Search This Blog

Thursday 17 November 2022

SIRI : MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA - 2

 






Simulizi : Siri: Maisha Na Kifo Cha Melanie Chuma

Sehemu Ya Pili (2)









Akiwa amepitiwa na usingizi sofani,Gosu Gosu alihisi kama mikono laini inamgusa shingo yake.Akajaribu kufumbua macho kweli kulikuwa na mtu mbele yake “Sandra” akasema Gosu Gosu “Samahani kwa kukatisha usingizi wako”akasema Sandra “It’s okay” akasema Gosu Gosu na kunyanyuka haraka akainyakua bastora yake “Any danger?akauliza “Relax Gosu Gosu.Hakuna hatari yoyote.Kumekucha tayari.Ni muda wa kuendelea na kazi” akasema Sandra na kuelekea katika kompyuta “Sikufumba macho toka nilipoanza uchunguza kompyuta hizi za Tamar na nimefanikiwa kupata mambo kadhaa.Nadhani tungekutana wote ili niwaeleze kile nilichobahatika kukipata” akasema Sandra.Gosu Gosu akaenda kuwaamsha Austin na Agatha wote wakakutana ofisini “Kuna mambo kadhaa nimefanikiwa kuyapata katika kompyuta hii kubwa ya Tamar.Kwanza kabisa Tamar amekuwa akipokea fedha kutoka katika akaunti moja kwenye benki ya Autum iliyoko Ufaransa.Sijaweza kumpata mmiliki wa akaunti hiyo kwani amefichwa lakini inaonyesha ni fedha nyingi amekuwa akipokea.Akaunti yake iliyoko katika benki moja hapa nchini ina shilingi bilioni mbili na milioni mia sita sabini na tisa”Sandra akanyamaza “Ni fedha nyingi sana” akasema Austin “Ndiyo maana hakuona ugumu kunipatia zaidi ya milioni moja kila siku” akasema Agatha “Tamar ni mtu makini sana na amekuwa makini katika kuchunga mawasiliano yake kama nilivyowaambia kwamba nilimtengenezea program maalum ya kufuta rekodi za mawasiliano yake yote ya simu na ndivyo anavyofanya katika kompyuta yake kila anapowasiliana na mtu hufuta kila kitu.Kwa bahati mbaya kwake na nzuri kwetu nilikuta kuna barua pepe ambayo aliisoma na kusahau kuifuta ambayo iliingia jana usiku.Imetoka kwa mtu anaitwa Dinosaur” “Dinosaur? Akauliza Gosu Gosu na kutoa kicheko kidogo “Wanyama hawa wamekwisha toweka duniani miaka mingi.” Akasema Austin kwa utani “Mtu huyo anajiita Dinosaur amemtumia Tamar ujumbe huu” akasema Sandra na kuwaonyesha akina Austin ule ujumbe uliotumwa na Dinosaur “Awamu ya kwanza na ya pili zimemalizika vyema,jiandae kwa awamu kubwa ya tatu.Nimetaarifiwa njiwa anaandaliwa na muda wowote atatua Dar es salaam.Maandalizi yamekamilika? Hivi ndivyo ulisomeka ujumbe ule aliotumiwa Tamar.Ukimya ulitanda pale sebuleni baada ya muda Austin akasema “Kama alivyosema Gosu Gosu kazi bado tunayo kubwa.Huyo Dinosaur ni nani? Umeweza kufuatilia barua pepe yake na kumgundua mahala alipo?akauliza Austin “Nimejaribu lakini sijafanikiwa.Ni mtandao wa watu makini na wenye utaalamu mkubwa katika kuficha mambo yao” akasema Sandra “Kuna mpango mkubwa unaandaliwa kati ya Tamar na huyo Dinosaur.Kuna mtu anakuja Dar es salaam ambaye katika maelezo haya ametajwa kama njiwa.Dinosaur pia ametaja kumalizika kwa awamu ya kwanza na ya pili na sasa wanaingia katika awamu ya tatu inaonekana kuna mpango mkubwa unaoendelea ambao una awamu tatu na mbili tayari zimekamilika na sasa inafuata awamu ya tatu ambayo ndiyo hiyo inamuhusisha huyo njiwa anayetarajiwa kuingia nchini hivi karibuni.Tumebaki njia panda”akasema Austin “Hili ni fumbo kubwa tulimuhitaji sana Tamar aweze kutupa majibu ya maswali haya”akasema Gosu Gosu “Tamar hayupo,hivyo basi tuna kazi kubwa mbele yetu.Tayari tuna huyu mtu anaitwa Dinosaur.Tunatakiwa kumfahamu ni nani yuko wapi na nini mipango yao na Tamar.Kuna ile akaunti ambayo imekuwa ikitumika kumtumia Tamar fedha katika akaunti yake hiyo nayo tunapaswa kuifahamu ni ya nani.Kazi nyingine kubwa ambayo tunayo ni kumfahamu mtu ambaye ametajwa kwa jina la njiwa ni nani?Hiyo ndiyo kazi kubwa iliyoko mbele yetu” akasema Austin “Bado haikuishia hapo” akasema Sandra “Katika kompyuta hii pia nimegundua kuna faili moja lilikuwa limefichwa sana lina video mbili.Katika video hizo anaonekana Tamar na mtu ambaye naamini ni Rais Dr Fabian wakifanya mapenzi lakini Dr Fabian anaonekana akimuingilia Tamar kwa nguvu”akasema Sandra “What?akauliza Gosu Gosu na Sandra akacheza video moja.Katika video hiyo Tamar anaonekana akiwa kitandani amejipumzisha akiwa na nguo ya ndani na mara akatokea mtu mmoja ambaye sura yake ilikuwa inafanana na Dr Fabian akaenda kulala pembeni yake na kuanza kumtomasa Tamar.Kulitokea kutokuelewana kati yao na Tamar akamnasa kofi.Dr Fabian akaonekana kukasirika akamnasa Tamar makofi mfululizo Tamar akajikunja kitandani akilia,Dr Fabian akachukua waya akamfunga Tamar mikono kwa nyuma halafu akaanza kumuingilia huku akiwa amemziba mdomo.Alipomaliza akavaa nguo zake na kumfungua ule waya aliomfunga halafu akaondoka zake akamuacha Tamar kitandani akilia.Baada ya muda akainuka na kwenda kuizima kamera iliyokuwa ikichukua video ile.Video ya pili anaonekana Tamar akitoka kuwasha kamera na vinywaji vikaonekana mezani.Baada ya muda akatokea Fabian akiwa anafunga vizuri suruali yake.Alionekana ametoka maliwato.Akaketi pembeni ya Tamar wakaanza kunywa pombe huku wakivuta sigara.Mara Fabian akambusu Tamar shavuni na kutaka kutoa ulimi wake akaupeleka katika mdomo wa Tamar ambaye hakuonekana kupendezwa na kitendo kile akamnasa kofi.Fabian alichukizwa na kitendo cha Tamar kumnasa kofi akasimama na kumnasa Tamar makofi mawili mfululizo halafu akamsukumia katika sofa na kuichana sketi aliyokuwa ameivaa Tamar halafu akaivuta nguo ya ndani akaitupa chini akashusha suruali yake na kuanza kumuingilia Tamar huku akimnasa makofi.Alipomaliza akavaa suruali yake na kuondoka.Tamar akaenda kuizima kamera.Sebule ilikuwa kimya kila mmoja alipatwa na mshangao mkubwa. “I can’t believe this ! akasema Gosu Gosu “Play that again.Nataka nihakikishe kama kweli huyu anayeonekana katika video hii ni Dr Fabian huyu Rais wetu au ni video ya kutengeneza.Teknolojia imekua sana zama hizi na watu wanaweza kutengeneza video kwa ajili ya kumchafua mtu Fulani” akasema Austin na Sandra akaicheza tena ile video. “Play it again ! akasema Austin ikachezwa tena. “Sandra unaweza ukanihakikishia kwamba anayeonekana katika video hii ni Rais Dr Fabian?akauliza Austin “Kuna progamu ya utambuzi wa sura ambayo inaweza kutusaidia kujua kama kweli huyu anayeonekana katika video hii ni Rais Dr Fabian.Tatizo ni kwamba program hiyo iko SNSA na ili kuipata lazima nitumie akaunti yangu.Je mtakuwa tayari nitumie akaunti yangu ya SNSA?akauliza Sandra “Do it” akasema Austin.Sandra akaingia katika akaunti yake ya SNSA akafungua program hiyo ya kutambua sura na kuchukua picha iliyoko katika ile video akaiingiza katika program ikaanza kutafuta.Baada ya sekunde chache program ikatoa majibu na ikathibitisha Yule ni Rais Dr Fabian. “Oh my God ! akasema Austin “Sasa nimeanza kupata picha kwa nini Dr Fabian amekuwa mwepesi sana kumsikiliza Tamar kila atakachomweleza.Ni kwa sababu ya video hizi.Tumejiuliza mimi na Austin kwa nini Dr Fabian anampa Tamar kipaumbele kikubwa namna hii sasa jibu tumelipata” akasema Gosu Gosu “Kuna kitu nimekiona katika video hizi mbili.Ukitazama video hizi mbili utaona kamera iliyokuwa inachukua videro hizi ilitegwa mahala ambako Dr Fabian asingeweza kuiona wala kujua kama wanarekodiwa.Tunaona baada ya matukio yote mawili kumalizika Tamar anainuka na kwenda kuzima kamera.Hii inaonyesha kwamba alitegemea kitendo kile kutokea” akasema Sandra “Nakubaliana na Sandra” akasema Austin “Inaonyesha wazi kabisa kwamba Tamar alitegemea matukio yale kutokea na akatega kamera ili arekodi.Nini hasa lengo lake kurekodi akitendewa vile na Dr Fabian?akauliza Austin “Nahisi Tamar amekuwa na mahusiano na Dr Fabian na inawezekana hii ni tabia ya Dr Fabian na alikuwa akimtendea hivi mara kwa mara ndiyo maana akaamua kumrekodi.Na mimi narejea swali lako kwa nini amrekodi? Gosu Gosu akauliza “Nahisi Tamar alitumiwa na watu ili kurekodi video zile”akasema Agatha “Walimtumia kwa madhumuni yapi? Video hizi zinaonyesha ni za muda mrefu kabla ya Dr Fabian hajawa Rais.Je kama ni watu walimtumia Tamar kurekodi ile video walijua kama Dr Fabiuan atakuwa Rais wa Tanzania? Akauliza Sandra “Tuna mengi bado ya kuyatafutia majawabu” akasema Austin “Jamani nina wazo.Tuna mambo mengi ya kuyatafutia majawabu kama alivyosema Austin lakini mikono yetu imefungwa.Austin unatafutwa na SNSA,Agatha anatafutwa na SNSA mimi pia nitakuwa ninatafutwa kwa vile ni mtu wa mwisho kuwasiliana na Tamar simuni.Kazi yetu itakuwa ngumu sana hivyo nina ushauri” “Go ahead” akasema Austin “Tumetoa jasho jingi kuhakikisha Rais anakuwa salama.Haikuwa kazi nyepesi kuzipata rekodi zile ambazo kama zingetumika zingemuweka pabaya sana Rais wetu,maisha ya watu pia yamepotea katika kuzitafuta zile video lakini Rais hajui kitu kinachoendelea.Kwa kazi hii kubwa tuliyoifanya we need something in return.Tumtake Rais amteue mmoja wetu hapa awe mkuu wa SNSA baada ya Tamar kufariki.Kama tukifanikiwa kumpata mmoja wetu katika nafasi hiyo basi tutaweza kufanikisha mipango yetu iliyobaki.Pale SNSA kuna kila kitu tunachokihitaji ili kutusaidia kufanikisha mipango yetu”akasema Sandra “That’s a good idea.Una akili sana Sandra”akasema Austin “Wazo hili linastahili tuzo” akasema Gosu Gosu na wote wakatoaa kicheko “Ahsante kama nyote mnakubaliana na wazo hili.Nani basi kati yetu ambaye tumpendekeze awe mkuu wa SNSA endapo Rais atakubali? Akauliza Sandra “Austin anafaa sana” akasema Agatha “Mimi hapana.Tayari mimi ni mkuu wa kikosi cha operesheni maalum hivyo nafasi yangu naomba ibaki hivyo hivyo.Kwa nini asiwe Gosu Gosu? “Me ?akauliza Gosu Gosu na kucheka “I’m a killer.Nikipewa nafasi hiyo kila siku watu watakuwa wanakufa” akasema Gosu Gosu na wote wakacheka “Seriously I’m not fit for that position lakini kuna mtu ambaye anaweza akafaa sana katika nafasi hiyo” akasema na kunyamaza “Nani ?akauliza Austin “Ruby” “Ruby? “Ndiyo.Anafaa sana kwa nafasi hii.Tukimuweka pale SNSA nina uhakika kila kitu kitakwenda vizuri” “Whos’s she?akauliza Sandra “Ruby ni mchawi wa kompyuta.Anaijua kompyuta kuliko aliyeigundua.Kwa sasa yuko uingereza anafanya kazi katika mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza GCHQ” “Wow ! huyo anaonekana anaweza kuwa chaguo zuri”akasema Sandra “She’s more than perfect for this position” akasema Gosu Gosu “Wote tunakubaliana kwamba Ruby achukue nafasi hiyo? Akauliza Austin na wote wakakubaliana.Austin akachukua simu yake akaiwasha na kumpigia Dr Fabian “Austin ! Akauliza Dr Fabian kwa sauti iliyojaa wasiwasi “Mheshimiwa Rais ahsante kwa kupokea simu yangu.Nahitaji kuonana nawe” “After what you’ve done do you think I’m going to trust you again?akauliza Dr Fabian kwa ukali “I’ve done nothing bad to you Mr President.Tafadhali naomba uniruhusu nije kuonana nawe.Nina jambo la muhimu sana la kuzungumza nawe” “Austin sina muda wa kuonana nawe! Naku…………” akasema Dr Fabian lakini Austin akamkatisha “Mheshimiwa Rais kabla ya alasiri ya leo nchi itatikiswa kwa rekodi za mazungumzo yako na Rais Patrice Eyenga kuhusiana na mauaji ya Lucy Muganza” akasema Austin “Mazungumzo?! Akauliza DrFabian “Ndiyo utayafahamu hapo baadae mheshimiwa Rais” “Are you trying to threaten me young man?akauliza Dr Fabian “Hapana mheshimiwa Rais sina uwezo huo lakini naomba tusifike huko kwani madhara yake ni makubwa hasa kwa upande wako.Naomba tuonane mheshimiwa Rais tuzungumze”akasema Austin.Dr Fabian akafikiri kidogo kisha akasema “Fine.Saa tano za asubuhi njoo hapa ikulu” akasema Dr Fabian na kukata simu









Austin alifika ikulu lakini Dr Fabian hakuonyesha uchangamfu kama ambavyo huchangamka kila anapokutana na Austin.Sura yake ilija hasira.Baada ya Austin kupokelewa Ikulu waliingia katika chumba cha mazungumzo ya faragha kama wafanyavyo kila Austin afikapo ikulu kwa mazungumzo. “Kabla hujanieleza kile unachotaka kunieleza naomba nikufahamishe kwamba nimepokea taarifa za kifo cha Tamar kwa masikitiko makubwa na nimeapa yeyote Yule aliyehusika katika kifo hicho nitamsaka hadi apatikane awe mzima au amekufa.Hakuna aliyeshiriki atakayebaki salama ! akasema Dr Fabian kwa ukali “Mheshimiwa Rais usitumie nguvu kubwa sana kuongelea suala hilo au kumtafuta muuaji wa Tamar Axon wakati unaye mbele yako” “You?! Akauliza Dr Fabian “Yes me and my friends we killed her” “Jesus Chris ! akasema Dr Fabian “Dr Fabian naomba kwanza unisikilize kile ninachotaka kukwambia halafu mwisho utaamua kama unataka kunikamata na kunifungulia mashtaka au vinginevyo lakini kwanza nisikilize” akasema Austin.Dr Fabian hakujibu chochote aliendelea kumtazama kwa hasira “Mheshimiwa Rais ulitupa kazi mimi na wenzangu ya kumuua Lucy Muganza na tukaitekeleza kazi hiyo vizuri lakini baadae likaibuka tena suala la balozi Benjamin nalo ukatukabidhi sisi tumchunguze kwa bahati mbaya akafariki wakati uchunguzi unaendelea.Mpaka sasa hatujui nani walimuua balozi Benjamin na kwa nini” “Hamjui nani kamuua balozi Benjamin?Mnadhani mimi ni mtoto mdogo ambaye nitashindwa kugundua mchezo mlioufanya?Wewe na wenzako mlimuua balozi Benjamin” akasema Dr Fabian “Kwa nini tumuue mtu ambaye ulitutuma tumchunguze?akauliza Austin na Dr Fabian akawa kimya “Mheshimiwa Rais hatukumuua Benjamin.Kama kuna mtu amekueleza kwamba sisi tulimuua amekudanganya.Sikiliza namna ilivyokuwa.Tuligundua kwamba balozi Benjamin amealikwa katika hafla ya uchangishaji fedha za mabweni ya watoto waishio kwenye mazingira magumu na sisi kwa vile tulikwisha anza kumfuatilia tulikuwepo ukumbini.Benjamin alitoka ukumbini akaenda katika lifti na akiwa ndani ya lifti mwanamke mmoja alimuwekea bahasha katika mfuko wake wa koti na mtu wangu aliyekuwamo ndani ya lifti akimfuatilia Benjamin alikiona kitendo hicho.Tulimuandama Yule mwanamke tumjue ni nani na amempa nini balozi Benjamin kwa siri namna ile.Tulifanikiwa kumpata mwanamke huyo na baada ya kumuhoji akadai yeye ni mfanyakazi wa SNSA.Kazi yake kubwa ni mdukuaji.Alitueleza kwamba kwa muda wa wiki kadhaa amepewa kazi maalum ya kudukua simu yako na kuhifadhi mazungumzo yako yote ya simu,hivyo mheshimiwa Rais fahami kila simu unayopiga au kupigiwa inasikilizwa na SNSA” “Simu yangu unadukuliwa? Dr Fabian akahamaki “Ndiyo mheshimiwa Rais.Simu yako inadukuliwa na SNSA” Dr Fabian akasimama na kushika kiuno. “Mheshimiwa Rais mawasiliano yako yote ya kila siku hurekodiwa na kisha huwekwa katika faili maalum” “SNSA hawawezi kudukua simu ya Rais ! That’s a big lie ! akafoka Dr Fabian “Nisikilize kwanza mheshimiwa Rais” akasema Austin “Mkurugenzi wa SNSA Tamar Axon ndiye aliyetoa maelekezo kwamba simu yako idukuliwe” “Tamar ! akazidi kuhamaki Dr Fabian “Tamar hawezi kabisa kufanya kitu kama hicho ! akasema Dr Fabian “Hiki si kitu cha kubuni mheshimiwa Rais.Ni kweli jambo hilo linafanyika na aliyekuwa akifanya ndiye aliyetueleza kinachoendelea.Katika kukusanya rekodi za mawasiliano yako Agatha aligundua uliwasiliana na Rais Patrice Eyenga wa Congo na mlikuwa mnazungumzia kuhusu mauaji ya Lucy Muganza.Rekodi zako zote ulizozungumza kuhusu mauaji ya Lucy Muganza Agatha alizificha hakumuonyesha Tamar.Agatha alipewa diski mweko na Tamar ampelekee balozi Benjamin na alipokuwa njiani aliichunguza kujua kuna nini ndani akakuta kuna rekodi mbili za mazungumzo yako na Rais Patrice Eyenga kuhusu mauaji ya Lucy Muganza” “Real?!! Akauliza Dr Fabian Austin akatikisa kichwa “Tamar anaweza kweli akanifanyia mambo kama hayo? Dr Fabian akabaki anashangaa “Ni kweli mheshimiwa Rais” akasema Austin “Ni vigumu kuamini” Austin akatoa diski mfukoni akaichomeka katika kompyuta na Rais akaanza kusikiliza rekodi za mazungumzo yake ya simu.Austin akamchezea rekodi mbili akizungumza na Patrice Eyenga. “Mheshimiwa Rais ziko nyingi hizi ni mbili tu nimekuchezea” akasema Austin. “A..A..AAAA…Austin I don’t know what to say ! “Don’t say anything Mr President.Siku ile tulipokwenda nyumbani kwa Tamar kufanya uchunguzi ukatuzuia tulikuwa tunatafuta faili lenye rekodi hizi” “Austin I’m sorry .I didn’t know anything.Kwa nini hukunieleza jambo kubwa kama hili mapema? “Nilitaka kukueleza lakini hukunipa nafasi na badala yake ukatengeneza mtego ili nikamatwe na SNSA” “Austin…”akasema Dr Fabian na kushindwa kuendelea.Alikosa neno la kusema “Mheshimiwa Rais,Jana usiku tumevamia nyumbani kwa Tamar na kufanikiwa kulipata faili lenye rekodi zote tumezifuta na zilizobaki ni hizi hapa” akasema Austin na kumpatia Dr Fabian ile diski mweko.Dr Fabian akashusha pumzi “Thank you Lord” akasema na kuichukua ile diski “Una hakika hakuna sehemu nyingine zilipo rekodi hizi? “Hakuna mheshimiwa Rais.Tulipandikiza kirusi katika mfumo wa kompyuta wa SNSA na kuharibu kila kitu rekodi zilikuwa zimebaki katika kompyuta ya Tamar” “Good job Austin.Ahsanteni sana wewe na wenzako kwa kazi hii kubwa mliyoifanya.Naomba unisamehe sana kwa yale niliyokufanyia” “Mheshimiwa Rais,Tamar alijiua mwenywe kwa kujipiga risasi.Tunaamini alikuwa anashirikiana na balozi Benjamin lakini mpaka sasa hatujui nani waliomuua balozi Benjamin na kwa nini.Japokuwa wote wawili wamefariki dunia lakini hatari bado haijaisha.Kuna mambo tumeyagundua kwanza Tamar alikuwa anapokea fedha kutoka katika akaunti iliyoko Ufarnsa ambayo mmiliki wake amefichwa.Amekuwa akipokea fedha nyingi kupitia akaunti hiyo.Tunatafuta kujua mmilikiwa hiyo akaunti na fedha hizo zote zina malengo gani.Katika akaunti yake tumekuta ana zaidi ya bilioni mbili.Tumegundua pia mawasiliano yake na mtu anaoitwa Dinosaur.Bado hatujafahamu mtu huyu yuko wapi lakini barua pepe tuliyoikuta katika kompyuta ya Tamar inasomeka hivi” akasema Austin na kumuonyesha Rais barua pepe waliyoikuta katika kompyuta ya Tamar.Dr Fabian akazidi kuchanganyikiwa “Ukisoma barua pepe hii utagundua Tamar na huyo Dinosaur wana mipango mikubwa inayokwenda kwa awamu na tayari awamu mbili zimekamilika na sasa wanaingia awamu ya tatu na njiwa anayetaja hapa si njiwa mnyama bali ni mtu anategemewa kuwasili muda wowote.Bado hatumjui ni nani na anakuja kufanya nini” “Dah ! siamini macho yangu.Tamar ?!! akasema Dr Fabian “Nilimuamini sana kumbe ni chui.Umesema anatumiwa fedha kutoka akaunti iliyoko Ufaransa,balozi Benjamin pia anatokea Ufaransa,Lucy na Laurent Muganza makazi yao wote ni Ufaransa,Rais wa umoja wa Ulaya anatokea Ufaransa na hata ukiangalia wale waliotuma jumbe katika kurasa zao zao za twitter Benjamin na Rais Michael wote wanatoka Ufaransa.Leo nimekuwa na malumbano makubwa na Rais wa Ufaransa kuhusu kifo cha Benjamin.Ukiunganisha haya yote unapata picha kwamba mchezo huu tunacheza na Ufaransa.Ukijiuliza kwa nini tucheze na Ufaransa?Jibu ni rahisi jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Baada ya kuingia madarakani Rais Patrice Eyenga amekata mirija yote ya mataifa makubwa kunufaika kwa kuchota rasilimali za Congo hasa madini na sasa wanatafuta namna ya kurudi.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inazidi kuimarisha ukuta wa kuzuia uchotwaji wa rasilimali zake kwa kujiunga na jumuiya ya Afrika mashariki ndiyo maana mataifa haya ambayo yanataka kurejea Congo kwa nguvu wanataka kuanza na kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki halafu waingie Congo.Kama Tamar alikuwa na mahusiano na balozi Benjamin basi ni wazi anashirikiana pia na umoja wa Ulaya na ndiye aliyekuwa akimpatia balozi Benjamin siri za nchi kwani SNSA ina siri nyingi za nchi.Ukifuatilia mtiririko wa mambo ulivyo toka alipouawa Lucy Muganza utaona kabisa kwamba balozi Benjamin na wenzake walihisi serikali ya Tanzania inahusika na mauaji yale hivyo wakawa wanatafuta ushahidi.Ninamshukuru sana huyo ambaye alificha rekodi za mazungumzo yangu na Patrice Eyenga.Alifanya jambo kubwa na la kishujaa” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais hii ni vita na ulipaswa kutuamini vijana wako lakini ulituzuia hatakuendelea na operesheni yetu.Licha ya kutuzuia lakini bado tumeendelea kuweka hatarini maisha yetu na kupambana hadi tukafanikiwa kupata rekodi hizo.You are safe now Mr President” akasema Austin “Austin nimeishiwa maneno ya kusema.Mimi ni rais wako lakini ninajiona mjinga sana kwa mambo niliyoyafanya.Kwa nini nilishindwa kukuamini Austin?Nisamehe sana kijana wangu najua nilichokif……….” “Usijali mheshimiwa Rais” Austin akamkatisha Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kuna jambo la mwisho” “Jambo gani Austin? “Wakati tunapekua kompyuta ya Tamar tumekuta kuna video hizi” akasema Austin na kumchezea Dr Fabian video moja kati ya mbili walizozikuta katika kompyuta ya Tamar. “Stop it ! akafoka Dr Fabian.Alikuwa anahema haraka haraka “Mr President can you say something about this?akauliza Austin Dr Fabian akafikiri kwa muda halafu akasema “Kuna mwingine yeyoye ambaye ameziona video hizi? “Hapana ni sisi pekee” akajibu Austin na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “Kwa miaka saa nimekuwa nikiteseka kwa ajili ya video hizi na nimelipa gharama kubwa sana mpaka sasa.Kuna nyakati nilitamani hata nife niondokane na adha nilizokuwa nazipata kutoka kwa Tamar kwa sababu ya video hizi” akanyamaza na kuchukua kitambaa akafuta jasho usoni akainamisha kichwa akazama mawazoni “Mheshimia Rais naomba unihakikishie je video hizi ni za kweli na zimetengenezwa?akauliza Austin “Video hizo ni za kweli kabisa Austin.Unaowaona ndani ya hiyo video ni mimi na Tamar.Labda nikupe picha tu kwamba mimi na Tamar tulikuwa na mahusiano ya kimapenzi lakini yalikuwa ya siri.Tamar alikuwa ndiye mwanamke niliyepaswa kumuoa lakini sikufanya hivyo kutokana na tabia yake ya kuwa na wanaume wengi nikamuoa Millen.Mimi na Tamar tuna mtoto mmoja wa kiume anaishi na mama yake mdogo nchini Hungary,hivyo Tamar alikuwa sehemu ya maisha yangu.Nilimjengea jumba kubwa Afrika kusini nikampa mahitaji yale yote aliyohitaji lakini bado Tamar hakuacha tabia yake ya kutoka na wanaume wengine japo kila mwisho wa wiki nilikuwa nakwenda Afrika kusini kwa ajili yake.Niliweka watu wa kumfuatilia na wakanitumia picha zake akiwa na wanaume tofauti ndani ya nyumba niliyojenga mimi.Nilikasirishwa na kitendo hicho ndiyo maana nikafanya vile nilivyofanya.Ilikuwa ni hasira tu” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais mimi na wenzangu hatuna haja ya kufahamu chochote wala kuingilia maisha yako binafsi lakini kuna kitu tumekiona katika video hizi.Inaonekana Tamar alitegemea kitendo kile kutokea hivyo akatega kamera mahala ambako usingeweza kuiona na akarekodi matukio yale.Katika video zote mbili baada ya wewe kuondoka Tamar anaonekana akiinuka na kwenda kuzima kamera”akasema Austin “Sijawahi kuona kipande hicho.Mimi alinitumia kipande kidogo na ndicho ambacho amekuwa akikitumia kunitisha kwamba atakiachia hadharani watu wakione.Sikuwa tayari kwa hilo ndiyo maana nilimtimizia kila alichokitaka” akasema Dr Fabian na Austin akamuonyesha mwisho wa video zile Tamar akiinuka na kwenda kuzima kamera. “Shetani mkubwa Yule ! akasema kwa hasira “Mheshimiwa Rais unaweza kukubaliana nasi kwamba Tamar alifanya vile makusudi kabisa kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe?akauliza Austin “Inaweza kuwa kweli kwani toka alipopata video hiyo amekuwa akinipa vitisho vingi na mimi sikutaka kupoteza heshima yangu katika jamii ndiyo maana nikawa tayari kumtimizia kila anachokihitaji” “Uliwahi kumueleza nia yako ya kuwania urais kabla ya tukio hili kutokea?akauliza Austin “Austin tayari umekwisha fahamu siri zangu hivyo siwezi kukificha kitu.Mimi nilianza kuandaliwa kuwa Rais miaka minne kabla ya rais aliyepita kumaliza muda wake.Mipango hii ilipoanza nilimshirikisha pia Tamar.Kujibu swali lako ni kweli alifahamu kama ninaandaliwa kwa nafasi ya urais.Baada ya mimi kuwa Rais ndipo alipoanza vituko vyake kutaka nimtimizie kila anachokihitaji kwa madai ya kuachia video ile endapo nisipomtimizia.Aliyekuwa mkurugenzi wa SNSA alifariki dunia nchini Afrika kusini na Tamar alinitaka nimteue yeye kuwa mkurugenzi wa SNSA.Baada ya kupitia taarifa zake za kielimu na kuona ana vigezo nikamteua kuwa mkurugenzi mkuu wa SNSA” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais napenda kukutoa hofu kwamba sasa uko salama.Kila kitu tunacho mikononi mwetu na hakutakuwa tena na kitisho chochote kwako.Sisi tuko kwa ajili yako.Tutakulinda kama tulivyofanya” “Ahsante sana Austin.Ninajiona mjinga sana kwa mambo niliyotaka kukufanyia kumbe wewe ndiye mkombozi wangu.Tamar ndiye aliyekuwa ananiongoza kutaka nikupoteze na mimi kwa ujinga wangu na kwa kumuogopa nilitekekeleza kila alichonitaka.Usiku ule mlipokwenda nyumbani kwake ni yeye aliyenipigia simu na kunitaka niwatake muondoke haraka sana nyumbani kwake na mimi nikafanya hivyo japo nilijua lazima kuna jambo la muhimu lililowapeleka pale.Ni yeye aliyetengeneza ule mtego ili uende pale Dino’s hotel ukamatwe oh my God ! akasema Dr Fanian na kuinama akisikitika “Mheshimiwa Rais hayo yote yamebaki historia sasa tunakwenda kuufungua ukurasa mpya sisi na wewe” akasema Austin na kumtazama Dr Fabian “Tumefanya kazi kubwa mheshimiwa Rais kuhakikisha unakuwa salama lakini na sisi kuna kitu tunakihitaji” “Sema Austin mnahitaji nini? “Kwa sasa baada ya Tamar ambaye ni mkurugenzi wa SNSA kufariki idara ile haina mkurugenzi.Tunataka umteue mtu kutoka katika watu wangu kuwa mkurugenzi wa SNSA” akasema Austin akimkazia macho Dr Fabia ambaye alivuta pumzi ndefu na ksuema “Are you blackmailing me Austin?! Akauliza Dr Fabian “Hapana mheshimiwa rais.Bado tuna kazi kubwa ya kufanya.Bado hatari haijakwisha.Bado vita inaendelea .Kuna maswali mengi ya kuyatafutia majawabu.Tunahitaji kujua nani waliomuua balozi Benjamin?nani anamtumia fedha Tamar?Dinosar ni nani?Wana mipango gani dhidi ya nchi yetu?Mwisho tunahitaji kujua mtu ambaye anatarajiwa kuingia nchini hivi karibuni kutekeleza awamu ya tatu ya mpango wa Dinosaur na Tamar ni nani?Tutaweza kuyapata majibu hayo kama mmoja wa watu wangu atakuwa mkurugenzi wa SNSA.Idara ile ni nyeti sana na kazi yake ni kubwa kwa nchi inatakiwa iongozwe na mtu muadilifu sana lakini ilikuwa imeshikwa na madalali wa mebapari.Tunataka kuirejesha heshima ya idara hii” akasema Austin “Austin sijui niseme nini kwa hili jambo zito ulilolizungumza.SNSA ni idara nyeti kabisa ya usalama wa nchi lakini niliiweka mikononi mwa makuwadi wa wanyonyaji.Nataka wewe uwe mkuu wa SNSA kama itakupendeza” akasema DrFabian “Mheshimiwa Rais mimi ni kiongozi wa kikosi muhimu kabisa naomba niendelee kubaki hapohapo katika nafasi yangu lakini kuna mtu ninampendekeza kwako anaitwa Ruby Rafael Magalla.Huyu ni mtanzania mwenye uraia wa Uingereza.Kwa sasa anafanya kazi katika mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia Uingereza.Ninamfahamu Ruby nimewahi kufanya naye kazi ni mtu mwenye akili nyingi na ana uwezo mkubwa sana wa kucheza na kompyuta.Nina hakika akiwekwa pale SNSA atakuwa na msaada mkubwa sana” akasema Austin “Austin huna haja ya kunielezea kwa undani kuhusu huyo mtu unayempendekeza.Ninakua mini.Sina shaka na uzalendo wako hata kidogo ninaamini mtu huyo uliyempendekeza anafaa kabisa.Mimi sina shida yoyote ya kumteua kuwa mkurugenzi wa SNSA.Swali ni je yeye mwenyewe yuko tayari? Akauliza Dr Fabian “Ruby anaipenda sana Tanzania na si mara moja amekuwa akija Tanzania kushiriki katika misheni mbali mbali toka wakati wa Rais aliyepita” “Real? “Ndiyo mheshimiwa Rais” “Basi vizuri.Nipe mawasiliano yake nitazungumza naye mimi mwenyewe na kumuomba aje Tanzania.Nitamshawishi kwa kila namna hadi akubali” akasema Dr Fabian “Nakushukuru sana mheshimiwa Rais” “Kama kuna kitu kingine chochote nieleze tafadhali” “Hakuna mheshimiwa rais kilichonileta hapa kwako ni hayo niliyokueleza” “Austin najua nimekukosea wewe na wenzako.Najua haitakuwa rahisi kuniamini tena lakini naomba tusameheane kwa yale yaliyotokea na tufungue ukurasa mpya.Tuna vita kubwa inatukabili mbele yetu nahitaji watu kama ninyi wazalendo wa kweli kwa nchoi yenu ambao mko tayari hata kuyatoa maisha yenu kwa ajili ya Tanzania.” “Sisi hatuna tatizo lolote nawe mheshimiwa Rais kikubwa tunachokitaka toka kwako tuamini” “Siwezi kurudia tena makosa niliyoyafanya Austin.Lakini nakuomba hizo rekodi na hizo video ziharibuni kabisa” “Usihofu kuhusu hilo mheshimiwa Rais.Zote zitaharibiwa na hakutakuwa na kitisho kingine chochote dhidi yako” akasema Austin na kuzifuta rekodi zile na video mbele ya Rais Austin na Dr Fabian walimaliza mazungumzo yao na kuagana Austin akaondoka RAMALLAH – PALESTINA Mathew Mulumbi alifumbua macho baada ya kusikia sauti za watu wakikimbia karibu na dirisha la chumba alimolala.Alitoka kitandani akajinyoosha halafu akaenda kufunua pazia akachungulia nje.Mara mlago wake ukagongwa akavaa shati na kwenda kuufungua akakutana na Ammar “Abu Al zalawi” akasema Ammar “Ammar” “Unaendeleaje Abu? “Ninaendelea vizuri sana Ammar” “Nafurahi kusikia hivyo.Abu naomba nikutoe hofu kwa lile tukio la jana halitajirudia tena.Wewe ni mtu wetu wa muhimu sana hivyo unastahili heshima kubwa.Naomba utambue kwamba mimi kama kiongozi wa kikundi hiki ninakuamini asilimia mia moja hivyo usiwe na hofu yoyote” akasema Ammar “Ahsante sana Ammar kwa kuniamini” akasema Mathew “Abu nimekuja kukuaga ninatoka kidogo kuna sehemu ninakwenda kuangalia kazi za zinavyokwenda,wewe utaendelea kupumzika hapa ukihudumiwa.Unatakiwa upone kabisa mjeraha yako yote na utakapokuwa umepona kabisa tutaanza kazi” akasema Ammar “Ahsante sana Ammar.Ninahudumiwa vizuri sana hapa.Ninajihisi nyumbani” akasema Mathew na Ammar akatabasamu “Abu sikufanya makosa kuamua kuungana nawe.Ninapata picha ya kundi letu kuwa kubwa na hatari baada ya kujiunga kwetu” akasema Ammar “Usijali Ammar tutafanya mambo mengi sana pamoja.Tuzidi kuomba uzima” akasema Mathew. “Majeraha yako yanaendeleaje?akaliza Ammar.Mathew akavua shati na Ammar akamtazama akasikitika “Watu wale ni wanyama sana.Atakuja Nawal kukuganga,ana taaluma ya uuguzi na amekuwa akisaidia sana watu wangu kila pale wanapopatwa na majeraha” akasema Ammar na kuondoka Kupitia dirishani Mathew aliweza kuona msafara wa magari ukiondoka akarejea kitandani kukaa. “Natakiwa kuwajulisha Mossad kwamba tayari nimekwisha jiunga na kikundi cha Ammar brigades lakini sijui namna ya kuwasiliana nao” akawaza Mathew na picha ya Peniela mke wake ikamjia kichwani “Peniela na wanangu ndio wanaonipa nguvu ya kuendelea kuvumilia mateso hata pale ninapokuwa nimekata tamaa kabisa.Nitahakikisha ninajitahidi kutoka salama mahala hapa ili nikaungane nao tena” akawaza Mathew na kumkumbuka Ruby “Sipati picha Ruby atakuwa alilia machozi kiasi gani alipopata taarifa kwamba nimefariki dunia.Yule mrembo ananipenda kupindukia na alikuwa tayari kuacha kila kitu kwa ajili yangu.Alikuwa tayari hata kuhama London na kuishi Tanzania kwa ajili yangu.Sikuwahi kumpa jibu kama nimekubali ombi lake la mimi na yeye kuwa wapenzi nilitaka kumpa jibu baada ya kurejea kutoka kuwakomboa Olivia na Coletha lakini kwa bahati mbaya sikurejea.Hii itakuwa ilimuumiza mno.Je tayari amekwisha pata mwanaume mwingine kama Peniela?Ni miaka mitatu tu lakini tayari Peniela amekwisha pata mwanaume.Je alikubaliana na taarifa kwamba nimefariki dunia?Alikubali vipi nimekufa bila kuiona maiti yangu? Alijaribu hata kidogo kuutafuta ukweli na kujiridhisha kweli nimekufa? Akajiuliza Mathew “Anyway nisimlamu sana haya yote yaliyotokea ni kwa sababu yangu.Kama ningejiweka mbali na hizi kazi hivi sasa ningekuwa nafurahi na familia yangu.Vipi kuhusu wenzangu akina Gosu Gosu?Nao pia wamekubali kweli nimefariki? Gosu Gosu sikuwa naye usiku ule hiv……” Mathew akatolewa mawazoni baada ya mlango kugongwa.Akaenda kuufungua akakutana na Nawal “Habari za asubuhi Abu Al zalawi” akasema Nawal “Habari nzuri Nawal,karibu” akasema Mathew na kumkaribisha Amar ndani.Alikuwa amebeba sinia lililokuwa na kifungua kinywa vile vile alikuwa ni kikapu ambacho kilikuwa na dawa “Abu nimeelekezwa nije kukuganga majeraha yako” akasema Nawal.Mathew akavua shati na Nawal akastuka baada ya kuyaona majeraha makubwa mgongoni mwa Mathew “Pole sana Abu.Wamekuumiza sana” akasema Nawal akaanza kuyasafisha majeraha yale “Abu kwa nini uko hapa?akauliza Nawal wakati akiendelea kumganga Mathew “Kwa nini unauliza hivyo Nawal? “Hauonekani kama ni gaidi.Sura na tabia za magaidi ninazifahamu lakini wewe si mmoja wao.Unatafuta nini hapa?akauliza Nawal “Nilimuua mkuu wa Mossad afrika Mashariki na majasusi wengine wawili.Niko hapa kupambana na Israel” akasema Mathew “Jina lako halisi ni nani?akauliza Nawal “Naitwa Abu Al zalawi” akasema Mathew “Jina lako si Abu Al Zalawi,wala wewe si gaidi” akasema Nawal “Amini utakavyo Nawal lakini mimi jina langu ni hilo” akasema Mathew Nawal akaacha kazi aliyokuwa anaifanya akaenda kukaa mbele ya Mathew.Muda wote walikuwa wakizungumza kiarabu lakini mara Nawal akabadili lugha wakaanza kuzungumza kiingereza “Your real name is Mathew Mulumbi and not Abu Zalawi.You are from Tanzania and not from Kenya.You are an agent and not a terrorist(jina lako ni Mathew Mulumbi na si Abu Zalawi.Unatokea Tanzania na si Kenya.Wewe ni jasusi na si gaidi)” akasema Nawal.Mathew alihisi tumbo linaanza kuunguruma kwa mstuko alioupata.Akahisi kijacho kumtoka GCHQ LONDON – UINGEREZA Ruby akiwa katika ofisi yake akiendelea na majukumu simu yake ikaita.Zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake na simu ile ilitokea Tanzania “Ni nani huyu?akajiuliza Ruby akiwa ameishikilia ile simu akizitazama zile namba “Anayefahamu namba hii kutoka Tanzania ni Gosu Gosu pekee.Kama ni yeye kwa nini ananipigia muda huu wakati nilikwishamuonya asinipigie wakati niko kazini?akajiuliza Ruby akionekana kukasirika.Simu ilikatika ikaanza kuita tena akaipokea “Hallow” akasema “Hallow” ikasema sauti ambayo Ruby hakuwa akiifahamu haikuwa sauti ya Gosu Gosu aliyokuwa ameitegemea “Nazungumza na nani? Akauliza “Naongea na Ruby Rafael Magalla? Ruby akastuka jina lake lilipotajwa “Ndiyo unazungumza na Ruby.Wewe ni nani?Umepata wapi namba zangu?akauliza Ruby kwa sauti ya ukali kidogo “Naitwa Dr Fabian Kelelo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania” akasema Dr Fabian na Ruby akabaki anashangaa.Alistuka sana “Hallow Ruby” “Nimestuka kidogo mheshimiwa Rais” “Ruby samahani kwa kukupigia simu hii bila taarifa lakini nimelazimika kukupigia kwa ajili ya jambo moja la muhimu sana” “Nakusikiliza mheshimiwa Rais” akasema Ruby “Ruby nimeamua kukupigia simu mimi mwenyewe kukujulisha kwamba nimekuteua uwe mkuu wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi SNSA” “What? Ruby akashangaa “Ni kweli Ruby nimekuchagua kuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi” Ruby akacheka kidogo na kusema “Mheshimiwa Rais sijui niseme nini lakini nimestuka sana.Kwanza sifahamu umenifahamuje hadi ukaniona ninafaa?Pili mimi si raia wa Tanzania japo wazazi wangu ni watanzania ambao baadae walichukua uraia wa Uingereza” “Ruby tafadhali usiseme hapana.Nimekuteua kwa kuwa ninaamini unaweza ukaiongoza idara hii kwa ufanisi mkubwa.Sikuwa ninakufahamu lakini wenzako akina Austin wamekupendekeza kwangu kwamba unafaa kwa nafasi hii” “Umesema Austin?! Ruby akashangaa “Ndiyo.Ninamuamini sana Austin.Aliponieleza kuwa unafaa kuongoza idara hii sikuwa na shaka nawe hata kidogo.Ruby nchi yetu kwa sasa iko katika vita kubwa ya kiuchumi na tunaitegemea sana idara hii ambayo nataka uiongoze.Ruby nafahamu nimekustukiza jambo kama hili ila naomba utafakari na unipe majibu kama utakuwa tayari” “Mheshimiwa Rais nashukuru.Naomba nipe muda nitafakari halafu nitakujibu” akasema Ruby na kuagana na Rais “Mstuko kama huu nilioupata leo niliupata siku ile nilipoambiwa kwamba Mathew amefariki dunia.Japo mstuko huu hawezi kulingana na ule wa taarifa ya kifo cha Mathew lakini nimestuka sana.Rais anataka niwe mkurugenzi wa SNSA ! Dah hiki si kitu kidogo.Idara ile ni kubwa sana na inahitaji mtu makini.Ni idara ambayo aliiongoza Devotha ambaye alitaka kuniua kwa risasi.Siwezi kusahau kitendo kile” akawaza Ruby.Kazi zake zote zilisimama alishindwa kuendelea na kazi “Lazima iko sababu kubwa hadi Austin anipendekeze kwa Rais niwe mkurugenzi wa SNSA.Huu ni mtihani mkubwa kwangu kwani hata hapa wananitegemea sana lakini asili yangu ni Tanzania.Toka ndani ya moyo wangu ninaipenda Tanzania kwani ndiko atokako Mathew Mulumbi mwanaume nimpendaye kuliko wote ambaye mpaka leo hii bado siamini kama kweli amefariki dunia.Nadhani nafasi hii imekuja kwa kusudi maalum kwani nikiwa mkurugenzi wa idara ile nitafahamu mambo mengi ya nchi,siri nyingi za nchi nitazijua na nitapata nafasi nzuri ya kuupata ukweli kuhusu Mathew Mulumbi.Sina haja ya kukataa nafasi kama hii wala kujiuliza mara mbili kama nikubali au nikatae” akawaza Ruby na kuchukua simu akapiga namba zile za Rais “Ruby” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais sina sababu ya kutafakari jambo kama hili wakati nchi inanihitaji.Japo kwa sasa ni raia wa nchi nyingine lakini Tanzania ni nyumbani na nina mapenzi makubwa na nchi yangu hivyo nimekubali uteuzi” “Ahsante sana Ruby.Ahsante sana.Nimefurahi mno.Nchi inahitaji vijana kama wewe.Lini utakuja Tanzania? “Kwanza itanilazimu kuanza mchakato wa kuacha kazi hapa ninapofanya kazi” akasema Ruby na kunyamaza kidogo “Mheshimiwa rais halitakuwa jambo jepesi na la haraka kuacha kazi hapa kwani kazi ninayoifanya ni nyeti sana lakini kwa namna yoyote ile lazima nihakikishe nimefanikiwa kuacha kazi hapa.Ninachokuomba jambo hili la uteuzi wangu liwe siri lisitangazwe” akasema Ruby “jambo hili ni la siri kubwa na anayefahamu ni Austin na wenzake na siwezi kumweleza mtu yeyote.Ruby nafasi hii hatapewa mtu mwingine zaidi yako hivyo basi kamilisha taratibu zako uje nyumbani tunakusubiri” akasema Dr Fabian na kuagana na Ruby USIKOSE SEHEMU IJAYO……………..





RAMALLAH – PALESTINA Mathew aliendelea kumtazama Nawal kwa mshangao alishindwa amwambie kitu gani.Maneno aliyoambiwa yalimstua sana.Kwa ndani alihisi kutetema.Nawal alilitambua hilo “Usihofu Abu Zalawi,hakuna anayelifahamu hilo zaidi yangu” akasema Nawal huku akitabasamu “Kwa nini uko hapa?akauliza Nawal “Huyu mwanamke amenifahamuje.Tayari kila kitu kimeharibika. ? Sikutegemea kufahamika mapema namna hii” akawaza Mathew “Mathew nakuuliza kwa nini uko hapa?Unatafuta nini?akauliza Nawal “Nawal naomba iwe mwanzo na mwisho kuniita kwa jina hilo mimi si Mathew Mulumbi bali ni Abu Al Zalawi” akasema Mathew kwa sauti ndogo lakini ya ukali “Abu usihofu sintakuita kwa jina hilo lakini ninafahamu hilo si jina lako na wewe ni Mathew Mulumbi jasusi kutoka Tanzania.Ninataka kukusaidia hivyo ninataka kujua nini kimekuleta hapa?akauliza Nawal Mathew akawa kimya “Abu ninakuuliza hivyo kwa sababu yawezekana umekuja mahala ambako si sahihi na unaweza ukapoteza hata maisha yako.Hii ni sehemu hatari sana na hawa jamaa wakigundua kwamba wewe si mwenzao bali uko hapa kwa misheni maalum watakuua.Nataka nikusaidie ili uweze kufanikisha misheni yako lakini nitakusaidia endapo utanieleza ukweli” akasema Nawal na kuzidi kumchanganya Mathew “Nahisi hawa jamaa tayari wamekwisha nifahamu na wanamtumia Nawal ili kujiridhisha kwamba kweli mimi ni jasusi kutoka Tanzania na si gaidi mwenzao kama nilivyojitambulisha kwao.Napaswa kuwa makini sana na mtego huu vinginevyo nitaangamia kabla ya kukamilisha misheni yangu” akawaza Mathew “Mathew mbona hunijibu?akauliza Nawal “Nawal najua wamekutuma uje kunichunguza kama kweli mimi ni jasusi lakini wamekosea sana.Mimi si huyo mtu unayemtaja Mathew Mulumbi.Mimi ni Abu Al Zalawi.Tafuta taarifa zangu katika mtandao wa Mossad utazipata” akasema Mathew “Mathew oh samahani Abu” akasema Nawal na Mathew akakasirika akamkaba shingo “Nitakuua Nawal kama ukiendelea kuniita kwa jina hilo ! akasema Mathew akiwa amekasirika Nawal akaogopa “Nani amekutuma uje unichunguze?akauliza Mathew na kumuachia Nawal ambaye alianza kukohoa “Ammar amekutuma uje unipeleleze? Akauliza tena “Hakuna aliyenituma kwako.Sikiliza nikueleze ukweli” akasema Nawal na kukohoa kidogo halafu akafungua mlango akachungulia kama kuna mtu karibu akaenda kuangalia pia dirishani halafu akasema “Mimi ninafanya kazi na shirika la ujasusi la Marekani CIA” “CIA ? Mathew akashangaa “Ndiyo.Niko katika kitengo cha D.U.A” “D.U.A ni nini”akauliza Mathew “Deep undercover agent” “Oh my God !! akasema Mathew “Niko hapa kwa misheni maalum ya kumtafuta mtu mmoja anaitwa Abdul Yasin Al Nasser.Huyu ni gaidi ambaye anahusika katika mashambulio manne makubwa ya kigaidi yaliyotokea katika miji miwili nchini Marekani na kuua watu zaidi ya mia moja na hamsini.Abdul Yasin ni ndugu na Ammar ndiyo maana niko hapa”akasema Nawal na kumuacha Mathew katika mshangao .Baada ya dakika moja akaendelea “Mimi ndiye niliyewasaidia Mossad wakaweza kumpata Ammar kupitia kwa CIA.Nilipoelezwa kwamba wewe ndiye uliyemsaidia Ammar akaweza kutoka gerezani sikuamini taarifa hizo kwani gereza alilokuwa amefungwa Ammar lina ulinzi mkali mno na hajawahi kutoroka mfungwa yeyote na ndipo nilipoanza kukuchunguza nikagundua kwamba wewe si gaidi kama inavyotajwa bali ni jasusi na nikajua kwamba kutoroka gerezani ulikuwa ni mpango maalum” akasema Nawal.Akatoka na kwenda kufungua mlango akachungulia nje kama kuna mtu pale karibu “Lazima nichukue tahadhari kwani hakuna anayeifahamu siri hii hadi sasa.Nimekwambia wewe kwa sababu ninataka kukusaidia” akasema Nawal na kumtazama Mathew “Baada ya kukueleza siri yangu kubwa sasa ni zamu yako.Nataka unieleze kwa nini uko hapa? Akauliza Nawal Mathew akatafakari kidogo halafu akasema “Mimi niko hapa kwa ajili ya kushirikiana na Ammar kupambana na Israel” “Abu unaniudhi sana unapoukwepa ukweli.Nimekueleza siri yangu kubwa kwa nini hutaki kuniamini?Usihofu tafadhali hakuna atakayefahamu siri hii”akasema Nawal “Kwa nini unataka kufahamu kilichonileta hapa?akauliza Mathew “Kwa sababu nataka nikusaidie uweze kumaliza misheni yako uondoke .Uwepo wako hapa unaweza ukasababisha misheni yangu kuharibika kwani hawa jamaa wanaweza wakakugundua kabla hujatekeleza misheni yako hivyo lengo langu ni kukupa msaada “ akasema Nawal “Huu ni mtihani mgumu sana.Nashindwa kufanya maamuzi je huyu mwanamke anachokiongea ni kitu cha kweli au ni mtego?Ni vipi kama nikikubali mimi ni Mathew Mulumbi halafu kumbe ametumwa aje anichunguze?Nitakuwa nimeharibu kila kitu na sintatoka hapa salama.Lakini ni vipi kama ni kweli haya anayoniambia halafu nikakataa kushirikiana naye?Kama ni kweli huyu mwanamke ni CIA anaweza akawa na msaada mkubwa sana kwangu” akawaza Mathew na kumtazama Nawal kwa makini “Ngoja nicheze kamari nijaribu kumuamini na kama kutatokea tatizo lolote nitakabiliana nalo” akawaza na kukohoa kidogo akasema “Ni kweli.Mimi ni Mathew Mulumbi jasusi kutoka Tanzania na niko hapa kwa ajili ya misheni maalum.Ninamtafuta Habiba Jawad” “Habiba Jawad?Nawal akashangaa “Ndiyo ninamtafuta Habiba Jawad na ndiyo maana niko hapa.Unamfahamu? “Kwa nini unamtafuta.Kwa nini umetumia njia ya hatari namna hii hadi ukafika hapa?akauliza Nawal “Miaka mitatu iliyopita kulifanyika shambulio la kigaidi nchini Tanzania lililofanywa na kundi la kigaidi la IS.Wakati wa kulichunguza suala hilo tukagundua kwamba kundi hilo la IS linafadhiliwa na Habiba Jawad na kwa sasa kundi hilo limejielekeza katika kujitanua barani Afrika.Habiba Jawad kutokana na utajiri wake amekuwa ndiye uti wa mgongo wa makundi mengi ya kigaidi na hata kundi hili la Ammar brigades nalo limo katika orodha ya makundi ya kigaidi yanayofadhiliwa naye.Ni hadithi ndefu hadi nimefika hapa lakini naomba nikueleze kwa kifupi tu.Mossad walingia nchini Tanzania na kumteka mtu mmoja anaitwa Edger Kaka aliyekuwa mbunge katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye alikuwa na mahusiano ya karibu na Habiba Jawad na kutengeneza ajali ambayo ilituaminisha wote kwamba Edger amekufa lakini baadae kikundi cha IS wakagundua kwamba Edger hajafariki na wakadhani serikali ya Tanzania ndiyo iliyotengeneza uongo ule kwamba Edger amefariki dunia hivyo wakaandaa mpango wa kumshinikiza Rais wa Tanzania kumuachia huru Edger ambaye waliamini anashikiliwa na serikali ya Tanzania.Mpango yhuo wa kumshinikiza Rais wa Tanzania amuachie Edger Kaka uliambatana na mambo mengi ikiwemo mauaji na utekaji wa watu.Katika kulichunguza tukio moja la utekaji nilibain kwamba Edger Kaka ambaye IS walikuwa wanamtafuta alikuwa ametekwa na Mossad na alifichwa katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi.Niliongoza timu kwenda Nairobi kumuokoa.Hapo ndipo ugomvi na Israel ulipoanza kwani ilinilazimu kuua mkuu wa Mossad Afrika Mashariki na majasusi wengine wawili ili kumpata Edger ili kumkabidhi kwa IS abao walikuwa wamemteka mtoto wa Rais na ili kuwaachia huru walimuhitaji Edger kaka.Wakati tukifanya mabadilishano ya mateka likatokea shambulio la kustukiza” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Mlishambuliwa na nani? Nawal akauliza “Vikosi vya Israel.Sifahamu walipataje taarifa za mabadilishano yale lakini ndio waliotuvamia wakaniteka mimi na Edger Kaka.Nilipelekwa Israel ambako kwa miaka mitatu nimekuwa nikiteswa wakinitaka nikiri na niwataje wenzangu niliokuwa nao wakati ninavamia ubalozi wa Israel jijini Nairobi na aliyenituma kufanya hivyo.Kwa miaka mitatu ya mateso makali sikuwahi kufumbua mdomo wangu kuzungumza chochote na ndipo walipoamua kumtuma mmoja wa watu wao kwenda kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mke wangu na wakanionyesha picha za wawili hao wakiwa katika mapenzi mazito.Niliumia sana na ndipo nlipokubali kuzungumza nikakubaliana nao kwamba nitawasaidia kumpata Habiba Jawad ili niweze kuwa huru.Ninataka kumpata Habiba Jawad ili kulifanya kundi la IS na mengine ya kigaidi yanayofadhiliwa naye yakose nguvu ya kiuchumi na kutoweka taratibu kutokana na kushindwa kujiendesha.Ili kupata sehemu ya kuanzia ilinilazimu kujenga mahusiano na mmoja wa watu ambao Israel walikuwa wanawashikilia kwa ugaidi na wakanikutanisha na Ammar nikajenga mahusiano naye na kupanga mpango wa kutoroka.Lengo la kumtorosha Ammar ni ili niweze kuingia katika mtandao wa kigaidi na hatimaye niweze kumfikia Habiba Jawad.Nadhani nimejibu maswali yako uliyoniuliza kwamba kwa nini nilimtorosha Ammar gerezani na kwa nini niko hapa” akasema Mathew “Pole sana Abu lakini njia uliyoipita ni ndefu na ya hatari kubwa” akasema Nawal “Hakukuwa na namna nyingine ya kuweza kuingia katika mtandao wa kigaidi kama nisingetumia njia hii” “Nalifahamu hilo lakini hofu yangu hawa jamaa wakigundua kwamba wewe ni jasusi na una misheni yako ya siri watakuua kabla hujakamilisha misheni yako.Hapa ni sehemu hatari sana” akasema Nawal “Hatari niliyonayo mimi na wewe unayo vile vile kwani hawa jamaa wakikugundua kwamba wewe unafanya kazi na CIA watakuua.Hivyo basi tunatakiwa tusaidiane ili tukamilishe malengo yetu.Huyo gaidi unayemtafuta umekwisha fanikiwa kujua mahala alipo?akauliza Mathew “Hapana bado sijafanikiwa kujua mahala alipo. Hawa jamaa wanajitahidi sana kuficha mambo yao ndiyo maana mpaka sasa bado sijafanikiwa kumpata Yasin Al Nasser lakini hatua niliyopiga ni kubwa hadi sasa.Nimepata mambo mengi yanayohusiana na mitandao ya kigaidi.” akasema Nawal “Katika muda uliokaa hapa umewahi kumuona au kumsikia Habiba Jawad? “Habiba jawad sijawahi kuonana naye ana kwa ana lakini nimemsikia akitajwa sana na Ammar.Kama ulivyosema ni mfadhili mkubwa wa makundi haya ya wanamgambo na magaidi na kama ukiendelea kuwa na ukaribu na Ammar unaweza ukafahamu mahala alipo lakini naomba uwe makini sana kwani hawa jamaa hawapaswi kukutilia shaka hata kidogo vinginevyo watakuua.Kwa sasa endelea kuwa karibu na Ammar kwani ametokea kukuamini sana.Usimuulize maswalimengi kuhusu kikundi chake nenda naye taratibu.Watakushirikisha katika mipango yao mbalimbali ya kigaidi wakiamini wewe ni mwenzao na chochote watakachokutaka ufanye usionyeshe wasiwasi wala kuuliza maswali kwani wanakutambua kama gaidi hivyo mipango mingi watakushirikisha.Hata wakikutuma uniue mimi usisite fanya hivyo” akasema Nawal “Nitajitahidi kufanya kila niwezalo kumfanya Ammar aendelee kuniamini lakini nina ombi moja kwako.Nahitaji kuwasiliana na Mossad kuwajulisha kwamba tayari niko katika kundi hili la Ammar brigades”akasema Mathew “Siwezi kukusaidia kwa hilo Abu kwa sababu inaweza ikaniharibia hata mimi.Niko hapa kwa siri kubwa hivyo sitaki Mossad wajue kama kuna mtu wa CIA ndani ya kundi hili.Hata hivyo nitaangalia namna ya kukusaidia” akasema Nawal “Sawa nimekuelewa lakini naomba unisaidie kufanya uchunguzi kuhusu mahala alipo Habiba Jawad ” akasema Mathew “Si jambo jepesi kama unavyodhani kwani hawa jamaa wanamlinda sana kwa kuwa wanajua anatafutwa nay eye ndiye muwezeshaji wao.Hawa jamaa wanajua sana namna ya kujificha kwa mfano kwa miaka zaidi ya mitatu sasa nimekuwa nikimtafuta Yasin Al Nasser bila mafanikio ila naamini niko karibu sana kujua mahala alipo” akasema Nawal “Nawal wewe uko karibu sana na Ammar hivyo utakapoona kuna hatari yoyote inanikabili nijulishe mara moja” akasema Mathew “Nitajitahidi kwa kila namna usiingie katika hatari na kama nitagundua hatari yoyote nitakujulisha haraka sana” “Hata hivyo ilikuaje hadi ukafika mahala hapa na kuolewa na Ammar?akauliza Mathew “Ni hadithji ndefu nitakusimulia siku nyingine .Sitaki kutumia muda mwingi humu ndani ili watu wasianze kuwa na wasiwasi kuhusu mimi na wewe.Nikipata nafasi nitamuomba Ammar unisindikize kwenda mjini siku moja na nitakueleza mengi huko” akasema Nawal akamalizia kumganga Mathew majeraha halafu akaondoka. “Daah ! dunia hii imejaa siri nyingi.Kumbe Nawal ni CIA !” akawaza Mathew “Hata hivyo mwanamke huyu ni jasiri anastahili sifa kubwa.Kitendo cha kuja kujipachika kwa watu hatari kama hawa ni kitendo cha kishujaa mno.Ameweka rehani maisha yake kwa ajili ya nchi yake.Wamarekani wako salama lakini yawezekana hawajui kama kuna watu kama hawa ambao wameyaweka rehani maisha yao ili wao wawe salama.Wakati mwingine yawezekana hata nchi yako unayoipigania isikuthamini kama ilivyonitokea mimi.Baada ya kutekwa na Mossad sina hakika kama kuna juhudi zozote zilifanyika kunitafuta na kujua mahala nilipo” akawaza Mathew na kuanza kukumbuka usiku ule waliposhambuliwa na watu wasiowafahamu na yeye akajikuta katika mikono ya Mossad. “Lilikuwa ni shambulio la ghafla sana ambalo hakuna aliyekuwa amelitegemea.Nakumbuka tulishambuliwa kutoka kila upande.Nilipigwa risasi mbili.Sina hakika kama Olivia na Coletha walifanikiwa kuokolewa.Huwa sipendi sana kukumbuka kuhusu usiku ule kwani ni tukio baya mno katika maisha yangu.Ni siku ambayo ilibadili kabisa maisha yangu.Huwa najiuliza kuhusu Rais Dr Evans, nilipambana kumuokoa mwanae lakini yeye amefanya juhudi gani za kunitafuta? Sitaki kuwaza zaidi jambo hili linaumiza sana.Yaliyopita yamekwisha pita na kwa sasa niko hapa peke yangu sina msaada wowote nchi yangu wanaamini nimekwisha fariki hivyo basi ni juhudi zangu binafsi ndizo zitakazoniokoa.Nimeamua kuja sehemu hatari kama hii ambako dakika yoyote mtu unaweza ukjapoteza maisha lakini sikuwa na namna nyingine ya kujiokoa zaidi ya kuamua kuja hapa na lengo ni kuendelea kupambana kuhakikisha watu wanakuwa salama.Mtandao wa IS umeotesha mizizi pia hata nyumbani Tanzania hivyo nikifanikiwa kumuondoa Habiba nitakuwa nimelea pia usalama nchini kwangu hivyo kwa namna yoyote ile lazima mfadhili huyu wa ugaidi apatikane” akawaza Mathew na kwenda kuchungulia nje kulikuwa kimya na walinzi wachache akarudi kitandani kujipumzisha PARIS – UFARANSA Rais Michael Weren wa Ufaransa alipomaliza kikao na baadhi ya watendaji wake akajulishwa kuhusu kuwasili kwa mgeni muhimu aliyekuwa na miadi ya kuonana naye siku hiyo.Michael akaelekeza mgeni wake apelekwe katika chumba maalum cha mazungumzo ya faragha yeye akaenda ofisini kwake akakutana na mshauri wake mmoja wakajadiliana kuhusu suala Fulani halafu akatoka kwenda kuonana na mgeni wake “Devotha Adolph.Karibu sana” akasema Michael “Nashukuru sana mheshimiwa Rais.Kuna taarifa gani umeniletea?akauliza Michael “Mheshimiwa Rais taarifa niliyokuja nayo si taarifa nzuri” akasema Devotha na Rais Michael akastuka kidogo “Kuna taarifa gani mbaya?akauliza “Tamar Axon amefariki dunia usiku wa kuamkia leo? “Nini?! Tamar amefariki?akauliza Michael kwa mshangao “Samahani mheshimiwa Rais kwa kukustua lakini ni kweli Tamar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo”akasema Devotha na Rais Michael akasimama “Devotha tafadhali niambie kama jambo hili si la kweli” “Ni kweli mheshimiwa Rais.Tamar amefariki dunia” akasema Devotha na Michael akasimama akaenda katika kabati lake la vitabu akaegemea na kuinamisha kichwa halafu akarejea tena katika kiti alichokuwa amekaa “Amepata ajali?akauliza “Hapana.Ameuawa” “Ameuawa? “Ndiyo mheshimiwa Rais.Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba kuna watu walimvamia nyumbani kwake wakamuua kisha wakaichoma nyumba yake” akasema Devotha na kimya kikatawala ndani ya kile chumba.Rais Michael alichanganyikiwa “Kweli hii ni taarifa mbaya sana umeniletea.Tamar ni mtu ambaye tulikuwa tunategemea mno katika mipango yetu.Nani waliomuua?Kuna yeyote ambaye amekamatwa mpaka sasa kuhusiana na mauaji hayo? akauliza “Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo” akasema Devotha Ulipita ukimya wa dakika mbili halafu Rais Michael akauliza “Devotha hili jambo limetokeaje? “Kwa mujibu wa taarifa nilizozipata ni kwamba Tamar alivamiwa na watu wasiofahamika wakamuua wakamtoa ndani wakamuweka katika gari lake halafu wakaichoma nyumba yake na kuharibu kila kitu.Wauaji walijua kuna kamera za ulinzi za siri nyumbani kwa Tamar hivyo ili kuzuia wasijulikane wakaichoma nyumba na kuharibu kila kitu hivyo hakuna kumbu kumbu yoyote iliyopatikana” akasema Devotha “Devotha nimechanganyikiwa.Sikutege mea kabisa jambo kama hili kutokea hasa kwa wakati kama huu ambao tulimuhitaji mno Tamar.Unadhani waliomuua Tamar kuna kitu walikigundua kuhusu kushirikiana na balozi Benjamin? “Kuna kila dalili kwamba wauaji hao kuna kitu walikifuata kwa Tamar na yawezekana baada ya kupata walichokifuata wakamuua.Waliomuua si majambazi bali ni watu wenye ujuzi mkubwa sana kwani nyumba ya Tamar ina mfumo mkubwa wa ulinzi na majambazi hawawezi kuingia lazima watakuwa ni watu hatari sana” “Unahisi serikali inaweza kuwa na mkono wake katika kifo hiki cha Tamar?akauliza Michael “Sina uhakika sana wa hilo lakini inawezekana pia.Kitu muhimu ni kufanya uchunguzi na kujihadhari”akasema Devotha na ukimya ukapita kisha Rais Michael akauliza “Tamar alifahamu nani waliomuua balozi Benjamin? “Hapana hafahamu chochote.Naye kama walivyo watu wengine anaamini serikali ya Tanzania inahusika katika mauaji yale ya balozi Benjamin. Niliwatumia vijana wengine kabisa kama tulivyokuwa tumekubaliana” akasema Devotha na ukimya ukapita halafu Rais Michael akasema “Devotha sikufichi nimestushwa mno na taarifa hii ya kifo cha Tamar.Mipango yetu yote kwa kiasi kikubwa ilimtegemea sana yeye.Kila kitu kilikuwa kinakwenda vizuri sana hadi baada ya kuzipokea taarifa hizi mbaya.Hivi sasa tulikuwa tunajiandaa kuingia katika awamu ya tatu ambapo Theresia Muganza anaandaliwa kwa ajili ya kwenda Tanzania na Tamar ndiye aliyekuwa anafanya maandalizi ya jambo hilo.Kifo chake kitasababisha mkwamo mkubwa katika mipango yetu.Kuna nini Tanzania? Lucy Muganza ameuawa Tanzania na sasa Tamar.Kwa nini Tanzania imekuwa inatukwamisha katika mipango yetu yote? Akauliza Rais Michael na kugonga meza kwa hasira “Ninaapa nitapambana na nchi hii ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwetu.Ni aibu kukubali kuyumbishwa na nchi kama Tanzania ! akasema Michael “Mheshimiwa Rais naomba nikutoe wasiwasi.Kifo cha Tamar si mwisho wa mipango yetu.Kila tulichokipanga kitaendelea kama kawaida na tutafanikiwa” akasema Devotha “Tanzania wameturudisha nyuma kiasi kikubwa sana ! “Mheshimiwa Rais nakubali kwamba Tamar alikuwa ni nguzo yetu na kifo chake kimeturudisha nyuma sana hata hivyo bado tunaweza kuendelea na mipango yetu”akasema Devotha “Ni jinsi gani tutaweza kuendelea na mipango yetu bila Tamar? Akauliza Rais “Mheshimiwa Rais ni kweli tutapata ugumu kuendelea na mipango yetu bila ya Tamar lakini tunaweza kuendelea na mipango yetu yote hata bila ya yeye kuwepo” “Ni hapo ndipo ninapotaka kupafahamu tutaendelea vipi bila Tamar? Yule alikuwa ndiye jicho letu katika serikali.Nataka kusikia mawazo yako tafadhali”akasema Michael “Mheshimiwa Rais pamoja na hili ililotokea la kuuawa Tamar lakini hatua tuliyopiga katika mpango wetu si ndogo.Mpaka sasa Tanzania imekwisha chafuka kimataifa.Duniani kote wanafahamu kwamba Tanzania hakuna usalama na tukitaka kuisambaratisha Afrika Mashariki lazima tuanze kwanza na Tanzania kwani ndipo ilipo mizizi ya jumuia hii.Tanzania ikidhoofika jumuiya hii itakosa nguvu.Tanzania ikichafuka eneo zima la Afrika Masharikilitachafuka hivyo hatua tuliyopiga mpaka sasa si ndogo.Dunia nzima wanajua Tanzania inahusika katika mauaji ya balozi Benjamin Hudson kufuatia ujumbe alioandika katika ukurasa wake wa twitter akiwataka raia wa kutoka nchi za umoja wa Ulaya kutotembelea au kuwa makini wanapokuwa Tanzania.Nina imani kufuatia kifo cha balozi Benjamin Watalii wanaotembelea Tanzania na Afrika Mashariki watapungua kwa hofu ya usalama wao na hilo ni jambo kubwa sana kwetu.Hata hivyo bado tunayo kazi kubwa ya kufanya na kwa sasa baada ya Tamar kuuawa tunatakiwa kubadili mbinu za kuendelea na mpango wetu” akasema Devotha “Nakusikiliza Devotha endelea” akasema Rais Michael “Kipaumbele kwa sasa ni kuhakikisha Theresia Muganza anaingia Tanzania na ili aweze kufanikisha vyema kazi yake ya kusambaratisha Afrika Mashariki tunahitaji mtu ndani ya idara ya SNSA.Kuna mtu ndani ya idara ya SNSA anaitwa Edwin mbeko huyu alikuwa msaidizi wa Tamar na ndiye niliyemtumia katika mauaji ya balozi Benjamin.Huyu anaweza kuwa mbadala wa Tamar na kuna uwezekano Rais akamteua kuwa mkurugenzi wa SNSA kushika nafasi ya Tamar.Nashauri tuendelee kumtumia huyu jamaa ambaye nilimfundisha kazi mimi mwenyewe wakati ninaongoza idara ile.Sijamueleza chochote kwa sasa hadi utakaporidhia kwamba awe ndiye mbadala wa Tamar” akasema Devotha na Rais Michael akafikiri na kusema “Unamuamini anaweza akaifanya kazi yake kikamilifu kama Tamar?akauliza Rais Michael “Ndiyo ninamuamini.Kama nilivyokueleza ndiye niliyemtumia katika mauaji ya balozi Benjamin Hudson.Ni mtiifu,msikivu na anafanya kazi yake kwa umakini mkubwa sana” akasema Devotha “Mimi sina tatizo .Kama unaamini anaweza akawa mbadala wa Tamar basi tumtumie” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Devotha “Jambo la pili .Wakati tukiendelea na mchakato wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kumtumia Theresia Muganza ,kwa upande wa pili lazima tuendelee na mpango wa kumuondoa madarakani Rais Dr Fabian Kelelo.Huyu ni kikwazo kikubwa sana katika mipango yetu.Natakiwa kukalia kiti chake haraka sana kama tulivyokuwa tumekubaliana ili niweze kusaidia katika mpango huu mkubwa”Devotha akanyamaza na Rais Michael akauliza “Tukianzia na mpango wa kwanza wa kumuingiza Theresa nchini Tanzania uUnadhani Theresia ataingiaje chini Tanzania? Umesema tumtumie msaidizi wa Tamar ni vipi kama Rais Dr Fabian hatamteua kuwa mkurugenzi wa SNSA na badala yake akateua mtu mwingine? Nataka nisikie mpango yako katika hilo.Kumbuka hiki ni kipimo kwako kama endapo tutakusaidia ukachukua urais utaweza kweli nafasi hiyo na ukatekeleza mipango yetu yote? Akasema Rais Michael “Baada ya Tamar kutolewa katika picha ninao mpango mwingine wa kumuingiza Theresia nchini Tanzania na kumuwezesha kutekekeza mipango yetu bila matatizo.Hapa Paris kuna bilionea anaitwa Peniela.Nadhani umewahi kumsikia” “Ndiyo ninamfahamu.Ni bilionea mkubwa na hakuna asiyemfahamu”akasema MIchael “Japo kwa sasa ana uraia wa Ufaransa lakini Peniela anatokea Tanzania” akasema Devotha “Nalifahamu hilo” akasema Rais Michael na Devotha akaendelea “Peniela na mume wake wamewekeza miradi mbali mbali nchini Tanzania.Mume wa Peniela aliitwa Mathew Mulumbi ambaye kwa sasa ni marehemu.Kutokana na mumewe kufariki mali za Peniela ambazo ziko Afrika Mashariki zinakosa usimamizi makini kwani Peniela anaichukia sana Tanzania” “Anaichukia Tanzania nchi yake?akauliza Rais Michael “Ndiyo.Kwa sababu ya kifo cha mumewe.Mathew alikuwa anafanya kazi ya ujasusi na hata mimi nimewahi kufanya naye kazi.Alifariki akiwa katika misheni aliyotumwa na Rais hivyo basi kitendo hicho kimemuumiza mo Peniela na kumfanya asitake tena kurejea Tanzania.Theresa atakwenda kwa Peniela akimuomba amuuzie baadhi ya makampuni yake yaliyoko Tanzania na ataingia Tanzania kama muwekezaji” akasema Devotha.Ulipita muda kidogo na Rais Michael akasema “Huo unaonekana ni mpango mzuri lakini kama Peniela tayari ana chuki na Tanzania kufuatia kifo cha mumewe,hatuwezi kumshirikisha katika mpango wetu huu? Akauliza Rais Michael “Hapana.Hatuwezi kumshirikisha.Si mtu ambaye tunaweza kumuamini” “Sawa.Basi mpango huo wa kumpeleka Theresia Tanzania kama muwekezaji ni mpango mzuri.Unaamini Peniela atakuwa tayari kuuza baadhi ya mali zake nchini Tanzania? “Nina watu ambao wako karibu na Peniela ambao wamenihakikishia kwamba Peniela ana mpango huo wa kuuza mali zake zote nchini Tanzania kwani hana mpango wa kurudi tena huko”akasema Devotha “Sawa endelea kulishughulikia hilo suala.Baada ya Theresia kupona atapelekwa kwanza mafunzoni kisha mchakato wa kuelekea Tanzania utaanza.Hata hivyo nina ushauri .Naamini mpango wetu wa kumuandaa Lucy Muganza kuchukua urais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ulivuja ndiyo maana akauawa.Kuuawa kwa Tamar kunadhihirisha kwamba tayari Tanzania wanafahamu kila kitu kuhusu mipango yetu ndiyo maana wanajaribu kwa kila wawezavyo kuhakikisha hatufanikiwi. Ushauri wangu kwa sasa inatubidi tutulie kwanza huku tukiendelea kujipanga kimya kimya kwa ajili ya operesheni mpya.Tumfanye Rais Fabian ajue kwamba baada ya kumuua Tamar basi mambo yamekwisha.Nitawashawishi pia wenzangu wa umoja wa Ulaya kutulia kimya wasiongee chochote kuhusu Tanzania kwa sasa.Katika mpango huu mpya tujihadhari sana usije ukavuja.Unadhani hawataweza kugundua kama Tamar alikuwa na mawasiliano nawe? Akauliza Rais Michael “Jina Devotha Adolph limekwisha sahaulika Tanzania hakuna anayejua kama niko hapa Paris.Kingine kizuri ni kwamba Tamar alikuwa anatumia program maalum katika simu yake ambayo kila amalizapo kuzungumza na simu basi kumbu kumbu zote hufutwa haraka sana hivyo hakuna rekodi zozote za mazungumzo ya simu watakazozipata katika simu ya Tamar kama wakitaka kufuatilia kujua alikuwa anawasiliana na nani”akasema Devotha ukapita ukimya kidogo na Rais Michael akasema “Devotha ulijunga nasi katika mpango wetu wa kutaka kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sharti kwamba unataka tukusaidie ushike nafasi ya Urais wa Tanzania .Mimi na wenzangu wa umoja wa Ulaya hatuna kipingamizi katika suala hilo kwani utakuwa na manufaa makubwa kwetu.Tanzania ni kioo cha Afrka Mashariki hivyo licha ya kwamba malengo yetu makubwa ya mpango huu ni jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini Tanzania tunaihitaji pia hivyo tunahitaji kumuweka mtu wetu madarakani.Usiwe na hofu Devotha fanikisha Theresia aingie Tanzania,mimi na wezangu tutakuweka madarakani kwani uwezo huo tunao.Kwa sasa twende kwanza na jambo moja tukilifanikisha tutaanza jambo la pili.Narudia tena kukusisitiza kwamba hakikisha mpango huu hauvuji kama ilivyokuwa kwa mpango ule wa kwanza” akasema rais Michael BAADA YA WIKI NNE PARIS – UFARANSA Saa kumi na moja za jioni Rais Michael Weren aliwasili katika jumba lake kubwa ambalo huwa analitumia kwa mapumziko na familia yake.Katika jumba hili ndimo anamoishi Theresia Muganza akiendelea kupatiwa matibabu na jopo la madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa plastiki kubadilisha muonekano wake.Alifika hapa kumtazama Theresa baada ya kutaarifiwa na madaktari kwamba kwa asilimia tisini Theresa alikuwa amepona. Rais Michael alipokewa na daktari mkuu wa lile jopo la madaktari waliopiga kambi katika jumba lile kuhakikisha wanaikamilisha kazi waliyopewa na Rais,kisha wakaelekea ndani ambako alisalimiana na madaktari wengine na kabla hajaingia katika chumba alimo Theresa akapewa taarifa na mkuu wa jopo lile la madaktari kuhusiana na kazi waliyoifanya.Alionyeshwa picha mbili tofauti.Picha ya kwanza ilimuonyesha Theresa Muganza kablaya upasuaji na ya pili ilimonyesha baada ya upasuaji.Zilikuwa ni sura mbili tofauti zilizomuacha Rais Michael mdomo wazi “Haya ni maajabu.Mtu unaweza ukabadilishwa kabisa mwonekano wako na watu wakashindwa kukutambua” akawaza Baada ya kupokea taarifa ile ya madaktari akaingizwa katika chumba kikubwa alimokuwamo Theresa ambaye alikuwa amejilaza katika sofa. “Theresa ! akasema Rais Michael kwa mshangao.Alipoonyeshwa zile picha mbili hakuwa bado akiamini sana akataka athibitishe mwenyewe kwa kumtazama.Alichokiona mbele yake kilimshangaza sana.Theresa alikuwa amebadilika.Hakuwa Theresa Yule wa wiki kadhaa zilizopita.Huyu wa sasa alikuwa ni mwanamke mwenye umbile la aina yake.Alikuwa na sura nzuri iliyochongwa na kuvutia mno.Alipotabasamu uzuri uliongezeka mara dufu.Rais Michael akageuka na kumpa mkono daktari mkuu akampongeza kwa mara nyingine tena kwa kazi ile kubwa.Madaktari wakatoka wakamuacha Rais na Theresa. “Karibu sana mheshimiwa Rais.Sikutegemea kama ungekuja leo” akasema Theresa huku akitabasamu “Nilitaarifiwa na madaktari kwamba wamekamilisha kazi yao hivyo nikaona nije niangalie kile walichokifanya.Nimeishiwa maneno ya kusema kwa namna walivyoifanya kazi yao kwa umahiri mkubwa.Hivi ndivyo nilivyokuwa nataka.Umekuwa tofauti kabisa na Theresa Yule wa mwezi uliopita.Wanastahili sifa madaktari hawa” akasema Rais Michael bado akiendelea kumtazama Theresa huku akitabasamu “Unauonaje muonekano wako mpya?Unaufurahia?akauliza “Nimeufurahia sana mwonekano huu.Nimekuwa mrembo zaidi ya nilivyotegemea.Nakushukur u sana mheshimiwa Rais” akasema “Ninapaswa kukushukuru wewe kwa kukubali kubadili mwonekano wako.Si jambo jepesi hata kidogo”akasema Rais Michael na kumtazama Theresa tabasamu halikukauka usoni kwake. “Sikuwahi kufikiria kufanya kitu kama hiki lakini kwa ajili ya wazazi wangu waliouawa kinyama imenilazimu nifanye hivi.Nataka kufahamu je mpaka sasa kuna mtu yeyote amekwisha kamatwa kuhusiana na mauaji yale?akauliza Theresa “Hapana.Hakuna mpaka sasa mtu aliyekamatwa kufuatia mauaji yale.Watu ambao walitajwa kuhusika katika tukio lile la mauaji ambao ni majambazi waliuawa siku ile ile ile ya tukio hivyo mpaka leo hii hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kwa mauaji yale.Huo ni upande mmoja wa taarifa iliyotolewa na serikali.Upande wa pili tumefanikiwa kupata taarifa ya daktari aliyefanyia uchunguzi wa miili ya marehemu.Taarifa hiyo inaonyesha risasi zilizotumika kuwaua marehemu haziendani na silaha walizokutwa nazo wale watu wanaotajwa kufanya mauaji yale.Aina ya silaha iliyotumika ni bunduki zinazotumiwa na wadunguaji.Ni bunduki nzito sana na ambazo mara nyingi huwa zinamilikiwa na jeshi.Taarifa nyingine tuliyonayo inatuonyesha kwamba Tanzania wanazo bundukiza aina hiyo walizinunua kutoka Marekani.Taarifa hizi zinatufanya tuamini kwamba serikali ya Tanzania wanahusika katika mauaji yale.Tulianza kufanya uchunguzi wa suala hili lakini bado hatujapata majibu kwani aliyekuwa anatusaidia kufanya uchunguzi wa suala hili ameuawa wiki chache zilizopita na tunaamini haya yote yanafanywa na serikali ya Tanzania” “Nimeishi Tanzania ni nchi ya amani sana.Kwa nini waliua wazazi wangu? Akauliza Theresa na http://deusdeditmahunda.blogspot.com/machozi yakaanza kumtoka “Usilie Theresa.Muda wa kulia umekwisha” “Inaumiza sana mheshimiwa Rais.Wazazi wangu waliuawa kikatili sana na mimi mwenyewe nilipona kwa bahati tu mpaka leo ninapojitazama siamini kama nilinusurika katika tukio lile.Ninahitaji kujua kwa nini wazazi wangu waliuawa? Akasema Theresa. “Theresa nitakueleza ukweli” akasema Rais Michael na kunyamaza kwa sekunde kadhaa halafu akaendelea “Baada ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kufanyika,Patrice Eyenga aliibuka mshindi.Baada ya kushinda uchaguzi Patrice Eyenga alikutana na makundi ya waasi wakazungumza kuhusu kumaliza vita vya miaka mingi vya wenyewe kwa wenyewe.Katika majadiliano hayo namna ya kumaliza vita hivyo walikubaliana kugawana faida itakayotokana na rasilimali za madini yaliyoko nchini humo.Hiyo ndiyo siri ya waasi kuweka silaha chini nchini Congo DRC na amani kupatikana.Wawekezaji wengi walifukuzwa nchini humo na kuleta wawezekaji wengine ambao waliingia nao makubaliano.Kwa ufupi naweza kusema kwamba wanaofaidika kwa rasilimali za Congo ni kikundi cha watu wachache sana.Umoja wa Ulaya hatukuwa tayari kukubali kikundi cha watu wachache waendelee kufaidika na rasilimali za Congo na kuwaacha wananchi wakiendelea kuogelea katika lindi la umasikini.Tukaamua kumuandaa mtu ambaye atakuja kumaliza udhalimu huu unaoendelea nchini Congo na ndipo tulipomuandaa Lucy Muganza agombee urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hivi karibuni na tuliamini angeshinda uchaguzi lakini kwa bahati mbaya mpango wetu huo ulivuja na tunaamini ndiyo sababu ya wazazi wako kuuawa kwani mafisadi hawa walijua kwamba endapo Lucy angeshinda uchaguzi basi kiama chao kingewadia hivyo wakaona suluhisho ni kumuua”akasema Rais Michael “Serikali ya Congo nao walishiriki katika mauaji yale?akauliza Theresa “Hatuna ushahidi wa moja kwa moja lakini tunaamini serikali ya Congo na Tanzania wameshirikiana katika mauaji hayo.Tulikuwa tunadukua mawasiliano ya Rais wa Tanzania tujue wanawasiliana nini na Rais wa Congo lakini hatukufanikiwa kuna watu waliingilia zoezi hilo” akasema Michael “Roho inaniuma sana nikiwakumbuka wazazi wangu.Ninaumia mno” akasema Theresa. “Theresa kama utakumbuka hapo awali niliwahi kukueleza kwamba wewe ndiye utakayevaa viatu vya mama yako”akasema Michael “Siipendi kazi ya siasa.Kama mama yangu asingejiingiza katika masuala ya siasa hivi sasa angekuwa hai.Sitaki kuwa mwanasiasa wataniua hasa wakijua mimi ni mtoto wa Lucy Muganza” akasema Theresa “Hautaingia katika siasa.Licha ya kwamba tulimuandaa kwa ajili ya kushika urais wa Congo lakini Theresa alikuwa na kazi nyingine mahsusi ambayo ndiyo utakwenda kuifanya.Usihofu kuhusu usalama wako.Kwa nza kabisa hakuna atakayejua wewe ni Theresa Muganza.Kuanzia sasa hautajulikana tena kama Theresia Muganza bali utajulikana kwa jina la Melanie Davis bilionea na raia wa Ufaransa” akasema Rais Michael na kuichukua bahasha iliyokuwa mezani akaifungua na kutoa nyaraka kadhaa akamkabidhi Theresa “Kuanzia sasa jina lako ni Melanie Davis.Jina la Theresia Muganza tunalizika rasmi.Hizi hapa ni nyaraka mbali mbali zinakuonyesha wewe ni mzaliwa wa Ufaransa na unayemiliki utajiri mkubwa uliorithi kutoka kwa wazazi wako ambao wote wawili wamekwisha fariki dunia.Suala la kubadili mwonekano wako lilifanyika kwa siri kubwa na tulifanya hivi ili kuzuia siri hii kuvuja” akasema Rais Michael.Theresa akaendelea kuzipitia nyaraka zile alipomaliza akafuta machozi na kusema “Ahsante sana mheshimiwa Rais kwa kupambana kuyaokoa maisha yangu.Naamini kama ningeendelea kubaki Tanzania hivi sasa ningekwisha uawa.Ni gharama kubwa sana umeitumia.Naomba uniambie nini unataka nikifanye kama malipo ya haya uliyonifanyia?akauliza Theresa “Ninataka ukaifanye kazi aliyotakiwa kuifanya mama yako” “Niko tayari mheshimiwa Rais kwa kazi hiyo hata kama ni ya hatari lakini nitaifanya ” “Vizuri.Tunataka uongoze mapambano ya kuikomboa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” akasema Rais Michael na ukimya mfupi ukapita Theresa akasema “Mheshimiwa Rais nadhani jukumu hilo unalonipa ni gumu mno liko juu ya uwezo wangu.Mimi nikaikomboe nchi ya Congo?Siwezi mheshmiwa Rais nitauawa kabla sijatekeleza hilo jukumu” akasema Theresa kwa wasi wasi “Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nchi uliyozaliwa kwa sasa imeingia katika jumuiya ya Afria Mashariki.Rais Patrice Eyenga amefanya hivi makusudi ili kuendelea kujiimarisha kiutawala .Hatutaweza kuikomboa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo bila kwanza kuiondoa katika jumiya ya Afrika Mashariki .Jukumu kubwa la kwanza unalokwenda kulifanya ni kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki” akasema Michael na kunyamaza baada ya sura ya Theresa kuonyesha mstuko “Najua nimekustua Theresa lakini hilo ndilo jukumu kubwa la kwanza ambalo alikuwa nalo marehemu mama yako Lucy Muganza na sasa wewe ndiye unayekwenda kulitekeleza.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imejiwekea mwavuli baada ya kujiunga na jumuiya hii hivyo basi hakuna namna tunavyoweza kuondoa unyonyaji unaofanywa na Patrice Eyenga na genge la mafisadi wenzake wachache wanaoendelea kunufaika na rasilimali za nchi yako huku mamilioni ya watu wakiendelea kuogelea katika umasikini mkubwa.Ni jukumu kubwa lakini kumbuka kwamba waliopanga njama za kumuua mama yako ni hawa viongozi wa Afrika Mashariki hivyo basi pamoja na kwamba tunapambana kuikomboa nchi yako ya Congo lakini vile vile tunakwenda kulipiza kisasi kwa wale wote waliowaua wazazi wako kikatili.Usihofu hautakuwa mwenyewe bali sisi tuko nyuma yako na tutakuwezesha kwa kila kitu.Kazi yako itakuwa rahisi sana na wala hautakuwa katika hatari yoyote” akasema Rais Michael na Theresa akafuta machozi “Nini hasa ninatakiwa kukifanya huko mnakotaka kunituma? akauliza Theresa “Kabla ya kwenda huko Afrika Mashariki utapewa kwanza mafunzo ya nini unakwenda kukifanya.Lazima tukuandae kwa kazi hii.Kesho atakuja mtu kukuchukua na kukupeleka mahala utakapopewa mafunzo na pale utakapokuwa umehitimu mafunzo yako basi utakwenda Afrika Mashariki” “Ni mafunzo gani ambayo ninakwenda kupewa? Akauliza Theresa “Ni mafunzo maalum ya kukuandaa na kukujenga, kukuondoa kutoka Theresa Muganza na kuwa Melanie Davis.Narudia tena kukutoa hofu kwamba tutakuwa nyuma yako kukulinda kuhakikisha huingii katika hatari yoyote” akasema Rais Michael “Kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa wale wote waliowaua wazazi wangu kinyama niko tayari mheshimiwa Rais” akasema Theresa huku akidondokwa na machozi “Usilie Theresa.Muda wa kulia umekwisha pita hivi sasa ni muda wa kujiandaa kulipa kisasi kwa waliowaua wazazi wako na kikomboa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Utaelezwa mengi,utafundishwa mengi hivyo nakuomba zingatia yale yote utakayofundishwa” akasema Rais Michael na kuagana na Theresa akaondoka “Rais Michale amekuja kukitonesha kidonda kilichoanza kunyauka.Nina hasira sana na wale waliofanya kitendo kile cha kinyama.Waliwaua wazazi wangu kikatili sana.Naamini yalikuwa ni mapenzi ya Mungu nibaki hai ili niweze kuikamilisha kazi ambayo mama yangu alikuwa amejitolea kuifanya ya kuokoa rasilimali za nchi yangu ya Congo.Damu ya wazazi wangu haitapotea bure lazima nihakikishe ninawalipia kisasi.Hakuna aliyeshiriki katika mauaji haya atabaki salama.Sikuwahi kuwa na chuki kubwa moyoni mwangu kama niliyo nayo sasa.Nilikuwa ninasikia simulizi za watu ambao wazazi wao waliuawa kinyama na sikujua mateso ya namna gani wanayapitia hadi na mimi nilipopoteza wa kwangu.Ni mateso makubwa mtu kuwakatili uhai wazazi waliokuleta duniani na kukulea kwa upendo mkubwa.Wazazi wangu hawakuwahi kunifundisha kumchukia mtu lakini hawa watu makatili wamenifanya niwe na roho ya chuki.Ninawachukia wanasisasa,ninawachukia viongozi wa nchi yangu ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Afrika Mashariki. Kitu pekee kilichobaki ambacho naamini kinaweza kunipa amani ya moyo ni pale nitakapohakikisha kwamba wale wote walioshiriki katika mauaji ya wazazi wangu wanapata adhabu inayowastahili” akawaza Theresa. LONDON – UINGEREZA Baada ya Ruby kukubali uteuzi wa Rais Fabian Kelelo wa kuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi,aliwasilisha kwa uongozi wake wa wajuu wa mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia ya uingereza maombi ya kuacha kazi.Ulikuwa ni mstuko mkubwa kwa viongozi wa juu wa mamlaka ile hawakuwa wametegemea mtu kama Ruby angeweza kuamua kuacha kazi licha ya kuwa na mshahara mkubwa na mnono na alipata kila alichokihtaji.Ruby aliombwa awape viongozi wake muda wa kulijadili ombi lake kabla ya kutoa maamuzi. Sababu aliyoitoa Ruby ya kutaka kuacha kazi haikuwashawishi viongozi wake kulikubali ombi lake hivyo baada ya wiki mbili akaitwa tena kuzungumza na jopo la viongozi wakamjulisha kwamba ombi lake la kuacha kazi wamelikataa hivyo basi wakamtaka Ruby aendelee na kazi lakini bado aliendelea kuwa na msimamo ule wa kutaka kuacha kazi.Kikao kati yake na jopo la viongozi kilifanyika kwa muda wa saa nne bila maafikiano na wakaomba wapewe tena muda wajadiliane.Baada ya Ruby kutoka katika kikao hicho viongozi wale waliendelea na kikao na wote walionyesha wasi wasi wao kuhusu nia ya Ruby kuacha kazi.Waliamua kutumia idara ya ujasusi ya MI5 kumchunguza Ruby mienendo yake,mawasiliano yake ili kuona kama kuna sababu nyingine iliyompelekea Ruby kutaka kuacha kazi. Saa moja za jioni alipotoka kazini Ruby na wafanyakazi wenzake walifika katika mgahawa mmoja kupata chakula.Walikuwa na kawaida ya kila wamalizapo majukumu yao ya siku hukutana katika mgahawa huo kupata chakula na kinywaji kabla ya kwenda majumbani.Wakiwa wanasubiri chakula huku wakiendelea na mazungumzo na kupata kinywaji alifika muhudumu akiwa na sinia la chakula akajigonga katika meza na mchuzi ukammwagikia Ruby katika nguo yake.Muhudumu Yule akamuomba samahani na kumtaka ampeleke katika chumba chake akabadili shati lake jeupe lililochafuliwa kwa mchuzi ili lifuliwe.Ruby aliongozana na yule muhudumu hadi katika chumba cha kubadili mavazi cha wahudumu na alipoingia mle ndani alipatwa na mshangao mkubwa. “Joe ?! akauliza kwa mshangao baada ya kumkuta mtu anayemfahamu ndani ya kile chumba “Ruby usihofu nimetumia njia hii ili niweze kuonana nawe bila mtu yeyote kuwa na wasiwasi nawe” akasema Joe ambaye ni rafiki mkubwa wa Ruby na alikuwa ni mfanyakazi wa idara ya MI5 “Kuna nini Joe?Unajua namna ya kuwasiliana name.Unayo namba yangu ya simu kwa nini hukunipigia?akauliza Ruby.Joe akamshika Ruby bega “Ruby kuna tatizo ndiyo maana sikutaka kukupigia simu” “Tatizo gani joe? “MI5 wanakuchunguza” akasema Joe na sura ya Ruby ikaonyesha mstuko mkubwa “MI5 wananichunguza?akauliza “Ndiyo wanakuchunguza” “Nini wanakitafuta kwangu? “Wanachunguza kila kitu.Wanachunguza mawasiliano yako na kila unachokifanya.Kuna kamera za siri zimefungwa nyumbani kwako hivyo basi kuwa makini uwapo nyumbani kwani kila unachokifanya kinaonekana.Mawasiliano yako yote yanafuatiliwa.Kila unayekutana na kuzungumza naye anachunguzwa.Wanataka kujua sababu ya kuacha kazi” akasema Joe “Joe ahsante sana kwa kunipa taarifa hizi muhimu.Nilitegemea jambo kama hili kutokea kwani mpaka leo hii hawajakubali kuniacha niende ” akasema Ruby “Kwa nini umeamua kuacha kazi Ruby?akauliza Joe “Ninataka kupumzika” akajibu Ruby “Ni sababu hiyo tu ndiyo ambayo imekufanya uache kazi? “Ndiyo Joe.Ninataka kupumzika” “kwa nini usiombe upewe likizo hata ya muda mrefu upumzike kuliko kuamua kuacha kabisa kazi?akauliza Joe “Nimechoshwa na kazi hii Joe hivyo ninataka nipumzike huku nikitafakari nini cha kufanya lakini sitaki tena kufanya kazi GCHQ” akasema Ruby “Ruby ninayaheshimu sana mawazo yako lakini nakuomba uwe makini sana kuanzia sasa,kila unachokifanya fahamu kwamba kuna watu wako nyuma yako wanakufuatilia” akasema Joe “Joe ninashukuru sana kwa kunitahadharisha.Nitakuwa makini sana kwa kila nikifanyacho” “Nitalifuatilia kwa karibu sana hili jambo na kama kukiwa na hatari yoyote nitakujulisha haraka sana.Sitaki uingie katika hatari yoyote Ruby” akasema Joe “Nashukuru sana Joe.Kweli wewe ni rafiki wa kweli.Ninafurahi kuwa na rafiki kama wewe”akasema Ruby “Ruby siwezi kusahau misaada mbali mbali ambayo umekuwa ukinisaidia.Nisingefika hapa nilipo kama si wewe hivyo basi siwezi kukubali ukaingia katika hatari.Sasa badilisha shati lako urejee hotelini ukaungane na wenzako.Hakikisha unakuwa kawaida na usionyeshe mabadiliko yoyote yale.Endelea kutumia simu yako kama kawaida kwa mawasiliano ya kawaida na marafiki zako lakini kwa mawasiliano yale ya muhimu ya siri usitumie simu hii kwani inafuatiliwa” akasema Joe.Haraka haraka Ruby akavua lile shati lililomwagikiwa mchuzi akavaa shati lingine alilokuja nalo Joe akatoka kwenda kuungana na wenzake wakaendelea kupata chakula.Baada ya chakula wakaondoka kila mmoja akielekea nyumbani kwake “Nilijua toka awali kwamba haitaweza kuwa rahisi GCHQ kukubali niache kazi.Nimekuwa mtu muhimu sana katika mamlaka hii na tayari ninazifahamu siri nyingi na hilo ndilo linalowapa ugumu wa kukubali niache kazi.Wana hofu labda nikiondoka ninaweza kutoa siri za nchi ninazozifahamu ndiyo maana wananichunguza kujua ninawasiliana na nani na kuzungumza nini.Kabla hata Joe hajanieleza kinachoendelea tayari nilikwisha anza kuchukua tahadhari kubwa ndiyo maana nimekuwa makini sana ninapowasiliana na Rais Dr Fabian ili wasijue kama ninakwenda Tanzania kuwa mkurugenzi wa SNSA.Kwa namna yoyote ile wakatae wasikatae lazima niondoke hapa Uingereza niende Tanzania.” akawaza Ruby. Alifika nyumbani kwake na kama alivyokuwa ameelekezwa na Joe hakuonyesha mstuko wowote kama kuna kamera za siri zimefungwa nyumbani kwake.Alikwenda chumbani kwake akavua mavazi yake akabakiwa na nguo za ndani halafu akaenda sebuleni akajilaza sofani akitazama filamu huku chupa ya mvinyo laini ikiwa mezani akiendelea kupiga mafunda taratibu.Alipitiwa usingizi sofani na baada ya kustuka akaenda chumbani kwake kulala Saa kumi na mbili za asubuhi aliamka na kuanza kujiandaa kwenda kazini.Wakati akipata kifungua kinywa akafungua kompyuta yake ili kutazama jumbe alizotumiwa na moja ya ujumbe ulitoka kwa mkuu wake aliyemtaka akaonane naye siku ile.Alipokuwa tayari akafunga mlango wa nyumba yake na kuondoka.Kitu cha kwanza alichokifanya baada ya kufika ofisini kwake ni kwenda kuonana na mkuu wake akamsalimu kisha mkuu Yule akaongozana naye wakaenda hadi katika ofisi ya mkurugenzi mkuu ambako kulikuwa na jopo la viongozi wa GCHQ.Hakuwa ametaarifiwa kuhusiana na kikao kile. “Ruby karibu.Habari za asubuhi” akasema mkurugenzi mkuu baada ya Ruby na mkuu wake wa idara kuingia mle ofisini “Habari nzuri kabisa mkurugenzi.Habari zenu wakuu wangu wengine” akasema Ruby kwa adabu wakaitikia wote halafu akaketi kitini. “Ruby hatukuwa tumekujulisha kuhusu kikao hiki lakini kwa ufupi ni kwamba kikao hiki ni cha dharura na mada kuu ni lile suala lako la kutaka kuacha kazi” akasema mkurugenzi mkuu na kumtazama Ruby “Ruby kwa mara nyingine tena napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha kwamba suala lako limekuwa linatuumiza vichwa vyetu sana toka ulipoliwasilisha kwetu.Hiyo ni kwa sababu wewe ni muhimu sana kwetu na umefanya kazi ambayo naweza kusema ni ya kutukuka kabisa.Wewe ni mmoja wa wafanyakazi bora kabisa hapa.Kinachotuumiza vichwa vyetu na kutufanya tuendelee kukutana kila uchao kujadili jambo hili ni umuhimu wako kwa mamlaka hii.Bado tunakuhitaji sana na hatuoni sababu ya kukuacha uende.Tumeichambua sababu yako ya kutaka kuacha kazi lakini bado hatujaona kama ni sababu yenye mashiko hivyo napenda kukujulisha kwamba kwa mara nyingine tena msimamo wa mamlaka ni kwamba ombi lako la kuacha kazi GCHQ limekataliwa” akasema mkurugenzi Yule mwenye umbo kubwa.Ruby akavuta pumzi ndefu halafu akasema “Mkurugenzi ninashukuru sana kwanza kwa kupokea ombi langu na kulijadili.Ninashukuru vile vile kwa maamuzi yenu ambayo mmefikia.Lakini kwa bahati mbaya na mimi pia bado msimamo wangu ni ule ule kwamba ninataka niache kazi hapa GCHQ”akasema Ruby na ofisi ile ikatawaliwa na ukimya “Ruby” akasema mkurugenzi mkuu na kumtazama Ruby “Kama nilivyokueleza kwamba umuhimu wako ni mkubwa sana katika mamlaka yetu hivyo basi kuna mambo ambayo idara tumeamua kuyafanya ili kukushawishi ubadilishe mawazo yako ya kuacha kazi katika mamlaka yetu.Sababu uliyoitoa ya kuacha kazi haijatushawishi hivyo kutufanya tuamini kuna sababu nyingine kubwa kwani mshahara wako hapa ni mzuri na unapata kila kitu hata hivyo tumeamua kukuongeza mshahara mara saba ya mshahara unaolipwa sasa” akasema mkurugenzi mkuu na sura ya Ruby ikaonyesha mshangao .Hakutegemea kulipwa mshahara mkubwa kiasi kile.Mshahara wake ulikuwa mkubwa lakini uliongezwa mara saba zaidi ili kumshawishi abaki kazini. “Haya sasa ni majaribu.Mshahara mkubwa sana huu ambao wanataka kunipa” akawaza Ruby “Ukiacha mshahara huo pia tutakupandisha cheo utakuwa ni mkuu wa idara.Mkuu wako wa sasa wa idara atapangiwa kazi nyingine.Utapewa nyumba kubwa na nzuri zaidi .Utapewa walinzi wa kukulinda kila mahala uendako.Hayo ni yale makubwa ambayo tunatarajia kukufanyia lakini kuna mengi ambayo yapo katika makataba huu tuliouandaa ambao tunataka ukaupitie na kuona yaliyomo halafu utatujulisha”akasema mkurugenzi mkuu wa GCHQ na kumsogezea Ruby faili akainuka akaenda kulichukua.Akapitia haraka haraka nyaraka zilizomo “Huu ni mtego mkubwa wameniwekea.Nikiendelea kukataa watajua lazima kuna sababu kubwa na ninaweza hata kuuawa na nikashindwa kufikia malengo yangu ya kwenda Tanzania.Ninachotakiwa hapa ni kulegeza msimamo wangu ili kuwapa moyo” akawaza Ruby “Ruby” akaita mkurugenzi na Ruby akainua kichwa “Una maoni gani? “Mkurugenzi nimeupokea mkataba huu na ninakwenda kuupitia nione kilichomo ndani yake halafu nitakuja tena kwako tutazungumza lakini nina ombi moja kwenu” “Omba chochote Ruby” “Nahitaji siku saba za mapumziko” akasema Ruby na ofisi ikawa kimya.Baada ya muda mkurugenzi mkuu akasema “Kwa nini unahitaji siku saba za mapumziko Ruby?Kwa nini isiwe siku mbili ? “Nimekuwa nikifanya kazi mfululizo bila kupumzika siku nyingine kwa saa ishrini na nne nahitaji siku chache za kupumzisha mwili na akili”akajibu Ruby Mkurugenzi akamtaka Ruby akaendelee na kazi atamjulisha baadae kile watakachokuwa wamekiamua kuhusu maombi yake ya likizo fupi ya siku saba. Baada ya Ruby kutoka,mkurugenzi mkuu akachukua simu na kupiga.Hazikupita dakika mbili mtu mmoja akaingia akiwa na kompyuta mpakato. “Tueleze nini umekigundua kwa Ruby?akauliza mkurugenzi mkuu.Yule jamaa akaifungua kompyuta yake na kusema “Nilichokigundua ni kwamba Ruby ana kitu anacho hataki kukiweka wazi.Nadhauri tuendelee kumchunguza” akasema yue jamaa ambaye ni mtaalamu wa kuchunguza watu kupitia maneno na matendo yao kujua kama wanasema ukweli ama wanadanganya.Baada ya kuwasilisha taarifa yake akatoka na wakuu wale wakaendelea na kikao chao. “Mmemsikia mtaalamu wetu alichokisema.Ruby kuna kitu anakificha na hataki kuwa muwazi.Pamoja na taarifa ya mtaalamu lakini nyote mmeshuhudia mstuko aliouonyesha Ruby baada ya kutamkiwa kwamba ataongezwa mshahara mara saba zaidi ya ule anaolipwa sasa.Hakuwa ametegemea kama tungeweza kumlipa kiasi kikubwa namna hii cha fedha ndiyo maana hata msimamo wake umelegea hadi akaamua kuchukua mkataba ule akaupitie.Hapo ndipo alipokosea” akasema mkurugenzi mkuu na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Sikuwa nimewajulisha dhumuni la kutaka kumuongezea Ruby mshahara mara saba zaidi ya mshahara wake wa sasa.Nadhani hata ninyi nyote mmestuka sana baada ya kusikia jambo hilo kwani nililifanya siri.Kama Ruby akilipwa mshahara mara saba ya mshahara wake wa sasa ninyi nyote ambao ni viongozi wake mtakuwa chini yake na atakuwa ananikaribia sana kufikia mshahara wangu mimi.” Akanyamaza tena kwa sekunde chache “Sikuwa nimedhamiria kumlipa Ruby kiasi kile kikubwa cha fedha kama nilivyomtamkia bali ulikuwa ni mtego nimemuwekea.Nilitaka kumpima msimamo wake mbele ya fedha.Mtakumbuka toka alipowasilisha ombi lake la kuacha kazi tumekuwa tukikaa naye na kuzungumza kujaribu kumshawishi asiache kazi na kama haitoshi mimi binafsi nimekuwa nikimpigia hata simu kumuomba abadili maamuzi yake lakini amekuwa na msimamo usioyumba.Niliwahi kumgusia kumuongeza mshahara lakini hakuwa tayari kubadili msimamo wake.Leo baada ya kumtamkia kwamba ataongezwa mara saba zaidi ya mshahara wake wa sasa amelegeza msimamo wake na amekubali kuchukua mkataba akaupitie na kuna kila dalili kwamba anaweza akakubali na kuendelea na kazi.Mtego wangu ulikuwa hapa kutaka kumpima Ruby msimamo wake mbele ya fedha.Ameonyesha shida yake ni fedha kwani kama shida yake si fedha asingelegeza msimamo wake lakini anaonekana shida yake ni fedha ndiyo maana amekubali kuchukua mkataba akaupitie.Wasi wasi wangu ni kwamba kama fedha imemfanya akalegeza msimamo wake ni vipi kama akitokea mtu au nchi na wakamlipa fedha mara kumi ya fedha tunayomlipa sisi kwa lengo la kutaka kupata siri Fulani za nchi yetu hamuoni kama anaweza akauza siri huyu mwanamke?akauliza mkurugenzi mkuu “Nadhani mmenielewa ninachokimaanisha.Kama ni hivyo huyu mwanamke ni hatari sana kwetu.Hatupaswi kuendelea kuwa naye katika mamlaka yetu.Tunapaswa kumuondoa haraka.Anafahamu mengi hadi sasa na madhara yake yanaweza kuwa makubwa kama akiamua kuuza kile anachokifahamu kuhusu nchi yetu.Sioni sababu ya kuendelea kumshikilia mtu mmoja kana kwamba akiondoka basi mamlaka haitakuwepo tena.Yeye ni mfanyakazi wa kawaida tu kama wengine.Narudia tena uamuzi wangu ni huo kwamba mwanamke huyu ni hatari na lazima tutafute namna ya kumuondoa hivyo timu inayoendelea kumchunguza iwe makini sana.Nitampigia simu kumjulisha kwamba nimekubali ombi lake la mapumziko ya siku saba na katika muda huo tumchunguze anachokifanya na tutafute namna ya kumuondoa.Tutumie utaalamu mkubwa kumuondoa na ionekane amejiua kutokana na msongo wa mawazo.Na sisi tutalithibitisha hilo kwamba aliomba mapumziko ya siku saba na alionekana ana msongo wa mawazo.Nadhani mmenielewa” akasema mkurugenzi mkuu na wote wakakubaliana naye. “Ahsanteni sana kwa kunielewa lakini nawakumbusha tena kwamba suala hili ni siri kubwa.Najua Ruby ni mwanamke mwenye akili nyingi na anayeweza kutambua hatari iliyoko mbele yake lakini vile vile ana marafiki wengi katika mamlaka na katika vyombo mbali mbali vya kiusalama hivyo basi suala hili lihusishe watu wachache sana ili kuzuia kuvuja” akaelekeza mkurugenzi mkuu na majadiliano yakaendelea kwa nusu saa kisha wakuu wale wakatoka kwenda kuendelea na majukumu yao.Mkurgenzi mkuu akampigia Ruby na kumtaka aende ofisini kwake ambako alimjulisha kwamba wamekubali aende mapumziko ya siku saba kama alivyokuwa ameomba. Baada ya ombi lake la mapumziko kukubaliwa Ruby hakutaka tena kuendelea kukaa ofisini akakusanya baadhi ya vitu vyake vichache vya muhimu akatoka.Moja kwa moja akaelekea katika ofisi za shirika la ndege la Misri ambako alikata tiketi ya ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea Misri asubuhi ya siku inayofuata halafu akaelekea nyumbani kwake kupumzika Taarifa ya Ruby kukata tiketi ya ndege kwa lengo la kusafiri kuelekea Misri zilimfikia mkurugenzi mkuu wa GCHQ kupitia kwa timu ya majasusi waliowekwa kumfuatilia Ruby na mara tu alipoipata taarifa ile akaitisha kikao cha dharura. “Jamani nimewaiteni tena kwa dharura kufuatia taarifa niliyoipata kutoka kwa timu ya watu wanaoendelea kumfuatilia Ruby.Nimetaarifiwa kwamba baada ya kutoka hapa Ruby alielekea katika ofisi za shirika la ndege la Misri akakata tiketi kwa ajili ya kuelekea Misri kwa ndege ya shirika hilo itakayoondoka kesho saa tatu asubuhi. Ruby anataka kuondoka nchini na hatujui kwa nini anakwenda Misri?akasema mkurugenzi mkuu “Labda niwakumbushe viongozi wenzangu kwamba mwaka 2013 Edward Snowden wa Marekani aliomba likizo kwa ajili ya mapumziko ya kiafya akaelekea Hong Kong na huko alivujisha siri za serikali ya Marekani.Ruby amekuwa akifanya kazi katika idara nyeti kabisa na siri nyingi anazifahamu.Sitaki kilichotokea Marekani kitokee na hapa kwetu.Nadhani mpaka hpa tayari mmekwisha pata picha ya nini kinaendelea” akasema mkurugenzi na majadiliano yakaendelea Ruby akiwa nyumbani kwake akipumzika,akapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama muhudumu wa mgahawa ambao Ruby amekuwa akienda mara kwa mara na wenzake kupata chakula cha usiku baada ya kumaliza kazi.Muhudumu Yule akamkumbusha Ruby kwamba shati lake ambalo lilichafuliwa na mchuzi kwa bahati mbaya lipo tayari na apite kulichukua.Ruby akamuahidi Yule muhudumu kwenda kulichukua shati lake jioni ya siku ile vile vile akaweka oda ya chakula kwa ajili yake na wenzake “Huyu lazima atakuwa ni Joe anataka nikaonane naye.Kuna taarifa atakuwa ameipata anataa kunipa” akawaza Ruby na kuendelea kutazama filamu.Alijua anaangaliwa kupitia kamera za siri hivyo basi hakutaka kuoyesha kama ameipania sana safari ile hivyo alijitahidi kwa kila namna aweze kuonyesha kwamba safari ile ilikuwa ya kawaida na haikuwa na uzito wowote. Alipochoka kutazama filamu akajilaza kitandani hadi ilipotimu saa kumi na mbili za jioni.Akaamka akajiandaa kisha akatoka kwenda kukutana na marafiki zake katika mgahawa wanapokutana kila mara.Wenzake tayari walikwisha fika na walikuwa wanaendelea kupata kinywaji Ruby akaungana nao na katika mazungumzo yao akawajulisha kwamba siku inayofuata anasafiri kwenda Cairo Misri.Wenzake wote walimshangaa kwa safari ile ya ghafla “Kwa nini Misri? Akauliza mmoja wao. “Ninapenda kusoma historia za mataifa mbali mbali na historia ya nchi ya Misri imenivuia sana.Nataka nikashuhudie kwa macho namna walivyokuwa wakiwazika wafalme wao wa zamani .Kuna mambo mengi nataka nikajifunze kule Misri” akajibu Ruby .Muhudumu akafika na kumtaka Ruby akachukue shati lake akawaomba radhi wenzake na kuelekea upande wa ndani katika vyumba vya wahudumu ambako kama alivyokuwa ametegemea akakutana na Joe. “Habari yako Joe” akasema Ruby “Habari nzuri Ruby.Nimefurahi kukuona” “Mimi pia nimefurahi kukuona.Nilipojulishwa na muhudumu kuhusu shati moja kwa moja nikajua ni wewe.Vipi kuna taarifa gani?akauliza Ruby “Ruby tayari wanafahamu kwamba kesho unasafiri kwenda Misri” akasema Joe “Nalitambua hilo.Wananifuatilia kila kona hivyo nisingeweza kuficha kuhusu safari yangu.Naamini hivi sasa wako nyumbani kwangu wakipekua kutafuta kwa nini ninasafiri kesho” akasema Ruby “Ruby uko katika hatari kubwa sana.GCHQ wamepanga kukuua” akasema Joe na Ruby akastuka “Wanataka kuniua? “Ndiyo.Ulifanya kosa kubwa kukubali kuchukua ule mkataba waliokuandalia.Ulikuwa ni mtego” akasema Joe na Ruby akavuta pumzi ndefu “Usijali Ruby tayari ninafahamu mpango mzima namna ulivyopangwa na nitakusaidia.Utafuata kile nitakachokueleza.Nilijua toka awali kwamba GCHQ wasingekuacha salama hivyo nikaanza kujiandaa kwa ajili ya kukusaidia.Usiwe na wasi wasi Ruby.Mimi nipo nitakusaidia” akasema Joe na kumuelezea Ruby kwa ufupi namna watakavyofanya. “Ahsante sana Joe”akasema Ruby na kumkumbatia Joe. “Tayari tumeelewana.Hivyo nenda sasa ukajumuike na wenzako ili wale wanaokufuatilia wasije wakaanza kuwa na wasiwasi nawe” akasema Joe na Ruby akatoka akaenda kuungana na wenzake.





Saa kumi na mbili za asubuhi tayari Ruby alikwisha amka akijiandaa kwa safari ile.Ni vitu vichache tu aliviweka katika sanduku lake dogo kwani alijua anaonekana kupitia kamera.Katika sanduku lile aliweka nguo chache na vitu vingine vidogo vidogo kama vpodozi.Kompyuta yake akaifungia katika kabati lake kwa lengo la kuwatoa wasi wasi wale waliokuwa wanamfuatilia.Aliandaa kifungua kinywa akakaa mezani na wakati akipata mlo ule wa asubuhi akawapigia simu marafiki zake kadhaa kuwajulisha kwamba anasafiri asubuhi ile kueleka Cairo Misri lakini atarejea baada ya siku nne. “Sasa muda umewadia.Today is victory or death.Lakini namuamini sana Joe ni mmoja wa majasusi hatari kabisa ndani ya MI5.Sijui nitamshukuruje kwa msaada huu mkubwa alionisaidia.Bila yeye nisingefahamu kama kuna mpango mkubwa umepangwa wa kuniua.Kwa hili alilonifanyia Joe hata yeye mwenyewe amehatarisha maisha yake lakini amefanya hivi kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwangu.Ananipenda mno na siku zote amekuwa ananitaka tuwe wapenzi lakini moyo wangu umekuwa mgumu kufunguka kwake.Moyo wangu bado uko kwa Mathew Mulumbi.Bado kuna kitu ndani ya nafsi yangu kinaniambia Mathew yuko hai lakini kama amekufa basi nitakutana naye huko wanakoenda wafu.Nampenda Mathew pekee”akawaza Ruby akijitazama katika kioo akaridhika na mwonekano wake halafu akachukua simu yake na kuita taksi ikafika na kumpeleka uwanja wa ndege wa kimataifa wa heathrow. Dakika mbili baada ya Ruby kuondoka nyumbani kwake gari moja aina ya Van lenye rangi nyeusi likafika nyumbani kwa Ruby wakashuka watu watatu waliovaa sare maalum za kazi wakiwa na kofia vichwani mwao wakazunguka mlango wa nyuma kisha wakafunika nyuso zao na kuacha macho wakafungua mlango wa nyuma na kuingia ndani mwa Ruby.Haraka haraka wakaenda katika chumba cha kulala Ruby wakafungua kabati ambamo Ruby aliweka kompyuta yake ndogo wakaichukua halafu wakatoka haraka sana. Watu wale wakiwa ndani ya nyumba ya Ruby waliweza kuonekana katika kompyuta za timu ya MI5 waliokuwa wakimfuatilia Ruby.Wote walishangazwa sana na kitendo cha wale jamaa kuingia na kuchukua kompyuta ya Ruby na kuondoka haraka namna ile.Hakukuwa na timu yoyote ya MI5 iliyokuwa karibu na eneo lile la nyumbani kwa Ruby kwani timu nzima ilihamishiwa uwanja wa ndege alikoelekea Ruby. Ruby akiwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote.Alikuwa amekaa na abiria wengine wakisubiri ndege huku akichezea simu yake.Alipokea simu chache kutoka kwa marafiki zake wakimtakia safari njema “Mungu anisaidie Joe aweze kufanikisha mpango wake kwani kama si hivyo leo ninakwenda kufa.Ninawaona majasusi kadhaa wa MI5 wako hapa uwanjani naamini wananifuatilia.Ninamuamini Joe lazima mpango wake utafanikiwa” akawaza Ruby Hatimaye abiria waliokuwa wakisubiri ndege ile aliyokuwa anaisubiri Ruby wakatangaziwa kuingia ndani ya ndege.Ruby akiwa na abiria wengine wakaingia ndegeni tayari kwa safari.Ruby hakuonyesha wasiwasi wowote lakini kwa ndani alikuwa na woga usioelezeka.Aliketi kitini akiwa na tabasamu usoni. “Kweli hawa jamaa wamedhamiria kunipoteza.Nimewaona majasusi wawili wa MI5 wakinifuatilia hadi humu ya ndege kuhakikisha nimeingia ndegeni halafu wakatoweka naamini watakuwa wameshuka” akawaza Ruby Baada ya dakika kadhaa akainuka na kuacha mkoba wake mdogo pamoja na simu katika kiti chake ili kumthibitishia mtu yeyote kuwa angerejea muda wowote akaelekea chooni Gari la ngazi likaondolewa taratibu na mlango wa ndege ukafungwa ishara kwamba ndege ilikuwa tayari kuondoka.Ndege ilipoanza kuondoka taratibu iligundulika kwamba abiria mmoja hakuwepo katika kiti chake huyu alikuwa ni Ruby.Mkoba na simu yake vilikuwepo katika kiti chake na hii ikawafanya wahudumu waamini kwamba yawezekana amebanwa yuko chooni na angerejea. Gari la ngazi liliambaa taratibu.Ndani ya gari lile walikuwamo watu watatu wote wakiwa wamevaa sare za wafanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo.Ukiacha dereva wengine waliokuwamo ndani ya gari lile ni Joe na Ruby aliyekuwa amevaa mavazi yalimyomfanya muonekano wake ubadilike.Gari lile lilikwenda hadi mahala linakoegeshwa gari dogo la kampuni ile ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni “Ahsante sana Bobby” akasema Joe na kufungua mlango akaangalia nje kama kuna hatari yoyote kisha akamtaka Ruby ashuke garini wakaingia katika lile gari dogo na kuondoka.Wakati wakiondoka pale uwanjani ndege ya shirika la ndege la Misri aliyotakiwa kupanda Ruby ikapaa “Joe nakushukuru sana kwa jambo hili kubwa ulilolifanya.Umehatarisha maisha yako kwa sababu yangu” akasema Ruby “Usinishukuru Ruby bado tuna kazi kubwa ya kufanya.Natakiwa kuhakikisha nimekuondoa hapa nchini kabla hawajagundua kwamba hauko ndegeni”akasema Joe huku akiendesha gari kwa umakini na uangalifu mkubwa akichunguza mara kwa mara kama wanafuatiliwa.Hatimaye baada ya mizunguko kadhaa wakaingia katika nyumba Fulani ambako waliwakuta watu watatu.Joe akawasalimu halafu akampeleka Ruby katika mojawapo ya chumba mle ndani akamtaka abadili mavazi.Alivaa gauni refu lenye nakshi za kupendeza,kichwani akavaa wigi lenye nywele ndefu akafunika macho kwa miwani kubwa myeusi na kisha akajitanda ushungi.Alipojitazama katika kioo akatabasamu.Haikuwa rahisi kutambulika. “Itachukua muda kwa mtu kuweza kukutambua” akasema Joe aliyekuwa na Ruby mle chumbani akimsaidia katika kubadili mwonekano “Ahsante sana Joe.Sijui bila wewe ningefanya nini” akasema Ruby .Joe akatoka akaenda sebuleni kukutana na wale jamaa waliowakuta mle ndani baada ya muda akarejea chumbani alimo Ruby “Ruby kompyuta yako hii hapa.Niliwatuma vijana wangu waende wakaichukue mara tu ulipoondoka pale nyumbani kwako kama tulivyokuwa tumepanga” “Ahsante sana Joe”akasema Ruby na Joe akachukua bahasha nyingine ndogo akampatia Ruby “Humo kuna hati ya kusafiria yenye jina la Annabel Jones ambalo ndilo jina utakalolitumia kuanzia sasa.Humo ndani ya ndege kuna tiketi ya treni utakwenda hadi Paris Ufaransa na pale utakutana na binamu yangu ambaye atakusaidia kuweza kupata usafiri wa kuelekea kokote unakotaka kwenda duniani tayari nimekwisha mpa maelekezo.Nitakupa kijana mmoja ataongozana nawe kukulinda endapo kutatokea hatari yoyote” akasema Joe Hakukuwa na muda wa kupoteza wakaingia garini na kuelekea katika kituo cha treni ya kuelekea jijini Paris. “Joe sina neno zuri la kukushukuru kwa kuyaokoa maisha yangu.Sintakusahau katika maisha yangu” akasema Ruby baada ya kufika katika kituo cha treni. “Ruby ingia ndani ya treni,jitahidi sana kuchukua kila aina ya tahadhari”akasema Joe.Ruby akaingia ndani ya treni huku machozi yakimtoka.Joe hakuondoka pale kituoni hadi alipohakikisha treni imeondoka kuelekea Paris SAA MOJA BAADAE Taarifa za ndege aina ya Boeing 747 ya shirika la ndege la Misri iliyokuwa na abiria wapato 257 ndani yake ikitokea London kuelekea Cairo kupoteza mawasiliano ikiwa angani zilianza kusambaa na mamlaka husika zilianza kuitafuta.Baada ya saa moja ilitangazwa kwamba ndege hiyo ilianguka katika kisiwa cha Sardina na watu wote 257 waliokuwamo ndani ya ndege hiyo walipoteza maisha. Ilikuwa ni taarifa iliyoistua dunia RAMALLAH – PALESTINA Maisha katika kambi ya kikundi cha Ammar Nazari Brigades kwa upande wa Mathew Mulumbi yaliendelea vizuri.Tayari amekwisha anza kushirikishwa katika masuala mbali mbali yanayohusiana na operesheni za kikundi hicho.Amekuwa karibu sana na Ammar na kwa muda huu wote amekuwa akijifunza mambo mambo mbali mbali yanayohusiana na mapambano dhidi ya Israel.Katika kipindi hiki cha mwezi mmoja maroketi kadhaa yalirushwa katika upande wa Israel lakini hayakusababisha kifo chochote. Jioni moja baada ya kupata chakula cha usiku Ammar alimtaka Mathew akapumzike kujiandaa kwa safari muhimu siku inayofuata.Mathew alipoingia chumbani kwake akajitupa kitandani alihisi uchovu mwingi kwani siku ile walikuwa na mizunguko mingi. “Umekwisha pita mwezi sasa nikiwa na hawa jamaa.Hakuna shaka yoyote hadi sasa tayari wananiamini na tayari mimi ni mwenzao.Licha ya Ammar kunipa upendeleo mkubwa lakini hata watu wengine nao tayari wamekwisha niamini na wananipenda.Siri zao nyingi nimezifahamu namna wanavyoandaa na kurusha maroketi upande wa Israel,mahala yalipo mahandaki yao,namna wanavyopata silaha na mambo mengine kadhaa.Kubwa ninalolilenga kwa sasa ni kumtafuta Habiba Jawad.Toka nimefika hapa sijawahi kumgusia lolote Ammar kuhusiana na Habiba Jaw………..”Mlango wa Mathew ukagongwa na kumuondoa mawazoni akainuka kwenda kuufungua akakutana na Nawal aliyekuwa amebeba nguo zilizokuwa zimefuliwa. “Nawal kwa nini usingesubiri hadi kesho ndipo uniletee hizi nguo? Wewe ni mke wa mtu na kuonekana huku kwangu usiku huu haitaleta picha nzuri wanaweza wakaanza kuhisi vingine na tukaharibu kila kitu”akasema Mathew “Abu unaponitamkia mimi ni mke wa Ammar unanikumbusha machungu ninayopata kwa uwepo wangu hapa.Nyote hamjui kile ninachokipitia lakini ninayavumilia kwa ajili ya nchi yangu na watu wangu.Tuachane na hayo nimekuja kukupa taarifa muhimu sana”akasema Nawal “Taarifa gani Nawal” akasema Mathew huku akjiweka sawa kuipokea taarifa hiyo. “Kuna shambulio linaandaliwa kufanyika kesho jijini Jerusalem na wewe ndiye unayepangwa kwenda kufanya shambulio hilo” akasema Nawal na Mathew akastuka sana “Shambulio? “Ndiyo.Kuna bomu linaandaliwa kwenda kulipuliwa kesho wewe ndiye utakayebeba kilipuzi.Nimeona nije kukutaarifu mapema ili uanze kujiandaa” “Nawal kwa nini tusiwataarifu Mossad kuhusu shambulio hilo ili waanze kujiandaa?akauliza Mathew “Hapana Abu hatupaswi kuwajulisha Mossad.Shambulio hilo lazima lifanyike na lifanikiwe ili hawa jamaa waendelee kuwa na imani nawe.Endapo Mossad watafahamu kuhusu shambulio hilo na likashindwa kufanikiwa wanaweza watatafuta kwa nini siri hiyo imevuja kwani mpango huu wameuandaa kwa siri kubwa”akasema Nawal “Kwa sasa nchini Israel ninajulikana kama mtu hatari gaidi niliyetoroka gerezani nitaingia vipi Jerusalem?Mathew akauliza “Hawa jamaa wana mtandao mrefu hata ndani ya Israel hivyo usihofu wamejiandaa vya kutosha.Ninachokuomba hakikisha bomu hilo linalipuka kesho.Maisha ya watu wasio na hatia yatapotea lakini hakuna namna ya kuweza kuwaokoa lazima bomu lilipuke ” akasema Nawal na Mathew akainamisha kichwa akafikiri kidogo na kusema “Nawal siko tayari kwa watu wasio na hatia kupoteza maisha huku nikishuhudia.Lazima tuwajulishe Mossad” akasema Mathew “Abu hapana na ninakuonya ukithubutu kufanya jambo lolote na kusababisha bomu hilo kushindwa kulipuka basi misheni yako itakuwa imefika mwisho hautafanikiwa tena kumpata Habiba Jawad .Hawa jamaa watachunguza na wakikugundua watakuua na mimi sintakuwa na msaada wowote kwako hivyo fanya ninavyokuelekeza.Wakati mwingine katika misheni kama hizi lazima tukubali kushindwa ili kuupata ushindi.Umenielewa Abu?akauliza Nawal “Nimekuelewa” akajibu Mathew kwa sauti ya chini “Ahsante.Tafadhali usionyeshe kama kuna kitu kinakusumbua wala usihoji maswali fanya utakachoelekezwa na uonyeshe kufurahia bomu lile kulipuka” akasema Nawal na kutoka akimuacha Mathew katika mawazo mengi. ”Maisha ya watu wasio na hatia yanakwenda kupotea hiyo kesho na mimi ndiye nitakayebeba swichi itakayolipua hilo bomu.Mimi ndiye nitakayetoa roho za watu hao wasio na hatia.Kwa nini lakini nimefikia hatua hii? Ni lazima kuwatoa sadaka watu hao kwa ajili ya mtu mmoja tu Habiba jawad?akajiuliza Mathew “Lakini ngoja nifuate ushauri wa Nawal kwamba natakiwa kuendelea kujiweka karibu zaidi na hawa watu ili waendelee kuniamini na kuniona ni mwenzao.Lazima bomu hilo lilipuke” akawaza Mathew “Kwa miaka mingi nimekuwa nikipambana na magaidi hawa wanaoua watu lakini leo hii nimejiunga nao na kushiriki katika mauaji ya watu wasio na hatia.Damu yote itakayomwagika kesho haiwezi kupotea bure lazima Habiba Jawad apatikane na hapo ndipo vikundi kama hivi vya akina Ammar vitajikuta vikifa taratibu kwani havitakuwa na vyanzo vingine vya mapato.Wote hawa wanamtegemea sana Habiba kuwapa fedha za kujiendesha” akaendelea kuwaza Mathew





Saa tisa za usiku mlango wa chumba cha Mathew ukagongwa akaamka na kuufungua akakutana na mmoja wa walinzi wa Ammar ambaye alimjulisha Mathew kwamba ajiandae anahitajika katika kikao “Mambo yameanza.Nadhani kikao hicho ni kwa ajili ya kujadili mauaji ya watu wasio na hatia yanayokwenda kufanyika leo” akawaza Mathew akiwa bafuni akinawa uso halafu akatoka na kwenda kuhudhuria kikao. “Habari za asubuhi Abu Zalawi” akasema Ammar akiwa katika sura yenye tabasamu “Ahsante sana Ammar.Habari zenu nyote” akasema Mathew “Abu samahani kwa kukuamsha mida hii lakini kama ujuavyo sisi ni jesho hivyo hufanya kazi muda wote” akasema Ammar “Usijali Ammar ninalifahamu hilo” akasema Mathew “Sasa tumekamilika tunaweza kuendelea” akasema Ammar “Kwa muda wote niliokaa gerezani mashambulio dhidi ya Israel yalipungua sana.Mashambulo yaliyofanyika si mengi na waisrael waliouawa idadi yao bado ni ndogo.Israel imeendelea kupanua makazi ya wayahudi katika ardhi yetu.Nimerudi mwenyewe kamanda wa vita na mapambano yanaanza upya na safari hii lazima Israel watasalimu Amri”akasema Ammar na kuwatazama watu wake waliokuwa makini wakimsikiliza “Mwezi mmoja sasa umepita toka nimerejea na kipindi chote hicho tumekuwa tukifanya maandalizi ya kufanya shambulio kubwa na sasa wakati umefika.Tunakwenda kuanzisha tena vita na Israel na kuwataka wasitishe mpango wao wa kupanua makazi ya wayahudi katika ardhi yetu.Baadae leo tutafanya shambulio kubwa la bomu na kumwaga damu ya waisrael.Abu Al Zalawi wewe ndiye utakayeongoza mapambao haya ya leo na hii itakuwa ni kazi yako ya kwanza tangu ujiunge nasi” akasema Ammar na kumtazama Mathew ambaye alitabasamu na kusema “Nakushukuru sana Ammar kwa kunichagua mimi niongoze shambulio la leo.Nimekuwa nikiisubiri sana siku kama hii ili niweze kumwaga damu ya waisrael.Bado nina hasira nao sana” akasema Mathew “Abu Zalawi kauli yako inadhihirisha wewe kweli ni mpiganaji.Kwa muda wote ambao nimekuwa katika mapambano haya sijawahi kukutana na mtu ambaye alifurahia alipopewa jukumu la kwenda kutekeleza shambulio la bomu.Ni moja kati ya mashambulio ambayo wengi wanayaogopa lakini wewe umelipokea kwa ujasiri mkubwa” akasema Ammar “Ammar nina hasira kubwa sana na Israel ndiyo maana najisikia fahari kubwa kumwaga damu nyingi ya viumbe hawa” akasema Mathew Mulumbi “Mungu atanisamehe kwa maneno haya lakini ninafanya hivi ili kujenga imani kwa hawa magaidi wakati ninatengeneza njia ya kwenda kwa Habiba Jawad.Ninaapa siku za hawa jamaa zinahesabika kwani damu hii inayokwenda kumwagika kwa mashambulizi haya haitapotea bure” akawaza Mathew Ramani kubwa ikaletwa na kuwekwa mezani. “Kesho shambulio linakwenda kufanyika katika kituo kikuu cha treni.Kwa kawaida katika kituo hiki huwa kuna mkusanyiko mkubwa wa watu hasa nyakati za asubuhi.Treni inapofika kunakuwa na idadi kubwa ya watu wanaoshuka na wengine wanaoingia na hapo ndipo tutalilipua bomu letu.Abu wewe utakuwa umejificha sehemu Fulani na utakuwa na kifaa cha kulipulia bomu hivyo shughuli hii nzima inakutegemea sana wewe.Hakikisha unalilipua bomu pale tu ambapo utaona kuna idadi kubwa ya watu eneo lilipo bomu” akaelekeza Ammar. Majadiliano yakaendelea kwa muda wa saa nzima na kisha Mathew akaenda kujiandaa kwa safari.Alipewa suti nzuri mpya ili awe katika muonekano nadhifu. “Ee Mungu nisamehe kwa hili ninalokwenda kulifanya leo” akaomba Mathew kabla hajatoka chumbani kwake. Gari mbili ziliondoka katika makazi ya Ammar kuelekea Jerusalem umbali wa kama kilometa kumi na sita.Mida hiyo ilikuwa ni saa kumi na moja za alfajiri. Walipita njia zilizojificha ili kukwepa vizuizi vya askari na walipofika sehemu Fulani wakakuta kuna gari moja limeegeshwa chini ya mti.Ammar na watu wake wakashuka na kutoka ndani ya lile gari walilolikuta njiani akashuka mwanamke mmoja mwembamba.Ammar na Yule mwanamke wakasalimiana halafu akamtambulisha Mathew kwa Yule mwanamke “Huyu ni mwenzangu anaitwa Abu Al Zalawi na ndiye atakayesimamia zoezi la leo” akasema Ammar na kumgeukia Mathew “Abu huyu ni mshirika wetu anaitwa Nadya yeye anaishi Jerusalem.Yeye ndiye atakayewapa kila aina ya msaada mnaouhitaji ili kufanikisha zoezi la leo” akasema Ammar. Nadya akaaga na na Ammar kisha sanduku lenye bomu likaingizwa katika gari la Nadya.Mathew na kijana ambaye ndiye atakayebeba sanduku lile lenye bomu wakaingia katika gari lile la Nadya na kuondoka. “Jukumu langu ni kuhakikisha mnaingia Jerusalem na kutekeleza shambulio lenu hivyo mtafuata maelekezo nitakayowapa na sitaki kuulizwa swali lolote.Tumeelewana?akauliza Nadya “Hakuna tatizo Nadya” akajibu Mathew Saa kumi na mbili kasoro waliwasili jijini Jerusalem na kuelekea katika nyumba Fulani wakapumzika na kupitia tena mpango wa shambulio lile halafu wakaondoka kuelekea mahala ambako kulipangwa kufanyika shambulio. Nadya aliegesha gari katika maegesho ya kituo cha treni.Watu walikuwa wengi asubuhi hii wengi wakitaka kupanda treni kuwahi makazini na katika shughuli mbalimbali “Tumefika” akasema Nadya.Walitumia dakika kadhaa ndani ya gari Mathew akijaribu kufanya uchunguzi kuona kama kuna hatari yoyote halafu Yule kijana akachukua sanduku na kuungana na abiria wengine waliokuwa wakiingia ndani ya kituo kile cha treni.Kwa muonekano wake kila mmoja aliamini kijana Yule ni msafiri kama wengine na haikuwa rahisi kumuhisi kama amebeba bomu kwani alionekana ni kijana nadhifu na mwenye maisha mazuri.Nadya na Mathew nao wakashuka garini kisha wakaelekea katika sehemu ya kukatia tiketi wakaingia ndani .Watu walikuwa ni wengi ndani ya kituo . Treni waliyokuwa wakiisubiri akina Mathew ilitangazwa kuwa ndiyo itakayofuata.Mathew ambaye alikuwa makini sana aliweza kumuona vyema kijana wake akiliweka chini sanduku lililokuwa na bomu.Treni ile waliyoishubiri ikafika na milango ikafunguliwa watu wakaanza kushuka huku wengine wakijiandaa kuingia.Watu walikuwa ni wengi.Mathew alimuona Yule kijana wake akiondoka taratibu eneo lile huku akiliacha sanduku lake chini. Mwili ulimtetemeka. “Ee Mungu nisamehe” akawaza Mathew kisha akatoka upande ule na kuiingia upande wa kusubiria treni ambako alimuona Nadya akamfanyia ishara atoke wakaongozana kuelekea nje “Muda umefika” akasema Nadya Kwa kutumia kidole gumba cha mkono wa kulia Mathew akabonyeza kile kilipuzi kilichokuwa mfukoni.Kishindo kikubwa kikasikika kikiambatana na moto na moshi mzito.Kishindo cha mlipuko ule kilikuwa kikubwa na kulitetemesha eneo lile.Mathew akawahi kumdaka Nadya na kumkinga.Watu waliokuwa nje ya kituo walianza kukimbia hovyo kunusuru maisha yao.Mathew na Nadya wakainuka na kuelekea katika gari lao na kumkuta Yule kijana wao akiwasubiri.Wakaingia garini na kuondoka. “Kazi nzuri sana Abu.Mapambano haya yataendelea hadi Israel watakapoondoka katika ardhi yetu” akasema Nadya “Uko sahihi Nadya ni wakati wa Israel kulipa uovu wao” akasema Mathew “Abu wewe unatokea wapi? NI nadra sana kuona mtu mweusi katika mapambano haya ya Israel na Palestina” akauliza Nadya “Asili yangu ni Misri.Baba yangu alkiuawa na majeshi ya Israel hivyo niliweka kiapo cha kupambana na Israel.Niliishi Kenya ambako nilimuua mkuu wa Mossad Afrika Mashariki na ndipo nilipokamatwa na Israel nikafungwa na gerezani nikakutana na Ammar tukafanikiwa kutoroka” akasema Mathew “Sipendi maswali kama haya.Sipendi kurudia kujieleza mimi ni nani! Akawaza Mathew “Unafanya kazi gani hapa Jerusalem?akauliza Mathew “Ninasoma” akajibu Nadya akiwa makini katika usukani.Ukimya ulitawala mle garini TEL AVIV – ISRAEL MAKAO MAKUU YA SHIRIKA LA UJASUSI ISRAEL (MOSSAD) “Mimi Ammar Al Nazari,Bin Khalfan bin Said kiongozi wa kikundi cha Ammar Nazari brigades ninayo furaha kubwa kuitangazia dunia kwamba shambulio lililotokea leo katika kituo kikuu cha treni jijini Jerusalem limetekelezwa na kikundi changu.Kikundi changu cha Ammar Nazari Brigades kimepanga kufanya mashambulizi makubwa katika miji mbali mbali ya Israel na kumwaga damu nyingi ya waisrael.Kilichotokea leo ni sehemu ndogo tu ya mashambulizi makubwa tutakayoyafanya.Tunataka walowezi wa kiyahudi waondoke katika ardhi yetu na mpango wa kupanua makazi ya wayahudi katika ardhi ya wapalestina usitishwe haraka sana.Kupuuzia kuyafanya hayo ni kuruhusu damu zaidi ya waisrael kumwagika kila uchao kwani sisi na vikundi vingine vya kupigania haki za wapalestina tumejipanga vizuri na kila siku damu nyingi itamwagika. Vita hii haitakoma na itaendelea viazi hata vizazi hadi pale tutakapoipata ardhi yetu” Hii ilikuwa ni video ambayo ilitoka muda mfupi baada ya shambulio la bomu kutokea katika kituo kikuu cha treni jijini Jerusalem ikimuonyesha Ammar Nazari kiongozi wa kikundi cha Ammar Nazari brigades akijitapa kikundi chake kufanya shambulio lile lililoua watu ishirini na moja na wengine wengi kujeruhiwa . Katika chumba cha mikakati walimokuwamo viongozi wa Mossad hali ilikuwa ya ukimya mkubwa baada ya kuitazama video ile. “Tayari wataalamu wetu wamekwisha tuthibitisha kwamba anayeonekana katika video hiyo ni Ammar Nazari”akasema Moshe Levine mkurugenzi mkuu wa Mossad. “Ilituchukua muda mrefu kumpata Ammar na tunawashukuru CIA ambao ndio walitusaidia tukaweza kumpata.Alipokuw gerezani mauaji kama haya yalipungua .Tulifanya maamuzi ya kumuachia Ammar atoroshwe na Mathew Mulumbi kwa mategemeo kwamba tungeweza kumpata Habiba Jawad lakini mpaka sasa umepita mwezi mzima hakuna mafanikio yoyote wala mawasiliano yoyote kutoka kwa Mathew.Kundi la Ammar brigades limepata nguvu mpya baada ya kiongozi wao kutoka gerezani na tayari limeanza kumwaga damu ya waisrael.Kama alivyosema katika video hii kwamba wamejipanga kwa ajili ya kufanya mashambulizi mengine zaidi ndani ya ardhi yetu” akasema Moshe na kunyamaza akawatazama viongozi wale “Nataka kufahamu kuna taarifa yoyote kutoka kwa Mathew Mulumbi?akauliza Moshe “Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kutoka kwa Mathew Mulumbi.Taarifa yenye uhakika tuliyo nayo ni kwamba baada ya kutoka gerezani Mathew Mulumbi aliambatana na Ammar Nazari kuelekea k atika kambi yao na toka wakati huo hatujawahi kusikia chochote kutoka kwa Mathew Mulumbi” akasema Efraim Dagan “Mna uhakika Mathew Mulumbi bado yuko hai? Nina wasiw asi yawezekana Ammar amemgundua kuwa ni pandikizi na wamemuua.Lazima tukubali tulifanya kosa kubwa kumuachia Ammar na sasa ameanza kutushambulia.Hatuwezi tena kuendelea kumsubiri Mathew Mulumbi.Hatujui kama yuko hai au ameuawa hivyo basi lazima tuchukue hatua za haraka sana kumdhibiti Ammar.Watu waliouawa leo ni wengi na ameahidi kuendelea kumwaga damu zaidi hivyo ni jukumu letu sisi kuhakikisha mipango yake hiyo haitimii.Waziri mkuu amekwisha weka vikosi katika utayari ili viweze kuvamia makazi ya wapalestina na kuanza msako wa nyumba kwa nyumba hadi wahakikishe wanampata Ammar.Njia hii kama mnavyojua ina madhara makubwa kwani maisha ya watu wengi wasio na hatia hupotea.Waziri mkuu anataka kusikia Ammar Nazari ameuawa hivyo basi suala la Mathew Mulumbi limekwisha rasmi na mkakati ulioko kwa sasa ni kuhakikisha Ammar anauawa.Wazri mkuuameniagiza nizungumze na mkurugenzi mkuu wa CIA ili waweze kutupatia taarifa zozote walizonazo kuhusu Ammar naili vikosi vya jeshi viweze kumteketeza yeye na kizazi chake chote.CIA walitusaidia awali kumpata Ammar na ninahakika wanaweza kuwa na taarifa zinazoweza kutusaidia kumpata Ammar” akasema Moshe akionekana kuwa na hasira “Mkurugenzi” akaita Efraim “Unasemaje Efraim? “Binafsi bado nina imani kubwa na Mathew Mulumbi.Ninaamini ….” Efraim akanyamaza baada ya Moshe kumkatisha “Nini kinakupa imani kuhusu Mathew Mulumbi? Suala lake tayari limefungwa.Kama yuko kwa Ammar naye atateketezwa kama wengine ! akasema Moshe “Nina imani Mathew Mulumbi hakuwa akidanganya.Alikuwa na ya dhati ya kumpata Habiba Jawad na vile vile anahitaji sana kuwa huru.Hawezi kukimbia kwani anaamini sisi tuko nyuma yake na akijaribu kufanya kitu chochote cha kijinga basi atakuwa anaiweka familia yake katika hatari”akasema Efraim “Efraim naomba usiwe na mawazo hayo tena.Yule jamaa alicheza na akili zetu na sisi tukajikuta tukiingia katika mtego wake tukamuamini akatoroka gerezani na sasa hatutaweza tena kumpata.Tumempoteza yeye na mtu hatari sana Ammar.Tukubali tulifanya makosa na sasa faili lake ninalifunga rasmi” akasema Moshe “Mkurugenzi naomba tulipe muda suala hili ili tuweze kujiridhisha kama kweli Mathew yuko kwa Ammar” akasema Efraim “Utafanikisha vipi suala hilo?Una mawasiliano naye?akauliza Moshe na Efraim Dagan akabaki kimya.Alikosa jibu “Hakuna namna yoyote ile ya kuweza kufahamu kama kweli Mathew Mulumbi yuko na Ammar Nazari.Aligoma tusimuwekee kifaa cha kutuwezesha kumfuatilia kwa kuwa alikuwa na mipango yake ya kutoweka na sisi tukakubali.Tunastahili mzigo wa lawama kwa haya yote yanayoendelea kutokea katika ardhi yetu.Nawahakikishia dam u hii iliyomwagika leo na inayoendelea kumwagwa yote inatulilia sisi kwa kuwa tulikubali kumuachia muuaji aende zake.Sitaki tena mjadala kuhusu jambo hili ninachokwenda kukifanya ni kuzungumza na mkurugenzi wa CIA kumuomba atusaidie kufahamu mahala alipo Ammar na kisha tutatoa taarifa kwa vikosi vya jeshi ambavyo viko katika utayari na kumsambaratisha Ammar na kizazi chake chote.Hiyo ndiyo adhabu pekee ambayo Ammar anastahili” akasema Moshe “Mkurugenzi utanisamehe kwa maswali yangu lakini nataka ufafanuzi mdogo.Umesema mpango ulioko mezani kwa sasa ni kumteketeza Ammar kwa bomu endapo tutafanikiwa kufahamu mahala alipo.Swali langu ni vipi kama Mathew Mulumbi atakuwa bado yuko kwa Ammar?Ninauliza hivyo kwa sababu naamini haiwezi kuwa rahisi kwa magaidi wale kumuamini Mathew haraka haraka na kuanza kumshirikisha katika mipango yao.Kabla ya kuletwa hapa makao makuu nimewahi kuwa andakava kwa miaka mitatu nikifuatilia mtandao wa kuuza silaha kwa magaidi na si kitu chepesi.Unaweza ukauawa muda wowote.Sitaki kumtetea Mathew lakini kuna kitu kinaniambia ndani yangu kwamba Mathew bado yuko upande wetu na tuvute subira.Nahisi anajitahidi kujenga mahusiano mazuri na Ammar na kundi lake na pale atakapokuwa amefanikiwa basi atatufahamisha.Mkumbuke kwamba dhumuni kubwa la Mathew ni kumfikia Habiba Jawad ambaye ndiye uti wa mgongo wa makundi karibu yote ya kigaidi yaliyoko Palestina ambayo yanaendelea kumwaga damu ya watu wetu wasio na hatia.Tukimuua Ammar bila kumkamata au kumuua Habiba Jawad bado hatutakuwa tumetatua jambo hili kwani kwani mauaji,mashambulizi ya mabomu,maroketi na kujitoa mhanga havitakoma bado vitaendelea kila uchao.Kama Mathew Mulumbi bado yuko hai basi ni msaada mkubwa kwetu.Yule ni jasusi na hastahili kuwekwa katika kundi la magaidi” akasema Efraim na ukimya ukatawala mle ndani “Efraim umejaribu kuelezea kwa umakini mkubwa kuhusu umuhimu wa Mathew na ninakubaliana nawe kwamba kama angefanya kwa mujibu wa makubaliano yetu basi kusingekuwa na tatizo lakini shida inakuja kwamba hatujui mpaka leo kama bado ni mzima au ameuawa,hatujui kama yuko na Ammar au ametokomea zake anakojua yeye na kikubwa zaidi ni kwamba hatuwezi kusubiri zaidi kwani Ammar anapanga mashambulizi mengine.Efraim naomba ufahamu si kwamba mawazo yako ninayapuuza lakini hali halisi ilivyo unaiona.Ammar anaendelea kumwaga damu ya waisrael na hatuwezi kukaa tukimuangalia tukitegemea tuna mtu tumempandikiza katika kundi lake.Katika hili suala tukubali kwamba tulijaribu na tumeshindwa hivyo tuje na mkakati mpya ambao ni kumteketeza Ammar na uzao wake wote.Kama vitaendelea kuibuka vikundi vingine vya wanamgambo tutakabiliana navyo pia.Kama Mathew Mulumbi bado yupo na Ammar atatusamehe kwani hatuna jinsi lazima naye ateketee.Mimi kama mkurugenzi mkuu wa Mossad ninasema tuhitimishe suala hili na tuanze kushughulikia suala la kumuua Ammar Nazari” akasema Moshe na wakuu wale wa idara mbali mbali ndaniya Mossad wakatoka Baada ya wakuu wale wa idara mbali mbali kutoka,Moshe akampigia simu mkurugenzi mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani (CIA) Jason Washington. “Habari yako Bwana Moshe” akasema Jason “Bwana Washington.Habari za huko? “Huku kwema kabisa.Poleni sana kwa shambulio lililotokea” “Ahsante sana”akajibu Moshe “Nimeiona video ya Ammar Nazari akijitapa kutekeleza shambulio lile,imekuaje akawa huru wakati alikuwa gerezani?akauliza Jason “Ni kweli alikuwa gerezani lakini kuna jambo lilitokea hivi karibuni na Ammar akawa huru” akasema Moshe “Sihitaji kujua nini kilitokea lakini Ammar hakupaswa kuwa huru” akasema Jason “Ni kweli Jason ndiyo maana nimekupigia kuomba msaada wako” “Unahitaji msaada gani Moshe? “CIA mlitusaidia mara ya kwanza tukafanikiwa kumpata Ammar tunaomba tena safari hii mtusaidie tuweze kufahamu mahala alipo.Hatutaki kumkamata tena tunataka kumteketeza yeye na kizazi chake chote” akasema Moshe na ukimya wa sekunde kadhaa ukapita halafu Jason Washington akasema “Hilo jambo litakuwa na gumu kwa sasa.Nasikitika kusema kwamba hatutaweza kuwasaidia katika hilo” “Kwa nini Jason?CIA na Mossad tumekuwa na mashirikiano ya karibu kwa muda mrefu na kusaidiana kila pale inapolazimika.Shambulio la leo ni baya na kama ulivyoona kwenye video ya Ammar ametishia kufanya mashambulizi zaidi.Tunajua kumkamata tena halitakuwa jambo jepesi hivyo tunataka kufahamu mahala alipo ili tumteketeze kwa bomu” akasema Moshe “Moshe kama nilivyokueleza awali ni kwamba hatutaweza kuwasaidia kwa sasa katika jambo hilo” akajibu Jason “Jason Marekani na Israel wote tuko kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.Tumekuwa na utamaduni wa kubadilishana taarifa za kiintelijensia kuhusiana na mitandao ya kigaidi au watu wanaosakwa kwa ugaidi.Mfano mzuri ni miezi minne iliyopita majasusi wetu wa wamefanikiwa kuwakamata wahusika wawili waliotekeleza shambulio la kigaidi huko Florida waliokuwa wamekimbilia nchini Misri.Ushirikiano wa namna hii umekuwepo kwa miaka mingi ndiyo maana tumekuja tena kwenu kuwaomba mtusaidie kupata taarifa za mahala alipo Ammar Nazari ili tumteketeze kabla hajaendelea kutekeleza mashambulio yake aliyoahidi kuendelea kuyatekeleza.Tafadhali Jason” akasema Moshe “Moshe nakubali mashirikiano yetu na ninyi ni mazuri na tumefanikiwa mambo mengi katika ushirikiano huo lakini katika suala hili kuna ugumu kidogo” “Ugumu gani Jason? “Ugumu uliopo ni kwamba tuna mtu wetu ndani ya kikundi cha Ammar Nazari brigades ambaye amepandikizwa kwa kazi maalum ambayo bado hajaikamilisha.Kitendo chochote cha kumkamata Ammar kwa sasa au kumuua ni hatari kwa mtu wetu aliyeko huko ambaye jukumu lake ni kubwa sana.Endapo Ammar atakamatwa tena lazima wataanza kuwa na hisia kwamba kuna mtu anatoa taarifa za mahala alipo hivyo wanaweza wakaanza kufanya uchunguzi na wakamgundua huyo mtu wetu na kumuua.Kuhusu kumteketeza Ammar nao niI mpango hatari kwa mtu wetu ambaye tumetumia gharama kubwa kumpandikiza hapo na anafanya kazi nzuri sana.Kwa sababu hizo Moshe siwezi kukusaidia katika mpango huu” akasema Jason “Jason umenishangaza sana.Kwa muda huu wote una mtu wako ndani ya kikundi cha Ammar bila kutujulisha?Ammar ni mtu muhimu sana kwetu kwa sasa.Naomba utusaidie kumpata tafadhali” “Moshe mtu wangu aliyemo katika kikundi cha Ammar Nazari brigades yuko pale kwa jambo kubwa sana na la muhimu hivyo kwa namna yoyote ile siwezi kukubali akawa katika hatari hasa kwa wakati huu ambao amepiga hatua kubwa katika kazi tuliyomtuma akaifanye” “Moshe una maana kwamba tumuache Ammar aendelee kutekeleza mipango yake ya mashambulizi na kumwaga damu ndani ya ardhi yetu?akauliza Moshe “Tafuteni njia mbadala ya kuweza kudhibiti mipango yake lakini kuhusu kumuua au kumkamata kwa sasa hilo jambo halitawezekana kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeharibu misheni yetu ya muda mrefu.Tuliwasaidia pale mwanzo mkafanikiwa kumpata Ammar lakini mkampoteza.Nimeamua kukueleza siri hii kwa sababu Ammar hatakiwi kuguswa kwa namna yoyote ile” “Jason tafadhali nihakikishie kwamba humaanishi kauli yako hiyo” akasema Moshe “Utanisamehe Moshe.Ninamaanisha kile ninachokisema.Naomba Ammar Nazari asiguswe kwa sasa kwani mkimgusa kwa namna yoyote ile mtakuwa mmevuruga misheni kubwa ya CIA ambayo imeandaliwa kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu.Hatuko tayari kwa hilo” akasema Jason Washington na Moshe Levine akavuta pumzi ndefu “Jason kwa mara ya kwanza leo umenisikitisha sana.Siamini kama kweli CIA wako tayari kumuona Ammar Nazari akiendelea kufanya mashambulio katika ardhi ya Israel na kumwaga damu ya watu wasio na hatia” akasema Moshe “Moshe nimejitahidi sana kukuelewesha kuhusu umuhimu wa Ammar na ninaomba uyazingatie yale niliyokueleza.Tunafuatilia kwa makini sana jambo hili hivyo msijaribu kufanya kitu chochote kwa siri” akasema Jason na kukata simu.Moshe akakasirika na kugonga meza kwa hasira. “CIA ni washirika wetu wakubwa sana lakini leo nimeshangaa kwa matamshi ya Jason kwamba wako tayari Ammar aendelee kumwaga damu ya waisrael ili kulinda misheni yao.Siko tayari kwa hilo .Siko tayari kumuona Ammar akiendelea kutamba akimwaga damu za waisrael” akawaza Moshe na kuinua mkono wa simu akampigia katibu muhtasi wake “Naomba niletee faili la Mansur Al Mustapha” akasema Moshe.Baada ya muda katibu muhtasi akaingia na kumletea Moshe faili la Mansur Al Mustapha.Akalifungua faili lile akaanza kupitia ukurasa baada ya ukurasa.Alilifunika faili lile akaegemea kiti chake akafikiri kwa muda halafu akachukua lile faili akaelekea lilipo gari lake akampa maelekezo dereva sehemu wanakoelekea. Kutoka makao makuu ya Mossad Moshe alielekea hadi katika gereza moja kubwa wanakofungwa watu wenye makosa makubwa ya mauaji na magaidi ambako alitumia kama nusu saa kisha akatoka na kuelekea katika ubalozi wa Marekani ulioko jijini Jerusalem.Balozi wa Marekani nchini Israel Sarah Howard akajulishwa ujio ule wa mkurugenzi wa Mossad na akaelekeza akaribishwe ofisini kwake.Moshe akakaribishwa ofisini kwa balozi “Moshe karibu sana”akasema Sarah “Ahsante sana Sarah.Habari za hapa? “Nzuri kabisa.Nimestushwa kidogo na ujio wako huu wa ghafla” akasema Sarah “Usihofu mheshimiwa balozi nimekuja kwa dharura kuna kitu nataka kuzungumza nawe” akasema Moshe “Moshe unazidi kunipa hofu na ujio wako huu.Kuna tatizo gani?akauliza balozi Sarah “Miaka mitatu iliyopita ubalozi wa Marekani hapa Jerusalem ulilipuliwa kwa bomu na takribani watu sabini waliokuwa wakifanyakazi katika ubalozi huo waliuawa na mmoja wa watu waliouawa katika shambulio lile ni mumeo Mike Howard” akasema Moshe na sura ya Sarah ikabadilika ghafla.Alikumbushwa mbali sana kwani wakati shambulio lile linatokea yeye ndiye aliyekuwa balozi na kwa wakati huo hakuwepo lakini mume wake ambaye naye alikuwa ni mfanyakazi wa ubalozi huo aliuawa. “Moshe sipendi sana kukumbushwa kuhusu jambo hilo kwani bado kidonda chake hakijapona.Nini hasa kimekuleta hapa kwangu?Kama kuna kitu kingine kimekuleta nieleze tafadhali na tusizungumzie suala la yale mauaji” akasema balozi Sarah. “Mheshimiwa balozi kilichonileta hapa kwako ni hicho.Nataka tuzungumzie tukio lile.Nafahamu nimekukumbusha mbali lakini utanisamehe.” Akasema Moshe na kunyamaza kimya “Toka tukio lile lilipotokea bado mpaka leo hii muhusika mkuu wa shambulio lile hajapatikana.Najua ungetamani sana kumuona mtu aliyefanya unyama ule akipatikana na haki kutendeka” akasema Moshe “Ni Mungu pekee anayejua ni mateso gani niliyoyapita na ninayoyapitia kwa kifo cha mpenzi wangu Mike.Alikuwa ni kila kitu kwangu na pengo lake halitazibika.Kingine kinachoniumiza ni kwamba kama ningekuwepo ofisini siku ile na mimi pia ningekuwa katika orodha ya waliofariki.Nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara kujua kama waliotekekelza shambulio lile wamekamatwa lakini mpaka leo hi hawajakamatwa.Hili linaniumiza sana” akasema balozi Sarah Howard.Baada ya muda mfupi Moshe akasema “Mossad tunamfahamu aliyefanya shambulio lile” “Mnamfahamu?akauliza Sarah kwa mshangao “Ndiyo tunamfahamu” “Mungu wangu ! kwa muda huu wote tumekuwa tukimsaka mshambulaji huyo kwa nini hamjatupa taarifa?akauliza Sarah “Muuaji huyo amefungwa katika gereza moja hapa Israel kwa makosa hayo hayo ya mauaji.Ni mtu muhimu sana kwetu hivyo hatuwezi kumkabidhi kwa Marekani” “Marekani na Israel tumekuwa na mashirikiano makubwa hasa linapokuja suala la kupambana na ugaidi.Moshe tafadhali naomba mtu huyo akabidhiwe kwa Marekani ili aweze kupatiwa adhabu stahiki kwani mauaji aliyoyafanya ni ya kinyama sana” akasema Sarah “Sarah ni kweli ulichokisema kwamba Marekani na Israel tumekuwa na mashirikiano makubwa hasa linapokuja suala la kupambana na ugaidi.Lakini kuna sababu kwa nini hatujawajulisha CIA kuhusu kukamatwa kwa mtu aliyefanya shambulio lile baya.Hata hivyo nimekuja kwako kukupa taarifa hii kwa kuwa nina hakika una kisasi na huyo mtu na ungependa kumuona akipata adhabu stahiki” akasema Moshe “Sijakuelewa Moshe unamaanisha nini? “Kuna kitu nakihitaji hivyo kama ukinisaidia kukipata basi nitakupatia huyo muuaji” akasema Moshe na balozi Sarah akapiga piga kalamu katika meza yake “Unataka nini Moshe? ` “Nataka kupata orodha ya majasusi wa siri wa Marekani walioko hapa Israel na Palestina na misheni zao” akasema Moshe.Balozi Sarah alistuka sana “Unataka orodha ya majasusi wa Marekani? “Ndiyo” “Kwa nini? “Sarah sitaki kuzungumza kwa undani suala hilo lakini kama unataka kuiona haki ikitendeka kwa mtu aliyemuua mume wako na watu wengine basi nisaidie niweze kupata hiyo orodha” akasema Moshe na Sarah akasimama “Moshe hilo nijambo lisilowezekana.Hayo ni mambo ya siri kubwa na mimi sina uwezo wa kuyapata na hata kama ningekuwa na orodha hiyo siwezi kukupatia” “Sarah naomba nikuweke wazi kwamba Mossad haina lengo baya na orodha ya majasusi hao.Labda nikueleze japo kidogo kwa nini ninataka orodha hiyo.Umesikia shambulio lililotokea leo asubuhi katika kituo cha treni na kuua watu wengi.Aliyetekeleza shambulio lile anaitwa Ammar Nazari.CIA wana taarifa za mahala alipo Ammar Nazari.Nimezungumza na mkurugenzi mkuu wa CIA nikamuomba anisaidie kujua mahala alipo Ammar lakini alikataa kwa madai kwamba kuna jasusi wa siri wa CIA yuko katika kundi hilo la Ammar akitekeleza misheni maalum.Sisi pia tuna mtu wetu ndani ya kundi hilo lakini tumepoteza mawasiliano naye na hatujui kama bado yuko hai hivyo tunataka kumtumia jasusi huyo wa CIA kuweza kujua kama mtu wetu huyo yuko hai.Jambo lingine ni kwamba jeshi la Israel linajiandaa kufanya mashambulizi ya anga katika kambi mbali mbali za wanamgambo na kuna hatari mojawapo ya kambi hizo ni ya Ammar hivyo basi maisha ya jasusi wa CIA yako hatarini.Ninataka kuokoa maisha yake kabla majeshi yetu hayajaanza kufanya mashambulizi” akasema Moshe.Sarah akafikiri kidogo na kusema “Kama mkurugenzi wa CIA alikataa kukupa orodha hiyo basi kuna sababu ya msingi sana halafu mambo kama haya ni ya siri kubwa” “Nalifahamu hilo Sarah ndiyo maana nimekufuata wewe” akasema Moshe.Sarah akafikiri na kusema “Moshe natamani sana kama ningeweza kuipata orodha hiyo unayoitaka lakini sina uwezo wa kuipata”akasema Sarah “Unao uwezo wa kuipata taarifa hiyo Sarah.Naamini unao watu ndani ya CIA ambao unaweza ukawatumia kuipata taarifa hiyo na mimi nikakubabidhi mtu huyo ambaye unaweza ukamfanya unachokitaka” akasema Moshe na kumfanya balozi Sarah azame mawazoni.Moshe akafungua mkoba wake na kutoa faili akaliweka mezani “Huyo ndiye aliyelipua ubalozi wa Marekani na ndiye aliyemuua mumeo” akasema Moshe na Sarah akalifungua faili lile akaanza kulipitia.Kila alivyofungua ukurasa sura yake ilizidi kubadilika “Mtu huyu aliwahi kufanya kazi CIA?akauliza Sarah kwa mshangao “Ndiyo alikuwa ni jasusi wa CIA.Nilifanya naye mahojiano kabla ya kuja hapa” akasema Moshe na kutoa diski mweko(flash disc) akampa Sarah ambaye aliichomeka katika kompyuta yake na kuanza kuangalia mahojiano ya Moshe na mtu ambaye alilipua ubalozi wa Marekani Video ilianza kwa Moshe kuonekana peke yake ndani ya chumba lakini baada ya dakika chache akaingia mtu mmoja aliyekuwa amefungwa pingu miguu na mikono akaketi kitini na Moshe akaanza kumuhoji “Mansur Al Mustapha” akasema Moshe “Unaendeleaje?Vipi maisha ya gerezani?akauliza.Mansur akamtazama kwa macho yaliyojaa hasira kubwa. “Kitu gani kimekuleta hapa? Akauliza Mansur “Mansur nimekuja hapa kuzungumza nawe jambo muhimu sana” “Mimi nawe hatuna cha kuzungumza” “Tunacho cha kuzungumza” akasema Moshe na kunyamaza akamtazama Mansur kwa makini kisha akasema “Muda mfupi kabla ya kuja hapa nimetoka kuzungumza na mkurugenzi mkuu wa CIA Jason Washington.Kuna taarifa nyeti sana nilikuwa nazihitaji kutoka kwake na hakuwa tayari kunipatia taarifa hizo vivyo nikamuahidi kumpatia kitu chenye thamani kubwa ili anipe taarifa hiyo.Bado sijamwambia kama kitu hicho ninachotaka kumpatia ni wewe” akasema Moshe na kumtazama tena Mansur kwa sekunde kadhaa “Marekani wanakutafuta sana ila hawajui kama umefungwa hapa.Ninataka nikukabidhi kwa Marekani lakini kabla sijafanya hivyo nimeona nije nizungumze nawe kwanza” akasema Moshe “Unataka nini kutoka kwangu?akauliza Mansur “Mansur ulikuwa jasusi wa Marekani umefanya kazi CIA kwa muda mrefu ukitumika katika eneo la mashariki ya kati lakini ni wewe ambaye ulilipua ubalozi wa Marekani jijini Jerusalem na kuua watu kadhaa na miononi mwao wapo waisrael.Nataka kujua kwa nini ulibadilika na kushambulia ubalozi wa Marekani?akauliza Moshe Mansur akatazama chini “Najua umeulizwa swali hili mara nyingi na hujawahi kunijbu lakini leo nataka unijibu kwani niko hapa kwa ajili ya kukusaidia” akasema Moshe.Mansur alionekana kukasirishwa na swali lile akamtazama Moshe kwa macho makali kisha akasema “Ndege za marekani ziliangusha bomu katika hoteli ambayo familia yangu walikuwa wamefikia jijini Damascus.Mke wangu na watoto wawili wakafariki dunia.Niliumia mno kwa kitendo hicho ingawa waliomba radhi baadae wakidai ni bahati mbaya lakini baada ya kufuatilia nikagundua haikuwa bahati mbaya kwani kuna mtu walikuwa wamemlenga aliyekuwamo ndani ya ile hoteli ndiyo maana wakailipua.Hiyo ndiyo sababu ya kuamua kulipua ubalozi wa Marekani jijini Jerusalem” akasema Mansur. “Huyo unayemona hapo ndiye Mansur Al Mustafa ambaye alilipua ubalozi wa Marekani na mumeo akafariki” akasema Moshe huku Sarah akiirudia kuitazama video ile “Moshe namuhitaji huyu mtu ! akasema Sarah kwa hasira “Nisaidie niweze kuipata orodha hiyo haraka nami nitakukabidhi mtu huyu” akasema Moshe. Sarah alichukua simu yake akapiga namba Fulani akazungumza na mtu kwa takribani dakika kumi halafu akaombwa asubiri “Kuna mtu wangu yuko makao makuu ya CIA nimezungumza naye anisaidie niweze kuipata taarifa hiyo.Ni mtu mzito hivyo usiwe na wasi wasi.Tuvute subira” akasema Sarah na kuendelea kuitazama video ile ya Moshe na Mansur “Nilikuwa naota siku moja niweze kukutana na muuaji Yule na leo amepatikana” akawaza Sarah akiuma meno kwa hasira. Zilipita dakika kumi ofisi ikiwa kimya simu ya sarah ikaita akaipokea akapewa maelekezo Fulani halafu akafungua katika barua pepe yake na kukuta kuna ujumbe katumiwa akaufungua akausoma.Ilikuwa ni orodha ya majasusi wa Marekani walioko katika nchi za Israel,Palestina,Misri,Iran,Ir aq,Syria na Jordan. “Tayari nimeipata orodha hiyo lakini sintakupatia hadi pale nitakapokuwa nimemtia mikononi muuaji wa mume wangu” akasema Sarah “Usiwe na shaka.Nitakupeleka kwenda kumuona mtu huyo kisha utaamua mwenyewe umfanye nini” akasema Moshe wakatoka na kuingia katika gari la Moshe wakaelekea katika gereza alikofungwa Mansur. “Tumefika gerezani.Hapa ndipo alipofingwa mtu huyo” akasema Moshe.Sarah akavuta pumzi ndefu halafu akasema “Moshe mtu huyo nataka nimhukumu mimi mwenyewe” akasema Sarah. “Usihofu kuhusu hilo” akasema Moshe.Waliingia ndani ya gereza wakasalimiana na mkuu wa gereza.Moshe akazungumza naye kwa muda muda na mkuu wa gereza akatoa maelekezo.Mansur akatolewa ndani ya gereza akiwa amefunikwa mfuko kichwani akaingizwa katika gari la Moshe wakaondoka.Hakukuwa na mazungumzo garini.Sarah alikuwa anafuta machozi mara kwa mara.Kitendo cha kukutana na mtu aliyemuua mume wake kilimuumiza sana. Walifika katika nyumba Fulani akapiga honi na geti likafunguliwa wakaingia ndani.Moshe akatoa maelekezo Mansur akatolewa garini akaingizwa katika chumba maalum. “Sarah hapa ni nyumba yetu ya mahojiano.Ni sehemu ya mateso.Hapa ndipo utakapotoa hukumu yako kwa mtu aliyemuua mumeo.Kuna mabadiliko yoyote?akauliza Moshe “Siwezi kubadilisha mawazo yangu Moshe.Ninataka kumuhukumu kwa mkono wangu”akasema Sarah na Moshe akamuongoza hadi katika chumba maalum ambacho Mansurhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ alikuwa amewekwa.Moshe akautoa ule mfuko kichwani kwa Mansur kisha akasogea pembeni akamuacha Sarah akiwa amesimama karibu na Mansur.Uso wake ulijaa hasira “Mansur Al Mustafa.Miaka mitatu iliyopita ulilipua ubalozi wa Marekani na kuua watu wengi miongoni mwa watu waliouawa alikuwepo pia mume wangu.Baada ya kukutafuta kwa muda mrefu hatimaye leo umepatikana.Sintakupeleka Marekani nitakuhukumu hapa hapa kwa mkono wangu”akasema Sarah huku akielekea katika meza iliyokuwa na vifaa vingi vya kutesea. “Sarah kabla hujaendelea na zoezi naiomba kwanza ile orodha” akasema Moshe.Sarah akachukua kompyuta yake na kumtumia Moshe ile orodha. “Sasa unaweza kuendelea” akasema Moshe baada ya kuhakikisha ameipata orodha ile na kuituma kwa katibu wake muhtasi ili kuipitia Sarah akachukua kisu kikali na kumfuata Mansur akamuamuru asimame lakini Mansur akagoma.Sara akainua kiti na kumpiga nacho kichwani Mansur akaanguka chini na damu zikaanza kumtoka kichwani mahala alikochanika.Moshe akamfuata akamuinua na sara kwa kutumia kile kisu kikali akaichana chana nguo aliyokuwa ameivaa Mansuri akabaki mtupu “Unataka kunifanya nini kahaba wewe?! Akauliza Mansur na kumtemea mate Sarah ambaye alipandwa na hasira zaidi na kukipisha kisu kile kikali kwa nguvu katika uume wa Mansur ukaanguka chini.Mansur akapiga kelele kubwa.Sarah akazidi kupandwa na hasira akamfuata pale chini akamkalia kifuani. “Uliwaua watu bila huruma na leo ni zamu yako kupata mateso waliyoyapata ! akasema Sarah na kukiingiza kisu kile mdomoni akamkata ulimi.Kama hiyo haitoshi akaanza kumchoma choma na kisu kile usoni akamtoboa ,macho yote mawili.Ndani ya muda mfupi Mansur hakuwa akitazamika. “Nipe bastora! Akasema Sarah na Moshe akampa bastora iliyokuwa na kiwambo cha sauti akaanza kummiminia risasi Mansur hadi zilipokwisha kwenye bastora.Tayari Mansur hakuwa na uhai tena.Akamtazama kwa hasira “Natumai umekwisha kutana na wale wote uliowakatili uhai kikatili shetani we! akasema Sarah.Alikuwa amechafuka damu mwili mzima “Moshe ahsante.Huko aliko mume wangu atafurahi nimemlipia kisasi.Sasa nina amani.Nipeleke nyumbani kwangu” akasema Sarah.Moshe akamuingiza katika chumba kingine kwa ajili ya kunawa kuondoa damu zilizotapaka kila sehemu mwilini.Moshe akatoa maelekezo ya kufanyiwa usafi mle chumbani wakaondoka hadi nyumbani kwa balozi Sarah wakaagana “Moshe suala hili ni siri kubwa kati yetu tafadhali asifahamu mtu yeyote” akasema Sarah akashuka garini na kuingia ndani.Moshe akaondoka kurejea makao makuu.Aliitisha kikao cha dharura cha wakuu wa idara ndani ya Mossad na kuwapa taarifa za kupatikana kwa orodha ile ya majasusi wa siri.Bila kupoteza muda wakaanza kuipitia orodha ile na kumpata jasusi aitwaye Nawal Hashim ambaye alipandikizwa na CIA katika kikundi cha Ammar RAMALLAH Kuonyesha furaha kubwa aliyokuwa nayo baada ya shambulio la bomu kufanikiwa katika jiji la Jerusalem Ammar Nazari alichinja ngamia wawili na kufurahi pamoja na watu wake.Kilipikwa chakula kizuri na watu walikula nyama huku ngoma zikipigwa na kucheza kufuraha kitendo kile cha kinyama ambacho wao walikiona ni kitendo cha kishujaa.Mathew Mulumbi ambaye ndiye aliyelipua lile bomu alipongezwa sana na wenzake wakimuita shujaa. Wakati sherehe zikiendelea Nawal aliyekuwa na wanawake wengine wakipika chakula,simu yake ikaita akaitoa katika gauni lake refu alilovaa na kutazama mpigaji.Zilikuwa ni namba ngeni.Kutokana na kuwepo kwa kelele nyingi za muziki na ngoma akasogea pembeni akaipokea ile simu “Hallow nani mwenzangu?akauliza “Nawal tafadhali naomba kama uko karibu na watu usionyeshe mstuko wowote sogea pembeni kuna jambo la muhimu nataka kuzungumza nawe” ikasema sauti ya kiume upande wa pili “Wewe ni nani unataka nini? “Naitwa Moshe Levine mkurugenzi mkuu wa shirika la ujasusi la Israel Mossad” “Kwa nini umenipigia?Umepata wapi namba yangu ya simu?akauliza Nawal kwa wasiwasi.Alishtuka sana “Nawal tunafahamu wewe ni jasusi wa CIA na uko hapo katika kundi la Ammar Nazari brigades kwa misheni maalum” akasema Moshe na kuzidi kumshangaza Nawal “Nashindwa kukuelewa.Tafadhali umekosea namba”akasema Nawal “Usikate simu tafadhali.Naomba unisikilize.Asubuhi ya leo kumefanyika shambulio la bomu katika kituo kikuu cha treni na watu wengi wamepoteza maisha shambulio ambalo limetekelezwa na kikundi cha Ammar Nazari brigades na Ammar ametishia kuendeleza mashambulizi zaidi.Tayari tumekwisha gundua mahala alipo Ammar na hivi ninavyozungumza nawe jeshila anga la Israel linajiandaa kufanya shambulio kubwa sana hapo katika makazi ya Ammar.Tunafahamu wewe ni jasusi wa CIA hivyo tunataka kukuokoa.Hivi sasa ndege ziko angani na ninakupa dakika ishirini tu za kuondoka mahala hapo kabla ya eneo hilo kugeuzwa juu chini kwa mabomu mazito” akasema Moshe na Nawal akatazama angani “Kwa nini CIA wasinipigie wanijulishe kama kuna jambo hilo?akauliza Nawal huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio “CIA hawajui chochote kuhusu shambulio hilo” “Kama hujaelezwa na CIA umefahamuje kuhusu mimi? Akauliza Nawal “Nawal hatuna muda wa kupoteza.Tafadhali fanya kile ninachokueleza.Shambulio kubwa litafanyika hapo muda si mrefu.Ondoka hapo haraka sana” akasema Moshe na kukata simu.Nawal alichanganyikiwa. “Misheni yangu imeharibika na siwezi tena kumpata mtu ambaye nilikuwa nikimsaka kwa muda huu wote niliokuwa hapa.Nimeumia sana lakini ngoja kwanza nifanye jitihada za kujiokoa kisha nitajua kitakachoendelea.Natakiwa pia kumuokoa Abu siwezi kumuacha hapa” akawaza Nawal na kuelekea mahala ambako wanamgambo walikuwa wakicheza ngoma huku Ammar na Mathew wakishangilia.Nawal akamfuata Ammar akamnong’oneza kitu halafu Ammar akamshika Mathew bega akamtaka waondoke.Nawal aliwaongoza hadi katika kijichumba kidogo ambacho Ammar hukitumia kwa mazungumzo ya faragha “Nawal kuna nini mbona umetuleta humu?akauliza Ammar huku akitabasamu.Nawal akaufunga mlango halafu akamwambia Ammar ampatie bastora yake.Ammar huku bado akishangaa akatoa bastora na kumpatia Nawal “Nawal kuna nini?Mbona sikuelewei?akauliza Ammar “Ammar nimekuleta hapa kuna jambo ambalo nataka ulifahamu” “Jambo gani Nawal?akauliza Ammar “Kuhusu mimi” “Kuhusu wewe?akauliza Ammar kwa mshangao “Huyu Nawal anataka kufanya kitu gani tena? Anataka kumweleza Ammar ukweli yeye ni nani? Mathew akajiuliza “Kwa muda wote tuliokaa wote nikiwa mke wako hujafanikiwa kunifahamu lakini mimi ni jasusi wa CIA na niko hapa kwa misheni maalum” “Nawal ! akasema Mathew “Abu nyamaza ! akafoka Nawal.Sura ya Ammar ilibadilika “Sijakuelewa Nawal ! akasema Ammar huku sauti yake ikiwa na kitetemeshi ndani yake “Nimekwambia mimi ni jasusi kutoka shirila la ujasusi la Marekani CIA na niko hapa kwa misheni maalum” akasema Nawal na Ammar akamtazama kwa macho makali yaliyoonyesha ukatili mkubwa. “Nawal haya unayonieleza ni ya kweli?akauliza “Ndiyo.Mimi ni CIA” akajibu Nawal na ghafla Ammar akachomoa kisu na kutaka kumrushia Nawal lakini Mathew aliyekuwa karibu yake akamuwahi akamrukia na kumuangusha chini akamtandika ngumi mfululizo uso wa Ammar ukaloa damu. “Abu zalawi kwa nini unanifanyia hivi? Unaungana na huyu shetani?akauliza Ammar na Mathew akamtandika ngumi nyingine nzito kisha akainuka.Nawal akakichukua kile kisu cha Ammar “Shetani ni wewe ambaye umeua watu wengi bila huruma na sasa ni zamu yako” akasema Nawal na kukizamisha kile kisu shingoni mwa Ammar akakichomoa na kukichoma tena halafu akachoma kifuani mahala ulipo moyo.Mathew alikuwa amesimama akiangalia “Kwa nini umemuua?akauliza Mathew lakini Nawali hakumjibu akampatia kisu “Mkate kichwa haraka sana! Akasema Nawal na Mathew akafanya kama alivyoelekezwa akamkata Ammar kichwa chake “Huu ndio mwisho wa Ammar Nazari brigades” akasema Nawal halafu akachukua simu yake na kuupiga picha mwili wa Ammar “Sasa ni wakati wa kuondoka mahala hapa” “Tunakwenda wapi? “Abu sitaki maswali nataka ufuate maelekezo yangu” akasema Nawal Mathew akajifuta damu mikononi halafu wakatoka hadi chumbani kwa Ammar na kuchukua simu pamoja na kitabu chenye jalada gumu jekundu ambacho Ammar hukitumia kuhifadhi kumbu kumbu zake muhimu.Wakachukua pia bastora kadhaa “Tuondoke” akasema Nawal wakaingia katika gari dogo la Nawal alilopewa zawadi na Ammar wakaondoka.Geti la kuingilia katika makazi ya Ammar likafunguliwa na gari la Nawal likatoka.Hakuna aliyemuuliza chochote kwani wanalifahamu gari lile. “Nawal umenishangaza sana.Nini kimesababisha ukafanya vile?Kwa nini umeamua kumuua Ammar?Tunaelekea wapi?akauliza Mathew wakiwa garini lakini Nawal hakumjbu kitu akaongeza mwendo wa gari Dakika chache baada ya kuondoka katika makazi yale ya Ammar simu ya Nawal ikaita,akaitambua namba ile ilikuwa ni ya Moshe Levine,akasimamisha gari na kuipokea simu “Nawal tayari umekwisha ondoka?akauliza “Ndiyo nimekwisha ondoka” “Naomba unithibitishe kwamba Ammar yuko katika makazi yake” “Ndiyo nimemuacha pale,wanasherehekea mafanikio ya shambulio lile walilolifanya leo ” akasema Nawal “Nawal nilisahau kukuuliza pale awali.Kuna mtu anaitwa Abi Al Zalawi umewahi kumuona? Alitoroka gerezani akiwa na Ammar” akauliza Moshe na Nawal akageuka kumtazama Mathew “Hapana sijawahi kumuona huyo mtu” akajibu Nawal “Ahsante Nawal.Kama kuna msaada wowote utauhitaji tafadhali nijulishe lakini usirejee tena katika makazi yale ya Ammar kwani muda mfupi ujao eneo lote hakutakuwa na makazi tena” akasema Moshe na kukata simu.Nawal akawasha gari safari ikaendelea “Ulikuwa unazungumza na nani?akauliza Mathew “Nitakueleza kila kitu lakini kwa sasa kuna kitu ambacho tunatakiwa kukishuhudia” akasema Nawal akazima gari wakashuka na kupanda katika kilima kidogo na kutazama walikotoka “Tunatazama nini Nawal?Mathew akauliza lakini Nawal hakumjibu kitu Baada ya dakika mbili moshi mkubwa mweusi ukaanza kuonekana angani na kwa mbali kishindo cha milipuko ya mabomu kikasikika “Israel wameshambulia kambi ya Ammar Nazari brigades.Huu ndio mwisho wa kikundi hiki” akasema Nawal na Mathew akashangaa “Israel wamefahamuje mahala alipo Ammar?akauliza Mathew “Niliyekuwa nazungumza naye simuni ni Moshe Levine mkurugnzi wa Mossad ambaye alinipigia simu na kunitaka niondoke mahala pale haraka sana kwani majeshi ya Israel yanategemea kufanya shambulio” “Moshe ndiye aliyekupigia simu?Mossad wamefahamuje kuhusu wewe? Wamejulishwa na CIA?akauliza Mathew “Kwa mujibu wa Moshe Levine CIA hawajui chochote kuhusiana na hiki walichokifanya Israel.Sifahamu wamewezaje kupata namba yangu ya simu”akasema Nawal “Wamekuuliza chochote kuhusu mimi? “Ndiyo lakini nimemdanganya.Nimemwam bia kwamba sijawahi kukuona.Mossad hawana mpango nawe tena na walitaka ufe katika mashambulio yale” akasema Nawal na ukimya mfupi ukapita “Kwa sasa tunaelekea wapi ? Akauliza Mathew “Misheni yangu ya kumtafuta Abdul Yasin Al Nasser tayari imevurugika.Natakiwa kuwajulisha CIA kuhusu kuvurugika kwa misheni yangu ili wanipe maelekezo mengine.Kuhusu wewe nitakusaidia uweze kufika kwa Habiba Jawad na ukamilishe misheni yako” akasema Nawal “Unafahamu alipo Habiba Jawad?akauliza Mathew “Sifahamu alipo lakini hapa tunayo simu ya Ammar na hiki kitabu ambacho huandika mambo yake ya muhimu.Naamini tunaweza kupata taarifa muhimu kuhusu Habiba Jawad” akasema Nawal “Nawal nina wazo”akasema Mathew na kunyamaza baada ya kishindo kikubwa kusikika.Mashambulizi ya mabomu yaliendelea katika kambi ya Ammar “Una wazo gani Abu?akauliza Nawal “Habiba Jawad amekuwa ndiye mfadhili mkuu wa makundi haya ya wanamgambo na magaidi na ninaamini lazima atakuwa anamfahamu Abdul Yasin Al Nasser.Tujitahidi kufanya kila linalowezekana tuweze kufika kwa Habiba” akasema Mathew “Ni wazo zuri lakini kabla ya kufanya chochote lazima kwanza niwajulishe CIA kile kilichotokea” akasema Nawal na kupiga makao makuu ya CIA akawajulisha kilichotokea.CIA walimtaka aende haraka sana katika ubalozi wa Marekani nchini Israel ulioko katika jiji la Jerusalem. “Jambo hili lililofanywa na Mossad kumuua Ammar limewashangaza sana CIA hawakuwa wamelitegemea.Hata hivyo wamenitaka niende katika ubalozi wa Marekani Jerusalem lakini sintaenda huko tunaendelea na operesheni yetu lazima tufike kwa Habiba Jawad” akasema Nawal DAR ES SALAAM – TANZANIA Wakati taarifa ya kuanguka kwa ndege ya shirika la ndege la Misri na kuua abiria wote waliokuwemo ndani yake zikiendelea kusambaa kwa kasi duniani kote,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo alikuwa ofisini kwake amechanganyikiwa.Kilichom canganya ni kuliona jina la Ruby Rafael Magalla katika orodha ya abiria waliokuwemo ndegeni.Alijaribu kumpigia Austin lakini simu iliita bila kupokelewa.Akiwa amejawa na mawazo mengi simu yake ikaita zilikuwa ni namba ngeni zilizotoka nje ya nchi akaipokea “Hallow” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais unazungumza na Ruby” “Ruby?! Akashangaa Dr Fabian na kusimama. “Ruby ni wewe kweli? “Ndiyo mheshimiwa Rais ni mimi”akasema Ruby na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu na kuinua mkono juu “Mungu wangu kweli una nguvu.Ahsante baba” akasema kwa sauti ndogo “Ruby nimeliona jina lako katika orodha ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege iliyoanguka ya shirika la ndege la Misri na kuua watu wote.Nilikuwa nimechanganyikiwa sikujua nifanye nini” “Mheshimiwa Rais ni kweli jina langu limo katika orodha ya watu waliofariki katika ajali ile lakini sikuwamo ndani ya ndege.Mheshimiwa Rais nimekupigia kukujulisha kwamba niko salama” “Uko wapi kwa sasa? “Mheshimiwa rais kwa sasa siwezi kukueleza niko wapi kwa ajili ya usalama wangu lakini naomba ufahamu kwamba niko salama na sijafa.Niko katika safari yangu ya kuja huko.Siwezi kukueleza nitafika lini lakini naomba uamini nitafika huko” akasema Ruby “Ruby tafadhali naomba unieleze kama kuna kitu chochote ninaweza kukusaidia.Ninaweza kutuma ndege ije ikuchukue mahala ulipo” “Ninashukuru sana mheshimiwa Rais ninafahamu unaweza kunisaidia lakini kwa sasa usihofi nitakuwa salama.Nitakujulisha pale nitakapohitaji msaada wowote.Ninachokuomba suala hili liwe ni siri yako kubwa.Usimueleze mtu yeyote kama nimekupigia simu niko hai.” akasema Ruby “Ruby kwa nini nisitume ndege ikaja kukuchukua mahal aulipo? Kama ni usalama niko tayari kutuma kikosi maalum kuhakikisha una kuwa salama” “Usihofu mheshimiwa Rais.Hakuna ulazima wa kutuma kikosi wala ndege.Ninakuja Tanzania lakini itanichukua muda kidogo ila fahamu kwamba nitafika niko njiani.Kwa heri kwa sasa mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kukata simu Dr Fabian akashusha pumzi baada ya Ruby kukata simu “Nini kimetokea hadi jina la Ruby likaonekana katika orodha ya watu waliofariki katika ajali ya ndege lakini hajafa? Nahisi Ruby atakuwa katika hatari lakini kwa nini hakunipa nafasi nimsaidie? Ningeweza kumtumia ndege mahala alipo pamoja na ulinzi ili kuhakikisha anakuwa salama lakini vyote hivyo amevikataa.Ngoja niendelee kumsubiri hadi atakapofika kama alivyoahidi yeye mwenyewe naamini anayo siri kubwa.Mungu amlinde katika safari yake hii ya hatari” akawaza Dr Fabian PARIS – UFARANSA “Ruby uko tayari kwa safari?akauliza Joseph ambaye ndiye aliyempokea Ruby jijini Paris. “Niko tayari tunaweza kuondoka” akajibu Ruby Waliingia katika gari na kuondoka kuelekea katika bandari ya Le havre “Ruby utanisamehe kwa usafiri huu utakaoutumia kwani ndio ambao nimeweza kuupata kwa haraka lakini ndio usafiri salama.Itakuchukua muda mrefu kidogo kufka Tanzania ila naamini utafika salama kuliko kama ungetumia usafiri wa ndege”akasema Joseph “Usijali Joseph.Ninakushukuru sana kwa msaada huu mkubwa ulionisaidia.Nimeupenda usafiri huu kwani ni salama zaidi kwangu kwa sasa” akasema Ruby “Nahodha wa meli utakayoondoka nayo ni ndugu yangu hivyo atahakikisha unakuwa salama na unafika salama huko uendako” akasema Joseph Iliwachukua saa mbili kufika katika bandari ya Le havre.Meli ambayo alitakiwa kuondoka nayo Ruby tayari ilikwisha pakia mzigo na aliyekuwa akisubiriwa ni Ruby ili waanze safari. Joseph alimkabidhi Ruby kwa nahodha wa meli ile kubwa ya mizigo wakaagana na Ruby akaingizwa melini.Safari ya kuelekea Afrika ikaanza. “Kwa heri Ulaya.Ninarejea katika nchi yangu ambako nitatumia ujuzi na maarifa yangu yote kuitumikia kuliko kuwatumikia watu hawa ambao nimewafanyia kazi kwa uaminifu mkubwa kwa muda mrefu lakini hawajauthamini mchango wangu kwao na badala yake wanataka kuniua.Huko waliko wanaamini kwamba tayari nimekwisha kufa na lengo lao limetimia.Namshukuru sana Joe ambaye ndiye aliyenisaidia hadi nimefika hapa.Sikujua kama kuna mpango wowote unaandaliwa wa kuniua lakini ni yeye ambaye alinidokeza uwepo kwa mpango huo na akajitolea maisha yake kunisaidia nikaweza kuukwepa mtego ule na na endapo wakigundua kwamba yeye ndiye aliyenisaidia nikatoroka lazima watamuua.Namuomba Mungu amsaidie aweze kuwa salama.Safari hii ya majini ni safari ndefu lakini nitavumilia kwani ndiyo njia pekee salama kwa mimi kufika Tanzania kuliko kama ningetumia ndege.Nitavumilia” akawaza Ruby akiwa amepumzika katika chumba chake alichopewa ndani ya meli ile kubwa ya mizigo



Geti la kuingilia katika jumba kubwa la bilionea Peniela lilifunguliwa na gari moja likaingia.Watu wawili wakashuka toka ndani ya gari lile la kifahari wakapokewa na Dinah ambaye ndiye mratibu wa shughuli zote za Peniela.Aliwakaribisha katika sebule kubwa na nzuri ambayo Peniela huitumia kukutana na wageni wake wa muhimu.Muhudumu alifika haraka na kuwahudumia wageni vinywaji .Wakati wageni wale wakiendelea na mazungumzo na Dinah akaingia Peniela ambaye jioni hii alikuwa amevaa suruali nyeusi na shati laini rangi nyeusi vile vile. “Karibuni wageni”akasema Peniela na kuwakaribisha wageni wake “Tunashukuru sana” wakasema wageni wale “Jamani wageni wetu huyu ndiye bilionea Peniela” akasema Dinah “Tunafutahi kukufahamu.Mimi nilizoea kukuona katika picha magazetini ni furaha yangu leo nimekutana nawe ana kwa ana.U mrembo sana” akasema mmoja wa wageni wale na Peniela akatabasamu “Peniela hawa ndio wale wageni wako niliokueleza.Yule pale anaitwa Devotha Adolph na huyu malaika hapa anaitwa Melanie David” akasema Dinah “Nimefurahi sana kukutana nanyi jamani karibuni sana.Dinah aliniambia kwamba mlitaka kuonana nami wiki iliyopita lakini niliomba tuvute muda kidogo kwani nilikuwa na matatizo.Nilivamiwa na watu wasiojulikana na walinzi wangu wakauawa” “Pole sana” wakasema Melanie na Devotha “Ahsanteni sana” akasema Peniela “Niliambiwa kuna jambo la muhimu mnataka kujadiliana nami” akasema Peniela “Ndiyo madam kuna jambo limetuleta hapa kwako.Nisiwe mzungumzaji mkubwa nimuachie muhusika mkuu ambaye ni huyu Melanie aweze kuzungumza nawe”akasema Devotha “Naitwa Melanie Davis kama nilivyojitambulisha.Ni mtoto wa pekee kwa wazazi wangu ambao wote wamekwisha tangulia mbele za haki” “Pole sana” akasema Peniela “Ahsante sana” “Wazazi wangu wanatokea jamhuri ya kidemokrasia ya Congo” “Ouh kumbe wanatokea Afrika Mashariki” akasema Peniela huku akitabsamu “Ndiyo wanatokea Afika mashariki ndiyo maana unaniona ninaweza kuzungumza Kiswahili vizuri.Walikuwa wafanya biashara na makazi yao yalikuwa Ufaransa lakini mimi nimesoma elimu yangu ya juu nchini Tanzania katika chuo kikuu cha Dar es salaam.Ninaipenda sana Tanzania” akasema Melanie. “Nimefurahi kusikia umesoma Tanzania.Mimi pia ni mtanzania japo kwa sasa nina uraia wa Ufaransa na kama unavyofahamu kwamba nchi yetu haikubali uraia wa nchi mbili.Niliamua kuukana uraia wangu wa kuzaliwa kwa sababu mbali mbali za kiuchumi.Devotha nawe unatokea wapi?Manake unazungumza Kiswahili safi kabisa” “Mimi pia ni mtanzania lakini nimeishi sana nje ya nchi na kwa sasa makazi yangu ni hapa Paris.Bado sijachukua uraia wa nchi nyingine kwani nina mpango wa kurejea nyumbani siku moja” akasema Devotha na Melanie akaendelea “Wazazi wangu walikuwa wafanya biashara matajiri kama nilivyoeleza.Walipouawa utajiri wote nilirithi mimi.Kwa sasa baada ya kumaliza masomo ninataka kujikita katika kusimamia biashara walizoacha wazee na kuongeza nyingine zaidi.Ninataka kuwekeza katika eneo la Afrika Mashariki ambako nimeziona fursa nyingi za kibiashara.Ninataka kuwekeza sehemu mbali mbali kama vile kwenye madini,biashara za vyakula nakadhalika.Wakati nikifikiria ni wapi nitawekeza nilipata tetesi kwamba kuna mtu anaitwa bilionea Peniela amewekeza sana Afrika Mashariki lakini kwa sasa anataka kuuza baadhi ya mali zake zilizoko Afrika mashariki nikaona hii itakuwa ni fursa nzuri ya kuja kuzungumza nawe kama jambo hili ni la kweli ili niweze kununua mali hizo kuliko kuanza kuwekeza kutoka chini” akasema Melanie.Peniela akanywa funda dogo la kinywaji na kusema “Ni kweli nimewekeza sana Afrika Mashariki.Niliamua kuwekeza sana nyumbani kabla ya kuwekeza nje ya nchi.Katika kusimamia biashara zetu mimi na mume wangu tuligawana yeye akawa anasimamia miradi yetu iliyoko Tanzania na mimi nikawa nasimamia miradi iliyoko Ulaya na Asia.Kwa bahati mbaya mume wangu amefariki miaka mitatu iliyopita na kwa sasa biashara zote zilizoko Tanzania zinasimamiwa na rafiki wa mume wangu anaitwa Papii Gosu Gosu naye ana asili ya Congo.Ninataka kuuza makampuni yangu na biashara zilizoko Tanzania kwani siwezi kusimamia miradi hii yote mingi peke yangu”akasema Peniela “Pole sana kwa kifo cha mumeo” Devotha na Melanie wakasema “Ahsante nimekwisha poa” akajibu Peniela “Kwa hiyo Melanie ni kweli ninauza mali zangu zote zilizoko Tanzania kama utakuwa tayari tunaweza kufanya mazungumzo na nitakupa upendeleo mkubwa wewe kwani kuna wengi wameonyesha nia ya kuzinunua” akasema Peniela “Peniela kama unauza mali zako Tanzania mimi nitazinunua zote tafadhali usimuuzie mtu mwingine mali hizo” akasema Melanie Mazungumzo kati ya Peniela na wageni wake yalikuwa marefu na walipata wote chakula cha usiku pale pale nyumbani.Peniela alimuomba Melanie ampe siku mbili ili aweze kumuita msimamizi mkuu wa mali zake nchini Tanzania pamoja na wanasheria ili waweze kuanza mchakato wa kuuziana mali zile “Sina sababu ya kuendelea kuishi Tanzania.Ni nchi yangu lakini baada ya Mathew kufariki sina hamu tena ya kutia mguu wangu kule ndiyo maana ninataka kuuza biashara zangu zote ili nisiwe na sababu yoyote ya kunipeleka huko.Laiti kungelikuwa na kaburi la Mathew ningekuwa na sababu ya kuendelea kuwekeza lakini hata kaburi lake halipo waliniambia eti mume wangu aliliwa na fisi.Walimuacha akafa kifo cha kinyama sana ndiyo maana wamenifanya niwe na chuki na nchi yangu.Si kwamba biashara hazifanyi vyema kwani yupo Gosu Gosu anasimamia vizuri lakini kila nikikumbuka kuhusu Mathew ninapatwa na hasira nyingi ndiyo maana nataka niuze kila kitu nisiwe na sababu yoyote ya kwenda tena Tanzania” akawaza Peniela akiwa chumbani kwake baada ya akina Melanie kuondoka. “Nakumbuka siku ile kabla ya kuuawa Nahum aliniambia kwamba nimtafute Mathew Mulumbi yuko hai lakini siamini maneno yake.Amefahamu vipi kama Mathew yuko hai?Hajawahi kufika Tanzania na wala hamfahamu Mathew ndiyo maana hata maneno yale nimeyapuuzia.Mathew amekwisha fariki na hakuna namna anayoweza kuwa hai.Nilitumiwa ujumbe na Rais wa Tanzania aliyemaliza muda wake na kujulishwa kwamba Mathew alifariki katika operesheni ya kuwakomboa mateka waliokuwa wametekwa na kikundi cha kigaidi cha IS.Ngoja niachane na hili suala linaweza kuanza kunitoa machozi muda huu” akawaza na kuchukua simu akampigia simu Gosu Gosu akamtaka afanye kila awezalo aende Paris haraka iwezekanavyo RAMALLAH - PALESTINA Mathew Mulumbi na Nawal walikaa chini ya jiwe Nawal akikipitia kitabu kile ambacho Ammar huandika kumbu kumbu zake mbali mbali.Kwa muda wa saa moja toka alipoanza kukipitia kitabu kile hakuwa amepata kitu chochote kinachoweza kuwasaidia kufahamu au kufika kwa Habiba Jawad. “Hakuna kitu cha maana humu.Yote aliyoyaandika ndani ya hiki kitabu ni mambo yanayohusiana na shughuli zinazofanywa na kikundi chake”akasema Nawal na kuzama katika mawazo.Mathew akapanda juu ya mwamba ule na kuangalia kama kuna mtu yeyote anayemfuata na akiwa kule juu akasikia sauti ya Nawal akiimuita akashuka haraka “Kuna nini Nawal?akauliza “Nimekumbuka kitu.Kuna mwanamama mmoja anaitwa Fatma huyu nadhani ni mshirika wa Ammar.NImewahi kufika nyumbani kwake mara mbili nikiwa na Ammar na yeye mwenyewe Fatma amewahi kuja kwetu mara kadhaa.Kila wanapokutana huwa wanazungumza pembeni na hakuna anayejua huwa wanazungumza nini.Nilihisi labda watu wale wana mahusiano ya kimapenzi na Ammar anataka kuoa mke wa tatu lakini akanihakikishia kwamba Fatma ni mshirika wake na hawana mahusiano yoyote.Nadhani Fatma anaweza akatusaidia kufahamu au kumpata mtu anayeweza kufahamu alipo Habiba Jawad” akasema Nawal “Ni wazo zuri sana.Twende tukajaribu” akasema Mathew wakashuka katika mwamba na kuingia ndani ya gari lao safari ikaanza kuelekea Ramallah anakoishi Fatma. “Nawal usijali utampata Abdul Yasin Al Nasser.Nina uhakika mkubwa kama tukifanikiwa kumpata Habiba tutajua mahala alipo Abdul Yasin Al Nasser.Hawa wote mfadhili wao ni mmoja Habiba Jawad” akasema Mathew baada ya kumuona Nawal akiendesha gari lakini akiwa na mawazo mengi “Katika mashambulizi ya mabomu aliyoyafanya Abdul baba yangu pia ni mmoja wa waliouawa hivyo siwezi kuondoka bila kumpata Abdul.Lazima nihakikishe anapatikana”akasema Nawal Safari iliendelea wakaingia katikati ya jiji la Ramallah.Nawal akapunguza mwendo baada ya kuingia katika mtaa Fulani wenye maduka makubwa.Baada ya mwendo wa dakika mbili akakata kulia na kufuata ujia ulio elekea katika geti la rangi ya bluu.Akamtaka Mathew abaki garini akafungua mlango akashuka na kwenda kuzungumza na jamaa mmoja aliyekuwa amesimama mlangoni.Walizungumza kwa muda mfupi na Yule jamaa akachukua simu akapiga halafu akafungua geti.Nawal akarejea garini akaingiza gari ndani. Mandhari ya ndani ya jumba lile yalikuwa ya kuvutia sana.Kulipandwa maua mazuri na miti ya kupendeza.Kulikuwa na nyumba tatu nzuri na mojawapo kati ya hizo ilikuwa ya ghorofa.Kulikuwa na njia nzuri zimetengenezwa kueleka katika kila nyumba.Nawal akafuata njia iliyoelekea katika nyumba ya ghorofa akasimamisha gari nje ya nyumba ile “Ni hapa tumefika” akasema Nawal na kufungua mlango akashuka Mathew naye akashuka.Mwanamamama mmoja mnene aliyevaa gauni refu na kujitanda mtandio mwepesi akatokeza katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni “Nawal ! akasema Yule mama “Fatma” akasema Nawal na kukumbatiana na Yule mama halafu akasalimiana na Mathew “Karibu sana Nawal” akasema Yule mama na kuwakaribisha ndani akamuita muhudumu akawahudumia wageni chai “Nashukuru sana Nawal kwa kunitembelea.Ammar niliwasiliana naye jana lakini hakuniambia kama utakuja mjini leo” akasema Fatma “Fatma kuna jambo limetokea leo” akasema Nawal “Kumetokea nini?akauliza Fatma akionekana kuwa na wasiwasi “Ammar ameuawa” “Ameuawa? “Ndiyo.Ameuawa a vikosi vya Israel.Vimefanya mashambulizi katika makazi yetu.Kwa bahati nzuri wakati mashambulizi yameanza Ammar alifanya kila aliloweza kuhakikisha ananiokoa mimi na wenzangu lakini aliuawa wakati akiwa katika harakati hizo.Wenzangu pia hawakubahatika kutoka salama.Mke mkubwa na familia yake waliokuwa katika gari lingine walilipuliwa na bomu.Ninamshukuru sana Abu Zalawi ambaye alipambana kuhakikisha ninakuwa salama.Huyu ni mtu wa karibu na Ammar na ndiye aliyemsaidia hata kutoroka gerezani” akasema Nawal “Nimestuka sana.Sijazipat a taarifa hizo bado.Pole sana Nawal” akasema Fatma akionekana kustuka “Israel wamemtafuta Ammar kwa muda mrefu sana na hatimaye wamefanikiwa kumpata.Imeniumiza mno” akasema Fatma na kufuta machozi “Asubuhi ya leo nimeiona video ya Ammar akitangaza kikundi chake kuhusika katika shambulio la bomu lililotokea jijini Jerusalem.Nilifurahi sana.Kila mmoja alifurahi mno kwa kile alichokifanya Ammar na hakuna aliyejua kama muda mfupi baadae angefariki dunia.Hata hivyo Ammar amekufa kishujaa.Tutaendelea kumuenzi siku zote kama mmoja wa mashujaa waliomwaga damu yao akilipigania taifa lake” akasema Fatma na kufuta machozi “Ammar alimtuma Abu Zalawi kutekeleza shambulio lile” akasema Nawal na Fatma akastuka “Kumbe wewe ndiye uliyetekeleza shambulio lile?akauliza Fatma “Ndiyo ni mimi” “Hongera sana Abu Zalawi.Wewe u shujaa mkubwa” akasema Fatma “Ukiacha shambulio la leo asubuhi,Abu Zalawi ndiye aliyemtorosha Ammar kutoka gerezani” “Mungu mkubwa.Nimefurahi kukutana nawe Abu.Yawezekana hauna asili ya eneo hili lakini u mtu muhimu sana kwetu” akasema Fatma “Nilikuwa nimefungwa gerezani baada ya kumuua mkurugenzi wa Mossad Afrika mashariki pamoja na majasusi wawili wa Israel nchini Kenya.Nilikamatwa na kuletwa Israel nikafungwa na hapo ndipo ndipo nilipokutana na Ammar tukapanga mpango wa kutoroka gerezani tukafanikiwa” akasema Mathew “Poleni sana Nawal na Abu.Lakini huu si mwisho wa mapambano.Kumuua Ammar hakuwezi kudhoofisha mapambano ya kudai haki ya maeneo yetu.Mapambano yataendelea” akasema Fatma “Fatma nimekuja kwako nataka utusaidie tuweze kufika kwa Habiba Jawad” “Habiba Jawad?! Fatma akastuka. “Ndiyo” akajibu Nawal.Fatma akashusha pumzi.Akafikiri kidogo na kusema “Kuna chochote Ammar amewahi kukueleza kuhusu Habiba Jawad?akauliza Fatma “Ammar hakunielekeza chochote kwa Habiba lakini aliwahi kunieleza kuwa ni mtu muhimu sana kwake.Ninataka kuonana naye kwa mambo mawili.Kwanza ni mimi mwenyewe nahitaji hifadhi baada ya Ammar kuuawa.Pili ni Abu Zalawi.Ana jambo la kuzungumza na Habiba” “Abu unamfahamu Habiba Jawad?akauliza Fatma “Nimekuwa nikimsikia lakini sijawahi kumtia machoni” “Una jambo gani unalotaka kuzungumza naye? “Ni kuhusu mtu anaitwa Edger Kaka” “Edger Kaka ni nani?Fatma akauliza “Huyu aliwahi kuwa mbunge katika bunge la jamhuri ya mungano wa Tanzania na alikuwa mtu wa karibu sana na Habiba Jawad” akasema Mathew “Sijakuelewa bado Abu” akasema Fatma “Naomba nikupe maelezo kidogo.Makazi yangu yalikuwa Nairobi Kenya na ndiko nilikomuua mkurugenzi wa Mossad Afrika mashariki.Nikiwa Nairobi nilifahamiana na na mtu anaitwa Rashid ambaye huyu alikuwa ni mwanachama wa kundi la IS nchini Kenya.Siku moja aliniomba nikaungane naye katika mabadilishano ya mateka.Alikuwa amewateka watu wawili ambao ni mtoto wa Rais wa Tanzania pamoja na mwanamke mwingine na Tanzania wao walikuwa wamemteka Edger Kaka.Nilikubali kwenda kumsaidia katika mabadilishano hayo na wakati tukibadilishana mateka hao ndipo likatokea shambulio kubwa na mimi kutekwa lakini sikuwa peke yangu nilitekwa pia na Edger Kaka tukaletwa Israel.Nilipewa mateso makali sana na siku moja nilipoteza fahamu nikapelekwa katika hospitali moja ambako nilipozinduka nilifanikiwa kumuona Edger kaka ambaye alikuwa katika hali mbaya.Ninataka kuonana na Habiba Jawad kumueleza kuhusu mtu huyo ambaye nilielezwa na Rashid kwamba ni mtu muhimu sana kwake” akasema Mathew na Fatma akatafakari kidogo “Ndugu zangu naomba niwaweke wazi kwamba Habiba si mtu ambaye unaweza ukaonana naye kirahisi.lakini kwa sababu ya Nawal ninaweza kuwasaidia ila mtapitia mlolongo mrefu kidogo hadi kumfikia.Abu umesema huyo mtu ambaye ulielezwa ana ukaribu na Habiba Jawad anaitwa nani?akauliza Fatma “Anaitwa Edger Kaka” akasema Mathew na Fatma akatoka akaenda chumbani kwake akapiga simu akazungumza na mtu na baada ya dakika tatu akarejea “Abu una uhakika mtu ambaye ulitekwa naye ni Edger kaka? Akauliza Fatma “Ndiyo nina uhakika.Baada ya kutekwa katika yale mabadilishano nilipelekwa sehemu Fulani kama pango nikaingizwa humo na kwa kuwa nilikuwa nimejeruhiwa kwa risasi nikaanza kupatiwa matibabu lakini wakati nikipatiwa matibabu akaletwa mtu akalazwa katika kitanda cha pembeni yangu na nilipotazama alikuwa ni Edger kaka.Nilipoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta nikiwa katika gereza nchini Israel.Niliteswa sana na siku moja baada ya kupatiwa mateso makali nilipoteza fahamu nikapelekwa katika hospitali ya gereza na ndiko nilikomuona Edger Kaka akiwa katika hali mbaya.Alikuwa amewekewa mipira ya kumsaidia kupumua.” Akajibu Mathew na Fatma akarejea tena chumbani kuzungumza na simu. Baada ya dakika chache akarejea tena na sura yake ilionyesha mabadiliko “Inaonekana huyu mtu unayemsema ni mtu muhimu sana kwa Habiba Jawad.Nitalazimika mimi mwenyewe kusafiri nanyi na kuhakikisha mnakwenda kuonana na Habiba Jawad.Kwanza itawalazimu kukaa hapa kwa muda wa siku mbili ili niweze kushughulikia hati zenu za kusafiria halafu ndipo safari ianze” akasema Fatma BAADA YA SIKU 3 PARIS - UFARANSA Ni jioni tulivu ndani ya jiji la Paris katika himaya ya biliona Peniela,tayari Papii Gosu Gosu alikwisha wasili kuitika mwito wa Peniela aliyemtaka kwenda Paris mara moja.Kwa muda wa siku nzima walikuwa wamejifungia katika ofisi ya nyumbani ya Peniela na kazi kubwa waliyokuwa wakiifanya ni kupitia kwa uangalifu nyaraka zote za usajili na umiliki wa biashara mbali mbali za Mathew Mulumbi ambazo Gosu Gosu alikuwa amezipeleka kwa Peniela.Vile vile walikuwa na kazi ya kupitia mahesabu na mwenendo mzima wa biashara zote.Baada ya kazi ile ngumu ya siku nzima Peniela akamtaka Gosu Gosu watoke na kwenda kupumzika bustanini. “Gosu Gosu ninakushukuru sana kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kusimamia miradi hii yote baada ya Mathew kuondoka.Miradi ni mingi na si kazi nyepesi kuisimamia lakini wewe umeweza kuifanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa sana na katika taarifa zote za fedha hakuna hata mradi mmoja unaoonyesha kujiendesha kihasara na vile vile hakuna upotevu wowote wa fedha.Umesimamia miradi hii kama mali yako.U mtu mwaminifu mno.Endapo biashara hizi zingekuwa katika mikono ya mtu mwingine hivi sasa zingebaki nyaraka tu za umiliki lakini kusingekuwa na senti yoyote inayoingia.Mathew hakukosea kukuamini”akasema Peniela na Gosu Gosu akatabasamu. “Mathew ni mtu wangu wa muhimu sana.Ninajua mwenyewe mahala alikonitoa na kunifikisha hapa.Kwangu mimi Mathew si rafiki bali ni zaidi ya ndugu” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana kwa mara nyingine tena” akasema Peniela na kunyamaza kwa muda kidogo kisha akasema “Gosu Gosu pamoja na usimamizi mkubwa na mzuri unaoufanya lakini nimeamua kuuza mali zote” akasema Peniela na kunyamaza akatazama angani.Gosu Gosu akavuta pumzi ndefu “Unataka kuuza mali zote? Akauliza Gosu Gosu “Ndiyo ninataka kuuza mali zote.Si kwa sababu ya kushindwa kusimamia au hasara bali sina mpango kuendelea kuwekeza Tanzania.Kifo cha Mathew kimenifanya nikafikia hatua hii lakini usiogope nitakuachia baadhi ya mali utaendelea kuziendesha wewe mwenyewe zitakuwa za kwako.Nitakuachia nyumba ile unayoishi pamoja na nyumba nyingine mbili.Magari yote aliyokuwa anayatumia Mathew utabaki nayo.Umefanya kazi kubwa na kwa uaminifu mkubwa hivyo basi unastahili kuwa na maisha mazuri ndiyo maana nakuomba usistuke kwa maamuzi haya ya kuuza mali hizo” akasema Peniela “Peniela nimekosa neno la kusema linaloweza kueleza shukrani zangu kwako kwa kuniamini na kunikabidhi mali zenu zote zilizoko Tanzania nizisimamie .Wako watu wengi ambao ungeweza kuwaamini ukawapa mali hizo waziendeshe lakini ukawaacha wote ukanichagua mimi.Ahsante sana kwa kuniamini.Ninashukuru vile vile kwa mali ulizonipatia.Ninajiona kama sistahili kupata mali hizi nyingi” “C’mon Gosu Gosu unastahili kupata mali hizi.Kazi uliyoifanya ni kubwa sana.Ningeweza kukuachia mali zote uendelee kuziendesha lakini nataka niitoe Tanzania katika akili yangu.Kitendo walichomfanyia Mathew kimeniumiza sana.Mathew nimetoka naye mbali na sisiti kusema kwamba yeye ndiye sababu ya mimi kufika hapa nilipofika.Mathew amekuwa ni kila kitu kwangu.Mathew aliipenda sana nchi yake na ndiyo maana hata baada ya kuachana na shughuli za ujasusi lakini bado aliendelea kufanya kazi mbali mbali za nchi kila alipotakiwa kufanya hivyo lakini kupenda huko kazi yake ndiko kumemsababisha akafa kifo cha kinyama sana.Kwa mambo aliyoyafanya Mathew alistahili hata kujengewa mnara wa kumbu kumbu.Ni mambo makubwa ameyafanya lakini aliachwa afe peke yake porini na maiti yake ikaliwa na fisi.Jambo hili linaniumiza sana na ndiyo maana nataka niisahau Tanzania japo ni nchi nilikozaliwa” akasema Peniela.Ukapita ukimya mfupi halafu Gosu Gosu akasema “Madam utaniwia radhi kwa hiki ninachotaka kukuuliza” “Uliza Gosu Gosu usiwe na hofu yoyote kuwa na amani” akasema Peniela “Hujawahi kufikiria kama yawezekana Mathew Mulumbi yuko hai bado?akauliza Gosu Gosu na maneno ya Nahum yakapita kichwani kwa Peniela “Nisikilize Peniela.Mathew Mulumbi yuko hai.Tafadhali mtafute” “Nahum alirudia maneno haya kwa zaidi ya mara moja.Alimaanisha kile alichokuwa anakisema au alikuwa anaweweseka akijua atauawa?Natamani nimweleze Gosu Gosu jambo hili lakini naona aibu kwani Mathew ni rafiki yake.Ngoja niachane na hili suala” akawaza Peniela na kumgeukia Gosu Gosu “Kwa nini umeuliza hivyo Gosu Gosu? “Madam kuna hisia huwa zinakuja kwamba Mathew hajafa.Sijui kwa nini ninakuwa na hisia kama hizo” akasema Gosu Gosu.Ukimya ukapita tena halafu Peniela akasema “Gosu Gosu hizo ni hisia tu na kila mtu ambaye alikuwa na ukaribu na Mathew anazo hisia hizo.Hata mimi nilikuwa na hisia kama hizo lakini kilichonisaidia ni kwamba ninamfahamu Mathew sana kama angekuwa hai angekwisha wasiliana name.Kifo chake kina utata mwingi ndiyo maana unakuwa na hisia hizo lakini tukubali Mathew amekwisha fariki dunia.Nikupe mfano mpaka leo hii bado kuna idadi kubwa ya watu duniani wanaoamini kwamba Tupac Shakur Yule mwanamuziki wa Marekani hajafa.Hii ni kwa sababu ya mazingira ya kifo chake lakini ukweli ni kwamba alifariki dunia na hiki ndicho tunachokipitia kwa Mathew Mulumbi.Hakuna aliyeuona mwili wake na hicho kinatufanya tuamini labda Mathew bado yuko hai lakini ukweli ni kwamba Mathew amekwisha fariki dunia.Hakuna namna anayoweza kurejea tena kwetu.Nakusihi Gosu Gosu endelea na maisha yako” akasema Peniela na mara akakumbuka kitu “Gosu Gosu una mke? “Hapana bado sina mke” “Unasubiri nini kuwa na mke?Sikiliza Gosu Gosu maisha haya ni mafupi sana hivyo tunapaswa kutumia kikamilifu muda tunaoupata.Umri unapanda juu haushuki chini hivyo ni wakati muafaka wa kufikiria kuwa na familia.Vipi kuhusu mchumba unaye? “Hapana hata mchumba sina” “Hata mchumba huna? Peniela akashangaa “Ndiyo madam” “Is everything okay with you? I mean are you…...” Kabla Peniela hajamaliza sentensi yake Gosu Gosu akamkatisha “Hapana siko hivyo.Mimi ni rijali” akasema huku akicheka “Kama ni rijali kwa nini huna mchumba mpaka leo wakati una mafanikio.Umekuwa ukisimamia miradi mingi,you have money,nice cars and everything”akasema Peniela “Mara chache nimekuwa nikitoka na wanawake just for one night stand”akasema Gosu Gosu “Sikiliza Gosu Gosu.Wewe ni mtu wa muhimu sana kwetu hivyo ninakushauri ni wakati sasa wa kufikiria kuhusu mke na kuanzisha familia.Unataka kuwa na familia ukiwa tayari na miaka hamsini? “Madam si kwamba sipendi kuwa na familia au kuwa na watoto lakini hofu yangu ni kwamba sintakuwa mume au baba mzuri” “Kwa nini Gosu Gosu? “Historia yangu si nzuri” “Mathew aliwahi kunidokeza kidogo kuhusu wewe lakini kama hutajali unaweza ukanieleza kwa ireful zaidi kuhusu historia yako”akasema Peniela “Utanisamehe madam lakini naomba nisikueleze kuhusu historia yangu ila nitaendelea kumshukuru Mathew kwani ni yeye aliyenitoa huko nilikokuwa na akanfikisha hapa” akasema Gosu Gosu “Nimekuelewa Gosu Gosu lakini kuna jambo naomba tuelewane” “Nakusikiliza madam” “Ninataka kukutafutia mwanamke” akasema Peniela na GosuGosu akacheka “Madam unataka kunitafutia mwanamke! Akasema na kuendelea kucheka “Ndiyo na ninamaanisha ninachokisema.Siwezi kukuacha ukaendelea na maisha hayo ya kuishi mwenyewe .Sahau historia ya nyuma lakini kwa sasa wewe ni gosu gosu mpya.Una kila kitu.Wewe ni milionea hivyo una kila sababu ya kuwa na mwanamke wa maana.Kuna mwanamke mmoja ni binti mwenye uzuri wa kimalaika.Uzuri wake ni wa ajabu kabisa huyo ndiye nitakuunganisha naye.Naamini atakufaa” “Yuko wapi huyo malaika manake umempa sifa kubwa sana” akasema Gosu Gosu “Anaitwa Melanie Davis na huyo ndiye ninayemuuzia biashara zangu.Bado umri wake mdogo lakini ni bilionea.Amerithi utajiri kutoka kwa wazazi wake.Huyo naamini atakufaa” akasema Peniela “Madam nakushukuru sana kwa kunijali lakini mimi ninapendelea mwanamke wa kawaida asiye tajiri.Hao wenye uzuri wa malaika na fedha nyingi wanasumbua sana na mara nyingi huwa hawadumu katika mahusiano.Unadhani binti mwenye sura ya kimalaika anaweza akakubali kuwa na mwanaume wa aina yangu?akauliza Gosu Gosu na Peniela akacheka kidogo “Si kila mwanamke mwenye pesa basi anakuwa mkorofi na hadumu katika mahusiano.Tazama mimi na Mathew.Mbona tunaishi vizuri na kwa kupendana japo mimi ndiye chanzo cha utajiri wetu.Siwezi sema kwamba matatizo hayapo kwani sisi si malaika lakini heshima ni kubwa.Gosu Gosu kinachomvutia mwanamke si sura bali upendo wa dhati.Mwanamke anahitaji kujaliwa,kupendwa na kutunzwa hata kama ana pesa kama mchanga.Ukimfanyia hayo atakuheshimu.Mwanamke ni kiumbe laini hivyo usimpeleke kwa mabavu,tumia lugha nzuri unapozungumza naye.Lugha unayotumia ukiwa na mke wako iwe tofauti na unavyozungumza na wanawake wengine huko mtaani.Mwanamke anataka heshima,anahitaji ulinzi.Si kwamba umlinde kama mlinzi bali anatakiwa ajisikie amani na salama akiwa nawe.Mwisho mwanamke anahitaji kuridhishwa haja zake za mwili.Nakuhakikishia ukiyafanya hayo mwanamke uliye naye atakulinda kama mboni ya jicho ili wale macho juu wanaopita wakikodolea waume wa wenzao wasikuibe” akasema Peniela na Gosu Gosu akacheka.Alifurahi sana “Ahsante sana madam kwa somo hilo zuri nitazingatia hayo uliyoyasema” akasema Gosu Gosu. “Vipi kuhusu suala nililokwambia?Nakuhakikish ia Gosu Gosu ukimuona huyo malaika ninayekwambia wewe mwenyewe moyo utakuruka” akasema Peniela “Madam wewe na Mathew ni walezi wangu hivyo siwezi kusema hapana.Niunganishe na huyo malaika” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana Gosu Gosu.Naamini wewe mwenyewe ukimuona utakubali haya ninayokwambia.She’s an angel” “Hana mpenzi?akauliza Gosu Gosu “Usihofu kuhusu mpenzi.Hata kama akiwa naye tunafanya mapinduzi.Ukimpata mtunze kama malkia.Mkiwa kitandani hakikisha unamfikisha mahala ambako hakuna mwanaume amewahi kumfikisha na ninakuapia hata kama alikuwa amevishwa pete ya uchumba ataivua” akasema Peniela wakaendelea na mazungumzo kisha wakaenda kupata chakula







Siku nyingine jijini Paris.Siku hii Gosu Gosu alikuwa amevaa suti kali iliyompendeza “Kuanzia sasa huo ndio muonekanao unaotakiwa kuendelea nao.Unatakiwa kuwa mtu wa suti kila wakati” akasema Peniela baada ya Gosu Gosu kumaliza kujiandaa.Walipata kifungua kinywa kisha wakaingia katika gari tayari kwenda kukutana na ujumbe wa Melanie Davis.Kikao kilifanyika katika hoteli moja kubwa jijini Paris inayomilikiwa na Peniela.Peniela na ujumbe wake ndio waliokuwa wa kwanza kuwasili hivyo kuwalazimu kuwasubiri akina Melanie. “Are you nervous?Peniela akamuuliza Gosu Gosu “Kidogo sana.Hamu yangu kubwa ni kumuona uyo malaika ambaye jana ulimpa sifa lukuki” akasema Gosu Gosu “Usijali utamuona atafikahapa” akasema Peniela.Waliendelea kusubiri kwa dakika kama ishirini hivi kisha msafara wa magari matano ukawasili pale hotelini.Melanie na ujumbe wake wakapokewa na Peniela wakakaribishwa ukumbini.Wakati watu wakijiandaa wakiweka sawa makabrasha yao Peniela akamuita pembeni Melanie.Gosu Gosu jicho lilimtoka kama fisi alipomuona Melanie akitembea. “Daah ! Peniela hakukosea kumpa sifa zile.Huyu kweli ni malaika.Melanie ana uzuri wa ajabu sana.Nilipomuona hadi nimemuogopa.Viumbe wa namna hii wanaweza wasiwe binadamu wa kawaida.Mnaweza mkadhani ni mwanadamu mwenzenu kumbe ni kiumbe toka sayari nyingine manake uzuri huu si wa kawaida.Kuanzia kwenye unywele hadi miguuni mtoto huyu anavutia.Amekamilika kila kitu.Sura ina tabasamu ambalo ni adimu sana kupatikana mguu wake daaah nashindwa hata kumuelezea huyu mtoto.Nimebahatika kuzunguka zunguka katika baaadhi ya nchi nimekutana na wanawake warembo lakini huyu ametia fora” akawaza Gosu Gosu “Mwanamke mwenye uzuri kama huu anaweza akanikubali mtu kama mimi kweli?I’m so ugly siendani naye kabisa.Lakini Peniela alinihakikishia kwamba ataniunganisha naye.Anajua mwenyewe namna atakavyofanya lakini mimi kumuingia mwenyewe mtoto kama huyu ni ngumu sijui nitaanzia wapi halafu sina ujuzi sana wa kutongoza wanawake ndiyo maana hupenda kuchukua wale wa usiku mmoja ninamlipa pesa zake tunamalizana.Lakini endapo mtoto kama huyu akiingia kwenye anga zangu naapa hatabanduka.Nitampa mapenzi hadi atasahau kama kuna wanaume wengine ndani ya hii dunia.Ataniona mimi peke yangu” akawaza Gosu Gosu Peniela alitoka ndani ya ule ukumbi na kusimama na Melanie katika korido. “Habari za toka majuzi Melanie?akauliza Peniela “Habari nzuri kabisa Peniela.Unaendeleaje? “Ninaendelea vyema sijui wewe”: “Mimi niko safi kabisa” “Naona umejiandaa vya kutosha.Mimi pia nimekwisha kamilisha kila kitu” “Vizuri sana” “Melanie kabla ya kuanza kwa kikao kuna mtu ambaye ninataka ukutane naye” “Nani huyo?akauliza Melanie “Nipe dakika mbili” akasema Peniela na kufungua mlango wa ukumbi akamtuma muhudumu amuite Gosu Gosu.Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio baada ya kusikia mwito ule wa Peniela.Alijua anakwenda kukutanishwa na Melanie.Aliinuka akatengeneza vizuri tai yake halafu akaanza kutembea kutoka nje akaufungua mlango na kuwaona Peniela na Melanie wamesimama wakimuangalia.Akahisi kama miguu inamtetemeka baada ya kugonganisha macho na Melanie.Akajikaza na kupiga hatua akawafuata “GosuGosu samahani kwa kukutoa ukumbini nimekuita hapa ili nikukutanishe na mtu muhimu sana.Huyu anaitwa Melanie Davis yeye ndiye ambaye leo hii ninamuuzia mali zangu .Usimuone mdogo mdogo lakini ana utajiri wa kutisha” akasema Peniela na kutoa kicheko kidogo Gosu Gosu naye akacheka kidogo “Melanie huyu anaitwa Gosu Gosu.Huyu ndiye ambaye amekuwa akisimamia biashara zangu zote Tanzania baada ya mume wangu kufariki.Ni mtu maminifu na mchapakazi.Mambo aliyonifanyia katika biashara ni makubwa na nina uhakika anaweza akawa na msaada mkubwa sana kwako”Akasema Peniela na Melanie akatabasamu kisha akanyoosha mkono na kumpa Gosu Gosu “Gosu Gosu nafurahi sana kukutana nawe” Mapigo ya moyo wa Gosu Gosu yalitaka kusimama baada ya kuugusa mkono wa Melanie “Hata mimi nafurahi kukutana nawe” akajibu Gosu Gosu “Jamani ni hilo tu ambalo nimewaitia hapa nadhani baadae jioni ya leo tutakutana sisi watatu na tutakuwa na mazungumzo ya kina zaidi.Kwa sasa tukaendelee na kikao” akasema Peniela wakarejea ndani ya ukumbi.Gosu Gosu damu ilimchemka hakuweza kutulia tena. Peniela alifungua kikao kile kwa kufanya utambulisho kwa wajumbe wa upande wake halafu Melanie naye akafanya utambulisho wa wajumbe aliokuja nao kisha mambo yakaanza. ******************** Tayari kiza kimekwisha Melanie Davis aliwasili katika jumba la Peniela akapokewa na kukaribishwa sebuleni.Usiku huu alikuwa amependeza sana alivaa gauni fupi jeupe.Alipendeza mno.Melanie alifika hapa usiku huu kufuatia mwaliko wa Peniela aliyemkaribisha nyumbani kwake kwa chakula cha usiku.Dakika chache baadae Peniela akajitokeza sebuleni akiwa naye amevaa gauni refu jeupe kama vile aliambizana na Melanie wavae wote rangi moja. “Melanie karibu sana.Umependeza sana usiku huu” akasema Peniela “Hata wewe umependeza sana Peniela” akasema Melanie “Huyu mtoto ni mzuri jamani.Kama ningekuwa mwanaume katu nisingekubali kumkosa kimwana huyu.Hata hivyo lazima nihakikishe ninamuunganishia Gosu Gosu” akawaza Peniela “Ahsante sana kwa kufika Melanie.Kama hutajali naomba tuzunguke kidogo bustanini wakati wahudumu wanaendelea kufanya maandalizi” akasema Peniela na Melanie akaungana naye wakatoka kuelekea bustanini. “Melanie najua huu si wakati mzuri wa kuzungumza masuala ya biashara kwani kutwa nzima ya leo tumekuwa tunazungumza masuala hayo lakini napenda nikushukuru kwa mchakato kwenda vizuri” “Mimi ndiye ninayepaswa kukushukuru kwa kukubali kuniuzia biashara zako.Japo nimetoa fedha lakini naona kama vile umenipa bure”akasema Melanie “Lini umepanga kwenda Tanzania?akauliza Peniela “Mapema iwezekanavyo.Ndani ya siku mbili au tatu zijazo nitakuwa nimefika Tanzania” akajibu Melanie “Vizuri sana.Kuna swali la kizushi nataka kukuuliza kama hutojali” “Uliza usihofu” akasema Melanie “Una mchumba tayari? Akauliza Peniela na Melanie akatabasamu “Hapana sina mchumba” akajibu Melanie “Malaika kama wewe unakosaje mchumba?Au wanaume wanakuogopa kutokana na uzuri wako? Akauliza Peniela na Melanie akacheka “Niliamua mimi mwenyewe nisiwe katika mapenzi” akasema Melanie Peniela alitumia zaidi ya nusu saa kumchombeza Melanie aweze kumkubali Gosu Gosu.Muda wote ambao Peniela alikuwa akimuelezea Gosu Gosu Melanie alikuwa anatabasamu kutokana na namna alivyomuelezea Gosu Gosu.Melanie alimueleza Peniela kwamba angehitaji kupata nafasi ya kuzungumza na Gosu Gosu.Walirejea ndani ambako walimkuta Gosu Gosu sebuleni akiwasubiri.Usiku huu alikuwa amevaa suti nzuri ya kijivu.Baada ya kusalimiana Peniela akawakaribisha katika chumba cha chakula kulikoandaliwa chakula maalum kwa ajili yao.Baada ya kumaliza kupata chakula Peniela akawaomba waelekee katika chumba cha mapumziko ambamo kulikuwa na runinga kubwa .Wakiwa mle Peniela akatoka na kuwaacha Gosu Gosu na Melanie.Ukimya ulikuwa umetawala mle katika chumba cha mapumziko hadi pale Melanie alipoinuka na kumfuata Gosu Gosu katika sofa na kukaa pembeni yake. “Unaonekana una hofu Gosu Gosu.Nini kinakupa hofu?akauliza Melanie “Sina hofu Melanie” akajibu Gosu Gosu.Baada ya sekunde kadhaa Melanie akasema “Madam Peniela amenipa ujumbe wako.Kwa nini hukunieleza wewe mwenyewe hadi ukamtumia Peniela?akauliza Melanie “Naomba niwe muwazi kwako Melanie.Nilishindwa namna ya kuzungumza nawe suala lile” “Gosu Gosu“ akasema Melanie kwa sauti laini na mwili wa Gosu Gosu ukazidi kusisimka “Nini kilikupa hofu ya kuja kunieleza jambo lile?Melanie akauliza “U mzuri mno Melanie hadi nikaogopa.Kwa kawaida wanawake wazuri kama wewe si rahisi kuwa na watu wa aina yangu.Ndiyo maana nikamuomba Peniela anisaidie” akasema Gosu Gosu “Usiwe mwoga Gosu Gosu.Ukimtaka mwanamke usimtumie mtu wa katikati bali mfuate wewe mwenyewe mweleze na ataamua mwenyewe akukubali au vipi lakini kitendo cha kumtumia mtu mwingine kinakufanya uonekane hujiamini” “Ninajiamini Melanie lakini kuna utofauti mkubwa sana kati yangu nawe na hilo ndilo lililonipa woga” “Hukupaswa kuogopa.Ni vipi nikikwambia kwamba hata mimi nilivutiwa nawe mara tu nilipokuona?akasena Melanie na moyo wa Gosu Gosu nusura usimame kwa mstuko alioupata. “Me?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo Gosu Gosu.Mimi sioni woga kukutamkia kwamba nilivutiwa nawe mara tu nilipokuona ” “Oh my God ! nini kimekuvutia kwangu? “Sikiliza Gosu Gosu mimi najifahamu ni mzuri.Ni mzuri sana lakini sipenzi wanaume wenye sura nzuri.Mara nyingi ukiwa na mwanaume mzuri inakufanya uwe katika mashindao na wanawake wengine nje ambao wanamtolea macho kama mwewe aliyeona kifaranga.Nikiwa nawe watu wanaweza wakanicheka kwamba imekuwaje mwanake mzuri kama huyu akawa na mtu kama huyu?Simaanishi kwamba wewe ni mbaya but you are not handsome.Hakuna mwanamke ambaye atataka kushindana nami kukupata hivyo utakuwa wangu peke yangu na hicho ndicho ninachokitaka.Kwa uzuri huu nilio nao hata wewe hautasumbuka kutafuta mwanamke mwingine kwani nimewazidi wengi uzuri.Pamoja na hayo…” akasema Melanie na kuinua glasi akanywa funda moja akaendelea “I have everything in life.Ninachohitaji mwanaume nitakayekuwa naye awe na uwezo wa kunitosheleza kitandani.Hiyo ndiyo starehe yangu kubwa Usistuke Gosu Gosu mimi ni muwazi sana hivyo napenda kukuweka wazi kwamba napenda sana kufanya mapenzi.Mwanaume ninayemtaka lazima awe na uwezo wa kuniridhisha.Nimewahi kuwa na wanaume kadhaa lakini walikimbia wenyewe walishindwa kutimiza mahitaji.Mimi nataka kama dozi ya dawa kutwa mara tatu au nne” akasema Melanie na wote wakacheka “Huo ndio ukweli Gosu Gosu na ndiyo maana wanaume wale niliowahi kuwa nao ambao ninaweza kuwaita wavulana walishindwa na kuondoka zao.Nataka mwanaume anayeiweza shughuli na sitaki Yule anayetumia dawa za kuongeza nguvu.Nataka nguvu za asili.Nilipokuona wewe Gosu Gosu sijui kwa nini nilivutiwa nawe lakini unaonekana uko tofauti kidogo na wengine.Peniela aliponipa ujumbe wako nilihisi kama vile moyo wangu umepigwa na radi kwa mstuko.Nilifurahi sana kwamba hata wewe ulikuwa umevutiwa nami.Nataka kukuthibitishia kwamba ombi lako nimelipokea lakini kabla ya yote kabla sijatamka kitu nataka kuhakikisha kama hisia zangu kwamba wewe ni tofauti ni za kweli.Usiku wa leo nataka tukalale wote”akasema Melanie na bado GosuGosu hakuwa ameamini.TaratibuMelanie akaupitisha mkono wake hadi maeneo ya ikulu kwa Gosu Gosu ambako hali ilikuwa mbaya . “Mbona uko kimya Gosu Gosu?akauliza Melanie huku akiupitiasha mkono wake maeneo yale ambako kulikuwa kumefura vibaya sana “Wow it looks so big ! akasema Melanie na kuzidi kumchanganya Gosu Gosu “Devotha aliniambia nifanye juu chini niweze kumteka huyu jamaa Gosu Gosu.Aliniambia kwamba ni mtu ambaye anaweza akanisaidia sana katika kazi ninayokwenda kuifanya Afrika Mashariki kwani ni muuaji hatari sana.Alinipa historia ya huyu jamaa kwamba aliwahi kupigana vita ya msituni kwa muda mrefu hivyo ni mwanajeshi mzuri na mimi nahitaji mtu kama huyu.Mpaka hapa tayari nimekwisha mpata na anaonekana ni mdhaifu sana kwa wanawake.Mtazame alivyopoa kama maji ya mtungi” akawaza Melanie na kutolewa mawazoni baada ya Peniela kuingia mle ndani na kustuka kwa hali aliyoikuta “Sorry guys” akasema Peniela “Usijali madam Peniela mimi na Gosu Gosu tulikuwa na mazungumzo kidogo hata hivyo tulikuwa tunakusubiri uje ili tukuage leo ninaondoka na Gosu Gosu nitamrejesha hapa kesho.Nataka nikamuonyeshe uzuri wa jiji la Paris” akasema Melanie “Hakuna tatizo lakini hakikisha Gosu Gosu anakuwa salama” akasema Peniela huku akitabasamu Baada ya mazungumzo mafupi Gosu Gosu na Melanie wakaondoka “Nataka nimchanganye kwa mapenzi mwanaume huyu hadi afanye kila nitakachomuamuru.Hadi hapa naamini nimekwisha mpata kwa asilimia sabini” akawaza Melanie wakiwa garini





Mlio wa simu ya mkononi ulimstua Melanie akaamka na kutazama mpigaji.Katika kioo lilitokea jina Dev likiwa na maana ya Devotha.Tayari kulikwisha pambazuka. “Nilikuwa na usingizi mzito sana sikujua kama tayari kumepambazuka” akawaza Melanie na kuelekea sebuleni akaipokea ile simu “Hallow”akasema “Melanie sauti yako ya uchovu sana bado umelala?akauliza Devotha “Simu yako ndiyo iliyonitoa usingizini” “Vipi mipango ilifanikiwa? “Kila kitu kilikwenda vizuri” “safi sana.Jiandae baadae leo unakwenda kukutana na Rais” akasema Devotha “Sawa ahsante kwa taarifa” akasema Melanie na kukata simu “Dah ! usiku wa jana sintausahau.Huyu jamaa kweli mwanajeshi na inaonekana ana muda mrefu hajakutana na mwanamke kwani mambo aliyonifanyia jana hadi mimi mwenyewe nilishindwa kuhimili.Ana nguvu za kutosha.Alinipeleka mizunguko minne hadi nikaishiwa nguvu kabisa na kumuomba aniache nilale ndiyo maana nimelala kama chatu.Kweli hapa nimepata mtu ninayemuhitaji” akawaza na kutabasamu baada ya matukio ya usiku ule kumjia kichwani “Ulikuwa ni usiku mzuri sana.Sijawahi kupelekeshwa kama nilivyopelekwa jana” akaendelea kuwaza halafu akaingia chumbani na kumkumbatia Gosu Gosu “Devotha alinitaka niwe na mahusiano na huyu jamaa kwa ajili ya kunisidia katika mipango yangu lakini nahisi tayari nimeanza kumpenda” akawaza Melanie na kumtazama Gosu Gosu aliyekuwa amelala.Akamuamsha kwani ni muda wa kuondoa kwenda kuendelea na majukumu mengine Saa tano za asubuhi iliwakuta Devotha na Melanie Davis katika ikulu





Saa tano za asubuhi iliwakuta Devotha na Melanie Davis katika ikulu ya Ufaransa kwa ajili ya kukutana na Rais Michael Weren. “Devotha na Melanie karibuni sana.Nimefurahi kukuona Melanie .Kwa uzuri huo utaitingisha dunia” akasema Michael na wote wakaangua kicheko. “Melanie nimetaarifiwa kwamba ulikamilisha mafunzo na ukafanya vyema na sasa uko tayari kwa kazi.Nimejulishwa pia na Devotha kwamba mipango yote imekwenda vizuri na muda wowote utaelekea Afrika mashariki tayari kuanza kazi”akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Tunazo taarifa kwamba mkutano mkubwa wa wake za maraisi duniani unatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam Tanzania mwezi ujao.Mkutano huo umeandaliwa na taasisi ya mke wa Rais wa Tanzania Millen Kelelo.JIna lake linafanana sana na lako.Mkutano huu unakuja miezi michache baada ya mauaji ya wazazi wako na mauaji ya balozi wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania.Tunaamini lengo la mkutano huo ni kwa ajili ya kuidhihirishia dunia kwamba Tanzania ni nchi salama ndiyo maana wake wa marais wote duniani wamealikwa.Mkutano huu ukifanikiwa basi lengo letu la kuichafua Tanzania na Afrika Mashariki litakuwa limefeli.Unakwenda kufanya kazi ya kuisambaratisha Afrika mashariki na kazi yako itaanzia katika mkutano huo wa wake za marais.Afrika Mashariki itaanzia kusambaratika hapo. Kwa kuanzia nataka mke wa Rais wa Rwanda auawe nchini Tanzania na ionekane nchi ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inahusika katika mauaji hayo.Nataka mahusiano ya Rwanda na Congo DRC yavunjike.Nchi mbili hizi zikianza malumbano ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki zitasababisha jumuiya kutetereka.Wakati Rwanda na Congo zikilumbana nataka uibuke mgogoro mwingine kati ya Tanzania na Rwanda.Balozi wa Rwanda anatakiwa naye auawe.Tukifanikisha kuibua migogoro hiyo tayari tutakuwa tumetoboa tobo na meli itaanza kuzama taratibu.Huu ni mpango mkubwa na Devotha ambaye ndiye anayeratibu kila kitu atakupa maelezo mengi zaidi ya nini unatakiwa ufanye lakini usiwe na hofu yoyote kuhusu usalama wako.Utakuwa salama kwani kuna majasusi wa siri wamekwisha andaliwa kwa ajili ya kukulinda na hutawaona ila fahamu kila unapokwenda watakuwepo na watahakikisha unakuwa salama.Unapokuwa katika utekelezaji wa jukumu hili usisahau kwamba tunayafanya haya kwa ajili ya kwanza kulipiza kisasi na pili kuikomboa Congo.Umekwisha fundishwa kila kitu na ninachokifanya hapa ni kukukumbusha tu jukumu lako.Kwa namna yoyote ile usikubali ukaenda nje ya lengo.Macho na akili yako vyote vielekeze katika kazi uliyopewa.Ukienda tofauti na kazi uliyopewa hautakuwa ukiwatendea haki wazazi wako ambao wameuawa kikatili na wapinga maendeleo hivyo basi lengo letu ni kuhakikisha kwamba yeyote Yule ambaye ana mkono wake katika mauaji ya wazazi wako habaki salama lakini kubwa zaidi ni kuhakikisha kwamba Congo inatoka katika jumuiya ya Afrika Mashariki na kuliondoa genge la watu wachache wanaojinufaisha na rasilimali za nchi hiyo.Nadhani umenielewa Melanie” akasema Michael Weren “Nimekuelewa mheshimiwa Rais.Tayari nimekwisha pewa mafunzo ya kutosha na ninaelewa nini ninakwenda kukifanya Afrika Mashariki na ninakuahidi kwamba nitafanya kwa umakini mkubwa kazi niliyotumwa na sintakuangusha” akasema Melanie “Nashukuru kwa maneno hayo yenye kutia moyo.Basi mimi sina la ziada nakutakia kila la heri na taarifa za maendeleo yako nitakuwa nikizipata kutoka kwa Devotha” akasema Rais Michael Weren na kuagana na akina Melanie MPENZI MSOMAJI - BAADA YA KUNUSURIKA KATIKA MTEGO WA KUUAWA RUBY YUKO NJIANI AKIELEKEA DAR ES SALAAM.JE ATAFIKA SALAMA? - MATHEW MULUMBI TAYARI YUKO KATIKA HARAKATI ZA KUONANA NA HABIBA JAWAD JE ATAFANIKIWA? - THERESA MUGANZA AMBAYE KWA SASA ANAJULIKANA KAMA MELANIE DAVIS ANAANZA SAFARI YA KUELEKEA DAR ES SALAAM KATIKA MISHENI NZITO YA KUISAMBARATISHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JE ATAFANIKIWA? KWA MAJIBU YA MASWALI HAYA MPENZI MSOMAJI USIKOSE SEHEMU IJAYO…





DAR ES SALAAM – TANZANIA Msafara wa mke wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Millen Kelelo uliwasili katika ukumbi ambao mkutano mkubwa wa wake za marais duniani utafanyikia.Alipokewa na meneja wa ukumbi ule kisha Millen na ujumbe wake wakaingia ndani kukagua shughuli za maandalizi ya ukumbi zinavyokwenda.Walizunguka sehemu mbali mbali za ukumbi na kwa kiasi kikubwa maandalizi yalikuwa yanaridhisha.Millen akatoa maelekezo kadhaa kwa meneja wa ukumbi ule halafu yeye na ujumbe wake wakaondoka wakaelekea Swala hoteli moja kati ya hoteli kubwa ya nyota tano ambayo baadhi ya wageni ambao ni wake za marais watafikia.Hapo napo Millen alipokewa na meneja wa hoteli na kutembezwa sehemu mbali mbali za hoteli kujionea namna walivyokuwa wamejiandaa kuupokea ugeni ule mkubwa kabisa.Maandalizi yalikuwa makubwa na ya kuridhisha.Millen na ujumbe wake walizungukia baadhi ya mahoteli mengine ili kujiridhisha na maandalizi na kikubwa hasa walichokuwa wakikitazama ni suala la usalama wa wageni wawapo katika hoteli hizo.Baada ya kumaliza kuzungukia mahoteli,Millen na msafara wake wakaeleka katika soko kuu la bidhaa za kiutamaduni ambako wageni wanatarajiwa kupelekwa hapo ili kutazama bidhaa mbali mbali za utamaduni wa mtanzania.Millen alizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo na kuwataka wajiandae vilivyo kwa ugeni ule mkubwa wa wake za marais ambao watakwenda kutembelea soko hilo na kununua bidhaa mbali mbali.Toka hapo sokoni Millen alielekea moja kwa moja katika ofisi za taasisi yake ambako alikuwa na mkutano na waandishi wa habari.Kabla ya kuingoa katika ukumbi kuzunguza na wanahabari aliingia kwanza ofisini kwake na baada ya dakika kadhaa akajulishwa kwamba kila kitu kiko tayari na akatoka kwenda kukutana na wanahabari. Ukumbi wa mikuano ulio katika jengo zilimo ofisi za taasisi yake ulijaa waandishi wa habari waliokuwa tayari kusikiliza na kuwafikishia wananchi kile ambacho mke wa Rais alikusudia kukisema.Kama kawaida yake Milleen ambaye tabasamu huwa halikauki usoni akatoa kicheko kidogo na kusema. “Samahani sana kwa kuwachelewesha ndugu zangu” Wanahabari walitikia lakini hawakusikika nini walikiongea kwani walikuwa wanazungumza kwa sauti ya chini y kunong’ona.Millen akaendelea “Ndugu wanahabari nimewaiteni hapa leo ili kupitia kwenu watanzania waweze kupata taarifa za kile kinachoendelea kuhusiana na maandalizi ya mkutano mkubwa wa kimataifa wa wake za marais wa dunia unaotarajia kufanyika hapa nchini mbili zijazo.Mkutano huu ni mkubwa na wa kipekee mno ambao ni mara ya kwanza unafanyika barani afrika na utafanyikia hapa kwetu Tanzania.Karibu wake za marais wa nchi zote za dunia wamepelekewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo na asilimia themanini tayari wamekwisha thibitisha kushiriki katika mkutano huo.Tunaendelea kuwasiliana na wale waliobaki ili kupata uhakika kuhusu ushiriki wao lakini naamini asilimia tisini na tisa ya wake za marais watahudhuria mkutano huo mkubwa. Ndugu wanahabari lengo kuu la kuandaa mkutano huu mkubwa hapa kwetu Tanzania ni kujadili kwanza mwanamke na mabadiliko ya sayansi na teknolojia,pili mwanamke na mabadiliko ya tabia nchi na tatu ni ongezeko la vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.Kama wote tunavyofahamu kumekuwa na mabadiliko makubwa na ya kasi ya teknolojia hivyo tunataka kujadili tuone katika mabadiliko hayo mwanamke anasimama wapi? Mwanamke anawezaje kunufaika na mabadiliko hayo ya teknolojia? Athari zipi hasi anakumbana nazo kufuatia mabadiliko hayo? Ndugu wanahabari kuhusu mwanamke na mabadiliko ya tabia nchi naamini nyote mnafahamu kuhusu mabadiliko makubwa ya tabia nchi yanayoendelea kutokea sehemu mbali mbali duniani na kwa kiasi kikubwa kupelekea mfumo wa maisha kubadilika.Tutajadili kwa kina changamoto anazopata mwanamke katika mabadiliko haya ya tabia nchi na kutafuta majawabu nini kifanyike na wake hawa wa marais watakaporejea katika nchi zao ambako karibu kila mmoja anayo taasisi yake watakwenda kujikita katika kutoa elimu katika yale ambayo tutakuwa tumekubaliana katika mkutano huo.Hayo ni machache tu ambayo tutayajadili katika mkutano huo lakini mada ni nyingi na tumewaawalika pia watu kutoka mashirika mbali mbali ya kimataifa watahudhuria pia. Ndugu wanahabari itoshe tu kusema kwamba mkutano huu ni mkubwa na wa kipekee kabisa kuwahi kufanyika nchini kwetu hivyo ninapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba watanzania tujiandae kwa ugeni huu mkubwa unaokuja nchini kwetu.Ukiacha faida kubwa zitakazopatikana kutokana na maazimio yatakayotolewa na mkutano huo lakini kuna faida nyingine kubwa za kiuchumi.Mkutano huo utasaidia katika kuitangaza nchi yetu kimataifa.Katika kipindi chote cha mkutano huo macho yote ya dunia yataelekezwa Tanzania.Hiyo ni fursa yetu ya kukuza utalii kwa kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwetu.Katika hilo wageni hawa watakapomaliza mkutano wao watapelekwa kutembelea vivutio mbali mbali vya kitalii vilivyopo hapa nchini.Wengine watapelekwa mbuga ya Serengeti na wengine watakwenda Ngorongoro na katika sehemu nyingine mbali mbali.Wakitoka huko watakuwa ni mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vyetu na tunategemea idadi ya watalii wanaotembela hifadhi zetu kuongezeka baada ya mkutano huo.Faida nyingine ni kwamba wageni hawa kila mmoja atakuja na ujumbe wake hivyo wenye mahoteli watafaidika.Ugeni huu mkubwa pia utatembelea sehemu mbali mbali kama vile soko la bidhaa za utamaduni pale watanunua bidhaa mbali mbali mbali za wajasiriamali.Hizo ni faida chache tu ambazo nimeweza kuzielezea zitakazopatikana kutokana na mkutano huu lakini faida ziko nyingi hivyo nawaomba watanzania hasa wana Dar es salaam muupokee ugeni huu mkubwa na muhakikishe mnanufaika na uwepo wa wageni hao hapa Dar es salaam. Ndugu wana habari leo nimefanya ziara ya kuzungukia kutazama maandalizi ya mkutano huu yanavyokwenda na nimeridhishwa na maandalizi yake.Nimezungukia ukumbi utakaotumika kwa mkutano na mikutano mingine midogo midogo,nimezungukia pia mahoteli ambako wageni wetu watafikia na sehemu nyingine mbali mbali na kuridhika na maandalizi mazuri yanayofanyika.Kwa ujumla kila sehemu wamekwisha jiandaa kikamilifu kwa ugeni huu.Naamini ndani ya siku chache zijazo maandalizi yote yatakuwa yamekamilika Ndugu zangu lengo kuu la kuwaiteni hapa leo ni kuwapa taarifa hiyo kuhusiana na maandalizi ya mkutano huo mkubwa wa wake za marais duniani na ninaomba kupitia kwenu taarifa ziwafikie wananchi na muwaelemishe juu ya faida zitakazopatikana kutokana na mkutano huo mkubwa.Nawashukuru sana ndugu zangu kwa kufika kwenu na ninawaomba muendelee kuitika wito kila pale tutakapowahitaji kwani ili kufanikisha mkutano huu tutawahitaji sana.Ahsanteni sana ndugu zangu na mchana mwema” akasema Millen na kusimama kwa ajili ya kuondoka lakini mwandishi mmoja wa habari akapaza sauti akitaka kuuliza swali.Millen akatazama saa ya mkononi halafu akasema “Ndugu zangu najua mnayo maswali mengi mnataka kuuliza lakini kwa siku ya leo muda hauniruhusu kwani nina kikao tena sehemu nyingine muda mfupi ujao.Nawaahidi kwamba tutaandaa tena mkutano mwingine na nitajibu maswali yenu yote” akasema Millen “Mama naomba nikuulize swali moja tu ! akaendelea kusisitiza Yule mwandishi.Millen akatabasamu na kusema “Sawa nitaruhusu swali moja tu kwa niaba ya wote” “Ahsante sana mama” akasema Yule mwandishi wa habari huku Millen akiketi kusikiliza swali “Mama umetutuma tufikishe taarifa kwa wananchi kuhusiana na mkutano huo mkubwa na sisi tutaifanya hiyo kazi kwani kwani ni jukumu letu kuhabarisha umma.Swali langu ni hili.Miezi michache iliyopita kulitokea matukio ya mauaji ambayo yalisababisha nchi za umoja wa Ulaya kuwatahadharisha raia wao wasifike au wachukue tahadhari wawapo hapa nchini.Wageni wanaokuja ni wake za marais nataka kujue je serikali ya Tanzania imejiandaa vipi kiusalama? Akauliza Yule mwandishi “Swali zuri sana ndugu yangu.Ni kweli kulitokea matukio kadhaa hapo siku za nyuma ya mauaji ambayo yalipelekea nchi yetu kuchafuka kimataifa hata hivyo serikali ya Tanzania imechukua kila aina ya tahadhari katika kuhakikisha kwamba wageni wote watakapofika hapa nchini kuhudhuria mkutano huo mkubwa wanakuwa salama.Siwezi kuingia ndani zaidi katika masuala hayo ya kiusalama lakini itoshe tu kuwathibitisha wananchi kwamba nchi iko salama na wageni wetu wote watakaokuja watakuwa salama wao na ujumbe wao hadi watakapoondoka.Nawaomba vile vile ndugu watanzania ulinzi wa amani yetu ni wetu sote hivyo kama kuna mtu atakuwa na taarifa za mtu au kikundi chochote cha watu watakaotaka kuvuruga amani watoe taarifa mara moja kwa vyombo husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na kwa haraka.Ahsanteni sana ndugu zangu” akasema Millen na kuinuka akatoka huku akiwaacha waandishi wa habari wakiwa bado na kiu ya kutaka kuuliza maswali. Baada ya kumaliza kikao na waandishi wa habari Millen aliingia garini akaondoka kurejea ikulu “Mwandihishi Yule wa habari ameuliza swali muhimu sana.Usalama ni kitu kinachopewa kipaumbele kikubwa mno katika mkutano huu ambao lengo lake kuu ni kuidhihirishia dunia kwamba Tanzania ni nchi salama kuishi,kuwekeza na hata kutembelea.Serikali imekwisha chukua kila aina ya tahadhari katika kuhakikisha mkutano huu unafanikiwa lakini bado nina hofu.Japo mambo yametulia hivi sasa lakini naamini nchi zile ambazo tuliingia katika msuguano nazo hazitapenda kuona mkutano huu ukifanikiwa.Nchi hasa zile za umoja wa Ulaya zikiongozwa na Ufaransa ziliwatangazia hadi raia wao wasifike Tanzania au kuchukua tahadhari za kiusalama wawapo hapa,hawatapenda kuona mkutano huu ukifanyika na kufanikiwa hivyo watafanya kila aina ya juhudi kuhakikisha hatufanikiwi.Huwa naingiwa na wasiwasi sana nikiliwaza hilo lakini Rais amekwisha nihakikishia kwamba usalama ni mkubwa na wa kutosha kabisa.Ameniahidi nisiwe na wasiwasi hivyo lazima nimuamini” akawaza Millen Alifika katika makazi yao ikulu na kuungana na mume wake Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo katika chakula cha mchana “Vipi mambo yamekwendaje huko ulikotoka? Akauliza Dr Fabian “Mambo mazuri.Maandalizi yanakwenda vizuri.Nimekagua ukumbi ambao umekarabatiwa upya na kwa asilimia tisini umekamilika kuna sehemu chache tu za kumalizia pia nimetoa maelekezo ya sehemu za kurekebisha.Nimekagua pia baadhi ya hoteli ambako wageni watafikia kote kuko vizuri wamejiandaa vya kutosha.Nikatoka hapo nikaenda kukagua soko la bidhaa za utamaduni ambako wageni watakwenda kutembelea nako huko maandalizi yako vizuri baada ya hapo nikarejea ofisini kuzungumza na wanahabari nikawataka watoe elimu kwa wananchi kuhusiana na mkutano huu na umuhimu wake.Kwa ujumla naweza kusema kwamba kwa kiasi kikubwa maandalizi yanakwenda vizuri sana.Kila idara inatekeleza majukumu yake vizuri.Fabian tumekaribia sana kuitimiza ndoto yetu ya kuihakikishia dunia kwamba Tanzania ni sehemu salama” akasema Millen “Nashukuru kama kila kitu kinakwenda vizuri.Kama kuna chochote kitakwama nieleze mara moja” akasema Dr Fabian “Kuna mwandishi mmoja aliniuliza swali akitaka kujua kuhusu usalama wa wageni akitolea mfano matukio yale ya mauaji yaliyotokea wakati ule”akasema Millen “Ulimjibu nini?akauliza Dr Fabian “Nilimtaka akawahakikishie wananchi kwamba usalama ni mkubwa na wasihofu”akajibu Millen “Ulimjibu vizuri.Usalama ni mkubwa sana.Kila aina ya tahadhari imechukuliwa katika kuhakikisha kwamba kila mgeni atakayekuja nchini kwetu kuhudhuria mkutano huo anakuwa salama.Vyombo vyote vinavyohusika na ulinzi wa taifa viko macho kuhakikisha hakuna kitisho chochote cha usalama kabla na baada ya mkutano huo.Kwa sasa kila siku jioni wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi hukutana na kubadilishana taarifa za siku nzima kuhusiana na usalama.Kuhusu hilo usiwe na wasiwasi wowote” akasema Dr Fabian Baada mapumziko ya mchana Rais alirejea ofisini kuendelea na majukumu yake na mara tu alipofika ofisini akampigia simu Edwin Mbeko ambaye ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya ukurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi baada ya kifo cha Tamar Axon “Mheshimiwa Rais” akasema Edwin kwa adabu “Edwin habari za mchana” “Nzuri kabisa mheshimiwa rais” “Edwin,mke wangu ametoka kufanya ukaguzi wa maandalizi ya ule mkutano mkubwa wa wake za marais.Kwa ujumla maandalizi yanakwenda vizuri lakini nimekupigia kukupa msisitizo uongeze nguvu zaidi katika kubaini kama kuna kitisho chochote cha usalama kabla ya mkutano huo.Vyombo vyote vya ulinzi na usalama hivi sasa macho yao vimeyaelekeza katika kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa amani na idara yako pia inaendelea na jukumu hilo kwa siri lakini nataka nguvu iongezwe zaidi.Kipaumbele kikuu cha idara yako kwa sasa kiwe ni mkutano huu mkubwa.Umenielewa Edwin? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” “Ahsante sana” akasema Dr Fabian na kukata simu PARIS – UFARANSA Devotha Adolph akiwa na gari lake la kifahari akiendeshwa na dereva wake huku mbele kukiwa na gari la walinzi wake aliopewa na Rais Michale Weren wamlinde,aliwasili katika jumba kubwa anakoishi Theresia Muganza ambaye kwa sasa anajulikana kama Melanie Davis.Mmoja wa walinzi wake akawahi kushuka katika gari na kumfungulia mlango akashuka akavaa kofia yake nyeupe ya mduara akaanza kutembea kuelekea ndani. “Haya ndiyo maisha ninayoyataka.Nataka niheshimiwe,nataka niwe na sauti nataka niwe na nguvu ya kumuamrisha mwanaume atii kile ninachokitaka.Huu ni mwanzo tu,harakazi zangu hazitakoma hadi nihakikishe siku moja ninaingia katika lile jumba jeupe pale Dar es salaam.Lazima siku moja niwe Rais wa Tanzania.Hii ni ndoto yangu ya muda mrefu na ninaamini siku moja itatimia.” akawaza Devotha wakati akipanda ngazi kuingia ndani huku walinzi wa jumba lile wakiwa wamesimama kwa adabu wakati akipita.Aliingia ndani na kupokewa kwa furaha na Melanie. “Karibu sana Devotha”akasema Melanie na kumkaribisha Devotha chumbani kwake “You look tired”akasema Devotha “Sijui hata niseme nini lakini toka nimekutana na Gosu Gosu hakuna kulala.Yule jamaa ana minguvu kama nyati.Akikukamata huwezi kufurukuta hata kidogo” akasema Melanie huku akitabasamu “Kuwa makini sana na Gosu Gosu.Kama nilivyokueleza kwamba he’s a killer.Si mtu wa kuamini wala kumfanyia masihara anaweza akakutoa roho sekunde yoyote” akasema “Niko makini sana” akasema Melanie “Vipi muelekeo wake hadi sasa?Unaweza kuwa na uhakika kwamba tayari umemuweka mikononi?akauliza Devotha “Naweza kukuhakikishia kwamba tayari ameingia mtegoni na amenasa.Hawezi kutoka tena.Kwa yeye kunipata mwanamke kama mimi ni kama kuokota gari lililojaa dhahabu.Mpaka sasa haamini kama ameweza kulala nami”akasema Melanie “Safi sana.Gosu Gosu ni mtu muhimu sana katika mpango huu.Lakini hakikisha asifahamu kama mimi na wewe tuna mawasiliano.Hatakiwi kabisa kujua kama niko hapa Paris.Akijua kama tuna mawasiliano mimi na wewe kila kitu kitaharibika hivyo kuwa makini sana” “Mmewahi kuwa na mahusiano?akauliza Melanie “Hapana sijawahi kuwa na mahusiano naye ila mimi naye tumewahi kushiriki katika misheni fulani na hapo ndipo nilipomfahamu.Sitaki kueleza zaidi lakini siku zote kumbuka huyu mtu ni hatari na ukikosea kidogo tu atavuruga kila kitu lakini pia ni mtu muhimu sana kwetu.Anao marafiki zake wengine ambao unapaswa kuwa muangalifu sana nao,mmoja anaitwa Austin January.Huyu ni mkuu wa kikosi cha jeshi kinachoshughulika na operesheni maalum.Naye pia ni mtu hatari.Kaa naye mbali kabisa.Kuna mwingine anaitwa Ruby.Huyu ni mwanamke hatari.Si muuaji bali anaitwa mchawi wa kompyuta.Ana uwezo mkubwa sana wa kucheza na kompyuta.Huyu makazi yake ni nje ya Tanzania hivyo si mtu wa kuhofia sana lakini ni hatari.Uwezo wake katika masuala haya ya mawasiliano unashangaza mno.Hawa wote kiongozi wao anaitwa Mathew Mulumbi” akasema Devotha na kunyamaza picha ya Mathew Mulumbi ikamjia kichwani akashusha pumzi na kusema “Mathew Mulumbi ni mtu mbaya mno lakini kwa bahati nzuri kwa sasa hayuko Tanzania na hatarejea tena Tanzania na yawezekana tayari amekwisha fariki huko mahala alikokuwa,hivyo mtu wa kuchunga sana ni Gosu Gosu.Anaweza kuwa na faida kwetu lakini tukikosea anaweza akawa na hasara kubwa.Jitahidi sana kumpa mapenzi mazito ili achanganyikiwe” akasema Devotha “Usihofu kuhusu hilo.Gosu Gosu hawezi kufurukuta tena kwangu.Ndani ya sku hizi mbili nimekwisha maliza kila kitu”akajigamba Melanie “Good.Nimepokea taarifa kutoka Tanzania kwa mtu anaitwa Edwin Mbeko ambaye ni mkuu wa idara ya serikali inaitwa SNSA,amenijulisha maandalizi yote yamekamilika”akasema Devotha “SNSA ni nini? Akauliza Melanie “Secret National security agency.Hii ni idara ya siri ya serikali ya Tanzania inayojishughulika na usalama wa ndani wa nchi.Mimi ndiye niliyeianzisha na ndiye niliyekuwa mkurugenzi wake wa kwanza.Baada ya mimi akafuata Kaiza akaja Tamar na sasa ni Edwin Mbeko.Utakapofika Tanzania umeandaliwa jina lingine ambalo utakuwa ukilitumia ambalo litakutambulisha kama mtanzania na utajulikana kama Melanie Chuma.Hivyo utakuwa na majina mawili.Melanie Davis raia wa Ufaransa na mwekezaji aliyenunua mali zilizokuwa zinamilikiwa na Mathew Mulumbi ambaye amefariki dunia,Vile vile kuna Melanie Chuma ambaye ni mtanzania mfanya biashara.Kutakuwa na tofauti kati ya Melanie Davis na Melanie Chuma.Unapokuwa Melanie Davis unakuwa kawaida kama ulivyo sasa lakini pale utakapohitaji kuwa Melanie Chuma utafanya mabadiliko kidogo katika mwonekano wako.Kuna ngozi ndogo imetengenezwa ambayo utaibandika chini ya jicho lako ikiwa na kidoti cheusi halafu kuna ngozi nyingine utaibandika pembeni ya kidevu ikiwa na alama kama kovu lililotokana na kidonda.Vile vile kuna ngozi utabandika katika vidole vyako ili kubadli alama za vidole kama kuna mtu atahitaji kuchukua alama” akasema Devotha na kutoa mkebe kutoka katika mkoba wake akaufungua.Ndani ya ule mkebe kulikuwa na ngozi hizo alizozisema.Akamuonyesha Melanie namna ya kuzibandika “Unapokuwa Melanie Davis jitahidi sana kuzungumza kifaransa kila wakati na ikikulazimu kuzungumza Kiswahili utazungumza Kiswahili kibovu ukidai kwamba bado unajifunza.Ukiwa Melanie Chuma utazungumza Kiswahili safi kama mtanzania.Kitu pekee cha kuchunga ni Gosu Gosu.Huyu amekufahamu kama Melanie Davis na kamwe asikutambue kama Melanie Chuma hivyo basi Gosu Gosu hapaswi hata itokee nini kuingia ndani ya chumba chako na wala usimkaribishe katika nyumba yako.Wafanyakazi wako wa ndani watatoka hapa hapa Ufaransa na si wafanyakazi tu bali ni majasusi ambao wamepewa mafunzo maalum kukusaidia lakini vile vile ni kuongeza ulinzi kwako kuhakikisha unakuwa salama na una kamilisha kazi uliyotumwa.Jambo lingine ni kama alivyokueleza Rais kwamba kuna watu ambao watakuwa wakikulinda bila ya wewe kujua.Hawatajionyesha kwako lakini fahamu kila uendako watakuwa wakikulinda.Utalindwa angani na ardhini.Kila unakoenda utaonekana na utafuatiliwa.Mambo yote kuhusu ulinzi umekwisha elekezwa hivyo sitaki kurudia tena.Tofauti nyingine kuhusu Melanie Davis na Melanie Chuma ni makazi.Melanie chuma atakuwa na nyumba nyingine ambayo imeandaliwa.Edwin atakuelekeza kila kitu kwani mambo hayo yote amekwisha yashughulikia.Yatakuwepo magari ya Melanie Davis na Melanie chuma lengo kuwa likiwa ni kuwatofautisha watu hawa wawili.Hayo ni machache tu ambayo nimekuja kukukumbusha kabla hujaondoka hapo kesho mengine tutaendelea kuelekezana pale utakapokuwa Dar es salaam.Kumbuka kujielekeza katika misheni yako uliyotumwa ambayo ni kuhakikisha kwamba Afrika Mashariki inasambaratika na nchi ya Congo inabaki peke yake ili iweze kuwa rahisi kuliondoa genge la http://deusdeditmahunda.blogspot.com/watu wachache wanaotafuna rasilimali za nchi hiyo vile vile usisahau kwamba misheni hizi zinajielekeza moja kwa moja kwa watawala wa nchi hivyo basi ni misheni hatari sana na ndiyo maana tumetumia gharama kubwa kuziandaa hivyo umakini mkubwa mno unatakiwa lakini usihofu kila hatua unayopiga sisi tuko nyuma yako.Usisahau vile vile kwamba watawala hawa tunaowalenga ndio waliowaua wazazi wako hivyo hakutakuwa na hata chembe ya huruma kwao” akasema Devotha na Melanie akashusha pumzi halafu akasema “Ni jukumu zito lakini nitalifanya kwa ajili ya wazazi wangu.Niliweka ahadi kwamba hakuna aliyehusika katika vifo vya wazazi wangu atakabaki salama lazima wote walipe uovu wao.Hata hivyo nataka kufahamu nini hatima yangu mwisho wa misheni hii?akauliza Melanie. “Mwisho wa misheni hii ni wewe kukalia kiti cha urais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Unachokwenda kukifanya hivi sasa ni kutengeneza njia ya kuelekea huko hivyo kaa ukijua kwamba siku moja utakuwa mtawala wa Congo na utazitimza ndoto za mama yako” akasema Devotha “Sihitaji urais na nimekwisha mueleza hata Rais Michael.Sitaki kuwa mwanasiasa” akasema Melanie “Nina uhakika maneno hayo yatabadlika siku moja.Hata mimi niliwahi kuwa na mawazo kama hayo wakati fulani nilichukia siasa na wanasiasa lakini kwa sasa nahitaji sana kuwa Rais wa Tanzania” “Unataka kuwa Rais wa Tanzania? Melanie akashangaa “Ndiyo Melanie.Nataka kuwa Rais wa Tanzania na mipango hiyo inaendelea.Pale jumuiya ya Afrika mashariki itakapovunjika basi nitachukua urais wa Tanzania.Wakati mimi nikiwa Rais wa Tanzania wewe utakuwa unaandaliwa kuwa Rais wa Congo” akasema Devotha huku akitabasamu “Kwa nini unataka kuwa Rais wa Tanzania? Huogopi? Akauliza “Mimi siogopi kitu.I was born a leader.Hii ni ndoto yangu na lazima niitimize kwa namna yoyote ile” akasema Devotha “Lakini Devotha kwa haya unayoyafanya endapo yakigundulika yatakuharibia safari yako ya kuelekea ikulu kwani utaonekana msaliti kwa nchi yako”akasema Melanie na Devotha akacheka kidogo “Kwanza hakuna atakayefahamu.Mambo haya ni mipango mikubwa na ninaungwa mkono na nchi kubwa za Ulaya.Ngoja nikufahamishe kitu Melanie Davis.Bara la Afrika ni tajiri mno.Mungu ametupa mali nyingi kuanzia mwanzo wa bara hadi mwisho wake.Kila sehemu ni utajiri aidha wa madini ama wa vitu vingine.Nchi zilizoendelea kiviwanda kwa kiasi kikubwa zinategemea malighafi kutoka nchi za Afrika ndiyo maana japo nchi nyingi za Afrika zinajitawala zenyewe zinafanya uchaguzi wa viongozi lakini ukiangalia wengi wa viongozi wa sasa wanaochaguliwa katika bara la Afrika kuna nchi tajiri ziko nyuma yao ambazo ziliwawezesha wakashinda uchaguzi.Mimi ninaungwa mkono na nchi kubwa za umoja wa Ulaya hivyo uhakika wa kuingia madarakani ni mkubwa.Siasa za Afrika bado zimetawaliwa na nguvu kubwa kutoka nje ya bara la Afrika” akasema Devotha “Endapo nchi za ulaya au yoyote kubwa itakusaidia ukaweza kuingia madarakani hudhani kwamba wanafanya hivyo kwa ajili ya wewe kuwasaidia kupata kitu Fulani wanachokihitaji?Hudhani huo ni usaliti kwa nchi yako?akauliza Melanie “Umesaidiwa kupata madaraka hivyo lazima kuwe na malipo and I don’t care.Ninachohitaji mimi ni kitu kimoja tu ambacho ni kupata madaraka” akasema Devotha “Sasa nimejua kwa nini nchi nyingi za bara la Afrika ni masikini japo Mungu amezipa utajiri mkubwa.Tatizo ni viongozi wetu ambao wengi waliingia madarakani kwa nguvu ya mataifa makubwa ambayo yanachohitajini kuchota rasilimali huku nchi zikiendelea kubaki masikini.Hii ni laana na ndiyo maana sipendi kuwa mwanasiasa” akasema Melanie “Huyu mjinga anaongea nini tena?Mbona anaanza kubadilika? Akawaza Devotha akichukizwa na maneno yale ya Melanie “Sikiliza Melanie.Hiki kitu kilikuwepo,kipo na kitaendelea kuwepo.Hata mama yako kama angekuwa Rais wa Congo zipo nchi tajiri ambazo zilikuwa nyuma yake na mojawapo ni Ufaransa.Tuachane na hayo masuala ya kisiasa tujielekeze katika jukumu kubwa lililoko mbele yako.Fahamu umebeba jukumu kubwa ambalo mwisho wake ni kuisaidia nchi ya Congo.Nenda katimize ndoto za mama yako ambaye alitaka kuiona siku moja Congo ikinufaika na rasilimali zake ilizojaliwa na Mungu” akasema Devotha “Nimekuelewa Devotha,usiwe na hofu yoyote.Kila kitu kitakwenda kufanyika kama kinavyotakiwa” akasema Melanie Walikuwa na mazungumzo marefu yaliyohusiana na operesheni anayokwenda kuifanya Melanie Afrika Mashariki.Baada ya mazungumzo yao Devotha akaaga na kuondoka kwa miadi ya kukutana tena siku inayofuata ambapo Melanie atakuwa akiondoka kuelekea Tanzania “Ama kweli maisha yanaweza yakabadilika ndani ya sekunde chache.Sikuwahi kuhisi kama siku moja ningeweza kufikia hatua hii.Ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuwa mwanasayansi mkubwa na nililenga siku moja kufika hadi anga za juu lakini leo hii niko hapa nikiandaa mpango mzito wa mauaji tena ya watu wakubwa.Sikutaka kufikia hatua hii lakini nimelazimishwa niwe hivi.Watu waliowaua wazazi wangu wamenilazimisha niwe mkatili na lazima niwe mkatili.Hawakuona huruma kutoa uhai wa wazazi wangu na mimi sintaona huruma kutoa uhai wao.Walikosea sana kuniacha hai kama wangejua wangenipiga risasi ya kichwa nife pale pale” akawaza Melanie na picha ya tukio la mauaji ya wazazi wake ikamjia “Naamini huko waliko waliopanga mauaji ya wazazi wangu wametulia wakiamini mambo yamekwisha bila kujua kuna ziraili anayeziwinda roho zao anakuja.Narudia tena kuapa hakuna aliyeshiriki katika mauaji ya wazazi wangu atakayebaki salama.” akawaza Melanie RIYADH – SAUDI ARABIA Mathew Mulumbi alifumbua macho baada ya kusikia mlango wa chumba alicholala ukigongwa.Akainuka pale kitandani na kuelekea mlangoni akiwa katika tahadhari kubwa.Hakuwa na bastora hivyo ilimlazimu kujihami kwa kutumia mikono yake.Alipoufungua mlango akakutana na jamaa aliyekuwa na bunduki akamsalimu na kumtaka ajiandae kuna sehemu wanaelekea. “Nawal yuko wapi?akauliza Mathew “Yuko katika chumba kingine.Yuko salama usihofu” akajibu Yule jamaa mwenye bunduki. Mathew na Nawal wakiwa wameongozana na Fatma waliwasili katika jiji la Riyadh Saidi Arabia wakitokea Ramallah saa tisa za usiku na moja kwa ,moja wakaletwa katika nyumba hii na kutokana na uchovu waliokuwa nao Mathew alijitupa kitandani na kulala kama chatu aliyemeza mbuzi hadi alipoamshwa na hodi ya mlinzi aliyekuja kumuamsha akimtaka ajiandae. Mathew akaenda dirishani akachungulia nje walikuwa juu ghorofani.Ilikuwa ni nyumba nzuri yenye mandhari ya kuvutia.Chini aliwaona walinzi wanne karibu na geti na wawili kati yao walikuwa na bunduki “Yawezekana hii ikawa ni mojawapo ya nyumba za Habiba Jawad.Ni nyumba nzuri na ina ulnzi mkubwa” akawaza Mathew na kuingia bafuni akaoga.Baada ya kuoga akakaa kitandani akisubiri kile kitakachofuata “Ammari Nazari tayari ameondoka na sasa anayefuata ni Habiba Jawad.Haitakuwa kazi nyepesi kumuua Habiba lakini lazima auawe au akamatwe.Baada ya hapo nitaanza tena mpango mpya wa kunirejesha Tanzania nikaanze maisha mapya.Kwa miaka hii mitatu nimepitia mambo mazito mno ambayo sijawahi kukutana nayo kwa kipindi chote ambacho nimekuwa katika kazi ya ujasusi hivyo basi ni muda wangu kuachana na kazi hizi.Kwenye soka mtu anapotaka kustaafu wana msemo wao wanasema anatundika daruga.Nataka kutundika daruga ili nianze maisha mapya na familia yangu ambayo bado wananihitaji sana.Watoto wangu,mke wangu……” Mara alipomkumbuka Peniela akaikumbuka ile picha aliyoiona Peniela akiwa chumbani na Nahum wakifanya mapenzi “Picha ile itanitesa sana kwa miaka mingi lakini siwezi kumlaumu Peniela kwa kuwa mimi ndiye niliyesababisha haya yote yakatokea.Kama nisingekubali kuendelea na kazi hii hivi sasa ningekuwa karibu na familia yangu na Peniela asingekuwa na Yule mwanaume.Simlaumu kwa kuwa anaamini tayari nimekufa na sintoweza kurudi tena ndiyo maana ameamua kuendelea na maisha yake.Ni vipi pale atakapojua kwamba niko hai?Atanipokeaje?Watoto wangu watanipokeaje? Dah ! sifahamu nini kitatokea lakini naomba Mungu anisaidie waweze kunipokea na kunikubali” akawaza Mathew na kuinamisha kichwa akisikitika. “Ukitafuta mzizi wa mimi kufika hapa ni Peniela.Nilijikuta katika misheni ya kumuokoa Olivia ambaye nilikuwa natoka naye kimapenzi kwa siri.Lakini kwa nini nikatoka na Olivia? Ni kwa sababu Peniela ambaye ni mke wangu alikuwa mbali nami.Kwa muda mrefu kumekuwa na tatizo la umbali kati yetu.Peniela amechukua uraia wa Ufaransa na mimi siko tayari kuukana uraia wangu wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine hiki kimekuwa ni kigezo cha kutufanya tuishi mbali mbali kwa kipindi kirefu na ndiyo maana nikajikuta nikianzisha mahusiano na Olivia.Kama Peniela angekubali tukaishi Tanzania haya yote yasingetokea lakini haitaki nchi yake alikozaliwa na mimi siwezi kuwa raia wa nchi nyingine kwani hakuna sababu yoyote ya kunifanya niukatae uraia wangu.Swali linakuja kama nitafanikiwa misheni yangu ya kumuua Habiba Jawad na kurejea nyumbani nini kitatokea?Je mfumo wa maisha yangu utabadilika?Je Peniela atakubali kuishi Tanzania au bado ataendelea na msimamo wake wa kuishi Ufaransa?Ni vipi kama akikataa kuishi Tanzania nitalazimika kubadili uraia na kuifuata familia yangu Ufaransa? Haya ni mambo ambayo lazima niyatafutie majawabu.Kama hakutakuwa na muafaka katika suala hili sijui nini kitatokea” akawaza Mathew na kuondolewa mawazoni baada ya mlango kugongwa akainuka akaenda kuufungua.Alikuwa ni Yule mlinzi akamtaka waelekee katika chumba cha chakula kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.Dakika mbili baada ya kuingia katika kile chumba akaingia Nawal “Abu Zalawi” akasema Nawal “Nawal unaendeleaje? Akauliza Mathew “Ninaendelea vizuri.Vipi wewe hali yako? “Mimi niko vizuri ni uchovu tu wa safari.Ilikuwa ni safari ndefu sana ile” akasema Mathew. Walipata kifungua kinywa kimya kimya wakiwa wamesimamiwa na walinzi wawili na baada ya kumaliza Nawal akawaomba walinzi wale kama watawaruhusu waende wakapumzike juu ya lile ghorofa.Walipanda juu ya ghorofa lile na wakaishuhudia mandhari nzuri ya jiji la Riyadh kwani jumba lille lilijengwa kilimani.Hata wakiwa kule juu ya ghorofa bado walinzi wale wawili waliendelea kuwalinda lakini walikuwa mbali kidogo na kuwapa uhuru wa kuzungumza mambo yao “Mathew katika chumba nilimolala nimegundua kuna kamera ya siri imetegwa.Naamini hata katika chumba chako ulicholala ni hivyo hivyo.Hawa jamaa wanatutazama.Wanachungu za kila tunachokifanya” akasema Nawal “Bado hawatuamini ndiyo maana wanatuchunguza.Safari ya kuelekea kwa Habiba Jawad bado ndefu.Fatma yuko wapi?akauliza Mathew “Fatma sijamuona toka nilipoamka.Inaonekana hakulala hapa alipotufikisha akaondoka zake” akajibu Nawal. Ukimya ulipita Mathew akiwa ameyaelekza macho yake kutazama namna watu walivyokuwa wakiendelea na shughuli zao za kawaida “Abu uko mbali sana kimawazo.Unaogopa? Nawal akauliza “Hapana siogopi kitu” “Nini kinakupa awazo hayo mengi? Akauliza Nawal “Nimeona namna watu wale kule chini wanavyoendelea na majukumu yao ya kawaida nikawaonea wivu.Natamani sana kuishi maisha ya kawaida kama wale watu kule chini.Wana furaha na amani wanaendelea na maisha yao kama kawaida.Tazama sisi hatuna furaha hata kidogo.Tuko hapa hatuko huru tunalindwa na bunduki kama wafungwa.Hatujui nini hatima yetu,hatujui kama tutaamka salama siku ya kesho.Tunaishi maisha ya mashaka.Kama Mossad wasingweza kupata namba yako ya simu wakakuonya kuhusu mashambulio yale waliyoyafanya katika kambi ya Ammar hivi sasa tungekwisha kuwa majivu .Nimechoshwa na maisha ya namna hii.Natamani kurejea maisha yangu ya kawaida” akasema Mathew “Nimechoka kabisa”akasema Mathew akisikitika na kuinamisha kichwa chini.Ulipita muda kidogo Nawal akasema “Wakati ninakuganga majeraha yako nilisoma maandishi uliyoyaandika katika mgongo yanayosomeka”People sleep peaceably in their beds at night only because rough men stand ready to do violence on behalf” akasema Nawal na kunyamaza. “Naamini ulikuwa na sababu maalum ya kuyaandika maneno yale.Sisi ndio wale uliowataja ambao hatulali ili kuhakikisha wengine wanakuwa salama” akasema Nawal “Kinachonisikitisha zaidi hakuna anayejua mateso tunayoyapitia.Kwa mfano hivi sasa hakuna anayejua kama siku chache zilizopita tumenusurika na mabomu ya Israel.Hakuna anayejua kama tuko hapa tunalindwa na askari wenye bunduki,hakuna oh Mungu wangu..! akasema Mathew na kuinamisha kichwa akisikitika “Zipo kazi nyingi ambazo tungeweza kuzifanya lakini tulichagua kazi hii kwa ajili ya kuhakikisha nchi zetu na ndugu zetu wanakuwa salama.Watu ambao tumeyatoa maisha yetu kuwalinda hawapaswi kujua kile tunachokifanya wala kukipitia katika kuhakikisha wao wanakuwa salama.Ni Mungu pekee ambaye anaona kile tunachokipitia na atatulipa kwa mazuri tunayoyafanya kwa nchi zetu”akasema Nawal “Nawal una bahati walau nchi yako inakuthamini.Mimi hakuna anayenijali wala hakuna anayesumbuka kunitafuta.Inaniumiza sana hasa nikiifikiria familia yangu amabo hivi sasa wanaamini tayari nimekwisha fariki” akasema Mathew “Una familia? Nawal akauliza “Ndiyo nina mke na watoto wanne” “watoto wanne? “Ndiyo” akasema Mathew “Kwa nini basi ukaendelea kujishughulisha na shughuli hizi wakati tayari una familia kubwa namna hiyo? Akauliza Nawal “Nilikwisha achana na hizi kazi lakini kazi hii bado iko damuni kwani kila mara ninajikuta tena katika misheni mbali mbali zinazohusiana na nchi.Kwa mfano kama ilivyoanza misheni hii sikutegemea kama leo ingenifikisha hapa” akasema Mathew “Nini kimekufikisha hapa? “Rafiki yangu alitekwa nyara na kilichoniponza ni kuamua kuacha shughuli zangu na kumtafuta.Mambo yote yalianzia hapo.Huwa najilaumu sana kama nisingekutana na Olivia yasingenikuta haya yaliyonikuta” “Mkeo anaitwa Olivia? “Hapana.Olivia ni rafiki yangu wa kawaida lakini nilikuwa natembea naye na hii ilisababishwa na umbali uliopo kati yangu na mke wangu”akasema Mathew “Uliponiambia kwamba uliamua kuacha kila kitu kwa ajili ya kumtafuta rafiki yako aliyetekwa nilikuwa najiuliza ni rafiki gani huyo anayeweza akakufanya ukajitoa namna hiyo kumbe ni mtu wa karibu zaidi” akasema Nawal huku akitabasamu “Vipi kuhusu wewe una familia? Mathew akauliza “Niliwahi kuwa na mpenzi lakini ni mimi niliyemuomba tuachane kwani kwa kazi yangu hii nisingeweza kuwa karibu naye muda wote na sikutaka kumkwaza hivyo basi nikamuomba tuachane na toka wakati huo sijawahi kuwa na mpenzi hadi nilipoingia katika ndoa na Ammar Nazari”akasema Nawal “Unaweza ukanieleza namna ulivyofika kwa Ammar hadi ukaolewa naye?akauliza Mathew na Nawal akazama mawazoni “Sipendi sana kulizungumzia hilo jambo.Ni moja kati ya mambo ambayo yananiumiza sana kwamba nilikubali kuwa mke wa mtu katili na muuaji.Mke wa gaidi.Lakini nilifanya hivyo kwa ajili ya nchi yangu.Haikuwa rahisi kuishi ndani ya kundi la magaidi ambao kila siku wanachokipanga ni kutoa roho za watu.Halikuwa jambo rahisi kuishi na watu ambao una hakika kwamba wanaweza wakakugundua muda wowote na pindi wakikugundua basi adhabu yake ni kifo.Nikiwa pale tayari nilikwisha weka sahihi ya kifo kwani nilijua nikikosea kidogo nitauawa.Haikuwa rahisi kuishi bila kujua kama utaiona kesho.Haikuwa rahisi kumvulia nguo yangu Yule gaidi ambaye hajui mapenzi hata chembe.Ni maisha ambayo sitaki kuyakumbuka na ninamshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha nimetoka pale salama” akasema Nawal “Pole sana Nawal” akasema Mathew. “Chloe ! akasema Nawal na Mathew akageuza shingo akamtazama. “Chloe Bennet ndilo jina langu.Nina damu ya kiarabu mama aliniambia kwamba baba yangu alikuwa na asili ya Libya.Katika shambulio lililofanywa na Abdul Yasin Al Nasser baba yangu ni mmoja wa watu waliouawa ndio maana kwa kila namna lazima nihakikishe nimempata” akasema Nawal na kunyamaza kwa muda “Kama wewe ulivyonikataza nisikuite Mathew Mulumbi naomba nawe usiniite Chloe tafadhali.Endelea kuniita Nawal” akasema Nawal “Sawa ntafanya hivyo” akajibu Mathew na wote wakawa kimya kila mmoja akiendelea kutazama watu wakiendelea na maisha yao ya kawaida mitaani “Nini mpango wako baada ya kukamilisha operesheneni hii ngumu uliyonayo? Akauliza Mathew “Abu maswali yako magumu.Sina mpango mwingine.Nitaendelea kufanya kazi hii ya ujasusi kwani ndiyo kazi ninayoipenda” “Hujawahi kufikiria kuachana na kazi hii na kuwa na familia yako siku moja? Akauliza Mathew “Sina uwezo wa kuzaa hivyo sifikirii kuwa na familia.Niliomba kuondolewa kizazi kwa kuhofia nisije nikabeba mimba ya Yule gaidi na kama nlivyokuwa nimewaza ndiyo ilivyokuwa.Kikubwa ambacho Ammar alikuwa anakihitaji sana kwangu ni kuzaa naye mtoto.Amejitahidi sana ili niweze kubeba mimba bila mafanikio na haifahamu siri hii.Kwa upande mwingine nawashukuru Israel kwa kumuua kwani alikuwa amepanga mwezi ujao twende hospitali nikapimwe kwa nini sipati mimba?Angegundua siri yangu angeniua.Ammar ni mkatili mno zaidi ya unavyofahamu” akasema Nawal “Kwa upande wangu mimi kinachoniumiza kichwa ni namna familia yangu watakavyonipokea kwani wanaamini tayari nimekwisha fariki.Wamekwisha endelea na maisha yao na mke wangu tayari ana mpenzi mwingine.Ninawaza nini kitatokea pale nitakapojitokeza?Naamini nitaharibu kabisa maisha yao.Haitakuwa rahisi kunikubali.Naamini watoto wanaweza wakafurahi kwamba nimerejea na ninaweza nikawaeleza kwamba taarifa ya kifo changu haikuwa sahihi lakini kwa mke wangu haitakuwa rahisi.Hata kama atanielewa maisha yetu hayatakuwa kama zamani” akasema Mathew na Nawal akamtazama kwa huruma “Tuachane na hayo kwa sasa tujielekeze katika misheni yetu.Katika simu yako ulikumbuka kufuta zile picha ulizopiga za Ammar?akauliza Mathew baada ya kumuona mmoja wa wale walinzi wawili akiwasogelea “Niliwatumia CIA kisha nikazifuta katika simu” akasema Nawal.Yule mlinzi akawataka warejee ndani kila mmoja akatakiwa kuingia katika chumba chake.Akiwa ndani ya chumba chake mlango ukafunguliwa wakaingia watu wawili,Mathew akatakiwa kunyoosha mikono yake akafungwa pingu halafu akafunikwa mfuko mweusi kichwani na kuinuliwa akatolewa mle chumbani “Mnanipeleka wapi?akauliza Mathew lakini hakuna aliyemjibu.Alishushwa ngazi taratibu na kuingizwa katika gari ambalo hakujua ni la aina gani akasikia mlango ukifungwa na gari likawashwa likaondoka.Hakujua anapelekwa wapi. “Nawal aliniambia katika vyumba tulivyolala kulikuwa na kamera za siri hawa jamaa walikuwa wanatuchunguza.Lakini hata kama wakinichunguza hawataweza kugundua chochote kama mimi ni jasusi badala yake watakutana na taarifa kwamba mimi ni gaidi niliyetoroka gerezani nikiwa na Ammar Nazari ambazo zimewekwa na Mossad.Nadhani kuna mahala ninapelekwa.Vipi kuhusu Nawal?Kwa nini yeye ameachwa?akajiuliza Mathew “Hii ni sababu kwa nini Israel mpaka leo wameshindwa kumpata Habiba Jawad.Si rahisi kumfikia.Kama ili kumfikia inakupasa upitie taratibu hizi basi hataweza kupatikana.Nashukuru walau nimepiga hatua katika kufahamu mahala alipo Habiba Jawad.Aombe kwa miungu yake yote anayoifahamu kwani siku zake zinahesabika.Labda niuawe kabla sijafanikiwa kuonana naye” akawaza Mathew Mulumbi huku gari lilkienda kwa kasi. Ilichukua mwendo wa kama saa mbili gari lile alilopanda Mathew likasimama mlango ukafunguliwa Mathew akashushwa.Bado alikuwa na mfuko kichwani.Alichokuwa anakisikia ni milango kufunguliwa na kufungwa na mwishowe akakalishwa katika kiti mikono ikafunguliwa pingu na kufungwa kwa kamba nyuma ya kiti halafu akasikia mlango ukifungwa kukawa kimya “Nadhani wamenileta hapa kwa mahojiano.Ee Mungu nisaidie”akawaza Mathew Zilipita dakika kumi akasikia hatua za mtu na mlango ukafunguliwa wakaingia watu zaidi ya mmoja mle ndani.Akasikia viti vikivutwa halafu sauti ikaamuru avuliwe ule mfuko kichwani.Mathew akajikuta katika chumba kikubwa na watu watano walikuwa wamejipanga kuzunguka meza kubwa.Pembeni kulikuwa na walinzi wawili wakiwa na bunduki wakimlinda. “Abu Al Zalawi assalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuh” akasema jamaa aliyejifunga kilemba kichwani akionekana ndiye mkuu wa jopo lile. “Wa alaykum s salam wa rahmatullahi wa barakatuh” akajibu Mathew “Abu Zalawi karibu sana Riyadh.Pole kwa safari ndefu ya kufika hapa na pole sana kwa yote yaliyowapata.Utatusamehe pia kwa namna tulivyokuchukua na kukufikisha hapa.Hizi ni taratibu zetu za kawaida za kuchukua tahadhari” akasema Yule jamaa “Jina langu naitwa Abdel Fattah Sarraf” akasema Yule jamaa aliyekuwa kiongozi wa jopo lile.Mathew alikuwa kimya akiwatazama “Abu Zalawi tunaomba utueleze wewe ni nani, umetokea wapi na kwa nini uko hapa?akauliza Abdel Fattah “Ee Mungu nisaidie huu usiwe mtego nimewekewa na hawa jamaa ili waweze kunipima kama ninasema kweli” akawaza Mathew “Naitwa Abu Al Zalawi.Ni mtoto wa Khalid Al Zalawi na Dalia Sultan ambao wotre tayari wamekwisha tangulia mbele za haki.Baba yangu Khalid alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kundi la Abu Hafs Al Masri,kundi lililokuwa na mafungamano na kundi la Alqaeda na lilikuwa pia likisaidiana na baadhi ya makundi ya wanamgambo wa kipalestina katika harakati za kudai haki ya ardhi yao ndipo alipouawa na vikosi vya Israel.Kitendo cha baba yangu kuuawa na Vikosi vya Israel kilinipelekea na mimi niingie katika vita dhidi ya Israel.Nilikwenda Kenya ambako ni asili ya mama yangu nikaishi huko na ndiko nilikoanzia harakati zangu za kupambanana na Israel.Nilimuua mkuu wa Mossad Afrika mashariki aliyeitwa Avi na majasusi wengine wawili.Nikiwa nchini Kenya nilifahamiana na mtu anaitwa Rashid ambaye alikuwa ni mfuasiwa kikundi cha IS.Siku moja Rashid aliniomba nikamsaidie kufanya mabadilishano kati yake na vikosi vya serikali ya Tanzania kwani IS walikuwa wamemteka mtoto wa Rais wa Tanzania na serikali ya Tanzania nao kuna mtu walikuwa wanamshikilia ambaye IS walikuwa wanamuhitaji.Rashid aliniambia kwamba mtu huyo ambaye anashikiliwa na serikali ya Tanzania anaitwa Edger Kaka na ni mtu muhimu na wakaribu mno kwa Habiba Jawad” Mathew akanyamaza na kuwatazama watu wale wakiwa kimya kabisa wakimsikiliza.Akaendelea “Mabadilishano yalifanyikia sehemu ya mpakani mwa Tanzania na Kenya na wakati mabadilishano hayo yakifanyika lilitokea shambulio kubwa la ghafla.Tulishambuliwa kutoka kila upande na mimi nilipigwa risasi tatu sikuweza tena kukimbia nikatekwa na watu hao ambao walikuwa wamefunika sura zao nikapelekwa katika pango lililokuwa karibu na mahala pale.Nilipokuwa mle ndani ya pango aliingizwa pia Edger kaka ambaye ndiye IS walikuwa wanamuhitaji.Nilichomwa sindano ya usingizi na nilipozinduka nilijikuta katika chumba chenye giza na baadae nikagundua tayari nilikuwa nimepelekwa nchini Israel.Niliteswa sana nikitakiwa kukiri kumuua mkuu wa Mossad Afrika Mashariki na kutaja mtandao wa kigaidi ninaoshirikiana nao.Miaka mitatu ya mateso makali lakini sikuweza kufumbua mdomo wangu kuzungumza chochote.Baada ya kuona wameshindwa kunifanya niongee waliamua kunifunga gerezani wakanipeleka katika chumba ambamo kulikuwa na mtu mmoja.Nilikuwa katika hali mbaya nilikuwa na vidonnda mwili mzima.Mtu Yule aliyekuwa amefungwa ndani ya kile chumba alinisaidia nikaweza kupata nafuu na ndipo nilipomfahamu mtu Yule kama Ammar Nazari.Nilitokea kuelewana sana na Ammar na ndipo tulipoanza harakati za kuandaa mpango wa kutoroka gerezani na tukafanikiwa.Wakati tukitoroka Ammar alipigwa risasi mbili lakini sikuweza kumuacha nilimbeba tukatoka mle gerezani.Baada ya kutoroka gerezani sikuwa na sehemu ya kwenda Ammar akanikaribisha katika kundi lake nikajiunga nao na tukaendeleza harakati za mapambano dhidi ya Israel.Mimi ndiye niliyelipua lile bomu katika kituo cha treni jijini Jerusalem na kuua watu wengi.Ammar aliandaa sherehe kubwa kujipongeza kwa ushindi ule dhidi ya Israel lakini wakati sherehe zikiendelea ndipo tulipovamiwa na vikosi vya Israel na kitu cha kwanza alichokifanya Ammar ni kuhakikisha familia yake inakuwa salama.Alinitaka mimi niondoke na Nawal na kuhakikisha anakuwa salama.Nilimchukua Nawal na kumuondosha eneo lile huku mashambulio ya mabomu mazito ya Israel yakiendelea.Nilimficha Nawal ndani ya handaki mlimani na mashambulizi yalipokoma ndipo tukatoka na akaelekeza twende Ramallah kwa mtu aliyeitwa Fatma ambaye alikuwa na ukaribu mkubwa na Ammar.Wakati nikiwa bado gerezani ninateswa kule Israel,niliwahi kupoteza fahamu nikapelekwa katika hospitali kubwa ya gereza kutibiwa na huko nilionyeshwa Edger kaka akiwa katika chumba maalum hana fahamu amewekewa mashine za kumsaidia kupumua.Nilimueleza Ammar kuhusu Edger kaka akasema kwamba tutakapotoka gerezani atatafuta nafasi ya kukutana na Habiba Jawad ili tuweze kumpa taarifa hiyo kuhusu Edger Kaka.Lengo kuu la kumfuata Fatma ni kumuomba atusaidie tuweze kuonana na Habiba Jawad ili nimpe taarifa za huyo mtu wake muhimu Edger Kaka.Nawal yeye alihitaji msaada wa kutafutiwa hifadhi baada ya mume wake kuuawa.Fatma alitutafutia hati za kusafiria na ndiye aliyetufikisha hapa Riyadh.Hiyo ndiyo historia yangu kwa ufupi hadi nimefika hapa kwenu” akasema Mathew “Abu Zalawi ahsante sana kwa kutupa historia yako ambayo inakuonyesha wewe ni mtu shujaa.Hongera kwa kulipua bomu lile juzi katika kituo cha treni.Hongera pia kwa kufanikisha kumtoa gerezani Ammar Nazari.Pamoja na hayo yote uliyotueleza bado kuna maswali machache tungependa kukuuliza.Umesema kwamba uliwahi kujiunga na kundi la Abu Hafs Al Masri na…” Abdel Fattah akakatishwa na Mathew “Si mimi bali ni baba yangu Khalid Al Zalawi ndiye aliyekuwa mmoja wa viongozi wa kundi hilo” akasema Mathew.Abdel Fattah akafungua moja ya faili lililokuwa mezani akasema “Hili faili mbele yangu ni la kikundi cha Abu Hafs Al Masri brigades.Majina yote ya viongozi wa kundi hilo wa sasa na waliopita yamo humu lakini sijaliona jina la Khalid Al Zalawi” akasema Abdel Fattah “Yawezekana kuna makosa katika hiyo orodha lakini Khalid Al Zalawi alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi hilo na aliuawa na vikosi vya Israel.Kutakuwa na makosa katika uandishi wa orodha hiyo ya viongozi kwani haiwezekani baba yangu asiwemo katika orodha hiyo” akasema Mathew “Orodha hii nimeipata kutoka katika ofisi kuu ya Abu Hafs Al Masri brigades na hawamfahamu mtu huyo anayeitwa Khalid Al Zalawi” akasema Abdel Fattah “Mambo yameanza kuharibika.Nilipewa taarifa hizi na Israel nizitumie na wala mtu huyo Khalid Zalawi simfahamu,hata historia yake.Hawa jamaa wanaonekana wanalifahamu kundi hili vizuri na leo hapa ninaumbuka.Lakini Israel wasingeniopa taarifa zile nizitumie kujiiunga na magaidi bila kuzifanyia kwanza utafiti.Ninachohitajikukifany akwa sasa ni kuwa na msimamo mmoja.Nikitetereka kidogo hawa jamaa watajuaninadanganya na wataniua.Ee Mungu nisadie”akawaza Mathew “Abu Zalawi hebu tueleze kidogo kuhusu baba yako Khalid Al Zalawi,maisha yake kabla hajauwa,mlikuwa mkiishi wapi nchini Misri?Marafiki zake wakuu walikuwa akina nani? Akauliza Abdel Fattah.Mathew akatabasamu kidogo na kuuliza “Nini maana yake?Hamniamii hadi nitoe maelezo hayo yote? “Jibu swali uliloulizwa Abu Zalawi” akasema Abdel Fattah na Mathew akachukau sekunde kadhaa kuyakumbuka maelekezo aliyopewa na Israel “Khalid Al Zalawi marafiki zake wakubwa ninaowafahamu ni Mohammed Atef kwa jina la utani Hafs,vile vile alikuwa na urafiki na Ayman Mohammed Rabie al Zawahiri.Marafiki zake walikuwa wengi sana na wengine siwafahamu kwa majina.Khalid alishiriki katika mashambuluo kadhaa yaliyotekelezwa na kikundi hicho cha cha Abu Hafs Al Masri brigades kwa mfano shambulio katika ofisi kuu za umoja wa mataifa Baghdad Iraq mwaka 2003,mashambulio ya mabomu katika sinagogi nchini Uturuki mwaka 2003,shambulio la bomu katika hoteli jijini Jakarta Indonesia 2003 na mashambulio mengine kadhaa” akasema Mathew “Abu umejitahidi kutoa maelezo lakini maelezo hayo uliyotoa yanahusiana na kundi la Abu Hafs Al Masri brigades na si Kahlid Al Zalawi ambaye unadai ndiye baba yako.Huna maelezo ya kumuelezea baba yako?akauliza Abdel Fattah “Nini mnakitafuta kwangu?Hamniamini haya niliyowaeleza? Mathew akawa mkali “Abu Zalawi,si kwamba hatukuamini lakini tunataka kujiridhisha na taarifa uliyotupa kwani jina la Khalid Al Zalawi halipo katika orodha ya viongozi wa kundi la Abu Hafs Al Masri brigades hivyo tunapatwa na wasiwasi kuamini kwamba kweli wewe ni Abu Al Zalawi” “Mimi ni Abu Al Zalawi” akasema Mathew “Jina lingine la baba yao alitwa nani? ‘Hakuwa na jina lingine.Jina lake ni Khalid Al Zalawi”akajibu Mathew “Abu Zalawi hatuwezi kukuamini kabisa kwa kuwa mtu unayesisitiza ni baba yako hatambuliki na hajawahi kujiunga na kundi la Abu Hafs Al Masri brigades.Umetudanganya” akasema Abdel Fattah kwa ukali “Sijawadanganya nimewaeleza ukweli” akasema Mathew. “Umetudanganya” akasema Abdel Fattah na kufungua faili lingine akamuonyesha Mathew “Huyu mtu katika hili faili ndiye Abu Al Zalawi.Umechukua jina la mtu mwingine.Ulidhani hatutagundua?akauliza Abdel Fattah kwa ukali “Hapana sijawadanganya.Jina langu ni Abu Zalawi ! akasema Mathew “Umetudanganya.Abu Al Zalawi si wewe bali ni huyu ambaye faili lake tunalo hapa.Abu Zalawi wa kweli hahusiki katika masuala yoyote ya ugaidi.Tunataka utueleze wewe ni nani? Akauliza Abdul Fattah “Mimi ndiye Abu Zalawi” akasema Mathew “Abu tunataka utueleze ukweli wewe ni nani?Tunafahamu wewe si Abu Zalawi hivyo tunataka kujua wewe ni nani? Sema ukweli”akasema Abdel Fattah “Mimi ni Abu Zalawi.Sina jina lingine”Mathew akaendelea kusisitiza Abdu Fattah akainuka na kuwapa ishara wale walinzi wawili wamtoe Mathew mle chumbani.Akavishwa mfuko ule mweusi akatolewa mle ndani na kuingizwa katika chumba kingine mikono ikafungwa katika pingu zilizounganishwa na meza nzito ya chuma mfuko ukatolewa kichwani.Mathew akakitambua kile chumba kilikuwa chumba cha mateso “Abu chumba hiki nichumba cha mateso na mara chache sana watu hutoka salama humu.Tunataka utueleze ukweli wewe ni nani? Ukisema ukweli wako tunaweza kufikiria kukupa adhabu nyingine kuliko ile ambayo unastahili kuipata kwa kutudanganya.Tunauthamini mchango wako kwa kulipua lile bomu kwenye kituo cha treni hivyo basi hatuoni sababu ya kukutesa na unaweza ukawa na msaada mkubwa kwetu lakini endapo utaendelea kusisitiza kwamba wewe ni Abu Zalawi wakati siye utaniudhi na nitaamrisha nguvu itumike” akasema Abdul Fattah “Mimi ni Abu Zalawi” akasema Mathew “Nakuuliza kwa mara ya mwisho wewe ni nani?akauliza Abdul Fattah “Mimi ni Abu Al Zalawi” Mathew akaendelea kusisitiza na mara mmoja wa walinzi aliyekuwa amesimama nyuma ya Mathew akakishika kiganja chake cha mkono akakiweka mezani na kuzamisha kisu. “Aaaaghhh !! Mathew akatoa mguno wa maumivu “Wewe ni nani?akauliza Abdel Fattah “Abu Zalawi ! akasema Mathew kisu kikiwa bado kimezama katika kiganja chake cha mkono.Yule jamaa akachomoa kile kisu na damu ikaanza kumwagika.Mathew akahisi maumivu makali “Wewe ni nani? Tueleze ukweli ! akafoka Abdel Fattah “Nimekwisha waambia mimi ni Abu Zalawi ! akasema Mathew damu ikiendelea kutoka katika kiganja chake cha mkono mara akapigwa ngumi nzito shavuni kabla hajakaa sawa akapigwa tena ngumi nyingine na damu ikaanza kumtoka mdomoni ‘Tueleze wewe ni nani?akaliza Abdel Fattah “Mimi ni Abu Zalawi ! akasema Mathew kwa ukali Mmoja wa wale jamaa waliokuwa wakimtesa Mathew akachukua kichupa kidogo akakishika kiganja cha mkono ule uliochomwa kisu akamimina kimiminika mahala penye jeraha na Mathew akafumba macho akigugumia kwa ndani maumivu makali aliyohisi. “Maumivu ni makali lakini lazima nivumilie kwa kutokuonyesha udhaifu wowote” akawaza Mathew “Jina lako nani?akauliza Abdel Fattah “Abu Zalawi ! akajibu Mathew.Mkono wake wa kushoto ukakamatwa kwa nguvu na kuwekwa mezani na Yule jamaa mwenye kisu akakizamisha katikati ya kiganja cha mkono. “Wewe ni nani?akauliza Abdel Fattah “Abu Zalawi ! Mbona hamnielewi ng’ombe ninyi?!! Akasema Mathew akiwa amepandwa na hasira huku akihisi maumivu makali.Kimiminika kutoka katika kichupa kidogo kikamiminwa mahala alipochomwa kisu na maumivu aliyoyapata hayaelezeki lakini aliendelea kuvumilia. “Wewe ni nani?Sema ukweli ili mateso haya yamalizike” akasema Abdel Fattah. “Endeleeni kunitesa lakini jina langu ni Abu Zalawi ! akasema Mathew Abdel Fattah akatoa maelekezo mengine na Mathew akavuliwa nguo na kwenda kufungwa katika wavu maalum.Akamwagiwa maji na kisha Abdul akashika nyaya za umeme akazigusanisha zikatoa cheche “Tueleze wewe ni nani?akauliza “Abu Zalawi ! akasema Mathew.Abdel akazigusisha nyaya zile katika kile chuma na Mathew akapitiwa na chaji za umeme. “Aaaagghhhh !! akagugumia kwa maumivu “Wewe si Abu Zalawi tuambie wewe ni nani?akauliza Abdel ‘Mtaniua jamani mimi ni Abu Zalawi ! Mathew akaendelea kusisitiza na Abdel akagusisha tena nyaya zile kwenye chuma na kumuuliza tena Mathew jina lake lakini aliendelea kusisitiza yeye ni Abu Zalawi.Akaamuru afunguliwe akaenda kufungwa katika meza na ndoo ya maji ikaletwa.Alifahamu kile wanachokwenda kukifanya. “Tueleze wewe ni nani?Mateso haya yataendelea hadi pale utakaposema ukweli au la utakufa ! “Mimi ni Abu Zalawi sina jina lingine” akasema Mathew na Abdel Fattah akafanya ishara mateso yaendelee.Mathew akafunikwa na taulo usoni halafu akaanza kumwagiwa maji.Alihangaika kutafuta hewa halafu taulo lile likatolewa akakohoa mfululizo “Jina lako nani? “Abu Zalawi ! akasema Mathew na zoezi lile likaendelea hadi ndoo nzima ya maji ilipomalizika lakini Mathew hakulegeza msimamo wake aliendelea kusisitiza yeye ni Abu Zalawi.Abdul Fattah akatoa tena maelekezo mengine.Mathew akachukuliwa na kufungwa mikono nyuma kwa pingu halafu akaenda kuwekwa katika pipa,maji baridi yakafunguliwa na kujazwa hadi usawa wa kifua kisha kukamiminwa dawa yenye kuwasha na pipa lile likafunikwa na mfuniko uliokuwa na sehemu ndogo ya kupitisha hewa kisha watu wale wakaondoka wakimuacha Mathew akiwashwa mwili mzima “Ee Mungu naomba nipe nguvu ya kuhimili mateso haya makali.Kama nitafariki kabla sijatimiza malengo yangu naomba unisamehe makosa yangu yote,unifutie adhabu zake na unikaribishe katika ufalme wako.Najua nimekukosea sana.NImetenda dhambi nyingi.Nimevunja amri zako.Pamoja na yote niliyokukosea lakini kuna jambo moja tu ambalo naamini nimelifanya kwa ukamilifu mkubwa nimeipenda nchi yangu ya Tanzania kwa moyo wangu wote sijawahi kuisaliti” akafanya maombi ya kimya kimya na kushindwa kuendelea baada ya muwasho kuzidi huku akishindwa kujikuna kwa kuwa mikono ilikuwa imefungwa kwa nyuma. “Je ni kweli Khalid Zalawi hakuwahi kuwa kiongozi katika kundi la Abu Hafs Al Masri brigades? Akajiuliza akia ndani ya maji “Mossad ndio walionipa taarifa zile nizitumie je walinipa bila kufanya uchunguzi na kuwa na uhakika nazo? Hapana wasingeweza kunipa taarifa ambazo hawana uhakika nazo.Naamini kabla ya kunipa taarifa zile nizitumie lazima walishafanya uchunguzi wa kutosha kujiridhisha kuhusu Khalid Zalawi.Kama ni hivyo kwa nini hawa jamaa wanaendelea kusisitiza kwamba mimi si Abu Zalawi?Yawezekana kuna kitu tayari wamekigundua ndiyo maana wanataka kufahamu mimi ni nani.Nimejileta mimi mwenyewe katika mdomo wa Mamba.Sielewi yupi ni mkweli kati ya Mossad na hawa jamaa.Kitu cha muhimu ni kuendelea na msimamo wangu ule ule hata wakinitesa vipi au hata kama wakitishia kuniua lazima niendelee kusisitiza kwamba mimi ni Abu Zalawi.” akawaza Mathew “Watu hawa ni akina nani?Fatma yuko wapi?Nawal yuko wapi? Akaendelea kujiuliza maswali Wakati Mathew akiwa katika pipa lililojaa maji ya baridi yenye kuwasha,upande wa pili wa nyumba ile Nawal naye alikuwa katika mateso makali pia.Mwili wake ulikuwa umechafuka damu.Wanawake watatu wenye sura za kikatili walikuwa wanaongoza mateso yale.Alikuwa amevuliwa nguo zote na kubaki mtupu. “Kwa nini lakini mnanitesa namna hii?akauliza Nawal “Tunataka kujua Israel walifahamu vipi mahala alipo Ammar Nazari?Kwa miaka mingi wamekuwa wakimtafuta Ammar lakini walishindwa kugundua mahala anapoishi hadi baada ya shambulio lile la bomu jijini Jerusalem” akauliza mmoja wa wale wanawake aliyeongoza mateso.Alikuwa na mikono iliyojaa na sura ya kikatili. “Nimekwisha waeleza sifahamu walifahamuje kuhusu Ammar” akajibu Nawal “Nawal umetueleza kuwa umeishi kwa muda wa miaka kadhaa na Ammar Nazari lakini kwa muda huo wote uliokaa naye Israel hawakuweza kutambua mahala alipo Ammar lakini amekuja huyu mtu Abu Zalawi na Ammar ameuawa.Tueleze ukweli kuhusu huyu mtu kwani sisi tayari tumekwisha fahamu kuwa jina analotumia si jina lake halisi” “Sikuwahi kuwa katika ngazi zozote za uongozi wa Ammar Nazari brigades hivyo siwezi kufahamu chochote kuhusu huyo mtu mnaye msema.Nilitambulishwa kwake kama Abu Al Zalawi kama ana jina lingine siwezi kujua” akasema Nawal “Baada ya kunusurika katika shambulio lile la Israel kwa nini ulimpeleka Abu Zalawi kwa Fatma? “Abu Zalawi aliniokoa na alihitaji kuonana na Habiba Jawad.Sikufahamu mahala ninakoweza kupata taarifa za Habiba Jawad ndiyo maana nikaenda kwa Fatma” “Ulifahamuje kama Fatma anamfahamu Habiba Jawad?akauliza Yule mwanamama “Mimi na Ammar tulifika nyumbani kwa Fatma mara kwa mara na hata Fatma alikuwa akifika katika makazi yetu na nilianza kuhisi labda wana mahusiano ya kimapenzi na niliwahi kumuuliza akasema kwamba Fatma humletea maagizo kutoka kwa Habiba Jawad ndiyo maana nikaenda kwake nikijua lazima atakuwa akimfahamu Habiba Jawad na anaweza akatusaidia kufika kwake:” “Nawal hukuwa na sababu yoyote ya kutaka kuonana na Habiba bali huyu jamaa Abu Zalawi ndiye aliyekupa shinikizo la kutaka umsaidie aweze kuonana na Habiba Jawad.Huyu mtu taarifa alizozitoa kwamba anaitwa Abu Zalawi si taarifa za kweli hivyo nataka utueleze ukweli huyu mtu ni nani? Kwa nini akakuokoa wewe peke yako? Kama aliweza kumtoa Ammar Nazari gerezani kwa nini alishindwa kumuokoa kutoka katika shambulio la Israel? Tueleze ukweli tafadhali ama sivyo mateso yataendelea hadi pale utakaposema ukweli” “Sifahamu chochote kuhusu Abu.Sifahamu kama amedanganya jina lake” akasema Nawal.Yule mwanamke akamnong’oneza mmoja wa wale wanawake aliyekuwa naye mle ndani,akatoka na baada ya dakika chache akarejea akiwa na mbwa mkubwa. “Nawal huyu mbwa amepewa mafunzo maalum na nitakapompa maelekezo ataanza kukuingilia.Naamini hutapenda kitu kama hicho kikutokee na hata sisi hatupendi kukufanyia kitu hicho lakini kwa kuwa umeshindwa kuonyesha ushirikiano kwetu basi hatuna budi kutumia njia hii.Nitakutaka kwa mara ya mwisho utueleze kuhusu huyu mtu anayejiita Abu Zalawi ni nani? akauliza Yule mwanamke. “Ninaomba tafadhali msinifanyie hivyo jamani.Mimi ni mwanamke mwenzenu.Nimekwisha waeleza kuwa huyu mtu mimi simfahamu vyema.Nilitambulishwa kwake kama mtu aliyemsaidia Ammar kutoka gerezani na toka hapo tulimfahamu kama mwenzetu.Sifahamu chochote kama jina hilo si lake” akasema Nawal na kutandikwa kofi kali kisha mwanamke Yule akawaelekeza wale wanawake wengine wawili wamshike vyema Nawal wakamuinamisha tayari kuingiliwa na Yule mbwa. “Nafasi ya mwisho.Tueleze kuhusu Abu Zalawi ! akafoka Yule mwanamke.Nawali alikuwa anamwaga machozi. “Jamani msinifanyie ukatili wa namna hii” “Nitahesabu mpaka tatu na kama bado hautakuwa tayari kutueleza chochote nitaamuamuru mbwa huyu akuingilie”akasema Yule mwanamke “Moja ! akaanza kuhesabu na Nawal ambaye alikuwa mtupu alikuwa ameshikwa barabara huku akilia.. “ Mbili ! akaendelea kuhesabu “Tatu ! akasema na kukunja sura akamshika shika Yule mbwa akampa maelekezo na kumuachia.Yule mbwa ambaye alimrukia Nawal kwa nyuma na kabla hajafanya chochote Nawal akalia kwa sauti “Nitasema ! Nitawaeleza kila kitu ! akasema Nawal na Yule mwaname akamuondoa Yule mbwa.Nawal alikuwa analia huku akihema kwa kasi “Haya tueleze ! akasema Yule mwanamama. “Tafadhali muondoeni huyo mbwa haraka humu ndani ! akasema Nawal huku akitetemeka. “Haondoki humu ndani.Utakaposhindwa kueleza ukweli kuhusu Abu Zalawi ataendelea na kazi yake ! akasema Yule mwanamama na Nawal akavuta pumzi ndefu mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja akaingia ndani. “Amefunguka? Akauliza Yule jamaa “Bado ila anataka kutueleza ukweli” “Abdel amesema mpeni mapumziko kwa muda.Mlowekeni katika maji hadi baadae” akasema Yule jamaa.Nawal akachukuliwa na kuingizwa katika pipa la maji yanayowasha kisha mfuniko ukafunikwa na watu wale wakatoka wakamuacha Nawal akiwashwa ndani ya maji. PARIS – UFARANSA Ndani ya chumba kikubwa chenye kuta zilizopamba kwa nakshi za kupendeza,Devotha Adolph alikuwa amekaa sofani huku katika meza ndogo mbele yake kukiwa na chupa ya mvinyo na mkononi alikuwa na sigara inayotoa moshi.Alivuta mkupuo mmoja wa sigara akapuliza moshi halafu akainua glasi akanywa funda moja la mvinyo “Lazima nijipongeze kwa kazi kubwa niliyoifanya hadi sasa.Haikuwa kazi nyepesi kuandaa mpango wa kuisambaratisha Afrika Mashariki.Kila kitu kimekaa sawa na kesho Melanie Davis anaingia Tanzania tayari kuanza kufanya kazi.Kwa mbali naanza kuhisi harufu ya ikulu.Dunia itashangaa sana pale nitakapotangazwa Rais mpya wa Tanzania.Nitaibuka kutoka kusikojulikana na kuingia ndani ya jumba lile.Hii imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu na lazima niitimize” akawaza Devotha akavuta mkupuo mkubwa na kupuliza moshi mwingi na kumbu kumbu ikamjia kichwani DAR ES SALAAM TANZANIA MIAKA MITATU ILIYOPITA Gari aina ya Landcruiser V8 liliwasili katika makazi ya Devotha likafunguliwa geti na kuingia ndani.Devotha ambaye usiku huu alikuwa amependeza vilivyo akatoka ndani na kuingia katika gari lile likaondoka.Kutoka katika makazi yake safari iliishia katika makazi ya balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Rafael Berger.Gari lilisimama karibu na kibaraza cha nyumba ile na balozi Rafael tayari alikuwepo nje ya nyumba yake kumpokea Devotha.Mlinzi akamfungulia Devotha mlango akashuka na balozi akampokea “Devotha karibu sana” akasema balozi Rafael “Nashukuru sana mheshimiwa balozi” akasema Devotha.Balozi alimuongoza hadi ndani akamtambulisha kwa familia yake.Baada ya dakika ishirini akawasili tena mtu mwingine ambaye alitambulishwa kwa Devotha kama Emmanuel Antoine.Wote wakaungana pamoja kwa chakula cha usiku kisha balozi,Devotha na Emmanuel wakawa na mazungumzo hivyo wakaenda bustanini.Bila kupoteza muda balozi akafungua mazungumzo “Devotha ninashukuru kwa kukubali mwaliko wangu na kufika hapa” akasema “Hata mimi ninashukuru kwa kunialika hapa kwako.Ni mara ya kwanza tunakutana mimi na wewe”akasema Devotha “Ni kweli ni mara ya kwanza kukutana.Hata hivyo mimi si mzungumzaji nitamuachia bwana Emmanuel aweze kuendelea” akasema balozi Rafael “Jina langu kama nilivyotambulishwa ninaitwa Emmanuel Antoine ninatokea Ufaransa na nimekuja hapa mahsusi kuzungumza nawe Devotha” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Kwa miaka mingi jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ilikuwa katika mapigano yasiyokwisha.Vikundi vya waasi vilikuwa vikiibuka kila uchao na kupambana na majeshi ya serikali.Kulikuwa na makundi mengi kama vile Alliance of Democratic Forces for the Liberation of Congo,Armed Forces of the Congolese People , Bana Mura ,Bundu dia Kongo,Congolese National Liberation Front,Forces for Renewal,Mai-Mai,March 23 Movement,Movement for the Liberation of the Congo,National Congress for the Defence of the People,Patriotic Forces for the Liberation of Congo,Patriotic Resistance Front of Ituri,Popular Front for Justice in the Congo,Rally for Congolese Democracy,Rally for Congolese Democracy– Goma,Resistance Patriots of Congo,Revolutionary Movement of the Congo,Union of Congolese Patriots.Haya ni makundi machache ambayo nimeweza kuyataja lakini yalikuwa mengi.Kwa sasa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imetulia na hakuna tena makundi ya waasi wala vita.Hata hivyo umewahi kujiuliza kwa nini makundi yote haya niliyoyataja yalikuwa yakitokea nchini Congo? Kundi moja likipotea basi liliibuka kundi lingine.Jibu ni jepesi tu kwamba makundi haya yalikuwa yanaanzishwa kwa malengo maalum na kinachosababisha haya yote kutokea kwa sababu nchi ya Congo ina utajiri mkubwa wa madini adimu kabisa duniani ambayo yanahitajika mno katika viwanda.Karibu makundi yote yanayoanzishwa ili kupambana na serikali hudhaminiwa na mataifa ya nje na kupewa silaha na zana za kijeshi na wanufaik ahuwa ni viongozi wa makundi hayo huku wapiganaji na wananchi wakibaki masikini.Ziko faida ambazo zinapatikana kutokana na mapigano hayo yanayoendelea huko Congo.Nchi zinapata masoko ya kuuza silaha na vile vile kujipatia malighafi kama vile madini adimu,maliasili za misitu nk.Nataka nikiri nchi yetu pia ni moja ya nchi ambazo zimefaidika sana na uwepo wa migogoro isiyokwisha katika nchi ya Congo” akatulia kidogo halafu akaendelea “Rais Patrice Eyenga ambaye ameingia madarakani mwaka uliopita amefanya kitu ambacho dunia haikuwa imekitegemea.Mara tu baada ya kuingia madarakani Rais Patrice amekuwa na mazungumzo na makundi ya waasi na kwa pamoja wamekubaliana kuweka silaha zao chini,kuacha mapigano na kuijenga upya nchi yao.Mabadiliko makubwa yamefanyika nchini Congo.Makampuni mengi yaliyokuwa yamewekeza nchini Congo katika sekta ya madini yamefurushwa na wametafutwa wawekezaji wengine wapya.Kiujumla nchi ya Congo imeanza kupiga hatua kiuchumi.Kupatikana kwa amani na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika kusimamia rasilimali za Congo zimetuathiri sisi mataifa makubwa ambao kwa kiasi kikubwa tulikuwa tukitegemea rasilimali hizo kutokana na mapigano ya serikali na vikosi vya waasi na sasa mshirika mkubwa wa Congo ni China na ndiye anayeuziwa madini muhimu yanayohitajika sana katika utengenezaji wa vifaa mbali mbali vya kielektroniki” akanyamaza kwa muda akamtazama Devotha “Tunajitaji malighafi kwa viwanda vyetu vya kutengeneza vifaa vya kielektroniki ambayo ni madini.Ni China pekee ambayo inapata kiasi kikubwa cha madini hayo kutoka Congo hivyo tunataka kutafuta njia ya kutuwezesha kupata tena madini hayo kutoka Congo.Njia pekee inayoweza kutuhakikishia kupata tena mafuriko ya madini ni kwa kuanzisha tena machafuko.Pale amani itakapopotea ndipo nasi tutaingia na kupeleka vikosi vya kulinda amani.Tutawezaje kuivuruga amani ya Congo? Hilo ni swali ambalo limenileta hapwa kwako kutafuta majibu” akasema Emmanuel na kunyamaza “Mimi ninahusiana nini na suala hilo?Mimi si raia wa Congo.Sina mahusiano yoyote na Congo” akasema Devotha “Nimekuja kwako kwa sababu tuna mpango kubwa wa kuvuruga amani na kuleta machafuko tena Congo na wewe ndiye utakayeongoza mpango huo” akasema Emmanuel na Devotha akapatwa na mshangao “Mimi?! Akauliza Devotha “Ndiyo.Wewe ndiye ambaye tumekuchagua uongoze harakati hizo za kuleta tena machafuko Congo” “Emmanuel nadhani umekosea kunichagua mimi niwafanyie kazi hiyo.Mimi sina uwezo wowote wa kuweza kuvuruga amani na kuleta machafuko nchini Congo” akasema Devotha “Devotha Adolph sijakosea kuja kwako na wala hatujakosea kukuchagua.Tulihitaji mtu ambaye anaweza akaifanya kazi hiyo kwa ufanisi na wewe umetokea kuwa na sifa za mtu tunayemuhitaji”akasema Emmanuel “Sifa zipi?akauliza Devotha “Tumefanya utafiti wetu na tukagundua historia yako inaonyesha uliwahi kulipukiwa na bomu nchini Kenya na kupoteza familia yako ukapelewa nchini Marekani ambako ulipatiwa matibabu na baadae ulipata mafunzo ya kijasusi ulifanya kazi na idara ya kupambana na ugaidi Marekani na rekodi zinaonyesha ulifanya vizuri sana na baadae ulikuja Tanzania na taarifa tulizo nazo ni kwamba unaongoza idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi” akasema Emmanuel na Devotha akabaki ameduwaa “Tuishie hapo Devotha tunafahamu kila kitu kuhusu wewe hivyo tunataka uandae mpango ambao utaifanya nchi ya Congo iweze kuzama tena katika machafuko na vile vile mpango ambao utaweza kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki” “Emmanuel hapana.Siwezi kufanya hivyo”akasema Devotha “Unaweza Devotha.Nisingeweza kuja kwako kama sina uhakika unaweza kufanya jambo hilo.Usihofu tunajua kitu tunachokutaka ukifanye ni cha hatari kubwa lakini malipo yake ni makubwa pia.Umeandaliwa jumba kubwa la kifahari jijini Paris.Kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinaweza kukuwezesha ukaishi kifahari miaka kumi na tano bila kufanya kazi yoyote.Kama haitoshi kila mwezi utakuwa ukipokea asilimia mbili ya madini yatakayokuwa yakipatikana kutoka nchini Congo.Hayo ni machache tu ambayo tuko tayari kukupatia lakini yako mengine mengi” akasema Emmanuel na Devotha akabaki kimya kwa muda wa dakika tatu hadi Emmanuel alipomstua “Devotha nahitaji kusikia maoni yako” akasema Emmanuel “Sihitaji hivyo vyote ulivyovitaja” akasema Devotha na Emmanuel akashangaa “Devotha wewe ni binadamu wa kwanza kukataa utajiri mkubwa kiasi hicho” akasema Emmanuel “Nahitaji kitu kingine”akasema Devotha “Nini unahitaji?akauliza Emmanuel. “Ndoto yangu kubwa ni kuingia katika siasa.Nataka nishike madaraka makubwa.Nataka niwe Rais wa Tanzania.Kama mnaweza mkanisaidia katika hilo mimi pia nitakuwa tayari kuwasaidia katika mpango wenu” akasema Devotha na Emmanuel akatabasamu “Devotha u mwanamke wa kipekee kabisa.Wanawake wengi wa aina yako wangechagua pesa na mali nyingi lakini wewe umekataa hivyo vyote na umechagua madaraka.Ninakupongeza sana kwa hilo.Nikuweke wazi kwamba asilimia kubwa ya siasa za bara la afrika zina shinikizo kutoka nje.Nchi nyingi za magharibi kwa sasa zinawekeza katika siasa za bara la Afrika kwa kutafuta wagombea wao na kuwasaidia kuwaweka madarakani ili wawe na manufaa kwao.Wanafanya hivyo kutokana na utajiri mkubwa wa bara hili.Kumekuwa na wimbi hivi sasa la mapinduzi barani Afrika unadhani ni kweli wananchi ndio wanaoanzisha mavugu vugu hayo ya kuwatoa viongozi madarakani?La hasha.Wapo watu ambao huanzisha vuguvugu hizo na kuwashawishi wananchi kwa ahadi ya maisha bora kama wangefanikiwa kuwatoa viongozi wao madarakani na wananachi kwa kutokujua kwao kilicho nyuma ya pazia huingia mitaani kuandamana na lengo lao hutimia lakini hakuna mabadiliko yanayotokea katika maisha yao kama walivyoahidiwa.Sitaki nikupe mifano wewe mwenyewe unafahamu kinachoendelea barani Afrika hivi sasa.Nimekwambia hayo ili upate picha kwamba siasa za bara la Afrika zimetawaliwa na nchi kubwa na wao huamua nani awe Rais.Vyama pinzani hupewa sapoti kubwa kwa kuanzisha vurugu,kuwahadaa wananchi waione serikali yao haifai na mambo mengine mengi.Devotha itoshe tu kusema kwamba sisi mataifa makubwa tunalitawala bara la Afrika lakini si moja kwa moja kama ilivyokuwa enzi zile za ukoloni bali tunatawala kwa kuwatumia waafrika wenyewe tena wazawa wa nchi hiyo hiyo.Kujibu ombi lako sisi hatuna tatizo na ombi lako.Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo bado siasa zake hazijaweza kuingiliwa na mataifa ya nje kiasi cha kuthubutu kuwachagulia nani awe rais wa nchi lakini kwa kuwa umeliomba tutaanza kulifanyia kazi kwani uwezo huo tunao.Nitaliwasilisha ombi lako kwa wenzangu tutaanza kulifanyia kazi.Halitakuwa jambo la haraka kwani lazima kwanza tuanze kujipenyeza taratibu katika siasa za nchi hii” akasema Emmanuel Kumbu kumbu ile ikamfanya Devoitha atabasamu akamimina mvinyo na kunywa “I chose power over money.Hivi sasa ningekuwa mtu tajiri mno kwa ahadi zile ambazo niliahidiwa lakini mimi ndoto yangu kubwa ni siku moja kuingia ndani ya lile jumba jeupe pale kandoni mwa bahari.Nataka niwe kiongozi wa watu zaidi ya milioni hamsini.Nataka niheshimike nataka watu hasa wanaume wanaowadharau na kuwaona wanawake ni viumbe dhaifu waione nguvu ya mwanamke pale nitakapotwaa madaraka.Nafurahi baada ya maandalizi ya muda mrefu kupanda na kushuka kwingi lakini sasa mipango imeanza kwenda vizuri na ninaelekea katika kuitimiza ndoto yangu na siku moja nitaitwa mheshimiwa Rais Devotha Adolph” akawaza na uso wake ukajenga tabasamu kubwa akainua glasi yake akanywa tena funda lingine kubwa halafu akasimama “Sipati picha siku hiyo nimeshika kitabu cha dini kati kati ya maelfu ya watu uwanjani nikiapa kuwa Rais wa Tanzania.Mimi Devotha Adolph naapa kwamba…”akatolewa mawazoni simu yake ilipoita.Akaichukua na kutazama aliyempigia alikuwa ni Edwin Mbeko akaipokea haraka “Hallow Edwin” akasema Devotha “Madam habari za huko? “Huku kwema kabisa.Unasemaje? “Nimekupigia kukujulisha kwamba leo nilikuwa na mazungumzo na Rais.Kikubwa alinisisitiza kwamba kipaumbele cha SNSA kwa sasa ni kuhakikisha mkutano wa kimataifa wa wake za marais unafanyika kwa amani na utulivu.Nimemuhakikishia kwamba hakutakuwa na tatizo lolote” akasema Edwin “Safi sana Edwin kwa kunipa taarifa.Melanie anatarajia kutua kesho hapo Tanzania hivyo basi hakikisha kila kitu kinakwenda vizuri.Wewe ndiye utakayekuwa msimamizi wake mkuu kwa upande huo na kama kuna chochote kitashindwa kwenda vizuri basi lawama zitakuwa juu yako” “Usijali madam maandalizi ni makubwa na hakutakuwa na tatizo lolote.Kila kitu kiko vizuri” akasema Edwin “Edwin operesheni hii ni muhimu sana na hakuna makosa yanatakiwa kufanywa.Kila kitu kiende kama kilivyopangwa.Liweke hilo katika akili yako na uliimbe kila siku katika mdomo wako.Umenielewa lakini? “Nimekuelewa madam usihofu” “Kuna shida nyingine yoyote,fedha au kitu chochote? “Hakuna madam.Kila kitu kipo na kama nikihitaji kitu nitakujulisha” “Ahsante Edwin” akasema Devotha na kukata simu





Mashuka yote na mito vilivyokuwa kitandani vilianguka chini kuashiria kwamba kulikuwa na shughuli pevu iliyofanyika mle chumbani.Mwangaza ulikuwa hafifu na muziki wa ala ulisikika kwa mbali.Kitandani Gosu Gosu na Melanie Davis walikuwa wamejilaza wamejipumzisha baada ya mtanange mzito.Melanie alikuwa anakichezea kifua cha Gosu Gosu “Gosu Gosu sijui nikueleze nini mpenzi wangu kwa raha unazonipatia.Ninapenda kufanya mapenzi na haijawahi kunitokea hata siku moja nikatosheka na kusema basi lakini kwako ninatosheka hadi ninasema basi.Wewe ni wa kipekee kabisa” akasema Melanie na Gosu gosu akatabasamu huku akizichezea nywele ndefu laini za Melanie “NInakwambia kweli Gosu Gosu.Hakuna mwanaume ambaye aliwahi kutembea na mimi akaniridhisha zaidi yako.Nimekupata na sitaki nikupoteze tena.Kuna kitu nataka nikwambie Gosu Gosu lakini naoma usistuke wala usikasirike” “Niambie chochote Melanie usiogope”akasema Gosu Gosu..Melanie akavuta pumzi ndefu na kusema “Kama nilivyokwambia kwamba nimehangaika kwa muda mrefu kukupata mtu kama wewe na nimefanikiwa kukupata hivyo sitaki kukupoteza.Nataka mimi nawe tuishi miaka mingi”akanyamaza na kumtazama Gosu Gosu na kumkumbatia akambusu “Nataka tufunge ndoa” akasema Melanie na kukilaza kichwa chake katika kifua cha Gosu Gosu.Zilipita dakika tano Melanie akainua kichwa chake na kuuliza “Umenisikia Gosu Gosu? “Nimekusikia lakini nilikuwa natafakari jibu gani nikupe” “Hujapendezwa na wazo langu?Don’t you love me Gosu Gosu? “Wazo lako si baya na kuhusu kukupenda usiwe na shaka ninakupenda mno Melanie lakini imekuwa haraka sana.Kwa nini tusilipe muda suala hili? “C’mon Gosu Gosu nini kinakuogopesha? We have everything in life.Sisi ni matajiri wakubwa kwa nini tuendelee kusubiri? Nataka nikuweke juu sana Gosu Gosu.Nataka nikuamini uwe ndiye taa yangu ya kuniongoza uwe msimamizi wangu wangu wa kila kitu kuanzia mwili wangu hadi biashara.Nataka tufunge ndoa tuwe mwili mmoja tuishi pamoja tupate watoto” akasema Melanie “Melanie mpenzi wangu nakupenda sana.Kwangu mimi mpaka leo sijaamini kama kweli nimeweza kukupata malaika kama wewe na nitaendelea kumshukuru Mungu kwa kukuleta katika maisha yangu.Kwa muda huu mfupi niliokuwa nawe nimepata furaha ya ajabu ambayo sijawahi kuipata maishani.Kunitaka tufunge ndoa kunaonyesha ni namna gani unavyonipenda na ninatamnai sana kusema ndiyo kwa ombi lako hilo lakini kuna mambo yananifanya nisite kusema ndiyo” “Nini kigumu Gosu Gosu?Una mwanamke mwingine tayari? “Hapana sina mwanamke mwingine” “Nini basi kinakupa ugumu Gosu Gosu kama huna mwanamke mwingine?akauliza Melanie “Melanie kinachonipa wasiwasi ni historia yangu ya huko nyuma ambayo inanifanya nihofie kusema ndiyo kwani yawezekana huko mbeleni nisiwe mume mzuri au baba mzuri kama tukifanikiwa kuwa na mtoto” akasema Gosu Gosu “Historia ipi Gosu Gosu.Nieleze tafadhali kwani mapenzi yetu ni ya wazi hakuna kufichana kitu” akasema Melanie.Gosu Gosu akafumba macho akafikiri kwa muda na kumuelekeza Melanie historia yake namna alivyochukuliwa akiwa mtoto mdogo na kupelekwa msituni kupigana vita. “Dah pole sana Gosu Gosu.Sikujua kama historia yako iko namna hii” akasema Melanie huku macho yake yakilengwa na machozi “Hiyo ndiyo sababu kuu iliyonifanya hadi sasa nisiwe na mke au watoto.Ninahofia naweza nisiwe mume au baba mzuri” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu pamoja na hayo yote uliyonieleza umeyapitia lakini sasa yamekwisha.Wewe ni Gosu Gosu mpya.Ninakupenda vile ulivyo.Sijali umewahi kuua watu wangapi lakini ninataka kuwa nawe.Niko tayari kuvumilia kila kitu hata kama hautakuwa mume mzuri kwa sababu nakupenda sana Gosu Gosu na lengo langu ni ili tutakapofika Dar es salaam tayari niweze kuishi nawe pamoja.Hata hivyo siwezi kukuharakisha kufunga ndoa ila nitakuomba ulitafakari jambo hili kwa kina na unipe jibu.Niko tayari kusubiri jibu lako hata kama itachukua miaka kwa sababu wewe ndiye mwanaume wa pekee kabisa kwangu”akasema Melanie “Ahsante sana Melanie kwa kunionyesha ni namna gani unanipenda hadi kuamua kutaka kufunga nami ndoa.Ahsante pia kwa kunipa muda ili niiweke sawa akili yangu kwa jambo hili kubwa na ninakuahidi pale nitakapokuwa tayari nitakujulisha”akasema GosuGosu na Melanie akamkumbatia akambusu “Nitatumia kila njia hadi nikuweke katika chupa niwe ninakuamuru kufanya kitu chochote na utatii.Nataka niwe mfalme wako nawe uwe mtumwa wangu kila nitakachokutuma lazima ukifanye” akawaza Melanie RIYADH – SAUDI ARABIA Mlango ulifunguliwa na wale jamaa wakaingia tena ndani ya kile chumba ambamo Mathew alikuwa amewekwa katika pipa.Watu wawili wakamnyanyua na kumtoa wakamtupa chini na kummwaga maji baridi kwa kutumia mpira.Mathew hakuwa na nguvu na mwili wake ulikuwa umevimba kutokana na ile kemikali ya kuwasha.Baada ya kumwagiwa maji akapelekwa tena katika kile chumba cha mahojiano akafungwa katika kiti “Nadhani tayari umepumzika vya kutosha na sasa tunaanza awamu ya pili.Tueleze wewe ni nani?Usiniambie wewe ni Abu Zalawi kwani Abu Zalawi ni huyu ambaye tunalo faili lake hapa” akasema Abdel Fattah.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema “Mimi…ni..aaah !akashindwa kuongea na kuinaisha kichwa.Abdel Fattah akamnasa kofi zito “Tafadhali zungumza ! akafoka Abdul “Mimi ni Abu Zalawi.Hata mkiniua bado hamtaweza kubadili jina langu.Nimechoka sasa kuteswa bila kujua kosa langu.Naombeni mniue kwani sikuja hapa kwa ubaya.Ninataka nimjulishe Habiba Jawad kuhusu mahala alipo Edger Kaka .Kama mnamfahamu mnaweza mkamfikishia ujumbe kwamba Edger Kaka yupo katika hospitali moja jijini Tel Aviv na ni mgonjwa sana.Hicho ndicho kilichonifikisha hapa lakini badala yake mnanitesa bila kosa.Naombeni mniue niko tayari” akasema Mathew, na Abdel Fattah akamtandika ngumi nzito na damu nyingi ikaanza kumtoka mdomoni.Wakati akijiandaa kurusha ngumi nyingine mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja akamueleza kwamba kuna simu yake ya muhimu.Abdul akatoka na kuwaacha watu wale wakiendelea kumpiga Mathew.Baada ya dakika tatu Abdul akarejea na kuwataka wasiendelee kumpiga Mathew.Akaelekeza wamfungue wakamvalisha kanzu ya kijivu na kumuingiza katika gari akiwa amevalishwa mfuko kichwani na gari lile likaondoka.Baada ya mwendo wa saa moja gari lile likaingia katika nyuma Fulani kisha haraka haraka Mathew akashushwa na kuingizwa ndani ya ile nyumba akapelekwa katika chumba akalazwa katika kitanda na ule mfuko aliofunikwa kichwani ukatolewa akajikuta katika chumba chenye vifaa vingi vya hospitali.Macho yake yakaanza kupunguza taratibu nguvu ya kuona na kitu cha mwishoi alichokiona ni sura ya mwanamke aliyevaa koti jeupe akimuinamia akimsemesha lakini Mathew hakuweza kufumbua mdomo wake kujibu chochote.





Mathew alifumbua macho na kujikuta katika chumba kizuri kilichosheheni vifaa mbali mbali vya matibabu.Alikuwa amelala juu ya kitanda cha wagonjwa na mkononi alikuwa na mpira wa chupa ya maji iliyokuwa inaning’inia katika chuma.Kulikuwa na mashine kadhaa zikionyesha mifumo mbali mbali ilivyokuwa ikifanya kazi katika mwili wake. “Nimeletwa hospitali” akawaza na kujaribu kujigeuza lakini alihisi maumivu katika sehemu bali mbali za mwili wake “Walinitesa sana wale jamaa wameniumiza kila sehemu” akawaza na kujaribu kujiinua ili akae kitandani lakini mgongoni kote alikuwa na vidonda vilivyosababishwa na kipigo alichokipata “Watu hawa watakuwa wamegundua mimi si Abu Zalawi na ndiyo maana walinitesa sana ili niwaeleze mmi ni nani.Yawezekana tayari wamekwisha fahamu mimi ni pandikizi na ni sababu ya Ammar Nazari kuuawa na Israel.Natakiwa kutafuta namna ya kujiokoa kutoka kwa hawa jamaa haraka sana ama sivyo wataniua.Walinileta hapa baada ya kuogopa ningeweza kupoteza maisha.Hii ni fursa ambayo natakiwa kuitumia kutoroka.Nawal yuko wapi?Siwezi kuondoka hapa nikamuacha lazima nijue mahali alipo ili niondoke naye.Nitatafuta namna nyingine ya kumtafuta Habiba Jawad” akawaza Mathew na mara mlango ukafunguliwa akaingia mwanadada mmoja aliyevaa koti jeupe la daktari.Alikuwa ameongozana na muuguzi mmoja na watu wawili wenye silaha. “la bas ya shabab , yumkinuk albaqa' fi alkharij” Yulke daktari akawaambia wale jamaa wenye silaha watoke nje na kisha akamsogelea Mathew “Naitwa Abiha Seif,ndiye daktari ninayekuhudumia.Nataka kujua unajisikiaje?akauliza Dr Abiha kwa sauti laini. “Nahisi maumivu makali kila sehemu ya mwili.Nimeumizwa sana.Kichwa kinaniuma mno”akasema Mathew “Pole sana” akasema Dr Abiha na kumuelekeza muuguzi kuondoa ile chupa ya maji aliyotundikiwa Mathew ambayo ilikaribia kumalizika na kumuelekeza akalete dawa Fulani “Uliletwa hapa jana usiku ukiwa hujitambui,nashukuru kwa sasa hali yako inaendelea vizuri” akasema Dr Abiha huku akitazama mashine ya kuonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo akachukua kiti na kuketi karibu na kitanda cha Mathew “Jina lako nani?akauliza Dr Abiha “Naitwa Abu Zalawi”akajibu Mathew “Abu Zalawi.Nimefurahi kukufahamu.Watu wale waliokuleta hapa jana unawafahamu? “Hapana siwafahamu lakini mmoja alijitambulishwa kwangu anaitwa Abdel Fattah Sarraf” “Ni wao ndio waliokutesa namna hii?akauliza http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Dr Abiha “Ndiyo ni wenyewe.Unawafahamu? akauliza Mathew “Ilikuaje ukajikuta mikononi mwa hawa jamaa? Nieleze ukweli tafadhali”akasema Dr Abiha “Nilifika hapa nikitokea Palestina nikiwa na mwenzangu ambaye sifahamu yuko wapi hivi sasa tukimtafuta mtu Fulani.Tulikuwa tumeongozana na mtu ambaye anamfahamu huyo mtu tuliyemfuata hapa.Mimi na huyo mwenzangu ni wageni katika jiji hili la Riyadh hivyo tulimtegemea mwenyeji wetu tuliyekuwa tumeongozana naye na kwa kuwa tulifika hapa jijini usiku alitupeleka katika nyumba Fulani tukalala hadi asubuhi na yeye hatukumuona tena.Nilichukuliwa na kuingizwa katika gari na watu ambao nilidhani wametumwa na Yule mwenyeji wetu na kupelekwa sehemu ambako nilikutana na Abdel Fattah Sarraf na wenzake na wakaanza kunipa mateso” akasema Mathew “Kwa nini walikutesa?akauliza Dr Abiha Mathew akabaki kimya “Usiogope kunieleza ukweli mimi naweza kuwa rafiki yako na msaada mkubwa kwako” akasema Dr Abiha “Kuna mambo walitaka kuyafahamu kuhusu mimi na tuliposhindwa kuelewana wakaanza kunitesa” “Mambo gani walitaka kuyafahamu kuhusu wewe? “Walitaka kufahamu jina langu na kwa nini niko hapa nikawatajia jina langu lakini wakasisitiza kwamba hilo si jina langu na wakanitaka niwaeleze jina langu halisi na ndipo walipoanza kunitesa” “Kwa nini hawakuamini ulipowatajia jina lako?Kuna kitu wanakifahamu kuhusu wewe?akauliza Dr Abiha “Sifahamu kwa nini walikuwa na wasiwasi nami.Wamenitesa sana wakinilazimihsa nikatae jina langu na nikubali kuwa mimi ni mtu mwingine jambo ambalo sikuwa tayari kulikubali.Nilikuwa tayar kufa kuliko kulazimishwa kukana jina langu” akasema Mathew “Pole sana Abu Zalawi kwa mateso makali uliyoyapata.Naomba nikuweke wazi kwamba umeingia katika mikono ya watu hatari sana na ambao wanaweza wakakuua muda wowote.Abdul Fattah anaongoza genge hatari na ni mtu anayeogopwa sana.Nyumba hii inamilikiwa na kundi lake na mimi huwa ninaletwa hapa kuhudumia wagonjwa mbali mbali wanaoletwa hapa wakiwa na hali mbaya kutokana na mateso wanayoyapata.Ninakuonea huruma sana hupaswi kuteseka kiasi hiki.Ninaweza kukusaidia” akasema Dr Abiha na kufunga dirisha kisha kwa sauti ndogo akamuuliza Mathew “Kuna walinzi hapo nje sitaki wasikie mazungumzo yetu.Una hati ya kusafiria? “Ndiyo ninayo lakini kila kitu kitu kimebaki katika nyumba ile ambayo tulifikia usiku ule” akasema Mathew “Unaweza ukakumbuka mahala hapo ni wapi? “Mimi ni mgeni hapa Riyadh hivyo siwezi kupakumbuka mahala hapo” “Natamani sana kukusadia Abu Zalawi kuondoka hapa lakini sifahamu nitakusaidiaje bila kuwa na hati ya kusafiria.Kama ungekuwa nayo ningeweza kukusaidia ukaondoka hapa nchini na kurejea ulikotoka.Kwani unatokea nchi gani? “Ninatokea Palestina” “Wewe ni mpalestina?akauliza Dr Abiha “Hapana mimi si mpalestina.Asili yangu ni Misri” akasema Mathew “Kama nikitaka kukusaidia uweze kuondoka hapa nchini unataka kuelekea nchi gani?akauliza Dr Abiha “Dr Abiha kuna mtu niliyekuja kumtafuta hapa Riyadh na siwezi kuondoka hapa bila kuonana naye.Ni muhimu sana nikaonana naye” “Ni nani huyo unayemtafuta? “Namtafuta mtu anaitwa Habiba jawad” “Habiba jawad? “Ndiyo.Unamfahamu? “Hapana ila nimewahi kumsikia sikia.Una shida gani na huyo Habiba Jawad? “Ninazo taarifa muhimu sana za kumpa” akasema Mathew na Dr Abiha akaonekana kama kuna kitu anakikumbuka halafu akasema “Huyu Habiba unayemtaja kwamba umekuja kumtafuta hapa Riyadh nimewahi kusikia akitajwa kujihusisha na masuala ya ugaidi.Samahani kuuliza je wewe nawe unajihusisha na masuala hayo?akauliza Dr Abiha na Mathew akawa kimya “Usihofu Abu Zalawi unaweza ukaniamini” “Sifahamu kama Habiba anajihusisha na masuala ya ugaidi lakini kuna jambo lingine kabisa ambalo nataka kuzungumza naye.Kama unataka kunisaidia nisaidie niweze kuonana na Habiba Jawad.Hata kama si yeye bali hata mtu wake wa karibu” akasema Mathew “Nitaangalia kama nitaweza kukusaidia kwa hilo lakini utaendelea kukaa hapa hapa hospitali kwa siku tatu au zaidi ili kuuguza majeraha haya makubwa uliyoyapata.,Jumba hili limezungukwa na walinzi kila sehemu hivyo usithubutu kutaka kutoroka.Mimi ndiye ninajua namna gani nitakusaidia kutoroka mahala hapa hivyo fuata maelekezo yangu” akasema Dr Abiha. “Ahsante sana Dr Abiha lakini kama sintakuwa ninakusumbua naomba unisaidie kufahamu mahala alipo mwenzangu niliyekuja naye anaitwa Nawal” “Sawa nitakusaidia kutafuta taarifa zake” akasema Dr Abiha na kutoka mle ndani DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa mbili za usiku ndege ya shirika la ndege la Ufaransa ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea Paris kupitia Nairobi Kenya.Miongoni mwa Abiria waliokuwamo ndani ya ndege hii ni Melanie Davis na Gosu Gosu.Baada ya kushuka ndegeni walikamilisha taratibu za uhamiaji na kisha wakaruhusiwa kuingia nchini.Mara tu walipotokeza sehemu ya abiria wanaowasili mwanamke mmoja aliyevaa suti nyeusi akamfuata Melanie.Alikuwa na uso wenye tabasamu “Melanie Davis.Karibu sana Dar es salaam” akasema Yule mwanamke na kumsaidia Melanie kusukuma torori lenye mabegi yake.Melanie akaitumia nafasi hiyo kuzungumza na Gosu Gosu “Gosu Gosu ningetamani sana kama ningeongozana nawe usiku wa leo lakini wenyeji wangu hawatakubali.Hata hivyo tutaonana kesho tayari kuanza kazi” akasema Melanie na kumbusu Gosu Gosu “Usijali Melanie tutakuwa na muda mrefu sana pamoja” akasema Gosu Gosu na Melanie akamfuata Yule mwanadada aliyekuja kumpokea hadi katika gari wakaondoka pale uwanjani.Gosu Gosu hakuwa amemjulisha mtu yeyote kama angerejea siku hii hivyo akachukua taksi na kuondoka kuelekea nyumbani kwake “Kwa siku hizi chache nilizokuwa Paris na Melanie nimekuwa Gosu Gosu mpya.Nimekuwa mwenye furaha na kujiamini zaidi.Melanie amenifanya niyafurahie maisha.Hapo awali nilikuwa ninaishi tu ili mradi siku zinasonga lakini baada ya kukutana na Yule mtoto malaika nimeonja raha ya maisha.Ninamshukuru sana Peniela kwa kuniunganisha na mtoto Yule ambaye imetokea bahati tu kumpata” akawaza Gosu Gosu na kutabasamu akayakumbuka mazungumzo yake na Melanie usiku uliopita kuhusu kufunga ndoa “Gosu Gosu pamoja na hayo yote uliyonieleza umeyapitia lakini sasa yamekwisha.Wewe ni Gosu Gosu mpya.Ninakupenda vile ulivyo.Sijali umewahi kuua watu wangapi lakini ninataka kuwa nawe.Niko tayari kuvumilia kila kitu hata kama hautakuwa mume mzuri kwa sababu nakupenda sana Gosu Gosu na lengo langu ni ili tutakapofika Dar es salaam tayari niweze kuishi nawe pamoja” “Melanie alinistukiza kwa ombi lile la kutaka tufunge ndoa.Sikuwa nimelitegemea kabisa kulisikia kutoka katika kinywa chake.Naamini ni kwa sababu ya mapenzi mazito niliyompatia ndiyo maana hataki kuishi mbali nami” akawaza na kutabasamu tena “Melanie anapenda kufanya mapenzi na ndiyo starehe yake kubwa na ukimpata mtoto kama yule lazima uwe na uwezo mkubwa wa kumridhisha.Hapa kwangu amefika kwani ninampeleka hadi mbingu ya saba mpaka yeye mwenyewe anasema imetosha na hicho ndicho kimempagawisha na kumfanya atangaze ndoa.Melanie hajui kama mimi pia nimeoza kwake.Sijawahi penda katika maisha yangu kama ninavyompenda Melanie.Amenifanya niyafurahie mapenzi.Natamani kama ningekuwa naye usiku huu,nahisi kama huko aliko kuna watu watamuiba” akatabasamu “Huu ni wivu tu unanisumbua.Sipaswi kuwa na hofu yoyote.Melanie ni wangu na atakuwa wangu peke yangu.Ninaapa yeyote ambaye atajipendekeza aidha kwa cheo chake au mali zake atakutana na mimi na nitamuondoa uhai.Sitaki mtu aniingilie katika mapenzi yangu” akaendelea kuwaza Gosu Gosu Alifika nyumbani na kupokewa na watumishi wake akaenda kuoga na kuandaliwa chakula “Naona hadi chakula si kitamu.Nimezoea Paris kula na Melanie au Peniela lakini hapa ninakula peke yangu.Nyumba imepoa sana hii nitazungumza na Melanie ili walau mara mbili au tatu kwa wiki awe akilala hapa.Najua hawezi kukataa” akawaza Gosu Gosu akiendelea kupata chakula na alipomaliza akaenda chumbani kujipumzisha Gari alimopanda Melanie Davis kutoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere liliingia katika moja ya mtaa wenye majumba makubwa eneo la Kisamawati.Hili ni eneo tulivu lililoko karibu na bahari ya Hindi.Ni eneo ambalo linajulikana kwa jina lingine kama kijiji cha mabilionea kutokana na wengi wanaoshi eneo hili kuwa ni wafanya biashara na matajiri wakubwa.Yule mwanamke aliyekuwa akiendesha gari akapunguza mwendo na kukata kulia akashika njia iliyoelekea katika jumba moja kubwa lililokuwa linawaka taa nyingi.Walipolikaribia geti Yule mwanamke ambaye alijitambulisha kwa Melanie anaitwa Joyce alitoa kiunga mbali akakielekeza katika geti likaanza kufunguka taratibu gari likaingia ndani geti liajifunga.Gari likasimama mbele ya jumba lile kubwa na zuri la ghorofa mbili . “Melanie karibu sana Dar es salaam.Hali ya hewa hapa ni joto tofauti na Paris” akasema Joyce “Nimewahi kuishi hapa hivyo ninaifahamu hali ya hewa ya jiji hili” akajibu Melanie.Mabegi yakashushwa toka ndani ya gari na mlango ukafunguliwa wakaingia ndani “Melanie hii ndiyo nyumba yako utakayokuwa ukiishi.Ni nyumba ya ghorofa mbili.Eneo hili linaitwa Kisamawati au kwa jina maarufu lililozoeleka hapa mjini ni kijiji cha mabilionea.Wanapaita hivyo kutokana na wengi wanaoishi eneo hili kuwa ni watu wenye uwezo mkubwa kifedha” akasema Joyce “Ni eneo tulivu sana.Nimepapenda” akasema Melanie “Ni kweli ni eneo tulivu sana na ukiwa hapa katika jumba hili bahari haiko mbali.Waweza siku moja ukaamua kutembea kwenda kupumzika baharini.Tumechagua uishi katika nyumba hii kwa sababu za kusalama” “Ahsanteni sana kwa kuchagua nyumba hii.Ninapenda kuishi karibu na bahari” akasema Melanie kisha Joyce akamuomba amtembeze katika sehemu mbali mbali za jumba lile. “Kama nilivyokueleza jumba hili ni kubwa na lina vyumba vingi.Kuna sebule tatu moja ya kawaida nyingine ya wageni muhimu na moja ya kwako na wageni wako binafsi.Kuna vyumba vitano vya kulala na vyote vinajitosheleza kila kitu ndani.Vipo vyumba vingine vinne vya kulala ambavyo ni vya kawaida.Kuna majiko mawili na wewe una jiko lako binafsi linalojitegemea.Kuna chumba cha mazungumzo ya faragha,vyumba viwili vya mapumziko,chumba cha filamu,chumba cha muziki ambamo kuna piano kubwa.Kuna chumba cha mazoezi na vile vile kuna saluni yako.Huna haja ya kwenda katika saluni za kulipia.Nje kuna bwawa kubwa la kuogelea na sehemu za kupumzikia vile vile kuna bustani nzuri” akasema Joyce na kumtembeza Melanie katika sehemu mbali mbali za jumba lile “Melanie jumba hili halina mlinzi lakini limezungukwa na kamera za siri za ulinzi.Ukiwa chumbani kwako unaweza ukafuatilia kujua kila kinachoendelea ndani na nje ya nyumba yako.Ukiwa chumbani kwako mtu yeyote ambaye atafika katika geti la nyumba yako utajulishwa na utaamua kumkaribisha ndani kwa kumfungulia geti au kutomfungulia.Kwa ufupi ni kwamba nyumba hii ina mfumo mkubwa wa ulinzi na huhitaji mlinzi.Kuna silaha zimefichwa sehemu na kama kuna hatari yoyote unaweza ukamshambulia yoyote kwa kutumia silaha zilizofichwa ukiwa chumbani kwako hivyo ukiwa hapa usiwe na wasiwasi kuhusu usalama wako.Uko salama sana” akasema Joyce na mara ukasikika mlio Fulani “Huo ni mlio kuashiria kwamba kuna mtu getini na ukiangalia katika Runinga kweli kuna mtu na huyu ni Edwin Mbeko” akasema Joyce na kumuelekeza Melanie namna ya kuutumia mfumo ule.Joyce akashuka chini kwenda kumpokea Edwin na kumpeleka juu katika sebule ya Melanie. “Melanie karibu sana Dar es salaam” akasema Edwin na kumpa mkono Melanie “Nashukuru sana nimekwisha karibia” akasema Melanie “Naitwa Edwin Mbeko naamini tayari umekwisha pata taarifa zangu kutoka kwa Devotha Adolph” akasema Edwin “Devotha amekwisha nieleza kila kitu kuhusu wewe.Amekupa sifa nyingi kwa kuwa mwepesi katika kutekeleza maelekezo yote unayopewa”akasema Melanie na Edwin akatabasamu “Ninaongoza idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi idara ambayo yeye mwenyewe Devotha amewahi kuiongoza na ndiye aliyeianzisha.Binafsi ndiye aliyeniingiza katika idara ile na kunifundisha mambo mengi.Devotha amebobea sana katika masuala ya ujausi.Pole na safari” “Safari ilikuwa ndefu lakini nashukuru nimefika salama.Vipi hapa mambo yanakwendaje? “Hapa kila kitu kinakwenda vizuri kama alivyokuelekeza Devotha.Maandalizi yote yamekamilika.Kwanza ni sehyemu yako ya makazi.Tumekutafutia nyumba hii ambayo naamini utaipenda” “Joyce amekwisha nitembeza sehemu mbali mbali za jumba hili na kwa ujumla nimelipenda sana.Karibu kila kitu ninachokihitaji kipo.Ahsante sana” akasema Melanie “Ahsante pia kama umelipenda hili jumba.Katika kulichagua tumezingatia mambo mengi na kubwa zaidi likiwa ni usiri na usalama.Usalama ni mkubwa sana ndani ya jumba hili naamini Joyce amekwisha kujulisha” “Amekwisha nijulisha kila kitu” akasema Melanie “Katika jumba hili utaishi na watumishi wawili.Wote wanatoka Ufaransa na watawasili kesho.Wote wawili ni watu waliopitia mafunzo ya ujasusi na wanakuja hapa kwa kazi maalum ya kukusaidia wewe tu.Wanajua kila kinachoendelea na wanajua watakusaidia vipi na vile vile watakuwa ni kama walinzi wako humu ndani.Kutakuwa na timu ya walinzi wa siri ambao hutawaona lakini watakuwa nawe kila uendako kuhakikisha unakuwa salama.Pale kutakapotokea kitisho chochote cha usalama wako walinzi hao watajitokeza.Awali tulipanga Walinzi hao watoke Ufaransa lakini baada ya kutathmini kwa kina tukaona tuwatumie watu wa hapa hapa Tanzania.Kuna watu nimewaandaa wenye umahiri mkubwa sana.Ni vijana ambao nimekuwa nikiwatumia katika shughuli mbali mbali katika idara yangu lakini kwa sasa nimewaweka pembeni kazi yao itakuwa moja tu kukulinda wewe.Utakuwa pia na dereva maalum kwa ajili ya kukupeleka sehemu mbali bali unazotakiwa kwenda.Dereva wako atakuwa ni Joyce Yule ambaye amekupokea uwanja wa ndege usiku huu.Joyce pamoja na kuwa atakuwa dereva wako lakini atakuwa pia mlinzi wako.Joyce ana mafunzo makubwa sana ya ujasusi na alipelekwa mafunzoni na Tamar kupata mafunzo maalum .Alimuandaa ili awe mlinzi wake binafsi lakini kwa bahati mbaya akauawa.Joyce pia atakuwa akiishi nawe ndani ya jumba hili.Ukiacha walinzi hao ambao watakuwa wanakufuata kwa siri kila uendako kutakuwa na timu nyingine ambao wao watakuwa wakikufuatilia kwa kutumia vifaa maalum.Watatumia satelaiti katika kukufuatilia vile vile watakuwa na uwezo wa kudukua kamera zote za barabarani na katika majengo mbali mbali utakamopita na kuingia lengo ni kuhakikisha unakuwa salama.Utakuwa na katibu wako muhtsasi huyu naye alipelekwa nje ya nchi katika mafunzo na Tamar.Nimemrejesha nyumbani aje kushiriki katika operesheni hii.Kwa ujumla tumejipanga vyema kila sehemu kuhakikisha unakuwa salama” akasema Edwin “Ahsante sana Edwin kwa maandalizi haya makubwa uliyoyafanya” akasema Melanie “Tukiachanana na masuala hayo ya ulinzi tugeukie sasa katika ile kazi yenyewe iliyokuleta hapa Tanzania.Si kazi nyepesi ni kazi ngumu lakini hauko peke yako sisi tuko nyuma yako kuakikisha kwamba unafanikisha kila kitu kama kinavyotakiwa” akasema Edwin na kutoa mkebe katika koti lake uliokuwa na sigara kubwa akachomoa moja. “Cigar? akamuuliza Melanie “No thank you” akasema Melanie na Edwin akaiwasha ile sigara kubwa akaanza kuvuta na kusema “Mkutano mkuu wa wake za marais duniani unatarajiwa kufanyika hapa Tanzania wiki mbili ijayo na kwa kiasi kikubwa maandalizi yake yamekwisha kamilika.Ni mkutano mkubwa na wake za marais wengi duniani wamethibitisha kushiriki katika mkutano huo isipokuwa wake za marais wa mataifa makubwa kama vile Marekani,Ufaransa nk.Ulinzi ni mkubwa sana ili kuhakikisha kwamba mkutano unafanyika vizuri na kwa amani.Idara yangu ya SNSA nayo imepewa jukumu kubwa la kuhakikisha mkutano huo unafanyika bila kuwepoo kwa kitisho chochote cha usalama kabla na baada ya mkutano.Maelekezo yaliyotolewa na Devotha ni kumuua mke wa Rais wa Rwanda mara atakapokuja katika mkutano huo na tumeelekezwa tuhakikishe mauaji hayo yaonekane kama vile yamefanywa na serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Tayari tunazo taarifa za hoteli atakayofikia bi Uwineza Ntezimana mke wa Rais wa Rwanda.Kazi iliyoko mbele yetu ni namna ya kuihusisha nchi ya Congo na mauaji yake”akasema Edwin “Sikiliza Edwin suala hili lazima liwe kubwa na lilete mtikisiko mkubwa katika jumuiya ya Afrika mashariki.Kwa sasa nchi za Rwanda na DRC hazina mahusiano mazuri na Uganda.Rwanda na Uganda zimekuwa zikitupiana maneno makali.Uganda na DRC pia hazina mahusiano mazuri baada ya majeshi ya Congo kuwafurusha waasi na kuvuka hadi mpaka wa Uganda na inadaiwa waliua raia kadhaa na jambo hilo limeleta mvutano mkubwa sana na kuifanya Uganda kuimarisha vikosi vyake katika mpaka wake na Congo na Rwanda.Misuguano hii inashughulikiwa ndani ya jumuiya Afrika mashariki lakini kabla haijamalizika tunaweza kulitumia kama dirisha la kutekeleza mpango wetu.Mke wa Rais wa Rwanda na mke wa Rais wa Congo wanapaswa kuuawa kwa pamoja na serikali ya Uganda ndiyo itakayobeba mzigo huo.Tukilifanikisha hilo msuguano utaongezeka na kuwa mkubwa zaidi.Rwanda na Congo zitailaumu Uganda kwa mauaji hayo.Tanzania pia italaumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi kwa wake hao wa viongozi na Afrika Mashariki itaingia katika mzozo mkubwa.Unauonaje mpango huo?akauliza Melanie “Ni mpango mzuri na utalifanya jambo hili kuwa kubwa zaidi.Kikubwa ni namna ya utekelezaji wake” “Usihofu kuhusu utekelezaji wake.Nataka hadi kufikia kesho saa mbili asubuhi nipate taarifa za kuhusiana na balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hapa nchini” akasema Melanie. Walizungumza mkakati mbali mbali ya namna ya kutekeleza mipango yao na kisha Edwin akaaga akaondoka. Baada ya Edwin kuondoka Melanie akiwa chumbani kwake akafungua kompyuta yake na kuitafuta picha ya Rebecca Eyenga mke wa Patrice Eyenga rais wa jamhuri ye kidemokrasia ya Congo akaitazama “Mume wako ameshiriki katika mauaji ya wazazi wangu na wewe siku zako zinahesabika.Lazima Patrice Eyenga naye apate uchungu mkubwa wa kupotelewa na mtu wake wa muhimu kama uchungu ninaoupata mimi kwa wazazi wangu kuuawa.Nimekwisha weka kiapo kwamba hakuna aliyeshiriki katika mauaji ya wazazi wangu atabaki salama” akawaza na kufuta machozi “Wiki hii natakiwa kwenda jijini Kinshasa kutembelea makaburi ya wazazi wangu.Sikuhudhuria mazishi yao hivyo nataka kuona mahala walikopumzishwa.Baada ya kutoka huko na kupata Baraka zao ndipo nitaanza rasmi kazi yangu.”akawaza Melanie







Saa kumi na mbili za asubuhi Melanie alipigiwa simu na Edwin Mbeko akamjulisha kwamba amemtumia taarifa za balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hapa nchini katika barua pepe yake.Melanie akaamka na kuelekea katika chumba cha mazoezi ambako alimkuta Joyce naye amekwisha amka akifanya mazoezi.Waliungana pamoja katika mazoezi kisha kila mmoja akaelekea chumbani kwake kujiandaa kwa ajili ya kuianza siku.Hawakuwa na mtumishi bado hivyo Joyce akaandaa kifungua kinywa.Wakati Joyce akiandaa kifungua kinywa Melanie alikuwa chumbani kwake akijiandaa,siku hii alivaa suti ya rangi nyeupe ambayo sketi yake iliishia juu kidogo ya magoti na kuwa na mpasuo mdogo kwa nyuma.Alijiangalia kwenye kioo akatabasamu “Walionitengeneza namna hii wanastahili pongezi kubwa.Kwa muonekano huu hakuna mwanaume anayeweza kuponyoka kama nikimuhitaji” akawaza na kuchukua moja ya simu kati ya simu tatu zilizokuwa mezani ambazo alipewa na Edwin kwa ajili ya mawasiliano.Akaziandika namba za simu alizopewa na Gosu Gosu akampigia “Hallow” akasema Gosu Gosu baada ya kupokea simu akiwa hafahamu namba zile ni za nani “Halo mpenzi wangu.Habari za asubuhi?akauliza Melanie “Melanie.Habari yao malaika wangu.Umeamka salama? “Nimeamka salama mpenzi sijui wewe” “Hata mimi nimeamka salama kabisa.Mawazo yote juu yako” akasema Gosu Gosu na Melanie akatabasamu “Darling hiyo ndiyo namba yangu nitakayoitumia hapa Tanzania muda wowote ukitaka kunitafuta utanitafuta katika namba hiyo.Kwa shughuli zote za kiofisi itatumika namba hiyo” akasema Melanie “Ahsante sana Melanie.Vipi kuhusu ratiba yako ya siku ya leo? “Nitakuwa na mizunguko kadhaa leo lakini kabla ya mizunguko yangu nataka kwanza nijitambulishe kwa wafanyakazi ili wanifahamu na mimi niwafahamu na kazi hiyo ya kunitambulisha utaifanya wewe.Nataka niifahamu ofisi yako halafu ndipo nitaendelea na shughuli nyingine.Nielekeze tukutane wapi?akauliza Melanie “Nielekeze mahala ulipo nije nikuchukue” akasema Gosu Gosu “Usijali Gosu Gosu ninaye dereva ambaye anaweza akanileta mahala ulipo” “Ouh safi sana.Basi mwambie akulete ofisi kuu za MAPEN GROUP CO LTD.Mimi nitakuwepo pale nikikusubiri” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana Gosu Gosu tutaonana muda si mrefu.Nakupenda sana” akasema Melanie “Nakupenda pia Melanie” akasema Gosu Gosu na Melanie akakata simu Melanie akatoka chumbani kwake na kuelekea chini ambako alimkuta Joyce akiwa tayari amejiandaa lakini hakuwa peke yake alikuwa na mwanamke mmoja mfupi mwenye weusi wa kung’aa. “Hello ladies” akasema Melanie na Yule mwanamke aliyekuwa anazungumza na Joyce akastuka baada kumuona Melanie “Madam Melanie huyu anaitwa Frimina Mbozi ndiye atakayekuwa katibu wako muhtasi” akasema Joyce “Hallow Frimina” akasema Melanie na kumpa mkono Frimina “Hallow madam Melanie.Naamini tayari taarifa zangu unazo” “Hutajali nikikuita Mina badala ya Frimina? Akauliza Melanie “Hakuna tatizo Madam Melanie” “Good.Mina taarifa zako tayari ninazo karibu sana” akasema Melanie na wote wakaenda kupata kifungua kinywa na baada ya kumaliza safari ikaanza.Kituo cha kwanza ilikuwa ni katika ofisi kuu za MAPEN Group .Gosu Gosu ambaye alikwisha wasili toka mapema ndiye aliyempokea Melanie.Siku hii alikuwa amevalia suti nzuri nyeusi na kila mmoja alimsifia kwa muonekano ule.Wengi hawakuzoea kumuona aiwa amependeza namna ile.Baada ya kupokelewa Melanie akatembezwa katika ofisi mbali mbali za jengo lile la ghorofa tatu halafu akaingizwa katika ofisi yake kubwa ambayo ilikuwa ni ofisi ya Mathew Mulumbi kisha ikatumiwa na Gosu Gosu na sasa ni Melanie Davis. “Ofisi nzuri sana hii nimeipenda” akasema Melanie halafu akaenda kukutana na wafanyakazi ambao walitaarifiwa kuacha kila kitu na kukusanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano.Walifahamu kuna ugeni lakini hawakujua mgeni Yule ni nani.Aliyefahamu ni Gosu Gosu pekee Gosu Gosu akiwa ameongozana na Melanie na katiku wake Frimina waliingia katika ukumbi wa mikutano.Gosu Gosu akawasalimu wafanyakazi wale halafu akatumia nafasi ile kuwatangazia rasmi kwamba kuanzia wakati ule Melanie Davis ndiye mmiliki mpya wa kampuni ya MAPEN.Wafanyakazi wote walipatwa na mshangao mkubwa Gosu Gosu akawaeleza sababu za mmiliki wa kampuni ile kuamua kuuza biashara zake kwa mtu mwingine.Melanie akakaribishwa kuzungumza na wafanyakazi akazungumza nao kwa muda mfupi na kuwahakikishia hakutakuwa na mabadiliko yoyote,kila kitu kitaendelea kuwa kama kilivyokuwa awali na kuwaomba wafanyakazi ushirikiano mkubwa.Baada ya mkutano ule na wafanyakazi Melanie akarejea ofisini kwake na rasmi Gosu Gosu akamkabidhi ofisi “Gosu Gosu huna haja ya kunikabidhi ofisi.Hii itaendelea kuwa ni ofisi yako.Mimi nitatafuta ofisi nyingine.Wewe bado ni meneja mkuu wa makampuni haya yote.Kama alivyokuamini Peniela na mimi pia ninakuamini vile vile.Kila kitu kitakuwa chini yako”akasema Melanie na kumfuata Gosu Gosu akambusu “Japo bado nasubiri jibu lako kuhusu kufunga ndoa lakini wewe tayari ni mume wangu Gosu Gosu.Wewe ni mfalme wangu na kila kilicho changu ni cha kwako”akasema Melanie na kumbusu “Ahsante sana Melanie kwa kuniamini.Nitahakikisha hujutii kuniamini” akasema Gosu Gosu huku Melanie akichezea tai yake “Gosu Gosu kulala usiku mmoja bila uwepo wako pembeni yangu naona kama ni miezi mitatu.Jioni ya leo nitakuja nyumbani kwako japo sintalala”akasema Melanie na kumbusu tena halafu akamuaga kwamba anakwenda katika mizunguko yake mingine wataonana jioni kisha Melanie akaondoka katika ofisi kuu za MAPEN GROUP huku akiacha gumzo watu wakijadili uzuri wake. Kutoka ofisi za MAPEN group Melanie alielekea katika ubalozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Alipokewa vizuri akajitambulisha kama yeye ana asili ya Congo lakini ametokea Ufaransa na anahitaji kuonana na balozi wa DRC nchini Tanzania.Balozi hakuwa na mtu yoyote ofisini hivyo Melanie akakaribishwa ndani. “Mheshimiwa balozi” akasema Melanie akitumia lugha ya kifaransa huku akitabasamu na kumpa mkono balozi “Hallow habari yako.Karibu sana”akasema balozi na kumuelekeza Melanie katika sofa nzuri zilizokuwamo mle ofisini. “Naitwa Melanie Davis nina asili ya Congo lakni ninaishi Ufaransa” akasema Melanie “Nafurahi kukufahamu Melanie.Mimi naitwa Germinus Mapupu balozi wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hapa Tanzania.Karibu sana katika ubalozi wetu hapa Dar es salaam” “Nashukuru sana mheshimiwa balozi” akasema Melanie na kukaa vizuri kwani sketi yake fupi aliyovaa ilikuwa imepanda sana juu na kuyaacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi “Niite Mr Mapupu inatosha” akasema balozi huku akitabasamu “Kaona paja tu tayari amekwisha anza kujichekesha chekesha”akawaza Melanie “Mhehimiwa balozi Mr Mapupu,kama nilivyokujulisha mimi nina asili ya Congo,wazazi wangu wote wawili ni wazaliwa wa Congo lakini walihamia Ufaransa kibiashara.Kwa sasa wote wawili wametangulia mbele za haki na mimi ndiye niliyebaki nikisimamia mali walizoziacha.Ninataka kupanua biashara walizoacha wazazi wangu nataka kuogeza uwekezaji zaidi hasa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Tayari nimenunua makampuni kadhaa hapa Tanzania na sasa nataka nikawekeze pia nyumbani Congo”akasema Melanie “Hongera sana Melanie kwa uamuzi huo mkubwa wa kuamua kuja kuwekeza nyumbani.Wapo watu wengi wa kutoka bara la Afrika wamepata fedha nyingi huko ughaibuni na hawakumbuki tena kurejea kuwekeza nyumbani na kuwapatia ajira ndugu zao.Wewe umefanya maamuzi mazuri sana.Tunahitaji sana uwekezaji kutoka nje na kwa hivi sasa nchi ya Congo imeweka sera nzuri sana za kuvuta wawekezaji na wewe ukiwa kama ni mkongo basi utapewa kipaumbele kikubwa.Ni sekta zipi unataka kuwekeza?akauliza balozi Mapupu “Bado sijajua ni sekta ipi ninaweza kuwekeza na kupata faida ndiyo maana nimekuja hapa kwako nikitaka kupata kibali cha dharura niweze kuingia nchini Congo nikaonane na idara inayohusika na uwekezaji nizungumze nao na nikitoka huko ntakuwa nimepata picha kamili ni sehemu gani ninaweza kuwekeza” akasema Melanie. Balozi Mapupu alielekeza Melanie aandaliwe nyaraka za kumuwezesha kuingia nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na ndani ya ya dakika kumi na tano kila kitu kilikuwa tayari “Hapa Dar es salaam unapatikana sehemu gani? Akauliza balozi Mapupu.Melanie akatoa simu na kumpatia balozi namba zake naye balozi akampatia za kwake “Nitakaporejea kutoka Congo nitakupigia kukujulisha na kama utakuwa na nafasi basi tunaweza kukutana jioni moja kwa chakula na kinywaji tukabadilishana mawazo” akasema Melanie huku akitabasamu “Nitafurahi sana Melanie.Utakaporejea tafadhali usiache kunipigia simu” akasisitiza balozi Mapupu na kumsindikiza Melanie hadi katika gari lake wakaagana akaondoka “Balozi Mapupu tayari amekwisha ingia katika kitabu changu chekundu.Mate yamemtoka hasa alipoliona paja linavyong’aa.Sikuwahi kujua kama wanaume ni wadhaifu kiasi hiki.Walionitengeneza nikawa na umbo hili nitaendelea kuwasifu siku zote kwa akili kubwa waliyotuma walijua kabisa nikiwa na umbo la namna hii hakuna mwanaume anaweza akanikatalia jambo lolote.” Akawaza Melanie na kutabasamu RIYADH – SAUDI ARABIA Dr Abiha aliingia katika chumba alimo Mathew Mulumbi,kama kawaida alikuwa ameongozana na wale jamaa waliokuwa na silaha akawataka wamsubiri nje amuhudumie mgonjwa “Habari yako Abu Zalawi” akasema Dr Abiha “Nzuri kabisa Dr Abiha” “Vipi maendeleo yako? “Ninaendelea vizuri tofauti na jana” “Nafurahi kusikia hivyo” akasema Dr Abiha na kumpima Mathew halafu akasema “Unaendelea vizuri Abu Zalawi” “Ahsante kwa huduma nzuri Dr Abiha.Ulifanikiwa kupata taarifa zozote kuhusiana na Yule mwenzangu Nawal? Akauliza Mathew “Hapana bado sijafanikiwa kupata taarifa zake zozote.Unaweza ukanielezea zaidi kuhusu huyo mwenzako?Ni mpenzi wako?akauliza Dr Abiha “Hapana si mpenzi wangu.Ni mke wa kiongozi wangu” akasema Mathew “Wewe ni mwanachama wa kikundi kipi?Abiha akauliza “Mimi ni mwanacahama wa kikundi cha Ammar Nazari brigades ambacho kinapambana na Israel kudai haki ya taifa la Palestina” akasema Mathew “Wewe ni Mpalestina? “Hapana mimi si mpalestina.Asili yangu ni Misri baba yangu alijulikana kama Khalid Al Zalawi na aliuliwa na majeshi ya Israel.Baada ya hapo ndipo nilipoamua kuingia katika mapambano na Israel.Nilijiunga na kundi la Ammar Nazari brigades na huko tumekuwa tukiendeleza mapambano dhidi ya Israel na juzi kiongozi wetu ambaye ni Ammar Nazari ameualiwa na vikosi vya Israel.Yule mwanamke niliyekuwa naye Nawali alikuwa mke wa Ammar Nazari na alinikabidhi nimlinde nihakikishe anakuwa salama” akasema Mathew “Kwa nini unamtafuta Habiba Jawad?akauliza Dr Abiha “Kuna taarifa muhimu nataka kumpatia” “Kuhusu nini?akauliza Dr Abiha “Kuna mtu wake wa muhimu ambaye ninafahamu mahala alipo” akasema Mathew “Abu Zalawi utakataa nikisema kwamba wewe ni gaidi?akauliza “Mimi si gaidi” akajibu Mathew “Kama si gaidi kwa nini mnaua watu wasio na hatia? “Haya ni mapambano Dr Abiha na ni mapambano ya kudai haki.Wapalestian wana haki ya kupigana kwa ajili ya ardhi yao ambayo inakaliwa kimabavu na Israel.Kwa nini Israel wanapoua wapalestina dunia inaona sawa lakini wapalestina wanapoua waisrael viongozi wa mataifa wanasimama na kulaani? Palestina wanapigana kwa haki ya ardhi yao na Israel hawana budi kurejesha ardhi hiyo na kuacha ukandamizaji inaowafanyia wapalestina” akasema Mathew “Abu wewe ni muislamu na ninaamini unasoma kitabu chetu kitukufu.Unaweza ukaniambia kitabu chetu kinasemaje kuhusu kuua watu wasiokuwa na hatia?akauliza Dr Abiha “Mwenyezi Mungu Subhanahu wa ta’ala ameagiza kwamba tusiue nafsi ambayo amekataza”akajibu Mathew “Kwa nini saa mnaua watu wasio na hatia?akauliza Dr Abiha “Katika Surah Al Baqarah 2:190 – 192 tunaaambiwa “Na piganeni katika njia ya Allaah na wale wanaokupigeni, wala msipundikie mipaka (mkawapiga wasiokupigeni). Kwani Allaah hawapendi warukao mipaka. Na waueni popote muwakutapo, na muwatowe popote walipokutoweni; kwani kuwaharibu watu na dini yao ni kubaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao karibu na Msikiti Mtakatifu (wa Makka) mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni (huko) basi nanyi pia wapigeni. Namna hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri. Lakini kama wakikoma, Allaah ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa kurehemu” akasema Mathew na Dr Abiha akabaki anamtazama. “Sina haja ya kueleza zaidi kwani maelezo hayo yanajitosheleza”akasema Mathew “Kweli yanajitosheleza”akasema Dr Abiha “Lini utanisaidia niweze kutoka humu ndani? Vipi kuhusu Habiba Jawad umepata taarifa zake zozote?akauliza Mathew “Ninaendelea kutengeneza mpango wa kukutorosha pale nitakapokuwa tayari nitakujulisha” akasema Dr Abiha “Dr Abiha tafadhali naomba unisaidie kupata taarifa za Habiba Jawad.Ninahitaji sana kumuona”akasema Mathew “Sawa nitakusaidia Abu Zalawi “ akasema Dr Abiha na kutoka mle ndani akamauacha Mathew “Niliwahi kukaa Libya miaka miwili nikiwa kule nilipata mafunzo ya lugha ya kiarabu na kupata mafunzo kuhusu Uislam.Kama nisingepata mafunzo yale swali aliloniuliza Dr Abiha lingeniumbua.Anaonekana ana nia ya dhati ya kunisaidia.Namuomba afanye haraka anisaidie kwani wale jamaa wakijua nimepata nafuu watanirejesha tena kuendelea kunitesa.Akinitoa hapa lazima nifanye juu chini nimpate Habiba Jawad.Naamini yuko hapa Saudi Arabia na siwezi kuondoka bila kuonana naye” akawaza Mathew KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO Ndege ndogo iliyokodiwa kutoka Dar es salaam Tanzania iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa.Ndani ya ndege hiyo alikuwa amepanda Melanie Davis na dereva wake Joyce.Ndege ilipotua wakashuka na kufuata taratibu za pale uwanjani kisha wakaruhusiwa kuingia jijini Kinshasa.Nje ya uwanja tayari gari kutoka kampuni ya kukodisha magari lilikuwa linawasubiri.Kabla ya kufika Kinshasa maandalizi yote yalikwisha fanyika.Melanie na Joyce wakaingia katika gari lile la kukodi wakaelekea mahala ambako Melanie alielekeza nje kidogo ya jiji la Kinshasa. Siku hii Melanie alikuwa amevaa mavazi meusi na macho yake aliyafunika kwa miwani mikubwa myeusi kwani yalikuwa mekundu kutokana na kulia sana usiku kila alipowakumbuka wazazi wake.Safari ilikuwa ya kimya kimya hadi walipofika katika shamba walilokuwa wanalimiliki wazazi wake ambako ndiko walikozikwa.Kulikuwa na geti lenye walinzi na Melanie akajitambulisha kwamba amekuja kutoa heshima za mwisho kwa Lucy na Laurent Muganza.Walimuhoji yeye ni nani na akawadanganya kwamba anatokea Ufaransa na marehemu Lucy Muganza aliwahi kumsomesha ndiyo maana amefunga safari kutoka Paris kuja kutoa heshima za mwisho.Walinzi wale wakamjulisha mtu mmoja ambaye ni mdogo wake Laurent Muganza naye akaelekeza watu wale waruhusiwe kuingia ndani.Lilikuwa shamba kubwa na kutoka getini hadi kufika mahala iliko nyumba kubwa ni umbali wa kilometa moja.Shamba lilisheheni mazao mbali mbali Walifika katika jumba lile kubwa na kupokewa na mdogo wake Laurent Muganza.Melanie alipomuona alishindwa kuyazuia machozi kumtoka kwani alikuwa amefanana mno na baba yake.Walikaribishwa ndani. “Hii ni nyumba yetu nilizoea kuja kukaa hapa mara nyingi nirudipo kutoka likizo kutokana na utulivu unaopatikana mahala hapa lakini leo hii ninakaribishwa kama mgeni.Hakuna anayenifahamu tena.Hata nikiwaeleza mimi ni Theresia Muganza hakuna atakayeniamini” akawaza Melanie “Karibuni sana jamani” baba yake mdogo Melanie akasema “Tunashukuru sana.Mimi naitwa Melanie Davis na huyu mwenzangu anaitwa Joyce.Ninatokea Paris Ufaransa na nimekuja hapa kwa ajili ya kutoa heshima kwa marehemu Lucy na Laurent Muganza” akasema Melanie “Karibu sana” “Ahsante baba.Lucy na mumewe walikuwa watu wakarimu sana na waliwahi kunilipia ada ya chuo kikuu pale nilipofiwa na wazazi hivyo ni watu wangu wa muhimu sana.Nilipata taarifa za kuuawa kwao nikiwa nchini Urusi hivyo nikashindwa kuhudhuria mazishi.Baada ya kupata nafasi nimeona nije nami nitoe heshima zangu kwa watu hawa wema ambao wamenifikisha hapa nilipofika” akasema Melanie na kufuta machozi “Pole sana Melanie.Kifo cha Laurent na mke wake kinaumiza sana.Walikuwa ni watu wema hawakuwa na maadui na walipendwa na kila mtu.Hata sisi imetuumiza mno.Mimi ni mdogo wake na Laurent” akasema Yule jamaa “Mmefanana sana”akasema Melanie halafu ukimya mfupi ukapita “Vipi kuhusu waliofanya mauaji haya wamekwisha kamatwa hadi sasa?Melanie akauliza “Kuna utata mwingi.Serikali ya Tanzania inadai kwamba waliofanya mauaji yale ni majambazi lakini hadi leo hii hawajatoa tena taarifa nyingine na hawataki kuruhusu wachunguzi wa kimataifa wakalichunguze hili suala.Kwa upande wa serikali ya Congo imekuwa kimya kabisa na hawajahi kutoa taarifa zozote” “Unadhani mauaji haya yanaweza kuwa ni sababu za kisiasa?Melanie akauliza “Tunahisi hivyo kwa sababu siku walipouawa ni siku ambayo Lucy alikuwa atangazwe na chama kikuu cha upinzani kama mgombea wa urais na Dar es salaam alipita ili kumchukua mwanae Theresia ili waje wote Kinshasa lakini hawakufika tena Kinshasa” akasema Yule baba mdogo wa Melanie “Vipi kuhusu mtoto wa marehemu yeye yuko wapi?akauliza Melanie “Theresia alinusurika katika shambulio lile na alipelekwa nchini Ufaransa kwa matibabu.Tumekuwa tunafuatilia kwa ubalozi wa Ufaransa ili kupata taarifa za maendeleo ya Theresia lakini jibu ambalo tumekuwa tukipewa ni kwamba hatuwezi kuzungumza naye kwani amefichwa mahala pa siri akiendelea kupatiwa matibabu.Kuna tetesi kwamba toka alipotolewa Tanzania akapelekwa Ufaransa hajawahi kuzinduka.Amewekwa katika mashine za kumsaidia kuishi” “Mungu amsaidie aweze kupona”akasema Melanie “Tunasali usiku na mchana Theresa aweze kupona na kurejea.Wazazi wake wameacha mali nyingi sana ambazo zinamsubiri yeye aweze kuziendeleza.Hivi sasa tunaendelea na mchakato wa kuorodhesha mali zote za marehemu wazazi wake na kuziweka tayari kumsubiri aje azisimamie”akasema Yule jamaa.Melanie akavua miwani na kufuta machozi “Ninaweza tafadhali kupelekwa mahala walikozikwa wazee hawa?akasema Melanie na Yule mzee akawaongoza kuelekea mahala walikozikwa Lucy na Laurent Muganza.Kulikuwa na nyumba nzuri sana ambayo ndani yake kulijengwa makaburi mawili ya Lucy na Laurent Muganza.Mlango ukafunguliwa na Melanie akaomba apewe faragha.Alilia machozi mengi sana juu ya makaburi ya wazazi wake “Ninawaahidi wazazi wangu yeyote ambaye alishiriki katika kuwakatili roho zenu hatabaki salama.Nitawatafuta kokote waliko na mmoja mmoja lazima walipe.Damu yenu haiwezi kupotea bure.Ninapotoka ndani ya nyumba hii mlimolala ninakwenda kuanza kazi ya kuwasaka wale wote waliowalaza humu kabla ya wakati wenu”Melanie akatamka maneno hayo na kuzibusu picha za wazazi wake zilizokuwa katika makaburi akafuta machozi kisha akatoka.Hakutaka tena kukaa eneo lile wakaagana na Yule baba yake mdogo kisha wakaondoka.Hakutaka tena kupita sehemu yoyote akarejea uwanja wa ndege ambako ndege ilikuwa inawasubiri wakapanda na kuondoka kurejea Dar es salaam “Kidonda changu kimetoneshwa leo kwa kuyaona makaburi ya wazazi wangu.Nimeumia sana” akawaza Melanie.Hakukuwa na mazungumzo mengi ndani ya ndege muda mwingi Melanie alikuwa ameinamisha kichwa akiwaza na kulia. Hatimaye ndege ikawasili salama jijini Dar es salaam tayari ilikuwa ni saa kumi na mbili za jioni.Mara tu waliposhuka ndegeni,Melanie akampigia simu Gosu Gosu na kumjulisha kwamba anakwenda kwake kisha wakachukua gari lao walilolicha pale uwanjani wakaondoka.Walifika nyumbani kwa Gosu Gosu ambaye aliwapokea na kuwakaribisha sebuleni.Melanie akamtaka waende chumbani wakazungumze faragha.Mara tu walipoingia chumbani Melanie akamrukia Gosu Gosu na kumuangusha kitandani kisha akaanza kutoa nguo.Mambo yalikwenda kimya kimya na Gosu Gosu alielewa kile anachotakiwa kukifanya na akashika usukani.Ulikuwa ni mtanange mzito sana lakini Gosu Gosu aliumiliki vilivyo. “Ahsante sana Gosu Gosu,ahsante sana mpenzi wangu” akasema Melanie huku akimbusu Gosu Gosu mfululizo na kumkumbatia kwa nguvu baada ya kumaliza mtanange ule “Melanie ulinipania sana siku ya leo” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu ni kweli.Sijui ningefanya nini kama ningekukosa.Ahsante tena”akasema Melanie “Nimekutafuta siku nzima ya leo simu yako haikuwa ikipatikana na hata ofisini sijakuona” akasema Gosu Gosu “Ni kweli.Kutwa nzima ya leo simu yangu ilikuwa imezimwa nilikuwa na mizunguko mingi” akasema Melanie “Pole sana.Kila kitu kimekwenda vyema?akauliza Gosu Gosu “Usihofu kila kitu kimekwenda vizuri.Nashukuru nimeimaliza siku nikiwa kifuani kwako” akasema Melanie na kuendelea kukilaza kichwa chake kifuani kwa Gosu Gosu “Gosu Gosu nakupenda sana na niko tayari kufanya jambo lolote kwa ajili yako.Je wewe uko tayari kufanya chochote kwa ajili yangu?akauliza Melanie “Melanie nadhani jibu unalifahamu kwamba niko tayari kufanya chochote kwa ajili yako” akasema Gosu Gosu “Nashukuru kwa kauli hiyo” “Kuna nini Melanie?Mbona kama leo hauko hauko sawa? “Kuna kitu nitakuomba unisaidie” “Sema Melanie nikusaidie nini? “Kwanza kabla sijakueleza ninachokitaka kwako naomba nikueleze siri yangu.Naomba tafadhali uitunze siri hii kwani sijawahi kumueleza mtu mwingine yeyote” “Usihofu Melanie.Siri yako iko salama kwangu” akasema Gosu Gosu “Baba yangu na Rais Patrice Eyenga wa DRC walikuwa marafiki na kabla Patrice hajawa Rais walikuwa wanafanya biashara pamoja.Walimiliki kampuni kadhaa kwa pamoja.Patrice alipotaka kuwania urais wa Congo kiasi kikubwa cha fedha za kuendesha kampeni yake alitegemea kutoka katika biashara walizokuwa wamechanga na baba.Alitumia fedha nyingi katika kampeni kwa ahadi ya kuzirejesha pale atakapokuwa ameshinda urais.Baada ya kufanikiwa kushinda urais baba alimtaka aanze kurejesha zile fedha ambazo ni nyingi ili kunusuru biashara zao lakini Rais Patrice Eyenga alitengeneza mpango na wazazi wangu wakauawa” akasema Melanie na Gosu Gosu akastuka na kuinuka akakaa.Alihisi mwili wote ukimsisimka kumbu kumbu ya mauaji ya Lucy na Laurent ikamjia “Wazazi wako waliuawa namna gani? Akauliza kwa wasi wasi kidogo “Walifariki katika ajali ya gari ambayo tunaamini ilitengenezwa.Gari lao dogo liligongana na gari kubwa la mizigo na wote wawili wakafariki hapo hapo.Ripoti ya wachunguzi wa kujitegemea inaonyesha kwamba ajali ile ilikuwa ya kutengenezwa.Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomuhusisha Rais Patrice Eyenga na ajali ile lakini tunaamini anahusika kwa sababu kifo cha baba kilitokea mara tu ulipoanza mzozo kati yake na Patrice kuhusu fedha” “Pole sana Melanie” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana.Nimekwisha lia sana kwa miaka mingi na machozi yamekauka.Hivi sasa sina tena machozi.Gosu Gosu kilichopo katika akili yangu kwa sasa ni jambo moja tu.Ninataka kulipa kisasi kwa Rais Patrice Eyenga kwa kile alichonifanyia” akasema Melanie na Gosu Gosu akabaki kimya.Alishindwa aseme nini “Unanisikia Gosu Gosu?akauliza Melanie baada ya kumuona Gosu Gosu amebaki kimya “Nimekusikia Melanie” “Naamini utaniunga mkono katika harakati zangu.Nataka Patrice Eyenga naye apate maumivu makali kwa kumpoteza mtu wake wa karibu sana kama mimi nilivyopata maumivu makali kwa kuwapoteza wazazi wangu” akasema Melanie na Gosu Gosu akahisi kama kuna kitu kimekwama katika koo lake akakohoa kidogo “Gosu Gosu umekuwa kimya ghafla baada ya kukueleza jambo langu kuna tatizo lolote?akauliza Melanie “Hapana niko sawa Melanie” “Unasemaje kuhusiana nahiki nilichokueleza?akauliza Melanie “Niko nawe Melanie katika jambo lolote.Siwezi kukuacha nyuma.Katika jambo lolote lile nitatangulia mbele na wewe utakuwa nyuma yangu nitakulinda dhidi ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza.Pole sana kwa mara nyigine kwa kifo cha wazazi wako na Patrice Eyenga anapaswa kulipa uovu wake aliokufanyia.Nini unafikiria kukifanya katika mpango wako wa kulipiza kisasi?akauliza Gosu Gosu “Ahsante kwa kuniunga mkono.Nitahitaji msaada wako Gosu Gosu” “Unahitaji nifanye nini Melanie?Niambie chochote nitakifanya” akasema Gosu Gosu Melanie akavuta pumzi ndefu na kusema “Nahitaji kuonana na James Kasai”akasema Melanie na Gosu Gosu akahisi kama tumbo lake limekuwa tupu ghafla “James Kasai yupi?akauliza Gosu Gosu “Kwa miaka mingi umekuwa katika mapigano msituni.Humfahamu James Kasai?akauliza Melanie “James Kasai ninamfahamu kama kiongozi wa kundi la waasi walio furushwa kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na na kukimbilia katika misitu ya Uganda.Wakati James na kundi lake wanafurushwa jeshi la Congo lilivuka mpaka na kuingia Uganda katika kuwatafuta waasi hao ambao walikataa kuweka silaha zao chini.Uganda iliita kitendo hicho cha wanajeshi wa Congo kuvuka mpaka kama kitendo cha uvamizi na kuongeza majeshi yake mpakani.Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inailaumu Uganda kuwa inawahifadhi waasi hao na Uganda inailaumu Congo kwa jeshi lake kuvuka mpaka na kuua raia wake” “Safi sana kumbe bado unafuatilia masuala hayo kwa karibu.Huyo James Kasai ambaye alikimbilia Uganda baada ya kufurushwa Congo ndiye ambaye ninataka kuonana naye.Nitakuachia wewe kazi hiyo ya kutafuta namna ya mimi kuweza kuonana naye.Sifahamu utafanyaje lakini ninachohitaji mimi ni kupata nafasi ya kuonana na James Kasai” akasema Melanie “Sawa Melanie nitajitahidi kutafuta namna ili uweze kuonana na huyo mtu unayemuhitaji” akasema Gosu Gosu “Ndiyo maana nakupenda sana Gosu Gosu” akasema Melanie na kuanza kumwagia mabusu mazito kisha wakaingia katika raundi nyingine ya mtanange. “Gosu Gosu jambo hili nililokueleza ni siri kubwa hivyo asifahamu mtu yeyote”akasema Melanie wakati akijiandaa kuondoka “Mimi ni mwanajeshi ninafahamu maana ya kutunza siri hivyo usiwe na wasiwasi mpenzi wangu” akasema Gosu Gosu “Nakupenda sana Gosu Gosu” akasema Melanie na kumbusu Gosu Gosu kisha akaelekea katika gari lake wakaondoka.Baada ya Melanie kuondoka Gosu Gosu akarejea ndani akiwa ameinamisha kichwa alihisi kitu kama nyundo inagonga kichwa chake.Moja kwa moja akaelekea katka baa yake ndogo iliyoko mle ndani akachukua chupa ya pombe kali akaelekea chumbani kwake akamimina katika glasi akanywa yote akaweka tena mara ya pili akanywa yote kisha akashusha pumzi “Melanie ametaka kunipasua moyo wangu leo.Mstuko nilioupata pale aliponitamkia kwamba Patrice Eyenga anahusika katika vifo vya wazazi wake ni mkubwa.Nashukuru wazazi wakehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ walifariki huko Ufaransa” akawaza Gosu Gosu na kunywa funda la kinywaji kile kikali akafumba macho “Kwa nini Melanie anataka kuonana na James Kasai?Huyu ni mtu mbaya na katili sana.Ni mtu ambaye amekuwa anatafutwa ili afikishwe katika mahakama ya uhalifu wa kivita kutokana na ukatili mkubwa ambao kundi lake liliufanya wakati likipambana na majeshi ya serikali ya Congo.Hadi leo bado James ameshindwa kukamatwa kwa sababu anakingiwa kifua na nchi ya Uganda ambao inadaiwa wamempa hifadhi.Nahisi kwamba Melanie anataka kuandaa mipango ya kulipiza kisasi kwa Rais Patrice Eyenga na anataka kumtumia James Kasai” akawaza na kujiegemeza sofani “Sikutaka tena kujiingiza katika masuala yoyote ya mauaji,nilitaka niishi maisha ya amani lakini siwezi kumuacha Melanie peke yake katika suala hili.Lazima nisimame naye.Ninampenda na huu ni wakati mzuri wa kumuonyesha ni namna gani ninampenda na kumthamini.Kama ni kuua niko tayari kuua kwa ajili yake.Nitatafuta namna ya kumpata James Kasai” akawaza Gosu Gosu na kuchukua simu yake.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog