Simulizi : Siri
Sehemu Ya Tatu (3)
Devotha aliwasili kitalu 1 alikopelekwa Mathew Mulumbi akitokea katika makaburi ya midizini.Aliingiza gari katika maegesho chini ya jengo akashuka na kuelekea ndani.Juhudi za kuunganisha mfumo mpya wa mawasiliano ziliendelea chini ya usimamizi wa Kaiza.Devotha akamuita Kaiza ofisi kwake “Nipe ripoti Kaiza mambo yanavyokwenda hapa”akasema Devotha “Hapa mambo yanakwenda vizuri.Kama nilivyokueleza tumefanikiwa kumpata Mathew Mulumbi yuko hapa.Tumeanza kumpatia mateso.Tulimuweka chumba cha baridi na sasa tumemuweka white room tukisubiri maelekezo yako.Kingine kinachoendelea hivi sasa ni kuunganisha vitalu vyetu vyote katika mfumo mpya.Vipi huko utokako mambo yamekwendaje?akauliza Kaiza “Huko mambo ni vile vile kama yalivyokuwa.Olivia amegoma kufunguka kabisa”akasema Devotha “Devotha nilikushauri jana kwamba tubadili mbinu za kumuhoji Olivia.Kwa kutumia nguvu katu hatutaweza kupata chochote toka kwake hata kama tukimuhoji kwa mwaka mzima.Kama aliweza kushuhudia baba yake akipigwa risasi na hakufunguka hakuna namna tutakayoweza kumfungua kwa kutumia nguvu” akasema Kaiza “Ulikuwa sahihi Kaiza,matumizi ya nguvu hayatasaidia.Nimefuata ushauri wako nikazungumza naye kirafiki na katika mazungumo hayo kuna kitu nimekipata” akasema Devotha “Umepata kitu gani kutoka kwa Olivia?akauliza Kaiza “Jana alipozungumza na Rais Olivia alizungumza kitu Fulani ambacho wote tulimuona kama mtu aliyechanganyikwa.Alisema kwamba Edger Kaka ambaye wote tunafahamu alifariki katika ajali ya gari miaka mitatu iliyopita yuko hai.Nilipozungumza naye pia akaendelea kusisitiza jambo hilo na kusisitiza kwamba Edger kaka yuko hai na akaenda mbali zaidi akadai kwamba Rais Dr Evans anafahamu jambo hilo na ndiyo maana akamuambukiza mtoto wake virusi alivyovitengeneza yeye mwenyewe ili kumshinikiza Rais ampe taarifa za mahala aliko Edger Kaka.Leo tena baada ya kuzungumza naye amerudia tena jambo hilo nikamkumbusha kwamba Edger kaka amekwisha fariki dunia na hakuna namna ya kumrejesha akaendelea kusisitiza kwamba Edger hajafariki dunia yuko hai.Akanihakikishia kwamba ana ushahidi mkubwa kwamba Edger hajafa.Olivia akadai alichukua sampuli za mabaki ya mwili ule uliozikwa katika kaburi la Edger akaenda kufanya uchunguzi akabaini kwamba mwili ule haukuwa wa Edger Kaka” akasema Devotha. “Amefanyia uchunguzi mwili wa Edger? How?akauliza Kaiza “Anadai amechukua mabaki ya mwili uliozikwa katika kaburi la Edger akaenda kufanya uchunguzi ndipo akagundua kwamba mwili ule haukuwa wa Edger” “Amewezaje kugundua kama ule mwili si wa Edger?Ni mwili wa nani?akauliza Kaiza “Hakutaka kunieleza kwa undani jambo hili lakini amekiri kwamba kuna siri kubwa ambayo hatuifahamu na kama ninataka anieleze kila kitu basi nimsaidie kupata taarifa za mahala alipo Edger Kaka” akasema Devotha “Devotha tujiulize kwa nini Olivia aibuke sasa na kudai Edger ambaye wote tunafahamu amefariki miaka mitatu iliyopita yuko hai?Amekuonyesha ushahidi alio nao kuhusiana na hicho anachokizungumza?akauliza Kaiza “Hajanionyesha ushahidi wowote lakini kwa kumtazama tu usoni anaonekana anamaanisha anachokisema” “Do you believe her?akauliza Kaiza “Simuamini moja kwa moja lakini kuna kitu ninakiona katika suala hili” akasema Devotha “That woman is a damn lier! Don’t trust her! Akasema Kaiza “Kaiza ukilitazama suala hili kwa upana utagundua kuna kitu ndani yake ambacho hatukijui bado_Olivia asingeweza kulisisitiza jambo hili kama halina ukweli na isitoshe amemuelekezea mzigo wote Rais.Kwa nini awaache watu zaidi ya milioni hamsini na ajielekeze kwa mtu mmoja tu?Hapa lazima kuna jambo ndiyo maana baada ya kuachana naye nilikwenda katika makaburi ya midizini alikozikwa Edger kaka kulichunguza.Nimelikagua kaburi na hizi ndizo picha nilizozipata” akasema Devotha na kuzihamishia picha alizopiga katika kaburi la Edger kwenye kompyuta yake akamuonyesha Kaiza. “Umegundua nini katika hizo picha Kaiza?akauliza Devotha “Sioni chochote katika hizi picha zaidi ya kaburi la Edger” “Ukilitazama hili kaburi kwa makini utagundua kuna kitu hakiko sawa.Tazama upande wa kulia wa kaburi kunaonekana kumetitia kidogo tofauti na upande wa kushoto.Kwa mujibu wa Olivia ni kwamba upande huu wa kulia wa kaburi la Edger ulichimbwa ndipo akaweza kuingia ndani ya kaburi akapata sampuli za mabaki ya mwili uliozikwa akaenda kufanya uchunguzi akagundua mwili ule haukuwa wa Edger.Ukilitazama kaburi hili utaona ni kweli upande huu unaonekana umewahi kuchimbwa japo si hivi karibuni lakini umechimbwa na hii inanipa uhakika kwamba yawezekana anachokisema Olivia ni kitu cha kweli” akasema Devotha “Bado nafsi yangu inakuwa nzito sana kukubaliana na hicho anachokisema Olivia.Edger kaka amekwisha fariki dunia na hakuna namna anayoweza kuwa hai”akasema Kaiza “Ni vipi kama ni kweli Edger hajafa?akauliza Devotha “Haiwezekani Devotha.Huyu mwanamke anataka kucheza na akili zetu.Taarifa zinadai ni yeye mwenyewe aliyekwenda hospitali baada ya ajali na kuutambua mwili wa Edger iweje leo aibuke na kudai mwili ule haukuwa wa Edger?akauliza Kaiza “Sikiliza Kaiza mambo kama haya yanatokea sana hasa katika nchi za wenzetu ambazo teknolojoa ni kubwa.Watu wanaghushi vifo vyao na inaonekana kweli wamekufa lakini kumbe bado wako hai.Sishangai hata hili tukio la Edger likawa kweli ni la kutengeneza kama anavyodai Olivia.Haya mambo yapo na yanafanyika sana ila hapa kwetu bado ni mageni”akasema Devotha “Kwa hiyo umepanga kufanya nini Devotha kuhusiana na suala hilo?akauliza Kaiza “Siwezi kulipuuza.Kuna vitu vinanipa hamu ya kutaka kulichunguza hili jambo kwa undani na kuufahamu ukweli wake”akajibu Devotha “Devotha ushauri wangu tusipoteze muda katika suala hilo.Yule mwanamke anashirikiana na magaidi na hapaswi hata kidogo kuaminiwa.Jukumu letu ni kuhakikisha kwa namna yoyote ile tunamfanya atueleze kila kitu kuhusu mtandao wao na mipango yao yote.Hili suala alilolianzisha la kuhusu Edger linataka kutupotezea mwelekeo na kutuvuruga.Ndivyo magaidi wanavyofanya mambo yao hutafuta jambo la kuwapoteza watu muelekeo na wao hupata mwanya wa kufanya mambo yao.Tusiwape nafasi hiyo Devotha”akasema Kaiza “Kaiza nitafanya uchunguzi wa jambo hili kuufahamu ukweli.Olivia hawezi akasisitiza jambo hili kama halina ukweli,zaidi ya yote Olivia ana mambo mengi anayafahamu na hataweza kutueleza hadi pale atakapopata taarifa za kuhusiana na alipo Edger hivyo lazima uchunguzi ufanyike katika jambo hili na ukweli ujulikane” akasema Devotha “Rais anafahamu kuhusu hicho unachotaka kukifanya?akauliza Kaiza “Rais hafahamu chochote na hapaswi kujua kama uchunguzi huu unafanyika.Olivia amemlenga yeye moja kwa moja kuwa anafahamu mahala alipo Edger hivyo akifahamu kama tunafanya uchunguzi wa hili jambo utaibuka mtafaruku mkubwa”akasema Devotha “Rais mwenyewe umezungumza naye ukamuuliza kama analifahamu hili jambo?akauliza Kaiza “Nimezungumza naye nikamuuliza akakana kabisa kulifahamu.Olivia hawezi akamlenga mtu mzito kama Rais bila kuwa na sababu.Lazima Dr Evans kuna kitu anakifahamu hivyo lazima tuchunguze tuujue ukweli” akasema Devotha “Ni vipi kama kweli anafahamu mahala alipo Edger? Kaiza akauliza “Kama kweli anafahamu suala hili husika atakuwa na la kutueleza kwa nini alifanya hivi na wapi alipo Edger.Olivia ameahidi kunieleza siri kubwa endapo atapata taarifa za mahali alipo Edger Kaka hivyo lazima kufanya juu chini kulichuguza hili jambo na kuupata ukweli” akasema Devotha “Devotha utanisamehe kwa hili nitakalolisema lakini sidhani kama hayo ni maamuzi mazuri.Sisi tuko chini ya Rais na kila tufanyalo lazima tumjulishe.Kufanya uchunguzi huo kwa siri bila kumjulisha Rais hauleti picha nzuri.Akigundua tunamchunguza tutakuwa katika matatizo.Hatatuamini tena.Sikushauri Devotha tufanye hivyo.Tuachane na hili jambo na tujielekeze katika jambo la msingi la kuchunguza kuhusu Olivia na IS” akasema Kaiza.Maneno yale ya Kaiza hayakumfurahisha Devotha “Kaiza toka lini ukanifundisha namna ya kufanya kazi yangu?Naomba iwe mwanzo na mwisho kunifundisha kazi.Mimi ndiye mkubwa hapa na hakuna wa kuuliza swali kwa chochote nitakachokifanya.Mimi ndiye ninayepanga nini kifanyike na nini kisifanyike na kwa sasa ninasema kwamba uchunguzi kuhusu Edger kaka lazima ufanyike hata kama Rais anahusika.Umenielewa Kaiza? Akauliza Devotha “Ninakuelewa Devotha na hata siku moja sijawahi kupingana nawe katika chochote unachokiamua.Wewe ni mkubwa wangu na ninapokea maelekezo yote kutoka kwako lakini katika hili nina mashaka makubwa kwamba kama uchunguzi ukifanyika na rais akagundua tunamchunguza tutakuwa tumejiweka katika matatizo makubwa” akasema Kaiza “Haijalishi kama Rais anahusika au hahusiki katika suala la Edger lakini lazima tulichunguze na kuufahamu ukweli.Kama kweli Edger kaka yuko hai lazima tujue yuko wapi ili tuweze kupata taarifa muhimu kutoka kwa Olivia.Sitaki tena mjadala katika suala hili” akasema Devotha na kusimama akachukua kompyuta yake ndogo “One more thing” akasema Devotha na kumgeukia Kaiza “Nilichokwambia kinabaki kati yetu hatakiwi mtu mwingine yeyote kufahamu” “Sawa Devotha” “Good.Ninataka kuzungumza na Mathew Mulumbi.Nataka kamera zote zizimwe” “Unataka kumuhoji Mathew nje ya kamera?akauliza Kaiza “Ndiyo.Nataka kuzungumza naye nje ya kamera” “Kwa nini Devotha?akauliza Kaiza “Kaiza hii ni mara ya mwisho nitakuonya kuhusu kuhoji maelekezo yangu” “I’m sorry Devotha.It wont happen again” akasema Kaiza na Devotha akatoka.Kaiza akamfuata nyuma hadi katika chumba maalum kwa ajili ya kufuatilia kamera zote akawaelekeza watu waliokuwemo ndani ya kile chumba kuzima kamera zote katika chumba alimo Mathew.Olivia akaongozana na watu wanne wakiwa na silaha kuelekea chini aliko Mathew.Mlango wa chumba alimowekwa Mathew ukafunguliwa na Mathew akiwa amevishwa mavazi meupe akaonekana akiwa amekaa kwenye kiti mikono yake ikiwa imefungwa katika pingu zilizokuwa katika meza. “I need a room” akasema Devotha na watu wote wakatoka nje akabaki peke yake ndani ya kile chumba.Kila kitu ndani ya kile chumba kilikuwa cheupe akavuta kiti na kumsogelea Mathew “Hallow Mathew Mulumbi” akasema Devotha.Mathew akamtazama hakusema chochote “Kabla ya yote napenda nikujulishe kuwa kamera zote zimezimwa na hakuna hakuna yeyote anayetazama wala kusikia mazungumzo yetu.Nimefanya hivi kwa kuwa nataka tuzungumze kwa uhuru” akasema Devotha na ukimya ukapita “Naitwa Devotha Adolph” akaendelea “Ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi.Tunashughulika na mtu au kikundi cha watu wanaojaribu kuhatarisha usalama wa ndani wa nchi yetu kwa namna yoyote ile.Kama jina lake lilivyo idara yetu inafanya mambo yake kwa siri kubwa bila kujulikana.Mfano mdogo tu kama utakumbuka kwa siku za karibuni kulikuwa na viashiria vya kuibuka kwa vikundi vidogo vidogo vyenye milengo ya kigaidi hapa nchini lakini sasa hivi hakuna tetesi zozote za kuwepo kwa vikundi kama hivyo tena ni kwa sababu kila vilipojaribu kuibuka tumekuwa tunavimaliza kabla havijaleta madhara yoyote kwa nchi,hilo ndilo hasa jukumu letu kuhakikisha nchi inakuwa salama”akasema Devotha “Ninyi ndio mliomteka Olivia Themba?Mathew akauliza “Ndiyo ni sisi” akajibu Devotha “Kwa nini mlimteka Olivia?Naye ni hatari kwa usalama wa nchi?akauliza Mathew “Tutazungumza hayo baadae.Kwa sasa nataka kufahamu mahusiano yako na Olivia Themba” “Mahusiano yetu ni ya kawaida ya kirafiki”akajibu Mathew “Unaweza ukanieleza wewe na Olivia mna muda gani toka mmefahamiana? “Ni miezi kadhaa sasa sikumbuki mingapi lakini hatuna muda mrefu sana” “Mahusiano yenu ni ya kimapenzi? “Mwanzo tulianza kama marafiki wa kawaida lakini baadae tukajikuta kila mmoja akimtamani mwenzake”akajibu Mathew “Ulimpa namba Fulani Olivia ukamtaka azipige kila pale atakapokuwa katika hatari.Olivia amekwisha tueleza kila kitu hivyo usishangae nimefahamuje.Nieleze nini hasa lilikuwa lengo la kumlinda Olivia hadi ukamtengenezea program ile maalum? “Programu ile ni kwa ajili ya familia yangu.Mwanangu aliwahi kutekwa nyara na watu wasiojulikana wakatishia kumuua na kudai fedha nyingi.Baada ya hapo ndipo nilipotengeneza program ile kwa ajili ya kunijulisha kama mmoja wa wanafamilia yangu yuko katika hatari.Olivia kama mtu wangu wa karibu nilimuweka pia katika programu ile ili nifahamu pindi anapokuwa katika hatari” akasema Mathew “Why Olivia?akauliza Devotha.Mathew akamtazama hakujibu kitu “Mathew unao marafiki wengi wa karibu lakini kwa nini Olivia pekee ndiye uliyempa programu hiyo? “NI kwa sababu Olivia ni mtu wangu wa karibu sana,zaidi ya rafiki na kingine kikubwa nilihisi usalama wake uko mashakani ndiyo maana nikampa programu ile” “Kitu gani kilikufanya uhisi usalama wa Olivia uko shakani? “Baada ya kufahamiana naye niligundua alikuwa na tatizo linalomsumbua nikamtaka anieleze kitu gani kinamsumbua akaniambia ana matatizo na watu Fulani ambao hakutaka kuniweka wazi.Ili kuhakikisha anakuwa salama niliamua kumpa namba zile ili nifahamu kila pale atakapokuwa katiak hatari”akajibu Mathew “Unasema Olivia alikueleza kuwa ana matatizo na watu Fulani.Kwa nini hukutaka kuwafahamu watu wanaohatarisha usalama wa mwanamke unayempenda? “Ni kwa sababu alinihakikishia nisiwe na wasi wasi kwani ni suala lililo ndani ya uwezo wake na anaweza kulitatua hivyo sikutaka kuendelea kumghasi anieleze ni watu gani” akajibu Mathew “Kwa hisia zako unadhani watu hao ni akina nani? “Ninaamini watu aliokuwa katika matatizo nao ni wale ambao wamemteka Nyara” “Unamaanisha sisi? “Ndiyo.Naamini alikuwa katika matatizo na ninyi ndiyo maana mkamteka nyara.Olivia ninamfahamu vyema,she’s an angel hana tatizo na mtu.Ni mwanamke mwenye heshima zake na hata familia yake ni watu wanaoheshimika hapa nchini.Kitendo mlichokifanya ni uonevu mkubwa sana na ninaapa lazima nihakikishe ninamuokoa hata mkimficha wapi” akasema Mathew na Devotha akacheka kidogo. “Mkeo anafahamu mahusiano yako na Olivia?akauliza Devotha “Hayo ni masuala yangu binafsi hutakiwi kuyajua” “Mr Mathew Mulumbi nitakosea nikisema kuna mtu au watu wamekutuma umlinde Olivia?akauliza Devotha “Watu gani wamenituma nimlinde Olivia?Mathew naye akauliza “Wewe ndiye unayewafahamu.Nataka unitajie watu hao ni akina nani?akauliza Devotha.Mathew akamtazama kwa muda halafu akasema “Jina lako Devotha Adolph,right?akauliza Mathew “Yes I’m Devotha Adolph” akajibu Devotha “Devotha,kwa nini unahisi kuna mtu au watu walionituma nimlinde Olivia? Ninaonekana kama mtu ninayeweza kufanya kazi kwa malipo?Devotha inaonekana hunifahamu vyema.Mimi ni bilionea nina fedha za kutosha na siwezi kufanya kazi kwa malipo”akajibu Mathew “Mathew naamini yupo mtu au watu waliokupa kazi ya kumlinda Olivia na kuhakikisha anakuwa salama na ni hao ndio waliokupa huo ubilionea.Ninataka kuwafahamau watu hao ni akina nani? Akauliza Devotha “Narudia tena kukuhakikishia Devotha hakuna mtu au watu walinituma nimlinde Olivia.Ninamlinda Olivia na nitaendelea kufanya hivyo dhidi ya wale wote wenye kuhatarisha usalama wake.Devotha umeolewa?Una watoto wangapi?akauliza Mathew “Hayo mambo hayakuhusu Mathew.Nataka kufahamu kwa nini uchague kuhatarisha maisha yako kumlinda Olivia na si mtu mwingine? Wewe una familia yako kwa nini uamue kupoteza muda kumlinda mtu kama Olivia?Akauliza Devotha Mathew akawa kimya “Devotha umekwisha niuliza swali hilo na nimekujibu tayari” “Mathew tayari tunafahamu wewe na Olivia mmekuwa mnatumiwa na kikundi fulani cha watu katika kufanikisha mambo yao hapa nchini.Lengo letu la kuwashikilia wewe na Olivia ni kutaka kuwafahamu watu hao ni akina nani? Akauliza Devotha “Bado sijakuelewa unaposema kuna watu ambao wanatutumia mimi na Olivia.Ni akina nani watuhao?Labda jaribu kutafuta lugha nzuri ya kuuliza swali lako ili nikuelewe”akasema Mathew “Nazungumzia watu mnaoshirikiana nao ambao wanawatumia wewe na Olivia katika kufanikisha mipango yao hapa nchini.Tukiwafahamu hao ninakuhakikishia Mathew hamtakuwa katika hatari yoyote lakini kama mtaendelea kuwaficha mtaendelea kujiweka katika hatari kubwa” “Devotha kuna kitu ninakiona katika maelezo yako lakini hutaki kukiweka wazi unakizunguka.Kuwa muwazi ili nielewe unachokitaka” akasema Mathew “Mathew Olivia tayari amekwisha hojiwa na amekiri kuwa mnatumiwa na kikundi Fulani kufanikisha mipango yao hapa nchini.Sasa ni zamu yako.Ninataka na wewe unieleze kuhusiana na watu mnaoshirikiana nao na mipango yenu hapa nchini.Mathew sitaki tuanze kutumia nguvu kukutesa wakati tunaweza kulimaliza hili suala bila matumizi yoyote ya nguvu”akasema Devotha “Kidogo nimeanza kukuelewa Devotha lakini mimi na Olivia hatuna watu tunaoshirikiana nao.Kama amewaeleza hivyo amewadanganya.Kwani amesema tunashirikiana na akina nani?akauliza Mathew “Mathew tafadhali usilifanye suala hili likawa gumu kwa upande wako_Olivia tayari amekwisha eleza kila kitu na sasa ni zamu yako.Nieleze ukweli wote hakuna anayesikia Zaidi yangu ndiyo maana kamera zote zilizomo humu ndani zimezimwa hivyo usihofu kunieleza ukweli. Nieleze tafadhali akina nani mnashirikiana nao? “Devotha bado jibu langu ni lile lile kwamba hakuna mtu ninayeshirikiana naye” “Nani alikutuma umlinde Olivia? “No one” akajibu Mathew “Mathew tunafahamu umewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na kutokana na ujuzi wako umekuwa unatumiwa na watu Fulani katika kuhakikisha Olivia anakuwa salama ndiyo maana ukampa program ile maalum ya kukujulisha pindi anapokuwa katika hatari ambayo ilikusaidia kufahamu mahala alikokuwa amefichwa baada ya kutekwa na ukajipanga kwenda kumuokoa.Nataka kufahamu nani waliokupa kazi ya kumlinda Olivia? Mathew akacheka kidogo halafu akasema “Kwa nini unapenda kurudia rudia maswali ambayo nimekwisha kujibu?Kama umeishiwa maswali naomba na mimi unijibu kwa nini mmemteka Olivia?Ana mahusiano gani na usalama wa nchi?akauliza Mathew “Mathew naomba tuweke mzaha pembeni.Nchi iko katika kitisho kikubwa cha kutumbukia katika machafuko makubwa,ni wewe na Olivia ndio tunaowategemea kutusaidia katika kuliepusha hilo lisitokee.Mathew umefanya mambo mengi makubwa kwa nchi hii lakini naomba haya yote mazuri uliyoyafanya yasiharibiwe na fedha unazolipwa na IS.Mathew n……………” “Umesema IS?akauliza Mathew na kumkatisha Devotha “Ndiyo.Mbona unajifanya kustuka? “Nimestuka kusikia jina hilo likitajwa na hasa ulipotamka kuwa mambo mazuri niliyoyafanya yasiharibiwe na fedha ninazolipwa na IS.Una maanisha nini Devotha? “Mathew huu ni wakati wa kuweka wazi kila kitu.Tayari tunafahamu wewe na Olivia mnatumiwa na kikundi cha IS na wanawalipa fedha nyingi sana ambazo ndizo chanzo cha utajiri wenu mkubwa.Tunao ushahidi wa kutosha kuhusu ninyi kushirikiana na IS hivyo tuokoe muda nataka kuufahamu mtandao wenu wote hapa Tanzania na nini malengo yenu? “Devotha hicho unachonieleza kimenistua sana.Nani kawapa taarifa kuwa ninashirikiana na IS? Hiki ni kikundi cha kigaidi ninawezaje kushirikiana na magaidi?Kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya kazi ya kupambana na magaidi hawa iweje leo nibadilike na kushirikiana nao?Kingine utajiri wangu hautokani na fedha haramu bali ni utajiri halali kabisa na nimekuwa tajiri hata kabla ya kufahamiana na OIivia.Fuatilia chanzo cha utajiri wangu utajua.Aliyewapa taarifa kuwa mimi au Olivia tunashirikiana na kikundi cha IS amewadanganya.Hakuna kati yetu anayeshirikiana na IS” akasema Mathew “Mathew hatujakurupuka .Tunao ushahidi mkubwa wa jambo hili kwamba wewe na Olivia mnashirikiana na IS” akasema Devotha “Devotha nimekuwa katika kazi hizi kwa nusu ya umri wangu nilionao sasa.Nimepitia mambo mengi na ninazifahamu mbinu nyingi za magaidi hasa pale wanapotaka kutekekeleza mpango wao sehemu Fulani hutafuta namna ya kuwapoteza watu ambao wanaona watakuwa kikwazo kwao.Kama kuna mpango wowote wa kufanyika kwa shambulio la kigaidi hapa nchini basi mmenasa kwenye mtego wao na tayari wamewapoteza mwelekeo kwa kuwaaminisha kwamba ninashirikiana na kikundi cha IS” “Mathew tumefanya uchunguzi na tumegundua wewe na Olivia mmekuwa na mashirikiano na kikundi cha IS.Nchi iko katika hatari na binafsi siko tayari kukubali nchi ikaingia katika hatari.Kazi ya idara yangu ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na wananchi wake wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.Nitakutaka kwa mara ya mwisho unipe majina ya watu ambao mnashirikiana nao waliopo hapa nchini na walio nje ya nchi kabla sijafikia maamuzi ya kuufungua ukurasa mpya kati yangu nawe” akasema Devotha na kusimama “Devotha nakuomba ukae tuzungumze” akasema Mathew na Devotha aliyekuwa amesimama akaketi “Uliniambia kamera zote zilizopo katika chumba hiki zimezimwa na hakuna mtu yeyote anayefuatilia mazungumzo yetu.Nataka kujua kwa nini? Huogopi kuwa katika chumba kimoja na mtu unayedai ana mashirikiano na magaidi? “Wewe ni jasusi mzoefu,umepitia mambo mengi unafahamu mbinu zote za mateso unajua kutunza siri,sioni sababu ya kukutesa.Naamini hata ukipewa mateso ya aina gani hautaweza kutoa siri ndiyo maana nikaamua kuja hapa kuzungumza nawe kirafiki.Kuna vitu vingi ninaweza kuvipata kwako kama nikizungumza nawe ana kwa ana nje ya kamera na bila kuingiliwa na mtu yeyote” “Good.Kwa kuwa mazungumzo yetu haya ni ya kirafiki nataka tuzungumze kweli kama marafiki.Ninataka kuuliza swali na nitaomba uwe muwazi kwangu” akasema Mathew “Go ahead” “Ulisema mnao ushahidi wa kutosha kutuhusisha mimi na Olivia kushirikiana na kikundi cha IS. Yawezekana mmekuwa mnafuatilia mawasiliano yangu na mkagundua ninawasiliana na watu wa IS.Kama ndiyo niambie bila kunificha kwamba Mathew umekuwa ukiwasiliana na mtu Fulani kutoka IS na mmezungumza mambo Fulani.Kama mnao ushahidi huo nieleze tafadhali na sintakataa kama ni kweli” akasema Mathew. “Huu ni mtego.Huyu jamaa anajiamini sana.Hatuna ushahidi wowote wa kumuhusisha na IS.Nikimtazama haonekani kama ana mashirikiano nao.Hapa amenibana ngoja nimueleze ukweli” akawaza Devotha “Mathew naomba nikueleze ukweli kwamba hatuna ushahidi wa moja kwa moja wa kukuhusisha wewe na kikundi cha IS yawezekana ni kwa kuwa unafahamu sana namna ya kujificha lakini mwenzako Olivia tayari tuna kila ushahidi kwamba anashirikiana na kikundi cha IS” “Olivia anashirikiana na IS? Kivipi? akauliza Mathew akionekana kushangaa “Mstuko huu ni wa kweli au anaigiza? Akajiuliza Devotha baada ya kuuona mstuko katika uso wa Mathew aliposikia Olivia anashirikiana na IS “Tulipata taarifa za kiintelijensia kwamba Olivia amekutana na Seif Almuhsin jijini Kinshasa.Seif Almuhsin ni mmoja kati ya watu muhimu katika kikundi cha IS na anatajwa kuwa ndiye anayeendesha zoezi la usajili wa vijana wanaojiunga na IS kisha kupelekwa katika kambi za mafunzo kuandaliwa kwa mambo ya kigaidi.Olivia na Seif walifikia hoteli moja jijini Kinshasa”akasema Devotha na kumuonyesha Mathew picha za Olivia akiwa na Seif Almuhsin jijini Kinshasa.Mathew alishangaa sana “Kitendo cha Olivia kukutana na Seif Almuhsin jijini Kinshasa” akaendelea Devotha “Kilitupa maswali mengi na tukaanza kumfuatilia kujua kama ana mahusiano na magaidi wa IS.Aliporejea nyumbani kutokea Kinshasa tulimteka nyara na baada ya kupekua mawasiliano yake tukagundua amekuwa na mawasiliano na mtu anaitwa Sayid Omar” “Sayid Omar?Who is he? Mathew akauliza “Mathew sipendi mzaha.Humfahamu Sayid Omar?akauliza Devotha “Devotha hizi ni taarifa mpya kabisa kwangu ninazisikia kwa mara ya kwanza toka kwako” akasema Mathew “Sayid Omar ni mfanya biashara mkubwa na anatajwa kuwa ni mfadhili mkubwa wa kikundi cha IS.Tumekuta mawasiliano ya barua pepe kati yake na Olivia katika kompyuta ya Olivia” “Subiri kidogo Devotha,walikuwa wanawasiliana kuhusu nini?akauliza Mathew “Hatujaweza bado kufasiri mazungumzo yao kwani wametumia lugha ya kiarabu.Kwa bahati mbaya katika idara yetu tulikuwa na mtu mmoja tu aliyekuwa na umahiri katika lugha ya kiarabu na kwa sasa hayupo hivyo tumeshindwa kujua ambacho Olivia na Sayid walikuwa wanawasiliana hadi hapo tutakapompata mtu anayeifahamu vyema lugha hiyo”akajibu Devotha “Ninaweza kuyaona mawasiliano hayo?akauliza Mathew na Olivia akamtazama “Nina ifahamu vyema lugha ya kiarabu.Ninaweza kuyaona mazungumzo yao nikakusaidia kujua walikuwa wanaongelea nini? akasema Mathew Devotha akaendelea kumtazama Mathew kwa makini “Tafadhali niamini Devotha.Nionyeshe barua pepe hizo tujue nini hasa walichokuwa wanawasiliana” akasema Mathew.Devotha akafungua mojawapo ya faili katika kompyuta yake na kumuonyesha Mathew ambaye aliisoma halafu akasema “Katika barua pepe hii Sayid Omar anamuuliza Olivia kuhusiana na maendeleo ya mpango wa kutengeneza kirusi.Olivia anamjibu kwamba anaendelea vizuri na uandaaji wa kirusi” akasema Mathew huku mstuko mkubwa ukionekana usoni pake. “Una uhakika walikuwa wanawasiliana kuhusu kirusi?akauliza Devotha naye akionekana kushangaa “Ndivyo inavyosomeka hapa” akajibu Mathew Devotha akafungua tena barua pepe nyingine akamuonyesha Mathew akaisoma “Katika barua pepe hii,Sayid anamkumbusha Olivia kua taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya mradi wa kutengeneza kirusi.Olivia anamjibu kwamba anaendelea vyema na utafiti wake na amefikia sehemu nzuri.Katika hii barua pepe nyingine Sayid anamkumbusha Olivia ajitahidi kufanya haraka kukamilisha kirusi kwani muda unakwenda na operesheni itaanza mara moja.Olivia anamjibu kwamba yuko katika hatua za mwisho za majaribio ya kirusi” “My God ! Kumbe huu ni mpango wa IS” akasema Devotha kwa sauti ndogo “Devotha unafahamu chochote kuhusiana na hiki kinachozungumzwa katika barua pepe hizi? Una hakika barua pepe hizi zinatoka kwa Olivia Themba?akauliza Mathew.Devotha akamtazama halafu akasema “Mathew usiniambie hulifahamu jambo hili” akasema Devotha. “Devotha sikulazimishi uniamini lakini hii nakwambia ukweli,hii ni mara ya kwanza ninalifahamu jambo hili.Nimekuwa karibu na Olivia kwa miezi kadhaa sasa lakini sikuwahi kuhisi kama anaweza akafanya kitu kama hiki.Nimestuka sana Devotha.Naomba tafadhali unieleze nini hasa kinachoendelea hapa?akauliza Mathew lakini Devotha hakuonekana kumuamini “Please Devotha tell me what’s going on.Olivia ni mtu muhimu sana kwangu hivyo nataka kujua kama kweli anashirikiana na magaidi wa IS.Nataka kujua mipango wanayoipanga.Tafadhali Devotha” akaomba Mathew. “Sawa nitakueleza.Tulipofahamu kuwa ana mawasiliano na Sayid Omar tulitaka atupe maelezo ya kina kuhusu Sayid na akatupa namba ambazo alituambia zitatusaidia kufahamu alipo Sayid Omar na baada ya kupiga namba zile ndipo mfumo wetu wote wa mawasiliano ukajifunga hakuna kompyuta iliyofanya kazi tena.Ili kufungua mfumo wetu ilihitaji namba maalum na Olivia aligoma kutupa namba hiyo hadi atakapoona na Rais.Nilifanya mpango wa kumkutanisha na Rais wakazungumza ndipo Olivia alipomstua Rais kwa kumwambia eti anamtaka Edger Kaka” “Edger Kaka?Mathew akashangaa “Edger Kaka aliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na alifariki katika ajali ya gari miaka mitatu iliyopita” akasema Devotha “Wakati suala hili linatokea nilikuwa nje ya nchi” akasema Mathew “Olivia ameibuka na kudai kuwa Edger Kaka hakufariki katika ile ajali bali yuko hai” “Yuko hai?Kivipi?Mathew akauliza “Anadai kuwa ni mchezo ulichezwa lakini Edger hakufa katika ile ajali” “Ana uhakika gani kuwa Edger hajafariki?Mathew akauliza “Anadai kuwa amefanya uchunguzi wake akagundua kuwa mwili ule uliozikwa ambao wote tuliamini ni wa Edger haukuwa mwili wa Edger.Olivia alimlenga moja kwa moja Rais Dr Evans kuwa anafahamu aliko Edger Kaka na ili kumshinikiza aweze kumuonyesha mahala alipo alitengeneza virusi ambavyo amemuambukiza Coletha mtoto wa rais na kama Rais asipotekeleza maagizo ya Olivia katika muda aliompatia basi mwanae atapoteza maisha.Nimestuka baada ya kugundua kuwa kumbe mpango huu ameshirikiana na IS kutokana na ushahidi tulioupata kutoka katika barua pepe hizi alizokuwa anawasiliana na Sayid Omar.Tuliamini Olivia alikuwa anatumiwa na wanasiasa kutaka kumchafua rais na serikali yake lakini kumbe ni IS walio nyuma ya mpango huu na Olivia anatumika tu” akasema Devotha “Devotha sasa nimekuelewa kwa nini mlimteka Olivia.Ninakuhakikishia sikuwa nikifahamu chochote kuhusiana na Olivia kushirikiana na IS.Nimestushwa mno na hiki nilichokifahamu.Olivia alinieleza ana matatizo na watu Fulani lakini ni tatizo analoweza kulimaliza.Kwa kuwa ni mtu wangu wa karibu nikampa namba zile za programu maalum ya kuniwezesha mimi kufahamu mahala alipo kila pale atakapokuwa amepatwa na matatizo.Nikiwa mkutanoni Arusha nikapokea ujumbe kutoka katika ile namba niliyompa Olivia.Baada ya kufuatilia nikagundua kuwa Olivia alikuwa ametekwa nyara.Programu ile ilinionyesha mahala namba ile ilikopigwa hivyo ikanilazimu kuondoka Arusha haraka sana kurejea Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kumuokoa Olivia na nilikua naendelea na harakati za kumuokoa hadi pale na mimi nilipotekwa asubuhi ya leo kufuatia mtego mlioweka mkishirikiana na Lucy Themba mke wa Agrey Themba.Sikuwa nikifahamu kama Olivia ana siri kubwa namna hii”akasema Mathew “Tulikuchukua kwa vile u mtu wa karibu na Olivia na tuliamini mnashirikiana na kazi yako kubwa ni kuhakikisha anakuwa salama.Ulifahamu mahala alikofichwa Olivia baada ya kutekwa na ukawa mbioni kwenda kumuokoa na katika harakati hizo za kumtafuta uliua watu wetu kumi na tatu kitu ambacho hakijawahi kutokea toka idara hii toka ilipoanzishwa.Kwa gharama zozote zile ilikuwa lazima tukupate kwani tayari ulikwisha kuwa mtu hatari kwetu na ulikuwa mbioni kuharibu mipango yetu yote” akasema Devotha “Devotha nakuhakikishia mimi siwezi kuwa na mahusiano na IS na wala sikujua kama Olivia ana mahusiano na watu hao.Kama ningefahamu ana mahusiano nao ningekwisha mmaliza mwenyewe kitambo sana kwani siwapendi magaidi.Samahani kwa tukio la jana lakini nilifanya tukio lile bila kujua kama wale ni watu wenu,nilijua ni kikundi cha watu wanaoteka watu kwa lengo la kujipatia fedha.Naomba uniamini Devotha” akasema Mathew “Mathew hivi tunavyoongea mtoto wa Rais yuko hospitali na kuna hatari anaweza akapoteza maisha endapo Rais hatamueleza Olivia mahala alipo Edger Kaka.Nimezungumza na Olivia asubuhi hii na ameendelea kusisitiza kuwa Edger yuko hai na Rais Dr Evans anafahamu mahala alipo.Kutokana na msisitizo huo niliamua kulifanyia uchunguzi jambo hilo kuufahamu ukweli wake lakini baada ya kufahamu kuwa ni jambo linalowahusisha pia IS nimeishiwa nguvu ya kuendelea kulichunguza hili suala.Nimeanza kuyaamini maneno ya Rais kuwa huu ni mpango maalum wa kutaka kuleta machafuko hapa nchini.IS wanatambua Edger alikuwa na watu wengi sana wanaomuunga mkono hasa vijana unadhani nini kitatokea wakisikia kuwa Edger yuko hai na serikali ndio wanaomshikilia?Ni wazi kutatokea machafuko makubwa na hicho ndicho wanachokitaka IS ili waweze kujipenyeza na kufanya mambo yao.Ahsante sana Mathew kwa kunisaidia kufahamu mawasiliano ya Olivia na Sayid.Sina haja ya kuendelea tena kulichunguza jambo hili kwani ni moja ya mipango ya IS kutaka kuleta machafuko hapa nchini na hakuna ukweli wowote” akasema Devotha “Devotha nisikilize.Kuna maswali ambayo nimejiuliza kufuatia maelezo yako.Kwanza kuna nini kati ya IS na Edger Kaka?akauliza Mathew “Mathew huu ni mchezo unataka kuchezwa na IS.Hakuna ukweli wowote katika suala hili.Edger kaka amekwisha fariki muda mrefu wanataka kuzua mtafaruku katika jamii na kuleta machafuko.Wanajua Edger alikuwa anapendwa na watu na kifo chake kiliwahuzunisha wengi hivyo wakija na taarifa kuwa Edger yuko hai na anashikiliwa na serikali moto mkubwa utawaka” akasema Devotha “Devotha ninakushauri endelea kulichunguza hili suala hadi uufahamu ukweli wake”akasema Mathew “Mathew hakuna haja ya kupoteza nguvu kufanya uchunguzi wakati tayari ukweli umekwisha bainika kuwa huu ni mpango wa IS na lengo lao ni kutaka kuleta machafuko nchini na wao kupata mwanya wa kupenya.Kitu kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa lengo lao halifanikiwi na hakuna machafuko yatakayotokea”akasema Devotha “Devotha ninakushauri uendelee kulichunguza hili jambo kwa sababu kuna kitu ninakiona ndani yake.Hebu jiulize kuna nini kati ya IS na Edger Kaka? Kwa nini Olivia ajiunge na IS katika mpango huu? Kwa nini IS waibuke sasa na kudai Edger hajafa? Nini wanakitafuta hapa nchini je ni kuleta machafuko kama unavyodai? Ni wazi kuwa mashabiki wa Edger wakisikia kuwa yuko hai na anashikiliwa na serikali moto mkubwa utawaka.Je lengo lao ni hilo? Lakini tunapaswa kujiuliza vile vile je ni kweli Edger yuko hai? http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Kama kweli yuko hai yuko wapi? Umeniambia kwamba Olivia amemlenga Rais kuwa anafahamu mahala alipo Edger na ndiyo maana akatengeneza virusi maalum na kumuambukiza mtoto wake je ni kweli Rais analifahamu jambo hili? Hadi utakapoyapatia majibu maswali hayo ndipo utafikiria kuachana na suala hili lakini kwa sasa ni suala muhimu mno na linatakiwa kuendelea kuchunguzwa hadi majibu yake yapatikane” akasema Mathew “Mathew hili jambo kweli ni kubwa kama ulivyosema na limejaa maswali mengi magumu kuyapatia majibu.Nilipozungumza na Olivia alinieleza kuwa anayo siri kubwa na kama ninataka kuifahamu basi nimpatie taarifa alipo Edger Kaka” akasema Devotha “Unaamini anayo siri hiyo?akauliza Mathew “Kwa kumtazama machoni utagundua Olivia anayo siri kubwa” “Kama unaamini Olivia anayo siri kubwa na atakueleza siri hiyo pale utakapofanikisha kupata taarifa alipo Edger Kaka basi endelea na uchunguzi hadi uhakikishe umeupata ukweli kama kweli yuko hai au amekufa”akasema Mathew na ukimya ukatawala.Mathew akauvunja ukimya “Devotha naamini ninyi ndio mliomteka Agrey Themba baba yake Olivia.Unaweza ukaniambia sababu ya kumteka? “Mathew hayo ni mambo ambayo hupaswi kuyafahamu na ninaomba tafadhali usiniulize chochote” “Mlitaka kumtumia ili kumfanya Olivia aongee kila kitu,ninazifahamu mbinu hizi.Mlifanikiwa?akauliza Mathew “Mathew shut up!! Akafoka Devotha “Devotha I can help you.Ninaweza kumfungua Olivia na kumfanya afunguke na kueleza kila kitu.Tafadhali kubali nikusaidie katika suala hili.Kuniweka humu ndani hakutasaidia chochote mimi sina mahusiano yoyote na IS kama mlivyoaminishwa.Nisaidie nitoke humu ndani na ninakuahidi kuupata ukweli wa suala hili.Nipe nafasi ya kumuhoji Olivia na ataeleza kila kitu” “Mathew japo umejitahidi sana kunishawishi kuwa hauhusiki kwa namna yoyote na Olivia lakini bado haiwezi kunifanya nikuamini.Nitaendelea na uchunguzi wangu wa suala hili na kuufahamu ukweli na kama hauhusiki na mtandao wa IS.Sikuahidi utaachiwa huru kwa sababu umefanya mauaji makubwa ya watu wetu kumi na tatu,umekwisha zifahamu siri zetu hivyo utaendelea kukaa sana huku shimoni.Kwa taarifa yako ni kwamba hapa ulipo ni mita mia mbili chini ya ardhi hivyo hautaweza kutoka kamwe”akasema Devotha “Devotha tafadhali naomba uniamini.Ni makosa makubwa mnayafanya kuniweka humu ndani wakati nchi iko katika hatari.IS wana mipango mikubwa hapa nchini na mtu kama mimi ninaweza kuwa na msaada mkubwa kwa nyakati kama hizi! Akasema Mathew “Mathew nimekwisha kueleza kuwa hakuna namna utakayoweza kutoka humu.Omba sana Mungu akusaidie lakini kutoka humu sahau” akasema Devotha “Devotha !” akaita Mathew “Mathew please !” akasema Devotha kwa ukali “Devotha hata kama maisha yangu yataishia ndani ya shimo hili lakini naomba nisaidie katika jambo hili.Naomba unisikilize japo kwa dakika mbili” Akasema Mathew. “Nini unataka kuniambia Mathew? Akauliza Devotha “Mchunguze Rais” “Nimchunguze Rais? “Ndiyo.Kama Olivia ameelekeza jambo hili kwake na kudai anafahamu kila kitu kuhusu Edger basi sehemu ya kuanzia uchunguzi ni kwa Rais.Dukua simu yake na fuatilia mawasiliano yake wiki moja kabla ya Edger kupata ajali na wiki moja baada ya ajali.Angalia amewasiliana na watu gani na utapata jibu kama kweli anafahamu kuhusu jambo hili” “Mathew huo ni mtihani mgumu sana.Kudukua simu ya Rais si kitu kidogo” “Nafahamu ni jambo zito lakini ndiyo sehemu pekee ya kuanzia uchunguzi wa hili jambo.Kama ukigundua Rais anafahamu jambo hili itakuwa rahisi kwako kujua mahala alipo Edger na kama hajui basi utakuwa ni mwanzo mzuri pia wa kutafuta ukweli kupitia Olivia kwa nini wamemlenga Rais” “Mathew ahsante kwa ushauri huo nitautafakari” akasema Devotha “One more thing” akasema Mathew “Jambo gani Mathew? “Ninayo timu yangu ambao ni watu wenye uwezo mkubwa.Mmoja anaitwa Papii Gosu gosu na mwingine anaitwa Ruby.Hawa wanaweza wakakusaidia mno katika uchunguzi wako.Ukihitaji msaada muda wowote watafute hao kuanzia saa kumi na mbili jioni ya leo utawata nyumbani kwangu watakuwa wamewasili kutoka nje ya nchi.Nitakuelekeza nyumbani kwangu na nitakupa pia namba ya simu ya nyumbani kwangu utapiga na kuzungumza nao” akasema Mathew na kumpatia Devotha namba za simu za nyumbani kwake na Devotha akainuka ili aondoke lakini akakumbuka kitu “Mathew ile programu uliyompa Olivia iliufunga mfumo wetu wa mawasiliano.Ili kuufungua kunatakiwa namba maalum.Hakuna tena ulazima wa kuendelea kuushikilia mfumo wetu wakati kila kitu unakifahamu.Nipe namba za kuufungua mfumo wetu” akasema Devotha.Mathew akampa namba za kuufungua mfumo ule Devotha akatabasamu na kuinuka akaelekea mlangoni akabonyeza kengele mlango ukafunguliwa akamkuta Kaiza akiwa na walinzi wakimsubiri. “Mpelekeni Mathew A3”Devotha akawaelekeza walinzi na kumtaka Kaiza waondoke “Devotha why A3?akauliza Kaiza lakini Devotha hakumjibu kitu wakaelekea katika lifti kupanda juu “Kaiza ofisini kwangu tafadhali” akasema Devotha baada ya kushuka katika lifti.Waliingia katika ofisi ya Devotha akafunga mlango “Kaiza nilikuonya awali kuhoji maamuzi yangu.Kwa nini kila nikifanya maamuzi yangu unanihoji?Who is the boss here?akauliza Devotha “Wewe ndiye mkubwa Devotha.Samahani nilistuka kidogo ulipoelekeza Mathew apelekwe A3 ambako ni sehemu maalum kwa ajili ya viongozi.A3 ni sehemu ya starehe sehemu iliyotengwa maalum kwa ajili ya watu wakubwa kuhifadhiwa pale wanapokuwa katika hatari na mtu kama Mathew ambaye anashirikiana na IS na ameua watu wetu kumi na tatu hakustahili kupewa heshima hiyo ya kukaa sehemu ya kustarehe kama yuko nyumbani kwake.Samahani sana Devotha kama nimekukwaza kwa kuuliza lakini nadhani Mathew hastahili kwenda A3” akasema Kaiza “Kaiza mimi ndiye mwenye maamuzi ya mwisho hapa hivyo sitaki wewe wala Rais au mtu mwingine yeyote ahoji maamuzi yangu,umenisikia? “Nimekusikia Devotha” “Good.This is the last warning.Muite Leon haraka sana” akasema Devotha na Leon mtaalamu mkuu wa mifumo yote ya mawasiliano akaitwa. “Leon nimepata namba za kuufungua mfumo wetu wa zamani” akasema Devotha na kumpatia namba zile akajaribu kuifungua kompyuta ya Devotha ikafunguka na wote wakatabasamu “Rudisheni mfumo wa zamani na huu mpya mnaoendelea kuushughulia ukae kama akiba ila wekeni kinga kubwa katika mfumo mpya hata ule wa zamani ili asitokee mtu akafanya kitu kama hiki walichokifanya Mathew na Olivia” akasema Devotha “Leon tazama pia kama watu hawa watakuwa wamepata taarifa zetu zozote” akasema Kaiza wakati akitoka na Leon ofisini kwa Devotha “Mathew hana mahusiano yoyote na IS.Maelezo aliyonipa nimeyaamini.Hakumfahamu Olivia kama ana mahusiano na kikundi cha IS.Ninamfahamu mtu anayesema ukweli na sina mashaka Mathew anasema kweli.Lengo lake lilikuwa ni kumlinda Olivia na niliuona mstuko alioupata baada ya kusikia kuwa Olivia ana mahusiano na IS.Hata hivyo ataendelea kukaa hapa hadi hapo mambo haya yatakapokwisha kwani akitoka atavuruga kila kitu katika uchunguzi wa suala hili.Nashukuru amenisaidia kufahamu suala la Edger Kaka limetoka kwa IS.Kinachoniumiza akili yangu hata kama ni mpango wa IS je ni kweli Edger yuko hai? Kama yuko hai yuko wapi? Kama you hai kwa nini IS waliibue suala hili?Watafaidika na nini kama Edger akipatikana? Kwa nini Rais Dr Evans awe ndiye mlengwa mkuu katika suala hili? Hawawezi kuibuka na kumlenga Rais moja kwa moja kama hakuna anachokifahamu.Kuna siri kubwa iko hapa kama alivyosema Olivia ambayo lazima niifahamu na kuipata siri hiyo lazima kwanza nifahamu mahala alipo Edger kama kweli yuko hai” akawaza Devotha na kuelekeza macho yake dirishani “Mathew amenipa ushauri mzuri kama nikitaka kulichunguza suala hili nianzie kwa kumchunguza Rais Dr Evans.Natakiwa kudukua mawasiliano yake na kujua amekuwa anawasiliana na nani hasa katika tarehe zile Edger alipopata ajali.Nahitaji kumpata mtu atakayenisaidia kudukua mawasiliano ya Rais.Hili jambo kubwa na la siri kwani kama nikibainika maisha yangu yatakuwa yameharibika na Rais hatakuwa na msamaha na mimi hata hivyo siwezi kuogopa nitafanya uchunguzi na lazima nidukue simu ya Rais.Nitahitaji mtu ambaye ni msiri atakayeifanya hii kazi” akawaza Devotha na kuzama mawazoni halafu akampigia simu Saada Amiri. “Madam Director” akasema Saada baada ya kupokea simu “Saada naomba uje ofisini kwangu mara moja”akasema Devotha.Baada ya dakika chache Saada akafika “Saada chukua kompyuta yako na vifaa vyako vyote tunaondoka” akasema Devotha na Saada akaenda kuchukua vifaa vyake akarejea katika ofisi ya Devotha wakatoka. “Tunakwenda wapi madam Devotha?akauliza Saada “Kuna kazi Fulani tunakwenda kuifanya” akasema Devotha. “Niko tayari madam Devotha”akasema Saada na Devotha akaondoa gari “Saada wewe ni mtu ninayekuamini kuliko wote katika idara yetu.Kuna kazi ambayo nataka tuifanye lakini ni kazi ngumu kidogo na inahitaji ujasiri na usiri mkubwa” akasema Devotha “Madam usiwe na hofu na mimi niko tayari kwa kazi yoyote ile hata kama ni ya hatari” akasema Saada “Tunakwenda ikulu kudukua simu ya Rais” akasema Devotha na Saada akaonyesha mstuko kidogo “Kudukua simu ya Rais? “Ndiyo nataka tudukue simu ya Rais.Wewe ndiye mdukuzi pekee ninayekuamini” akasema Devotha “Madam Devotha unaweza ukanieleza kwa nini tudukue simu ya Rais? “Kuna taarifa Fulani za muhimu sana ninazitafuta na hakuna sehemu nyingine ya kuzipata bali katika simu ya Rais” “Nimeingiwa na hofu kidogo baada ya kusikia kwamba natakiwa kudukua simu ya Rais.Hili ni jambo la hatari sana” akasema Saada “Usiwe na hofu Saada.Hautaingia katika hatari yoyote.Katika jukumu letu la kulinda usalama wa nchi kuna nyakati tunajikuta tukilazimika kufanya mambo ya hatari sana kama haya lakini lengo ni kuiweka nchi salama.Are you ready?akauliza Devotha “Yes madam I’m ready” akasema Saada ingawa sura yake ilionyesha wasi wasi.Devotha akasimamisha gari pembeni ya barabara akashuka upande wa dereva kumuachia Saada aendeshe akatoa simu na kumpigia Dr Evans “Devotha mambo yanakwendaje?akauliza Dr Evans baada ya kupokea simu “Mheshimiwa Rais nimekupigia ninahitaji kukuona kuna suala la dharura nataka tulijadili” akasema Devotha. “Devotha suala hilo haliwezi kusubiri? “Hapana mheshimiwa Rais haliwezi kusubiri.Nahitaji kukuona tuzungumze” akasema Devotha “Sawa Devotha njoo ninakusubiri” akasema Dr Evans na kukata simu “Tunakwenda ikulu kuonana na Rais.Tukifika nitamtaka tukazungumze naye katika chumba cha faragha na wewe ukiwepo na tukiingia ndani ya chumba hicho wakati mimi nikizungumza naye wewe utaendelea na zoezi lakuunganisha simu yake na programu ya kuidukua” akasema Devotha “Hilo halina tatizo madam Devotha,progamu ninayotaka kuitumia kujiunganisha na simu ya Rais ni ile ya kujiunganisha na simu ukiwa naye karibu bila yeye kujua.Haihitaji kuipata simu yake na kuingizaprogramu.Swali langu ni vipi kama Rais hatakuwa na simu yake wakati ukizungumza naye?Nivipi kama atakuwa ameiacha simu yake ofisini au iko kwa mlinzi wake?akauliza Saada “Nimekuwa na ukaribu na Rais nimekwisha msoma vyema.Simu yake hupenda kuiweka katika mfuko wa ndani wa koti.Hana kawaida ya kuacha simu yake ofisini au kumpa mlinzi wake hivyo nina uhakika mkubwa kwamba hata tutakapokuwa tunazungumza naye atakuwa na simu yake” akasema Devotha “Madam nitakuomba tukiingia ndani ya hicho chumba nawe uzime simu yako ili niwe na kazi ya kuitafuta simu moja tu ya Rais” “Usihofu kuhusu hilo Saada” akasema Devotha na Saada akaongeza mwendo wa gari “Mpaka sasa sijapata jibu kwa nini IS waje na mpango huu wa kudai Edger hajafariki dunia.Nini hasa wanakilenga katika mpango wao huu?Ni kuleta machafuko?Kuichafua serikali?Nini hasa wanakitafuta? Akajiuliza Devotha “Baada ya kuidukua simu ya Dr Evans nitaupata ukweli kama kweli anahusika na jambo hili au hahusiki.Yeye ndiye mlengwa namba moja ambaye wanatumia nguvu kumlazimisha aonyeshe mahala alipo Edger.Kama atakuwa anafahamu chochote kuhusu suala hili tutafahamu kupitia mawasiliano yake yake na nitampa taarifa hizo Olivia ili anipe siri aliyonayo anayodai ni kubwa.” akaendelea kuwaza Devotha Waliwasili ikulu kwa ajili ya kuonana na Rais “Saada we’re here.Get ready” Devotha akamweleza Saada walipowasili ikulu “Wow ! ni pazuri mno.Ni mara yangu ya kwanza kufika mahala hapa” akasema Saada huku akitabasamu Rais DrEvans alikuwa na ratiba iliyombana sana siku hii alikuwa na wageni wengi aliohitaji kuonana nao na kazinyingine mbalimbali hivyo bila kupoteza muda baada ya akina Devotha kuwasili wakaelekea moja kwa moja katikachumba cha mazungumzo ya faragha “Devotha mtanisamehe leo nina muda mfupi sana ratiba yangu imenibana mno hivyo naomba twende moja kwa moja katika kitu kile cha msingi unachotaka kunieleza” akasema Dr Evans “Samahani pia mheshimiwa Rais kwa ujio huu wa dharura lakini hatutachukua muda mrefu” akasema Devotha “Devotha mambo mengine si lazima uje kuonana nami tunaweza kuzungumza kwenye simu hakuna tatizo lolote.Siyo kila wakati lazima tuonane.Halafu watu wanaweza kuanza kuhisi kuna nini kati yetu.Idara yako ni ya siri sana tusiwape watu nafasi ya kuhoji mambo hadi wakaifahamu.Nini hasa kikubwa Devotha?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais nilisahau kukutambulisha.Huyu anaitwa Saada Amir ni mmoja wa watu wangu ninaowaamini sana.Ni mara ya kwanza anafika hapa” akasema Devotha “Saada karibu sana”akasema rais “Ahsante sana mheshimiwa Rais” akajibu Saada.Akafungua mkoba wake na kutoa kompyuta akaiweka mapajani na kufungua programu ambayo ilianza kuitafuta simu ya Rais bila yeye kufahamu. “Mheshimiwa Rais kilichonileta hapa nilitaka tujadiliane kuhusu AgreyThemba” “Kuna nini kuhusu Agrey? Akauliza Dr Evans “Tulimchukua Agrey kwa lengo la kusaidia kumfungua Olivia lakini mpango wetu unaonekana kushindwa kufanikiwa.Olivia amegoma kabisa kufunguka hata baada ya baba yake kupigwa risasi” “Unataka kusemaniniDevotha? “Nimekuja tujadiliane hatima ya Agrey Themba.Binafsi sioni sababu ya kuendelea kumshikilia na kuzua taharuki katika jamii” akasema Devotha Katika kompyuta ya Saada ulisikika mlio na ujumbe ukajitokeza “New device found” Kwa wepesi wa aina yake Saada akaendelea kucheza na kompyuta yakehalafu akakohoa kidogo.Devotha akaitambua ishara ile kuwa tayari zoezi la kuiunganisha simu ya Rais lilikamilika. “Saada tafadhali unaweza ukamsubiri mkuu wako hapo nje nataka kuzungumza naye kwa dakika chache” akasema DrEvans na Saada akainuka akaiweka kompyuta yake katika mkoba akatoka nje. “Devotha kamwe usithubutu kuwaza suala la kumuachia Agrey Themba.Utakuwa umefanya kosa kubwa sana kwani mipango yetu yote itaharibika.Ataeleza kila kitu kilichomtokea.Nilikwisha kueleza kuwa huu ni mwisho wa Agrey Themba kwani pale tutakapokuwa hatuna matumizi naye tutamuua kwa sababu lazima atafahamu kuwa mimi niko nyuma ya jambo hili nahii inaweza kuleta mtafaruku mkubwa mno hivyo Agrey tayari ni mfu.Nadhani umenielewa Devotha” akasema Dr Evans “Sawa nimekuelewa Dr Evans” “Devotha,mwanangu yuko hospitali hali yake hairidhishi hata kidogo ingawa madaktari wako katika harakati za kutafuta tiba kutokana na virusi alivyoambukizwa na Olivia.Nina hasira sana na Olivia kwa ukatili mkubwa aliomfanyia mwanangu.Coletha hana kosa lolote alilolifanya kwa Olivia kumtendea hivi.Hicho anachokisema kuhusu Edger Kaka ni kitu kigeni kabisa kwangu na sifahamu chochote.Alitakiwa anifuate mimi mwenyewe aniulize kuhusu jambo hilo kuliko kuanza kutesa familia yangu bila kosa.Nataka umfungue Olivia,nataka aeleze sababu za kwa nini wametunga uongo huu mkubwa na kuuelekeza kwangu akidai kuwa ninafahamau alipo Edger Kaka.Kama hatakuwa tayari kufunguka nitaiteketeza familia yake yote pamoja na yeye mwenyewe.Sina mzaha katika hili !! akasema DrEvans na sekunde kadhaa zikapita za ukimya “Devotha nataka nikikupigia simu jioni ya leo uwe tayari na taarifa kutoka kwa Olivia.Umenielewa Devotha? “Nimekuelewa mheshimiwa Rais” akasema Devotha “Good.Vipi kuhusu Mathew?Tayari mmeshaanza kumuhoji? “Kwa sasa tumeanza kumtesa kihisia ili kutengeneza mazingira ya woga.Baadae tutaanza kumuhoji” “Vizuri.Hakikisha kila kitu kinakwenda kama nilivyokuelekeza Devotha.Nataka kabla ya siku ya leo kuisha tuwe tumepata majibu yote.Kuna lingine unataka kunieleza? akasema Dr Evans “Mheshimiwa Rais lililonileta ni hilo tu la Agrey Themba.Samahani kwa kukupotezea muda sikutaka kulizungumza jambo kama hili simuni.Nitafuata maelekezo yako” “Good.Jitahidi kila pale unapokuwa na tatizo kunipigia simu kama nitaona kuna ulazima wa kuonana nitakujulisha lakini si kila wakati lazima tuonane” akasema Dr Evans na kuinuka wakatoka ndani ya kile chumba na kumkuta saada akiwa nje akisubiri.DrEvans akaagana nao wakaondoka “Saada natakakujua kama mpango wetu ulifanikiwa” akauliza Devotha wakielekea katika gari “Kila kitu tayari madam Devotha.Nilikupa ishara naamini uliielewa” “Niliewa ishara uliyonipa.Nilitaka tu kujiridhisha kuwa kila kitu kimekwenda vizuri” akasema Devotha wakaingia garini na kuondoka. “Saada thank you so much for doing this.Nimesababisha ukafanya jambo la hatari kubwa lakini ni kwa ajili ya usalama wa nchi” “Usijali madam Devotha.Hii ni kazi yangu na sijutii kuifanya” akasema Saada Kutoka ikulu walielekea moja kwa moja nyumbani kwa Devotha “Madam nyumba yako ni nzuri sana sikujua kama unaishi sehemu nzuri kama hii” akasema Saada akitabasamu.Devotha akampeleka katika chumba chake cha ofisi “Hii ni ofisi yangu ndogo ya nyumbani.Utafanyia kazi zako hapa” akasema Devotha “Niko tayari kwa kazi madam.Nielekeze nini hasa unachokitaka” akasema Saada akiendelea kubonyeza kompyuta yake harakaharaka.Devotha akaingia mtandaoni kutafuta tarehe aliyofariki Edger kaka.Akaandika kijikaratasi na kumpatia Saada. “Nataka kujua mawasiliano ya Rais katika tarehe hizo” akasema Devotha na Saada akaanza kazi.Devotha akamuacha saada akiendelea na kazi akaenda chumbani kwake “Dr Evans amedhamiria kabisa kumuua Agrey Themba.Hanakosa lolote yule mzee.Ninawaza namna ya kumsaidia ili kuokoa maisha yake.Ngoja kwanza niachane na mawazo hayo kwa sasa nijielekeze katika jambo moja tu kuutafuta ukweli kuhusu Edger kaka.Leo lazima ukweli ujulikane kama Edger yuko hai kama anavyodai Olivia na kama Rais analifahamu jambo hili” akawaza na kwenda kusimama dirishani akatazama nje “Kitu gani IS wanapanga kukifanya hapa nchini hadi waje na mpango kamahuu wa kudai Edger yuko hai? Kwa nini Edger Kaka?Wana maslahi gani na jambo hili?akajiuliza “Naamini hawawezi wakapanga jambo kama hili liwe la kweli au si kweli kama halina maslahi makubwa kwao.Nitahakikisha ninalichunguza jambo hili hadi niufahamu ukweli wake na sehemu pekee ya kuanzia ni kwa kufahamu kama kweli Edger yuko hai” akawaza Devotha
Rais Dr Evans akiwa katika mazungumzo na wageni waliofika kumtembelea akaingia mmoja wa walinzi wake akamnong’oneza kitu sikioni.DrEvans akawaomba radhi wageni wale na kuwaahidi atawakaribisha siku nyingine kwa mazungumzo kuna suala la dharura anahitaji kulishughulikia.Akaagana nao wakaondoka “Nini kimetokea Richard? Umenistua sana”akauliza DrEvans “Kuna kitu kimetokea mheshimiwa Rais.Naomba tukazungumze katika chumba cha siri” akasema Richard na kumuongoza Rais hadi katikachumba cha mazungumzo ya siri ambamo kulikuwa na watuwawili “Isaack,Bakari kuna nini kimetokea?akauliza DrEvans kwa wasiwasi “Samahani mheshimiwa Raiskuna jambo limetokea tukaona ni vyema ukalifahamu kwa haraka”akasema Isaack “Nini kimetokea? Akauliza DrEvans na mlinzi wake akamvutia kiti akaketi “Mheshimiwa Rais simu yako imeunganishwa na mfumo maalum ili kuzuia isiingiliwe na wadukuzi hivyo kuifanya iwe salama muda wote.Mfumo huo unaweza kutambua haraka sana kama kuna mtu anajaribu kutaka kudukua simu yako,au ya makamu wa Rais na waziri mkuu na kutujulisha na sisi huchukua haua za haraka kudhibiti jaribio hilo” akanyamaza kidogo akabonyeza kompyuta yakena kuendelea “Muda mfupi uliopita tumegundua kuna mtu amefanikiwa kuvuka ukuta uliowekwa na kuingia katika simu yako na amekuwa anafuatilia mawasiliano yako” Dr Evans akavuta pumzi ndefu “Amedukua simu yangu?Mmefanikiwa kumtambua mtu huyo ni nani?Tayari mmemdhibiti? “Mheshimiwa Rais baada ya kufuatilia tumegundua mtu huyo anayedukua simu yako anafanya kazi zake kutoka katika nyumba hii ambayo tumeifuatilia mmiliki wake anaitwa Devotha Adolph” Dr Evans alihisi kama kitu kizito kimegonga kichwa chake “Umesema Devotha Adolph? “Ndiyo mheshimiwa Rais” “My God!! Akasema Dr Evans akalegeza tai yake “Mnaweza kumzuia huyo mtu asiendelee na kile anachokifanya?akauliza Dr Evans “Ndiyo tunaweza mheshimiwa Rais lakini tunahitajikuwa na simu yako ndiyo maana tumekuita hapa ili utukabidhi simu yako tuifanyie kazi” akasema Isaack na kwa haraka Dr Evans akaitoa simu yake mfukoni akampatia “Simu hii hapa.Hakikisha unamzuia haraka sana mtu huyo asiendelee kufanya hicho anachokifanya.Lakini amewezaje kuvuka ukuta mliouweka hadi akaingia katika simu yangu? “Mheshimiwa Rais huyu mtu aliyefanya jambo hili anaonekana ni mdukuzi mwenye ujuziwa juu sana ndiyo maana akaweza kuuvuka ukuta tulioweka na akaingia katika simu yako” “Stop them now!! Akasema Dr Evans hukuakihema haraka haraka.Isaack na Bakari wakaanza harakakufanya kazi ya kuwadhibiti wadukuaji “Mheshimiwa Rais kuna maelekezo yoyote unayatoa kuhusiana na hawa watu waliojaribu kudukua simu yako?akauliza Richard “Nothing for now” akasema Dr Evan akiwatazama Isaack na Bakari wakiendelea na zoezi lao la kuwadhibiti wadukuzi.Zilipita dakika kadhaa Isaack akasema “Tayari mheshimiwa Rais.Tumekwisha wadhibiti wadukuaji lakini inabidi tuangalie kwa kina zaidi namna huyu mdukuaji alivyoweza kuvuka ukuta uliowekwa na kuweza kudukuasimu yako.Tutauangalia mfumo huu kwa kina zaidi ili tujue wapi kuna mwanya na kuuimarisha zaidi na kama tukiona inafaa tutabadili na kuweka mfumo mwingine” akasema isaack “Unaweza kujua kitu gani hasa walichokuwa wanakichunguza katika simu yangu?akauliza Dr Evans “Tunakwenda kulifanyia kazi hilo kujua nini hasa walichokifanya katika katika simu yako” akasema Isaack “Isaack ninawashukuru sana kwa kazi hii kubwa mliyoifanya.Tafadhali endeleeni kuwadhibiti watu hawa na wale wote wanaodiriki kutaka kufanya kitendo hiki cha kudukua simu yangu na vyombo vya mawasiliano vya viongozi wengine” akasema Dr Evans “Tutafanya hivyo mheshimiwa Rais.Tutahakikisha hakuna mtu atakayeweza kufanya hivi tena.Hawa watuwaliofanya hivi tunafahamu mahala walipo kama ungependa wafuatiliwe na kutiwa nguvuni”akasema Isaack “Kwa sasa endeleeni kulifanyia uchunguzi suala hili kujua namna walivyoweza kudukua simu yangu na kama wamepata msaada wowote kutoka kwa mtu aliye katika ofisi yenu.Hayo masuala mengine niachie nitayafanyia kazi” akasema Dr Isaack na kutoka akaeleka ofisini kwake.Mara tu alipoingia ofisini akampigia simu Kaiza “Mheshimiwa Rais” akasema Kaiza baada ya kupokea simu “Kaiza nataka kufahamu mahala ulipo sasa hivi? “Kwa sasa niko hapa kitalu 1.Nilisimamia zoezi la kumkamata Mathew Mulumbi tukalifanikisha na sasa tunasubiri maelekezo ya Devotha” “Devotha yuko wapi? “Alitoka hapa hajamueleza mtu yeyote anaelekea wapi” “Unadhani amekwenda nyumbani kwake? “Sina hakika kama amekwenda nyumbani kwake ngoja nijaribu kumtafuta nifahamu mahala alipo” “Hapana usifanye hivyo.Kaiza nataka kufahamu nini kinachoendelea hapo sasa hivi?Nieleze ukweli” “Kinachoendelea kwa sasa mheshimiwa Rais ni kuwahoji hawa watu tunaowashikilia” “Unaweza ukaniambia kwa nini mpaka sasa Olivia hajaweza kufunguka?Mmeshindwa kumfungua ili nitafute watu wanaoweza kuifanya kazi hiyo?Nieleze ukweli Kaiza bila kunificha kuna tatizo gani?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa Rais hatujashindwa kumfungua Olivialakini kuna mambo yanaendelea hapa ambayo binafsi yananishangaza” “Nieleze Kaiza ni mambo gani hayo?Kuwa muwazi kwangu” “Mheshimiwa Rais ni kuhusu mkurugenzi wetu Devotha.Kuna mambo amekuwa anayafanya ambayo binafsi siyaafiki.Leo asubuhi alifika hapa na akanieleza kuwa ametoka kuonana na Olivia akasema kwamba anataka kulifanyia uchunguzi jambo aliloambiwa na Olivia kuhusiana na Edger Kaka.Anataka kufanya uchunguzi kujua kama kweli Edger yuko hai.Nilimzuia asifanye hivyolakini alinionya kuwa yeye ndiye mkubwa hapa na sipaswi kumuingilia katika maamuzi yake.Baada ya hapo akataka kuzungumza na Mathew Mulumbi lakini bila kamera wala sauti.Tulizima kila kitu akaenda kuzungumza naye na alipomaliza kuzungumza naye akaondoka bila kutuaga anaelekea wapi.Mheshimwia Rais mtu kama Mathew ambaye jana ameua watu wetu kumi na tatu alistahili mateso makali lakini imekuwa tofauti,Devotha ameelekeza Mathew apelekwe chumba A3 ambako ni sehemu maalum kwa ajili ya viongozi wakuu pale wanapokuwa katika hatari.Nimehojikuhusu Mathew kupewa hadhi hiyo lakini bado jibu nililopewa sikulifurahia.Mheshimiwa Rais nina uhakika mkubwa kwamba bado hatujashindwa kuwafungua Mathew wala Olivia lakini kwa namna Devotha anavyoendesha mambo katu hatutaweza kupata chochote toka kwao” akasema Kaiza “Kaiza ninashukuru sana kwa kuwa muwazi kwangu.Sasa naomba unisikilize kwa makini haya maagizoninayokupa ambayo nataka yatekelezwe haraka sana” akasema Dr Evans “Nakusikiliza mheshimiwa Rais” akasema Kaiza “Nataka uende ukamtoe Olivia kitalu 2 na umpeleke mahala nitakapokuelekeza ili akahojiwe huko.Sitaki Devotha afahamu chochote kuhusu jambo hili.Ninataka ufanye kila linalowezekana kuhakikisha kabla ya jua kuzama leo Olivia awe amefunguka kila kitu kuhusu yeye na IS” “Sawa mheshimiwa Rais nitafanya kama ulivyoelekeza” http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Unaniahidi kwamba utafanya kama nilivyoeleza?Utamfungua Olivia? “Mheshimiwa Rais nakuahidi nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha Olivia anafunguka” “Good.Ondoka hapo ulipo kimya kimya bila kumueleza mtu yeyote na nitakuelekeza sehemu ya kumpeleka Olivia.Jambo lingine kuanzia sasa Devotha hatakuwa kiongozi tena badala yake wewe ndiye utakayeongoza idara hiyo.Nataka Devotha afungiwe kilakitu kuanzia simu na aondolewe katika mtandao asiweze kupata chochote.Kila kitu kibadilishwe haraka sana na mwisho nataka Devotha akamatwe” akasema Dr Evans na kukata simu “Siamini Devotha ameamua kumuamini Olivia kuhusu suala la Edger Kaka na ameamua kufanyauchunguzi kubaini kama kweli ninafahamu mahala alipo Edger.Kwa nini ameshindwa kuniamini nilipomwambia kwamba hichoanachokisema Olivia ni uongo mkubwa na mimisifahamu chochote?Ninamuamini sana Devothana kumtegemea sana katika mambo mengilakini nimesikitishwa na kitendo chake cha kushindwa kuniamini na badala yake ameanza kunichunguza.Sina hakika kama ninaweza kuendelea kumuamini kwa hili alilolifanya.Siwezi kufanyakazi na mtu ambaye haniamini.Amekosea sana kufanya hiki alichokifanya” akawaza Dr Evans
Saada alitoka ndani ya ofisi kwa kasi akatazama huku na huko akimtafuta Devotha “Madam Devotha !! akaitakwa nguvu.Alionekana kuchanganyikiwa “Madam Devotha ! akaita tena mara akatokea mtumishi wa ndani “Madam Devotha yuko chumbani kwake anapumzika”akasema yule mtumishi “Naomba umuite tafadhali.Mwambie namuhitaji haraka sana” akasema Saada na kurejea katika ofisi ya Devotha.Baada ya dakika tatu Devotha akafika akamkuta saada akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa “Saada kuna nini?akauliza “Madam Devotha !! akasema Saada akihangaikakubonyeza kompyuta yake “Saada nieleze tafadhali nini kimetokea? “Madam tayari tumejulikana” “Kivipi?akauliza Devotha “Wamekata mawasiliano kati yangu na simu ya Rais.Nimejaribu kuunganisha tena lakini haiwezekani tena kuna ukuta mzito.Madam zoezi limeishia hapa nashauri tusiendelee tena,tumejiweka katika hatari kubwa” akasema Saada. “Relax saada.Usiwe na hofu.Let me handle this” “Madam Devotha hadi kufikia hatua ya kukata mawasiliano kati yangu na simu ya Rais tayari wanafahamu niko wapi hivyo yawezekana muda huu wako njiani wakinifuata hapa.Madam ….” “Usihofu Devotha nilikuahidi kuwa sintakuingiza katika hatari yoyote.Funga kila kitu chako tunaondoka” akasema Devotha na kwenda chumbani kwake akachukua funguo ya gari akarejea mle ofisini “Kabla hawajakubaini na kukata mawasiliano tayari ulikuwa umepata taarifa zozote kuhusiana na ile kazi niliyokupatia?akauliza Devotha “Sikuwa nimefanikiwa bado kupata namba zile nilikuwa naendelea na maandalizi.I’m sorry madam I failed you”akasema Saada “Usiwe na hofu Saada.Hata hivyo tumejaribu” akasema Devotha wakatoka na kuelekea garini “Nimemuweka Saada katika hatari hata hivyo sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kudukua simu ya Dr Evans kuutafuta ukweli.Japo hatujafanikiwa kupata kile nilichokikusudia lakini nimejaribu na sasa natakiwa kumtafutia Saada sehemu salama ya kujificha kwa muda wakati nikiweka mambo sawa.Sehemu pekee ambako naamini haitakuwa rahisi kwake kujulikana ni nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambako ni sehemu ya mwisho kabisa ambayo mtu yeyote anaweza akafikiria kwenda kumtafuta Saada.Atakaa pale kwa muda na hadi kufikia jioni ya leo nitakuwa nimepata namna nzuri zaidi ya kumsaidia Saada” akawaza Devotha Alifuata maelekezo aliyopewa na Mathew akafika katika geti la nyumba yake akajitambulisha kwa mlinzi kwamba ni rafiki wa Mathew Mulumbi na amewaelekeza wafike pale wakaruhusiwa kuingia ndani wakapokewa na mtumishi wa ndani wa Mathew aitwaye Theresa “Sisi ni marafiki zake Mathew,ametuelekeza tufike hapa kumsubiri”akajieleza Devotha “Karibuni sana.Na ninyi pia mnatoka nje ya nchi?akauliza Theresa “Hapana sisi hatutoki nje ya nchi.Wanaotoka nje ya nchi ni wengine” akasema Devotha wakakaribishwa sebuleni wakahudumiwa vinywaji “Saada hapa ulipo ni sehemu salama na hakuna yeyote atakayejua kama uko hapa.Kitu muhimu cha kufanya zima kabisa vifaa vyako vyote vya mawasiliano na usiwashe hadi pale nitakapokujulisha kupitia simu ya humu ndani.Usijaribu kuwasiliana na mtu yeyote yule.Nataka nikaliweke sawa suala hili na hadi kufikia jioni ya leo kila kitu kitakuwa sawa.Umenielewa Saada?akauliza Devotha “Nimekuelewa madam Devotha” akasema Saada “Good.Mimi ninakwenda nitafika tena baadae kukuchukua” akasema Devotha na kumtaka Theresa amuandalie Saada chumba cha kupumzika “Mtu ninayetakiwa kuonana naye kwa sasa ni Olivia.Natakiwa kuzungumza naye kumueleza kuwa nimeshindwa kupata uhakika kama Dr Evans analifahamu suala la Edger kaka kupitia simu yake na nitamtaka kama ana namna nyingine ya kunisaidia kuthibitisha kuwa Dr Evans analifahamu suala hili anipatie ili niweze kumsaidia kumtafuta Edger” akawaza Devotha na kuchukua simu akampigia Kaiza lakini simu yake haikuwa ikipatikana akaendelea na safari yake. Alifika kitalu 2 akafunguliwa geti akaingia ndani mara tu aliposhuka garini akamuelekeza mlinzi kumleta Olivia ofisini kwake akaelezwa kuwa Kaiza akiwa na wenzake kwenye magari matatu walifika pale na kumchukua Olivia wakaondoka naye bila kueleza wanaelekea wapi.Taarifa ile ilimstua sana Devotha akataka akahakiki kama kweli Olivia hayupo ndani ya chumba chake akaamuru mlango ufunguliwe ili ahakiki kama alichoelezwa ni kitu cha kweli.Chumba kilikuwa kitupu.Akachukua simu ili kumpigia Kaiza lakini akasikia ujumbe uliomstua kuwa simu yake ilikuwa imezuiwa kwa muda “What’s going on? Kwa nini simu yangu imezuiliwa?Kwa nini Olivia akaondolewa bila mimi kujulishwa?akajiuliza Devotha.Akazitafuta namba za Rais akajaribu kupiga lakini jibu likawa lile lile kuwa simu yake imezuiliwa.Akatoka kwa haraka ndani ya kile chumba akaelekea katika ofisi yake akafungua kompyuta yake akajaribu kuingia katika mtandao wa idara yao lakini namba za siri za kuingilia katika mfumo zilikuwa zimebadilika. “Damn !! akasema na kupiga meza kwa hasira.Akiwa ameinamisha kichwa akiwaza mara mlango wake ukagongwa wakatokea watu watatu ambao ni makachero wa idara yake. “Karibuni” akasema Devotha na kuwakaribisha watu wale ofisini kwake. “Mnasemaje James?akauliza Devotha huku akipanga mafaili yake “Madam Devotha please come with us”akasema James “Come with you where?akauliza Devotha “Please madam we have orders to take you” akasema James. “Take me where?Nani kawatuma kwangu?akauliza Devotha “Tafadhali madam naomba uongozane nasi” akaendelea kusisitiza James “What if I say no?! akauliza Devotha “Madam please usilifanye jambo hili likawa gumu” akasema James.Olivia akaushika mkoba wake na kutaka kuuinua wale jamaa wote kwa kasi kubwa wakingiza mikono katika makoti yao na kutoa bastora “Usiguse kitu chochote!! Devotha akaamriwa “Easy ! easy gentlemen !! akasema Devotha “Kama mmetumwa kuja kunichukua hakuna haja ya kutumia nguvu.Siku zote nimekuwa kiongozi wenu nyote mnanifahamu vyema.Twendeni kwa amani huko mlikotumwa mnipeleke” akasema Devotha “Come over here slowly with your hands up !! akasema James kwa sauti kali.Devotha akainua mikono juu.Ghafla Devotha akafanya kitu ambacho hakuna aliyekitegemea.Alibonyea chini ya meza akateleza kwa kasi kubwa na kumvaa James akamkata mtama.Kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana ambacho hawakuwa wamekitarajia.James alianguka chini kama furushi kwa kuwa hakuwa ametegemea kitu kile kutokea.Wakati wenzake wakijiuliza kilichotokea akamtandika James teke kali katika korodani akatoa mlio wa maumivu makali akaachia bastora aliyokuwa ameishika na kupeleka mikono yake yote mahala alikopigwa teke.Tayari Devotha alikwisha waona wale jamaa namna walivyokaa mle ndani akachukua chupa moja kubwa iliyokuwa pembeni na kumrushia mmoja wao ambaye aliinama ili kuikwepa na Devotha akaitumia nafasi hiyo akageuza jicho lake kama kinyonga na kumuona jamaa mwingine akimuelekezea bastora akajigeuza kama kima na kumtandika mateke mawili haraka haraka,alimpiga teke la mkono bastora ikamponyoka kisha akamtandika teke kali la kifua lililompeleka ukutani kabla hajakaa sawa akamkata mtama akaanguka chini na kichwa chake kikagonga meza akainyakua bastora ya yule jamaa na kumuelekezea yule aliyemkosa na chupa “Weka chini bastora yako haraka sana!! Akaamuru Devotha Yule jamaa akaonekana anasita.Bila ajizi Devotha akachia risasi mbili zikapita pembeni ya uso wake.Jamaa alitetemeka mikono na bila ubishi akaiweka chini bastora yake na kuipiga teke kumuendea Devotha. “Chukua ule waya wafunge wenzako!! Akaamuru Devotha yule jamaa akachukua waya wa umeme na kuwafunga wenzake mikono kwa nyuma pamoja na miguu halafu akamuelekeza ageukie ukutani na ainue mikono yake juu.Akafuata maelekezo aliyopewa na Devotha akamfunga mikono kwa waya. “Nani kawatuma kwangu?akauliza Devotha lakini hakujibiwa.Akafungua mkoba wake na kutoa bastora yenye kiwambo cha sauti na kumpiga James risasi katika mguu wake “Nani kawatuma kwangu?akauliza Devotha “Kaiza !! tumepewa maelekezo na Kaiza !! akalalama James “Damn you Kaiza!! Akasema Devotha akiuma meno kwa hasira akachukua mkoba wake akaweka baadhi ya vitu vyake muhimu akatoka mle ofisini.Alipotoka nje akawakuta walinzi watatu “Na ninyi pia mmetumwa kwangu?akauliza Devotha aliyejawa hasira “Tumesikia mlio wa risasi tukajiuliza nini kimetokea humo ndani”akajibu mmoja wao “Kaiza akifika hapa mwambieni ujumbe wake nimeupata” akasema Devotha akipiga hatua kuelekea katika gari lake akaingia na kuondoka. “Wameniwekea vizingiti kila mahali.Nahisi tayari Dr Evans ametambua kuwa ni mimi niliyekuwa nadukua mawasiliano yake na akatoa maelekezo nikamatwe pamoja na kuondolewa kabisa katika mifumo yote.Yawezekana vile vile amepewa taarifa na Kaiza kuwa ninamfanyia uchunguzi kwani ni yeye pekee niliyemueleza jambo hilo.Kaiza hakukubaliana nami na nina hakika ni yeye aliyemueleza Rais kuwa ninamchunguza.Naanza kuhisi maelekezo haya ya kufungiwa simu na mtandao pia yametoka kwa rais na yawezekana ni kweli anahusika katika suala hili la Edger na ndiyo maana hataki nichunguze jambo hili.Sasa nimeanza kumuamini Olivia kuna siri kubwa ambayo siifahamu.Kikubwa ninachopaswa kukifanya kwa sasa ni kuwatafuta Olivia na baba yake kujua wamepelekwa wapi” akawaza Devotha “Hili jambo tayari limekuwa kubwa.Nahitaji mtu wa kunisaidia siwezi kupambana peke yangu.Mtu pekee ambaye ninamuamini kwa sasa ni Saada lakini yeye ni mtaalamu wa kompyuta na hafahamu chochote kinachohusiana na mapambano,nahitaji mtu ambaye anaweza kupambana” akawaza na kukumbuka kitu “Mathew aliniambia anao watu wake ambao anawaamini na wanaweza wakanisaidia.Alisema watu hao wanatokea nje ya nchi.Nadhani itakuwa vyema nikiwatumia watu hao wa Mathew katika kumtafuta Olivia” akaendelea kuwaza Devotha na kuingiwa na hofu “Hili ni wazo zuri la kuwatumia hao watu wa Mathew lakini nitalazimika kuwaeleza ukweli wote kuhusu Mathew.Naamini watanielewa na watakubali kushirikiana nami.Lakini kuna wazo nimelipata kwa nini nisisaidiane na hao jamaa kumuokoa Mathew? Nimemuhoji mimi mwenyewe na haonekani kuwa na muunganiko wowote na kikundi cha IS.Lengo lake kuu lilikuwa kumlinda Olivia na hakuwa akifahamu kama Olivia ana mahusiano na IS.Hili ni wazo zuri.Kama nikifanikiwa kumpata Mathew naamini kabisa tukiungana tunaweza tukaupata ukweli wa jambo hili.Ngoja nikakutane na hao jamaa zake nizungumze nao na tuanze haraka mikakati ya kumuokoa Mathew Mulumbi kutoka kitalu 1” akawaza Devotha na kuelekea nyumbani kwa Mathew
Geti jeusi lilifunguliwa na gari tatu nyeusi zikaingia katika nyumba moja ambayo ilikuwa na magari mengi mabovu.Kulikuwepo pia matairi mengi ya magari yaliyotumika yamepangwa katika mafungu.Nyumba hii ilionekana kama ni gereji ya magari.Kulikuwa na nyumba ya wastani ambayo ilikuwa umechafuka kuta zake na mafuta ya magari.Hatua chache kutoka nyumba ile watu watano walikuwa katika injini ya gari wakiitengeneza na mara tu magari yale matatu yalipoingia wakaacha kazi waliyokuwa wanaifanya wakaelekea katika yale magari.Kutoka ndani ya ile nyumba akatokea jamaa mmoja aliyevaa koti refu jeupe kama wavaayo madaktari.Kaiza akashuka garini akamfuata wakasalimiana “Karibuni.Naitwa Dr Alex ndobe” “Naitwa Kaiza” Baada ya kutambulishana Dr Alex akawatambulisha wale jamaa waliokuwa wanatengeneza injini ya gari halafu mmoja wao akauliza gari lililombeba mgonjwa.Kaiza akaelekeza gari ambalo alikuwa amewekwa Olivia dereva wake akaombwa aliingize katika chumba kimoja kilichokuwa na ukubwa wa kuweza kukaa gari mbili.Baada ya muda mfupi sehemu ya sakafu liliposimama gari lile ikazama chini taratibu pamoja na lile gari.Kaiza alibaki anashangaa.DrAlex akamjulisha kuwa kuna nyumba ya chini ambayo kila kitu kinafanyika huko na akamtaka amfuate wakaingia katika chumba kingine akaufungua mlango kwa kadi maalum wakashuka chini hadi mahala lilipo lile gari alimo Olivia.Kaiza akaamuru Olivia ashushwe.Buti la gari likafunguliwa akashushwa Olivia akiwa amefunikwa mfuko mweusi kichwani Dr Alex akaelekeza aingizwe katika chumba Fulani kisha akamchukua Kaiza katika chumba kidogo kwa ajili ya maongezi “Kaiza karibu sana.Mimi na wewe ni mara yetu ya kwanza tunakutana.Sitaki kufahamu mmetokea wapi lakini nimepewa maelekezo na rais kuhusu ujio wenu hapa hivyo karibuni.Hapa ni sehemu ya siri ambayo hutumika katika kutesa wale watu ambao ni hatari kwa nchi na ambao wana taarifa muhimu zinazohitajika.Magaidi,majamba zi sugu hata wale wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya huletwa hapa”akasema Dr Alex “Nashukuru pia kukufahamau Dr Alex.Rais amenielekeza nije hapa ambapo ni sehemu sahihi kabisa.Kuna mtu ambaye ana taarifa nyeti sana kwa ajili ya usalama wa nchi na amegoma kufunguka kutupa taarifa hizo tunazozihitaji mno.Tumemleta hapa kwa ajili ya kumfanya afunguke na atueleze kila kitu” akasema Kaiza “Usihofu Kaiza mahala hapa panaitwa gate of hell.Kama nilivyokueleza ni sehemu maalum ambayo huletwa wale watu ambao ni hatari kwa nchi ambao wamegoma kufunguka huko walikokuwa wanashikiliwa.Hapa ni sehemu iliyojaa mateso ya kila aina.Nimekuwa hapa kwa miaka kumi nikiongoza kikosi hiki maalum kabisa na vijana uliowaona hapo nje wakitengeneza injini ndio watesaji wakubwa mimi ni kiongozi wao.Naomba nikupe siri moja ya hapa Kaiza.Hakuna aliyewahi kuletwa hapa akatoka hai ndiyo maana panaitwa ni geti la kuelekea huko wanakoenda baada ya kufa.Wote wanaoletwa hapa huletwa kuja kuuawa na kupotea kabisa.Hicho ndicho kikubwa kinachofanyika hapa hivyo kama mmemleta mtu wenu hapa ninakuhakikishia kwamba atafunguka lakini hatatoka hai” akasema Dr Alex “Hakuna tatizo katika hilo Dr Alex.Kikubwa ninachokihitaji kutoka kwa huyu mtu tuliyemleta hapa ni taarifa alizonazo ambazo ni muhimu sana kwa usalama wa nchi” akasema Kaiza “Vizuri,basi naomba tusipoteze muda kazi ikaanze mara moja” akasema Dr Alex wakatoka na kuingia katika chumba kimoja chenye mitambo mingi. “Hiki ndicho Chumba ambacho kila kitu hufanyika.Hii yote unayoiona hapa ni mitambo ya kutesea watu” akasema Dr Alex akimuonyesha Kaiza kitanda ambacho hutumiwa kutesea watu. “Watu wangapi mnawapokea hapa kila mwezi? Akauliza Kaiza “Hakuna idadi maalum.Tunaweza kumaliza hata miezi mitatu bila kupokea mtu yeyote” akasema Dr Alex na Kaiza akaelekeza Olivia aingizwe katika kile chumba,akalazwa katika kitanda maalum kinachoendeshwa na kompyuta.Mikono na miguu yake ikabanwa kwa pingu maalum.Kiunoni akafungwa mkanda.Shingoni akawekewa kifaa Fulani cha kubana shingo lakini kinachoruhusu hewa kupita.Baada ya kumaliza kumuandaa,mfuko uliofungwa kichwani ukatolewa.Dr Alex akapatwa na mstuko mkubwa.Alihisi miguu ikimtetemeka baada ya kugundua mtu yule alikuwa ni Olivia Themba. “Dr Olivia Themba?akajiuliza “Sikujua kama mtu waliyemleta hapa kutolewa uhai wake ni huyu.Oh my God! amefanya nini Olivia hadi akaingia katika mikono ya hawa jamaa?akaendelea kujiuliza Dr Alex.Olivia naye alistuka sana kumuona Dr Alex. “Dr Alex?! Anafanya nini hapa?akajiuliza “Dr Alex is everything okay?akauliza Kaiza baada ya hali ya Dr Alex kubadilika ghafla alipomuona Olivia na kushindwa kuuzuia mstuko wake “Dr Alex is everything okay?akauliza tena Kaiza “I’m okay.Nimestuka kidogo baadaya kumuona huyu mrembo.Tumezoea kupokea watu wenye sura za kutisha za kikatili.Huyu ni mwanamke wa pili kuletwa hapa” akasema Dr Alex na kutoa maelekezo kadhaa kwa vijana wake.Mashine kubwa ikaletwa karibu yake nyaya zikaunganishwa kutoka katika mashine ile na kubandikwa kichwani,kifuani na sehemu nyingine mbali mbali za mwili wa Olivia.Dr Alex akamfanyia ishara Kaiza aweze kuzungumza na Olivia kabla ya zoezi la kumtesa kuanza.Kaiza akamsogelea Olivia na kumtazama huku sura yake ikiwa imejikunja kwa hasira “Olivia kwa jina naitwa Kaiza,ni mara ya pili ninakutana nawe.Safari hii tumekutana katika mazingira magumu zaidi kwako.Kama unavyoona,humu ndani kuna mitambo mbali mbali na yote hii kazi yake ni moja tu kutesa watu.Ukiingia ndani ya chumba hiki utapata mateso ya kila aina na siri moja ya chumba hiki ni mara chache sana walioingizwa ndani ya chumba hiki wametoka salama.Ni wachache sana wale waliokubali kutoa ushirikiano na kueleza kila kitu.Olivia hata wewe kutoka kwako salama ndani ya chumba hiki itategemea na ushirikiano utakaoutoa lakini kama hautatoa ushirikiano kwetu this will be the end of you” akasema Kaiza akimuangalia Olivia kwa macho makali “Chumba hiki kinaitwa gate of hell kwani ukiingizwa humu tayari kufuli la geti la kuelekea huko wanakoenda waliokufa linakuwa limefunguliwa hivyo muda wowote geti linaweza likafunguliwa na ukaingizwa huko.Ni sehemu ambayo huletwa watu wajeuri ambao hawataki kufunguka na kutoa taarifa muhimu.Hapa ni sehemu yako ya mwisho na kama hautakuwa tayari kufunguka basi utakuwa ni mwisho wako.Kabla sijafanya chochote nataka ushuhudie kile ambacho huwapata wenzako kama wewe ambao wanakuwa viburi na kuletwa hapa” akasema Kaiza na kumfanyia ishara Dr Alex ambaye alimuelekeza mmoja wa watu wake awashe runinga kubwa iliyokuwamo mle chumbani. Runingani alionekana mtu aliyechafuka damu akiwa amelala juu ya kitanda kile alichokuwa amelala Olivia.Kitanda kilikuwa kimechafuka kwa damu.Uso wa mtu yule ulifunikwa kitambaa maalum kiasi cha kutoweza kumtambua,akatokea Mtu yule aliyeficha sura yake akamvalisha kofia ya chuma.Kofia ile iliunganishwa na umeme.Mtu mwingine akaonekana katika sehemu iliyokuwa na mtambo wenye kuwaka taa za rangi mbali mbali.Akabonyeza kitufe chekundu na yule jamaa kitandani akaanza kutetemeka.Alitetemeka sana na baada ya muda akatulia tuli tayari alikwisha farik Olivia akafumba macho hakutaka tena kutazama. “Olivia hiyo ni picha moja tu umeiona.Hivyo ndivyo wanavyofanywa wale wote ambao ni hatari kwa usalama wa nchi wanaoletwa hapa na kugoma kufunguka.Kwa sasa wewe pia ni mmoja kati ya watu hatari kwa usalama wa nchi hivyo kama hautafunguka yatakukuta kama yaliyowakuta hao unaowaona runingani.Olivia si nia yetu kuua watu au kuwatesa lakini inatulazimu kufanya hivyo ili kuliweka taifa letu salama.Tunataka raia wa nchi hii waishi na kufanya kazi zao bila hofu yoyote ya usalama wao ndiyo maana sisi tumekula kiapo cha kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa nchi inakuwa salama na tunaondoa kitisho chochote cha kuhatarisha usalama wa ndani ya nchi hivyo pale inapotulazimu kuondoa uhai wa mtu ambaye tunaamini ni hatari tunafanya hivyo bila ajizi” akasema Kaiza “Olivia wewe u mwanamke mrembo sana,mwenye elimu na taaluma kubwa unaheshimika mno hapa nchini na inaniuma kukufanyia hivi,lakini umetulazimisha wewe mwenyewe tukufanyie hivi.Bado unayo nafasi ya kuyamaliza mambo haya kwa kuamua kufunguka ukweli ambao utasaidia kuiweka nchi salama” Kaiza akanyamza tena halafu akawataka watu wote mle ndani watoke akabaki yeye na Olivia pekee,akavuta kiti na kuketi karibu na Olivia “Olivia sasa tuko peke yetu.Nimefanya hivi ili uwe huru kujieleza.Umekuwa na mawasiliano na hata kukutana na baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi la IS.Ulikwenda Kinshasa kukutana na Seif Almuhsin ambaye anafahamika kwa kazi yake kubwa ya kusajili vijana ambao hupelekwa katika kambi za mafunzo za IS ambako hupatiwa mafunzo ya kigaidi na kupelekwa sehemu mbali mbali kupigana.Kama haitoshi umekuwa vile vile na mawasiliano na Sayid Omar ambaye anadaiwa ni mfadhili mkubwa wa kikundi cha IS.Nataka kufahamu mahusiano yako na IS.Tuanzie hapo” akasema Kaiza. “Macho ya huyu jamaa yanaonyesha ukatili mkubwa.Ni wazi hapa ni sehemu yangu ya mwisho na kama nisipofanya juhudi binafsi uhai wangu unaweza kuondolewa.Natamani nife niondokane na mateso haya lakini halitakuwa suluhisho kwani Edger Kaka yuko hai,anaweza akapatikana na siri yake isijulikane hivyo IS wakaendelea na mipango yao hapa nchini na yawezekana akashika hata nafasi ya urais.Sitaki hilo litokee na ndiyo maana itanilazimu kuvumilia mateso yote ili kuhakikisha kwamba mipango yangu inatimia.Natakiwa kuhakikisha kabla ya kufa niwe nimempata Edger na nikahakikisha anaondoka hapa nchini kama tulivyokubaliana na mama yake Habiba.Endapo atapatikana nikiwa nimekufa hakuna mtu yeyote hapa nchini atakayefahamu siri yake.Yuko wapi Mathew Mulumbi?Alinipa namba zile akaniahidi kwamba mara tu nitakapopiga atajua mahala nilipo na atatafuta msaada mbona namba zile zimepigwa na hajatokea?Alikuwa ananidanganya? Hajui kama nimetekwa?.Tumaini pekee nimelipata baada ya kumuona Dr Alex.Nimestuka sana baada ya kumuona hapa.DrAlex niliwahi kukutana naye tukiwa katika mazoezi ya vitendo katika hospitali moja nchini Urusi na baadae tukaja kukutana hapa Tanzania.Hatuna ukaribu mkubwa lakini ni mtu ambaye tunafahamiana na tumekuwa tunakutana mara kwa mara sehemu mbali mbali.Amewahi kumleta mgonjwa wake wakati ninafanya kazi hospitali kuu ya moyo nikamsaidia.Nimemuona machoni namna alivyostuka aliponiona hakutegemea kuniona mahala hapa.Hakuwaeleza hawa jamaa kama ananifahamu na hii ni dalili tosha kuwa anataka kunisaida” akawaza Olivia na kutolewa mawazoni na kaiza. “Olivia nimekuachia muda wa kutafakari sasa ni muda wa kuanza mazungumzo yetu tafadhali. Nijibu tafadhali kile nilichokuuliza.”akasema Kaiza kwa ukali “Nimekwisha waambia ni rais pekee ninayeweza kuzungumza naye na si ninyi.Mmenileta hapa kunitesa hivyo anzeni haraka kunitesa” akasema Olivia.Kaiza hakuonekana kufurahishwa na kauli ile ya Olivia “Olivia nimekueleza kuwa hii ni sehemu ya mwisho itakayoamua hatima ya maisha yako na yawezekana usitoke hai ndani ya chumba hiki.Umeona kile kinachowapata wale wanaoletwa hapa na wakaendelea kuwa kiburi.Nataka ufunguke mahusiano yako IS”akasema Kaiza “Ulisema hili ni geti la kuingilia kuzimu? Naombeni msipoteze muda lifungueni geti hilo nipelekeni huko mnapoteza muda wenu kunihoji kwani hamtapata kitu chochote” akasema Olivia.Kaiza akamtazama Olivia kwa hasira. “Huyu ni mwanamke wa namna gani? Magaidi wale wamekwisha muharibu.Wamempa ujasiri mkubwa na yuko tayari kufa kuliko kusema chochote.Pamoja na vitisho vyote hivi bado anakuwa mgumu kusema chochote.Nilimuahidi rais kumfungua Olivia na lazima nifanye kila kinachowezekana kuhakikisha Olivia anafunguka kuhusu mahusiano yake na IS.Nataka afunguke kila kitu” akawaza Kaiza na kubonyeza kengele iliyokuwa ukutani mlango ukafunguka wakaingia watu watatu waliojaza miili yao walikuwa wamevaa fulana nyeusi zilizowabana.Sura zao zilionyesha ukatili mkubwa.Olivia akatetemeka kwa ndani baada ya kuwaona “Hata ukiziangalia sura za hawa jamaa wanaonekana ni wakatili,ni wauaji lakini silaha yangu pekee ni kutoonyesha woga wa aina yoyote.Japo nina hofu kubwa lakini ninapaswa kuendelea kushikilia msimamo wangu na kuendelea kujiamini.Hata wakinipa mateso ya namna gani sipaswi kuonyesha kutetereka” akawaza Olivia.Kaiza akamsogelea karibu “Olivia hawa unaowaona hapa kazi yao kubwa ni kufungulia watu geti la kuelekea kuzimu.Kwa kuwa umeonyesha kiburi,safari yako ya kuelekea kuzimu inaanza sasa hivi lakini bado unayo nafasi ya kuweza kuzuia hiki kinachokwenda kutokea.Please talk to me” akasema Kaiza “Niko tayari kwenda huko kuzimu unakosema lakini kabla hamjanipeleka huko rais anafahamu hiki mnachotaka kunifanyia?Mtoto wake anaumwa yuko hospitali.Mkiniua mimi,Coletha mtoto wa rais naye atakufa pia kwani hakuna anayeweza kukumtibu zaidi yangu.Kabla hamjaniua mjulisheni kwanza mkuu wenu kile mnachotaka kukifanya lakini mkiniua bila yeye kufahamu mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana”akasema Olivia. “Olivia hii ni nafasi ya mwisho ninakupa ya kufunguka”akasema Kaiza “Nimekwisha waeleza fanyeni kile mnachotaka kukifanya lakini nimewapa tahadhari kuhusu kuniua muulizeni kwanza mkuu wenu” akasema Olivia.Kaiza akatoka na baada ya muda akarejea akiwa na Dr Alex akampa maelekezo kuwa kazi ianze mara moja.Dr Alex akaiwasha mashine ile ambayo nyaya zake ziliunganishwa katika mwili wa Olivia.Wale jamaa watatu waliojazia miili yao wakakisogelea kitanda cha Olivia. “Charging 75%” akasema Dr Alex “Start with 150% “ akasema Kaiza “Hapana Kaiza haiwezekani.Lazima kuanza na kiwango cha chini.150% ni kiwango kikubwa sana na hakifai kwa mwanamke” “Usimuonee huruma huyu mwanamke she’s a devil.Anao uwezo mkubwa sana wa kuvumilia mateso hata yakiwa makali kiasi gani.Ameshuhudia baba yake akipigwa risasi mbili na hakutetereka!! Akasema Kaiza “Pamoja na hayo Kaiza hapa kuna taratibu zake ambazo lazima tuzifuate.Tunaanza na 75%” akasema DrAlex. “Sawa Dr Alex.Lakini nina uhakika mkubwa sana kiwango hicho ni kidogo na huyu mwanamke anaweza akakihimili” akasema Kaiza “Usihofu Kaiza.Tutapandisha kiwango taratibu” akasema Dr Alex na Olivia akawekewa kifaa mdomoni “Okay do it ! akasema Kaiza.Dr alex akabonyeza kitufe Fulani katika ile mashine halafu akashika kidude chenye rangi ya kijani akakizungusha.Olivia akaanza kutetemeka mwili .Chaji za umeme zilipita mwilini mwake.Baada ya sekunde kadhaa Dr Alex akazima ile mashine.Olivia bado alikuwa anatetemeka.Kaiza akamsogelea na kumvua kile kifaa alichokuwa amewekewa mdomoni na kumuita “Olivia!! Olivia hakuitika alikuwa anatetemeka mwili “Olivia unaruhusu tuendelee au uko tayari kuongea?akauliza Kaiza.Olivia hakujibu kitu “Tuendelee tena.Charge 120” akasema Kaiza na mashine ikawashwa.Baada ya sekunde kadhaa Olivia akaanza kutokwa povu mdomoni.Mashine ikazimwa haraka zile nyaya zikaondolewa mwili mwake.Dr Alex akachukua kifaa cha kupimia mapigo ya moyo na kumpima “Nini kimetokea? Is she breathing? akauliza Kaiza “Tuliweka kiwango kikubwa sana cha chaji.We nearly killed her” akajibu daktari na kuchukua sindano akamchoma Olivia. “Doctor please don’t let her die !! akasema Kaiza baada ya kushuhudia kilichokuwa kimetokea Olivia.Alipochomwa sindano ile baada ya muda mfupi akatulia “Will she be okay? akauliza kaiza .Dr Alex akachukua tena kipimo chake cha mapigo ya moyo akampima Olivia na kumgeukia Kaiza “Yuko salama lakini inabidi kumpumzisha kwanza kabla ya kuendelea na zoezi hili” akasema daktari “Atapumzika kwa muda gani?Kaiza akauliza “Nashauri tumpumzishe kwa masaa mawili au matatu kabla ya kuendelea” akasema Daktari “Hatuna saa tatu za kusubiri.Nitaruhusu apumzike kwa nusu saa halafu tuendelee na zoezi” “Hapana Kaiza.Hali ya Olivia ni mbaya na anatakiwa apumzishwe kabla ya kuendelea na mateso mengine”akasema Dr Alex “Sikiliza Dr Alex.Huyu mwanamke anazo taarifa za muhimu mno ambazo tunatakiwa kuzipata na ameletwa hapa ili aweze kufunguka na si kulala kitandani.Nataka uhakikishe anakuwa tayari ndani ya dakika thelathini.Umenisikia Dr Alex?akauliza Kaiza kwa ukali.Dr Alex hakufurahishwa na kauli ile ya Kaiza “Mr Kaiza mimi ndiye daktari na ninachosema mimi ndicho kinatakiwa kifuatwe.Zaidi ya yote mimi ndiye mkubwa wa hapa na kauli yangu ndiyo ya mwisho!! Akasema Dr Alex “Dr Alex usitake mimi na wewe tufungue ukurasa mpya wa kuonyeshana nani mkubwa.Fanya kazi yako na uhakikishe ndani ya nusu saa Olivia anakuwa tayari.Fanya kazi yako vyema ukishindwa nitakuondoa hapa na kumleta mtu mwingine ambaye anaifahamu kazi yake!! Akasema Kaiza kwa ukali. “I don’t take orders from you Kaiza !!akasema Dr Alex “Imeanza leo.From today you’ll be taking orders from me !! akasema Kaiza na Dr Alex akakunja vidole vyake kwa hasira akatazamana na Kaiza “I need a room !! akasema Dr Alex na wale jamaa wote wakatoka nje akabaki peke yake akashusha pumzi. “Kaiza ni nani hadi anipe amri? Sijapendezwa na kauli zake chafu.Nimekuwa katika chumba hiki kwa zaidi ya miaka kumi sasa na hajawahi kutokea mtu yeyote aliyenitamkia maneno kama aliyonitamkia Kaiza” akawaza Dr Alex na kumgeukia Olivia aliyekuwa amelala kitandani “Namfahamu sana Dr Olivia.Mimi na yeye tulikutana kwa mara ya kwanza nchini Urusi toka hapo tukawa marafiki.Japo mimi na yeye hatuna ukaribu mkubwa sana lakini ni marafiki na nimewahi kumpeleka shangazi yangu katika hospitali ya moyo alikokuwa anafanya kazi Olivia kabla ya kuanzisha kituo chake cha utafiti wa magonjwa na Dr Olivia alihakikisha amehudumiwa na akapona.Amefanyaje hadi akaingia katika mikono ya hawa jamaa? Nimesikia anaulizwa kuhusu mahusiano yake na kikundi cha IS,msomi kama huyu anawezaje kushirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS? Siamini kama hilo linawezekana.Familia ya Olivia ni matajiri wakubwa na Olivia hana sababu ya kujiunga na kikundi cha kigaidi.Watakuwa wamemleta mtu ambaye si sahihi.Olivia hapaswi kuwepo mahala hapa” akawaza Dr Alex na kumsogelea Olivia akampima mapigo ya moyo. “Mapigo ya moyo yanakwenda vizuri” akawaza Dr Alex huku akiweka kile kifaa cha kupimia mfukoni.Wakati akijianda kuchukua kifaa kingine Olivia akafumbua macho. “Dr Alex” akaita Olivia kwa sauti ya kunong’ona.Dr Alex akastuka halafu akamuinamia kana kwamba anampima kisha kwa sauti ndogo akasema “Fumba macho yako kuna kamera kila kona humu ndani wakijua umefumbua macho watakuja na kuendelea kukutesa” akasema Dr Alex huku akijitahidi kumkinga Olivia “Dr Alex please help me” akasema Olivia akiwa amefumba macho “Olivia kwa nini uko hapa? Hawa jamaa wamekutoa wapi?Hupaswi kuwepo sehemu kama hii ni sehemu ya hatari kubwa.Kwa nini umeingia katika mikonoi ya hawa jamaa?akauliza Dr Alex “Ni hadithi ndefu Dr Alex kama tukijaliwa uhai nitakueleza lakini kwa sasa unisaidie kutoka humu.Please don’t let them kill me” akasema Olivia “Olivia ni vigumu sana kutoka sehemu hii hata hivyo nitajitahidi kutafuta namna ya kukusaidia” akasema Dr Alex “DrAlex naomba mtafute mtu anaitwa Mathew Mulumbi muelekeze mahala nilipo yeye atajua namna ya kuja kuniokoa” akasema Olivia “Olivia I can’t do that ! “Dr Alex fikisha ujumbe kwa Mathew Mulumbi kuwa niko hapa.Yeye atatafuta namna ya kuja kuniokoa” “Olivia hapa ni sehemu ya siri na hapaswi mtu yeyote kupafahamu” akasema Dr Alex “Dr Alex please help me.Don’t let them kill me” akasema Olivia “What have you done Olivia?akauliza Dr Alex “Dr Alex something is going to happen in this country.Ni mimi pekee ambaye ninaweza nikazuia jambo hilo lisiweze kutokea hivyo naomba unisaidie” akasema Dr Olivia “Nini kinakwenda kutokea Olivia?Kwa nini hawa jamaa wamekuleta hapa? Nimesikia wanakutuhumu kuwa una mahusiano na kikundi cha kigaidi cha IS je ni kweli unahusiana na kikundi hicho?akauliza Dr Alex “Dr Alex sina muda wa kuelezea lakini naomba unisaidie kufikisha ujumbe kwa Mathew Mulumbi ni mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha Masai milk.Mpe taarifa kuwa niko hapa yeye atajua namna ya kunisaidia”akasema Olivia “Olivia..” Dr Alex akastuka baada ya mlango kufunguliwa akaingia Kaiza akiwa na watu wake wawili. “How’s she?akauliza Kaiza “Bado hali yake si nzuri anahitaji mapumziko” akasema Dr Alex na kuvuta dawa katika sindano akamchoma Olivia. “Dr Alex nimekwambia ninamuhitaji Olivia ndani ya nusu saa.Leo lazima afunguke” “Kaiza na mimi nimekwisha kueleza kuwa hali ya Olivia si nzuri anatakiwa kupata mapumziko ya walau saa moja au mbili” “Hatuna muda huo Dr Alex.Nataka ndani ya nusu saa awe tayari kuendelea na mahojiano”akasema Kaiza Mara ghafla Olivia akaanza kutetemeka. “What’s going on? akauliza Kaiza “I don’t know.Hali yake imebadilika ghafla” akasema Dr Alex.Mashine ya kusoma mgandamizo wa damu ilikuwa inatoa mlio na kuonyesha mgandamizo ni mkubwa kupita kawaida “Mgandamizo wa damu umekuwa mkubwa sana nahitaji kufanya jitihada za kuushusha” akasema Dr Alex na kukimbia nje baada ya dakika mbili akarejea akiwa na vichupa kadhaa vya dawa akamchoma Olivia na baada ya dakika tatu mashine ile ikaacha kutoa mlio na mgandamizo ukaanza kushuka.Kaiza akashusha pumzi “Kaiza tafadhali naombeni mnisikilize.Mimi ni daktari na nimekuwa hapa kwa miaka zaidi ya kumi sasa na kila anayeletwa hapa mimi ndiye humpima na kujua anahitaji kiwango gani cha mateso.Kwa Olivia uwezo wake wa kustamihili mateso makali kama haya ya kuchomwa na umeme ni mdogo ndiyo maana hali yake imekuwa namna hii na kama mkilazimisha aendelee kuteswa atapoteza maisha na mtapoteza kila kitu mnachokitaka toka kwake.Nawaomba mzingatie ushauri wangu wa kumuacha apumzike kwa muda niliowaelekeza” akasema Dr Alex Kaiza akamuita pembeni Dr Alex “DrAlex samahani kwa maneno niliyokutamkia awali lakini ukweli ni kwamba huyu mwanamke anazo taarifa nyeti sana kwa ajili ya usalama wa nchi ambazo tunahitaji kuzipata kutoka kwake ndiyo maana tumemleta hapa ambako tunaamini atafunguka.Anashirikiana na kikundi cha kigaidi cha IS na tunataka kujua ni mambo gani wanayapanga hapa nchini hivyo naomba ufanye kila lililo ndani ya uwezo wako kuhakikisha anakuwa salama na muda wa kupumzika upunguzwe ili tuweze kumuhoji.Naomba mapumziko yawe ni saa moja.Tusaidie kwa hilo tafadhali” akasema Kaiza “Sawa Kaiza nitajitahidi lakini naomba heshima iwepo kati yetu” “Usihofu kuhusu hilo Dr Alex” akasema Kaiza “Sasa mnaweza mkatoka.Niachieni nafasi niweze kumuandaa huyu mtu kwa ajili ya mahojiano” akasema Dr Alex,Kaiza na watu wake wakatoka nje “Kaiza anadai Olivia anazo taarifa nyeti kwa ajili ya usalama wa nchi na kwamba anajihusisha na kikundi cha kigaid cha IS.Olivia naye anadai kuna jambo kubwa linakwenda kutokea hapa nchini na ni yeye pekee mwenye uwezo wa kulizuia lisitokee.Nani mkweli kati yao? Sitaki kujua nani mkweli ninachohitaji ni kumsaidia Olivia.Sitaki kufahamu amefanya nini au kama taarifa za kuwa anashirikiana na kikundi cha IS ni za kweli lakini lazima nimsaidie kuyaokoa maisha yake.Nimekuwa nikishuhudia watu wakiuawa kila wanapoletwa humu ndani lakini kwa mara ya kwanza ninahisi kutaka kumsaidia Olivia aepukane na kifo.Naamini ameletwa hapa kimakosa.Olivia haonekani kama ni mfuasi wa IS.Familia yao ni watu wenye uwezo mkubwa na hana ulazima wowote wa kujiunga na makundi ya kigaidi” akawaza Dr Alex akiwa amesimama pembeni ya kitanda cha Olivia “Olivia amenitaka nimtafute Mathew Mulumbi, hili jina si geni kulisikia.Amesema ni mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha Masai Milk.Anadai huyu anaweza akamsaidia akifahamu kama yuko hapa.Hii ni sehemu ya siri na hatakiwi mtu mwingine asiyehusika kufahamu kinachoendelea ndani ya nyumba hii lakini kwa mara ya kwanza nitavunja kanuni kwa ajili ya kumsaidia Olivia.Siwezi kushuhudia kwa macho yangu akiuawa” akawaza na kumtazama tena Olivia “Olivia anasema kuna jambo kubwa linakwenda kutokea hapa nchini na ni yeye pekee mwenye uwezo wa kulizuia.Ni jambo gani hilo?Nafsi yangu inaniambia Olivia ana jambo kubwa hivyo nalazimika kumsaidia.I have to do something” akawaza Dr Alex na kutoka mle ndani ya chumba alimo Olivia ambapo mlangoni kulikuwa na mlinzi mmoja mwenye silaha aliyekuja na Kaiza.Dr Alex akaenda katika chumba kilichokuwa na runinga kubwa iliyoonyesha kamera mbali mbali zilizozunguka lile jumba akawaona Kaiza na watu wake aliokuja nao wakiwa wamekaa katika viti vya kupumzikia.Haraka haraka akaingia mtandaoni na kuitafuta kampuni ya maziwa ya Masai akapiga simu ikapokelewa na muhudumu wa kike,akaomba kuzugumza na mkurugenzi Mathew Mulumbi.Alitaarifiwa kuwa Mkurgenzi hajafika kazini akapewa namba ya simu ya mkononi ya Mathew akapiga lakini haikuwa ikipatikana.Akapiga tena na kumjulisha muhudumu kuwa namba zile hazipatikani akaomba apatiwe namba nyingine ili aweze kuzungumza na Mathew jambo la muhimu sana akapewa namba ya simu ya nyumbani kwake ili ajaribu kuwasiliana na nyumbani kwa Mathew.
Saada akiwa amejipumzisha katika moja ya chumba cha wageni nyumbani kwa Mathew alisikia mlango ukigongwa.Akainuka haraka haraka na kuelekea mlangoni “Yawezekana Devotha amekuja” akawaza wakati akikinyonga kitasa kuufungua mlango akakutana na mtumishi wa ndani “Dada samahani kwa kukusumbua” akasema yule mtumishi “Bila samahani ,karibu” akasema Saada “Kuna mtu amepiga simu anamtafuta kaka Mathew.Anadai ana jambo la muhimu sana la kumueleza amepiga simu kazini kwake akaambiwa hajafika akapiga namba zake za simu hapatikani.Hata mimi nimepiga namba zake zote za simu ninazozifahamu lakini hapatikani.Imenishangaza kwa kuwa haijawahi kutokea kaka Mathew akashindwa kupatikana simuni.Muda wote simu zake huwa hewani.Nimekuja kwako nataka kufahamu mahala mlikomuacha” akasema yule mtumishi wa ndani akimuangalia kwa wasi wasi “Mathew hapatikani simuni?akauliza Saada “Ndiyo hapatikani simuni.Mlisema mlikuwa naye na akawaelekeza mje hapa nyumbani” “Ndiyo tulikuwa naye na akatuelekeza tutangulie hapa nyumbani kwake na yeye atafuata baadae” “Kwani ninyi mmetokea wapi dada?akauliza Theresa.Kabla Saada hajajibu kitu,simu yake ikaita akaipokea akazungumza kwa muda mfupi halafu akasema “Nimepigiwa simu kuna mgeni wa kaka ngoja nikampokee ninakuja sasa hivi” akasema na kumuacha Saada akiwa na hofu kubwa. “Tumemdanganya huyu msichana kuhusu Mathew na sasa ameanza kuwa na wasiwasi.Hii inaweza kuwa mbaya kwetu kwani tayari amekwisha anza kuhoji mahala aliko Mathew.Devotha yko wapi?” akawaza Saada na kwenda kukaa kitandani “Nimeingia katika matatizo makubwa.Naamini hivi sasa nitakuwa ninasakwa kwa kitendo cha kudukua simu ya rais.Sikupenda kufanya vile lakini nisingeweza kukataa ombi la madam Devotha.Ni mtu ninayemuheshimu sana,amenitoa mbali hadi akanifikisha hapa nilipo leo.Kikubwa ninachokiona kwa sasa ni kuondoka hapa nchini hadi hapo mambo yatakapotulia.Akija hapa nitamshauri ili niweze kwenda nje ya nchi kupumzika kwa muda hadi hapo mambo yatakapokaa sawa kwani kama nikiendelea kukaa hapa nchini lazima nitakamatwa na nikikamatwa Devotha naye atakuwa katika matatizo makubwa” akaendelea kuwaza Saada Katika kibaraza kikubwa cha kuingilia ndani taksi nyeupe iliegesha mlango ukafunguliwa akashuka jamaa mmoja aliyevaa suruali ya jeanz nyeusi na fulana nyeupe,shingoni alikuwa na mkufu mkubwa wa dhahabu.Macho yake aliyafunika kwa miwani mizuri ya jua. “Theresa ! akasema yule jamaa baada ya kushuka garini na kumuona mtumishi wa ndani wa Mathew akiwa amesimama kibarazani “Gosu gosu ! akasema Theresa akamfuata wakasalimiana.Dereva wa taksi akashusha mizigo ya Gosu gosu na Theresa akaiingiza ndani. “Pole na safari” akasema Theresa “Ahsante.Habari za hapa? “Hapa kwema kabisa”akajibu Theresa Theresa anamfahamu Papii Gosu gosu kwani amekuwa akifika hapa mara kwa mara kutokana na kusimamia biashara za Mathew zilizopo nje ya nchi “Mathew yuko wapi?akauliza Gosu gosu “Imekuwa vyema umefika.Kuna jambo limetokea hapa muda mfupi kabla hujawasili” akasema Theresa “Kumetokea nini?akauliza Gosu gosu akionekana kuwa na hofu kidogo “Ni kuhusu kaka Mathew” “Nini kimetokea Theresa? “Mathew aliondoka hapa nyumbani asubuhi leo akatoa maelekezo tuandae vyumba kwa ajili yako na dada Ruby.Mchana huu walifika watu wawili wakadai kuwa wameelekezwa na Mathew wafike hapa na wamsubiri.Baadae mmoja akaondoka akabaki mmoja nikamuandalia chumba chumba cha wageni akaenda kupumzika.Muda mfupi uliopita kuna mtu amepiga simu akadai anataka kuzungumza na Mathew kama yuko hapa nyumbani.Anadai amemtafuta bila mafanikio.Nilishangaa kwa kuwa kaka Mathew hajawahi kuzima simu zake.Muda wote anapatikana hewani.Nini kimetokea leo hadi simu zake zote zisipatikane ?” akasema Theresa “Theresa unasema toka Mathew alipoondoka asubuhi hajarejea hadi mida hii? akauliza Gosu gosu “Hajaonekana tena toka alipoondoka asubuhi.Si kuonekana tu hata kupiga simu hajapiga”akajibu Theresa “Something is not right” akawaza Gosu gosu “Huyo mtu aliyepiga simu amejitambulisha yeye ni nani ?akauliza “Hakusema yeye ni nani lakini alionekana kuwa na shida sana ya kuzungumza na Mathew.Inaonekana kuna jambo la muhimu sana alitaka kumueleza.Aliacha namba zake za simu ili Mathew ampigie atakapofika” akasema Theresa “Huyo mgeni ambaye anadai ameelekezwa na Mathew aje hapa umewahi kumuona? “Ni mara yangu ya kwanza kumuona” akajibu Theresa na simu yake ikaita akaipokea na kuzungumza kwa sekunde chache halafu akamgeukia Gosu gosu “Nilikueleza kuwa wageni wale walikuwa wawili na mmoja wao akaondoka akabaki moja,nimejulishwa na walinzi wa getini kuwa yule mwenzake amerejea” “Good.Niachie mimi nitamuhoji ili tujue mahala aliko Mathew” akasema Gosu gosu.Wote waliyaelekeza macho yao nje na muda mfupi likafika gari jeusi likaegesha mbele ya nyumba akashuka mwanamke mmoja mwenye umbo zuri. “Ni yule pale” akasema Theresa wakimtazama mwanamke yule akishuka garini “She’s so pretty !! akanong’ona gosu gosu Mwanamke yule akagonga mlango Theresa akaenda kuufungua na kumkaribisha ndani. “Mpaka sasa sijalifahamu jina lako” akauliza “Ninaitwa Theresa.Wewe unaitwa nani? “Naitwa Devotha” “Nafurahi kukufahamu Theresa.Habari za toka wakati ule? “Nzuri kabisa karibu tena mama Devotha” akasema Theresa “Ahsante sana” akasema Devotha na kuyaelekeza macho yake kwa Gosu gosu “Hi”akasema “Hi”akajibu Gosu gosu “Mama Devotha huyu ni rafiki wa kaka anaitwa papii Gosu gosu.Amefika muda mfupi uliopita kutoka nje ya nchi” “Karibu sana Papii..ouh gosh jina lako refu” “Papii Gosu gosu” akasema Gosu gosu “Gosu gosu.Nafurahi kukutana nawe.Habari za wapi? “Nimetokea Dubai” akajibu Gosu gosu “Ninaitwa Devotha Adolph ni rafiki wa Mathew” “Nafurahi kukufahamu Devotha” akajibu Gosu gosu “Mathew hajafika bado?akauliza Devotha “Bado hajaonekana” akajibu Theresa “Yule msichana wangu niliyemuacha hapa yuko wapi?akauliza “Yuko chumba cha wageni anapumzika” “Nipeleke nikaonane naye” akasema Devotha huku akiinuka “Devotha we need to talk! Akasema Gosu gosu “Unasemaje Gosu gosu? “Umenisikia vizuri.We need to talk.Please follow me ! akasema Gosu gosu na kuinuka,Devotha akamfuata wakaelekea katika chumba cha maongezi “Devotha mimi si mzungumzaji mzuri.Maneno yangu huwa machache sana.Nataka kufahamu mahala alipo Mathew” “Mbona unaonekana kuwa na hofu gosu gosu?Mathew is fine” “Mathew hapatikani simu zake zote zimezimwa.Ulimwambia Theresa kuwa aliwaelekeza mfike hapa.Where is he? “Gosu gosu naomba usiwe na wasiwasi tafadhali.Mathew ni rafiki yangu.Mimi na yeye tulikuwa na mazungumzo Fulani ya kibiashara na yule msichana niliyenaye anaitwa Saada.Ni Mtanzania lakini kwa sasa anaishi nchini Msumbiji.Mathew alielekeza nimlete Saada hapa nyumbani kwake na tumsubiri hadi atakapofika ili tufanye mazungumzo.Kwa kuwa nilikuwa na mizunguko mingine ya kufanya ilinilazimu kumuacha Saada hapa na kuondoka.Kwa nini Mathew hapatikani simuni?akauliza Devotha.Gosu gosu akavua miwani yake na kumtazama Devotha kwa macho makali yenye kuogofya. “Mimi ndiye msimamizi mkuu wa biashara za Mathew na kila anachotaka kukifanya huwa ananishirikisha.Nataka kufahamu ni biashara gani wewe na Mathew mnataka kuifanya na huyo Saada?akauliza Gosu gosu “Ni biashara ya madini” “Madini?akauliza Gosu gosu na kutoa kicheko kidogo “Mathew hajawahi kufikiria kufanya biashara ya madini.Ni mara ya kwanza ninasikia kutoka kwako kuwa Mathew anataka kufanya biashara ya madini.Mathew ni billionea ana miradi mingi mikubwa inayomuingizia fedha nyingi hajawahi kufikiria kujiingiza katika biashara hiyo ya madini” akasema Gosu gosu “Kweli kabisa mimi na yeye tunataka kuingia ubia ili tununue mgodi wa kuchimba dhahabu” akasema Devotha “Mathew anao washauri wake wa biashara na mimi nikiwa mmoja wao,kila anachofikiria kukifanya huwa kinaletwa kwetu tunakichambua kama kinaweza kuwa na faida na tunamshauri.Mathew anaiamini mno timu yake hiyo ambayo ndiyo iliyomsaidia sana kwa biashara zake kukua na kuwa kubwa.Hajawahi kuleta kwetu wazo la mradi wa madini” akasema Gosu gosu. “Unataka kusema nini Gosu gosu? Mimi muongo?akauliza Devotha “Sijasema hivyo lakini ninapata ukakasi kidogo kuamini hicho unachoniambia.Nataka nikazungumze na Saada pia.Devotha mimi ni mtu mbaya sana naomba usithubutu kunidanganya.Nikigundua umenidanganya………” akasema Gosu gosu “Gosu Gosu let’s talk” akasema Devotha wakati Gosu Gosu akipiga hatua kutoka mle chumbani “Please sit down! Akasema Devotha “Niambie haraka hicho unachotaka kuniambia” akasema Gosu gosu “I know where Mathew is”akasema Devotha “Where is he? akauliza Gosu Gosu.Tayari sura yake ilikwisha badilika “Kabla ya kukueleza chochote kuhusiana na mahala alipo Mathew kuna mambo ambayo nataka uyafahamu” akasema Devotha “Go ahead” akasema Gosu Gosu “Naitwa Devotha Adolph.Ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi…” “Devotha ninachotaka kukifahamu kutoka kwako ni kitu kimoja tu.Mathew yuko wapi? Hizo habari za usalama sijui wa nchi sizihitaji” akasema Gosu Gosu kwa sauti kali “Taratibu Gosu Gosu.Ili ufahamu mahala alipo Mathew unahitaji kupata maelezo kwanza.Tafadhali naomba unisikilize” akasema Devotha “Idara ninayoiongoza ina jukumu kubwa la kuhakikisha inang’amua viashiria vyote vya kuhatarisha usalama wa nchi na kuviondoa kabla ya kuleta madhara” akanyamaza kidogo kisha akasema “Tulipata taarifa kuna mtanzania mmoja amekutana na mtu kutoka kundi la kikaidi la IS jijini Kinshasa.Tulimgundua mtu huyo ni daktari anaitwa Dr Olivia Themba.Tulimfuatilia toka alipokuwa Kinshasa na aliporejea http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Dar es salaam tulimteka lengo likiwa ni kufahamu mahusiano yake na kikundi cha IS.Tulipochunguza mawasiliano yake tuligundua alikuwa akiwasiliana na mtu anaitwa Sayid Omar ambaye anatajwa kuwa mfadhili mkubwa wa IS.Tulimtaka atupe maelezo kuhusiana na Sayid Omar na akatupa namba Fulani akidai zingetuwezesha kufahamu alipo Sayid Omar.Namba zile zilifunga mtandao wetu wa mawasiliano.Baadae tuligundua kwamba namba zile alipewa na Mathew Mulumbi hivyo tukaanza kumfuatilia Mathew pia,tukaweka mtego na leo asubuhi tulifanikiwa kumpata Mathew na amehifadhiwa sehemu Fulani kwa mahojiano” akasema Devotha Gosu Gosu akainuka uso wake ukiwa umejikunja akakunja ngumu.Devotha tayari alikwisha msoma Gosu Gosu naye akasimama. “Easy Gosu Gosu..Take it easy..Sit down and let me finish” akasema Devotha “Nakupa nafasi ya kumaliza hicho unachotaka kunieleza na sentensi ya mwisho nataka ieleze alipo Mathew” akasema Gosu Gosu..Wakatazamana kwa muda Devotha akaendelea “Olivia alitaka kuonana na rais.Nikafanya juhudi akaonana naye wakazungumza na hapo ndipo jambo jipya likabainika” akasema Devotha na kumueleza Gosu Gosu kila kitu kuhusiana na madai ya Olivia kuwa Edger kaka yuko hai. “Baada ya kuona msisitizo mkubwa aliouweka Olivia katika suala hili la Edger kaka niliamua kulipa uzito na kulichunguza kufahamu ukweli wake.Olivia alinihakikishia endapo nitafanikiwa kufahamu alipo Edger kaka angenieleza siri kubwa ambayo anaamini ninahitaji sana kuifahamu.Nilionana na Mathew pia nikamuhoji na akanipa ushirikiano mkubwa ambao sikuutegemea na..”kabla hajamaliza sentensi yake Gosu Gosu akamkatisha “Where is he?! Akauliza Gosu Gosu huku akigonga meza “Gosu Gosu easy ! Let me finish ! “Devotha hili si suala la kufanyia mzaha hata kidogo.Hayo yote unayonieleza yanapita sikio hili na kutokea lingine.Ninachohitaji kufahamu ni kitu kimoja tu Mathew yuko wapi? Kila unapotoa maelezo yako na kumtaja Mathew unazidi kunipandisha hasira!! Akasema Gosu Gosu kwa ukali “Tafadhali Gosu Gosu nipe dakika chache nimalizie kukupa maelezo yangu” akasema Devotha “Go ahead” akasema Gosu Gosu “Nimekwambia nilizungumza na Mathew akanipa ushirikiano mkubwa na alinisaidia kuyasoma hata mawasiliano ya Olivia na Sayid Omar yaliyoandikwa kwa Lugha ya kiarabu.Baada ya kumuhoji niligundua Mathew hahusiki na chochote kuhusu IS bali lengo lake lilikuwa ni kumlinda Olivia.Kwa bahati mbaya nisingeweza kumtoa mahala alipo kwa haraka hivyo bado anaendelea kuwepo mahala hapo lakini nakuhakikishia yuko salama kabisa.Alinishauri niendelee kulichunguza suala hili la Edger Kaka na akanieleza anao watu wawili ambao wanaweza wakanisaidia sana katika jambo hili wanatoka nje ya nchi naamini mmoja wao ni wewe.Alinielekeza niwafuate na kuwataka mnisaidie katika kulichunguza hili jambo” akanyamaza akamtazama Gosu Gosu halafu akaendelea “Kitu alichonishauri nikifanye ni kudukua mawasiliano ya rais jambo ambalo nililifanya” “Ulipata nini kutoka katika simu ya rais? akauliza Gosu Gosu “Nothing.Waliwahi kugundua haraka kuwa simu ya rais imedukuliwa na hatukuweza kuendelea tena.Ikanilazimu kumchukua Saada ambaye ndiye aliyekuwa anaifanya kazi hiyo ya udukuzi na kuja kumficha hapa ambako ninaamini ni sehemu salama kwake.Baada ya hapo niliamua kwenda kuonana na Olivia kuzungumza naye kwa kina lakini nilipofika mahala alipokuwa anahifadhiwa sikumkuta.Tayari aliondolewa na kupelekwa mahala kusikojulikana.Tayari rais amegundua kuwa ni mimi niliyedukua mawasiliano yake hivyo waliniwekea mtego wanikamate.Kwa bahati nzuri uwezo wangu ni mkubwa kuliko watu waliotumwa kuja kunikamata hivyo niliwachakaza vibaya na kuondoka kuja hapa kutafuta msaada.Gosu Gosu suala hili ni kubwa na mimi peke yangu siwezi ninaomba uniamini na tushirikiane kwa pamoja kumtafuta Olivia na kuujua ukweli.Hapa nilipo ninaamini ninatafutwa na nimewekewa vizuizi kila kona.Simu yangu imefungwa na siwezi kuingia hata katika mtandao wetu.Nimezuiliwa kila mahali” akasema Devotha. “Devotha kama Mathew alikuelekeza kupata msaada kutoka kwetu ,basi karibu sana.Yule ni mkuu wetu ni kaka yetu na maelekezo yake ni amri kwetu.Tutashirikiana nawe lakini kwa sharti moja tu” “Sharti gani Gosu Gosu? “Mathew lazima awe wa kwanza kukombolewa.Tusaidie tumpate Mathew na kisha tutakusaidia umpate Olivia” “Mathew yuko sehemu salama.Olivia hajulikani alipo.Nashauri nguvu kubwa tuielekeze kumtafuta Olivia kwanza halafu nitawasaidia kumpata Mathew Mulumbi” “Mathew first ! akasema Gosu Gosu “Fine.Lakin……..” akanyamaza Devotha baada ya Theresa mtumishi wa ndani wa Mathew kuonekana katika mlango wa kioo “Karibu Theresa” akasema Gosu Gosu “Kaka,yule mtu amepiga tena anauliza kama nimefanikiwa kuwasiliana na Mathew” akasema Theresa “Naomba simu niwasiliane naye” akasema Gosu Gpsu “Nani anayemtafuta Mathew?akauliza Devotha “Kuna mtu amepiga simu anamtafuta Mathew anadai ana jambo la muhimu sana la kuzunguma naye.Hii ni mara ya pili anapiga.Yawezekana ana jambo la muhimu”akasema Gosu Gosu “Wait ! Unamfahamu mtu huyo?Devotha akauliza “Hapana simfahamu.Kuna njia moja tu ya kujua tatizo lake.Anaonekana hamjui Mathew nitampigia na kujifanya mimi ndiye Mathew halafu tutajua kwa nini anamtafuta Mathew”akasema Gosu Gosu na kwa kutumia simu ya nyumbani kwa Mathew akampigia yule mtu simu ikapokelewa “Hallow” akasema jamaa wa upande wa pili aliyepokea simu “Hallow,Mathew Mulumbi hapa.Ninazungumza na nani?akauliza Gosu Gosu “Naitwa Dr Alex.Nimekutafuta sana.Kuna jambo nataka tuzungumze la muhimu” “Jambo gani Dr Alex? “Ni kuhusu Olivia” “Olivia?akauliza Gosu Gosu na kumtazama Devotha “Nakusikiliza DrAlex” akasema Gosu Gosu na mara akasikia sauti ikiuliza kwa ukali “Dr Alex unazungumza na nani? “Nazungumza na rafiki yangu!! Akajibu Dr Alex “Unamueleza nani kuhusu Olivia?ikauliza sauti ile kali.Gosu Gosu alisikia kila kitu kupitia simu yake kwani Dr Alex hakuwa ameikata “Nakuuliza unazungumza na nani? ikauliza sauti ile kwa ukali “I can explain Kaiza”akasema Dr Alex na mara simu ikakatwa “Gosu Gosu kuna nini kuhusu Olivia?” akauliza Devotha.Gosu Gosu akamueleza kila kitu alichokisikia “ My God !! Kaiza alikuwa msaidizi wangu na ninaamini yuko na Olivia.Wako wapi hospitali? Huyo Dr Alex ni nani? Akauliza Devotha “Yawezekana Dr Alex anataka kumsaidia Olivia na ndiyo maana alikuwa anamtafuta Mathew.Nadhani alitaka kumjulisha mahala alipo ndipo huyo jamaa Kaiza akaingia” “Gosu Gosu yawezekana hali ya Olivia ni mbaya ndiyo maana amepelekwa hospitali.Yawezekana ameteswa sana hali yake ikabadilika.Tunatakiwa tukamuokoe Olivia haraka kabla hajapoteza maisha”akasema Devotha “Mathew first! Akasisitiza Gosu Gosu “Gosu Gosu nadhani itakuwa vyema kama tukianza kushughulikia suala la Olivia.Ni muhimu sana.Maisha yake yako hatarini” “Devotha hakuna kitu kitakachofanyika bila ya Mathew kupatikana.Ukitaka mimi na wewe tuzungumze lugha moja nionyeshe mahala alipo Mathew Mulumbi” akasisitiza Gosu Gosu.Devotha akavuta pumzi ndefu halafu akasema “Mathew yupo mahala panaitwa Kitalu1.Idara yetu ina sehemu zake mbali mbali na zimepewa majina ya vitalu na kila kitalu kina namba.Mahala alipo Mathew pamepewa hadhi ya namba 1 kutokana kuwa sehemu salama zaidi kuliko zote tulizonazo.Ni sehemu pekee ambayo hata kiongozi wa nchi anaweza akajificha hapo hata kwa mwaka mzima pale panapokuwa na kitisho cha usalama wake.Nataka kufahamu mko wangapi jumla?akauliza Devotha “Niko peke yangu kama unavyoniona” “Peke yako?Devotha akashangaa “Ndiyo niko peke yangu.Mathew alikueleza tuko wawili,mwingine hajawasili bado anaitwa Ruby nategemea atawasili jioni ya leo akitokea Uingereza”akasema GosuGosu “Hapa kuna tatizo Gosu Gosu.Kitalu 1 ni sehemu yenye ulinzi wa kutosha na inahitaji watu wa kutosha wakiwa na silaha kama kweli tunataka kumuokoa Mathew Mulumbi.Kumefungwa kamera kila mahali hivyo kila tutakachokifanya kitaonekana.Ninahitaji tupate watu kama kumi hivi” akasema Devotha “Hakuna watu kumi.Niko peke yangu”akasema GosuGosu na Devotha akaendelea kumshangaa “Gosu Gosu tafadhali tusiweke mzaha katika suala hili.Tuangalie namna tutakavyoweza kupata watu wa kutusaidia katika suala hili” akasema Devotha “Devotha mimi peke yangu ni kikosi kinachojitosheleza” akasema Gosu Gosu “Sijakuelewa Gosu Gosu unamaanisha nini? “Hakuna haja ya kuwa na watu kumi au zaidi mimi peke yangu ninatosha kabisa” “Gosu Gosu usifanye mzaha katika mambo muhimu kama haya.Usalama wa Mathew Mulumbi na Olivia unatutegemea sisi kwa sasa hivyo tunapaswa kuwa na kikosi cha watu wasiopungua kumi.Hakuna mahala tunakoweza kupata watu hata kwa kuwakodi na kuwalipa? “Mimi ni mwanajeshi.Nimekulia msituni na toka nikiwa mdogo nimekuwa nikipigana vita.Ninajiamini mimi peke yangu ni zaidi ya kikosi” akasema Gosu Gosu.Devotha alikosa neno la kusema akabaki anamtazama. “Usishangae Devotha.Nilichokwambia ni kitu cha kweli kabisa.Hata Mathew ananifahamu vyema ndiyo maana alinipigia simu nikiwa Dubai na kunitaka nifike haraka Dar es salaam kumsaidia kumtafuta rafiki yake aliyetekwa ambaye naamini ni Olivia”akasema Gosu Gosu.Wakatazamana kwa sekunde chache “Ninachokihitaji kwa sasa ni kupata silaha..”akasema Gosu Gosu “Usihofu kuhusu silaha utapata kila aina ya silaha unayoitaka”akasema Devotha “Good.Kingine ninachohitaji ni kuipata ramani ya jengo lilivyo hadi kufika mahala alipo Mathew naamini unalifahamu vyema jengo hilo” akasema Gosu Gosu wakaelekea katika maktaba ndogo hapo nyumbani kwa Mathew naDevotha akaanza kuichora ramani ya jengo lile ilivyo.Gosu Gosu akakumbuka kitu “Ulisema mtu aliyekusaidia kudukua simu ya rais yuko hapa?Gosu Gosu akauliza “Ndiyo anaitwa Saada.Ni mtaalamu sana wa mambo hayo” “Huyo anaweza akawa na msaada mkubwa kwetu.Ulisema jengo hilo lina kamera za ulinzi.Nitahitaji mtu wa kudukua mtandao wenu ili kucheza na kamera za ulinzi zilizomo humo ndani kutuwezesha kuingia bila kujulikana.Unadhani Saada anaweza akaifanya hiyo kazi?akauliza Gosu Gosu “Ndiyo anaweza” akasema Devotha na Saada akaitwa.Devotha akamueleza kila kitu wanachotaka kukifanya.Saada akawasha kompyuta yake akajaribu kuingia katika mtandao wa idara yao lakini hakufanikiwa “Kuna tatizo” akasema Saada “Kuna tatizo gani? akauliza Devotha “Namba zangu za siri za kuingilia katika mtandao wa idara zimebadilishwa na siwezi kuingia tena” akasema Saada “Nilitegemea kitu hicho kutokea.Wamebadilisha kila kitu nadhani lengo ni kunidhibiti mimi.” akasema Devotha “Devotha wewe umekuwa kiongozi wa idara hii naamini lazima kuna watu ambao ni watiifu kwako hata kama litatokea jambo gani.Kuna yeyote unayeweza kumpigia akakusaidia kuingia katika mtandao?akauliza Gosu Gosu.Devotha akatafakari na kusema “Wapo kama watatu hivi ambao naamini wako tayari kwenda nami kaburini” “Good.Tutatumia simu ya humu ndani kumpigia mmoja wao na utamuomba akusaidie ili Saada aweze kuingia katika mtandao wa idara yenu na kufuatilia Kamera” akasema Gosu Gosu na kwenda kuchukua simu akampatia Devotha akaziandika namba na kupiga simu ikaanza kuita baada ya muda ikapokelewa “Hallow” ikasema sauti upande wa pili baada ya kupokea simu “Zai tafadhali usistuke wala kutamka jina langu” akasema Devotha “Baba shikamoo.Habari za huko?akasema Zai huku akisimama na kutoka mahala alipokuwa akaenda kujificha mahala kusiko na watu “Hallo madam” akasema Zai kwa sauti ndogo akiwa amejifungia ndani ya chumba Fulani “Zai nina tatizo ninahitaji msaada wako” akasema Devotha “Madam kuna nini?Imekuja taarifa kwamba kuanzia sasa nafasi yako imeshikwa na Kaiza” “Zai kuna tatizo limetokea nitakueleza siku nyingine lakini kwa sasa kuna msaada nahitaji” “Nikusaidie nini Madam?akauliza Zai “Ninataka kuingia katika mtandao wa idara.Namba zangu zimebadilishwa nataka unisaidie kuifungua kadi yangu ambayo huwa ninaitumia hadi nyumbani kwangu” “Madam hilo ni jambo la hatari sana wanaweza wakagundua ni mimi niliyekusaidia nikajiweka katika matatizo makubwa” “Usiogope Zai.Siku zote nimekuwa kinga yako hata pale ulipoharibu kazi.Naomba na mimi leo unisaidie hili jambo dogo.Niunganishe katika mtandao.Hakuna atakayejua” akasema Devotha Zai akafikiri kidogo na kusema “Sawa madam naomba namba yako ya kadi” Devotha akamtajia namba za kadi yake,Zai akaenda katika chumba Fulani kulikokuwa na kompyuta nyingi akakaa katika kompyuta moja na kuanza kuifanya kazi ile baada ya dakika tano akampigia simu Devotha “Madam tayari kadi yako nimeifungua.Ninaomba itumie ndani ya saa mbili tu kisha haitafanya kazi tena.Kama kuna kitu ambacho unataka kukifanya basi kifanye ndani ya muda huo kabla ya muda niliouweka kumalizika.Namba za siri utakazotumia kuingia katika mtandao wetu ni Alpha- Bravo-660” “Zai nakushukuru sana” akasema Devotha na kukata simu akampatia Saada zile namba za siri akaingiza wakafanikiwa kuingia katika mtandao wa idara ya siri ya usalama wa nchi. “Good.Kinachofuata sasa ni silaha”akasema Gosu Gosu “Silaha tunazipata nyumbani kwangu.Ninazo silaha za kutosha” akasema Devotha wakaingia katika gari wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Devotha.Waliingia haraka haraka Gosu Gosu akachukua silaha alizozihitaji kisha wakaondoka Kutoka nyumbani kwa Devotha wakaelekea Lupai hotel ambayo haiko mbali sana na kitalu 1.Pale wakachukua chumba na kumuacha Saada “Saada utakaa katika chumba hiki na utaongoza kila kitu kutokea hapa” akasema Gosu Gosu na kujaribu kifaa alichokiweka sikioni kwa ajili ya mawasiliano halafu akamgeukia Devotha “Devotha are you ready?akauliza Gosu Gosu “I’m ready” akasema Devotha wakaingia garini na kuondoka kuelekea kitalu 1.Devotha alikaa kiti cha mbele na Gosu Gosu akajificha nyuma akiwa na silaha.
“Dr Alex nataka unieleze ni nani uliyekuwa unawasiliana naye kuhusu Olivia?Kaiza akamuuliza Dr Alex aliyekuwa amekestishwa kitini amefungwa mikono. “Nina binti yangu anaitwa Olivia anasoma shule ya Ukombozi International,nilipaswa kwenda kumchukua shuleni lakini kutokana na kazi iliyopo hapa sintaweza.Niliyekuwa nawasiliana naye ni rafiki yangu nilitaka kumuomba aende shuleni akamchukue mwanangu” akasema Dr Alex.Kaiza akamtazama kwa makini Kaiza akachukua simu na kumtaka DrAlex ampatie namba za simu za mkuu wa shule anakosoma mwanae halafu akampigia simu “Dr Alex kama unanidangan….” Akasema Kaiza na simu aliyopiga ikapokelewa “Hallow” ikasema sauti ya mwanamama upande wa pili “Hallow.Hapo ni Ukombozi international school?akauliza Kaiza “Ndiyo nikusaidie nini tafadhali? “Kuna mwanafunzi anaitwa Olivia Alex anasoma katika shule yako? “Ndiyo anasoma katika shule hii” “Sawa ahsante sana” akasema Kaiza na kukata simu “Umeamini sasa? akauliza Dr Alex akiwa amekunja sura kwa hasira “Samahani Dr Alex nilitaka kuwa na uhakika,nilistuka niliposikia ukimjulisha mtu kuhusu Olivia nikadhani unamuongelea huyu mwanamke tuliyenaye ambaye naye anaitwa Olivia”akasema Kaiza “Naamini Olivia atakuwa tayari muda huu.Tunaweza kuendelea na zoezi letu”akasema Kaiza “Sina hakika sana lakini tunaweza kuendelea” akasema Dr Alex wakaelekea katika chumba alimo Dr Olivia.Kaiza akamsogelea karibu na kumuita.. “Olivia..!.Olivia ! ..Olivia hakuinua hata ukope. “Dr Alex are you sure she’s okay?akauliza Kaiza.Dr Alex akachukua kipimo akampima halafu akamgeukia Kaiza “Kaiza naomba tuahirishe zoezi hali ya Olivia si nzuri” “Dr Alex nimekwisha kueleza umuhimu wa huyu mtu hivyo jitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anakuwa tayari kuhojiwa” akasema Kaiza “Naomba tumpe muda zaidi apumzike.Mwili wake bado hauwezi kuhimili mateso mengine zaidi na kama mkilazimisha kutaka kumtesa mtamuua na mtakosa kile mnachokitafuta kutoka kwake” akasema Dr Alex.Kaiza akaitazama saa yake halafu akasema “Dr Alex ninaongeza saa moja pekee.Jitahidi ndani ya huo muda awe amekuwa tayari kuhojiwa.Kama ndani ya saa moja hatakuwa tayari tutafanya tunavyojua sisi” akasema Kaiza na kutoka ndani ya kile chumba akamuacha Dr Alex peke yake.Jasho lilikuwa linamtoka “Nilitaka kuharibu kila kitu.Hawa jamaa hawana imani na mimi na wananifuatilia.Kuna kitu wamekwisha kihisi.Natakiwa kuwa makini sana” akawaza Dr Alex akifuta jasho lililokuwa linamtoka usoni “Nashukuru nilimpata Mathew Mulumbi ingawa sikumueleza chochote kuhusiana na Olivia hawa jamaa wakaniwahi lakini naamini atakuwa amefahamu Olivia yuko katika matatizo kwani sikuikata simu makusudi ili aweze kusikia kila kilichotokea.Tatizo ni kufahamu mahala alipo Olivia.Siwezi tena kuwasiliana naye kumfahamisha zaidi kwani simu yangu wameichukua hawa jamaa.Natakiwa kutafuta namna nyingine ya kuhakikisha ninamsaidia Olivia.Nilimchoma dawa kumfanya awe dhaifu ili hawa jamaa wasiweze kumtesa natakiwa kuendelea kutafuta mwanya wa kumuokoa Olivia ndani ya saa moja alilotoa Kaiza” akawaza Dr Alex. Kaiza alitoka ndani ya kile chumba akawaita vijana wake wakaenda kukaa katika chumba cha kupumzikia “Simuamini kabisa huyu DrAlex.Nataka tumuelekezee macho kila anachokifanya.Nataka mtu mmoja akae katika chumba alimo Olivia ili kufuatilia kila kinachoendelea.Ninahisi kuna mchezo unaendelea hapa”akaelekeza Kaiza na kuwapanga vijana wake mara simu yake ikaita akaipokea “Deo kuna taarifa gani?akauliza “Kaiza nimepokea taarifa kutoka kitalu 2 kuna jambo limetokea” “Kumetokea nini?Devotha amepatikana?akauliza Kaiza “Hapana mkuu” “Sasa kumetokea nini? “Nimejulishwa kuwa wale makachero niliowaweka kitalu 2 kwa ajili ya kumkamata Devotha wameshindwa kuifanya kazi ile na badala yake wote wamekutwa wamefungwa katika ofisi ya Devotha” Kaiza akashusha pumzi “Watu watatu wameshindwaje kumkamata Devotha? Deo nimekuteua uwe msaidizi wangu kwa muda hivyo huu ni mtihani wako wa kwanza,nataka nitakapomaliza hapa niwe tayari nimepata taarifa za kukamatwa Devotha.Sitaki kusikia eti mmeshindwa kumkamata yule mwanamke.Tunao watu wengi wenye uwezo mkubwa,tengeneza timu nzuri ya watu ambao unaamini wataweza kumpata Devotha.Sitaki hadi machweo yanaingia Devotha awe bado hajapatikana.Umenisikia Deo? “Nimekusikia mkuu” “Good.Jipange vizuri kumsaka Devotha.Nimekuteua uwe msaidizi wangu kwa kuwa naufahamu uwezo wako hivyo achana na kila kitu na uelekeze nguvu katika suala moja tu la kumtafuta Devotha.Wekeni mitego kila sehemu kuanzia nyumbani kwake hadi sehemu zote anazopenda kutembelea.Wataarifu walinzi katika vitalu vyote waimarishe ulinzi na ikitokea Devotha akaenda katika kituo chochote akamatwe mara moja” akasema Kaiza na kukata simu “Damn ! Watu watatu wameshindwaje kumkamata yule mwanamke? Kwa uzembe wao sasa Devotha ameshafahamu anatafutwa na kuifanya kazi ya kumkamata iwe ngumu zaidi.” akawaza Kaiza “Kwa vyovyote vile lazima Devotha apatikane.Kama lisingekuwa hili suala la Olivia ningemtafuta mimi mwenyewe na kuhakikisha anapatikana lakini ninashughulikia suala muhimu sana na nilimuahidi rais siku haitakwisha leo kabla Olivia hajafunguka.Ninazidi kuchanganyikiwa muda unavyokimbia na bado sijapata chochote kutoka kwake.Zoezi linazidi kuwa gumu kutokana na hali ya Olivia kutokuwa ya kuridhisha.Naamini baada ya saa moja atakuwa amerejea katika hali yake ya kawaida na leo ni leo lazima atasema ukweli wote”akaendelea kuwaza.
Dr Neerav patel daktari bingwa wa figo akiwa ameshika faili mkononi alitembea haraka haraka akaingia ndani ya jengo kubwa la ghorofa sita ambalo lina wodi maalum wanazokaa watu wenye uwezo mikubwa kifedha na viongozi wa serikali.Katika jengo hili ndiko alikokuwa amelazwa Coletha mtoto wa Rais Dr Evans.Dr Neerav alikwenda hadi katika lifti na kubonyeza namba sita akielekea katika ghorofa ya juu kabisa alikokuwa amelazwa Coletha.Alikuwa peke yake katika lifti akapanda hadi katika ghorofa ya sita milango ya lifti ikafunguka akashuka.Mara tu aliposhuka akakutana na watu wawili waliovaa suti wakiwa na vifaa ambavyo walimkagua kila anayeshuka katika lifti ili kuthibitsha hana silaha.Dr Neerav hakukaguliwa akawaslimu wale wanausalama akaenda zake. Katika mfuko wa koti wa upande wa kulia alipachika kitu mfano wa nembo Fulani na hakuna aliyekitilia maanani kitu kile lakini ile ilikuwa ni kamera ndogo ya siri yenye uwezo mkubwa wa kuchukua picha hata katika mazingira yenye giza.kamera ile ilikuwa inaendelea kuchukua picha na kuzihifadhi. Kulikuwa na walinzi kadhaa katika njia ya kuelekea katika chumba alimolazwa Coletha.Dr Neerav alikaribia kufika katika chumba cha mwisho kabisa ambamo ndimo alimolazwa Coletha.kila aliyekaribia chumba kile alizuiliwa na maafisa usalama na kuhojiwa anakoelekea.Aliwapita akina dada wawili waliokuwa wamesimamishwa wakihojiwa ambao walijitambulisha ni marafiki wa Coletha.Dr Neerav hakusimamishwa akawapita maafisa wale wa usalama waliopata wanne akaenda hadi katika mlango wa chumba alimolazwa Coletha ambao ulikuwa wazi akaingia ndani ya kile chumba na kumkuta mwanadada mmoja aliyekuwa amekaa katika sofa akitazama runinga na katika kitanda alilala msichana mmoja ambaye hata bila kuambiwa alionekana ni mgonjwa “Karibu daktari” akasema yule mwanadada aliyekuwa amekaa sofani aliyeonekana ni mlinzi wa Coletha “Ahsante sana anaendeleaje mgonjwa?akauliza Dr Neerav “Hali yake inabadilika badilika lakini daktari anasema hakuna tatizo” akasema yule mwanadada.Dr Neerav akaenda katika kadi iliyokuwa katika kitanda alicholala Coletha akaisoma halafu akaaga na kuondoka moja kwa moja akaelekea katika lifti akaingia na kushuka chini kabisa.Alishuka katika lifti na kutoka ndani ya lile jengo akaelekea katika ofisi yake iliyoko kitengo cha figo.Akachukua simu yake akapiga “Hallow Dr Neerav” akasema jamaa aliyepokea simu “Fahad nimemaliza lile zoezi” “Good.Vipi ulinzi chini ukoje?akauliza Fahad “Nje ya jengo kuna walinzi wawili waliovaa sare za kampuni binafsi ya ulinzi wakiwa karibu na mlango mkuu wa kuingilia ndani ya jengo.Kwa ujumla naweza kusema hakuna ulinzi kwa upande wa nje” “Safi sana.Vipi kwa upande wa ndani? Akauliza Fahad “Kwa upande wa ndani wapo walinzi kadhaa kwa haraka haraka niliowaona ni kama sita au saba hivi wote wakiwa wamevalia mavazi yao yale ya suti” “Umefanikiwa kumuona Coletha na kuhakikisha yumo mle ndani?akauliza Fahad “Nimeingia hadi katika chumba alimolazwa nimefanikiwa kuonana naye” “Vipi hali yake? “Hali yake hata kwa kumtazama tu utagundua ni mgonjwa.Nilikuwa na kamera yangu nimechukua picha nyingi nitazituma kwako ili uzipitie” “Nashukuru sana Dr Neerav.Naomba tafadhali endelea kufuatilia kwa karibu kama kutakuwa na mabadiliko yoyote au kama atahamishwa usiku wa leo tunakuja kumchukua” “Ninaendelea kufuatilia Fahad na kama kutatokea mabadiliko yoyote nitakujulisha” akasema Dr Karim na kukata simu “Usiku wa leo Tanzania itatikiswa tena pale tutakapofanya shambulio katika hospitali na kumchukua mtoto wa rais.Naamini kabla ya kufika asubuhi ya kesho rais atakuwa ametujulisha mahala aliko Edger Kaka.Olivia alikosea sana kuamua kushirikiana na serikali bila kujua kuwa tayari IS inao mtandao mkubwa hapa nchini ambao hakuna anayeufahamu zaidi ya Edger Kaka.Edger Kaka alipata mafanikio makubwa na kujulikana hapa nchini bila watu kujua kama kuna timu nyuma yake inayomnyanyua.Tutaitikisa nchi hii hadi tumpate Edger” akawaza Fahad
Devotha aliikaribia barabara ya kuelekea kitalu 1. “Saada ninakaribia kuingia barabara ya kuelekea Kitalu 1.Kila kitu umekiweka sawa?akauliza Devotha “Kila kiti kiko sawa madam.Utakapoingia katika barabara ya kuelekea kitalu 1 nitazima kamera inayochukua picha za kila gari linaloekea katika geti.Hamtaweza kuonekana hivyo mtaingia ndani ya jengo kirahisi” akasema Saada. Baada ya dakika mbili Devotha akamwambia Saada “Ndani ya sekunde ishirini nitakuwa nimeingia katika barabara ya kuelekea kitalu1” Tayari alikwisha washa taa kuashiria kwamba anakata kona.Sekunde chache kabla ya kukata kona Saada akampa taarifa kuwa tayari kamera imezimwa na hawataonekana “Thank you Saada” akasema Devotha na kukata kona akaingia katika barabara inayoelekea katika jengo la kitalu1.Akaichukua kadi yake akaipachika katika kifaa Fulani halafu akamgeukia GosuGosu “Gosu Gosu kaa tayari.Kazi inaanza” akasema Devotha Alilikaribia geti akakinyoosha kifaa kile alichopachika kadi yake akabonyeza namba kadhaa na geti likajifungua.Gari la Devotha likaingia ndani na geti likajifunga taratibu.Kitendo cha geti kufunguka na gari kuingia ndani bila walinzi kuliona katika kamera kiliwastua sana na kuwafanya watoke ndani ya nyumba yao kwa kasi wakiwa na silaha.Devotha akasimamisha gari baada ya walinzi kumuelekezea silaha.Akashusha kioo na walinzi wote wakastuka “Mama Devotha!! Walinzi wake waliokuwa tayari na silaha zao wakashangaa.Devotha hakuwasemesha kitu akavua miwani yake na kuiweka pembeni “Madam tafadhali shuka garini haraka! Akaamuru mmoja wa walinzi wale “Benard ! akaita Devotha “Madam shuka garini haraka sana” akasema Benard. “Get out Devotha” akasema Gosu Gosu kwa sauti ndogo.Devotha akafungua mlango na kushuka garini “Geukia gari na uinue mikono juu” akasema Benard kwa ukali.Mmoja wa walinzi akamsogelea Devotha kwa lengo la kumfunga pingu lakini Gosu Gosu aliyekuwa amejificha katika kiti cha nyuma alikwisha jiweka tayari na bastora mbili mkononi.Walinzi wale walijielekeza kwa Devotha bila kuwa na taarifa kama kuna mtu mwingine ndani ya gari.Kwa kasi ya ajabu Gosu Gosu akashusha kioo cha gari na kuutoa mkono wake wenye bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti akamlenga Benard kati kati ya paji la uso akaanguka chini.Kitendo kile kilimpa Devotha nafasi akageuka kwa kasi ya umeme na kumtandika ngumi mfululizo yule mlinzi ambaye tayari alikwisha mfunga pingu mkono mmoja akaanguka chini.Wakati Devotha akiendelea kupambana na yule jamaa Gosu Gosu tayari alikwisha watanguliza kuzimu wale walinzi wengine wawili “Madam naomba msiniue tafadhali” akasema yule mlinzi aliyeanguka chini. Devotha akamuamuru kuinuka na kuwavuta wenzake na kuwaficha katika vichaka vya maua yaliyokuwa katika ukuta wa kwanza.Devotha akasikia mlio wa risasi kutoka katika bastora yenye kiwambo cha sauti.Akageuka haraka haraka na kumkuta yule mlinzi akiwa ameanguka chini akivuja damu.Gosu Gosu alimpiga risasi “Hakukuwa na ulazima wa kumuua,hakuwa na madhara yoyote”akasema Devotha “I’m a soldier and any soldier is trained to kill enemies.Ndani ya jengo hili kila mtu ni adui yangu hivyo nitaua kila nitakayekutana naye hadi nitakapompata Mathew Mulumbi” akasema Gosu Gosu “Hata macho yake yanaonyesha kweli ni muuaji” akawaza Devotha akimtazama Gosu Gosu usoni. “Saada tumemaliza hapa nje tunaelekea ndani” akasema Devotha wakaelekea katika gari na kulivuka geti la pili ambalo alilifungua kama alivyofungua geti la kwanza.Hakukuwa na mlinzi yeyote katika geti la pili “Saada tunakwenda katika maegesho chini ya jengo” Devotha akamjulisha Saada “Tayari nimezima kamera ya eneo la maegesho” akasema Saada Devotha aliingiza gari katika maegesho yaliyokuwa chini ya lile jengo.Akafungua mlango na kushuka.Gosu Gosu akachukua silaha zake akaziweka kwenye begi na kubakiwa na bunduki mbili ndogo alizozishika mkononi.Devotha alikuwa na bastora moja. “Saada tuko maegesho tunaelekea ghorofani katika chumba iliko lifti itakayotushusha chini aliko Mathew.Zima kamera katika lifti tunaelekea huko” akasema Devotha wakiwa katika mlango.Akapitisha kadi na mlango ukafunguka.Kulikuwa kimya kabisa. “Saada updates please.Tunakaribia chumba cha lifti.Kuna walinzi wangapi unawaona karibu?akauliza Devotha “Sioni mlinzi yeyote” akasema Saada “Good” akajibu Devotha Katika chumba kilichokuwa na runinga kubwa mbili,picha kutoka katika kamera zote zilizozunguka eneo lile la kitalu 1 zilionekana.Watu wanne waliokuwamo ndani ya kile chumba waliendelea na shughuli zao kama kawaida huku wakizungumza na kupata vitafunwa mara mmoja aliyekuwa amekaa kiti namba 4 akastuka ghafla baada kugundua kuna kitu hakiko sawa katika kamera. “Guys something is not right” akasema “Kuna nini Cosmas?akauliza mwenzake “Kuna kitu kimenishangaza kidogo” akasema Cosmas “Camera 5 ambayo iko katika maegesho kubwa haikuwa ikionyesha picha lakini sekunde chache zilizopita imerejea na kuanza kuonyesha tena picha” akasema Cosmas “Cosmas is right.Kuna kitu kweli hakiko sawa.Kamera 7A ambayo ni ya kwenye lifti pia haionekani hapa” akasema mwingine “What’s happening?akauliza Cosmas Haraka haraka kila mmoja akakaa katika kiti chake wakaanza kutafuta chanzo cha tatizo.Baada ya muda Charles akasema “Kuna mtu amejiunga na mtandao wetu na ndiye anayeziongoza kamera zetu” akasema Charles aliyegundua tatizo lile huku akiendelea kubonyeza kompyuta yake. “Inaonyesha mtu huyu hayuko mbali na hapa.Inanionyesha yupo…oh wait a second”akasema na kuendelea kubofya kompyuta yake “Mdukuaji yuko hapa”akasema Charles “Lupai hotel ?! akauliza Cosmas kwa mshangao “Ni nani huyo anayeweza kufanya hivi? Nini anakitafuta?akauliza “Kaiza anatakiwa ajulishwe haraka jambo hili” akasema Charles na kuchukua simu akampigia Kaiza lakini simu iliita bila kupokelewa “Kaiza hapokei simu” akasema “Tunatakiwa kumtafuta mtu huyo ni nani na kumtia nguvuni ili tujue sababu za kudukua mtandao wetu.Kama Kaiza hapokei simu tumjulishe Deo ambaye ndiye msaidizi wake wa muda.Yeye anaweza akatuma timu ya watu wakafika hapo hotelini haraka” akashauri Cosmas na Charles akampigia simu Deo “Hellow Charles” akasema Deo “Deo kuna tatizo” “Tatizo gani Charles? “Tumegundua kuna mtu anadukua mtandao wetu.Amekuwa anacheza na kamera zetu” “Mmemfahamu ni nani? “Bado hatujafahamu ni nani ila amejiunga na mtandao wetu kutokea mbali.Tumefuatilia mahala alipo na kugundua yuko Lupai hotel ambayo haiko mbali na hapa” “Good job Charles.Endeleeni kumfuatilia mimi na timu yangu tunaelekea hapo Lupai kumtafuta huyo mtu.One more thing,mmegundua sababu ya kudukua kamera zetu? “Bado hatujui tunaendelea na uchunguzi” akasema Charles “Endeleeni kufanya uchunguzi.Yawezekana huu ukawa ni mchezo wa Devotha.Jambo kama hilo haliwezi kufanywa na mtu wa kutoka nje lazima linafanywa na mtu wa ndani.Hakikisheni ulinzi unaimarishwa kila kona.Mathew Mulumbi ahamishwe mahala alipo na apelekwe seli 12B” akaelekeza Deo na kukata simu. Devotha na Gosu Gosu waliingia katika lifti na kuelekea ghorofa ya tano iliko lifti itakayowapeleka chini aliko Mathew Mulumbi “Guys we have problem.Kuna watu wanne ghorofa ya tano wanasubiri lifti,wana silaha” Saada akawajulisha akina Devotha GOSU GOSU NA DEVOTHA WANAUNGANA KUMUOKOA MATHEW MULUMBI JE WATAFANIKIWA?OLIVIA ATAFANIKIWA KUKOMBOLEWA? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII
Devotha akagueka na kumtazama Gosu Gosu baada ya kupewa taarifa ile na Saada. “Don’t panic.Niachie mimi hiyo kazi,nitawamaliza wote” Gosu Gosu akamweleza Devotha “Gosu Gosu nakuomba jitahidi kujizuia kuua hadi pale itakapolazimu.Hawa ni watu wangu nimekuwa nao muda mrefu kama ndugu hivyo sipendi kuwaua hovyo.Sikufurahi ulivyoua wale walinzi getini” akasema Devotha “Kaa nyuma yangu let me handle this!! akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu please..”akasisitiza Devotha lakini Gosu Gosu hakusema chochote alikuwa amejiweka tayari kukabiliana na watu wale. “Madam Devotha tayari nimezima kamera ya nj….” Saada akamtaarifu Devotha lakini kabla hajamaliza maelezo yake milango ya lifti ikajifungua na kwa wepesi wa aina yake Gosu Gosu akaruka nje na kuwastua wale jamaa wanne waliokuwa na silaha wakisubiri kuingia katika lifti. “Taratibu wekeni silaha zenu chini na kila mmoja ainue mikono juu!! Akaamuru Gosu Gosu.Wale jamaa walipatwa na mstuko mkubwa sana,walimtazama Gosu Gosu kama wamekutana na dudu la kutisha.Sura yake alikuwa ameikunja,macho na sauti yake vilitosha kuonyesha kuwa hakuwa na mzaha na angeweza kutoa roho ya mtu muda wowote “Fanyeni mlivyoamriwa.Wekeni silaha zenu chini” Devotha akasema naye akiwa na sura iliyoonyesha hakuwa na masihara.Taratibu wale jamaa watatu waliokuwa na bunduki kila mmoja akaiweka chini silaha yake na ghafla kwa kasi ya aina yake mmoja ambaye hakuwa na bunduki akachomoa bastora lakini Gosu Gosu aliyekuwa na jicho kama la kinyonga alikiona kitendo kile akaizinga bunduki yake na kumchakaza yule jamaa kwa risasi.Wale jamaa watatu waliobaki walitetemeka kwa woga. Haraka haraka Devotha akatumia kadi yake akafungua mlango uliokuwa karibu akawaamuru wale jamaa kuingia na kuuingiza pia mwili wa yule mwenzao aliyeuawa na GosuGosu.Kwa kutumia waya wale jamaa wakafungwa miguu na mikono.Gosu Gosu akakata mashati yao na kujaza vitambaa midomoni mwao. “Tunaelekea wapi baada ya hapa?akauliza Gosu Gosu “Kuna sehemu mbili ambazo tunatakiwa kudhibiti.Kwanza chumba cha kamera na pili kuna chumba kinaitwa control room.Humo ndimo kuna mifumo yote ya kuongoza kila kitu ndani ya hili jengo” akasema Devotha “Hakuna tatizo nielekeze njia ya kufika huko” “Tutaanzia chumba cha Kamera” akasema Devotha “Saada tunaelekea katika chumba cha kamera” Devotha akamjulisha Saada “Sawa Madam Devotha hakuna tatizo lolote mnaweza kwenda njia zote naona ni nyeupe” akasema Saada Gosu Gosu akafungua mlango akachungulia nje hakukuwa na mtu yeyote. “It’s clear ! akasema kisha akatangulia na Devotha akamfuata nyuma Katika chumba cha kamera zoezi la kumfuatilia mdukuaji lilikuwa linaendelea.Kamera ziliendelea kuzimwa na kuwashwa tena baada ya muda mfupi wote wakazidi kushangaa “Nini hasa lengo la huyu mdukuaji?Kwa nini anazima na kuwasha kamera zetu?akauliza Charles “Guys hapa kuna jambo linaendelea.Angalieni mtiririko a namna kamera zinavyozimwa.Ukifuatilia utaona imezimwa kwanza kamera ya maegesho kubwa chini ya jengo. Ikafuata kamera 7A ambayo ni kamera iliyoko ndani ya lifti,ikazima tena kamera 12CC iliyoko katika korido ghorofa ya tano.Kuna kitu mnakiona hapa?akauliza Charles “Kuna jambo hata mimi ninaliona hapa.Hizi kamera haziwezi kuzimwa bila kuwa na sababu ya msingi.Huyu mdukuaji anaonekana ni mtu anayelifahamu jengo hili vyema na kwa namna anavyozima kamera zetu inaonekana kuna jambo analificha lisionekane.Tunatakiwa kufahamu anaficha kitu gani?akauliza Charles “Jamani tuko kwenye hatari.Huyu mdukuaji atakuwa anawaficha wavamizi ndiyo maana utaona mtiririko wake wa kuzima kamera ameanza na ile ya chini kabisa ya jengo.Ili kujihakikishia kuwa kweli tumevamiwa chunguza kama kamera ya getini iliwahi kuzimwa.Tumeanza kustuka kuwa kamera zinazimwa katika kamera ya maegesho.Yawezekana …….” akasema Jonathan na kustuliwa na sauti ya mshangao ya Charles “It’s true.Anachokisema Jonathan ni kitu cha kweli kabisa.Kamera mbili zilizimwa kabla ya ile tuliyoanza kuigundua.Kama alivyosema Jonathan yawezekana tuko kwenye hatari.Yawezekana kweli kuna uvamizi unafanyika..” akasema Charles na mara Cosmas akatoa sauti ya mstuko “Oh my God !!. “Nini Cosmas?akauliza Charles “Mathew Mulumbi ! Tunamshikilia hapa na anahisiwa kushirikiana na mtandao wa IS.Kama kuna wavamizi ni wazi watakuwa wamekuja kwa lengo la kumkomboa yeye tu hakuna kingine” akasema Cosmas.Wote mle ndani ya chumba wakatazamana.Walipatwa na mstuko. “Jamani kama ni wavamizi wamewezaje kupita getini?Huwezi kuvuka getini kama si mmoja wetu ,kamahaupo katika mfumo wetu”akasema Steven “Fuatilia getini kama kuna mtu yeyote amepita hapo muda mfupi uliopita” akasema Cosmas.Charles akapiga simu getini lakini haikupokelewa,akapiga tena lakini hali ilikuwa ile ile simu haikupokelewa. “Simu haipokelewi.Hii inashangaza sana kwa watu wa getini kutokupokea simu” “Jibu ni jepesi tu kwamba hakuna mtu getini” akasema Jonathan “Where are they?akauliza Steve sauti yake ikionyesha woga mkubwa “May be they’re dea……………….” Kabla Charles hajamaliza kile alichotaka kukisema mlango ukafunguka wakaingia watu wawili.Alitangulia Devotha na nyuma yake akafuata Gosu Gosu aliyekuwa na bunduki mbili ndogo zilizofungwa kiwambo cha sauti.Ulikuwa ni mstuko mkubwa kwa wale watu mle ndani ambao hawakuutarajia “Tafadhali kaeni mbali na kompyuta zenu na kila mmoja ainue juu mikono yake” akasema Devotha aliyekuwa na bastora mkononi. “Madam Devotha!! Akasema Charles “Mmesikia mlichoambiwa.Kila mmoja ainue mikono yake juu haraka sana!! Akasema Gosu Gosu. Ghafla Charles akarukia ukutani na kubonyeza kitufe chekundu ambacho ni kengele ya kuashiria kuna hatari ndani ya jengo.Taa nyekundu iliyokuwa juu ikaanza kuwaka na mlio wa king’ora ukasikika.Mkono wa Gosu Gosu ulikuwa mwepesi sana kabla Charles hajageuka baada ya kubonyeza ile kengele tayari alikwisha izinga bunduki yake na kumimina risasi.Charles akaanguka chini.Hakuwa na uhai tena.Haraka haraka Devotha akaenda katika kifaa Fulani chenye namba akabonyeza namba kadhaa na ile kengele ya hatari ikatoweka. “Nawaonya! Yeyote atakayejifanya mjuaji na kutaka kufanya kinyume na maelekezo atapoteza maisha yake kama Charles.Tafadhali fuateni maelekezo mnayopewa! akasema Devotha kwa ukali “Madam Devotha Please don’t kill us tutafuata maelekezo yote.” akasema Cosmas aliyekuwa anatetemeka.Haraka haraka Devotha akakata waya na kuwafunga wote mikono na miguu wakawaziba midomo na kuwafungia katika chumba kilichokuwa pembeni . “Gosu Gosu we need to hurry.Ile Kengele aliyoibonyeza Charles ni kiashiria kwamba kuna hatari ndani ya jengo.Kila ofisi ina kengele hiyo ambayo ikibonyezwa hupeleka taarifa katika chumba kinaitwa control room na taarifa ikifika pale milango yote katika jengo hili hujifunga.Taarifa pia hutumwa kwa kikosi maalum ambacho hushughulikia masuala ya dharura pekee.Kikosi hiki hukaa katika ghorofa ya tatu ya jengo hili.Mara waipatapo taarifa hiyo ya hatari hufuatilia imetoka wapi na kufika hapo haraka sana kujua tatizo.We need to get out very quick kwani hawa jamaa muda wowote watafika hapa” akasema Devotha akaenda katika mlango akapitisha kadi yake lakini mlango haukufunguka. “Tayari milango yote imekwisha jifunga kama nilivyokueleza” akasema Devotha “Hakuna namna yoyote ya dharura ya kuweza kuifungua milango ikitokea hali ya namna hii?Gosu Gosu akauliza “Hakuna namna nyingine hadi kuwasiliana na watu walio katika control room ndio pekee wanaweza kufungua milango inapotokea hali kama hii” akasema Devotha “Isiwe taabu Devotha” akasema Gosu Gosu na kuvua begi lake akatoa kifaa Fulani na kukipachika katika mlango halafu akamtaka Devotha wasogee mbali kidogo akakilenga kifaa kile kwa risasi na ukatokea mlipuko mlango ule ukasambaratika king’ora cha hatari kikaanza kulia. “Hurry let’s go!! Akasema Devotha “Hawa jamaa wataendelea kutufuatilia katika kamera mahala tunakoenda.We need to destroy this room” akasema Gosu Gosu na kutoa bomu dogo la mkono katika begi lake,akang’oa kifuniko chake Devotha akachungulia nje “It’s clear” akasema Devotha,Gosu Gosu akasogea mlangoni wakatoka nje ya kile chumba halafu akalirusha lile bomu dogo katika kile chumba cha kamera likalipuka akawahi kumkumbatia Devotha wakaanguka chini. “Tunakwenda control room.Kushuka chini mahala aliko Mathew lazima tushuke kwa kutumia lifti na kwa sasa hakuna lifti yoyote inayofanya kazi hivyo lazima tuingie pale control ro….” Devotha akastuka baada ya kuchungulia na kuwaona watu watatu wakielekea mbio upande ule waliokuwepo.Akamfanyia ishara GosuGosu kuwa watu watatu wanakuja.Walipokaribia Gosu Gosu akajitokeza na kucheza na bunduki zake mbili wale jamaa wote wakaanguka chini.Mara ikasikika milio ya risasi “Aaaagghh !!! Devotha akatoa mguno wa maumivu akaanguka chini.Gosu Gosu akageuka na kumkuta Devotha akiwa ameanguka chini akivuja damu. “Gosu Gosu take cover !! Akasema Devotha na kwa haraka Gosu Gosu akajificha nyuma ya nguzo huku risasi zikipiga upande wa pili wa ile nguzo.Devotha aliyekuwa amepigwa risasi katika bega la kushoto akaivuta bastora yake iliyoanguka sentimeta chache na kwa kutumia mkono wake wa kulia akaachia risasi kadhaa na kuwafanya wale jamaa waliokuwa wanawashambulia wajifiche na risasi zikawa zinarushwa kwa kuviziana,hii ilimpa Gosu Gosu aliyekuwa bado amejificha katika nguzo nafasi ya kuwasoma wale jamaa namna walivyokaa.Jamaa mmoja akajitokeza ili aachie risasi lakini akamkuta tayaro Gosu Gosu amejiandaa akamlenga kati kati ya paji la uso akaanguka na bunduki yake ikaruka pembeni.Gosu Gosu akapata nafasi akaruka na kumuendea Devotha.Akamkagua alikuwa amepigwa risasi katika bega la kushgoto. “Risasi haijatokeza upande wa pili bado iko ndani” akasema Gosu Gosu akavua begi alilolivaa mgongoni akavua na fulana yake aliyoivaa na kuweka mahala alikopigwa risasi Devotha “Weka mgandamizo mahala hapo ili kuzuia damu kutoka kwa wingi.Tukimaliza zoezi hili tutaitoa risasi hiyo” akasema Gosu Gosu “Thank you Gosu Gosu.Tunatakiwa kuhakikisha tunafika control room haraka” akasema Devotha na Gosu Gosu akamsaidia kunyanyuka.Mara tu walipojitokeza katika korido zikaanza kuvuma risasi.Gosu Gosu akamkinga Devotha kwa kuachia risasi mfululizo wakarejea mahala walipokuwa wamejificha. “Sikiliza Devotha hawa jamaa wamekwisha jipanga.Hakuna njia nyingine ya kufika huko control room? “Hakuna njia nyingine zaidi ya hii” “Good” akasema Gosu Gosu na kufungua begi lake akatoa kopo akang’oa kifuniko chake na kulirusha katika korido.Moshi mzito mweusi ukaanza kutoka katika lile kopo na kusambaa.Akatoa lingine na kulirusha mbele zaidi na baada ya muda mfupi eneo lote likawa na moshi mzito kiasi cha kutoweza kumuona mtu aliyeko mbele yako.Gosu Gosu alikuwa amejiandaa akavaa miwani yenye kifaa maalum ya kumuwezesha kuona sehemu zenye giza na katika moshi mzito.Gosu Gosu akamtaka Devotha aendelee kukaa pale pale.Akatembea kwa kunyata kuelekea upande ule ambako wale jamaa walikuwa wamejificha.Alipokaribia aliwaona jamaa watatu wakiwa wamejibanza katika uchochoro uliokuwa na dirisha.Gosu Gosu hakupoteza muda ndani ya sekunde chache akawakata pumzi kwa risasi mfululizo.Haraka haraka akamfuata Devotha “It’s clear.Twende” akasema Gosu Gosu na kumuinua Devotha wakaanza kutembea taratibu hadi walipokunja kona na kufuata korido la upande wa kulia kisha wakafuata korido la kushoto na hatua chache ikasikika milio ya risasi Gosu Gosu akamvuta Devotha pembeni.Kulikuwa na watu mbele yao wakiwashambulia.Gosu Gosu alitumia zaidi ya dakika tano kupambana na watu wale wanne akawamaliza kisha akamuongoza Devotha hadi katika lile lango ambalo lilikuwa limefungwa.Akatoa kifaa kama kile alichokitumia katika chumba cha kamera akakipachika mlangoni kisha akakipiga risasi na lango likafunguka akarukia ndani ambako kulikuwa na mkanyagano mkubwa baada ya mlipuko ule kutokea mlangoni kila mtu akikimbia kunusuru maisha yake.Gosu Gosu akapiga risasi juu na kutaka watu wote watulie.Mle ndani kulikuwa na zaidi ya watu kumi na tano.Devotha akaingia na kumuita Zai ambaye ndiye aliyemsaidia kumuunganisha tena na mtandao wa idara akamtaka afungue milango yote.Zai akakaa kitini na kubonyeza kompyuta yake baada ya muda milango yote ikaanza kufunguka.Devotha akawataka wale watu kutoa kila walicho nacho na kutupa chini halafu akawataka waingie katika chumba kilichokuwa pembeni.Akamtaka Zai aufunge ule mlango kupitia kompyuta yake ili isiwe rahisi kwa waliokuwa ndani kuufungua.Gosu Gosu bado alikuwa mlangoni tayari kukabiliana na chochote ambacho kingejitokeza.Milango yote ilipofunguka na kila kitu kurejea kawaida Devotha akamtaka Zai awafuate wakatoka ndani ya kile chumba wakaelekea katika lifti kushuka chini.Milango ya lifti ikafunguka wakatoka na Devotha akawaongoza Gosu Gosu na Zai kuelekea katika chumba cheupe “Wakati ninaondoka Mathew alikuwa huku niliagiza atolewe apelekwe katika chumba kingine.Tuanzie huku kwanza kutazama kama alihamishwa” akasema Devotha.Milango yote ilikuwa wazi wakaelekea katika chumba cheupe lakini Mathew hakuwepo “Watakuwa wamemuhamisha Mathew kama nilivyoelekeza.Twendeni VIP” akasema Devotha wakatoka ndani ya chumba kile walipopiga hatua chache milio ya risasi ikasikika.Gosu Gosu akamrukia Devotha akamuangusha chini na kugeuka kwa kasi ya ajabu akawaona watu wanne wakiwa na silaha akamimina risasi wawili wakaanguka chini wawili wakakimbia kuelekea katika lifti.Kabla hawajaingia mmoja wao akapigwa risasi ya mguu mwenzake akageuka akavurumisha risasi halafu akamvuta yule aliyepigwa risasi akamungiza ndani ya lifti akaendelea kuvurumisha risasi kuwazuia akina Gosu Gosu kupiga risasi yoyote.Milango ya lifti ikajifunga na lifti ikapanda juu.Baada ya wale jamaa wawili kunusurika na kuondoka,Gosu Gosu akamuendelea Zai aliyekuwa amelala chini akivuja damu akamgeuza lakini Zai hakuwa na uhai tayari alikwisha fariki alikuwa amepigwa risasi nyingi kifuani. “She’s gone” Gosu Gosu akamwambia Devotha ambaye alikosa cha kuongea akabaki anamtazama Gosu Gosu “Devotha watu wale tayari wanafahamu tuko huku chini hivyo wanapeleka taarifa kwa wenzao na muda wowote wanaweza wakaja wengi tukashindwa kupambana nao.Tumtafute Mathew haraka tuondoke eneo hili”akasema Gosu Gosu “Nimeumia sana Gosu Gosu,mimi ndiye nimesababisha kifo cha Zai.Najuta kwa nini nilimtumia” akasema Devotha “Devotha hakuna tunachoweza kukifanya kwa Zai tayari amekwisha kufa.Our priority is Mathew Mulumbi” akasema Gosu Gosu na kumfuata Devotha akamuinua wakaelekea katika sehemu ambako alielekeza Mathew apelekwe.Lango la kuingia katika sehemu ya VIP lilikuwa wazi wakaingia ndani na kuingia katika kibao kimeandikwa A3.Mle ndani kulikuwa na watu watatu wenye silaha wakiwa wamemzunguka Mathew aliyekuwa amefungwa pingu mkononi “Wekeni silaha zenu chini ni mimi Devotha” akasema Devotha.Mmoja wao akauelekezea mtutu wa bunduki kichwani kwa Mathew. “Madam Devotha tayari tunakufahamu wewe ni nani,tafadhali naomba usimame hapo hapo usijaribu kunyanyua hata hatua moja.Taratibu wewe na mwenzako wekeni silaha zenu chini !! akasema kwa sauti kali mmoja wa wale jamaa “Evans kama kuna kitu umeambiwa kuhusu mimi wamekudanganya.Unanifahamu vizuri mimi nimekuwa kiongozi wenu mnanifahamu vizuri.Tafadhali ondokeni hapo nataka kuzungumza na Mathew” “Madam tafadhali fanya nilivyokuelekeza ama sivyo Mathew atakufa.Tunajua ulichokuja kukifanya huku chini ni kumtorosha.Tunayo maagizo ya kumlinda Mathew kwa gharama zozote.Nitahesabu hadi tatu nataka muweke silaha zenu chini !! akasema Evans kwa ukali. “Okay tunaweka silaha zetu chini” akasema Devotha na kuanza kuinama chini taratibu kuweka bastora yake.Gosu Gosu aliyekuwa karibu na Devotha alifanya kitu cha ghafla sana ambacho wale jamaa hawakukitegemea,alimsukuma Devotha akaanguka naye chini huku akimimina risasi jamaa wawili wakaanguka,Mathew aliyekuwa amekaa sofani alijibinua akaanguka na kiti kisha akaipiga teke ile bunduki iliyokuwa imeelekezwa kichwani kwake,akajibinua zaidi na kumtandika yule jamaa teke la shingo akayumba na kuanguka akamkaba kabali kwa miguu yake hadi yule jamaa alipokata pumzi akamuachia. “Mathew are you okay brother? Gosu Gosu akamuuliza Mathew “Gosu Gosu you are a ghost ! sikutegemea kabisa kukuona mahala hapa” akasema Mathew.Hakuamini kabisa kama angeweza kumuona Gosu Gosu mahala pale. “Nafurahi kukukuta ukiwa mzima Mathew.Tutazungumza zaidi baadae kwa sasa tunatakiwa kutafuta namna ya kuondoka katika hili shimo” akasema Gosu Gosu huku akizifungua pingu alizofungwa Mathew kwa kutumia kifaa kidogo alichokitoa katika begi lake “Gosu Gosu thank you so much” akasema Mathew “Don’t thank me.Thank her ! akasema Gosu Gosu akimuonyeshea Devotha. Mathew akamfuata Devotha pale chini alipokuwa amekaa.Alikuwa amechafuka damu.Bado aliendelea kushikilia sehemu alikopigwa risasi “Devotha.Pole sana”akasema Mathew “Devotha amepigwa risasi begani katika jitihada za kufika hapa kukukomboa.Ni zamu yetu kuhakikisha tunamtoa humu salama na kumpatia matibabu.Tayari amekwishapoteza damu nyingi” akasema Gosu Gosu “Devotha we’ll get you out of here I promise you” akasema Mathew “Guys ninahisi nguvu zinaniishia.Tufanyeni haraka tutoke humu.Kuna njia ya siri ya kutoka huku.Hatutaweza kupita kule juu wako wengi” akasema Devotha.Mathew akamsaidia akanyanyuka “Mathew hawajakuumiza hawa jamaa?Unaweza kutembea?Gosu Gosu akamuuliza Mathew “Hawakunip amateso makubwa zaidi ya kuniweka katika chumba cha baridi.Shukrani kwa Devotha kwani yeye ndiye aliyesababisha nisiteswe.Nina deni kubwa kwake” akasema Mathew.Devotha akaelekza ufunguliwe mlango wa chooni akaingia,Mathew akamfuata na Gosu Gosu aliyekuwa kifua wazi akiwa na bunduki zake mbili ndogo akawa nyuma kukabiliana na chochote.Ndani ya kile choo kulikuwa na kisanduku mfano wa tanki dogo la maji limetundikwa ukutani,Devotha akabonyesa sehemu Fulani likafunguka,akakibandua kifuniko cheupe akakuta kitu mfano wa simu akabonyeza namba Fulani na mara ukuta ukajiachia ikaonekana ngazi ya kushuka chini. “C’mon hurry up we need to leave” akasema Devotha.Mathew na Gosu Gosu wakaingia haraka baada ya kusikika hatua za watu wakiingia mle chumbani.Devotha akabonyeza namba Fulani kwa ndani na ule ukuta ukajifunga na haikuwa rahisi kwa mtu kufahamu kama nyuma ya ukuta ule kulikuwa na njia. “Njia hii ni ya siri na ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kuwatorosha viongozi pale watakapokuwa na matatizo.Njia hii inakwenda kutokea karibu na bahari.Wanaoifahamu njia hii ni mimi na Ka……” Akasema Devotha na kutaka kuanguka Mathew aliyekuwa nyuma yake akamdaka. “Davotha..! Devotha !..” Mathew akamuita lakini Devotha hakuwa na nguvu.Mathew akamlaza chini na kumchunguza. “She’s still breathing.Tuharakishe tutoke humu akapatiwe matibabu haraka” akasema Mathew “Mathew ni Devotha pekee anayeifahamu njia.Tutafanyaje kutoka huku chini?akauliza Gosu Gosu “Papii,it’s just you and I now.We need to find a way.Nitambeba Devotha” akasema Mathew “No Mathew I’ll do it” akasema Gosu Gosu na kumpatia Mathew zile bunduki na lile begi kisha akambeba Devotha wakaendelea kufuata ujia ule ambao Devotha aliwaeleza unakwenda kutokea karibu na bahari. “Mathew ninafahamu namna ya kutoa risasi kwa nini tusimtoe Devotha risasi?akauliza Gosu Gosu “Hata mimi ninao uwezo wa kutoa risasi lakini Devotha tayari amepoteza damu na kama tukimtoa risasi kienyeji ataendelea kupoteza damu nyingi.Tunahitaji kumpeleka hospitali akaongezewe damu na kufanyiwa upasuaji kuondoa risasi.Pili ni muda.Hatuna muda mrefu wale jamaa wanaweza wakatukuta hapa” akasema Mathew “Mathew are sure she’s going to make it? Akauliza Gosu Gosu “Kama siku yake haijafika hatapoteza maisha.Keep moving” akasema Mathew. Walitembea kwa takribani dakika kumi na mbili kisha wakakuta ngazi zinapanda na baada ya kuzipanda ngazi zile wakakuta kuna kifaa kama kile walichokikuta chooni. “Tumekwama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Huu ni mlango wa kutokea nje lakini hatujui namba za kufungulia tuweze kutoka” akasema Gosu Gosu “Hatujakwama.Ninazifaham u namba za kufungulia.Nilimuona Devotha wakati akifungua ule mlango kule chooni na mimi nina sifa moja ninapoziona namba hata kama ni nyingi mara moja huziweka kichwani” akasema Mathew na kuzibonyeza namba zile ambazo Devotha alizitumia kufungulia mlango kule chooni na taratibu lango likajifungua wakatabasamu na kutoka nje.Ilikuwa ni sehemu yenye mwanga kandoni mwa bahari na mlango ule ulitengenezwa kwa mfano wa mwamba na haikuwa rahisi kwa mtu kujua kama katika mwamba ule kulikuwa na mlango wa kuingilia katika njia ya chini kuelekea kwenye jengo la kitalu 1.Jengo lile waliliacha kwa kama mita mia nne hivi.Dakika mbili baada ya kutoka ndani ya ile njia lango likajifunga “Oh ahsante Mungu tumetoka salama” akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu we’re not safe yet.Tunatakiwa kutafuta namna ya kuondoka eneo hili,bado tuko karibu sana na lile jengo la hawa jamaa” akasema Mathew “Mathew barabara haiko mbali na hapa.Tuendelee na safari.Nitambeba Devotha and you’ll cover me”akasema Gosu Gosu “Gosu Gosu hali ya kiusalama kwa sasa hapa nchini si nzuri matukio ya utekaji watu yameshika kasi na watu wakituona tukiwa katika hali hii tutajiweka katika matatizo mengine.Tazama tulivyochafuka damu.Hatuna simu wala chombo chochote cha mawasiliano.Ninachofikiria nenda katafute gari mimi nitabaki hapa na Devotha” akasema Mathew.Bila ubishi Gosu Gosu akamuachia Mathew silaha akaondoka kwenda kutafuta usafiri wa kuondoka nao. “Sikutegemea kama Devotha angeweza kuwageuka wenzake na kuungana na Gosu Gosu kuja kuniokoa.Yawezekana amepima na akagundua kwamba walifanya makosa kunikamata ndiyo maana akaenda kumtafuta Gosu Gosu wakashirikiana hadi wakafanikiwa kunikomboa.Haikuwa kazi rahisi kuniokoa” akawaza Mathew akimtazama Devotha ambaye hakuwa na fahamu. “Ee Mungu tafadhali naomba umponye Devotha.Amejitolea kuniokoa kwa kuwa anafahamu umuhimu wangu katika kuisaidia nchi yangu dhidi ya hila na mipango ya magaidi.Ninamuhitaji sana katika kazi kubwa iliyoko mbele yetu” Mathew akaomba kimya kimya Dakika chache baadae Gosu Gosu akarejea akikimbia na kumjulisha kuwa tayari amepata gari wakasaidiana kumbeba Devotha wakapanda mwamba ule hadi juu ambako Gosu Gosu aliegesha gari wakamuingiza garini na Gosu Gosu akaliondoa gari kwa kasi “Umepata wapi hili gari?akauliza Mathew “Mwenye gari yuko kwenye buti.Usihofu atakuwa huru baada ya kazi yetu kumalizika. Tunaelekea wapi?akauliza Gosu Gosu “Sehemu pekee ambako tunaweza kumpeleka kwa sasa ni kwa Dr Philip.Yule pekee ndiye ninayemuamini anaweza akamuhudumia Devotha kwa siri” akasema Mathew
Deo akiwa na vijana wake alifika Lupai hotel akampigia simu Charles lakini simu haikupokelewa.Akapiga tena simu ikaita bila kupokelewa.Akampigia Cosmas lakini naye vile vile simu yake ilita bila kupokelewa. “Kuna nini kinaendelea mbona hawapokei simu hawa jamaa?akajiuliza Deo akaendelea kuwapigia watu zaidi ya watatu lakini wote simu zao ziiita bila kupokelewa “Kitu gani kinaendelea kitalu 1? Mbona wote hawapokei simu? akajiuliza Deo na kuzidi kuingiwa na wasiwasi akamgeukia mmoja wa watu wake aliyekuwa naye garini “Najaribu kuwasiliana na kitalu 1 lakini hakuna anayepokea simu.Kitu gani kinaendelea kule?Tumekuja hapa kumtafuta mtu anayedukua kamera zetu na ambaye kwa mujibu wa Charles yuko hapa hotel Lupai.Tutampataje mtu huyo bila kupata msaada kutoka kwa watu wetu kitalu 1? akauliza “Ni vigumu kumpata mtu huyo bila kupata msaada kutoka kitalu1.Hoteli hii ni kubwa ina vyumba vingi na hatujui mdukuaji huyo yuko chumba gani” akajibu yule jamaa “Nikweli,bila kupata msaada wa watu wa kitalu 1 hatutaweza kufahamu mahala alipo.Twendeni kitalu 1 tukajue kinachoendelea kwa nini watu wote hawapokei simu” akasema Deo wakaondoka kuelekea kitalu 1. Katika chumba 86 ndani ya hoteli Lupai ambamo alikuwemo Saada,mawasiliano kati yake na Devotha yalikatika. “Sina kitu cha kufanya hapa.Devotha hapatikani tena simuni.Mara ya mwisho nilichokisikia ni milio ya risasi na baada ya hapo sijampata tena Devotha.Nina wasiwasi yawezekana tayari amekwisha uawa.Natakiwa kuondoka hapa haraka sana kabla sijakutwa.Nina wasiwasi wanaweza wakafuatilia na kugundua niko hapa” akawaza Saada huku akipakia kompyuta yake katika mkoba akafungua mlango na kuingia katika lifti akashuka chini akaelekea zilipo teksi akaingia katika mojawapo ya teksi akamuelekeza dereva ampeleke sehemu Fulani.
Deo na timu yake waliwasili katika geti la kuingilia kitalu 1 na kukuta kuna watu wawili kutoka katika kikosi cha dharura.Alistuka kwani si kawaida kwa kikosi hiki kulinda geti.Akashuka getini na kuuliza kilichotokea na akaelezwa kila kitu kilichokuwa kinaendelea ndani ya jengo lile.Haraka haraka akakimbilia ndani na kukuta kukiwa na taharuki kubwa.Kitu kikubwa alichotaka kukifahamu ni kama Mathew Mulumbi bado yupo.Alihisi kuishiwa nguvu baada ya kujulishwa kwamba Devotha ndiye aliyefanya uvamizi ule na lengo lake kubwa ni kumuokoa Mathew Mulumbi.Kulikuwa na sintofahamu mle ndani namna akina Devotha walivyoweza kupotea katika mazingira ya kutatanisha.Deo akalazimika kushuka chini ili kuthibitisha kweli Mathew Mulumbi ametoweka na kukuta vyumba vyote vikiwa vitupu Mathew hayupo.Akampigia simu Kaiza kumpa taarifa zile “Deo kuna taarifa gani?Naomba unieleze haraka ninajiandaa kuanza kumuhoji Olivia” akasema Kaiza “Kaiza kuna jambo limetokea hapa kitalu 1 si la kawaida” akasema Deo na kumsimuliza Kaiza kila kitu kilichotokea.Kaiza alichanganyikiwa hakujua afanye nini “Devotha ni shetani.Kwa nini akafanya usaliti mkubwa namna hii kwa idara ambayo ameiunda yeye mwenyewe? Kwa nini amechagua kumuamini Olivia akaungana na magaidi na kumsaliti hadi rais wake? Akajiuliza Kaiza “Kaiza” akaita Deo baada ya kuona Kaiza amekuwa kimya “Deo nini kinachoendelea hapo kwa sasa?akauliza Kaiza “Kwa sasa zinaendelea jitihada za kufahamu mahala walikojificha akina Devotha.Inaaminika bado hawajatoka ndani ya jengo hili hivyo unaendelea upekuzi wa kila chumba kuhakikisha wanapatikana”akasema Deo “Hamuwezi kuwapata.Tayari wamekwisha ondoka” akasema Kaiza “Kwa mujibu wa watu waliokuwepo hapa wanadai akina Devotha hawakufanikiwa kutoka ndani ya jengo hivyo wanaamini bado wako humu ndani” “Kama wavamizi hao waliongozwa na Devotha amini nakwambia tayari wamekwisha ondoka hawako ndani ya hilo jengo” akasema Kaiza “Kaiza hakuna sehemu wanakoweza kutoka bila kuonekana nah ii ndiyo inayotupasua vichwa kwa sasa .Kama wametoka wamepita wapi wasionekane?akauliza Deo “Deo ninakuja huko sasa hivi,kama mtafanikiwa kuwapata kabla sijafika hapo utanijulisha” akasema Kaiza na kukata simu akawaita watu wake “Nimepewea taarifa kuna dharura imetokea kitalu 1.Nimetaarifiwa kuna watu wamevamia kitalu 1 na wamemtorosha Mathew Mulumbi ambaye ni mshirika mkubwa wa Olivia.Ninataka kwenda huko kuthibitisha kama hizo taarifa ni za kweli.Mambo hapa yatasimama hadi hapo nitakaporejea lakini ninyi mtabaki mtaendelea kumlinda Olivia.Elekezeni sana macho kwa huyu Dr Alex mimi sina imani naye kabisa” Kaiza akatoa maelekezo kwa watu wake halafu akamfuata Dr Alex “Dr Alex nimepata dharura kuna sehemu ninahitajika mara moja.Tutasimamisha zoezi kwa muda hadi hapo nitakaporejea.Nataka uutumie muda huu kuhakikisha Olivia anaandaliwa kwa ajili ya mahoijiano ili nitakaporejea kazi iendelee.Watu wangu wote wanabaki hapa kuhakikisha usalama unakuwepo ninakuonya usijaribu kufanya jambo lolote la kipuuzi” akasema Kaiza “Usiwe na hofu Kaiza.Hii ni ofisi yangu na niko hapa kwa zaidi ya miaka kumi.Huna sababu ya kuwa na hofu na mimi.Ninaifahamu kazi yangu” akasema Dr Alex.Kaiza akaingia katika gari na kuondoka kuelekea kitalu 1. “Devotha ndiye aliyempa rais wazo la kuanzisha idara hii ya siri ya usalama wa ndani wa nchi na toka idara hii ilipoanzishwa amefanya kazi kubwa na nzuri.Rais anamuamini mno na idara yetu sasa inaanza kuwa kubwa na mipango imeanza ili isambae kila mkoa hapa Tanzania.Sifahamu kwa nini Devotha amechagua kuyaacha mafanikio haya makubwa na kuchagua kuisaliti idara aliyoianzisha yeye mwenyewe.Kwa nini achague kumuamini Olivia mtu anayeshirikiana na magaidi ambao wanahatarisha usalama wa nchi?Kwa nini ameamua kumsaliti rais?Mbaya zaidi ameshiriki kufanya mauaji ya watu wake mwenyewe ambao amefanya nao kazi kama ndugu zake.Sifahamu ni shetyani gani amemuingia hadi akafanya haya aliyoyafanya.Nimepata funzo la kutomuamini kiumbe anaitwa mwanadamu.Anaweza akakusaliti dakika yoyote” akawaza Kaiza “Kitendo cha Devotha kumuamini Olivia na kuamua kushirikiana naye kumtafuta Edger Kaka ni wazi ameamua kushirikiana na magaidi wale wanaoshirikiana na Olivia ambao lengo lao kubwa ni kutaka kuleta vurugu nchini kwa kuwaaminisha watu kuwa Edger Kaka ni mzima anashikiliwa na serikali.Ameamua kumtorosha Mathew ambaye naye anashirikiana na magaidi na kinachofuata atatafuta uwezekano wa kumtorosha pia Olivia.Ameamua kujiunga upande wa maadui zetu hii inamfanya awe ni mmoja wa maadui zetu na adui wa nchi hii pia.Ninaweka ahadi ya kumsaka kokote aliko na kumpa stahili yake kwa usaliti huu mkubwa alioufanya.Kitu kikubwa kwa sasa ni kumlinda Olivia kwa nguvu zote kwani ni mtu pekee ambaye anaweza akatusaidia kuutambua na kuusafisha mtandao huu wa IS hapa nchini.Nitakaporejea sintajali litakalotokea lazima nihakikishe anasema kila kitu kuhusiana na mtandao wao hapa nchini”akaendelea kuwaza Kaiza Aliwasili Kitalu 1 na hakuamini macho yake kile kilichotokea.Aliumia sana alipowakuta watu wote waliouawa wakiwa wamewekwa katika chumba kimoja “Huu ni ukatili mkubwa usiovumilika.Devotha ninaapa lazima atalipa uovu huu mkubwa alioufanya!! Akawaza Kaiza akiitazama miili ile.Kaiza akaendelea kuzungukia sehemu nyingine za jengo lile kuangalia uharibifu uliofanyika halafu akaenda chini mahala alikokuwa amehifadhiwa Mathew. “Kaiza inashangaza sana namna Devotha na wenzake walivyopotea.Hawakufanikiwa kupanda kule juu lakini tumebaki tunajiuliza namna walivyotoweka katika mazingira ya kutatanisha mno.Tuliamini labda wamejificha humu ndani lakini tumepekua kila mahali hatujawaona.Wametoweka kimiujiza” akasema Deo . “Hapana hakuna muujiza uliofanyika” akasema Kaiza na kwenda katika choo kilicho kwenye chumba cha A3 akakuta tanki dogo jeupe lililopachikwa ukutani limefunguliwa “Damn you Devotha!! Akasema akilitazama tanki lile.Akabonyeza namba katika kifaa kilichokuwamo ndani ya tanki lile dogo na ukuta ukajiachia ikaonekana njia kubwa wote aliokuwa nao wakabaki wanashangaa. “Huku ndiko walikopita Devotha na akina Mathew.Hii ni njia ya siri ambayo ilitengenezwa maalum kwa ajili ya kuwatorosha viongozi wakuu kama kuna hatari yoyote.Njia hii inakwenda kutokea karibu na bahari hivyo kumuwezesha Rais au kiongozi yoyote mkubwa kutoroka kirahisi.Tunaoifahamu siri hii ni sisi wawili mimi na Devotha pekee” akasema Kaiza kisha wakaingia ndani ya njia ile hadi walipofika mwisho wake hawakuwakuta akina Devotha.Kaiza akalifungua lango wakatokeza nje hakukuwa na mtu.Wakarejea kitalu 1 na Kaiza hakuwa na namna nyingine Zaidi ya kumjulisha Rais kile kilichotokea. “Kaiza nini kinaendelea hapo?akauliza Dr Evans baadaya kupokea simu ya Kaiza “Mheshimiwa rais nimekupigia kukujulisha kuwa nimelazimika kuja hapa kitalu 1 kuna tatizo limetokea” “Tatizo gani limetokea Kaiza? akauliza Dr Evans Kaiza akamueleza Dr Evans kila kitu kilichotokea. “Hivyo ndivyo ilivyotokea mheshimiwa rais na kunilazimu nirejee hapa kitalu 1 kushughulikia hili suala” akamalizia “Kaiza sikutegemea kabisa kusikia kitu kama hicho kutoka kwako.Nilikupa maelekezo ya kuhakikisha Devotha anadhibitiwa na asiweze kuingia katika mfumo wetu.Nilitoa maelekezo haya kwa kufahamu ni mtu hatari anaufahamu mfumo wa idara yenu kwa undani na kama asingedhibitiwa angeweza kufanya chochote.Mmepuuzia maelekezo yangu na haya ndiyo matokeo yake.Amepata mwanya ameutumia na sasa anazidi kutupa wakati mgumu hata wa kumkamata”akasema Dr Evans kwa ukali “Tulifanya kama ulivyoelekeza mheshimiwa rais na Devotha aifungiwa kila kitu kuanzia simu yake hata kadi zake zote ambazo zingemuwezesha kuingia katika mfumo wetu”akasema Kaiza “Kama mlifanya nilivyowaelekeza amewezaje kuingia katika mfumo wenu na akafanya anavyotaka hata akaingia hadi kitalu 1 mahala ambako tunaamini ni salama Zaidi na akafanikiwa kumtorosha Mathew mtu ambaye alikuwa muhimu sana kwetu? “Mheshimiwa rais tunataka kufanya uchunguzi kubaini namna alivyoweza kufanikiwa kuingia katika mfumo wetu na akafanikiwa kuingia hapa kitalu 1”akajibu Kaiza “Kaiza ninachokihitaji kukisikia kutoka kwako ni kuwa Mathew na Devotha wamekamatwa.Hawa ni watu ambao wataharibu kila kitu kama tusipowadhibiti.Devotha amechagua kuungana na watu wanaoshirikiana na magaidi na ninaamini malengo yake ni kumkomboa pia Olivia.Kama tayari amemtoa Mathew basi anayefuata ni Olivia.Nataka kusikia watu hawa wamekamatwa kabla hawajaleta madhara yoyote.Hawa tayari ni maadui zetu wakubwa.Devotha na Mathew Muumbi ni watu wenye mafunzo makubwa na yawezekana kukawa na ugumu katika kuwakamata ninatoa maelekezo kama kutakuwa na ulazima watakapoonekana wapigwe risasi na kufa kwani ni watu hatari sana kwa usalama wa nchi yetu.Nataka msako wa kuwatafuta uanze haraka sana.Kama mkishindwa niambieni nitumie vyombo vyangu vingine ingawa sitaki kushirikisha idara nyingine katika mambo haya ya siri”akasema Dr Evans “Nimekuelewa mheshimiwa rais na suala hili tunakwenda kulifanyia kazi”akajibu Kaiza “Vipi kuhusu Olivia?Umefikia wapi kumfungua?Amesema chochote? akauliza Dr Evans “Imenilazimu kusimamisha kila kitu na kuja huku kitalu 1 baada ya tukio hili kutokea lakini hadi ninaondoka kuja huku sikuwa nimefanikiwa kupata chochote kutoka kwa Olivia hali yake haikuwa nzuri baada ya kumpitisha katika mashine ya umeme.Dr Alex alishauri tumpe muda wa kupumzika kabla ya kuendelea tena na mahojiano.Ninakuahidi mheshimiwa rais kwamba jua halitazama leo kabla Olivia hajasema chochote.Nakuhakikishia mheshimiwa rais lazima tutawapata Devotha na wenzake wote”akasema Kaiza “Kaiza ninapata wakati mgumu wa kuyaamini maneno yenu.Hata Devotha naye aliniahidi hivyo hivyo lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichopatikana.Kuna ugumu gani katika kumfanya Olivia aongee?Nimewasaidia hata kumpata baba yake lakini mmeshindwa kumtumia kumfanya Olivia afungue mdomo.Ugumu uko wapi?akauliza Dr Evans “Naomba uniamini mheshimiwa rais kwamba haya ninayokwambia ni ya kweli kabisa.Nitakapokupigia simu lazima nitakuwa na taarifa zote za kuhusiana na mtandao wa IS hapa nchini kutoka kwa Olivia” akasema Kaiza” “Kaiza tafadhali naomba ulimalize hili suala.Nina mambo mengi sana ya kushughulikia na sitaki kuendelea kupigiwa simu kuelezwa matatizo badala ya kuelezwa mafanikio.Endapo mtashindwa katika hili sintakuwa na namna nyingine Zaidi ya kuifunga hii idara kwani itakuwa imeshindwa kufanya kazi yake na haitakuwa na maana tena.Naamini umenielewa Kaiza” “Nimekuelewa mheshimiwa rais tutajitahidi”akajibu Kaiza “Good.Shughulikia suala hilo limalizike.Nina mambo mengi natakiwa kuyashughulikia nimechoka kusikia kila wakati matatizo kutoka kwenu.Nataka ufanisi !! akasema Dr Evans kwa ukali na kukata simu “Rais amekasirika sana.Devotha amesababisha Rais asiwe na Imani nasi tena” akawaza Kaiza. “Ukiyachunguza maneno ya rais yawezekana kweli kuna uzembe umefanyika hapa.Imewezekanaje Devotha akafanikiwa kuingia hapa na kumchukua Mathew Mulumbi?Zipo kamera za ulinzi ambazo hata ukirusha sindano ndogo itaonekana wameshindwaje kumuona Devotha wakati akiingia hapa hadi akaua watu wetu na kumchukua Mathew? Rais ana haki ya kuwa mkali.Tunalipwa vizuri tunaishi maisha mazuri hivyo lazima tuonyeshe ufanisi mkubwa katika majukumu yetu.Rais hana Imani tena nasi na kazi yangu kubwa ni kurejesha Imani kwa Rais na hilo litawezekana kama tukifanikiwa kuwapata Devotha na Mathew Mulumbi.Tutaanzia wapi kuwatafuta watu hawa? Akajiuliza Kaiza “Devotha tayari anafahamu kuwa anatafutwa hivyo kumpata haitakuwa kazi nyepesi.Kitu kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha tunamlinda kwa kila namna Olivia kwani yeye ndiye njia yetu pekee ya kutusaidia kuweza kuufahamu mtandao wake wote na kupitia kwake tutawapata hata akina Devotha”akaendelea kuwaza Kaiza
Devotha alipokelewa katika hospitali inayomilikiwa na Dr Philip hali yake haikuwa nzuri hata kidogo na bila kupoteza muda akaingizwa katika chumba cha upasuaji na zoezi la kuondoa risasi likaanza haraka likisimamiwa na Dr Philip ambaye aliwahi kufanya kazi na Mathew katika idara ya ujasusi kabla ya kufungua hospitali yake mwenyewe baada ya kukopeshwa kiasi kikubwa cha fedha na Mathew.Wakati upasuaji ule ukiendelea Mathew akaomba kuzungumza pembeni na Dr Philip “Dr Philip ninamkabidhi mgonjwa huyu kwako naomba ufanye kila linalowezekana kuhakikisha anakuwa salama.Mimi nitakuja tena baadae kuangalia maendeleo yake”akasema Mathew “Mathew umejingiza kwenye jambo gani tena? Lini utaachana na mambo haya?akauliza Dr Philip “Dr Philip tutazungumza baadae kwa kirefu lakini kwa sasa naomba nguvu kubwa ielekeze katika kuhakikisa Devotha anakuwa salama.Nakuomba sana Dr Pilip unisaidie katika suala hili” akasema Mathew “Mathew usiwe na hofu kuhusu mgonjwa wako nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha anakuwa salama ila nakushauri ndugu yangu ungeachana na hizi shughuli.Waachie wengine na wewe endelea na maisha yako.Umekwisha fanya mambo mengi pumzika sasa na jikite katika biashara” akasema Dr Philip “Dr Philip si kwamba ninazitafuta kazi hizi bali zinanifuata zenyewe na ninajikuta siwezi kukataa kuifanya kwa manufaa makubwa ya nchi.Jambo lingine kazi hii tayari iko damuni hivyo nitaendelea kuifanya kila pale nitakapolazimika kuifanya” akasema Mathew na kumuomba Dr Philip ampatie simu yake akampigia Jordan dereva wa kampuni yake akamtaka aende Tumaini cark parking ghorofa ya tano amuwekee gari pale kisha wakaagana na Dr Pilip wakaondoka pale hospitali. “Tutaliacha gari hili Tumaini car parking hatulihitaji tena” akasema Mathew baada ya kuondoka hospitali “Pole sana Mathew” akasema Gosu Gosu aliyekuwa katika usukani “Nashukuru sana Gosu Gosu.Sikufanya makosa kukuita uje kwani bila wewe sijui kama ningetoka mle ndani salama.Ahsante sana kwa kuniokoa” akasema Mathew “Usijali Mathew.Kwa sasa baada ya kukuokoa tujielekeze kumtafuta Olivia” “Tayari umepata habari zake?Mathew akauliza “Ndiyo.Devotha amenieleza kila kitu kilichotokea kwa nini walimteka Olivia na hadi walivyokuteka wewe.Alisema ulimuelekeza kwangu kwa ajili ya msaada na akanitaka nimsaidie kumtafuta Olivia lakini nilikataa na kumwamba kama anahitaji msaada wangu kitu cha kwanza ambacho tunatakiwa kukifanya ni kukuokoa kwanza wewe.Hakuwa na kipingamizi tukaanza taratibu za kufika mahala ulipokuwa umeshikiliwa” Gosu Gosu akamueleza Mathew kila kitu kilichotokea hadi walipofanikiwa kumuokoa “Sikutegemea kabisa kama Devotha angeweza kuniamini na kuamua kuwasaliti wenzake.Alikuja kuzungumza nami akanihoji maswali mengi kuhusiana na mahusiano yangu na Olivia nikamueleza kila kitu bila kumficha na ndipo akanieleza mambo yote ya Olivia kushirikiana na kikundi cha IS.Mungu amsaidie apone haraka kwani ana nia ya dhati ya kutaka kuufahamu ukweli wa jambo hili linaloendelea” akasema Mathew “Simfahamu Olivia lakini kwa maelezo aliyonipa Devotha yamenifanya nijiulize maswali mengi kuhusiana na yeye kujiunga na kikundi cha kigaidi cha IS.Ume……”akasema Gosu Gosu na Mathew akamkatisha. “Suala hilo hata mimi limenistua sana nilipolisikia.Devotha alinionyesha baadhi ya picha ambazo zinamuonyesha Olivia akiwa jijini Kinshasa na mtu anaitwa Seif Almuhsin ambaye ni mtu wa IS na kazi yake kubwa ni kukusanya vijana ambao hujiunga na kikundi cha IS kisha kupelekwa katika kambi zao za mafunzo ya kigaidi.IS kimekuwa ni kikundi tishio kwa sasa duniani na wameanza mikakati ya kujitanua Zaidi barani Afrika.Kitendo cha Olivia kukutana na Seif kinazua maswali mengi.Kama haitoshi baada ya kupekua kompyuta yake amekutwa akiwasiliana na mtu mwingine anaitwa Sayid Omar ambaye anatajwa kuwa ni mfadhili mkubwa wa IS.Devotha alinipa nisome baadhi ya barua pepe ambazo Olivia alikuwa anawasiliana na Sayid kwa lugha ya kiarabu.Nilishangaa sana,sikujua kama Olivia anaifahamu lugha ya kiarabu.Katika barua pepe zile Olivia na Sayid walizungumzia kuhusiana na utengenezwaji wa kirusi na kwa mujibu wa Devotha,Olivia ametengeneza kirusi ambacho amemuambukiza mtoto wa rais na kwa sasa binti huyo wa rais yuko hospitali hali yake si nzuri.Olivia amefanya hivi ili kumshinikiza rais amueleze mahala alipo Edger Kaka” “Edger Kaka?!! Gosu Gosu akashangaa “Ni nani huyo? “Edger Kaka aliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.Alifariki katika ajali ya gari miaka mitatu iliyopita lakini Olivia ameibukana kudai kuwa Edger Kaka hajafa yuko hai” akasema Mathew na Gosu Gosu akatoa kicheko kidogo “Kwa nini anadai hivyo? akauliza “Hilo ni swali analotakiwa kulijibu yeye mwenyewe.Kwa maelezo aliyompa Devotha anadai ajali ile iliyotokea ilikuwa ya kutengeneza na hata mwili uliozikwa haukuwa wa Edger Kaka.Olivia anadai anao ushahidi wa kuthibitisha hilo na amekwenda mbali zaidi kwa kumnyooshea kidole rais Dr Evans kwamba anahusika katika jambo hilo na anafahamu mahala alipo Edger na ndiyo maana anamshinikiza amuonyeshe alipo kwa kumuambukiza mwanae virusi na kama rais asipofanya hivyo basi mwanae anaweza kupoteza maisha.Mambo kama haya yanatokea sana katika ulimwengu wa sasa na yawezekana hata hili analolisema Olivia likawa kweli lakini swali linaloibuka hapa ni je hili suala lina mahusiano gani na IS? .Olivia ni kama chambo tu lakini nyuma yake wapo IS ambao ameshirikiana nao katika kutengeneza kirusi hicho ili kumshinikiza rais aeleze mahala alipo Edger.Tujiulize IS wana maslahi gani katika suala hili?Mwenye kuweza kutupa majibu ya suala hili ni Olivia ambaye hatujui mahala alipo hivyo kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kuhakikisha tunampata Olivia Themba.Tayari tunafahamu anashikiliwa na idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi ambayo iko chini ya rais na hapo hapo ikumbukwe kwamba Rais ndiye amenyooshewa kidole na Olivia kuhusiana na mpango huu wa kutengeneza kifo cha Edger Kaka na yawezekana kuna ukweli ndani yake na Olivia anaweza akauawa ili jambo hili liendelee kuwa siri hivyo basi ili kuupata ukweli wote kuhusu suala la Edger Kaka,kuhusu IS lazima tumpate Olivia” akasema Mathew na kunyamaza kidogo wakalipita gari lililokuwa mbele yao halafu akasema Gosu Gosu akauliza “Mathew ulikutana vipi na Olivia? “Nilikutana na Olivia katika klabu moja ya usiku tukawa marafiki.Baadae urafiki wetu ukawa mkubwa Zaidi nadhani unanielewa.Ninao uwezo mkubwa sana wa kumsoma mtu na toka nilipofahamiana naye niligundua kuna kitu ananificha na siku moja baada ya kumdadisi akanieleza kuwa ana tatizo na watu fulani ingawa hakutaka kunieleza ni akina nani.Sikutaka kuingilia mambo yake binafsi lakini Kwa kuwa tayari ni mtu wangu wa karibu na sikutaka aingie katika hatari zozote nilimpa namba za ile programu aliyoitengeneza Ruby ili atakapopata matatizo nijue yuko wapi.Nikiwa mkutanoni Arusha nilipokea ujumbe kutoka katika namba ile niliyompa Olivia na taarifa zikaanza kusambaa mitandaoni kuwa Olivia ametekwa nikalazimika kuja Dar es salaam haraka sana kwani tayari nilikuwa nafahamu sehemu ya kuanzia kumtafuta.Nilifika hadi mahala ambako namba zile zilipigwa lakini Olivia alikwisha hamishwa.Nilipokuwa narudi baada ya kumkosa Olivia nikapigiwa simu na mama yake Olivia akanijulisha kuwa mume wake amepigiwa simu na mtu ambaye alijifanya ni mimi na akamdanganya kuwa amempata Olivia na kumtaka wakutane mahala.Nilifika mahala hapo nikalikuta gari la baba yake Olivia lakini yeye mwenyewe hakuwemo, tayari alikwisha tekwa.Nilianza kuhisi kuna mtu anayeshirikiana na watekaji ambaye ana ukaribu mkubwa na familia ya akina Olivia.Usiku huo huo nikaenda kuonana na Lucy Themba mama yake Olivia nikamtaka anieleze kama kuna mtu yeyote walimwambia kuhusu mimi kufahamu mahala alipo Olivia.Lucy alikana kabisa kumweleza mtu yeyote.Niliporejea nyumbani Ruby akanijulisha amegundua Olivia ametekwa na idara ya serikali inayojulikana kama idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi.Nilijiuliza maswali kwa nini idara ya serikali wamteke Olivia na baba yake?Nilitaka kuufahamu ukweli ndipo nilipowaomba wewe na Ruby mje mara moja kunisaidia katika suala hili”akasema Mathew “Usijali Mathew tayari nimekaribia” akasema Gosu Gosu.Ukapita kimya mfupi Mathew akasema “Mapema alfajiri leo nilipigiwa simu na Lucy Themba akanitaka niende nyumbani kwake kuna jambo anatakakunieleza.Sikuwa na wasi wasi wowote nikaenda kuonana naye.Nilifanya kosa kutochukua tahadhari kumbe ulikuwa ni mtego.Nilivamiwa na kundi la watu wenye silaha wakanichukua na kunipeleka mahala pale mliponikuta.Niliwekwa katika chumba cha baridi kali halafu wakanitoa na kunipeleka katika cumba chenye mwanga mkali mweupe.Baadae akaja Devotha akajitambulisha kwangu kama ndiye mkurugenzi wa idara ile ya siri ya usalama wa ndani ya nchi.Devotha alinihoji kuhusu mahusiano yangu na Olivia nikamueleza kila kitu bila kumficha.Alinihoji maswali mengi akitaka kujua kwa nini nilimpa Olivia namba zile za kunijulisha pindi akipata matatizo.Nilimweleza sababu ya kumlinda Olivia na bada ya mazungumzo alitaja kuwa mimi na Olivia tunatumiwa na IS kufanikisha mipango yao hapa Tanzania.Nilistuka na kumtaka anipe ushahidi wa mimi kujihusisha na mtandao wa kigaidi wa IS.Alikiri kwamba hakuwa na ushahidi wowote wa mimi kujihusisha na mtandao huo ila walikuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu Olivia kujihusisha na mtandao huo.Alinieleza namna walivyopata taarifa za Olivia kuonekana akiwa na watu wa IS jijini Kinshasa na hadi walivyomfuatilia na kumteka.Alinionyesha barua pepe ambazo Olivia amekuwa akiwasiliana na mtu anaitwa Sayid Omar ambaye anatajwa kuwa mfadhili mkubwa wa kikundi hicho.Mawasiliano yao yalikuwa katika lugha ya kiarabu.Nilisoma barua pepe zile,Olivia na Sayid walikuwa wanawasiliana kuhusiana na maendeeleo ya mradi wa kutengeneza kirusi ambacho Devotha aliniambia walimuambikiza mtoto wa rais ili kumshinikiza awaeleze mahala alipo Edger Kaka.Nilimtaka Devotha aniachie huru ili niweze kumsaidia kuutafuta ukweli wa jambo hili lakini hakuwa tayari kufanya hivyo ndipo nikamweleza kama akihitaji msaada Zaidi awatafute wewe na Ruby mtamsaidia.Nilimpa vile vile maelekezo ya kufanya kwa kumtaka aidukue simu ya rais ili kufahamu kama rais analifahamu suala lile la Edger Kaka kwani yeye ndiye amekuwa mlengwa mkubwa.Sikujua tena kilichoendelea hadi pale mlipojitokeza na kuniokoa”akasema Mathew “Devotha alifanya kama ulivyomuelekeza” akasema Gosu Gosu “Aliidukua simu ya rais.Kuna dada mmoja anaitwa Saada ambaye ndiye aliyemsaidia katika kuidukua simu ya rais lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kupata kitu chochote kwani waligundulika mapema.Nadhani Rais aligundua kwamba ni Devotha ndiye aliyedukua simu yake hivyo akafungiwa kila kitu kuanzia simu yake,na hakuweza tena kuingia katika mtandao wa idara yake.Yeye na Saada baada ya kuhisi wako katika hatari walikimbilia nyumbani kwako.Nilipowasili nilikutana na Theresa akanijulisha kuwa kuna mtu alipiga simu pale nyumbani anakutafuta anadai ana jambo la muhimu sana la kukueleza lakini hupatikani simuni.Theresa alijaribu naye kukutafuta katika namba zako zote za simu hukuwa unapatikana na hii ikampa wasiwasi.Muda huo huo Devotha akawasili nikamuhoji na kumtaka anieleze mahala ulipo akanieleza kila kitu kilichotokea na mahala ulipo.Wakati nikizungumza na Devotha mtu yule aliyekuwa anakutafuta simuni akapiga tena simu ya nyumbani kwako nikalazimika kuzungumza naye nikijifanya mimi ni Mathew nikamuliza anachonikufutia akasema anazo taarifa kuhusu Olivia.Kabla ajaeleza chochote ikasikika sauti ikimuuliza kwa ukali yule jamaa anazungumza na nani na simu ikakatwa” “Alisema anazo taarifa za Olivia?Mathew akauliza “Ndiyo.Alitaka kunieleza kitu Fulani kuhusu Olivia lakini akazuiwa na mtu baqda ya hapo simu yake ikakatwa na haikupatikana tena” akasema Gosu Gosu “Kwa namna alivyokuwa anazungumza unadhani alitaka kunieleza nini kuhusu Olivia? Mathew akauliza “Sina hakika lakini alichotaka kukueleza kinahusiana na Olivia.Kwa taarifa tu ni kwamba Olivia amehamishwa kutoka mahala alipokuwa na hata Devotha mwenyewe hafahamu mahala alipo” akasema Gosu Gosu.Mathew akafikiri kidogo na kusema “Ninahisi Olivia alimtumia huyo jamaa kufikisha ujumbe kwangu lakini akagundulika kabla hajafikisha ujumbe.Kama ni kweli Olivia alimtumia huyo jamaa kutaka kunifikishia ujumbe na akagundulika basi kitendo hicho kinamuweka katika hatari Zaidi.Kikubwa tunachopaswa kukifanya kwa sasa ni kutafuta mahala ambako huyo jamaa alikuwepo wakati akipiga simu.Kwa bahati mbaya Ruby bado hajawasili yeye ndiye mtaalamu sana wa haya mambo ya mawasiliano” akasema Mathew “Tunaye Saada.Anao ujuzi wa kutosha katika mambo haya.Ndiye aliyemsaidia Devotha kudukua simu ya rais na ndiye aliyetusadia kuingia pale mahali ulipokuwa umefungwa kwa kucheza na kamera.Tulimchukulia chumba Lupai hotel ili aendelee na zoezi la kucheza na kamera za jengo lile tungeweza kumfuata lakini kwa bahati mbaya Lupai Hoteli iko karibu sana na lile jengo la wale jamaa”akasema Gosu Gosu “Tafuta namba za hoteli mpigie simu na muelekeze sehemu ya kukutana anaweza akatusaidia kufahamu mahala alipo huyo jamaa aliyekuwa ananitafuta” akasema Mathew “Sawa nitafanya hivyo.Vipi Paul naye anakuja?akauliza Gosu Gosu “Hapana Paul hatakuja.Tutakuwa na Ruby” akasema Mathew “Tulikuwa na timu nzuri sana wakati ule tukiwa kikosi cha siri” “Usijali kila kitu kitakwenda vizuri.Tutampata Olivia na tutajua kila kitu kuhusu yeye na kikundi cha IS na kama kuna mipango yoyote wanayoipanga hapa nchini tutahakikisha haifanikiwi” akasema Mathew na ukimya ukatawala garini “Bado ninajiuliza maswali mengi kuhusiana na Olivia na IS.Kuna nyakati najikuta nikikataa Olivia hawezi na hana sababu ya kujihusisha na watu wa IS lakini upo ushahidi mkubwa wa jambo hili na kuna sauti ndani mwangu inaniambia nilifuatilie hili jambo hadi mzizi wake na kuufahamu kweli.Nitahakikisha ninafahamu kuhusiana na hili suala” akawaza Mathew na kuivuta picha ya Olivia kichwani kwake “She’s an angel.Ana sura nzuri ya kimalaika.Akicheka vishimo hutokea katika mashavu yake.Ana sauti nyororo kama Wema,ana kila sifa ya mwanamke mzuri.Inawezekanaje msichana mzuri kama huyu akajihusisha na mtandao wa kigaidi?Ni kwa ajili ya kujipatia fedha?Sidhani kama Olivia ana shida na fedha kwani anatoka katika familia bora kabisa na yeye mwenyewe ni msomi mzuri,Olivia ana kila kitu anachokihitaji katika maisha yake hana sababu ya kujiunga na magaidi kwa ajili ya fedha kitu gani basi kimempelekea akafanya haya aliyoyafanya? Jambo hili hata watu wakilisikia litawapa ugumu sana kuamini lakini huo ndio ukweli.Olivia anashirikiana na magaidi na kwa kushirikiana na Sayid Omar wametengeneza kirusi ambacho wamemuambukiza mtoto wa Rais ili kumshinikiza awaonyeshe mahala alipo Edger Kaka.Huyu Edger Kaka ana nini hadi IS wamtafute kwa gharama kiasi hiki?Ana maslahi gani kwao? Bado mtu mwenye kuweza kusaidia kupata majibu ya maswali haya yote anabaki kuwa ni Olivia pekee” akawaza Mathew Walifika Tumaini Car praking,jengo la ghorofa nane ambalo ni maalum kwa ajili ya kuegesha magari.Walipanda hadi ghorofa ya tano ambako Mathew alimiuelekeza Jordan apeleke gari.Alishuka garini akaenda kulitafuta gari alilomuelekeza Jordan amletee akalipata.Milango yake haikuwa imefungwa na katika droo ya gari kulikuwa na funguo.Mathew akaingia na kuliwasha.Gosu Gosu akafungua buti la ile gari waliyokuwa wameitumia akakata Kamba alizomfunga dereva. “Kila kitu chako kiko garini hakuna kilichopotea” akasema Gosu Gosu na kutoa bunda la dola za kimarekani akamega nusu yake na kumrushia yule jamaa ndani ya buti “Samahani sana kwa usumbufu” akasema huku akimfanyia ishara kuwa afunge mdomo wake.Akachukua silaha zao akaelekea katika gari alimokuwamo Mathew wakaondoka “Una hakika yule dereva hataweza kuwa na madhara?Mathew akauliza “Hana madhara.Nimempooza na kiasi cha kutosha cha dola” akasema Gosu Gosu Mathew ndiye aliyeshika usukani na safari ikawa ya kimya kimya hadi walipofika nje ya nyumba yenye geti jeusi eneo la Buti mbili.Mathew akashuka garini akaenda katika geti akafunua mfuniko wa kasha Fulani dogo ambalo ndani yake kulikuwa na vitufe kadhaa vya namba akabonyeza namba na geti likafunguka akamtaka Gosu Gosu aingize gari ndani kisha akalifunga geti Ilikuwa ni nyumba ya wastani iliyokuwa na vyumba vitatu vya kulala,sebule,jiko,chumba cha chakula pamoja na chumba kingine kidogo kwa ajili ya maktaba. “Nani anaishi hapa? Akauliza Gosu Gosu “Hii pia ni nyumba yangu.Nimeinunua kutoka kwa rafiki yangu na ninaendelea na ukarabati.Ninapenda wakati mwingine kuja kupumzika hapa kuna utulivu mwingi.Ninawekeza sana katika majengo kwani thamani yake haishuki bali inapanda kila mwaka” akajibu Mathew “Hongera.Ni nyumba ndogo lakini nzuri sana” akasema Gosu Gosu wakaingia ndani “Kuna vyumba vitatu humu ndani.Kimoja ni cha kwangu ,kingine atatumia Ruby na kingine utatumia wewe.Operesheni yote itafanyika kutokea hapa” akasema Mathew na kuingia katika chumba chake cha kulala baada ya muda akatoka akiwa na simu tatu amkapatia moja Gosu Gosu “Mimi ni mtu wa tahadhari muda wote .Sifahamu ni wakati gani nitakutana na hatari hivyo basi huwa nina kawaida ya kuhifadhi vitu muhimu vya mawasiliano katika baadhi ya sehemu zangu muhimu.Simu hiyo utatumia wewe hii nyingine ataitumia Ruby.Mpigie yule msichana uliyesema mlimuacha hotelini tunamuhitaji tuanze kazi” akasema Mathew.Gosu Gosu akajisachi mfukoni alikuwa na risiti waliyotumia kufanya malipo akanakili namba za simu za Lupai Hoteli akapiga na kuomba kuzungumza na chumba 86 akaunganishwa lakini simu ikaita bila kupokelewa. “Saada atakuwa amendoka pale hotelini au yuko katika matatizo? akawaza Gosu Gosu na kumfuata Matew chumbani kwake “Simu ya chumbani kwa Saada inaita haipokelewi” akasema Gosu Gosu “Usiogope.Tutamsubiri Ruby si muda mrefu toka sasa atawasili.Wakati tunamsubiri kuna mahala nataka twende” akasema Mathew wakaingia garini na kuondoka bila kumueleza Gosu Gosu wanakoelekea
Kaiza alikaa katika iliyokuwa ofisi ya Devotha akakiegemeza kichwa kitini.Alizama katika lindi la mawazo akiitazama picha ya Devotha iliyokuwa mezani akitabasamu “Devotha ndiye aliyeniingiza katika idara hii.Siku zote nimekuwa nikimuheshimu kama dada yangu na siamini kama tumefikia hapa.Kwa nini lakini akafanya maamuzi haya ambayo nayaita ya kijinga kujiunga na watu wanaoshirikiana na magaidi?Kwa nini amechagua kuwa adui yetu? Rais ametoa ruhusa ya kumpiga risasi kokote atakapoonekana,inaniumiza kwa amri hii lakini yote haya ameyataka yeye mwenyewe.Kitendo cha kuua watu ambao amekuwa akiishi na kufanya nao kazi kama ndugu kimeniumiza sana na kuna wakati inaniwia ugumu kuamini kama kweli aliyefanya unyama huu ni Devotha huyu ninayemfahamu mimi ambaye amekuwa ni kama dada yangu.Amenisaidia katika mengi lakini sintaweza kumsaidia katika hili alilolifanya.Rais amekwisha toa maelekezo lazima yafuatwe.” akawaza Kaiza na kuifunika picha ile ya Devotha “Lakini amri hii ya rais ni kubwa mno.Naamini ametoa amri hii kwa hasira.Tulipaswa kumkamata Devotha akahojiwa na kufahamu sababu iliyompekekea akafanya hivi alivyofanya.Hata hivyo hatuwezi kumpinga,maagizo yke ni amri kwetu na lazima yatekelezwe.Kikubwa ninachopaswa kuumiza kichwa kwa sasa ni namna ya kumpata.Devotha anaifahamu idara hii kama nyuma ya kiganja chake cha mkono na anafahamu mbinu zetu zote hivyo kumpata inaweza kuwa ngumu sana kwetu lakini…”Kaiza akatabasamu kwa mbali baada ya kukumbuka kitu “Asubuhi baada ya kumuhoji Mathew Mulumbi,Devotha aliondoka hapa bila kuaga anakwenda wapi na ninakumbuka aliondoka akiwa na Saada.Sasa nimepata picha.Yawezekana alimtumia Saada katika kudukua simu ya rais kwani Saada ni mmoja wa wadukuzi tunaowategemea hapa katika idara yetu.Nina uhakika mkubwa tukimpata Saada tutakuwa tumempata pia Devotha au tutafahamu mahala alipo Devotha.Kwa nini sikuwa na wazo hili toka mapema?Tusingesumbuka namna hii na pengine mida hii tungekwisha mpata Devotha” akawaza Kaiza akainua simu na kupiga akauliza kama Saada alikuwepo wakati Devotha aliovamia akajibiwa hakuwepo. “Tayari nimepata jibu.Saada anatumiwa na Devotha.Ipo namna rahisi ya kumpata Saada.Kuna kifaa kidogo sana huwa tunawawekea mwilini watu wote wa idara yetu bila wao kuna na tunaofahamu siri hii ni mimi na Devotha pekee.Kila mtu anayejiunga huchomwa sindano ya usingizi na huwekewa kifaa Fulani kidogo mithili ya punje ya mchele ambacho hutuwezesha sisi kufahamu mahala alipo kwa siri bila wao kuwa na taarifa.Sijui kwa nini sikuwa na wazo kama hili toka mapema” akawaza Kaiza na kuufunga kabisa mlango wa ofisi ile halafu akaingiza namba za siri katika kompyuta yake na kuanza kutafuta kitu Fulani na baada ya muda akakipata alichokuwa anakitafuta “Sasa amepatikana.Tayari nimekwisha ona mahala alipo” akawaza Kaiza na kutoka akaelekea control room.Hali ya simanzi kubwa ilikuwa imetanda.Watu walikuwa wameketi vitini wengine wakilia “Naombeni tusikilizane jamani” akasema Kaiza na kila mmoja akakaa sawa kumsikiliza “Poleni sana kwa kile kilichotokea.Tumeumizwa mno kwa wenzetu tuliowapenda kuuawa.Kibaya na kinachoumiza Zaidi ni kwamba aliyefanya jambo hili ni mwenzetu,ndugu yetu ambaye kwa muda wote amekuwa akituongoza lakini leo amebadilika na kufanya hivi alivyofanya.Hili halivumiliki na lazima tuhakikishe wale wote waliofanya hivi wanapatikana wakiwa hai au wamekufa! Akasema Kaiza na kunyamaza akawatazama watu wale waliokuwa wameyaelekeza macho yao kwake kisha akaendelea. “Nimekuwa ofisini nikijaribu kutafakari kama aliyefanya jambo hili ni Devotha huyu ninayemfahamu mimi au ni mwingine anayefanana naye lakini jibu ni jepesi kwamba ni Devotha huyu huyu ambaye amekuwa kiongozi wetu ndiye aliyebadilika na kufanya haya yaliyotokea.Nimemjulisha rais kilichotokea naye pia amestushwa mno na hiki alichokifanya Devotha ambaye alimuamini sana.Kwa hiyo basi Rais ameelekeza kwamba Devotha ni mtu hatari sana ambaye amekuwa adui yetu na adui yetu ni adui wa Tanzania hivyo basi kokote atakapoonekana anatakiwa kuuawa.Si yeye peke yake bali na wale wote anaoshirkiana nao akiwemo Mathew Mulumbi ambaye yeye na Olivia wanashirikiana na kikundi cha IS.Mkumbuke watu hawa wana mafunzo makubwa hivyo yawezekana kuwakamata ingawa ngumu kwetu ndiyo maana rais ametoa maelekezo hayo kwamba kokote wakatakoonekana wapigwe risasi na kufa.Nafahamu wengi hapa mtashangaa kwa amri hii ya rais kwa sababu tumekuwa na Devotha na tunampenda lakini kwa hili alilolifanya hatuna namna Zaidi ya kutekeleza amri ya rais.Anastahili adhabu ya kifo kama alivyoua wenzetu” akasema Kaiza na kunyamaza akawatazama wale watu mle ndani ambao nyuso zao zilijaa simanzi kubwa. “Asubuhi ya leo Devotha alipoondoka hapa alikuwa ameongozana na Saada ambaye wote tunamfahamu uwezo wake mkubwa katika udukuzi.Devotha alimchukua Saada ili akamsaidie kazi zake za udukuzi na nina uhakika mkubwa kwamba ni yeye aliyemsaidia Devotha kuingia hapa ndani na haya yote yakatokea.Ili kumpata Devotha tunatakiwa kumpata Saada.Ninaamini aidha wako pamoja au anafahamu mahala alipo.Kuanzia sasa Saada naye anaingia katika orodha ya wale tunaowatafuta.Ninawahakikishi a kwamba tukimpata Saada tutakuwa tumempata Devota.Ninafahamu mahala tunakoweza kumpata Saada hivyo nitaongozana na timu ya watu tutakwenda huko kumchukua na akipatikana atatupa ukweli wote mahala alipo Devotha.Wakati sisi tunakwenda kumtafuta Saada wengine mtaendelea na kazi kama kawaida.Hiki ni kipindi kigumu sana kwetu hivyo lazima na sisi tusimame imara kuhakikisha kwamba tunaibuka washindi.Siku zote kushindwa kwetu ni mwiko.Lazima tuhakikishe tunashinda na kuwatia mikononi Devotha na mtandao wake wote.Rais anatutegemea sana sisi,Tanzania inatutegemea pia hivyo basi lazima tuhakikishe tunakiondoa kitisho cha usalama kinachoikabili nchi yetu kwa sasa kutoka kwa IS” akasema Kaiza na kuchagua watu wanne akawataka waongozane kwenda kumtafuta Saada.Hakumueleza mtu yeyote wapi wanaelekea au amefahamuje mahala alipo Saada.Safari ilikuwa ya kimyakimya na Kaiza ndiye aliyekuwa anatoa maelekezo wapi waelekee.Macho yake hayakubanduka katika simu yake.
Saada baada ya kutoka Lupai hotel,alifikiria sehemu ya kwenda akaogopa kwenda nyumbani kwake kwani alihisi anaweza akafuatiliwa huko.Hakutaka tena kurejea nyumbani kwa Mathew kwani aliyempeleka pale alikuwa Devotha ambaye alipoteza mawasiliano naye na hakujua angempata wapi.Sehemu pekee ambako aliamini ni salama kwake kwa muda ule ni kwa mpenzi wake Aziz Mubarak anayeishi katika maghorofa ya Kaumbe. Toka Lupai hotel Saada akamuelekeza dereva wa ile taksi aliyopanda ampeleke katika maghorofa ya Kaumbe.Alikuwa na ufunguo mmoja wa kuingia katika nyumba ya mchumba wake Aziz.Alimlipa dereva pesa yake akapanda lifti hadi ghorofa ya saba anakoishi mpenzi wake.Akaingia ndani ya nyumba ya mpenzi wake akafunga mlango.Hakutaka kuwasha simu yake kwa kuwa aliogopa anafuatiliwa.Mle ndani ilikuwemo kompyuta ya Aziz akawasha na kumpigia simu kupitia mtandao akamjulisha kuwa amekwenda pale kwake.Aziz akamjulisha kuwa atafika pale muda si mrefu.Baada ya dakika kumi na tano Aziz akawasili kama alivyoahidi.Saada hakumueleza kitu chochote kilichotokea na hata Aziz alipomtaka wafanye mapenzi hakutaka kwani hakutaka kuonyesha kama kuna jambo limemtokea. Kaiza na vijana wake waliwasili katika maghorofa ya Kaumbe.Kaiza akiwa na simu yake ambayo ilimuelekeza mahala aliko Saada aliwaongoza vijana wake wakafika hadi katika mlango wa kuingia katika nyumba ya Aziz akagonga mlango na Aziz akainuka akaenda kuufungua.Alistuka sana alipowaona wale jamaa.Hakuwahi kuwaona maeneo yale “Karibuni” akasema kwa wasiwasi “Samahani kaka.Namuulizia dada mmoja anaitwa Saada Amiri” akasema Kaiza na Aziz akastuka “Aliwalekeza anaishi hapa?akauliza “Hajatuelekeza hivyo lakini tunafahamu yuko humu ndani hivyo tunaomba tuzungumze naye” akasema Kaiza “Ninyi ni akina nani?Ni polisi?akauliza Aziz “Hapana sisi si polisi ni wafanyakazi wenza na Saada.Tunamuomba tuzungumze naye tafadhali ni mambo ya kiofisi usiwe na hofu” akasema Kaiza.Aziz akageuka na kurejea ndani “Darling kuna mtu yeyote ulimjulisha kuwa unakuja hapa?akauliza Aziz “Hapana darling sijamjulisha mtu yeyote Zaidi yako.Kuna nini kwani?akauliza Saada “Una hakika?Azizi akauliza “Ndiyo nina uhakika hata simu yangu nimeizima ndiyo maana nikawasiliana nawe kwa kutumia mtandao.Kwani kuna nini Aziz? “Kuna watu wanakuulizia.Wanadai ni wafanyakazi wenzako.Twende ukawasikilize wanadai wamekufuata kwa mambo ya kiofisi.Kama hujawaeleza uko hapa nashangaa wamefahamuje?akauliza Aziz. Saada alipatwa na mstuko mkubwa sana aliposikia kuna watu wanamtafuta. “Darling mbona umestuka sana?akauliza Aziz “Devotha ameniingiza katika matatizo makubwa” akawaza huku akiinuka na kuvaa nguo zake “Darling kuna tatizo lolote?akauliza Aziz “Hakuna tatizo Darling” akasema Saada na kisha akafungua mlango wa chumbani na kutoka.Wakiwa sebuleni Saada akasimama akawaza.Aziz aliendelea kumtazama.Saada akamfuata akamkumbatia na kumbusu “Nakupenda sana Aziz” akasema kisha akatembea hatua tatu kama kuna kitu anakifuata ukutani ghafla akachomoka hadi dirishani akajirusha nje.Aziz akapiga ukelele mkubwa uliowafanya Kaiza na vijana wake kuingia ndani ndipo wakashuhudia kile kilichokuwa kimetokea.Wote walibaki na mshangao mkubwa.Aziz alitoka mbio kushuka chini huku akipiga kelele kama chizi.Kaiza akawaelekeza watu wake wafanye upekuzi wa haraka mle ndani wakakuta mkoba wa Saada uliokuwa na vifaa vichache wakachukua kompyuta mbili walizozikuta mle ndani wakaondoka haraka. “Damn you Devotha.Umesababisha binti wa watu akaamua kujitoa uhai kwa woga.Damu yake na wale wote uliowatoa uhai itaendelea kukulilia siku zote za maisha yako.Nitahakikisha ninakukamata” akawaza Kaiza akiwa garini.Kaiza akawataka vijana wake kuchukua taksi warejee kitalu 1 yeye akabaki na gari lake akaelekea mahala aliko Olivia
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saada baada ya kutoka Lupai hotel,alifikiria sehemu ya kwenda akaogopa kwenda nyumbani kwake kwani alihisi anaweza akafuatiliwa huko.Hakutaka tena kurejea nyumbani kwa Mathew kwani aliyempeleka pale alikuwa Devotha ambaye alipoteza mawasiliano naye na hakujua angempata wapi.Sehemu pekee ambako aliamini ni salama kwake kwa muda ule ni kwa mpenzi wake Aziz Mubarak anayeishi katika maghorofa ya Kaumbe. Toka Lupai hotel Saada akamuelekeza dereva wa ile taksi aliyopanda ampeleke katika maghorofa ya Kaumbe.Alikuwa na ufunguo mmoja wa kuingia katika nyumba ya mchumba wake Aziz.Alimlipa dereva pesa yake akapanda lifti hadi ghorofa ya saba anakoishi mpenzi wake.Akaingia ndani ya nyumba ya mpenzi wake akafunga mlango.Hakutaka kuwasha simu yake kwa kuwa aliogopa anafuatiliwa.Mle ndani ilikuwemo kompyuta ya Aziz akawasha na kumpigia simu kupitia mtandao akamjulisha kuwa amekwenda pale kwake.Aziz akamjulisha kuwa atafika pale muda si mrefu.Baada ya dakika kumi na tano Aziz akawasili kama alivyoahidi.Saada hakumueleza kitu chochote kilichotokea na hata Aziz alipomtaka wafanye mapenzi hakutaka kwani hakutaka kuonyesha kama kuna jambo limemtokea. Kaiza na vijana wake waliwasili katika maghorofa ya Kaumbe.Kaiza akiwa na simu yake ambayo ilimuelekeza mahala aliko Saada aliwaongoza vijana wake wakafika hadi katika mlango wa kuingia katika nyumba ya Aziz akagonga mlango na Aziz akainuka akaenda kuufungua.Alistuka sana alipowaona wale jamaa.Hakuwahi kuwaona maeneo yale “Karibuni” akasema kwa wasiwasi “Samahani kaka.Namuulizia dada mmoja anaitwa Saada Amiri” akasema Kaiza na Aziz akastuka “Aliwalekeza anaishi hapa?akauliza “Hajatuelekeza hivyo lakini tunafahamu yuko humu ndani hivyo tunaomba tuzungumze naye” akasema Kaiza “Ninyi ni akina nani?Ni polisi?akauliza Aziz “Hapana sisi si polisi ni wafanyakazi wenza na Saada.Tunamuomba tuzungumze naye tafadhali ni mambo ya kiofisi usiwe na hofu” akasema Kaiza.Aziz akageuka na kurejea ndani “Darling kuna mtu yeyote ulimjulisha kuwa unakuja hapa?akauliza Aziz “Hapana darling sijamjulisha mtu yeyote Zaidi yako.Kuna nini kwani?akauliza Saada “Una hakika?Azizi akauliza “Ndiyo nina uhakika hata simu yangu nimeizima ndiyo maana nikawasiliana nawe kwa kutumia mtandao.Kwani kuna nini Aziz? “Kuna watu wanakuulizia.Wanadai ni wafanyakazi wenzako.Twende ukawasikilize wanadai wamekufuata kwa mambo ya kiofisi.Kama hujawaeleza uko hapa nashangaa wamefahamuje?akauliza Aziz. Saada alipatwa na mstuko mkubwa sana aliposikia kuna watu wanamtafuta. “Darling mbona umestuka sana?akauliza Aziz “Devotha ameniingiza katika matatizo makubwa” akawaza huku akiinuka na kuvaa nguo zake “Darling kuna tatizo lolote?akauliza Aziz “Hakuna tatizo Darling” akasema Saada na kisha akafungua mlango wa chumbani na kutoka.Wakiwa sebuleni Saada akasimama akawaza.Aziz aliendelea kumtazama.Saada akamfuata akamkumbatia na kumbusu “Nakupenda sana Aziz” akasema kisha akatembea hatua tatu kama kuna kitu anakifuata ukutani ghafla akachomoka hadi dirishani akajirusha nje.Aziz akapiga ukelele mkubwa uliowafanya Kaiza na vijana wake kuingia ndani ndipo wakashuhudia kile kilichokuwa kimetokea.Wote walibaki na mshangao mkubwa.Aziz alitoka mbio kushuka chini huku akipiga kelele kama chizi.Kaiza akawaelekeza watu wake wafanye upekuzi wa haraka mle ndani wakakuta mkoba wa Saada uliokuwa na vifaa vichache wakachukua kompyuta mbili walizozikuta mle ndani wakaondoka haraka. “Damn you Devotha.Umesababisha binti wa watu akaamua kujitoa uhai kwa woga.Damu yake na wale wote uliowatoa uhai itaendelea kukulilia siku zote za maisha yako.Nitahakikisha ninakukamata” akawaza Kaiza akiwa garini.Kaiza akawataka vijana wake kuchukua taksi warejee kitalu 1 yeye akabaki na gari lake akaelekea mahala aliko Olivia
Mathew na Gosu Gosu waliwasili katika makazi ya bilionea Agrey Themba.Aliwakuta walinzi wawili nje ya geti.Walikuwa ni walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi na mmoja wao alikuwa na bunduki.Akawasalimu na kuwaeleza shida yake ya kutaka kuonana na Lucy Themba.Walinzi wale wakamueleza kwamba hakuna mgeni yeyote anayeruhusiwa kuingia ndani bila ruhusa ya Lucy Themba hivyo wakawataka akina Mathew wasubiri ili wamuulize Lucy.Mmoja wa wale walinzi akaingia ndani na kumuacha nje yule mwenye bunduki.Mathew akampa ishara Fulani Gosu Gosu halafu akamuita yule mlinzi “Samahani kaka nataka kuuliza” akasema Mathew yule mlinzi ambaye bunduki yake ilikuwa begani akasogelea gari la akina Mathew. “Unasemaje? akauliza “Wewe uko hapa mara kwa mara kuna tetesi zozote za kupatikana kwa Olivia na baba yake Agrey?akauliza Mathew.Gosu Gosu akafungua mlango wa gari akashuka na kuzunguka nyuma ya gari akajifanya anatazama matairi huku akimsogelea yule jamaa “Swali hilo muwaulize watu wa familia mimi kazi yangu ni kulinda.Sina muda wa kufuatilia mambo ya ndani” akasema yule jamaa na kutaka kugeuka aondoke ghafla akajikuta akizuiliwa na GosuGosu aliyemuwekea bastora tumboni “Ingia garini haraka sana ama sivyo nitausambaza utumbo wako sasa hivi” akasema Gosu Gosu.Mathew aliyekuwa ndani ya gari naye akatoa bastora akamnyooshea yule jamaa halafu akafungua mlango kwa ndani Gosu Gosu akamuingiza garini yule mlinzi.Kabla hajakaa sawa yule mlinzi akajikuta amepigwa vichwa viwili mfululizo kutoka kwa Gosu Gosu akaanguka kitini hakuwa na fahamu.Akaichukua silaha yake akaitupa nyuma ya gari. Mathew akashuka garini haraka na kwenda katika ule mlango mdogo akausukuma taratibu akachungulia na kumuona yule mlinzi akiwa ndani ya nyumba ndogo ya walinzi akiinua mkono wa simu Mathew hakutaka kumpa nafasi akaingia ndani na kwa kutumia bastora yenye kiwambo cha sauti akakipiga risasi kiganja cha mkono wa yule jamaa akaanguka chini.Kufumba na kufumbua tayari Mathew alikwisha ingia mle katika nyumba ya walinzi. “Usithubutu kupiga kelele nitakumaliza.Nataka uniambie Lucy Themba yuko ndani? “Ndiyo yuko ndani” akasema yule jamaa “Kuna watu wangapi mle ndani?Mathew akauliza “Yupo Lucy na Teddy mtumishi wa ndani” akajibu yule mlinzi.Mathew akampiga pigo zito akalala sakafuni hakuwa na fahamu.Bila kupoteza muda Mathew akafungua geti Gosu Gosu akaingiza gari ndani Mathew akamuelekeza amshughulikie yule jamaa aliyepigwa risasi mkononi ili damu isiendele kumwagika yeye akapiga hatua ndefu kuelekea mlango mkuu wa kuingilia sebuleni,akakinyonga kitasa mlango ukafunguka akaingia sebuleni hakukuwa na mtu yeyote.Akanyata taratibu kuelekea katika chumba cha chakula.Akasikia sauti ya mwanamke akiimba.Sauti ile ilitokea jikoni akanyata taratibu na kumuona msichana mmoja akiosha vyombo huku akiimba.Mathew akakohoa kidogo msichana yule akastuka na kugeuka sahani aliyoishika ikamponyoka na kuanguka chini baada ya kujikuta akitazamana na bastora.Mwili wote ulimtetemeka. “Shhhhhh !! Mathew akamfanyia ishara asipige kelele. “Nionyeshe alipo Lucy! “Yuko chumbani kwake” akajibu yule msichana huku akitetemeka Mathew akamtaka amuongoze kuelekea chumbani kwa Lucy.Alimuonyesha mlango wa chumba cha Lucy na Mathew akamtaka agonge mlango naye akafanya kama alivyoelekezwa akagonga mlango “Nani? Ikauliza sauti kutokea ndani “Mama ni mimi” akajibu yule mtumishi “Unasemaje Teddy?akauliza Lucy Themba akiwa chumbani kwake. “Mwambie kuna kitu unataka kuuliza”akasema Mathew kwa sauti ya chini sana “Mama kuna kitu nataka kukuuliza” akasema Teddy na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa.Lucy Themba alipatwa mstuko mkubwa mno kama vile ameona jitu la kutisha baada ya kumuona Mathew Mulumbi akiwa na bastora.Alitaka kuufunga mlango Mathew akawahi akaupiga teke mlango ukambamiza Lucy akaanguka chini Mathew akachumpa ndani na kumuelekezea bastora “Simama tafadhali !! akasema Mathew “Niue tu shetani wewe.Siendi kokote!akasema Lucy “Lucy nakupa sekunde tano uwe umeinuka mwenyewe !! “Nimesema niue siendi kokote” akasema Lucy Mathew akailenga taa kubwa iliyokuwa juu ikasambaratika na kutoa mlio.Lucy alikuwa anatetemeka mwili kwa woga.Mathew akamuinua “Lucy tafadhali fanya kile ninachokuelekeza ili uwe salama” akasema Mathew na kumuamuru Lucy atoke wakaenda sebuleni “Ninakuhakikishia Mathew hautafika mbali na huu mchezo unaoufanya.Kwa taarifa yako unatafutwa kila kona.Tayari serikali inafahamu kila kitu kuhusu wewe”akasema Lucy lakini Mathew hakumjibu kitu. “Mathew tumekukosea kitu gani hadi ututese namna hii?Ni kitu gani unakitafuta kwetu?Unahitaji fedha?Sema ni kiasi gani unataka tukupatie utuache salama kuliko kuendelea kututesa kiasi hiki ! Akasema Devotha.Mathew hakujibu kitu aliendelea kumtazama Lucy halafu akaweka bastora mezani na kusema “Mama kwanza kabisa nakuomba samahani kwa hiki kilichotokea.Imenilazimu kutumia njia hii ya nguvu kwani isingekuwa rahisi wewe kukubali kuzungumza nami kwa kuwa tayari unafahamu mimi ni mtu mbaya na nina malengo mabaya na familia yako.Mama nimekuja hapa kwa mazungumzo muhimu nawe.Naomba unipe dakika kadhaa na unisikilize kwa makini” akasema Mathew Lucy Themba akaendelea kumtazama kwa hasira “Mama naomba niende moja kwa moja katika jambo la msingi lililonileta hapa.Ulinipigia simu asubuhi leo ukanitaka nifike nyumbani kwako kuna jambo unataka kuniambia nikafika kwako na kumbe ulikuwa ni mtego umeandaliwa nikatekwa.Nimekuja kukueleza kile ambacho nimekigundua huko mahala nilikokuwa nimepelekwa baada ya kutekwa.Naomba unisikilize kwa makini sana” akasema Mathew na kumtazama Lucy Themba “Waliponitoa hapa walinilipeleka mahala kunaitwa Kitalu 1 nikafungiwa ndani ya chumba kilicho zaidi ya mita mia chini ya ardhi.Nilihojiwa na mwanamama anaitwa Devotha ambaye ndiye mkurugenzi wa idara hiyo na kikubwa alitaka kufahamu kuhusu mahusiano yangu na Olivia.Nilimweleza kila kitu bila kumficha akataka kufahamu kwa nini ninamlinda Olivia hadi nikampa namba maalum za kunijulisha mahala alipo pindi anapokuwa katika hatari.Nilimueleza Devotha kila kitu na ndipo alipoamua kufunguka ukweli kwamba sababu iliyowafanya wanishikilie ni ukaribu wangu na Olivia.Mama kuna kitu ambacho nadhani hamkifahamu kuhusu Olivia na hata mimi sikuwa nikikifahamu hadi asubuhi ya leo” Mathew akanyamaza tena kidogo halafu akaendelea “Olivia anashirikiana na magaidi wa kikundi cha IS” akasema Mathew na kunyamaza baada ya kuuona mstuko mkubwa katika uso wa Lucy Themba. “Hapana ! Hilo jambo si kweli !! akasema Lucy na kusimama “Mama naomba kaa chini tafadhali ! akasema Mathew “Hakuna utakachoniambia kuhusu huo uongo wako nikaukubali.Olivia ni mwanangu nimemzaa na kumlea mwenyewe.Ninamfahamu alivyo kulio mtu yeyote.Ninazifahamu tabia zake ninafahamu kila kitu kuhusu Olivia na ninadiriki kusema katu hawezi akafanya kitu kama hicho.Katu hawezi akajihusisha na magaidi!! Akasema Lucy Themba kwa ukali “Mama naomba unisikilize bado ninaendelea” akasema Mathew.Lucy Themba akaonekana kutulia kusikiliza “Olivia ametekwa na idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi” akasema Mathew na Lucy akastuka tena “Unasema mwanangu ametekwa na idara ya serikali?akauliza “Mama naomba tafadhali endelea kunisikiliza” akasema Mathew “Idara ya usalama wa taifa ya nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo walipata taarifa za kiintelijensia kwamba kuna mtu kutoka kikundi cha Islamic States anaitwa Seif Almuhsin anaelekea nchini kwao hivyo wakaanza kumfuatilia toka alipoingia Congo na katika kumfuatilia wakagundua kwamba Seif alikutana na kufanya mazungumzo na mtanzania.Kwa bahati mbaya sina picha zake hapa lakini alipigwa picha na zikaletwa Dar es salaam kwa rais.Mtanzania huyo aliyekutana na Seif Almuhsin akatambulika kuwa ni mwanao Olivia Themba”akasema Mathew na Lucy akahamaki “No ! No ! That’s impossible !! akasema Lucy kwa ukali “Nisikilize mama” akasema Mathew “Idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi walitaka kujua sababu ya Olivia kukutana na kufanya mazungumzo na Seif mtu ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya vijana kutoka nchi za ukanda wa afrika mashariki na kati na kuwapeleka katika makambi ya IS ambako hufundishwa ugaidi hivyo wakaandaa mpango wa kumteka mara tu atakapotua nchini akitokea Kinshasa” “Mathew naomba usicheze na akili yangu baba.Unaniambia mwanangu ametekwa na idara ya serikali?akauliza Lucy “Baada ya kutekwa Olivia alihojiwa na katika kumpekua wakakuta mawasiliano ya barua pepe kati yake na mtu anaitwa Sayid Omar ambaye anatajwa kuwa mfadhili mkubwa sana wa kikundi cha IS.Walimtaka Olivia awaeleze kwa kina kuhusu kinachoendelea kati yake na IS.Katika mahojiano akawapa namba ambazo nilimpa mimi apige pindi atakapokuwa katika hatari ili kunijulisha akidai zinaweza kuwasaidia kufahamu alipo Sayid Omar.Namba zile ni kirusi na ambacho kiliufunga kabisa mfumo wote wa mawasiliano wa idara hiyo ya siri ya serikali.Baada ya kila kitu kusimama Olivia aliombwa aufungue mfumo huo lakini akagoma kuufungua hadi atakapozungumza na Rais hivyo ikawalazimu viongozi wa idara hiyo kufanya mpango na kumuita Rais akakutana na Olivia”Mathew akanyamza baada ya Lucy kusimama na kuweka mikono kichwani “Mathew unataka kuniambia Rais alionana na Olivia? Rais anafahamu kuhusu jambo hili la kutekwa Olivia?akauliza Lucy huku akihema haraka haraka “Ndiyo mama.Rais nafahamu na alikwenda kuonana na Olivia.Katika mazungumzo yao Olivia alimueleza kusudi la kutaka kuonana naye.Alimweleza Rais kwamba mwanae anayeitwa Coletha ameambukizwa virusi ambavyo amevitengeneza yeye mwenyewe Olivia na Coletha anaweza kupoteza maisha kama rais hatatekeleza kile atakachomuelekeza.Naomba nikurudishe nyuma kidogo mama.Nilikueleza kwamba Olivia alikuwa anawasiliana na Sayid Omar na nilibahatika kuzisoma barua pepe walizokuwa wanatumiana ambazo zilikuwa katika lugha ya kiarabu na katika mawasiliano yao walikuwa wanawasiliana kuhusiana na mradi wa kutengeneza kirusi ambacho ndicho hicho ameambukizwa Coletha mtoto wa rais”akasema “Mathew unataka kuupasua moyo wangu.Olivia mwanangu huyu anaweza akafanya kitu kama hicho?Anaweza akatengeneza kirusi kwa lengo la kumuua mtoto wa rais?Hapana si kweli”akasema Lucy Themba “Lengo la Olivia si kumuua Coletha bali ni kumshinikiza Rais aweze kutimiza matakwa yake na ili kumfanya rais amsikilize ndiyo maana akamuambukiza mwanae virusi hivyo na ni yeye pekee mwenye tiba yake.Hivi sasa Coletha yuko hospitali akiendelea kufanyiwa uchunguzi na hali yake inaendelea kuwa mbaya” “Jesus Christ !! akasema Lucy.Mathew akamtazama na kuendelea “Kuna jambo ambalo Olivia analitaka kutoka kwa rais.Nadhani unamkumbuka mtu anaitwa Edger Kaka.Aliwahi kuwa mbunge na akapata ajali akafariki miaka mitatu iliyopita” “Ninamkumbuka.Olivia ndiye aliyeokoa maisha yake kwa kumpeleka hospitali Israel na alipata ajali na kufariki dunia wakati akielekea nyumbani kwake baada ya kurejea nchini akitokea Israel” akasema Lucy.Mathew akaendelea “Olivia anadai kwamba Edger Kaka hajafariki yuko hai” “Edger Kaka hajafariki?Kivipi?Lucy Themba akashangaa “Hakuna anayefahamu hadi sasa kwa nini ametoa madai hayo lakini hicho ndicho anachoendelea kukisisitiza kwamba Edger kaka hakufariki katika ile ajali na anadai kuwa amefanya uchunguzi wake akagundua mwili ule uliozikwa katika kaburi la Edger haukuwa wa Edger bali ni wa mtu mwingine kabisa hivyo Edger yuko hai” “Nashindwa kukuelewa Mathew.Tulikuwa tumetoka kumpokea Olivia uwanja wa ndege akirejea nchini yeye na Edger Kaka wakitokea Israel.Wakati wa kuondoka uwanja wa ndege Edger na msafara wake wakatangulia sisi tukaondoka dakika chache baade.Tukiwa njiani tulipitwa na magari mawili ya zimamoto na mbele kidogo tukakuta ajali kubwa na magari yakiwaka moto,tukajulishwa kuwa imetokea ajali na miongoni mwa magari yaliyopata ajali ni gari la mbunge Edger Kaka.Baada ya moto kuzimwa miili iliyokuwa imeungua ikatolewa na kupelekwa hospitali.Olivia alitaka kuhakikisha ni kweli Edger amefariki katika ajali ile tukampeleka hospitali. Ni mimi niliyemshika mkono Olivia katika chumba cha maiti na akautambua mwili wa Edger Kaka uliokuwa umeungua na hautambuliki lakini aliugundua kutoka na mkufu wa shingoni pamoja na pete za vidoleni.Iweje leo aibuke na kudai kuwa Edger hajafa? Yawezekana mwanangu amepatwa na matatizo ya akili!! Akasema Lucy “Olivia hana tatizo lolote la kiakili mama.Amesimama katika kauli yake na anachodai ni kuwa ajali ile ni ya kutengeneza na kwamba Edger yuko mahala amefichwa.Amekwenda mbali Zaidi kwa kumtaja muhusika mkuu wa mchezo huo kuwa ni rais Dr Evans na kitendo cha kumuambukiza mwanae virusi ni ili kumshinikiza aweze kumuonyesha mahala aliko Edger Kaka.Olivia ameendelea kulisisitiza jambo hili na amedai kama rais hatamuonyesha mahala alipo Edger basi mwanae atakufa.Ili kumshinikiza Olivia aweze kufunguka na kueleza ukweli wote kuhusu mashirikiano yake na IS iliwalazimu kumteka pia baba yake Agrey Themba ili kusaidia kumfungua Olivia lakini bado haikusaidia kitu Olivia hajafunguka na bado anaendelea kusisitiza kuwa Edger hajafa na anamtaka rais amuonyeshe mahala alipo.Dr Evans ameulizwa kuhusu suala hilo akakiri hajui chochote kuhusu Edger Kaka kuwa hai.Baada ya kuendelea kusisitiza jambo hilo mkuu wa idara ya usalama wa ndani ya nchi anaitwa Devotha akaamua kuanza kulichuguza hili jambo ili kuubaini ukweli.Alianza kwa kudukua simu ya rais ili afahamu kama Rais analifahamu jambo hilo lakini hakufanikiwa na akagundulika kuwa amedukua simu ya rais hivyo akaanza kutafutwa.Ilimlazimu kufanya kila juhudi kunitoa mahala nilikokuwa nimefungiwa akisaidiwa na mwenzangu yuko nje anaitwa Gosu Gosu na katika harakati za kuniokoa Devotha amepigwa risasi na hivi sasa yuko hospitali anayapigania maisha yake.Mimi na mwenzangu tunaendelea na suala ili kuutafuta ukweli wa jambo hili analosema Olivia kuwa Edger yuko hai na vile vile kujua kwa nini Olivia anashirikiana na magaidi.Kwa hiyo mama nimekuja hapa ili kukupa taarifa hizo ujue kinachoendelea hivi sasa kuhusu mwanao” akasema Mathew.Lucy Themba akafuta machozi. “Nataka kufahamu jambo moja tu je rais anafahamu pia kuhusu kutekwa kwa mume wangu Agrey?akauliza Lucy Themba “Kila kinachofanyika katika idara hiyo ya siri ya mambo ya ndani ya nchi,Rais anakifahamu hivyo naamini hata kutekwa kwa Agrey Themba anafahamu pia” akasema Mathew “Nihakikishie mume wangu na Olivia wako salama” akasema Lucy akiendelea kufuta machozi “Mama hakuna anayefahamu hadi sasa mahala walipo Olivia na baba yake Agrey Themba lakini naamini wako salama.Mimi na mwenzangu Gosu Gosu jukumu letu ni kuwatafuta na kufahamu mahala walipo na kuufahamu ukweli wa hili jambo.Nimekuleta hapa mama kukueleza suala hili na kukuthibitishia kuwa uko salama.Ninachokuomba toka kwako ni kuniamini.Nilikuja kwenu nikawaomba ruhusa niweze kusaidia kumtafuta Olivia ukaniruhusu lakini baadae ukabadilika ukashirikiana na wale jamaa waliomteka mwanao mkaweka mtego nikatekwa.Mimi si mtu mbaya.Olivia ni rafiki yangu na mimi nina nia ya dhati ya kumtafuta.Nina uzoefu mkubwa wa mambo haya ya kiuchunguzi na ninakuhakikishia kwamba Olivia na baba yake watapatikana lakini ni pale tu utakapokuwa tayari kushirikiana nami” akasema Mathew.Lucy Themba alimuangalia Mathew kwa macho ya huruma “Mama haya yote niliyokueleza ni ukweli mtupu naomba uniamini.Bila kuunganisha nguvu hatutaweza kuwapata Olivia wala baba yake.Agrey Themba hana kosa lolote na hajui kama mwanae anashirikiana na magaidi hivyo lazima tuhakikishe tunamuokoa lakini kwa Olivia tunataka kumpata ili kufahamu kwanza kuhusu mashirikiano yake na magaidi na pili kupata uhakika wa hicho anachokisisitiza kuwa Edger Kaka you hai.Yawezekana ni kweli Edger Kaka yuko hai na yawezekana ni kweli Rais anahusika katika suala hili na kama hayo yote ni kweli basi Olivia atakuwa katika wakati mgumu sana na kuna hatari anaweza akapotezwa ili jambo hili liendelee kubaki siri.Jukumu letu ni kumuokoa Olivia na kuufahamu ukweli”akasema Mathew “Mathew nashindwa niseme nini.Ulichonieleza kimenistua mno na ulimi wangu unakuwa mzito hata kutamka chochote.Kwanza ni kuhusu mwanangu Olivia kushirikiana na magaidi na pili ni kuhusu hicho anachodai eti Edger Kaka yuko hai lakini kubwa Zaidi ni Rais kulifahamu suala hili la kutekwa Olivia.Ninatamani sana kuyaamini hayo unayoyasema Mathew lakini ninashindwa”akasema Lucy “Kitu gani kinakuwia ugumu kuniamini mama? “Yote uliyonieleza.Kwanza kuhusu Olivia kushirikiana na magaidi.Ninamfahamu vyema Olivia hawezi katu kufanya kitu kama hicho.Nimemlea katika maadili mazuri na ninarudia tena kwamba hana sababu yoyote ile ya kujiunga na magaidi kama mnavyodai.Pili ni kuhusu rais Dr Evans.Huyu ni rafiki mkubwa sana wa familia yetu na amekuwa anasaidiana nasi kwa hali na mali kumtafuta Olivia toka tukio hili lilipotokea.Anatumia uwezo wake wote katika kuhakikisha Olivia na baba yake wanapatikana.Dr Evans hawezi katu akafanya jambo kama hilo kwa familia yetu.Jambo lingine,Olivia hawezi kabisa kumfanyia Coletha jambo lolote baya.Wanapendana na wanaishi kama ndugu hivyo hawezi kabisa akamtengenezea virusi vinavyoweza kumdhuru.Olivia hana roho mbaya ya namna hiyo” akasema Lucy “Hivi sasa Coletha yuko hospitali amelazwa anaumwa.Unaweza ukalithibitisha hilo kwa muda wako lakin..” Mathew akataka kusema kitu Lucy akainuka Mathew akamtaka aketi “Ninataka kuwasiliana na rais ili kuthibitisa hilo unalolisema lakini simu yangu iko chumbani” akasema Lucy. “Mtume mtumishi wako wa ndani akuletee nataka uzungumze hapa mbele yangu” akasema Mathew na Lucy akamuita Teddy akamtuma amletee simu yake na ilipoletwa akazitafuta namba za simu za rais akampigia. “Weka sauti kubwa nataka kusikia kile mnachokizungumza” akasema Mathew “Hallow Lucy” akasema Dr Evans baada ya kupokea simu “Dr Evans samahani kwa usumbufu nimekupigia kutaka kujua maendeleo.Sijapata mrejesho wowote kutoka kwako toka asubuhi Mathew alipochukuliwa.Kuna taarifa zozote hadi hivi sasa za kuhusu Olivia na baba yake? Mathew amesema chochote?akauliza Lucy “Samahani Lucy sikuwa nimekujulisha kile kilichokuwa kinaendelea.Vijana wangu bado wanaendelea kumuhoji Mathew Mulumbi ili aweze kufunguka na kueleza kila kitu.Yule jamaa aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na ni mtu anayefahamu mbinu zote za mateso hivyo si rahisi kumfungua na kumfanya asema kila kitu lakini usihofu Lucy nitakujulisha kila pale nitakapopata taarifa kutoka kwa watu wangu.Bado juhudi za kuwatafuta Olivia na baba yake zinaendelea.Ninaendelea kuwasiliana na jeshi la polisi wamenihakikishia kwamba wamefika sehemu nzuri katika kufahamu mahala walipo Olivia na baba yake na kwa kuwa ni mapema bado siwezi kuweka wazi taarifa za kiuchunguzi ninachokuomba niamini na tuliamini jeshi la polisi wanafanya kazi nzuri sana kuhakikisha Olivia na Agrey wanapatikana wakiwa salama salimini” akasema Dr Evans “Ninashukuru sana Dr Evans kwa namna ulivyojitoa katika jambo hili.Kabla sijasahau nimepata taarifa kuwa Coletha amelazwa hospitali.Hizi ni taarifa za kweli?akauliza Lucy na swali lile likaonekana kumstua Dr Evans “Dr Evans” akaita Lucy baada ya Dr Evans kuwa kimya “Lucy ni kweli Coletha amelazwa hospitali.Samahani sikukueleza jambo hili” “Nimeshangaa sana kwa mtoto kulazwa hospitali bila kutujulisha.Nimepata taarifa hizo kutoka kwa watu wengine kabisa” “Nisamehe sana Lucy kwa kutokufahamisha” “Nini kinamsumbua Coletha?akauliza Lucy “Kulitokea tukio la moto chuoni kwao na katika harakati za kujiokoa akapoteza fahamu na toka wakati huo hajisikii vizuri ndiyo maana nikamchukua na kumpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi kufahamu nini kinachomsumbua.Lakini maendeleo yake ni mazuri” akasema Dr Evans “Nashukuru Dr Evans.Nitakwenda kumjulia hali nikipata nafasi” “Sawa Luvy lakini kesho anaweza akatoka hospitali kwa mujibu wa madaktari” akasema Dr Evans “Mpe pole sana.Usiache kunijulisha maendeleo yake vile vile kile kinachoendelea katika utafutaji wa familia yangu” akasema Lucy “Nitakujulisha Lucy” akasema Dr Evans wakaagana na kukata simu.Lucy akamtazama Mathew “Nadhani sasa umejihakikishia mwenyewe kwamba ninachokueleza ni kitu cha kweli kabisa.Coletha anaumwa yuko hospitali na kinachomsumbua ni virusi alivyoambukizwa na Olivia akishirikiana na watu wa IS.Mama ninayokueleza yote haya ni ukweli mtupu”akasema Mathew “Kidogo ninaanza kukuamini Mathew.Dr Evans amekuwa na ukaribu mkubwa sana kwetu na toka jambo hili lilipotokea amekuwa karibu kutufariji na kutuhakikishia kuwa Olivia atapatikana.Itaniumiza sana kama nikihakikisha ni yeye aliye..”akasema Lucy na kukatishwa na Mathew “Ninakuhakikishia mama rais Dr Evans anafahamu kila kitu kuhusu suala hili na anafahamu mahala walipo Olivia na baba yake.Hayo maneno ya kwamba jeshi la polisi wako karibu kuwapata ni uongo mkubwa anakupa moyo wakati anafahamu fika kuwa hawatajua mahala alipo”akasema Mathew.Lucy akafikiri kidogo na kusema “Kwa haya uliyonieleza kuna picha Fulani ninaanza kuipata.Jana usiku ulipoondoka hapa nikampigia simu rais na kumfahamisha kuwa Agrey amepotea.Nilimueleza kila kitu namna alivyotoweka na aliposikia jina lako likitajwa akasema moja kwa moja kuwa wewe unahusika katika suala hilo na kwamba lazima ukamatwe ili ueleze mahala walipo Olivia na Agrey.Ni yeye aliyewatuma watu wake wakaja kuweka mtego na kukuchukua nikiamini maneno yake kuwa unahusika na utekaji ule wa Olivia na baba yake.Maneno unayonieleza kuwa anafahamu kila kinachoendelea yameukata kabisa moyo wangu.Nimechanganyikiwa niambie nifanye nini Mathew?akauliza Lucy “Kwa sasa usifanye chochote.Nimekuja kukueleza mambo haya ili kukuweka sawa ufahamu kile kinachoendelea.Usimweleze chochote Dr Evans kwamba umefahamu yeye yuko nyuma ya haya matukio ya utekaji wa familia yako.Msikilize kila atakachokueleza.Mimi na timu yangu tunaendelea na zoezi la kuwatafuta Olivia na baba yake na tayari tuna chanzo kizuri cha kujua mahala alipo Olivia.Tukimpata Olivia itakuwa rahisi kufahamu ukweli wa kile kinachoendelea.Kama nitahitaji msaada wako wowote nitakuja kukuomba lakini nakuomba usimweleze mtu yeyote haya tuliyoyazungumza.Dr Evans akifahamu kuwa umeifahamu siri yake utakuwa katika hatari kubwa hivyo jizuie kuzungumza lolote.Narudia tena kukuhakikishia mama kuwa mimi na wenzangu tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunafahamu mahala waliko Olivia na mzee Agrey” akasema Mathew “Mathew sijui nikwambie nini baba lakini naomba samahani sana kwa kile nilichokufanyia kijana wangu.Niliaminishwa na Dr Evans kwamba wewe ni mtu mbaya na kwamba ndiye unayehusika na matukio yote ya kutekwa kwa Olivia na Agrey.Nilifanya makosa makubwa sana kuamini taarifa hizi.Nisamehe sana.Bila wewe nisingeyafahamu haya yote.Ahsante kwa kuja kunieleza siri hii uliyoifahamu” akasema Lucy “Mama usijali.Kila kitu huongozwa na Mungu.Kama nisingetekwa tusingeifahamu siri hii.Narudia tena kukuomba mama usimueleze mtu yeyote hili jambo hadi hapo tutakapokuwa tumewapata Olivia na Agrey”akasema Mathew “Mathew nawaombea Mungu awatangulie muweze kuwapata Olivia na mume wangu Agrey.Chochote mnachokihitaji nielezeni nitawapatia” akasema Lucy “Ninashukuru mama kama kuna msaada nitahitaji kutoka kwako nitakujulisha.Narudia kukuomba mama Jambo hili ni siri kubwa asifahamu mtu mwingine yeyote.Hata unapotaka kuwasiliana name usitumie simu yako ya kawaida naamini watakuwa wanafuatilia simu zako.Tafuta simu nyingine na utawasiliana nami kupitia namba hizi za simu” akasema Mathew na kumpatia Lucy namba za simu anazotumia kisha akainuka kwa ajili ya kuondoka “Mama kabla sijasahau kuna mlinzi wako mmoja amejeruhiwa mkononi katika harakati za kutaka kuingia hapa ndani naomba atibiwe na uwaonye wasiseme chochote kwa mtu yeyote kuhusu mimi kuja hapa” Mathew akamuelekeza Lucy “Nitafanya hivyo Mathew” akasema Lucy akaongozana na Mathew hadi lilipo gari lao wakaagana na kuondoka zao. “Maneno ya Mathew kuhusu Dr Evans kufahamu kutekwa kwa Olivia na Agrey ninaweza kuyakubali.Amekuwa mstari wa mbele sana kutupa moyo na kutuhakikishia kuwa Olivia atapatikana tusihofu hata alipopotea Agrey amekuwa karibu nami sana kunifariji na kunihakikishia kuwa watapatikana.Sikutegemea kama Dr Evans anaweza akatufanyia hivi.Sisi tumekuwa ni kama n dugu zake iweje atutese namna hii? Nimemchukia ghafla kwa hili alilotufanyia.Natamani hata sasa nimpigie simu nimjulishe tayari ninafahamu kila kitu anachotufanyia lakini Mathew ameniomba sana nisimueleze chochote Rais ili nimpe nafasi ya kuweza kuwatafuta Olivia na Agrey” akawaza Lucy na kuhisi baridi pale alipoyakumbuka maneno ya Dr Evans namna alivyokuwa akiwapa moyo “Nilifanya makosa makubwa kumuamini Dr Evans aliponidanganya kuhusu Mathew.Alisisitiza Mathew lazima akamatwe kwa sababu alijua tayari anafahamu nani waliomteka Olivia na angeweza kuvuruga mipango yao.Ninahisi yawezekana Agrey aliwasiliana naye akamjulisha kuhusu Mathew kufahamu mahala alipo Olivia na ndiyo maana Olivia akahamishwa mahala alipokuwa amefichwa.Evans ametufanyia kitu kibaya mno ambacho sikukitegemea kabisa..”Lucy akastuka kama mtu aliyekuwa ndotoni baada ya kukumbuka kitu “Mathew anadai Olivia anashirikiana na magaidi wa IS.Hii taarifa bado kidogo inipasue moyo wangu.Mwanangu Olivia anashirikiana na magaidi?!! Kama ni kweli kitu gani kimemuingia na kumfanya aamue kufanya kitu kama hiki?Amekosa nini Olivia hadi akaamua kujiunga na magaidi?Balaa gani hili anatuletea katika familia yetu?akajiuliza Lucy na kumtafakari Olivia kiundani. “Hapana siamini kama Olivia wangu amebadilika na kuwa gaidi.Nakubaliana na Mathew kwamba uchunguzi ufanyike ili tuufahamu ukweli wa hili jambo” Lucy alihisi kuchanganyikiwa akaenda chumbani kwake
“Nilikueleza kilichotokea jana nilipokwenda kumuokoa Olivia” Mathew akamwambia Gosu Gosu walipoondoka nyumbani kwa Lucy “Ndiyo ulinieleza” akasema Gosu Gosu “Baada ya kumkosa Olivia na kutekwa kwa Agrey Themba niliamini kuna mtu mwenye ukaribu na familia ya akina Olivia ambaye anashirikiana na watekaji na leo nimepata jibu kuwa ni rais Dr Evans.Yeye na Agrey Themba ni marafiki wakubwa na walikuwa wanamshirikisha kila kinachoendelea.Jana usiku walimjulisha kuhusu mimi kufahamu mahala alipo Olivia na mipango yangu ya kwenda kumuokoa bila kujua kama anafahamu kila kitu.Rais aliwasiliana na watu wake wa idara ya usalama wa ndani ya nchi waliokuwa wamemteka Olivia na wakamuondoa Olivia haraka sana kabla sijafika na nilipofika nikaambulia patupu.Ninaanza kuyaamini maneno aliyosema Olivia kuwa Edger kaka hajafa na kwamba Dr Evans anahusika katika suala hili na anafahamu mahala alipo” Akasema Mathew na kumueleza Gosu Gosu kila kitu alichozungumza na Lucy Themba “Tuliweke pembeni hilo la Edger Kaka na tushughulikie kwanza kumpata Olivia ambaye ndiye mwenye ukweli wote.Kwa kuwa tunao muda mchache kabla Ruby hajawasili tupite madukani tununue vifaa alivyoelekeza nimuandalie kwa ajili ya kufanyia kazi yake” akasema Mathew “Inaumiza sana kwa familia ya Olivia kugundua kwamba rais ambaye ni mtu wao wa karibu analifahamu suala hili la utekaji na amekuwa akiwadanganya”akasema Gosu Gosu “Inaumiza sana.Nilimuona namna Lucy alivyostuka alipofahamu kuwa rais anafahamu kila kitu kuhusu kutekwa kwa Olivia na baba yake” “Una hakika hawezi akaharibu mambo yule mama?akauliza Gosu Gosu “Hapana hataweza kuharibu kitu kwani tumani pekee la kuwapata Olivia na mume wake liko kwangu hivyo atafuata maelekezo yote nitakayompa” akasema Mathew
Baada ya kumaliza kuzungumza na Lucy Themba simuni,Dr Evans akasimama na kushika kiuno “Mambo yanazidi kuwa magumu.Nilitegemea hadi muda huu Mathew awe amekwisha funguka na tujue kila kitu kinachoendelea kuhusu mipango ya IS lakini ametoroshwa na hajulikani alipo.Alikuwa ni mtu muhimu sana kwetu.Devotha amefanya kitu kibaya mno kuamua kumtorosha Mathew.Nguvu kubwa kwa sasa ni kuielekeza kwa Olivia.Kama bado ataendelea kuwa mgumu nitaagiza hata mama yake naye achukuliwe aunganishwe na baba yake.Akiwaona wazazi wake wanavyopata mateso atafunguka” akawaza Dr Evans akachukua simu na kumpigia Dr Mbeula ikiwa ni mara ya tatu kumpigia toka asubuhi “Mheshimia rais” akasema Dr Mbeula “Dr Mbeula nataka kufahamu maendeleo ya mwanangu.Kuna hatua yoyote mmepiga hadi hivi sasa?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais tumeendelea na zoezi la kuvifahamu kwa undani virusi hivi ili tuone namna ya kuvikabili lakini kadiri muda unavyokwenda ndivyo tunavyozidi kugundua mambo mengine Zaidi kuhusu virusi hivi.Kwanza kabisa virusi hivi vina tabia ya kujibadili umbo.Kila vinapokutana na dawa au kemikali aina Fulani hujibadili umbo lake. Hivyo inatupa ugumu kupata dawa ya kupambana navyo.Pili virusi hawa wakiingia katika mwili wa binadamu wanatengeneza kemikali ambayo inaua kinga ya mwili.Mhes….” “Dr Mbeula samahani kwa kukukatisha” Rais akasema “Endelea mheshimiwa rais” “Ninachotaka kusikia kutoka kwako ni kama uwezo wa kupambana na virusi hivyo mnao.Kama unadhani hamna uwezo nijulishe haraka ili nimpeleke mwanangu nje ya nchi kwa matibabu Zaidi kabla hali yake haijawa mbaya” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais kwa namna tunavyoendelea na zoezi letu nina uhakika mkubwa tutafanikiwa kuwafahamu vyema virusi hawa na kupambana nao lakini haitakuwa kwa haraka” “Una uhakika mtafanikiwa Dr Mbeula? “Ndiyo mheshimiwa rais ninao uhakika.Naomba uniamini”akajibu Dr Mbeula “Vipi hali ya Coletha hivi sasa anaendeleaje?akauliza Dr Evans “Hali yake inandelea vyema mheshimiwa rais” “Sawa Dr Mbeula.Nitakuja baadae jioni kumjulia hali mgonjwa.Naombeni mjitahidi sana” akasema Dr Evans “Tunajitahidi mheshimiwa rais lakini bado kuna kitu nataka kukifahamu” akasema Dr Mbeula. “Kitu gani Dr Mbeula? akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais ninataka kujua kama unafahamu kitu chochote kuhusiana na virusi hivi.Ninataka kufahamu chanzo chake na kama kuna wagonjwa wengine ambao wameambukizwa virusi hivi” akasema Dr Mbeula. “Dr Mbeula kwa sasa jielekezeni katika kutafuta ufumbuzi wa kupambana na virusi hao.Hayo masuala mengine achana nayo kwanza”akasema Dr Evans wakaagana “Olivia ! Olivia !! akasema Dr Evans kwa hasira “Ni Olivia aliyesababisa haya yote.Kwa nini lakini akanifanyia kitendo cha kikatili namna hii?Kwa nini anataka kumuangamiza mwanangu? Nimemkosea nini hadi akaamua kunifanyia hivi?Atapata faida gani kama Coletha akipoteza maisha? Ninaapa kama mwanangu Coletha akifariki dunia nitaiteketeza familia yake yote bila kujali kama ni marafiki zangu.Mwanangu hawezi kupoteza maisha bila hatia halafu nikae kimya!! Akawaza Dr Evans na kumpigia simu Kaiza “Mheshimiwa rais”akasema Kaiza “Kaiza nipe habari.Nini kinaendelea mpaka sasa?akauliza Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa rais tunaendelea kumtafuta Devotha na tulifanikiwa kumfahamu mtu ambaye angetupa taarifa muhimu za kuweza kumpata Devotha lakini kwa bahati mbaya tumempoteza” “Mmempoteza?! Dr Evans akashangaa “Tumempoteza mheshimiwa rais.Aliwahi kujirusha ghorofani kabla hatujamkamata akafariki dunia.Hivi sasa vijana wanaendelea kupitia kompyuta yake na ili kufahamu kama wanaweza wakapata kitu chochote kitakachopelekea kumpata Devotha.Kwa sasa nimefika hapa mahala alipo Olivia ninataka kuendelea na mahojiano naye”akasema Kaiza “Kaiza tafadhali hakikisha Olivia anafunguka na anasema kila kitu.Ninakupa huu ni mtihani wako wa mwisho ukishindwa kumfungua nitatafuta watu wengine wanaoweza kuifanya hiyo kazi” akasema Dr Evans “Nitajitahidi kufanya kila niwezalo kuhakikisha tunapata kila taarifa kutoka kwa Olivia” akasema Kaiza na rais akakata simu kwa hasira “Rais amepoteza kabisa Imani na sisi kwa sababu ya Olivia.Nikishindwa katika hili hataniamini tena na aligusia hata kuifutilia mbali idara yetu.Natakiwa kumfanya atuamini tena na hii itawezekana kama tukimfungua Olivia” akawaza Kaiza wakati akishuka ndani ya gari. NAIROBI KENYA Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia iliwasili katika uwanja wa ndeje wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi ikitokea Tel aviv Israel kupitia Adis Abbaba Ethiopia.Miongoni mwa abiria wawili waliokuja na ndege hii ni majasusi wawili wa shirika la ujasusi la Israel Mossad,Fishel na Ehud ambao walitumwa nchini Kenya kwa kazi maalum. Siku tatu zilizopita roketi lililorushwa na wanamgambo wa kipalestina wakishirikiana na kikundi cha Islamic state lilitua katika shule ya chekechea na kusababisha vifo vya watoto kumi na mbili.Shambulio hilo lililolaaniwa kila kona ya dunia lilimpelekea waziri mkuu wa Israel aitishe kikao cha dharura na wakuu wa shirika la ujasusi la Israel Mossad.Katika kikao hicho waziri mkuu alitaka kufahamu namna Mossad walivyojipanga kuwamakata viongozi wakuu wa kikundi cha IS ambacho kinashirikiana na vikundi vingine vya wanamgambo wa kipalestimna kuendesha mashambulizi katika ardhi ya Israel na kuua watu. Mkurugenzi mkuu wa Mossad alimueleza waziri mkuu mikakati ya Mossad kuwa ni kuwapata wafadhili wakuu wa vikundi vile ambao ni Habiba Jawad na Sayid Omar.Alimpa taarifa za kuwepo kwa mtu wanayemshikilia katika sehemu ya siri nchini Kenya anaitwa Edger Kaka ambaye ana mahusiano na watu hao wawili wanaowatafuta sana.Alimkumbusha kuhusu operesheni iliyofanyika nchini Tanzania na Edger akatekwa. “Baada ya kumteka nchini Tanzania tulimpeleka Kenya ambako tumemuhifadhi kwa miaka mitatu sasa.Aliwahi kuhojiwa na kutoa taarifa chache lakini hazikusaidia kuwapata Habiba Jawad na Sayid Omar ambao wameendelea kufadhili vikundi vya kigaidi vinavyoendeleza mauaji dhidi ya waisrael.Tuliamua kumuacha kwa muda mrefu bila kumuhoji huku akiishi katika mateso na upweke mkubwa ndani ya chumba chenye giza na mateso mengine ya kumuumiza kiakili ili kumfanya awe tayari kutupa taarifa zote za kuwahusu Habiba na Sayid pale tutakapoamua kumuhoji.Naamini sasa ni muda muafaka wa kumuhoji.Kwa mateso aliyoyapata kwa miaka mitatu atakuwa tayari kuzungumza.”akasema mkuu wa Mossad Baada ya kikao kile ndipo Fishel na Ehud wakatumwa nchini Kenya kumfanyia mahojiano Edger Kaka na kuhakikisha anaeleza kila kitu. Katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta majasusi hao walipokewa na afisa kutoka ubalozi wa Israel nchini Kenya wakaelekea moja kwa moja katika hoteli walikoandaliwa kufikia.Kutoka hotelini wakachukuliwa na kupelekwa hadi katika ubalozi wa Israel nchini Kenya ambako Mossad walikuwa na ofisi zao. “Karibuni sana Nairobi,karibuni sana Afrika”akasema Avi mkuu wa Mossad Afrika mashariki “Tunashukuru sana tumekaribia” akasema Ehud “Nini kinachoendelea hapa kuhusu Edger Kaka?akauliza Fishel “Edger yuko hapa ubalozini kwa muda wa miaka mitatu sasa na kwa muda huo ameendelea kuishi katika mateso bila kufanyiwa mahojiano yoyote.Tumekuwa tunamtesa kisaikolojia ili pale tutakapoanza kumuhoji awe ameteseka vya kutosha na aeleze kila kitu.Watu kama hawa wenye mahusiano na magaidi kwa kawaida wanakuwa wagumu mno kufunguka na kutoa siri hivyo mateso kama haya huwafanya wawe tayari kusema kila kitu” akasema Avi na kuwasha runinga na mtu mmoja aliyekuwa mtupu akiwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni amelala katika sakafu yenye baridi akaonekana. “Yule ndiye Edger Kaka”Akasema Avi “Haya ndiyo mateso ambayo amekuwa akipewa kwa miaka mitatu sasa.Amekuwa akipewa chakula mara moja kwa siku.Chumba alimo kuna baridi na amekuwa akiishi hivyo bila mavazi yoyote.Kikubwa ambacho tumekuwa tunakiwekea mkazo mkubwa ni kuhakikisha hapati magonjwa yoyote.Kila siku daktari humkagua kujiridhisha na maendeleo yake.Anaonekana dhaifu lakini hana tatizo lolote la kiafya” akasema Avi Edger kaka alikuwa amejikunyata katika pembe akiwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni.Alikuwa mtupu kabisa Alitia huruma sana.Alikuwa ameota ndevu nyingi na haikuwa rahisi kutambulika kwa haraka.Ehud akamtazama kwa makini na kusema “Kwa namna anavyoonekana tayari amekwisha kata tamaa” “Hatua ya kwanza tunayoanza nayo ni kumtoa katika mateso aliyonayo sasa na kumuweka katika maisha mazuri.Anatakiwa anyolewe nywele na ndevu aogeshwe na avishwe mavazi mengine mapya.Baada ya hapo tutaendelea na hatua inayofuata.Kitu kingine kabla ya kuanza kumuhoji Edger tunatakiwa kuifahamu historia yake alikokotoka hadi hapa alipofika.Naamini kwa muda huu mrefu mtakuwa mmekusanya taarifa za kutosha za kumuhusu” akasema Ehud na Avi akapiga simu akaomba kutumiwa faili la Edger Kaka katika ile ofisi alimokuwemo.Baada ya sekunde chache faili likatumwa akatoka akawaacha akina Ehud wakiendelea kupitia taarifa zilizokuwa zimekusanywa kuhusu Edger. “Taarifa yake ni nzuri haina hata chembe ya mashaka.Ni mbunge aliyependwa sana,amekuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi.Ni mbunge aliyejizoea umaarufu mkubwa sana na ni mmoja wa wanasiasa vijana waliokuwa wanatajwa kufaa kushika nafasi ya urais.Imetokeaje mtu kama huyu akajiunga na kikundi cha ugaidi?akauliza Fishel “Hata mimi inanishangaza.Sikujua kama alikuwa mtu maarufu nchini mwao kiasi cha watu kumtaja hata kushika nafasi ya urais” akasema Ehud Edger Kaka alifunguliwa minyororo akatolewa katika kile chumba,hakuweza kutembea akabebwa na kupelekwa bafuni akaogeshwa akanyolewa nywele na ndevu halafu akavishwa mavazi mengine mapya.Ngozi yake ambao haikuonja hata tone la mafuta kwa muda wa miaka mitatu ilikuwa imekakamaa hakuwa Edger yule mtanashati.Alibadilika mno.Hakuweza kutembea akawekwa katika kiti cha magurudumu akasukumwa hadi katika chumba kimoja kulikoandaliwa chakula kizuri.Harufu nzuri ya vyakula vilivyoandalia ilimsisimua sana Edger ambaye hakuwa ameisikia harufu nzuri kama ile kwa muda mrefu.Alihisi njaa kali alitamani akivamie chakula kile akimalize chote lakini mwili wake haukuwa na nguvu.Baada ya dakika tatu wakaingia watu wawili wakakaa mezani na Edger akasogezwa karibu na meza akashushwa kutoka katika kiti kile cha magurudumu na kuweka katika kiti cha kulia chakula.Mikono ilikuwa inamtetemeka alipoona chakula kile kizuri. “Edger karibu chakula,tumia kadiri uwezavyo” akasema Fishel na kumsogezea Edger sahani na kumpakulia uji mzuri katika bakuli.Edger akajaribu kushika kijiko akashindwa.Mikono haikuwa na nguvu.Fishel akasohgeza kiti akakaa karibu yake akamnywesha uji ule hadi bakuli lilipomalizika.Taratibu Edger akaanza kuhisi mikono inapata nguvu akaomba tena chakula kingine.Fishel akampakulia chakula akaendelea kumlisha sambamba na kumnywesha kinywaji.Edger hakuamini kama amekula tena chakula kile kizuri ambacho hakuwa na matumaini ya kukiweka tena katika ulimi wake.Hakutaka kuacha alitaka aendelee kula lakini Fishel akamzuia akamtaka apumzike kwanza.Edger akatolewa katika kile chumba cha chakula akapelekwa katika chumba kingine kizuri chenye kitanda kikubwa na godoro zuri.Machozi yalimtoka alipobebwa kutoka kwenye kiti na kukalishwa kitandani. “Siamini kama nimeweza tena kulala katika godoro zuri kubwa na laini.Sifahamu ni kwa muda gani nimekaa katika kile chumba chenye giza lakini naamini ni muda mrefu.Nimeteseka na kulala mtupu katika sakafu yenye baridi nikiteseka kwa njaa na kiu.Nini kimetokea leo hadi wakanitendea hivi?akajiuliza Edger akiendelea kutiririkwa na machozi.Taratibu akahisi macho mazito na haukupita muda akapitiwa na usingizi akalala “Nimemtazama machoni anaonekana wazi amechoka na mateso aliyoyapata.Hakuamini alipoweka tena mdomoni chakula kizuri.Naamini tutakapoanza kumuhoji atakuwa tayari kusema kila kitu” akasema Ehud “Ni mateso makubwa sana miaka mitatu kukaa ndani ya chumba chenye giza huoni mwangaza wa jua.Naamini hatakubali tena kurejea katika mateso yale” akasema Fishel. Edger aliachwa apumzike katika kitanda kile kikubwa akaamshwa na kupelekwa katika chumba kingine ambamo walikuwemo Fishel na Ehud “Edger Karibu.Tumekutana tena.Unajisikiaje?akauliza Fishel “Kwa sasa ninahisi nguvu kidogo” akasema Edger kwa sauti dhaifu ambayo haikuwa inasikika vyema. “Edger mimi na mwenzangu tuna mazungumzo kidogo nawe lakini kabla ya kuzungumza nataka upumzike kwa dakika kumi.Wakati ukipumzika tunataka uangalie filamu hii halafu tutarudi kuzungumza” akasema Fishel.Edger akashushwa kutoka katika kile kiti cha magurudumu akakalishwa sofani.Fishel na Ehud wakatoka wakamuacha peke yake.Baada ya dakika tano toka Fishel na Ehud watoke mle chumbani akaingia mtu mmoja akamfunga Edger kifaa Fulani mkononi halafu akawasha runinga kisha akatoka akamuacha Edger peke yake ndani ya chumba. “Ifuatayo ni historia fupi ya mbunge Edger Kaka aliyefariki katika ajali ya gari siku mbili zilizopita” Ndivyo ilivyoanza taarifa ile na kumstua mno Edger.Alitamani kunyanyuka lakini miguu haikuwa na nguvu.Akabaki anashuhudia picha zake mbali mbali zikionyeshwa zilizoambatana na historia yake.Mdomo ulibaki wazi akishangaa Wakati Edger akiendelea kutazama taarifa ile iliyohusiana na kifo na mazishi yake Fishel na Ehud walikuwa katika ofisi yao wakimfuatilia Edger kwa makini kupitia kamera.Pamoja nao alikuwepo mtu mwingine aliyekuwa katika kompyuta akiangalia grafu iliyokuwa inapanda na kushuka “Ameonyesha mstuko mkubwa sana baada ya taarifa kuanza.Inaonyesha hafahamu chochote kilichotokea.Hajui kama alikwisha fariki na kuzikwa” akasema yule jamaa aliyekuwa anafuatilia chati ile katika kompyuta.Wakati Edger akiendelea kutazama rekodi ile runingani akionekana kuchanganyikiwa mara akapatwa na mstuko mkubwa baada ya kumuona mwanadada mmoja akiwa amevaa gauni refu jeusi na kilemba cheusi kichwani na macho yake aliyafunika kwa miwani mikubwa akiwa amesimama katika mimbari akisoma historia ya Edger Kaka.Alishindwa kumalizia aya ya mwisho akaangua kilio akatokea mwanamke mmoja na kwenda kumshika mkono akamrejesha kitini kuketi. “Olivia !! akasema Edger Kaka akiwa ameyatumbua macho.Alipatwa na mstuko mkubwa sana “Huyu mwanamke ni nani?akauliza Fishel “Huyu ni daktari wake anaitwa Olivia Themba.Ndiye aliyekuwa naye nchini Israel”akajibu yule jamaa aliyekuwa anafuatilia grafu “Edger amestuka mno baada ya kumuona Olivia.Grafu imepanda hadi kupita kile kiwango chake cha kawaida.Kwa mstuko huu lazima Olivia ni mtu muhimu sana kwake”akasema yule jamaa.Ehud na Fishel waliendelea kumtazama Edger mara wakastuka baada ya Edger kuanguka chini.Walisubiri kwa dakika mbili kama atainuka lakini aliendelea kulala pale chini.Haraka haraka wakatoka mbio na kwenda katika chumba alimo Edger na kumkuta amepoteza fahamu.Wakamtoa ndani ya kile chumba na kumuingiza katika chumba kingine daktari akaitwa akafika haraka na kumpima na akawatoa wasiwasi kwamba Edger hakuwa na tatizo bali alipoteza fahamu kutokana na mstuko. “Ni mstuko uliopelekea akapoteza fahamu lakini hana tatizo lolote”akasema daktari. Edger aliachwa katika chumba chenye hewa ya kutosha hadi alipozinduka.Baada ya kuzinduka akaachwa kwa muda wa robo saa halafu akapelekwa tena katika chumba kingine walimo Fishel na Ehud “Edger pole sana kwa kilichotokea” akasema Fishel aliyezungumza kwa upole mkubwa “Ninyi ni watu wakatili sana.Kwa nini mmenifanyia hivi? Kwa nini mmenionyesha video ile?akauliza Edger machozi yakimtoka.Bado sauti yake ilikuwa dhaifu sana “Jina lako nani?akauliza Fishel “Naitwa Edger Kaka” “Edger unatokea wapi? “Mimi ni mtanzania” “Hapa ulipo unafahamu ni wapi? “Sifahamu niko wapi.Maisha yangu yamekuwa katika chumba chenye giza nikisubiri Mungu aichukue roho yangu lakini naye ameniacha nikiteseka hataki kunichukua” akasema Edger akionekana kukata tamaa kabisa na maisha yake “Siku 1095,saa 26280 ndizo ulizokaa humu ndani ambazo ni sawa na miaka mitatu.Najua hufahamu muda ambao umekaa ndani ya kile chumba lakini ni miaka mitatu sasa.Hiki ni kipindi kirefu,mambo mengi yamefanyika duniani.Binadamu wa kwanza ametua katika sayari ya Mars.Chaguzi nyingi zimefanyika katika nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania.Kikubwa kuliko yote ulifariki ukazikwa na tayari jina lako limesahaulika limebaki katika kumbu kumbu kwamba aliwahi kutokea mtu anaitwa Edger Kaka” akasema Ehud “Mimi sijafariki bado niko hai.Kilichoonekana katika filamu ile ni uongo mkubwa.Mimi niko hai” akasema Edger “Video ile uliyoitazama muda mfupi uliopita ambayo imesababisha ukapoteza fahamu imekuonyesha kila kitu kwamba tayari umefariki dunia na tayari umezikwa.Umeyaona mazishi yako namna watu walivyohuzunika kwa kifo chako.Wengi walivaa fulana zenye jina lako wakikulilia,wakipita mbele ya jeneza lako wakitoa salamu za mwisho.Edger wewe tayari umekwisha fariki”akasisitiza Ehud “Nashindwa kuwaelewa.Kwa nini mnanisisitiza kwamba nimekufa wakati niko hai? Mimi niko hai sijafa ! Mimi ni binadamu si mzimu.Nini kimefanyika hadi nionekane nimekufa?akauliza Edger “Edger tayari umekufa.Naomba nikukumbushe namna ulivyopoteza maisha.Ulikuwa unaelekea nyumbani kwako ukitokea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Ulikuwa umerejea nchini kwako kutokea Israel ulikoenda kwa matibabu.Muda mfupi baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere msafara wako ulipata ajali.Tayari umepata picha ya kilichotokea?akauliza Fishel.Edger akabaki kimya “Edger unakumbuka chochote kuhusiana na ajali ile?akauliza Ehud “Ndiyo nimekumbuka kila kitu na kitu cha mwisho ninachokumbuka ni kishindo kikubwa na kukawa kiza kinene.Sifahamu kama ilikuwa ni ajali au nini lakini nilipokuja kupata fahamu nilijikuta katika chumba chenye giza nikiwa nimefungwa minyororo na watu wakaanza kunihoji kuhusu kikundi cha IS.Nimeshangaa kuona video ile watu wakinililia eti nimekufa.Nimestuka sana sikutegemea kitu kama hiki ndiyo maana nikapoteza fahamu.Nini kiliwekwa ndani ya lile sanduku ili kuwaaminisha watu kuwa nimekufa”akauliza Edger “Edger ulifariki usiku ule na tayari umekwisha zikwa na hili hapa ni kaburi lako” akasema Ehud akatoa picha katika faili akamuonyesha Edger akaitazama huku mikono ikimtetemeka “Haya mambo nashindwa kuyaelewa.Kwa nini nimefanyiwa hivi?kwa nini mmeniteka na kunizushia kifo wakati niko hai?Mwili ule ambao ulizikwa ndani ya jeneza linalodaiwa ni la kwangui ni mwili wa nani?akauliza Edger “Sikiliza Edger.Katika siku 1095 waisrael 59 wamepoteza maisha.Kumekuwa na urushwaji wa maroketi kutokea upande wa Palestina kunakofanywa na vikundi vya wanamgambo wa kipalestina wakisaidiwa na kikundi cha kigaidi cha IS.Siku tatu zilizopita roketi limerushwa na kutua katika shule ya watoto wadogo na kuua idadi kubwa ya watoto.Matendo kama haya ya kikatili yanayofanywa na wanamgambo wa kipalestina wakisaidiwa na kikundi cha kigaidi cha IS yameendelea kushika kasi kutokana vikundi hivi kuwezeshwa kwa fedha na silaha hivyo kuwa na uwezo wa kujipanga na kufanya mashambulio katika ardhi ya Israel.Baada ya uchunguzi wa kina imebainika kwamba mfadhili mkubwa wa vikundi hivi anaitwa Habiba Jawad.Huyu ni mwanamke tajiri.Aliwahi kuolewa na mwanaume tajiri ambaye alikuwa na asili ya Palestina na aliutumia utajiri wake kufadhili makundi ya wanamgambo kuua waisrael na ndipo vikosi vya Israel vilipompiga risasi akafariki.Habiba Jawad alirithi utajiri wa mumewe na akaendelea kufadhili vikundi vya kigaidi.Ili asigundulike kuwa ni yeye anayefadhili vikundi hivi anamtumia mtu anaitwa Sayid Omar.Kwa muda mrefu Habiba na Sayid wamekuwa wakitafutwa sana na serikali ya Israel lakini hawajapatikana hadi sasa.Wamekuwa wakisaidiwa na serikali ya Saudi Arabia kujificha” Fishel akasema na kumtazama Edger kwa muda halafu akaendelea “Ukiwa hospitalini nchini Israel ulitembelewa na watu wawili ambao ni Habiba Jawad na Sayid Omar ukaonana nao mkazungumza.Kitendo cha Habiba Jawad na Sayid Omar kuhatarisha maisha yao kwa kuingia katika ardhi ya Israel wanakotafutwa sana kwa lengo moja tu la kuja kuonana nawe ni kiashiria tosha kuwa wewe ni mtu muhimu sana kwao.Ukaribu wako na Habiba na Sayid unakufanya uwe mtu wetu muhimu sana ndiyo maana uko hapa kwa miaka mitatu sasa na yawezekana ukaendelea kuishi hapa kwa miaka mingi Zaidi yawezekana hadi mwisho wa uhai wako kwani katika ulimwengu wa kawaida tayari umefariki,umezikwa na umesahaulika.Jina lako limebaki historia.Hakuna anayekutafuta tena.Tumekuacha kwa miaka mitatu bila kukuuliza chochote ili kukuonyesha kwamba tunaweza kukuacha ukateseka hadi siku utakapopoteza maisha yako.Siku ya leo tumekutoa katika chumba cha giza na tumekurejesha katika maisha ya kawaida japo kwa muda mfupi kukumbusha kwamba unayo nafasi ya kurejea katika maisha yako ya kawaida.Bado unayo nafasi Edger ni juu yako kuitumia”Fishel akanyamaza tena akamtazama na kusema “Edger historia yako inaonyesha wewe uliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ukiwa ni mbunge mwenye umaarufu mkubwa.Ulikuwa kinara wa kupambana na ufisadi na kutokana na juhudi zako katika kuwapigania na kuwasemea wanyonge walianza kukutaja kuwa ni mmoja wa watu wanaofaa hata kupewa nafasi ya kuongoza nchi.Nyota yako tayari ilikwisha anza kung’ara lakini hukuweza kutimiza malengo yako na ukajikuta mahala hapa ambako kumezima ndoto zako zote.Edger tumekufungulia dirisha dogo ambalo unaweza ukalitumia kutoka na kurejea katika maisha yako ya awali.Uchaguzi ni wako mwenyewe kama utoke kupitia nafasi hii uliyoipata au uendelee kubaki hapa kwa maisha yako yote ukiendelea kuteseka hadi pale roho yako itakapokutoka.Kipi unakichagua?Kutoka au kuendelea kukaa katika chumba kile cha giza?Kumbuka hakuna mtu yeyote anayefahamu kuwa uko hai au uko hapa hivyo mwenye kuamua hatima ya maisha yako ni wewe mwenyewe” akasema Fishel.Edger akainamisha kichwa akatafakari kwa muda halafu akasema “Nimechoka na mateso haya.Mmenitesa vya kutosha sitaki kurejea tena katika kile chumba.Niambieni nini mnakitaka ili kuniondoa katika mateso haya na kunirejeshea maisha yangu ya uhuru?akauliza Edger “Umefanya uchaguzi mzuri.Huo ni uamuzi wa busara sana.Nataka unijibu unawafahamu Habiba Jawad na Sayid Omar? Akauliza Ehud “Ndiyo ninawafahamu” akajibu Edger “Tunataka utupe taarifa ambazo zitatusaidia kuwapata watu hawa wawili.Habiba Jawad na Sayid Omar wanaendelea kufadhili vikundi vya wanamgambo wa kipalestina ambao wanafanya mauaji dhidi ya waisrael.Ni hilo tu ambalo tunalihitaji na kama ukitusaidia tukawapata watu hao nakuhakikishia kwamba tutakurejeshea maisha yako.Tutakuachia huru na tutakupa pia ulinzi mkubwa pamoja na kukupeleka ukaishi mahala ambako utakuwa salama salimini na utaendesha maisha yako kimya kimya.Uko tayari kutueleza ukweli?akauliza Fishel.Edger akavuta pumzi ndefu akainamisha kichwa akazama mawazoni.Fishel na Ehud wakamuacha atafakari.Zilipita dakika tatu Edger akainua kichwa na kusema “Nimekaa katika chumba cha giza kwa miaka mitatu na sielewi chochote kinachoendelea huko duniani hivyo ni ngumu sana kwangu kujua mahala waliko Habiba Jawad au Sayid” akasema Edger “Wote wawili walikuja kukutembelea hospitali nchini Israel.Una mahusiano gani nao?akauliza Ehud “Sina mahusiano yoyote nao” akajibu Edger “Kama huna mhusiano nao kwa nini walikuja kukutembelea hospitali mara mbili?akauliza Fishel “Sikuwa nikifahamiana na Habiba au Sayid Omar hadi walipokuja kunitembelea hospitali.Kilichowaleta hospitali walitaka niwasaidie kufanikisha mradi wao wa kuanzisha kampuni ya mafuta nchini Tanzania” “Habiba Jawad na Sayid ni watu ambao wanatafutwa na serikali ya Israel lakini hawakuhofia usalama wao na wakaingia Israel kwa sababu moja tu ya kuja kukuona hospitali.kwa nini wewe na asiwe mtu mwingine?akauliza Fishel “Walipataje taarifa za wewe kulazwa hospitali Israel? akauliza Ehud “Sifahamu walipataje taarifa zangu na sielewi kwa nini walinichagua mimi” akajibu Edger “Edger hiki unachokieleza tunajua ni uongo mtupu.Tunajua unawafahamu vyema Habiba na Sayid na hospitali pale haikuwa mara ya kwanza kuonana.Edger tambua hapa tunazungumzia maisha ya waisrael wanaoendelea kuuawa kila siku,maisha ya wapalestina ambao wanaendelea kuuawa kutokana na vurugu zinazosababishwa na wanamgambo wa kipalestina wanaofadhiliwa na akina Habiba.Vile vile tunazungumzia hatima ya maisha yako.Najua unafahamu kila kitu kuhusu Habiba na Sayid lakini unaogopa kusema.Nakuhakikishia Edger unakosea sana kwani hao unaojaribu kuwaficha hawana msaada tena kwako.Tayari wanajua umefariki na wamekwisha kusahau.Hakuna ambaye atakusaidia kukuondoa mahala hapa.Hatima ya maisha yako utaiamua wewe mwenyewe.Tupe kile tunachokitaka tuokoe maisha ya watu wetu na sisi tukurejeshee maisha yako mazuri.Tunajua kile utakachotueleza kina gharama hivyo tuko tayari kutoa malipo ambayo ni kukusaidia kuanza maisha mapya.Hii ni nafasi pekee umeipata na hautaipata tena nafasi nyingine kama hii hivyo ukishindwa kuamua leo utarudishwa tena katika kile chumba na huo utakuwa ni mwisho wako” akasema Fishel “Sipendi kukaa katika chumba kile nimechoka na mateso haya ninayoyapata lakini sina chochote cha kuwaeleza kuhusu Habiba au Sayid Omar.Nilichowaeleza ni ukweli mtupu siwafahamu watu hawa na mara yangu ya kwanza kukutana nao ilikuwa ni hospitali kabla ya hapo sikuwahi kuonana nao.Tulipanga kuwasiliana nao baada ya kufika Tanzania ili kuwasaidia kwa taratibu za kuanzisha kampuni ya mafuta.Habiba alinieleza kwamba ana visima vya mafuta.Hakuwahi kunipa maelezo yoyote kuhusu yeye wala mahala anakoishi hivyo sifahamu chochote.Naombeni mniamini ndugu zangu.Mnanitesa bure bila kosa mkinihusisha na watu nisiowafahamu” akasema Edger na kwa mbali macho yake yakalengwa na machozi “Edger macho yako ingawa yanalengwa machozi lakini yanaonyesha wazi unadanganya.Kwa nini unakubali kuteseka kwa ajili ya watu ambao hawatakuwa na msaada kwako? Kwa nini unawaficha watu ambao wanajua umekwisha fariki? Hakuna yeyote katika dunia hii ambaye atakusaidia.Uko peke yako hivyo jiokoe mwenyewe.Sahau kuhusu Habiba,Sayid au IS hakuna ambaye atakuja hapa kukuokoa.Edger narudia tena kukuhakikishia kwamba endapo ukiamua kushirikiana nasi tutakulinda dhidi ya IS.Serikali ya Israel itakusaidia uweze kupata sehemu salama ya kuishi ambako utaanza upya maisha yako.Taarifa utakazotupa ni muhimu sana na ambazo zitasaidia kuokoa maisha ya watu wengi hivyo lazima na sisi tuhakikishe unakuwa na maisha mazuri wewe na wale uwapendao” akasema Ehud.Walimpa tena Edger nafasi ya kutafakari kisha akasema “Natamani sana kupata nafasi nyingine ya kuishi maisha mazuri yenye furaha na amani lakini sintaweza kuyapata maisha hayo kwa kuwa sifahamu chochote kuhusu Habiba Jawad au mtandao wa IS.Laiti ningefahamu kitu chochote hata kidogo cha kuweza kusaidia kuwapata watu hao ningewaeleza lakini sina chochote cha kuwasaidia” “Uko tayari kurejea tena katika kile chumba cha giza kuendelea na mateso? akauliza Fishel lakini Edger hakujibu akabaki kimya “Edger nimekuuliza hivyo kwa sababu hii ni mara yako ya mwisho utaipata nafasi kama hii,kama hautaitumia vyema hakuna tena dirisha lolote litakalofunguliwa kukuruhusu upite.Itumie vyema nafasi hii kujiondoa kutoka katika mateso haya.Narudia tena kukuhakikishia kwamba watu hao ambao unawaficha na hutaki kutupa taarifa zao hawana msaada wowote kwako.Wakati wewe unateseka kwa miaka mitatu ndani ya chumba cha giza wao wanaendelea na maisha yao mazuri ya kifahari,wanakula vizuri wanalala sehemu nzuri wanasafiri kwa magari ya kifahari na wanapata kila wanachokihitaji kwenye maisha yao.Wewe uko katika chumba ambacho hakina mwangaza ukilala katika sakafu yenye baridi tena ukiwa mtupu,ukipata chakula kidogo mara moja kwa siku huku ukinateseka kwa kiu.Si Habiba,Sayid au IS wanafahamu ni mateso gani unayapitia.Edger nakukumbusha tena uko peke yako hivyo jisaidie wewe mwenyewe” akasema Ehud “Naridia tena kukuhakikishia kwamba utakuwa na maisha mazuri ukitoka hapa,utaishi katika nyumba nzuri,gari zuri la kifahari na utapata kila unachokihitaji.Kama kuna kitu kingine chochote unataka tukupatie ili utupe taarifa za Habiba na Sayid tueleze.Sisi tukohapa kwa niaba ya serikali hivyo chochote utakachokitaka utakipata” akasema Fishel.Edger akafikiri na kusema “Ninataka kurejea tena katika kile chumba changu cha giza nikaendelee na mateso,sihitaji kitu kingine chochote” akasema Edger .Fishel na Ehud wakatazamana.Hawakutegemea jibu lile “Edger unalifunga dirisha ambalo halitafunguliwa tena.Tumekupa nafasi ya kuchagua wewe mwenyewe aina ya maisha unayotaka kuishi na kama ukichagua kurudi katika kile chumba cha giza sisi hatuna kipingamizi tutakurejesha lakini fahamu kuwa hakuna tena nafasi nyingine itakayofunguliwa kwako” akasema Ehud “Nirejesheni nikaendelee kuteseka” akasema Edger. “Edger kabla ya kukurejesha tena katika chumba kile kuna kitu nataka ukifahamu” akasema Fishel na kufungua faili akatoa picha akamuonyesha Edger ambaye sura yake ilibadilika baada ya kuiona picha ile. “Unamfahamu huyu?akauliza “Ndiyo.Huyu ni Olivia Themba daktari wangu ambaye aliyaokoa maisha yangu nilipotaka kuuawa kwa sumu” akajibu Edger “Kila unapoiona picha yake unastuka sana.Kuna nini kinaendelea kati yenu?akauliza Ehud “Huyu mtu mwenye umuhimu mkubwa kwangu.Bila yeye hivi sasa tayari ningekwisha fariki na hata ninyi msingep[ata nafasi ya kunitesa.Watu walitaka nifariki dunia lakini yeye alipambana akayaokoa maisha yangu hivyo nitaendelea kumshukuru hadi mwisho wa maisha yangu” akasema Edger “Kwa namna unavyomuangalia Olivia inaonyesha wazi kuna jambo linaendelea zaidi ya urafiki wa kawaida.Unampenda Olivia?Fishel akauliza “Olivia ni rafiki yangu”akajibu Edger “Jibu swali unampenda?akauliza Ehud Edger akawa kimya “Naomba nikupe taarifa kwamba Olivia ametekwa na watu wasiojulikana siku mbili zilizopita na mpaka leo hii hajulikani mahala alipo” akasema Fishel Mstuko mkubwa ulionekana usoni kwa Edger. “Mstuko mkubwa ulioupata unaonyesha jinsi gani Olivia alivyo muhimu kwako” akasema Fishel na kumuonyehsa Edger taarifa mbali mbali za kuhusiana na tukio la kutekwa Olivia kupitia kompyuta yake. “Nani wamemteka Olivia?akauliza Edger “Edger ni vipi kama tukikusaidia ukakutana tena na Olivia na ikiwezekana mkaanzisha maisha yenu sehemu tulivu ambako hakuna atakayewasumbua?akauliza Fishel.Edger akaitazama tena ile picha Ya Olivia. “Mnao uhakika wa kumuokoa Olivia kutoka kwa watekaji?akauliza Edger “Sisi tuna mtandao mkubwa na tunaweza kukusaidia kumpata Olivia na tukakukutanisha naye tena” akasema Fishel “Tafadhali kama mnao uwezo wa kumuokoa Olivia fanyeni hivyo.Ni mwanamke wa kipekee kabisa ambaye huwezi kumfananisha na wengine na hastahili kufanyiwa kitendo hiki alichofanyiwa” akasema Edger “Edger tunaweza kumuokoa Olivia kwa vile wewe umetutuma tufanye hivyo lakini kabla ya kuandaa operesheni ya kumtafuta Olivia tunataka kufahamu kwa nini unataka tumuokoe?Ni kwa sababu alikusaidia kuokoa maisha yako au kuna sababu nyingine?Tupe sababu ya msingi ili tuone uzito wake”Akauliza Ehud “Olivia ni mwanamke nimpendaye kuliko wote.Sijawahi kupenda mwanamke kama ninavyompenda Olivia” akasema Edger “Ulipotoweka tayari mlikuwa wapenzi? “Sikuwa nikimfahamu Olivia hadi nilipofumbua macho na kujikuta hospitali nchini Israel na ndipo nilipomuona Olivia kwa mara ya kwanza.Nilimpenda sekunde ya kwanza nilipomtia machoni.Nilimueleza hisia zangu na tulikubaliana kulipa suala hilo nafasi ya kutosha tutakaporejea nyumbani kwa bahati mbaya hilo halikutokea tena mlinichukua na kunileta hapa sikumuona tena Olivia hadi nilipomuona leo katika ile filamu.Ninampenda Olivia tafadhali muokoeni kama uwezo mnao” “Ahsante kwa kutueleza ukweli.Tutakusaidia katika hilo.Tutakwenda Tanzania kumtafuta Oliviana lakini kabla ya kufanya hivyo na sisi tutaomba utueleze kuhusiana na Habiba Jawad na Sayid Omar” akasema Fishel “Nitawaeleza kila kitu pale nitakapomuona Olivia mbele ya macho yangu”akasema Edger “Usihofu Edger sisi tunakwenda kumtafuta Olivia na tuna uhakika wa kumpata lakini kabla hatujaingia katika operesheni hiyo nataka kwanza utupe maelezo kuhusu Habiba na Sayid Omar ni jinsi gani tutaweza kuwapata? “Nimewaambia nitawaeleza kila kitu lakini hadi hapo nitakapomuona Olivia mbele ya macho yangu niishike mikono yake na kuhakikisha kweli ni yeye mwanamke nimpendaye” akasema Edger “Sawa Edger tunakwenda kufanya operesheni katika nchi ya watu na kumchukua raia wa nchi nyingine bila ruhusa au kibali cha mamlaka husika,hili ni jambo kubwa sana hivyo kabla hatujafanya hivyo tunataka kupata uhakika kuwa hiki tunachokwenda kukifanya kina manufaa kwetu” “Awali uliniambia kwamba nichague kitu chochote ninachokitaka kutoka kwenu ili niweze kuwapa taarifa mnazozihitaji.Ninachokihitaji ni kumpata OIlivia Themba na nitawaeleza kila kitu mnachokihitaji.Kingine nataka mniandalie nyumba mahala ambako nitaishi na Olivia kwa amani” akasema Edger “Sawa Edger.Tutafanya kama unavyotaka.Tutamleta Olivia mbele ya macho yako lakini kama hautakuwa tayari kutueleza kile tunachokitaka utakuwa umemuweka Olivia katika matatizo makubwa kwani hautamuona tena na kwa kuwa atakuwa ameifahamu siri hii na yeye pia atafungwa katika chumba cha giza kwa maisha yake yote.Nataka uwe na uhakika kuwa utatupa taarifa zote za kuwahusu Habiba Jawad na Sayid Omar kabla hayujamleta Olivia” akasema Fishel “Naombeni mniamni nitawaeleza kila kitu pale nitakapomuona Olivia mbele yangu.Kwa ajili yake niko tayari kuweka kila kitu bayana hivyo hakikisheni mnafanya kila mnaloweza kumpata Olivia.Aliyaokoa maisha yangu na sasa ni zamu yangu kuyaokoa maisha yake” akasema Edger “Sawa Edger nimeyapokea maneno yako na sisi tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunampata Olivia lakini ukumbuke nilivyokueleza.Kama ukienda kinyume na makubaliano yetu utakuwa umempoteza pia Olivia kwani hautamuona tena na utakuwa umemsababishia mateso makubwa” akasema Fishel “Msiwe na wasiwasi na mimi.Nitawaeleza kila kitu nikimuona Olivia” akasema Edger. “Vizuri.Kwa kuwa umetuhakikishia kwamba uko tayari kuzungumza na kutueleza ukweli wote hatutakurejesha tena katika kile chumba cha giza utaendelea kuishi maisha mazuri katika chumba kipya ukipata kila unachokihitaji” akasema Ehud kisha wakamuita Avi na kumpa maelekezo kwamba Edger aendelee kuishi maisha mazuri katika kile chumba kipya asiendelee tena na mateso Fishel na Ehud wakarejea katika ofisi yao kujadiliana kuhusiana na kile walichokipata kutoka kwa Edger “Hatimaye Edger amekubali kueleza ukweli wote kama akimuona Olivia.Ninaiona nguvu ya mwanamke.Kikubwa sasa ni namna ya kumpata huyo Olivia.Nani kamteka na kwa nini? Akauliza Fishel “Fishel japo tumemuahidi Edger kwamba tunao uwezo wa kumpata Olivia lakini si jambo rahisi hata kidogo.Hatujui hata tuanzie wapi” akasema Ehud “Ehud hilo lisikupe shida.Tulichokuwa tunakitafuta ni kupata taarifa kutoka kwa Edger ambaye amekubali kueleza kila kitu lakini hadi atakapomuona Olivia hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunampata Olivia.Tunakwenda Tanzania na tutahakikisha tunampata Olivia” akasema Fishel “Fishel kwa mtazamo wangu tumetengeneza operesheni mpya ambayo haikuwa na ulazima.Tungetumia nguvu tungeweza kupata taarifa zote kutoka kwa Edger bila kulazimika kuingia tena katika operesheni nyingine.Tayari amekwisha choshwa na mateso yale na lazima angefunguka” akasema Ehud “Kuna siri kubwa ambayo Edger anaificha hapa na ndiyo maana alikubali kurejea tena katika kile chumba akaendelea kuteseka kuliko kuisema na hata kama tungetumia nguvu ya kiasi gani asingeweza kusema chochote.Ameteseka kwa miaka mitatu lakini ameona ni bora arudi tena katika mateso akaendelee kuteseka kuliko kusema chochote hadi tulipomgusia http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Olivia ndipo akawa tayari kufunguka.Nina uhakika mkubwa sana tukimleta Olivia atafunguka na atatueleza kila kitu” akasema Fishel “Una uhakika atatueleza au atakuwa anacheza na akili zetu? “Atafunguka.Niamini mimi” akasema Fishel “Fishel bado moyo wangu unakuwa mgumu sana katika suala hili kwani litatuingiza tena gharama za kufanya operesheni katika nchi nyingine na hatuna uhakika kama tutampata Olivia kama ulivyomuahidi Edger” akasema Ehud “Ehud kwa ajili ya taifa teule la Israel kila kitu kinawezekana.Lazima tufanye kila linalowezekana kuhakikisha taifa teule linakuwa salama.Tutaingia Tanzania na kumtafuta Olivia tutamleta hapa ili Edger aweze kutueleza mahala alipo Habiba Jawad na Sayid Omar ambao kwa kutumia fedha zao wanaendelea kufadhili vikundi vya wana mgambo ambavyo vinaendesha mauaji dhidi ya waisrael” akasema Fishel na kutazama na Ehud kwa muda halafu akasema “Tuwasiliane na makao makuu tuwajulishe kuhusu suala hili” akasema Fishel na kuomba waunganishwe na makao makuu baada ya muda mkurugenzi mkuu wa Mossad akawa hewani “Fishel habari za Nairobi?Nimeambiwa mnataka kuzungumza nami.Kuna kitu gani kinaendelea huko?Kuna chochote mmeshakipata kutoka kwa yule jamaa?akauliza mkurugenzi “Mkurugenzi tumefika salama kabisa Nairobi na bila kuchelewa tumeanza kazi iliyotuleta hapa.Tumemtoa Edger katika chumba cha giza na kumrejesha katika maisha mazuri kisha tukaanza kuhojiana naye.Alikana kuwafahamu Habiba Jawad na Sayid Omar na akatuomba tumrejeshe katika chumba cha giza akaendelee kuteseka.Hakuwa tayari kusema lolote hadi tulipomuonyesha picha ya mwanamke mmoja anaitwa Olivia.Huyo mwanamke ni daktari ambaye ndiye aliyeyaokoa maisha yake kwa kumpeleka Israel baada ya kupewa sumu.Edger amekiri kumpenda Olivia na ameahidi kutueleza kila kitu tunachohitaji kama tukimkutanisha tena na Olivia” akasema Fishel “Hiyo ni hatua nzuri sana.Kama amekubali kueleza kila kitu endapo atampata huyo mwanamke ni jambo zuri sana.Huyo mwanamke anapatikana wapi?akauliza mkurugenzi “Mkurugenzi hapa kuna tatizo kidogo.Huyo mwanamke anapatikana nchini Tanzania” “Tanzania ni karibu sana na Kenya na tuna ubalozi wetu pale hivyo kumpata huyo mwanamke itakuwa kazi nyepesi.Tutatuma timu ya watu kwenda kumtafuta na kumleta Nairobi.Mossad tunao utajiri mkubwa wa majasusi mahiri” akasema mkurugenzi “Tatizo lililopo mkurugenzi ni kwamba mwanamke huyo ametekwa nyara siku mbili zilizopita na watu wasiojulikana na hadi leo hii bado hajapatikana” “Ametekwa?!! “Ndiyo mkurugenzi.Ametekwa nyara na watu wasiojulikana”akajibu Fishel “Pamoja na kutekwa nyara lakini bado ni mtu wa muhimu kwetu.Edger anazo taarifa nyeti sana tunazozihitaji hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunampata huyo Olivia.Tutatuma majasusi wetukwenda Tanzania kumtafuta Olivia lakini kabla ya kutuma kikosi cha majasusi Tanzania ninataka wewe na Ehud mtangulie Tanzania.Nitatoa maelekezo kwa balozi wetu ili muweze kupatiwa kila msaada mnaouhitaji mkiwa Tanzania.Nataka mkafanye uchunguzi wa tukio hilo la kutekwa kwa Olivia na kisha mnipe taarifa haraka namna gani tunaweza kufanya yetu ya kumtafuta na kumpata Olivia.Naombeni mlipe uzito suala hili muhimu mno.Maroketi yanaendelea kurushwa katika ardhi ya Israel na ili kuwadhibiti wanamgambo hao wanaofanya mashambulio haya lazima tukate mrija unaowaunganisha na kisima cha fedha kwa kuwakamata Habiba na Sayid.Tuwasiliane mtakapofika Tanzania” akasema mkurugenzi na kukata simu.Fishel na Ehud wakatazamana “Fishel tumenunua kazi nyingine ambayo haikuwa na ulazima wowote.” akasema Ehud “Ehud nini hasa tatizo lako?Unaonekana hujafurahia kabisa suala la kumtafuta Olivia ili Edger aweze kutupa taarifa muhimu” akasema Fishel “Ni kweli sijafurahishwa na jambo hili.Tulikuja hapa kumfanya Edger afunguke na atupe taarifa zile muhimu sana tunazozihitaji lakini mwenzangu umekuwa mwepesi sana kukubali matakwa yake”akasema Ehud “Ehud hakuna ambacho tungekipata kwa Edger,yuko tayari kuendelea kuteseka kuliko kueleza chochote.Hata kama tungetumia nguvu kumtesa tungeweza kumuua kabla ya kupata chochote toka kwake kwani afya yake ni dhaifu mno.Lakini baada ya kumgusia kuhusu Olivia amekubali kutueleza kila kitu kama tukimleta Olivia,huoni kama hayo ni mafanikio makubwa Ehud” akasema Fishel. “Japokuwa mkurugenzi ameridhia lakini binafsi sijapendezwa na hili jambo” akasema Ehud “Ehud nakufahamu wewe unapenda matumizi ya nguvu lakini kwa hali aliyonayo Edger hatuwezi kutumia nguvu.Tutatumia nguvu kumsaka Olivia na kisha tutapata taarifa nyeti toka kwa Edger.Haya tayari ni maelekezo tumepewa hatuna haja ya kuendeleza mjadala kinachotakiwa kwa sasa ni kuanza kujiandaa kuelekea Tanzania.Twende tukaonane na balozi kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea Tanzania” akasema Fishel. TANZANIA.. Hali ya Olivia Themba iliendelea kuwa mbaya kadiri muda ulivyozidi kusonga.Hakuwa na fahamu.Hii ilitokana na mateso makali aliyopewa na Kaiza akiwa na watu wake.Dr Alex alikuwa amefungwa katika kiti pembeni akishuhudia Olivia alivyokuwa akiteswa baada ya kutokea mzozo kati yake na Kaiza kuhusiana na mateso aliyokuwa akimpa Olivia.Pamoja na jitihada zote za Kaiza lakini hakuweza kupata chochote kutoka kwa Olivia.Alichanganyikiwa kwani tayari kiza kiliingia na hakuwa amekamilisha kazi aliyopewa na rais.Akamgeukia Dr Alex “Dr Alex unatakiwa ufanye kila linalowezekana kumuamsha Olivia.Lazima afunguke.lazima aseme kila kitu leo!! Akasema Kaiza kwa ukali “Siwezi Kaiza.Siwezi kufanya chochote tena.Umekataa kusikia ushauri wangu na hayo ndiyo matokeo yake.Olivia is going to die and you’ll get nothing !! Ungenisikia ushauri wangu usingefika hapa ulipofika.Sina chochote cha kukusaidia kwa sasa.Let her die!! Akasema Dr Alex maneno yaliyompandisha hasira Kaiza akamrukia Dr Alex teke zito la kifua lililompeleka chini.Akaenda ukutani na kupiga ukuta kwa mikono yake alipandwa na hasira.Akageuka kumtazama Olivia hali yake bado haikuwa nzuri. “Dah ! nitafanya nini?Hali ya Olivia ni mbaya na huyu daktari amegoma kufanya chochote.Lazima nitafute msaada siwezi kumuacha Olivia akafariki kwani ni my muhimu sana kwetu” akawaza Kaiza akatoka ndani ya kile chumba na kumpigia simu Dr Evans “Kaiza naamini tayari zoezi limekamilika” akasema Dr Alex mara tu alipopokea simu “Mheshimiwa rais”akasema Kaiza “Nini Kaiza?akauliza Dr Evans “Zoezi halijafanikiwa mheshimiwa rais.Mpaka sasa hatujafanikiwa kupata chochote kutoka kwa Olivia.Nimetumia kila aina ya mateso lakini hajafungua mdomo wake kusema chochote na kwa bahati mbaya hali yake imebadilika ghafla hana fahamu nina wasiwasi anaweza akapoteza maisha muda wowote” “What?! Akauliza Dr Evans kwa mstuko “Ndiyo mheshimiwa rais,hali yake si nzuri hata kidogo” “Kaiza don’t let her die !! Umenisikia? “Mheshimiwa rais..” “Sikiliza Kaiza,nimetoka hospitali kumtazama mwanangu Coletha na hali yake si nzuri hata kidogo.Madaktari wanahangaika kutafuta tiba lakini mpaka sasa hawajafanikiwa.Mwenye kuifahamu tiba ya mwanangu ni Olivia pekee ambaye ndiye aliyetengeneza virusi vinavyomtesa mwanangu.Kwa namna yoyote ile Olivia hatakiwi kufa bado namuhitaji sana” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais….” “Kaiza sihitaji maelezo nataka kusikia Olivia anazinduka na anakuwa salama tena asiendelee kupatiwa mateso yoyote.Namuhitaji sana kwa ajili ya uhai wa mwanangu.Olivia akifa utakufa naye!! “Mheshimiwa rais ninahitaji msaada natakiwa kumpeleka Olivia hospitali kwa matibabu” akasema Kaiza “Dr Alex yuko hapo mtumie kuhakikisha Olivia anakuwa salama” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais hata Dr Alex mwenyewe amekiri hawezi kufanya kitu.Olivia anatakiwa kupelekwa hospitali.Mheshimiwa rais kuna kitu ambacho nadhani itakuwa vyema ukakifahamu kuhusu Dr Alex.Sifahamu kwa nini lakini amekuwa mgumu sana kutoa ushirikiano kwetu na kuna wakati nilimkamata akizungumza na mtu kwenye simu kuhusu Olivia na nilipomuhoji akadai anamzungumzia Olivia mwanae.Mheshimiwa rais sina imani na huyu mtu kabisa kuna mchezo anatuchezea” akasema Kaiza na ukimya mfupi ukapita halafu Dr Evans akasema “Sikiliza Kaiza,Olivia hatakiwi kupelekwa hospitali.Kila mtu anafahamu Olivia amepotea hivyo akionekana tayari kila kitu kitakuwa kimeharibika na tutashindwa kupata taarifa za muhimu.Nitakuelekeza shambani kwangu,mtoe Olivia hapo na utampeleka shambani kwangu kuna nyumba kubwa pale.Ninamtuma daktari wangu anakwenda kule akiwa na vifaa vyote vinavyotakiwa mtamkuta kule na yeye ndiye atakayebeba jukumu la kuhakikisha Olivia anazinduka.Inaniuma kusema hivi lakini wakati mnaondoka hapo muue Dr Alex na watu wake wote.Sehemu hiyo itakuwa chini yenu.Umenielewa Kaiza? Akauliza Dr Evans “Nimekuelewa mheshimiwa rais” akasema Kaiza na Dr Evans akamueleza mahala lilipo shamba lake na bila kupoteza muda maandalizi ya kuondoka mahala pale yakaanza.Dr Alex akafunguliwa na kusaidiana na akina Kaiza kumtoa Olivia mle ndani na kumpakia garini.Kabla hawajaondoka Kaiza akamuomba Dr Alex warejee ndani wakazungumze. “Dr Alex imelazimu kumuhamisha Olivia tunampeleka hospitali.Ahsante sana kwa msaada wako mkubwa uliotupatia na ninakuomba samahani kwa yale yaliyotokea.Kuna uwezekano tukarejea tena hapa kuendelea na zoezi letu pale Olivia atakapokuwa tayari”akasema Kaiza “Hata mimi ninashukuru sana Kaiza.Tusahau yaliyopita tuangalie ya mbele.Kabla haujaondoka ninaweza kuipata simu yangu tafadhali?akauliza Dr Alex.Kaiza akaingiza mkono mfukoni kama vile anaitoa simu yake lakini kwa kasi ya ajabu mkono wake ukaenda katika bastora aliyokuwa ameichomeka nyuma kiunoni akaichomoa na kuachia risasi mfululizo Dr Alex akaanguka chini na hakuwa na uhai tena Kaiza akamtazama halafu akamtemea mate na kutoka mle ndani.Wakati Kaiza akiwa ndani ya ofisi vijana wake ambao tayari alikwisha wapa maelekezo waliwavamia wale watu wa Dr Alex na kuwamaliza wote Kaiza alipotoka alikuta kazi imemalizika. “Kila kitu tayari?akauliza Kaiza “Ndiyo mkuu kila kitu tayari” “Good.Let us go” akasema Kaiza wakaingia katika magari na kuondoka eneo lile kuelekea mahala walikoelekezwa na rais shambani kwake.
Tayari Kiza kimekwisha tanda angani ndege ya shirika la ndege la Misri ilipotua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Miongoni mwa abiria waliokuja na ndege hii ni Ruby ambaye baada ya kukamilisha taratibu akatoka na kupokewa na Mathew na Gosu Gosu wakaingia garini na kuondoka haraka eneo lile “Ruby karibu tena Tanzania.Nimefurahi sana kukuona tena” akasema Mathew wakiwa garini “Sikuwa na mpango wa kuja Tanzania hivi karibuni lakini imenilazimu kuja kwa ajili ya hili suala muhimu sana.Nini kinaendelea hivi sasa?akauliza Ruby na Mathew akamsimulia kila kitu kilichotokea hadi mahala walikofika “Poleni sana kwa kila kilichotokea.Suala lolote ambalo ndani yake kuna mkuu wa nchi lazima liwe zito sana.Suala hili lina mkusanyiko wa mambo kadhaa ndani yake.Kuna suala la Olivia kujihusisha na mtandao wa IS,suala la Edger Kaka ambalo rais amehusishwa nalo na ninaamini kadiri tunavyoendelea kulichimba hili suala kuna mengi zaidi yatajitokeza” akasema Ruby baada ya kupata picha nzima ya namna jambo lile linavyokwenda Baada ya kutoka uwanja wa ndege walielekea moja kwa moja katika hospitali ya Dr Philip kujua maendeleo ya Devotha waliyemuacha pale. “Devotha anaendelea vyema.Tulifanikiwa kutoa risasi mbili alizokuwa amepigwa begani.Anaendelea vyema yuko katika chumba maalum anapumzika” DrPhilip akamwambia Mathew kisha akawaongoza kuelekea katika chumba alimokuwa amelazwa Devotha ambaye alikuwa amekaa kitandani akitazama runinga.Dr Philip akakinyonga kitasa na kuufungua mlango wakaingia.Sura ya Devotha ikapatwa na mstuko halafu akatabasamu “Hello Devotha” akasema Dr Philip “Oh thank you Lord ! akasema Devotha “Nilikuwa na wasiwasi sana kama mlifanikiwa kutoka salama” akasema Devotha “Usihofu tulitoka salama.Unaendeleaje?akauliza Mathew “Ninaendelea vyema.Nawashukuru madaktari wamenihudumia.Ahsanteni sana kwa kuokoa maisha yangu” akasema Devotha “Devotha mimi ndiye ninayepaswa kukushukuru kwa kuyaokoa maisha yangu.Bila wewe hivi sasa bado ningeendelea kuwapo ndani ya lile shimo”akasema Mathew “Nini kinaendelea hivi sasa Mathew?akauliza Devotha “Devotha nitakuja kukujulisha kila kinachoendelea lakini kwa sasa usiwaze chochote endelea kupumzika” akasema Mathew.Devotha akarusha shuka pembeni “Dr Philip I’m okay now.Tafadhali nahitaji kuondoka” “Devotha pumzika tafadhali.Tutakujulisha kila kinachoendelea” akasema Mathew “Hapana Mathew.I need to get out of here.Kuna mambo mengi yanayoendelea na siwezi kuendelea kulala hapa na kuwaacha mfanye kazi peke yenu” akasema Devotha “Devot…….” Dr Philip akataka kusema kitu Devotha akamzuia “Dr Philip unakwenda kutoa huu mrija wa maji au niuondoe mwenyewe?akauliza Devotha “Let her go” akasema Mathew na Dr Philip akauchomoa mrija wa maji aliyokuwa ametundikiwa Devotha “Utanisamehe Dr Philip najua ulipenda niendelee kukaa hapa lakini baada ya kuwaona wenzangu hawa nimepata nguvu ya ghafla na siwezi kuendelea kukaa tena hapa hospitali”akasema Devotha na kulivua lile gauni la wagonjwa alilokuwa amevaa akavaa nguo zake “Wow ! she’s so hot ! akawaza Gosu Gosu akimshuhudia Devotha akivaa mbele yao “Tunaweza kuondoka” akasema Devotha Dr Philip akamuomba asubiri amletee dawa za kutumia kisha wakaondoka “Pole sana Devotha” akasema Gosu Gosu “Ahsanteni sana” akasema Devotha “Mathew unaweza ukanieleza nini hasa kilitokea pale kitalu 1?Mliwezaje kuufungua mlango wa kutokea nje?akauliza Devotha “Devotha tujielekeze katika masuala mengine ya muhimu ya kumtafuta Olivia.Unahisi anaweza kuwa wapi?akauliza Mathew “Olivia alihamishwa kutoka kitalu 2 na sifahamu mahala alikopelekwa.Niligundulika nimedukua simu ya Rais nikaanza kutafutwa na nikafungiwa kila kitu.Sikuwa na sehemu nyingine salama ya kukimbilia Zaidi ya nyumbani kwako ambako nilipokelewa vyema na Theresa mtumishi wako mimi na Saada msichana ambaye alinisaidia kudukua simu ya rais.Niliamua kumfuata Olivia kitalu 2 nikaonane naye sikumkuta tayari alikwisha hamishwa na sikuweza kujua mahala aliko kwani sikuweza tena kuingia katika mfumo wa idara yetu. Nilirejea nyumbani kwako ndipo nikakutana na Gosu Gosu ambaye naye alikuwa amefika muda huo tukazungumza na kuanza mikakati ya kukuokoa .Mathew sifahamu alipo Olivia.Naamini watakuwa wamempeleka mafichoni mahala ambako sipafahamu kwa kuhofia ninaweza kumtorosha” akasema Devotha na safari ikaendelea kimya kimya “Gosu Gosu umewasiliana na Saada?Yuko salama?akauliza Devotha “Nimepiga simu hotelini nikaunganishwa na chumba chake ili nizungumze naye lakini simu ya chumbani kwake inaita bila kupokelewa” akasema Gosu Gosu “Au atakuwa amekamatwa na akina Kaiza baada ya kugundua kuwa anacheza na kamera za kitalu 1?” akauliza Devotha. “Tumuombee awe salama” akasema Gosu Gosu Safari iliendelea hadi walipofika katika nyumba ya Mathew wanayoitumia kama ofisi yao.Wakashuka garini na kuingia ndani “Karibuni ndani jamani,hapa ni nyumbani kwangu ni sehemu ambayo naamini itakuwa salama kwetu na kila kitu kitafanyika kutokea hapa” akasema Mathew na kuwakaribisha Devotha na Ruby “Mathew una nyumba ngapi hapa Dar es salaam?akauliza Ruby “Ninazo nyumba zaidi ya ishirini hapa Dar es salaam.Ninawekeza katika majengo kwani thamani yake inapanda kila wakati tofauti na magari ambayo kila mwaka thamani yake hushuka hivyo msiwe na hofu kama tukigundulika tuko hapa tutahama na kwenda sehemu nyingine bado ninazo nyumba za kutosha” akasema Mathew na kuwaonyesha Ruby na Devotha chumba chao “Devotha ingekuwa vyema kama ungepumzika.Mimi na wenzangu tutaendelea na utakapokuwa tayari utajiunga nasi”akasema Mathew. “Hapana Mathew huu si muda wa kupumzika ni muda wa kupambana.Siwezi kulala kitandani wakati wenzangu mnaendelea kupambana hili ni jeraha dogo ambalo haliwezi kunizuia kupambana.Count me in Mathew” akasema Devotha kisha Mathew akawataka wote waelekee chumba cha kusomea ambacho kilikuwa kikubwa kidogo. “Awali ya yote nawashukuru sana nyote kwa kufika kwenu hasa wale mliotoka mbali Gosu Gosu na Ruby.Najua niliwapa taarifa ndani ya muda mfupi na mkasitisha shughuli zenu kuja kunisaidia nawashukuru sana kwa upendo wenu huo.Kabla sijaendelea Zaidi naomba nifanye utambulisho mdogo.Gosu Gosu n Ruby kutaneni na Devotha ambaye alikuwa mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi.Devotha tayari umekwisha kutana na Gosu Gosu na ninaomba usiku huu ukutane pia na Ruby ambaye anatokea nchini Uingereza huyu ninamuita mtu mashine.Anaifahamu kompyuta kuliko hata aliyeigundua.Kuna nyakati humuita jini kutokana na uwezo wake wa ajabu wa kucheza na kompoyuta.Huyu ndiye aliyetengeneza ile programu ambayo ilifunga mfumo wenu.Ni mtu ambaye ananisaidia sana kila pale ninapokuwa na kazi na amekuja kushirikiana nasi katika kumtafuta Olivia” Akasema Mathew “Nimefurahi sana kukufahamu Olivia” akasema Devotha “Mimi pia nimefurahi kukutana nawe” akasema Ruby “Baada ya utambulisho sasa tunaendelea.Ndugu zangu mbele yetu tunalo jambo kubwa linatukabili.Ni jambo ambalo ndani yake kuna mambo mengine kadhaa yamejitokeza ambayo yanaongeza utata.Kwa ufupi ni kwamba nina urafiki na mrembo mmoja anaitwa Olivia Themba.Siku mbili zilizopita alitekwa na watu wasiojulikana na lengo la kuwaita Gosu Gosu na Ruby ni ili mnisaidie kumtafuta lakini katika suala hilo yameibuka mambo mengine makubwa.Devotha idara yako inahusika kwa kiasi kikubwa sana na suala hili,nataka uwe wa kwanza kutueleza kwa kina kila kitu kuhusiana na Olivia,Karibu” akasema Mathew. “Idara ya usalama wa taifa ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo walipata taarifa kwamba kuna mtu anaitwa Seif Almuhsin ambaye kazi yake kubwa ni kukusanya vijana kutoka katika nchi za Afrika mashariki na kati na kuwapeleka katika kambi za mafunzo za IS anaelekea nchini kwao.Akiwa jijini Kinshasa Seif alikutana na mtu ambaye baada ya kumchunguza waligundua ni mtanzania anaitwa Olivia Themba.Rais wa Congo alimtuma mjumbe maalum kuleta ujumbe kwa rais wa Tanzania kumjulisha kuhusu Olivia kukutana na mtu wa kikundi cha IS,Rais naye akatukabidhi sisi jukumu hilo tukaandaa mpango wa kumteka Olivia mara tu alipotua nchini akitokea Congo.Tulimpeleka mafichoni na kuanza kumfanyia mahojiano.Tukagundua alikuwa na mawasiliano pia na mtu anaitwa Sayid Omar ambaye baada ya kumchunguza tukagundua ni mfadhili wa kikundi cha IS.Tulimbana Olivia atueleze kuhusiana na mahusiano yake na watu wale wa IS na akatupa namba Fulani akatutaka tuzitumie zitatusaidia kujua mahala alipo nabaada ya kuziingiza namba zile mtandao wote wa idara yetu ukajifunga.Olivia akadai kuwa ili kuufungua tena mtandao wetu anataka kuzugumza na rais.Niliwasiliana na rais akafika akazungumza naye lakini hawakuelewana.Olivia alimueleza rais kwamba mwanae Coletha ameambukizwa virusi ambavyo kama hatatibiwa kwa muda wa siku kumi na mbili atapoteza maisha.lengo la kumuambukiza Coletha virusi hivyo ambavyo alivitengeneza yeye mwenyewe ni kumtaka rais amuelekeze mahala alipo Edger Kaka.Huyu Edger aliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na alifariki dunia katika ajali iliyotokea siku aliporejea nchini akitokea Israel alikoenda kwa matibabu.Olivia anadai kuwa Edger hajafa na kwamba rais Dr Evans anafahamu mahala alipo.Anadai ajali ile iliyotokea ni ya kutengenezwa na kwamba serikali ndio waliofanya tukio lile na Rais anafahamu mahala Edger alipo.Tumemtesa Olivia ili atupe taarifa za kuhusu yeye na IS lakini bado ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa Edger hajafa na rais anafahamu mahala alipo.Nilimuuliza rais kuhusu tuhuma zile akakana kufahamu chochote kuhusu Edger Kaka.Baadae nilitaarifiwa na rais kuwa kuna mtu anaitwa Mathew Mulumbi aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa tayari anafahamu mahala alipo Olivia na alikuwa katika mikakati ya kwenda kumuokoa.Tulimuhamisha Olivia haraka kutoka mahala alipokuwa amehifadhiwa na tukaweka kikosi cha kulinda mahala pale na ili Mathew atakapofika atiwe nguvuni kwa bahati mbaya karibu kikosi chote kiliuawa.Mathew naye akaingia katika orodha ya watu tunaowatafuta na tuliamini naye pia ni mmoja wa watu wa IS na kazi yake kubwa ni kumlinda Olivia.Ili kumshinikiza Olivia aweze kutueleza kila kitu tulimteka baba yake mzee Agrey Themba.Tulimtesa sana Agrey huku Olivia akishuhudia lakini hakufunguka.Usiku huo huo nikapokea maelekezo kutoka kwa rais ya kutuma timu nyumbani kwa Lucy Themba alfajiri kwa ajili ya kumkamata Mathew na mtego huo ukafanikiwa tukishirikiana na Lucy Themba mama yake Olivia.Asubuhi ya leo nilianza kwa kumuhoji tena Olivia na akanieleza kuwa ni kweli Edger yuko hai na kama nikitaka kupata uhakika nifanye uchunguzi nitajua.Nililazimika kumuamini na kuamua kulichunguza hilo suala.Nilikwenda kuonana pia na Mathew nikamuhoji na katika mahojiano hayo akanisaidia kuzisoma barua pepe ambazo Olivia alikuwa anawasiliana na Sayid Omar na ndipo nikagundua kwamba Olivia na Sayid Omar walikuwa wanashirikiana kuandaa kirusi ambacho amemuambikiza mtoto wa rais kushinikiza kupewa taarifa za mahala alipo Edger kaka.Nilikata tamaa baada ya kugundua IS wako pia katika mpango ule wa kushinikiza rais aeleze mahala alipo Edger Kaka.Mathew alinishauri nisiache kuchunguza na akanishauri nianze kwa kumchunguza rais.Nilimtumia Saada tukadukua simu ya rais lakini hatukupata chochote kwani tuligundulika mapema.Baada ya kugundulika nilifungiwa mawasiliano yote siwezi kupiga simu wala kuingia katika mtandao wetu na ndipo nilipoamua kukimbilia kwa Mathew kuomba msaada kwani alinieleza anao watu wake wawili wanaoweza kunisaidia ambao ndio nyie Gosu Gosu na Ruby.Nilimueleza Gosu Gosu kila kitu nashukuru akanielewa na tukaanza mikakati ya kumuokoa kwanza Mathew na katika harakati hizo nikapoteza fahamu hadi nilipozinduka na kujikuta nikiwa hospitali.Kwa ufupi hayo ndiyo yaliyojiri kwa upande wa idara yangu” akasema Devotha “Ahsante Devotha kwa maelezo hayo ambayo naamini kila mmoja wetu ameyaelewa.Kufuatia maelezo hayo tunaweza kuichora chati yetu namna hii.Kwanza kabisa tunaye Olivia Themba.Huyu ana mawasiliano na Seif Almusin na Sayid Omar ambao hawa wote ni watu wa kundi la IS.Hapa lazima tufahamu Olivia ana mahusiano gani na hawa watu wa IS?Ni mwenzao au wanamtumia tu kufanikisha mipango yao?Olivia nimekuwa naye karibu ni mtu mwenye kila kitu na binafsi sioni sababu ya yeye kujiunga na kikundi cha IS.Olivia na IS wanamleta mtu anaitwa Edger Kaka.Tunatakiwa kumfahamu huyu Edger Kaka ni nani?Ana mahusiano gani na Olivia na hawa watu wa IS?Huyu Edger aliwahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania je anahusianaje na IS? Hawawezi kupoteza nguvu kubwa na fedha kama suala hili halina maslahi kwao.Baada ya kumfahamu Edger Kaka na mahusiano yake na Olivia na IS linakuja swali je ni kweli yuko hai kama wanavyodai?Kama bado yuko hai yuko wapi? Kama yuko hai Rais anafahamu mahala alipo? Ili kupata baadhi ya majibu ya maswali yetu tunatakiwa kumpata Olivia ambaye ametekwa na hajulikani yuko wapi.Tunayo sehemu ya kuanzia kufahamu mahala alipo Olivia.Kuna mtu alipiga simu nyumbani kwangu akazungumza na GosuGosu naamini hata wewe Devotha ulikuwepo,mtu huyo alikuwa ananitafuta mimi na Gosu Gosu akajifanya ni mimi akazungumza naye mtu huyo akamueleza kwamba anataka kumpa taarifa za kuhusiana na Olivia.Kwa bahati mbaya hakueleza chochote cha msingi kwani simu ilikatika.Ruby ni wewe tuliyekuwa tunakusubiri uje ili uifanye kazi hii.Tunataka kujua huyo jamaa alipiga simu hii kutoka wapi? Hii ndiyo sehemu ya kwanza kuanzia kazi yetu.Kuna yeyote mwenye swali la kuuliza kabla hatuaendelea mbele?Akauliza Mathew “Olivia anashirikiana na magaidi na ndiyo sababu anashikiliwa na idara ya serikali.Nataka kufahamu kwa nini sisi tunamtafuta?Kwa nini tunataka kumtoa kutoka katika mikono ya idara ambayo wanaweza wanao mtandao mpana Zaidi wa kupambana na magaidi?Endapo tutafanikiwa kumpata Olivia hamuoni kwamba tutakuwa tunafifisha juhudi za idara ya serikali kupambana na magaidi? Akauliza Ruby “Ruby umeuliza swali zuri kwa nini tunamtafuta Olivia na Kutaka kumtoa katika mikono ya serikali?Kikubwa kinachotufanya tumtafute Olivia ni kutaka kuufahamu ukweli kuhusiana na suala la Edger Kaka.Tunataka kupata uhakika kama kweli yuko hai au amekufa.Kama kweli Edger yuko hai na Rais anahusika na suala hilo basi Olivia hataachwa salama hivyo basi tunatakiwa kumuokoa na kujua kuhusu suala hili kwa upana wake na vile vile kujua IS wameingiaje katika suala hili na wana maslahi gani nalo?Majibu ya maswali haya tutayapata kwa Olivia pekee.Nadhani umenielewa Ruby” akasema Mathew “Nimekuelewa Mathew” akasema Ruby “Good.Endelea kufanya mambo yako kila kitu ulichoelekeza nikuandalie kipo tayari” akasema Mathew na kumuonyesha Ruby vifaa mbali mbali alivyokuwa amemuandalia akaanza kuvifunga tayari kuanza kazi.Wakati Ruby akiendelea kufanya maandalizi ya kuanza kazi akisaidiwa na Gosu Gosu,Mathew akatoka nje Devotha akamfuata “Unajisikiaje Devotha?akauliza Mathew “Mathew nina wasiwasi sana na Saada.Sijui atakuwa katika hali gani.Ninatamani kwenda kumtafuta kujua hali yake” akasema Devotha “Devotha sahau kuhusu Saada kwa sasa.Elekeza akili yako katika suala kubwa lililo mbele yetu la kumpata Olivia.” akasema Mathew “Mathew huyo Saada ninayemzungumzia ndiye aliyefanikisha sisi tukakufikia mahala ulikokuwa umefungwa.Bila yeye kucheza na mtandao wetu kuzima na kuwasha kamera tusingekufikia kwa urahisi na kukukomboa”akasema Devotha “Nalifahamu hilo Devotha na ninashukuru lakini kwa sasa tuna kazi kubwa ya kufanya kumtafuta Olivia.Naamini huyo mtu wako anafahamu namna ya kuchukua tahadhari na atakuwa salama.Baadae kama tukipata nafasi ya kutosha tutaangalia namna ya kumtafuta” akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita “Naamini sikufanya kosa kuchagua kusaliti idara yangu na kujiunga nawe Mathew” akasema Devotha “Ulifanya uamuzi sahihi na hautajutia uamuzi huo” akajibu Mathew na kurejea ndani akamuacha Devotha pale nje.
Ving’ora vya magari ya wagonjwa vilisikika na magari matatu ya wagonjwa yaliyokuwa katika mwendo mkali yakawasili katika hospitali kuu ya taifa ya Mtodora.Geti likafunguliwa na magari yale yakapita.Ving’ora vile viliwafanya wauguzi na madaktari kutoka kwa haraka kujua ni aina gani ya wagonjwa walioletwa na magari yake “Kuna ajali imetokea watu kadhaa wamefariki dunia na majeruhi tumewakimbiza hapa” akasema mmoja wa wauguzi wa gari la wagonjwa.Haraka haraka majeruhi wale wa ajali wakashushwa katika yale magari wakapelekwa katika chumba cha upasuaji kwani wengi walikuwa wamechafuka damu na haikujulikana ni sehemu zipi walizokuwa wameumia.Walikuwa jumla majeruhi nane.Wanaume saba na mwanamke mmoja. Dakika mbili toka magari yale ya wagonjwa yawasili pale hospitali,gari mbili aina ya Noah zenye rangi nyeusi zikawasili pale hospitali akashuka mwanaume moja akajitambulisha kuwa wamefika pale kujua hali za ndugu zao ambao wamepata ajali ya gari.Waliruhusiwa kuingia ndani na kuegesha magari yao maegesho wakashuka wanaume watatu na wanawake saba ambao walikuwa wamevaa mavazi marefu ya kufunika uso na kuacha macho tu.Walikwenda mapokezi na kujulishwa kuwa wagonjwa waliopata ajali wamepelekwa katika chumba cha upasuaji na wakawataka watu wale wakasubiri nje ya chumba cha upasuaji kulikokuwa na sehemu ya kupumzika.Baada ya muda mfupi zikawasili gari nyingine mbili nao wakadai pia ni ndugu wa majeruhi wa ajali ya gari walioletwa pale.Waliruhusiwa kupita na mara tu walipofunguliwa geti kuingia ndani vioo vya gari la nyuma vikafunguliwa na mitutu ya bunduki zilizofungwa viwambo vya sauti ikajitokeza na walinzi wote waliokuwa getini wakamiminiwa risasi.Magari yale yakasimama wakashuka watu wanne na kuwamalizia kwa risasi walinzi wawili waliokuwa ndani ya chumba cha walinzi kisha wakawakusanya wale walinzi wote waliouawa kwa risasi na kuwafungia katika kile chumba.Mmoja wao akachukua simu na kupiga “We have control of the main gate”akasema Nje ya chumba cha upasuaji jamaa mmoja aliyevaa kanzu ya kijivu alimaliza kuzungumza na mtu simuni akaiweka mfukoni halafu akamsogelea jamaa mmoja akampa maelekezo na bila kupoteza muda akaelekea katika mlango wa chumba cha upasuaji akakinyonga kitasa lakini ulikuwa umefungwa kwa ndani akagonga kwa nguvu na baada ya dakika mbili ukafunguliwa na muuguzi ambaye alingiwa na baridi ya ghafla baada ya kujikuta akitazamana na mtutu wa bunduki uliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti.Haraka haraka watu sita waliovaa mavazi ya kufunika nyuso zao wakionekana kama wanawake wakaingia ndani ya chumba cha upasuaji na kutoka ndani ya mavazi yao wakachomoa bunduki walizokuwa wameshika.Yule kiongozi wao akaachia risasi na kuisambaratisha taa kubwa inayotumika katika upasuaji kisha akawaamuru watu wote mle ndani kukaa pembeni ya meza zile za upasuaji.Madaktari na wauguzi waliokuwa ndani ya chumba kile walipatwa na mstuko mkubwa baada ya kuwaona wale majeruhi wa ajali waliokuwa wamelala vitandani wakiinuka baada ya wenzao kuingia mle ndani. Haraka haraka madaktari wakavuliwa mavazi na vitambaa walivyokuwa wamevaa midomoni vikaingizwa ndani ya midomo yao kuwazuia kupiga kelele kisha wote wakafungiwa katika chumba kimoja.Jamaa wawili wakavaa mavazi ya madaktari na wanawake wawili wkavaa sare za wauguzi.Mtu mmoja akalala katika kitanda cha wagonjwa kisha wakatoka wakikisukuma kitanda kile.Pembeni ya mtu yule aliyelala kitandani kama mgonjwa zilipangwa silaha na kufunokwa na shuka ili watu wasizione.Ndani ya chumba kile cha upasuaji walibaki watu wawili wakilinda ili asitokee mtu yeyote akaharibu operesheni kabla haijakamilika. Yeyote aliyewaona watu wale aliamini ni madaktari wakiwa na mgonjwa.Nyuma yao walifuatwa na watu wengine sita waliokuwa wamevaa mavazi marefu kama wanawake na kuficha nyuso zao wakionekana kama ndugu wa mgonjwa aliyekuwa anasukumwa katika kitanda.Walikuwa wanaelekea katika jengo kubwa maarufu kama jengo la wagonjwa binafsi ambako kuna wodi wanakolazwa watu wenye uwezo mkubwa kifedha pamoja na viongozi.Ni katika jengo hili ndiko alikolazwa Coletha mtoto wa rais.Kiongozi wa kundi lile akachukua simu na kupiga “Kila mtu akae katika nafasi yake tunakaribia kufika katika jengo” akasema yule jamaa na kukata simu.Jamaa aliyepewa maelekezo naye akatoa maelekezo kwa wenzake waliokuwa nje ya chumba cha upasuaji na taratibu wakaanza kutawanyika wakielekea katika jengo lile aliko mtoto wa rais. Lango la kuingilia jengola wagonjwa binafsi lilikuwa wazi na kitanda kile kikaingizwa ndani.Kulikuwa na meza ya mapokezi na wauguzi waliokuwepo pale wakastuka baada ya kuona kitanda kikiingizwa bila wao kupewa taarifa kama kuna mgonjwa anapelekwa ili waandae chumba.Kulitokea mabishano kidogo kati ya wauguzi wa ile wodi na wale jamaa mmoja wa wale wauguzi akataka kupiga simu lakini lilikuwa ni kosa kubwa kwani risasi kama mvua zilitoka kwa mmoja wa wale watu waliokuwa wamejitanda mavazi marefu akionekana kama mwanamke na ndani ya vazi lile alikuwa ameshika bunduki ndogo.Wakati wauguzi wakishughulikiwa,nje ya jengo walinzi wawili waliovaa sare za kampuni ya ulinzi walijikuta wakiminiwa risasi bila maelezo na watu waliovalia mavazi yale marefu.Haraka haraka wauguzi wale wakafichwa nyuma ya meza yao kubwa.Kiongozi wa magaidi wale akatoa simu na kupiga “Tunaelekea ghorofa ya juu”akasema Waliingia katika lifti na kuelekea ghorofa ya sita.Milango ya lifti ilipofunguka kulikuwa na watu watatu waliokuwa nje ya lifti wakiwa na kazi maalum ya kuwakagua watu waliokuwa wakiingia ghorofa ya sita kuhakikisha hakuna anayeingia na silaha.Hakukuwa na muda wa kuulizana kwani tayari ramani nzima tayari waliifahamu hivyo kabla wale walinzi hawajafanya chochote wakamiminiwa risasi za kustukiza halafu wakaingizwa na kufungiwa katika chumba cha pembeni.Safari ikaendelea wakisukuma kitanda kile na mara wakakutana na madaktari watatu waliostuka.Wakawasimamisha na kutaka kupata maelezo kuhusiana na mgonjwa yule aliyekuwa kitandani.Miongoni mwa madaktari wale alikuwemo Dr Stanslaus Mbeula ambaye ndiye anayeongoza jopo la madaktari wanaochunguza virusi alivyoambukizwa Coletha. “Mgonjwa huyu anakwenda wapi?Nani katoa ruhusa aletwe huku? Utaratibu wa hapa hamuufahamu?akauliza Dr Mbeula baada ya kuona maelezo ya wale jamaa yanajichanganya.Kitendo kile cha Dr Mbeula kuwafokea wale madaktari kwa kupeleka mgonjwa katika wodi ile bila kufuata utaratibu kikawavuta walinzi waliokuwa wakimlinda Coletha waliokuwa wamezagaa katika ghorofa ile ya sita.Ghafla wale magaidi waliovaa sare za madaktarina wauguzi wakabonyea chini ya kitanda na risasi zikaanza kuvuma kutoka kwa watu waliokuwa nyuma yao waliokuwa wamevaa mavazi marefu meusi,Dr Mbeula na wenzake wakaanguka chini.Kitendo kile kiliwastua walinzi wa Coletha ambao walianza kurusha risasi kuwaelekea wale jamaa.Yule mgonjwa aliyekuwa amelala kitandani akalitupa shuka pembeni na kuwapa nafasi wenzake waliokuwa chini ya kitanda kuchukua silaha.Wakati akijiandaa kushuka kitandani akapigwa risasi za kifua akaanguka juu ya kitanda na kufa hapo hapo.Mapambano makali yakaanza kati ya walinzi wa Coletha na wale magaidi. “Red six ! Red six !!..akasema mmoja wa walinzi wa Coletha akiwajulisha wenzake kuwa wamevamiwa. Bastora za walinzi wa Coletha hazikuwa na viwambo vya sauti hivyo milio ya risasi ilisikika na kuzua taharuki kubwa.Magaidi zaidi walikimbilia ndani ya jengo lile kuwasaidia wenzao wakiwa na bunduki nzito.Walinzi wa Coletha wakazidiwa nguvu na kuuawa.Kiongozi wa magaidi wale akaingia ndani ya chumba alimolazwa Coletha na kumkuta akiwa amekumbatiwa na msaidizi wake “Tafadhali naomba msituue!! http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Akalia yule msaidizi wa Coletha na bila huruma yule kiongozi wa magaidi akamchapa risasi na kumuua.Coletha akayafunika macho kwa mikono yake aliogopa sana “Usihofu Coletha hatutakuua.Tunakupeleka sehemu salama” akasema yule jamaa na kitanda kikaingizwa Coletha akapandishwa wakatoka haraka mle chumbani hadi kwenye lifti tayari kwa kushushwa chini.Hawakuiacha maiti ya mwenzao aliyeuawa kwa risasi.Baada ya kushuka chini kitanda alichopanda Coletha kikaanza kusukumwa kwa kasi kubwa kuelekea mahala yalikoegeshwa magari.Magaidi wale walikuwa wamejipanga vyema kukabiliana na hatari yoyote ambayo ingetokea.Baada ya kukamilisha kazi yao wakakimbilia katika magari yao na kuondoka.Mara tu walipovuka geti kuu la kuingilia hospitali mlipuko mkubwa ukatokea katika jengo la wagonjwa binafsi.Bomu lililipuka
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment