwanangu.Nimelia sana lakini nimefurahi kuweza kumzika mwanangu mimi mwenyewe kwani kule Israel angezikwa kama mzoga.Ahsante sana kwa hilo.Mimi na familia yangu yote tumefurahi sana na kwa niaba yao nakushukuru sana.” Akasema Habiba “Naamini haikuwa rahisi kuuleta mwili wa Seif lakini umepambana na ukafanikiwa kuufikisha hapa nyumbani.Mossad waliuwekea mwili ule kifaa maalum cha kuwawezesha kuufuatilia na kujua unaelekea wapi.Wewe pia uliwekewa kifaa katika mkono wako wa kushoto hapo mahala penye jeraha.Nilikuwa na taarifa hizi kabla hata hujaondoka Israel.Nilifahamu kila ulichowaeleza Mossad katika kikao mlichojadili kuhusu kuutumia mwili wa Edger Kaka kufahamu mahala nilipo” akasema Habiba na kucheka kidogo. “Nimefurahishwa sana na kile ulichokifanya.Ngoja nikuweke wazi Mathew kwamba huu ulikuwa ni mtihani wako wa kwanza na umefaulu.Kwanza kwa namna ulivyowashawishi viongozi wa Mossad na wakakuelewa wakakupa mwili wa Seif,pili ni namna ulivyoweza kupambana hadi ukafanikiwa kuondoa kifaa kile katika mwili wa Seif.Nimekwambia kwamba nilifahamu kuhusu kifaa kilichowekwa katika mwili wa Seif na nilitaka kuona ungefanya nini.Je ungekubali mwili ule wa Edger uje na kifaa kile na kuwapa nafasi Mossad ya kufahamu mahala nilipo? Hukuacha hilo litokee na ukapambana kuhakikisha unakiondoa kile kifaa.Endapo ungechagua kushirikiana na Mossad basi ungekuwa ni mwisho wako kwani usingefika kokote.Umewasaliti wenzako waliokuamini kwa ajili yangu.Hili ni jambo kubwa sana umelifanya.Umeweka mbele maisha yako kwa ajili yangu na kuhakikisha mwili wa Seif unafika nyumbani ukiwa safi na salama.Ahsante sana kwa hilo. Wewe ni mtu mahiri sana.Umeiva katika kazi yako.Ni majasusi wachache sana wanaofikia uwezo wako” akasema Habiba na Mathew alihisi fulana yake aliyoivaa ndani ikiloa jasho. “Huyu mama anazidi kunichosha.Kama ameweza kufahamu kila nilichozungumza na Mossad ni mtu wa namna gani huyu?Ni binadamu wa kawaida kweli huyu? Ninajiuliza kwa sababu mambo yake yananishangaza sana.Au anatumia nguvu za giza?Mathew akajiuliza maswali “Mathew nataka kufahamu kwa nini uliamua kufanya vile ulivyofanya? Nakuuliza hivyo kwa sababu umepita njia ngumu sana hadi kunifikia.Ulikubali kufanya jambo la hatari sana la kumtorosha Ammar Nazari gerezani na ukajiunga na kundi lake yote hiyo ikiwa ni kwa ajili ya kutafuta njia ya kufika kwangu.Nafahamu maisha ndani ya Ammar Nazari brigades hayakuwa rahisi na kama hitoshi bado ukaenda kulipua lile bomu kule Israel na kuua watu.Yote hii ni katika kuhakikisha unatengeneza mazingira ya kuweza kufika mahala nilipo.Umelipa gharama kubwa sana kufika hapa ulipofika.Ulikuwa na uwezo wa kuwaeleza Mossad kila kitu kuhusu mimi na namna wanavyoweza kunifikia lakini hukufanya hivyo.Ilikuwa ni nafasi yako ya dhahabu kuhitimisha misheni yako lakini hukufanya hivyo badala yake ukawapa taarifa za uongo kuhusu mimi na wakakuamini.Kwa nini ulifanya hivyo? Akauliza Habiba.Ilimchukua Mathew muda kidogo kutafakari kisha akasema “Hata mimi sielewi kwa nini nilifanya vile” akasema Mathew na Habiba akatabasamu kwa mbali.Kimya kifupi kikapita halafu Habiba akasema “Mathew ngoja nikufahamishe kitu kimoja cha muhimu.Hukuweza kufanya hivyo kwa sababu hapa ndipo mahala unapotakiwa kuwepo.You belong here ! akasema Habiba na Mathew akatoa kicheko. “Unanifurahisha mama.Hapa ndipo sehemu ninapotakiwa kuwa? This is not my place.I don’t belong to terrorists” akasema Mathew “Mathew bado una mengi ya kujifunza” akasema Habiba. “Nini hasa unakitafuta kwangu mama Habiba?akauliza Mathew “Ninachokitafuta kwako? Habiba akauliza “Ndiyo.Umenieleza namna nilivyopita njia ngumu kwa ajili ya kutaka kufika kwako na lengo langu likiwa moja tu kukuua.Kama ulilifahamu lengo langu na ulikuwa na uwezo wa kuniua kwa nini hukuniua?Kwa nini ukanikaribisha mimi adui yako katika makazi yako?Una uhakika gani kwamba sintabadilika kesho na kukuua? Akauliza Mathew na Habiba akacheka kidogo “Sikuelekeza uuawe kwa sababu ninafahamu hapa ndipo mahala unapotakiwa uwe.Kuhusu kuniua huwezi kufanya hivyo si leo,kesho wala kesho kutwa.Sikiliza Mathew nimempoteza mtoto wangu wa kwanza and I need you as my son” “Me ? “Yes you” akajibu Habiba “Hilo haliwezekani.Siwezi katu kuwa mtoto wako.Mimi siko katika dunia ya ugaidi” akasema Mathew “Unasema hivyo kwa sababu bado mambo mengi huyafahamu Mathew.Nataka nikufumbue macho yako na kukuonyesha dunia ambayo huifahamu.Kuna mambo makubwa ambayo huyajui na siku ukiyajua utashangaa hutaamini macho yako.Nitakupeleka huko.Nitayabadili maisha yako na utakuwa mtu mkubwa” “Sihitaji kuwa mtu mkubwa.Maisha niliyonayo sasa yananitosha” akasema Mathew “Haya si maisha yako Mathew.Maisha yako ni makubwa zaidi ya unavyofikiri.Kwa kuanzia…..” Habiba akanyamaza kidogo kupisha helkopta iliyopita maeneo yale na kusababisha kelele “Helkopta hii hufanya doria katika eneo hili kila siku kuhakikisha hakuna hatari yoyote.Hii pia ni salamu kutoka kwa mfalme” akasema Habiba na helkopta ilipopita akaendelea “Nilikuwa nakueleza kwamba utajiri wangu niliugawa katika sehemu nne.Kila mtoto wangu alikuwa na sehemu yake ya utajiri na sehemu moja ilikuwa ya kwangu.Seif ameondoka na sehemu yake ya utajiri haina mtu.Wewe utachukua sehemu yake.Utajiri wako wote uliopotea nakurejeshea” akasema Habiba “Mama najua nia yako ni nzuri sana lakini siwezi kulikubali jambo hilo.Siwezi kukubali kupata utajiri ambao sijui chanzo chake.Nina nguvu bado na nitaendelea kupambana kuhakikisha ninapata tena mali kutokana na jasho langu.Kukubali utajiri huo ni sawa na kukubali kuwa gaidi.Siwezi” akasema Mathew. “Watch your tongue son! Akasema Habiba kwa sauti ya ukali akachukua kichupa kidogo cha dawa ya mafua akakifugua akanusa halafu akasema “Nimejishusha kwako isiwe sababu ya kuzungumza nami vile utakavyo.Who do you think you are? Wakubwa wa dunia hii wananyenyekea wanapozungumza nami na wanaitafuta nafasi ya kukaa nami namna hii wanaikosa,kwa nini wewe umeipata halafu unakosa adabu? Akafoka Habiba “Samahani mama” akasema Mathew “Na iwe ni mara ya mwisho kuzungumza nami kama uko na vijana wenzio.Mtu unayezungumza naye laiti ungemfahamu hata kidogo tu ungezugumza naye ukiwa umelala chini kwa adabu ! “Nisamehe mama” akasema Mathew “Ninakupenda ndiyo maana ninazungumza nawe namna hii.Hata watoto wangu wa kuzaa mwenyewe sijawahi kukaa nao tukazungumza namna hii.Wananiogopa na kuzungmza nami kwa adabu kubwa” akasema Habiba tayari uso wake ulionyesha kukasirika “Nataka ubadilike.Jifunze kuwa na adabu.Niheshimu sana kwani mimi ndiye ambaye nitayabadili maisha yako.Habiba Jawad hajui jibu hapana.Neno langu ni amri ! Umenisikia?akauliza Habiba kwa ukali “Ndiyo mama” akajibu Mathew na ukimywa wa dakika mbili ukapita “I’m sorry sikutarajia kuwa mkali na si tabia yangu kuwa mkali hadi pale ninapokorofishwa.Mathew hukuzaliwa hapa lakini wewe ni wa hapa.You belong here.This is your home.I’m not your biological mother but from now on I’m going to be your mother.Hili si ombi hii ni amri .Umenielewa Mathew?akauliza Habiba jawad “Nimekuelewa mama” “Ahsante” akajibu Habiba na ukimya ukatawala.Baada ya muda akasema “Kesho unakwenda Dubai” akasema na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Utaambatana na Najma.Anakwenda kuniwakilisha katika mazungumzo muhimu.Utahudhuria mazungumzo hayo lakini hupaswi kuchangia chochote.Tazama jifunze hadi wakati wako utakapofika.Najma atazungumza badala yangu.Bado tuna majonzi lakini kazi haziwezi kusimama.Maisha lazima yaendelee kwani hata tukisimamisha kila kitu Seif hatarejea” akasema Habiba na kunyamaza baada ya dakika mbili akasema “Tayari kila kitu kimekwisha andaliwa kwa ajili ya safari kesho asubuhi.Mtaondoka na ndege binafsi kuelekea Dubai.Mtapumzika kwa muda wa wiki moja ndipo mtarejea.Nimefanya hivi ili wewe na Najma muweze kupata muda mzuri wa kufahamiana” akasema Habiba na kukaa tena kimya “Mathew ninayafanya haya kwa faida yako mwenyewe.Siku moja utanishukuru kwa haya ninayoyafanya hivyo nakuomba usikasirike wala kuniona mkatili.Kitu kikubwa ambacho ninaendelea kukusisitiza ni kuwa mwangalifu.Mimi nina macho mawili lakini yanatazama kila sehemu.Nina masikio mawili lakini yanasikia mambo mengi hivyo usijaribu kufanya jambo lolote la kipuuzi.Nadhani umenielewa vizuri” akasema Habiba “Nimekuelewa mama” akasema Mathew “Vizuri.Kuhusu Nawal bado ataendelea kusubiri taratibu za dini zikamilike kwani mwanamke ambaye amefiwa na mumewe kwa taratibu za dini yetu atakaa eda kwa miezi minne na siku kumi ndipo atakapoolewa tena” akasema Habiba “Mama Habiba samahani sana kwa hiki ninachotaka kuuliza lakini sina nina mbaya” akasema Mathew “Uliza usihofu” “Mimi na Nawal unatufahamu vyema.Sisi si waislamu lakini tumejiingiza huku katika uislamu kutokana na hizi kazi zetu lak…………”akasema Mathew na Habiba akamkatisha “Nalifahamu hilo na hiyo ni siri yetu mimi na ninyi hadi kuingia kaburini.Sijali kuhusu imani zenu kwani Mungu tunayemuabudu ni Yule Yule mmoja lakini kwa kuwa mmekwisha ingia kwenye uislamu basi mtaendelea kuwa waislamu.Ninakachokueleza hapa ndicho nitakachomueleza Nawal. Umenielewa Mathew? Akauliza Habiba “Nimekuelewa mama” akajibu Mathew “Vizuri sana.Sasa nenda kapumzike tutazunguza utakaporejea kutoka Dubai” akasema Habiba huku akiinuka.Mathew naye akainuka wakaanza kuondoka pale bustanini “Mathew usiwe na wasi wasi kuhusu Najma.Ninaamini utampenda” akasema Habiba huku akitabasamu Walirejea ndani na kupata chakula kisha Habiba akampeleka Mathew kupumzika katika nyumba moja ya ghorofa mbili.Ilikuwa ni nyumba nzuri sana yenye samani za kuvutia mno iliyojengwa juu ya kilima. “Hii ni nyumba ambayo niliijenga maalum kwa ajili ya Seif kwa bahati mbaya hajawahi kuingia hata ndani.Kuanzia sasa nyumba hii ni yako kama nilivyokwambia kwamba kila kilichokuwa cha Seif kitakuwa chako” akasema Habiba “Nashukuru sana mama” akasema Mathew na Habiba akamuonyesha sehemu mbali mbali za nyumba ile kisha akamuacha apumzike.Mathew akaenda katika kioo akajitazama. “Huyu ninayemuona katika kioo ndiye Yule Mathew Mulumbi ambaye alikula kiapo cha kumuua Habiba Jawad? Nini kimemtokea? Akajiuliza na kwenda kukaa kitandani “Nini kimenitokea? Nimepitia mchakato mgumu hadi kumfikia Habiba lakini baada ya kumuona mipango yangu yote imeyeyuka kama mshumaa.Nimekutana ana kwa ana na mfahdili mkuu wa ugaidi duniani.Nimekosa ujasiri nimejikuta nikikubali kila anachonieleza.Nimepewa sehemu ya utajiri wa Edger Kaka na hii inanihalalisha kwamba mimi tayari nimeingia katika mtandao wa kigaidi.Sifahamu Yule mwanamke ana nguvu gani kwani ukiwa karibu yake unajikuta ukikubali kila unachoelezwa” akaendelea kuwaza kisha akasimama “No ! This is not me.This is not Mathew Mulumbi I know. Mathew Mulumbi katu hawezi kuwa gaidi.This isn’t over.Natakiwa kuendelea na misheni yangu ya kumuua Habiba Jawad.I m ust kill her ! akawaza na kugonganisha mikono kwa hasira “Lazima nikiri nimeteleza baada ya kuonana na Habiba lakini siwezi kuanguka na kulala hapo hapo lazima niinuke na niendelee na misheni yangu.Hata kama itanichukua miaka kutimiza misheni yangu lakini lazima nihakikishe nimeitimiza.Kwa sasa suala hili limekwisha kuwa kubwa tofauti na nilivyotegemea.Natakiwa kutumia akili kubwa sana kujipanga.Nitaendelea kujifanya mjinga huku nikiendelea kujipanga taratibu.Bado hawajamfahamu vizuri Mathew Mulumbi”akaendelea kuwaza. “Siku ilikuwa ndefu sana.Napaswa kupumzisha kichwa changu.Bado nina safari ndefu” akawaza na kujilaza
Mathew aliamshwa saa moja za asubuhi na mtumishi aliyekuwa ameambatana na watu wengine wawili ambao walijitambulisha kama wataalamu wa mitindo na waliokwenda kumuandaa Mathew kwa ajili ya safari ya Dubai.Bila kupoteza muda wataalamu wale wakaanza kazi yao ya kumuandaa Mathew.Kwanza walianza kwa kumpima halafu mmoja akaondoka na mwingine akaendelea na kazi.Baada ya nusu saa Yule jamaa aliyeondoka akarejea akiwa na masanduku mawili makubwa yaliyokuwa yamesheheni nguo.Zilikuwa ni suti za gharama kubwa na nguo nyingine pamoja na viatu. Saa moja ilimalizika na Mathew akawa tayari.Alipojitazama kwenye kioo akatabasamu. “Hii dunia ina maajabu sana.Jana nilikuwa mtu niliyechakaa nisiye na mwonekano wowote lakini tazama leo hii mwonekano wangu umebadilika kabisa nimerudia mwonekano wangu wa awali na hata zaidi.Dah ! wamenikumbusha mbali sana hawa jamaa” akawaza Mathew na mmoja wa wale jamaa akamuuliza kama ameridhika na mwonekano wake na Mathew hakuwa na tatizo lolote. “Kwa mujibu wa maelekezo niliyopewa nitaambatana nawe Dubai kwa ajili ya kuhakikisha kila siku unakuwa katika mwonekano nadhifu kabisa” akasema mmoja wa wale wanamitindo Muhudumu akamchukua Mathew na kumpeleka kwa Habiba Jawad ambaye naye alipatwa na mshangao baada ya kumuona Mathew “Abu Zalawi umebadlika kiasi hata mimi nimetaka kukupotea” akasema Habiba na kusalimiana na Mathew kisha wakajumuika katika kifungua kinywa.Sayid Omar naye akafika na kujiunga nao kila mmoja aliustaajabia muonekano mzuri wa Mathew.Wakati wakiendelea kupata kifungu akinywa akaingia mwanamke mmoja mrefu kidogo aliyejitanda nguo ndefu hadi miguuni na ushungi uliofunika nywele zake.Macho yake aliyafunika kwa miwani kubwa myeusi. “Huyu lazima atakuwa ndiye Najma.Amefanana na Habiba Jawad.Pamoja na mavazi haya aliyoyavaa ya kufunika mwili wote lakini ni mzuri.Huyu ndiye ninayetakiwa kumuoa.” Akawaza Mathew na kugonganisha macho na Habiba,Mathew akatabasamu.Habiba akatoa salamu kwa wote waliokuwepo pale mezani kisha akavuta kiti akaketi “Kila kitu tayari? Akauliza Habiba “Ndiyo mama kila kitu tayari” akajibu Yule msichana. “Abu Zalawi kutana na Najma” akasema Habiba “Najma huyu ndiye Abu Zalawi” Habiba akaendelea na utambulisho “Karibu sana Abu Zalawi nafurahi kukufahamu”akasema Najma “Mtapata nafasi nzuri ya kuzungumza na kufahamiana pale mtakapokuwa Dubai” akasema Habiba.Nadya akamuomba mama yake wakazungumze pembeni pale mezani wakabaki Mathew na Sayid Omar “Abu Zalawi itumie vyema nafasi ya Dubai kuwa karibu sana na Najma.Ni mwanamke mwenye sifa zote na mpaka sasa hana mwanaume yeyote” akasema Sayid Omar huku akitabasamu.Mathew hakujibu kitu akatabasamu Najma alimaliza mazungumzo na mama yake wakarejea katika chumba cha chakula. “Abu Zalawi muda umefika twende tuondoke” akasema Najma.Mathew akaagana na Habiba na Sayid akaungana na Najma wakaelekea nje kulikokuwa na gari wakaondoka kuelekea katika uwanja wa ndege.Najma alikuwa ameongozana pia na wanawake wengine wawili katika safari ile.Uwanja wa ndege waliokuwa wanaelekea ni ule ambao walitua na ndege ya Rayan Jaber wakati wakiurejesha mwili wa Edger Kaka kutoka Israel. Habiba Jawad na familia yake walimiliki ndege kadhaa kubwa na ndogo na asubuhi hii zilikuwepo uwanjani ndege tatu.Baada ya kushuka katika magari Najma akasalimiana na jamaa wengine wanne waliokuwa wamevalia kanzu zao nzuri na baada ya maongezi mafupi yaliyochukua kama dakika kumi hivi Najma akawaongoza watu wale wakapanda ndege ile ya kifahari ya Habiba Jawad na safari ya Dubai ikaanza.Kutoka Riyadh hadi Dubai walitegemea kutumia saa mbili na nusu kutokana na mwendo mkali wa ile ndege.Ndani ya ndege Najma alikuwa na mazungumzo na wale jamaa wanne waliowakuta uwanja wa ndege.Mathew alikuwa peke yake katika sehemu maalum ambako hukaa Habiba Jawad kama akisafiri kwa kutumia ndege hii. “Mathew ngoja nikufahamishe kitu kimoja cha muhimu.Hukuweza kufanya hivyo kwa sababu hapa ndipo mahala unapotakiwa kuwepo.You belong here ! Mathew akayakumbuka maneno ya Habiba Jawad wakati wakizungumza jana usiku. “Je ni kweli hapa ndipo mahala ninapotakiwa kuwepo? Akajiuliza huku akipata juisi ya matunda “Sifahamu alimaanisha nini lakini yawezekana labda ninatakiwa kuwepo hapa katika ulimwengu huu wa magaidi ili niweze kuufahamu mtandao wao wote na namna wanavyoendesha shughuli zao.Yawezekana mimi ndiye nikasaidia dunia kupambana na ugaidi kwani hapa nilipo ndipo kitovu chake.Sasa nimeanza kupata picha kamili ni kweli ninatakiwa kuwepo mahali hapa.It’s true I belong here” akawaza Mathew na kuinua glasi yake ya kinywaji akanywa. “Wakubwa wa dunia hii wananyenyekea wanapoizungumza nami na wanaitafuta nafasi ya kukaa nami namna hii wanaikosa,kwa nini wewe umeipata halafu unakosa adabu? Akaendelea kukumbuka mazungumzo yao usiku uliopita “Alimaanisha nini kwa kauli yake hii kwamba wakubwa wa dunia hii wananyenyekea wanapozungumza naye?Ni wakubwa gani aliowamaanisha?Ni viogozi wa mitandao ya kigaidi au akina nani?akaendelea kujiuliza maswali “Kuna mengi ya kufahamu kwa Habiba Jawad.Kuna kauli moja alisema http://deusdeditmahunda.blogspot.com/”Nataka nikufumbue macho yako na kukuonyesha dunia ambayo huifahamu.Kuna mambo makubwa ambayo huyajui na siku ukiyajua utashangaa hutaamini macho yako.Nitakupeleka huko.Nitayabadili maisha yako na utakuwa mtu mkubwa” “Kitu ninachotakiwa kukifanya ni kuwa mvumilivu na nitafahamu mambo mengi kutoka kwa Habiba.Natakiwa kufaham…………….” “Hallo Abu” Sauti nzuri ya Najma ikamtoa Mathew Mawazoni “Samahani Abu Zalawi kwa kukuacha peke yako.Nilikuwa nawapa maelekezo wale wajumbe wangu” akasema Najma na kujimiminia kinywaji katika glasi kisha akaketi sofani akanywa funda moja na kutazama saa yake ya dhahabu mkononi “Tumebakiza dakika chache kutua Dubai.Naamini mama amekwisha kufahamisha kwamba tutakuwa hapo kwa muda wa wiki moja” akasema Najma “Ndiyo amekwisha nijulisha suala hilo” “Vizuri” akasema Najma na kabla hawajaendelea na maongezi akaja mtu mmoja akamuita Najma akatoka “Ni mwanamke mzuri sana.Ana umbo zuri,ana adabu na anaonekana ni mchapa kazi mzuri sana kiasi cha mama yake kumuamini kumtuma akamuwakilishe katika kikao hicho muhimu. Hapa ndipo ninapochanganyikiwa kwani yawezekana nikajikuta nikimpenda Najma na kusahau misheni yangu.” Akawaza Mathew na kutabasamu “Kwa namna yoyote ile lazima niikamilishe misheni yangu na ili kuikamilisha sina budi kumuoa Najma” akaendelea kuwaza Mathew huku akiyatafakari maisha yake alikotoka na alipo sasa. DUBAI Ndege ya akina Mathew ilitua jijini Dubai na baada ya kukamilisha taratibu wakatoka na kuingia katika magari maalum yaliyokuwa yakiwasubiri. “Jiji hili nilikuwa nikifika mara kwa mara kwa ajili ya biashara zangu” akawaza Mathew wakiwa garini.Walifikia katika hoteli moja yenye gharama za juu mno yenye hadhi ya kifalme. “Hoteli hii ninaifahamu ni hoteli yeye gharama za juu mno kuliko zote Dubai na wageni wake wengi ni wafanyabiashara mabilionea au viongozi wakuu wa nchi.Mimi na utajiri wangu niiokuwa nao sikuwahi kuthubutu kufikia hoteli kama hii” akawaza Mathew wakaingia katika chumba chao.Wahudumu wakapanga mabegi na Najma akatoa maelekezo kadhaa ya kufanyika mle chumbani.Kuna baadhi ya maua akaagiza yaletwe na alihitaji mwonekano Fulani ndani ya kile chumba. “Abu Zalawi hiki ndicho chumba ambacho tutakitumia kwa muda wa wiki nzima tutakayokuwa hapa Dubai.Nilikichagua mwenyewe,Unakionaje?Umekip enda? akauliza Najma “Ni chumba kizuri sana nimekipenda” “Kitu gani hasa unakipenda kiwepo katika chumba chako cha kulala?akauliza Najma “Kuwe na kitanda kizuri na godoro” akasema Mathew na Najma akacheka kidogo “Kitanda pekee? “Najma hutajali nikikuita Naj badala ya Najma?akauliza Mathew na Najma akatabasamu “Huyu mtoto anapenda kutabasamu kama mama yake” akawaza Mathew “Hakuna tatizo Abu niite upendavyo”akasema Najma “Ahsante.Naj naamini mama amekupa taarifa zangu kwamba ninatokea katika kundi la Ammari Nazari brigades ambalo limekuwa likiendesha mapigano na serikali ya Israel.Sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa katika ugaidi hivyo maisha yetu sisi ni ya shida ndiyo maana usishangae nikikwambia ninahitaji kitanda na godoro tu katika chumba changu cha kulala” akasema Mathew “Nalifahamu hilo Abu lakini maisha yale yamekwisha.Tayari umetoka huko na hautarudi tena.Hapa unaanza maisha mapya na utaishi kama mfalme ndiyo maana nimechagua hoteli hii kubwa na nzuri kwa ajili yako Abu.Nataka usahau tabu zote ulizowahi kupitia huko nyuma.Nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha unasahau yote na kuanza maisha mengine” “Nashukuru sana Naj” “Tutazungumza mengi lakini kwa sasa nataka twende tukafanye manunuzi ya vitu mbali mbali” akasema Najma “Naj ahsante sana lakini ninahitaji kupumzika.Nenda kafanye manunuzi utanikuta mimi hapa ninapumzika”akasema Mathw “Basi hakuna tatzo.Chochote ukihitaji utawajulisha hotelini watakuhudumia.Usihofu kuhusu usalama ni mkubwa sana mahala hapa” akasema Najma na kuondoka “Natamani ningekwenda na Najma kufanya manunuzi lakini ninaogopa.Watanzania ni wengi hapa Dubai na ninaweza kukutana na wanaonifahamu hasa Gosu Gosu ambaye huwa anakuja hapa Dubai mara kwa mara” Mathew alipomkumbuka Gosu Gosu akajikuta akitabasamu “Nimemkumbuka sana Gosu Gosu.Sijui kwa sasa atakuwa wapi.Je Peniela bado anaendelea kumtumia katika biashara au tayari naye ameendelea na maisha yake? Yawezekana naye tayari amekwisha nisahau na anaamini nimefariki dunia.Yule jamaa siwezi kumsahau katika maisha yangu.Alikuwa ni msaidizi wangu mkubwa.Ninashukuru sana kumfahamu.Kwa kule kwetu anaitwa Jembe.Ni mchapakazi mzuri,haogopi chochote lakini ni mtu hatari sana.Ni mwepesi mno kutoa uhai wa mtu nadhani ni kwa sababu ya maisha aliyopitia kwani kwa mujibu wa maelezo yake alichukuliwa na kundi la waasi angali akiwa mdogo akapelekwa msituni akaanza kufundishwa kupigana.Kuna nyakati hata mimi huwa ninamuogopa ninapokuwa naye katika misheni lakini ninachoshukuru ni kwamba kwangu mimi ana adabu sana.Ananiheshimu mno na hajawahi katu kunidharau au kupuuza chochote nilichomuelekeza.Gosu Gosu kwangu ni zaidi ya rafiki.Natamani sana kama ningekuwa naye huku kwa Habiba lakini angeweza kuharibu misheni Yule ana hasira za karibu sana.Ngoja tu niendelee mwenyewe naamini kama tunaendelea kuwa hai tutaonana siku moja”akawaza Mathew na kutabasamu “Siwezi kumkumbuka Gosu Gosu nikacha kumkumbuka Ruby.Sifahamu yuko wapi hivi sasa na anafanya nini.Sjui ni machozi kiasi gani alilia baada ya kupata taarifa kwamba nimefariki dunia.Ruby alinipenda mno na alinieleza wazi wazi namna anavyonipenda na anavyotaka kuwa na mimi katika mahusiano ya kimapenzi.Nimekuwa naye karibu kwa miaka mingi na amenisaidia sana katika misheni mbali mbali za hatari lakini mara zote nilipomuita hata katika misheni za hatari hakuwahi kusema hapa.Muda wowote nilipomuta aliitika ndiyo.Ruby ni mtu wa pekee kabisa kwangu. Kama nisingeingia katika matatizo haya na kufika huku niliko hivi sasa ningekuwa naye katika mahusiano.Tayari nilikwisha fanya maamuzi ya kuwa naye katika mahusiano ya siri kwani alikuwa tayari kuishi mahala kokote nitakakoishi kitu ambacho mke wangu Peniela hakuwa tayari kukifanya.Hakuwa tayari kuishi Tanzania lakini Ruby alikuwa tayari” akawaza na mwili ukamsisimka baada ya kukumbuka tukio la Ruby kupigwa risasi na Devotha “Nimekumbana na matukio mengi mabaya lakini lile la Ruby kupigwa risasi na Devotha ni tukio lililoniumiza sana na ninakumbuka nilifanya tukio moja baya ili kuokoa maisha ya Ruby.Sasa ndipo ninaamini kweli Ruby yuko moyoni mwangu.Maumivu niliyoyapata yalikuwa makubwa.Nilipanga baada ya sakata lile kumalizika ningekwenda naye sehemu tukatulie tupumzike na nilikuwa na mipango ya kuzaa naye mtoto mmoja au hata zaidi.Kwa bahati mbaya sana mpango huo haukufanikiwa.Sijui kama atakuwa ameolewa kwa sasa au bado? Daah ! sikutegemea kabisa maisha yangu kubadilika namna hii” akawaza Mathew DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa tatu za asubuhi balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nchini Tanzania Germinus Mapupu aliwasili katika jengo zilimo ofisi za mke wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Millen Kelelo.Alipokewa na wahudumu wa mapokezi na akaeleza shida yake ya kuonana na mke wa Rais.Kwa kuwa Millen hakuwa amefika bado akapigiwa simu na wale wahudumu na kujulishwa kwamba balozi Mapupu alikuwepo pale ofisini akihitaji kuonana naye.Millen akamtaka balozi Mapupu aendelee kusubiri atafika pale ndani ya kipindi kifupi. Saa nne na dakika ishirini mke wa Rais wa Tanzania Millen Kelelo akawasili katika ofisi zake.Siku hii alikuwa amevaa suti nzuri ya suruali ya rangi nyekundu.Alipendeza sana.Kisha shuka garini akaelekea ofisini akapita kuwasalimu watu wa mapokezi halafu akaelekea katika ofisi yake ambako alimkuta balozi Mapupu akimsubiri “Balozi Germinus” akasema Millen huku akitabasamu “Madam first lady” akasema balozi Mapupu wakasalimiana na kumkaribisha ofisini kwake “Karibu sana mheshimiwa balozi.Ungenijulisha kama unakuja ofisini kwangu leo ningewahi zaidi” “Usijali mama Kelelo.Nilikuwa na haki ya kusubiri kwa kuwa nimevamia bila taarifa” “Karibu sana” akasema “Madam first lady sitaki kuchukua muda wako mwingi lakini kuna suala la muhimu sana lililonileta hapa kwako” Akasema balozi Mapupu “Usijali mheshimiwa balozi tunao muda wa kutosha” akasema Millen “Kwanza kabisa napenda nikupongeze sana kwa kuandaa mkutano mkubwa utakaowakutanisha wake za marais wa dunia nzima.Rebeca Eyenga mke wa rais wa Congo naye tayari amekwisha thibitsha kushiriki.Kama unavyofahamu kwa muda wa miaka kadhaa hivi sasa mahusiano ya nchi yangu na Rwanda yamekuwa si mazuri sana.Nimefikiria kuutumia mkutano huo kama chanzo cha kutafuta amani kwa nchi zetu hizi mbili.Nimepanga kuandaa chakula maalum na kuwakaribisha mke wa Rais wa Congo na mke wa Rais wa Rwanda na huo utakuwa ni mwanzo wa kupatikana amani.Wanawake hawa wawili wakiweza kukaa meza moja wakazungumza nina uhakika mkubwa watawashawishi waume zao kuweka kando tofauti zao na amani itapatikana” “Hilo ni wazo zuri sana mheshimiwa balozi.Kama ukianza kuwakutanisha wanawake hawa wawili wakaelewana na wakaondoa tofauti zao basi uhakika wa marais wa Rwanda na Congo kumaliza vita yao ya maneno ni mkubwa sana.Nakupongeza sana mheshimiwa balozi kwa wazo hili zuri” akasema Millen “Madam Millen,ahsante kwa kulikubali ombi langu lakini nitahitaji msaada wako” akasema balozi Mapupu “Nikusaidie nini mheshimiwa balozi? “Kutokana na msuguano uliopo baina ya waume zao,upo ugumu wa kuwaleta wanawake hawa katika meza moja.Kumpata mke wa Rais wa Rwanda itakuwa ni kazi ngumu ndiyo maana nahitaji msaada wako” “Ni kweli hilo unalolisema mheshimiwa balozi.Nini unataka nikifanye? Akauliza Millen “Ninachokiomba kwako ni hiki.Mimi nitaandaa kila kitu lakini nitakukaribisha wewe na wewe ndiye utakayewakaribisha wanawake hao katika chakula.Utakaa nao meza moja na watajikuta wakizungumza na kuweka kando tofauti zao.Ninakuomba sana mama ukubali kunisaidia kwa hilo” akasema balozi Mapupu “Mimi sina tatizo kabisa na suala hilo.Ni suala jema sana ambalo lazima tuliunge mkono.Siwezi kukataa kusaidia katika suala hili.Hawa wote ni wageni wangu na ninakubali kuwaleta wote mezani.Nitakusaidia kwa hilo.Utanieleza namna ulivyopanga kulifanya hilo jambo ili na mimi nifanye maandalizi” “Nashukuru sana madam first lady.Nitakuja tena kukupa mrejesho wa namna ninavyoliandaa jambo hilo lakini narudia tena kukushukuru kwa kulikubali ombi langu.Hili ni jambo kubwa sana umelifanya kwa nchi yangu” akasema Balozi mapupu kisha akaagana na Millen akaondoka kwa miadi ya kurejea tena kumpa Millen mrejesho wa namna anavyoandaa chakula hicho cha pamoja cha wake za marais wa Congo na Rwanda DUBAI Saa kumi na mbili za jioni iliwakuta Najma na Mathew tayari wamekwishajiandaa kwenda kukutana na wageni wao ambao Mathew hakuwa amejulishwa wanatoka wapi na hakutaka kuuliza.Kikao kilipangwa kufanyika ndani ya hoteli ile ile waliyokuwa wamefikia.Wakiwa wameongozana na watu wengine wanne pamoja na walinzi wawili wakaingia katika ukumbi maalum wa mikutano unaoweza kuchukua watu kumi na tano.Wageni waliokuwa wanawasubiri hawakuwa wamefika na Najma akaomba wasubiri kidogo ndani ya dakika tano mlango ukagongwa mlinzi akaufungua na mwanamke mmoja mwenye umbo na uzuri wa kipekee kabisa akaingia.Wote mle ndani walikuwa kama wamepigwa na butwaa kwa sekunde chache.Ilikuwa ni kama waliona kitu cha kuwashangaza. “Huyu ndiye tunayemsubiri au amepotea njia?akajiuliza Mathew “Naamini sijakosea chumba” akasema Yule mgeni baada ya kuona namna watu wote mle chumbani walivyopigwa na butwaa wakimuangalia. “Hapana hujakosea chumba” akasema Najma ambaye jioni hii alikuwa amevaa suti nzuri nyeusi iliyomkaa vyema na kulionyesha umbo lake zuri “Karibu sana” akasema Najma na kusalimiana na Yule mwanamke mzuri akamkaribisha kiti “Karibu sana.Uko mwenyewe au kuna wengine wanakuja? Najma akauliza “Hakuna mwingine ni mimi mwenyewe”akasema Yule mwanamke mwenye uzuri wa kimalaika “Basi hakuna haja ya kupoteza muda tunaweza kuanza kikao chetu” akasema Najma “Sawa tunaweza kuendelea” akasema yule mwanamama “Kwanza tuanze kwa utambulisho.Mimi naitwa Najma Hanifnejad ndiye kiongozi wa jopo hili lililokuja kukutana nawe.Pembeni yangu anaitwa Abu Al Zalawi” akasema Najma na kuendelea kutambulisha watu wote alioongozana nao. “Ninashukuru sana kuwafahamu” akasema Yule mwanamke mrembo “Mimi ninaitwa Melanie Davis ninatokea Tanzania.Ni mwekezaji ambaye ninamiliki makampuni kadhaa makubwa.Nimefurahi sana kukutana nanyi” akasema Melanie “Hata sisi tumefurahi sana kukutana nawe Melanie.Naamini huu ni mwanzo mzuri wa mashirikiano makubwa baina yetu” akasema Najma.Mathew alihisi mwili wake ukitetemeka aliposikia Melanie akitaja kwamba ametokea Tanzania. “Abdallatif Al Hashimi naomba utufungulie kikao hiki kwa kutupa maelezo ya utangulizi” akasema Najma “Bismillahir Rahmnair Raheem” akasema Abdallatif “Jina langu ni Abdalatif Al Hashimi bin Abdul Aleem.Ninatoka IS kitengo cha fedha” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Kikundi cha IS kina mpango mkubwa wa kujiimarisha katika bara la Afrika na tumechagua eneo la Afrika Mashariki na kati kama sehemu muhimu kwa ajili ya kujenga kambi maalum ya kuandaa watu wetu na kuwapeleka katika mapambano sehemu mbali mbali duniani. Katika utafiti wetu tuligundua kwamba sehemu nzuri ambayo tunaweza kujenga kambi kubwa ya mafunzo ni katika misitu mikubwa ya jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo.Ili suala hilo liweze kufanikiwa ilitulazimu kuingia makubaliano ya mashirikiano na mtu anaitwa James Kasai ambaye anaongoza kundi la waasi waliotimuliwa huko Kivu ya Kaskazini nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kukimbilia Kaskazini mwa Uganda ambako yeye na kundi lake wamejificha msituni.Kwa sasa James na kikundi chake cha waasi wako katika hali mbaya ya kiuchumi kwani chanzo pekee cha fedha walichokuwa wanakitegemea ni biashara ya madini ambayo kwa sasa yanadhibitiwa na serikali.Tumekuwa na majadiliano na James na amekubali kushirikiana nasi na mambo yote ambayo tunayahitaji ameyakubali lakini ombi lake kubwa ni kupatiwa msaada wa fedha na vifaa vya kijeshi.James anataka kurejea tena msituni kupambana na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hivyo anahitaji silaha na zana za kisasa za kivita.Sisi tumemuahidi kumsaidia kwa kila kitu kumpatia fedha na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya kupambana na serikali ya DR Congo.Ugumu ulikuwepo njia yakuweza kumfikishia fedha kwani serikali nyingi hivi sasa ziko macho sana katika suala la usafirishaji wa fedha wakiogopa fedha za dawa za kulevya na fedha za kufadhili ugaidi.Hilo limetukwamisha kwa muda mrefu hadi pale James alipotufahamisha kwamba amekwisha pata mshirika ambaye tutapitishia kwake fedha ambaye ni wewe” akasema Abdallatif “Ni kweli mimi ndiye mshirika wa James Kasai na nimekuja hapa kama alivyowaeleza kuanza mchakato huo wa kifedha”akasema Melanie Davis na majadiliano yakaanza.Saa tatu za usiku kikao kilisimama kwa wajumbe kupata chakula cha usiku kisha kikao kikaendelea hadi saa tisa za usiku.Kila kitu kilitakiwa kumalizika usiku ule kwani asubuhi siku iliyofuata Melanie alitakiwa kuondoka kurejea Tanzania Kikao kilimalizika kwa mafanikio makubwa wakaagana na Melanie akaondoka kurejea hotelini alikofikia.Najma akampeleka Mathew chumbani kupumzika yeye akarejea kuendelea na kikao na wale wajumbe wa IS. “Chumba kilikuwa na ubaridi wa kutosha wa kiyoyozi lakini mwili wote umeloa jasho baada ya kushuhudia kwa macho yangu namna Habiba anavyofadhili ugaidi.IS wanataka kujiimarisha Afrika Mashariki na kati na wana mikakati mizito ya kuanzisha kambi kubwa ya mafunzo itakayokuwa ikifundsha ugaidi.Nimesisimkwa mwili kwa vile jambo hili linalofanyika ni lile ambalo nimekuwa nikipambana nalo kwa miaka mingi lakini leo hii nimekuwa mjumbe nikishuhudia kwa macho yangu kundi la kigaidi la IS likipokea ufadhili wa fedha nyingi kutoka kwa Habiba Jawad katika harakati zake za kujitanua na kujiimarisha katika eneo la Afrika Mashariki na kati.Magaidi ambao wanakwenda kuzalishwa katika kambi hiyo ya mafunzo wataua idadi kubwa ya watu duniani.Kama magaidi wakiwa na kambi yao ya mafunzo nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo basi eneo zima la Afrika Mashariki halitakuwa salama.Nimeshuhudia mikataba ya fedha na silaha ikifanyika ambayo inakwenda kumuimarisha huyo mtu anayeitwa James Kasai ambaye ndiye atakayewasaidia IS waweze kupata eneo la kujenga kambi ya mafunzo”Akawaza Mathew akiwa amevua shati akipata ubaridi “Kwa nini Habiba Jawad ametaka niyashuhudie haya? Nini anakitafuta kwangu?Huyu mwan…….” Mathew akastuka baada ya mlango kufunguliwa Najma akaingia.Haraka haraka Mathew akataka kuvaa fulana yake lakini Nadya akamzuia “Abu usivae kwanza hiyo fulana yako” akasema Najma na kumsogelea Mathew.Alipatwa na mshangao mkubwa alipouona mwili wa Mathew ukiwa na makovu mengi ya vidonda. “Nini kimekutokea Abu hadi ukawa katika hali hii? Akauliza “Usijali Naj haya ndiyo maisha yetu” akasema Mathew “Hapana hili si jambo la kawaida.Huu ni ukatili mkubwa uliopitiliza.Mwili wa binadamu hauwezi kuharibiwa namna hii na likaonekana jambo la kawaida” akasema Nadya huku akiukagua mwili wa Mathew “Nilifungwa Israel miaka mitatu nikiteswa kila uchao na makovu haya unayoyaona niliyapata huko.Haya majeraha mengine ambayo yameanza kupona niliyapata katika mchakato wa kufika kwa mama yako Habiba.Haikuwa rahisi kufika kwake ilinilazimu kupitia mateso makali” “Sikulifahamu hilo.Kwa nini umepitia mateso haya? Kwa nini uliteswa na Israel kwa muda huo wote wa miaka mitatu? Akauliza Najma “Nilimuua mkuu wa Mossad ukanda wa Afrika Mashariki na ndipo nilipokamatwa na Israel na kufungwa kwa miaka mitatu nikiteswa na baadae nikiwa gerezani nikafahamiana na Ammar nazazi mkuu wa kikundi cha Ammar Nazari brigades,tukafanya mpango na tukatoroka gerezani nikaenda kujiunga naye na kuendelea mapambano dhidi ya Israel.Hivi majuzi Israel walifahamu maficho ya Ammar wakatuvamia.Kwa bahati nzuri niliwahi kumtorosha Nawal lakini wengine wote waliuawa.Baada ya kunusurika katika mashambulio yale nilihitaji kumuona Habiba ili kumpa taarifa za mwanae Seif ambaye nilikuwa nafahamu mahala alipo na ndipo iliponilazimu kuyapitia haya niliyoyapitia ili kufika kwake” “Pole sana Abu Zalawi kwa haya uliyoyapitia.Hukupaswa kupitia mateso haya lakini kuanzia sasa hutapitia tena mateso kama haya” akasema Najma na kuanza kulia. “Nyamaza kulia Najma.Haya ni maisha yangu ya kawaida nimeyazoea” akasema Mathew akimbembeleza “Sikujua kama umepitia haya kufika kwetu” akasema Najma akiendelea kulia “Haya ni maigizo au nini?.Analia kwa kuona vidonda mwilini mwangu kwa nini halii kwa watu wanaopoteza maisha kwa kuuawa na makundi ya ugaidi wanayoyafadhili? Muda mfupi uliopita ameweka sahihi kiasi kikubwa cha fedha kilipwe kwa James Kasai ambaye atazitumia fedha hizi kwa mauaji,haya ni maigizo tu” akawaza Mathew akimtazama Najma akilia “Naj nyamza usiendelee kulia.Haya yamekwisha pita na itabaki ni kumbu kumbu yangu hivyo yasikuumize sana”akasema Mathew na kuchukua kitambaa akamfuta machozi “Abu Zalawi nikufanyie kitu gani uwe na furaha katika maisha yako na usahau mambo hayo magumu uliyoyapitia?Niambie chochote unachokitaka nitakufanyia ili uwe na furaha.Naamini kwa haya uliyoyapitia hutakuwa na furaha kamwe katika maisha yako” akasema Najma.Mathew akamfuta machozi na kushika mikono akamtaka ainuke wakaenda sofani.Mathew akamtazama Najma usoni na kusema “Naj sihitaji kitu chochote.Pole uliyonipa inatosha sana” akajibu Mathew na ukimya ukapita halafu Najma akasema “Sijawahi kuwa na mwanaume katika maisha yangu nina maanisha mpenzi.Hilo limewafanya watu wajiulize maswali mengi sana kuhusu mimi kwa nini sitaki kuwa na mpenzi?Hata mimi sifahamu ni kwa nini hali ile imenitokea lakini nimejikuta tu sitaki kuwa na mwanaume yeyote katika mahusiano ya kimapenzi.Mama amewahi kuniuliza mara kadhaa kwamba kwa nini sitaki kuwa na mwanaume nikamjibu hata mimi sifahamu kwa nini.Moyoni niliamini kwamba maisha yangu nitakuwa mwenyewe na sintahitaji mwanaume yeyote” akanyamaza na kufuta machozi “Kwa nini mwanamke mzuri kama wewe Naj hutaki kuwa na mpenzi? U mzuri wa sura na umbo na ninaamini wapo wanaume wengi wanakupenda na huko waliko wanaomba siku moja wapate bahati ya kuwa nawe”akauliza Mathew “Hata mimi sifahamu Abu nini kimenitokea lakini nimejikuta nikiwa hivyo” akajibu Najma na kukaa kimya kidogo halafu akaendelea “Baba yangu anatokea nchini Iran” akasema na kunyamaza kidogo “Nimeishi naye kwa muda mrefu hadi nilipomaliza masomo yangu ya udaktari nchini Urusi ndipo nilipoamua kuhamia Saudi Arabia kwa mama.Kilichoniondoa Iran ni kijana mmoja ambaye alikuwa ananifuatilia mno akinitaka tuwe wapenzi kitu ambacho sikuwa tayari.Hata baba yangu alikuwa akimfahamu kwani ni mtoto wa tajiri mwenzake.Niliamua kuja huku kujiepusha na kero za kijana huyo.Nashukuru kwa hapa Saudi kidogo wananielewa kwamba sipendi mahusiano ya kimapenzi” akasema Najma na kunyamaza kwa sekunde chache hakutaka kumtazama Mathew usoni. “Hivi majuzi mama aliniita na kunieleza kwamba anafahamu sihitaji mahusiano ya kimapenzi lakini kuna mtu mmoja atakuja ambaye anaamini anaweza akanifaa.Alinieleza kila kitu kuhusu Abu Zalawi na nikajikuta nikimfahamu kabla hata sijamtia machoni.Mama alikiri kwamba yeye binafsi anampenda na angependa awe sehemu ya familia yetu.Alinitaka nijaribu japo kwa mara ya kwanza kuingia katika mahusiano na kama nikishindwa basi hatanishawishi tena kuingia katika mahusiano yoyote.Sifahamu nini kilinitokea lakini nilijikuta nikimkubalia mama kwamba nitajaribu.Hata yeye binafsi hakuamini nilipompa jibu lile kwamba nitajaribu kuingia katika mahusiano na Abu Zalawi.Sifahamu kama kuna nguvu yoyote ambayo mama aliitumia kunishawishi lakini nilijikuta nikikubali kuingia katika mahusiano na mtu ambaye sijawahi kumtia machoni pangu.Inashangaza sana” akasema Najma na kutoa kicheko kidogo halafu akaendelea. “Mara ya kwanza kukuona kwa macho yangu mawili ni leo asubuhi kabla ya kuondoka kuja huku.Nilistuka nilipokuona.Sifahamu sababu ya mstuko ule lakini nilistuka sana.Nilihsi kitu cha tofauti kinanitokea.Kwa mara ya kwanza nilihisi mwili unanisisimka baada ya kumuona mwanaume.Abu Zalawi umekuwa ni mwanaume wa kwanza kunisisimua na kwa mara ya kwanza najihisi kupenda na kutaka kuingia katika mahusiano” akasema Najma na kunyamaza kidogo akatazama chini kama vile anaona aibu “Nilipoona mgongo wako nilistuka kwa namna ulivyochafuliwa na makovu na vidonda.Toka ndani ya moyo wangu nimeumia sana kukuona ukiwa katika hali hii.Naamini haya uliyoyapitia yataendelea kukutesa ndani ya moyo wako kwa miaka mingi ndiyo maana ninataka nifanye kila lililo ndani ya uwezo wangu kukufanya uwe na furaha.Abu Zalawi naomba nikiri kwako kwamba toka ndani kabisa ya moyo wangu niko tayari kuwa na mahusiano nawe.Umenigusa moyo wangu kwa namna ya ajabu” akasema Najma na kunyamaza akatazama chini kwa muda halafu akainua kichwa akamtazama Mathew “Abu yawezekana ikawa vigumu kwako kuufungua moyo wako kwangu na nitalipokea hilo lakini niruhusu japo niwe sehemu ya maisha yako.Niruhusu nikupe furaha ya maisha.Niruhusu nikusahaulishe maisha yako ya nyuma uliyopitia mateso mengi.Nataka nikupe pumziko” akasema Najma kwa hisia kali sana “Dah ! huyu mtoto anaongea kwa hisia kali mpaka ninasisimka mwili” akawaza Mathew “Abu Zalawi sisi ni matajiri wakubwa.Tuna fedha nyingi mno lakini nakuhakikishia kwamba sintatumia utajiri tulionao kukunyanyasa.Siku zote nitakuwa chini yako,nitakuwa mnyenyekevu kwako,nitaitika haraka kila pale utakaponiita,nitakuwa mwepesi kuomba msamaha kila pale nitakapokosea,katu sintasimama kujibizana nawe na neno lako ni amri kwangu kwani wewe utakuwa ni mfalme nami kijakazi wako” akasema Najma “Maneno mazito sana haya ameyatamka Naj na anaonekana anamaanisha anachokisema” akawaza Mathew “Najma huna sababu ya kuendelea kulia.Maneno uliyoyatamka ni mazito na yamenigusa hadi ndani ya moyo wangu.Ni nadra sana kwa dunia ya sasa kumpata mwanamke wa aina yako ambaye anaogelea katika utajiri na akatamka maneno mazito kama hayo uliyonitamkia.Naweza kusema nina bahati ya kipekee kwanza kuwa mwanaume wa kwanza ambaye nimeugusa moyo wako hadi ukaamua kubadili msimamo wako na kujikuta ukitamani kuingia katika mahusiano.Pili ninajiona mwenye bahati sana kutamkiwa maneno kama hayo ya unyenyekevu mkubwa mimi ambaye sina mbele wala nyuma” akasema Mathew “Usiseme hivyo Abu.Moyo wangu unaumia sana kwa maisha magumu uliyopitia” akasema Najma “Huo ndio ukweli Naj ambao siwezi kuona haya kuusema.Mimi ni masikini hohehahe na ninamshukuru sana mama Habiba kwa kuguswa na maisha yangu na kuamua kunisaidia kuyaanza maisha mapya.Kama alivyokushauri wewe kufikiria kama unaweza ukaanzisha mahusiano nami ndivyo alivyonishauri na mimi kufikiria kama ninaweza kuanzisha mahusiano nawe na hatimaye tukafunga ndoa na kuishi kwa furaha na amani.Sifahamu kitu gani mama amekiona kwetu na kuhisi tunaweza tukaendana hadi akatushauri tuanzishe mahusiano.Naamini kuna kitu amekiona kwetu na mimi ni nani wa kumpinga? Siwezi kukataa japo itatuchukua muda kwa kila mmoja kumfahamu vyema mwenzake yukoje kwani mimi nina mapugufu yangu nawe pia unayo yako lakini kama kweli tukiamua tuwe na furaha na amani basi hakuna kitakachoshindikana” akasema Mathew “Abu Zalawi ni hicho tu ambacho nilitaka kukisikia kutoka kwako.Kuhusu madhaifu hayo ni ya kawaida nitayabeba yote na kuyavumilia.Nataka unihakikishie je lile ombi la mama la kutaka mimi na wewe tuoane unalikubali?Usikubali tu kwa vile mama amekushauri lakini usikie moyo wako unakuambia nini.Usishinikizwe na mtu yeyote.Kama hauko tayari kwa hilo nitaelewa.Niambie ukweli tafadhali” akasema Najma.Mathew akamtazama na kutabasamu kidogo halafu akasema “Mama alitoa ushauri na kunitaka nifikirie kama ushauri alioutoa utafaa na ndiyo maana akaniruhusu niambatane nawe huku Dubai kwa lengo la kufahamiana na kila mmoja ajitafakari kama mwenzake anaweza akamfaa.Mimi kwa upande wangu ninamshukuru sana mama kwa kuwa na maono makubwa na mtazamo wa mbali.Ameyaona maisha yangu na yalivyokuwa na ameyaona yatakavyokuwa na akajua mtu pekee ambaye anaweza akanifaa ambaye atanipa furaha katika maisha yangu ni wewe Najma.Kwa hili nitaendelea kumshukuru mama Habiba siku zote.Kujibu swali lako ndiyo nimelikubali ombi lake.Nitawezaje kusema hapana kwa malaika kama wewe? Akasema Mathew na tabasamu likajengeka katika sura ya Najma “Ahsante Abu Zalawi.Kama nilivyokuahidi kwamba nitakuwa mke mwema na muaminifu kwako,nitakuheshimu kwa maisha yangu yote lakini kuna jambo moja ambalo nataka unihakikishie” akasema Najmana kunyamaza “Naj sema chochote” “Nataka unihakikishie kwamba katika mahusiano haya yetu sintatoa machozi na kujutia maamuzi yangu” akasema Najma na Mathew akatabasamu “Najma mimi ni mgumu sana kutoa ahadi ambayo siwezi kuitekeleza lakini kwa hili ninakuahidi kwamba hutatoa machozi.Nitakulinda kama mboni ya jicho langu na hutajutia maamuzi yako”akasema Mathew “Abu kila nionapo midomo yako ikitamka maneno ninazidi kusisimkwa mwili.Nimevumilia kwa muda mrefu nadhani siwezi tena kuendelea kuvumilia.Tafadhali nao…..” Najma hakumaliza alichotaka kukisema kwani tayari Mathew alikwisha muelewa naye hakupoteza wakati akamnyanyua na kumpeleka kitandani.Kila mmoja alionekana kuwa na kiu kubwa na mtanange ule hivyo hakukuwa na kupoteza muda kipute kikaanza mara moja. WIKI MOJA BAADAE RIYAD – SAUDI ARABIA Ndege ya kifahari ilitua katika uwanja wa ndege unaomilikiwa na familia ya Habiba Jawad.Ndege hii ilitokea Dubai na ndani yake alikuwepo Mathew Mulumbi akiwa na Najma.Kwa muda wa wiki moja waliyokaa na kustarehe Dubai mapenzi mazito yaliibuka kati yao na wazo la Habiba Jawad la kuwataka wafunge ndoa lilipita bila kupingwa.Wawili hawa walionekana ni wenye nyuso za furaha sana walipowasili Riyadh Saudi Arabia Walishuka ndegeni na kuingia katika gari safari ya kuelekea nyumbani kwa Habiba ikaanza. “Nina hakika mama atafurahi sana pale atakaposikia kuhusu maamuzi yetu ya kufunga ndoa” akasema Najma “Lazima afurahi kwa kuwa yeye ndiye mwasisi wa jambo hili” akajibu Mathew “Abu Zalawi sikuuliza swali hili.Ungependa lini ndoa yetu ifungwe?akauliza Najma akiwa amemuegemea Mathew “Hakuna chochote cha kutuzuia hivyo ningependa iwe mapema iwezekanavyo” akajbu Mathew “Hata leo hii? “Hata sasa tukishuka kwenye gari mimi niko tayari” akajibu Mathew na kumuacha Najma akiwa na tabasamu kubwa sana Waliwasili katika makazi ya Habiba Jawad na kupokewa na Sayid Omar akawakaribisha ndani ambako walikutana na Habiba Jawad ambaye alitoa tabasamu kubwa baada ya kuwaona “Karibuni wageni” akasema Habiba.Baada ya mazugumzo ya dakika kumi na tano Habiba akasema “Nimefurahi kuwaoneni mmerejea salama wanangu.Najma wewe nenda kaendelee na shughuli zako tutazungumza baadae kwa sasa nataka kwanza kuzungumza na Abu Zalawi” akasema Habiba na Najma akatoka Habiba akamgeukia Sayid Omar “Na wewe pia Sayid naomba utupishe kwanza nina mazungumzo muhimu na Abu” akasema Habiba na Sayid akaaga akaondoka wakabaki Habiba na Mathew “Abu habari za huko Dubai? Sikumpigia simu Najma sikutaka kumsumbua lakini kwa nyuso zenu namna ninavyoziona mlivyoondoka na mlivyorejea nadhani mambo si mabaya” akasema Habiba huku akitabasamu “Mambo yamekwenda vizuri mama.Ilikuwa ni safari nzuri ambayo naweza kusema ilikuwa na mafanikio.Mimi na Najma tulipata nafasi nzuri sana ya kufahamiana na kwa bahati nzuri tumejikuta wote kila mmoja akimuhitaji mwenzake.Binafsi nimekubali kumuoa Najma” akasema Mathew na uso wa Habiba ukachanua kwa tabasamu pana “Utanifanya nipasuke kwa furaha Abu Zalawi. Ni kweli umefanya maamuzi hayo ya kumuoa Najma? “Ndiyo mama.Nimeamua nitamuoa Najma” akasema Mathew “Abu kauli hiyo ni nzito sana ninakuomba ujipe muda ujitafakari tena na ujiridhishe kama kweli uko tayari kumuoa Najma.Sitaki nikushinikize kwani unayekwenda kumuoa ni mwanangu na sitaki apatwe matatizo” akasema Habiba “Usiwe na hofu mama.Nimekwisha jitafakari vya kutosha na kujiridhisha kwamba ninamuhitaji Najma.Mama wewe mwenyewe unayafahamu maisha yangu….” “Shhhh…” akasema Habiba na kumzuia Mathew asiendelee “Tukiwa hapa ndani hatuzungumzi masuala yale kwani anaweza akaingia mtu yeyote na kusikia hivyo chunga sana.Tutazungumza masuala yale tukiwa sehemu salama kama kule bustanini.Umenielewa Abu” “Nimekuelewa mama” akasema Mathew “Abu naomba nikuweke wazi kwamba kuna siku chache sana katika maisha yangu ambazo nimewahi kufurahi na siku ya leo ni mojawapo.Nimefurahi sana kwa maamuzi yako ya kumuoa Najma.Sina hakika kama amekueleza historia yake” “Amenieleza mama” akasema Mathew “Vizuri kama amekueleza.Alichokueleza ni kitu cha kweli kabisa.Najma hakuwahi kuwa na mpenzi na hakutaka kuwa na mpenzi.Hiki ni kitu kilichomshangaza kila mtu kwa nini hataki kuwa na mpenzi? Nimezungumza naye mara kadhaa lakini hata yeye pia alikiri kwamba hafahamu kwa nini amekuwa hivyo.Nimejaribu kumkutanisha na wanaume mbalimbali wenye sura nzuri na uwezo mkubwa kifedha lakini imeshindikana.Mwana mfalme wa Saudia anampenda mno Najma lakini hata naye ameshindwa kupata nafasi.Sifahamu nilipata wapi wazo la kumgusia kuhusu wewe.Nilishangaa nilipomueleza kuhusu wewe alionyesha mabadiliko na akataka kuonana nawe.Ni mara ya kwanza Najma alinipa jibu hilo na ndipo nilipokuomba umuoe mwanangu kwani alionekana kukupenda kabla hata hajakutia machoni.Jibu ulilonipa kwamba uko tayari kumuoa ni jibu ambalo limenipa furaha kubwa ambayo siwezi kuielezea na ndiyo maana ninakuomba ulitafakari kwa kna suala hilo na kujiridhisha kama kweli uko tayari kumuoa Najma.Nataka Najma awe na furaha katika maisha yake.Nataka awe na familia yenye furaha.Sitaki aje kumwaga machozi na kujutia maamuzi yake” akasema Habiba “Mama sina sababu ya kukudanganya,nimeamua kwa dhati ya moyo wangu kumuoa Najma.Ninamuhitaji katika maisha yangu na ninakuahidi kwamba hata mara moja hataangusha chozi na kujutia maamuzi yake ya kuolewa nami” akasema Mathew.Ukapita muda kidogo na Habiba akasema “Ninashukuru kwa kunihakikishia hilo.Sifahamu kwa nini nimekuamini namna hii hadi nikaamua kukuomba umuoe mwanangu.Yawezekana ni kwa sababu ninakuchukulia kama mwanangu na ndiyo maana nina mipango mikubwa ya kuyabadili maisha yako.Nataka nikutoe katika yale maisha yako ya awali ya mateso na mahangaiko na kukuingiza katika maisha mapya yaliyojaa amani na furaha tele ndiyo maana nimekupitisha katika mitihani kadhaa ambayo umefanikiwa kuishinda” akasema Habiba na kukaa kimya kidogo halafu akaendelea “Utakumbuka kabla ya kwenda Dubai nilikueleza kwamba nitakupatia sehemu ya utajiri wa Seif .Ni utajiri mkubwa sana ambao naweza kusema ni mara kumi zaidi ya ule utajiri wako uliokuwa nao.Hautakuwa na ulazima wa kufanya kazi kwani pesa inaingia tu na huku wewe mkeo na watoto mtakaojaliwa kuwapata mkiishi maisha ya starehe” akasema Habiba na kunyamaza akamtazama Mathew “Mama mimi ninakushukuru sana kwa kuniamini hadi kufanya maamuzi hayo ya kunipa utajiri kubwa uliokuwa wa Seif Jawad.Najiuliza mimi ambaye unafahamu kabisa kwamba nia yangu ilikuwa ni kukuua kwa nini ukanifanyia haya? Kwa nini ukanipokea na kunifanya mwanao?akauliza Mathew “Kuna jambo moja ambao sikuwa nimetaka kukuweka wazi bado lakini kwa kuwa umeuliza nitakueleza.Ninataka uwe msaidizi wangu” “Nini?Mathew akauliza kwa mshangao “Ninataka uwe msaidizi wangu.Kama unavyoniona umri wangu unazidi kusogea hivyo utafika wakati ambao itanibidi na mimi nipumzike.Nataka pale nitakapoamua kupumzika basi wewe usimame badala yangu” akasema Habiba “Kwa nini mimi?akauliza Mathew “Kwa sababu unafaa na una sifa za kuwa mrithi wangu” akasema Habiba “Mama una watu wengi wanaokuzunguka.Sayid Omar na hata mwanao Abu Dahir kwa nini umewaacha hao wote na ukanichagua mimi? “Hao wote na wengine ambao hukuwataja hawana sifa za kushika nafasi yangu pale nitakapokuwa nimeamua kupumzika.Ni wewe pekee na msaidizi wako atakuwa Nawal” akasema Habiba “Mama utanisamehe kama nitakuwa nimekukosea lakini wewe una fadhili ugaidi duniani na juzi Dubai nimeshuhudia ukifadhili kundi la IS katika harakati zake za kuanzisha kambi yake ya mafunzo nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Je unataka mimi nije kurithi kazi hiyo ya kufadhili ugaidi na kusababisha watu wasio na hatia kuuawa? Akauliza Mathew na Habiba akacheka kidogo “Bado una mengi huyafahamu kijana wangu.Bado una safari ndefu ya kujifunza kuhusu hayo unayoyasema hivyo kaa tayari kujifunza.Usiwe na haraka ya kutoa majibu na maamuzi,kuwa na subira.Kule Dubai nilifanya makusudi kabisa ili uweze kushuhudia tukio lile na bado utaendelea kushuhudia mengine mengi ila nakuomba uwe mvumilivu.Endelea kujifunza.Kuna mengi bado utatakiwa kuyafahamu.Tuachane na hayo” akasema Habiba na kunyamaza kidogo halafu akasema “Lini mnataka kufunga ndoa?Mmekwisha lijadili hilo?akauliza Habiba. “Mapema iwezekanavyo.Hakuna sababu ya kuchelewa” akasema Mathew na Habiba akatoa kicheko kikubwa “Kweli Abu Zalawi umenifanya niwe na furaha kubwa.Kwa nini umeamua iwe mapema hivyo?Hamuhitaji kupata muda wa kufahamiana zaidi kabla ya kuingia katika ndoa? “Hakuna kitu cha kutuzia tusifunge ndoa.Mimi na Najma kila mmoja anamuhitaji mwenzake,kila mmoja amekwisha ridhika na mwenzake hivyo hatuhitaji kuvuta muda.Jambo la heri kama hili halihitaji kuvuta muda.Labda kama una kipingamizi kinachoweza kutufanya tusifunge ndoa” akasema Mathew “Mimi sina kipingamizi chochote cha kuwafanya mkachelewa kufunga ndoa yenu.Kama maamuzi yenu ni hayo mimi sina kipingamizi nitazungumza na wenzangu na maandalizi yaanze mara moja” “Ahsante mama lakini kuna kitu kinaniumiza kichwa kidogo” akasema Mathew “Kitu gani Abu? “Najma hajui chochote kuhusu historia yangu ya nyuma.Najiuliza ni vipi endapo akija kufahamu ukweli kuhusu mimi? Kwamba huko nitokako nina mke na watoto? “Kwa nini umeuliza Abu? “Nimeuliza kwa sabau dunia imekuwa ndogo sana hivi sasa” “Hatalifahamu hilo na hata akilifahamu italazimu aufahamu ukweli hivyo jambo hilo lisikuumize kichwa” akasema Habiba BAADA YA SIKU TATU Nyumbani kwa Habiba Jawadi kulikuwa na heka heka za maandalizi ya harusi ya Najma na Mathew.Ni siku ya tatu tu toka waliporejea kutoka Dubai na Mathew kutamka kwamba anataka kumuoa Najma.Maandalizi makubwa yalifanywa katika bustani nzuri ambako ndiko sherehe zingefanyika. Mathew Mulumbi alisimama dirishani katika nyumba yake akichungulia namna maandalizi yalivyokuwa yakindelea bustanini “Nimefanya maamuzi magumu ya kuamua kumuoa Najma.Nasikia kuna sauti mbili ndani mwangu zinakinzana kuhusu maamuzi haya lakini naamini nimefanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka kabisa.Sikuwa na namna nyingine ya kuendelea na misheni yangu zaidi ya kumuoa Najma.Hii ni misheni nzito na kubwa zaidi ya nilivyotegemea na inahitaji maamuzi kama haya.Lakini bado kuna mambo ambayo bado najiuliza kuhusu Habiba Jawad.Anafahamu mimi ni nani anafahamu kwa nini niko hapa,lakini juzi aliniambia kwamba anataka mimi niwe mrithi wake kwa nini hanioni mimi kama mtu hatari kwake? Inanibidi niwe makini sana na nifikiri mara mbili zaidi yake kwani vinginevyo nitashindwa kutimiza misheni yangu.Niko kwenye uti wa mgongo wa ugaidi na lazima niuvunje ili ugaidi ukose nguvu.Lakini kama alivyosema Habiba kwamba nina mengi ya kujifunza bado.Alisema kuna mengi bado siyafahamu na ili niyafahamu hayo yote,maamuzi haya niliyoyafanya ya kumuoa Najma ni sahihi”akawaza na sura ya Najma ikamjia akatabasamu “Ni mwanamke mzuri mwenye adabu na mnyenyekevu.Wanawake wa aina yake ni nadra sana kupatikana zama hizi.Nitajitahidi kufanya kila niwezalo ili kumlinda siku moja asijitie uamuzi wake wa kuolewa nami japokuwa nina uhakika siku moja lazima ataufahamu ukweli na utaumia sana.Lakini ni vipi kama nitajikuta nimezama mapenzini na kuamua kusahau kila kitu kuhusu misheni yangu? Kwa mwanamke kama Najma hilo linawezekana kabisa”akawaza na kutabasamu “Kama hilo likitokea na nikajikuta nimeamua kukubaliana na ile kauli ya Habiba kwamba hapa ndipo mahala ninapotakiwa niwepo basi nitakuwa nimekubali kuwa mrithi wa Habiba na kuendelea kufadhili makundi ya kigaidi’ akawaza na kucheka kidogo. “Hiki ni kichekesho.Mathew Mulumbi kutoka ujasusi hadi kuwa mfadhili wa ugaidi”akawaza na kucheka tena “Wengi hawatanielewa lakini iko siku nitakuwa shujaa wa dunia” akawaza Mathew DAR ES SALAAM – TANZANIA Nyumbani kwa Germinus Mapupu balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nchini Tanzania maandalizi ya chakula cha jioni kwa ajili ya wake za marais wa Congo na Rwanda yalikuwa yanaendelea.Asubuhi na mapema gari maalum lililowabeba wapishi wa kimataifa walioletwa na nchini na Melanie Davis liliwasili na bila kupoteza muda wakaanza maandalizi.Wapambaji nao walifika na kuanza kuandaa sehemu watakapokutana akina mama hao.Ulinzi uliimarishwa sana toka asubuhi na kila aliyeingia mahala hapa alipekuliwa.Kwa bahati nzuri gari la wapishi liliwahi sana kufika kabla ya askari hawajawasili hivyo hawakukaguliwa. Wake za marais kutoka nchi mbali mbali tayari walikwisha anza kuwasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mkutano mkubwa wa wake za marais na miongoni mwa wageni wa mwanzo kabisa kuwasili ni wake za maraisi wa Congo na Rwanda.Kwa siku nzima mke wa Rais wa Tanzani Millen Kelelo alikuwa na kazi ya kuwapokea wake za marais walioendelea kuwasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mkutano ambao ungefunguliwa siku ya jumapili na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo.Ulinzi uliimarishwa mno katika jiji la Dar es salaam na hasa katika mahotel ambako wageni walifikia.Hadi wageni walipoanza kuwasili hakukuwa na taarifa yoyote ya kiintelijensia iliyoonyesha kuwapo kwa kitisho cha usalama. Hadi ilipofika saa kumi na moja za jioni tayari wake za marais hamsini na nne walikwisha wasili.Millen Kelelo alirejea ikulu kujiandaa kwa ajili ya kuhudhuria katika chakula cha usiku nyumbani kwa balozi Germinus Mapupu kwani kwa jioni ile hakukuwa tena na mgeni mwingine aliyetarajiwa kuwasili Akiwa katika maandalizi ya kuelekea katika chakula hicho cha jioni akaingia mumewe Dr Fabian Kelelo “Mambo yamekwendaje? “Siku imekuwa fupi sana mambo ni mengi.Wageni hamsini na nne wamekwisha wasili hadi hivi sasa na wengine watawasili kesho.Katika hao waliokwisha wasili wengi wanatoka nchi za Afrika” “Vipi kuhusu nchi za Ulaya,Asia na Amerika?akauliza Dr Kelelo “Nadhani wengi watawasili kesho.Usiwe na hofu Fabian watakuja.Wengi wamekwisha nihakikishia kwamba watafika na nina uhakika watakuja” akasema Millen “Hakuna tatizo hata wasipofika lakini hao waliofika wanatosha kabisa kufikisha ujumbe kwa dunia” akasema Dr Fabian na kumshika mkewe mikono “Millen nakuhakikishia mkutano huu utafanikiwa.Ahsante sana kwa kulileta wazo hili.Dunia nzima kwa sasa macho yao yameelekezwa Tanzania.Dunia nzima inajua kuna kitu kinaendelea Tanzania” akasema Dr Fabian na kumbusu mkewe “Ahsante sana Millen” “Fabian umekwisha nishukuru zaidi ya mara hamsini kwa siku hii ya leo” akasema Millen huku akicheka “Hata nikisema ahsante mara elfu kumi bado haitoshi.Jambo hili unalolifanya ni jambo kubwa kwa nchi.Umepambana kuhakikisha jina la Tanzania kisiwa cha amani linarejea kutamkwa na dunia nzima na katika kulithibitisha hilo wake za marais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda wanakwenda kuufungua ukurasa mpya usiku wa leo na nina uhakika huu utakuwa ni mwanzo mzuri wa kumaliza msuguano unaoendelea hivi sasa baina ya nchi zao.Hongera sana Millen kwa kulifanikisha hilo” akasema Dr Fabian na kumbusu tena mke wake kisha akamuacha amalizie kujiandaa.Baada ya kumaliza kujiandaa akamuaga mumewe na kuondoka kuelekea nyumbani kwa balozi wa Congo nchini Tanzania Ulinzi ulikuwa kali na walioruhusiwa kuingia mle ndani ni watu maalum tu waliopewa mwaliko.Jeshi la polisi liliimarisha ulinzi eneo lote la kuzunguka makazi yale ya balozi Mapupu.Saa moja na nusu Millen Kelelo mke wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akawasili katika makazi ya balozi Mapupu.Alipokelewa na balozi Mapupu na mke wake akakaribishwa na burudani nzuri ya ngoma za asili.Dakika kumi na tano baadae Rebeca Eyenga mke wa Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo akawasili akapokewa na Millen na balozi Mapupu na kukaribishwa ndani.Dakika chache baadae mke wa Rais wa Rwanda akawasili naye kama ilivyokuwa kwa wengine akapokewa na Millen na kukaribishwa ndani.Alistuka sana alipomkuta Rebeca mle ndani.Hakuwa ametegemea “Kwa nini hukuniambia kama huyu naye umemulika?Mke wa Rais wa Rwanda akamnong’oneza Millen “Usiwe na hofu.Kuwa na amani” akasema Millen. Burudani ya ngoma za asili ikatolewa kisha balozi Mapupu akazungumza machache na kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Millen Kelelo ambaye alianza kwa kumshukuru balozi Mapupu kwa kumkaribisha jioni ile vile vile akawashukuru wote waliohudhuria chakula kile “Balozi Germinus aliponialika nyumbani kwake kwa chakula aliniambia kwamba utakuwa ni usiku wa kipekee kabisa na nilikuwa najiuliza ameandaa kitu gani cha kuufanya usiku huo kuwa wa kipekee? Mimi alinipa kazi moja tu ya kuhakikisha ninamualika mke wa Rais wa Rwanda na nilifanya hivyo naye kwa heshima kubwa amehudhuria.Baada ya kuingia hapa ndani ndipo nikagundua kitu kikubwa alichokifanya balozi Mapupu.Ukiangalia mahala hapa kuna wakongomani,wapo wanyarwanda na watanzania pia.Naamini wapo wakristu,waislamu pia wa dini nyingine.Ujumbe ambao tunaupata kwa hiki alichokifanya balozi Mapupu ni kwamba mipaka ya kijiografia haiwezi kututenganisha.Sisi ni ndugu moja.Wakongo,wanyarwanda,w arundi ,watanzania nakadhalika sote tu ndugu moja.Mipaka yetu isitugawe na kujenga hasama baina ya nchi zetu.Kuanzia usiku huu tunakwenda kuidhihirishia dunia kwamba Afrika Mashariki ni moja na watu wake ni wamoja” akasema Millen na kuwainua wake za marais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda akawashika mikono na kusimama kati kati yao.Akamuita balozi wa Rwanda na kumtaka akae upande ule wa Rebeca Eyenga na balozi wa Congo akamtaka akae pembeni ya mke wa Rais wa Rwanda. “Usiku wa leo tunaufungua ukurasa mpya wa kutafuta amani katika nchi zetu.Kwa muda sasa nchi ya Rwanda na nchi ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hazina maelewano mazuri lakini usiku wa leo tunataka kuanzisha vuguvugu la kutafuta amani.Nitawaomba kwanza wanawake hawa wawili kutoka ndani ya mioyo yao washikane mikono wasalimiane na kumaliza tofauti zao.Nataka watakaporejea nchini kwao wakawe chachu ya kutafuta amani katika nchi zao.” akasema Millen .Rebeca Eyenga na mke wa Rais wa Rwanda huku wote wakitabasamu na makofi mengi yakipigwa wakashikana mikono na kukumbatiana.Watu wakashangilia.Wakazungumza na kukumbatiana tena.Mabalozi wa Congo na Rwanda nao wakasalimiana na kukumbatiana kwa furaha.Wageni waliokuwa wamealikwa nao wakaanza kusalimiana kwa furaha.Lilikuwa ni tukio la aina yake. Baada ya tukio lile watu wakaa mezani kwa ajili ya kupata chakula.Wageni wakajipanga mstari na kuanza kupata chakula.Baada ya wageni wote kupata chakula wahudumu wakaanza kupita na meza kubwa za magurudumu zilizosheheni vinywaji mbali mbali na baada ya meza zote za wageni kusheheni vinywaji meza tatu za magurudumu zikapangwa vinywaji mbali mbali kwa ajili ya wageni waalikwa kujihudumia wenyewe pale watakapohitaji.Ni meza ambazo zilikuwa zimefunikwa kwa vitambaa safi na hakuna ambaye angeweza kuhisi chochote kibaya.Wakati wageni wakiendelea kupata chakula wapishi na wahudumu wakakusanyika mahala walikokuwa wametengeneza jiko lao la muda “Kazi tumeimaliza.Mabomu yote yamekwisha tegwa ndani ya zile meza na kilichobaki ni kuyalipua.Kinachofuata kwa sasa ni kuanza kutoka humu ndani.Hakikisheni wote mnatoka.Mnafahamu lile gari letu lilikoegeshwa hivyo kila mmoja akaingie humo.Nataka ndani ya dakika kumi kila mtu awe nje na tuondoke mahala hapa” akaelekeza Yule mkubwa wao kisha wapishi na wahudumu wakaanza kupungua taratibu mle ndani.Hakuna aliyeweza kuligundua hilo kwa haraka.Ndani ya dakika kumi tayari wote walikwisha toweka mle ndani na kuingia katika gari lao lililokuwa nje.Kiongozi wao akahakikisha wote wako salama.Gari lao likawashwa na kuondoka. taratibu “Sasa ni ule wakati wa kuibadili historia” akasema kiongozi wa kundi lile na kuchukua kifaa Fulani mithili ya simu akabonyeza namba kadhaa halafu akabonyeza kitufe chekundu na mara mlipuko mkubwa ukatokea na kulitingisha lile eneo. Wakiwa ndani ya gari Yule kiongozi wao akachukua simu na kumpigia James Kasai akamjulisha kwamba wamemaliza kazi.James akawapongeza halafu naye akampigia simu Melanie Davis akamjulisha kwamba kazi imemalizika.Melanie Davis akampigia simu Edwin Mbeko akamuelekeza kwamba wale watu wake wamemaliza kazi hivyo anatakiwa ahakikishe wameondoka nchini salama kuelekea Uganda. “Kazi ndiyo kwanza imeanza.Afrika Mashariki itawaka moto” akawaza Melanie na kuwasha runinga ambako kulikuwa habari mpasuko kuhusiana na tukio lile.Kikosi cha uokoaji na zimamoto kilikuwa cha kwanza kufika eneo lile la tukio na kufuatiwa na vikosi vingine vya usalama.Hali ya mahala pale ilitisha.Maiti zilisambaa kila kona.
Dakika arobaini baada ya mlipuko ule kutokea,ilianza kusambaa video ikimuonyesha kiongozi wa kundi pekee la waasi lililosalia kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo James Kasai akijitapa kuhusika katika shambulio lile kwa kushirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS huku akieleza kwamba mashambulio mengine zaidi yatafuata.Mwisho James akaahidi kwamba anajiandaa kurejea Congo kwenda kuikomboa nchi hiyo. Dr Fabian Kelelo akiwa katika makazi yake ikulu alichanganyikiwa akiwataka wasaidizi wake wampeleke eneo la tukio ili akahakiki kama mke wake yuko hai ama amekufa.Rais hakuruhusiwa kutoka mle ndani kwa ajili ya usalama wake na hakuruhusiwa hata kushika simu.Kila kitu kilifanywa na wasaidizi wake. Akiwa amekaa sofani ameinamisha kichwa huku machozi yakimdondoka mmoja wa wasaidizi wake akamsogelea akiwa ameshika simu. “Mzee kuna simu kutoka kwa Rais Patrice Eyenga” akasema Yule msaidizi na kumuibua Dr Fabian Kelelo kutoka katika dimbwi la mawazo.Dr Fabian akaichukua simu ile na kusogea pembeni huku wasaidizi wake wakiwa makini sana “Hallo Patrice” “Dr Fabian tafadhali nihakikishie kama Rebecca yuko salama” akasema Patrice Eyenga “Sifahamu Patrice.Sifahamu kama yuko hai ama vipi.Hapa nilipo nimechanganyikiwa ninasubiri taarifa kutoka kwa watu wangu walioko eneo la tukio kujua kama kuna mtu amenusurika” akasema DrFabian “Dr Fabian hili jambo limetokeaje? Uliihakikishia dunia kwamba usalama ni mkubwa sana nini kimetokea?Nataka kusik…………”Dr Fabian akaitoa simu sikioni baada ya mmoja wa wasaidizi wake aliyekuwa ameshika kompyuta mpakato kumfanyia ishara kwamba kuna suala la muhimu sana analotakiwa kulitazama. “Patrice naomba dakika moja nitakupigia” akasema na kukata simu “Kuna nini? Akauliza na kuonyeshwa video ile ya James Kasai akijitapa kufanya shambulio lile. “Aaaaghhh !! akasema kwa hasira Dr Fabian na kupiga ngumi meza.Wasaidizi wake wakamshika na kumsihi atulie “Tafadhali niacheni.Huyu muuaji ndiye ame….oh my God ! akasema kwa hasira na kushika kichwa.Baada ya dakika kadhaa mmoja wa wasaidizi wake akamsogelea akiwa na simu “Mzee kuna simu kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini” akasema Yule jamaa na Rais akaichukua haraka “Hallo” akasema “Mheshimiwa Rais” akasema mkuu wa jeshi la polisi nchini “IGP tafadhali niambie mke wangu yuko salama ! akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais niko hapa eneo la tukio na vikosi vya uokoaji.Hali ni mbaya na yaliyolipuka ni mabomu matatu yaliyokuwa yamefichwa katika meza za vinywaji.Miili yote ya waliofariki imekwisha ondolewa hapa kupelekwa hospitali na tumepata jumla ya maiti arobaini na sita na majer………..” “Kamanda unazidi kunichanganya kwa taarifa ndefu.Nataka kujua mke wangu yuko salama?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nasikitika kutamka kwamba mkeo ni mmoja wa waliofariki dunia katika tukio hilo pamoja na wake za marais wa Congo na Rwanda bila kusahau mabalozi wa Congo na Rwan……” “Oh Millen..!! akasema Dr Fabian na kuanguka chini akapoteza fahamu.Haraka haraka akachukuliwa na kukimbizwa katika chumba cha huduma ya kwanza.
Melanie Davis akiwa katika chumba chake akifuatilia habari za kuhusiana na tukio lile huku mezani akiwa na chupa ya shampeni simu yake ikaita alikuwa ni Edwin Mbeko “Hello Edwin” akasema Melanie “Madam wale watu tayari wamekwisha ondoka na ndege inayoelekea Nairobi Kenya” “Ahsante sana Edwin.Kazi nzuri.Endelea kufuatilia kwa karibu sana taarifa zote za usalama na unijulishe kama kutakuwa na tatizo lolote kwa upande wetu” akasema Melanie na kukata simu “Damu ya wazazi wangu haitamwagika bure.Lazima itaondoka na watu wengi na kama nilivyoahidi huu ni mwanzo tu” akawaza na kuchukua glasi ya shampeni akanywa “Sikutegemea kama siku moja ninaweza nikawa mkatili namna hii lakini ni wao wenyewe ndio walionifanya mimi niwe mkatili kiasi hiki kwa kuwaondoa wazazi wangu kikatili.Walifanya makosa makubwa sana kushindwa kuniua na sasa nitawawinda usiku na mchana na wote walioshiriki suala hili watalipa uovu wao” akawaza Melanie na simu yake ikaita alikuwa ni Devotha. “Hallo Devotha” akasema Melanie “Melanie nini umekifanya?akauliza Devotha kwa ukali “Devotha kwa nini badala ya kunipongeza unaanza kunifokea?Melanie akahamaki “Ninakufokea kwa kitendo ulichokifanya ! akaendelea kufoka Devotha “Kwa kitendo nilichokifanya ! Melanie akashagaa “Nilichokifanya si ndicho nilitumwa kukifanya? Sasa nimekosea wapi?akauliza Melanie “Umekosea sana Melanie.Kwa nini umewashirikisha IS? Kwa nini umeshirikiana na magaidi? Akauliza Devotha kwa ukali “Devotha mlinituma Afrika Mashariki kwa ajili ya misheni maalum hivyo basi ni jukumu langu kuhakikisha misheni inafanikiwa bila kujali ninashirikiana na nani.Ninaomba msianze kunivuruga niacheni nitekeleze kazi mliyonituma niitekeleze” akasema Melanie kwa ukali “Melanie hujui kwamba kwa kushirikiana na magaidi wa IS unalifanya suala hili kuwa kubwa zaidi tofauti na tulivyokuwa tumelipanga? “Nimekwisha kueleza Devotha na ninarudia tena kukueleza kwamba hii ni misheni yangu na ninaitekeleza vile nitakavyo.Naomba kama huna lingine la kunieleza tafadhali kata simu ! akasema Melanie kwa ukali “Nisikilize Melanie.Kuanzia sasa hakuna tena mashirikiano baina yako na hao magaidi wala kikundi kingine chochote.Unafanya kitu cha hatari sana Melanie.Mpango huu ni wa siri kubwa lakini kwa hiki ulichokifanya cha kuwashirikisha waasi na magaidi kitaufanya mpango wetu huu kufahamika.Ninakuelekeza kuanzia sasa vunja kabisa mahusiano yoyote uliyo nayo na hao watu.Umenielewa Melanie?! Akauliza Devotha “Devotha kwa mara ya mwisho ninarudia kukusisitiza kwamba mmenituma kufanya kazi na nitaifanya kwa jinsi nitakavyo mimi.Naomba iwe ni mara ya mwisho kunifokea bila kujua ni magumu gani nimepitia hadi kufanikisha tukio lile kubwa ! akasema Melanie na kukata simu “Huyu Devotha kwa nini ananilazimisha nimuondoe kabla ya wakati wake?Yeye pia yumo katika orodha ya watu ambao lazima damu yao imwagike kwani ni yeye aliyemfuata mama yangu na kumshawishi ajiunge katika siasa.Kwa kuwa anaonekana kutaka kunipanda kichwani dawa yake ni ndogo tu.Lazima nimuondoe na kazi hii ataifanya Gosu Gosu.Nitamtuma kwenda Ufaransa kumuua Devotha” akawaza Melanie na kuinua glasi yake ya shampeni akanywa. NDUGU MSOMAJI TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………..
KAMPALA – UGANDA Saa tatu za asubuhi televisheni ya taifa ya Uganda ilikatisha vipindi vilivyokuwa vinaendelea na kujiunga na matangazo ya moja kwa moja kutoka katika kambi kubwa ya kijeshi iliyoko nje kidogo ya jiji la Kampala ambako Rais wa Uganda Jenerali Akiki Rwamirama alitarajiwa kulihutubia taifa kutokea katika kambi hiyo. Msafara wa Jenerali Akiki uliwasili katika kambi hiyo kubwa akapokewa na mkuu wa majeshi wa Uganda,wimbo wa Taifa ukapigwa halafu mkuu wa majeshi akazungumza machache na kumkaribisha Rais azungumze na wanajeshi waliokuwa na hamu ya kumsikiliza na kupitia kwao taifa zima liweze kupata ujumbe.Jenerali Akiki akaelekea katika mimbari iliyoandaliwa na kuwasalimu wanajeshi ambao waliitika kwa sauti kubwa akatabasamu na kuendelea “Mheshimiwa waziri wa ulinzi,mkuu wa majeshi,makamanda wote wa vikosi na wote mlioko hapa itifaki ikiwa imezingatiwa” akanyamaza na kuwatazama wanajeshi halafu akaendelea “Awali ya yote napenda kwa niaba ya serikali yangu na wananchi wa Uganda kuchukua nafasi hii kuwapa pole nyingi ndugu zetu wa Tanzania,Congo na Rwanda kwa tukio baya lililotokea usiku wa jana jijini Dar es salaam la mlipuko wa bomu,tukio ambalo lilisababisha watu wengi kuuawa na miongoni mwao ni wake za marais wa Tanzania,jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda waliokuwa wamekwenda nchini Tanzania kuhudhuria mkutano mkubwa wa wake za marais ulioandaliwa na mke wa Rais wa Tanzania.Tunawapa pole sana wote waliofiwa na tunawahAkikishia kwamba ndugu zao wa Uganda tuko pamoja nao kwani huu ni msiba wa Afrika Mashariki.Shambulio lile ni la kinyama kabisa na tunalilaani kwa nguvu zetu zote” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Nadhani mpaka sasa wengi wenu tayari mmekwisha itazama video iliyoanza kusambaa toka jana usiku ambayo inamuonyesha mtu anayejulikana kama James Kasai akitamba kuhusika katika tukio lile la mauaji akishirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS.Huyu James Kasai ni kiongozi wa kikundi cha waasi ambaye amekuwa akiendesha mapambano na serikali ya Congo kwa muda mrefu na baada ya kutimuliwa kutoka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inadaiwa alikimbilia katika misitu iliyoko Kaskazini mwa nchi yetu.Nchi za Rwanda na Congo zimekuwa zikitulaumu sisi kwamba tunamuhifadhi James Kasai lakini ukweli ni kwamba hatuna uhakika wa uwepo wake katika misitu yetu kama inavyodaiwa.Toka shutuma hizo zilipoanza,tumefanya operesheni za kijeshi zaidi ya mara mbili kumsaka James Kasai lakini hatujafanikiwa kumpata huko mahala wanakodai amejificha.Tunaamini James Kasai atakuwa bado amejificha katika misitu ya Congo na si nchini Uganda kama inavyodaiwa” akanyamaza tena kidogo kisha akaendelea Kuanzia saa tisa za usiku wa kuamkia leo,ndege za kivita za Rwanda zimeingia katika anga letu na kufanya mashambulizi katika vijiji vilivyoko kandoni mwa misitu ya Kaskazini mwa nchi yetu.Bado hatujapata idadi kamili ya watu waliouawa lakini uharibifu uliofanyika ni mkubwa.Mashambulizi hayo yamefanywa kwa kisingizio cha kumtafuta James Kasai.Vikosi vyetu mahiri vya Anga vilifanikuwa kuziangusha ndege vita mbili za jeshi la Rwanda zilizoingia katika anga letu kwa lengo la kufanya mashambulio.Kitendo hiki ni cha kichokozi na serikali ya Uganda kamwe haiwezi kukivumilia ! akasema kwa ukali Rais Akiki na wanajeshi wakashangilia “Narudia tena kwamba kitendo hiki kilichofanywa na serikali ya Rwanda kutuvamia,kufanya mashambulio na kuua watu wetu katu serikali ninayoiongoza haiwezi kukivumilia !! akasema kwa ukali na kunyamaza akawatazama wanajeshi halafu akaendelea “Kwa muda mrefu sasa Rwanda wamekuwa wakiendesha chokochoko dhidi ya nchi yetu lakini tumekaa kimya hatujawajibu chochote na sasa wameamua kutuvamia na kutushambulia.Ninasema kwa mara ya tatu hiki walichokifanya ni uchokozi wa wazi na hatuwezi kuukubali uchokozi huu ukaendelea.Tuko tayari kupambana na taifa lolote lile liwe kubwa au dogo ambalo litathubutu kutuchokoza hivyo basi tayari nimemuelekeza mkuu wa majeshi aweke vikosi vyetu vyote vya jeshi katika utayari wa vita na vikosi vingine vitangulie katika mpaka wetu na Rwanda.Tunataka kutoa ujumbe kwa dunia kwamba Uganda si mahala pa kufanyia majaribio ya kijeshi.Ukiingiza pua yako Uganda tutakukata hadi miguu.Damu ya watu waliouawa bila hatia haiwezi kumwagika bure lazima tulipe na tukomeshe uovu huu uliofanywa na Rwanda ! akasema Rais Akiki na wanajeshi wakamshangilia kwa nguvu “Kwa wananchi wa Uganda nawaomba muwe watulivu na muendelee na shughuli zenu kama kawaida.Jeshi lenu lenye wanajeshi walio na ari kubwa ya kuitetea nchi yao http://deusdeditmahunda.blogspot.com/liko imara kuwalinda dhidi ya adui yeyote kutoka nje anayetishia amani na usalama wenu na ndiyo maana jana usiku liliweza kuzima mashambulio ya ndege za jeshi za Rwanda na kuangusha ndege mbili.Hatutaishia katika kuangusha ndege mbili tu la hasha,tunataka tuende mbali zaidi na kumfundisha adabu huyu mvamizi wetu ! Jenerali Akiki akaendelea kushangiliwa kwa nguvu Narudia tena kuwaomba ndugu zangu tusimame pamoja katika hili na kupinga aina yoyote ya uvamizi kwa taifa letu.Mimi na serikali ninayoiongoza ambao tulikula kiapo cha kuilinda mipaka ya nchi yetu nawaahidi kwamba tutapamba na yeyote hadi tone la mwisho la damu yetu katika kuilinda nchi yetu.Jambo la mwisho ambalo nataka kuwasisitiza wananchi wa Uganda fuatilieni sana vyombo vya habari kwani kila hatua tutakayoichuikua tutakuwa tukiwajulisha Ahsanteni Mungu Ibariki Uganda Jenerali Akiki akamaliza hotuba yake fupi kisha akaongozwa na mkuu wa majeshi kuelekea sehemu ambako kikao cha faragha kingefanyika kati ya Rais na makamanda wa vikosi mbali mbali vya jeshi.Kikao hicho kilidumu kwa saa mbili kisha Rais akaondoka akiwa katika ulinzi mkali sana kurejea ikulu.Akiwa njiani akapigiwa simu na mke wake aliyekuwepo jijini Dar es salaam. “Hallow” akasema Jenerali Akiki “Hallo mpenzi habari za huko.Nilikuwa naitazama hotuba yako” akasema Dr Natukunda Rwamirama mke wa Rais wa Uganda “Unasemaje kuhusu hotuba ile? Huko Dar es salaam wanaiongeleaje? Akauliza Jenerali Akiki huku akitabasamu “Watu wana hofu kwamba kwa hotuba ile uliyoitoa leo,kuna uwezekano mkubwa kukazuka vita baina ya Uganda na Rwanda” akasema Dr Natukunda “Uwezekano ni mkubwa sana.Katu hatuwezi kuvumilia kitendo ilichokifanya serikali ya Rwanda.Wametuvamia na kutushambulia hatuwezi kukaa kimya lazima tujibu.Ninaapa kuifanyia Rwanda kitu kibaya sana ! akasema Jenerali Akiki “Lakini mume wangu sioni sababu ya kuanzisha vita na Rwanda” “Umefurahia Rwanda ilichokifanya? Wamevamia wakafanya mashambulio na kuua watu wetu.Hilo ni jambo zuri?akauliza Jenerali Akiki kwa sauti ya ukali kidogo. “Si jambo zuri walilolifanya lakini Rwanda walikuwa na sababu ya kufanya vile.Wanafahamu kwamba tunamuhifadhi James Kasai na kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia jambo hili kwani wakati akiendesha mapambano yake nchini Congo James Kasai aliua wanyarwanda wengi pia.Rwanda wamekuwa wakishinikiza tumfukuze au tumkamate James lakini tumekuwa tukikanusha kwa nguvu kwamba James Kasai hayupo Uganda.Unadhani Rwanda hawajui kama James yupo Uganda na sisi tumempa hifadhi?Wanajua na ndiyo maana wakafanya operesheni ile ili waweze kumuondoa wao wenyewe baada ya sisi kuendelea kumkumbatia.Mpenzi wangu kwa hiki alichokifanya James sidhani kama kuna ulazima wa kuendelea kumpa hifadhi na kumtetea.Ni wakati wa kumtaka aondoe vikosi vyake.Tukiendelea kumuhifadhi yeye na kundi lake atatusababishia matatizo makubwa sana.Namlaumu sana mdogo wangu kwa kukubali kuolewa na mwanaume kama Yule ambaye hana hata chembe ya ubinadamu” akasema Dr Natukunda.Jenerali Akiki akavuta pumzi ndefu halafu akauliza “Mke wangu hilo suala ni gumu kidogo.Japo James amefanya kitendo hicho lakini hatuwezi kumuondoa kwa haraka namna hiyo.Wewe mwenyewe unafahamu namna tunavyofaidika na huyu mt……….” Akasema Jenerali Akiki na mke wake akamkatisha “Mume wangu niko hapa Dar es salaam nimeshuhudia kile alichokifanya ni kitendo cha kinyama sana.James hafai kabisa na sasa ameharibu zaidi baada ya kujiunga na magaidi wa IS.Tumuondoe haraka kwani huko tunakoelekea atakuja kutushambulia hata sisi wenyewe” akasema Dr Natukunda “Sawa nimekuelewa vipi kuhusu safari ya kurudi? Akauliza Jenerali Akiki “Nimeahirisha kidogo ili nishiriki miili ya marehemu ndipo niondoke.Hawa waliouawa walikuwa marafiki zangu.Millen Kelelo alikuwa ni rafiki yangu sana na siwezi kuondoka Tanzania bila kumuaga.Mkutano tuliokuja kuhudhuria haupo tena hivyo baada tu ya kuaga miili ya marehemu nitaanza safari ya kurejea Uganda”akasema Dr Natukunda “Vipi kuhusu usalama wako? “Usalama hapa ni mkubwa usiwe na wasiwasi” akasema “Sawa hAkikisha baada tu ya zoezi hilo kukamilika basi unarejea nyumbani mara moja” akasema Jenerali Akiki na kukata simu “Nadhani Natukunda yuko sahihi ni wakati wa James kuondoa vikosi vyake katika ardhi ya Uganda.Tumekuwa tukimfadhili katika mapambano yake na serikali ya Congo na sisi tumekuwa tukifaidika kwa kupata madini na rasilimali nyingine kupitia kwake hivyo yeye ataendelea kubaki hapa Uganda lakini vikosi vyake lazima viondoke.Nitawasiliana naye ili aweze kuondoa kimya kimya vikosi vyake kwa muda huu ambapo hali ya hewa imechafuka.Baadae hali itakapotulia atavirejesha.Kuhusu Rwanda lazima niwafundishe adabu.Nitawachapa kuanzia mpakani hadi mji wao mkuu wa Kigali.” Akawaza Jenerali Akiki Alipofika ikulu moja kwa moja akaelekea chumbani kwake akachukua simu ya satelaiti na kumpigia James Kasai “Mheshimiwa Rais”akasema James Kasai baada ya kupokea simu “James habari yako” “Mheshimiwa Rais naamini simu hii umenipigia kuhusiana na kile kilichotokea Dar es salaam jana”akasema James Kasai “James kwa nini ulifanya vile? Kwa nini hukunijulisha kama kuna shambulio unalipanga nchini Tanzania? Akauliza Jenerali Akiki kwa ukali “Mheshimiwa Rais …….” Akasema James lakini Jenerali Akiki akamkatisha “Nisikilize James.Kwa sababu ya kile ulichokifanya hivi sasa tunajiandaa kuingia katika vita na Rwanda.Usiku wa kuamkia leo ndege za vita za Rwanda zimevamia ardhi yetu na kufanya mashambulio katika vijiji vilivyo kandoni mwa misitu yetu.Wamefanya hivyo ili kulipiza kisasi kwa kile ulichokifanya kumuua mke wa Rais wa Rwanda,balozi pamoja na raia wengine.Rwanda wanafahamu kwamba unapewa hifadhi na Uganda lakini na hii imekuwa ni sababu ya kutokuelewana nao kwa muda mrefu.Ulichokifanya jana kimefanya mahusiano yetu kuwa magumu zaidi.Tayari nimepeleka vikosi vya jeshi katika mpaka wetu na Rwanda,tuko tayari kwa vita.Katika hili sintarudi nyuma lazima niishikishe adabu Rwanda.Sifahamu kuhusu Congo na Tanzania wao watachukua hatua gani kwani toka lilipotokea shambulio lile sijaweza kuwasiliana na viongozi wake.Rais wa Congo hatuna mahusiano mazuri lakini Rais wa Tanzania hakupokea simu yangu nilipompigia.James kwa hiki ulichokifanya ambacho sasa kinakwenda kuigharimu nchi yetu nimefikia maamuzi ya kukutaka uondoe vikosi vyako nchini Uganda.Tumekuhifadhi kwa muda wa kutosha sasa ni wakati wa kuondoa vikosi kwenda kutafuta hifadhi sehemu nyingine Uganda si sehemu salama tena kwa vikosi vyako.Pale hali itakapotulia utavirejea tena lakini wewe utaendelea kubaki hapa hapa Uganda” akasema Jenerali Akiki na James akashusha pumzi “Mheshimiwa Rais nafahamu nilich………” “James hakuna tena mjadala katika suala hili tayari nimekwisha fanya maamuzi hivyo anza kuandaa vikosi kwa ajili ya kuondoka.Utajua mwenyewe utavipeleka wapi aidha Congo au Sudan lakini nakupa siku mbili uwe tayari umeondoa vikosi vyako katika ardhi ya Uganda.Nadhani umenielewa James si kwamba ninakufukuza bali ni kwa ajili ya usalama wa watu wako” akasema Jenerali Akiki “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” “Sawa.Nasubiri utekelezaji.Kama kutakuwa na tatizo lolote au utahitaji msaada nijulishe tafadhali”akasema Jenerali Akiki na kukata simu DAR ES SALAAM – TANZANIA Ndege ya Patrice Eyenga Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Waziri wa mambo ya nje ya nchi alikuwepo uwanjani pale kumpokea kisha wakaelekea ikulu ambako alikutana na Rais Dr Fabian Kelelo “Pole sana Patrice” akasema Dr Fabian baada ya kumpokea Patrice Eyenga ikulu “Dr Fabian bado sijaamini mpaka sasa kama kweli mke wangu Rebeca amefariki dunia” akasema Patrice Eyenga “Ni ngumu kuamini Patrice lakini ni kweli Rebeca na Millen wamefariki dunia.Hata mimi iliniwia ugumu kuamini nikalazimika kwenda hospitali jana usiku kuthibitisha na kweli wamefariki”akasema Dr Fabian.Patrice Kelelo alichanganyikiwa.Alisimama na kwenda kusimama dirishani.Akatoa kitambaa akafuta machozi “Nimeumia sana Dr Fabian.Rebeca alikuwa ni kila kitu kwangu.Nisingeweza kufika hapa nilipofika leo kama si yeye.Amekuwa ni taa yangu inayoniongoza.Dah ..! Ninakosa hata neno la kusema” akasema Patrice Eyenga “Patrice inaumiza mno.Tukio hili ni la kinyama sana”akasema Dr Fabian “Dr Fabian tukio hili limetokeaje?Hakukuwa na ulinzi wa kutosha?akauliza Patrice “Ulinzi ulikuwa wa kutosha sana” akajibu Dr Fabian “Kama kulikuwa na ulinzi wa kutosha magaidi hao waliwezaje kupenya na kufanya shambulio? Akauliza Patrice “Hilo ndilo ambalo vyombo vyetu vya uchunguzi vinalifanyia kazi kujua namna magaidi hao walivyoweza kupenya na kuingia nyumbani kwa balozi wakatekeleza shambulio lle.Pale uchunguzi utakapokuwa umekamilika tutajua nini hasa kilitokea,lakini kiulinzi tulikuwa tumejiandaa sana” akasema Dr Fabian. “Kama ningejua Rebeca wangu anakuja kufa nisingemruhusu laini sikuwa na wasiwasi wowote na usalama wake ndiyo maana nikamruhusu aje” akasema kwa uchungu Patrice “Patrice lazima tumpate huyu mtu James Kasai.Kwa namna yoyote ile lazima apatikane na alipe kwa hiki alichotufanyia ! akasema Dr Fabian “James Kasai ! akasema Patrice huku akiuma meno kwa hasira “James Kasai bazazi mkubwa Yule ameniulia mke wangu.Ninaapa sintafumba jicho hadi nihAkikishe ametiwa nguvuni ! akasema Patrice Eyenga Wakati mazungumzo yakiendelea Dr Fabian akajulishwa kwamba Rais Benjamin Ntezimana wa Rwanda tayari ametua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na alikuwa njiani kuelekea ikulu “Rais Benjamin tayari ametua na muda wowote atafika hapa”Dr Fabian akamweleza Patrice Eyenga “Benjamin naye anakuja?! akauliza Patrice kwa hamaki “Patrice nafahamu wewe na Benjamin hamtazamani machoni lakini kwa wakati huu wekeni pembeni tofauti zenu.Huu ni wakati ambao mnapaswa kuonyesha mshikamano mkubwa sana na kuunganisha nguvu kupambana na adui yetu mkubwa.Suala hili ni zaidi ya tunavyofikiria.James Kasai katika video yake amesema kwamba ametekeleza tukio lile kwa ajili ya kulipiza kisasi kwako lakini kwa namna ninavyolitazama tukio hilo ni zaidi ya kulipiza kisasi” “Dr Fabian kuna jambo lolote ambalo unalifahamu kuhusiana na tukio lile na hujanieleza?akauliza Patrice “Bado ni mapema sana kusema chochote Patrice lakini kwa namna ninavyolitazama suala hili lilivyopangwa nalazimika kuamini kwamba ni zaidi ya kulipiza kisasi kwa Rebeca” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo halafu akasema “Millen alinifuata siku moja akanieleza kwamba balozi wa DRC Germinus Mapupu alimfuata ofisini kwake na kumueleza kuwa anataka kuwakutanisha wake za marais wa Congo na Rwanda kwa chakula watakapokuwa hapa nchini kuhudhuria mkutano wa wake za marais wa dunia na akamuomba naye ahudhurie na amualike pia na mke wa Rais wa Rwanda kwani asingeweza kukataa mwaliko wake.Mimi nilimuunga mkono kwa suala lile zuri na kumuahidi kumpa ushirikiano mkubwa.Kila mara alikuwa akinipa taarifa za maendeleo ya mpango huo na mimi nilivikabidhi vyombo vya usalama kuhAkikisha ulinzi unaimarishwa.Hadi siku ya tukio niliwasiliana na watu wa usalama na wakanihAkikishia kwamba usalama umeimarishwa lakini usiku nikapewa taarifa kwamba mabomu matatu yamelipuka na mke wangu amefariki dunia” akasema Dr Fabian na kuinamisha kichwa chini “Ningejua kama anakuja Tanzania kuuawa nisingemruhusu aje ! akasema Patrice “Hakuna aliyejua kama tukio lile lingetokea.Wote tuliamini tuko salama na ndiyo maana nilimruhusu hata mke wangu kwenda” akasema Dr Fabian Wakati wakiendelea na maongezi wakajulishwa kwamba Rais Benjamin Ntezimana tayari alikuwa amewasili ikulu.Dr Fabian akatoka kwenda kumpokea akamkaribisha ndani wakazungumza faragha kwa dakika ishirini halafu wakawa na kikao cha pamoja kati ya marais watatu kutoka Tanzania,Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Melanie Davis aliwasili katika makazi ya Gosu Gosu na kumkuta akimsubiri kwani alimpigia simu mapema sana na kumtaka asiende kazini siku ile atakuwa na mazungumzo naye muhimu. “Karibu sana malaika wangu” akasema Gosu Gosu baada ya Melanie kuwasili “Gosu Gosu mpenzi wangu nafahamu tuna mengi ya kuzungumza lakini unafahamu kabla ya kitu chochote nini ninahitaji” akasema Melanie na Gosu Gosu hakutaka mazungumzo zaidi akamfuata pale sofani akambusu na kumuinua akambeba kuelekea chumbani.Mle chumbani hakukuwa na kupoteza muda mtanange ukaanza mara moja.Gosu Gosu ambaye alikuwa na pumzi kama farasi alikwenda mizunguko miwili bila kuchoka na kumpuuza Melanie aliyekuwa akimuomba Gosu Gosu wapumzike kwani alikwisha fika kilele zaidi ya mara tatu. “Leo ulikuwa umenipania sana” akasema Melanie huku akimpiga Gosu Gosu kijikofi kidogo na wote wakaangua kicheko “Sote tulikuwa tumekamiana sana siku ya leo ndiyo maana mchuano ulikuwa mkali sana.Unawezaje kwenda mizunguko miwili bila kuchoka?Kuna kitu unatumia cha kukuongezea nguvu? Akauliza Melanie na Gosu Gosu akaangua kicheko “Situmii chochote cha kuniongezea nguvu.Ninakula vizuri na kuutunza mwili wangu kwa mazoezi ndiyo maana nina uwezo mkubwa namna hii.Kama usingepiga kelele ningeendelea hadi mzunguko wa tatu” akasema Gosu Gosu na wote wakaangua kicheko “Nakupenda sana Gosu Gosu.Sijui nikuelezaje ili ujue namna ninavyokupenda” akasema Melanie “Nafahamu Melanie namna unavyonipenda.Mimi pia nakupenda zaidi ya ninavyoweza kukueleza” akajibu Gosu Gosu na kumbusu Melanie “Ule mpango wa kulipiza kisasi ulifanikiwa vizuri sana.Hongera” akasema Gosu Gosu na Melanie akatoa tabasamu “Mpango wangu umekwenda vizuri sana.Lengo lilikuwa ni kumuua Rebeca peke yake lakini ilishindikana kumuua mwenyewe bila wale wenzake” “Ni tukio kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa wake watatu wa marais kuuawa katika shambulio moja.Naamini uchunguzi mkubwa utafanyika.Nina wasiwasi sitaki uingie katika matatizo mpenzi wangu” akasema Gosu Gosu Melanie akatabasamu na kusema “Relax my Gosu Gosu.Hawana tena haja ya kufanya uchunguzi wakati aliyefanya shambulio lile tayari wanamfahamu.Unadhani kwa nini tulimfuata James Kasai?Ni kwa sababu ya jambo hili.Hivi sasa nguvu yote inaelekezwa kumtafuta yeye” “Ni vipi kama James akikamatwa na akakutaja kwamba unashirikiana naye?Gosu Gosu akauliza “Kwanza si rahisi kukamatwa na pili hata kama akikamatwa na kunitaja mimi sijali kwani nilichokuwa nakitaka kimetimia.Hivi sasa Patrice Eyenga yuko katika majonzi makubwa sana.Moyo wake unakatwa taratibu na kisu kikali.Patrice atakufa taratibu sana kwa mateso anayoyapata kwa kifo hiki cha mke wake” akasema Melanie huku akitabasamu “Vipi kuhusu IS kuhusika katika shambulio lile? “IS ? “Ndiyo.Hawa ni magaidi ambao James amekiri kushirikiana nao” “Gosu Gosu usiwe na wasi wasi wowote tafadhali.Mimi ninayemtambua ni James Kasai na si IS.Kama yeye anashirikiana na magaidi ni juu yake.Gosu Gosu wewe ni mwanajeshi na hupaswi kuwa na wasiwasi wowote” akasema Melanie “Lazima niwe na wasiwasi kwa sababu sitaki uingie katika matatizo” akasema Gosu Gosu “Tuachane na hayo Gosu Gosu kwani leo ni siku ya furaha sana kwa kufanikiwa kulipiza kisasi kwa Patrice Eyenga” akasema Melanie huku Akikichezea kifua cha Gosu Gosu “Gosu Gosu uliwahi kunitamkia kwamba uko tayari kufanya chochote kwa ajili yangu” “Ndiyo Melanie.Niko tayari kufanya chochote kwa ajili yako” “Ahsante sana Gosu Gosu.Kuna mtu nahitaji kumuondoa pia” “Niambie ni nani huyo mtu nikamtoe roho yake hata sasa hivi? Akauliza Gosu Gosu “Hayuko hapa Tanzania.Yuko Paris Ufaransa” akasema Melanie na Gosu Gosu akashusha pumzi na kumuangalia “Ni nani huyo mtu na amefanya nini?akauliza Gosu Gosu “Usitake kujua amefanya nini.Mtu yeyote ambaye ninataka kumuondoa duniani fahamu kwamba amenifanyia jambo zito hivyo hata huyu ambaye nataka kumtanguliza huko waendako wafu amenifanyia jambo baya kabisa.Ninachotaka kujua ni je uko tayari kunisaidia? Akauliza Melanie huku akitabasamu “Melanie nadhani jibu tayari unalo kwamba mimi niko tayari muda wowote ule kufanya chochote kwa ajili yako.Nielekeze mahala anakopatikana mtu huyo na mimi nitakwenda kumtoa roho yake” akasema Gosu Gosu. “That’s my Gosu Gosu” akasema Melanie na kumbusu.Nitakupa taarifa zake zote baadae ila anza kufanya maandalizi kwani unatakiwa kesho kutwa uondoke kuelekea Paris” “Hakuna tatizo Melanie.Nitaanza maandalizi mara moja na nitakwenda kumtoa uhai wake huyo mtu unayemtaka.Kuanzia sasa usihangaike tena kwenda kwa akina James Kasai au kwingineko.Kama unataka kumuondoa mtu uhai niambie mimi nitatekeleza” akasema Gosu Gosu “Nakupenda Gosu Gosu na sitaki kukuingiza katika hatari ndiyo maana ninawatumia watu kama akina James Kasai katika mipango yangu ya kulipiza kisasi.” akasema Melanie huku akitabasamu “Ni watu wangapi ambao bado wako katika orodha ya wale ambao unataka kuwaondoa duniani? Gosu Gosu akauliza “Sina orodha bali nina watu wachache tu ambao nataka walipe uovu wao wakimalizika hao nitakuwa nimewatendea haki wazazi wangu kwani niliwaahidi kuwalipia kisasi” akasema Melanie.Baada ya dakika chache wakaingia tena katika mzunguko mwingine wa tatu halafu Melanie akaondoka kuelekea nyumbani kwake akamuacha GosuGosu akijiandaa kwenda kushughulikia safari ya kuelekea Paris.
Kikao cha faragha baina ya marais wa Tanzania,Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kilichochukua saa tatu kilimalizika halafu marais wote watatu wakajitokeza mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wamekusanyika ikulu wakisubiri kikao kile kimalizike ili wapate walau neno kutoka kwa marais wale.Toka lilipotokea shambulio lile baya Rais wa Tanzania Dr Fabian hakuwa amezungumza lolote.Vituo karibu vyote vya matangazo vilikatisha matangazo yao na kujiunga moja kwa moja ikulu kusikiliza hotuba ya Rais. Ndani ya ukumbi watu wote wakasimama baada ya marais kuingia.Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais hakupoteza muda akamkaribisha moja kwa moja Rais Dr Fabian aweze kusema neno kwa niaba ya marais wenzake wa Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. “Poleni sana ndugu waandishi wa habari kwa kutusubiri muda mrefu.Tulikuwa na kikao kizito kidogo ndiyo maana tumechelewa” akasema Dr Fabian halafu akaitazama karatasi yake na kuendelea “Ndugu wanahabari awali ya yote nipende kuwashukusu sana kwa kufika kwenu kwa wingi.Nimeelezwa kwamba wengi wenu mmefika hapa toka asubuhi lakini hamjakata tamaa kusubiri ili kuwapelekea watanzania taarifa” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Ndugu zangu siku ya jana nchi yetu na jumuiya ya Afrika Mashariki imepata pigo kubwa.Watu wasio na hata chembe ya huruma wamefanya shambulio ambalo limepelekea mauaji ya watu hamsini na saba kupoteza maisha na miongoni mwao ni wake za marais wa Rwanda,jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na mke wangu mimi,pia mabalozi wa Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wao wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na familia zao wamepoteza maisha.Hili ni moja ya tukio baya kabisa. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ndugu Germinus Mapupu ambapo walikuwa wamehudhuria hafla ya chakula cha jioni ambacho balozi Germinus Mapupu alikuwa amekiandaa kwa ajili ya bi Rebeca Muyenga mke wa Rais wa Congo na Agatha Ntezimana mke wa Rais wa Rwanda.Lengo kubwa la kuandaa chakula hicho lilikuwa ni kuwakutanisha pamoja wake hao za marais ikiwa ni katika jitihada za kuondoa tofauti zao.Kama mnavyofahamu kwa muda sasa nchi za Rwanda na Congo hazina maelewano mazuri na balozi Mapupu alitaka kutumia fursa hii ambayo wake hao za marais wote wanakutana hapa Dar es salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kutafuta maelewano baina ya nchi zao lakini lengo lake hilo jema halikuweza kufanikiwa kwani wote waliuawa.Ni ukatili mkubwa sana ambao haukubaliki. Baada ya tukio lile la mauaji hayo ya kinyama mtu anayejiita James Kasai alijitokeza na kusambaza video akidai kuhusika katika shambulio hilo akishirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS ambacho kwa miaka ya karibuni kimekuwa kikijiimarisha sana katika bara la Afrika hususan ukanda huu wa Afrika Mashariki.Si mara ya kwanza kwa kikundi cha IS kufanya shambulio katika nchi yetu.Watanzania bado hawajasahau kitendo walichokifanya IS miaka michache iliyopita pale walipoteka wanafunzi na kuwachinja kama kuku na sasa wamerejea tena” Dr Fabian akanyamaza kwa sekunde chache halafu akasema Huyu mtu anayeitwa James Kasai ni nani? Akauliza Dr Fabian na kunyamaza akameza mate “James Kasai anatokea nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na anaongoza kikundi cha waasi ambao kwa miaka zaidi ya kumi wamekuwa wakipigana na serikali.Alipoingia madarakani Rais Patrice Eyenga aliwaita mezani viongozi wa makundi yote ya serikali ambayo kwa miaka mingi yalikuwa yakipigana na serikali kwa lengola kutafuta amani lakini ni James Kasai pekee ambaye alikataa kushiriki katika majadiliano ya kuleta amani ya Congo na aligoma kuweka silaha chini hivyo akafurushwa na jeshi la Congo na inaaminika alikimbilia katika misitu ya Kaskazini mwa Uganda na sasa ameamua kushirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS na kufanya shambulio baya katika ardhi yetu.James Kasai amekuwa ni tishio kubwa si kwa Tanzania tu bali kwa jumuiya nzima ya Afrika Mashariki na hatuwezi kumuacha akaendelea kuwa tishio kwa nchi zetu lazima uovu wake ufike mwisho Mimi na wenzangu marais wa Rwanda na jamhuri ya kidemokrasi ya Congo tumekuwa na kikao kizito cha faragha na katika kikao hicho tumeazimia kuunganisha nguvu kuhAkikisha tunampata James Kasai akiwa mzima au amekufa.Kila nchi itatoa kikosi cha wanajeshi na tutaunda kikosi kimoja ambacho kitakuwa na silaha na zana kali za kivita ambacho kitakwenda kumsaka James Kasai kokote aliko.Kitapanda milima na mabonde,kitavuka mito na bahari,misitu na nyika na kuhAkikisha James Kasai anatikana akiwa mzima au mfu.Narudia tena tutapanda milima na mabonde,tutavupa mito na bahari,misitu na nyika tukimsaka James Kasai na lazima tumpate akiwa mzima au amekufa. Tunaamini James Kasai yuko katika misitu iliyo Kaskazini mwa Uganda na tunaamini serikali ya Uganda wanalifahamu hilo lakini wamekuwa wakimkingia kifua hivyo basi tunaitaka serikali ya Uganda ihAkikishe inashirikiana na kikosi ambacho kitaundwa kwa ajili ya kumtafuta James Kasai.Mtu huyu mkatili asiye na hata chembe ya ubinadamu yuko ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kwa mujibu wa taratibu za jumuiya ya Afrika Mashariki kunapotokea kitisho chochote katika mojawapo ya nchi wanachama basi nchi nyingine zote wanachama hujitolea vikosi vya jeshi ambavyo vitakwenda kupambana kuhAkikisha kwamba nchi hiyo inakuwa salama.James Kasai ni hatari si kwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo pekee bali kwa jumuiya nzima ya Afrika Mashariki hivyo nchi wanachama zinatakiwa kuunganisha nguvu kupambana na adui huyu na ninawaahidi wana Afrika mashariki tutamfutilia mbali James Kasai.Siku zake zinahesabika” Dr Fabia akanyamaza baada ya mpambe wake kumsogelea na kumpa kijikaratasi kilichosomeka “Miili iko tayari kuelekea uwanja wa ndege” Dr Fabian akakisoma kijikaratasi kile halafu akaendelea na hotuba yake Narejea tena kuwapeni pole wana jumuiya ya Afrika Mashariki kwa msiba huu mzito uliotupata.Mimi nikiwa mwenyekiti wa jumuiya hii ninawahAkikishia kwa kushirikiana na wenzangu tutahAkikisha jumuiya yetu inakuwa salama.TutahAkikisha hakuna tena kitisho chochote cha namna hii na watu kama hawa wanaondolewa haraka sana katika jumuiya yetu pale tu wanapoibuka. Mungu ibariki Afrika Mashariki Ahsanteni kwa kunisikiliza Dr Fabian akamaliza hotuba yake fupi na hakukuwa na nafasi yoyote ya kuuliza maswali.Akawaongoza wale maraisi wenzake kutoka ndani ya ukumbi ule wakaelekea nje ambako magari yalikuwa yameandaliwa na kwa pamoja wakaondoka kuelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ambako miili ya marehemu ilikuwa inapelekwa tayari kwa kusafirishwa kuelekea katika nchi zao. Msafara wa marais watatu uliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambako kuliandaliwa shughuli maalum kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu kabla ya kusafirishwa.Marais walichukua nafasi zao wakindelea kusubiri miili iwasili.Watu walikuwa wengi wakiwa wamekaa kwa utulivu mkubwa na simanzi katika mahema huku kwaya ikiwa jukwaani ikiimba kuwafariji .Ulinzi ulikuwa mkali mno eneo lote la uwanja wa ndege. Dakika chache baada ya marais kuwasili pale uwanja wa ndege wa Julus Nyerere magari yaliyobeba majeneza yenye miili ya marehemu yakawasili na kufuata utaratibu majeneza yakashushwa na kupangwa.Viongozi wa dini waliokuwepo mahala pale wakapewa nafasi ya mwanzo ya kuwaombea marehemu.Hakukuwa na hotuba yoyote iliyopangwa kutolewa pale uwanjani hivyo baada ya viongozi wa dini kuwaombea marehemu likafuata zoezi dogo la kuaga miili ya marehemu.Waliopangwa kuaga miili ile pale uwanjani ni wafanyakazi wa balozi za Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vile vile raia wa nchi hizo wanaoishi hapa nchini.Kulikuwepo vile vile na kundi la wake za marais walikuwa wamefika nchini kuhudhuria mkutano wa wake za marais ulioandaliwa na mke wa Rais wa Tanzania marehemu Millen Kelelo.Majeneza hayakufunguliwa bali watu walipita mbele yake kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.Wakati zoezi likiendelea,taratibu ndege mbili za jeshi zilianza kusogea na kujipanga vizuri.Zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa miili ile ya marehemu lilimalizika na wanajeshi wakasogea wakabeba jeneza lenye mwili wa marehemu Agatha Ntezimana mke wa Rais wa Rwanda wakaupeleka katika ndege ya jeshi,ukafuatia mwili wa balozi wa Rwanda na mke wake pamoja na watu wengine wa kutoka Rwanda waliouawa katika shambulio.Lango la ndege likafungwa na ndege ikaondoka.Kikosi kingine cha askari wakabeba jeneza lenye mwili wa marehemu Rebeca Eyenga mke wa Rais Patrice Eyenga wa jamhuri ya kidemokrasia na kuupakia katika ndege ikafuatia miili ya balozi Germinus Mapupu na mingine ya watu kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo waliouawa katika shambulio.Lango la ndege likafungwa na ndege ikapaa kuelekea Kinshasa.Lilikuwa ni tukio lililoleta simanzi kubwa.Dakika tatu baada ya ndege za jeshi kuondoka,ndege ya Rais Patrice Eyenga ikasogea akakumbatiana na Dr Fabian Kelelo pamoja na Rais Benjamin Ntezimana kisha akaelekea katika ndege yake ambayo haikuchukua muda ikapaa na kuondoka.Baada ya muda mfupi ndege ya Rais Benjamin nayo ikasogea akaagana na Dr Fabian akapanda ndegeni naye akaondoka kuelekea Kigali. Rais Dr Fabian Kelelo akaenda kuwasalimu wanakwaya waliofika pale kuwafarijji waombolezaji,akasalimiana pia na viongozi wa dini,akaagana na baadhi ya wake za marais waliokuwa wamekuja kuhudhuria mkutano wa wake za marais kisha akaondoka pale uwanjani kurejea ikulu “James Kasai ! akawaza Dr Fabian akiwa garini.Jina hili lilipita kichwani kwake kila mara na kumfanya akunje sura kwa hasira “Bazazi huyu nitamfundisha adabu.Hiki alichokifanya atalipa kwa gharama kubwa sana” akawaza na kuchukua simu akazitafuta namba za simu za Rais wa Uganda akampigia na kuelezwa kwamba yuko katika kikao muhimu “Huyu ndiye ambaye amemuhifadhi James Kasai nchini Uganda japokuwa amekuwa akikanusha vikali kufanya hivyo lakini ukweli tunao kwamba James Kasai yuko nchini Uganda na sintajali kama mimi na yeye ni marafiki,tunakwenda kuvamia Uganda kumtafuta James Kasai.Sijali kitakachotokea kama ni vita niko tayari kuingiza nchi vitani lakini lazima James apatikane” akawaza Dr Fabian ambaye sura yake ilitawaliwa na majonzi makubwa. Alipokaribia kufika ikulu simu yake ikaita alikuwa ni Jenerali Akiki Rwamirama Rais wa Uganda.Dr Fabiana akaitazama simu ile kwa hasira kisha akaipokea “Hallow mheshimiwa Rais” akasema Dr Fabian “Dr Fabian nimeikosa simu yako nilikuwa katika kikao muhimu” “Mheshimiwa naomba nikupigie simu baada ya dakika tano” akasema Dr Fabian na kukata simu.Gari lilifika ikulu akashuka na kuelekea chumbani kwake akachukua simu na kuvuta pumzi ndefu kisha akampigia Jenerali Akiki “Dr Fabian habari yako.Pole sana kwa tukio lililotokea.Mara tu nilipopata taarifa za tukio lile nilikupigia simu kukupa pole lakini simu yangu haikupokelewa.Kwa niaba ya wananchi wa Uganda ninakupa pole sana kwa tukio lililotokea.Tuko pamoja na msiba huu ni wetu sote.Pole sana mheshimiwa Rais” akasema Jenerali Akiki na sura ya Dr Fabina ikajikunja kwa hasira “Jenerali Akiki hauko pamoja na sisi na usinidanganye kwamba msiba huu umekugusa! “Kwa nini unasema hivyo mheshimiwa Rais? Sisi ni ndugu.Uganda na Tanzania tuna mahusiano ya kindugu hivyo msiba huu ni msiba wa Tanzania ni msiba wa Uganda na ni msiba wa Afrika mashariki.Uganda tunalia kama mnavyolia watanzania Congo na Rwanda” akasema Jenerali Akiki “Kama kweli msiba huu umekugusa nataka unieleze mahala alipo James Kasai ! akasema Dr Fabian “James Kasai? “Ndiyo.Humfahamu? “Ninamfahamu James Kasai lakini hayupo Uganda ! “Usinidanganye Jenerali Akiki.James Kasai yuko Uganda na umempa hifadhi” “Hilo si kweli Dr Fabian.James Kasai hayupo nchini Uganda.Taarifa nilizonazo ni kwamba James Kasai amejificha katika misitu ya Congo.Tafadhali usiziamini taarifa zinazotolewa na Congo na Rwanda wakidai kwamba James Kasai yuko Uganda” “Jenerali Akiki,tunao ushahidi wa kutosha kwamba James yuko nchini Uganda na kwa kuwa hutaki kuweka wazi mahala alipo,sisi tunaandaa kikosi ambacho kitaingia katika misitu ya Uganda kuendesha operesheni ya kumsaka.Itakuwa ni operesheni kubwa kuwahi kufanywa na vikosi vya afrika mashariki.Tutapita msitu kwa msitu hadi tuhAkikishe James Kasai anapatikana akiwa mzima au mfu ! akasema Dr Fabian ambaye uso wake ulionyesha hakuhitaji masihara.Zilipita sekunde kadhaa Jenerali Akiki akasema “Usiku wa kuamkia jana,ndege za jeshi la Rwanda zilivamia anga letu na kufanya mashambulizi katika vijiji vilivyopo kandoni mwa misitu iliyopo Kaskazini ambako wanadai James Kasai amejificha.Katika mashambulio hayo watu tisa waliuawa na vijiji kadhaa kharibiwa vibaya.Vikosi vya jeshi letu la anga vilifanikiwa kuangusha ndege mbili za Rwanda zilizoingia katika anga letu kwa lengo la kufanya mashambulizi” akanyamaza kidogo na kuendelea “Asubuhi ya leo nimezugumza na vikosi vya jeshi na nimeagiza vikosi vyote vya jeshi vikae katka utayari wa vita.Tayari nimepeleka vikosi katika mpaka wetu na Rwanda na muda wowote vikosi vitaingia Rwanda kulipiza kisasi kwa kile ambacho tunakiita ni uchokozi mkubwa.Rwanda wametuvamia na kuua watu wetu bila hata kuwa na uhakika kama kweli James Kasai yupo nchini Uganda.Kitendo kile hakivumiliki na hakiwezi kuachwa hivi hivi lazima tuchukue hatua kali ndiyo maana nataka niifanye nchi ya Rwanda kama mfano kwa wale wengine wote ambao wanataka kufanyia mchezo Uganda.Naomba nikuweke wazi Dr Fabian kwa kuwa wewe ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwamba ninajiandaa kuingia katika vita na Rwanda na nchi nyingine yoyote ambayo itathubutu kuvamia Uganda” akasema Jenerali Akiki “Jenereali Akiki tafadhal usithubutu kufanya hicho unachotaka kukifanya.Ukithubutu kuivamia kijeshi Rwanda basi nchi zote za Afrika mashariki zitamuunga mkono Rwanda” “Hilo haliniogopeshi Dr Fabian.Umekwisha nihAkikishia kwamba mmekutana Dar es salaam na marais wa Rwanda na Congo na tayari mmepanga kuivamia Uganda.Ninawaonya msithubutu kufanya hivyo.Msithubutu kamwe kutuma wanajeshi wenu nchini Uganda kwani hawatafika kokote nitawafyekelea mbali.Jeshi langu limekwisha jiandaa na liko tayari kwa vita.Siogopi kama mtaunganisha nguvu lakini nataka kukuhAkikishia jambo moja kwamba jeshi langu linao uwezo wa kupambana na majeshi yenu yote.Nakuonya Dr Fabian usiingize nchi yako vitani utajutia uamuzi wako.Jeshi la Uganda la sasa si lile la Iddi Amin mliyemchakaza wakati ule.Hili ni jeshi jipya ambalo lina uwezo wa kupambana na majeshi ya nchi yoyote.Ninawakaribisha wanajeshi wenu lakini chimbeni makaburi ya kutosha kwani hakuna atakayerejea nyumbani salama.Hakuna ambaye atavamia ardhi ya Uganda akatoka akiwa salama.Hivi si vitisho nazungumza ukweli na kama hamuamini ninachokisema basi subirini muone kile kitakachotokea nchini Rwanda ! akasema Jenerali Akiki na kukata simu “Aaagh !! akasema kwa hasira Dr Fabian “Hakuna nchi yoyote ndani ya Afrika Mashariki inayoweza kuitisha Tanzania kijeshi.Akiki akitaka kupigana na Tanzania utakuwa ndio mwisho wake.Tutatuma kwanza kikosi cha umoja kwenda kumtafuta James Kasai na kama ikionekana upo ulazima basi nitalituma jeshi la wananchi kwenda Uganda lakini operesheni kama hii ni ndogo.Kikosi kidogo tu kitakwenda kikishirikiana na vikosi vingine kutoka Rwanda na Congo” akawaza Dr Fabian na simu yake ikaita akajulishwa kuwa anahitajika katika kamati ya maandalizi KAMPALA – UGANDA Baada ya kumaliza mazungumzo na Dr Fabian,Jenerali Akiki akampigia simu James Kasai “Mheshimiwa Rais” akasema James Kasai “James nimekupigia tena.Nimetoka kuzungumza na Rais wa Tanzania muda mfupi uliopita na mazungumzo yetu hayakwenda vizuri.Kwa mara ya kwanza tumefokeana na kutoleana vitisho vya kushambuliana kijeshi.Jambo lingine ni kwamba marais wa Congo na Rwanda wote wamekutana nchini Tanzania na kwa pamoja wamekubaliana kuunda kikosi ambacho kitafanya operesheni ya kijeshi kukusaka.Hivi tuzungumzavyo tayari maandalizi ya kikosi hicho yameanza na pale kitakapokuwa tayari kitatumwa Uganda.Wanafahamu mahala vilipo vikosi vyako hivyo kwa usalama wao nakuomba uviondoe ili kikosi hicho kitakapofika wakute tayari wamekwisha ondoka” akasema Jenerali Akiki “Nimekuelewa mheshimiwa Rais na tayari maandalizi yamekwisha anza ya kuondoka.Nategemea usiku wa leo vijana wataanza safari.Nitakujulisha pale watakapokuwa wameanza kuondoka” “Vizuri sana.Endapo kuna msaada wowote utauhitaji usisite kunijulisha mara moja nitakusaidia” akasema Jenerali Akiki “Nashukuru sana mheshimiwa Rais kwa kila kitu.Pale nitakapokuwa na uhitaji wa chochote basi nitakujulisha” akasema James Kasai na kuagana na Rais. “Pamoja na umuhimu wake kwetu lakini James Kasai ameniingiza katika matatizo makubwa sana.Amevuruga mahusiano yetu mazuri na nchi nyingine za Afrika Mashariki na hadi tumefikia hatua ya kutishiana kijeshi.Sikupenda kabisa kulumbana na Rais wa Tanzania ambao wamekuwa ni ndugu zetu kwa miaka mingi lakini imelazimu kufanya hivyo kwa ajili ya kumlinda James.Sitaki kuingia katika vita na Tanzania kwani ina jeshi bora mno…” akawaza Jenerali Akiki na kukuna kichwa. “Kwa sasa mambo yamekwisha haribika nimekwisha tunisha misuli hivyo sitakiwi kulegea.Natakiwa kuendelea kutunisha misuli ili kuonyesha kweli nimedhamiria kupigana na jeshi la nchi yoyote ambayo itathubutu kuvuka mpaka na kuingia Uganda.Kwa nchi ya Rwanda lazima niipe onyo ili siku nyingine wasirudie kitendo walichokifanya cha kuvuka mpaka na kushambulia Uganda” akawaza Jenerali Akiki na kumpigia simu waziri wa mambo ya nje wa Uganda akamtaka awarejeshe nyumbani mabalozi wa Uganda walioko katika nchi za Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na vile vile akamtaka awaelekeze mabalozi wanaoziwakilisha nchi hizo nchini Uganda waondoke haraka sana Uganda ndani ya saa ishirini na nne. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ilikaribia saa moja za jioni jijini Dar es salaam muda ambao Melanie Davis alikuwa akijiandaa kwenda nyumbani kwa Gosu Gosu kwani waliahidiana kukutana jioni ya siku ile kwa ajili ya mazungumzo.Akiwa chumbani kwake akijiandaa simu yake ikaita akatazama mpigaji alikuwa ni katibu wake muhtasi Frimina “Mina unasemaje?akauliza Melanie “Madam kuna tatizo” akasema Frimina na Melanie akastuka kidogo “Kuna tatizo gani? akauliza “Nimepata taarifa muda si mrefu kwamba Gosu Gosu amepigwa risasi” “Gosu Gosu ! Oh my God ! Melanie akastuka sana na kuangusha kifaa alichokuwa amekishika mkononi “Madam Melanie ! akaita Frimina “Mina kuna kitu kimoja tu ambacho nataka kukisikia kutoka kwako.Is he okay? “Nimeambiwa kwamba amekimbizwa hospitali na hali yake ni mbaya sana” “Yuko hospitali gani?akauliza Melanie “Nimeambiwa amepelekwa hospitali kuu ya Mtodora” akasema Frimina na Melanie akahisi miguu yake inaisha nguvu akakaa kitandani. “Gosu Gosu jamani ! akasema Melanie.Hakupoteza muda akachukua mkoba wake na kutoka mbio akamfuata Joyce akamtaka ampeleke katika hospitali ya Mtodora “Gosu Gosu tafadhali naomba usiniache.Bado ninakuhitaji sana katika maisha yangu.Una umuhimu mkubwa” akawaza Melanie huku machozi yakimporomoka “Ni nani hawa waliompiga risasi Gosu Gosu na kwa nini? Akaendelea kujiuliza maswali. “Endapo Gosu Gosu akifariki dunia litakuwa ni pigo lingine kubwa kwa upande wangu.Ni mtu ninayemtegemea kwa mambo mengi.Kama si yeye nisingeweza kuonana na James Kasai.Ni yeye ambaye kila wakati anaifanya akili yangu ikae sawa.Ni mtu muhimu sana katika maisha yangu” akaendelea kuwaza huku gari likiwa katika mwendo mkali kuelekea hospitali.Mara kwa mara alivua miwani na kufuta machozi “Gosu Gosu kupigwa risasi imetonesha kidonda changu.Kitendo hiki kimenikumbusha machungu ya wazazi wangu.” akawaza na kuendelea kufuta machozi Walifika katika hospitali ya Mtodora na Melanie akashuka na kukimbia hadi katika jengo la mapokezi akajitambulisha kuwa ndugu yake amepigwa risasi na ameletwa pale hospitali. “Kuna wagongwa kadhaa wamepokelewa hapa hospitali jioni hii wakiwa na majeraha ya sirasi.Ndugu yako anaitwa nani?akauliza muuguzi wa mapoezi “Gosu Gosu”akatamka Melanie na Yule muuguzi akatazama katika kompyuta yake “Papi Gosu Gosu” akasema Yule muuguzi “Ndiyo” “Mgonjwa wako yuko hapa hospitali lakini kwa sasa ameingizwa katika chumba cha upasuaji” akasema Yule muuguzi na kumuelekeza Melanie kilipo chumba cha upasuaji kisha kwa haraka akiwa na Joyce wakaelekea huko. Mlango wa chumba cha upasuaji ulikuwa umefungwa na hakuruhusiwa mtu asiyehusika kuingia ndani ya chumba kile hivyo kuwalazimu akina Melanie kusubiri nje. “Ee Mungu naomba umponye Gosu Gosu” hii ndiyo kauli ambayo Melanie alibaki anaitamka kimoyo moyo.Alishindwa kukaa akanyanyuka na kuanza kuzunguka zunguka “Madam Melanie kaa upumzike tafadhali.Hatujui upasuaji huo utachukua muda gan..” akasema Joyce na mara mlango ukafunguliwa akatoka muuguzi mmoja aliyevaa mavazi ya kijani Melanie akamkimbilia “Dada samahani” akasema Melanie na Yule muuguzi akasimama “Ndugu yangu ameingizwa humu kufanyiwa upasuaji amepigwa risasi vipi hal….” “Bado yuko kwenye upasuaji.Endeleeni kusubiri hadi upasuaji ukimalizika mtajulishwa kila kitu” akasema Yule mwanadada na kuendelea na safari “Madam Melanie kaa utulie utachoka sana ukiendelea kusimama.Yawezekana upasuaji ukachukua muda mrefu” akasema Joyce “Nashindwa kukaa Joyce.Ninapata wakati mgumu sana” akajibu Melanie na kuchukua simu akampigia Frimina “Frimina tayari niko hapa hospitali lakini Gosu Gosu ameingizwa katika chumba cha upasuaji niko hapa na Joyce tunasubiri upasuaji umalizike.Nataka uniambie tukio hili limetokea wapi? “Gosu Gosu leo hakuwepo kazini kwa siku nzima lakini jioni ya leo alikuja ofisini kwake kuna vitu alikuja kuchukua akaniaga kwamba atakuwa na safari ya Paris kesho kutwa.Muda mfupi baada ya kuondoka nikapigiwa simu na walinzi kwamba Gosu Gosu amepigwa risasi wakati akijiandaa kuingia barabara kuu.Inadaiwa kwamba walijitokeza watu wawili waliokuwa na pikipiki kubwa wote wakiwa wamevaa mavazi meusi na kofia ngumu kichwani hivyo sura zao hazikuweza kuonekana.Mmoja aliyekuwa nyuma alikuwa na bunduki ndogo akaanza kulimiminia risasi gari la Gosu Gosu huku mwenzake akimimina risasi juu kuzuia watu wasisogee eneo lile na baada ya kuhAkikisha kwamba wamemimina risasi za kutosha wakaondoka na hakuna mpaka sasa aliyewatambua watu hao ni akina nani” akasema Frimina “Dah ! akasema Melanie na kushika kiuno “Ahsante Frimina.Nitaendelea kuwasiliana nawe kuhusiana na kile kinachoendelea hapa” akasema Melanie na kukata simu “Ni nani hawa waliomshambulia Gosu Gosu?Nini walikuwa wanakihitaji kutoka kwake?Nadhani hawa jamaa lengo lao lilikuwa ni kumuua tu” akaendelea kuwaza Walikaa pale nje kwa muda wa saa tano ndipo alipotoka daktari na kuwapa taarifa “Poleni sana kwa kusubiri.Tumefanya upasuaji wa kuondoa risasi mwilini mwa mgonjwa wenu.Jumla alikuwa amepigwa risasi kumi na mbili katika sehemu mbali mbali za mwili wake.Risasi mbili alipigwa katika bega la kulia,risasi moja katika kiganja cha mkono wa kulia,saba katika sehemu ya juu ya paja,na mbili sehemu ya chini ya mguu wa kulia.Inaonekana mshambuliaji alikuwa upande wa kulia kwani ndio hasa ulioshambuliwa.Risasi nyingine zaidi ya kumi hazikuweza kuingia mwilini mwake kwa kuwa alikuwa amevaa fulana isiyopenya risasi na bila fulana hiyo asingeweza kuwa hai hadi sasa kwani inaonekana washambuliaji hao walikuwa na lengo la kuua kabisa.Kwa sasa atapelekwa katika chumba cha uangalizi maalum huku tukiangalia hali yake kwa ukaribu zaidi” akasema daktari “Daktari nakushukuru sana kwa kazi kubwa mliyoifanya lakini naomba ufanye kila lililo ndani ya uwezo wako kuhAkikisha ndugu yangu anapona na kama utaona kuna ulazima wa kumpeleka nje ya nchi basi usisite kunishauri hivyo daktari nakuomba sana” akasema Melanie huku michirizi ya machozi ikionekana machoni pake “Usijali mama.Ni kazi yetu kuhAkikisha tunaokoa maisha ya kila mgonjwa anayeletwa hapa hospitali.Nakuahidi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhAkikisha mgonjwa wako anapona”akasema Melanie na kuelekeza macho mlangoni ambako mlango mkubwa ulifunguliwa na kitanda kikatolewa kikisukumwa na wauguzi.Juu ya kitanda kile alikuwa amelala Gosu Gosu akiwa hana fahamu.Melanie na Joyce wakawafuata wauguzi wale hadi katika chumba cha uangalizi maalum ambako akina Melanie hawakuruhusiwa kuingia kwa usiku ule “Madam hakuna tunachoendelea kukifanya hapa twende nyumbani ukapumzike kisha tutakuja tena kesho alfajiri kujua maendeleo ya mgonjwa.Kama kutakuwa na mabadiliko yoyote wauguzi wapo watatujulisha” akasema Joyce “Ni kweli Joyce.Twende tukapumzike” akasema Melanie.Joyce akazungumza na wauguzi na kuwataka wawajulishe endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote kwa mgonjwa. Waliondoka pale hospitali huku kichwa cha Melanie kikiwa kizito kwa mawazo akijiuliza ni nani waliofanya tukio lile na kwa nini Gosu Gosu amepigwa risasi? “Joyce twende nyumbani kwa Gosu Gosu.Nataka nikazungumze na mtumishi wake wa ndani” akasema Melanie na Joyce akaendesha gari hadi nyumbani kwa Gosu Gosu.Walinzi wote walikuwa wakimfahamu hivyo wakamkaribisha ndani na kumuamsha mtumishi wa ndani wa Gosu Gosu kama Melanie alivyokuwa ameelekeza. “Karibu sana mama Melanie” akasema Yule mtumishi ambaye alionekana kutofahamu chochote kilichokuwa kimetokea “Ahsante nashukuru” akasema Melanie “Mama chumbani kwa kaka kuko wazi kama unataka kwenda lakini yeye bado hajarudi hadi mida hii” akasema Yule mtumishi “Lucy hilo ndilo hasa lililonileta hapa”akasema Melanie na kunyamaza kidogo “Nimetokea hospitali.Gosu Gosu amepatwa na matatizo” “Matatizo gani?akauliza Lucy kwa mstuko “Amepigwa risasi na watu wasiojulikana” akasema Melanie na Lucy akaangua kilio “Tafadhali usilie Lucy.Gosu Gosu hajafa lakini hali yake si nzuri yuko katika chumba cha uangalizi maalum baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi alizokuwa amepigwa” akasema Melanie na kumlazimu Joyce kumbembeleza Lucy anyamaze “Nimekuja hapa kukupa taarifa hizo kwani niliamini bado hujazipata hata hivyo kuna jambo nataka unisaidie kulifahamu” “Jambo gani? “Nataka kujua kama kuna mtu yeyote wa karibu wa Gosu Gosu unayemfahamu aidha ndugu au rafiki” akasema Melane na Lucy akamtazama kwa wasi wasi mkubwa. “Usihofu Lucy Gosu Gosu ni mzima” akasema Melanie baada ya kuutambua wasiwasi mkubwa aliokuwa nao Lucy “Rafiki yake mkubwa ambaye ninamfahamu anaitwa Austin” “Austin? “Ndiyo” “Anaishi wapi huyo Austin? “Sifahamu anaishi wapi lakini ninazo namba zake za simu kama ukitaka kuwasiliana naye” akasema Lucy na kwenda chumbani akachukua simu yake na kumpa Melanie namba za simu za Austin akaziandika katika simu yake akampigia “Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili baada ya kupokea simu “Hallow Austin” akasema Melanie “Nani mwenzangu? Akauliza Austin kwa mshangao kidogo “Naitwa Melanie Davis.Unamfahamu Papi Gosu Gosu? “Ndiyo ni rafiki yangu.Kuna nini? Akauliza Austin “Naomba nikujulishe kwamba Gosu Gosu amepatwa na matatizo” “Matatizo gani? “Amepigwa risasi na watu wasiojulikana jioni ya leo” “Tafadhali usinitanie”akasema Austin “Si utani ni kitu cha kweli kabisa.Alikimbizwa hospitali amefanyiwa upasuaji na kwa sasa amewekwa katika chumba cha uangalizi maalum.Nimetoka huko sasa hivi”akasema Melanie “Wewe uko wapi hivi sasa” akauliza Austin’ “Kwa sasa niko hapa nyumbani kwake na mfanyakazi wake Lucy ndiye aliyenipa namba zako” “Ahsante sana kwa taarifa hii.Ninaelekea hospitali sasa hivi” akasema Austin na Melanie akakata simu akaagana na Lucy wakaondoka kurejea nyumbani. Alipofika nyumbani kwake akapitiliza moja kwa moja chumbani akautupa mkoba sofani “Kichwa kinaniuma sana” akawaza Melanie na kwenda kuchukua chupa ya mvinyo akaenda kuketi sofani na kuanza kunywa.Mara akasikia mlio fulani ukitoka katika mojawapo ya simu yake.Ulikuwa ni mlio wa kumfahamisha kwamba kwamba kuna mtu alimpigia simu lakini akamkosa.Akainuka akaenda kuzitazama simu zake na mojawapo ya simu iliyopigwa ni ya Devotha. “Devotha anataka nini ?Amepiga simu mara sita ! akawaza na kuamua kumpigia “Hallo Devotha” akasema Melanie baada ya simu yake kupokelewa “Hallo Melanie.How’s Gosu Gosu?akauliza Devotha kwa sauti yenye kicheko kidogo ndani yake “Gosu Gosu? “Ndiyo anaendeleaje?Is he dead? Akauliza Devotha na Melanie akawa kimya huku akihema haraka haraka.Sura yake ilibadilika “Sikiliza Melanie” akasema Devotha “Usihangaike kuumiza kichwa chako nani waliompiga risasi Gosu Gosu?My people did” akasema Devotha “What?! You wanted to kill him?Why Devotha ?! akauliza Melanie kwa uchungu “Nilitaka kumuua kabla hajaniua” akasema Devotha.Melanie akastuka sana kwa kauli ile ya Devotha “Kwa nini unasema hivyo? Akauliza Melanie “Melanie Davis bado u mchanga sana katika mambo haya hivyo siku zote usitake kushindana na wakubwa zako.Ulidhani sintajua kama umemtuma Gosu Gosu aje Paris kuniua? Akauliza Devotha na Melanie akawa kimya “Nafahamu mipango yako yote ninafuatilia kila unachokifanya Melanie.Ninafahamu Gosu Gosu alikuwa aondoke kesho kuja Paris kuniua.Ulifikiria nini kumtuma Gosu Gosu aje kuniua Melanie?Do you think it’s easy to kill someone like me? Akauliza Devotha huku akitoa kicheko “Bahati yake Yule jamaa ana maisha marefu kama paka lakini ule ni ujumbe kwamba hata wewe ninaweza nikakumaliza muda wowote ninaotaka hivyo nataka uende katika mstari tunaotaka sisi.Nikikuelekeza fanya jambo Fulani tekeleza na ukitaka kwenda kinyume chake matokeo yake hayatakuwa mazuri.Hili ni onyo la mwisho kwako na ukithubutu tena kutaka kufanya mambo unavyotaka wewe nitakuondoa haraka bila kusita na kumuweka mtu mwingine.Umenisikia Melanie?akauliza Devotha.Melanie alikuwa anatetemeka kwa ndani. “Melanie umenielewa? “Nimekuelewa” “Good.Prepare yourself for the next mission” akasema Devotha na kukata simu. “Oh my God ! akasema Melanie na kuvuta pumzi ndefu akaitupa simu kitandani “Is this real or I’m dreaming?akajiuliza “Devotha amefahamuje kama nimepanga mipango na Gosu Gosu ya kwenda kumuua?Kwa vyovyote vile lazima kuna namna ambayo amesikia mazungumzo yetu.Hakuna mwingine ambaye nimemueleza jambo hili zaidi ya Gosu Gosu pekee.Nadhani ipo namna ambayo hawa watu wamefanya ili kuwawezesha kufuatilia kila ninachokifanya na kusikia kila ninachokizungumza.Naamini hivyo kwa sababu sifahamu Devotha alifahamu vipi kuhusu mimi kumfuata James Kasai? Niliporejea kutoka Uganda alinipigia na kunieleza kwamba anafahamu nimetoka kuonana na James Kasai.Nilijiuliza sana amefahamu vipi sikupata jibu lakini sasa nimefahamu.Swali ninalojiuliza ni je kitu gani wameniwekea ambacho kinawafanya waweze kunifuatilia kila ninachokifanya? Kipo kitu wameniwekea ambacho lazima nikifahamu kwani bila kukifahamu hakuna mpango wangu utakaofanikiwa” akawaza Melanie Zaidi ya saa moja Melanie alikuwa amekaa sofani akiwaza namna Devotha anavyoweza kunasa mazungumzo yake akashindwa kupata jibu “Kuna teknolojia kubwa imetumika hapa na kufahamu walichokifanya itanilazimu nifanye majaribio kadhaa.Kwanza nitahama hiki chumba na kuhamia katika chumba kingine ambacho nitaweka kila kitu kipya.Nitanunua kila kitu kipya kuanzia mavazi hadi urembo.Hii mikufu,heleni zote nitaziacha sintazivaa tena yawezekana kuna kifaa wameniwekea ambacho kukibain itanichukua muda mrefu.Nitaweka mfumo mpya wa ulinzi katika chumba change nitakachohamia ili asiweze kuingia mtu mwingine wakati sipo”akawaza Melanie na kulala RIYADH – SAUDI ARABIA “Abu Zalawi unaonekana kuguswa sana na tukio lililotokea Tanzania.Umekuwa unalifuatilia kwa karibu sana” akasema Najma wakiwa sebuleni ndani ya jumba lao kubwa wakitazama runinga huku Mathew akibadilisha chaneli mbalimbali kutafuta taarifa za kina za tukio lile.Ulipita muda kidogo Mathew akasema “Fedha zile ulizosaini Dubai kumtumia James Kasai ndizo zimesababisha mauaji haya” “Ni kweli.Tulipokwenda Dubai nilisaini mkataba wa kumtumia fedha James Kasai ambaye ameingia mashirikiano na kikundi cha IS.Usiniambie umeguswa na kilichotokea wakati nawe umewahi kuwa gaidi na hizi ndizo zilikuwa shughuli zenu kuua watu” akasema Najma “Uko sahihi nimepitia huko katika ugaidi lakini kwa sasa ninaanza kuondoka huko taratibu” “Usijali Abu Zalawi sisi kazi yetu ni kutoa fedha kwa IS na wanachokwenda kukifanya sisi hakituhusu” akasema Najma “Lakini ni ufadhili huu wa fedha kwa vikundi vya kigaidi ndiyo sababu inayomfanya Habiba Jawad atafutwe sana na mashirika makubwa ya kijasusi duniani.Anatafutwa na Mossad,CIA n.k. Kwa nini tusiachane na mambo haya ya kufadhili ugaidi tukaendelea na maisha yetu ya kawaida? Hatutakuwa na maisha ya furaha na amani kama tutaendelea na mambo haya ya kufadhili ugaidi” akasema Mathew akionekana kuumizwa na kile kilichotokea Tanzania “Abu Zalawi usiwe na hofu sisi tuko salama”akajibu Najma “Hatuko salama Najma.Hujui ni namna gani Habiba Jawad anatafutwa na mataifa makubwa ambayo yanaongoza katika kupiga vita ugaidi duniani hasa Marekani na Israel.Sikuwa nimekueleza jambo hili lakini haikuwa rahisi kuufikisha mwili wa seif Jawad hapa.Majasusi wa Mossad waliuwekea kifaa maalum cha kuufuatilia kufahamu mahala ulipo wakiamini kwamba unaweza ukawasaidia kufika kwa Habiba Jawad.Kwa bahati nzuri niliweza kukigundua kifaa hicho na kukiondoa.Kama nisingeweza kukigundua mama angekuwa katika matatizo makubwa na yeye akiingia katika matatizo sisi sote mnakuwa kwenye matatizo.Ninadhani ni wakati wa mama Habiba kuachana na mambo haya ya kufadhili ugaidi akajielekeza katika biashara zake” akasema Mathew Najma akabaki kimya “Najma mimi nilikuwa gaidi na katika harakati zangu nimekwisha ua watu wengi.Si siku nyingi sana nililipua bomu katika kituo cha treni jijini Jerusalem na katika shambulio lile watu wengi walipoteza maisha.Baada ya kunusurika katika mashambulio ya Israel nilijiuliza nini sababu ya kuendelea kuua watu? Nimekuwa nikisoma mafundisho mbali mbali ya dini yetu na nimegundua kwamba nilikuwa ninafanya kosa kubwa kutumia kigezo cha dini kuendesha mambo ya kigaidi.Dini yetu ni dini safi na hairuhusu ugaidi.Uislamu si ugaidi bali wapo magaidi ndani ya Uislamu.Binafsi nimeama kuachana na mambo yale ya ugaidi na kumcha mwenyezi Mungu Subhanahu wa ta’ala.Naamini hata wewe ndicho kitu unachokitaka kwani nakumbuka siku ile tukiwa Dubai ulistuka sana baada ya kuuona mgongo wangu na ukanihAkikishia kwamba maisha yale yamekwisha” akasema Mathew “Abu Zalawi hayo yote uliyoyasema ninayafahamu na ninatamani sana kutoka katika maisha haya niishi maisha ya kawaida ya amani.Hata mimi sifurahii kufadhili ugaidi na kila ninaposikia kundi Fulani la kigaidi ambalo tunalifadhili fedha limefanya shambulio moyo wangu huumia sana kwani katika mauaji hayo wapo watoto,wanawake,wapo waislamu na wasio waislamu.Lakini mikono yangu imefungwa na siwezi kufanya chochote.Ninafuata maelekezo ya mama.Kwa sasa mimi ndiye ambaye amekuwa akinituma sehemu mbali mbali kumuwakilisha katika shughuli zake mbali mbali na mikataba mingi ya fedha mimi ndiyo husaini badala yake” “Ahsante sana Najma kwa maneno hayo ambayo nilihitaji sana kuyasikia.Lakini umewahi kukaa na mama yako ukajaribu kuzungumza naye kuhusiana na athari za kufadhili ugaidi? “Hapana sijawahi kuzungumza naye chochote.Kuna mambo ambayo siwezi kuzungumza naye na mojawapo ni suala hilo.Ni mama yangu lakini Habiba Jawad anatisha na akikasirika wanasema huwa ni mbaya sana ingawa sijawahi kumuona akiwa amekasirika.Nasikia kuna mambo ambayo ameyapiga marufuku kuyazungumzia na hilo ni kubwa ambalo hataki lizungumzwe na neno la Habiba Jawad ni amri” akasema Najma “Nitazungumza naye kesho juu ya suala hili” akasema Mathew na Najma akamtazama kwa mshangao “Unataka kwenda kuzungumza naye jambo hili? “Ndiyo nitazungumza naye” “Utaanzaje Abu Zalawi?akauliza Najma “Usihofu nitazungumza naye kesho.Nitamfuata nyumbani kwake” akasema Mathew na Najma akaonyesha wasiwasi kidogo “Mbona unaonyesha hofu Najma? “Usimfuate nyumbani kwake.Hapendi kufuatwa kwake na kama ana jambo la kukueleza basi atakuita yeye mwenyewe.Labda umsubiri atakapotoka kwenda kupata kifungua kinywa ndipo uombe kuzungumza naye lakini usimfuate katika nyumba yake ya kulala” akasema Najma “Hujawahi kuingia katika nyumba yake? “Nimeingia mara nyingi lakini pale tu yeye mwenyewe aliponiita kwenda kuzungumza au kunipa maagizo mbali mbali” “Kwa nini hapendi watu waingie ndani ya nyumba yake?Kuna siri yoyote anaificha? “Mama yangu ni mtu mwenye siri nyingi nadhani ndiyo maana anachunga sana watu kuingia ndani mwake.Kwa mfano ofisi yake ipo ndani ya jumba lake lakini hakuna anayefahamu iko sehemu gani bali yeye peke yake.Nasikia kuna handaki ambalo anaweza akajificha na kukaa humo hata miaka mitano bila kutoka nje lakini hakuna anayefahamu mahala lilipo wala mlango wa kuingilia.Kuna mtu mmoja tu anayefahamu mengi kuhusu jumba lile la mama naye ni bi Nasrat Jazer.Huyu ninaambiwa amekuwa mtumishi wa ndani wa mama toka akiwa msichana na hadi sasa amekuwa mzee.Huyu ndiye ambaye mama anamuamini sana kati na ndiye pekee ambaye anaweza akaingia na kutoka muda wowote ndani ya jumba la Habiba Jawad” akasema Najma “Naj nakushukuru sana kwa maelezo haya uliyonipa lakini kesho nitamtafuta Habiba nizungumze naye.Najua haitakuwa rahisi kunielewa lakini nitajaribu” akasema Mathew akazima runinga na kuelekea chumbani kulala. “Nimeumizwa sana na tukio lile la kigaidi nchini Tanzania.Nilishuhudia wakati fedha zikisainiwa ambazo zimekwenda kumfadhili James Kasai ambaye ametekeleza shambulio lile.Kuua wake watatu wa marais kwa mara moja pamoja na mabalozi nini hasa kusudio lake?Huyu James anatokea jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na inasemekana anaishi nchini Uganda kwa nini akashambulia Tanzania ambayo kwa miaka mingi imekuwa ni mhifadhi mkuu wa wakimbizi wengi kutoka nchini Congo? Wanajeshi wa Tanzania wamemwaga damu yao nchini Congo wakiipigania amani ya Congo kwa nini leo huyu mtu mmoja aibuke na kufanya mauaji yale makubwa?Au hii ni mipango ya Habiba Jawad kulipiza kisasi kwa kifo cha mwanae Edger Kaka? Nadhani ndilo hasa lilikuwa lengo lake kumfadhili James Kasai fedha nyingi ili aweze kufanya shambulio lile.Nimeumizwa sana na kitendo kile na ninaapa lile litakuwa ni tukio la mwisho.Sintakubali tena kundi lolote la kigaidi kushambulia Tanzania.Kesho nakwenda kuzungumza na Habiba Jawad anieleze ukweli kama shambulio lile ni yeye ndiye aliyelipanga na nini kusudio lake?Nadhani uvumilivu unaanza kunishinda siwezi tena kuendelea kuvumilia kuona ugaidi ukiendelea wakati ninao uwezo wa kuzuia.Niko tayari kupoteza maisha lakini niwe nimemuua Habiba Jawad.Yule mama bado hajanifahamu vyema mimi ni kiumbe wa aina gani” akawaza Mathew DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa kumi na mbili za asubuhi juu ya alama ilimkuta tayari Melanie amewasili hospitali ya Mtodora kwenda kumtazama Gosu Gosu.Alichokikuta hospitali pale kilimmaliza nguvu.Hali ya Gosu Gosu ilibadilika usiku na kulazimika kumuwekea mashine ya kumsaidia kupumua.Melanie hakuruhusiwa kuingia ndani bali alimuona Gosu Gosu kupitia kioo kikubwa. “Maskini Gosu Gosu mpenzi wangu usiniache.Tafadhali usiondoke na kuniacha peke yangu ! Melanie akawaza huku akimtazama Gosu Gosu kupitia kioo.Mara akashikwa bega na kugeuka “Habari yako dada” jamaa mmoja mwenye mwili uliojengeka akamsalimu.Melanie hakuwa akimfahamu yule jamaa.Akafuta machozi na kusema “Nzuri habari yako” “Naitwa Austin January ni rafiki wa karibu wa Gosu Gosu.Natumai wewe ndiye uliyenipigia simu jana usiku kunijulisha masahibu haya yaliyompata mwenzetu” akasema Austin “Ndiyo ni mimi.Naitwa Melanie Davis” “Melanie pole sana.Ni mara ya kwanza tunaonana je wewe ni ndugu yake? Akauliza Austin “Gosu Gosu ni mchumba wangu” akasema Melanie na Austin akastuka kidogo halafu akatabasamu “Nafurahi kukufahamu.Mimi ni rafiki yake mkubwa” akasema Austin “Nilifika jana nyumbani kwake baada ya kutoka hapa hospitali nikamuuliza mtumishi wake wa ndani kama anamfahamu rafiki au ndugu wa karibu wa Gosu Gosu akanipa namba zako nikakupigia” akasema Melanie “Gosu Gosu ana asili ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini kwa sasa ni Raia wa Tanzania.Hana ndugu ninaye mfahamu huku Tanzania na toka nilipokutana naye mimi ndiye nimekuwa ndugu yake.Nilikutanishwa naye na mtu mmoja ambaye sasa ni marehemu anaitwa Mathew Mulumbi na toka wakati huo tumekuwa watu wa karibu mno.Nashukuru kwa kunipa taarifa.Nataka kufahamu tukio hili limetokeaje? “Kwa mujibu wa taarifa nilizopewa ni kwamba Gosu Gosu alikuwa anatoka ofisini kwake jana jioni na wakati akisubiri kuingia barabara kuu wakatokea watu wakiwa katika piki piki na mmoja aliyekaa nyuma alikuwa na bunduki akaanza kumimina risasi katika gari la Gosu Gosu.Mimi nilipewa taarifa hizo na katibu wangu muhtasi ndipo nikaja moja kwa moja hospitali kujua maendeleo yake” akasema Melanie “Nimejaribu kupiga simu polisi kufuatilia kama kuna mtu yeyote aliyepatikana lakini mpaka sasa hawajampata mtu yeyote uchunguzi unaendelea” akasema Austin na ukimya ukapita. “Nimejiuliza sana sababu ya Gosu Gosu kushambuliwa nimekosa jibu.Ninawaza je ni sababu za kibiashara au ni kulipiza kisasi? Akauliza Austin “Nadhani tutapata jibu pale jeshi la polisi watakapokamilisha uchunguzi wao na kuwapata watu waliofanya shambulio hili” akasema Melanie “Nakuahidi Melanie mtu huyu lazima atapatikana.Iwe mvua au jua lazima atapatikana. Kwa sasa tuendelee kumuombea Gosu Gosu aweze kupona.Hali yake si nzuri na kwa mujibu wa daktari niliyezungumza naye amenipa ukweli kwamba hali hii aliyonayo sasa kupona ni hamsini kwa hamsini hivyo tujiandae kwa lolote litakalotokea” akasema Austin na Melanie akaangua kilio “Gosu Gosu wangu jamani !!! Austin akamnyamazisha “Tafadhali Melanie jizuie kumwaga chozi.Kwa sasa tunahitaji sana kuwa majasiri.Gosu Gosu anatuhitaji sana” akasema Austin na Melanie akafuta machozi.Austin akamshika bega na kusema “Sikiliza Melanie.Ninamfahamu Gosu Gosu ni mpambanaji.He’ll fight this.Believe me Gosu Gosu will fight this ! “Austin najua unajaribu kunipa moyo lakini hali haisi ya Gosu Gosu inaonekana.Uwezekano wa kupona ni mdogo sana.Oh jamani mimi !! “Melanie eneo hili halihitaji kelele ! Austin akawa mkali “Jitahidi kujizuia kumwaga machozi eneo hili.Ndugu za Gosu Gosu ni sisi wawili pekee hivyo basi ninahitaji kushirikiana na mtu mwenye ujasiri.Kama hautakuwa na ujasiri tafadhali kaa nyumbani usifike hapa ! akasema Austin “Samahani nimekuelewa Austin” “Good.Sasa nenda nyumbani kapumzike mimi nitaendelea kukaa hapa na kama kuna chochote kitatokea nitakujulisha”akasema Austin na kumshika mkono Melanie akamsindikiza hadi katika gari lake ambamo alikuwemo Joyce dereva wake “Melanie kuwa jasiri,Gosu Gosu atapambana na atapona.Ninamfahamu vyema ni mpambanaji” akasema Austin na kuagana na Melanie akaondoka “Dah ! Gosu Gosu amemtoa wapi Yule mtoto?Halafu mbona hajanieleza chochote kama tayari ana mchumba?Siku hizi ameanza kuniweka mbali katika masuala yake ndiyo maana hata suala hili hakutaka kunishirikisha.Hata hivyo anastahili kupongezwa kwa kumpata mwanamke mzuri kama yule” akawaza Austin na kurejea ndani.
Saa kumi na mbili za alfajiri Rais wa Tanzania Dr Fabian Kelelo alitaarifiwa kwamba Dr Evans rais mstaafu tayari alikuwa amewasili ikulu.Dr Fabian akatoka kwenda kukutana naye akamkaribisha katika chumba cha mazungumzo ya faragha. “Ahsante sana kwa kukubali kuonana nami asubuhi hii Dr Fabian kwani bila kuwahi asubuhi hii sidhani kama tutaweza kuonana hapo baadae na kuzungumza” akasema Dr Evans “Mzee nakushukuru sana kwa kufika.Toka tukio lile lilipotokea nimekusahau kabisa.Uliponipigia simu alfajiri ya leo ndipo nikakukumbuka.Ahsante sana kwa kuja kuniona mzee wangu nakuhitaji sana kwa wakati kama huu” akasema Dr Fabian “Pole sana Dr Fabian.Hata mimi nilijua kijana wangu lazima atanihitaji sana kwa wakati huu” akasema Dr Evans ukimya mfupi ukapita “Mzee ulisema una jambo la msingi unataka kunieleza” akasema Dr Fabian “Ni kweli kuna jambo ambalo ninataka kukueleza linalohusiana na hiki kilichotokea” “Nakusikiliza mzee”akasema Dr Fabian “Nimetafakari sana kuhusu tukio lile na kuna jambo moja limenijia akilini.Ninadhani tukio lile ni la kulipiza kisasi” “Kulipiza kisasi gani?akauliza Dr Fabian akionyesha mshangao kidogo “Miezi michache iliyopita ukishirikiana na Patrice Eyenga mlituma timu ya watu ikawaua Lucy Muganza na mume wake na baada ya hapo kukatokea tena matuko tukio ya mauaji akauawa balozi wa umoja wa ulaya halafu ghafla kukawa shwari.Nimetafakari sana sababu za James Kasai kufanya shambulio lile tena ndani ya ardhi ya Tanzania lakini sababu alizotoa haziniingii akilini.Kama angekuwa na nia ya kulipiza kisasi kwa Rais Patrice Eyenga angekwisha fanya hivyo muda mrefu lakini kwa nini asubiri hadi sasa? James Kasai hana ugomvi wowote na Tanzania lakini ukichunguza kwa undani sana tukio lile lilivyopangwa utagundua kwamba liliwalenga sana mkeo Millen na Rebeca Eyenga ambao ni wake za marais waliopanga mauaji ya Lucy Muganza”akasema Dr Evans na Dr Fabian akaonekana kuzama katika mawazo akakunja sura na kusema “Dr Evans kuna picha Fulani nimeanza kuipata kufuatia maelezo yako.Nakumbuka wiki iliyopita Millen alinieleza kwamba alifuatwa ofisini kwake na balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Germinus Mapupu akamueleza kuwa anataka kuwaleta pamoja wake za marais wa Rwanda na Congo hivyo ataandaa chakula maalum cha usiku na akamtaka Millen amsaidie kumleta mezani Agatha Ntezimana mke wa Rais wa Rwanda.Tulifurahi kwa jitihada hizo za balozi kutumia mkutano ule kutafuta suluhu ya mgogoro unaofukuta baina ya nchi zao mbili na Millen alikubali kusaidia kuwapatanisha wake za marais hao.Kama mauaji yale yalikuwa ni ya kulipiza kisasi basi lazima balozi Germinus Mapupu alitumiwa katika kuandaa mpango ule wa kuwaleta mezani Rebeca na Agatha.Swali linakuja nani waliokuwa nyuma ya mpango huo? Ninaamini kama balozi Germinus angefahamu kuwa mpango ule utasababisha mauaji asingethubutu kushiriki” “Exactly !! akasema Dr Evans “Nadhani umeanza kunielewa ninachokimaanisha.Balozi Germinus Mapupu aliandaa hafla ile kwa kujua kwamba ni jambo jema ambalo litasaidia kuleta amani katika nchi zao na hakujua kama mpango ule ulikuwa na lengo lingine.Umeuliza swali zuri nani yuko nyuma ya mpango ule? Kama unakumbuka Lucy Muganza alikuwa anatumiwa na umoja wahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ulaya na hasa hasa nchi ya Ufaransa na kazi zake kubwa alizotakiwa kufanya ni kwanza kuvuruga jumuiya ya Afrika Mashariki na pili kuleta machafuko nchini Congo.Ukilitazama kwa kina jambo hili utagundua kwamba kinachotokea sasa kina mlengo kama ule wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Vita inanukia kati ya Rwanda na Uganda.Rwanda wameshambulia maeneo ya Uganda na kuua watu na Uganda wameandaa vikosi vyao kwa ajili ya vita.Rwanda nao wamekwisha weka tayari vikosi vyao kukabiliana na yeyote atakayethuibutu kuvamia ardhi yao.Jamhuri ya kidemokrasa ya Congo imeweka vikosi vyake katika utayari na imepeleka vikosi vingine katika mpaka wake na Uganda.Tayari Uganda imewataka mabalozi wake walioko katika nchi za Rwanda na Congo warejee nyumbani mara moja na imewatimua mabalozi wa nchi hizo walioko Uganda.Ukiacha hayo wewe na nchi za Rwanda na Congo mnaandaa kikosi cha pamoja ambacho kitafanya operesheni ya kumsaka James Kasai.Kikosi hicho kitavamia misitu ya Kaskazini mwa Uganda inakodaiwa James Kasai amejificha na Uganda haiko tayari kwa kikosi hicho kuvamia ardhi yake itafanya mashambulizi na huo utakuwa ni mwanzo wa vita.Rwanda na Congo zitavamia Uganda na hapo hakutakuwa tena na jumuiya ya Afrika Mashariki.Fabian mmeingia katika mtego na mmenasa.Mlifanya maamuzi bila kutulia na kutafakari.Sasa basi tujiulize nani ambao wanataka jumuiya ya Afrika Mashariki ivunjike?Nani wanataka machafuko yarejee nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo?Jibu ni umoja wa Ulaya na si nchi zote za umoja wa Ulaya bali Ufaransa ambayo imejificha chini ya kivuli cha umoja wa ulaya.Unanielewa lakini Dr Fabian? “Mzee ninakuelewa vizuri sana” “Ahsante kwa kunielewa lakini hayo ni mawazo yangu tu sijamanisha kwamba ndiyo ukweli wenyewe” “Mzee umenifumbua macho yangu na nimepata mwangaza mkubwa kwa haya uliyonieleza.Sikuwa nimeyafikiria kabisa.Sasa unanishauri nifanye nini mzee wangu? “Ninakushauri ufanye uchunguzi wa siri sana kujua nani walio nyuma ya mpango ule wa marehemu balozi Mapupu kuandaa chakula na kuwaita wake za marais.Hakuwa peke yake lazima wapo watu waliomshawish kuandaa mpango ule wakidai ni mpango wa amani.Pili sitisha mipango yote ya kutaka kuivamia Uganda kijeshi kwa kigezo cha kumtafuta James Kasai” “Mzee mtu huyu ni muuaji na ameweka wazi kwamba mashambulio yataendelea na kibaya zaidi huyu mtu tayari anashirikiana na kundi la kigaidi la IS.Hatuwezi kumuacha akendelea kufanya atakavyo na kuua watu….” Dr Fabian akasema kwa ukali “Dr Fabian nisikilize na unielewe.Huu ni mtego mmetegewa na tayari mmenasa.Mkithubutu kutumia nguvu za kijeshi mtaitumbukiza jumuiya ya Afrika mashariki katika machafuko makubwa na pale machafuko hayo yatakapomalizika hakutakuwa tena na jumuiya ya Afrika mashariki.Kila nchi itajikuta peke yake na hicho ndicho maadui zenu wanachokihitaji.Uchumi wa nchi za Afrika Mashariki utayumba sana.Dr Fabian nakusihi sana usikubali kutumia njia za kijeshi katika jambo hili” akasema Dr Evans “James Kasai ni mtu hatari ana jeshi lake tutawezaje kumpata bila ya kutumia nguvu za kijeshi?akauliza Dr Fabian “Inatakiwa ifanyike operesheni ya kimya kimya.Tengeneza kikosi cha siri ambacho kitafanya kazi hiyo ya kumsaka James Kasai kwa siri kubwa na hatimaye watamtia nguvuni.Tunacho kikosi cha jeshi kinachojihusisha na operesheni maalum kinachoongozwa na Austin January,kitumie kikosi hicho wana uwezo mkubwa wa kumpata James Kasai” akasema Dr Evans “James Kasai yuko kati kati ya kundi la waasi na wana silaha kali.Kikosi chetu ni kidogo ukilinganisha na kundi kubwa la waasi tena wanaomiliki silaha nzito nzito.Tutakwenda kuwapoteza vijana wetu” akasema Dr Fabian “Kikosi kile maalum kabisa kilianza wakati wa uongozi wangu unadhani kwa nini nilikianzisha kikosi kama kile? Ni kwa ajili ya operesheni kama hizi.Kikosi kile kina watu mahiri sana ambao wamepitia mafunzo ya hali ya juu mno.Wanao uwezo mkubwa wa kupigana kwenye hali zote iwe majini,ardhini,msituni jangwani n.k.Ni kikosi chenye watu wachache kutokana na gharama kubwa ya mafunzo kwa mwanajeshi mmoja.NakuhAkikishia Dr Fabian ukitumia kikosi hiki utafanikiwa kumpata James Kasai”akasema Dr Evans na Dr Fabian akashusha pumzi. “Mzee umenipa ushauri mzuri sana lakini nina wasi wasi kwamba ushauri huu umechelewa kwani tayari mipango imekwisha andaliwa na baadae leo vikosi kutoka Rwanda na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vitawasili kwa ajili ya kuungana na kile cha Tanzania kwa mazoezi ya wiki moja kisha wataelekea Uganda kumtafuta James Kasai” “Dr Fabian ninajua una hasira za kuondokewa na mkeo.Si wewe peke yako bali hata wenzako wa Rwanda na Congo nao pia wana hasira ndiyo maana nyote kwa pamoja mmekubaliana kirahisi sana kutuma kikosi cha jeshi kuvamia Uganda kumsaka James Kasai bila kupima athari za kile mnachotaka kukifanya.Unapokalia kiti cha urais hupaswi kukurupuka.Unapaswa kuwa na subira.Kila jambo linapotokea jitahidi kwanza kufanya tafakari ya kina kabla ya kutoa maamuzi.Naweza kusema kwamba mmekurupuka sana katika maamuzi yenu ya kuunda kikosi cha pamoja mkasahau hata kuwashirikisha wanachama wengine wa jumuiya ya Afrika mashariki.Ni vipi kama wanachama hao wengine hawatakubaliana na hatua mnazozichukua? Dr Fabian ninaiona jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika vipande vipande na mbaya zaidi jumuiya inakwenda kusambaratika ikiwa katika mikono yako.Utaandikwa katika vitabu vya historia kwamba ulichangia kwa jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika na utasomwa kwa vizazi hadi vizazi.Tafadhali usiruhusu jambo hili litokee katika utawala wako.Fanya maamuzi magumu ambayo yatainusuru jumuiya” akasema Dr Evans na Dr Fabian akainamisha kichwa akiwaza “Dr Fabian kilichonileta kwako asubuhi hii ni kuwasilisha mawazo yangu na ushauri lakini ninakuachia wewe mwenyewe kila kitu utapima na kuona kama yanafaa na utaangalia namna ya kuyafanyia kazi.Ahsante sana kwa kunisikiliza mheshimiwa Rais na kwa mara nyingine tena pole sana” akasema Dr Evans huku akisimama “Mzee nakushukuru sana kwa kuja kuniona na kunipa mawazo mazuri.Naomba nipe muda nitafakari nini cha kufanya lakini nakuahidi mawazo haya mazuri lazima nitayafanyia kazi” “Ahsante sana Dr Fabian.Sasa ninaweza kuondoka” akasema Dr Evans na Rais akamsindikiza hadi katika gari lake akaondoka. “Aliyoyasema Dr Evans yanaweza kuwa na ukweli.Ukilitazama kwa kina tukio lile kuna uwezekano mkubwa sana likawa na malengo ya kulipiza kisasi na kwa upande mwingine ukawa ni mwendelezo wa kile alichotakiwa kukifanya Lucy Muganza yaani kusambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki.Ushauri wa Dr Evans kuhusu kutotumia nguvu za kijeshi kumsaka James Kasai ni mzuri na ukilitazama jambo hili kwa kina ni kweli jumuiya ya Afrika Mashariki inaelekea kusambaratika.Jana Rwanda imeshambulia Uganda na hivi sasa kila nchi inaandaa vikosi vyake vya jeshi tayari kwa vita.Ni kweli yataibuka machafuko makubwa sana katika eneo hili la afrika mashariki kama juhudi za haraka zisipochukuliwa.Suala hili lipo katika mikono yangu kwa sasa na ndiye nitakayeamua juu ya uhai wa hii jumuiya.Je nisimamishe operesheni ya kijeshi ambayo tumepanga kuifanya kumtafuta James Kasai?akajiuliza Dr Fabian “Endapo tutasimamisha operesheni ya kijeshi tunayoiandaa kwa ajili ya kumsaka James Kasai Rais wa Uganda atajaa kiburi na atajiona mkubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki.Anaweza akavamia nchi yoyote kwa kujua kwamba hakuna nchi inayoweza kuitisha Uganda.Lazima achapwe kidogo kupewa fundisho ingawa ushauri wa Dr Evans nao ni mzuri lakini dah ! sijui nifanye nini.I think I need to talk to Austin” akawaza na kuchukua simu akazitafuta namba za Austin
Austin akiwa nje ya chumba alimolazwa Gosu Gosu mara simu yake ikaita akaitoa mfukoni kutazama mpigaji alikuwa ni Dr Fabian Kelelo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Akastuka kwani ni muda umepita hawakuwa wamewasiliana “Mheshimiwa Rais” akasema Austin “Austin habari yako” “Nzuri kabisa mheshimiwa Rais” “Austin samahani kwa usumbufu asubuhi hii” “Bila samahani mheshimiwa Rais.Kwanza pole sana mzee kwa msiba mzito uliokupata” “Ahante sana.Austin nakuhitaji mara moja hapa ikulu” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais utanisamehe sintaweza kufika hapo kwa wakati niko hapa hospitali ya Mtodora toka jana usiku mmoja wa rafiki yangu ambaye nimeshirikiana naye katika misheni mbali mbali amepigwa risasi jana jioni” “Ooh Pole sana.Ni nani huyo? “Ni Gosu Gosu mheshimiwa Rais” akasema Austin “Ulikuwa naye katika ile misheni ya Lucy? “Ndiyo mheshimiwa Rais” “Vipi hali yake? “Hali yake si nzuri mheshimiwa Rais.Kwa mujibu wa madaktari chochote kinaweza kutokea” “Dah ! hili ni pigo kubwa sana.Nitazungumza na daktari mkuu wa hapo hospitali ili kuweka uzito mkubwa katika kumuhudumia.Kuna kingine chochote ambacho unadhani ninaweza kusaidia? “Hapana mheshimiwa Rais pale nitakapokuwa na chochote ninachohitaji nitakujulisha” akasema Austin “Sawa Austin basi endelea kukaa hapo hapo hospitali kumuhudumia mgonjwa na chochote kitakachojiri utanijulisha.Austin tafadhali kuweni makini sana.Chukueni kila aina ya tahadhari kuanzia sasa” “Sawa mheshimiwa rais” akajibu Austin na Dr Evans akakata simu. “Huyo jamaa aliyepigwa risasi alishiriki katika mauaji ya Lucy Muganza.Yawezekana Dr Evans yuko sahihi kwamba haya ni matukio ya kulipiza kisasi” akawaza Dr Evans na kumpigia simu Edwin Mbeko mkuu wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi akamtaka afike ikulu mara moja
Edwin Mbeko aliwasili ikulu kwa haraka kama alivyotakiwa na Rais,akapokewa na kupelekwa katika chumba cha mazungumzo ya faragha. “Edwin habari za asubuhi” “Nzuri mzee shikamoo” “Marahaba.Edwin nina ratiba ndefu sana siku ya leo na nisingeweza kupata nafasi ya kuzungumza nawe baadae ndiyo maana nimekuita hapa asubuhi hii ili nikupe maelekezo” akasema Dr Evans “Niko tayari mkuu kupokea maelekezo” akasema Edwin “Tutazungumza kwa kirefu tutakapopata muda kuhusiana na kilichotokea lakini kwa sasa kuna jambo nataka wewe na idara yako mlichunguze.Marehemu balozi Germinus Mapupu aliandaa hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwake kwa ajili ya wake za marais wa Rwanda na Congo,nataka kufahamu alishirikiana na nani kuandaa hafla ile? Nina uhakika hakuwa peke yake hivyo tukimfahamu ambaye alisaidiana naye kuandaa tutakuwa na sehemu nzuri ya kuanzia uchunguzi wetu.Nataka idara yako ijielekeze katika suala hilo.Masuala mengine yatashughulikiwa na idara za polisi na vyombo vingine.Tumeni kila uwezo mlio nao kuhAkikisha mnajua mtu au watu ambao walishirikiana na balozi Mapupu” akasema Dr Fabian “Sawa mheshimiwa Rais tutalifanyia kazi suala hilo” “Nitazungumza nawe tena jioni ya leo nataka hadi muda huo tayari kuwe kuna chochote mmekipata” akasema Dr Fabian na kuagana na Edwin. Baada ya kutoka ikulu Edwin Mbeko alikwenda moja kwa moja ofisini kwake.Alifunga ofisi yake kwa funguo ili mtu mwingine asiweze kuingia ndani kisha akampigia simu Devotha “Edwin Mbeko” akasema Devotha baada ya kupokea simu “Devotha habari za muda huu” “Nzuri kabisa.Kuna taarifa gani asubuhi hii?akauliza Devotha “Nimetoka ikulu muda mfupi uliopita kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania” “Amekuambia nini? “Ametoa maelekezo kwa idara yangu tuchunguze tujue balozi Mapupu alishirikiana na nani katika kuandaa hafla ile ya chakula cha jioni” “Tayari ameanza kuwa na wasiwasi kwamba kuna mtu au watu walio nyuma ya balozi Mapupu.Edwin hAkikisha Melanie hajulikani kama ni yeye aliyefadhili hafla ile” akasema Devotha “Tumekwisha lifanya hilo madam na tayari tumekwisha futa mawasiliano yote ya balozi Mapupu na Melanie hivyo usiwe na wasi wasi wowote tunamlinda Melanie kwa kila uwezo tulio nao” akasema Edwin “Good.Kuna jambo lingine hAkikisha Melanie hafahamu kama vijana wako ndio waliompiga risasi Gosu Gosu.Akijua mambo yanaweza kuwa mabaya” akasema Devotha “Hawezi kujua chochote lakini kuna kitu Fulani kimetokea ambacho kinanipa wasiwasi kidogo.Nmejulishwa asubuhi na timu wanaomfuatili Melanie kwamba mawasiliano yamekatika na hawawezi kumpata Melanie.Inaonekana amegundua kuhusu zile saa zake tulizozibadilisha ambazo tumeziwekea vifaa maalum kama ulivyoelekeza pamoja na zile simu zake na hajavitumia kabisa leo”akasema Edwin Mbeko “Ni mimi ndiye niliyefanya kosa nilimwambia kwamba ninafuatilia kila anachokifanya.Sikutakiwa kumueleza jambo hilo.Nadhani ametafuta ni namna gani tumeweza kufuatilia mazungumzo yake na Gosu Gosu na akagundua tumemuwekea vifaa katika saa zake na kuna mchezo umefanyika katika simu yake ndiyo maana leo hajavitumia kabisa vifaa hivyo.Kitu cha msingi ni kuwalinda wale wadada wawili nyumbani kwake akigundua kwamba tuliwatumia kufanya mchezo huo atawafanyia kitu kibaya.Melanie amebadilika sana anahitaji ” akasema Devotha “Nimekuelewa madam.Nitafanya kama ulivyoelekeza” akasema Edwin Mbeko na kumuaga Devotha RIYADH – SAUDI ARABIA Saa moja za asubuhi simu ya Najma ikaita akainuka na kuichukua. “Mama anapiga” akasema na kuipokea wakasalimiana halafu Habiba akasema “Nawataka kwangu asubuhi hii kwa ajili ya kifungua kinywa” akasema Habiba na Najma akabaki ameduwaa “Najma umenisikia? Akauliza Habiba “Nimekusikia mama.Nitamjulisha Abu” akasema Najma na Habiba akakata simu “Kuna nini?akauliza Mathew baada ya kuona uso wa Najma ukiwa na mabadiliko “Mama anataka twende nyumbani kwake kupata kifungua kinywa” akasema Najma “Ni kama vile alijua kuwa ninahitaji kuzungumza naye” akasema Mathew Najma akaamka na kwenda maliwato “Huyu Habiba Jawad ni mwanamke wa aina gani? Amefahamu vipi kama ninahitaji kuonana naye siku ya leo?Anazidi kunishangaza na kuna nyakati najikuta nikiingiwa na hofu.Yawezekana anatumia nguvu za giza si bure.Ni jana tulikuwa tunajadiliana namna ya kuweza kuzungumza naye halafu asubuhi ya leo anatukaribisha kwake.Hii ni ajabu kwa kweli” akawaza Mathew akainuka na kukaa kitandani “Mpenzi unamuwaza Habiba Jawad?akauliza Najma baada ya kumkuta Mathew akiwa amekaa kitandani akiwaza “Nimeshangaa kidogo kwani ni jana tulikuwa tunajadiliana namna ya kuzungumza naye na leo asubuhi anatualika nyumbani kwake” “Usimuwaze Habiba ndivyo alivyo.Tumekwisha mzoea.Ana uwezo mkubwa wa kuhisi mtu unawaza kitu gani.Tulale kidogo kabla ya kuelekea kwa Habiba” akasema Najma huku akimkumbatia Mathew “Ninatamani hata sasa nimfuate Habiba nyumbani kwake.Sijapata usingizi usiku wa leo nikiwaza kuhusu shambulo la Tanzania.IS wamefanya mauaji ya kikatili sana wakisaidiana na James Kasai.Kinachoniumiza zaidi nilishuhudia utiaji saini wa mabilioni ya fedha ambayo alipewa James Kasai kuimarisha kikosi chake cha waasi.IS wanataka kujiimarisha katika eneo la Afrika Mashariki na kati,wanataka kujenga kambi kubwa ya mafunzo ya kigaidi nchini Congo na magaidi hao watasambazwa sehemu mbalimbali duniani kuua watu wasio na hatia.I won’t let that happen..! “Abu mpenzi ! akaita Najma kwa sauti laini na kumstua Mathew toka mawazoni “Uko mbali sana kimawazo.Nini kinakusumbua? “Najaribu kujipanga namna nitakavyozungumza na Habiba” akasema Mathew na Najma akacheka “Liweke kando jambo hilo nakuhitaji” akasema Najma na Mathew akaelewa alichotakiwa kukifanya akampa Najma haki yake ya asubuhi. Baada ya kipute cha asubuhi wakaingia bafuni kuoga kisha wakajiandaa wa ajili ya kwenda kupata kifungua kinywa nyumbani kwa Habiba Jawad.Walipokuwa tayari wakatoka na kutembea kuelekea katika jumba la Habiba.Himaya ya Habiba ilikuwa na majumba nane makubwa ya ghorofa na jumba lake lilikuwa katikati ya majumba yote.Zilikuwepo pia nyumba nyingine ndogo ndogo kumi na tano.Katika Himaya hii Habiba aliishi na watumishi wake,wasaidizi wake wa karibu,walinzi na sasa waliongezeka Mathew na Najma.Mwanae Abu Dahir alikuwa na makazi yake sehemu nyingine ambako huko nako Habiba alikuwa na nyumba yake ambayo hufikia kama akiamua kwenda kumtembelea mwanae. Kutoka katika nyumba yao hadi nyumbani kwa Habiba hakukuwa na umbali na kulitengenezwa njia nzuri sana za kutembea kwa miguu kutoka jengo moja hadi jingine.Walifika katika nyumba ya Habiba wakakaribishwa ndani na mmoja wa watumishi wa ndani wa Habiba.Ilikua ni mara ya kwanza kwa Mathew kuingia ndani ya jumba la Habiba Jawad. “Uzuri wake ni kama lile jumba la Jaber kule Jordan lakini tofauti ni kwamba Habiba hajaweka viti vya dhahabu kama Yule jamaa kule Jordan” akawaza Mathew wakiwa sebuleni wakimsubiri Habiba.Baada ya dakika chache Habiba akatokea Mathew na Najma wakasimama na kumsalimu kwa adabu. “Karibuni sana wanangu.Abu Zalawi ni mara yako ya kwanza kuingia hapa.Umelizoea lile jengo lingine ambalo tumekuwa tukikutana mara kwa mara kwa chakula na maongezi lakini hili ndilo jengo langu binafsi hata akina Najma ni nadra sana kuingia humu” akasema Habiba “Nashukuru sana mama kwa kutukaribisha” akasema Mathew kisha Habiba akawachukua hadi katika chumba maalum kwa ajili yam lo wa asubuhi pekee.Kulikuwa na meza yenye viti sita ambayo ilishehenezwa vyakula vya aina mbalimbali.Habiba akawakaribisha mezani wakapata kifungua kinywa.Baada ya kumaliza Habiba akasema “Najma ninamuhitaji Abu Zalawi nina mazungumzo naye.Tutakapomaliza mazungumzo yetu atakuja nyumbani” akasema Habiba na Najma akaondoka akamuacha Mathew pale nyumbani kwa Habiba “Abu Zalawi kwa mara nyingine tena karibu sana hapa nyumbani kwangu.Wewe ni mmoja wa watu wachache sana ambao wamewahi kukaribishwa ndani ya nyumba hii” akasema Habiba na kumtaka Mathew amfuate. Ni jumba lililokuwa na vyumba na kona nyingi na hatimaye wakafika katika mlango sehemu ambako walikutana na ukuta wa rangi nyeupe.Taa nyeundu ikawaka na sauti ikasikika ikimtaka Habiba atamke jina lake. “Voice recognized” ikasikika sauti baada ya Habiba kutamka jina lake na mara vikasikika vyuma vikilia na sehemu ya ukuta ikajifungua “Abu Zalawi karibu sana katika makazi yangu” akasema Habib akimuongoza Mathew kuingia katika sebule nzuri sana yenye uzuri wa ajabu “Kumbe Habiba anayo sebule nyingine nzuri kushinda ile niliyoiona kule chini” akawaza Mathew alipoingia katika sebule ile nzuri na kubwa Habiba akaboyeza kidude Fulani ukutani na mlango ukajifunga. “Karibu sana Mathew Mulumbi.Hapa tuko huru kuzungumza kitu chochote bila kuhofia mtu yeyote” akasema Habiba “Sikujua kama una sebule nyingine nzuri namna hii mama.Ahsante kwa kunikaribisha”akasema Mathew “Nimekuleta hapa ili tuzungumze kwa uhuru.Leo nataka tuzungumze kwa Kiswahili kwani hakuna anayetusikia” akanyamaza kidogo halafu akasema “Mathew kwa siku nzima ya jana haukuwa katika hali yako ya kawaida.Hii ilisababishwa na tukio lililotokea Tanzania ambalo IS wametajwa kuhusika.Nikiutazama uso wako una maswali zaidi ya elfu moja ya kuniuliza lakini kuna kitu ambacho nataka ukifahamu” Habiba akanyamaza akamtazma Mathew na kuendelea “Nilikutuma uongozane na Najma kwenda Dubai kwa makusudi kabisa na nilitaka ushuhudie James Kasai akifadhiliwa fedha.Sikutaka ufanye chochote bali uwe shuhuda tu.Uliporejea uliniuliza swali kwa nini nilitaka ushuhudie jambo lile? Akasema Habiba na kukaa kimya tena “Mathew nimewahi kukutamkia zaidi ya mara moja kwamba ninakupenda na nimekuchagua kutoka katika kundi la mamilioni ya watu.Usinielewe vibaya ninakupenda kama mwanangu na ndiyo maana nimediriki kukupa mali zote ambazo alistahili Seif.Pembeni ya hilo kuna jambo lingine kubwa.Niliwahi kukudokeza na leo ninarejea tena kwamba ninataka uchukue nafasi yangu” akanyamaza akatazama chini “Nilipokueleza jambo hili ulistuka sana ukajibu kwamba huwezi kuwa mfadhili wa magaidi.Leo tena narejea kusema kwamba wewe ndiye ambaye nimekuchagua ushike nafasi yangu.Kwa nini ninakuandaa wewe? Ni kwa sababu unaweza ukafanya kile ninachotaka ukifanye.Kuna siri ambazo nitakueleaza ambazo hakuna anayezifahamu hata watoto na wasaidizi wangu wa karibu” akasema Habiba “Siri ya kwanza ambayo nataka uifahamu ni kwamba I’m dying” “You are dying?akauliza Mathew “Yes I’m dying.Kwa sasa naomba nisikueleze chochote lakini fahamu kwamba ninakufa.Hii ni siri yangu kubwa ambayo sijamueleza mtu yeyote wa karibu na hata wanangu hawajui.Ninajua una kifua cha kuficha siri hivyo iweke kifani kwako siri hii.Hapaswi mtu yeyote kuifahamu.Umenielewa Mathew?akauliza Habiba Jawad. “Nimekuelewa mama lakini… “Hicho unachotaka kuuliza siku nyingine nitakueleza.Najua unataka nikufafanulie kauli yangu kwamba ninakufa lakini muda bado utafahamu hapo baadae” akasema Habiba “Mama umenistua sana” “Usistuke Mathew.Lengo lako la kunitafuta llikuwa ni kuniua na pale nitakapokuwa nimekufa basi misheni yako itakuwa imetimia.Habiba jawad atakuwa amekufa na ugaidi utakuwa umekomeshwa duniani” akasema Habiba na kucheka “Mama ni kweli malengo yangu yalikuwa ni kukuua lakini baada ya kufanikiwa kuonana nawe ana kwa ana mtazamo wangu ulibadilika kabisa.Tazama niko hapa sasa nimeoa mwanao na nimeingia katika orodha ya watoto wako…” akasema Mathew na Habiba akatoa kicheko kidogo “Mathew Mulumbi ninakupenda sana” akasema na kuendelea kucheka “Ninakufahamu Mathew Mulumbi zaidi ya vile ujuavyo.Nafahamu pamoja na yale yote ambayo nimekufanyia lakini bado akili yako inawaza siku moja utaniua na kuondoka hapa na misheni yako itakuwa imekamilika” “Hapana si hivyo mama” akasema Mathew “Huwezi kunidangnya Mathew ninajua.Ninakuomba ondoa mawazo hayo.Kama nilivyokwambia kwamba hapa ndipo mahala unapotakiwa kuwepo.Hapa ni nyumbani kwako.Una misheni kubwa sana zaidi ya ile ya kuniua hivyo endelea kufuata maelekezo yangu.Tuachane na hilo turejee nchini Tanzania” akasema Habiba “James Kasai amefanya shambulio kubwa ambalo limepelekea vifo vya watu zaidi ya hamsini kwa mujibu wa taarifa niliyonayo.Huyu James Kasai ni nani?Kwa nini ametekeleza shambulio lile?akauliza Habiba Jawad “James Kasai anaongoza kikundi cha waasi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana na jeshi la serikali ya jamhuri ya kidemokrasiaya Congo.Kwa muda wa miaka mingi kumekuwa na vita isiyokwisha nchini Congo na kwa kiasi kikubwa vita hiyo imekuwa ikisababshwa na nguvu kubwa kutoka nje ya nchi hiyo.Zipo nchi za Ulaya ambazo zimekuwa zikifadhili makundi mbali mbali ya waasi ili kuanzisha mapigano na serikali ya Congo kwa maslahi yao.Hii ndiyo sababu utaona kumekuwa na makundi mengi ya waasi yakiibuka mara kwa mara.Kwa miongo kadhaa wananchi wa Congo wamekuwa wakiishi katika machafuko hadi pale Patrice Eyenga aliposhinda urais na kuwaita mezani viongozi wote wa makundi ya waasi wakazungumza na kukubaliana kumaliza tofauti zao.Ni James Kasai pekee ambaye hakuwa tayari kuweka silaha chini hivyo akafurushwa na majeshi ya serikali akakimbilia nchini Uganda.James Kasai hakuwa amefadhiliwa na mataifa ya Ulaya kama ilivyokuwa kwa makundi mengine mengi ya waaasi baliyeye alikuwa akifadhiliwa na moja wapo ya nchi jirani na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na ndiyo maana aliweza kumiliki silaha nzito nzito na kufanikiwa kushika sehemu kubwa ya Congo hasa miji ile yenye utajiri mkubwa wa madini.Nchi iliyomfadhili ilikuwa ikifaidika kwa kiasi kikubwa cha madini kilichoibwa kutoka katika migodi mikubwa” akasema Habiba na kumtazama Mathew aliyekuwa kimya akimsikiliza “Watu wengi wanadhani kwamba vikundi vya waasi nchini Congo vilikuwa vikifadhiliwa na mataifa ya nje pekee lakini hawajui kama zipo nchi jirani ambazo zilikuwa zikifadhili vikundi vya waasi nchini Congo.Baada ya kufurushwa kutoka Congo,James Kasai alikimbilia Uganda ambako amepewa hifadhi na serikali ya Uganda katika misiti ya Kaskazini mwa Uganda.Nchi iliyokuwa inamfadhili James Kasai haitoi ufadhili tena hivyo kumfanya awe katika hali mbaya kifedha na hapo ndipo IS walipoingia.IS wanataka kupanua mtandao wao na kujiimarisha barani Afrika.Wanatafuta sehemu ya kujenga kambi kubwa ya mafunzo ya kigaidi na wakaona katika misitu mikubwa ya Congo kunafaa sana kujenga kambi yao hivyo basi wakaenda kuzungumza na James Kasai wakataka kuingia naye makubaliano ya masharikiano ili aweze kuwasaidia waweze kujenga kambi kubwa ya mafunzo nchini Congo.James alikubali kushirikiana na IS kwa sharti la kulipwa kiasi kikubwa cha fedha na silaha.Huo ndio ule mkataba ulioushuhudia Dubai” akasema Habiba na kunyama kidogo halafu akaendelea “Kuingia madarakani kwa Rais Patrice Eyenga kulikuwa na athari kubwa hasa kwa mataifa yale ambayo yalikuwa yananufaika kupitia migogoro ya Congo na hii ikasababisha nchi hizo kutafuta njia za kuwarejesha tena kuendelea kuchuma rasilimali za Congo na njia pekee ambayo ingeweza kuwasaidia kurejea tena nchini Congo ni kwa kuanzisha machafuko.Ukatengenezwa mpango wa kumuondoa Patrice Eyenga madarakani kwa kupitia uchaguzi mkuu uliopita.Aliandaliwa mtu anaitwa Lucy Muganza ili aweze kuchuana na Patrice Eyenga katika uchaguzi mkuu.Huyu Lucy Eyenga alikuwa ni mfanyabiashara bilionea aliyependwa sana nchini Congo.Kwa bahati mbaya Lucy hakuweza kufika katika uchaguzi mkuu kwani aliuawa yeye na mumewe nchini Tanzania” akanyamaza kidogo na kusema “Ninajaribu kukupa historia hii kwa sababu najua huifahamu kwani wakati haya yote yakitokea wewe hukuwa na habari” “Ni kweli mama mambo haya ni mara ya kwanza ninayasikia kutoka kwako sikuwa nikiyafahamu” akasema Mathew “Mataifa haya makubwa yakiongozwa na nchi ya Ufaransa wana mpango pia wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Kwa nini wanataka kuisambaratisha jumuiya hii? Jibu ni kutokana na uimara wake.Bila kuivunja vipande vipande jumuiya hii itawawia ugumu kuweza kuanzisha machafuko nchini Congo kwani kwa sasa tayari Congo ni mwanachama wa jumuiya hiyo na kwa taratibu zilivyo za jumuiya hiyo endapo kutatokea nchi au kikundi chochote toka ndani au nje ya jumuia ya Afrika Mashariki kikatishia amani ya mojawapo ya nchi mwanachama basi nchi zote za jumuiya zitaungana pamoja na kuunda jeshi moja ambalo litakwenda kuisaidia nchi hiyo.Jumuiya ikivunjika Congo itabaki peke yake na hata pale machafuko yatakapotokea basi hakuna nchi itakayoisaidia.Shambulio lile la James Kasai lina malengo hayo pia ya kuanzisha machafuko yatakayopelekea jumuiya ya Afrika Mashariki kusambaratika.Kama umefuatilia vyombo vya habari ni kwamba vikosi vya anga vya nchi ya Rwanda vilivamia katika misitu ya Kaskazini mwa Uganda ambako inaaminika James Kasai amejificha na kushambulia vijiji kadhaa na kuua watu.Rais wa Uganda ametangaza kwamba kitendo kile cha Rwanda ni cha kichokozi na ni tangazo la vita.Vikosi vya Uganda vimesogezwa katika mpaka wake na Rwanda tayari kuishambulia Rwanda.Nchi ya Rwanda nayo imeapa kila risasi moja itakayorushwa katika upande wake zitarejea risasi elfu moja.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nayo imesogeza vikosi vyake katika mpaka wake na Uganda.Nchi tatu za Tanzania Rwanda na Congo zimeunda kikosi kimoja cha jeshi kwa ajili ya kwenda kufanya operesheni ya kijeshi nchini Uganda na serikali ya Uganda imeapa kukifyekelea mbali kikosi hicho.Tayari Uganda imewarejesha nyumbani mabalozi wake kutoka nchi za Rwanda na Congo.Kwa ujumla hali ya Afrika Mashariki ni tete na endapo hakutachukuliwa juhudi za haraka jumuiya ya Afrika mashariki itavunjika vipande vipande na hicho ndicho wakubwa hao wanachokitafuta.Kuna mpango mkubwa sana umeandaliwa wa kuivuruga Afrika Mashariki na tayari mambo yameanza.Naamini mambo yakiendelea kama yalivyo kwa muda wa wiki moja hakutakuwa tena na jumuiya ya Afrika Mashariki” akanyamaza Habiba na kumtazama Mathew halafu akatabasamu “Kama kawaida yako nikikutazama ninaona maswali zaidi ya elfu moja katika sura yako lakini sitaki leo uniulize swali lolote” akasema Habiba na kunyamaza tena halafu akamkazia macho Mathew na kusema “Mathew Mulumbi ninakutuma uende Tanzania” “Tanzania?Mathew akauliza kwa mshangao “Ndiyo nataka uende Tanzania.Unakwenda kwa misheni maalum” akasema Habiba na Mathew akashusha pumzi “Najua umestuka lakini nakuomba usistuke.Nataka urudi nyumbani Tanzania kwa ajili ya misheni maalum nitakayokutuma mimi” akasema Habiba “Niko tayari mama.Misheni gani unanituma Tanzania?akauliza Mathew. “Unakwenda kuikomboa Afrika mashariki.Nataka ukamuue James Kasai na vile vile kuung’oa mzizi wa IS nchini Tanzania na Afrika Mashariki na kati.Si operesheni nyepesi lakini ndiyo itakayoinusuru Afrika Mashariki.James Kasai ana nguvu kubwa hivi sasa na kama asipodhibitiwa ataleta maafa makubwa sana katika Afrika mashariki hivyo unakwenda kummaliza” akanyamaza na kumtazama Mathew “Naona kuna jambo limekukaba koo unataka kulisema” “Mama Habiba mimi sina tatizo kabisa na misheni hii unayonituma na ninakuahidi kuitekeleza kwa ukamilifu mkubwa sana lakini swali langu kwako umeonyesha kuguswa na kile alichokifanya James Kasai lakini ametekeleza tukio lile kwa kutumia fedha zako.Kwa nini ulikubali kumfadhili mtu ambaye ulifahamu fika ni muuaji na anakwenda kuua watu wasio na hatia? Kwa nini umemuacha akatekeleza shambulio lile baya hadi sasa Afrika Mashariki inataka kusambaratika ndipo unaamua auawe? Kwa nini ..oh my God ! akasema Mathew na kushika kichwa kwa mikono yake “You still have so much to learn my son” akasema Habiba “Umekuwa unaniambia maneno hayo kila wakati kwamba bado kuna mengi natakiwa kujifunza.Wapi nikajifunze hayo unayosema natakiwa kujifunza?akauliza Mathew “You don’t understand……”akasema Habiba na Mathew akamkatisha “Make me understand then! akasema kwa ukali na kusimama.Habiba akamtazama kwa macho makali kisha akasema “Sit down ! Mathew akaketi “Nilikuonya na leo tena ninarudia kukuonYa likiwa ni onyo la mwisho kwamba unapozungumza nami chunga sana ulimi wako.Usirudie tena kusimama na kuninyooshea kidole.Umenisikia Mathew?! Akauliza Habiba kwa ukali “Samahani mama” “Ninafahamu unauchukia ugaidi na karibu nusu ya maisha yako umekuwa ukipambana na magaidi lakini vita ya ugaidi si rahisi kama unavyodhani ndiyo maana ninakuambia kwamba kaa jifunze.Unadhani hakuna mwingine ambaye ninaweza kumuweka katika nafasi yako?Wako wengi sana.Mamilioni ya majasusi lakini nimeamua kukuchagua wewe miongoni mwao hivyo tafadhali fuata kile ninachokuelekeza ! akasema Habiba kwa ukali “Sawa mama nimekuelewa.Samahani sana” akasema Mathew “Unakwenda Tanzania kwa kazi moja tu ya kumuua James Kasai vile vile kuung’oa mzizi wa IS afrika Mashariki.Hii si misheni nyepesi lakini nitakupa kila aina ya msaada kuhAkikisha unafanikiwa.Ukiwa Dar es salaam nitakupa maelekezo yote ya mahala alipo James Kasai na vile vile kuhusiana na mtandao wa IS.Utaanza kwanza na James Kasai halafu utamalizia na IS.Sikupangii namna utakavyoendesha operesheni yako lakini usimweleze mtu yeyote kuhusu mahala ulipokuwa na kuhusu mimi.Narudia usimueleze chochote mtu yeyote kuhusu yale uliyoyapitia toka kutekwa na Mossad hadi kufika kwangu kwani kama nilivyokueleza jambo hili ni siri yangu nawe” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Utaondoka toka hapa hadi Cairo Misri kwa kutumia hati ya kusafiria ya Abu Al Zalawi raia wa Saudia Arabia na kutoka Misri utapanda ndege ya moja kwa moja kuelekea Tanzania.Kila kitu kwa ajili ya safari hiyo kimekwisha andaliwa na muda wako wa kukaa katika eneo la Afrika Mashariki ni siku thelathini.Utakapomaliza misheni yako utatoweka na asifahamu mtu yeyote umeelekea wapi.Utarejea hapa kuja kuendelea na kile ambacho nimekuleta hapa ukifanye.Nitakupa maelekezo namna ya kuweza kuondoka Tanzania bila mtu yeyote kujua umeelekea wapi” akasema Habiba “Mama kwa mara nyingine tena ninakuomba samahani kwa kukukwaza hata hivyo kuna kitu nataka kuuliza kama utaniruhusu” “Uliza usihofu” akasema Habiba “Kwa nini umeguswa na Afrika mashariki hadi ukanitaka nikamuue mmoja wa washirika wako?akauliza Mathew na Habiba akatabasamu “Ni kwa sababu sitaki eneo unakotoka liingie katika machafuko ndiyo maana nataka ukahAkikishe unamaliza hatari yoyote inayoweza kusababisha mvurugano afrika Mashariki.Nimefanya hivi kutokana na mapenzi makubwa uliyo nayo kwa nchi yako.Umepitia magumu mengi yote ni kwa ajili ya nchi yako Tanzania na kwa kuwa ninakupenda kama kijana wangu sitaki kukuona ukiumia kwa sababu ya kile kinachotokea katika nchi yako ndiyo maana nataka ukamalize hatari hiyo inayoikabili nchi yako na pale utakapohAkikisha iko salama basi utarejea hapa kuendelea na misheni nyingine.Naamini sasa umeanza kunielewa kwa nini nilikwambia kwamba hapa ndipo mahala unapotakiwa uwepo” akasema Habiba “Kweli mama nimeanza kukuelewa kwa nini uliniambia vile na ninashukuru sana kwa kunipa fursa ya kwenda kuipigania nchi yangu na kuokoa jumuiya ya Afrika mashariki isivunjike hata hivyo bado ninajiuliza namna nitakavyoweza kupambana na James Kasai ambaye ana kikosi kikubwa chenye zana nzito za vita na mimi nikiwa peke yangu au na watu wangu wachache ambao nitawateua wanisaidie katika operesheni yangu” “Kuna siri ambayo wengi hawaifahamu kuhusu James Kasai.Huyu mtu haishi porini kama watu wanavyodhani.James Kasai anaishi jijini Kampala tena maisha ya kifahari sana.Tanzania,Rwanda na Congo zinaandaa kikosi kwa ajili ya kwenda kuvamia misitu kumsaka James lakini hawatafanikiwa kumpata.James haishi msituni anaishi Kampala.Utakapofika Dar es salaam ndipo nitakapokupa maelekezo kuhusiana na mahala alipo James.Hii ni siri ninakupa ambayo hata wakuu wa nchi za Afrika Mashariki hawaijui” akasema Habiba “Mama mambo haya yote unayafahamu vipi?akauliza Mathew “Narejea tena ile kauli yangu tulia ujifunze.Utafahamu mambo mengi sana kama ukiwa mvumilivu na utanishukuru badala ya kunichukia” akasema Habiba “Kitu kingine,Najma asifahamu chochote kama unakwenda Tanzania.Utamweleza nimekutuma kazi nchini Misri.Ukifika Tanzania lazima utakutana na ndugu jamaa na marafiki zako na mkeo Peniela lazima atapata habari kwamba uko hai lakini siku zote muweke Najma mbele kwani anakupenda sana na furaha yake iko kwako.Nadhani umenielewa Mathew” “Nimekuelewa mama.Ninakushukuru kwa mara nyingine tena kwa fursa hii uliyonipa ya kwenda kuisaidia nchi yangu.Sasa nimeanza kukuelewa ulivyosema kwamba uko tofauti na watu wanavyodhani.Ahsante kwa kunipa nafasi ya kukufahamu japo kidogo” akasema Mathew na mazungumzo yakaishia pale Habiba akamtoa Mathew mle ndani akamruhusu aondoke. “Mtu niliyekula kiapo cha kumuua pale nitakapomtia machoni leo hii ndiye amegeuka msaada kwa nchi yangu.Imenishangaza sana sikutegemea kama Habiba Jawad angeweza kufanya kitu kama hiki alichokifanya.Japo kuna maswali mengi ambayo ningependa kumuuliza lakini ngoja nikafanye kama alivyonitaka.Ninamshukuru hata kwa hiki kidogo alichonisaidia kwa nchi yangu” akawaza Mathew akielekea nyumbani kwake baada ya kuondoka kwa Habiba Jawad “Hatimaye ninarejea tena nyumbani.Natamani ningekuwa na mbawa nipae hata sasa hivi kwa furaha niliyonayo ya kwenda tena nyumbani lakini siendi kustarehe.Ninakwenda katika misheni ambayo si misheni rahisi.Ninakwenda kumuua James Kasai mmoja wa watu hatari kabisa katika Afrika Mashariki.Haitakuwa operesheni nyepesi kama alivyosema Habiba.James Kasai ni mtu aliyejizatiti sana kiulinzi na mbaya zaidi ni kwamba anahifadhiwa na serikali ya Uganda hivyo maficho yake si mahala ambapo panaweza kuingilika kirahisi hata hivyo nitahAkikisha ninamtia mikononi na kumuua.Habiba amenishangaza pia aliposema kwamba anataka nikaung’oe mzizi wa IS nchini Tanzania na Afrika mashariki.Hiki ni kikundi ambacho amekuwa anakifadhili fedha kwa nini leo hii anataka nikaung’oe mzizi wake Tanzania?akajiuliza Mathew “Nisiumize kichwa changu kwa mawazo ninachotakiwa ni kuanza kujipanga namna nitakavyotekeleza operesheni hii muhimu sana.Nahitaji kutafuta watu watakaonisaidia katika operesheni hiyo.Kwa namna yoyote ile namuhitaji sana Gosu Gosu.Yule ni mwanajeshi asiyeogopa chochote.Sifahamu nitampata wapi,nitajua nikifika Tanzania.Ninamuhitaji vile vile Ruby.Huyu naye sifahamu nitampata wapi lakini nitakapofika Tanzania nitajua” akasimama baada ya picha fulani kumjia akilini “Austin January ! akawaza na sura yake ikabadilika “Ni mtu ambaye anaweza kuwa muhimu sana anaweza akanisaidia mno lakini sifahamu kama naye alinusurika usiku ule tuliposhambuliwa na kikosi cha Mossad.Lilikuwa ni shambulio baya sana.Haya yote nitayajua nikifika Dar es salaam” akawaza na kumkumbuka Peniela “Peniela mke wangu na watoto wangu.Sijui watakuwa katika hali gani pale watakaposikia kwamba niko hai.Dah ! kweli mambo yamevurugika sana lakini kila kitu kitakwenda kujulikana huko huko mbele ya safari” akawaza Mathew DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa tano za asubuhi mwili wa Millen Kelelo mke wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania uliwasili katika viwanja vya ikulu kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Tukuyu Mbeya kwa mazishi.Watu walikuwa ni wengi na ulinzi ulikuwa mkali sana.Kila aliyepita alikaguliwa na mitambo maalum kuhAkikisha hakuna anayeingia na silaha au kitu chochote cha hatari. Vilio vilisikika pale mwili wa Millen ulipokuwa unashushwa garini na kupelekwa ndani ambako wanafamilia walipewa nafasi ya kwanza ya kuuaga mwili wa mpendwa wao kabla ya waombolezaji wengine.Ni wazazi na Dr Fabian pekee walioruhusiwa kuuona mwili wa Millen kwa mara ya mwisho kwani ulikuwa umeharibika sana.Jeneza likafunguliwa na Dr Fabian akalisogelea machozi yakamporomoka “Oooh Millen kwa nini umekufa kifo kibaya namna hii?Umewakosea nini hawa watu hadi wakuue kikatili namna hii?Endapo ningefahamu kama unakwenda kufa kifo cha namna hii nisingekuruhusu uende.Nani atabaki mshauri wangu?Maisha yangu yatakuwaje bila wewe Millen? Sijawahi lia machozi mengi namna hii katika maisha yangu ninakuahidi wale wote waliofanya kitendo hiki watalipa kwa gharama kubwa sana.Ninaapa mmoja baada ya mwingine lazima watalipa ukatili huu waliokufanyia.Kwa heri Millen tutakutana huko kwa muumba wetu kwani wote safari yetu ni moja” Dr Fabian aliyaongea maneno haya kimoyo moyo akimuaga mke wake kipenzi Millen Kelelo.Alipotoka wakafuata wazazi kisha jeneza likafungwa wengine walitoa heshima zao za mwisho wakati jeneza limefungwa. Wakati wanafamilia wakiendelea kuuaga mwili wa Millen,Dr Fabian akajulishwa kwamba Rais wa Kenya tayari ametua uwanja wa ndege na alikuwa njiani kuelekea ikulu kushiriki katika zoezi lile la kuuaga mwili wa Millen.Dr Fabian akatoka nje akachukua simu na kumpigia Patrice Eyenga. “Patrice nimetoka kuutazama mwili wa Millen sasa hivi.Kilichofanyika kilikuwa ni unyama uliovuka mipaka.Huyu mwanaharamu James Kasai lazima apatikane kwa namna yoyote ile.Sijali kama tutaingia vitani na Uganda au vipi lakini lazima apatikane akiwa mzima au amekufa.Kitendo alichokifanya hakivumiliki” akasema Dr Fabian “Dr Fabian hivi tunavyozungumza kikosi kwa ajili ya operesheni ya kumsaka James Kasai kiko uwanjani wakijiandaa kuondoka kuja Tanzania kuungana na wenzao” “Safi sana Patrice.Tayari maandalizi yamekamilika kwa ajili ya kikosi hicho” “Ahsante sana Dr Fabian tutaendelea kuwasiliana” akasema Patrice wakaagana na kukata simu “Nilikwisha anza kufikiria kuachana na mpango wa kutumia kikosi cha jeshi kumsaka James Kasai lakini baada ya kuona ukatili aliomfanyia mke wangu nimeamua kuendelea na maandalizi ya kikosi cha jeshi cha pamoja.Hawezi akafanya ukatili wa namna hii halafu akaachwa hai.Jenerali Akiki ni rafiki yangu sana,Uganda ni ndugu zetu lakini katika hili ninaweka kila kitu pembeni na nitapeleka kikosi kwenda kumsaka James Kasai hata kama Uganda hataki jambo hilo.Tayari Jenerali Akiki amekwisha dai kwamba kupeleka kikosi maalum kumtafuta James Kasai ni kitendo cha uvamizi na ameahidi kujibu lakini akithubutu kuua hata mwanajeshi mmoja ataiona nguvu yangu.Nitamchapa vibaya sana na hata kumuondoa madarakani” Dr Evans akatolewa mawazoni baada ya kujulishwa kwamba tayari wanafamilia na ndugu wa karibu wamekwisha maliza zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.Akarejea ndani na kushauriana jambo na wasaidizi wake pamoja na mkuu wa kamati ya maandalizi ya shughuli ile.Wakati wakijadiliana akajulishwa kwamba rais wa Kenya David Njoroge alikuwa amewasili.Akatoka kwenda kumpokea akamkaribisha ndani wakawa na mazungumzo ya faragha ya dakika chache “Pole sana Dr Fabian kwa kilichotokea” akasema Rais David “Ahsante sana David.Ahsante sana kwa kuja kunifariji” “Nilikuwa na ziara ya kwenda Afrika Kusini lakini imenibidi kuahirisha ili kuja kuungana nawe katika wakati huu mgumu.Mke wangu yeye nimemtuma aende Rwanda akaniwakilishe na makamu wangu wa Rais amekwenda jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Msiba huu ni mkubwa.Si msiba wenu peke yenu ni msiba wa wana afrika mashariki wote” akasema David “Kilichofanyika ni ukatili uliovuka mipaka ya ubinadamu.Ni kitendo ambacho hakiwezi kuvumilika hata kidogo ! akasema Dr Fabian “Dr Fabian pamoja na kuwa katika wakati mgumu sana lakini kuna jambo ambalo ninataka kuzungumza nawe” “Jambo gani David? “Ni kuhusu hatua unazotaka kuchukua kuhusu mtu ambaye anadaiwa kuhusika katika shambulio hili James Kasai.Nimejulishwa kwamba mmekubaliana na marais wa Rwanda na Congo kuunda kikosi kimoja kitakachokwenda Uganda kufanya operesheni ya kumsaka na kumtia nguvuni James Kasai” “Ni kweli David.Tumekubaliana kuunda kikosi ambacho kitakwenda Uganda kuhAkikisha James Kasai anapatikana.Hivi tunavyozungumza kikosi cha kutoka Congo kiko uwanja wa ndege kikijiandaa kuja Tanzania kuungana na vikosi vya Tanzania na Rwanda.Watafanya mazoezi ya pamoja ya wiki moja kisha wataelekea katika misitu ya Kaskazini mwa Uganda ambako ndiko aliko James Kasai na wataendesha operesheni ya kijeshi hadi watakapompata James.Safari hii hatapona lazima atiwe nguvuni” akasema Dr Fabian “Dr Fabian umekwisha wasiliana na Rais wa Uganda ukamjulisha kuhusu mpango huo?akauliza David “Nimezungumza naye lakini hatukuelewana na Jenerali Akiki akadiriki kunitolea vitisho.Kwa nini anamkingia kifua James Kasai?Kwa nini hataki kutoa ushirikiano?Mimi na wenzangu tumekwisha amua kwamba Jenerali Akiki akubali au akatae lazima tuingie Uganda kumsaka James Kasai na kama akithubutu kuua hata mwanajeshi mmoja kutoka katika kikosi hicho kama alivyoahidi atakiona cha moto,nitamchakaza ! akasema Dr Fabian “Dr Fabian nimekuja kukushauri ndugu yangu simamisha kwanza shughuli zozote za kijeshi mnazotaka kuzifanya nchini Uganda ili tujaribu kutafuta suluhu kwa njia ya mazungumzo.Kabla sijapanda ndege kuja huku nimepewa taarifa kwamba vikosi vya Uganda na Rwanda vilikuwa vinashambuliana mpakani.Kwa ujumla hali si shwari na kuna hatari kubwa eneo zima la Afrika Mashariki likaingia katika machafuko.Kila nchi imeweka vikosi vyake katika utayari wa vita na tayari Uganda imekwisha waondoa mabalozi wake katika nchi za Rwanda na Congo hii inaashiria tayari kuna uhasama mkubwa sana baina ya nchi zetu.Kitendo cha kutumia nguvu za kijeshi kitakuwa ni kama kuongeza mafuta kwenye moto.Kitazidisha mzozo.Nashauri hatua zozote za kijeshi dhidi ya Uganda zisimamishwe kwanza na tuwashawishi Rwanda na Congo warejeshe majeshi yao nyuma ili yafanyike mazungumzo na kupata suluhu ya jambo hili” “David ahsante sana kwa kuguswa na jambo hili lakini naomba nikuhAkikishie kwamba mimi na wenzangu tumekwisha azimia kwamba kwa namna yoyote ile lazima James Kasai apatikane na ili kumpata lazima tutumie nguvu za kijeshi.James tayari amekuwa hatari kwa nchi zetu na tukimuacha atakuwa na madhara makubwa mno.Tayari amekwisha fanya ukatili mkubwa sana huko Congo hadi kufikia hatua ya kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya uhalifu wa kivita.Hatuwezi kumuacha akaendelea lazima tummalize na mwisho wake umewadia.Hatutarudi nyuma katika maamuzi haya na kama Uganda hawatatuunga mkono katika suala hili sisi tutaendelea na operesheni hadi tuhAkikishe James Kasai amepatikana.Endapo Jenerali Akiki ataamua kuanzisha vita sisi tuko tayari na tutamchakaza vibaya sana” akasema Dr Fabian na kunyanyuka “Mheshimiwa Rais nadhani tutaendelea na mazungumzo badae leo tuna ratiba ndefu sana.Baada ya kumaliza shughuli za hapa tunatarajia kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mazishi siku ya kesho” “Ahsante sana Dr Fabian kwa kunipa dakika hizi chache tukazungumza.Nakuomba ukipata nafasi yatafakari hayo niliyokueleza.Ni wewe ambaye unaweza ukainusuru jumuiya yetu isiingie katika machafuko” akasema David “Ahsante kwa ushauri David nitauzingatia” akasema Dr Fabian kisha wakatoka kwenda kuendelea na ratiba nyingine.
Melanie Davis hakutoka katika chumba chake alikuwa anafuatilia katika runinga shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Millen Kelelo mke wa Rais wa jamhuri ya uungano wa Tanzania.Pembeni ya kitanda chake alikuwa na simu yake ambayo aliitumia kuwasiliana na Austin juu ya maendeleo ya GosuGosu.Kwa mujibu wa taarifa ya Austin hadi mchana ule bado hali ya Gosu Gosu haikuwa nzuri. “Ninaogopa hadi kwenda hospitali kumtazama Gosu Gosu kwani ni mimi ambaye nimesababisha haya yote yakamtokea.Kama nisingemtuma akamuue Devotha haya yote yasingemtokea.This isn’t over Devotha.Mimi nawe tutapambana.Ulifanikiwa mara ya kwanza sintakupa nafasi ya kufanikiwa mara ya pili..”akatolewa mawazoni na mlio wa simu akaichukua kutazama mpigaji alikuwa ni Devotha na sura yake ikajikunja. “Huyu shetani ninamuwaza kumbe naye ananiwaza ! akawaza Melanie huku akiitazama simu kwa hasira halafu akaipokea “Hallo”akasema “Melanie samahani sana kwa maneno niliyokutamkia mara ya mwsho tulipozungumza simuni.Kuna maneno ambayo niliyatam…….” “Devotha hayo yamekwisha pita nieleze sababu ya kunipigia simu” akasema Melanie na kumkatisha Devotha “Melanie kutokana na matokeo mazuri ya kile ulichokifanya ndiyo maana nimetangulia kwa kukuomba samahani kwa yale niliyokutamkia.Pokea salamu nyingi za pongezi kutoka kwa Rais Michael Weren.Anakupongeza kwa hiki ulichokifanya ambacho ndicho hasa tulichokuwa tunakitaka na ndicho tulikutuma ukakifanye.Japokuwa ulifanya kwa kutumia njia unazozijua wewe lakini matokeo yake ndiyo yale ambayo tulikuwa tukiyatafuta.Kutokana na matokeo haya makubwa kuanzia sasa mashirikiano yako na James Kasai yamebarikiwa na unaweza ukaendelea.Hakuna atakayehoji kama James anashirikiana na magaidi ama vipi lakini tunachohitaji sisi ni mipango yetu iende vyema kwa hiyo uko huru Melanie kushirikiana na yeyote ili mradi uhAkikishe kwamba mashirikiano hayo hayatakuwa na athari kwetu” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Jambo la pili ni kwamba baada ya kumaliza awamu ya kwanza sasa unaingia katika awamu ya pili ambayo ni kumuondoa Rais Patrice Eyenga wa Congo.Jumuiya ya Afrika mashariki haina muda mrefu itasambaratika hivyo tunaelekeza macho yetu nchini Congo.Lazima tumuondoe Rais Patrice Eyenga.Hivyo basi fanya mazungumzo na James Kasai muone namna jambo hilo linavyoweza kutekelezeka.Kama kuna chochote ambacho James Kasai atahitaji sisi tuko tayari kumpatia” akasema Devotha,Melanie akashusha pumzi ndefu na ukimya mfupi ukapita kisha Devotha akauliza “Umenielewa Melanie nilichokwambia? “Nimekuelewa Devotha nitalifanyia kazi” akasema Melanie “Good.Naomba tuweke tofauti zetu pembeni na tumalize salama misheni yetu”akasema Devotha “Lakini hii haina maana kwamba nimekusamehe kwa kitendo ulichokifanya cha kutaka kumuua Gosu Gosu ! akasema Melanie “Kama nisingemuwahi angeniua mimi.Ninamfahamu Gosu Gosu vizuri.Kwa nini lakini ukataka kuniua Melanie?Kitu gani kibaya kimesababisha unichukie kiasi hiki?Tusichukiane tafadhali hadi kufikia hatua ya kutaka kuuana.Mimi nawe ni kitu kimoja” akasema Devotha “Lazima nikuue shetani wewe ! akawaza Melanie “Sawa Devotha naomba na wewe usirudie tena kunikaripia kama mtoto mdogo” “Nimekuelewa Melanie na samahani sana.Haitajirudia tena.Tukiachana na hayo nimezungumza na Edwin Mbeko anasema amepewa jukumu na Rais la kuchunguza nani waliokuwa wakishirikiana na balozi Germinus Mapupu katika kuandaa hafla ile ya chakula cha usiku kwa wake za marais.Usihofu kila kitu iko safi kwani hawataweza kugundua chochote kuhusu wewe” akasema Devotha na kuagana na Melanie “Wenyewe wameanza kunikubali kwa jambo nililolifanya.Devotha leo hii amekuwa mdogo kama nini.Ameona mwenyewe mimi si mtu wa kufanyia mchezo.Baada ya mafanikio makubwa sasa wanataka niende mbali zaia nimuue Patrice Eyenga.Ninakubaliana nao kwa kuwa Patrice Eyenga ni mmoja watu waliomo katika orodha ya wale ninaohitaji kuondoa roho zao.Alishiriki katika mauaji ya wazazi wangu hivyo hakuna msamaha lazima aondoke.Baada ya Patrice Eyenga atafuata Rais wa Tanzania Dr Fabian na Devotha ajiandae.Pale nitakapohAkikisha wale wote waliohusika katika kuwaua wazazi wangu wameondoka duniani ndipo nitakapoanza kuyapanga upya maisha yangu.Kwa sasa akili yangu yote naielekeza katika kulipiza kisasi” akawaza Melanie akainuka na kuchukua glasi yenye mvinyo mkali “Nitazungumza na James Kasai na tutapanga namna tutakavyoweza kumuondoa Patrice Eyenga.Kama tumeweza kumuondoa mke wake hatutashindwa kumuondoa Patrice Eyenga lakini huu ni mpango mkubwa sana ambao lazima upangwe kwa ustadi mkubwa mno.Ngoja niwasiliane naye sasa hivi bila kuchelewa nione ataniambia nini” akawaza Melanie na kuchukua simu ambayo huutumia kuwsiliana na James akampigia “Habari yako Melanie” akasema James Kasai baada ya kupokea simu “Nzuri James habari yako” “Hamsini kwa hamsini siwezi kusema nzuri au mbaya.Unasemaje Melanie kwani muda huu si wa kuzungumza simuni na nimepokea simu yako kwa kuwa ni mtu muhimu sana kwangu” “James samahani kwa usumbufu na ahsante kwa kupokea simu yangu.James nahitaji kuzunguza nawe pale utakapokuwa na nafasi.Nina jambo kubwa na la muhimu la kujadiliana” akasema Melanie “Jambo gani Melanie?Unaweza ukanigusia japo kwa ufupi nione uzito wake kama tunaweza kuzungumza sasa hivi au hadi tupate nafasi ya kutosha.Kuwa huru usiogope” akasema James Kasai “Baada ya awamu ya kwanza kuwa na mafanikio makubwa sasa nataka kuingia katika awamu ya pili nayo ni kumuua Patrice Eyenga” akasema Melanie na James Kasai akawa kimya kwa muda “James ! akaita Melanie “Melanie suala lako ni zuri na zito sana hatuwezi kulizungumza simuni.Tafadhali njoo Uganda.Nitampa maelekezo Eddie Okello atawasiliana na Gosu Gosu” “Gosu Gosu alipatwa na matatizo alipigwa risasi yuko katika hali mbaya sana” akasema Melanie “Gosu Gosu amepigwa risasi? “Ndiyo amepigwa risasi na watu wasiofahamika” “Pole sana.Namuombea apone haraka sana.Basi Eddie atawasiliana nawe moja kwa moja na kukupa maelekezo” akasema James na kuagana na Melanie “Gosu Gosu kupigwa risasi kunawastua watu wengi.Namshukuru Yule rafiki yake Austin ambaye amenipa moyo kwamba Gosu Gosu atapona.Yule jamaa Austin ndiye Yule ambaye Devotha alinieleza nikae naye mbali? Nakumbuka alinitajia majina kadhaa na mojawapo ni hili la Austin.Itanilazimu nifanye uchunguzi nijue kama ni yeye kweli ili niweze kumuepuka haraka sana.Baadae jioni ya leo nitakwenda hospitali.Hata hivyo he’s very handsome” akawaza na kutabasamu kidogo akachukua glasi yenye kinywaji akanywa “Afrika Mashariki nywele zimewasimama kwa tukio lile dogo la kuuawa kwa wake za marais sasa wasubiri mengine makubwa ambapo wataondoka Patrice Eyenga na swahiba wake Dr Fabian.Kama kuna rais mwingine ambaye alishiriki kupanga mauaji ya wazazi wangu naye pia ajiandae” akanywa mvinyo “Sikutegemea kama katika maisha yangu nitakuwa mkatili namna hii.Lakini wakati mwingine walimwengu ndio wanaosababisha watu wakawa makatili”
Bado hali ya Gosu Gosu iliendelea kuwa tete.Austin January hakubanduka hospitali akifuatilia kwa karibu sana hali ya Gosu Gosu akihofia yawezekana waliotaka kumuua wangeweza kumfuata pale hospitali.Akiwa ametulia nje akitafakari mara akawaona watu wawili wakijana walipofika karibu akamtambua mmoja wao alikuwa ni Melanie Davis.Akasimama “Melanie” akasema Austin na kumpa mkono Melanie “Austin” akasema Melanie na Austin akawakaribisha katika viti wakaketi “Usingesumbuka kuja huku usiku huu ungepiga tu simu kuulizia maendeleo ya mgonjwa” akasema Austin “Austin hujui tu hali gani ninapitia kwa sasa kwa tukio hili la Gosu Gosu kushambuliwa.Nashindwa kula wala kunywa.Natamani nikae hapa hospitali nikimtazama mpenzi wangu muda wote.Gosu Gosu ni kila kitu kwangu” akasema Melanie na kuchukua kitambaa akafuta machozi “Nyamaza kulia Melanie.Kama nilivyokueleza awali kwamba Gosu Gosu ni jasiri na atashinda vita hii ya kupigania maisha yake” akasema Austin “Austin najua hayo ni maneno ya kunipa moyo lakini ukweli halisi ni kwamba Gosu Gosu hatapona” akasema Melanie na kuanza tena kulia na kuangusha kichwa chake mapajani mwa Austin ambaye alimuinua na kumpiga piga mgongoni “Melanie usilie tafadhali.Gosu Gosu anatuhitaji sana sisi muda huu tuwe majasiri.NinakuhAkikishia kwamba Gosu Gosu atapona.Naomba uniamini” akasema Austin. Na Melanie akafuta machozi “Kuwa jasiri Melanie.Gosu Gosu atapona ninakuhAkikishia” akasema Austin.Joyce aliyekuwa amefuatana na Melanie akainuka kama vile anazungumza na simu akaenda kusimama pembeni. “Austin nakushukuru sana kwa kuacha shughuli zako na kuja kushinda hapa na mgonjwa usiku na mchana” akasema Melanie “Kama nilivyokueleza Gosu Gosu ni ndugu yangu hivyo niko tayari kuacha kila kitu kwa ajili yake” akasema Austin “Unafanya kazi gani Austin? “Mimi ni mfanya biashara” “Biashara gani? “Ninafanya biashara ya kuuza magari” “Ouh vizuri sana.Magari ya aina gani unauza?Unaweza kunielekeza lilipo duka lako nije kutembelea? “Mimi sina duka la magari bali biashara yangu ni kuingiza gari mbili au tatu natafuta wateja ninawauzia kisha naagiza nyingine au wakati mwingine watu wanaohitaji magari wamekuwa wakinitumia sana mimi kuwaagizia magari nje ya nchi” akasema Austin “Kwa nini usifungue duka lako mwenyewe la kuuza magari kuliko kuagiza gari moja moja? “Mtaji wangu bado mdogo ndiyo maana ninafanya hivyo lakini pale mtaji wangu utakapokuwa mkubwa nina mpango wa kufungua duka” akasema Austin na ukimya ukapita “Nitakapohitaji gari nitakuja kukuona.Mimi ni mpenzi sana wa magari ya kifahari” “Usijali pale utakapohitaji njoo unione nitakusaidia kupata gari la ndoto yako” akasema Austin na Melanie akaomba akamuone Gosu Gosu.Austin akazungumza na muuguzi Melanie akavishwa mavazi maalum na kuingizwa ndani ya chumba alimo Gosu Gosu aliyekuwa akipumua kwa msaada wa mashine Melanie alitumia dakika zaidi ya kumi ndani ya chumba kile cha Gosu Gosu kisha akatoka huku machozi yakimtiririka “Austin I need to go home.Ninahisi kama kichwa change kinataka kupasuka baada ya kumuona Gosu Gosu akiwa katika hali ile.Tutaendelea kuwasiliana.Kesho sintafika hapa hospitali nitakuwa na safari ya muhimu sana.Hata hivyo nitajitahidi kuwasiliana nawe kujua maendeleo” akasema Melanie na Austin akawasindikiza hadi katika gari lao wakaondoka “Umefanikiwa kuipata picha ya Austin?Melanie akamuuliza Joyce “Ndiyo madam.Nimefanikiwa kumpiga picha kadhaa bila yeye kutambua” “Good” akasema Melanie na kuchukua simu ya Joyce akazitazama zile picha za Austin ambazo Joyce alimpiga bila yeye kujua. “He’s such a handsome guy.Ameanza kunivutia.Kama Gosu Gosu hatapona basi nitakuwa na huyu Austin.Ana sura nzuri,umbo zuri anapangilia maneno yake wakati wa kuongea na anajali.Hata hivyo natakiwa kuthibitsha kama kweli ni yeye yule ambaye Devotha alinionya nikae naye mbali” akawaza na kuzihamisha zile picha kutoka katika simu ya Joyce kwenda katika simu yake halafu akamtumia Devotha akimuuliza kama Yule ndiye Austin aliyemuonya akae naye mbali “Kaa mbali sana na huyu mtu.Usimpe nafasi akakufahamu wewe ni nani.Huyu ndiye mmoja wa wale niliokukanya usiwe karibu nao” Devotha akamjibu Melanie “Pamoja na onyo hili la Devotha lakini tayari Austin amekwisha nivutia sana.Nitamsogeza karibu.If he’s a killer like Gosu Gosu He’ll be killing for me.Hakuna mwanaume katika dunia hii anayeweza kusema hapana kwa Melanie” akawaza Melanie na kutabasamu Muda mdupi baada ya akina Melanie kuondoka pale hospitali,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akampigia simu Austin “Habari yako Austin” akauliza Dr Fabian “Nzuri kabisa mheshimiwa Rais” “Vipi maendeleo ya mwenzako? “Hali yake bado si nzuri hata kidogo” “Tunaweza kumsafirisha kumpeleka nje ya nchi? “Nimewauliza madaktari wamesema kwamba kwa hali yake hii haitawezekana.Kwa sasa anapumua kwa msaada wa mashine” “Sawa Austin utaendelea kunijulisha kile kitakachokuwa kinaendelea hapo hospitali.Kesho tutamzika mke wangu kisha nitarejea Dar es salaam nitafik hapo hospitali kumtazama mwenzako.Ulisema anaitwa nani? “Papi Gosu Gosu” “Sawa nitafika hapo kumtazama Gosu Gosu.Bado naendelea kusisitiza umakini sana kwani hatujui waliomshambulia Gosu Gosu walikuwa na malengo gani” akasema Dr Fabian “Ninachukua tahadhari kubwa mheshimiwa Rais ndiyo maana sijabanduka hapa hospitali nikihofia pengine waliofanya kitendo hiki wakijua bado yuko hai wanaweza wakamfuata hapa hospitali” “Austin nakutakia usiku mwema.Tutaonana kesho” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Austin na Rais akakata simu
Afrika Mashariki iliamshwa na taarifa za vikosi vya Uganda na Rwanda kushambuliana usiku kucha katika mpaka wa nchi zao.Wakati hayo yakijiri katika mpaka wa Uganda na Rwanda,nchini Tanzania kikosi maalum cha jeshi kilichojumuisha wanajeshi kutoka nchi za Tanzania Rwanda na Congo kilikwisha kutana na kuanza mazoezi ya pamoja kabla ya kuelekea nchini Uganda kumsaka James Kasai. Pamoja na hali hiyo tete iliyozikumba baadhi ya nchi za Afrika Mashariki bado biashara kati ya Tanzania na Uganda ziliendelea kama kawaida.Safari za ndege ziliendelea vile vile safari za treni na mafuta yaliendelea kusafirishwa kama kawaida kutoka Uganda kwenda Tanzania. Katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere,Melanie Davis alikuwa mmoja wa abiria waliokuwa ndani ya ndege ya shirika la ndege la Tanzania ikielekea jijini Kampala Uganda.Taratibu ndege ikaanza kuondoka kisha ikashika kasi na kupaa kuelekea Kampala. Iliwachukua muda wa saa tatu na dakika thelathini kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda.Hali ilikuwa shwari kabisa na hakukuwa na kitisho chochote kwa abiria japokuwa ulinzi ulikuwa mkali mno uwanjani pale . Melanie na abiria wengine wakashuka ndegeni na kwenda kukamilisha taratibu za uhamiaji kisha wakaruhusiwa kuingia Uganda.Eddie Okello alikuwepo uwanjani kumpokea Melanie “Melanie karibu tena kwa mara nyingine Uganda” akasema Eddie baada ya kumpokea Melanie “Ahsante Eddie nashukuru” akasema Melanie na Eddie akamuongoza katika gari lake la kifahari wakaondoka pale uwanjani “Nataka kujua maendeleo ya Gosu Gosu”akasema Eddie “Hali yake si nzuri kama nilivyokueleza simuni.Mpaka sasa anapumua 0kwa msaada wa mashine.Madaktari wanasema kwa hali aliyofikia ni hamsini kwa hamsini na loloet linaweza kutokea hivyo tuzidi kumuombea” “Nimemfahamu Gosu Gosu kwa miaka mingi toka tukiwa wadogo msituni.Ni mpiganaji asiyekata tamaa na nina uhakika atapambana kwa ajili ya maisha yake na wale anaowapenda” akasema Eddie “Yawezekana kweli Gosu Gosu akapona kwani huyu ni mtu wa pili sasa anatamka hivyo.Namuombea apone bado ninamuhitaji”akawaza Melanie “Nani lakini waliomshambulia Gosu Gosu?Tayari wamepatikana?akauliza Eddie “Mpaka sasa haijulikani bado nani waliomshambulia na hajakamatwa mtu yeyote kuhusiana na tukio lile” “Ilikuwa ni bahati watu hao walimuwahi kwani kama wangempa upenyo kidogo wasingefanikiwa.Ninamfahamu Gosu Gosu ana uwezo mkubwa wa kucheza na silaha na alikuwa akishika silaha sote tulikuwa tunaingiwa hofu kwani hubadilika na kuwa mtu mwingine kabisa”akasema Eddie “Kwa bahati mbaya siku alipopigwa risasi hakuwa na silaha yoyote garini.Alichokumbuka ni fulana ya kuzuia risasi ambayo huwa haachi kuivaa kila mara.Hiyo ndo iliyomsaidia kwani alipigwa risasi nyingi tumboni .Bila fulana ile hivi sasa tyari tungekwisha mzika.Waliomshambulia walikusudia kumuua kabisa” Akasema Melanie “Tuzidi kumuombea apone haraka” akasema Eddie “Kampala kunaonekana shwari kabisa kama vile hakuna kitisho chochote cha usalama” Akauliza Melanie “Kampala kuko shwari.Shughuli zinaendelea kama kawaida na hakuna kitisho chochote cha usalama.Mapigano yanaripotiwa kuendelea huko mpakani lakini huku hakuna chochote” akajibu Eddie na kupunguza mwendo kidogo halafu akaendelea “Hawa mataifa wanaotaka kuungana kumtafuta James wanajisumbua bure hawataweza kumpata James hata wafanye nini badala yake wanawapeleka wanajeshi wao kwenda kuuawa” akasema Eddie.Melanie alikuwa kimya kabisa akimsikiliza.Eddie alipoona Melanie haongei chochote akaweka mziki na safari ikaendelea bila mazungumzo yoyote hadi walipofika katika barabara moja nzuri iliyopandwa maua mazuri pembezoni.Baada ya muda wakafika katika geti lililokuwa linalindwa na askari wenye silaha.Eddie akashusha kioo na kusalimiana na kiongozi wa askari wale ambaye aliamuru geti lifunguliwe na gari la Eddie likaingia ndani.Eddie akamfungulia mlango Melanie akashuka na kushangaa kwa madhari nzuri aliyoiona.Kulikuwa na jumba kubwa zuri sana Eddie akamkaribisha ndani akamtambulisha kwa wahudumu wanne wa jumba lile ambao walikuwa wamevaa sare maalum.Mwanamama mmoja ambaye alionekana ndiye msimamizi mkuu wa jumba lile akawaongoza Melanie na Eddie kuelekea katika chumba cha mapumziko “Melanie karibu sana.Hapa ni sehemu salama kabisa usiwe na hofu” akasema Eddie “Hapa ni wapi?Mbona kunalindwa na polisi?akauliza Melaniehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hii ni nyumba ya wageni”akajibu Eddie na kunywa kinywaji kidogo walichoandaliwa “Nyumba gani ya wageni inalindwa na askari wenye silaha?akauliza Melanie akionekana kuwa na hofu kidogo “Hii ni nyumba ambayo wageni maalum wa Rais wa Uganda hufikia ndiyo maana unaona inalindwa na askari wenye silaha” “Wageni wa Rais?Melanie akashangaa “Ndiyo hii ni nyumba ya kufikia wageni maalum wa rais” “Mimi si mgeni wa Rais.Mimi nimekuja kuonana na James Kasai na sina mahusiano yoyote na Rais.Au amenileta hapa kwa sababu za kiusalama? Akauliza Melanie “Sifahamu chochote Melanie lakini yeye malekezo niliyopewa ni kukuchukua na kukuleta hapa na mimi ninatekeleza maelekezo hayo” “Yuko wapi James?akauliza Melanie “Siwezi kujibu swali hilo” akasema Eddie na kusimama “Melanie nimekufikisha mahala nilipoelekezwa mimi ninaondoka ninakwenda kuendelea na shughuli zangu tutaonana tena” akasema Eddie “Sasa nitaonana vipi na James?Melanie akauliza “Usihofu Melanie.James utaonana naye.Kuwa na amani” akajibu Eddie na kuondoka
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment