Simulizi : Siri
Sehemu Ya Tano (5)
Ndege waliyopanda akina Gosu Gosu ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kisha ikapaa kuendelea na safari ya kulekea Nairobi Kenya.Devotha aliyekuwa amekaa upande wa dirishani alionekana kutabasamu muda wote “You are always smilling” Gosu Gosu aliyekuwa amekaa pembeni ya Devotha akaanzisha maongezi.Devotha akageuka na kumtazama Gosu Gosu “Hivi ndivyo nilivyo.Kila wakati sura yangu inatabasamu hata nikifa bado nitaendelea kutabasamu” akasema Devotha na kumfanya Gosu Gosu naye atabasamu “Nadra sana kukuona ukitabasamu Papii” akasema Devotha akitoa kicheko cha chini chini “Natabasamu kwa sehemu muhimu tu na nimeanza kutabasamu hivi karibuni.Kabla ya hapo sijawahi kuweka tabasamu usoni pangu.Sira yangu imekaa kikazi zaidi” akasema Gosu Gosu “Ngoja nikufundishe kitu Papii,jifunze na jizoeshe kutabasamu kila wakati.Tabasamu linaficha mengi na linaepusha mengi.Tabasamu ni silaha kubwa ya ushindi” akasema Devotha na kutazama nje akaendelea kutabasamu “What a beautiful country! Akasema halafu mara tabasamu likapotea usoni pake.Bado Gosu Gosu alikuwa amegeuza shingo yake akimuangalia “Umeona nini?Mbona tabasamu limepotea ghafla?akauliza “Kuna wazo limenijia, ni vipi kama sintarudi tena nyumbani?What if I die there?akauliza Devotha “That won’t happen.We’ll all come home together.I’ll protect you” akasema Gosu Gosu kwa sauti ndogo ili watu wasisikie maongezi yao.Devotha akamtazama akatabasamu tena “Gosu Gosu you are a killer but to me you are so sweet.So soft.Why?akauliza Devotha lakini Gosu Gosu akajifanya kama vile hajasikia alichoulizwa “Umesemaje? “Nilipokabwa na Mathew ulikuja ukaniokoa.Sikutegemea kama ungesimama kunitetea kwani ninyi ni washirika.Kwa nini ulinisaidia?Kwa nini ulimzuia Mathew?Devotha akauliza “Hivyo ndivyo nilivyo.Nina sura mbili.Kuna wakati ninakuwa shetani na kuna wakati ninakuwa malaika” akajibu Gosu Gosu na Devotha akatoa kicheko kidogo. “Wewe na Mathew ni watu ambao ni vigumu sana kuwaelewa.Mathew anaonekana ni mkatili sana lakini kuna wakati anakuwa mpole.By the way where is your family? “Family? “Ndiyo” “Sina familia”akajibu Gosu Gosu “Huna familia? “Ndiyo.Sina mke,sina watoto sina mpenzi.Familia yangu mimi ni Mathew na Ruby hao ndio watu wangu wa karibu wanaonijali na ndio ndugu zangu” “You and Ruby why you worship Mathew so much like he’s you God?akauliza Devotha “You don’t know him yet.Once you know him well I hope you’ll worship him as well” akajibu Gosu Gosu.Devotha akainamisha kichwa kidogo akafikiri halafu akauliza “Mathew na Ruby ni wapenzi? “Sifahamu kama wana mahusiano hayo kwani mimi nimefahamiana nao tayari wakiwa marafiki” “Mke wa Mathew yuko wapi? “Mke wa Mathew anaishi Ufaransa.Mbona unaonekana kutaka kumfahamu sana Mathew? Gosu Gosu akauliza “Ndiyo ninataka kumfahamu.Ni mtu ambaye amenishangaza sana kwa mambo anayoyafanya ndiyo maana ninataka kumjua ni mtu wa aina gani”akajibu Devotha “Mathew hapendi kuchunguzwa so let’s not talk about him.Vipi kuhusu wewe una mume na watoto? Akauliza Gosu Gosu na muhudumu akapita na torori lililojaa vinywaji Devotha akachukua glasi ya mvinyo unaotengenezwa Dodoma akanywa funda moja halafu akatabasamu “Mvinyo bora kabisa huu unaotengenezwa na zabibu ya hapa hapa nyumbani” akasema Devotha “Devotha nilikuuliza swali naomba unijibu” “Sina mume wala watoto na sijawahi kufikiria kuwa na mume” “Kwa nini?Gosu Gosu akauliza “Sitaki mume.Sitaki kuwa chini ya mwanaume.Ninao uwezo wa kufanya yale yote anayoyafanya mwanaume.I can shoot and kill,I can give men orders and they obey hivyo sina haja ya kuwa na mwanaume ambaye ataniweka chini yake.I want to control not to be controlled you understand me? Akauliza Devotha “Nimekutana na wanawake kama wewe vitani ambao walikuwa na mawazo kama yako lakini siku zote mwanamke atabaki kuwa chini ya mwanaume.Mathew amenifanya nikakutana na watu mbali mbali na mmoja wao ni mchungaji Crintson Davis ambaye amenisaidia sana kunitoa katika dunia niliyokuwepo na kuanza kujifunza neno la Mungu.Nitakutolea mifano michache.Katika 1 Wakorinto 11:9 maandiko yanasema " Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume." Tukirudi katika kitabu cha mwanzao 2:18 Bwana Mungu akasema si vyema huyo mtu awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”.Maandiko haya mawili ni mfano tu kwamba siku zote mwanamke atakuwa chini ya mwanaume.Ukisema kwamba hutaki kuwa chini ya mwanaume unakwenda kinyume na maandiko na unamkosoa aliyekuumba mwanamke” akasema Gosu Gosu na Devotha akatabasamu “Gosu Gosu unaonekana wewe bado u mchanga sana katika maandiko.Biblia hiyo hiyo imeonyesha nguvu kubwa aliyonayo mwanamke.Tukianzia na hapo hapo ulipoishia.Mungu alimuumba mwanamke baada ya kuona kwamba wajibu aliompa mwanaume katu asingeweza kuutekeleza ndipo akamleta mwanamke.Mwanaume ni dhaifu bila mwanamke na mimi siwezi kuongozwa na kiumbe dhaifu wakati nimepewa nguvu kubwa.Si nguvu ya misuli bali nguvu ya ndani.Mwanamke ndiye aliyeiharibu dunia kwa kula tunda alilokatazwa na Mungu.Unadhani kwa nini shetani aliamua kumfuata na kumshawishi mwanamke kula tunda?Ni kwa sababu aliifahamu nguvu yake kwamba anao uwezo wa kumfanya mwanaume afanye kitu chochote.Sitaki kwenda ndani zaidi lakini mwanamke ni kiongozi wa mwanaume.Atakaloliamua mwanamke mwanaume hawezi akalipinga.Hiyo ni nguvu kubwa sana aliyopewa mwanamke” “Hizo ni dharau kwa wanaume Devotha ! akasema Gosu Gosu ambaye hakupendezwa na maneno yale ya Devotha “Gosu Gosu wanaume ninawaheshimu lakini si kuwa chini yao na kuwaacha wawe na maamuzi katika kila jambo” “Kwa maneno hayo unataka kuniambia kwamba wewe hautaolewa katika maisha yako yote? “Don’t you get it Papii? Sitaki kuwa chini ya mwanaume.Nikiolewa nitakuwa chini ya mwanaume ambaye atataka kunitawala na mimi sitaki kutawaliwa ninataka nitawale.Kama nikimpata mwanaume ambaye atakubali kuwa chini yangu nimtawale niwe na maamuzi ya mwisho ndani ya nyumba nitakuwa tayari kuolewa” akasema Devotha “Mwanaume wa aina hiyo utasubiri sana.Siku zote katika ndoa mwanaume ndiye kichwa cha nyumba.Ukitaka wewe kuwa kichwa utasubiri sana na yawezekana utaishi hivyo kwa maisha yako yote” “I don’t care.Hata kama nikiishi mwenyewe kwa maisha yangu yote hakuna ubaya.Isitoshe mwili wangu huu mzuri sitaki uanze kuharibiwa kushikwa shikwa hovyo kutumikishwa kingono na mwishowe nianze kuchujuka.Sitaki hilo” akasema Devotha “Ni hicho tu ndicho kinakuogopesha kutumikishwa na mwanaume? “Papii nimekwambia ninataka kuwa mtawala na si mtawaliwa.I wish ningekuwa na….”akasema Devotha na kunyamaza “Ungekuwa na nini?akauliza Gosu Gosu “Ningekuwa na sehemu za siri za mwanaume..” “Ah ! don’t go there.Huko unakotaka kuelekea si kuzuri hata kidogo.Wewe ni mwanamke na utabaki kuwa mwanamke.Jikubali ! akasema Gosu Gosu kwa sauti ya ukali kidogo halafu kukawa kimya “Gosu Gosu umechukia? “Maneno ulioyasema hayajanifurahisha mimi kama mwanaume” ‘I’m sorry lakini huo ni ukweli Papii.Sipendi kutawaliwa ninataka nitawale niwe na sauti.Ninafikiria hata siku moja niwe Rais wa nchi” akasema Devotha na Gosu Gosu akatoa kicheko kidogo “Mbona unacheka Gosu Gosu siwezi kuwa Rais?Ninapenda sana uongozi kuwa na sauti” “Devotha nieleze ukweli katika maisha yako hujawahi kuwa na mwanaume? “You’ve been so nice to me hivyo nitakuwa mkweli kwako.Nimewahi kuwa na wanaume kadhaa kwa ajili ya kujifurahisha tu lakini si kwa ajili ya mapenzi lakini katika wanaume wote ambao nimetembea nao sijawahi kufurahia hilo tendo hata mara moja.Ninaona kama vile ninakereka tu” “Kutokana na uzuri wako mwanaume ambaye unaweza ukatoka naye ni yule mwenye wadhifa au mwenye pesa ambaye kwake pesa na kazi ndivyo vipaumbele na ndiyo maana wakashindwa kukuridhisha na wakasababisha utuone wanaume wote hatuna maana.You need to try with a rough man like me,I swear you’ll forget your name ! akasema Gosu Gosu na kumfanya Devotha aangue kicheko kikubwa hadi abiria wengine wakageuka kumtazama. “Kitu gani kimekufurahisha?akauliza Gosu Gosu “Umenifurahisha sana Papii.You can’t afford me hata kwa mfano.Mimi na wewe hatuendani.Ni kama mafuta na maji”akasema Devotha “Devotha I need to sleep.Usiku mzima wa jana sijalala naomba nitumie dakika chache tulizonazo kabla ya kufika Nairobi nijipumzishe” akasema Gosu Gosu na kufumba macho. “Katika wanawake wote wa hii dunia kwa nini moyo wangu umemuangukia Devotha? Ni mara ya kwanza nimejikuta nikimpenda mwanamke lakini mwanamke mwenyewe ambaye moyo wangu umemuangukia ana utata mkubwa ila sikati tamaa nitahakikisha ninampata Devotha.Mimi ni mpiganaji nitapigana pia katika hili hadi nihakikishe anatua mikononi mwangu.Kinachotakiwa hapa ni kumbadili mtazamo wake na kumfanya ahitaji kupendwa” akawaza Gosu Gosu
Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.Abiria walishuka na miongoni mwao walikuwemo Gosu Gosu,Tino na Devotha.Gosu Gosu ndiye aliyekuwa wa kwanza kukamilisha taratibu za uhamiaji, akawasubiri wenzake nje na wote walipokamilisha na kuingia nchini Kenya wakachukua taksi na kumuomba Dereva awapeleke Sadena hoteli.Ni moja kati ya hoteli kubwa ya nyota tano jijini Nairobi.Tino na Devotha walionekana kulifahamu vyema jiji la Nairobi tofauti na Gosu Gosu ambaye alikuwa kimya akitazama nje. Sadena hoteli walipokewa vizuri na wahudumu.Gosu Gosu na Tino wakachukua chumba kimoja kikubwa na Devotha akachukua chumba chake peke yake.Wahudumu wakawasindikika hadi katika vyumba vyao.Baada ya kuonyeshwa vyumba vyao wote wakakutana na kuanza kupanga mikakati. “Tayari tumefika Nairobi na hakuna kupoteza muda tunaanza kazi.Devotha wewe ndiye tunayekutegemea sana katika vipi mipango yako? akasema Gosu Gosu “Mpango uko namna hii,nitawasiliana na Avi mkuu wa Mossad afrika Mashariki na kupanga kuonana naye hapa hotelini.Zitafungwa kamera katika chumba change na mtakuwa mkifuatilia kile kitakachokuwa kinaendelea chumbani kwangu.Namfahamu Avi ana udhaifu mkubwa kwa wanawake,nitampa vishawishi ili tufanye mapenzi.Wakati mimi nikifanya naye mapenzi mmoja ataingia ndani na kupekua mavazi ya Avi .Tunachokitafuta ni kadi anayoitumia kuingilia ofisini kwake.Tutachukua taarifa zote za muhimu za kadi hiyo na tutatengeneza kadi ambayo itatusaidia kuingia ndani ya ubalozi wakati wa operesheni.Zoezi la kuchukua taarifa za muhimu katika hiyo kadi likimalizika kadi itarudishwa na mlango ugongwe mara mbili haraka haraka nitajua kazi imekalika na mimi nitaingia katika awamu ya pili ambayo nitamtaka Avi anipeleke katika ubalozi wa Israel nikaonane na Edger Kaka na kujua mahala alipo.Nitakuwa nimevaa kamera ndogo ya siri ambayo itawezesha ninyi kuipata ramani kamili ya mahala alipo Edger Kaka.Kama mpango huu ukifanikiwa basi tutakuwa tumerahisisha sana kazi yetu” akasema Devotha “Ni mpango mzuri sana tuombe ufanikiwe.Na kama ikishindikana una plani nyingine? Akauliza Gosu Gosu na Devotha akatabasamu “Nina plani zaidi ya mia moja kichwani msiwe na wasiwasi” akasema Devotha “Vizuri sasa.Kwa ajili ya zoezi hilo tunahitaji kupata vifaa muhimu vya kutuwezesha kulifanikisha.Nina watu wangu hapa Nairobi ambao watanisaidia kupata vifaa mbali mbali tutakavyovihitaji katika zoezi hilo na vile vile usisahau kuwajulisha watu wa Dar es salaam kama tumefika salama” akasema Tino na kutoka akaenda mapokezi kuomba huduma ya gari.Hoteli hii ya Sadena hutoa huduma ya usafiri kwa wageni wake wanaotaka kuzunguka sehemu mbali mbali za jiji la Nairobi.Tino analifahamu vyema jiji la Nairobi hivyo hakuhitaji dereva alipewa gari akaondoka mwenyewe. Baada ya Tino kuondoka,Devotha akaenda chumbani kwake akachukua simu ambayo ni maalum kwa mawasiliano na Mossad pale anapokuwa nje ya Dar es salaam akaiwasha na kupiga namba Fulani akatakiwa kutaja namba zake za utambulisho akazitaja na baada ya sekunde kadhaa sauti ya mwanamke ikasema “Karibu sana Devotha jijini Nairobi.Nikusaidie nini tafadhali? “Ninataka kuzungumza na mkurugenzi Avi Abramson” akasema Devotha na kutakiwa kusubiri sekunde chache aunganishwe.Zilipita sekunde hamsini na sauti ya kiume ikasikika “Devotha habari yako?Nimeshangaa kuambiwa uko Nairobi.Mbona umekuja bila kutoa taarifa? “Dr Yonathan Cohen hajakujulisha kuhusu ujio wangu? “Hapana hajanipa taarifa zozote kama unakuja Kenya” “Dr Yonathan anafahamu kuhusu safari yangu ya dharura nchini Kenya na nilitegemea akujulishe” akasema Devotha “Hakijaharibika kitu.Yawezekana ametingwa na mambo mengi ndiyo maana hajanijulisha.Nikusaidie nini Devotha?Uko hapa kwa shughuli gani? “Kikubwa kilichonileta hapa ni kuonana nawe Avi” “Unataka kuonana nami? “Ndiyo ninataka kuonana nawe.Nina mazungumzo ya muhimu mno nawe” akasema Devotha “Haikuwezekana kunipigia simu tukazungumza hadi uamue kuja mwenyewe Nairobi?akauliza Avi “Ndiyo Avi nimeamua kuja mwenyewe kuzungumza nawe ana kwa ana kwa kuwa suala lenyewe ni kubwa na hatuwezi kuzungumza simuni” akasema Devotha “Umefikia wapi hapa Nairobi? “Nimefikia Sadena hotel chumba 204” “Unataka tukutane wapi na saa ngapi?akauliza Avi “Nifuate hapa katika chumba changu saa kumi na moja za jioni kwa sasa nahitaji kupumzika.Ukifika mlangoni gonga mara moja halafu subiri kidogo gonga tena mara mbili halafu subiri kidogo kisha gonga mara tatu nitajua ni wewe” “Sawa Devotha nitafika hapo” “Ahsante” akasema Devotha na kukata simu halafu akamfuata Gosu Gosu “Kila kitu tayari.Avi atafika hapa saa kumi na moja za jioni naamini hadi wakati huo maandalizi yote yatakuwa yamekamilika” akasema Devotha wakaendelea na mazungumzo mengine Katika ubalozi wa Israel,Avi Abramson mkuu wa Mossad katika ukanda wa afrika mashariki na kati alibaki na maswali mengi kichwani kwake baada ya kumaliza kuzungumza na Devotha.Kikubwa kilichokula akili yake ni kile kilichompeleka Devotha Nairobi.Mara akainua mkono wa simu ya mezani na kumpigia Dr Yonathan jijini Dar es salaam.Baada ya kusalimiana Avi akauliza “Dr Yonathan nimekupigia kukujulisha kwamba nimetoka kuzungumza na Devotha muda mfupi uliopita yuko hapa Nairobi.Ulifahamu kuhusu safari yake ya Nairobi? “Utanisamehe sana kwa kutokujulisha mapema Avi.Ni kweli ninazo taarifa zake.Aliondoka hapa mchana wa leo akiwa na Fishel na Ehud wakaelekea Arusha kuna uchunguzi wanakwenda kuufanya lakini aliniambia kwamba akifika Kilimanjaro atawaacha akina Ehud waelekee Arusha na yeye ataunganisha na ndege hadi Nairobi anataka kuonana nawe halafu atarejea tena Arusha kuendelea na uchunguzi wanaoufanya na akina Ehud”akasema Dr Yonathan “Alikueleza sababu ya kunifuata Nairobi?akauliza Avi “Hapana hakunieleza sababu yoyote lakini anaonekana ana jambo kubwa anataka kuzungumza nawe.Nahisi ni kuhusiana na suala la Olivia” “Vipi kazi niliyowatuma akina Fishel inakwendaje? Akauliza Fishel “Kila kitu kinakwenda vyema na Devotha atakupa maelezo ya kutosha kuhusu suala hilo” akasema Dr Yonathan “Ahsante Dr Cohen naamini nitafahamu mengi pale nitakapokutana na Devotha baadae”akasema Avi na kuagana na Dr Yonathan.
Tino alirejea hotelini akiwa ameongozana na mtu mwingine.Akamtambulisha mtu Yule kwa akina Gosu Gosu kuwa anaitwa Abdallah ni mtaalamu wa masuala ya mawasiliano.Mtu Yule ambaye alionekana si muongeaji sana alianza kusaidiana na Tino kufunga kamera katika chumba cha Devotha.Walifunga kamera nne ndani ya chumba kile ambazo zote ziliunganishwa na kompyuta iliyokuwemo katika chumba cha akina Gosu Gosu.Picha kutoka chumbani kwa Devotha zikaanza kuonekana.Wote wakazihakiki na kufanya marekebisho kidogo halafu kila kitu kikakaa sawa.Katika chumba cha akina Gosu Gosu kulikuwa na kompyuta tatu.Moja iliunganishwa kamera na nyingine mbili zilikuwa kwa ajili ya kazi nyingine.Abdallah baada ya kumaliza kazi yake akaaga na kuondoka Tino akamsindikiza na baada ya dakika chache akarejea chumbani “Abdallah ni mmoja wa marafiki zangu walioko hapa jijini Nairobi.Ni mtaalamu sana wa mambo ya mawasiliano.Kwa sasa ofisi imekamilika na kinachofuata ni kujiunganisha na Dar es salaam ili nao waweze kufuatilia kila kinachoendelea hapa” akasema Tino na kumpigia simu Mathew “Tino habari za Nairobi? Umekwisha rejea?Nilijulishwa na Devotha ulikuwa umetoka kidogo” “Ndiyo nilikuwa nimetoka kidogo nilikwenda kufuatilia vifaa na tayari tumekwisha tengeneza ofisi kilichobaki ni kujiunga nanyi huko ili muweze kufuatilia kila kinachoendelea hapa” akasema Tino kisha akaanza kufuata maelekezo ya Ruby na baada ya dakika chache tayari wakawa wamejiunga na akina Mathew Dar es salaam. “Good job guys.Mmekuwa na mwanzo mzuri nawatakia kila la heri pale mtakapokuwa tayari mtatujulisha” akasema Mathew
Saa kumi na moja na dakika ishirini na nane mkurugenzi wa Mossad ukanda wa Afrika Mashariki Avi Abramson akawasili Sadena hotel.Ndani ya gari alikuwa na dereva pamoja na mlinzi wake mmoja ambao aliwataka wabaki garini yeye akashuka na kuelekea ndani ya hoteli akapanda lifti hadi ghorofa ya tano akakitafuta chumba 204 akagonga kama alivyoelekezwa.Mlango ukafunguliwa na Devotha aliyekuwa amevaa gauni jepesi ambalo liliweza kuyaonyesha hadi mavaziya ndani.Kwa sekunde kadhaa Avi alibaki amesimama mlangoni akimshangaa Devotha.Hakuwa ametarajia kumkuta akiwa katika hali ile “Avi karibu ndani ” akasema Devotha “Devotha..” akasema Avi akionekana kuendelea kumshangaa “Samahani nilikuwa ninajiandaa kwenda kuoga sikutegemea kama ungeweza kuja mida hii.Umewahi sana” “Tulikubaliana tukutane saa kumi na moja jioni na nilipotoka kazini nimekuja moja kwa moja hapa” akasema Avi “Karibu naomba unisubiri nikaoge kwanza.Utatumia kinywaji gani? Akauliza Devotha huku akilitikisa umbo lake na kuzidi kumpagawisha Avi “Kitu chochote ulichonacho humu ndani nitatumia malaika wangu” akasema Avi Devotha akaenda katika kabati akachukua chupa ya mvinyo akaiweka mezani na kumuwekea David katika glasi. “Devotha U mrembo sana” akasema Avi akiwa na tabasamu pana sana.Devotha naye akatabasamu “Devotha hakuna ubaya wowote tukiendelea kuzungumza ukiwa katika mavazi hayo.Ninafurahi sana kuliona umbo lako zuri.Mungu amekujalia uzuri wa kipekee kabisa.Ninamshukuru na kumsifu kwa uumbaji huu uliotukuka” akasema Avi akiwa katika tabasamu pana sana “Ouh Avi” akasema Devotha akiilegeza sauti yake na kuwa laini sana “Kweli kabisa Devotha.Uzuri wako si wa kawaida” akasema Avi na Devotha akabaki amesimama akitabasamu “Ahsante sana Avi.Nisubiri dakika mbili nikaoge” akasema Devotha na kuanza kupiga hatua kuelekea katika mlango wa chumba cha kulala na mara tu alipokishika kitasa akageuka na kumtazama Avi ambaye bado alikuwa anamtazama kwa uchu. “Ungependa kuoga nami Avi?akauliza huku kidole kimoja akiwa amekiweka mdomoni.Avi akatabasamu na kubabaika “Ninakutania Avi” akasema Devotha akitoa kicheko kidogo “Hakuna tatizo Devotha.Kuna mtu yeyote unayemtegemea hapa kuja mida hii?akauliza Avi “Hakuna ninayemtegemea.Hapa Nairobi nimekuja kuonana nawe pekee sina miadi na mtu mwingine” akasema Devotha na Avi akasimama akavua koti “Basi hakuna tatizo nitajumuika nawe.Hakuna mwanaume anayeweza kukataa ombi la kuoga na malaika kama wewe” akasema Avi huku akivua shati haraka haraka na kulitupa katika sofa akaufungua mkanda wa suruali lakini akasita halafu akapiga hatua kuelekea mlangoni akaufunga mlango kwa funguo halafu akavua suruali na kubakiwa na nguo ya ndani “Niko tayari malaika wangu” akasema Avi na kumfuata Devotha bafuni.Devotha akafungua mkanda wa ile nguo laini aliyokuwa ameivaa akaiachia ikaanguka chini akabaki amevaa mavazi ya ndani.Kitendo kile kilileta vurugu ikulu kwa Avi ambako kulichachamaa na kufura kwa hasira.Devotha huku akitabasamu akamtaka Avi amsaidie kuifungua sidiria yake kwa nyuma.Wakati Avi akimfungua akayagusisha makalio yake kwa makusudi ikulu kwa Avi. “Kwisha habari yake.Nikiwaambia viumbe hawa ni wadhaifu wanakasirika lakini huo ndio ukweli angalia macho yanavyomtoka Avi mwili wote unamchemka kama ningekuwa na nia ya kumuua ningemtoa roho yake sasa hivi” akawaza Devotha halafu akamshika mkono Avi wakaingia bafuni wakakaa katika beseni kubwa la kuogea. “Tunahitaji mvinyo” akasema Devotha akitaka kuinuka “Usiinuke Devotha nielekeze nikachukue” akasema Avi na kutoka ndani ya maji akaenda kuchukua chupa ya mvinyo wakaendelea kuoga huku wakipata mvinyo.Mkono wa kulia wa Devotha ulikuwa ukiisugua sugua ikulu ya Avi ambaye alifumba macho kwa raha alizohisi.Mara akakumbuka kitu “Devotha karibu sana Nairobi.Nimefurahi kukuona japo ujio wako umekuwa wa ghafla sana” “Hata mimi sikuwa nimetarajia kama ningekuja Nairobi lakini imenilazimu kuja kwa dharura” “Nini hasa sababu ya kuja Nairobi?Kuna tatizo gani? “Usihofu Avi nitakueleza kila kitu lakini kwanza tu…” akasema Devotha huku akiinuka na Avi akajua alichokitaka Devotha.Hakumpa nafasi na kumaliza sentensi yake akamkamata sawa sawa na mtanange ukaanza bafuni. Tino na Gosu Gosu walikuwa wakishuhudia kila kinachoendelea katika chumba cha Devotha kupitia kamera wakiwa chumbani kwao.Akina Mathew Dar es salaam nao pia walikuwa wanashuhudia pia kinachoendelea Nairobi “Ni muda wa kuingia kuichukua kadi” akaelekeza Mathew baada ya kuona Devotha na Avi wakiwa wamezama mapenzini.Tino akatoka ndani ya chumba chao akatazama pande zote kulikuwa kimya akaenda katika mlango akaingiza vitu Fulani katika kitasa akaanza kukichokonoa na ndani ya muda mfupi akafanikiwa kufungua kitasa akakinyonga na taratibu akaingia ndani.Moja kwa moja akaenda katika mavazi ya Avi yaliyokuwa sofani akalichukua koti akaanza kulipekua na katika mfuko wa ndani wa koti akaikuta kadi waliyokuwa wanaitafuta. “Hiyo ndiyo kadi tunayoitafuta” akasema Ruby ambaye naye alikuwa akishuhudia kila kitu akiwa na Mathew Dar es salaam.Taratibu Tino akatoka ndani ya kile chumba cha Devotha akarejea katika chumba chao “Good job Tino” akasema Mathew Katika kamera bado mtanange ulikuwa unaendelea bafuni.Devotha aliendelea kumpeleka Avi vilivyo. Baada ya kuipata ile kadi kazi ikaanza na usukani akaushika Ruby akiwa Dar es salaam.Tino akaanza kufuata maelekezo aliyopewa na Ruby akaingiza kadi ile katika kifaa Fulani kilichounganishwa na kompyuta ambacho kilimuwezesha Ruby kuweza kupata taarifa alizozihitaji kutoka katika ile kadi.Baada ya dakika saba akamtaka Tino aitoe kadi ile. “Guys kazi yetu tumeimaliza nimepata taarifa zote ninazozihitaji katika hiyo kadi sasa mnaweza kuirejesha” akasema Ruby.Tino akichukua kadi ile na kuirejesha katika chumba cha Devotha,baada ya kutoka akagonga mlango mara mbili kama alivyokuwa ameelekeza Devotha halafu akaelekea chumbani kwake.Akiwa bafuni Devotha alisikia mlango ukigongwa kama alivyokuwa ameelekeza mara moja akajua kazi imekwisha “Avi imetosha.Tutaendelea baadae kama ukitaka” akasema Devotha “Devotha mbona unaniacha kati kati?Tuendelee malaika wangu” akasema Avi huku akitweta “Usijali Avi tutaendelea hata baadae lakini kwanza nataka tuzungumze kile kilichonileta hapa Nairobi” akasema Devotha na kutoka ndani ya lile beseni la kuogea akajifuta maji.Avi alibaki anashangaa lakini Devotha akamtaka atoke ndani ya maji “Sawa Devotha tuzungumze kile kilichokuleta Kenya.Kuna tatizo gani? Kwa nini umetaka kuniona?akauliza Avi huku akivaa mavazi yake “Avi usiku wa jana nilikutana na watu wako wawili uliowatuma Tanzania Fishel na Ehud.Walinieleza kile kilichowaleta Tanzania kwamba ni kuandaa operesheni ya kumtafuta Olivia ambaye ametekwa na watu wasiojulikana na mpaka sasa bado vyombo vyote vinaendelea kumsaka ikiwemo na idara yangu lakini bado hatujampata.Ili niweze kuwasaidia kuandaa operesheni yao nilitaka kwanza kufahamu sababu ya Mossad kumtafuta Olivia.Fishel na Ehud walilazimika kunieleza sababu ya kumtafuta Olivia.Walinipa siri kubwa ambayo sikuwa nikiifahamu kuwa Edger Kaka ambaye aliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani ambaye sisi sote tunaamini alifariki dunia katika ajali,yuko hai” akasema Devotha na sura ya Avi ikaonyesha mshangao mkubwa “Najua hili ni suala la siri kubwa lakini mimi kama mtu wenu ambaye mnanitumia katika masuala yenu mbali mbali sikupaswa kuwekwa gizani hadi ninakuja kufahamu hivi sasa”akasema Devotha “Devotha hukupaswa kufahamu jambo hili na hata hao waliokueleza wamefanya makosa makubwa mno kukupa taarifa hizi za siri” akasema Avi “Avi tayari nimekwisha fahamu siri hii na usiwalaumu sana watu wako kwani hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kunieleza ukweli ili niwasaidie nami nitawasaidia kumpata Olivia na ndiyo maana nimekuja hapa.Kikubwa kilichonileta kwako ninataka kuonana na Edger Kaka.Nataka nizungumze naye” akasema Devotha “Hilo haliwezekani Devotha.Edger yuko mahala pa siri na wanaoruhusiwa kuonana naye ni watu wachache tena maalum tu.Wewe hauko katika kundi hilo la watu wanaoweza kuonana na Edger Kaka”akasema Avi “Avi nafahamu Edger anazo taarifa nyeti sana mnazozitafuta na ili awape taarifa hizo lazima mumpate Olivia.Ili kumpata Olivia lazima nifanye mahojiano na Edger Kaka yeye anafahamu mahala alipo Olivia,anafahamu waliomteka” “Olivia ametekwa na IS?akauliza Avi “Tunahisi hivyo ndiyo maana ninataka kuhojiana naye.Edger anampenda Olivia na lazima atanipa ushirikiano wa kujua mahala alipo.Avi naomba unipe dakika tano tu nizungumze na Edger na ninakuahidi Olivia atapatikana” akasema Devotha na Avi akazama mawazoni huku akiendelea kumtazama Devotha “Avi nisingeweza kuja hapa kama sina uhakika wa hiki ninachokuomba.Tafadhali naomba unipe dakika tano tu za kuzungumza na Edger Kaka na ninakuhakikishia zitakuwa na msaada mkubwa sana” akasema Devotha lakini Avi alionekana kuwa na wasi wasi na kumuangalia Devotha kwa macho makali. “Huyu jamaa tayari ameonyesha wasiwasi.Kuna kitu amekihisi kuhusu Devotha.Guys we need to get in there fast.Tukichelewa Devotha atakuwa katika hatari kubwa! akasema Gosu Gosu “Wait ! akasema Mathew “Mathew Devotha yuko katika hatar…” “Ninasema subiri Gosu Gosu.She knows what she’s doing” akasema Mathew “Devotha nataka uniambie ukweli nani aliyekupa taarifa za Edger Kaka?akauliza Avi “Nimekwambia Avi taarifa hizo nimezipata kutoka kwa watu uliowatuma kwangu niwasaidie kumpata Olivia Fishel na Ehud”akajibu Devotha “Hapana si kweli.Fishel na Ehud ni majasusi wakubwa sana na wanafahamu umuhimu wa siri hii ambayo hata watu wengi ndani ya Mossad hawaifahamu na majasusi wetu wamekula kiapo cha kutokutoa siri zozote.Nataka uniambie ukweli aliyekupa taarifa hizi” akasema Avi Devotha akawa kimya akimtazama “Nijibu Devotha,nani amekupa siri hii? Akauliza Avi “Avi najua unawaamini sana watu wako lakini ni mimi ndiye niliyewafanya hadi wakavunja kiapo chao na kunipa siri hii kwani sikuwa tayari kuwasaidia kumpata Olivia kama wasingenieleza sababu ya kumtafuta.Kama ni lawama mimi ndiye ninastahili.Avi kwa nini usinipeleke mara moja nikaonana na Edger Kaka halafu tutakuja kuendelea pale tulipoishia?akasema Devotha na kumfuata Avi akaanza kuchezea maeneo ya ikulu “Devotha una uhakika kwamba Edger anaweza kuwa na msaada katika kumtafuta Olivia?akauliza “Nisingeweza kuja hapa Nairobi kama nisingekuwa na uhakika Avi.Naomba dakika tano tu na nitakuwa na jibu mahala alipo Olivia.Edger anafahamu kila kitu” akasema Devotha “Lakini Edger amekaa ndani kwa miaka mitatu sasa hafahamu chochote kinachoendelea huko nje na kikubwa zaidi hafahamu chochote kuhusu kutekwa kwa Olivia Themba” akasema Avi “Avi niamini ninachokwambia.Nisingewez a kupoteza nauli yangu kutoka Dar es salaam kuja hapa Nairobi kama nisingekuwa na uhakika kwamba Edger anaweza akasaidia kupatikana kwa Olivia” akasema Devotha “Devotha vipi kuhusu serikali yako,una hakika hawataweza kugundua kama tunamtafuta Olivia? “Usihofu hawataweza kufahamu chochote” akajibu Devotha.Avi akamtazama kwa makini halafu akasema “Sawa nitakupa dakika tano tu za kuzungumza naye lakini hii ni siri kubwa na ninaomba upate majibu ya mahala alipo Olivia.Jambo lingine ni kwamba hii ni siri kubwa na asifahamu mtu mwingine jambo hili.Tukigundua kwamba umetoa siri tutakuua.Umenielewa? akauliza Avi na kusimama “Ahsante sana Avi” akasema Devotha “Tusipoteze muda twende mara moja” akasema Avi wakatoka mle ndani.Devotha alikuwa amevaa suti ya kijivu na kifuani upande wa kushoto aliweka ua jekundu ambalo kati kati yake kulikuwa na kamera ndogo ambayo ingewawezesha wenzake kufuatilia kile kinachoendelea ndani ya ubalozi wa Israel MPENZI MSOMAJI - DEVOTHA ATAFANIKIWA KUONANA NA EDGER KAKA? - OPERESHENI YA KUVAMIA UBALOZI WA ISRAEL ITAFINIKIWA? - NINI HATIMA YA OLIVIA NA COLETHA? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII
Gari la Avi Abramson mkuu wa Mossad ukanda wa Afrika Mashariki lilikaribia kufika katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi akatoa simu na kupiga akazungumza na mtu simuni akamtaka azime kamera zote za ulinzi ubalozini hapo kwa muda wa dakika kumi na tano. Gari lilifika getini na kwa haraka walinzi wakafungua geti na kuingia ndani ya jengo la ubalozi.Mlinzi wa Avi akawahi kushuka garini na kuangaza pande zote kama kuna hatari yoyote halafu akamfungulia mkuu wake mlango wa gari Avi akashuka.Bila kuonekana Devotha akabonyeza ile kamera aliyoivaa katika koti lake naye akafunguliwa mlango akashuka. Mara tu Devotha alipobonyeza kamera,akina Gosu Gosu waliokuwa ndani ya chumba cha hoteli Sadena wakaanza kupata picha. “She’s in”akasema Tino na kuwajulisha akina Mathew Dar es salaam waliokuwa wanafuatilia kila kinachoendelea Nairobi “Good job” akasema Mathew Baada ya kushuka garini Avi akamuita Devotha pembeni “Nimeelekeza kamera zote zizimwe kwa muda wa dakika kumi na tano ili uweze kuonana na Edger.Sitaki mtu yeyote afahamu kama nimekuleta hapa ukaonana naye.Naomba tusipoteze muda twe….” Akasema Avi “Avi kabla hatujaenda huko una hakika mtu uliyemuelekeza azime kamera kweli amezima kamera zote? Akauliza “Nina uhakika amezima.Kwa nini umeuliza? “Yawezekana akajiuliza maswali mengi kwa nini kamera zote katika jengo hili zizimwe? Anaweza akapata ushawishi wa kuacha baadhi ya kamera ili ajue kinachoendelea.Nakushauri ufanye uhakiki kama kweli kamera zote zimezimwa ili yasije kutokea matatizo kwa upande wako baada ya mimi kuondoka” akasema Devotha “Ninawaamini watu wangu lakini ulilolisema lina msingi yawezekana kweli mtu niliyemuelekeza azime kamera akataka kuchunguza kujua nini kinaendelea” akasema Avi na kumtaka Devotha amfuate wakaelekea ofisini kwake akawasha kompyuta yake.Kulikuwa na sehemu ya kuweka namba za siri na Devotha akaielekeza kamera yake makusudi katika kompyuta ya Avi ili wenzake wanaoendelea kumfuatilia wazione namba zile za siri atakazoandika Avi.Huu ulikuwa ni ujanja wa Devotha kumleta Avi ofisini kwake ili waweze kuipata namba ya siri anayoitumia kuingia katika mtandao wao.Avi akabonyeza kompyuta yake na kujiridhisha kamera zote zilikuwa zimezimwa. “Kamera zote zimezima” akasema Avi huku akizima kompyuta yake “Ni vyema umejiridhisha” akasema Devotha wakatoka nahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kuelekea mahala aliko Edger kaka Timu ya akina Mathew waliokuwa wakimfuatilia Devotha walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanaipata vyema ramani ya njia ya kupita kuelekea mahala alikofichwa Edger Kaka. Avi alitumia kadi yake kufungulia mlango mkubwa wakaanza kushuka ngazi kuelekea chini ya jengo hadi walipofika katika lango lingine kubwa akalifungua kwa kutumia kadi ile ile wakatokea katika sebule nzuri yenye sofa za kuvutia. “Hapa ndipo anapoishi Edger Kaka” akasema Avi na kwenda kuufungua mlango mwingine akaingia Devotha akamfuata.Ndani ya chumba kile kulikuwa na kitanda kikubwa ambacho alikuwa amelala mtu mmoja aliyedhoofu sana. “Edger unaendeleaje?akauliza Avi “Naendelea vyema.Kuna taarifa zozote umeniletea?Olivia amepatikana?akauliza Edger “Nimekuletea mgeni.Atajitambulisha yeye ni nani na kwa nini yuko hapa” akasema Avi na kumgeukia Devotha akamnong’oneza sikioni “Una dakika tano tu za kuzungumza naye,usithubutu kufanya kitu chochote cha kijinga” akasema Avi na kutoka akaufunga mlango.Devotha akachukua kiti akaketi.Edger alikuwa anamshangaa hakuwahi kumuona hapo kabla “Edger kaka”akasema Devotha “Wewe ni nani?Unataka nini?akauliza Edger ambaye bado sauti yake ilikuwa dhaifu “Naitwa Devotha ninatokea Tanzania”akasema Devotha na kumstua Edger “Tanzania?akauliza “Ndiyo” akajibu Devotha na woga mkubwa ulionekana machoni pa Edger “Umefahamuje kama niko hapa?akauliza Edger “Ninafanya kazi na Mossad hivyo ninafahamu kila kinachoendelea na kwa nini uko hapa.Nimepewa dakika tano tu za kuzungumza nawe hivyo nataka kujielekeza moja kwa moja katika suala la msingi lililonileta kwako” akasema Devotha na kumkazia macho Edger “Hivi sasa nchini Tanzania shirika la ujasusi la Israel Mossad,wanaandaa operesheni kubwa ya kumtafuta Dr Olivia Themba ambaye ametekwa na watu wasiojulikana.Ili uweze kuwapa Mossad taarifa za muhimu wanazozitafuta kuhusu mtandao wenu wa IS,umeelekeza wahakikishe wanamtafuta na kumpata Olivia.Mimi ndiye wakala wa Mossad nchini Tanzania na operesheni nzima ya kumtafuta Olivia inaniegemea mimi.Katika uchunguzi wetu wa awali tumebaini kwamba Olivia ametekwa na watu wa mtandao wako wa IS hivyo nimekuja kwako kukuomba utoe ushirikiano ili tuweze kumpata Olivia” akasema Devotha “Olivia ametekwa na watu wa IS?akauliza Edger “Ndiyo ametekwa na IS.Kama ulimaanisha ulichokisema kuwa Olivia ni mwanamke pekee unayempenda ,huu ni wakati wako wa kutoa ushirikiano mkubwa ili tuweze kumuokoa kutoka katika mikono ya IS” akasema Devotha “Kwa nini IS wamteke Olivia Themba?akauliza Edger “Mimi siwezi kuwa na jibu lakini wewe unafahamu kila kitu kwa nini wamteke Olivia” “Sifahamu chochote dada yangu.Nimekaa mahala hapa ambapo sijui ni wapi kwa muda wa miaka mitatu na sielewi chochote kinachoendelea huko nje.Siwezi kujua sababu ya IS kumteka Olivia” “Edger umekuwa hapa kwa muda wa miaka mitatu na katika muda huo wote watu wako wa IS hawajui kama uko hai hivyo hakuna yeyote atakayekusaidia.Unapaswa kuyapigania maisha yako wewe mwenyewe.Umeanza vyema kwa kuahidi kueleza kila kitu japo umetoa masharti ya kupata Olivia ninakuahidi tutampata lakini nataka utupe ushirikiano mkubwa katika hilo kwani Olivia kama nilivyokuelea anashikiliwa na watu wa mtandao wako.Nataka unipe orodha ya watu walio katika mtandao wa IS nchini Tanzania ambao unamini wanaweza kuwa wanahusika na kutekwa kwa Olivia Themba” akasema Devotha “Sifahamu mtu yeyote wa IS Dar es salaam” akajibu Edger “Edger ulikiri mwenyewe kwamba unampenda Olivia,huu ni wakati wako wa kulithibitisha hilo kwa kutoa taarifa ambazo zitasaidia kumpata.Waliomteka ni wenzako wa IS na yawezekana lengo lao ni kumuua.Kama kweli unampenda Olivia nipe majina ya watu walio katika mtandao wa IS nchini Tanzania ili tuweze kumuokoa Olivia” akasema Devotha “Dada yangu sifahamu mtu yeyote ambaye anashirikiana na IS nchini Tanzania” akajibu Edger na Devotha akamtazama kwa hasira “Edger unaonyesha wazi kwamba maneno yale uliyoyasema kwamba unampenda Olivia si maneno ya kweli bali ulikuwa ni uongo.Huna mapenzi yoyote kwa Olivia kwani kama ungekuwa unampenda ungedhihirisha hilo kwa kutoa taarifa ambazo zingesaidia kumuokoa kutoka katika mikono ya watu ambao hatujui lengo lao ni nini kwake.Edger Olivia alikuokoa pale ulipowekewa sumu kwa sasa yuko matatizoni ni wakati wako na wewe kuhakikisha unamsaidia kuyaokoa maisha yake kama alivyofanya kwako” akasema Devotha.Edger hakujibu kitu aliendelea kumtazama Devotha “Edger muda wangu unakwisha tafadhali naomba unijibu ili tuweze kumuokoa Olivia ambaye hastahili kupitia mateso kama haya anayoyapitia hivi sasa” akasema Devotha lakini bado Edger aliendelea kuwa kimya.Mlango ukagongwa. “Edger muda wangu umekwisha.Nitakapotoa mguu wangu ndani ya chumba hiki bila kupata jibu lako naomba ufahamu kuwa hakutakuwa na uwezekano tena wa kumpata Olivia.IS are going to kill her !! akasema Devotha.Bado Edger aliendelea kuwa kimya.Devotha akainuka “Edger nina sekunde chache zimebaki nieleze tafadhali! Akasema Devotha “Sifahamu mtu yeyote” akajibu Edger.Devotha akamtazama kwa hasira na kumfuata pale kitandani akamshika na kumuinua lakini kabla hajafanya chochote Avi akaingia “Devotha !! akasema Avi na Devotha akamuachia Edger “Muda umekwisha.Twende tuondoke” akasema Avi “Olivia akifariki dunia damu yake itakuwa juu yako” akasema Devotha kwa ukali na kutoka ndani ya kile chumba “Muda nilioelekeza kamera kuzimwa umekaribia kumalizika hivyo unapaswa kuwa tayari umetoka ndani ya jengo pale kamera zitakapowashwa” akasema Avi huku wakitembea haraka haraka kutoka ndani ya jengo wakaingia katika gari la Avi na kuondoka katika ubalozi wa Israel. Hakukuwa na mazungumzo garini baada ya kuondoka katika ubalozi wa Israel hadi walipofika Sadena hotel.Avi na Devotha wakashuka garini wakaelekea chumbani. “Umepata ulichokuwa unakitafuta kwa Edger Kaka?akauliza Avi “Hapana sikufanikiwa kupata chochote muda ulionipa wa kuzungumza naye ni mdogo sana” akasema Devotha “Nafahamu ni muda mfupi lakini ulipaswa kuutumia kikamilifu na kuweza kupata taarifa kutoka kwa Edger.Devotha hata kama ningekupa masaa manne ya kuzungumza naye Edger asingeweza kukueleza chochote.Kama ameweza kukaa kwa muda wa miaka mitatu bila kuzungumza chochote usingeweza kupata chochote kutoka kwake kwa muda wa dakika tano” akasema Avi “Edger alikuwa karibu sana kufunguka.Kwa ajili ya Olivia yuko tayari kueleza kitu chochote.Ungenipa muda zaidi wa kuzungumza naye nakuhakikishia ningeweza kupata kile nilichokuwa nakitafuta kwake” “Devotha unapaswa ushukuru kwa hata dakika zile chache nilizokupatia ukaweza kuonana na Edger Kaka.Kuna watu wako ndani ya ubalozi wetu hawafahamu kama kuna mtu anaitwa Edger ameishi pale ndani kwa miaka mitatu” “Ninalifahamu hilo Avi lakini kama ningeweza kupata nafasi nyingine ya kuzungumza naye nina uhakika mkubwa wa kuweza kupata kile ninachokitafuta” “Devotha hakutakuwa na nafasi nyingine tena ya kuonana na Edger kaka na ninaomba hiki tulichokifanya kibaki kuwa siri kwani ikijulikana ni mimi nitakuwa katika matatizo makubwa.Naomba uitunze siri hii” akaomba Avi “Usijali Avi.Ninafahamu umuhimu wa siri hii kubwa na ninakuhakikishia nitakwenda nayo kaburini” akasema Devotha “Kwa sasa baada ya kukosa taarifa kutoka kwa Edger nini mipango yako ya kumpata Olivia? Akauliza Avi “Bado yapo matumaini makubwa.Kuna taarifa fulani tunazifuatilia jijini Arusha ambako niliwaacha Fishel na Ehud.Nikitoka hapa ninakwenda kuungana nao.Nina uhakika taarifa hizo zinaweza kutupa mwanga.Usihofu Avi lazima tutampata Olivia” akasema Devotha na kwenda kumkalia Avi mapajani “Avi nimemaliza kile kilichonileta Nairobi japo sijafanikiwa lakini nimejaribu.Unataka tuendelee pale tulipoishia?akauliza Devotha huku akikuna kidevu cha Avi na kumfanya atabasamu halafu akaanza kumfungua tai yake akamuinamia na kumbusu. “Unasemaje Avi tuendelee?akauliza Devotha akiendelea kumbusu Avi “Mhh ! Avi akaguna “Unasemaje Avi?Unahitaji tuendelee pale tulipoishia?Nataka nikuonyeshe namna wanawake wa kiafrika wanavyoyafahamu mapenzi” akasema Devotha akiendelea kumfanyia uchokozi Avi ambaye tayari damu ilikuwa inamchemka.Akamvua koti na kulitupa pembeni akaanza kumvua shati.Avi mashetani yake yakampanda akajikuta akiufungua mkanda wa suruali yake akaivua na kuitupa sakafuni.Akamvuta Devotha na kuanza kumbusu akamfungua vifungo vya koti,Devotha akainuka akamshika mkono Avi akamuongoza hadi katika chumba cha kulala na kumlaza kitandani akamvua nguo ya ndani na kuanza kufanya utundu mkubwa ikulu kwa Avi kwa kutumia ulimi wake halafu akambusu Avi na kusema “Avi ninahitaji kupata vinywaji nisubiri dakika mbili nikachukue kinywaji nikipendacho halafu nitarejea” akasema Devptha “Kwa nini usiwapigie simu walete kinywaji hicho hapa hapa chumbani?HUna haja ya kwenda wewe mwenyewe” akasema Avi “Ngoja nikachukue mwenyewe nirudi haraka.Wahudumu wanaweza wakachelewa kuja na mimi huwa ninapata starehe sana nikinywa kinywaji nikipendacho.Nipe dakika mbili tu” akasema Devotha na kumbusu Avi kisha akatoka na kwa haraka akaingia katika chumba cha akina Gosu Gosu “Mambo yanakwendaje huku? Mmefuatilia kila kitu?akauliza Devotha “Devotha umefanya kazi nzuri.Tumekufuatilia kila ulichokifanya” akasema Gosu Gosu na mara katika picha za kamera Avi akaonekana akiishika simu yake “Guys Avi ameishika simu yake kuweni makini kufuatilia kile anachokizungumza” akasema Mathew na wote wakageukia runinga kumtazama Avi “Ongeza sauti tusikie kile anachokizungumza” akasema Mathew na Tino akaongeza sauti “Hallow Nabil” akasema Avi baada ya mtu aliyempigia kupokea simu.Baada ya sekunde chache akasema “Nabil kuna kazi ambayo nataka uifanye usiku wa leo.Kuna mwanamke mmoja ametoka Tanzania nataka kumkata pumzi usiku wa leo.Nitakupa maelekezo baadae kidogo anza kujiandaa” akasema Avi na kukata simu. “Guys Avi hajafurahishwa na kitendo cha Devotha kufahamu siri yao na kuonana na Edger Kaka na sasa anasuka mpango wa kumuua.Siri hii ya Edger Kaka kuwepokatika ubalozi wao hawataki ijulikane.Devotha umefanya kazi nzuri sana.Kwa sasa wote tuna uhakika Edger Kaka yuko hai na tumethibitisha hilo.Baada ya kufahamu mpango wa Avi kumuua Devotha kuna mambo mawili ambayo lazima tuyafanye” akanyamaza kidogo na kusema. “Tunatakiwa kuhakikisha Avi,mlinzi na dereva wake hawatoki salama ndani ya hoteli.Tunatakiwa kuwaua wote.Devotha utarejea ndani ya chumba chako na kumtaka Avi awapigie simu watu wake aliowaacha ndani ya gari ambao ni dereva na mlinzi wake ili waweze kupata kinywaji wakati wewe ukiendelea kumstarehesha.Akiwapigia utawafuata utawachukua na kuwapeleka katika chumba cha akina Gosu Gosu.Wakiingia humo waueni wote na atabaki Avi peke yake hiyo itakuwa ni kazi ya Devotha kummaliza.Kabla ya saa tatu usiku wa leo watu hao wawe wameuawa.Gosu Gosu unajua namna ya kufanya baada ya kuwaua watu hao.Tino ni mwenyeji hapo Nairobi atakusaidia namna ya kuihifadhi miili ya watu hao isionekane” akasema Mathew “Sawa Mathew nimekuelewa”akasema Gosu Gosu “Jambo la pili,baada ya kuwaua hao jamaa,Tino utachukua gari la Avi na utakwenda katika ubalozi wa Israel.Wanalifahamu gari la Avi wakiliona watakuruhusu kupita getini na kama kutakuwa na tatizo lolote waambie wapige simu ya Avi ambayo itaunganishwa na mfumo wetu na Ruby ataipokea na kuzungumza na hao jamaa kwa kutumia sauti ya Avi ambayo imerekodiwa.Ukivuka geti tutakuongoza kuelekea katika ofisi ya Avi kwani tayari tumeipata ramani muda ule alipokuwa na Devotha.Tunataka kuingia katika mtandao wa Mossad ili tuweze kupata taarifa zote za muhimu zitakazotuwezesha kufanikisha operesheni yetu.Ukishaingia katika ofisi hiyo Ruby atakupa maelekezo nini cha kufanya.Nadhani mmenielewa” akasema Mathew. “Tumekuelewa Mathew,hakuna muda wa kupoteza mimi ngoja nirejee chumbani nikamshawishi ili awapigie simu watu wake kule garini” akasema Devotha “Devotha kuwa makini sana ili Avi asigundue kwamba tayari tunafahamu kile anachotaka kukifanya” akasema Mathew “Niko makini usihofu” akasema Devotha kisha akatoka katika kile chumba na kurejea tena chumbani kwake akamfuata Avi pale kitandani ambaye alikuwa mtupu akambusu “Mbona umerejea bila vinywaji?akauliza Avi huku akiuchezea uume wake “Avi kuna kitu kimenirudisha” “Kitu gani?akauliza Avi “Umewaacha ndani ya gari mlinzi na dereva wako wanakusubiri na hawajui utatoka humu ndani saa ngapi.Haipendezi wakati sisi tunastarehe wao waendelee kupigwa na baridi ndani ya gari.Itapendeza kama tukiwatafutia sehemu nao waweze kupata nafasi ya kupumzika wakati sisi tunaendelea na mambo yetu”akasema Devotha “Usihofu Devotha watanisubiri hata kama nikitoka saa tisa usiku,ni kazi yao” akasema Avi “Avi nakubali ni kazi yao lakini wakati mwingine tuwe na ubinadamu.Kuna ubaya gani wakati sisi tukistarehe wao wakiendelea kupata kinywaji na chakula cha jioni?Yawezekana ukatoka humu saa nne za usiku.Muda huo wote watakuwa garini wanakusubiri?Wapigie simu tafadhali wajulishe kwamba ninakwenda kuwachukua ili wapate kinywaji kidogo wakati sisi tunastarehe.Avi unajua kunikuna na ninataka nikupe vitu adimu sana leo hadi umsahau mke wako”akasema Devotha na kumbusu Avi akamletea simu yake.Avi akaweka dole gumba simu ikafunguka akampigia mlinzi wake akamjulisha kwamba kuna mtu anakwenda kuwachukua ili wapate kinywaji kwani yeye atachelewa kidogo “Ahsante Avi.Umefanya jambo jema ninawafuata sasa hivi ili nao waendelee kuburudika kwa vinywaji” akasema Devotha na kutoka akashuka chini hadi katika maegesho ya magari akagonga mlango wa gari kioo kikashushwa “Amewapigia simu Avi? Twendeni mkapumzike kidogo mpate chakula na vinywaji kuna sehemu mmeandaliwa.Avi atachelewa kidogo” akasema Devotha wale jamaa hawakuwa na wasiwasi kwani wamekwisha pewa ruhusa na mkuu wao wakashuka garini na kumfuata Devotha wakaelekea ndani.Moja kwa moja akawapeleka hadi katika chumba cha akina Gosu Gosu akakiminya kitasa na kuufungua mlango “Karibuni ndani”akasema Devotha David Kioko dereva wa Avi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani ya kile chumba ambamo aliwakuta Gosu Gosu na Tino “Karibu kaka” akasema Tino na kulazimisha tabasamu usoni.Mlinzi wa Avi naye akapiga hatua kuingia ndani ya kile chumba lakini alipochunghulia ndani akasita kuingia.Devotha aliyekuwa nyuma yake kwa kasi ya umeme akamrukia teke kali la mgongo Yule jamaa akaangukia ndani.Gosu Gosu aliyekuwa karibu na mlango alimpokea Yule mlinzi wa Avi kwa ngumi nzito iliyompeleka chini kisha akamtandika tena teke zito la uso na Yule jamaa akaanza kutoa damu mdomoni.Gosu Gosu akatoa bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti “Msiniue jamani ! akasema dereva aliyekuwa akitetemeka lakini Gosu Gosu hakupoteza muda akaizinga bastora yake na kuachia risasi tatu akimlenga kifuani Yule mlinzi wa Avi. “Ndugu zangu msiniue nawaomba sana” akaomba Yule dereva lakini masikio ya Gosu Gosu yalikuwa yameziba akaachia risasi kadhaa na Yule dereva akaanguka sakafuni.Gosu Gosu akawavuta akawaingiza chooni akawapekua na kuchukua simu zao zote akazizima kabisa kisha akafuta damu iliyosambaa pale sebuleni. “Kazi nzuri Gosu Gosu,Devotha usichukue muda mrefu nenda kaendelee na sehemu yako.Tino jiandae uelekee katika ubalozi wa Israel hapo muachie Gosu Gosu ataendelea kumlinda Devotha”akaelekeza Mathew. Devotha akatoka na kurejea katika chumba chake “Tayari wanapata chakula na kinywaji.Sisi tuendelee”akasema Devotha akivua koti lake “Ahsante Devotha una roho nzuri sana.Ngoja niwakumbushe wasinywe kupitiliza sintakawia sana hapa” akasema Avi na kuchukua simu yake lakini Devotha akamshika mkono na kuichukua simu akaitupa pembeni. “Usiwasumbue Avi wale ni watu wazima wanafahamu wanachotakiwa kukifanya.Waache nao waburudike kidogo” akasema Devotha na kuanza kumporomoshea mabusu mfululizo na taratibu Avi akazidiwa na kipute kikaanza. Tino alitoka chumbani kwao akaufungua taratibu mlango wa chumba cha Devotha na kuingia sebuleni akapekua mavazi ya Avi akachukua kadi ya Avi ya kufungulia milango halafu akatoka na kurejea chumbani kwao akachukua funguo za gari akaenda maegesho akalitafuta gari la Avi akaingia na kuondoka kuelekea katika ubalozi wa Marekani akiwa ameweka kifaa cha mawasiliano sikioni ili aweze kuwasiliana na akina Mathew “I’m on move” akasema Tino “Tunakufuatilia Tino” akasema Mathew.Tayari kiza kilikwisha ingia Hotelini chumbani kwa Devotha kipute kilikiwa kinaendelea na Devotha alimpeleka Avi vilivyo.Hadi mzunguko mmoja ulipomalizika Avi alikuwa hoi akihema kama mkimbiaji wa mbio ndefu.Devotha akamuacha pale chumbani amelala kitandani akaenda sebuleni akatazama kamera.Hii ilikuwa ni ishara kwa akina Gosu Gosu “Gosu Gosu hakuna kupoteza muda ni wakatiwa kummaliza Avi ” akaelekeza Mathew na Gosu Gosu ambaye sura yake ilikuwa imejikunja kwa hasira akaificha bastora yake kiunoni akachungulia nje hakukuwa na mtu akaenda katika mlango wa chumba cha Devotha akakiminya kitasa taratibu na mlango ukafunguka akamkuta Devotha sebuleni akichomoa bastora yake akanyata na kuingia chumbani akamkuta Avi amelala kitandani hoi.Kijiusingizi kilianza kumpitia “Hey ! Gosu Gosu akamstua Avi alistuka akainua kichwa akajikuta akitazamana na bastora.Alitaka kuinuka lakini alichelewa kwani kidole cha Gosu Gosu tayari kilikwisha izinga bastora na risasi zikatoka na kuzama kifuani kwa Avi.Gosu Gosu aliyeonekana kuwa na hasira kali alimchakaza Avi kwa risasi hadi zilipomalizika katika bastora. “Papii imetosha,tayari amekufa ! akasema Devotha aliyekuwa amesimama mlangoni akishuhudia Gosu Gosu akifanya mauaji yale “Mfiche bafuni tutamuondoa baadae” akasema Gosu Gosu na kutoka mle chumbani “Ama kweli safari hii nimekutana na watu wa aina yake.Gosu Gosu ni muuaji hata macho yake yanaonyesha kwake kutoa roho ya mtu ni kitu chepesi mno.Ilitosha kumuua Avi kwa risasi mbili lakini amemimina risasi zote katika bastora yake.Kuna nyakati hata mimi ninaogopa sana kuwa karibuna watu hawa?akawaza Devotha akamvuta Avi toka kitandani akampeleka bafuni akampekua na kuchukua kila kitu alichokuwa nacho kisha akatoka na kwenda chumbani kwa Gosu Gosu. “Kazi nzuri Devotha.Kwa sasa tunasubiri Tino aingie ndani ya ubalozi.Anafanya jambo la hatari tumuombee arejee salama”akasema Mathew aliyekuwa akishuhudia kila kitu “Tino tupe mrejesho tafadhali” akasema Devotha “Ninakaribia kufika ubalozini nimechelewa njiani msongamano mkubwa sana jioni hii hapa Nairobi.Nitawajulisha kitakachoendelea” akasema Tino Alikaribia kufika katika geti la kuingilia ndani ya balozi akapewa ishara na walinzi ya kusimama akapunguza mwendo lakini walipogundua ni gari la Avi haraka haraka wakakimbia kufungua geti.Lilikuwa na vioo vyeusi hivyo hawakuweza kuona aliyekuwa ndani ya gari ni nani. “Guys I’m in.Nimepita getini bila taabu wakidhani ni Avi.Nahitaji maelekezo ya kufika katika ofisi ya Avi” akasema Tino “Safi sana Tino.Katika mzunguko fuata njia ya kushoto halafu utapinda kulia utaona kibao kimeandikwa VIP parking.Huko ndiko alikoegesha gari Avi wakati nimekwenda naye” akasema Devotha na Tino akafuata maelekezo aliyopewa akafika katika maegesho aliyoelekezwa “Tayari nimefika maegesho” akasema Tino “Shuka garini nenda katika mlango mkubwa utapitisha kadi mlango utafunguka utaingia ndania” akaelekeza Devotha. Tino akavuta pumzi ndefu nakusema “Pray for me guys” Akashuka garini na kuangaza pande zote kulikuwa kimya na ofisi chache zilikuwa zinawaka taa.Alipohakikisha hakuna tatizo lolote akatembea kwa kujiamini kuelekea katika mlango mkubwa akatoa kadi ya Avi akaipitisha na mlango ukafunguka akaingia ndani akakuta kuna lifti nne “Tayari nimeingia kuna lifti nne ninaziona” akasema Tino “Kuelekea ofisini kwake panda lifti ya kushoto kwako hadi ghorofa ya sita ndiko ziliko ofisi za Mossad.Ukishuka kwenye lifti fuata korido hadi chumba cha mwisho kabisa kwenye kona hiyo ndiyo ofisi ya Avi” akasema Devotha na Tino akaingia ndani ya lifti hadi ghorofa ya sita akashuka na kuanza kutembea kuelekea katika chumba cha mwisho kama alivyoelekezwa.Wakati akielekea katika ofiosi ya Avi mara mlango wa ofisi moja ukafunguliwa wakatoka jamaa wawili lakini Tino hakuwajali akajiamini na kupishana nao.Jamaa wale nao hawakumjali kabisa waliamini Tino ni mmoja wao kwani asingeweza kuingia katika ghorofa ile kama si muhusika wa Mossad. Alifika chumba cha mwisho ambacho ndicho ofisi ya Avi kwa mujibu wa maelekezo ya Devotha akapitisha kadi ile mlango ukafunguka akaingia ndani. Mara tu Tino alipoingia ndani ya ofisi ya Avi,katika chumba walimo Gosu Gosu na Devotha simu ya Avi ikaanza kutoa mlio. “Tino hebu jaribu kutoka ndani ya hicho chumba” akasema Devotha na Tino akatoka ndani ya kile chumba Mara tu Tino alipotoka ndani ya kile chumba ule mlio katika simu ya Avi ukakoma “Nadhani kuna muunganiko kati ya ofisi na simu ya Avi.Ulipofungua tu mlango simu ikaanza kutoa mlio ulipotoka ikaacha” akasema Devotha “Kuna kitu hata mimi nimekigundua ambacho si kawaida katika ofisi hii.Hakuna hewa na hakuna kitu chochote kinachowaka hata taa ya ndani haiwaki” “Ofisi hiyo” akasema Ruby akiwa Dar es salaam “Ina mfumo maalum ambao unamtambua Avi pekee na ndiyo maana wakati ule alipoingia na Devotha hakukuwa na tatizo lolote.Akiwa nje ya ofisi na mlango wa ofisi yake ukafunguliwa atajulishwa kwa kutumia simu yake ya mkononi iliyounganishwa na mfumo huo.Lazima iko namna ya kuweza kuufungua mfumo huo kwa kutumia simu ya Avi.Tino ingia tena katika hiyo ofisi na mlio ukianza katika simu ya Avi ichukue na ujaribu kuifungua uizime kengele ” akasema Ruby “Sawa nimekusikia Ruby” akasema Tino na kufungua tena mlango wa ofisi ya Avi akaingia ndani na simu ya Avi ikaanza tena kutoa mlio. “Devotha ichunguze simu hiyo ya Avi kwa haraka lazima kuna namna ya kuweza kuufungua mfumo” akasema Ruby na Devotha akaichunguza simu ile akakuta mahala kuna alama ya kuweka dole gumba Gosu Gosu akatoka mbio http://deusdeditmahunda.blogspot.com/akaenda chumbani kwa Devotha na kukata dole gumba la Avi kisha akaliweka katika ile sehemu inayohitaji dole gumba la Avi na mara simu ikafunguka na Devotha akapekua akaipata sehemu iliyoandikwa unlock the system akaibonyeza na ofisini kwa Avi taa zikawaka. “Tino nini kimetokea hapo?akauliza Devotha “Taa zimewaka” akasema Tino “Good sasa nataka uende katika kompyuta ya Avi uiwashe” akaelekeza Devotha na kwa haraka Tino akaenda katika kompyuta ya Avi akaiwasha na kukutana na sehemu inayomtaka aingize namba za siri.Ruby tayari alikuwa na namba za siri za kufungulia kompyuta ile ya Avi akamtajia Tino akaziingiza namba zile na kompyuta ya Avi ikafunguka. “Elekeza kamera yako katika kompyuta ya Avi” akasema Ruby na Tino akaelekeza kamera katika kompyuta ya Avi akaanza kumuelekeza namna ya kuiunganisha na kompyuta ndogo aliyokuwa nayo Tino.Haraka haraka Ruby akaanza kazi yake akiwa Dar es salaam huku akimuelekeza Tino kufanya mambo kadhaa katika kompyuta ile ya Avi.Baada ya muda wa dakika kadhaa mafaili yakaanza kuhamishwa kutoka katika kompyuta ya Avi kuingia katika kompyua ya Tino.Asilimia zilihesabu haraka haraka namna mafaili yalivyokuwa yakihama kutoka katika kompyuta ya Avi.Ilipofika asilimia mia moja Tino akaelekezwa kitu cha kufanya halafu akaizima ile kompyuta ya Avi akatoka ndani ya ile ofisi na kuufunga mlango akaanza kutembea kwa tahadhari hadi katika lifti akashuka na kuelekea maegesho alikoacha gari la Avi akaingia na kuondoka,akafunguliwa geti bila kuulizwa chochote walinzi wakidhani ni Avi ndiye aliyekuwamo ndani ya gari. “Nimetoka salama” akasema Tino “Kazi nzuri sana sasa rejea hotelini” akasema Mathew. Kabla ya kurejea hotelini Tino akapita kuchukua baadhi ya vifaa ambavyo aliagizwa na Gosu Gosu kisha akarejea hotelini. “Mathew tayari nimefika hotelini salama” Tino akawajulisha akina Mathew\ “Tino kazi nzuri sana.Sasa ni wakati wako Gosu Gosu unajua nini cha kufanya wakati Ruby akiendelea kupitia kile ambacho tumekipata kutoka katika kompyuta ya Avi.” akasema Mathew.Gosu Gosu akachukua vifaa alivyokuja navyo Tino ambavyo ni shoka dogo kali,panga na kisu kikubwa kikali na bila huruma akaanza kuikata kata miili ya dereva na mlinzi wa Avi ikafungwa vizuri katika mifuko ya nailoni na kuingizwa ndani ya masanduku makubwa akaenda pia chumbani kwa Devotha na kufanya hivyo pia kwa Avi halafu usafi mkubwa ukafanyika kabla ya miili ile iliyokuwa ndani ya masanduku kuondolewa mle hotelini.Gosu Gosu Anita wakayakokota masanduku yale matatu hadi katika lifti wakashuka chini wakatoka nje ya hoteli hadi katika gari la Avi.Tino alibaki nyuma ili kuhakiki usalama wa wenzake.Baada ya kuhakikisha wenzake wameingia garini na yale masanduku Tino naye akawafuata akaingia garini wakaondoka.Walielekea mtaa Fulani ambako Tino akawataka Gosu Gosu na Devotha wabaki garini yeye akashuka baada ya dakika kama kumi hivi akarejea akiwa na watu wengine wawili wakaingia garini na safari ikaanza wakaingia katika kiwanda kikubwa haraka haraka masanduku yale matatu yakashushwa kutoka garini watu wale wawili wakiongozana na Tino wakaingia ndani ya nyumba Fulani Gosu Gosu na Devotha wakabaki garini.Dakika ishirini zikapita Tino akarejea na wale jamaa wawili wakaingia garini na kuondoka pale kiwandani.Safari ilikuwa ya kimya kimya kurejea hotelini. DAR ES SALAAM “Mathew kupitia haya mafaili ambayo Tino ameyachukua katika kompyuta ya Avi tumefanikiwa kupata mambo mengi ya Mossad kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.Siri zao nyingi sasa tunazo.Tunayo orodha ya majasusi wote wa Mossad walioko eneo la Afrika Mashariki na kati na kusini.Orodha ya operesheni zao zote ,watu wanaowafuatilia na mambo mengine mengi lakini kikubwa ni kuipata ramani ya jengo zima la ubalozi na Israel nchini Kenya ambayo inaonyesha kila kitu kuanzia mfumo wote wa ulinzi,njia za dharura za kujiokoa endapo kumetokea shambulio,mahala zinapohifadhiwa silaha na mambo mengine mengi” akasema Ruby baada ya kumaliza kuyapitia mafaili ambayo waliyapata kutoka katika ofisi ya Avi. “Good job Ruby.Vijana wamefanya kazi kubwa sana kule Nairobi.Ramani hii ndiyo ambayo tulikuwa tunaitafuta sana na hatukujua kama tungeweza kuipata mapema namna hii hivyo basi usiku wa leo tunakwenda Nairobi kumchukua Edger Kaka” akasema Mathew “Usiku wa leo?akauliza Ruby “Ndiyo.Kila kitu kitamalizika usiku wa leo.Hatuna tena muda wa kuendelea kusubiri.Avi,dereva wake na mlinzi wote wameuawa na siku ya kesho wataanza kutafutwa na wasipopatikana tayari wataanza kuhisi wameuawa na kufanya operesheni yetu kuwa ngumu hivyo lazima tuhakikishe kila kitu kinamalizika usiku wa leo.Kikosi cha jeshi cha operesheni maalum ambacho tutashirikiana nacho kipo tayari muda wowote kwa kazi hivyo sioni sababu ya kuendelea kusubiri.Everything ends tonight and we’ll bring Edger Kaka home” akasema Mathew. “Mathew una hakika hakuhitajiki maandalizi zaidi kabla ya kuvamia ubalozi huo?akauliza Ruby “Ruby usihofu.Kikosi ambacho utashirikiana nacho ni kikosi hatari kabisa na wao muda wotewapo tayari kwa kazi hawahitaji maandalizi.Kikubwa kwao ni kujua wapi wanakwenda na kufanya nini.Tunayo ramani ambayo inatuongoza katika kila kitu hivyo hakuna haja ya kupoteza muda kufanya maandalizi.Tukitaka kuvuta muda zaidi tutatengeneza mazingira magumu.Avi ni mtu mkubwa na shughuli nyingi za Mossad zinamtegemea yeye,simu yake tumeizima na itakapofika asubuhi bado hapatikani simuni na hajulikani alipo wataanza kuingiwa na wasi wasi na juhudi za kumtafuta zitaanza mara moja na wasipompata hadi kufika kesho mchana wataamini amepatwa na jambo baya hivyo basi tahadhari kubwa itachukuliwa na kuifanya kazi ya kumchukua Edger kaka iwe ngumu ndiyo maana ninataka usiku wa leo operesheni hiyo imalizike.Sisi tuko tayari,kikosi kiko tayari,hakuna cha kusubiri” akasema Mathew na kuchukua simu akampigia Dr Evans “Mathew habari yako kijana wangu.Umekuwa kimya sana nini kinaendelea?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais kabla sijasema chochote nataka kufahamu kama wale jamaa wamekupigia simu siku ya leo” akasema Mathew “Hawajanipigia simu na hata mimi nashangaa kwa ukimya wao.Waliniahidi kunipigia simu kunipa maelekezo mengine ya nini wanakitaka lakini nashangaa mpaka sasa hawajawasiliana nami na hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui hali ya mwanangu ikoje.Nimejaribu kupiga namba zile walizotumia kunipigia hazipatikani.Nifanye nini Mathew? Akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais usiwe na hofu mwanao atakuwa salama.Hawatakubali mwanao afe watahakikisha kwa kila namna anakuwa mzima ili waweze kumtumia katika mabadilishano na Edger Kaka.Bado wanaamini kwamba wewe unafahamu mahala alipo Edger na ndiyo maana wanamshikilia mwanao hivyo basi watahakikisha kwa namna yoyote ile mwanao anakuwa salama na ndiyo maana wakamtaka kwanza Olivia ili aweze kumtibu virusi vile alivyomuambukiza” akasema Mathew “Mathew ahsante sana kwa kunipa moyo lakini yule ni mwanangu lazima niwe na wasi wasi.Ukimya wao unanipa mashaka sana kwamba yawezekana wanashindwa kuwasiliana nami kwa kuwa mwanangu tayari amefariki” “Tusiombe hayo yatokee mheshimiwa Rais,nina uhakika mkubwa kwamba mwanao atakuwa mzima kabisa.Nina uzoefu na hawa magaidi namna wanavyofanya operesheni zao na Coletha watakuwa wanamchunga sana kwa kila namna wawezavyo.” “Tuachane na hayo nataka kufahamu mmefikia wapi katika maandalizi yenu?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais nimekupigia kukujulisha kwamba timu niliyoituma kwenda Nairobi kufanya maandalizi ya operesheni,imefanya kazi nzuri na tayari tumefanikiwa kuipata ramani ya jengo la ubalozi na tayari tumefahamu mahala alipo fichwa Edger kaka na kikubwa zaidi sote tumefanikiwa kumuona na kuthibitisha kuwa ni yeye japo amedhoofu mno”akasema Mathew “Hongera sana Mathew na timu yako kwa kupiga hatua hiyo kubwa ndani muda mfupi.Sikutegemea kabisa kama mngeweza kulifanikisha jambo hilo mapema namna hii” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais,katika kuifanikisha kazi waliyotumwa watu wetu wamelazimika kutoa uhai wa watu watatu akiwemo mkuu wa Mossad Afrika mashariki na kati dereva wake na mlinzi.Mhshimiwa Rais naamini tumeupanua zaidi mgogoro huu lakini hakukuwa na namna nyingine ililazimu watu hao wauawe ili tupate tunachokihitaji” “Ni kweli Mathew hiki kilichofanyika kinaongeza mafuta kwenye moto lakini kama ilikuwa lazima watu hao wauawe ili tupate tunachokihitaji mimi sina tatizo.Kwa hiyo nini mipango yenu baada ya kupata mlichokuwa mnakihitaji? “Mheshimiwa Rais operesheni yetu ya kumchukua Edger Kaka inakwenda kufanyika usiku wa leo” “Usiku wa leo?akauliza Dr Evans kwa mshangao kidogo “Ndiyo mheshimiwa Rais lazima tuifanye usiku wa leo.Aliyeuawa ni mkuu wa Mossad Afrika Masjhariki hivyo asipopatikana hasi asubuhi ya kesho wataamini ameuawa hivyo kuifanyakazi ya kwenda kumchukua Edger kuwa ngumu ndiyo maana ninataka kila kitu kimalizike usiku wa leo” akasema Mathew “Mathew hatuwezi kuzungumza suala hili simuni nataka ufike hapa ikulu mara moja.Mmoja wa wasaidizi wangu ambaye nimemuweka hapo awasaidie atakuleta hapa ikulu mara moja” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa Rais” akajibu Mathew na Dr Evans akakata simu.Mathew akampigia Tino Nairobi “Tino mnaendeleaje huko? “Tunaendelea vyema Mathew.Tumetoka kumalizia kuiteketeza miili ya wale jamaa” “Good.Avi ni mtu muhimu sana kwa Mossad na lazima atatafutwa,mna hakika hawataweza kupatikana na kugundulika wameuawa?akauliza Mathew “Haitakuwa rahisi kupatikana kwani miili yao imetupiwa katika tanuru kubwa la moto na hivi tunavyoongea imekwisha kuwa majivu.Hakuna hat mfupa utakaoonekana” “Good.Tino nataka kuwapa mrejesho wa kile ambacho tumefanikiwa kukigundua kutoka katika yale mafaili tuliyoyachukua ofisini kwa Avi.Tumefanikiwa kupata siri nyingi za Mossad afrika mashariki lakini kikubwa tumefanikiwa kupata ramani ya jengo la ubalozi yenye kuonyesha kila kitu.Baada ya kuipata hiyo ramani hatuna tena muda wa kuendelea kusubiri hivyo basi tunakwenda kumchukua Edger Kaka usiku wa leo” “Usiku wa leo?akauliza Tino “Ndiyo Tino,usiku wa leo tutamaliza kila kitu na kuondoka Nairobi.Hamtakiwi kuwepo hapo Nairobi hadi kufika kesho asubuhi kwani Avi ataanza na ninyi ndiyowatu wa mwisho kuonekana naye hivyo mtakuwa katika hatari kubwa.Kila kitu kinakwenda kufanyika usiku wa leo kabla Avi hajaanza kutafutwa” akasema Mathew na kunyamaza baada ya mlango kufunguliwa akaingia mmoja wa wasaidizi wa Rais Mathew akamfanyia ishara asubiri dakika mbili “Tino ninakwenda kuonana na Rais muda si mrefu ili kupanga namna tutakavyotekeleza operesheni hii na baada ya kutoka huko nitawapa taarifa nini kinaendelea lakini kwa muda huu anzeni kujiandaa na hakikisheni mkiondoka hapo hotelini mnaacha kila kitu kiko salama.Kama kuna kamera za usalama hapo hotelini fanyeni kila namna mnayoweza kufuta kumbukumbu zote.Tino wewe unao utaalamu huo” akasema Mathew “Sawa Mathew tunaanza kujiandaa na utakapokuwa tayari utatujulisha mambo yanavyokwenda” akasema Tino na Mathew akakata simu akamuaga Ruby ambaye aliendelea kupitia mafaili yale waliyoyapata kutoka katika ofisi ya Avi akaingia katika gari na kupelekwa ikulu.
Mathew alifika ikulu akapokewa na kupelekwa mahala aliko Rais ambaye alikuwa na mtu mmoja aliyevaa sare maalum za jeshi. “Karibu sana Mathew Mulumbi” akasema Dr Evans “Ahsante sana mheshimiwa Rais”akajibu Mathew “Mathew kutana na mkuu wa kikosi cha operesheni maalum anaitwa Austin January”Dr Evans akafanya utambulisho Mathew akaonyesha mshangao kidogo “Austin January?akauliza “Ndiyo.Mbona umeshangaa? “Jina na sura hii si vigeni kwangu lakini sina kumbu kumbu tumewahi kuonana mahali.Nikumbushe tafadhali kama tumewahi kuonana sehemu Fulani” akasema Mathew “Hata mimi jina na sura yako si vigeni kwangu lakini kama ilivyo kwako hata mimi nahisi kukufahamu japo sijui tumewahi kuonana wapi” akasema Austin “Mtakumbushana baadae ni wapi mmewahi kukutana lakini kwa sasa tujielekeze katika kile kitu cha muhimu kilichotukutanisha hapa ila kwa kukusaidia Mathew ni kwamba Austin January amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi ya Taifa na alikuwa anaishi na kuendesha biashara zake nchini Afrika kusini lakini alipata misuko suko mikubwa kule alivamiwa shamba lake likachomwa mke na watoto wake kuuawa na ndipo serikali kwa kushirikiana na ubalozi wetu Afrika kusini wakamsaidia akarejea nyumbani salama ambako alianza upya maisha yake na kwa kuwa anafahamika sana kwa umahiri wake nililetewa mapendekezo ya kumjumisha katika kikosi cha jeshi kinachoshughulika na operesheni maalum na kwa sasa ndiye kiongozi wa kikosi hicho.Ninyi nyote mmewahi kufanya kazi idara moja ndiyo maana imekuwa rahisi kile mmoja kumkumbuka mwenzake.Mtaendelea kukumbushana taratibu” akasema DrEvans “Ahsante sana mheshimiwa Rais kwa kusaidia kunipa picha hii ndogo itanisaidia kukumbuka ni wapi mimi na Austin tumewahi kukutana” akasema Mathew “Austin,Mathew Mulumbi ana historia kama yako kwani naye aliwahi kupatwa na matatizo kama yaliyokupata ya kupoteza familia yake yote na ndipo alipoamua kuacha kabisa kazi ya ujasusi na kuanza kufanya biashara kwa sasa ni mfanya biashara mkubwa ni mmoja wa mabilionea wakubwa tulio nao hapa nchini lakini pamoja na hayo bado anaendelea kulitumikia taifa kila pale anapolazimika.Kwa ujumla ninafurahi kuwa na nchi yenye hazina kubwa ya vijana kama ninyi ambao wanaweza wakafanya kazi kubwa ya kulilinda taifa lao” akasema Dr Evans “Ninashukuru pia kukutana na Mathew Mulumbi.” akasema Austin “Mathew nimemuita Austin hapa na ninashukuru amefika kwa haraka kwani kikosi chake ndicho tutakachokitumia katika operesheni hii.Toka jana nilikwisha mpa maelekezo ya kuandaa kikosi cha watu kumi kwa ajili ya kufanya operesheni maalum lakini sikuwa nimemueleza kwa undani ni operesheni gani na inakwenda kufanyika wapi.Ninataka utumie nafasi hii kumpa picha pana kabisa ya kile kinachokwenda kufanyika na kwa nini tunahitaji kikosi chake” akasema Dr Evans. Mathew akaanza kumueleza Austin toka mwanzo wa sakata lile la kutekwa Olivia “Muda hautoshi kueleza kila kitu lakini kikubwa ni kwamba tulifanikiwa kufahamu kuwa Edger Kaka ambaye aliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ambaye alifariki katika ajali na kuzikwa miaka mitatu iliyopita,yuko hai.Israel wakitumia shirika lao la ujasusi la Mossad walitengeneza ajali ile na kutuaminisha Edger amefariki lakini kumbe ni mzima wamemficha Nairobi wakimuhoji kutaka kupata taarifa za mtandao wa IS .Inasadikiwa Edger Kaka ana mahusiano na kikundi cha IS” “Nimekuelewa vizuri Mathew.Ninapenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa jitihada zote ulizofanya hadi kulifikisha hapa hili jambo.Kama alivyoagiza Rais tayari kikosi cha watu kumi kimekwisha andaliwa na kiko tayari kwa kazi muda wowote tutakapopata maelekezo”akasema Austin “Ahsante Austin.Kwa sasa Edger amefichwa katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi na operesheni yetu tunayoiandaa ni kwenda kumchukua hapo ubalozini.Tukifanikiwa kumpata yeye tutaweza kuwapata Olivia na Coletha na vile vile tutapata taarifa za mtandao wa IS hapa nchini” “Mathew mimi na vijana wangu tuko tayari hata sasa kwa kazi tunahitaji maelekezo tu”akasema Austin “Ili kuweza kumchukua Edger Kaka ubalozini hapo ililazimu kwanza kuipata ramani ya jengo lote la ubalozi na kufahamu mfumo wote wa ulinzi ulivyo.Nilituma timu kwenda Nairobi kufanya kazi hiyo na tayari wameikamilisha kazi niliyowatuma.Tumeipata ramani ya jengo la ubalozi wa Israel nchini Kenya hivyo basi kilichobaki ni kuvamia ubalozini hapo usiku wa manane leo hii na kumchukua Edger Kaka kumrejesha nyumbani” akasema Mathew “Austin nadhani umemsikia Mathew na kumuelewa.Ninaamini vijana wako wamekwisha jiandaa kwa operesheni hii na mimi ninatoa ruhusa kwamba operesheni hiyo ifanyike.Ninataka Mathew na Austin sasa mkakae na mjadili kwa kina namna mtakavyoiendesha operesheni hii.Kama kuna kitu chochote ambacho mnadhani mtakihitaji kwangu mnijulishe haraka sana” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwa upande wangu kila kitu kutuwezesha kufanya operesheni hiyo tunacho”akasema Austin “Sawa Austin.Mathew tusiendelee kupoteza muda nataka niwaache wewe na Austin mkajadili namna ya kufanya operesheni hii.Mimi nitaendelea kuwasiliana nanyi mara kwa mara kujua maendeleo yenu” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais ninakushukuru sana kwa kutupa ruhusa kuifanya operesheni hii.Nitaendelea kuwasiliana nawe kukujulisha kila hatua tunayopiga.Ninakuhakikishi a kwamba tutarejea hapa nyumbani tukiwa na Edger Kaka.Kama wale jamaa watakupigia simu jitahidi kuvuta muda hadi pale tutakapokuwa tumerejea”akasema Mathew “Mathew hili mnalokwenda kulifanya ni jambo ambalo linaweza kuibua mgogoro mkubwa sana kwanza na majirani zetu Kenya na pili kwa marafiki zetu Israel endapo itagundulika kama ni sisi,hivyo nawaomba mjitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hakuna chochote kitakachoweza kututambulisha kwamba ni sisi ndio tuliofanya tukio hilo”akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais ninakuomba ondoa hofu kabisa kuhusu suala hili.Tayari tumekwisha chukua kila tahadhari kuhakikisha hatujulikani kama sisi ndio tuliovamia ubalozi na kumchukua Edger Kaka.Tunafanya hivi kwa ajili ya kujilinda sisi wenyewe na kuilinda nchi yetu” akasema Mathew “Kitu kingine ambacho tunatakiwa kukifanya ni kujiepusha kuua watu wengi bila sababu.Kama inawezekana tujitahidi kusiwe na idadi kubwa ya vifo” akasema Dr Evans “Tutajitahidi mzee kufuata maelekezo yako”akajibu Mathew “Sawa vijana wangu ninawaachia kila kitu na ninaamini mtafanya operesheni hii kizalendo kwa maslahi mapana ya nchi yetu na vile vile kusaidia kuwaokoa watu wetu wawili Coletha na Olivia.Ninawapa Baraka zangu na ninawatakia kila la heri” akasema Dr Evans na kusimama akapeana mikono na akina Mathew wakatoka. “Mathew tunaelekea katika kambi yetu ambako safari itaanzia hapo” akasema Austin wakaingia katika gari lake wakaondoka “Sikujua kama kuna viongozi ambao wanakuwa na sura mbili.Machoni wanaonekana wazalendo lakini kumbe ndani ni chui wakali.Nimesikitika sana kwa taarifa hii niliyoipata leo kuhusiana na Edger Kaka kujihusisha na kikundi cha kigaidi cha IS” akasema Austin “Mungu alifanya jambo kubwa sana la kutuficha kufahamu mawazo ya mwenzako vinginevyo tungekwisha malizana.Hakuna aliyetegemea kama Edger kaka angeweza kujihusisha na magaidi.Mpaka sasa bado hatujapata jibu nini hasa lilikuwa lengo la kuungana na magaidi hawa?Ni kujipatia fedha? Majibu haya yote tutayapata pale tutakapomtia mikononi” akasema Mathew na safari ikaendelea hadi walipofika katika kambi ya kikosi cha jeshi kinachoshughulika na operesheni maalum.Ilikuwa ni mara ya kwanza Mathew kuingia katika kambi hii nzuri.Austin akamuongoza wakaenda hadi katika chumba cha mipango ambako kulikuwa na watu sita,wote walisimama na kutoa heshima kwa mkuu wao halafu wakakaa. Kuta za chumba hiki zilijazwa runinga kubwa zenye kuonyesha picha mbali mbali.Kulikuwa na kompyuta nyingi na mitambo mbali mbali “Gentlemen tumepata mgeni lakini huyu si mgeni wa kawaida ni mgeni maalum kabisa anaitwa Mathew Mulumbi.Huyu ni mmoja kati ya majasusi nguli kabisa kuwahi kutokea hapa nchini kwetu na yuko hapa kwa sababu maalum hivyo msishangae kwa mara ya kwanza mtu ambaye si mwanajeshi kuingia katika chumba hiki.Huyu ni mwenzetu katika ulinzi wa taifa” akasema Austin na kumtambulisha Mathew wale makamanda waliokuwemo mle ndani. “Nilipigiwa simu na Rais jana usiku akanipa maelekezo niandae kikosi cha watu kumi kwa ajili ya operesheni ambayo atanifahamisha pale muda utakapofika.Nilifanya kama alivyonielekeza na usiku huu ameniita ikulu na kunifahamisha kwamba ile operesheni ambayo alinitaka niandae kikosi inakwenda kufanyika usiku huu.Mathew Mulumbi ambaye ndiye kiongozi wa operesheni hiyo maalum atawafafanulia zaidi.Karibu Mathew” akasema Austin “Ahsante Austin.Miaka mitatu iliyopita Israel kwa kutumia shirika lake la ujasusi la Mossad walifanya operesheni ya siri hapa nchini wakafanya mauaji na kumteka raia wetu ambaye alikuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania anayeitwa Edger Kaka.Walitengeneza ajali ambayo ilituaminisha wote kwamba Edger kaka amefariki dunia lakini kumbe haikuwa kweli.Edger Kaka yuko hai na amefichwa katika ubalozi wa Israel nchini Kenya.Baada ya kupata taarifa hizo za Edger kaka kuwa hai tulifanya uchunguzi wa kutosha kujiridhisha kama taarifa hizo ni za kweli na mapema usiku huu wa leo timu ambayo niliitanguliza Nairobi kufanya uchunguzi wa jambo hilo imepata majibu”akasema Mathew na kuiwasha kompyuta yake ambayo ikaunganishwa na picha za video ambazo walizipata Devotha alipoingia ndani ya ubalozi wa Israel jijini Nairobi kuonana na Edger Kaka zikaanza kuonekana katika runinga kubwa ukutani. “Mmoja wa watu wangu walioko Nairobi alifanikiwa kuingia ndani ya ubalozi wa Israel jijini Nairobi akiwa amevaa kamera ya siri na hizi ndizo picha tulizozipata kutoka katika kamera hiyo.Huyo anayeonekana pichani ndiye Edger Kaka raia wa Tanzania anayeshikiliwa mateka na Israel katika ubalozi wake nchini Kenya” akasema Mathew na baada ya wale makamanda kuitazama video ile mmoja wao akauliza “Kwa nini Israel wakamteka nyara mbunge wetu na kwenda kumficha Kenya? “Kuna maelezo marefu kidogo hapo lakini kwa ufupi tu kuokoa muda ni kwamba Edger Kaka ana mahusiano na watu ambao wanafadhili kikundi cha kigaidi cha IS na vikundi vingine vya wanamgambo wa kipalestina ambavyo vimeendelea kufanya mashambulizi katika ardhi ya Israel na kuua watu.Walimteka Edger ili awasaidie kuwapa taarifa za namna ya kuwapata watu hao lakini mpaka leo hii Edger hajafunguka chochote” akajibu Mathew “Hii ni taarifa ya kushangaza sana.Mbunge wa Tanzania anajihusisha na kundi la kigaidi.Kwa nini vyombo husika vya uchunguzi havikuweza kumbaini?akauliza mwingine “Hilo ndilo swali ambalo tunalitafutia majibu lakini inaonekana hayuko peke yake kuna mtandao wao hapa nchini na inaonekana kuna watu wapo hadi ndani ya serikali ndiyo maana imekuwa vigumu kwa Edger kaka kujulikana”akajibu Mathew “Misheni yetu ni nini hasa?akauliza mwingine “Misheni yetu tunakwenda Nairobi kumchukua raia wetu Edger kaka anayeshikiliwa mateka katika ubalozi wa Israel nchini Kenya” “Wow ! It’s more than a mission.It’s a war” akasema mmoja wao “They started this war.Waliingia nchini kwetu wakaua raia na kuteka hivyo tunachofanya sisi ni kwenda kumkomboa raia wetu anayeshikiliwa mateka na njia pekee ya kumkomboa raia wetu ni kwa kuvamia ubalozi huo.Makamanda hii ni operesheni ya siri sana na mpaka sasa hivi serikali ya Israel haifahamu chochote kuhusiana na operesheni hii tunayokwenda kuifanya na wala hawajui kama tayari tunafahamu kuwa Edger Kaka yuko hai na anashikiliwa katika ubalozi wao.Jambo hili ni kubwa ndugu zangu lakini naomba nisitumie muda mwingi kuwaeleza kwani kweni ninyi kubwa ni operesheni inayokwenda kufanyika usiku wa leo.Tayari tunayo ramani ya jengo hilo lilivyo na mfumo wote wa ulinzi tunaufahamu hivyo operesheni yetu haiutakuwa ngumu” akasema Mathew na kuwafungulia ramani ya jengo la ubalozi wakaitazama kimya kimya “Hiyo ndiyo ramani ya jengo la ubalozi wa Israel nchini Kenya lakini Edger Kaka yuko chini ya jengo hili” akasema Mathew “Kwa namna jengo hili lilivyokaa” akasema Austin “Tunahitaji kujigawa katika timu mbili.Timu ya kwanza ambayo itakuwa ni Oscar team wataingia kwa juu na kulidhibiti jengo kutokea juu na timu ya pili ambayo itajulikana kama Mike team wao wataingia kwa kupitia lango kuu na kuidhibiti sehemu yote ya nje ili kuwapa nafasi Oscar team watakaopitia juu ya jengo kuweza kuigia ndani na kumchukua mateka wetu.Mathew una timu ya watu wangapi kule Nairobi?akauliza Austin “Ninao watu watatu”akajibu Mathew “Ni wapiganaji?Wanaweza wakaungana na timu yetu itakayopita upande wa chini?akauliza Austin “Wawili ni wanajeshi.Mmoja alikuwa komandoo wa jeshi na mwingine amepigana vita vya msituni nchini Congo kwa muda mrefu wa mwisho ni mwanamke ambaye ndiye tuliyemtumia ku….” Akasema Mathew lakini Austin akamkatisha “I’m sorry Mathew we don’t include women in our missions.Si kwamba ni ubaguzi lakini ni kutokana na aina ya mafunzo tunayoyapitia ambayo kwa mwanamke inakuwa ngumu hivyo tutawajumuisha katika Mike team hao wanajeshi wawili lakini huyo mwanamke hatutamjumuisha” akasema Austin “Austin this woman is not just a woman ni mpiganaji hatari.Anatakiwa kujumuishwa katika kikosi na baada ya operesheni kukamilika wote wanarejea nyumbani hakuna atakayebaki nyuma hivyo basi kwa mara ya kwanza itawalazimu kwenda nje ya taratibu zenu na kumjumuisha mwanamke katika misheni.Msiwe na hofu ninamuamini Devotha” akasema Mathew “If you trust her it’s fine lakini sisi tuna taratibu moja tuwapo katika misheni kama kuna mmoja kati yetu ambaye anaonekana kutaka kuwa mzigo na kuharibu misheni tunamuua hapo hapo na kama huyo mwanamke ataonekana kuwa mzigo kwetu nasikitika kwamba hatutakuwa na namna nyingine zaidi ya kumuua” akasema Austin. “Hakuna tatizo sina shaka kabisa na Devotha” akasema Mathew “Good.Oscar team ambao watapitia juu watakuwa watu saba na Mike team ambao itawajumuisha pia na watu wako walioko Nairobi itakuwa na watu nane jumla tutakuwa watu kumi na tano.Mathew naomba ufahamu kwamba watu wangu wana mafunzo ya hali ya juu mno na usiwe na wasi wasi wowote.Nitaongoza Mike team na wewe utaongoza Oscar team.Tutatumia helkopta tatu zinazotumia teknolojia ya hali ya juu sana ambazo hazina mlio kama helkopta nyingine na sifa yake nyingine haziwezi kuonekana katika rada.Lakini kuna jambo linatakiwa lifanyike.Umeme unatakiwa kukatika katika eneo lote la kuzunguka jengo la ubalozi ili ndege zetu zisionekane wakati zikitua.Tutakuwa tumevaa miwani ya kuonea gizani na mavazi ambayo yatatufanya tusionekane kwa urahisi” akasema Austin “Hilo la umeme tayari nimekwisha litolea maelekezo na mmoja kati ya watu wangu walioko Nairobi analishughulikia hilo.Swali la kujiuliza hapa ni vipi watakuwa na jenereta la dharura wakaliwasha? akasema Mathew “Tutakapokuwa tayari tumekaribia jengo tutamjulisha huyo mtu wako na umeme ukikatika helkopta ya Oscar team itatua juu ya jengo na kama kutakuwa na jenereta la dharura basi kazi ya kwanza itakayofanyika itakuwa ni kuliharibu ili kulifanya eneo liendelee kuwa na giza na kuwapa Mike team nafasi ya kutua.Hii haitachukua dakika tano.Watu wako watakao ambatana na Mike team wanapaswa kuandaa sehemu ya wenzao kutua.Baada ya kutua itarushwa angani kamera ambayo itakuwa inalizunguka jengo lote na watu wa Dar es salaam wataweza kuangalia kila kitu kinachoendelea nje ya jengo kupitia kamera hiyo na watatujulisha kama kuna hatari yoyote inakaribia eneo hilo.Mike team tutahakikisha tunalidhibiti eneo la nje ka haraka sana ili ninyi muweze kupata nafasi nzuri ya kumchukua Edger Kaka.Unauonaje huo mpango?akauliza Austin “Mpango ni mzuri hata mimi nilikuwa ninafikiria hivyo hvyo kama ulivyopanga” akasema Mathew kisha wakaendelea kuchambua ramani ile na kuweka mikakati zaidi namna watakavyoweza kutekeleza operesheni yao. “Mathew nafahamu wewe na timu yako mnayo ofisi yenu na pamoja na taratibu zenu za kufanya operesheni mbali mbali lakini hii ni operesheni ya kijeshi hivyo inapaswa kuongozwa kutokea hapa na tukishaikamilisha tutawakabidhi mtu wenu nanyi mtaendelea na taratibu zenu wenyewe.Nadhani hakutakuwa na tatizo katika hilo”akasema Austin “Hakuna tatizo Austin.Haijalishi operesheni inaongozwa kutoka wapi kikubwa ni kuikamilisha.Hata hivyo kuna mtu wangu mmoja ningeomba aje kuungana nanyi hapa katika kuongoza operesheni hiyo” akasema Mathew “Mathew utanisamehe ndugu yangu kwa taratibu zetu hapa mtu ambaye si mwanajeshi au hahusiki kwa namna yoyote na kikosi hiki haruhusiwi kuingia katika chumba hiki hata wewe mwenyewe uko hapa kwa agizo la Rais vinginevyo usingekuwa eneo hili.Hii ni sehemu nyeti sana kuna mambo mengi yanayofanyika ya kiulinzi ndani ya chumba hiki ambayo tunaopaswa kuyafahamu ni sisi pekee wahusika” akasema Austin “Ninalifahamu hilo Austin lakini ninakuomba umkubali huyo mwanadada ninayekwambia.Anaitwa Ruby ninamuita mchawi wa kompyuta na mambo yote ya kielektroniki.Ni mtu ambaye naamini tunamuhitaji sana awepo katika chumba cha kuongozea operesheni kwa usiku huu” akasema Mathew “Mathew..” Austin akataka kusema kitu lakini Mathew akamkatisha “Austin tafadhali ndugu yangu,Ruby ninamuamini sana na ninakuhakikishia kwamba msaada wake ni mkubwa.Vile vile ninataka awepo hapa kwa ajili ya usalama wake amenusurika kuuawa kwa risasi na siwezi kukubali tena akauawa.Ni mtu mtu muhimu sana kwangu” akasema Mathew .Austin akafikiri kidogo halafu akasema “Sawa hakuna tatizo tutaruhusu aje hapa lakini hatajihusisha na kitu chochote hadi pale msaada wake utakapohitajika.Ninayo timu ya kutosha yenye ujuzi mkubwa wa mambo haya na wamekuwa wakiongoza operesheni mbali mbali kwa miaka mingi.” “Ahsante sana Austin.Kabla ya kwenda kuzungumza na makamanda wako nataka tuzungumze na timu iliyoko Nairobi kuwajulisha kuhusu mipango ya operesheni na kitu wanachotakiwa kukifanya” akasema Mathew na kupewa simu maalum ili aweze kuwasiliana na watu wake kwani ukiwa eneo lile huruhusiwi kutmia simu za kawaida za mkooni bali zipo simu maalum.Mathew akaandika namba na kumpigia Tino “Hallow” akasema Tino baada ya kupokea simu akiwa hajui nani aliyempigia “Tino it’s me Mathew.Mnaendeleaje hapo? “Tunaendelea vyema.Tayari tumekwisha rejea hotelini tumejianda tunasubiri maelekezo yako” akasema Tino “Kama nilivyowaeleza kwamba operesheni itafanyika usiku wa leo.Nimetoka ikulu kujadiliana na Rais kuhusu operesheni ya usiku wa leo ametoa baraka zake ifanyike na amenikabidhi kwa mkuu wa kikosi cha jeshi kinachohusika na operesheni maalum ambaye amenileta katika kambi yao tumejadili kwa mapana namna tutakavyotekeleza operesheni yetu”akasema Mathew na kumpa Tino maelekezo yote wanayotakiwa kuyafanya “Upande wa timu ya Nairobi hakuna tatizo sasa tukazungumze na vijana wako” akasema Mathew wakaelekea katika chumba cha mikutano ambako waliwakuta watu kumi na mbili wote wakasimama baada ya kumuona mkuu wao,akawataka waketi “Toka jana niliwataka mfanye mazoezi makali kwa ajili ya operesheni maalum.Namini tayari mmekwisha jiandaa vya kutosha.Usiku wa leo tutakuwa na operesheni maalum.Kabla sijawaeleza kile tunachokwenda kukifanya usiku wa leo nataka niwatambulishe kwenu mgeni niliyekuja naye anaitwa Mathew Mulumbi ni mmoja kati ya majasusi nguli kabisa kuwahi kutokea hapa nchini.Yeye ndiye kiongozi wa operesheni hii na nitamuomba awafafanulie kwa ufupi umuhimu wa operesheni ya usiku wa leo” akasema Austin na bila kupoteza muda Mathew akasema “Miaka mitatu iliyopita Israel kupitia shirika lake la ujasusi la Mossad walifanya operesheni ya siri hapa nchini na kuua watu kadhaa kisha wakamchukua mateka mbunge wa bunge la jamhuri ya muuungano wa Tanzania na kutuaminisha kwamba mbunge huyo aliyejulikana kama Edger Kaka amefariki katika ajali waliyoitengeneza.Jambo hili limekuwa siri kubwa hadi hivi majuzi tulipogundua kwamba Edger Kaka raia wetu aliyetekwa yuko hai na amefichwa katika ubalozi wa Israel nchini Kenya.Edger Kaka anatajwa kuwa na mahusiano na wafadhili wakuu wa vikundi vha kigaidi kama vile IS na vikundi vingine vya wanamgambo ambavyo vinaendesha mashambulizi na kuua watu katika ardhi ya Israel na hii ndiyo sababu ambayo Israel walimteka ili aweze kuwapa taarifa zitakazosaidia kuwapata wafadhili hao wa ugaidi ambao wamekuwa wakitafutwa kwa miaka mingi.Japokuwa ana mahusiano na magaidi lakini bado ni raia wetu ambaye ametekwa hivyo basi tunakwenda usiku wa leo kumchukua Edger Kaka na kumrejesha nyumbani.Ni operesheni ya siri ambayo tunataka baada ya kuikamilisha serikali ya Kenya wala Israel wasigundue kama ni sisi ndio tuliofanya uvamizi huo katika ubalozi wa Israel.Maandalizi ya kutosha yamekwisha fanyika kutuwezesha kuikamilisha operesheni hii. Mimi na mkuu wenu Austin tumejipanga vyema kuhakikisha kwamba tunawalinda nyote na mnarejea nyumbani salama.Hakuna atakayebaki nyuma awe mzima,amejeruhiwa au amekufa.” akasema Mathew na kumuachia Austin aendelee kutoa maelekezo “Nadhani mmesikia tunachokwenda kukifanya usiku wa leo.Tutajigawa katika timu mbili timu Oscar na timu Mike.Timu Oscar itaongozwa na Mathew na timu Mike itaongozwa na mimi.Oscar team wataingia ndani ya jengo kwa kupitia upande wa juu na Mike team tutaingia kwa kutumia lango kuu ili tuweze kulidhibiti jengo kwa nje” akasema Austin na kutoa maelekezo ya kile kinachotakiwa kufanywa usike ule katika operesheni.Baada ya kutoa maelekezo Mathew akalazimika kuondoka kwenda kumchukua Ruby “Mambo yamekwendaje huko?akauliza Ruby mara tu Mathew aliporejea katika makazi waliypopewa na Rais “Mambo yamekwenda vizuri.Kila kitu tayari kimeandaliwa nimekuja kukuchukua unahitajika sehemu Fulani” akasema Mathew na kumfafanulia Ruby kila kitu.Ruby hakuwa na tatizo akakubali kuongozana na Mathew kwenda katika kambi ya kikosi cha operesheni maalum. Saa saba na dakika moja za usiku helkopta ya kwanza iliyowabeba wanajeshi wa kikosi maalum ikapaa na kuondoka kuelekea Nairobi.Hawa walikuwa Oscar team wakiongozwa na Mathew Mulumbi ambaye usiku huu naye alikuwa amevaa sare za kikosi hiki na mkononi akiwa na bunduki kubwa.Baada ya dakika tatu helkopta ya pili iliyobeba team Mike wakiongozwa na Austin nayo ikapaa ikaelekea Nairobi.
Simu ya Rais iliyokuwa katika mfuko wa koti lake ilianza kutetema kuashiria kuna mtu anapiga.Alikuwa amepumzika sebuleni kwake akiwa mchovu na mwenye mawazo mengi.Akaitoa simu ile na kutazama mpigaji akahisi mwili wote unaingiwa baridi.Aliogopa kuipokea.Zilikuwa ni zile namba zinzotumiwa na wale magaidi waliomteka mwanae.Aliitazama simu ikiita na kukatika “Ni wenyewe wanapiga,naogopa hata kuipokea simu yao” akawaza Dr Evans na mara simu ile ikaanza kuita tena.Kabla hajaipokea akachukua simu nyingine akapiga namba za Mathew lakini simu yake haikuwa ikipatikana “Ngoja niipokee nisikie wanachokitaka” akawaza Dr Evans na kuipokea ile simu “Hallow” akasema “Mheshimiwa Rais habari za usiku huu.Ni mimi Yule rafiki yako nimekupigia tena ili tuzungumze” “Kabla ya yote nataka kuhakikisha kama mwanangu yuko salama” akasema Dr Evans “Mwanao ni mzima hana tatizo lolote anaendelea vyema” akajibu Yule jamaa “Ili mimi na ninyi tuweze kuzungumza nataka unihakikishie kwanza kama mwanangu yuko hai na anaendelea vyema kwa sababu mlimchukua akiwa mgonjwa” akasema Dr Evans “Naomba dakika mbili” akasema Yule jamaa na kukata simu.Dr Evans akavuta pumzi ndefu na kuchukua kitambaa akafuta jasho “Hawa jamaa wamenitikisa sana.Hakuna kitu kinachoniumiza kama wanavyocheza na uhai wa mwanangu.Ngoja niwe mvumilivu kama alivyoshauri Mathew” akawaza Dr Evans na simu ikaita tena akaipokea na kumshuhudia mwanae Coletha akiwa kitandani amekaa anasoma kitabu.Afya yake ilionekana kuimarika “Coletha my queen nitatumia kila njia kuhakikisha ninakutoa katika mikono ya hao magaidi.Ninaamini hawataweza kukuua kama alivyosema Mathew”akawaza Dr Evans kwa sauti ndogo na video ile ikakatwa baada ya sekunde kadhaa simu y akaaida ikapigwa akaipokea “Mheshimiwa Rais naamini sasa umepata uhakika kuwa mwanao yuko hai na yuko salama hivyo tunamuhudumia vizuri sana.Sasa tunaweza kuendelea na maongezi yetu” akasema Yule jamaa “Nini mnakitaka tena?Nimekwisha wapatia Olivia mnataka nini kingine? Akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais kuna kitu kingine tunakitaka kutoka kwako” “Sema mnataka nini? “Tunamtaka Edger Kaka” akasema Yule gaidi na Dr Evans akatoa kicheko kidogo “Mheshimiwa Rais usicheke tafadhali hili ni jambo zito sana.Tunamuomba Edger Kaka na sisi tutakurejeshea mwanao” “Niwaambie lugha gani mnielewe ninyi watu? Edger Kaka hayuko hai amekwisha fariki miaka mitatu iliyopita na mimi si Mungu sina uwezo wa kumfufua na kuwakabidhi” “Mheshimiwa Rais tunafahamu kuwa Edger kaka hajafariki dunia bali wewe na watu wako mlitengeneza ajali ili kudanganya wananchi kwamba Edger amefariki dunia kumbe yuko mahala amefichwa.Tunamuomba tafadhali.Ukitukabidhi tunakuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba tutakurejeshea mwanao”akasema Yule gaidi “Edger Kaka amekufa na hakuna namna ya kumrejesha tena duniani na hata kama angekuwa hai nisingeweza kumkabidhi kwenu kwani ni msaliti kwa taifa na angestahili adhabu kali sana kwa kitendo cha kushirikiana na magaidi ! akasema Dr Evans kwa ukali kidogo “Mheshimiwa Rais nakuomba tafadhali utekeleze hilo tunalokutaka na tunatoa muda hadi kesho saa mbili za asubuhi uwe umemuandaa Edger Kaka.Nitakupigia simu saa mbili kamili za asubuhi na kukupa maelekezo zaidi mahala pa kumpeleka na namna utakavyompata mwanao” akasema Yule jamaa “Naombeni mnisikilize vizuri nyie watu na fikisha ujumbe huu kwa wakubwa zako kwamba sintafanya tena makubaliano yoyote na ninyi.Tanzania haifanyi majadiliano na magaidi na ninakuhakikishia kwamba nitawasaka kokote mliko na kumchukua mwanangu !! akasema Dr Evans kwa ukali.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa Yule mtu simuni akasema “Rudia tena kauli yako mheshimiwa Rais sijakusikia vizuri ! “Ninaomba unisikie vizuri.Nimesema sintafanya majadiliano tena na ninyi.Tanzania hatufanyi majadiliano na magaidi bali tunawafyekelea mbali.Damu mliyomwaga ya watu wasio na hatia inatosha na sasa inafuata zamu yenu.Ninatangaza vita na ninyi na ninawahakikishia kwamba nitampata mwanangu akiwa mzima na kitakachowatokea kitakuwa ni historia kwenu na kwa vizazi vyenu.Umenipa hadi saa mbili za asubuhi niwe nimemrejesha Edger Kaka na mimi ninawapa hadi muda huo muwe mumemrejesha mwanangu ama sivyo nitawachapa kichapo kitakatifu” akasema Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais kwanza kabisa nataka kukusahihisha kwamba hatujamwaga damu Tanzania.Bado hakuna damu iliyomwagika.Umekosea sana kwa hiki ulichokitamka kwamba unatangaza vita na sisi.Kwa kauli hiyo umetulazimsha tufanye kile ambacho hatukuwa tumetaka kukifanya.Kwa kuwa umekuwa kiburi,hatuna budi kukulazimisha ufanye kile tunachokutaka ukifanye na hapo ndipo utakapoiona damu halisi ikimwagika.Mheshimiwa Rais vita yetu ni vita takatifu ya vizazi hadi vizazi na ninarudia tena umekosea sana kutangaza vita na sisi” Dr Evans akiwa amefura kwa hasira akasema “Mnadhani ninaogopa hata mkitishia kumuua mwanangu? Fanyeni kile mnachotaka kukifanya lakini mjue kwamba siku zenu zinahesabika.Mpaka saa mbili asubuhi kesho nataka unipigie simu unijulishe alipo mwanangu ama vinginevyo mjiandae! Akasema Dr Evans na kukata simu “I need my pills.Naona hali imebadilika” akawaza Dr Evans na kuchukua kopo dogo lenye dawa akatoa mbili akameza “Nimetangaza vita na magaidi na kwa kufanya hivi nimeyaweka mashakani maisha ya mwanangu Coletha.Sifahamu magaidi hawa watamfanya nini lakini sina hakika kama wataweza kumuua.Hata hivyo nimefanya vyema kuonyesha msimamo vinginevyo kama ningewakubalia kila kitu wanachokisema wangeweza kunitaka hata niachie urais.Mathew amenifanya niwe jasiri sana kabla sijakutana naye sikuwa na ujasiri wa kuweza kuzungumza na magaidi na kuwatisha kama nilivyofanya leo.Naamini muda huu watakuwa angani wakielekea Nairobi kumchukua Edger kaka nawaombea wafanikiwe kumpata” akawaza Dr Evans na kujifuta jasho usoni “Kinachofuata sasa ni kuhakikisha ulinzi unaimarishwa kila sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu kwani magaidi hawa wanaweza wakafanya shambulio sehemu yoyote ile hasa zenye mikusanyiko mikubwa ya watu” akawaza Dr Evans na kumpigia simu waziri wa mambo ya ndani Deus Mkuza “Deus nimekupigia simu usiku huu kuna maelekezo ninataka yafanyiwe kazi haraka sana” “Nakusikiliza mheshimiwa Rais” akasema waziri Deus Mkuza “Kuna vitisho vya kutokea kwa mashambulio zaidi ya kigaidi hapa nchini vikifanywa na wale wale waliofanya shambulio la Mtodora.Ninataka kuanzia sasa ulinzi uimarishwe katika sehemu zote zenye mkusanyiko mkubwa wa watu katika vituo vya mabasi,mahoteli,maduka makubwa,misikiti ,makanisa na kokote kule ambako idadi kubwa ya watu wanakusanyika kwa wakati moja.Sitaki shambulio lingine litokee wakati tayari vipo viashiria vya kuonyesha kwamba kuna shambulio lingine linapangwa.Nataka maelekezo haya yafanyiwe kazi haraka sana kuanzia usiku huu”akasema Dr Evans “Nimekuelewa mheshimiwa Rais ninatoa maelekezo hayo kwa jeshi la polisi sasa hivi” akasema waziri Deus “Ahsante Deus.Usiku mwema” akasema Dr Evans na kukata simu “Lazima kila jitihada ifanyike kuhakikisha kwamba IS wanadhibitiwa wasifanye shambulio lingine hapa nchini.Nilifanya makosa makubwa kutekeleza takwa lao la kuwapa Olivia kama si Mathew kutokea na unifumbua macho wangeniendesha sana washenzi wale.Kwa sasa sina hofu tena nitakabiliana nao kwa kila nguvu niliyonayo.Naamini akina Mathew watakuwa wamerejea kabla ya saa mbili za asubuhi kesho,tutakaa na kujadiliana namna ya kufanya kukabiliana na hawa magaidi.Hii vita lazima tushinde” akawaza Dr Evans Jijini Nairobi,Fahad ambaye alikuwa anawasiliana na Rais Dr Evans alipandwa na hasira kali baada ya Dr Evans kukata simu. “Nadhil ! akafoka Fahad “Kuna nini Fahad mbona umebadilika hivyo?akauliza Rashid “Rais amebadilika ghafla.Sikutegemea kama angeweza kubadilika namna hii.Rais niliyezungumza naye sasa hivi si Yule ambaye nilizungumza naye awali ambaye alikuwa na sauti yenye woga akiwa tayari kutekeleza kila tutakachomuamuru,lakini usiku huu amekuwa na sauti yenye ujasiri ,ukali na haonyeshi kuogopa kitu tena.Amediriki hata kutamka kwamba anatangaza vita na sisi na ametupa hadi kesho saa mbili za asubuhi tuwe tumemrejesha mwanae ama sivyo atatufyekelea mbali” akasema Fahad na Rashid akalazimika kutoa kicheko kidogo “Ni Rais wa Tanzania Dr Evans ndiye aliyetamka maneno hayo au kuna mtu mwingine aliyejifanya Rais? “Ni yeye mwenyewe.Hata mimi nimeshangaaa sana.Ametoa wapi ujasiri wa kutamka maneno kama haya?akauliza Fahad “Nilijaribu kumsihi asitamke maneno kama yale kwani yatakuwa na athari kubwa sana kwa nchi yake lakini hakutaka kunisikia na badala yake akatoa vitisho na kikubwa zaidi haonyeshi kujali tena kuhusu mtoto wake kutekwa” akasema Fahad “Nini maamuzi yako baada ya kauli yake? Tuvute subira labda atabadili mawazo?akauliza Rashid “Hatabadili mawazo badala yake ataendelea na juhudi za kutusaka kama alivyoahidi” “Nini basi unashauri kifanyike?Rashid akauliza “yurid alharb , falanuqatil alharb”akasema Fahad kwa lugha ya kiarabu akimaanisha “ametaka vita twendeni tukapigane” “Twendeni tukamuonyeshe kwamba IS tupo Tanzania na tunao uwezo wa kufanya chochote tukiamua.Ametulazimisha yeye mwenyewe tumwage damu na sasa damu inakwenda kumwagika” akasema Fahad ambaye alikuwa na hasira kali “Nini unakifikiria Fahad kitakachomfanya Rais atii maelekezo yetu?akauliza Rashid.Fahad akafungua sehemu anakohifadhi majina katika simu yake akatoka nje akazungumza na mtu Fulani kwa zaidi ya dakika kumi halafu akarejea ndani akitabasamu “Tayari nimepata suluhisho.Kuna shule moja ya wasichana iko nje kidogo ya jiji inamilikiwa na kanisa inaitwa St Getrude secondary school.Ni moja kati ya shule bora kabisa Tanzania.Tunavamia shule hiyo usiku wa leo na kuwachukua mateka baadhi ya wasichana na kuwapeleka mafichoni halafu tutazungumza tena na Rais tuone kama ataendelea kuwa kiburi.Tutampa Rais muda wa kutekeleza maelekezo yetu na kama akipuuza tutaanza kuua mwanafunzi mmoja baada ya mwingine huku wananchi wakishuhudia kupitia simu zao na hiyo itasaidia sana kumpa Rais shinikizo aweze kutekeleza kile tunachokitaka.Wananchi lazima watashikwa na hasira wakiona watoto wao wanachinjwa kama kuku hawatakaa kimya lazima wataitaka serikali kufanya kila wawezalo kuwakomboa watoto na Rais atakuwa ndani ya shinikizo kubwa hivyo lazima atatekeleza kile tunachokitaka.Kwa njia hii tutaua ndege wawili kwa jiwe moja,tutampata Edger Kaka na tutamuondoa Rais madarakani kwani tutahamasisha maandamano yasiyokwisha ya kumtaka Rais aachie madaraka na kisha tutamuweka madarakani mtu wetu” akasema Fahad “Fahad hili ni suala zuri lakini linahitaji maandalizi ya kutosha ili kulitekeleza”akasema Rashid “Hatuna muda wa kujiandaa Rashid.Tunao vijana ambao wako tayari kwa kazi muda wowote watakapopewa maelekezo na hii ndiyo faida ya kutengeneza mtandao.Tunayo timu ya kutosha Dar es salaam ambao wanatosha kabisa kuifanya kazi hii usiku wa leo.Hakuna mtu anayetegemea tukio kama hilo kutokea na tutawastukiza usiku wa manane wakiwa wamelala tutavamia na kuchukua wasichana na kuondoka nao.Huu utatumika kama moja ya mpango wa kumuweka mtu wetu madarakani.Tulishindwa kwa Edger Kaka lakini safari hii hatuwezi kushindwa tena”akasema Fahad “Kuna ulazima wa kumjulisha mama Habiba kabla hatujafanya jambo hilo?akauliza Rashid “Habiba alitukabidhi sisi kazi tuhakikishe tunafanya kila tunaloweza kumpata Edger Kaka hivyo hakuna ulazima wa kupata Baraka zake kwa kila tunachokifanya.” akasema Fahad. NAIROBI – KENYA Helkopta ya kwanza iliyowabeba Oscar team wakiongozwa na Mathew Mulumbi ilivuka anga la Tanzania na kuingia anga la Kenya.Ilipata saa tisa na dakika kumi za usiku.Kwa kuwa helkopta hizi zilitengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ya kutoonekana kwenye rada haikuweza kugundulika ilipoingia katika anga la Kenya. “Tino tayari tumeingia katika anga la Kenya” Mathew akamjulisha Tino “Sisi huku tunawasubiri mtakapofika jijini Nairobi mtatujulisha ili kazi ianze mara moja” akasema Tino. Baada ya kufika katika jiji la Nairobi Mathew akampigia simu Tino akamjulisha kwamba tayari wamekwisha fika katika jiji la Nairobi na walikuwa tayari kuelekea katika jengo la ubalozi wa Israel Mara tu Tino alipopokea taarifa kutoka kwa Mathew kuwa wamekwisha fika katika jiji la Nairobi Tino akapiga namba Fulani katika simu yake na dakika mbili baadae umeme ukazima katika jiji zima la Nairobi .Wakiwa angani akina Mathew waliweza kushuhudia namna umeme ulivyokatika “Kila kitu kimekwenda kama tulivyotaka sasa kazi inaanza” akasema Mathew na helkopta ile ikaelekezwa katika jengo la ubalozi wa Israel.Kulikuwa giza lakini helkopta ile ilikuwa na teknolojia ya hali ya juu mno ya kumuwezesha Rubani kuona na kutua salama sehemu anakotakiwa kutua.Wakati helkopta ya team Oscar ikikaribia kutua juu ya jengo la ubalozi wa Israel,helkopta iliyowabeba team Mike ilijiandaa kutua katika sehemu ya nje ya ubalozi huo na Tino akatakiwa kutoa ishara.Akavua shati na kulichoma moto na ishara ile ikaonekana kisha moto ule ukazimwa na helkopta ile ikaanza kushuka na ilipokaribia chini Austin na kundi lake wakashuka kwa kutumia kamba kisha helkopta ikapaa. Bado jiji zima la Nairobi lilikuwa giza.Mike team walijipanga na kulikaribia geti kuu la kuingilia ndani ya ubalozi.Wote walikuwa na miwani maalum ya kuwasaidia kuona kwenye giza.Katika geti kuu walinzi wawili walikuwa wamekaa katika viti wakizungumza mmoja akivuta sigara huku bunduki zao wakiwa wameziweka mapajani.Wawili walionekana wakiwa wamelaza vichwa vyao katika meza na kofia zao zikiwa pembeni hawakuwa na habari kama kulikuwa na watu wakiwatazama bila wao kuwaona.Ilikuwa ni operesheni inayokwenda kwa muda maalum hivyo hakukuwa na muda wa kupoteza.Tayari walinzi wale wote walikwisha lengwa na bunduki kubwa za team Mike zilizofungwa viwambo vya kuzuia risasi.Austin akatoa ishara na risasi mfululizo kutoka katika bunduki zao zikawakata uhai walinzi wale ambao hawakuwa na habari yoyote kama wamevamiwa.Haraka haraka Austin na timu yake wakaenda katika geti kuu “Mathew tayari tumelidhibiti geti kuu” akasema Austin kisha akamtaka mmoja wa watu wake aliyebeba ndege ndogo yenye kamera aiwashe na kuirusha ili kuwawezesha watu walioko Dar es salaam kuweza kufuatilia kila kinachoendelea pale nje ya jengo kujua kama kuna hatari yoyote. “Dar es salaa tayari tumerusha kamera angani,mnaweza kutuona sasa” akasema Austin “Tayari tumeiona na tunapata picha nzuri.Tunaizungusha jengo zima kujua kuna walinzi wangapi” akasema kamanda aliyeko Dar es salaam katika chumba cha kuongozea operesheni ile. Mathew na kundi lake la Oscar walifanikiwa kuingia ndani ya ubalozi kwa kupitia sehemu ya juu ya ghorofa.Ni usiku mwingi tayari ofisi nyingi hazikuwa na watu hivyo walishuka bila vikwazo vyovyote hadi walipofika katika ghorofa ya sita ambako ndiko kuna ofisi za Mossad.Katika ghorofa hii kulisikika milio ya betri za kutunza umeme wa kompyuta na ilionyesha kulikuwa na watu wanafanya kazi wakihifadhi data zaso kabla ya kompyuta kuzima.Mathew na timu yake wakaanza kunyata kuelekea katika chumba mlio ule wa betri ulitokea.Mlango mmoja ulikuwa wazi na kwa kuwa walikuwa na miwani ile ya kuwawezesha kuona katika giza waliweza kuwaona watu sita wakijitahidi kuhifadhi mafaili katika kompyuta kabla hazijazima. “Hii ndiyo adha ya Afrika,hakuna umeme wa uhakika bado.Nini sababu ya kukatika umeme usiku huu?Kuna matengenezo gani usiku hu...!” Mmoja wao akasikika akilalama lakini hakumaliza sentensi yake kwani alipigwa risasi ya kichwa kutoka katika bunduki yenye kiwambo cha sauti akaanguka chini.Hakuna aliyebaki hai ndani ya kile chumba baada ya kuhakikisha wamewaua wote wakatoka na kuendelea kushuka chini.Hawakukutana na kikwazo chochote. “Mike one,tayari tumefika jengo la chini kabisa.Vipi huko nje?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/akasema Mathew akiwasiliana na Austin “Tumedhibiti eneo lote la nje” “Good.Oscar team tunaelekea mahala aliko Edger Kaka.” akasema Mathew na kuelekea katika mlango mkubwa ulioonekana kama mlango wa lifti kukabandikwa kifaa Fulani kilichounganishwa na waya mrefu na kisha akina Mathew wakakaa mbali kidogo baada ya sekunde chache kifaa kile kikalipuka na mlango ukasambaratishwa,haraka haraka wakafuata ujia ulioelekea chini wakaukuta mlango mwingine ambao nao waliulipua kama walivyofanya ule wa kwanza.Kabla ya kukifikia chumba alimo Edger Kaka wakaukuta mlango wa chuma ambao iliwalazimu waweke kifaa kikubwa zaidi na kishindo kikatokea kikubwa wakapata nafasi ya kupita hadi katika chumba alimo Edger Kaka ambaye alikutwa amekaa kitandani jasho likimtoka kutokana na woga baada ya kusikia kishindo kile kikubwa.Alimulikwa na tochi kubwa yenye mwanga mkali “Edger kaka? akaita Mathew lakini Edger alikuwa anatetemeka mwili wote kwa woga baada ya kuliona kundi la watu wakiwa na silaha nzito wakiingia mle ndani. “Mike team we have Edger Kaka” akasema Mathew “Are you sure it’s him?akauliza Austin “100% it’s him” akasema Mathew “Good job Oscar team” akasema Austin. “Who are you?Where are you taking me?akauliza Edger Kaka “Edger Kaka we’re here to rescue you.We’re taking you home” “Home? Where?akauliza Edger bado alikuwa anatetemeka “Tanzania” akasema Mathew “No ! please don’t take me there ! please kill me right here don’t take me there” akasema Edger Kaka “Wewe ni Raia wa Tanzania ambaye unashikiliwa mateka na tumekuja kukukomboa kukurejesha nyumbani.Can you walk?akauliza Mathew lakini Edger alionekana kuchanganyikiwa.Mathew akaelekeza afungwe pingu na abebebwe.Akachukua karatasi na kalamu akaandika maneno kwa lugha ya kiarabu “aqad khadhna rajlna. hadhih harb muqadasat walan tantahi abdaan. hadhih hi albidayat faqat alkthyr min al'umur hataa tati 'iilaa 'ard falistina. la 'iilah 'iilaa allah ” Akimaanisha “tumemchukua mtu wetu.Hii ni vita takatifu na isiyokoma.Huu ni mwanzo tu bado kuna mengi yanakuja hadi pale mtakaporejesha ardhi ya wapalestina.Hakuna Mungu zaidi ya Allah” Ujumbe ule akauweka juu ya meza kisha akaamuru Edger abebwe na kutolewa mle ndani kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kutembea “Mike team,tunatoka sasa” akasema Mathew akiwa ametangulia mbele mkononi akiwa na bunduki kubwa.Bado Edger kaka alikuwa analalama akitaka asipelekwe Tanzania ikawalazimu kumziba mdomo kwa gundi ya plastiki ili asipige kelele.Bado jengo lilikuwa giza umeme haukuwa umerudi.Walipanda hadi ghorofa ya juu na kuikuta helkopta yao tayari imetua ikiwasubiri.Edger kaka ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingizwa ndani ya Helkopta.Mathew alihakikisha watu wake wote wameingia ndani ya Helkopta na yeye akawa wa mwisho “Mike Team,Oscar team tuko tayari kwa kuondoka.Kuna tatizo lolote?akauliza Mathew “Hakuna tatizo lolote,Mike team wote wako salama na wamekwisha ingia ndani ya helkopta tayari kwa kuondoka” “Good job guys now we can go back home” akasema Mathew na helkopta ikapaa halafu akabonyeza kitufe chekundu katika kifaa Fulani alichokuwa nacho na bomu walilokuwa wamelitega katika chumba kikubwa walimowakuta watu wa Mossad likalipuka na kusambaratisha kila kitu.haukuwa mlipuko mkubwa lakini ulitosha kusambaratishakila kitu ndani ya kile chumba. DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa kumi na mbili na dakika ishirini na moja helkopta ya kwanza iliyowabeba Oscar team ikatua katika kambi ya jeshi ya kikosi cha operesheni maalum,Mathew Mulumbi akawa wa kwanza kushuka kisha Edger Kaka akashushwa na kwenda kuhifadhiwa katika chumba maalum.Helkopta ya pili ikatua na Mike team wakiongozwa na Austin January wakashuka.Austin akamfuata Mathew “Mathew Mulumbi hongera sana kwa kufanikisha vyema operesheni yetu” akasema Austin “Hongera nawe Austin na timu yako.Kila mmoja amesimama katika nafasi yake vyema kabisa.Ninashukuru kwa kuwa hakukuwa na majeruhi wala hatujampoteza mtu yeyote” akasema Mathew “Operesheni imekuwa nyepesi sana zaidi ya nilivyotegemea” “Hawakuwa wamejiandaa na hawakujua kama wangeweza kuvamiwa.Ilikuwa ni operesheni ya siri sana na itawawia vigumu kujua kama ni sisi ndio tuliofanya uvamizi ule kwani mle ndani ya chumba cha Edger niliacha ujumbe ambao unaonyesha IS ndio waliofanya uvamizi ule na kumchukua mtu wao” akasema Mathew “Mathew kwa upande wetu nadhani tumemaliza kazi yetu na tunawaachia ninyi muendelee na taratibu zenu”akasema Austin “Ahsante Austin.Ninataka kuwashukuru wote walioshiriki katika operesheni hii.Baada ya hapa mimi na timu yangu tutaendelea na taratibu zetu lakini nitaomba Edger aendelee kukaa hapa hadi hapo tutakapokuwa tumepata sehemu muafaka ya kumuhifadhi”akasema Mathew “Hakuna tatizo Mathew hapa ni sehemu salama sana” akasema Austin na kumuongoza Mathew hadi katika chumba cha mikutano ambako wote walioshiriki katika operesheni ile walikuwa wamekusanyika.Autin na Mathew walipoingia wote wakasimama “Gentlemen poleni kwa uchovu.Mathew hapa ana neno la kusema” akasema Austin na kumpa nafasi Mathew “Sina maneno mengi ya kusema lakini kubwa ninataka kuwashukuruni sana kwa namna mlivyojitoa kuhakikisha operesheni hii inafanikiwa.Kila mmoja alisimama vyema katika nafasi yake ndiyo maana operesheni imekwenda vizuri na imeonekana nyepesi kuliko wengi mlivyotarajia.Hakuna aliyeumia au kupoteza maisha na wote tumerejea nyumbani salama.Ahsanteni sana” akasema Mathew kisha akawapa wote mikono wakaagana.Austin akampeleka Mathew katika chumba cha kuongozea operesheni.Mara tu alipoingia Ruby ambaye alionekana kuwa na tabasamu kubwa usoni akainuka katika kiti na kwenda kumkumbatia Mathew “Ahsante Mungu umerejea salama Mathew”akasema Ruby “Ahsante sana Ruby.Sote tumerejea salama” akasema Mathew na kuwageukia makamanda waliokesha wakiwaongoza katika operesheni ile. “Gentlemen sina neno zuri la kuwashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya usiku wa leo ya kutuongoza tumekwenda salama na kurejea salama.Operesheni yetu imefanikiwa na tumemrejesha nyumbani raia wetu aliyekuwa anashikiliwa mateka nchini Kenya.Ahsanteni sana” akasema Mathew na kuanza kuwapa mikono kuwapongeza kwa kazi kubwa waliyoifanya. “Mathew Mulumbi” akasema kamanda mmoja ambaye umri wake ulikuwa mkubwa kidogo “Nimefurahi sana nimefanya kazi nawe lakini nina ombi moja kwako kama utakuwa tayari.Tunamuhitaji sana Ruby.Amekuwa na msaada mkubwa sana kwetu kiasi ambacho hatukuwa tumetegemea.Uwezo wake ni mkubwa na wa kushangaza kabisa.Tunamuhitaji katika chumba hiki” akasema Yule kamanda na Mathew akatabasamu na kumtazama Austin “Kwa bahati mbaya Ruby haishi hapa nchini makazi yake ni Uingereza vile vile hii ni operesheni yake ya mwisho kushiriki.Amenursurika kuuawa hivyo hatashirii tena katika shughuli hizi atafanya kazi nyingine” akasema Mathew na kumtaka Ruby akae katika kiti ili amsukume watoke lakini Ruby akagoma akataka kutembea. “I’m okay now Mathew” akasema Ruby kisha wakatoka ndani ya kile chumba wakaenda katika ofisi ya Austin ambako Mathew alitaka kuwasiliana na Rais Dr Evans.Akampigia simu kwa kutumia simu maalum ya Austin “Austin” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais” “Niliisubiri sana simu hii.Naamini tayari mmekwisha rejea” “Ndiyo mzee tumerejea saa kumi na mbili za asubuhi” “Ahsante Mungu.Mmefanikisha salama operesheni yenu? “Mheshimiwa Rais yuko hapa Mathew Mulumbi ambaye atakueleza kila kitu” “Mzee shikamoo” “Marahaba Mathew poleni sana kwa kazi kubwa.Ninashukuru mmerejea salama.Nyote mu wazima? “Mzee tunashukuru kila kitu kimekwenda vizuri.Operesheni imemalizika salama na kwa mafanikio makubwa tumempata Edger Kaka na kumrejesha nyumbani kwa hivi sasa amehifadhiwa hapa katika kambi hii hadi hapo utakapotoa maelekezo mengine” “Dah ! Mathew sijui niwashukuruje kwa kazi hii kubwa mliyoifanya” “Mheshimiwa Rais wale jamaa wamekupigia tena simu?akauliza Mathew “Mathew naomba tuwasiliane kwa kutumia simu yako” akasema DrEvans “Sawa mzee nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Mathew kisha akamuaga Austin wakapewa gari na dereva kwa ajili ya kuwarejesha katika makazi yao.Mathew na Ruby walikuwa wa kwanza kuingia garini kisha wakafuata Tino,Gosu Gosu na Devotha ambaye alisita kuingia ndani ya gari baada ya kumuona Ruby “Devotha get in ! akasema Mathew kwa sauti kali na Devotha akaingia garini wakaondoka. Baada ya kuondoka katika kambi ile Mathew akachukua simu yake akaiwasha na kumpigia DrEvans ambaye alipokea haraka “Mathew nimefurahi sana nyote mmerejea nyumbani salama salimini.Hizi ni taarifa njema kabisa” akasema DrEvans “Mheshimiwa Rais tunashukuru Mungu sote tumerejea salama kabisa hakuna hata mmoja wetu aliyepata jeraha au kupoteza maisha ilikuwa ni operesheni yenye mafanikio makubwa na kama nilivyokujulisha awali kwamba tumefanikiwa kumpata Edger kaka ambaye amehifadhiwa katika kambi ile ya kijeshi tukisubiri hatua nyingine” akasema Mathew “Kazi nzuri sana Mathew mmeifanya.Hakukuwa na tatizo lolote ambalo linaweza kupelekea tukagundulika kuwa ni sisi ndio tuliofanya uvamizi huo? “Tumejtahidi sana mheshimiwa Rais kuwa makini mno ili kutoacha alama yoyote ya kuwawezesha Israel na serikali ya Kenya kujua kama ni sisi ndio tuliofanya uvamizi ule”akajibu Mathew “Ahsante sana Mathew kwa uhakika huo japo tunatakiwa kuendelea kuwa makini sana kufuatilia taarifa za tukio hili” “Tutafanya hivyo mheshimiwa Rais.Hata hivyo kuna suala lingine nilikuwa nalifikiria” akasema Mathew “Suala gani Mathew? “Dr Yonathan Cohen anafahamu kile kilichotokea na sina uhakika sana kama ataendelea kuificha siri hii kwa miaka yote bila kuiweka wazi.Yawezekaa kwa sasa akawa kimya lakini nina wasi wasi yawezekana hapo baadae akaamua kuiweka wazi siri hii na kuibua mgogoro” “Unashauri nini kuhusu huyo mtu Mathew? “Kwa sasa sishauri tumfanye chochote lakini upo ulazima wa kumuweka katika uangalizi mkubwa” “Hakuna tatizo utaratibu kila kitu unachoona kinafaa Mathew nimekupa ruhusa hiyo.Si kila jambo lazima uniambie mimi ili kupata ruhusa yangu,kama kuna jambo unaona lina umuhimu lifanye haraka na utanijulisha baadae” “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Mathew mmerejea asubuhi hii na yawezekana bado hamjasikia kilichotokea usiku wa kuamkia leo” “Hatujapata taarifa zozote mheshimiwa Rais nini kimetokea?akauliza Mathew “Usiku wa kuamkia leo yapata saa tisa kuelekea saa kumi za usiku watu wasiojulikana wamevamia shule ya sekondari ya wasichana ya St Getrude wameua walinzi na kuwateka wanafunzi wapatao sitini na sita na walimu wao watatu.Msako mkali umekwisha anza kuwatafuta wanafunzi hao.Mathew nakuhitaji hapa ikulu kwa ajili ya maongezi muhimu ya faragha” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa Rais nitafika hapo” akasema Mathew “Ninakusubiri asubuhi hii” akasema Dr Evans na kukata simu Mathew akashusha pumzi “Vipi Mathew kuna tatizo?akauliza Gosu Gosu “Wakati tukiwa katika operesheni yetu kule Nairobi,hapa nyumbani kumefanyika tukio la utekaji.Watu wasiojulikana wamevamia shule ya sekondari ya wasichana ya St Getrude na kuteka wasichana wapatao sitini na sita na mpaka sasa hawajulikani walipo” “Nani wanaoweza wakafanya tukio kama hilo?akauliza Ruby “Hakuna wengine wanaoweza kufanya tukio kama hili zaidi ya magaidi.Wamekuwa wakifanya utekaji ili kushinikiza serikali kuwatekekelezea mambo yao wanayoyataka.Tuliona mwaka 2014,wanafunzi wa kike 276 walitekwa kutoka katika shule ya sekondari ya serikali katika mji wa Chibok jimbo la Borno nchini Nigeria.Ninaamini hata hapa nyumbani waliofanya tukio hilo la kuteka wasichana ni magaidi ambao bado hatujui ni kikundi gani cha kigaidi na nini lengo lao” akasema Mathew “Another mission?akauliza Tino “Bado hatujafahamu nani waliofanya tukio hilo na kwa nini hata hivyo vipo vyombo vya kushughulikia suala hilo hivyo sisi hatutajihusisha” akajibu Mathew “Mathew naomba niliweke wazi hili mapema.Sihitaji tena kushirikishwa katika operesheni nyingine kama itajitokeza.Nimetoa msaada katika operesheni hii na imefanikiwa hivyo nahitaji sasa kuendelea na shughuli zangu kama kuna kitu utahitaji kutoka kwangu you know where to find me” akasema Tino. “Tino nakushukuru sana kwa msaada wako mkubwa ulioutoa katika operesheni hii.Ninakwenda kuonana na Rais muda mfupi ujao na nitamueleza kuhusu mchango wako mkubwa katika operesheni hii.Tafadhali naomba usifunge milango kila pale tutakapokuwa na shida na kuhitaji msaada wako au hata ushauri” “Mathew milango iko wazi na unakaribishwa muda wowote” akasema Tino Walifika katika makazi yao ya muda Mathew hakupoteza muda akamtaka mmoja wa wasaidizi waliopewa na Rais ampeleke ikulu lakini kabla hajaondoka akamfuata Ruby katika chumba alimokuwa anatibiwa akamuomba daktari dakika mbili azungumze na Ruby daktari akatoka nje “Ruby ninaelekea ikulu kuonana na Rais amenitaka nikaonane naye asubuhi hii.Nitapata muda baadae wa kukushukuru kwa kazi kubwa uliyoifanya licha ya kuumwa na kutuwezesha kufanikisha kumpata Edger lakini kuna kitu nataka nikuombe” Akasema Mathew na kumtazama Ruby “Najua hauna amani kumuona Devotha hapa lakini nakuomba uvumilie.She’s part of us.Amekuwa na mchango mkubwa sana naye katika operesheni hii lakini kama haujisikii vizuri I can let her go” akasema Mathew “Mathew siwezi kuwa muongo kwamba kila kitu kiko sawa kuhusu mimi na Devotha.Alitaka kuyaondoa maisha yangu na kila ninapomuona ninapata mstuko lakini kama ulivyosema amekuwa na mchango mkubwa sana katika operesheni hii na kwa ajili ya hilo nitajitahidi kuweka kando kile kilichotokea baina yetu.I’ll try to act like nothing happened” “Thank you Ruby.Aliyekupa jina hili hakukosea kabisa wewe u mwanamke wa kipekee kabisa.Nitakaporejea tutajua nini kinachoendelea” akasema Mathew na kumbusu Ruby shavuni halafu akatoka akaenda katika chumba alimokuwa Devotha akamkuta amejilaza kitandani “Hello Devotha”akasema Mathew Devotha akainuka na kukaa “Mathew nimemaliza kile mlichotaka nikifanye,can I go home now?akauliza Devotha “Usiwe na hofu Devotha nyumbani utakwenda lakini bado hatujamaliza operesheni yetu.Kumpata Edger Kaka si mwisho bado kuna mambo mengi tutahitaji kuyafahamu kutoka kwake.Suala hili ni pana zaidi hivyo utaendelea kubaki nasi hapa.Ninakwenda kuonana na Rais na yawezekana nikarudi na maelekezo mapya hivyo kwa sasa siwezi kusema chochote hadi nitakaporejea.Kuna kitu kimoja nataka kukuomba,najua wewe na Ruby bado hamuangaliani usoni lakini naomba uwe mvumilivu.Kitendo kile ulichokifanya hawezi kukisahau kwa haraka naomba mpe muda.Kwa sasa usizungumze naye kitu chochote hadi nitakaporejea” akasema Mathew “Mathew do you think she’s okay for me to be here?akauliza Devotha “Ruby hana tatizo isipokuwa bado kuna kitu kimemkaba kooni na hakiwezi kuondoka kwa urahisi kama nilivyokueleza.She needs time” “Unadhani ataweza kusahau tukio lile?Unadhani anaweza akanisamehe?akauliza Devotha “I don’t know yet but she’ll try.Devotha tutazungumza baadae nitakaporejea” akasema Mathew na kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni halafu akageuka “Hongera ulifanya kazi nzuri sana Nairobi” akasema Mathew na Devotha akatabasamu “Thank you” akajibu na Mathew akatoka akamfuata Gosu Gosu “Gosu Gosu ninakwenda kuonana na Rais.Kuna jambo ambalo hakuweza kunieleza katika simu ndiyo maana akanitaka nimfuate ikulu ninadhani linahusiana na tukio la kutekwa kwa wale wasichana.Kuwa macho sana na hawa wanawake wawili Ruby bado ana hasira na Devotha japokuwa nimejaribu kumtuliza na amenielewa lakini viumbe hawa si wa kuwaamini sana anaweza akabadilika sekunde.Najua umechoka lakini jitahidi kuwachunga” “Usijali Mathew hakuna kibaya kitakachotokea wakiwa chini ya uangalizi wangu.Nenda tafadhali usichelewe” akasema Gosu Gosu na Mathew akatoka akaingia katika gari ambalo lilikuwa linamsubiri akaelekea Ikulu kuonana na Rais. “Naamini lipo jambo kubwa ambalo Rais ameshindwa kunieleza katika simu ndiyo maana akanitaka nikaonane naye tuzungumze faragha.Hata hivyo ninashukuru kwa operesheni yetu imekwenda vyema na sasa tunaye Edger Kaka na hapa ndipo mchezo unaponoga kati yetu na IS.Lazima kwa kila namna Olivia na Coletha wapatikane.Sijawahi kupambana na magaidi hawa nikashindwa na hata sasa hawatanishinda labda wawahi kuniua lakini kama bado niko hai nitapambana bao kwa kila uwezo nilio nao kuhakikisha ninawakomboa Olivia na Coletha” akawaza Mathew akiwa garini na kwa mbali akahisi macho yanakuwa mazito hakuwa amepata usingizi kwa siku ya pili “Nahisi macho yameanza kuwa mazito ngoja kwa dakika hizi chache kabla ya kufika ikulu nisinzie kidogo kwani sifahamu nitakalolikuta huko kwa Rais” akawaza Mathew na kulaza kiti akasinzia NAIROBI – KENYA Taarifa kuu iliyoliamsha taifa la Kenya ni tukio la kuvamiwa kwa ubalozi wa Israel jijini Nairobi.Iligundulika kuwa ubalozi wa Israel umevamiwa na watu wote waliokuwemo ndani kuuawa.Waliogundua jambo hilo ni walinzi waliokuwa wakiingia zamu ya asubuhi kuchukua nafasi za wale waliokuwa zamu ya usiki kukuta wenzao wote wameuawa.Kenya ni moja wapo ya nchi ambayo mashirika mengi makubwa ya habari duniani yalikuwa na ofisi zake hivyo taarifa za kilichotokea katika ubalozi wa Israel zilisambaa kwa haraka duniani kote “Kumetokea tukio la uvamizi katika ubalozi wa Israel usiku wa kuamkia leo” kiliripoti chombo kimoja kikubwa cha habari chenye makao yake makuu nchini Uingereza katika taarifa yake ya habari ya asubuhi.Taarifa hiyo iliendelea “Watu wasiofahamika,wamevamia jengo la ubalozi wa Israel jijini Nairobi Kenya usiku wa kuamkia leo na inadaiwa watu wote waliokuwamo ndani ya jengo usiku huo wameuawa.Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa hadi sasa kuhusiana na nani waliofanya uvamizi huo wala sababu ya kuvami aubalozi huo lakini taarifa za awali zinaonyesha kwamba hilo ni tukio la ugaidi.Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo katika taarifa zetu mbali mbali za habari” taarifa hiyo ilimalizia Vyombo vingi viliripoti kwa ufupi kuhusiana na tukio lile wakati wakisubiri taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka zinazohusika ili kujua nini hasa kilichotokea.Lilikuwa ni tukio lililoleta mshangao mkubwa kwa wakazi wa jiji la Nairobi hasa namna wavamizi hao walivyoweza kuingia ndani ya Jengo hilo na wengi walijiuliza sababu ya kuvamia ubalozi huo Balozi wa Israel nchini Kenya alifika kwa haraka sana baada ya kupata taarifa ya ofisi yake kuvamiwa.Alikuta tayari askari wa kikosi maalum cha kupambana na ugaidi nchini Kenya wamekwisha wasili na kuimarisha ulinzi kuzunguka jengo lote akazungushwa kuona namna wavamizi wale walivyofanya mauaji na kuingia ndani.Walikwenda hadi katika ofisi yake lakini haikuwa imeguswa.Katika ghorofa yenye ofisi za Mossad kulifanyika uharibifu mkubwa katika mojawapo ya ofisi na watu waliuawa.Balozi akakumbuka kitu na kupatwa na mstuko mkubwa sana akawataka askari wale wasiendelee na chochote na watoke kwanza nje ya jengo waachie wenyewe kwanza wafanye uchunguzi wao.Askari wale walitii maelekezo ya balozi na kuendelea na zoezi la kuimarisha ulinzi nje ya jengo na balozi akarejea ofisini kwake akihema akawaita ofisini kwake baadhi ya maofisa wa Mossad ambao tayari walikuwa wamewasili pale ubalozini. “Kabla ya yote nataka kujua Edger Kaka yuko salama?akauliza na hakuna aliyekuwa na jibu balozi akawataka waelekee chini mahala alikokuwa amefungwa Edger.Walistuka baada ya kukuta mlango mkubwa wa kuelekea chini mahala aliko Edger ukiwa umesambaratishwa na mlipuko wakatazamana na kisha wakashuka chini wakakuta milango kadhaa yote ikiwa imelipuliwa.Mlango wa chumba alimokuwa Edger Kaka ulikuwa chini baada ya kulipuliwa na mlipuko .Wote walihisi kuishiwa nguvu kwani tayari jibu walikuwa nalo.Waliingia ndani ya kile chumba lakini kilikuwa kitupu Edger Kaka hakuwemo.Balozi alichanganyikiwa alikosa cha kuzungumza.Mmoja wa maafisa akamletea karatasi iliyokuwa mezani akaichukua akaisoma akahisi mwili wote unaingiwa baridi.Yalikuwa ni yale maandishi aliyoandika Mathew kwa lugha ya kiarabu na kuyaacha mezani.Balozi alijaribu kumpigia simu mkuu wa Mossad Afrika Mashariki Avi Abramson lakini simu yake haikuwa ikipatikana balozi akazidi kuchanganyikiwa akarejea ofisini kwake
“Mathew Mulumbi karibu sana kijana wangu” akasema Dr Evans baada ya Mathew kuwasili ikulu “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Kwa kukutazama tu unaonekana umechoka na una usingizi.Pole sana” “Ahsante mzee.Kwa siku ya pili mfululizo hatujafunga ukope tumekuwa kazini hivyo lazima mwili uchoke” “Pole sana Mathew na timu yako kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya.Natamani ningekufahamu toka awali kabla sijafuata maelekezo ya washenzi wale na kuwapa Olivia naamini hivi sasa tungekuwa katika sehemu nzuri sana ya kumpata mwanangu” “Usijali mzee mimi na wenzangu tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunawapata Olivia na Coletha”kasema Mathew “Nalifahamu hilo Mathew na ninaamini mtawapata lakini kama mzazi ninaumia sana kila ninapowaza mwanangu yuko katika mikono ya wale makatili ambao wanaweza wakamuua muda wowote.Anyway tuweke pembeni hayo.Nataka kuwapeni pongezi nyingi kwa kazi kubwa mliyoifanya.Kwa dhati kabisa ninasema mnastahili tuzo ya kipekee kwa namna mnavyojitoa kwa taifa lenu.Nawaomba msichoke kwani bado tunayo kazi ya kufanya kusafisha nchi na kuwaondoa hawa magaidi ambao wameanza kuleta hofu nchini.Mafanikio mliyoyapata usiku wa leo ni makubwa na ya kupongezwa sana,Edger Kaka amerejeshwa nchini na ninaamini kupitia kwake tutafahamu mambo mengi.Nimetazama taarifa za habari za mashirika mbali mbali makubwa ya habari duniani na habari kuu iliyopewa kipaumbele kile kilichotokea jijini Nairobi katika ubalozi wa Israel.Wengi wametoa taarifa kwa ufupi sana wakiahidi kutoa taarifa zaidi baadae.Kazi nzuri sana mmeifanya lakini kama nilivyosema tuendelee kutega masikio kusikia kile kinachoendelea huko Nairobi” akasema Dr Evans “Usiwe na hofu mzee tumejitahidi sana kuhakikisha kwamba tunaifanya operesheni kwa umakini mkubwa bila kuacha nyayo yoyote nyuma inayoweza kusababisha watu wakafuatilia na kugundua ni sisi.Imekuwa ni operesheni ya siri kama walivyofanya Mossad katika ardhi yetu” akasema Mathew na Dr Evans akainama akavuta pumzi ndefu na kusema “Jana usiku mida ya saa saba hivi nilipigiwa simu na wale jamaa na kama tulivyokuwa tumehisi ni kweli walitaka niwapatie Edger kaka ili waweze kumuachia mwanangu.Niliwaeleza ukweli kwamba hatutafanya makubaliano tena na magaidi.Walinipa hadi saa mbili za asubuhi ya leo niwe nimemuandaa Edger Kaka na watanipigia kunipa maelekezo zaidi.Sikuwaogopa nami nikawaeleza kwamba itakapofika muda huo huo wawe wamemrejesha mwanangu kwani nitatumia kila nguvu niliyo nayo kuhakikisha ninawafyeka wote.Mazungumzo yale yalikuwa ni kama tamko la vita.Usiku mida ya saa tisa kuelekea saa kumi nilipigiwa simu na mkuu wa jeshi la polisi akinijulisha kwamba kumetokea tukio baya katika shule ya sekondari ya wasichana ya St Getrude ambako watu wasiojulikana wamevamia wakaua walinzi na kisha kuwateka wasichana sitini na sita a walimu wao watatu.Usiku huo huo jeshi la polisi lilianzisha msako mkali sana kuwatafuta watekaji hao na hadi kumepambazuka bado hakuna taarifa zozote za kuwapata watekaji wala wasichana.Saa kumi na moja na nusu za asubuhi nilipigiwa simu tena na wale jamaa wakanijulisha kwamba wao ndio waliowateka wasichana wale na wakanitaka niwapatie Edger kaka ama wasichana wote watauawa.Wameendelea kusisitiza kwamba ikifika saa mbili kamili za asubuhi watapiga simu kujua kama tayari nimemuandaa Edger Kaka na kama sintakuwa nimemuandaa basi wataanzia hapo kuua msichana mmoja baada ya mwingine hadi pale nitakapotekeleza ombi lao.Mathew nimechanganyikiwa na sijui nifanye nini kibaya zaidi mmoja wa wasichana waliotekwa katika shule hiyo ni mtoto wa waziri mkuu” akasema Dr Evans na kutulia kidogo. “Katika matukio yote yalitotokea ndani ya kipindi hiki kifupi nimekuwa kimya na sijamueleza mtu jambo lolote kama ninafahamu watu wanaoyatekeleza imekuwa ni siri kubwa.Hata alipotekwa mwanangu sijamweleza mtu yeyote kama ametekwa na magaidi bali nimekuwa nikiwaeleza kwamba mwanangu yuko sehemu salama.Nilikuwa nataka kulimaliza suala hili kimya kimya kwani nikiliweka wazi mambo mengi ya siri yataibuka ambayo sitaki yajulikane na kubwa zaidi ni hii idara ya siri ya mambo ya ndani ya nchi ambayo wengi hawaifahamu kama ipo.Idara hii inanisaidia sana mimi binafsi katika kutekeleza majukumu yangu.Mathew sitaki watu wafahamu kwanza kuhusu idara ile ya siri,pili kuhusu Edger Kaka kuwa hai na vile vile kuhusu kutekwa kwa Olivia,Agrey themba na Coletha.Sitaki watu wajue kama nimekuwa nikiwasiliana na magaidi kwa siri na kujadiliana nao kuwapa kile wanachokitaka ili wamrejeshe mwanangu.Kinachonipa hofu ni kwamba magaidi wale wanaweza wakaanza kuwaua watoto waliowatea kama walivyoahidi ili kunishinikiza kuwapa Edger Kaka.Siko tayari na siwezi kuwapa kile wanachokitaka na kichwa changu kinapouma.Nishauri Mathew nini tukifanye? akasema Dr Evans “Mzee kwanza kabisa pole sana kwa huu mtikisiko unaoendelea ninachoweza kukushauri ni kwamba usilegeze msimamo wako.Kama umeamua jambo hili liwe siri basi liendelee kuwa siri wakati tukilitafutia ufumbuzi.Kuna mambo mengi yanaambatana na jambo hili ambayo hayatakiwi kujulikana” “Mathew nina wasiwasi sana na hili jambo ndiyo maana nimekuwa kimya nikisubiri kwanza urejee ili unishauri nini cha kufanya.Sitaki jambo hili la siri lijulikane ndiyo maana nataka unishauri nini cha kufanya.Mathew kuna wakati ninajikuta ninawaza kwa nini jambo hili sikuliweka wazi mapema? Yawezekana ningeliweka wazi na kuwakabidhi vyombo husika hivi sasa tayari magaidi hawa wangekuwa wamekwisha dhibitiwa na mateka wote wameokolewa.Nina wasi wasi mwingi Mathew nini kitatokea itakapofika saa mbili za asubuhi? Je nivitaarifu vyombo vya uchunguzi jambo hili? Ninawaza hadi nahisi kichwa kinataka kupasuka” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais japo suala hili linazidi kuchukua sura mpya lakini nakuomba usikate tamaa.Bado tunao uwezo wa kupambana na hawa magaidi na kuwakomboa watu wetu kimya kimya bila mambo yale ya siri kujulikana.Tunaye mtu wao muhimu sana wanayemtafuta na ambaye tunaweza kumtumia kuwapata watu wetu.Naomba kibali cha kukumhoji Edger kaka na kupata taarifa za muhimu kutoka kwake kuhusiana na mtandao wao na namna ya kuweza uwapata Olivia na Coletha.Mheshimiwa Rais endelea kulifanya suala hili kuwa siri kwani endapo utaamua kuliweka wazi litafumua mambo mengi yaliyofichika.Ukiamua kuliweka wazi fahamu kwamba hakutakuwa tena na idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi ambayo ni muhimu na inafanya kazi nzuri,uvamizi wetu katika ubalozi wa Israel lazima utajulikana na maisha yangu na watu wangu tuliofanya uvamizi huo yatakuwa shakani Mossad watatuandama sisi na familia zetu hadi wahakikishe wamelipa kisasi.Mheshimiwa Rais kwa namna yoyote ile suala hili halipaswi kujulikana linapaswa kuendelea kuwa siri kwani ndani yake kuna mkusanyiko wa mambo mengi” akasema Mathew “Mathew si kwamba na mimi ninapenda iwe hivyo lakini hawa magaidi wananilazimisha nifanye hivyo.Hawa watu ni wakatili kuliko wanyama wa mwituni na kwao kutoa uhai wa mtu ni kitu chepesi sana hivyo basi hawatasita kutoa uhai wa watoto wale kama walivyoahidi kwa lengo la kumpata mtu wao.Hapo ndipo akili yangu inapokwama nifanye nini kuwanusuru watoto wale wasio na hatia yoyote wasiuawe?Je niendelee kulifanya siri jambo hili na kuyaweka hatarini maisha ya watoto wale ambao hawafahamu chochote? Je niliweke wazi hili jambo na kukubali kifo changu cha kisiasa?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais mimi ushauri wangu ni jambo hili liendelee kuwa siri.Endapo itajulikana kwamba ulikuwa unafahamu kilichotokea na umekuwa na mawasiliano na magaidi na mkafanya majadiliano bila kuhusisha vyombo husika vyenye dhamana na ulinzi wa taifa kitakuwa ni kifo chako kisiasa kama ulivyosema lakini si wewe tu bali sisi sote,watu wote wanaofanya kazi katika idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi ambao wamekuwa wakiendesha mambo yao kimya kimya bila kujulikana.Hatutabaki salama mheshimiwa Rais.Bado ninaamini kwamba tunao uwezo wa kuwadhibiti magaidi hawa na kuwakomboa mabinti zetu waliotekwa pamoja na akina Olivia.Ninaomba jambo hili utuachie mimi na timu yangu tuendelee kulishughulikia hadi mwisho wake.Nina uhakika mkubwa kwamba tutalifikisha mwisho na kuwakomboa watu wetu.Ninaposema hivi simaanishi kwamba vyombo vingine vya ulinzi na usalama havina uwezo wa kulishughulikia hili jambo lakini ni kwa ajili ya kukulinda wewe mheshimiwa Rais na sisi pia ambao tumeshirikiana nawe katika hili jambo” “Mathew nakuamini sana kijana wangu kila pale ninapokuwa nimekata tamaa unanipa moyo na tumaini la kusonga mbele.Ninauchukua ushauri wako na kuendelea kuufumba mdomo wangu kama vile sifahamu chochote kuhusiana na suala hili.Ninachokutaka Mathew japo umechoka lakini wewe na timu yako mnapaswa kuendelea na hili jukumu mtapumzika pale kazi hii itakapokuwa imekamilika.Nataka umuhoji Edger Kaka.Make him talk.Sifahamu wala sijali njia utakazotumia ninachohitaji mimi ni Edger kaka afunguke taarifa za muhimu zitakazotusaidia kuweza kuwapata wasichana waliotekwa pamoja na akina Olivia.Wewe ni mzoefu katika mambo hayo unafahamu njia nyingi za kumfungua mtu kama huyu.Nataka kabla ya kufika saa mbili za asubuhi muda ambao hawa jamaa wanataka wampate Edger,uwe umefanikiwa kupata chochote cha kutusaidia kuwapata watoto wetu.Nimeitisha kikao cha dharura cha baraza kuu la usalama wa taifa saa mbili na nusu za asubuhi hivyo nataka hadi kufika muda huo tayari muwe mmepata taarifa kutoka kwa Edger Kaka ambazo zitatuwezesha kujua mahala walipo watekaji.Nataka tuufahamu mtandao wao wote.Mathew naomba kazi hii kubwa tuliyoifanya isiende bure” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwa mara nyingine tena ninakutoa hofu na kukuahidi kwamba mimi na wenzangu tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba tunapata taarifa muhimu za kutusaidia kuwapata watu wetu waliotekwa na IS.Vile vile bado naendelea kukusisitiza kuendelea kuliweka jambo hili siri” “Nitafanya hivyo Mathew.Nawategemea sana ninyi katika hili suala vinginevyo hali itakuwa mbaya sana kwa upande wangu.Endapo watapiga tena simu hawa jamaa nitakujulisha” akasema DrEvans “Nashukuru mheshimiwa Rais mimi ngoja nikaendelee na kazi” akasema Mathew kisha wakaagana akaondoka. “Magaidi ni watu wenye roho mbaya kuliko hata Simba na bila kufanya juhudi watoto wetu watachinjwa ili kumshinikiza Rais aweze kuwapatia wanachokihitaji.Kwa namna yoyote ile Edger Kaka hataweza kuingia katika mikono yao.Yule ndiye atakayetusaidia sisi kuwafahamu magaidi hao na mtandao wao.” akawaza Mathew Alirejea katika makazi yao na kuwaita Devotha na Gosu Gosu.Ruby alikuwa chumbani kwake akipumzika “Nimetoka kuonana na Rais na mambo niliyoyakuta huko ni makubwa.Ndugu zangu bado tunayo kazi kubwa mbele yetu.Magaidi wa IS ndio waliowateka wasichana usiku wa leo na wanataka kuwatumia wasichana hao kumshinikiza Rais aweze kuwapatia kile wanachokitaka yaani Edger Kaka.Rais yuko katika wakati mgumu sana hivyo tunapaswa kumsaidia.Kwa nini ninasema hivyo ni kwa sababu hili suala lina mambo mengine mengi ndani yake ambayo hayapaswi kujulikana ndiyo maana Rais amekuwa kimya kuanzia kutekwa kwa Olivia hadi kutekwa kwa wasichana usiku wa kuamkia leo.Magaidi wale wameahidi kumpigia simu Rais leo saa mbili asubuhi kujua kama tayari amemuandaa Edger Kaka na kamabado basi wataanza kuua wasichana waliowateka. Ndugu zangu najua mmechoka sana lakini kazi bado inaendelea na hatuna muda wa kupumzika hadi tuhakikishe tumewakomboa wasichana wote waliotekwa,Olivia na Coletha hivyo tunarejea tena katika ile kambi ya jeshi tulikomuhifadhi Edger kaka na kuanza mahojiano naye Rasmi.Leo lazima atafunguka” akasema Mathew “Nilidhani kwa kumpata Edger tutakuwa tumekaribia kulimaliza hili suala lakini kumbe mchezo umeanza upya” akasema Devotha “Mathew usiwe na hofu kama ulivyosema tutapumzika pale tutakapokuwa tumelimaliza hili jambo”akasema Gosu Gosu “Ahsanteni sana” akasema Mathew na kwenda kumuaga Ruby wakaondoka. *************** Gari aina ya fuso lililowabeba wasichana waliotekwa kutoka shule ya sekondari ya St Getrude huku likisindikizwa na gari nyingine mbili lilikatisha katika viunga vya jiji la Dar es salaam bila kutiliwa shaka yoyote hadi lilipofika katika nyumba moja kubwa eneo la magetini iliyozungushiwa uzio mkubwa na kilichoweza kuonekana ukiwa nje ni bati la kijani.Miti mbali mbali ya kivuli na minazi viliizungka ile nyumba.Geti la nyumba ile likafunguliwa na gari zile zikaingia ndani.Lile gari kubwa aina ya Fuso ambamo ndimo wanafunzi wote walikuwa wamepanda likafunguliwa mlango mkubwa wa nyuma na watu nane wakashuka wakiwa na silaha.Nazil Jalib kiongozi wa opereseheni ile naye akashuka kutoka kutoka katika gari dogo na kuwafuata wale jamaa akaanza kuwapongeza “eamal jayid !!(kazi nzuri) ndiyo maneno aliyokuwa akiyasema Nazil kwa lugha ya kiarabu kila alipokuwa anampongeza mmoja wa watu wale waliofanikisha kuwateka wale wasichana.Baada ya kumaliza kuwapongeza,wote wakasimama kimya kumsikiliza ‘ana saeid lilghayat alyawm bima faealtaha. ma faealtuh alyawm hu bidayat alharb alty la tantahi dida alwilayat almutahidat al'amrikiati. 'uqsim biaism allah 'anahum sayadfaeun thmnaan bahzaan jdaan likuli ma faealuh lana. ma faealtuh alyawm hu 'iieadat tashkil jil 'iilaa jilin.( “Nimefurahi leo kwa yale mliyoyafanya.Mlichokifanya leo ni mwanzo wa vita vya kudumu dhidi ya maadui zetu.Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu,watalipa kwa gharama kubwa sana kwa kila kitu ambacho wametufanyia.Kwa mlichokifanya leo mtakumbukwa na vizazi hadi vizazi”) Baada ya maneno yale aliyoyatamka Nazil watu wake wakainua bunduki zao juu kuonyesha ishara ya utii halafu Nazil akasema “Haraka sana washusheni wasichana wote wapelekwe katika chumba kilichoandaliwa halafu hao walezi wao wapelekwe katika chumba kingine wakafungiwe” akaelekeza Nazil na kwa haraka wasichana wale wakaanza kushushwa kutoka katika lile gari walimokuwamo aina ya Fuso wakaingizwa ndani huku wakihesabiwa.Jumla walikuwa wanafunzi sitini na sita. Ndani ya lile jumba kubwa kulikuwa na chumba kikubwa ambacho hutumiwa kwa ajili ya ibada na wanafunzi wale wote wakawekwa ndani ya chumba kile,walimu wao watatu wakafungiwa ndani ya chumba kingine. “Msiogope mabinti.Sisi si watu wabaya lakini serikali yenu ndiyo mbaya.Tumewaleteni hapa kwa muda ili kuishinikiza serikali yenu kutupa kile tunachokitaka na wakishatupatia tunachohitaji tutawaacha huru lakini kama hawatakuwa tayari kutupa kile tunachohitaji tutawauweni mmoja baada ya mwingine” akasema Nazil Jalib na wasichana wale wakaanza kulia “Quiety ! akafoka na wasichana wale wakatulia “Sijawaambia kwamba tunaanza kuwaua bali tunasubiri kwanza utekelezaji wa serikali yenu kwa kile tunachokitaka na kama wakitekeleza tunavyotaka sisi basi tutawaachia huru” akasema Abdul na kuagiza wanafunzi wale wapewe maji ya kunywa.Maboksi ya chupa za maji yakaingizwa wakaanza kupewa maji ya kunywa Nazil alienda katika chumba kimoja chenye vifaa mbali mbali ya mawasiliano akampigia simu Fahad “Mambo yanakwendaje Nazil?Akauliza Fahad akiwa nchini Kenya “Fahad kila kitu kimekamilika tayari wasichana wamefikishwa hapa kwako wote wako salama tumewahifadhi tukisubiri maelekezo yako” akasema Nazil “Kazi nzuri sana Nazil. Ni wakati wa kumuonyesha Rais wa Tanzania kwamba sisi hatuna mchezo hata kidogo.Tukisema kitu tunakimaanisha.Kwa sasa endeleeni kuwachunga hao wasichana mimi nitaondoka hapa Nairobi kwa ndege ya saa kumi na mbili za asubuhi nitafika Dar es salaam saa moja na nusu .Saa mbili kamili za asubuhi nitampigia simu Rais kumuuliza kama tayari anaye Edger Kaka na kama akiendelea kuwa kiburi basi tutaanza zoezi la kuua wanafunzi mmoja mmoja hadi pale atakapoamua kutekeleza kile tunachokitaka.Tutawaua mubashara huku watu wakishuhudia hivyo anzeni maandalizi ya tukio hilo kubwa ambalo watanzania hawajawahi kulishuhudia nchini kwao” akasema Fahad akiwa jijini Nairobi. “Sikufikiria kumwaga damu ya watanzania hasa watoto ambao hawana kosa lolote lakini yote haya ameyataka Rais wao kwa kutaka kushindana nasi.Nitamuonyesha nguvu yetu pale nitakapoanza kutoa uhai wa msichana mmoja baada ya mwingine” akawaza Fahad.
Rais wa Zanzibar akiwa ameongozana na makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar waliwasili ikulu jijini Dar es salaam tayari kuhudhuria kikao maalum cha dharura cha baraza la usalama la taifa kilichoitishwa na Rais kujadili hali ya usalama wa taifa kufuatia mfululizo wa matukio ya kigaidi.Baraza hili la usalama la taifa hujumuisha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama mwenyekiti,makamu wa Rais wa Tanzania,Rais wa Zanzibar,makamu wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na waziri mkuu wa Tanzania kama katibu.Viongozi wengine walioalikwa katika kikao hicho ni wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama vilivyopo nchini. Mara tu baada ya Rais wa Zanzibar kuwasili kikao kikaanza bila kuchelewa. “Ndugu wajumbe wa baraza hili na wengine waalikwa karibuni sana.Nimelazimika kuitisha kikao hiki cha dharura kufuatia mfululizo wa matukio ambayo yanahatarisha amani na usalama wa nchi.Ndani ya kipindi kifupi sana kumetokea matukio ambayo yameleta hofu kubwa kwa raia wetu.Tukio la kwanza lilikuwa ni kutekwa kwa Olivia Themba na baba yake Agrey Themba.Mpaka leo hii hawajapatikana.Lilitokea tena tukio lingine la shambulio katika hospitali ya Mtodora na watu kadhaa kuuawa.Kabla tukio hilo halijapoa wametekwa tena wasichana wengine sitini na sita.Matukio haya yote yametokea ndani ya wiki moja tu,vyombo vyetu vya ulinzi wa taifa viko wapi?Kwa nini mpaka sasa matukio haya yanaendelea kutokea nchini? Akina nani wanaofanya matukio haya?Mmefikia wapi hadi sasa katika kuwabaini na kuwatia nguvuni? Kuna maswali mengi sana yanayoibuka kufuatia matukio haya ambayo yanahitaji majibu.Tuanzie kwanza na tukio lililotokea usiku wa leo la kutekwa kwa wasichana sitini na sita katika shule ya sekondari ya St Getrude.Jeshi la polisi hebu tupeni picha halisi nini hasa kimetokea huko?Watoto hawa wametekwa katika mazingira gani? Hatua gani mmepiga hadi sasa katika kufahamu mahala walipo na nani waliowateka?akauliza Dr Evans kana kwamba hafahamu chochote. “Mheshimiwa Rais” akasema mkuu wa jeshi la polisi “Mida ya saa kumi alfajiri ya leo nilipigiwa simu na kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam akanijulisha kuwa amepata taarifa za kutokea kwa uvamizi katika shule ya sekondari ya St Getrude na wakati ananipigia simu alikuwa njiani akielekea huko akiwa na kikosi ha askari waliojihami silaha kali kwenda kuthibitisha taarifa hizo.Walipofika huko walikuta ni kwelli tukio hilo limetokea na wanafunzi sitini na sita wakiwa wametekwa pamoja na walimu wao watatu huku walinzi wanne wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi.Taarifa za awali ambazo jeshi la polisi tunazo zinaonyesha kwamba watu hao walifika shuleni hapo mida ya saa tisa usiku kuelekea saa kumi na kufanya tukio hilo ovu.Jeshi la polisi tayari tumekwisha anza uchunguzi wa awali wa tukio hilo tukifuatilia picha za kamera za barabarani ambako tunahisi watu hao walipita baada ya kuwateka watoto.Kimeundwa kikosi maalum kwa ajili ya kulishughulikia suala hili mheshimiwa Rais na wako kazini.Kuhusu matukio yale mengine ya nyuma..” akasema mkuu wa jeshi la polisi lakini Rais akamkatisha “Jeshi la polisi tumechoka na chunguzi zisileta majibu.Tunataka matokeo ya haraka,tunataka kujua watoto wako wapi na waliowateka ni akina nani.Tunataka kufahamu wapi alipo Olivia Themba na baba yake Agrey Themba,tunataka kujua nani waliofanya shambulio katika hospitali ya Mtodora na kusababisha vifo vya watu wasio na hatia.Nataka kusikia mipango inayoweza kutupa majibu ya haraka kuwafahamu watu hao ni akina nani hasa katika suala hili la wanafunzi kutekwa nyara.Hatujui lengo la watu hao ni nini kwa kuwateka hao wanafunzi.Hili jambo lipewe uzito mkubwa sana” “Mheshimiwa Rais toka yalipoanza matukio haya jeshi la polisi hatujalala tuko macho saa ishirini na nne tukichunguza na tunaendelea vizuri.Mheshimiwa Rais watu hawa wanaotekeleza haya matukio ni watu waliojiandaa vyema na wanafanya kitaalamu sana wakijihadhari kutokuacha nyayo zozote nyuma zinazoweza kusababisha wakagundulika ndiyo maana uchunguzi umechukua muda lakini tuko pazuri”akasema mkuu wa jeshi la polisi “Idara ya kudhibiti na kupambana na ugaidi nini kinaendelea kwa upande wenu?Mko kimya sana na matukio ya ugaidi yanaendelea kufululiza hapa nchini,jukumu lenu kubwa ni kupambana na kudhibiti ugaidi lakini hamuonekani kutekeleza jukumu lenu na kuwaachia magaidi uwanja mpana wa kutawala na kufanya kile watakacho.N…..” Dr Evans akanyamaza baada ya kusikia mtetemo katika koti lake,akaitoa simu kutazama mpigaji akahisi kuchanganyikiwa akatazama saa ukutani ilikuwa ni saa mbili kamili za asubuhi.Akaitazama simu ile ikiita na kukata.Wote mle ndani ya chumba walikuwa kimya wakimtazama Rais,simu ikaanza kuita tena akashindwa kuipokea. “Tuendelee.Nataka kupata taarifa kutoka kwa idara ya kupambana na kudhibiti ugaidi.Katika matukio haya yote yaliyotokea ninyi mmepiga hatua gani katika kuwabaini waliotekeleza….”akanyamaz a Rais baada ya simu yake kuita tena.Akaomba radhi akatoka nje ili aweze kupokea.Alikuwa na hasira nyingi zilizochanganyika na woga,akawataka walinzi wake wasogee mbali kidogo wampe nafasi kisha akaipokea ile simu “Nilikupa hadi saa mbili kamili uwe umemrejesha mwanangu umefanya hivyo tayari?akauliza Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais nataka unisikilize vizuri.Ulitangaza vita na sisi na tayari vita hiyo imeanza.Kama nilivyokujulisha kwamba tayari tunawashikilia wasichana sitini na sita na walimu wao watatu.Hatima ya maisha yao iko mikononi mwako.Utaamua kama unataka kuwaokoa au kama unataka kuwaangamiza.Kuwaokoa wasichana hao tunataka utupatie Edger Kaka na kwa kuwa umekuwa kiburi na kutaka kupambana nasi tutafanya majadiliano mengine kuhusu mwanao Coletha” “Bastard ! akasema Dr Evans kwa hasira “Mheshimiwa Rais hatuhitaji kuwafanya kitu chochote hawa wasichana wasio na kosa hivyo basi ninakuongezea saa moja hadi saa tatu kamili.Nitakupigia tena simu na wakati huo nataka tayari uwe na Edger Kaka kisha nitakupa maelekezo wape apelekwe na wapi pa kwenda kuwachukua wasichana wenu.Baada ya hapo tutaanza majadiliano kuhusu mwanao.Endapo utashindwa kutekeleza maelekezo hayo hadi kufika saa tatu kamili za asubuhi tutaanza kuua msichana mmoja kila baada ya dakika thelathini kwa kumchinja shingo na kitendo hicho kitafanyika huku watanzania wakishuhudia mubashara kupitia simu zao.Nakuonya tena mheshimiwa Rais usijaribu kupambana nasi.Sisi ni jeshi kubwa na tumesambaa hapa nchini na ukijaribu kupambana na sisi Tanzania itageuka nyekundu kwa damu nyingi itakayomwagika.Tutazungu mza tena saa tatu kamili” akasema Yule jamaa na kukata simu.Dr Evans alijikuta akihisi baridi na kushindwa kutamka chochote.Akaitazama simu yake kwa sekunde kadhaa halafu akazitafuta namba za Mathew akampigia lakini simu ya Mathew haikuwa ikipatikana akazidi kuchanganyikiwa akarejea tena katika chumba cha mikutano kuendelea na kikao kile na wajumbe wa baraza la usalama la taifa
Geti la kambi ya kikosi cha operesheni maalum likafunguliwa na gari la akina Mathew likapita.Tayari walikwisha wasiliana na Austin na kumjulisha kuwa wanakwenda kuanza mahojiano na Edger Kaka.Wote wakazima simu zao kwani ukiwa ndani ya kambi ile huruhusiwi kutumia simu ya mkononi bali zipo simu maalum unazoweza kutumia kupiga.Walifika hadi katika jengo la utawala wakapokewa na kuongozwa moja kwa moja hadi katika ofisi ya Austin “Karibuni tena ndugu zangu”akasema Austin “Ahsante Austin.Utatuwia radhi kwani tutaendelea kuwa wageni wako na tutafika hapa mara kwa mara kila pale tutakapokuwa na uhitaji na mtu wetu” “Mathew msijali tafadhali kuweni na amani.Hili ni suala la kitaifa hivyo basi lazima tuhakikishe linakamilika” “Ahsante sana Austin.Tumelazimika kurejea tena kuja kuanza kumuhoji Edger.Usiku wa kuamkia leo watu wa IS wamevamia na kuteka wasichana sitini na sita katika shule ya sekondari ya St Getrude na lengo kubwa la kuwateka wasichana hao ni kumshinikiza Rais aweze kumuachia Edger Kaka” akasema Mathew “Wana uhakika kama Rais anafahamu mahala alipo Edger? Akauliza Austin “Hawajui chochote kuhusu Edger Kaka kama alitekwa na Mossad na alikuwa Nairobi,wao wanaamini yuko hai na mchezo ule ulifanywa na serikali ya Tanzania ndiyo maana wanatumia kila njia kushinikiza Rais aweze kumuachia mtu wao”akajibu Mathew “Saa mbili kamili za asubuhi watampigia simu Rais kujua kama tayari amekwisha muandaa Edger na kama hatatekeleza hilo basi wataanza kuwaua wale wasichana.Tumelazimika kuja tena hapa kumuhoji Edger Kaka atusaidie kufahamu mtandao wao hapa nchini ili tuweze kuwaokoa wale wanafunzi pamoja na mtoto wa Rais” akasema Mathew “Sawa Mathew nimekuelewa hapa tuna chumba maalum kwa ajili ya mahojiano mtakitumia chumba hicho kumuhoji Edger na kama mkihitaji kuingia katika hatua nyingine zaidi ya kutumia nguvu kipo chumba maalum kwa ajili hiyo na wapo wataalamu wa kuifanya hiyo kazi” akasema Austin huku akiinuka “Tunaye mtaalamu wetu wa kutesa ambaye ni Gosu Gosu.Hakuna aliyewahi kuingia katika mikono yake akashindwa kufungua mdomo wake lakini kwa afya ya Edger Kaka tunataka kwanza kumuhoji bila kutumia nguvu” akasema Mathew wakatoka mle ofisini na Austin akawaongoza hadi katika chumba cha mahojiano kulimokuwa na meza na viti viwili.Mathew akaingia mle ndani na baada ya dakika tatu Edger Kaka akiwa amefungwa pingu mkononi akaingizwa ndani ya kile chumba akiwa anasukumwa katika basikeli ya magurudumu kwani bado hakuwa na uwezo wa kutembea.Mathew akaamuru afunguliwe mikono abaki huru na watu wote watoke nje akabaki na Edger, akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema “Edger Kaka pole sana kwa masahibu yote yaliyokupata kwa muda wa miaka mitatu.Lakini yote hayo yamekwisha sasa umerejea nyumbani.Unajisikiaje kurejea tena nyumbani? Akauliza Mathew.Edger akajaribu kuzungumza lakini sauti ikamkwama Mathew akaomba kuletewa maji Edger akanywa “Sasa niambie Edger unajisikiaje kurejea nyumbani ? Akauliza Mathew “Unataka nikwambie nina furahi?I’m not happy at all.Mlikosea sana msingesumbuka kuja kunikomboa na kunirejesha tena Tanzania” akasema Edger kaka “Kwa nini unasema hivyo Edger? Hupendi Tanzania?Hupendi kurejea nyumbani? Akauliza Mathew “Because I’m dead already.Nimeonyeshwa video ya mazishi yangu namna watu walivyonililia wakijua nimefariki dunia wengine wakipoteza fahamu baada ya kupita katika jeneza ambalo waliamini kuna maiti yangu lakini kumbe ulikuwa ni mchezo umetengenezwa.Imeniumiza sana baada ya kulifahamu hilo jambo na siwafichi ninatamani hata sasa mnipige risasi nife niondoke kabisa katika dunia hii” akasema Edger “Edger waliofanya tuko lile si Tanzania bali ni Israel wakitumia shirika lao la ujasusi la Mossad na ndiyo maana baada ya kufahamu kwamba uko hai tukafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kukukomboa na kukurejesha nyumbani.Tumetengeneza mgogoro mkubwa sana wa kidiplomasia kati yetu na Israel kwani tumelazimika kuua watu wao wengine wa muhimu kabisa ili tuweze kukukomboa.Naweza kusema kwamba serikali ya Tanzania kwa kukuthamini imetumia gharama kubwa kukukomboa na kukurejesha nyumbani.Unapaswa kufurahi”akasema Mathew “Ninashukuru kwa kunitoa katika nyumba ile ya mateso lakini haikuwa na ulazima wowote wa kutumia gharama kubwa kunikomboa”akasema Edger “Edger wewe ni mtanzania na ilikuwa lazima kwa gharama zozote zile tukurejeshe nyumbani”akasema Mathew na kumtazama Edger kwa sekude kadhaa halafu akasema “Edger unaweza ukatueleza sababu za Israel kutumia gharama kubwa kutengeneza kifo chako wakati bado uko hai?akauliza Mathew na Edger akabaki kimya “Nijibu Edger swali nililokuuliza” “Sifahamu chochote” akasema Edger “Edger jina langu ninaitwa Mathew Mulumbi ndiye niliyeongoza operesheni ya kuja kukukomboa na kukurejesha nyumbani.Hapa uko sehemu salama na mateso yote uliyoyapata kwa miaka mitatu yamekwisha.Hapa ndipo patakuwa chimbuko la maisha yako mapya.Mheshimiwa Rais anafahamu kuwa uko hapa na ndiye aliyetoa kibali cha kufanya operesheni ile ya siri ya kukukomboa na yuko tayari kukufanyia kitu chochote unachokihitaji ili uanze maisha yako upya lakini amenituma hapa kwako nije kuzungumza nawe ili tuufahamu ukweli wote kwa nini ulitekwa na Israel?Usihofu hapa uko sehemu salama na hakuna anayefahamu kama uko hapa hivyo kuwa huru”akasema Mathew na Edger akainamisha kichwa akazama mawazoni “Edger please usiipoteze hii nafasi uliyoipata.Hii ni tiketi ya kuelekea maisha mapya hivyo itumie kikamilifu” akasema Mathew “Sifahamu chochote kwa nini waliniteka nyara na kunipa mateso yale makali kwa miaka mitatu.Watu wale ni wanyama mno! Akasema Edger na sura ya Mathew ikaanza kubadilika “Who is Habiba Jawad? Akauliza Mathew na Edger akastuka “Umesema nani? “Habiba Jawad ni nani? “Si..simfahamu” akajibu Edger.Mathew akamtazama kwa macho makali “Edger Kaka narudia tena kauli yangu kwamba hapa panaweza kuwa chimbuko la maisha yako mapya au panaweza kuwa ni mwisho wa maisha yako hivyo ni jukumu lako kuchagua nini unakitaka kuishi au kufa.Mimi ninayezungumza nawe hapa ninamuwakilisha Rais hivyo sihitaji mzaha.Ninapokuuliza nataka unipe majibu ya kweli kama ukitaka kuwa kiburi nakuhakikishia hautafika kokote Edger.Mateso uliyoyapata nchini Kenya kwa miaka mitatu yanatosha sana hatutaki kuendelea kukutesa hata hapa nyumbani hivyo funguka,kuwa mkweli tueleze nini kilitokea na sisi tutajua namna ya kukusaidia.We need information from you” akasema Mathew “Mathew Mulumbi,right?akauliza Edger “Ndiyo”akajibu Mathew “Nakwambia kweli kabisa kwamba sifahamu sababu ya kutekwa na kupelekwa mafichoni kwa miaka mitatu.Kama kuna taarifa zozote mlizopewa kuhusu mimi si taarifa za kweli hata kidogo”akasema Edger “Mzaha umeisha ngoja nikueleze ukweli.Edger wewe unashirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS.Ukiwa katika matibabu nchini Israel ulitembelewa na watu wawili ambao ni wafadhili wakuu wa kundi hili na mengine mengi ya kigaidi ambao ni Habiba Jawad na Sayid Omar na hapo ndipo Israel walipoanza kukufuatilia na hatimaye kukuteka wakaenda kukuficha jijini Nairobi katika ubalozi wao wakitaka kupata taarifa za mahala walipo Habiba Jawad na wenzake wanaofadhili ugaidi” akasema Mathew na jasho likaonekana usoni kwa Edger “Taarifa zinaonyesha kwamba chanzo cha ugonjwa wako uliosababisha upelekwe nchini Israel ni sumu Dr Olivia Themba aliyapigania maisha yako hadi ukapona,aliweka rehani maisha yake kwa ajili yako lakini umemuingiza katika mtandao wa IS.Haya ndiyo malipo kwa mtu kama huyu ambaye alipambana kuokoa maisha yako? Akauliza Mathew kwa ukali “Sikuwahi kumuingiza Olivia katika IS” akajibu Edger Kaka “Kama si wewe nani aliyemuunganisha Olivia na kundi la IS? “Olivia hayupo katika kundi la IS” akajibu Edger “Umejuaje kama Olivia si mfuasi wa IS?akauliza Mathew na Edger akabaki kimya.Mathew akapiga meza kwa nguvu “Answer me Edger !! “Olivia is not IS ! akasema Edger kwa sauti ya juu halafu akainamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa na kusema “Look guys Olivia ni mtu muhimu mno kwangu.She saved my life.Kama si yeye kupigania maisha yangu hivi sasa wala msingekuwa mnanihoji ningekwisha kufa zamani sana.Hakuna kiasi chochote cha pesa kinachoweza kufikia thamani ya Olivia kwangu.Thamani yake ni kubwa kuliko tani ya dhahabu,almasi na kila kito cha thamani unachokifahamu.Zaidi ya yote kuna kitu ambacho hamkifahamu.Mimi na Olivia tulikuwa tunaelekea kuwa wapenzi.Ni mwanamke pekee ambaye moyo wangu umemuangukia na kumpenda hata yeye pia alikwisha tokea kunipenda” akasema Edger “Muongo mkubwa we !Ungekuwa unampenda Olivia usingemuingiza katika kundi lenu la kigaidi.Umeyaharibu maisha yake.Olivia wa sasa si Olivia Yule unayemfahamu wewe.Amekuwa muuaji hana huruma hata chembe kutoa roho ya mtu.Kwa kushirikiana na IS ametengeneza kirusi cha maangamizi ambacho wanataka kukitumia kufanya mashambulio yao ya kigaidi.Kwa nini ukakubali mwanamke unayempenda ageuke kuwa mkatili namna hii? Akauliza Mathew “Mimi sijamuingiza Olivia IS na siwezi kufanya kitu kama hicho.Mara ya mwisho kuonana na Olivia ni uwanja wa ndege wa Julius Nyerere tulipotoka Israel.Tuliagana kwa miadi ya kuonana kesho yake lakini huo ukawa ni mwisho wa kuonana naye kwani hiyo kesho haikunikuta Tanzania tayari nilikuwa nimetekwa na sifahamu chochote kilichokuwa kinaendelea wakati nikiwa nimeshikiliwa na Mossad.Taarifa za kwamba mimi ndiye niliyemuingiza Olivia IS si za kweli.Kwanza Olivia hafahamu chochote kuhusu IS” akasema Edger.Mathew akamtazama kwa macho yaliyojaa hasira halafu akasema “Walipokuja wale majasusi wa Mossad kukuhoji uliwaambia wakusaidie kumtafuta Olivia na utawaeleza kila kitu wanachokitaka.Hapo ulionyesha kweli unampenda Olivia na uko tayari kufanya kitu chochote ili kumpata.Nataka kufahamu kama unaendelea kusimama katika kauli yako kwamba ukimpata Olivia utakuwa tayari kufunguka”akasema Mathew “Olivia ninampenda kuliko kitu chochote na sintoacha kumpenda ndiyo maana niliwaamba wale watu wa Mossad waniletee Olivia mwanamke ninayempenda nami nitawaeleza kile wanachotafuta kwangu.Niko tayari kufanya chochote kwa ajili yake” “Ahsante kwa kuweka wazi namna unavyompenda Olivia.Lakini kuna tatizo katika kumpata.Olivia yuko katika mikono ya IS hivi sasa” “Mikono ya IS kivipi?akauliza Edger “Ngoja nitumie dakika chache kukupa maelezo kidogo.Idara ya usalama wa taifa ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo walipata taarifa kwamba mmoja wa watu wa IS anaitwa Seif Almuhsin anatembelea nchini kwao hivyo wakaanza kujiandaa kumfuatilia.Alipofika Kinshasa wakaanza kumfuatilia na wakagundua kwamba alikutana na mwanamke mmoja wa kitanzania ndipo taarifa zilipotumwa huku Tanzania na akagundulikwa kwamba ni Olivia Themba.Ililazimu idara zinazihusika na usalama wa nchi kumteka Olivia mara tu aliporejea kutokea Kinshasa na lengo likiwa ni kutaka kujua mahusiano yake na watu wa IS.Kuthibitisha kwamba Olivia ni mtu wao IS walishambulia hospitali ya Mtodora wakaua watu na kumteka mtoto wa Rais wakimshinikiza Rais awakabidhi Olivia na Rais katika jitihada za kutaka kumkomboa mwanae akalazimika kuwapa Olivia na mpaka sasa hatujui yuko wapi ndiyo maana tunahitaji sana msaada wako tuweze kumpata ili utueleze kile tunachotaka kukisikia kuhusu IS.Edger machoni pa watu tayari umekwisha kufa na kusahaulika hata IS hawajui kama uko hai hivyo basi ni wakati wako wa kuachana nao na kuishi maisha mapya.Rais yuko tayari kukusaidia kuanza maisha mapya kwa kukutafutia nchi ambako utakwenda kujificha huko ukiwa na Olivia.Huo ndio msaada pekee ambao Rais wa Tanzania yuko tayari kukusaidia kama nawe utakuwa tayari kutusaidia” akasema Mathew na Edger akainamisha kichwa “Edger tafadhali tusaidie tukusaidie.IS wana mipango miovu sana dhidi ya nchi yetu.Usiku wa kuamkia leo wamevamia shule ya sekondari ya wasichana na kuteka wasichana sitini na sita ambao mpaka sasa hawajulikani walipo.Edger umekuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano na ulijizolea sifa nyingi sana kutokana na utendaji wako wa kazi hasa katika kupiga vita ufisadi.Una mapenzi makubwa na nchi hii na siamini kama uko tayari kuona IS wakihatarisha amani na usalama wa nchi yetu.Watu wanaishi kwa hofu hivi sasa kwani IS wametishia kufanya mashambulizi mengi hapa nchini.Kama uliona video ya mazishi yako ya bandia utakuwa umeona namna watu walivyokuwa na mapenzi makubwa nawe,wengi walipoteza fahamu kukulilia.Edger upendo ule ni mkubwa na ninaamini hauko tayari kuwaona watu wale ambao walikupenda na wakawa na matumaini makubwa kwako wakiishi kwa mashaka na kukosa amani.Tusaidie kuufahamu mtandao wa IS hapa nchini na sisi tutakupatia kila unachokihitaji ili kuyaanza maisha mapya.Mwanamke unayempenda yuko katika mikono ya IS,wasichana sitini na sita wasio na hatia wanashikiliwa mateka na wanaweza wakapoteza maisha kama juhudi za haraka za kuwatafuta hazitafanywa.Tunakutegeme a sana Edger tafadhali tusaidie” akasema Mathew.Edger akafikiri kidogo na kusema “Hili jambo la Olivia kujiunga na IS linanishangaza sana.Limetokeaje? “Edger muda unakwenda mbio sana kama una nia ya dhati ya kutusaidia kumpata Olivia muda ni huu”akasema Mathew lakini bado Edger Kaka aliendelea kuinamisha kichwa. “Edger unaufahamu vyema mtandao wa IS hapa nchini nataka kujua ni wapi unahisi amefichwa Olivia? Tafadhali…” akasema Mathew “Sifahamu chochote nimekuwa mateka kwa miaka mitatu na sijui kinachoendelea hapa nchini” akasema Edger “Tupe majina ya viongozi wa IS hapa Tanzania” akasema Mathew na Edger akamtazama na kusema “I’m not IS” Kauli ile ilimkasirisha sana Mathew akasimama “Edger we don’t want to destroy you.We want to help you.Ili tukusaidie lazima na wewe utusaidie kuutambua mtandao wa IS hapa Tanzania na kuwakomboa watu wanaowashikilia mateka” “Guys I’m not IS.Siufahamu mtandao wowote wa IS hapa Tanzania” akasema Edger na Mathew akaendelea kumtazama kwa jicho kali “Kitu gani ulitaka kuwaeleza Mossad? Akauliza Mathew Edger akawa kimya.Mathew akapiga meza kwa hasira “Answer me Edger !! “Sifahamu chochote ! akajibu Edger.Mathew akamtazama na kusema “Ninakupa dakika kumi nitakaporejea nitahitaji kupata taarifa za mtandao wote wa IS hapa nchini ama sivyo tutafungua ukurasa mpya” akasema Mathew na kutoka ndani ya kile chumba akaingia katika chumba kingine ambacho Austin,Gosu Gosu na Devotha walikuwa wanafuatilia mahojiano yale. “Bastard ! akasema Mathew kwa hasira akiwa ameshika kiuno “Natamani kumuharibu haribu Yule mtu lakini ninasita kwanza afya yake mbovu na vile vile bado tunamuhitaji sana”akasema Mathew “Usijali Mathew ni mwanzo mzuri.Ulimchanganya kwa maswali na mwenyewe akajikuta akikiri kuwa ni IS.Ninaamini katika awamu ya pili tunaweza kupata jambo toka kwake” akasema Austin “Akiendelea kujifanya kiburi nipe dakika tano tu nicheze naye atasema kila kitu” akasema Gosu Gosu “Usihofu Gosu Gosu atafunguka tu” akasema Mathew na kumgeukia Austin “Austin I need to call president” akasema Mathew na Austin akamchukua wakaelekea katika ofisi yake akampatia simu ili aweze kuzugumza na Rais “Mathew ahsante kwa kupiga.Hapa nilipo nimechanganyikiwa na sijui nifanye nini.Nimekutafuta katika simu yako haupatikani”akasema DrEvans “Niko hapa katika kambi ya kikosi maalum na simu zetu tumezima.Nini kinaendelea huko?Saa mbili kamili imekwisha pita wale jamaa wamepiga simu? “Ndiyo Mathew wamepiga simu na wamenipa hadi saa tatu za asubuhi niwe nimewapa Edger Kaka ama sivyo wataanza kuwachinja wale wasichana waliowateka.Mmekwisha anza kumuhoji Edger?akauliza “Ndiyo mheshimiwa Rais,tumekwisha anza kumuhoji lakini tunakwenda naye taratibu na atafunguka” “Mathew tafadhali fanya haraka kupata taarifa kutoka kwa huyo mtu kwani inakaribia saa tatu na wale jamaa wameahidi mpaka kufikia saa tatu kama sijawatimizia wanachokitaka wataanza kuua watoto.Fanya kile unachoweza kuhakikisha unapata taarifa muhimu kabla ya muda huo” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwa hali ya Edger Kaka ilivyo hatuwezi kutumia nguvu afya yake ni dhaifu sana ndiyo maana tunajaribu kutumia njia ya ushawishi ili aweze kukubali kufunguka na tuna uhakika huo kwamba atafunguka” “Mathew zimebaki dakika chache kufika saa tatu kamili muda ambao wale jamaa wametoa unadhani kuna chochote ambacho tutakuwa tumekipata hadi kufikia muda huo?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais siwezi kukuahidi chochote kwa muda huu mfupi lakini kama wakipiga tena hiyo saa tatu kamili kama walivyoahidi,buy time” akasema Mathew “Mathew I don’t know what to do.Tegemeo langu lote ni kwako.Niko katika kikao cha baraza la usalama la taifa na nimejitahidi kufanya kama ulivyonielekeza kuendelea kuliweka siri hili suala lakini nina wasi wasi yawezekana ukafika muda nikashindwa kuendelea kuliweka siri hili jambo pale watakapoanza kufanya mauaji ya watoto na mimi sina njia nyingine ya kufanya” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwa namna yoyote ile hakikisha huliweki wazi hili jambo.Ninakuahidi kufanya kila linalowezekana kuwakomboa hao wasichana na wengine wote wanaoshikikliwa na IS lakini usijaribu kabisa kufunguka suala hili mbele ya viongozi tutaharibu kila kitu.Siwezi kukuahidi chochote kwa sasa mheshimiwa Rais lakini nina imani kubwa tutawakomboa hao wasichana wote waliotekwa nyara” akasema Mathew “Mathew nina kuamini sana lakini tatizo ni muda ambao tutautumia kuwakomboa hao mateka kabla magaidi hawajaanza kuwaua.Hapa nilipo katika kikao viongozi wote wana hasira kali na wanataka itumike nguvu kubwa kuwasaka magaidi na kuwakomboa watoto.Ninasita kuruhusu nguvu kubwa itumike kwa sasa kuogopa kumpoteza kabisa mwanangu.Hapo ndipo akili yangu inapokwamia” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais relax.Umetupa kazi ya kuwakomboa watoto hivyo usiwe na wasiwasi tutaifanya hiyo kazi.Ninachokuomba tu kama wale jamaa watapiga muda huo wa saa tatu jitahidi kuvuta muda wakati sisi tukiendelea utafuta mbinu za kuwasaka hao magaidi” “Sawa nitafanya hivyo Mathew lakini naomba ufahamu hili suala linazidi kuwa zito kwangu na kama usipopatikana msaada wa haraka basi litanishinda nguvu.Tutawasiliana tena baadae ninakwenda kuendelea na kikao kusubiri ifike saa tatu kamili” akasema Dr Evans na kukata simu. “Saa tatu kamili magaidi wameahidi uanza kuua watoto kama Rais hatauwa ametekeleza ombi lao.Tunapaswa kujitahidi sana tumfungue Edger kwa haraka” akasema Mathew
Geti la kambi ya kikosi cha operesheni maalum likafunguliwa na gari la akina Mathew likapita.Tayari walikwisha wasiliana na Austin na kumjulisha kuwa wanakwenda kuanza mahojiano na Edger Kaka.Wote wakazima simu zao kwani ukiwa ndani ya kambi ile huruhusiwi kutumia simu ya mkononi bali zipo simu maalum unazoweza kutumia kupiga.Walifika hadi katika jengo la utawala wakapokewa na kuongozwa moja kwa moja hadi katika ofisi ya Austin “Karibuni tena ndugu zangu”akasema Austin “Ahsante Austin.Utatuwia radhi kwani tutaendelea kuwa wageni wako na tutafika hapa mara kwa mara kila pale tutakapokuwa na uhitaji na mtu wetu” “Mathew msijali tafadhali kuweni na amani.Hili ni suala la kitaifa hivyo basi lazima tuhakikishe linakamilika” “Ahsante sana Austin.Tumelazimika kurejea tena kuja kuanza kumuhoji Edger.Usiku wa kuamkia leo watu wa IS wamevamia na kuteka wasichana sitini na sita katika shule ya sekondari ya St Getrude na lengo kubwa la kuwateka wasichana hao ni kumshinikiza Rais aweze kumuachia Edger Kaka” akasema Mathew “Wana uhakika kama Rais anafahamu mahala alipo Edger? Akauliza Austin “Hawajui chochote kuhusu Edger Kaka kama alitekwa na Mossad na alikuwa Nairobi,wao wanaamini yuko hai na mchezo ule ulifanywa na serikali ya Tanzania ndiyo maana wanatumia kila njia kushinikiza Rais aweze kumuachia mtu wao”akajibu Mathew “Saa mbili kamili za asubuhi watampigia simu Rais kujua kama tayari amekwisha muandaa Edger na kama hatatekeleza hilo basi wataanza kuwaua wale wasichana.Tumelazimika kuja tena hapa kumuhoji Edger Kaka atusaidie kufahamu mtandao wao hapa nchini ili tuweze kuwaokoa wale wanafunzi pamoja na mtoto wa Rais” akasema Mathew “Sawa Mathew nimekuelewa hapa tuna chumba maalum kwa ajili ya mahojiano mtakitumia chumba hicho kumuhoji Edger na kama mkihitaji kuingia katika hatua nyingine zaidi ya kutumia nguvu kipo chumba maalum kwa ajili hiyo na wapo wataalamu wa kuifanya hiyo kazi” akasema Austin huku akiinuka “Tunaye mtaalamu wetu wa kutesa ambaye ni Gosu Gosu.Hakuna aliyewahi kuingia katika mikono yake akashindwa kufungua mdomo wake lakini kwa afya ya Edger Kaka tunataka kwanza kumuhoji bila kutumia nguvu” akasema Mathew wakatoka mle ofisini na Austin akawaongoza hadi katika chumba cha mahojiano kulimokuwa na meza na viti viwili.Mathew akaingia mle ndani na baada ya dakika tatu Edger Kaka akiwa amefungwa pingu mkononi akaingizwa ndani ya kile chumba akiwa anasukumwa katika basikeli ya magurudumu kwani bado hakuwa na uwezo wa kutembea.Mathew akaamuru afunguliwe mikono abaki huru na watu wote watoke nje akabaki na Edger, akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema “Edger Kaka pole sana kwa masahibu yote yaliyokupata kwa muda wa miaka mitatu.Lakini yote hayo yamekwisha sasa umerejea nyumbani.Unajisikiaje kurejea tena nyumbani? Akauliza Mathew.Edger akajaribu kuzungumza lakini sauti ikamkwama Mathew akaomba kuletewa maji Edger akanywa “Sasa niambie Edger unajisikiaje kurejea nyumbani ? Akauliza Mathew “Unataka nikwambie nina furahi?I’m not happy at all.Mlikosea sana msingesumbuka kuja kunikomboa na kunirejesha tena Tanzania” akasema Edger kaka “Kwa nini unasema hivyo Edger? Hupendi Tanzania?Hupendi kurejea nyumbani? Akauliza Mathew “Because I’m dead already.Nimeonyeshwa video ya mazishi yangu namna watu walivyonililia wakijua nimefariki dunia wengine wakipoteza fahamu baada ya kupita katika jeneza ambalo waliamini kuna maiti yangu lakini kumbe ulikuwa ni mchezo umetengenezwa.Imeniumiza sana baada ya kulifahamu hilo jambo na siwafichi ninatamani hata sasa mnipige risasi nife niondoke kabisa katika dunia hii” akasema Edger “Edger waliofanya tuko lile si Tanzania bali ni Israel wakitumia shirika lao la ujasusi la Mossad na ndiyo maana baada ya kufahamu kwamba uko hai tukafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kukukomboa na kukurejesha nyumbani.Tumetengeneza mgogoro mkubwa sana wa kidiplomasia kati yetu na Israel kwani tumelazimika kuua watu wao wengine wa muhimu kabisa ili tuweze kukukomboa.Naweza kusema kwamba serikali ya Tanzania kwa kukuthamini imetumia gharama kubwa kukukomboa na kukurejesha nyumbani.Unapaswa kufurahi”akasema Mathew “Ninashukuru kwa kunitoa katika nyumba ile ya mateso lakini haikuwa na ulazima wowote wa kutumia gharama kubwa kunikomboa”akasema Edger “Edger wewe ni mtanzania na ilikuwa lazima kwa gharama zozote zile tukurejeshe nyumbani”akasema Mathew na kumtazama Edger kwa sekude kadhaa halafu akasema “Edger unaweza ukatueleza sababu za Israel kutumia gharama kubwa kutengeneza kifo chako wakati bado uko hai?akauliza Mathew na Edger akabaki kimya “Nijibu Edger swali nililokuuliza” “Sifahamu chochote” akasema Edger “Edger jina langu ninaitwa Mathew Mulumbi ndiye niliyeongoza operesheni ya kuja kukukomboa na kukurejesha nyumbani.Hapa uko sehemu salama na mateso yote uliyoyapata kwa miaka mitatu yamekwisha.Hapa ndipo patakuwa chimbuko la maisha yako mapya.Mheshimiwa Rais anafahamu kuwa uko hapa na ndiye aliyetoa kibali cha kufanya operesheni ile ya siri ya kukukomboa na yuko tayari kukufanyia kitu chochote unachokihitaji ili uanze maisha yako upya lakini amenituma hapa kwako nije kuzungumza nawe ili tuufahamu ukweli wote kwa nini ulitekwa na Israel?Usihofu hapa uko sehemu salama na hakuna anayefahamu kama uko hapa hivyo kuwa huru”akasema Mathew na Edger akainamisha kichwa akazama mawazoni “Edger please usiipoteze hii nafasi uliyoipata.Hii ni tiketi ya kuelekea maisha mapya hivyo itumie kikamilifu” akasema Mathew “Sifahamu chochote kwa nini waliniteka nyara na kunipa mateso yale makali kwa miaka mitatu.Watu wale ni wanyama mno! Akasema Edger na sura ya Mathew ikaanza kubadilika “Who is Habiba Jawad? Akauliza Mathew na Edger akastuka “Umesema nani? “Habiba Jawad ni nani? “Si..simfahamu” akajibu Edger.Mathew akamtazama kwa macho makali “Edger Kaka narudia tena kauli yangu kwamba hapa panaweza kuwa chimbuko la maisha yako mapya au panaweza kuwa ni mwisho wa maisha yako hivyo ni jukumu lako kuchagua nini unakitaka kuishi au kufa.Mimi ninayezungumza nawe hapa ninamuwakilisha Rais hivyo sihitaji mzaha.Ninapokuuliza nataka unipe majibu ya kweli kama ukitaka kuwa kiburi nakuhakikishia hautafika kokote Edger.Mateso uliyoyapata nchini Kenya kwa miaka mitatu yanatosha sana hatutaki kuendelea kukutesa hata hapa nyumbani hivyo funguka,kuwa mkweli tueleze nini kilitokea na sisi tutajua namna ya kukusaidia.We need information from you” akasema Mathew “Mathew Mulumbi,right?akauliza Edger “Ndiyo”akajibu Mathew “Nakwambia kweli kabisa kwamba sifahamu sababu ya kutekwa na kupelekwa mafichoni kwa miaka mitatu.Kama kuna taarifa zozote mlizopewa kuhusu mimi si taarifa za kweli hata kidogo”akasema Edger “Mzaha umeisha ngoja nikueleze ukweli.Edger wewe unashirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS.Ukiwa katika matibabu nchini Israel ulitembelewa na watu wawili ambao ni wafadhili wakuu wa kundi hili na mengine mengi ya kigaidi ambao ni Habiba Jawad na Sayid Omar na hapo ndipo Israel walipoanza kukufuatilia na hatimaye kukuteka wakaenda kukuficha jijini Nairobi katika ubalozi wao wakitaka kupata taarifa za mahala walipo Habiba Jawad na wenzake wanaofadhili ugaidi” akasema Mathew na jasho likaonekana usoni kwa Edger “Taarifa zinaonyesha kwamba chanzo cha ugonjwa wako uliosababisha upelekwe nchini Israel ni sumu Dr Olivia Themba aliyapigania maisha yako hadi ukapona,aliweka rehani maisha yake kwa ajili yako lakini umemuingiza katika mtandao wa IS.Haya ndiyo malipo kwa mtu kama huyu ambaye alipambana kuokoa maisha yako? Akauliza Mathew kwa ukali “Sikuwahi kumuingiza Olivia katika IS” akajibu Edger Kaka “Kama si wewe nani aliyemuunganisha Olivia na kundi la IS? “Olivia hayupo katika kundi la IS” akajibu Edger “Umejuaje kama Olivia si mfuasi wa IS?akauliza Mathew na Edger akabaki kimya.Mathew akapiga meza kwa nguvu “Answer me Edger !! “Olivia is not IS ! akasema Edger kwa sauti ya juu halafu akainamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa na kusema “Look guys Olivia ni mtu muhimu mno kwangu.She saved my life.Kama si yeye kupigania maisha yangu hivi sasa wala msingekuwa mnanihoji ningekwisha kufa zamani sana.Hakuna kiasi chochote cha pesa kinachoweza kufikia thamani ya Olivia kwangu.Thamani yake ni kubwa kuliko tani ya dhahabu,almasi na kila kito cha thamani unachokifahamu.Zaidi ya yote kuna kitu ambacho hamkifahamu.Mimi na Olivia tulikuwa tunaelekea kuwa wapenzi.Ni mwanamke pekee ambaye moyo wangu umemuangukia na kumpenda hata yeye pia alikwisha tokea kunipenda” akasema Edger “Muongo mkubwa we !Ungekuwa unampenda Olivia usingemuingiza katika kundi lenu la kigaidi.Umeyaharibu maisha yake.Olivia wa sasa si Olivia Yule unayemfahamu wewe.Amekuwa muuaji hana huruma hata chembe kutoa roho ya mtu.Kwa kushirikiana na IS ametengeneza kirusi cha maangamizi ambacho wanataka kukitumia kufanya mashambulio yao ya kigaidi.Kwa nini ukakubali mwanamke unayempenda ageuke kuwa mkatili namna hii? Akauliza Mathew “Mimi sijamuingiza Olivia IS na siwezi kufanya kitu kama hicho.Mara ya mwisho kuonana na Olivia ni uwanja wa ndege wa Julius Nyerere tulipotoka Israel.Tuliagana kwa miadi ya kuonana kesho yake lakini huo ukawa ni mwisho wa kuonana naye kwani hiyo kesho haikunikuta Tanzania tayari nilikuwa nimetekwa na sifahamu chochote kilichokuwa kinaendelea wakati nikiwa nimeshikiliwa na Mossad.Taarifa za kwamba mimi ndiye niliyemuingiza Olivia IS si za kweli.Kwanza Olivia hafahamu chochote kuhusu IS” akasema Edger.Mathew akamtazama kwa macho yaliyojaa hasira halafu akasema “Walipokuja wale majasusi wa Mossad kukuhoji uliwaambia wakusaidie kumtafuta Olivia na utawaeleza kila kitu wanachokitaka.Hapo ulionyesha kweli unampenda Olivia na uko tayari kufanya kitu chochote ili kumpata.Nataka kufahamu kama unaendelea kusimama katika kauli yako kwamba ukimpata Olivia utakuwa tayari kufunguka”akasema Mathew “Olivia ninampenda kuliko kitu chochote na sintoacha kumpenda ndiyo maana niliwaamba wale watu wa Mossad waniletee Olivia mwanamke ninayempenda nami nitawaeleza kile wanachotafuta kwangu.Niko tayari kufanya chochote kwa ajili yake” “Ahsante kwa kuweka wazi namna unavyompenda Olivia.Lakini kuna tatizo katika kumpata.Olivia yuko katika mikono ya IS hivi sasa” “Mikono ya IS kivipi?akauliza Edger “Ngoja nitumie dakika chache kukupa maelezo kidogo.Idara ya usalama wa taifa ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo walipata taarifa kwamba mmoja wa watu wa IS anaitwa Seif Almuhsin anatembelea nchini kwao hivyo wakaanza kujiandaa kumfuatilia.Alipofika Kinshasa wakaanza kumfuatilia na wakagundua kwamba alikutana na mwanamke mmoja wa kitanzania ndipo taarifa zilipotumwa huku Tanzania na akagundulikwa kwamba ni Olivia Themba.Ililazimu idara zinazihusika na usalama wa nchi kumteka Olivia mara tu aliporejea kutokea Kinshasa na lengo likiwa ni kutaka kujua mahusiano yake na watu wa IS.Kuthibitisha kwamba Olivia ni mtu wao IS walishambulia hospitali ya Mtodora wakaua watu na kumteka mtoto wa Rais wakimshinikiza Rais awakabidhi Olivia na Rais katika jitihada za kutaka kumkomboa mwanae akalazimika kuwapa Olivia na mpaka sasa hatujui yuko wapi ndiyo maana tunahitaji sana msaada wako tuweze kumpata ili utueleze kile tunachotaka kukisikia kuhusu IS.Edger machoni pa watu tayari umekwisha kufa na kusahaulika hata IS hawajui kama uko hai hivyo basi ni wakati wako wa kuachana nao na kuishi maisha mapya.Rais yuko tayari kukusaidia kuanza maisha mapya kwa kukutafutia nchi ambako utakwenda kujificha huko ukiwa na Olivia.Huo ndio msaada pekee ambao Rais wa Tanzania yuko tayari kukusaidia kama nawe utakuwa tayari kutusaidia” akasema Mathew na Edger akainamisha kichwa “Edger tafadhali tusaidie tukusaidie.IS wana mipango miovu sana dhidi ya nchi yetu.Usiku wa kuamkia leo wamevamia shule ya sekondari ya wasichana na kuteka wasichana sitini na sita ambao mpaka sasa hawajulikani walipo.Edger umekuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano na ulijizolea sifa nyingi sana kutokana na utendaji wako wa kazi hasa katika kupiga vita ufisadi.Una mapenzi makubwa na nchi hii na siamini kama uko tayari kuona IS wakihatarisha amani na usalama wa nchi yetu.Watu wanaishi kwa hofu hivi sasa kwani IS wametishia kufanya mashambulizi mengi hapa nchini.Kama uliona video ya mazishi yako ya bandia utakuwa umeona namna watu walivyokuwa na mapenzi makubwa nawe,wengi walipoteza fahamu kukulilia.Edger upendo ule ni mkubwa na ninaamini hauko tayari kuwaona watu wale ambao walikupenda na wakawa na matumaini makubwa kwako wakiishi kwa mashaka na kukosa amani.Tusaidie kuufahamu mtandao wa IS hapa nchini na sisi tutakupatia kila unachokihitaji ili kuyaanza maisha mapya.Mwanamke unayempenda yuko katika mikono ya IS,wasichana sitini na sita wasio na hatia wanashikiliwa mateka na wanaweza wakapoteza maisha kama juhudi za haraka za kuwatafuta hazitafanywa.Tunakutegeme a sana Edger tafadhali tusaidie” akasema Mathew.Edger akafikiri kidogo na kusema “Hili jambo la Olivia kujiunga na IS linanishangaza sana.Limetokeaje? “Edger muda unakwenda mbio sana kama una nia ya dhati ya kutusaidia kumpata Olivia muda ni huu”akasema Mathew lakini bado Edger Kaka aliendelea kuinamisha kichwa. “Edger unaufahamu vyema mtandao wa IS hapa nchini nataka kujua ni wapi unahisi amefichwa Olivia? Tafadhali…” akasema Mathew “Sifahamu chochote nimekuwa mateka kwa miaka mitatu na sijui kinachoendelea hapa nchini” akasema Edger “Tupe majina ya viongozi wa IS hapa Tanzania” akasema Mathew na Edger akamtazama na kusema “I’m not IS” Kauli ile ilimkasirisha sana Mathew akasimama “Edger we don’t want to destroy you.We want to help you.Ili tukusaidie lazima na wewe utusaidie kuutambua mtandao wa IS hapa Tanzania na kuwakomboa watu wanaowashikilia mateka” “Guys I’m not IS.Siufahamu mtandao wowote wa IS hapa Tanzania” akasema Edger na Mathew akaendelea kumtazama kwa jicho kali “Kitu gani ulitaka kuwaeleza Mossad? Akauliza Mathew Edger akawa kimya.Mathew akapiga meza kwa hasira “Answer me Edger !! “Sifahamu chochote ! akajibu Edger.Mathew akamtazama na kusema http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Ninakupa dakika kumi nitakaporejea nitahitaji kupata taarifa za mtandao wote wa IS hapa nchini ama sivyo tutafungua ukurasa mpya” akasema Mathew na kutoka ndani ya kile chumba akaingia katika chumba kingine ambacho Austin,Gosu Gosu na Devotha walikuwa wanafuatilia mahojiano yale. “Bastard ! akasema Mathew kwa hasira akiwa ameshika kiuno “Natamani kumuharibu haribu Yule mtu lakini ninasita kwanza afya yake mbovu na vile vile bado tunamuhitaji sana”akasema Mathew “Usijali Mathew ni mwanzo mzuri.Ulimchanganya kwa maswali na mwenyewe akajikuta akikiri kuwa ni IS.Ninaamini katika awamu ya pili tunaweza kupata jambo toka kwake” akasema Austin “Akiendelea kujifanya kiburi nipe dakika tano tu nicheze naye atasema kila kitu” akasema Gosu Gosu “Usihofu Gosu Gosu atafunguka tu” akasema Mathew na kumgeukia Austin “Austin I need to call president” akasema Mathew na Austin akamchukua wakaelekea katika ofisi yake akampatia simu ili aweze kuzugumza na Rais “Mathew ahsante kwa kupiga.Hapa nilipo nimechanganyikiwa na sijui nifanye nini.Nimekutafuta katika simu yako haupatikani”akasema DrEvans “Niko hapa katika kambi ya kikosi maalum na simu zetu tumezima.Nini kinaendelea huko?Saa mbili kamili imekwisha pita wale jamaa wamepiga simu? “Ndiyo Mathew wamepiga simu na wamenipa hadi saa tatu za asubuhi niwe nimewapa Edger Kaka ama sivyo wataanza kuwachinja wale wasichana waliowateka.Mmekwisha anza kumuhoji Edger?akauliza “Ndiyo mheshimiwa Rais,tumekwisha anza kumuhoji lakini tunakwenda naye taratibu na atafunguka” “Mathew tafadhali fanya haraka kupata taarifa kutoka kwa huyo mtu kwani inakaribia saa tatu na wale jamaa wameahidi mpaka kufikia saa tatu kama sijawatimizia wanachokitaka wataanza kuua watoto.Fanya kile unachoweza kuhakikisha unapata taarifa muhimu kabla ya muda huo” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwa hali ya Edger Kaka ilivyo hatuwezi kutumia nguvu afya yake ni dhaifu sana ndiyo maana tunajaribu kutumia njia ya ushawishi ili aweze kukubali kufunguka na tuna uhakika huo kwamba atafunguka” “Mathew zimebaki dakika chache kufika saa tatu kamili muda ambao wale jamaa wametoa unadhani kuna chochote ambacho tutakuwa tumekipata hadi kufikia muda huo?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais siwezi kukuahidi chochote kwa muda huu mfupi lakini kama wakipiga tena hiyo saa tatu kamili kama walivyoahidi,buy time” akasema Mathew “Mathew I don’t know what to do.Tegemeo langu lote ni kwako.Niko katika kikao cha baraza la usalama la taifa na nimejitahidi kufanya kama ulivyonielekeza kuendelea kuliweka siri hili suala lakini nina wasi wasi yawezekana ukafika muda nikashindwa kuendelea kuliweka siri hili jambo pale watakapoanza kufanya mauaji ya watoto na mimi sina njia nyingine ya kufanya” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwa namna yoyote ile hakikisha huliweki wazi hili jambo.Ninakuahidi kufanya kila linalowezekana kuwakomboa hao wasichana na wengine wote wanaoshikikliwa na IS lakini usijaribu kabisa kufunguka suala hili mbele ya viongozi tutaharibu kila kitu.Siwezi kukuahidi chochote kwa sasa mheshimiwa Rais lakini nina imani kubwa tutawakomboa hao wasichana wote waliotekwa nyara” akasema Mathew “Mathew nina kuamini sana lakini tatizo ni muda ambao tutautumia kuwakomboa hao mateka kabla magaidi hawajaanza kuwaua.Hapa nilipo katika kikao viongozi wote wana hasira kali na wanataka itumike nguvu kubwa kuwasaka magaidi na kuwakomboa watoto.Ninasita kuruhusu nguvu kubwa itumike kwa sasa kuogopa kumpoteza kabisa mwanangu.Hapo ndipo akili yangu inapokwamia” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais relax.Umetupa kazi ya kuwakomboa watoto hivyo usiwe na wasiwasi tutaifanya hiyo kazi.Ninachokuomba tu kama wale jamaa watapiga muda huo wa saa tatu jitahidi kuvuta muda wakati sisi tukiendelea utafuta mbinu za kuwasaka hao magaidi” “Sawa nitafanya hivyo Mathew lakini naomba ufahamu hili suala linazidi kuwa zito kwangu na kama usipopatikana msaada wa haraka basi litanishinda nguvu.Tutawasiliana tena baadae ninakwenda kuendelea na kikao kusubiri ifike saa tatu kamili” akasema Dr Evans na kukata simu. “Saa tatu kamili magaidi wameahidi uanza kuua watoto kama Rais hatauwa ametekeleza ombi lao.Tunapaswa kujitahidi sana tumfungue Edger kwa haraka” akasema Mathew
Tayari chumba ambacho Fahad na kundi lake wangekitumia kwa ajili ya kurusha moja kwa moja tukio la mauaji kwa wasichana waliowateka ili kumshinikiza Rais awakabidhi mtu wao Edger Kaka,kilikwisha andaliwa.Macho ya Fahad yalikuwa katika saa ya mkononi akisubiri ufike muda wa kumpigia simu Rais ili kujua kama ametekeleza takwa lao.Mshale ulipogonga saa tatu kamili akawasha simu yake na kumpigia Rais.Simu ikaita bila kupokelewa akapiga tena ikaita na kukatika bila kupokelewa.Akapiga mara ya tatu simu haikupokelewa. “Hataki kupokea simu.Huyu Rais bado hajatufahamu vizuri.Tunatakiwa kumuonyesha kwamba tunamaanisha kila tunachokisema.Tuendelee na zoezi letu.Kila kitu kiwekwe tayari” akasema Fahad na kuchukua kofia ya kufunika uso akavaa akabaki anaonekana macho.Kamera ikawashwa kisha akapewa ishara kwamba aanze kuzungumza “Ndugu watanzania mimi ni kiongozi wa kikundi cha Islamic state hapa Tanzania ambao tumekuwa tukiendesha mfululizo wa matukio.Ni sisi tuliofanya shambulio katika hospitali ya Mtodora na usiku wa kuamkia leo tumevamia shule ya sekondari ya St Getrude na kuteka wanafunzi sitini na sita na walimu wao watatu.Tunayo madai yetu kwa Rais wa nchi na amekuwa akiyapuuza hivyo basi kumuonyesha kwamba hatutanii kwa kile tunachokisema tutaua msichana mmoja baada ya mwingine miongoni mwa hawa tuliowateka kila baada ya nusu saa.Tutaendelea kumwaga damu nchini Tanzania hadi pale Rais wenu atakapotupatia kile tunachokihitaji.Tutaendelea na zoezi hili la kuua wanafunzi hawa hadi watakapomalizika na kama hatakuwa ametekeleza kile tunachokitaka tutafanya tukio lingine kubwa zaidi ya hili” akasema Fahad na kutoa ishara mwanafunzi mmoja akaletwa mbele ya kamera na mtu aliyejifunika sura yake.Mwanafunzi Yule aliyekuwa katika mavazi ya kulalia akapigishwa magoti mbele ya kamera.Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia. “Binti unaitwa nani? Akauliza Fahad “Naitwa Lucy Nswami” “Lucy una miaka mingapi? “Nina miaka kumi na tano.Tafadhali naomba msituue.Ongeeni na baba yangu ni tajiri anafanya biashara ya madini atawapa kiasi chochote cha pesa mnachohitaji.Tafadhali naomba msituue….”akasema Lucy na Fahad akasema “Lucy angalia ile kamera na umuombe Rais wako awaokoe kwa kutupa kile tunachomdai” Huku uso wake umefunikwa na machozi Lucy akaiangalia kamera na kusema “Mheshimiwa Rais baba yetu, tunaomba utuokoe.Tumetekwa na tunahitaji msaada wako.Tumeambiwa kwamba usipowapatia wanachohitaji watatuua wote. Tunakuomba Rais tuokoe tusiuawe.Sisi bado ni wasichana wadogo na tuna malengo mengi ya maisha.Tuokoe mheshim……..” akashindwa kuendelea akaangua kilio. “Ndugu watanzania,wasichana hawa wanakwenda kupoteza uhai wao angali wadogo kwa sababu ya ukaidi wa Rais wenu.Narudia tena kila baada ya dakika thelathini mwanafunzi mmoja atapoteza uhai” Akasema Fahad na kumpa ishara Fulani Yule mtu aliyekuwa amesimama karibu na Yule binti.Akaenda katika meza akachukua kamba akamfuata Lucy na kumfunga mikono akaikaza barabara na kumfunga kitambaa cheusi usoni halafu akachukua panga kali akamsogelea na kuliinua juu.Panga liliposhuka chini kichwa cha Lucy kikatengana na kiwiliwili. “Huyu ni wa kwanza .Tutaendelea kuua kila baada ya dakika thelathini” akasema Fahad na kamera ikazimwa. “Fanyeni usafi na muuhifadhi huu mwili.Zoezi hili ni endelevu hadi pale Rais atakapotekeleza ombi letu” akasema Fahad na kuvua ile kofia akatoka ndani ya kile chumba IKULU – DAR ES SALAAM Wakati kikao cha baraza la usalama la taifa kikiendelea katika ikulu Dar es salaam,mmoja wa wasaidizi wa Rais akaingia na kumnong’onza kitu Rais sikioni halafu akatoka “Nimetaarifiwa kuna video imeanza kusambaa mtandaoni ambayo inasemekana inatoka kwa watekaji” akasema Dr Evans na kuwasha runinga iliyokuwa ukutani na video ile ikaanza kuonekana.Chumba cha mikutano kilibaki kimya na watu wote mle ndani wakiwa katika taharuki kubwa sana.Hawakutegemea kabisa kama wangeona ukatili mkubwa kama ule.Dr Evans kama ilivyo kawaida yake awapo katika mstuko midomo ilikuwa inamtetemeka hakujua aseme nini. “Oh my God I can’t believe this ! akasema waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Evarist Mlukola.Minong’ono ya chini chini ikaanza na Elizabeth wimara mkurugenzi msaidizi wa idara ya kudhibiti na kupambana na ugaidi alishindwa kujizuia kudondosha machozi. “Mr President can you say anything about this video?akauliza waziri mkuu ambaye uso wake ulikuwa umejikunja kwa hasira “Niseme nini mheshimiwa waziri mkuu? Sote tumeshuhudia video hii na tumeona kilichotokea.Tumeona unyama uliofanywa na hawa magaidi.Kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni kufanya kila juhudi kuhakikisha watekaji hawa wanapatikana na vile vile kuwakomboa wasichana waliotekwa”akasema Dr Evans “With all due respect Mr President you must have to explain something to us.Sote tumesikia alichokisema huyu kiongozi wa magaidi ambaye ameelekeza lawama zote kwako kwamba wewe ndiye sababu ya wao kufanya mashambulizi kadhaa likiwamo lile la Mtodora na kama haitoshi wamewateka wasichana usiku wa leo na wameanza kuwachinja kama kuku kukushinikiza uwapatie kile ambacho wanakitaka.Mheshimiwa Rais katika hili tunahitaji maelezo ya kina ! Kwa nini wasimtaje mtu mwingine na wajielekeze moja kwa moja kwako?Wanataka nini? Umekuwa na mawasiliano nao? Akauliza waziri mkuu akiwa amekasirika “Guys nawaombeni mtulie.Tulikuwa tunakwenda vyema na kikao chetu video hii isije kutuvuruga.Hii ni vita na hawa magaidi wanatumia kigezo hicho cha kuelekeza lawama kwangu moja kwa moja ili kutuvuruga lakini ukweli ni kwamba sifahamu chochote.Sina mawasiliano nao na sifahamu wanataka nini” “Mr president please if you know something please tell us so we can save the innocent children.Watoto wale wanachinjwa kama kuku hawana kosa lolote ! akasema waziri mkuu akionekana kupandisha jazba “Mheshimiwa waziri mkuu naomba utulize jazba kwani jambo hili linatakiwa lijadiliwe kwa umakini mkubwa.Ninafahamu wasi wasi wako kwani mtoto wako ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa,lakini tunatakiwa kujadili jambo hili kwa busara na kufikia maamuzi ya namna bora ya kukabiliana na watu hawa.Tukienda kwa papara tutawapoteza watoto wetu na watu wengi watakufa.” Akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais muda hausimami.Muda mfupi ujao wasichana wengine watauawa.We need to act faster.Kama unalo la kutuambia mheshimiwa Rais this is the time.Kama kuna kitu wanakihitaji hawa magaidi tuweke wazi ili tuweze kujadili namna ya kufanya” Akasema waziri mkuu kwa jazba.Tayari alikwisha pandwa na hasira.Dr Evans naye alionekana kukerwa na maneno ya waziri mkuu “Ndugu waziri mkuu,nchi haiendeshwi namna hiyo.Janga hili ni kubwa na lazima itumike busara na mbinu kubwa katika kulishughulikia.Nimekwisha sema kwamba magaidi hawa lengo lao ni kutuvuruga kwa kutunga uongo na ninaanza kulichukulia jambo hili kama mbinu ya kunichafua mimi kisiasa.Yawezekana wanatumiwa na watu wa ndani na wa nje kwa madhumuni yao ya kisiasa lakini mimi sifahamu chochote.Siwafahamu watu hawa na wala sifahamu wanachokitaka.Suala kwamba ninajua wanachokitaka ni uongo mkubwa.Ninachowaomba ndugu zangu kitu kikubwa kwa sasa ni kuviachia vyombo vya usalama vilishughulikie hili suala na kuwakomboa wasichana wetu” “Mheshimiwa Rais watoto wetu wanachinjwa kama kuku lakini huonekani kuguswa kabisa!!.Please Mr president wake up.Act like a president…!! akasema kwa ukali waziri mkuu.Dr Evans naye akafura kwa hasira na kumtaka waziri mkuu watoke wakaongee nje. “Mheshimiwa waziri mkuu sintavumilia tena kitendo chako cha dharau mbele ya wajumbe.Umenionyesha dharau kubwa sana.Mimi ndiye Rais na ndiye mwenye maamuzi ya nini kifanyike.Kama una njia bora ya kuweza kulishughulikia suala hili tueleze tukusikie.Tuko katika kipindi kigumu tunatakiwa tushikamane,tuwe kitu kimoja ,tukianza kuvurugana sisi viongozi hatutaweza kukabiliana na suala hili.Hii ni vita na hawa jamaa wamedhamiria kutuvuruga kwanza ili waweze kutupiga vizuri”akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais samahani sana kwa kile kilichotokea mle ndani ya kikao nadhani unafahamu namna nilivyo mtiifu kwako,sijawahi kupingana nawe hata mara moja,nakiri nilichokifanya ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi wangu mkuu naomba msamaha sana lakini sikuwa nimekusudia kubishana nawe mheshimiwa Rais ni kutokana na hasira na uchungu nilio nao kujua kwamba mwanangu ni mmoja wa watoto walio mikononi mwa magaidi na muda wowote anaweza akachinjwa.Naamini hata wewe kama mwanao angekuwa mikononi mwa magaidi hawa wasio na hata chembe ya huruma ungejua nini ninakimaanisha mheshimiwa Rais ndiyo maana ninakuomba kama kuna kitu hawa magaidi wanakitaka angalia namna ya kuwapatia ili tuweze kuwakomboa hawa watoto wasio na hatia wanaochinjwa kama ndege.Mheshimiwa Rais wewe unafahamika ni Rais mwenye msimamo na watu wanakupenda sana unadhani nini kitatokea baada ya sakata hili?Litakuwa ni anguko kubwa la kisiasa na si kwako tu bali kwetu sote na chama chetu pia hivyo basi wewe pekee ndiye unayeangaliwa na kila mtu hivi sasa.Tukio hili linaweza kukujenga zaidi kisiasa au kukubomoa kabisa” akasema waziri mkuu na kuanza kupiga hatua kuondoka Dr Evans naye akamfuata ndani ya kile chumba cha mikutano. “Guys we need a break.Waziri mkuu nakuhitaji ofisini yangu.Baada ya dakika ishirini turejee tena hapa tumalizie kikao chetu” akasema Dr Evans na kuongozana na waziri mkuu kuelekea ofisini wakaketi sofani “Nakusikiliza mheshimiwa Rais”akasema waziri mkuu baada ya kumuona Dr Evans akiwa ameinamisha kichwa katika kiti chake toka walipoingia mle ofisini “Mr Evarist sijui nianzie wapi lakini naomba kile nitakachokueleza hapa kibaki kuwa siri yetu na nimeamua kukueleza kwa sababu ninakuamini” “Usihofu mheshimiwa Rais.Unanifahamu vyema namna nilivyo mtiifu kwako,nieleze chochote na kitabaki ndani ya kuta za chumba hiki” akasema waziri mkuu Dr Evans akavuta pumzi ndefu na kusema “Unachokipitia waziri mkuu na mimi ndicho ninachokipitia”akasema DrEvans “Sijakuelewa una maanisha nini mheshimiwa Rais” “Mwanangu Coletha pia ametekwa na hao magaidi” “Coletha..! Ametekwa..aagh I don’t understand..how ?Waziri mkuu akapatwa na mshangao “Ni hadithi ndefu lakini shambulio la juzi katika hospitali ya Mtodora lilimlenga mwanangu na walifanikiwa kumteka na hadi hivi sasa tunavyoongea wako naye na yuko katika hatari ya kuuawa kama wengine” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais sijaelewa sababu ya Coletha kutekwa nyara na magaidi” akasema waziri mkuu “Kuna kitu ambacho hawa magaidi wanakitaka” akanyamaza tena kwa sekunde chache akasema “Wanamtaka Edger Kaka” “Edger kaka? Akauliza waziri mkuu na kutoa kicheko kidogo “Ndiyo wanamtaka Edger Kaka” “Huo ni upuuzi.Wanamtaka marehemu? Hawajui kama Edger kaka amekwisha fariki miaka mitatu iliyopita? “Edger kaka is not dead” akasema Dr Evans “What? Waziri mkuu akashangaa “Ni kweli.Edger Kaka hajafariki yuko hai” akasema Dr Evans na waziri mkuu akasimama akamtazama Dr Evans kwa mshangao mkubwa “Mheshimiwa Rais najaribu kutaka kuamini kile unachonieleza lakini ninashindwa kwa sababu sote tulihudhuria msiba wa Edger Kaka na tukamzika sasa unaponiambia kwamba Edger yuko hai ni kitu cha ajabu sana.Hicho ni kitu cha kufikirika.Yuko hai kimwili au umeonekana mzimu wake?akauliza waziri mkuu “Edger Kaka ni mzima kabisa hakufa katika ile ajali kama wengi tunavyoamini.Naomba ukae nikueleze japo kwa ufupi” akasema Dr Evans na waziri mkuu akaketi. “Siku chache zilizopita kupitia vyanzo vyangu nilipata taarifa za Edger Kaka kuwa hai.Nilianza kuzifuatilia taarifa hizi kujua ukweli wake na nikathibitisha kwamba kweli Edger Kaka yuko hai.Ajali ile ambayo ilichukua uhai wake ilikuwa ya kutengenezwa” “Ajali ile ilitengenezwa?akauliza waziri mkuu “Ndiyo ilikuwa ajali ya kutengenezwa” “Nani walioteneneza ajali ile na kwa nini?akauliza waziri mkuu “Israel” “Israel?!! Waziri mkuu akazidi kushangaa “Ndiyo.Israel kupitia shirika lao la ujasusi la Mossad ndio waliotengenezea ajali ile.Sababu kubwa ya kutengeneza ajali ile ni ili kumpata Edger Kaka ambaye waligundua ana mahusiano na wafadhili wakuu wa kikundi cha kigadi cha IS ambao wanaendesha mashambulizi ndani ya Israel.Hiyo ndiyo sababu ya wao kutengeneza ajali ile wakafanikiwa kumpata Edger Kaka na kumpeleka mafichoni” “Mheshimiwa Rais unazidi kunichanganya.Edger kaka ana mahusiano na kikundi cha IS? Akauliza waziri mkuu “Ndiyo.Ana mahusiano na kikundi cha IS”akajibu Dr Evans “Haya ni maajabu.Edger Kaka ni IS?Alikuwa ni mmoja wa wabunge wenye kuaminiwa sana hapa nchini,alisimama kidete na kupigana vita dhidi ya ufisadi na kutokana na juhudi zake wengi tulimtabiria kufika mbali kisiasa taarifa za kwamba ana mahusiano na kikundi cha IS zimenistua mno” akasema waziri mkuu “Nilipigiwa simu na kiongozi wa kikundi cha IS akanifahamisha kwamba wamemteka mwanangu na wakanipa maelekezo kwamba kama ninamtaka mwanangu akiwa hai basi nisimueleze mtu yeyoite jambo hili la mwanangu kutekwa ndiyo maana mpaka leo sijamweleza mtu yeyote kama mwanangu katekwa kila mtu ninamwambia kwamba mwanangu yuko sehemu anapumzika lakini ukweli ni kwamba ametekwa na magaidi.Pili magaidi hao wakanitaka nimuachie Edger Kaka.Magaidi hao wanafahamu kwamba Edger Kaka yuko hai lakini hawajui yuko wapi na wanaamini kwamba serikali ya Tanzania ndio tuliotengeneza ajali ile na kwamba tunafahamu mahala alipo Edger.Jana walinipigia simu na kunitaka leo saa mbili za asubuhi niwe nimemuandaa Edger Kaka na watanipa maelekezo sehemu ya kumpeleka lakini niliwaonya kwamba nitawasaka kwa nguvu zangu zote hadi nihakikishe nimewafyekelea mbali na hapo ndipo vita ilipopamba moto na wakavamia shule ya sekondari wakateka wasichana na sasa wameanza kuwaua.Kauli ya kwamba kuna kitu wanakidai kutoka kwangu ni huyo Edger kaka” akasema Dr Evans “Jesus Christ ! akasema waziri mkuu. “Mheshimiwa Rais ulipaswa kuliweka wazi suala hili ili lishughulikiwe na vyombo husika kabla jambo hili halijawa kubwa kama lilivyo sasa.Hukupaswa kulifanya jambo hili kuwa siri.Tumefika hapa tulipofika kwa sabab……….” Akasema waziri mkuu lakini Dr Evans akamkatisha “Jambo hili ni kubwa zaidi ya unavyofikiri.Si kwamba sikuwa na uwezo wa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuwatafuta magaidi hawa lakini nililazimika kulifanya siri kwa sababu maalum” “Mheshimiwa Rais hili si suala la kufanya siri.”akasema waziri mkuu “Ni suala la siri ! akasema Dr Evans “Kuna sababu gani ya kulifanya suala hili kuwa siri na kuwaacha magaidi wafanye watakacho ndani ya ardhi yetu? Wameteka watu na wanaanza kuwaua.Hii haikubaliki kabisa mheshimiwa Rais.Tusiwape nafasi magaidi ya kufanya wakitakacho.Tanzania hatuwezi kuwaogopa magaidi ! akasema waziri mkuu. “Si kwamba kulifanya suala hili liwe siri ni kuwapa nafasi magaidi watambe.Kuna operesheni ya chini kwa chini inayoendelea kuwatafuta magaidi hawa mahala walipo na kuwakomboa watoto wote waliotekwa” akasema DrEvans “Nani wanafanya hiyo operesheni? “Nina kikosi cha majasusi mahiri ambao wanalioshughulikia hili suala na wako katika hatua nzuri hivi sasa” akasema Dr Evans “Ni akina nani hao? “I’m sorry I can’t tell you right now ni akina nani wanaolishughulikia hili jambo” “Mheshimiwa Rais unanishangaza sana kwa namna jambo hili unavyolifanya kuwa siri.Kuna kitu gani hapa ambacho hutaki kukiweka wazi?Ninashindwa kukuelewa mheshimiwa Rais” “I have my reasons! Akasema Dr Evans “Ni sababu zipi hizo ambazo zinakusababisha kutolifikisha suala hili kwa vyombo husika?Umekuwa unawalaumu wakuu wa vyombo vya usalama kwamba hawafanyi kazi zao vyema wakati kumbe unazo taarifa zote za magaidi hawa lakini uko kimya.Mheshimwa Rais ….”akasema waziri mkuu Rais akamkatisha “Waziri mkuu nimesema kwamba suala hili ninalishughulikia kwa namna ninavyojua mimi na ninakuomba yale niliyokueleza yawe siri yako sitaki jambo hili livuje.Umenielewa? akauliza Dr Evans akionekana kukasirika “Mheshimiwa Rais mwanangu anashikiliwa na magaidi na hatujui yawezekana yeye akawa ni wa pili kuchinjwa unadhani nitakuelewa vipi unaposhindwa kuchukua hatua madhubuti za kupambana na magaidi hawa? “Si mwanao tu ambaye anashikiliwa na magaidi hawa.Hata mimi pia nina uchungu pia kwani sijui hali ya mwanangu ikoje.Sifahamu kama ni mzima au wamekwisha muua lakini pamoja na uchungu huo ninalichukulia suala hili kwa umakini mkubwa sana na ndiyo maana sijataka suala hili lijulikane kwa sababu inaonekana huu ni mtandao mkubwa na wengine wamepandikiwa katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.Edger Kaka hakuwa peke yake lazima wapo watu aliokuwa anashirikiana nao hivyo basi kuliweka wazi hili jambo taarifa zitawafikia magaidi na mipango yetu yote itajulikana ndiyo maana ninalishughulikia kimya kimya” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais utaniona mtovu wa nidhamu lakini hapa tunazungumzia maisha ya watoto wasio na hatia wanaoendelea kuuawa.Wananchi hawatatuelewa kama hatutachukua hatua za haraka kuwazuia magaidi hawa wasiendelee kufanya mauaji ya watoto wetu.Lazima tuwadhibiti haraka sana kwa kila namna tuwezavyo” akasema waziri mkuu. “Magaidi watadhibitiwa lakini si kwa haraka kama unavyotaka wewe.Tunakwenda taratibu” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais suala hili si la kwenda nalo taratibu.Magaidi wameahidi kuua watoto wetu kila baada ya nusu saa hatupaswi kulichukulia rahisi hili jambo.Nchi iko katika taharuki wananchi hawana uhakika na usalama wao macho yao yote yako kwetu sisi lazima tuchukue maamuzi magumu ya kulimaliza hili jambo na kuwakomboa watoto wetu wanaoshikiliwa na magaidi” akasema waziri mkuu.Dr Evans akafikiri kidogo na kusema “Kwa mtazamo wako unashauri nini kifanyike?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais kwanza nataka kufahamu Edger Kaka yuko wapi?Je umejiridhisha ni kweli yuko hai?akauliza waziri mkuu “Ni kweli Edger Kaka yuko hai nimejiridhisha kwa hilo na tayari kikosi kinachoshughulika na suala hili kimefanikiwa kumkomboa kutoka mahala alikokuwa amefichwa na serikali ya Israel na yuko hapa nchini.Hivi tunavyoongea anafanyiwa mahojiano” “Pongezi kubwa kwa hilo mheshimiwa Rais lakini mimi ushauri wangu ni huu.Taifa liko katika taharuki kubwa sana.Kitendo walichokifanya magaidi hawa cha kuwachinja kama kuku wanafunzi waliowateka hakijawahi kuonekana hapa nchini na kimeleta hofu kubwa mno.Ili kuirejesha nchi katika hali ya kawaida ninashauri kwamba tukubaliane na hawa magaidi tuwapatie kile wanachokitaka”akasema waziri mkuu na Dr Evans akasimama “Mheshimiwa waziri mkuu niambie haumaanishi hicho unachokisema” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais ninamaanisha.Hatuna ujanja hawa jamaa tayari wamekwisha tubana katika kona na lazima tukubaliane nao ili tuwaokoe wasichana wetu.Timu inayoshughulikia hili suala hatuna uhakika kama itafanikiwa kuwapata magaidi hawa leo.Mheshimiwa Rais watu hawa kabla ya kufanya shambulizi lolote lile wanakuwa tayari wamekwisha jipanga vya kutosha kukabiliana na nguvu yoyote itakayotumika kuwatafuta.Ninaamini hadi kikosi hicho unachokitumia kifanikiwe kuwapata mahala walipo tayari idadi kubwa ya watoto wetu kama si wote watakuwa wamechinjwa ndiyo maana nashauri kwamba tuwape hicho wanachokitaka halafu tujipange upya namna ya kuwakabili.Kuwapa kile wanachokitaka kwa ajili ya kuwakomboa watoto wetu si kushindwa vita ni jambo la kawaida.Edger Kaka hana msaada wowote kwetu kwa muda ambao tulijua amefariki dunia hakuna shughuli yoyote iliyosimama hapa nchini hivyo hakuna kitu tutakachopungukiwa.Watu wote hapa nchini wanajua Edger amefarki dunia na hata tukiwapa magaidi mtu wao hakuna atakayejua bado jambo hili litaendelea kuwa siri kama unavyotaka na watoto wetu watakombolewa na baada ya hapo tutaanza kufanya uchunguzi kuubaini mtandao huu hapa nchini” akasema waziri mkuu na kumfanya DrEvans azame mawazoni. “Mheshimiwa Rais muda unakwenda mbio.Muda si mrefu kutoka sasa magaidi hawa watarusha tena video ya pili wakimchinja mtoto mwingine kama ndege.Siri hii tutaifahamu sisi watu wachache.Kama Edger kaka atakuwa na umuhimu mkubwa bado tutaendelea kumsaka na kumtia mikononi kwa kutumia vyombo vyetu” akasema waziri mkuu.Baada ya tafakari ya dakika tatu Dr Evans akasema “Mawazo yako si mabaya mheshimiwa waziri mkuu.Kuna kitu cha msingi nimekiona ndani yake.Nadhani tukubaliane na hawa jamaa na tuwape kile wanachokitaka ili tuweze kuwakomboa watoto wetu na nchi itulie” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais hayo ndiyo maamuzi kama Rais.Si kila wakati tutashinda kuna nyakati tutashindwa na katika hili si kwamba tumeshindwa bali tumekubali yaishe lakini tutajipanga tena upya kuwakabili vilivyo magaidi hawa”akasema waziri mkuu.Dr Evans akachukua simu na kumpigia Austin January mkuu wa kikosi cha jeshi cha operesheni maalum “Mheshimiwa Rais” akasema Austin “Austin nataka kujua kinachoendelea hapo sasa hivi kuhusiana na Yule mtu wetu Edger Kaka” “Kwa sasa kinachoendelea ni mahojiano.Mathew amempa Edger mapumziko mafupi kabla ya kurejea tena kuendelea kumuhoji” “Kuna mategemeo ya kupata kitu chochote kutoka kwake?akauliza Dr Evans “Mategemeo yapo lakini si kwa haraka.Inahitaji subira kidogo kwani kila mbinu zinatumika” akasema Austin “Sawa Austin nimekuelewa.Nimekupigia simu ili tuzungumze jambo moja la muhimu sana” “Nakusikiliza mheshimiwa Rais” “Nadhani tayari unazo taarifa kwamba usiku wa kuamkia leo magaidi walivamia shule moja ya sekondari wakateka watoto na tayari wameanza kuwachinja wakitaka tumuachie Edger Kaka.Baada ya tafakari ya kina nimeona hakuna haja ya kuendelea kumshikilia Edger Kaka wakati magaidi wanaendelea kuua watoto wetu.Nimeamua kuwapa kile wanachokitaka yaani Edger Kaka.Najua ni maamuzi yatakayowastua sana akina Mathew hasa baada ya kazi kubwa na ngumu ya kumrejesha nyumbani lakini sina namna ya kufanya kwa haraka kuzuia watoto wetu wasiendelee kuuawa.Magaidi tayari wamemuua binti mmoja na wameahidi kuendelea kuua watoto wengine kila baada ya nusu saa hivyo nimeamua kuwapa wakitakacho.Naomba jambo hili liwe siri yako na usiwaeleze akina Mathew.Kuna mtu ninamtuma sasa hivi anakuja hapo kambini kumchukua Edger Kaka” akasema Dr Evans na katika line ya simu kukawa na ukimya mkubwa “Austin are you there?akauliza Dr Evans “Nipo mheshimiwa Rais” “Good.Umenielewa nilichokisema? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais,nitafanya kama ulivyoelekeza” akajibu Austin na DrEvans akakata simu “Mheshimiwa Rais hakuna namna unayoweza kuwasiliana na hawa jamaa ukawajulisha kwamba wasifanye tena mauaji mengine ya watoto kwani ombi lao unalifanyia kazi? Akauliza waziri mkuu “Wao ndio hupiga simu pale wanapohitaji kuzungumza nami.Naamini kabla ya kufanya mauaji mengine lazima watanipigia simu” akasema Dr Evans na kumuita mmoja wa wasaidizi wake akampa maelekezo ya kwenda katika kambi ya kikosi cha operesheni maalum akamchukue Edger Kaka na kisha asubiri maelekezo “Ni namna gani tutafanya makabidhiano na hao jamaa? Tutakuwa na uhakika gani kama tukiwapa mtu wao watarejesha watoto wetu?akauliza waziri mkuu “Shida yao ni kumpata Edger Kaka pekee hivyo watakapompata hawatakuwa na sababu ya kuendelea kuwashikilia watoto wetu” akanyamaza Dr Evans baada ya simu yake kuita.Akazitazama mpigaji halafu akamtazama waziri mkuu “Wenyewe wanapiga” akasema Dr Evans na kutazama saa “Why don’t we trace that call na kufahamu mahala walipo? “They are not stupid.They are very smart people.This phone is untraceable! Akasema Dr Evans “Sawa waambie wasiue tena watoto tunawapa mtu wao” akasema waziri mkuu na Dr Evans akapokea simu “Mheshimiwa Rais sina maneno mengi nadhani salamu zetu tayari umekwisha zipata.Zoezi tulilolianza linaendelea nimekupigia kukujulisha kwamba ndani ya dakika chache zijazo tutaondoa shingo ya mwanafunzi mwingine.Ninataka kufahamu kuna mabadiliko yoyote au bado msimamo wako ni ule ule? “Tafadhali msiue tena mwanafunzi mwingine.Ninyi ni watu makatili sana mmetoa uhai wa mwanafunzi asiye na hatia ! akafoka Dr Evans “Damu ya mwanafunzi Yule na wote tutakaoendelea kuwatoa uhai iko juu yako mheshimiwa Rais.Wewe ni sababu ya watoto hawa wasio na hatia kuuawa.Kama unataka kuokoa maisha yao tekeleza kile tunachokitaka na wataendelea kuwa salama lakini ukitaka kushindana nasi utawapoteza wote.Sisi hatuogopi kufa mheshimiwa Rais hapa tulipo tumevaa mabomu tayari kujilipua na watoto hawa pale itakapolazimu kufanya hivyo” “Tafadhali msiue tena mtoto mwingine.Nitawapa kile mnachokitaka.Nitawapa Edger Kaka.Ninaomba mnipe muda zaidi ili niweze kumuandaa kwa ajili ya kuwakabidhi ila naomba mtakapompata mtu wenu msiendelee tena na mauaji ya watu wasio na hatia” “Mheshimiwa Rais tupe mtu wetu na sisi tutasitisha mauaji na hautasikia tena kuna mtu ameuawa na IS hapa nchini kwako.Kwa kuwa umekubali kuimaliza hii vita nitakupigia baada ya nusu saa na kama utakuwa unanidanganya nitawakata vichwa wanafunzi saba.! Akasema na kukata simu. “Wameongeza tena nusu saa.Kama hatutakuwa tumewakabidhi mtu wao wataua wanafunzi saba” “Mheshimiwa Rais hawa jamaa hawatanii kabisa.Ni watu wenye roho za kikatili mno” akasema waziri mkuu “Ndani ya muda huo tayari Edger atakuwa amepatikana na tutasubiri maelekezo yao mahala pa kumpeleka na mahala tutakapowapata watoto wetu” akasema Dr Evans “Nimewahi kufanya kazi na Edger Kaka bungeni alikuwa mmoja wa wabunge mahiri mno katika kuchangia mambo mbali mbali.Kila aliposimama bunge lilikaa kimya kumsikiliza.Bado ninatafakari taarifa hizi kwamba ana mahusiano na kikundi cha IS” akasema waziri mkuu.
Austin January aliegemea meza ya ofisi yake baada ya kumaliza kuzungumza na Rais.Alikuwa katika mawazo mengi. “Nini kimetokea hadi Rais anataka kumkabidhi Edger Kaka kwa magaidi ambao wanafanya mauaji ndani ya ardhi yetu?Hapa Rais amekosea.Nilikula kiapo cha kumtii Rais lakini kwa hiki anachotaka kukifanya niko tayari kuvunja kiapo changu.Edger ni mshirika wa magaidi na kamwe hawezi kukabidhiwa kwa magaidi.Hatuwezi kusalimu amri kwa magaidi hata siku moja.Lazima nikiri hapa Rais ameonyesha udhaifu mkubwa.Ana uhakika gani kama akiwapa wanachokitaka watawaachia watoto wanaowashikilia?Ni vipi kama akiwapa mtu wao na wasiwaachie watoto na wakaanzisha tena madai mengine? Wanaweza wakasema hivyo kwani tayari wamekwisha muona ana udhaifu” akawaza Austin na kutoka haraka ofisini kwake akaelekea katika chumba cha mahojiano akawakuta Gosu Gosu na Devotha wakifuatilia mahojiano ya Mathew na Edger “Kuna chochote kimepatikana?akauliza “Mathew ameingia muda mfupi uliopita kuendelea kumuhoji Edger”akajibu Gosu Gosu na Austin akafungua mlango akaingia ndani ya kile chumba cha mahojiano “Mathew excuse me can I talk to you for a second? akasema na Mathew akatoka “Mathew we need to get out of here now ! “Nini kimetokea?akauliza Mathew kwa mshangao “Listen to me Mathew we’re leaving this place now ! “I don’t understand you Austin.Nini kimetokea?Tunakwenda wapi?Vipi kuhusu mahojiano na Edger?akauliza Mathew “Tunamchukua tutakwenda kuendelea na mahojiano naye huko mbele ya safari.We need to hurry.Tusaidiane tumbebe tuondoke! Akasema Austin na Mathew akamuita Gosu Gosu wakasaidiana wakambeba Edger Kaka wakamfuata Austin hadi katika gari la Mathew aina ya land cruiser v8 rangi nyeusi wakamuingiza Edger sehemu ya nyuma na kumlaza Gosu Gosu akapewa kazi ya kumchunga na Austin akaondoa gari. “Austin what happened? Akauliza Mathew baada ya kulivuka geti. “Something happened nitawaeleza mbele ya safari”akasema Austin “Tunakwenda wapi?akauliza Mathew ambaye alistushwa sana na mabadiliko yale ya Austin “Somewhere safe”akajibu Austin huku akiwa makini kufuatilia kama kuna gari yoyote inawafuata.
Kitendo cha magaidi kurusha mtandaoni video wakimchinja mmoja wa wanafunzi waliomteka kiliamsha hasira kali kwa wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamekusanyika katika shule ya sekondari ya St.Getrude ambako wanafunzi waliotekwa walikuwa wanasoma.Umati mkubwa wa wazazi na watu wengine ulikuwa umekusanyika katika shule hii kupata taarifa za kilichotokea na kujua hatima ya watoto wao.Mkuu wa polisi wa kituo kilichokaribu na shule ile ambaye alikuwepo pale shuleni na timu ya makachero wakiendelea na uchunguzi wa tukio lile aliwasihi wananchi wale wawe watulivu kwani suala lile linashughulikiwa na jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Video ya mwanafunzi akichinjwa mabayo ilisambaa mtandaoni kwa kasi kubwa iliamsha hasira kali kwa wananchi wale na vilio vikasikika.Illazimu kuongeza askari polisi zaidi eneo lile kwani tayari kulikwisha anza kuonekana viashiria vya kuvunjika amani.Askari polisi baada ya kuona hali imebadilika na hasira miongoni mwa wananchi wale imepanda wakawataka wazazi wale kutawanyika eneo lile kwani suala la watoto wao kutekwa linashughulikiwa na watapewa taarifa.Kutoka ndani ya gari moja jeupe ambalo lilikuwa limeegeshwa pembeni kabisa ya shule akashuka mtu mmoja akiwa na kipaza sauti akapanda juu ya gari na kuanza kutangaza. “Jamani watoto wetu wametekwa,wanauawa na hatupati jibu lenye uhakika kuhusu juhudi za kuwatafuta.Tukiendelea kukaa hapa hatutawapata watoto wetu.Twendeni tuanze maandamano kuelekea ikulu kwa Rais kushinikiza juhudi za kuwatafuta watoto wetu.Bila kutoa shinikizo kwa serikali watoto wetu hawatapatikana.Twendeni ikulu hatuogopi mabomu,tunaandamana wa amani kushinikiza serikali iwatafute watoto wetu.Tuko pamoja jamani? akauliza Yule jamaa na wananchi wote wakamuunga mkono na maandamano yakaanza kutoka pale shuleni wakitembea kwa mguu kuelekea ikulu.Waliingia katika barabara kuu na kulazimisha magari kusimama kwa muda kuwapisha wapite.Kadiri walivyozidi kusonga mbele ndivyo taarifa zilizvyozidi kusambaa na idadi ya watu kuzidi kuongezeka.Jeshi la polisi lililazimika kuchukua hatua za kuyatawanya maandamano yale yasiyokuwa na kibali ambayo yalianza kugeuka kero kwa watu waliokuwa wakiendelea na shughuli zao kwani kila walikopita ililazimu shughuli zote kusimama kwa muda. Gesi ya kutoamachozi na maji ya kuwasha vilitumika katika kuwatawanya waandamanaji wale na kusababisha mtafaruku mkubwa.Mtifuano ule kati ya polisi na waandamanaji ulikuwa ni kama kuongeza mafuta katika moto kwani idadi ya watu ilizidi kuongezeka,biashara kufungwa shughuli zikasimama na wengi wakajiunga katika maandamano yale ya kuishinikiza serikali iweze kupambana na magaidi wale na kuwakomboa watoto waliotekwa. Taarifa za maandamano yale makubwa zilifika ikulu katika chumba ambamo mkutano wa dharura wa baraza la usalama la taifa ulikuwa unaendelea na kumlazimu Rais kuahirisha kwa muda kikao kile hadi jioni ili waweze kushughulikia lile suala lililojitokeza.Yeye na waziri mkuu wakaelekea ofisini “Mheshimiwa Rais nadhani sasa umeamini maneno yangu niliyokwambia kwamba suala hili litakuwa kubwa sana na tayari moto umeanza kuwaka.Wananchi wana hasira kali ndiyo maana wameingia barabarani wakiandamana kushinikiza serikali kufanya juhudi za kuwakomboa watoto wao waliotekwa na magaidi”akasema waziri mkuu “Ulikuwa sahihi kabisa.Hakuna tena haja ya kuendelea kupambana na hawa jamaa tuwape kile wanachokitaka na tuwapate watoto wetu” akasema Dr Evans na kuchukua simu akampigia Austin lakini simu ikaita bila kupokelewa.Akapiga tena bado simu iliendelea kuita bila kupokelewa. “Kwa nini Austin hapokei simu?akajiuliza Dr Evans na kumpigia simu mtu aliyemtuma kwenda kumchukua Edger kaka “Mheshimiwa Rais” akasema Yule jamaa baada ya kupokea simu “Ben umefika wapi? “Mheshimiwa Rais tayari nimefika hapa mahala uliponituma lakini kuna tatizo nimelikuta hapa na nilikuwa katika harakati za kukupigia simu kukujulisha” “Kuna tatizo gani? akauliza “Austin hayupo hapa kambini na kwa taarifa nilizopewa ameondoka hapa kambini kama dakika kumi na tano zilizopita.Nimepelekwa kwa msaidizi wake nikampa maagizo uliyonipana akaniambia kwamba mtu niliyetumwa kuja kumchukua Edger Kaka ambaye ameletwa kutoka Nairobi alfajiri ya leo amechukuliwa na akina Austin na hajui wamempeleka wapi” “What ? That can’t be.Nimezungumza na Austin na kumpa maagizo kwamba nitatuma mtu kwenda kumchukua Edger kaka sasa iweze aondoke naye?Hebu mpe simu huyo msaidizi wake nizungumze naye ! akasema Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais” ikasema sauti ya upande wa pili “Derick nataka kufahamu Austin amekwenda wapi? “Hakuna anayejua amekwenda wapi mheshimiwa Rais,ameondoka hapa bila kumjulisha mtu yeyote mahala anakoenda” “Alikuwa ameongozana na nani? “Kwa mujibu wa waliomuona wakati akiondoka alikuwa ameongozana na wale jamaa aliokuwa nao katika operesheni ya Nairobi jana usiku,Mathew Mulumbi na wenzake vile vile walimchukua Edger Yule mtu waliyekwenda kumkomboa Nairobi na hakuna anayejua wamekwenda wapi” akasema Derick “Bastard ! akasema DrEvans na kugonga meza kwa hasira “Derick hakuna namna mnayoweza kumfuatilia Austin kufahamu mahala alipo? “Mheshimiwa Rais haitakuwa rahisi kwa kuwa hawajumia gari la kikosi wametumia gari walilokuja nalo akina Mathew Mulumbi.Magari yetu ya kikosi ingekuwa rahisi kufuatilia kwa sababu yote yana mfumo ambao unatuwezesha kufahamu mahala yalipo” “Oh my God ! Kwa nini Austin amenifanyia hivi?akauliza Dr Evans na ukimya mfupi ukapita halafu akasema “Derick ninakupa kazi ya kumtafuta Austin.Tumia njia zozote unazozijua kumtafuta na ukifanikiwa kujua mahala alipo nijulishe haraka sana.Ninakuahidi zawadi kubwa mno kama ukilifanikisha hilo.Nitakupa hata uwaziri kama utafanikiwa kumpata Austin.Derick ninamaanisha ninachokisema kwani suala hili ni muhimu mno kwa taifa.Austin amefanya kosa kubwa sana.Umenielewa Derick? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” “Good.Tumia kila aina ya uwezo mlio nao hapo kikosini kumtafuta Austin mahala alikoelekea.Watumie wataalamu wote mlio nao hapo na kama mkifanikisha kumpata nitawazawadia shilingi bilioni moja mgawane na ahadi yangu ya kuupa nafasi kubwa ndani ya serikali iko pale pale.Derick umenielewa ninachokimaanisha? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais na ninakwenda kuianza kazi hiyo sasa hivi” “Good.Nijulishe ukipata chochote” akasema Dr Evans na kuiweka simu mezani “Nini kimetokea mheshimiwa Rais?akauliza waziri mkuu “That bastard Austin is gone.Edger Kaka is gone! “Sijakuelewa mheshimiwa Rais ametoweka vipi? “Give me a second” akasema Dr Evans na kumpigia simu Kaiza “Mheshmiwa Rais shikamoo mzee” akasema Kaiza “Kaiza nataka nikupe kazi ambayo ukiifanya kikamilifu nitakupa zawadi kubwa ambayo hukuwahi kuitegemea.Safari hii sitaki mzaha” akasema DrEvans “Niko tayari mheshimiwa Rais kwa kazi yoyote” “Good.Nataka utumie kila aina ya uwezo ulio nao kumtafuta Devotha.Ninamuhitaji sana tena kwa haraka.Ukifahamu mahala alipo nijulishe haraka sana.Nakuahidi Kaiza kama uifanikiwa kumpata Devotha nitakupa nafasi kubwa sana ambayo hukuwa umeitarajia” “Mheshimiwa Rais ahsante kwa jukumu hilo naomba unipe muda nilifanyie kazi kwa kutumia kila uwezo nilio nao” akasema Kaiza na Dr Evans akakata simu “Mheshimiwa Rais nini kinaendelea?Nini kimetokea?Hao uliokuwa unazungumza nao ni akina nani?akauliza waziri mkuu “Edger is gone.Siamini kama Austin amenifanyia kitu kama hiki.oh my God ! “Who is Austin? “Ni mkuu wa kikosi nilichokituma kwenda kumchukua Edger kaka mahala alikokuwa amefichwa.Baada ya kufanikiwa kumrejesha Edger kaka nyumbani nilielekeza ahifadhiwe mahala salama kitu cha kushangaza baada tu ya kumwambia kwamba ninatuma mtu kwenda kumchukua,Mathew amemtorosha na hawajulikani wamekwenda wapi.I’m sure this was Mathew’s idea ! “Mathew ! who is he? Akauliza waziri mkuu “Mheshimiwa kwa sasa tujielekeze katika kutafuta plan B.Tayari kumeanza kuonekana mkwamo katika mpango wetu wa kumkabidhi Edger kaka kwa IS” “Mheshimiwa Rais sijakuelewa nini hasa kimetokea? Kwa nini Edger asipatikane?akauliza waziri mkuu “Waziri mkuu hili limekuwa ni tatizo kubwa kwa sasa tujaribu kubuni namna nyingine ya kulishughulikia hili suala wakati jitihada za kuwasaka hao jamaa waliomtorosha Edger zinaendelea” “Mheshimiwa Rais hao watu kwa nini wamemtorosha Edger? “Siwezi kufahamu.Naomba tusipoteze muda mheshimiwa waziri mkuu tujitahidi kutafuta namna ya kukabiliana na hili suala.Kumbuka wale jamaa wameahidi kuua wasichana saba kama hatutawapatia Edger katika muda huo walioutoa” “Nimechanganyikiwa mheshimiwa Rais na sijui nifanye nini” akasema waziri mkuu na kuzama katika tafakari ya muda mfupi halafu akasimama “Mheshimiwa Rais sasa nimekuelewa lakini naomba nikufahamishe kitu kimoja kwamba mimi si mtoto mdogo unayeweza kucheza na akili yangu.Nafahamu yote hii ni michezo yako unataka kunichezea lakini nakuhakikishia kwamba haitafanikiwa kamwe.Mpaka sasa sijafahamu kitu gani ambacho unakificha na hutaki kuliweka wazi hili suala kwa vyombo husika vilifanyie kazi.Sitaki tena kupoteza muda kujua kitu gani unakificha lakini siwezi kamwe kuendelea kukaa hapa kupoteza muda wakati watoto wetu wakiendelea kuchinjwa kama kuku ! akasema kwa ukali waziri mkuu na kugeuka akaanza kupiga hatua kuelekea mlangoni Dr Evans akabaki amepigwa na butwaa “Mheshimiwa waziri mkuu !! akaita Dr Evans lakini waziri mkuu hakugeuka akaufungua mlango na kutoka hakupoteza muda akachukua simu na kumpigia kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam na kumtaka asiwatawanye waandamanaji bali awaache wakusanyike yeye anakwenda mahala hapo.Baada ya kuzungumza na kamanda wa polisi waziri mkuu akainga katika gari na msafara wake ukaondoka ikulu.Akiwa garini akaamuandikia mtu Fulani ujumbe mfupi “Our plan is working.Ninaelekea kwenye maandamano.Tukutane hapo” Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam alifika sehemu ambako maandamano ya wananchi waliokuwa wanakwenda ikulu kutaka kumshinikiza Rais kufanya juhudi za kuwakomboa wasichana waliotekwa yalizuiliwa.Kwa kutumia kipaaza sauti aliwatangazia waandamanaji warejee sehemu ile na wawe watulivu wamsubiri waziri mkuu ambaye alikuwa njiani akielekea mahala pale kuzungumza nao.Polisi wote waliondolewa na kuingia katika magari yao ili kuondoa hofu kwa waandamanaji Dakika kumi na saba msafara wa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ukawasili eneo ambalo maandamano yalizuiliwa.Watu walikuwa wamekusanyika tena baada ya tamko lile la kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam.Baada ya kufika eneo la tukio waziri mkuu akazungumza na kamanda wa kanda maalum halafu akajitokeza juu ya gari lake akapewa kipaza sauti “Habari za asubuhi ndugu zangu” akawasalimu watu wale waliokuwa wamekusanyika.Watu wengine waliokuwa wametawanyika na kujificha wakiogopa askari polisi wakajtokeza na kuanza kurejea baada ya kumuona waziri mkuu. “Kwanza kabisa nachukua nafasi hii kuwapeni pole sana kwa kile kilichotokea usiku wa kuamkia leo baada ya magaidi kuwateka watoto wetu sitini na sita.Kama haitoshi wamefanya unyama mwingine mkubwa kwa kuanza kuwaua watoto wetu.Huu ni ukatili uliopitiliza na hauvumiliki. Ndugu zangu nimekuja hapa kama mzazi kwani na mimi pia mwanangu ni mmoja wa watoto waliotekwa.Nimekuja kuungana nanyi katika kuishinikiza serikali iweze kufanya kila iwezalo kuhakikisha watoto wetu wanakombolewa”akasema waziri mkuu na watu wakashangilia “Najua wengi mtashangaa sana kwa nini nije kuungana nanyi wakati mimi ni sehemu ya serikali ambayo inatakiwa kuhakikisha inafanya kila juhudi za kuwakomboa watoto wetu lakini hapa sipo kama waziri mkuu ninaungana nanyi kama mzazi na tutaandamana wote kwa pamoja kwa amani huku tukishindikizwa na polisi tukielekea ikulu kumshinikiza Rais aweze kutumia nguvu yake kuwakomboa watoto wetu.Rais anao uwezo wa kuwakomboa watoto wetu na kuzuia wasiuawe na magaidi hivyo tunakwenda ikulu na hatutaondoka pale hadi tutakapohakikisha watoto wetu wamekombolewa.Msiogope ndugu zangu lazima tushikamane imara kuhakikisha watoto wetu wanarejeshwa” akasema waziri mkuu huku akishangiliwa akashuka garini na kwenda kuungana na waandamani wakashikana mikono na safari ya kuelekea ikulu ikaanza.Maandamano yale ambayo sasa yaliongozwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yaliendelea kuzoa idadi kubwa ya watu na kulifanya jiji la Dar es salaam kusimama kwa muda.
Baada ya kutoka katika kambi yao,Austin aliwapeleka akina Mathew hadi katika nyumba Fulani iliyokuwa na ukuta wa mawe.Haikuwa nyumba kubwa sana ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala sebule jiko chumba kidogo cha kupumzika na chumba cha kusomea. “Karibuni ndani jamani” akasema Austin na kumsaidia Gosu Gosu kumbeba Edger na kumuingiza ndani wakampeleka katika moja wapo ya chumba na kumfunga pingu mkononi katika dirisha lililokuwa karibu na kitanda alicholazwa. “Whats’s going on Austin?akauliza Mathew “Wakati ukiendelea kumuhoji Edger nilipokea simu kutoka kwa Rais akanieleza kwamba anatuma mtu kuja kumchukua Edger Kaka kwani amefanya maamuzi ya kumkabidhi kwa magaidi.Alinielekeza kwamba nisiwataarifu kuhusu jambo hili.Baada ya simu ile nilitafakari nikaona haitakuwa sawa.Huyu mtu amewahi kuwa kiongozi na ana mahusiano na magaidi yawezekana akawa ni pandikizi na alikuwa anatumiwa kuwapa magaidi siri za nchi.Kuna mambo mengi ambayo hatuyafahamu kuhusu Edger kaka hivyo nikaamua kupingana na Rais na kumchukua Edger kumleta hapa.Naamini baada ya kugundua kwamba nimemtorosha Edger Rais atakasirika sana na mpaka sasa nimekwisha poteza kazi yangu na tayari nimeingia katika mgogoro mkubwa na mkuu wa nchi lakini hilo si tatizo kwangu kwani nilichoamua kukifanya ni kwa manufaa ya taifa.Maamuzi ya Rais ni maamuzi ya uoga na yanafaa kupuuzwa.Ni maamuzi ya kutatua tatizo kwa muda mfupi bila kufahamu kama kuna mtandao mkubwa wa IS hapa nchini.Kuanzia sasa mimi ni mwenzenu tutashirikiana pamoja katika kupambana na hawa magaidi wanaotishia amani na usalama wa nchi yetu” akasema Austin “Dah ! akasema Mathew akiwa katika mshangao “Nimekosa neno la kusema kwa hiki alichotaka kukifanya Rais.Austin una hakika kweli ni Rais ndiye aliyekupa maelekezo hayo na si mtu mwingine aliyetumia simu ya Rais?akauliza Mathew “Ni Rais.Nimekuwa nazungumza na Rais mara kwa mara na kama angekuwa ni mtu mwingine ametumia simu yake ningegundua lakini aliyenipigia simu na kunipa maelekezo yale ni Rais Dr Evans” akasema Austin “Oh my God ! ni akili yake kweli au kuna mtu kamshauri afanye hivi?Tumeyaweka maisha yetu rehani kwa ajili ya kwenda kumkomboa Edger Kaka nchini Kenya lakini kumbe alikuwa na mipango yake,amenisikitisha sana sikutegemea kabisa kama angeweza kutufanyia kitu kama hiki.Ahsante sana Austin kwa hiki ulichokifanya,usijali kuhusu kazi hapa tunalitanguliza taifa kwanza.Kuanzia sasa tutambue kwamba operesheni hii tuko peke yetu na hatuna tena msaada wa Rais” akasema Mathew “Kwa namna ninavyomfahamu Dr Evans akigundua kwamba tumemtorosha Edger tayari tutakuwa maadui zake na atatumia nguvu kubwa kutusaka.We must prepare ourselves for that” akasema Devotha. “Vipi kuhusu Ruby na Yule mke wa balozi? Akauliza Gosu Gosu “We must go get her.Ruby ni muhimu sana katika operesheni hii.” akasema Mathew “So what’s the plan?akauliza Austin “Plan ya kwanza ni kuwakomboa watoto waliotekwa ambao tayari IS ameanza kuwaua.Naamini Rais amewaahidi kuwa atawapa mtu wao lakini baada ya kumkosa hali itakuwa mbaya lazima watawachinja watoto kwa hasira.Tunatakiwa tusimamishe mauaji hayo na kuwakomboa watoto”akasema Mathew “How are we going to do it?akauliza Devotha “We have Edger kaka.Huyu atatusaidia sana kuweza kuufahamu mtandao wao” akasema Mathew “Mathew unadhani anaweza akafunguka kwa haraka na tukazuia mauaji yale ya watoto yasiendelee?Tayari wameua mmoja na wametishia kuendelea kuua kila baada ya muda Fulani”akasema Austin “Let me try once again.Lazima kila mbinu itumike kuhakikisha Edger anaongea.Guys let’s not waste time.Gosu Gosu na Devotha mnakwenda kuwachukua Ruby na mke wa balozi mimi na Austin tutaendelea hapa” akasema Mathew “Mathew I don’t think that’s a good idea.Laiti kama ungekuwepo ingesaidia lakini nikienda peke yangu na Gosu Gosu anything can happen.Ruby bado ana hasira na mimi”akasema Devotha “I’ll go.Nitakwenda badala ya Devotha” akasema Austin na Mathew hakuwa na kipingamizi wakaondoka akabaki na Devotha.Mathew akamuacha Devotha akichunga usalama yeye akaingia katika chumba alimo Edger Kaka “Edger kaka tumelazimika kukuhamisha na kukuleta hapa kwa sababu maalum.Israel tayari wamekwishafahamu kwamba ni sisi tuliokuteka nyara na hivi tunavyoongea umeibuka mzozo mkubwa sana kati yao na sisi ndiyo maana Rais akaelekeza tukuondoe pale haraka sana.Wewe ni Raia wa Tanzania na hatuwezi kukukabidhi kwa Israel kwani watakuua.Rais ana mpango mzuri sana juu yako Edger anataka kukusaidia ili uweze kuishi maisha mazuri yenye amani ukiwa na mwanamke umpendaye Olivia.Lakini ili tukusaidie nawe pia hauna budi kutusaidia kufahamu mtandao wa IS hapa Tanzania na kuwapata Olivia pamoja na watoto waliotekwa usiku wa leo.Edger wasichana wale hawana hatia yoyote na tayari IS wamekwisha anza kuua mtoto mmoja baada mwingine kwa kuwakata vichwa.Huu ni ukatili mkubwa sana na usiovumilika.Wasichana wale hawafahamu chochote na hawastahili kutendewa ukatili wa namna hii.Wasichana sitini na sita wote watauawa kama hatutafanya juhudi za kuwakomboa” akasema Mathew na Edger akaendelea kumtazama bila kusema chochote.Mathew akasema “Edger nataka kujua kitu kimoja toka kwako.Uliendesha harakati kubwa sana hapa nchini za kufichua ufisadi uliokuwa unafanywa na watu mbali mbali serikalini ukajenga jina kubwa na wananchi wakakuamini.Nataka kufahamu je mambo yale uliyokuwa unayafanya ni kweli uliyafanya kwa dhamira ya dhati ya kupambana na kufichua ufisadi au ilikuwa ni moja ya njia zako ya kutafuta umaarufu ili kuficha maovu yako? Bado Edger Kaka alikuwa kimya “Edger please.Muda unakimbia nijibu swali langu ni kweli ulikuwa na dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi au ilikuwa ni moja ya mipango yako kujenga taswira nzuri mbele ya jamii ili kuficha mambo yako unayoyafanya? akasema Mathew na kumtazama Edger machoni “Don’t say it.Tayari nimepata jibu.It was all lies.Mapambano yale yalikuwa ni kiini macho kuwalaghai wananchi,kujenga jina lako katika jamii.Nini hasa lilikuwa lengo lako au lengo lenu?Naamini haukuwa peke yako katika hili.Mlikuwa na mipango gani?akauliza Mathew Edger aliendelea kuwa kimya “Nani ni kiongozi wa mtandao wenu hapa Tanzania? Naamini si wewe bali yupo mkubwa wako na wewe ulikuwa unatumika tu.Nani kiongozi wako?akauliza Mathew lakini bado Edger aliendelea kuwa kimya akimtazama Mathew “Edger unaniudhi sana ninapokuuliza unakaa kimya.Ninao uwezo wa kukuharibu hapa hapa lakini ninayaheshimu maelekezo ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ana malengo mazuri ya kukusaidia ili ukaishimaisha mazuri mahala ambako hakuna atakayekugundua.Nataka unisaidie tuweze kuwakomboa wale wasichana ambao wanakatwa shingo kikatili huku watu wakishuhudia mtandaoni.Ni kitendo cha kikatili sana walichokifanya.Watoto wale wanaouawa wana ndoto zao ambazo wanataka kuzitimiza katika maisha yao lakini wanakatishwa ndoto zao kikatili.Edger your not a killer.You are not like them.Macho yako yanaonyesha haujawahi kutoa roho ya mtu hivyo basi waonee huruma watoto wale wanaouawa bila kuwa na kosa lolote.Naomba utusaidie tuwapate wale watoto” akasema Mathew.Edger akainamisha kichwa akaonekana kuzama mawazoni “Edger hakuna tena kitu cha kuficha kuhusu IS.Hawana msaada tena kwako.Kwao umekwisha fariki na hauna thamani tena hivyo ni wewe na sisi tu.Tusaidie na sisi tukusaidie ili uishi maisha yenye raha mustarehe mahala ambako hakuna atakayekufahamu ukiwa na mwanamke Yule umpendaye” akasema Mathew na baada ya dakika mbili Edger akainua kichwa akaonekana kusikitika na kusema “Fine,let’s end this.Nitawaeleza kile ninachokifahamu lakini ninataka kuzungumza na rais ili nipate uhakika kutoka kwake kwamba baada ya kuwapa kile mnachokitaka nitapatiwa kile ninachokitaka” akasema Edger “Baada ya kitisho cha magaidi ulinzi wa Rais umeongezeka na hivi tunavyozungumza Rais yuko mahala pa siri na hakuna namna utakayoweza kuzungumza naye kwa sasa.Niko hapa kwa niaba yake hivyo utazungumza na mimi.Rais tayari amekwisha weka wazi kuwa anataka kukusaidia.Zungumza nami nieleze chochote unachokitaka na utakipata” akasema Mathew. “I need a new passport with new name,I need a house.Si nyumba tu mradi nyumba nataka nyumba nzuri ya ghorofa yenye hadhi huko Uswisi.I need two cars,luxury ones.Nahitaji mtaji mkubwa utakaoniwezesha kuwekeza katika kilimo,mwisho namuhitaji Olivia.Mkinihakishia kwamba nitapata hivyo vyote niko tayari kuwasaidia kuwapa taarifa”akasema Edger “Edger,Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania yuko tayari kufanya chochote kile utakachokihitaji ili uweze kutupa taarifa muhimu.Hesabu kwamba haya yote umeyapata” akasema Mathew “Not so simple Mr…what’s your name again?akauliza Edger “Mathew ..Mathew Mulumbi” “Mr Mathew Mulumbi mambo hayaendi kirahisi namna hiyo.Nahitaji uhakika kutoka kwa Rais pekee na si mtu mwingine” akasema Edger “Kama nilivyokwambia kwamba Rais haitawezekana kuzungumza naye kwa sasa kutokana na kupelekwa sehemu salama kufuatia vitisho vya mashambulio ya kigaidi na badala yake nipo mimi.Usihofu mambo yako yote yatatekelezwa.Lakini wakati hayo yakitekelezwa kwa nini tusianze kwanza kumtafuta Olivia? Kila unachokitaka kitapatikana lakini kitakosekana kimoja tu,Olivia Themba.Nipe taarifa ambazo zitatusaidia kumuokoa Olivia.Ninakuhakikishia kila kile unachokihitaji kitapatikana.I give you my word” akasema Mathew “Mathew wewe mwenyewe unafahamu namna mambo haya yanavyokwenda ninahitaji uhakika kwamba kweli yale ninayoyataka yanakwenda kutekelezwa.Convince me! Akasema Edger Kaka.Mathew akamtazama usoni kwa makini halafu akasema “Unataka kutumia jina gani jipya? Edger akafikiri kidogo na kusema “Nickson Robert” “Sawa nisubiri nitarejea”akasema Mathew na kutoka “Bastard ! akasema Mathew kwa ukali. “Nini kimetokea?akauliza Devotha “Edger yuko tayari kufunguka lakini kuna masharti ametoa” akasema Mathew “Ametoa sharti gani? “Anataka nyumba ya kifahari Uswisi,anataka magari mawili ya kifahari anataka mtaji wa kuwekeza katika kilimo na anataka hati mpya ya kusafiria yenye jina jipya na mwisho kabisa anataka kuondoka na Olivia Themba.Tukimtekelezea hayo yote yuko tayari kutupa maelezo ya kutusaidia kuwakomboa watoto pamoja na Olivia” “Vitu alivyovitaka ni vikubwa mno viko nje ya uwezo wetu.Tutafanya nini kuvipata na mahusiano yetu na Rais yamevunjika?Kama bado tungekuwa na mahusiano naye,Rais anao uwezo wa kutekeleza hayo yote”akasema Devotha “Forget about president.We’ll move on without him.Edger anahitaji kitu cha kumridhisha kwamba maombi yake yanafanyiwa kazi” “What are we going to do Mathew? “I need to call my wife in Paris” “Your wife? Akauliza Devotha “Ndiyo” “Mkeo anaingiaje katika sakata hili? “Ni bilionea mkubwa.Anafahamiana na matajiri wakubwa sehemu mbali mbali duniani,nataka anisaidie kupata nyumba ya kununua nchini Uswisi ambayo itanunuliwa kwa jina la Nickson Robert ambalo amechagua Edger” “Mathew kwa nini unataka kuingia hasara? “I don’t care ninachohitaji ni kupata taarifa za kutuwezesha kuwakomboa Olivia,Coletha na watoto waliotekwa.Tuwasubiri akina Gosu Gosu warejee na vifaa ili niweze kupiga simu kwa mke wangu.Tukinunua nyumba hiyo ataridhika na atatueleza kila kitu” akasema Mathew
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliendelea kuongoza maandamano ya wananchi kuelekea ikulu kumshinikiza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutumia nguvu kuwakomboa watoto waliotekwa nyara ambao walianza kuuawa na magaidi. Akiwa ofisini kwake Dr Evans alipewa taarifa ya waziri mkuu kuungana na wananchi katika maandamano ya kuelekea ikulu kushinikiza kuwakomboa watoto waliotekwa.Zilikuwa ni taarifa zilizomstua sana Dr Evans. “Traitor ! akasema kwa ukali huku akitazama maandamano yale yaliyokuwa yanarushwa mubashara runingani “Nilifanya kosa kubwa sana kumuamini waziri mkuu na kumpa siri za kile kinachoendelea.Bahati nzuri sikumpa siri zote hasa kuhusiana na ile idara ya siri wala kutekwa kwa akina Olivia.Sikujua kama angeweza kunigeuka namna hii na sasa ameamua kulifanya jambo hili kama mtaji wake wa kisiasa.Kwa nini nikakubali kumsikiliza na kufuata ushauri wake? Ni kwa sababu yake nimewapoteza akina Mathew hadi Austin January ambaye siku zote amekuwa mtiifu mno kwangu.Wote wameniona mimi ni mpuuzi kwa sababu waliyaweka rehani maisha yao kwa ajili ya kwenda kumkomboa Edger Kaka na kumleta nyumbani lakini mimi nimetaka kuwageuka na kumkabidhi kwa magaidi.Nimerud……………. ” akastuka baada ya simu yake kuita akahisi mikono inamtetemeka akaitazama simu ile ikiita akaogopa kuipokea.Simu ikakatika na kuanza kuita tena akaamua kuipokea “Hallo” akasema “Mheshimiwa Rais nusu saa tuliyokuongezea imemalizika nataka kufahamu kama tayari unaye Edger Kaka” ikasema sauti ya upande wa pili “Kitendo mlichokifanya cha kumuua mmoja wa wanafunzi mliowateka kimeleta matatizo makubwa sana.Maandamano makubwa yanafanyika hivi sasa watu wanaandamana kuja ikulu na hadi viongozi wa serikali wamejiunga na maandamano hayo makubwa.Mmesababisha mtikisiko mkubwa sana k……” Dr Evans akakatishwa “Mheshimiwa Rais yote haya umeyataka wewe mwenyewe kama ungetupa kile tunachokihitaji kwa amani tusingefika hapa tulipofika.Sasa nataka kufahamu tayari umekwisha muandaa Edger Kaka? “Kumuandaa Edger Kaka si kitu chepesi inahitaji taratibu zifanyike kumtoa mahala alipo.Nimewatuma wasaidizi wangu huko na wanaendelea kulishughulikia.Tafadhali nahitaji muda zaidi niweze kuwakamilisha kile mnachokitaka” “Mheshimiwa Rais bado unaonekana hujali na una moyo mgumu kama Farao.Kutokana na kuendelea kutudharau hakutakuwa na majadiliano tena na kila baada ya nusu saa tutaua watoto wawili hadi pale utakapokuwa umekamilisha hitaji letu.Itakapofika saa nane na haujatupatia mzigo wetu tutaongeza idadi ya watoto na kuwa watano ambao watachinjwa kila baada ya nusu saa.Ikifika saa kumi na mbili za jioni bado hujatupatia mzigo wetu tutaongeza tena idadi tunataka hadi itakapofika saa sita za usiku wa leo tuwe tumewamaliza wasichana wote.Nitawasiliana nawe tena baada ya nusu saa” “Tafadhali msiue tena watoto nitawapatia kile mn……….”akasema Dr Evans lakini tayari simu ilikwisha katwa. “Sijawahi kukutana na mtihani mkubwa kama huu katika maisha yangu.Hawa makatili wanakwenda kumuua mtoto mwingine” akawaza na kuchukua simu akampigia mkuu wa jeshi la polisi akazungumza naye lakini hakukuwa na taarifa zozote zenye kuleta matumaini ya kuwapata watekaji.Dr Evans akazidi kuchanganyikiwa.
Austin na Gosu Gosu walirejea wakiwa na Ruby na mke wa balozi ambaye alikuwa amefungwa kitambaa usoni wakaingizwa ndani. “Samahani sana Ruby kwa usumbufu huu” akasema Mathew huu akimsaidia Ruby kuketi sofani “It’s okay Mathew.What’s going on? Wametuchukua bila kutueleza nini kinaen…..” akasema Ruby mara akatokea Devotha wote wakabaki kimya wakitazamana kwa jicho la chuki. “Look ladies” akasema Mathew na kuwatazama kwa zamu “Najua nyote hamtazamani usoni kutokana na kile kilichotokea lakini kwa wakati huu tuko katika dharura kubwa sana tunahitaji ushirikiano mkubwa ili kuweza kufanikisha misheni yetu hivyo basi ninawaomba ninyi wawili ambao wote ni muhimu sana katika misheni hii muweke kando tofauti zenu na mfanye kazi kwa pamoja.I know it’s hard but do it for the country.Do it for the girls we’re trying to rescue.Are we clear ?! akauliza Mathew “Yes we’re clear ! akajibu Devotha Ruby akabaki kimya “Ruby are we clear ?! akauliza Mathew “Yes we’re clear” akajibu Ruby “Good.Kwa ufupi sana Ruby nataka nikupe taarifa ya kile kilichotokea.Ni kwamba Rais ametugeuka na amekusudia kumkabidhi Edger Kaka kwa magaidi kwa lengo la kuwakomboa mateka wanaowashikilia.Hiyo ndiyo sababu tuko hapa.Hatuko tayari Edger Kaka akabidhiwe kwa magaidi” akasema Mathew “Is he crazy? How could he do that? Akauliza Ruby.Austin na Gosu Gosu nao wakaingia pale sebuleni. “Ahsanteni sana Austin na Gosu Gosu kwa kufanikiwa kuwaleta Ruby na mke wa balozi.Naamini mmechukua kila kifaa muhimu tunachokihitaji” akasema Mathew “Tumekuja na kila kitu muhimu” akasema Ruby na kuomba apewe kompyuta yake. “Nilifanya mahojiano tena na Edger Kaka na safari hii amekubali kutoa ushirikiano lakini ametoa masharti ambayo ni kupatiwa hati mpya ya kusafiria,kutafutiwa nyumba Uswisi,Kutafutiwa gari la kifahari na mtaji wa kuwekeza katika kilimo.Kama mnavyoona mambo haya anayoyataka Edger ni makubwa sana na yanahitaji fedha nyingi.Kama tungeendelea kuwa na ukaribu na Rais ingekuwa rahisi kwetu kuweza kuyatimiza hayo lakini kwa sasa hii ni misheni yetu wenyewe bila kumshirikisha Rais hivyo inatulazimu kutafuta namna ya kumfanya Edger aweze kufunguka.Nimefikiria kufanya jambo hili.Nitampigia simu mke wangu aliyeko Paris Ufaransa.Ni bilionea na anafahamiana na wafanya biashara wengi wakubwa duniani kote.Nataka anunue nyumba nchini Uswisi kwa jina la Nickson Robert ambalo amelichagua Edger ili kumpa moyo kwamba maombi yake yanafanyiwa kazi.Ni gharama kubwa sana lakini hakuna namna we have to do everything we can to save the girls” akasema Mathew “Kwa upande wangu sina tatizo na hilo kwani tunachohitaji ni taarifa zitakazotusaidia kufahamu mahala wasichana walipo na kuufahamu mtandao wa IS hapa nchini” akasema Gosu Gosu. “Kuna yeyote mwenye wazo mbadala?akauliza Mathew na wote wakabaki kimya “Inaonekana wote tumekubaliana na hiki ninachotaka kukifanya.Ruby nahitaji kompyuta yako nizugumze na mke wangu” akasema Mathew na kuchukua kompyuta ya Ruby akaingia mtandaoni na kumtafuta mke wake akampigia simu ikapokelewa “Hello sweetheart I had a very bad dream about you.Are you okay my love?akauliza Peniela mke wa Mathew “C’mon my Peny I’m more than fine.watoto wanaendeleaje?Miss you guys so much” akasema Mathew “We miss you too darling.When are you coming home?akauliza “Soon.Very soon” akajibu Mathew “Ouh Mathew It’s hard without you.I love you more than I can say.Please come very soon.Missed your kisses,the way you hold me in your strong arms,they way you take me to the moon,the way you…ouh gosh ! akasema Peniela na kunyamaza “Just say it” akasema Mathew huku akitabasamu “Forget it.How you doing out there?akauliza Peniela na Mathew akageuza shingo kamtazama Ruby “Uko na nani?Unaangalia nini huko pembeni? Akauliza Peniela “Niko mwenyewe usihofu darling” “Mathew please don’t you ever try cheat on me.Nikigundua uko na mwanamke mwingine huko Tanzania I swear I’ll kill myself.Mathew you are mine and mine alone” “Usihofu darling you know me I can’t do that.You are my one and only angel” akasema Mathew na uso wa Peniela ukatakata kwa tabasamu kubwa “Darling nimekupigia ninahitaji unisaidie kitu kimoja” “Unataka nini Mathew? “Nataka kununua nyumba Uswisi.It’s very urgent” “Uswisi?! Peniela akashangaa “Ndiyo.Nataka nyumba Uswisi.A luxury one” “Luxury house?What for?akauliza Peniela “I’ll explain later darling just find me a house.Nitafutie nyumba tatu nzuri za kifahari zinazouzwa unitumie nichague moja itakayonifaa” akasema Mathew “Mathew what’s going on? Are you buying this for someone?A woman? “C’mon Peniela just do as I say.I’ll explain to you later” akasema Mathew “Sawa Mathew.Let me make some calls.Nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Peniela na kukata simu “Ruby kwa nini usiende kupumzika pale tutakapokuhitaji tutakujulisha.Let me take you to the room” akasema Mathew na kumshika mkono Ruby wakaelekea chumbani “She don’t know what you are doing out here” akasema Ruby wakati wanaelekea chumbani “Tayari ameukana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine kitu ambacho mimi siwezi kukifanya ndiyo maana muda mwingi ninakuwa hapa Tanzania.I was born here and I will die here.I love this beautiful country.I’m a man and I have needs and she knows that.Do you understand me?akauliza Mathew “I understand you Mathew but you must be very carefull.Akifahamu…...” “I’m not a saint.I need love,Ineed someone when she’s not here but she’s still my wife and I love her so much” “I’m here Mathew to give you love,to take her place when she’s not around.Niko tayari kuishi Tanzania au sehemu yoyote ile ulipo” akasema Ruby “Thank you Ruby.Pumzika kwa sasa” akasema Mathew na kumbusu Ruby shavuni akatoka akarejea sebuleni. “What happened out there?akauliza Mathew “Haikuwa rahisi kuwachukua lakini imetulazimu kutumia nguvu”akasema Austin “You didn’t kill those guys,right?akauliza Mathew “No we didn’t” “Mathew kuna kitu kinaendelea huko nje ambacho si cha kawaida” akasema Gosu Gosu “Nini kinaendelea?akauliza Mathew “Kuna maandamano makubwa ya wananchi yanafanyika kuelekea ikulu kumshinikiza Rais atumie nguvu katika kupambana na magaidi ili kuwakomboa watoto waliotekwa wasiendelee kuuawa” akasema Gosu Gosu “Wanaelekea ikulu?Mathew akashangaa “Ni maandamano makubwa sana ya watu barabara nyingi zimefungwa na kikubwa zaidi waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndiye anayeongoza maandamano hayo” “Waziri mkuu?! “Ndiyo.Ni tukio la kushangaza sana.Inadaiwa kwamba mwanae ni mmoja wa mabinti waliotekwa na magaidi ndiyo maana ameamua kuungana na wananchi kuandamana kuelekea ikulu kuishinikiza serikali kutumia nguvu kubwa kuwakomboa watoto” akasema Gosu Gosu “It doesn’t make sense to me.Waziri mkuu ni mtu mkubwa serikalini na hata kama mwanae ametekwa nyara alipaswa kushirikiana na viongozi wenzake serikalin….” Mathew akakatisha mazungumzo baada ya simu katika kompyuta kuita “It’s her.Peniela” akasema na kuipokea “Mathew nimefanya mawasiliano ya haraka kuna nyumba tatu nimepata ambazo ninakutumia picha na maelezo yake sasa hivi ili uchague ipi unaitaka” “Thank you Peny.Nitumie sasa hivi” akasema Mathew na simu ikakatwa “Tayari amepata nyumba” akasema huku akifungua akaunti yake ya barua pepe akakuta picha za nyumba ambazo ametumiwa na Peniela. “Twendeni kwa Edger akachague nyumba ipi anaitaka” akasema Mathew na kuchukua kompyuta ile wakaenda katika chumba alimo Edger Kaka. “Hallow Edger I’m back.Nataka kukuthibitishia kwamba tunaamisha kile tunachokisema.Nimekuletea nyumba tatu uchague moja utakayoipenda” akasema Mathew na kumsogezea Edger kompyuta akaanza kumuonyesha zile nyumba.Zilikuwa ni nyumba za kifahari haswa. “Is this real or is your game ?akauliza Edger “Edger hatufanyi mchezo hapa.Kila kitu ni halisi.Chagua nyumba unayoipenda na itanunuliwa hapa hapa ukishuhudia.Chagua nyumba” akasema Mathew na Edger akachagua nyumba anayoitaka.Mathew akampigia simu Peniela na kumpa maelekezo ya kuinunua nyumba ile.Baada ya dakika kumi Peniela akampigia simu na kumjulisha kwamba tayari malipo yamekwisha fanyika na nyumba ile imekwisha nunuliwa.Mathew akapiga simu katika kampuni ile ambayo waliuza nyumba na kuthibitishiwa kwamba nyumba ile imenunuliwa na Nickson Robert mfanyabiashara kutoka Tanzania. “Done.Umehakikisha wewe mwenyewe.Mambo yameanza kushughulikiwa nyumba tayari umepata mengine yanafuata.It’s your turn.Give me information” akasema Mathew na Edger akatazama chini halafu akainua kichwa na kusema “I don’t know his name” “You don’t know what? Akauliza Gosu Gosu kwa ukali huku akimsogelea Edger “Gosu Gosu please” akasema Mathew “Nimesema sifahamu jina lake.Ni mtu mmoja ana asili ya kiarabu lakini anazungumza Kiswahili safi na anaishi hapa Dar es salaam ila sifahamu wapi” “C’mon Edger we’re using billions of money that’s not the information I want! Akafoka Mathew “I real don’t know his name lakini huyo ndiye ambaye hunipa maelekezo na taarifa mbali mbali.Ufisadi wote niliokuwa naufichua taarifa na nyaraka zote nilipata kutoka kwa huyo jamaa ambaye sikupaswa kumuuliza jina lake wala kufahamu taarifa zake” “Mlikuwa mnawasilianaje? Akauliza Austin “Nilikuwa napokea ujumbe katika simu yangu unaosema LUNCH.Kila nilipopokea ujumbe ule nilijua maana yake na nilikwenda Masjid Hidaya kuonana na huyo jamaa ambaye husali hapo kila siku.Baada ya swala hunipa kama ana ujumbe wowote” akasema Edger “Unaweza ukazikumbuka namba zake za simu alizokuwa anazitumia kuwasiliana nawe?Mathew akauliza “Hapana sizikumbuki” akasema Edger “Remember the number dammit ! akafoka Gosu Gosu na kurusha kofi zito Mathew akamdaka mkono “Easy gentlemen” akasema Mathew na kutuliza jazba iliyoanza kupanda mle ndani “Edger I’m going to ask you one more question” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Huyu mtu ambaye humfahamu jina lake unaweza ukanieleza muonekano wake?akauliza Mathew “Ndiyo” akajibu Edger na Mathew akaomba aletewe kalamu ya risasi na karatasi.Edger akaanza kumuelezea mwonekano wa Yule jamaa huku Mathew akifuata maelezo yale kuchora picha.Alipomaliza kuchora akamuonyesha Edger “Wow ! This is amazing.Haya ni maajabu.Nilikuwa nasikia kwamba wapo watu wana uwezo wa kumchora mtu kwa kufuata maelezo nilidhani ni uongo kumbe ni kitu cha kweli kabisa.Huyo mtu yuko hivyo hivyo ulivyomchora” akasema Edger “Thank you Edger pumzika tutakuja kuzungumza tena baadae” akasema Mathew wakatoka mle ndani “Mathew huyu jamaa anacheza na akili zetu.Nyumba ile ina thamani zaidi ya milioni mia moja na hailingani kabisa na taarifa hii aliyotupa !! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu asili yako wewe ni mpiganaji hivyo unapaswa kujifunza mambo haya ya kipelelezi.Katika kazi hii taarifa ndogo sana inaweza ikanunuliwa kwa gharama kubwa na ikawa na msaada mkubwa mno ndiyo maana hainiumizi kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa taarifa ile aliyotupa Edger.Kwa sasa tunatakiwa kwanza kumfahamu mtu huyu ni nani.Muite Ruby” akasema Mathew na Ruby akaitwa “Ruby tunataka kumfahamu mtu huyu ni nani.Huyu ndiye ambaye alikuwa anawasiliana na Edger Kaka” akasema Mathew na kumpatia Ruby ile karatasi.Ruby akaichukua ile picha akaiingiza katika kompyuta yake na kuanza kumtafuta mtu Yule ni nani.Picha zilipita haraka haraka katika kompyuta na mara program ikasimama. “Hakuna picha inayofanana na hii” akasema Ruby. “That can’t be.Search again” akasema Mathew na kuchukua ile picha akaenda kwa Edger “Edger huu si mchezo wa kuigiza.Nataka uniambie picha hii inafanana kweli na mtu ambaye ulikuwa unawasiliana naye? “Ndiyo.Ni yeye mwenyewe” “Tumejaribu kumtafuta hakuna picha inayofanana na hii” “Mathew nilichokwambia ni kitu cha kweli kabisa.Find that man.” akasema Edger Mathew akatoka na kuwafuata wenzake “Mmepata chochote? “Hakuna picha inayofanana na hiyo” akasema Ruby “Keep on searching.Mimi na Austin tunakwenda Masjid Hidaya ambako Edger anadai ndiko amekuwa akikutana na huyo jamaa.Gosu Gosu na Devotha mtabaki hapa mkilinda usalama.Tunaye mtu muhimu mno hapa ndani hivyo unahitajika ulinzi wa kutosha” akasema Mathew na kumuita pembeni Gosu Gosu “I don’t trust Devotha keep an eye on her.Usimpe nafasi asije akafanya kama alivyomfanyia Ruby” akasema Mathew hawakupoteza muda wakaingia garini na kuondoka. “Mathew inawezekanaje Edger asilifahamu jina la mtu ambaye wamekuwa wakiwasiliana naye? Una hakika anasema kweli? Akauliza Austin “I believe him.Edger alikuwa anatumika kwa ajili ya misheni maalum ndiyo maana hawakutaka afahamu jina la Yule aliyekuwa anawasiliana naye.Tutamfahamu tu usijali” akasema Mathew. Kulikuwa na heka heka nyingi mitaani.Barabara zilijaa magari kufuatia baadhi ya barabara kufungwa kutokana na maandamano ya wananchi kushinikiza serikali iwakomboe wasichana waliotekwa “Kuna kitu mliniambia kilinishangaza kidogo.Waziri mkuu kuamua kuungana na wananchi kuandamana hiki ni kitu cha ajabu sijawahi kukishuhudia.Waziri mkuu ni mtu mkubwa hata kama mwanae ni mmoja wa waliotekwa hauapswa kufanya alivyofanya alipaswa kushirikiana na viongozi wenzake serikalini kuhakikisha watoto wanapatikana” akasema Mathew “Ni kweli inashangaza sana” akajibu Austin ambaye tayari alikwisha vua sare za kijeshi na kuvaa mavazi ya kawaida Austin na Mathew walifika Mikunguzi na kuitafuta Masjid Hidaya.Ulikuwa ni msikiti mzuri sana na magari kadhaa yaliegeshwa nje.Pale nje walinunua kofia na kuvaa “Sijawahi kuingia msikitini” akasema Austin “Nimeishi nchi za kiarabu nifuate ninavyofanya tukifanikiwa kuingia ndani tujitahidi kuangaza kila kona kumtafuta huyu jamaa” akasema Mathew na kuelekea sehemu ya kufanya maandalizi kabla ya kuingia katika swala.Austin akamfuatisha Mathew anavyofanya kisha wakaingia ndani ambako tayari swala ilikuwa inaendelea.Macho ya Mathew na Austin hayakutulia sehemu moja yalizunguka kama kinyonga kumtafuta Yule jamaa bila mafanikio.Wengi wa waliokuwamo ndani ya msikiti walikuwa ni watu wenye asili ya arabuni Swala ilimalizika na watu wakaanza kutoka.Mathew ambaye alikaa karibu na mlango alizungusha macho kuangaza lakini hakumuona mtu Yule na mwisho Austin naye akatoka “Nothing.Hayupo huyu mtu.Sina hakika kama Edger ametuambia kitu cha kweli” akasema Austin “Wait for me here” akasema Mathew na kumfuata Imamu wa msikiti “As salamu alaykum” Mathew akamsalimu “Wa Alaikum Salaam” akajibu Imam “U mgeni hapa,umetokea wapi?akauliza Imamu “Ni kweli mimi ni mgeni nina shida nawe Imamu” akasema Mathew na Imamu akamchukua hadi pembeni kidogo ya msikiti “Nikusaidie nini ndugu yangu?akauliza Imamu Yule mwenye ndevu nyingi.Mathew akatoa karatasi mfukoni na kuikunjua “Unamfahamu huyu mtu?Umewahi kumuona hapa msikitini? Imamu Yule akaitazama picha ile na kusema “Hapana simfahamu” “Imamu tazama vizuri hiyo picha.Mtu huyu husali hapa masjid Hidaya unamfahamu? “Hapana simfahamu.Ninashindwa kumtambua katika picha ya kuchora.Huna picha yake halisi? “Imamu jaribu kutazama vizuri hii picha unaweza kuwa unamfahamu mtu huyu” akasema Mathew na Yule imamu akaitazama picha kwa mara nyingine “Sina kumbu kumbu kama nimewahi kumuona mtu mwenye sura hii hapa katika mskikiti huu.Tunaosali hapa si watu wengi na tunafahamiana ndiyo maana ilikuwa rahisi mimi kukutambua wewe kuwa ni mgeni hapa” akasema Imamu na kumtazama Mathew kish akauliza “Wewe ni askari? “Hapana mimi si askari” “Kwa nini basi unamtafuta huyu mtu kama si askari? “Huyu ni mtu muhimu kwangu.Nisaidie tafadhali kujua mahala alipo” akasema Mathew lakini Yule imamu akamrejeshea picha yake “Picha yako hii huyu mtu simfahamu na sijawahikumuona hapa.Jaribu labda misikiti mingine” akasema Imamu na kuanza kuondoka Mathew akamfuata “Mzee naomba unisikilize.Mimi natoka katika idara ya kupambana na ugaidi”akasema Mathew na imamu yule akastuka “Nilihisi kitu kama hicho.Kwa nini kila mnapofanya misako yenu ya kuwatafuta magaidi huwa mnakimbilia katika nyumba zetu za ibada kana kwamba sisi ndio huwaficha watu hao?akauliza Imamu akionekana kukereka Mathew hakumjali “Huyu mtu ambaye ninataka unisaidie kumtambua ana mahusiano na kikundi cha magaidi ambao wamefanya shambulio la bomu katika hospitali ya Mtodora na kuua watu wasio na hatia na kama haitoshi wamewateka tena wanafunzi na wameanza kuwaua kikatili kwa kuwachinja kama kuku” “Kwa kweli kitendo kile nimekiona na kimeniumiza sana.Hata sisi mchana huu tumefanya dua maalum ili watu hao wanyama waweze kupatikana” akasema Imamu “Huyu tunayemtafuta ana mahusiano na watu hao.Tafadhali tusaidie tuweze kumtambua” akasema Mathew na Imamu Yule akaiomba tena ile picha akaitazama vizuri. “Imamu huyu mtu amekuwa akisali katika msikiti huu na kama ulivyosema kwamba watu wote wanaosali katika huu msikiti mnafahamiana lazima utakuwa unamfahamu.Huyu ni mtu hatari sana na kama hautatusaidia kumfahamau utatufanya tuamini kwamba mnawahifadhi magaidi katika msikiti huu..” “Hapo unakosea ndugu yangu.Uislamu ni dini safi na isihusishwe na ugaidi.Kamwe uislamu haujawahi kushabikia ugaidi.Hii ni dini inayohubiri amani ndiyo maana salamu yetu inasema As salamu alaykum maana yake amani iwe kwako.Muislamu yeyote analazimika kusambaza na kutangaza amani kwa muislamu mwenzake na asiye muislamu hivyo basi itendo chochote cha kumnyima mtu yeyote amani hakikubaliki ndani ya uislamu.Magaidi ni watu wanaotumia nguvu kulazimisha matakwa yao yafanikiwe aidha kiimani au kisiasa.Mwenyezi Mungu Subhaanahuu wataala kupitia Quran tukufu Surah An-Nisa 4 aya ya 93 anakemea mauaji “walakun klu min yaqtul mwmnaan ean eamad – falmukafa’at hi aljahim,hayth Yuthbit ‘iilaa al’abad,waqad ghadib allah ealayh washatamah wa’aeada lah eqabaan Kbyraan…..Tafsiri ya Kiswahili inasema “Lakini yeyote anayemuua mwamini kwa makusudi malipo yake ni Jahannamu ambako atakaa milele na Mwenyezi Mungu amekasirika naye na amemlaani na amemtayarishia adhabu kubwa” akasema Imamu na kumtazama Mathew Aya hiyo na nyingine kadhaa zinatufundisha ubaya wa kuua nafsi iso na hatia na hata kujiua mwenyewe.Kuna somo refu hapa ambalo linafundisha namna uislamu usivyofungamana na ugaidi lakini muda wangu hauruhusu ila nimekupa hayo machache kukuthibitishia kwamba uislamu haukumbatii ugaidi.Katika matendo hayo ya kigaidi wanaoathirika pia wamo waislamu.Katika wasichana waliotekwa wamo pia waislamu hivyo basi itoshe tu kusema kwamba Uislamu si dini ya kigaidi kama inavyoendelea kujengeka kwa wengi” “Nimekuelewa Imam hata mimi nimewahi kuishi katika nchi za kiarabu ninaifahamu dini ya kiislamu vizuri na hata kiarabu ninakizungumza vyema.Turejee katika suala letu.Huyu mtu ni muhimu sana naomba tafadhali unisaidie kupata taarifa zake” akasema Mathew. “Nasema ukweli na Mwenyezi Mungu Subhaanahuu wataala ananisikia,huyu mtu mimi simfahamu kwa sababu nina miezi minne tu toka nimehamia katika msikiti huu.Yupo imamu wa zamani kwa sasa anasumbuliwana maradhi labda tukifanikiwa kumpata huyo anaweza akawa anamfahamu” “Unafahamu mahala anapoishi huyo imamu wa zamani?akauliza Mathew “Ndiyo ninapafahamu.Si mbali sana na hapa” akasema Imamu na bila kupoteza muda wakaingia katika gari na kuondoka kuelekea kwa imamu wa zamani wa Masjid Hidaya. “Nimestuka sana kusikia kwamba katika msikiti wangu anasali mtu ambaye anajihusiana na vitendo vya kigaidi.Mambo haya tumekuwa tunayapinga kwa nguvu kubwa”akasema Imamu “Magaidi hawana alama ni watu tunaoishi nao katika jamii na kushiriki nao mambo mbalimabli hata ibada”akasema Austin Walifika katika nyumba ya imamu wa zamani ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu,wakamkuta amekaa nje akipunga upepo wakamsalimu na bila kupoteza muda wakamueleza kile kilichowapeleka pale.Imamu Sadiq akaitazama ile picha kwa makini sana na kusema “Ni kweli huyu mtu alikuwa anasali katika msikiti wetu na alipenda sana kuhudhuria Swalat Dhuhri.Hakuwa mtu wa kuchangama sana na wenzake aliondoka baada ya swala kumalizika.Mara chache alikuja kunisalimu na alikuwa mchangiaji mzuri sana kila pale kulipohitajika michango mbalimbali.Nimestuka kusikia kwamba anahusishwa na matendo ya kigaidi yanayoendelea kutokea hapa nchini” akasema Imamu Sadiq “Mzee tunahitaji utusaidie namna ya kumpata huyu mtu.Unafahamu mahala anapoishi?akauliza Mathew “Huyu mtu simfahamu vyema zaidi ya kumuona msikitini,sifahamu anaishi wapi wala kazi yake..”akasema Imam Sadiq na kunyamaza “Lakini kuna kitu nimekikumbuka.Kuna wakati aliwahi kumtuma mwanamama mmoja anaitwa Zulfa aniletee mchango wake wa ujenzi wa choo cha madrasa.Naamini huyo Zulfa anaweza akawa anamfahamu vyema huyu jamaa” akasema Imam Sadiq. “Zulfa yupi mzee?akauliza Imam Shafii. “Zulfa mtoto wa Ustaadh Shabani ana duka lake la kuuza vitambaa mtaa wa Mkongoro” akasema Imam Sadiq na kuwaelekeza akina Mathew lilipo duka la Zulfa wakamuaga mzee Yule na Mathew akamuachia shilingi lakini tatu kwa ajili ya kumsaidia katika matibabu wakaondoka.
“Mathew alikuita nje akaenda kukueleza nini?Devotha akamuuliza Gosu Gosu wakiwa sebuleni wakipumzika baada ya akina Mathew kuondoka “Kwa nini unataka kujua?akauliza Gosu Gosu “Alikwambia unichunge.Bado haniamini hata kidogo” akasema Devotha huku akitabasamu “Hapana hakusema hivyo kuna maelekezo mengine alinipa” “Gosu Gosu yawezekana bado hunifahamu vyema.Mimi ninao uwezo mkubwa sana wa kusikia kuliko kawaida.Ninao uwezo wa kusikia hata sisimizi akipita mbele yangu” “That’s impossible ! akasema Gosu Gosu “It’s true.Huifahamu historia yangu ndiyo maana unadhani haiwezekani.Kwa ufupi tu ni kwamba niliwahi kulipukiwa na bomu nikiwa bado msichana mdogo nikapelekwa Marekani kwa matibabu nimefanyiwa operesheni nyingi kuutengeneza mwili wangu huu unaoniona leo na katika operesheni hizo ndipo nilipooongezewa uwezo wa kusikia.Sifahamu walifanyaje lakini uwezo wangu ni mkubwa mno na niliwasikia mkinong’onezana na Mathew akikutaka unichunge nisije nikageuka na kufanya kama nilivyofanya kwa Ruby” akasema Devotha na Gosu Gosu akabaki kimya “Nakubali nilifanya kosa na inaniumiza mno.Nilikuwa katika harakati za kuutafuta ukweli huu ambao tunautafuta sasa.Naomba mniamini mimi si msaliti na siwezi tena kufanya hivyo” akasema Devotha “I trust you Devotha” “Kitu gani kinakufanya uniamini? “Macho yako yananifanya nikuamini” akasema Gosu Gosu na Devotha akatoa kicheko. “Nina jicho moja tu hili lingine ni bandia” “I don’t care but I do trust you” akasema Gosu Gosu “Papii nakiri sijawahi kukutana na katili kama wewe.Nilishuhudia namna ulivyowakata kata watu kule Nairobi lakini unapokuwa nami ukatili ule unapotea,unaongea vizuri,unasimama kunitetea,kwa nini? “Imenitokea hivyo.Ninapokuwa karibu nawe nahisi tofaut…..” “Wait ! akasema Devotha na kuongeza sauti ya runinga http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Ndugu watazamaji wetu sasa tunawaunganisha na waandishi wetu walioko katika maandamano makubwa ya wananchi yanaoelekea ikulu hivi sasa” akasema mtangazaji na kujiunga na waandishi wao walikuwa wakifuatilia maandamano yale makubwa yaliyoongozwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. “Hii haijawahi kutokea.Waziri mkuu aliyeko madarakani kuungana na wananchi kuandamana kuishinikiza serikali ambayo na yeye ni sehemu yake ! akasema Devotha “Inasemekana yeye pia mwanae ni mmoja wa wasichana waliotekwa ndiyo maana ameungana na wananchi kuishinikiza serikali kufanya juhudi za kuwakomboa watoto”akasema Gosu Gosu “Vipi kuhusu nafasi yake ya uwaziri mkuu?Ataendelea nayo baada ya hiki alichokifa………..”Devotha akanyamaza baada ya kutokea vikosi vya askari polisi wa kutulia ghasia wakiwa wamejihami kwa silaha na vifaa tayari kuyazuia maandamano yale yasiendelee kuelekea ikulu.Waziri mkuu aliyekuwa kiongozi wa maandamano yale akasimamana watu wote wakasimama.Amri ikatolewa na mkuu wa kikosi kile cha kutuliza ghasia kwamba maandamano yale si halali na kuwataka wananchi watawanyike ama sivyo jeshi litalazimika kutumia nguvu Waziri mkuu aliyekuwa kiongozi akaomba kipaza sauti na kupewa “Jeshi la polisi,ninayezungumza hapa ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na maandamano haya ni ya amani ndiyo maana nimeungana na wananchi kuwaonyesha kwamba tuko pamoja nao.Naomba mturuhusu tafadhali tuweze kuendelea na maandamano yetu hadi ikulu,wananchi hawa wanaandamana kwa amani bila vurugu zozote” akasema Waziri mkuu na kushangiliwa na watu “Mheshimiwa waziri mkuu,umeongoza wananchi kuvunja sheria ya kuandamana bila kibali naomba uwatake wananchi watawanyike tafadhali ama sivyo jeshi la polisi litatumia nguvu” “Kamanda nakuhakikishia kwamba kama mwananchi yeyote atapigwa kuuawa au kuumizwa wewe na kikosi chako chote mkatafute kazi nyingine za kufanya” akasema waziri mkuu “Mheshimiwa waziri mkuu hakuna aliye juu ya sheria na sisi tuko hapa kwa mujibu wa sheria.Tafadhali nawaomba wananchi mtawanyike haraka sana maandamano haya hayana kibali hivyo si halali.Mkikaidi tutatumia nguvu” akasema mkuu wa kikosi kile lakini bado watu waliendelea kushikana mikono kuonyesha mshikamano huku wakiimba kwa nguvu wakitaka serikali iwakomboe watoto wao. Jeshi la polisi walifuata taratibu za kuwataka watu watawanyike na walipokaidi wakaanza kuwatawanya kwa gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.Mvurugano mkubwa ukatokea.Devotha akasimama na kusogelea runinga zaidi kuna kitu alikiona katika runinga kikamstua “Papii we need to get this video.Kuna kitu nimekiona kimenisua sana” “Umeona nini katika mvurugano huu mkubwa? “Muite Ruby” akasema Devotha na Gosu Gosu akamuita Ruby lakini Ruby akagoma akadai hajisikii vyema “Kuna kitu nimekiona hapa muhimu sana kukifuatilia.” akasema Devotha “Umeona nini? “Siwezi kukwambia kwa sasa lakini lazima tuipate video ile.Tuwasubiri akina Mathew warejee kwani ni yeye pekee anayeweza kumpa kazi Ruby akaifanya” akasema Devotha
Akina Mathew walifika mtaa wa Mkongoro wakalitafuta duka waliloelekezwa na Imam Sadiq wakalipata.Wakashuka garini na kuingia ndani mara tu walipoingia Imam Shafii akasalimiwa na sauti ya mwanamke “As salamu alaykum” Imam Shafii akageuka na kutazamana na mwanamke aliyevaa gauni refu jeusi “Wa Alaikum Salaam.Wajionaje hali” akajibu Imam “Mimi mzima sana.Karibu sana Imam Shafii leo umekuja dukani kwetu kumchukulia bi Khadija kitambaa?akauliza Yule mwanamke Imam shafii akatoa kicheko kidogo.Hakuna anamfahamu lakini Yule mwanamke alikuwa anamfahamu “Ni kweli nimekuja kumtafutia bi Khadija kitambaa kizuri lakini vile vile nimekuja kuonana na bi Zulfa.Natumai ndiye wewe” akasema Imam Shafii “Hapana mimi ni mdogo wake naitwa Zaituni” “Ouh Zaituni.Mmefanana sana.Huyu mama Zulfa yeye yuko wapi?akauliza Imam Shafii “Ametoka amekwenda katika mizunguko yake nimwambiaje akifika”akauliza Zaituni “Naomba unipatie namba yake nitazungumza naye kuna mchango wa kuwapeleka watoto wetu wa madrasa ziara jijini Arusha na tunataka watembelee pia mbuga za wanyama ndiyo maana ninazunguka kutafuta michango kwa wafadhili mbali mbali.Nimeambiwa dada yako ni mchangiaji mzuri sana wa maendeleo ya msikiti wetu” akasema Imam Shafii na kuchukua namba za simu za Zulfa kisha akachagua kitambaa kimoja kikubwa na kuwaonyesha akina Mathew “Unaonaje hiki si kitampendeza bi Khadija:?akauliza na Mathew akatoa fedha akakilipia kile kitambaa wakaondoka “Mambo haya magumu nusura ningeharibu kwani mtu mwenyewe tunayemtafuta simfahamu lakini wao wananifahamu” akasema Imam Shafii “Usijali ulifanya vizuri hujakosea” “Nini kinandelea baada ya hapa?akauliza Shafii. “Imam Shafii sisi tunakushukuru sana kwa ushirikiano mkubwa uliotupa.Kwa sasa kazi yako imemalizika na kama tukihitaji tena msaada tutakuja kukuona.Tutakuacha hapo mbele utachukua taksi kwani hatutaweza kukurejesha nyumbani” akasema Mathew “Jamani hata mimi nawashukuruni sana kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kupambana kuwakomboa watoto wetu.Naombeni msikate tamaa na muda wowote mkihitaji kitu chochote kutoka kwangu nitafuteni nitawasaidia.Kabla sijashuka nataka niwaombee dua Mwenyezi Mungu awatangulie katika kazi hii na mfanikiwe kuwakomboa wote waliotekwa na kuwatia nguvuni magaidi hawa” akasema Imamu Shafii na kuwaombea dua halafu Mathew akampatia shilling laki mbili kama ahsante kwa ushirikiano aliowapa wakamuacha katika kituo cha taksi wakaendelea na safari. Baada ya kumshusha Imam Shafii,Mathew akampigia simu Ruby kwa kutumia simu mpya walizonunua na kumtaka aifuatilie namba atakayoipigia kufahamu mahala mtu anayempigia alipo.Ruby akaweka sawa program zake na kumjulisha Mathew kila kitu tayari na Mathew akaipiga ile namba ya Zulfa simu ikaanza kuita “Hallow”ikasema sauti laini ya mwanamke “As salamu alaykum bi Zulfa” akasema Mathew “Wa Alaikum Salaam.Nani mwenzangu? Akauliza Zulfa “Naitwa Hassan ninasali Masjid Hidaya.Nilikuwa na Imam Shafii ndiye aliyenipa namba zako nikupigie nikujulishe kwamba kuna mchango unafanyika ili kuwapeleka watoto wetu wa madrasa waende ziara jijini Arusha na kuzungukia vivutio mbali mbali vya kitalii.Mchango huu ni wa hiyari na unatoa kile ulichonacho.Kwa kuwa wewe umekuwa mchangiaji mkubwa wa miradi mingi tumeona tukujulishe na kama hali itaruhusu badi unaweza ukatuchangia chochote.” “Nashukuru sana kwa taarifa hiyo.Hilo ni jambo jema sana Inshallah tukijaaliwa nitachangia” “ahsante sana bi Zulfa unaweza ukatuelekeza mahala ulipo hivi sasa tukufuate tuchukue mchango huo? “Kwa sasa niko katika mizunguko yangu ila mwambie Imam Shafii nitamfikisha mchango wangu jioni au kesho asubuhi” “Ahsante sana nashukuru bi Zulfa.Uwe na siku njema” “Amina” akasema Zulfa na kukata simu Mathew akampigia Ruby “Umefanikiwa kupata mahala alipo? akauliza Mathew “Give me a second” akasema Ruby na baada ya dakika kama mbili akapiga “Mathew nimefanikiwa kupata mahala alipo huyo mtu uliyempigia.Ninakutumia sasa hivi katika simu yako ramani ya mahala hapo” akasema Ruby na baada ya dakika moja ujumbe ukaingia katika simu ya Mathew akaufungua ilikuwa ni ramani aliyotumiwa na Ruby ikionyesha mahala alipo Zulfa .Mathew na Austin wakaitazama ramani ile kisha Mathew akasema “Huu ni mtaa wa Saada Thabit.Huu ni mtaa maarufu kwa kuwa na maduka mengi ya vifaa vya elekroniki.Ramani inaonyesha Zulfa yuko katika moja wapo ya jengo katika mtaa huu.Tuelekee huko” akasema Mathew Austin aliyekuwa katika usukani akawasha gari wakaingia barabarani wakaendelea na safari.
“Ruby tayari umepata satellite? Tumekaribia kufika mtaa wa Saada Thabit” Mathew akamwambia Ruby “Yes I have it.Baada ya muda mfupi nitaanza kupokea picha za mahala mlipo” akasema Ruby “Thank you.Tujulishe pale utakapokuwa tayari” akasema Mathew na kukata simu. Mwendo ulikuwa wa taratibu katika mtaa huu wenye pilika pilika nyingi.Simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Ruby “Mathew tayari kila kitu kimekaa sawa nimeanza kupokea picha.Mtu wetu yupo katika jengo lililo pembeni ya jengo refu lenye rangi ya dhambarau “Ni Savanna hotel” akasema Mathew “Basi jengo la pembeni yake ndimo alimo mtu wetu uliyempigia simu” akasema Ruby “Good Job Ruby tutafika hapo baada ya muda mfupi” akasema Mathew Austin aliendesha gari taratibu hadi walipofika Savanna hotel wakaipita hoteli ile kubwa na pembeni yake kulikuwa na jengo la ghorofa moja. “Nafikiri tumefika mahala hapo” akasema Mathew na kumpigia simu Ruby “Ruby tayari tumefika mahala hapo.Tupe mrejesho mtu wetu bado yumo ndani ya jengo hili?akauliza “Ndiyo.Bado hajatoka ndani ya hilo jengo” “Good.We’re going in” akasema Mathew Wakaegesha gari mbele ya jengo lile lenye maduka matano makubwa yaliyokuwa upande wa chini na upande wa juu kulikuwa na maduka mawili na saluni kubwa ya wanawake. “Austin pitia maduka ya chini kagua mimi naelekea juu.Naamini lazima huyo Zulfa atakuwa anafanana na Yule mdogo wake tuliyemkuta kwenye lile duka la vitambaa” akasema Mathew na kupanda ngazi zilizokuwa pembeni ya jengo lile kuelekea juu huku Austin akianza kukagua maduka yaliyokuwa chini.Mathew alitembea taratibu hadi katika mlango wa chumba cha saluni ile kubwa akachungulia ndani.Kulikuwa na wanawake kadhaa. “Mathew the target is moving.She’s talking to someone on phone” Ruby akamtaarifu Mathew na mara mlango ukafunguliwa wakatoka wanawake wawili mmoja aliyevaa gauni refu la rangi nyekundu akizungumza na simu. “Thank you Ruby.Tayari nimemuona” akasema Mathew na kuanza kutembea taratibu kumfuata mwanamke Yule.Mathew akampigia simu Austin akamtaka aelekee garini kwani tayari amekwisha muona mtu waliyekuwa wanamtafuta. Mwanamke Yule alielekea moja kwa moja katika gari lake aina ya Mercedece benz rangi nyeusi akaingia na kuondoka huku akizungumza na simu.Austin akakimbia kumfuata Mathew garini wakaondoka kumfuata Yule mwanamke. “Mathew nimefuatilia simu yake anazungumza na mtu anaitwa Habib Hussein.Ninakutumia ramani ya mahala alipo huyo Habib” akasema Ruby “Sawa Ruby endelea kumfuatilia na sisi tuko gari tatu nyuma yake” akasema Mathew na baada ya dakika moja ukaingia ujumbe katika simu yake ni ramani ikionyesha mahala alipo Habib Hussein ambaye alikuwa anazungumza na Zulfa simuni Waliendelea kumfuatilia Zulfa akaiacha barabara ya Mtambikile akaingia katika mtaa wa misheni. “Where’s she going?akauliza Mathew kwa sauti ndogo akakata kona kungia katika mtaa alioingia Zulfa.Kulikuwa na watu wengi mtaa huu hivyo mwendo haukuwa mkali.Ruby akapiga simu “Mathew inawezekana huyu mtu wetu anakwenda kuonana na Habib kwani inaonyesha anaelekea uelekeo alipo Habib” akasema Ruby na Austin akaitazama ramani waliyotumiwa na Ruby ni kweli walikuwa wanaelekea mahala alipo Habib. “Ruby is right.Kuna uwezekano Zulfa anamfuata Habib” akasema Austin “Tutaendelea kumfuata hadi pale tutakapompata ili atuonyeshe mahala alipo huyu mtu ambaye alikuwa na mawasiliano na Edger” akasema Mathew. Gari za Zulfa liliwasha taa kuonyesha ishara ya kukata kona kuingia upande wa kushoto. “Gaming house ! Mathew akashangaa “Anakwenda kufanya nini hapa?akauliza “Nadhani ndipo alipo Habib” akajibu Austin. Gari la Zulfa liliingia katika jengo lenye bango kubwa linalosomeka Dar es salaam gaming house.Hapa ni mahali ambapo inachezwa michezo mbali mbali ya kubahatisha kwa kutumia mashine mbali mbali.Zulfa hakwenda katika maegesho ya kawaida wanakoegesha watu wengine akaelekea katika mlango mkubwa uliokuwa upande wa kushoto wa jumba lile na lango likajifungua akaingiza gari ndani. “Huyu anaonekana ni mzoefu sana wa mahala hapa ndiyo maana amepita moja kwa moja katika lile lango na kuingia ndani” akasema Mathgew “Tumsubiri akitoka tumfuate na tukipata nafasi nzuri tumchukue kwani hatuwezi kufanya chochote hapa kuna watu wengi” akasema Austin “Austin hatuna muda wa kusubiri.Magaidi wanaendelea kuchinja watoto hivyo lazima tuhakikishe tunawakomboa watoto haraka sana.I’m going in there nataka kuchunguza kama nitaweza kumuona Zulfa.Wewe utabaki hapa nje kwa tahadhari ukilichunguza jengo hili.Nikikupigia simu haraka sana uje ndani” akasema Mathew na kabla hajashuka garini Ruby akapiga simu “Mathew I’ve lost them.Simu zao zote zimezimwa”akasema Ruby “Kwa nini wote wazime simu kwa wakati mmoja?akauliza Mathew “Sifahamu nini kimetokea hadi wakazima wote simu kwa wakati mmoja.Mathew ……”akasema Ruby na kunyamaza “Nini Ruby?Mathew akauliza “Wameua watoto wengine wawili muda mfupi uliopita.Mathew we must hurry to find the kids,wanawaua kikatili mno” akasema Ruby “Arlight.Ninakwenda mle ndani kumtafuta Zulfa.Lazima tuhakikishe kwa namna yoyote ile tunampata ili atuelekeze kwa mtu huyo ambaye tunaamini anaweza kuwa na majibu ya mahala walipo wasichana waliotekwa.Ruby I promise you,we’ll get the kids very soon” akasema Mathew na kukata simu. “Change of plan,we’re going in together” akasema Mathew na kushuka garini wakatembea kwa tahadhari kuelekea ndani ambako watu walikuwa wanacheza michezo mbali mbali.Mathew na Austin wakaingia ndani ya jengo lile wakatawanyika kile mmoja akaenda upande wake wakaanza kuchunguza kama wangeweza kumuona Zulfa.Kulikuwa na kamera kadhaa zimefungwa mle ndani “Ninaziona kamera humu ndani lazima kuna chumba ambacho kinatumika kwa ajili ya kuangalizia kila kinachoendelea humu ndani.Hii ina maanisha kwamba kuna ofisi ziko mahala ndani ya jengo hili yawezekana huko ndiko alikoenda Zulfa” akawaza Mathew huku akiendelea kuchunguza.Wakati akiendelea kuzunguka ukaingia ujumbe katika simu yake ulitoka kwa Austin “Tukutane maliwato” Mathew hakupoteza muda akaelekea iliko maliwato akamkuta Austin akinawa mikono. “Nini umegundua?akauliza Mathew “Kuna kamera zimefungwa katika kila chumba na kuna watu wanaofuatilia kila kinachoendelea humu ndani.Wakati nikiwa ninachunguza kuna mlango mmoja karibu na block F ulifunguliwa akatoka jamaa mmoja ambaye alikuja kutazama mashine moja ambayo haikuwa ikifanya kazi vizuri akatoa maelekezo isitumike hadi itakapotengenezwa kisha akareja tena ndani.Kuna ofisi zipo katika jengo hili nahisi ndiko alikoenda Zulfa” “Nimekuelewa Austin.Kuna kitu kingine pia nimkigundua katika jengo hili kuna vifaa vya kuhisi hatari ya moto kabla haujatokea.Katika gari letu tunayo makopo yale ya kutoa moshi na kwa kawaida vifaa hivi huweza kupiga kelele pale vinapohisi moshi mwingi.Utakwenda katika gari utachukua kopo moja kisha utakuja nalo huku chooni na kulifungua.Moshi utaanza kutoka na vifaa vile vitapiga kelele na itatokea taharuki humu ndani.Mimi nitakuwa karibu na mlango ule na utakapofunguliwa tu nitazama ndani kumtafuta Zulfa wewe utakwenda kunisubiri katika gari” akasema Mathew “Looks like a good plan” akasema Austin na kutangulia kutoka mle maliwato baada ya dakika tatu Mathew naye akatoka akaenda block F akauona ule mlango aliousema Austin na ili kupoteza muda akalazimika kucheza katika moja wapo ya mashine iliyokuwa karibu na ule mlango.Wakati akiendelea kucheza akamuona Austin akielekea chooni na baada ya dakika moja akatoka Mathew akaanza kujiweka tayari.Dakika moja na nusu toka Austin atoke mle chooni moshi mzito ukaanza kutoka kupitia chini ya mlango na kuzua taharuki kubwa kwa watu waliokuwa wakicheza mle ndani wakaanza kuulizana chanzo cha ule moshi na mara kengele za tahadhari ya moto zikaanza kulia.Walinzi wakaingia ndani na kuanza kuwatoa watu nje ya jengo.Kulikuwa na taharuki kubwa.Kama alivyokuwa ametazamia Mathew mlango ule aliokuwa amesimama pembeni yake ulifunguliwa na watu wawili waliotoka kwa haraka sana kuja kushuhudia kilichokuwa kimetokea na Mathew akapata upenyo akaingia ndani.Hakuna aliyekuwa anamfuatilia kwani watu walikuwa katika heka heka za kujiokoa.Alipoingia upande huu wa pili Mathew akakutana na meza mbili zilizokuwa na kompyuta mbili ambazo hazikuwa na watu.Akakipita chumba kile na kukutana na korido ambako aliona watu wakitoka katika ofisi zao wote wakijiuliza kilichotokea.Akalifuata korodo lile na kumkuta mwanadada mmoja aliyevaa shati jeupe na sketi fupi ya kijivu akitoka ndani ya ofisi moja Mathew akamgonga akaanguka akamshika mkono akamuinua.. “Samahani,kuna dada mmoja ameingia huku amevaa gauni refu jekundu la kung’aa.Mimi ni dereva wake aliniacha nje nimsubiri baada ya kengele ya tahadhari ya moto kuita nimelazimika kuja kumtafuta.Kama unafahamu alipon ielekeze tafadhali” akasema Mathew “Yule ni mchumba wa Habib.Mfuate katika ofisi ya Habib nyoosha halafu pinda kushoto mlango wa pili ndimo ofisi ya Habib” akasema Yule mwanadada na kuanza kukimbia.Mathew naye akakimbia kuelekea katika ofisi ya Habib kama alivyoelekezwa.Akaitoa bastora yake akakinyonga kitasa lakini mlango ulikuwa wazi akaingia ndani chumba kilikuwa kitupu hakukuwa na mtu yeyote akachukua simu akampigia Austin “Austin nimeipata ofisi ya Habib lakini hayuko humu chumba ni kitupu.Kaa macho huko nje kama anatoka” akasema Mathew na kuelekea mezani akaanza kupekua makaratasi na mafaili aliyoyakuta pale juu kuangalia kama anaweza akapata kitu cha kumsaidia lakini hakupata chochote akaenda katika kabati kubwa akavunja kioo na kuanza kupekua mafaili mara akastuliwa na sauti kali “Taratibu sana inua mikono yako juu” ikasema sauti ya mwanaume. “Taratibu geuka nitazame” akasema Yule jamaa na Mathew akageuka taratibu akajikuta akitazama na bastora mbili na kilichomstua zaidi ni kumuoa mtu aliyekuwa akimtafuta Zulfa akiwa na bastora pi.Zulfa na Yule jamaa walionekana kushangaa hawakumfahamu Mathew “Who are you?akauliza Yule jamaa “Habib Hussein” akasema Mathew na Yule jamaa akastuka sana na kutazamana na Zulfa “Slowly drop down your gun” akasema Habib na Mathew akatii taratibu akaichomoa bastora yake akaiweka chini huku mkono mmoja akiwa ameuinua. “Nini unakitafuta katika ofisi yangu?Nimekuona kupitia simu yangu ukiingia katika ofisi yangu nikarudi haraka.Nakuuliza tena wewe ni nani?Unatafuta nini humu? Akauliza Habib “Listen to me guys.Kuna bomu ndani ya nyumba hii na muda si mrefu litalipuka.Let’s talk outside ! akasema Mathew Habib akastuka akageuka kumtazama Zulfa aliyekuwa mlangoni.Ni fursa hiyo ambayo Mathew alikuwa anaitafuta.Kwa kasi ya umeme akairukia bastora yake iliyokuwa sakafuni “Habib !! akapiga ukelele Zulfa kumstua Habib ambaye aligeuka ghafla na kutaka kuizinga bastora yake lakini Mathew aliyekuwa mwepesi kama kima tayari alikwisha inyakua bastora yake akaizinga na kuachia risasi tatu zilizompata Habib kifuani akaanguka chini.Baada ya Habib kuanguka chini Zulfa akageuka haraka na kuachia risasi mbili kumlenga Mathew aliyekuwa chini lakini jicho la Mathew lililozunguka kama kinyonga lilikwishaona uelekeo ambao Zulfa alikuwa ameulenga hivyo akajirusha pembeni haraka na kufumba na kufumbua Zulfa alikuwa amepotea.Mathew akainuka na kwenda mlangoni akachungulia lakini hakumuna Zulfa alikwisha toweka “She’s gone” akasema Mathew na kuchukua simu akampigia Autin huku akikimbia. “Austin kuwa makini huko nje Zulfa ametoweka huku ndani.Angalia ule mlango alikoingilia”akaelekeza Mathew na mara akajikuta amepigwa na kitu usoni akaanguka chini.Kabla hajajua kilichompiga akapigwa teke kali la tumbo akatoa mgumo wa maumivu.Mathew alihisi maumivu makali sana ya kichwa lakini akajitahidi kufumbua macho na kitu cha kwanza alichokishuhudia ni mwanamke aliyevaa suruali nyeusi na gauni jekundu akiwa amelipandisha na kulifungia kiunoni. “Zulf..” akapigwa teke kali la usoni damu ikaanza kumtoka mdomoni “Huyu mwanamke anaonekana ni hatari sana katika kupigana natakiwa kumdhibiti haraka sana.Mathew akajifanya akigugumia kwa maumvu makali na Zulfa akiwa na bastora mbili akaanza kumsogelea. “Who are you son of b…………” hakumaliza alichotaka kukisema Mathew akajigeuza kwa kasi ya ajabu na kumkata mtama akaanguka chini lakini kwa umahiri mkubwa akajibiringisha na kusimama tena lakini kabla hajafanya chochote Mathew naye alikwisha simama Zulfa akazunguka mateke mawili Mathew akayaona na kukwepa halafu akamtandika teke zito lililompeleka ukutani na kutoa mguno wa kuumia.Ghafla Zulfa akachomoa bastora nyingine Mathew akarukia nyuma ya mtungi mkubwa wa maua risasi zikapiga mtungi ule na kuupasua kisha Zulfa akatoka mbio.Mathew akaokota simu yake na bastora zile mbili alioziacha Zulfa na kuanza kumfuatilia.Akasikia mlango ukibamizwa na piki piki ikiwashwa.Akawahi mlango ule lakini ulikuwa umefungwa kwa ndani .Akaruka teke zito na kuuvunja lakini alichelewa tayari Zulfa alikuwa ameondoka na pikipiki kubwa akielekea katika mlango mkubwa wa kutokea nje.Mathew akaanza kuachia risasi lakini Zulfa alikuwa makini akashika usukukani kwa mkono mmoja akageuka na kuanza kuachia risasi ikamlazimu Mathew kujificha Zulfa akasimama katika mlango mkubwa akisubiri ufunguke huku akiachia risasi kumzuia Mathew asimsogelee.Mathew akampigia simu Austin “She’s coming out.Yuko na piki piki ! akasema Mathew mlango ukafunguka Zulfa akatoka “Tayari nimemuona.What do you suggest I take her down or we follow her? “Take her down we don’t have much time” akasema Mathew.Austin ambaye alikuwa karibu na lango lile alilotokea Zulfa akajiweka tayari na mara tu lango lilipofunguliwa Zulfa akatoka akiwa katika mwendo mkali Austin bila kujali watu wengi waliokuwepo pale nje akaachia risasi kadhaa na piki piki ile ikaanguka chini.Zulfa alirushwa na kuanguka mbali lakini kwa umahiri wake akatua chini kifundi hivyo hakuumia lakini hakuweza kutembea kwani risasi mbili kati ya zile alizoachia Austin zilimpata mguuni.Bila kupoteza muda Austin akamfuata akamfunga pingu haraka haraka akamuinua na kumkimbiza hadi katika gari lao akamuweka kiti cha nyuma na kumpigia simu Mathew “Mathew tayari nimempata.Come quick” “Good job Austin.Nilikuwa napekua gari lake kuna vitu nimevipata.I’ll be there in a second” akasema Mathew na kukata simu. Watu waliokuwapo pale nje walishuhudia kile alichokifanya Austin na kwa haraka walinzi wawili waliokuwa na silaha wakaanza kulisogelea gari lake “C’mon guys don’t do this !akasema Austin kwa sauti ndogo mara wote wawili wakaanguka chini.Mathew Mulumbi aliyetokea ndani aliwaona na kuwamaliza wote kwa bastora yake yenye kiwambo cha sauti kisha akakimbia hadi katika gari akaurushia mkoba aliokuwa nao garini akarukia katika usukani na kuwasha gari kisha wakaondoka kwa kasi kubwa huku Austin akiwa dirishani na bastora akiendelea kuachia risasi na kulifanya eneo lote liwe jeupe kabisa.Walitoka mtaa wa misheni wakaingia barabara ya Mtambikile kisha wakakunja kulia na kuingia barabara ya Fidel ambayo haikuwa na magari mengi na hapo mwendo ukawa mkali wakakata kulia na kuingia barabara ya Ngorongoro “Austin Make sure no body is following us” akasema Mathew “Hakuna anayetufuatilia Mathew.Just drive ! akasema Austin.Jeraha la Zulfa lilikuwa linatoa damu nyingi “Una boksi la huduma ya kwanza humu?akauliza Austin na Mathew akamuelekeza lilipo Austin akachukua pamba na kuigandamiza katika jeraha la Zulfa ambaye alikuwa anagugumia kwa maumivu makali. “I’ll kill you bastard !! akalia Zulfa akihisi maumivu makali.
Austin na Mathew waliwasili katika makazi yao,haraka Zulfa akashushwa garini na kuingizwa ndani. “Mathew tunahitaji kuziondoa risasi katika mguu wa Zulfa amepoteza damu nyingi” akashauri Austin “I need to call a doctor” akasema Mathew “There is no need.Hatuna muda wa kumsubiri hadi daktari afike hapa.I’ll do it” “Can you remove the bullets? “That’s why we’re special unit.Tunafundishwa kila kitu ili hata tukiwa katika misheni Fulani na mmoja wetu akapigwa risasi tunamuhudumia sisi wenyewe” akasema Austin “Good.Let’s do it” akasema Mathew na Zulfa akaingizwa katika chumba alimo mke wa balozi kulimokuwa na meza.Austin akaenda kuchukua sanduku lake dogo la vifaa na kulileta mle chumbani.Mathew akawaacha Austin na Gosu Gosu akamfuata Ruby “Ruby you did a great job thank you” “You’re welcome” akajibu Ruby huku akitabasamu Mathew akampatia kompyuta aliyoitoa katika gari la Zulfa ili aichuguze kama kuna kitu anaweza akakipata. “Gosu Gosu mshike mikono mzuie kwa nguvu kwani hatuna sindano ya ganzi wala usingizi hivyo nitamuwekea dawa Fulani katika jeraha kisha nitazitoa risasi.Atapiga ukulele kwani dawa inauma sana” akasema Austin na Gosu Gosu akamshika Zulfa mabegani. “Hey ! listen to me lady.I’m going to remove the bullets.It’s goin to hurt lakini nakupa hii uma na meno” Austin akamwambia Zulfa na kumpa kitu Fulani aweke mdomoni “You go to he……..aaghh” Zulfa akapiga ukelele mkubwa wa maumivu baada ya Austin kumwagia dawa katika jeraha. “Easy gentlemen..easy !! akasema mke wa balozi aliyekuwamo mle chumbani akainuka na kusogelea pale mezani “Please stay away maam” akasema Gosu Gosu “I can help.I’m a doctor” akasema Yule mama Austin akageuka na kumtazama “Are you sure?akauliza “Yes”akajibu na kisha akaanza kusaidia na Austin kutoa risasi katika mguu wa Zulfa “Mimi na Yonathan tulikutana jeshini”akasema Yule mke wa balozi “Sote tulikuwa tunahudumia askari walioumia katika mapigano na wapalestina”akaendelea kuwapa historia yake namna alivyokutana na balozi Yonathan Cohen wakawa wapenzi na hatimaye wakafunga ndoa Walifanikiwa kutoa risasi mbili katika mguu wa Zulfa,wakayafunga majeraha.Zulfa alikwisha poteza fahamu “You need to take her to hospital ! akasema mke wa balozi Austin hakumjibu kitu akafanya usafi na kisha wakambeba Zulfa na kumpeleka katika chumba kidogo ambacho alikitumia kama stoo ambamo kulikuwa na kitanda kidogo wakamlaza Wakati Ruby akiendelea na jitihada za kuipekua kompyuta ya Zulfa Mathew akaelekea katika chumba alimo Edger “Hallow Edger” akasema Mathew “Mmefanikiwa kumpata Yule jamaa?akauliza Edger “Bado hatujafanikiwa kumpata lakini tumempata mtu ambaye anaweza akatufikisha kwake.Umewahi kumuona au kumsikia mwanamke mmoja anaitwa Zulfa? “Zulfa? “Ndiyo.Ni mtu wa karibu na jamaa tunayemtafuta” akasema Mathew “Hapana simfahamu huyo Zulfa na sijawahi kumuona” “Una hakika hajawahi kutumwa kwako hata mara moja kukuletea ujumbe wowote?akauliza Mathew “Kama nilivyokwambia kwamba mimi nilikuwa nawasiliana na Yule jamaa pekee na hajawahi kumtuma mtu mwingine yeyote kuniletea ujumbe” “Are you sure? “yes I’m sure” akajibu Edger “Good.Nitakujulisha pale tutakapokuwa tumempata” akasema Mathew na kuanza kutoka mle chumbani alipofika mlangoni akageuka. “Magaidi tayari wamechinja watoto wanne na wanaendelea kuchinja zaidi.Kuna chochote ambacho unaweza ukaniambia kinachoweza kusaidia kuwapata watoto wale zaidi ya huyu jamaa? “Hakuna chochote ninachokifahamu kinachoweza kusaidia zaidi ya taarifa hiyo niliyokupa Mathew.Find that man ! akasema Edger na Mathew akatoka na kuwakuta aina Austin tayari wamemaliza kumtoa Zulfa risasi.Wakamjulisha kuwa mke wa balozi ni daktari na ametoa msaada katika kumtibu Zulfa. “Good job to you all.Hatimaye tumempata mtu ambaye tuna hakika anaweza akatufikisha kwa mtu ambaye alikuwa anawasiliana na Edger Kaka.Mwanamke huyu ni hatari sana ana uwezo mkubwa wa kupigana bila kutumia silaha na akiishika silaha ni mtumiaji mzuri pia.Sikuwa nimetegemea kabisa kama angeweza kuwa hatari namna ile.Haikuwa rahisi kumpata”Akasema Mathew na kuwataka wenzake wapumzike wakati wakiendelea kumsubiri Zulfa azinduke na papo hapo kusubiri kama Ruby anaweza akapata kitu katika kompyuta ya Zulfa. “Kuna chochote umekipata Ruby?akauliza Mathew “Still searching” akajibu Ruby na Mathew akasimama nyuma yake akiangalia namna Ruby alivyokuwa akiifanya kazi yake mara akafuatwa na Gosu Gosu “Mathew can we talk for a second” akasema Gosu Gosu wakatoka ndani ya kile chumba “Mlipoondoka mimi na Ruby tulikuwa tunatazama runinga namna maandamano yalivyokuwa yanaendelea.Maandamano hayo yalisimamishwa na askari wa kutuliza ghasia kwa hayakuwa halali na waliyatawanya.Mimi sikuwa nimetilia maanani sana kutazama kilichokuwa kinaendelea lakini Devotha aliyekuwa makini kufuatilia kuna kitu alikiona ambacho alisema si cha kawaida na akataka kuipata video ile ya namna maandamano yalivyotawanywa na askari.Tulimuomba Ruby atusaidie kuipata video hiyo ili Devotha aweze kuchunguza zaidi hicho alichokisema hakikuwa cha kawaida lakini kwa kuwa Ruby na Devotha bado hawajakaa sawa ilikuwa vigumu kwa Ruby kukubali.Nimeona bora nikueleze jambo hili ulifahamu ili tujue kitu gani ambacho Devotha alikiona”akasema Gosu Gosu “Hakukueleza nini aliona?akauliza Mathew “Hapana hakunieleza”akasema Gosu Gosu wakatoka kwenda nje kuonana na Devotha “Gosu Gosu ameniambia kwamba kuna kitu Fulani ulikiona wakati askari wa kutuliza ghasia wakitawanya maandamano.Can you tell me what you saw?Mathew akamuuliza Devotha “Ni kweli kuna kitu nilikiona ambacho kilinishangaza kidogo ndiyo maana nikataka kupata kipande kile cha video ya askari wakitawanya waandamanaji ili nijiridhishe na kile nilichokiona ni kitu cha kweli” “Uliona nini?akauliza Mathew “Wakati maandamano yamesimamishwa na polisi,kulitokea majibizano kati ya kamanda wa polisi na waziri mkuu.Wakati majibizano hayo yakiendelea I saw someone”akasema na kunyamaza kidogo “Ulimuona nani? “Nyuma ya waziri mkuu kulikuwa na mwanamke mmoja aliyevaa suti ya suruali rangi ya kijivu na pembeni ya huyo mwanamama kulikuwa na mtu mmoja amevaa miwani myeusi na suti nyeusi.Nilipomuona huyo mtu nikastuka na kumuelekezea macho nikamuona akizungumza na simu halafu akampatia simu mwanamama ambaye alikuwa nyuma ya waziri mkuu aliyekuwa akizungumza katika kipaza sauti wakati huo.Alipomaliza,yule mwanamama akamsogelea waziri mkuu na kumnong’oneza kitu sikioni.Kamera ilihama na sekunde chache baadae gesi ya machozi ikaanza kurushwa waandamanaji wakatawanyika.Nilitaka kupata kipande kile nijiridhishe kama mtu niliyemuona kweli ni mwenyewe au wamefanana” “Mtu huyu uliyemuon….” Akasema Gosu Gosu lakini Devotha akamkatisha “Sijamaliza bado” “Go ahead” akasema Mathew “This man I saw…” akasita kidogo halafu akasema “Wakati idara yetu inaanzishwa jukumu letu la kwanza lilikuwa ni kuvitafuta na kuvisafisha vikundi vya kigaidi vilivyoanza kuchipuka na kutishia hali ya amani.Kuna kikundi kimoja ambacho kiongozi wake alijulikana kama Nazil Jalib kiliwahi kuvamia kijiji, kuiba mali na kuua watu hamsini.Tulifanikiwa kukiondoa kikosi hicho hatari na nyumba ya kiongozi wake Nazil iliteketezwa kwa bomu na tuliamini kwamba amefariki lakini mtu niliyemuona leo katika maandamano yale anafanana vile vile na Nazil.Ninataka kuipata video ile ili kujiridhisha kama kweli mtu Yule ni Nazil kama ni yeye basi mtu huyu ni hatari sana na kama ni yeye ana ukaribu gani na waziri mkuu?akauliza Devotha “Usihofu D……” akasema Mathew na Austin akatokea “Guys Ruby ana jambo amelipata anataka kutueleza.Am I missing something here?akauliza “Kuna jambo Fulani Devotha alikuwa ananieleza” akasema Mathew wakaelekea ndani “Ruby umepata nini?akauliza Mathew. “Kuna kitu ambacho kimenishangaza kidogo”akanyamaza na kuvuta pumzi “Nimeipekua kompyuta hii ya Zulfa haina kitu chochote cha maana zipo program za kawaida za kuiwezesha kompyuta kufanya kazi.Kompyuta hii haitumiki kwa mawasiliano yoyote ya barua pepe au mitandao yoyote ya kijamii” akasema Ruby “Kompyuta hii nimeikuta katika mkoba uliokuwamo katika gari lake pamoja na vifaa vyake vingine vidogo vidogo nikajua ndiyo kompyuta yenye taarifa zake zote.Haiingii akilini atembee na kompyuta ambayo haitumii katika shughuli zake.Haitumii kwa mawasiliano au hata kwa program za kiofisi.Una hakika hakuna mafaili ameyafuta? “Kama kuna mafaili ameyafuta ningejua lakini hakuna kilichofutwa” akasema Ruby “Austin unadhani Zulfa ataamka saa ngapi? “Sina hakika lakini hatachukua muda mrefu” “Tunahitaji kumfanya mahojiano haraka.Magaidi wanaendelea kuua watoto kila baada ya muda” akasema Mathew na Ruby akasema “Sijamaliza bado.” Akasema Ruby na kufumba macho akionekana kuwa katika maumivu “Ruby are you oay?akauliza Mathew “Yeah I’m fine” akajibu Ruby “Wakati naendelea kuipekua hii kompyuta kuna ujumbe ulijitokeza ghafla.Nikaufungua ujumbe ule ulikuwa ni mchezo wa kompyuta.Ulisomeka hivi “Hello Zay come online let’s play” akasema Ruby “A computer game! Mathew akashangaa “Yes a computer game” akasema Ruby “Let me see it” akasema Mathew “Unahitaji namba za siri za kufungulia huo mchezo ili uweze kucheza” akasema Ruby.Mathew akafikiri kidogo na kusema “Ruby unaweza kuitafuta namba ya siri anayotumia Zulfa kufungulia mchezo huu?akauliza Mathew “Yes I can” akajibu Ruby “Good.Find it” akasema Mathew. “Wakati Ruby anatumia program yake ya kutafuta namba za siri za kuufungulia mchezo huu Devotha endelea na lile suala ulilokuwa unatueleza” akasema Mathew “Niliwaeleza kuwa Nazil Jalib ni mtu hatari sana ambaye tuliamini amekufa katika mlipuko wa bomu pamoja na watu wengine saba waliokuwemo katika nyumba mlipuko ulipotokea lakini kumuona mtu kama Yule pale leo tena karibu na waziri mkuu nimestuka sana.Ni mtu hatari na kama yuko hai anapaswa kutafutwa” “Mtu huyu ni nani hasa? “Anajiita invisible.Ni mtu ambaye hatukuwahi kufanikiwa kupata taarifa zake za kutosha.Nahitaji kupata kile kipande cha video ili kujiridhisha kama kweli ni yeye ama vipi.Kuna jambo lingine vile vile ambalo sina hakika mtalipokeaje lakini kama tukithibitisha kweli ni Nazil italazimu kumshirikisha Kaiza” akasema Devotha ‘That bastard works for president !! akafoka Mathew “Ili kujiridhisha kwamba huyu niliyemuona leo katika maandamano ni Nazil Jalib italazimu kumtafuta Kaiza kwani kwa sasa yeye ndiye kiongozi wa idara niliyokuwa ninaiongoza na kumbu kumbu zote za Nazil ziko pale” “Fine.We’ll see what we can do” akasema Mathew na kumfuata Ruby “Kuna chochote umekipata?akauliza Mathew “Program still searching” akasema Ruby “How long it’ll take” “It depends.Let’s wait for program to finish” akasema Ruby.Mathew akatoka na kuingia katika chumba alimokuwamo mke wa balozi ambaye alistuka sana na kuanza kuogopa,Mathew akamsogelea “Unajisikiaje?akauliza ‘Naendelea vizuri.Lini nitakuwa huru?akauliza “Nimeambiwa ulichokifanya muda mfupi uliopita.Tunashukuru sana kwa msaada uliotoa kwa mgonjwa tuliyemleta hapa” akasema Mathew “Taaluma yangu ni daktari ndiyo maana nikawasaidia” “Mama kwanza kabisa naomba ufahamu kwamba sisi si watu wabaya.Sisi siyo wakatili kama unavyodhani na usiwe na hofu yoyote ukiniona mimi au mwenzangu yeyote ameingia humu ndani.Tuko katika kutekeleza kazi moja nzito sana kwa ajili ya usalama wa taifa.Magaidi wamevamia shule na kuteka watoto sitini na sita na hivi tuzungumzavyo tayari wamekwisha anza kuwachinja mmoja baada ya mwingine na tunafanya jitihada za kuwakomboa” “Mimi na mume wangu tunahusika nini na hao magaidi?akauliza mke wa balozi “Jioni ya leo utarejea nyumbani kwako,hatuna tena sababu ya kuendelea kukuweka hapa na yeyote atakayekuuliza mahala ulipokuwa utamueleza ulipata safari ya dharura.Ningekupeleka nyumbani kwako muda huu lakini tunayo shughuli nzito ya kuwakomboa watoto waliotekwa na magaidi” akasema Mathew na mlango ukafunguliwa Gosu Gosu akaingia “Mathew program imekubali” akasema Gosu Gosu na Mathew akatoka akamfuata Ruby “Nimefanikiwa kuzipata namba za siri za kuingia katika mchezo huu” akasema Ruby na kuufungua mchezo ule Mathew akautazama kisha akasema “Oh thank you Heaven Father” akasema Mathew na kuwatazama wengine “This is how terrorist communicates.Wanafahamu kwamba wanafuatiliwa sana katika simu na mitandaoni hivyo siku hizi wanatumia michezo kama hii kwa mawasiliano kitu ambacho si rahisi kwa mtu kuweza kutilia shaka” akasema Mathew na kuanza kuwaelezea wenzake namna magaidi wanavyowasiliana kwa kutumia michezo. “Mkitaka kuamini ninachokisema ngoja tujaribu” akasema Mathew na kuanza kucheza “Nimeanzisha mchezo ili kuwapa taarifa kwamba niko hewani” akasema Mathew Baada ya muda mtu mwingine akacheza na kisha ujumbe ukajitokeza chini “uko wapi?Tunakutafuta sana.Kwa nini umezima simu siku kama ya leo?akauliza Yule mtu wa upande wa pili “Mmeona namna wanavyowasiliana?akauliza Mathew na kucheza tena halafu akaandika ujumbe chini “Kulifanyika uvamizi Habib ameuawa mimi nimefanikiwa kutoka salama na kukimbia.Msihofu ni wezi walitaka kupora fedha” Baada ya muda ujumbe ukajibiwa “Z kuna mabadiliko ya dharura yamefanyika naamini bado hujapata taarifa.Hatutakutana kwa Zahara kama ilivyokuwa imepangwa bali tutakutana Mellisa hotel ukumbi no 5.Utamkuta Zeno atakupokea” akasema Yule jamaa mwingine “Nini sababu ya mabadiliko? Mathew akauliza “Kuna jambo linakwenda kufanyika hapo fika bila kukosa.Saa tisa kamili” akasema Yule jamaa “Sawa ninakuja” Mathew akajibu na Yule mtu akatoka hewani na meseji zote walizotumiana zikafutika “Nadhani mmeona namna wanavyofanya mawasiliano yao.Si rahisi kwa mtu mwingine kugundua kama kuna mawasiliano yanafanyika.Wote wana mchezo huu katika simu au kompyuta zao na wameunganishwa na mtandao wao hivyo basi kunapokuwa na jambo hujulishana kwa kupitia njia hii” “These people are smart” akasema Gosu Gosu “No ! They are stupid ! akajibu Austin “Tayari tumepata uhakika kwamba wanakutana mchana wa leo Mellisa hotel.Tutakuwa wageni wao kwani na sisi tutakwenda kuhudhuria katika kikao chao kujua wanachokijadili.Sasa tumepata uhakika mkubwa kwamba kweli Zulfa anashirikiana na magaidi wa IS ambao tayari wana mtandao wao mkubwa hapa nchini.Kitu kikubwa kwa sasa ni kutafuta namna ya kuweza kuingia katika hicho kikao” akasema Mathew “Ninaamini kikao hicho kitahudhuriwa na watu wengi na muhimu wa IS hapa nchini ambao tunawatafuta sana so this is the chance.Hakuna wakati ambao tutawapata wengi kwa pamoja kama katika kikao hiki na ninaamini kutokea pale tutaweza kupata taarifa za mahala walipo watoto waliotekwa nyara”akasema Austin “Anachokisema Austin ni kitu cha msingi sana na kama tukifanikiwa kuingia katika kikao hicho tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana.Guys we’re so close to know where the kids are”akasema Mathew “Nina wazo” akasema Devotha “Mellisa hoteli ni moja ya hoteli kubwa hapa nchini.Viongozi wengi wa kimataifa wanapokuja nchini hufikia pale kutokana na hadhi yake.Ni hoteli yenye ulinzi mkubwa.Nimefika pale mara nyingi katika shughuli zangu hivyo ninapafahamu vyema.Kumbi zake za mikutano zinaaminika sana na hata vikao vingi vya siri hufanyika pale ndiyo maana kupata ukumbi pale kwa mikutano ni shida kwa kuwa kila siku kumbi zake zimejaa.Tunatakiwa kutafuta namna ya kuweza kuwapata ambayo kwanza haitawafanya wastuke na waahirishe kikao,pili kuwachukua bila kutumia nguvu” “Nini ushauri wako?akauliza Mathew “Maya B virus”akasema Devotha “Whats that? Akauliza Mathew “It’s a sleeping Virus.Hiki ni kirusi ambacho kinasambaa kwa njia ya hewa na mtu yeyote akivuta hewa yenye kirusi hiki basi hupatwa na usingizi wa ghafla na kulala.Tukiwa na kirusi hiki tutatumia mfumo wa usambazaji hewa wa pale hotelini na hewa yenye kirusi hicho itambaa hoteli nzima na watu wote hotelini mle watalala usingizi.Baada ya kuwalaza tutaleta gari la wagonjwa na kuwapakia watu wetu na kuondoka nao”akasema Devotha “Hii ni njia nzuri sana.Nataka kufahamu zaidi kuhusu hicho kirusi,mtu akivuta hewa yenye kirusi hicho inamchukua muda gani kulala na inachukua muda gani kuamka? Hakuna madhara yoyote ya kiafya kwa mtu aliyevuta hewa yenye kirusi hicho?Mathew akauliza “Inamchukua mtu dakika tano hadi kumi kulala usingizi toka avute hewa yenye kirusi Maya naakisha lala inamchukua dakika thelathini ndipo anaamka.Kuhusu madhara hakuna madhara yoyote.Kirusi hiki kimetengenezwa maalum kwa ajili ya kumfanya mtu alale.Hiki ni kirusi kipya kabisa ambacho kimetengenezwa na jeshi la Marekani na kinatumika kama silaha.Wanapokuwa katika mapambano dhidi ya vikosi mbali mbali vya kigaidi hutumia teknolojia ya ndege ndogo zisizo na rubani kwenda kusambaza kirusi hiki mahala walipo magaidi ambao hulala na kujikuta wamevamiwa.Mtu akiamka baada ya dakika mbili atakuwa mzima tena na hakuna madhara mengine msihofu” akasema Devotha “Nadhani njia hii aliyoipendekeza Devotha ni njia nzuri sana labda kama kuna mtu ana wazo mbadala”akasema Mathew na wote wakakubaliana na wazo lile la Devotha la kutumia kirusi Maya B “Okay sote tumekubaliana kutumia kirusi hicho.Swali ni wapi tutakipata hicho kirusi? Mathew akauliza “Ninacho nyumbani kwangu”akajibu Devotha “Good.Kama kirusi kipo tayari tujadili namna ya kwenda kukiingiza katika mfumo wa hewa wa pale hotelini” “I’ll do it.Nimefika katika ile hoteli mara nyingi na ninaifahamu vyema kila sehemu.Nitachukua kirusi na kwenda kukiingiza katika mfumo wa hewa safi.Kabla sijaingiza kirusi hicho katika mfumo wa hewa nataka gari la wagonwa liwe limeandaliwa na kuwepo karibu na nitakapojulishwa kuwa kila kitu tayari basi nitaingiza kirusi na baada ya dakika tano kupita mnatakiwa kufika haraka sana na kuwachukua watu tunaowahitaji” “Good plan.mambo yatakwenda namna hii.Devotha na Austin ninyi mtakwenda hotelini.Austin utamlinda Devotha hadi uhakikishe amefanikisha kuingiza kirusi hicho katika mfumo wa hewa kisha mtanijulisha.Mimi ninakwenda kufanya mpango wa gari la wagonjwa na baada tu ya kupewa taarifa nitafika hapo mara moja na wote tutasaidiana kuweza kuwabeba watu wetu na kuwapakia garini.Gosu Gosu wewe utabaki hapa kulinda usalama tunao watu wawili hatari humu ndani.Kuna yeyote mwenye wazo mbadala kabla hatujatawanyika kwenda kujiandaa kwa kazi hii?akauliza Mathew hakukuwa na mwenye wazo mbadala bila kupoteza muda Austin akaingia chumbani kwake akavaa suti nzuri nyeusi kisha wakaingia katika gari la Mathew wakaondoka hadi nyumbani kwa Devotha Mathew akawaacha pale yeye akaondoka kwenda kuonana na Dr Hiran.
Devotha na Austin waliwasili hoteli Mellisa wakiwa katika gari la kifahari aina ya Rolls Royce phantom rangi ya fedha mali ya Devotha.Ukimya ulikuwa mkubwa sana katika hoteli hii iliyokuwa imezungukwa na msitu wa miti ya kivuli.Sauti za ndege mbali mbali ndizo zilizosikika.Ulinzi katik ahoteli hii ulikuwa wa kielektroniki.Gari linapofika getini tayari linakuwa limeonekana na kukaguliwa kama lina silaha ndani,mlipuko au kitu kingine chochote cha hatari na baadaya ukaguzi geti hifunguliwa na gari huingia ndani.Endapo gari litakutwa na tatizo lolote geti halitafunguka na kengele maalum hulia kuwapa taarifa kikosi cha walinzi ambao wana sehemu yao maalum ndani ya hoteli. Baada ya kufika getini walitumia dakika moja gari likakagulia kisha geti likafunguliwa wakaingia ndani moja kwa moja wakaelekea katika maegesho.Devotha akafungua sehemu ya siri ndani ya gari lake anakohifadhi silaha na ambapo si rahisi kuonekana katika mitambo ya usalama akatoa bastora mbili zilizofungwa viwambo vya sauti akampatia moja Austin.Akachukua vifaa vingine pamoja na kirusi kile kilichokuwa katika chupa ndogo inayofanana na chupa za uturi akaviweka katika mkoba wake “Sasa tuelekee ndani.Ninaifahamu hoteli hii vyema na hata badhi ya wafanyakazi wa hapa wengi wananifahamu kutokana na kuja mara kwa mara.Kabla ya kuachia kirusi nitakupigia simu halafu utaelekea maliwato kule utavaa maski kujikinga na hewa yenye kirusi hicho”akasema Devotha wakashuka na kuelekea ndani ya hoteli. Mara tu walipoingia ndani ya hoteli Devotha akasalimiwa na baadhi ya wafanyakazi waliomfahamu kisha wakaenda kuchukua meza wakakaa na kuagiza chakula.Watu walikuwa wachache ndani ya hoteli hii ni kutokana n gharama za juu sana za hoteli hii ndiyo maana inajulikana kama hoteli ya mabilionea.Chakula kililetwa wakaanza kula wakivuta muda kusubiri muda wa kuanza kikao ufike.Wakati wakiendelea na chakula simu ya Devotha ikaita alikuwa ni Mathew “Tayari nimekwisha andaa gari kubwa la wagonjwa ninawasubiri ninyi” akasema Mathew “Sisi tayari tunasubiri muda wa kuanza kikao ufike na kwa mujibu wa saa yangu zimebaki dakika chache.Nitajulisha kila kitu kitakapokuwa tayari” akasema Devotha na kukata simu akaitazama yake Muda ule alioambiwa Zulfa wa kuanza kikao ulipofika Devotha akachukua mkoba wake na kuinuka pale mezani kama vile anaelekea upande wa pili lakini akakunja kona na kufuata ujia uliokuwa upande wa kulia akakutana na mlango wa kioo na ndani yake kulikuwa na mtu mmoja akipata chakula huku akiyaelekeza macho katika kompyuta yake.Devotha akagonga mlango na Yule jamaa akainuka haraka akamfuata “Nikusaidie nini mama?akauliza Yule jamaa aliyevaa suruali nyeusi na shati zito jeupe lenye nembo ya Mellisa group. “Samahani nimepotea na kujikuta nimefika hapa.Natafuta njia ya kwenda juu sitaki kutumia lifti “Rudi ulikotoka utakutana na kibao kimeelekez…………..” kabla hajamaliza maelekezo yake Devotha alichomoa bastora kutoka katika koti lake na kumtandika risasi mbili Yule jamaa akaangukia ndani.Devotha akageuka kutazama kama kuna mtu lakini alikuwa peke yake haraka haraka akaingia ndani na kumvuta Yule jamaa akamficha chini ya meza halafu akachukua simu na kumpigia Austin akamtaka aelekee maliwato kwani muda wowote angeweza kuingiza kirusi kile katika hewa.Bila kupoteza muda akaufungua mlango mwingine wa chumba na kuingia katika mashine ya kuzalisha hewa safi na kuisambaza katika hoteli.Akatafuta sehemu nzuri akavaa mask na kumpigia simu Austin kuwa avae mask halafu akatoa kile kichupa chenye kirusi akang’oa kifuniko na kirusi kile kikaanza kutoka ndani ya chupa kwa kasi na kuingia katika hewa.Alipomaliza akaelekeza macho katika saa akihesabu dakika baada ya dakika tano akampigia simu Mathew “Tayari tumemaliza kazi unaweza ukaja” akasema Devotha kisha akazima mtambo ule wa kupeleka hewa ili kuacha hewa ile yenye kirusi isambae akatoka mle ndani akaelekea katika ukumbi wa chakula.Yalikuwa ni mambo ya kushangaza sana kwani watu wachache waliokuwemo mle ukumbini walikuwa wamelalia meza zao kana kwamba wamekufa lakini hii ni baada ya kuvuta hewa yenye kirusi.Moja kwa moja akaelekea jikoni ambako alikuta hali ile ile akazima majiko ili kuzuia ajali ya moto isitokee.. Devotha akamjulisha Austin kila kitu tayari,Austin akatoka maliwato akamfuata “I’ve never seen something like this.Hoteli yote wamelala usingizi ndani ya kipindi hiki kifupi?Austin akashangaa “C’mon Austin we have job to do.Follow me! Akasema Devotha wakakimbia kuelekea ulipo ukumbi ambao Zulfa alielekezwa.Nje ya ukumbi ule walikuta walinzi wawili wakiwa wamekaa chini wamepitiwa na usingizi.Kwa haraka haraka ungeweza kudhani watu wale wamekufa lakini walikuwa wamelala “Ni hapa” akasema Devotha na kukiminya kitasa cha mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.Austin akaurukia teke mlango ukafunguka wakaingia ndani ya chumba kile ambamo kulikuwa na watu kumi na tano na wote walikuwa wamelala usingizi. “Hurry up.We have to collect everything.Kompyuta,simu na kila walichonacho ambacho kinaweza kusaidia” akasema Devotha wakaanza mara moja zoezi la kukusanya kila kitu kilichokuwa mezani mara Devotha akastuka baada ya kumuinua kichwa mmoja wa watu waliokuwa wamelalia meza “This is unbelievable !! akasema kwa sauti na kumstua Austin ambaye naye akainua kichwa kutazama kilichomstua Devotha naye akajikuta akiupatw ana mshangao mkubwa “Waziri mkuu!! Ni yeye kweli au ni mtu aliyefanana naye?akauliza Austin “Ni yeye mwenyewe” akasema Devotha huku akimpekua na kuchukua simu yake akaitenga tofauti na zile za wengine Haraka haraka Devotha akampigia simu Mathew “Mathew umefika wapi? “Tayari ninapita hapa getini wewe uko wapi?akauliza Mathew na Devotha akampa maelekezo mahala walipo.Mathew na Dr Hiran wakiwa wamevaa makoti meupe pamoja na vifaa vya kujikinga na hewa ile yenye kirusi wakashuka garini wakiwa na machela na kukimbia kuelekea mahala waliko akina Devotha wakaingia ndani “Devotha haya ni maajabu ya karne.Are you sure they’ll be fine?Mathew akauliza “They’re fine.Wote wataamka” akasema Devotha na kumfanyia ishara Mathew atazame katika kiti na Mathew akapatwa na mshangao mkubwa “Waziri mkuu ?! What is he doing here?akauliza “Tumemkuta humu anaonekana ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hiki,atatueleza alichokuwa anakifanya humu ndani ni kitu gani atakapoamka” akasema Devotha na kazi ya kuwaondoa wale watu mle ndani ikaanza mara moja.Mathew akamuinua waziri mkuu akamuweka katika kitanda cha magurudumu Dr Hiran na Devotha wakasukuma kitanda kile kumtoa nje.Mathew akamuinua mtu mwingine akamuweka begani Austin naye akafanya hivyo hivyo na kuelekea kwenye lifti wakashuka chini na kuwapakia watu wale ndani ya gari.Devotha na Dr Hiran wakabaki wakiwalinda watu wale wakati Mathew na Austin wakiendelea na zoezi la kuwatoa wengine ndani ya kile chumba.Walitumia dakika ishirini kumaliza zoezi la kuwaondoa watu wale kumi na tano waliokuwemo mle ndani ya chumba na kuchukua kila kitu walichokuwa nacho na bila kupoteza muda wakaondoka kwa kasi kubwa huku gari lile likipiga king’ora na kuachiwa njia barabarani.Austin aliwafuata nyuma akiwa na gari la Devotha “Simu ya waziri mkuu hii hapa” Devotha akamkabidhi Mathew “Devotha kitu ulichokifanya leo sijawahi kukiona sehemu yoyote hata katika filamu.Bado najiuliza ni kweli kile nilichokishuhudia ama ni mazingaombwe? Akauliza Mathew na Devotha akatabasamu “Hiki ni kirusi kipya kimetengenezwa na kinatumika kama silaha japo kwa siri mno.Kirusi kama hiki hakiwezi kutangazwa wala kuruhusiwa kutumika kwani kinaweza kusababisha maafa makubwa duniani.Kinaweza kutumika katika uhalifu mkubwa na hata mauaji ndiyo maana ni moja kati ya vitu vya siri kubwa katika jeshi la Marekani.Wamekuwa wanatumia kirusi hiki katika kuwatafuta magaidi ambao wamekuwa wakijificha milimani” “Wewe ulikipata vipi? Mathew akauliza “Niliwahi kufanya kazi katika idara ya kupambana na ugaidi ya Marekani na ndiko nilikopata kirusi hiki na ni siri yangu kubwa.Hawataki teknolojiayao ijulikane”akasema Devotha na Mathew akayaelekeza macho yake kwa waziri mkuu. “Ulikuwa sahihi ulipoingiwa na shaka kuhusiana na waziri mkuu.Bado siamini kama kiongozi mkubwa kama huyu ana mahusiano na magaidi.Kumbe Edger Kaka hakuwa peke yake,mtandao wao ni mpana sana na ndiyo maana hawakutaka Edger aufahamu.”akasema Mathew “Mathew mimi tayari nilikwisha ingiwa na wasi wasi kwanza kwa kitendo chake cha kuamua kuungana na wananchi katika maandamano.Ni kitendo cha kushangaza sana.Pili nilistuka baada ya kumuona akiwa karibu na Yule mtu ambaye nina uhakika ni Nazil jalib ambaye ni gaidi na muuaji mkubwa.Baada ya kumkuta huku katika kikao na watu wa IS sina shaka kabisa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anashirikiana na magaidi.Kwa nini kiongozi mkubwa kama huyu aliyebeba dhamana kubwa kabisa akafanya hivi?Nini anakitafuta? Au alitumwa na Rais kuja kufanya majadiliano na hawa magaidi namna ya kufanya makabidhiano? kauliza Devotha ambaye alikuwa anaendelea na zoezi la kuwafunga watu wale mikono kwa pingu za plastiki “Tayari nimefahamu anachokitafuta.Ni madaraka.Ameisaliti serikali na kujiunga na wananchi kwa lengo la kutafuta umaarufu.Anachochea wananchi waichukie serikali yao na yeye aonekane shujaa kwa kushiriki nao katika maandamano.Kwa kitendo hicho anajitengenezea mazingira ya kuwania nafasi ya urais na kama akishinda huo utakuwa ni ushindi kwa IS.Katika kutafuta madaraka wanasiasa wako tayari kufanya jambo lolote lile ili waweze kutimiza malengo yao.Wapo vibaraka wa mabeberu ambao wako tayari kuweka rehani nchi na rasilimali zake kwa mabeberu ili wasaidiwe kupata madaraka makubwa.Lakini mwisho wake umefika na mipango yake haitaweza kufaniki………..”akanyamaza Mathew baada ya simu ya wazirihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ mkuu aliyokuwa ameiweka mfukoni kutetema.Mathew akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji jina liliandika Nazil. “Nazil ?!! Mathew akashangaa na kuipokea ile simu akaiweka sikioni “Mheshimiwa tayari nimefika na nimetoa maelekezo kwa Fahad.Mtoto atakayefuata ni mwanao lakini itakuwa ni kwa kutishia tu hatauawa hivyo usiwe na wasi wasi.Fahad yuko mtandaoni kwa sasa”akasema Nazil na Mathew akakata simu halafu akamuandikia ujumbe mfupi “Kila kitu kiende kama kilivyopangwa mimi niko kwenye kikao”akautuma ujumbe ule halafu akamgeukia Devotha “Devotha we have the kids vile vile sina shaka tena waziri mkuu anashirikiana na magaidi” akasema Mathew “Mtu aliyempigia simu waziri mkuu sasa hivi jina lake limeandikwa Nazil jina ambalo linafanana na yule mtu ambaye ulimuona katika maandamano akiwa karibu na waziri mkuu.Nazil alikuwa anamjulisha waziri mkuu kwamba tayari amefikisha ujumbe kwa Fahad.Inaonekana huyu Fahad ndiye ambaye anafanya mauaji ya watoto waliowateka.Kwa mujibu wa maelezo yake inaonekana waziri mkuu alimtuma kupeleka ujumbe kwa Fahad akimtaka atishie kumuua mtoto wake ambaye ni mmoja wa mabinti waliotekwa.Nadhani hii ni kutaka kumpa shinikizo zaidi Rais kwani hawezi kukubali kuona mtoto wa waziri mkuu wake akichinjwa hivyo atafanya kila awezalo kuhakikisha anamuokoa.Nadhani lengo la kumtumia mwanae ni hilo” akasema Mathew.Devotha kwa kutumia simu yake alitazama mtandaoni ambako kulirushwa video ambayo watekaji wa watoto walitishia kumuua mtoto wa waziri mkuu. “Ni kweli.Imerushwa video nyingine wakitishia kuua mtoto wa waziri mkuu.Kumbe suala zima la kuteka watoto wale wa shule limeratibiwa na waziri mkuu.Anathubutuje kumfanyai mwanae kitu kama hiki? akasema Devotha na mara mtu wa kwanza akapiga chafya na kufumbua macho “Wameanza kuamka”akasema Mathew “I told you” akasema Devotha akitabasamu. Ndani ya dakika tano tayari wote walikuwa wameamka na walishangaa baada ya kujikuta wakiwa wamefungwa mikono na wakiwa wameelekezewa bastora “Who are you people?akauliza waziri mkuu baada ya kuzinduka na kutoka usingizini.Alijaribu kujitikisa lakini alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma “Nifungueni mikono yangu ng’ombe nyie.!! akafoka waziri mkuu. “Mimi ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hiki mnachokifanya ni kosa kubwa mno na ninawaambia wazi kwamba adhabu yake ni kubwa mno.This is a kidnap!! Akaendelea kufoka waziri mkuu lakini hakujibiwa.Devotha akachukua gundi ya nailoni na kuanza kuwabandika midomoni ili wasiweze kupiga kelele Walichukua muda mfupi kufika katika makazi yao kwani gari lile la wagonjwa liliachiwa njia ya kupita barabarani.Baada ya kuwasili wote wakashushwa wakaingizwa ndani na kujazwa katika chumba kimoja “Guys natamani niwashukuru kwa kazi hii kubwa lakini bado tunayo kazi ya kufanya mbele yetu.We need to find the girsl” akasema Mathew na kuwaeleza kile alichokipata katika simu ya waziri mkuu.Akampatia simu ile Ruby na kumtaka atafute mahala ambako Nazil alikuwepo wakati akipiga ile simu.Haraka haraka Ruby akaanza kucheza na kompyuta ili kufahamu mahala alipo Nazil “Tukifanikiwa kupata mahala alipo Nazil hapo ndipo walipo wasichana waliotekwa” akasema Mathew na wote wakawa kmya wakimsubiri Ruby awape jibu.Baada ya dakika tatu Ruby akasema “Nimempata.Alikuwa hapa wakati akipiga simu” akasema Ruby na kuwaonyesha katika ramani mahala alipokuwa Nazil wakati akimpigia simu waziri mkuu. “Thank you Ruby.Guys mahala hapo alipo Naziri ndipo walipo watoto.Tunakwenda kuwaokoa watoto lakini tutahitaji msaada.Hatuwezi peke yetu.Hawa watu lazima watakuwa wamejiandaa vilivyo kiulinzi kwani wanajua nguvu kubwa inatumika kuwasaka watoto wale.Austin we need your team” akasema Mathew “Nakubaliana nawe Mathew kwamba tunahitaji msaada lakini kwa sasa mimi si kiongozi tena wa kikosi kile baada ya kupuuza agizo la Rais” “Usihofu I’m going to talk to president” “President?! Devotha akashangaa “Yes” “He betrayed us.Hatuwezi kumuamini tena” “Tunahitaji timu ya watu kutusaidia kupambana na magaidi ni yeye mwenye uwezo wa kutusaidia kupata timu tunayoihitaji” akasema Mathew kisha akachukua simu yake ya zamani akaiwasha na kumpigia Rais. “What do you want?akauliza Dr Evans kwa ukali baada ya kupokea simu “Mheshimiwa Rais nahitaji msaada wako” “You go to hell Mathew !! Mambie na Aus………….” “Mheshimiwa Rais naomba unisikilize kwanza.Tayari tumefahamu mahala walipo watoto waliotekwa” akasema Austin na Dr Evans akasikika akishusha pumzi “Are you sure?akauliza Dr Evans “Ndiyo mheshimiwa Rais tuna uhakika” “Ni wapi? “Mheshimiwa Rais ninahitaji kikosi cha operesheni maalum kitusaidie tuweze kuwakomboa watoto hao.Mahala walipo tunaamini magaidi watakuwa wamejihami vilivyo kwa silaha hivyo tunahitaji nguvu ya kutosha” “Mathew I don’t kno what to say …” akasema Dr Evans na kuvuta pumzi ndefu “Mathew niko tayari kuwasaidia kila mnachokihitaji.Uko na Austin hapo karibu?Nipe nizungumze naye”akasema Dr Evans na Mathew akampa Austin simu “Mheshimiwa Rais” akasema Austin “Austin nataka utumie kikosi chako katika kuwakomboa wasichana hao waliotekwa.Tusameheane katika yale yaliyotokea” akasema Dr Evans “Nashukuru mheshimiwa Rais” akasema Austin na kumrejeshea simu Mathew “Mathew nimekwisha mpa maelekezo Austin mtatumia kikosi chake na hakikisheni mmewakomboa wasichana wote waliotekwa” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa Rais”akasema Mathew na kukata simu.Bila kupoteza muda Austin akapiga simu kikosini na kutoa maelekezo wajiandae.Kulitokea mabishano kidogo kati yake na msaidizi wake hadi pale alipomthibitishia kwamba lile ni agizo la Rais. Ofisi ya muda ililazimu kuhama kutoka katika nyumba ile na kurejea katika kambi ya kikosi cha operesheni maalum.Waziri mkuu na wenzake wakapaiwa katika gari.Edger akapakiwa katka buti ya gari la Devotha kisha mke wa balozi na Zulfa aliyekuwa analindwa na Gosu Gosu wakaingia katika gari la Devotha wakaondoka mahala pale kuelekea katika kambi ya kikosi cha operesheni maalum.
“Mike team,Oscar team tunakaribia kufika sehemu lengwa.Mmefika wapi ? Mathew Mulumbi akauliza wakiwa ndani ya gari wakikaribia kufika eneo la magetini wakiifuata nyumba ambayo wanaamini ndiko waliko watoto waliotekwa nyara.Ulikuwa ni msafara wa gari tatu ambazo ndani yake zilijaza wanajeshi kutoka kikosi cha jeshi cha operesheni maalum “Oscar team,Mike team tumekaribia sana kufika sehemu hiyo ndani ya dakika chache tutakuwa tumefika hapo” akasema Austin ambaye alikuwa anaongoza kikosi kilichokuwa katika helkopta “Main tower what’s your status?akauliza Mathew “Kwa kuhesabu ninawaona watu zaidi ya kumi wakiwa nje ya nyumba hiyo wakiwa na bunduki.Saba wako upande wa mbele ya nyumba na wengine wako upande wa nyuma”akasema kamanda kutoka katika ofisi kuu ya kuongozea operesheni ambao walikuwa wanafuatilia kinachoendelea kupitia satelaiti maalum Ndani ya nyumba ile katika chumba ambacho magaidi walikuwa wanatumia kurushia matangazo yao mtandaoni namna wanavyowachinja wanafunzi waliowateka,mwanafunzi mmoja alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma akiwa wamepigishwa magoti.Fahad akiwa amevaa kofia ya kumziba asionekane sura akajitokeza na kamera ikawashwa “Ndugu watanzania nimekuja tena.Bado Rais wenu amegoma kutekeleza matakwa yetu,ameendelea kuwa na kiburi na sisi hatuna namna nyingine zaidi ya kuendelea kuwachinja watoto tuliowateka.Hapa ninaye mtoto wa waziri mkuu ambaye naye tutamchinja kama tulivyofanya kwa wengine.Niliwapa muda Rais na serikali yake ili wamuokoe mtoto wa kiongozi mwenzao lakini wamepuuza hivyo tunakwenda kuondoa kichwa cha mtoto huyu.Baada ya saa moja tutaongeza idadi hadi kufika saa sita usiku wa leo lazima watoto wote tuliowateka wawe wamemalizika na hapo tutaufungua ukurasa mpya.Tayari tumekwisha jipanga na tutaigeuza Tanzania nyekundu kwa damu hadi pal…….” Akanyamaza baada ya kusikika mtikisiko kutokana na milio ya helkopta. “Nini hicho?akauliza akiwa na wasiwasi “Kata kamera!! Akasema kwa sauti kubwa halafu akavua kofia Milio ya risasi ilianza kusikika nje ya ile nyumba. Helkopta mbili kutoka katika kikosi anachokiongoza Austin zilifika katika nyumba ile na kuanza kushambulia kwa risasi walinzi waliokuwa nje na silaha wakilinda.Wakati mashambulizi yakiendelea wanajeshi wengine walikuwa wanashuka toka ndani ya helkopta kwa kamba.Risasi ya kwanza ilipolia iliwasha taa ya kijani kwa akina Mathew wakashuka magarini na mmoja akapanda geti hadi ndani akalifungua wakaingia. Milio ile ya helkopta iliwastua waliokuwa ndani wakaanza kutoka wakikimbia kuja kushuhudia kinachoendelea nje lakini walikutana na timu ya akina Mathew ambao walikuwa wanaelekea ndani na kuwamaliza mmoja mmoja “Nazil tumevamiwa.Tayari wanafahamu mahala tulipo.You know what to do” Fahad akamwambia Nazil aliyeonekana kuchanganyikiwa. “Wewe na wewe nendeni mkawalete watoto wote hapa we’ll die with them !! akasema Fahad lakini wale jamaa aliowatuma hawakuweza kuinua hata hatua moja kwani tayari mvua ya risasi ilianza kunyesha.Nazil aliyepigwa risasi ya bega la kushoto akachomoa bomu kutoka katika kizibao alichovaa na kung’oa funguo kisha akalirusha. “Gurunetiiiii !! Mathew akawajulisha wenzake na kufanya kitendo ambacho wote hawakukitarajia.Aliitupa chini bunduki yake akaruka kulidaka bomu lile kabla halijagusa chini kisha akasimama na kutoka mbio mle ndani akaenda katika dirisha akapiga ngumi kioo na kulitupa bomu lile nje likalipuka akasimama akihema huku akivuja jasho mwili mzima.Kilikuwa ni kitendo cha hatari sana. Baada ya kunusurika kulipukiwa na bomu,Gosu Gosu akaliendea panga ambalo magaidi walikuwa wanalitumia kuwakatia vichwa wasichana waliowateka akamfuata Nazil “Mliwachinja watoto wetu kama kuku sasa ni zamu yenu ! akasema kwa hasira na kuliinua panga juu na kulishusha kwa nguvu akatenganisha kichwa cha Nazil na kiwili wili. “Haya ndiyomalipo ya uovu wenu kenge nyie !! Mvua ya risasi ilikoma baada ya magaidi wote kuanguka chini.Walikuwa wamechakazwa vibaya sana kwa risasi. Tayari nyumba yote ilikuwa imedhibitiwa.Mathew akatoa picha mfukoni akampatia Gosu Gosu “Find this man” akasema Mathew na mara akaingia mmoja wa makamanda “Mr Mathew Mulumbi tumezunguka nyumba yote na hakuna tena gaidi mwingine.Wote wamejeruhiwa au kuuawa.Habari njema ni kwamba tayari tumewapata wasichana wote waliobaki waliokuwa wanashikiliwa mateka pamojana walimu wao” “Ahsante sana Kamanda.Good job” akasema Mathew “Mike team,this is Oscar team.Tumefanikiwa kuwapata wasichana waliotekwa.Ninarudia tumewapata wasichana waliotekwa” akasema Mathew akiwajulisha akina Austin halafu akachukua simu akampigia Rais Dr Evans “Mathew nini kinaendelea?akauliza Dr Evans akiwa na wasi wasi “Misheni imekamilika mheshimiwa Rais na tumewapata wasichana wote waliotekwa pamoja na miili mine ya wale waliouawa” “Ouh Mungu wangu ! akasema Dr Evans na kukaa kimya kwa muda “Mheshimiwa Rais” akaita Mathew “Mathew nimeishiwa maneno.Sijui niseme nini” “Mheshimiwa Rais tunawachukua watoto hawa na kuwapeleka katika kambi ya kikosi cha operesheni maalum ambako watapumzika kabla ya ratiba nyingine kuendelea.Mr President I need to see you.Kuna mambo mazito ambayo unatakiwa uyafahamu.Vile vile jeshi la polisi wanatakiwa kufika hapa kuchukua miili hii ya magaidi na kuifanyia uchunguzi nyumba hii” akasema Mathew “Mathew mtakaporejea kambini nifahamisheni ili niweze kufika huko mara moja kuja kuwapa pole watoto hao.Kwa sasa natakiwa kulihutubia taifa ili kuwajulisha kwamba watoto waliotekwa na magaidi wamekombolewa ili kutuliza hali ya wasiwasi mkubwa iliyotanda” akasema Rais na kuagana na Mathew. “Mathew Mulumbi ahsante sana.Umefanya kitendo cha kishujaa mno kudaka bomu lile.Umetuokoa wote ndani ya chumba vinginevyo tungekufa wote” akasema mmoja wa wanajeshi wa kikosi kile na kumpa mkono Mathew kumpongeza. “Mathew ! akaita Gosu Gosu “Nimempata yule mtu wetu ni huyu hapa lakini amepigwa risasi amefariki dunia” akasema Gosu Gosu na kumpatia Mathew simu ya Yule jamaa. “We needed him alive.Lakini hakuna ubaya kwani tumefanikiwa kumfikia na kumuua” akasema Mathew “Mathew Yule mtu aliyerusha bomu ukalidaka ni Yule ambaye Devotha alimuona katika maandamano na akamtilia shaka.Ni gaidi wa muda mrefu na kwa mujibu wa Devotha alikuwa anajiita mtu asiyeonekana lakini leo ameonekana na umekuwa ni mwisho wake” “Good job Gosu Gosu”akasema Mathew Wasichana wale walipakiwa katika helkopta na wengine katika magari kisha wakaondoka kurejea kambini.
Matangazo katika runinga na redio ya taifa yalikatishwa ghafla na wimbo wa taifa kupigwa.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akajitokeza “Ndugu watanzania wenzangu,nimejitokeza kwenu muda huu kuwapeni taarifa kwamba muda mfupi uliopita,vijana wetu hodari wakishirikiana na kikosi cha jeshi cha operesheni maalum wamefanikiwa kuvamia nyumba ambayo magaidi waliitumia kuwaficha wasichana waliowateka na kufanya mauaji ya kikatili.Katika uvamizi huo vijana wetu shupavu wamefanikiwa kuwaua magaidi wote na kuwakomboa wasichana sitini na mbili na walimu wao watatu pia miili minne ya wasichana wengine waliouawa na magaidi imepatikana.Ndugu watanzania huu ni ushindi mkubwa tumeupata dhidi ya magaidi hawa waliojaribu kutaka kuvuruga amani yetu Ninawahakikishia kwamba tutausaka mtandao wote wa magaidi hapa nchini na kumkamata hadi gaidi wa mwisho.Ninawaomba tuendelee kuwa watulivu wakati vyombo husika vikiendelea kutekeleza majukumu yake.Tutaendelea kuwajulisha kila kinachoendelea katika sakata hili. Kwa wazazi ambao watoto wao wamekombolewa mtajulishwa wakati gani watoto wenu watarejeshwa kwenu na kwa wale ambao watoto wao wameuawa serikali itagharamia mazishi yao.Mtaendelea kupewa taarifa zaidi za kile kinachoendelea Mungu ibariki Tanzania Ahsanteni kwa kunisikiliza Ilikuwa ni hotuba fupi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akilijulisha taifa kuhusiana na kukombolewa kwa wasichana waliotekwa nyara na magaidi. “Sijui nitawatazama vipi vijana wale machoni kwa jambo nililowafanyia la kuwageuka na kutaka kumkabidhi Edger Kaka kwa magaidi.Sikuwa nimepanga kufanya hivyo bali yalikuwa ni mawazo ya waziri mkuu ambayo niliona ni mazuri na kuamua kuyafuata.Nilikosea sana kumshirikisha waziri mkuu jambo hili kubwa halafu akanigeuka na kuungana na waandamanaji.Mpaka sasa sifahamu nini hasa ilikuwa dhamira yake ya kwa kitendo kile alichokifanya.Kwa alichokifanya ameonyesha kutokuiamini serikali ambayo yeye ni sehemu yake na amepoteza sifa za kuwa waziri mkuu.Ngoja kwanza nikakutane na watoto wale waliokombolewa nataka nijue kuhusu Olivia na Coletha” akawaza Dr Evans na kuelekeza helkopta ya Rais iandaliwe
Kikosi kilichokwenda kuwakomboa wasichana waliotekwa kilirejea kambini na wasichana wote wakakusanywa katika bwalo la chakula ambako walianza kupewa huduma mbali za matibabu kwa wale waliokuwa na majeraha na vile vile wakapewa chakula chepesi Wakati wakiendelea kupongezana kwa ushindi ule mkubwa helkopta ya Rais ikaonekana angani na ikaelekezwa sehemu ya kutua.Mara tu Rais alipotua akapokelewa na Austin January mkuu wa kikosi kile na kuelekea moja kwa moja ofisini kwake “Karibu sana mheshimiwa Rais” akasema Austin “Ahsante sana Austin.Mathew Mulumbi yuko wapi? “Alikuwa anaangaliwa na daktari amepata majeraha madogo” “Please call him.I need to see you both” akasema Dr Evans na Austin akapiga simu katika hospitali ya kambi na hazikupita dakika tano Mathew akafika “Mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Mathew na Austin sipati maneno mazuri ya kuwaambia lakini kabla sijasema ahsante nataka niwaombe sana msamaha kwa yale yote niliyowatendea.Nitawaeleza kila kitu pale tutakapokuwa tumepata muda lakini toka ndani ya moyo wangu I’m deeply sorry” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais yale yamekwisha pita.Sisi ni binadamu na wote tunakosea.Kwa sasa tutazame ya mbele.Bado tunayo kazi ya kufanya.Hatujafika mwisho” akasema Mathew na kumueleza Rais namna operesheni ile ilivyofanyika hadi wakafanikiwa kuwakomboa mateka.Austin na Mathew wakamuongoza Rais kuelekea katika bwalo la chakula kuonana na wasichana wale waliokombolewa.Baada ya kuwasalimu akaenda pia katika chumba cha maiti pale kambini na kuiona miili ya wasichana wale waliouawa na magaidi kisha akawageukia akina Mathew “Kazi nzuri sana vijana.Ahsanteni kwa kuwafyekelea mbali makatili hawa ambao wamekatisha uhai wa wasichana wadogo wasio na hatia” “Mheshimiwa Rais kuna jambo lingine ambalo unatakiwa ulishuhudie kwa macho yako” akasema Mathew na kumuongoza Dr Evans hadi katika chumba walimowahifadhi waziri mkuu na wenzake. “Huyu ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Anafanya nini hapa? Akauliza Dr Evans alipatwa na mshangao mkubwa “Mheshimiwa Rais nchi hii imebarikiwa kupata viongozi wazuri lakini wapo viongozi wachache ambao wako tayari kufanya chochote ili kutimiza matakwa yao ya kisiasa.Mbele yako ni waziri mkuu wa Tanzania ambaye tumemkuta katika mkutano na watu wa IS.Mpango huu wa kuwateka wanafunzi umepangwa na magaidi pamoja na huyu waziri mkuu na tunao ushahidi wote kupitia simu yake ambayo amekuwa akiitumia kuwasiliana na magaidi.Mmoja wa mag…………..” Mathew hakumaliza kutoa maelezo kwa Rais ghafla Dr Evans akachomoka na kumfuata waziri mkuu akaanza kumporomoshea makonde mazito.Mathew na Austin wakamshika “Sasa nimepata picha.Huyu mtu ndiye aliyenipa wazo la kumkabidhi Edger Kaka kwa magaidi.Kumbe ni mwenzao.Kwa nini sikulitambuahili mapema?Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu sikujua kama niko na nyoka mwenye sumu !! akasema DrEvans na kutaka kumfuata tena kwenda kumuadhibu lakini akina Mathew wakamzuia “Imetosha mheshimiwa Rais ataadhibiwa na sheria” akasema Mathew “Kwanza alikuwa Edger Kaka na sasa ni kiongozi mkubwa kabisa naye anashirikiana na magaidi.Nani nimuamini? Akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais hawa wengine wote unaowaona humu ni washirika wa mtandao wa IS.Tunaamini hawa ni baadhi tu lazima wapo wengine kwani inaonekana tayari IS wamekwisha jenga mtandao mkubwa hapa nchini.Vyombo vinavyohusika vitachunguza na kuubaini mtandao wote wa IS hapa nchini.Tumechukua simu zao kompyuta na kila kifaa chao cha mawasiliano tutavikabidhi kwa chombo kitakachokuwa kinalishughulikia suala hili” akasema Mathew kisha akamchukua Rais na kumpeleka katika chumba kingine alimokuwamo Edger Kaka. “Mhshimiwa Rais huyu ni Edger Kaka”akasema Mathew “Hallow Edger” akasema Dr Evans “Hello” “Nimefurahi kukuona tena” “Me too Mr President” Hakukuwa na maongezi ndani ya kile chumba Mathew akamchukua wakaenda katika hospitali ya kikosi akamuonyesha Zulfa ambaye naye ni mfuasi wa IS halafu akampeleka kwa mke wa balozi wa Israel “Mama ahsante kwa uvumilivu wako kwa muda wote uliokaa na hawa vijana.Jioni ya leo utarejeshwa kwako lakini kinachotakiwa ni kufuata masharti utakayopewa” akasema Dr Evans wakatoka “Vijana mmefanya kazi kubwa sana ambayo sijui niwalipe nini.Hata hivyo nataka kufahamu mipango ya kuwatafuta akina Olivia na Coletha” “Kuna mtu mmoja ambaye amekuwa akihusika na utekaji anaitwa Fahad ameuawa katika uvamizi na kama tungeweza kumpata huyo angetusaidia kufahamu walipo Olivia na Coletha.Itatulazimu kuzungumza tena na Edger Kaka ili atusaidie kutupa taarifa zilizosaidia kuwapata wasichana hawa na atatusaidia pia kujua mahala walipo Coletha na Olivia.” akasema Mathew na kumueleza Rais kile ambacho walikuwa wamekubaliana na Edger Kaka kisha wakaelekea katika sehemu ya kupumzika viongozi na Edger Kaka akaletwa mbele ya Rais “Hallow Edger.Karibu tena Dar es salaam karibu tena Tanzania.Sikutegemea kabisa kama tungeweza kuonana lakini imetokea tumekutana” “Ahsante mheshimiwa Rais” akasema Edger “Edger tayari tunafahamu kila kitu kuhusu wewe na ndiyo maana tukafanya kila juhudi ili tuweze kukupata na sasa ni wakati wa mimi na wewe kuzungumza” akasema Dr Evans na kunyamaza kidogo halafu akaendelea “Nilimpa ruhusa Mathew Mulumbi ya kuzungumza nawe kwa niaba yangu na umemtajia vitu ambavyo unavihitaji ili kuweza kutupa taarifa tunazozihitaji sana kuhusu mtandao wa kikundi cha IS hapa Tanzania.Mathew amenikabidhi orodha ya vitu ulivyoviorodhesha tukupatie na tayari vimekwisha anza kuvifanyia kazi mfano nyumba tayari umeipata na hivi vingine vinaendelea kufanyiwa kazi na utavipata vyote.Ninakupa nafasi nyingine ya kuanza maisha mapya.Ningeweza kukufunga mahala katika shimo ukaishi huko kwa miaka yako yote au ningeamua kukuteketeza kabisa kwani kila mtu anafahamu umekwisha kufa lakini sitaki kufanya hivyo nataka nikupe nafasi nyingine ya kufurahia maisha ila fursa hii haitakuja hivi hivi you’ll have to pay me something.Nataka unipe taarifa za mahala walipo Coletha na Olivia Themba.Nataka kuwakomboa ili nimchukue mwanangu na wewe umchukue Olivia mkaishi maisha mazuri yenye amani mahala ulikochagua kwenda kuishi” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais ninashukuru kwanza kwa kuja kuniona na kunipa nafasi nyingine ya kwenda kuanza maisha yangu.Natamani sana ningekuwa na msaada zaidi lakini nimekuwa ndani ya chumba cha giza kwa miaka mitatu na sijui chochote kinachoendelea huku nje.Sifahamu mahala walipo mwanao na Olivia.I’m sorry Mr President” akasema Edger “Edger hii ni nafasi ya mwisho ya kutengeneza maisha yako.Ukishindwa kuitumia ni hiyari yako lakini baada ya hapa hakutakuwa na majadiliano tena kwani utapelekwa mahala ambako utateseka hadi siku yako ya mwisho ya maisha hapa duniani.Kwa nini ukubali mateso Edger?Hutaki kuishi maisha mazuri sehemu salama ambako hakuna anayekufahamu huku ukiwa na mwanamke unayempenda Olivia Themba? Watu wako wa IS hawana kumbu kumbu tena nawe wamekwisha kusahau ni wakati wako na wewe kuwasahau ili ukaendelee na maisha yako hawana tena msaada kwako.Tumia vyema fursa hii uliyoipata kwani ukiamua kuiacha utaijutia kwa maisha yako yote” akasema Dr Evans “Edger ulikuwa mbunge kijana mwenye maisha marefu sana ya kisiasa na sote tuliamini kwamba utakuwa kiongozi mkubwa mbeleni na wengi walikwisha anza kukutabiria mambo makubwa,kwa nini ukaamua kujiunga na magaidi hao wasio na huruma hata chembe? Nini hasa ulikuwa unakipata kutoka kwao? Sitaki kulizungumzia sana hilo ninaliweka pembeni itabaki kuwa siri yetu sisi tuliomo humu ndani ya hiki chumba ninachotaka nisaidie niweze kuwapata mwanangu na Olivia Themba” akasema Dr Evans na Edger akainamisha kichwa akafikiri kwa muda halafu akaomba apewe kalamu na karatasi akaandika namba Fulani na kumpa Rais “Sina hakika kama bado zinatumika lakini jaribu kupiga namba hizo.Ukiulizwa jina watajie namba W0023S12 kisha utazungumza na Habiba Jawad.Yawezekana yeye anaweza akawa na taarifa za mahala walipo Coletha na Olivia” “Ni nani huyu Habiba Jawad?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais piga namba hizo na pengine unaweza ukafahamu mahala walpowatu wako.Sina maelezo zaidi” akasema Edger “Mheshimiwa Rais habiba Jawad ni mfadhili mkuu wa kikundi cha IS na ana ukaribu mkubwa na Edger hata alipokuw hospitali Israel alikwenda kumtembelea nay eye ndiye sababu ya Mossad kumteka Edger” akasema Mathew “Austin waambie watu wako wafuatilie namba hii aliyotoa Edger tufahamu mahala alipo huyu Habiba.”Dr Evans akamwambia Austin lakini Edger akaingilia kati “You can’t trace that number.Watajua mnawafuatilia.Wana teknolojia kubwa ya kuficha mawasiliano yao.Ukijaribu kufuatilia hiyo namba unaweza ukawakosa watu wako” akasema Edger na Dr Evans akamtazama Mathew “Do it Mr President” akasema Mathew na Dr Evans akapiga zile namba simu ikaanza kuita.Kama alivyokuwa amesema Edger simu ilipokelewa na Dr Evans akaulizwa jina lake akataja namba zile alizopewa na baada ya muda ikasikika sauti nyingine ya mwanamke “Hallow Seif” “Hallow.Unazungumza na Dr Evans Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Nazungumza na Habiba Jawad? akauliza Dr Evans na ukimya ukapita “Hallow! Akaita DrEvans “Naamini Edger Kaka ndiye aliyekupatia namba hizi unipigie.Ninaomba umuachie haraka sana ama sivyo kutatokea umwagikaji mkubwa sana wa damu hapo Tanz……..” akasema Habiba na Dr Evans akamkatisha “Hakuna mnachoweza kukifanya tena Habiba Jawad,sehemu kubwa ya mtandao wenu tumewakamata na wengine wameuawa na tunaendelea kuwafuatilia wengine waliosalia.Tunaye hadi waziri mkuu ambaye mlikuwa mnashirikiana naye” akasema DrEvans na ukimya mfupi ukapita “Najua hujanipigia simu kunieleza namna mlivyofanya mauaji.Unataka nini?Habiba Jawad akauliza “Habiba pamoja na haya yote yaliyotokea lakini bado mimi na wewe tunaweza kuzungumza tukafikia makubaliano” “Nini unataka kukubaliana nami?akauliza Habiba “Watu wako waliwateka watu wangu wawili ambao ninawahitaji” “Waliwateka watu wako baada ya wewe kugoma kutekeleza matakwa yetu ya kutukabidhi mtu wetu.Je uko tayari sasa kutukabidhi mtu wetu na sisi tukukabidhi watu wako? “Habiba niko tayari kuwapa kile mnachokitaka lakini na mimi mnirejeshee watu wangu wawili mnaowashikilia” akasema Dr Evans na wote mle ndani wakapatwa na mshangao “Hatimaye umekubali kumuachia Edger Kaka ! akasema Habiba “Tutafanya mabadilishano.Nitawapa mtu wenu na ninyi mtanipa watu wangu.No more blood.Mko tayari kwa sharti hilo? Akauliza Dr Evans “Sina tatizo na hilo.Kama ungekubali toka mwanzo kufanya makubaliano nasi haya yote yaliyotokea kamwe yasingetokea” akasema Habiba “Nataka kujua namna tutakavyofanya mabadilishano” “Ndugu Rais kwanza naomba ufahamu kwamba mwanao na Olivia Themba hawako Tanzania” “Hawako Tanzania? DrEvans akastuka “Ndiyo ndugu Rais.Hawapo Tanzania.Baada ya saa moja nitakupigia kukujulisha namna tutakavyofanya mabadilishano na mahala yatakapofanyika.Maelekezo yatakayotolewa yafuatwe tafadhali ama ukijaribu mchezo wowote wa kijinga utawakosa watu wako” akasema Habiba na kukata simu “Edger ninakurejesha kwa watu wako ili niweze kuwapata watu wangu lakini yale tuliyokubaliana yataendelea kubaki vile vile na utakabidhiwa vitu vingine vyote vilivyobaki” “Vipi kuhusu Olivia? Edger akauliza “Baada ya kumpata Olivia tutamrejesha kwanza nyumbani halafu baadae atawasiliana nawe mtapanga namna ya kukutana.Huu ni wakati wa kutengeneza amani hatutaki tena damu imwagike na jambo hili litabaki kuwa siri yetu sisi tuliomo humu ila ninakuonya ukiondoka hapa usithubutu kukanyaga mguu Tanzania.Umenielewa? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” akasema Dr Evans na kutoka mle ndani akiwa ameongozana na akina Mathew “Mheshimiwa Rais una hakika unataka kumrejesha Edger kwa magaidi?akauliza Mathew “Once you get Coletha and Olivia,make sure you kill that Zombie.Anzeni kujiandaa kwa hilo.We can’t let him go” akasema Dr Evans
Saa sita za usiku katika mpaka wa Tanzania na Kenya helkopta mbili za kikosi cha jeshi cha operesheni maalum zikatua upande wa Tanzania mita kadhaa kutoka mahala ambako mabadilishano yangefanyika.Ni helkopta ambazo hazina mlio na hazionekani katika rada.Kikosi cha wanajeshi kumi na mbili waliojihami kwa silaha wakashuka na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea eneo ambako mabadilishano yangefanyika.Kikosi hiki kiliongozwa na Austin January “Mike team tunatoa taarifa tumekwisha tua na sasa tunaelekea eneo la tukio”Austin akatoa taarifa kwa ofisi yao Dar es salaam waliokuwa wanawaongoza katika operesheni ile “Tumewapata Mike team,Oscar team wako njiani wanaelekea eneo la tukio ndani ya dakika kumi watakuwa wamefika”akasema kamanda Linus kutoka ofisi kuu Dar es salaam Wakati wakikaribia eneo la tukio wakapokea taarifa kutoka ofisi kuu “Mike team kuna gari tatu zinawasili eneo la tukio” “Unaweza kuhesabu kuna watu wangapi?Austin akauliza “Hawajashuka katika magari nitawajulisha watakapoanza kushuka” akasema kamanda Linus kutoka ofisi kuu Magari matatu yaliwasili eneo la tukio na baada ya dakika tatu wakashuka watu wanne waliojifunga vitambaa vichwani wakiwa na bunduki nzito.Wakashuka tena watu wengine kumi na tano wakajipanga mstari wakiwa na bunduki zao za kivita.Eneo lilikuwa na giza na mwangaza ulitoka katika taa za magari yaliyowashwa. Austin na kikosi chake walifika eneo la mabadilishano.Wote walikuwa wamevaa miwani ya kuwasaida kuona usiku hivyo waliweza kuwaona wale jamaa walivyokuwa wamejipanga. “Mike team we’re in position” akasema Austin akiwajulisha Dar es salaam kwamba wako tayari Dakika chache baadae helkopta ikasikika ikielekea eneo lile. “Mike team,Oscar team wanakaribia kufika eneo la tukio” Austin akajulishwa.Taa kubwa yenye mwangaza mkali kutoka katika helkopta ilimulika chini na likapatikana eneo zuri la kutua na helkopta ile ikatua wakashuka wanajeshi kumi waliokuwa na silaha nzito baada ya kushusha katika helkopta akina Mathew wakajipanga vizuri kisha Mathew akiwa na mwanajeshi mmoja wakaanza kupiga hatua taratibu kuwafuata wale jamaa na walipofika katikati wakasimama.Watu wawili kutoka upande wa Kenya wakaanza kupiga hatua kuwafuata akina Mathew “Karibu Kenya Mathew Mulumbi” akasema kiongozi wa kile kikundi “Thank you Rashid.Nahitaji kuwaona watu wangu nijiridhishe ! akasema Mathew kwa sauti kubwa kutokana na muungurumo wa helkopta “Only you.”akasema Rashid “Fine” akasema Mathew na Rashid akamuongoza hadi katika mojawapo ya gari mlango ukafunguliwa na tochi ikamulikwa ndani Mathew akawashuhudia Coletha na Olivia wakiwa.Olivia hakuweza kumtambua Mathew kutokana na mavazi ya kijeshi aliyokuwa ameyavaa “Nataka kumuona wa kwangu” akasema Rashid na Mathew akamuongoza hadi katika helkopta akamuona Edger Kaka na kuthibitisha ni yeye. “Now let’s make the exchange.Waruhusu watu wangu watembee na mimi nitamuachia Edger Kaka.Hawezi kutembea hivyo mtu wangu mmoja atamsukuma katika kiti kumleta kwenu.Wakati watu wangu wanakuja na mtu wako naye atakuwa analetwa.Umenielewa?akauli za Mathew “Nimekuelewa” “Good.Nitakapopiga alama nyekundu juu mabadilishano yaanze haraka” akasema Mathew na Rashid akarejea upande wao.Edger Kaka akatolewa katika helkopta na kuwekwa tayari.Taa kubwa ikawashwa ili kulifanya eneo lile liwe na mwanga.Baada ya kila kitu kukamilika Mathew akapiga alama nyekundu juu kuashiria mabadilishano kuanza “Mike team stand by ! Austin akawajulisha watu wake.Taratbu Edger Kaka aliyekuwa katika kiti cha magurudumu akaanza kusukumwa na wakati huo huo Olivia na Coletha wakaanza kutembea taratibu kuelekea upande wa Tanzania waliko akina Mathew.Sehemu zote mbili watu walikuwa makini wamejiandaa kama kungetokea aina yoyote ya shambulio_Olivia alikutana kati kati na Edger Kaka “Olivia ! akasema Edger kaka na Olivia akastuka sana akataka kumfuata Edger lakini Yule mwanajeshi aliyekuwa anamsukuma katika kiti akamzuia.Olivia alikaribia sana kufika mahala walipo akina Mathew. “C’mon Olivia hurry up” akasema Mathew kwa sauti ndogo. Kabla Olivia hajawafikia akina Mathew ukatokea mlipuko wa bomu katikati ya walipokuwa akina Mathew na wale watu wa IS na kuzua taharuki kubwa kisha ikafuata mivumo ya risasi.Mathew alikimbia na kuwarukia Olivia na Coletha akawaangusha chini huku Risasi nyingi zikipigwa. “Mike team,Mike team there is an ambush we need help !! akasema Mathew aliyekuwa amelala chini akiwakinga akina Coletha “I repeat there is an ambush we need help !! akasema na kuwainua akina Olivia akawashika mikono wakaanza kukimbia kuelekea ilipo helkopta yao.Kabla hawajaifikia ukatokea mlipuko helkopta ikasambaratika ililipuliwa kwa bomu.Ilimlazimu Mathew kusimama ghafla baada ya mlipuko ule kutokea na mara akatoa mgumo baada ya risasi mbili kupiga bega lale la kushoto.Aligeuka ili kutazama nyuma lakini akapigwa risasi ya mguu akaanguka chini “Olivia take Coletha Run !! akasema Mathew ambaye aliiokota bunduki yake akaanza kupiga risasi hovyohovyo ili kuwakinga akina Olivia. “Aaagghhhhhh ! akapiga ukelele na kuangusha bunduki chini baada ya risasi kupiga mkono aliokuwa ameshika bunduki.Risasi ziliendelea kuvuma eneo lile na mara Mathew akamulikwa kwa tochi yenye mwanga mkali sana.Alikuwa amezungukwa na mitutu saba ya bunduki kutoka kwa watu waliofunika nyuso zao na kuacha macho.Haraka haraka akafungwa pingu na kunyanyuliwa akabebwa na kupelekwa sehemu Fulani kulikokuwa na pango .Ndani ya pango hilo kulikuwa na taa zenye mwanga mkali kulikuwa pia na vitanda vinne na vifaa mbalimbali vya matibabu.Inaonekana watu wale walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya matibabu endapo itatokea watu wao wakapata majeraha.Haraka haraka Mathew akaanza kuhudumiwa ili kuzuia damu kutoka kwa wingi.Mara wakaingia tena watu sita wakiwa wamefunika nyuso zao na walimbeba mtu ambaye walimtupa katika kitanda kilichokuwa karibu na Mathew.Mathew akageuza shingo kumtazama alikuwa ni Edger Kaka.Mathew akastuka akataka kumsemesha lakini akachomwa sindano ya usingizi taratibu nguvu ya macho ikaanza kupunguza “Edger Kaa..Edger..Edg…E..E…..” akashindwa kuendelea kutamka akalala. Hatimaye milio ya risasi na milipuko vilivyodumu kwa dakika kumi na tano vikakoma.Austin aliyekuwa amejificha mahala akiwa na Olivia na Coletha akachukua redio yake na kuanza kuita “Mike team please respond ! akasema Eneo lote lilikuwa kimya kabisa.Austin alianza kuwatafuta watu wake kwa kutumia redio na akawapata wote isipokuwa watatu. “Oscar team please respond ! akasema lakini hakupokea taarifa zozote “I repeat Oscar team please respond ! akasema tena lakini hakupokea taarifa zozote.Akawaita Mike team wakakusanyika kisha wakaanza kuwatafuta wenzao.Timu yote ya Mathew hakuna aliyebaki hai wote walikuwa wamekufa.Miili ya watu wote waliokuwa wameuawa ikakusanywa sehemu moja. “Mathew Mulumbi is missing ! Lazima tumtafute tumpate.Hatuwezi kurejea nyumbani bila yeye.We have to bring him home dead or alive,let’s find him ! akasema Austin wakaingia tena kumtafuta Mathew na wakalazimika kufika hadi eneo la upande wa pili la Kenya walikokuwa IS ndipo walipogundua kwamba karibu magaidi wote walikuwa wameuawa. “Tumewamaliza wote.! Akasema mmoja wa Mike team “Si wote.Edger Kaka haoinekani hapa.Wengine wametoroka naye” akasema Austin wakaendelea kumtafuta Mathew Nje ya pango ambamo Mathew alikuwa anatibiwa kulikuwa na watu wawili wakiwa ndani ya gari lililofichwa kwa kufunikwa na matawi ya miti.Hili ni gari maalum la mawasiliano. “Sasa tunawarudishia mawasiliano yao” akasema mmoja wao na kubonyeza kitufe Fulani na baada ya muda mfupi redio ya Austin ikaanza kuita “Mike team..Mike? “Dar es salaam tunawapata vizuri.Tumejaribu kuwatafuta lakini hamkuwa mkipatikana.Nini kimetokea?akauliza Austin “Mawasiliano yalikatika ghafla na hata sisi hatukuweza kuwapata.Tuko hapa na Rais.Nini kinaendelea huko? “Kumefanyika shambulio la kustukiza,tumepoteza watu kumi na tatu na sisi tumefanikiwa kuua watu karibu wote wa IS lakini kuna wachache wametoweka na Edger Kaka” “Austin Rais hapa ninaongea.Shambulio hilo limetokeaje?Hamkuwa mmejiandaa?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais shambulio hilo limefanyika ghafla sana kabla hata makabidhiano hayajamalizika” “Lilikuwa shambulio kubwa kiasi gani hadi tukapoteza watu wengi kiasi hicho? “Mheshimiwa Rais lilikuwa shambulio kubwa na lenye kutumia nguvu nyingi.Tumepoteza pia helkpota moja” “Jesus Christ ! akasema Dr Evans “Vipi kuhusu watu wetu mmefanikiwa kuwaokoa? “Ndiyo mheshimiwa Rais,Coletha na Olivia wote tumewaokoa lakini Mathew Mulumbi hatujui yuko wapi.Tumetafua eneo lote hajapatikana.Tunahisi yawezekana amejificha au yuko mahali amepoteza fahamu tunaendelea kumtafuta” akasema Austin “Austin mnatakiwa haraka sana muondoke eneo hilo kwani tayari ni hatarishi.Watu hao walionusurika yawezekana wamekwenda kutoa taarifa kwa wenzao na muda wowote watarudi tena hapo wakiwa na nguvu kubwa” “With all due respect Mr President we can’t leave without Mathew.We need to find him and bring him back home dead or alive.We don’t leave anybody behind” akasema Austin “Austin you are coming home that’s an order from president.The mission is complete.We’ll find Mathew but for now I command you bring my people home! akasema DrEvans. “Sawa mheshimiwa Rais”akasema Austin na kuwajulisha marubani wa helkopta zao maalum ambazo zilikuwa mbali na eneo lile ambazo zilifika mara moja.Miili yote ikapakiwa wakaondoka kurejea Tanzania.Austin January alishindwa kujizuia machozi kumtoka walipoondoka eneo lile bila ya Mathew “Ni mara ya kwanza ninapoteza watu wengi kiasi hiki.Ni mara ya kwanza vile vile ninaondoka na kumuacha mtu nyuma.Yawezekana Rais akawa sahihi kwani kuendelea kukaa pale kungekuwa ni kuhatarisha maisha ya hawa walionusurika na yawezekana watu wale wangerejea na nguvu kubwa.Inaniumiza sana kumuacha Mathew” akawaza Austin “Lakini shambulio lile limetokeaje? Mbona tulifanya uhakiki wa eneo lile na kujiridhisha waliokuwepo ni wale watu wa IS?Mawasiliano kati yetuna ofisi yetu ya Dar es salaam yalikatika vipi? Akajiuliza Austin akakosa majibu “Watanzania wameondoka.Narudia tena watanzania wameondoka.Tumenasa mawasiliano wakizungumza na Rais wao akiwataka kurejea nyumbani haraka” akasema mmoja wa wale jamaa waliokuwa katika gari lenye mitambo ya mawasiliano akiwajulisha wenzao waliokuwa ndani ya pango ambao walianza kupongezana.Gari tano zikafika pale pangoni na watu wale wakaanza kuingia katika magari wakapakia kila kitu na kuondoka eneo lile. DAR ES SALAAM Devotha hakuwa na usingizi usiku huu.Alikuwa amejilaza katika kitanda chake kikubwa huku pembeni yake kukiwa na chupa ya mvinyo na glasi.Alikuwa amevaa gauni fupi la kulalia la rangi nyeupe.Macho yake aliyaelekeza katika runinga kubwa iliyokuwa ukutani akitazama filamu. Simu yake ikaita alikuwa ni Gosu Gosu. “Gosu Gosu,nilikuwa nasubiri sana simu yako.Are you coming? Akauliza Devotha huku akitabasamu “Devotha nimepigiwa simu na Ruby muda mfupi uliopita amenipa taarifa za kilichowatokea wenzetu usiku huu waliokwenda mpakani kufanya mabadilishano” “Nini kimetokea Papii?akauliza Devotha na kukaa kitandani “Kumetokea shambulio la kustukiza na tumepoteza watu kumi na tatu.Kibaya zaidi…” akanyamaza “Papii !! akaita Devotha “Mathew is missing.They left him ! “What ? They left him?Why? akauliza “Nimechanganyikiwa Devotha.Ninasubiri warejee ili niweze kujua nini kimetokea” akasema Gosu Gosu “Ahsante sana Papii kwa taarifa hii ya kusikitisha.Please keep me posted” akasema Devotha na kukata simu.Akaichukua simu yake ambayo huitumia kuwasiliana na Mossad akapiga na kutaja namba yake ya siri “Devotha nilikuwa najiandaa kukupigia simu kukushukuru kwa msaada wako mkubwa uliotusaidia.Tumefanikiwa kumpata tena Edger Kaka na vile vile Mathew Mulumbi kiongozi wa kuvamia ubalozi wetu wa Nairobi na kuua watu wetu.Watasafirishwa kwenda Israel ambako Mathew atapata adhabu stahiki kwa makosa aliyoyafanya.Amevamia balozi zetu akaua watu wetu,wengine wakiwa ni wa muhimu sana” akasema mkurugenzi wa Mossad “Ninachowaomba msimuue.Mpeni adhabu yoyote mnayoona anastahili lakini msimuue ni mtu muhimu sana na mwenye taarifa nyingi za kumuhusu Edger Kaka.Hata ninyi pia anaweza akawa na msaada kwenu” akasema Devotha “Ni mapema sana kusema adhabu atakayoipata Mathew Mulumbi lakini kwa mauaji aliyoyafanya sina hakika kama kutakuwa na msamaha.Nitaendelea kukujulisha.Jitahidi sana usigundulike” akasema mkurugenzi “Nitajitahidi” akasema Devotha na kukata simu “Kazi imemalizika.Kwa heri Mathew.I’m just doing my job” akasema Devotha kwa sauti ndogo na kumimina mvinyo katika glasi akanywa wote “I’m done here.I’m done with this job.I need new life somewhere far from here.Ninacho kiasi cha kutosha cha fedha ambacho kinaweza kunitosha kuyaanza maisha yangu mapya.Nimeshuhudia mengi katika sakata hili la akina Olivia hadi kwa Edger Kaka,nimeshuhudia mauji ya kutisha yaliyovuka ubinadamu.I need to change my life.Time for me to disappear ” akawaza Devotha
Helkopta mbili zikitokea katika operesheni ya kuwakomboa Coletha na Olivia zilitua katika kambi ya kijeshi ya kikosi cha operesheni maalum.Austin alikuwa wa kwanza kushuka ndani ya helkopta kisha majeruhi wakashushwa na kusaidiwa na mwisho ikashushwa miili ya waliouawa “Mheshimiwa Rais” akasema Austin “Poleni sana Austin.” Akasema Dr Evans na mara akasikia sauti ikimuita “Dady ! alikuwa ni Coletha akiwa amevalishwa blanketi kumkinga baridi.Nyuma yake alikuwepo Olivia Themba. “Coletha my princess” akasema Dr Evans na kukumbatiana na mwanae “Ahsante sana baba kwa kufanya juhudi za kutukomboa” “Anything for you my daughter.Sijui nimshukuruje Mungu kwa kuonana nawe tena” akasema Dr Evans na kumkumbatia tena mwanae “Vipi hali yako? Hawajakuumuza wale mashetani? “Kwa sasa ninajisikia vyema.Olivia alinitibu na hali yangu kwa sasa ni nzuri kabisa” akasema Coletha na Dr Evans akamtazama Olivia aliyekuwa amesimama pembeni yao “Olivia.Come here my daughter” akasema Dr Evans na kukumbatiana na Olivia. “Umeyaokoa maisha ya mwanangu.Thank you” akasema Dr Evans “Ahsante nawe mheshimiwa Rais kwa kufanya kila juhudi kuja kutuokoa.Mheshimiwa Rais ninahitaji kuzungumza nawe” “Not now Olivia” “Mheshimiwa Rais ni muhimu sana.We have to talk tonight” akasema Olivia Dr Evans akawapa pole makamanda wote walioshiriki katika operesheni ile kisha akazungumza na Austin halafu akaondoka kuelekea ikulu akiwa garini na Olivia na Coletha Baada ya kufika ikulu Dr Evans akawa na mazungumzo ya faragha na Olivia “Olivia nimekwisha kushukuru kwa kuokoa maisha ya mwanangu pili nakupa pole sana kwa yote mliyoyapitia lakini kubwa nataka kutumia nafasi hii kuzungumza kuhusu wewe na hatima yako.Umekuwa na mashirikiano na magaidi ambao wamemwaga damu nyingi ya watanzania wasio na hatia yoyote.Tumekwisha wakamata watu kadhaa wanaohusika katika mtandao huu na wengine wameuawa.Uchunguzi mkali sana utaanza kuanzia kesho kuwatafuta wale wote ambao wanajihusisha na IS na nimekula kiapo kwamba hakuna hata mmoja ambaye ana mahusiano na IS atabaki salama.Lazima tuwatafute kokote waliko hapa nchini.Olivia wewe ni kama mwanangu,mimi na baba yako ni kama ndugu hivyo nataka kukupa nafasi nyingine sitaki upotee.Kabla sijakueleza zaidi nataka kusikia kutoka kwako kile ambacho umesisitiza kwamba unataka kuniambia” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais na mimi ninakushukuru tena kwa kufanya juhudi za kutukomboa lakini nimeumia sana kumuacha Mathew Mulumbi.Alipigwa risasi wakati akituokoa mimi na Coletha.Yawezekana walimuua lakini hatukupaswa kumuacha nyuma.Imeniumiza sana”akasema Olivia na kufuta machozi “Olivia mahala mlipokuwa hapakuwa sehemu salama hata kidogo.Watu wale waliowavamia wangeweza kurejea tena na kuwamaliza wote.Operesheni ile ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakomboa wewe na Coletha na kwa kuwa tayari mlikwisha kombolewa hakukuwa tena na sababu ya kuendelea kuwaweka katika hatari ndiyo maana nikaamuru muondoke haraka sana.Usihofu kuhusu Mathew he’ll be fine.Nitatuma timu ya kwenda kumtafuta kama alijeruhiwa au ameuawa atapatikana” akasema Dr Evans “Sijapendezwa na hilo lakini tuliweke pembeni kwanza.Mheshimiwa Rais nataka kufahamu hali ya baba yangu ikoje? “Anaendelea vyema” “Mambo tayari yamemalizika.Lini ataachiwa huru? “Olivia maswali kama hayo si ya kunipotezea muda wangu.Nina mambo mengi ya kushughulikia yanayohusu usalama wa nchi na si kupoteza muda kujibu maswali kama hayo.Kama hauna kitu cha kunieleza tuendelee kujadili suala lako la kushirikiana na magaidi wa IS” akasema Dr Evans kwa sauti kali kidogo “Mheshimiwa Rais kwanza kabisa mimi si gaidi naomba ulifahamu hilo” “But you are working with them so you are one of them” akasema Dr Evans “Hufahamu chochote kuhusu mimi mheshimiwa Rais na sikutaka kuweka wazi kitu chochote nikisubiri wakati kama huu.Leo nitakueleza kila kitu” “Nieleze nielewe kwa nini unakana wewe si gaidi wakati unashirikiana nao” “Mheshimiwa Rais jambo hili linaanzia katika ugonjwa wa Edger Kaka”akasema Olivia na kumsimulia Rais namna alivyopambana hadi kumpeleka Edger Kaka Israel na kilichotokea kule hadi waliporejea nyumbani. “Niliagana na Edger uwanja wa ndege kwa miadi ya kuonana naye kesho ili tukatoe pole kwa familia ya yule msichana aliyeuwa nchini Israel lakini hatukuonana tena kwani ilitokea ajali ambayo ilihusisha msafara wa Edger na ikadaiwa kwamba amefariki dunia.Ni mimi ndiye niliyeutambua mwili wake na kilichonifanya niutambue mwili ule ni mkufu aliouvaa na pete.Tulimzika na tukasahau”akanyamaza kwa muda halafu akaendelea “Miaka mitatu baadae nikiwa kazini nilifuatwa na meneja wa hoteli Fulani kubwa hapa jijini akanieleza kwamba kuna mgeni wangu ambaye natakiwa kuonana naye ambaye anazo taarifa kuhusiana na Edger Kaka.Nilikwenda kuonana naye na akajitambulisha kwangu anaitwa Abu Dahir.Alidai yeye ni kaka wa Edger Kaka na akanipa maelezo kuwa yeye na Edger mama yao ni mmoja ambaye ni Habiba Jawad.” Olivia akanyamza kidogo baada ya Dr Evans kuonyesha mshangao “Habiba Jawad ni mama wa Edger Kaka? “Ndiyo mheshimiwa Rais.Habiba Jawad ni mzaliwa wa Kenya lakini ana asili ya Somalia aliolewa na Nasser Jawad mfanya biashara tajiri na wakamzaa mtoto aitwaye Seif Jawad ambaye ndiye huyu Edger Kaka.Jina Edger alipewa baada ya kuhamishiwa Tanzania.Wazazi wake walimuhamishia Tanzania akiwa chini ya uangalizi wa walezi wa kitanzania waliolipwa fedha nyingi na Habiba na ndipo akapewa jina la Edger Kaka lakini jina lake halisi ni Seif Jawad” “My God ! haya mambo ni mageni kabisa.Kumbe Edger Kaka si mtanzania? Akauliza Dr Evans “Edger Kaka si mtanzania”akajibu Olivia “Baada ya mumewe kufariki dunia,Habiba aliolewa na mwanaume mwingine tajiri mwenye asili ya Palestina na wakazaa mtoto ambaye ndiye huyo Abu Dahir ambaye alinifuata hapa Tanzania.Abu dahir alinieleza kwamba Edger Kaka hajafariki dunia na akaniomba kwa kuwa nilikuwa na ukaribu na Edger basi tushirikiane kuutafuta ukweli na kumsaidia Edger.Alinitaka niachane na kazi yangu ya udaktari na badala yake atanipa fedha ambazo nitajenga kituo cha utafiti wa magonjwa mbali mbali ya binadamu na wanyama na ndicho kituo kile nilichokijenga.Hiyo ilikuwa hatua ya kwanza.Baada ya kituo kukamilika Abu Dahir akaniita nchini Saudi Arabia kwa ajili ya hatua ya pili na kwa mara ya kwanza nikakutana na mama yake Edger ambaye ni Habiba Jawad.Nilizungumza naye akanieleza mengi historia yake na yote anayoyafanya na alikiri kwangu kwamba anafadhili kikundi cha IS na vikundi vingine vidogo dogo vya kigaidi.Alinitaka tuingie katika hatua ya pili nayo ni kuufanyia uchunguzi mwili ule ambao wote tuliamini ni wa Edger kaka.Nilichukua sampuli za masalia ya mwili ule mimi mwenyewe na kuzifanyia uchunguzi nikabaini kweli mwili ule haukuwa wa Edger Kaka na hapo ndipo tulipoingia katika hatua ya tatu ambayo ni kumtafuta Edger Kaka mahala alipo.IS waliamini kwamba waliohusika katika kutengeneza ajali ile ya Edger ni serikali ya Tanzania hivyo wakanitaka niandae kirusi ambacho tutakitumia kumuambukiza mwanao ili kukushinikiza uweze kumuachia Edger.Hilo likafanyika na nilikwenda Congo kukutana na Seif Almuhsin ili kupata matokeo ya kirusi nilichokitengeneza na niliporejea hapa ndipo nikatekwa.Mheshimiwa Rais IS walinitaka niwafanyie kila wanachokitaka na kama nikikataa basi watawaua familia yangu ndiyo maana nikakubali kufanya nao kazi.Mheshimiwa Rais historia nzima ya mimi na IS ni hiyo.Mimi si gaidi na wala si mmoja wao na siwezi kuwa mmoja wao japo nimeshiriki katika baadhi ya mipango yao”akasema Olivia na kunyamaza “Olivia maelezo hayo yamenitoa jasho.Kwa nini hukunieleza haya yote nilipokuja kuonana nawe pale katika idara ya siri ya mambo ya ndani? “Lengo langu lilikuwa kumpata Edger kaka ili niweze kumalizana na IS ndiyo maana sikutaka kukueleza kitu chochote.Mheshimiwa Rais narudia tena kusisitiza kwamba mimi si gaidi na hata nilipomuambukiza Coletha kile kirusi nilikuwa na uhakika hatakufa kwa kuwa nilikuwa na dawa ya kumtibu” “Sasa nimekuelewa Olivia.Kila mtu alikuwa anajiuliza maswali mengi sababu ya wewe kujiunga na IS na sasa nimepata jibu.Pole sana kwa yote uliyopitia” akasema DrEvans “Ahsante sana mheshimiwa Rais lakini nataka nikueleze kwamba hukupaswa kumuacha Edger kaka.Yule ndiye gaidi na alikuwa hapa nchini kwa malengo maalum.Kwanza si mtanzania lakini ameishi hapa nchini kama Mtanzania na hadi akapata uongozi.IS walikuwa wanamuandaa Edger kuwa Rais wa Tanzania” “Kuwa Rais? Dr Evans akashangaa “Ndiyo.Alikuwa anaandaliwa kuwa Rais na wametumia gharama kubwa kumtengeneza hadi pale alipofika” “Kwa hilo nakubaliana nawe Olivia.Baada ya kushindwa kwa mpango wao kwa Edger Kaka walianza kumuandaa waziri mkuu wa sasa kwa ajili ya nafasi hiyo” “Waziri mkuu? “Ndiyo.He was one of them” akasem Dr Evans na kumueleza Olivia kile kilichotokea mchana wa siku iliyopita hadi waziri mkuu alivyokamatwa. “Mheshimiwa Rais mmefanya mambo makubwa sana siku ya leo lakini kuna makosa pia yamefanyika.Kwanza mtu aliyeyafanikisha haya yote ambaye ni Mathew Mulumbi hakupaswa kuachwa porini afe mwenyewe.Pili Edger Kaka hakupaswa kabisa kutoka mikononi mwetu.Alipaswa kuendelea kushikiliwa hapa hapa nchini” akasema Olivia “Nakubaliana nawe Olivia kwamba hayo ni makosa yamefanyika lakini mafaniko pia ni makubwa.Watoto waliotekwa nyara wamepatikana,magaidi wamekamatwa na wengine kuuawa na kubwa zaidi wewe na Coletha mmrejea nyumbani.Plani yetu iilikuwa ni kumuua baada ya mabadilishano lakini mambo hayakwenda kama tulivyotaka na wakafanikiwa kumtorosha Edger Kaka.Hata hivyo pamoja na kukimbia lakini hatarejea tena Tanzania.Umenifumbua macho Olivia na sasa tunakwenda kufanya uhakiki upya wa nani ni mtanzania na nani siye tukianza na viongozi.Kuna mengi yanakwenda kufanyika nchi itatikisika kwa muda lakini itakaa sawa.Kilichotokea kimenipa funzo kubwa.Hata hivyo kuna jambo ambalo nataka msaada wako” “Jambo gani mheshimiwa Rais? “Nimeikosea sana familia yako hasa baba yako.Agrey si rafiki bali ni zaidi ya ndugu.Mimi na yeye tuna historia ndefu.Najua akifahamu hiki kilichotokea urafiki wetu utafika mwisho jambo ambalo sitaki litokee.What can I do?akauliza DrEvans “Ni kweli mheshimiwa Rais umetokea mvurugano mkubwa lakini nataka nikiri kwamba aliyesababisha haya yote ni mimi.Mimi na wewe sote tunatakiwa kuwaeleza wazazi wangu ukweli wote wa kile kilichotokea.Itachukua muda urafiki wenu kurejea kama zamani lakini nina uhakika mkubwa mambo haya yatamalizika” akasema Olivia “Tutamaliza mambo haya kesho lakini kwa sasa utakwenda kupumzika umeandaliwa chumba hapa hapa.Please don’t call anyone hadi pale muda utakapofika” akasema Dr Evans
Saa nne na nusu za asubuhi msafara wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania uliwasili katika kambi ya jeshi ya kikosi cha operesheni maalum.Alishuka garini na kupokewa na waziri wa ulinzi na kusalimiana na mku wa majeshi na makamanda wengine wakubwa wa jeshi akiwamo Austin January mkuu wa kikosi kile cha operesheni maalum.Baada ya Rais kuwasili ratiba iliyopangwa kwa ajili ya kuiaga miili ya wanajeshi waliopoteza maisha katika operesheni ya kuwakomboa Coletha na Olivia ikaanza.Viongozi wa dini walianza kwa dua na sala mbali mbali za kuwaombea marehemu wale na ratiba ikaendelea.Miili ya wanajeshi wale ikaagwa na Rais akaondoka kurejea ikulu ambako alitarajiwa kulihutubia taifa “Ndugu watanzania wenzangu ni siku nyingine tena nimekuja mbele yenu kuzungumza nanyi.Awali ya yote narudia tena kuwapeni pole wale wote mliofiwa na wapendwa wenu katika matukio ya kigaidi yaliyotokea hapa nchini.Tunawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani Amina. “Ndugu watanzania,nchi yetu ambayo amani imetamalaki,ilipatwa na majanga ya mashambulio mawili ya kigaidi,moja ni bomu lililolipuliwa katika hospitali ya Mtodora na shambulio lingine ni kutekwa kwa wanafunzi sitini na sita katika shule ya sekondari ya St Getrude.Katika shambulio la hospitali ya Mtodora walifariki watu ishirini na moja na wengine wengi kujeruhiwa wengine vibaya sana na katika wanafunzi waliotekwa wameuawa watoto wanne na tukafanikiwa kuwakomboa wanafunzi sitini na mbili na walimu wao watatu.Wanafunzi wote waliokombolewa watakabidhiwa kwa wazazi wao kwa sasa wanaendelea kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kuwaweka vizuri kwani kitendo kilichowatokea kimewasababishia mstuko mkubwa.Kwa wale waliouawa taratibu zinafanywa ili miili yao ikabidhiwe kwa familia zao kwa ajili ya mazishi ambayo yatagharamiwa na serikali.Tunawapa pole sana wote mliofiwa na watoto na ndugu zenu katika mashambulio haya tunawaombea uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. “Ndugu watanzania wenzangu magaidi wanapofanya shambulio mahali Fulani huwa na sababu zao aidha kulipiza kisasi au kulazimisha wapewe au kutimiziwa mambo Fulani yenye manufaa kwao.Hapa kwetu walifanya hivyo kuna mambo walikuwa wanayahitaji na wakafanya mashambulio yale ili kushinikiza serikali iwatimizie madai yao.Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haijawahi na haitafanya makubaliano yoyote na magaidi.Jukumu letu ni kuhakikisha tunawafyekelea mbali kila pale wanapojaribu kujipenyeza nchini kwetu na ndivyo tulivyofanya.Alasiri ya jana majasusi wetu wakishirikiana na kikosi cha jeshi cha operesheni maalum walifanikiwa kugundua maficho ya magaidi hao wakavamia na kuwakomboa watoto sitini na mbili na walimu wao watatu.Magaidi wote waliokuwamo katika nyumba hiyo waliuawa.Hatuna huruma na gaidi yeyote.Msako mkali ulianza jana hiyo hiyo na tayari tumefanikiwa kuwakamata watu kadhaa ambao wana mahusiano na kikundi cha kigaidi cha IS na tunaendelea kukamata wengine hadi tutakapohakikisha magaidi wote wametiwa mikononi.Nawaahidi kwamba hakuna gaidi atakayebaki,tutawakamata wote na kuufyekelea mbali mtandao wao wote hapa nchini. Usiku wa jana pia kumetokea mapigano makubwa kati ya kikosi chetu cha operesheni maalum na magaidi katika mpaka wa Tanzania na Kenya na katika mapigano hayo makali tumewapoteza vijana wetu kumi na tatu na kuwasambaratisha magaidi wote.Tunawaombea vijana wetu hao mashujaa wapumzike kwa amani kwani wamemwaga damu yao kwa kulipigania taifa lao Ndugu watanzania katika watu tuliowakamata wakihusiana na mtandao wa kigaidi wamo pia viongozi wa serikali.Wapo baadhi ambao tunawashikilia tunaendelea kuwachunguza na pale uchunguzi utakapokamilika tutawafikisha mahakamani.Katika sakata hili pia tumegundua kwamba kuna watu ambao si raia wa nchi hii lakini wanaishi hapa nchini na tayari wamekwisha ingia hadi katika ngazi za uongozi.Tunaanza kufanya uhakiki wa viongozi wote wa serikali kujiridhisha kama kweli ni raia wa Tanzania.Tumebaini mchezo unaofanywa na watu wasiotutakia mema wa kupandikiza watu wao hapa nchini toka wakiwa wadogo kwa malengo ya kuwatumia katika mipango yao na watu hao wanaopandikizwa wamediriki kushika hadi nafasi za uongozi.Tutakuwa makini katika mipaka yetu kudhibiti wahamiaji haramu ninatoa rai kwenu watanzania wenzangu kama unamfahamu mtu yeyote ambaye si raia wa nchi hii lakini anaishi hapa nchini toa taarifa katika vyombo husika ili aweze kushughulikiwa haraka sana kwani wengiwa magaidi hawa ni wageni ambao wamekuwa wakiishi hapa nchini wakifadhiliwa na wenyeji Ndugu watanzania matukio haya yametufundisha kwamba upo ulazima wa kuviongezea nguvu kubwa vyombo vyetu vinavyohusika katika mapambano na ugaidi ili viwe na uwezo mkubwa wa kubaini matukio ya kigaidi kabla hayajatokea na kuyadhibiti.Hilo tutalifanya haraka sana.Mwisho kabisa nataka kuwajulisha kwamba kuanzia leo hii nimelivunja baraza langu la mawaziri nitateua baraza jipya hapo baadae. Narudia tena wito wangu wa kuwataka watanzania tuwe wavumlivu na tuviache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake Mungu ibariki Tanzania Ahsanteni kwa kunisikiliza BAADA YA MWEZI MMOJA Tayari umekwisha pita mwezi mmoja toka yalipofanyika mashambulio ya kigaidi.Nchi imetulia na wananchi wanaendelea na maisha yao kama kawaida.Rais Dr Evans ameunda baraza jipya la mawaziri.Baada ya uchuguzi kukamilika aliyekuwa waziri mkuu wa jamhuri ya munganowa Tanzania na wenzake sitini na saba walifikishwa mahakamani wakituhumiwa kwa makosa ya ugaidi.Dr Olivia Themba alikikabidhi serikalini kituo cha utafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama ambacho alikijenga kwa fedha kutoka kwa watu wa IS na yeye akaanza ujenzi wa hospitali kubwa ya magonjwa ya moyo pembeni kidogo ya kituo kile. Mathew Mulumbi alitafutwa bila mafanikio na hakuna aliyefahamu yuko wapi.Timu iliyotumwa kumtafuta ilirejea bila ya Mathew Mulumbi na kutoa ripoti yake kwamba kuna uwezekano mkubwa alifariki na kuliwa na fisi kwani eneo lilipotokea shambulio lile kuna fisi wengi.Rais Dr Evans alituma ujumbe maalum kwenda Paris Ufaransa kwa Peniela mke wa Mathew kupeleka salamu za pole kufuatia kifo cha Mathew.Ujumbe ule uliongozwa na Austin January ambaye alikuwa na Mathew eneo la tukio.Ruby aliondoka nchini kwenda kuendelea na shughuli zake lakini Gosu Gosu aliombwa na Peniela kubaki nchini kuendelea kusimamia miradi yote ya Mathew ombi ambalo Gosu Gosu alilipokea kwa mikono miwili. Mahusiano kati ya Dr Evans na Agrey Themba yaliendelea baada ya Dr Evans kueleza ukweli wa kile kilichotokea na kumuomba rafiki yake yule mkubwa msamaha wakasameheana na maisha yakaendelea kama ilivyokuwa awali lakini kilichotokea kilibaki kuwa siri kati yao Siku tatu baada ya shambulio la mpakani kutokea Devotha aliondoka nchini kwa ndege akielekea Dubai na hakuna mwenye mawasiliano naye tena wala kufahamu mahala alipo. Idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi iliimarishwa zaidi na Rais aliamua kuitambulisha rasmi idara hii kwa viongozi wa juu wa serikali na ulinzi ili wafahamu uwepo wake.Kaiza alipewa ukurugenzi wa idara hii.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TAMATI
MWISHO WA SIMULIZI YA SIRI PART 1
USIKOSE SEHEMU YA PILI YA SIRI IITWAYO MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
0 comments:
Post a Comment