Search This Blog

Thursday 17 November 2022

SIRI : MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA - 1

 






IMEANDIKWA NA : PATRICK CK



*********************************************************************************



Simulizi : Siri: Maisha Na Kifo Cha Melanie Chuma

Sehemu Ya Kwanza (1)



SIRI PART 2 MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA

SEASON 1 SEASON 2 SEASON 3 SEASON 4 SEASON 5 SEASON 6 SEASON 7 SEASON 8 SEASON 9 SEASON 10



ARUSHA Kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Arusha Tanzania kilimalizika kwa mafanikio makubwa.Kikao hicho cha kawaida kilichohudhuliwa na marais kutoka nchi zote sita zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki,kilipokea na kujadili taarifa mbali mbali zinazohusu jumuia hiyo ikiwamo taarifa kuhusiana na mchakato wa uanzishwaji wa sarafu moja ya Afrika Mashariki ulikofikia.Kikao hicho pia kilijadili ombi la nchi ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kujiunga na jumuiya hiyo na kuikubali kuwa mwanachama wa saba wa jumuiya hiyo.Jambo lingine lililofanyika katika kikao hicho ni nchi ya Tanzania kuchukua nafasi ya uenyekiti wa jumuiya kwa muda wa mwaka mmoja. Baada ya kikao kumalizika na wakuu wa nchi kuzungumza na wana habari kuhusu yale yaliyojiri katika kikao hicho,wakuu wote wa nchi walielekea katika hoteli ya Kobe Village kwa ajili ya kupata chakula cha mchana na baada ya chakula baadhi ya wakuu wa nchi waliondoka na walibaki wachache waliokuwa na mazungumzo binafsi na Rais wa Tanzania na baada ya kumaliza mazungumzo yao marais wa Kenya na Burundi wakaondoka akabaki Rais Patrice Eyenga wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambaye alikuwa na mazungumzo binafsi na mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki rais wa Tanzania Dr Fabian Kelelo. Dr Fabian alimkaribisha Rais Patrice katika chumba chake kwenye hoteli kubwa jijini Arusha Kobe village kwa ajili ya mazungumzo maalum.Walinzi wote wa marais hawa wawili wakabaki nje na kuwapa nafasi wakuu wao wazungumze faragha. “Karibu sana ndugu Patrice” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais Dr Fabian kwanza ninakushukuru sana kwa namna ulivyojitahidi katika kikao kuwashawishi marais wakubali ombi la nchi yangu kujiunga na jumuiya hii.Ni muda mrefu tumekuwa tukiitafuta nafasi ya kujiunga na jumuiya ya Afrika mashariki lakini migogoro na mapigano yasiyokwisha nchini kwetu ndivyo vimetuchelewesha.Ninashuk uru sana kwa kutukubali na sisi tuingie katik ajumuiya hii.Ni furaha kubwa kwa wananchi wa Congo kujiunga na wenzao ” akasema Rais Patrice Eyenga “Mheshimiwa Patrice ninakupongeza sana kwa maamuzi haya makubwa ya kuiunganisha nchi yako na jumuiya ya Afrika mashariki.Ninaamini nchi yako itanufaika sana na fursa zilizomo katika jumuiya hii.Kuna maombi mengi ya nchi zinazotaka kujiunga na jumuiya hii lakini tumeyachambua na baaadhi ya nchi zimekataliwa nyingine tunaendelea kuzijadili lakini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tumewakubali kwa kuwa ninyi ni ndugu zetu tunafanya biashara pamoja na kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kiuchumi hivyo mnastahili kabisa kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki” akasema Dr Fabian “Kwa niaba ya wananchi wa Congo ninashukuru sana” akasema Patrice na ukimya ukapita mle ndani “Karibu sana tuijenge afrika Mashariki” akasema Dr Fabian na ukimya mfupi ukapita kisha Patrice akasema “Dr Fabian tukiachana na hilo la kukubaliwa uanachama kuna jambo lingine kubwa ambalo nataka kuzungumza nawe ili kwa pamoja tuone namna ya kulitatua” akasema Rais Patrice “Karibu” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,Tanzania na Congo tumekuwa marafiki na ndugu kwa miaka mingi.Tanzania imekuwa ni nyumbani kwa watu wa Congo.Kila pale kulipokosekana amani nchini kwetu wengi wa watu wa Congo walikimbilia huku.Watu wetu wameishi hapa kwa amani miaka nenda rudi na kwa sasa baada ya machafuko vita na mauaji kumalizika,raia wote wa Congo waliokuwa wakiishi katika nchi mbalimbali kama wakimbizi wameanza kurejea nyumbani na kwa pamoja tunaijenga Congo mpya.Uchumi wetu umeanza kukua,viwanda vingi vinajengwa,miundo mbinu inaboreshwa na kwa nafasi hii tuliyoipata ya kujiunga na jumuiya ya Afrika mashariki nina imani tutapiga hatua kubwa sana na ndani ya miaka michache ijayo nchi ya Congo uchumi wake utapaa kwa kasi ya kushangaza kwani ni nchi tajiri imejaa rasilimali.Tunataka raia wa Congo wafaidike na rasilimali ambazo Mungu amewajalia.Kwa ujumla tunakwenda vizuri” akasema Patrice na kunyamaza kidogo “Patrice binafsi ninapenda sana kukupongeza kwa namna ulivyofanikiwa kuirejesha amani ya Congo.Wamepita maraisi wengi na wamefanya mengi lakini katika suala la amani wamejaribu wakashindwa.Umetokea wewe na kuishangaza dunia kwa kuirejesha amani Congo.Nakushauri Patrice hakikisha hakutokei tena chokochoko zozote za kuweza kuvuruga amani hii mliyoipata baada ya kuikosa kwa miaka mingi na amabyo mmeipata k3a gharama kubwa.Damu nyingi imemwagika katikakuipata amani hii hivyo dhibiti viashiria vyovyote vile ambavyo vinaweza kusababisha mkarejea mahala mlikotoka katika mapigano.Nchi ya Congo mlipaswa kuwa nchi inayoongoza kwa uchumi mkubwa barani Afrika lakini mmecheleweshwa kwa sababu ya migogoro isiyokwisha.Narudia tena kukupongeza wewe kwa juhudi zako na watu wako kuamua kuweka silaha chini na kuijenga nchi.Bado mnayo safari ndefu na wewe kama kiongozi wa safari hiyo simama imara nina uhakika mkubwa mtafika mahala ambako mnataka kufika”akasema Dr Fabian “Dr Fabian hicho ndicho hasa kilichonileta hapa kwako.Tunakaribia kuingia katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.Hivi sasa ni mchakato wa teuzi ndani ya vyama unaendelea na chama changu tayari kimekwisha niteua mimi niwanie tena urais kwa muhula mwingine.Chama cha CDP ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani wao wamemteua Lucy Muganza kuwa mgombea wao.Lucy Muganza ni mwanamama bilionea,ana viwanda vingi vikubwa na amewekeza sana katika sekta ya madini.Huyu mwanamama ana ushawishi mkubwa katika siasa za Congo na ni mmoja wa watu anayependwa sana.Kwa miaka mingi amekuwa akisaidia walemavu,akina mama na vijana.Ana taasisi zake zinazosaidia watu masikini na watu wengi wamefanikiwa kujikwamua katika umasikini kupitia yeye na ndiyo CDP walipomtangaza kuwa mgombea wao,kulikuwa na shangwe karibu kila kona ya Congo kuonyesha kufurushishwa na nia yake ya kutaka kuwania urais.Binafsi najiamini nimefanya mambo makubwa na ninanguvu kubwa katika uchaguzi ujao lakini kuchaguliwa kwa Lucy Muganza kumebadili upepo wa uchaguzi na nina hakika nitakutana na wakati mgumu sana.Pamoja na mengi mazuri aliyoyafanya pamoja na kukubalika kwake lakini watu wa Congo hawamfahamu Lucy Muganza ni nani.Naamini kama wangemfahamu wasingeingia mitaani kushangilia uteuzi wake” Patrice akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Tetesi za Lucy kuteuliwa kugombea urais na chama cha CDP nilizipata muda mrefu na kama kawaida yetu wanasiasa nilijua lazima kutatokea mchuano mkali kati yangu naye na nikaweka timu maalum ya majasusi ambao wamekuwa wakimchunguza kwa siri nyendo zake ndipo nikagundua kuwa Lucy ni hatari sana kwa usalama wa Congo” akanyamaza tena kwa sekunde chache na kuendelea “Tulichogundua ni kwamba,Lucy anatumiwa na mataifa ya magharibi kutaka kuivuruga Congo na hata kugombea urais si utashi wake bali amesukumwa na nchi za Magharibi afanye hivyo.Utajiuliza nini sababu ya Lucy kutumiwa na nchi tajiri kutaka kuiharibu Congo? Sababu kubwa ni hii.Nilipoingia madarakani nchi ya Congo bado ilikuwa katika vita na mauaji.Bado rasilimali zetu za madini zilikuwa zinatoroshwa na kuzifaidisha nchi tajiri.Tulichokifanya mimi na serikali yangu ni kwanza kurejesha amani Congo na tukafanikiwa.Baada ya mapigano kumalizika kilichofuta kilikuwa ni kukata mirija yote ya wanyonyaji wa rasilimali zetu na hili halikuwapendeza wakubwa wa huko nje waliokuwa wakifaidika kwa kiasi kikubwa na rasilimali za madini kutoka Congo ndiyo maana wanataka kutumia uchaguzi huu kikamilifu kuhakikisha mtu wao ambaye atawarejesha katika kuendelea kuchota rasilimali za Congo anashinda uchaguzi.Taarifa nilizonazo ni kwamba Lucy ambaye yuko ufaransa kwa sasa,ameendelea kufanya vikao vya siri na watu hao wanaomtaka awe rais wa Congo wakijadili mikakati mbali mbali ya kupata ushindi.Ninakiri Lucy ana nguvu kubwa sana nchini Congo na kuna nyakati ninakuwa na hofu kwamba ninaweza nikashindwa na yeye akaibuka mshindi katika uchaguzi mkuu ujao.Endapo Lucy atashinda uchaguzi basi lengo la watu walio nyuma yake ni kuirejesha nchi ya Congo kule ilikotoka katika machafuko na kuwapa mabeberu nafasi ya kuendelea kunyonya rasilimali zetu wakati sisi tukipigana kwani ili watunyonye lazima kwanza watuvuruge tushindwe kuelewana wenyewe kwa wenyewe na hapo wanapata nafasi nzuri ya kuchota madini yetu na rasilimali nyingine bila huruma” akanyamaza na kunywa funda la maji halafu akaendelea “Lucy Muganza si hatari kwa Congo pekee bali kwa jumuiya nzima ya Afrika Mashariki.Kitendo cha Congo kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki hakijawafurahisha hawa wakubwa hivyo wanao mkakati wa kuisambaratisha jumuiya hii ambayo uwepo wake ni kikwazo kikubwa kwao katika kuendeleza unyonyaji wa rasilimali za nchi wanachama kwani nchi zote ndani ya jumuiya zinasimama pamoja na kuzungumza lugha moja hasa linapokuja suala la kulinda rasilimali zilizopo katika nchi zetu.Jumuiya ya Afrika Mashariki imestawi sana na kuwa mfano barani Afrika kiasi cha kuvutia nchi nyingi kutaka kujiunga itasambaratika endapo Lucy Muganza atafanikiwa kushinda uchaguzi na kuingia madarakani” akasema Patrice na kunyamaza.Dr Fabian bado alikuwa kimya akisikiliza “Ipi mikakati yao kuihujumu jumuiya ya Afrika Mashariki?akauliza Dr Fabian “Dr Fabian unajua ni kwa nini sikutaka kulizungumza jambo hili mbele ya maraisi wengine? Ni kwa sababu kuna baadhi ya maraisi tayari wana mahusiano ya karibu na ya siri sana na Lucy Muganza.Hata kabla ya kushinda uchaguzi tayari amekwisha anza mikakati ya kuisambaratisa jumuiya.Upo mpango wa siri unaandaliwa wa kuunda jumuiya nyingine ndogo ya nchi tatu pale jumuiya hii ya nchi saba itakapokuwa imesambaratishwa.Mwanam ke huyu ni nyoka mkubwa na anapaswa kukanyagwa kichwa haraka sana kabla hajaleta madhara” akasema Patrice “Hilo ni suala zito sana Patrice.Sikuwahi kufikiri kama ndani ya jumuiya hii kunaweza kutokea jambo la namna hiyo.Hili unalonieleza kuhusu baadhi ya marais kutaka kujiunga na Lucy kuanzisha jumuiya yao ndogo una uhakika nalo?akauliza Dr Fabian “Ndiyo Dr Fabian.Ninao uhakika mkubwa kwamba kuna jumuiya mpya ya nchi tatu inataka kuanzisha baada ya jumuiya hii kubwa kusambaratishwa”akajibu Patrice “Ni marais gani ambao tayari Lucy ameanza kuzungumza nao juu ya jambo hilo?akauliza Dr Fabian.Patrice akaufungua mkoba wake akatoa faili na kumpatia DrFabian. “What is this?akauliza Dr Fabian “Tumekuwa tukifuatilia mawasiliano yote ya Lucy na ndani ya faili hilo kua mawasiliano yake yote anayoyafanya na marais hao wawili na kupanga mipango yao ya kuanzisha jumuiya mpya ya nchi tatu” akasema Patrice na Dr Fabian akaanza kufungua kurasa moja moja “Nitakuachia faili hilo utaendelea kulipitia taratibu.Kila kitu kiko humo kuanzia mawasiliano ya simu,barua pepe na katika hiyo diski kuna kuna rekodi za mazungumzo yao ya simu” akasema Patrice.Dr Fabian akalifunika lile faili halafu akasimama akazunguka mle chumbani huku akitazama juu halafu akajiegemeza katika meza na kusema “Wakoloni hawa wametutawala tukawa watumwa wao,wamechukua rasilimali zetu na kutajirisha nchi zao huku wakituachia umasikini mkubwa.Tunapofanya juhudi za kujikomboa wao wanatumia uwezo walio nao kuhakikisha hatusongi mbele tunabaki pale pale tulipo na kama haitoshi bado wanaendelea na mipango ya kutaka kuendelea kutuibia.Ni kwa sababu yao mifarakano katika bara la Afrika haiishi.Kila mahala ni vurugu na ukichunguza chanzo chake utakuta kuna mkono wa mataifa makubwa.Wanasema Afrika imelaaniwa,ninakataa Afrika hatujalaaniwa bali wao wanaokuja kutuibia rasilimali zetu tulizopewa na Mungu ndio waliolaaniwa.Inashangaza sana kuona mpaka sasa bado kuna watu tena viongozi wakubwa wanaendelea kuwaabudu hawa mabeberu na wako tayari kufanya jambo lolote kwa ajili yao hata kumwaga damu za ndugu zao ili mradi kuwafurahisha mabeberu.Patrice tunatakiwa kusimama na kusema hapana kwa unyonyaji huu.Wazee wetu akina mzee Nyerere,Lumumba na wengineo walijioa kupambana kuhakikisha tunajikomboa kutoa katika makucha ya wanyonyaji ni jukumu letu na sisi kusimama imara kuhakikisha unyonyaji huu hauendelei.Jumuiya ya Afrika mashariki kweli ni mwiba kwao kwani tumekata mirija ya wanyonyaji na sasa wanahangaika kutaka kuivunja” akasema Dr Fabian “Ahsante kwa kunielewa Dr Fabian sasa tunazungumza lugha moja.Tanzania imechukua uongozi wa jumuiya hii sitaki isambaratikie mikononi mwako ndiyo maana ninataka tufanye kila linalowezekana kuhakikisha kwamba lengo la mabeberu hawa halitimii.Tupambane tuiokoe Congo na tuiokoe jumuiya ya Afrika mashariki ambayo wenzetu wanafikiria kuivunja.Binasi siko tayari nchi yangu irejee kama ilivyokuwa zamani Congo ya vita na mauaji yasiyokwisha.Imetugharimu miaka mingi na gharama kubwa kuipata amani hii tuliyonayo sasa.Siko tayari kuipoteza na kuwaacha mabeberu wakiendelea kufaidika na rasilimali zetu,nitapambana hadi tone la mwisho la damu kuifia nchi yangu.Hata kama ni kutawala kwa lazima nitafanya hivyo kuilinda amani ya Congo na kuzuia mabeberu wasithubutu tena kukanyaga katika ardhi yetu ndiyo maana nimekuja kwako rafiki yangu na ndugu yangu kuomba msaada wako.Tanzania mmekuwa nasi wakati wote wa machafuko na hamjawahi kutuacha hata mara moja na ninaamini hamtatuacha hata sasa tunapohitaji kuilinda amani yetu kwa gharama zozote”akasema Patrice.Dr Fabian akamtazama kwa makini halafu akauliza “Nini ushauri wako katika hili Patrice? Akauliza Dr Fabian.Ilipita dakika moja Patrice akasema “Ni kumuua Lucy Muganza” akasema na kunyamaza kwanza ili kile alichokitamka kimuingie Dr Fabian halafu akaendelea “Hiyo ndiyo njia pekee iliyobaki ya kuliepusha taifa la Congo kurejea kule lilikotoka,kuikoa jumuiya ya Afrika mashariki na kuzima kabisa ndoto za mabeberu za kutaka kuendelea kunyonya nchi zetu.Ni uamuzi mgumu lakini ndiyo njia pekee ya kulimaliza hili suala.Binafsi nimeishi katika shida kubwa,nimesoma kwa taabu ninafahamu mateso waliyokuwa wakiyapata watu wa Congo ndiyo maana yeyote anayecheza na amani ya Congo ni adui yangu mkubwa.Lucy Muganza ni hatari sana kwa amani yetu ndiyo maana ninashauri tumuondoe” akasema Patrice na ukimya ukatawala mle ndani halafu Dr Fabian akasema “Patrice sina kipingamizi chochote na hicho unachokisema lakini nina maswali machache.Huyu mama kama ulivyosema ni maarufu sana nchini Congo na ana wafuasi wengi,kama tukimuua hudhani wafuasi wake wanaweza wakahisi ni serikali ndiyo waliofanya mpango huo wa mauaji na vurugu kubwa zikaanza?Jambo lingine hata kama akiuawa Lucy hawa wakubwa walioko nyuma yake hawataweza kutafuta mtu mwingine ambaye atachukua nafasi ya Lucy na kuendeleza mikakati yao?Kama wakifanya hivyo tutaendelea kuua kila atakayeteuliwa? “Mtu mwingine wanaweza wakampata ili kuendelea na mipango yao lakini hatakuwa na umaarufu mkubwa kama Lucy.Huyu mama licha ya kuungwa mkono na nchi za Magharibi lakini hata yeye binafsi nguvu yake ya ushawishi ni kubwa.Angeweza hata kusimama peke yake bila ya kuungwa mkono na nchi za magharibi na akashinda uchaguzi.Tukimuondoa huyu mama itawapa hata wao wakati mgumu wa kutafuta mtu ambaye ana uwezo kama Lucy na hii itanihakikishia mimi ushindi.Kuhusu vurugu haitakuwa rahisi kutokea kwani Lucy hatauawa akiwa Congo.Atauawa akiwa hapa Tanzania” “Tanzania?! Dr Fabian akashangaa “Ndiyo.Akiuliwa hapa Tanzania haitakuwa rahisi mtu yeyote kuhisi kama serikalio ya Congo inahusika na mauaji hayo”akasema Patrice na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “Ni vipi kama ukifanyika uchunguzi na ikagundulika kwamba sisi ndio tuliotekeleza mauaji hayo,huoni kwamba Tanzania itachafuka kimataifa jambo ambalo sitaki litokee.Tunasifika duniani kote kwa amani sitaki sifa hii nzuri iharibike kwa kufanya mauaji hayo katika ardhi ya Tanzania”akasema Dr Fabian “Dr Fabian nadhani umewahi kusikia kuhusu kufanya maamuzi magumu na katika mambo kama haya ndipo maamuzi magumu hufanyika.Usiwe na hofu nitatuma kikosi changu kuja kumuua Lucy ili kuiepusha nchi yao na lawama.Dr Fabian ninakuomba tufanye hivi kwa maslahi ya Congo na jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.”akasema Patrice “Tatizo si kumuua Lucy bali ni kumuua katika ardhi ya Tanzania.Unafahamu namna nchi hii inavyoheshimika kimataifa,sitaki nchi yangu ichafuke kama ambavyo wewe hutaki nchi yako ichafuke”akasema Dr Fabian “Dr Fabian wewe ni mgeni katika uongozi una mwaka mmoja tu sasa na humfahamu vyema Lucy Muganza na inawezekana hujawahi hata kumtia machoni lakini ni mwanamke mwenye nguvu kubwa na ndiyo maana hata mimi binafsi ninamuogopa kwamba akiachwa anaweza akachukua nchi na ninavyomfahamu akichukua nchi atairudisha ilivyokuwa awali.Ataleta machafuko katika nchi za maziwa makuu.Nchi na nchi hazitaelewana,ule umoja wetu utatoweka na kila nchi itasimama yenyewe.Hilondilo wanalitaka hawa wakubwa ili waweze kuingia na kutuibia mali zetu.Ni sisi wawilitu ambao tunaweza kuzia hayoyasitokee na njia pekee ya kuzuia yasitokee ni kwa kumuua Lucy Muganza” akasema Patrice.Dr Fabina alikaa kimya kwa muda halafu akauliza “Umekwisha andaa mpango wa kumuua Lucy? “Kama nilivyosema kwamba kuna timu ya majasusi ambayo inamfuatilia Lucy kwa siri kubwa sana.Kwa sasa Lucy yuko Ufaransa ambako amekuwa na mfululizo wa vikao na hao wakubwa wakifanya mikakati ya kuhakikisha Lucy anashinda uchaguzi mkuu ujao.Jumamosi ya wiki hii atarejea nyumbani lakini kabla ya kuelekea Kinshasa atakuja kwanza Tanzania.Hapa ana mtoto wake anayesoma katika chuo kikuu cha Dar es salaam anaitwa Theresia Muganza.Katika safari hiyo Lucy pia atakuwa ameongoza na mume wake Laurent na lengo la kuja Tanzania ni kumchukua binti yao Theresia ili waelekee Kinshasa kama familia ambako mapokezi makubwa yanamsubiri Lucy kutoka kwa malefu ya wafuasi wa chama cha CDP.Nataka atakapotia mguu hapa Tanzania asiondoke hai bali jeneza lake ndilo lirejeshwe Congo.Ninacho kikosi nimekiandaa kwa ajili ya kazi hiyo ambacho kama ukiniruhusu nitakituma kuja kumuondoa Lucy hapa Tanzania” akasema Patrice Dr Fabian akawaza kidogo na kusema “Patrice wewe ni rafiki yangu mkubwa,tumekutana masomoni nje ya nchi na sasa wote tumeshika nafasi za urais na siwezi kukukatalia ombi lako kwa ajili ya kulinda Afrika Mashariki na kuilinda amani ya Congo.Lucy atauawa hapa Tanzania lakini na watu wangu.Sitaki watu wa nje waje kufanya mauaji katika ardhi yetu.Ninao vijana mahiri wanaoweza kuifanya hiyo kazi.Nitakachohitaji kutoka kwako ni mawasiliano kati ya timu yako inayomchunguza Lucy na timu yangu nitakayoiandaa kwa ajili ya kumuondoa” akasema Dr Fabian.Maongezi yaliendelea kwa takribani nusu saa kisha wakaagana Patrice akaondoka kuelekea Kinshasa.Kiongozi wa mwisho kuondoka Arusha alikuwa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo.Akiwa ndani ya ndege alikuwa kimya akilipitia faili lile alilopewa na Patrice.Akaichomeka diski aliyopewa na Patrice katika kompyuta na kuanza kusikiliza mazungumzo yaliyorekodiwa ya Lucy Muganza na baadhi ya viongozi wa nchi zilizo katika jumuiya ya Afrika Mashariki “Patrice yuko sahihi mwanamke huyu ni hatari sana kwa uhai wa jumuiya yetu ya Afrika mashariki na anapaswa kuondolewa haraka sana kabla hajaleta madhara.Kinachonishangaza marais hawa ambao Lucy amekuwa akiwasiliana nao wakipanga mikakati ya kuanzisha jumuiya yao ndogo ni watu walio mstari wa mbele sana katika kuhimiza mshikamano madhubuti miongoni mwa wanachama wa jumuiya hii kumbe wana siri kubwa wanatembea nayo.Nitapambana kuhakikisha jumuiya hii haivunjikii mikononi mwangu.Nitailinda jumuiya hii kwa gharama zozote katika wakati wangu kama mwenyekiti japo wapo viongozi ambao wako tayari ivunjike lakini watasubiri hadi pale nitakapokuwa nimemaliza muda wangu wa uongozi lakini nina hakika kama tukimuondoa Lucy na mipango yao yote ya kuanzisha jumuiya yao ndogo nayo itayeyuka” akawaza na kulifunika lile faili “Lakini bado kuna kitu kinanipa ukakasi katika akili yangu.Lucy Muganza ni tegemeo la mataifa ya magharibi katika kufanikisha mipango yao ya unyonyaji wa rasilimali zetu ni vipi kama walio nyuma yake wakiamua kufanya uchunguzi wa kifo chake na wakabaini kwamba ninahusika?Nitakuwa nimeingia katika mgogoro mwingine mkubwa na nchi za magharibi.Nifanye nini?Nijitoe katika mpango huu wa kumuua Lucy Muganza?akajiuliza “Hapana siwezi kujitoa katika mpango huu.Tayari nimekwisha muhakikishia Patrice kwamba niko pamoja naye katika suala hili.Hata mimi siko tayari kuona machafuko yakirejea tena Congo kama ilivyokuwa zamani.Watu wa Congo wameitafuta amani kwa miaka mingi na wametumia gharama kubwa hadi kuipata.Ni jukumu letu sisi majirani zao kuhakikisha amani waliyo nayo haipotei tena.Kibaya zaidi ni mipango yao ya kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Nadhani kumuua Lucy ndiyo njia pekee ya kulitatua hili jambo hata hivyo umakini mkubwa sana unatakiwa.Ni suala ambalo linapaswa kupangwa kitaalamu mno” akawaza Dr Fabian Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye katika historia ya marais waliowahi kuingia madarakani yeye ndiye anayetajwa kuwa kijana kuliko wote na mwenye sura ya kuvutia. DAR ES SALAAM Ni saa saba na dakika ishirini na moja za usiku lakini bado Dr Fabian hakuonekana kuwa na usingizi.Alikuwa ameketi sofani akiwa na lundo la vitabu pembeni yake.Millen mke wake alimfuata pale sofani na kukaa karibu yake akakifunika kitabu alichokuwa anakisoma mume wake na kumbusu “What’s wrong darling.Uliondoka hapa kuelekea Arusha ukiwa na furaha kubwa lakini umerejea ukiwa katika hali ya mawazo mengi na haujazungumza nami kitu chochote kuhusiana na safari ya Arusha.Nini kimetokea huko?akauliza Millen mwanamke mwenye weupe wa kung’aa na sura ya upole yenye tabasamu muda wote.Dr Fabian akamtazama mke wake halafu akatabasamu na kusema “Usijali Millen.Kila kitu kiko sawa” “Hapana.Ninakufahamu vyema Fabian hauko sawa.Something is wrong with you.Nini kimetokea Arusha? Niambie tafadhali kama kuna tatizo lolote nijue”akasema Millen “Fine” akasema Dr Fabian na kuvuta pumzi ndefu “Arusha mambo yamekwenda vizuri hakukuwa na tatizo lolote.Tumechukua uenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda wa mwaka mmoja.Kwa ujumla kila kitu kilikwenda vizuri kabisa” “Kama kila kitu kilikwenda vizuri nini hasa kinakusumbua kichwa chako mpenzi wangu?Si kawaida yako kukaa hapa hadi muda huu.Nini kinakusumbua? “Ni kweli Millen nina tatizo lakini naomba nisikwambie kwa sasa ni tatizo gani” “Hapana nieleze Fabian.Hakuna tatizo lako ambalo haujawahi kunieleza” akasema Millen.Dr Fabian akamtazama mkewe halafu akasema “Toka nimeingia madarakani nimekutana na mtihani wangu wa kwanza mkubwa ambao lazima niushinde” “Mtihani upi? Akauliza Millen na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “I need to silence someone very dangerous” akasema na kukaa kimya baada ya kuuona mstuko katika uso wa mke wake “You mean killing somebody?akauliza Millen na Dr Fabian akatikisa kichwa kukubali “Kuna mataifa makubwa ambayo hayapendi kuona jumuiya ya Afrika mashariki inastawi na wanajaribu kutumia kila njia kuisambaratisha.Kuna mtu ambaye wanamtumia katika kulifanikisha hilo.Njia pekee ya kumaliza mipango na njama zao ovu ni kwa kumuondoa huyo ambaye wanataka kumtumia lakini jambo hilo linatakiwa lifanywe kitaalamu sana ndiyo maana ninasoma vitabu hapa kuhusu vifo mbali mbali vya watu maarufu vilivyowahi kutokea duniani na ambavyo mpaka leo hii havijawahi kupatiwa ufumbuzi.I want this one to be unsolved murder” “Fabian hakuna namna nyingine ya kuweza kulishughulikia suala hilo zaidi ya kuua?I’m scared” akasema Millen “Millen nimekushirikisha jambo hili la siri kubwa ambalo sikupaswa kukueleza.Natamani ningekuwa na njia nyingine ya kuweza kuliondoa tatizo hilo zaidi ya hii ninayotaka kuifanya lakini hakunanjia nyingine.It’s hard even for me but I have to do it.Mtu huyo ni hatari na si kwa jumuiya ya Afrika mashariki pekee bali ni hatari pia kwa amani ya Congo.Umewahi kufanya kazi katika shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi unafahamu mateso na taabu wanazopitia wakimbizi,mtu huyo anataka kutumiwa kuirejesha Congo katika machafuko ili mabeberu waweze kurejea tena na kuendelea kuchota rasilimali za nchi hiyo.I won’t let that happen ! akasema Dr Fabian “Hofu yangu Dr Fabian ni vipi kama ukifanyika uchunguzi na ikabainika kwamba unahusika na mauaji hayo?akauliza Millen “That won’t happen.Ni jambo ambalo litafanywa kitaalamu mno ndiyo maana nikakwambia kwamba nataka jambo hili lisiweze kupatiwa ufumbuzi hata kama wataamua kulichunguza” akasema Dr Fabian.Mke wake hakuzungumza tena kitu kingine akamshika mkono mumewe na kumuongoza kwenda chumbani kupumzika kwani muda ulikuwa umekwenda sana.



Saa tatu na nusu za asubuhi gari tatu ziliwasili ikulu jijiji Dar es salaam.Kutoka katika mojawapo ya gari akashuka Rais mstaafu wa jamhuri ya muungao wa Tanzania Dr Evans ambaye alipokewa na Rais Dr Fabian akamuongoza ndani.Moja kwa moja wakaelekea sehemu ya mazungumzo ya faragha. “Mambo yanakwenda vipi hapa mheshimiwa Rais?akauliza Dr Evans “Mambo yanakwenda vyema mzee,tunaendelea vizuri” akajibu Dr Fabian “Hongera sana mheshimiwa Rais.Ni kweli mambo yanakwenda vizuri hata sisi tulio huko nje tunaona.Kila kitu ni kizuri.Ongeza juhudi zaidi” “Nashukuru sana mzee” “Hongera pia kwa kuchukua uenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza” “Ahsante mzee ninashukuru sana.Vipi maisha ya ustaafu? “Maisha yanakwenda vizuri.Ninapumzika vya kutosha sasa na hata mwili wangu umeanza kunawiri” akasema Dr Evans na wote wakacheka “Mzee nimekuita hapa kwa mazungumzo ya faragha ningeweza kukufuata kwako mimi mwenyewe lakini kama unavyojua taratibu za hapa ni ngumu kidogo” “Hakijaharibika kitu mheshimiwa Rais ninafahamu kila kitu hivyo usihofu” “Ahsante mzee.Nimekuita hapa ninahitaji sana msaada wako wa mawazo” “Ndiyo nakusikiliza” “Jana tumeipokea rasmi jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika jumuiya ya Afrika mashariki na kufanya jumla ya nchi wanachama kuwa saba katika jumuiya hiyo” “Hilo ni jambo jema sana.Jumuiya inazidi kupanuka na kuimarika zaidi.Kwa miaka michache ijayo jumuiya hii itakuwa ni moja kati ya jumuiya kubwa kabisa zenye nguvu barani Afrika”akasema Dr Evans “Ni kweli mzee hayo unayoyasema.Jumuiya ya Afrika Mashariki imestawi sana na kuzifanya nchi nyingi kutaka kujiunga lakini nyingine kama Somalia zimekataliwa kwa sasa hadi baadae”akanyamaza kidogo na kuendelea “Baada ya mkutano kumalizika nilikuwa na mazungumzo marefu ya faragha na Rais Patrice Eyenga wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Patrice alinieleza kuhusiana na mchakato wa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unavyoendelea nchini Congo lakini hapo hapo likaibuka tatizo.Chama cha upinzani cha CDP kimemteua mwanamama Lucy Muganza kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu ujao” “Nilisikia taarifa hizo.Lucy Muganza nimewahi kumsikia.Ni mwanamama bilionea nchini Congo”Akasema Dr Evans “Ndiye huyo.Ni mwanamama mwenye nguvu sana nchini Congo na ni mpinzani mkubwa wa Rais Patrice.Pamoja na nguvu yake kubwa ya ushawishi aliyonayo mwanamama huyo lakini kuna jambo kubwa nyuma yake.Anatumiwa na mataifa ya magharibi ambayo hayajafurahishwa na utawala wa Rais Patrice ambaye amekata mirija ya unyonyaji na anataka Congo inufaike na rasilimali ilizo nazo.Kwa miaka mingi nchi ya Congo imekuwa katika machafuko lakini baada ya kuingia madarakani Rais Patrice amefanya kazi kubwa na hatimaye amani imepatikana Congo.Mambo aliyoyafanya Patrice hayajawafurahisha mataifa yaliyokuwa yakinufaika na rasilimali za Congo hivyo basi wanataka kuweka mtu wao katika madaraka ambaye atairejesha tena Congo katika machafuko ili wao warejee tena kuendelea kuchota rasilimali.Mtu huyo ambaye wanataka kumtumia ni Lucy Muganza.Kama haitoshi wana mpango pia wa kuivuruga jumuiya ya Afrika Mashariki.Kutokana na uimara wake jumuiya hii imekuwa ni mwiba kwa mabeberu waliozoea kuchota rasilimali zetu na kufaidisha nchi zao.Kitendo cha jamhuri ya kidemokrasia kukubaliwa kujiunga na jumuiya ya Afrika mashariki kinawanyima usingizi kwani wanaamini itakuwa vigumu tena kwao kuendeleza unyonyaji wao kutokana na uimara wake hivyo kwa gharama zozote wanataka kuhakikisha jumuiya hii inasambaratika.Lucy Muganza amekwisha anza mipango hiyo na tayari amefanya mawasiliano na baadhi ya wakuu wa nchi zilizo katika jumuiya ya Afrika Mashariki na tayari viongozi wa nchi mbili wamekwisha kubaliana kwamba mara tu uchaguzi utakapofanyika na yeye akawa mshindi basin chi hizo zitajiondoa kutoka katika jumuiya ya Afrika Mashariki na kuunda jumuiya yao ndogo ya nchi tatu” akanyamaza kidogo kwa muda halafu akaendelea “Baada ya majadiliano na Rais Patrice tumeona hakuna njia nyingine ya kupambana na mabeberu hawa na kuififisha mipango yao miovu zaidi ya kumuondoa Lucy Muganza” akanyamaza “Unaonekana unaogopa Dr Fabian” akasema Dr Evans huku akitabasamu “Mzee napenda nikiri ni kweli ninaogopa.Ni mara yangu ya kwanza toka nimekalia kiti hiki kukutana na mtihani mgumu kama huu ambao unanilazimu nitoe uhai wa mtu” “Karibu Dr Fabian katika ulimwengu wa mitihani ya urais.Mambo ndiyo kwanza yameanza.Mitihani kama hii itakuja mingi na unatakiwa kuishinda.Unachotakiwa ni kufanya maamuzi ya haraka,sahihi na kwa wakati muafaka.Usiwe mwoga katika kufanya maamuzi wewe ni rais na watu zaidi ya milioni hamsini wanakutegemea wewe kwa usalama wa maisha yao,afya zao na mustakabali mzima wa maisha yao hivyo kama kuna kitisho chochote kwa nchi kiondoe haraka mno kabla hakijaleta madhara makubwa bila kujali gharama.Nadhani umenielewa” akasema Dr Fabian “Nimekuelewa mzee ndiyo maana mimi na Rais Patrice tumeamua kwa pamoja kumuondoa Lucy Muganza.Ambacho kinanipa wasi wasi ni how to do it?Kwa usiku mzima nimekuwa nikitafakari sana namna ya kulifanya tukio hilo kuwa unsolved nimekosa jibu ndiyo maana nimekuita hapa unisaidie mawazo mzee wangu.Wewe umekuwepo madarakani kwa miaka kumi umepitia mengi na ninaamini unazo mbinu nyingi za kuweza kulishughulikia suala hili” akasema Dr Fabian na Dr Evans akamtazama na kuinuka akaanza kuzunguka mle ndani “How to do it” akasema kwa sauti ndogo “Fabian my president you don’t know how to do it?Please don’t let me down.Nilikupendekeza,nikak upigania kwenye chama na hata katika kampeni because I saw something special in you.Nilimuona Rais ambaye ataipeleka Tanzania mbali zaidi ya hapa tulipoifikisha mimi na wengine wote waliopita.Rais mwenye nguvu ambaye ataogopwa ndani na nje.Imekuaje leo unaniita na kutaka nikufudishe namna ya kutatua tatizo dogo kama hili?akauliza Dr Evans kwa ukali “Mzee ninahitaji ushauri na namna bora ya kuweza kulitatua suala hili.Wewe unao uzoefu mkubwa sana zaidi yangu mimi” “C’mon Dr Fabian you are a president ! You have everything in your power.Kwa nini unakuja kwangu?Tafadhali Fabian usiniangushe mimi ambaye nilipambana kuhakikisha unaingia madarakani.Make me proud.Tumia nguvu uliyo nayo dhidi ya mtu yeyote wa ndani au wa nje ya nchi ambaye anatishia amani yetu.Usisite kuchukua hatua haraka kila pale linapojitokeza suala lolote la hatari.Usitegemee watu wengine wafikiri badala yako watakupoteza.Nimekuwa nakuelekeza mambo haya kila wakati” akasema Dr Evans na kumtazama Dr Fabian ambaye alikuwa ameinamisha kichwa.Maneno yale ya Dr Evans yalimuingia “What do you need?akauliza Dr Evans “Kwa kuwa Lucy Muganza ni tegemeo kubwa kwa nchi za Magharibi nina uhakika mkubwa baada ya kumuua watakuja kufanya uchuguzi.I want it to be unsolved” akasema Dr Fabian “Unataka tukio lifanyike hapa Tanzania? “Ndiyo mzee.Likifanyika Congo watajua ni mpango umesukwa wa kumuua ndiyo maana tunataka tukio hilo lifanyike hapa Tanzania” “Una ila kitu Dr Fabian cha kukusaidia.Idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi ipo chini yako kwa nini unashindwa kuitumia wakati ina watu wenye ujuzi mkubwa wa kuweza kulifanya jambo hilo?akauliza Dr Evans “Mzee ni kweli unalolisema lakini suala hili ni la siri kubwa ndiyo maana sitaki lijulikane.Zaidi ya yote bado sina mtandao wa watu ninao waamini kuwashirikisha katika mambo makubwa na ya siri kama haya” “That’s the problem Dr Fabian.Huwezi kuwa peke yako bila kuwa na watu unaowaamini.Huwezi kufanya kila jambo siri lazima uwe na watu ambao unawaamini na unawashirikisha mambo makubwa kama haya japo unapaswa uwe makini sana si kila mtu anapaswa kuaminiwa”akasema DrEvans “Mheshimiwa Rais ulisalitiwa na waziri mkuu wako mtu ambaye ulimuamini sana na kitendo hicho kinanipa woga hata mimi kuwaamini watu walio karibu yangu na kuwashirikisha mambo makubwa kama haya” “Unalolisema ni la kweli Dr Fabian.Katika mambo haya ya uongozi umakini mkubwa unatakiwa kujua nani unamshirikisha nini na kwa nini.Si kila mtu anapenda wewe uwepo mahali hapa.Wapo watu ambao wanawaza kukushusha kutoka mahali hapa ulipofika lakini hawataweza.Hata hivyo unatakiwa uwe na watu wachache ambao unawaamini na watakusaidia sana katika mambo yako.Kuna mtu mmoja ambaye wakati wangu nilimuamini sana na alikuwa na msaada mkubwa.Ni mkuu wa kikosi cha jeshi cha operesheni maalum anaitwa Austin January.Ni mtu makini,mtiifu na mtunza siri.You can trust him” akasema Dr Evans “Austin January” akasema Dr Fabian “Ni kijana kama wewe japo umemzidi kidogo lakini mnaweza mkaelewana sana.Binafsi ni mtu ambaye nilimtumia sana katika mambo yangu mbali mbali na amenisaidia mno japo kuna wakati tulitofautiana lakini niliyekuwa mkorofi ni mimi.Nakushauri mtumie sana huyu mtu”akasema Dr Evans “Ahsante sana mzee kwa ushauri wako huu.Vipi kuhusu idara ya siri ya mambo ya ndani?Ninaweza kuwaamini kuwashirikisha katika mambo makubwa ya siri? “Ni idara yenye msaada mkubwa kwa Rais lakini nakushauri kwa mambo makubwa kama haya usiwashirikishe.Watumie kwa mambo mengine ya kawaida ya usalama wa ndani ya nchi” “Mzee ninakushukuru sana kwa ujio wako huu ambao umenipa nguvu mpya”akasema Dr Fabian “Ninashukuru kwa kuniita.Kwa kuongezea kabla sijaondoka,tukio hilo lifanye lionekane ni tukio la ujambazi.Austin anafahamu mambo yote haya na atakuelekeza nini cha kufanya” akasema Dr Evans “Mzee nakushukuru kwa mara nyingine tena kwa ujio wako huu ambao umekuwa na msaada mkubwa kwangu.Usinichoke pale nitakapokuita tena kukuomba msaada.Mimi bado ni kijana wako ninaendelea kujifunza mambo na bado ninakutegemea”akasema Dr Fabian “Mr president please don’t call me again to come here labda iwe ni kwa sherehe.Sifanyi hivi kwa nia mbaya bali kukupa wewe uwanja mpana wa kufanya mambo yako.Huu ni wakati wako,sisi tumekwisha maliza muda wetu na tunakupa na wewe nafasi ya kuongoza nchi kwa uhuru.Usitutegemee sana sisi” akasema Dr Evans wakaagana akaondoka ikulu. “Dr Evans ameongea maneno mazito lakini yenye maana kubwa.Mimi ni Rais nina kila kitu ninapaswa kusimama kama Rais na si kuonyesha woga wa aina yoyote.Natakiwa kuilinda nchi yangu kwa gharama zozote zile hicho ndicho kiapo nilichokula” akawaza DrFabian na kuinua mkono wa simu akampigia katibu muhtasi wake na kumtaka atume ujumbe kwa Austin January mkuu wa kumtaka afike ikulu jioni ya siku ile kwa ajili ya kupata chakula cha usiku na Rais ***************** Saa moja na nusu za jioni Austin January akiwa na dereva wake aliwasili ikulu akapokewa na mwenyeji wake ambaye ni Rais Dr Fabian.Usiku huu Austin alivaa suti nzuri ya rangi nyeusi iliyomkaa vyema.Ilikuwa ni mara ya kwanza kufika ikulu tangu Rais Dr Fabian alipochukua madaraka. “Austin January karibu sana ikulu.Nimefurahi leo kuonana nawe ana kwa ana”akasema Dr Fabina akimkaribisha Austin “Nshukuru sana mheshimiwa Rais hata mimi nimefurahi kukutana nawe.Ahsante sana kwa kunikaribisha”akasema Austin “Utanisamahe hata hivyo kwa kuchelewa kukutana na mtu kama wewe.Mambo ni mengi ndiyo maana kuna vitu vingine kama kukutana na watu muhimu kama ninyi ninasahau lakini hakijaharibika kitu.Leo tumekutana na utakuwa ni mwanzo wetu mzuri wa kujenga mahusiano mazuri na kuendelea kukutana mara kwa mara”akasema Dr Fabian “Nashukuru sana mheshimiwa Rais.Ni heshima kubwa kwangu kukutana nawe kwa mara ya kwanza toka umeingia madarakani” akasema Austin. Chakula maalum kiliandaliwa na Austin akakaribishwa.Alihisi furaha kubwa kukaribishwa ikulu na kupewa heshima ya namna ile.Baada ya chakula Dr Fabian akamtaka Austin waelekee katika chumba cha mapumziko. “Austin kwa mara nyingine tena ninakushukuru kwa kuitika wito na kuja kunitembelea” Dr Fabian akaanzisha maongezi “Hata mimi ninakushukuru mheshimiwa Rais kwa kunialika” “Austin pamoja na kutaka kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri na watu kama wewe,kuna jambo ambalo ninahitaji msaada wako.Kama unavyojua mimi nina mwaka mmoja tu tangu nichukue nafasi hii ya urais bado kuna mambo mengi naendelea kujifunza ikiwamo kutafuta watu wa karibu ambao nitawaamini na kuwashirikisha kati9ka mamo mazito ya nchi.Wewe ni mmoja wa watu ambao ninategemea kufanya naye kazi kwa ukaribu sana.” “Nashukuru sana mheshimiwa Rais kwa kuniamini”akasema Austin “Nimejifunza mengi kutoka kwa watangulizi wangu hasa Dr Evans na kubwa zaidi ni kuwa na watu wachache ninaowaamini ambao nitawaeleza zile siri ambazo watakwenda nazo kaburini.Ni Dr Evans ndiye aliyenifumbua macho kuhusu wewe.Amekumwagia sifa lukuki namna ulivyomsaidia wakati alipokuwa madarakani.Huko aliko hatasahau uaminifu wako mkubwa kwake ndiyo maana akanishauri uwe mmoja wa watu nitakaowaamini na mimi ninamuamini sana Yule mzee neno lake ni kama amri kwangu hivyo nimekuita hapa kukufahamisha kwamba kuanzia sasa wewe ni mmoja wa watu wangu wachache ambao nitakuwa nao karibu sana” “Ahsante mheshimiwa Rais kwa heshima hii kubwa uliyonipa.Nakuahidi uaminifu mkubwa na utendaji uliotukuka” akasema Austin “Austin kuna jambo ambalo nataka kujadiliana nawe ili tushauriane njia bora zaidi ya kulimaliza.Ni jambo ambalo tunatakiwa kulimaliza kwa haraka lakini kimya kimya na kwa usiri mkubwa” akasema Dr Evans na kunyamaza kidogo halafu akasema “Wewe si mwanasiasa hivyo sintajikita sana katika masuala ya kisiasa lakini kwa ufupi ni kwamba nimepata taarifa kuna watu wanapanga mipango ya kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki.Zipo nchi kubwa na tajiri ambazo zilizoea kunufaika na rasilimali zilizoko katika nchi wanachama wa jumuiya hii lakini kutokana na uimara wa jumuiya na nchi zote wanachama kuweka msimamo mmoja katika kusimamia rasilimali zake imekuwa vigumu sana kwa nchi hizo kubwa kuendelea na unyonyaji wao wa rasilimali zetu.Jana katika mkutano wa jumuiya ya Afrika Mashariki tumeipokea jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kama mwanachama mpya na kufanya jumla ya nchi wanachama kuwa saba.Kama unavyofahamu jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamekuwa katika machafuko ya muda mrefu jambo lililopelekea rasilimali zake nyingi ziibwe kwa muda mrefu.Baada ya kuingia madarakani Rais Patrice Eyenga amejitahidi kuirejesha amani ya Congo na sasa nchi imetulia na Congo imeanza kupiga hatua kimaendeleo.Patrice na serikali yake wamekata mirija yote ya wanyonyaji na kutaka rasilimali za Congo ziwanufaishe watu wa Congo.Kitendo cha serikali ya Congo kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuziba mianya yote ya wizi wa rasilimali zake na kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki,havijawafurahish a nchi za Magharibi hasa zile ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikinufaika kupitia mwanya wa migogoro isiyokwisha.Kwa sasa nchi ya Congo na jumuiya nzima ya Afrika Mashariki tupo katika vita kubwa ya kiuchumi na nchi kubwa” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Ili kukwamisha juhudi zote zilizofanywa na serikali ya Congo katika kuikwamua nchi hiyo kiuchumi,nchi hizo kubwa wameamua kuutumia uchaguzi mkuu wa Rais utakaofanyika hapo baadae kumuweka madarakani mtu wao wanayemtaka ambaye wana uhakika atakuwa na msaada mkubwa kwao katika kuendelea kuchota madini na mali nyingine za Congo.Jambo lingine wanalopanga kulifanya wakubwa hao ni kuisambaratoisha jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwao katika uchotaji wa rasilimali kwa nchi za Afrika Mashariki.Mtu ambaye anatumiwa na mabeberu hao ambaye wanataka kumuingiza katika ikulu ya Congo ni mwanamama Lucy Muganza.Huyu ni mwanamama bilionea ana biashara kubwa kubwa nchini Congo na anatajwa kuwa ni mtu mwenye nguvu sana kisiasa na ambaye wengi wanatarajia anaweza akamshinda Rais wa sasa Patrice Eyenga.Kama huyu mama akifanikiwa kushinda uchaguzi basi Congo itarejea kule illikotoka na vile vile jumuiya yetu ya Afrika Mashariki itasambaratika.Tumenasa mawasilianyo ambayo Lucy amekuwa akiyafanya na maraisi wa nchi mbili wanachama wa Afrika Mashariki na kuwashawishi wakubali kujiunga pamoja kama nchi tatu na kutengeneza jumuiya yao ndogo.Mwanamama huyu ni hatari sana” akanyamaza Dr Fabian akasimama “Mazungumzo haya ni mazito Austin I think we need a drink” akasema na kuindea simu iliyokuwemo mle chumbani akapiga na kuomba waletewe mvinyo.Baada ya muda mfupi akafika mtumishi akiwa na sinia lenye chupa ya mvinyo na glasi mbili akawamiminia wakaendelea na maongezi yao. “Jumamosi wiki hii Lucy Muganza atafika hapa nchini kwa ndege yake binafsi akitokea Ufaransa akiwa na mumewe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Hapa Tanzania yupo mwanae anasoma katika chuo kikuu cha Dar es salaam na lengo la kutua hapa ni kumpitia mwanae ili kwa pamoja kama familia waelekee Congo kwani siku hiyo ndipo atakapotambulishwa rasmi kama mgombea urais kupitia chama cha CDP na kumeandaliwa mapokezi makubwa sana.Atakapoingia hapa Tanzania sitaki atoke hai.Nataka jeneza lake ndilo lirudi Congo.I want her dead” akasema Dr Fabian na kuchukua glasi lake akanywa funda la kinywaji “Are you with me Austin?akauliza “Nimekuelewa mheshimiwa Rais unachokimaanisha” “Good.Nina uhakika mkubwa kifo chake kitawastua sana wale ambao wanamtumia na watataka kufanya uchunguzi wa kna kubaini sababu za kifo chake hivyo nataka tukio hilo lionekane kama ni tukio la uporaji.Ionekane kama vile ameuawa na majambazi ambao walitaka kumpora fedha. Nadhani umenielewa Austin” “Nimekuelewa mheshimiwa rais na ninakuhakikishia kwamba suala hilo litakwisha.Umeniambia kwamba anapokuja hapa Tanzania atakuwa ameongoza na mumewe na anakuja kumchukuamwanae,vipi kuhusu hao wawili mumewe na mwanae?Wao wanaachwa? “Hapana.Kill them all ! akasema Dr Fabian “Sawa mheshimiwa Rais.Nitakachohitaji ni kupata taarifa zote za kuhusiana na huyo mwanamama ili mimi na watu wangu tuweze kujipanga vizuri” akasema Austin “Kesho nitakuunganisha na timu ya majasusi ambao wanaendelea kumfuatilia huyo mwanamama kwa siri na watakupa taarifa zake zote.Austin nakukumbusha kwamba suala hili ni muhimu mno na linatakiwa kuandaliwa kitaalamu sana.Lingine nataka nikukumbushe kuhusu usiri.Tunapanga kumuondoa mtu ambaye anaungwa mkono na mataifa makubwa yenye nguvu hivyo basi usiri mkubwa unatakiwa”akasisitiza “Nafahamu ninachotakiwa kukifanya mheshimiwa Rais na ninakuahidi kulishughulikia suala hiki kwa umakini mkubwa na usihofu kuhusu siri.Mimi na wenzangu ambao tutafanya hii kazi siri hii tutakwenda nayo kaburini”akasema Austin “Utii wako ndiyo sababu ambayo imemfanya Dr Evans aendelee kukukumbuka kila wakati.Austin nakuahidi kama tukiendelea na mashirikiano mazuri namna hii utakuwa na nafasi nzuri sana katika uongozi wangu” akasema Dr Fabian na maongezi yakaendelea.Saa tatu kamili Austin akaondoka katika makazi yale ya Rais “Nimefurahi kukutana na Rais Fabian.Sikuwa na mategemeo ya kuonana naye au kuwa karibu naye kama nilivyokuwa na Dr Evans lakini namshukuru mzee Yule amenisemea vizuri kwa Rais mpya na sasa nimekuwa na ukaribu pia na Rais Fabian.Ni Rais kijana bado na anayeweza kushaurika.Pamoja na furaha niliyo nayo ya kukutana naye lakini amenitwisha jukumu zito la kumuondoa Lucy Muganza.Hili ni jukumu kubwa kumuua kipenzi cha wengi.Ni jukumu langu la kwanza kupewa na Rais huyu hivyo lazima nihakikishe ninalifanikisha kama alivyotaka ili kujenga uaminifu kwake” akawaza Austin “Hata hivyo kazi hii haitakuwa kazi ya kikosi change bali nitaifanya na watu wangu ninaowaamini walio nje ya kikosi.Mtu wa kwanza ambaye ninamuhitaji ni Papaa Gosu Gosu.” akawaza Austin na kuchukua simu yake akazitafuta namba za Gosu Gosu akampigia na simu ikapokelewa “Kamanda Austin” akasema Gosu Gosu “Papaa uko wapi? “Niko hapa Rombo hotel nimekuja kupumzisha akili kuna burudani nzuri ya muziki”akajibu Gosu Gosu “Nahitaji kukuona Papaa ninakuja hapo sasa hivi.Wait for me” akasema Austin na kukata simu “Gosu Gosu ni mpiganaji mzuri na ndiyo maana aliaminiwa mno na Mathew Mulumbi” Austin akahisi mwili unamsisimka alipomkumbuka Mathew Mulumbi “It’s been three years hakuna taarifa zozote kuhusu Mathew Mulumbi.Bado kuna mkanganyiko mkubwa sana kuhusu suala hili kama Mathew yuko hai au amekufa.Picha ya kilichotokea usiku ule tulipokwenda kuwakomboa Olivia na Coletha bado haijatoka kichwani mwangu.Nimejaribu kuwaza na kuwazua ilitokeaje Mathew akapotea mpaka sasa sijapata majibu.Kwa wengine tayari wamekata tamaa lakini mimi bado sijakata tamaa.Kuna kitu kinanifanya niamini kwamba kuna uwezekano mkubwa Mathew yuko hai.Japo iliundwa timu ambayo ilifanya uchunguzi kuhusu Mathew na ikaja na majibu kwamba alifariki na wanahisi aliliwa na fisi lakini kwangu mimi ninakataa kabisa.Naamini Mathew yuko hai.Yuko wapi anafanya nini na kwa nini hataki kujitokeza kama yuko hai ni maswali ambayo yanaendelea kunitesa mno na nitaendelea kuteseka katika maisha yangu yote kwa kuwa kwa mara ya kwanza niliondoka na kumuacha mtu muhimu sana kwa nchi nyuma.Kwa hili sintajisamehe” Sura ya Austin ilibadilika na kujaa mawazo baada ya kumkumbuka Mathew Mulumbi Walifika Rombo hotel akamuacha dereva wake akimsubiri garini akaingia ndani kumtafuta Gosu Gosu na kumkuta amekaa katika meza peke yake akifuatilia muziki wa bendi iliyokuwa inatumbuiza katika hoteli ile.Mara tu Gosu Gosu alipomuona Austin namna alivyopendeza akainuka na kumpa mkono huku akitabasamu “Austin kulikoni leo umependeza kiasi hicho? Akauliza Gosu Gosu na Austin akavuta kiti akaketi. “Habari za siku Papaa?akauliza Austin “Inakaribia miezi mitano hatujaonana” “Ni kubanwa na majukumu Papaa.Si unajua hizi kazi zetu.Vipi unaendeleaje na maisha?akauliza Austin “Ninaendelea vyema.Kila kitu kinakwenda vizuri” akasema Gosu Gosu muhudumu akafika na kuagizwa kinywaji “Umetoka kutoa posa leo?akauliza Gosu Gosu “Papaa nimetoka ikulu niliitwa na Rais” “Uliitwa na Rais? “Ndiyo alikuwa na mazungumzo na mimi” “Una bahati sana Austin.Kuitwa na Rais ikulu si jambo dogo” akasema Gosu Gosu “Kikubwa ilikuwa ni kufahamiana.Alipata taarifa zangu kutoka kwa Dr Evans na akataka kuniona hivyo akaniomba tuonane jioni ya leo kwa chakula cha usiku ndiyo maana umenioa nimevaa namna hii.” akasema Austin “How’s the new president? Akauliza Gosu Gosu huku akiinua glasi yake na kunywa funda moja “Ni kijana bado, si mwongeaji sana anaongea kwa vituo na yuko makini sana katika kuchagua kipi cha kuongea wapi na muda gani.Kwa ujumla naweza kusema ni mtu mwelewa sana na anapokea ushauri kuliko Yule mzee wetu Dr Evans” akasema Austin na Gosu Gosu akacheka “Umenikumbusha mbali sana mzee Yule namna alivyokuwa akibadilika badilika.Hakuwa na msimamo” akasema Gosu Gosu na wote wakacheka “Papaa pamoja na kufahamiana lakini Rais aliniita na kunipa kazi” “Kazi?! Gosu Gosu akashangaa “Ndiyo.” Akasema Austin na kumueleza Papii kila kitu kuhusiana na kazi ile aliyopewa na Rais “Dah ! si kazi nyepesi hii Austin”akasema Gosu Gosu “Ndiyo maana nimekuja kwako Papaa.Nataka tushirikiane katika hii kazi” “Me?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo Papaa.Nimekutafuta kwa ajili ya kazi hii” “Hapana umekosea Austin kutaka kunijumuisha katika kazi hii.Mimi tayari nimekwisha achana na hayo mambo toka tulipompoteza Mathew” “Papaa kupotea kwa Mathew ni jambo ambalo linatuumiza sote.He was our friends lakini pamoja na kupotea kwake bado mambo mengine yanapaswa kuendelea.Huyu mwanamama Lucy Muganza ni hatari sana kwa usalama wa nchi yetu,jumuiya ya Afrika Mashariki na zaidi sana nchi yako ya kuzaliwa Congo.Siwezi kuifanya kazi hii peke yangu ndiyo maana nimekuja kwako Papaa kuomba msaada” “Austin wewe ni kongozi wa kikosi una watu wengi kwa nini usitumie watu wako kuifanya kazi hiyo hadi unifuate mimi.Mimi siko tena katika hayo mambo.Kwa sasa ni mfanyabiashara.Ninayo miradi kadhaa mikubwa hapa nchini ninaisimamia hivyo sitaki kujiingiza katika masuala mengine.Siwezi kufanya kazi yoyote ya serikali tena.What they did to Mathew was unfair” akasema Gosu Gosu “I know that and I agree with you.It was unfair lakini yalikuwa ni maamuzi ya kijasiri ya Rais”akasema Austin na sura ya Gosu Gosu ikabadilika “Maamuzi ya kijasiri?Unayaita maamuzi yale ya kijasiri?Ule si ujasiri.Ni uoga na ujinga! Akafoka Gosu Gosu “Papaa natamani ungekuwepo ili ushuhudie kilichotokea.Hayakuwa maamuzi mepesi kwa Rais kuamuru tuondoke na tumuache Mathew.Lengo la operesheni ile lilikuwa ni kuwakomboa mateka waliokuwa wanashikiliwa na IS na tayari tulifanikiwa kuwaokoa hivyo kuendelea kukaa mahala pale ni ilikuwa ni kuendelea kuhatarisha usalama wetu na wa watu tuliowakomboa ndiyo maana Rais akafanya maamuzi yale magumu.Inaumiza sana kumpoteza rafiki yetu lakini haikuwa rahisi hat akwa Rais mwenyewe naamini hata wewe ungekuwa mahala pa Rais ungefanya vile alivyofanya.It was a tough call” “Tough call? Akauliza Gosu Gosu “You can’t be serious Austin.Rais aliamuru mrejee nyumbani na kumuacha nyuma Mathew ili kumuondoa mwanae katika hatari lakini alisahau kama mtu aliyeachwa nyuma ndiye aliyefanikisha kupatikana kwa mwanae.It hurt Austin.Inaumiza sana.Najaribu sana kutaka kulisahau jambo hili lakini ninashindwa.Kinachoniumiz a sikuwepo karibu nisingekubali ujinga kama huu kufanyika.Ningebaki naye porini”akasema Gosu Gosu “Papaa,Mathew alikuwa rafiki yetu na sote tunaumizwa na kilichotokea lakini ile ni vita na katika vita hata watu wema huwa wanapotea.Wewe I mpiganaji unalifahamu hilo” akasema Austin “You call him your friend? You left him behind and you call him your friend?Austin ujio wako hapa umekuja kutonesha kidonda nilichonacho.Hakuna siku ambayo sijaangusha chozi nikimlilia Mathew.Hufahamu chochote kuhusu Mathew.Sisi ambao tuko naye karibu ndio tunaoumia.I was a criminal,a killer lakini amenitoa kule nilikokuwa na amenirejesha katika ubinadamu.Kwangu mimi unapomzungumzia Mathew Mulumbi unamzungumzia mtu muhimu mno”akasema Gosu Gosu “Papaa uko sahihi kwamba yawezekana simfahamu vizuri Mathew kama vile unavyomfahamu wewe lakini hata mimi kitendo cha kuondoka na kumuacha Mathew nyuma kinaniumiza mno na sintajisamehe kwa kile kilichotokea lakini mimi ni mwanajeshi wewe pia umekuwa mwanajeshi na unafahamu kitu kikubwa tunachofundishwa jeshini ni utii hasa kwa viongozi.Amri ilitolewa na amiri jeshi mkuu na mimi nisingeweza kuipinga kwa namna yoyote ile.Papii suala la Mathew naomba lisitufanye tukashindwa kufanya majukumu mengine.We can’t cry for him forever.We have to stop ! akasema Austin kwa sauti yenye amri na kumtazama Gosu Gosu “Nimekuja hapa kuomba msaada wako.Let’s do this for the our countries and Mathew either he’s dead or still alive will be proud of us.Kumuenzi Mathew ni kufuata nyayo zake.He was a super billionaire lakini linapokuja suala la ulinzi wa taifa Mathew aliweka utajiri wake kando akaingia katika mapambano na hivyo ndivyo anavyotaka sisi pia tufanye.Muda wowote tuwe tayari kukubali kufanya kazi yoyote kwa ajili ya taifa letu.Our countries needs us” akasema Austin na Gosu Gosu akainamisha kichwa chini. “Papaa inua kichwa nitazame” akasema Austin na Gosu Gosu akainua kichwa akamtazama “Tazama watu wote hawa humu ukumbini they’re all happy lakini wapo watu ambao hawalali kuhakikisha kwamba watu hawa wanakuwa salama siku zote na sisi ni miongoni mwa watu hao ambao tumechaguliwa kuifanya kazi hiyo.Hatuwezi kuikimbia kazi yetu tunatakiwa kuitika ndiyo kila pale tunapoitwa kwa ajili ya taifa letu.Taifa linatuita na tuitike ndiyo.Hivyo ndivyo Mathew angefanya hajawahi kuitika hapana.Kila pale alipoitwa aliitika ndiyo.Mimi tayari nimeitika ndiyo nataka kusikia kutoka kwako ndiyo au hapana.If it’s yes I’ll stay but if it’s no I’ll go away and I’ll never come bother you again” akasema Austin.Gosu Gosu akabaki kimya akitafakari “Papaa I need the answer” akasema Austin “Yes”akajibu Gosu Gosu “Good.Let’s do this for Mathew,for Tanzania,for Congo and for East Africa Community” akasema Austin.Gosu Gosu akachukua glasi yake ya kinywaji “I’m doing this for Mathew” akasema Gosu Gosu.Austin naye akainua glasi “Fo Mathew” akasema wakagonganisha glasi na wote wakanywa halafu Gosu Gosu akauliza “What’s the plan? “Plani ni hii.Tukio hilo linatakiwa lionekane ni tukio la kihalifu.Kazi yetu sisi ni kumuua Lucy,mume wake,mtoto na walinzi.Upande wa pili tutatafuta majambazi ambao tutawapa taarifa kwamba ndani ya gari lile la Lucy kuna fedha nyingi ili wapange mipango ya kumvamia.Wakati huo huo tutakuwa tumewajulisha polisi kuhusu uwepo wa mpango wa majambazi hayo kufanya uporaji ila hatutawaeleza wanataka kumpora nani na tutawapa namba za gari ambalo majambazi hao watalitumia.Sisi tukifanya mauaji hayo polisi kwa kuwa wanafahamu mpango wa majambazi na wanalifahamu gari lao wataamini kwamba mauaji hayo yamefanywa na majambazi na hapo itaibuka vita mpyakati ya polisi na majambazi hao na sisi tutakuwa tumemaliza zoezi tutaondoka kimyakimya.Dunia nzima watajua kwamba Lucy Muganza ameuawa na majambazi.Unaonaje mpango huo? Akauliza Austin na kwa mbali sura ya Gosu Gosu ikajenga tabasamu “It’s one of the best plan” “Thank you.Tatizo ni namna ya kuweza kuwapata hao majambazi” akasema Austin “I know someone who can help us.Tutakwenda kuonana naye kesho hapendi kutembelewa usiku.Ni Mathew pekee aliyekuwa na uwezo wa kumfuata usiku.Kitu kingine tunahitaji kupata taarifa za huyo mama ambaye kama anakuja siku ya jumamosi ni siku mbili tu kutoka leo hivyo maandalizi yanatakiwa yafanywe haraka” akasema Gosu Gosu. “Taarifa nitaanza kuzipata kesho kutoka kwa majasusi ambao wanamfuatilia Lucy Muganza” akasema Austin na kuagiza tena kinywaji “By the way where is Devotha? Have you heard from her?akauliza Austin “I don’t know where she is.Nimejitahidi kumtafuta bila mafanikio.Austin do you mind if I ask a question? “Just ask” akasema Austin na kunywa bia kidogo “I know I’ve asked you a hundred times but I’m going to ask you again.What real happened that night? Akauliza Gosu Gosu.Austin akachukua kinywaji chake akanywa halafu akashusha pumzi na kusema “Umeniuliza swali hili mara nyingi lakini bado jibu nililonalo ni lile lile ambalo nimekuwa nikikupa siku zote.Kila unapouliza huwa ninakueleza kile nilichokishuhudia mimi kwa macho yangu usiku ule.Tulivamiwa wakati mabadilishano yakiendelea.Sisi tulimuachia Edger Kaka aende kwa watu wa IS na wao waliwaachia Olivia na Coletha.Mimi na kikosi change tulikuwa tumejibanza tukisubiri kama kungetokea tatizo lolote na lengo letu lilikuwa baada ya kuwapata akina Olivia basi tumuue Edger Kaka lakini ghafla tulianza kushambuliwa kwa silaha kali kutoka kila upande.Lilikuwa ni shambulio ambalo hatukuwa tumelitegemea.Tulipotezana na kila mmoja alifanya juhudi binafsi za kujikomboa.Baada ya hali kutulia tukajikusanya na kugundua timu yote ya Mathew walikuwa wameuawa lakini Mathew hakuwepo.Magaidi wote tuliwaua lakini Edger Kaka hakuwepo.Hicho ndicho ninachokumbuka” akasema Austin na kunywa tena glasi yake ya kinywa ukimya wa dakika tatu ukapita Gosu Gosu akasema “Austin kufuatia hicho ulichonieleza kuna swali ambalo nataka kukuuliza and please be honest with me” “Uliza chochote usihofu papaa” akasema Austin.Gosu Gosu akamtazama usoni kwa muda wa dakika moja halafu akauliza “Do you believe Mathew is dead? Austin akashusha pumzi akaegemea kiti akazama katika tafakari kisha akajibu “No I don’t.Kuna sauti ninaisikia ndani yangu ikiniambia Mathew hajafa.Hisia hizo ninazo kwa muda mrefu na siamini kama kweli Mathew amekufa”akajibu Austin “Ni hilo tu nililotaka kulisikia kutoka kwako.Hata mimi nina mawazo kama yako.Siamini kabisa kama Mathew amefariki dunia.Austin nadhani umefika wakati wa kuutafuta ukweli kuhusu Mathew” “Hata mimi nilikuwa na mawazo hayo ya kulichimba suala hili la Mathew lakini kwanza tumalize hii kazi ya Rais ndipo tuingie katika mambo mengine kwani tukitaka kuanza kumtafuta Mathew tunahitaji kujipanga kisawa sawa” akasema Austin wakaendelea na maongezi kuhusiana na mpango wao wa mauaji ya Lucy Eyenga na saa sita za usiku Austin aliachana na Gosu Gosu akarejea kambini kupumzika.



Saa nne za asubuhi siku iliyofuata Austin aliwasili katika makazi ya Mathew Mulumbi ambako kwa sasa anaishi Gosu Gosu.Siku hii Austin hakuwa katika sare za kijeshi alikuwa amevaa suruali ya jeans rangi ya bluu na fulana nyeupe.Alikaribishwa ndani na Gosu Gosu wakawa na mazungumzo kidogo kabla hawajaendelea na kile walichopanga kukifanya siku ile “Any word from president?akauliza Gosu Gosu “Amenipigia simu asubuhi ya leo akaniambia kwamba atanipigia baadae kuniunganisha na timu ya majasusi ambao wanamfuatilia Lucy Muganza” “Good.Tunakwenda kuonana na Tino”akasema Gosu Gosu “Tino? Austin akashangaa “Ndiyo.Tulikuwa naye Nairobi katika operesheni ya kumchukua Edger kaka” “Nimemkumbuka Tino.Where is he now? “Tino ni rafiki mkubwa wa Mathew Mulumbi.Biashara yake kubwa ni silaha na anafahamiana na majambazi wengi wa Afrika Mashariki kwani wengi hununua silaha kutoka kwake.Huyu ndiye atakayetuunganisha na majambazi tunaowahitaji katika misheni hii.Nimekwisha zungumza naye simuni nikamueleza nitakwenda kwake kumuona nina shida naye akaniahidi kunisubiri saa tano za asubuhi hivyo hatuna muda wa kuoteza twende tumfuate” akasema Gosu Gosu wakaingia katika gari la Mathew na kuondoka. Walifika nyumbani kwa Tino ambaye alikuwa anawasubiri akawakaribisha ndani “Gosu Gosu kwa nini hukuniambia kama unakuja na kamanda Austin?akaulizaTino “Sikutaka kukupa hofu” “Karibuni sana jamani.Ni muda umepita hatujaonana”akasema Tino “Kweli zimepita siku nyingi hatujaonana” akajibu Gosu Gosu “Save yourself a drink” akasema Tino akiwaelekeza akina Austin kujihudumia vinywaji. “So guys tell why you are here?Najua hamko hapa kwa ajili ya kunijulia hali” akasema Tino “Ni kweli Tino.Tuko hapa kwa sababu maalum.We need you and we need your help” akasema Austin na Tino akaonekana kustuka kidogo akaweka chini glasi ya kinywaji aliyokuwa ameshika “You need me and you need my help” akasema Tino “Yes” akajibu Austin na Tino akatabasamu kidogo “You guys you are just like Mathew.You look for me only whe you have problems.So what is it this time? Akauliza Tino Austin akamuelezea kila kitu kuhusu Lucy Muganza.Tino akanywa kinywaji kidogo na kusema “Aren’t you guys tired of being used everytime? These people they use you for nothing.Bado sijasahau kuhusu Mathew.Moyo wangu unaniuma mpaka leo hii kumpoteza na alipotea katika mambo kama haya mnayotaka niwasaidie.Guys I’m done.Nimekwisha achana na hayo mambo na kwa sasa nina biashara nyingine zinazoniingizia fedha sitaki tena kuhatarisha maisha yangu” akasema Tino “Tino suala la Mathew Mulumbi linatuumiza sote.He was our friend.Inaniuma zaidi hasa mimi ambaye nilikuwa naye hadi dakika za mwisho.Guys wote hapa ni wanajeshi.Wote tumekwisha wapoteza wenzetu muhimu sana katika mapambano na Mathew si mtu wa kwanza.Look at me nimepoteza familia yangu yote.Walichomwa moto na kuungua mpaka kuwa mkaa but here I am I’m still fighting.Ninachowaomba ndugu zangu suala la Mathew lisitufanye tushindwe kutimiza majukumu yetu mengine kwa taifa.Huyu mama ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.Kama akifanikiwa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki hatashindwa kuvuruga muungano wetu.Naamini hakuna ambaye yuko tayari kuona hilo likitokea.Papaa hapa amepigana vita msituni kwa miaka mingi wakiitafuta amani na leo nchi alikotoka kuna amani na taratibu watu wameanza kusahau kule walikotoka lakini huyu mama anakuja kutumiwa kuleta mgawanyiko tena nchini Congo ili mabeberu waweze kuendelea na mchezo wao wa kuchota rasilimali.Hakuna kati yetu anayetaka hilo litokee.Kama Mathew angekuwepo hapa asingejiuliza mara mbili angevaa silaha na kuingia katika mapambano.Ndugu zangu tuna majonzi kuhusu Mathew lakini njia pekee ya kumuenzi ni kwa kushika silaha na kupambana dhidi ya yeyote Yule anayeonekana kitisho kwa usalama wa nchi yetu.Rais anatutegemea sana” akasema Austin “Rais ana vyombo vingi vinavyoweza kulifanya hili jambo kwa nini sisi?akauliza Tino “Kuna mambo mengine ambayo ni ya siri kubwa na huwezi ukamshirikisha kila mtu bali watu wachache tu unaowamini” “He knows us?He knows me?akauliza Tino “He knows and trust me and I trust you guys.Misheni hii ni ya siri mno na Rais ameamua iwe hivyo kwa sababu lazima uchunguzi utafanyika hivyo hataki serikali ya Tanzania au Congo zionekane zinahusika katika kifo hicho” akasema Austin na baada ya ukimya fupi Tino akauliza “Mnataka mimi nifanye nini?Niwasaidie kitu gani katika misheni hii? “Misheni hii haitakiwi kuonekana kama ni tukio la mauaji ya kupangwa bali lionekane kama ni tukio la ujambazi.Tunataka kutafuta kikundi cha majambazi ambao tutawapa taarifa kwamba gari atakalopanda Lucy Muganza litakuwa na mamilioni ya fedha ndani yake hivyo basi watapanga mipango ya kulivamia na wakati huo huo tutawajulisha jeshi la polisi na kuwapa taarifa zote za mipango ya majambazi hao na wataanza kuwafuatilia watu hao kwa karibu.Wakifika mahala ambako tutakuwa tumepanga kutekeleza mpango wetu tutawaondoa Muganza na wengine kwa haraka na kazi itabaki kwa polisi na wale majambazi.Tutawamaliza Muganza na familia yake tukiwa mbali hivyo polisi wataamini kwamba majambazi ndiyo waliotekeleza mauaji hayo katika kufanikisha mpango wao wa kupora hivyo watajihami na kutaka kuwadhibiti.Majambazi wakiona polisi wanawafuata wataanza kuwarushia risasi na hapo utatokea mvurugano na kwa umahiri wa askari wetu naamini watawamaliza majambazi hao ndani ya muda mfupi hivyo basi moja kwa moja tukio hili litaonekana ni tukio la ujambazi na hakuna ambaye ataingiza hisia kwamba serikali inahusika na tukio hilo.Wewe unawafahamu watu wanaojihusisha na hayo masuala ya ujambazi hivyo utatusaidia kuandaa mpango huo na wao.Baadae leo nitaanza kuwasiliana na kiongozi wa kikundi cha majasusi wanaomfuatilia Lucy na watatupa taarifa zote za kuhusiana na Lucy na tutazitumia taarifa hizo kutengeneza mpango wetu wa kumuondoa”akasema Austin “Sawa.Kwangu hilo ni suala dogo sana” akasema Tino kisha wakapanga wakutane jioni ya siku hiyo kwa ajili ya mikakati zaidi





Saa mbili za usiku iliwakuta,Austin na Tino tayari wamekwisha fika nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambako Gosu Gosu alikuwa akiwasubiri kwa ajili ya kuendelea na mipango yao.Baada ya kupata chakula cha usiku wakaelekea katika chumba maalum ambacho Mathew hukitumia kama ofisi yake “Guys bila kupoteza muda tuendelee na majadiliano pale tulipokuwa tumeishia mchana.Austin what have you got for us?akauliza Gosu Gosu “Tayari nimekwisha pata mawasiliano na mkuu cha kikosi cha majasusi ambao wanaendelea kumfuatilia Lucy nchini Ufaransa.Kwa taarifa walizonazo ni kwamba Lucy atawasili hapa Tanzania kesho kutwa Jumamosi saa nne za asubuhi.Lengo la kuja Dar es salaam ni kumchukua mwanae anayesoma katika chuo kikuu cha Dar es salaam anaitwa Theresia Muganza kisha wataelekea nchini Congo ambako kumeandaliwa mapokezi makubwa ambapo Lucy atatambulishwa rasmi na chama cha CDP kama mgombea urais kupitia chama hicho.Majasusi hao wanaomfuatilia Lucy wataendelea kumfuatilia hadi pale Lucy atakapoondoka Paris na baada ya hapo she’ll be ours hivyo mipango yote ya kumuondoa ni juu yetu.Tunatakiwa kuifahamu ratiba yake atakapokuwa hapa Tanzania.Tujue akishuka uwanja wa ndege ataelekea wapi,atatumia usafiri upi na bila kusahau ulinzi.Kwa kuwa ni mtu ambaye anatumiwa na nchi kubwa hawawezi kumuacha hivi hivi lazima watamuwekea ulinzi mkubwa wa kutosha hivyo lazima tujiandae kwa hilo” akasema Austin “Nadhani taarifa za kutosha kuhusu ratiba nzima ya Lucy Mganza hapa Tanzania tutaipata kwa mwanae Theresia.Lazima watakuwa wanawasiliana na atakuwa anafahamu kila kitu.Kuna yeyote amewahi kumuona au kumsikia huyo Theresia au kujua mahala anakoishi?akauliza Tino lakini wote hawakumfahamu Theresia Muganza. “Wote hatumfahamu na hatujawahi kumuona Theresia.Nashauri tuanze kwa kumfuatilia na kumfahamu halafu tudukue mawasiliano yake na tujue wanaongea nini na mama yake.”akashauri Tino “Wazo zuri sana hilo Tino.Hiyo itakuwa ni ratiba yetu ya kwanza asubuhi ya kesho.Vipi kuhusu wale jamaa ambao tulikupa kazi ya kuwatafuta? Austin akauliza “Tayari nimekwisha fanya mawasiliano na kundi Fulani nikawaambia wajiandae nitawaletea taarifa za kazi ya mamilioni ya fedha na kwa kuwa wananiamini wamekubali.Kwa upande huo hakuna wasi wasi kabisa.Ninachohitaji kufahamu tumejipangaje kumuondoa Lucy? “Mpango ninaofukiria mimi uko hivi.Mpaka Lucy atakapokuwa ametua hapa nchini tayari tutakuwa tumekwisha pata taarifa za ratiba yake yote.Tutaanza kumfuatilia kuanzia atakaposhuka ndegeni hadi sehemu ambako tutakuwa tumepanga kufanya misheni yetu.Ninaamini lazima Theresia atakuwepo uwanjani kuwapokea wazazi wake kisha wataelekea mahali aidha hoteli au kama ana nyumba hapa Tanzania wataelekea huko.Mchezo wote tutaumalizia barabarani” akasema Austin na kuufungua mkoba wake akatoa karatasi kubwa ilikuwa ni ramani ya jiji la Dar es salaam akaiweka mezani “Hii ni barabara ya Serengeti ambayo inatoka uwanja wa ndege hadi katika mzunguko wa sanamu ya kifaru.Pale kuna barabara tatu.Ipo barabara ya Arusha,barabara ya Fidel na barabara ya Twiga.Hapa ndipo misheni yetu itakapofanyika.Eneo hili ni eneo ambalo lina biashara na shughuli nyingi.Tunatakiwa kujipanga vizuri hapa.Ukitoka barabara ya Serengeti kama ukielekea barabara ya Arusha pale kuna hoteli Jacombo.Gosu Gosu na Tino mtakuwa hapa.Ni hoteli ambayo iko pembezoni mwa barabara.Mtachukua chumba na kujiweka tayari.Ng’ambo ya barabara kwa upande wa Mashariki kuna hoteli 442 hapa nitakuwepo mimi na mtu mwingine nitakayemuongeza katika timu yetu.Lucy atakapofika katika mzunguko kama ataelekea barabara ya Arusha basi Gosu Gosu na Tino mtafanya kazi ya kumuondoa lakini endapo ataelekea barabara ya Twiga basi Mimi na huyo nitakayekuwa naye tutamaliza mchezo.Nina imani wote ni wataalamu katika kulenga shabaha na tutatumia bunduki za hali ya juu za masafaa marefu aina ya Barret M82” akasema Austin “Mpango huu ni mzuri lakini nina waza.Hatujui Lucy anaweza kutumia gari la aina gani.Kama ulivyosema kwamba Lucy anatumiwa na mataifa makubwa hivyo lazima wahakikishe wanamlinda na yawezekana labda gari lake likawa halipenyi risasi.Jambo la pili yawezekana gari lake likawa na vioo vyeusi na kutupa ugumu wa kuona ndani.Tutafanikishaje mpango wetu?akauliza Tino “Ahsante kwa wazo hilo.Ili kufanikisha mpango wetu lazima tuwaone vyema watu tunaotaka kuwaua hivyo basi tunahitaji kufanya kitu ambacho kitawafanya waliomo ndani ya gari la Lucy kufungua vioo vya gari kama vitakuwa vimefungwa watakapofika katika mzunguko wa Kifaru ili kutupa sisi nafasi ya kuweza kuwaona vyema namna walivyokaa ndani na kuwaondoa”akasema Austin “Tutengeneze ajali” akashauri Gosu Gosu. “Tuligonge kwa nyuma au ubavuni gari hilo la Lucy Muganza na watalazimika kusimama na kushuka kuangalia kitakachokuwa kimetokea” akasema Gosu Gosu “Wazo la kutengeneza ajali ni wazo zuri lakini ni vipi kama ajali hiyo itasababisha watu wajae eneo hilo kwa haraka na tukashindwa kutekeleza misheni yetu? Kama unavyojua hapa Dar es salaam ajali ndogo hujaza watu ndani ya sekunde chache”Akasema Austin “Mara tu milango itakapofunguliwa tutaweza kuona ndani na kuwaondoa Lucy na familia yake haraka sana kabla watu hawajajaa eneo hilo la ajali” akasema Gosu Gosu “Ni vipi kama atakuwa na msafara wa gari zaidi ya moja? Ninahisi yawezekana kukawa na gari la walinzi wake au gari la ndugu zake bila kusahau wapo wakongo waishio hapa nchini ambao wapo wanaomuunga mkono na wanaweza wakajitokeza pia kumpokea” akasema Tino “ I have an idea.Dhumuni letu sisi ni kumfanya Lucy Muganza aidha afungue madirisha atakapofika eneo la mzunguko wa Kifaru au ashuke kabisa ili tuweze kupata nafasi nzuri ya kumdungua.Nashauri tutege bomu kwenye gari”akasema Gosu Gosu “That’s a terrorism.Tunaweza kuua na watu wasio na hatia.Tunaye muhitaji ni Lucy na familia yake pekee hivyo tujielekeze hapo na tusifikirie kumwaga damu za watu wasio na hata.Ni magaidi pekee wanaofanya hivyo” akasema Austin “Listen guys.Lucy tunahitaji kumuondoa Lucy kwa gharama zozote zile.Endapo ikitokea tukashindwa kumuua na akafanikiwa kuondoka salama hapa nchini madhara yake ni makubwa tofauti na kama wangekufa watu wawili au watatu.Tutatafuta gari kuukuu na kuliweka pembeni ya barabara.Mara tu gari la Lucy litakapofika katika mzunguko lazima watasubiri kidogo kuingia katika mzunguko na tutaitumia nafasi hiyo kulipua bomu hilo.Ninaamini kutakuwa na taharuki kubwa sana na lazima atatolewa katika gari ili kuondolewa katika hatari na hapo ndipo tutakapoanza kuwadondosha mmoja baada ya mwingine” akasema Gosu Gosu “Sasa nimekuelewa Papaa unachokimaanisha.Kwa kuitazama ni plani nzuri lakini tukio letu tunataka kulifanya lionekane ni tukio la kijambazi hivyo tukitumia mlipuko kwanza linaweza kuonekana kama shambulio la kigaidi na vile vile linaweza kuvuruga kabisa mpango wetu kwani bomu litakapolipuka itaibuka taharuki kubwa sana eneo lile na watu watasambaratika.Mpango wetu utakuwa umevurugika” akasema Austin. “Wazo lingine” akasema Tino “Tutaanza kumfuatilia Lucy toka atakaposhuka ndani ya ndege hadi atakapoingia barabarani.Wazo langu ni atakapofika katika mzunguko wa Kifaru kabla hajaingia mzungukoni tutayapiga risasi matairi yaliyo upande wetu na wakati huo huo ninyi Austin na mwenzako mtayadungua matairi ya upande wenu gari halitaweza tena kutembea.Wote walio ndani ya gari watalazimika kushuka baada ya gari kushindwa kutembea ili kuangalia kilichotokea na hapo ndipo tutakapoitumia nafasi hiyo kumuondoa Lucy” “That’s a good plan.Nadhani tukubaliane na wazo hili la Tino” akasema Austin na wote wakakubaliana na wazo lile “Jambo la mwisho nadhani upo ulazima wa kuongeza pia watu wachache katika mpango huu.Nitawashirikisha watu wachache kutoka katika kikosi changu ili kuongeza nguvu” akasema Austin JUMAMOSI – DAR ES SALAAM Ndege aina ya Gulfstream III iliwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Ndege hii ya kifahari ilimilikiwa na mwanamama bilionea Lucy Muganza “Ndege imetua tayari.Narudia tena ndege imetua” Mtu aliyewekwa ndani ya uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kumfuatilia Lucy Muganza akawajulisha wenzake akina Austin.Wote walikuwa na vifaa vya mawasiliano masikioni mwao hivyo basi taarifa ile iliwafikia wote. “Lucy amekwisha shuka ndegeni?akauliza Austin “Ndege imetua muda si mrefu sana na mlango bado haujafunguliwa” akasema Yule jamaa “Endelea kufuatilia kutujulisha atakayeshuka ndani ya hiyo ndege pale mlango utakapokuwa umefunguliwa” akasema Austin “Osmund nini kinaendelea hapo nje ya uwanja?akauliza Austin “Theresia Muganza yuko hapa sehemu ya kupokelea abiria wanaowasili.Yuko na watu kadhaa na wote wanaonekana wanamsubiri Lucy” “Good.Endelea kutujulisha kile kinachoendelea upande huo.Tino na Papaa tafadhalini nijulisheni kama mko tayari katika sehemu zenu” akasema Austin “Tuko tayari katika sehemu nzuri tunaweza kuyaona kwa urahisi magari yote ambayo yanatokea barabara ya Serengeti” akasema Gosu Gosu “Good.Sisi pia tko vizuri hapa” akasema Austin. Mlango wa ndege ya bilionea Lucy Muganza ulifunguliwa na baada ya dakika mbili wakashuka wasichana wawili halafu baada ya muda mfupi akajitokeza mwanamama akiwa ameongozana na mtu mmoja mrefu mwembamba aliyevaa suti nzuri iliyomkaa vyema.Mwanamama Yule alikuwa amevaa gauni zuri lililompendeza sana bila kuisahau vito vya thamani alivyovaa shingoni.Nyuma yao kulikuwa na watu wanne watatu wakiwa wazungu na mmoja mwafrika. “Lucy ameshuka ndegeni akiwa na mumewe na walinzi wanne.Narudia tena Lucy ameshuka ndegeni akiwa na mume wake na walinzi wanne” akasema Barack aliyekuwa ndani ya uwanja wa ndege akimfuatilia Lucy “Barack are you sure? “100%.Hivi sasa anaelekea katika jengo la uwanja”akajibu Barack “Osmund standby.Lucy ameingia katika jengo la uwanja na muda si mrefu atatoka” akasema Austin Lucy Muganza akiwa na mume wake Laurent Muganza na walinzi wao wanne walikamilisha taratibu za uhamiaji wakaruhusiwa kuingia nchini. Mara tu walipotokea katika sehemu ya abiria wanaowasili Theresia aliruka kwa furaha na kwenda kuwakumbatia wazazi wake.Ulikuwa ni wakati wa furaha kubwa kwa familia hii kukutana pamoja. “Karibuni sana Dar es salaam” akasema Theresia “Ahsante sana Theresia.Vipi maendeleo yako?akauliza Lucy “Ninaendelea vyema kabisa.Nimewakumbuka mno” akasema Theresia “Maam we need to go”mmoja wa walinzi akamwambia Lucy kisha wakasalimiana na marafiki kadhaa wa Theresia waliofika pale uwanjani kumpokea na kutoka nje “Austin this is Osmund.Lucy tayari ametoka nje anaelekea kwenye gari”akasema Osmund aliyekuwa nje ya uwanja “Good Osmund endelea kufuatilia kila hatua” akaelekeza Austin. Gari tatu zilijipanga tayari kabisa kwa kuondoka pale uwanjani.Gari la kwanza lilikuwa ni Mercedece benz rangi nyeusi na gari la kati kati lilikuwa ni aina ya Limuosine nalo likiwa na rangi nyeusi na gari la tatu likiwa ni Mercedece benz.Lucy mume wake na Theresia wakaingia katika gari la kati kati aina ya Limousine na safari ikaanza “Lucy anaondoka hapa uwanjani” akasema Osmund “Zimeongozana gari tatu lakini Lucy na familia yake wamepanda gari la kati kati aina ya Limousine.Mlinzi mmoja amepanda mbele katika Limousine na walinzi waliobakia wamepanda gari la nyuma.Hapa uwanjani kazi imekamilika sisi tunawafuata kwa nyuma” akasema Osmund “Good job Osmund.Endeleeni kuwafuatilia na kutujuza kama kutakuwa na mabadiliko yoyote” akasema Austin “Tino na Papaa jiwekeni tayari Lucy amekwisha ondoka uwanja wa ndege na si muda mrefu sana atafika mahala hapa.Kila kitu kiende kama kilivyopangwa tafadhali” akasema Austin akiwaweka wenzake katika utayari halafu akachukua simu yake na kupiga namba Fulani “Christopher tayari mmejipanga?akauliza “Tumekwisha jipanga kuanzia saa mbili za asubuhi tunakusubiri wewe utupe maelekezo kaka” “Safi sana.Tayari Yule mama amekwisha shuka uwanja wa ndege hivi sasa ameingia katika gari na kuondoka kuelekea mjini.Sanduku lenye madini limeingizwa kwenye gari aina ya Limousine.Mbele ya hiyo Limo kuna mercedece benz na nyuma yake kuna mercedece nyingine jumla kuna walinzi wanne ambao nina hakika mnaweza kuwaondoa bila matatizo” “Ahsante sana Austin kwa taarifa hizo.Tumekwisha jipanga vizuri na madini hayo tutayachukua” akasema jamaa aliyekuwa akizungumza na Austin simuni. “Chris kwa kuwakumbusha tu mnatakiwa kutumia gari yenye nguvu na uwezo mkubwa wa kukimbia pale mtakapokuwa mmeyapata madini.Mnatumia gari gani? “Tunatumia gari langu lile Prado lakini nimebadili namba na kuweka za bandia.” “Ok good.Kila la heri” “Austin ahsante sana kwa kutupa taarifa hizi.Nakuahidi kama tukifanikiwa basi mgawo utakuwa sawa kwa sawa” akasema Chris “Shukran sana Chris.Tutawasiliana tena baadae pale kazi itakapokuwa imekamilika” akasema Austin na kukata simu halafu akampigia simu kamanda wa polisi akamjulisha kuwa wale jamaa aliomueleza kuwa wanajiandaa kufanya tukio la ujambazi tayari wamekwisha jiandaa hivyo polisi wawe tayari kwani uporaji huo unapangwa kufanyika katika mzunguko wa kifaru.Alimueleza kila kitu kuhusu gari wanalotumia waporaji.Polisi nao wakaanza kujipanga vizuri ili kukabiliana na majambazi hao. Gari aina ya Limousine alilopanda Lucy Muganza liliwapita akina Chris mahala walipokuwa wameegesha gari lao nao wakaingia barabarani wakiwa nyuma yao kwa magari mawili.Ndani ya gari lile la kifahari maongezi na vicheko vilitawala Lucy na familia yae hawakujua kama kuna jambo kubwa linakwenda kutokea muda mfupi baadae Mwendo wa gari ulianza kupungua baada ya kuanza kuongezeka magari hasa yale yaliyokuwa yakitokea barabara ya umoja wa wa Afrika kuingia katika barabara ya Serengeti. “Austin,Lucy amekaribia sana kufika katika mzunguko wa sanamu ya Kifaru.Get ready” akasema Osmund. “Tino,Jose na Papaa nadhani mmemsikia Osmund.Tujipange tayari” akasema Austin Magari matatu ya msafara wa Lucy Muganza yalifika katika mzunguko wa Kifaru.Tayari akina Austin walikwisha liona gari alilopanda Lucy “Tino and Papaa please confirm if you have a clear shot ! akasema Austin na akina Tino wakathibitisha kuwa wameliona gari na wako katika nafasi nzuri. “It’s show time” akasema Austin na ndani ya sekunde chache wote kwa pamoja wakaachia risasi wakiyalenga matairi ya lile gari la kifahari alimopanda Lucy Muganza. Dereva wa gari lile alistuka baada ya kuhisi kuna kitu kisicho cha kawaida katika gari.Lilibonyea chini ghafla akafungua dirisha na kuchungulia nje akastuka baada ya kuona tairi zote hazina upepo akapiga usukani kwa hasira.Haraka haraka akashuka pamoja na mlinzi aliyekuwemo ndani ya ile gari na kukagua tairi zote hazikuwa na upepo akawasiliana na wenzake haraka haraka.Magari yalikuwa yamesimama yakipiga honi wakimtaka dereva alisogeze gari lile pembeni kwani lilisababisha msongamano.Walinzi wengine nao wakashuka kwa haraka kutoka katika gari walimokuwemo kwenda kushuhudia kilichotokea na wakafanya maamuzi ya haraka baada ya kugundua matairi yale yalitobolewa na risasi “Madam kuna tatizo.Shukeni haraka sana muingie katika gari lingine” akasema mmoja wa walinzi.Mlango wa Limosuine ukafunguliwa huku walinzi wa Lucy wakiwa makini sana wakiangaza huko na huko kama kuna hatari yoyote.Askari polisi nao baada ya kuliona tukio lile wakaanza kujiweka tayari wakajua wale majambazi wanajiandaa kufanya ujambazi.Lucy,mumewe na Theresia wakashuka garini na walinzi wale wakaanza kuwaongoza kwa haraka kuelekea katika gari lingine lakini kabla mlango wa lile gari haujafunguliwa kikatokea kitendo cha ghafla ambacho hawakuwa wamekitarajia.Ndani ya sekunde chache walinzi wote wanne walikuwa chini.Lucy,mumewe na Theresia wakabaki peke yao wamesimama wakishangaa kilichotokea mara Lucy akatoa mguno na damu zikaruka akaanguka chini alikuwa amepigwa risasi ya kichwa “Luc………” Laurent hakumaliza kulitaja jina la mke wake naye akapigwa risasi akaaguka chini. “Theresia kimbia !! akapiga kelele dereva wake laini Theresa aliponyanyua tu mguu akapigwa risasi ya kifua akaanguka chini. Kitendo kile cha akina Lucy kupigwa risasi kiliwastua polisi ambao waliamini majambazi wale wameanza kufanya kazi yao hivyo kwa haraka wakaanza kuwasogelea.Majambazi wale walistuka kuona askari polisi wakijipanga na kuelekea katka gari lao wakajua tayari wamegundulika wakaanza kujihami kwa kuwarushia risasi polisi.Eneo lile lilibaki tupu baada ya mvua ya risasi kuanza kunyesha watu wote walikimbia na kuacha magari.Mapambano ya askari na majambazi yalidumu kwa dakika tano na askari wakafanikiwa kuwaua majambazi wote waliokuwemo ndani ya ile gari.Baada kuwamaliza wale majambazi wakaenda kuwatazama wale watu waliopigwa risasi ni mmoja tu Theresia aliyepigwa risasi kifuani upande wa kulia ndiye alionekana akiwa hai lakini wengine wote hawakuwa na uhai.Haraka haraka polisi wakataka kwanza kuokoa maisha ya Yule aliyekuwa hai.Wakampakia Theresa katika gari lao na kuondoka kwa kasi kubwa kumuwahisha hospitali. “Good job guys.Now let’s go home.Our country is safe” akasema Austin na wote wakaanza kufungua silaha zao na kuziweka katika mabegi yao kisha wakaondoka eneo lile ambalo tayari lilijaa askari. **************** Hospitali ya mtendeni ndiyo ilikuwa hospitali ya karibu na mahala pale tukio lilipotokea.Gari la polisi likaingia hospitali hapo na haraka haraka Theresia akashushwa akaingizwa ndani. “Amepigwa risasi katika tukio la ujambazi.Tafadhali okoeni uhai wake” akasema mmoja wa askari.Haraka haraka Theresia akaingizwa katika chumba cha upasuaji akageuzwa ili kuangalia kama risasi imetokea upande wa pili lakini haikutoka hivyo ilikuwa ndani,ikaletwa mashine ya mionzi na kupiga picha kifuani wakaiona risasi moja “Anahitaji kufanyiowa upasuaji mkubwa kuondoa risasi hii na hapa hospitalini kwetu hatuna uwezo wa kufanya upasuaji mkubwa kama huo.Tutakachokifanya ni kuzuia damu kuendelea kuvuja halafu atakimbizwa katika hospitali kuu ambako atafanyiwa upasuaji mkubwa wa kuondoa risasi ambayo iko sehemu mbaya” akasema daktari Yule na kwa haraka likafanyika zoezi la kuzuia damu kuendelea kuvuja katika jeraha halafu akapakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa katika hospitali kuu ya Mtodora kwa ajili ya upasuaji.





Taarifa za kuuawa Lucy Muganza na mumewe Laurent zilisambaa kwa haraka na kumfikia balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Rafael Berger ambaye alifika haraka sana hospitali kuu ya Mtodora ambako miili ilipelekwa.Alionyeshwa miili ya Lucy na mumewe akajiridhisha kuwa ni wenyewe.Wakati balozi Rafael akiwa katika chumba cha maiti ndani ya chumba cha upasuaji madaktari walikuwa katika heka heka za kuokoa maisha ya Theresia aliyekuwa amepigwa risasi kifuani.Upasuaji mkubwa ulikuwa unafanyika kuondoa risasi aliyokuwa amepigwa kifuani Balozi Rafael akiwa ameongozana na daktari mkuu alipelekwa katika chumba cha upasuaji akiwa amevaa mavazi maalum kushuhudia madaktari wakiendelea na heka heka za kuokoa maisha ya Theresia.Aliridhika na kazi iliyokuwa ikifanyika akatoka nje akaagana na daktari akaelekea katika gari lake akaondoka pale hospitali.Akiwa ndani ya gari balozi Rafael akampigia simu Rais wa Ufaransa Michael Weren “Nipe taarifa Rafael kuhusu taarifa hizi za kuuawa Lucy Muganza” akasema Michael na Rafael akavuta pumzi ndefu na kusema “Ni kweli mheshimiwa Rais Lucy na Laurent wameuawa.Nimeiona miili na nimethibitisha ni wenyewe.Binti yao Theresa yeye amenusurika.Amepigwa risasi ya kifua na hivi sasa yuko katika chumba cha upasuaji madaktari wakiendelea na jitihada za kuokoa maisha yake.Nimeingia hadi ndani ya chumba cha upasuaji nikajiridhisha na namna madaktari wanavyofanya kazi yao” akasema balozi Rafael na ukimya mfupi ukapita halafu Rais Michael akauliza “Tukio hilo limetokea katika mazingira gani? “Mara tu baada ya kupokea taarifa hizo niliwasiliana na mkuu wa jeshi la polisi Tanzania ambaye ni rafiki yangu na akaniambia kwamba hata yeye amepokea taarifa hizo lakini hakuwa na taarifa kamili za nini kilichotokea ameahidikunipa taarifa baadae atakapokuwa amepata taarifa kamili lakini taarifa ya awali inasema kwamba lilikuwa ni tukio la ujambazi na watu watano wameuawa katika tukio hilo.Inasemekana walitaka kumvamia Lucy na kumpora wakiamini anazo fedha nyingi ndani ya gari lake” akasema Rafael na ukimya ukapita tena kisha Rais Michael akasema “Rafael tukio hili ni kubwa na limenistua sana hata hivyo kuna jambo ambalo tunatakiwa tulifanye kwa haraka nalo ni kumuondoa Theresa hapo Tanzania na kumleta Ufaransa kwa matibabu na usalama zaidi.Hatuna uhakika bado kama Lucy ameuawa kweli na hao majambazi kama inavyodaiwa au vinginevyo hadi pale tutakapofanya uchunguzi wetu hivyo basi kumuacha Theresia hapo Tanzania ni kuendelea kuhatarisha maisha yake.Nitaelekeza ndege ya jeshi kutoka katika kambi yetu ya kijeshi iliyoko Djibouti ije haraka Tanzania kumchukua Theresia.Tafadhali hakikisha hadi muda huo ndege itakapowasili hapo Tanzania Theresa anakuwa salama” akasema Michael Weren Rais wa Ufaransa “Mheshimiwa Rais unahisi kwamba yawezekana hili ni tukio la kupangwa na si la ujambazi kama inavyodaiwa? Akauliza Rafael “Toka alipotangaza nia ya kugombea urais Lucy amekuwa na maadui wengi hasa kutoka nchini mwake ndiyo maana tumemuongezea ulinzi lakini nashangaa kusikia leo ameuawa.Tukio hilo linaonekana limepangwa kitaalamu sana lakini tutachunguza na kupata majibu lakini kwa sasa lazima tumuhamishe kwanza Theresia yeye atatusaidia sana kufahamu kile kilichotokea” akasema Rais Michael “Sawa mheshimiwa Rais nitaomba ulinzi kutoka vyombo vya ulinzi hapa Tanzania wamlinde Theresia wakati tukisubiri ndege hiyo ifike” akasema balozi Rafael “Hapana usifanye hivyo,hatujui nani wanahusika katika suala hili hivyo basi suala la kumuondoa Theresia hapo Tanzania ni suala la siri na halitakiwi kujulikana.Endelea kubaki hapo hapo hospitali usibanduke hadi pale ndege itakapofika na kumuhamisha” akasema Rais Michael



Baada ya kumaliza kazi,Austin na timu yake walikutana nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambako anaishi Gosu Gosu “Misheni imekwenda vizuri kama tulivyokuwa tumepanga.Ninawashukuru sana jamani kwa kazi hii kubwa.” akasema Austin “Baada ya kuimaliza kazi hii sasa nataka tulijadili suala la Mathew Mulumbi kama tulivyokuwa tumekubaliana” akasema GosuGosu “Kuna nini cha kujadili kuhusu Mathew Mulumbi?akauliza Tino “Mimi na Austin tulifanya majadiliano awali na tukajikuta mawazo yetu yanafanana kwamba Mathew bado yuko hai” akasema Gosu Gosu “Nini kimewafanya muamini hivyo kwamba Mathew yuko hai?akauliza Tino “Ni kutokana na mazingira ya tukio la kupotea kwake ndiyo maana tunahisi yawezekana Mathew yuko hai” akasema Gosu Gosu.Tino akavuta pumzi ndefu na kusema “Imepita miaka mitatu sasa toka Mathew alipopotea na mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizowahi kupatikana kama yuko hai.Limekuwa ni kama fumbo kubwa na hakuna wa kulifumbua” akasema Tino “Ni kweli ni fumbo kubwa lakini tunataka kulifumbua.Binafsi na hata Austin tunaamini kwamba Mathew bado yuko hai” “Kama yuko hai where is he?akauliza Tino “Hapo ndipo mahala pa kuanzia” akasema Gosu Gosu Tino akamgeukia Austin “Austin ulikuwepo katika operesheni hiyo ya kwenda kuwakomboa mtoto wa rais na Olivia hebu tueleze nini hasa kilitokea?Kwa nini unaamini Mathew yuko hai?akauliza Tino.Austin akaonekana kuzama mawazoni halafu akasema “Guys I real don’t know what real happened.Kwa muda wa miaka mitatu sasa kila siku usiku ninapofumba macho hujaribu kuvuta picha ya usiku ule ili walau niweze kukumbuka kilichotokea na kupata picha kama Mathew yu mzima au alikufa lakini kwa muda wote huu picha ninayoipata ni ile ile.Olivia anadai kwamba Mathew alipigwa risasi akaanguka chini na akawataka yeye na Coletha wakimbie.Hakumbuki nini kiliendelea lakini kwa kauli ile ya Olivia inaonyesha wazi kwamba upo uwezekano labda Mathew alifariki dunia.Baada ya shambulio kukoma mimi na vijana wangu tulizunguka eneo lote tukimsaka Mathew bila mafanikio.Hapo ndipo kichwa kinapoanza kuniuma na maswali mengi yalianzia hapo je kama alijeruhiwa alitoroka eneo lile na kwenda kujificha?Kama alitoroka je yu mzima au alifariki dunia? Kikosi kilichotumwa kwenda kufanya uchunguzi na kumtafuta siku iliyofuata baada ya lile tukio kilitoa taarifa yake kwamba hawakufanikiwa kumpata Mathew na walihisi yawezekana aliliwa na fisi kwani eneo lile lilikuwa na fisi wengi.Hapo ndipo mjadala ulipoishia kwamba Mathew amekufa” akasema Austin na ukimya ukatawala mle ndani. “Kitu gani mlikuwa mmepanga kukifanya kuhusu suala hili?akauliza Tino “Tulianza kwa kujenga wazo hilo kwamba Mathew yuko hai lakini bado hatujajua wapi tuanzie kulifanyia kazi hilo wazo” akasema Gosu Gosu “Guys mimi nadhani tuliweke pembeni suala hili kwa muda.Give me time to think.Nikipata chochote ambacho kitatusaidia katika uchunguzi wetu nitawaeleza”akasema Austin “Nadhani Austin yuko sahihi.Suala hili ni gumu sana.Kama Mathew yuko hai yuko wapi?Kwa nini kwa muda huu wote hajataka tujue mahala alipo?Nadhani tuachane na hili jambo na kama Mathew yuko hai basi siku moja atarejea” akasema Tino “We have to fight for him.He’s our friend and we don’t have to stop searching for him.Tutatulia pale tutakapothibitisha kweli amekufa lakini mpaka sasa hivi hakuna ushahidi wowote wa kutuonyesha Mathew amekufa” akasema Gosu Gosu “Nakubali Papaa,Mathew ni mwenzetu na lazima tuupate ukweli kama kweli amekufa au ni mzima.Give me a little time and I’ll come to you” akasema Austin na kuchukua simu akampigia Dr Fabian “Hallo Austin” akasema Dr Fabia “Mheshimiwa Rais nimekupigia kukujulisha kwamaba ile kazi tumeimaliza” “Ahsante sana Austin kwa kazi nzuri.Nimekwisha pata taarifa tayari kuhusiana na kilichotokea.Mmetumia akili nyingi sana kwani hivi sasa kila mtu anaamini kwamba tukio lile lilikuwa ni la kijambazi.Nifikishie salamu kwa vijana wote mlioshirikiana katika kutekeleza jukumu hili waambie nitapanga nafasi ya kukutana nao kuwashukuru kwa kazi hii kubwa kwa taifa lao”akasema Dr Fabian “Kwa niaba yao mheshimiwa Rais nashukuru sana kwa kutuamini na kutupatia jukumu hili kubwa kwa nchi yetu” “Pamoja na hayo” akasema Dr Fabian na kunyamaza kwa muda halafu akasema “Kuna jambo dogo halikwenda sawa lakini si tatizo.Nimepokea taarifa kwamba Theresia mtoto wa Lucy amenusurika yeye alipigwa risasi ya kifua na hivi sasa yuko mahututi na madaktari wanaendelea na jitihada za kuokoa maisha yake.Lakini hili si tatizo kwani mlengwa mkuu alikuwa ni Lucy Muganza.Huyu Theresia hana hatari yoyote kwetu.” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais tunashukuru sana.Imekuwa heshima kwetu kuaminiwa nawe”akasema Austin “Nitafurahi kukutana nanyi wote na kujenga timu imara na nitapenda kuwatumia katika operesheni zangu mbali mbali za siri” akasema Dr Fabian wakaagana na kukata simu. TEL AVIV – ISRAEL Mlipuko mkubwa wa bomu la kujitoa mhanga ulitokea katika bustani ya watoto wadogo katika jiji la Tel Aviv.Mwanamke mmoja aliyejitanda vazi refu jeusi alifika katika bustani hiyo akiwa na mwanae pamoja na kikapu kilichojaa pipi akaingia ndani ya bustani hiyo akawakusanya watoto na kuanza kuwagawia pipi na dakika tano baadae akajilipua.Watoto kumi na sita walifariki pale pale akiwemo mlipuaji na mtoto aliyekuwa ameongozana naye.Vikosi vya uokozi vilifika haraka sana eneo hilo la bustani na kuanza kazi haraka ya kuokoa manusura wa tukio lile.Wakati vikosi vikiendelea na zoezi la uokozi katika bustani ya watoto bomu lingine kubwa lililotegwa katika gari lililipuka katika kituo cha kulelea wazee na kusababisha vifo vya wazee tisa. Muda mfupi baada ya matukio yale ya milipuko ile ya mabomu kutokea,iliwekwa video mtandaoni ikimuonyesha Ibrahim Seif Al Nasir mmoja wa viongozi wa juu wa kikundi cha IS akijigamba kwamba kikundi chao ndicho kilichotekeleza mashambulio yale mawili na akaendelea kuonya kwamba wamejipanga vyema na kwamba mashambulio zaidi yataendelea bila kukoma hadi pale ardhi ya wapalestina itakaporejeshwa.Alitoa angalizo kwa waisrael wajiandae kwani damu nyingi zaidi inakwenda kumwagika. Video ile ya kikundi cha IS ilimpelekea waziri mkuu kuitisha kikao cha dharura cha wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini Israel IDF,AMAN,AFI,BP,NI,GSS, RPPC na MOSSAD.Kikao hicho kizito kilichukua zaidi ya saa sita kikijadili kwa kina mashambulio yale mawili ya mabomu,hali ya usalama ya Israel na namna ya kupambana na kikundi cha IS ambacho kilitishia kuendelea kufanya mashambulio zaidi katika ardhi ya Israel hadi pale maeneo ya wapalestina ambayo yanakaliwa kimabavu na Israel yatakaporejeshwa.Baada ya kikao hicho kilichoongozwa na waziri mkuu wa Israel kumalizika,mkuu wa shirika la ujasusi la Israel Moshe Levine akarejea ofisini kwake na kuitisha kikao cha dharura na watendaji wakuu wa shirika hilo pamoja na wakuu wa idara zote zilizo ndani ya Mossad ambao walifika kwa haraka sana na kikao kuanza “Nimetoka katika kikao kizito na waziri mkuu.Agenda kuu ya kikao hicho ni usalama wa Israel hasa kufuatia milipuko miwili ya mabomu iliyoua watu ishirini na tisa.Kama haitoshi kikundi cha IS ambao wametekeleza mashambulizo hayo wameendelea kutishia kumwaga damu zaidi katika ardhi yetu.Israel hatuko tayari kwa vitisho vya namna hii na lazima tuwaonyeshe kwamba ukimwaga damu ya muisrael mmoja malipo yake ni makubwa.Huu ni mwisho wa kuvumilia na sasa tunakwenda kulimaliza kundi hili la kigaidi na kulinda maisha ya watu wetu” akasema Moshe na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Nimeulizwa maswali katika kikao ambayo sikutoa majibu ya kuridhisha.Nimeulizwa kwa nini hadi leo hii tumeshindwa kuwakamata au hata kufahamu waliko wafadhli wakuu wa kikundi cha IS na vikundi vingine vinavyofanya mauaji katika ardhi yetu? Mossad ni chombo kikubwa kina majasusi wenye uwezo mkubwa mno kuliko vyombo vingi vya kijasusi duniani,tumefanikiwa operesheni nyingi sana duniani lakini kwa nini mpaka leo hatujui alipo Habiba Jawad na wenzake wanaovifadhili vikundi hivi vya kigaidi?Vyombo vyote vya ulinzi hapa Israel vinatutegemea sisi kupata taarifa za mahala walipo watu hao ambao ni wafadhili wakuu wa vikundi hivi lakini toka tulipoanza kumtafuta Habiba Jawad mpaka leo hii ni miaka kadhaa imepita na hakuna majibu yopote ya kuridhisha kuhusu mahala alipo Habiba na wenzake.Jibu nililowapa ni kwamba tayari tuna mipango tunaendelea nayo katika suala hilo na nikaomba tupewe muda kidogo.Waziri mkuu ametupa muda wa wiki mbili tuwe tumepata majibu kutoka katika hiyo mipango yetu.Waziri mkuu yuko sahihi kabisa kuwa mkali kwani suala hili limechukua miaka mingi kitu ambacho hakijawahi kutokea katika shirika letu.Jambo hili linakaribia miaka kumi sasa na hatuwezi kuendelea kumfuatilia mtu mmoja kwa miaka hiyo yote lazima jambo hili lifike mwisho na tufahamu mahala alipo Habiba na tumtie nguvuni na kuhitimisha ugaidi katika ardhi yetu.Nataka leo nipate taarifa za mipango yetu inakwendaje.Tuanze na Dr Daniel.Nimekuita hapa ili utupe taarifa kuhusiana na Edger Kaka.Kuna matumaini yoyote unayaona kwake?Kuna mabadiliko yoyote unayategemea? Akauliza Moshe na Dr Daniel akajibu “Kama nilivyoeleza katika taarifa yangu ya mara ya kwanza baada ya kumpima Edger Kaka mara tu alipoletwa kutoka Kenya na kwa mujibu wa vipimo ambavyo nimeendelea kumpima mara kwa mara hakuna tena mabadiliko yoyote yaliyotokea wala yanayotegemewa kutokea.Edger hataamka tena.Ubongo wake umekufa na hakuna namna ya kuweza kumuamsha.Kinachomfanya aonekane yuko hai ni mashine zile alizofungiwa lakini kiuhalisia Edger amekwisha fariki kitambo”akasema Dr Daniel “Dr Daniel ahsante kwa taarifa hiyo.Uliwahi kutueleza mapema jambo hili lakini tulikuomba uendelee kumuweka katika mashine ya kumsaidia kuishi tukitegemea labda kutakuwa na mabadiliko mbeleni lakini imepita miaka mitatu sasa na hakuna mabadiliko yoyote na kwa mujibu wa taarifa yako ya leo ni kwamba Edger tayari amefariki dunia hivyo basi hakuna haja ya kuendelea naye.Ni wakati wa kuzima mashine zote na kumuacha apumzike” akasema Moshe na chumba chote kikawa kimya “Edger Kaka tunamuondoa rasmi katika mipango yetu na sasa tunabaki na mtu mmoja ambaye tunaamini anaweza akawa na msaada kwetu ambaye ni Mathew Mulumbi.Huyu aliwahi kuwa jasusi nchini Tanzania na ndiye aliyeongoza kikosi kilichovamia ubalozi wetu Nairobi wakaua watu na kumchuua Edger Kaka kutoka mafichoni tulikomficha.Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa aliyekuwa wakala wetu nchini Tanzania,Mathew na wenzake ndio waliowaua Avi Abramson dereva na mlinzi wake.Wakala wetu huyo aliyetupa taarifa zote anadai baada ya kumchukua Edger Kaka kutoka Nairobi Mathew alifanya mawasiliano na Habiba kwa ajili ya kufanya mabadilishano ya mateka yaani yeye awape Edger Kaka na wao IS waachie huru rafiki yake anaitwa Olivia na mtoto wa Rais wa wakati huo ambao walikuwa wametekwa na magaidi wa IS.Ni kwa sababu hiyo Mathew anakuwa ni mtu muhimu sana kwetu kwa sasa.Tunataka kujua namna alivyoweza kuwasiliana na habiba Jawad.Kwa bahati mbaya toka ameletwa hapa Israel Mathew Mulumbi hajawahi kufungua mdomo wake kulia au kutamka chochote.Ni binadamu wa ajabu sana.Niliagiza kiwango cha mateso kipande hadi kufikia daraja la kwanza lakini pamoja na mateso hayo yote bado huyu jamaa hajathubutu kusema chochote.Nimevutiwa sana na aina ya majasusi wa aina hii ambaye yuko tayari kufa kuliko kutoa siri.Amekubuhu vilivyo katika ujasusi” akasema Moshe na kunyamaza kwa sekunde chache “Njia ya mateso haikuonekana kuzaa matunda hivyo tukaamua kubadili mbinu.Katika taarifa tulizopewa na huyo wakala wetu ni kwamba Mathew ni mtu tajiri sana.Yeye na mke wake wanamiliki makampuni na biashara kubwa kubwa sehemu mbali mbali duniani.Mke wake na watoto wao wawili wanaishi Paris Ufaransa.Tumeamua kuitumia familia yake kumfungua mdomo wake na nina uhakika safari hii lazima atafunguka kwani takwimu zinaonyesha njia hii imekuwa na mafanikio makubwa kila pale inapotumiwa.Efraim Dagan wewe ndiye msimamizi wa operesheni hii hebu tupe mrejesho nini kinaendelea hivi sasa katika mpango wetu wa kuitumia familia ya Mathew? Akauliza Moshe Levine “Tayari tumemtuma mmoja wa watu wetu Nahum Yatom kwenda jijini Paris.Akiwa pale Nahum atakutana na Peniela na kujenga naye mahusino ya kibiashara kwani anakwenda pale kama mfanya bisahara tajiri.Nahum ni kijana mtanashati sana mwenye umbo na sura nzuri yenye kuvutia wanawake wengi na yeye ni maalum kabisa kwa misheni kama hizi za kujenga mahusiano na wanawake ambao tumewalenga.Ni mtaalamu sana katika upande huo na anajua nini cha kufanya.Hajawahi kushindwa.Anazo mbinu zote za kuweza kumteka mwanamke.Baada ya kuanzisha mahusiano ya kibiashara na Peniela jukumu lake la pili ni kuanzisha mahusiano naye ya kimapenzi na tayari amekwisha fanikiwa kwa hilo.Amekutana na kufanya mapenzi na Peniela mara mbili katika hoteli alikofikia na sasa Peniela amemualika nyumbani kwake.Nahum hataki kufanya haraka kwenda nyumbani kwa Peniela ili kumfanya asistuke chochote.Atakapokwenda nyumbani kwa Peniela atafunga kamera za siri ambazo zitatuwezesha kumuona yeye na Peniela katika mahaba mazito na hapo ndipo tutamuonyesha Mathew Mulumbi picha hizo ambazo tunaamini zitamuumiza sana na atafunguka.” akasema Efraim na kwa mbali Moshe akatabasamu “Huu ni mpango mzuri sana.Linapokuja suala la familia watu wengi hata wawe wagumu kiasi gani hushindwa kuvumilia na kufunguka.Nina uhakika mkubwa kwa mpango huu Mathew Mulumbi atakapomuona mke wake akiwa na mwanaume mwingine katika mahaba lazima atafunguka kila kitu anachokifahamu kuhusu Habiba Jawad.Hata hivyo nataka Nahum asiendelee kuvuta muda mwingi kufika nyumbani kwa Peniela.Kama tayari amekwisha muweka Peniela kiganjani hakuna kuchelewa.Afanye haraka kazi aliyotumwa huko.Mwambie kwamba nataka baada ya siku tatu awe amekamilisha kila kitu na zoezi lifanyike ili Mathew ashuhudie.Hatuwezi kusubiri zaidi ya hapo” akaelekeza Moshe BAADA YA SIKU 3 FACILITY 1391 TEL AVIV Mlango mzito wa chumba uliafunguliwa wakaingia watu sita watatu kati yao akiwa na silaha.Taa ikawashwa na watu wale wakaonekana wakiwa wamezifunika nyuso zao zisionekane. “Mathew Mulumbi muda wa safari” akasema mmoja wao na kumsogelea Mathew ambaye alikuwa amejikunyata katika godoro akiwa amevalishwa mavazi meusi akitetemeka kwa baridi.Mkono wake mmoja ulikuwa umefungwa pingu na mnyororo mrefu ukaunganisha pingu ile na chuma kizito kilichofukiwa katika sakafu yenye zege zito.Mathew Mulumbi ambaye alikuwa na ndevu nyingi na nywele ndefu akafunguliwa pingu ile ndefu akafungwa nyingine mikono yote halafu akafunikwa mfuko mweusi kichwani na kutolewa ndani ya kile chumba akaingizwa katika gari maalum ambalo liliondoka katika jela hii ya siri ambamo hufungwa magaidi na watu hatari kwa usalama wa Israel. Baada ya dakika arobaini gari likasimama mlango ukafunguliwa na Mathew Mulumbi akashushwa garini bado akiwa na mfuko kichwani.Watu wale waliomuongoza hawakuwa wakizungumza.Mathew alihisi wakipanda lifti na baada ya muda mfupi milango ya lifti ikafunguliwa wakatembea kidogo na mlango wa chumba ukafunguliwa akaingizwa ndani na kukalishwa sofani halafu mfuko ule mweusi ukatolewa kichwani akajikuta katika chumba kimoja kikubwa kizuri chenye samani za kupendeza.Alishangaa kwani kwa muda wa miaka mitatu Mathew alikuwa analala katika godoro kuu kuu ndani ya chumba chenye baridi kali.Akiwa bado katika kukishangaa chumba kile kizuri mmoja wa wale jamaa akamwambia “Ingia bafuni uoge” akasema Yule jamaa na kumfugua pingu akamuonyesha Mathew mlango wa bafu.Taratibu Mathew akainuka na kuufungua mlango wa bafu akaingia.Lilikuwa ni bafu zuri sana lakini kabla hajafanya chochote akapatwa na mshangao mkubwa baada ya kujitazama katika kioo “Nimekuwa hivi?Nyumbani wakiniona katika hali hii watadhani mimi ni msukule.Ninatisha.Sijawahi kujitazama kwenye kioo toka nilipotekwa na hawa jamaa.Uso wangu umeharibika ninaonekana kama shetani” akawaza Mathew akiendelea kujitazama katika kioo.Pembeni akaiona mashine ya kunyolea pamoja na dawa mbalimbali akaishika mashine ile akaitazama. “Sijui hata nianzie wapi kwa namna ninavyotisha.Ni muda mrefu sijatia maji mwilini mwangu.Nini hasa wanataka kunifanyia hawa jamaa? Akajiuliza “Hii ni moja ya njia za majasusi kutaka kupata taarifa kutoka kwa mtu wanayemshikilia kwa kujifanya wanakutendea wema baada ya njia ya mateso kushindikana.Lakini hapa wamefika hata kama wakitumia njia hii hawatapata kitu kutoka kwangu.Niko tayari kufa kuliko kuwaeleza kitu chochote hawa jamaa” akawaza na kuanza kuvua ile nguo nyeusi aliyokuwa amevaa na akagundua kwamba nguo ile ilikuwa imeshikana na mwili kufuatia vidonda alivyokuwa navyo mwilini.Akaitoa kwa nguvu na kuhisi maumimu makali kwani alitonesha baadhi ya vidonda.Akafumba macho na kusikilizia maumivu yale. “Kwa muda mrefu hawa jamaa wamekuwa wananitesa wanataka nikiri kwamba nilihusika katika uvamizi wa ubalozi wao Nairobi na papo hapo niwataje watu nilioshirikiana nao. Katu siwezi kuwaeleza chochote.Niko tayari kufa lakini si kusema chochote kwa hawa jamaa” akawaza na kuvua suruali akajitazama katika kioo namna mwili wake ulivyoharibka.Mwili wote ulijaa vidonda.Taratibu Mathew akaingia katika beseni kubwa la kuogea akafumba macho na kukukumbuka maisha yale aliyokuwa akiishi “Nilikuwa na maisha kama haya kabla sijatekwa nyara.Masikini familia yangu sijui watakuwa katika hali gani hadi muda huu sijatokea.Peniela atakuwa Amelia mno_Oh my God Ruby,sipati picha namna atakavyokuwa akihuzunika.Kila ninapowawaza hawa watu wangu wa karibu,familia yangu ,Ruby,Gosu Gosu ninapatwa na nguvu ya kuendelea kuvumilia mateso makali ninayoyapata hapa.Naamini iko siku nitatoka katika mateso haya,iko siku nitarejea nyumbani kuungana nao tena” akawaza Mathew akiwa ndani ya beseni lile la kuogea “Kila ninapofumba macho picha ya usiku ule hunijia.Nakumbuka namna tulivyovamiwa na kuanza kushambuliwa.Nilipigwa risasi kadhaa na wakanichukua.Kwa inavyoonekana wale jamaa walinilenga zaidi mimi na Edger Kaka kwani baada ya kutupata mapambano yalikoma.Waliotushambulia kilikuwa ni kikosi cha Israel.Kitu ambacho nimekuwa ninajiuliza kwa muda mrefu walifahamuje kama tunafanya mabadiliano ya mateka na IS?Mpango ule ulikuwa wa siri na ninahisi kwamba lazima kuna mtu ambaye aliwapa Israel taarifa za kuwepo kwa mpango ule wa mabadilishano.Akilini mwangu anakuja Devotha lakini kuna wakati ninakataa kwamba Devotha hawezi akafanya hivyo.Tumekuwa naye katika operesheni nzima hadi mwisho na ameshiriki kikamilifu katika kuvamia ubalozi wa Israel Nairobi.Lakini swali lingine linalokuja kama si yeye ni nani basi anaweza akafanya hivyo? Waliofahamu kuhusu mabadilishano yale ni Gosu Gosu na Devotha na kati ya hao ni Devotha ambaye alikuwa na mahusiano na Mossad.Sitaki kuamini moja kwa moja kama kweli ni yeye aliyeuza taarifa zetu kwa Mossad kwani nilimuamini sana lakini endapo nikifanikiwa kutoka hapa nitafanya uchunguzi na kumbaini mtu aliyesababisha ninateseka namna hii” akawaza na kuendelea kuoga halafu akatoka ndani ya beseni lile la kuogea akaenda katika kioo akachukua mashine na kunyoa ndevu zote na nywele “Afadhali hapa kidogo ninaonekana binadamu.Mungu atawabariki kwa wema huu mdogo walionitendea lakini naamini kuna kitu wanakitafuta ndiyo maana wamefanya hivi” akawaza.Alipomaliza akatoka bafuni na kukuta nguo zikiwa zimewekwa kitandani. “Vaa hizo” akasema mlinzi aliyekuwemo mle chumbani.Mathew akavaa nguo zile alizoletewa akajitazama katika kioo “Kidogo kwa sasa ninaonekana binadamu” akawaza akiwa amesimama mbele ya kioo halafu Yule mlinzi akamtaka aketi sofani.Baada ya dakika mbili akaingia mwanamke mmoja aliyevaa sketi fupi nyeusi na shati jeupe akiwa na sinia lenye chupa ya mvinyo na glasi akamuwekea Mathew mezani “Karibu mvinyo safi” akasema Yule mlinzi.Mathew akaitazama chupa ile ya mvinyo halafu akatikisa kichwa ishara ya kukataa kutumia mvinyo ule.Aliendelea kukaa sofani mawazo mengi yakizunguka kichwani kwake na mara mlango ukafunguliwa wakaingia watu wanne “Ahsanteni vijana sasa mnaweza mkaniacha na Mathew” akasema mtu mmoja aliyekuwa amewekwa kati kati na walinzi wote mle ndani wakatoka na Yule jamaa akaenda kuketi sofani akitazamana na Mathew.Akaiinua chupa ile ya mvinyo akaitazama na kutabasamu “Mallacan 1946 mvinyo ghali kabisa duniani.Nimekuletea mvinyo huu ishara ya kufungua mahusiano mapya kati yetu.Ninaitwa Efraim Dagan ni mkuu wa idara ya operesheni za kimataifa ndani ya Mossad.Kama hutajali tunaweza kutembea kidogo?akauliza Efraim na kuinuka Mathew akasita kusimama “Usihofu Mathew,uko salama.Tafadhali inuke tutembee kidogo” akasema Efraim na Mathew akajaribu kusimama akahisi miguu haina nguvu.Efraim akamfuata akamshika mkono akamsaidia kusimama wakatoka ndani ya kile chumba wakaanza kutembea katika korido huku walinzi wakiwa nyuma yao.Mathew alionekana dhaifu hivyo mwendo ulikuwa mdogo sana.Ni Efraim ambaye alikuwa akiongea lakini Mathew hakuonekana kumsikiliza.Waliingia katika chumba Fulani kilichokuwa na runinga nane kubwa na watu kadhaa walikuwa wanaendelea na kazi katika kompyuta zao.Efraim akamuongoza Mathew hadi katika sofa nzuri wakaketi wakitazama runinga kubwa “Mathew Mulumbi kwa muda wa miaka mitatu tumekuwa tukihitaji kusikia http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kauli yako ukikiri kuhusika katika uvamizi wa ubalozi wetu jijini Nairobi ukaua na kuchukua mateka lakini umekuwa kiburi na hauko tayari kufanya hivyo.Tumekupa kila aina ya mateso lakini unaonekana u mvumilivu mno wa mateso na kwa ajili hiyo basi umetulazimisha kufanya kile ambacho hatukuwa tumekusudia kukifanya.Naomba nipeleke Paris” akasema Efraim akimuelekeza mmoja wa vijana waliokuwamo ndani ya kile chumba.Mara katika runinga zikaanza kuonekana picha na Mathew akapatwa na mstuko mkubwa “Penny !! Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu Mathew Mulumbi akafungua mdomo na kutamka baada ya kumuona mke wake Peniela akiwa chumbani na kijana mmoja mwenye sura nzuri.Walikuwa wamelala kitandani wakiwa watupu kabisa na ilionekana walikuwa wametoka kufanya mapenzi.Peniela alionekana ni mwenye furaha na walifanyiana utani kwa kurushiana mito na Yule kijana “No this is not true ! akasema Mathew kwa sauti ndogo na kunyanyuka.Walinzi waliokuwa karibu wakamsogelea. “Kaa chini Mathew Mulumbi” akasema Efraim na walinzi wakamfuata Mathew wakamkalisha chini. “Hii si kweli.Hii picha mmeitengeneza kutaka kuniumiza.Peniela mke wangu hawezi akafanya kitu kama hiki” akasema Mathew “Hiki si kitu cha kutengeneza Mathew.Hiki ni kitu cha kweli.Tazama saa.Sisi na Patris tumepishana kwa saa moja tu.Unachokiona ni kitu ambacho kinaendelea sasa hivi katika nyumba yako iliyoko Paris.Kijana unayemuona runingani anaitwa Nahum na kwa sasa yuko na Peniela mke wako ambaye anaamini tayari umekwisha fariki dunia.Tunao pia watu wetu ambao wanawafuatilia binti yako Malaika na mwanao Patrick.Mathew tunao uwezo wa ………..” Efraim hakumaliza alichotaka kukisema Mathew akapatwa na nguvu za ajabu akainuka na kuwasukuma walinzi akamuendelea Efraimu akamtandika ngumi nzito iliyomuangusha sofani mara Mathew akaanguka chini na kupoteza fahamu baada ya kuwekewa mgongoni kifaa chenye chaji za umeme alichokuwa amekishika mmoja wa walinzi. “Mpelekeni chumbani mfungeni mikono na miguu.Mtu hatari sana huyu” akaelekeza Efraim aliyekuwa anavuja damu mdomoni.Mathew akachukuliwa akapelekwa katika chumba kingine kilichokuwa na kitanda kidogo akafungwa miguu na mikono kwa pingu maalum zilizounganishwa katika kitanda hicho. “Ana mikono migumu kama jiwe Yule jamaa lakini tumempata.Hatimaye baada ya miaka mitatu leo ameongea.Ameumizwa na kile alichokiona na lengo letu limefanikiwa kwani tulitaka aumie na sasa atakuwa tayari kufanya kitu chochote hata kutueleza kitu chochote kile kutokana na hasira alizonazo” akawaza Efraim





Mathew Mulumbi alirejewa na fahamu baada ya dakika kumi na tano na kujikuta akiwa amefungwa miguu na mikono katika kitanda akajaribu kujitikisa lakini hakuweza alikuwa amefungwa barabara. “Kile nilichokiona runingani ni kitu cha kweli au nilikuwa njozini? Niliyemshuhudia katika video ile alikuwa ni Peniela mke wangu au ni katuni? Akawaza “Lakini mwanamke niliyemshuhudia ni Peniela mke wangu.Video ile inaonekana ni video halisi kabisa na mle chumbani walimokuwamo kweli ni chumbani kwangu.Naamini watu hawa wamenionyesha video ile kwa ajili ya kuniumiza baada ya njia zao zote za mateso kushindikana.Kwa hili walilolifanya wamefanikiwa wameniumiza mno.Peniela ninampenda mno pamoja na wanangu” akawaza Mathew na michrizi ya machozi ikaonekana machoni “Peniela..ouh Pen…………….” Akatolewa mawazoni Mathew baada ya mlango kufunguliwa akaingia Efraim akiwa ameweka pande la barafu mahala alipopigwa ngumi na Mathew.Alikuwa ameongozana na walinzi wake.Mathew alipomuona hasira zikazidi akajaribu kujitikisa lakini alikuwa amefungwa barabara. “Mathew najua umeumia sana kwa video ile uliyoina ya mkeo.Tulitaka tukuonyeshe kile kinachoendelea huko nje.Watu wako wote wanaamini tayari umekufa ndiyo maana hata mkeo Peniela ameamua kuwa na mwanaume mwingine ambaye ni mtu wetu.Familia yako iko mikononi mwetu na tukiamua muda wowote tunaweza kuifanya kitu chochote.Mathew hakuna wa kukuokoa hapa ulipo bali ni juhudi zako wewe mwenyewe ndizo zitakuokoa.Chaguo ni lako kama unataka kuendelea kukaa hapa au kuiokoa familia yako.” akasema Efraim.Mathew akauma meno kwa hasira na kuuliza “Nini mnataka kutoka kwangu?akauliza Mathew na Efraim akatabasamu “Tunataka kuzungumza nawe.” Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema “Niko tayari kwa mazungumzo lakini tafadhali naombeni msiiguse familia yangu” “Safi sana.Kama uko tayari kwa mazungumzo tutaonana baada ya muda mfupi” akasema Efraim na kutoka ndani yakile chumba “Kwa ajili ya Peniela na watoto wangu niko tayari kufanya kitu chochote ili kuwa nao tena.Hawa jamaa wanaweza kweli wakawafanyia kitu kibaya ili kunilazimisha niwaeleze kile wanachokitaka.Simlaumu Peniela kwa kuingia katika mahusiano na mwanaume mwingine kwani imepita miaka mitatu bila kuniona na anaamini tayari nimekwisha fariki hivyo ameamua maisha yaendelee.Wa kulaumiwa hapa ni mimi mwenyewe ambaye kila ninaposema sitaki tena kazi hizi lakini ninajikuta nikizifanya bila kutarajia.Ni mimi ndiye ninayeiweka familia yangu njia panda hivi sasa kama ningeamua kukaa mbali na hizi kazi haya yote yasingetokea.Nimekuwa mtiifu na muaminifu mno kwa nchi yangu lakini hapa nilipofika ni mwisho.Ni muda wa kupambana kwa ajili ya familia yangu” akawaza Mathew “Kuna nyakati najutia kwa nini nilifahamaiana na Olivia Themba kwani ni yeye aliyenifanya nikaingia katika sakata lile na mwisho wangu umekuwa hapa.Lakini sipaswi kujilaumu sana kwani nilipambana na kuhakikisha nimemuokoa Olivia,mtoto wa Rais na wale wasichana waliokuwa wametekwa na magaidi.Katika mapambano yale ndipo tulibaini kuwa kuna mtandao mkubwa wa IS nchini kwetu.Yawezekana wote sasa hivi wamekwisha nisahau wakiamini nimefariki dunia.Kama mke wangu amekwisha nisahau hakuna atakayenikumbuka tena hivi sasa.Hakuna atakayejaribu hata kunitafuta.Sina msaada mwingine kwa hivi sasa kutoka kwa watu wangu msaada pekee ni kumuomba Mungu anionyeshe njia ya kuweza kutoka hapa nilipokwama” akaendelea kuwaza Mathew na mlango wa chumba alimokuwemo ukafunguliwa wakaingia watu watano.Akafunguliwa mikono na kufungwa pingu halafu akafunguliwa miguu na kufungwa pingu yenye mnyororo mrefu halafu akavalishwa mfuko mweusi na kutolewa ndani ya kile chumba akapelekwa katika chumba Fulani akakalishwa katika kiti halafu akavuliwa ule mfuko kichwani akajikuta akiwa kati kati ya chumba huku akitazamana na watu kumi na tano waliokuwa katika meza tatu zilizokuwa mbele ya kile chumba.Efraim Dagan alikuwa kati kati yao akasema “Mathew Mulumbi karibu sana.Mbele yako ni jopo la viongozi na wakuu wa idara mbali mbali ndani ya Mossad” akasema Efraim “Ndugu wajumbe wa kikao hiki mbele yenu ni Mathew Mulumbi ambaye alifanya kazi katika idara ya ujasusi ya Tanzania,yuko hapa mbele yetu kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa ambayo ataulizwa” Efraim akawaeleza wale watu alikuwa nao ndani ya kile chumba halafu akamgeukia Mathew “Mathew Mulumbi muda mfupi uliopita ulinieleza kwamba uko tayari kuzungumza nasi.Tumefurahi kwa uamuzi wako huo kwani ni miaka mitatu imepita sasa na jitihada mbali mbali za kuipata sauti yako zilishindikana.Kwa kuanzia tungependa ulithibitishie jopo hili lililoko mbele yako kwamba wewe ndiye uliyevamia ubalozi wa Israel jijini Nairobi na kuua watu wetu akiwemo mkuu wa Mossad Afrika Mashariki Avi Abramson kisha kumteka Edger Kaka aliyekuwa anahifadhiwa ubalozini hapo” Mathew Mulumbi akageuza shingo akafanya ishara kuwa anataka maji ya kunywa.Haraka haraka chupa ya maji ikaletwa na kuwekwa mezani.Hakutaka kutumia glasi akachukua chupa ile akaigugumia yote ikamalizika.Akawaangalia wajumbe wale halafu akasema “Naitwa Mathew Mulumbi ni mtanzania.Nimewahi kufanya kazi katika udara ya ujasusi ya Tanzania” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Miaka mitatu iliyopita nilivamia ubalozi wa Israel jijini Nairobi na katika operesheni ile watu kadhaa waliuawa akiwamo Avi Abramson aliyekuwa mkuu wa Mossad kwa ukanda wa Afrika mashariki.” Akanyamaza kidogo baada ya minong’ono kusikika “Miaka mitatu kabla ya tukio lile kutokea” akasema na watu wote wakanyamaza “Kikosi maalum cha majasusi wa Mossad waliingia nchini Tanzania wakafanya operesheni ya kimya kimya wakaua na kumteka Edger Kaka na kwenda kumficha katika ubalozi wa Israel nchini Kenya.Nilichokifanya mimi na wenzangu niliowaongoza ni kwenda kumkomboa raia wetu aliyetekwa nyara na Israel.Nilichokifanya ulikuwa ni muendelezo wa kile mlichokianzisha ninyi.Mnaamini ninyi ni taifa kubwa lenye nguvu na mnaweza mkafanya chochote mnachotaka katika nchi yoyote ndiyo maana mkaingia katika ardhi yetu mkaua na kuchukua mateka raia wetu.Kama haitoshi bado mliwatuma majasusi wengine kuandaa operesheni nyingine ya kimya kimya nchini Tanzania ili muweze kumchukua mateka raia mwingine lakini majasusi hao mliowatuma niliwaua.Niliwaua majasusi hao ili kuwapa salamu muwe na heshima.Tanzania ni nchi huru inayojitawala yenyewe na hamuwezi kuingia katika ardhi yake mkafanya kile mkitakacho.Lile lilikuwa ni onyo kwamba msithubutu kukanyaga ardhi ya Tanzania.” akasema Mathew ambaye alianza kupandwa na hasira akawatazama watu wale mle ndani akaendelea “Edger Kaka ambaye mlimteka na kumficha katika ubalozi wenu Nairobi ana mahusiano na magaidi wa kikundi cha IS ambao wamekuwa wakiendesha mashambulio katika ardhi yenu na kwa sasa wamejitanua zaidi katika nchi za Afrika.Walijenga mtandao mkubwa nchini kwetu wakateka na kuua watu.Miongoni mwa watu waliotekwa ni rafiki yangu Olivia pamoja na mtoto wa Rais wa wakati huo ambaye naamini hivi sasa atakuwa amekwisha maliza muda wake wa uongozi.IS waliwateka watu hao wakishinikiza kuachiwa huru kwa Edger Kaka ambaye waliamini anashikiliwa na serikali ya Tanzania.Tunao ushahidi wa kutosha kwamba mliingia ndani ya ardhi yetu mkaua na kuteka.Yawezekana mlifanya hivyo kwa lengo zuri la kutaka kupata taarifa za kuhusiana na kikundi cha IS lakini mlikosea kufanya jambo hili kimya kimya.Mlipaswa kuzitaarifu mamlaka husika nchini Tanzania juu ya Edger Kaka na kwa pamoja mngesaidiana katika kumdhibiti.Binafsi sijutii kwa kile nilichokifanya kwani nilifanya kwa ajili ya kuirejesha heshima ya nchi yangu na vile vile kuwakomboa watu waliotekwa na sintasita tena kufanya hivyo kila pale nchi yangu itakapochezewa na taifa lolote liwe kubwa au dogo” akasema Mathew kwa kujiamini na watu wote mle ndani walikuwa kimya wakimsikiliza. “Katika matukio haya yote mawili ya ninyi kumteka Edger na sisi kuvamia ubalozini kwenu na kumchukua Edger ,Yote yamefanyika katika harakati za kujaribu kupambana na kikundi cha IS.Adui yetu hapa sisi na ninyi ni mmoja ambaye ni IS.Mmenifunga gerezani kwa miaka mitatu mkinitesa kila uchao mkiniadhibu kwa kuvamia ubalozi wenu huku IS wakiendelea kushambulia na kuua watu wenu.Badala ya kuendelea kunitesa,mimi na ninyi kwa nini tusikae pamoja na kuweka mikakati ya kupamba na adui huyu mmoja tuliye naye? IS ni adui wa dunia nzima na si Israel peke yake hivyo kama mtakuwa tayari mimi na ninyi tunaweza kuunganisha nguvu na kupambana na IS” akasema Mathew na minong’ono ikasikika ndani ya kile chumba.Mathew akawaacha wajadiliane halafu baada ya muda Efraim akasema “Mathew Mulumbi umeongea kitu kikubwa sana na sisi tunakubaliana na mawazo yako.Tuyaweke pembeni hayo yote yaliyotokea na tuufungue ukurasa mpya sisi na wewe.Kama ulivyosema sisi na wewe wote adui yetu ni mmoja ambaye ni kikundi cha kigaidi cha IS.Tulimchukua Edger Kaka baada ya kubaini kwamba ana mahusiano na wafadhili wakuu wa kikundi hicho ambao ni Habiba Jawad na Sayid Omar.Kwa miaka mingi tumekuwa tukimtafuta Habiba Jawad na wenzake ambao wamekuwa wakifadhili vikundi mbali mbali vya kigaidi vinavyoendelea kufanya mauaji katika ardhi ya Israel.Siku chache zilizopita yamefanyika mashambulio ya kigaidi kutoka kwa IS na kuua watu zaidi ya thelthini wengi wakiwa ni watoto na wazee wasiojiweza.Kumekuwa pia na mashambulio mengine madogo madogo ya maroketi karibu kila siku na watu wanaendelea kupoteza maisha.Tunataka kulimaliza suala hili na kukomesha mauaji yanaoendelea hapa nchini.Tunataka kuuondoa mtandao wote wa kigaidi unaoendesha mashambulizi hayo” akasema Efraim na kunyamaza kidogo “Kuna mtu mmoja ambaye tumekuwa tunamtafuta kwa miaka mingi bila mafanikio Habiba Jawad.Tunahisi anafichwa na serikali ya Saudia ndiyo maana mpaka leo juhudi zetu zote za kumsaka zimegonga mwamba.Tunataka tuungane sisi na wewe kumsaka na kumpata Habiba Jawad na wenzake ambao wanaendeleza mauaji katika ardhi ya Israel.IS ni kitisho si kwa Israel pekee bali ni hata kwa nchi yenu na dunia nzima.Tunataka taarifa ambazo zinaweza kutusaidia kumpata Habiba Jawad na wenzake ambao ni wafadhili wakuu wa kikundi cha IS na vikundi vingine vya kigaidi” akasema Efraim na kunyamaza.Wote wakayaelekeza macho yao kwa Mathew. “Tunaamini unaweza kuwa na msaada mkubwa sana katika kutusaidia kulipiga vita kundi hili hatari.Habiba Jawad bado anaendelea kuwa ni mtu hatari sana kwa dunia kwani yeye ndiye uti wa mgongo wa mitandao hii ya kigaidi.Kama tukifanikiwa kumuondoa huyu mwanamama naamini ugaidi utakoma kama si kupungua kabisa duniani.Huyu mama ni tajiri mno na anautumia utajiri wake katika kufadhili ugaidi.Kama una chochote ambacho unadhani kinaweza kutusaidia kumpata Habiba tueleze tafadhali na sisi tutaona namna ya kukusaidia” akasema Efraim.Zilipita dakika mbili Mathew akiwa kimya akitafakari halafu akasema “Ninao uwezo wa kuwasaidia kumpata Habiba Jawad lakini nataka mimi na ninyi tuingie makubaliano” akasema Mathew “Nini unakihitaji kutoka kwetu Mathew?akauliza Efraim “Nataka kuwa huru” akasema Mathew na zikapita sekunde kadhaa za ukimya halafu Efraim akasema “Mathew Mulumbi tunaweza kufikiria ombi lako endapo taarifa utakazotupa zinaweza kuwa na msaada kwetu hivyo kama unazo taarifa zozote tupe tuzichambue tuzifanyie kazi tuone kama zinaweza kutufaa halafu tutaona namna ya kukusaidia” akasema Efraim “Ngoja niwaambie jambo ninyi mnaojiita taifa teule.Hamtafanikiwa katika vita hii kutokana na viburi mlivyonavyo kujiona ninyi ni bora zaidi kuliko wengine.Hamuonyeshi kama mna nia ya dhati ya kutaka kumpata Habiba Jawad na kukomesha mauaji yanayoendelea katika ardhi yenu.Kama mngekuwa na nia ya dhati ya kumtafuta Habiba msingejiuliza mara mbili kuhusu ombi langu la kutaka kuachiwa huru pale nitakapowasaidia kumpata au kumuondoa kabisa Habiba Jawad na wenzake.Nawaambia ukweli kwa sasa Habiba amewabana kwenye kona na mimi ndiye pekee ninayeweza kusaidia kumpata.Ni uamuzi wenu kama mnataka kumaliza ugaidi na mauaji katika nchi yenu kwa kunipa uhuru wangu au kuendelea kuniweka hapa na kunitesa huku mauaji yakiendelea kila uchao” akasema Mathew.Efraim akaelekeza Mathew atolewe nje kwa dakika kadhaa wakabaki wao wakijadiliana “Nimewabana vizuri.Wana shida na Habiba Jawad hivyo hawana ujanja wa kukataa.Lazima wataniachia huru pale nitakapokuwa nimefanikisha kazi yao.Hata mimi ninamtafuta sana Habiba Jawad.Huyu kama bado yuko hai ataendelea kufadhili makundi mbalimbali ya magaidi na nina uhakika mkubwa lazima watarejea tena Tanzania na kutengeneza mtandao wao.Hii ni nafasi nimeipata ya kuweza kummaliza na kumaliza kabisa nguvu ya kikundi cha IS” akawaza Mathew na mlinzi aliyekuwa akimlinda akapewa maelekezo ya kumrejesha Mathew ndani. “Mathew tumefanya majadiliano mafupi tukiwashirikisha pia viongozi wetu wa ngazi za juu na wamekubali ombi lako lakini endapo utatupa taarifa zitakazosaidia kumpata Habiba Jawad.” “Ninataka uthibitisho wa barua iliyosainiwa na waziri mkuu kwa sababu naweza kuwapa taarifa za kuwasaidia halafu mkaniua au kunirejesha gerezani” akasema Mathew “Mathew nasikitika kwamba hicho unachokitaka hakitawezekana” “Basi hamna nia ya dhati ya kuniachia huru mlikuwa mnanidanganya.Naombeni mnirejeshe gerezani nikaendelee kuteseka” akasema Mathew “Mathew unaitupa nafasi pekee ambayo inaweza kukusaidia.Hakutakuwa na nafasi nyingine kama hii uliyoipata” “Sihitaji nafasi nyingine.Naombeni mnirejeshe kule gerezani mnakonifunga kwenye giza nikaendelee na maisha ya kule” akasema Mathew na kuufumba mdomo wake.Kila alichoulizwa hakujibu.Efraim akaelekeza Mathew arejeshwe katika kile chumba kizuri. “Hawana ujanja lazima watarudi kwangu.Kwa sasa mimi ndiye tegemeo lao katika kumpata Habiba Jawad” akawaza Mathew wakati akirejeshwa katika chumba kile kizuri “Hawanirejeshi tena kule katika gereza kule walikonifunga kwa miaka mitatu hii ni ishara kwamba wananihitaji.Ninauona mwanga wa mimi kuondoka hapa japo njia nitakayopita inaonekana itakuwa na mawe na miiba mingi lakini mwisho wa siku nitafanikiwa kuondoka hapa na kurudi nyumbani” akawaza na kujilaza katika kitanda kile kikubwa “Katika maisha yangu ndani ya kazi hii ya ujasusi sijwahi kukutana na wakati mgumu kama huu.Nimepitia mateso ambayo sijawahi kupitia lakini nimevumilia na sikuwahi kuwasaliti wenzangu nilioshirikiana nao katika operesheni ile.Kinachonishangaza Mossad wanazo taarifa zote kuhusiana na kila nilichokifanya.Lazima yupo mtu ambaye aliwapa taarifa hizi.Bado akili yangu inanituma lazima atakuwa ni mtu wangu wa karibu na bado jina la Devotha linakuja kichwani kwangu kila ninapowaza kuhusu usaliti huu mkubwa niliofanyiwa.Kama kweli ni yeye atakuwa amefanya jambo baya sana kwani jambo nililolifanya ni kwa manufaa ya taifa.Halafu Rais Dr Evans licha ya kuyaweka maisha yangu hatarini kumuokoa mwanae kwa nini hakufanya juhudi zozote kunitafuta na kujua mahala nilipo?Na yeye anaamini nimefariki dunia?Vipi kuhusu watu wangu Gosu Gosu na Austin?Wako wapi?Nao wanaamini nimefariki? Dah ! niko mwenyewe.Sina msaada wowote.Msaada pekee ni Mungu wangu ambaye siachi kumuomba kila siku aniangazie njia niweze kutoka katika mateso haya.Endapo nikifanikiwa kutoka hapa salama nataka nitulie na familia yangu. Peniela tayari ana mahusiano na mtu mwingine akiamini tayari nimekufa.I’ll be back my love.Kwa sababu yako nitafanya kila ninaloweza ili kutoka hapa” akaendelea kuwaza na kutokana na uchovu aliokuwa nao taratibu akaanza kusinzia Mathew alistuliwa kutoka katika usingizi mzito na mtu aliyekuwa akimtikisa akafumbua macho na kujikuta akitazamana na watu saba. “Mathew Mulumbi amka tafadhali” akasema Efraim “Mnanirejesha gerezani?akauliza Mathew “Hapana hatukurejeshi gerezani” akasema Efraim na kumtaka Mathew waketi sofani.Akaufungua mkoba wake na kutoa karatasi akampa Mathew aisome “Hiki nini?akauliza Mathew “Hiyo ni hati ya makubaliano iliyosainiwa na waziri mkuu wa Israel.Tutakuachia huru pale utakapotupa taarifa kuhusiana na Habiba Jawad” akasema Efraim.Mathew akaipitia hati ile kwa makini na kutabasamu “Mathew hakuna kupoteza muda tuanze sasa hivi.Tunahitaji kuzipata taarifa hizo haraka” akasema Efraim “Yuko wapi Edger kaka?akauliza Mathew “Wa nini Edger Kaka? Akauliza Efraim “Ninahitaji kuzungumza naye.Hafahamu mahala alipo Habiba lakini anaweza akatusaidia kutupa mawasiliano yake na tukajua mahala alipo Habiba” “Kuna tatizo lilitokea wakati wa kumchukua Edger Kaka kule Nairobi.Kwa bahati mbaya usiku ule Edger alianguka katika jiwe na kugongesha kichwa akapoteza fahamu na mpaka leo hii hajaamka.Kwa mujibu wa daktari ni kwamba ubongo wake umekufa na hataweza kuamka tena.Kinachomfanya aonekane kuwa hai mpaka leo hii ni mashine lakini kiuhalisia Edger amekwisha fariki dunia hivyo tupe taarifa nyingine ambazo hazitamuhitaji Edger” akasema Efraim na Mathew akazama mawazoni kwa muda kisha akasema “Sasa naombeni mnisikilize.Nilitegemea kupata taarifa kutoka kwa Edger lakini kwa kuwa hayupo tena tutafanya vile nitakavyoelekeza mimi” akasema Mathew “Mathew haikuwa rahisi kuweza kupata sahihi ya waziri mkuu katika suala hili hivyo tunachokihitaji ni taarifa na si vinginevyo” akasema Efraim “Mnalo gereza ambalo mnawahifadhi watu wanaohusika na makosa ya ugaidi hapa Israel” “Ndiyo.Kituo 1391 ndilo gereza la siri ambako wote wanaohusika na mitandao ya kigaidi au mauaji ndani ya Israel hufungwa” akajibu Efraim “Vizuri.Nataka nipelekwe huko na niwekwe chumba kimoja na mmoja kati ya magaidi hatari kabisa mnaowashikilia katika gereza hilo kutoka katika moja ya kikundi cha wanamgambo wanaoendesha mapambano dhidi ya Israel” akasema Mathew na kumstua Efraim “Hizo si taarifa tunazozitafuta” akasema Efraim “Nisikilize tafadhali.Huu ni mpango ambao utanifikisha kwa Habiba Jawad.Kwa sasa sina taarifa zozote kuhusu mahala alipo kwani nilimtegemea Edger Kaka lakini kwa kupitia mpango huu ninaokueleza ninaamini nitafahamu alipo au kumfikia Habiba Jawad.Nitalazimika kuungana na kufanya kazi na magaidi ili waweze kujenga imani kwangu na wakati huo nikiendelea kuusoma mtandao wao na kufahamu alipo Habiba Jawad” “Hapana Mathew huu ni mpango wa hatari sana ambao siwezi kuruhusu ukaufanya.Wakifahamu wewe si mwenzao lazima watakuua na tutakua tumerudi nyuma sana” akasema Efraim “Nalifahamu hilo Efraim lakini hakuna njia nyingine ya kuweza kumpata Habiba Jawad zaidi ya hii ninayokueleza.Niwekeni chumba kimoja na huyo gaidi nitajenga urafiki naye na kumfanya aniamini halafu tutafanya mpango wa kutoroka hapo gerezani na huo utakuwa ni mwanzo wa mimi kushirikiana na magaidi hao na itakuwa ni njia ya kuelekea kwa Habiba Jawad” “Mathew siwezi kutoa jibu lolote kuhusiana na mpango huu kwa sasa.Nitahitaji kuzungumza na viongozi wangu wakuu juu ya mpango huu na wao watatoa maelekezo” akasema Efraim na kuondoka “Nimeamua kufanya jambo la hatari sana lakini ndiyo njia pekee ya kuweza kumfikia au kufahamu mahala alipo Habiba Jawad na wale wote wanaofadhili ugaidi.Kama serikali ya Saudi wanachangia kumficha basi njia pekee ya kumfikia ni kujiunga na magaidi.Ni maamuzi magumu sana haya lakini lazima niyafanye ili niweze kuwa huru.Hakuna namna nitakavyoweza kutoka katika mikono ya Mossad kama sintatumia njia hii.Pili nahitaji sana kummaliza Habiba Jawad ambaye ufadhili wake unalifanya kundi la kigaidi la IS kujitanua na kusambaa sehemu mbali mbali duniani.Tukifanikiwa kumuondoa huyu tutakuwa tumefanikiwa kuupunguza nguvu ugaidi.Shughuli za kigaidi zitakosa nguvu baada ya kukosa fedha” akawaza Mathew “Hatari ya mpango huu kwanza haitakuwa rahisi kwao kuniamini lazima nitapitia wakati mgumu sana hadi waniamini na pili ni pale watakaponigundua kwamba ni pandikizi ninawachunguza.Adhabu yake ni kifo.Pamoja na hatari hiyo iliyopo lakini lazima nitumie njia hii ya kujiunga na magaidi.Mungu atasimama nami” akaendelea kuwaza na haukupita muda akalala. PARIS – UFARANSA “Nimehakikishiwa na serikali ya Tanzania kwamba wale wote waliofanya mauaji haya hakuna atakayebaki salama.Waliuawa watu watano siku ya tukio na wengine bado wanaendelea kusakwa.Tumeumizwa na msiba huu mkubwa lakini ninawaomba tuwe na subira wakati vyombo vyetu vikiendelea kulifanyia kazi suala hili na ninawahakikishia kwamba wale wote waliofanya mauaji haya watapatikana. Sipati maneno mazuri ya kumuelezea Lucy Muganza lakini alikuwa ni mwanamke shupavu na jasiri mwenye maono makubwa na zaidi sana aliyeipenda mno nchi yake ya Congo” Haya ni baadhi ya maneno yaliyokuwamo katika hotuba ya Rais Patrice Eyenga wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo aliyoitoa katika hotuba yake wakati wa mazishi ya Lucy na mumewe Laurent Muganza waliouawa nchini Tanzania.Maelfu na maelfu ya wananchi wa Congo na wafuasi wa chama cha CDP walihudhuria mazishi hayo. Wakati mazishi ya Lucy na mumewe Laurent Muganza yakifanyika nchini Congo,binti yao Theresia ambaye alinusurika katika shambulio lile alikuwa nchini Ufaransa katika hospitali moja kubwa alikohamishiwa baada ya kutolewa Tanzania. Tayari alikwisha fahamu kuwa wazazi wake walifariki dunia lakini hakuruhusiwa kuhudhuria au kutazama mazishi hayo kutokana na afya yake kuwa dhaifu. Katika chumba cha mikutano ndani ya makazi ya Rais wa Ufaransa,Rais Michael Weren alikuwa katika kikao na jopo la madaktari kumi na mbili mabingwa wa upasuaji wakiongozwa na Dr Alex McKnees bingwa wa upasuaji wa plastiki kutoka New York Marekani.Kilichowakutanish a hapa ni kujadiliana kuhusu upasuaji mkubwa wanaotarajia kuufanya “Ahsanteni sana kwa kufika natumai timu nzima ninayoihitaji kwa ajili ya kazi yangu imetimia.Kikubwa nilichowaitia hapa kuna upasuaji mkubwa ambao ninataka muufanye.Kuna binti ambaye nataka afanyiwe upasuaji na kubadili kabisa muonekano wake” akasema Rais Weren na kuwasha runinga kubwa iliyokuwa nyuma yake na picha za Theresia Muganza zikaanza kuonekana “Anaitwa Theresia Muganza.Ni msomi wa chuo kikuu.Huyu ni mtoto wa mabilionea Lucy na Laurent Muganza ambao waliuawa nchini Tanzania katika shambulio siku chache zilizopita na leo hii wanazikwa nchini Congo.Tunaamini watu waliowaua wazazi wake wataendelea kumsaka hadi wahakikishe wamempata na kumuua kwani lengo lao lilikuwa ni kuwaua familia nzima.Ili kumlinda na hatari hiyo nataka afanyiwe upasuaji wa kubadili mwonekano wake.Ninyi ni mabingwa wa upasuaji huo mnajua nini cha kufanya lakini ninachohitaji mimi baada ya bandeji kuondolewa mwilini mwake Theresia anatakiwa awe ni mtu mpya.Nataka mumtengeneze awe na uzuri wa kipekee.Awe ni mwanamke ambaye ataitikisa dunia kwa uzuri atakaokuwa nao.Sitaki kuwafundisha kazi yenu kwani mnajua kila kitu lakini kwa ujumla nataka mnitengenezee malaika ambaye kila apitapo mtaani watu wageuze shingo zao kumtazama.Naamini mmenielewa” akasema Rais Weren wakaendelea na majadiliano na madaktari wale kisha wakaomba siku mbili wakalijadili suala lile na namna watakavyofanya upasuaji ule mkubwa. TEL AVIV – ISRAEL Mathew Mulumbi alishinda ndani ya chumba alichohamishiwa akiwa chini ya ulinzi mkali sana.Hakuruhusiwa kutoka au hata kufungua pazia kuchungulia nje.Muda wote ndani ya chumba kulikuwa na walinzi wenye silaha na alikuwa amefungwa mkono mmoja kwa pingu iliyounganishwa na mnyororo mrefu na kufungwa katika chuma kizito. Saa kumi na moja za jioni waliingia watu wanne ndani ya kile chumba wakamfungua Mathew pingu na kumvisha mfuko mweusi kichwani wakamtoa ndani ya kile chumba wakamuingiza ndani ya gari na kuondoka.Mathew hakujua anapelekwa wapi.Baada ya dakika ishirini gari lile likasimama mlango ukafunguliwa Mathew akashushwa na kuingizwa katika lifti baada ya muda mfupi mlango ukafunguka wakatoka ndani ya lifti wakatembea kidogo wakasimama kwa sekunde chache mlango ukafunguliwa wakaingia ndani ya chumba.Mathew hakuweza kuona kilichokuwa kinaendelea.Alikalishwa katika kiti akafunguliwa pingu za mikono na mfuko uliokuwa kichwani ukatolewa.Alijikuta katika ofisi nzuri na mbele yake kulikuwa na watu watano.Mtu aliyweza kumtambua katika wale watano ni Efraim Dagan ambaye walionana usiku uliopita. “Mathew Mulumbi karibu.Tumekutana tena mimi na wewe lakini naomba nikutambulishe wenzangu ambao niko nao hapa” akasema Efraim na kuwatambulisha watu wale walikuwemo mle ndani na wa mwisho kutambulishwa alikuwa ni Moshe Levine mkurugenzi wa Mossad. “Kufuatia mazungumzo yetu ya jana” akaendelea Efraim “Tumekuwa na mazungumzo marefu sana mimi na wenzangu tangu asubuhi kujadili wazo lako.Tumemaliza majadiliano muda mfupi uliopita tumeona tukuite hapa tuje kuzungumza nawe” akasema Efraim “Mathew Mulumbi” akasema Moshe mkurugenzi wa Mossad “Efraim alifikisha kwangu wazo lako jana usiku na tukalazimika kukutana kulijadili.Ninataka kujua kwa nini unataka kufanya hivi ulivyoshauri kujiunga na magaidi?akauliza Moshe “Mkurugenzi kama nilivyomwambia Efraim kwamba sisi sote adui yetu ni mmoja ambaye ni IS.Mambo yote yaliyotokea na kupelekea mimi kuwa hapa ni kwa sababu ya mapambano dhidi ya IS.Kikundi hiki ni tishio si kwa Israel pekee bali hata nchini kwangu tayari tumeonja athari za ugaidi hivyo ninataka kusaidiana nanyi kulimaliza kundi hili hatari kama si kulimaliza nguvu kwa kumuondoa Habiba Jawad.Nilitegemea kumtumia Edger Kaka lakini baada ya kutaarifiwa kwamba Edger hataweza kuamka tena ndipo nilipoamua kutumia mbinu hii ya kujiunga na magaidi”akasema Mathew “Mathew Mulumbi mbinu hii ni hatari na inaweza ikakuletea matatizo makubwa” akasema Moshe “Nalifahamu hilo mkurugenzi lakini hatuna namna nyingine kwa sasa ya kumfikia Habiba Jawad bali kwa mbinu hii.Alinieleza Efraim kwamba mmemtafuta Habiba kwa miaka mingi bila mafanikio na kuna hisia kwamba anafichwa na serikali ya Saudia hivyo basi kumpata mtu kama huyu ni vigumu sana.Ninafahamu haitakuwa rahisi kuwafanya magaidi hao waniamini nitapitia nyakati ngumu sana lakini nina uhakika mkubwa kwamba nitafaulu kujenga imani kwao na nitafanikiwa kujua mahala alipo Habiba Jawad.Ikitokea nikagundulika na kuuawa nitakuwa nimekufa nikijaribu lakini nakuahidi kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha ninakamilisha misheni yangu” akasema Mathew “Mathew ninafurahishwa sana na ujasiri wako.Unachotaka kukifanya ni kitu cha hatari mno ambacho sintaweza kumruhusu mtu wangu akakifanya kwani ni kuhatarisha uhai” “Mimi si mmoja wa watu wako hivyo hata ikitokea nikapoteza maisha hakuna hasara yoyote mtakayoipata”akasisitiza Mathew “Kwa nini unasisitiza sana kutaka kutumia mbinu hii ya kujiunga na magaidi?akauliza Moshe “Wakati nikipambana kuokoa watu aliokuwa wametekwa na kundi la IS wakishinikiza kuachiwa kwa Edger Kaka,niligundua kwamba tayari walikuwa na mtandao mkubwa na walikwisha otesha mizizi hadi katika ngazi za juu za uongozi wa nchi yetu kwani aliyekuwa waziri mkuu wa wakati ule alikuwa ni mmoja wa waliokuwa katika mtandano wao na walikuwa wanamuandaa aje kuwa rais.Karibu nusu ya mtandao mkubwa wa IS uliokuwa nchini Tanzania tulifanikiwa kuutambua na kuwakamata wahusika lakini sikufanikiwa kufika mwisho wa sakata lile na kujua hitimisho lake lakini hatua kubwa ilikuwa imepigwa.Mafanikio yale yalikuwa ya muda tu ili kulimaliza kabisa tatizo la ugaidi ni kuukata kabisa mzizi ambao ni Habiba Jawad na wenzake wanaotumia utajiri wao kufadhili ugaidi.Ninasisitiza kutaka kutumia mbinu hii ya hatari kwani kama tukifanikiwa kumuondoa Habiba Jawad na wenzake wafadhili wakuu wa ugaidi tutakuwa tumesaidia si Israel pekee bali hata nchi za Afrika ambako magaidi wameanza kuotesha mizizi yao.Jambo lingine ambali linanilazimu kutaka kutumia mbinu hii ya kujiunga na magaidi ninataka kwenda nyumbani kama nikifanikiwa kumaliza salama” akasema Mathew “Mathew kama alivyokueleza Efraim kwamba tunamuhitaji sana Habiba Jawad.Kwa muda mrefu tumekuwa tukimsaka bila mafanikio.Tunaamini tukifanikiwa kumpata au kumuua Habiba basi kundi la IS na vikundi vingine vinavyofanya mashambulio ya maroketi na kujitoa mhanga vitaishiwa nguvu na kufa kabisa.Kwa hiyo basi sisi tunataka kushirikiana nawe kwa kutumia njia hiyo uliyoipendekeza lakini huu utakuwa ni mpango wa siri sana kwani tunaamini hata hapa Israel Habiba anao watu wake wanaomsaidia kwani aliwahi kuingia hapa Israel bila kujulikana.Tunataka tukulinde ili usiweze kugundulika ndiyo maana ninasema kwamba operesheni hiyo utakayoifanya iwe ya kimya kimya na tutakaofahamu ni sisi watu wachache pekee.Usishangae kusikia kwamba hata ndani ya Mossad wapo watu ambao wanashirikiana na Habiba Jawad” akasema Moshe na kumuachia Efraim aendelee “Tutakuwekea mwilini kifaa maalum ambacho kitatuwezesha sisi kukufuatilia kila mahala utakapokuwa na kufahamu kama uko mzima.Kila mahala utakapokuwa unakwenda kutakuwa na kikosi cha majasusi wakikufuata kwa kutumia kifaa hicho utakachowekewa mwilini.Tutakupa kifa kingine kidogo cha mawasiliano kitakacho……” “Hakuna haja” akasema Mathew na kumkatisha Efraim “Hawa jamaa ni watu waliojipanga vizuri.Wanazifahamu mbinu zote za ujasusi.Naamini watanichunguza na wakinikuta na kifaa chochote ambacho kitaniunganisha mimi na ninyi nitakuwa nimenunua kifo change,wataniua.Sihitaji kwenda nikiwa na kifaa chochote” akasema Mathew “Mathew lazima tufuatilie kila utakachokuwa unakifanya huko mahala utakapokuwa unakwenda.Tunapaswa kuwa na mawasiliano kati yetu na wewe.Ni sisi tunaopaswa kukulinda na kuhakikisha unakuwa salama.Hivyo basi lazima uwe na kifaa ambacho kitatuwezesha sisi kukufuatilia” akasema Moshe “Sihitaji kifaa chochote”akasisitiza Mathew “Tutawasiliana vipi nawe bila kuwa na kifaa cha mawasiliano?akauliza Moshe “Naombeni mniamini.Ninajua ninachokwenda kukifanya.Nitajua namna ya kuwasiliana nanyi nikiwa huko.Ninachokitaka kutoka kwenu ni kuniunganisha na magaidi halafu kitakachoendelea huko nitajua mimi lakini nawahakikishia kwamba nitatafuta kila namna ya kuweza kuwasiliana nanyi na kuwajulisha kila hatua nitakayokuwa ninapiga”akasema Mathew “Mathew Mulumbi natamani niseme hapana lakini kwa vile umesisitiza basi tutafanya unavyotaka ingawa matumaini kama utaweza kumfikia Habiba Jawad au kufahamu mahali alipo ni madogo sana.Hata hivyo ninatoa ruhusa kwa mpango huu uendelee” akasema Moshe na Efraim akasimama akasogea mbele kulikokuwa na runinga akaiwasha na katika runinga akaonekana mtu mmoja mwenye macho ya kikatili “Huyu anaitwa Ammar Al Nazari.Huyu ni kiongozi wa kikundi kimoja cha wanamgambo kinachoitwa Ammar Nazari Brigades kinachoendesha mapambano dhidi ya Israel na chenye mahusiano ya karibu na IS.Habiba Jawad ni mfadhili wa kikundi hiki pia.Ammar Nazari brigades wanahusika katika kufanya mashambulizi kadhaa nchini Israel yaliyoua watu wengi.Mpaka sasa idadi ya watu wanaotajwa kuuawa na mashambulio ya kikundi hiki inakaribia mia moja ishirini na nane.Tunataka ujenge mahusiano na huyu mtu na kupitia huyu utaweza kupata taarifa zote kuhusiana na Habiba Jawad” akasema Efraim na Mathew akayaelekeza macho yake runingani akimtazama Yule jamaa Ammar Nazari mwenye macho yaliyojaa ukatili. “Ili mpango wetu ukamilike lazima Ammar atoke gerezani na utokaji wenyewe unapaswa kuwa wa kutumia nguvu yaani kutoroka” akasema Mathew “Ammar ni mtu ambaye tulifanya kazi kubwa kumtafuta hadi kumpata.Toka alipokamatwa kundi lake limefifia na kukosa nguvu japo bado wanaendelea na mashambulizi ila kwa kiasi kidogo tofauti na wakati ule kabla hatujamkamata.Kumuachia mtu kama huyu ni jambo linaloumiza sana” akasema Moshe “Hakuna ujanja mkurugenzi lazima mtu huyu aachiwe kwani kutoka kwake kutakuwa na faida kubwa zaidi kuliko kuendelea kukaa ndani” akasema Mathew “Unadhani itachukua muda gani kwa wewe kujenga mahusiano na Ammar?akauliza Efraim “Simjui mtu huyu,sijawahi kukutana naye lakini naamini ndani ya siku nne au tano nitaweza kujenga mahusiano naye.Mpango utakuwa hivi nitapigwa hadi nipoteze fahamu kisha nitapelekwa katika chumba alimo Ammar na kutupiwa humo.Akiniona na majeraha niliyonayo atatamani kujua mimi ni nani.Nitagoma kuzungumza naye na nitagoma kula kwa siku mbili na hali hiyo lazima itamtisha na ataamua kutoa taarifa kwa askari wa gereza nitatolewa ndani ya kile chumba na kwenda kutibiwa halafu baadae nitarejeshwa tena na safari hii nitakuwa na kisu kidogo.Naamini huo utakuwa ni mwanzo wangu mimi na yeye kuwa marafiki” akasema Mathew “Mipango yako Mathew Mulumbi inaonekana ni mizuri lakini ya hatari kubwa sana.Ni vipi kama Ammar hatanasa katika mtego wako?akauliza Moshe “Niamini mkurugenzi nina uhakika mkubwa lazima atanasa.Ninawafahamu magaidi” akasema Mathew “Wakati unaendelea kujenga urafiki na Ammar sisi tutakuwa tunaandaa mpango wa wewe kutoroka na pale utakapotolewa chumbani kupeleka katika hospitali ya gereza utaelezwa kila kitu namna mpango huo utakavyokuwa.Kitu cha msingi jitahidi sana kuhakikisha anakuwa karibu yako” akasema Efraim “Nina uhakika nitafanikiwa.Ninachowasisiti za katika mpango huo mtakaouandaa wa kutoroka hakikisheni uwe ni mpango unaoonekana kweli tumetoroka.Ikiwezekana katika mpango huo Ammar apigwe risasi sehemu kama vile kwenye mguu au mkononi ili aone mpango huo wa kutoroka ni wa kweli.Vile vile nitaomba Edger Kaka asiondolewe katika mashine zinazomuweka hai kwani nitamtumia pia katika kutafuta njia ya kufika kwa Habiba Jawad” “Edger Kaka hana msaada wowote kama nilivyokueleza.Amekwisha fariki na kinachomuweka hai mpaka sasa ni mashine”akasema Efraim “Ninalifahamu hilo lakini ninashauri msiondoe mashine hizo kwa sasa yawezekana tukamtumia pia.Inaweza ikawa ni njia moja wapo ya kuniweka karibu zaidi na Habiba Jawad pale nitakapofanikiwa kuonana naye” akasema Mathew na majadiliano yakaendelea kuhusiana na mpango ule. “Mathew tumekuwa na majadiliano mazuri kuhusu mpango huu hivyo kinachofuata sasa ni utekelezaji.Ninachosisitiza ni usiri wa mpango huu.Mtandao wa Habiba ni mkubwa na nina uhakika hata ndani ya Mossad anao watu wake hivyo usiri unatakiwa sana katika mpango huu.Mimi na wenzangu hawa tutaendelea kufuatilia kwa karibu zaidi mpango huu lakini hakikisha siku zote unajitahidi kuwa salama na kujitahidi kwa kila namna kufanya mawasiliano nasi ili tujue mahala ulipo na kama utahitaji msaada wowote.Kumbuka operesheni hii ni muhimu si kwa Israel pekee bali hata kwa nchi yako na dunia kwa ujumla.Endapo ukiifanikisha vyema makubaliano yetu yanabaki vile vile utakuwa huru lakini usijaribu kufanya kitu chochote cha kijinga cha kutaka kutoroka kwani hautafika mbali kabla hatujakutia mikononi.Ninakutakia kila la heri”akasema Moshe “Usiwe na hofu kuhusu mimi kwamba ninaweza kutoroka.Nimeamua kwa hiyari yangu kufanya jambo hili na ninafahamu manufaa yake ni makubwa kwenu na kwetu pia” akasema Mathew na kisha akaongozana na Efraim kutoka ndani ya ile ofisi. PARIS – UFARANSA Hali ya Theresa muganza iliendelea vizuri.Ulinzi ulikuwa mkali sana katika wodi alimolazwa. Saa tatu za usiku akiwa amelala kitandani huku pembeni yake akiwepo muuguzi mlango ukafunguliwa wakaingia watu wanne na nyuma yao akatokea mtu ambaye Theresa alizoea kumuona katika runinga na taarifa mbali mbali za habari za kimataifa,Rais wa Ufaransa Michael Weren akiwa ameongozana na madaktari.Daktari akatoa maelezo kuhusu maendeleo mazuri ya mgonjwa na Rais Weren akawataka watu wote mle ndani watoke akabaki na Theresa.Akavuta kiti akamsogelea Theresa kitandani ambaye aliinuka na kukaa. “Theresa pole sana” akasema Weren “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akajibu Theresa na Rais Weren akatabasamu “Kumbe unanifahamu mimi ni nani” “Hakuna asiyekufahamu wewe ni nani mheshimiwa Rais” akajibu Theresa “Vipi unajisikiaje? “Hali yangu inaendelea vizuri.Nashukuru sana kwa kunileta huku na kuokoa maisha yangu.Ninapata huduma nzuri sana na sasa sijambo.Ninapata nafuu kubwa kila uchao.Ninakushukuru sana wewe binafsi mheshimiwa Rais kwa jitihada zako kuhakikisha ninahamishiwa huku na kupatiwa huduma nzuri.Sina hakika kama ningeendelea kubaki kule Afrika kama ningekuwa ninazungumza nawe muda huu” akasema Theresa na kuanza kumwaga machozi.Rais Weren akatoa kitambaa na kumpatia afute machozi “Pole sana Theresa.Tukio lile ni baya na la kinyama sana lakini nakuomba uwe na ujasiri.Huu si wakati wa kuendelea kumwaga machozi.Wazazi wako wamekufa kishujaa na watu mashujaa hatuwaenzi kwa kulia bali kwa kuendelea yale waliyoyapigania.Mama yako alikuwa mstari wa mbele kupigania usawa na mgawanyo sahihi wa rasilimali za taifa la Congo ndiyo maana akaamua kugombea urais ili ahakikishe rasilimali zinawanufaisha watu wote.Najua bado unaumwa na sitaki kukuongezea maumivu lakini lazima ufahamu kwamba kifo cha mama yako kinahusiana na yeye kutaka kuwania urais wa Congo.Haya ni mauaji ya kisiasa na si ujambazi kama inavyodaiwa” akasema Rais Michael Weren na Theresia akafuta machozi “Tumefanya uchunguzi wa risasi ambazo zilikuwa katika miili ya marehemu ni risasi za bunduki za hali ya juu sana ambazo hutumiwa na wadunguaji.Bunduki kama hizo hutumiwa na vikosi vya majeshi na si rahisi kwa mtu wa kawaida kuwa nayo.Kama kweli majambazi hao kama inavyodaiwa walikuwa na hiyo silaha basi walipewa na serikali ili watekeleze mpango huo wa mauaji”akasema Rais Michael “Masikini mama yangu niliwahi kumuonya kuhusu mpango wake wa kutaka kugombea urais lakini akanitaka nisiwe na hofu.Kwa nini lakini hakutaka kunisikia na sasa ameniacha yatima? Akasema Theresa akiendelea kumwaga machozi “Mama yako Lucy Muganza alikuwa na malengo makubwa sana kuhusu Congo na alitaka kuifikisha mbali kiuchumi.Mimi binafsi na baadhi ya maraisi wa nchi kubwa tulimuunga mkono baada ya kuyaona mawazo yake yanahitajika sana kwa wakati huu.Hivi sasa amani inayodaiwa iko nchini Congo ni amani bandia.Wakuu wa serikali na waliokuwa viongozi wa waasi wamewekeana mikataba ya kupeana utajiri.Wanaendelea kuinyonya Congo.Ni watu wachache wanaoendelea kufaidika na rasilimali za Congo huku wananchi wengi wakiendelea kuogelea katika umasikini mkubwa.Haya ndiyo mambo ambayo Lucy Muganza alikuwa anayapinga kwa nguvu zake zote hadi akaamua kugombea urais ili aweze kuikomesha dhuluma hii kubwa kwa watu wa Congo lakini kwa bahati mbaya hakuyweza kutimiza lengo lake wakawahi kuondoa uhai wake” akasema Rais Michael.Theresa akafuta machozi na kuuliza “Serikali ya Congo wanahusika katika mauaji ya wazazi wangu? Rais Michael hakujibu kwa haraka swali lile akainuka na kwenda kutazama mojawapo ya mashine iliyokuwepo mle chumbani halafu akarejea kitini akaketi na kusema “Hatuna uhakika bado nani wameshiriki katika mauaji yale tunaendelea na uchnguzi lakini kwa namna yoyote ile itakavyokuwa lazima serikali ya Congo itakuwa na mkono wake.Si serikali ya Congo peke yake bali tunahisi hata nchi nyingine za afrika mashariki kama Tanzania watakuwa wameshiriki katika mpango huu wa mauaji ya wazazi wako”akasema Rais Michael “Mheshimiwa Rais ninaomba hawa wote waliohusika na mauaji ya wazazi wangu wasakwe na waadhibiwe vikali.Mauaji ya namna ila hayakubaliki ni mauaji ya kinyama mno” akasema Theresa “Theresa kama nilivyokueleza kwamba tunaendelea na uchunguzi wa kuwabaini waliofanya tukio lile lakini naomba ufahamu kwamba watu waliotekeleza mauaji yale ni wataalamu na walijipanga vyema.Walijua fika Lucy ni mtu mkubwa na lazima uchunguzi wa kina utafanyika baada ya kumuua hivyo wakajitahidi kutokuacha kitu chochote cha kuweza kuwatambulisha.Uchunguzi huo unaweza ukachukua miaka na kuna uwezekano tusimpate muuaji ni nani kwani kwa namna tukio lile lilivyotengenezwa ni mfumo wa matukio yale ambvayo yanakosa majibu na hubaki yakielea.Majambazi wanaodaiwa kumuua Lucy wote wameuawa na hakuna tena mtu wa kumuhoji.Limebaki ni fumbo.Kosa kubwa walilolifanya ni kukosea kukupiga risasi na ukanusurika” “Nimepona kwa huruma ya Mungu.Kuna wakati ninaona ni bora ningekufa mimi na wazazi wangu wangu wabaki hai waendelee kuipigania nchi yangu isiendelee kunyonywa” akasema Theresa na kuanza tena kulia “Usilie Theresa kwani bado hakijaharibika kitu.Utakwenda kuifanya kazi ambayo mama yao alikusudia kuifanya” “Siasa?! Akauliza Theresa kwa mshangao kidogo “Theresa jukumu lako kubwa ni kuvaa viatu vya mama yako na kuendeleza kazi aliyoianzisha kuhakikisha utajiri wa Congo unawanufaisha watu masikini” akasema Rais Weren na kunyamaza akamtazama Theresa “Unamaanisha nini mheshimiwa Rais?akauliza Theresa akionekana kuwa na wasi wasi mwingi “Tunakuandaa kuwa Rais wa Congo” akasema Rais Weren na mstuko mkubwa ukaonekana usoni kwa Theresa “Mimi ?! Rais? Theresia akauliza “Ndiyo Theresa.Tunakuandaa ili uje ushike madaraka ya urais uendeleze maono ya mama yako.Usihofu si sasa hivi bali tutakujenga kwanza na kukuandaa kushika nafasi hiyo na muda wako ukifika basi tutakuingiza madarakani.Hata mama yako tulianza kwanza kwa kumuandaa na alipokuwa tayari ndipo akatangaza kuwania urais lakini hawa watu wamezima ndoto zake.Nilisema kwamba walikosea sana kukuacha hai kwani utakwenda kutimiza ndoto zote za mama yako” akasema Rais Weren “Mheshimiwa Rais sina hakika kama ninahitaji nafasi hiyo kubwa.Siipendi siasa kwani imesababisha nikabaki yatima wazazi wangu wote wameuawa kwa sababu ya chuki za kisiasa” akasema Theresa “Usihofu Theresa.Sisi tupo tutakuongoza na kukusimamia.Tutakulinda dhidi ya hatari yoyote” “Katika kauli zako unazungumza uwingi.Wewe na nani mlikuwa nyuma ya mama yangu?akauliza Theresa “Tuko viongozi wa mataifa kadhaa ambao tunayapigania maslahi ya Congo.Tunataka rasilimali za Congo ziwanufaishe watu wote wa Congo na si kikundi cha watu wachache” “Mheshimiwa Rais ninashukuru sana kwa mawazo hayo mazuri juu yangu lakini nadhani mimi si mtu sahihi kwa nafasi hiyo.Watu waliomuua mama walitaka kuiteketeza familia yote na mimi nimepona kwa mkono wa Mungu.Nikisema nikubali ombi lako sintaweza kufika mbali kwani hawa jamaa lazima wataniua tu.Kama waliweza kuwaua wazazi wangu hata kama mlikuwa mmewapa ulinzi hawatashindwa kuniondoa na mimi” akasema Theresa “Usihofu hakuna atakayejua kama wewe ni Theresa Muganza” “Watashindwaje kujua kama ni mimi? “Tutakubadili muonekano wako na utakuwa mtu mpya kabisa na jina jipya hakuna atakayeweza kuhisi wewe ni Theresa Muganza na hapo ndipo kazi itakapoanzia” akasema Rais Weren na midomo ya Theresa ikamcheza akionekana kutaka kuongea kitu lakini Rais Weren akamtoa wasiwasi “Najua taarifa hizi zimekustua sana lakini naomba usistuke Theresa.Tuko pamoja nawe na tunakuandaa kwa mipango mikubwa sana.Nimekuja mwenyewe kukupa taarifa kwamba kesho utafanyiwa upasuaji mkubwa wa kubadili muonekano wako.Tayari timu ya madaktari bingwa kumi na mbili kutoka sehemu mbali mbali duniani mabingwa wa upasuaji wa plastiki wako hapa Paris wakiandaa upasuaji huo.Baada ya upasuaji huo kukamilika utakuwa mtu mwingine kabisa,Theresia Muganza atawekwa pembeni na utaanza na jina jipya,maisha mapya.Safari ya kuelekea katika ndoto kubwa ya mama yako kuliongoza taifa la Congo itaanza.Ninachokuomba usiwe na hofu madaktari hawa ni mabingwa wa upasuaji huo na ninakuhakikishia watakapokuondoa bandeji usoni utakuwa ni malaika,kiumbe mpya kabisa” akasema Weren na baada ya maongezi na Theresa akamuaga na kuondoka “Muda si mrefu moto unakwenda kuwaka Afrika Mashariki.Naamini waligundua kitu kuhusu Lucy kutumika katika mpango wa kuisambaratisha Afrika Mashariki ndiyo maana wakamuua lakini bado hawajafanya kitu kwani sisi tunazo mbinu nyingi zaidi yao na mipango ya kuisambaratisha Afrika Mashariki iko pale pale.Anguko lao linakuja si muda mrefu sana” akawaza Rais Weren akiwa garini baada ya kutoka kuonana na Theresa. TEL AVIV - ISRAEL Mlango mkubwa wa chuma wa mojawapo ya chumba ndani ya gereza la siri wanakofungwa magaidi na wale wote wenye kuendesha mashambulizi dhidi ya Israel,ulifunguliwa na mtu mmoja aliyeonekana hana fahamu na aliyeloa damu mwili mzima akasukumiwa ndani kisha mlango ukafungwa. Ammar Nazari ambaye ndiye aliyekuwa akilala ndani ya kile chumba akastuka sana baada ya kumuona Yule mtu.Akamsogelea akamgeuza na kumtazama.Uso wake ulikuwa umevimba na hakuwa akitazamika kwa damu iliyokuwa inamvuja. “Huyu mtu ni nani?Kwa nini wamekuja kumtupia humu?akawaza akiendelea kumtazama vizuri mtu yule. “Huyu ni mwafrika.Wamemtoa wapi?Ni mara chache sana kumuona mtu mwenye asili ya Afrika katika gereza hili.Humu ndani tumejaa waarabu hasa wapalestina na wengine ambao tunaendeleza harakati za mapambano dhidi ya dhuluma za Israel.Huyu amefanya nini hadi akafika hapa?Ni jambazi?Ameua? akaendelea kujiuliza Ammar huku akivua kilemba chake akakipasua na kuanza kumfuta damu. “Huyu jamaa atakuwa amefanya kosa kubwa sana.Ameumizwa mno.Mwili wake wote una viodonda.Inaonekana ameteswa sana kisha wakaja kumtupa humu ndani” akawaza Ammar na kwenda kuchukua maji katika chombo chake cha kuhifadhi maji ya kunywa akaanza kumfuta damu Yule mtu “Huu ni ukatili usioelekezeka.Hawa watu ni wakatili mno.Unawezaje ukamtesa mwanadamu mwenzako kiasi hiki?Hii ndiyo sababu inayonifanya niendelee kuwa na chuki na hasira dhidi ya watu hawa na ninaapa kama itatokea siku moja nikawa huru nitaendelea kupambana nao hadi tone la mwisho la damu yangu.Nitaendelea kuua waisrael hadi pale watakaporejesha ardhi yetu waliyoipora” akawaza Ammar akiendelea kumfuta damu. Katika moja wapo ya chumba ndani ya lile gereza Efraim Dagan akiwa na baadhi ya maafisa wa Mossad wakiwa na viongozi wa lile gereza walikuwa wakitazama kila kinachoendelea katika chumba kile cha Ammar kupitia runinga iliyunganishwa na kamera ya siri iliyomo katika chumba kile.Efraim akachukua simu na kumpigia Moshe mkurugenzi mkuu wa Mossad “Efraim mambo yanakwendaje? Akauliza Moshe Levine “Mkurugenzi nimekupigia kukujulisha kuwa mambo yameanza.Tayari Mathew amekwisha ingizwa katika chumba cha Ammar na hivi tuongeavyo tunamtazama kupitia kamera ya siri iliyomo humo chumbani.Amestushwa sana na hali ya Mathew na anamsaidia kwa kumfuta damu iliyotapaa mwili mzima.Inaonekana ana hamu sana ya kutaka kumfahamu Mathew ni nani pale atakapokuwa amezinduka.Mwanzo umekuwa mzuri” akasema Efraim “Kazi nzuri sana.Endeleeni kumfuatilia kwa karibu sana kujua kila kinachoendelea humo ndani.Ammar ni mtu mbaya sana akimgundua kwamba ni pandikizi atamuua” “Tuko makini mkurugenzi kumfuatilia Mathew na kama tukigundua kuna jambo lolote lisilo la kawaida tutamtoa Mathew haraka sana lakini mpaka hapa tunaona kuna mwelekeo mzuri” “Kuhusu Mathew Mulumbi unamuamini?Haweze akabadilika na kutoweka? Akauliza Moshe “Kuna kila dalili kwamba hataweza kwenda kinyume na makubaliano yetu japo hatuwezi kumuamini asilimia mia moja kwa sasa.Tunaendelea kufuatilia mwenendo wake” akasema Efraim “Nashauir pale atakapokuwa ametolewa ndani ya chumba hicho baada ya siku mbili achomwe sindano ya usingizi na afungwe kwa siri kifaa kitakachotuwezesha sisi kumfuatilia na kujua mahala alipo.Sina imani naye huyu mtu anaweza akatoroka” akasema Moshe na kukata simu. Chumbani bado Ammar aliendelea kumsaidia Mathew Mulumbi kwa kumfuta damu halafu akamlaza katika kitanda kimoja kwani ndani ya chumba kile kulikuwa na vitanda viwili akaendelea kumpepea kutokana na hali iliyokuwemo mle ndani ya chumba kuwa ni joto .Alikuwa anavuja jasho jingi usoni Zilipita dakika arobaini Mathew akafumbua macho. “Allahu Akbar ! akasema Ammar baada ya Mathew kuzinduka. “mrhbana,aistarkhaa.sat akun bikhayr” akasema Ammar akimtaka Mathew atulie atakuwa salama.Akaenda katika chombo anachohifadhi maji ya kunywa akatikisa na kukuta kuna maji kidogo akamimina katika kikombe cha bati na kumpatia Mathew “ashrb ma'(kunywa maji) akasema Ammar na kumsogezea Mathew kikombe cha maji lakini Mathew akakipiga kofi kile kikombe kikaanguka na maji yakamwagika.Ammar akamtazama “sawf tamut huna 'iidha kunt la tashrib alma'(utakufa humu kama hutakunywa maji)akasema Ammar lakini Mathew hakumjibu kitu.Ammar akakaa kwenye kiti cha mbao akimtazama Mathew. “min 'ant? madha faelt?(wewe ni nani?Umefanya nini?) akauliza Ammar lakini Mathew hakumjibu kitu “laqad qatalat shakhsana? laqad qatalat alyahud?(umeua mtu?Umeua wayahudi?) akauliza Ammar lakini bado Mathew hakumjibu alikuwa kimya. “la takhafuu manya. asmaa eammar nazaraa. ma asmaka? min 'ayn 'ant?(Usiniogope.Naitwa Ammar Nazari.Jina lako nani?Umetokea wapi?) akauliza Ammar bado Mathew hakuweza kuzungumza Ammar akafunua bakuli lililokuwa pembeni ya chumba akatoka mkate “aistayqaz wa'akal min fidlik. tahtaj 'iilaa alttaqat min ajl albaqa' huna(inuka ule tafadhali.Unahitaji nguvu uweze kuishi humu) akasema Ammar Mathew hakutaka kumtazama akafumba macho. “kayf yumkinuni masaeiduk? 'ant la turid 'an takul 'aw tashrub. 'ant turid 'an tamut? (Nikusaidiaje? Hutaki kula wala kunywa.Unataka kufa?) akauliza Ammar “daeni 'atrikuk alan lilrraha. sanatahadath lahqaan(Ngoja nikuache kwa sasa upumzike,tutazungumza baadae” akasema Ammar na kwenda kujilaza katika kitanda kingine. “Mambo mazuri.Nataka niunganishwe na kila kinachoendelea ndani ya chumba kile niwe nikifuatilia kwa karibu” akasema Efraim akitaka kuunganishwa katika simu yake ili aendelee kufuatilia kila kinachoendelea katika chumba kile kisha akatoka “Umekuwa ni mwanzo mzuri sana.Kuna kitu ndani yangu kinanifanya nimuamini sana huyu Mathew Mulumbi.Ninakiri toka nimeingia katika mambo haya ya ujasusi sijawahi kukutana na mtu kama Mathew.Ni mtu wa ajabu sana.Kwa miaka mitatu ameweza kuvumilia mateso na hajatamka hata neno moja” akawaza Efraim. - LICHA YA LUCY MUGANZA KUUAWA LAKINI BADO MIPANGO YA KUISAMBARATISHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI IKO PALE PALE NA SASA ANAANDALIWA MWANAE THERESA KUVAA VIATU VYA MAMA YAKE - MATHEW MULUMBI KATIKA JITIHADA ZA KUTAKA KUJIKOMBOA KUTOKA MIKONO YA MOSSAD ANAANDAA MPANGO WA KUJIUNGA NA MAGAIDI ILI AWEZE KUMPATA HABIBA JAWAD.JE MIPANGO YAKE ITAFANIKIWA?MPENZI MSOMAJI USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI HII KATIKA SEHEMU IJAYO….







DAR ES SALAAM Saa tatu za asubuhi Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo alipata ugeni ambao ni balozi wa umoja wa Ulaya ndugu Benjamin Hudson ambaye aliomba kuonana na Rais ili kuzungumza mambo muhimu. “Karibu sana mheshimiwa balozi.Ni furaha yangu kuonana nawe leo”akaanzisha maongezi Dr Fabian “Ahsante sana mheshimiwa Rais kwa kukubali ombi langu kuja kuonana nawe”akasema balozi Benjamin “Tanzania tuna mahusiano mazuri na umoja wa Ulaya hivyo nisingeweza kukataa ombi la kuonana na mwakilishi wao hapa Tanzania” “Ni kweli mheshimiwa Rais mahusiano ya Tanzania na umoja wa Ulaya ni makubwa na yanakwenda vizuri hata hivyo nimetumwa nikuletee salamu za umoja huo.Kwanza pongezi kwa maendeleo mazuri na ya kuridhisha ya kiuchumi lakini pili ni ombi nimetumwa niliwasilishe kwako” “Ahsante kwa pongezi.Umoja wa Ulaya wanaomba kitu gani?akauliza Dr Evans na balozi Benjamin akavuta pumzi ndefu na kusema “Mheshimiwa Rais hivi majuzi kumetokea mauaji ya bilionea Lucy Muganza na mume wake Laurent Muganza.Laurent Muganza alikuwa ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Congo lakini vile vile alikuwa ni mmoja kati ya wafanyakazi wa ngazi za juu katika makao makuu ya umoja wa ulaya jijini Brussels.Nafahamu kwamba tayari taarifa ya awali ya mauaji yale imekwisha tolewa na inatajwa kwamba chanzo cha mauaji yale kilikuwa ni ujambazi.Tunaheshimu vyombo vya ndani vya Tanzania lakini umoja wa Ulaya umenituma niwasilishe ombi maalum kwako la kutaka kutuma timu maalum ya wachunguzi kuja kufanya uchunguzi wa mauaji hayo hasa ukizingatia kwamba Laurent Muganza alikuwa afisa katika umoja wa Ulaya.Kwa mujibu wa maelekezo niliyopewa ni kwamba timu hiyo itakuwa na watu nane ambao ni wabobezi katika mambo ya uchunguzi” akasema balozi Benjamin na Dr Fabian akawa kimya kwa muda halafu akasema “Mheshimiwa balozi sitaki nieleweke vibaya lakini suala hili la mauaji ya Lucy Muganza na mumewe linaendelea kushughulikiwa na vyombo vya uchunguzi vya hapa nchini na watakapokamilisha uchunguzi wao watatoa taarifa.Kuruhusu timu nyingine ya kutoka nje kuja kufanya uchunguzi wakati vyombo vya ndani havijakamilisha uchunguzi wao kwanza ni kudhalilisha vyombo vya ndani kwamba haviwezi kuchunguza matukio makubwa kama haya na pili tunawavunja moyo vijana wetu ambao hawalali wakitafuta kupata ukweli wa tukio lile.Ushauri wangu kwa umoja wa Ulaya ambao ni wadau wetu wa maendeleo wasiwe na wasi wasi na waviamini vyombo vyetu vya ndani ya nchi na waviache vifanye uchunguzi vikikamilisha watatoa taarifa na kama hawataridhika na taarifa hiyo tutaangalia kama kutakuwa na ulazima wa kuruhusu wachunguzi kutoka nje ya nchi lakini kwa sasa hakuna ulazima wowote wa kuleta wachunguzi kutoka nje ya nchi” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ombi la kutaka kuleta wachunguzi wa nje si kwamba hatuviamini vyombo vya Tanzania bali tunataka kutanua zaidi wigo wa uchunguzi.Aliyeuawa ni afisa mkubwa katika umoja wa Ulaya na yawezekana majambazi wale walitumika tu lakini wahusika wa mauaji hayo ni wengine kabisa.Tunataka kuchimba kiini cha mauaji yale.Tunahisi zipo njama za kuwadhuru maafisa wetu hivyo kupitia uchunguzi huo utakaofanyika na timu maalum,itajulikana nani ambao wanapanga njama hizo za kudhuru maafisa wetu”akasema balozi Benjamin “Mheshimiwa balozi pamoja na sababu ulizozitoa lakini bado sioni ulazima wa kuruhusu wachunguzi wa kutoka nje kuja kufanya uchuguzi wa mauaji yaliyotokea Tanzania.Nasema katu siwezi kuruhusu jambo la namna hiyo.Tanzania tunavyo vyombo vya uchunguzi vyenye watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi na kwa ujumla vyombo vyetu vinafanya kazi nzuri sana hivyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi wowote.Fikisha salamu zangu kwa umoja wa Ulaya kwamba wasiwe na wasiwasi wasubiri taarifa itakayoptolewa na vyombo vyetu na kama hawataridhika nayo basi tutaangalia namna nyingine lakini kwa sasa hatutaruhusu wachunguzi wowote kutoka nje ya nchi” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,Tanzania ni nchi ambayo ina heshima kubwa sana kimataifa.Mauaji haya ya Laurent na mke wake Lucy yameistua dunia na kuzifanya nchi nyingi zigeuke na kuitazama Tanzania kutaka kujua kulikoni mauaji yale yakatokea hapa katika nchi iliyojaa amani na utulivu.Tanzania imepata doa kutokana natuko lile na njia pekee ya kulifuta doa hilo ni kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kufanya uchunguzi lakini kama hamtaruhusu timu hiyo kufanya uchunguzi wake Tanzania itachafuka kimataifa jambo ambalo inaweza kuwa na athari kubwa hasa kiuchumi”akasema balozi Benjamin “Mheshimiwa balozi kauli yako inalenga kuonyesha kwamba Tanzania inahusika na mauaji hayo ya Laurent na mke wake.” Akasema Dr Fabian “Hakuna mwenye ushahidi na hilo mheshimiwa Rais lakini fahamu kwamba Tanzania inanyooshewa kidole kuhusiana na mauaji hayo na njia pekee ya kujisafisha na kuondoa doa ambalo nchi yako imelipata kwa mauaji yale kutokea katika ardhi yenu ni kuruhusu timu ya wachunguzi wa kimataifa kufanya uchunguzi wao.Kama hamtaruhusu wachunguzi hao itajengeka hisia kwamba Tanzania kuna kitu inaficha kisijulikane kuhusu mauaji yale” “Mheshimiwa balozi sasa nimepata picha kamili ya kwa nini mnataka timu ya wachunguzi wa kimataifa waje kufanya uchunguzi.Tayari mnaamini kwamba Tanzania ina mkono wake katika mauaji yale.Naomba niwatoe wasiwasi kwamba katu Tanzania haiwezi kupanga njama za kumuua Laurent na mke wake.Subirini uchunguzi ukamilike na mtawajua watu wanaohusika na mauaji hayo lakini kuihusisha Tanzania ni kutaka kuipaka matope” “Mheshimiwa Rais hakuna mpaka sasa anayeamini kama Tanzania inaweza ikahusika katika mauaji hayo lakini kitendo cha kugoma kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kama nilivyosema kinaweza kuitia doa serikali yako na kuvuruga mahusiano mazuri na jumuiya ya Ulaya” akasema balozi Benjamin na Dr Fabian akamtazama kwa muda kisha akauliza “Kwa nini Laurent Muganza?Mbona kumewekwa uzito mkubwa sana kutaka kufahamu chanzo cha kifo chake hadi kutaka kuingilia taratibu zetu za ndani ya nchi? akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais niliweka wazi kwamba kuna wasi wasi kuna njama za kuwadhuru maafisa wa umoja wa Ulaya na tunahisi mipango hiyo tayari imeanza hivyo basi tunataka kuanza kufanya uchunguzi kwa kuanzia na kifo cha Laurent” “Nani anataka kuwadhuru maafisa wa umoja wa Ulaya?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais hayo ni mambo ya ndani sana ya kiusalama na hata mimi siwezi kufahamu.Ninachokuomba litafakari ombi hilo la umoja wa Ulaya na uwaruhusu wachunguzi wa kimataifa kuja kufanya uchunguzi wa jambo hili” “Balozi Benjamin nadhani mimi na wewe tumekwisha maliza hapa.Jibu langu halitabadlika.Hatutaruhusu wachunguzi wowote wa kimataifa nchini kwetu.Nifikishie salamu hizo kwa umoja wa Ulaya”akasema Dr Fabian na kutaka kuinuka lakini Benjamin akamuomba ampe dakika mbili kuna kituanataka kumueleza “Mheshimiwa Rais kabla sijaondoka kuna jambo nataka ulifahamu ambalo ndilo hasa chanzo cha wasiwasi kuhusu mauaji yale hadi kutaka kutuma wachunguzi wa kimataifa” akasema balozi Benjamin na kufungua mkoba wake akatoa mafaili mawili. “Mheshimiwa Rais hizi ni taarifa mbili tofauti.Moja ni taarifa ya awali ya jeshi la polisi kuhusina na mauaji yale na nyingine ni taarifa ya daktari iliyotolewa baada ya miili ya Lucy na Laurent kufanyiwa uchunguzi” akasema balozi Benjamin “Mheshimiwa rais hizi si taarifa za siri bali ni taarifa za wazi kabisa na mtu yeyote anaweza kuwa nazo.Hii taarifa ya daktari nimeipata kutoka kwa ndugu za marehemu na hii ya jeshi la polisi iko mtandaoni” “Kuna nini katika taarifa hizi?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa rais katika taarifa hizi mbili kuna jambo dogo lakini lenye kuibua maswali mazito.Taarifa ya awali ya jeshi la polisi inaonyesha kwamba majambazi ambao wanadaiwa kumuua Lucy na mumewe pamoja na walinzi wao,waliuawa wote na walikutwa wakiwa na silaha mbali mbali ambazo zimeorodheshwa hapo ambazo ni bunduki za vita aia ya SMG pamoja na bastora kadhaa.Ripoti ya jopo la madaktari walioifanyia miili uchunguzi inaonyesha kwamba risasi zilizowaua Laurent na mkewe Lucy ni kubwa tofauti na risasi za SMG.Baada ya kuzifanyia uchunguzi risasi hizo zimebainika ni za bunduki aina ya Barret M82.Mheshimiwa Rais hizi ni bunduki hatari sana zenye nguvu na zinazotumiwa na wadunguaji.Kwa kawaida bunduki kama hizi hutumiwa au kumilikiwa na majeshi au vikosi maalum.Majambazi waliouawa hawakuwa na bunduki hizo.Taarifa nilizonazo zinanionyesha kwamba Tanzania mnazo bunduki za namna hiyo na mlizinunua kutoka Marekani.Maswali yanaanzia hapo mheshimiwa Rais.Nadhani unakubaliana nami kwamba suala hili ni kubwa na linahitaji uchunguzi mkubwa pia.Siamini kama Tanzania inahusika katika suala hili lakini zitajengeka hisia hizo pale ambapo utakataa wachunguzi wa kimataifa waje kuchunguza suala hili mheshimiwa Rais” akasema balozi Benjamin na uso wa Dr Fabian ukajikunja kwa hasira. “Balozi taarifa kama hizo za silaha tulizo nazo unazipata wapi?Kwa hilo balozi umevuka mipaka ya kazi yako ya uwakilishi wa jumuiya ya Ulaya na sasa unaanza kufanya uchunguzi wa mambo yasiyokuhusu.Masuala ya silaha ni masuala nyeti kabisa ya usalama wa nchi.Hili sintalifumbia macho balozi.Lazima umoja wa Ulaya watueleze kama walikutuma hapa kuja kuwawakilisha au kufanya ujasusi.Ahsante kwa kufika mheshimiwa balozi” akasema Dr Fabian akiwa amekasirika na balozi Benjamin akasimama “Mheshimiwa Rais nakuomba jipe muda litafakari suala hili na ufanye maamuzi yenye kufaa kwa nchi yako.Wachunguzi hao hawataingilia suala lolote la nchi yako bali watachunguza kifo cha raia wa kigeni hivyo kuwazuia kufanya uchunguzi ni mwanzo wa kuibuka kwa mjadala mpya wenye swali la kwa nini?Ahsante mheshimiwa rais nakushukuru kwa kunikaribisha na kunisikiliza.Nategemea kupata simu yako baada ya tafakari ya kina” akasema balozi Benjamin na kusimama.Dr Fabian akamuelekeza mmoja wa wasaidizi wake amsindikize balozi nje katika gari lake yeye akaelekea ofisini kwake. “Mambo yameanza.Sasa nimeamini kumbe Lucy Muganza alikuwa mtu muhimu sana kwao ndiyo maana wanafanya shinikizo la kutaka iruhusiwe timu ya wachunguzi wa kimataifa kuingia nchini na kuchunguza.Ni vipi kama nitaruhusu timu hiyo kuingia nchini na kuchunguza halafu wakabaini sisi ndio tuliomuua Lucy Muganza na mumewe?Moja kwa moja nitakuwa nimejivisha kitanzi.Lakini nisiporuhusu wachunguzi hao kuingia nchini lazima watajiuliza maswali kuna kitu gani tunakificha? Halafu huyu balozi amepata wapi taarifa nyeti kama hizo za sisi kumiliki bunduki za Barret M82? Suala hili limeanza kuchukua sura mpya na litakuwa kubwa zaidi.Inaonekana tayari wamekwisha hisi sisi ndio tuliomuua Lucy na wanachokitafuta hivi sasa ni ushahidi wa kutosha na ushahidi huo wataupata endapo watatuma timu yao hapa nchini.Something must be done.Hili si suala la kuachia hivi hivi inaonekana kuna watu mtandao wa watu wa ndani pia wanaosaidiana na umoja wa Ulaya katika kutafuta ukweli wa hili jambo.Lazima tuwafahamu ni akina nani hao na kuwadhibiti haraka sana” akawaza Dr Fabian





Geti la nyumbani kwa Rais mstaafu Dr Evans lilifunguliwa na gari lililobeba shehena ya matunda likaingia.Yalikuwa ni matunda kutoka katika shamba la matunda la Dr Evans.Watumishi walianza kupakua matunda yale yaliyokuwa katika masanduku na kuyaingiza ndani katika chumba maalum cha baridi kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya shambani yenye kuharibika haraka kama vile matunda.Wakati zoezi likiendelea la kupakua matunda Dr Evans akatoka ndani.Siku hii alivaa suruali ya jeans ya khaki shati jeupe na kofia ya mzunguko ya rangi nyeupe.Akalisogelea lile gari akasalimiana na wafanyakazi kisha akashika tunda moja akalitazama na kutabasamu halafu akamuagiza mtumishi wake amuandalie juisi kutoka katika matunda yale yaliyotoka shambani siku ile.Dr Evans akazunguka zunguka katika makazi yake akisalimiana na wafanyakazi na kukagua namna shughuli zilivyokwenda halafu akaenda kukaa katika sehemu ya kupumzikia pembeni ya bwawa la kuogelea. “Maisha ya kustaafu baada ya kulitumikia taifa ni mazuri sana.Ninapata kila kitu ninachokitaka,ninakwenda sehemu yoyote ninayoitaka lakini kuna kitu kimoja tu ambacho nimekikosa.Ningekuwa na mke furaha yangu ningefurahia zaidi maisha ya kustaafu.Nimeishi mwenyewe kwa muda mrefu toka mama yake Coletha alipofariki dunia.Kwa nini nisitafute mwanamke wa kuishi naye?Naamini siwezi kukosa mwanamke mtu mzima mstaafu mwenzangu na ambaye hana mume ili niishi naye wakati huu.Siwezi kuk………………” DrEvans akatolewa mawazoni baada ya simu yake kuita.Akaichukua na kutazama aliyepiga akalazimika kuinuka na kukaa vizuri.Alikuwa ni Rais Dr Fabian Kelelo. “Mheshimiwa Rais” akasema Dr Evans baada ya kuipokea simu “Mzee shikamoo” “Marahaba.Habari yako Dr Fabian? “Naendelea vyema mzee wangu.Habari za hapo nyumbani? “Mimi mzima kabisa.Nina siku mbili tu nimerejea kutoka Afrika kusini nilikwenda kumtembelea binti yangu anafanya kazi huko”akasema Dr Evans na mtumishi wake akamletea juisi akamuwekea pembeni “Mzee samahani kwa kukusumbua.Nina jambo nahitaji ushauri wako.Najua ulisema nisikusumbue lakini sina mwingine ambaye ninaweza kumkimbilia kwa suala hili muhimu ” akasema Dr Fabian “Una tatizo gani mheshimiwa Rais? Akauliza Dr Evans “Unakumbuka lile suala la Yule mama Lucy Muganza? “Ndiyo.Nakumbuka aliuawa”akajibu Dr Evans “Ni kweli aliuawa lakini kuna tatizo limejitokeza nahitaji unipe ushauri nifanye nini” akasema Dr Fabian na kukaa kimya kwa muda kisha akasema “Balozi wa umoja wa Ulaya ametoka hapa ikulu si muda mrefu sana ameniletea taarifa kuwa kufuatia mauaji yale ya Lucy na mumewe,umoja wa Ulaya wanataka kutuma wachunguzi wao kuja kuchunguza kujua chanzo cha mauaji yale” “Umoja wa Ulaya?akauliza Dr Evans “Ndiyo mzee.Umoja wa Ulaya wanataka kutuma timu ya wachunguzi wa kimataifa kuja nchini kufanya uchunguzi wa mauaji yale ya Lucy Muganza na mume wake Laurent kwa madai kwamba Laurent alikuwa ni afisa katika makao makuu ya umoja wa Ulaya hivyo lazima umoja huo ujiridhishe sababu za kuuawa kwake”akasema Dr Fabian “Kama umoja wa Ulaya nao wameingilia kati na kutaka kufanya uchunguzi,hii inatoa picha ya wazi kwamba hawa watu wawili Lucy na mumewe walikuwa ni watu muhimu sana kwao.Ulifanya vyema kuwaondoa mapema na Dr Fabian huu ni wakati wako wa kuonyesha msimamo mkali kama Rais.Usiwaruhusu wachunguzi hao wa umoja wa ulaya kuingia nchini kwa namna yoyote ile” akasema Dr Evans “Lakini mzee nikisema niwazuie wachunguzi hao wasiingie nchini italeta picha kwamba kuna jambo ninalificha kuhusu mauaji hayo” akasema Dr Fabian “Dr Fabian tatizo lako unataka uwe mwema na mzuri kwa kila mtu kitu ambacho hakiwezekani.Usifanye mambo kwa kutaka watu wakuone mzuri sana bali fanya jambo kwa maslahi ya nchi.Huu ni mtego umewekewa na ukienda kichwa kichwa utanasa.Usiwaruhusu kamwe wachunguzi hao waje hapa nchini kufanya uchunguzi.Weka msimamo kwamba hilo ni suala la ndani ya nchi na linashughulikiwa na vyombo vya ndani.Huhitaji wachunguzi kutoka nje.Ukithubutu kuwakaribisha sebuleni wataingia hadi chumbani hivyo nakushauri usiwape nafasi kabisa katika suala hilo.Simama na msimamo mmoja kwamba uchunguzi utafanywa na vyombo vya ndani.Umenielwa Dr Fabian? “Nimekuelewa mzee” “Good.Unapaswa kusimama kama Rais mwenyehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ msimamo mkali usiyoyumba lakini ukiwachekea hawa na ukaonyesha uoga watakutawala na utafanya kila wakitakacho wao.Usitishwe na mtu yeyote au taifa lolote liwe kubwa au dogo.Hii ni vita na mpaka hapa hesabu kwamba vita hii kwa asilimia kubwa umeshinda kwani walimtegemea mno Lucy Muganza ndiyo maana hivi sasa wanahaha.Hata hivyo kuna kitu nataka kujua.Kwa nini wawe na wasi wasi hadi watake kutuma watu wao kuja kuchunguza mauaji hayo? Kuna kitu wamekiona au kuna taarifa yoyote wameipata inayowapa wasiwasi? Akauliza Dr Evans “Kuna jambo alinieleza balozi ambalo mimi nadhani hata timu niliyowatumia katika kufanikisha jambo lile hawakulitilia maanani.Aina ya risasi zilizokutwa katika miili ya akina Lucy ni za bunduki aina ya Barret M82.Hizi ni bunduki kubwa na hutumika kwa udunguaji.Bunduki hizi zipo katika kikosi cha jeshi cha operesheni maalum kwani kuna wadunguaji wako pale.Majambazi ambao wanatajwa kuwa walimuua Lucy walikuwa na bunduki aina ya SMG na bastora.Umoja wa Ulaya wamelibaini hilo na ndiyo maana wanataka wafanye uchunguzi.” akasema Dr Fabian “Kweli hapo lazima tukubali kuna kosa lilifanyika.Ilitakiwa baada ya kufanya mauaji yale wafuatilie hadi katika ripoti ya daktari lakini wao walipomuua Lucy wakajua wamemaliza kila kitu.Umoja wa Ulaya wanayo hoja ya msingi ya kutaka kuleta wachunguzi wao lakini jambo pekee ni kusimama kidete kukataa hakuna mchunguzi yeyote kuingia nchini”akasema Dr Evans “Kitu kingine kilichonistua kwa balozi Benjamin ni kuwa na taarifa kwamba Tanzania tunazo bunduki za aina ile iliyotumika kumuua Lucy na anafahamu tumezinunua wapi bunduki hizo” “Anazo taarifa za silaha zetu?Amezipata wapi? Akauliza Dr Evans kwa mshangao “Hata mimi nimeshangaa kama ulivyoshangaa wewe.Nimefikiria kumtimua nchini kwa kufanya ujasusi badala ya kazi iliyomleta” akasema Dr Fabian kwa ukali “Hapana usimtimue.Huyu ni mtu anayepaswa kuchunguzwa sana kujua amepata wapi taarifa hizo nyeti.Naamini lazima kuna watu hapa nchini anashirikiana nao hadi akafanikiwa kupata taarifa hizo nyeti.Ukimtimua nchini utashindwa kujua anaoshirikiana nao hivyo nakushauri muache lakini kuanzia sasa anza kumchunguza kwa siri naamini kuna mengi utayafahamu kutoka kwake.Kama ameweza kupata taarifa kwamba tunazo bundukio aina ya Barret M82 basi hashindwi kujua tuna vifaru vingapi,mizinga mingapi kwa ujumla huyu mtu anachokifanya ni ujasusi lakini mvumilie na umchunguze kwa siri mno.Ni mtu hatari sana kwa taifa”akashauri Dr Evans “Mzee nakushukuru sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi” “Fabian” akaita Dr Evans “Naam mzee” “Samahani nakuita Fabian kwani hapa nataka kuzungumza nawe kama mwanangu na ninaomba unisikilize vizuri” “Nakusikiliza mzee” “Umeingia katika vita ya kiuchumi.Hii ni vita mbaya sana kuliko vita ya silaha.Unatunishiana misuli na mataifa makubwa yenye uchumi mkubwa,teknolojia kubwa na zaidi sana ambayo tunayahitaji katika ukuaji wa uchumi wetu lakini kwa kiasi kikubwa uchumi huo mkubwa wa mataifa hayo unategemea sana rasilimali zetu kama vile madini,mazao ya kilimo maliasili n.k.Kwa miaka mingi wamekuwa wakifaidika kwa kubeba rasilimali zetu na kitendo cha kuvuruga mipango yao ya kutaka kuendelea kunufaika na rasilimali zetu kinakufanya uwe ni adui kwao na kwa kuwa wana nguvu basi wafanya kila waliwezalo kuhakikisha kwamba wanakudhoofisha au wanakundoa katika nafasi yako wewe na wenzako ambao mnasimama pamoja.Hii ni vita mbaya lakini kitakachokusaidia ni uimara wako na kufanya maamuzi sahihi yasiyoyumba.Watakutikisa lakini usikubali kutikisika.Kutokana na misimamo yako nchi inaweza ikayumba lakini wewe kama kiongozi mkuu simama imara ipeleke nchi sehemu salama.Katika vita hii jaribu kuwa na watu wachache sana ambao utawaamini ambao watakusaidia sana kupambana.Mapambano yanatatakiwa yawe ni ya siri kubwa hata viongozi wenzako wakuu hawapasi kujua kwani miongoni mwao wako wasaliti wakubwa.Ichunge sana jumuiya ya Afrika mashariki isivunjike na hasa kuvunjikia mikononi mwako.Naamini umenielewa Dr Fabian” akasema Dr Evans “Mzee nimekuelwa vizuri sana.Ninakushukuru tena kwa ushauri wako mzuri ninakuahidi nitaufanyia kazi” akasema Dr Fabian akaagana na Dr Evans “Yule mzee amekuwa na msaada mkubwa sana kwangu kila pale ninapokuwa nimetingwa na suala zito.Amenipa ushauri mzuri ambao napaswa kuuzingatia.Kweli hii ni vita japo si ya vifaru na mizinga lakini ni vita ya uchumi.Nitajitahidi kusimama imara kupambana” akawaza na kuchukua simu akampigia Austin na kumtaka afike ikulu jioni ana mazungumzo naye. “Austin na wenzake walifanya kosa dogo ambalo sasa linakwenda kutugharimu hata hivyo bado nitaendelea kumuamini na kufanya naye kazi nyingi za siri” akawaza Dr Fabian PARIS – UFARANSA Hali ya ubaridi iliyokuwepo nje ilimfanya bilionea Peniela aendelee kulivuta blanketi zito alilokuwa amejifunika.Kikubwa kilichomfanya asitake kubanduka kitandani licha ya kwamba tayari imekwisha gonga saa mbili za asubuhi ni mtu aliyekuwa pembeni yake ambaye asubuhi hii bado alionekana kuzidiwa sana na usingizi. “Nahum ! Nahum ! ..Peniela akamuita Yule jamaa aliyekuwa naye kitandani huku akimtikisa.Nahum akaitika kwa sauti iliyojaa uchovu mwingi.Peniela akamkumbatia na kumbusu “Kumekucha haraka sana leo” akasema Nahum huku akifikicha macho “Usiku mzima wa jana hatujalala.Una pumzi za ajabu Nahum.Hukutaka kuniachia kila mzunguko ulipoisha uliunganisha mwingine.Sikumbuki hata nilifika kilele mara ngapi jana.Wanaume kama wewe ni nadra sana kupatikana zama hizi.Nina bahati kwani hata mum…..” Peniela akasita na kumtazama Nahum ambaye alikuwa anatabasamu “Mbona unasita?Unaogopa kumtaja aliyekuwa mumeo Mathew Mulumbi? Akauliza Nahum na Peniela akastuka “Umemfahamu vipi Mathew?akauliza na Nahum akatabasamu “Kabla ya kukutongoza nilitafuta kwanza taarifa zako na kuambiwa kwamba mumeo alikuwa anaitwa Mathew Mulumbi na alifariki nchini Tanzania.Sikutaka kuwa na mahusiano na mtu mwenye mume wake.Nilipopata uhakika kwamba uko mwenyewe ndipo nilipoamua kukufuata” akasema Nahum na Peniela akawa kimya “Nini kilimuua Mathew Mulumbi?akauliza Nahum “Samahani Nahum huwa sipendi sana kuzungumzia suala hilo.Tafadhali naomba tusiongelee tena habari za Mathew.Tuko hapa mimi na wewe tufurahie wakati wetu huu.Masuala yote ya Mathew tuyaweke pembeni” akasema Peniela “Samahani mpenzi wangu” akasema Nahum na kumbusu Peniela “Naomba dakika mbili nikawatazame watoto kama wamekwisha kwenda shule” akasema Peniela na kumbusu Nahum halafu akafunga vizuri nguo yake na kutoka Baada ya Peniela kutoka Nahum akaiwasha simu yake iliyokuwa imezima,zikaingia jumbe mbali mbali akazipitia kwa haraka haraka na kisha akalitafuta jina la Efraim akampigia “Nahum kulikoni ukazima simu yako kwa usiku mzima?akauliza Efraim baada ya kupokea simu “Nililazimika kuzima simu nilikuwa na Peniela chumbani kwake na huwa ninachukua tahadhari kubwa kila ninapokuwa naye” akajibu Nahum “Kuanzia sasa usithubutu kuzima simu” akasema Efraim “Nitajitahidi Efraim” “Vizuri.Nilikuwa nakutafuta kukujulisha kwamba misheni imekamilika na unatakiwa kuondoka haraka sana huko Paris kurejea Israel” akasema Efraim “Misheni imekamilika?akauliza Nahum “Ndiyo.Ulitumwa huko kwa ajili ya kazi maalum ambayo tayari imekamilika na kitu tulichokuwa tunakitafuta tumekipata.Mathew Mulumbi ameongea hivyo hakuna tena sababu ya wewe kuendelea kukaa huko.Rudi nyumbani haraka sana” akasema Efraim na ukapita ukimya “Nahum unanisikia? “Ninakusikia Efraim lakini..” “Hakuna lakini,rudi nyumbani haraka sana kazi uliyotumwa imekamilika”akasema Efraim “Efraim naomba unipe muda wa wiki mbili ili nimuandae Peniela kabla sijatoweka” akasema “Nahum tayari umeanza kupenda? akauliza Efraim na Nahum akawa kimya alishindwa kujibu “Nahum hii ni kazi na hupaswi kuuruhusu moyo wako kupenda hata siku moja.Umekutana na wanawake wengi wazuri na haujawahi hata mara moja kutaka kuanguka mapenzini nakuonya isitokee kwa huyo mwanamke mweusi.Narudia tena kukuonya usithubutu kutaka kumpenda Peniela.Ukithubutu kuufungua moyo wako tu utakufa kabla haujatimiza lengo lako hivyo nakuonya chunga sana hicho unachofikiria kukifanya.Nakupa siku tatu kuanzia leo uwe umerejea nyumbani baada ya siku hizo tatu akaunti zote zenye fedha zinazokutambulisha kama bilionea zitafungwa kadi zako zote hazitatumika tena utabaki na hati yako ya kusafiria tu kwa ajili ya kurejea nyumbani.Narudia tena siku tatu kuanzia sasa uwe nyumbani.Kitu kingine kwa kuwa misheni imekamilika tafadhali usiendelee kutumia fedha hovyo kwani tunaona namna unavyotumia fedha kwa fujo” akasema Efraim na kukata simu.Nahum alikuwa kama mtu aliyemwagiwa maji baridi.Alibaki amekaa kitandani ameishikilia simu yake.Alikuwa katika lindi la mawazo. “Sikuwahi kuona ugumu wa kazi hii hapo kabla lakini leo kwa mara ya kwanza ninadiriki kuichukia hii kazi.Nimetengenezwa kwa ajili ya kazi moja tu ya kujenga mahusiano na wanawake wale ambao tunawahitaji katika misheni zetu.Nimekutana na wanawake mbali mbali masikini,matajiri,wake za watu,viongozi lakini sikuwahi hata mara moja kufikiri kama itatokea siku moja moyo wangu utamuangukia mtu ambaye ninamchunguza.Imenitokea kwa Peniela.Nakiri sijawahi kukutana na mwanamke kama huyu.Sifahamu kama kuna kitu anatumia kunivuruga akili yangu lakini nimechanganyikiwa kwake.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nahisi kumpenda mwanamke ambaye ni huyu Peniela.Nahisi furaha,raha ya ajabu kila ninapokuwa naye lakini masharti ya kazi yangu hayaniruhusu kupenda na ninatakiwa ndani ya siku tatu niwe nimeondoka Paris kurejea Israel.Nitafanya nini?akajiuliza. “Mathew Mulumbi alikuwa anafaidi sana.Wanawake kama hawa ni nadra sana kupatikana zama hizi.Nitawezaje kumuacha Peniela? Hapa ndipo ninabaki njia panda je niitike wito wa kurudi nyumbani au niendelee kuwa na Peniela? Akajiuliza “Hapana siwezi kumuacha Peniela.Niko radhi kuachana na kazi yangu na kuwa naye.Mathew Mulumbi hataweza kutoka tena katika mikono ya Mossad hivyo sina cha kuhofia.Ninayo nafasi kubwa na hata Peniela mwenyewe ananipenda pia” Mlango wa chumbani ukafunguliwa Peniela akarejea na haraka haraka Nahum akaificha simu yake “Nimerejea” akasema Peniela na kujirusha kitandani na kumwagia mabusu Nahum “Vipi watoto wanaendeleaje?akauliza Nahum “Tayari wamekwenda shule.Nimekosa kuwasalimu asubuhi hii” “Napenda namna unavyowapenda wanao” akasema Nahum “Ni kweli ninawapenda sana Malaika na Patrick.Unajua watoto hawa si wa kuwazaa mimi” “Siyo wanao? “Si wanangu wa kuwazaa lakini baba yao ni Mathew.Kuna wakati mimi na yeye tuliwahi kukwaruzana na kila mmoja akaenda kuendelea na maisha yake na huko alikoenda aliishi na mwanamke mwingine na wakazaa watoto wawili kwa bahati mbaya Yule mwanamke alifariki na kumuachia Mathew watoto.Tulipomaliza tofauti zetu na kurudiana niliwachukua na kuanza kuwalea kama mama yao.Kwa sasa baada ya baba yao kufariki mimi nimebaki ndiye baba yao na mama yao” akasema Peniela Nahum akabaki kimya “Masikini Peniela hajui kama mume wake yuko hai anaendelea kupata mateso makali.Kwa nini tunawatesa watu namna hii?Kila mtu tayari anafahamu kuwa Mathew Mulumbi amefariki dunia.Hata watoto wake wanajua baba yao hayup….” “Nahum ! akaita Peniela na kumstua Nahum kutoka katika mawazo “Mbona umezama katika mawazo ghafla?akauliza Peniela “Kuna kitu nimekumbuka nitakueleza siku nyingine.Vipi kuhusu watoto wako uliozaa na Mathew wako wapi? “Mimi na Mathew tumezaa watoto wawili na wote wako masomoni Canada.Unatamani kuwaona? “Nina hamu sana ya kuonana nao.Unadhani watanikubali?Unadhani ninaweza kuvaa viatu vya baba yao? Akauliza Nahum.Peniela akamtazama na kutabasamu “Hakuna atakayeweza kuvaa viatu vya Mathew.Ni mwanaume wa pekee kabisa ambaye mguu wake ni mkubwa na kila atakayejaribu kuvaa viatu vyake vitampwaya.Mathew atabaki kuwa Mathew” akasema Peniela “Kwa kunitazama unadhani ninaweza kuwa na asilimia ngapi ya Mathew?akauliza Nahum na Peniela akacheka “Wewe bado mtoto wa mama,umekulia katika utajiri hujui kuhangaika huwezi kuwa hata na asilimia moja ya Mathew.Kidogo labda pumzi ya kitandani lakini hata hapo bado huwezi kumfikia Mathew.Yule alikuwa na mapafu ya farasi.Mwendo wake si wa kawaida” akasema Peniela na Nahum akamrukia “Kumbe unawapenda wanaume wenye mapafu ya farasi basi ngoja nikuonyeshe kwamba si Mathew pekee mwenye mapafu ya farasi” akasema Nahum na kuanza utundu wake lakini peniela akamsukuma “Nahum hatuwezi kufanya saa hizi tunatakiwa kwenda katika kikao cha bodi leo kujadili kuhusiana na ule mradi wa mvinyo tunaotaka kuanzisha” Peniela alipogusia masuala ya bodi Nahum akapatwa na mstuko mkubwa “Peniela kwa nini tusiahirishe kikao hicho hadi siku nyingine?Leo ninataka nipate muda mwingi wa kuwa nawe au wewe hupendi tupate muda wa kutosha wa kuwa pamoja?Kama ni miradi tutafanya tu.Wewe ni bilionea mimi ni bilionea hivyo hatuna shida na pesa.Maisha haya ni mafupi sana kwa kuwa tayari tunazo pesa basi tujipe muda wa kutosha wa sisi kufurahi.Hakuna anayejua kesho yake.Sitaki itokee nimekufa halafu huko niliko nijilaumu kwa nini sikutumia muda wangu vizuri na Peniela” akasema Nahum na Peniela akatabasamu “Unataka kikao kifanyike lini? “Baada ya siku nne kutoka sasa” “Siu nne? “Ndiyo.Nataka siku hizi zote niwe nawe tukistarehe tu.Peniela maisha haya ni mafupi sana huwezi kujua nini kinaweza kutokea kesho hivyo basi tutumie vyema muda tunaoupata” akasema Nahum na kumvuta Peniela akambusu na kuanza utundu wake haukupita muda kipute kikaanza. **************** Jopo la madaktari bingwa wa upasuaji wa plastiki lilikamilisha upasuaji wa kubadili muonekano wa Theresia Muganza kwa mafanikio makubwa.Upasuaji huu ulifanyika kwa siri kubwa katika hospitali moja kubwa ya jeshi na baada ya upasuaji kukamilika Theresa alihamishiwa katika jumba moja kubwa linalomilikiwa na Rais wa Ufaransa kwa ajili ya mapumziko.Kwa ajili ya Theresa jumba hilo liliwekwa vifaa mbali mbali vya matibabu ambavyo vingehitajika wakati wa kumuuguza na madaktari waliendelea kukaa karibu na Theresa kumuhudumia.Kazi yao haikuwa imekamilika bado hadi pale ambapo bandeji alizofungwa katika sehemu mbali mbali za mwili wake zitakapoondolewa ndipo kazi yao itakapokuwa imekamilika. TEL AVIV – ISRAEL Ni siku ya pili tangu Mathew Mulumbi aginizwe katika chumba alimo Ammar Nazari kiongozi wa kundi la wanamgambo la Ammar Nazar Brigades.Toka ameingia ndani ya chumba kile Mathew hakufungua mdomo wake kutamka hata neno moja.Licha ya kutotaka kuzungumza Mathew hakuweka kitu chochote mdomoni.Hali ile ilimtisha sana Ammar ambaye alijitahidi kwa kila namna kumsaidia Mathew aweze kula lakini ilishindikana.Mathew Mulumbi alianza kutetemeka mwili ikamlazimu Ammar kubonyeza kitufe kilichokuwa karibu na mlango na mara wakafika askari sita. “Kuna nini humu?akauliza mmoja wa askari wa gereza “Huyu mtu ameletwa humu ndani ni siku ya pili leo hazungumzi wala hataki kula chakula wala kunywa chochote.Hali yake inazidi kuwa mbaya.Anahitaji msaada anaweza akapoteza maisha” akasema Ammar.Mlango ule mkubwa ukafunguliwa askari wakaingia ndani na kumuinua Mathew Mulumbi wakambeba wakamtoa mle ndani mlango ukafungwa “Ni nani Yule mtu?Ni mtu wa ajabu sana Yule.Toka ameletwa humu ndani hajafungua mdomo wake kutamka chochote,hataki kula wala kunywa.Nini hasa lengo lake?Anataka kufa?Anaonekana amekata tamaa kabisa hasa kutokana na mateso makali aliyoyapata.Ameteswa mno.Ana vidonda kila sehemu ya mwili wake.Nahisi kuna jambo kubwa amelifanya lililompelekea akateswa kiasi kile.Hata hivyo anaonekana ni mtu jasiri sana.Natamani kumjua zaidi” akawaza Ammar Mathew baada ya kutolewa mle chumbani akapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya gereza,hali yake haikuwa nzuri kutokana na kukosa nguvu.Haraka haraka akaanza kuhudumiwa.Efraim Dagan alikuwepo pale hospitali kuhakikisha kila kitu kina kwenda vizuri kwa mujibu wa mpango wao. Baada ya saa tatu Mathew tayari alikuwa anajihisi vizuri akatolewa ndani ya kile chumba akapelekwa katika ofisi ya mkuu wa gereza ambako alimkuta Efraim dagan na watu wengine watatu “Hongera Mathew kazi nzuri sana.Tumefuatilia kwa makini toka ulipoingia mle ndani ya kile chumba na mpaka sasa kila kitu kimekwenda vizuri” akasema Efraim “Nimekuwa nikimsoma Ammar anaonekana ni mtu ambaye anataka sana kunifahamu nimetoka wapi na nimefanya nini.Amekuwa akiniuliza maswali kila mara kuhusu hilo na kubwa zaidi alichotaka kufahamu ni kama nimeua muisrael.Nadhani sintapata ugumu kujenga naye urafiki” akasema Mathew “Tumemaliza awamu ya kwanza na sasa tunaingia awamu ya pili ambayo ni kujenga urafiki na Ammar halafu kutoroka gerezani.Mpango wa kutoroka gerezani unaadaliwa na kabla ya kukueleza namna utakavyotoroka hapa gerezani na Ammar tunataka kwanza kujiridhisha kwamba urafiki madhubuti kati yako na Amar umejengeka.Tukijiridhisha kuwa Ammar yuko tayari kutoroka gerezani tutakuwekea kitu Fulani chini ya sahani ya chakula.Hakikisha kila unapopewa chakula unapitisha mkono chini ya sahani na utakapokuta kuna ktu kimebandikwa chini ya sahani ya chakula ujue kwamba muda umefika.Askari atakayepita kukusanya vyombo utamvamia na kutaka kumshambulia lakini askari wengine watakudhibiti na kukutoa mle ndani kisha utaletwa hapa ofisini na kuelekezwa namna utakavyoweza kutoroka pale gerezani” akasema Efraim “Mpaka hapa tayari amekwisha onyesha kutaka kunifahamu na kuwa karibu nami.Amekuwa mwema kwangu na ananionea huruma.Nitakaporejea kazi itaanza” akasema Mathew “Kuwa mwangalifu sana Mathew,Ammar anaweza akaonekana ni mtu mwema machoni lakini ni mtu hatari sana usimuamini haraka.Jina utakalotumia ni Abu Al zalawi,raia wa Kenya mwenye asili ya Misri.Baba yako aliitwa Khalid Al Zalawi.Alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kundi la Abu Hafs al-Masri Brigades kundi ambalo linabeba jina la la muasisi wake ambaye ni Abu Hafs kutoka nchini Misri aliyekuwa na mafungamano ya kindugu na aliyekuwa kiongozi wa kundi la Alqaeda Osama Bin Laden baada ya binti yake kuolewa na mtoto wa Osama.Baba yako Khalid aliuawa na majeshi ya Israel na toka hapo umekuwa ukiendesha mashambulio dhidi ya Israel sehemu mbali mbali duniani.Mama yako alifariki angali u mdogo na aliitwa Dalia.Picha yako itawekwa katika orodha ya watu wanaotafutwa sana na Israel na maelezo hayo niliyokupa ndiyo yatakayoambatana na picha yako.Tunaamini watataka kukufahamu wewe ni nani,utawapa maelezo hayo na lazima watataka kuthibitisha taarifa utakazowapa hivyo wakitafuta watakutana na hayo maelezo kwamba wewe ni mtu hatari unayetafutwa na Israel.Makazi yako yatakuwa ni Nairobi Kenya na hapa unatakiwa uwe unazifahamu vyema sehemu mbali mbali za jiji la Nairobi kwani wanaweza pia wakataka kufahamu mahala unapoishi Nairobi.Nadhani umenielewa Mathew” akasema Efraim “Nimekuelewa Efraim”akajibu Mathew “Mathew kwa kukubali kufanya hivi jina lako linaingia katika orodha ya magaidi lakini ni kwa muda tu hivyo usiwe na wasi wasi wowote.Baada ya kumaliza kazi yako tutakuondoa kutoka katika orodha hiyo” “Sina tatizo na hilo” akajibu Mathew.Wakaendelea kuelekezana halafu Mathew akaachwa apumzike. Alipumzika kwa saa tatu halafu akarejeshwa ndani ya kile chumba alimo Ammar Nazar.Mlango wa chumba cha Ammar ulipofunguliwa Mathew akapigwa teke la mgongo na askari akaangukia ndani kisha mlango ukafungwa.Mathew alijibamiza ukutani na kuanguka chini.Amar aliyekuwa kitandani akainuka haraka na kwenda kumuinua. “hal tadhit?(Umeumia?) akauliza Ammar na kumsaidia Mathew kukaa.Alikuwa ameumia usoni baada ya kujibamiza ukutani na damu ilikuwa inamtoka.Ammar akachukua kitambaa akamsaidia Mathew kufuta damu usoni. “aqad yudhik kathirana(wamekuumiza sana hawa jamaa) akasema Ammar akiendelea kumfuta Mathew damu. “khudh raha (pumzika) akasema Ammar “shukraan jazilaan(nashukuru) akasema Mathew na Ammar akatabasamu “alhamd lilh.hal tastatie altahaduth bialearabia?(Ahsante Mungu.Unaweza kuzungumza kiarabu? “nem fielaan(Ndiyo) akajibu Mathew na tabasamu kubwa likajengeka usoni kwa Ammar “Vipi hali yako kwa sasa?akauliza Ammar kwa kiarabu “Kwa sasa ninaendelea vizuri” akajibu Mathew kwa kiarabu safi “Hali yako ilinitisha sana.Kwa nini ulitaka kujiua kwa kukataa kula?akauliza Ammar “Nimekuwa hapa kwa miaka mitatu nikiteswa kila uchao na hakukuwa na dalili zozote za mimi kutoka hapa ndiyo maana niliona ni bora nife niepukane na mateso haya.Tazama mwili wangu kila sehemu ni vidonda vitupu” akasema Mathew “Sikiliza ndugu yangu mimi nina miaka mitano nimefungwa hapa katika gereza hili.Wapo wengine wana miaka zaidi ya kumi lakini hata siku moja hawajakata tamaa.Bado tuna matumaini kwamba siku moja tutatoka hapa na kuendeleza mapambano.Hatutakata tamaa kuendelea kupambana kwa ajili ya ardhi yetu.Yawezekana sisi tukaishia njiani na tusiuone ushindi lakini kwa sababu ya mapambano yetu ya leo na kutokukata tamaa watoto wa watoto wetu wanaweza wakayaona matunda ya mapambano yetu pale ardhi yetu itakapokuwa imerejeshwa.Gereza hili limejaa mateso.Tunateswa mno lakini hakuna ambaye amewahi kusalimu amri kwao.Japokuwa sisi tuko ndani lakini huko nje naamini mapambano yanaendelea.Nimekueleza haya ili kukupa moyo kwamba usikate tamaa kwa kile unachokiamini” akasema Ammar na Mathew akatikisa kichwa kukubaliana naye “Kwa nini uko hapa?Kwa nini wanakutesa namna hii? Akauliza Ammar “Naitwa Abu Al Zarawi.Ni mtoto wa Khalid Al Zalawi kutokea Misri.Baba yangu alikuwa ni kamanda wa ngazi za juu katika kundi linaloitwa Abu Hafs al – Masri Brigades kundi ambalo muasisi wake ni Mohammed Atef au kwa jina maarufu Abu Hafs ambaye alikuwa mwanachama wa kundi la Ayman al-Zawahiri’s al- Jihad.” “Ninamhamu Ayman al- Zawahiri mmoja wa viongozi wakubwa kabisa wa Alqaeda.Anatajwa ndiye aliyeratibu mashambulio mawili ya mabomu katika balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya.Kwa sasa ndiye aliyechukua nafasi ya Osama Bin Laden baada ya Marekani kumuua” akasema Ammar na Mathew akaendelea “Baba yangu Khalid al- Zalawi aliuawa na majeshi ya Israel na ndipo nilipoapa kulipiza kisasi kwa kuua waisrael kokote waliko duniani.Nilikwenda nchini Kenya nikiwa la lengo la kuanzisha kikundi cha kijihad.Nikiwa Kenya nilimuua mkuu wa Mosad Afrika Mashariki alikuwa anaitwa Avi Abramson.Si huyo tu bali niliwaua pia majasusi wengine wawili wa Mossad na hapo ndipo nilipoanza kusakwa na Israel hadi waliponikamata na kunileta hapa”akasema Mathew na tabasamu kubwa likaonekana usoni kwa Ammar “Kumbe wewe ni mwenzetu.Nilijuliza sana sababu ya wewe kuteswa namna hii nikahisi kwa mateso haya unayoyapata lazima utakuwa umefanya jambo kubwa na ili upate mateso makubwa kama haya lazima uwe umeua waisrael”akasema Ammar “Nilimuua mtu wao muhimu sana na wameniwinda kwa muda mrefu hadi wakanikamata” “Ilikuaje wakakukamata?akauliza Ammar “Kuna rafiki yangu anaitwa Rashid yeye ni mfuasi wa IS aliniomba niungane nao katika mabadilishano ya mateka na watanzania ambao walikuwa wanamshikilia mtu mmoja aliyeitwa Edger Kaka ambaye ana mahusiano na Habiba Jawad” akasema Mathew na sura ya Ammar ikaonyesha mstuko “Habiba Jawad? “Ndiyo.Unamfahamu?ak auliza Mathew “Ndiyo ninamfahamu” “Basi kuna mtu ambaye ana mahusiano naye ya karibu anaitwa Edger Kaka ambaye alikuwa anashikiliwa nchini Tanzania alitakiwa kufanyiwa mabadilishano na watu wawili waliokuwa wametekwa na IS.Tukiwa katika mabadilishano hayo ya mateka tulivamiwa na vikosi vya Israel na wakaniteka wakanileta huku.Pamoja nami alikuwepo pia Edger Kaka ambaye ana mahusiano na Habiba Jawad” akasema Mathew “Ninafurahi kukufahamu Abu Zalawi.Mimi ninaitwa Ammar al-Nazari.Ni kiongozi wa kundi linaitwa Ammar Nazari brigades.Lengo la kundi hili ni kuendeleza mapambano ya kudai ardhi yetu inayokaliwa kimabavu na Israel.Tumekuwa tukifanya mashambulio nchini Israel na tumefanikiwa kuua waisrael wengi.Pamoja na mimi kuwepo hapa lakini bado kundi langu pamoja na makundi mengine yanaendelea na mapambano ya kudai haki yetu na nina uhakika mkubwa iko siku hata kama mimi na wenzangu hatutatoka humu basi lazima haki yetu itapatikana” akasema Ammar Waliendelea na mazungumzo halafu Ammar akauliza “Huyo mtu ambaye unadai ana mahusiano na Habiba Jawad yuko wapi? “Sifahamu yuko wapi kwani nilipofumbua macho nilijikuta sehemu yenye giza na nimeishi mahala hapo nikiteswa kwa miaka mitatu hivyo sifahamu mahala alipo Edger Kaka.Unadhani wanaweza kuwa wamemuua? “Sina hakika kama wanaweza wakamuua.Israel wanamtafuta sana Habiba Jawad lakini bado hawajafanikiwa kumpata mpaka leo hii ndiyo maana wakamteka huyo mtu mwenye mahusiano na Habiba” “Ni nani huyo Habiba Jawad? Mathew akauliza “Ni mtu muhimu sana katika harakati zetu.Ni tajiri mkubwa sana na ambaye ndiye anawezesha harakati nyingi za vikundi mbali mbali kufanyika.Naweza kusema yeye ndiye uti wa mgongo wa vikundi vingi vinavyoendesha mapambano dhidi ya udhalimu wa Israel” akasema Ammar “Natamani siku moja ningekutana naye nimueleze kuhusiana na mtu wake Edger Kaka.Yawezekana haujui mahala alipo kwani ni miaka mitatu imepita sasa tangu tulipotekwa” “Habiba si mtu wa kuonekana kirahisi.Kama tungekuwa nje ya gereza ningeweza kukusaidia ukaonana naye lakini ni mchakato mrefu hadi kumfikia”akasema Ammar na ukimya wa dakika kadhaa ukapita Mathew akasema “Ammar mimi sina lengo la kuendelea kukaa humu gerezani” “Umekata tamaa kuendelea kupambana?akauliza Ammar “Hapana sijakata tamaa lakini siwezi kuendelea kukaa humu ndani ya gereza nikiteseka lazima nitafute namna ya kutoka humu” akasema Mathew na Ammar akaangua kicheko “Abu gereza hili ni moja ya gereza lenye ulinzi mkali sana.Hajawahi kutoroka mtu hapa kutokana na ulinzi uliopo.Hizo ndoto achana nazo kwani utakufa kabla haujatimiza lengo lako.Endelea kusali kumuomba Mungu anaweza akafungua njia na tukatoka lakini suala la kutoroka usiliweke kichwani mwako.Unadhani watu wangu wangeshindwa kuja kunikomboa?Lakini hawawezi kutokana na ulinzi wa mahala hapa” akasema Ammar “Ngoja nikueleze ukweli.Baada ya kutolewa kule kwenye giza nililetwa humu na kwa muda wa siku mbili sikuweza kuzungumza nawe chochote pia sikula wala kunywa.Si kwamba nilikuwa nimedhamiria kufa kama ulivyodhani bali ule ulikuwa ni mpango maalum” “Mpango maalum?akauliza Ammar “Ulikuwa ni mpango maalum ili niweze kutoka humu ndani na kupelekwa hospitali.Kuna mitu nilihitaji kuonana naye” “Ulikuwa unahitaji kuonan na mtu?Kwa dhumuni gani?akauliza Ammar huku akijiweka vizuri “Ni kwa ajili ya mpango wangu wa kutoroka” akasema Mathew “Abu nakushauri tena mpango huo wa kutoroka achana nao utapoteza maisha bure.Tumuombe Mungu atatufungulia milango na siku moja tutatoka humu” “Israel wametumia gharama kubwa kutusaka hivyo hawawezi kutuacha huru.Tutafia humu.Nitajaribu mpango wangu wa kutoroka na kama nikifa nitakuwa nimekufa kishujaa” akasema Mathew “Abu una familia? “Wakati ninakamatwa nilikuwa na mchumba ni mrembo sana anaitwa Nawal lakini mpaka sasa hajui mahala nilipo.Ninampenda sana na yeye ni moja ya sababu za mimi kutaka kutoroka humu gerezani” “Nawal? Ammar akashangaa “Ndiyo.Kwa nini mbona umestuka? “Mke wangu mdogo pia anaitwa Nawal.Imekuwa bahati wote tuna wapenzi wenye majina yanayofanana.Abu kama kweli unampenda huyo mchumba wako Nawal naomba unisikie tafadhali.Usijaribu kutoroka.Ukombozi utakuja.Iko siku tutatoka humu gerezani na kwenda kukutana naye tena” “Ammar tazama nilivyoteseka.Tazama mwili wangu wote una vidonda.Imetosha na sitaki kuendelea tena.Nataka kujaribu kutoroka hapa gerezani.Ninataka nikaendeleze mapambano huko nje.Yawezekana siku moja nikaja kukukomboa hapa gerezani” akasema Mathew “Abu unajiamini vipi kama kweli utafanikiwa mpango wako wa kutoroka?Ammar akauliza “Sijui kama nitafanikiwa lakini lazima nijaribu.Siwezi kukaa humu ndani kusubiri muujiza.Hakuna muujiza utakaotokea hapa lazima nipambane mwenyewe” akasema Mathew na wote wakabaki kimya.Ammar alionekana kuzama mawazoni.Mathew akapanda kitandani akajilaza “Tayari nimerusha ndoano na anaonekana kutaka kuisogelea.Atanasa tu na nitamuondoa humu.Ameniamini kwa haraka sana baada ya kusikia kwamba nimeua waisrael.Nitakapomtoa humu huyu ndiye atakayenipeleka kwa Habiba Jawad kwani amekiri mwenyewe kwamba anamfahamu.Nitakwenda kuukata uti wa mgongo wa ugaidi duniani.Wengi wanawafahamu magaidi wakubwa kama akina Osama,Ayman al-Zawahiri na wengine wengi waliouawa na walio hai lakini hawajui watu hawa wanatoa wapi nguvu na uwezo wa kuendesha makundi makubwa ya kigaidi na kupanga mashambulizi ya kigaidi.Yote haya yanawezeshwa na watu kama akina Habiba ambao wanatumia utajiri wao katika kufadhili makundi ya kigaidi.Haitakuwa kazi nyepesi lakini Mungu atanitangulia na nitafanikisha kumuondoa.Kikubwa ni huyu jamaa Ammar lazima anase katika ndoano yangu.Huyu ndiye njia ya kunifikisha kwa Habiba Jawad” akawaza Mathew. Ammar alifungua kitabu alichokuwa nacho akasoma halafu akainua kichwa akamtazama Mathew “Abu ni kweli umedhamiria kutaka kutoroka?akauliza Ammar “Tayari anaelekea kwenye ndoano” akawaza Mathew “Ndiyo Ammar.lazima nijaribu.Siwezi kuendelea kukaa humu ndani.Nimeumizwa sana na lazima nikalipe kisasi.Hii ni vita lazima nipambane.Siogopi kufa.Tumekwisha poteza watu wengi katika haya mapambano wengine ni wa muhimu sana hivyo siogopi chochote.Sisi kama viongozi wa mapambano haya lazima tuonyeshe njia kwa tunaowaongoza kwamba tunapaswa kuendelea kupambana kwa kile tunachokitafuta hata kama ikilazimu kutoa uhai wetu.Mimi nitaondoka hapa gerezani kama nikishindwa nitakufa nikiwa nimejaribu” akasema Mathew baada ya sekunde chake Ammar akauliza “Umepanga kutoroka vipi? Akauliza Ammar.Mathew hakumjibu “Abu tayari unao mpango wowote wa kukuwezesha kutoroka?akauliza tena “Ammar kwa kuwa wewe ni mwenzangu ntakueleza ukweli.Toka nilipoletwa hapa nilikuwa ninatafuta namna ya kuweza kutoroka ndipo nikakutana na daktari moja anaitwa Abeba anatothea Ethiopia anafanya kazi katika hospitali ya gereza.Nilipelekwa hospitali nikiwa sijitambui akanihudumia nikapata nafuu alinionea huruma sana na akaahidi kunisaidia kutoroka.Alisema ananiandalia mpango wa kutoroka na utakapokuwa tayari atanijulisha” “Anakuandalia mpango gani? Akauliza Ammar “Ananiandalia ramani ya gereza na njia za kupita ili niweze kufanikiwa kutoroka.Nilipoletwa hapa chumbani kwako nilikuwa natafuta namna ya kuweza kuonana tena na Abeba nijue amefikia wapi kuhusu ramani ile aliyokuwa ananiandalia ndiyo maana nikatumia njia ile ya kugoma kula chakula ili nipelekwe hospitali na mpango wangu ulifanikiwa nilionana na Abeba akanieleza kwamba ndani ya siku tatu niende tena hospitali atakuwa amefanikisha kuipata ramani hiyo.Nina uhakika nikiipata na kujua njia za kupita nitaondoka hapa gerezani” akasema Mathew “Huyo Abeba imekuwaje hadi akaamua kukusaidia kutoroka?Haogopi kugundulika? Akauliza Ammar “Mimi ndiye niliyemuomba anisaidie niweze kutoroka hapa gerezani.Alinionea huruma kwa mateso niliyokuwa nayapata akaahidi kuisaidia” “Una uhakika atakusaidia au anakuweka katika mtego? “Nina uhakika atanisaidia” “Unamuamini vipi? “Ninao uwezo wa kumsoma mtu kama ana maanisha anachokisema au ananidanganya na kwa Abeba nina uhakika anamaanisha anachokisema” akasema Mathew.Zilipita dakika tatu za ukimya halafu Ammar akauliza “Endapo mpango wako wa kutoroka utafanikiwa utakwenda wapi? “Bado sijajua nitaelekea wapi lakini nitakapokuwa nimetoka nje ya gereza nitajua nielekee wapi.Nina mpango wa kujiunga na kikundi kimoja wapo cha jihad niendeleze mapambano dhidi ya Israel.Sina mpango wa kurejea tena Kenya kwani hawa jamaa watanifuata kule”akasema Mathew na kukawa kimya.Ammar akaendelea kusoma kitabu chake. DAR ES SALAAM - TANZANIA Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo alipomaliza kikao na wageni wake waliofika kumtembelea akarejea ofisini kwake na kumpigia simu Benjamin Hudson balozi wa umoja wa ulaya nchini Tanzania “Mheshimiwa Rais habari za muda huu?akauliza Balozi Benjamini baada ya kupokea simu “Habari nzuri mheshimiwa balozi” “Ahsante sana mheshimiwa Rais kwa kunipigia simu ninategemea ni kuhusiana na lile suala tulilozungumza asubuhi” “Ni kweli ni kuhusiana na lile suala.Mheshimiwa balozi nimekupigia kukujulisha kwamba msimamo wangu haujabadilika bado ni ule ule kwamba hakuna mchunguzi yeyote wa kimataifa atakayeruhusiwa kuingia nchini kufanya uchunguzi wa mauaji ya Lucy na Laurent Muganza.Uchunguzi utafanywa na vyombo vya ndani na vitatoa taarifa kwa hiyo naomba ufikishe ujumbe huo kwa umoja wa Ulaya” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ninashukuru kwa majibu hayo na nitayafikisha sehemu husika kama yalivyo” “Kingine mheshimiwa balozi nakuomba usithubutu kuendelea kufanya mambo yasiyokuhusu.Endapo utarudia tena kufanya mambo yaliyo nje ya majukumu yako nitakufukuza nchini” “Nimekuelewa mheshimiwa Rais na ahsante sana kwa ushirikiano wako” akasema balozi Benjamin na Dr Fabian akakata simu Dakika ishirini baada ya kuzungumza na balozi Benjamin simuni,akaingia ofisini mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais akiwa na kompyuta ndogo “Mheshimiwa Rais kuna jambo ambalo nadhani unapaswa kulijua” akasema na kumuonyesha Rais ujumbe wa twitter aliouandika balozi Benjamin.Katika ujumbe wake Benjamin aliwaonya watu wanaotoka nchi za umoja wa Ulaya kuchukua tahadhari kubwa wawapo nchini Tanzania na kuwataka wale wanaopanga kuja Tanzania kutafakari mara mbili “Mshenzi huyu !! akasema kwa hasira Dr Fabian na kugonga meza. “Si huyu peke yake aliyefanya hivi bali hata Rais wa Ufaransa Michael Weren naye ameandika katika ukurasa wake” akasema mkurugenzi Yule wa mawasiliano wa rais.Rais Michael yeye aliwaonya raia wa Ufaransa wanaotembelea Afrika mashariki akawataka wawe waangalifu sana kutokana na hali ya usalama kutokuwa ya kuridhisha. “Tunafanya nini kuhusu kauli hizi mheshimiwa rais? “Kwa sasa hatufanyi chochote.Nipe muda kidogo wa kufikiria nini cha kufanya” akasema Dr Fabian na kuegemea kiti chake “Dr Evans alikuwa sahihi kwamba tunaingia vitani na tayari vita imeanza.Kauli hizi mbili za balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini na ya rais wa Ufaransa zote zinalenga kuitangazia dunia kwamba Tanzania si mahala salama kutembelea wala si mahala salama kuwekeza.Idadi ya watalii itapungua sana na tutapoteza fedha nyingi za kigeni,mapato ya nchi yatapungua kwani utalii unaingizia nchi fedha nyingi sana.Kushuka kwa mapato ya serikali ni chanzo cha miradi mingi ya maendeleo kushindwa kutekelezeka,huduma za kijamii kuzorota na uchumi kushuka.Hicho ndicho wanachokitaka hawa jamaa kutudidimiza kiuchumi na tuone kwamba hatuwezi kupiga hatua bila wao” akawaza Dr Fabian “Vita ya uchumi kama alivyosema Dr Evans ni vita mbaya sana na kupigana kwake hakuhitaji mabavu.Ni akili nyingi inapaswa kutumika.Kwa sasa hatutawajibu chochote kufuatia kauli zao walizozitoo katika mitandao.Tutakaa kimya huku tukijipanga namna bora ya kuweza kukabiliana na misuko suko mikubwa inayokuja mbeleni.Kitu kikubwa kwa sasa ni kumfuatilia balozi Benjamin kufahamu nyendo zake.Nataka kujua anashirikiana na akina nani hapa nchini.Naamini hayuko peke yake bali kuna watu anaoshirikiana nao ambao walimpa taarifa zile za Tanzania kumiliki aina ya bunduki za udunguzi ambazo zinadhaniwa ndizo zilitumika kuwaua Lucy na Laurent Muganza.Namshukuru Dr Evans kwa kunishauri vyema kwani bila ushauri wake hivi sasa tayari ningekwisha mtimua nchini Yule balozi.Ngoja niwe mvumilivu niusome mchezo huu unakwendaje sitakiwi kwenda kichwa kichwa….”akawaza Dr Fabian





Saa moja za jioni Austin January aliwasili ikulu kama alivyokuwa ametakiwa na rais.Kabla ya kupata chakula wakaelekea sehemu ya mapumziko ambako Rais alikuwa na mazungumzo na Austin. “Austin karibu tena ikulu.Mahala hapa utafika mara nyingi sana wakati wa uongozi wangu na tafadhali usichoke” akasema Dr Evans “Siwezi kuchoka mheshimiwa Rais ni heshima kubwa kwangu kuwepo hapa”akajibu Austin “Austin nilikueleza awali kwamba wewe utakuwa msiri wangu na nitakushirikisha katika mambo makubwa ya nchi na ninaamini kwamba yale yote ambayo mimi nitakuamini kwayo yatabaki kifuani kwako na utakwenda nayo kaburini” “Mheshimiwa Rais usiwe na shaka kabisa na mimi.Nimeapa kutunza siri utakazonieleza na ninakuahdi kila nitakachoona kusikia au kutenda nitakwenda nacho kaburini.Si mimi tu bali na timu nzima ninayoshirikiana nayo katika kazi mbali mbali utakazotupa” “By the way wanaendeleaje wenzako?Natamani sana kukutana nao nitapanga muda niwaalike tukutane tufahamiane.Fikisha salamu zangu nyingi kwao” “Nitafikisha mheshimiwa rais” “Mapema leo asubuhi alinitembelea balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini anaitwa Benjamin Hudson.Aliniletea ujumbe kutoka umoja wa Ulaya na ujumbe huo unanitaka niwaruhusu wachunguzi wa kimataifa kuja kufanya uchunguzi wa vifo vya Laurent na Lucy Muganza.Vifo vya watu hawa wawili vimewastua na wanahaha hawajui la kufanya na hii inadhihirsha wazi kwamba walikuwa ni watu wao wa muhimu sana na walikuwa na mipango nao mikubwa.Lauret Muganza alikuwa ni mfanyakazi katika umoja wa Ulaya hivyo wanatumia kigezo hicho kulazimisha turuhusu wachunguzi wa kimataifa wakidai eti kuna mpango wa siri wa kuwadhuru maafisa kutoka umoja wa Ulaya hivyo wanataka kujua nani aliyemuua Laurent.Nilikataa kwamba hatuwezi kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kwa kuwa suala hilo linachunguzwa na vyombo vya ndani.Baada ya kuonyesha msimamo wangu wa kutotaka kuwaruhusu wachunguzi kutoka nje akanieleza sababu kubwa inayowafanya watake kuleta watu wao kuja kufanya uchunguzi.Akanionyesha taarifa mbili moja ni taarifa ya awali ya polisi kuhusiana na tukio lile na nyingine ni taarifa ya daktari baada ya miili kufanyiwa uchunguzi.Taarifa ya polisi ilionyesha kwamba tukio lile lilikuwa ni la kijambazi na watu kadhaa waliuawa kuhusiana na tukio hilo lakini risasi zilizokutwa katika miili ya marehemu haziendani na silaha walizokutwa nao hao majambazi.Risasi zilizokutwa katika miili ya marehemu ni za bunduki za hali ya juu sana zinazotumiwa na wadunguaji ambazo majambazi wale hawakuwa nazo.Alienda mbali zaidi na kunieleza kwamba Tanzania tunamiliki bunduki za aina hiyo tulizinunua kutoka marekani.Nilistuka na kukasirika kwa balozi huyu kuanza kufanya mambo yasiyomuhusu kama kufuatilia kuhusu silaha tunazomiliki kama nchi.Nilitamani kumtimua nchini lakini nikapata wazo kwamba yeye peke yake asingeweza kuipata taarifa nyeti kama ile lazima kuna watu anaoshirikiana nao hapa nchini.Kama nikimtimua hatutaweza kuwafahamu watu wanaoshirikiana naye.Tulifanya kosa dogo katika operesheni ile kwamba baada tu ya kuwamaliza akina Lucy hatukuwa na wazo kwamba miili ile ingefanyiwa uchunguzi hata hivyo kosa hilo dogo limetusaidia katika kufahamu kuwa tuna wasaliti humu nchini ambao wamekuwa wakishirikiana na hawa watu”akasema Dr Fabian na kunyamaza akamtazama Austin “Nakubali mheshimiwa Rais tulifanya kosa hilo dogo.Hatukuwa na wazo la kuendelea kufuatilia zaidi baada ya kumuua Lucy na hatukujua kama lingechukua sura mpya namna hii.Tusamehe sana mheshimiwa Rais” “Usijali Austin.Hata mimi mwenyewe sikuwa nikifikiria kitu kama hicho lakini kwa kuwa lengo kuu ambalo ni kumuua Lucy lilitimia hakuna tatizo.Mchana wa leo nilimpigia tena simu balozi nikarudia kumuhakikishia kwamba hakuna mchunguzi wa kimataifa atakayeruhusiwa kuingia nchini.Muda mfupi baadae katika ukurasa wake wa twitter balozi aliandika ujumbe wa kuwaonya watu kutoka jumuiya ya Ulaya wanaotembelea Tanzania kuwa makini.Si yeye peke yake bali hata Rais wa Ufaransa aliandika pia ujumbe wa twitter akiwataka raia wa Ufaransa wanaotembelea Afrika Mashariki kuwa makini kwa sababu za kiusalama.Jumbe hizi mbili zinalenga kuiaminisha dunia kwamba Tanzania si mahala salama kutembelea au hata kuwekeza.Hii inaweza kuwa na athari kubwa sana kiuchumi kwani mapato yatokanayo na utalii yatashuka na watu ambao walitaka kuja kuwekeza nchini hawatakuja tena” “Dah ! akasema Austin “Hii ni vita Austin.Ni vita ya uchumi.Mataifa haya makubwa kwa kila namna yanataka kutudhoofisha kiuchumi ili tuweze kuwapigia magoti na kuwaacha waendelee kutunyonya.Siko tayari kwa hilo.Nitaongoza mapambano haya na nina uhakika mkubwa tutashinda vita hii.Hatutashinda kwa mabomu au vifaru lakini tutashinda kwa msimamo wetu.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa kwanza ni kutambua kuwa tayari tuko vitani na tunapambana na mataifa yaliyotuzidi kila kitu,kiuchumi,kiteknolojia kijeshi hivyo haitakuwa vita nyepesi.Kazi ambayo nataka kuwapa wewe na timu yako ni kumfuatilia balozi Benjamin Hudson kila anachokifanya hapa nchini.Nataka kujua anakotoa siri za nchi.Fautilia mawasiliano yake….” Akanyamaza baada ya kitu Fulani kumjia kichwani. “Mara zote ninapowasiliana na huyu balozi hutumia simu ya mezani ya ofisini kwake au simu ya mezani ya nyumbani sifahamu kama ana simu ya mkononi lakini haya yote ni sehemu ya kazi yenu ya kumchunguza.Chunguzeni kila kitu kuhusu huyu mtu.Nadhani umenielewa Austin” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nimekuelewa sana na nimeelewa nini tunatakiwa kukifanya.Nakutoa wasi wasi kwamba tutaifanya kazi hii kwa umakini mkubwa sana na kujua kila anachokifanya huyu balozi na watu wote anaoshirikiana nao” “Nafurahi kusikia hivyo Austin.Hii ni misheni muhimu sana kwa nchi hivyo naomba ifanyike kwa umakini mkubwa sana.Benjamin anajua anachokifanya na anafanya kwa kujiamini sana hivyo muwe makini mno mnapomchunguza.Naamini umeniuelewa vizuri Austin” “Mheshimiwa Rais nakutoa tena wasi wasi kwamba nitalisimamia jambo hili kwa umakini mkubwa sana.Itanilazimu kuchukua likizo ya mwezi mmoja kazini ili niweze kulishughulikia suala hili kikamilifu” “Ahsante Austin ninakutegemea sana.Tutakapopata kitu chochote kutoka katika uchunguzi huo tutajua nini kifuate lakini kwa sasa nguvu kubwa iwekezwe katika kumfuatilia Benjamin” akasema Dr Fabian. Waliendelea na mazungumzo kidogo kisha wakapata chakula na Austin akaondoka.Alipotoka tu nje ya ikulu akampigia simu Gosu Gosu “Papaa uko wapi? “Ninaelekea nyumbani.Leo nimechoka sana nataka nikapumzike” “Sawa Papaa ninakuja hapo nyumbani kwako nisubiri” akasema Austin “Rais yuko sahihi tulifanya kosa kujiamini kwamba tumemaliza kazi kumbe tukasahu kama maiti zile zingeweza kufanyiwa uchunguzi na kujua ni risasi za aina gani zilizowaua akina Lucy.Anyway makosa madogo madogo kama haya huwa yanajitokeza kitu cha muhimu ni kujitahidi kuwa makini kusitokee tena makosa yoyote kama hili.Lakini kwa upande wa pili kosa tulilolifanya limemuibua balozi Benjamin na sasa tunajua tunapambana na watu wa aina gani.Kama tungefuatilia na kuchukua zile risasi tusingejua kama kuna mtu ambaye anazo siri za nchi na hatujui anazipata wapi.Tutamuonyesha kwamba Tanzania si nchi ya mchezo.Wametuzidi kwa kila kila kitu lakini tutawapa somo la kujifunza na hawatathubutu tena kutuchezea” akawaza Austin





Baada ya Austin kuondoka Dr Fabiana alijihisi mchovu naye akaelekea chumbani kwake kujipumzisha.Siku hii hakutaka hata kutazama taarifa ya habari.Millen alimfahamu vyema mumewe na alijua kuna jambo linamsumbua hivyo akamfuata chumbani na kupanda kitandani akajilaza pembeni yake akambusu “Pole sana Fabian.Haya mambo yatakwisha.Usiumize mno kichwa chako na ujipange vizuri namna ya kukabiliana nao” akasema Millen “Tayari unajua kinachoendelea?akauliza Dr Fabian “Ndiyo ninafahamu kuhusu kauli za balozi Benjamin na Rais wa Ufaransa katika mtandao wa twitter zikiwaonya watu wao wawe makini wanapokuja kutembea au kuwekeza Tanzania kwani hali ya kiusalama ni mbaya.Hiyo ndiyo habari kubwa iliyoviteka vyombo karibu vyote vya habari ulimwenguni jioni ya leo” akasema Millen “Millen tayari vita imeanza na hii ni vita ya kiuchumi.Hii inatajwa kama vita mbaya na ngumu kuliko hata vita ya kutumia silaha.lakini Mungu yuko nasi na atatupigania tutashinda” “Fabian uko sahihi tutashinda hii vita japo tutakuwa tumeumizwa sana kwani kauli zile mbili tu tayari zina athari kubwa kiuchumi.Pato litokanalo na utalii litashuka na mambo yetu mengi hapa nchini kushindwa kufanikiwa”akasema Millen “Haitaishia hapo Millen mambo ndiyo kwanza yameanza na yatakuja mengi makubwa zaidi ya hilo.Tutawekewa vikwazo vya kiuchumi,tutafungiwa masoko ya bidhaa zetu na mambo kadha wa kadha ili mradi kutudhoofisha.Mimi kama kiongozi wa nchi ninasema nitapambana kuhakikisha Tanzania inasonga mbele na hatutasalimu amri kwao.Nitawaeleza wananchi wangu washikamane kuipigania nchi yao na umoja huo ndio utakaotufanya tushinde vita hii” akasema Dr Fabian “Nina wazo Fabian ambalo linaweza kuwa na msaada” akasema Millen “karibu” “Lengo la kauli zile mbili zilizotolewa kuhusu usalama Tanzania ni kuihakikishia dunia kwamba Tanzania si salama hivyo watalii na wawekezaji wasije.Ni vipi kama ninaweza kuitisha mkutano mkubwa wa wake za marais kutoka ulimwenguni kote na mkutano huo ukafanyika hapa Dar es salaam? “Can you do that?akauliza Dr Fabian akainuka na kukaa “Yes I can.Ninaweza kuitisha mkutano mkubwa wa wake za marais duniani na ukafanyika hapa Dar es salaam.Ni gharama kubwa itatumika lakini hii itasaidia kuuonyesha ulimwengu kwamba Tanzania ni sehemu salama kwani wake za marais watakuja na kuondoka salama.Kama mkutano huo ukifanikiwa itakuwa ni jibu kwa hao mabeberu kwamba Tanzania ni nchi salama na amani imetamalaki” “Una akili nyingi sana Millen.Sina cha kumlipa Mungu kwa kunipa mwanamke mwenye upeo mkubwa kama wewe.Sikuwa na wazo kama hilo.Ni wazo kubwa na kama likifanikiwa itakuwa ni ushindi mkubwa kwetu.Ahsante kwa hilo Millen” akasema Dr Fabian “Sambamba na hilo nashauri kufanyike kampeni mbali mbali kama vile za kutokomeza malaria nchini ili mradi tu kampeni hizo ziwe kubwa na za kitaifa na katika uzinduzi wa kampeni hizo waalikwe wanamuziki wakubwa wa kimataifa wa kutoka Marekani na kwingineko na yafanyike matamasha makubwa ya muziki.Wanamuziki wale wakubwa wanafuatiliwa duniani kote na kama akifanya tamasha Tanzania basi dunia nzima watafahamu na huu utakuwa ni ujumbe kwa dunia kwamba Tanzania ni nchi salama.Wapo vijana waliobobea katika masuala hayo ya burudani unaweza ukakaa nao mkajadiliana na kikubwa ni kuwawezesha.Hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa kujibizana na hawa jamaa sisi tutawajibu kwa namna nyingine kabisa na dunia itatuelewa”akasema Millen “Ahsante sana Millen kwa mawazo hayo makubwa na mazuri.Tuanze kuyafanyia kazi.Japo ni gharama kubwa lakini kama yakifanikiwa itakuwa ni faida kubwa sana kwetu” “Usihofu kuhusu gharama kwani jambo tunalolifanya lina manufaa makubwa kuliko gharama tutakazotumia.Hata hivyo gharama zote zitakuwa chini ya taasisi yangu na tutaanza kwa kuwatafuta wafadhili hasa wa ndani.Nitazungumza na wafanya biashara wakubwa ambao watatumia mkutano huo kutangaza biashara zao nao watatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha mkutano huo.Licha ya kutumika kuitangazia dunia kwamba Tanzania ni nchi ya amani lakini pia mkutano huo utakuwa na manufaa kiuchumi.Wanawake hao hawatakuja peke yao watakuwa wameambatana na ujumbe mkubwa.Mahoteli yetu yatajaa watu,wajasiriamali watauza bidhaa zao.Tutapanga vile vile safari ya kwenda katika mojawapo ya vivutio vyetu vilivyopo hapa nchini na tutatumia fursa hiyo kutangaza pia utalii wetu na lengo la hao mabeberu litakwama kwani watalii wataendelea kumiminika kila uchao hapa nchini kwetu” akasema Millen “Millen sijui nikushukuruje kwa mawazo kama haya.Sikuwahi kabisa mkufikiria kitu kama hicho” “Usijali mheshimiwa Rais niko nyuma yako nitasimama nawe katika vita hii na tutashinda.Ukiwa na tatizo lolote tafadhali niamini” akasema Millen





Austin alifika nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambako kwa sasa anaishi Gosu Gosu.Alimkuta Gosu Gosu akimsubiri akamkaribisha kinywaji “Kwa muonekano huo lazima utakuwa umetoka ikulu” akatania Gosu Gosu na Austin akaangua kicheko kikubwa “Hujakosea Papaa.Ni kweli nimetoka ikulu.Niliitwa na Rais” akasema Austin “Kila utokapo kuonana na Rais na ukanitafuta lazima kunakuwa na tatizo.Kuna nini leo?akauliza Gosu Gosu.Austin akaenda katika friji akachukua bia baridi akanywa funda kadhaa halafu akasema “Kuna tatizo Papaa.Kwanza katika ile misheni yetu ya hivi majuzi kuna kosa dogo tulilifanya” akasema na Gosu Gposu aliyekuwa ameishika glasi akitaka kuipeleka mdomoni akaiweka chini ‘Tulikosea nini? Akauliza Gosu Gosu akionekana kuwa na wasi wasi “Usiwe na wasi wasi Papaa.Misheni ilikwenda vyema lakini ni kosa dogo tulilifanya.Baada ya kumuua Lucy tulidhani tumemaliza kazi kumbe tukasau kama tumeacha risasi katika miili ya marehemu” “Jesus ! Gosu Gosu akastuka “Miili ya marehemu ilifanyiwa upasuaji na kutolewa risasi na baada ya kuzichunguza wakagundua kwamba risasi zile ni za bunduki kubwa za udunguaji ambazo wale majambazi tuliowauzia kesi hawakuwa nazo.Kufuatia sintofahamu hiyo umoja wa Ulaya unataka kuleta wachunguzi wa kimataifa waingie nchini kulichunguza suala lile lakini kwa bahati nzuri Rais ameweka msimamo kwamba hakuna mchunguzi wa kimataifa ambaye ataruhusiwa kuingia nchini kwani suala lile la mauaji ya Lucy na mumewe linachunguzwa na vyombo vya ndani.Balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini anaitwa Benjamin Hudson alimueleza Rais kwamba anayo taarifa kwamba Tanzania tulinunua bunduki za aina ile kutoka Marekani hivyo kama hataruhusu wachunguzi wa kimataifa kutakuwa na wasi wasi kwamba kuna kitu Tanzania tunakificha kuhusiana na mauaji yale ya Lucy.Kuna kila dalili kuna kitu wanakifahamu kuhusu mauaji yale lakini bado hawana uhakika wanatafuta ushahidi ndiyo maana wanashinikiza kuruhusu wachunguzi wa kimataifa.Pamoja na shinikizo lote alilopewa Rais lakini bado ameshikilia msimamo wake kwamba hakuna mchunguzi yeyote wa kimataifa atakayeruhusiwa nchini.Alasiri ya leo balozi Benjamin Hudson na Rais wa Ufaransa kwa nyakati tofauti wote wameandika ujumbe katika kurasa zao za twitter wakiwaonya raia wa Ufaransa na wale wanaotoka katika nchi za jumuiya ya Ulaya kuwa waangalifu wanapokuwa nchini Tanzania au kufikiria mara mbili.Matamko haya yanalenga kupunguza idadi ya watalii na wawekezaji wanaokuja nchini hivyo kuzorotesha uchumi wetu.Haya yote yameibuka baada ya kifo cha Lucy Muganza na sasa tunapata picha ya wazi kwamba Lucy Muganza alikuwa ni mtu muhimu sana kwao na walipanga kumtumia katika mipango yao miovu dhidi ya nchi zetu.Baada ya njama zao kushindwa sasa tumeingia katika vita ya uchumi nao na baada ya matamko haya mawili ya leo tutegemee mambo mengine makubwa zaidi” akasema Austin “Dah ! Kumbe hatukukosea kumuondoa Yule mama kwani alikuwa kibaraka wa mataifa makubwa” akasema Gosu Gosu “Hatukukosea kabisa kumuondoa lakini sasa tunaanza kuona athari za kile tulichokifanya.Tumeuondoa mtu muhimu kwa mataifa makubwa ambayo yametuzidi kwa kila kitu na siyo siri tunawategemea wakubwa hawa katika ukuaji wa uchumi wetu hivyo basi tutegemee kukumbana na misukosuko mikubwa.Mashambulizi makubwa hivi sasa yanaelekezwa moja kwa moja kwa Rais wetu kwa lengo la kumdhoofisha na kama akionekana kuwa imara zaidi wanaweza wakamuondoa madarakani kwa njia zozote zile hata kwa kumuua kwani uwezo wanao.Tuna kazi kubwa ya kumsaidia Rais wetu katika mapambano haya.Vita hii inapiganwa nje na hata ndani.Kuna watu wako humu nchini ambao wanashirikiana na mabeberu hao katika kuihujumu nchi na kumdhoofisha Rais.Ushahidi wa hilo ni taarifa ya silaha aliyonayo balozi Benjamin.Balozi Yule hawezi kuipata taarifa ile nyeti kama hakuna mtu au watu anaoshirikiana nao.Tujiulize kama balozi huyo ameweza kujua tunazo bunduki ngapi aina ya Barret M82,ni mambo mangapi ya siri anayafahamu kuhusu nchi yetu? Nani wanampa taarifa hizi za siri? Hiyo ndiyo kazi ambayo rais anataka tuifanye.Tumchunguze balozi Benjamin Hudson na tufahamu nyendo zake na anapata wapi taarifa zile za siri” “Kweli hii ni vita.Kwa nini Rais asimtimue nchini? He’s spying on us ! akafoka Gosu Gosu “Angeweza kumtimua hata usiku huu lakini kikubwa anachokitaka Rais ni kufahamu watu anaoshirikiana nao huyu balozi wanaompa taarifa nyeti za nchi.Kama akimtimua hatutaweza kuwajua wasaliti hao” akasema Austin “Nini hasa Rais anataka tukifanye katika suala hili?Gosu Gosu akauliza “Rais anataka tumchunguze balozi Benjamin.Tujue kila anachokifanya,watu anaokutana nao na watu anaowasiliana nao.Kikubwa hapa ni kujua anashirikiana na akina nani”akasema Austin “It’s a taugh mission.Kumchunguza mtu mkubwa kama huyu si kazi nyepesi.Hapa ndipo ninapomkumbuka Mathew Mulumbi.Misheni kama hizi zilimfaa sana” akasema Gosu Gosu “Papaa,Mathew is not here.It’s just us.Tunaweza kufanikiwa hata kama Mathew Mulumbi hayupo.Mimi nimewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi kwa muda mrefu nina uzoefu mkubwa katika masuala haya hivyo usihofu.” “Ninakuamini Austin lakini siwezi kumsahau Mathew.Nimekuwa naye katika misheni mbalimbali.Tunaanzia wapi katika misheni hii? akauliza Gosu Gosu “Kwa kuanzia ni nyumbani kwa balozi.Tunapaswa kumchunguza kila anachokifanya nyumbani kuanzia anapoamka asubuhi anafanya nini.Tutamfuatilia anapotoka kila anakoenda na kuwafahamu watu wote anaokutana nao na kufanya nao mazungumzo.Tujue anazungumza nini nao.Si kazi nyepesi hii” akasema Austin “Ndiyo maana nilisema awali kwamba ni kazi nzito.Sisi wawili peke yetu hatuwezi.Lazima tuongeze timu yetu iwe kubwa.Tupate watu ambao watakuwa wakimfuatilia balozi toka atakapoondoka nyumbani kwake na watu hawa lazima wawe wakibadilika badilika na hata magari watakayokuwa wakitumia lazima yawe yakibadilika.Ni zoezi pia ambalo litahitaji fedha” “Uko sahihi papaa tunahitaji kuongeza watu.Kuna watu wangu watatu wako likizo nitazungumza nao ili niwajumuishe katika timu hii ninawaamini sana.Kuhusu fedha usijali tuko vizuri.Rais amenipa kadi ya akaunti Fulani ya benki na kunitaka nitoe kiasi chochote cha fedha nitakachokihitaji hivyo hakuna wasiwasi wowote wa ukosefu wa fedha.Tutaanza kwa kuingia nyumbani kwa balozi kisha tutafunga kamera za siri ambazo zitatusaidia tuweze kumfuatilia balozi nyumbani kwake kila anachokifanya.Tutasikia mazunguzo yake yote” akasema Austin na kukumbuka kitu “Nimekumbuka rais alinieleza kwamba balozi huyu hana simu ya mkononi au kama anayo huitumia kwa siri.Mawasiliano yake yote hutumia simu ya mezani ya ofisini na simu ya mezani ya nyumbani” “Balozi wa umoja wa Ulaya ni mtu mkubwa na haiwezekani akakosa simu ya mkononi.Anawasiliana vipi na wenzake pale anapokuwa mbali na simu ya mezani ya ofisini kwake au ya nyumbani?Nimepata wazo” akasema Gosu Gosu “Wazo gani papaa?akauliza Austin “Ruby anaweza akatusaidia sana kujua mawasiliano ya balozi huyo” “Ruby? “Ndiyo.Umeshamsahau? “Hapana siwezi kumsahau Ruby yule mchawi wa kompyuta.Uwezo wake wa kucheza na kompyuta unashangaza sana.Yuko wapi hivi sasa? Mnawasiliana? akauliza Austin “Kwa sasa Ruby anafanya kazi Mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza, GCHQ” “Anafanya kazi GCHQ? Akauliza Austin “Ndiyo anafanya kazi katika mamlaka hiyo” “Hawajakosea walioamua kumuajiri hapo.Anastahili kabisa kuwepo mahala hapo.Watu kama wale walipaswa kuwepo hapa nchini kuisaidia nchi.Una mawasiliano naye? “Ndiyo huwa ninawasiliana naye mara kwa mara.Ninataka atusaidie kutafuta mawasiliano ya balozi Benjamin.Lengo ni kutaka kujua anawasiliana vipi na ofisi yao kuu ya umoja wa Ulaya kama hana simu ya mkononi?akasema Gosu Gosu “Fine.Call her.Naamini atakuwa na msaada kubwa kwetu kwani kwa mahala alipo ana uwezo wa kufahamu mambo mengi ya Benjamin na umoja wa Ulaya” akasema Austin na bila kupoteza muda Gosu Gosu akampigia simu Ruby simu ikapokelewa “Hallow Ruby ! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu nilikwisha kwambia usitumie namba hii kunipigia wakati niko kazini.Nitakupigia baada ya dakika tano” akasema Ruby na kukata simu “Amekata simu?akauliza Austin “Atapiga baada ya dakika tano” akajibu Gosu Gosu Baada ya dakika tano kama alivyoahidi Ruby akapiga simu “Unasemaje Gosu Gosu?akauliza Ruby “Samahani sana Ruby kwa kukupigia katika namba hii” “Usijali.Lakini wakati mwingine nitafute katika namba yangu ya nyumbani na kama ukinikosa acha ujumbe’ “sawa nitafanya hivyo Ruby” “Ulikuwa unasemaje?akauliza Ruby “Ruby nimekupigia nina shida.Kwanza kabisa fahamu kuwa niko na Austin January” “Austin?! Akauliza Ruby “Ndiyo .Niko naye hapa” “Austin January ni jina ambalo sitaki kulisikia kabisa katika maisha yangu.Aliondoka na kumuacha Mathew porini.Sijasahau hilo jambo hata kidogo.Bora usingeniambia uko naye kwani siku yangu tayari imeharibika” “samahani sana Ruby kwa kukuharibia siku.Suala hilo linatutesa sote lakini hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuubali kwamba tumempoteza Mathew na maisha yaendelee”akasema Gosu Gosu na Ruby akasikika akivuta pumzi ndefu “tayari umekata tamaa?akauliza Ruby “Hapana Ruby siwezi kukata tamaa kuhusu Mathew lakini ni wapi tutaanzia kumtafuta? “I’ve never given up on him.Something is telling me Mathew is still alive.Bado nina imani kubwa kwamba siku moja Mathew atarudi.I know Mathew than anyone else and he can’t just die like that” akasema Ruby na ukimya ukapita “I’m sorry Gosu Gosu kila ninapomkumbuka Mathew akili huwa inahama kabisa.Tuyaache hayo.Ulikuwa unasemaje?Najua simu hii haikuwa kwa ajili ya kunisalimu” akasema Ruby “Ni kweli Ruby nimekupigia nina tatizo” “Sema una tatizo gani? “We’re in a mission? “A mission?akauliza Ruby kwa mshangao “Ndiyo.It’s a tough mission” “Hujaachana na hayo mambo?Gosu Gosu usishiriki tena katika hizo misheni utapotea kama alivyopotea Mathew.Don’t trust that Austin” akasema Ruby “Ruby I’m doing this for the Nation and for Mathew” “Nini kinaendelea?Uko kwenye misheni gani?Ruby akauliza “Nadhani ulisikia siku chache zilizopita mwanamke mmoja anaitwa Lucy Muganza na mumewe Laurent waliuawa hapa Tanzania” “Ndiyo nilisikia.Limekuwa suala kubwa kwa sasa”akasema Ruby “We did it” akasema Gosu Gosu “You what? “We killed them” “Usinitanie Gosu Gosu” “Kweli kabisa.Mwanamke Yule alikuwa hatari sana kwa nchi na jumuiya ya Afrika Mashariki.Alikuwa anatumiwa na nchi kubwa kutaka kusambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki ndiyo maana tukamuondoa.Baada ya mauaji hayo umoja wa ulaya wametaka kutuma wachunguzi wa kimataifa kufanya uchunguzi lakini Rais amegoma.Balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini na rais wa Ufaransa kila mmoja katika ukurasa wake wa twitter wameandika ujumbe wakiwaonya watu kutoka nchi za umoja wa ulaya kuchukua tahadhari au kutokufika kabisa Tanzania.Kilichonifanya niombe msaada wako ni kwamba tunamchunguza balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini Benjamin Hudson.Huyu amekuwa akishirikiana na baadhi ya watu hapa nchini na wamekuwa wakimpa siri za nchi.Mpaka sasa tayari anafahamu kuhusu silaha tulizo nazo.Rais alitaka kumtimua lakini amesita kumtimua anataka tuwafahamu kwanza watu anaoshirikiana nao.Ninachotaka utusaidie ni kufahamu mawasiliano yake.Katika uchunguzi wetu tumegundua hana simu ya mkononi tumejiuliza anawasiliana vipi na wenzake? Naomba utusaidie kwa hilo” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu sikushauri uendelee na misheni hiyo.Umeingia katika misheni ya hatari sana” akasema Ruby “Usihofu Ruby I’ll be fine” “Nimekwambia hivyo kwa sababu ninamfahamu Benjamin Husdon ni mtu hatari.Amewahi kufanya kazi ya ujasusi katika shirika la ujasusi nchini Ufaransa.Ni mtu ambaye anafahamu kila kitu kuhusu ujasusi hivyo si mtu rahisi kumfuatilia” “Ruby unanisaidia kwa hilo nililokuomba au?akauliza Gosu Gosu “Nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Ruby na kukata simu Baada ya kusubiri kwa dakika kumi Ruby akapiga “Gosu Gosu kama nilivyokwambia kwamba huyu mtu amekaa muda mrefu sana katika ujasusi hivyo anafahamu kila kitu na amekuwa akichukua tahadhari kubwa katika mawasiliano yake hivyo mawasiliano yake hutumia simu ya satelaiti.Hicho ndicho nilichokipata.Nitaendelea kuchimba zaidi kama nikipata chochote nitakujuza lakini kuweni makini huyo mtu mnayemchunguza ni hatari sana”akasema Ruby “Ruby ninashukuru sana kwa taarifa hizo ambazo nina uhakika mkubwa zitatusaidia.Naomba kama ukipata chochote kingine unachodhani kinaweza kutusaidia basi tujulishe” “Sawa Gosu Gosu nitafanya hivyo” akasema Ruby na kukata simu “Ruby anadai kuwa Benjamin anatumia simu ya Satelaiti kuwasiliana na ofisi yao kuu.Inaonekana huyu jamaa yuko hapa nchini kimkakati zaidi kwani anaonekana ni mtu mwenye kujificha mambo yake na kuchukua tahadhari kubwa.Kuna kitu tutakipata tukiendelea kumchunguza huyu jamaa” “Kama anatumia simu ya satelaiti tunatakiwa kujua anaitumia saa ngapi na akiwa wapi.Kesho asubuhi na mapema nitatuma vijana wawili waende karibu na makazi ya balozi huyo kwa ajili ya kuanza kumfuatilia.Mara tu atakapotoka sisi tutakwenda hapo tukijifanya ni watu wa kutoka Tanesco tunakwenda kukagua mita ya umeme na tutafunga kamera sebuleni,chumba cha kulala balozi,na vyumba vingine tutakavyoona inafaa.Ninao vijana wawili pale kikosini ni wataalamu sana wa hayo mambo watakwenda kuifanya hiyo kazi.Baada ya hapo tutafanya mpango wa kuweka kifaa katika gari lake ili tuweze kujua kila mahala anakoenda na maongezi yote yanayofanyika katika gari” akasema Austin





Saa tano na dakika kumi na nane za usiku Benjamin Hudson balozi wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania aliingia katika ofisi yake ndogo iliyoko nyumbani akafunga mlango.Pembeni ya meza kulikuwa na kasiki dogo akabonyeza namba kadhaa likafunguka akatoa ufunguo akafungua droo ya moja ya kabati lake akatoa sanduku dogo jeusi akaliweka mezani akalifungua.Sanduku lile kwa kuliangalia waweza kudhani ni sanduku linalotumika kubebea nyaraka mbalimbali za kiofisi lakini sanduku hili lilikuwa na matumizi mengine kabisa.Hii ilikuwa ni simu maalum ambayo Benjamin hutumia kuwasiliana na watu wake.Akafungua sehemu Fulani akachomoa eria kama ya redio akaivuta juu halafu akachukua kidude kidogo akakiweka sikioni akabonyeza sehemu anakohifadhi namba akazitafuta namba Fulani akapiga na simu ikapokelewa “Mheshimiwa Rais Michael” akasema Benjamin akiongea kwa lugha ya kifaransa baada ya simu yake kupokelewa. “Benjamin habari za Tanzania?akauliza Rais wa Ufaransa Michael Weren “Huku salama kabisa mheshimiwa Rais” “Benjamin nashukuru sana kwa kazi nzuri uliyoifanya.Mpaka sasa tuna uhakika asilimia kubwa kwamba Tanzania imefanya mauaji yale hilo halina ubishi.Kama wangekuwa hawajafanya wangeruhusu wachunguzi lakini wamegoma kwa vile wanafahamu fika kwamba ukweli utajulikana.Kazi tuliyonayo kwa sasa ni kutafuta je nani alitoa maelekezo ya Lucy na Laurent kuuawa? Na je Tanzania walifanya mauaji haya peke yao au kuna watu walishirikiana nao?Nina uhakika mkubwa kwamba lazima suala hili linahusisha zaidi ya nchi moja.Nina wasiwasi sana na Patrice Eyenga lazima atakuwa anahusika katika suala hili.Ninahisi hivyo kwani baada tu ya kukubaliwa kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki ndipo mauaji yale yakatokea.Hakuna mazungumzo yoyote umeyanasa kuhusu Dr Fabian na Patrice Eyenga wakizungumzia mauaji hayo? Akauliza rais Michael. “Mheshimiwa Rais,nimekuwa ninafuatilia mawasiliano ya Rais Dr Fabian kila siku lakini mpaka sasa sijapata mazungumzo yoyote ya Dr Fabian akizungumza chochote na Patrice Eyenga au hata kuzungumzia suala lile la mauaji ya Lucy” akasema Benjamin “Benjamin tafadhali hakikisha unalichimba suala hili kiundani.Rais ana mbinu njia nyingi za mawasiliano.Unatakiwa kupata kila anachokizungumza.Tunatum ia fedha nyingi sana katika jambo hili hivyo tunahitaji kuona matunda yake” akasema Rais Michael “Mheshimiwa Rais,nimeahidiwa na chanzo changu cha taarifa kuwa kesho kutwa nitapata taarifa nyeti sana na muhimu” “Chanzo kimesema ni taarifa gani hiyo? ‘Bado sijaambiwa ni taarifa gani lakini nimeambiwa ni nyeti na ya muhimu sana” “Sawa Benjamin endelea kulifanyia kazi hilo suala.Baada ya kutuma ujumbe ule twitter Rais amekupigia simu akakwambia chochote?akauliza Rais Michael “Hapana hajanipigia simu.Amekaa kimya.Nimeambiwa kwamba ameitisha kikao cha baraza la mawaziri kesho asubuhi nadhani ajenda kubwa ya kikao hicho ni kujadili kile tulichokiandika katika kurasa zetu za twitter”akajibu Benjamin “Benjamin endelea kufuatilia kwa karibu sana hilo suala ni muhimu sana.Tunahitaji sana kupata ushahidi wa kumuhusisha Rais Fabian na mauaji yale ya Lucy na Laurent.Jambo lingine nataka kukufahamisha kwamba maandalizi ya Theresa yanakwenda vizuri.Tayari amekwisha fanyiwa upasuaji wa kubadili na madaktari wamenithibitishia kwamba ulikuwa ni upasuaji wenye mafanikio makubwa.Kwa sasa anaendelea kuhudumiwa na atakapopona tu ataanza kupewa mafunzo ya nini anatakiwa kufanya kisha atakuja Afrika Mashariki kituo chake kitakuwa Tanzania.Misheni yake kubwa ni kuisambaratisha afrika Mashariki.Tafadhali endelea kumuandalia mazingira mazuri ili atakapokuja asipate ugumu kuifanya kazi yake” akasema Michael “Mpaka sasa nimekwisha muandalia mazingira mazuri na ninaendelea kumuandalia hivyo atakapokuja haitamuwia ugumu kuifanya kazi yake” akasema Benjamin wakaagana na kukata simu







Austin aliwasili katika makazi ya Gosu Gosu saa tatu kasoro dakika nane za asubuhi na kukaribishwa ndani na mwenyeji wake.Hakuwa peke yake alikuwa ameambatana na watu wawili “Papaa kutana na Stanley na Nasibu.Hawa ni vijana wangu,wataalamu sana wa masuala ya elektroniki.Watatusaidia katika masuala ya Kamera” akasema Austin na Gosu Gosu akasalimiana na wale vijana alioambatana nao Austin “Kama nilivyokueleza simuni kwamba tayari nimetuma vijana wawili kuanzia asubuhi kumfuatilia balozi Benjamin na taarifa niliyopewa muda mfupi uliopita kabla sijafika hapa ni kwamba mke wa balozi ndiye aliyetangulia kuondoka nyumbani balozi alifuata muda mfupi baadae.Hivi sasa vijana wanaendelea kumfuatilia na watatupa taarifa baadae.Kuondoka kwa balozi Benjamin kunatuwashia taa ya kijani kuwa sasa tunaweza kwenda nyumbani kwake” akasema Austin “Tukifika pale tutajitambulisha kama watu wa Tanesco tunaopita nyumba kwa nyumba kukagua mita za umeme.Tayari nimekwisha tengeneza vitambulisho vyetu vikituonyesha kama wafanyakazi wa Tanesco.Nimetaarifiwa kuna mlinzi mmoja getini hivyo tutamuonyesha vitambulisho na kuingia ndani.Nina uhakika mita hiyo ya umeme itakuwa nje hivyo basi vijana wangu wawili wataingia ndani kujifanya wanakagua mfumo mzima wa umeme huku wakifunga kamera za siri.Ni zoezi ambalo halitachukua muda mrefu litakuwa limekamilika” akasema Austin kila mmoja akachukua kitambulisho chake wakaingia garini na kuondoka.Wakiwa njiani bado Austin aliendelea kuwasiliana na vijana aliowatuma kumfuatilia Benjamin na wakamjulisha kwamba balozi tayari amewasili ofisini kwake na wako nje wakimsubiri. Walifika katika makazi ya balozi Benjamin.Kulikuwa na askari mmoja mwenye silaha akilinda.Austin akashuka garini na kumsalimia vizuri Yule askari halafu akamueleza kwamba wao ni watu wa kutoka tanesco ambao wanapita nyumba baada ya nyumba kukagua mita za umeme.Walimuonyesha vitambulisho na askari Yule akaridhika akapiga simu ndani akatoa taarifa kwamba kuna wageni.Mtumishi wa ndani akatoka na kwenda kuwapokea.Austin alijitabulisha kwamba wao ni maafisa wa kutoka shirika la umeme tanesco na wanatembelea nyumba mbali mbali kukagua mita.Mfanyakazi Yule wa ndani wa balozi hakuonyesha wasi wasi wowote wala hakutaka kutazama vitambulisho akawapeleka moja kwa moja ilipo mita ya umeme.Austin akiwa na kifaa cha kupimia umeme akapima halafu akamgeukia Yule mfanyakazi akamtaka akawaonyeshe vijana wake vifaa vyote vikubwa vinavyotumia umeme ndani.Bila kusita mfanyakazi Yule aliyekuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu na fulana neykundu akawazungusha mle ndani akiwaonyesha vifaa mbali mbali vinavyotumia umeme halafu wakatoka nje.Austin akampa Yule msichana mita aishike halafu akawataka Stanley na Nasibu waingie ndani waanze kuzima kifaa kimoja kimoja cha umeme. “Zima friji ! akasema kwa sauti Austin na Stanley akaenda kuzima friji.Wakati zoezi hilo likiendelea Nasibu alikuwa na kazi moja ya kufunga kamera za siri katika vyumba bali mbali.Kwanza alifunga sebuleni halafu akafunga jikoni kisha akafunga chumba cha mapumziko na chumba cha mwisho alichotakiwa kufunga ni chumba cha kulala balozi ambacho kilikuwa kimefungwa kwa funguo.Mlango wa chumba kile ulikuwa na kifaa maalum cha kupiga kelele kama utafunguliwa endapo balozi au mke wake hayupo.Nasibu akachomoa kifaa Fulani katika begi lake akakiweka karibu na kifaa kile cha kutoa ukelele halafu akachukua vyuma Fulani vidogo akaufungua ule mlango akaingia ndani.Akafunga kamera mahala ambako si rahisi kuonekana .Wakati akishuka akaona kitu Fulani mezani.Ilikuwa ni kadi ya mwaliko.Akaisoma akairudisha mahala pake na kutoka akaufunga mlango akachukua kile kifaa chake chenye usumaku ambacho kilizuia kelele kutoka katika kile kifaa kilichowekwa mlangoni halafu akatoka nje.Austin alipomuona akajua kila kitu tayari akamaliza zoezi la kupima na kumjulisha Yule mfanyakazi kwamba hakuna tatizo lolote wakaaga na kuondoka. “Kila kitu tayari mkuu.Nimefunga kamera sebuleni,jikoni,chumba cha mapumziko na chumba cha kulala balozi” akasema Nasibu “Good job guys” akasema Austin “Katika chumba cha kulala balozi kuna kitu nimekiona”akasema Nasibu “Umeona nini? “Nimekuta kuna kadi ya mwaliko.Balozi amealikwa katika hafla ya uchangishaji fedha itakayofanyika kwa ajili ya mabweni ya kulala watoto wanaoishimazingira magumu.Hafla hiyo itafanyika Zimba hotel siku ya ijumaa” “Hizo ni habari njema.Ni kesho kutwa hivyo tujipange.Tutamfuata balozi kila mahala atakapokwenda.Tutamfuata kama kivuli anapoamka hadi anapokwenda kulala” akasema Austin Baada ya kutoka nyumbani kwa balozi walielekea moja kwa moja nyumbani kwa Gosu Gosu ambako ndiko kila kitu kitafanyika kutokea hapo.Vijana wale mahiri Stanley na Nasib walifanya mambo haraka haraka na wakaanza kupata picha kutoka katika kamera walizozifunga nyumbani kwa balozi Benjamin. “Okay guys,ninyi makazi yenu yatahamia hapa kwa muda.Kazi yenu kubwa itakuwa ni kufuatilia kila kinachofanyika mle ndani.Hakikisheni mnafuatilia simu zote zinazopigwa,watu wote wanaoingia mle ndani na kila anachokifanya balozi. “Tunafanya zoezi hili kwa muda gani mkuu?akauliza Nasibu “Hakuna muda maalum hadi pale tutakapopata kile tunachokitafuta” akasema Austin “Msijali kila kitu mtakipata hapa ndani.Kitu cha msingi ni macho yenu yasibanduke katika kompyuta kufuatilia kila kinachoendelea ndani ya nyumba ile” “Yule mfanyakazi ulikuwa naye nje wakati sisi tunafanya mambo yetu ndani una hakika hajahisi chochote? Akauliza Stanley “Hapana hajahisi chochote.Ameamini asilimia mia moja kwamba sisi ni watu kutoka tanesco.Hata Yule askari aliamini hivyo” akajibu Austin kisha akamuaga Gosu Gosu kwamba anakwenda kufuatilia masuala yake ya likizo ya dharura. TEL AVIV – ISRAEL Inakaribia saa moja za jioni katika chumba cha gereza walimo Mathew Mulumbi na Ammar Nazari.Ni siku ya tatu toka Mathew alipoanza kuzungumza na Ammar na wa muda huo tayari walikuwa marafiki wakubwa.Walizungumza mambo mengi sana kuhusiana na harakati zao na Ammar alikubali kujiunga na Mathew katika mpango wake wa kutoroka pale gerezani na alimtaka watakapofanikiwa kutoroka basi akajiunge na kundi lale la Ammar Nazari Brigades ombi ambalo Mathew alilikubali. Siku hii ndiyo ambayo ilipangwa Mathew akapewe maelekezo yote kuhusu namna watakavyotoroka pale gerezani.Ammar aliamini alivyoambiwa na Mathew kwamba kuna mwanamke anayeitwa Abeba raia wa Ethiopia ndiye anayemsaidia kutoroka kwa kumpa ramani ya gereza.Jioni ya siku hiyo waliandaa mpango ambao ungemfanya Mathew aweze kutolewa mle chumbani na kupelekwa hospitalini “Muda unakaribia Ammar.Tafadhali tufanye kama vile tulivyokubaliana.Kwa namna yoyote ile leo hii lazima nitoke humu nikaonane na Abeba kwani aliniahidi leo hii tayari atakuwa amepata ramani ya gereza itakayoniwezesha kutoroka” akasema Mathew “Usijali Abu kila kitu kitakwenda kama tulivyokubaliana” akajibu Ammar Saa moja na nusu za jioni wapishi wakiwa na torori kubwa la chakula walikuwa wakipita chumba hadi chumba kugawa chakula wakiwa wameongozana na askari wa gereza.Mlango wa akina Mathew ukafunguliwa akaingia mpishi kuwapa chakula.Mathew akaishika sahani ile ya chakula akakitazama na kuirusha ile sahani “Nimechoka kula aina moja ya chakula kila siku.Sisi pia ni binadamu kama ninyi !! akasema kwa ukali “Tafadhali kuwa na adabu kwa chakula unachopewa.Unadhani imewachukua muda gani kwa wapishi kuandaa chakula hiki?Siku nyingine ukirudia kitendo kama hicho nitakuadhibu vikali” akasema kwa ukali Ammar “Unasemaje ?! akauliza Mathew na kumsogelea Ammar akamvuta kilemba chake Ammar akakasirika na kumtandika ngumi nzito Mathew akaanguka chini lakini akawahi kuinuka akamfuata Ammar na kumuangusha chini Ammar akachukua uma ya kulia chakula akamchoma nayo mkononi damu zikaanza kumtoka askari wakaingia na kuwaamua “Samahani ndugu zangu nilikuwa namfunza adabu huyu mwenzangu kwa kosa la kudharau chakula.Mpelekeni akatibiwe jeraha lake” akasema Ammar na Mathew akatolewa mle ndani na kupelekwa hospitali akatibiwa jeraha lile kisha akatolewa na kupelekwa katika ofisi ya mkuu wa gereza alikomkuta Efraim Dagan na maafisa wengine wa gereza na wa Mossad wakimsubiri. “Mathew Mulumbi karibu tena.Kwanza pole kwa maumivu lakini vile vile hongera kwa kazi nzuri.Tumekuwa tunakufuatilia kila unachokifanya mle ndani na tunafurahi kwa kuwa umefanikiwa kumshawishi Ammar hadi akakuamini” akasema Efraim Dagan “Haikuwa kazi nyepesi lakini nashukuru ameniamini na yuko upande wangu” akasema Mathew “Baada ya hatua ile kukamilika sasa kinachofuata ni mpango wa kutoroka gerezani.Tayari tumekwisha andaa mpango huo” akasema Efraim Dagan na kumpa nafasi mmoja wa maafisa wa gereza kuendelea.Wote wakaelekeza macho yao katika runinga kubwa iliyokuwa mbele ikawashwa na ramani ikaonekana “Hii ni ramani ya gereza lote.Hapa kwenye mduara mwekundu ndipo chumba mlimo wewe na Ammar.Mpango tulioutengeneza utakuwa hivi.Siku ya kutoroka utajifanya umepoteza fahamu ghafla na Ammar atabonyeza kengele ya dharura na watafika askari wawili haraka kujua kumetokea nini.Atawaeleza kwamba umeanguka na kupoteza fahamu kisha mmoja wa askari hao atakusogelea kujua nini kimekutokea na hapo ndipo utakapokurupuka kama Mamba na kumrukia na wakati huo huo Ammar atamdhibiti askari mwingine.Hakikisha askari hao hamuwaui bali wapotezeni fahamu tu.Mtachukua mavazi yao pamoja na redio ya mawasiliano kisha mtaondoka kwa kufuata ramani tutakayokupa.Baada ya dakika tano kitalia king’ora cha hatari kuashiria kwamba kuna wafungwa wanatoroka na ninyi mtakuwa na redio ya mawasiliano kutoka kwa wale askari na mtakuwa mkisikiliza kila kinachoendelea.Mkifika hapa geti kumi na moja tutaweka askari mdunguaji ambaye atamdungua Ammar kwa risasi ya mguu na wewe utaachia risasi kadhaa kama vile unamlenga askari huyo kisha utambeba Ammar.Mtapita katika mfereji huu wa maji machafu utakaowatoa nje ya gereza ambako tutakuwa tumewaondoa askari wanaolinda upande huo na kuwataka waingie ndani ili kusaidia kuwatafuta wafungwa waliotoroka.Mfereji huu ni mrefu na unakwenda kuungana na mfumo mwingine wa maji taka toka sehemu nyingine za jiji lakini kabla ya kufika sehemu ambapo mfereji huu unaungana na mifereji mingine mtakuta kuna ngazi ya kupanda na juu kuna mfuniko mtatoka nje na hapo tayari mtakuwa mko nje ya gereza.Baada ya kutoka nje mtafuata barabara kuelekea Kaskazini na kwa dakika kama saba hivi mtakuta daraja mtajificha chini ya daraja kisha atakuja Dr Abeba atamulika tochi na kuzima mara tatu utamtambua kisha atawapeleka sehemu ambako Ammar atapatiwa matibabu na kutoka hapo atawasaidia kuondoka Israel” akasema Yule afisa wa gereza “Mathew unasemaje kuhusu mpango huo? Akauiza Efraim “Ni mpango mzuri lakini kuna maboresho nataka yafanyike.Kwa namna mpango ulivyo tutatoka bila kutumia nguvu nyingi na itaonekana ni rahisi kutoroka.Gereza hili lina sifa ya ulinzi mkali hivyo basi lazima ionekane tumetoka ndani ya gereza kwa bahati” akasema Mathew na kutoa maelekezo kadhaa ya kuboresha mpango ule kisha akapewa karatasi yenye ramani ya gereza ikionyesha njia watakazopita kisha akarudishwa katika chumba chake “Mambo yamekwendaje? Akauliza Ammar akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua namna mambo yalivyokwenda “Mambo yamekwenda vizuri.Nimefanikiwa kuipata ramani” akasema Mathew na kutoa karatasi katika nguo yake ya ndani akaikunjua ilikuwa ni ramani ya gereza.Ammar akashindwa kulizuia tabasamu katika uso wake baada ya kuiona ramani ile.Hakuamini kama kile alichokuwa anakiona ni kitu cha kweli. “Ninaona haya kama maajabu.Sikuitegemea hata siku moja kama ningeweza kuikamata ramani ya gereza hili.Hii itatusaidia sana tutakapotoka hapa kuandaa kuja kuvamia na kuwawachukua watu wetu waliofungwa hapa” akasema Ammar na Mathew akaanza kumuelekeza namna mpango wote utakavyokuwa na njia watakazopita. DAR ES SALAAM – TANZANIA Ni siku ya ijumaa ikiwa ni siku ya tatu toka akina Austin walipoanza kumfuatilia balozi Benjamin Hudson.Kwa muda wa siku zote tatu Stanley na Nasibu hawakubandua macho katika kompyuta wakifuatilia kila kinachofanyika nyumbani kwa balozi Benjamin lakini kwa muda wote huo wa siku tatu hawakuwa wamepata kitu chochote cha muhimu.Timu iliyokuwa inamfuatilia balozi Benjamin kila aendako nao walifanya kazi yao kwa umakini mkubwa na kupata picha ya kila aliyezungumza na balozi Benjamin.Ubao uliokuwemo katika ofisi yao ulikuwa na picha za watu mbali bali ambao Benjamin alikutana nao katika siku hizo tatu na wote walifanyiwa uchunguzi lakini bado hawakuwa wamepata mtu ambaye walimuhisi anaweza kuwa anashirikiana na balozi Benjamin na kumpa siri mbali mbali. Austin January akiwa amevalia suti nyeusi jioni hii alikuwa ameegemea meza akitazama picha za watu kadhaa waliofanya mazungumzo na Benjamin “This dude is very clever” akasema Austin “Anajua sana kuficha mambo yake.Karibu watu wote hawa aliokutana nao ni watu wa kawaida sana.Katika siku hizi zote tatu hatujamuona na simu yoyote ya mkononi.Tumekuwa tukifuatilia simu zote zinazopigwa nyumbani kwake lakini hakuna simu yoyote tuliyoitilia shaka.Anafanyaje mawasiliano yake? akauliza Austin “Kuna kitu kimoja ambacho mimi na wenzangu tumekiona na tukajiuliza.Kila ifikapo saa tano usiku Benjamin hutoka chumbani kwake”akasema Stanley “Huelekea wapi? Austin akauliza “Hatujajua huelekea wapi kwani kamera tumeweka chumbani kwake,sebuleni,jikoni na katika chumba cha mapumziko” “Tulipaswa kuweka kamera kila sehemu ili tujue kila kinachofanyika mle ndani.kama anatoka kila saa tano usiku lazima kuna mahala huwa anakwenda” akasema Austin “Kwa hiyo tunafanya nini kuhusu hilo?akauliza Gosu Gosu “Lazima tutafute namna ya kurudi tena mle ndani kufunga kamera nyingine sehemu mbali mbali kujua usiku huo akitoka Benjamin huenda wapi.Kwa sasa tujielekeze katika tukio la usiku wa leo ambapo Benjamin amealikwa katika hafla ya uchangiaji fedha kwa ajili ya mabweni ya watoto waishio katika mazingira magumu.Mimi,GosuGosu,na Nasibu wote tutakuwemo ndani ya ukumbi huo.Macho yetu wote tutayaelekeza kwa mtu mmoja tu Benjamin Hudson.Wote tutakuwa tumevaa kamera ambazo zitamuwezesha Stanley atakayekuwa amebaki nyumbani kupata picha za kila kinachoendelea mle ndani ya ukumbi.Tuhakikishe tunapata picha ya kila anayezungumza na Benj……” akanyamaza Austin baada ya simu yake kuita.Walikuwa ni vijana wanaomfuatilia Benjamin “Hallow” akasema Mathew baada ya kuipokea simu “Mkuu,huyu jamaa ametoka na ndani ya gari yuko yeye na mke wake” “Nadhani wanaelekea katika hafla waliyoalikwa jioni hii ya leo.Endeleeni kumfuatilia na sisi tunaelekea ukumbini” akasema Austin na kukata simu. “Tayari balozi Benjamin anaelekea ukumbini.Tusipoteze muda tuelekee huko” akasema Austin.Ni Stanley pekee aliyebaki pale nyumbani wengine wote wakaingia katika magari na kuondoka.Austin alikuwa na Nasib Gosu Gosu alikuwa peke yake. Zimba hoteli usiku huu iling’aa kwa mataa ya rangi mbali mbali yaliyozunguka hoteli hii ya hadhi ya nyota tano.Usiku huu mahala hapa kulikuwa na hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha kulelea watoto cha Mama wa Afrika.Watu wengi walialikwa kuhudhuria hafla hiyo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga mabweni ya watoto hao waishio katika mazingra magumu.Katika sehemu ya kuegesha magari kulikuwa na watu watatu wakiongoza magari kwani usiku huu kulikuwa na magari mengi ya watu waliofika katika hoteli hii kuhudhuria hafla hiyo.Akina Austin waliwahi kufika kabla ya balozi hajafika.Hawakuwa na kadi za mwaliko kwani kadi zilitolewa kwa watu maalum tu lakini kwa wengine ambao waliguswa na kutaka kuchangia walikaribishwa pia hivyo akina Austin walikuwa katika kundi hili wakaingia ndani ya ukumbi.Watu walikuwa wengi na bado waliendelea kuingia ukumbini.Nasib alipanda sehemu ya juu,Gosu Gosu na Austin kila mmoja akachukua sehemu yake. Wakiwa mle ukumbini Austin akapigiwa simu na vijana wake kwamba balozi Benjamini tayari amefika hapo ukumbini na ameshuka garini yeye na mkewe wanaelekea ukumbini.Austin akawatumia ujumbe Gosu Gosu na Nasibu kuwajulisha kwamba muda wowote balozi Benjamin ataingia ukumbini hivyo wajiandae. Balozi Benjamin akiwa ameongoza na mkewe na watu wawili walioonekana ni walinzi wake,wakaingia ndani ya ukumbi.Toka alipoingia ukumbini macho ya Nasibu yalimng’aza na kuelekeza kamera kumfuatilia.Alipokewa na mtu maalum aliyewekwa kwa ajili ya kupokea wageni.Alielekezwa kukaa katika meza ya tatu kutoka meza ya mbele.Kulikuwa na watu wengine watatu katika meza hiyo wakasalimiana.Wakati wakiendelea na mazungumzo,Austin akainuka kama vile anakwenda maliwato lakini aliporejea hakwenda tena kukaa katika meza ile aliyokuwa amekaa badala yake akaenda kukaa karibu na meza ya balozi huku macho yae akiyageuza kama kinyonga kutazama kila kinachoendelea katika meza ile aliyokaa balozi.Wote walikuwa wamevaa kamera za siri ambazo zote walizielekeza kwa balozi. Muongoza shughuli aliposhika kipaza sauti na kutangaza kwamba muda si mrefu shughuli itaanza,Benjamin akaitazama saa yake ya mkononi halafu akainuka na kutembea kama vile anaelekea maliwato Gosu Gosu naye akasimama akaelekea huko.Nasibu naye akashuka ghorofani na kumfuata Gosu Gosu.Benjamin aliingia maliwato baada ya dakika mbili akatoka lakini hakurejea ukumbini akachepuka na kufuata korido akaelekea baa.Akaenda kaunta na kununua chupa ya bia.Gosu Gosu akabaki nyuma akamuacha Austin aingie mle baa.Balozi Benjamin akamimina bia ile katika glasi akanywa huku akiangaza huku na kule halafu akalipa na kumuachia muhudumu chenji akatoka mle baa na kuelekea katika lifti.Wakati akisubiri lifti iliyokuwa juu Nasibu naye akafika akaungana naye kusubiri lifti.Baada ya muda mfupi milango ya lifti ikafunguka wakaingia walikuwa jumla watu sita.Balozi akaomba abonyezewe namba sita akimaanisha anakwenda ghorofa ya sita.Nasibu akawaandikia ujumbe akina Gosu Gosu kwamba balozi anaelekea ghorofa ya sita.Haraka haraka Gosu Gosu aliyefika katika eneo lile la lifti akaingia katika lifti ya pembeni ambayo haikuwa na mtu na kubonyeza ghorofa ya sita lifti ikaondoka. Milango ya lifti ikafunguka ghorofa ya sita lakini balozi hakushuka badala yake akaingia mwanamke Fulani aliyekuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu na fulana nyeupe iliyombana na viatu virefu vya bluu.Mwanamke Yule alimsogelea zaidi balozi ambaye alikuwa karibu na Nasib.Hakuna aliyemjali akachomoa mfukoni bahasha ya khaki na kumuwekea balozi kwenye koti.Mwanamke Yule alishuka ghorofa ya nane Nasibu naye akashuka.Baada ya kushuka mwanamke Yule akaanza kushuka ngazi kwa miguu.Nasibu akajibanza mahala na kupiga simu kwa Austin “Kuna mwanamke amepanda lifti ghorofa ya sita na akamuwekea balozi bahasha ya khaki kwa uficho.Mwanamke huyo ameshukia ghorofa ya nane na anashuka kwa kutumia ngazi za kawaida.Amevaa suruali ya jeans ya bluu,fulana nyeupe ya kumbana na viatu vya bluu ana mkoba mweupe” “Kazi nzuri sana Nasib shuka taratibu rejea chini uendelee kumfuatilia balozi” akasema Austin halafu akampigia simu Gosu Gosu aliyekuwa ghorofa ya sita akamjulisha amfuatilie mwanamke Yule anayeshuka ngazi. Milango ya lifti ilifunguka na balozi Benjamin akatoka na kuelekea baa akasimama kaunta akaangaza angaza kama vile anamtafuta mtu halafu akaondoka akaelekea ukumbini. “Anarejea ukumbini” Nasibu akamjulisha Austin. Balozi aliingia ukumbini na kukuta tayari hafla imeanza akaenda kuketi katika meza yake. Gosu Gosu aliendelea kumfuatilia taratibu mwanamke Yule akapita baa halafu akatoka nje na moja kwa moja akaelekea katika maegesho.Gosu Gosu naye akaelekea katika maegesho.Mwanamke Yule akaingia katika gari la kifahari aina ya range rover e vogue rangi nyekundu akaliwasha na kuondoka Gosu Gosu naye akawasha gari lake na kuanza kumfuatilia “Ameondoka hapa hotelini.Ninamfuatilia kumfahamu ni nani” Gosu Gosu akamwambia Austin “Sawa Gosu Gosu endelea kumfuatilia sisi tunaendelea kumfuatilia balozi tayari amerejea ukumbini.Tunahitaji kujua bahasha aliyopewa ina nini? Naamini ina kitu kikubwa hadi akaenda kumpa kiuficho namna hiyo.Ruby alikuwa sahihi huyu jamaa ni mtu anayechukua tahadhari kubwa sana katika mambo yake.Tafadhali hakikisha unapata majibu mwanamke huyo ni nani na amempa nini balozi.Kama utahitaji msaada nijulishe haraka sana” akasema Austin Baada ya kutoka Zimba hoteli mwanamke Yule akaenda hadi Dar es salaam supermarket.Gosu Gosu naye akaenda hapo akaegesha gari na kumuachia mlinzi shilingi elfu kumi amlindie lile gari atakuja kulichukua baadae akamfuata dereva wa boda boda akamtaka waelekee sehemu fulani lakini akamtaka wasubiri kuna gari wanalifuata.Dakika kama kumi baadae gari la Yule mwanamke likatoka na Gosu Gosu akamuelekeza Yule dereva wa boda boda walifuate. Mwanamke Yule aliingia katika jumba moja kubwa la ghorofa moja lililokuwa na geti lenye nakshi za kuvutia.Gosu Gosu na Yule dereva wakalipita jumba lile na kwenda mbele kidogo kisha Gosu Gosu akamlipa Yule dereva kiasi cha pesa alichohitaji akaondoka zake.Gosu Gosu akaanza kurejea taratibu katika jumba lile.Ni mtaa uliokuwa na majumba mazuri na kwa muda ule hakukuwa na watu wengi barabarani.Kulikuwa na taa kubwa getini iliyotoa mwangaza mkubwa.Gosu Gosu akaenda kuegemea nguzo ya umeme akatazama pande zote halafu akachomoa bastora yake yenye kiwambo cha sauti akailenga ile taa ikapasuka.Eneo lile likawa na mwanga hafifu sana halafu akatulia pale kwa muda akiangaza pande zote kama kuna mtu.Zilipita piki piki mbili na magari matatu halafu akavuka barabara na kwenda katika geti akajaribu kuusukuma mlango mdogo wa geti ulikuwa umefungwa kwa ndani haraka haraka akavua viatu na kurudi nyuma hatua kadhaa halafu akatoka mbio na kuruka akashika kingo za juu za geti akapanda na kuchungulia ndani.Aliliona gari la Yule dada likiwa limeegeshwa mbele ya nyuma akajirusha ndani na kutua bila kelele.Akaangaza angaza mara akasikia muungurumo wa mbwa mkubwa aliyemsogelea kimya kimya kwa wepesi wa aina yake Gosu Gosu akaizinga bastora yake na mbwa Yule akaanguka chini kimya kimya.Akamvuta na kumtupa pembeni kwenye maua akatembea taratibu hadi katika kibaraza akachungulia ndani sebuleni akamuona mwanamke mmoja amekaa sebuleni akitazama filamu.Yule mwanamke aliyempa bahasha balozi hakuwepo.Akazunguka kwa nyuma akajaribu kuusukuma mlango ulikuwa wazi akaingia ndani akatokea jikoni hakukuwa na mtu akatokea sehemu ya kulia chakula akasikia hatua za mtu akajibanza pembeni katik anguzo kwa bahati mbaya akagonga glasi ikaanguka na kuvunjika. “Dada ? akaita Yule msichana aliyekuwa akipita akitokea sebuleni lakini alipoona kimya akaamua kuingia katika chumba cha chakula kuangalia kwa nini glasi ile imevunjika.Mara tu alipoingia akajikuta akitazamana na mtu mwenye bastora “Mamaaaa ! akapiga kelele “Shhhh !! usipige kelele nitakufumua kichwa kwa risasi ! akasema Gosu Gosu.Yule msichana alikuwa anatetemeka mwili kwa woga “Dada yako yuko wapi?akauliza Gosu Gosu “Yuko chumbani kwake”akajibu Yule msichana akitetemeka “Nipeleke chumbani kwake haraka sana” akasema Gosu Gosu na mara ikasikika sauti ikiita “Nancy ! “Nancy ! “Dada ananiita” akasema Yule msichana “Itika” akasema Gosu Gosu na Yule msichana akaitika “Nimesikia unapiga kelele kuna nini huko?akauliza “Hakuna kitu dada” akasema Nancy “Kamuangalie mtoto kama amelala” akasema Yule dada kule juu “Nipeleke katika chumba alimo mtoto” akasema Gosu Gosu na Yule msichana Nancy akampeleka katika chumba alimo mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa kama miaka mitano. “Anaitwa nani huyu mtoto?akauliza Gosu Gosu ‘Anaitwa Teddy” akajibu Yule Nancy na Gosu Gosu akampa pigo kichwani akaanguka chini na kupoteza fahamu akamuinua Yule mtoto aliyekuwa usingizini akambeba na kuelekea ghorofani kilipo chumba cha Yule dada.Akagonga mlango “Nancy ! akaita yule dada mle chumbani na Gosu Gosu akagonga kwa mara ya pili na mlango ukafunguliwa.Yule dada hakuamini alipojikuta akitazama na Gosu Gosu aliyekuwa na bastora huku akiwa amembeba mwanae. “Who are you? Akauliza Yule dada ambaye mstuko alioupata ulikuwa mkubwa “Sit down ! akasema Gosu Gosu na Yule dada akatii na kukaa kitandani.Gosu Gosu akaichukua bastora iliyokuwa mezani ya Yule dada akaifutika kiunoni akamtazama Yule dada ambaye midomo ilikuwa inamtetemeka “Wewe ni nani?Unataka nini?Tafadhali naom……” akasem Yule dada lakini Gosu Gosu akamnyamazisha “Quiety ! “Nina muda mfupi sana hapa nataka unijibu maswali nitakayokuuliza kiufasaha na kama utathubutu kuleta jeuri au kujaribu kutaka kufanya ujinga wowote nitakuua wewe na mwanao.Umenielewa?akauli za “Nimekuelewa.Tafadhali naomba usimdhuru mwanangu.Unataka nini? Pesa? Akauliza Yule mwanadada “Jina lako nani? “Naitwa Rahel” “Rahel unafanya kazi wapi? “Mimi ni mfanya biashara wa vipodozi” “Are you sure? “Ndiyo mimi ni mfanya biashara” “Usiku huu ulikutana na balozi wa umoja wa ulaya katika hoteli ya Zimba una mahusiano naye yapi? “Balozi wa Ulaya?akauliza Rahel “Ndiyo” “Simfahamu wala sijafika Zimba hoteli usiku huu.Nilipotoka kwenye biashara zangu nimekuja moja kwa moja nyumbani.Utakuwa umenifananisha” “Nilikwambia nina muda mfupi sana hapa.Nakupa nafasi ya mwisho unieleze una mahusiano gani na balozi wa Ulaya hapa nchini bwana Benjamini Hudson?akasema Gosu Gosu.Huku machozi yakimtoka Rahel akajibu “Naomba uniamini kaka yangu sina mahusiano yoyote na huyo balozi wala simjui ni nani” “Nilikutaka uwe mkweli kwangu,kwa kuwa umekuwa muongo nitaanza kumpiga risasi moja moja mwanao hadi utakapokuwa tayari kunieleza ukweli” akasema Gosu Gosu na kumuelekezea yule mtoto bastora mguuni “Nitahesabu mpaka tatu kama hautakuwa tayari nitaufumua mguu wake kwa risasi” akasema Gosu Gosu “Tafadhali kaka yangu nakuomba sana usimuumize mwanangu.Unamuonea bure mimi simfaham…….” “Tatu ! akasema Gosu Gosu kwa ukali “Kaka nakuomba ..” akasema Rahel huku akitaka kuinuka “Usiinuke hapo nitakuchakaza kwa risasi.Mbili ! akasema kwa ukali “M….” Kabla Gosu Gosu hajamaliza kutamka mlango ukapigwa teke zito na bomu dogo la kurusha kwa mkono likatupiwa mle ndani “Oh my God ! akasema Gosu Gosu.Rahel macho yakamtoka pima.Picha ya Mathew Mulumbi akidaka bomu na kulirusha nje walipokuwa katika misheni ya kuwakomboa watoto waliotekwa na magaidi ikapita haraka haraka kichwani kwake “Mathew Mulumbi aliwahi kudaka bomu na kulitupa nje” akawaza na kufanya kitendo ambacho Rahel hakuwa amekitarajia.Gosu Gosu alimrusha Teddy kitandani huku akimrushia Rahel bastora ambaye aliidaka kiufundi sana akaanguka chini na kumimina risasi mlangoni .Gosu Gosu aliruka akalishika lile bomu na kulirusha katika dirisha lililokuwa wazi bomu lile likaenda kutua ndani ya bwawa la kuogelea.Alikuwa anatweta.Hakuamini kama walikuwa wamenurusika.Akainuka na kuelekeza macho yake mlangoni watu wawili walikuwa wameanguka wakivuja damu.Ilikuwa kazi ya Rahel.Aliwachakaza watu wale kwa risasi kutoka katika bastora aliyopewa na Gosu Gosu Gosu.Akawasogelea watu wale akawachunguza walikuwa wamekufa.Akamgeukia Rahel aliyekuwa amejibanza pembeni ya meza ya vipodozi alikuwa anatetemeka “Are you okay?akauliza. “I’m..I’m … fine” akajibu kwa kitetemeshi. “Good job Rahel” akasema Gosu Gosu “Thank you.Umeokoa maisha yangu na ya mwanangu” akasema Rahel na kwenda kumkumbatia mwanae aliyekuwa kitandani akilia.Gosu Gosu akamtaka asitoke mle chumbani akashuka chini kwenda kuangalia kama kuna watu wengine lakini hakukuwa na mtu akarejea chumbani kwa Rahel “Unawafahamu watu hawa?akauliza Gosu Gosu “Hapana siwajui”akajibu “Okay we need to get out of here immediately.Hapa tayari ni sehemu hatarishi kwenu.Zima kompyuta na simu zako zote”akasema Gosu Gosu na Rahel akafungua zimu zake mbili akatoa laini zake “Unatupeleka wapi? “Sehemu salama” akasema Gosu Gosu na kumtaka Rahel akusanye kila kitu chake cha muhimu akaweka katika sanduku dogo wakatoka mle chumbani akaenda katika chumba cha chakula akambeba Yule msichana ambaye mpaka sasa bado hakuwa na fahamu akamuingiza garini.Akarudi tena ndani na kuibeba miili ya wale jamaa waliouawa akaipakia garini na kuifunika na turubai “Hao unawapeleka wapi?akauliza Rahel kwa wasiwasi “Miili hii haipaswi kuendelea kukaa mle ndani mwako ninakwenda kuitupa.Polisi hawatakiwi wajue kuhusiana na tukio hili” akasema Gosu Gosu akiwa katika usukani.Bado Rahel alikuwa amemkubatia mwanae aliyekuwa anatetemeka.Alichokishuhud ia usiku ule kilimstua sana.Safari ilikuwa ya kimya kimya wakielekea nje kidogo ya jiji hadi walipokuta vichaka Fulani Gosu Gposu akazima gari na kushusha miili ya wale jamaa akaitupa vichakani kisha wakaanza safari ya kurejea jijini. “Who are you?akauliza Rahel “You’ll soon know who I am” akajibu Gosu Gosu “Tafuta sehemu salama tuliache hili gari hatupaswi kuendelea kulitumia” akasema Rahel “Kwa nini Rajel? “Kwa sababu wanatufuatilia.Wanajua hivi sasa tuko wapi” akasema Rahel na Gosu Gosu akamtazama “Akina nani wanatufuatilia? “Do as I say ugly man ! akasema Rahel kwa ukali “Fine” Gosu Gosu akaiingiza gari ile katika baa moja wakashuka wakashuka halafu wakachukua taksi hadi Dar es salaam supermarket ambako Gosu Gosu aliacha gari lake wakaingia garini na kuondoka “Huyu mwanamke anaonekana ana mambo makubwa sana.Alisema hawajui watu wale waliokuja kumuua na sasa anasema kwamba tunafuatiliwa.Kuna jambo analifahamu nidyo maana akataka kuuawa” akawaza Gosu Gosu Walipokaribia kufika katika makazi ya Gosu Gosu ndipo alipokumbuka kutaka kuwasiliana na wenzake akina Austin lakini kumbe simu yake ilikuwa imepata hitilafu katika ule mshike mshike na ikazimika.Alipofika katika makazi yake akawakaribisha ndani Rahel na mwanae pamoja na Nancy yule msichana aliyekuwa amepoteza fahamu ambaye tayari alikwisha rejewa na fahamu.Bila kupoteza muda akamuelekeza mtumishi wa ndani awaandalie wageni wale chumba cha wageni na baada ya muda mfupi chumba kikawa tayari Rahel akaenda kumlaza mwanae na Yule mdogo wake.Wakati Rahel akimbembeleza mwanae alale Gosu Gosu akabadili simu na kumpigia Austin akamjulisha kila kilichoendelea. “Pole sana Papaa.Niliingiwa na wasiwasi mkubwa baada ya simu yako kutopatikana kila nilipojaribu kupiga”akasema Austin “Hata mimi mwenyewe sikuwa nakumbuka kabisa kuhusu simu hadi nilipofika nyumbani.Austin I saw death today” akasema Gosu Gosu “Pole sana Papaa.Umefanya kazi kubwa sana hadi ukafanikiwa kumpata huyo mwanamke ambaye naamini atakuwa na msaada mkubwa kwetu.Kwa sasa mpe muda apumzike ila usimruhusu kufanya mawasiliano na mtu yeyote Yule na kila kitu chake kizimwe kwani wanaweza wakamfuatilia wakajua mahala alipo.Mimi nitawaachia vijana waendelee kumfuatilia balozi ninakuja hapo nyumbani sasa hivi kuungana nawe tumuhoji huyo mwanamke.Kuna mambo mengi ambayo tunahitaji kuyafahamu kutoka kwake” akasema Austin Alipomaliza kuzungumza na Austin Gosu Gosu akachukua bia baridi katika friji akaigugumia yote halafu akasimama akiwa ameegemea friji. “Haikuwa siku yangu ya kufa leo lakini tayari nilikwisha chungulia kaburi.Kama nisingepata ujasiri wa kuliokota bomu lile na kulirusha nje mimi na wote mle ndani tungekwisha kufa.Namshukuru Mathew kwa kunipa ujasiri kwani naye pia aliwahi kudaka bomu akalirusha nje akatuokoa wote na leo nimefanya kama alivyofanya yeye.” Akawaza na kuvuta pumzi ndefu sana na kuelekea katika chumba cha wageni waliko akina Rahel akagonga kidogo halafu akaruhusiwa kuingia akausukuma mlango akaingia ndani.Rahel alikuwa amekaa kitandani mwanae Teddy na Yule msichana Nancy walikuwa wamelala “Wanaendeleaje?akauliza Gosu Gosu “Nashukuru wamepata usingizi lakini mstuko walioupata ni mkubwa”akasema Rahel “You need something to drink?Wine,beer or whisky? Akauliza Gosu Gosu “No thank you”akajibu Rahel “Rahel kama hutajali naomba tuzungumze tafadhali” akasema Gosu Gosu na Rahel akainuka pale kitandani wakaelekea sebuleni.Gosu Gosu akafungua friji akatoa chupa ya maji ya kunywa akamminia Rahel katika glasi akampa yeye akachukua chupa ya bia “Rahel hapa ulipo ni sehemu salama hakuna anayeweza kukufuata hapa hivyo jisikioe amani.Baada ya yote yaliyotokea nadhani sasa ni wakati muafaka wa kuzungumza.Niliweka hatarini maisha yangu kukuokoa wewe na mwanao hivyo ninahitaji kuufahamu ukweli.Nataka unieleze ukweli bila kunificha na mimi nitakusaidia lakini kama ukiamua kunidanganya utakuwa unajidanganya wewe mwenyewe kwani watu wale ambao walikufuata kukuua hawatachoka wataendelea kukutafuta usiku na mchana hadi watakapohakikisha wamekumaliza.Nataka kufahamu wewe ni nani?Unafanya kazi wapi na nani unashirikiana naye na kwa nini watu wale walikuja kutaka kukuua?akauliza Gosu Gosu.Rahel akainama akafuta machozi halafu akamtazama Gosu Gosu “Nilikudanganya.Jina langu si Rahel.Naitwa Agatha”akanyamza kidogo halafu akaendelea “Kabla sijakueleza chochote nataka unihakikishie usalama wangu na familia yangu.Hawatachoka kunitafuta hadi pale watakapohakikisha nimeuawa.I was so stupid to believe them” akasema Agatha “Agatha nimekuokoa kutoka kwa wale watu usiku wa leo na nitaendelea kukulinda.Nakuahidi wewe na familia yako mtakuwa salama” “You don’t know what you’re talking about Gosu Gosu.The people I’m talking about they’re dangerous than you think.I know their secrets so they must find and kill me” akasema Agatha “Agatha nakutoa hofu kwamba utakuwa salama.Mimi na wenzangu tutakulinda na kuhakikisha unakuwa salama.Niambie ni akina nani hao watu? “This place is not http://deusdeditmahunda.blogspot.com/safe for me why don’t you understand?akauliza Agatha kwa ukali “Find me somewhere safe and I’ll tell you everything I know” akasema Agatha “Agatha tafadhali naomba unisikilize.This place is very safe for you and for your family.Hakuna anayejua uko hapa na hakuna atakayejua kama uko hapa.Ninaibeba dhamana ya usalama wako wewe na familia yako.Naomba uniamini tafadhali.Mimi ndiye peekee unayeweza ukaniamini kwa maisha yako kwa wakati hii.Me and my friends we’ll keep you guys safe I give you my word” akasema Gosu Gosu.Rahel akamtazama kwa muda halafu akasema “I work for SNSA” “SNSA? What’s that?akauliza Gosu Gosu “Secret Nation security Agency.Idara ya siri ya usalama wa nchi inayojishughulisha na usalama wa ndani wa nchi” akasema Agatha na picha ya Devotha ikapita kwa haraka katika akili ya Gosu Gosu “Idara ya siri? Akauliza “Ndiyo.Hii ni idara inayofanya kazi zake kwa siri kubwa hapa nchini na ni watu wachache sana ambao wanafahamu uwepo wake.Mimi nilikuwa katika kitengo cha udukuzi.Kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na kitengo hiki ambayo watu hawayafahamu.Kila siku maelfu ya simu zinadukuliwa tunasikiliza mawasiliano yao bila wao kujua.Tumekwisha ingia katika mitandao yote ya simu iliyopo hapa nchini na tunao uwezo wa kufuatilia kila simu tunayoitaka bila ya wao kujua.Tunaweza kuwasha mikrofoni ya simu bila mtu kujua hata kama simu yake ikiwa imezimwa na kumfuatilia.Mtu yeyote tunayemtilia shaka tunao uwezo wa kumfuatilia ” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Nilipewa kazi ya maalum ya kudukua mawasiliano yote ya Rais kujua anawasiliana na nani na wanawasiliana kuhusu nini.Hukusanya mawasiliano ya Rais kwa siku nzima na kuyaweka katika faili maalum ambalo mwenye uwezo wa kulifungua ukiacha mimi ni Tamar.Kila jioni ninapowasilisha taarifa ya siku Tamar hunipatia shilingi milioni moja na nusu kama malipo ya kazi niliyoifanya na hii ni nje ya mshahara ndiyo maana sikuacha kuifanya kazi hii kwani ilikuwa na malipo mazuri” “Pesa hizo nyingi Tamar alizipata wapi? Na kwa nini akulipe kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa kazi ambayo ungeweza kuifanya kama sehemu ya kazi yako ya siku?akauliza Gosu Gosu “Alinilipa fedha nyingi ili kunifanya kwanza nitunze siri na pili nipate moyo wa kuendelea kuifanya ile kazi kwa kujua kwamba ina malipo mazuri.Kuhusu anakotoa fedha sikuhitaji kujua lakini ninachofahamu Tamar ni tajiri.Anamiliki magari ya kifahari sana” akajibu Agatha “Ulifahamu rekodi zile anazipeleka wapi ukishazihifadhi? Gosu Gosu akauliza “Hapana sikujua anazipeleka wapi na nilitamani sana kufahamu lakini kutokana na malipo makubwa aliyokuwa akinilipa sikutaka kufuatilia”akajibu Agatha “Usiku wa leo umempa balozi Benjamin bahasha ya khaki ilikuwa na kitu gani ndani yake?akauliza Gosu Gosu “Kama nilivyokueleza kwamba kazi yangu mimi ilikuwa ni kukusanya rekodi zote za mawasiliano ya Rais na kuzihifadhi katika faili maalum na baada ya hapo kazi yangu huwa imekwisha ninachukua fedha zangu na kurudi nyumbani.Siku chache zilizopita nilinasa mawasiliano ya Rais Dr Fabian na Rais wa Congo Patrice Eyenga.Ilikuwa ni muda mchache baada ya Yule mwanamama tajiri Lucy Muganza na mumewe kuuawa jijini Dar es salaam.Katika mazungumzo yao Dr Fabian alimjulisha Rais Patrice kwamba kazi imekamilika na Lucy Muganza tayari ameuawa,Congo na Afrika Mashariki watakuwa na amani.Nilistuka sana baada ya kunasa mazungumzo hayo na sikuyaweka katika orodha ya mawasiliano niliyompa Tamar.Nilinasa tena mazungumzo mengine Dr Fabian akimjulisha Rais Patrice Eyenga kwamba kulifanyika makosa madogo katika operesheni ya kumuua Lucy Muganza na umoja wa Ulaya umekwisha anza kuwa na wasi wasi kwamba ni serikali yake ndiyo waliotekeleza mauaji yale na wametaka wachunguzi wa kimataifa waingie nchini kuja kuchunguza kuhusu mauaji hayo.Rais Patrice alimpa pole Dr Fabian kwa kumsababishia yeye na nchi yake matatizo yale makubwa lakini Dr Fabian alimuhakikishia kwamba suala lile watalimaliza asiwe na wasi wasi.Niliingiwa na hofu ya kumuonyesha Tamar maongezi hayo kati ya Rais wetu na Patrice Eyenga na hivyo nikayaficha.Kutokana na kufanya kazi mfululizo bila kupumzika,Tamar alinipa mapumziko ya siku tatu kuanzia jana lakini leo aliniita na kunipa maelekezo ya kwenda Zimba hotel kukutana na balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini bwana Benjamin Hudson.Alinipa maelekezo yote ya namna nitakavyoweza kukutana naye na kumpatia bahasha ile” ‘Benjamin hakuwa na simu ya mkononi uliwezaje kufanya mawasiliano naye hadi mkakutana katika lifti? “Benjamin anatumia saa yake ya mkononi katika kuwasiliana.Ana saa maalum inayotumika kama simu hivyo ukimpigia katika namba yake,huonyesha katika saa na kisha hubonyeza kidude katika saa yake na sikioni huwa ameweka kifaa maalum kidogo sana cha kusikilizia maongezi.Hivyo ndivyo hufanya mawasiliano yake.Niliyajua haya yote kutoka kwa Tamar” akajibu Agatha “Endelea” akasema Gosu Gosu “Nikiwa njiani nilipata hamu ya kujua kuna nini ndani ya ile bahasha nikasimamisha gari na kuifungua nikakuta kuna flashi ya kuhifadhia kumbukumbu nikaichomeka katika kompyuta yangu nikakuta kuna rekodi za yale mazungumzo ya Rais Dr Fabian na Rais Patrice Eyenga ambayo sikutaka kumpa Tamar.Inaonekana kuna kitu alikigundua ndiyo maana akanipa siku tatu za kupumzika na wakati nikiwa mapumzikoni akapitia upya rekodi zote za Rais na kugundua kuna baadhi ya rekodi nilizificha.Hapo ndipo nilipogundua kuwa rekodi zile huwa anampatia Benjamin lakini sikujua nini hasa lengo la kufanya vile” akasema Agatha. “Pole sana Agatha.Ahsante kwa kuwa mkweli lakini nataka kufahamu kwa nini hukutaka kumuonyesha Tamar rekodi hizo za mazungumzo ya Rais Dr Fabian na Patrice Eyenga?Gosu Gosu akauliza “Niliponasa mazungumzo yale nikajua Rais wetu pamoja na Patrice wote wawili wanahusika katika mauaji yale ya Lucy Muganza hivyo sikutaka jambo hilo lijulikane ndiyo maana nikayaficha.Kabla ya kuingia SNSA nilikuwa nafanya kazi ikulu na Rais aliyepita Dr Evans ndiye aliyenipeleka SNSA kwa ajili ya kumpa taarifa zote zinazoendelea pale.Baada ya kuja Rais mpya Dr Fabian bado nimeendelea kubaki pale pale.Nikiwa nafanya kazi ikulu nilikula kiapo cha kulinda siri hivyo nilijihisi hatia kubwa sana kufanya kile nilichokuwa nakifanya kudukua mawasiliano ya Rais lakini sikuweza kukataa kwani yalikuwa ni maagizo ya wakubwa wangu” “Good job Agatha.Unadhani…oh my God ! Gosu Gosu akashindwa kuendelea na kushika kichwa. “Suala hili limekuwa kubwa.Idara nyeti ya serikali tayari imekwisha ingiliwa” akawaza Gosu Gosu “Nataka uniambie kuhusu Tamar ?Who is she? Akauliza Gosu Gosu “Ndiye kiongozi wa SNSA kwa sasa” “Kuna mtu anaitwa Kaiza.Do you know him? “Kaiza? “Ndiyo.Unamfahamu? “Kaiza is dead.Alifariki mwaka jana.Alikutwa amefariki katika chumba cha hoteli nchini Afrika kusini”akasema Agatha “Baada ya Kaiza kufariki dunia ndipo alipoletwa Tamar kuchukua nafasi yake.Umemfahamuje Kaiza? “He was a friend of mine” “Unafahamu kuhusu idara hii ya siri?akauliza Agatha “Ndiyo ninaifahamu kidogo.Aliwahi kunieleza Kaiza” akasema Gosu Gosu “Who are you?akauliza Agatha “Naitwa Gosu Gosu.Mimi na kikosi cha rafiki zangu tulipata taarifa kwamba Lucy Muganza anakuja Tanzania.Mwanamke Yule tajiri alikuwa anatumiwa na mataifa makubwa ya nje kwanza kwa ajili ya kutaka kuisambaratisha jumuiya ya Afrika mashariki na pili kuleta machafuko nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ili mabeberu hao wanaomtumia waweze kupata nafasi ya kuendelea kuchota rasilimali.Mimi na wenzangu ndiyo tuliofanya tukio lile.We killed her.” Akasema Gosu Gosu na Agatha akamtazama kwa mshangao. “Najua nimekustua Agatha lakini ni kweli mimi na wenzangu ndiyo tuliomuua Lucy Muganza.Mwanamke Yule alikuwa hatari sana kwa nchi yetu na jumuiya ya afrika Mashariki.Kuna mpango mkubwa unaandaliwa na nchi kubwa kwa ajili ya kusambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Mpango unaandaliwa pia kwa ajili ya kuiondoa madarakani serikali ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo na Lucy Muganza ndiye aliyekuwa ameandaliwa kwa ajili ya kushika nafasi ya Rais wa Congo.Baada ya kugundua mpango huo ikatulazimu kumuondoa na kitendo hicho kimeleta mtafaruku mkubwa sana.Kuna vita kubwa ya chini chini inaendelea hivi sasa baada ya Lucy Muganza kuuawa.Umoja wa Ulaya wanataka wachunguzi wa kimataifa waweze kuingia nchini kufanya uchunguzi wa kifo hicho.Kikubwa wanachokitafuta hapa ni ushahidi wa kumuhusisha Rais wetu na mauaji hayo.Ulifanya jambo la kizalendo sana kutowapa rekodi za mazungumzo kati ya Rais wetu na Rais Patrice Eyenga.Naamini walikuwa wanazitafuta sana taarifa hizo lakini tumechelewa kwani tayari wamekwisha zipata kupitia flashi ile uliyompa balozi Benjamin usiku huu”akasema Gosu Gosu “Hapana bado hawajazipata.Nilipogundua kilichomo ndani yake nilifuta rekodi zile na kupandikiza kirusi katika ile flashi nadhani baada ya kugundua nilichokifanya ndipo walipoanza kunitafuta waniue”akasema Agatha “Ulifahamu fika kwamba wangegundua ulichokifanya lakini bado ukafanya.Kwa nini?Ulijiamini nini? Akauliza Gosu Gosu “I have money.Lot’s of money hivyo nilikuwa nimejiandaa kesho niondoke zangu nchini.Tayari nilikuwa na tiketi za ndege kwa ajili ya kuelekea nchini China” “Agatha unadhani Tamar kiongozi wako anashirikiana na balozi Benjamin kwa ajili ya fedha au kuna jambo lingine? “I think it’s more than money.Baada ya kunielezea kile kinachoendelea hivi sasa hapa nchini nimeanza kupata picha kamili kuhusu Tamar.There’s must be something bigger than money.Ili kujua kinachoendelea kati yao lazima kwanza mumchunguze Tamar”akasema Agatha. “One more thing” akasema Agatha na kutulia kidogo “Sikumpa balozi Benjamin ile flashi niiyotumwa nimpelekee lakini haina maana kwamba hataweza kupata zile rekodi kwa kuwa bado zipo katika hifadhi za SNSA.Ili kujihakikishia kwamba Rais yuko salama katika hili tunapaswa kuharibu mfumo mzima wa kuhifadhi kumbukumbu za SNSA na vile vile……….” Akanyamaza kidogo “Endelea Agatha “Kuipata kompyuta ya Tamar.Kila jioni huhifadhi rekodi zote nilizozipata kwa siku katika faili maalum ambalo tunaoweza kulifungua ni mimi na Tamar pekee na faili hilo limeunganishwa na compyuta ya Tamar na anaweza akalifungua hata akiwa mbali na ofisi yake” akasema Agatha na kunyamaza baada ya Austin kuingia mle ndani.Agatha akaonyesha woga kidogo “Agatha huyu anaitwa Austin January ni mkuu wa kikosi cha jeshi cha operesheni maalum na ndiye kiongozi wangu.Mimi na yeye tunashirikiana katika yale niliyokueleza na huyu ndiye kiongozi wangu” Gosu Gosu akafanya utambulisho na kisha akamueleza Austin yale yote aliyoelezwa na Agatha. “Dah ! Pole sana Agatha na hongera pia kwa ujasiri mkubwa uliouonyesha.Hapa ulipo uko sehemu salama kabisa na mimi na wenzangu tunakuahidi kukulinda kwa kila namna tunavyoweza.Ahsante sana kwa kutupa taarifa hii muhimu.Kwa sasa kitu ambacho tunatakiwa kukifanya kwa haraka ni kuharibu hilo faili ambalo umekuwa ukihifadhi rekodi zote za mazungumzo ya simu ya Rais”akasema Austin “Ili kuharibu faili hilo ninapaswa kuharibu mfumo wote wa SNSA.Ninaweza kupandikiza kirusi katika mfumo huo na kuuharibu lakini nina hofu yawezekana hadi sasa tayari nitakuwa nimekwisha ondolewa katika mfumo na sintakuwa na uwezo wa kuingia na kufanya chochote.We need someone from inside” akasema Agatha “Kuna mtu yeyote unayemuamini anayeweza kukusaidia bila kuhatarisha maisha yako? Akauliza Austin.Agatha akafikiri kidogo na kusema “Kuna kijana mmoja anaitwa Samson.Huyu nimekuwa nikimsaidia na kumfundisha mambo mengi.Anaweza akanisaidia” “Good.You can call him” akasema Austin na kumpatia simu yake akapiga “Hallow ! ikasema sauti ya kiume upande wa pili “Hallo Sam it’s me Agatha.Where are you?akauliza Agatha “Niko barabarani ninaelekea nyumbani.Agatha nini kimetokea leo?Ujumbe umesambazwa kwamba kuanzia sasa wewe ni mtu hatari sana kwa idara na yeyopte atakayekuona au kujua mahala ulipo atoe taarifa haraka sana.Umefanya nini? “Samson sina muda wa kueleza kwa sasa ila kuna jambo kubwa linaloendelea hapo katika idara yetu.Nitakueleza siku nyingine,kwa sasa nimekupigia nahitaji msaada wako” akasema Agatha “What do you need?akauliza Samson “I need access to our system” “What?Are you Crazy Agatha? How can you access the system? Tayari umekwisha ondolewa katika mfumo nakushauri tafadhali huko uliko endelea kujificha kwani ukijaribu kufanya chochote watajua mahala ulipo” “Sikiliza Samson.Nataka unisaidie niingie katika mfumo kwa kupitia akaunti yako.Kuna mambo nataka niyafanye ambayo kama nisipoyafanya yataniletea matatizo makubwa.Samson ni wewe pekee ninayekutegemea kwa sasa unisaidie katika hili.Nimekuwa msaada kwako kwa muda mrefu sasa ni wakati wako kunisaidia.Please Samson I need help” akasema Agatha.Zilipita sekunde kadhaa Samson akasema “Agatha unaniweka katika hatari kubwa.Hata hivi nnavyozungumza nawe ni hatari kubwa kwani wanaweza wakajua” “Samson please.Help me” akasema Agatha “What do you want me to do? “I need you to go back there to the server room and I’ll direct you what to do” akasema Agatha “Sawa Agatha naomba unipe dakika kumi nirejee ofisini nitakupigia nikishafika” “Ahsante sana Sam and I’m so sorry for this.Sina mtu mwingine wa kumkimbilia zaidi yako” akasema Agatha “Usijali Agatha” “Sam jambo lingine naomba usilitaje jina langu utakapokuwa unazungumza na mimi ili watu wasijue.Sitaki kukuweka katika matatizo” “I’m already in touble anyway” akasema Samson na kukata simu kisha Agatha akaelekea chumbani kuchukua kompyuta yake Baada ya muda mfupi Agatha akarejea akiwa na kompyuta yake akaiwasha akajaribu kuingia katika mfumo wa SNSA lakini namba alizoingiza hazikuwa sahihi “Nilijua tu tayari nimekwisha fungiwa” akasema Agatha “Agatha wakati tunamsubiri Samson afike ofisini nataka kumfahamu vizuri huyu Tamar.Umekuwa naye karibu hadi akakuamini kufanya kazi ya hatari kama hii ya kudukua mawasiliano ya Rais.Nataka kumfahamu ni mtu wa aina gani?Austin akauliza “Ni kweli nimekuwa na ukaribu na Tamar na hakuona mtu mwingine wa kumpa kazi ile zaidi yangu na nimeifanya kwa uaminifu mkubwa kuhusu Tamar ni mtu msiri sana.Ni mtu mwenye kuchukua tahadhari kubwa kila wakati.Hapendi mambo yake binafsi yajulikane.Anaishi peke yake na mfanyakazi wake hajawahi kuzungumzia chochote kuhusu kuwa na familia…” akanyamaza Agatha baada ya simu ya Austin kuita “Samson” akasema Austin na kumpatia simu Agatha “Hello Sam” akasema Agatha “Tayari nimefika.Nipe maelekezo unayotaka” akasema Samson kwa sauti ndogo “Good.Nataka unipe namba za kufungulia akaunti yako” akasema Agatha na Samson akampa namba zake Agatha akaifungua akaunti ya Samson halafu akaenda hadi katika faili lile anakohifadhi rekodi zote za Rais akajaribu kulifuta lakini Samson hakuwa na uwezo wa kulifuta faili lile ambalo waliokuwa na uwezo wa kuingia na kulifuta ni Agatha na Tamar pekee “Nimejaribu kuingia katika mfumo kwa kutumia akaunti ya Samson lakini imeshindikana kulifuta faili.Only one option left.To destroy the whole system” akasema Agatha “Do it”akasema Austin na Agatha akapandikiza kirusi katika mfumo wao na mara tu Samson alipoufungua ujumbe wenye kirusi kile kikaanza kusambaa kwa haraka katika mfumo na ndani ya muda mfupi mfumo wote ukasambaa kirusi na kuanza kuleta mauza uza. “Done” akasema Agatha na kuifunga akaunti ya Samson na “Samson nakushukuru sana kwa msaada wao.Nitakutafuta nikueleze nini kilichonitokea” “What have you done? akauliza Samson “Get out of there now Samson” akasema Agatha na kukata simu “Nimemaliza.Mfumo wote umeharibika kinachofuata ni kuitafuta kompyuta ya Tamar ambayo lazima itakuwa na hifadhi ya zile rekodi” akasema Agatha “This is another mission.Hakuna kulala usiku huu wa leo lazima tuhakikishe kwa namna yoyote ile tuanipata kompyuta ya Tam……….” akasema Austin na kunyamaza baada ya Stanley kutokea alikuwa anahema kwa kasi “Stanley kuna nini?akauliza Gosu Gosu “Limetokea shambulio katika ukumbi walimo akina Nasib.Nikiwa nafuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini mle kupitai kamera ya Nasb waliingia watu wapatao sita wakiwa wamefunika nyuso zao na kuanza kumimina risasi hovyo.Sijaweza tena kupata pich a nyingie kwani mawasiliano na Nasibu yamekatika” akasema Stanley na Austin akachukua simu na kupiga namba ya Nasib simu ikaanza kuita lakini haiupokelewa.Akapiga tena lakini haikupokelewa.Wote wakabaki wamesimama wakitazamana. “We need to go back there” akasema Austin “Austin mahala pale ni hatari sana kwa sasa” ` “I have my men in there.I need to g………..” Austin akanyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni Nasib.Austin akaipokea haraka haraka “Nasibu mambo yanakwendaje huko? “Mkuu …” akasema Nasibu akihema kwa nguvu. “Nasibu nini kimetokea hapo?akauliza Austin “Something happened here” “Nini kimetokea?Nieleze tafadhali” “balozi Benjamin ameuawa” “What?Austin akastuka “Balozi Benjamin ameuawa” Austin akashusha pumzi na kuuliza “Nasib tafadhali naomba unieleze kama taarifa hizo ni za kweli” “Kweli kabisa mkuu.Balozi Benjamin amefariki.Ameuawa muda mfupi uliopita” “Kauawa?Nani kamuua?akauliza Austin “Wakati sherehe zikiendelea waliingia watu sita wakiwa na silaha huku wakiwa wamefunika nyuso zao wasionekane.Walianza kumiminia watu risasi hovyo hovyo na kuwaua.Balozi Benjamin alikuwa mmoja wa watu waliopigwa risasi kwa haraka sana baada ya watu wale kuingia ukumbini na akafariki pale pale.Mimi nilikuwa sehemu ya juu hivyo niliweza kuona kilichokuwa kinaendelea upande wa chini.Nilimuona jamaa mmoja akimfuata balozi na kuanza kummiminia risasi ili kuhakikisha amekufa kabisa halafu akamvua saa ya mkononi,akamsachi mfukoni na kuchukua vitu fulani.Inaonekana waliyekuwa wamemlenga ni balozi Benjamin kwani baada tu ya kuhakikisha amekufa wakaondoka zao” “Wewe na vijana wengine wote mko salama? “Wote tuko salama kabisa mkuu.Mimi nilikuwa upande wa juu nikajificha katika nguzo huku nikishuhudia kilichokuwa kinaendelea upande wa chini.watu wengi wameuawa hapa lilikuwa ni tukio la kinyama sana.Wenzangu waliokuwa upande wa nje wanasema kwamba watu wale waliondoka kwa kutumia magari mawili ambayo hayakuwa na namba huu wakipiga risasi hovyo.Tukio hilo limetokea haraka sana na hatukuweza kufanya chochote” “Poleni sana Nasib.Hakuna mnachoweza kufanya hapo kwa sasa.Rudini hapa nyumbani tujipange”akasema Austin na kukata simu “Balozi Benjamin ameuawa”akasema Austin “Mungu wangu ! akasema Agatha “Kwa mujibu wa Nasib kuna watu sita waliokuwa na silaha wameingia ukumbini nak uanza kuwafyatulia watu risasi hovyo na balozi alikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kushambuliwa kwa risasi.Kuonyesha kwamba balozi ndiye aliyekuwa amelengwa mmoja wa washambuliaji alimfuata na kummiminia risasi kuhakikisha wanamuua kabisa”akasema Austin “Haya lazma ni mauaji ya kupangwa na ninakubaliana na Austin kwamba aliyekuwa mlengwa hapa ni balozi Benjamin.Nani anaweza kuwa amefanya mauaji haya?akauliza Gosu Gosu “Ni vigumu kwa sasa kujua nani aliyepanga mauaji haya lakini sababu kuu ilikuwa ni kumuua balozi Benjamin” “Wameturudisha nyuma sana.Tayari tulikwisha anza kupata mwangaza lakini kifo cha Benjamin kimeuzima mwangaza ule”akasema Gosu Gosu “Natakiwa kumpigia simu Rais kumjulisha kuhusu jambo hili” akasema Austin na kumpigia simu Dr Fabian “Austin habari za usiku huu? “Habari si nzuri sana mheshimiwa Rais.Kuna tukio limetokea usiku huu muda mfupi uliopita.Balozi Benjamin ameuawa akiwa katika hafla ya uchangiaji ujenzi wa mabweni ya watoto waishio katika mazingira magumu” “Ameuawa? Dr Fabian akashangaa “Ndiyo mheshimiwa Rais.Balozi Benjamin ameuawa.Ukumbi ulivamiwa na watu wasiojulikana waliofunika nyuso zao wakaanza kumimina risasi ukumbini na kuua watu hovyo.Balozi Benjamin na mke wake wameuawa na inaonekana wao walikuwa walengwa wakuu wa shambulio kwani baada ya kuhakikisha wamefariki dunia wauaji hao wakaondoka zao”akasema Austin ukapita ukimya mfupi “Mheshimiwa Rais” akaita Austin “Austin nimestushwa sana na taarifa hizo.Wewe ndiye wa kwanza kunijulisha.Nitawasiliana na vyombo vya ulinzi kupata taarifa kamili ya nini kimetokea hapo na watu wangapi wameuawa.Kuna chochote mlichokuwa mmekipata kabla ya balozi kuuawa?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais,kuna jambo tulikuwa tumelipata na tunaendelea kulifuatilia tutakapolikamilisha nitakuja kukufahamisha” akasema Austin “Austin hakikisha mnawajua nani waliomuua balozi Benjamin kwani suala hili linaonekana ni kubwa zaidi ya tunavyodhani” akasema Dr Fabian “Sawa mheshimiwa tutafanya hivyo” akajibu Austin na Dr Fabian akakata simu Austin akamgeukia Gosu Gosu “Rais anataka tuwapate waliomuua balozi Benjamin.Sehemu pekee ya kuanzia uchunguzi wetu kuwafahamu waliomuua Benjamini ni kwa Tamar.Nina uhakika kubwa anaweza kuwa na mahusiano na mauaji hayo”akasema Austin “Kwa nini Tamar ahusike katika kumuua balozi Benjamin ambaye ni mshirika wake mkubwa?Kwa maelezo ya Agatha picha tunayoipata ni kwamba rekodi zile alizokuwa anazikusanya Tamar alikuwa anazipeleka kwa balozi Benjamin na nina uhakika kwamba fedha alizokuwa akilipwa Agatha zilitoka kwa Benjamin.Tamar naye lazima alikuwa akipata fedha nyingi sana kwa ajili ya kazi hiyo.Kama alikuwa akifaidika wa kudukua mawasiliano ya Rais kwa nini ashiriki kumuua mtu aliyekuwa anamuuzia taarifa hizo? Akauliza Gosu Gosu “Hata mimi napata shaka kama Tamar anaweza kuhusika na mauji hayo lakini tukirejea katika taarifa ya Nasib ni kwamba watu wale walipoingia tu Benjamin alikuwa ni mtu wa mwanzo kulengwa risasi na kuonyesha kwamba walimlenga yeye mmoja wa wauaji alimfuata akamuongeza risasi na kisha akamvua saa ya mkononi halafu akampekua na kuchukua kila kitu alichokuwa nacho na hii ina maanisha kwamba ile flashi aliyopewa na Agatha wameichukua hawa wauaji.Kwa picha hii inaonyesha wazi kwamba wauaji walifahamu fika kwamba balozi Benjamin anatumia saa ya mkononi katika kuwasiliana pili walifahamu kuhusu flashi aliyopewa na Agatha.Aliyepanga mauaji haya ni mtu ambaye anamfahamu vizuri sana Benjamin Hudson na katika watu ambao lazima tuwachunguze Tamar ni mmoja wao” akasema Austin na kunyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni Dr Fabian “Mheshimiwa Rais” akasema Austin “Austin nimepata taarifa sasa hivi kwamba nyumba ya balozi Benjamin inawaka moto hivi sasa.Unadhani moto huo unaambatana na tukio la kuuawa kwake? “Nahisi hivyo mheshimiwa rais kwani muda wa kutokea kwa matukio haya mawili umekaribiana sana.Nalazimika kuamini kwamba waliomuua Benjamin ni hao waliochoma nyumba yake” “Mpaka sasa kuna lolote mmekwisha lipata kuhusu mauaji hayo?akauliza Dr Fabian “Mpaka sasa bado hatuna fununu zozote lakini tunajipanga kuanza uchunguzi wetu” akasema Austin “Taarifa niliyoipata kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi ambaye yuko eneo la tukio ni kwamba mpaka sasa watu hamsini na sita wamefariki dunia na wengine wamekimbizwa hospitali na kuna uwezekano idadi ya vifo ikaongezeka.Tafadhali fanyeni juu chini kuweza kujua aliyemuua balozi Benjamin” akasema Dr Fabian akakata simu “Nyumba ya balozi Benjamin inawaka moto ndiyo taarifa aliyonipa Rais” akasema Austin “Dah ! akasema Gosu Gosu.Taarifa ile ilimshangaza sana “Hata mimi nalazimika kuamini kwamba walioichoma nyumba ya Benjamin ni wale wale waliomuua.Swali ninalojiuliza kama kumuua tu haikutosha kwa nini wakaenda kuichoma nyumba yake kuna nini hapa wanakificha?akauliza Gosu Gosu “Swali hilo ndilo tunatakiwa kulitafutia majibu.Agatha tuelekeze tafadhali nyumbani kwa Tamar.Suala hili haliwezi kusubiri.Tunaanza kumfuatilia usiku huu huu” akasema Austin PARIS – UFARANSA Milio ya wadudu ndiyo iliyotawala usiku huu katika sehemu tulivu kuzunguka ziwa dogo ambako Peniela na mpenzi wake Nahum walikwenda kupumzika.Angani kulikuwa na mbalamwezi kali ikimulika na wapenzi hawa walikuwa wamekaa nje katika kibaraza huku moto wa kuni ukiwaka mbele yao.Walinzi wa Peniela walikuwa wamejipanga mbali kidogo kuwapa wapenzi hawa nafasi ya kuwa peke yao. “Peniela kwa muda huu mfupi niliokutana nawe ninakiri kwamba nimeishi maisha yangu yote hata nikifa leo sina wasi wasi.Nimeipata ile furaha yote ya maisha yangu niliyoihitaji” akasema Nahum “Nahum mpenzi una nini leo?Kutwa nzima ya leo umekuwa ukizungumzia masuala ya kufa”akasema Peniela Nahum akatabasamu na kuuchukua mkono wa Peniela akambusu kiganjani. “Maisha haya ni mafupi sana Peniela.Ukipata nafasi ya kufurahi itumie kikamilifu kwani huwezi kujua nini kinafuata mbele yako.Kifo kimetuzunguka kila mahali” akasema Nahum “Nahum sitaki kusikia ukizungumzia habari ya kifo tena.Tumekuja hapa kufurahi na si kuhuzunika.Kifo kipo na sote tutakufa hivyo tusiongelee masuala hayo kwa sasa” akasema Peniela “Sawa malaika wangu,lakini naomba ufahamu wewe ni mwanamke wa pekee kabisa ambaye sijawahi kukutana naye katika maisha yangu.Naomba nikiri jambo moja kwako” “Nakusikiliza” akasema Peniela huku akitabasamu “Kwa muda mrefu nimekuwa mchezeaji tu wanawake na sikuwahi kupenda.Nimekutana na wanawake wengi na ……..” Nahum akanyamaza baada ya mmoja wa walinzi wao kutokea akikimbia “Ingieni ndani harak……..” Hakumaliza alichokuwa anawaeleza akina Peniela akapigwa risasi ya mgongo akaanguka chini.Kwa kasi ya aina yake Nahum akaruka kutoka mahala alipokuwa amekaa akamrukia Peniela wakaanguka chini ya kiti. “Peniela nisikilize.Watu hawa wananitafuta mimi wamekuja kuniua hivyo kama nikifa nakuomba umtafute Mathew Mulumbi.Yuko hai” “Nahum !! akasema Peniela “Nisikilize Peniela.Mathew Mulumbi yuko hai.Tafadhali mtafute” akasema Nahum na kusimama akitaka kukimbia akapigwa risasi tatu na kuanguka chini akafa pale pale. Peniela mwili ulimtetemeka alikosa nguvu akabaki amejificha chini ya kiti.Baada ya dakika tano kupita akasikia sauti ikimuita “Mama Peniela ! Mama Peniela ! ilikuwa ni sauti ya mmoja wa walinzi wake.Peniela hakuweza kufungua mdomo wake kuitika.Walinzi wale walikuwa na tochi wakamulika eneo lile ambalo liikuwa giza baada ya taa kupasuliwa wakamuona Peniela akiwa amejificha chini ya kiti.Hatua chache mbele yake alilala Nahum akiwa hana uhai.Mmoja wa walinzi wale akamfunika Peniela koti kisha wakamuinua na kumpeleka katika gari wakaondoka kwa kasi eneo lile wakipishana na magari ya askari waliojulishwa kuhusu kutokea kwa mauaji yale. “Nini kimetokea?Nani kafanya mauaji yale?Peniela akawauliza walinzi wake “Mpaka sasa hatujui nani kafanya mauaji yale lakini nilichokishuhudia mimi ni watu waliovaa makoti marefu na kufunika nyuso zao wakiwa na bunduki za kulenga masafa marefu wakitoweka katika msitu.Usihofu mama tutachunguza na tutajua ni nani waliofanya tukio lile” akasema mmoja wa walinzi “Hivi ni kweli Nahum amekufa au niko ndotoni?akajiuliza Peniela na kuendelea kumwaga machozi ,akakumbuka namna alivyomuona Nahum akipepesuka huku akichakazwa risasi “Huu ni mkosi gani unanikuta mimi?Kila mwanaume ambaye ninakutana naye na moyo wangu ukampenda hadumu.Mathew alipotea na sasa Nahum”akawaza na kuendelea kulia TEL AVIV – ISRAEL Simu ya Efraim Dagan aliyekuwa na maafisa wengine wa Mossad pamoja na maafisa wa gereza ambalo Mathew Mulumbi alifungwa,ikaita akatoika nje na kuipokea “Hallow” akasema Efraim “Mkuu tumeimaliza kazi.Nahum tayari amekufa” “Kazi nzuri sana.Mna hakika hakutakuwa na tatizo lolote? “Tumemuondoa kiumakini sana hakutakuwa na tatizo lolote hata hivyo tulilazimika kuwaua pia walinzi wachache wa Peniela ndipo tukaweza kumfikia Nahum” “Ahsanteni sana kwa kazi hii nzuri” akasema Efraim na kukata simu “Nahum alikuwa ni mmoja wa watu wetu wa muhimu sana lakini alichagua mapenzi akasahau kazi na hivyo kuhatarisha maisha yake mwenyewe na ya shirika.Amekipata alichokihitaji” akawaza Efraim na kurejea ndani walikuwa wanaendelea kufuatilia kile kinachoendelea chumbani alimo Mathew Mulumbi na Ammar Nazari “Ammar muda umewadia.Nataka kupata tena uhakika kutoka kwako kama uko tayari kuendelea na mpango wetu wa kutoroka” akasema Mathew.Ammar akawaza kidogo halafu akasema “Tuendelee na mpango wetu Abu.Ninataka kuondoka humu ndani” akasema Ammar “Safi sana.Kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga” akasema Mathew na Ammar akatikisa kichwa kukubaliana naye halafu Mathew akalala sakafuni kama mtu aliyepoteza fahamu.Ammar akasogea karibu na mlango akanyoosha mkono na kubonyeza kitufe cha kengele ya dharura. “Mambo yameanza” akasema Efraim akiwa katika ofisi ya mkuu wa gereza. Askari wawili wa gereza walifika katika mlango wa chumba cha akina Mathew na kuuliza kuna nini,Ammar akawajulisha kwamba mwenzake Abu ambaye ni Mathew ameanguka ghafla na kupoteza fahamu.Mlango ukafunguliwa na askari wale wakaingia ndani,Ammar akatakiwa kusogea kwenye kona wakati askari mmoja akienda kumtazama Mathew.Akammulika tochi machoni halafu akapiga magoti ili aweze kumtazama vizuri mara kwa kasi ya ajabu akajikuta amedakwa shingo yake akageuzwa na kuangushwa chini akataka kuinuka lakini akapigwa ngumi nzito akalala sakafuni.Lilikuwa ni tukio lililotokea kwa kufumba na kufumbua.Mara tu Mathew alipomvamia askari Yule aliyekuwa anamuangalia,askari aliyekuwa na Ammar akageuka kutazama nini kimetokea ndipo Ammar akamrukia kama Simba anayerukia windo akampiga kichwa kizito akaanguka chini halafu akaiokoa bunduki akampiga na kitako kichwani akamuinua na akamkaba na kumvunja shingo kisha akamtupa chini “Nimeingia kwenye ulimwengu wa makatili” akawaza Mathew.Ammar akachukua mto akaukunja halafu akachukua bastora ya Yule askari aliyekuwa amedhibitiwa na Mathew akamuwekea kichwani akaachia risasi na kumfumua kichwa. “Tulipanga kutokuua askari lakini huyu jamaa ameamua kuua.Nikimzuia anaweza akaingiwa na mashaka” akawaza Mathew na haraka haraka wakawavua sare wale askari wakavaa na kuchukua redio ya mawasiliano pamoja na kadi ya kufungulia milango.Wakawaficha askari wale chini ya kitanda “Uko tayari?akauliza Mathew “Niko tayari” akajibu Ammar.Mathew akachukua ramani ile ya gereza wakaipitia kisha wakatoka kwa tahadhari wakafunga mlango. “Tulikubaliana kutokuua askari.Mbona wameua askari wangu?akafoka mkuu wa gereza. “Kama Mathew angemzuia Ammar kutokuua wale askari angeweza kuingiwa na wasi wasi ndiyo maana akaamua kumuacha awaue”akajibu Efraim Mathew na Ammar wakifuata ramani ile waliyopewa walipita korido la kwanza halafu wakatokea katika ngazi wakapanda na kutokea katika korido la pili.Kwa mbele wakawaona askari wakajibanza wakasubiri askari wale wapite halafu wakatembea haraka haraka wakakuta kuna njia mbili wakafuata njia ya kushoto wakaifuata njia ile na mara tu walipolifikia geti la kwanza king’ora cha hatari kikalia.Askari wakaanza kukimbia kwenda kujua nini kimetokea.Walipitisha kadi katika geti lile la kwanza likafunguka wakavuka na kukimbia hadi katika ujia ambao walikuta askari watatu wakikikimbia ,Ammar akawamiminia risasi.Mathew akaitazama ramani akakuta lazima waruke ukuta kuingia upande wa pili haraka haraka akamtaka Ammar kuinama akapanda juu ya mgongo na kushika kingo za ukuta kisha akamvuta Ammar naye akapanda wakajirusha upande wa pili.Walikwaruzwa na seng’enge zilizokuwa juu ya ukuta.Mathew akainuka na kumtaka Ammar waendelee baada ya kusikia katika redio kwamba wafungwa waliotoroka wamevaa sare za askari.Mathew akiwa ametangulia mbele mara ghafla wakamulikwa na tochi zenye mwanga mkali na kutakiwa kusimama.Kwa kasi ya aina yake Mathew aliyekuwa ametangulia mbele akajitupa chini na Ammar akamimina risasi askari watatu wakaanguka chini kisha wakakimbia kuelekea katika geti la pili.Wakati Mathew akijandaa kufungua geti lile mara Ammar akatoa mguno wa maumivu alikuwa amepigwa risasi ya mguu akaangua chini. “Nimepigwa risasi ya mguu !! akalalama Ammar.Mathew akageuka na kumimina risasi halafu akamfuata Ammar akamuinua na kumtaka ajitahidi wamekaribia. “Ammar jitahidi utembee tunakaribia sana kufika katika ule mfereji mkubw..” akasema Mathew na risasi zikaanza kuvuma akamkinga Ammar na kuanza kumimina risasi halafu akamuinua na kuvuka geti mara Ammar akapigwa tena risasi nyingine ya mguu ikamlazimu Mathew kumuinua na kumuweka begani “Naona mambo yanaanza kuwa magumu.Mpango ulikuwa apigwe risasi moja lakini amepigwa mbili.Yawezekana kuna askari ambao hawajui kuhusu huu mpango wa kutoroka.Kinachofuata kwa sasa ni kuwafagia tu kila atakayetukaribia kwani tukifanya mchezo wanaweza wakatumaliza hawa.” Akawaza Mathew na mara taa zikazima.Hii ilikuwa ni ishara kwamba wanakaribia kufika katika mfereji mkubwa wa maji taka.Katika mfuniko wa kuingilia katika mfereji wa maji taka kulikuwa kimya lakini Mathew akageuka na kumimina risasi kwa nyuma kana kwamba kuna watu walikuwa wanawafuatilia halafu akamuweka chini Ammar akalifungua geti akambeba Ammar hadi katika mfuniko.Akachana shati lake na kumfunga Ammar pajani halafu akautafuta mfuniko akauona.Ulikuwa ni mfuniko mkubwa wa zege akajitahidi kuusogeza pembeni akashindwa “Natakiwa kujitahidi vinginevyo wakitukuta hapa watatuua” akawaza Mathew na kukusanya nguvu akausukuma mfuniko ule ukasogea akajitahidi tena ukasogea zaidi akamulika ndani na kuziona ngazi za kushukia chini.Haraka haraka akamfuata Ammar akamsogeza pale kwenye shimo na kuanza kumshusha chini taratibu kisha wakaanza kutembea katika maji yaliyokuwa na harufu.Baada ya dakika kumi na moja wakazikuta ngazi ambazo kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa Mathew zinatokea barabarani Mathew akapanda na kuusukuma mfuniko wa chuma akachungulia nje ni kweli walikuwa barabarani.Akampandisha Ammar na kuufunika mfuniko ule wa chuma akamtegemeza wakavuka barabara wakaanza kutembea hadi walipokuta daraja wakaingia kwa chini wakajificha “Tuko nje ya gereza sasa” akasema Mathew “Ahsante sana Abu.Bado naona kama ni ndoto”akajibu Ammar akihisi maumivu makubwa “Si ndoto ni kweli kabisa tuko nje ya gereza.Kinachotakiwa sasa ni kutafuta namna ili uweze kupata matibabu kwanza kuondoa risasi ambazo umepigwa na pili kuongezewa damu.Dr Abeba atafika kutupeleka sehemu salama” “Unamuamini huyo Abeba?akauliza Ammar “Ndiye aliyetusaidia tukafika hapa na ndiye atakayetusaidia tuweze kuondoka hapa Israel salama” akasema Mathew na magari kadhaa yakapita pale juu ya daraja. “Tutafute namna nyingine ya kujiokoa huyo mtu wako hawezi kuja tena.Ninazidi kupoteza damu nitakufa”akasema Ammar akiwa katika maumivu baada ya kusubiri kwa muda bila Abeba kutokea “Vuta subira atakuja.Ninamtegemea yeye kwa kila kitu” akasema Mathew na kuendelea kusubiri Baada ya dakika kadhaa likapita gari moja na kwenda kusimama mbele kidogo ya daraja halafu mlango ukafunguliwa.Tochi ikawashwa na kuzimwa mara tatu kisha Mathew akajitokeza.Alikuwa ni Abeba.Wakasaidiana kumbeba Amar wakamungiza katika gari na kuondoka “Nashukuru sana Abeba kwa msaada huu mkubwa.Nadhani hii ni mara ya kwanza watu wanafanikiwa kutoroka katika gereza lile” akasema Ammar lakini Abeba hakujibu kitu.Aliendesha gari hadi nje kidogo ya mji wakaingia katika shamba la matunda kulikuwa na nyumba wakaingia ndani na bila kupoteza muda Abeba akaanza kumshughulikia Ammar.Wakafanikiwa kutoa risasi mbili katika mguu wake na kumuongezea damu kwani Abeba alikuwa amekwenda na akiba ya damu. Baada ya kumuhudumia Ammar ikafuata zamu ya Mathew akamganga majeraha mbalimbali aliyoyapata wakati akiwa mle gerezani. “Mnatakiwa kabla ya mapambazuo muwe mmeondoka hapa Israel kwani picha zenu zitasambazwa kila mahali kwamba ni wahalifu na mnatafutwa.Wapi mnaelekea ili niwapeleke?akauliza Abeba na Mathew akamtazama Ammar aliyekuwa amelala kitandani “Naomba unisaidie simu tafadhali” akasema Ammar na Abeba akampa simu Ammar akaandika namba na kupiga.Simu ilipopokelewa akazungumza na mtu na kumpa maelekezo kadhaa halafu akamuelekeza Abeba sehemu ya kuwapeleka. Chupa ya damu ilipomalizika wakaingia garini na safari ikaanza kuelekea Ramallah huku Ammar akimuelekeza Abeba njia ya kupita kukwepa vizuizi vya wanajeshi.Safari ilikuwa ya kimya kimya na baada ya mwendo wa saa moja wakasimamishwa na kundi la watu wenye silaha.Mathew akaiweka sawa bunduki yake lakini Ammar akamzuia “Hawa ni watu wangu niliwaelekeza niwakute hapa” akasema Ammar na kumshukuru Abeba kwa msaada mkubwa aliowasaidia.Kundi lile la watu wenye silaha wakalisogelea gari lile na Ammar akafungua mlango akashuka.Watu wake walipomuona wakambeba huku wakishangilia na kupiga risasi juu “Be safe” Abeba akamwambia Mathew “Go now.This place is too dangerous” akasema Mathew na Abeba akageuza gari akaondoka zake.Mathew akabaki amesimama.Ammar akapelekwa katika gari kisha akaagiza Mathew aletwe katika gari alimo na msafara wa magari ukaondoka eneolile huku watu wakishangilia na kupiga risasi juu “Abu nashukuru sana rafiki yangu.Bado sijaamini kama niko nje ya gereza lile.Siamini kama leo ninakwenda nyumbani kwangu.Sina namna nzuri ya kukushukuru kwa msaada huu mkubwa.Karibu sana katika himaya yangu.Eneolote hili ni la kwangu” akasema Ammar Abeba baada ya kuwaacha akina Mathew akasimamisha gari na kusubiri huku akiwatazama kupitia kiona mbali maalum chenye uwezo wa kuona kwenye giza akaona Mathew akiingizwa katika gari alimo Ammar na msafara wa magari ukaondoka akachukua simu na kumpigia Efraim “Mathew na Ammar tayari wamekutana na wanamgambo wa Ammar Nazari Brigades wamewachukua na wameondoka” “Kazi nzuri Abeba.Sasa unaweza ukarudi.Tumuombee Mungu aweze kufanikisha mpango wetu.Kwa namna ulivyomuona Ammar anawasi wasi wowote kuhusu Mathew? “Hana wasi wasi wowote.Furaha yake haielezeki” “Safi sana.Hii ni bahati nasibu tumecheza tuendelee kusubiri” akasema Efraim







Katika makazi ya Ammar Nazari sherehe kubwa ilikuwa inaendelea.wafuasi wake walikuwa wakicheza ngoma na kufurahi.Msafara wa magari uliwasili na furaha ikazidi.Ammar akashushwa garini na kuingizwa ndani akasalimiana na mke wake na watoto. “Abu kutanana familia yangu.Nina watoto tisa na wake wawili” akasema Ammar na kumtambulisha Mathew kwa wake zake na watoto. “Huyu anaitwa Abu Al zalawi ni mwenzetu katika mapambano dhidi ya Israel na ndiye aliyefanikisha mimi kuwepo hapa leo.Ni mtu muhimu sana kwangu na nina deni kubwa kwake” akasema Ammar na kuelekezwa Mathew apewe chumba maalum katika makazi yake na ahudumiwe kwa kila kitu.Mke mdogo wa Ammar akamchukua Mathew na kumpeleka katika chumba cha wageni muhimu katika jumbe lile la Ammar “Karibu jisikie nyumbani.Naitwa Nawal.Ni mke mdogo wa Ammar” akasema Nawal na kumtaka Mathew akaoge. “Mathew Mulumbi karibu katika ulimwengu wa magaidi.Mpaka hapa naamini Ammar ameniamini vya kutosha kwani nimefanikiwa leo hii amewasili nyumbani kwake.Uhakika wa kumpata Habiba Jawad ni mkubwa sana” akawaza Mathew akiwa bafuni akajitazama katika kioo “Ninatisha.I look like hell.Hata Peniela akinitazama leo anaweza akanipotea.Tazama mwili wangu ulivyokuwa na makovu na vidonda kila mahali.Sijawahi pitia kipindi kigumu katika maisha yangu na katika kazi yangu ya ujasusi hadi sasa.Nimeteseka mno na kama nikifanikiwa kutoka salama katika sakata hili sintajishughulisha tena na mambo haya.It’s over.Nataka nitulie na familia yangu” Mathew alipokumbuka familia yake akajikuta akipandwa na hasira za ghafla. “Peniela anaamni tayari nimekwisha fariki na ameamua kuendelea na maisha yake akaanzisha mahusiano na na Yule mtu wa Mossad.Inaniuma sana kwa mke wangu ninayempenda kuchezewa kiasi hiki.Mossad wanamtumia kwa ajili ya kunitaka nifanye wakitakacho.Siwezi kumlaumu sana kwani haya yote nimeyataka mimi mwenyewe.Lakini naapa kama nikifanikiwa kutoka salama na kumkuta Yule jamaa anaendelea na mahusiano na Peniela nitamnyonga kwa mikono yangu nimalize hasira zangu zote nilizonazo” akawaza Mathew na kuoga maji alipotoka akakuta kuna nguo zimewekwa kitandani akavaa halafu akakaa kitandani “Najaribu kuwaza ni vipi kama wakigundua mimi nimetumwa na Mossad?Hakutakuwa na kingine zaidi ya kuuawa.Natakiwa kuwa makini sana kuhakikisha sifanyi kosa hata dogo kwani kosa dogo sana linaweza kuniletea matatizo makubwa” Mlango ukagongwa akaenda kuufungua akakutana na Nawal akamkaribisha seheu ya chakula ambako alikuwepo Ammar na watu wengine watano waliokuwa na ndevu nyingi.Wale jamaa walimuangalia Mathew kwa makini sana akawasalimu halafu akaketi katika mkeka pamoja nao.Ammar akamtambulisha Mathew kwa wale jamaa ambao ni viongozi wa juu wa kundi la Ammar Nazari Brigades “Ndugu zangu viongozi wenzangu huyu anaitwa Abu Al Zalawi ni raia wa Kenya lakini mwenye asili ya Misri.Amekuwa akiendesha mapambano dhidi ya waisrael nchini Kenya na amefanikiwa kumuua mkuu wa Mossad Afrika mashariki aliitwa ..” akasema Ammar na kumtazama Mathew “Aliitwa Avi Abramson” akasema Mathew. “Vile vile aliua watu wengine wawili wa Mossad hadi alipokamatwa na kuletwa katika gereza nililokuwa nimefungwa.Kwa bahati nzuri mimi nay eye tulielewana na kuwa marafiki na yeye ndiye aliyefanikisha mimi kuwepo hapa muda huu.Yeye ndiye aliyenisaidia hadi kunifikisha hapa.Nilipigwa risasi na kushindwa kutembea angeweza kuniacha na kuendelea kutoroka lakini hakuniacha alinibeba na kuhakikisha tunatoka wote gerezani.Ndugu zangu huyu ni mgeni muhimu sana kwetu na tuna deni kubwa kwake.Baada ya kutoka gerezani hatarejea tena chini kwake kwani tayari taarifa za kutoroka kwake zitakuwa zimesambaa hivyo atabaki hapa ataungana na sisi katika mapambano” akasema Ammar na watu wale wakamkaribisha Mathew kwa furaha.Baada ya kupata chakula Ammar akaelekeza Mathew apelekwe akapumzike Baada ya Mathew kuondoka Ammar akawa na kikao kizito na wasaidizi wake wakampa kwa muhtasari yale yote yaliyofanyika wakati akiwa gerezani akawapongeza kwa kuendeleza mapambano hata wakati akiwa amefungwa.Baada ya maongezi marefu yaliyochukua saa tatu Habib msaidizi mkuu wa Ammar akasema “Ammar sote tunashukuru sana kwamba umerejea salama kutoka gerezani.Lakini kuna kitu kinanipa wasiwasi sana” “Nini kinakupa wasi wasi? “Huyu jamaa uliyekuja naye.Una uhakika gani kweli ni mpiganaji?Hudhani kwamba anaweza kuwa ni pandikizi la waisrael wakitaka kutuchuguza na kupata taarifa zetu?akauliza Habib “Msiwe na wasi wasi ndugu zangu.Abu Zalawi ni mtu mzuri na si pandikizi.Haikuwa rahisi kwangu kumuamini lakini baada ya kumchunguza nikamuamini ni mwenzetu.Ameteswa kwa miaka mitatu na hata mngebahatika kumona mgongo wake wote umejaa vidonda.Msiwe na shaka naye hata kidogo” akasema Ammar “Ammar wewe ni kiongozi wetu na hata siku oja hatuwezi kukupinga kwa kila ukisemacho lakini binafsi bado nina mashaka na huyu mtu.Kama mtakubaliana name kabla ya kumuingiza katika jeshi letu tumchunguze na kumjua ni nani na tumpime kwa kumpa jaribio kama kweli anaweza kuwa ni muaminifu kwetu” akasema Habib na ukimya ukatawala mle chumba baada ya muda Ammar akauliza “Kwa nini mnakuwa na wasi wasi kuhu huu mtu?Kwa mambo aliyonifabnyia hatustahili hata kumchunguza kwani ni mtu safi na hana tatizo.Huyu ni mwenzetu anastahili heshima kubwa” akasema Ammar akionekana kukereka na maneno yale ya Habib “Ammar utanisamehe kama maneno yale yalionyesha utovu wa nidhamu lakini ni kanuni ya jeshi letu kabla ya kumuingiza mtu yeyote lazima kwanza tumchunguze na tujiridhishe kama kweli ni mtu safi na anaweza akatufaa.Hata huyu pia lazima tumchunguze tumjue ni nani na katokea wapi.Naomba unipe ruhusa nimchunguze huu mtu na kama nikikuta kuna chembe ya kasoro basi nitakupa taarifa” “Sawa hakuna tatizo fanya hivyo” akasema ammar na kikao kikaishia hapo kwani hakuonyesha kufurahishwa na kitendo kile cha kutaka kumchunguza Mathew Habib hakutaka kusubiri hadi asubuhi akawachukua vijana wawili wakiwa na kifaa Fulani wakaenda katika chumba cha Mathew wakagonga akaamka na kufungua mlango wakaingia ndani. “Abu Zalawi unajisikiaje?akauliza Habib “Ninajisikia maumivu mwili mzima” akasema Mathew “Pole sana.Mimi naitwa Habib ni kamanda mkuu wa vikosi vyote vya Ammar Nazari Brigades.Ammar amenipa maelekezo ya kukujumuisha katika jeshi letu hivyo basi kabla ya kukuingiza rasmi jeshini kuna mchakato ambao lazima uupitie” akasema Habib na kuwapa ishara wale vijana aliokuwa nao wafaye ukaguzi.Kifaa kile walichokuwa nacho kikawashwa na kuanza kupitishwa katika mwili wa Mathew lakini hawakukuta kuna kitu chochote ambacho Mathew alikuwa amepandikizwa mwilini ili kuwajulisha Mossad mahala alipo.Habib akaagiza warudie tena lakini hakukuwa na kitu chochote.Akaelekeza nguo zote alizokuja nazo Mathew zichunguzwe lakini hakukuwa na kifaa chochote “Uko safi sasa tunaomba tuongozane”akasema Habib na Mathew akainuka akaongozana na wale jamaa “Nilijua mambo kama haya yanaweza kutokea ndiyo maana nilikataa kufungwa kifaa chochote cha kuwajulisha Mossad mahala nilipo.Kama ningekuwa na kifaa kile hivi sasa yangekuwa ni mambo mengine.” Akawaza Mathew Waliingia katika chumba kimoja kikubwa chenye mitambona vifaa vingi vya mawasilano “Watu hawa wameendelea sana.Ofisi hii ni kubwa utadhani ofisiya Mossad” akawaza Mathew na kuingizwa katika chumba kidogo chenye meza na viti viwili.Akakaa mle na baada ya muda akaingia kijana mmoja aliyevaa kanzu ya rangi ya kijivu.Alikuwa amevaa miwani na hakuwa na ndevu nyingi kama wenzake.Mkononi alikuwa na faili akaliweka mezani. Habib na wenzake walikuwa wanafuatilia mahojiano yale ya Mathew na Yule kijana kupitia runinga kubwa katika chumba kingine “Naitwa Mustapha.Nimekuja hapa nataka kuchukua taarifa zako hivyo naomba unipe taarifa za kweli ili tuweze kukufahamu na kukuingiza katika mfumo wetu”akasema Mustapha. “Nafurahi kukufahamu Mustapha.Natumai tutafanya kazi pamoja”akajibu Mathew huku akitabasamu “Nataka kufahamu jina lako nani?akauliza Mustapha “Naitwa Abu Al Zalawi” “Unaweza ukatupa historia yako kwa ufupi umetokea wapi hadi ukafika hapa?akauliza Mustapha “Kama nilivyosema naitwa Abu Al zalawi,raia wa Kenya mwenye asili ya Misri.Baba yangu aliitwa Khalid Al Zalawi.Alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kundi la Abu Hafs al-Masri Brigades.Baba yangu Khalid aliuawa na majeshi ya Israel na hapo ndipo nilipoapa kuendeleza mapambano na Israel.Mama yangu alitokea Kenya hivyo haikuwa kazi kwangu kupata uraia wa Kenya.Nikiwa Kenya nilimuua Avi Abramson mkuu wa Mossad Afrika Mashariki pamoja na majasusi wengine wawili ndipo nilipoanza kutafutwa na serikali ya Israel” Wakati Mathew akimuelezea Mustapha historia yake katika chumba kile walichokuwemo akina Habib vijana walikuwa na kasi ya aina yake na mara tu alipotaja jina lake wakalitafuta na sura na picha yake vikaonekana Runingani.Abu Zalawi alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wanatafutwa sana na serikali ya Israel. “Anachokisema ndicho kilichoandikwa na Israel” akawaza Habib Mathew aliulizwa maswali mengi kuhusu maisha yake na hadi namna walivyofanikisha kutoroka. “Majibu yake yanaridhisha kabisa na yanashawishi kumuamini lakini bado nafsi yangu inakuwa nzito kumuamini moja kwa moja.lazima nimpe mtihani kesho” akawaza Habib na kumrejesha Mathew chumbani kwake. “Nashukuru Mossad wameweza kufanya kama walivyoelekeza.Taarifa zote nilizowapa ziko mtandaoni na wameridhika mimi ni Abu Zalawi lakini huyujamaa Habib bado haonyeshi kunikubali.Amesema tutaonana asubuhi.Sijui anataka afanye nini tena” akawaza Mathew na kujilaza kitandani alikuwa amechoka sana Saa kumi na mbili za asubuhi mlango wa chumba alimolala Mathew ukagongwa akaingia Habib. “Abu kumekucha kazi inaanza.Sisi hatuna muda wa kupumzika” akasema Habib na Mathew bila hata kunawa uso akatoka wakaingia katika gari na kuondoka.Ulikuwa ni mwendo mrefu hadi ilipofika saa nne za asubuhi wakasimamisha gari sehemu na Habib akasema “Abu wewe ni mtu shujaa.Tunakushukuru sana kwa kumuokoa mkuu wetu na kuamua kuungana nasi katika mapambano dhidi ya waisrael.Jana ulinieleza hasira ulizo nazo kuhusu Israel na uliapa kulipiza kisasi kwa kitendo cha kumuua baba yako.Kilometa chache kutoka hapa kuna soko kubwa la samaki na watu wengi kutoka upande wa Israel huja kununua samaki.Ulinieleza kwamba umeteswa kwa miaka zaidi ya mitatu gerezani.Ni wakati wa kulipa kisasi.Tunakwenda kuondoa maisha ya waisrael” akasema Habib na kufungua sanduku lililokuwa nyuma likaonekana bomu kubwa. “Jesus Christ ! akawaza Mathew baada ya kuliona bomu lile. “Abuu nadhani mpaka hapa umekwisha fahamu ninachokimaanisha” “Nimekuelewa Habib” akasema Mathew huku akijitahidi kutokuonyesha woga wowote. Walikwenda hadi katika soko kubwa la samaki.Magari kadhaa yalikuwa yamejipanga yakiuza samaki wabichi.Gari walilopanda akina Mathew likapenya na kuingia kati kati ya magari yale ya kuuza samaki. “Abu tumefika.Muda utakapowadia utabonyeza kitufe hiki bomu litalipuka na damu ya waisrael itamwagika.Wewe ni mpambanaji nadhani unafahamu thamani ya hiki unachokwenda kukifanya” “Ninafahamu Habib” akasema Mathew.Habib akamfanyia dua halafu akabonyeza saa iliyokuwa mbele halafu akashuka akafungua mlango. “Mathew dunia itakukumbuka kwa ushujaa huu wa leo na sote tutakutana ahera” akasema Habib na kushuka garini akamuacha Mathew “Nimenusurika mara nyingi kupoteza maisha hadi watu wananiambia nina maisha marefu kama paka lakini leo hii nadhani maisha yangu yamefika ukingoni.Hakuna namna nitakavyoweza kupona.Bomu litalipuka na kuua watu wengi na mimi nikiwemo.Najuta kilichonileta huku.Bora ningebaki gerezani Israel kuliko kuja kufa kigaidi huku nikiua watu wengine wasio na hatia” akawaza Mathew huku uso wake ukiwa umeloa jasho akitazama sekunde zinavyozidi kukimbia kwa kasi “Mathew Mulumbi leo ninakufa kifo cha kijinga sana.Ile sifa yangu yote ya mtu shujaa lakini leo inafutika na kufa kama gaidi.Nadhani muda huu uliobaki wa dakika mbili niutumie kwa maombi” akawaza Mathew na kufumba macho “Ee Mungu ni wewe pekee mwenye kuona hadi ndani ya mioyo yetu na kujua dhamira zetu nadhani unanitazama hivi sasa dhamira yangu si kuua watu wako wasio na hatia.Nimefika hapa kutokana na mapenzi makubwa niliyo nayo kwa nchi yangu na lengo langu ni kuhakikisha ninapambana na magaidi hawa wasio na huruma hata chembe lakini nimejikuta mikononi mwao na wananilazimisha kujiua na mimi kuua wengine.Nimekukosea mambo mengi ee Mungu wangu naomba unisameheme yale yote niliyokukosea makubwa na madogo.Mungu wangu,Musa aliwaondoa waisrael utumwani Misri lakini hakuweza kufika nchi ya ahadi,ninaomba baada yangu umuinue mtu mwingine aweze kuiendeleza hapa nilipofika na kuutokomeza kabisa ugaidiNinakufa nikiwa na mapenzi makubwa na nchi yangu Tanzania na ndilo neno langu la mwisho kulitamka.Nakupenda Tanzania” akafumbua macho na kutazama saa zilibaki sekunde tano. “It’s time” akawaza na kutazama nje halafu akatazama saa sekunde zilibadilika tatu ,mbili moja “Allahu akbar ! akasema Mathew na kubonyeza kitufe alichoelekezwa

 MPENZI MSOMAJI USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI HIIKATIKA SEHEMU IJAYO…





DAR ES SALAAM Muziki uliofunguliwa kwa sauti ndogo ulisikika katika sebule kubwa nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambamo Austin na Gosu Gosu walikuwa kimya na kila mmoja alionekana kuzama mawazoni.Life goes on wimbo wa mwanamuziki marehemu Tupac Shakur ndio uliokuwa ukichezwa mle sebuleni.Huu ni wimbo ambao Austin January hupenda sana kuusikiliza hasa pale anapokuwa na mawazo mengi.Alifuatisha mdundo kwa kichwa huku akiimba mashairi ya wimbo ule alioonekana kuufahamu vizuri.Gosu Gosu alikuwa amejilaza sofani na mbele yake kulikuwa na meza ndogo yenye chupa tatu za bia.Hawakuwa wakizungumza na kila mmoja sura yake ilionekana kujawa na mawazo. Wimbo ulimalizika na Austin akaendelea kusikiliza nyimbo nyingine za marehemu Tupac.Aliinuka sofani akaenda katika friji akafungua na kuchukua chupa ya bia akaenda kusimama dirishani akanywa funda moja na kuchungulia nje.Tayari kulianza kupambazuka.Milio ya ndege ilianza kusikika,akageuka na kumtazama Gosu Gosu ambaye naye alionekana kuwa mbali sana kimawazo “Papaa kumepambazuka.What are we going to do?akauliza Austin.Gosu Gosu akainuka akakaa na kuchukua chupa akanywa funda kubwa na kusema “Hatuna cha kufanya.Umesikia alichokisema mkuu wa nchi kwamba tuachane na suala hili.Hatuwezi kupingana na kauli yake.We have to stop” akasema Gosu Gosu.Austin naye akanywa funda moja halafu akaenda kuketi sofani “Papaa una hakika kweli unataka kukata tamaa?Kuna jambo linaloendelea hapa na tunapaswa kulifahamu” akasema Austin “Austin kaka yangu,nadhani tuyaheshimu mawazo ya Rais.It’s over ! Tukiendelea kutaka kulazimisha jambo hili tutaingia katika vita ambavyo hatutashinda.Yule ni mkuu wa nchi na lazima tutii maelekezo yake.Amesema tuachane na hili suala hakuna namna tunavyoweza kuendelea nalo” akasema Gosu Gosu “Unadhani Mathew angekuwepo angekubali suala hili liishie hapa?akauliza Austin.Ilimchukua muda kidogo kwa Gosu Gosu kujibu swali lile. “We’re not Mathew.Yule alikuwa ni mtu wa kipekee kabisa hivyo basi hatuwezi kujifananisha naye.Austin hakuna unachoweza kunieleza kitakachonishawishi niendelee na operesheni hii”akasema Gosu Gosu “C’mon Papaa.Kwa nini unakuwa hivyo?Inakuingia akilini kwa Rais kututaka tuachane na operesheni hii? Lazima kuna jambo hapa si bure” akasema Austin “Austin kama nilivyosema,kuwe na jambo kusiwe na jambo mimi sihusiki tena.Kwa sasa naendelea na maisha yangu ya kawaida na sitaki tena kujihusisha na masuala haya.Tulikwisha jitoa kumsaidia Rais katika mapambano haya lakini ni yeye mwenyewe aliyekuja kutuzuia tusiendelee hivyo basi hakuna haja ya kuendelea tena.Rudi kambini kwako endelea na majukumu yako ya kawaida” akasema Gosu Gosu “I can’t believe this !! akasema Austin kwa sauti ndogo.Hakuamini kuyasikia maneno yale ya Gosu Gosu “Austin kapumzike kaka.Umepata likizo hivyo nenda mahala ukapumzishe akili yako aidha Zanzibar au sehemu nyingine mbali na hapa” “Natamani Mathew Mulumbi angekuwepo hapa.Asingeweza kukubali kuliacha jambo hili likielea hewani” akasema Austin na Gosu Gosu akainuka kwa hasira akagonga meza iliyokuwa na chupa za bia zikaanguka akamfuata Austin akamkunja shati “Usithubutu kuzungumza kuhusu Mathew wakati ni wewe uliyemuacha porini.Usitake kunipandisha hasira.Please go ! akafoka Gosu Gosu.Austin aligundua Gosu Gosu hakuwa akitania tayari sura yake ilikwisha badilika akachukua begi lake na kuondoka kimya kimya MASAA MANNE YALIYOPITA MAKAO MAKUU YA IDARA YA SIRI YA USALAMA WA NDANI WA NCHI Juhudi kubwa zilikuwa zinafanywa na wataalamu wa usalama wa mtandao kudhibiti kirusi hatari kilichopandikizwa katika mfumo wa kompyuta wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Kwa saa mbili sasa juhudi ziliendelea bila mafanikio.Mkuu wa idara hiyo Tamar Axon alikuwepo ofisini kwake kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri.Iligundulika kwamba kirusi kile kiliingia katika mfumo kupitia akaunti ya Samson Mkuza ambaye hakuwa akipatikana hewani.Ilitumwa timu ya watu watatu kwenda kumfuatilia na kujua mahala alipo lakini timu ile ilirudisha majibu kwamba Samson alijipiga risasi ya kichwa baada ya kugundua anataka kukamatwa. “Huyu lazima atakuwa ni Agatha ! Ninaapa kumtafuta kwa namna yoyote ile hadi apatikane.Nilimuamini sana na kumfanya aishi maisha mazuri ya kifahari lakini ndiye aliyekuja kunisaliti.Amenisikitisha sana.Huko aliko muda wake unahes…..” Tamar akatolewa mawazoni baada ya mlio Fulani kusikika katika simu yake ya mkononi.Akaitazama haraka haraka kuna picha zilitumwa katika simu yake akazifungua kuzitazama.Kulikuwa na watu nyumbani kwake “Nani hawa wamevamia nyumbani kwangu?akajiuliza.Alihisi kiubaridi kwa ndani.Alikuza picha zile zilizotumwa katika simu yake kutoka katika kamera ya siri iliyofungwa nyumbani kwake akazitazama vyema “Huyu mmoja ninamfahamu.Ni Austin January.Ni mkuu wa kikosi cha jeshi cha operesheni maalum.Anatafuta nini nyumbani kwangu?akajiuliza akiendelea kushuhudia kupitia simu yake namna akina Austin walivyokuwa wanahangaika nyumbani kwake. “Wanatafuta nini hawa jamaa? Akajiuliza “Agatha ! akasema kwa sauti ndogo iliyojaa hasira “Lazima watakuwa wanafanya kazi na Agatha na ndiye aliyewaelekeza nyumbani kwangu.Stupid ! akawaza na kutafuta namba za Rais akampigia “Hallow Tamar” akasema Dr Fabian Kelelo “Fabian ninakutumia picha Fulani sasa hivi halafu nitakupa maelekezo” akasema Tamar na kumtumia Rais picha zile za Austin na Gosu Gosu wakiwa nyumbani kwake wakihangaika kuingi ndani “Umewatambua hao watu ?akauliza Tamar na Dr Fabian akababaika kujibu “Fabian umewatambua hao watu?akauliza tena Tamar “H..N..Ndiyo.Ninamfaha mu mmoja ni mkuu wa kikosi cha operesheni maalum” akasema Dr Fabian “Good.Nilidhani ungekana humjui.Hawa watu wamevamia nyumbani kwangu na sijui wanachokitafuta hapo ni nini.Nataka waondoke mara moja kabla hayajawakuta mambo makubwa” akasema Tamar na kukata simu “Austin na wenzake wamekwenda kutafuta nini nyumbani kwa Tamar? Kama kuna kitu walitaka kwenda kukichunguza kwa nini hawakunijulisha kabla ya kujiamulia wenyewe kwenda kuvamia nyumbani kwa Tamar? Ni kweli mimi ndiye niliyewatuma kazi lakini walipaswa kunijulisha kama wanakwenda kuvamia nyumbani kwa Tamar.Yule ni mtu mkubwa sana na hawakupaswa kuvamia nyumbani kwake kama mhalifu.Hii sijaipenda” akawaza Dr Fabian na kumpigia simu Austin Austin na Gosu Gosu wakiwa tayari wameingia nyumbani kwa Tamar wakikitafuta chumba cha kulala cha Tamar mara simu ya Austin ikatetema.Akaitoa akatazama mpigaji alikuwa ni Rais “Rais ! Austin akastuka akaiacha simu ile ikiita na kukatika ikaanza kuita tena akaamua kuipoea “Mheshimiwa Rais ! akasema Austin “Austin ninafahamu mahala mlipo na ninaomba muondoke hapo haraka sana! akasema Dr Fabian kwa ukali “Mheshim………..” “Austin sasa hivi nataka muondoke hapo! Akafoka Dr Fabian “Mheshimiwa Rais kuna jambo la msingi sana tunalifuatilia ndiyo maana tuko hapa.Umefaham…” Austin akakatishwa na Dr Fabian “Austin you have three minutes to get out of there.This is an order ! akasema Dr Fabian.Austin alibaki ameduwaa asijue la kufanya “Austin C’mon ! akasema Gosu Gosu baada ya kumuona Austin amesimama “Papaa we have to go ! “What?!! Gosu Gosu akashangaa “Tuondoke” akasema Austin “Austin acha masihara.Tulikuja hapa kufanya upekuzi kutafuta kile kitakachoweza kutusaidia kufahamu nani waliomuua balozi Benjamin.Tutaondoka vipi kabla hatujafanya kazi iliyotuleta?akauliza Gosu Gosu “It’s an order from president” “President? “Ndiyo.Ametutaka tuondoke haraka sana eneo hili.Ametoa dakika tatu” akasema Austin “Rais amejuaje kama tuko hapa? “Sijui amefahamu vipi lakini tayari anafahamu kama tuko hapa na ametutaka tuondoke haraka sana.Hajaonekana kufurahishwa na ujio wetu hapa” akasema Austin kisha akageukana kuanza kuondoka “Austin ! akaita Gosu Gosu lakini Austin hakugeuka akaendelea na harakati zake za kutoka.Nyumba ile likuwa kimya kabisa hakukuwa na mtu yeyote.Gosu Gosu alisimama akimtazama Austin akiondoka hakuwa na la kufanya akapiga ngumi ukuta kwa hasira naye akaondoka.Walitoka nje ya lile jumba la Tamar wakaingia katika gari lao na kuondoka eneo lile. “Austin tafadhali nipe jibu kwa nini Rais ametutaka tuondoke pale wakati tunafuatila jambo la muhimu sana? Amefahamu vipi tuko hapa?akauliza Gosu Gosu “Nilimueleza kuwa tuko pale kwa sababu maalum,kuna jambo tunalifuatilia la muhimu lakini hakunielewa akatutaka tuondoke haraka sana” “Nashindwa kuelewa maamuzi haya ya Rais.Kwanini hukumweleza kama Tamar anadukua mawasiliano yake na anashirikiana na balozi Benjamin?akauliza Gosu Gosu “Tulipanga tumueleze jambo hili baada ya kuzipata zile rekodi hata hivyo hakunipa nafasi ya kumueleza” akasema Austin na ukimya ukapita “Rais ndiye aliyetupa kazi hii tuifanye ninashindwa kuelewa kwa nini basi aamue kuzuia tusifanye uchunguzi wetu? Tamar ni mtu muhimu mno katika suala hili” akasema GosuGosu “Papaa hili jambo linachanganya sana,kwanza ni namna Rais alivyofahamu kuhusu uwepo wetu pale.Nani alimweleza tuko nyumbani kwa Tamar?akauliza Austin “Austin jambo hili haliwezi kuisha hivi hivi lazima tumuulize Rais tujue kwa nini ametuzuia tusiendelee kumchunguza Tamar? Ikiwezekana tumweleze ukweli ili aturuhusu kuitafuta kompyuta hiyo yenye rekodi zinazomuhusu yeye”akasema Gosu Gosu “Papaa sisi sote ni wanajeshi na tunafundishwa kutii amri za viongozi wetu.Rais ni kiongozi wetu na ametoa amri hivyo lazima tuitekeleze bila kuhoji chochote” “Austin hii si operesheni ya jeshi.Tumeyaweka maisha yetu hatarini na kukubali kufanya kazi ya Rais kwa nini yeye mwenyewe aingilie na kutuzia tusiendelee na kazi aliyotupa?akauliza Gosu Gosu na safari ikaendelea kimya kimya. Walifika katika makazi ya Gosu Gosu wakakaa sebuleni. “Austin mpigie Rais.Lazima atueleze kwa nini ametuzuia tusimchunguze Tamar?Wakati anatupa kazi hakutupa masharti kwamba kuna watu ambao hawapaswi kuguswa katika uchunguzi wetu hivyo basi tunahitaji kujua sababu za kutomchunguza Tamar” akasema Gosu Gosu.Austin akafikiri kidogo na kuchukua simu akampigia Dr Fabian.Simu iliita bila kupokelewa “Hapokei simu” akasema Austin “Call him again” akasema Gosu Gosu na Austin akampigia tena simu ikapokelewa “Austin unasemaje?akauliza Dr Fabian “Mheshimiwa Rais tayari tumekwisha sitisha lile zoezi letu kama ulivyoelekeza na kuondoka mahala pale” “Safi.Naomba msiendelee tena na hili zoezi hadi pale nitakapowapa maelekezo zaidi”akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais ! akasema Austin kwa mshangao “Austin kwa sasa operesheni yenu itasimama hadi pale nitakapowaelekeza tena.Waambie vijana wako kila mmoja akaendelee na shughuli zake za kawaida hadi hapo utakapowajulisha tena”akasema Dr Fabian na kukata simu.Austin akaitupa simu sofani kwa hasira “Anasemaje Rais? “Amesitisha tusiendelee na chochote hadi hapo atakapotoa maelekezo mengine” akasema Austin na Gosu Gosu akatoa kicheko “Nashindwa kuelewa kinachoendelea hapa Austin hadi Rais atuzuie tusiendelee na kazi aliyotupa” akasema Gosu Gosu na kuinuka akaenda katika friji akachukua chupa tatu za bia akaziweka katika meza ndogo akakaa na kuanza kunywa “Upo msemo usemao kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi.Pakacha letu limevuja na ninafuu kwetu.Hatujui tumeepushwa na jambo gani huko mbele kama tungeendelea.Yawezekana baada ya balozi Benjamin kuuawa Rais anadhani mambo yamekwisha kumbe mambo ndiyo kwanza yameanza.Austin mimi nimekubali na kutii agizo lake nitakaa pembeni lakini nakuomba usinifuate tena kunieleza eti kuna kazi ya Rais” akasema Gosu Gosu huku akiendelea kukata bia







Toka kulipopambazuka Rais Dr Fabian amekuwa akipokea simu kutoka wa viongozi wa mataifa mbali mbali wakimpa pole kuhusiana na shambulio lile lililotokea katika hoteli ya Zimba na kusababisha vifo vya watu sitini na tatu.Shambulio lile ilikuwa ni habari kubwa katika vyombo mbali mbali vya habari duniani. Wakati akipata kifungua kinywa Dr Fabian alikuwa anapitia magazeti ya hapa nchini ambayo nayo habari kuu ilikuwa ni shambulio lile kubwa “Mauaji makubwa sana haya na ya kikatili.” Akasema Millen mke wa Dr Fabian “Haijawahi kutokea nchini mwetu watu wengi kiasi hiki wakauawa kikatili namna hii.Wauaji hawa lazima wasakwe kila kona na wapatikane! Akasema Dr Fabian kwa ukali “Balozi wa umoja wa Ulaya alikuwemo mle ukumbini na ni mmoja wa watu waliouawa unahisi mauaji yale yanahusiana na hiki kinachoendelea hivi sasa baina ya nchi yetu na nchi za Ulaya?akauliza Millen “Siwezi kuhusisha moja kwa moja tukio hili na hiki kinachoendelea japo naamini umoja wa Ulaya wataamini kwamba mauaji haya ni mpango wa serikali kulipiza kisasi kwa balozi wao kwa kuiandika vibaya Tanzania” akasema Dr Fabian. “Ni kweli lazima watahisi hivyo kwa sababu balozi Benjamin ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba Tanzania si mahala salama kutembelea.Picha itakayojengewa ni kwamba Tanzania wameamua kumuua balozi huyu kufuatia ujumbe ule alioutuma katika akaunti yake ya twitter.Kuna kazi kubwa hapa ya kuwatafuta waliomuua balozi huyu kwani Tanzania inazidi kuchafuka.Watu waliouawa ni wengi sana na hii ina athari kwetu kwani hivi sasa dunia nzima wanaamini Tanzania si mahala salama tena” akasema Millen “Lazima wauaji wapatikane haraka sana kwa namna yoyote ile.Lakini pamoja na tukio hili usiache kuendelea na mpango wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa wake za marais duniani.Kwa namna yoyote ile mkutano huo lazima ufanyike na utatusaidia kuithibitishia dunia kwamba Tanzania ni sehemu salama” akasema Dr Fabian na baada ya kupata kifungua kinywa akaondoka kwenda kuanza majukumu yake ya siku. Dakika chache baada ya kuingia ofisini kwake,akataarifiwa kwamba Rais wa Ufaransa alikuwa katika laini ya simu akitaka kuzungumza naye. “Mambo yameanza.Huyu ndiye aliyekuwa akishirikiana na Benjamin katika kushinikiza uchunguzi ufanyike kuhusiana na kifo cha Laurent Muganza” akawaza Dr Fabian na kuelekea katika chumba cha mawasiliano ya moja kwa moja.Katika runinga alionekana Rais wa Ufaransa. “Mr Michael Weren” akasema Dr Fabian bila kupoteza wakati “Mheshimiwa Rais Dr Fabian.Poleni sana kwa tukio baya la usiku wa jana.Kwa niaba ya nchi yangu na kwa niaba ya ya umoja wa Ulaya ninatoa salamu nyingi za pole kwa madhira haya yaliyotokea” akasema Rais Michael “Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania ninasema ahsante sana” akasema Dr Fabian “Naweza kusema kwamba hili ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Tanzania.Hili ni tukio la ugaidi.Kuna mtu yeyote ambaye amekamatwa hadi sasa kuhusika katika mauaji hayo?akauliza Rais Michael “Mheshimiwa Rais Michael,tayari vyombo vyetu vimekwisha anza kulichunguza jambo hili na tutatoa taarifa nani waliohusika katika mauaji yale” “Mheshimiwa Rais,balozi wa umoja wa Ulaya na mke wake ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo na hili si tukio la kwanza kwa watu wanaohusiana na umoja wa Ulaya kuuawa nchini Tanzania.Siku chache zilizopita aliuawa Laurent Muganza hapo hapo Dar es salaam na jana kauawa balozi wa Umoja wa Ulaya.Sitaki kusema moja kwa moja kwamba yawezekana shambulio hilo la jana lilimlenga balozi Benjamin kwani sina ushahidi wa kutosha lakini ninakuomba kwa mara nyingine tena waruhusu wachunguzi wa umoja wa Ulaya waje wasaidie kuchunguza suala hili.Ninakuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba wachunguzi hao hawatahusika na mambo mengine zaidi ya kusaidia katika uchunguzi” akasema Rais Michael “Mheshimiwa Rais,yalipotokea mauaji ya Lucy na Laurent Muganza uliniomba jambo hilo nikakataa kwani suala lile bado linachunguzwa na vyombo vya ndani.Katika suala hili pia hatutaruhusu wachunguzi wowote kutoka nje ya nchi kwani linashughulikiwa na vyombo vyetu vya ndani lakini pale tutakapohitaji msaada wa kutoka nje hatutasita kuomba.Kwa hiyo ninasema hapana kwa ombi lako” akasema Dr Fabian “Mheshimwia Rais kitendo cha Tanzania kuendelea kukataa kuruhusu wachunguzi wa kutoka nje ya nchi kusaidia katika kuchunguza kuhusu mauaji haya kinatia shaka sana na kuwafanya watu wahisi yawezekana kuna mambo serikali yako haitaki yajulikane ndiyo maana kumekuwa na ugumu mkubwa katika kuruhusu wachunguzi wa kimataifa.Hili ni doa kwa serikali yako na kuliondoa doa hili ni kuruhusu timu ya wachunguzi iweze kuja kusaidia uchunguzi” akasema Rais Michael “Hatuna chochote cha kuficha mheshimiwa Rais baada ya uchunguzi kukamilika kila kitu kitawekwa wazi na kama hakuna lingine mheshimiwa Rais,nina majukumu mengine pia ya kufanya” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais nakuomba ulitafakari suala hilo kwani athari zake zitakuwa ni kubwa kwa nchi yako”akasema Rais Michael “Jibu nililolitoa mheshimiwa Rais halitabadilika.Hakuna mchunguzi wa kimataifa atakayeruhusiwa kuingia nchini.Ahsante kwa kupiga simu mheshimiwa Rais” akasema Dr Fabian na kuzima kamera,akashusha pumzi.Akatoka katika kile chumba na kurejea ofisini kwake akaketi na kuvuta pumzi ndefu wakati akitafakari simu yake ya mkononi ikaita alikuwa ni Tamar. “Habari yako Tamar” “Nzuri kabisa habari yako Fabian? “Nzuri.Unaendeleaje Tamar? “Ninaendelea vizuri.Nimekupigia kukujulisha kwamba tumepata tatizo.Mfumo wetu wote wa kompyuta umeingiliwa na kirusi hatari” akasema Tamar “Mfumo umeingiliwa na kirusi?akashangaa Dr Fabian “Ndiyo Fabian mfumo wetu umeingiliwa na kirusi hatari hivyo kila kitu hapa kimesimama.Nimekesha hapa na wataalamu wakijaribu kutafuta kila njia ya kudhibiti kirusi hicho” “Lini limetokea hilo tatizo?akauliza Dr Fabian “Limeanza jana usiku” “Imewezekanaje mkashambuliwa na kirusi wakati mfumo wenu wa kompyuta hapo una ulinzi wa hali ya juu sana?akauliza Dr Fabian “Kuna mmoja wa mfanyakazi wetu hapa anaitwa Agatha ambaye tuligundua kwamba alikuwa anaiba siri za idara na hatujui alikokuwa anazipeleka.Baada ya kujua tumemgundua alitoweka na mpaka sasa hajapatikana.Tunaamini huyo ndiye aliyepandikiza kirusi hicho katika mfumo wetu kwa kupitia katika akaunti ya mfanyakazi mwingine aliyekuwa na ukaribu naye.Picha za kamera zinaonyesha kwamba kijana huyo aitwaye Samson alimaliza majukumu yake akaondoka lakini baadae akarejea tena na moja kwa moja akaelekea katika chumba cha seva.Tumefuatilia chanzo cha kirusi hicho tukagundua kilianzia katika akaunti yake na kilitumwa kutoka katika kompyuta ambayo mpaka sasa bado hatujaweza kutambua ni ya nani na yuko wapi.Baada ya kugundua hilo tulimfuata Samson ili atueleze chanzo cha kirusi kile lakini alijipiga risasi na kujiua kabla watu wetu hawajamkamata.Tulibahatik a kuipata simu yake na tulipoipekua tumegundua jana usiku aliwasiliana na Austin January na muda waliowasiliana ndio muda huo ambao kirusi kiliingia katika mfumo wetu”akasema Tamar “Austin Janury?! Dr Fabian akashangaa “Ndiyo Fabian.Simu iliyotumika kuwasilina na huyo kijana ni ya Austin January.Hata hivyo aliyekuwa anaitumia simu hiyo kuwasiliana na Samson ni mwanamke ambaye baada ya kuihakiki sauti yake tumegundua ni Agatha ambaye tunamtafuta kwa kuiba siri za idara.Tunaamini Austin na Agatha wanafanya kazi pamoja na Austin anafahamu mahala alipo Agatha.Sifahamu nini hasa wanachokitafuta katika idara yetu au wamepewa taarifa gani na Agatha hadi wakafikia kufanya kitendo hiki walichokifanya.Kama haitoshi walijaribu kuvamia nyumbani kwangu na kwa bahati nzuri nina mfumo wa ulinzi ambao ulinitumia picha za wavamizi hao katika simu yangu ndipo nikawasiliana nawe.Ningeweza kuwafanya chochote kibaya watu wale waliovamia nyumbani kwangu lakini tunamuhitaji Austin.Tunahitaji kufahamu alipo Agatha” akasema Tamar na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “Tamar kuna jambo ambalo nataka ulifahamu.”akasema na kunyamaza kidogo “Austin nilimtuma kazi maalum ya kuwatafuta wauaji wa balozi Benjamin Hudson sasa nashangaa amefikaje fikaje hadi katika idara yako na kuleta uharibifu mkubwa namna hiyo” akasema Dr Fabian na Tamar akatoa kicheko kidogo “Fabian toka lini ukaanza kuwatumiwa wanajeshi katika operesheni kama hizi wakati idara yangu ipo na ndiyo inayoshughulika na masuala hayo? Ukiacha sisi kuna polisi na vyombo vingine kwa nini ukaviacha hivyo vyote na kuamua kumpa jukumu Austin January?Don’t you trust us anymore?Hatufanyi kazi vizuri? Akauliza Tamar “Tamar si hivyo.Kuamua kumtumia Austin hakumaanishi kwamba nimepoteza imani na idara yako au idara nyingine lakini nilikuwa na sababu zangu binafsi kufanya hivyo ,naomba usinielewe vibaya.Mmekuwa mkifanya kazi nzuri siku zote na nina imani kubwa na ninyi” akasema Dr Fabian “Fabian sitaki kufahamu sababu zako za kuamua kumtumia Austin katika kuwatafuta wauaji wa balozi Benjamin lakini ninachokihitaji kwa sasa ni kufahamu mahala alipo Agatha na anayefahamu mahala alipo ni Austin.Ninahitaji kumpata Austin nimuhoji na kufahamu alipo Agatha hivyo naomba msaada wako” akasema Tamar na Dr Fabian akawa kimya “Fabian najua jambo hili limekustua kidogo lakini kumpata Austin ni lazima kwetu ili atuonyeshe mahala alipo Agatha na vile vile tujue ni siri zipi za idara ambazo amekuwa akipewa na Agatha.Fabian hawa watu wawili lazima watakuwa na mpango mkubwa sana wa kuhujumu idara yetu na lazima tuwadhibiti haraka” akasema Tamar.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu alishindwa aseme nini. “Fabian say something ! akasema Tamar “Tamar nashindwa niseme nini kwani Austin ni mtu wangu wa muhimu sana na amekuwa akinisaidia katika shughuli zangu mbali mbali hivyo inaniwia ugumu kusaidia kumteka.Niachie suala hilo nitazungumza naye mimi mwenyewe na kumuhoji alipo Agatha halafu nitakujulisha” akasema Dr Fabian “Fabian you don’t understand.Huyu mtu amekuwa anashirikiana na Agatha mfanyakazi wetu humu kuiba siri za idara na sielewi kwa madhumuni yapi.Huyu mtu ni hatari lazima kuna mahala anazipeleka siri hizo ambazo nyingi zinahusiana na usalama wa nchi hivyo hata ukizungumza naye hatakueleza chochote.Tusaidie sisi tumpate tutamfungua kwa mateso” akasema Tamar.Picha ya Austin ikazunguka katika kichwa cha Dr Fabian halafu akasema “Tamar hapana,siwezi kuruhusu Austin akafanyiwa chochote kabla sijamuhoji kujua kwa nini alifanya hivyo alivyofanya na kwa nini anashirikiana na Agatha” akasema Dr Fabian “Fabian unanifanya niamini kwamba yawezekana wewe ndiye uliyemtuma Austin afanye haya aliyoyafanya” akasema Tamar “Mimi nilimpa kazi nyingine kabisa ambayo haihusiani na idara yako.Kama kuna taarifa yoyote ninaitaka katika idaya yako ningeweza kuagiza niletewe hivyo basi siwezi kumtuma mtu aibe siri za idara”akasema Dr Fabian “Kama hukumtuma alikuwa anatafuta nini nyumbani kwangu? You sent him to spy on me? Tamar akauliza “I didn’t send him to spy on you.Kwa nini nifanye hivyo?akauliza Dr Fabian “Kama hukumtuma kwa nini unamkingia kifua?Nina uhakika mkubwa huyu jamaa kuna kitu anakifanya katika idara yetu,nina uhakika mkubwa ananichunguza kwa nini hutaki nijue kinachoendelea?akauliza Tamar “Tamar nina mambo mengi ya kufanya leo hivyo naomba tulimalize hili suala.Sitaki Austin aguswe.Nitazungumza naye mimi mwenyewe na atanieleza kile anachokitafuta katika idara yako” akasema Dr Fabian “Fabian sasa unanifanya niamini kwamba unamtumia Austin kunichunguza.Umeniudhi sana na sasa naomba unisikilize vyema.Utake usitake nitamchukua Austin nimuhoji nifahamu kile anachokitafuta katika idara yetu,nijue sababu ya kwenda kuvamia nyumbani kwangu na vile vile nijue mahala alipo Agatha.Please don’t try to stop me” akasema Tamar.Kauli ile ya Tamar ilionyesha kumchukiza sana Dr Fabian “Tamar nakuonya usinijaribu ! Mimi si mtu wa kujaribu.Mimi ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzan……” akasema Dr Fabian na simu ikakatwa “Huyu mwanamke mshenzi sana anataka kunipanda kichwani na kunitawala.Nimempa cheo kikubwa na sasa anataka kukitumia vibaya.Nitamuondoa haraka sana asifanye mchezo na mimi.Akithubutu kumgusa Austin nitammaliza” akawaza Dr Fabian na mara ukasikika mlio wa ujumbe mfupi wa simu.Akaufungua ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Tamar.Ilikuwa ni video fupi.Dr Fabian alipoitazama video ile akahisi jasho likimtoka usoni na muda huo huo simu yake ikaita akaipokea “Tamar what’s the meaning of this?akauliza Dr Fabian kwa ukali “Nimekutumia kukukumbusha tu kwamba wewe ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania lakini mimi nina nguvu zaidi yako ninaweza kukuondoa katika nafasi yako uliyo nayo hivyo unapaswa kuniheshimu sana na kunisikiliza kila ninachokitaka.Tusifike huko.I need Austin” akasema Tamar.Dr Fabian alihisi joto akalegeza tai na kushusha pumzi “Mnataka nifanye nini?akauliza “Mpigie simu mwambie saa mbili usiku leo aende Dino’s hotel ambako kuna mtu utamtuma ampelekee taarifa Fulani ya siri.Akishafika pale sisi tutajua namna tutakavyomchukua”akasema Tamar “Sawa nitafanya hivyo” akasema Dr Fabian “Thank you Mr President.I’m reminding you don’t try to warn him or let him escape” akasema Tamar “Tamar this will be the last warning to you stop blackmailing me !.Please destroy this video.Sintakuonya tena kuhusu jambo hili ! akafoka Dr Fabian na simu ikakatwa Dr Fabian alihisi kuchanganyikiwa akaendelea kuzunguka mle ofisini akitoka pembe moja hadi nyingine “Nilifanya makosa makubwa sana kumuweka Tamar katika ile nafasi na tayari amekwisha nibana kwenye kona kwa kuwa anajua anayo ile video ! akawaza Dr Fabian na kugonganisha mikono kwa hasira “Austin ni mtu muhimu sana kwangu kwa wakati huu.Ni yeye ndie aliyefanikisha mauaji ya Lucy Muganza na ni mtu ambaye nimechagua kumuamini na kumtumia katika operesheni mbali mbali za siri.Kwa nini nimtoe kafara mtu muhimu kama huyu?Kuna nini kinaendelea hapa hadi akavamia nyumbani kwa Tamar?Kuna swsali la kujiuliza pia nini kilimpelekea Austin kwenda nyumbani kwa Tamar? Ni kweli anashirikiana na mmoja wa wananyakazi wa SNSA kuiba siri za idara?Kama ni kweli kwa madhumuni gani? Nilifanya makosa makubwa kukubali agizo la Tamar la kuwaondoa Austin na wenzake nyumbani kwa Tamar walikokuwa wamevamia bila kumuhoji na kujua kinachoendelea” akawaza Dr Fabian na kuegemea meza. “Naanza kuamini yawezekana ni kweli Austin anashirikiana na huyo Agatha mfanyakazi wa SNSA kuiba siri za idara na kuna taarifa walikwenda kuitafuta pale nyumbani kwa Tamar.Kwa nini lakini Austin afanye hivi? Kama kuna taarifa anaihitaji kutoka SNSA angenieleza ili nimsaidie kuipata kuliko kushirkiana na mmoja wa wafanyakazi kuiba siri kitu ambacho ni kibaya sana.Ninaanza kuwa na wasi wasi yawezekana hata mauaji yale ya jana Austin anahusika kwa sababu ni yeye niliyempa jukumu la kumfuatilia balozi Benjamin na kuna uwezekano walisuka mpango wa kumuua balozi Benjamin kimya kimya” akawaza Dr Fabian “Naanza kuiona pointi ya msingi ya Tamar.Kuna mambo mengi ambayo hatuyajui kuhusu Austin na anapaswa kuhojiwa aeleze kila kitu.Mambo kama haya ndiyo yanayonifanya niwe muoga wa kuwaamini watu.Kila unayemuamini anakuwa na kasoro zake.Tayari nilikwisha anza kumuamini Austin lakini kwa kitendo cha kuanza kuiba siri za idara nyeti ya usalama wa ndani wa nchi inaonyesha wazi hapaswi kuaminiwa” akaendelea kuwaza Dr Fabian na kuishika simu yake mara akaikumbuka ile video aliyotumiwa na Tamar.Akaifuta haraka haraka na kushusha pumzi akaegemea kiti “Mpaka lini Tamar ataendelea kunilazimisha nifanye kila akitakacho kwa sababu ya video hii?Hapo mwanzo nilichukulia rahisi lakini kwa sasa naona hili jambo linaanza kuwa kubwa na ameanza kuvuka mipaka yake.Anataka anitawale na nimtimizie kila anachokihitaji hata ambacho hakiwezekani.Natakiwa haraka sana kutafuta namna ya kuweza kumdhibiti kwani bila kufanya hivyo ataniletea matatizo makubwa sana huko tuendako kwani anaweza akanitaka hata niachie ngazi.Ningeweza kumuondoa but …oh my God I can’t ! akawaza Dr Fabian na baada ya muda akachukua simu na kumpigia Austin “Mheshimiwa Rais” akasema Austin baada ya kuipokea simu “Austin nina shughuli nyingi sana leo sintaweza kuonana nawe ila kuna jambo la muhimu ambalo nilitaka nikuonyeshe lakini nitamtuma mtu wangu.Fika Dino’s hotel saa mbili za usiku utakutana naye na atakupa hizo nyaraka.Ukishazipitia utanipa mrejesho” “Sawa mheshimiwa Rais” “Ahsante Austin” “Mhesh…….” Austin akataka kusema kitu lakini tayari simu ilikwisha katwa. “I have no choice Austin.I’m so sorry” akasema Dr Fabian baadaya kukata simu







“Gosu Gosu” Sauti laini ya mwanamke ilimstua Gosu Gos kutoka katika usingizi mzito.Alifumbua macho na kujikuta akiwa amelala sofani.Mezani kulikuwa na chupa kadhaa za bia.Akafikicha macho na kuinuka akakaa “Agatha” akasema “Mlirudi saa ngapi kutoka kwa Tamar?akauliza Agatha “Ahsante kwa kuniamsha.Ninahisi kichwa kizito sana.I need to take a bath” akasema Gosu Gosu na kuchukua bastora yake akaelekea chumbani kwake akajimwagia maji baridi “Nimelala usingizi mzito sana halafu mbaya zaidi niliweka bastora mezani.Hii ni hatari,angeweza kuingia mtu mbaya na kunimaliza” akawaza Gosu Gosu “Lakini usingizi huu umesababishwa na bia nilizokunywa jana.Si kawaida yangu kulala namna hii” akaendelea kuwaza “Sitaki kushiriki tena kazi yoyote ile atakayoniomba Austin.Jana Rais ametufanyia kitu kibaya sana na mpaka sasa bado sifahamu kwa nini alifanya vile.Kwa nini hakutuacha tukaendelea na zoezi letu na badala yake akaamuru tuondoke haraka nyumbani kwa Tamar tulikofuata jambo muhimu tena kwa faida yake yeye mwenyewe? Anyway, I’m done.Sitaki tena kushiriki katika operesheni yoyote ya serikali.Toka wakati wa Mathew mambo kama haya yalikuwa yanatokea.Viongozi ndani ya serikali hawaeleweki na hawaaminiki.Ninaweka nukta katika mambo haya na ninataka kujikita zaidi katika kusimamia biashara za Mathew” akawaza Gosu Gosu na kuitazama picha kubwa ya Mathew ukutani “What happened to you Mathew Mulumbi? Are you real dead ?If not where are you brother?akajiuliza Gosu Gosu na mlango wake ukagongwa akaufungua alikuwa ni mtumishi wake wa ndani aliyemjulisha kwamba kifungua kinywa tayari.Kabla ya kwenda katika chumba cha chakula Gosu Gosu akaenda katika chumba cha wageni walimolala akina Agatha.Mlango ukafunguliwa akatoka Agatha “Gosu Gosu” akasema Agatha “Watoto wanaendeleaje?akauliza “Bado wako katika mstuko.Bado wanaogopa” akajibu Agatha “Ni kweli lilikuwa tukio baya.Itachukua muda tukio lile kuwatoka vichwani mwao” akasema Gosu Gosu “It’s breakfast time” akasema Gosu Gosu “Sina hakika kama watakubali kutoka humu chumbani.Bado wanaogopa sana” “It’s okay.Mtumishi atawaandalia kifungua kinywa humo humo chumbani” akasema Gosu Gosu na kuelekea katika chumba cha chakula kupata kifungua kinywa. “Lazima nitafute namna ya kuwasaidia Agatha na familia yake waweze kuwa salama.Nina uhakika mkubwa lazima Tamar na idara yake wataelekeza nguvu zao nyingi kumsaka na kuhakikisha anapatikana” akawaza akiwa mezani.Alipomaliza akaenda tena katika chumba cha Agatha akagonga mlango na kumtaka Agatha wazungumze wakaelekea katika bwawa kubwa la kuogelea “Usiwe na hofu Agatha hapa uko sehemu salama na nitahakikisha wewe na familia yako mnakuwa salama,naomba uniamini” “Ahsante nashukuru” “Kwa sasa mtaendelea kukaa hapa kwangu hadi pale tutakapopata sehemu salama zaidi mtakapoishi kwa amani bila bughudha.Kitu chochote mtakachokihitaji usisite kunijulisha” “Nakushukuru sana Gosu Gosu kwanza kwa kutuokoa jana na pili kwa kuhakikisha tunaendelea kuwa salama.Bila wewe hivi sasa mimi na familia yangu tungekwisha uawa.Nashukuru vile vile kwa huduma nzuri tunazopatiwa hapa.Ukiacha mstuko ambao bado watoto wanao lakini tunajihisi tuko nyumbani”akasema Agatha huku akitabasamu “Msiwe na hofu jisikieni nyumbani.Jumba hili ni kubwa na mko huru kuzunguka sehemu mbali mbali.Kuna bustani nzuri na sehemu za michezo ya watoto.Unaweza ukawatoa ndani ukawaleta hapa kuja kupumzika” akasema Gosu Gosu “Hujanieleza kuhusu jana.Mlifanikiwa kupata chochote nyumbani kwa Tamar?akauliza Agatha. “It was complicated” “Complicated? How?akauliza Agatha “Tulifanikiwa kuingia nyumbani kwa Tamar na wakati tukielekea katika chumba chake cha kulala Austin akapigiwa simu na Rais akamtaka tuondoke haraka sana mahala pale” “Rais? Akauliza Agatha “Ndiyo.Rais alipiga simu na kututaka tuachane na zoezi lile na tuondoke haraka sana mahala pale” “Kwa nini akafanya vile? Si yeye aliyewapa kazi hii kwa nini basi awazuie msitekeleze kazi aliyowapa?akauliza Agatha akionyesha mshangao mkubwa “Hilo ndilo swali ambalo hata sisi tumekuwa tunajiuliza.Imetokea nini hadi Rais akafanya maamuzi kama haya?Tulikwenda pale kwa nia ya kumsaidia yeye mwenyewe ili rekodi za mawasiliano yake zisiwafikie wabaya wake lakini dah ! Gosu Gosu akashindwa kuendelea akainamisha kichwa “Alifahamuje kama mko pale?akauliza Agatha “Agatha sisi hatufahamu chochote.Anyway naomba tuachane na suala hilo kwani hata sisi tumeamua kuachana nalo.Kwa vile aliyetupa kazi ambaye ni Rais ameamua kutuingilia katika kazi aliyotupa hatuna haja ya kuendelea na hili jambo.Kipaumbele changu kwa sasa ni kuhakikisha wewe na familia yako mnakuwa salama” akasema Gosu Gosu na ukmya ukatanda mahala pale.Baada ya kama dakika tano hivi Agatha akasema “Gosu Gosu hampaswi kuliacha jambo hili hewani.Rais yuko katika hatari kubwa.Zile rekodi kama zikitoka katika kompyuta ya Tamar basi Rais atakuwa katika hatari kubwa.Je mlijaribu kumweleza jambo hilo na hatari inayomkabili?akauliza Agatha “Hapana hatujamweleza bado.Tulitaka tuipate kwanza kompyuta ya Tamar tuhakikishe tunazo rekodi ndipo tumueleze Rais kilichokuwa kinaendelea” “That’s a mistake.Rais anapaswa kuambiwa nini kinaendelea.Yawezekana hajui kuna bomu linalokaribia kumlipukia” akasema Agatha “Agatha tuachane na hayo mambo.Wanasiasa wa aina yake ambao ni vigeu geu dawa yao ni kuwaacha wafe na misalaba yao.Hakuna haja ya kupoteza muda na kuhatarisha maisha kumsaidia mtu ambaye haoni thamani ya msaada wetu.Let him be.Hilo bomu likimlipukia atajua mwenyewe” akasema Gosu Gosu. Ukimya ukapita tena halafu Agatha akasema “Gosu Gosu nafahamu umeshafanya mengi kwangu lakini kuna msaada nina uhitaji” “Sema unahitaji nini Agatha? “Nahitaji kuzungumza na Samson” “I’m sorry Agatha hutakiwi kuzungumza na mtu yeyote kwa sasa.Watu wako wanaweza wakafuatilia simu na kujua mahala ulipo” “Nalifahamu hilo ndiyo maana nataka tukawasiliane naye mbali kidogo na hapa ili hata kama wakinifuatilia wasigundue kwamba niko hapa.Nakuomba sana Gosu Gosu nisaidie kwa hilo” akasema Agatha “Sauti yako ina ushawishi mkubwa na hakuna anayeweza kusema hapana.Jiandae twende ukawasiliane na huyo mtu wako” akasema Gosu Gosu na Agatha akainuka kuelekea chumbani kwake kujiandaa.Gosu Gosu akabaki kwenye kiti akimtazama “Mtoto ameumbwa kiafrika haswaa.Sura yake nzuri ya upole,sauti yake tamu laini,macho yake malegevu dah naona taratibu anaanza kuingia katika ubongo wangu” akawaza Gosu Gosu huku akitabasamu naye akainuka na kuelekea chumbani kwake kuchukua bastora Agatha alivaa suruali ya jeans rangi ya bluu na shati jeusi kichwani akavaa kofia na miwani mikubwa myeusi ili isiwe rahisi kutambulika.Wakaingia garini na kuondoka “Do you mind if I ask?akauliza Gosu Gosu “Uliza chochote Gosu Gosu” “Mumeo yuko wapi?akauliza “Alikwisha fariki kwa ajali.Alifariki wakati mwanangu akiwa na mwaka mmoja” “Pole sana.Nini kilifuata baada ya hapo? “Una maanisha nini?Agatha akauliza “Uliolewa tena au bado uko peke yako? “Sikutaka kuolewa tena kwani uwezo wa kumtunza mwanangu ninao hivyo sikuona sababu ya kutafuta mwanaume mwingine”akasema Agatha na Gosu Gosu akatoa kicheko “Nini kimekufurahisha?akauliza Agatha “Wanawake mnanifurahisha sana.Hukutaka kuolewa kwa vile uwezo wa kumsomesha mwanao unao.Lakini kama usingekuwa nao ungeolewa?Why you always thinking of ..” akanyamaza “Say it” akasema Agatha “Tuachane na hilo jambo”akasema GosuGosu “Sema tu we always thinking of money? “I didn’t mean that.But isn’t it true? akasema Gosu Gosu “Umewaza nini hadi ukauliza hivyo? Agatha akauliza “Zama hivi fedha na mali vimepewa kipambele sana katika mahusiano kuliko upendo alio nao mtu na hii iko sana kwa upande wa wanawake.Wengi wanamkubali mtu kutokana na uwezo wake wa kifedha bila kujali kama mtu huyo ana mapenzi ya kweli kwake au hapana.Ninazungumza kitu ambacho nina uzoefu nacho.Hapo kabla sikuwa hivi nilivyo,sikuwa na fedha wala mali,I was no body.Ilikuwa kazi ngumu sana kumtongoza mwanamke akanikubali kutokana na hali yangu ya wakati huo lakini kwa sasa baada ya kuwa mtu ninauona usumbufu mwingi sana kutoka kwa wanawake.They call me handsome,baby na majina yote ya kimahaba.Wengine kwa sura hii hii wananiambia eti nimefanana na P didy.Nyie wanawake Mungu anawaona” akasema Gosu Gosu na wote wakaangua kicheko “Mkeo yuko wapi?akauliza Agatha “Sina mke” “Kwa nini mtu mwenye mafanikio makubwa kama haya usiwe na mke mpaka leo?Utaruka ruka hadi lini? Au unasubiri ufungue shirika la ndege ndipo uamue kuwa na familia?akauliza Agatha “Ngoja nikueleze ukweli Agatha mali hizi unazoziona,jumba lile kubwa,magari si vyangu.Mimi ni msimamizi tu.Mali hii ina mwenyewe hivyo usione kama nimefanikiwa” akasema Gosu Gosu na sura ya Agatha ikaonyesha mshangao kidogo “Nimeona nikwambie ukweli mapema ujue kwani wanaume wengi hawapendi kusema ukweli.Sipendi kumdanganya malaika kama wewe kwamba mali hizi ni zangu.Mimi ni msimamizi tu yupo mwenyewe” akasema Gosu Gosu na Agatha akacheka “Nimekuwa malaika tena” “Hujioni katika kioo ulivyo Agatha?Mungu amekupendelea na kukupa ile sura ya kimalaika.Wanawake wachache sana waliojaliwa uzuri wa aina yako” akasema GosuGosu na Agatha akatabasamu “Una maneno mengi sana Gosu Gosu.By the way what’s your real name?akauliza Agatha “Jina langu mimi ni hilo hilo Gosu Gosu sina jina lingine” “Una lafudhi ya kikongo.Umewahi kuishi kule? “Ndiyo mimi asili yangu ni jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini kwa sasa ni mtanzania.Ninafurahi sana kuwa mtanzania” akasema Gosu Gosu Walifika kati kati ya jiji Gosu Gosu akaegesha gari katika mgahawa Fulani wakashuka na kuingia ndani wakaagiza supu.Agatha akaiwasha simu yake na kumpigia Samson. Katika idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi,simu ya Samson ilikuwa imewekwa katika kifaa maalum na mara tu ilipoita jina la Agatha likaonekana.Lucas ambaye alikuwa amekabidhiwa jukumu la kuifuatilia simu ile haraka haraka akainua simu na kumpigia Tamar akamjulisha kwamba Agatha anapiga.Haraka haraka Tamar akatoka ofisini kwake na kumfuata Lucas katika meza yake. “Umefuatilia kujua anapiga kutokea wapi?akauliza Tamar.Lucas akabonyeza kompyuta yake kisha ramani ikatokea katika runinga kubwa. “Yuko mtaa wa Ali Mzawa” “Good job.Alex chukua kikosi cha watu watano mumfuate Agatha haraka sana.Yuko mtaa wa Ali Mzawa tutakuwa tunawapa maelekezo kila mahala atakakoenda” akasema Tamar “Nitakupata Agatha.Hutaweza kunikimbia.Huna sehemu ya kujificha kahaba wewe nchi hii yote ninaiona katika kiganja changu! Nitakapokutia mikononi nitakuonyesha raha ya usaliti” akawaza Tamar na kurejea ofisini kwake Agatha alipiga simu mara ya kwanza lakini haikupokelewa,akapiga mara ya pili lakini haikupokelewa. “Something is not right.Samson huwa ana kifaa cha kupokelea simu sikioni na haijawahi kutokea hata mara moja nikapiga simu mara mbili bila kupokelewa”akasema Agatha na kunyamaza kidogo wakatazamana “He must be in trouble” akasema Akasema Agatha na kuizima simu yake akachomoa betri. “Twende tuondoke hapa haraka sana.Lazima watakuwa wanaifuatilia simu yangu na watajua niko hapa” akasema Agatha GosuGosu akamrushia muhudumu noti mbili za elfu kumi kumi kulipia supu ile ambayo ilikwisha letwa mezani wakaondoka “Tunaelekea wapi? Akauliza Gosu Gosu “Nataka twende nyumbani kwake tukajue kama ana tatizo lolote.Nina wasi wasi yawezekana wakawa wamegundua kwamba kirusi kile nilichokipandikiza katika mfumo wao kilipitia katika akaunti yake.Kama wakiligundua hilo nitakuwa nimemuweka katika wakati mgumu sana” akasema Agatha na kumuelekeza GosuGosu anakoishi Samson Iliwachukua zaidi ya dakika hamsini kuwasili katika mtaa anakoishi Samson.Mara tu walipokaribia katika nyumba ya Samson walikutana na umati mkubwa wa watu na magari ya polisi. “Nini kimetokea pale?Ni karibu sana na nyumbani kwa Samson” akasema Agatha kwa woga.Gosu Gosu akaegesha gari pembeni “Stay in the car.Ninakwenda kuangalia nini kimetokea”akasema Gosu Gosu na kushuka garini akaenda kuungana na umati ule mkubwa wa watu “Kuna nini hapa” akamuuliza kijana mmoja aliyekuwa karibu yake “Kuna kijana mmoja amejipiga risasi asubuhi ya leo” “Unamfahamu kijana huyo? “Ndiyo ninamfahamu kwa sura lakini nimesikia watu wanaomfahamu vyema wanamuita Samson” “Wanadai nini sababu ya kujipiga risasi?akauliza GosuGosu “Hakuna anayefahamu hadi sasa chanzo cha kujipiga risasi lakini wengine wanadai ni sababu za kimapenzi ila hakuna mwenye uhakika” akajibu Yule kijana.Gosu Gosu hakutaka kuendelea kupoteza muda akarejea garini “He’s dead.Samson is dead.Amejiua kwa kujipiga risasi leo asubuhi” akasema Gosu Gosu.Agatha akainama na kuangua kilio.Gosu Gosu akawasha gari wakaondoka “Agatha usilie tafadhali huu ni wakati wa kuwa imara sana.Mambo ndiyo kwanza yameanza” akasema Gosu Gosu “Samson asingeweza kujiua na hakuwa na sababu ya kujiua lazima watakuwa wamegundua kile nilichokifanya kupita akaunti yake na ili kujiepusha na matatizo akaamua kujiua.Moyo unaniuma sana ni mimi ambaye nimesababisha kifo chake”akasema Agatha akiendelea kulia “Agatha usijilaumu tafadhali kwa kile ulichokifanya” “I did that to protect President but…….” Agatha akanyamaza na kufuta machozi “Inauma kwani juhudi zote hizi za kumsaidia Rais lakini yeye ndiye amekuwa mstari wa mbele kuturudisha nyuma.Gosu Gosu please help me to get out of the country.Kama nikiendelea kukaa hapa Tanzania mimi na familia yangu tutauawa.Hakuna mahala ndani ya Tanzania ambako tunaweza kujificha na kuamini tuko salama” akasema Agatha “Agatha usihofu.Nitakulinda na utakuwa salama” “Gosu Gosu you don’t know these people they’re powerfull.Wana uwezo wa kufika kokote kule” akasema Agatha “Naomba uniamini tafadhali.Nitakulinda kama nilivyokuahidi” akasema Gosu Gosu na mara ukaingia ujumbe katika simu yake.Mwendo wa gari ulikuwa wa taratibu sana kutokana na foleni.Akaufungua ujumbe ujumbe ule akausoma “Tukutane sasa hivi Msanzi hotel.Kuna jambo la muhimu sana.Austin” Ndivyo ulivyosomeka ujumbe ule “Austin kwa nini ameamua kutumia namba nyingine kunitumia ujumbe?Kwa nini hajatumia namba yake ya kawaida?akajiuliza Gosu Gosu na kuamua kumpigia kupitia namba ile aliyotumiwa ujumbe. “Hallow”akasema Gosu Gosu “Papaa najua umeshangaa lakini hiyo ni namba yangu nyingine ambayo huwa ninaitumia kwa dharura.Naomba tafadhali tukutane mahala nilipokuelekeza”akasema Austin “Kuna nini Austin?akauliza Gosu Gosu “Nitakueleza utakapofika Papaa lakini ni jambo la muhimu sana” akasema Austin “Sawa ninampeleka Agatha nyumbani halafu nitakuja hapo”akajibu Gosu Gosu







Gosu Gosu aliwasili Msanzi Pub ambako Austin alikuwa anamsubiri “Karibu Papaa ahsante sana kwa kufika” akasema Austin muhudumu akafika kwa haraka Gosu Gosu akaagiza bia. “Nimeshangaa sana kwa nini hukutumia ile namba yako ya kawaida niliyoizoea?akauliza Gosu Gosu “Gosu Gosu kuna kitu nimekuitia hapa.Najua umekwisha kata tamaa kabisa na hutaki kusikia chochote kutoka kwangu lakini lazima nikushirikishe jambo hili” “Usijali Austin.Kuna nini? “Tulipoachana asubuhi nilikwenda nyumbani kambini kupumzika.Nikiwa napumzika natafakari kile kilichotokea jana usiku Rais akanipigia simu” akasema Austin na kunyamaza baada ya kuona sura ya Gosu Gosu imebadilika “Usikasirike Papaa najua hutaki kusikia chochote kuhusu Rais”akasema Austin. “Austin umenichafua kabisa kusikia kuwa Rais alikupigia simu.Naomba nikuweke wazi kabisa kama kuna kazi amekupa mimi usinihusishe! Akasema Gosu Gosu “tafadhali nisikilize kwanza Papaa”akasema Austin “Rais aliniambia kwamba kuna nyaraka muhimu atamtuma mtu aniletee jioni ya leo hivyo natakiwa kwenda Dino’s hotel kukutana na huyo mtu na nikisha zipitia nyaraka hizo nitakazoletewa nimjulishe” akasema Austin.Gosu Gosu akainuia chupa ya bia akanywa funda kubwa “Tatizo liko wapi Austin?Kama anataka kukupa nyaraka nenda kazichukue uzifanyie kazi”akasema Gosu Gosu “Hapo ndipo kuna tatizo Papaa.Huoni kama jambo hili lina ukakasi? “Ukakasi kivipi Austin? “Kwanza kabisa Rais Dr Fabian ni msiri sana na hapendi mambo yake ya siri yajulikane.Alinihakikishia kwamba mpaka sasa hana mtu anayemuamini kumshirikisha katika mambo yake ya siri na ndiyo maana rais aliyepita Dr Evans akamuelekeza kwangu kwamba anaweza akaniamini na nikafanya naye kazi za siri.Kitendo cha kutaka kumtuma mtu kwangu kuniletea nyaraka za siri tena hotelini kinanishangaza kidogo kwa sababu hana utaratibu huo.Kama kuna jambo lolote la siri anataka kunieleza huwa ananiita ikulu tunazungumza ana kwa ana lakini leo hii anataka kumtuma mtu kwangu kuniletea taarifa ya siri.Hainiingii akilini Papaa.Tukiliweka hilo pembeni turejee katika suala la usiku wa jana.Rais alifahamuje kama tumekwenda nyumbani kwa Tamar?Baada ya kufahamu kwa nini hakutuacha tuendelee na kile kilichotupeleka pale na badala yake akatutaka tuondoke?Kama haitoshi akapiga tena simu na kututaka tuachane na uchunguzi tuliokuwa tunaufanya hadi hapo atakapotueleza.Ukilitazama vizuri jambo hili utagundua kwamba kuna mawasiliano kati ya Rais na SNSA na unapozungumzia SNSA unamzungumzia Tamar.Ninaamini Rais alipata taarifa zetu jana kutoka kwa Tamar.Ninahisi pale nyumbani kwa Tamar kuna kamera za siri ambazo zimeunganishwa na mtambo maalum ambao humjulisha Tamar kama kuna mtu ameingia nyumbani kwake wakati hayupo.Baada ya kupewa taarifa hizo ndipo akamjulisha Rais” akasema Austin.Ukimya ukapita kila mmoja akipiga mafunda kadhaa ya kinywaji halafu Austin akaendelea “Kama ni hivyo linaibuka swali.Baada ya kujua tumevamia kwake Tamar angeweza kupiga simu polisi akawajulisha kwamba kuna watu wamevamia nyumbani kwake,angeweza kutuma vijana wake mahiri kutoka SNSA wakatufuata pale na kutuweka chini ya ulinzi au angeweza kutufanya chochote lakini alimjulisha moja kwa moja Rais ambaye naye alitutaka tuondoke pale haraka sana na akatutaka tusiendelee tena na uchunguzi wowote.Kwa nini Tamar alimjulisha Rais kuhusu sisi kuvamia nyumbani kwake? Kabla hatujapata jibu turejee katika lile suala letu la kwanza.Rais ananitaka nikaonane na mtu atakayemtuma jioni ya leo hotelini hudhani kama huo ni mtego nimetegewa?akauliza Austin.Gosu Gosu akatikisa kichwa “Austin umenifumbua macho na kuna kitu ninakiona katika hayo uliyonieleza.Kweli hapa kunaonekana kuna jambo halijakaa vyema.Nakubaliana nawe kwamba yawezekana huu ukawa ni mtego.Kuna kitu nimekumbuka.Jana usiku tukiwa nyumbani ulimpa simu yako Agatha kuwasiliana na Samson ambaye alimsaidia katika kuingiza kirusi kwenye mfumo wa kompyuta wa SNSA.Kabla ya kuja hapa Agatha aliniomba nimpeleke mahala akawasiliane na Samson,alimpigia simu lakini simu yake haikupokelewa.Tukaenda nyumbani kwake na kukuta amejipiga risasi.Yawezekana SNSA walikuta namba yako ya simu katika simu ya Samson na wanaamini kwamba lazima utakuwa unafahamu mahala alipo Agatha ambaye anafahamu siri nyingi za SNSA hivyo wanataka kutengeneza mtego wakukamate kwa lengo la kufahamu alipo Agatha” akasema Gosu Gosu “Kama ni hivyo kwa nini basi wamtumie Rais? Akauliza Austin “SNSA iko chini ya Rais.Malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hii ya siri ni kumsaidia Rais katika kutawala hivyo kila wanachokifanya lazima Rais ajue hivyo watakuwa wamemtumia yeye ambaye ni mtu wa karibu kwako ili kukupeleka katika mtego” akasema Gosu Gosu “Lakini idara hiyo hiyo ambayo iko chini ya Rais ndiyo inayotumiwa kutaka kumuhujumu Rais.Kwa nini anashindwa kuliona hilo? Akauliza Austin na baada ya tafakari Gosu Gosu akasema “Austin kuna kitu kinaendelea hapa ambacho hatukifahamu.Rais amebadilika ghafla sana na kuleta wasiwasi mkubwa” akasema Gosu Gosu “NIkweli mabadiliko ya Rais yanashangaza na anatulazimisha tuhisi kuna jambo linaloendelea” akasema Austin “What’s the plan?akauliza Gosu Gosu “Papaa naomba nikuweke wazi kwamba mimi sina mke,sina mtoto sina familia.Sina kitu chochote cha kupoteza hivyo basi nimeamua kuondoka zangu.Siwezi kushindana na Rais yeye ana mtandao mrefu.Nimefikiria sana na hayo ndiyo maamuzi yangu”akasema Austin.Gopsu Gosu akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema “Are you sure Austin that you want to run away? “I’m sure.I’m done here”akasema Austin na kuchukua chupa yake akanywa funda kadhaa za bia. “Austin siwezi kupingana na maamuzi yako ya kutaka kuondoka kuepukana na matatizo lakini naomba nikukumbushe kitu kimoja kwamba kukimbia si suluhisho la hili jambo.Hata ukikimbia hawa watu wana mashirikiano na nchi mbali mbali hivyo unaweza ukakamatwa au ukamalizwa kimya kimya”akasema Gosu Gosu na kunyamaza “Nini ushauri wako? Austin akauliza “Sikushauri ukimbie.Nashauri tulikabili hili jambo hadi mwisho wake.Tuchimbe zaidi na kuufahamu ukweli wa mabadiliko haya ya ghafla ya Rais” akasema Gosu Gosu “Papaa unaposema tukabiliane na hili suala unamaanisha kwamba tupambane na SNSA na Rais?Hatuna uwezo wa kupambana na hawa watu.SNSA wana uwezo wa kumpata mtu yeyote wanayemtaka hapa nchini hivyo sidhani kama tunaweza kup……..” “Austin remember we’re soldiers.Hatuogopi chochote na kazi yetu sisi ni kupambana.Mimi nitakuunga mkono katika mapambano haya ili tuweze kujua kile kinachoendelea nyuma ya pazia” akasema Gosu Gosu kisha wakaendelea na majadiliano mengine RAMALLAH – PALESTINA Soko kubwa la samaki liliendelea kujaa watu.Ndani ya gari moja lililokuwa pembeni kidogo ya lile soko Habib, msaidizi wa Ammar Nazari alikuwa na watu wengine watatu wakiwa wameyaelekeza macho yao katika kompyuta.Walikuwa wanamuangalia Mathew Mulumbi aliyekuwa ndani ya gari ambalo kuliwekwa kamera za siri zilizounganishwa na kompyuta ile waliyokuwa wakiitazama. Mathew alifumba macho baada ya muda kufika halafu akabonyeza kitufe alichoelekezwa na Habib lakini hakukutokea mlipuko.Habib na wenzake wakatazamana na kutabasamu “Huyu kweli ni mpiganaji.Atatufaa sana” akasema Habib Ndani ya gari alimo Mathew Mulumbi jasho lilimtiririka usoni kama mtu aliyesimama kwenye matone ya mvua. “Nini kimetokea?Mbona bomu halijalipuka?akajiuliza na kufumbua macho.Akatazama kama kuna kitu amekosea lakini kila kitu kiko vile vile kilivyoachwa na Habib.Mara mlango ukafunguliwa akaingia Habib “Nimefanya kila ulichonielekeza lak……….”akasema Mathew Habib akamkatisha “Hongera sana Abu.Huu ulikuwa ni mtihani kwako na umeushinda vizuri.Hili bomu halikuwa limeunganishwa hivyo usishangae kwa nini halikulipuka.” akasema Habib na kuwasha gari wakaondoka “Kila mtu ambaye anajiunga na sisi lazima apewe mitihani kumpima kama kweli ana nia ya dhati ya kujiunga nasi na moja ya mtihani ambao hupewa ni kama wanaweza wakajitoa mhanga kujilipua na bomu.Wengi wamekuwa wanakwama kila wanapopewa mtihani kama huu na wengine hutoka ndani ya gari wakakimbia.Si kazi nyepesi kujitoa mhanga hivyo ni moja kati ya mtihani mgumu sana ambao ili ukubaliwe kujiunga nasi lazima uupitie.Hongera Abu wewe ni jasiri na unafaa kuwa mmoja wetu” akasema Habib lakini Mathew hakujibu kitu bado aliendelea kutokwa na jasho. “Naomba Mungu anisaidie niweze kutoka salama kwa hawa wauaji.Mimi ni mtu jasiri sana lakini leo ujasiri wangu wote umeingia mfukoni.Nimetetemeka.Ni vipi kama lile bomu lingekuwa la kweli?Hivi sasa ningekwisha kuwa marehemu.Nimezoea kuua watu lakini leo nimenusa kifo.Nimeogopa sana” akawaza Mathew bado mwili uliendelea kumtetemeka. “Nashukuru kwamba sasa wananiamini na hili ni jambo zuri kwani lengo langu la kuelekea kuonana na Habiba Jawad linakwenda kutimia.Naomba Mungu aendelee kunikinga na hawa jamaa ili niweze kumfikia Habiba Jawad” akaendelea kuwaza Mathew. “Abu naomba usiwe na wasiwasi wowote kuhusu sisi.Hizi ni taratibu zetu za kawaida kwa kila ambaye anataka kujiunga nasi na katika wote ambao nimewahi kuwafanyia usaili wewe umeshinda kwa kiwango cha juu sana.Nini mipango yako?akauliza Habib “Mipango yangu kama nilivyomueleza Ammar ni kwamba nataka kuendelea kupambana na Israel.Ni hilo pekee ndilo lililopelekea kuamua kujiunga na Ammar” akasema Mathew “Ulikutana vipi na Ammar gerezani?akauliza Ammar “Ni hadithi ndefu lakini ninamshukuru sana Ammar kwani ni mtu aliyenisaidia sana tukiwa gerezani.Nilipokutana naye nilikuwa katika hali mbaya.Nilikuwa nimeteswa mno na nilikuwa nimekata tamaa.Ni Ammar ambaye alikuwa karibu nami akanisaidia hadi nikawa tena binadamu.Kwa bahati nzuri tukakutana mimi na yeye sote tuna malengo sawa na akanishauri tutakapofanikiwa kutoroka gerezani basi nijiunge naye” akasema Mathew “Gereza mlilokuwa mmefungwa ni gereza linalosifika kwa ulinzi mkali sana.Mliwezaje kutoroka gerezani? Akauliza Habib “Ni hadithi ndefu sana hiyo.Nitakueleza siku tukipata nafasi.Kwa sasa nahitaji kupumzika” akasema Mathew na kujiegemeza kitini akafumba macho akajifanya amelala “Natakiwa haraka sana kuanza kutafuta njia ya kujinasua kutoka kwa hawa watu.Sitaki kutumia muda mrefu sana nikiwa na mgaidi hawa” akawaza Mathew na kusinzia Walirejea katika makazi ya Ammar wakashuka na kuingia ndani ya jumba kubwa la Ammar “Karibuni sana” akasema Ammar aliyekuwa amejilaza katika godoro pale sebuleni “Ahsante sana Ammar.Vipi maendeleo yako?akauliza Mathew “Ninaendelea vyema kabisa” akasema Ammar na kumgeukia Habib “Habib nataka unieleze mlikuwa wapi?Ulimpeleka wapi Abu?akauliza Ammar huku akiinuka na kukaa. “Kama tulivyokuwa tumekubaliana jana Ammar nimetoka kumpa Abu mtihani kidogo”akasema Habib “Amefuzu?akauliza Ammar “Ndiyo amefuzu vyema kabisa.Ni mtu jasiri na ninaweza kusema kwamba ni mtu ambaye tunamuhitaji sana” akasema Habib “Nashukuru kusikia hivyo” akasema Ammar na kumfanyia ishara mmoja wa wasaidizi wake asogee karibu halafu akamtuma aende akawaite watu wote waliokuwa nje waiingie ndani.Sebule ilikuwa ndogo kwani watu waliokuwa nje walikuwa wengi wengine wakabaki nje.Walikuwa na hamu sana ya kutaka kusikiliza kile ambacho mkuu wao alitaka kukisema.Ammar akamtaka msaidizi wake amsaidie kusimama na kujitegemeza kwa kutumia fimbo “Naombeni mnisikilize ninyi nyote ! akasema Ammar “Ninamshukuru Mungu baada ya miaka kadhaa ya kufungwa gerezani hatimaye nimeweza kutoka gerezani na sasa nimekuja kuungana nanyi tena.Ninawashukuru sana kwa kuendeleza mapambano hata wakati ambao sikuwepo.Kwa hiki mlichokifanya nina uhakika mkubwa sana kwamba hata nikifa leo hautakuwa mwisho wa mapambano.Bado mapambano yataendelea.Ninawahakikish ia kwamba jeshi letu litakuwa imara sana na damu nyingi inakwenda kumwagika Israel” akasema na kunyamaza “Jambo la pili ambapo nataka kuzungumza nanyi ni kwamba mimi ndiye kiongozi wa kundi hili la Ammar Nazari brigades na hata nitakapokuwa kaburini bado kundi hili litaendelea kubeba jina langu.Nikiwa kama kiongozi ninahitaji heshima na kauli yangu mimi ni ya mwisho.Nitakachokisema lazima wote mkitii” akasema na kunyamaza kidogo “Nimetoka gerezani kwa msaada mkubwa wa Abu” akasema akimnyooshea kidole Mathew “Mimi na yeye tulikuwa tumefungwa gereza moja na yeye ndiye aliyenisaidia mimi hadi nikatoroka.Mpango wa kutoroka ulikuwa wa kwake lakini hakutaka kuniacha akaondoka nami.Nimepigwa risasi mara mbili angeweza kuniacha gerezani lakini kwa ujasiri mkubwa hakuweza kufanya hivyo alinibeba na kuhakikisha anaondoka nami.Narudia tena ni kwa sababu yake niko nanyi hapa leo” akasema Ammar na kunyamaza kidogo “Sisi tunazo taratibu zetu kwa mtu ambaye anataka kujiunga nasi na ninyi nyote mmepitia huko kila mmoja kwa namna yake.Tunafanya hivyo ili kupata uhakika kwamba ni kweli mna nia ya dhati ya kujiunga nasi.Abu ni mtu ambaye kwa kile alichokifanya cha kunisaidia nikatoka gerezani tayari amekwisha onyesha uaminifu kwetu kwani aliyaweka maisha yake hatarini kwa ajili yangu.Baada ya kufika hapa kuna baadhi ya wenzangu ambao hawakutaka kumuamini na walitaka kumfanyia majaribio.Licha ya kuwaeleza kwamba Abu ni mtu mwaminifu kwetu na hakuna haja ya kumsumbua kwa kumfanyia majaribio lakini bado wameendelea kusisitiza kutaka kumfanyia majaribio.Sijapendezwa na hiki walichokifanya hawa wenzangu wakiongozwa na Habib.Kitendo cha kushindwa kuniamini hata mimi kiongozi wenu ni kitendo cha dharau na kimenisikitisha sana.Leo nataka kutoa fundisho kwamba nimerudi mwenyewe na sitaki dharau.Nitakachokisema nataka kitekelezwe.Kauli yangu mimi ni ya mwisho ! akasema Ammar kwa ukali akamfanyia ishara mmoja wa wasaidizi wake ampatie bastora na akafanya kitendo ambacho wote hawakuwa wamekitegemea. Alimnyooshea bastora Habib na kumpiga risasi ya kichwa akaanguka chini akafa palepale. “Hili ni onyo kwenu nyote kwamba sitaki dharau.Nitakachokisema mimi ni amri na kila mtu lazima akitekeleze” akasema Ammar na kuwataka watu wote watoke mle ndani.Akamgeukia Mathew “Abu samahani sana kwa yote yaliyotokea.Wewe ni mtu muhimu sana kwetu hukupaswa kufanyiwa hivi walivyokufanyia.Huwa tunawafanyia hivi wale ambao ni wageni kabisa katika mapambano haya lakini wewe si mgeni.Wewe ni mpiganaji mkubwa na unapaswa kuwa kiongozi wa ngazi za juu kabisa katika kundi letu.Habib ni mtu wangu wa karibu sana nimetoka naye mbali lakini nimemuua kwa heshima yako.Mimi kama kiongozi wao sina mashaka yoyote nawe na ninakuamini kwa asilimia mia moja lakini yeye ameonyesha dharau kwangu kwa kuamua kwenda kukufanyia majaribio.Ni vipi kama huko mlikoenda mngekamatwa na majasusi wa Israel waliotapakaa kila sehemu?Naomba usinione mkatili sana nilichokifanya ni kudumisha nidhamu katika kundi langu.Pole sana na samahani kwa yote Abu.Sasa nenda ukapumzike” akasema Ammar na Mathew akaelekea katika chumba chake kujipumzisha. “Mambo ndiyo kwanza yameanza.Bado nitakutana na mambo mengi makubwa yaliyojaa ukatili mkubwa lakini sipaswi kukata tamaa.Nimekuja hapa kupambana na lazima nipambane.Lazima nifikie lengo langu la kumfikia Habiba Jawad.Natakiwa kuwa karibu sana na Ammar ambaye naamini ndiye atakayeniongoza kufika kwa Habiba.Haitakuwa rahisi kufika kwa Habiba lakini nitajitahidi hadi nifike na nimuondoe kwani utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa dunia.Huyu ndiye uti wa mgongo wa ugaidi duniani kama huyu akiondoka basi ugaidi utakosa nguvu” akawaza Mathew akavua nguo na kuingia bafuni kuoga “Nilitaarifiwa mapema kwamba Ammar ni mtu mbaya sana na leo nimelithibitisha hilo kwa kitendo chake cha kumuua mshirika wake wa karibu Habib.Hakuna aliyetegema kitu kama kile kutokea.Umakini mkubwa unatakiwa huyu jamaa hana rafiki” akawaza Mathew na kutoka bafuni baada ya kumaliza kuoga akabadili nguo na kujilaza kitandani. “Natamani kupata nafasi ya kuwajulisha Mossad kwamba tayari nimekwisha fika na niko salama lakini sina simu na sijui nitapata wapi simu.Lazima nitafute njia ya kuwasiliana nao” akawaza Mathew na kutolewa mawazoni baada ya mlango wa chumba chake kugongwa.Akamruhusu mgongaji kuingia ndani.Alikuwa ni Nawal mke mdogo wa Ammar aliyekuwa amebeba birika la chai na sinia la vitafunwa akamuandalia Mathew mezani “Karibu chai” akasema Nawal Mathew akainuka na kushika kikombe akanywa chai kidogo halafu akasema “Nashukuru sana Nawal” Nawal aliendelea kusimama akimtazama Mathew “Kwa nini umemsaidia Ammar?Kwa nini umemtoa gerezani?akauliza Nawal kwa sauti ndogo na Mathew akatabasamu “Nakuuliza Abu kwa nini umemsaidia Ammar?Unamfahamu vyema?akauliza Nawal “Ammar ni rafiki yangu na nisingeweza kumuacha katika mpango wangu wa kutoroka gerezani” akasema Mathew “Ulifanya kosa kubwa sana Abu.Hukupaswa kumtoa Ammar gerezani”akasema Nawal “Kwa nini Nawal.Hujafurahi kwa mumeo kurejea nyumbani?akauliza Mathew “Sijafurahi na wala siwezi kufurahi.Humfahamu vizuri Ammar ni mtu katili sana” akasema Nawal na sura yake ilionyesha alimaanisha alichokisema.Mathew akaweka kikombe chini na kumtazama Nawal “Nawal uko sahihi ni kweli simfahamu vyema mumeo nimekutana naye gerezani tukawa marafiki” akasema Mathew “tafadhali ondoka.Hapa si sehemu sahihi kwako” akasema Nawal “Kwa nini unasema hivyo Nawal? “Nikikutazama macho yako hayaonyeshi ukatili hauonekani kama ni gaidi.Mahala hapa wamejaa magaidi ambao ni watu makatili sana na wanaweza wakakuua.Tafadhali ondoka” akasema Nawal “Nawal sina sehemu nyingine ya kwenda,hapa nimefika nyumbani.Ninataka kufanya kazi na Ammar na kundi lake” akasema Mathew na Nawal akaondoka kwa hasira “Huyu mwanamke inawezekana ametumwa kuja kunichunguza na kuniwekea mtego.Siamini kabisa hawa watu kwani wataniwekea mitego mbali mbali ili kunipima kama kweli nina nia ya dhati ya kujiunga nao.Bado nina safari ndefu kidogo lakini lazima nifanyue kila juhudi kuwafanya waniamini.Haiwezekani mke wake asifurahi mumewe kutoka gerezani.Nimekwisha utambua mtego wao wanataka kumtumia Nawal kunichimba kwa undani.Hapa wamekwama,hawatapata chochote” akawaza Mathew PARIS – UFARANSA Katika jumba la bilionea Peniela hali ilikuwa ya ukimya japo shughuli za hapa na pale ziliendelea kama kawaida.Maafisa wa usalama walikuwa wanaingia na kutoka katika jumba hili la kifahari wakitaka kupata taarifa za kina kuhusiana na tukio la mauaji ya walinzi wanne wa Peniela pamoja na mpenzi wake Nahum baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.Waandishi wa habari nao walipiga kambi nje ya jengo la Peniela wakitafuta habari za kile kilichojiri. Saa tano za asubuhi Peniela akiwa amevaa mavazi meusi aliingia katika gari lake la kifahari na msafara wake ukaondoka kuelekea hospitali.Ulinzi wake uliimarishwa sana siku hii. “Siamini kama leo ninakwenda kumuaga mpenzi wangu Nahum.Jana nimeshinda naye kutwa nzima tukifurahi na kupeana raha lakini leo hii siko naye tena na ninakwenda kumuaga.Kweli dunia haina usawa kabisa.Kwa nini kila pale ninapoipata furaha ya maisha yangu dunia inanikatili?Kwanza alikuwa ni Mathew ambaye alitoweka na mpaka leo hii hata kucha zake sikuwahi kuziona.Baada ya Mathew amekuja Nahum ambaye kidogo alinivutia na nikaanzisha mahusiano naye akanisaidia kuyapunguza machungu ya kuondokewa na Mathew lakini naye amenyakuliwa kama upepo.Mimi nina mkosi gani?Kwa nini dunia inaniadhibu kiasi hiki? Sipaswi kupenda au kuwa na mpenzi? Akajiuliza Peniela akiwa garini.Picha mbali mbali akiwa na Nahum wakifurahi zikaendelea kupita kichwani kwake “Ni vigumu kuamini lakini ni kweli ninakwenda kumuaga Nahum.Siku nzima ya jana alikuwa anazungumza masuala ya kufa hadi nikamtaka asiendelee tena kutamka maneno yale yanayohusiana na kifo.Ni kama vile alijua atakufa.Nani lakini waliomuua Nahum? Akawaza Peniela akachukua kitambaa na kujifuta machozi “Kuna kitu kinaniumiza kichwa sana kuhusu mauaji haya ya Nahum.Alikuwa na mabadiliko ya ghafla na hakutaka tena kuendelea na mambo yoyote ya kibiashara na badala yake akataka tutumie muda mwingi kustarehe.Kutwa nzima ya jana hakuonekana kuwa na raha na alikuwa anazungumzia sana masuala ya kufa hadi nilipomtaka asiendelee kuongelea mambo hayo.Je alijua atakufa ndiyo maana akawa katika hali ile?akajiuliza Peniela na kuanza kukumbuka namna tukio lile lilivyotokea. “Peniela nisikilize.Watu hawa wananitafuta mimi wamekuja kuniua hivyo kama nikifa nakuomba umtafute Mathew Mulumbi.Yuko hai” Peniela akayakumbuka maneno aliyoambiwa na Nahum dakika chache kabla ya kuuawa.Akafuta machozi “Alijuaje kama watu wale wamekuja kumfuata yeye kumuua ? akawaza na kuendelea kufuta machozi “Kuna maneno Nahum aliyasema ambayo yananichanganya zaidi ! akawaza na kuikumbuka sauti ya Nahum “Nisikilize Peniela.Mathew Mulumbi yuko hai.Tafadhali mtafute” “Alimaanisha nini kwa kauli hii? Akajiuliza “Nahum aliirudia kauli hii mara mbili tena kwa msisitizo mkubwa kwamba Mathew yuko hai akinitaka nimtafute.Oh my God what’s going on?Who was he? Akajiuliza Peniela “Ngoja kwanza niachane na hili jambo litaniumiza kichwa change,nimalize kwanza misiba hii iliyonikuta niwazike walinzi wangu halafu nitakaa na kutafakari kwa kina hiki kilichotokea.Kwa sasa akili yangu imechoka kabisa na kuendelea kutafakari jambo kubwa kama hili ni kuendelea kujichosha zaidi na sintapata muafaka wowote.Naliweka jambo hili pembeni kwa muda” akawaza Peniela. DAR ES SALAAM Saa kumi na moja za jioni Gosu Gosu alirejea katika makazi yake akiwa na mwanaserere mkubwa.Alipoingia ndani akawakuta Agatha na mwanae Teddy pamoja na Nancy wakiwa katika chumba cha mapumziko wakitazama filamu. “Hallo” akasema http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Gosu Gosu akitabasamu. “Karibu Gosu Gosu” akasema Agatha na Gosu Gosu akamfuata Teddy akapiga magoti na kumpatia Yule mwanasesere. “Sweetheart this is the gift from your uncle” akasema Gosu Gosu na Teddy akamchukua Yule mwanasesere “Thank you uncle” akasema Teddy “Mmeshindaje hapa?akauliza Gosu Gosu “Tumeshinda salama.Tunaendelea vizuri.Any news?akauliza Agatha “Hakuna habari yoyote” “Uncle what’s your name?akauliza Teddy “My name?akauliza Gosu Gosu huku akitabasamu “Yes” “My name is uncle Gosu Gosu” “Uncle Gosu Gosu do you have children? I want someone to play with”akasema Teddy “Do you want to play? “Yes I want to play” akajibu Teddy na Gosu Gosu akawataka watoke mle ndani wakaeleka bustanini ambako kulikuwa na bembea na michezo mbali mbali ya watoto.Mathew alikuwa ameitengeneza bustani hii maalum kwa ajili ya wanae kila wanapokuja kutembea. Gosu Gosu akaenda na Teddy kwenye bembea akaanza kumsukuma taratibu.Teddy alifurahi sana.Baada ya muda Gosu Gosu akamuacha Teddy na Nacy akamfuata Agatha “Thank you so much Gosu Gosu”akasema Agatha na Gosu Gosu akatabasamu “Kwa mara ya kwanza toka nimepatwa na matatizo nimejikuta nikitabasamu.Nilikuwa na mawazo mengi sana kuhusu Teddy kama angeweza hata kucheza kutokana na hali aliyokuwa nayo leo asubuhi.Hakutaka hata kutoka nje.Ahsante kwa kumfanya atabasamu tena” akasema Agatha huku akilengwa na machozi “Usijali Agatha,nilikuahidi kwamba nitafanya kila niwezalo kuhakikisha mnakuwa salama na wenye furaha tena” “Alikuuliza swali kuhusu watoto wako hukumjibu” akasema Agatha na wote wakacheka “Lilikuwa swali gumu sana.Mwanao ana akili nyingi anasoma shule gani? “Anasoma shule moja ya kimataifa ndiyo maana hata lugha anayozungumza muda mwingi ni kiingereza zaidi” “Jitahidi sana kumuwekea misingi mizuri ya kielimu.Tukiachana na hayo kuna jambo limetokea leo ambalo limetushangaza kidogo kuhusu Rais” akasema Gosu Gosu na kumueleza Agatha kuhusiana na hofu yao kwa mambo anayoyafanya Rais “Mwenendo huu wa Rais unatufanya tujiulize maswali mengi hasa kuhusu mahusiano yake na Tamar Axon.Anaonekana anamsikiliza mno Tamar na ndiyo maana baada tu ya kufahamishwa kwamba tuko katika nyumba ya Tamar akatuamuru tuondoke haraka sana na kama haitoshi akatutaka tusiendelee na kazi ile aliyotupatia.Tamar anashirikiana na watu ambao tunaamini hawana malengo mazuri na nchi yetu na afrika mashariki kwa ujumla.Tamar ana malengo mabaya sana na Rais na tunajiuliza kwa nini Rais anamsikiliza Tamar kiasi hiki?Kuna chochote unachokifahamu kuhusu Tamar na Rais? Akauliza Gosu Gosu “Kama nilivyokueleza jana kwamba Tamar ni msiri sana na mambo yake mengi hapendi yajulikane.Ninachokifahamu mimi ni kwamba SNSA iko chini ya Rais na hakuna jambo linalofanyika bila Rais kujulishwa.Tamar yuko chini ya Rais na hawezi akamuamuru kitu chochote” “Tamar alikupa kazi ya kudukua mawasiliano ya rais.Katika udukuzi wako uliwahi kupata mawasiliano ya Rais na Tamar?akauliza Gosu Gosu na Agatha akababaika kidogo “Mawasiliano ya Rais na Tamar? “Ndiyo.Uliwahi kuyanasa? “Hapana sijawahi kunasa mawasiliano ya Rais na Tamar” “SNSA iko chini ya Rais na uliniambia kwamba kila kinachofanyika katika idara ile lazima Rais awe na taarifa.Wanawasiliana vipi kumpa rais taarifa?Nani mwenye jukumu la kumpa Rais taarifa za kila siku za idara ya SNSA? “Jukumu la kumjulisha Rais kuhusu shughuli za SNSA ni za mkurugenzi mkuu ambaye ni Tamar lakini sifahamu wanawasiliana vipi”akasema Agatha “Agatha umekuwa karibu na Tamar na unayafahamu mambo yake mengi tafadhali tusaidie tuweze kumfahamu vyema huyu mwanamke hatari” “Nimekueleza yote ninayoyafahamu kuhusu Tamar.Ni mwanamke msiri sana ambaye hapendi mambo yake mengi yajulikane” akasema Agatha “Sawa Agatha ninashukuru hata kwa taarifa hizi chache ulizotusaidia” akasema Gosu Gosu na kuelekea ndani akawaacha akina Agatha bustanini akaenda kujiandaa kwa ajili ya mpango waliokuwa wameupanga na Austin jioni hiyo. OFISI KUU SNSA “Listen to me everyone! Sauti kali ya Tamar ikawafanya wote waliokuwa katika meza zao wakiendelea na shughuli katika ukumbi mkubwa,waache kila walichokuwa wanakifanya wakageuka kumtazama mkuu wao. “Kama mnavyofahamu kwamba mfumo wetu umeingiliwa na kirusi ambacho tunaamini kilipandikizwa na mmoja wa watu wetu Agatha akimtumia mwenzetu mwingine Samson ambaye amejiua leo asubuhi tulipokwenda kumkamata.Kirusi hicho hatari kimeharibu kabisa mfumo wetu.Kwa bahati nzuri tulikuwa tumejiandaa kwa mfumo wa akiba bila hivyo hali ingekuwa mbaya sana.Bado hatujajua nini hasa malengo ya Agatha kupandikiza kirusi katika mfumo wetu lakini tunachokifahamu ni kwamba Agatha anashirikiana na kikundi cha watu na mmoja wa watu ambao anashirikiana nao ni huyu hapa” akasema Tamar na kubonyeza kiunga mbali na picha ya Austin January ikatokea katika runinga kubwa “Huyu anaitwa Austi January.Ni mkuu wa kikosi cha jeshi kinachohusika na operesheni maalum.Austin amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi Tanzania na baadae akaenda kuishi nchini Afrika kusini akifanya biashara lakini alirejea nchini baada ya kutokea vurugu kubwa zilizopelekea familia yake kuuawa.Baada ya kurejea nchini akajiunga na kikosi hicho cha operesheni maalum.He’s someone very dangerous.Huyu ndiye ambaye amekuwa akishirikiana na Agatha na tukifanikiwa kumpata huyu tutafahamu mahala alipo Agatha,hivyo basi jioni ya leo tunakwenda kumchukua hoteli Dino’s.Tayari mpango umekwisha andaliwa na Sandra ndiye atakayeongoza operesheni hiyo.Austin tayari amekwisha elekezwa afike Dino’s hotel tayari kukutana na Sandra.Chumba namba 109 kimeandaliwa kwa ajili ya Sandra na Austin kukutana na tayari Sandra amekwisha pewa maelekezo yote na atakapofika hapo hotelini atamfuata Austin na kumchukua kuelekea chumba hicho kilichoandaliwa.Akiwa humo chumbani Sandra anajua nini atafanya na sisi tutavamia na kumchukua Austin.Operesheni hii ni ya kimya kimya na hakuna mauaji yoyote labda kama ikilazimika lakini timu itakayokwenda huko tujitahidi sana kujizuia kuua.Tunayemuhitaji ni Austin peke yake hivyo basi tujielekeze katika lengo hilo moja.Lakini tukumbuke kwamba Austin hayuko peke yake kuna watu anashirikiana nao kwa siri hivyo basi umakini mkubwa unatakiwa.Justin utaongoza timu hiyo itakayokwenda kumchukua Austin hapo hotelini.Wengine wote kazi yetu itakuwa ni kuwasaidia wenzetu waweze kufanikisha shughuli yao” akasema Tamar na kuondoka akaelekea katika chumba kimoja alimokuwamo Sandra msichana mwembamba mrefu mwenye weusi wa kung’aa. “Are you ready?akauliza “Yes I’m ready” akajibu Sandra.Taar akamtazama halafu akasema “Sandra,Austin is very dangerous.Are you sure you want to do this?akauliza Tamar “Yes I want to do this.Nataka nianze na mimi kujifundisha taratibu na kupata uzoefu” akajibu Sandra “Good. Justin na timu yake watakuwepo karibu kuhakikisha unakuwa salama.Jitahidi usionyeshe woga wowote utakapokutana na Austin” akasema Tamar “Usihofu Tamar nitajitahidi” akasema Sandra.Wakaagana Sandra akatoka akaingia katika gari lake na kuondoka.Tamar akarejea katika ukumbi ule mkubwa akamfuata Hamisa “Austin amepiga simu yoyote kwa kutumi namba ile ya simu tunayotumia kumfuatilia?akauliza Tamar “Hapana hajapiga simu yoyote kutwa nzima ya leo kwa kutumia namba ile ya simu tunayoifuatilia” akasema Hamisa “Good.Keep following him” akasema Tamar na kuelekea ofisini kwake.Akachukua simu na kumpigia Dr Fabian “Tamar” akasema Dr Fabian baada ya kupokea simu “Fabian muda umefika.Mwambie Austin aanze kuelekea eneo la tukio” akasema Tamar “Sawa Tamar.Lakini mmejipanga vizuri?akauliza Dr Fabian “Ndiyo tumejipanga vyema.Tayari timu yetu imeelekea huko.Mwambie aanze safari sasa hivi and Fabian don’t try to do anything stupid ! Akasema Tamar na kukata simu.Baada ya dakika chache akapigiwa simu na Hamisa kwamba tayari Austin amepigiwa simu na Rais na amekwisha anza safari kuelekea Dino’s hotel.







Austin alifika Dino’s hoteli.Akaegesha gari halafu akachukua simu nyingine akampigia Gosu Gosu “Papaa tayari nimefika hapa Dino’s hotel.Uko wapi?akauliza Austin “Ninakaribia kufika hapo” “Ok good.Kila kitu kama tulivyopanga” akasema Austin “Usihofu Austin.Niko nyuma yako” akasema Gosu Gosu. “Just to remind you Papaa kama mtego huu unawekwa kati ya Rais na SNSA basi huyo mtu atakayetumwa hatakuwa peke yake lazima kutakuwa na timu ya watu hivyo tusitegemee urahisi” akasema Austin “Usihofu Austin.Mimi peke yangu ni kikosi cha watu kumi na mbili.Hujawahi kunishuhudia katika mapambano” akasema Gosu Gosu. Austin akaichukua ile simu aliyoitumia kuwasiliana na Gosu Gosu akaiweka katika mfuko wa ndani wa koti bila kuikata ili kumuwezesha Gosu Gosu aweze kusikia kila kinachoendelea.Taratibu akafungua mlango na kushuka akaangaza angaza kwa sekunde kadhaa halafu akaanza kutembea kuelekea ndani “Tayari ameshuka garini anaelekea ndani” mmoja wa watu wa SNSA aliyekuwa katika timu ya Justin akawajulisha wenzake.Austin akaingia ndani ya hoteli akaelekea upande wa baa akaenda kukaa kaunta akaagiza glasi ya mvinyo akaanza kunywa taratibu. Gosu Gosu naye akafika pale hotelini akaegesha gari.Sikioni alikuwa ameweka kifaa cha kumuwezesha kufuatilia kile simu ile ya Austin ambayo hakuizima.Akachukua begi lake la mgongoni akavaa kofia kichwani halafu akashuka na kutembea taratibu kuelekea upande wa baa kwani tayari Austin alikwisha mpa maelekezo yote.Alipoingia ndani ya baa akamuona Austin amekaa kaunta akipata kinywaji taratibu akaenda kukaa katika meza ambayo haikuwa na mtu akaagiza kinywaji. Baada ya dakika kama kumi hivi,akatokea mwanamke mmoja mrefu mwembamba mwenye weusi wa kung’aa.Usiku huu alivaa sketi nyeusi iliyombana na juu akavaa blauzi nyeusi ambayo ilifunguliwa vifungo maeneo ya kifua hivyo kuonyesha sidiria yake nyeusi iliyoyabeba matiti yaliyojaa.Shingoni alivaa mkufu wenye madini ya kung’aa.Nywele zake ndefu alizibana kwa nyuma kwa ujumla alikuwa amependeza.Mwanamke Yule akamfuata Austin na kukaa karibu yake “Hello handsome” akasema huku akitabasamu na kukaa katika stuli ndefu iliyokuwa pembeni mwa Austin “Hi” akasema Austin naye akitabasamu “Naitwa Sandra.Mgeni wako uliyekuwa unanisubiria” akasema Sandra “Ouh kumbe ni wewe.Nimefurahi kukuona.Karibu sana” akasema Austin na kumtaka muhudumu amsikilize Sandra kinywaji anachotumia “Ahsante sana Austin kwa kinywaji lakini ingependeza zaidi kama tungeburudika baada ya kumaliza kwanza mazungumzo ya muhimu” akasema Sandra “Ni jambo zuri pia.Mheshimiwa amekupa ujumbe gani?akauliza Austin “Hatuwezi kuzungumza hapa mambo nyeti.Nimechukua chumba” akasema Sandra “I’m not comfortable in the room.Hatuwezi kutafuta sehemu tukakaa na kuzungumza?Kuna sehemu nyingi hapa hotelini zinazofaa kwa mazungumzo ya faragha” akasema Austin na Sandra akatabasamu na kumsogelea Austin “Mazungumzo nyeti yanazungumzwa sehemu maalum.Nimeandaa chumba maalum ambako tutakuwa huru bila kuingiliwa na mtu yeyote.Usiogope kuwa na amani” akasema Sandra huku akiichezea tai ya Austin “Okay.Tunakwenda chumba namba ngapi?Nataka utangulie mimi nitakufuata nyuma haitapendeza tukiongozana.Hii ni kwa ajili ya usalama wetu” akasema Austin “Chumba namna 109” akasema Sandra na kuanza kuondoka kuelekea katika kikwezi (lifti) “Ninaelekea chumbani” Sandra akawajulisha wenzake akielekea upande kilipo kikwezi. Mazungumzo yote ya Sandra na Austin,Gosu Gosu aliyasikia kupitia kifaa cha kupokelea simu alichokiweka sikioni kwani simu ya Austin haikuwa imezimwa.Mara tu Sandra alipoanza kuondoka pale kaunta Gosu Gosu naye akainuka na kuelekea katika kikwezi.Milango ilifunguka wakashuka watu sita.Ndani ya kikwezi waliingia watu wanne,Gosu Gosu,Sandra na watu wengine wawili walioonekana kuwa ni wapenzi.Sandra akabonyeza kitufe namba nne akimaanisha anashuka ghorofa ya nne Gosu Gosu akamuomba ambonyezee kitufe namba tano.Mara tu kikwezi kilipoanza kuondoka Ghafla Gosu Gosu akatoa kifaa chenye chaji ya umeme na kuwapitishia wale wapenzi wawili kwa haraka na wote wakaanguka na upoteza fahamu halafu kwa kasi ya aina yake akatoa bastora na kumnyooshea Sandra kisha akaweka kidole mdomoni ishara ya kumtaka akae kimya.Sandra alitetemeka Gosu Gosu alipomsogelea “Don’t try to move or scream.You are going to do what I tell you to do ! akasema Gosu Gosu kwa sauti ndogo. “Give me your phone” akasema na kuichukua simu ile ya Sandra.Milango ya kikwezi ilifunguka walipofika ghorofa ya nne lakini hawakushuka.Gosu Gosu akauvuta mkufu wa Sandra na kuurusha nje milango ikajifunga wakaendelea juu hadi ghorofa ya saba ambayo ni ya mwisho wakashuka na kupanda juu kabisa ya ghorofa.Gosu Gosu akachukua simu ya Sandra na kuandika namba ya simu ya Austin ambayo inafuatiliwa na SNSA. “Mwambie Austin kwamba tayari” akasema Gosu Gosu na kumnyooshea Sandra bastora. Austin aliitoa simu mfukoni akaipokea “Hallow” akasema “Austin tayari” akasema Sandra na Gosu Gosu akachukua simu ile akaikata na kuikanyaga kanyaga halafu akachukua simu yake na kumuandikia Austin ujumbe “Done” Gosu Gosu akafungua begi lake na kutoa mavazi meusi ya wanawake akamrushia Sandra avae na yeye akavaa kanzu.Sandra akajifunika hadi usoni akaacha macho pekee.Haikuwa rahisi kumtambua. Simu ya Austin ilipoita makao makuu ya SNSA waliona “Simu ya Austin inaita” akasema Hamisa “Unaweza ukajua nani anampigia?akauliza Tamar aliyekuwa na timu ya wataalamu wakifuatilia zoezi lile “Ni Sandra anapiga” akasema Hamisa “Justin,Sandra anampigia simu Austin” akasema Tamar akiwajulisha timu yake walioko pale hotelini lakini ghafla akastuka “Something is strange ! akasema Tamar “Mpango ulikuwa Sandra amchukue Austin na ampeleke katika chumba kilichoandaliwa.Nini kimetokea hadi Sandra aamue kumpigia simu Austin?Something is not right.Call Sandra now ! akasema Tamar na Hamisa akampigia simu Sandra lakini simu yake haikuwa ikipatikana. “Oh my God ! Can you see the tracker?akauliza Tamar “Yes.I can see it but it’s not moving” akasema Hamisa. “Justin we have a problem” akasema Tamar “Kuna tatizo gani?akauliza Justin “Austin bado yuko baa? “Ndiyo bado ninamuona hapa baa anakunywa” “Good.Tuma mtu haraka sana aende chumba 109 akamtazame Sandra.Kuna kitu kimetokea hapa kinaleta mashaka kidogo” akasema Tamar na Justine akamtuma mtu haraka kwenda chumba 109 kumtazama Sandra.Baada ya dakika mbili mtu aliyetumwa na Justin kwenda kumtazama Sandra chumbani akarejea na kumnong’oneza “Sandra is not there ! I repeat Sandra is not in the room ! Justin akamjulisha Tamar “Oh my God ! Find her !akasema Tamar “Justin hakikisha humpotezi Austin ! Tamar akaendelea kutoa maelekezo. “Everyone get inside.Sandra is missing! Justin akawajulisha watu wa timu yake Wakati akiendelea kutoa maelekezo kwa timu yake kumtafuta Sandra Justin mara katika runinga kubwa ukutani katika ofisi za SNSA ule mduara mwekundu uliokuwa unaonekana ambayo ilikuwa ni simu ya Austin ukatoweka. “We’ve lost the signal.Austin amezima simu” akasema Hamisa “Justin simu ya Austin imezimwa.Bado unamuona hapo baa?akauliza Tamar na kumfanya Justin apatwe na mstuko mkubwa sana baada ya kugeuka na kutomuona tena Austin “Oh my God ! He’s gone” akasema Justin “Justin make sure you find him ! akafoka Tamar na kuvua spika za masikioni akazitupa mezani kwa hasira. Katika eneo la maegesho gari ziliendelea kuingia na kutoka.Miongoi mwa gari zilizokuwa zinatoka ni gari la Gosu Gosu.Ndani ya gari hakuwa peke yake alikuwa na Sandra aliyekuwa amevaa mavazi meusi ya kufunika hadi uso na kuacha macho akiwa na pingu mkononi.Taratibu gari lilitoka katika geti la hoteli na kuingia barabara kuu.Mita kadhaa Gosu Gosu akapunguza mwendo na kusimamisha gari. “C’mon Austin where are you?akajiuliza Gosu Gosu akiwa anaangaza angaza nje huku bastora yake ikiwa mkononi.Mara mlango wa nyuma ukafunguliwa na Austin akaingia ndani. “Let’s go ! akasema Austin na Gosu Gosu akaondoa gari. Justin na timu yake walizunguka hoteli nzima wakiwatafuta Austin na Sandra bila mafanikio.Katika ghorofa ya sita waliweza kuupata mkufu wa Sandra ambao ulikuwa na kifaa maalum cha kuwawezesha kujua mahala alipo na juu kabisa ya hoteli walikuta mavazi ya Sandra na viatu vyake “We’ve lost them ! Ninarudia tena tumewapoteza.Austin ametoweka na Sandra haonekani.Tunahisi atakuwa ameondoka naye” akasema Justin “Justin hii imetokeaje?Una timu kubwa ambayo mngeweza kujipanga vyema na kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa.Kwa nini mkashindwa kumpata Austin? ! akauliza Tamar kwa ukali “Tulijipanga vizuri madam Tamar lakini sijui nini kimetokea hapa hadi tukampoteza Austin na Sandra.I’m sorry madam ! akasema Justin “Rudini hapa haraka sana tuanze mchakato upya wa kuwatafuta Austin na Sandra.” akasema Tamar na kuelekea ofisini kwake alihisi kichwa kizito.Akachukua simu na kumpigia Rais. “Hallow Tamar” akasema Dr Fabian “Fabian we have a problem” “Kuna tatizo gani Tamar?akauliza Dr Fabian “Tumeshindwa kumpata Austin” “Hamjampata Austin?Kwa nini? akauliza Dr Fabian “Timu niliyoituma kumfuatilia Austin wamememfuatilia hadi dakika za mwisho lakini amepotea katika mazingira ya kutatanisha sana.Si yeye tu bali hata Yule msichana ambaye tulimtumia naye ametoweka na hatujui yuko wapi.Tunahisi Austin lazima atakuwa ameondoka naye” akasema Tamar “Tamar huu ni uzembe mkubwa sana umefanyika.Kwa nini watu wako wakamuacha Austin akatoweka?Hamuoni sasa mambo yanazidi kuwa magumu?akauliza Dr Fabian “Fabian huu si muda wa kuanza kutoleana lawama.Ninachokuomba tusaidie tuweze kumpata Austin”akasema Tamar “It’s too late.Mpaka sasa tayari atakuwa amekwisha fahamu kwamba nilitumika kuandaa ule mtego na hii itakuwa mbaya sana kwangu.Oh my God ! akasema Dr Fabian “Fabian do something ! Call him.Mwambie chochote akuelewe.Mwambie kwamba mpango ule ulivuja…ouh gosh I don’t know ! akasema Tamar na kushika kiuno.Alichanganyikiwa. “Tamar listen to me.Tayari tumeharibu.Kama Austin anaye huyo msichana uliyemtumia basi muda huu tayari atakuwa amekwisha jua kwamba ule ulikuwa ni mtego na baada ya kulifahamu hilo mimi nitakuwa adui yake mkubwa hivyo siwezi kumpigia simu kumueleza chochote”akasema Dr Fabian “Tutafanya nini Fabian kumpata Austin?akauliza Tamar “Njoo ikulu.We need to discuss something important” akasema Dr Fabin “Sawa ninakuja” akasema Tamar na kukata simu “Aaagghhh ! akasema Tamar kwa hasira na kutawanya mafaili yaliyokuwa mezani. “Huyu Austin kwa nini anacheza na akili yangu nana hii? Lakini nitampata tu na kumuonyesha mimi ni nani.Hawezi akanikimbia.Ngoja kwanza nikaonane na Fabian nijue ana jambo gani anataka kuniambia” akawaza Tamar na kufunga ofisi yake akaondoka bila kuaga mtu yeyote







Geti la mojawapo ya bohari linalomilikiwa na makampuni ya Mathew Mulumbi,likafunguliwa na gari la akina Gosu Gosu likaingia ndani.Sandra akashushwa na kuingizwa katika kijichumba kimoja kidogo ndani ya lile bohari lililokuwa na bidhaa mbali mbali.Akakalishwa katika kiti kisha akatolewa gundi aliyokuwa amezibwa mdomoni. “Jamani naombeni msiniue! Akasema Sandra kwa woga “Binti naomba nikufahamishe kwamba sasa umeingia katika mikono ya ziraili ambaye muda wowote anaweza akaitoa roho yako.Kitakachokuokoa ni ukweli ! akasema Gosu Gosu na kumtazama Sandra kwa macho makali. “Narudia tena kwamba kitakachokuokoa ni ukweli.Kuna mambo ambayo tunataka kuyafahamu kutoka kwako na kila tutakachokuuliza tafadhali kuwa mkweli.Ukithubutu kutudanganya hautatoka salama humu ndani.Umenisikia?akauliza “Nimekusikia kaka” akajibu Sandra huku akitetemeka “Jina lako nani?akauliza Austin “Naitwa Sandra Benard” akajibu Sandra bado alikuwa anatetemeka “Sandra relax.Take a deep breath ! akasema Austin na Sandra akavuta pumzi ndefu “Good.Sandra nataka kufahamu wewe ni nani?Unafanya kazi gani? Akauliza Austin lakini Sandra akasita kujibu.Gosu Gosu aliyekuwa karibu yake akamnasa kofi zito akaanguka chini “Easy papaa.We don’t need to hurt her yet”akasema Austin.GosuGosu akamuinua Sandra na kumketisha kitini. “Ukiulizswa swali unajibu mara moja bila kujishauri” akasema Gosu Gosu kwa ukali “Narudia tena kukuuliza Sandra unafanya kazi gani? akauliza Austin “Ninafanya kazi katika idara ya serikali” “Zipo idara nyingi za serikali.Idara ipi unafanya kazi?akauliza Austin “Idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.SNSA” akasema Sandra “Nani aliyekutuma kwangu?Ni Rais?akauliza Austin “Hapana si Rais.Nimetumwa kwako na Tamar ambaye nndiye mkurugenzi wa SNSA” akajibu Sandra.Austin na Gosu Gosu wakatazamana “Sema ukweli wako Sandra vinginevyo utakuwa katika matatizo makubwa sana” akasema GosuGosu “Nasema kweli kabisa.Nimetumwa na Tamar” “Hujatumwa na Rais? “Hapana.Sijatumwa na Rais nimetumwa na Tamar” “Tamar alikutuma nini kwangu?akauliza Austin.Sandra akabaki kimya.Gosu Gosu akainua mkono wake “Nitajibu msiniumize” akasema Sandra “Jibu haraka ! akafoka Gosu Gosu “Nilitumwa kwako nijifanye nimetumwa na Rais halafu nikuchukue nikupeleke chumba 109 ili nikakupe maagizo yake.Tukiwa chumbani nilitakiwa kukushawishi tufanye mapenzi na wakati tukiendelea na kitendo hicho iliandaliwa timu kwa ajili ya kuja kuvamia na kukuteka” akasema Sandra.Austin akavuta pumzi ndefu na kuuliza “Kwa nini ninatafutwa na idara yenu? “Tamar ametueleza kwamba unashirikiana na Agatha kuiba siri mbali mbali za idara na vile vile unahusika katika kupandikiza kirusi katika mfumo wetu wa kompyuta” akasema Sandra. “Ahsante kwa kunieleza ukweli.Sasa nataka kufahamu kuhusu Tamar.Anatumia njia gani kuwasiliana na Rais? Akauliza Austin “Sina ukaribu mkubwa na Tamar na mambo yake mengi siyajui lakini kuna mtu mmoja ambaye nina uhakika mkubwa atakuwa anafahamu mambo yake mengi kutokana na ukaribu wao mkubwa na ambaye tumeambiwa kwamba mnashirikiana naye” akasema Sandra “Ni nani huyo? “Agatha” “Agatha? “Ndiyo.Agatha ni mtu wa karibu sana na Tamar kwani wanashiriki mapenzi ya jinsia moja” “Real ? akauliza Gosu Gosu kwa mshangao “Ndiyo.Tamar na Agatha ni wapenzi japo wamekuwa wakifanya jambo hilo kwa siri” “Wewe umefahamu vipi hilo suala?akauliza Austin “Tamar aliwahi kuniita nyumbani kwake siku moja usiku alikuwa na tatizo katika kompyuta yake na nilipofika nikawakuta yeye na Agatha na alinionya nilichokiona iwe ni siri yangu nisithubutu kumweleza mtu.Agatha ni mtu anayemfahamu sana Tamar” akasema Sandra. “Unafanya kazi gani SNSA?akauliza Austin “Mimi ni mtaalamu wa kutengeneza program za kompyuta pale SNSA” “Unafahamu chochote kuhusu udukuzi unaofanywa na idara yenu katika simu za watu na mitandao ya mawasiliano?akauliza Austin na Sandra akawa kimya “Jibu ! akasema Gosu Gosu “Ndiyo ninafahamu” “Unafahamu kama simu ya Rais nayo inadukuliwa? “Hapana sifahamu hilo.Ninachofahamu mimi tumekuwa tukidukua simu za watu mbali mbali ambao tunawafuatailia kuhusiana na usalama wa nchi lakini sifahamu kama simu ya Rais inadukuliwa”akasema Sandra.Austin na Gosu Gosu wakatazamana na kupeana ishara kisha Gosu Gosu akachukua kitambaa na kumfunga Sandra usoni “Ahsante Sandra kwa ushirikiano uliotupa but you are coming with us” akasema Gosu Gosu na kumbeba Sandra akamuingiza katika gari wakaondoka pale katika bohari







Tamar Axon mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi aliwasili ikulu alikoitwa na Rais Dr Fabian.Baada ya kupokelewa waliekea sehemu ya mazungumzo ya faragha. “Tamar nini kimetokea hadi mkashindwa kumpata Austin?akauliza Dr Fabian “I real don’t know what happened lakini nilituma timu ya vijana mahiri kabisa na tulikuwa tumejipanga vyema.Wote tumeshangazwa na hiki kilichotokea namna Austin alivyotoweka” “Vipi kuhusu huyo msichana ambaye ulimtumia?Kuna taarifa zake zozote umezipata hadi sasa?akauliza Dr Fabian “Mpaka sasa hatujapata chochote na tuna uhakika yawezekana Austin ndiye amemteka”akasema Tamar Dr Fabian akavuta pumzi ndefu “Kushindwa kumpata Austin ni mgogoro mwingine mkubwa mmeutengeneza na mimi ndiye ambaye ninajiweka katika wakati mgumu zaidi” akasema Dar Fabian “Nalielewa hilo Fabian..” “No you don’t understand Tamar.You real don’t.Kama ungekuwa unafahamu ni madhara gani yatanipata kama mngemkosa Austin usingekubali vijana wakampoteza ! akasema Dr Fabian kwa sauti kali kidogo “Fabina kwa nini na wewe hutaki kunielewa ninapokwambia kwamba haikuwa dhamira yetu kushindwa kumpata Austin? Tunamsaka kwa udi na uvumba kwa kuwa ni mtu ambaye anashirikiana na Agatha kuiba siri zetu ambazo ni siri za nchi.Mimi na idara yangu tusingekubali kumpoteza hivi hivi.Nakiri kuna makosa madogo yanaweza kuwa yalifanyika hivyo naomba unielewe na mimi” akasema Tamar “Tamar sikurushii wewe lawama lakini ninazungumzia uhalisia uliopo.Mimi ndiye niliyempigia simu Austin na kumtaka aende pale hotelini na kumdanganya kwamba kuna mtu ninamtuma akampelekee ujumbe.Kama amefanikiwa kutoroka basi lazima atakuwa amegundua kwamba ule ulikuwa ni mtego na kama atakuwa amemteka huyo msichana uliyemtumia basi lazima atafahamu kwamba sikumtuma Yule msichana bali ametumwa na SNSA.Nilikubali kufanya vile kwa kuamini kwamba baada ya kutekwa ungekuwa ni mwisho wake lakini imekuwa tofauti” akasema Dr Fabian “We’ll get him” akasema Tamar “Muda huo ambao mtampata tayari tutakuwa tumechelewa sana kwani tayari anajua mambo mengi ” akasema Dr Fabian “Fabian hatuwezi kuumiza vichwa vyetu na mtu mmoja.Niachie mimi jukumu hilo na nitahakikisha ninampata Austin” akasema Tamar “Tamar kuna jambo ambalo unapaswa kulifahamu kuhusu Austin”akasema Dr Fabian na kunyamaza akavuta pumzi ndefu “Jambo gani Fabian? Akauliza Tamar “I used him to kill Lucy Muganza” “You did what ?akauliza Tamar kwa mshangao “I killed Lucy Muganza.Austin January ndiye aliyetekeleza misheni hiyo” akasema Dr Fabian na Tamar akashusha pumzi “Najua umestuka lakini ..” “Ni kweli nimestuka Fabian.Kwanza sikutegemea kabisa kama ungeweza kufanya jambo la hatari kama hili lakini pili sikutegemea kama ungeweza kuviacha vyombo vyote vilivyo chini yako ambavyo vingeweza kulifanya jambo hili kwa umakini mkubwa sana na ukaamua kumtumia Austin.Tatu kwanini Lucy Muganza? Why you killed her? Akauliza Tamar.Dr Fabian akamtazama Tamar kwa muda halafu akasema “Lucy Muganza alikuwa ni hatari kwa taifa letu na jumuiya nzima ya afrika mashariki.Alikuwa anatumiwa na mataifa makubwa ya nje katika mpango wao mkubwa wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Mimi kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo sikuwa tayari jambo hilo litokee na suluhu pekee ilikuwa ni kumuondoa Lucy Muganza” akasema Dr Fabian “Fabian taarifa hizo za kiintelijensia kwamba Lucy anatumiwa na mataifa makubwa katika mpango wa kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki umezipata wapi? Halafu siku zote unapopata taarifa nyeti kwa usalama wa nchi kama hizo umekuwa ukiziwasilisha kwa idara yetu au idara nyingine za serikali kwa ajili ya kufanyiwa kazi kwanini safari hii ulipozipata taarifa hizo za Lucy Muganza ukaamua kuchukua hatua kimyakimya bila kutushirikisha?akauliza Tamar “Sikiliza Tamar,jambo hili ni la siri kubwa na sikutaka kuzihusisha taasisi za serikali ili hata kama ukifanyika uchunguzi basi serikali isihusishwe bali kikundi kidogo cha watu ndiyo maana nikaamua kumtumia Austin ambaye alitekeleza misheni hiyo akishirikiana na watu wachache” akasema Dr Fabian “Fabian umenisikitisha sana kwa kushindwa kuniamini na kunishirikisha katika suala hili” “Si kwamba sikuamii Tamar lakini nilitaka jambo hili lifanyike kwa siri” “Why are you telling me now?akauliza Tamar “Because it’s complicated” “Complicated ?How? “Austin na wenzake walifanikiwa kumuua Lucy Muganza kama nilivyowaelekeza lakini kuna kosa dogo walilifanya ambalo limezua utata mkubwa.Miili ya Lucy na mumewe ilifanyiwa uchunguzi na kukutwa na risasi ambazo ni za bunduki kubwa za wadunguaji ambazo majambazi wanaodaiwa kutekeleza shambulio lile hawakuwa nazo.Laurent Muganza mume wa Lucy alikuwa ni mfanyakazi katika ofisi za umoja wa Ulaya hivyo umoja huo unataka wachunguzi kutoka umoja wa Ulaya waruhusiwe kuingia nchini kuja kufanya uchunguzi wa suala hilo.Nilikataa jambo hilo na kuwaeleza kwamba uchunguzi unafanywa na vyombo vya ndani na hapo ndipo mgogoro ulipoanzia.Aliyekuwa balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini Benjamin aliandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba Tanzania si mahala salama kutembelea halikadhalika rais wa Ufaransa naye alifanya hivyo kwa kuandika katika ukurasa wake akiwaonya raia wa Ufaransa na wa nchi nyingine za Ulaya kuwa waangalifu wanapotembelea Afika Mashariki na hasa Tanzania” akanyamaza akameza mate kulainisha koo halafu akaendelea “Balozi Benjamin alinishangaza kwa kuwa na taarifa nyeti kabisa za nchi.Niliamini lazima kuna watu anashirikiana nao ndipo nikawataka Austin na timu yake waanze kumchunguza lakini jana nikapewa taarifa kwamba watu wasiojulikana wamevamia ukumbi alimokuwamo balozi Benjamin na kumuua kwa risasi.Kifo cha Benjamin kimezidi kuiweka pabaya Tanzania kwani dunia nzima hivi sasa wanaamini serikali ya Tanzania wanahusika katika kifo hicho.Nimekuwa na malumbano makubwa siku ya leo na viongozi wa umoja wa ulaya wakitaka wachunguzi wa kimataifa waruhusiwe kuingia nchini kuchunguza kifo hiki cha Benjamin na kile cha Laurent Muganza lakini nimeendelea kushikilia msimamo wangu kwamba hakuna mchunguzi yeyote wa kimataifa ambaye ataruhusiwa kuingia hapa nchini kuchunguza.Austin anafahamu siri hii na kwa hiki kilichotokea leo siri hii haiko salama tena,hivyo basi kwa namna yoyote ile lazima tuhakikishe Austin anapatikana” akasema Dr Fabian.Ulipita ukimya halafu Tamar akauliza “You are so stupid Fabian” akasema Tamar “Stupid ! akahamaki Dr Fabian “Tamar iwe ni mwanzo na mwisho kunidharau kiasi hicho.Unaponidharau mimi unawadharau watanzania walioniweka hapa.Mimi ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na unapaswa kuniheshimu.Kama huwezi kuniheshimu mimi kama Fabian basi heshimu nafasi niliyo nayo.Ukiingia ndani ya jumba hili tukufu kabisa unapaswa uwe na heshima ! akasema kwa ukali Dr Fabian “Fabian sijakudharau kwamba huna akili lakini nimekudharau kwa sababu umeyatafuta matatizo wewe mwenyewe halafu yanakushinda kuyatatua.Kwa nini ulishindwa kuniita ukanieleza na mimi nikakushauri namna bora ya kulishughulikia suala hili lakini badala yake ukaamua kutumia magenge ya wahuni kwa misheni kubwa kama hii.Hujiamini?Huniamini hata mimi?Fabian unatakiwa ubadilike vinginevyo utashindwa kuongoza nchi hii” akasema Tamar na ukimya ukapita “Fabian tuyaweke pembeni yote yaliyotokea.Makosa yamekwisha fanyika na jukumu letu ni kujisahihisha na kusonga mbele.Nataka kujua nini kinafuata baada ya hapa?akauliza Tamar “Kinachofuata hapa ni kuhakikisha siri hii haivuji na ili kuizuia siri hii ni kuhakikisha Austin anapatikana”akasema Dr Fabian “Fabian kuna jambo nataka nikuulize na ninaomba uwe muwazi kwangu.Je unahusika na mauaji ya Benjamin? “Hapana sihusiki.Sikutaka Benjamin auawe kwani nilikuwa naendelea kumchunguza kujua mtandao wake” “Ahsante kwa kunieleza ukweli Fabian lakini swali lingine ni namna gani tutaweza kumpata Austin? Nimeuliza hivyo kwa kuwa wewe ndiye unayemfahamu zaidi kuliko mimi”akasema Tamar “Kuna mtu ambaye nitamuuliza kuhusu Austin ambaye anamfahamu vizuri.Usiwe na hofu Tamar uhakika wa kumpata Austin ni mkubwa” “Fabian naomba nikukumbushe kwamba suala hili ni zito kwani Austin kwa sasa atakuwa na watu wawili kutoka katika idara yetu na wote hao ni watu muhimu.Agatha ni mtu muhimu sana katika udukuzi na Sandra ni mtu tunayemtegemea sana katika kutengeneza program mbali mbali za kompyuta tunazozitumia.Wote hawa wawili wanafahau siri nyingi za idara yetu na nina wasiwasi kwamba Austin akizipata siri hizo, nchi inaweza ikaingia katika kitisho cha usalama kwani hatujui dhumuni lake ni nini” akasema Tamar “Tamar ninahisi akili yangu imechoka na haifikiri sawa sawa.Ninahitaji mapumziko.Hadi kesho saa nne za asubuhi nitakuwa nimepata taarifa za kutosha kuhusiana na huyu mtu Austin January.Ninachokuomba Tamar nimekushirikisha katika siri hii kubwa naomba tuungane tuwe kitukimoja kwa manufaa ya nchi.Tofauti zetu tuziweke pembeni” “Usihofu Fabian.Mimi ninashukuru kwa kunishirikisha siri hii kubwa.Naomba kuanzia sasa kusiwe na usiri tushirikishane katika masuala yote nyeti ya taifa.Mimi na watu wangu tunakwenda kujipanga kuhakikisha tunafahamu alipo Austin.Nawe pia ukipata taarifa zozote zinazoweza kutusaidia kujua mahala alipo nijulishe mara moja” akasema Tamar akaagana na Dr Fabian akaondoka







Katika makazi ya Mathew Mulumbi kulikuwa na nyumba mbili ndogo ambazo hutumika kama nyumba za wageni.Austin na Gosu Gosu wakamuingiza Sandra katika mojawapo ya nyumba hizo halafu Gosu Gosu akaenda katika chumba alimo Agatha akagonga mlango “Gosu Gosu” akasema Agatha “Agatha wanaendeleaje watoto?akauliza Gosu Gosu “Wanaendelea vizuri.Tayari wamepumzika” “Good.Tunaweza kuzungumza kidogo?akauliza Gosu Gosu “Hakuna tatizo” akasema Agatha na kutoka akamfuata Gosu Gosu hadi katika ile nyumba walikompeleka Sandra. “Agatha sitaki kuchukua muda mrefu kuna jambo nataka kukuuliza na ninaomba unipe jibu la kweli” akasema Gosu Gosu na Agatha akaonyesha wasiwasi kidogo “Jambo gani Gosu Gosu?Uliza tu kama nina jibu nitakupa” “Nataka kufahamu namna Tamar anavyowasiliana na Rais” “Uliniuliza swali hili na nikakujibu kwamba sifahamu chochote kuhusu mawasiliano ya Tamar” akajibu Agatha “Are you sure Agatha? “Yes I’m sure.Kwani kuna nini Gosu Gosu?akauliza Agatha “Agatha nimegundua kwamba unanidanganya na kwamba wewe na Sandra mna ukaribu mkubwa sana kwa kuwa ninyi wawili mna mahusiano ya kimapenzi.Mnashiriki mapenzi ya jinsia moja” akasema GosuGosu kwa ukali.Midomo Agatha ikamtetemeka akakosa cha kusema.Alistuka sana. “Kwa nini ukanidanganya Agatha? I saved your life,nimeweka maisha yangu mbele kukulinda wewe na wanao kwa nini ukanidanganya? Gosu Gosu akauliza “Gosu Gosu nani kakupa taarifa hizo? Agatha akauliza “Haijalishi nani kanipa h izo taarifa ninachohitaji ni kufahamu je ni kweli ama si kweli? “Hapana si kweli.Hizo ni taarifa za uongo” akajibu Agatha. “Agatha sipendi kudanganywa.Utanifanya nikuchukie.Niambie ukweli tafadhali” akasema GosuGosu “Gosu Gosu aliyekupa taarifa hizi amekudanganya mimi sifanyi hayo mambo.Ukaribu wangu na Tamar ni wa mtu na kiongozi wake wa kazi,hakuna zaidi ya hapo” akasema Agatha.GosuGosu akapiga makofi na mlango wa chumba ukafunguliwa akatokea Austin akiwa ameongozana na Sandra.Agatha akasimama kwa mshangao.Hakuamini kile alichokiona mbele yake “Sandra ?!! akauliza kwa mshangao “Sit ! akaamuru Gosu Gosu “Ladies we don’t have much time.Sandra nataka unithibitishe mbele ya Agatha zile taarifa ulizotueleza” akasema Austin “Ni kweli kama nilivyowaeleza huyu ndiye mtu wa karibu na Tamar.Mambo yake yote huyu ndiye anayeyafahamu kwa kuwa ni mpenzi wake.Agatha naomba ukatae mbele yangu halafu nionyeshe vithibitisho” akasema Sandra.Agatha akainama alikosa jibu “Agatha ! akaita Gosu Gosu “Usiiname chini tunahitaji majibu ! “I’m so sorry guys.It’s true.Nimekuwa nikishiriki mapenzi ya jinsia moja na Tamar”akasema Agatha na kuanza kulia “Oh my God ! akasema Gosu Gosu akiwa ameshika kiuno “Watu kama hawa ndiyo wanaosababisha Mungu atupunguzie umri wa kuishi duniani.Hili ni chukizo kubwa sana kwake.Amekosa mwanaume mtoto mzuri kama huyu hadi akashiriki mapenzi na mwanamke mwenzake?Mwanamke mzuri ana kila sifa nzuri ya kike lakini kasoro yake ni hiyo moj….” Gosu Gosu akatolewa mawazoni na Austin “Nyamaza kulia Agatha.Naamini machozi hayo ni ishara ya kwamba unajutia kile ulichokuwa unakifanya.Nadhani umegundua si kitu sahihi na hakikubaliki katika jamii yetu.Yawezekana tumesoma nje ya nchi au tumekaa sana huko lakini tusiige pia na tamaduni zao na kuzileta huku kwetu.Tazama GosuGosu anavyokutazama kwa macho makali anakushangaa.Hakutegemea mwanamke mzuri kama wewe ungeweza kushiriki katika mambo kama hayo.Anyway hatuko hapa kukuhukumu bali tunakushauri uachane na hayo mambo” akasema Austin na Agatha akafuta machozi “Sandra mimi naitwa Austin January nadhani tayari unanifahamu,mwenzangu pale anaitwa Gosu Gosu.Sisi kwa pamoja tunashughulika na operesheni mbali mbali za siri hapa ndani ya nchi na nyingi ya operesheni zetu zinakuwa ni za serikali.Kama mtakumbuka miaka mitatu iliyopita kulitokea tukio la kigaidi hapa nchini ambapo magaidi waliteka watoto na sisi ndio tuliofanikisha kuwakomboa watoto wale.Maisha yetu tumeyatoa kwa ajili ya kuhakikisha nchi inakuwa salama” akasema Austin na kuwatazama akina Sandra “Siku chache zilizopita Rais Dr Fabian alipata taarifa za kiintelijensia kwamba kuna mtu ambaye anaandaliwa na mataifa makubwa kuwa Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na mtu huyo anataka kutumiwa katika kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Mtu huyo ni Lucy Muganza.Baada ya kupata taarifa hiyo Rais aliinita akanipa kazi mimi na wenzangu ya kumuondoa Lucy Muganza.Naomba mfahamu kwamba mimi na huyu mwenzangu hapa ndio tuliomuua Lucy Muganza na mumewe Laurent lakini tulifanya hivyo kwa amri ya Rais na kwa maslahi mapana ya nchi yetu,jumuiya ya Afrika Mashariki na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Baada ya kumuondoa Lucy Muganza mambo ndipo yalipoanza.Kwanza umoja wa Ulaya ulitaka kuleta wachunguzi wake hapa nchini na Rais akakataa.Nyote mnajua kile alichokiandika balozi Benjamin katika ukurasa wake wa twitter.Balozi Benjamin alikuwa na taarifa kuhusiana na silaha zetu.Hizi ni taarifa nyeti sana za nchi na Rais akatupa maelekezo tumfuatilie.Katika kumfuatilia ndipo tulipokutana na Agatha” akasema Austin na kunyamaza kidogo. “Agatha alipewa kazi na Tamar ya kudukua simu ya Rais.Kila siku alikusanya rekodi zote za mawasiliano ya Rais na kuzihifadhi katika faili aliloelekezwa na kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba kila siku alikuwa akipewa kitita cha fedha kwa kazi ile.Katika harakati zake za udukuzi Agatha alinasa mawasiliano ya Rais Dr Fabian na Rais Patrice Eyenga wa Congo ambayo yalizungumzia mauaji yale ya Lucy Muganza.Alinasa rekodi zaidi ya moja lakini hakuzijumisha katika zile rekodi alizokuwa anazihifadhi.Kwa maelezo aliyotupa anadai kwamba hakujua rekodi zile Tamar alikuwa anazipeleka wapi.Jana Tamar alimtuma Agatha apeleke bahasha kwa balozi Benjamin.Akiwa njiani Agatha aliifungua bahasha aliyopewa akakuta kuna diski mweko(flashdisc).Alipoifungu a akakuta kuna rekodi mbili za mazungumzo ya Rais Dr Fabian na Patrice Eyenga.Alizifuta rekodi zile na kuweka kirusi katika hiyo diski mweko.Sisi pia tulikuwa tunamfuatilia balozi Benjamin na ndipo tulipogundua kwamba alipewa bahasha na Agatha tukaanza kumuandama tukafanikiwa kumpata na kumuokoa kutoka katika jaribio la kuuawa.Toka jana tuko naye hapa tunamuhifadhi na kumlinda.Kitendo cha Tamar kumpatia balozi Benjamin rekodi zile za Rais ambazo ni wazi zinazungumzia mauaji ya Lucy Muganza kinaashiria malengo mabaya kwa Rais.Usiku wa jana Balozi Benjamin aliuawa na watu wasiojulikana.Tuliamua kuanza uchunguzi wetu nyumbani kwa Tamar.Tulifanikiwa kuingia lakini kabla hatujafanya chochote nilipigiwa simu na Rais akatutaka tuondoke mahala pale haraka sana.Kama haitoshi Rais akatutaka tusiendelee tena na zoezi lile alilotupa la kuchunguza watu wanaoshirikiana na Benjamin.Mchana wa leo nimepigiwa simu na Rais akanieleza kwamba jioni niende Dino’s hotel pale kuna mtu nitakutana naye atanipa ujumbe muhimu.Kumbe ulikuwa ni mtego nimetegewa ili nikamatwe lakini kwa bahati nzuri mimi na mwenzangu Gosu Gosu tuliweza kung’amua mapema mtego huo na tukajipanga tukautegua na kumchukua Sandra”akanyamaza tena kwa sekunde kadhaa halafu akaendelea “Nimewapa maelezo haya marefu ili kuwapa picha halisi ya kile kinachoendelea hivi sasa.Rais yuko katika hatari kubwa sana.Rekodi zile za mazungumzo yake na Patrice Eyenga bado ziko katika kompyuta ya Tamar ambaye alikuwa na mahusiano na balozi Benjamin kutoka umoja wa Ulaya ambao walikuwa wanamuandaa Lucy Muganza awe Rais wa Congo na vile vile kuisambaratisha jumuiya ya Afrika Mashariki.Kitu kinachonishangaza ni kwamba Rais anaonekana kumsikiliza sana Tamar ndiyo maana nilimuuliza swali Agatha kwamba kwa nini katika rekodi zote alizokuwa anadukua za Rais hakuwahi kupata mazungumzo ya Rais na Tamar? Au Tamar alikuzuia kufuatilia mawasiliano yake na Rais? Nataka kujua Tamar na Rais wanazungumza nini wanapowasiliana kwani kuna kitu nakiona hakiko sawa” akasema Austin “Austin na Gosu Gosu naombeni mnisamehe sana.Jana sikuwaeleza ukweli wote kuna mambo niliyaficha kuhusu Tamar” akasema Agatha “Endelea” akasema Austin “Mazungumzo ya Tamar na Rais si rahisi kupatikana kwa sababu Tamar anatumia progamu Fulani ambayo kila amalizapo kuzungumza na mtu simuni basi program hiyo hufuta kumbukumbu zote za maongezi hayo haraka sana hivyo ni vigumu kupata rekodu zozote za mazungumzo ya Tamar sin a rais tu bali na mtu yeyote.Programu hiyo alimtengenezea Sandra”Akasema Agatha.Gosu Gosu na Austin wakamgeukia Sandra “Ni kweli Sandra?akauliza Austin “Ni kweli.Tamar alinitaka nimtengenezee progamu hiyo hivyo hakuna kumbu kumbu yoyote ya simu za Tamar inayobaki ndiyo maana inakuwa vigumu kupata rekodi za mazungumzo yake na Rais” akasema Sandra “She’s very smart”akasema Austin “Ni muangalifu sana kwa kila anachokifanya” akasema Sandra “Sandra na Agatha,naomba mfahamu kwamba kwa sasa nchi iko vitani na mataifa makubwa ambayo yanatafuta kila njia iliwaweze kuingia katika nchi zetu na kuchta rasilimali zetu.Kiongozi mkuu katika mapambano haya ni Rais wetu ambaye ameendelea kuwa na misimamo isyiyumba kuhusu rasilimali za nchi na hili linamfanya awe ni mlengwa namna moja.Mabeberu hawa watatafuta kila namna ya kuweza kumdhoofisha Rais wetu na kama ikiwezekana hata wamundoe madarakani na kuweka mtu wanayemtaka wao.Wanachokitafuta sasa ni kupata ushahidi wa kutosha kumuhusisha Rais na mauaji ya Lucy Muganza na wanawatumia watu wa karibu na Rais kama Tamar.Nadhani mnaweza kuona hatari aliyonayo Rais wetu.Hivyo basi jukumu letu sisi ni kumlinda Rais kwani inaonekana wazi hajui kinachoendelea nyuma ya pazia.Tusiwaache wafanikishe lengo lao.Tunawahitaji sana ninyi wawili katika mapambano haya.Je mko tayari kuungana nasi kumlinda Rais? Akauliza Austin “Mimi niko tayari ndiyo maana nilizifua rekodi za Rais ambazo zingeweza kumuhusisha na mauaji yale ya Lucy Muganza” akasema Agatha “Good ! Vipi kuhusu wewe Sandra uko tayari? “Let me honest with you guys” akasema Sandra “Baba yangu alikuwa ni rafiki wa Dr Fabian na hata alipofariki miezi mitano iliyopita Dr Fabian aligharamia mazishi yake.Ni mtu ninayemuheshimu sana.Mwili umenisisimka baada ya kusikia maelezo yako na hatari aliyonayo Dr Fabian.Mimi siwezi kusema hapana katika mpango huu kwani Dr Fabian ni mtu muhimu kwangu.Naamini hata kufika kwangu hapa ni kwa mpango wa Mungu kwani nilisikia wanatafuta mtu wa kwenda kukutana na Austin nikajikuta najitolea.Mimi sina utaalamu sana na mambo hayo ya kiuchunguzi bali nimebobea katika mambo ya kompyuta.Kama kuna chochote kitahitajika kwa upande huo mimi nitashughulikia” akasema Sandra “Ahsante sana Sandra.Tunahitaji mno msaada wako.Tunahitaji mtu ndani ya SNSA wa kumchunguza Tamar.Tunahitaji pia kuzifuta rekodi zote za mazungumzo ya Rais na Patrice Eyenga zilizopo katika kompyuta ya Tamar haraka na kazi hiyi Sandra utakwenda kuifanya.Tunataka vile vile kupata mawasiliano ya Tamar tujue anaowasiliana nao na wanawasiliana nini.Can you help us with that?akauliza Austin “It’s a tough job but I can do it to save president” akasema Sandra “Mpango utakuwa namna hii.Tutakutelekeza mtaa wa Chambo pale kuna makahaba wengi.Utakuwa umesawajika na utawaeleza makahaba wale kwamba ulitekwa na watu usiowafahamu wakakupeleka mahala wakakufanyisha mapenzi kwa nguvu kisha wakaenda kukutupa pale.Makahaba wale watakuhurumia utawaomba simu umpigie Tamar na kumtaka aje kukuchukua na utakuwa umerejea tena SNSA.Utamweleza kwamba nimekuachia huru baada ya kugundua kwamba hujui chochote na hauna taarifa zozote za kunisaidia.Kesho asubuhi utarejea ofisini tunataka haraka sana utafute kila njia ili uweze kufuta zile rekodi zote za maongezi ya Rais zilizopo katika kompyuta ya Tamar.Vile vile nataka uondoe programu uliyoitengeneza ya kufuta kumbukmbuzote za mawasiliano ya Tamar” akasema Austin “Guys” akasema Agatha na wote wakamgeukia “I think you all don’t know madhara ya zile rekodi.Nawahakikishia kwamba rekodi zile ni mbaya na hatupaswi kuchukua muda mrefu kuziondoa katika kompyuta ya Tamar.Tukisema tumtumie Sandra hataweza kuipata kompyuta ya Tamar kwa wakati na kadiri tunavyozidi kuchelewa ndivyo Tamar anavyopata muda wa kutekeleza mipango yake.Kama ni kuzifuta rekodi basi iwe ni leo”akasema Agatha “Nini wazo lako?akauliza Gosu Gosu “Nataka nijitolee mimi niende” akasema “No you can’t.! akasema GosuGosu “Tamar anakujua wewe ni msaliti na unashirikiana na Austin akiuona tu lazima atakuua” “She won’t kill me.Ninamfahamu Tamar vizuri kuliko mtu yeyote I know how I can handle her.I know how I can make her believe me.Ninawahakikishia kwamba ataniamini na nitapata nafasi ya kuingia katika kompyuta yake na kufuta rekodi zote za Rais” akasema Agatha “Agatha nakubaliana na Gosu Gosu kwamba huo mpango ni wa hatari kubwa sana.Tamar hatakuamini hata kidogo kwani anajua unashirikiana na Austin na kwa sasa katika idara nguvu kubwa imeelekezwa katika kukutafuta wewe na Austin.Hakuna ambaye atakuamini.Niache mimi niende na nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba ninaipata kompyuta ya Tamar”akasema Sandra “Naombeni mniamini ndugu zangu kwamba Tamar ataniamini.Ninajua namna ya kumfanya aniamini” Agatha akaendelea kusisitiza “Utafanya nini kumfanya Tamar akuamini tena?akauliza Austin “Nitamwambia niligundua kwamba balozi Benjamin anafuatiliwa ndiyo maana nikafuta zile rekodi zilizokuwamo katika diski mweko aliyonipa nikapandikiza kirusi na nilipofika nyumbani nikavamiwa na mtu aliyeniteka na kunipeleka mahala nisipopajua na ndipo nilipokutan na Austin ambaye alikuwa ana uwezo wa kuingia katika kompyuta zetu na kuchukua siri mbali mbali.Alinitaka nimsaidie kudukua kompyuta yako ndipo nilipomdanganya na kuingiza kirusi katika mtandao wetu ambacho kimeweza kuharibu pia hata kompyuta zake na kufuta siri zote ambazo amekwisha ziiba kutoka kwetu.Mpaka hapo Tamar atakuwa ameniamini na ntaweza kuichukua kompyuta yake na kufuta zile rekodi” akasema Agatha. “Unaonekana ni mpango mzuri lakini Tamar anaweza akakuuliza umewezaje kutoroka kutoka kwetu? Lazima kutafuta maelezo ya kutosha ili kumthibitishia Tamar kwamba kweli umefanikiwa kutoroka”akasema Austin “You’ll shoot me ! akasema Agatha “Shoot you?akauliza Gosu Gosu kwa mshangao “Ili kumfanya aniamini kwamba nilitoroka lazima nipigwe risasi.Tamar akijua nimepigwa risasi hatakubali nikatibiwe hospitali atanipeleka kwake na mimi lengo langu kubwa ni kwenda nyumbani kwake ili nikafute zile rekodi pia kufanya uchunguzi wa mambo mengine yanayomuhusu Tamar” akasema Agatha “Vipi kuhusu familia yako?Akikuuliza wanao wako wapi utampa jibu gani?GosuGosu akauliza Agatha akabaki kimya.Alikosa jibu “Guys,Tamar is very smart.Tukifanya kosa hata dogo anaweza akagundua kwamba ni mchezo tumeucheza hivyo tutakosa kila kitu na kuwaweka ninyi hatarini.Ninao ushauri kama mtaona unafaa” akasema Gosu Gosu “Go ahead” akasema Austin “Mpango wa kumtumia Sandra ulikuwa mzuri sana na hauwezi kuwa na mashaka kwani ni rahisi kuaminiwa na Tamar hivyo nashauri tuendelee na mpango huo lakini kutokana na unyeti wa rekodi hizo nashauri tusichukue muda mrefu sana kwani Tamar anaweza akazihamisha au akazituma mahali hivyo hatuna njia nyingine zaidi ya kumvamia na kumchukua Tamar na hiyo kompyuta usiku wa leo.” akasema Gosu Gosu.Walikaa kimya wakitafakari halafu Austin akasema “I think that’s the best option right now” akasema Austin “Sawa kama mmeamua hivyo” akasema Agatha “Agatha si kwamba mpango wako ulikuwa mbaya lakini ulikuwa na hatari.Tamar yuko makini sana na anaweza akagundua kwamba ni mchezo umechezwa hivyo kukuweka katika hatari ya kuuawa” akasema Austin Baada ya majadiliano marefu wakakubaliana watumie njia ile aliyoipendekeza Gosu Gosu. “Baada ya wote kukubaliana na njia hii kuna jambo la mwisho ambalo lazima tulifanye ambalo ni kumfanya Sandra aonekane kweli alikuwa katika mateso makali.Utatusamehe Sandra kwani hakuna namna ya kuepuka maumivu” akasema Austin “Hakuna tatizo” akasema Sandra.Gosu Gosu akaenda ndani na kuja na vifaa mbali mbali vya kutesea akamchoma sindano Fulani “Hii sindano itakusaidia usihisi maumivu makali” akasema Gosu Gosu na kusubiri kwa dakika chache halafu akamtaka Sandra avue lile gauni alilovaa akabakiwa na nguo za ndani akamfunga katika kiti na kuanza kumchapa.Mwili wa wa Sandra ulianza kuvimba na kuanza kuonyesha alama huku damu ikichuruzika. “Imetosha” akasema Sandra akilia.GosuGosu akamfungua na kisha akalichana chana lile gauni lake likapakwa damu halafu akalivaa.Sandra alitengenezwa kama walivyotaka yaani aonekane mtu aliyetoka katika mateso makali. “Nadhani kila kitu tayari sasa tuendelee na mpango wetu” akasema Austin baada ya maandalizi yote kukamilika na Sandra akapelekwa garini.Alihisi maumivu makali.Kabla ya kuingia garini Gosu Gosu akamuita pembeni Agatha “Agatha tutampata Tamar usiku wa leo.Tukimpata tutamleta hapa.Will that be a problem to you?akauliza Gosu Gosu “Hakuna tatizo lolote” “Good” akasema Gosu Gosu na kuingia garini wakaondoka







Mtaa wa Chambo unasifika sana kwa kuwa na wanawake wengi wanaofanya biashara ya ukahaba hasa ifikapo nyakati za usiku.Austin alisimamisha gari na baadhi ya makahaba wakaanza kulisogelea wakidhani ni mteja mara wakashuhudia mlango ukifunguliwa na mwanamke mmoja akasukumwa nje kisha gari lile likaondoka kwa kasi.Makahaba wale wakamfuata Yule mwanamke aliyesukumwa kutoka ndani ya gari,alikuwa ameeumizwa sana. “Naombeni mnisaidie jamani wale jamaa walitaka kuniua” akasema Sandra na kutaka kunyanyuka akaanguka.Wanawake wawili wakamsaidia kunyanyuka wakampeleka katika kijichumba Fulani ambacho huwa wanakitumia kwa shughuli zao za ukahaba. “Nini kimekupata?akauliza mmoja wao “Nilikuwa klabu mimi na wenzangu nikakutana na wale wanaume wakataka niondoke nao.Walikuwa na fedha tukanywa pombe kisha tukaondoka.Nilipoingia katika gari lao wakanifunga kitambaa usoni wakanipeleka mahaa nisipopajua wakanibaka na kutishia kuniua.Hawajanipa chochote wamenipora kila kitu hadi nguo zangu wakanivisha hili gauni na kuja kunitupa hapa” “Pole sana shoga.Wanaume wa siku hizi unapaswa kuwa mwangalifu sana.Tena wewe una bahati kubwa wamekuacha hao wengine huwa wanabakwa na kuuawa au hata kutupwa porini” “Unaishi wapi kwani?akauliza mwingine “Naombeni mnisaidie simu niwasiliane na dada yangu aje anichukue siwezi kutembea katika hali hii” akasema Sandra na mmoja wa wale makahaba akampa simu,akaandika namba za Tamar na kupiga.Simu ikaita bila kupokelewa.Akapiga mara ya pili simu haikupokelewa akapiga mara ya tatu ikapokelewa “Hallow” akasema Tamar “Sandra hapa ninaongea”akasema Sandra akiwa katika maumivu “Sandra ! akasema Tamar kwa mshangao. “Is that real you?akauliza Tamar “Tamar it’s me Sandra” “Oh my God ! where are you? “Tamar naomba uje unichukue.Nimekutwa na matatizo makubwa” “Uko wapi Sandra? Akauliza Tamar na Sandra akamueleza mahala alipo. “Endelea kukaa hapo hapo usiondoke” akasema Tamar na kukata simu Mita chache kutoka mahala pale alipokuwapo Sandra,Austin na Gosu Gosu walikuwa ndani ya gari wakifuatilia kila kinachoendelea.Sandra alikuwa amepewa kifaa Fulani kidogo akibonyeze pale tu atakapoona na Tamar ambacho kitawapa ishara mahala alipo. “Papaa nina wasi wasi kidogo kuhusu huu mpango” akasema Austin “Usiwe na wasi wasi wowote Austin.Nina uhakika mkubwa wa kumpata Tamar usiku wa Leo na lazima tumpate” akasema Gosu Gosu “Kuna wakati ninavunjika moyo kwani mtu ambaye tunapambana na kuhatarisha maisha kwa ajili yake hajui chochote na wala hatuthamini” akasema Austin “Austin usifanye ili uthaminiwe fanya kwa sababu ni jambo sahihi kulifanya.Rais alifanya jambo la busara kumuondoa Lucy na ni kwa maslahi ya nchi zetu hivyo lazima tuhakikishe tunamlinda dhidi ya hatari yoyote ile hata kama yeye mwenyewe hataki tumlinde.It’s our job ! akasema Gosu Gosu “Sawa ngoja tuendelee.Lakini pata picha kama tusingeung’amua mapema mtego ule na ningekamatwa na SNSA nani sasa hivi angekuwa anahangaika kwa ajili ya usalama wake? Akauliza Austin “Austn we have a job to do.Hayo mambo mengine siku nafasi ikipatikana utamuuliza” akasema Gosu Gosu Sandra akiwa bado ndani ya kile chumba kidogo alichohifadhiwa,mara akaingia Yule mwanamke aliyetumia simu yake kuwasiliana na Tamar “Kuna mtu wako anakupigia simu” akasema Yule mwanamke na kumpa simu Sandra “Hallow” akasema Sandra “Kuna gari iko hapo nje nenda ingia uondoke mahala hapo haraka sana” akasema Tamar na kukata simu.Sandra akawashukuru wale wanawake halafu akatembea kwa kuchechemea akatoka nje akaliona gari moja jeusi limeegeshwa pembeni ya barabara.Taa za gari lile zikawaka na kuzima akaitambua ishara ile na kufungua mlango wa gari akaingia na gari likaondoka.Gosu Gosu na Austin ambao hawakuwa mbali na eneo lile walimshuhudia Sandra akitoka ndani ya kile kijichumba na kuingia katika gari akaondoka “Papaa tumeliwa.Mbona hajabonyeza kitufe kutupa taarifa?akauliza Austin “Usihofu Austin.Kumbuka tulimwambia hadi atakapohakikisha amemuona Tamar ndipo atupe taarifa.Usiogope Austin Sandra atatufikisha kwa Tamar” akasema Gosu Gosu





Gari lililombeba Sandra lilifika karibu na jengo la biashara la Mawingu tower.Sandra akashuka kutoka ndani ya lile gari akaelekezwa kuingia katika gari lingine lenye rangi nyeusi.Kitendo kile kilifanyika haraka haraka sana na magari yale yakaondoka kila moja njia yake.Wakati kitendo kile kinafanyika Austin na Gosu Gosu walikuwa wameegesha gari umbali wa mita kadhaa na walishuhudia kila kilichofanyika kwa kutumia kiona mbali.Pamoja na kuingia katika gari lingine bado Sandra hakuwa amebonyeza kile kidude alichopewa. “These people are very smart.Wanachukua tahadhari kwa kila wanachokifanya” akasema Gosu Gosu “Lazima wachukue tahadhari kuhakikisha kwamba hawafuatiliwi.Lakini sina amani kabisa na Sandra” akasema Austin “Kuwa na amani Austin.Nina uhakika mkubwa kwamba tutampata Tamar usiku wa leo” akasema Gosu Gosu wakaendelea kulifuatilia lile gari alimopanda Sandra Gari lile lilifika hadi nje ya klabu moja gari lile likasimama mlango ukafunguliwa na haraka haraka Sandra akashuka akaenda katika gari lingine jeupe aina ya Range rover e vogue akaingia na kufunga mlango.Mara katika simu ya Gosu Gosu ukasikika mlio kutoka katika kile kidude alichokuwa nacho Sandra “Thank you Lord.Tumempata Tamar.Sandra amebonyeza kile kitufe.Kumbe mbadilishano wote huu wa magari mwisho wake ulikuwa kwa Tamar” akasema Gosu Gosu Sandra alipoingia katika gari aliloelekezwa aingie akamkuta Tamar.Kwa haraka akabonyeza kile kidude kuwapa taarifa akina Austin “Funga mkanda” akasema Tamar mara Sandra akaweka mkono mdomoni akitaka kutapika akafungua mlango na kushuka chini akainama katika mtaro wa karibu.Lengo lake lilikuwa ni kukitupa kile kifaa alichokuwa nacho.Akakitupa katika mtaro na kurejea garini “Are you okay?akauliza Tamar “I’m okay” akajibu Sandra na Tamar akaondoa gari.Austin na Gosu Gosu ambao walikuwa wanafuatilia kila kitu wakiwa umbali wa mita kadhaa nao wakaendelea na zoezi lao la kumfuatilia Tamar kwani walikwisha liona gari lake “Ahsante kwa kunipa moyo Papaa.Mimi tayari nilikwisha kata tamaa kabisa na Sandra”akasema Austin Ndani ya gari la Tamar kulikuwa na ukimya mkubwa Tamar akiwa makini katika usukani “Unajisikiaje hali yako Sandra? Umeumizwa? akauliza “Nimepigwa sana.Mwili umevimba” “Umeumizwa sana nikupeleke hospitali?akauliza Tamar “Hapana nipeleke sehemu salama” akajibu Sandra na safari ikaendelea kimya kimya.Baada ya muda Tamar akasema “Sandra I’m real sorry.Sikupaswa kukuruhusu uende ukafanye kazi hii ya hatari wakati hauna uzoefu na mambo yale.Yote yaliyokupata ni kwa sababu yangu” akasema Tamar “Usijali Tamar.I wanted to learn the field work” akasema Sandra na kufumba macho kwa maumivu “I’m sorry Sandra” akasema Tamar akimuonea huruma Sandra kwa maumivu aliyokuwa nayo Hakukuwa na mazungumzo mengine garini hadi walipofika katika jumba la Tamar na kwa kutumia kiunga mbali akafungua geti wakaingia ndani.Tamar akashuka haraka haraka akamfungulia mlango Sandra akamsaidia kushuka.Sandra alikuwa anachechemea Tamar akasaidia wakaingia sebuleni “Sandra pole sana” akasema Tamar huku akimvua Sandra lile gauni alilokuwa amevaa na kuona namna mwili wake ulivyovimba kwa kipigo. “Mashetani hawa wamekuumiza sana Sandra.Pole” “Ahsante sana” akasema Tamar “Tamar I’m sorry I failed you! Akasema Sandra “Shhhhh !! akasema Tamar akimtaka Sandra anyamaze “Usiseme chochote tafadhali.You did great.Kitu kikubwa nashukuru u mzima japo wamekuumiza.Twende bafuni nikakusafishe majeraha.Utalala hapa kwangu na kesho daktari atakuchunguza kujua kama umeumizwa kwa ndani” “Ahsante Tamar”akasema Sandra wakainuka na kuelekea katika bafu lililomo chumbani kwa Tamar akachemsha maji na kuanza kumkanda Sandra aliyekuwa akitoa kelele za maumivu. “Wamemuumiza sana huyu mtoto.Hili ni kosa langu kwani nilimruhusu aende katika kazi ya hatari wakati hana uzoefu wowote na mambo haya.Ninaapa lazima nimpate Austin na wenzake” akawaza Tamar. Akiwa bafuni akiendelea kumkanda Sandra mara akasikia mlio Fulani ukitoka chumbani kwake.Akamtazama Sandra kwa macho makali “What have you done?akauliza Tamar kwa ukali “Sijafanya chochote ! akasema Sandra “Wait for me here.Usitoke tafad…..” akasema Tamar na kabla hajapiga hatua moja mlango wa bafuni ukapigwa teke zito ukafunguka mtu mmoja akaingia mle bafuni akiwa na bunduki.Alikuwa ni Gosu Gosu “Tamar Axon ! akasema Gosu Gosu kwa sauti kali “Piga magoti tafadhali kisha weka mikono yako kichwani !! akasema Gosu Gosu Taratibu Tamar akaanza kupiga magoti lakini ghafla akajigeuza kwa kasi ya ajabu na kuinyakua chupa iliyokuwa katika meza ndogo akamrushia Gosu Gosu ambaye alipinda ili kuikwepa na hicho ndicho Tamar alichokuwa anakitafuta.Kabla Gosu Gosu hajakaa sawa akakatwa mtama na kuanguka chini kama furushi akasindikizwa na teke kali la mbavuni lililomfanya Gosu Gosu atoe mguno wa maumivu kisha Tamar akainyakua bunduki ndogo aliyokuwa nayo Gosu Gosu. “Simama ju……” Kabla Tamar hajamlizia kumuamuru Gosu Gosu asimame akapigwa chupa ya kichwani na Sandra akapepesuka kisha Gosu Gosu akamsindikiza na teke zito lililomsukuma akaenda kuangukia kioo kikubwa kilichotenganisha bafu na choo kikavunjika huku Tamar akitoa ukulele wa maumivu. “Gosu Gosu are you okay?akauliza Sandra “Thank you Sandra.I’m okay.Mshenzi huyu ameniumiza mbavu zangu”akasema Gosu Gosu na kunyanyuka akaichukua bunduki yake na kumfuata Tamar aliyekuwa anagugumia kwa maumivu “Help me ! Help me ! akalia Tamar.Alikuwa amekatwa na kioo tumboni na utumbo ulianza kutoka nje. “Sandra tafadhali tafuta kitambaa kisafi leta haraka sana”akasema Gosu Gosu na kumfuata Tamar pale chini “Tamar ! Tamar ! akasema Gosu Gosu na kugeuka kumtazama Sandra aliyemtuma kitambaa.Akaamua kuinuka yeye mwenyewe kwenda kutafuta kitambaa.Gosu Gosu alifanya kosa kuacha bastora yake pale chini Tamar akanyoosha mkono na kuishika akajilenga kichwani na kuachia risasi. Gosu Gosu alikipata kitambaa na kurejea haraka bafuni lakini akapatwa na mstuko mkubwa kwa kile alichokiona mle ndani.Tamar alikuwa amejipiga risasi kichwani. “Nooooooo !! akasema Gosu Gosu na kumfuata akamtazama tayari Tamar alikwisha kufa.Akasimama na kushika kiuno huku akihema kwa kasi. “She’s gone.Tulimuhitaji akiwa mzima” akasema Gosu Gosu akimtazama Sandra aliyekuwa nyuma yake “Anastahili kifo cha namna hii shetani huyu” akasema Sandra “Jiandae tunaondoka hapa sasa hivi.Pekua tafuta kama kuna kitu chochote humu ndani ambacho unadhani kinaweza kutusaidia” akasema Gosu Gosu na kutoka akaelekea katika ofisi ya Tamar alikokuwa Austin. “She’s gone”akasema Gosu Gosu “You killed her? Austin akauliza “Hapana amejiua mwenyewe.Umepata nini? “Nimepata kompyuta mbili,kadi za benki na hati ya kusafiria.Bado naendelea kupekua mafaili yake kuona kama kuna kitu cha muhimu kwetu” akasema Austin “Austin we need to go.Tulichokuwa tunakitafuta ni kompyuta yake na tayari tumeipata.Nina uhakika ndani ya hiyo kompyuta kuna mengi tutayapata” Walifanya upekuzi wa haraka haraka wakachukua kila walichoona kina umuhimu kwao na kujiandaa kuondoka. “Austin kabla hatujaondoka nataka nikukumbushe kwamba nyumba hii ina kamera za siri hivyo basi hatutakuwa salama kama tutaondoka hapa bila kuharibu kamera hizo ambazo naamini zimeturekodi wakati tukiingia hapa.Tuichome nyumba” akasema Gosu Gosu “Tuichome nyumba? “Ndiyo.Hatuna muda wa kuanza kuzitafuta hizo kamera mahala zilipo.Tukichoma nyumba kila kitu kitateketea na hakutakuwa tena na ushahidi wowote” akasema Gosu Gosu “Guys kabla hatujaondoka kuna kitu ambacho lazima mkifahamu.Tumefanikiwa kuipata kompyuta ya Tamar lakini kompyuta hii ili ifunguke nywila yake ni jicho la kulia la Tamar.Tutafanyaje kuifungua?akauliza Sandra.Gosu Gosu hakupoteza muda akachomoa kisu na kuondoa jicho la kulia la Tamar akalifunga katika kitambaa.Sandra alitetemeka kwa woga.Hakuwahi kushuhudia jambo kama lile Baada ya kila kitu kukamilika Tamar akatolewa ndani ya nyumba akaingizwa ndani ya gari lake nyumba ikawashwa moto kisha waondoka ***************** “Guys poleni sana.Mambo yamekwendaje huko?akauliza Agatha baada ya akina Gosu Gosu kurejea “Mambo yamekwenda vizuri.Tumepata tulichokihitaji,tumeipata kompyuta ya Tamar na vitu vingine kadhaa” akasema Gosu Gosu “Where is she?akauliza Agatha “She’s gone” akajibu Gosu Gosu na sura ya Agatha ikabadilika akalengwa na machozi “Agatha utalia baadae right now we still have job to do” akasema Gosu Gosu wakaingia ndani katika ofisi yao. “Jamani usiku wa leo umekuwa mfupi sana lakini wenye mafanikio kwa upande wetu.Kikubwa tulichokuwa tunakitafuta tumefanikiwa kukipata ambacho ni kompyuta hii ya Tamar.Kitu cha kwanza ambacho tunatakiwa kukifanya ni kuzitafuta rekodi zile za Rais na kuzifuta kabisa halafu tutaanza kumchunguza mahusiano yake na balozi Benjamin wa umoja wa Ulaya aliyeuawa” akasema Austin Agatha akaitambua kompyuta ile ya Tamar ambayo huhifadhi zile rekodi ikawashwa na kutakiwa kuingiza nywila.Gosu Gosu akalifungua lile jicho la Tamar kutoka katika kitambaa na kulielekeza katika kompyuta ile ikafunguka. “Mlimuondoa jicho lake?akauliza Agatha kwa mshangao “Agatha jielekeze katika kazi ! akasema Gosu Gosu Agatha akalitafuta faili lile linalohifadhi rekodi za Rais akalipata “Nimelipata” akasema Agatha na kuwaonyesha wenzake “Hatuna haja ya kusikiliza mazungumzo ya rais lifute moja kwa moja” akasema Austin “Kwa nini tusihifadhi katika diski na kumuonyesha Rais kitu tulichokifanya?Lazima ajue kwamba hayuko salama na ili atuamini lazima tumuonyeshe kile kilichokuwa kimefanywa na Tamar” akasema Gosu Gosu “That’s a good idea.Tufanye hivyo” akasema Austin na faili lile likahifadhiwa katika diski mweko na kufutwa kabisa katika kompyuta ya Tamar huku wote wakishuhudia http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Congraturations guys.Our president is safe now” akasema Austin “Tujipongeze kwa hatua hii kubwa tuliyopiga lakini kazi ndiyo kwanza imeanza.Tamar alikuwa na mahusiano na balozi Benjamin na ndiye aliyempa rekodi zile za mazungumzo ya Rais.Tunatakiwa kujua nini mipango yao? Je ni Tamar ndiye aliyekuwa akimpatia balozi Benjamin siri mbali mbali za nchi?Kama ndiyo kwa nini? Swali lingine tunalohitaji kulitafutia majawabu nani waliomuua balozi Benjamin Hudson?Bado tunayo kazi kubwa mbele yetu” akasema Gosu Gosu “Ni kweli tunayo kazi kubwa ya kufanya lakini kwa muda huu uliobaki kabla ya mapambazuko tupumzishe miili yetu halafu kesho tutajua wapi pa kuanzia”akasema Austin “Mimi sintalala,nataka nizipitie kompyuta hizi kila faili nifanyie uchunguzi kila kitu ili tujue kila kilichomo” akasema Sandra “I’ll stay here with her” akasema Gosu Gosu “Thank you” akasema Sandra.Agatha na Austin kila mmoja akaenda chumbani kwake kupumzika wakawaacha Gosu Gosu na Sandra sebuleni.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog