Search This Blog

Thursday, 17 November 2022

SIRI - 4

 






Simulizi : Siri

Sehemu Ya Nne (4)







Kwa maelekezo waliyopewa na Ruby,Mathew na Gosu Gosu walifanikiwa kufika katika jengo ambalo ndimo mtu aliyepiga simu akitaka kumjulisha Mathew kuhusu Olivia alikuwemo wakati akipiga simu.Nyumba ilikuwa giza na haikuwa ikiwaka hata taa moja.Geti halikuwa limefungwa,Mathew akalisukuma taratibu na kuingia ndani wakiwa katika tahadhari kubwa.Ndani ya ile nyumba kulikuwa na magari mengi mabovu “Mathew unadhani tuko sehemu sahihi?Mbona hapa panaonekana kama gereji?akauliza Gosu Gosu “Ninamuamini sana Ruby hawezi akatuelekeza sehemu ambayo si sahihi.Tuchunguze mahala hapa vizuri.Mara nyingi sehemu kama hizi hutumika kama maficho kwani si rahisi mtu kutilia shaka kama kuna kitu kinaendelea” akasema Mathew Walinyata kwa tahadhari wakipita gari baada ya jingine wakichungulia na walipokaribia kufika katika mlango wa kuingia ndani ile nyumba waligundua kuna miili ya watu ndani ya gari wakiwa wamekufa.Mathew akawasha tochi akawamulika walikuwa wamekufa.Akamgeukia Gosu Gosu “Tuko sehemu sahihi kabisa.Kuna kitu kimetokea hapa tumekikosa !! akasema Mathew huku Gosu Gosu akiwa makini kujihami na hatari yoyote ambayo ingetokea. Mlango wa kuingilia ndani ulikuwa wazi wakaingia kwa tahadhari.Haikuwa nyumba kubwa.Ilikuwa na vyumba vichache wakakagua vyumba vyote hakukuwa na kitu chochote cha maana zaidi ya vifaa vya magari . “Nini kinachofanyika katika nyumba hii? Ukiangalia kwa haraka haraka shughuli kubwa inayofanyika mahala hapa ni ufundi wa magari lakini kitendo cha watu wale kuuawa kinawasha taa nyekundu kutuonyesha kuwa kinachofanyika hapa ni zaidi ya kutengeneza magari.Yule mtu aliyepiga simu akinitafuta ukazungumza naye alipiga simu kutokea hapa” “Mathew unadhani Olivia alikuwepo hapa? Nyumba yote imejaa vifaa vya magari hakuna sehemu ambako Olivia anaweza akafichwa” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu naamini lazima kuna kitu hapa.Tujiulize nani kawaua watu wale? Lazima ipo sababu ya kuuawa kwao na si bahati mbaya” akasema Mathew na kwenda tena katika gari ilimowekwa miili ya wale jamaa waliouawa.Wakaitoa miili ile na kuanza kuichunguza.Walikuta vitu mbalimbali kutoka kwa wale jamaa lakini wote waliwakuta wakiwa na kadi maalum za kufungulia mlango. “Wote wana kadi hizi ambazo ni maalum kwa ajili ya kufungulia milango.Mlango upi hapa ndani unafunguliwa kwa kadi?akauliza Mathew kisha wakaelekea tena ndani ya nyumba wakaanza kuchunguza milango yote kupata mlango ambao kadi zile walizokutwa nazo wale jamaa hutumika kuufungua.Wakati wakiendelea kuchunguza Gosu Gosu akamuita Mathew “Kuna kitu nimekiona katika chumba hiki” akasema Gosu Gosu na kumuonyesha Mathew kitu Fulani Mathew akajaribu kupitisha moja ya kadi waliyoipata kutoka kwa wale jamaa na mlango ukajifungua kukaonekana ngazi za kushuka chini. “Nilijua tu lazima kuna kitu kinaendelea katika nyumba hii” akasema Mathew na kumtaka Gosu Gosu aendelee kubaki pale pale juu kulinda usalama endapo kungetokea hatari yoyote.Taratibu akashuka chini akiwa katika tahadhari kubwa.Mara tu baada ya kushuka ngazi kitu cha kwanza alichokishuhudia ulikuwa ni mwili wa mtu aliyelala chini akiwa amekufa kwa kupigwa risasi.Alikuwa amevaa koti la kidaktari.Mathew akamchunguza kwa makini akampekua lakini hakumkuta na kitu chochote.Alimuacha yule jamaa akaanza kupitia chumba kimoja baada ya kingine akikagua na mwisho akakifikia chumba kikubwa kilichokuwa na mitambo kadhaa ambayo aliigundua ni mitambo maalum ya kutesea watu. “Hii sehemu inaonekana ni maalum kwa ajili ya mateso,naamini Olivia aliletwa hapa kuteswa .Devotha alieleza kuwa Olivia alihamishwa kwa siri na hajui alipelekwa wapi naamini aliletwa hapa.Hawa waliouawa ni akina nani?Je ni wale waliokuwa wanamshikilia Olivia? Kama ndiyo nani kawaua?Ninaanza kuwa na wasiwasi yawezekana labda wamevamiwa wakauawa na kisha wavamizi wakaondoka na Olivia” akawaza Mathew na kwenda kumpiga picha yule jamaa aliyeuawa akiwa na koti la kidaktari halafu akamtumia Ruby na kumpigia simu “Ruby tumefika mahala hapa ulipoelekeza,tumekuta shughuli kubwa inayoendelea ni ufundi wa magari” akasema Mathew na kumuelezea Ruby namna eneo lilivyo “Lakini tumegundua kuna nyumba ya siri iko chini ya nyumba hii ndogo iliyo juu ambako ndiko shughuli mbali mbali za utesaji zinaendelea.Kuta zina damu na inaonekana unyama mkubwa sana hufanyika hapa katika hii nyumba.Kuna vyumba kadhaa na kimoja kina mitambo na zana mbali mbali za kutesea watu.Hakuna mtu yeyote tuliyemkuta eneo hili bali tumekuta kuna watu wameuawa na kufichwa ndani ya gari na huku chini nimekuta ameuawa mtu mmoja.Nimekutumia picha ya huyo mtu nataka umuonyeshe Devotha kama anamfahamu.Nataka kujua kama anamfahamu” akasema Mathew na Ruby akamuonyesha Devotha ile picha aliyotumiwa na Mathew baada ya muda mfupi Devotha akasema “Mathew huyu mtu simfahamu kabisa.Hayuko katika idara yangu” “Devotha hiyo ndiyo hali tuliyoikuta hapa.Yamefanyika mauaji na huyo mtu ni mmoja wa wale walioua….” “Mathew..!! akaita Devotha “Kuna nini Devotha? “Mathew ninatazama runinga sasa hivi kuna habari mpasuko.Umetokea mlipuko mkubwa katika jengo la wagonjwa binafsi katika hospitali kuu ya Mtodora.Jengo hilo linalodaiwa kulipuliwa ndimo alimokuwa amelazwa Coletha mtoto wa rais.Chanzo cha mlipuko huo inasadikiwa ni bomu la kutegwa.Taarifa za awali zinaeleza kwamba kikundi cha watu wasiofahamika walifika hospitali hapo wakiwa na magari ya kubebea wagonjwa wakidai kupeleka majeruhi wa ajali ya gari.Waliwateka madaktari wakawavua mavazi yao wakavaa na inasemekana walielekea katika jengo alimokuwa amelazwa mtoto wa rais.Mpaka sasa hakuna idadi kamili ya vifo au majeruhi iliyotolewa” akasema Devotha “Oh my God !! akasema Mathew na kukuna kichwa. “Kuna taarifa zozote hadi hivi sasa kuhusiana na Coletha kama ni mzima? “Hakuna taarifa yoyote hadi hivi sasa iliyotolewa” akasema Devotha.Mathew akafikiri kidogo na kusema “Hakuna shaka wavamizi hao walikuwa na shida na Coletha.Naamini lazima watakuwa ni watu wa IS wakiendelea na mpango wao wa kumtaka rais awaeleze mahala alipo Edger Kaka.Devotha naomba umpatie simu Ruby” akasema Mathew “Hallo Mathew” akasema Ruby “Ruby kama nilivyokueleza awali kwamba ninaamini Olivia alikuwepo mahala hapa.Nimegundua nyumba hii imezungukwa na kamera za siri,kuna chumba ambacho kina runinga kubwa zilizounganishwa na kamera zinazoizunguka nyumba hii.Kamera hizi zinaweza kutusaidia kufahamu kilichotokea na kinachofanyika mahala hapa.Ninataka tupitie kumbu kumbu zote zilizohifadhiwa kuanzia asubuhi ya leo”akasema Mathew na Ruby akamtaka aende katika chumba hicho chenye kuonyesha picha zote za kamera.Akaketi na kuanza kufuata maelekezo yote ambayo Ruby alimpa.Baada ya dakika tano Ruby akaweza kudukua kamera zile na kuanza kupitia kumbu kumbu za kamera akianzia na kamera iliyokuwa katika geti la kuingilia ndani.Aliipeleka mbele kamera hadi pale aliposhuhudia geti likifunguliwa na magari matatu yenye rangi nyeusi yakiingia “There stop ! ..Devotha aliyekuwa pembeni ya Ruby akasema “Hizi ni gari zetu” akazitazama kwa makini halafu akamtaka Ruby apeleke mbele.Milango ya magari ikafunguliwa na watu kadhaa wakashuka “Kaiza !! akasema Devotha kwa hasira “Unamfahamu?Ruby akauliza “Ndiyo.Alikuwa msaidizi wangu” akajibu Devotha Kaiza alisalimiana na mtu aliyevaa koti jeupe.Baada ya muda lango kubwa la moja wapo ya chumba likafunguliwa na gari moja kati yay ale waliyokuwa nayo akina Kaiza likaingia.Ruby akahamisha kamera baada ya watu wote kuonekana wakiingia ndani. Katika kamera nyingine walimshuhudia Olivia akiwa amefungwa kitandani. Walifuatilia kila kilichokuwa kimetokea katika kile chumba alimokuwa amefungwa Olivia akiteswa. “Nimekuwa mkurugenzi wa idara ya siri ya mambo ya ndani ya nchi lakini sipafahamu mahala hapa ni wapi.Nakubaliana na Mathew kwamba mahala hapa ni maalum kwa ajili ya kutesea watu.Kaiza amepafahamuje mahala hapa? akawaza Devotha Walifuatilia kila kitu hadi pale Olivia alipondolewa katika kile chumba akapakiwa garini na kuondoka. “Ahsante sana Ruby kwa msaada huu mkubwa na sasa tumepata uhakika kuwa Olivia alikuwa hapa na amehamishwa na kupelekwa mahala kusikojulikana.Tunao uhakika bado yuko mikononi mwa idara ya usalama wa ndani ya nchi.Swali linaloibuka wamempeleka wapi?akauliza Mathew “Kwa kuwa tumepata uhakika kuwa Olivia yuko katika mikono ya Kaiza njia nyepesi ya kufahamu mahala alipo ni kwa kumpigia simu Kaiza na kufahamu mahala alipo.” akasema Devotha “Hilo ni wazo zuri.Fanyeni hivyo kisha mtatujulisha,sisi tunaondoka hapa” akasema Mathew kisha akatoka kule chini akakutana na Gosu Gosu wakaelekea garini na kuondoka mahala pale.Mathew akamueleza kila kitu kilichotokea akiwa kule chini. “Ukiacha hilo la Olivia kuwepo hapa kuna lingine kubwa limetokea” akasema Mathew “Kumetokea nini tena? “Hospitali kuu ya Mtodora imevamiwa na watu wasiofahamika wamefanya mauaji na kulipua jengo la wagonjwa binafsi alimokuwa amelazwa mtoto wa rais” Mathew akasema “Nani waliofanya kitendo hicho? akauliza Gosu Gosu “Naamini waliofanya kitendo hiki ni magaidi wa IS ambao wanataka kumshinikiza rais awaeleze mahala alipo Edger Kaka na japo haijawekwa wazi bado lakini nina uhakika mtoto wa rais ndiye sababu ya wao kuvamia hospitali hapo.Ninazidi kujiuliza umuhimu wa Edger Kaka kwa kikundi cha IS.Mtu pekee ambaye anaweza akatusaidia kutuondoa katika wingu hili lililotanda ni Olivia ambaye mpaka sasa hatujui mahala alipo” akasema Mathew na simu yake ikaita alikuwa ni Ruby “Hallow Ruby” akasema Mathew “Mathew tumejaribu kumpigia simu Kaiza lakini hapatikani kwa namba zile anazozifahamu Devotha” akasema Ruby “Hakuna namna nyingine ya kumpata Kaiza? Ninaomba kuzungumza na Devotha” akasema Mathew “Hallow Mathew” “Devotha nataka unielekeze mahala anakoishi Kaiza” “Kwa nini Mathew? Unataka kumfuata kwake? “Nataka kuichukua familia yake” “Mathew hapana hilo si jambo zuri” “Kwa nini Devotha? “Kaiza ana watoto wadogo mapacha wana miezi miwili hawastahili kuingizwa katika jambo hili.Tutafute namna nyingine ya kumtafuta Olivia na si kuwaumiza familia ya Kaiza ambao hawana kosa lolote” akasema Devotha “Devotha ninaomba usiwe kikwazo cha kukwamisha mambo yetu.Sijali kama ana watoto mapacha hata kama angekuwa na watoto hamsini lakini tayari Kaiza ni mtu muhimu sana kwetu hivyo kila njia inapaswa kutumika kuhakikisha tunampata Olivia” akasema Mathew “Hapana Mathew tutafute namna nyingine lakini binafsi siko tayari kuwaingiza malaika wale katika hatari.Hawana kosa lolote” akasema Devotha “Listen to me lady.This is my mission and we’re going to do it my way.Wewe ni nani wa kunizuia nisitekeleze mipango yangu? Akauliza Mathew kwa ukali “Mathew this is my mission too” akasema Devotha kwa ukali “Devotha you don’t know me well.Naomba tusibishane tafadhali nieleze anakoishi Kaiza” akasema Mathew akionekana kukasirishwa sana na maneno yale ya Devotha “Usinitishe Mathew” akasema Devotha na kukata simu “Damn it !! akasema Mathew kwa hasira “Simuelewi huyu mwanamke.Kwa nini amegoma kunielekeza anakoishi Kaiza?Tumekwama Gosu Gosu turejee nyumbani nikamuonyeshe huyu mwanamke mimi sipendi mzaha” akasema Mathew.







Taarifa ya kuvamiwa kwa hospitali ya Mtodora na kutokea kwa mlipuko katika jengo alimokuwa amelazwa Coletha mtoto wake zilimstua mno Dr Evans.Alitaka kuelekea huko haraka kujua hali ya mwanae lakini walinzi wake wakamzuia kwani eneo lile tayari ni hatari kwa usalama wake. “Kwa nini mnanizuia wakati jengo lililolipuliwa amelazwa mwanangu?akauliza kwa ukali “Mheshimiwa rais jukumu letu ni kukulinda wewe na kuhakikisha unakuwa salama hivyo hatuko tayari kukuacha ukaenda mahala ambako si salama.Tunaomba utulie hapa na tutafuatilia kujua kama mwanao ni mzima” akasema Hassan kiongozi wa kikosi cha kumlinda rais.Dr Evans alikuwa anatokwa na jasho usoni kama amemaliza mbio ndefu. “Hassan my pills please” akaomba apewe dawa zake akameza na kutulia sofani “Hassan tafadhali nataka haraka taarifa za kilichotokea hospitali.Nataka kujua kama mwanangu ni mzima” akasema Dr Evans. “Mzee tayari vikosi mbali mbali viko eneo la tukio na jitihada za uokozi zinaendelea.Watu wetu pia wameelekea huko na muda si mrefu tutapata jibu” akasema Hassan “Nani hawa waliofanya jambo hili? Huu ni unyama mkubwa sana kuvamia hospitali na kuua watu! Wanyama hawa lazima wapatikane !! akasema Dr Evans na kumpigia simu mkurugenzi wa idara ya kudhibiti na kupambana na ugaidi. “Mheshimiwa rais” akasema mkurugenzi wa idara ya kupambana na ugaidi “Mkurugenzi nataka kupata taarifa za hiki kilichotokea hospitali ya Mtodora” akasema Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa rais tayari timu yetu imekwisha fika eneo la tukio na uchunguzi unaendelea ila kwa taarifa ambazo zimepatikana hadi sasa ni kwamba usiku huu zilifika gari tatu za wagonjwa zikiwa na majeruhi wa iliyodaiwa ni ajali ya gari.Haraka haraka majeruhi wale walichukuliwa na kukimbizwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kupatiwa huduma kwani walikuwa wamechafuka damu na walionekana kuumia mno.Wakati madaktari wakiendelea kuwachunguza majeruhi wale ili kujua sehemu walizoumia walifika tena watu wengine ambao walidai ndugu zao wamepata ajali na kukimbizwa pale hospitali.Kwa mujibu wa madaktari waliokuwemo katika chumba cha upasuaji wanadai kwamba wakati wakiendelea na zoezi la kuwahudumia majeruhi wale mara wakajikuta wakivamiwa na watu wenye silaha na kitu cha kushangaza wale majeruhi waliokuwa katika vitanda wakihudumiwa wakainuka wote kumbe hawakuwa wameumia kokote ulikuwa ni mpango wa kuwawezesha kuingia pale hospitali.Magaidi wale waliwavua nguo madaktari wakavaa wao kisha wakasukuma kitanda kuelekea katika jengo lililolipuliwa.Haijajulikana bado kitu gani walikwenda kukifanya katika jengo hilo.Timu yetu wakishirikiana na idara nyingine wanaendelea na uchunguzi na pale tutakapopata taarifa Zaidi tutakujulisha mheshimiwa rais” akasema mkurugenzi wa idara ya kupambana na ugaidi “Mkurugenzi idara yako imepewa jukumu la kuhakikisha inang’amua kuwepo kwa mashambulio ya kigaidi.Hamkupata viashiria vyovyote vya kutokea kwa shambulio hili?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais hatukuwa tumepata viashiria vyovyote vya kufanyika kwa shambulio kama hili la kigaidi” “Nataka muhakikishe mnawafahamu waliofanya tukio hilo ni akina nani na kuwatia nguvuni haraka sana.Vile vile hakikisheni mnafahamu kama kuna mashambulio mengine Zaidi yamepangwa kufanyika na muhakikishe mnazuia kufanyika kwa shambulio lingine tena la kigaidi hapa nchini.Nataka taarifa za kila mtakachokuwa mnakigundua kuhusiana na tukio hili” akasema Dr Evans “Nitakujulisha mheshimiwa rais” akajibu mkurugenzi na rais akakata simu “Mwili wote unatetemeka kila nikimuwaza mwanangu Coletha.Je atakuwa mzima?akajiuliza Dr Evans na mara simu yake ikaita.Zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake akaipokea. “Hallow” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais habari za usiku huu.Mimi ni kiongozi wa kikundi kilichofanya shambulio usiku huu katika hospitali kuu ya Mtodora.Kama uko na watu karibu usionyeshe mstuko wowote sogea pembeni ninataka kuzungumza nawe,usijaribu kutaka kuifuatilia simu hii nitagundua” akasema mtu wa upande wa pili wa simu aliyekuwa anazungumza Kiswahili safi.Dr Evans akawafanyia walinzi wake ishara kwamba anaingia chumbani kwake kuzungumza na simu.Mwili ulikuwa unamtetemeka “Hallow” akasema Dr Evans kwa woga “Mheshimiwa rais nilikueleza kwamba mimi ni kiongozi wa kikundi kilichofanya shambulio usiku huu katika hospitali kuu ya Mtodora.Napenda kukujulisha usihangaike kumtafuta mwanao tumemchukua tunaye sisi.Hali yake si nzuri anaumwa sana na anaweza akapoteza maisha hivyo ili kuokoa uhai wake unapaswa kusikiliza na kutekeleza kila kile tutakachokuelekeza” akasema yule jamaa na kumfanya Dr Evans ashushe pumzi “Kwa nini mmemteka mwanangu?Amewakosea nini? Ninawaonya kuwa mmekosea kuanzisha vita na mimi.Matokeo yake ni mabaya mno kwenu !! akasema Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais tunafahamu nguvu kubwa uliyonayo lakini kwa usalama wa mwanao utafuata kila tutakachokuelekeza ukifanye na kama ukipuuzia utamkosa mwanao na mashambulio Zaidi yataendelea katika sehemu mbali mbali hapa Dar es salaam.Tumejipanga vizuri katika sehemu mbali mbali zenye mikusanyiko ya watu na pindi utakapokataa kutekekeleza matakwa yetu basi Tanzania itageuka nyekundu.Hatutanii.Tukio la usiku huu katika hospitali ya Mtodora ni ishara kwamba tunaweza kuingia sehemu yoyote tukiamua” akasema yule jamaa “Punguani wewe !! akasema Dr Evans kwa hasira “Mheshimiwa rais hivi sasa kisu kiko shingoni kwa mtoto wako Coletha na unayeweza kuzuia kifo chake ni wewe kwa kutekeleza maagizo yetu” “Mnataka nini kutoka kwangu?akauliza Dr Evans “Tunataka mambo kadhaa na jambo la kwanza tunataka utupatie mtu anaitwa Olivia Themba ambaye anashikiliwa na serikali.Nataka tumpate Olivia ndani ya nusu saa kuanzia sasa na kama hautatekeleza hilo basi tegemea kusikia mambo mengine makubwa sana usiku wa leo.Usiku huu utakuwa ni usiku wa damu.Tekeleza hicho nilichokueleza na utaokoa maisha ya maelfu ya watanzania ambao watapoteza maisha yao usiku wa leo kama hautakuwa tayari kutekeleza kile tulichokuelekeza.Dakika ishirini kutoka sasa nitakupigia simu na ninataka hadi muda huo Olivia awe ameandaliwa tayari kupelekwa mahala nitakapokuelekeza.Tekeleza hilo nililokuelekeza na mwanao atakuwa salama.Ninaanza kuhesabu muda kuanzia sasa”akasema yule jamaa na kukata simu.Dr Evans akabaki ameshikilia simu sikioni “Haya ni majaribu makubwa sana kuwahi kuyapata katika uongozi wangu.Nilikuwa sahihi nilipohisi waliofanya shambulio hilo lengo lao lilikuwa ni kumpata mwanangu Coletha.Lazima hili ni kundi la IS na ndiyo maana wametaka kwanza wampate mtu wao kabla ya kitu kingine chochote.Watu hawa hatari natamani nitumie nguvu yangu kubwa kuwasaka lakini ninahofia usalama wa mwanangu Coletha.Kwanza ni mgonjwa na pili hawa jamaa wanaweza wakamuua.Ni watu wakatili mno.Kwa nini Olivia akajiunga na watu hawa?Anapata nini kutoka kwa magaidi?akajiuliza Dr Evans “Ninafikiria nivishirikishe vyombo vya usalama kuwatafuta hawa jamaa lakini linapokuja suala la mwanangu ninaingiwa na hofu.Sitaki kuhatarisha usalama wa mwanangu.Magaidi hawatanii wanaweza wakautoa uhai wa mwanangu.Wamenibana kwenye kona na sina namna nyingine ya kufanya Zaidi ya kuwasikiliza kwa ajili ya usalama wa mwanangu.Hiki ni kitendo cha ukatili mkubwa sana na hakivumiliki.Nitawaonyesha mimi ni nani pale nitakapokuwa nimempata mwanangu” akawaza Dr Evans na kumpigia simu Kaiza “Kaiza anaendeleaje Olivia? “Kwa sasa hali yake inaendelea vyema.Daktari uliyemtuma amemuhudumia na hali yake inaridhisha” akajibu Kaiza “Kaiza nataka umchukue Olivia na uende naye kitalu 2.Nataka ndani ya dakika ishirini uwe umefika pale” akasema Dr Evans na Kaiza akashangaa “Kuna nini mheshimiwa rais?akauliz “Kaiza fanya kama nilivyokuelekeza.Ndani ya dakika ishirini uwe umefika kitalu 2 ukiwa na Olivia.Anza safari sasa hivi” akasema Dr Evans na kukata simu. “I’m doing this for Coletha but you’ll pay for this you bastards.Lazima watalipa kwa gharama kubwa sana kitendo hiki walichokifanya cha kumwaga damu za watu na kumteka mwanangu.Kwa nini wananiandama kiasi hiki?Wameanza kwa kumuambukiza mwanangu virusi na kama haitoshi wakaona wamteke kabisa.Je ni hili suala la Edger Kaka ndilo linasababisha haya yote?Kwa nini hawataki kunielewa nikiwaeleza kuwa sifahamu chochote kuhusu suala hilo?Safari hii wamevuka mstari na lazima nitawaonyesha mimi ni nani”akawaza Dr Evans akiwa amekunja uso kwa hasira.





Mathew na Gosu Gosu walirejea katika makazi yao “Nataka nimuonyeshe Devotha sihitaji mzaha ninapokuwa kazini” akawaza Mathew baada ya kushuka garini akipiga hatua ndefu kuingia ndani Gosu Gosu akiwa nyuma yake.Mara tu alipofungua mlango wa sebuleni akakutana na kitu ambacho hakuwa amekitarajia.Akasimama pale mlangoni kwa sekunde kadhaa asiamini kile alichokishuhudia kwa macho yake “Jesus Christ !! akasema Mathew kwa sauti ndogo “Kuna nini Mathew?akauliza Gosu Gosu aliyekuwa nyuma yake. Mathew akatoka mbio na kumfuata Ruby ambaye alikuwa amelala sakafuni katika dimbwi la damu. “Ruby !! Ruby !! akaita Mathew na kumgeuza Ruby “Ruby !! akaita Mathew na Ruby akafungua macho.Hakuwa na nguvu.Alikuwa amepigwa risasi haikujulikana ni risasi ngapi kwani mwili wake wote ulikuwa umechafuka kwa damu “My God !! akasema Gosu Gosu “Please don’t die Ruby!! Akasema Mathew na kumuinua “Gosu Gosu tunatakiwa kumuwahisha Ruby hospitali” akasema Mathew akambeba Ruby hadi garini kisha wakaondoka kwa kasi kubwa.Gosu Gosu akiwa katika usukani na Mathew akiwa amemshikilia Ruby “De…dev..D..dd…” Ruby akalalama “Ruby !! akaita Mathew “Devot….” Akasema na kukohoa akatema damu “Ruby usiseme chochote..You’ll be fine.!! Akasema Mathew “De…Devoth….aaaa…sh..o..o t..m..m..eee!! akasema Ruby kwa taabu.Mathew akahisi kama nyundo kubwa imetua kichwani kwake “Devotha ?!! Mathew akasema kwa mshangao. “Dd…” Ruby akataka kusema lakini akashindwa fahamu zikampotea. “Ee Mungu baba nakuomba mponye Ruby.Bado namuhitaji sana katika operesheni hii.Nchi iko katika vitisho vya mashambulio ya magaidi,watu wengi watapoteza maisha na huyu ana msaada mkubwa katika mapambano haya” Mathew akaomba kimya kimya “Kwa nini Devotha ametaka kumuua Ruby?Japo sijajua sababu ya kutaka kumuua Ruby lakini Devotha amekosea sana.Ruby ni mtu wangu wa muhimu na yeyote anayemgusa ananigusa mimi moja kwa moja.Nitamsaka katika kila pembe ya dunia na nitahakikisha ninampata.” akawaza Mathew na kumsisitiza Gosu Gosu aongeze mwendo wa gari kuwahi hospitali. MPENZI MSOMAJI - RUBY ATAPONA?NINI SABABU YA KUSHAMBULIWA? DEVOTHA YUKO WAPI? - MAGAIDI WATAFANIKIWA KUMPATA OLIVIA? - FISHEL NA EHUD WANAKUJA TANZANIA KUMTAFUTA OLIVIA WATAMPATA? - MPENZI MSOMAJI USIKOSE SEHEMU IJAYO

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Mathew na Gosu Gosu waliwasili katika hospitali ya Dr Philip.Kabla gari halijasimama vizuri tayari Mathew alikwisha fungua mlango akaruka nje na kumshusha Ruby akambeba na kuanza kukimbia naye kuelekea mapokezi “Please Ruby don’t die!! Akasema Mathew Wauguzi walipomuona Mathew akiwa amembeba mgonjwa aliyechafuka damu haraka haraka wakaleta kitanda na kumtaka Mathew amlaze mgonjwa kitandani “Huyu mgonjwa amepata ajali?akauliza muuguzi mmoja “Dr Philip yuko wapi? Akauliza Mathew “Dr Philip yuko katika chumba cha upasuaji anafanya upasuaji kwa mgonjwa” akasema mmoja wa wauguzi . “Gosu Gosu” Mathew akasema na kumfanyia ishara Gosu Gosu asukume kile kitanda yeye akatangulia akikimbia kuelekea katika chumba cha upasuaji.Hospitali ile alifahamu vyema kwani amekuwa akifika pale mara kwa mara.Wauguzi walibaki wameduwaa wakishangaa. Mathew aliufungua mlango wa chumba cha upasuaji na Gosu Gosu akaingiza kitanda kile alichokuwa amelala Ruby.Muuguzi aliyekuwa mezani katika mapokezi ya chumba cha upasuaji akastuka na kusimama kwa hasira “Nini kimetokea?Nani karuhusu mgonjwa huyu aletwe hapa bila kufuata utaratibu?akauliza yule mwanamama muuguzi kwa ukali. “Dr Philip yuko wapi?akauliza Mathew “Kaka samahani naombeni mumtoe huyo mgonjwa wenu nje haraka sana.Hapa si mahali pa kuingia kila mtu anavyotaka.Zipo taratibu za kufuata kabla ya mgonjwa kuingizwa hapa.!! Yule mwanamama akaendelea kuwa mbogo. “Daktari gani ameruhusu mgonjwa wenu aletwe hapa? Akauliza yule mwanamama kisha akaenda katika simu iliyokuwa mezani kwake akapiga na kuanza kuzungumza kwa ukali “Rahel nani karuhusu mgonjwa aletwe chumba cha upasuaji bila kufuata utaratibu? Ninataka kumfahamu yule ambaye ameruhusu jambo hili litokee!! Hamjui kuna upasuaji mkubwa unaendelea hapa ndani ? Tafadhali naombeni tusiharibiane kaz….”Akasema kwa ukali na mara mkono wake uliokuwa umeshika simu ukashikwa na kushushwa chini akageuka kwa hasira na kujikuta akitetemeka baada ya kujikuta akitazamana na mdomo wa bastora. “Fungua huo mlango haraka sana mgonjwa aingizwe ndani akafanyiwe upasuaji !! akasema Mathew. “T..tt..taf……” akasema yule muuguzi akibabaika “Fungua mlango haraka sana!! Akafoka Mathew na yule muuguzi akafungua mlango Mathew akaingia ndani ya chumba cha upasuaji ambako upasuaji ulikuwa unaendelea kwa mgonjwa.Gosu Gosu akasukuma kitanda na kukiingiza ndani.Madaktari na wauguzi waliokuwa wanaendelea na upasuaji wakastuka .Dr Philip aliyekuwa anaongoza upasuaji ule akavua kitambaa alichokuwa amekivaa mdomoni “Mathew !! akasema kwa mshangao uliochanganyika na hasira na kumfuata Mathew “What are you doing here Mathew?! Akauliza Dr Philip kwa hasira “Tuko kati kati ya upasuaji kwa nini umefanya hivi Mathew? Kwa nini unakosa adabu hata kidogo tu? akaendelea kuuliza Dr Philip “Dr Philip hatuna muda mrefu wa mazungumzo nataka kila kitu kinachoendelea sasa kisimame na mgonjwa wangu ashughulikiwe kwanza ndipo muendelee na mambo yenu mengine” akasema Mathew “Mathew are you crazy?!!Tumelifumua tumbo la mgonjwa na hatuwezi kusimamisha upasuaji kwa sababu ya mgonjwa wako.Tuna kitanda kimoja tu humu ndani cha upasuaji.Nakushauri kama mgonjwa wako yuko katika hali mbaya mpeleke katika hospitali nyingine kuokoa maisha yake lakini kwa hapa hatutaweza kumsaidia kwa sasa atapoteza maisha.Tusiendelee kubishana muwahishe hospitali nyingine” akasema Dr Philip “Dr Philip huyu ni Ruby amepigwa risasi.Ni mtu muhimu mno kwangu na ninahitaji umshughulikie haraka apone” “I can’t do that Mathew !!Please get out of here now !! akafoka Dr Philip na kumsukuma Mathew atoke nje mara kwa hasira Mathew akamkaba shingoni akamsukuma na kumbana ukutani.Madaktari na wauguzi walipoona tukio lile wakahamaki na kutaka kumfuata Mathew wapambane naye Gosu Gosu akatoa bastora na kuwaelekezea “Kila mtu asimame mahala alipo asithubutu hata mtu mmoja kunyanyua mguu ama nitamfumua kwa risasi!! Akafoka Gosu Gosu akiwa amewaelekezea bastora “Dr Philip katika watu wote humu ndani ni wewe pekee unanifahamu vizuri mimi ni nani.Naomba usilifanye suala hili kuwa gumu.Muhudumie mgonjwa wangu haraka sana.Ukiacha akipoteza maisha nakuhakikishia hakuna atakayetoka salama humu ndani.I’ll kill you all!! akasema Mathew na kumuachia Dr Philip ambaye aliinama na kukohoa mfululizo “You are a devil Mathew !! How could you do this to me?Kwa miaka hii yote nimekuwa msaada mkubwa kwako iweje leo unanifanyia hivi?akauliza Dr Philip “Dr Philip sitaki maneno mengi.Are you going to do it or not?akauliza Mathew “What if I say no? ‘Dr Philip try to say no and I swear I’m going to kill all of you right now !! akasema Mathew na kumuelekezea bastora. Dr Philip alivimba kwa hasira alimtazama Mathew kwa jicho kali. “Arlight ! Weka silaha yako chini Mathew! Siamini kama umekuwa na roho ya kishetani namna hii !! akasema Dr Philip taratibu Mathew akashusha chini mkono wake ulioshika bastora.Dr Philip akaenda katika meza ile ambayo mgonjwa alikuwa amelazwa akiendelea kufanyiwa upasuaji “Jamani hatuna namna Zaidi ya kusimamisha upasuaji vinginevyo yataibuka mambo mazito humu ndani” “Dr Phill…….” Daktari mmoja akafungua mdomo wake akataka kusema kitu lakini Mathew aliyekuwa karibu akamuonya “Shut up !! Sitaki kusikia mtu akiongea humu Zaidi ya Dr Philip.Fanyeni kile atakachowaelekeza!! Akafoka Mathew Mashine kadhaa alizokuwa amefungwa yule mgonjwa aliyekuwa kitandani akifanyiwa upasuaji zikafunguliwa na mara mashine ya kuonyesha mapigo ya moyo ikaanza kutoa mlio na kusoma sifuri.Dr Philip akatikisa kichwa kwa uchungu.Mgonjwa yule waliyekuwa wakimfanyia upasuaji alifariki dunia.Akashushwa na kuwekwa katika kitanda cha wagonjwa kisha Ruby akalazwa katika kitanda cha upasuaji haraka haraka mashine zikaunganishwa wakaanza kuzitafuta risasi kwa kutumia mashine maalum za kupiga picha wakaziona risasi kisha upasuaji ukaanza haraka.Nyuso za madaktari wale bado zilionyesha simanzi kubwa kwa kile kilichokuwa kimetokea kwa mgonjwa yule kufariki dunia. “Mathew tumekwisha kubali tunamshughulikia mgonjwa wako tafadhali naomba mtoke nje.Chumba hiki ni kwa watu maalum tu.Show some respect ! akasema Dr Philip “I’m not going anywhere.Nataka nihakikishe kila kinachoendelea humu na ikitokea mgonjwa wangu akafariki ninawahakikishia ninyi nyote hakuna atakayetoka salama ndani ya chumba hiki! akasema Mathew akamfanyia ishara Gosu Gosu atoke nje kuhakikisha kunakuwa shwari. “Let’s do everything to save this woman.Anamaanisha anachokisema huyu jamaa he’s going to kill us all mwanamke huyu akifa.Tufanyeni kila kinachowezekana” akasema Dr Philip taratibu “Do you know him?akauliza daktari mwingine lakini Dr Philip hakujibu kitu. “Kwa nini Devotha amefanya jambo kama hili? Kwa nini ametaka kumuua Ruby?Ni kweli alikuwa na nia ya dhati ya kushirikiana nasi katika kuutafuta ukweli au alikuwa na lengo lake lingine? Mathew akajiuliza “Nilifanya kosa kubwa kumuamini Devotha kwa haraka kiasi kile lakini sipaswi kujilaumu sana kwa namna alivyojitolea kuniokoa na yeye mwenyewe kuhatarisha maisha yake mtu yeyote lazima angemuamini.Nitampata tu na atanipa majibu kwa nini alitaka kumuua Ruby mtu wangu wa muhimu sana” akawaza Mathew na kuyaelekeza macho yake pembeni alikokuwa amelazwa mgonjwa yule aliyefariki dunia baada ya upasuaji kusimama. “Mungu atanisamehe kwa hiki nilichokifanya lakini nimelazimika kufanya hivi ili kuokoa maisha ya Ruby.Nchi iko katika hatari kubwa ya mashambulizi ya kigaidi na katika kuwatafuta magaidi hawa ninamuhitaji mno Ruby” akawaza Mathew na kumtazama Dr Philip “Dr Philip ni rafiki yangu mkubwa na kwa muda mrefu amekuwa ni msaada mkubwa kwangu.Kila pale ninapokuwa katika operesheni zangu na kuhitaji msaada wa kitabibu humkimbilia yeye.Nimemuumiza sana kwa hiki nilichokifanya leo na ninaamini utakuwa ni mwisho wa urafiki wetu” akawaza Mathew akiendelea kushuhudia risasi zikitolewa katika mwili wa Ruby Risasi tatu zilitolewa huku Mathew akishuhudia zikawekwa katika kisahani cha bati.Ulikuwa ni upasuaji uliochukua saa mbili.Baada ya kuhakikisha hakuna tena risasi iliyobaki mwilini Dr Philip akaelekeza sehemu zilizopasuliwa zianze kushonwa,akaondoka pale mezani akiwa amejaa hasira akamfuata Mathew “Mathew let’s talk! Akasema Dr Philip kwa ukali na kumuongoza Mathew wakaingia katika chumba cha kubadilishia mavazi akamtazama Mathew kwa hasira “Tumefanya ulichokitaka.Tumeua mgonjwa kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumuokoa mgonjwa wako.Ninakuapia Mathew damu ya mgonjwa yule ambaye ameuawa bila hatia itakuandama kwa maisha yako yote” akasema Dr Philip na kuendelea kumtazama Mathew kwa hasira “Siamini Mathew kama kweli ni wewe ndiye uliyefanya hivi.Mathew ninayemfahamu mimi hawezi akafanya kitu kama hiki ulichokifanya leo.Nani amekuharibu kichwa chako namna hiyo Mathew?Hiki uli…” “Enough !..akasema Mathew kwa ukali “Sijutii nilichokifanya Dr Philip” akasema Mathew na kuendelea kumtazama Dr Philip kwa macho makali “Sikiliza vyema Dr Philip.Nchi iko katika kitisho kikubwa cha mashambulio ya kigaidi.Usiku huu kumefanyika shambulio la kigaidi katika hospitali ya Mtodora na mpaka sasa haijulikani watu wangapi wamepoteza maisha.Magaidi wamejipanga kufanya mashambulizi Zaidi na juhudi za kuwadhibiti magaidi hao zinaendelea.Mwanamke yule aliyepigwa risasi ana umuhimu mkubwa sana katika kuwatafuta magaidi hawa.Kuna mambo makubwa yanaendelea hapa nchini huyajui hivyo nilichokifanya ni kitu sahihi kabisa.Kwa namna Ruby alivyo muhimu katika vita hii ilikuwa lazima nifanye chochote kile ili aweze kupona.” akasema Mathew kwa ukali kisha wakaendelea kutazamana “Look Dr Philip.Najua nilichokifanya hakijakufurahisha lakini nimefanya kwa ajili ya usalama wa taifa.Tuko katika operesheni nzito sana hapa nchini na Ruby ana umuhimu mkubwa katika opresheni hiyo.N…..” “Mathew sitaki kusikia tena kitu chochote kutoka kwako.Tumekwisha ua mgonjwa asiyekuwa na hatia kwa sababu ya mgonjwa wako.Kitu pekee ninachokitaka sasa hivi…………..” akasema Dr Philip na kunyamaza akamtazama Mathew “Wanamalizia kufunga sehemu zilizopasuliwa na baada ya kumaliza utaondoka na mgonjwa wako sitaki kumuweka hapa katika hosptali yangu.Utampeleka kokote unakojua wewe lakini si katika hospitali hii.One more thing Mathew..” akanyamaza tena na kuvuta pumzi ndefu na kusema “Utakapoondoka hapa iwe ni mwisho wako kukanyaga tena hapa.Forget about me,sahau kama tumewahi kuwa marafiki kwani urafiki wetu wa muda mrefu umeishia hapa!! Akasema Dr Philip “Dr Philip !!akasema Mathew “Usiseme chochote Mathew.It’s over !! We’re over !! akasema Dr Philip na kutoka ndani ya kile chumba akarejea katika kitanda cha upasuaji ambako madaktari walikuwa wanaendelea kushona sehemu walizopasua “Tunampeleka wodi gani huyu mgonjwa?akauliza mmoja wa wauguzi “Hatuna nafasi ya kumuweka katika hospitali yetu.Mtu wake aliyemleta ataondoka naye na kumpeleka anakojua yeye! akasema Dr Philip na Ruby akawekwa katika kitanda akiwa hana fahamu.Dr Philip akamfuata tena Mathew “Mathew mgonjwa wako tayari tumekwisha mfanyia upasuaji na sasa uko huru kumpeleka mahala unakotaka lakini siwezi kumuweka katika hospitali yangu!! Akasema Dr Philip “Dr Philip please don’t do this to me” akasema Mathew “Mathew nilichokisema hakitabadlika.Tafadhali mtoe mgonjwa wako na umpeleke mahala unakotaka.Tafadhali Mathew tunahitaji kuendelea na shughuli nyingine kuna wagonjwa wengine wanahitaji upasuaji” akasema Dr Philip.Mathew akamtazama kwa muda kisha akasema “Fine.I need an ambulance.Mgonjwa huyu siwezi kumuweka katika gari dogo” akasema Mathew “Hilda piga simu gari la wagonjwa lifike hapa haraka sana” akaelekeza Dr Philip na Hilda yule mwanamama wa mapokezi ya chumba cha upasuaji akapiga simu na baada ya dakika mbili likafika gari la wagonjwa Ruby akaingizwa garini. “Tunaelekea wapi?akauliza dereva wa gari lile la wagonjwa “Shuka garini” akaamuru Mathew na yule dereva akashuka “Gosu Gosu nifuate na gari letu nitaendesha hili gari la wagonjwa” Mathew akamwambia Gosu Gosu na kuingia katika gari la wagonjwa akandoka pale hospitali akiwaacha watu wote katika mshangao mkuwa.Kilichotokea pale kilikuwa ni kama filamu lakini ni tukio halisi. “Let’s get back to work! Dr Philip akawaambia madaktari na wauguzi ambao bado walikuwa katika taharuki kubwa kufuatia tukio lile. “One more thing ! akasema Dr Philip “Kilichotokea hapa kitabaki humu humu.Hakuna mtu mwingine wa nje kufahamu kwani itakuwa mbaya Zaidi kwa upande wetu hasa mimi hivyo naomba kila mmoja ajitahidi kuufunga mdomo wake kama vile hakujatokea kitu chochote” akaelekeza Dr Philip na kazi zikaendelea kama kawaida Mathew baada ya kutoka nje ya hospitali ya Dr Philip akapunguza mwendo wa gari na kutoa simu yake akaandika namba na kupiga simu ikaita na kupokelewa “Hallow Mathew Mulumbi”ikasema sauti ya upande wa pili “Dr Hiran habari yako” akasema Mathew “Mimi mzima kabisa Mathew.Vipi wewe mzima?Uko kimya sana siku hizi Mathew” akasema Dr Hiran “Dr Hiran uko wapi sasa hivi? “Niko hapa hospitali ninajiandaa niondoke” “Usiondoke tafadhali ninakuja hapo sasa hivi nina shida nahitaji msaada” “Karibu sana Mathew utanikuta hapa” akasema Dr Hiran “Mungu aendelee kumpigania Ruby apone.Nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha anapona.Nitamlilia Mungu kwa machozi yote asimchukue Ruby bado ninamuhitaji sana” akawaza Mathew Alifika hospitali anakofanya kazi Dr Hiran akampigia simu akamtaka amfuate. “Mathew ! akasema kwa mshangao Dr Hiran baada ya kumona Mathew katika gari la wagonjwa. “Dr Hiran nimekuja kwako kuomba msaada wako.Ninaye mgonjwa wangu amefanyiwa upasuaji katika hospitali Fulani lakini nataka akatibiwe nyumbani kwangu.Nimekufuata unisaidie kwa hilo ndugu yangu.Niko tayari kwa gharama zozote hata mara mbili Zaidi kwa ajili ya kumuhudumia mgonjwa wangu huyu nyumbani.Tafadhali sana Dr Hiran” akasema Mathew.Dr Hiran akafungua mlango wa gari na kumtazama Ruby ambaye bado hakuwa na fahamu “Nini tatizo lake huyu mgonjwa hadi akafanyiwa upasuaji?Kwa nini hutaki akae hospitali ambako ni rahisi sana kupatiwa msaada kila pale hali yake itakapokuwa mbaya? Kwa namna alivyofanyiwa upasuaji anahitaji uangalizi wa karibu sana na ninashauri alazwe hapa hospitali” akasema Dr Hiran “Dr Hiran sitaki alazwe hospitali kwa sababu ya usalama wake.Kama inawezekana nyumba yangu inaweza kuwa hospitali ya muda kwa ajili ya mgonjwa wangu.Usihofu kuhusu pesa nitalipa kiasi chochote kitakachohitajika hata na Zaidi lakini ninachohitaji ni uangalizi wa mgonjwa wangu akiwa nyumbani” akasema Mathew na Dr Hiran akazama katika mawazo “Dr Hiran muda unakimbia sana naomba jibu tafadhali” “Huko walikomfanyia upasuaji walifanya makosa makubwa sana kuruhusu ukaondoka na mgonjwa akiwa bado kwenye hali hii.Anahitaji uangalizi wa karibu sana kwani hali yake inaweza kubadilika muda wowote.Ngoja nikaandae vifaa ambavyo nitavihitaji” akasema Dr Hiran na kurejea ndani baada ya dakika chache akarejea akiwa na gari ambalo lilikuwa na vifaa ndani yake safari ikaanza akilifuata gari la Mathew hadi walipofika nyumbani kwa Mathew.Ruby akashushwa garini na kuingizwa ndani.Gosu Gosu akamsaidia Dr Hiran kushusha vifaa alivyokuja navyo wakaingiza ndani na mashine kadhaa zikafungwa kumsaidia Ruby “Mashine hizi tunazifunga tu kusaidia mifumo ya mwili wake ifanye kazi lakini hali yake inaendelea vyema.Nimekuja na chupa kadhaa za damu ili kumuongezea damu.” Akasema Dr Hiran na kuchukua sampuli ya damu akapima kujua ni aina gani ya damu aliyonayo Ruby kisha akamtundikia chupa ya damu. “Kwa sasa kilichobaki ni kusubiri mgonjwa azinduke” akasema Dr Hiran “Nashukuru sana Dr Hiran.Fanya kila uwezalo bila kujali suala la fedha” akasema Mathew “Mathew suala la fedha halina kipaumbele sana kitu kikubwa ni kuokoa uhai.Lakini nini hasa tatizo la mgonjwa?Kwa nini alifanyiwa upasuaji?akauliza Dr Hiran “Alipigwa risasi” “Dah ! Ni nani huyo mkatili aliyefanya kitendo hicho kwa mrembo kama huyu?akauliza Dr Hiran huku akimtazama Mathew “Mathew una hakika hapa tulipo tuko salama?akauliza tena “Usihofu Dr Hiran tuko salama na ndiyo maana nimemleta mgonjwa wangu hapa.Endelea kumtazama mgonjwa mimi na mwenzangu tuna mazungumzo kidogo” akasema Mathew kisha akamchukua Gosu Gosu wakaenda katika ofisi yao “Najaribu kutafakari sababu ya Devotha kufanya hivi alivyofanya lakini sijapata jibu” akasema Gosu Gosu “Hata mimi nimetafakari sana jambo hili.Tulimuamini Devotha kama mwenzetu na sijui kwa nini amebadilika na kutaka kumuua Ruby.Hatutaweza kupata jibu kwa nini amefanya hivi hadi pale tutakapomtia mikononi.Tumuombee Ruby aweze kuzinduka na kutueleza nini kilichotokea hapa.Wakati tukimsubiri Ruby azinduke tuendelee kutafuta namna ya kumpata Kaiza ambaye ndiye aliye na Ol……………..” Mathew akastuka ghafla “Nini Mathew?akauliza Gosu Gosu baada ya kuuona mstuko wa Mathew “Nimekumbuka komyuta moja haipo hapa.Ni ile ndogo aliyokuwa anaitumia Ruby ambayo ameweka program zake zote” “Unadhani Devotha ameondoka nayo?akauliza Gosu Gosu “Hakuna mwingine anayeweza kuondoka nayo zaidi yake.Tulimuacha humu ndani yeye na Ruby na tuliporejea tumemkuta Ruby peke yake akiwa amepigwa risasi.Nashawishika kuamini lazima Devotha ndiye aliyeondoka nayo.Vile vile ameondoka na simu ile aliyokuwa anaitumia Ruby.Itakuwa rahisi sana kufahamu mahala alipo kwa kufuatilia ile simu ninazifahamu namba zake.Kuna vitu hata mimi ninavifahamu katika teknolojia ya kompyuta na mawasiliano.Nimekuwa karibu sana na Ruby kuna vitu vingi nimejifunza toka kwake” akasema Mathew “Kama unaweza kufuatilia simu ile na kufahamu mahala alipo itakuwa vyema sana.Mimi ufahamu wangu wa kompyuta ni mdogo sana na nimeifahamu kompyuta hivi karibuni baada ya kuanza kufanya kazi kwako.Nimekulia msituni nikipigana vita.Hatukuwa na kompyuta kule na hata kama tungekuwa nayo hakuna muda wa kujifunza” akasema Gosu Gosu.Mathew akakaa katika kompyuta na kuanza kuitafuta programu ambayo ingemuwezesha kufuatilia simu ile aliyoondoka nayo Devotha.Baada ya muda akaegemea kiti “Vipi Mathew?akauliza Gosu Gosu “Nimeshindwa kuipata programu ambayo tunaweza kuitumia kufuatilia simu ile aliyoondoka nayo Devotha.Haya mambo yanahitaji utaalamu mkubwa.Mimi utaalamu wangu ni katika mapambano na si katika mambo haya ya teknolojia” akasema Mathew na kuzama katika tafakari mara akakumbuka kitu. “Nisubiri dakika mbili” akasema na kuelekea chumbani kwake akafungua kabati kubwa la nguo na ndani ya sanduku hilo kulikuwa na kasiki dogo akalifungua na kutoa kitabu Fulani akafunua kurasa haraka haraka akatabasamu baada ya kupata kile alichokuwa anakitafuta akarejea katika chumba cha kusomea “Nina kawaida ya kuweka kumbu kumbu ya vifaa vyangu vyote vya mawasiliano.Kuna namba Fulani za siri ndani ya simu ni muhimu sana kuzifahamu ambazo zinaweza kusaidia kufahamu mtumiaji wa simu mahala alipo” akasema Mathew na kuchukua simu yake akaandika namba Fulani kutoka katika kile kitabu akapiga “Hallow” ikasema sauti ya mwanadada upande wa pili wa simu “Sasha unazungumza na Mathew Mulumbi hapa kutoka Tanzania”akasema Mathew “Mathew Mulumbi?akauliza Sasha “Ndiyo.Umenisahau?aka uliza Mathew “Nikumbushe tafadhali tumeonana wapi?Najaribu kukumbuka jina hilo lakini sikumbuki kama nimewahi kukutana na mtu kutoka Tanzania” akasema Sasha “Tuliwahi kukutana Mumbai katika klabu moja.Kuna mtu ulikuwa unamfuatilia lakini akagundua Kamba unamfuatilia akatuma kundi lake wakakuvamia kukuteka kwa bahati nzuri nilikuwepo karibu nikakusaidia kupambana na wale jamaa tukawashinda.Tayari umenikumbuka? “Ouh ni wewe kumbe?Sasa nimekukumbuka Mathew.Nimelikumbuka na hili jina.Ni muda wa miaka kadhaa umepita sasa hatukuwahi kuwasiliana ndiyo maana imekuwa rahisi kusahau jina lako lakini sura yako bado naikumbuka.Habari za Tanzania?akauliza Sasha “Tanzania salama kabisa.Vipi wewe unandeleaje? “Ninaendelea vyema Mathew.Uliniahidi utakuja Marekani lakini mpaka sasa kimya.Lini utakuja kutembea huku.Nitafurahi sana kukuona” “Nitakuja Sasha kama nilivyokuahidi” “Mathew nashukuru sana kwa kunikumbuka.Umenikumbus ha mbali sana” akasema Sasha “Bado uko CIA?akauliza Mathew “Ndiyo.Kwa sasa nimerudishwa hapa makao makuu Langley.Siko tena katika kazi za nje,kwa nini umeuliza? Sasha akauliza “Sasha ninahitaji msaada wako” “Sema unahitaji nini Mathew? “Nahitaji unisaidie kufuatilia simu Fulani kujua mtumiaji wake mahala alipo” akasema Mathew na Sasha akaomba ampe namba za siri za hiyo simu pamoja na namba za laini ya simu akamuomba asubiri kwa dakika chache “Mathew hujawahi kuishiwa maarifa.Sikujua kama unaye mtu ndani ya CIA anayeweza akatusaidia” akasema Gosu Gosu “Ninao marafiki zangu kutoka katika mashirika mbalimbali ya kijasusi duniani ambao huwatumia kuomba msaada pale ninapokuwa nimebanwa na jambo.Huyu Sasha nilifahamiana naye Mumbai nilimsaidia kumuokoa kutoka katika genge la wahuni.Toka hapo tukawa marafiki lakini ni muda mrefu umepita hatujawasiliana ndiyo maana imenilazimu kumkumbusha” akasema Mathew na kunyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni Sasha “Mathew nimefuatilia simu hiyo na kuipata mahala ilipo.Ninakutumia sasa hivi katika simu yako ramani ya mahala ilipo simu hiyo utaendelea kuifuatilia.Kama kuna msaada Zaidi utauhitaji utanijulisha” akasema Sasha “Ninashukuru sana Sasha” akasema Mathew na katika simu yake ukaingia ujumbe uliotumwa na Sasha akaufungua.Ilikuwa ni ramani iliyoonyesha mahala simu ile aliyoondoka nayo Devotha ilipo “Tumempata.Kwa mujibu wa ramani hii simu inaonekana ipo katika bustani ya Kiembe kavu.Ninahisi kuna mtu amemfuata mahala hapo.Nitakwenda kumfuatilia wewe utabaki hapa kufuatilia hali ya Ruby na kulinda usalama.Hakikisha yule daktari habanduki mle ndani na kama kutatokea hatari yoyote basi utakabiliana nayo.Bado naamini tuko katika hatari kwani hatujui lengo la Devotha kutugeuka na kukimbia.Umakini mkubwa sana unahitajika” akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akabadili mavazi akachukua bastora mbili na kuingia garini akaondoka kuelekea bustani ya mapumziko ya Kiembe kavu kumfuata Devotha “Devotha alifikiri hataweza kupatikana.Alikosea sana,hana sehemu ya kukimbilia nitamsaka kila kona hadi nihakikishe amepatikana na atalipa kwa hiki alichokifanya.Kama ni kutusaliti angeondoka kimya kimya bila kumpiga risasi Ruby ambaye ni mtu wangu wa muhimu mno.Nataka nimuonyeshe kwamba yeye bado ni mchanga sana katika hizi kazi”akawaza Mathew Ilimchukua dakika ishirini kufika katika bustani ya Kiembe kavu.Bado simu ile iliendelea kuonekana katika ramani aliyotumiwa na Sasha. “Devotha anafanya nini hapa bustanini?Mbona imekuwa ni muda mrefu haondoki eneo hili?Kuna mtu anamsubiri?akajiuliza Mathew wakati akiegesha gari akashuka na kuanza kuifuatilia simu ile kwa tahadhari kubwa.Alifika hadi sehemu ambayo ilionyesha katika ramani kuwa ndipo ilipo simu.Eneo lile hakukuwa na mtu.Kulikuwa na viti vya mbao vya kupumzikia lakini vilikuwa tupu. “Where is she?akajiuliza Mathew akiangaza kila upande kwa tahadhari kubwa lakini hakukuwa na mtu eneo lile.Kilichomshangaza bado aliendelea kuiona simu ile eneo lile.Akaamua kuipiga ili kupata majibu na mara akasikia mlio wa simu katika maua yaliyokuwa pembeni ya kiti cha kupumzikia.Akapekua maua na kuikuta simu “Damn you Devotha!! Akasema Mathew kwa hasira “Huyu mwanamke ni mjanja sana na inaonekana mbinu nyingi za kijasusi anazifahamu.Alijua tunaweza kumfuatilia kwa kutumia simu hii ndiyo maana akaja akaitupa hapa ili kutupoteza mwelekeo.Huu si mwisho Devotha nitakupata tu.Muda wako unahesabika” akawaza Mathew na kumpigia simu Gosu Gosu akamueleza kilichotokea “Huyu mwanamke ni mjanja sana anafahamu mbinu za kijasusi hata hivyo atapatikana tu muda si mrefu.Vipi hali ya Ruby?Mathew akauliza “Bado daktari yuko hapa anaendelea kumuangalia anasema maendeleo yake ni mazuri” akasema Gosu Gosu “Sawa Gosu Gosu nitakupigia tena baada ya muda” akasema Mathew na kukata simu “Devotha hakuondoka na simu hii kwa ajili ya kuja kuitelekeza hapa.Lazima kuna mtu aliwasiliana naye” akawaza Mathew na kuangalia katika kumbu kumbu za simu zilizopigwa lakini hakukuwa na rekodi zozote. “Amefuta rekodi zote za mawasliano na hii inaonyesha kuna mtu aliwasiliana naye na ndiyo maana amefuta kila kitu” akawaza Mathew na kumpigia simu Sasha “Sasha samahani kwa kukusumbua tena.Nimefuatilia simu ile na kuipata lakini nimeikuta imetelekezwa na aliyeichukua hayupo.Ninataka unisaidie kujua namba ya mwisho kuwasiliana na simu hii usiku huu” akasema Mathew na Sasha akamuomba asubiri kidogo.





Gari dogo la rangi nyeusi lilisimama nje ya nyumba moja ya ghorofa moja Devotha akashuka na kumlipa dereva fedha halafu akatembea kuelekea katika geti.Akabonyeza kengele ya getini na baada ya dakika mbili mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na msichana ambaye anamfahamu Devotha “Karibu sana dada Devotha” akasema yule msichana na Devotha hakujibu kitu akaongoza moja kwa moja kuelekea ndani.Aliingia sebuleni na kumkuta mwanadada mmoja mweupe sana aliyekuwa sofani amejilaza akitazama runinga “Devotha karibu sana”akasema yule mwanadada na kuinuka akakaa “Nashukuru sana Bella”akasema Devotha na kukaa huku akifumba macho kwa maumivu “Devotha are you okay?akauliza Bella “I’m okay usihofu” akasema Devotha “Utakunywa kinywaji gani?akauliza Yule msichana aliyemfungulia geti “No thank you” akajibu Devotha “Devotha kuna tatizo gani?Si kawaida yako kufika hapa usinywe hata maji?akauliza Bella. “Jane samahani naomba nizungumze na Bella” Devotha akamwambia yule msichana na alipotoka akamfuata Bella sofani “Bella watoto wako wapi?akauliza Devotha “Wamelala.Kuna nini? Akauliza Bella kwa wasiwasi “Sina muda wa kuelezea kwa sasa lakini naomba uwaandae watoto tunandoka” “Tunaondoka?Tunakwen da wapi? “Mko katika hatari kubwa.Kuna watu wanajiandaa kuja kuwachukua watoto wako.Please Bella sina muda wa kuelezea tafadhali jiandae tuondoke” akasema Devotha “Devotha sikuelewi.Nani wanataka kuja kumchukua mwanangu na kwa nini?akauliza Bella “Bella tafadhali tusiendelee kupoteza muda.Nitakueleza mbele ya safari.Jiandae tunaondoka” akasema Devotha “Hapana Devotha siwezi kuondoka hapa hadi utakaponieleza kuna tatizo gani” akasema Bella Devotha akafungua vifungo vya shati alilokuwa amevaa na Bella akastuka “Umefanya nini? “Nimeshambuliwa na watu hao ambao wanapanga kuja kuwachukua wanao.Tafadhali Bella naomba uniamini na ufanye kama ninavyokuelekeza” akasema Devotha na Bella akasimama akabaki anamuangalia Devotha “Kaiza anafahamu suala hili? “Sina mawasiliano yake.Naomba unipe simu niwasiliane naye tafadhali” akasema Devotha na Bella akazitafuta namba za simu za mume wake akampigia lakini simu haikuwa ikipatikana “Hapatikani katika namba zake za simu”akasema Bella “Hata mimi nimemtafuta katika namba zake za simu hapatikani.Nenda kajiandae Bella wale jamaa watafika hapa muda si mrefu .Tutamjulisha Kaiza jambo hili” akasema Devotha.Bella akaenda chumbani kwake akawatazama watoto wake mapacha waliolala katika kitanda pembeni ya kitanda chao kikubwa. “Siko tayari mtu yeyote ahatarishe usalama wenu.Ninawapenda kuliko kitu chochote” akasema Bella na kufungua droo katika meza yake ya vipodozi akatoa kitabu akatafuta namba Fulani ambazo mume wake Kaiza alimuelekeza azitumie kumpigia kama kuna dharura akaziandika katka simu na kupiga simu ikapokelewa haraka “Bella kuna tatizo? Akauliza Kaiza baada ya kupokea simu “Kaiza nimekutafuta simuni hupatikani” “Nilikuelekeza utumie namba hizi kama kuna dharura kubwa tu.Kuna tatizo gani? Akauliza Kaiza kwa ukali kidogo “Kaiza kuna jambo limetokea hapa nyumbani muda huu.Amekuja Devotha..” “Devotha?! Kaiza akastuka sana “Ndiyo amekuja hapa muda si mrefu na amenitaka niwakusanye watoto tuondoke.Anadai kuna watu wanapanga kuja kuwateka watoto” “Kuwateka watoto?akauliza Kaizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Ndiyo.Anadai hivyo kwamba kuna watu wanataka kuja kuwachukua watoto” akasema Bella “Bella nisikilize vizuri.Mwanamke huyo ni muongo mkubwa” “Kaiza nini kimetokea?akauliza Bella “Bella naomba unisikilize tafadhali” akasema Kaiza “Katika kasiki langu dogo kuna bastora iko humo.Nilikupeleka katika mafunzo ya kutumia silaha nikiamini nyakati kama hizi zinaweza kujitokeza.Nataka uichukue hiyo bastora na ufanye kila unaloweza kuwalinda watoto wetu.Jitahidi kuvuta muda kuna watu ninawatuma hapo sasa hivi wanakuja kumdhibiti Devotha.Mwanamke huyo ni hatari mno wala usimpe nafasi ya kuwakaribia watoto wetu.Umenielewa Bella?akauliza Kaiza “Kaiza I’m so scared.Umeniogopesha sana” “Usiogope Bella.Tafadhali kuwa jasiri.Devotha si mtu mzuri na ukimpa nafasi ataondoka na watoto wetu.Tafuta namna ya kufanya kuvuta muda wakati timu ninayoituma inakuja hapo muda si mrefu” akasema Kaiza “Sawa Kaiza ngoja nijaribu” akasema Bella na kukata simu akavuta pumzi ndefu “Kuna nini kinaendelea?Devotha amekuwa kiongozi wa Kaiza na amekuwa akifika hapa mara kwa mara amekuwa rafiki yetu mkubwa,nini kimetokea leo hadi Kaiza akatamka maneno yale?Lazima kuna suala kubwa limetokea.Ngoja nifuate ushauri wa mume wangu yeye ndiye anayejua kinachoendelea huko katika shughuli zao.Mtihani kwangu ni namna ya kumdhibiti Devotha hadi hao watu atakaowatuma Kaiza watakapofika.Sina uwezo wowote wa kupambana lakini nitafanya kila niwezavyo kwa ajili ya wanangu.Siwezi kukubali Devotha akawachukua wanangu.Anataka awafanyie nini?akajiuliza Bella wakati akifungua kasiki na kutoa bastora akaitazama na kuvua gauni refu alilokuwa amevaa kisha akavaa suruali ya jeans na fulana pana ndefu akaichomeka bastora ile kiunoni akajitazama katika kioo bastora haikuwa inaonekana akashuka chini.Devotha alipomuona Bella anashuka akasimama “Bella tayari umewaandaa watoto”akauliza Devotha “Devotha kuna kitu naomba ukanisaidie” akasema Bella na kupanda ngazi Devotha akimfuata kwa nyuma.Waliingia katika chumba ambacho hakikuwa na kitu kilikuwa kinafanyiwa ukarabati. “Nikusaidie nini Bella” akauliza Devotha mara Bella akaitoa bastora kiunoni akamuelekezea Devotha “Naomba piga magoti tafadhali !! akasema Bella kwa ukali “Bella unataka kufanya nini?Weka chini bastora tafadhali !! akasema Devotha “Devotha piga magoti chini haraka sana!! Akasema Bella “Bella please !! You are doing a mistake !! akasema Devotha “Devotha sitaki utani katika hili.Piga magoti na inua mikono juu!! akasema Bella “Bella you wont shoot me..Please put your gun down !! This is a mistake!! Akasema Devotha akapiga hatua moja kutaka kumsogelea Bella “Devotha tafadhali usinisogelee!! Ukijaribu kupiga hatua moja nitakupiga risasi ! akasema Bella.Devotha akamtazama na kusema “No Bella you won’t shoot me.Nimekuja kukuokoa wewe na familia yako.Nimekuwa karibu na familia yenu ndiyo maana siko tayari watoto wako malaika wasio na kosa waingie katika mikono ya watu wabaya.Tafadhali weka chini silaha yako Bella” akasema Devotha “Devotha piga magoti !! akafoka Bella “Bella kwa nini unakuwa mbishi?Weka silaha yako chini tafadhali na unisikie kile ninachokisema.Watu wabaya wanawatafuta wanao” akasema Devotha “Kwa nini wanawatafuta wanangu?akauliza Bella “Sikiliza Bella kuna jambo kubwa linaloendelea hivi sasa hapa nchini na linaihusisha idara yetu.Kuna watu wanataka ku….” Akasema Devotha akiwa ameyaelekeza macho yake kama kinyonga katika bastora aliyokuwa ameishika Bella “Devotha don’t move !! akasema Bella “Weka bastora chini Bella!! Akasema Devotha akipiga hatua ya pili “Devotha nitakupiga risasi tafadhali!! Akasema Bella “No Bella you wont shoot me !! akasema Devotha na kuinua mguu kabla hajaweka mguu chini ukasikika mlio wa risasi.Jicho la Devotha lilikuwa katika kidole cha Bella na alifahamu Bella anakwenda kupiga risasi akawahi kujirusha pembeni kwa wepesi mkubwa.Bella alipatwa na mstuko mkubwa baada ya mlio ule wa risasi kusikika.Aliduwaa kwa muda na sekunde hizo ndizo alizozihitaji sana Devotha akainua ndoo iliyokuwa na rangi iliyoganda akampiga nayo Bella mkononi akapepesuka na kuweka mkono mmoja ukutani na kabla hajageuka Devotha alikwisha fika na kumtandika teke zito akaanguka chini na kitu cha kwanza alichokiwahi Devotha ni bastora. “Bella why are you so stupid? Nimekuja hapa kukusaidia wewe na familia yako kwa nini hutaki kunielewa?akauliza Devotha.Bella alikuwa chini akitetemeka. “Devotha tafadhali usiwachukue watoto wangu !! akasema Bella akilia “You fool !! ninataka kukusaidia Bella.Sina nia mbaya na watoto wako.Ninawapenda kama watoto wangu ndiyo maana niko hapa.Tafadhali inuka twende tukawachukue watoto tuondoke hapa” akasema Devotha “Devotha tafadhali usiwachukue watoto wangu.Devotha niko chini ya miguu yako !! akalia Bella “Inuka !! akafoka Devotha “Devotha kuliko kukuona ukiwachukua watoto wangu niko tayari uniue.Niue sasa hivi Devotha kisha ukawachukue watoto wangu uwafanye unachokitaka” akasema Bella akilia.Devotha akamtazama na kuvuta pumzi ndefu na kumrushia Bella bastora “Take the gun.Kill me if you want” akasema Devotha na Bella akabaki anashangaa “Simama ! akasema Devotha na Bella akasimama “Sina nia mbaya nawe Bella.Sijaja hapa kukudhuru wewe na wanao.Ninawapenda sana na niko hapa kwa ajili ya kuwasaidia.Naomba uniamini Bella ninataka kuwasaidia lakini kama hamtaki msaada wangu fine.Nitaondoka lakini msinilaumu kwamba sikuwaonya.Mko tayari niwasaidie au mnasubiri watoto waje wachukuliwe?akauliza Devotha lakini Bella alikuwa kimya “Nijibu Bella kama mnataka msaada wangu na kama hamtaki niondoke zangu” akasema Devotha.Bado Bella alikuwa anatetemeka mikono.Alishindwa aseme nini. “Fine.Hamtaki msaada wangu ninaondoka lakini kitakachowakuta msinilaumu” akasema Devotha na kukishika kitasa cha mlango akaufungua. “Wait ! akasema Bella “Tafadhali niweke wazi Devotha nini hasa kinachoendelea?Nani wanataka kuwachukua watoto wangu?Nieleze tafadhali nielewe” “Bella nimekuwa rafiki yenu kwa muda mrefu nimekuwa nikija hapa kwenu mara kwa mara na watoto wenu ninawapenda sana.Kitu gani kinachokufanya uwe na wasiwasi na mimi leo?akauliza Devotha.Bella akavuta pumzi ndefu na kusema “Nilipokwenda chumbani niliwasiliana na Kaiza kupitia namba za siri alizonipatia nimpigie endapo kuna dharura nikampata nikamueleza umefika hapa na unataka kutuchukua mimi na watoto akanieleza akanionya nisikupe nafasi ya kuwachukua watoto.Wewe na Kaiza mmekuwa watu wa karibu kwa muda mrefu na wewe ndiye mkuu wake wa kazi.Nini kimetokea hadi Kaiza anipe onyo lile?Nieleze tafadhali kila kitu.Kama kweli umekuja kwa lengo la kutusaidia mimi na wanangu nieleze kila kitu bila kunificha” akasema Bella.Devotha akamtazama na kusema “Bella kuna jambo kubwa linaendelea katika idara yetu ambalo limezua tofauti kubwa kati yangu na Kaiza.Kwa ufupi tu ni kwamba siko tena katika idara ile ya siri ya mambo ya ndani ya nchi na hivi sasa wananitafuta ndiyo maana Kaiza amekuonya usinipe nafasi ya kuwasaidia akiamini labda lengo langu ni kuwadhuru.Sina nia hiyo Bella na ndiyo maana niko tayari kuwaacha na kuondoka zangu endapo hamuhitaji msaada wangu tena.Kitu ninachotaka ukifahamu ni kwamba kuna watu wanapanga mipango ya kuja kuwachukua hapa wewe na wanao” akasema Devotha “Devotha hicho ndicho ninachotaka kukifahamu.Watu hao ni akina nani na kwa nini wanataka kuwachukua watoto wangu?akauliza Bella “Bella hiyo ni hadithi ndefu na inahitaji muda wa kutosha kukuelezea.Tafadhali fanya maamuzi kama unataka niwasaidie na kama hutaki msaada wangu mimi niondoke zangu” akasema Devotha Bella alibaki amesimama akitafakari “Bella muda unakimbia fanya maamuzi.Ni wewe mwenye kufahamu uchungu wa watoto na si Kaiza hivyo wewe ndiye unayepaswa kufanya maamuzi ya usalama wao.Ninakupa sekunde kumi za kufanya maamuzi” akasema Devotha.Bella alikuwa anahema haraka haraka “Sekunde kumi zimekwisha na umeshindwa kufanya maamuzi mimi ninaondoka lakini kitakachowatokea msinilaumu kwamba sikuwaonya” akasema Devotha na kuanza kupiga hatua. “Devotha subiri” akasema Bella “Bella please don’t waste my time.Fanya maamuzi!! Akafoka Devotha “Please help us ! akasema Bella “Are you sure? Akauliza Devotha “Tafadhali tusaidie Devotha.Usiache wanangu wakatekwa na watu wabaya.Kama unaweza kutusaidia tafadhali fanya hivyo” akasema Bella huku macho yake yakiwa na machozi “Wako wapi watoto?Haraka sana twende tukawaandae” akasema Devotha na kumfuata Bella wakaingia katika chumba chao cha kulala “What a beautifull angels ! akasema Devotha na kutabasamu alipowaona watoto wale wakiwa wamelala katika kitanda chao.Bella akamuelekeza mlezi wao awaandae watoto kwa ajili ya safari. “Devotha unatupeleka wapi ukitutoa hapa?akauliza Bella “Somewhere safe” akajibu Devotha Wakati watoto wakiendelea kuandaliwa Devotha akasikia kama vishindo vya mtu “Bella kuna watu wangapi mnaishi humu?akauliza “Ni sisi unaotuona hapa na Kaiza hakuna mwingine” akajibu Bella “Fungua mlango chungulia nje kama kuna mtu” akasema Devotha na kuchomoa bastora yake.Bella akaonyesha wasi wasi “Bella fungua mlango angalia kama kuna mtu hapo nje ya mlango! Akasema Devotha.Kwa woga Bella akaenda mlangoni na kukinyonga kitasa mlango ukafunguka akajikuta amesukumwa akaanguka chini na watu watatu wakarukia ndani.Devotha alikuwa mwepesi sana mara tu Bella aliposukumwa akaanguka chini tayari alikwisha rukia katika kitanda na kumnyakua mmoja wa watoto akamuweka kifuani kwake na kumuelekezea bastora kichwani. “Devotha weka silaha yako chini tafadhali !! akaamuru mmoja wa wale jamaa “Ayoub wewe ni mtu mdogo sana kunipa mimi amri! Akasema Devotha “Devotha ninakuamuru kwa mara nyingine tena weka silaha yako chini na mlaze mtoto kitandani.I have orders to shoot you !! akasema Ayoub akiwa amekunja sura kuonyesha hana masihara “C’mon Ayoub you won’t shoot me.Najua mmetumwa na Kaiza lakini hata yeye hatakubali kuona watoto wake wakiuawa.Kabla haujaizinga bastora yako na kunipiga risasi watoto hawa wawili ambao Kaiza amehangaika kuwapata watakuwa wamekufa.Kwa nini tuwaue malaika hawa?Niko hapa kuokoa maisha yao na si kuwadhuru hivyo wekeni silaha zenu chini na mniache niendelee na zoezi langu la kuwaokoa watoto hawa” akasema Devotha “Devotha tafadhali naomba uweke silaha chini na umlaze mtoto huyo kitandani ! akasema Ayoub “Ayoub ninawapa wewe na wenzako sekunde kumi kuweka silaha zenu chini ama sivyo watoto hawa watakufa!! “One ! akaanza kuhesabu Devotha “Two ! “Devotha please don’t kill my children !! akalia Bella aliyekuwa amesimama mlangoni “Three !! akasema Devotha.Ayoub na wenzake wakajipanga vyema “Four !! akasema Devotha “five ! Devotha akaendelea kuhesabu.Bella akakurupuka na kwenda kusimama kati kati ya Devotha na wale jamaa waliotumwa na Kaiza “Tafadhalini wekeni silaha zenu chini.Devotha hayuko hapa kuidhuru familia yangu she’s here to help us.Sikieni anachokisema na muweke chini silaha zenu haraka! Akasema Bella “Mama tafadhalisogea pembeni tupe nafasi ya kutekeleza maagizo!! Akasema Ayoub “Ninyi na huyo aliyewatuma hamfahamu chochote.Devotha hana tatizo lolote she’s here to help us.Tafadhali naombeni muweke silaha zenu chini na muondoke hapa haraka sana!! Akafoka Devotha “Mama sogea pembeni tafadhali usitulazimish….” Akasema Ayoub lakini Bella akamkatisha kwa ukali “Kama mnataka kumpiga risasi Devotha anzeni kwanza na mimi !! akasema Bella akimkaribia Devotha akainyakua simu yake iliyokuwa mezani na kwa haraka akampigia Kaiza “Bella vijana wangu wamefika hapo nyumbani tayari?akauliza Kaiza baada ya kupokea simu “Kaiza waambie watu wako waweke silaha zao chini na waondoke hapa ndani haraka sana” “Kwa nini bella?Nimewatuma waje wamdhibiti Devotha na kuwanusuru watoto wetu”akasema Kaiza “Devotha hana tatizo kama unavyodai.She’s here to help us.She’s here to save our family!! Akasema Bella huku akilia “Bella sikuelewi una maanisha nini? Nimekueleza Devotha ni mtu hatari sana.Tafadhali waache vijana wangu wafanye kazi yao niliyowatuma.Nahitaji sana kumpata Devotha” “Kaiza hali ya humu ndani ni mbaya na watoto wangu ndio wako katika hatari.Watu wameelekezeana bastora na muda wowote wanaweza wakashambuliana na waathirika wakubwa watakuwa watoto wangu.Tafadhali Kaiza naomba uwaamuru watu wako waweke silaha zao chini.Hivi tuzungumzavyo kuna bastora katika kichwa cha mtoto wangu na muda wowote anaweza akapigwa risasi.Limalize hili jambo tafadhali!! Akasema Bella “Damn !! akasema Kaiza kwa hasira na kumtaka Bella ampe simu Ayoub azungumze naye “Zungumza na mkuu wako” akasema Bella na Ayoub akachukua ile simu akazungumza na Kaiza kisha akampa simu Bella na kuwageukia wenzake “Stand down ! Ayoub akawaeleza wenzake na wote wakashusha silaha zao chini. “Nyote mtaendelea kukaa ndani ya chumba hiki hakuna atakayeruhusiwa kutoka nje ya chumba hiki.Yeyote atakayethubutu atapigwa risasi bila huruma.Hayo ni maelekezo kutoka kwa kiongozi wetu!! Akasema Ayoub “Kuna watu wanataka kuja kuwachukua watoto hawa.Lazima tuwatoe hapa kwa usalama wao !! akasema Devotha “NImesema hakuna atakayeruhusiwa kutoka ndani ya chumba hiki bila sababu.Kwa yeyote atakayepuuza agizo hili tutampiga risasi hivyo endeleeni kukaa humu humu ndani! Yeyote atakayekuja hapa kwa lengo hilo la kuwachukua watoto atatukuta hapa tutapambana naye” akasema Ayoub na kuwaelekeza vijana wake watoke nje na kufunga mlango.Watu wawili wakabaki mlangoni pale wakilinda kuhakikisha hakuna mtu anayetoka ndani ya kile chumba wengine wakajipanga sehemu mbali mbali za nyumba ile kuhakikisha hakuna anayeingia wala kutoka. Bella akawachukua wanae akawakumbatia machozi yalikuwa yanamtoka “Bella kwa nini hukuniambia kama kuna watu wametumwa na Kaiza kuja kunikamata?akauliza Devotha “Nisamehe Devotha.Huu ulikuwa ni mpango wa Kaiza lakini niliamini tungewahi kuondoka hapa kabla ya watu hawa aliowatuma hawajafika” akasema Bella “Do you trust me?akauliza Devotha “I do” akajibu Bella “Ulipaswa kunieleza jambo hili haraka.Chukua simu na umjulishe mume wako nahitaji kuonana naye aje hapa nyumbani haraka” akasema Devotha.Bella akachukua simu akampigia mume wake akamjulisha kile kilichokuwa kimetokea pale nyumbani. “Bella kwa nini umefanya hivi? Kwa nini umemuamini Devotha na kusimama kumtetea?akauliza Kaiza kwa ukali “Kaiza,Devota hana tatizo lolote.She’s here to save us! “Sikiliza Bella humfahamu Devotha.Huyo ni mwanamke hatari sana na sitaki kabisa akae karibu na familia yangu!! “Bella naomba nipe simu nizungumze na Kaiza” akasema Devotha na Bella akampa simu “Hallow Kaiza!! Akasema Devotha “Devotha you are a devil.Kitu gani unakitafuta kwa familia yangu?Nakuhakikishia hautatoka salama humo ndani! akasema Kaiza “Sikiliza Kaiza nakutaka uje hapa nyumbani kwako haraka sana.Ninakusubiri hapa.Ninakuonya usijaribu kutaka kufanya mpango wowote wa kutuma watu wako waje wanikamate.Niko hapa na familia yako na jaribio lolote la kutaka kunikamata litaiweka familia yako katika hatari kubwa.Njoo haraka sana nyumbani nataka kuzungumza nawe” akasema Devotha na kukata simu.







“Mheshimiwa rais tayari nimefika hapa kitalu 2 nasubiri maelekezo yako” Kaiza akamjulisha Rais baada ya kufika kitalu 2 mahala alikoelekezwa ampeleke Olivia “Kuna mtu nimemtuma hapo anakuja kumchukua Olivia” “Anakuja kumchukua Olivia?Anampeleka wapi? Mbona bado tunaendelea kumuhoji? Kaiza akauliza “Ninamuhitaji mimi” akajibu Dr Evans kwa ukali kidogo “Vipi kuhusu baba yake? “Agrey Themba endeleeni kumuhifadhi pale pale mahala nilipokuelekeza hadi hapo nitakapowapa maelekezo mengine.Umenielewa Kaiza? “Nimekuelewa mzee” “Good.Vipi zoezi la kuwatafuta Devotha na Mathew Mulumbi limefikia wapi?akauliza Dr Evans na Kaiza akastuka akabaki kimya “Kaiza !! akaita Dr Evans baada ya Kaiza kuwa kimya. “Mheshimiwa rais kuna muelekeo mzuri sana kuna taarifa zenye uhakika za mahala alipo Devotha.Tunaendelea kuzifanyia kazi taarifa hizo ili kujua kama zina ukweli wowote na kisha tutafika mahala hapo kumchukua Olivia.” akasema Kaiza “Good.Nitafurahi sana nitakapopata taarifa za kupatikana kwa Devotha na wenzake.Kaiza weka uzito mkuwa sana katika suala hilo” “Sawa mheshimiwa Rais usiku huu hakuna kulala msako unaendelea hadi tuhakikishe tunampata Olivia” akasema Kaiza na Dr Evans akakata simu “Mpaka Rais kuamua kumchukua Olivia akazungumze naye ni wazi amekwisha poteza kabisa imani na sisi.Nahisi ule usemi wake kwamba ataifunga idara hii endapo tutashindwa kupata taarifa muhimu kutoka kwa Olivia kuhusu kikundi cha kigaidi cha IS sasa unaelekea kutimia.Kitu pekee ambacho kitamfanya arudishe imani kwetu ni kwa kumpata Devotha.Tayari ninafahamu mahala alipo hivyo sipaswi kuipoteza nafasi hii ambayo ni muhimu sana kwangu.Nataka rais aniamini ninaweza kazi na nitaanzia kwa Devotha” akawaza Kaiza Baada ya kupita dakika kumi akawasili mtu aliyetumwa na rais.Olivia akatolewa ndani akiwa amefungwa mfuko kichwani akaingizwa katika buti la gari lile kisha yule jamaa akaondoka naye “Mzee tayari nimemchukua yule mtu” akasema yule jamaa akiwa garini baada ya kumchukua Olivia “Safi sana.Nenda mahala nilipokuelekeza usubiri maelekezo yangu” akasema Dr Evans Baada ya mjumbe yule wa rais kuondoka,Kaiza hakutaka kupoteza muda akaingia katika gari lake na kuondoka kuelekea nyumbani kwake. “Imekuaje Bella akamuamini Devotha na hata kudiriki kumtetea eti hana tatizo na amekwenda pale kuwakinga dhidi ya watu wanaotaka kuiteka familia yangu?Yule mwanamke hapaswi kuaminiwa kabisa ni muongo na muuaji.Laiti Bella angefahamu mambo aliyoyafanya Devotha leo asingethubutu kusimama na kumtetea” akawaza Kaiza “Ninamuamini sana Bella na lazima iwepo sababu ya yeye kuamua kuchukua upande wa Devotha.Yawezekana ameamua kujiweka upande wake ili niweze kupata nafasi ya kumpata Devotha bila kutumia nguvu.Sasa nimeuelewa mchezo alioucheza Bella.Ana akili nyingi sana yule mwanamke hadi akaweza kumuingia Olivia na kumteka kiakili” akawaza Kaiza na kutabasamu kwa mbali “Mwisho wa Olivia umefika kwani hataweza kutoka mle ndani salama na ataeleza kila kitu.Alifanya makosa makubwa sana kuamua kujiunga na akina Olivia ambao wanatumiwa na kikundi cha IS.Namuonea huruma sana Devotha kwa kile kitakachomkuta lakini ameyataka yeye mwenyewe kwa kuchagua kushirikiana na magaidi na mbaya Zaidi akadiriki kuua hata watu wetu ambao hawalali kuhakikisha nchi inakuwa salama.” Akaendelea kuwaza Kaiza





Simu ya Dr Evans iliita na kumfanya ahisi baridi.Alizifahamu namba zile alizoziona katika kioo cha simu yake.Ni namba alizopigiwa na wale magaidi waliofanya shambulio katika hospitali ya Mtodora na kumteka mwanae.Mikono ilimtetemeka alipoishika ile simu “Ee Mungu naomba ujasiri wa kulikabili hili jambo” akaomba kimya kimya na kuipokea ile simu “Hallow” akasema Dr Evans “Nilikuahidi kukupigia baada ya dakika thelathini muda umefika.Nataka kujua umetekeleza maelekezo yetu?akauliza yule jamaa “Ndiyo ninaye mtu mnayemtaka.Kabla sijawapa mtu mnayemtaka nataka kujua namna nikatakavyompata mwanangu” akasema Dr Evans “Si rahisi hivyo kama unavyodhani mheshimiwa rais.Mwanao utampata lakini kwa wakati ule tunaotaka sisi na kama utaendelea kutekeleza kila kile tutakachokuelekeza.Usihofu bado tutakuwa na mazungumzo marefu mimi na wewe lakini kwa sasa nataka Olivia apelekwe Mkumbira mtaa wa Binti Kassim.Nyuma ya soko la mfenesini kuna msikiti na mbele kidogo ya msikiti kuna miembe mitatu ambako kuna gari limeegeshwa hapo.Nataka Olivia aingizwe katika gari hilo.Gari litakalomleta Olivia mahala hapo nataka awepo mtu mmoja pekee ndani.Tunafuatilia na kama tukiona kuna watu wawili ndani yake au kuna gari linafuata utamkosa mwanao.Kuwa makini sana wakati huu” akasema yule jamaa “Vipi kuhusu mwanan………….” Dr Evans akataka kuuliza lakini tayari simu ilishakatwa. “Bastard !! akasema Dr Evans na kuitupa simu kitandani akashika kiuno “Natamani nitume kikosi kikawasambaratishe hawa magaidi lakini ninasita kufanya hivyo kwa sababu ya mwanangu kwani anaumwa.Wameshika mpini hawa jamaa ninatakiwa kufanya kile wanachokitaka.Ngoja nitoe maelekezo Olivia apelekwe mahala walipoelekeza” akawaza Dr Evans na kumpigia simu yule mtu wake ambaye alimtuma kumchukua Olivia Kitalu 2 akampa maelekezo ya mahala kwa kumpeleka Olivia SAA TATU ZILIZOPITA “Devotha umekosea sana kubishana na Mathew.Unatakiwa kumfahamu Mathew vyema kama unataka kufanya naye kazi.Hapendi kubishana.Hata kama kuna kitu unataka kumuelekeza tafuta namna nzuri ya kumuelekeza na si kufanya kama ulivyofanya wewe.Hata mimi sikufurahi namna ulivyojibizana naye” Ruby akamwambia Devotha mara tu alipomaliza kuzungumza na Mathew simuni.Devotha akamtazama na kuuliza “Umefanya kazi na Mathew kwa muda gani? “Nimekuwa nafanya kazi na Mathew kwa muda mrefu sasa.Kwa nini umeuliza? “Unaonekana u mtiifu sana kwake na ndiyo maana umeweza kufanya naye kazi muda mrefu.Mimi sijazoea kupewa amri kama alivyofan…” akasema Devotha na kunyamaza baada ya kuhisi mtetemo katika mkono wake wa kushoto. “Excuse me ! akasema Devotha na kutoka akaelekea bafuni akavua ile glovu ambayo amekuwa akivaa mkononi.Devotha hakuwa na vidole viwili katika mkono wake wa kushoto hivyo basi huvaa glovu maalum ambayo imewekewa vidole vya bandia na kumfanya aonekane ana vidole vilivyokamilika.Kutoka ndani ya ile glovu akatoa kidole kimoja akakifungua na kutoa kitu Fulani mfano wa kadi ndogo halafu akavaa tena ile glovu akatoka na kumfuata Ruby “Ruby naweza kutumia simu yako?akauliza Devotha “Hii simu Mathew ameiweka maalum kwa ajili ya kuwasiliana sisi kwa sisi katika operesheni yetu na hatutakiwi kupiga namba tofauti zaidi ya ile ya Mathew au Gosu Gosu” “Nataka kumtafuta Saada.Huyo ndiye alitusaidia tukaweza kumuokoa Mathew lakini mpaka sasa hakuna anayejua mahala alipo” akasema Devotha.Ruby akasita “Nisaidie Ruby.Saada ni mtu muhimu sana kwangu.Lengo langu ni kufahamu kama ni mzima na yuko wapi” akasema Devotha na Ruby akampatia ile simu akatoka akaenda chooni “Simuamini huyu mwanamke.Anaonekana ana jambo hata ukimuona usoni macho yake yanaonyesha wasi wasi.Au amepatwa na wasiwasi baada ya kumueleza kuwa alifanya kosa kubishana na Mathew? Nahisi hivyo kwa sababu alionyesha kupata mstuko wakati tukilizungumzia suala hilo.Anataka kuwasiliana na nani? Ni kweli anataka kuwasiliana na huyo mtu wake kujua mahala alipo? Kama kweli anataka kuwasiliana na huyo mtu wake kwa nini amekwenda kujificha chooni?Hapa kuna kitu anakificha” Akawaza Ruby na kuinuka akanyata kumfuata Devotha kule chooni. Devotha akaingia chooni akajifungia na kufungua ile simu ya Ruby akaweka ile kadi ndogo aliyoitoa katika glovu yake kisha akawasha simu na ujumbe ukaingia katika simu ile akausoma.Kilichoandikwa katika ujumbe ule ni namba ambazo alihitaji kuwasiliana nazo.Devotha akapiga simu katika zile namba alizotumiwa “Hallow” akasema Devotha “Your Identification number please! Ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili “BRAVO 15E 361 A” Akasema Devotha “Thank you Devotha,wait for three seconds” ikasema sauti ya yule mwanamke “Nilijua tu huyu mwanamke anatudanganya.Ngoja niendelee kusikiliza nijue mtu anayewasiliana naye” akawaza Ruby aliyekuwa amesimama mlangoni akisikiliza kila alichokizungumza Devotha “Devotha”ikaita sauti upande wa pili “Hallo Dr Yonathan ! akasema Devotha “Nahitaji kuonana nawe usiku huu” akasema Dr Yonathan “Kuna nini Dr Yonathan?akauliza Devotha “Ninakusubiri ofisini kwangu.Fika haraka sana” akasema Dr Yonathan “Sawa ninakuja hapo ubalozini mud..” Devotha akastuka baada ya kuhisi kuna mtu mlangoni.Akasogea mlangoni na kuufungua akachungulia nje hakuona mtu akaufunga tena ule mlango “Dr Yonathan nitakuja hapo muda si mrefu” akasema Devotha na kukata simu akaichomoa ile kadi “She was listening to me !! akawaza Devotha akairejesha ile kadi ndogo katika kile kidole ndani ya glovu halafu akajitazama katika kioo. “She’s such a pretty lad but she’s forcing my hand !! akawaza Devotha na kuikunja sura yake halafu akatoka mle bafuni akarejea chumbani alikokuwa Ruby na kumrejeshea simu yake “Umefanikiwa kumpata uliyekuwa unamtafuta?akauliza Ruby na Devotha akawa kimya kwa muda halafu akasema “Ruby mimi unanionaje?akauliza Devotha “Kwa nini unauliza hivyo Devotha? “Just answer me Ruby ! akasema Devotha “Nakuona wa kawaida tu” akajibu Ruby akiendelea na kazi yake katika kompyuta “Umekosea sana Ruby mimi siko kawaida kama unavyodani.Mimi ni binadamu lakini waweza niita binadamu mashine.Unionapo hapa nina jicho moja linalofanya kazi lakini wengi hawalifahamu hilo.Mwili wangu uliwahi kuharibiwa vibaya sana kwa bomu na nilifanyiwa operesheni Zaidi ya thelathini na nane hadi mwili wangu ukawa hivi unavyoniona leo.Ninaposema ninao utofauti na wanadamu wengine ninamaanisha hivyo.Nikupe mfano mdogo tu kwamba ninao uwezo mkubwa sana wa kusikia kuliko uwezo wa mwanadamu wa kawaida.Ninaweza kusikia hata sisimizi akipita kitu ambacho katika hali ya kawaida hakiwezekani.Nilitengenezw a hivi kwa sababu maalum ndiyo maana ninasema mimi ni binadamu mashine” akanyamaza na kumtazama Ruby ambaye alionekana kuwa na wasiwasi “Nilipokuwa maliwatoni nilikusikia ukiwa umejibanza mlangoni ukisikiliza kile ninachozungumza.Sikufurahi shwa na kitendo kile.Kwa nini ukanifuatilia kusikiliza mazungumzo yangu?akauliza Devotha “Hapana sijakufuatilia Devotha” akasema Ruby na Devotha akamnasa kofi kali lililombabatiza Ruby kabla hajakaa sawa akapigwa teke kali lililompeleka hadi chini.Devotha akaichukua bastora iliyokuwa juu ya meza. “Ulikuwa na wasi wasi na mimi? Ulitaka kufahamu ninafanya nini? Ulikosea sana.Umejitafutia kifo chako wewe mwenyewe.I’m sorry Ruby !! akasema Devotha na kuizinga bastora akaachia risasi tatu zilizompata Devotha.Akachukua simu ya Devotha pamoja na kompyuta yake akaviweka katika mkoba wake na kutoka.Alijaribu kufungua geti akashindwa kwani lilihitaji namba maalum za kufungulia ambazo hakuzifahamau akarejea ndani akachukua kiti na kukiweka ukutani akaruka na kushika kingo za ukuta akapanda na kujirusha nje.Akabaki pale chini akigugumia kwa maumivu makali sehemu ile ya bega alikokuwa na jeraha la risasi.Akapeleka mkono akahisi maji maji,jeraha lilikuwa linatoa damu.Akainuka na kuanza kupiga hatua za haraka kisha akaandika namba Fulani katika simu ile ya Ruby na kupiga. “Anthony naomba uje mara moja unichukue nimekwama sehemu Fulani” akasema Devotha akimpigia dereva taksi ambaye humtumia katika manunuzi ya vitu mbali mbali akamuelekeza sehemu ya kumkuta. “Natakiwa kuwahi kumuokoa Bella na wanae kabla Mathew Mulumbi hajafika hapo na kuwachukua.Japokuwa sijamuelekeza mahala wanakoishi lakini naamini lazima atatfuta mbinu nyingine hadi apafahamu.Yule jamaa ana macho ya kikatili mno anaweza akachinja wale watoto” akawaza Devotha “Licha ya kwamba sitaki watoto wale wapate msuko suko wowote kutoka kwa Mathew lakini nahitaji kutumia jambo hili kama njia ya kunikutanisha tena na Kaiza.Ninahitaji tena kujenga mahusiano kati yangu naye ili niweze kumpata Olivia.Kaiza amechukua nafasi yangu na ndiye anayeaminiwa na Rais hivi sasa na kikubwa zaidi anafahamu alipo Olivia hivyo basi lazima nitafute namna ya kuwa karibu naye na kumfanya aniamini” akawaza Devotha “Mossad wana nini hadi watake kuonana nami usiku huu? Haijawahi kutokea nikaitwa usiku namna hii lazima litakuwa ni suala muhimu mno la dharura.Ngoja nikawasikilize” akawaza Devotha





Gari jeusi aina ya BMW lilifika katika soko la Mifenesini katika mtaa wa binti Kassim likapunguza mwendo.. “Naliona gari moja linakaribia sokoni nina wasi wasi ndilo linalomleta Olivia” akasema jamaa mmoja aliyekuwa na redio ndogo ya mawasiliano akiwa juu ya mti mkubwa wa mwembe. “Abbas unaweza ukatazama ndani kuna watu wangapi?akauliza mtu mwingine “Linakaribia kufika hapa nilipo nitaangalia na kuwajulisha” akasema Abbas. Gari lile lililokuwa linakwenda taratibu sana lilifika katika ule mwembe aliokuwa amejificha Abbas.Akajitahidi kuchungulia ndani kwa kutumia hadubini ndogo aliyokuwa nayo “Abbas unaona chochote? “Idris gari lina vioo vyeusi kiasi kwamba ni vigumu kuona ndani” akajibu Abbas Gari lile lilipita na kuelekea eneo la msikiti “Amefika msikitini” akasema Isa aliyekuwa amejificha katika pembe moja ya ukuta uliozunguka msikiti. “Unaweza kuona ndani kuna watu wangapi?akauliza Idris “Namuona dereva peke yake sioni mtu mwingine” akajibu Isa. Gari lile liliupita msikiti likaelekea katika miembe mitatu ambako kuna gari lilikuwa limeegeshwa. “Anakaribia miembe mitatu.Mlioko eneo hilo hakikisheni mtu anayeshushwa ni Olivia” Idris mkuu wa operesheni ile akasema Gari lile lilifika katika miembe mitatu na kuegesha nyuma ya gari moja lililokuwa limeegeshwa pale.Baada ya dakika mbili mlango wa dereva ukafunguliwa akashuka jamaa mmoja na kwenda kufungua buti ya gari.Muda huo wote alikuwa anaangaliwa na watu waliojificha sehemu mbali mbali za eneo lile na mara tu alipofungua buti ya gari wakatokea watu watano na kumtaka dereva wa lile gari kusogea pembeni wakamtoa mtu aliyekuwa ndani ya buti akiwa amefunikwa mfuko kichwani wakamvua ule mfuko na kummulika mmoja wao akatoa picha na kuifananisha akatikisa kichwa kuwaelekeza wenzake kuwa yule ni Olivia.Haraka haraka wakamshusha kutoka katika ile gari na kumpakia katika gari lao na kumuamuru dereva yule kuondoka haraka eneo lile.Alifuatiliwa hadi alipoondoka kabisa ndipo gari nyingine nne zilizokuwa zimefichwa maeneo yale zikajitokeza na wale wote waliokuwa wamejificha sehemu mbali mbali wakajitokeza wakaingia katika magari na kuliweka kati kati gari lile aliokuwa amewekwa Olivia wakaondoka.Idris kiongozi wa operesheni ile akampigia simu Fahad mkuu wao “Fahad tayari tumempata Olivia” akasema Idris “Kazi nzuri sana Idris.Hakukuwa na tatizo lolote?akauliza Fahad “Hakukuwa na tatizo lolote.Rais ametekeleza kila kitu kama ulivyomuahidi” akajibu Idris “Sawa tunawasubiri.Chukueni tahadhari kuhakikisha Olivia hajawekewa kitu chochote kitakachowawezesha kumfuatilia na kujua mahala alipo” akasema Fahad “Tayari tumekwisha mchunguza na hatujapata kitu chochote alichofungwa” akajibu Idris Baada ya kuzungumza na Idris,Fahad akampigia simu Dr Evans “Umeanza vyema kwa kutekeleza kile tulichokuelekeza.Tumempata Olivia na mwanao ana nafasi kubwa ya kuendelea kuwa hai” “Mmekwisha pata mlichokuwa mnakihitaji.Naombeni mnipatie mwanangu” akasema Dr Evans “Tunakwenda taratibu mheshimiwa rais.Utampata mwanao lakini si rahisi namna hiyo.Endelea kututegea sikio nitakuja kuzungumza nawe tena lakini narudia tena kukuonya endelea kuwa mkimya na jambo hili ulifahamu wewe peke yako” akasema Fahad na kukata simu huku akitabasamu na kupiga simu kwa Habiba Jawad. “Fahad habar za huko?akauliza Habiba “Huku kwema Habiba tunaendelea vizuri” “Kuna taarifa gani Fahad? “Ninazo taarifa njema kwamba tumefanya shambulio usiku huu katika hospitali kuu ya Mtodora na tayari tunao Coletha mtoto wa Rais pamoja na Olivia Themba” akasema Fahad “Hizo ni taarifa nzuri sana Fahad.Hongereni mno kwa kazi hii kubwa.Huu ni ushindi mkubwa sana” akasema Habiba “Mama ninawataka msiwe na hofu tutampata Edger muda si mrefu sana kwa sasa kinachoendelea ni kumtibu mtoto wa Rais kwani hali yake si nzuri sana kisha tutazungumza na rais kumtaka atuonyeshe mahala alipo Edger.Kwa sasa tumembana kwenye kona na atatueleza kila kitu tunachokitaka kwa kuwa tayari tunaye mwanae hana ujanja.Tuanze maandalizi ya kumpokea Edger kwa sababu uhakika wa kumpata ni mkubwa sana” akasema Fahad “Fahad nataka nikuombe kitu kimoja.Tafadhali usimuue Olivia kama alivyoelekeza Khalid Radwan.Muhoji taratibu sana ufahamu ukweli sababu ya kutekwa kwake.Siamini kama kweli anatumiwa na serikali ya Tanzania kuchota siri zetu.Jambo lingine unalopaswa kulifahamu ni kwamba Seif anampenda sana Olivia.Endapo akipatikana na akijua mwanamke ampendaye tumemuua hatafurahi hata kidogo_Olivia amemfanyia Seif mambo mengi hivyo basi muhoji taratibu kujua ukweli.Nisikilize mimi na si Khalid.Umenisikia Fahad?akauliza Habiba “Ndiyo mama Habiba nimekuelewa nitafanya kama ulivyoelekeza” “Ahsante sana nawatakia kila la heri katika kufanikisha mpango huu.Nijulishe tafadhali kila kinachoendelea ili na sisi tujiandae” akasema Habiba na kuagana na Fahad. “Sasa uhakika wa kumpata mwanangu Seif ni mkubwa sana.Kama tayari wamefanikiwa kumpata mtoto wa Rais pamoja na Olivia basi muda si mrefu Seif atapatikana.Tunatakiwa kuanza maandalizi mara moja ya kumpokea Seif.Sijui nitafanya sherehe gani kwa kumuona tena mwanangu” akawaza Habiba na kumpigia Sayid Omar simu akampa taarifa zile halafu akampigia simu Khalid Radwan akamjulisha kuhusu taarifa zile alizozipokea kutoka kwa Fahad “Hizo ni habari njema sana Habiba.Nilijua tu njia pekee ya kumpata Seif ni kwa kumshikilia mtoto wa rais na sasa atatueleza mahala aliko Seif.Nimefurahi pia kusikia kwamba yule msaliti Olivia amepatikana.Ametufanyia jambo baya na mpaka sasa hatufahamu ni mambo gani amewaeleza serikali ya Tanzania kuhusu sisi.Kitakachompata kitakuwa ni fundisho kwa wengine wenye tabia kama hii ya usaliti.Wakati mwingine Habiba usiwaamini watu kwa haraka kama ulivyofanya kwa Olivia.Hakupaswa kabisa kufahamu chochote kuhusu sisi.Kwa kuwa amepatikana adhabu yake ni kumuondoa kichwa! Akasema Khalid “Khalid nilimuamini Olivia kwa kuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwetu.Bila yeye tusingefika hapa tulipofika.Ni kwa sababu yake Seif hakupoteza maisha alipowekewa sumu.Ni kwa sababu yake tuna uhakika leo kwamba Seif yuko hai.Hatupaswi kuamini kwa haraka hivyo kwamba Olivia alikuwa anatumiwa na serikali.Tunatakiwa kumuhoji taratibu kuupata ukweli na ndivyo nilivyomuelekeza Fahad.Olivia tumetoka naye mbali ninamfahamu vyema na sina hakika kama anaweza kuwa anatumiwa na serikali kutuchunguza kama unavyodai.Ushauri wangu ni kumfanyia mahojiano na kumchunguza kama kweli anatumiwa na serikali kutuchunguza.Tukijiridhisha kama kweli anatumiwa basi nitaridhia auawe lakini endapo hatutagundua chochote kuhusu kutumiwa na serikali Olivia bado ni mtu muhimu sana kwetu” akasema Habiba “Habiba mimi sijawahi kukutana na Olivia hivyo siwezi kubishana nawe kama unahisi Olivia hawezi kuwa msaliti ufanyike uchunguzi kama ulivyoelekeza na endapo watu wetu wakijiridhisha kwamba hana mahusiano na serikali mimi sina tatizo naye kabisa lakini nina uhakika mkubwa kwamba amekuwa akitumiwa na serikali na ninaamini uchunguzi wa kina ukifanyika mtagundua hilo.Tukiweka pembeni hilo suala la Olivia kuna jambo ambalo nataka lifanyike kwa haraka ikiwezekana usiku huu.Nataka Coletha na Olivia waondolewe Tanzania.Nataka wapelekwe nchini Kenya ambako tunazo nyumba zetu kadhaa wakahifadhiwe huko na kila kitu kitaendelea kutokea kule sitaki tuendeshe operesheni kutokea Dar es salaam kwani kuna uwezekano mkubwa wakafahamu mahala walikofichwa Olivia na mtoto wa Rais.Pale Dar es salaam watabaki watu wachache.Rais atakapoelekeza mahala alipo Seif watu wetu ambao watakuwa katika utayari watamchukua haraka sana na kumpeleka nchini Kenya na kutokea pale atasafirishwa kuja huku.Nitakapomaliza kuzungumza nawe nitampa maelekezo Rashid kule Kenya afanye maandalizi ya kuwapokea watu hao muhimu na kuhakikisha wanakuwa salama.Habiba huu ni ushindi mkubwa sana tumeupata.Tumehangaika sana kuingia Tanzania na kuijenga himaya yetu na seif ni mtu pekee ambaye tulimjenga na kumtegemea sana kwa ajili ya kuishika Tanzania lakini likatokea hili jambo lililotokea na kuvuruga mipango yetu yote.Kwa sasa baada ya kuwa na uhakika wa kumpata Seif tunatakiwa kuendelea na mipango yetu ya kuhakikisha tunampata Rais ambaye atakuwa na mahusiano nasi ambaye atatusaidia kujenga mtandao wetu.Tukifanikiwa kujenga mtandao wetu Imara nchini Tanzania tutakuwa tumeliteka bara zima la Afrika.Tanzania ni kioo cha Afrika na tukifanikiwa kujiotesha pale kusambaa kwenda katika nchini nyingine Afrika ni jambo jepesi sana” akasema Khalid “Mawazo yako ni mazuri Khalid hata mimi nakubaliana nawe kuhusu kuwahamisha Olivia na mtoto wa Rais kuwapeleka nchini Kenya.Naamini kila kitu cha kuwawezesha kuwahamisha watu hao kutoka Tanzania kwenda Kenya wanacho hivyo basi kama kuna uwezekano zoezi hilo lifanyike kabla hakujapambazuka Afrika Mashariki.Kama kuna chochote kitahitajika kutoka kwangu nijulisheni haraka” akasema Habiba “Kila kitu cha kuwawezesha kufanya hilo zoezi wanacho.Tumewekeza sana katika tawi letu la Nairobi kwani ndiyo makao makuu kwa nchi za Afrika mashariki na kati.” Akasema Khalid kisha akaagana na Habiba akampigia simu Rashid ambaye ni mkuu wa IS tawi la Afrika Mashariki anayeishi Mombasa. “Rashid kuna taarifa njema.Ile timu uliyoituma kwenda Dar es salaam wakishirikiana na wenzao waliowakuta pale wamefanikiwa kuwapata mtoto wa Rais pamoja na yule mwanamke aliyetusaliti Olivia.Hii ni dalili njema kuwa tumekaribia sana kumpata Seif”akasema Khalid “Mungu ni mkubwa sana” akasema Rashid “Kufuatia ushindi huo mkubwa ninataka ufanye yafuatayo.Tuma boti haraka sana iende Dar e salaam nataka Olivia na huyo mtoto wa Rais wahamishiwe nchini Kenya.Kuendelea kuwaweka nchini Tanzania ni hatari wanaweza wakagundulika mahala walipo na tukawapoteza na tukiwapoteza tutakuwa tumeharibu operesheni nzima.Baada ya kuwaondosha Tanzania kila kitu kitaendeshwa kutokea Kenya.Rashid narudia tena kukukumbusha kwamba operesheni hii ni muhimu mno.Tunamuhitaji Seif na tuko karibu sana kumpata na nina uhakika yawezekana usiku wa leo au kesho tukafahamu mahala alipo.Nadhani umenielewa Rashid” akasema Khalid “Nimekuelewa Khalid.Kila kitu kitakamilika usiku wa leo” akasema Rashid “Naamini kila kitu mnacho cha kuwawezesha kukamilika opresheni hii.Kama kutakuwa na tatizo au mtahitaji chochote tujulisheni haraka sana” “Khalid kila kitu tunacho na kama tukihitaji chochote tutawajulisha” akasema Rashid. Baada ya kuzungumza na Rashid nchini Kenya Khalid akampigia simu Fahad nchini Tanzania na kumjulisha kuhusu mpango wa kuwahamisha Olivia na Coletha kuwapeleka Kenya na maandalizi yakaanza haraka.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kaiza alifika nyumbani kwake na kuwakuta watu wake aliowatuma kumchukua Devotha wakiwa wamejipanga kuimarisha ulinzi kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayetoka au kuingia ndani ya nyumba ile “Devotha bado yuko ndani? Kaiza akamuuliza Ayoub “Ndiyo mkuu bado yumo ndani” “Familia yangu pia imo ndani?Wapo salama?akauliza Kaiza kwa wasiwasi “Wote wako salama kabisa” akajibu Ayoub “Good.Ninakwenda ndani jiwekeni sawa nikiwapa ishara mtavamia chumbani haraka sana na kumchukua Devotha” akasema Kaiza na kuelekea chumbani kwake akaufungua mlango na kuingia ndani akawakuta Devotha na Bella wakiwa wamekaa wanazungumza wakionekana hawana tatizo lolote baina yao.Kaiza akawatazama “My love karibu” akasema Bella akiinuka na kumfuata mume wake akamshika mkono na kumketisha sofani.Macho ya Kaiza aliyaelekeza kwa Devotha “You are such a devil.Hujatosheka na watu uliowaua hadi ukaifuata familia yangu?Sikujua kama una roho ya kikatili namna hii Devotha.Watoto wangu wamekosa nini hadi uwafuate na kuhatarisha maisha yao?Huna hata huruma na hawa malaika ambao hawafahamu chochote?akauliza Kaiza kwa ukali lakini Devotha hakumjibu kitu “Love,punguza hasira na usubiri Devotha azungumze nawe.Hayuko hapa kwa ubaya au kuhatarisha uhai wa watoto wetu.She’s here to save us.Tafadhali msikilize” “Bella kitu gani amekuambia huyu mwanamke hadi ukamuamini.Huyu ni shetani hana hata chembe moja ya huruma.She’s not who you think she is.Usikubali hata kidogo akaingia ndani ya kichwa chako na kukupa maneno mazuri ukamuamini.She’s a …..” “Enough !! akasema Devotha kwa ukali na kusimama.Kaiza naye akasimama. “What !! You want to kill me now? Akauliza Kaiza kwa ukali. “Love,relax !! akasema Bella akimpiga piga mumewe mgongoni. “We need to talk Kaiza.Bella give us a room.Take out the twins” akasema Devotha.Bella na yule mtumishi wake wakawabeba watoto wakawatoa nje ya kile chumba na kuwaacha Kaiza na Devotha “Sit down ! akasema Devotha “No I can’t.Huna tena uwezo wa kuniamuru chochote.Kama kuna chochote unataka kuniambia make it quick na wala usijidanganye kwamba utatoka hapa salama.Ninakupa muda wa dakika tano kueleza kile unachotaka kunieleza! Akasema Kaiza “Look Kaiza ,I’m not here to harm your family.Ninawapenda watoto wako na kamwe siwezi kuwadhuru! Akasema Devotha “So why are you here ? akauliza Kaiza kwa ukali “I’m here to save them ! akajibu Devotha “You are here to save my children? Akasema Kaiza na kutoa kicheko kidogo. “Wewe Devotha unaweza kumuonea huruma mtu? Mambo uliyoyafanya leo hakuna anayeweza akakuamini tena.I don’t trust you anymore.Nilikuwa nakuamini kuliko watu wote.Nilifuata kila ulichonieleza lakini kwa yale uliyoyafanya leo mauaji makubwa ya bila huruma siwezi kukuamini tena.You’ve become a devil.I don’t know you anymore ! You are not Devotha I know ! akasema Kaiza “I’m sorry for what happened today !! Hata mimi inaniumiza kwa yale niliyoyafanya lakini ilikuwa lazima niyafanye.I did that for a reason” akasema Devotha “You betrayed us.Sisi ni rafiki zako,ndugu zako tumekuwa pamoja kwa muda mrefu lakini umetusaliti.Umeua marafiki zako,umeua ndugu zako.Hakuna sababu inayoweza kukufanya ukamwaga damu nyingi vile.You are a killer Devotha!! Akasema Kaiza kwa ukali akatazamana na Devotha “Saada ambaye ulimchukua akusaidie katika mambo yako amejirusha toka ghorofani na kufariki dunia kwa sababu yako.Huna chochote cha kunieleza Devotha.Nina hasira na kila mmoja wetu ana hasira kali mno na wewe kwa mambo uliyoyafanya.Natamani hata hapa nitoe bastora nikuchakaze kwa risasi” akasema Kaiza Devotha akamtazama kisha akatoa bastora na kumpatia Kaiza “Take the gun.Fanya kile ambacho kinaweza kukuondolea hasira ulizo nazo juu yangu” akasema Devotha na kusimama mbele ya Kaiza ambaye uso wake ulikuwa umejikunja kwa hasira akainua mkono ule ulioshika bastora akamnyooshea Devotha “Shoot me !! akasema Devotha kwa ukali.Kaiza akaendelea kumtazama Devotha kwa hasira huku akihema kwa kasi “Kaiza don’t you know how to shoot? Akauliza Devotha kwa ukali “Aaaagghh !! akasema Kaiza kwa hasira “Shoote me Kaiza.Maliza hasira zako.Hii ni nafasi pekee umeipata na ukishindwa kuitumia hii nafasi hautapata nafasi nyingine tena ya kuniua.So let us end this.Kill me now !! akafoka Devotha Mara Kaiza akaushusha mkono uliokuwa na bastora na kujishika kiunoni. “Umeipata nafasi ya kuniua na kumaliza kabisa hasira zako umeshindwa kuitumia na hautaipata tena.Sasa ni wakati wangu” akasema Devotha huku Kaiza akiendelea kumtazama kwa hasira. “Devotha wewe ni shetani kabisa !.Nilik…………….” Kaiza akataka kusema lakini Devotha akamzuia “Stop Kaiza ni wakati wangu.Nilikupa nafasi ukashindwa kuitumia na sasa naomba unisikilize” akasema Devotha Kaiza akatoa kitambaa na kufuta jasho lililomjaa usoni “I’m sorry for what happened today!Nafahamu nimewaumiza sana watu wote.Tumekuwa pamoja kama ndugu na hata mimi sikutegemea kama siku moja kungeweza kutokea jambo kama hili”akasema Devotha na Kaiza akatikisa kichwa “Siamini hata neno moja utakalonieleza Devotha.Wewe ni shetani” akasema Kaiza “Tafadhali nisikilize hadi nitakapomaliza” akasema Devotha “Una haki ya kuniita majina yote unayotaka lakini nataka ufahamu sababu ya kufanya hivi nilivyofanya.Olivia tayari amekwisha ingiwa na itikadi za kigaidi na hakuna namna ambayo tungeweza kumfanya ili atupe taarifa za mtandao wa IS hivyo nikaamua kujifanya ninakuwa upande wake ili aniamini.Lengo kuu likiwa ni kutaka kuufahamu mtandao wao na nini hasa malengo yao hapa nchini.Nilianza kwa kudukua simu ya rais ili nifahamu kama ana uhusika wowote na kile alichokisema Olivia kwamba Rais anafahamu mahala alipo Edger kaka.Sikufanikiwa kupata chochote kutoka katika simu ya Rais kwani niligunduliwa haraka na kuanzia hapo nikafungiwa kila kitu na wewe ukachukua nafasi yangu.Niliposhindwa kupata chochote katika simu ya rais nikaamua kurejea tena kwa Olivia lakini sikumkuta tayari ulikwisha muondoa na kumpeleka mafichoni.Baada ya kumkosa Olivia nikakumbuka tunaye Mathew Mulumbi ambaye ana mahusiano na Olivia nikaandaa mpango wa kwenda kumtoa pale kitalu 1.Tayari nilikwisha ondolewa katika nafasi yangu ya ukurugenzi wa idara na nilikuwa natafutwa hivyo basi hakuna ambaye angeweza kuniruhusu kuingia ndani ya kitalu 1 ndiyo maana nikalazimika kuingia kwa nguvu na ndipo yakatokea yale yaliyotokea lakini kwa namna yoyote ile ilikuwa lazima nimpate Mathew Mulumbi”akasema Devotha na kumtazama Kaiza ambaye bado sura yake ilikuwa imejikunja akimtazama Devotha kwa hasira kali. “Hili ni tukio ambalo katu sintaweza kulisahau katika maisha yangu.Licha ya watu wangu kuuawa lakini hata mimi nimenusurika kifo” akasema Devotha na kufungua shati lake na kumuonyesha Kaiza jeraha ambako alipigwa risasi. “Kitendo cha kumtoa Mathew Mulumbi kitalu 1 kilimfanya aniamini kwamba mimi ni mwenzao na nikapata nafasi ya kuwa nao karibu na kuwasoma vyema na hicho ndicho kitu nilichokuwa nakitaka” “Kuwa karibu yao?Wako wangapi?akauliza Kaiza na ile mistari iliyojikunja usoni ikatoweka “Mathew Mulumbi ana watu wake anaofanya nao kazi” “IS?akauliza Kaiza “Nimegundua kwamba Mathew Mulumbi hana mahusiano na kikundi cha IS bali ana mahusiano na Olivia Themba.Mathew hakufahamu kama Olivia ana ushirika na kikundi cha IS” “How come you trust him so easily? Mathew na Olivia ni wote ni washirika wa IS” akasema Kaiza “Hata mimi niliamini hivyo mwanzoni na ndiyo maana nikataka kuufahamu ukweli na nikatumia njia hii ya kuwa karibu nao ili niweze kufahamu kila kitu kutoka kwao na ndipo nikagundua kwamba Mathew hana mahusiano yoyote na IS na wala hakujua kama Olivia ana mashirikiano na IS.Baada ya kuufahamu ukweli kuhusu Olivia na IS Mathew na watu wake ..” akasema Devotha na Kaiza akamkatisha “Mathew na watu wake akina nani?akauliza Kaiza “Mathew aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na kwa sasa anashughulika na mambo yake binafsi ya biashara.Pamoja na kuachana na mambo ya ujasusi lakini kutokana na ujuzi wake mkubwa amekuwa akitumiwa wakati mwingine na serikali katika operesheni kadhaa hivyo anao watu wake anaosaidiana nao katika kazi zake.Yupo mmoja anaitwa Gosu Gosu huyu anadai ni mwanajeshi amewahi kupigana vita ya msituni kwa miaka mingi na mwingine anaitwa Ruby alikuwa ni mtaalamu mkubwa sana wa kompyuta.Sijawahi kukutana na mtu anayeifahamu kompyuta kama yeye” “Unasema alikuwa mtaalamu where is she? “I shot her.I killed her !! akasema Devotha “Kwa nini ulimuua? “Nilimuua kwa sababu ya kuikoa familia yako” “Kwa ajili ya kuiokoa familia yangu kivipi?akauliza Kaiza “Kuna mtu alipiga simu mchana nyumbani kwa Mathew akimtafuta Mathew akadai kwamba anazo taarifa za kumuhusu Olivia.Kwa msaada wa Ruby walifanikiwa kujua mahala mtu yule alipokuwa wakati akipiga ile simu ,Mathew na Gosu Gosu wakaenda na kukuta kuna watu watano wameuawa na kufichwa garini vile vile wakagundua kuna nyumba ya chini ambayo hutumika kwa ajili ya kutesea watu” “Jesus Christ ! Kaiza akasema kwa mstuko “Nilikwambia Ruby ni mwanamke hatari ambaye anaifahamu kompyuta kuliko aliyeigunudua hivyo aliweza kufanikiwa akiwa mbali kupata kumbukumbu za kamera zilizozunguka nyumba ile na kila kitu kikawa wazi.Tuliona kila kitu kilichofanyika katika nyumba ile.We sawa you Kaiza.Tulikuona toka ulivyofika pale na ukamuingiza Olivia ndani ya nyumba na mateso yote uliyompatia.” Akasema Devotha baada ya Kaiza kutoa kitambaa mfukoni na kufuta jasho “Baada ya mateso mengi ulionekana kupitia Kamera,ukimuingiza Olivia garini akiwa hajitambui na kuondoka.Wewe ndiye mtu pekee unayefahamu mahala alipo Olivia.Mathew Mulumbi baada ya kumkosa Olivia alitaka kufahamu mahala unakoishi.Nilitaka kufahamu sababu ya kutaka kujua mahala unakoishi akadai kwamba anataka kuiteka familia yako kukushinikiza ueleze mahala alipo Olivia.Sikuwa tayari kwa hilo kwa kuwa nilibaki na Ruby pekee ndipo nilipoamua kufanya jambo ili kuja kuwaokoa familia yako.Nilimpiga risasi Ruby ili niweze kupata nafasi ya kutoka mahala pale na ndipo nilipokuja mpaka hapa kuwahi kuwachukua watoto wako na kuwapeleka sehemu salama.Hivyo ndivyo ilivyotokea” akasema Devotha “Kaiza naomba uniamini kwamba haya yote niliyoyafanya ni kwa ajili ya kuutafuta ukweli wa kuhusu Olivia.Kwa sasa baada ya kuwa na uhakika kuwa Mathew hana mahusiano na IS tunabaki na Olivia pekee ambaye tunapaswa kuhakikisha tunamlinda kwa kila namna tuwezavyo kwani Mathew na wenzake lengo lao kubwa ni kumpata na wanatumia kila uwezo walio nao kuhakikisha wanampata.Kaiza hili suala la Olivia si suala dogo.Ipo siri kubwa ndani yake.Shambulio lililotoka leo usiku katika hospitali ya Mtodora ni mwanzo tu wa mipango ya IS hapa nchini na kubwa ni kumshinikiza rais Dr Evans aweze kuwaonyesha mahala alipo Edger Kaka.Jengo lililolipuliwa alikuwa amelazwa mtoto wa rais na inawezekana shambulio lile lilimlenga yeye.Haya yote Olivia anayafahamu na kama tukijiweka karibu yake anaweza akatueleza kila kitu lakini ili atueleze kuhusu mipango yao yote lazima tupate kwanza taarifa za kumuhusu Edger Kaka na sehemu pekee ambako tunaweza kupata taarifa za Edger ni kwa kumchunguza rais Dr Evans.Msisitizo huu unaowekwa na IS kwa Rais kuonyesha alipo Edger unatoa picha kwamba Rais analifahamu jambo hili na ndiyo maana nilidukua simu yake kuutafuta ukweli.Olivia yuko tayari kueleza kila kitu lakini hadi akipata taarifa za mahala alipo Edger” akasema Devotha na kunyamaza kidogo akamtazama Kaiza halafu akaendelea. “Kaiza kazi yetu ni ..” “Devotha don’t say we.Sisi si washirika tena.Toka ulipoamua kutusaliti na kufanya mambo yako peke yako you are not one of us anymore” “Kaiza nimejaribu kukueleza kwa kirefu sababu ya mimi kufanya hivi nilivyofanya” “Lakini mpango wako haujazaa matunda yoyote Zaidi ya kusababisha vifo kwa watu wetu” akasema Kaiza “Kaiza tafadhali naomba unielewe.Tuyaweke pembeni yote yaliyopita na tuungane tena kuweza kuzuia mashambulio Zaidi ambayo IS wamepanga kuyafanya.Naamini mashambulizi Zaidi yatakuja na sisi tunao uwezo wa kuzuia yasitokee hivyo lazima tufanye kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunaifahamu mipango ya IS na kuizuia.Thats what we’ve been doing for years.Nchi iko salama kwa sababu hatulali tukihakikisha hakuna vitisho vyovyote vya amani yetu na ndivyo tunavyotakiwa kufanya hata sasa.Tuhakikishe hakuna tena damu ya mtanzania itamwagika lakini hatuwezi kufanya hivyo kama hatutaweza kuungana na kufanya kazi kwa pamoja”akasema Devotha “How can I trust you again Devotha? “Niamini kama ulivyokuwa unaniamini zamani.Usiwe na wasi wasi na mimi” “Natamani kukuamini Devotha lakini nashindwa.Is this is one of your games? “A game? This isn’t a game.Ingekuwa ni mchezo ninataka kuucheza nisingemuua Ruby kwa ajili ya kuwaokoa familia yako.Hivi sasa Mathew na wenzake naamini wananitafuta kwa kumuua mwenzao.Pamoja na hilo nililolifanya kwa familia yako you still don’t trust me?akauliza Devotha “Please trust me Kaiza.Tumepata nafasi tuitumie vyema” akasema Devotha.Kaiza akazama mawazoni kwa muda halafu akauliza “Devotha hata kama IS wana mipango ya kufanya mashambulio mengine hapa nchini tutawezaje kujua? “Kwa nini unauliza hivyo Kaiza?We have a solution.Olivia.Yeye ndie ambaye atatuongoza kufahamu mipango yote ya IS hapa nchini na kama kuna mashambulio mengine yanapangwa lakini atatueleza hayo yote kama tukifanikiwa kupata taarifa za kumuhusu Edger Kaka” akasema Devotha.Kaiza akamtazama kwa macho yaliyoonyesha kukata tamaa “Kuna nini Kaiza? Akauliza Devotha “Devotha,Olivia is gone” “What? She’s gone? Devotha akashangaa “Where is she?Is she dead?akauliza “Hajafa ni mzima kabisa ila amechukuliwa na rais” “Rais amemchukua?How?akauliza Devotha akiendelea kushangaa na Kaiza akamueleza kila kitu kilichotokea kuhusu Olivia “I can’t believe this.Rais anataka kumpeleka wapi Olivia?akauliza “Kuna kitu alikitamka kwamba haridhishwi na namna tunavyofanya kazi zetu na akadai kwamba ataifuta idara yetu naamini hata kitendo cha kumchukua Olivia ni kutokana na kupoteza imani na sisi” akasema Kaiza.Devotha akafikiri kidogo na kusema “Hapana Kaiza.Rais anatuamini sana.Toka idara hii imeanzishwa tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa weledi mkubwa sana na hatujawahi kumuangusha.Nilichokifanya mimi hakimaanishi kwamba idara nzima ni mbovu hadi akatishia kuifuta.Kuna kitu ninakihisi.Usiku huu magaidi wamevamia hospitali alikokuwa amelazwa mwanae na nina uhakika mkubwa kwamba mlengwa mkuu wa uvamizi ule alikuwa mwanae.Ninaamni shambuluo lile ni muendelezo wa shinikizo la IS kumtaka Rais awaonyeshe mahala alipo Edger kaka.” “Nini unakimaanisha Devotha?akaulizia Kaiza “Ninamaanisha kwamba kama magaidi walivamia hospitali na katika jengo moja tu alilokuwa amelazwa mtoto wa Rais hii ina maana kwamba walichokuwa wanahitaji ni kumpata mtoto wa Rais.Kwa kuwa hakuna taarifa rasmi hadi hivi sasa kuhusiana na watu wangapi wamefariki katika shambulio hilo kuna mambo mawili ambayo yananijia kichwani.Kwanza kuna uwezekano mkubwa magaidi wakawa wamemteka mtoto wa Rais na kwa sababu hiyo basi Rais akamtaka Olivia ili aweze kuzungumza naye na kumtumia ili kumpata mtoto wake.Pili yawezekana magaidi tayari wanaye mtoto wake na wamemshinikiza rais awapatie Olivia ambaye ni mtu wao.Yote haya mawili yanawezekana hivyo basi kitu cha kwanza kufahamu ni kama mtoto wa rais ambaye alikuwa amelazwa katika jengo lililoshambuliwa yuko wapi.Je ni mzima au amekufa? Jibu tutakalolipata litatuongoza kufahamu kwa nini Rais amemchukua Olivia” akasema Devotha “Hapo ndipo kwenye tatizo Devotha” “Usihofu Kaiza kila kitu niachie mimi.Ninachohitaji kutoka kwako ni ushirikiano wako na uniamini.” akasema Devotha “Devotha tafadhali huu usiwe ni moja ya michezo yako.Naomba suala hili liwe la kweli na tushirikiane kuwapata hawa watu ambao wanatishia amani ya nchi yetu”akasema Kaiza “Tutawapata Kaiza.Ninakuhakikishia lazima tutawapata” akasema Devotha na ukimya ukapita wakaendelea kutazamana.Devotha akakumbuka kitu “Ninahitaji kwenda sehemu Fulani na nitakaporejea hapa nitakuwa na jibu la wapi tuanzie” akasema Devotha “Vipi kuhusu Mathew Mulumbi unadhani ataweza kufika hapa kama alivyokuwa amepanga?akauliza Kaiza kwa wasiwasi “Hata kama akifika hapa tayari unao watu wa kutosha kukulinda lakini sina uhakika kama anaweza akafika hapa kwani mtu pekee ambaye walikuwa wakimtegemea awape maelekezo ya mahala unapoishi ni mimi na hawataweza kunipata.Kwa usiku huu watakuwa na mstuko wa kifo cha mwenzao Ruby” akasema Devotha “Devotha yule mtu ameweza kuua watu kumi na tatu ambao tuliwaamini na kuwategemea sana katika operesheni mbali mbali nina hakika akifahamu mahala nilipo hawa vijana nilionao hawataweza katu kumzuia.I’m so scared” akasema Kaiza “Usiwe na wasiwasi Kaiza.Kwa kuwa tayari umekwisha fahamu kuna hatari waelekeze watu wako wajipange vyema kuikabili hatari yoyote ile itakayokuja.Kaiza suala hili la mimi na wewe kuonana ni siri kubwa kati yetu na waelekeze vijana wako wasifungue midomo yao kwa kile walichokiona humu” akasema Devotha “Nitafanya hivyo Devotha” akasema Kaiza “Kama hakuna lingine niruhusu niondoke kwa muda nitarejea baadae” “Kuna jambo moja nataka kulifahamu ulitaka kuwapeleka wapi familia yangu ambako ulidai ni salama?akauliza Kaiza “Hakuna haja ya kuwapeleka huko tena kwa kuwa tayari umekwisha fika.Sina gari naweza kutumia gari lako?” akauliza Devotha.Kaiza akasita kidogo halafu akaongoza ana Devotha hadi katika gari lake akampa funguo na Devotha akaondoka. “Naamini sijafanya kosa tena kumuamini Devotha.Kama huu ni moja ya mchezo wake naapa sintomsamehe kamwe! Akawaza Kaiza wakati Devotha akitoka getini na gari lake “Nimemaliza upande mmoja.Haikuwa rahisi kumshawishi Kaiza akubali kuwa upande wangu lakini nashukuru ameniamini sasa ngoja nielekee ubalozi wa Israel nikajue Mossad wanataka kitu gani” akawaza Devotha akiwa katika mwendo mkali “Dr Evans kwa nini amemchukua Olivia?Anataka kumpeleka wapi?akajiuliza “Kwa namna yoyote ile lazima kumpata Olivia.Bila kumpata haya yote niliyoyafanya leo yatakuwa ni kazi bure.Damu yote iliyomwagika leo itakuwa imemwagika bure” akawaza Devotha







“Wakati ninamsubiri Sasha anipe jibu ngoja nirejee maskani nikajue hali ya Ruby kwani sifahamu itamchukua Sasha muda gani kupiga tena.Yawezekana naye yuko katika shughuli zake” akawaza Mathew akiwa bado katika bustani ya Kiembe kavu na kuingia garini akaondoka “Nitakesha usiku wa leo nikimtafuta Devotha na nikimpata atajuta kunitoa ndani ya lile shimo” akawaza Mathew na kuvuta kumbu kumbu namna alivyohojiana na Devotha na hadi alivyoongoza operesheni ya kumkomboa “Aliua watu wa idara yake kwa ajili ya kunikomboa mimi kwa nini sasa ametugeuka? I was so stupid to trust her ! Kama ningechukua tahadhari ya kutosha mapema haya yote yasingetokea na Ruby asingekuwa katika hatari.Yeye mwenyewe alinusurika kupoteza maisha kwa kupigwa risasi wakati akinikomboa nini hasa lilikuwa lengo lake?Alitaka kuwa upande wetu na kujua mipango yetu? Akajiuliza “Majibu yote nitayapata pale nitakampomtia mikononi” akaendelea kuwaza Mathew akiendelea kukanyaga mafuta. Hadi alipowasili katika makazi yao bado Sasha hakuwa amempigia simu kumpa jibu la namba zilizowasiliana na simu ile ya Ruby aliyotoroka nayo Devotha. “Mambo yanakwendaje hapa?akauliza Mathew baada ya kuingia katika chumba alimolazwa Ruby “Kila kitu kinakwenda vyema.Mpaka sasa sijaona tatizo lolote kwa Ruby mifumo yake yote inakwenda vyema na pale dawa ya usingizi itakapokwisha basi atazinduka.Msiwe na wasi wasi wowote” akasema Dr Hiran “Dr Hiran nakushukuru sana kwa msaada huu mkubwa” “Usihofu Mathew hii ni kazi yangu hata hivyo marafiki lazima tusaidiane naamini iko siku na mimi nikiwa na tatizo utakuwa tayari kunisaidia” akasema Dr Hiran “Wewe ni rafiki wa kweli Dr Hiran muda wowote ukiwa na tatizo usisite kunieleza nami nitakusaidia” akasema Mathew akiwa ameyaelekeza macho yake kwa Ruby “Unadhani itamchukua muda gani kuzinduka kutoka usingizini?akauliza Mathew “Sina hakika lakini atazinduka tu msiwe na hofu” akasema Dr Hiran kisha Mathew akamuita Gosu Gosu wakaenda katika chumba cha kusomea “Gosu Gosu yule mwanamke anacheza na akili zetu.Alifahamu kwa alichokifanya lazima tutamfuatilia na akacheza mchezo wa kutuchanganya akili zetu tushindwe sehemu ya kuanzia kumtafuta lakini nakuhakikishia lazima atapatikana.Kama si usiku wa leo basi haitavuka kesho lazima atapatikana.Ninaamini simu hii hakuichukua kwa ajili ya kwenda kuitelekeza pale bustanini bali alikuwa na kazi nayo.Ninasubiri jibu la Sasha kujua ni namba zipi ambazo Devotha aliwasiliana nazo baada ya kutoka hapa” akasema Mathew “Mathew nina wazo kwa nini usimpigie tena simu huyo Sasha? Yawezekana amekwisha sahau kama unasubiri jibu toka kwake” akashauri Gosu Gosu “Ni wazo zuri ngoja nimpigie” akasema Mathew na kumpigia simu Sasha “Mathew nisamehe sana nilikwisha sahau kama nilikuahidi kukupigia” akasema Sasha baada ya kupokea simu “Usijali Sasha nafahamu majukumu yako” “Mathew nimefuatilia ile simu nitakutumia namba mbili za mwisho kuwasiliana nayo” akasema Sasha na kumtumia Mathew namba ambazo ziliwasiliana na ile simu aliyoondoka nayo Devotha “Sasha nashukuru sana kwa msaada huu mkubwa” “Karibu tena Mathew” akasema Sasha na kukata simu “Gosu Gosu ulikuwa sahihi kabisa.Tayari Sasha alikwisha nisahau.Amenitumia namba hizi mbili ambazo zimewasiliana na simu hii ya Ruby ninaamini ni Devotha aliyepiga” akasema Mathew na kuzitazama zile namba halafu akaipiga namba ya kwanza ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa “Your Identification number please! Ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili wa simu na Mathew akakata simu “Nimeulizwa namba ya utambulisho.Naamini ni Devotha aliyetakiwa kutaja namba yake ya utambulisho” akasema Mathew “Yawezekana labda alipiga simu katika idara yao” akasema Gosu Gosu “Yawezekana lakini ukumbuke tayari amewasaliti wenzake na anatafutwa” akasema Mathew “Kama si idara yake ni nani hawa wanaohitaji namba ya utambulisho? Akauliza Gosu Gosu “Ninavyofahamu mimi mifumo kama hii yenye kuhitaji namba za utambulisho huwa ni katika mashirika ya kijasusi au taasisi nyingine za usalama” akasema Mathew na kuipiga ile namba ya pili ikaita na baada ya muda ikapokelewa “Hallow” ikasema sauti ya mwanaume “Hallow habari yako ndugu yangu” akasema Mathew “Nzuri kabisa habari yako” “Salama.Nikusaidie nini? “Nahitaji kukufahamu ndugu yangu nimekuta namba yako katika simu ya mpenzi wangu” “Mpenzi wako nani?akauliza yule jamaa kwa ukali kidogo “Devotha.Unamfahamu? “Ouh kumbe Devotha.Ninamfahamu sana amekuwa ananituma kazi nyingi mara kwa mara kama kwenda kumfanyia manunuzi mbalimbali.Mimi ni dereva taksi naitwa Antony” akasema “Nafurahi kukufahamu Anthony.Unapatikana sehemu gani? “Mimi hupatikana hapa Queen tower hotel” “Sawa Anthony imekuwa vizuri nimekufahamu ila kuna kitu nataka kuuliza” “Uliza usihofu” “Devotha amekupigia simu usiku huu kuna kazi yoyote alikutuma umfanyie? “Mbona una wasiwasi kaka? Kuna tatizo lolote?akauliza Anthony “Hakuna tatizo Antony kuwa na Amani” “Devotha aliponipigia simu usiku huu hakunituma kazi bali alinitaka nimpeleke sehemu Fulani” “Unaweza ukanipeleka mahala hapo?akauliza Mathew na Antony akasita “Usihofu Antony.Nitakulipa kiasi kizuri cha pesa.Labda kwa kukudokeza tu ni kwamba nimepanga kumvisha Devotha pete ya uchumba lakini sijamwambia.Nimetoka safari nje ya nchi usiku huu na ninataka kumshangaza kwa kumfuata mahala alipo kumvisha pete ya uchumba.Nataka kumfanyia sprise.Nisubiri hapo tafadhali ninakuja ndani ya dakika kumi na tano” akasema Mathew na kukata simu “Sasa jibu limepatikana.Baada ya kutoka hapa Devotha aliwasiliana na Anthony ambaye ni dereva taksi akamtaka ampeleke sehemu Fulani.Naamini Antony atakubali kutupeleka mahala alikompelelka Devotha.Tujiandae tuelekee huko” akasema Mathew “Vipi kuhusu Ruby? “Atabaki hapa na Dr Hiran.She’ll be fine.Naamini mahala alipo Devotha hivi sasa atakuwa na ulinzi hivyo tunahitaji kwenda sote wawili” akasema Mathew na kumfuata Dr Hiran “Dr Hiran mimi na Gosu Gosu tunatoka kwa muda kuna sehemu tunaelekea kisha tutarejea.Ninakuomba endelea kumuhudumia Ruby na hakikisha anakuwa salama.Kama kuna kitu chochote kitatokea nijulishe haraka sana” akasema Mathew “Usiwe na wasi wasi Mathew.Nafahamu umuhimu wake kwenu hivyo nitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha anakuwa salama” akasema Dr Hiran “Ahante sana Dr Hiran” akasema Mathew wakatoka na kuingia garini wakaondoka. “Mathew una hakika Ruby atakuwa salama hapa peke yake? Nina wasiwasi sana na Devotha kwani anapafahamu mahala hapa na kama lengo lake lilikuwa kutuchunguza sisi anaweza akawaleta wenzake hapa” akasema Gosu Gosu “Tumkabidhi Mungu atamlinda lakini hatuna namna ya kufanya,Devotha ni muhimu sana kupatikana kwa sasa” akasema Mathew Walitumia chini ya dakika ishirini kufika Queen tower hotel kutokana na mwendo mkali ambao Mathew alikuwa anaendesha.Baada ya kufika katika maegesho Mathew akatoka ndani ya gari na kumpigia simu Antony “Antony tayari nimefika hapa Queen Tower hotel.Nielekeze mahala ulipo tafadhali” akasema Mathew baada ya Antony kupokea simu kisha akamuelekeza mahala alipo. “Gosu Gosu ninamfuata Antony,wewe utatufuata kwa nyuma na kama kuna hatari yoyote unaiona utanijulisha” akasema Mathew na kutembea kuelekea mahala zinakoegeshwa taksi akampata Antony “Karibu sana kaka” akasema Antony akionekana kuwa na wasiwasi. “Ahsante Antony.Nashukuru kukufahamu.Naomba unipeleke ile sehemu tafadhali” akasema Mathew huku akifungua mlango na kuingia garini.Antony akawasha gari na kuondoka kumpeleka Mathew mahala alikompeleka Devotha. **************** Devotha aliwasha taa ya kushoto ya gari na kukata kona akaifuata barabara inayoelekea katika ubalozi wa Israel nchini Tanzania.Toka akiwa mbali akawashiwa taa ya kumuashiria apunguze mwendo wa gari na apunguze ukali wa taa.Alipunguza mwendo na kuendesha gari taratibu hadi alipokaribia getini akasimamishwa na walinzi wenye silaha akajitambulisha kwamba ana miadi ya kukutana na balozi wa Israel nchini Tanzania.Gari la Olivia likakaguliwa kama lina hatari yoyote kama vile mlipuko akakutwa na silaha.Mmoja wa walinzi wale akapiga simu ndani ya ubalozi kumjulisha balozi kwamba mgeni wake amekwisha fika na akatoa maelekezo aruhusiwe kuingia ndani.Kabla hajaruhusiwa Devotha akatakiwa kwanza kuacha silaha yake kwa walinzi halafu akaingia ndani.Anaifahamu ofisi ya balozi kwani si mara ya kwanza amefika hapa lakini kabla hajaingia katika chumba cha lifti akamkuta mlinzi mmoja aliyevaa suti nyeusi akamuelekeza aingie katika chumba kimoja akakaguliwa na mashine kama ana hatari yoyote halafu akaruhusiwa kupita moja kwa moja akaelekea katika ofisi ya balozi na kugonga mlango akaruhusiwa kuingia ndani.Hakuwa peke yake ndani ya ile ofisi alikuwa na watu wengine wawili “Dr Yonathan” akasema Devotha “Devotha karibu sana” akasema Dr Yonathan akainuka na kwenda katika meza iliyokuwa na chupa kadhaa za mvinyo akamimina katika glasi na kumpatia glasi moja Devotha “Nashukuru Dr Yonathan lakini kwa leo sintatumia kinywaji kwani ninatumia dawa” “Unaumwa nini?akauliza Dr Yonathan “Ni matatizo ya kawaida.Habari za hapa?akauliza Devotha na Dr Yonathan akagugumia mvinyo wote uliokuwemo katika glasi halafu akamtazama Olivia “Samahani kwa kukusumbua usiku huu lakini nashukuru kwa kufika” “Usijali Dr Yonathan” akasema Devotha “Devotha kama unavyoona humu ndani ninao wageni wawili ambao ni Fishel” akasema Dr Yonathan na Fishel akatikisa kichwa huku akitabasamu “Mwingine ni Ehud” Ehud naye akatikisa kichwa baada ya kutajwa “Ehud na Fishel kutaneni na Devotha Adolph ni wakala wa Mossad hapa Tanzania” akasema Dr Yonathan.Devotha akasimama na kuwapa mikono majasusi wale “Nimefurahi kukutana nanyi.Karibuni sana Tanzania” akasema Devotha “Sisi pia tumefurahi kukutana nawe” akajibu Fishel “Devotha baada ya kufahamiana sasa tuelekee moja kwa moja katika kile kilichotukutanisha hapa usiku huu” akasema Dr Yonathan na kunyamaza kwa muda halafu akaendelea “Fishel na Ehud wametokea Tel Aviv wametumwa na Mossad hapa Tanzania kwa ajili ya kazi maalum na wewe ukiwa kama wakala wa Mossad hapa Tanzania ni jukumu lako kuhakikisha kwamba wanafanikiwa kile kilichowaleta hapa Tanzania” akasema Dr Yonathan na ukimya mfupi ukapita “Ningependa kufahamu nini hasa kilichowaleta hapa Tanzania?akauliza Devotha.Fishel akakohoa kidogo kurekebisha koo halafu akasema “Tumekuja kwa ajili ya kufanya maandalizi ya operesheni kabambe ya Mossad itakayofanyika hapa Tanzania siku chache zijazo” akasema Fishel na kunyamaza kidogo “Operesheni gani ambayo Mossad wanataka kuifanya hapa Tanzania?akauliza Devotha “Operesheni ambayo Mossad wanataka kuifanya hapa Tanzania ni kumtafuta mtu anaitwa Olivia Themba” akasema Fishel na Devotha akapatwa na mstuko mkubwa “Olivia Themba?!akauliza “Ndiyo,Olivia Themba” akajibu Fishel “Nimestuka kidogo kusikia Mossad wanamtafuta Olivia Themba” akasema Devotha “Tunafahamu kwamba Olivia ametekwa nyara na watu wasiojulikana mpaka sasa hajapatikana wala hajulikani alipo na ndiyo maana tumekuja sisi kuandaa operesheni ya kumtafuta” akasema Fishel “Nini hasa sababu ya Mossad kumtafuta Olivia?akauliza Devotha “Swali hilo hatutaweza kukujibu Devotha.Jukumu lako kama wakala wetu ni kuhakikisha unatusaidia sisi kuweza kuandaa na kufanikisha operesheni yetu na kumpata Olivia” akasema Fishel na Devotha akajikuta amekosa neno la kuongea “Devotha wewe ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi naamini kabisa kwamba mara tu baada ya tukio hili kutokea idara yako imekuwa inashughulikia suala hili kwa karibu sana.Nataka kufahamu namna tukio hili la kutekwa Olivia lilivyotokea na mwisho nataka kufahamu ni wapi idara yako imefikia hadi sasa kufahamu waliomteka Olivia ni akina nani na mahala alipo” akasema Fishel.Devotha akameza mate kulainisha koo kwani alihisi kama sauti inashindwa kutoka.Akawatazama majasusi wale kwa zamu ambao walikuwa wamemkazia macho “Pamoja na ujasiri wangu lakini hapa nimegonga ukuta hawa jamaa wamenibana kwenye kona.Sikujua kama Mossad nao wanamtafuta Olivia.Najuta kuamua kuwa wakala wao hapa Tanzania.Hata hivyo sintawaeleza ukweli kuhusu Olivia.Siko tayari wampate Olivia kwani ni mtu muhimu sana ambaye hata mimi ninamsaka kwa udi na uvumba”akawaza Devotha “Devotha !! akaita Dr Yonathan baada ya kumuona Devotha amezama mawazoni “Nilikuwa natafuta namna ya kuanza kulieleza suala hili” akasema Devotha “Olivia alitekwa katika geti la nyumbani kwake alipokuwa akitoka jijini Kinshasa”akasema Devotha na Ehud akamkatisha “Mnazo taarifa zozote za nini alikwenda kufanya nchini Congo DRC?akauliza Ehud “Taarifa tulizonazo ni kwamba alikwenda jijini Kinshasa kwa shughuli zake za kiutafiti.Olivia ni daktari ambaye anaendesha kituo cha utafiti wa magonjwa mbali mbali ya wanadamu na wanyama.Zilikutwa sampuli za damu katika gari lake na baada a kuzipima zikagundulika ni damu za wanyama Sokwe ambazo alizikusanya kwa ajili ya kuzifanyia utafiti katika kituo chake” akasema Devotha.Ukimya mfupi ukapita Fishel akasema “Endelea Devotha” “Watekaji walikuwa wamejiandaa vyema walitumia helkopta kuusimamisha msafara wake na kufanya mashambulizi wakaua walinzi wa Olivia kisha wakamchukua na kuondoka naye.Helkopta iliyotumika katika utekaji huo ilipatikana imetelekezwa na ikabainika watekaji waliiba helkopta ile wakaitumia katika shughuli yao ile kisha wakaitelekeza mahali nje kidogo ya jiji.Vyombo vyote vya uchunguzi hapa nchini vinashirikiana katika kumtafuta Olivia na mpaka sasa hakuna taarifa zozote za nani aliyemteka Olivia wala mahala alipo.Idara yangu mimi ni ya siri na hata shughuli zake pia zinafanyika kwa siri bila kushirikisha idara yoyote ya serikali lakini hata sisi mpaka sasa bado hatujapata ufumbuzi wowote wa jambo hili.Tunachohisi waliofanya jambo hili ni watu kutoka nje wakisaidiwa na watu kutoka ndani ya nchi” “Nina swali Devotha” Akasema Ehud “Uliza usihofu” “Umesema kwamba watekaji waliua walinzi wa Olivia.Mmefuatilia na kujua kwa nini Olivia alikuwa na walinzi wa kumlinda?Alihisi kuna hatari yoyote inamkabili hadi akaamua kuajiri walinzi wa kumlinda?akauliza Ehud “Kumekuwa na matukio ya utekaji nyara kwa siku za hivi karibuni ndiyo maana wengi wa matajiri hasa waliopo hapa Dar es salaam wameajiri walinzi kwa ajili ya kuwalinda na ndivyo alivyofanya Olivia” “Mmechunguza kama walinzi wa Olivia walikuwa ni watu wa aina gani? Je walipitia mafunzo ya ulinzi? Ehud akauliza “Hilo hatujalifanya.Hatukuwa tumeliwekea uzito wowote” akajibu Devotha “Endelea Devotha.Ulisema mnahisi waliomteka Olivia ni watu kutoka nje ya nchi wakisaidiwa na watu wa hapa nchini.Kwa nini mnahisi hivyo?akauliza Fishel “Kwa namna tukio lile lilivyotekelezwa limefanywa na watu wenye ujuzi mkubwa sana ambao tunaamini wametoka nje ya nchi.Tunaamini ni watu wa kutoka nje ya nchi kwa sababu kumekuwa na mfululizo wa matuko ya utekaji wa watu matajiri hapa nchini kwa siku za hivi karibuni na watekaji wamekuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya kujipatia kipato.Kwa mujibu wa jeshi la polisi mtandao wa watekaji wa watu umeanzia nchini Afrika kusini na Nigeria na kwa sasa wameanza kusambaa katika nchi za Afrika mashariki ambako matukio kama haya hayajazoeleka.Katika matajiri watatu waliotekwa hivi karibuni na kupatikana baada ya kutoa kiasi kikubwa cha fedha ilibainika wateka walitoka nchini Afrika kusini na ndiyo maana hata tukio hili tunaamini watekaji wametokea nje ya nchi.Tunaamini sababu kuu ya kumteka Olivia ni kujipatia kipato_Olivia anatoka katika familia ya mabilionea Agrey na Lucy Themba.Olivia pia ana utajiri mkubwa na watekaji wamelenga kujipatia fedha nyingi kutoka kwa familia ya Olivia” “Mna mawasiliano na wazazi wa Olivia kujua kama watekaji wamewasiliana nao kudai kiasi cha fedha? akauliza Fishel “Tuna wasiliana mara kwa mara na mpaka sasa bado hawajapata simu yoyote kutoka kwa watekaji lakini naamini watekaji hao lazima watawasiliana nao na wameahidi kutujulisha pindi wakipokea simu yoyote kutoka kwa watekaji” akasema Devotha “Unaweza ukatukutanisha na familia ya Olivia tukazungumza nao?akauliza Fishel na swali lile likambabaisha kidogo Devotha “Devotha unaweza ukatukutanisha na familia ya Olivia tukazungumza nao? Fishel akauliza “Familia ya Olivia ni watu wa karibu sana na Rais hivyo baada ya kutokea kwa tukio hili ulinzi mkali umewekwa kuilinda familia hiyo na si rahisi kuonana nao.Kuna watu wachache na maalum ambao wanaruhusiwa kuonana nao hata hivyo nitajaribu kufanya mipango ili muweze kuonana nao.Nini sababu ya kutaka kuonana nao?akauliza “Kuna mambo tunataka kuyafahamu kutoka kwao”akasema Fishel “Sidhani kama hilo ni wazo zuri.Familia hii wana ukaribu mkubwa sana na rais na ninyi mko hapa Tanzania hamna kibali cha kufanya operesheni yenu taarifa zinaweza kumfikia Rais na kila kitu kikaharibika.Ninawaomba muwe watulivu na mfuate kile nitakachowaelekeza.Mimi ndiye wakala wenu hapa Tanzania na nitasaidiana nanyi kuhakikisha mnampata Olivia lakini msijaribu kutaka kufanya kitu chochote ambacho kinaweza kuhatarisha usalama wenu hapa Tanzania na kinachoweza kuniweka mimi pia katika hatari.Hakuna anayefahamu kama mimi ni wakala wa Mossad hapa Tanzania” akasema Devotha. “Sawa Devotha sisi tunakusikia wewe ambaye ndiye wakala wetu lakini tunataka kufahamu namna utakavyotusaidia kuandaa operesheni yetu na hatimaye tuweze kumpata Olivia” akasema Ehud “Ninaomba mnipe muda hadi asubuhi ili niweze kuandaa mpango mzuri wa namna ya kuwasaidia kutekeleza operesheni yenu” akasema Devotha. “Hakuna tatizo Devotha nenda katuandalie mpango mzuri ambao utatuwezesha kufanikisha operesheni yetu hapa Tanzania.Kikubwa tunachokihitaji ni kupata walau fununu za mahala alipo Olivia ili majasusi wetu waweze kuingia hapa nchini na kumchukua.Timu ya majasusi iko katika utayari wakisubiri kupata taarifa muda wowote kutoka kwetu ili waweze kuingia hapa nchini” akasema Fishel “Msihofu kila kitu kitakwenda vizuri” akasema Devotha.Hakukuwa na mazungumzo Zaidi Devotha akaagana na balozi Yonathan akaondoka. “Nimepatwa na mstuko mkubwa sana ambao sikuutegemea kiasi kwamba nahisi kama ile sehemu niliyoshonwa inaanza kuachia” akawaza na kupeleka mkono mahala penye jeraha akagusa maji maji “Hili jeraha sitakiwi kulifanyia mzaha linaweza kuniletea matatizo makubwa.Nahitaji kulitibu haraka kabla halijaleta madhara.Kwa hali ya mambo inavyokwenda nahitaji kuwa na afya njema” akawaza na kuvuta pumzi ndefu “Sikuwahi kupatwa na mstuko kama nilioupata leo baada ya kusikia kwamba Mossad nao wanamtafuta Olivia.Sikujua kama suala hili la Olivia lingekuwa kubwa kiasi hiki kiasi cha kuwafanya shirika kubwa la ujasusi Mossad nao kutaka kufanya operesheni ya kumtafuta.Kwa nini Israel wanamtafuta Olivia? Wamekuwa wagumu kueleza sababu ya kumtafuta Olivia.Kama ningejua mapema alichoniitia Dr Yonathan ni suala hili la Olivia katu nisingekwenda kuonana naye” akawaza Devotha “Nimewadanganya sikutaka kuwaeleza ukweli.Siko tayari wampate Olivia ambaye ana siri kubwa tunayohitaji kuipata.Endapo Mossad watampata Olivia hatutaweza tena kuipata siri hiyo ambayo Olivia aliniambia atanieleza pale nitakapokuwa nimepata taarifa za mahali alipo Edger Kaka.Kuna siri kubwa imejificha hapa katika suala hili la Edger Kaka na kubwa ni ushiriki wa IS katika suala hilo.Mpaka sasa hakuna anayefahamu IS wanahusikaje na Edger Kaka? Limebaki ni fumbo lakini mtu pekee mwenye majibu ya fumbo hili ni Olivia Themba ambaye hatujui mahala aliko hadi hivi sasa.Hatujui Rais amempeleka wapi.Mossad hawapaswi kumpata Olivia kabla yetu.Nitahakikisha hakuna operesheni yoyote ya Mossad itakayofanyika hapa nchini kabla hatujampata Olivia.Nimefanya mambo makubwa ikiwemo kutoa uhai wa watu wangu kwa ajili ya kutaka kuifahamu siri aliyonayo Olivia hivyo siwezi kuwapa nafasi Mossad wakampata Olivia kabla yangu” akaendelea kuwaza Devotha na kuongeza ubaridi ndani ya gari kwani ubaridi uliokuwepo haukutosha bado alihisi joto. “Kwa sasa ngoja nielekee nyumbani kwangu.Tayari nimekwisha elewana na Kaiza hakuna tena kitu cha kuhofia.Nahitaji kuwasiliana na Mary aje anitazame hili jeraha” akawaza Devotha akielekea nyumbani kwake “Kuna kitu nimekigundua kwa Devotha sijui kama na ninyi mmekigundua” akasema Ehud baada ya Devotha kuondoka “Kuna kitu hata mimi nimekiona” akasema Fishel “Devotha kuna kitu anatuficha hataki kutueleza ukweli.Baada ya kuombwa atukutanishe na familia ya Olivia kwanza alistuka na kisha akasema hilo haliwezekani.Ameonyesha wasi wasi mkubwa baada ya kusikia tunataka kuonana na wazazi wa Olivia.Binafsi mstuko huu aliouonyesha Devotha unanifanya niwe na wasiwasi kama maelezo haya aliyotupa yana ukweli ndani yake.Nina uhakika mkubwa sana kuna jambo Devotha analificha” akasema Ehud “Kama mna wasiwasi na Devotha anaweza asiwezeshe operesheni yenu kufanikiwa nini mnashauri kifanyike?akauliza Dr Yonathan “Kwa upande wangu nakubaliana na Ehud kwamba Devotha hawezi akatueleza kila kitu na ushauri wangu ni kwamba tusimtegemee sana katika operesheni yetu ila tuwe na mpango mbadala lakini papo hapo tuendelee kuwa nyuma yake na tumuonyeshe tunamtegemea sana yeye ili asiwe na wasiwasi wowote na sisi kwamba kuna mambo tunayafanya nyuma yake.Sehemu ya kwanza ambako nashauri tuanzie kufanya uchunguzi wetu kwa siri ni kwa familia ya Olivia.Tukionana nao wanaweza wakatupa picha pana Zaidi ya suala hili la kutekwa kwa Olivia.Kuna mambo ambayo tunaweza kuyapata yakatusaidia sana kufahamu nani kamteka Olivia na pengine kufahamu hata mahala alipo” akasema Fishel “Mawazo ya Fishel ni mazuri sana na yatatusaidia kuweza kupata taarifa za kutekwa Olivia” akasema Ehud.Walifanya majadiliano kisha wakapelekwa katika sehemu walikoandaliwa kupumzika.







Hakukuwa na maongezi mengi garini kati ya Mathew na Anthony hadi walipofika katika nyumba ambako Antony alimpeleka Devotha. “Nilimleta katika nyumba hii” akasema Antony “Una uhakika ni hapa?akauliza Mathew “Ndiyo nilimleta hapa”akasema Mathew na kutoa kitita cha noti kwa ajili ya kumpa Antony ghafla akatokea jamaa mmoja akipiga hatua kubwa kuelekea gari la akina Mathew.Hatua kadhaa kabla hajalifikia gari la akina Mathew akaanguka chini na bastora ikaanguka pembeni yake.Antony akastuka sana baada ya kuiona bastora ile. “Ana bastora !! akasema huku akitazama nyuma ili aweze kuondoa gari. “Relax don’t panic” akasema Mathew baada ya kujua ile ilikuwa kazi ya Gosu Gosu aliyekuwa katika gari la nyuma yao.Akamkabidhi Antony kitita cha fedha na kujiandaa kushuka lakini ghafla wakatokea watu watatu wakiwa na bastora. “Antony ondoa gar…………”kabla Mathew hajamaliza risasi zikaanza kuvuma.Mathew akamvuta mkono Anthony kumlaza chini ya kiti lakini alichelewa kwani risasi nyingi zilipigwa upande ule wa dereva.Kwa kasi ya aina yake Mathew akafungua mlango na kuruka nje.Akazama chini ya uvungu wa gari akatambaa na kuchungulia aliwaona watu wale watatu wakiwa wamelala chini wakivuja damu.Ilikuwa ni kazi ya Gosu Gosu aliyewazimisha wote kwa risasi Kutokea pale chini ya uvungu wa gari Mathew akailenga taa kubwa iliyokua getini iliyokuwa na mwangaza mkali ikasambaratika na eneo lile la nje likawa na mwangaza hafifu kutoka kwa taa zilizokuwa ndani ya jumba lile.Mathew akarejea garini kumtazama Antony hakuwa na uhai tayari alikwisha fariki. “Mathew ! Gosu Gosu akamuita Mathew kwa sauti ndogo “He’s gone” akasema Mathew na kutoka ndani ya ile gari “Tayari wanajua tuko hapa na kama kuna wengine ndani watakuwa wanajipanga kutusubiri tuingie ndani” akasema Gosu Gosu “Vyovyote itakavyokuwa lazima tuingie ndani na kumpata Devotha.She’s in there.Hata kama litakuja jeshi zima tutapambana.Kama ni kufa tufe tukijaribu” akasema Mathew. “Kitu cha kufanya ili kutusaidia tuweze kuingia ndani kiurahisi ni kulifanya eneo liwe na giza.Tuziondoe zile taa kubwa zinazoleta mwangaza mkubwa pale ndani ili tupate nafasi ya kuing…..” Kabla Mathew hajamaliza sentensi yake taa zote zikazimika “Kama vile walikuwa katika mawazo yetu” akasema Mathew “Usihofu Mathew uko na mwanajeshi.Huu ni mchezo mdogo sana.Nimepambana kwa miaka mingi vita ya usiku.Nifuate mim……..aaagghh..!! Gosu Gosu akatoa mguno na kuanguka chini. “Gosu Gosu are you okay?akauliza Mathew “Nimekoswa na risasi imenikwaruza shingo.Usihofu I’m okay Mathew”akasema Gosu Gosu “Kuna wadunguaji.Tayari wametuona mahala tulipo.We need to do something ! akasema Mathew Mathew akaingia ndani ya lile gari la Antony akamtoa na kisha akaligeuza kulielekea geti na Gosu Gosu akaleta jiwe Mathew akaliweka katika pedeli ya mafuta gari lile likaanza kutembea huku Mathew na Gosu Gosu wakiwa nyuma yake.Mivumo ya risasi ikasikika na vioo vya gari vikivunjwa kwa risasi.Hii iliwapa nafasi akina Mathew kufahamu kirahisi mahala walipokuwa wamejificha watu waliokuwa ndani ya nyumba na kuwapa urahisi wa kuwaondoa.Mara milio ya risasi ikakoma baada ya kulikaribia geti.Lile gari halikuwa na dereva likagonga geti na kishindo kikasikika.Mathew na Gosu Gosu wakajibanza kusubiri kama kuna mtu yeyote ambaye atajitokeza baada ya kusikia kishindo kile cha geti kugongwa na gari lakini zilipita dakika mbili bila hatua ya mtu kusikika Gosu Gosu akausukuma mlango mdogo wa geti wakaingia ndani.Kulikuwa kimya sana na hakukuwa na dalili za kuwepo mtu. “Kuko kimya sana yawezekana kuna watu wamejificha wakisubiri tujitokeze.Cover me ! akasema Mathew na kuanza kukimbia kuelekea katika kibaraza.Alipofika akajibanza nyuma ya sanamu kubwa ya kifaru iliyokuwa katika kibaraza cha nyumba ile.Gosu Gosu naye akakimbia kumfuata Mathew hakukuwa na mlio wowote wa risasi tena.Eneo lote la nyumba ile lilikuwa giza kulikuwa na mwangaza hafifu kutoka katika taa za nyumba za jirani. “Umeme katika nyumba hii ulizimwa makusudi kabisa.Katika nyumba nyingi kifaa cha kukata a kuwasha umeme huwekwa sebuleni naamini hata humu itakuwepo sebuleni.I’m going to look for it cover me” akasema Mathew wakaingia sebuleni.Mathew akajibanza na kuangaza pande zote kama kuna mtu yeyote ataonekana lakini kulikuwa kimya hakukuwa na mtu yeyote.Mathew akawasha tochi ya simu yake na kuanza kuchunguza ukutani na kama alivyokuwa amehisi akafanikiwa kukiona kifaa cha kuwashia na kukatia umeme akawasha na taa zote zikawaka wakachukua nafasi haraka haraka kuangalia kama kuna mtu yeyote atakayejitokeza kisha wakaanza kupanda ghorofani wakiingia katika chumba kimoja baada ya kingine.Walishangaa kwa ukimya uliokuwepo “Wamekwenda wapi watu wote?akauliza Gosu Gosu “Hata mimi nashangaa.Au yawezekana tumewamaliza wote? Akasema Mathew Chumba cha mwisho walichoingia ni chumba kikubwa cha kulala ambacho kilikuwa kitupu hawakukuta mtu yeyote. “Tumemkosa !! akasema Gosu Gosu “She was here.Lazima kuna namna ametoroka.Wakati ule ilipozimwa taa ndipo alipoweza kutoroka” akasema Mathew wakashuka na kuanza kufanya uchunguzi wakagundua kulikuwa na mlango wa nyuma uliokuwa wazi. “Lazima atakuwa ametoroka kupitia mlango huu” akasema Mathew “Hata kama ameondoka hatakuwa mbali sana.Tukifuata njia hii ya huku nyuma tunaweza kumpata” akasema Gosu Gosu “Hatutaweza kumpata.Tayari ametuponyoka.!! akasema Mathew na kumtaka Gosu Gosu warejee ndani. “Tuchunguze nyumba hii kwa makini yawezekana kuna kitu tunaweza kukipata kinachoweza kutusaidia kumpata Devotha” akasema Mathew wakarejea ndani moja kwa moja katika kile chumba cha kulala.Katika meza iliyokuwemo mle chumbani kulikuwa na picha zimeangushwa.Mathew akachukua picha moja akaitazama na kustuka. “This is Kaiza” akasema na kuchukua tena picha nyingine akamuona Kaiza akiwa na mwanamke mmoja wakitabasamu. “Hapa ni nyumbani kwa Kaiza?akajiuliza na kuzipitia picha zile na zote zilikuwa za Kaiza.Akamuita Gosu Gosu aliyekuwa katika chumba kingine “Kuna kitu nimekigundua.Hapa ni nyumbani kwa Kaiza yule ambaye alikuwa na Olivia.Tazama hizi zote ni picha zake” akasema Mathew na Gosu Gosu akazipitia zote “Devotha na Kaiza tayari walikwisha ingia katika mgogoro mkubwa baada ya Devotha kuwasaliti wenzake na kuungana nasi.Imewezekanaje Devotha akaja kuonana na Kaiza?akauliza Gosu Gosu “She played us.Huyu mwanamke ni mjanja sana ametumia akili nyingi kujifanya anakuwa upande wetu ili kutuchunguza lakini kumbe bado anashirikiana na idara yake na ndiyo maana katika ile namba ya simu ya kwanza niliyopiga nilitakiwa kutaja namba ya utambulisho.Naamini namba ile ni ya mtandao wa idara ya akina Devotha.Nini hasa alichokuwa anakitafuta kwetu hadi afanye yale yote?akauliza Mathew “Sasa nimepata jibu kwa nini alikuwa mgumu kuelekeza mahala anakoishi Kaiza kwa kuwa alifahamu kuwa bado ni mwenzake na hakutaka kuiweka familia yake katika hatari na ndiyo maana baada ya kutoka pale kwetu alikuja moja kwa moja hapa na ninaamini alikuja kumuonya Kaiza kwamba familia yake iko katika hatari.Lakini hizi zote ni mbio za sakafuni hatafika mbali” akasema Mathew “Nini kinafuata? akauliza Gosu Gosu “Twende tukajipange upya” akasema Mathew wakatoka na kuelekea katika gari lao wakaondoka “Mathew nimepata wazo” akasema Gosu Gosu “Mchana wakati tukijiandaa kuja kukukomboa nilihitaji silaha,Devotha akanichukua hadi nyumbani kwake na kuniingiza katika chumba cha silaha nikachukua kila nilichokihitaji.Ninapakumbu ka mahala anapoishi,kwa nini tusimfuate huko? Yawezekana tukampata na vile vile tunahitaji silaha pia” “Wazo zuri twende huko” akasema Mathew na Gosu Gosu aliyekuwa katika usukani akaongoza njia kuelekea nyumbani kwa Devotha Muda mfupi baada ya akina Mathew kuondoka nyumbani kwa Kaiza,mfuniko wa moja ya shimo kati ya mashimo manne ya maji machafu ukafunuliwa na mtu mmoja akatokeza kichwa akachungulia halafu akatoka na kuelekea ndani akachunguza nyumba yote kama kuna mtu halafu akarejea tena katika lile shimo “It’s clear ! akasema na watu wakaanza kutoka ndani ya lile shimo ambalo halikuwa shimo la kuhifadhi maji machafu bali lilitengenezwa maalum kwa ajili ya kujificha pale inapotokea hatari.Kaiza akawasaidia mke wake na watoto kutoka ndani ya lile shimo wakarejea ndani “Devotha alikuwa anasema kweli kuhusu wale jamaa kuja kuvamia na kuwachukua watoto wangu.Sehemu hii imekwisha kuwa hatari.Hakuna haja ya kuendelea kukaa hapa wale jamaa wanaweza wakarejea tena.Siwezi kuacha familia yangu wawe katika hatari.I need to take them to safe place” akawaza Kaiza na kuwapa maelekezo vijana wake wawili aliokuwa nao ndani ya lile shimo wakusanye miili ya wale wenzao waliouawa kisha waipeleke kitalu 1.Yeye akaingia gereji akachukua gari la mke wake akaiingiza familia yake na kuondoka haraka “Tunaelekea wapi Kaiza?akauliza Bella ambaye bado alikuwa amewakumbatia watoto wake “To the safe place” akasema Kaiza “Devotha yuko wapi? Will she be safe? “Sifahamu yuko wapi hana simu hivyo hatuwezi kujua kama yuko salama au vipi” akasema Kaiza “Please Kaiza don’t leave us again.Tuko katika hatari na tunakuhitaji sana” Bella akasisitiza.Kaiza hakujibu kitu alikuwa katika mawazo mengi





Wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwa Devotha,simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Dr Hiran. “Dr Hiran anapiga” akasema Mathew kwa wasiwasi akamtazama Gosu Gosu halafu akaipokea ile simu “Hallow Dr Hiran” akasema Mathew “Mathew nimekupigia kukujulisha kwamba mgonjwa wetu amezinduka”akasema Dr Hiran na Mathew akashusha pumzi “Thank you Lord! Akasema kwa sauti ndogo “Vipi maendeleo yake?akauliza Mathew “Anaendelea vyema.Lakini kuna maneno ambayo amekuwa anayatamka kwa kuyarudia rudia nimeyaandika nikihisi pengine yanaweza kuwa na maana” “Anatamka maneno gani?akauliza Mathew “BRAVO 15E 361 A” akajibu Dr Hiran “Dr Hiran nashukuru sana endelea kuandika kila anachokitamka tuko njiani tunarejea sasa hivi” akasema Mathew na kukata simu “Gosu Gosu we need to go back” “Kwa nini Mathew?Kuna mabadiliko katika hali ya Ruby? “Ruby amezinduka na kwa mujibu wa Dr Hiran anaendelea vyema lakini kuna maneno amekuwa anayatamka kwa kuyarudia rudia BRAVO 15E 361 A” akasema Mathew “This looks like some codes” akasema Gosu Gosu “Ndiyo inaonekana ni namba Fulani ya siri.Ruby ameitamka namba hii kwa kuirudia rudia kwa sababu ndicho kitu kikubwa anachokikumbuka kwa sasa.Tunatakiwa kufahamu amezipata wapi namba hizi? Akasema Mathew.Gosu Gosu akageuza gari na kushika njia ambayo inaelekea nyumbani kwao “Vipi kuhusu Devotha?akauliza Gosu Gosu “Baadae tutamtafuta lakini kwa sasa hili ni la muhimu sana” akasema Mathew “Yule mwanamke ana maisha marefu kama paka.Hata hivyo atapatikana tu hana sehemu ya kujificha” akaendelea kuwaza Mathew Iliwachukua saa moja na na dakika ishirini kuwasili katika makazi ya Mathew.Mathew alishuka garini haraka haraka kabla hata gari halijasimama vizuri akakimbilia ndani “How’s she! Akamuuliza Dr Hiran “Relax Mathew.Anaendelea vyema.Kwa sasa ametulia ameacha kuweweseka” akasema Dr Hiran “Aliendelea kuzungumza maneno mengine?Umeyarekodi?akaul iza Mathew “Maneno pekee ambayo ameendelea kuyatamka ni yale yale niliyoyaandika.Alikuwa anayarudia hadi pale alipotulia” akajibu Dr Hiran “Dr Hiran naweza kuzungumza naye?akauliza Mathew na Dr Hiran akawa kimya “Please Dr Hiran ni muhmu sana.Anazo taarifa za muhimu ambazo natakiwa kuzipata kutoka kwake” akasema Mathew “Anatakiwa kuachwa apumzike lakini kama ana jambo la muhimu unaweza ukazungumza naye” akasema Dr Hiran na kuongozana na Mathew hadi katika kitanda cha Ruby “Ruby…Ruby !! akaita Mathew na Ruby akafumbua macho “It’s me Mathew” “Ma..ma…” Ruby akataka kutamka lakini akaanza kukohoa “Easy.Easy Ruby” akasema Mathew “Mathew nadhani tumuache kwanza apumzike”akasema Dr Hiran.Ruby akamfanyia Mathew ishara asogee karibu.Mathew akainama ili kumsikiliza Ruby “The codes !! akasema Ruby kwa sauti ndogo. “What codes?akauliza Mathew “BRAVO 15E 361 A” “Umezipata wapi hizi codes? Akauliza Mathew “Devo…” “Devotha” akasema Ruby kwa sauti ndogo “Umezipata kwa Devotha?akauliza Mathew “She made the call…follow the codes!! Akasema Ruby “Ruby this is very important.Please tell me everything” Ruby akakohoa kidogo na kusema “She shot me ! Before that she made the call.I heard her mention that codes.Please find her !! akasema Ruby na macho yake yakajaa machozi “Pole sana Ruby.Yamekwisha,you are safe.I’ll protect you” akasema Mathew na kumfuta Ruby machozi “Mathew promise you’ll find her! Akasema Ruby “I promise you pretty angel I’m going to find her.I’ll get her” akasema Mathew “Thank you Mathew.Thank you for saving my life.” Akasema Ruby “Ruby wewe ni mtu muhimu sana kwangu hivyo yeyote anayecheza na maisha yako ananigusa moja kwa moja hivyo nitamuonyesha Devotha kwamba alikosea mno kucheza na maisha yako.Pumzika Ruby daktari yuko hapa ataendelea kukuangalia.Mimi na Gosu Gosu pia tuko hapa.Hakuna chochote kitakachokutokea tena” akasema Mathew na kumbusu Ruby katika paji lake la uso akatoka nje na kumkuta Gosu Gosu akiwa na Dr Hiran. “Dr Hiran thank you so much .Naomba tafadhali uendelee kumuangalia Ruby usihofu kuhusu malipo” akasema “Mathew niko hapa hadi kutakapopambazuka na sintafumba jicho http://deusdeditmahunda.blogspot.com/langu kuhakikisha Ruby anakuwa salama.Mpaka hapa hayupo tena katika hatari hivyo msihofu” akasema Dr Hiran na Mathew akamuita Gosu Gosu wakaenda katika chumba cha kusomea “Ruby amenieleza kwamba Devotha alipiga simu na alimsikia akitaja zile namba ambazo Dr Hiran alitutumia.Naamini namba hizi za siri Devotha alizitumia katika ile namba ambayo nilipiga na kutakiwa kutaja namba ya utambulisho.Ni wakati wa kufahamu alikuwa anawasiliana na nani” akasema Mathew na kuchukua ile simu ya Ruby akapiga zile namba ambazo alitumiwa na Sasha “Simu inaita” Mathew akamwambia Gosu Gosu na kuiweka simu ile katika sauti kubwa “Your Identification number please! Ikasema sauti ile ile ya mwanamke aliyoisikia mwanzo alipopiga simu. “BRAVO 15E 361 A” Akasema Mathew.Baada ya sekunde mbili sauti ile ikasema “Thank you Devotha,wait for three seconds” Baada ya sekunde tatu kama alivyoahidiwa sauti ile ya mwanamke ikasema “Devotha Dr Yonathan amenituma nikwambie yuko kwenye kikao muhimu na wale wageni kutoka Tel Aviv atakutafuta baada ya nusu saa”ikasema sauti ya Yule mwanamke na Mathew akakata simu. “Dr Yonathan ! who is he? Akauliza Gosu Gosu “Kuna mambo mawili hapa yamejitokeza.Kwanza ni Dr Yonathan na pili ni wale wageni kutoka Tel Aviv.Kwa kauli hii ya huyu mwanamke inaonekana Devotha anawafahamu watu hao waliotoka Tel aviv.Tunatakiwa kumfahamu huyo Dr Nathan kabla ya kuwafahamu watu hao waliotoka Tel Aviv wana mahusiano gani na Devotha” akasema Mathew “Ruby was here and I hope she heard everything” akasema Mathew na kutoka mle ndani Gosu Gosu akamfuata nyuma wakaelekea katika chumba alimo lala Ruby.Dr Hiran alikuwa na sindano mkononi akitaka kumchoma Ruby “Dr Hiran subiri kidogo.Nahitaji kuzungumza naye kuna jambo la muhimu mno” akasema Mathew na kuwafanyia ishara Dr Hiran na Gosu Gosu watoke mle ndani.Mathew akakaa katika kitanda cha Ruby “Ruby nimekuja tena kuomba msaada wako.Nataka unieleze kila kitu ulichokisikia akikizungumza Devotha” “Umezipata namba alizopiga Devotha? Umetumia zile namba nilizokupa? “Ndiyo Ruby na ndiyo maana nimerudi tena kwako.Nimetumia zile namba na tumegundua ni namba za utambulisho za Devotha.Baada ya muda tukapewa jibu kwamba Dr Yonathan hawezi kuzungumza na Devotha kwa sasa yuko kwenye kikao na wageni wale kutoka Tel Aviv.Tunataka kumfahamu huyu Dr Yonathan ni nani? Nini ulisikia wakizungumza?akauliza Mathew.Ruby akafumba macho “Ruby ! akaita Mathew kwa sauti ndogo “Baada ya kutaja zile namba nilimsikia Devotha akizungumza na Dr Yonathan na ilionekana kama vile huyo Dr Yonathan alimtaka Devotha waonane usiku huu na nikamsikia Devotha akimjibu kwamba atafika ubalozini muda si mrefu.Niliishia kusikiliza hapo kwani alihisi ninamsikiliza nikaondoka” “Kwa maelezo haya uliyoyasikia inaonekana kama vile huyu Dr Yonathan ni mtu mwenye wadhifa na yupo katika ubalozi Fulani hapa Tanzania.Inawezekana huyo Dr Yonathan akawa ni balozi” akasema Mathew na kusimama “Ruby thank you.Endelea kupumzika” akasema Mathew na kutoka mle ndani haraka akamtaka Gosu Gosu warejee katika ofisi yao akamueleza kila kitu alichoelezwa na Ruby “Gosu Gosu nahisi huyu Dr Yonathan akawa ni balozi.Njia rahisi ya kuupata ukweli ni kutafuta mtandaoni” akasema Mathew na kukaa katika kompyuta akaingia mtandaoni na kutafuta orodha ya mabalozi wote wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.Mara akastuka baada ya kuliona jina Dr Yonathan Cohen akiwa ni balozi wa Israel hapa Tanzania “Israel !! akasema Mathew kwa mshangao “Devotha ana mahusiano na Israel na mtu aliyekuwa anazungumza naye Dr Yonathan Cohen ni balozi wa Israel hapa nchini.” “Cette affaire deviant plus belle et plus grande”akasema Gosu Gosu kwa sauti ndogo kwa lugha ya kifaransa akimaanisha suala hili linazidi kuwa kubwa “Kuna ushirikiano gani kati ya Devotha na balozi wa Israel hapa nchini? Kadiri tunavyoendelea na hili suala ndivyo tunavyozidi kuchimbua mambo zaidi.Mwanzo ilikuwa Olivia na IS sasa ni Devotha na Israel”akasema Mathew “Tunafanya nini Mathew?akauliza Gosu Gosu “Kitu pekee cha kufanya hapa ni kumfuata balozi Dr Yonathan.Ni yeye pekee mwenye kuweza kutusaidia kumpata Devotha na vile vile atatueleza kinachoendelea kati ya ubalozi wake na Devotha hadi wakutane usiku huu tena kwa mawasiliano maalum”akasema Mathew akainamisha kichwa akafikiri kidogo na kusema “Gosu Gosu I have to be honest with you brother” akasema Mathew na kumtazama Gosu Gosu “Tunachoenda kukifanya ni kitu cha hatari kubwa na kinaweza kusababisha hata mvutano mkubwa baina ya nchi hizi mbili lakini pamoja na hatari yake bado ni jambo la muhimu sana ambalo lazima tulifanye.Ninakutegemea sana lakini kama haujisikii kushiriki katika operesheni hii you can stay I’ll go there alone I’m not scared”akasema Mathew “Mathew I’m a soldier.Nimekuwa napigana vita toka nikiwa mdogo.Muziki niliouzoea masikioni mwangu ni milio ya risasi na mabomu.Hivyo basi siogopi na sintoogopa chochote.Nitume kokote nitaenda.Hata kama nitashindwa kupita lakini nitakufa nikijaribu.I’m with you Mathew.This is our country and this is our war.We must fight” akasema Gosu Gosu “Thank you Gosu Gosu.Tunachokihitaji sasa ni silaha kwani balozi Yule analindwa na ulinzi mkali”akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema “I know where we can get weapons.Tujiandae tuondoke” akasema Mathew na kurejea katika chumba alimo Ruby ambaye tayari alikuwa amelala Mathew akambusu katika paji la uso “You’ll be safe Ruby” akasema na kumuaga Dr Hiran wakaondoka







Baada ya kutoka nyumbani kwao Kaiza alielekea moja kwa moja nyumbani kwa Devotha ambaye aliwapokea na kuwakaribisha ndani “Karibuni sana.Sikutegemea kuwaona hapa usiku huu” akasema Devotha na kustuka baada ya kuziona sura za akina Kaiza zikiwa zimejaa wasiwasi mkubwa “Nini kimetokea?akauliza. Kaiza akavuta pumzi ndefu na kusema “Ulikuwa sahihi Devotha” “Kuhusu nini? “Kuhusu Mathew Mulumbi.Ni kweli amevamia nyumbani kwangu usiku huu akiitafuta familia yangu” Kaiza akamueleza kila kitu kilichotokea na namna walivyoweza kujiokoa. “Poleni sana”akasema Devotha “Devotha nimeamua kuileta familia yangu hapa nikiamini ni sehemu salama.Nina uhakika mkubwa lazima Mathew atarajea tena.Pale nyumbani kwangu si salama tena kwa familia yangu kuwepo” akasema Kaiza “Usihofu Kaiza hapa ni nyumbani kwako na familia yako watakuwa salama” akasema Devotha na kuwataka wamfuate akaenda kuwaonyesha chumba cha kulala.Nyumba ile ya Devotha ilikuwa na vyumba vya kutosha vya kulala.Devotha na Kaiza wakaenda sebuleni kuzungumza “Kaiza usihofu tena familia yako iko salama.Mathew hapafahamu mahala hapa” akasema Devotha “Nashukuru sana Devotha.Utanisamehe kwa maneno yale yote machafu niliyokutamkia sikuwa nikielewa chochote” “Kaiza tuyaweke pembeni yote yaliyotokea na tujielekeze katika suala moja la muhimu sana ambalo ni kumpata Olivia” akasema Devotha “Devotha Olivia amechukuliwa na rais kama nilivyokueleza”akasema Kaiza “Kaiza we must find her.Kwa namna yoyote ile lazima tumpate Olivia.Ni muhimu sana” akasema Devotha “Nafahamu umuhimu wa kumpata Olivia lakini namna ya kumpata ndiyo changamoto” “Sikiliza Kaiza kwa sasa una ukaribu na Rais.Mpigie simu na muulize kama Olivia amefika salama na muulize saa ngapi atarejeshwa ili tupate walau picha ya kinachoendelea kati yake na Olivia” akasema Devotha.Kaiza akafikiri kidogo halafu akatoa simu yake ambayo huitumia kwa mawasiliano na Rais akampigia “Kaiza kunani usiku huu?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais samahani kwa usumbufu lakini ninataka kufahamu kama Olivia amefikiswa salama” “Usijali amefika salama” akajibu Dr Evans kwa ufupi “Mheshimiwa Rais ninataka kufahamu vile vile atarudi saa ngapi kwani niko na timu yangu tunamsubiri ili tuendeleze mahojiano naye” akasema Kaiza “Kaiza nitakujulisha atakapokuwa tayari kurejea kwenu lakini kwa sasa endeleeni na operesheni nyingine ya kuwatafuta Devotha na Mathew Mulumbi” akasema Dr Evans na ukimya mdogo ukapita “Kaiza kuna lingine?akauliza Dr Evans “Hakuna mheshimiwa Rais ni hayo tu niliyotaka kuyafahamu” akasema Kaiza “Basi wekezeni nguvu kubwa katika kuwatafuta Devotha na Mathew” akasema Dr Evans na kukata simu.Kaiza akashusha pumzi “Umesikia jibu alilolitoa.Atanijulisha pale Olivia atakapokuwa tayari kurejea kwetu” akasema Kaiza “Maneno haya ya Rais yanatoa picha ya wazi kwamba Olivia hatarejea tena.Tutafute namna nyingine ya kujua mahala alipo” akasema Devotha “Devotha ushauri wangu mimi tuachane na hili suala litatuweka katika matatizo makubwa” “Usiwe muoga Kaiza.Hii ni kazi yetu kuhakikisha nchi inakuwa salama hivyo lazima tuhakikishe kwa kila namna Olivia anapatikana” akasema Devotha “Hilo nalifahamu Devotha lakini ugumu ni namna ya kumpata Olivia” “Kuna njia moja tu ya kuweza kufahamu mahala alipo Olivia nayo ni kumchunguza Rais” “Una maana kudukua mawasiliano yake?akauliza Kaiza kwa wasi wasi na Devotha akatingisha kichwa kukubaliana naye “Hapana Devotha.Hatuwezi kufanya hivyo hilo ni jambo la hatari kubwa sana.Tazama kilichokutokea wewe ulipojaribu kudukua simu ya rais.Sitaki jambo hilo linitokee na mimi pia” akasema Kaiza “Kaiza hatuna namna nyingine ya kufanya.Kama tunataka kufahamu mipango yote ya IS hapa nchini na kama tunataka kuzuia mashambulio mengine yaliyopangwa na IS basi ni lazima tumpate Olivia.Mtu pekee ambaye anafahamu mahala alipo Olivia ni Rais hivyo lazima tutafute kila mbinu kuhakikisha tunapata taarifa kutoka kwake za mahala alipo Olivia.” akasema Devotha na kunyamaza akamtazama Kaiza ambaye alikuwa na wasi wasi mwingi “Kaiza hili ni suala dogo ambalo haliwezi kutushinda.Tumesoma na tunazifahamu mbinu mbali mbali hivyo lazima tuhakikishe tunafahamu alipo Olivia.Are you with me or not?akauliza Devotha “I don’t know Devotha.Rais ni mtu mwenye nguvu kubwa na sitaki kuingia katika mgogoro naye.Unafahamu amri aliyoitoa kuhusu wewe na Mathew Mulumbi.Shoot to kill !! akasema Kaiza kisha wakatazamana “Uko hai mpaka sasa kwa sababu nimetaka iwe hivyo na hiki nilichokifanya ni usaliti mkubwa kwa Rais na akigundua kwamba nina shirikiana nawe hata mimi nitakuwa katika matatizo makubwa.Devotha naomba tusiingie tena katika matatizo na Rais.Kama ni kumtafuta Olivia tutafute namna nyingine ya kuweza kumpata lakini si kwa kudukua mawasiliano ya Rais ni hatari sana” akasema Kaiza “Niambie ni njia ipi unadhani inaweza kutusaidia kumpata Olivia?akauliza Devotha Kaiza akabaki kimya “Niambie Kaiza kama kuna njia yoyote unaifahamu inayoweza kutusadia kumpata Olivia” akasema Devotha akionekana kuanza kukasirika “Tell me ?! akauliza Kwa ukali “Devotha wewe ni mtu mwenye akili nyingi na unazo mbinu nyingi ninaamini hujaishiwa mbinu nyingine ya kufanya ili kufahamu mahala alipo Olivia zaidi ya hii ya kudukua simu ya Rais.Tafuta mbinu nyingine Devotha na mimi nitakuwa nyuma yako” akasema Kaiza “Kaiza hadi nimefikia maamuzi haya ni kwamba tayari nimekwisha tafuta kila namna ya mbinu nimekosa” akajibu Devotha. “Hata kama ukisema tudukue simu ya Rais how are we going to do it?Tulikuwa na mtu mmoja tu ambaye alikuwa na ujuzi na uwezo mkubwa katika udukuaji ambaye tayari amekwisha fariki.Devotha huu mpango umekwisha kwama tutafute namna nyingine” akasema Kaiza “Aaaagghhh ! akasema Devotha kwa hasira “Kaiza unaniudhi unavyonikatisha tamaa!! “Sikukatishi tamaa Devotha ninazungumza uhalisia.Ni wazi mpango huu hauwezekani kabisa” akasema Kaiza. “Hapana Kaiza.Siwezi kukubali kushindwa kirahisi namna hiyo.Sijawahi kukata tamaa katika maisha yangu.Nitapata mbinu nyingine ya kufahamu mahala alipo Olivia.Nahitaji kumfahamu mtu aliyekuja kumchukua Olivia pale Kitalu 2” “What?akauliza Kaiza “Ulikuwepo kitalu 2 alipokuja Yule jamaa aliyetumwa na Rais kumchukua Olivia.Nahitaji kumfahamu mtu huyo.Elekeza watu wako wakutumie kumbu kumbu za kamera za kitalu 2” akasema Devotha “Devotha ndiyo maana nikakwambia kwamba huu mpango hauwezekani kwani wewe na watu wako mliharibu mfumo wetu wote wa kuhifadhi kumbu kumbu za kamera kutoka katika vitalu vyetu hivyo basi hakuna kumbu kumbu yoyote tunayoweza kuipata” akasema Kaiza na Devotha akamtazama kwa hasira “Kaiza naona unajaribu kufanya kila uwezalo kuhakikisha mpango wangu haufanikiwi.Why are you doing this to me?akauliza Devotha “Devotha usinielewe vibaya lakini ninajaribu kukueleza kitu cha kweli.Tukubali kwamba suala hili la Olivia liko nje ya mikono yetu kwa sasa hivyo tujielekeze katika mambo mengine.Nadhani suala la msingi kwa sasa ni kuanza kutafuta namna ya kuhakikisha unakuwa salama.Ushauri wangu ni kuondoka hapa nchini haraka.Devotha Rais ana hasira kubwa na wewe na anaisaka roho yako sana hivyo njia pekee ya wewe kuendelea kuwa salama ni kuachana na suala hili la Olivia na kuondoka nchini.Nitakusaidia katika hilo.Nenda ukakae nje ya nchi kwa muda halafu utarejea hapo baadae wakati Rais amekwisha maliza muda wake.Ninas……” “Kaiza !! akasema Devotha kwa hasira na Kaiza akanyamaza “Kaiza unanifahamu vyema mimi ni mtu wa aina gani pale ninapokasirika.Umenikasiris ha sana Kaiza sikutegemea kabisa kusikia maneno hayo kutoka kwako.Bahati yako mkeo na watoto wako hapa lakini ningeweza kukifumua kichwa chako kwa risasi sasa hivi ! “Devotha nilichokueleza ni kitu cha ukweli kabisa.Nataka nikusaidie kuondoka hapa nchini wakati bado ninao uwezo kwani sifahamu nini kitatokea kesho.Wewe ni rafiki yangu kubali nikusaidie” akasema Kaiza.Devotha akamtazama kwa macho yaliyojaa hasira na kusema “Go to hell you witch ! akasema huku akianza kupiga hatua halafu akageuka “Sikufahamu kama u mwoga kiasi hiki.Nitakuonyesha nguvu yangu.Utaiona nguvu ya mwanamke” akasema Devotha na kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake







Mathew na Gosu Gosu walifika eneo la Manziki. “Sijawahi kufika eneo hili.Kunaitwaje huku?akauliza Gosu Gosu “Kunaitwa Manziki” akajibu Mathew na kusimamisha gari nje ya nyumba moja kubwa ambayo ujenzi wake ulikuwa unaendelea. “Nani anaishi hapa?akauliza Gosu Gosu “A friend of mine” akajibu Mathew na kuchukua simu akampigia Tino “Mathew” akasema Tino baada ya kupokea simu “Tino samahani sana kwa usumbufu usiku huu.Nina shida kubwa kaka” akasema Mathew ukapita ukimya Tino akasema “Uko wapi Mathew” “Niko hapa nje ya nyumba yako? “C’mo Mathew acha utani” “Seriously niko hapa nje” akasema Mathew.Baada ya dakika tatu mlango ukafunguliwa akatoka Tino.Mathew akafungua mlango wa gari akashuka.Tino akamfuata. “Mathew ni mara ngapi unataka nikuonye kuhusu namna unavyokuja kwangu? Nimekwisha kueleza kwamba sipendi njia unayotumia kuja kwangu ! akasema Tino akionekana kutokufurahishwa na ujio ule wa Mathew “Ninafahamu Tino lakini nina shida na sina namna nyingine ya kufanya ni kwako pekee ninakoweza kupata msaada.Tafadhali usinifungie milango Tino nimekwama na ninahitaji sana msaada wako” akasema Mathew.Tino akamtazama na mara mlango wa gari ukafunguliwa akashuka Gosu Gosu.Tino akamtazama Mathew kwa hasira “Who is he?akauliza “Niko naye.Anaitwa Gosu Gosu”akajibu Mathew. “Come inside” akasema Tino wakaingia ndani “What do you want?akauliza Tino “Nahitaji silaha”akajibu Mathew kwa ufupi “Bado hujafanikiwa kumpata Yule mtu wako?akauliza Tino “Mpaka sasa sijafanikiwa kumpata.Jambo hili limekuwa kubwa tofauti na nilivyodhani.” akasema Mathew. “Kama mpaka sasa hujafanikiwa kumpata mpenzio basi suala hili ni kubwa.Ninavyokufahamu Mathew Mulumbi ukisema suala ni kubwa basi ni kubwa kweli.Anyway unahitaji silaha zipi?akauliza Tino “Nipeleke kwenye chumba cha silaha nikachague” akasema Mathew na Tino akainuka wakamfuata hadi katika chumba anakohifadhi silaha zile nyeti kabisa anazoziuza kwa magenge ya waalifu nje ya nchi.Gosu Gosu akatabasamu baada ya kuingia ndani ya kile chumba wakachagua silaha na vifaa wanavyovihitaji “Mathew chukua kila unachokihitaji sitaki uje tena hapa.Wewe ni mtu mwenye maadui wengi na hujui kwa sasa nani anakufuatulia hivyo kuja kuja hapa kunaweza kuniletea hata mimi matatizo.Ukiwa na tatizo ni bora ukanipigia simu kuliko kunifuata nyumbani” akasema Tino. “Nimekuelewa kaka.nashukuru sana kwa msaada huu mkubwa” akasema Mathew huku akisimama Tino akamtaka aketi “Nini hasa kinachoendelea huko na kusababisha hadi sasa ushindwe kumpata huyo mtu wako?akauliza Tino. “Tino suala hili ni pana sana na nikianza kukueleza litachukua muda mrefu kidogo.Kuna sehemu muhimu tunakwenda usiku huu na nikipata nafasi nitakuja kukueleza kila kitu” “Mathew nimeuliza ili nipate picha ya namna suala hili linavyokwenda and may be I can help” akasema “Tatizo ni kwamba suala hili hadi serikali wana mkono wake na si serikali tu hata nchi za nje nao wana mkono wao katika jambo hili.Kwa mfano tukitoka hapa tunakwenda kuvamia makazi ya balozi wa Israel hapa nchini.Kuna mtu muhimu sana ambaye tunamtafuta.Nadhani hadi hapo umekwisha pata picha namna suala hili lilivyo kubwa” akasema Mathew “How many are you?akauliza Tino “ Just the two of us” akajibu Mathew “Only you two?akauliza Tino na kutoa kicheko kidogo “Mathew usinifanye nicheke.Ninyi wawili pekee mnataka kwenda kuvamia makazi ya balozi wa Israel?akauliza Tino “Kaka unaonekana tayari umekwisha nisahau mimi ni nani.Ukiacha uwezo wangu ninaye Papii Gosu Gosu ambaye ni sawa na jeshi la mtu mmoja” akasema Mathew.Tino akafikiri kidogo na kusema “I’m coming with you” akasema “Tino hapana.Huko tuendako ni hatari sana.Please stay ! akasema Mathew “Mathew wewe ni rafiki yangu siwezi kukuacha.Nitakuunga mkono” “Tin….” “Don’t say anything Mathew.Tunakwenda wote” akasema Tino na kuelekea chumbani kwake “Tino aliwahi kuwa komandoo jeshini alifukuzwa kazi baada ya kufanya vurugu kubwa za kupiga watu na toka wakati huo amekuwa akijishughulisha na biashara ya silaha.Si biashara halali lakini ni mtu anayefahamika na kila mkuu wa chombo cha usalama.Ni mtu ambaye anawasaidia kupata taarifa nyingi za kiusalama kwa sababu anafahamiana na wahalifu wengi wa ndani na nje ya nchi.Kila linapotokea tukio kubwa la uhalifu hapa nchini Tino huwa wa kwanza kuulizwa kama anawafahamu waliofanya uhalifu huo.Amekuwa ni chanzo kikubwa cha taarifa kwa vyombo vya usalama.” Mathew akamweleza Gosu Gosu “Kwa jeshi hili la watu watatu tunaweza hata kupindua nchi”akasema Gosu Gosu na kuta kicheko kidogo.Tino akatokea akiwa amevaa tayari kuingia katika mapambano. “I’m ready” akasema Tino na kuzunguka nyuma ya nyumba na kutoa gari dogo lenye muundo wa basi.Wakaingiza silaha zao katika gari lile kisha wakaondoka. Walikaribia kufika eneo la Kilimani kilipo kijiji cha mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.Tino akasimamisha gari “Mlikuwa mmepanga kuingia vipi katika nyumba ya balozi wa Israel?akauliza Tino “Tukifika tutajitambulisha kama mafundi wa kutengeneza viyoyozi.Tutadai tumepigiwa simu kuna shida ya viyoyozi katika nyumba ya balozi.Lengo ni kutafuta nafasi ya kuwadhibiti walinzi ili tuweze kuvuka kuingia ndani.Please don’t kill the cops” akasema Mathew. “What if they….” Akataka kusema kitu Tino,Mathew akamzuia “We’re killing only terrorists not cops.Polisi wanafanya kazi kubwa ya kujitolea kulinda maisha ya watu we have to respect them.Ni wenzetu katika ulinzi wa taifa hivyo tutawadhibiti kwa muda ili kupata nafasi ya kuingia ndani.Are we clear?akauliza Mathew “Hakuna tatizo” akasema Gosu Gosu. “Tino are we clear?akauliza Mathew “We’re clear” akajibu Tino “Good” akasema Mathew “Gari langu hili limekamilika ni maalum kwa operesheni kama hizi.Lina vifaa vyote vya ujasusi.Naamini lazima kuna kamera za ulinzi zimefungwa huko t uendako hivyo nitazima zote kama zipo ili wasiweze kufuatilia na kufahamu ni akina nani waliofanya uvamizi huu” akasema Tino. “Good.Kila kitu kiwekwe tayari” akasema Mathew na gari likawashwa safari ikaendelea.Walikuta bango kubwa likiwa na maandishi kijiji cha mabalozi. “Tumekaribia ni kilometa moja kutoka hapa” akasema Mathew. Kwa mbali wakaliona geti na mara wakajitokeza watu wawili wakiwa na tochi kubwa zenye mwanga mkali wakamulika gari like na Tino aliyekuwa katika usukani akapunguza mwanga wa taa.Gosu Gosu akachukua hadubini na kutazama “Nimeona askari polisi wanne.Wawili wana silaha.Vile vile kuna mbwa mmoja.Inaonekana kuna geti kabla ya kuvuka kwenda katika nyumba za mabalozi”akasema Gosu Gosu “Damn it.Nimewahi kufika hapa muda mrefu kidogo na wakati huo hakukuwa na geti.Nilijua tunavuka moja kwa moja kwenda katika nyumba ya balozi.Hata hivyo hakijaharibika kitu tutavuka lazima tufike nyumbani kwa balozi” akasema Mathew. Askari mmoja akanyoosha mkono kumtaka dereva asimamishe gari. “Get ready” akasema Mathew huku wakiwasoma wale askari namna walivyokaa.Tino akasimamisha gari na kushusha kioo.Askari aliyekuwa amemshika mbwa akasogelea gari na mmoja akasogelea kioo “Wakuu habari zenu” akasema Tino “Mnaelekea wapi usiku huu?akauliza askari aliyesogea dirishani “Tunaelekea kwa balozi wa Israel.Tumetoka kampuni ya kurekebisha viyoyozi.Tumepigiwa simu kwamba kuna shida katika nyumba ya balozi viyoyozi vyote havifanyi kazi” “Mmeitwa na balozi?Mbona hajatupa taarifa zozote kama kuna watu watakuja usiku huu?Utaratibu wa hapa kama balozi ana wageni wake hutoa taarifa kwetu ili tuwaruhusu wageni wake” “Nimekuelewa afande nadhani ni yeye mwenyewe amekosea ngoja nimpigie simu nimjulishe kwamba tayari tuko hapa” akasema Tino na mbwa akaanza kubweka. “Kuna nini ndani ya gari?akauliza Yule askari “Ni vifaa vya matengenezo” akajibu Tino “Shukeni wote ndani ya gari” akasema Yule askari.Alikosea sana kuwataka akina Mathew washuke garini.Kufumba na kufumbua Tino aliupiga teke mlango ule ukampiga askari Yule aliyekuwa akimuhoji akaanguka chini.Mathew na Gosu Gosu wakaufungua mlango mkubwa kama umeme wakaruka nje wakiwa na silaha.Tino akaruka nje na kumuwahi Yule askari aliyepigwa na mlango na kumkaba kabali.Lilikuwa ni tukio lililotokea kwa ghafla mno na ambalo askari wale hawakuwa wamelitegemea “Wekeni silaha zenu chini!! Akaamuru Mathew. “Hatuhitaji kuua askari yeyote.Tafadhali wekeni silaha zenu chini haraka sana!! Akafoka Mathew.Mmoja wa askari aliyekuwa na silaha akaiweka chini na mwingine naye akafanya vile vile.Gosu Gosu akatoa pingu katika sanduku lao la silaha pamoja na kamba akawafunga askari wale na kuwaziba midomo wasiweze kupiga kelele kisha wakafungua geti na kuwaficha katika kichaka cha maua kilichokuwa karibu na geti mbwa akafungwa katika mti kisha wakaingia garini na kuingia katika kijiji cha mabalozi.Kulikuwa na vibao vilivyoelekeza kila nyumba ya balozi wakafuata kibao kilichoelekeza ilipo nyumba ya balozi wa Israel.Kulikuwa na askari mmoja katika geti la nyumba ya balozi akalisimamisha gari .Tino akasimamisha gari na kushusha kioo “Habari yako Afande” akasema “Nzuri habari yako” “Sisi ni mafundi wa viyoyozi tumekuja hapa mara moja baada ya kupigiwa simu na balozi” “Mmepigiwa simu na balozi?Mbona hajanijulisha chochote? “Tayari amekisha wasiliana na geti kubwa ndiyo maana wakaturuhusu kupita” Wakati Tino akizungumza na Yule askari Gosu Gosu alitoka garini taratibu kwa kutumia kioo cha upande wa pili na kuingia chini ya uvungu wa gari.Miguu yake yenye nguvu mithili ya chuma ikamkata mtama askari Yule akaanguka na kabla hajajua kilichomuangusha tayari Mathew alikwisha ruka nje “Usithubutu kupiga kelele” akasema Mathew na kuchukua silaha yake.Gosu Gosu akamuinua na kumtandika kichwa kizito akapoteza fahamu. “Good job Gosu Gosu” akasema Mathew wakampakia Yule askari katika gari lao.Tino akatoka katika kiti cha dereva akachukua kamera ndogo ya kuruka juu akairusha huku akiifuatilia katika kompyuta yake.Aliizungusha kamera ile katika nyumba yote na kugundua kulikuwa na kamera nne za ulinzi katika kile upande wa nyumba. “Tayari nimekwisha ziona ni kamera za aina gani” akasema Tino na kuanza kucheza na kompyuta yake na baada ya muda akasema “We can go now.Kamera zote zimezima” akasema Kila mmoja akachukua silaha yake na vifaa,Gosu Gosu akawa wa kwanza kupanda geti akaingia ndani na kulifungua Mathew na Tino wakaingia kisha wakanyata kuelekea katika mlango.Kulikuwa na gari mbili katika banda la kuhifadhia magari. Katika mlango kulikuwa na kifaa maalum kwa ajili ya kupiga kelele pale mlango unapokuwa umefunguliwa.Mathew akatoa kifaa Fulani kidogo katika begi na kukibandika mlangoni akabonyeza namba Fulani halafu akachukua vifaa vingine na kuchokonoa kitasa mlango ukafunguka na kifaa kile hakikutoa sauti yoyote wakaingia ndani.Taa zilikuwa zimezimwa ndani kulikuwa na mwangaza hafifu uliotoka katika taa za nje. Walitembea kwa kunyata wakikitafuta chumba cha balozi.Kulikuwa na ukimya mkubwa katika nyumba hii.Katika moja wapo ya chumba walichofunga wakamkuta msichana mmoja akiwa amelala akataka kupiga kelele Gosu Gosu akamuwahi na kumziba mdogo “Usipige kelele hatutakudhuru”akasema Mathew “Tuonyeshe chumba cha balozi” akasema Mathew .Gosu Gosu akamuinua Yule msichana huku akiwa amemziba mdomo akawaongoza hadi katika chumba cha balozi Dr Yonathan Cohen.Mathew akatumia vifaa vyake akachokonoa kitasa cha mlango wa chumba cha balozi kikafunguka akakinyoga taratibu na kuingia ndani.Sauti ya mlango kufungulia ikamstua Dr Yonathan aliyekuwa amelala kitandani na mke wake akawasha taa iliyokuwa pembeni ya kitanda na moyo ulitaka kumpasuka baada ya kuwaona watu wenye silaha wakiwa wameingia mle chumbani. “Amkeni haraka sana!! Akaamuru Mathew.Dr Yonathan huku akitetemeka akamuasha mke wake. “Ninyi ni akina nani?Mnataka nini?Mmewez……” Dr Yonathan aliuliza maswali lakini Mathew akamtaka anyamaze na kumuelekeza Gosu Gosu awafunge kamba “Nini mnahitaji kutoka kwetu?Niambieni tafadhali nitawapatia chochote” akasema Dr Yonathan.Mke wake alikuwa analia “Balozi muda wetu ni mdogo sana wa kuwepo hapa.Tunachohitaji kutoka kwako ni ukweli.Endapo utatupa ukweli wa kile tunachokihitaji wewe na mke wako mtakuwa salama lakini endapo utaamua kutudanganya basi wewe na mke wako safari yenu ya maisha itaishia hapa.Tutawaua.Umenielewa ?akauliza Mathew “Mnahitaji kufahamu nini?Chochote mnachokitaka nitawaeleza tafadhali msituue”akasema balozi “Usiku wa leo umewasiliana na mwanamke mmoja anaitwa Devotha ambaye namba yake ya utambulisho ni BRAVO 15E 361 A” Sura ya balozi Dr Yonathan ilibadilika alipomsikia Mathew akitamka namba zile za utambulisho za Devotha.Mathew akauona mstuko ule wa balozi halafu akaendelea “Nataka kufahamu kilichowakutanisha usiku huu na vile vile nataka kujua mahala alipo” akasema Mathew.Balozi Dr Yonathan alikuwa anatetemeka “Umeulizwa swali jibu haraka sana! Akasema Gosu Gosu aliyekuwa nyuma ya balozi na kumsindikiza na kofi zito la shingo balozi akaanguka chini. “Balozi hatuna haja ya kuwaumiza au hata kuwatoa uhai lakini mkitulazimisha tufanye hivyo hatutasita kuwatoa roho zenu hapa hapa.Utakapotupa majibu tunayohitaji tutawaacha mkiwa salama salimini” akasema Mathew “Simfahamu mtu anayeitwa Devotha” akasema Dr Yonathan na sura ya Mathew ikabadilika “Humfahamu Devotha? “Ndiyo simfahamu mtu huyo.Kama kuna mtu aliyewaambia kwamba nimeonana naye amewadanganya.Simjui na sijawahi kukutana naye” akasema Dr Yonathan ` “Dr Yonathan ninafahamu kila kitu.Umekutana na Devotha usiku huu ubalozini kwako.Nakuuliza kwa mara ya mwisho nini kilichowakutanisha usiku huu? Yuko wapi hivi sasa?akauliza Mathew “Simfahamu mtu huyo.Mmekosea kuja kwangu mimi sina mahusiano yopyote na huyo Devotha.Kwanza ni nani huyo mwanamke?akauliza Dr Yonathan.Mathew akamtazama kwa macho yaliyojaa hasira halafu akasema “Dr Yonathan kwa mara ya mwisho kabisa naomba unieleze ukweli wa kile nilichokuuliza.Sitaki nikutendee ubaya wowote ule.Nipe majibu ya kile ninachokitaka na ninakuahidi nitakuacha hai wewe na mke wako” akasema Mathew “Vijana nawaeleza ukweli mtupu simfahamu huyo Devotha mnayemzungumzia.Aliyewae lekeza kwangu amewadanganya” Dr Yonathan akaendelea kusisitiza ` “Gosu Gosu huyu mzee bado hajatufahamu vyema anatulazimisha kufanya kile ambacho hatukuwa tumekusudia kukifanya” akasema Mathew na kumuangalia tena Dr Yonathan halafu akamgeukia Gosu Gosu “Ondoa kidole kimoja kimoja katika mikono ya mke wake hadi pale atakapokuwa tayari kutupa majibu” Mathew akasema na bila kupoteza muda Gosu Gosu akachomoa mkasi mdogo mgumu katika mfuko wa suruali.Dr Yonathan macho yakamtoka.Alipatwa na woga mkubwa.Bila huruma Gosu Gosu akakishika kiganja cha mkono wa mke wa Dr Yonathan na kwa nguvu akakikata kidole kimoja.Mke wa Dr Yonathan akaanguka chini akigala gala kwa maumivu makali.Gosu Gosu akachukua kitambaa na kumfunga mdomoni asiweze kutoa sauti.Dr Yonathan akiwa amefungwa mikono akapandwa na hasira akataka kusimama kumvaa Mathew lakini Tino tayari alikwisha muona akamuwahi kumtandika teke kali akaanguka chini. “Kwa nini mnatutenda hivi?Kwa nini mnamtesa mke wangu kiasi hiki nyie wanyama?akauliza Dr Yonathan huku akitetemeka kwa hasira baada ya kumuona namna mke wake alivyokuwa anagala gala chini kwa maumivu. “Dr Yonathan sisi ni wanyama sana kama ulivyosema na hapa bado haujauona unyama wetu.Nakuhakikishia kwamba tutamkata mke wako kiungo kimoja kimoja na atakata roho kwa mateso makali sana huku ukishuhudia.Nataka uniambie uko tayari kuzungumza au tuendelee na zoezi letu?akauliza Mathew. “Aaaagghh !! akasema kwa hasira Dr Yonathan. “Gosu Gosu endelea” akasema Mathew na Gosu Gosu akakishika kwa nguvu kiganja cha mkono wa mke wa Dr Yonatha na kukikata kidole cha pili.Ni maumivu makali sana aliyoyapata mwanamama Yule lakini sauti ya kilio cha uchungu haikuweza kusikika kwa kuwa alikuwa amefungwa kitambaa mdomoni. “Mashetani ninyi kwa nini mnamtesa mwanamke huyu asiye na kosa lolote?Kama ni kunitesa niteseni mimi.Kwa nini mnakuwa wakatili kiasi hiki?akauliza Dr Yonathan kwa hasira huku akimtazama mke wake namna alivyokuwa anagalagala kwa maumivu makali. “Uko tayari kuzungumza? Akauliza Mathew lakini bado Dr Yonathan aliyaelekeza macho yake kwa mke wake.Gosu Gosu akamnasa kofi kali “Jibu ulichoulizwa ! akasema kwa ukali “Dr Yonathan nakuuliza kwa mara ya mwisho.Uko tayari kuzungumza?akauliza Mathew “Tafadhali naombeni mumuache mke wangu.Kwa nini mnamtenda hivi?Nani kawatuma mtufanyie hivi?akauliza Dr Yonathan.Mathew akapandwa na hasira akamfuata mke wa Dr Yonathan akamuinua akachomoa kisu na kukiweka chini ya jicho. “Ninaliondoa jicho la mkeo kama hautakuwa tayari kuzungumza!! Akasema Mathew kwa ukali na taratibu kisu kile kikaanza kukata ngozi damu ikaanza kuchuruzika “Basi ! basi ! nitawaeleza kila kitu.Tafadhali msiendelee kumuumiza mke wangu!! Akapiga kelele Dr Yonathan.Mathew akamsukuma mwanamama Yule akaanguka chini halafu akamfuata Dr Yonathan “Haraka sana nieleze kila kitu kuhusu Devotha.Kwa nini mlikutana naye usiku wa leo?akauliza Mathew “Tafadhali naombeni kwanza mumsaidie mke wangu asiendelee kupoteza damu” akasema Dr Yonathan “Nieleze kwanza kile ninachokitaka halafu tutamshughulikia mke wako kama ukishindwa kuwa mkweli mkeo atapoteza damu nyingi na atafariki dunia huku ukishuhudia” akasema Mathew. “Tafadhali kuweni na huruma.Nitawaeleza kila kitu” akaomba Dr Yonathan.Mathew akamuelekeza Gosu Gosu amuhudumie Yule mama. “Wakati mke wako anaendelea kupatiwa matibabu kuzuia damu kuendelea kumwagika endelea kunipa maelezo! Akasema Mathew.Dr Yonathan akainama akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema “Ni kweli nilikutana na Devotha usiku huu baada ya kuelekezwa kufanya hivyo na makao makuu ya Mossad Tel Aviv”akaanza kutoa maelezo Dr Yonathan “Devotha ana mahusiano gani na Mossad?akauliza Mathew “Devotha ni wakala wa Mossad kwa hapa Tanzania na kila pale Mossad wanapokuwa na jambo lao la kufanya hapa Tanzania humshirikisha yeye.Namba ile uliyoitaja ndiyo namba yake ya utambulisho”akajibu Dr Yonathan “Endelea” akasema Mathew “Mossad wanaandaa operesheni hapa Tanzania ndiyo maana nilimuhitaji Devotha usiku huu ili aweze kukutana na watu waliotumwa na Mossad kuja kuandaa operesheni hiyo”akasema Dr Yonathan na kugeuka kumtazama mkewe ambaye alikuwa anabubujikwa machozi “Operesheni gani ambayo Mossad wanaiandaa hapa Tanzania? Mathew akauliza “Mossad wanamtafuta msichana mmoja ambaye ametekwa siku chache zilizopita na watu wasiojulikana anaitwa Olivia Themba.Wametuma watu wao kuja kufanya uchunguzi na kuandaa namna operesheni hiyo itakavyofanyika kabla ya kutuma kikosi kuja kumtafuta Olivia” akasema Dr Yonathan “Umesema Olivia Themba?Mathew akauliza “Ndiyo anaitwa Olivia Themba”akajibu Dr Yonathan “Olivia Themba ana mahusiano gani au ana umuhimu gani kwa Mossad hadi waandae operesheni ya kuja kumtafuta? “Sifahamu zaidi ya hapo.Maagizo niliyopewa ni kumtafuta Devotha na kumkutanisha na majasusi hao wa Mossad sifahamu sababu ya kumtafuta Olivia” “Dr Yonathan tulikubaliana utatutueleza ukweli wote lakini umevunja makubaliano yetu na umeniudhi.Nitakuomba kwa mara ya mwisho unieleze kila kitu kuhusiana na Olivia na Mossad” “Naomba mniamini jamani hayo niliyowaeleza ndiyo ninayofahamu.Msiendelee kututesa tafadhali sifahamu zaidi ya hapo” akasema balozi “Balozi kwa kuwa umevunja makubaliano yetu nakuomba umuage mkeo kwa mara ya mwisho” akasema Mathew “Tafadhali naomba msimuue mke wangu.Nimekwisha waeleza kile mlichotaka kukifahamu na sifahamu zaidi” akalia machozi Dr Yonathan “Tunaondoka na mke wako na hautamuona tena katika maisha yako.Naomba umtazame mkeo kwa mara ya mwisho na umuage” akasema Mathew “Jamani msitufanyie hivi.Niko chini ya miguu yenu nawaomba” akasema Dr Yonathan huku akilia machozi “Gosu Gosu mfunge huyo mwanamke tunaondoka naye” akasema Mathew na bila kupoteza muda Gosu Gosu akamuinua mke wa Dr Yonathan na kumuweka begani. “Kwa heri Dr Yonathan” akasema Mathew na kugeuka kuanza kuondoka na alipofika mlangoni Dr Yonathan ambaye mikono yake ilikuwa bado imefungwa kwa nyuma akamuita “Mrejesheni mke wangu nitawaeleza kila kitu” akasema Dr Yonathan.Mathew akageuka na kumtazama “Hii ni nafasi ya mwisho ninakupa !! akasema Mathew na kumtaka Gosu Gosu amrejeshe mke wa balozi chumbani akambwaga kitandani “Hatuna muda wa kupoteza balozi nieleze kila kitu” akasema Mathew “Ipo sababu kubwa ambayo Mossad wanamtafuta Olivia Themba” akasema Dr Yonathan na kuvuta pumzi ndefu halafu akaendelea “Miaka mitatu iliyopita mtu mmoja aliyefahamika kama Edger Kaka aliyewahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania alipatwa na ugonjwa wa ghafla akiwa bungeni na kupelekwa Dar es salaam katika hospitali kuu ya moyo alikopokelewa na Dr Olivia Themba na baadae hali yake ilipozidi kuwa mbaya Dr Olivia akafanya mpango na Edger akapelekwa nchini Israel ambako iligundulika kwamba alipewa sumu ili afe na kitendo hicho kilimlazimu waziri mkuu wa Tanzania wakati huo atume mlinzi maalum wa kwenda kumlinda Edger kwa siri bila yeye kujua kama analindwa.Mlinzi huyo kwa kushirikiana na mmoja wa majasusi wa Mossad waligundua kwamba mwanamke mmoja anayeitwa Habiba Jawad na mtu mwingine anaitwa Sayid Omar walifika hospitali usiku kumtembelea Edger.Watu hawa wawili wanatajwa kuwa ni wafadhili wakubwa wa kikundi cha IS ambacho kwa kushirikiana na vikundi vingine vidogo vidogo vya wanamgambo wamekuwa wakifanya mashambulio katika ardhi ya Israel na kuua waisrael.Serikali ya Israel imekuwa ikiwatafuta kwa muda mrefu hasa Habiba mwanamama tajiri bila mafanikio.Mara moja ilianza mipango ya kumpata Edger ili aweze kusaidia kuwapata Habiba na Sayid Omar na ndipo ilipotengenezwa ajali wakati Edger akirejea nchini kutokea Israel na Mossad wakafanikiwa kumchukua Edger wakati huku Tanzania ikiamini Edger alikufa katika ile ajali” “Edger kaka hajafariki dunia?! Akauliza Mathew kwa mshangao “Edger yuko hai lakini hii ni siri kubwa sana ya Mossad” akajibu Dr Yonathan “Kumbe Olivia alikuwa sahihi aliposisitiza kwamba Edger hajafa” akawaza Mathew “Rais wa Tanzania anahusika kwa namna yoyote ile na ajali hiyo iliyotengenezwa na Mossad?Anafahamu chochote?akauliza Mathew “Ilikuwa ni operesheni ya siri na ambayo serikali ya Tanzania hawajui chochote ndiyo maana mpaka sasa wanaamini Edger alifariki dunia.Rais wa Tanzania hafahamu chochote”akasema Dr Yonathan “Kwa nini Mossad wanamtafuta Olivia? Mathew akauliza “Kwa miaka mitatu Edger kaka amewekwa mafichoni akiteswa ili kumfanya aweze kutoa siri za maficho ya Habiba Jawad.Kufuatia mfululizo wa mauaji ya waisrael yanayoendelea hivi sasa kutoka kwa vikundi vya wanamgambo wa kipalestina majasusi wawili wametumwa kumuhoji Edger Kaka ili kufahamu namna ya kumpata Habiba Jawad lakini Edger aligoma kueleza chochote hadi pale atakapomuona Olivia mbele ya macho yake.Amekiri kwamba http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Olivia ndiye mwanamke pekee anayempenda kuliko wote hivyo kama Mossad wanataka awaeleze kila kitu wanachokitaka yuko tayari kuwaeleza lakini hadi atakapomuona tena Olivia ndiyo maana Mossad wanataka kufanya operesheni ya kumtafuta Olivia.” “Damn it ! akasema Mathew na kugonganisha mikono kwa hasira “Tayari nimewaeleza kila mnachokitaka naomba mtimize ahadi yenu mtuache huru” akasema Dr Yonathan “Devotha yuko wapi? “Sifahamu alipo kwa sasa” “Unafahamu namna ya kumpata? “Hap….Ndiyo ! akajibu Dr Yonathan baada ya kumuona namna Mathew alivyokuwa amebadilika “Katika mkono wake wa kushoto Devotha ana upungufu wa vidole viwili hivyo huvaa glovu ambayo imetengeneza maalum kama chombo cha mawasiliano.Ndani ya glovu hiyo kuna vidole vya bandia na mojawapo ya kidole hicho kina kadi maalum ambayo humtumia ujumbe kama ninataka kumuona.Ujumbe ukiingia hutoa mtetemo ambao yeye Devotha anaufahamu kisha huitoa kadi ile akaiweka katika simu na kuusoma ujumbe” akasema Dr Yonathan “Mtumie ujumbe haraka sana” akasema Mathew na kumfungua Dr Yonathna ambaye aliichukua simu yake akatuma ujumbe katika ile kadi ya Devotha na baada ya muda akasema “Ujumbe hajaupokelewa,kidole kile kimezimwa inaonekana ameweka katika chaji”akasema Dr Yonathan na Mathew akaichukua ile simu “Edger kaka yuko wapi?Amefichwa wapi?akauliza Mathew “Sifahamu mahala alipo.Ni siri ya Mossad.Mimi ni balozi tu na jukumu langu ni kutekeleza maelekezo ninayopewa na viongozi wangu” akasema Dr Yonathan “Hao majasusi ambao wamekuja kuandaa operesheni ya kumtafuta Olivia wako wapi? “Wako ubalozini kuna chumba wameandaliwa” “Utatupeleka huko ubalozini waliko hao jamaa” akasema Mathew “Vipi kuhusu mke wangu? “Tunaondoka naye tunakwenda kumtibu” akasema Mathew na kumuelekza Gosu Gosu ambebe mke wa Dr Yonathan wakatoka mle mle ndani haraka.Wakaingia katika gari lao na kumshusha yule askari ambaye bado hakuwa na fahamu wakamuwekea bunduki yake pembeni na kuondoka.Dr Yonathan bado alikuwa katika mshangao mkubwa sana. “Mke wangu mnampeleka kutibiwa wapi?akauliza Dr Yonathan. “Nyamaza !! akafoka Gosu Gosu.Safari ikaendelea kimya kimya na baada ya muda Dr Yonathan akauliza “Nyie ni akina nani?Nini hasa mnachokihitaji kwetu?Mnafahamu athari za hiki mlichokifanya? “Nimekwambia unyamaze.Kama hautaki kutii nitakufunga mdomo kama mke wako” akasema Gosu Gosu. Kutoka nyumbani kwa balozi wa Israel walielekea moja kwa moja katika makazi yao. “Dr Hiran anaendeleaje Ruby?akauliza Mathew “Anaendelea vyema .Kwa sasa amelala” “Ahsante sana.Dr Hiran kuna mgonjwa mwingine tumekuja naye nitakuomba umuhudumie ameumia sana” akasema Mathew na Dr Hiran akaenda kumtazama mke wa balozi na kutoa wazo apelekwe hospitali. “Hospitali atakwenda lakini naomba kwanza apatiwe huduma ya kwanza hapahapa” akasema Mathew na kumgeukia balozi “Mke wako atabaki hapa atapatiwa huduma na daktari na baadae ndipo atapelekwa hospitali” “Hapana.Mke wangu ameumizwa sana hawezi kubaki hapa” “Balozi tafadhali fuata kile ninachokuelekeza ili wewe na mke wako muendelee kuwa salama” akasema Mathew na kumtaka balozi atoke nje akaingia garini,kabla hawajaondoka Mathew akamfuata Dr Hiran. “Dr Hiran tfadhali usimpe mwanamke huyu nafasi ya kutoka humu chumbani au kuwasiliana na mtu yeyote hadi nitakaporejea” akasema Mathew na kukimbilia katika gari wakaondoka Safari ilikuwa ya kimya kimyakimya hadi walipofika katika ubalozi wa Israel.Wakasimamishwa na walinzi Dr Yonathan akatokeza kichwa na kujitambulisha kwamba yeye ni balozi wa Israel na amekuja ofisini kwake kwa dharura.Geti likafunguliwa wakaingia ndani.Wakashuka garini na Dr Yonathan akawaongoza kuelekea katika jengo lenye vyumba walikolala wale majasusi wawili. “Ni katika chumba kile pale ndipo walipo hao jamaa” akasema Dr Yonathan.Mathew akawafanyia ishara wenzake wajihadhari akamsogeza balozi hadi pale mlangoni na kumpa maelekezo agonge mlango na azungume kwa lugha ya kiingereza ili wamuelewe anachokisema. “Nani wewe? Ikauliza sauti kutokea ndani ya kile chumba “Ni mimi balozi Dr Yonathan.Kuna dharura imetokea ndiyo maana nimekuja ghafla kuja kuwaona” akasema Dr Yonathan na baada ya ya dakika mbili mlango ukafunguliwa na mtu mmoja aliyekuwa kifua wazi na mkononi akiwa na bastora. Mara tu alipotokeza mkono wake uliokuwa umeshika bastora ukapigwa teke kali na bastora ile ikamponyoka,akataka kurudi ndani na kuubamiza mlango lakini Tino akaurukia teke zito mlango ukafunguka akarukia ndani.Gosu Gosu naye akachumpa kama nyani na kurukia ndani. “Tulieni hivyo hivyo” akasema Tino. “Weka silaha yako chini ! Tino akamuamuru Fishel aliyekuwa kitandani akijiandaa kuamka na mkononi akiwa na bastora.Taratibu Fishel akaiweka bastora chini na kuisukuma kuelekea kwa Tino.Mathew akaingia ndani akiwa na balozi.Ilikuwa ni kama ndoto kwa wale jamaa hawakuwa wametegemea jambo kama lile kutokea.Mathew akampigisha magoti balozi pamoja na akina Fishel na Ehud halafu akasema “Sina muda wa kupoteza hapa kuna jambo moja tu ambalo ninataka ninyi watatu mnijibu ! akasema Mathew “Nataka mniambie wapi alipo Edger Kaka?Akauliza Mathew lakini wote wakawa kimya “Nauliza tena wapi aliko Edger Kaka? Akauliza tena Mathew lakini wale jamaa wakaendelea kuwa kimya.Mathew akamuendea mmoja wao na kumuelekezea bastora “Jina lako nani? “Fishel” akajibu “Fishel wapi alipo Edger Kaka?Nijibu ili ujiokoe” akasema Mathew ambaye macho yake yalionyesha ukatili mkubwa “Sifahamu alipo Edger Kaka” akajibu Fishel “Fishel sihitaji mchezo wowote wa kupotezeana muda.Nitakuuliza kwa mara ya pili wapi alipo Edger Kaka? Akauliza Mathew “Sifahamu alipo Edger Kaka” akajibu Fishel.Mkono wa Mathew ulikuwa mwepesi sana akaizinga bastora yake yenye kiwambo cha sauti na kuachia risasi Fishel akaaguka chini ubongo ukasambaa sakafuni. “Nimewaambia sihitaji mchezo ninachohitaji ni majibu!! Akasema Mathew kwa ukali akamuendea Ehud “Zamu yako.Nataka unieleze aliko Edger Kaka! Akasema Mathew “Sifahamu ! akajibu Ehud bila woga “Narudia kwa mara ya pili wapi alipo Edger Kaka?akauliza Mathew “Sifahamu” akajibu Ehud Kama alivyomfanya Fishel,Mathew akaachia risasi mbili na Ehud akaanguka chini.Mathew akamgeukia balozi Dr Yonathan. “Ni zamu yako sasa.Umeona kilichowapata wenzako?Sina utani hata kidogo nieleze haraka mahala alipo Edger Kaka” akasema Mathew “Sifahamu alipo Edger Kaka” akasema Dr Yonathan “Nitahesabu mpaka tano,kama usiponipa jibu na wewe yatakukuta kama yaliyowakuta hawa wenzako” akasema Mathew “Nakuhakikishia kwamba sifahamu chochote kuhusu mahala alipo Edger kaka” “Tano ! akaanza kuhesabu “Nasema kweli jamani sifahamu chochote! Akalia balozi “Nne ! “Jamani mtafanya makosa makubwa sana kama mtaniua.Israel na Tanzania ni nchi marafiki na hiki mlichokifanya kitakuwa na athari kubwa sana kwa nchi yenu.Nawasihi msiniue na nitawasaidia msiingie katika matatizo makubwa” akasema Dr Yonathan “Tatu ! akasema Mathew kwa ukali “Nawaomba vijana wangu msifanye hivyo.Msiniue tafadhali ! akasema balozi “Mbili ! akasema Mathew.maneno aliyoyatamka balozi hayakuonekana kumuingia kabisa “Moj…..” “Msiniue tafadhani nitasema ukweli” akasema balozi.Uso wake ukiwa umeloa jasho. “Wapi alipo Edger Kaka?akauliza Mathew kwa ukali “Edger Kaka amefichwa katika ubalozi wa Israel nchini Kenya” “Una hakika? “Ndiyo nina uhakika.Edger Kaka yuko katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi” akajibu balozi Dr Yonathan.Mathew akamuangalia na kumtaka anyanyuke wakatoka na kurejea katika gari lao wakaondoka. “Mathew mimi nitaishia hapa.Msaada wangu ulikuwa kuwasaidia kuingia salama nyumbani kwa balozi wa Israel operesheni iliyofanikiwa.Ninaomba mnirejeshe nyumbani na ninyi mtaendelea na mambo yenu.Mtakaponihitaji muda wowote niko tayari kutoa msaada” akasema Tino “Tino tunakushukuru sana kwa msaada wako mkubwa.Bado tutaendelea kuhitaji msaada wako” akasema Mathew . Walimrejesha Tino nyumbani kwake halafu wakachukua gari lao waliloliacha pale wakaendelea na safari hadi nyumbani kwa Mathew.Mke wa balozi alikuwa amehudumiwa na alikuwa amelala baada ya kupewa dawa ya kumfanya alale ili asiendelee kuhisi maumivu makali aliyokuwa anayapata.Dr Yonathan akafungiwa katika chumba kimoja na Mathew akamtaka Gosu Gosu waelekee katika chumba cha kusomea wanachokitumia kama ofisi yao. “Gosu Gosu tumefanya jambo kubwa na la hatari sana kuvamia makazi ya balozi wa nchi nyingine na kumteka yeye na mke wake na kama haitoshi tumevamia ubalozi wa Israel na kuua watu wawili.Hili ni suala kubwa na linaloweza kuleta mgogoro mkubwa wa kidiplomasia baina ya nchi zetu hizi mbili.Kwa namna yoyote ile serikali ya Israel lazima wataitaka serikali ya Tanzania itutafute na kuhakikisha tunapata adhabu stahiki kwa jambo tulilolifanya.Kwa upande wangu sijutii kile tulichokifanya kwani ilitulazimu kukifanya na tumeweza kugundua kitu kikubwa sana.Tumepata uhakika Edger Kaka hajafa na ajali ile ilikuwa ya kutengenezwa na waliofanya hivyo ni Israel wakitumia shirika lao la kijasusi la Mossad.Olivia alikuwa sahihi kusisitiza kuwa Edger hajafa nadhani tayari alikuwa na taarifa.Kitu ambacho hakuwa sahihi ni kumuhusisha Rais na tukio lile.Kwa mujibu wa Dr Yonathan,operesheni ile ya kumteka Edger ilikuwa ya siri na serikali ya Tanzania hawakufahamu chochote na hata Rais hajui chochote.Sifahamu kwa nini OIivia ameendelea kusisitiza kwamba Rais anafahamu mahala alipo Edger Kaka.Usiku wa leo tumegundua pia kwamba Edger Kaka ana mahusiano na watu wanaofadhili kikundi cha kigaidi cha IS na hii inamuhusisha moja kwa moja na kikundi hicho.Kwa maelezo ya balozi ninahisi Edger ndiye aliyemuunganisha Olivia na kikundi cha kigaidi.Kwa nini mtu kama Edger Kaka ambaye alikuwa ni mbunge mwenye heshima kubwa ajiunge na magaidi?Kwa nini ameyaharibu maisha ya Olivia kwa kumuunganisha na magaidi?Atanieleza hili nitakapomtia mikononi” akasema Mathew na kunyamaza akiwa na hasira nyingi “Edger Kaka anadai eti anampenda Olivia.Huu ni upuuzi mkubwa sana.Huko aliko aombe kwa miungu yake yote asiingie katika mikono yangu.Ameyaharibu maisha ya Olivia kwa kumuunganisha na magaidi na kwa hili atajuta kwa nini alikuja duniani!! Mathew akatolewa mawazoni na Gosu Gosu “Mathew pamoja na yote tuliyoyagundua usiku huu lakini bado tunarudi pale pale kwamba tunamuhitaji sana Olivia” akasema Gosu Gosu.Mathew akafikiri kidogo na kusema “Kuna jambo moja ambalo tunatakiwa kulifanya” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Jambo gani Mathew?akauliza Gosu Gosu “Tunatakiwa kuonana na Rais kabla ya mapambazuko” “Rais? Gosu Gosu akastuka “Ndiyo Gosu Gosu.Tunatakiwa kuonana na Rais.Edger Kaka anashirikiana na magaidi hivyo kwa kila namna lazima tumpate.Olivia anatafutwa hivi sasa na Mossad na Rais hana taarifa hizi hivyo kama tukionana naye na tukamueleza itakuwa rahisi sisi kumpata.Jambo lingine ni hiki tulichokifanya usiku wa leo kuvamia makazi ya balozi na kumteka nyara pia kuwaua majasusi wawili wa Mossad.Kwa hiki tulichokifanya Israel hawatatuacha salama.Tunahitaji kinga na mtu pekee anayeweza kutusaidia katika suala hili ni Rais” “Mathew nimeshangazwa kidogo na maamuzi ya kutaka kuonana na Rais.Huyu Rais ndiye aliyeelekeza idara ya siri ya usalama wa mambo ya ndani ya nchi wakuteke.Mpaka sasa Rais anaamini wewe pia ni mmoja wa watu wanaoshirikiana na magaidi.Kitendo cha Devotha kukutoa katika jumba lile kinazidi kumfanya Rais awe na hasira nawe zaidi.Una hakika anaweza akakubaliana nasi? “Tumegundua jambo kubwa sana na Rais lazima atusikilize.Nitakwenda ikulu kuonana na Rais usiku huu huu.Wewe utabaki hapa ukiwalinda balozi na mke wake.Hatutawaachia hadi nitakapokuwa nimeonana na Rais” “Mathew I’m so scared ! “Me too.I’m scared.I’m not sure about this but it is the only option we have right now.Kama sintarejea mpaka itakapofika saa mbili asubuhi hakikisha balozi unaendelea kumshikilia kwani ni yeye atakayeniokoa.Mtumie yeye kumshinikiza Rais aniachie huru lakini ninaamini mambo yatakwenda vyema.Nitaonana na Rais na atanielewa.Mlinde sana Ruby,hakikisha anakuwa salama” akasema Mathew “Mathew utatumia njia gani kuonana na Rais usiku huu? Akauliza Gosu Gosu “I don’t know yet but I’ll find a way.Lazima nionane na Rais usiku huu” akasema Mathew na kuagana na Gosu Gosu akaingia garini na kuondoka. “Mungu mlinde Mathew arejee salama.Hiki anachokifanya ni kitu cha hatari kubwa” akaomba Gosu Gosu. - MATHEW NA WENZAKE WAMEMTEKA BALOZI WA ISRAEL NA MKEWE NA KUUA MAJASUSI WAWILI WA MOSSAD NINI KITATOKEA? - MATHEW ANAAMUA KWENDA KUONANA NA RAIS KUMUELEZA KILE ALICHOKIGUNDUA KUHUSU EDGER KAKA..JE LENGO LAKE LITAFANIKIWA?ATA REJEA SALAMA? MPENZI MSOMAJI USIKOSE SEHEMU IJAYO YA SIMULIZI HII…







“Lazima nionane na Rais usiku wa leo.Mambo haya makubwa tuliyoyagundua usiku huu anapaswa kuyafahamu tatizo ni namna ya kuweza kuonana naye kama atakuwa tayari kunipokea na kunisikiliza.Mimi na yeye tayari tumekwisha jenga ukuta mkubwa kati yetu na hadi hivi sasa anaamini kwamba mimi na Olivia tunashirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS.Pamoja na hayo lakini kwa umuhimu wa jambo hili lazima nifanye kila mbinu hadi nihakikishe nimeonana naye usiku huu wa leo kabla ya mapambazuko” akawaza Mathew akiwa katika mwendo mkali baada ya kuondoka nyumbani kwake “Siri tuliyoigundua ni kubwa hadi mwili unanisisimka.Edger Kaka ambaye alikuwa mbunge aliyejizolea umaarufu mkubwa sana kutokana na umahiri wake wa kupinga rushwa na mafisadi kumbe anashirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS.Imewezekanaje kwa muda huu wote aliokuwa mbunge vyombo vyetu vya usalama vimeshindwa kumfuatilia na kufahamu kuwa anashirikiana na magaidi?Ninaanza kupata picha kwamba yawezekana hayuko peke yake lazima upo mtandao.Kwa siku za karibuni IS wamekuwa wanajitanua sana barani Afrika hususan katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.Ninahisi yawezekana zile harakati zake zote za kupambana na mafisadi zilikuwa ni kwa ajili ya kuficha mambo yake aliyokuwa anayafanya nyuma ya pazia akishirikiana na IS.Nini hasa malengo yao? Je Edger alijiunga na IS kwa ajili ya fedha au kuna sababu nyingine? Akajiuliza Mathew “Kibaya zaidi kinachonifanya niwe na hasira naye,ni kumuingiza Olivia katika kikundi cha magaidi.Ameyaharibu maisha ya Yule mrembo_Olivia hastahili kuishi maisha ya namna hii.Pamoja na kuyaharibu maisha yake bado ameendelea kudai kwamba anampenda na anawataka Mossad wamtafute ili awaeleze kile wanachokitaka kutoka kwake.Mwendawazimu huyu hatafanikiwa kumuona tena Olivia katika maisha yake.Nitampata Olivia na kumuondoa katika maisha haya aliyoingia” Mathew akaendelea kuwaza na alipokumbuka kuhusu Mossad akahisi baridi “Mossad ni mojawapo ya mashirika makubwa ya ujasusi duniani ambalo nimeingia nalo katika mgogoro mkubwa.Nimeua majasusi wao wawili na kama haitoshi nimemteka balozi wa Israel hapa nchini.Hili si jambo dogo.Huu ni mgogoro mkubwa sana wa kidiplomasia na taifa la Israel hata hivyo siogopi kwani wao ndio walioanza uchokozi wao kwa kuingia na kufanya operesheni kwenye ardhi yetu wakaua Rais na kumteka Edger.Kama walikuwa wanamuhitaji Edger Kaka wangewasiliana na mamlaka za hapa Tanzania wakashirikiana kumpata na si kuingia katika ardhi yetu wakafanya watakacho na kuondoka kwa vile tu wao ni taifa lenye uwezo mkubwa wanadhani wana haki ya kuingia katika nchi yoyote na kufanya watakacho.Hii ni dharau kubwa kutoka kwa haya mataifa yaliyoendelea na lazima tuwaonyeshe kwamba japokuwa sisi hatujaendelea kama wao lakini tunao uwezo mkubwa kama wao.Sijali kitakachotokea lakini ninachokitaka mimi ni kumpata Edger Kaka” akawaza na kuongeza mwendo wa gari akalipita gari kubwa la mafuta “Kama mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ameweza kushirikiana na magaidi wa IS bila kujulikana kuna ulazima mkubwa wa kuwachunguza kwa kina viongozi wetu kabla ya kuwachagua au kuwapa nyadhifa.Wengine wanakuwa ni mamluki wanatumiwa kwa maslahi ya mataifa na vikundi vilivyoko nje.Sijui watanzania hasa wale waliokuwa wafuasi wakubwa wa Edger Kaka watazipokeaje taarifa za kuwa mbunge wao,kiongozi wao anashirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS.Naamini zitakuwa ni taarifa mbaya sana kwao na wengi hawataamini.Kitu kingine ambacho nakifikiria ni kwamba huyu Edger hakuwa peke yake kuna watu ambao amekuwa akishirikiana nao hapa nchini na nina uhakika mkubwa tayari IS wamekwisha jenga mtandao wao ndani ya Tanzania na ndiyo maana ukitazama shambulio la leo katika hospitali ya Mtodora linaoneka na kufanyika kwa wepesi sana.Ninaapa kuufumua kabisa mtandao wote wa IS hapa nchini” akawaza Mathew Kichwa cha Mathew Mulumbi kilijaa mawazo mengi akiwa barabarani.Aliendesha gari hadi nje ya nyumba Fulani nzuri iliyozungushiwa ukuta wa rangi nyeupe na pembeni ya ukuta kukiwa na maua mazuri.Mlinzi aliposikia muungurumo wa gari akafungua dirisha dogo akachungulia halafu akafungua mlango mdogo wa geri akatoka nje.Mathew akashuka garini “Habari yako kaka” Mathew akamsalimu Yule jamaa “Habari nzuri.Nini shida yako hapa usiku huu?akauliza Yule mlinzi ambaye alionekana akutoka usingizini “Ninaitwa Mathew Mulumbi nimekuja kuonana na mzee Meshack.Ni muhimu sana tafadhali”akasema Mathew “Unataka kuonana na mzee usiku huu?Haitawezekana ndugu subiri hadi kesho asubuhi.Muda huu amelala na hapendi usumbufu akiwa amepumzika” “Nalifahamu hilo ndugu yangu lakini naomba umjulishe kwamba Mathew Mulumbi yuko hapa na ataruhusu nikaonane naye”akaomba Mathew “Ndugu yangu naomba unisikilize.Ondoka hapa urejee asubuhi.Hakuna namna ninayoweza kukuruhusu usiku huu ukaonane na mzee” akasema Yule mlinzi.Mathew hakutaka kubishana naye akarejea garini. “Nimegonga mwamba.Huyu mlinzi hataweza kuniruhusu kuonana na Meshack Jumbo na sitaki kutumia vurugu kuingia ndani.Ninasita kumpigia simu Meshack kwani namba zake sizikumbuki vyema lakini ngoja nijaribu” akawaza Mathew na kuziandika namba katika simu yake akapiga.Hakuwa na uhakika na zile namba “Sina uhakika kama namba hizi ni sahihi lakini lazima nijaribu” akawaza Mathew wakati simu ile ikiita ikakatika bila kupokelewa akazitazama tena zile namba na kupiga simu ikaanza kuita na baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa.Akashusha pumzi baada ya kuitambua sauti ile iliyopokea simu. “Ahsante Mungu” akasema Mathew Mulumbi kwa sauti ndogo “Hallow ! ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Mathew aliitambua ni ya mzee Meshack Jumbo mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi “Mzee Jumbo samahani kwa kukusumbua usiku huu ni mimi Mathew” “Mathew ! Jumbo akashangaa “Ndiyo mzee.Samahani sana kwa kukusumbua usiku huu” “Una tatizo gani Mathew?akauliza mzee Jumbo huku akiinuka kitandani “Mzee nimekuja nina tatizo niko hapa nje ya geti lako” “Uko hapa nyumbani kwangu? “Ndiyo mzee lakini mlinzi wako amenizuia amegoma hata kukupigia simu” akajibu Mathew “Sawa ninampigia mlinzi akuruhusu uingie ndani.Hajakosea anafuata maelekezo yangu niliyompa” akasema Meshack Jumbo na kukata simu.Hazikupita sekunde kumi Mathew akamuona mlinzi akitoa simu mfukoni akaipokea halafu akafungua geti na kumruhusu Mathew aingie ndani.Mathew akaegesha gari na kushuka,mlango wa sebuleni ukafunguliwa Meshack Jumbo akatoka akiwa amevaa mavazi ya kulalia “Mathew karibu sana” akasema Meshack na kumkaribisha Mathew ndani “Habari za hapa mzee.Samahani sana kwa kukusumbua usiku huu” akasema Mathew “Bila samahani Mathew kuwa na amani.Kwema huko utokako? “Huko nitokako si kwema mzee wangu ndiyo maana nimekuja kwako usiku huu” akasema Mathew “Nini kimetokea?Ni kuhusiana na shambulio lililotokea usiku wa leo katika hospitali ya Mtodora?akauliza Meshack “Hilo nalo linahusiana na kile kilichonileta hapa.Mzee kwa kuwa muda si rafiki sana nitakueleza kwa ufupi kile kinachoendelea” “Mathew Mulumbi unanifahamu mimi sipendi kufahamu mambo kwa kifupi.Nataka unieleze jambo kwa kirefu ili nielewe na hata kama unahitaji msaada wangu nijue nitakusaidia vipi.Nieleze kwa kirefu kila kitu” akasema Meshack Jumbo na Mathew akaanza kumuelezea kila kitu toka alivyokutana na Olivia Themba hadi yale waliyoyagundua usiku ule. “I think I need a drink” akasema Meshack Jumbo na kutoka baada ya dakika chache akarejea akiwa na chupa kubwa ya mvinyo akamimina katika glasi akanywa funda kubwa. “You need some?akauliza “No thank you! Akajibu Mathew “Mathew sijui nianzie wapi kusema chochote kwa hiki ulichonieleza.Nimestuka sana.Kwanza kwa magaidi kuweza kupiga hatua kubwa kiasi hiki na kufanya kila wakitakacho.Kuna udhaifu katika vyombo vyetu vinavyohusika na kudhibiti ugaidi hapa nchini ndiyo maana magaidi wameweza kupata mwanya wa kufanya kile wakitakacho.Pili ni kuhusu Edger Kaka.Huyu alikuwa ni mbunge mwenye jina kubwa hapa nchini na alifanya kazi kubwa ya kufichua ufisadi mkubwa uliokuwa unafanywa na watu mbali mbali hususan viongozi walioko serikalini.Alijijengea umaarufu mkubwa sana kwani aliweza kuwataja mafisadi hadharani bila woga.Aliaminiwa mno na alikuwa mmoja wa wanasiasa vijana waliotabiriwa kufika mbali sana katika uongozi lakini taarifa kwamba anahusiana na kikundi cha kigaidi cha IS imenistua sana.Sikutegemea kabisa.Kwanza kusikia kwamba yuko hai ni mstuko mkubwa kwangu.Sote tunaamini alifariki katika ile ajali kumbe ulikuwa ni mchezo tu.Kwa kweli sijui niseme nini” akasema Meshack Jumbo na kumimina tena mvinyo katika glasi akanywa “Mzee kwa hapa nilipofika nimekwama ninahitaji msaada ndiyo maana nimekuja kwako” “Sema Mathew unahitaji nikusaidie nini? “Nahitaji kuonana na Rais usiku huu.Kama nilivyokueleza Rais anaamini mimi na Olivia wote tunatumiwa na kikundi cha IS na hivi sasa idara ya siri ya mambo ya ndani ya nchi wananisaka kila kona wakiamini ninashirikiana na magaidi hivyo siwezi kupata nafasi ya kuonana na Rais ndiyo maana nimekuja kwako ili utafute namna ya kunikutanisha na Rais usiku huu niweze kuzungumza naye ayafahamu haya tuliyoyagundua.Hata yeye mwenyewe haufahamu ukweli wa hili suala hivyo nataka nimueleze kwa kina ajue namna suala hili lilivyokaa.Kingine ninachohitaji kuonana na Rais ni kuhusu Olivia.Yeye anafahamu mahala alipo Olivia na kama tukiweza kumpata basi atatusaidia kufahamu mambo mengi kuhusiana na mtandao wa IS na mipango yao hapa nchini.Jambo lingine ni kwamba tayari tumeingia katika mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kwa kuvamia makazi ya balozi wa Israel na kumteka vile vile kuwaua majasusi wawili wa Mossad waliotumwa hapa nchini kuandaa operesheni ya kumtafuta Olivia ili wamtumie katika kumlazimisha Edger Kaka awaeleze mahala walipo watu ambao wanafadhili kikundi cha IS ambao yeye Eger anawafahamu na walikwenda kumtembelea alipokuwa amelazwa hospitali nchini Israel.Huu ni mgogoro mkubwa na Rais lazima aufahamu kwani ni yeye anayeweza kutusaidia.Jambo lingine mzee tunahitaji kumpata Edger Kaka ambaye anashikiliwa katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi.Hii ni operesheni kubwa na nzito na mimi sina uwezo wa kuitekeleza mwenyewe ninahitaji msaada mkubwa na mtu pekee anayeweza akaniwezesha ni Rais hivyo mzee ninaomba unisaidie niweze kuonana naye kwa usiku huu” akasema Mathew.Meshack Jumbo akainamisha kichwa akafikiri kwa muda na kusema “Mathew jambo hili ni kubwa sana na Rais wa nchi lazima alifahamu lakini tatizo ni namna ya kukutana na Rais.Siwezi kukudanganya kijana wangu nimekuwa serikalini kwa miaka mingi na nimekuwa na ukaribu na marais karibu wote waliopita lakini huyu wa sasa sina ukaribu naye kabisa na hata mawasiliano naye sina” akasema Meshack Jumbo “Mzee hatuwezi kukwama.Tafuta namna ya kuniwezesha kukuonana na Rais naamini huwezi kushindwa kupata mbinu yoyote” akasema Mathew na Meshack akazama katika tafakari halafu akasema “Nimepata wazo.Mke wangu anaye mdogo wake ameolewa na aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama wa taifa ambaye amestaafu miaka mitatu iliyopita.Huyu anaweza akawa na ukaribu na Rais na anaweza akatusaidia kuonana naye lakini lazima naye tumshirikishe alifahamu jambo hili.Anaitwa Joel Mshana” akasema Meshack Jumbo “Hakuna tatizo mzee ninachohitaji mimi ni kuonana na Rais” akasema Mathew na Meshack Jumbo akainuka akaenda chumbani kwake na kumkuta mke wake akiwa amekaa kitandani “Kuna nini Meshack?Nimekusikia ukizungumza na mtu sebuleni.Kuna mgeni? “Kuna mgeni amekuja.Sikutaka kukuamsha usingizini lakini mgeni mwenyewe ni Mathew Mulumbi” “Kuna tukio gani?Mathew hawezi kuja usiku huu kama hakuna tukio limetokea” “Nitakueleza baadae lakini kwa sasa nataka kuzungumza na shemeji Diana” “Diana? Mke wa Meshack Jumbo akastuka aliposikia mumewe anataka kuzungumza na mdogo wake usiku ule “Diana amefanya nini? “Ninataka kuzungumza na mumewe” akasema Meshack “Kuna tatizo gani Meshack?Nieleze tafadhali kama mdogo wangu yuko kwenye hatari” “Hakuna hatari yoyote usihofu.Ninataka kuzungumza na mume wake.Mathew ana shida ya kuonana na Rais na amekuja kwangu ili nimsaidie kumkutanisha naye lakini sina ukaribu na Rais huyu wa sasa ndiyo maana ninataka kuomba msaada wa Joel yeye amestaafu kazi si miaka mingi na nina uhakika mkubwa atakuwa ana mawasiliano ya karibu na Rais” “Una uhakika ni hilo tu na Diana hayuko katika hatari? “Niamini darling si Diana wala mume wake walio katika hatari.Tunataka kutafuta njia ya kumsaidia Mathew kuonana na Rais” akasema Meshack na kuchukua simu yake akatoka akarejea sebuleni halafu akazitafuta namba za simu za shemeji yake Diana akampigia. “Mzee Meshack” akajibu Diana baada ya kuipokea simu “Umeniogopesha sana kwa simu hii ya usiku.Kuna tatizo lolote huko?akauliza Diana kwa wasi wasi “Diana naomba unisamehe sana kwa simu hii ya usiku.Huku kwema kabisa hakuna tatizo lolote” “Haujawahi kunipigia simu usiku mwingi namna hii ndiyo maana nimestuka sana” “Usihofu Diana.Nimepiga simu usiku huu ninataka kuzungumza na Joel na mimi sina namba zake za simu” “Kuna tatizo lolote? Akauliza Diana “Hakuna tatizo usihofu ila kuna suala nataka kuzungumza naye la muhimu” akajibu Meshack Jumbo “Sawa subiri kidogo” akasema Diana na kumpatia simu mume wake “Hallow Meshack” akasema Joel Mshana “Joel samahani sana kwa kukuamsha usiku huu” “Usijali Meshack.Vipi huko kwema? “Joel ninahitaji kuzungumza nawe jambo Fulani.Kama hutajali naomba nije hapo kwako usiku huu kuna suala la muhimu sana” “Suala gani Meshack?Kuna tatizo hapo nyumbani? “Ni suala linalohusiana na usalama wa nchi.Naomba tafadhali nije hapo kwako tuzungumze” akasema Meshack “Meshack unaniogopesha kidogo.Unaweza ukanieleza japo kidogo tu suala hilo linahusiana na nini? “Usijali Joel nitakuja kukueleza nikifika si suala la kuzungumza simuni.Ndani ya dakika arobaini naamini nitakuwa nimefika hapo kwako” akasema Meshack “Sawa karibu sana Meshack ninakusubiri hapa” akasema Joel na Meshack akakata simu. “Joel amekubali.Tusipoteze muda twende tukaonane naye” Meshack akamwambia Mathew akaenda chumbani akamuaga mke wake wakaingia katika gari la Mathew na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Joel Mshana “Mathew bado natafakari kuhusu Edger Kaka.Taarifa kwamba anashirikiana na magaidi imenistua sana.Nini hasa malengo yake ya kushirikiana kwa siri na watu hawa?akauliza Meshack Jumbo “Kwa maelezo niliyoyapata kutoka kwa balozi wa Israel Dr Yonathan Cohen,Edger Kaka akiwa hospitali alitembelewa na watu wawili ambao wanatafutwa sana na serikali ya Israel kwa kufadhili kikundi cha kigaidi cha IS pamoja na vikundi vingine vya wanamgambo wa kipalestina wanaoua waisrael hivyo basi kitendo hicho kinaonyesha moja kwa moja kwamba lazima ana mahusiano ya karibu na watu hao wawili na ndiyo maana Israel wakamteka na kutufanya tuamini kwamba amekufa lengo lao ni kumuhoji kupata taarifa za watu hao wanaowatafuta”akasema Mathew “Kama watu hao wanaotafutwa na serikali ya Israel waliweza kuvuka mpaka na kuingia Israel wakaenda kumuona Edger hospitali inaonyesha wazi kuna watu ndani ya serikali ya Israel ambao wanawasaidia katika kutekeleza mipango yao.Huu Lazima ni mtandao mkubwa.Nadhani ni wakati wa Israel sasa kuyaachia maeneo ya wapalestina inayoyakalia kimabavu ili kumaliza vita hii ambayo na sisi pia tumejikuta tukiingia bila kutaka.Wafadhili hao wa ugaidi wanafadhili vikundi ambavyo vinafanya mashambulio katika makazi ya waisrael na kuipelekea serikali ya Israel kufanya operesheni ya kimya kimya ndani ya nchi yetu na kumchukua Edger Kaka na huu ni mgogoro mmoja.Mgogoro mwingine ni pale ambapo balozi wao ametekwa na watu wao wawili kuuawa.Kama kusingekuwa na mapigano haya ya waisrael na wapalestina haya yote yasingekuwepo ndiyo maana ninasema kwamba ninadhani ni wakati muafaka kwa serikali ya Israel kuwarejeshea wapalestina maeneo yao wanayoyakalia kimabavu ili kuumaliza huu mzozo”akasema Meshack Jumbo “Mzozo wao hautuhusu.Kinachonipa hasira ni dharau za mataifa haya yaliyoendelea kwa mataifa yetu yenye uchumi mdogo.Wameingia hapa nchini kwetu wakafanya operesheni yao kimya kimya na kumchukua raia wetu bila sisi kufahamu na kama haitoshi bado wana mipango ya kuja tena kufanya operesheni nyingine ya siri hapa nchini ya kumtafuta Olivia wamchukue kama walivyomchukua Edger Kaka.Hii ni dharau kubwa sana kwani hata kama Edger Kaka ana mahusiano na magaidi serikali yetu ilipaswa kujulishwa lakini hawakufanya hivyo.Mgogoro huu wameuanzisha wao wenyewe na sasa ni zamu yetu kuwaonyesha kwamba hata sisi tunao uwezo mkubwa kama wao na tunaweza kufanya mambo kama wanayoyafanya wao.Watashangaa namna tutakavyokwenda kumchukua Edger Kaka katika ubalozi wao.Sijali kitakachotokea lakini kitu cha muhimu ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama” akasema Mathew akionekana kuwa na hasira “Huyu mwanamke Olivia kuna chochote unachotaka kunieleza kuhusu yeye?akauliza Meshack “Najua unachotaka kukifahamu mzee.Urafiki wetu ulikwenda mbali zaidi.Nadhani tayari umekwisha nielewa” “Lakini Mathew wewe una mke wako kwa nin………..” “Mzee naomba tusizungumzie masuala hayo.Tujielekeze katika jambo linaloikabili nchi kwa sasa” akasema Mathew Safari iliendelea kukiwa na maongezi machache hadi walipofika nyumbani kwa Joel Mshana ambaye walimkuta anawasubiri. “Karibu sana Meshack” akasema Joel Mshana.Meshack na Mathew wakaingia sebuleni “Joel awali ya yoite naomba uniwie radhi sana kwa usumbufu huu mkubwa niliowapa usiku huu” akasema Meshack Jumbo “Usihofu Meshack.Naamini lazima kuna sababu ya msingi hivyo ondoa hofu kabisa” akasema Joel “Ahsante sana Joel.Kabla hatujaendelea naomba nikutambulishe huyu ni Mathew Mulumbi.Amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi wakati wangu” akasema Meshack Jumbo “Mathew Mulumbi ! Huyu si mgeni kwangu.Ninamfahamu japo sina hakika kama naye ananifahamu na ndiyo maana nilipokuona naye nikajua lazima kuna jambo kubwa” akasema Joel “Joel ni kweli kuna jambo kubwa na tumekuja hapa kwa ajili ya kuomba msaada wako” “Ulinieleza ni suala linalohusiana na usalama wa Taifa.Ningependa kulifahamu suala hilo na msaada upi mnauhitaji?Kama utakuwa ndani ya uwezo wangu ninawaahidi kuwasaidia” akasema Joel Mshana. “Joel kumekuwa na mfululizo wa matukio yasiyo ya kawaida kwa siku za karibuni kwa mfano matukio ya utekaji nyara.Alitekwa Olivia Themba na baadae akatekwa baba yake mzee Agrey Themba.Wakati bado jitihada za kuwatafuta zikiendelea usiku wa leo kumetokea shambulio la kigaidi katika hospitali ya Mtodora na mpaka sasa idadi kamili ya vifo na majeruhi bado haijatolewa.Usiku wa leo amenifuata Mathew na kunifumbua macho kuhusiana na haya mambo ambayo yamekuwa yanaendelea hapa nchini kuanzia utkwaji wa Olivia na hili la usiku wa leo katika hospitali ya Mtodora.Ni mambo mazito sana.Lengo la Mathew kuja kwangu alinitaka nimsaidie aweze kuonana na Rais ili amueleze masuala haya makubwa lakini mimi sina mahusiano ya karibu na Rais ndiyo maana nikaona tuje kwako utusaidie kwa hilo.Naamini wewe na Rais mna mahusiano ya karibu na itakuwa rahisi kuonana naye kupitia kwako” akasema Meshack Jumbo.Joel Mshana akafikiri kidogo na kusema “Hujakosea Meshack.Japokuwa nimestaafu kazi lakini bado nina mahusiano ya karibu na Rais na hata yalipotokea matukio haya hasa la usiku wa leo nimempigia nikampa pole kwa kile kilichotokea katika hospitali ya Mtodora.Uwezo wa kuwasaidia kuonana na Rais ninao lakini siwezi kufanya hivyo bila kufahamu sababu hasa ya kutaka kuonana naye.Rais ni mtu mkubwa na ili niweze kuwasaidia kuonana naye nataka kufahamu sababu”akasema Joel “Mzee Joel,ninazo taarifa nyeti sana za kuhusiana na kile kinachoendelea hivi sasa hapa nchini ninazotaka kuzifikisha kwa Rais usiku huu.Muda wetu ni mfupi na siwezi kukueleza kila kitu lakini kuna mambo nyeti sana ambayo Rais anapaswa kuyafahamu kuhusiana na shambulio lililotokea usiku huu na kile kinachoendelea hapa nchini”akasema Mathew “Mathew nahitaji kufahamu ni taarifa gani ulizonazo ili na mimi nipime kama zina uzito wa kuonana na Rais.Usihofu kuhusu mimi nimewahi kuwa mkuu wa idara ya usalama wa Taifa na nimestaafu miaka mitatu iliyopita.Nieleze tafadhali taarifa ulizonazo” akasema Joel “Mzee Joel nakufahamau wewe ni nani na ninakuamini lakini Rais anapaswa kuzisikia taarifa hizi kwanza kabla yako.Naomba umuamini mzee Meshack Jumbo na utusaidie kwenda kuonana na Rais na utasikia kila kitu” akasema Mathew “Mathew nasikitika kwamba nitashindwa kukusaidia ombi lako bila kufahamu sababu ya kutaka kuonana na Rais.Hamuwezi kwenda peke yenu lazima niwapeleke mimi na ili niwapeleke huko lazima niwe ninafahamu kile ambacho kimewapeleka.Lazima iwe ni sababu kubwa ili nimshawishi akubali kuonana nawe” akasema Joel.Meshack Jumbo akakohoa kidogo na kusema “Joel mimi na wewe tunafahamiana vyema,tumekuwa marafiki kwa muda mrefu,tumeshirikiana katika mengi na isitoshe sisi ni ndugu kwani tumeoa nyumba moja naomba uniamini katika hili ninalokuomba utusaidie.Mathew ana mambo ya muhimu sana ambayo anataka kuyafikisha kwa Rais.Kama ningekuwa na ukaribu na Rais nisingekujak ukusumbua usiku huu lakini sina ukaribu naye ndiyo maana ninakuomba utusaidie Joel” “Meshack sina tatizo lolote nawe.Wewe ni ndugu yangu lakini tatizo ni kwamba nitamueleza nini Rais akitaka kujua sababu ya kutaka kwenda kuonana naye usiku huu?Ni hicho pekee ambacho ninataka kukifahamu” “Mweleze ni suala muhimu kwa usalama wa Taifa” akasema Mathew.Joel akageuka na kumtazama Meshack Jumbo “Tusaidie tafadhali Joel” akasema Meshack na Joel akainamisha kichwa “Meshack mmenipa mtihani mgumu sana” “Usihofu Joel ninaamini hata Rais mwenyewe atakushukuru kwa hiki atakachokwenda kuambiwa na Mathew” akasema Meshack Jumbo. Joel akaenda chumbani kwake akachukua simu na kurejea sebuleni akazitafuta namba za Rais akapiga. “Hallow Joel” akasema Dr Evans baada ya kupokea simu “Mheshimiwa Rais samahani sana kwa kukusumbua usiku huu” akasema Joel “Bila samahani Joel.Nimemaliza kikao na wakuu wa vyombo vya usalama muda mfupi uliopita hivyo usihofu kitu kazi zinaendelea” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais nimekwisha kupa pole awali lakini naomba nikupe tena pole kwa mara ya pili kwa suala lililotokea leo” “Nashukuru sana Joel” “Mheshimiwa Rais pamoja na kukupa pole lakini simu hii ni kwa ajili ya jambo lingine kabisa” “Nakusikiliza Joel” “Mheshimiwa Rais japokuwa tumestaafu kazi lakini kwa nyakati kama hizi ambazo taifa letu linapitia wakati mgumu tunalazimika kuvaa tena gwanda kuingia katika uwanja wa mapambano.Yawezekana hatuwezi kushika bunduki na kupambana lakini tunao uzoefu mkubwa sana katika masuala haya ya usalama ambao tunaweza tukautumia” “Uko sahihi Joel,kama Taifa tunapitia wakati mgumu sana na kila mzalenzo wa taifa hili ambaye anadhani anaweza kuwa na msaada wa kuwafahamu hawa waliofanya matukio haya maovu tunamkaribisha.Mtu kama wewe Joel uzoefu wako unahitajika sana kwa wakati kama huu” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais hilo ndilo hasa ambalo limenipelekea nikupigie simu usiku huu.Naomba pia utambue kwamba niko hapa na Meshack Jumbo” “Meshack Jumbo?akauliza Dr Evans “Ndiyo.Ni mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi” “Mheshimiwa Rais tunataka kuja kuonana nawe usiku huu kuna jambo la muhimu sana tunataka kuzungumza nawe linalohusiana na haya mambo yanayoendelea hivi sasa hapa nchini” akasema Joel na ukimya mfupi ukapita “Mheshimiwa Rais” akaita Joel “Nafahamu huu si utaratibu na sisi kama wastaafu wa tuliokuwa vyombo vya usalama tunafahamu taratibu zilivyo lakini tunaomba utukubalie ombi letu la kutaka kuonana nawe usiku huu mheshimiwa Rais.Nimuhimu sana”akasema Joel “Sipati kigugumizi kukutana nanyi Joel lakini suala hilo mnalotaka kunieleza haliwezi likaahirishwa hadi kesho asubuhi tukaonana mkanieleza?Muda mfupi ujao nitakuwa na kikao kingine tena ndiyo maana ninawaomba kama ikiwezekana tuonane asubuhi” akasema Dr Evans. “Mheshimiwa Rais suala hili ni muhimu sana na haliwezi kusubiri hadi asubuhi ndiyo maana tunataka kuonana nawe usiku huu huu kabla ya mapambazuko”Joel akasisitiza “Joel unaweza ukanigusia suala hilo ni kuhusu nini? “Mr President it’s the matter of national security so I can’t tell you on phone” akasema Joel “Joel kwa kuwa wewe ni mtu ambaye tumefanya kazi vizuri ninakufahamu vyema nitaahirisha kwa muda kikao ambacho kilikuwa kifanyike muda mfupi ujao kwa ajili ya kuja kuonana nanyi.Mtahitaji usafiri nitume vijana wangu waje wawachukue mahala mlipo?akauliza Dr Evans “Tunashukuru mheshimiwa Rais lakini tutatumia usafiri binafsi.Tunashukuru sana kwa kukubali kuonana nasi tutafika hapo ikulu si muda mrefu sana kutoka sasa” “Ninawasubiri” akasema Dr Evans na kukata simu.Joel Mshana akavuta pumzi ndefu “Rais amekubali kuonana nasi kwa sababu ananiamini mno.Nimekubali kuubeba mzigo huu kutokana na namna ninavyomuamini Meshack Jumbo.Naamini asingeweza kufika hapa kwangu usiku huu kama kusingekuwa na suala nyeti hivyo nawaomba ndugu zangu heshima yangu kwa Rais isishuke kama hamna jambo zito ambalohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ linastahili Rais kuahirisha kikao muhimu kulisikiliza” akasema Joel “Usihofu Joel” akasema Meshack.Hawakupoteza muda wakaingia katika gari la Mathew na safari ya ikulu ikaanza huku ndani ya gari kukiwa na mazungumzo machache.Kila mmoja alionekana kuzama katika mawazo. Iliwachukua dakika hamsini kufika ikulu na kwa kuwa tayari taarifa zao zilikwisha wasilishwa kwa walinzi wa ikulu waliruhusiwa kupita baada ya kukaguliwa na bastora ya Mathew kubaki kwa walinzi.Walipokewa na walinzi wawili na kuigizwa ndani aliko Rais.Mara tu walipoingia Rais akasimama kuwasalimu. “Joel Mshana karibu sana.Nimefurahi kukuona tena mzalendo wa kweli” akasema Dr Evans “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Joel wakapeana mikono kusalimiana “Mheshimiwa Rais kutana na Meshack Jumbo,mkurugenzi mstaafu wa idara ya ujasusi” “Mzee Jumbo karibu sana.Nimefurahi kuonana nawe” akasema Dr Evans “Hata mimi nimefurahi sana kukutana nawe mheshimiwa Rais” Mara Rais akastuka kama ameona dude la kutisha “I think I know this man ! akasema Dr Evans kwa mshangao kidogo.Tayari sura yake ilikwisha badilika “Yes Iknow this this man.Joel what’s the meaning of this ?! akauliza Dr Evans akwa ukali “Mr Pres…………..” Joel akataka kusema kitu lakini Mathew akamzuia “Mheshimiwa Rais naitwa Mathew Mulumbi ! akasema Mathew na Dr Evans akapandwa na hasira. “Joel what is this?! What is your plan? Akauliza Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais ..” akataka kusema kitu Meshack Jumbo lakini Dr Evans akamzuia. “This man is a terrorist.Huyu ni mshirika mkubwa wa magaidi na hapaswi kuingia katika nyumba hii yenye heshima kubwa.Joel na huyo mwenzako nani sijui sikutegemea kabisa kwa namna ninavyokuamini ukafanya hivi ulivyofanya kumleta gaidi ikulu.Watu wengi wamepoteza maisha usiku wa leo katika shambulio la kigaidi na mpaka sasa mwanangu hajulikani kama ameuawa ama yuko wapi.Huyu ambaye mmeongozana naye anahusika moja kwa moja na tukio lile.Oh my God !! akasema Dr Evans na kuelekea katika simu iliyokuwa mezani akainua mkono wa simu. “Mheshimiwa Rais kabla hujapiga hiyo simu kuwataka walinzi wako waje wanikamate naomba unipe dakika tatu nizungumze nawe na baada ya hapo nitajisalimisha kwako na walinzi wako watanikamata na kunipeleka sehemu yoyote utakayo” akasema Mathew “Mheshimiwa Rais umekubali kuonana nasi kutokana na imani yako kubwa kwangu.Ninaomba uniamini mimi na umsikilize huyu kijana anachotaka kukueleza.Tafadhali mheshimiwa Rais niko chini ya miguu yako” akasema Joel Mshana. “Joel sikutegemea kabisa.Narudia tena sikutegemea kabisa kama ungeweza kumleta huyu gaidi katika nyumba hii tukufu” “I’m not a terrorist ! akafoka Mathew na Meshack Jumbo akamzuia “Mathew please.Kuwa mvumilivu” akasema Meshack kwa sauti ndogo “Joel na mwenzako ninyi ni watu wenye heshima kubwa sana katika nchi hii kwa nini mmekubali kuivunja heshima yenu kwa kuungana na huyu gaidi? Akauliza Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais naomba unisikilize.Mimi ni Meshack Jumbo nimewahi kuwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi kwa miaka ishirini na tatu.Ni mimi niliyempokea Mathew Mulumbi katika idara yangu na kufanya naye kazi na alikuwa mmoja wa majasusi wa kuaminiwa mno na amekwisha fanya mambo mengi makubwa kwa nchi hii ambayo sitaki kupoteza muda wako kuyataja.Ninamuamini Mathew Mulumbi sana.Tafadhali nakuomba umsikilize.Ana jambo la kukueleza” akasema Meshack Jumbo “Hakuna chochote mtakachonieleza kitakachonibadili msimamo wangu.Huyu ni mtu ambaye ninamtafuta kwa udi na uvumba.Tena ninawashukuru kwa kunirahisishia kazi yangu ya kumtafuta na ninawashukuru vile vile kwa kunipotezea muda wangu.Sikutegemea kabisa Joel kama ungew..….” “Mheshimiwa Rais tafadhali” akasema Joel Mshana na kupiga magoti “Mr Mshana please stand up! Akasema Mathew kwa ukali “Usipige magoti.Tuko hapa kwa ajili ya kulipigania taifa letu lakini mtu ambaye tumempa dhamana ya kuwaongoza watanzania hajali maisha ya watanzania yanavyopotea.Let him do whatever he wants to do.Go ahead Mr president make the call.Lakini kabla haujapiga hiyo simu naomba usikie haya machache.Ninafahamu unanitafuta kwa udi na uvumba na maamuzi yangu ya kuja kukuoan hayakuwa rahisi na nilifahamu fika kwamba ninakuja mwenyewe kwenye mdomo wa mamba na sintaweza kutoka salama lakini sikuogopa kwa kuwa kilichonileta hapa ni kulipigania taifa langu.Kesho asubuhi kama sintaonekana mtaani taarifa zitaanza kusambaa katika mitandao yote ya jamii hapa nchini kuhusiana na kutekwa kwa Olivia Themba na baba yake Agrey Themba.Watanzania wote watafahamu nani aliye nyuma ya utekaji ule.Unataka watu wafahamu nani aliye nyuma ya tukio la kutekwa Olivia Themba na baba yake Agrey?akauliza Mathew na Dr Evans akabaki kimya “Answer me Mr President !! akasema Mathew kwa ukali “Mheshimiwa Rais naomba tusifike huko Mathew anakotaka tufike.Mambo haya ni nyeti mno na tusianze kuanika siri za taifa hili na kuuweka usalama wetu mashakani.Ninakuomba mheshimiwa Rais mpe dakika chache umsikilize kile anachotaka kukueleza” akasema Meshack Jumbo.Dr Evans akamtazama Mathew kwa macho yaliyojaa hasira “You want to challenge me young man?! Akauliza “Mheshimiwa Rais siko hapa kushindana nawe na sina uwezo wala nguvu ya kushindana nawe.Niko hapa kwa ajili ya kukupa taarifa muhimu kwa usalama wa nchi hivyo naomba unisikilize kile ninachotaka kukueleza na baada ya hapo utaamua wewe mwenyewe kitu cha kufanya” akasema Mathew “Mheshimiwa Rais msikilize tafadhali Mathew kile anachotaka kukueleza.Kama kuna tofauti yoyote baina yenu tuziweke kando kwa muda na tuyaweke mbele maslahi ya taifa” akasema Meshack Jumbo “Ninyi nyote hamjui mnachokiongea.This man is a threat to this country.Ni mtu mbaya sana huyu na sifahamu amewaeleza nini hadi mkakubali kuacha usingizi wenu na kumsindikiza hapa kwenye nyumba tukufu ya watanzania !! Akaendelea kufoka Dr Evans “Mheshimiw Rais naendelea kukuomba niamini mimi niliyemleta Mathew hapa kwako na umsikilize japo kwa dakika chache na baada ya hapo utaamua kitu cha kumfanya yeye pamoja na sisi ambao tumemleta hapa kwako.Naomba sana mheshimiwa Rais” akasema Joel.Dr Evans akamtazama Mathew kwa dakika zipatazo mbili akiwa na sura iliyojikunja akionyesha hasira za wazi kisha akasema “Nieleze hicho unachotaka kunieleza lakini wakati unanieleza andaa majibu yote kuhusiana na mtandao wenu na mahala alipo mwanangu Coletha.Bila kupata majibu hayo I swear I’m going to eat you alive!! akasema Dr Evans kwa ukali “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew na kushusha pumzi “Mheshimiwa Rais ninaitwa Mathew Mulumbi.Niliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na huyu hapa mzee Meshack Jumbo ndiye aliyekuwa mkurugenzi wangu hadi nilipoachana na kazi hizo na kwa sasa ninajishughulisha na biashar…………….” “Tafadhali sitaki unipotezee muda wangu nina kazi nyingi za kufanya usiku huu kuhakikisha taifa linakuwa salama hivyo sitaki hadithi.Ninakufahamu tayari wewe ni nani hivyo nenda moja kwa moja katika kile kilichokuleta hapa !! akafoka Dr Evans “Mheshimiwa Rais bado hujanifahamu mimi ni nani na yawezekana taarifa ulizonazo hazijakupa picha halisi ya kuhusiana na mimi hata hivyo sitaki kupoteza muda ngoja nijielekeze moja kwa moja katika suala la msingi lililonileta hapa”akanyamaza kidogo na kuendelea “Siku moja nikiwa katika klabu ya usiku nilikutana na mwanamke mmoja ambaye alijitambulisha kwangu kama Olivia Themba na tukawa marafiki wakubwa.Katika urafiki wetu nilibaini kwamba kuna jambo lililokuwa linamsumbua Olivia na siku moja nilipomdadisi akanieleza kwa ufupi kwamba ana matatizo na watu Fulani ambao hakutaka kuniweka wazi ni akina nani.Kwa kuwa ni mtu wangu wa karibu nilichukua jukumu la kuhakikisha anakuwa salama hivyo nikampa namba Fulani ambazo nilimtaka azipige wakati akihisi hatari au akiwa katika hatari na kupitia namba hizo mimi nitafahamu mahala alipo kisha nitakwenda kumsaidia.Nikiwa jijini Arusha katika mkutano wa wadau wa maziwa nchini nikapokea ujumbe kutoka katika zile namba nilizompa Olivia na baada ya muda nikapata taarifa kwamba Olivia Themba ametekwa na watu wasiojulikana.Kupitia program ile niliyompa Olivia niliweza kugundua mahala namba zili zilipopigwa hivyo nikalazimika kuondoka Arusha haraka na kurudi Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kumuokoa Olivia.Kabla ya kwenda kumuokoa nililazimika kuonana kwanza na wazazi wake nikawaeleza ninachotaka kukifanya na wakaniruhusu nikamuokoe binti yao.Nilipofika mahala ambako niliamini Olivia alikuwa amefichwa nikakuta ameondolewa na nikakutana na kikosi cha watu walioandaliwa kwa ajili ya kunimaliza.Nilifanikiwa kupambana nao na kuwashinda.Baada ya kuondoka mahala hapo nilipigiwa simu na Lucy Themba mama yake Olivia akanijulisha kwamba mume wake Agrey Themba amepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mimi na akadai kwamba amempata Olivia na kumuelekeza sehemu ya kukutana.Nilistuka kwa taarifa ile ikanilazimu kufika mahala ambako mtu huyo alitaka akutane na Agrey lakini nilichelewa kwani tayari Agrey alikwisha tekwa.Nilimtaka Lucy Themba anieleze kama kuna mtu yeyote ambaye walimueleza kuhusu mimi kwenda kumuokoa Olivia akadai hakuna mtu yeyote waliyemueleza.Asubuhi Lucy alinipigia simu na kunijulisha kwamba anahitaji kuniona kuna jambo muhimu anataka kunieleza.Nilipofika nyumbani kwake kumbe ulikuwa ni mtego nikatekwa na kupelekwa mahala nisipopafahamu” akanyamaza akamtazama Rais halafu akaendelea “Nikiwa mahala hapo nilipofungwa baadaya kutekwa alikuja mwanamama mmoja akajitambulisha kwangu anaitwa Devotha ambaye ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi akanieleza kwamba wameniteka baada ya kubaini ninashirikiana na kikundi cha IS.Alinihoji maswali mengi na nikamueleza kila kitu kuhusu mimi na Olivia akaridhika kwamba sina mahusiano yoyote na IS lakini akanieleza kwamba Olivia anashirikiana na kikundi cha IS na kwa kuwa mimi ni mtu wake wa karibu waliamini lazima na mimi nitakuwa mmoja wao.Sifahamu nini kiliendelea lakini baadae nilikuja kukombolewa na Devotha akiwa na mmoja wa marafiki zangu.Nilimuuliza sababu ya kuniokoa akanieleza kwamba anataka kuutafuta ukweli na amenitoa ili nimsaidie kuupata ukweli wa kile alichokieleza Olivia.Alinieleza kwamba Olivia alitoa madai yakuwa mbunge Edger Kaka ambaye alifariki katika ajali ya gari miaka mitatu iliyopita yuko hai na kwamba wewe Rais unalifahamu jambo hili na unafahamu mahala alipo ndiyo maana mwanao akaambukizwa virusi hatari ili kukushinikiza uwaonyeshe alipo Edger Kaka. Devotha anadai kuwa Olivia alimuhakikishia anayo siri kubwa na angempatia siri hiyo endapo angemsaidia kupata taarifa za mahala alipo Edger Kaka.Kutokana na msisitizo aliouonyesha Olivia,ilimlazimu Devotha kuamua kufanya uchunguzi wa suala hili ili kubaini ukweli na ndipo alipoamua kudukua simu yako kuchunguza kama unalifahamu jambo hili lakini hakufanikiwa kupata chochote kwani alibainika haraka.Aliposhindwa kudukua simu yako akaenda kuonana na Olivia akakuta amehamishwa na ndipo alipobaini kuwa amefungiwa kila kitu kuanzia simu hadi kadi zake zote na hivyo kumlazimu kufanya maamuzi magumu ya kuja kunitoa kutoka mahala nilikokuwa nimefichwa.Haikuwa kazi nyepesi kunitoa na ililazimu watu kadhaa kupoteza maisha.Baada ya kufanikiwa kunitoa nilianza kushirikiana na Devotha kuutafuta ukweli kuhusu Edger Kaka lakini wakati tukiendelea kuna jambo lilitokea.Devotha alimpiga risasi mmoja wa watu wangu halafu akatoweka na mpaka sasa sijajua sababu ni nini na ninaendelea kumtafuta” akanyamaza akamtazama Rais na wale wazee wawili wote walikuwa kimya wakimsikiliza “Nimekusikia unataja watu wako.Una jeshi,kikosi au ni watu wako wa IS?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais naomba niweke wazi kwamba mimi si gaidi!! Akasema Mathew akionekana kukerwa na maneno yale ya Rais “Endelea Mathew” akasema Meshack kwani anamfahamu Mathew akikasirika mambo yanaweza kuharibika.Mathew na Rais wakatazamana kisha akaendelea “Nilianza kumsaka Devotha kujua kwa nini alimpiga risasi Ruby na katika harakati za kumsaka nikagundua kwamba Devotha alikutana na Dr Yonathan Cohen balozi wa Israel hapa nchini” Mathew akanyamaza baada ya kuona sura ya Dr Evans imebadilika.Wale wazee wawili mle ndani nao wakatazamana “Kwa kuwa lengo langu lilikuwa kumpata Devotha,nililazimika kumfuata balozi Dr Yonathan nyumbani kwake kufahamu mahala alipo Devotha na sababu ya kukutana naye usiku huu” Mathew akakatishwa na Rais “Una maanisha ulivamia nyumbani kwa balozi wa Israel? akauliza Dr Evans “Ndiyo mheshimiwa Rais nililazimika kumvamia Dr Yonathan katika makazi yake” “Jesus Christ ! akasema Dr Evans na kumtazama Mathew kwa hasira zaidi midomo ikimtetemeka alishindwa kutamka kile alichotaka kukisema “Mheshimiwa Rais” Mathew akaendelea “Kuna mambo niliyagundua kutoka kwa balozi Dr Yonathan.Kwanza ni kuhusu Devotha” akanyamaza tena kidogo na kuendelea “Devotha ni wakala wa shirika la ujasusi la Israel,Mossad” “What?Dr Evans akastuka “Devotha ni wakala wa shirika la ujasusi la Israel na namba yake ya utambulisho ni BRAVO 15E 361 A” Uso wa Dr Evans ulionyesha mstuko mkubwa “Unamzungumzia Devotha yupi?akauliza Dr Evans “Devotha Adolph mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi” akajibu Mathew na Joel Mshana akastuka. “Wait ! akasema na kumtazama Mathew “Unasema kuna kitu kinaitwa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi? “Ndiyo mzee.Kuna idara hiyo” akajibu Mathew “Inashangaza nimekaa ndani ya serikali kwa miaka mingi na sijawahi kusikia kitu kama hicho.Kazi zake ni zipi hasa hiyo idara? Nani anaiongoza?Imeanzishwa kwa sheria gani?akauliza Joel “Joel achana na mambo hayo kwanza tujielekeze katika suala la msingi lililotuleta hapa” akasema Meshack Jumbo “Endelea Mathew” akasema Meshack.Dr Evans alikuwa kimya kabisa. “Israel kupitia shirika lake la ujasusi la Mossad wamekuwa wakimtumia Devotha katika mipango yao ya kijasusi hapa nchini.Usiku wa leo Devotha aliitwa kwenda katika ubalozi wa Israel kuonana na majasusi wawili waliotumwa na Mossad kuja Tanzania kufanya maandalizi ya kumtafuta Olivia Themba” “Olivia Themba?!! Dr Evans akastuka “Ndiyo mheshimiwa Rais.Mossad wanamtafuta Olivia Themba na wametuma watu wao wawili kuja kufanya maandalizi kabla ya kutuma kikosi cha majasusi kuja Tanzania kumtafuta Olivia na Devotha ndiye anayewasidia katika kuandaa operesheni hiyo” “Oh my God ! kwa nini kila mahali ni usaliti tu? Devotha nilimuamini sana lakini kumbe anashirikiana na nchi za nje !! akasema Dr Evans na kutikisa kichwa. “Hao Mossad kwa nini wanamtafuta Olivia?akauliza Dr Evans “Kuna historia fupi hapa.Miaka mitatu iliyopita mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Edger Kaka alipatwa na ugonjwa akiwa bungeni na akapelekwa nchini Israel ambako aliambatana na Olivia” “Ninafahamu hilo na mimi ndiye niliyetoa ndege impeleke huko Israel”akasema Dr Evans “Akiwa nchini Israel,iligundulika kwamba aliwekewa sumu kwa kusudi la kumuua.Waziri mkuu wa wakati huo alituma mtu maalum wa kumlinda Edger kwa siri akihofia kwamba wale waliotaka kumuua Tanzania wangeweza kumfuata kule Israel na kummalizia.Kachero huyo wakati akiendelea na shughuli zake za ulinzi kwa siri aligundua watu wawili waliofika kumtembelea Edger hospitali usiku wa manane.Ilimlazimu kumshirikisha rafiki yake kutoka Mossad na wakagundua kwamba watu wale ni Habiba Jawad na Sayid Omar ambao wamekuwa wakitafutwa na serikali ya Israel kwa kufadhili vikundi vya wanamgambo wa kipalestina ambao wamekuwa wakifanya mashambulio kwa raia wa Israel.Kitendo cha Edger kutembelewa na watu hao wawili kilimfanya awe ni mtu muhimu sana kwa Mossad na wakapanga mipango ya kumteka.Waliandaa operesheni kabambe na kumchukua Edger hapa Tanzania.Walitengeneza ajali ambayo sote tuliamini kwamba ndiyo iliyochukua uhai wa Edger Kaka lakini ukweli ni kwamba Edger Kaka hajafariki dunia.Yuko hai bado” akanyamaza baada ya kuona sura za Dr Evans na Joel Mshana zimebadilika “No this is not true ! Edger Kaka is dead !! akasema Dr Evans “Hapana mheshimiwa Rais.Wote tuliamini hivyo lakini ukweli ni kwamba Edger Kaka bado yuko hai” akasema Mathew.Ukapita ukimya. “Una uhakika gani kwa hili unalotueleza Mathew?akauliza Dr Evans “Nimehakikishiwa na balozi Dr Yonathan Cohen kuhusu suala hili.Nilimuuliza kama unafahamu jambo hili au kama unahusika kwa namna yoyote ile akakiri kwamba hufahamu chochote kuhusu jambo hili kwani ni siri kubwa ya Mossad.Kwa hiyo mheshimiwa Rais madai ya Olivia na IS kwamba unafahamu mahala alipo Edger Kaka si ya kweli nimelithibitisha hilo” akasema Mathew na Dr Evans akashusha pumzi “Thank you God ! akasema Dr Evans “Olivia na kundi lake walinituhumu kwamba ninafahamu mahala alipo Edger Kaka na wakamuambukiza mwanangu Coletha virusi hatari ili kunishinikiza niweze kuwaonyesha mahala alipo Edger kitu ambacho sikuwa nakifahamu kabisa.Mimi na watanzania wote tuliamini kwamba Edger Kaka tayari amekwisha fariki dunia katika ajali kumbe ajali ile ilikuwa ya kutengeneza.Mathew kwa mara ya kwanza nakushukuru sana kwa kuutafuta ukweli” akasema Dr Evans na kumtazama Mathew huku macho yake yakionyesha kama yanataka kulengwa na machozi. “Where is Edger Kaka now?akauliza Dr Evans “Baada ya kumteka Edger Kaka walimpeleka nchini Kenya katika ubalozi wa Israel ambako amekaa kwa miaka mitatu akiteswa na ndipo walipoamua kutuma majasusi wawili kutoka Tel Aviv kuja kumuhoji ili awaeleze mahala walipo Habiba Jawad na Sayid Omar.Edger Kaka aliwaambia majasusi wale wa Mossad kama wanataka awaeleze kila kitu wanachokitaka basi wamtafute na wampeleke Olivia Themba” “Why Olivia Themba?akauliza Dr Evans “Edger Kaka anadai kwamba Olivia ni mwanamke anayempenda kuliko wote na yuko tayari kuwaeleza Mossad kila kitu wanachokitaka kama wakimpata Olivia.Hiyo ndiyo sababu ya Mossad kutaka kutaka kufanya operesheni hapa nchini kumtafuta Olivia”Mathew akanyamaza na kumtazama Dr Evans “Mheshimiwa Rais nimemaliza kile nilichotaka kukueleza.Sasa ninajisalimisha kwako niko tayari kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zozote unazoona zinafaa” akasema Mathew na kumsogelea Dr Evans.Joel na Meshack Jumbo wakabaki wanashangaa.Dr Evans akamtaza Mathew kwa muda halafu akasema “Take a sit ! akasema Dr Evans na Mathew akaketi. “Mathew Mulumbi naomba toka ndani ya moyo wako unisamehe sana kwa yale yote niliyokufanyia bila kujua.Mathew kijana wangu sijui niseme nini unielewe kwamba nilifanya yale yote bila kujua nikiamini wewe ni mmoja wa IS lakini naomba unisamehe sana.Mambo niliyokufanyia ni makubwa.Ni mimi ndiye niliyeagiza ukamatwe na uwekwe kizuizini pale kitalu 1.Ni mimi ndiye .oh my God !! Dr Evans akashindwa kuendelea na kutazama chini.Mathew akasimama “Mheshimiwa Rais ninasubiri amri yako.Niko tayari kwa hatua zozote utakazozichukua dhidi yangu kwa yale yote niliyoyafanya! Akasema Mathew Mulumbi “Please Mathew take a sit ! akasema Dr Evans lakini bado Mathew aliendelea kusimama akimuangalia “Mr Presid…………...”Mathew akataka kusema kitu lakini Meshack Jumbo akamzuia. “Mathew obey the order please !! akasema Meshack Jumbo kwa sauti kali Mathew akageuka akamtazama halafu akaketi.Joel Mshana bado aliendelea kushangaa kama vile yuko ndotoni mambo aliyoyasikia yalimshangaza sana “Mathew please listen to me” akasema Dr Evans “Kwa mambo niliyokufanyia una haki ya kuwa na hasira juu yangu.Sistahili kabisa msamaha wako hata kama ningeomba mara elfu moja.Kitu kimoja ambacho nataka niweke wazi kwamba nilifanya mambo haya bila kujua na bila kufanya utafiti wa kutosha kama kweli unahusiana na mtandao wa IS kama wote tulivyokuwa tunaamini.Hata hivyo Mathew narudia tena kukuomba msamaha.Naamini haitakuwa rahisi kunisamehe lakini kwa sasa taifa letu linapitia kipindi kigumu mno.Mpaka sasa bado hatujapata idadi kamili ya wale waliopoteza maisha katika shambulio la bomu lililofanywa katika hospitali ya Mtodora na bado kuna vitisho vya kuwepo kwa mashambulio zaidi.Kama Rais wako,kama mzazi,kama mtanzania mwenzako ninataka nikuombe tuweke pembeni kila kitu kilichotokea na tuungane katika kuliondoa taifa letu katika hatari hii kubwa.Watu wameingiwa hofu na usalama wa maisha yao na jukumu letu ni kuhakikisha tunaiondoa hofu hiyo na waishi kwa amani” akanyamaza kidogo halafu akasema “Mathew licha ya vikwazo vyote ulivyokumbana navyo hukukata tamaa bali umeendelea kupambana na kuutafuta ukweli.Ulijua ninakutafuta lakini bado ulitafuta kila njia hadi ukaja kuonana name kunifikishia taarifa hizi nyeti mno.Mathew wewe ni mtu wa pekee na nchi yetu imebarikiwa sana kukupata mtu kama wewe.Nakuomba Mathew Mulumbi jambo hili uliloligundua na kuamua kuja kunieleza lisiishie hapa bali uhakikishe unalifikisha mwisho.Nataka nikukabidhi rasmi jukumu hili ulibebe na ulimalize wewe mwenyewe kwa namna unavyojua.Mimi nitatoa kila aina ya msaada unaohitajika.Naomba sana Mathew” akasema Dr Evans.Mathew akafikiri kidogo na kusema “Mheshimiwa Rais siku zote katika maisha yangu nimekuwa nikitanguliza kwanza nchi yangu na ndiyo maana kila pale linapotokea suala ambalo linanihitaji mimi kuwepo huwa sijiulizi mara mbili kulifanya kwa ajili ya nchi yangu.Mheshimiwa Rais licha ya yote yaliyotokea lakini bado mimi na wewe tunaweza kufanyakazi pamoja na kuiondoa nchi katika hatari.Nimelipokea ombi lako na ninakuahidi kuhakikisha ninatumia ujuzi na uzoefu wangu wote niliojaaliwa kulifikisha mwisho.Ninachohitaji ni ushirikiano mkubwa na kuaminiana” akasema Mathew “Mathew nashukuru sana kwa kukubali ombi langu.Ninakuahidi ushirikiano mkubwa sana na kukupatia kila kile utakachokihitaji.Wazee wangu Joel na Meshack ninawaomba msamaha sana kwa maneno niliyowatamkia hapo awali.Ni kweli nilikuwa na hasira na Mathew na ndiyo maana nikajikuta nikitamka maneno yale bila kujua.Nisameheni sana wazee wangu ninahitaji sana ushauri wenu katika jambo hili naomba tuungane pamoja tulivushe taifa katika wakati huu mgumu.” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais sisi tumestaafu utumishi katika taasisi lakini si kulitumikia taifa.Bado tuna nguvu na ari ya kulitumikia taifa letu na kila pale itakapotulazimu sisi tuko tayari kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha nchi inakuwa salama.Tuko tayari kuungana nawe mheshimiwa Rais pamoja na kijana wetu Mathew katika kuhakikisha tunamaliza kitisho hiki cha usalama hapa nchini kwetu” akasema Joel Mshana “Nawashukuru sana wazee wangu kwa kukubali kwenu.Ninawaomba sasa wote tuelekee katika chumba cha mazungumzo ya faragha ili tuweze kulijadili suala hili kwa kina” akasema Dr Evans. Waliinuka wote wakamfuata Rais wakaelekea katika chumba cha vikao vya faragha “Karibuni sana” akasema Dr Evans na baada ya wote kuketi akasema “Muda unakwenda kasi sana hivyo bila kupoteza muda tuanze mazungumzo” akasema Dr Evans “Mathew alizungumzia jambo lililomstua sana Joel Mshana kuhusiana na idara ya siri ya mambo ya ndani ya nchi.Ni kweli idara hii ipo lakini inafanya kazi zake kwa siri kubwa ndiyo maana hata ndani ya serikali haifahamiki.Idara hii iko chini yangu na mimi ndiye ninayeisimamia kwa kila kitu.Idara hii niliiunda mimi kwa siri kwa ajili ya kunisaidia katika kuhakikisha nchi inakuwa salama na kuniwezesha kutekeleza vyema majukumu yangu ya kuongoza nchi.Mtashangaa kwa nini niunde idara hii licha ya kuwa na majeshi na vyombo vingine vya usalama lakini idara hii ni muhimu sana kwangu mimi kama Rais.Hakuna fungu lolote la bajeti kutoka serikalini ni mimi mwenyewe ndiye ninayejua fedha za kugharamia idara hii ninazipata wapi.Idara hii imekuwa na mchango mkubwa sana katika kufanikisha shughuli zangu.Naomba nisiendelee zaidi kuizungumzia idara hii ya siri bali tujikite katika kile kilichotukutanisha usiku huu” akanyamaza Dr Evans baada ya sekunde chache akaendelea “Nilipokea mjumbe maalum kutoka kwa Rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambaye aliniletea ujumbe kwamba kuna raia wangu mmoja ameonekana jijini Kinshasa akifanya mazungumzo na mtu anaitwa Seif Almuhsin ambaye anatoka kikundi cha IS na kazi yake kubwa ni kukusanya vijana kutoka katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati na kuwapeleka katika kambi zao za mafunzo kuwafundisha ugaidi.Nilionyeshwa picha za mtu huyo nikamtambua kuwa ni Olivia Themba.Ilikuwa rahisi kumtambua Olivia kwa kuwa Mimi na baba yake Agrey Themba ni marafiki wakubwa toka tukiwa vijana.Nilishangazwa sana na Olivia kukutana na Yule gaidi hivyo nikaelekeza idara yangu ya siri kufanya uchunguzi kujua sababu ya Olivia kukutana na Yule mtu.Uliandaliwa mpango na Olivia akatekwa nyara aliporejea nchini akitokea Kinshasa.Naomba niwaweke wazi wazee wangu kwamba idara yangu ya siri ndiyo waliofanya tukio lile la utekaji wa Olivia lakini kwa nia nzuri ya kutaka kufahamu Olivia ana mahusiano gani na IS.Katika upekuzi akagundulika pia amekuwa na mawasiliano na mtu anaitwa Sayid Omar huyu anatajwa kuwa mmoja wa wafadhili wa IS.Alipohojiwa zaidi akawadanganya kwamba atawaelekeza mahala alipo Sayid Omar na akawapa namba ambayo aliwataka wapige akidai ni ya Sayid na walipopiga tu mfumo wote wa mawasiliano wa idara hiyo ya siri ukajifunga.Olivia alipotakiwa aufungue akadai lazima aonane kwanza na mimi.Nilijulishwa nikaenda kuonana naye na akakiri kwamba anashrikiana na IS akaenda mbali zaidi kwamba wamemuambukiza mwanagu Coletha virusi hatari na atapoteza maisha kama nisipowaeleza mahala alipo Edger Kaka.Olivia alisisitiza kwamba Edger Kaka hajafariki dunia na mimi ninafahamu mahala alipo.Nilidhani Olivia ana matatizo ya akili lakini aliendelea kuliwekea jambo hili msisitizo mkubwa.Baadae nilipata taarifa kutoka kwa Agrey Themba kwamba kuna mtu amekwenda nyumbani kwake anaitwa Mathew Mulumbi na anadai kuwa anafahamu mahala alipo Olivia na alikuwa mbioni kwenda kumuokoa.Ni kweli mahala alikosema Mathew ndiko alikokuwa Olivia.Nikatoa maelekezo Olivia ahamishwe na haraka kabla Mathew hajafika na kiwekwe kikosi maalum ili kumkamata mara tu atakapofika hapo,kwa bahati mbaya Mathew aliweza kupambana nao akawamaliza na alinusurika mtu mmoja pekee.Jithada za kumuhoji Olivia zilionekana kugonga mwamba nikaelekeza baba yake Agrey Themba atekwe ili kumshinikiza Olivia aongee lakini bado haikusaidia”akanyamaza akameza mate na kuendelea “Kwa kushirikiana na idara hiyo ya siri na mke wa Agrey Themba tuliweka mtego na kumkamata Mathew Mulumbi ambaye tuliamini anashirikiana na Olivia na wote wako katika mtandao wa IS.Niliagiza ahojiwe tujue kila kitu.Kama alivyoeleza Mathew nilifahamishwa na watu wangu kwamba kuna watu wanajariku kudukua simu yangu.Baada ya kufuatilia nikagundua ni Devotha.Nilishangaa sana kwa nini aamue kufanya vile ndipo nikaamua kumtoa kabisa katika nafasi yake ya ukurugenzi wa idara ya siri na kuelekeza akamatwe lakini kwa bahati mbaya akaponyoka na baadae nikapata taarifa kuwa amemtorosha Mathew Mulumbi.Nilikasirika sana na kuelekeza kwamba kokote wawili hawa watakapoonekana wapigwe risasi na kuuawa” akanyamaza “Nimeamua kuweka wazi kila kitu ili tufungue ukurasa mpya.Nilimkabidhi Kaiza kazi ya kumuhoji Olivia lakini hadi ilipofika jioni hakuwa amepata chochote na hali ya Olivia haikuwa nzuri nikaelekeza apelekwe shambani kwangu akahudumiwe.Wakati Olivia akiendelea kupatiwa matibabu likatokea shambulio la Mtodora.Katika hospitali hiyo alikuwa amelazwa mwanangu Coletha na jengo lililolipuliwa ndimo alimokuwa amelazwa.Muda mchache baada ya shambulio lile kutokea nilipigiwa simu na mtu ambaye alinijulisha kwamba yeye ni kiongozi wa kikundi kilichotekeleza shambulio lile katika hospitali ya Mtodora na kwamba wanamshikilia mwanangu Coletha” akanyamaza baada ya nyuso za Meshack na Joel kuonyesha mstuko. “Walinionya kwamba nisithubutu kumueleza yeyote suala hili wala nisijaribu kuelekeza vikosi vya usalama viwasake kwani wangemuua mwanangu Coletha.Walinitaka nifuate maelekezo watakayonipa ili mwanangu awe salama.Walinitaka niwapatie Olivia Themba” Sura ya Mathew ikaonyesha mstuko “Uliwapa walichokihitaji?akauliza Mathew “I’m so sorry Mathew.Nakiri kwamba I was stupid and coward.Sikuyatanguliza mbele maslahi ya Taifa na nikaamua kuwapa kile walichokitaka.I gave them Olivia” “Oh mon Dieu ! (Oh Mungu wangu) akasema Mathew kwa lugha ya kifaransa na kusimama “How could y…………” akasema Mathew lakini Meshack Jumbo akamzuia “Mathew ! Respect ! akasema Jumbo kwa sauti kali “I’m sorry” akasema Mathew na kuketi “Mathew una kila haki ya kuwa na hasira kwa hili nililolifanya lakini naamini hata kama ungekuwa wewe mahala pamgu ungefanya kama nilivyofanya mimi.Mwanangu anateseka hana kosa lolote na siko tayari apoteze maisha ndiyo maana nikawa tayari kutekeleza maelekezo waliyonipa” akasema Dr Evans “Nini kilifuata baada ya kuwapa Olivia Themba?Walimrejesha mwanao?Mathew akauliza “Hapana Mathew.Sijapewa mwanangu.Nimeambiwa niwe mvumilivu bado kuna mazungumzo kati yangu nao.Nahisi kuna vitu vingine watahitaji” “Damn it !! akasema Mathew kwa hasira “Mathew I was alone and scared.I didn’t know what to do.Nilichokuwa nakihitaji ni kumpata mwanagu akiwa salama na ndiyo maana nikafuata kila walichokitaka wale jamaa.Nimeyaweka haya mbele yenu nikiamini kwamba tunaanza upya na mwanangu atapatikana.Nina imani kubwa nawe Mathew kwamba utampata mwanangu Coletha akiwa mzima ndiyo maana ninakubali kwamba nilikosea”akasema Dr Evans na kumtazama Mathew “Mathew ninakuomba unisaidie kumtafuta mwanangu Coletha na umuokoe pia Oliv…..” “Ni hivi mheshimiwa Rais” akasema Mathew na kumkatisha Dr Evans “Olivia alikuwa mtu muhimu sana na ndiyo maana watekaji hao walimtaka kwa haraka kabla ya kitu kingine chochote.Tayari anafahamu mipango yote ya IS hapa nchini hivyo basi lazima na sisi tuhakikishe tunamsaka na kumpata kabla Mossad hawajampata kwani nao vile vile wanamtafuta sana.Ninataka unipe maelekezo yote namna walichomchukua” akasema Mathew na Dr Evans akamueleza kila kitu.Mathew akakuna kichwa. “Mheshimiwa Rais kwa maelezo hayo ni wazi itakuwa vigumu kujua mahala alipo Olivia lakini ipo namna moja tu ya kuweza kumpata Olivia na Coletha kutoka kwa hao watekaji” akasema Mathew “Nakusikiliza Mathew” “Tayari tumekwisha fahamu kwamba Edger Kaka yuko hai na mahala alipo,jambo lingine zuri ni kwamba IS hawafahamu mahala alipo bado wanaamini yupo hapa Tanzania kumbe yuko Nairobi Kenya.Tunatakiwa kuvamia ubalozi wa Israel nchini Kenya na kumchukua Edger Kaka kimya kimya.Tukifanikiwa kwa hilo tutakuwa na uhakika mkubwa wa kuwapata Olivia na Coletha” akasema Mathew “Kuvamia ubalozi wa Israel na kumteka Edger Kaka ?! akaulzia Dr Evans “Huo ni mgogoro mkubwa sana wa kidiplomasia tunataka kuuanzisha Mathew.Israel ni marafiki zetu wa muda mrefu na wamekuwa wakitusaidia sana katika mambo mbali mbali hatuwezi kuingia katika mgogoro nao” akasema Dr Evans akionyesha wasiwasi “Mheshimiwa Rais tayari tupo kwenye mgogoro mkubwa kati yetu nao” akasema Mathew na Dr Evans akaonyesha woga “Kwanza kabisa ni wao waliovamia ardhi yetu wakafanya operesheni wakaua na kumteka raia wetu.Hata kama Edger alikuwa na taarifa za muhimu za watu wanaowatafuta hawakupaswa kufanya walichokifanya.Walipaswa kuishirikisha serikali ya Tanzania katika jambo hilo lakini kwa makusudi kabisa waliingia katika ardhi yetu na kufanya walichotaka kukifanya.Mheshimiwa Rais walichokifanya Israel ni kitendo cha dharau kwa nchi yetu hivyo uchokozi waliuanzisha wao wenyewe.Kama haitoshi hivi sasa wanajiandaa kuja kufanya operesheni nyingine ya kimya kimya ndani ya ardhi yetu kumtafuta Olivia” akasema Mathew “Mheshimiwa Rais anachokisema Mathew ni sahihi kabisa.Israel walifanya makosa kuja kufanya operesheni ndani ya ardhi yetu wakaua watu wetu na kumchukua mateka raia wetu.Hiki ni kitendo cha uchokozi mkubwa na bado wanataka kurejea tena kufanya operesheni ndani ya ardhi yetu kimya kimya.Kitendo hiki hakivumiliki kabisa” akasema Joel Mshana “Usiku huu wa leo nimevamia makazi ya balozi wa Israel nikamteka nyara yeye na mkewe pamoja na kuwapa mateso hasa mkewe ili kutafuta taarifa za Edger Kaka.Kama haitoshi nimekwenda pia katika ubalozi wa Israel na nimewaua majasusi wawili ambao walitumwa kuja kuandaa mpango wa operesheni ya kumtafuta Olivia.Huu ni mgogoro mkubwa taya……” “Unasema umeua raia wawili wa Israel?!! Akauliza Dr Evans “Ndiyo mheshimiwa Rais nimeua raia wawili wa Israel ambao ni majasusi waliotumwa kuja nchini kuandaa operesheni ya siri ndani ya ardhi yetu” “Kwa nini umefanya hivyo Mathew?Unafahamu athari za hicho ulichokifanya?akauliza Dr Evans “Mzee bila kufanya vile nisingeweza kufahamu mahala alipo Edger Kaka ! akajibu Mathew “Hili jambo mbona linakuwa kubwa na gumu kulitatua? Naamini mapema asubuhi nitapigiwa simu na waziri mkuu wa Israel akimuulizia balozi wake na sintakuwa na jibu la kumpa” “Mheshimiwa Rais naomba unisikilize” akasema Mathew “Tunahitaji kufanya operesheni kubwa katika ubalozi wa Israel nchini Kenya na kumchukua Edger Kaka.Tulipaswa kuifanya operesheni hiyo usiku huu huu lakini tayari tumekwisha chelewa kwani yanatakiwa maandalizi ya kutosha.Nashauri operesheni hiyo ifanyike usiku wa kesho au kesho kutwa hivyo basi inatakiwa siku ya leo kusivuje taarifa zozote za kutekwa kwa balozi wa Israel hapa nchini wala wale majasusi wawili waliouawa ndani ya ubalozi wa Israel wasijulikane.Tukifanikiwa kwa hili tutapata nafasi nzuri ya kujiandaa kwa ajili ya operesheni ya kumtwaa Edger Kaka kutoka katika ubalozi wa Israel nchini Kenya”akashauri Mathew “Mathew bado napatwa kigugumizi namna hilo unalolishauri litakavyotekelezwa.Balozi ametekwa na raia wawili wameuawa.Oh God ! akasema Dr Evans akionekana kukata tamaa. “Mheshimiwa Rais jambo hili linahitaji sana nguvu yako kulimaliza” akasema Mathew “Hebu nielekezeni kitu gani ninatakiwa kukifanya?Kichwa changu kimechoka” akasema Dr Evans “Ili tuweze kuingia katika makazi ya balozi Dr Yonathan ilitulazimu kuwadhibiti kwanza askari waliokuwa getini” “Mliwadhibiti vipi? Mliwaua? akauliza Meshack Jumbo “Tuliwafunga ili wasiweze kutuzuia kufanya kazi yetu.Wamefungwa katika kichaka cha maua karibu na geti.Vile vile yuko mmoja ambaye alikuwa amepoteza fahamu huyu alikuwa analinda geti la nyumba ya balozi.Hawa askari wote wanatakiwa waondolewe pale haraka sana na wapelekwe sehemu wakahifadhiwe hadi pale tutakapokuwa tumemaliza operesheni yetu hiyo kesho.Jeshi la polisi hawapaswi kufahamu chochote kuhusu kutekwa kwa balozi kwa sasa.Baada ya kuwadhibiti kwanza askari wale atafuata balozi Dr Yonathan.Huyu kwa sasa anashikiliwa katika makazi yangu lakini nitamrejesha nyumbani kwake ili asubuhi aweze kwenda kazini.Lengo la kufanya hivi ni kuzuia watu wasijue chochote kilichotokea usiku huu”akasema Mathew “Una hakika gani kwamba balozi hatasema chochote kwa serikali yake?akauliza Dr Evans “Hataweza kwa sababu tunamshikilia mke wake.Tutampa masharti ayafuate na kama akienda kinyume tutatishia kumuua mke wake.Jambo la tatu usiku huu kabla ya kupambazuka tunatakiwa kuiondoa miili ile miwili ya wale majasusi wawili waliouawa ndani ya ubalozi wa Israel.Haya yanatakiwa kufanyika kabla ya mapambazuko.Tukisha yakamilisha haya ndipo tuanze kuandaa operesheni ya kuvamia ubalozi wa Israel nchini Kenya” Akasema Mathew “Mheshimiwa Rais Mathew ameeleza vizuri sana namna mambo yanavyotakiwa kufanyika na hata mimi ninakubaliana na mawazo yake.Nguvu yako inatakiwa sana katika suala hili”akasema Meshack Jumbo “Sina kipingamizi katika yale yote aliyoyaeleza ili mradi tu awe na uhakika kwamba yakitekelezwa yatakuwa na manufaa” “Mheshimiwa Rais hii ni hatua ya kwanza ya kuondoa mgogoro unaoweza kutokea kati yetu na Israel wakati tunajiandaa kwenda kuvamia ubalozi wao nchini Kenya.Nina uhakika mkubwa kama tukikamilisha haya niliyoelekeza kila kitu kitakwenda vyema” akasema Mathew “Basi hakuna muda wa kupoteza tuanze kwanza na hawa askari waliokuwa wanalinda geti la kijiji cha mabalozi” akasema Dr Evans na kuchukua simu akampigia simu mkuu wa jeshi la polisi “Mheshimiwa Rais” akasema mkuu wa jeshi la polisi “Afande IGP kuna jambo nahitaji msaada wako wa haraka sana” akasema Dr Evans “Ndiyo mheshimiwa Rais” “Katika kijiji cha mabalozi kuna askari wanalinda katika geti kuu.Kuna kazi Fulani niliwatuma vijana wangu wakaifanye usiku huu pale ndani na ikawalazimu kuwadhibiti wale askari lakini wote wako salama na silaha zao zote zipo.Ninawataka askari wale waondolewe haraka sana eneo lile na waletwe hapa ikulu.Nataka wasiulizwe chochote kuhusu kilichotokea na simu zao zote zichukuliwe ili wasiweze kuwasiliana na mtu yeyote” akasema Dr Evans “Nimekuelewa mheshimiwa Rais ninatakakufamu je ni askari wale tu wanaolinda geti kuu au askari wote wanaolinda kijiji cha mabalozi? “Kwani ulinzi ukoje katika kijiji cha mabalozi?akauliza Dr Evans “Kwa kawaida kuna kuwa na askari watano katika geti kuu la kuingilia kijijini,wawili wanakuwa na silaha wengine wawili hawana silaha na mmoja anakuwa na mbwa.Ukiingia ndani pia kuna kuwa na askari mmoja katika kila nyumba ya balozi” “Basi ninawataka wale walioko geti kuu na Yule anayelinda katika nyumba ya balozi wa Israel” “Sawa mheshimiwa Rais nimekuelewa” “Afande fuatilia suala hili ili litekelezwe haraka kama nilivyoelekeza” akasema Dr Evans http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Sawa mheshimiwa Rais” akasema mkuu wa jeshi la polisi na Rais akakata simu “Hilo la kwanza limemalizika.Askari wale wataletwa hapa na nitaelekeza wapelekwe katika nyumba ya mapumziko wakapumzike huko hadi kesho kutwa ndipo watakapoachiwa huru.Nini kinafuata baada ya hapo?akauliza Dr Evans “Kinachofuata ni kwenda kumchukua balozi na kwenda naye ubalozini ili kuichukua ile miili ya wale majasusi wawili waliouawa na kisha tutamrejesha balozi nyumbani kwake ili kuondoa wasi wasi kwani asipoonekana asubuhi kutakuwa na tatizo.Katika hilo la balozi tunahitaji sehemu salama kwa ajili ya kumuhifadhi mke wake pale katika makazi yangu si salama sana kwani tayari Devotha anapafahamu na anaweza akafanya chochote.Tunahitaji sehemu ambako tutamuhamishia mke wa balozi ambako ni salama zaidi” akasema Mathew “Kuhusu makazi salama hakuna tatizo nina mashamba mawili na yote yana nyumba.Tutatumia nyumba yangu iliyoko katika shamba la Mikindu ambako huitumia kama sehemu yangu ya mapumziko” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais ahsante kwa hilo.Nadhani ni wakati wa kwenda kuanza utekelezaji kwani muda unakimbia sana.Tutaendelea na majadiliano zaidi baada ya kuhakikisha tumelimaliza hili jambo” akasema Mathew na kusimama “Mathew ni vipi kama wale magaidi wakinipigia simu?akauliza Dr Evans “Usiwe na hofu mheshimiwa Rais.Hawataweza kumuua mwanao kwani wanaamini wewe unafahamu mahala alipo Edger Kaka hivyo basi wakikupigia simu jitahidi kutafuta namna ya kuvuta muda ili tujipange kwanza tumteke mtu wao na hapo ndipo mchezo utakaponoga” akasema Mathew “Mathew una hakika hawatweza kumuua mwanangu hawa jamaa?akauliza Dr Evans “Niamini mheshimiwa Rais,mwanao atakuwa salama.Hawataweza kumfanya kitu chochote” akasema Mathew.Akashikana mkono na Rais wakaagana “Mathew kabla hujaondoka” akasama Dr Evans na kumpatia Mathew namba zake za mawasiliano.Meshack Jumbo na Joel Mshana wakapewa gari la kuwarajesha majumbani ili kumpa nafasi Mathew ya kuwahi kutekeleza jukumu lake kabla ya mapambazuko. “Mungu ameniwekea roho ya ubishi ndani mwangu na kutokukata tamaa katika jambo lolote lile na kuna nyakati ninakuwa na ujasiri uliopitiliza.Nina wasiwasi siku moja roho hii ya ubishi na kutokubali kushindwa itaniweka katika matatizo makubwa.Kitendo nilichokifanya leo kilikuwa cha hatari kubwa.Nilijipeleka mimi mwenyewe katika mdomo wa Mamba.Ni vipi kama Rais angekataa kunisikiliza?Ningekuwa katika hatari kubwa.Hata hivyo ninashukuru Rais amenielewa japo haikuwa rahisi.Kwa sasa baada ya kuweka mambo sawa kinachofuata ni kupambana na magaidi kuhakikisha ninawafyekelea mbali wote na kumpata Olivia akiwa salama pamoja na Coletha.Lakini kubwa zaidi ni operesheni ya kuvamia ubalozi wa Israel nchini Kenya kumchukua Edger Kaka.Hili halitakuwa jambo rahisi na itakuwa ni operesheni inayohitaji maandalizi ya aina yake.Kwa namna yoyote ile lazima Edger Kaka apatikane! Akawaza Mathew akiwa garini akirejea katika makazi yake baada ya kutoka ikulu







Mathew aliwasili katika makazi yake na kumkuta Gosu Gosu akiwa amejiimarisha sawa sawa kiulinzi.Hakuamini kumuona Mathew akirejea akiwa mzima.Akainua mikono juu akamshukuru Mungu “Ahsante Mungu kwa kumrejesha salama Mathew.Sikujua kama ataweza kurejea salama” akasema Gosu Gosu na kumfuata Mathew aliyekuwa anashuka garini “Mambo yanakwendaje hapa?akauliza Mathew “Hapa ni salama kabisa hakuna tatizo lolote” akajibu Gosu Gosu “Vipi maendeleo ya wagonjwa? “Wote wanaendelea vyema.Vipi huko utokako?Kuna mafanikio?akauliza Gosu Gosu “Mungu mkubwa.Mafanikio yapo makubwa” akasema Mathew na kuelekea ndani akaenda kwanza kumtazama Ruby ambaye bado alikuwa amelala.Dr Hiran alikuwa amejilaza sofani aliposikia mlnago ukifunguliwa akaamka “Mathew” “Dr Hiran mgonjwa wangu anaendeleaje? “Anaendelea vyema.Wote wawili hawana tatizo lolote.Yule mwingine aliyekatika vidole nimempatia huduma ya kwanza lakini anahitaji matibabu zaidi” akasema Dr Hiran “Ahsante sana Dr Hiran kwa msaada huu mkubwa.Naomba usinichoke kila pale itakapokuwa ninakuhitaji.Kesho nitakuandikia hundi yako ya malipo” akasema Mathew “Mathew kitu cha muhimu ni wagonjwa wetu wawe wazima usiwaze sana kuhusu malipo” akasema Dr Hiran.Mathew akamchukua Gosu Gosu wakaelekea katika chumba cha kusomea ambacho wanakitumia kama ofisi yao “Gosu Gosu huko nilikotoka mambo ni mazuri japo muda ni mfupi kukuelezea kila kitu lakini mambo yamekwenda vyema kabisa.Nimetoka ikulu kuonana na Rais” “Dah ! Mathew wewe ni kiumbe wa ajabu sana na kuna nyakati ninakuogopa.Umewezaje kupenya hadi ukaingia ikulu kuonana na Rais?akauliza Gosu Gosu “Naweza kusema ni maongozi ya Mungu tu kwa sababu kuna mambo mengine yanatokea ambayo hata mimi nakuwa siyatarajii.Kwa ufupi nimefanikiwa kuonana na Rais.Haikuwa rahisi lakini nimemueleza kile tulichokipata katika uchunguzi wetu na kumfanya aingiwe baridi.Ni mambo makubwa ambayo hakuwa ametegemea kuyasikia.Kuokoa muda ni kwamba Rais yuko upande wetu sasa na tumeufungua ukurasa mpya.Tuko timu moja sisi na yeye” akasema Mathew “Ashukuriwe Mungu” akasema Gosu Gosu “Amenieleza kila kitu kilichotokea tukayaacha yaliyopita yaende na kuamua kuanza upya.Hata hivyo kuna mambo yametokea ambayo tusingeweza kuyafahamu kama nisingeonana naye.Kwanza ni kuhusu shambulio la Mtodora.Kama tulivyokuwa tunahisi shambulio lile lilimlenga mtoto wa Rais.Muda mfupi tu baada ya shambulio lile kutokea Rais alipigiwa simu na kiongozi wa kikundi kile kilichofanya shambulio lile hospitali na akamweleza kwamba wamemchukua mwanaye akamtaka afuate maelekezo watakayompa.Rais hajamueleza mtu yeyote jambo hili kwani ni moja ya masharti aliyopewa na watekaji hao ili mwanae aweze kuwa salama.Baada ya hapo watekaji hao ambao naamini ni IS walimtaka Rais awapatie Olivia.Ili kuhakikisha mwanae anakuwa salama Rais akalazimika kutekeleza kile walichokitaka na akawapatia Olivia.Mipango yetu imekwama kwani Olivia tayari yuko katika mikono ya magaidi.Njia pekee iliyobaki ni kumpata Edger Kaka.Tukifanikiwa kumpata huyu tutaweza kufahamu mahala walipo Olivia na Coletha pamoja na mambo mengine mengi kuhusiana na mtandao wa IS.Ili kumpata Edger lazima tuvamie ubalozi wa Israel nchini Kenya.Hii ni operesheni kubwa ambayo inatupasa kujipanga vilivyo.Tutaitumia siku nzima ya leo kujipanga na kama ikiwezekana na usiku wa leo au kesho tutavamia ubalozi huo na kumchukua Edger.Ili kupata nafasi nzuri ya kufanya maandalizi yetu tunapaswa kuhakikisha kwamba hakuna taarifa yoyote itakayovuja kuhusiana na hiki kilichotokea usiku huu kuvamiwa kwa balozi wa Israel na vile vile kuuawa kwa wale majasusi.Mambo haya yanapaswa kubaki siri Israel wakijua kila kitu kitaharibika na tutamkosa Edger.Hivi sasa tunamchukua balozi na tunakwenda ubalozini ambako tutachukua miili ile ya wale watu wawili tuliowaua na kuondoka nayo kwenda kuificha mahali ili kuondoa kabisa ushahidi halafu tutamrejesha balozi nyumbani kwake kujiandaa kwa shughuli za leo na kutakapopambazuka ataenda ofisini kwake ili watu wasijue kama kuna tatizo lolote limetokea.Mke wake tutaendelea kumshikilia na tutamuhamishia katika nyumba ya Rais ambako Rais ametutaka tufanyie kila kitu huko kutokana na usalama kuwa ni mkubwa sana mahala hapo”akasema Mathew kisha wakaenda katika chumba alimo balozi.Gosu Gosu akamfungua pingu “Mke wangu anaendeleaje? Ninaomba nikamuone tafadhali” akasema Balozi “Usihofu balozi mkeo utamuona lakini kwa sasa tuna mazungumzo muhimu na wewe” akasema Mathew “Kitu gani zaidi mnachokihitaji kutoka kwangu? Taarifa zote mlizozitaka nimewapa mnataka nini tena?Tafadhali naomba mtuachie mimi na mke wangu tuondoke” akasema Dr Yonathan “Dr Yonathan suala hili si rahisi kama unavyodhani.Tayari umeingia katika matatizo makubwa sana na nchi yako.Umetoa siri za taifa lako lakini ulifanya hivi kwa nia nzuri ya kujilinda wewe binafsi na kumlinda mke wako pia.Serikali ya Israel wakifahamu hiki ulichokifanya hawatakuacha salama.Maisha yako yote yaliyobaki utaishia gerezani. Hawataangalia ulitoa siri za nchi katika mazingira gani lakini watakachokitambua wewe ni msaliti kwa taifa la Israel na haufai kuwa kiongozi na utaishia gerezani na yawezekana ukapotea bila hata familia yako kujua na huo ukawa ni mwisho wako.Dr Cohen tunataka kukusaidia ili haya yote yaliyotokea usiku wa leo yabaki kuwa siri na tutakaofahamu ni sisi pekee”akasema Mathew na kumtazama Dr Yonathan “Nini hasa mnachokitafuta kwangu nyie vijana?Mmenilazimisha nikatoa siri za nchi na sasa bado mnataka kunilazim……..” “Hatukulazimishi Dr Cohen tunataka uamue wewe mwenyewe kama unataka suala hili libaki kuwa siri au unataka serikali ya Israel wafahamu kwamba ni wewe uliyetupa taarifa zote za kuhusu Edger Kaka ambaye ni mtu muhimu sana kwa serikali ya Israel na walitumia gharama kubwa kumpata.Tunakupa nafasi hii ili uweze kuamua hatima ya maisha yako.Muangalie mkeo,itazame familia yako na ufanye maamuzi sahihi.Dr Cohen hakuna mkamilifu hapa duniani kila mtu anakosea lakini wewe umelisaliti taifa lako kwa ajili ya familia yako hivyo basi usikubali familia yako ikateseka pale utakapokwenda gerezani.Tunataka kukusaidia Dr Cohen” akasema Mathew.Dr Yonathan akafikiri kwa muda na kusema “Hakuna namna mnavyoweza kulifanya suala hili likawa siri.Mliua askari wanaotulinda katika makazi yetu na kubwa zaidi mkaua wale majasusi wawili wa Israel tena ndani ya ubalozi wetu.Jambo hili haliwezi kubaki siri lazima lijulikane”akasema DrYonathan “Sikiliza Dr Yonathan.Askari wale wanaowalinda katika makazi yenu hawakuuawa bali walidhibitiwa tu na tunao uwezo wa kuwaziba midomo yao na tukio lile likabaki kuwa siri.Tunahitaji ushirikiano wako Dr Cohen ili jambo hili lisijulikane kwa serikali ya Israel.Uko tayari kushirikiana nasi? “Nini hasa mnataka kukifanya?akauliza Dr Yonathan “Tunataka utupeleke ubalozini usiku huu kabla ya mapambazuko tunakwenda kuichukukua miili ile ya wale majasusi waliouawa na kuificha.Baada ya hapo utarejea nyumbani kwako na utaendelea na shughuli zako kama kawaida ili asigundue mtu yeyote kilichotokea.Utawajulisha Tel Aviv kwamba majasusi wale wawili wanaendelea vyema na maandalizi ya operesheni yao na hakuna tatizo.Saa nne za asubuhi utaondoka ubalozini na utakwenda mahala nitakapokuelekeza.Mke wako tutakuwa naye na kama utafanya kinyume na maelekezo yetu hautamuona tena lakini ukifanya kama tunavyotaka basi suala hili litaendelea kubaki siri na utaungana tena na mkeo.Yeyote atakayekuuliza kuhusu mkeo mjibu amekwenda nje ya Dar es salaam kwa dharura.Usijidanganye tafadhali kufanya jambo lolote la kijinga,tunakufuatilia.Umeni elewa? akauliza Mathew “Nimekuelewa lakini mke wang…” “Usihofu kuhusu mkeo atapatiwa huduma zote na atakuwa salama.Tekeleza kile ninachokuelekeza na mkeo utampata.Narejea kukuonya kama ukifungua mdomo wako na kusema hiki kilichotokea hautamuona tena mkeo.Nadhani tumeelewana.Sasa inuka tunaelekea ubalozini.”akasema Mathew na kumfuata Dr Hiran “Dr Hiran tunaondoka tena nitakuacha hapa ukiendelea kuwahudumia hawa wagonjwa wetu wawili.Usihofu uko salama na endapo kutatokea hatari yoyote unijuze mara moja” akasema Mathew “Usihofu Mathew mimi niko hapa hadi kutakapopambazuka” akasema Dr Hiran Mathew akamuelekeza Gosu Gosu kukusanya vifaa vote watakavyovihitaji katika kazi ile kisha wakamchukua Dr Yonathan wakaingia garini na kuondoka kuelekea katika ubalozi wa Israel.



Gari tatu ziliwasili katika geti la kuingilia kijiji cha mabalozi.Hakukuwa na mlinzi yeyote pale getini.Mkuu wa jeshi la polisi alikuwa amefika katika kijiji cha mabalozi kutekeleza agizo la Rais.Alifunguliwa mlango akashuka eneo likakaguliwa kisha wakaanza kuwatafuta askari walipo.Mbwa aliyekuwa amefungwa katika mti ndiye aliyewasaidia kufahamu mahala walikokuwa wamefungwa askari wale.Pembeni kidogo ya mahala alikofungwa mbwa walikuwepo askari watano wakiwa wamefungwa na kubandikwa gundi midomoni mwao ili wasiweze kupiga kelele.Haraka haraka wakafunguliwa na kuhakikiwa kama wote ni wazima wakapelekwa ndani ya gari.Hawakuulizwa chochote kilichotokea.Silaha zao zilikuwa pembeni yao nazo zikachukuliwa na kuwekwa katika gari lingine.Mkuu wa jeshi la polisi akaelekeza afuatwe askari mwingine ambaye alikuwa analinda nyumba ya balozi wa Israel.Gari lilimfuata na baada ya muda naye akaletwa akaunganishwa na wenzake.IGP akatoa maelekezo ya kupelekwa kwa walinzi wengine haraka sana kuchukua nafasi za wale askari kisha wakaondoka kuelekea ikulu kama alivyoelekeza Rais.







Gari la Mathew lilisimamishwa katika geti la kuingilia ubalozi wa Israel.Balozi Dr Yonathan akashuka na kujitambulisha kwa walinzi wakaruhusiwa kupita.Moja kwa moja wakaegesha gari katika nyumba ambayo hutumiwa na wageni maalum wanaotembelea ubalozi huo.Gosu Gosu akashuka akiwa na masanduku mawili makubwa wakaingia ndani ya nyumba ile moja kwa moja hadi katika chumba ilimo miili ya majasusi wale waliouawa.Bila kupteza muda Gosu Gosu akatandika turubai chini halafu akachukua vifaa walivyokuja navyo shoka dogo,panga na kisu kikubwa kikali na kuanza kuikata miili ile vipanda vipande.Dr Yonathan akafumba macho asione kile kilichokuwa kinaendelea mle chumbani mara akaanza kutapika.Hakuwahi kushuhudia kitu cha namna ile kwa macho yake ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia mwili wa mtu ukikatwa vipande vipande kama nyama “Nimeingia katika mikono ya watu makatili mno wasio na huruma hata chembe.Sipaswi kuwafanyia mchezo watu hawa ni wanyama na wauaji.Wanakata kata wanadamu wenzao kama nyama.Huu ni ukatili mkubwa uliovuka mipaka” akawaza Dr Yonathan Gosu Gosu hakumuangalia mtu usoni aliendelea na zoezi lake la kuikata ile miili alipomaliza mwili wa Fishel akaviweka vipande vyote katika mfuko mkubwa wa nailoni halafu akauweka kwenye sanduku akalifunga akauchukua mwili wa Ehud na kuufanya vile vile kisha akaufunga katika sanduku.Akakusanya vifaa vyake akafanya usafi mle ndani.Walihakikisha kila kifaa chenye damu wamekiondoa na baada ya kujiridhisha kwamba hakuna wasiwasi wowote mle ndani wakayachukua masanduku yale mawili wakayakokota hadi katika gari lao wakaondoka.Bado Dr Yonathan alikuwa anatetemeka mwili kwa kitendo alichokishuhudia. “Dr Yonathan ahsante sana kwa ushirikiano wako mkubwa.Suala hili tumelimaliza na hakuna yeyote atakayefahamu kilichotokea.Itabaki kuwa siri yetu na wewe utaendelea kuwa salama.Tutakurejesha nyumbani kwako ujiandae kwa ajili ya siku ya leo usionyeshe utofauti wowote fanya kazi zako kama vile hakuna kitu chochote kilichotokea.Hakikisha umewasiliana na Tel Aviv ukawajulisha kuwa huku mambo yanakwenda vyema ili wasiwe na wasi wasi wowote.Saa nne za asubuhi nitakupigia simu na kukuelekeza sehemu utakayotakiwa uende.Tafadhali naomba ufanye kila nilichokuelekeza ili wewe na mkeo muwe salama.Sisi sio watu wabaya lakini ukitulazimisha tutakuwa wakatili sana.Umenielewa balozi?akauliza Mathew “Nimekuelewa” akajibu Balozi Dr Yonathan “Safi” akasema Mathew na kuelekea moja kwa moja katika makazi yake. “Gosu Gosu wewe utashughulikia kuihifadhi hiyo miili isigundulike mimi ninamrejesha balozi nyumbani kwake kwani mapambazuko yanakaribia.Tutakutana tena hapa kwa ajili ya awamu ya pili.Kama kuna tatizo lolote nijulishe haraka sana tafadhali.Tumia gari la Dr Hiran” akasema Mathew.Gosu Gosu akashusha yale masanduku yenye miili ya watu na kuyapakia katika gari la Dr Hiran.Mathew hakupoteza muda pale nyumbani akageuza gari na kuondoka kumrejesha Dr Yonathan nyumbani kwake. “Jamani naombeni mnipe nafasi walau nimuone mke wangu nijue maendeleo yake.Nimekubali kufanya kila mnachokitaka kwa sababu yake niruhusuni walau nimtazame”akaomba Dr Yonathan “Usihofu balozi,mkeo ni mzima na anaendelea vyema.Fuata maelekezo yangu na utaonana naye tena lakini ukienda kinyume na ninavyotaka hautamuona tena mkeo” akasema Mathew akiwa makini katika usukani “Watu hawa ni akina nani?Kitu gani wanakitafuta?Wamewezaje kufahamu kuhusu mawasiliano yangu na Devotha?Naanza kuhisi yawezekana hawa jamaa wakawa ni magaidi wa IS ambao wanamtafuta Edger Kaka” akawaza Dr Yonathan na kugeuza shingo akamtazama Mathew kwa jicho la wizi “Hawa lazima ni magaidi.Inaniumiza sana kuwapa siri mahala alipo Edger Kaka ambaye nchi yangu imetumia gharama kubwa kumpata na ambaye anategemewa sana kuonyesha mahala alipo Habiba Jawad mfadhili wa vikundi vya ugaidi.Lakini sikufanya hivi kwa kupenda bali kwa ajili ya kuokoa maisha yangu na maisha ya mke wangu.Kama nisingefanya vile wangeweza kutuua sote kama walivyowaua na kuwakata kata akina Fishel na Ehud bila huruma.Hawa si watu wa kufanyia mchezo hata kidogo.Ukatili wao umevuka kile kiwango cha ukatili.Hata wanyama si wakatili kiasi hiki.Ninachomuomba Mungu ni siri hii isijulikane kwamba ni mimi ndiye niliyewaeleza mahala alipo Edger Kaka.Maisha yangu yataishia gerezani.Nimelitumikia taifa langu kwa uaminifu kwa miaka mingi lakini nimekuja kuharibu mwishoni wakati karibu ninastaafu.Nitafanya kila linalowezekana ili jambo hili lisijulikane” akawaza Dr Yonathan. Hakukuwa na mazungumzo ndani ya gari hadi walipofika katika geti la kuingilia katika kijiji cha mabalozi ambako walisimamshwa na askari balozi akajitambulisha wakaruhusiwa kupita hadi katika nyumba yake ambako alikuta tayari amekwisha letwa askari mwingine.Mambo haya yakaendelea kumshangaza sana Dr Yonathan. “Dr Yonathan umefika nyumbani kwako utaendelea na ratiba zako kama kawaida asubuhi hii na usionyeshe kama kuna kitu chochote kimetokea.Kumbuka saa nne nitakupa maelekezo ya sehemu unakotakiwa uende na ufanye hivyo haraka sana.Unaweza kwenda” akasema Mathew na Dr Yonathan akafungua mlango akashuka akaenda chumbani kwake akamfungua mtumishi wao wa ndani ambaye alikuwa amefungwa kamba “Nyamaza usilie Mariana.Mambo yamekwisha” “Balozi watu wale ni akina nani?Mama yuko wapi?akauliza Mariana “Usihofu Mariana jambo lile limekwisha tayari tumekwishamalizana na wale watu nimewapa wanachokihitaji na sasa tuko salama.Mama yuko hospitali anapatiwa matibabu kwa majeraha aliyoyapata” akajibu balozi.Bado Mariana aliendelea kulia “Mariana naomba unisikilize” akasema Balozi Mariana akafuta machozi “Hiki kilichotokea hapa usiku wa leo kitabaki kuwa siri ya hapa sitaki kivuke nje ya mipaka ya nyumba hii.Hatakiwi mtu yeyote kufahamu.Hata akija mtu yeyote kukuhoji usimueleze chochote sema kwamba hakujatokea kitu.Atakayemuuliza mama mwambie amesafiri kwa siku chache atarejea.Umenisikia Mariana? “Nimekusikia” “Vizuri sana.Nitakuongeza mshahara wako na ninakuahidi nitakapoondoka hapa Tanzania pale muda wangu utakapokuwa umemalizika nitaondoka nawe kwenda kukutafutia kazi huko nchi za Ulaya ili uwe na maisha mazuri lakini itunze siri hii asiifahamu mtu yeyote” akasema balozi Dr Yonathan na sura ya Mariana ikajenga tabasamu. “Sasa nenda kapumzike kwa ajili ya kujiandaa kuikabili siku” akasema Dr Yonathan na Mariana akatoka mle chumbani. “Ee Mungu naomba umlinde mke wangu huko aliko awe salama hadi pale tutakapoungana tena” akaomba Dr Yonathan akiwa amekaa kitandani akiwa mwingi wa mawazo.Picha ya kile alichokifanya Gosu Gosu ubalozini ikamjia akakimbia chooni kutapika Mara tu Mathew alipotoka katika kijiji cha mabalozi akachukua simu na kumpigia Rais “Hallow Mathew” akasema Dr Evans baada ya kupokea simu “Mheshimiwa Rais nimekupigia kukupa taarifa kwamba tayari tumemaliza kazi kwa upande wa balozi na hivi ninavyozungumza nawe nimetoka kumrejesha nyumbani kwake anajianda kwa ajili ya kuanza shughuli zake za siku” “Kazi nzuri Mathew.Vipi kuhusu wale jamaa mliowaua kule ubalozini? “Nako tayari pia tumekwisha iondoa miili ile na hakuna tena kitu cha kuhofu.Vipi kuhusu wale askari? “Askari wale tayari wamekwisha ondolewa na nimeelekeza wapelekwe katika nyumba ya mapumziko na wakae huko hadi tutakapokamilisha operesheni yetu” “Ahsante sana mheshimiwa Rais” “Baada ya hatua hii ya kwanza kukamilika nini kinachoendelea?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais,baada ya awamu ya kwanza kukamilika nitahitaji kuwa na mazungumzo nawe ili kupanga mikakati ya namna ya kulitekeleza hili suala lakini kabla ya kuonana tunahitaji kuhamishia ofisi yetu ya muda katika shamba lako kama ulivyosema kwani mahala tulipo sasa si salama” “Sawa Mathew nitamtuma mtu wangu atakufuata mahala ulipo na ndiye atakayewapeleka huko shambani kwangu.Kitu gani kingine unakihitaji? “Nitahitaji daktari nina wagonjwa wawili ambao wanahitaji kuendelea kupatiwa matibabu” “Sawa Mathew lakini ningeomba tukutane asubuhi kabla ya saa tatu kwani nitakuwa na vikao vingi siku ya leo hivyo jitahidi tukutane mapema.Nadhani ingekuwa vyema wewe ukaja kuonana nami kwanza na hao wagonjwa wako watapelekwa shambani na watu wangu na baada ya kutoka huku utakwenda kuungana nao” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa Rais.Vipi kuhusu wale jamaa wamekupigia tena simu kutaka kitu chochote?akauliza Mathew “Hapana hawajanipigia bado lakini naamini watapiga asubuhi” akajibu Dr Evans “Kama tulivyokubaliana mheshimiwa Rais endapo wakipiga simu jitahidi kuvuta muda ili tuweze kupata nafasi ya kumaliza kwanza operesheni yetu” “Nitafanya hivyo Mathew usiwe na shaka” akasema Dr Evans na kuagana na Mathew akakata simu Tayari ni saa kumi na moja za asubuhi Mathew alipowasili katika makazi yake. “Dr Hiran wagonjwa wangu wanaendeleaje? “Wanaendelea vizuri Mathew.Wote tayari wako macho na maendeleo yao ni mazuri sana” akasema Dr Hiran “Nakushukuru sana Dr Hiran.Umenifanyia jambo kubwa sana na fedha peke yake haitoshi kulipia wema huu ulionisidia.Umekesha nami usiku kucha ukiwahudumia wagonjwa wangu.Nashukuru sana” “Usijali Mathew kama daktari ni jukumu langu kuhakikisha wagonjwa wanapona bila kujali kwanza masuala ya pesa” “Tayari kumepambazuka ni wakati wako wa kwenda kupumzika.Hundi yako italetwa baadae ofisini kwako na kama nitakuhitaji tena nitakujulisha” “Muda wowote Mathew ukihitaji msaada wangu mimi nipo tayari kukusaidia kama rafiki yako hivyo kuwa na amani” “Ahsante sana Dr Hiran.Utatumia gari langu kwa muda,gari lako aliondoka nalo Gosu Gosu baadae atalirejesha kwako” akasema Mathew na Dr Hiran akaenda kuwaaga wagonjwa Ruby na mke wa balozi kisha akaingia katika gari la Mathew na kuondoka.Baada ya Dr Hiran lkuondoka Mathew akaeleka katika chumba alimo Ruby “Mathew ! akasema Ruby.Mathew akamfuata pale kitandani akamuinamia na kumbusu katika paji la uso “Unaendeleaje Ruby” “Namshukuru Mungu sijambo.Ahsante kwa kuyapigania maisha yangu.Siamini kama ninaendelea kuvuta pumzi” akasema Ruby “Ruby sijui nimshukuruje Mungu kwa muujiza huu mkubwa.Nilimlilia sana asiichukue roho yako kwani bado ninakuhitaji sana Ruby.Mungu amesikia ombi langu na amekurejeshea tena uzima.Ashukuriwe sana aliye juu” akasema Mathew “Mathew pamoja na kumshukuru Mungu lakini napaswa kukushukuru sana wewe kwa namna ulivyopambana kuhakikisha ninapona.Ulifanikiwa kumpata Yule shetani Devotha? Akauliza Ruby “Mambo mengi yamefanyika usiku wa leo.Yameibuka mambo mengine ambayo hatukuwa tunayafahamu.Nitakueleza kila kitu pale utakapokuwa katika hali nzuri kwa sasa endelea kupumzika”akasema Mathew “Mathew I’m fine.Nieleze kila kitu kilichotokea.Tell me you killed that witch” akasema Ruby “Relax Ruby.Kwa hali yako ya sasa unahitaji mapumziko.Usiwaze sana kuhusu haya masuala yaliyotokea” “Mathew that devil almost killed me ! She shot me three times.Tell me you’ve killed her” akaendelea kusisitiza Ruby na macho yake yakaonyesha machozi “Ruby kama nilivyokueleza kwamba yametokea mambo mengi usiku wa kuamkia leo hivyo sikuweza kufanikiwa kumpata Devotha lakini nitampata.Nakuhakikishia kwamba lazima nitampata na atalipa kwa hili alilolifanya.Hataweza kukwepa” “Nini hasa kimetokea usiku kilichosababisha ukashindwa kumpata Devotha?akauliza Ruby “Nitakueleza baadae Ruby” “No Mathew tell me now !! akasema Ruby na kutaka kuinuka ili akae akagugumia kwa maumivu “Easy Ruby ! Easy” akasema Mathew na kumsaidia Ruby kukaa. “I’m fine Mathew.Nieleze kila kitu” akasema Ruby na Mathew akalazimika kumsimulia kila kitu kilichotokea kwa usiku mzima. “Pole sana Mathew kwa kazi kubwa uliyoifanya usiku wa leo.Mambo uliyoyagundua sikuwa nimewahi hata kuyaota ndotoni.Sikutegemea kama suala hili lingekuwa kubwa namna hii na hata kuhusiana mataifa mengine” akasema Ruby “Hata mimi nilipoanza kulichunguza hili suala sikutegemea kama lingeweza kuwa kubwa kiasi hiki.Sikutegemea kusikia Olivia anajihusisha na mtandao wa kigaidi wa IS.Sikutegemea kama suala hili litamuibua Edger Kaka ambaye nchi nzima wanafahamu alifariki katika ajali miaka mitatu iliyopita lakini kumbe yuko hai.Sikutegemea kama suala hili lingeniingiza katika mgogoro na Israel,katika mgogoro na Mossad” akasema Mathew “Mambo yaliyoibuka hasa usiku wa leo ni makubwa sana.Nini kinachoendelea sasa kuhusiana na suala hili?akauliza Ruby “Kikubwa ambacho ilikuwa lazima tukifanye ni kuhakikisha kwamba yale yote yaliyotokea kwa usiku wa leo yanabaki kuwa siri.Serikali ya Israel hawapaswi kufahamu kitu chochote kuhusiana na kuvamiwa kwa balozi wao na wala kuuawa kwa majasusi wao wawili na jambo hilo tumelikamilisha na kilichotokea kitabaki kuwa siri.Baada ya kukamilisha hatua ya kwanza kinachofuata ni kuvamia ubalozi wa Israel nchini Kenya na kumchukua Edger Kaka.Huyu ndiye atakayetusaidia kuwapata Olivia na Coletha.Vile vile atatusaidia sana katika kufahamu mipango yote ya IS waliyoipanga hapa nchini” akasema Mathew “Kuvamia ubalozi wa Israel?! Ruby akashangaa “Ndiyo.Lazima tuvamie ubalozi wa Israel na kumchukua Edger Kaka ambaye anahifadhiwa ubalozini hapo” “Hii ni operesheni kubwa sana Mathew na ya hatari” akasema “Ndiyo ni operesheni kubwa na ya hatari lakini lazima tuifanye.Lazima tumpate Edger Kaka kwa gharama zozote zile na ili tumpate lazima tuvamie ubalozi wa Israel jijini Nairobi” akasema Mathew “Operesheni yenyewe itakuwaje?akauliza Ruby “Ninakwenda kujadiliana na Rais asubuhi ya leo namna ya kuunda timu ya watu kwa ajili ya operesheni hii” “Tafadhali na mimi niweke katika hiyo timu” akasema Ruby “Ruby ! akasema Mathew “Mathew ninaomba na mimi uniweke katika hiyo timu.Unanihitaji sana” akasema Ruby “Ni kweli ninakuhitaji sana Ruby lakini bado unatakiwa kuendelea kukaa kitandani ukiuguza majeraha” “Usihofu Mathew nitakuwa salama.Nilikuja hapa Tanzania kufanya kazi na si kulala kitandani.Ni kweli nina maumivu lakini hayaweza kunizuia kufanya kazi.Naomba Mathew tusiweke mjadala katika hilo.Ninao uwezo wa kufanya kazi hata kama niko kitandani” akasema Ruby na Mathew akamtazama “Nafahamu unachotaka kukisema na tafadhali usikiseme Mathew kwani mimi ninao uwezo wa kufanya kazi hata nikiwa nimelala kitandani.Operesheni kama hii inanihitaji mno” akasema Ruby “Sawa Ruby kwa kuwa umesisitiza mimi sina kipingamizi chochote.Nitakujum………… …” akanyamaza baada ya Gosu Gosu kuwasili “Vipi mambo yamekwendaje huko? Akauliza Mathew “Kila kitu tayari.Safari yao imekwisha na wapumzike kwa amani.Hakuna atakayewaona tena” akasema Gosu Gosu “Good job.Sasa nenda kaoge ujiweke tayari muda wowote tutaondoka hapa kuelekea katika shamba la Rais ambako ndiko ofisi yetu itahamia” “Tunaondoka hapa?akauliza Ruby “Ndiyo Ruby tunaondoka hapa tunakwenda sehemu salama zaidi” akajibu Mathew.









Kijua kilikwisha chomoza wakati gari mbili zilipofunga breki katika geti la nyumba ya Mathew.Hawa walikuwa ni watu waliotumwa na Rais.Mathew akawapokea na kuwakaribisha ndani akapewa maelekezo ya Rais. “Gosu Gosu utaongozana na hawa jamaa wawili mimi natakiwa kuwahi ikulu sasa hivi kuonana na Rais.Nitakapotoka huko nitakuja moja kwa moja kuungana nanyi.Gari langu utaondoka nalo” Mathew akampa maelekezo kisha akaingia katika mojawapo ya zile gari mbili akaondoka akiwaacha akina Gosu Gosu wakijiandaa kuondoka kuhamia katika makazi mapya. Hakukuwa na mazungumzo katika gari ile alilopanda Mathew hadi walipofika ikulu akapelekwa moja kwa moja kuonana na Rais “Mathew karibu sana nimefurahi kukutana nawe tena.Pole kwa kazi kubwa uliyoifanya usiku wa leo”akasema Dr Evanbs “Nashukuru sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew na Rais akamuelekeza kiti aketi “Mathew leo ni siku itakayokuwa ndefu sana kwangu,ratiba yangu inaonyesha nitakuwa na mfululizo wa vikao ndiyo maana nimeona nizungumze nawe kwanza kabla ya mambo mengine yoyote.Kabla hatujaendelea una hakika kila kitu kimekwenda kama tulivyokubaliana? akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais tumejitahidi sana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.Nakutoa hofu mheshimiwa Rais hakuna tatizo litakalotokea” “Yule balozi una uhakika naye hataweza kuwaeleza watu wake kile kilichotokea? “Hapana mzee hataweza kwani mke wake tunamshikilia sisi na nimekwisha muonya kama akifanya ujinga wa aina yoyote ile hatamuona tena mke wake.Kingine ambacho kitamlazimisha asiweze kutamka chochote ni woga hataki Israel wagundue kwamba yeye ndiye aliyetupa siri zote kuhusiana na Edger Kaka.Usiwe na hofu na balozi mheshimiwa Rais lazima atatupa ushirikiano wa kutosha” “Sawa Mathew kama una uhakika hakutakuwa na tatizo lolote ninakuamini” akasema Dr Evans “Ahsante sana mheshimiwa Rais” “Sasa tujielekeze katika jambo hili linalotukabili.Nimekuachia wewe kila kitu ukiendeshe katika suala hili nataka kusikia namna ulivyojipanga kulimaliza hili suala na hatimaye mwanangu na Olivia wapatikane” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais kama nilivyokueleza usiku kwamba ili kulimaliza suala hili tunatakiwa kumpata Edger Kaka ambaye amefichwa katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi” “Mathew suala hili bado linanipa ukakasi mkubwa.Ninataka kumpata Edger Kaka lakini si kwa kuvamia ubalozi wa Israel.Hili ni suala zito Mathew na ninasita hata kulikubali lifanyike kwani endapo ikijulikana basi kutakuwa na mzozo mkubwa wa kidiplomasia na tutakuwa tumepoteza rafiki mzuri sana wa nchi yetu.Hicho kinanipa hofu sana Mathew” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais Israel wanamshikilia Edger Kaka kwa sababu wanaamini ana mahusiano na kikundi cha IS na ndiyo maana walifanya operesheni ile kubwa ya siri na kumchukua wakaenda kumficha Nairobi katika ubalozi wao.Waliomteka Coletha ni mtandao huu wa akina Edger Kaka na tayari wanafahamu kuwa Edger Kaka yuko hai.Ili kuwapata Coletha na Olivia lazima tumpate Edger Kaka na hakuna namna nyingine ya kumpata Edger zaidi ya kuvamia ubalozi wa Israel.Hili ni suala kubwa mheshimiwa Rais ni sawa na kuvamia nchi lakini hatuna namna nyingine ya kufanya lazima tumpate Edger Kaka kwa gharama zozote zile.Ni mtu muhimu sana kwetu na kuna maswali mengi ambayo anapaswa kuyajibu.”akasema Mathew “Mathew hicho ulichokisema ni kitu ambacho kimenistua sana hata mimi kusikia kwamba Edger Kaka ana mahusiano na magaidi.Hakuna anayeweza kuamini jambo hili kwani Edger alikuwa mmoja wa wanasiasa vijana aliyejizolea umaarufu mkubwa sana hasa katika mapambano ya ufisadi.Alikuwa mstari wa mbele katika kuanika ufisadi na aliwataja mafisadi bila woga wowote.Inashangaza mno kusikia kwamba mtu kama huyu ambaye alionekana kama mkombozi wa taifa kumbe anashirikiana na magaidi.Ni kweli kuna mambo mengi ambayo tunahitaji kuyafahamu kutoka kwa Edger Kaka.” akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais nadhani umeona umuhimu wa kumpata Edger Kaka kwa gharama zozote” akasema Mathew “Nakubaliana nawe Mathew kwamba Edger ni mtu muhimu sana lakini njia ambayo umependekeza kuitumia kumpata ndiyo inayonipa hofu” “Mheshimiwa Rais kuna njia yoyote nyingine ambayo unadhani inaweza kutusaidia kumpata Edger Kaka?akauliza Mathew.Dr Evans akafikiri kidogo na kusema “Njia nyingine ya kufanya kumpata Edger ni kwa kufanya majadiliano na serikali ya Israel” akasema Dr Evans “Hapana mheshimiwa Rais hatuwezi kufanya hivyo.Israel hawapaswi kabisa kujua kama tayari tunafahamu Edger yuko hai ndiyo maana nashauri tufanye operesheni ya kimya kimya bila wao kujua.Mheshimiwa Rais operesheni hii si operesheni rahisi lakini lazima tuifanye na ninakuhakikishia nitaiongoza mimi mwenyewe na tutarejea hapa nchini tukiwa n Edger Kaka.Ninachohitaji ni ruhusa yako mheshimiwa Rais” “Mathew ninaomba nikueleze ukweli kijana wangu ninatamani sana kuruhusu operesheni hii ifanyike lakini bado ninahofu kubwa.Kwanza tunavamia ubalozi wa nchi nyingine ndani ya nchi ya jirani..Dah ! Dr Evans akashika kichwa “Mheshimiwa Rais muda unakwenda na mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe.Mimi sina namna nyingine ya kuweza kumpata Edger Kaka na ninaomba ufahamu kuwa bila kumpata Edger Kaka itakuwa vigumu sana kwetu kuwapata Coletha na Olivia Themba” akasema Mathew na kumpa nafasi Dr Evans akatafakari halafu akasema “Mathew let us do it” akasema Dr Evans lakini bado macho yake yalionyesha woga “Ahsante mheshimiwa Rais najua haya ni maamuzi magumu umeyafanya lakini yana faida kubwa kwa nchi” “Tell me how’re you going to do it?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais operesheni hii ni kubwa mimi na watu wangu hatuwezi kuifanya peke yetu.Tunahitaji kuongezewa nguvu” “Nguvu ya namna gani unaihitaji? “Nahitaji watu mahiri” “Watu wa aina gani unawahitaji Mathew?akauliza Dr Evans “Ninahitaji watu wenye mafunzo ya hali ya juu na uwezo wa kupambana kwani hii ni vita hivyo lazima watu wanaokwenda kufanya operesheni hii wawe na ujuzi mkubwa katika mapambano” “Nitakupa kikosi maalum cha wanajeshi ambao hutumiwa katika operesheni maalum.Unadhani watu wangapi watatosha katika operesheni hii?akauliza Dr Evans “Naomba niongezewe watu kumi ukijumisha na watu wangu nilionao jumla tutakuwa watu kumi na nne.Tunatosha kabisa kuvamia ubalozi wa Israel na kumchukua Edger Kaka.Operesheni itakuwa namna hii.Tutatanguliza kwanza majasusi kwenda nchini Kenya kufanya uchunguzi namna jengo lile la ubalozi wa Israel lilivyo,namna tunavyoweza kuingia ndani na mahala alipo Edger Kaka.Tukipata ramani nzima ya jengo hilo na tukifahamau namna ulinzi ulivyo basi tutafanya mazoezi namna ya kuweza kuingia ndani ya hilo jengo na kumchukua Edger.Tutahitaji helkopta mbili za kijeshi ambazo hazitoi mlio na hazionekani katika rada na zoezi la uvamizi litafanyika usiku wa manane” akasema Mathew na kunyamaza baada ya simu ya Rais kuita akaitoa mfukoni na kuipokea akazungumza halafu akamgeukia Mathew “Mathew nimetaarifiwa kuwa nina wageni ambao napaswa kuonana nao muda huu.Mpango wako nimeusikia ni mzuri na mimi niko tayari kutoa kila aina ya msaada unaohitajika.Kwa kuwa bado maandalizi yanaendelea nitakuomba tukutane tena jioni hapa hapa ikulu ili tuwe na mazungumzo mapana zaidi na unijuze mahala mlikofikia.Nafahamu operesheni hii inahitaji fedha hivyo basi nimeandaa kiasi Fulani cha fedha kwa ajili ya kuanzia kazi” akainuka akafungua kabati na kutoa sanduku jeusi “Humu kuna milioni mia mbili thelathini na tatu.Hizi ni kwa ajili ya kugharamia operesheni hii hivyo basi sehemu yoyote inayohitaji kutumia fedha msisite kutumia fedha na kama ikimalizika mniambie nitatoa nyingine.Mathew ninakukabidhi kila kitu na ninaamini kwamba mambo yote yatakwenda vyema na mwisho wa operesheni hii nataka Coletha na Olivia wapatikane.Naomba nisikucheleweshe nenda sasa hivi mkaanze maandalizi kwa ajili ya operesheni hii.Jioni tutakutana hapa nataka uje na taarifa ya vifaa vyote utakavyovihitaji ili nivifanyie maandalizi” akasema Dr Evans na kuagana na Mathew wakatoka ndani ya kile chumba cha mazungumzo ya faragha.Moja kwa moja Mathew akaelekea katika gari lililomleta na kuondoka. “Nadhani hii itakuwa ni moja kati ya operesheni zangu kubwa kabisa kuwahi kufanya tangu nimeanza kazi hii ya ujasusi” akawaza Mathew “Katika operesheni hii namuhitaji vile vile Tino.” akaendelea kuwaza Mathew na kumuelekeza dereva wa lile gari sehemu ya kwenda halafu akatoa simu na kumpigia Tino “Mathew kuna habari gani?akauliza Tino “Tino ninakuja hapo nyumbani kwako kukuchukua” “Kuna nini Mathew?akauliza Tino kwa wasi wasi “Usiogope Tino muda si mrefu nitafika hapo ni kwa ajili ya ile kazi imekuwa kubwa zaidi kidogo” akasema Mathew na kukata simu. Kwa maelekezo ya Mathew dereva wa lile gari alifika hadi nyumbani kwa Tino Mathew akashuka na kuingia ndani “Karibu sana Mathew.Kuna tatizo gani?akauliza Tino akiwa amesimama akionekna kuwa na wasiwasi “Usihofu Tino hakuna tatizo lolote lakini kuna operesheni nyingine imejitokeza ambayo ninakuhitaji uwepo” “Unanihitaji mimi? “Ndiyo Tino.Nakuhitaji sana katika operesheni hiyo” “Inahusiana na nini hiyo operesheni? “Sitaki kuzungumzia hapa lakini kwa ufupi tu ni kuhusiana na kwenda kumchukua Edger Kaka kutoka katika ubalozi wa Israel jijini Nairobi” akasema Mathew na kumtazama Tino “Tino hii ni operesheni nzito na ya hatari sana hivyo nahitaji sana msaada wako.We need to do this for our country” “Mathe……” “Tino please don’t say no! I need you in this brother ! Tino akafikiri kidogo na kusema “Fine ! akaenda chumbani kwake akavaa shati na kutoka wakaingia katika gari wakaondoka. Mathew na Tino walipelekwa moja kwa moja katika nyumba ya mapumziko ya Rais iliyoko nje kidogo ya jiji.Tayari akina Gosu Gosu walikwisha fika.Kulikuwa na wahudumu wawili wa kike na mmoja wa kiume na tayari daktari alikwisha wasili alikuwa anawahudumia Ruby na mke wa balozi “Karibuni” akasema Gosu Gosu wakaelekea ndani “Kila kitu kiko vizuri mahala hapa? Akauliza Mathew “Nimekagua kila kitu kiko safi.Kuna watumishi watatu hapa ndani kwa ajili ya kutuhudumia na vyumba vipo vya kutosha.Kuna ofisi http://deusdeditmahunda.blogspot.com/mbili ambazo tunaweza kuzitumia zenye vifaa vya kutosha ambazo huzitumia Rais.Vile vile kuna chumba cha tiba hapa ndani chenye vifaa vingi ambacho unaweza kukiita ni hospitali ndogo hii ni kwa ajili ya Rais endapo atapatwa na ugonjwa wakati akiwa hapa.Humo ndimo wanamohudumiwa akina Ruby hivi sasa kwa ujumla naweza kusema kwamba nyumba hii imekamilika ina kila kitu ambacho kitatuwezesha kufanya kazi zetu bila wasi wasi” akasema Gosu Gosu na kumzungusha Mathew kwa haraka haraka katika nyumba ile halafu wakarejea sebuleni Mathew akamtaka Gosu Gosu awaite watumishi wa ile nyumba wakafika mara moja “Ndugu zangu samahani kwa kuwatoa katika kazi zenu lakini nimewaiteni hapa kwa ajili ya kufahamiana.Yawezekana mkawa mnajiuliza maswali mengi kuhusiana na sisi ni akina nani.Mimi naitwa Mathew Mulumbi huyu mwenzangu hapa anaitwa Papii Gosu Gosu na huyu hapa anaitwa Tino.Tuko hapa kwa ajili ya kazi maalum tuliyotumwa na Rais na tutakuwepo hapa kwa muda wa siku kadhaa kisha tutaondoka.Naomba kuwajulisha kwamba kuna zoezi litakuwa linaendeshwa hapa kwa siku hizo chache tutakazokaa hapa hivyo msiwe na wasi wasi pale mtakapoona watu wakiingia na kutoka humu ndani ambao hamuwajui,msiwe na wasi wasi mkisikia mtu anapiga kelele za maumivu au mkiona mtu akipigwa au hata mkisikia mlio wa risasi.Mko salama na msihofu kitu.Endeleeni na shughuli zenu kama kawaida.Kama kutakuwa na lolote la kuwajulisha tutawajulisheni lakini ninawaomba jambo moja.Usiri.Chochote kile mtakachokiona ndani ya nyumba hii hakipaswi kutoka nje.Naamini tayari mnalifahamu hilo” akasema Mathew na kuwataka wale watumishi wakaendelee na majukumu yao kisha akawachukua akina Gosu Gosu wakaenda katika moja ya ofisi ya Rais “Ni muhimu kuwaweka sawa watumishi hawa ili wafahamu kile kinachoendelea na wasistuke siku wakiona mtu anakatwa kichwa humu ndani.Tuachane na hayo tuendelee na mambo yetu.Nimetoka kuonana na Rais tumezungumza japo si kwa urefu sana kwani ratiba yake kwa siku ya leo imembana mno.Kitu kikubwa ambacho Rais alitaka kusikia kutoka kwangu ni namna tulivyojipanga kuhakikisha tunawaokoa mwanae na Olivia kutoka katika mikono ya magaidi wanaowashikilia hivi sasa.Nilimuweka wazi Rais kwamba njia pekee ya kuwapata watu hao ni kwanza tumpate Edger Kaka ambaye ana mahusiano na watu hao na kumpata Edger Kaka lazima tuvamie ubalozi wa Israel nchini Kenya ambako ndiko amefichwa.Ndugu zangu kuvamia ubalozi wa nchi nyingine tena ndani ya nchi nyingine ni jambo ambalo lina athari kubwa sana kidiplomasia lakini hatuna namna nyingine ya kufanya kumpata Edger Kaka zaidi ya kuvamia ubalozi huo.Baada ya majadiliano,Rais akakubali tufanye operesheni hiyo lakini akatoa angalizo kwamba tujitahidi kuifanya kwa umakini mkubwa sana na yeye yuko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha operesheni hii inafanikiwa.Ameahidi kutupatia makomandoo wa kikosi maalum cha jeshi ambao hutumiwa katika operesheni maalum hivyo tutakuwa na nguvu ya kutosha.Tutakuwa jumla watu kumi na nne kwani Ruby naye ameomba ajumuishwe katika operesheni hii lakini yeye atakuwa na kazi yake maalum kama mnavyojua yeye ni mtaalamu wa kompyuta kwa hiyo atakaa katika idara ya mawasiliano.Tutatumia helkopta za kikosi cha jeshi kinachohusika na operesheni maalum ambazo ni za kisasa hazina mlio wala haziwezi kuonekana katika rada” akanyamaza kidogo “Kitu kikubwa cha kwanza ambacho tunatakiwa kufanya ni kulifahamu vyema jengo hilo la ubalozi namna lilivyo ili tuweze kujipanga namna ya kuingia na kumchukua Edger.Tunatakiwa kuipata ramani ya jengo zima,kufahamu mfumo mzima wa ulinzi ulivyo ndani na nje ya jengo na jambo la tatu kubwa ni kufahamu mahala alipofichwa Edger Kaka.Hii ndiyo kazi kubwa ya kwanza tunayotakiwa kuifanya ambayo itatupa urahisi wa kuweza kuingia ndani ya jengo hilo” akasema Mathew “Uko sahihi Mathew operesheni nzima inategemea sana kama tutafaulu kulifahamu jengo hilo namna lilivyokaa na mpangilio wote wa ulinzi” akasema Tino. “Kufuatia nchi ya Kenya kuandamwa na mfululizo wa matukio ya kigaidi mara kwa mara ulinzi katika balozi mbali mbali hasa za nchi ambazo zimekuwa zikipambana na vikundi vya kigadi kwa muda mrefu kama Marekani na Israel umeimarishwa sana.Naamini jengo hilo litakuwa na teknolojia ya hali ya juu sana ya ulinzi hivyo ili tuufahamu mfumo mzima wa ulinzi hatuwezi kuwakwepa Mossad.Lazima tupate mtu ndani ya Mossad ambaye anaweza akatusaidia kutupa taarifa zote za mfumo mzima wa ulinzi ulivyo katika ubalozi huo” akasema Tino “Tino jambo unalolisema ni sahihi na ninakubaliana nalo lakini upo ugumu wa kumpata mtu ndani ya Mossad ambaye anaweza akatusaidia kupata taarifa nyeti kama hiyo.Ukumbuke Edger amehifadhiwa pale hivyo ni sehemu ambayo wanaitazama kwa macho matano” akasema Mathew “Kwa nini tusipandikize mtu ndani ya Mossad ambaye atatumika kama kirusi cha kuchota taarifa? akauliza Gosu Gosu. “Hilo nalo ni wazo zuri.Kama hatuwezi kumpata mtu ndani ya Mossad basi tupandikize wa kwetu” akasema Tino “It’s not that simple guys na inahitaji muda wa kutosha hadi mtu huyo kufanikiwa kumpandikiza mtu huyo ndani ya Mossad na sisi hatuna muda huo” akasema Mathew “Mathew nadhani nimepata jibu.Devotha” akasema Gosu Gosu “What?! Akauliza Mathew kwa ukali kidogo “Mathew najua hili halipenyi vyema katika masikio yako lakini tunaye mtu ambaye tunaweza kumtumia katika operesheni hii na akatusaidia sana ambaye ni Devotha” akasema Gosu Gosu.Mathew akatoa kicheko kidogo “Gosu Gosu umetoa wapi wazo kama hilo?Yaani tumshirikishe tena Devotha katika mipango yetu?That woman is a devil.She shot Ruby three times,she nearly killed her nitawezaje kumsamehe mtu kama huyu?Nitawezaje tena kumjumuisha mtu kama huyu katika timu yangu?Hakuna namna ninayoweza kufanya naye kazi tena na nimeweka kiapo popote nitakapomuona Devotha I’ll kill her ! akasema Mathew “Mathew wewe ni kaka yangu ni kiongozi wangu na ninakuheshimu sana.Sijawahi kukupinga katika jambo lolote,kila ulichonielekeza nimekifanya.Nafahamu unao ujuzi mkubwa sana katika mambo haya zaidi yangu.Mimi ni mwanajeshi tu na kazi yangu ni kupigana vita lakini kwa mara ya kwanza naomba unikubalie na mimi hiki ninachokisema ambacho ninaamini kinaweza kuleta mchango mkubwa katika operesheni hii.Nafahamu alichokifanya Devotha kinaumiza sana na hata mimi nina hasira naye lakini tunaweza kuweka pembeni tofauti zetu kwa muda na tukaungana kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya nchi na baada ya kumaliza kazi ndipo tukaendelea na mambo yetu binafsi.Samahani Mathew kama nitakuwa nimekukwaza kwa mawazo haya” akasema Gosu Gosu “Nadhani Papii amesema kitu cha msingi sana.Kama mwanamke huyo anayemzungumzia anaweza akawa na msaada katika operesheni hii basi nashauri ajumuishwe kama itaonekana inafaa.Hii operesheni ni kubwa sana na kila ambaye anaweza kuwa na msaada hata wa kupeleka karatasi muhimu sehemu Fulani basi atumike.Mathew naungana na Papii kukuomba kama utaona inafaa mwanamke huyo ajumuishwe katika operesheni hii” akasema Tino “Kwa nini alitaka kumuua Ruby?Alimkosea nini?Hili jambo limeniumiza sana na kumfanya Devotha awe ni adui yangu mkubwa.Ruby hakustahili kufanyiwa ukatili mkubwa kama ule” akasema Mathew “Mathew ninayafahamu haya yote na unayo haki ya kuwa na hasira na Devotha hata mimi nina hasira naye sana lakini kwa sasa lazima tukubali kwamba tunamuhitaji sana.” Akasema Gosu Gosu na Mathew akamtazama kwa macho makali “Gosu Gosu kwa nini unadhani tunamuhitaji Devotha katika operesheni hii?akauliza Mathew “Devotha ni wakala wa Mossad hivyo itakuwa rahisi kwake kuweza kuchota taarifa za mfumo wa ulinzi ulivyo katika ubalozi wa Israel pamoja na mahala alipo Edger Kaka ndani ya ubalozi huo.Hivi ndivyo tutakavyomtumia.Tutamtum a Devotha kwenda Nairobi.Akiwa kule Devotha ataomba kuonana na mkuu wa Mossad pale Kenya na hapo ndipo atakapotumia ujuzi na uzoefu wake kuchota taarifa zile tunazozihitaji.Simfahamu vyema Devotha lakini kwa namna nilivyofanya naye operesheni ile ya kuja kukukomboa ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa sana” akasema Gosu Gosu.Ilimchukua Mathew zaidi ya dakika mbili akitafakari halafu akasema “Sawa nimekuelewa Gosu Gosu.Japo moyo wangu haufurahii jambo hili lakini inabidi tulifanye kwa manufaa ya taifa.Kama tukitaka kumpata Devotha lazima tumtumie balozi Dr Yonathan.Yeye amekuwa akiwasiliana naye kwa kutumia mfumo wao wa mawasiliano.Baadae saa nne ninakwenda kukutana na balozi Samawati beach hotel.Pale pametulia sana na ninafahamika ni hoteli ya mmoja wa marafiki zangu.Nitamuelekeza balozi amjulishe Devotha naye afike hapo hotelini kabla yeye hajafika hapo na akishafika tutamalizana naye.Tino wewe utakwenda kushughulikia tiketi tatu za ndege ya saa saba mchana inayoelekea Nairobi.Mtasafiri nyote watatu wewe,Gosu Gosu na Devotha” akasema Mathew “Hakuna tatizo katika hilo” akajibu Tino.Mathew akachukua simu na kupigia Samawati beach hotel akaweka oda ya chumba akapewa chumba namba 98 halafu akampigia balozi Dr Yonathan “Hallow Mathew” akasema Dr Yonathan baada ya kupokea simu “Dr Yonathan nimekupigia kukukumbusha kwamba saa nne za asubuhi natakiwa kukutana nawe Samawati beach hotel” “Ninakumbuka Mathew kwamba nina miadi ya kuonana nawe mida hiyo” “Vizuri sana kama unakumbuka.Jambo lingine ninamuhitaji Devotha” akasema Mathew “Devotha? Dr Yonathan akauliza kwa mshangao “Ndiyo namuhitaji Devotha.Nataka utumie njia zako mnazotumia kuwasiliana na umtake afike Samawati beach hotel chumba namba 98 saa tatu na nusu mwambie una mazungumzo naye” “Sawa Mathew nitafanya hivyo.Vipi mke wangu anaendeleaje? “Usihofu anaendelea vyema kabisa hana tatizo lolote anapatiwa huduma nzuri” akajibu Mathew na kukata simu. “Tino wewe utakwenda kushughulikia hizo tiketi mimi na Gosu Gosu tutakwenda Samawati beach hotel kuonana na balozi na Devotha.Utatumia gari langu,sisi tutatumia gari la hawa wasaidizi wa Rais” akasema Mathew na kwenda katika chumba walimo Ruby na mke wa balozi.Kilikuwa ni chumba kikubwa ambacho kilionekana kama hospitali ndogokwani kulisheheni vifaa vya kila aina vya matibabu “Ruby” akasema Mathew akitabasamu baada ya kumkuta Ruby akiwa amekaa kitandani.Mathew akasalimiana na Daktari Yule aliyekuwa anawahudumia akina Ruby.Mke wa Dr Yonathan alipomuona Mathew alipatwa na mstuko mkubwa akashindwa kujizuia kuanza kulia.Mathew hakumjali akamfuata Ruby “Unaendeleaje Ruby?akauliza “Ninaendelea vizuri Mathew kama unavyoniona” “Sawa Ruby endelea kupumzika ninatoka kidogo nitakaporejea nitakuwa na mazungumzo marefu nawe” akasema Mathew “Mathew unakwenda wapi?Hapa ni wapi tulipoletwa? “Hapa ni sehemu salama sana kwa wakati huu Ruby usiwe na hofu yoyote hata nisipokuwepo” akasema Mathew “Mathew tayari umempata Yule shetani?akauliza Ruby “Usihofu Ruby mambo yanakwenda vyema nitakaporejea nitakuw na mengi ya kukueleza” akasema Mathew akambusu Ruby katika paji la uso akamuaga na kutoka mle chumbani akimuacha mke wa balozi akitetemeka.Mathew akazungumza na walinzi akawataka wahakikishe hakuna mtu yeyote kati ya Ruby au mke wa balozi anatoka ndani ya nyumba ile.Wakaingia garini na kuondoka “Hili wazo la kumshirikisha Devotha katika operesheni hii litamuumiza sana Ruby hata hivyo kama Devotha ataonekana kuwa na msaada kwetu hakuna ubaya tunaweza kumtumia halafu mimi na yeye tutamalizana baada ya operesheni hii kumalizika” akawaza Mathew wakiwa garini. ****************** Boti tatu ndogo za mwendo kasi zilikaribia jiji la Mombasa.Tayari ilikaribia saa tatu za asubuhi.Boti hizi zilikuwa zinatokea Pemba nchini Tanzania ambako walikwenda kwa ajili ya kazi maalum.Hiki kilikuwa ni kikosi kilichotumwa kwenda Tanzania kuwachukua Olivia Themba na Coletha.Mawasiliano yalikuwa makubwa kati ya wale jamaa waliokuwa katika zile boti na wenzao waliokuwa wanawasubiri sehemu Fulani kabla ya kufika jiji la Mombasa.Sehemu Fulani nje ya bahari walikuwepo watu kadhaa wakiwasubir wenzao waliokuwa wakija na zile boti.Kwa kufuata maelekezo waliyokuwa wanapewa na wenzao watu wale waliziongoza boti zao kuelekea ufukweni halafu boti zikasimama wakashuka watu na kuwashusha wanawake wawili waliokuwa wamefunikwa mifuko kichwani.Wakawatoa nje wakawakabidhi wanawake wale kwa wale jamaa waliokuwa nje wakiwasubiri na bila kupoteza muda wanawake wale wakaingizwa katika helkopta iliyokuwa mita chache kutoka ufukweni.Watu wawili kutoka katika zile boti nao wakaingia katika helkopta ile ikapaa na kuondoka kuelekea Nairobi TANZANIA Gosu Gosu aliyekuwa amejibanza sehemu fulani katika hoteli ya Samawati aliyaelekeza macho yake katika maegesho alimuona mwanamke mmoja mwenye umbo lenye la kumtoa udenda rijali yeyote akishuka kutoka ndani ya gari na kuanza kuelekea katika jengo la hoteli.Haraka haraka akachukua simu na kumpigia Mathew “Gosu kuna chochote huko?akauliza Mathew “Devotha amefika tayari na anapanda huko juu” “Good” akajibu Mathew Devotha aliingia katika lifti na kuelekea ghorofa ya nne kilipo chumba namba 98.Gosu Gosu naye akatoka katika mahala alipokuwa amejificha akaenda kupanda lifti nyingine naye akaelekea ghorofa ya nne alipo Mathew. Milango ya lifti ikafunguka ghorofa ya nne na Devotha akashuka kisha akaanza kutembea huku akiangalia namba za vyumba akikitafuta chumba namba 98.Siku hii alikuwa amevaa sketi ya jeans rangi nyeupe iliyomkaa vyema na fulana nyepesi ya rangi nyeupe iliyoubana mwili wake na kukifanya kifua chake kizuri kionekane vyema.Alikuwa amependeza sana.Alifika hadi chumba 98 akabonyeza kengele.Mathew aliyekuwa ndani ya chumba akachungulia katika kitundu kidogo kilichopo mlangoni akamuona Devotha.Mwili wote ukafura kwa hasira.Kwa kasi ya umeme akaufungua mlango na kumvuta ndani Devotha ambaye hakuwa amejiandaa kwa lolote akiamini kwamba anakwenda kukutana na Dr Yonathan,Mathew akaupiga mlango teke ukajifunga halafu akamkaba shingo Devotha akamgandamiza ukutani. “Hatimaye nimekupata shetani wewe !! akasema Mathew kwa hasira akiwa ameiweka bastora kichwani kwa Devotha ambaye mwili wote ulikuwa unamtetemeka. “Mathew ! akaita Gosu Gosu baada ya kuingia mle ndani na kumkuta Mathew akiwa amembana Devotha ukutani huku bastora ikiwa kichwani “Mathew please brother ! akasema Gosu Gosu “I promised to kill this witch and I have to fulfill my promise !! akasema Mathew akiwa ameuma meno kwa hasira.Gosu Gosu aliingiwa na hofu kubwa kwa hasira alizokuwa nazo Mathew. “Mathew ukimuua tutakosa kila kitu.We need her so much.Please don’t kill her ! akaomba Gosu Gosu.Mathew akamtazama halafu akamuachia Devotha akainama akikohoa mfululizo.Gosu Gosu akamfuata “Take a deep breath !! akamwambia Devotha ambaye alivuta pumzi ndefu haraka haraka.Bado Mathew alikuwa amesimama kati kati ya kile chumba akiwa na hasira. “Take a sit ! Gosu Gosu akamuelekeza Devotha aketi halafu akamsogelea Mathew “Mathew nadhani tungemalizana kwanza na Devotha kabla ya balozi hajafika” akasema Gosu Gosu kwa adabu.Mathew aliyekuwa amegeukia dirishani akageuka na kumtazama Devotha kwa hasira “Ulifikiria nini Devotha kumpiga risasi Ruby ?Alikukosea nini? Ulifikiri sintakupata? Devotha nakuhakikishia njia pekee ya kunikwepa mimi ni kufa.Kama uko hai ndani ya dunia hii nikiamua kukusaka ni lazima nikupate.Anyway tuyaweke pembeni hayo kwanza tuzungumze mambo ya msingi.” Akasema Mathew na kuiweka bastora yake pembeni. “Sifahamu nianzie wapi” akasema Mathew na kumtazama Devotha ilionyesha wazi kwamba hakuwa ameridhika kumuacha Devotha bila kumfanya chochote. “Edger Kaka ni kweli yuko hai” akasema Mathew na mstuko ukaonekana usoni kwa Devotha “Yuko hai?akauliza “Ndiyo_Olivia alikuwa sahihi kabisa.Edger Kaka yuko hai”akasema Mathew huku hasira zikionekana kuanza kupungua “Hata mimi nilihisi hivyo.Msisitizo aliouonyesha Olivia ni mkubwa.Yuko wapi Edger?Tayari mnafahamu mahala alipo?akauliza Devotha “Ndiyo tunafahamu mahala alipo” akajibu Mathew “Good.Sasa sikiliza Mathew.Nilizungumza na Olivia na akanihakikishia kwamba ana siri kubwa ambayo atanieleza endapo nitampa taarifa za mahala alipo Edger Kaka nadhani sasa ni wakati wa kuifahamu siri hiyo kubwa”akasema Devotha “I’m sorry Devotha unaonekana uko nyuma ya wakati sana.We don’t have Olivia”akasema Mathew “Olivia alichukuliwa na Rais jana usiku na tuk…” “Olivia hayuko kwa Rais” akasmea Mathew na kumkatisha Devotha “What do you mean?akauliza Devotha “Nadhani unafahamu jana usiku magaidi walifanya shambulio katika hospitali ya Mtodora.Mlengwa mkuu wa shambulio lile alikuwa ni Coletha mtoto wa Rais ambaye walifanikiwa kumchukua na kuondoka naye.Rais alipigiwa simu akajulishwa juu ya jambo lile na akaonywa afuate kila atakachoelekezwa ama sivyo mwanae atapoteza maisha.Kitu cha kwanza walichokihitaji magaidi wale ni Olivia Themba.Rais kwa kuwa alihitaji kumpata mwanae akalazimika kuwapatia kile walichokihitaji hivyo Olivia Themba yuko katika mikono ya magaidi hivi tunavyozungumza na hatujui yuko wapi” “Bastard !! akasema Devotha kwa hasira “Kwa nini Rais akafanya jambo kama hilo?Kwa nini akawakubalia magadi kile wanachokitaka?akauliza kwa ukali “Hakuwa na namna nyingine ya kufanya.Anahitaji kumuokoa mwanae na mtu yeyote angekuwa mahala pake angefanya kama vile alivyofanya Rais” akasema Mathew “So what’s going on now?akauliza Devotha “Devotha nataka kwanza utambue tayari tunafahamu kuwa wewe ni wakala wa Mossad hapa nchini”akasema Mathew Uso wa Devotha ulionyesha mstuko mkubwa sana “Mmef..fah…Oh my God ! Devotha akababaika “Jana usiku ulikwenda kuonana na balozi wa Israel Dr Yonathan Cohen katika ubalozi wa Israel hapa nchini na kikubwa kilichokupeleka kule ni kwenda kukutana na majasusi wawili wa Mossad waliotumwa Tanzania kwa kazi maalum ya kuandaa operesheni ya kumtafuta Olivia na wewe kama wakala wao wanakutumia katika kuwasaidia kuandaa operesheni hiyo” akasema Mathew bado sura ya Devotha ilikuwa katika mshangao.Hakutegemea kama akina Mathew wangeweza kufahamu jambo lile. “It’s not true ! akasema Devotha. “BRAVO 15E 361 A ndiyo namba yako ya utambulisho.Devotha we know everything about you.Hakuna siri tena.Naomba tusipoteze muda kubishana jambo hilo.Ninachotaka unieleze ni je majasusi wale walikueleza sababu ya kumtafuta Olivia Themba?akauliza Mathew.Zilipita sekunde kadhaa Olivia akasema kwa sauti ndogo “Hapana hawakunieleza.Niliwahoji sababu za kumtafuta Olivia lakini hawakutaka kuniweka wazi kwa nini wanamtafuta” akasema Devotha “Sawa.Hawakutakakuku weka wazi kwa sababu anayemuhitaji Olivia ni Edger Kaka” “What? Sijakuelewa una maanisha nini Mathew” “Japokuwa wewe ni wakala wa Mossad lakini hulifahamu jambo hili.Akiwa katika matibabu nchini Israel Edger Kaka alitembelewa na watu wawili ambao wanatafutwa na Mossad kwa muda mrefu kwa kufadhili kundi la IS na vikundi vingine vinavyofanya mashambulizi katika ardhi ya Israel na kuua watu.Mossad ndio waliotengeneza ajali ile ambayo ilituaminisha kwamba Edger amefariki dunia lakini kumbe bado yuko hai” akasema Mathew “Oh my God ! akasema Devotha akionekana kushangazwa sana na taarifa zile “Baada ya kumchukua Edger Kaka usiku ule walimpeleka kumuhifadhi katika ubalozi wa Israel nchini Kenya ambako yuko hadi hivi sasa.Kufuatia mfululizo wa matukio ya kurusha maroketi yanayofanywa na vikundi vya wanamgambo wa kipalestina katika ardhi ya Israel ambayo yamesababisha vifo vya wanafunzi kadhaa na walimu,walitumwa majasusi wawili kwenda nchini Kenya kumuhoji Edger kwani wamemuweka pale kwa muda wa miaka mitatu bila kumuhoji chochote.Katika mahojiano hayo Edger Kaka alikuwa tayari kuwaeleza Mossad kila kitu wanachokihitaji kwa sharti la kuhakikisha wanampata Olivia.Anadai kwamba anampenda Olivia na ndiye mwanamke anayetaka kuishi naye.Hiyo ndiyo sababu ya Mossad kuja kumtafuta Olivia nchini Tanzania”akasema Mathew “Binafsi sikuwa tayari kuwasaidia Mossad kumpata Olivia kwani ninafahamu umuhimu wake kwetu na hata taarifa nilizowapa hazikuwa za kweli.Niliwaahidi kuwasaidia lakini sina mpango huo wa kuwasaidia badala yake ninatafuta namna ya kufanya ili mpango wao huo usifanyike hapa nchini”akasema Devotha “Huna haja ya kuwa na wasiwasi nao tena.They’re gone” akasema Mathew “Gone?Where?akauliza Devotha “Dead.We killed them” “Jesus Christ ! You killed them? “Yes we did” akajibu Mathew “Ahsanteni sana kwa jambo hilo kubwa mlilolifanya ila hili ni tangazo la vita.Mossad watawawinda usiku na mchana hadi wahakikishe wamewapata watu waliowaua majasusi wao.Mathew mmeingia katika hatari kubwa sana”akasema Devotha “Tunajua,lakini hawatafahamu chochote kuhusiana na suala hilo kwani tayari limekwisha shughulikiwa kikamilifu” “Mathew samahani naomba nipewe nafasi ya kuuliza swali.Mmewezaje kufahamu mambo haya yote hadi kuwaua wale majasusi?Ni vipi mtafanya ili Mossad wasiweze kugundua kama majasusi wao wameuawa? Ninauliza hivyo kwa sababu mimi kama wakala wao lazima nitaulizwa mahala walipo Fishel na Ehud.Moja kwa moja tayari na mimi nimekwisha ingia katika hili jambo japo sikufanya mauaji hayo” akasema Devotha “Devotha hayo mambo mengine hayana umuhimu mkubwa.Akili na nguvu zetu zote tuapaswa kuvielekeza katika kuwatafuta Olivia na Coletha ambao hatujui mahala walipo hadi hivi sasa.Ili kuwapata akina Olivia lazima kwanza tuhakikishe tumempata Edger Kaka.Kuna njia moja tu ya kumpata Edger Kaka nayo ni kwa kuvamia ubalozi wa Israel nchini Kenya ambako ndiko amefichwa” “Mathew mnataka kuanzisha vita ! akasema Devotha “Thay started this war.Tunachokifanya sisi ni muendelezo wa kile walichokianzisha wao.Waliingia katika ardhi yetu wakaua na kuteka raia wetu wakiamini jambo hili litabaki siri na hatutalifahamu.Edger Kaka ni raia wetu ambaye ametekwa hivyo kila aina ya mbinu itatumika kumrejesha nyumbani na mbinu pekee ambayo inatakiwa kutumika kwa sasa ni kuvamia ubalozi wa Israel nchini Kenya na kumchukua na hapo ndipo wewe unaingia” akanyamaza Mathew akamtazama Devotha kisha akaendelea “Tunaandaa kikosi kabambe kitakachofanya operesheni ya aina yake ya kumchukua Edger.Kitu kikubwa kabla ya yote ambacho kitatuwezesha sisi kufanikisha operesheni hiyo ni kupata ramani ya jengo hilo lilivyo na vile vile kufahamu mfumo mzima wa ulinziulivyo na tatu tunatakiwa kufahamu alipo Edger Kaka ndani ya ubalozi huo.Tulihitaji kupandikiza mtu ndani ya Mossad lakini muda tulio nao ni mfupi sana ndiyo maana tukaamua kukutumia wewe ambaye tayari una mahusiano na Mossad” akasema Mathew. “Nini mnataka nikifanye?akauliza Devotha “Unakwenda Nairobi.Nataka ukatafute ramani ya jengo la ubalozi wa Israel nchini Kenya,mfumo wote wa ulinzi wa ubalozi huo na mahal alipofichwa Edger.Tumekuchagua wewe kwa kuwa tayari ni mtu wao wa karibu unawasiliana nao hivyo ni rahisi kuweza kuingia kati kati yao na kupata taarifa tunazozihitaji.Naomba ufahamu Devotha kwamba katika operesheni hii tunakutegemea sana.Ukishindwa kufanikiwa utakuwa umetuangusha sisi,umemuangusha Rais na umewaangusha pia watanzania kwani operesheni hii tunaifanya kwa ajili ya Tanzania hivyo nakuomba ufanye kila unaloweza kulifanya ili kupata taarifa hizo.Naomba utambue vile vile kwamba Rais Dr Evans ndiye aliyetoa kibali cha kufanyika kwa operesheni hii hivyo utaona namna ilivyo muhimu.Rais yuko pamoja nasi na ametutuma tuifanye kazi hii kwa niaba ya watanzania” akasema Mathew “Ni kweli mimi nina ukaribu na Israel kupitia shirika lao la ujasusi la Mossad na ninawaahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha ninazipata taarifa hizo.Makao makuu ya Mossad kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki yapo katika ubalozi wao nchini Kenya na ninafahamiana sana na Avi mkuu wa Mossad kwa ukanda huu.Nimekuwa nikiwasiliana naye mara kwa mara.Ninaamini kupitia kwake tutaweza kupata kila kitu tunachokihitaji.Mawazo yangu bado ni kwa wale majasusi wawili mliowaua.Nina wasiwasi kukosekana kwao kunaweza kuharibu kila kitu ninaweza kuulizwa maswali kuhusu wao nikashindwa kujibu”akasema Devotha “Usihofu Devotha.Balozi wa Israel Dr Yonathan Cohen yuko na sisi katika operesheni hii” “Yuko nasi?Kivipi? “Ni hadithi ndefu lakini fahamu kwamba yuko upande wetu.Yeye ndiye atakayesimamia suala la wale majasusi wawili kila taarifa zao zitakapotakiwa.Wewe ukiulizwa utasema kwamba kuna tetesi kwamba Olivia baada ya kutekwa amepelekwa jijini Arusha hivyo basi majasusi hao nao wamekwenda jijini Arusha kufanya uchunguzi.Balozi Dr Yonathan yeye ataendelea kuwahakikishia Mossad kwamba ana mawasiliano ya mara kwa mara na majasusi hao wakiwa jijini Arusha hadi pale tutakapomaliza operesheni yetu ambapo balozi atadai kuwa mawasiliano yamekatika ghafla na hajui kama majasusi hao wako salama” “Mmewezaje kumuingiza balozi Dr Yonathan katika suala hili?akauliza Devotha “Utafahamu hapo baadae lakini kwa sasa kama nilivyokueleza awali kwamba tujielekeze katika kuhakikisha operesheni hii inafanikiwa” akasema Mathew. “Sawa Mathew mimi niko tayari.Lini ninatakiwa kwenda huko Nairobi? “Unaondoka baadae leo.Utaambatana na Gosu Gosu na Tino” “Tino?Who is he? “Utamfahamu baadae.Kwa pamoja mtaunda timu ambayo mtahakikisha mnafanikiwa kuipata ramani hiyo ya jengo la ubalozi wa Israel na mtakuwa mkiwasiliana nasi huku Dar es salaam kwa kila mnachokifanya.Tino ni mtaalamu sana wa mawasiliano na atatuunganisha sisi na ninyi huko Nairobi” akanyamaza Mathew baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni balozi Dr Yonathan “Hallo balozi” “Mathew tayari nikefika hapa hotelini uliponielekeza tuonane” akasema Dr Yonathan “Njoo moja kwa moja chumba namba 98 ghorofa ya nne” akaelekeza Mathew “Devotha kabla sijasahu naihitaji ile kompyuta ambayo uliichukua kutoka kwa Ruby” akasema Mathew. “Guys I don’t know how to say this but I’m sorry.Nilichokifanya ni kitu kibaya na hata mimi mwenyewe ninakijutia.Sifahamu akili yangu ilikuwa inawaza nini hadi nikafanya kitendo kile.Naombeni sana mnisamehe” akasema na kumtazama Mathew “Is she….” “She’s not dead.Tumepambana kwa kila tulivyoweza na Mungu amesikia maombi yetu na kumrejeshea uhai ila tayari alikwisha chungulia kaburi” “Please forgive me Mathew” “Sifahamu nitaanzia wapi kukusamehe Devotha kwa hiki ulichokifanya.Umeniumiza sana.Hujui ni kwa namna gani Ruby alivyo mtu wangu wa muhimu.Lakini hayo yote tuyaweke pembeni kwanza naomba ukafanye kazi niliyokuag…………” Mlango ukagongwa na Mathew akanyamaza.Gosu Gopsu akainuka kwenda kuufungua,alikuwa ni balozi Dr Yonathan.Devotha akatazamana na Dr Yonathan “Huyu Mathew ni mtu wa kuogopwa sana.Amewezaje kumdhibiti balozi na kumfanya afanye kila anachomuamuru?Sikutegem ea kabisa kama angeweza kugundua jambo kama hili la mimi kuwa wakala wa Mossad lakini tayari anafahamu kila kitu hadi namba yangu ya utambulisho.Licha ya hilo ameweza vile vile kuwaua Ehud na Fishel.Huyu si mtu wa kawaida napaswa kumuogopa sana.Tayari amekwisha niandika kwa kalamu nyekundu hivyo napaswa kuwa makini sana kufuata maelekezo yake vinginevyo he’s going to kill me ! akawaza Devotha “Balozi karibu sana.Ahsante umefika kwa wakati tuliokubaliana.Nataka kufahamu huko utokako nini ninaendelea?Kuna tatizo lolote kuhusiana na kile kilichotokea jana? akauliza Mathew “Mpaka sasa kila kitu ni shwari kabisa.Hakuna tatizo lolote.Nimewasiliana na mamlaka za juu na kuwajulisha kwamba huku kila kitu kinakwenda vyema”akajibu balozi “Vipi kuhusu wale majasusi wawili?akauliza Mathew “Ehud na Fishel walipofika hapa nchini walifikia katika hoteli na baadae ndipo wakaja ubalozini ambako tuliwapa nyumba inayotumiwa na wageni wanaofika ubalozini hapo hivyo hawakuwa wamerudisha vyumba vyao.Wakati ninakuja huku nimepita katika hoteli walikofikia kuwafahamisha kwamba wageni wale hawatarejea tena pale hotelini na nikalipa kiasi chote cha fedha walichokuwa wanadaiwa.Viongozi wa Mossad niliwasiliana nao asubuhi ya leo nikawajulisha kwamba watu wao wanaendelea na maandalizi ya operesheni na wameelekea Arusha” akasema Dr Yonathan “Vizuri.Nafurahi kama mambo yamekwenda vyema” akasema Mathew “Vipi mke wangu anaendeleaje? Akauliza balozi “Yuko vizuri usihofu” akajibu Mathew “Balozi nimekuita hapa kuna mambo ambayo tunataka utusaidie”akasema Mathew na kumtazama balozi halafu akaendelea “Israel kwa kutumia shirika lao la ujasusi la Mossad walivamia ardhi yetu wakaua na kuteka raia wetu wakampeleka mafichoni.Walifanya kitendo kibaya sana na kama haitoshi wanajiandaa tena kuvamia ardhi yetu na kufanya operesheni nyingine ya kumteka raia mwingine wa Tanzania na kumtorosha na hatujui katika operesheni hiyo watanzania wangapi watapoteza maisha yao.Israel ni marafiki zetu lakini kwa hiki walichokifanya hatukubaliani nacho hata kidogo.Mheshimiwa balozi tunamuhitaji mtu wetu aliyetekwa na Israel na kwenda kufichwa katika ubalozi wenu nchini Kenya.Hatuhitaji majadiliano yoyote kwani wao wakati wakimchukua hawakujadiliana nasi hivyo na sisi tunataka kumchukua kama wao walivyomchukua yaani kimya kimya” akanyamaza akamtazama balozi aliyekuwa kimya akimsikiliza halafu akandelea “Nafahamu umuhimu wa Edger Kaka kwa Israel lakini huyu ni raia wa Tanzania na tunamuhitaji vilevile hasa kwa wakati huu hivyo basi tunaandaa operesheni ya kwenda kumchukua mahala alikohifadhiwa jijini Nairobi katika ubalozi wenu na tunahitaji msaada wako” Dr Yonathan alijitahidi kuficha woga alioupata lakini vidole vyake vilikuwa vinatetemeka.Mathew aliligundua hilo lakini hakumjali “Devotha ambaye ni wakala wa Mossad anakwenda jijini Nairobi ambako atakutana na mkuu wa Mossad katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ndugu Avi.Tunamtuma Devotha kwa kazi maalum katika ubalozi huo hivyo atahitaji msaada wako pale atakapohitaji”akanyamaza tena akamtazama balozi “Devotha atamjulisha Avi kwamba majasusi wale wawili wa Mossad wako jijini Arusha na Avi akikuuliza utamthibitishia hivyo kwamba kweli wako Arusha.Ukumbuke bado tunakufuatilia Dr Yonathan na kosa moja utakalolifanya litagharimu uhai wa mke wako na wewe pia.Hii ni operesheni ya kitaifa na lazima ifanikiwe kwa gharama zozote zile na kumrejesha Edger Kaka Nyumbani.Umenielewa? akasema Mathew “Kwa upande wangu nina wasiwasi mkubwa na hicho mnachotaka kukifanya.Ninawashauri msikifanye kwani ni hatari kubwa na kitazidi kuyaweka mahusiano ya nchi zetu mbili katika mashaka makubwa.Serikali ya Israel wakigundua hiki mlichokifanya mtajiletea matatizo makubwa ninyi na taifa lenu.Nawahakikishia kwamba hakuna atakayeshiriki katika jambo hili atakayebaki salama” akasema Dr Yonathan “Dr Yonathan naomba ufahamu kwamba tunachokifanya sisi ni muendelezo wa kile walichokianzisha Israel.Walivamia ardhi yetu wakaua na kumteka raia wetu,tunachokitaka sisi ni kumkomboa Raia wetu ambaye walimteka hivyo huu si uvamizi bali tunakwenda kumchukua raia wetu ka kutumia njia ile ile waliyoitumia wao”akasema Mathew “Edger Kaka ni mtu muhimu sana kwa nchi yangu.Ni yeye ambaye tunamtegemea atuonyeshe mahala walipo wafadhili wakuu wa vikundi vya ugaid ambavyo vinaendelea kuua waisrael” “Tunajua umuhimu wake kwa nchi yako lakini ukweli unabaki pale pale kwamba huyu bado ni raia wetu na kama Israel inamuhitaji basi wanatakiwa kufuata taratibu kwa kuwasiliana na mamlaka zetu husika.Edger Kaka ni mtu muhimu sana kwetu pia hivyo lazima tumrejeshe nyumbani” akasema Mathew “Siwashauri mfanye hivi jamani.Mtaibua jambo zito amb……….” “Dr Yonathan hauna uwezo wowote wa kutuzuia kufanya chochote.Tunakwenda Kenya kumchukua Edger Kaka na kumrejesha nyumbani na hakuna wa kutuzuia si wewe wala taifa lako la Israel.Ninataka utoe ushirikiano kila pale utakapotakiwa ufanye hivyo.Umenielewa Dr Yonathan? Akauliza Mathew “Sawa nimekuelewa lakini msije laumu huko mbeleni kwamba sikuwaonya” akasema Dr Yonathan Majadiliano yaliendelea kisha Dr Yonathan akaondoka zake. “Nadhani hakuna tena cha ziada kila kitu tayari kimewekwa wazi ni wakati wa kwenda kujiandaa kwa safari” akasema Mathew “Vipi kuhusu silaha.Hatujui huko tuendako tutakutana na hatari gani hivyo lazima tujihami kw……………”akasema Devotha lakini Mathew akamkatisha “Usihofu kuhusu hilo.Tino atashughulikia kila kitu na silaha zitapatikana” akajibu Mathew. “Kuna lingine unataka kulifahamu?akauliza “Mathew we have a problem” akasema Devotha “What problem? “Rais aliniamini akanipa idara niingoze lakini jana nilifanya mambo yaliyonifanya nikawa adui yake mkubwa.Nilidukua simu yake na vile vile kusababisha mauaji makubwa ya watu wa idara ya niliyokuwa naiongoza.Rais ametoa amri popote pale nitakaponekana nipigwe risasi.Itakuaje pale atakaposikia kwamba nimejumuishwa katika operesheni hii?Sina hakika kama atakubali niwepo” “Usihofu kuhusu Rais.Leave that to me I can handle it.Kuna lingine” akauliza Mathew “Hakuna” akajibu Devotha “Kama hakuna basi tumemaliza hapa kinachofuata ni kwenda kuanza maandalizi” akasema Mathew wote wakatoka “Devotha tunakwenda nyumbani kwako kuchukua kompyuta ya Ruby.Inahitajika sana katika operesheni hii ” akasema Mathew Kutoka Samawati beach hotel walielekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa Devotha.Gosu Gosu akamtaka Mathew abaki garini yeye akashuka na kumfuata Devotha ndani. “Gosu Gosu thank you.Uliniokoa sana pale ulipoingia mle ndani.Nilimuona Mathew machoni alikuwa amedhamiria kuniua na kama si wewe angenitoa uhai.Yule mtu ni hatari sana.Sikuwa nimetegemea kabisa kama ningeweza kumkuta mle chumbani.Halafu namna alivyoweza kunikamata na kuniingiza mle chumbani mpaka sasa ninajiuliza alifanyaje kwani kufumba na kufumbua nilijikuta nikiwa ndani” akasema Devotha “Don’t mess with him again.Mathew ni mtu mzuri lakini ni mbaya mno pale unapomkorofisha” akasema Gosu Gosu “Hata sasa bado naona hana imani na mimi.Nina wasi wasi nini kitatokea huko mbeleni” “Usihofu.Unachotakiwa kukifanya ni kufuata maelekezo yake na kufanya kile anachokuelekeza” “Nitafanya hivyo” akasema Devotha na kumpatia Gosu Gosu ile kompyuta ya Ruby “Vipi kuhusu Ruby,atanisamehe kweli kwa kile nilichokifanya?akauliza Devotha “I don’t know.Kwa sasa tujielekeze katika operesheni yetu na hayo mengine yatakuja baadae” akasema Gosu Gosu akabaki amesimama akimtazama Devotha “Mbona unaniangalia hivyo?akauliza Devotha “Nothing.Anza kujiandaa.Kumbuka hili ni jambo la siri kubwa sana.Funga mdomo wako usimwambie yeyote.We’re watching you”akasema Gosu Gosu na kuondoka “Siku zote nimekuwa nikiamini kwamba mimi ni mmoja wa watu mahiri sana katika mambo haya ya upelelezi lakini leo nimethibisha kwamba bado kiwango changu ni kidogo mno.Kuna watu ambao wako juu mno katika taaluma hii.Sikuwahi kuwaza kama Mathew angeweza kugundua siri yangu kubwa ambayo sikutaka watu wa hapa nchini waijue lakini tayari imejulikana.Kikubwa hapa ni kujaribu kujenga mahusiano mazuri na Mathew ili amani kati yangu naye iwepo.Anaonekana ni mtu mbaya na mkatili anayeweza kutoa uhai wa mtu kufumba na kufumbua.Sitakiwi kumfanyia masihara kabisa.Mathew amekuwa mwanaume wa kwanza kumuogopa” akawaza Devotha NAIROBI – KENYA Helkopta iliyowabeba Olivia na Coletha ilianza kushuka taratibu na kutua katika sehemu maalum ya kutulia helkpota iliyokuwa na herufi H ndani ya jumba moja kubwa la ghorofa tatu lililokuwa na uwanja mkubwa uliopandwa majani mazuri yenye ukijani uliokolea.Ndege na wanyama wa aina mbali mbali kama vile Farasi na Punda milia walionekana kwa mbali.Magari ya kifahari yalikuwa yamejipanga na hii ilikuwa ishara tosha kwamba aliyekuwa akiishi ndani ya jumba hili alikuwa ni mtu tajiri sana. Watu sita waliovalia suti nzuri nyeusi wakaisogelea helkopta ile na mlango ukafunguliwa akashushwa Olivia halafu Coletha wakawachukua na kuwapeleka ndani na kila mmoja akawekwa katika chumba chake.Fahad ambaye naye alikuwamo katika ile helkopta akashuka na kuongozwa na mmoja wa jamaa aliyevaa suti nyeusi hadi ndani ya jumba lile akapelekwa ghorofa ya pili.Mtu mmoja aliyekuwa ndani ya ofisi nzuri akawakaribisha wakaingia. “Fahad karibu sana Nairobi.Nimefurahi kukuona” akasema Yule jamaa mnene “Nimefurahi kukutana nawe pia Rashid” akasema Fahad na Rashid akamchukua wakaenda katika sebule nzuri “Vipi safari yenu haikuwa na tatizo lolote? Akauliza Rashid “Hakukuwa na tatizo lolote tumesafiri salama kabisa” “Nashukuru kusikia hivyo.Poleni kwa safari” “Tunashukuru sana” “Nilipokea maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu kwamba kila kitu kitaendeshwa kutokea hapa na maandalizi yote yamekwisha fanyika” “Nilielekezwa hivyo mimi pia.Kwa ujumla kila kitu kinakwenda vyema.Rais wa Tanzania anaendelea kutekeleza kila tutakachomuamuru na hivi sasa anasubiri kwa hamu kubwa tumuambie kitu gani kingine tunachokihitaji ili kumuachia mwanae.Kabla ya kumwambia kwamba tunamuhitaji Edger Kaka tunatakiwa kwanza kumtesa kihisia.Tutamuacha kwa muda bila kumpigia simu ili kuendelea kumpa hofu zaidi.Hatuna cha kuhofia kwani hakuna anayejua kama Olivia na mtoto wa Rais hawako tena Tanzania.Lilikuwa ni wazo zuri sana kuamua kuwaleta huku Kenya.Kwa kuwa hatuna haraka na Rais tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kumuhoji Olivia.Maelekezo yaliyotolewa na mama Habiba kuna wasiwasi kwamba Olivia anatumiwa na serikali ya Tanzania kuchota siri zetu na kutekwa kwake ulikuwa ni mpango wa serikali baada ya kupata taarifa za kutosha kuhusu sisi hivyo wakaamua kumteka Olivia kumficha wakati wanaendelea kujiandaa kutushughulikia” akasema Fahad. “Fahad naomba nikuulize kitu kimoja samahani lakini” “Uliza Rashid usihofu” “Una hakika kweli Olivia alikuwa anatumiwa na serikali ya Tanzania? “Sina uhakika sana na hilo lakini linawezekana” akajibu Fahad “Binafsi ninaingiwa na mashaka kwa sababu kama kweli angekuwa anatumiwa na serikali kupata taarifa zetu kwa muda huu wote tayari tungekwisha ona hatua kadhaa zikichukuliwa na serikali ya Tanzania katika kuwatafuta lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizowahi kuchukuliwa na serikali ya Tanzania kupambana nanyi hii ina maana kwamba Serikali ya Tanzania hawana uhakika au hawajui kama IS wana mtandao wao Tanzania” akasema Rashid “Nadhani wanajua ndiyo maana wakamteka Edger Kaka na kuidanganya dunia kwamba amefariki katika ajali.Nina uhakika mkubwa wanamfahamu Edger ni nani na hivi sasa watakuwa wanausaka mtandao wake.Haya yote tutayafahamu kwa kumuhoji Olivia” akasema Fahad. Rashid akamchukua Fahad hadi katika chumba ambacho kiliandaliwa maalum kwa ajili ya mahojiano.Kulikuwa na kiti ambacho nyuma yake kulikuwa na kitambaa cheusi chenye maandishi meupe yalioandikwa kwa lugha ya kiarabu.Kulikuwa na taa nne zenye mwangaza mkali vile vile kulikuwa na kamera tatu. “Maandalizi mazuri sana.Habiba anapaswa kufuatilia mubashara tunavyomuhoji Olivia” akasemaFahad na Rashid akachukua simu yake akampigia Habiba Jawad “Hallo Rashid” akasema Habiba baada ya kupokea simu “Mama Habiba habari za huko? “Huku kwema habari za Nairobi? “Huku salama kabisa.Nimekupigia kukujulisha kwamba timu ya Dar es salaam imekwisha wasili hapa Nairobi muda mfupi uliopita,wote wako salama kabisa” “Vizuri sana.Olivia na Yule mtoto wa Rais nao wako salama?akauliza Habiba “Wote wako salama” “Ahsante kwa taarifa hizo Rashid.Naweza kuzungumza na Fahad?akauliza Habiba “Ndiyo,huyu hapa zungumza naye” akasema Rashid na kumpatia simu Fahad “Mama Habiba”akasema Fahad “Fahad nakupeni hongera nyingi kwa kazi kubwa mliyoifanya vile vile poleni kwa safari” “Tunashukuru mama.Tuliondoka Dar es salaam salama tukaenda hadi Pemba ambako tuliwakuta wenzetu kutoka Mombasa wanatusubiri tukaingia katika boti na safari ya kuja huku ikaanza.Tunashukuru tumefika salama kabisa” “Baada ya kufika Kenya nini mipango yenu? “Kwa kuwa tumetoka nje ya Tanzania hatuna cha kuhofia tena hivyo tunataka kumtesa kwanza Rais kihisia.Hatutampigia simu kwa haraka na kwa muda huu tunataka kumfanyia mahojiano Olivia kama ulivyoelekeza” akasema Fahad “Vizuri sana.Itakuwa vyema kufahamu kama kweli alikuwa anatumiwa na serikali ya Tanzania kuchota siri zetu” “Kila kitu kiko tayari mama na tutakuunganisha moja kwa moja ushuhudie kile kinachoendelea hapa” “Nitafurahi sana” akasema Habiba na vijana waliokuwa katika chumba kingine kilichokuwa na mitambo na kompyuta kadhaa wakaelekezwa kumuunganisha Habiba ili aweze kushuhudia Olivia akihojiwa.Baada ya kila kitu kukamilika Fahad akaagiza Olivia aletwe katika kile chumba cha mahojiano.Akawekwa katika kiti na mikono ikafungwa mfuko ukatolewa kichwani.Alikuwa dhaifu mwili wake ulikuwa umevimba kutokana na kupigwa na mateso makali aliyoyapata kutoka kwa akina Kaiza.Kamera zikawashwa na Fahad akachukua kiti akamsogelea Olivia. “Olivia pole sana.Unajisikiaje sasa?akauliza Fahad “I’m fine” akajibu Olivia kwa sauti ndogo “Olivia unaweza kufahamu hapa uko wapi?akauliza Fahad Olivia akatikisa kichwa ishara kwamba hafahamu chochote “Can you guess?akauliza Fahad “I can’t” akajibu Olivia “Olivia japokuwa hali yako bado dhaifu lakini kuna mambo ambayo tunataka kuyafahamu kutoka kwako ndiyo maana uko hapa kuhojiwa” “Nini mnataka kukifahamu? Akauliza Olivia “Tunataka kufahamu namna ulivyotekwa na kile kilichotokea baada ya kutekwa” Akauliza fahad. “What is the meaning of this?Kwa nini mnanirekodi? Niko kwenye hukumu?akauliza Olivia “Olivia just answer the question! Akasema Fahad. “Nilitekwa wakati ninarejea nyumbani kutokea Kinshasa kuonana na Seif Almuhsin.Walioniteka ni idara ya serikali inayojulikana kama idara ya siri ya mambo ya ndani ya nchi.Walipata taarifa kuwa nimekwenda Kinshasa kukutana na Seif na wakaanza kunifuatilia.Kikubwa walichotaka kukifahamu kutoka kwangu ni mahusiano yangu na IS kwani katika kompyuta yangu walikuta barua pepe nilizokuwa ninawasiliana na Sayid Omar” akasema Olivia “Hii idara ya siri ya serikali walifahamuje kuhusu wewe kukutana na Seif Almushin? “Idara ya usalama wa taifa ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo walipewa taarifa kwamba Almuhsin anakwenda nchini Congo na wakaanza kumfuatilia na kugundua nilikuwa na mazungumzo naye wakaitaarifu serikali ya Tanzania na ndipo wakajiandaa na kuniteka” “Nini kiliendelea baada ya kukuteka?akauliza Fahad “Kama nilivyowaeleza kwamba walitaka kufahamu mahusiano yangu na IS na kwa kuwa walikuta mawasiliano yangu na Sayid Omar waliamini lazima nitakuwa na mahusiano nao.Ninaye rafiki yangu anaitwa Mathew Mulumbi huyu alinipa namba Fulani za siri nimpigie pale nitakapokuwa na matatizo na nikawapa namba hizo wapige nikiwadanganya kwamba ni namba za Sayid Omar walipopiga namba hizo mifumo yao yote ikazima” “Mifumo yao ikazima?Kivipi? “Idara hii ina mifumo yake ya mawasiliano ambayo yote ilijifunga baada ya kutumia simu yao kupiga namba zile” “Huyo Mathew ni nani? “Ni mpenzi wangu” “Anafanya kazi gani? “Ni mfanya biashara.Anao mfumo wqa ulinzi kwa ajili ya familia yake na mimi akaniunga na mfumo huo” “Endelea” “Walinitaka nifungue mfumo wao na mimi sikujua namna ya kuufungua nikawaambia wakitaka niwafungulie mfumo wao ninataka kuzungumza na Rais wakakubali na kumleta Rais,nikamueleza kwamba mwanae amechomwa sindano yenye virusi na atakufa kama hatatimiza kile ninachokitaka.Nilimuweka wazi ili mwanae apone anapaswa kunipa taarifa zote za mahala alipo Edger Kaka.Rais alikana kufahamu chochote kuhusiana na Edger Kaka.Nilianza kupewa mateso makali nikitakiwa kueleza kila kitu kuhusiana na mahusiano yangu na IS.Wamenitesa sana lakini sikufumbua mdomo wangu kusema chochote hadi niliporejea tena katika mikono yenu.Ahsanteni kwa kuniokoa” akasema Olivia “Olivia nakupa pole sana kwa mateso uliyoyapata.Pamoja na hayo kuna jambo nataka kukueleza.Baada ya kutekwa tumefanya uchunguzi wetu na tumegundua kwamba huu ulikuwa ni mchezo umechezwa kati yako na serikali ili ionekane umetekwa lakini ukweli ni kwamba wewe unatumiwa na serikali katika kutuchunguza na kuwapa taarifa zetu” akasema Fahad na mstuko mkubwa ukaonekana usoni kwa Olivia “Sijakuelewa hicho ulichokisema Fahad” “Olivia tumegundua kwamba unashirikiana na serikali na hata kutekwa kwako ulikuwa ni mchezo maalum ili kutuvuruga na kuwapa serikali nafasi ya kushughulikia taarifa zile ulizowapa” akasema Fahad “Are you crazy?Nani kawapa habari hizo zisizo na ukweli wowote?Kitu gani kimewafanya muhisi kwamba ninashirikiana na serikali kuwahujumu? Akauliza Olivia “Olivia tunataka majibu ni mambo gani ambayo umewaeleza serikali kuhusu sisi? Olivia hili si suala la mchezo na kama hautakuwa mkweli basi huu utakuwa ni mwisho wako.Tuambie ukweli wote na ninakuahidi tutakusamehe lakini kama utaendelea kuficha wakati tunafahamu kila kitu utajiweka katika mazingira mabaya sana ” akasema Fahad.Olivia akamuangalia kwa macho yaliyojaa hasira “Sikujua kama ninyi watu mko namna hii” akasema Devotha na kuvuta pumzi ndefu “Nilimsaidia mtu wenu Edger Kaka alipotaka kuuawa kwa sumu.Baadae mkanifuata na kuniambia Edger Kaka yuko hai na mkanitaka niwasaidie kufanya uchunguzi wa suala hilo.Nilikubali kuacha kazi yangu niliyokuwa naifanya kwa ajili ya kuwasaidia kuufahamu ukweli.Mliniingiza katika mtandao wenu bila mimi kutaka lakini bado niliendelea kushirikiana nanyi na hadi ukweli ukabainika kwamba Edger yuko hai.Kama haitoshi nimetengeneza hadi kirusi ambacho ameambukizwa mtoto wa Rais ambaye ni sawa na mdogo wangu.Ni moja ya jambo gumu sana ambalo nimewahi kulifanya katika maisha yangu kumuambukiza Coletha virusi vile lakini nimefanya kwa ajili ya kuwasaidia kumpata Edger Kaka.Pamoja na hayo yote niliyowafanyia bado mnasema nashirikiana na serikali?Kama ningekuwa nashirikiana na serikali ningekubali kuteseka namna hii?Nimeteswa mateso makali,nimechomwa na umeme na kila aina ya mateso ili kutoa taarifa za kuhusiana nanyi lakini sikufumbua mdomo wangu kusema chochote nimevumilia haya yote kwa ajili ya kuhakikisha Edger Kaka anapatikana.Kwa haya yote niliyoyafanya hivi ndivyo mnavyonilipa? Sikujua kama ninyi ni watu msio na shukran kiasi hiki” akasema Olivia akionekana kukasirika sana “Olivia nataka ufahamu kwamba hakuna kitu kibaya katika mtandao wetu kama usaliti.Kila tunapogundua msaliti ndani ya kundi letu adhabu yake ni kukatwa kichwa.Tunafahamu msaada wako mkubwa uliotusaidia lakini yote uliyoyafanya yameharibiwa na huu usaliti uliofanya na umegeuka adui yetu.Lakini kwa kuuthamini mchango wako kwetu tunakupa nafasi ya kukiri kosa lako na ukitueleza ukweli tutakusamehe ila ukiendelea kutudanganya utatulazimisha tuendelee na adhabu unayoistahili” akasema Fahad “Ninafahamu mambo mengi kuhusu ninyi na kama ningekuwa nashirikiana na serikali kama mnavyodai nyote msingekuwepo hapa muda huu.Kama ningekuwa msaliti msingeupata ukweli kuhusu Edger Kaka lakini kama mnaamini mimi ni msaliti nawapa uhuru wa kufanya kile mkitakacho.Kama ni kuniua I’m ready.Fikisheni salamu zangu kwa Habiba Jawad mwambieni ninashukuru kwa malipo aliyonilipa baada ya kuhangaika kumtafuta mwanae” akasema Olivia “Olivia tueleze ukweli tafadhali.Nakuhakikishia tutak…………….” Akasema Fahad na Olivi akamkatisha. “Niueni!! akasema Olivia Fahad akaenda katika pembe ya chumba akachukua panga kali akamsogelea Olivia “Olivia nafasi yako ya mwisho” “Sina cha kuwaeleza.Nimewasaidia kwa kila mlichokihitaji lakini mmeamua kunilipa kwa namna hii.Kill me! Akasema Olivia na kufumba macho.Fahad akaliinua panga “Fahad stop.Hana mashirikiano yoyote na serikali.Imetosha mfungueni mpelekeni akapumzike” akasema Habiba na Fahad akalishusha chini panga alilokuwa amelishika. “Open your eyes Olivia.It’s over” akasema Fahad na Olivia akafumbua macho akashangaa baada ya kumuona Fahad akitabasamu.Mtu mmoja akaenda kumfungua mikono “Mmeahirisha kuniua?akauliza Olivia “Olivia lile lilikuwa ni zoezi la kupima uaminifu wako.Tumejiridhisha wewe ni muaminifu” “Mmenisikitisha sana kwa kushindwa kuniamini hata baada ya kuwafanyia mambo mengi.Nimesikitishwa sana” akasema Olivia “Olivia usihofu.Ni utamaduni wetu kila pale tunapofanikiwa kumkomboa mwenzetu ambaye alikuwa ametekwa kumfanyia mahojiano kufahamu kilichotokewa wakati akiwa ametekwa.Kwa sasa utakwenda kupumzika” akasema Fahad na kuwataka watu wawili waliokuwamo mle ndani wamchukue Olivia na kumpeleka katika chumba chake alichoandaliwa akapumzike “Mama Habiba umeshuhudia mwenyewe mahojiano” akasema Fahad baada ya Olivia kutolewa mle chumbani “Olivia hana mashirikiano yoyote na serikali.Endeleeni na mipango mingine ya kumtafuta Seif.Mtoto wa Rais anaendeleaje? “Anaendelea vyema.Olivia alimtibu jana kabla ya kuanza safari ya kuja huku na sasa anaendelea vizuri” “Vizuri sana.Lini umepanga kumpigia simu Rais kumpa maelekezo kuhusu Seif? “Nitampigia simu kesho.Siku ya leo ninamuacha ateseke kwa mawazo” akasema Fahad. DAR ES SALAAM Mathew na Gosu Gosu waliwasili katika nyumba ya Rais waliyopewa waweke makazi ya muda.Aliposhuka garini akamfuata Ruby chumbani kwake na kumkuta amekaa kitandani “Ruby unaendeleaje? “Maendeleo yangu ni mazuri sana” akajibu Ruby “Namshukuru sana Mungu kwa maendelo haya mazuri.Ninakuhitaji sana” akasema Mathew “Mathew uliniahidi kunieleza kile kinachoendelea” “Nitakueleza Ruby lakini kwanza naomba nikurejeshee kompyuta yako ambayo Devotha aliichukua” “Oh Thank you Mathew.Tell me you’ve killed her ! akasema Ruby “Kuna mambo mengi yanaendelea Ruby nitakueleza kila kitu” akasema Mathew na kuanza kumsimulia Ruby kile kilichotokea katika usiku wa jana. Machozi yalimtiririka Ruby baada ya kusikia namna Mathew na Gosu Gosu walivyohangaika kuyaokoa maisha yake.Mathew akashindwa kuendelea akaanza kumbembeleza Ruby “Nyamaza kulia Ruby” “Mathew mimi ni nani hadi ukanifanyia haya? Akauliza Ruby “Ruby wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu na ndiyo maana nilikuwa tayari kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha unapata matibabu” “You killed for me Mathew.Oh my God ! Nitakulipa nini kwa hiki ulichonifanyia? Akauliza Ruby “Ruby toka tulipofahamiana ni mimi ambaye nimekuwa na deni kubwa kwako na kwa mambo ambayo umekuwa unanifanyia mpaka leo sina cha kukulipa.Nilichokifanya ni kidogo sana ukilinganisha na mambo ambayo umekuwa unanifanyia.Ni mimi ndiye mwenye deni kubwa kwako ambalo hata nikitumia utajiri wangu wote sintaweza kulilipa” “Mathew sifahamu niseme nini kwa hiki ulichonifanyia” akasema Ruby na kuushika mkono wa Mathew akaubusu. “Naomba niendelee kukueleza kile kilichotokea jana usiku kwani bado sijamaliza” akasema Mathew “Endelea tafadhali” akasema Ruby huku akifuta machozi “Baada ya kuhakikisha umepata matibabu tulianza kumsaka Devotha na kitu cha kwanza tulichokigundua alikuwa amewasiliana na Dr Yonathan Cohen balozi wa Israel hapa nchini na wakaenda kukutana katika ubalozi wa Israel.Baada ya kuligundua hilo kiguu na njia tukavamia makazi ya balozi na kuwateka yeye na mke wake ambaye yuko nasi hapa.Balozi akatueleza sababu ya kukutana na Devotha usiku wa leo na akatueleza kitu ambacho hatukuwa tunakifahamu.Kumbe Devotha ni wakala wa shirika la ujasusi la Israel.Mossad wametuma watu wao kuja kuandaa operesheni ya kumtafuta Olivia” Mathew akamueleza Ruby kila kitu kuhusiana na Devotha,Edger Kaka na mipango ya Mossad “Sikufikiria kama jambo hili ni kubwa kiasi hiki” akasema Ruby baada ya Mathew kumaliza kumpa maelezo ya kina kuhusiana na kile walichokuwa wamekigundua. “Baada ya kugundua hayo yote ikalazimu kwenda kuonana na Rais” Mathew akaendelea “Jitihada zilifanywa nikafanikiwa kukutana na Rais nikamueleza mambo haya yote na tofauti zetu za awali zikamalizika tukaungana na kuwa kitu kimoja.Hivi sasa tunawasiliana moja kwa moja na Rais” akasema Mathew “Hilo ni jambo kubwa sana umelifanya Mathew hongera.Nini mlikipanga baada ya kukutana na Rais? “Kama utakumbuka jana usiku lilifanyika shambulio la kigaidi katika hospitali ya Mtodora na shambulio hilo lilimlenga mtoto wa Rais na magaidi walifanikiwa kumteka wakaondoka naye kisha wakampigia simu Rais wakamjulisha na kumtaka awapatie Olivia.Rais hakuwa na namna ya kufanya akawapatia Olivia.Rais aliniomba sana nimsaidie kuwakomboa Olivia na Coletha.Ili kuwakomboa Olivia na Coletha lazima kwanza kumpata Edger Kaka ambaye anashikiliwa katika ubalozi wa Israel nchini Kenya.Kuna namna moja tu ya kuweza kumpata Edger Kaka nayo ni kuvamia ubalozi huo na kumchukua.Rais amekwisha toa ruhusu jambo hilo lifanyike na hivi sasa tuko katika maandalizi ya awali ya operesheni hiyo ya kwenda kumuokoa Edger Kaka.Ili tuweze kuingia ndani ya ubalozi huo tunahitaji kupata ramani ya namna jengo lilivyo na taarifa za kiusalama hivyo basi tunatanguliza timu ya watu watatu kwenda Nairobi mchana huu kuanza kuifanya kazi hiyo.Wakiwa kule watakuwa wakiwasiliana nasi huku Tanzania kutujulisha kila kinachoendelea hivyo nakuhitaji sana katika operesheni hiyo.Tunahitaji kuwa na mawasiliano kati ya ofisi ya Dar es salaam na watu wa Nairobi” akasema Mathew “Mathew hakuna tatizo katika hilo.Mimi niko zaidi ya tayari” akasema Ruby “Ahsante sana Ruby nafahamu muda wowote uko tayari lakini kuna tatizo kidogo” akasema Mathew “Kuna tatizo gani Mathew? Akauliza Ruby “Timu inayokwenda Nairobi mchana huu ni Gosu Gosu,rafiki yangu mwingine anaitwa Tino na ……” Mathew akasita “Mbona unasita Mathew?akauliza Ruby “Ruby kuna jambo limefanyika ambalo naamini halitakupendeza lakini imebidi lifanyike” “Jambo gani hilo Mathew nieleze tafadhali” akasema Ruby “Ili kuweza kupata ramani ya jengo na taarifa zote za ulinzi inatubidi tupandikize mtu ndani ya Mossad jambo ambalo ni gumu na linahitaji muda mrefu ambao sisi hatuna hivyo tumeamua kumtumia mtu ambaye tayari ana ukaribu na Mossad ili asaidie katika kupata taarifa hizo.” Mathew akanyamaza kidogo halafu akasema “Tumemshirikisha pia Devotha katika operesheni hii” Ruby akamtazama Mathew kwa mshangao mkubwa “Mathew naomba usinitanie tafadhali” akasema Ruby “Ruby haikuwa rahisi kwangu kufanya maamuzi haya niliyoyafanya lakini ni kwa ajili ya operesheni hii” akasema Mathew “Mathew that witch shot me three times.She’s supposed to be in hell right now.Unathubutuje kumrejesha ashirikiane nasi tena? Akauliza Ruby “Ruby imelazimu iwe hivyo kwani tunahitaji mtu ambaye anaweza kuingia ndani ya Mossad akatusaidia kupata taarifa muhimu za kutuwezesha kufanikisha operesheni yetu.Hata mimi nafsi yangu haitaki jambo hili lakini imebidi iwe hivyo.Nakuomba Ruby ukubali Devotha ashirikiane nasi na baada ya operesheni kumalizika nitajua adhabu ya kumpa lakini kwa sasa ni mtu wa muhimu sana” akasema Mathew. “Mathew sina cha kusema kwa sababu wewe ndiye kiongozi na ndiye mwenye kauli ya mwisho kama umeamua kumshirikisha mtu aliyetaka kuniua katika timu yetu sina cha kupinga lakini Mungu atanilipia” akasema Ruby “Ruby my dear do you trust me? “With all my life” akajibu Ruby “Ahsante kwa kuniamini Ruby” “Mathew nimekuwa ninakuamini toka siku ya kwanza nilipofahamiana nawe” “Ruby nakuomba uniamini pia katika hili.Niliumizwa na kitendo alichokifanya Devotha na adhabu niliyokuwa naifikiria kichwani kwangu ni kumuua lakini mwanamke huyu ana maisha marefu kama paka kwani nimejikuta sina namna zaidi ya kukubali kumtumia tena kutokana na umuhimu wake lakini this isn’t over yet.Mimi na yeye tutamalizana baada ya operesheni hii kumalizika” akasema Mathew “Mathew sina chochote ninachoweza kukupinga.Kauli yako ni ya mwisho na lazima niiheshimu hata kama moyo wangu hautaki”akasema Ruby na Mathew akamtazama kisha akauliza “Ruby kutakuwa na tatizo lolote kufanya kazi na Devotha? Ruby akafikiri kidogo halafu akasema “Hakuna tatizo lolote.I trust you” “Thank you my Ruby” akasema Mathew akambusu Ruby katika paji la uso na kutoka akamfuata Gosu Gosu “Nimezungumza na Ruby kuhusu Devotha” akasema Mathew “Amesemaje?akauliza Gosu Gosu akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua maamuzi ya Ruby “Haikuwa rahisi kumshawishi akubali kufanya kazi tena na Devotha lakini amekubali Devotha ashiriki katika operesheni hii na amekubali kufanya naye kazi.Najua amekubali kwa kuniridhisha mimi ila moyoni bado ana kinyongo” “Ahsante sana kwa kumshawishi Ruby.Nini kinafuata?Umewasiliana na Tino?akauliza Gosu Gosu “Kabla ya kuwasiliana na Tino natakiwa kwanza kuwasiliana na Rais na kumjulisha hatua tuliyofikia” akasema Mathew na kuchukua simu akampigia Dr Evans “Mathew nimelazimika kusimamisha kikao kwa muda ili kupokea simu yako kwani ni ya muhimu sana kwa sasa.Nini kinaendelea huko? “Mheshimiwa Rais samahani kwa usumbufu huu”akasema Mathew “Mathew nimekupa uhuru wa kupiga simu yangu muda wowote ambao utakuwa na jambo la kuniambia usione kama ni usumbufu tafadhali” “Ahsante mheshimiwa Rais kwa heshima hiyo.Nimekupigia kukujulisha kwamba mchana huu timu ya watu watatu itaondoka hapa Dar es salaam kuelekea Nairobi kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ile operesheni.Kila kitu tayari kimewekwa sawa” “Safi sana Mathew.Hilo ni jambo zuri.Lini mmepanga kufanya operesheni? “Mheshimiwa Rais operesheni inategemea na uhodari wa timu yetu inayokwenda Nairobi namna watakavyotekeleza yale tunayowatuma wakayafanye yaani kutafuta ramani ya jengo la ubalozi wa Israel nchini Kenya na mahala alipofichwa Edger.Kama wakiweza kuyakamilisha haya mchana huu basi hata usiku wa leo tunaweza kufanya operesheni yetu”akasema Mathew “Mathew kwa nini usiongozane na hao jamaa wanaokwenda Nairobi ili kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda haraka na kwa mafanikio?akauliza Rais “Usihofu mheshimiwa Rais watu ninaowatuma huko ninawaamini wanaweza wakaifanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi.Hata hivyo mawasiliano kati yetu ni makubwa na nitakuwa nikifuatilia kila kitu wanachokifanya kule nikiwa hapa hapa Dar es salaam.Mheshimiwa Rais kuna jambo nataka ulifahamu pia kuhusu timu ninayoituma Nairobi” “Ndiyo nakusikiliza Mathew” akasema Dr Evans “Katika timu hiyo ya watu watatu yupo pia Devotha Adolph” akasema Mathew na ukimya wa sekunde kadhaa ukapita “Mheshimiwa Rais” akaita Mathew “Nimestuka sana nilipolisikia jina la Devotha.Huyo mwanamke sihitaji kabisa kumuona mbele ya macho yangu.Nilimuamini sana lakini kwa aliyoyafanya hastahili kuendelea kuwa hai na sitaki ashiriki tena suala lolote linalohusiana na nchi yetu.Ni msaliti na atatuuza! akasema Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa Rais nafahamu kila kitu kuhusu Devotha na hata mimi nilikuwa namtafuta mno nimuadhibu kwa kitendo alichokifanya cha kutaka kumuua mmoja wa watu wangu wa karibu lakini mheshimiwa Rais kwa sasa Devotha ana umuhimu mkubwa sana katika operesheni yetu.Ni yeye ambaye tutamtanguliza mbele kutafuta ramani ya jengo la ubalozi tunalotaka kuvamia.Ni kwa umuhimu huo ndio maana nimeamua kumjumuisha katika kikosi hiki” “Mathew I real don’t like this ! akasema Dr Evans “Nafahamu mheshimiwa Rais na hata mimi sikutaka lakini imenilazimu.Naomba uniamini mheshimiwa Rais” Dr Evans akafikiri kidogo halafu akasema “Mathew kama unaona ana umuhimu wa kushiriki katika operesheni hiyo sawa mjumuishe lakini kwa sharti moja” akasema Dr Evans na kunyamaza kimya kwa sekunde kadhaa “Nakusikiliza mheshimiwa Rais” akasema Mathew “Baada ya operesheni kumalizika kill her ! Ilipita dakika moja ya ukimya Dr Evans akasema “Mathew umenisikia nilichokwambia? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” “Good.Akishamaliza kile ambacho umemtuma akifanye nataka auawe” akasema Dr Evans “Nitafanya hivyo mheshimiwa Rais” “Ahsante.Ninawatakia kila la heri katika maandalizi yenu kama kuna chochote mtakihitaji msisite kuniambia” “Ahsante mheshimiwa Rais kwa sasa ni hilo tu nililotaka kukufahamisha” “Keep me posted ! akasema Dr Evans na kukata simu “Rais amesemaje?akauliza Gosu Gosu.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema “Rais amekubali tumjumuishe Devotha lakini ameagiza baada ya kumaliza kazi tuliyomtuma tumuue” Gosu Gosu alistushwa na maagizo yale akamtazama Mathew kwa sekunde kadhaa na kuuliza “Mathew are you real going to kill her?akauliza Gosu Gosu “I don’t know yet” akajibu Mathew “Mathew please don’t kill her.She’s an asset.Kuna mambo mengi ambayo tutaendelea kumuhitaji.Mathew hatuna sababu ya kumuua Devotha badala yake tunapaswa kumsaidia kumuondoa katika hatari hii ya kuuawa.This is a win win situation.Anatusaidia na sisi tunapaswa kumsaidia” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu naomba tusiliongelee suala hili kwa sasa.Tujielekeze katika safari ya Nairobi” akasema Mathew na kumpigia simu Tino ambaye alimjulisha kwamba anakaribia kufika pale nyumbani. “Mathew wakati tukimsubiri Tino nataka tumalize lile suala la Devotha” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu Rais amekwisha toa maelekezo ambayo hatuna budi kuyafuata na isitoshe hata mimi bado nina hasira naye sana kwa alichomfanyia Ruby” “Mathew kama unakubaliana na alichokiagiza Rais kwamba tumuue Devotha basi tufanye hivyo kabla hajaenda Nairobi.Haitakuwa busara tumtume kazi atufanyie halafu tumuue.Mathew hatuna sababu ya kumuua Devotha.Nakubali amefanya kosa kubwa na hata mimi sikufurahia kitendo alichokifanya lakini Devotha bado ana msaada mkubwa kwetu.Atatusaidia mno” akasema Gosu Gosu Mathew akamkazia macho “Gosu Gosu unaonekana kumtetea sana Devotha,why?Mathew akauliza “The truth is,I don’t want her to die” akasema Gosu Gosu na mlango ukagongwa Gosu Gosu akaufungua alikuwa ni Tino amerejea. “Karibu Tino” akasema Mathew. “Ahsanteni sana.Nimerejea na huko nilikotoka nimefanikiwa kupata tiketi tatu katika ndege ya shirika la ndege la Tanzania inayoondoka saa saba mchana kuelekea Nairobi.Nimekata daraja la kwanza” akasema Tino “Safi sana” akasema Mathew “Vipi kwa upande wenu mambo yamekwenda vizuri?Tino akauliza “Kwa upande wetu kila kitu kimekwenda vyema.Tumekutana na balozi na Devotha na mambo yote yamewekwa sawa kilichobaki kwa sasa ni kujiandaa kwa safari ila kuna jambo moja ambalo nataka utusaidie Tino kama litakuwa ndani ya uwezo wako” “Jambo gani Mathew? “Mkiwa Nairobi mtahitaji vifaa vya mawasiliano kuhusu hilo hakuna tatizo kwani fedha zipo mtanunua lakini zitahitajika silaha kwa ajili ya kujilinda kabla ya operesheni.Unaweza ukatusaidia kwa hilo? “Mathew usiwe na hofu yoyote kuhusu silaha.Hilo ni jambo dogo sana kwangu.Ninao mtandao mkubwa wa watu Afrika Mashariki na Kenya ninao watu wangu ambao watanipatia hizo silaha” “Good.Pamoja na silaha kuna jambo lingine vile vile ambalo ninataka ukiwa Nairobi uanze kulishughulikia.Siku tutakayofanya operesheni tutalazimika kukata umeme eneo lote la karibu na ubalozi wa Israel.Tunatakiwa kuifanya operesheni yetu gizani hivyo basi kwa kuwa tayari unao mtandao wako jijini Nairobi anza kulifanyia kazi hilo suala” akasema Mathew “Hesabu hilo nalo limekwisha.Mtandao wangu unao watu wazito na hilo suala nitalifanikisha” akasema Tino. “Sawa ndugu zangu naona yale yote yalipangwa kufanyika asubuhi ya leo yamekamilika kinachofuata kwa sasa ni kujiandaa kwa ajili ya safari” Mathew,Gosu Gosu na Tino wakaingia katika gari la Mathew wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Mathew ambako Gosu Gosu alikuwa ameacha sanduku lake halafu wakaelekea nyumbani kwa Tino naye akachukua vitu vichache alivyovihitaji wakatoka na kuelekea nyumbani kwa Devotha ambaye tayari alikwisha jiandaa wakamchukua na kuelekea uwanja wa ndege “Guys this is it.Nawatakia kila la heri katika safari yenu hii mfike salama na mtekeleze jukumu mlilotumwa.Ninawategemea sana ndugu zangu na nchi inawategemea pia.Kumbukeni hamtarejea tena Tanzania hadi operesheni itakapokamilika hakikisheni mnakuwa salama” akasema Mathew na kuwaaga akina Gosu Gosu ambao waliingia ndani sehemu ya kusubiri ndege.Mathew hakuondoka hadi pale alipohakikisha ndege waliyopanda akina Tino imepaa “Mungu awatangulie tutakutana Nairobi” Mathew akasema kwa sauti ndogo akawasha gari lake na kuondoka akarejea katika makazi yao ya muda moja kwa moja akaelekea katika chumba cha Ruby. “Ruby akina Gosu Gosu tayari wameondoka kuelekea Nairobi.Tunahitaji kuwasiliana nao pindi tu wakifika hivyo basi tunapaswa kuanza kuandaa ofisi kwa ajili ya mawasiliano.Dar es salaam hadi Nairobi kwa ndege ni mwendo wa saa moja na nusu hivi hivyo maandalizi yanatakiwa yaanze mara moja” akasema Mathew.Ruby akamtazama akamshika mkono na kusema “Mathew moyo wangu hauko tayari kufanya kazi na mtu aliyetaka kuniua lakini nitafanya kwa ajili yako.You want to know why?akauliza Ruby “Ndiyo Ruby ningependa kujua”akasema Mathew.Ruby akamtazama Mathew machoni akafumbua midomo yake laini akasema ‘It’s because I love you Mathew” Mathew akatabasamu kidogo halafu akasema “I love you too Ruby” “Mathew naelewa unanipenda kama rafiki yako,kama mtu wako wa karibu lakini mimi ni tofauti kidogo.Nakupenda Mathew like I..ouh gosh I don’t know how to say it” akasema Ruby “Niambie Ruby chochote unachotaka kuniambia” akasema Mathew.Ilimlazimu Ruby kuvuta pumzi halafu akasema “Mathew nilikupenda sekunde ya kwanza nilipokutia machoni.Niliamini wewe ndiye mwanaume pekee ambaye ninastahili kuwa naye maishani.Mathew I know you have a wife and beautiful kids na hiyo ndiyo sababu iliyonifanya niishi na mzigo huu mzito moyoni mwangu kwa muda mrefu lakini siwezi kuendelea tena kubeba zigo hili.Nimechungulia kaburi na kwa hiki kilichonitokea ni kama vile nimekumbushwa kwamba maisha haya ni mafupi sana na uhai unaweza ukakutoka sekunde yoyote ile hivyo tunatakiwa kuyaishi maisha tuliyonayo sasa.Hakuna anayeijua kesho yake.Kama una kitu cha kumwambia mtu mwambie sasa na usisubiri hadi kesho kwani hujui kama utaiona hiyo kesho.Kwa nafasi hii niliyoipata baada ya kunusurika kifo ninataka nikueleze Mathew kwamba wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu.Nakuhitaji Mathew katika dunia yangu.Milango ya himaya yangu nimekwisha ifungua kwako muda mrefu sana ila bado hujaingia.Mathew nakutaka uwe mpenzi wangu” akasema Ruby.Mathew alibaki anamtazama Ruby akashindwa aseme nini “Ruby sijui niseme nin…” “Usiseme chochote Mathew kwani nafahamu utakachokisema na kitanivunja moyo wangu sana lakini naomba unisikilize.Najua una mke lakini niko tayari kuwa mpenzi wakjo wa siri bila mke wako kujua.Niko tayari kuzaa nawe mtoto.Kama uliweza kuwa na Olivia bila mkeo kujua naomba uwe na mimi pia.Sijali una wanawake wangapi pembeni ya mke wako lakini ninachohitaji ni penzi lako Mathew” akasema Ruby kwa hisia kali na kwa mbali macho yake yalilengwa machozi. “Look at me Mathew” akasema “I’m very pretty may be than your wife and your Olivia but….” Akashindwa kuendelea akamwaga machozi “Ruby nimekuelewa.Nyamaza kulia.Nimekuelewa yote uliyoniambia” akasema Mathew “Umenielewa? “Ndiyo nimekuelewa lakini ninaomba tuyazungumze baada ya operesheni yetu kumalizika.Tushike suala moja tulimalize kwanza halafu tutaingia tena katika suala lingine.Jambo hilo linazungumzika”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mathew nataka tulimalize suala hili hapa hapa.Nina hofu kubwa baada ya kunusurika kifo” “Ruby wewe unanifahamu mimi vizuri pengine kuliko mtu yeyote, nikisema tutalizungumza jambo hili amini hivyo.Nakuahidi Ruby mara tu operesheni hii itakapomalizika mimi na wewe tutakwenda mahala mbali na Dar es salaam tukiwa peke yetu tupumzike na tutazungumza mengi likiwamo suala hili.” akasema Mathew na kwa mbali tabasamu likaonekana usoni kwa Ruby.Mathew akamsaidia kusimama akamshika mkono wakatembea hadi katika ofisi akaketi kitini na kuanza kumpa Mathew maelekezo ya kufanya. “Sikutegemea kabisa kama Ruby angeweza kunitaka niwe mpenzi wake.Mimi na yeye tunaheshimiana sana na ninamchukulia kama mdogo wangu lakini kumbe mwenzangu amebeba mzigo mzito moyoni mwake.Ngoja kwanza nijielekeze katika operesheni nzito na baadae tutazungumza kwani hili si jambo dogo”akawaza Mathew akiendelea kuuganisha vifaa huku akielekezwa na Ruby aliyekuwa ameketi kitini











ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog