Simulizi : Siri
Sehemu Ya Pili (2)
HAIFA – ISRAEL Saa nane kasoro dakika ishirini kwa saa za Israel,mlango wa chumba alimolazwa Edger kaka ulifunguliwa na watu watano wakaingia wakiongozwa na mmoja aliyevaa koti la daktari,wawili wakabaki mlangoni.Edger alikuwa amelala fofofo yule jamaa mwenye koti la daktari akamuamsha. “Edger amka uzungumze na wageni wako” akasema yule jamaa aliyevaa koti la kidaktari.Edger akafumbua macho na kukuta kuna watu mle chumbani akainuka na kukaa akafikicha macho ili aweze kuona vizuri. Miongoni mwa watu wale alikuwemo mwanamama aliyejitanda ushungi kichwani. Baada ya Edger kuinuka na kukaa watu watatu wakatoka mle chumbani na kuwaacha watu wawili tu.Yule mwanamama akavua ule ushungi aliokuwa amejitanda na uso wa Edger ukachanua kwa tabasamu pana “Mama ! akasema Edger na kuinuka akaenda kumkumbatia mama yake “Edger ! Akasema mwanamama yule ambaye ni Habiba Jawad.Walikumbatiana kwa dakika mbili halafu Edger akapeana mkono na mtu aliyekuwa pembenmi “Sayid Omar,nafurahi kukuona” akasema Edger “Pole sana Edger” akasema Sayid.Edger akawakaribisha wageni wake katika sofa lililokuwamo mle chumbani “Mama nimefurahi sana kukuona.Ahsante kwa kuja kunitembelea” akasema Edger “Hata mimi nimefurahi sana kukuona Edger.Imenilazimu kufanya kila niwezalo kuja kukuona mwanangu.Nimeumizwa sana na hawa washenzi waliotaka kuyaondoa maisha yako.Ninakuahidi kwamba wote walioshiriki katika jaribio hili la kukuua tutawasaka na hakuna atakayebaki salama.Najua ni mtandao mkubwa wa maadui zako ambao hawalali wakipanga mipango ya kukuangamiza” akasema Habiba Jawad “Jaribio lao limeshindwa.Hali yangu ni nzuri kwa sasa” akasema Edger “Edger napenda pia kukuhakikishia kwamba kwa sasa kuwa na amani kwani uko salama.Kama alivyosema Habiba mtandao wa maadui zako ni mkubwa na walituma watu wao kukufuata hadi huku kutafuta namna ya kukumaliza.Watu waliotumwa kukufuatilia walitega vifaa humu chumbani kwako bila wewe kujua.Walitega kamera za siri na walikuwa wanaangalia kila unachokifanya,vilitegwa vifaa vingine pia ambavyo viliweza kunasa mawasiliano yako yote uliyokuwa unayafanya na kuwatumia wakuu wao.Ni mtandao mkubwa uliowahusisha pia watu wakubwa serikalini lakini taarifa nzuri ni kwamba tayari tumekwisha ubaini mtandao huo na tayari hatua za haraka za kuuondoa zimeanza na hivi tuongeavyo vijana wako kazini wakiendelea na kazi ya kuusafisha na hatabaki mtu yeyote tutahakikisha wote tumewasafisha” akasema Sayid Omar “Nashukuru sana Sayid kwa kuweza kulitambua hilo kwa haraka kwani mimi sikuwa na mawazo kama wangeweza kunifuata hadi huku.Unaweza ukanitajia baadhi ya watu waliomo katika mtandao huo niwafahamu? akauliza Edger “Hapana Edger sintaweza kukutajia kwa sasa lakini ninachoweza kukushauri ni kuwa makini sana.Kuanzia sasa usimuamini mtu yeyote yule.Yule unayemuamini ndiye huyo atakayekuingiza kwenye shimo la moto hivyo jaribu kuchagua watu wachache wa kuwaamini na kuwaweka karibu.Mipango yako usimueleze mtu ambaye hauna imani naye.Umenielewa Edger? Akauliza Sayid “Nimekuelewa Sayid” akajibu Edger “Edger” akaita Habiba “Naam mama” “Hiki kilichotokea kimezidi kutupa sababu ya wewe kugombea urais.Hadi sasa tayari umekwisha jenga maadui wengi na mtandao wao unazidi kutanuka na kila uchao wanapanga kukuangamiza.Wakati umefika kwa wewe kugombea urais.Hatuna tena muda wa kusubiri kwani tunavyoendelea kuvuta muda na kusubiri zaidi maadui zako wanaendelea kujipanga zaidi namna ya kukuangamiza.Edger tumekuandaa kwa muda mrefu kwa ajili ya nafasi hiyo na mpaka hapa tulipofika maandalizi yetu yanakwenda vizuri.Tayari umekwisha tengeneza wafuasi wengi ambao ndio mtaji mkubwa kwa mwanasiasa kushinda chaguzi.Nguvu yako ni kubwa na unazidi kuwapa hofu maadui zako.Kwa upande Fulani ninawashukuru hawa waliofanya jaribio hili la kukuua kwani wametufanya na sisi macho yetu yafumbuke zaidi na kung’amua kwamba wakati umefika.Ninashukuru Edger kwa kukubali kugombea urais kwani ile mipango yetu yote inakwenda kutimia” akasema Habiba “Mama sikuwa nimepanga kugombea urais kwa wakati huu,mipango yangu ilikuwa nigombee baada ya miaka mitano ijayo lakini kwa hili lililojitokeza na kwa ushauri nilioupata kutoka kwa Sayid nimeamua kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.Uko sahihi kwamba tayari nimekuwa na maadui wengi na wanaongezeka kila uchao na njia pekee ya kuweza kuwashinda maadui zangu ni kwa kuwa rais.Nina uhakika mkubwa wa kushinda uchaguzi kutokana na mtaji mkubwa wa wafuasi nilio nao.Tayari nimejenga jina kubwa na wananchi wengi wananiamini na nina hakika nitashinda kwa ushindi mkubwa. Lakini …”akanyamaza kidogo “Lakini nini Edger?akauliza Habiba “Nimeamua nitagombea kupitia chama cha upinzani cha Democratic ambacho tayari mazungumzo yamekwisha anza ili niweze kujiunga nao” “Hapana Edger” akasema Habiba “Hautagombea urais kupitia chama cha upinzani.Utagombea urais kupitia chama chako.Kuhama chama kunaweza kuzusha maswali mengi,utaonekana u mroho wa madaraka.Kampeni za rais ni gharama kubwa hivyo basi kwa vyama vidogo kama hicho unachotaka kuhamia lazima kitachunguzwa sana namna kilivyoweza kugharamia kampeni na wanaweza wakagundua mambo ambayo hatutaki yajulikane.Ukiwa ndani ya chama chako hakuna atakayeweza kukuhisi chochote kwani kampeni zako zitagharamiwa na chama chako ambacho ni kikubwa na kina rasilimali za kutosha hivyo basi utaendelea kugombea urais lakini kupitia chama chako”akasema Habiba Jawad “Mama hayo uyasemayo ninayafahamu na hata mimi ningependa sana kugombea urais kupitia chama changu lakini kuna tatizo ndiyo maana nikafikiria kuhama chama” “Kuna tatizo gani Edger?akauliza Sayid Omar “Tatizo ni kwamba nguvu yangu kubwa iko nje ya chama.Ndani ya chama sina nguvu kubwa na sina uhakika kama ninaweza kuteuliwa na chama kugombea.Kuna mchuano mkubwa ndani ya chama vigogo wenye nguvu wakichuana nani achaguliwe kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao.Kama nguvu yangu ingekuwa kubwa chamani ningekubaliana nawe mama lakini nguvu yangu kubwa iko nje ya chama ndiyo maana nikafikiria kuhama chama na kujiunga na chama kingine ili niweze kutumia nguvu yangu ya nje kushinda urais.Nikiwa ndani ya chama changu ninawahakikishia kwamba sintaweza kufika kokote” akasema Edger “Edger wasi wasi wangu ni kwamba kuhama chama kutakupunguzia mvuto.Ushauri wangu ni kwamba endelea kubaki ndani ya chama chako ila unachohitaji ni kuunda timu yenye nguvu ambayo itakuwezesha wewe uweze kuteuliwa ndani ya chama kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu ujao wa rais.Tutaunganisha baadhi ya vigogo wenye ushawishi chamani na watakubali kwani kinachoongea ni fedha.Tuachie sisi suala hilo tutalishughulikia lakini achana kabisa na mipango yoyote na vyama pinzani.Utagombea urais kupitia chama chako na utashinda” akasema Habiba “Mama nimeamua kugombea urais kupitia chama cha upinzani kwa sababu mimi ndiye niliye ndani ya chama na ninafahamu kinachoendelea ninafahamu fitina zilizopo ndani ya chama hivyo naombeni mkubaliane nami nijiunge na chama cha upinzani.Msihofu kitu kwani ninao mtaji mkubwa wa wafuasi na kokote nitakakoenda watanifuata.Wote wanafahamu namna ninavyoikososa serikali na kupambana na mafisadi ndani ya chama changu na wananiunga mkono.Kitendo cha mimi kuwekewa sumu pia kitakuwa ni kigezo kikubwa sana cha mimi kuhama chama na nitakapowaeleza wananchi wataniamini” akasema Edger.Habiba na Sayid wakatazamana kwa muda kisha Habiba akasema “Tunakwenda kulijadili suala hili tuone ipi itakuwa njia bora zaidi ya wewe kugombea urais aidha ukiwa ndani ya chama chako au ukiwa nje ya chama.Jibu tutakalopata tutakujulisha.Edger nimefurahi nimekuona na yawezekana hatutaweza kuonana tena kwani usalama wetu ni mdogo sana hapa Israel lakini tutaendelea kuwasiliana kama kawaida” akasema Habiba na kumkumbatia Edger wakaagana. “Sayid ameniambia kwamba walitumwa kuja kunichunguza ni watu wangu wa karibu,ni akina nani hao?Watu nilio nao karibu hapa hospitali ni Olivia na Judy je kuna mmojakati yao ametumwa kunichunguza?Nahisi labda anaweza kuwa Judy kwani sidhani kama Olivia anaweza akafanya hivyo.Yeye ndiye aliyenileta hapana kuokoa maisha yangu.Nilishuhudia vifaa vile vilivyotolewa humu chumbani vilivyotegwa kunifuatilia nina hofu kama wameweza kunasa mawasiliano yangu na Sayid wanaweza wakaniharibia kabisa mipango yangu yote ya kuwania urais.Wakigundua kwamba Sayid ni mfadhili mkubwa wa kikundi cha IS jina langu litachafuka mno na kitakuwa ni kifo changu cha kisiasa.Sitaki siri yangu ijulikane hadi hapo lengo langu litakapotimia.Sayid amenihakikishia kwamba wanalifuatilia suala hili na mtandao wote wataufagia.wanatakjiwa wafanye haraka sana kuufagia mtandao huu kabla hawajaleta madhara” Kichwa cha Edger kilikuwa na mawazo mengi sana baada ya Habiba na Sayid kuondoka pale hospitali TEL AVIV – ISRAEL Saa tatu za asubuhi katika chumba kimoja ndani ya jengo la makao makuu ya shirika la ujasusi la Israel Mossad, watu wanne walikuwa ndani ya chumba cha mikutano wanamsubiri mkurugenzi mkuu wa shirika hilo kwa ajili ya kikao muhimu.Mkurugenzi mkuu ambaye alikuwa njiani akitokea nyumbani kwake aliwasili ndani ya muda mfupi baada ya kupewa taarifa kwamba anahitajika kwa jambo muhimu la usalama wa taifa.Yitzhak Zamir mkurugenzi mkuu wa Mossad alipowasili katika chumba kile akaomba wajielekeze moja kwa moja katika kile kilichowakutanisha pale kwani alikuwa na mazungumzo na waziri mkuu saa tano asubuhi. “Mkurugenzi tumelazimika kukuita hapa asubuhi hii kuhusiana na suala muhimu” akasema David Shiloah na kumfanyia ishara Yair aendelee kutoa maelezo “Siku chache zilizopita rais wa Tanzania alimpigia simu waziri mkuu na kuomba mgonjwa wake ambaye ni mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyekuwa mahututi,aruhusiwe kuingia hapa nchini kupata matibabu.Kutokana na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Israel waziri mkuu alitoa maelekezo kwa mgonjwa huyo kuruhusiwa kuingia nchini kutibiwa na alipoletwa hapa nchini alipelekwa Haifa katika hospitali ya Rambam.Wakati wakimpatia matibabu madaktari waligundua kwamba mbunge alipewa sumu.” Yair akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Dr Olivia Themba kutoka hospitali kuu ya moyo nchini Tanzania ambaye ndiye aliyeambatana na mgonjwa huyo alimjulisha spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania suala hilo la Edger kuwekewa sumu na spika akamjulisha waziri mkuu.Inahisiwa sababu ya kutaka kuuawa kwa mbunge huyo ni chuki za kisiasa kwani amekuwa ni mahiri sana katika kufichua ufisadi unaofanywa nchini mwake hasa na watu wakubwa serikalini hivyo amejijengea maadui wengi.Baada ya kupata taarifa kuwa Edger aliwekewa sumu waziri mkuu wa Tanzania aliamua kuchukua hatua za kumlinda kwa kuhofia kwamba watu waliotaka kumuua wangeweza kumfuata hata kule Israel kummalizia.Nina urafiki na waziri mkuu wa Tanzania,aliwahi kunisaidia kupata hifadhi Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja nilipokuwa nawafuatilia wale magaidi waliokwenda kujificha Zanzibar.Kutokana na urafii wetu alinipigia simu akaniomba nimsaidie mmoja wa vijana wake ambaye atamtuma hapa Israel kumlinda Edger.Niliwasilisha suala hili kwa kiongozi wangu David nikamueleza na yeye akanipa ruhusa na kufanya hivyo.Nilifanya maandalizi na Dickson alipokuja hapa nilimpeleka katika ile hospitali akiwa kama mgonjwa kutokea nchini Zimbabwe.Dickson aliweka kamera za siri katika chumba cha Edger na aliweza kuona kila kinachofanyika ndani ya chumba kile.Usiku wa kuamkia jana watu wawili mwanamke na mwanaume waliingia ndani ya chumba cha Edger lakini hawakuweza kuongea naye kwa kuwa alikuwa amelala fofofo.Dick alinitumia picha za mwanamke yule akinitaka nimsaidie kumtambua na nilipomuona tu nilistuka baada ya kumuona mwanamke yule ni Habiba Jawad” “Habiba Jawad? Yitzhak akastuka “Ndiyo mkurugenzi” akajibu Yair “Mna uhakika ni mwenyewe Habiba Jawad?akauliza Yitzhak. “Ndiyo mkurugenzi.Tuna uhakika ni mwenyewe” akasema Yair na kutoa picha kutoka katika faili lililokuwa mbele yake akampatia mkurugenzi wake akazipitia “Endelea” akasema Yitzhak “Aliposhindwa kuzungumza na Edger,Habiba alimuachia ujumbe uliokuwa katika bahasha.Dick aliichukua bahasha ile akakuta kuna namba za simu ambazo Edger alielekezwa apige.Alinipigia simu na usiku ule ule bila kupoteza muda nilifika pale hospitali.Tuliamua kupiga namba zile za simu Habiba alizomuachia Edger ili kufahamu mahala alipo.Nilifanikiwa kupata simu ambayo ingetusaidia kufahamu mahala aliko Habiba na Dick akaitumia kupiga zile namba alizoacha Habiba lakini baada ya simu kupokelewa Habiba aligundua kwamba yule hakuwa Edger akakata simu haraka hivyo hatukuweza kujua mahala alipo.Hakukata tamaa Dick aligundua kwamba Edger alikuwa anatumia kompyuta yake kuwasiliana na watu wake muhimu kwa kutumia mtandao wa Skype hivyo siku iliyofuata Dick akafanikiwa kuipata kompyuta ya Edger na kugundua kwamba amekuwa na mawasiliano na Sayid Omar” “Sayid Omar bin Abdullah?akauliza Yitzhak “Ndiyo mkurugenzi.Edger amekuwa na mawasiliano naye”akajibui Yair “Sasa nimepata picha nzuri.Kwa mujibu wa taarifa za uchunguzi tulizonazo ni kwamba Habiba na Sayid ni washirika wakubwa na Sayid anatumiwa na Habiba katika kufadhili kikundi cha IS ambacho kinaendeleza harakati zake sehemu mbalimbali duniani.Kama huyo Edger ana mawasiliano na Sayid na akatembelewa hospitali na Habiba hii inatuhakikishia kwamba huyo mbunge ana mahusiano ya karibu sana na watu hao.Inashangaza sana kwa mbunge huyo kuwa na mahusiano na watu hawa hatari.Serikali ya Tanzania wanafahamau chochote kuhusiana na suala hili? Idara ya ujasusi Tanzania wanafahamu kama mmoja wa wabunge wa nchi yao ana mahusiano na watu wanaofadhili mtandao wa IS?akauliza Yitzhak “Hapo ndipo penye tatizo mkurugenzi.Dick alitumwa na waziri mkuu wa Tanzania kuja kumlinda Edger kwa siri na suala hili limejitokeza wakati akiendelea kutimiza jukumu lake la kumlinda Edger na hajamueleza mtu yeyote nchini Tanzania.Nilimshauri asimjulishe mtu yeyote bali tuendelee kufanya uchunguzi na kufahamu kinachoendelea kati ya Edger na hawa watu wa IS.Kwa bahati mbaya sana kabla hatujafika mbali na uchunguzi wetu Edger amefariki dunia” “Amefariki? Yitzhak akashangaa “Ndiyo amefariki dunia jana usiku na inadaiwa kwamba chanzo cha kifo chake ni kupanda ghafla kwa shinikizo la damu lakini hizo ni sababu tu naamini kabisa Dick ameuawa na IS.Nina uhakika waligundua kwamba alikuwa anamfuatilia Edger na wakamuua.Kulithibitisha hilo waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ndiye aliyemtuma Dick kuja hapa Israel kumlinda Edger naye pia ameuawa asubuhi ya leo katika mlipuko wa bomu lililotegwa nje ya ofisi yake.Naamini kabisa kwamba IS ndio waliofanya shambulio hilo kwa ajili ya kuficha siri ya Edger isigundulike.Waligundua kwamba Edger amekuwa na mawasiliano na waziri mkuu hivyo wakaamini kwamba lazima atakuwa amemueleza kuhusiana na Edger kukutana na Habiba hivyo wakalazimika kuwaua wote” akasema Yair “Habiba Jawad amekuwa akimtumia Sayid Omar kufadhili kikundi cha IS ambacho kimekuwa kinaendesha mauaji ya watu ndani ya ardhi ya Israel.Nimeshangazwa na kitendo cha watu hawa wawili kuingia nchini mwetu bila ya mamlaka kufahamu na kuwatia nguvuni.Nalazimika kuamini kwamba kuna watu ndani ya serikali ambao wamewasaidia watu hawa kuingia humu nchini na hadi kufika hospitali kuonana na Edger.Uchunguzi mkali sana unatakiwa kufanywa katika hili na kuwabaini hawa watu wanaoshirikiana na IS” akasema Yitzhak kwa ukali “Kitendo cha huyu mbunge kukutana na watu hawa wawili kinadhihirisha wazi kwamba wana mahusiano ya karibu na ninahisi kwamba yawezekana naye akawa ni mwanachama wa kikundi cha IS kwani kikundi hiki kina wanachama wengi na wamekuwa na wakipandikiza watu wao ndani ya serikali mbali mbali na ninaamini hata ndani ya serikali yetu wana watu wao ndiyo maana watu hawa wawili Habiba na Sayid wameweza kuingia nchini Israel bila mamlaka kuwa na taarifa.Ninashawishika kuamini kwamba huyo mbunge naye ni mmoja wa watu walipandikizwa na IS ndani ya serikali ya Tanzania.Nini mnafikiria kukifanya?akauliza Yitzhak “Tumelifikisha kwako suala hili tunasubiri maelekezo yako mkurugeni” akasema David.Yitzhak akatoa sigara akawasha na kuvuta mikupuo kadhaa halafu akasema “Tunamuhitaji sana Edger.Tumekuwa tunawatafuta Sayid na Habiba kwa muda mrefu na huyu anaonekana ni mtu wao wa karibu sana hadi wamehatarisha usalama wao kwa kuingia hapa Israel kuja kumtembelea hospitali.Hiki walichokifanya kinatuhakikishia kwamba huyu ni mtu wao wa muhimu sana hivyo basi tukimpata atatusaidia kwanza kufahamu walipo Habiba na sayid na pili kufahamu mambo mengi ya IS pamoja na mipango yao mbali mbali.Tuanze mikakati ya kuhakikisha kwamba tunampata huyu kijana.Yair utasimamia hili zoezi.Weka watu pale hospitali ambao watafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea kwa huyu jamaa.Chunguzeni watu anaokutana nao na kama akionekana Habiba au mtu mwingine yeyote watakayemtilia shaka basi wakujulishe haraka sana” akasema Yitzhak na kumgeukia David “David nataka iandaliwe operesheni maalum ya kumpata Edger.Nataka ufanyike uchunguzi kujua lini Edger atarejea nyumbani Tanzania.Operesheni kubwa iandaliwe ya kwenda kumchukua Edger nchini Tanzania muda mfupi atakapowasili akitokea huku Israel.Nasema ni operesheni nzito kwa sababu nataka Tanzania na dunia nzima wajue kwamba Edger amefariki dunia.Huyu ni mtu muhimu sana kwetu na serikali ya Tanzania haipaswi kufahamu chochote kuhusu operesheni hii kubwa tunayokwenda kuifanya.Uwezo wa kufanya operesheni kubwa kama hiyo tunao kwani shirika letu la ujasusi ni shirika kubwa na lenye uwezo mkubwa kabisa wa kufanya chochote katika nchi yoyote duniani. Tumekwisha fanya operesheni kubwa katika nchi mbali mbali duniani na hatujawahi kushindwa hivyo basi hatuwezi kushindwa pia katika operesheni hii.Hii ni operesheni muhimu sana na ipewe uzito mkubwa.Ninakwenda kuonana na waziri mkuu nitazungumza naye kuhusu suala hili ili atupe kibali chake na nitakaporejea nataka nikute mpango maalum umekwisha andaliwa namna operesheni hii itakavyoendeshwa” akasema Yitzhak na kuwaachia jukumu lile David na Yair kuandaa operesheni ile ya kumpata Edger
TANZANIA Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alilazimika kukatisha ratiba ya shughuli zake zote jijini Dar es salaam baada ya kupata taarifa za mlipuko uliotokea jijini Dodoma na kumuua waziri mkuu.Muda mfupi kabla ya kupokea taarifa ile ya kuuawa kwa waziri mkuu,rais alipokea taarifa kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini akimjulisha kuhusu mauaji ya mkubwa Donald Nkebo aliyekutwa ameuawa kwa kupigwa risasi katika nyumba moja yeye pamoja na watu wengine watano.Taarifa ya kuuawa Donald Nkebo ilimstua mno rais kwani ni mtu aliyekuwa anamtegemea sana katika kufanikisha mipango ya kuwamaliza wapinzani wake kisiasa.Rais alimuagiza mkuu wa jeshi la polisi nchini kuhakikisha kwamba analiagiza jeshi lake kufanya kila linalowezekana kuwapata watu waliofanya mauaji yale ya Donald Nkebo na vijana wake.Akiwa bado katika mstuko mkubwa wa kuuawa Donald Nkebo rais alizidi kutikiswa baada ya kupewa taarifa ya waziri mkuu kuuawa katika mlipuko.Ilikuwa ni taarifa mbaya sana kuipokea kwa siku ile.Mara tu baada ya kupata taarifa zile alilazimika kuitisha kwa haraka kikao cha baraza kuu la usalama la taifa.Kikao kile kiliwajumuisha yeye rais,makamu wa rais,rais wa Zanzibar ambaye alifika kwa haraka baada ya kupewa mwito wa kuwepo kwa kikao kile,alikuwepo pia makamu wa rais wa Zanzibar vile vile walikuwepo wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi. “Ndugu zangu ninawashukuru sana kwa kufika kwenu kwa haraka mara tu baada ya kupokea mwito.Kabla ya yote ninapenda tusimame kwa dakika moja tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika mashambulio yaliyotokea leo jijini Dodoma na katika mauaji mengine yaliyotokea hapa Dar es salaam” akasema Dr Evans kisha wote wakasimama kuwaombea marehemu wote waliofariki katika mashambulio yale mawili. “Ndugu viongozi wenzangu sijui nianzie wapi,lakini naomba nikiri kwamba nimetikiswa” akasema rais na kunayamza kidogo “Nilipigiwa simu na mkuu wa jeshi la polisi alfajiri ya leo akanipa taarifa kwamba mmoja wa wafanya biashara wakubwa hapa nchini Donald Nkebo amekutwa katika nyumba Fulani ameuawa pamoja na watu wengine watano.Donald ni mtu anayefahamika sana hapa nchini ni mmoja wa wawekezaji wakubwa ana viwanda vyake kadhaa na biashara nyingine kubwa kubwa na vile vile ni mmoja kati ya wafadhili wakubwa wa chama chetu.Binafsi ni mtu ambaye ninamfahamu na kumheshimu sana hasa kutokana na mchango wake mkubwa katika uchumi wetu.Mazingira ya kifo chake yalinistua sana na nikampa maelekezo mkuu wa jeshi la polisi kuhakikisha watu waliofanya mauaji hayo wanapatikana.Mpaka sasa kuna chochote ambacho kimepatikana kuhusiana na mauaji hayo?akauliza Dr Evans. “Mkuu,mara tu baada ya jeshi la polisi kupata taarifa za mauaji yale na kuyathibitisha nilikutaarifu na ukanipa maelekezo,tayari tumekwisha fungua jalada la uchunguzi na vijana wako kazini wakiendelea na kazi.Mimi mwenyewe baada ya kupokea taarifa hiyo niliondoka na kwenda eneo la tukio kuthibitisha kwani Donald ni mtu niliyekuwa nikifahamiana naye sana tulikutana tukiwa chuo kikuu cha Dar es salaam na toka hapo tumeendelea kuwa marafiki wakubwa.Mheshimiwa rais tunaendelea kuchunguza nyumba ile yalimofanyika mauaji kujua shughuli gani zilizokuwa zinaendelea kwani kumekutwa vifaa mbali mbali vya mawasiliano na inaonekana kulikuwa na kompyuta kadhaa lakini zote zimeondolewa.Inaonekana baada ya kutekeleza mauaji yale wauaji waliondoka na kompyuta zote zipatazo kumi.Tunahisi kuna kitu katika hizo kompyuta ndiyo maana zikachukuliwa na wauaji.Vile vile wauaji walichukua simu zote za watu waliowaua.Donald amekutwa akiwa ameuawa ndani ya gari akiwa amevaa mavazi ya kulalia,inaonekana aliondoka nyumbani kwake na kwenda katika nyumba ile usiku hivyo tunataka kujua mahusiano yake na wale watu waliouawa.Mheshimiwa rais timu maalum kutoka makao makuu iko kazini hivi sasa na nitakutaarifu kila pale nitakapopata taarifa yoyote kutoka kwao” akasema inspekta jenerali wa polisi “Kabla taarifa hiyo niliyopokea kutoka kwa IGP haijapoa nikapokea tena taarifa nyingine ya kifo cha waziri mkuu..” akasema Dr Evans na kuinamisha kichwa “I’m sorry,kifo cha waziri mkuu kimeniumiza mno” akasema Dr Evans naukimya ukatawala ndani ya chumba kile.Kila mmoja alikuwa na uso wenye simanzi. “Wakuu wote wa vyombo vya usalama mko hapa nataka kujua nini kimetokea Dodoma hadi bomu likategwa katika ofisi ya waziri mkuu na kumuua.Mmekwisha wajua watu waliofanya tukio hilo ni akina nani?akauliza Dr Evans na kuwatazama wakuu wale wa vyombo vya usalama “Inspekta jenerali tuanze na wewe.Jeshi la polisi ndio wanaolinda ofisi zote kuu za serikali.Imewezekanaje watu wakaingia na kutega bomu wakati jengo lile lina ulinzi saa ishirini na nne bila polisi kugundua?Askari wako walikuwa wapi?akauliza Dr Evans kwa sauti kali kidogo “Mheshimiwa rais ni kweli jengo la ofisi ya waziri mkuu linalindwa na askari polisi kwa saa ishirini na nne na kilichotokea kimetustua hata sisi ngazi za juu na tumejiuliza swali hilo hilo imewezekanaje hawa watu wakapenya na kutega mabomu katika geti la ofisi ya waziri mkuu ambako kuna ulinzi wa saa ishirini na nne?Askari wetu walikuwa wapi? Mheshimiwa rais ni mapema sana kupata majibu ya maswali haya kwani uchunguzi ndiyo kwanza umeanza,tayari timu maalum ya makachero mahiri kabisa ndani ya jeshi la polisi wamekwisha tua jijini Dodoma na tayari wameanza uchunguzi kuhusiana na tukio hili na mimi mwenyewe baada ya kumalizika kwa kikao hiki ninakwenda Dodoma kujua nini hasa kilichotokea na nitahakikisha ndani ya muda mfupi tunapata majibu” akasema Inspekta jenerali wa polisi.Ukimya ukapita tena halafu Dr Evans akasema “Idara ya kupambana na ugaidi ni kazi yenu kudhibiti matukio kama haya ya ugaidi,mlikuwa wapi na kuacha shambulio hili likatokea? Shambulio kama hili si la kupangwa kwa siku moja,lazima limechukua muda kuandaliwa.Ninyi kama idara yenye jukumu la kuzuia mambo kama haya yasitokee hamkuwa na viashiria vyovyote vilivyowaonyesha kwamba shambulio kama hili linaweza kutokea?Mmeshindwaje kubaini jambo kama hili kutokea hasa katika sehemu nyeti kama ofisi ya waziri mkuu?akauliza Dr Evans kwa ukali “Mheshimiwa rais” akasema Genevieve Nelson mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi. “Idara yangu haikuwa na taarifa zozote za kuweza kutokea kwa shambulio lile.Tayari idara yangu imekwisha ingia kazini kuwatafuta wale wote waliofanya tukio hili tukishirikiana na vyombo vingine.Timu ya watu nane tayari wamekwisha wasili jijini Dodoma.Nina uhakika mkubwa kwamba hadi kufika mchana wa leo tutakuwa tumepata jibu zuri la nani waliofanya shambulio hilo”akasema Genevieve “Kwa idara hii muhimu sana kushindwa kubaini kuwepo kwa shambulio hili ni udhaifu mkubwa sana.Najiuliza kama leo wameweza kutega bomu katika ofisi ya waziri mkuu bila chombo chochote kung’amua je watashindwa kuingia na kutega bomu ikulu?Kuna umuhimu gani wa kuwa na idara ya kudhibiti ugaidi ikiwa magaidi wanawza kupenya hata katika ofisi nyeti za serikali na kufanya mashambulio?akauliza Dr Evans kwa ukali akiwatazama wakuu wale wa vyombo vya usalama “CDF kuna nini upande wako? Akauliza Dr Evans “Baada ya kupata taarifa za tukio hilo nimeelekeza timu ya wataalamu wa mabomu ifike haraka sana eneo la tukio na tayari wako eneo la tukio wakisaidiana na wataalamu kutoka jeshi la polisi kukusanya kila kitu kwa ajili ya uchunguzi kubaini ni bomu la aina gani lililotumika na limetengenezwa wapi.” akasema mkuu wa majeshi.Ilimchukua Dr Evans dakika chache za kutafakari kisha akasema “7 Agosti 1998 tulionja adha ya mashambulio ya kigaidi baada ya ubalozi wa marekani hapa nchini kulipuliwa.Watu 11 walipoteza maisha na wengine 85 walijeruhiwa.Leo kwa mara ya pili tena magaidi wanatushambulia na safari hii wakimlenga kiongozi mkubwa kabisa wa serikali ambaye ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Hili ni jambo lisilokubalika na linaumiza sana.Damu ya watu hawa imepotea bila hatia yoyote.Nataka vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchi hii mshirikiane na muhakikishe kwamba watu hawa waliofanya unyama wa namna hii wanapatikana haraka sana na watueleze nini sababu ya kufanya hivi.Wametuchokoza na hatuwezi kukaa kimya.Yeyote aliyetuchokoza lazima apate majibu yake.Awe ni mtu,kikundi cha watu au taifa lazima ajulikane na apate stahili yake kwa unyama huu waliotufanyia.Nataka tutume ujumbe kwa dunia kwamba Tanzania si sehemu salama kwa magaidi na wale wote wenye kufikiria kufanya mashambulio katika ardhi yetu wasithubutu kufanya hivyo tena.Kwa kuwa bado ni mapema sana na hatuna taarifa zozote za nani wamefanya shambuliohili nataka tukutane tena hapa saa kumi na moja jioni na mpaka wakati huo kila mmoja aje hapa akiwa na taarifa idara yake imefikia wapi katika kuwatambua magaidi waliofanya unyama huu kwenye ardhi yetu” akasema Dr Evans na wajumbe wa kikao kile wakatawanyika na kuwaacha Dr Evans,makamu wa rais na rais wa Zanzibar katika mazungumzo mazito MAZISHI YA KITAIFA - BAADA YA SIKU 3 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ulifurika pomoni katika mazishi ya kitaifa ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyefariki katika mlipuko wa bomu jijini Dodoma.Viongozi kutoka nchi mbali mbali za Afrika waliwasili kuhudhuria mazishi yale ya kitaifa.Rais wa jamhuri ya muunganoi wa Tanzania Dr Evans akiwa na mke wake waliwasili katika uwanja wa taifa tayari kuwaongoza watanzania katika shughuli ile.Dakika chache baada ya rais kuwasili,mwili wa waziri mkuu ukaingizwa uwanjani kwa ajili ya kuagwa. Viongozi wa dini walifungua shughuli ile kwa kusoma dua kisha zikafuata salamu kutoka kwa wakuu mbali mbali wa nchi waliohudhuria mazishi yale na hatimaye ukafika wakati ambao rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akapewa nafasi ya kuhutubia hadhira ile kubwa ya watanzania waliofika kumuaga waziri mkuu. “Ndugu watanzania na wageni wetu mliotoka katika mataifa jirani kuja kuungana nasi katika mazishi haya ya kitaifa,awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kutukutanisha hapa sote siku ya leo katika shughuli hii ya kumuaga mpendwa wetu mheshimiwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania” Dr Evansa akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Dakika thelathini kabla ya uhai wake kukatishwa kikatili,nilizungumza naye na nikampa maelekezo katika mambo kadhaa na nilimuahidi kwamba mwisho wa wiki tungekutana jijini Dodoma.Nusu saa baada ya kuzungumza naye nilipewa taarifa za kifo chake,nilipatwa na mstuko ambao siwezi kuuelezea.Kifo hiki kimenigusa sana mimi binafsi,watanzania wote kwa ujumla na wapenda amani kote duniani.Nimepokea salamu za rambi rambi kutoka kwa mataifa mengi duniani wote wakiguswa na msiba huu mkubwa,nawashukuru sana nyote mliotufariji katika wakati huu mgumu” rais akanyamaza tena kidogo na kuendelea “Hakuna maneno mazuri ya kumuelezea mpendwa wetu huyu kwani hakuna asiyefahamu utendaji wake wa kazi.Binafsi amekuwa msaada mkubwa sana kwangu na serikali ninayoiongoza.Amekuwa msimamizi mzuri wa shughuli zote za serikali kwa umakini na weledi mkubwa sana.Muda hautoshi kumuelezea mpendwa wetu huyu itoshe tu kusema kwamba utendaji wake wa kazi ulitukuka na tumempoteza mtu muhimu mno. Kutokana na utendaji kazi wake http://deusdeditmahunda.blogspot.com/uliotukuka na uadilifu usio na kifani,alitengeneza maadui wengi wa ndani na nje ya nchi hasa wafujaji wa fedha za serikali,mafisadi na wahujumu uchumi.Hakusita kukemea ubadhirifu na kuchukua hatua stahiki kila pale alipoubaini.Maadui hawa aliowatengeneza hawakuona namna nyingine ya kupambana naye zaidi ya kuitoa roho yake.Walichokifanya ni unyama uliopitiliza na haukubaliki.Ninatuma salamu kwa wale wote waliofanya kitendo hiki,awe ni mtu,kikundi cha watu wa ndani au nje ya nchi siku zenu zinahesabika.Mmetuchokoza na sasa ni wakati wetu wa kujibu mapigo na majibu yetu hayatakuwa madogo.Tutawasaka magaidi hawa kila sehemu,iwe ardhini,majini au hata angani,hawana sehemu ya kujificha.Hakuna jiwe libaki juu ya lingine wote walioshiriki uovu huu watapata stahili yao” akasema Dr Evans kwa msisitizo mkubwa Wakati mazishi ya kitaifa yakiendelea katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam,katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ikitokea Tel Aviv kupitia Addis Ababa ilitua na abiria kuanza kushuka.Ndani ya ndege hii walishuka majasusi watano kutoka shirika la ujasusi la Israel Mossad.Majasusi hawa walikuja nchini kwa ajili ya kutekeleza operesheni maalum ya kumteka Edger kaka.Tayari walikwishapata taarifa kwamba Edger kaka alikuwa na mipango ya kurejea nchini siku ya mazishi ya waziri mkuu ili aweze kuwahi mazishi hayo kwani waziri mkuu alikuwa ni mmoja wa watu aliowaheshimu sana.Waliwahi kufika nchini kabla ya ndege aliyopanda Edger Kaka na Olivia ambayo ililazimika kuchelewa kuondoka nchini Israel kwa sababu za kiufundi.Ukweli ni kwamba hakukuwa na hitilafu yoyote katika ndege hiyo bali ulikuwa ni mpango maalum wa Mossad ili Edger achelewe kufika nchini Tanzania na kufika Dar es salaam usiku ili mpango wa kumteka uweze kutekelezwa kama ulivyopangwa. Majasusi wale baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji na kuruhusiwa kuingia nchini kila mmoja alipokelewa na mtu maalum kutoka ubalozi na kumpeleka katika nyumba anakoishi afisa mmoja wa ubalozi ambako ndiko mipango yote ya operesheni ile ilikuwa inafanyika.Siku mbili zilizopita majasusi wengine watatu waliwasili nchini kimya kimya kwa ajili ya kuandaa operesheni hiyo ya siri wakisaidiwa na maafisa wa ubalozi wa Israel nchini Tanzania. Baada ya kuhakikisha kila mmoja wao ameingia nchini salama na hakukuwa na tatizo lolote bila kupoteza muda kikao kikaanza “Poleni kwa safari na karibuni Tanzania” akasema Gershom Rabin mkuu wa operesheni ile. “Kwa siku tatu tulizokaa hapa tumekuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha tunaandaa operesheni kubwa ya aina yake ambayo itatuwezesha kumpata Edger kaka na kuiacha serikali ya Tanzania ikiamini kwamba Edger kaka amefariki katika ajali ya gari.Mpaka sasa mipango yote inakwenda vyema.Nimekuwa na mawasiliano na mawasiliano na watu wetu Noam na Yosef ambao wako ndani ya ndege aliyopanda Edger na wamenihakikishia kwamba Edger bado yuko ndegeni nimewasiliana pia na marubani wa ndege hiyo wamenihakikishia kwamba ndege itaingia Dar es salaam saa sita za usiku leo hivyo operesheni yetu bado inaendelea vizuri kama tulivyoipanga” akasema Gershom “Hapa mbele yetu kuna ramani” akasema Gershon na kuisogelea ramani ile. “Hii ni barabara ambayo inatoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kuja mjini.Shughuli yetu itafanyikia eneo hili hapa lenye mduara mwekundu.Ni kilometa kadhaa kutoka uwanja wa ndege na tumechagua eneo hili kwa kuwa hatutaki tukio lifanyike kati kati ya jiji ambako kwa nyakati hizo bado linaweza kuvuta watu.Ilan na Moshe mtakuwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kumsubiri Edger kisha mtawapokea Noam na Yosef halafu mtalifuata kwa nyuma gari atakalopanda Edger huku mkiendeleza kuwasiliana nasi.Sina haja ya kuwakumbusha nini mnapaswa kufanya kila mmoja anafahamu sehemu yake ni ipi na tumekwisha fanya mazoezi ya kutosha hivyo kilichobaki ni utekelezaji tu.Kikubwa ninachowasisitiza ni umakini mkubwa sana kwani operesheni hii ni ya siri na serikali ya Tanzania haifahamu chochote.Kosa moja hata dogo linaweza kutuletea matatizo makubwa hivyo epukeni kufanya kosa.Mwisho kabisa kumbukeni kunaweza kutokea mabadiliko katika operesheni hii hivyo kila mmoja awe makini katika kumlinda mwenzake” akasema Gershom kisha wakaendelea na majadiliano kuhusiana na operesheni ile.
******************* Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ambayo ilipaswa kuingia nchini saa sita za mchana iliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere saa sita za usiu.Hii ilitokana na sababu za kiufundi zlizotajwa kujitokeza na kuilazimu ndege ile kuchelewa.Ndani ya ndege hii ndimo alimokuwamo Edger kaka pamoja na Olivia Themba.Edger alichagua kupanda ndege hii ili awahi kufika Dar es salaam na kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya waziri mkuu vile vile lakini lengo lake halikufanikiwa kutokana na mpango wa shirika la ujasusi la Israel Mossad kuichelesha ndege ile ili waweze kutekeleza operesheni yao. Ndani ya ndege aliyopanda Edger Noan na Yosef majasusi kutoka Mossad walikuwa wanamfuatilia kila anachiokifanya huku wakiendelea kuwasiliana na wenzao walioko tayari jijni Dar es salaam. “Welcome home Olivia” akasema Edger baada ya ndege kutua.Dr Olivia akatabasamu “Welcome home Edger” akasema Olivia “Olivia nafahamu baada ya kushuka ndegeni kila mmoja ataenda uelekeo wake japo ningetamani sana tungepata walau hata dakika kumi za kuwa pamoja kabla ya kuachana ili niweze kukushukuru tena kwa yote uliyonifanyia.Nimekwisha kushukuru sana lakini bado haitoshi nitaendelea kukushukuru tena na tena kwa yale uliyonifanyia kwani siwezi kuyalipa kwa fedha zaidi ya kuendelea kukushukuru.Kwa muda huu mfupi tuliokuwa pamoja umekuwa mtu wangu wa karibu sana na ninajihisi vibaya kuachana nawe leo”akasema Edger.Dr Olivia akamshika mkono na kusema “Edger hupaswi kuendelea kunishukuru mimi bali mshukuru sana Mungu ambaye alinitumia mimi kuyaokoa maisha yako.Sifa na utukufu mrejee yeye ambaye amekupa tena nafasi nyingine.Ninakuahidi kwamba huu hautakuwa mwisho wa kuonana.Bado nitandelea kuonana nawe mara kwa mara kujua maendeleo yako.”akasema Dr Olivia “What about dinner tomorrow?akauliza Edger.Olivia akatabasamu na kusema “Sawa hakuna tatizo katika hilo” “Thank you Olivia.Nitakupigia simu kukujulisha ni saa ngapi na wapi tukutane kwa ajili ya chakula cha usiku” akasema Edger “Ahsante Edger.Ni wakati wa kushuka sasa” akasema Olivia “Olivia nimekumbuka kitu,kesho nitakwenda kuwapa pole wazazi wa Judy utapenda kuambatana nami?Ni vyema kama tutakwenda sote kwani Judy alikuja Israel kwa ajili ya kuniuguza hivyo lazima nikawape pole wazazi wake kwa kifo cha mtoto wao” “Usijali tutakwenda wote.Tutawasiliana asubuhi tujue tutakutana wapi” akasema Olivia akachukua mkoba wake mdogo na kuelekea mlangoni na nyuma yake alimfuata Edger Kaka wakashuka ndegeni bila kujua kama nyuma yao kuna majasusi wanawafuatilia. Edger na Olivia walikamilisha taratibu za uwanjani na kuingia nchini.Nje ya uwanja Edger alipokewa na rafiki yake mkubwa ambaye pia ni katibu wake Stanley pia walikuwepo viongozi wa chama cha Democratic na watu wengine kadhaa.Haikuwa imetangazwa kama Edger Kaka angerejea nchini na lengo kuu la kuweka siri ujio wake ni ili awashangaze watu kwa kufika ghafla ndani ya uwanja wa uhuru hivyo ni watu wachache waliofahamu kuhusu kurejea kwake na kufika uwanjani kumpokea. “Karibu tena nyumbani Edger” akasema Stanley kisha akamtambulisha Edger kwa viongozi wa juu wa chama cha Democratic aliokuwa nao pale uwanjani .Wakati Edger akiendelea kusalimiana na viongozi wa chama cha Democratic waliofika kumpokea,Dr Olivia alikuwa anasalimiana na familia yake waliofika pale kumpokea wakiongozwa na baba yake bilionea Aggrey Themba.Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwao kwa mtoto wao kurejea nchini salama “Olivia tunamshukuru sana Mungu umerejea salama”akasema Agrey “Hata mimi ninashukuru sana kurejea tena nyumbani salama na kuwaoneni tena familia yangu.Nilikuwa nawakumbuka kila dakika” akasema Olivia halafu akawachukua familia yake akaenda kuwatambulisha kwa Edger ambaye alifurahi sana kukutana nao na Aggrey akaahidi kumkaribisha rasmi Edger nyumbani kwao kwa ajili ya kufahamiana zaidi.Hakukuwa tena na muda wa kupoteza uwanjani pale Edger akaongozwa katika gari lililoandaliwa kumchukua na viongozi wale wa chama cha democratic wakaingia katika magari yao kisha msafara wa magari matatu ukaondoka pale uwanjani.Olivia na familia yake nao wakaingia katika gari lao na kuondoka.Majasusi Noam na Yosef waliokuwa wanamfuatilia Edger toka Israel wakaungana na majasusi wenzao wawili waliofika pale uwanjani kuwapokea wakaingia garini na kuondoka kuufuata msafara wa Edger. Hakukuwa na magari katika barabara ya kutoka uwanja wa ndege hivyo mwendo wa magari ya msafara wa Edger ulikuwa mkali.Kilometa tano kutoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere gari lililokuwa limetangulia mbele ya msafara ule wa Edger lilikutana uso kwa uso na lori la mafuta lililopoteza uelekeo na kishindo kikubwa kikasikika.Gari la pili ambalo ndilo alimokuwa amepanda Edger likagonga kwa nyuma gari lile la kwanza lililogongwa na lori la mafuta.Dereva wa gari la tatu naye alishindwa kulizuia gari lake akagonga kwa nyuma gari la Edger.Ilikuwa ni ajali mbaya. Mara tu baada ya ajali ile kutokea majasusi wanne kutoka katika gari lililokuwa linaufuatilia kwa nyuma msafara ule wa Edger wakashuka kama umeme na kulifuata gari la Edger.Kwa kasi ya aina yake wakaufungua mlango na kumkuta Edger akiwa amepoteza fahamu na alikuwa anavuja damu katika paji la uso.Kulikuwa pia na watu wengine wawili waliokuwamo ndani ya lile gari na mmoja wao alikuwa anagugumia kwa maumivu.Edger akatolewa haraka haraka na kukimbizwa katika gari lingine lililokuwa linalifuata lile lori la mafuta kwa nyuma kisha ukatolewa mwili kutoka katika ile gari ukavishwa pete za Edger pamoja na mkufu wa dhahabu wenye kidani chenye herufi E kisha mwili ule ukakimbizwa katika gari alimokuwamo Edger.Wakati zoezi la kubadilisha mwili ule likifanyika kwa kasi majasusi wengine walikuwa katika zoezi la kumtoa dereva wa lori la mafuta lililosababisha ajali ambaye alikuwa amebanwa miguu.Gorshem kiongozi wa opersheni ile akaitwa haraka kushuhudia namna dereva yule alivyobanwa miguu “Amebanwa sana na hatuna muda wa kuendelea kumnasua,tumuacheni tuondoke” akaelekeza na kisha tanki la mafuta likafunguliwa na mafuta yakaanza kusambaa,kifaa Fulani kikategwa na Majasusi wote wakakimbilia katika gari lao wakaondoka. Magari machache yaliyokuwa yanatoka uwanja wa ndege usiku ule yalilazimika kusimama kutokana na ajali ile.Gari la akina Olivia nalo likalazimika kusimama baada ya kukuta magari mengine yamesimama na wakajulishwa kwamba kuna ajali kubwa imetokea mbele na magari hayawezi kupita.Mara ghafla ukatokea mlipuko mkubwa.Gari lile la mafuta na magari mengine yaliyokuwa karibu yakafunikwa na moto mkubwa. Baada ya kukamilisha zoezi la kumtwaa Edger timu ya majasusi ikaelekea moja kwa moja sehemu Fulani kandoni mwa bahari ya Hindi kulikokuwa na boti mbili.Pale walikuta kuna gari nyingine mbili na haraka haraka Edger akashushwa kutoka ndani ya gari akaingizwa katika boti.Katika boti ile pia kulikuwa na familia ya dereva wa lile lori lililosabisha ajali na lengo lilikuwa ni kumuhamisha dereva yule na familia yake na kuwapeleka kuishi nchini Israel.Majasusi wale wakaagana na maafisa wa ubalozi waliowasindikiza wakaingia katika boti na kuondoka kwa kasi kubwa.Boti zile mbili zilikwenda kwa kasi kubwa hadi mataa ya jiji ya dar es salaam yalipoanza kuonekana kama nyota ndipo walipoikuta meli kubwa na Edger akashushwa kutoka katika ile boti akaingizwa melini akaanza kupatiwa huduma.Gershon kiongozi wa operesheni ile akakutana na watu wake katika mojawapo ya ofisi “Ninawapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya leo_Operesheni imekuwa na mafanikio makubwa sana na imekwenda kama tulivyokuwa tumeipanga japo nasikitika kwamba hatukuweza kuondoka na dereva yule kama tulivyokuwa tumekubaliana naye kwani kwa namna alivyokuwa amebanwa ingetuchukua muda kumnasua na sisi hatukuwa na muda lakini tunayo familia yake ambayo nitahakikisha wanakuwa katika mikono salama na watatunzwa kwa maisha yao yote.Hatujampoteza mtu yeyote katika operesheni hii na haya ni mafanikio makubwa sana kwetu.Operesheni hii ni muhimu sana katika vita dhidi ya magaidi ambao wamekuwa wakiendelea kuua watu wetu kila uchao.Kupitia mtu huyu tutafahamu mambo mengi sana kuhusiana na mtandao wa IS” akasema Gorshen. Jijini Dar es salaam magari ya zimamoto kutoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere yalifika kwa haraka sana eneo la tukio na kuanza kuuzima moto ule mkubwa uliokuwa unawaka na iliwachukua zaidi ya nusu saa kuuzima moto ule mkubwa.Ni mwenyekiti pekee wa chama cha Democratic aliyenusurika katika ajali ile kwani yeye alikuwa katika gari la tatu na baada ya ajali ile kutokea alifanikiwa kutoka salama na kuanza kukimbia kama mtu aliyechanganyikiwa huku akipiga kelele za kuomba msaada.Ulipotokea moto ule mkubwa yeye hakuwepo eneo lile alikuwa katika gari moja lililokuwa limesimama mbali kidogo akiomba msaada wa kuwaokoa wenzake waliopata ajali akiwemo mbunge Edger Kaka. Moto ulizimwa na miili ikatolewa katika magari ikiwa imeungua vibaya sana.Askari polisi walifika haraka sana na kulifunga eneo lile ili kuzuia umati watu wasilisogelee eneo lile.Taarifa za kutokea kwa ile ajali zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kama moto wa nyika na watu wakaanza kufika eneo lile hasa baada ya taarifa hizo kueleza kuwa mbunge Edger Kaka ni miongoni mwa wanaodaiwa kufariki katika ajali hiyo mbaya. Miili ya watu waliokuwemo katika magari yale yaliyoungua moto ikaanza kutolewa na haikuwa rahisi kutambulika kwani walikuwa wameungua vibaya sana.Mwili ambao ulidaiwa kuwa wa Edger uliweza kutambuliwa kwa kuwa ulikuwa na mkufu wenye kidani chenye herufi E pamoja na pete za kidoleni zote zikiwa na herufi E ikiwa ni herufi ya kwanza ya jina lake.Miili yote ilichukuliwa na kupelekwa hospitali kuhifadhiwa. Olivia Themba ambaye ndiye aliyekuwa na Edger nchini Israel alimuomba baba yake amkimbize hospitali ilikopelekwa miili ya marehemu ili kuhakiki kama taarifa zile za Edger kufariki katika ajali ile ni za kweli.Huku akimwaga machozi mengi aliweza kuutambua mwili wa Edger kutokana na mkufu ule aliokuwa amevaa wenye kidani chenye herufi E pamoja na pete za mkononi.Aliwahakikishia watu kwamba mwili ule ni wa Edger Kaka kwani mkufu ule alikuwa ameuvaa toka wakiwa Israel.Taarifa za kifo cha Edger zililistua taifa BAADA YA MIAKA MIWILI Tayari imekwisha pita miaka miwili toka lilipotokea shambulio la bomu jijini Dodoma lililomuua waziri mkuu wa Tanzania na watu wengine kadhaa.Kwa kipindi hiki chote cha miaka miwili bado vyombo vya uchunguzi havikuwa vimefanikiwa kuwapata watu waliofanya shambulio lile la kigaidi.katika kipindi hicho cha miaka miwili ,uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ulifanyika na Dr Evans Mwaluba akashinda uchaguzi huo kwa kura nyingi kwani hakupata upinzani mkubwa.Watu pekee aliokuwa akiwahofia ni Damian Mwamba na Edger kaka ambao wote walifariki dunia. Kifo cha Edger kaka bado kiliendelea kuzua maswali mengi namna kilivyotokea.Kulikuwa na maswalimengi yaliyokosa majibu kuhusiana na ajali ile lakini kilichowashangaza zaidi watu ni na hata wachunguzi wa ajali ile ni kupotea kwa familia ya dereva wa lori lililosababisha ajali ambayo haikujulikana mahala ilipo. Ni siku ya jumanne Dr Olivia Themba akiendelea na majukumu yake ya kazi,akapewa taarifa kwamba ana mgeni wake.Alipomaliza kuzungumza na mgonjwa akaenda katika sehemu ya mapumziko kwa madaktari na kuagiza mgeni wake apelekwe kule.Kijana mmoja nadhifu aliyevaa suti nzuri ya kijivu akajitokeza na kumfuata Dr Olivia ambaye alimtazama kijana hakuwa akimfahamu “Hallo” akasema Dr Olivia kijana yule akavua miwani aliyokuwa amevaa akatabasamu “Hallow Dr Olivia habari yako” akasema yule jamaa “Habari yangu nzuri”akajibu Dr Olivia huku naye akitabasamu. “Dr Olivia naamini ni mara yetu ya kwanza kuonana” akasema yule jamaa “Sina kumbukumbu kama tumewahi kuonana hapo kabla lakini mwenzangu unaonekana kunifahamu vizuri” akasema Dr Olivia “Naitwa Oscar Benard ni meneja wa Loll’s Hotel”akasema Oscar “Loll’s Hotel ninaifahamu” akasema Olivia “Unakaribishwa sana Dr Olivia kutembelea hoteli yetu kupumzika na kupata chakula” akasema Oscar “Nafurahi kukufahamu Oscar,nikusaidie nini?akauliza Dr Olivia “Nimekuja hapa kuonana nawe kwa shida mahsusi kabisa” “Karibu” akasema Olivia “Katika hoteli yangu amekuja mgeni toka nje ya nchi ni tajiri na amekuja maalum kwa ajili ya kuonana nawe” akasema na Dr Olivia akaonyesha mstuko “Amekuja kuonana na mimi? Ni nani huyo?Akauliza “Ndiyo amekuja kuonana nawe.Amenipa maelezo mafupi tu kwamba yeye ni ndugu wa Edger kaka hivyo anahitaji kukuona kuna mambo anataka kuzungumza nawe yanayomuhusu Edger”akasema Oscar “Ndugu wa Edger kaka?Dr Olivia akashangaa “Ndiyo anasema yeye ni ndugu wa Edger Kaka” “Anaitwa nani huyo mtu na ametokea wapi? akauliza Dr Olivia akionekana kuwa na wasi wasi “Dr Olivia kazi yangu mimi ilikuwa kufikisha ujumbe kwako kwamba kuna ndugu wa Edger Kaka amekuja na anahitaji kuzungumza nawe kuna jambo muhimu sana.Ninasubiri jibu kama uko tayari kuonana naye mkazungumza au hauko tayari” akasema Oscar “Oscar ninashindwa kutoa jibu kwa sasa kwani simfahamu mtu huyo ni nani na amenifahamuje mimi hadi akafunga safari kutoka huko alikotoka kunifuata mimi huku Tanzania.Isitoshe mimi si ndugu wa Edger kwa nini anifuate mimi badala ya kuwatafuta ndugu zake?Kwa nini yeye mwenyewe asinifuate hapa kazini akanieleza hilo analotaka kunieleza?akauliza Dr Olivia “Dr Olivia,mgenihuyo si mtu mdogo.Ni bilionea mkubwa na anafahamu kwamba hapa si sehemu ya maongezi ni sehemu ya kazi ndiyo maana akahitaji kupata muda maalum wa kuzungumza nawe.Nakuona una wasiwasi sana.Usihofu tafadhali hakuna chochote kibaya.Usalama upo wa kutosha katika hoteli yetu” akasema Oscar na Dr Olivia akazama katika tafakari kisha akasema “Edger hakuwahi kuniambia chochote kama ana ndugu yake tajiri nje ya nchi.Mtu huyo kama kweli nindugu yake kwa nini hakuwahi kuja kumuona hospitali nchini Israel wakati Edger anaumwa? Kwa nini hakujitokeza katika msiba wa Edger? Akauliza Olivia “Olivia maswali hayo ni yeye mwenyewe anayepaswa kuyajibu,mimi kazi yangu ni kufikisha ujumbe kuwa anataka kuonana nawe.Nakusihi ukaonane naye tafadhali kwani amekuja kuonana nawe lazima ana jambo la muhimu sana anataka kukueleza.Mimi ni meneja wa hoteli ile kubwa lakini nimelazimika kuacha majukumu yangu yote na kuja kuonana nawe.Nisingeweza kuja hapa kama nisingekuwa na uhakika kwamba ana jambo la muhimu la kukueleza.Ninakushauri Olivia nenda ukaonane naye”akasema Oscar na kumfanya Dr Olivia azame katika mawazo “Dr Olivia please !! akasisitiza Oscar “Anataka nikaonane naye wapi na muda gani? Dr Olivia akauliza “Utakutana naye leo jioni pale pale hotelini” akasema Oscar “Sawa Oscar nitafika hapo hotelini kuonana naye jioni.Nimeamua kuja kuonana naye kwa sababu ya kukuheshimu wewe”akasema Dr OLivia “Ahsante sana Dr OIivia ninakuhakikishia kwamba hautajutia muda wako.Usafiri utakuja nyumbani kwako kukuchukua” “Tafadhali nitatumia gari langu kuja hapo hotelini kuonana na huyo mgeni asiyekuwa na jina” “Tafadhali Olivia wewe ni mgeni muhimu wa mgeni wetu mkubwa hivyo mimi ndiye nitakayehakikisha nitashughulikia kila kitu kuhusu wewe kuonana na huyo mtu wako.Litakuja gari saa moja jioni nyumbani kwako kukuchukua kukupeleka hotelini” akasema Oscar wakaagana akaondoka “Edger hakuwahi kunieleza kama ana ndugu yake tajiri nje ya nchi.Nilikaa naye hospitali kwa muda mfupi lakini sikuwahi kumsikia akizungumzia suala la familia yake.Niliwahi kumuuliza suala hilo la ilipo familia yake lakini hakunijibu chochote na hakutaka kabisa kuliongelea suala hilo.Huyu aliyejitokeza na kudai kwamba yeye ni ndugu wa Edger ametoka wapi?Ametokea nchi gani?Kwa muda huu wote alikuwa wapi hadi aibuke leo?Alipofariki ilibainika kwamba hakuwa na ndugu wengine kwani ndugu zake walikwisha fariki wote huyu katokea wapi? Dr Olivia akajiuliza maswali mengi kuhusiana na mtu huyo anayedai ni ndugu wa Edger Kaka “Nitakwenda kuonana naye huyo mtu nifahamu kuhusu undugu wake na Edger ni undugu wa namna gani na kwa nini amejitokeza sasa”akawaza Dr Olivia. ***************** Saa moja za jioni kama alivyoahidiwa,likafika gari kumchukua Dr Olivia kumpeleka akaonane na mgeni wake ambaye hadi muda huo hakuwa akimfahamu.Bado kichwa chake kilijaa mawazo kuhusiana na mtu huyo anayekwenda kuonana naye. Alitoka ndani na kuingia katika gari lililokuja kumchukua akaondoka kuelekea Loll’s hotel. “Huyu mtu ametokea na kunikumbusha mambo mengi kuhusu Edger Kaka.Nilifahamiana naye kwa muda mfupi na tukajikuta tukiwa na ukaribu mkubwa japo kuna wakati tuliwahi kuingia katika sintofahamu pale aliponitamkia kwamba ananipenda.Alinieleza ukweli wake na kabla hatujaendelea zaidi na ukaribu wetu akafariki dunia kwa kifo cha kikatili sana.Inaniumiza kila nikimkumbuka ninaona kama alinipa mkosi kwani toka alipofariki ni miaka miwili sasa hajawahi kujitokeza mwanaume mwingine ambaye amewahi kunitamkia kwamba ananipenda.Yawezekana Edger alikuwa ndiye chaguo langu nililopewa na Mungu lakini hatukupata nafasi ya kuwa pamoja.Laiti angekuwa hai labda hivi sasa tungekwisha ingia katika mahusiano na yawezekana tungekwisha funga ndoa kwani hata mimi tayari nilianza kuvutiwa naye japo sikuwa tayari kumueleza” akawaza Dr Olivia akiwa garini akielekea Loll’s Hotel. “Miaka miwili sasa toka afariki lakini bado uchunguzi wa ajali ile haujakamilika.Suala hili limebaki hewani mpaka leo haijulikani kama ile ilikuwa ni ajali au ni moja kati ya mipango ya maadui zake ya kumuua.Yawezekana ajali ile ikawa ni moja ya mpango wao wa kummaliza baada ya kushindwa kumuua kwa sumu.Nilimkatalia Edger kwamba asirejee nyumbani mapema kwa ajili ya usalama wake hakutaka kunisikia.Huyo ndugu yake ambaye hakuwahi kujitokeza hata katika msiba amefahamuje kama nilikuwa na ukaribu na Edger? Akajiuliza Olivia. Gari lilifika Loll’s hotel,mlango ukafunguliwa Dr Olivia akashuka akapokewa na Oscar “Karibu Olivia.Umependeza sana usiku wa leo” akasema Oscar huku akimshika mkono Olivia na kumuongoza kuelekea ndani “Oscar nimekuja hapa usiku huu kwa sababu yako tafadhali naomba suala lililonileta hapa liwe ni suala la msingi.Nitasikitika sana kama kilichonileta hapa ni mambo tofauti na Edger” akasema Dr Olivia “Nashukuru kwa kuniamini Olivia.Nisingeweza kukuomba ufike hapa kama kusingekuwa na suala la muhimu” akasema Oscar Walipanda lifti hadi ghorofa ya ishirini na tatu wakashuka na kuelekea katika chumba chenye hadhi ya rais.Kulikuwa na walinzi wawili mlangoni waliovalia nadhifu kabisa,mmoja akafungua mlango Oscar na Dr Olivia wakaingia ndani ya chumba kile kikubwa na kizuri.Mtu mmoja mwenye asili ya kiarabu aliyevalia suti nzuri nyeusi akasimama huku akitabasamu akawakaribisha ndani “Karibuni wageni wangu”akasema yule jamaa “Ahsante sana” akajibu Oscar halafu akamgeukia Dr Olivia “Olivia kutana na Abu dahir mfanya biashara anatokea nchini Saudi Arabia na ndiye mgeni wako uliyekuja kuonana naye usiku wa leo”akasema Oscar na kumstua Dr Olivia “Abu Dahir kutana na Dr Olivia Themba huyu ndiye aliyeyaokoa maisha ya Edger kaka kwa kumpeleka nchini Israel” akasema Oscar “Ahsante sana Oscar kwa kumleta malaika huyu ambaye ninahitaji sana kumuona” akasema Abu dahir na kupeana mkono na Oscar “Dr Olivia I’ll be outside.Tafadhali usihofu kitu” akasema Oscar na kutoka “Olivia karibu sana jisikie amani.Najua una hofu kubwa lakini nakuomba ondoa hofu uko salama.Utatumia kinywaji gani?akauliza Abu dahir “Ahsante nitatumia maji”akajibu Dr Olivia na Abu dahiri akammiminia maji katika glasi “Olivia naomba kwanza nikushukuru sana kwa kukubali kuonana nami japo hunifahamu” akasema Abu dahir “Niliambiwa maongezi ni kuhusu Edger Kaka ndiyo maana nikakubali kuja kuonana naye.Wewe ni nani?akauliza Dr Olivia “Mimi kama alivyokueleza Oscar ninaitwa Abu dahir ni mfanya biashara ninaishi Saudi Arabia kwa sasa,baba yangu anatokea Palestina lakini mama yangu anatokea Saudi Arabia.Ninafanya biashara mbali mbali lakini kubwa ni biashara ya mafuta.Nina visima vya mafuta katika nchi za Iraq na Saudi Arabia” akasema Abu “Abu naomba tujielekeze moja kwa moja katika suala la msingi lililotukutanisha hapa ambalo ni Edger.Unahusiana vipi na Edger? Hakuwahi kuniambia kama ana ndugu yake tena mwenye asili ya arabuni.Ulikuwa wapi muda huu wote haukujitokeza hadi sasa?akauliza Olivia “Dr Olivia nitakueleza kila kitu lakini kwanza nakukaribisha tusipate chakula nilichokiandaa maalum kwa ajili yako halafu tutazungumza” akasema Abu dahir na kuinuka akamuongoza Dr Olivia katika chumba cha chakula ambako kulikuwa na meza iliyotawanywa vyakula vingi.Akamvutia kiti Dr Olivia akaketi
“Karibu Dr Olivia” akasema Abu ambaye alionekana ni mtu mstaarabu sana.Dr Olivia akaweka chakula kidogo katika sahani na kumtazama Abu “Nadhani tuendelee na maongezi.Nilikuuliza kuhusiana na mahusiano yako na Edger Kaka.Hakuwahi kunieleza kama ana ndugu yake tena ana asili ya kiarabu” akasema Dr Olivia “Dr Olivia kwanza kabla sijakujibu swali lako nataka nitumie nafasi hii kukushukuru sana kwa kukayaokoa maisha ya Edger.Kama si wewe Edger angefariki dunia”akasema Abu dahir.Dr Olivia akala vijiko kadhaa na kusema “Siku zote daktari anayeifahamu vyema kazi yake atafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba mgonjwa wake anapona na ndivyo nilivyofanya kuhakikisha kwamba Edger anapona” akasema Dr Olivia “Dr Olivia uliniuliza kuhusu mahusiano yangu na Edger kaka.Mimi na Edger ni ndugu.Edger ni kaka yangu” akasema Abu dahir na uso wa Olivia ukaonyesha mshangao mkubwa “Sijakuelewa Abu.Wewe na Edger undugu wenu ukoje?akauliza Dr Olivia kwa mshangao “Kama nilivyokueleza kwamba Edger ni ndugu yangu.Ni kaka yangu.Najua unajiuliza inawezekanaje mimi na yeye tukawa ndugu wakati yeye ni mwafrika na mimi ninaonekana kama mwarabu? Akauliza Abu na kucheka kidogo “Mimi si mwarabu kwa asilimia mia moja nimechanganya damu.Kwa ufupi ni kwamba mimi na Edger mama yetu ni mmoja”akasema Abu na Dr Olivia akaweka kijiko chini akamtazama “Inavyojulikana wazazi wote wa Edger wamekwishafariki dunia na wote walikuwa watanzania iweje wewe na Edger mama yenu awe mmoja? “Dr Olivia nitakueleza ukweli halisi lakini naomba kile nitakachokueleza kisikustue.Nimeamua kukueleza ukweli kwa sababu ninakuamini” akasema Abu na kunyamaza kidogo halafu akasema “Mama yake Edger au mama yetu anaitwa Habiba Jawad.Ni mzaliwa wa Kenya lakini asili yake ni Somalia.Aliolewa na Nasser Jawad mfanya biashara mkubwa nchini Kenya na wakafanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye ni Edger.Alipofikisha umri wa miaka mitano Edger akahamishiwa nchini Tanzania akiwa chini ya uangalizi wa mama mmoja anaitwa Genevieve msika.Jina halisi la Edger kaka ni Seif Jawad.Alipohamishwa kutoka Kenya kuja Tanzania akabidilshwa jina na kuitwa Edger Kaka akachukua jina la baba yake mlezi aliyeitwa Eliud kaka” akasema Abu na Olivia akamkatisha “Subiri kidogo Abu naona unazidi kunichanganya.Unasema kwamba jina halisi la Edger kaka ni Seif jawad na jina Edger alipewa alipohamishiwa Tanzania.Nini sababu ya wazazi wake kumuhamishia nchini Tanzania? “Seif kuhamishiwa Tanzania kulikuwa na sababu maalum na utaifahamu huko mbeleni”akasema Abu na kupiga vijiko kadhaa akafuta mdomo kwa kitambaa akaendelea “Nataka umfahamu kiundani Edger kaka ni nani na kwa nini ninakueleza haya yote” akasema Abu dahir “Nasser Jawad baba yake mzazi Edger alifariki dunia kwa ugonjwa wa saratani.Nasser alipofariki dunia Habiba aliolewa na mwanaume mwingine ambaye ni baba yangu anaitwa Abdul dahir.Baba alikuwa tajiri sana hivyo akamuhamisha mama kutoka Kenya wakaenda nchini Saudi Arabia na ndipo nilipozaliwa mimi hivyo Edger ni kaka yangu.Utofauti wetu ni kwamba baba yangu mimi alikuwa mwarabu na baba yake Edger alikuwa mweusi” akanyamaza kidogo na kumtazama Olivia,akaendelea. “Baba yangu aliuawa na vikosi vya Israel wakimtuhumu kuhusika katika kufadhili vikundi vya kigaidi ambavyo vimekuwa vikiendesha operesheni zake nchini Israel na kuua raia” akasema Abu dahir.Macho ya Dr Olivia yalizidi kuonyesha woga “Ni kweli alikuwa anafadhili makundi hayo ya kigaidi? akauliza Dr Olivia “Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba alikuwa anafadhili makundi hayo ya kigaidi lakini baba ni mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele sana katika kupigania haki za wapalestina na ndiyo sababu ya kuuawa kwake.Tuachane na hayo tujielekeze zaidi katika suala lililotukutanisha hapa kuhusu Edger kaka” akasema Abu na kunyamaza kidogo “Dr Olivia wewe ndiye uliyempeleka Edger Israel na ukayaokoa maisha yake na baada ya hali yake kuwa nzuri mkarudi wote Tanzania lakini hakuweza kufika nyumbani kwake akafia njiani.Unaweza ukanipa picha kidogo ya namna tukio lile lilivyotokea? Akauliza Abu dahir.Swali lile lilimfanya Dr Olivia kuacha kabisa kula chakula kwani lilimkumbusha mbali sana usiku ule ambao alishuhudia moto mkubwa ukiwaka na ndani ya moto ule Edger Kaka aliteketea.Machozi yakamtoka “Samahani Dr Olivia.Najua nimekukumbusha mbali sana” akasema Abu dahir “Ni kweli Abu nimekumbuka mbali sana.Kumbu kumbu ya tukio lile imenitesa kwa muda mrefu sana na kuna nyakati nikiwa peke yangu kumbukumbu ile hunijia kichwani na kuniumiza sana.Ni moja ya kumbu kumbu ambayo ninajaribu sana kuitafuta kichwani kwangu” akasema Dr Olivia na kufuta machozi akaendelea “Tulipokea taarifa kutoka bungeni Dodoma kwamba mbunge Edger kaka analetwa kwa matibabu katika hospitali yetu.Tulimpokea akiwa katika hali mbaya na baada ya jitihada za kumuhudumia ilionekana kwamba ugonjwa wake unahitaji matibabu zaidi nje ya nchi.Hospitali yetu ina ushirikiano mkubwa na hospitali ya Rambam iliyoko Haifa Israel tuliwasiliana nao wakakubali tumpeleke huko lakini baada ya kulifikisha suala hili kwa viongozi wake zilianza sarakasi na badala ya kukubaliana na pendekezo letu la kumpeleka Edger nje ya nchi wakafanya mpango ahamishwe kupelekwa katika hospitali ya Muhimbili.Mimi kama daktari ni jukumu langu kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba ninaokoa maisha ya mgonjwa hivyo nilitumia nafasi yangu na uwezo wangu kuhakikisha kwamba Edger anasafirishwa kwenda Israel.Baba yangu na rais ni marafiki wakubwa tangu utoto wao hivyo nilimtumia baba kumuomba rais atumie uwezo wake kumsaidia Edger na rais akakubali akazungumza na mamlaka za Israel na Edger akaruhusiwa kuingia Israel.Rais Dr Evans alitoa ndege yake ambayo ilitupeleka nchini Israel” Akanyamza akavuta pumzi kidogo halafu akaendelea “Baada ya kufika nchini Israel vipimo vilionyesha kwamba aliwekewa sumu.Kama unavyojua Edger alikuwa na maadui wengi hivyo walijaribu kumuua kwa sumu ile ambayo inahisiwa kwamba ilipakwa katika sabuni ya kuogea.Tukiwa Israel na hali yake ikiendelea vyema tulipata taarifa za kuuawa kwa waziri mkuu katika mlipuko wa bomu na jambo hili lilimuumiza sana Edger kwani alikuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwake katika mambo ya siasa hivyo akapanga lazima ahudhurie mazishi yake.Nilijaribu kumzuia asiondoke Israel asubiri hadi atakapopona kabisa lakini aliendelea na msimamo wake kwamba lazima akahudhurie mazishi ya waziri mkuu hivyo tukajiandaa na kuondoka.Ndege tuliyosafiri nayo ilipata hitilafu ya kiufundi hivyo tukachelewa sana kufika Tanzania.Badala ya kufika saa sita za mchana tukafika saa sita usiku na Edger hakuweza kuwahi mazishi ya kitaifa ya waziri mkuu kama alivyokuwa ametarajia.Baada ya kushuka ndegeni tuliagana kwa miadi ya kukutana tena siku inayofuata na Edger akaondoka uwanjani pale na watu wake waliokuja kumpokea.Kilometa chache baada ya kuondoka pale uwanjani ndipo ilipotokea ajali ile iliyochukua uhai wa Edger” akasema Dr Olivia “Pole sana kwa kumbukumbu hii yenye kusikitisha.Bado kuna kitu nataka kukifahamu kama hutajali.Nataka kupata walau picha ya namna ya ajali ile ilivyotokea”akasema Abu dahir “Sifahamu nini kilitokea kwani Edger aliwahi kuondoka pale uwanjani na mimi nilifuata muda mfupi baadae na nilikuta ajali tayari imetokea na moto mkubwa unawaka.Nilipoambiwa kwamba magari ya msafara wa Edger ndiyo yaliyopata ajali sikuamini na baada ya miili kutolewa nikalazimika kwenda hospitali kuhakikisha kama ni kweli Edger amefariki dunia na mimi ndiye niliyefanikisha kuutambua mwili wake uliokuwa umeungua vibaya sana na kilichonisaidia kuutambua mwili wake ni mkufu aliokuwa amevaa shingoni wenye kidani chenye herufi E na pete alizokuwa amevaa vidoleni.Hivyo ndivyo ilivyotokea na Edger akapoteza maisha” akasema Dr Olivia na kuinama.Abu dahir akafuta mdomo kwa kitambaa kisha akasema “Ahsante sana Dr Olivia kwa taarifa hii uliyonipa.Nilihitaji sana kufahamu kilichotokea na kuondoa uhai wa kaka yangu” akasema Abu na kimya kifupi kikapita halafu akauliza “Unadhani kwa nini mpaka leo hii hakuna maelezo ya kueleweka kuhusiana na ajali ile namna ilivyotokea? Kwa nini suala hili limebaki likielea? akauliza Abu dahir “Hilo suala hata mimi limekuwa linaniumiza sana kichwa kwani hakuna taarifa zozote mpaka sasa kuhusiana na suala hili.Limekuwa ni suala lililokosa ufumbuzi hadi leo” “Unahisi Edger aliuawa?akauliza Abu “Ninahisi hivyo kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.Edger alikuwa na maadui wengi na ndiyo maana walijaribu kumuua kwa sumu wakamkosa.Naamini maadui zake ndio waliopanga ajali ile siamini kama lile ilikuwa tukio la bahati mbaya” “Kwa nini unaamini hivyo Olivia?Abu akauliza “Ni kutokana na mazingira yenyewe ya namna tukio lilivyotokea.Kwa mfano mpaka leo familia ya dereva wa lile lori la mafuta lililosababisha ajali,inandelea kutafutwa na hawajulikani walipo.Kwa nini wapotee ghafla?Wako wapi?Nao wameuawa pia?Usiku ule dereva yule alikuwa anaelekea wapi? Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo yanaumiza kichwa sana na yamekosa majibu mpaka leo na ndiyo yanayonifanya niamini kwamba ajali ile ilipangwa” akasema Dr Olivia.Ukapita ukimya wa dakika mbili Abu dahir akasema “Olivia ulikuwa ni mtu wa karibu sana wa Edger na kuanzia sasa utakuwa mtu wangu wa karibu pia.Kuna jambo nimekuja kukueleza ambalo naamini litakustua lakini nakuomba usistuke sana” akasema Abu “Jambo gani Abu? “Edger hajafa” akasema Abu dahir.Dr Olivia akamtazama kwa mshangao mkubwa “Sijakuelewa unamaanisha nini” akasema Dr Olivia “Edger hajafariki dunia kama inavyoaminika”akasema Abu dahir.Dr Olivia akasimama “Si kweli Abu.Hizo ni hisia tu lakini ukweli ni kwamba Edger amefariki dunia na mimi ndiye niliyeutambua mwili wake” akasema Dr Olivia “Tafadhali keti Dr Olivia” akasema Abu na Olivia akaketi “Nikwambiacho ni kitu cha kweli kabisa,Edger hajafa kama inavyodaiwa.Tunazo kila sababu za kuamini kwamba Edger hakufa katika ile ajali”akasema Abu “Sikuelewi abu kwa nini unaamini hivyo? Mimi ndiye niliyekuwepo eneo la tukio na ndiye niliyeutambua mwili wake na tukauzika bila ndugu yeyote kujitokeza.Iweje leo ujitokeze na kudai kwamba ndugu yako yuko hai?akauliza Dr Olivia akionekana kukasirika “Dr Olivia nafahamu hili ni suala ambalo litakustua sana lakini huo ndio ukweli wenyewe kwamba Edger ni mzima hajafa.Kilichofanyika ni mpango wa hali ya juu sana ambao ulifanywa na majasusi wa hali ya juu na kuiaminisha dunia kwamba Edger amefariki dunia lakini kumbe bado yuko hai” akasema Abu “Abu hapo ndipo unaponichanganya.Kwa nini unasisitiza kwamba Edger yuko hai? Kama unadai kwamba ajali ile ilikuwa ni mpango mzito nani waliofanya mpango huo na kwa nini?Kama yuko hai yuko wapi?akauliza http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Dr Olivia “Olivia nisingeweza kuja kwako kukupa taarifa hizi kwamba Edger yuko hai kama nisingekuwa na uhakika na ushahidi wa kutosha wa kulithibitisha suala hilo lakini naomba uamini kwamba ni kweli Edger yuko hai na hakufariki dunia katika ile ajali kama inavyodaiwa” “Yuko wapi? akauliza Dr Olivia “Dr Olivia hata sisi hatujui mahala alipo Edger lakini tunaamini yuko hai.Kuna mambo kadhaa ambayo itatulazimu kuyafanya katika kuutafuta ukweli wa mahala alipo Edger.Olivia ili kufahamu ukweli kuhusiana na suala hili la Edger na mahala alipo tunakutegemea sana wewe”akasema abu dahir na Dr Olivia akaangua kicheko kidogo “Abu unanishangaza sana.Umeniletea taarifa kwamba Edger hajafa yuko hai halafu unasema tenba kwamba hujui mahala alipo na unahitaji msaada wangu.Ninashindwa kukuelewa nini hasa lengo lako kwangu” akasema Dr Olivia “Olivia sisi kama familia tuna hakika Edger hajafa bali alichukuliwa na anashikiliwa sehemu Fulani na tunao ushahidi wa kuamini hivyokwamba Edger yuko hai hata hivyo tunataka kuanza mchakato wa kuutafuta ukweli kuhusu Edger na wewe ndiye mtu ambaye tunakutegemea sana katika mchakato huo.Uliyaokoa maisha yake mara ya kwanza bila kuombwa na mtu yeyote lakini safari hii ninakuomba ukubali tena kumsaidia Edger.Huko aliko hatujui ni mateso gani anayapitia,hatujui maisha yake yakoje.Tafadhali Dr Olivia ninahitaji sana msaada wako” akasema Abu dahir .Baada ya kufikiria kidogo Dr Olivia akauliza “Unataka nikusaidie nini Abu dahir? “Kuna hatua tatu tutazipitia hadi kuupata ukweli kuhusu Edger.Tutaanza na hatua ya kwanza lakini kabla ya hatua hiyo itakulazimu kufanya kitu kimoja” akasema Abu “Kitu gani unataka nikifanye?akauliza Dr Olivia “Itakulazimu uachane na kazi unayoifanya sasa” “Nini?akauliza Dr Olivia kwa sauti ya ukali “Usistuke Dr Olivia.Tulia nisikilize hadi nimalize kile ninachotaka kukueleza” akasema Abu “Umenistua sana kuniambia eti niachane na kazi ninayoifanya sasa.Wewe ni nani wa kuniamuru kuacha kazi ninayoipenda?akasema Dr Olivia “Samahani kwa kukustua Dr Olivia lakini unapaswa unisikilize hadi mwisho.Nataka uachane na kazi hii unayoifanya sasa na badala yake utafungua kituo kikubwa cha kufanya tafiti za magonjwa mbali mbali ya binadamu na wanyama ambacho kitakuwa ni kikubwa katika ukanda huu wa afrika mashariki na kati.Gharama zote za ujenzi wa kituo hicho zitatoka kwangu na hautatumia hata shilingi yako moja ila utakachokifanya ni kuanzisha taasisi yako ambayo mimi na wenzangu tutachangia fedha ambazo utazitumia katika ujenzi wa kituo hicho kikubwa ambacho kikikamilika kitakuwa mkombozi mkubwa sana kwa watu wa ukanda huu kwani utafiti wa magonjwa mbali mbali utafanyika kupitia kituo hicho.Baada ya hatua ya kwanza kukamilika ambayo ni ujenzi wa kituo hicho ndipo itafuata hatu aya pili”akasema Abu dahir Haikuwa rahisi kwa Dr Olivia kukubaliana na kile alichokisema Abu dahir.Baada ya mjadala mzito uliochukua masaa zaidi ya mawili,hatimaye Dr Olivia akakubali ombi la Abu dahir la kuachana na kazi katika hospitali kuu ya taifa ya moyo na kuanzisha kituo kile cha utafiti.Baada ya mazungumzo yale marefu wakaagana na Dr Olivia akaondoka “Kuna ule msemo usemao ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.Haya aliyonieleza Abu dahir kwamba Edger hajafariki dunia yamenistua sana.Kama ni kweli ni maajabu makubwa kwangu.Inawezekanaje wakati mimi ndiye niliyeutambua mwili wa Edger hospitali na niliweza kuutambua kutokana na mkufu aliokuwa ameuvaa iweje leo niambiwe eti Edger hakufa na yuko hai?akajiuliza Dr Olivia akiwa ndani ya gari akirejeshwa nyumbani kwake baada ya kutoka kuonana na Abu dahir. “Mwili wangu unanitetemeka kila nikifikiria jambohili.Kama ni kweli Edger hajafariki dunia yuko wapi?I’m confused.Sitakiwi kuendelea kulifirikiria suala hili kwani litaniathiri sana kisaikolojia.Kwa sasa ngoja nielekeze nguvu katika ujenzi wa kituo hicho cha utafiti alichoelekeza Abu dahir.Nini hasa malengo ya kujenga kituo hiki hapa Tanzania? Kituo hicho kina mchango gani katika kumtafuta Edger? Nimekubali maombi yake kwa ajili ya Edger lakini kituo hicho pia kinaweza kuwa na msaada mkubwa sana katika kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali mbali ya binadamu na wanyama hasa haya yanayoibuka mara kwa mara na kuyatafutia tiba.Sioni tatizo kujenga kituo hicho kwa sababu sintantumia hata senti yangu moja” akaendelea kuwaza Dr Olivia “Kwa nini wazazi wa Edger walimleta Tanzania wakati walikuwa na uwezo wa kumlea na kumsomesha nchini Kenya?Abu dahir aliniambia kwamba Edger alihamishiwa Tanzania kwa shughuli maalum.Ni shughuli gani hiyo? Kwa nini hakutaka kuiweka wazi? Kuna mambo mengi yamejificha kuhusu Edger ambayo natakiwa kuyajua” akawaza Dr Olivia MWAKA MMOJA - BAADAE Ujenzi wa kituo kikubwa kabisa cha utafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama kilichojengwa nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ulikamilika.Kilikuwa ni kituo kikubwa na cha aina yake katika ukanda wa afrika mashariki na kati.Ujenzi wa kituo hicho uligharimu fedha nyingi ambazo zilichangwa na wafadhili wa taasisi ya Olivia trust. Kituo hicho cha aina yake cha utafiti kilifunguliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kazi za utafiti zikaanza mara moja.Wanasayansi wengi kutoka ndani na nje ya nchi waliajiriwa katika kituo hicho na magonjwa mbali mbali ya wanadamu na wanyama yalifanyiwa utafiti na kupatiwa tiba yake.Ndani ya miezi sita ya mwanzo tayari magonjwa zaidi ya matano yalikwisha fanyiwa utafiti na kutafutiwa tiba,mafanikio ya kituo hiki yalianza kuonekana Miezi sita baada ya kukamilika kwa kituo kile Dr Olivia aliitwa na Abu dahir nchini Saudi Arabia kwa ajili ya mazungumzo.Siku mbili baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia akachukuliwa na kupelekwa kuonana na Abu dahir.Wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara lakini haya yalikuwa ni mazungumzo maalum kabisa.Alikaribishwa katika himaya ya Abu dahir na kutambulishwa kwa familia yake kisha akamchukua hadi katika nyumba iliyokuwa pembeni ya jumba lake ambako kulikuwa na ulinzi mkali wakaingia ndani na kumkuta mwanamke mmoja mtu mzima aliyejitanda vito vya dhahabu. “Dr Olivia karibu sana,kutana na Habiba Jawad.Huyu ndiye mama yangu na ndiye mama yake Seif Jawad au Edger Kaka kama anavyofahamika”Abu dahir akafanya utambulisho. “Mama kutana na Dr Olivia Themba huyu ndiye aliyeyaokoa maisha ya Seif kwa kumpeleka Israel na ndiye aliyekuwa naye hadi siku ya mwisho alipopotea” akasema Abu na Habiba akatabasamu.Dr Olivia akamsogelea na kwa adabu akapiga magoti akamsalimu yule mama ambaye alimshika mkono akamuinua akamkumbatia “Nimefurahi sana kuonana nawe Olivia ana kwa ana.Nilikuwa ninakusikia na niliomba sana siku hii ifike haraka niweze kuonana nawe na kuushika mkono wako na hatimaye siku imefika na niko nawe leo.Karibu sana Olivia hapa ni nyumbani kwangu,huyu ni mwanangu Abu ambaye mnafahamiana tayari, mwanangu mwingine ni Seif au Edger kama unavyomfahamu” akasema Habiba akitumia Kiswahili safi. “Dr OIivia usiogope tafadhali jisikie nyumbani” akasema Habiba baada ya kumuona Dr Olivia akiogopa. “Olivia naomba tutembee kidogo katika himaya yangu” akasema Habiba Olivia akainuka wakatoka na kutembea taratibu kuelekea katika bustani nzuri “Habari za Tanzani Dr Olivia.Shughuli za utafiti zinakwendaje? Akauliza Habiba “Tanzania kwema kabisa na shughuli zinakwenda vizuri sana.Mpaka sasa tayari tumekwisha kamilisha tafiti za magonjwa matano ya binadamu na tiba yake kupatikana.Bado kuna tafiti nyingine nyingi zinaendelea.Kwa ujumla naweza kusema kwamba kituo kile kimekuwa ni msaada na mkombozi mkubwa sana kwa watu.Ninamshukuru Abu dahir kwa wazo la kujenga kituo kile ingawa malengo makubwa ya kujengwa kwa kituo kile niliambiwa ni hatua ya kwanza ya mchakato wa kumtafuta Edger” akasema Dr Olivia “Dr Olivia kituo kile kina dhumuni la kufanya tafiti za magonjwa mbalimbali na kuyatafutia tiba lakini kina kazi nyingine mbili maalum kabisa.Kabla ya kukueleza kuhusiana na kazi hizo ningependa kwanza kukujulisha kwamba naitwa Habiba jawad kama alivyonitambulisha Abu dahir.Mimi ndiye mama mzazi wa Edger kaka na Abu dahir.Alipokuja Tanzania kuonana nawe mwaka jana Abu alikueleza machache kuhusiana na Edger kaka ambaye jina lake halisi ni Seif Jawad.Mimi asili yangu ni Somalia lakini nilizaliwa na kukulia Kenya nikaolewa na tajiri mmoja anaitwa Nasser jawad tukabahatika kumpata mtoto mmoja tu ambaye ni Seif.Alipokuwa na umri wa miaka mitano seif alihamia nchini Tanzania akiwa chini ya uangalizi wa marafiki zetu na toka hapo maisha yake yote yamekuwa nchini Tanzania” akasema Habiba “Abu dahir alipokuja kuonana nami alinieleza hayo yote na nilimuuliza sababu ya Edger kuhamishiwa Tanzania lakini hakunipa jibu.Ninaamini leo nitapata jibu nini hasa ilikuwa sababu ya kumuhamishia Seif Tanzania?akauliza Olivia “Ipo sababu ya seif kuhamishiwa Tanzania na nitakueleza” akasema Habiba na kunyamaza kidogo kisha akaendelea “Wazazi wangu waliuawa nchini Tanzania nikiwa bado msichana mdogo.Baba yangu alikuwa anazunguka sehemu mbalimbali akitoa mihadhara ya kidini na alipokuwa nchini Tanzania yeye na mama yangu walivamiwa na kuuawa na watu wanaodaiwa ni majambazi.Vifo vya wazazi wangu viliniumiza sana kwani vilinifanya niishi maisha ya taabu kubwa na kutokana na magumu niliyoyapitia niliweka ahadi ya kuhakikisha kwamba wale wote waliowaua wazazi wangu wanapatikana na kulipa uovu wao hata kama itapita miaka mia moja.Nilipata tetesi kwamba mauaji ya wazazi wangu ulikuwa ni mpango maalum wa serikali za afrika mashariki kumuua baba wakidai kwamba baba yangu alikuwa anazunguka kuhamasisha watu kujiunga na vikundi vya ugaidi.Nilimuingiza Seif Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango wangu wa kulipiza kisasi kwa nchi za afrika mashariki kwa kuwaua wazazi wangu.Nilimuandaa seif kwa ajili ya kushika madaraka makubwa nchini Tanzania ili mpango wangu uweze kutimia.Nilitaka awe rais wa Tanzania” akasema Habiba na sura ya Dr Olivia ilionyesha mstuko mkubwa. “Usistuke Olivia ni kweli nilimuandaa Seif aje kushika madaraka makubwa ya nchi.Nilimkabidhi kwa familia ya watanzania ambao niliwawezesha kwa utajiri na wakamsajili Seif kama mtoto wao wa kumzaa wakambadili jina na kumuita Edger Kaka.Nasser baba yake Seif alifariki dunia kwa ugonjwa wa saratani, nikaolewa na mwanaume mwingine anaitwa Abdul dahir ambaye ndiye baba yake Abu dahir.Abdul alikuwa ni mpalestina na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za taifa la Palestina.Alikuwa tajiri sana hivyo alifadhili vikundi mbali mbali vilivyokuwa vinaendesha mapambano dhidi ya Israel.Naamini umekuwa ukisikia juu ya mzozo unaoendelea kati ya Palestina na Israel.Umekuwa ni mzozo wa muda mrefu na hakuna dalili zozote za kumalizika licha ya juhudi mbalimbali za kujaribu
kuumaliza mzozo huo kufanyika.Labda nikupe maelezo mafupi kuhusiana na mzozo huu wa palestina na Israel.Mzozo huu ulianza karne ya ishirini baina ya wakazi wayahudi na waarabu wa maeneo ambayo hivi sasa yako chini ya Israel na mamlaka ya palestina.Toka kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948 tayari taifa hili limekwisha pigana vita sita na majirani zake na hadi sasa mapambano yanaendelea na hakuna dalili zozote za kupata suluhisho la mzozo huu. Mwaka 1947 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipigia kura mpango w a ugawaji wa Palestina ambapo mataifa 33 yalipiga kura ya ndiyo,13 hapana na 10 hayakusimama upande wowote. Kufuatia kura hiyo eneo la Palestina lilitakiwa kugawiwa kwa dola la Kiyahudi,dola la Kiarabu na mji wa Yerusalemu. Waarabu walipinga ugawaji huo kwa kudokeza ya kwamba mpango wa ugawaji wakazi wangekuwa Waarabu.Sehemu kubwa ya ardhi katika sehemu ya Dola la Kiarabu ilikuwa mlimani na haikufaa vema kwa ajili ya kilimo. Wawakilishi wa Kiyahudi walisema idadi ya Wayahudi itaongezeka haraka kutokana na uhamiaji wa Wayahudi wengine kwani wakati ule bado kulikuwa na malaki ya wayahudi katika makambi kwenye nchi za Ulaya ambao hawakuuawa na Wajerumani Mara baada ya azimio hilo la umoja wa mataifa,mapigano yalianza katika Palestina.Vikundi vya wanamgambo wa Kiarabu vilishambulia makazi ya Kiyahudi kote nchini.Wayahudi pia walikuwa na vikundi vyao vya wanamgambo. Tarehe 14 Mei mkutano wa wawakilishi Wayahudi ulitangaza Dola la Israeli kama nchi mpya. Tarehe 15 Mei 1948 majeshi ya Misri, Yordani, Lebanoni, Syria na Irak yaliingia Palestina yakatwaa maeneo ya Kiarabu na kushambulia makazi ya Kiyahudi.Katika vita ya miezi 10 jeshi la Israeli lilifaulu kusimamisha wapinzani na kuwarudisha nyuma.Wakati wa kusimamisha mapigano Israeli ilikuwa imeongezeka maeneo yake ikatawala asilimia 78 ya eneo iliyokabidhiwa awali na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Dola la Kiyahudi pamoja na nusu ya maeneo yaliyokusudiwa kwa ajili ya Dola la Kiarabu. Zaidi ya wakazi Waarabu 700,000 walilazimika kukimbia kutoka miji na vijiji vyao,wakienda nje ya maeneo yanayotawaliwa sasa na Israeli.Waarabu takribani 150,000 walibaki ndani ya maeneo hayo kama raia Waarabu wa Israeli.Baada ya vita kumalizika Israeli ilikataa kurudi kwa watu waliokuwa wamekimbia na hii ndiyo asili ya wakimbizi Wapalestina wanaoishi Syria, Lebanoni, Jordani na Misri, pamoja na wale wanaoendelea kukaa katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi. Nchi zote za kiarabu isipokuwa Jordani zilikataa kuwapa wakimbizi hao haki za uraia,kwa hiyo hadi leo wajukuu wamebaki kama wakimbizi katika nchi za kigeni bila uraia,wakisafiri wanatumia vitambulisho vilivyotolewa na umoja wa mataifa,wanakosa haki ya kutafuta kazi au kushiriki katika siasa kama raia wa kawaida, hata kama familia zimeshaishi katika nchi hizo hadi kizazi cha tatu au nne.Nadhani unapata picha ni mateso kiasi gani wanayapata wapalestina ambao wametolewa katika ardhi yao.Baada ya vita ya 1948-1949 nchi jirani zilikataa kulitambua taifa la Israeli.Hali ya vita ikaendelea ingawa bila mapigano kati ya majeshi makubwa.Wanamgambo wa wafedayin wapalestina waliendelea kuvuka mpaka kutoka makambi ya wakimbizi na kushambulia vijiji vya Kiyahudi. Wanamgambo hao walipata mara nyingi silaha na mafunzo kutoka kwa majeshi ya Misri na Syria.Mwaka 1964 chama cha ukombozi wa Palestina PLO yaani Palestine Liberation Organization kilianzishwa kufuatia azimio la nchi za kiarabu.Huu ulikuwa ni muungano wa vikundi mbalimbali vya wapalestina na kiliendesha harakati za kushambulia mipaka ya Israel mara kwa mara.Olivia historia ya mzozo huu ni ndefu lakini kwa maelezo hayo mafupi naamini umepata picha halisi ya kwa nini raia wa Palestina wanamwaga damu zao kila uchao kupigania ardhi yao iliyoporwa.Abdul dahir alikuwa mmoja wa wafadhili wa vikundi hivi vidogo vilivyoendesha mapambano dhidi ya Israel hadi alipouawa” akanyamaza kidogo “Ninayafahamu mateso wanayoyapata ndugu zangu” akaendelea “Hivyo basi kifo cha Abdul hakikuzuia harakati za kudai haki kuendelea.Nilishika hatamu na kuendelea kutoa ufadhili kwa wapigania haki lakini nikimtumia mtu anayeita Sayid Omar.Huyu nilimuwezesha akawa tajiri mkubwa na ndiye ninayepitishia ufadhili wangu kwake.Harakati hizi hazitakoma hadi pale tutakapohakikisha kwamba ardhi ya wapalestina imerudishwa.Tukiachana na hayo turejee nyumbani Tanzania.Bado azma yangu ya kutaka kulipiza kisasi kwa wazazi wangu iliendelea na nilimtengeneza Seif kwa ajili ya hilo.Mipango ilikwenda vyema na Seif akaingia katika siasa,akashinda ubunge ,akawa na jina kubwa lengo kubwa likiwa ni kumuandaa kuwa rais wa Tanzania.Katika harakati zangu niliungana na kikundi cha IS na lengo letu ni kuanzisha himaya kubwa ya IS katika ukanda wa Afrika mashariki na dhumuni kubwa ni kuwaandaa vijana ambao watatusaidia katika mapambano ya kudai haki sehemu mbali mbali duniani.Kuna vijana wengi kutoika ukanda wa Afrika mashariki ambao wanasafiri umbali mrefu kujiunga na IS hivyo tunataka kuanzisha kambi za siri za kuwakusanya vijana na kuwapa mafunzo kisha kuwatumia katika mapambano yetu ” akasema Habiba na Dr Olivia akatoa kitambaa katika pochi yake akajifuta jasho usoni “Ee Mungu nisaidie niweze kutoka salama huku niliko.Nimejileta mwenyewe katika mto wenye Mamba niokoe ee Mungu wangu” akaomba Dr Olivia kimya kimya.Alikuwa anatetemeka ndani.Aliogopa sana.Habiba Jawad akalitambua hilo “Usiogope Olivia.Najua haya niliyokueleza yamekustua sana lakini ni lazima uyafahamu” akasema Habiba “Madam Habiba ni kweli nimestuka sana hasa baada ya kusikia kuhusu kikundi cha IS.Hiki ni kikundi cha kigaidi na kimekuwa kikiendesha mauaji ya kikatili sehemu mbali mbali duniani” akasema Dr Olivia kwa woga “Usiogope Dr Olivia.IS ni kikundi chenye kupigania haki za wanyonge waislamu na wasio waislamu kote duniani na ndiyo maana nikakubali kuungana nao na kwa sasa tunaelekeza nguvu katika kupambana na Israel” “Madam Habiba hakuna unachoweza kunieleza kuhusu IS nikakuelewa.Hiki ni kikundi cha kigaidi na kimekuwa kikifanya mauaji ya kinyama sehemu mbali mbali duniani.Hakitetei mtu yeyote zaidi ya kuendesha mauaji ya kinyama.Laiti ningejua kuhusu jambo hili mapema nisingekubali katu kuungana nanyi.Edger alifahamu kuhusu suala hili? Akauliza Dr Olivia “Edger anafahamu kila kitu”akajibu Habiba.Dr Olivia akashika kichwa “Oh my God ! “Sikiliza Olivia niliamua kujiunga na IS ili kuongeza nguvu kwa ajili ya kumsaidia Edger aweze kushika nafasi ya urais.Tunataka kulitumia eneo la Afrika mashariki kama eneo la mafunzo kupika watu wetu ambao watakwenda kufanya kazi sehemu mbali mbali duniani.Tumechagua Tanzania iwe ni kambi yetu kuu ya mafunzo na itakuwa rahisi kwetu kuanzisha kambi ya mafunzo endapo Edger atakuwa rais.Tuliwekeza muda na fedha nyingi kwake na tulifanikiwa kwa asilimia tisini na nane kumtengeneza mtu ambaye alipendwa sana,mtu ambaye alikuwa mtetezi wa wanyonge,anayepambana na mafisadi wanaohujumu uchumi wa Tanzania na tulikuwa na uhakika kwamba endapo angegombea urais angeshinda kwa asilimia kubwa sana lakini kwa bahati mbaya mpango wetu ulivurugwa katika dakika za mwisho kabisa” akasema Habiba. “Katika safari ya kumuandaa Edger kushika madaraka makubwa ya nchi tulijikuta tukitengeneza pia maadui ambao hawakumpenda na walipanga kumuua na mojawapo ya jaribio la kumuua ni lile la kumuwekea sumu jaribio ambalo lilishindwa na ninakushukuru sana kwa kuyaokoa maisha yake.Akiwa hospitali bado maadui zake waliendelea kumfuatilia kwa lengo la kumuua.Walitumwa watu Israel kumfuata kumuua.Katika chumba alimokuwa amelazwa kulifungwa kamera za ulinzi na vyombo vya kunasa mawasiliano ikiwa ni muendelezo wa mipango ya kumuua.Walikuwa wanafuatilia mawasiliano yake yote na hata alipoamua kurejea nyumbani walifahamu kwamba anarejea hivyo wakafanya jaribio lile la kumuua” akasema Habiba “Abu dahir aliniambia kwamba Edger hajafa.Kauli hii imenitesa kwa mwaka mzima nikitafakari hili linawezekanaje? Mimi ndiye niliyeutambua mwili wake hospitali uliokuwa umeungua sana na niliweza kuutambua kutokana na mkufu aliokuwa ameuvaa shingoni uliokuwa na kidani chenye herufi E na pete alizokuwa amevaa.Naamini leo nitapata majibu ya suala hilii” akasema Dr Olivia “Alichokueleza Abu ni cha kweli kabisa kwamba Seif hajafa.Kilichofanyika ulikuwa ni mpango maalum kabisa wa kumteka na kuiaminisha dunia kwamba Edger amefariki lakini ukweli ni kwamba Edger yuko hai”akasma Habiba Jawad “Madam Habiba bado mnaendelea kunichanganya.Kama yuko hai mnafahamu mahala alipo?Nani waliofanya mpango huo?akauliza Dr Olivia “Mpaka sasa bado hatufahamu mahala alipo Edger wala nani aliyefanya mpango ule lakini tunaamini kabisa kwamba yuko hai sehemu Fulani anashikiliwa” akasema habiba “Madam Habiba unakiri kwamba hamjui mahala alipo na wala wanaomshikilia mna uhakika gani kwamba Edger yuko hai?akauliza Olivia “Olivia najua jambo hili limekustua sana kusikia kwamba Edger yuko hai lakini nakuhakikishia kwamba Edger yuko hai hakufa katika ile ajali.Kuna sababu zinazopelekea tuamini hivyo.Nimekueleza kwa kirefu kuhusiana na mimi ni nani na maisha yangu kwa ujumla na kutokana na harakati zangu hizo za kupigania haki nimekuwa nikitafutwa sana na nchi ya Israel.Miezi kadhaa baada ya kuamini Edger amefariki katika ile ajali nilianza kufuatiliwa na majasusi wa Mossad ambao walivamia sehemu zangu mbali mbali za siri lakini kwa bahati nzuri hawakupata chochote kwani mambo yangu ninayafanya kwa umakini mkubwa sana.Tulijiuliza na wenzangu namna Mossad walivyoweza kupata taarifa zile kwani zilikuwa ni taarifa nyeti sana na waliokuwa wakifahamu maficho yangu ni watu wachache mno ambao hata itokee nini hawataweza kunisaliti ndipo hapo tulipoanza kuwa na hisia kama kweli Edger alifariki katika ajali ile.Tulianza uchunguzi mara moja na tukagundua kwamba kifo kile ulikuwa ni mpango maalum kabisa ulioandaliwa.Tulibaini kwamba ndege ambayo Edger aliondoka nayo ilichelewa kwa saa kumi zaidi ya muda ambao ilitakiwa kuwasili jijini Dar es salaam” akasema Habuba “Nalifahamu hilo.Edger alitaka kuwahi mazishi ya waziri mkuu na ndiyo maana tulichagua ndege ambayo ingetuwezesha kufika Dar es salaam saa sita mchana lakini kulitokea hitilafu za kiufundi zilizopelekea ndege ile ichelewe kuondoka Tel aviv hivyo tukachelewa sana kufika Dar es salaam.Badala ya kufika saa sita mchana tukafika saa sita za usiku”akasema Dr Olivia “Uchunguzi wetu unaonyesha kwamba hakukuwa na hitilafu yoyote katika ile ndege bali ulikuwa ni mpango maalum wa kuichelewesha ifike Dar es salaam usiku ili waweze kukamilisha mpango wao wa kumteka Edger na kutuaminisha kwamba amefariki lakini nina uhakika mkubwa kwamba Edger hajafa yupo sehemu Fulani anashikiliwa” akasema Habiba na kumfanya Dr Olivia azame mawazoni “Madam Habiba ninaanza kupata picha fulani kwa hayo maelezo yako.Taarifa ya ndege kuwa na hitilafu ilikuwa ya ghafla sana na ilimshangaza kila mtu.Hata mazingira ya ajali ile yanatia shaka sana.Ni miaka mitatu sasa lakini familia ya dereva wa lori lililogonga gari la Edger haijapatikana na hawajulikani walipo na hii inazidi kunifanya niamini kwamba yawezekana kweli Edger hajafa kama tunavyodhani” akasema Dr Olivia “Nashukuru kama umeanza kuipata picha kubwa ya jambo hili” akasema Habiba “Lakini madam Habiba kuna maswali ambayo nitahitaji majibu.Kama Edger hajafa ule mwili uliokutwa ndani ya gari lake ukiwa umevaa mkufu ule wa Edger ambao alikuwa ameuvaa toka tukiwa Israel ni wa nani?Na kama bado mzima yuko wapi na nani wanaomshikilia? akauliza Dr Olivia “Alikueleza Abu dahir kwamba kutakuwa na hatua kadhaa katika kuutafuta ukweli kuhusu Edger na hatua ya kwanza ilikuwa ni kujenga kituo kile cha utafiti ambacho kimekamilika na sasa tunaingia katika hatua ya pili ambayo ni kuupata ukweli kuhusu Edger kama kweli yuko hai.Mwili ule ambao ulikutwa ndani ya gari ukiwa na mkufu wa Edger na wewe ukautambua kwamba ni wa Edger tunataka kuufanyia uchunguzi kubaini kama kweli ni mwili wa Edger na hilo zoezi litafanyika katika kile kituo chako ambacho dhumuni kubwa la kujengwa kwake lilikuwa hilo.Tutachukua sampuli za mabaki ya ule mwili tutaupima vinasaba kupata ukweli kama kweli mwili ule ulikuwa wa Edger na kama vipimo vikituonyesha kwamba mwili ule si wake basi tutakuwa sahihikwamba Edger yuko hai na hapo tutaingia katika hatua ya tatu ya kumtafuta na kujua mahala alipo” akasema Habiba “Madam Habiba nakubaliana na wazo hilo la kuufanyia uchunguzi mwili ule ambao tunaamini ni wa Edger ili kuupata ukweli.Kama mwili ule utakuwa si wa Edger unadhani nani waliomteka nyara na kwa madhumuni gani? Yuko wapi? akauliza Dr Olivia “Ni mapema sana kusema anashikiliwa wapi na nani lakini baada ya kupata uhakika kwamba mwili ule si wa Edger hapo ndipo tutakapoanza uchunguzi wetu kuhakikisha tunafahamu mahala alipo na nani anamshikilia.Dr Olivia nina uhakika mkubwa sana kwamba Edger yuko hai na nitakuomba sana msaada wako ili tuweze kumpata.Huko aliko naamini atakuwa anateswa mno na tusipoharakisha kumuokoa watamuua.Dr Olivia ninaamini mambo niliyokueleza leo yamekustua sana na kukuogopesha lakini nakuomba usiogope.Lengo la mimi kushirikiana nawe ni kwa ajili ya kunisaidia kumpata Edger ambaye najua siwezi kumpata bila msaada wako hivyo nakuomba tushirikiane kuhakikisha kwamba Edger anapatikana akiwa mzima” akasema Habiba “Madam Habiba ni kweli mambo uliyonieleza leo yamenistua na kuniogopesha hasa baada ya kuifahamu historia ya Edger.Sikujua kama Edger ana mahusiano na kikundi cha IS.Sikujua kwa nini Edger alihamishiwa Tanzania.Baada ya kufahamu haya yote nimeingiwa na hofu kubwa” “Nini kinakupa hofu Dr Olivia?akauliza Habiba “Kila kitu nilichokifahamu leo.Ninawaogopa magaidi.Watu wengi wasio na hatia wanapoteza maisha sehemu mbali mbali duniani kutokana na vitendo vya ugaidi.IS ni kikundi cha kigaidi na kimekuwa kikifanya mauaji sehemu mbali mbali duniani.Nimeingiwa na woga kufahamu kuwa Edger ana mahusiano na kikundi hiki cha kigaidi” akasema Dr Olivia “Tafadhali usiogope Dr Olivia” akasema Habiba “Nchini Tanzania Edger ni mbunge ambaye ana jina kubwa sana,anapendwa na watu wengi na amekuwa mstari wa mbele katika kuendesha mapambano dhidi ya mafisadi na wahujumu uchumi.Hana woga wala aibu katika mapambano hayo.Amekuwa ni mtetezi wa wanyonge,amekuwa ni msemaji wa wale wasiokuwa na sauti ya kusema.Kutokana na nguvu yake kubwa ya ushawishi naamni kama angegombea urais angeshinda kwa kishindo kikubwa.Kinachonipa hofu kwamba nyuma ya mafaniko hayo yote makubwa aliyonayo ana siri kubwa ambayo watanzania hawaifahamu.Pindi watanzania wakijua kwamba mtu ambaye walikuwa tayari kumuamini awaongoze kwanza si mtanzania na pili ana mafungamano na kikundi cha IS sina hakika nini kitatokea.Huu unaweza ukawa ni mwisho wa Edger.Hiyo ni hofu yangu kubwa sana” akasema Dr Olivia.Habiba akatabasamu kidogo na kusema “Huna sababu ya kuwa na hofu Olivia.Hakuna atakayejua siri hiyo.Ni watu wachache sana wanaofahamu jambo hili na wote wamekula kiapo cha utii cha kwenda kaburini na hii siri.Hakuna atakayeweza kutoa siri hii kuhusiana na Edger.Katika watu wachache wanaoifahamu hii siri umeongezeka wewe hivyo utalishwa kiapo cha uaminifu kwamba hautatoa siri hii na siku ukifungua ulimi wako kutamka chochote kuhusiana na siri hii uliyoifahamu leo utakuwa ni mwisho wako wewe na ukoo wako wote.Hakuna serikali inayoweza kukusaidia tunao mtandao mkubwa na tunao uwezo wa kuingia sehemu yoyote.Sikuogopeshi Dr Olivia lakini tayari nawe ni mmoja wetu” akasema Habiba na Dr Olivia akahisi haja ndogo inataka kumtoka “Dr Olivia umestuka sana kusikia kwamba wewe tayari ni mmoja wetu lakini hilo lilikuwa ni angalizo tu kwamba umezifahamu siri zetu hivyo unapaswa ukae kimya.Hatuna tatizo na wewe hakuna atakayekugusa na badala yake sisi ndio tutakaokuwa tunakulinda na kuhakikisha unakuwa salama.Hatuna lengo lolote baya na Tanzania na ninakuhakikishia kwamba hakuna damu ya mtanzania itakayomwagika.Edger unamfahamu ni mtu mzuri,ana roho nzuri anaipenda Tanzania na ni mtu mwenye malengo makubwa sana na Tanzania.Nilikueleza awali kwamba mpango wa kumpeleka Edger Tanzania ilikuwa ni kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa wale waliowaua wazazi wangu lakini baada ya Edger kuupata ubunge na kuona mambo makubwa aliyokuwa anayafanya hasa katika kufichua wizi mkubwa wa rasilimali za nchi unaofanywa na vigogo niliamua kubadili malengo yangu na kuanza kumuunga mkono katika mapambano yake dhidi ya wanyonge.Alinieleza namna anavyoguswa na maisha wanayoishi watu masikini ukilinganishwa na utajiri mkubwa ulioko nchini ambao ni watu wachache wanaofaidika nao.Licha ya mipango yetu lakini umasikini wa watanzaniani jambo linalomgusa Edger kutoka moyoni.Aliniomba tuachane na mpango ule wa kuwatafuta watu watu waliowaua wazazi wangu bali tujielekeze katika kupambana na maadui wa kweli wa maendeleo ya Tanzania ambao ni mafisadi na baadhi ya mataifa makubwa ambayo yamekuwa yakizinyonya nchi ndogo na Tanzania ikiwemo.Wazo hili nililiona ni zuri na nikaamua kumuunga mkono,hivyo vita yetu ya sasa ni kwa mataifa makubwa ambayo yanazikandamiza nchi ndogo na Tanzania ikiwemo na vita hii ni ngumu na ndiyo maana ninataka Edger awe rais wa Tanzania ili tuwe na nguvu ya kupambana na mataifa haya ya magharibi” akasema Habiba. “Madam Habiba pamoja na nia hiyo mnayosema ni njema lakini hakuna atakayeelewa akisikia kuhusu Edger kuwa na mafungamano na IS.Bado machoni pa wengi hiki ni kikundi cha kigaidi na hakuna mtanzania ambaye atakubali kuongozwa na rais ambaye kwanza si mtanzania na pili ana mafungamano na kikundi cha kigaidi.Hata mimi siko tayari madam Habiba kwa Edger kuongoza nchi.Najua haya ni maneno ambayo hayakufurahishi lakini huo ni ukweli kwamba siko tayari kwa Edger kuwa rais wa Tanzania.Nchi yangu Tanzania ni nchi yenye kuheshimika duniani kote.Ni nchi ya mfano kwa mataifa mengine na ambayo amani imetamalaki kwa miaka na miaka na katu siko tayari kuona amani yetu ikianza kuchezewa.Endapo Edger akishinda urais utakuwa ni mwanzo wa kulisambaratisha taifa letu kwani zitaanza kupandikizwa chochochoko za dini na taifa lile zuri ambalo limekuwa ni kimbilio la wale wote wasio na kwao litabomoka na hilo ni pigo kubwa kwa Afrika nzima.madam habiba unapozungumzia Afrika unaizungumzia Tanzania ambayo kutokana nayo nchi nyingi zimekombolewa kutoka katika makucha ya wakoloni.Tanzania imekuwa msuluhishi wa mizozo katika nchi mbali mbali ndani ya bara la Afrika,imekuwa ni nyumba ya wakimbizi wanaokimbia mapigano katika nchi zao,sifa hii ya nchi hii nzuri iliyobarikiwa haitakiwi kuharibiwa.Tanzania inapaswa ibaki kama ilivyo yaani kisiwa cha amani” akasema Dr Olivia na kushindwa kuyazuia machozi kumtoka “Dr Olivia usilie tafadhali.Yote uliyoyasema nimeyasikia lakini nakuhakikishia kwamba hatuna malengo mabaya na Tanzania.Tuna malengo mazuri sana ya kuisaidia nchi yako unayoipenda.Hata kama Edger akiwa rais hakuna tatizo lolote litakalotokea” akasema Habiba.Ulipita ukimya halafu Dr Olivia akasema “Madam Habiba,mwanao Edger au Seif ni mtu wangu wa karibu katika kipindi kifupi nilichofahamiana naye alidiriki hata kunitamkia kwamba ananipenda japo sikumpa jibu lolote kwa sababu kwanza tulikuwa hospitali na pili kipindi tulichofahamiana kilikuwa kifupi sana lakini nakiri kwako kwako kwamba hata mimi nilikwisha anza kuwa na hisia na Edger japo sikumueleza.Nilitaka akitoka hospitali tuoate muda wa kutosha kuthibitsha kama hisia zetu ni za kweli lakini hatukupata huo muda akatoweka.Baada ya kuufahamu ukweli kuhusu Edger sina hakika kama hata akipatikana nitaendelea kuwa na urafiki naye lakini nitashirikiana nanyi katika kumtafuta.Pamoja na hayo mimi na wewe lazima tuwe na makubaliano” akasema Dr Olivia “Edger hakuwahi kunitamkia chochote kuhusu kumpenda mwanamke yeyote na sina hakika kama maneno hayo aliyokutamkia amewahi kumtamkia mwanamke mwingine.Kitu gani mimi na wewe unataka tukubaliane Olivia?akauliza Habiba.Dr Olivia akamtazama Habiba usoni kwa muda halafu akasema “Nitaendelea kushirikiana nanyi katika kumtafuta Edger lakini kwa sharti moja kwamba endapo akipatikana hatajishughulisha tena na mambo yoyote yanayohusiana na siasa na mpango wa kumtaka agombee urais hautakuwepo tena” akasema Dr Olivia.Habiba Jawad akatabasamu na kuuliza “Ni vipi kama nikisema hapana? “Sintashiriki katika mpango wowote wa kumtafuta Edger”akasema Dr Oliviana sura ya Habiba ikabadilika “Mungu nisaidie hiki ninachokifanya ni hatari kubwa watu hawa wanaweza wakaniua muda wowote.Natakiwa kuwa makini sana”akawaza Dr Olivia akitazamana na Habiba “Madam Habiba kwa sasa mnanihitaji sana katika mpango huu na ili nishiriki lazima mkubaliane na hicho ninachokitaka” akasema Dr Olivia.Habiba alimtazama Dr Olivia hadi akaingiwa na wasi wasi “Hakuna tatizo na hicho unachokihitaji.Ninachokitaka mimi ni mwanangu apatikane hata kama itakuwa ni kwa kuvuruga mipango yetu yote niko tayari,hata hivyo nawe lazima ulishwe kiapo cha kuilinda siri hii hadi kaburini.Hatakiwi mtu mwingine yeyote kujua” akasema Habiba. DAR ES SALAAM Dr Olivia alirejea Dar es salaam tayari kabisa kuanza mchakato wa kuutafuta ukweli kuhusu Edger Kaka ambaye kila ....
DAR ES SALAAM Dr Olivia alirejea Dar es salaam tayari kabisa kuanza mchakato wa kuutafuta ukweli kuhusu Edger Kaka ambaye kilamtu aliamini kwamba amefariki dunia na kuzikwa “Bado akili yangu inanituma kuamini kwamba yule tuliyemzika ni Edger Kaka .Hata hivyo ngoja tufanya uchunguzi ili tuubaini ukweli kama kweli amekufa au yuko hai kama mama yake anavyohisi” akawaza Dr Olivia akiwa ndani ya gari akielekea nyumbani kwake baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.Bila kuchelewa alipofika nyumbani kwake akampigia simu rafiki yake Walter kasuku. “Dr Olivia” akasema Walter “Walter ninahitaji kukuona uko wapi? “Niko katika mizunguko yangu mjini” “Unaweza ukaja nyumbani kwangu mida hii?Niko hapa ninakusubiri” akasema Dr Olivia na Walter akamuahidi kuwa angefika pale kwake muda si mrefu. “Ninajuta sana kuyaokoa maisha ya Edger kwani msaada wangu nilioutoa unanipeleka katika shimo la moto.Nimeingia katika hatari kubwa sana bila kutarajia. Hakuna anayeweza kuhisi kama Edger kaka tumaini la watu wengi si mtanzania na vile vile ana mafungamano na IS.Hii ni siri kubwa sana na ninajuta kuifahamu.IS ni kikundi hatari sana cha kigaidi lakini siwezi kwenda kinyume na maelekezo yao kwani wamekwisa nilisha kiapo cha kutunza siri hii niliyoifahamu na nimewahakikishia kwamba nitakwenda nayo kaburini”akawaza Dr Olivia “Ninajiuliza ni vipi kama nikigundulika kama ninawasiliana na Habiba Jawad ambaye ni mfadhili wa makundi ya kigaidi? Ni vipi kama ikigundulika kituo kile cha utafiti wa magonjwa kimejengwa kutokana na fedha za watu ambao ni wafadhili wa magaidi?Kuna wakati ninajiwa na wazo la kutaka kukiwasha moto kituo kile kiteketee kabisa ili mimi na hawa jamaa tusiwe na mawasiliano tena lakini kituo kile ni muhimu na kina msaada mkubwa sana” akawaza Dr Olivia na kuamua kunywa mvinyo mkali ili kuondoa mawazo yaliyojaa kichwani Walter Kasuku aliwasili katika makazi ya Dr Olivia na kukaribishwa ndani. “Walter karibu sana” Dr Olivia akamkaribisha Walter “Olivia are you okay?akauliza walter mara tu baada ya kumuona Dr Olivia “I’m okay.Nina uchovu wa safari nimerudi toka nje ya nchi mchana huu” akasema Dr Olivia “Pole na safari Dr Olivia.Baada ya kupata mwito wako nimeachana na kila kitu nimekuja kukusikiliza” akasema Walter na Dr Olivia akatabasamu “Walter nimekuita ninahitaji msaada” “Sema Olivia unahitaji msaada gani? “Nina kazi muhimu sana nataka unitafutie vijana majasiri ”akasema Dr Olivia.Walter akatabasamu na kutoa pakiti ya sigara “Ni kazi gani hiyo Dr Olivia?akauliza Walter huku akiwasha sigara “Ni kazi ngumu kidogo na inayohitaji usiri mkubwa” akasema Dr Olivia “Usiogope Dr Olivia niambie ni kazi gani,hata kama ni kuua mtu kwa ajiili yako mimi niko tayari wewe ni mtu wangu wa muhimu sana.Toka uliponisaidia mwanangu akafanyiwa upasuaji wa moyo wakati ule nikiwa sina hata shilingi kumi wewe si rafiki tu bali ni ndugu yangu kabisa.Niambie kazi gani unayo? akasema Walter huku akipuliza moshi wa sigara “Walter unanifurahisa sana ndugu yangu sijawahi kuwa na mawazo kama hayo ya kuua mtu” akasema Dr Olivia huku akicheka “Hata mimi nilikuwa nakutania Dr Olivia.Nieleze ni kazi gani unayo? “Unamkumbuka Edger Kaka?akauliza Dr Olivia “Ndiyo ninamkumbuka.Si yule mbunge aliyefariki katika ajali ya gari?akauliza Walter “Ndiyo” “Ni miaka mitatu sasa imepita toka alipofariki dunia.Ninataka kupata sampuli ya mabaki yake kwa ajili ya kufanya uchunguzi Fulani.Ninahitaji unitafutie vijana wanaoweza kuchimba vizuri na kuingia ndani ya kaburi kuchukua sampuli za mabaki ninazohitaji.Ni kazi ngumu na ya siri ila yenye malipo manono” akasema Dr Olivia.Walter akapuliza moshi mwingi na kusema “Olivia hiyo mbona ni kazi ndogo tu.Kwa kuwa ni kazi muhimu na ya siri nitaisimamia mimi mwenyewe na sihitaji malipo yoyote.Vijana watakaonisaidia nitawalipa mimi mwenyewe” “Walter hapana hupaswi kufanya hivyo.Nitakulipa fedha kama ambavyo ningemlipa mtu yeyote ambaye angeifanya hii kazi.Tafadhali naomba usiseme hapana” akasema Dr Olivia “Sawa Olivia wewe ni bosi na mimi ninakusikiliza.Lini unataka kazi hiyoifanyike? “Nataka kazi hiyo ifanyike usiku wa leo,ila na mimi nitakuwepo eneo la tukio ili nichukue sampuli ninazohitaji” akasema Dr Olivia “Usihofu Dr Olivia kila kitu kinawezekana.Mchana huu mimi nitakwenda katika makaburi ya midizini alikozikwa Edger nitafanya uchunguzi wa namna tutakavyoweza kuendesha zoezi hilo usiku wa leo_Olivia jambo hili hesabu tayari limekwisha” akasema Walter na kuagana na Dr Olivia “Bado akili yangu inakataa kabisa kwamba Edger yuko hai.Mimi ndiye niliyeutambua mwili wake hospitali.Japokuwa Habiba amejaribu sana kunielewesha kwa nini wanaamini Edger yuko hai lakini nikikumbuka namna ilivyokuwa na namna nilivyoweza kuutambua mwili wa Edger siamini kama ni kweli yuko hai.Lakini ukilichunguza kwa undani zaidi suala hili lina utata mwingi.Majibu yote tutayapata baada ya kufanya vipimo” akawaza Dr Olivia baada ya Walter kuondoka “I’m so scared.Ni vipi kama kweli mwili ule nilioutambua haukuwa wa Edger? Akajiuliza “Hili jambo linaniogopesha sana.Lakini vipimo vitatupa majibu” akaendelea kuwaza **************** Saa mbili za usiku Walter alikwenda kumchukua Olivia kwa ajili ya kuelekea katika zoezi la kwenda kuchukua sampuli za mabaki ya Edger Kaka. “Dr Olivia una hofu yoyote?akauliza Walter baada ya Dr Olivia kuingia garini “Ninahofu lakini hakuna tatizo lolote twendeni” akasema Dr Olivia.Ndani ya gari alikuwepo Walter na vijana wengine watatu safari ikaanza kuelekea makaburi ya Midizini “Sijawahi kuingiwa na woga wa namna hii katika maisha yangu.Usiku huu ninakwenda makaburini kufukua kaburi dah ! Nitaendelea kukijutia kitendo cha kumuokoa Edger kwani ndicho kimenifikisha hapa.Kama nisingemuokoa Edger hivi sasa ningekuwa naendelea na maisha yangu bila matatizo lakini sasa maisha yangu yamebadilika” akaendelea kuwaza Dr Olivia Walikaribia kufika katika makaburi ya Midizini ulikozikwa mwili wa Edger Kaka.Ni makaburi yaliyoko nje kidogo ya jiji na kulijengwa uzio mkubwa kuzunguka makaburi hayo na kulikuwa na ulinzi kwa saa ishirini na nne.Toka mchana Walter alifika eneo hilo na kufanya uchunguzi namna atakavyoweza kuingia ndani ya makaburi yale na akagundua kwamba kuna mtaro mkubwa wa maji ya mvua unaotoka ndani ya makaburi yale. Walisimamisha gari na kuliacha umbali wa kilometa mbili kutoka makaburi yale wakachukua vifaa vyao na kupita porini wakimuacha mtu mmoja akilinda gari.Waliufikia ukuta uliozunguka makaburi yale. “Kuna mageti matatu katika makaburi haya na yote yana walinzi hivyo tutaingia ndani kwa kupitia mtaro wa maji ya mvua.Msiogope nimekwisha fanya uchunguzi toka mchana na ramani yote ya mahala hapa ninayo.Nifuateni mimi nitakavyosema” akasema Walter wakaanza kuambaa na ukuta akiwaongoza wenzake hadi walipofika sehemu ambako mtaro ule unatokea ndani kulikuwa na wavu kwa ajili ya kuzuia watu kupenya na kuingia ndani.Walikuwa wamekamilika kwa vifaa hivyo likafanyika zoezi dogo la kuung’oa wavu ule wakaingia ndani kisha walter akawaongoza kuelekea katika kaburi la Edger.lilikuwa ni kaburi zuri lililopambwa kwa vigae vyenye kung’aa na picha ya Edger ikionekana katika mojawapo ya kigae. “Kaburi la Edger hili hapa.Kazi ianze mara moja” akasema Walter akiwaelekeza vijana wake waanze kazi ya kuchimba pembeni ya kaburi.Kazi ilifanyika haraka haraka na ndani ya saa moja walikuwa wamekwisha chimba shimo kubwa pembeni ya kaburi kisha wakatoboa tundu katika ukuta wa kaburi.Lilitobolewa tundu kubwa ambalo mtu angeweza kupenya na kuingia ndani ya kaburi.Walter akakaingia shimoni kuhakiki kazi iliyofanyika halafu akatoka na kumfuata Olivia “Dr Olivia kazi tayari.Uko tayari kuingia ndani ya kaburi kuchukua sampuli unazozihitaji? akauliza Walter.Dr Olivia alikuwa anaogopa sana “Dr Olivia kazi tayari.Ni wakati wa kuchukua sampuli” akasema Walter lakini bado Olivia alionekana kuogopa.Walter akamshika mkono “DrOlivia kila kitu tayari ni wakati sasa wa kuchukua sampuli unazozihitaji.Usiogope nitaingia ndani ya kaburi pamoja nawe”akasema Walter na kumuinua Dr Olivia hadi katika shimo lile akatangulia kuingia ndani ya lile shimo halafu akamshika Dr Olivia akamshusha ndani ya lile shimo.Dr Olivia alikuwa anatetemeka.Walter akawasha kurunzi ndogo na kupenya katika lile tundu akaingia ndani ya kaburi. “Olivia haraka ingia ndani tumalize kazi”akasema Walter na kumshika mkono Dr Olivia akamvuta na kumuingiza ndani ya kaburi lile alikuwa anatetemeka kwa woga.Walter akalifungua sanduku lile ambalo bado lilikuwa linang’aa kama limewekwa jana.Ndani ya sanduku lile kulilala mifupa ya mwanadamu. “Dr Olivia chukua unachotaka kuchukua tuondoke” akasema Walter.Dr Olivia akaondoa woga na kuchukua sehemu za mifupa alizozihitaji akaziweka katika mfuko maalum Walter akalifunga lile sanudku kisha wakatoka na kazi ya kulifukia shimo lile walilochimba ikaanza.Ilichukua nusu saa kulifukia lile shimo kisha wakaondoka hadi mahala walikoacha gari wakaingia na kuondoka.Dr Olivia alikuwa kimya kabisa bado mwili ulikuwa unamtetemeka hakuweza kuongea lolote hadi walipofika nyumbani kwake akaingia chumbani kwake na kutoka na bahasha nzito akamkabidhi Walter akamshukuru kwa kazi ile kubwa wakaagana “Walter kumbuka hii ni siri kubwa hapaswi mtu mwingine kufahamu” Dr Olivia akamsisitiza walter Baada ya akina walter kuondoka Dr Olivia akavua mavazi yale aliyokuwa ameyavaa na kuyatupia katika mashine ya kufulia akaingia bafuni kuoga “Mwili bado unatetemeka.Eneo lile linatisha mno usiku.Ahsante Mungu ametusaidia tumetoka salama.Nimeyaona tena masalia ya Edger pamoja na ule mkufu wake aliokuwa amevaa siku alipofariki” akawaza Olivia “Ninaamini si muda mrefu ukweli utajulikana kama kweli Edger yu hai au amekufa”akaendelea kuwaza akatoka mle bafuni nakuingia chumbani kwake akakaa kitandani “Siwezi kulala humu chumbani leo peke yangu.Jumba hili ni kubwa na mambo niliyoyaona kule makaburini yanatisha.Kila nikifumba macho picha inayonijia ni ile nikiwa ndani ya kaburi.Ni vipi kama tungekamatwa tukiwa ndani ya lile kaburi? Ingekuwa ni aibu isiyokuwa na kifani.Narudia tena kujilaumu sana kufahamiana na Edger kwani amenisababisha nikafanya mambo ambayo sikuwahi hata kuota kama nitayafanya” akawaza Dr Olivia na kukitazama tena chumba chake. “I need to go out.Siwezi kulala humu ndani peke yangu leo” akawaza Dr Olivia na kuchukua simu akampigia rafiki yake Monica “Olivia mbona umerudi kimya kimya?akauliza Monica rafiki wa Dr Olivia baada ya kupokea simu “Nimerudi mchana wa leo.Uko wapi Monica? “Niko nyumbani nimepumzika.Kuna nini Olivia? “Monica nataka kutoka nikapoteze mawazo.Una nafasi tutoke wote? “I’m sorry Olivia labda siku nyingine leo Eddy amekuja niko naye na siwezi kuondoka nikamuacha peke yake”akasema Monica “Usijali Monica.Msalimu sana Eddy” akasema Dr Olivia na kukata simu “Hata kama nimekosa mtu wa kutoka naye nitatoka peke yangu.Siwezi kulala mwenyewe humu ndani leo” akawaza Dr Olivia na kufungua kabati lake akachagua mavazi ambayo yangemfaa kwa usiku ule.Alichagua suruali ya jeans ya bluu na blauzi nyekundu.Nywele zake ndefu akazifunga kwa nyuma akajitazama na kutabasamu “Nimependeza.Kinachonifu rahisha kuhusu mimi nguo yoyote ile inanipendeza” akawaza na kuchukua pochi yake akatoka akingia garini na kuondoka. “Hakkas night club ni sehemu nzuri na muafaka kwenda kupoteza mawazo usiku huu.Ni klabu bora kabisa katika jiji hili kwani wateja wake wengi ni watu wastaarabu tena ni matajiri wenye hela zao hakuna vitendo vya vurugu.Hata ukienda mwanamke peke yako hakuna atakayekusumbua” akawaza Dr Olivia akiwa garini.Bado picha ya namna walivyoingia ndani ya kaburi la Edger iliendelea kumjia kichwani “Kila nikifikiria kitendo kile mwili unanitetemeka.Sikuitegemea kama siku moja ningefikia hatua kama hii ya kufukua makaburi.” akawaza Dr Olivia Alifika Hakkas night club moja ya sehemu zenye burudani ya kipekee kabisa jijini Dar es salaam.Ni klabu yenye kuheshimika kwani hata baadhi ya viongozi wa serikali hufika hapa kupumzisha akili baada ya shughuli za kutwa nzima.Kulikuwa na sehemu maalum kwa ajili ya watu maalum matajiri na watu wenye nyadhifa mbali mbali vile vile kukawa na sehemu za kawaida ambako mtu yeyote anaruhusiwa. Dr Olivia alishuka garini akaelekea katika mlango wa klabu ambako kulikuwa na walinzi wawili waliovalia sare maalum vile vile kukawa na wahudumu watatu waliovaa suti nyeusi wakamkaribisha ndani ya klabu ile.Ni utaratibu wa klabu hii wateja wote wafikapo hukaribishwa kwa furaha na wahudumu.Dr Olivia anaifahamu klabu hii amekuwa akifika hapa mara kwa mara kupata burudani hivyo alipitiliza moja kwa moja hadi katika upande wa watu maalum au VIP.Hakukuwa na watu wengi upande huu,akaketi sofani muhudumu akafika akamuhudumia kinywani kisha akaendelea kupata burudani ya mwnamuziki aliyekuwa akipiga gitaa na kuimba.Makofi yalikuwa mengi kila pale kijana yule alipomaliza wimbo na watu waliinuka kwenda kumtunza.Kilikuwa ni kipaji kikubwa.Uso wa Dr Olivia haukukauka tabasamu. “Hello maam” sauti ya kiume ilimstua Dr Olivia ambaye mawazo yake yote yalikuwa katika tumbuizo la yule mwanamuziki.Akageza shingo na kukutana na mtu mtanasahati aliyevalia suruali ya jeans iliyopauka kidogo fulana na koti zuri. “Hallo” akasema Dr Olivia “Naweza kukaa hapa?akauliza yule jamaa ambaye alikuwa na glasi ya kinywaji mkononi.Dr Olivi akamtazama kwa macho ya kumsaili halafu akasema “Hakuna tatizo” Yule jamaa akaketi pembeni ya Dr Olivia ambaye macho yake aliyaelekeza kwa yule mwanamuziki.Baada ya wimbo kuisha akapiga makofi ya furaha “Oh my gosh ! what a talent !Amenikosha sana yule kijana” akasema Dr Olivia na kufungua pochi yake akahesabu kitita cha noti na kuinuka akaenda kumtunza halafu akarejea mahala pale “Kijana yule ana kipaji kikubwa mno” akasema Dr Olivia baada ya kurejea kutoka kutunza.Yule jamaa aliyekuwa pembeni yake hakujibu kitu macho yake alikuwa ameyaelekeza katika simu yake ya mkononi na hakuonekana kufurahishwa na burudani iliyokuwa inatolewa.Dr Olivia akageuza shingo akamtazama kwa muda kisha akasema “Unaonekana haufurahii kabisa onyesho la yule kijana” Yule jamaa akainua kichwa na kusema “Mimi si mpenzi sana wa miziki ya namna hii ndiyo maana sijaguswa” “Why are you here then?akauliza Dr Olivia akionekana kumshangaa yule jamaa “Nimekuja hapa na marafiki zangu” “Where are they?Wameondoka na kukuacha peke yako?akauliza Dr Olivia “Wapo lakini wametawanyika kwenda kutafuta wanawake” “What about you?Aren’t you going to find one?akauliza Dr Olivia “I’m not interested” akajibu yule jamaa aliyeonekana kuwa na majibu mafupi.Dr Olivia akanywa kinywaji halafu akauliza “What’s your interest? You don’t like music,women,you are not having fun what exactly do you like?akauliza Dr Olivia yule jamaa akageuza shingo akamtazama na kuuliza “Are you waiting for someone? “Hapana sitegemei mtu yeyote.Nimekuja hapa mwenyewe”akajibu Dr Olivia “Malaika kama wewe kwa nini umekuja peke yako sehemu kama hii?akauliza yule jamaa “Nikusahihishe mimi si malaika.Mimi ni mwanadamu.Malaika wako huko juu mbinguni” akajibu Dr Olivia na yule jamaa akatabasamu “Finaly you are smilling.Nini kimekufanya utabasamu? “Hiyo kauli yako kwamba wewe si malaika” “Ni kweli mimi si malaika mimi ni mwanadamu.Malaika wanaishi na Mungu huko juu mbinguni” “Wanawake kama wewe ambao muumba wa mbingu na ardhi amewatunuku uzuri wa kipekee tunawaita malaika” akasema yule jamaa na Dr Olivia akatabasamu “Arlight Mr no interest I’m not an angel.My name is Olivia.Dr Olivia” “Wow! Are you a doctor?akauliza yule jamaa “Ndiyo mimi ni daktari.Nilikuwa nafanya kazi katika hospitali ya taifa ya moyo lakini kwa sasa nimefungua kituo changu cha utafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama” “Ouh kile kituo kikubwa kilichofunguliwa hivi karibuni cha utafiti wa magonjwa wewe ndiye mmiliki wake?akauliza yule jamaa na Dr Olivia akatikisa kichwa kukubaliana naye “Hongera sana,wewe ni mwanamke wa mfano kabisa.Nimewahi kusikia sifa zako namna unavyopambana kuokoa maisha ya watu.Nakupongeza kwa kufungua kituo kile kikubwa cha kisasa kabisa cha utafiti.By the way I’m Mathew..Mathew Mulumbi” akasema yule jamaa “Nice to meet you mr Mathew Mulumbi”akasema Dr Olivia na kuinua glasi yake iliyokuwa na kinywaji akanywa kidogo na kuuliza “Mathew unajishughulisha na nini? “Mimi ni mfanyabiashara.Nina kampuni zangu kadhaa hapa nchini” akasema Mathew na kumtajia Dr Olivia kampuni zake anazozimiliki “Wow kumbe niko na bilionea hapa.Ndiyo maana mawazo yako hayakuwa hapa kwani ninyi mabilionea muda wote mawazo yenu yako kwenye pesa” akasema Dr Olivia na wote wakacheka “Baba yangu pia ni mfanya biashara nadhani umewahi kumsikia Agrey Themba” “Bilionea Agrey Themba nimewahi kumsikia japo hatufahamiani” akasema Mathew Mulumbi. “Nitafurahi kama mkikutana,mnaweza kuwa marafiki wakubwa kwani tabia zenu zinaendana” “Dr Olivia hautajali nikikuita Olivia?akauliza Mathew “Kuwa huru.Call me Olivia” akasema Dr Olivia “Olivia si kwamba kila wakati ninawaza pesa.Kuna muda ambao unahitaji kupumzisha akili na ndiyo maana zikatengenezwa sehemu kama hizi zenye burudani ambako watu huja na kupumzisha akili zao”akasema Mathew “Kama umekuja kuburudika na kupumzisha akili kwa nini hauonekani kufurahi?Unaonekana kama umelazimishwa kuja hapa.Let me tell you one thing mr Mathew Mulumbi,ukiingia ndani ya jengo hili kama umekuja kufurahina kupoteza mawazo matatizo yako yote yaache getini utakutana nayo wakati wa kutoka.Kama unadaiwa na TRA,kama umegombana na mke wako yote hayo yaache getini.Ukiingia humu dance like no body is watching you,drink,have fun” akasema Dr Olivia na kuinuka akamuomba Mathew amsubiri “Leo nimekutana na kiboko yangu.Olivia ni muongeaji hakuna mfano halafu pombe imekwisha anza kumpanda kichwani” akawaza Mathew na mara Olivia akarejea akiwa na chupa ya whisky. “Mr Mathew Mulumbi kwa kuwa umekuja hapa kuburudika naomba sasa tuanze kuburudika.Usiniambie kwamba hata mvinyo hutumii.Tafadhali naomba tunywe mvinyo huu hadi tuumalize.Usihofu klabu hii haifungwi hadi asubuhi” akasema Olivia na kumimina mvinyo katika glasi ya Mathew.Wakagonganisha glasi na kila mmoja akaipeleka kinywani “Mhh ! so strong” akasema Mathew na Dr Olivia akatoa kicheko “Usinitie aibu Mathew” akasema Olivia na kumimina tena mvinyo mwingine katika glasi “Olivia hautajali nikikuuliza swali?akauliza Mathew “Uliza usihofu mr Bilionea” akasema Dr Olivia “Kwa nini umekuja hapa peke yako?Mwenzako yuko wapi? “Mwenzangu yupi? “Namaanisha mpenzi wako yuko wapi?Tumezoea kuona wanawake wengi wakija sehemu kama hizi huwa wanaambatana na waume au wapenzi wao lakini wewe umekuja mwenyewe yuko wapi mpenzio? akauliza Mathew. “Kwa nini unataka kujua kuhusu mpenzi wangu? Dr Olivia akauliza “Ninataka kujihadhari pindi akitokea hapa kwa sababu wanaume wengine hawapenzi kuwaona wapenzi wao wakiwa sehemu kama hizi na wanaume wengine” akasema Mathew .Dr Olivia akanywa kinywaji halafu akaelekeza macho yake katika glasi ile ya kinywaji akaitazama kwa muda halafu akasema “Sina mpenzi” Mathew akamtazama Dr Olivia kwa macho yenye kuonyesha mshangao kidogo “Vipi mbona umeshangaa? Ni ajabu mimi kutokuwa na mpenzi? akauliza “Si ajabu kutokuwa na mpenzi lakini nimewashangaa wanaume kwa nini mpaka leo hii malaika kama wewe uko mwenyewe? “Mathew si kwamba wanaume hawapo lakini ni mimi mwenyewe ndiye mwenye matatizo” “Tatizo gani Olivia? “Bado sijampata mwanaume yule ambaye naweza kusema ameuteka moyo wangu” “I see” akasema Mathew na wote wakatazamana “Vipi kuhusu wewe mbona uko peke yako?Mwenzako yuko wapi?akauliza Dr Olivia “Mimi nina mke na watoto wawili” “Hongera” “Ahsante sana” “Kama tayari unayo familia unafanya nini muda huu mahala hapa? Kwa nini usiende kukaa na familia yako nyumbani? “Familia yangu haiko hapa Tanzania.Wanaishi nchini Ufaransa” “Mkeo ni mzungu? “Hapana ni mtanzania lakini amechagua kuishi Ufaransa na tayari anao uraia wa kule” “Wewe kwa nini uko hapa?Kwa nini usiungane na familia yako nchini Ufaransa?akauliza Dr Olivia “Hilo jambo limenishinda kabisa.Siwezi kuukana utaifa wangu.Mimi ni mtanzania,nimekulia hapa na nitazikwa hapa na ndiyo maana nimechagua kuishi hapa” “How do you guys manage? Wewe uko hapa mkeo yuko Ufaransa.Mnawezaje kuishi kama mke na mume au mmeachana tayari? “Hapana hatujaachana tunaonana mara kwa mara.Mahusiano ya mbali ni magumu lakini tunajitahidi sana kuendelea kulinda penzi letu na familia yetu” akasema Mathew “Wewe uko hapa klabu na mwanamke mwingine mnakunywa pombe, unaamini huko aliko mke wako naye yuko mwenyewe muda huu?akauliza Dr Olivia “Hizo ndizo changamoto tunazokutana nazo lakini inalazimu tuishi kwa imani” “Hujawahi kumsaliti mkeo ukiwa huku?akauliza Dr Olivia na Mathew akacheka “Dr Olivia una maswali magumu sana” “Ugumu uko wapi Mathew just answer me.Hujawahi kumsaliti mkeo?Kuwa mkweli usiogope.Haya ni maongezi tu hakuna atakayejua” akasema Dr Olivia “Kusema ukweli nimewahi japo ni mara chache.Unajua kama mwanadamu kuna nyakati mwili unahitaji kutimiziwa mahitaji Fulani ya muhimu na kama mtu ambaye anaweza kukutimizia mahitaji hayo kwa muda huo hayupo basi unatafuta namna mbadala ya kuweza kutimiza haja zako lakini si kwamba simpendi au simheshimu yule niliyenaye ni mazingira tu ndiyo yanayopelekea hayo kutokea” akasema Mathew “Mr Bilionea unajua sana kujitetea.Anyway siwezi kukulaumu kwani umbali kati yako na mkeo unachangia mambo haya yote kutokea” akasema Dr Olivia wakaendelea na mazungumzo huku wakipata kinywaji.Ni Mathew aliyestuka baada ya kutazama saa na kukuta ni saa kumi kasoro za alfajiri “Olivia ni muda wa kuondoka sasa.Mapambazuko yanakaribia” akasema Mathew na Dr Olivia alipotazama saa yake akakubali waondoke “Olivia huwezi kuendesha gari ukiwa katika hali hiyo umekunywa sana pombe” akasema Mathew “Usijali Mathew I can Manage” “Hapana Olivia.Let me drive you home” akasema Mathew na kumpigia simu mmoja wa madereva wa kampuni yake na kumtaka aje kuchukua gari lake pale klabuni halafu atamuelekeza sehemu ya kumfuata.Aliacha ufunguo mapokezi ili apatiwe dereva wake atakapofika.Mathew akashika usukani wa gari la Dr Olivia ambaye baada tu ya kuingia garini akaegemeza kichwa katika kiti na kulala.Mathew akamuamsha na kumtaka amuelekeze mahala anakoishi halafu akamuacha alale. “Such a beautiful lady” akawaza Mathew huku akimtazama Dr Olivia aliyekuwa amezidiwa na kinywaji “Mwanamke mzuri kama huyu,msomi na anatoka katika familia yenye uwezo mkubwa kwa nini hana mpenzi hadi sasa?Alinieleza ukweli au alikuwa ananidanganya?Kingine kinachonipa maswali kuhusu mwanamama huyu ni namna alivyokuwa anakunywa mvinyo.Ni nadra kumuona mwanamke tena msomi kama huyu anakunywa pombe kiasi hiki.Kwa sisi ambao tunafahamu kuwasoma watu kwa kumtazama tu Olivia anaonekana kama vile ana tatizo Fulani anataka kujishaulisha ndiyo maana anakunywa pombe namna ile.Wanawake kama hawa mara nyingi tatizo lao huwa ni masuala ya mapenzi.Yawezekana ameachana na mpenzi wake na ndiyo maana anakunywa pombe kiasi hiki kujisahaulisha” akawaza Mathew. Kwa maelekezo aliyopewa na Olivia walifika katika makazi yake,mlinzi alipoliona gari la Olivia hakuuliza chochote akafungua mlango Mathew akaingiza gari ndani hadi katika kibaraza cha nyumba kubwa ya Olivia akasimamisha gari kisha akashuka garini akazunguka upande aliokuwa amekaa Olivia ambaye alikuwa amelala.Mtumishi wa ndani wa Olivia aliposikia gari limesimama mbele ya nyumba akatoka haraka haraka ili kumpokea Olivia na akapatwa na mshangao kwa kukutana na Mathew akamsalimu “Naitwa Mathew ni rafiki wa Olivia.Tulikuwa klabu lakini Olivia anaonekana kuzidiwa na kinywaji hivyo nimemrejesha nyumbani”akasema Mathew na kumshusha Olivia akambeba hadi sebuleni akamlaza katika sofa akamtaka yule mtumishi aliyejitambulisha kwa jina la Lucy akaandae kikombe cha kahawa.Ndani ya muda mfupi kahawa ikaletwa na Mathew akamuamsha Olivia akamsaidia kunywa kahawa ile halafu akamtaka mtumishi yule wa ndani amuonyesjhe kilipo chumba cha Olivia.Mathew akambeba Olivia hadi chumbani kwake akamlaza kitandani halafu akampigia simu dereva wake akamuelekeza mahala alipo ili amfuate.Alimuacha Olivia chumbani kwake amelala akashuka chini kwenda kumsubiri dereva wake ambaye hakuchelewa sana akafika Mathew akaagana na Lucy akaondoka. ***************** Saa tatu za asubuhi Dr Olivia akaamka.Kichwa chake kilikuwa kinagonga kama kinapigwa na jiwe gumu. “Oh gosh ! I feel headache like hell” akawaza na kuinuka kitandani akatoka mle chumbani akaenda jikoni akanywa glasi mbili za maji halafu akamtaka mtumishi wake amuandalie supu “Jana nimekunywa pombe nyingi kupita kawaida yangu”akawaza Olivia wakati akielekea chumbani kwake kujiandaa kwa ajili ya shughuli zake za siku “Ni Mathew ndiye aliyesababisha nikanywa pombe nyingi kiasi kile.Nilifurahi sana kukutana naye” akawaza na kukumbuka usiku wa jana kule klabu akatabasamu “Mathew ni mtu mcheshi sana.Nilivyokuwa namchukulia awali ni tofauti na alivyo baada ya kumzoea.Ni mtu ambaye anafaa sana kuwa naye karibu na kwa kiasi kikubwa naweza kusema kwamba alinisaidia sana kuupitisha usiku wangu jana.Nilikuwa na mawazo na woga mwingi na sikujua ni namna gani ningeweza kuumaliza usiku wa jana lakini nilipokutana na Mathew alinisaidia nikaweza kusahau matatizo niliyokuwa nayo.Natamani kama ningeonana naye tena lakini sijui nitaonana naye wapi na sikuchukua hata namba yake ya simu” akawaza Dr Olivia “It’s not a big deal sitakiwi kuumiza kichwa sana kuhusu Mathew kwanza ni mume wa mtu ninachotakiwa kufanya ni kujielekeza katika majukumu yangu na hasa jukumu kubwa nililo nalo la kufanya utafiti wa kuhusiana na Edger kaka.Tayari ninazo sampuli na kinachofuata ni kuufahamu ukweli.Je Edger ni mzima au amekufa na kama ni mzima yuko wapi?Majibu ya swali hilo yatategemea sana matokeo ya uchunguzi nitakaoufanya” akawaza Dr Olivia na kuingia bafuni kuoga Japo alihisi maumivu makali ya kichwa lakini ilimlazimu kuelekea ofisini kwake. “I’m working with terrorists.Hili jambo linanitesa sana ni vipi kama nikigundulika? akaongeza mwendo wa gari huku mwili wake ukihisi baridi Dr Olivia alifika katika kituo chake akaelekea moja kwa moja katika ofisi yake.Katika kituo kile kulikuwa na maabara ya siri ambayo aliyekuwa na uwezo wa kuingia ni Dr Olivia peke yake.Ilikuwa chini kabisa ya jengo lile na ili kuingia katika maabara hiyo inakulazimu kupita katika ofisi ya Olivia. Alipitia mafaili kadhaa yaliyokuwa mezani kwake halafu akafungua mkoba wake na kuchukua bahasha ile yenye sampuli za mifupa waliyoitoa katika kaburi la Edger akaitazama halafu akafunga ofisi yake na kufungua mlango uliokuwa ndani ya ofisi ile akaingia katika chumba
kilichokuwa na vifaa mbali mbali.Ndani ya chumba kile kulikuwa na mlango mwingine akaingiza namba ukafunguka akaingia katika chumba ambacho kulikuwa na lifti akaingia na kuelekea chini akashuka na kuelekeza jicho lake katika mlango uliokuwa mbele yake ukafunguka akaingia ndani ya chumba kikubwa cha maabara.Kabla ya kuingia katika maabara akaingia katika kichumba kidogo akavaa mavazi maalum halafu akaanza kazi. ************** Saa moja za jioni Dr Olivia akatoka ofisini kwake akaingia garini na kuondoka.Alihisi uchovu alikuwa amefanya kazi kwa muda wa siku nzima “Mwili umechoka natamani nifike nyumbani haraka nikapumzike.Zoezi limekwenda vyema na ninatumai kesho kupata majibu.Akili yangu itatulia baada ya kupata majibu ya kipimo kile na baada ya hapo nitajua nini kitaendelea” akawaza Dr Olivia Alipofika nyumbani kwake akakuta kuna gari la kifahari limeegeshwa nje akastuka “Gari la nani hili? Sina miadi na mtu yeyote kuja kwangu leo na sipendi kukaribisha wageni nyumbani kwangu hasa usiku”akawaza “Yawezekana ni baba amekuja lakini baba hii si kawada yake.Kama angekuwa na shida na mimi angenijulisha tuonane na hana mazoea ya kuja kwangu bila taarifa” akawaza Dr Olivia akachukua mkoba na mafaili yake akashuka garini.Mtumishi wake wa ndani akatoka haraka kwa ajili ya kumpokea mizigo “Lucy hili gari la nani?Nimekwisha wapa maelekezo msipokee mgeni yeyote bila ruhusa yangu kwa nini mmekiuka maelekezo yangu? akauliza Dr Olivia akionekana kuwa mkali kidogo “Samahani dada ni yule rafiki yako aliyekurudisha jana hapa nyumbani ndiye yuko ndani” akajibu Lucy huku akipokea mizigo “Rafiki yangu gani?akauliza Dr Olivia “Yule aliyekurudisha jana usiku anaitwa Mathew” “Oh my Gosh Mathew!!akasema Dr Olivia na kushusha pumzi “Ndiyo dada.Alipokuja alizuiliwa getini akaomba niitwe nikaenda nikamueleza kwamba haupo akasema atakusubiri.Sikuwa na wasi wasi naye kwa kuwa jana ulikuwa naye nikajua ni rafiki yako.Nilitaka nikujulishe akasema nisifanye hivyo kwani anataka akufanyie surprise.Samahani sana dada sintarudia tena” akasema Lucy na Dr Olivia akatabasamu “Usijali Lucy huyu hana tatizo lakini siku nyingine usirudie kukaribisha mtu bila ruhusa yangu.Unapaswa kuniuliza kwanza kabla hujafanya maamuzi yoyote” akasema Dr Olivia na kuingia “Hello Mr Bilionea” akasema Dr Olivia alipoingia sebuleni “Hello Olivia”akasema Mathew na kusimama wakashikana mikono Dr Olivia akajitupa sofani “Pole sana Olivia.Samahani kwa kuja bila taarifa lakini jana hatukuachana vyema.Nilikuacha ukiwa umelala haujitambui kwa kinywaji na sikuwa na namba yako ya simu ndiyo maana nimekuja leo ili kujua unaendeleaje.Nisamehe sana kwa uvamizi huu” akasema Mathew “Usijali Mathew lakini wakati mwingine kufanya hivi I don’t like suprises” akasema Dr Olivia “It wont happen again” akasema Mathew “Karibu sana Mathew.Ninashukuru jana ulinifikisha nyumbani salama.Kama ningeendesha gari mwenyewe nisingefika salama” akasema Dr Olivia “Niliona hali uliyokuwa nayo ndiyo maana nikaamua kukuleta nyumbani.Olivia ninashukuru nimekuona na kuhakikisha uko salama sasa ninaweza kuondoka” “Acha kunitania Mathew.Yaani umepoteza muda wako wote kunisubiri halafu nimefika tu unaondoka? Umekuja kwangu wewe ni mgeni wangu.Tupate chakula na maongezi kisha utakwenda kwako.Unakimbilia wapi wakati mkeo hayupo ?Au una miadi na mwanamke leo?akauliza Dr Olivia “Hapana sina miadi na mtu yeyote.Ninakuona umechoka sana ninataka kukupa nafasi ya kupumzika” “Hayo ni mawazo yako mimi sijasema kama nimechoka.Wait for me ninakuja baada ya muda mfupi” akasema Dr Olivia na kupanda chumbani kwake akaingia bafuni kuoga na kisha oga akachukua kompyuta yake na kumpigia simu Habiba Jawad.Mawasiliano yao yamekuwa ni katika mtandao “Olivia” akasema Habiba Jawad baada ya kupokea simu “Madam Habiba habari za huko? “Tunaendelea vyema vipi wewe unaendeleaje? “Ninaendelea vyema pia.Madam nimekupigia kukujulisha kwamba jana nimefika salama na usiku wa jana nikaanza kazi.Nilifanikiwa kupata baadhi ya sampuli kutoka katika kaburi lile la Edger” “Wow ! kazi nzuri sana Olivia.Wepesi wako umenishangaza sana” akasema Habiba “Usijali madam” “Nini kinaendelea baada ya kuzipata sampuli hizo? Lini tutegemee majibu ya vipimo? “Tutegemee kesho madam.Maabara ile ina uwezo mkubwa sana na inaweza kutoa majibu ya vipimo vya vinasaba kwa siku moja hadi mbili hivyo tutegemee kesho kupata majibu” “Olivia sijui niseme nini.Nina furaha kubwa na vile vile nina hofu” akasema Habiba “Madam habiba sote tuna hofu kubwa kwani majibu yatakayopatikana yatatupa picha kamili kuhusu Edger kama kweli ni mzima au amefariki dunia” akasema Dr Olivia “Dr Olivia tafadhali naomba uhakikishe kipimo hicho kimefanyika kwa uhakika mkubwa sana kwani lengo hasa la kujenga kituo hicho ni kwa ajili ya kufanya uchunguzi huo kwa hiyo kesho ndipo tutajua kama uamuzi wa ujenzi wa kituo hicho ulikuwa wa manufaa” akasema Dr Olivia “Usihofu Madam Habiba.Niko makini sana na suala hili na majibu yatakayopatikana yatakuwa na uhakika.NImeshughulikia suala hili mimi mwenyewe” akasema Dr Olivia “Ahsante sana Olivia.Mimi na familia yangu tunasubiri majibu kutoka kwako kwa hamu kubwa ili tujue nini kifuate” akasema Habiba “Tuombe Mungu majibu yawe mazuri” akasema Dr Olivia “Olivia kila la heri vile vile endelea kuwa makini sana hasa kwa wakati huu.Usimuamini mtu yeyote yule.Majibu yatakapotoka kesho tutaangalia namna ya kufanya ili uwe na ulinzi.Tafadhali tuwasiliane tena kesho” akasema Habiba na kukata simu.Dr Olivia akashusha pumzi “Olivia ..Olivia..Olivia..!! akasema Dr Olivia akiwa ameweka mikono kichwani. “Olivia ninakwenda kupotea hivi hivi nikiona.Kwa nini lakini nimekubali kufanya kazi na hawa watu ?akajiuliza “I’m not with them.I’m doing this for Edger! Majibu yakipatikana mimi na wao hatutakuwa na mahusiano tena na ikiwezekana hata kituo chao nitawaachia”akawaza na kuingiwa na woga “Nikienda kinyume na matakwa yao wataniua na familia yangu.Nifanye nini?akajiuliza “I’m confused.Nashukuru Mathew amekuja atanisaidia kuyaondoa mawazo haya na kukiweka sawa kichwa changu” akasema Dr Olivia na kushuka sebuleni. “Samahani kwa kukuweka muda mrefu Mathew ”akasema Olivia “Usijali Olivia” akajibu Mathew “Mathew nakushukuru umekuja.I real needed someone to talk to.The house is big and boring,ninapotoka kazini nimechoka ninakosa mtu wa kuongea naye ndiyo maana ninaamua kwenda klabu kupoteza mawazo” akasema Dr Olivia na Mathew akatabasamu “Tupate chakula kwanza I feel hungry !! akasema Dr Olivia na kumuongoza Mathew katika chumba cha chakula. Baada ya kupata chakula wakaelekea katika chumba maalum cha kupumzikia.Kulikuwa na sofa nzuri sana na luninga kubwa ukutani.Katika ukuta mwingine kulikuwa na kioo kikubwa ambaco ndanoi yake maji yalikuwa yanamwagika na kutoa sauti nzuri huku muziki wa ala ukisikika kwa mbali.Kilikuwa ni chumba cha kipekee kabisa “Ninapotaka kupumzika huwa ninakuja humu”akasema Dr OIivia na kumkaribisha Mathew halafu akafungua kabati na kutoa chupa zaidi ya nane za whisky. “Mathew let’s have some fun.Hakuna haja ya kwenda klabu tunaweza kufurahi hata hapa nyumbani.Kwa ufupi jana nilifurahi sana kupata kampani yako.Wewe ni mtu ambaye kila mtu angependa kutoka naye.Unajua namna ya kumfanya mtu afurahi na asijihisi mpweke.Mathew mkeo ana bahati sana.U wa kipekee mno” akasema Dr Olivia “Olivia nashukuru.Kitu ulichokihisi kwangu nami ndicho nilichokihisi kwako.Nilifurahi sana kuwa nawe jana.Nilikuwa nimeboreka na nilitaka kuondoka lakini baada ya kukutana nawe nilijikuta nikitamani kuendelea kuwa nawe hadi tukajikuta tukikaribia kufika asubuhi”akasema Mathew na wote wakaangua kicheko “Let’s have fun Mathew” akasema Dr Olivia wakaanza kupata kinywaji.Uwepo wa Mathew ulimpa faraja kubwa sana Dr Olivia.Walizungumza mambo mengi na Dr Olivia alionekana kuzidiwa kwa kinywaji akainuka na kumfuata Mathew sofani. “Mathew why are you here?akauliza Dr Olivia.Mathew akatabasamu akamtazama na kusema “Nadhani nilikueleza kwamba nilikuja hapa kwa ajili kujua maendeleo yako kwani jana nilikuacha katika hali ambayo haikuwa nzuri” “Are you sure Mathew? “Olivia mbona una wasi wasi na mimi?Nimefanya vibaya kuja kukujulia hali?akauliza Mathew “Hapana Mathew hujafanya vibaya.Ninataka kujua hasa nini kimekuleta kwangu hadi ukaamua kunisubiri? Akauliza tena Olivia “Olivia tayari umezidiwa na kinywaji nadhani ni wakati wa mimi kuondoka nikuache ukapumzike” akasema Mathew “C’mon Mathew you came here to have fun so let’s have fun” akasema Olivia akimshika mkono Mathew “Usihofu leo tuko nyumbani hata kama ukizidiwa na kilevi basi utalala hapa hadi asubuhi.Mathew samahani kama swali nililokuuliza limekukera lakini ninataka niufahamu ukweli.Kama hauko tayari kunieleza ukweli ngoja mimi nikueleze ukweli” akasema Dr Olivia na kunywa funda moja la kinywaji “I saw the way you were looking at me yesterday.I see love in your eyes.You like me”akasema Dr Olivia na kumsogelea zaidi Mathew “Mathew mimi nina tatizo moja nalo ni kusema ukweli.Hata kama unakwepa kunieleza ukweli lakini ninakuona machoni,ninaitazama midomo yako you like me.You came here for me.You need me”akasema Dr Olivia “Olivia nimekuja hapa kuk……”akasema Mathew lakinbi Dr Olivia akamzuia “Tatizo la wanaume wengi hamtaki kuwa wazi hata pale mnapoelezwa ukweli.Mathew ulichokifanya si kitu kibaya kwani hata mimi nilijiuliza sana ni namna gani ningeweza kukupata tena.Ninafurahi kuwa karibu yako.Ninajihisi furaha na amani nikiwa karibu yako.Natamani niwe karibu yako muda wote.Unanifanya nifurahi,nitabasamu.Mathew naamini hautanielewa vibaya kwa hiki nitakachokueleza lakini mimi na wewe nataka tujuane zaidi nataka tuwe karibu zaidi and for tonight I’m going to …” Dr Olivia hakumalizia sentensi yake mikono yenye nguvu ya Mathew ikamvuta na kumkumbatia kwa nguvu akaanza kumporomoshea mabusu mfululizo.Dr Olivia naye akajibu kwa busu,taa ya kijani ikawaka na safari ikaanzia hapo.Chumba cha mapumziko kiligeuka sayari ya mahaba.Walihama kutoka sofa moja hadi lingine. “Mathew this is not the right place.Twende chumbani kwangu” akasema Dr Olivia wakatoka mle katika chumba cha mapumziko wakapanda ghorofani chumbani kwa Dr Olivia.Wote wawili mahaba yalikwisha wazidi hivyo walipofika tu chumbani hakukuwa na maongezi Mathew akamshika Dr Olivia na kumuangusha kitandani ukaanza mtanange wa kukata na shoka “Mathew thank you so much.I needed this.It’s been a while” akasema Dr Olivia na Mathew akatabasamu.Walimaliza mzunguko mmoja “Ahsante pia nawe.Naomba nikiri kwamba ni kweli nilikufuata hapa nyumbani na na kilichonileta hapa ni hiki.Olivia nilipokuona jana ulinisisimua sana.Nilivutiwa sana nawe na ninaomba tuwe na ukaribu mkubwa zaidi” akasema Mathew “Nilikuona toka jana nikayasoma mawazo yako na nilipokuona hapa leo sikushangaa nilijua kilichokuleta na mimi nilikuwa nakihitaji sana.Mathew naomba tafadhali usinifikirie vibaya kwa sababu imekuwa rahisi mno kwangu kujiachia kwako na sijui imenitokeaje.Mimi ni mwanamke mgumu sana na ndiyo maana mpaka leo hii sijabahatika kuwa na rafiki wa kiume lakini wewe tumekutana jana tu na leo hii nipo juu ya kifua chako.Imenitokea hivyo na nisingejitendea haki kama ningekuacha ukaondoka.Ningejilaumu sana Mathew” akasema Dr Olivia.Mathew akaupeleka mkono katika nywele laini za Dr Olivia akazichezea na kusema “Olivia katu siwezi nikakuchukulia rahisi rahisi.Nitakuheshimu sana na urafiki wetu nitaupa thamani kubwa,na ningependa urafiki wetu uendelee zaidi na zaidi japokuwa nina familia lakini haiwezi kuwa kigezo cha kukuumiza wewe” “Mathew ninakuhitaji sana hasa kwa wakati huu.Naomba usimame na mimi.Ninahitaji mno mtu wa kunishika mkono naomba uwe karibu nami japo kwa muda huu ambao utakuwepo hapa Dar es salaam.Nimejikuta nikipata nguvu mpya na tumaini toka jana nilipokutana nawe.Sifahamu kwa nini ninajishi namna hii yawezekana Mathew kuna kizizi unakitumia” akasema Dr Olivia na wote wakaangua kicheko. “Natania Mathew siamini kabisa katika mambo hayo japokuwa wapo wanaoamini”akasema Dr Olivia “Dr Olivia nadhani ni wakati wangu wa kuondoka nikuache upumzike” “Hapana Mathew leo utalala hapa hapa utaondoka asubuhi.You are single and I’m single shida iko wapi?Kuwa na amani hapa ni sehemu salama kabisa.Nakuhitaji usiku wa leo Mathew.Please stay” akasema Dr Olivia.Mathew akamtazama machoni na kusema “Uko sahihi Olivia.Sina sababu ya kukimbia kwani niko peke yangu.Tuufanye usiku wetu uwe wa kipekee” akasema Mathew “Thank you Mathew.Thank you so much.We need champagne to celebrate our new beginning ” akasema Dr Olivia na kuvaa nguo akatoka mle chumbani akaenda kuchukua vinywaji. **************** Saa kumi na mbili za asubuhi Mathew aliamka akaoga na kuagana na Dr Olivia akaondoka zake. “Ninaapa sijawahi kuwa na usiku mzuri kama jana.Mathew ni mwanaume wa pekee kabisa.Sifahamu imenitokeaje lakini kwake nimejikuta nikiwa mrahisi mno lakini sijakosea kwani ananisaidia sana kupita katika kipindi hiki kigumu ninachopitia.Nikiwa naye ninakuwa na amani sana na tabasamu usoni lakini nikiwa peke yangu ninajiona kama vile ninaelekea kwenye kitanzi cha kuninyonga” akawaza Dr Olivia baada ya Mathew kuondoka “Ngoja nimuweke kando Mathew nijielekeze katika jukumu kubwa nililo nalo.Siku ya leo ni siku ya kipekee kabisa kwani ukweli unakwenda kujulikana kama Edger kaka alikufa katika ile ajali au bado mzima.I’m so scared” akawaza Dr Olivia akakaa kitandani akionekana kuwa na mawazo mengi.Akainuka na kuendelea kujiandaa. Alifika ofisini kwake saa nne za asubuhi na kabla ya kufanya shughuli yoyote alijiegemeza kitini “Ninaogopa kuufahamu ukweli.Nina wasi wasi maisha yangu yanaweza yakabadilika kuanzia siku ya leo.Hii ni siku ngumu sana kwangu” akawaza Dr Olivia Alikaa kitini kwa zaidi ya dakika kumi akiwaza halafu akainuka “Sipaswi kuogopa.Natakiwa kuufahamu ukweli” akasema Dr Olivia na kuvaa koti lake jeupe akaelekea katika maabara maalum Ilipofika saa kumi na moja jioni Dr Olivia tayari alikuwa na majibu.Mwili ulimtetemeka baada ya majibu kuonyesha kwamba mwili ule haukuwa wa Edger.Machozi yakamtoka “He’s alive..!He’s not dead ! akasema Dr Olivia.Alikuwa peke yake ndani ya maabara ile kubwa. “Haya mambo nimekuwa nikiyaona katika filamu na sikujua kama siku moja nitayashuhudia kwa maco yangu.Kila mtu anajua kwamba Edger amekufa.Oh my God where is he?akajiuliza Ni wazi Dr Olivia alikuwa katika wakati mgumu sana baada ya kupata majibu yale. “Habiba alikuwa sahihi kuamini Edger hajafa.Naniwaliofanya mchezo ule na kwa nini?Naamini waliofanya mchezo ule ni watu wataalamu mno kwani walifanikiwa kumuaminisha kila mtu kwamba Edger amefariki.Kama Habiba asingeingiwa na shaka ukweli usingeweza kujulikana lakini sasa ukweli umejulikana Edger hajafa na kinachofuata ni kutafuta mahala alipo” Akawaza Dr Olivia akatoka mle maabara akarejea ofisinikwake na kumpigia simu Habiba Jawad kupitia kompyuta yake “Dr Olivia naamini simu hii ina habari njema” akasema Habiba “Madam Habiba tayari ninayo majibu hapa” akasema Dr Olivia na Habiba Jawad akavuta pumzi ndefu “Nimesubiri kwa muda mrefu kuufahamu ukweli lakini sasa majibu yamepatikana ninapata hofu kuyapokea” akasema Habiba “Usiogope Madam Habiba.Kuwa jasiri na uyapokee majibu” akasema Dr Olivia “Haya nipe majibu Olivia” akasema Habiba na kufumba macho. “Madam niliingia mimi mwenyewe katika kaburi lile la Edger na kuchukua sampuli za mabaki nilizozihitaji na nimefanya kipimo mimi mwenyewe kwa usahihi mkubwa na majibu yaliyotoka ni …..” akasita kidogo “Nieleze Olivia unazidi kuniweka roho juu”akasema habiba “Majibu yanaonyesha kwamba mwili uliozikwa katika lile kaburi si mwili wa Edger ” akasema Dr Olivia na Habiba akafunika uso kwa viganja vyake vya mikono.Akakaa kimya kwa dakika mbili na alipotoa viganja vile uso wake ulikuwa umeloa machozi. “Ahsante Mungu.Nimesubiri kwa muda mrefu sana kuupata ukweli huu.Imenigharimu muda na fedha nyingi kuufahamu ukwelikwamba mwanangu Seif hajafa bali yuko hai.Olivia sijui nikushukuruje kwa jambo hili kubwa ulilolifanya” akasema Habiba akiendelea kumwaga machozi ya furaha. “Madam Habiba baada ya kuufahamu ukweli kwamba Edger hajafa nini kinafuata?akauliza Dr Olivia “Kinachofuata baada ya kuufahamu ukweli huu ni kuanza kumtafuta kila kona ya dunia kwani mpaka sasa bado hatujui mahala alipo na nani anamshikilia.Olivia ninakushukuru mno na ninaomba nikuache ili nikutane na watuwangu nizifikishe taarifa hizi njema kabisa.Nitawasiliana nawe baadae” akasema Habiba na kumuaga Olivia “Mimi mwenyewe sitaki kuendelea kukaa hapa kichwa changu kimevurugika kabisa.Majibuhaya yaliyopatikana yamezidi kunichanganya na kuniongezea hofu.Nani waliofanya jambo lile la kuidanganya dunia kwamba Edger amefariki dunia?Edger yuko wapi?Watu hao walifahamu kwamba Edger ni mshirika wa IS ndiyo maana wakamteka na kutunga kifo chake? Nitaendelea kujuta kumfahamu Edger kwa ajili yake nimejikuta nikiingia katika ulimwengu wa magaidi ambao wamenibana katika kona na sijui nifanye nini,sijui nimweleze nani jambo hili ambalo linaelekea kunipa uchizi.Ninayaona maisha yangu yakielekea shimoni kwani naamini ikosiku nitajulikana kuwa ninashirikiana na magaidi.Kila ninapowaza jambo hili ninazidi kuchanganyikiwa” akawaza Dr Olivia. “Ninamshukuru Mungu ameniona na kuniletea Mathew.Ni wakati kama huu ninamuhitaji sana mtu kama yule ambaye hunipa nguvu ya kusimama.Ninahisi amani,furaha na nguvu nikiwa naye” akawaza Dr Olivia na mara gari ziliposimama katika taa za barabarani akachukua simu akazitafuta namba za Mathew akampigia “Dr Olivia” akasema Mathew “Mathew uko wapi mida hii?akauliza “Nimetoka kazini muda si mrefu ninaelekea nyumbani.Wewe uko wapi?akauliza Mathew “Mathew kama hutajali tunaweza kukutana nyumbani kwangu?akauliza Dr Olivia “Kuna tatizo lolote Dr Olivia?akauliza Mathew baada ya kugundua utofauti katika sauti ya Dr Olivia “Ninakuhitaji Mathew” “Usijali Olivia,ninakwenda nyumbani kwangu kisha nitakuja kwako,nisubiri hapo tafadhali”akasema Mathew “Ahsante sana Mathew” akasema Dr Olivia na kukata simu “I real need someone like Mathew today.Nahitajimtu wa kunipa nguvu kwa sababu mambo yanayonikabili ni mazito” akawaza Dr Olivia Alifika nyumbani kwake na kujilaza kitandani kichwa kilikuwa kizito “Nimeingia kwenye ulimwengu wa magaidi na sijui namna ya kutoka.Nimeikamilisha kazi yao na sitaki kuendelea kushirikiana nao tena hawa jamaa lazima nitafute namna ya kuwakwepa.Hata hivyo duniahii ina maajabu sana.Mwili ule ambao watu wote tuliamini ulikuwa wa Edger ni wa nani? Haya aya mambo ni magumu sana na sitakikuendelea kuumiza kichwa changu zaidi” akawaza Dr Olivia na kuingia bafuni kuoga kisha akajilaza kitandani akimsubiri Mathew. Saa moja na nusu Mathew akafika nyumbani kwa Dr Olivia ambaye alifurahi sana kumuona akamkumbatia kwa nguvu “Mathew nimefurahi sana umekuja.Kila nikuonapo ninapata nguvu” akasema Dr Olivia na kumuongoza Mathew wakaenda kukaa nje sehemu maalum ya kupumzikia,Olivia akaleta chupa kadhaa za mvinyo “Olivia toka tumefahamiana juzi umekuwa unatumia sana kinywaji.Inaonekana kuna jambo linakusumbua na unataka kuliondoa kichwani kwako kwa kutumia kilevi.Unaweza ukanieleza una tatizo gani Olivia?You can trust me,Im here for you” akasema Mathew “Sina tatizo lolote Mathew nahitaji tu kufurahi.Ninaonekana kama nina tatizo linanisumbua?akauliza Dr Olivia “Ninajua kumsoma mtu hasa ambaye ana jambo linamsumbua na japokuwa hutaki kuniweka wazi lakini naamini kwamba unalotatizo.Nataka nikuelekeze kitu Dr Olivia,siku zote kama una tatizo usilitatue kwa kunywa pombe.Njia hiyo kamwe haitakusaidia kutatua tatizo lako.Sikulazimishi unieleze tatizo lako kwanini muda mfupi tu umepita toka tumefahamiana lakini kama hutajali unaweza ukaniamini na kunieleza kinachokusumbua” akasema Mathew. “Mathew hayoni mawazo yako,sina tatizo lolote linalonisumbua” akasema Dr Olivia huku akichukua chupa ya mvinyo na kutaka kuimimina katika glasi Mathew akamzuia “Olivia hakuna kutumia mvinyo leo.Today let’s have fun without alcohol.Kamauna tatizo tulitatue bila kutumia kilevi chochote” akasema Mathew “Mathew sina tatizo lolote linanisumbua.Tutumie mvinyo tafadhali”akasema Dr Olivia “Hapana Olivia.Leo hakuna kutumia mvinyo.Si mazoea mazuri kutumia mvinyo kila siku.Tuzungumze na kama kunakitu ambacho kinatufanya tufurahi basi tufanye lakini si kugeuza mvinyo sehemu ya maisha yetu” “C’mon Mathew siwezi kuwa kawaida kama sintatumia hata mvinyo kidogo” akasema Dr Olivia “Hap…………” Mathew akanyamaza baada ya simu ya Dr Olivia kuita.Akatazama mpigaji na sura yake ikabadilika. “Is there any problem Olivia?akauliza Mathew “Mathew I have to take this call” akasema Dr Oliviana kuelekea ndani. “Hallow madam Habiba” akasema Dr Olivia baada ya kuipokea simu ile ambayo ilipigwa kupitia mtandao wa skype. “Dr Olivia nimefikisha majibu yale kwa wenzangu na wote wamefurahi sana kwamba zile hisia zetu kuhusu Edger kuwa hai ni sahihi kabisa.Kinachofuata sasa ni hatua ya tatu ambayo ni kumtafuta Edger yuko wapi.Katika hatua hii ya tatu utakuwa ukiwasiliana na Sayid Omar yeye ndiye niliyemkabidhi jukumu lote la kuhakikisha Edger anajulikana yuko wapi na anapatikana kwa gharama zozote zile.Olivia ninakushukuru sanakwa jambo kubwa ulilolifanya la kuamua kushirikiana nasi naomba uendelee kuwa nasi na ninakuahidi kwamba lazima Edger atapatikana kwa gharama zozote.Ninachokusisitiza Olivia ni usiri.Endelea kuitunza siri uliyoifahamu hata kama itakulazimu kuhatarisha maisha yako lakini siri uliyoifahamu katu usifumbue mdomo na kumweleza mtu yeyote” akasema Habiba “Madam Habiba tumekwisha wekamakubaliano na ninaomba makubaliano yetu muyazingatie na mara tu baada ya Edger kupatikana utakuwa ni mwisho wetu mtaniacha niendelee na maisha yangu” “Usiogope tutalizingata hilo Olivia.Mimi ni mtu ninayeheshimu sana makubaliano.Naomba sasa uzungumze na Sayid Omar na atakupa maelekezo” akasema Habiba Jawad na katika simu akatokea mtu mmoja mwenye kipara na miwani “Hallow Olivia.Naitwa sayid Omar na kama alivyokuelekeza Habiba katika awamuhii ya tatu utakuwa na mimi.Katika awamu ya kwanza ulikuwa na Abu dahir,awamu ya pili ukawa na Habiba na sasa ni awamu ya tatu ambayo utakuwa na mimi.Awamu hii imegawanyika katika sehemu mbili.Sehemu ya kwanza ni kufahamu nani waliomchukua Edger na yuko wapi.Sehemu ya pili itakua ni kumchukua mahala alipo.Mpaka sasa hatuna uhakika ni nani waliofanya mchezo ule na kumchukua Edger.Nipe muda hadi kesho asubuhi kwa saa za kwenu Tanzania nitakupigia simu na kukueleza ni wapi tunahisi yupo Edger” akasema Sayid Omar na kuagana na Dr Olivia ambaye alihisi miguu inamuisha nguvu akakaa kitandani “Ee Mungu kwa nini umeniacha nikaingia katika mtihani huu? Nimeingia katika himaya ya magaidi,himaya ya watu makatili,wauaji na sioni mlango wa kutokea.Nionyeshe njia ee Mungu niweze kujitoa katika mikono ya watu hawa” akaomba Dr Olivia akilengwa na machozi “Kama watafanikiwa kumpata Edger utakuwa ni mwisho wa mahusiano yangu naye.Sitaki kuwa na ukaribu wowote na hawa magaidi” akawaza Dr Olivia na kukumbuka kwamba alimuacha Mathew peke yake akatoka na kurejea mahala alipokuwa Mathew “Mathew tafadhali naomba uniruhusu ninywe glasi hata moja tu ya mvinyo ili kichwa changu kikae sawa.Bila kupata mvinyo nahisi kichwa changu kitapasuka” akasema Dr Olivia.Mathew akamtazama na kuchukua chupa akamimina mvinyo katika glasi.Olivia akaishika glasi ile na kunywa pombe yote iliyokuwemo. “Oh my God !! akasema Dr Olivia “Olivia nieleze tatizo lako tafadhali.You can trust me” akasema Mathew.Dr Olivia akainamisha kichwa akazama mawazoni “Olivia mimi ni rafiki yako na kama tumeamua kuwa marafiki hakuna haja ya kufichana kama una jambo kubwa nieleze tafadhali yawezekana nikawa na msaada kwa tatizo lako” akasema Mathew. “Hata kama nikikueleza Mathew hautaweza kunielewa”akasema Dr Olivia “Usiogope Olivia nieleze nitakuelewa” akasema Mathew “Nina tatizo kubwa sana Mathew na ninahitaji msaada wa Mungu pekee kulitatua” akasema Dr Olivia “Olivia pole sana kwa tatizo ulilonalo lakini bado naendelea kukusisitiza unieleze tatizo lako kwani yawezekana Mungu amenituma kwako ili niwe msaada wa tatizo ulilo nalo.Usiogope Olivia hata kama tatizo ni kubwa kiasi gani nieleze na mimi nitakuelewa” akasema Mathew.Dr Olivia akafikiri kidogo na kusema “Hapana Mathew siwezi kukueleza.Tatizo nililo nalo nitalikabili mimi mwenyewe na kulimaliza”akasema Dr Olivia “Olivia kuna maana gani ya kuwa marafiki kama hatuwezi kushirikishana matatizo tunayopitia?Urafiki maana yake ni kushirikishana kila tatizo na kusaidiana.Kama rafiki yako niko tayari kukusaidia katika matatizo yote uliyonayo” akasema Mathew “Mathew sitaki kukuingiza katika matatizo.Nitakabiliana nao mimi mwenyewe” akasema Dr Olivia “Utakabiliana na akina nani? Are you in trouble with some people? akauliza Mathew “Mathew umenichanganya hadi nimejikuta nikitamka kitu ambacho sikupaswa kukitamka”akasema Dr Olivia “Niambie ukweli Olivia uko katika matatizo na watu gani? Dr Olivia akainamisha kichwa akafikiri halafu akasema “Mathew sipendi kukushirikisha katika tatizo langu lakini kwa kuwa umesisitiza nitakueleza kwa ufupi tu.Ni kweli nina tatizo na watu Fulani” “Matatizo gani? Ni akina nani?Mathew akauliza “Usihofu Mathew ni jambo ambalo ninaweza kulimaliza na ninajitahidi kulimaliza.Endapo nikishindwa kulitatua na kuhitaji msaada nitakujulisha.Naomba nisiingie kwa ndani zaidi” akasema Dr Olivia “Nimekuelewa Dr Olivia na ninakuomba kama ulivyoahidi kwamba endapo utashindwa kutatua tatizo lako mimi niko hapa tayari kukusaidia” “Ahsante Mathew.Nikishindwa nitakutafuta” akasema Dr Olivia “Olivia umeahdi kunitafuta pale utakapohitaji msaada wangu lakini mimi ninapenda kukupa msaada mdogo sana” “Msaada upi Mathew? “Nitakupa namba ambazo unatakiwa uziweke kichwani na utazitumia pale tu unapokuwa matatizoni.Ukipiga namba hizo zitaniwezesha mimi kujua pale unapokuwa na matatizo.Narudia tena kukupa angalizo kwamba namba hizi si za kutumia hovyo hadi pale utakapokuwa umepata matatizo.Namba hizo ni kirusi ambacho kinaweza kuchota taarifa kwa haraka na kunijulisha mahala ulipo na mimi nikatafuta msaada namna ya kukusaoid” akasema Mathew “Umewahi kusomea mambo haya ya teknolojia?Kirusi hicho kinakusaidia nini Mathew?akauliza Dr Olivia “Nina utaalamu kidogo wa haya masuala.Kirusi hiki kinanisaidia kwa familia yangu kujua kama wako katika hatari.Kuna wakati mwanangu mmoja aliwahi kutekwa ndipo nilipoamua kutumia njia hii kujua kama wako kwenye matatizo”akasema Mathew na kumtajia Dr Olivia namba zile akazihifadhi kisha wakaendelea na maongezi mengine.walipata chakula cha usiku na ilipofika saa tano Mathew akaaga ili aondoke lakini Dr Olivia akawa na ombi “Mathew naomba usinichoke tafadhali.Ninaomba na usiku wa leo uupitishe hapa kwangu.Ninakuhitaji sana Mathew” akasema Dr Olivia.Haikuwa rahisi kwa Mathew kukataa.
Dr Olivia Themba aliyaelekza macho yake katika saa kubwa ya ukutani akiangalia namna mishale inavyopishana.Ilikaribia saa mbili za asubuhi muda ambao Sayid Omar aliahidi kumpigia simu kumpa taarifa zakuhusiana na mahala alipo Edger kaka na mipango ya kumchomoa kutoka mahala anaposhikiliwa. “Nilitamani sana kujua ukweli kuhusu Edger Kaka lakini sasa baada ya kuufahamu ukweli nimeingiwa na hofu kub..” Olivia akatolewa mawazoni baada ya simu kuita katika kompyuta yake.Mpigaji alikuwa ni Sayid Omar.Akashusha pumzi na kuipokea “Hallo Sayid” “Habari za asubuhi Dr Olivia” “Habari nzuri kabisa Sayid” akajibu Dr Olivia “Dr Olivia nimekupigia kama nilivyokuahidi.Tumejitahidi sana kuchunguza lakini mpaka sasa bado hatujui Edger yuko wapi na nani anamshikilia,lakini uchunguzi wetu kuna viashiria kwamba yawezekana Edger akawepo nchini Tanzania.Tunahisi hivyo kutokana na mpango ule wa kumteka namna ulivyoratibiwa.Isingewezekana kufanyika jambo kama lile bila serikali kuwa na taarifa.Ukilitazama tukio lile kwa undani zaidi utaona kwamba lazima serikali ya Tanzania wana mkono wake.Tunahisi kwamba Mossad waliwapa taarifa serikali ya Tanzania na wakaratibu mpango ule kwa pamoja hivyo sehemu ya kuanza kumtafuta Edger na kufahamu mahala alipo ni Tanzania” akasema “Sayid mna uhakika kwamba Edger yuko hapa Tanzania?akauliza Dr Olivia “Hatuna uhakika mkubwa lakini tunahisi hivyo.Tukio lile la kutengeneza kifo chake lilitengenezwa kitaalamu sana na tunaamini lazima serikali ya Tanzania ilishirikiana na Israel hivyo Tanzania ni sehemu nzuri kuanzia uchunguzi wa kujua mahala Edger alipo.Kuna uwezekano mkubwa akawepo hapo hapo nchini amefungwa mahala Fulani akihojiwa.Zoezi letu litaanzia nchini Tanzania” akasema Sayid “Sayid,Tanzania ni kubwa.Mmejipanga kuanzia wapi uchunguzi huo?akauliza Dr Olivia “Ili kufanikisha operesheni kubwa kama ile lazima mkuu wa nchi awe anafahamu kila kitu na atoe idhini ya kufanya kwake” “Una maanisha rais? akauliza Dr Olivia “Ndiyo_Operesheni kubwa kama ile haiwezi kufanyika bila ya rais kufahamu.Nina uhakika mkubwa kwamba rais anafahamu kuhusu jambo hili na anafahamu alipo Edger hivyo basi uchunguzi wetu utaanzia kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania”akanyamaza kwa muda halafu akaendelea “Olivia tumegundua kwamba rais ana mtoto wake anayesoma katika shule moja ya kimataifa hapo Dar es salaam.Tunataka kumtumia huyo ili kumlazimisha rais atueleze kile kitu kuhusu Edger” akasema Sayid na kumstua Olivia “Mnataka kumtumia mtoto wa rais? “Ndiyo tunataka kumtumia mtoto wa rais ili kumfanya baba yake atusikilize na aturejeshee au http://deusdeditmahunda.blogspot.com/kutueleza mahala alipo Edger”akajibu Sayid “Sayid kabla ya kufanya lolote nashauri muwe kwanza na uhakika mkubwa kwamba serikali ya Tanzania inafahamu kuhusu suala hilo la Edger.Mkifanya mambo bila uchunguzi mtajikuta mkiumiza watu wengine ambao hawana kosa lolote kama huyo mtoto wa rais”akasema Dr Olivia “Usiogope Dr Olivia,tayari tunao uhakika mkubwa kwamba serikali ya Tanzania wanahusika katika suala hili na lazima rais anafahamu mahala alipo Edger na yeye ndiye atakayetupa mwangaza wote wa mahala alipo” akasema Sayid na Dr Olivia akashusha pumzi “Mpango tulioupanga umekaa namna hii.Kupitia kituo chako cha utafiti utatengeneza kirusi ambacho tutakitumia katika mpango huu.Tunataka kirusi hicho kiwe cha aina yake na ambacho kinaweza kumuathiri binadamu na kumuua.Kirusi hicho kiwe na uwezo wa kuua kwa kuanzia siku saba na isizidi siku kumi na mbili.Baada ya kutengeneza kirusi hicho utatengeneza pia kinga yake.Tutamchoma mtoto wa rais sindano yenye kirusi hicho na atakapoanza kuumwa tutamjulisha rais kwamba mwanae amechomwa sindano yenye kirusi hatari na hapo tutamtaka amuachie huru Edger ili tuweze kuokoa uhai wa mwanae.Unauonaje mpango huo?akauliza Sayid.Dr Olivia akabaki kimya akimtazama Sayid kupitia kompyuta yake “Dr Olivia” akaita Sayid baada ya kuona Dr Olivia akiwa kimya sana “Sayid naomba ufahamu jambo jambo moja” “Jambo gani Olivia? “Nilipokutana na Habiba Jawad mama yake Edger na alinieleza mambo mazito kwamba ninyi ni washirika wa IS na hata Edger naye ni mshirika wa mtandao huo.Niliogopa mno na sikutaka kuendelea kushirikiana naye lakini aliniomba sana nimsaidie aweze kumpata mwanae.Nilikubali kumsaidia kwa sharti kwamba baada ya Edger kupatikana sintaendelea kushirikiana nanyi tena na kwamba Edger akipatikana aondoke nchini Tanzania na wala asijihusishe tena na masuala yoyote ya kisiasa.Nimefanya kila lililowezekana na ukweli umebainika kwamba Edger yuko hai kaziyangu imeishia hapo.Jambo unaloniambia nilifanye kwamba nitengeneze kirusi ambacho mtakitumia katika mpango wa kumtafuta Edger limenishanganza na siwezi kufanya kitu kama hicho.Nimekwisha wasaidia mmempata uhakika kwamba Edger yuko hai imetosha”akasema Dr Olivia “Olivia sina sababu ya kuzungumza maneno mengi lakini kwa ufupi tu ni kwamba wewe ni mwenzetu.Toka ulipokubali kushirikiana na Abu dahir tayari ulikubali kuwa mwenzetu” akasema Sayid na Dr Olivia akamkatisha haraka “Mimi si mwenzenu.Mimi si IS.Mimi si gaidi !! Akasema Dr Olivia kwa ukali “Dr Olivia sahihi yako ipo katika vitabu vyetu hivyo tunakuhesabu ni mwenzetu na huo ni ukweli ambao hauwezi kuuepuka.Utaendelea kupokea maagizo na maelekezo kutoka kwetu.Wewe ni mtu muhimu kwetu na hatutakusumbua hadi pale tutakapokuwa na uhitaji na msaada wako na kwa sasa tunahitaji sana msaada wako ili tuweze kumpata Edger hivyo andaa mipango ya kutengeneza kirusi hicho kama nilivyokuelekeza.Atakuja mtaalamu mwingine wa masuala hayo ya utengenezaji wa virusi utashirikiana naye.Umenielewa Dr OIivia?akauliza Sayid Omar “Sayid nataka kwanza tuweke sawa jambo hili.Mimi si mmoja wenu.Mimi si IS.Mlinishirikisha katika shughuli zenu bila mimi kujua hivyo msinihesabu kama mwenzenu.Kama daktari ninayetambua wajibu wangu nilijitolea kuokoa maisha ya Edger hivyo sitaki jambo jema nililolifanya ligeuke shubiri kwangu.Msinifanye nijutie kitendo nilichokifanya cha kuokoa uhai wa Edger” akasema Dr Olivia na machozi yakimtoka “Dr Olivia samahani sana kwa maneno niliyoyatamka.Siku zote tunakupa heshima kubwa na ya kipekee kabisa kwani bila wewe hivi sasa Edger angekwisha fariki.Pamoja na yote uliyoyafanya lakini bado Edger yuko katika hatari maisha yake bado yako hatarini hivyo kile ulichokifanya cha kuokoa maisha yake bado kinaendelea na tunahitaji sana msaada wako.Lakini Olivia hayo yote hayaondoi ukweli kwamba umekwisha zifahamu siri zetu na umekula kiapo cha kutokufungua mdomo kusema chochote kuhusiana na yale uliyoyagundua hivyo wewe tayari ni mwenzetu lakini kama nilivyokueleza tutakutumia pale tu ambapo tutakuwa na uhitaji na msaada wako na kama hatuhitaji msaada wako hatutakuwa na shida nawe utaendelea na maisha yako kama kawaida.Kuwa mmoja wetu ni fursa ambayo itakuwezesha Dr Olivia kuingia katika ulimwengu wa watu wazito wenye nguvu na mabilionea.Kuna fursa nyingi zinakuja kupitia sisi.Olivia utakuwa mwanamke mwenye nguvu,tajiri,na hakuna ajuaye kwani siku moja unaweza ukashika nafasi ya juu ya uongozi.Hupendi siku moja kuwa rais wa kwanza mwanamke?Hupendi siku moja uongoze watu zaidi ya milioni hamsini?Hutaki jina lako kuingia katika vitabu vya historia ya nchi na dunia? Akauliza Sayid na Dr Olivia akabaki kimya “Kimya hicho kinanifanya niamini kwamba uko tayari.Olivia tuna mipango mikubwa sana juu yako.Endelea kuwa mtulivu na ufuate maelekezo yetu tutakayokueleza na utafika mbali sana.Ninakuhakikishia kwamba hautajutia kushirikiana nasi” akasema Sayid “Sayid suala hili linakuwa gumu kwangu kwa sababu rais ambaye tunataka kumtumia mtoto wake kumshinikiza atueleze mahala alipo Edger,ni rafiki mkubwa wa baba yangu na mimi ninamuita baba.Mtoto wake Coletha ninafahamiana naye ananiita dada.Sisi ni zaidi ya marafiki bali tunaishi kama ndugu hivyo sitaki kuwa sehemu ya kuitesa familia hii ya rais” akasema Dr Olivia “Dr Olivia sisi tunapokuwa katika kutimiza malengo hatuangalii kuhusu ndugu zetu.Kama italazimu kuwaumiza ndugu zetu ili kufanikisha shughuli yoyote muhimu tunafanya hivyo bila kusita hivyo basi suala la wewe kuwa na ukaribu na familia ya rais halina nafasi kwetu.Mpango wetu lazima utekelezwe.Kuna wakati ambao lazima tufanye maamuzi magumu” akasema Sayid “Sayid hapana siwezi kufanya jambo kama hilo.Siwezi kuiumiza familia ya rais ambayo ni sawa na familia yangu.Coletha ni mdogo wangu na siwezi kutengeneza kitu ambacho kitahatarisha uhai wake.Nashauri mtafute namna nyingine ya kufanya kumtafuta Edger na si kuitumia familia ya rais kwani mkiumiza familia hii mtakuwa mnaniumiza mimi pia.Nawasihi mkae tena mfikirie kwa undani namna nyingine ya kufanya” akasema Dr Olivia “Olivia nilikueleza muda mfupi uliopia kwamba wewe ni mtu muhimu sana kwetu na tuna mipango mikubwa juu yako lakini unanishangaza kwa namna unavyofanya jambo hili liwe gumu.Unanifanya nitamke kitu ambacho sikuwa nimetaka kukisema.Nafsi yangu inaniuma kusema hivi lakini Dr Olivia imefika wakati ambao itakulazimu kuchagua aidha familia yako au familia ya rais” akasema Sayid na kumstua Dr Olivia “Una maanisha nini Sayid?akauliza Dr Olivia “Namaanisha kwamba itakulazimu kuchagua familia moja aidha familia yako au familia ya rais kwani kama hautakuwa tayari kutekeleza mpango huu hatutakuwa na njia nyingine zaidi ya kuishikilia familia yako hadi pale utakapokuwa tayari kufanya kile ulichoelekezwa” akasema Sayid na Dr Olivia akastuka sana “Sayid ninakuomba sana familia yangu isihusishwe kwa namna yoyote na mambo yangu.Hawafahamu chochote kuhusiana na yale ninayoyafanya hivyo naomba msiwahusishe kwa namna yoyote ile” akasema Dr Olivia “Olivia familia yako itaendelea kuwa salama endapo utakuwa mvumilivu na kutekeleza yale tutakayokuelekeza kuyafanya hivyo nakuomba sana yapokee maelekezo yangu na ukubali kuyafanyia kazi lakini kama utakwenda kinyume nasi lazima tukuadhibu kwa kuishikilia familia yako na ninakuhakikishia endapo tukifanya hivyo itakuwa vigumu sana kuwaona tena.Sikutaka kuyasema hayo Dr Olivia na sitaki tufikie huko kwani sisi ni washirika na tuna mipango mingi mizuri kwako ambayo itategemea sana ushirikiano wako kwetu hivyo Dr Olivia ninakuomba sana tusaidie katika hili.Tumuokoe Edger na tuendelee na mipango mizuri tuliyonayo.Huyo binti wa rais ambaye unamuhofia hatutaki kumuua bali tunataka kumtumia kwa ajili ya kumshinikiza rais atueleze mahala aliko Edger” akasema Sayid.Dr Olivia alichanganyikiwa. “Dr Olivia” akaita Sayid.Dr Olivia akafuta machozi na kusema “Sayid tafadhali naomba msiiguse familia yangu nitafanya hicho mnachotaka nikifanye” akasema Dr Olivia “Safi sana Olivia.Ahsante kwa maamuzi hayo mazuri ninakuhakikishia kwamba hautajutia maamuzi hayo.Ninataka sasa uanze kufanya maandalizi ya kutengeneza kirusi hicho na nitamtuma mtaalamu mwingine aje akusaidie katika hilo zoezi “Hapana sihitaji mtu yeyote wa kunisaidia.Nitaifanya kazi hiyo mimi mwenyewe” akasema Dr Olivia “Una hakika hutaki mtu wa kukusaidia Dr Olivia?akauliza sayid “Sihitaji mtu wa kusaidiana naye.Nitaifanya kazi hii mimi mwenyewe” “Sawa Olivia.Unaweza ukaniambia itachukua muda gani kutengeneza kirusi hicho? “Sina hakika itachukua muda gani hadi hapo nitakapoanza kazi hiyo.Nipe muda wa kufanya utafiti kujua ni aina gani ya kirusi kinahitajika” akasema Dr Olivia “Sawa Olivia tutaendelea kuwasiliana mara kwa mara kujua maendeleo ya mpango huo lakini naomba jambo hili lisichukue muda mrefu sana kwani hatujui Edger yuko katika hali gani huko aliko” akasema Sayid na kuagana na Dr Olivia “Nitaendelea kujuta kila wakati kumfahamu na kumsaidia Edger.Wema na juhudi zangu vimegeuka shubiri.Nimejiingiza katika mtego nimenasa na siwezi tena kutoka.Familia yangu nayo imeingizwa katika suala hili na sasa wako katika hatari wanatishiwa kuuawa endapo sintafanya wanavyotaka.I won’t let that happen to my family.Wazazi na ndugu zangu hawafahamu kama nina mahusiano na watu wa IS.Hakuna ajuaye kama hata fedha za kituo kile ambacho kila mmoja anajua ni changu zimetoka kwao.Ee Mungu naomba unitoe katika shimo hili la moto nilimojitumbukiza” akawaza Dr Olivia akitoa machozi “Sijui itakuaje pindi wazazi wangu wakifahamu kwamba ninashirikiana na magaidi.Nitafanya nini mimi?akaendelea kujiuliza maswali “Sina ujanja IS wameniweka kwenye kona lazima nifanye wanachokitaka ili familia yangu waendelee kuwa salama.Lakini nitaendelea kuwa sehemu yao hadi lini?Nitaendelea kufanya kazi zao hadi lini? Akajiuliza na kukumbuka maneno ya Sayid Omar. “Olivia utakuwa mwanamke mwenye nguvu,tajiri,na hakuna ajuaye kwani siku moja unaweza ukashika nafasi ya juu ya uongozi.Hupendi siku moja kuwa rais wa kwanza mwanamke?Hupendi siku moja uongoze watu zaidi ya milioni hamsini?Hutaki jina lako kuingia katika vitabu vya historia ya nchi na dunia? “Nilikubaliana na Habiba Jawad kwamba kwa namna yoyote ile Edger akipatikana hataendelea na shughuli za siasa hapa nchini.Tulikubaliana kwamba mipango ya kumtaka Edger awanie urais wa Tanzania ifutwe na sasa wameanza kunifikiria mimi kunifanya niwe rais wa Tanzania.Hawa watu tayari wanao mtandao mkubwa hapa nchini na kwa uwezo wao mkubwa wa kifedha walio nao wanaweza wakalifanikisha hilo walitakalo.Kama waliweza kumtengeneza Edger Kaka akawa ni mmoja wa watu maarufu kabisa na ambaye ilibaki kidogo tu angeshika madaraka ya urais hawashindwi kunifanya mimi kuwa rais wa Tanzania” akawaza Dr Olivia na kwa mbali akatabasamu “Hakuna mtu katika dunia hii asiyependa kuwa mtu mkubwa.Hakuna anayeweza kukataa kushika madaraka ya urais na kwa kuwa watu hawa tayari wamekwisha anza kunifikiria kwa hilo lazima watahakikisha wanalifanikisha na siwezi kusema hapana kwani wanatumia kigezo cha kuiteketeza familia yangu.Wanazidi kunichanganya hawa watu ngoja kwanza niachane na masuala hayo nijielekeze katika hili kubwa la kutengeneza kirusi” akawaza Dr Olivia na kwenda katika chumba chake cha kusomea kilichojaa vitabu akachagua vitabu anavyovihitaji na kuviweka mezani akaanza kupitia kimoja baada ya kingine.Alizima kabisa simu yake ili asipate bughudha yoyote.Kwa siku nzima Dr Olivia alishinda katika chumba chake cha kusomea akipitia vitabu na machapisho mbali mbali alivyoamini vingemsaidia katika kile alichotaka kukifanya. MIEZI MITATU BAADAE
Kwa muda wa miezi mitano Dr Olivia Themba aliweka pembeni kazi zake zote akajielekeza katika jukumu moja tu la kutengeneza kirusi ambacho kingetumika katika mpango wa kumtafuta Edger.Olivia alifanikiwa kutengeneza kirusi SAB104 ambacho alikifanyia majaribio kwa Sokwe na kilionyesha mafanikio kama alivyokuwa amekusudia. Akiwa nyumbani kwake usiku akampigia simu Sayid ambaye wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara “Olivia habari za huko?akauliza Sayid “Huku kwema kabisa.Sayid nimekupigia simu kukujulisha kwamba rasmi sasa kirusi kiko tayari.Jina la kirusi hicho ni SAB104 kina uwezo wa kuua ndani ya siku kumi na nne kama mgonjwa hatakuwa amepata matibabu.Dalili za maambukizi ya kirusi hiki huanza kujitokeza siku moja tu baada ya kuingia mwilini.Mgonjwa huanza kuhisi mwili umechoka na usingizi wa mara kwa mara.Ndani ya …” “Olivia subiri kidogo” akasema sayid na kumkatisha Dr Olivia “Hizo ni habari njema sana ambazo nimekuwa nasubiri kuzisikia kwa muda mrefu.Nataka unielezee kwa kituo kuhusiana na kirusi hicho ili na mimi nikielewe kiundani” akasema sayid na Dr Olivia akamueleza kwa undani kuhusiana na kirusi kile. “Kazi nzuri sana umeifanya Dr Olivia ni kazi ambayo itamfurahisha kila mtu lakini kuna kitu kimoja ambacho nataka kifanyike.Umenieleza kwamba kirusi hicho umekifanyia majaribio kwa sokwe.Nataka kirusi hicho kifanyiwe majaribio kwa binadamu” akasema Sayid “Hakuna haja ya kufanya majaribio kwa binadamu.Majaribio niliyoyafanya ka Sokwe yanatosha sana” akasema Dr Olivia “Olivia hatutaki kubahatisha.Umefanya kazi kubwa na nzuri hivyo lazima tuwe na uhakika wa kile tunachotaka kukifanya hivyo atakuja mu wetu ambaye ni mtaalamu wa masuala hayo kuthibitisha kirusi hicho kama kinaweza kufanya kazi tunayoitaka.Atakuja mtu kesho kuchukua kirusi hicho ili tukifanyie majaribio kuona uwezo wake” akasema Sayid “Sayid mnataka kukijaribu wapi kirusi hicho? Nina wasiwasi kinaweza kusambaa na kuleta janga kubwa”akauliza Dr Olivia akionekana kuwa na wasiwasi “Usiwe na wasiwasi Dr Olivia.Tutakujulisha pale majaribio yatakapokuwa yamekamilika.Mpokee mtu atakayekuja kesho kuchukua kirusi hicho”akasema Sayid. “sayid sidhani kama hilo ni jambo zuri.Kirusi hiki nimekwisha kifanyia majaribio na nina uhakika nacho” akasema Olivia “Usihofu Olivia tunataka kujiridhisha kuhusu uwezo wake” akasema sayid na kukata simu. BAADA YA SIKU 1O Tayari zimekwisha pita siku kumi toka kirusi SAB104 kilipochukuliwa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa majaribio na akina Sayid.Dr Olivia akiwa ofisini kwake akapigiwa simu na Sayid “Habari yako Sayid”akasema Dr Olivia “Habari nzuri kabisa Olivia” “Kuna habari gani mpya?akauliza Dr Olivia “Olivia itakulazimu kwenda nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kesho kutwa”akasema Sayid “Nikafanye nini huko?akauliza Dr Olivia akishangaa “Ukifika Kinshasa utafikia hotel Zoela moja kati ya hoteli kubwa kabisa jijini Kinshasa.Chumba chako ni PS 3.Hotelini hapo utakutana na mtu anaitwa Seif Almuhsin ambaye atakuwa katika chumba PS1.Hivi ni vyumba vyenye hadhi ya rais hivyo usihofu usalama wako” “Seif almuhsin ni nani?Kwa nini nikaonane naye Kinshasa?akauliza Dr Olivia “Usiulize maswali mengi Olivia,anza kufanya maandalizi ya kwenda Kinshasa na kila kitu utakifahamu huko.Tiketi yako yako ya ndege italetwa ofisini kwako kesho asubuhi” akasema Sayid na kuagana na Dr Olivia “Nikafanye nini Kinshasa?Huyu Seif Almuhsin ni nani?Mbona sijawahi kumsikia wakimtaja? Akajiuliza Dr Olivia bila kupata majibu. KINSHASA – SIKU MBILI BAADAE Saa kumi na mbili za jioni Dr Olivia aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa.Uwanjani hapo alipokewa na mtu maalum na moja kwa moja akapelekwa Hotel Zoela ambako alipokelewa na kupelekwa moja kwa moja katika chumba chake ambacho kilikwisha andaliwa.Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye hadhi ya chumba cha rais.Dr Olivia hakushanganzwa na uzuri wa chumba kile kwani uzuri wa chumba chake ni mara mbili zaidi ya chumba hiki.Akaoga na kujilaza kitandani kwa ajili ya kujiandaa kukutana na Seif Almuhsin. “Mpaka sasa sielewi sababu ya kuja Kinshasa.Huyu Seif Almuhsin ni nani? Akajiuliza Dr Olivia “Siamini kama leo nimefikia hatua hii.Nilikuwa nayasoma mambo haya katika magazeti na kutazama katika luninga namna kikundi cha IS kinavyosumbua dunia kwa kufanya mauaji ya kinyama sehemu mbali mbali lakini leo hii ninakaa nao meza moja na kupanga mipango mbali mbali.Ni vipi endapo dunia itafahamu kwamba ninashirikiana na IS?Nitawaeleza nini familia yangu kuhusu suala hili wanielewe? Dah ! inaniumiza sana kuona maisha yangu yakiharibika nikijiona.Nimesoma sana lakini elimu yangu yote imeshindwa kuwa na manufaa kwa jamii yangu bali ninaitumia kuwasaidia hawa magaidi.Kuna wakati ninajiuliza kwa nini nisiitaarifu serikali kuhusu suala hili lakini ninaingiwa na hofu kwani mtandao wa hawa jamaa ni mkubwa na kwa kufanya hivyo nitaendelea kujiweka katika hatari kubwa kwani lazima wataniua mimi na familia yangu.Ngoja niendelee kufanya vile wanavyotaka lakini lazima nitafute njia ya kujitoa katika mtandao huu” akawaza Dr Olivia na kutolewa mawazoni baada ya muhudumu kugonga mlango.Dr Olivia akaenda kuufungua mlango na muhudumu akampatia kijikaratasi chenye ujumbe ukimuelekeza meza iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya chakula cha usiku.Hakupoteza muda akaanza kujiandaa.Baada ya kujiandaa akatoka na kuelekea katika ukumbi wa chakula akakaa katika meza aliyoelekezwa.Muhudumu akafika na kumuhudumia kinywaji. “Halow Olivia” sauti ikamstua Olivia aliyekuwa katika mawazo mengi.Mtu mmoja aliyevaa suti nyeupe akavuta kiti na kukaa.Bila kutambulishwa Dr Olivia akajua yule ndiye Seif Almuhsin,akamtazama kwa sekunde kadhaa na kuuliza “Seif Almuhsin? Akauliza Olivia na yule jamaa akamungalia Olivia huku akitabasamu “U mrembo sana Olivia.Nimefurahi kukutana nawe ana kwa ana” akasema Seif Wahudumu wakafika na kuandaa meza. “Olivia sura yako inaonyesha wasiwasi mkubwa”akasema Seif “Hayo ni mawazo yako Seif sina wasi wasi wowote” akasema Olivia Walipata chakula na kuzungumza mambo mengi na kisha Seif akamtaka waondoke waende katika chumba chake “Olivia karibu sana kuwa na amani usiwe na hofu yoyote,uko salama” akasema Seif baada ya kuingia chumbani. “Seif nimeelekezwa nije Kinshasa kukutana nawe lakini sijaambiwa sababu ya kuja hapa.Nataka kufahamu tafadhali kwa nini niko hapa?akauliza Dr Olivia “Dr Olivia uko hapa kwa ajili ya kushuhudia mafanikio kazi yako.Kama unakumbuka alikuja mtu kuchukua kirusi kile kwa ajili ya kukifanyia majaribio ambayo yalikuja kufanywa nchini Congo.Watu wawili walichukuliwa na kuchomwa sindano yenye virusi hivyo na wakahifadhiwa sehemu tukawafuatilia kwa makini sana toka siku ya kwanza walipopata maambukizi ya virusi hivyo” akasema Seif na sura ya Olivia ikaonyesha wasi wasi Seif akawasha kompyuta yake kisha akawasiliana na mtu Fulani akamtaka amuonyeshe picha ya mtu wa kwanza na baada ya muda Dr Olivia akamshuhudia mtu aliyelala chini akiwa anatokwa na damu puani na mdomoni alikuwa katika hali mbaya sana.Dr Olivia akastuka sana “Huyu ni mtu wa kwanza ambaye muda wowote atafariki dunia” akasema Seif na kumtaka yule jamaa amuonyeshe mtu wa pili “Huyu ni mtu wa pili ambaye hali yake ilikuwa mbaya lakini baada ya kuanza kutumia dawa uliyotengeneza ya kupambana na virusi wale hali yake imebadilika na anaendelea vyema lakini kama asingetumia dawa ile hali yake ingekuwa mbaya kama yule mtu wa kwanza” akasema Seif “Seif sitaki kuangalia picha hizi ziondoe tafadhali” akasema Dr Olivia akigeuza shingo kutazama upande mwingine.Seif akatoa maelekezo watu wale wawili wote wauawe kwani hawana kazi nao tena “Sasa rasmi nimeingia katika ulimwengu wa mauaji” akawaza Dr Olivia akitetemeka kwa ndani “Olivia hiki ulichokishuhudia ni matokeo ya kile ulichokitengeneza.Nathubutu kukwambia kwamba huu ulikuwa ni mtihani mkubwa kwako na umefaulu kwa alama za juu sana” akasema Seif “Kwa hiyo hamkuniamini?akauliza Dr Olivia “Dr Olivia ni kawaida yetu kuwa na uhakika wa kila tunachokifanya hivyo ilitulazimu kufanya majaribio ya kirusi kile kuthibitisha uwezo wake na sasa baada ya kuthibitisha uwezo wake tunaweza kukitumia katika mpango wetu.Tayari maandalizi yamekamilika na usiku huu mtoto wa rais atachomwa sindano yenye kirusi na baada ya siku mbili tutamtaka rais atuonyeshe mahala alipo Edger.Usihofu mipango inakwenda vizuri.Siku si nyingi tutafahamu mahala alipo Edger” akasema Seif almuhsin “Ni vipi kama rais atakataa kutoa ushirikiano? Ni vipi kama akigoma kufuata maelekezo atakayopewa?akauliza Dr Olivia “Dr Olivia unaonekana una wasi wasi mwingi.Usiwe na hofu tafadhali,tuna uhakika na kile tunachotaka kukifanya.Kwa namna yoyote ile rais lazima atatekeleza kile tunachokitaka” akasema Seif “Lazima niwe na wasiwasi kwani Coletha ni mdogo wangu familia zetu ni marafiki kwa muda mrefu,sitaki binti yule apoteze maisha” “Dr Olivia usihofu.Hatapoteza maisha.lazima rais atatekeleza kile tunachokitaka ndani ya muda atakaopewa na kama akishindwa kutekeleza maagizo basi hakuna namna mwanae atapoteza maisha.Olivia hii ni vita ya haki hivyo basi kupoteza ndugu katika mapambano ni jambo la kawaida.Sisi hatuogopi kufa au kuua.Olivia umekwisha ingia katika ulimwengu wetu hivyo mambo kama haya unapaswa kuyaozea.IS si watu watu wabaya kama inavyodhaniwa lakini sisi tunaendesha mapambano kwa ajili ya kudai haki na katika kudai haki wakati mwingine tunalazimika kuua kwani hata hao maadui zetu nao wanatuua.Mabomu yenye tani nyingi yanaangushwa katika kambi zetu kila uchao na kuua watu wetu hivyo na sisi lazima tujibu” “Hakuna kitu mtakachonieleza kikanifanya nikubali kuungana nanyi.Niko nanyi kwa shinikizo na ondoeni katika vichwa vyenu kwamba mimi ni mwenzenu.Katu siwezi kuwa sehemu yenu” akasema Dr Olivia na kumfanya Seif aangue kicheko “Olivia wewe ni mwenzetu tayari na muda utafika ambapo utakiri kwa ulimi wako kwamba ni mwenzetu.Wewe una umuhimu mkubwa sana kwetu Olivia na kuna mipango mingi mikubwa juu yako ambayo naamini tayari umekwishajulishwa hivyo endelea kuwa mtulivu na mvumilivu” akasema Seif ARUSHA - TANZANIA Mkutano wa wazalishaji wakubwa wa bidhaa za maziwa katika nchi za Afrika Mashariki ulikuwa unaendelea katika hoteli moja kubwa jijini Arusha.Wazalishaji hawa walikutana ili kujadili namna ya kutatua changamoto kadhaa wanazokutana nazo katika sekta yao ya maziwa.Mathew Mulumbi ambaye naye anamiliki kiwanda cha kutengeneza maziwa ya unga alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo Wakati mkutano ukiendelea bangili ya dhahabu aliyokuwa ameivaa Mathew ikatoa mlio na taa ndogo nyekundu ikawaka mfulululizo.Mathew akastuka na kuitazama bangili ile halafu katika kompyuta yake iliyokua mezani ukaingia ujumbe akaifunika kompyuta yake na kutoka akaelekea maliwato akatoa simu yake na kuangalia ujumbe ulioingia akastuka “Dr Olivia!! She’s in trouble “Akasema kwa mshangao Akapiga simu ya Olivia lakini haikuwa ikipatikana.Haraka haraka akatoka maliwato akaenda kukusanya vifaa vyake na bila kuaga mtu akatoka katika chumba cha mkutano akachukua taksi akarejea hotelini alikofikia.Haraka haraka akaifungua kompyuta yake kuutazama ujumbe ule ulioingia “Ramani inanionyesha kwamba taarifa imetumwa kutoka sehemu fulani Kigamboni.Olivia yuko Kigamboni I must help her” akawaza Mathew akiangalia ramani iliyoonekana katika kompyuta yake na sehemu Fulani katika ramani ile kulikuwa na mduara mwekundu ikionyesha ndipo mahala taarifa ilikotoka. “Olivia yuko katika matatizo gani? Kwa muda wa miezi kadhaa sasa toka tumefahamiana Olivia hayuko kawaida anaonekana kuna jambo kubwa linamsumbua.Nimejaribu kumuuliza mara kwa mara kutaka kujua tatizo lake lakini amekuwa mgumu kunieleza.Natakiwa kurejea Dar es salaam haraka sana kumsaidia” akawaza Mathew na kupiga simu ofisi za shirika la ndege la Tanzania kujua kama kuna ndege yoyote inayoondoka muda mfupi ujao kuelekea Dar es salaam.Alitaarifiwa kwamba ipo ndege ambayo itaondoka ndani ya saa moja kutoka muda ule kuelekea Dar es salaam,akakata tiketi na hakutaka kupoteza muda akaanza kukusanya vifaa vyake kwa ajili ya kuondoka.Wakati akipakia vifaa vyake sandukuni simu yake ikaita alikuwa ni rafiki yake Gibson. “Gibson mambo vipi?akauliza Mathew “Mambo poa Mathew habari za Arusha? “Huku kwema lakini ninajiandaa kurejea Dar es salaam” “Mkutano umemalizika? “Hapana bado lakini kuna dharura imetokea na kunilazimu niondoke kabla mkutano haujamalizika” “Mathew tayari umekwisha pata taarifa?akauliza Gibso “Taarifa zipi Gibson? “Hujapata taarifa zozote?Hujaingia katika mitandao ya kijamii kuona kilichotokea? “Toka asubuhi nilikuwa katika mkutano na sijapata muda wa kujua nini kinaendelea.Nijuze tafadhali” akasema Mathew “Nilidhani safari yako ya ghafla ni baada ya kupata taarifa za kilichotokea” “Sifahamu chochote Gibson.Nini kimetokea? “Ni kuhusu yule rafiki yako Dr OIivia.Mapema leo ametekwa nyara na watu wasiojulikana wakati akiingia nyumbani kwake akitokea uwanja wa ndege.Mpaka sasa bado hajapatikana.Hiyo ndiyo habari kubwa ya leo” akasema Gibson “Olivia ametekwa?Mathew akashangaa “Ndiyo ametekwa.Ni taarifa kubwa sana nikajua nawe tayari unafahamu” “Sifahamu kama Olivia ametekwa wewe ndiye wa kwanza kunijuza.Gibson ahsante sana kwa taarifa hizi tutazungumza zaidi nikirejea Dar es salaam baadae jioni’ akasema Mathew na kukata simu “Kumbe Olivia ametekwa nyara !! Nani hao waliomteka nyara?akawaza Mathew na kuingia katika mitandao ya kijamii kufuatilia taarifa zile.Alihisi mwili wote ukimsisimka baada ya kusoma taarifa mbali mbali namna tukio lile lilivyotokea. “Kwa taarifa zinavyoelezea,tukio hili la utekaji wa Olivia limefanywa kitaalamu mno na waliofanya hivi si watu wa mzaha ni watu wenye uwezo mkubwa.Walikuwa wamejipanga vyema kuhakikisha kwamba mpango wao unafanikiwa” akawaza Mathew “Nini sababu ya Olivia kutekwa? Watekaji hao ni watu wanaotaka kujipatia fedha au kuna suala lingine?Kwa haraka haraka namna tukio lilivyotokea siamini kama watu hao wamemteka Olivia kwa sababu ya fedha lazima kuna sababu kubwa.Nilifanya vyema kumpa program ile ya kunijulisha pindi anapokuwa katika hatari.Olivia ni mtu wangu wa karibu sana siwezi kukubali akawa katika hatari nitalibeba jukumu la kumtafuta kuhakikisha anapatikana.Ninarejea Dar es salaam na jiji litatikisika.Watekaji hao wamekosea sana kumteka mtu wangu wa karibu” akawaza Mathew na kupakia mizigo yake kisha akachukua gari la hoteli akaelekea uwanja wa ndege tayari kurejea Dar es salaam. MPENZI MSOMAJI * BILA KUTARAJIA DR OLIVIA ANAJIKUTA AKIINGIA KATIKA MIKONO YA KIKUNDI CHA IS NA ANAKUBALI KUFUATA MAELEKEZO YAO ILI WAZAZI NA FAMILIA YAKE WAWE SALAMA.ATAFANIKIWA KUJITOA KATIKA MIKONO YA IS?
DAR ES SALAAM MathewMulumbi aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam akitokea jijini Arusha.Alitoka ndani ya uwanja na kupokewa na dereva wake safari ya kuelekea nyumbani ikaanza “Tukio gani limetokea hapa jijini leo?Mathewakamuuliza dereva wake kana kwamba hajui chochote kilichotokea “Kumetokea tukio la utekaji leo.Yule rafiki yako Dr Olivia ametekwa nyara na watu wasiojulikana.Hujapata taarifa hizo mpaka muda huu?akauliza Athuman dereva wa Mathew “Tayari ninazo taarifa hizo nilitaka nipate uhakika kama taarifa hizo ni za kweli.Kuna taarifa zozote mpaka sasa kama amepatikana? “Mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa kama amepatikana lakini naamini bado hajapatikana kwani kama angekuwa amepatikana ingekwisha tangazwa” akasema Athumani.Ukapita ukimya Mathewakauliza “Athumani wewe unazunguka sehemu mbali mbali na unasikia mengi,kwa tetesi ulizozisikia huko mtaani nini yaweza kuwa sababu ya kutekwa kwake?akauliza Mathew “Mkuu kwa kweli mpaka sasa hakuna anayejua nini sababu ya Olivia kutekwa.Kila mtu anaongea la kwake.Wengi wanaamini kwamba watekaji wamefanya hivyo kwa ajili ya kutaka fedha kwani Dr Olivia ni mtoto wa bilionea na hata yeye mwenyewe ana mafanikio makubwa.Kikubwa kilichopo mtaani ni hicho kwamba watekaji lengo lao ni kujipatia fedha.Michezo kama hii ya kuteka watu na kudai fedha haikuwepo nchini kwetu imeibuka ghafla na kushika kasi.Wafanya biashara wakubwa na matajiri wako kwenye hatari kubwaya kutekwa na kulazimishwa kutoa fedha nyingi ili kuachiwa huru.Serikali inatakiwa kudhibiti mchezo huu usiendelee kwani unaleta hofu kubwa hasa kwa wafanya biashara wakubwa.Leo katekwa Dr Olivia kesho atakuwa nani? Hofu kubwa imetanda” akasema Athumani “Uko sahihi Athumani kwamba michezo kama hii ya utekaji haijazoeleka hapa nchini kwetu.Ni wajibu wa wananchi kushirikiana na serikali kudhibiti matukio kama haya yanayoanza kushika kasi hapa nchini.Wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi la polisi kila pale wanapokuwa na taarifa.Michezo kama hii ya utekaji hufanywa na watu kutoka nje wakisaidiwa na watu wachache wa ndani” akasema Mathewa safari ikaendelea kimya kimya “Wamekosea sana hawa jamaa kumteka Olivia.Hawakujua kama Olivia ni mtu wangu wa karibu?Nitahakikisha ninaingia katika mapambano na kumuooa Olivia kwa gharama zozote” akawaza Mathew “Lakini nini hasa sababu ya kumteka Olivia? Wanahitaji fedha? Nahisi lengo lao ni hilo la kujipatia fedha lakini papo hapo kuna kitu ndani mwangu kinakataa kwamba lengo la watekaji ni kujipatia fedha.Nahisi kuna kitu zaidi ya fedha.Toka nilipokutana na Olivia nimehisi ana tatizo linamsumbua na nilipomdadisi alikiri kweli ana tatizo na watu Fulani ambao hakutaka kuwataja.Je ni watu hao ndio walimteka nyara? Kama ni wao nini hasa tatizo lao? Je wamehitilafiana katika biashara? Kama ndiyo ni biashara gani anaifanya Olivia? Hajawahi kunieleza kama ana biashara nyingine tofauti na kumiliki kituo kile cha utafiti wa magonjwa lakini naamini hawezi kukosa biashara.Maisha ya Olivia yametawaliwa na usiri mwingi hapendi kuweka wazi maisha yake ndiyo maana linapotokea tatizo kama hili tunashindwa wapi tuanzie kumtafuta.Hata hivyo nitafanya uchunguzi na ukweli utabainika” akawaza Mathew Tayari kiza kilikwisha ingia alipofika nyumbani kwake.Akaenda chumbani kwake na kukaa kitandani akatafakari namna atakavyoufanya uchunguzi ule. “Tayari ninafahamu mahala alipo Olivia lakini siwezi kwenda huko kwa kukurupuka.Natakiwa kujipanga vyema kwani watekaji ni watu waliojiandaa.Kabla ya kufanya lolote natakiwa kwanza nikaonane na wazazi wa Olivia kujua kinachoendelea hadi sasa.Yawezekana Olivia amepatikana au yawezekana tayari watekaji wamewasiliana nao na kudai kiasi cha fedha.Vile vile natakiwa kuwaeleza azma yangu ya kumtafuta Olivia na wao waridhie na kunipa ruhusa ya kulichunguza jambo hili.Siwezi kukurupuka na kuanza kuchunguza bila kupata ridhaa yao” akawaza Mathewna kufungua kasiki lililkuwa chumbani kwake akatoa bastora akaiweka katika koti na kuondoka.Hakuhitaji dereva usiku huu aliondoka peke yake. “Nimewaza sana kuhusu sababu ya kutekwa Olivia lakini bado sijapata jibu.Sababu kwamba watekaji wanataka fedha hainingii kabisa akilini.Mgogoro aliowahi kunidokeza waweza ukawa ni sababu pia lakini kuna kitu wengi wanakisahau kuna sababu ya kimapenzi pia.Hii inawezekana ni mojawapo ya sababu pia.Yawezekana kuna kigogo mmoja anayemtaka lakini Olivia amekataa kumpa nafasi hivyo akaamua kutumia nguvu.Nikikutana na wazazi wake ninaweza kupata mwanga zaidi kwani wao wanamfahamu vyema kuliko mimi” Akawaza akiwa garini akielekea nyumbani wazazi wa Olivia Alifika eneo la Mikindani akautafuta mtaa wa Themba.Kutokana na umaarufu wake na namna alivyojitolea kusaidia jamii inayomzunguka wakazi wa eneo la Mikindani waliamua kumzawadia Agrey Themba mtaa ambao waliuita mtaa wa Themba.Mathewaliuliza ilipo nyumba ya bilionea Themba akaelekezwa akapunguza mwendo baada ya kulikaribia geti.Ulinzi ulikuwa mkali eneo lile.Gari la Mathewlikasimamishwa na walinzi waliokuwa wanalinda geti la kuingilia ndani kwa mlinzi mmoja akamfuata.Mathewakashusha kioo akasalimia naye na mlinzi yule akamtaka ajitambulishe yeye ni nani “Naitwa Mathewni rafiki wa Olivia nimekuja kuonana na wazazi wake”akasema Mathew “watu hawaruhusiwi kuingia ndani labda kwa miadi maalum hata kama ni ndugu” akasema yule mlinzi “Sina miadi ya kuonana na wazazi wa Olivia lakini mimi ni mwanafamilia ni mchumba wa Olivia”akasema Mathewyule mlinzi akamtazama kwa makini “Kaka usiwe na hofu mimi ni mwanafamilia,nimetoka safari Arusha jioni hii nikapata taarifa za tukio lililotokea nikaona nije moja kwa moja nyumbani” akasema Mathewambaye alikuwa ndani ya gari la kifahari sana hivyo mlinzi yule akaruhusu geti lifunguliwe na Mathewakaingia ndani.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia katika jumba lile kubwa.Magari kadhaa ya kifahari yaliyopata matano yalikuwa yameegeshwa.Kijana mmoja ambaye alionekana ndiye mpokeaji wa wageni akamuelekeza sehemu ya kuegesha magari,Mathewakashuka akapokewa na yule kijana akamkaribisha na kumuongoza kuelekea sebuleni ambako kulikuwa na watu kadhaa.Mathewakawasalimu wote aliowakuta mle ndani.Alimfahamu Agrey Themba ingawa hawakuwa marafiki.Pembeni yake alikaa mwanamama ambaye kwa haraka Mathewakamtambua kuwa alikuwa mama yake Olivia kwa namna walivyofanana.Muhudumu akafika haraka na kumuhudumia Mathewkinywaji. Dakika tano baada ya Mathewkuingia mle sebuleni wale wageni waliokuwamo wakaaga na kuondoka,Agrey akawasindikiza na pale sebuleni akabaki mama yake Olivia “Karibu sana baba”akasema bi Lucy Themba mama yake Olivia “Nashukuru mama.Pole sana kwa tatizo lililotokea” akasema Mathew “Tunashukuru baba.Dunia hii imekuwa na watu makatili sana.Siku hizi ubinadamu umetoweka.Watu wanatenda matendo ya kinyama mchana wa jua bila kuogopa.Mambo haya sijui yanatokea wapi.Yanataka kupoteza amani tuliyo nayo Tanzania” akasema bi Lucy “Ni kweli mama mambo haya ni mageni kabisa katika nchi yetu.Watanzania tumezoea amani na hatujazoea kusikia matukio kama haya ya kuteka watu tena mchana wa jua.Mambo kama haya yanatokea sana katika nchi za wenzetu lakini taratibu yameanza kutokea na hapa kwetu pia.Serikali kupitia vyombo vyake wanapaswa kudhibiti hali hii isiendelee kwani kama matukio ya namna hi yakiendelea yanaweza kuzua hofu kubwa hasa kwa wafanya biashara ambao ndio walengwa wakubwa” akasema Mathew na Agrey Themba akarejea mle sebuleni “Kijana karibu sana.Samahani hatukusalimiana vyema wakati ulipoingia” akasema Agrey na kumpa mkono Mathew “Karibu sana” akasema Agrey “Nimekaribia mzee.Poleni sana na tukio la leo”akasema Mathew “Tumekwisha poa kijana wangu.Ni jambo ambalo limetuacha katika simanzi kubwa”akasema Agrey huku akimtazama Mathewkwa makini sana “U mgeni kabisa machoni kwangu.Tumewahi kuonana sehemu fulani? Naomba unikumbushe tafadhali kwani uzee umekwisha piga hodi na kuna nyakati ninasahau” akasema Agrey “Mzee mimi nakufahamu ila wewe sidhani kama unanifahamu.Ninaitwa MathewMulumbi ni mfanyabia………….” Kabla Mathewhajaendelea Agrey akamkatisha“MathewMulumbi hili si jina geni kwangu.Wewe ndiye mwenye kiwanda cha kutengeneza maziwa cha Masai Milk? “Ndiyo mimi mzee” akajibu Mathew “Nimefurahi kukutana nawe Mathewkaribu sana.Ninamiliki shule kadhaa hapa jijini dare s salaam ambazo hupata huduma ya maziwa kutoka kiwandani kwako.Niliambiwa kiwanda kile kinamilikiwa na kijana mmoja anaitwa Mathewlakini sikuwahi kukutia machoni.Niliambiwa ukiacha kiwanda kile unazo pia biashara nyingine kubwa kubwa.” akasema Agrey “Ndiyo mzee.Nina biashara nyingine mbali mbali,viwanda mashamba nk” “Hongera sana Mathew.Nimefurahi nimekutana nawe leo ingawa tumekutana katika wakati kama huu wa matatizo.Naamini pale tatizo hili litakapokuwa limemalizika tutapata wasaa mzuri wa kukutana na kuzungumza mambo mengi hususan masuala yetu ya kibiashara”akasema Agrey “Ahsante sana mzee,nitafurahi sana kupata wasaa wa kuzungumza nawe mambo mengi na kupata mawazo mengi zaidi ya biashara” akasema Mathewukimya mfupi ukaputa Mathewakasema “Mzee na mama mtanisamehe kwa kuja bila taarifa lakini nimekuja kuwapeni pole kwa tukio lililotokea leo.Nilikuwa katika mkutano Arusha ndipo nilipopata taarifa za kutekwa Olivia hivyo ikanilazimu kukatisha mkutano na kurejea Dar es salaam.Dr Olivia ni rafiki yangu.Nimefahamiana naye miezi kadhaa iliyopita na amekuwa rafiki yangu mkubwa ndiyo maana nilipopata taarifa za kutekwa kwake nimelazimika kuja mara moja kuungana na familia yake katika wakati huu mgumu vile vile kusaidia katika kumtafuta”akasema Mathew “Mathewninakushukuru sana kwa kuguswa na suala hili.Wewe ni rafiki wa kweli na kwa hili ulilolionyesha la kuacha shughuli zako zote na kuja kuungana nasi kutufariji katika wakati huu mgumu limetugusa sana.Kwa nini Olivia hajawahi kututambulisha kwetu? Wewe unapaswa kuwa sehemu ya familia yetu.Olivia anao marafiki wengi lakini hakuna aliyeonyesha kuguswa kama wewe” akasema Agrey “Mzee mpaka sasa kuna taarifa zozote zimepatikana kujua mahala alipo Olivia?akauliza Mathew “Nimekuwa na mawasiliano ya karibu sana na rais,mkuu wa jeshi la polisi nchini na hao wote tunawasiliana kila mara na hadi nilipowasiliana nao kama dakika ishirini zilizopita bado Olivia hakuwa amepatikana.Jeshi la polisi linaendelea na juhudi zake na hakuna kulala hadi wahakikishe Olivia anapatikana.Rais amekwisha toa maelekezo kwa jeshi la polisi wahakikishe wanatumia kila uwezo walio nao kumtafuta Olivia na kumpata.Ninaamini mpaka kesho asubuhi tunaweza tukawa na taarifa nyingine nzuri lakini taarifa tuliyonayo hadi muda huu bado Olivia hajapatikana” akasema Agrey.Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa halafu Mathewakasema “Mzee samahani tunaweza kuzungumza faragha kidogo? “Sawa hakuna tatizo” akasema Agrey akamchukua Mathewwakatoka nje ya nyumba wakaelekea katika bustani ambako kulikuwa na sehemu za kukaa kupumzika “Nakusikiliza Mathew” Akasema Agrey “Mzee nitakuchukulia muda wako kidogo lakini nataka nipate picha ya namna tukio lile lilivyotokea.Mimi sijabahatika kufika eneo la tukio kama nilivyokueleza kwamba nilikuwa Arusha.Naamini utakuwa umefika eneo la tukio na utakuwa umeshuhudia namna tukio lilivyotokea.Nataka kufahamu mazingira ya namna tukio lile lilivyotokea kwani nimesoma tu mtandaoni na sijapata picha halisi” akasema Mathew.Agrey akamtazama Mathewkidogo na kusema “Niliwasiliana na Olivia asubuhi ya leo akiwa jijini Kinshasa na akanieleza kwamba atarejea leo nyumbani.Alirejea salama na tukio la kutekwa limetokea wakati akijiandaa kuingia ndani ya nyumba yake akitokea uwanja wa ndege.Kwa siku za karibuni Olivia aliamua kuwa na walinzi kwa kuwa wewe ni mtu wake wa karibu nadhani umekwisha waona akiwa nao sehemu mbali mbali.Aliamua kuwa na walinzi baada ya kuwa na wasi wasi na usalama wake hivyo alipotoka uwanja wa ndege alikuwa na magari mawili moja alikuwamo yeye na mlinzi wake mmoja pamoja na dereva na lingine walikuwemo walinzi wake wengine.Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba magari yalipokaribia katika geti la nyumba ya Olivia ilitokea helkopta na mtu mmoja akajitokeza katika helkopta ile akiwa na bunduki kubwa na kuanza kumimina risasi katika magari yale na dereva wa gari la Olivia akapigwa risasi akafa pale pale na gari la Olivia likaenda kugonga ukuta.Walinzi wake nao waliuawa wote.Taarifa kutoka kwa mlinzi wa getini ambaye alijificha wakati tukio lile linatokea alisema kwamba zilitokea gari mbili kwa kasi na kumchukua Olivia wakaondoka naye.Jeshi la polisi walijaribu kufuatilia picha za kamera za ulinzi lakini hawakuweza kuwatambua watu wale kwani walikuwa wamefunika nyuso zao na vile vile gari zote mbili zilikuwa na namba zinazofanana.Helkopta ile imepatikana imekutwa imetelekezwa sehemu nje ya jiji na dereva wake amekutwa ameuawa yeye na familia yake inaonekana helkopta ile iliibwa na watekaji wakaitumia kisha wakaitelekeza.Hapo ndipo walipofikia jeshi la polisi na uchunguzi unaendelea” akasema Agrey “Pole sana mzee wangu.Hili linaonekana ni tukio lililopangwa kitaalamu sana.Kuna mtu yeyote ambaye anashikiliwa hadi sasa kufuatia tukio hilo?akauliza Mathew “Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba hadi sasa watu zaidi ya ishirini wanashikiliwa na jeshi la polisi vile vile watumishi wote wa nyumbani kwa Olivia nao pia wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.Mtandao uliofanya tukio hili unaonekana ni mrefu ndiyo maana idadi hiyo kubwa ya watu inashikiliwa ndani ya kipindi kifupi” akasema Agrey na gari Fulani likaingia wakashuka watu wawili Agrey akamuomba Mathewamsubiri akawapokee wageni wale atarejea.Agrey akaenda kuwapokea wageni wake na kuwakaribisha ndani baada ya muda mfupi akarejea “Samahani kwa kukuacha mwenyewe Mathew,mgeni yule ni naibu waziri wa mambo ya nje amekuja kutupa pole,ni rafiki yangu sana.Tuendelee na mazungumzo yetu” akasema Agrey “Mzee nimeomba tuzungumze faragha kuna suala la muhimu sana la kujadiliana mimi na wewe na sikupenda mtu mwingine alifahamu’ akasema Mathew “Ni suala gani Mathew?akauliza Agrey. “Hakuna anayefahamu sababu ya Olivia kutekwa lakini wengi tunaamini yawezekana watekaji wanataka fedha kwani mchezo wa namna hii upo katika nchi mbali mbali na mara watekaji wanapomteka mtu hupiga simu kwa familia yake wakidai kiasi kikubwa cha fedha.Hamjapigiwa simu na mtu yeyote msiyemfahamu?akauliza Mathew “Hata sisi tunaamini hivyo kwamba watekaji hao yawezekana lengo lao ni kujipatia fedha lakini mpaka sasa hawajapiga simu na hatujapokea simu yoyote ambayo hatuifahamu” akajibu Edger “Kama lengo lao ni fedha basi watapiga simu na watakapopiga watatoa vitisho kwamba msiwasiliane na jeshi la polisi” “Tumekwisha eleweshwa tayari na jeshi la polisi kuhusiana na suala hilo na watakapopiga tutawasiliana na polisi haraka sana” akasema Agrey “Hata hivyo umakini mkubwa unatakiwa kwani watu hawa ni hatari na wamejipanga vyema hivyo kosa moja hata dogo linaweza kuweka uhai wa Olivia mashakani” akasema Mathew “Unaniogopesha Mathew.Unashauri wakinipigia simu kutaka fedha nisiwasiliane na polisi?akauliza Agrey “Sina maana kwamba usiwasiliane na jeshi la polisi lakini umakini mkubwa sana unatakiwa.Hata polisi wasipokuwa makini mnaweza mkapoteza fedha na Olivia msimpate.Tuachane na hilo kuna suala la pili ambalo nataka tuzungumze” akasema Mathewna kunyamaza kidogo kisha akasema “Nimefahamiana na Olivia miezi kadhaa iliyopita na tumekuwa marafiki wa karibu sana.Katika ukaribu wetu nimekugundua kwamba Olivia alikuwa na tatizo linalomsumbua na siku moja niliwahi kumuomba anieleze tatizo lake lakini alinieleza kwa kifupi kwamba ana matatizo na watu Fulani.Nilimtaka anieleze ni tatizo gani na watu hao ni akina nani lakini hakutaka kuliongelea suala hilo.Hali hiyo imeendelea kwa muda mrefu na baada ya tukio la leo nimeanza kupata picha kwamba yawezekana watu hao ambao alinidokeza kwamba ana matatizo nao watakuwa na mahusiano na kutekwa kwake.Nimekuja kwako kufahamu je hakuwahi kukueleza chochote wewe au mama kuhusiana na tatizo lililokuwa linamsumbua? Akauliza Mathew.Agrey akafikiri kidogo na kusema “Ni mara ya kwanza ninasikia kutoka kwako kwamba Olivia alikuwa na tatizo linamsumbua.Kwa tabia yake Olivia ni mtu msiri sana ni nadra kuweka wazi tatizo linalomsumbua.Akikueleza tatizo lake basi limemshinda kulitatua na anahitaji msaada.Anaamini sana katika kutatua matatizo yake yeye mwenyewe bila kuomba msaada.Kutokana na wote kuwa na shughuli nyingi,mimi naye tumekuwa tukionana mara chache na hata tunapoonana hajawahi kunieleza kama ana tatizo linamsumbua.Ni watu gani hao aliokuwa katika mgogoro nao? Inawezekana kabisa wakawa wanahusika katika tukio la leo kama unavyosema” akasema Agrey.
“Ngoja nikamuulize mama yake yawezekana amewahi kumueleza chochote kuhusiana na tatizo lake” akasema Agrey “Hakuna sababu ya kumsumbua mama.Naamini hajamweleza kwani kama angekuwa anafahamu chochote angekwisha kwambia” akasema Mathewna ukimya mfupi ukapita halafu Mathewakasema “Mzee ninaomba nikueleze jambo kubwa ambalo limenileta hapa lakini naomba jambo hilo libaki kati yetu” “Nakusikia Mathew” “Mimi nimewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi lakini kwa sasa nimeachana na shughuli hizo na ninaendelea na biashara zangu lakini kuna nyakati hulazimika kurejea tena katika kazi yangu hiyo ya zamani pale linapotokea jambo ambalo linanilazimu niwepo kulishughulikia.Mara nyingi nimekuwa nikiombwa na serikali kushughulikia masuala Fulani pale penye ulazima na siwezi kukataa kwani nina mapenzi makubwa na nchi yangu” akasema Mathew.Agrey Themba akamuangalia kwa macho yaliyojaa mshangao mkubwa “Wewe ni mpelelezi?akauliza Agrey “Ndiyo.Nimewahi kuifanya kazi hiyo lakini kwa sasa ninafanya shughuli zangu binafsi”akasema MathewMulumbi “Nimeshangaa sana Mathewsikutegemea kabisa bilionea kama wewe unaweza kuwa mpelelezi” akasema Agrey “Niliwahi kufanya kazi hiyo zamani lakini kwa sasa nimekwisha achana nao ninajishughulisha na biashara zangu kama nilivyokueleza awali.Mzee Themba,Olivia ni rafiki yangu mkubwa na kwa sababu yake nimeamua kutumia ujuzi wangu nilio nao katika masuala haya ya uchunguzi kumtafuta na kuhakikisha ninampata” akasema Mathew “Mathewahsante sana kwa kujitolea kutumia ujuzi wako kumtafuta mwanangu lakini suala hili tayari liko katika mikono ya jeshi la polisi na wanatumia kila nguvu waliyonayo kuhakikisha wanampata Olivia.Ninashauri kama unalo jambo lolote linaloweza kusaidia kupatikana kwa Olivia liwasilishe kwa jeshi la polisi walifanyie kazi kwani wao wana nguvu kubwa na mtandao mrefu.Hata hivyo nakushukuru sana Mathewkwa moyo wako wa kujitolea kwa ajili ya Olivia”akasema Agrey Themba “Mzee,kwa uzoefu wangu nimegundua watekaji hawa ni watu waliojiandaa na hawajakurupuka.Wanafahamu Olivia ni mwanao,wanafahamu ukaribu wako na rais na wanajua kabisa kwamba kutokana na ukaribu huo nguvu itakayotumika kumtafuta Olivia ni kubwa hivyo wamejiandaa vyema kukabiliana na nguvu http://deusdeditmahunda.blogspot.com/yoyote itakayotumika.Ukifuatilia namna walivyomchukua Olivia ndipo utagundua kwamba watu hawa si watu wa kufanyia mzaha na operesheni hii hawakukurupuka wamejipanga vyema.Operesheni kama hizi hufanywa na watu wenye utaalamu mkubwa hasa majasusi pale wanapomuhitaji mtu Fulani muhimu.Nimefanya kazi katika idara ya ujasusi nikiwa tegemeo hivyo mambo kama haya ninayafahamu vyema na ndiyo maana nimejitolea kumtafuta Olivia kwani nina uhakika mkubwa wa kumpata kwa kuwa ninazifahamu mbinu zote za kijasusi”akasema Mathew.Agrey akafikiri kwa muda na kusema “Mathewmaneno yako yanazidi kunipa woga kuhusu mwanangu kama huko aliko atakuwa salama ninatamani sana kukupa jukumu hili la kumtafuta mwanangu lakini tayari polisi wanaendelea na uchunguzi na hatuwezi kuwa na timu mbili za uchunguzi kwa wakati mmoja.Polisi wana mtandao mkubwa sana na wanaweza wakampata Olivia kwa haraka zaidi kuliko ukiwa peke yako.Ushauri wangu Mathewnitakuunganisha na mkuu wa jeshi la polisi uzungumze naye na kama kuna kitu chochote ambacho unadhani kinaweza kusaidia katika uchunguzi utawaeleza na wao watakifanyia kazi.Kwa sasa jeshi la polisi wanatafuta sana taarifa zozote ambazo zinaweza kusaidia kumpata Olivia wewe unaweza kuwa mtu muhimu sana kwao” akasema Agrey “Mzee suala hili la la Olivia ni pan asana na ninakuomba usilichukulie krahisi.Hatuwezi kuwaachia jeshi la polisi peke yao na ndiyo maana nimeamua kusaidia uchunguzi kwa kutumia uzoefu nilio nao lakini kwa mbinu zangu ninazozijua” akasema Mathew “Mathewnimekuelewa sana kijana wangu lakini hofu yangu ni kwamba nikikuruhusu ufanye uchunguzi wako peke yako unaweza ukaingiliana na jeshi la polisi na kumuweka Olivia katika hatari zaidi ndiyo maana nikashauri kwamba uungane na jeshi la polisi au kama una taarifa zenye msaada basi wape polisi.Binafsi bado nina imani kubwa na jeshi la polisi kwamba watampata Olivia ndani ya muda mfupi kwani nguvu waliyoanza nayo ni kubwa” akasema Agrey.Mathewakamtazama Agrey na kusema “Olivia ametekwa saa tano asubuhi,tayari giza limeingia na hakuna taarifa yoyote yenye kutia matumaini kuhusu mahala aliko Olivia.Mzee nafahamu juhudi kubwa zinafanyika kumtafuta Olivia lakini bado haitoshi.Nguvu zaidi inahitajika na ninaomba ridhaa yenu ili na mimi nitoe msaada wangu” akasema Mathew “Mathewbado imani yangu ni kubwa kwa jeshi la polisi kwamba watampata Olivia.Wamekwisha jipanga vyema kabisa na kwa mipango yao namna walivyonieleza wanakwenda vizuri.Kupitia tukio hili la Olivia jeshi la polisi wanataka kuchimba hadi mzizi wa mtandao huu wa watekaji hapa nchini na kuusafisha kabisa.Mathewnadhani hatuna cha kuzungumza zaidi nina wageni wananisubiri ndani.Kama utakuwa tayari kushirikiana na jeshi la polisi basi utanijulisha ili nikuunganishe na viongozi wa polisi” akasema Agrey Themba na kumpa mkono Mathewakimuaga “Mzee ni vipi nikikueleza kwamba tayari ninafahamu mahala alipo Olivia? akauliza Mathew “What?!! Agrey akapatwa na mstuko mkubwa. “Mzee nisikilize vizuri” akasema Mathewhuku Agrey akimtazama kwa macho yenye woga “Baada ya Olivia kunidokeza kwamba ana matatizo na watu fulani niliingiwa hofu kuhusu maisha yake na nilichokifanya nilimpa namba Fulani nikamtaka azipige namba hizo pindi anapokuwa katika matatizo.Namba hizo ni za program maalum ambayo ninaitumia kwa ajili ya usalama wa familia yangu.Nikiwa mkutanoni Arusha nilipata ujumbe ukinijulisha kuwa namba ile imepigwa nikatazama ni nani amepiga nikagundua ni Olivia.Programu ikanionyesha hadi mahala ambapo namba hiyo ilipigwa na ninaamini ndipo alipo Olivia”akasema Mathew “Jesus Christ !! akasema Agrey.Mathewakamtaka waelekee katika gari lake akachukua kompyuta na kumuonyesha Agrey “Namba zile nilizompa Olivia zilipigwa hapa kwenye huu mduara mwekundu ambako ramani hii inatuonyesha kwamba ni sehemu fulani Kigamboni”akasema Mathew.Agrey akaitazama ramani ile kwa makini huku midomo ikimtetemeka “Ma.mma…Mathewunachok isema ni cha kweli?akauliza “Ndiyo mzee ni kitu cha kweli kabisa.Nimerejea kutoka Arusha kwa sababu nina uhakika wa kumpata Olivia.Ninayo sehemu ya kuanzia kumtafuta Olivia.Kabla sijaenda mahala hapo niliona ni vyema nikafika kwanza hapa kuzungumza nanyi na kuwaeleza mipango yangu kuhusiana na kumpata Olivia.Mzee ninaomba mniruhusu nikamtafute Olivia.Ninawaahidi ninao uwezo mkubwa wa kumpata kwa haraka” akasema Mathew “Nadhani mama yake naye anatakiwa kulifahamu suala hili” akasema Agrey na kumpigia simu mke wake akamtaka awafuate pale bustanini ambaye alifika mara moja. “Lucy utatusamehe tulitoka nje kuna suala nyeti sana tulikuwa tunazungumza.Mathewameniel eza jambo zito sana” akasema Agrey “Ni jambo gani?akauliza Lucy “Mathewhebu mueleze mke wangu naye asikie”akasema Agrey,Mathewakamueleza kila kitu alichomueleza Agrey,Lucy akaanza kumwaga machozi “Lucy usilie tafadhali.Nimekuita hapa ili tushirikiane katika kutoa maamuzi nini kifanyike.Mathewamenieleza historia yake amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na ameomba atusaidie katika kumtafuta Olivia.Nilisita kumruhusu afanye hivyo kwa kuwa tayari jeshi la polisi wanalishughulia hili suala hivyo nikaogopa kusitokee mgongano katika uchunguzi” akasema Agrey “Agrey are you out of your mind? Mtoto wetu ametekwa na watu wasiojulikana na hatujui mpaka sasa hivi yuko wapi.Amekuja mtu mwenye taarifa nyeti kama hii ambayo inaweza ikasaidia kumpata mwanetu halafu hutaki kumpa ushirikiano!! Akafoka Lucy “Lucy si kwamba sitaki kumpa ushirikiano ninaogopa kuleta mgongano kwani tayari jeshi la polisi wanalishughulikia suala hili.Nimekuita hapa ili tujadiliane tuone nini cha kufanya” akasema Agrey “Agrey hupaswi kuweka mjadala katika suala hili.Kwa hapa tulipofika tunahitaji msaada wa kila aina kumpata Olivia.Hata kama jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi bado haizuii na sisi kuendelea na jitihada nyingine za kumtafuta Olivia.Hatuwezi kukaa na kulitegemea jeshi la polisi peke yake.We need to do something! Mungu amemleta huyu kijana ambaye ameacha shughuli zake zote na kuamua kutusaidia kumtafuta Olivia,lazima tumpe ushirikiano mkubwa” akasema Lucy “Mathewtunakusikiliza wewe una ushauri gani?akauliza Agrey “Kilichonileta hapa kuzungumza nanyi ni kuomba mnipe ruhusa ya kumtafuta Olivia.Nina uhakika mkubwa nitampata.Ninao uzoefu mkubwa sana katika masuala haya ndiyo maana nina uhakika wa kumpata Olivia na tayari ninayosehemu ya kuanzia.Naombeni wazee wangu mnikubalie niweze kumtafuta Olivia.Ninakuondoa hofu mzee wangu kwamba uchunguzi wangu hautaweza kuleta mgongano wowote au kuingilia uchunguzi wa jeshi la polisi.Ningeweza kufanya uchunguzi huu kimya kimya bila kumtaarifu mtu yeyote lakini nimeona haitakuwa vyema kufanya hivyo bila kupata Baraka zenu.Nafahamu si jambo jepesi,ni jambo la hatari sana lakini niko tayari kulifanya na nitahakikisha Olivia anapatikana” akasema Mathew “Mathewninatamani sana kusema nenda kamtafute Olivia lakini ninasita kukutuma uende huko peke yako Mathew.Nashauri taarifa hii tuwape jeshi la polisi wakaifanyie kazi,wao wana nguvu kubwa kuliko ukiwa peke yako”akasema Agrey “Mzee laiti ungenifahamu hata kidogo usingekuwa na hofu nami.Ninapoamua kuingia katika kazi hizi siogopi kitu.Hata hao waliomteka Olivia kama wananifahamu na wakasikia kwamba MathewMulumbi anajiandaa kumsaka Olivia mioyo yao itabadili mapigo wataingiwa na hofu kubwa kwa sababu wanajua ziraili ameanza kazi yake.Siogopi chochote mzee wangu kwa ajili ya Olivia.Ninaomba mnipe ruhusa niende nikaanze kazi usiku huu” akasema Mathew “Mathewhakuna mjadala katika suala hili.Tunahitaji sana msaada wako kumtafuta Olivia.Ninakupa Baraka zote kijana wangu nenda kamtafute Olivia.Tumia kila aina ya uwezo ulio nao kuhakikisha unasaidia kumpata mwanangu” akasema Lucy Themba mama yake Olivia.Agrey Themba alitaka kusema kitu mke wake akamzuia “Agrey nimekwisha toa Baraka zangu Mathewakasaidie kumtafuta Olivia sitaki maelezo zaidi.Mathewunaweza kwenda baba kama kuna tatizo lolote utalipata chukua namba yangu hii ya simu utawasiliana nami.Mimi ndiye nina uchungu mkubwa kwa mwanangu kupotea hivyo siwezi kukataa msaada wako Mathew” akasema Lucy Themba na kumpatia Mathewnamba zake za simu “Mzee ninaondoka tutaendelea kuwasiliana.Kila nitakachokipata nitawasiliana nanyi” akasema Mathewna kupiga hatua ndefu hadi katika gari lake akaondoka “Lucy sijafurahishywa na hiki ulichokifanya” akasema Agrey baada ya Mathewkuondoka “Sihitaji mjadala wowote katika suala hili Agrey na kama umechukia mimi sijali kwani ninachohitaji ni mwanangu apatikane.Kijana amekuja na anazo taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa Olivia kwa nini tusimpe nafasi ya kusaidia na isitoshe ni mpelelezi anazo mbinu nyingi za kuweza kusaidia kumpata Olivia.Kwa nini unakuwa na wasi wasi katika suala hili?Nashindwa kukuelewa Agrey” akasema Lucy “Lucy wote tuna uchungu mkubwa kwa tukio la leo lakini tunapaswa tuwe makini sana katika hatua tunazozichukua kwani nyingine zinaweza kusababisha madhara badala ya kuwa msaada kwetu.Jeshi la polisi hivi sasa wako kazini wakimtafuta Olivia.Wanakwamba lazima mwanao atapatikana.Msihi pia Lucy asiwe na wasi wasi,jeshi la polisi wako kazini na wanaendelea kufanya kila waliwezalo kuhakikisha kwamba wanampata Olivia.Mimi bado siamini kama jeshi la polisi wanaweza wakashindwa kumpata Olivia.Mtandao wao ni mkubwa sana na nguvu kubwa kwa sasa wameielekeza katika suala hili hivyo ninawatoa wasiwasi kwamba Olivia lazima atapatikana.Tuendelee kushikamana.Kama mtapata taarifa zozote zinazoweza kusaidia katika uchunguzi huu tuzifikishe haraka kwa jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi”akasema Dr Evans “Nimekuelewa Evans na ninakushukuru sana kwa kuweka uzito mkubwa katika suala hili.Nina imani kubwa na jeshi la polisi chini ya maelekezo yako kwamba Olivia atapatikana” akasema Agrey “Agrey nitaendelea kuwasiliana nawe na kukujulisha kila nitakachokuwa ninakipata kutoka kwa jeshi la polisi” akasema Dr Evans wakaagana “Agrey amenistua sana.Hili suala la Olivia litanipasua moyo wangu” akawaza Dr Evans na kuweka mkono kifuani mahala unakokaa moyo.Mapigo ya moyo wake yalibadilika na kwenda kwa kasi kubwa. “Siri imegundulika” akawaza “Yote ambayo huyo Mathewamemueleza Agrey ni ya kweli kabisa.Ni kweli Olivia yuko kitalu 7 Kigamboni.Maelezo niliyoyapata kutoka kwa Devotha ni kwamba walimtaka Olivia awape namba za Sayid Omar ambaye amekuwa akiwasiliana naye mara kwa mara na akawapa namba zile ambazo walipozipiga mfumo wote ukajifunga.Kompyuta zote zikazima na hakuna kilichoendelea hadi sasa.Kumbe namba zile Olivia alipewa na Mathew.Who is this MathewMulumbi?akajiuliza Dr Evans “Kwa kuwa tayari amekwisha fahamu mahala alipo Olivia hatua za haraka sana zinatakiwa kuchukuliwa ama sivyo mpango wetu utaharibika.Kwanza kabisa Olivia anatakiwa aondolewe haraka sana mahala pale na jambo la pili ni kuhakikisha kwamba huyo Mathewanapatikana kwa sababu tayari ni mtu hatari kwetu.Hiki ni kirusi hatari ambacho kinatakiwa kudhibitiwa haraka mno” akawaza Dr Evans na kuzitafuta namba za simu za Devotha Adolph akampigia “Mr president” akasema Devotha “Devotha uko wapi? “Niko hapa kitalu 7 mheshimiwa rais” “Devotha we have a big problem”akasema DrEvans “Tatizo gani mheshimiwa rais? “Nitakueleza lakini kwa sasa kuna mambo nataka ufanye kwa haraka.Kwanza kabisa nataka Twiga atolewe kitalu 7 na apelekwe kitalu 2 ambako ni salama zaidi”akasema Dr Evans “Kuna tatizo gani mheshimiwa rais?Kwa nini tumuhamishe?akauliza Devotha “Nisikilize Devotha na utekeleze kile ninachokuagiza.Hakikisha sasa hivi Twiga anaondolewa hapo kitalu 7 na kupelekwa kitalu 2.Peleka timu P3 unit hapo kitalu 7 wakalinde na wahakikishe kwamba hakuna mtu yeyote anayeingia mle ndani.Yeyote atakayekaribia eneo hilo akamatwe haraka sana.Nataka kila kitu kiondolewe hapo kitalu 7 na nyumba ibaki tupu.Tekeleza hayo yote haraka sana.Nitaonana nawe usiku huu kukueleza kuna nini kinaendelea”akasema Dr Evans na kukata simu “Natakiwa kuonana na daktari wangu naona mabadiliko makubwa ya kiafya.Hili suala la Olivia limeniletea matatizo makubwa” akawaza Dr Evans na jina la Mathewlikamjia kichwani “Who is this guy !! Is he real or a ghost? Huyu amekuja kuharibu kila kitu na anatakiwa adhibitiwe haraka sana kabla hajaharibu kila kitu.Kwa maelezo aliyonipa Agrey inaonekana Mathewanafahamu alipo Olivia lakini hajui anashikiliwa na akina nani ndiyo maana anataka kuchunguza.Naomba iwe hivyo asifahamu chochote” akawaza Dr Evans na kuchukua simu akazitafuta namba za mkurugenzi wa idara ya ujasusi akampigia “Mheshimiwa rais”akasema mkurugenzi wa idara ya ujasusi baada ya kupokea simu ya rais “Jacob habari za usiku huu” “Nzuri kabisa mheshimiwa rais” “Jacob nahitaji msaada.Nataka upitie katika kumbu kumbu za watu waliowahi kufanya kazi katika idara yako na angalia kama kuna mtu anaitwa MathewMulumbi” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa rais.Unahitaji jibu kwa usiku huu? “Now ! akasema Dr Evans kwa saui ya juu “I need the answer now!! Akasisitiza “Naomba dakika chache mheshimiwa rais” akasema Jacob silele mkurugenzi wa idara ya ujasusi Baada ya dakika tatu Jacob akapiga simu “Niambie Jacob” “Mheshimiwa rais nimezipata taarifa hizo.Ni kweli kuna mtu aliwahi kufanya kazi katika idara yetu ya ujasusi anaitwa MathewMulumbi” akasema Jacob.Dr Evans akashusha pumzi akatafakari kwa sekunde chache na kusema “Nataka unitumie faili lenye taarifa zake sasa hivi katika barua pepe yangu sasa hivi” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa rais”akasema Jacob “Damn ! akasema Dr Evans kwa hasira.Tayari walikwisha ingia ikulu gari likasimama akashuka haraka haraka na kuelekea ndani moja kwa moja katika ofisi yake ndogo akawasha kompyuta yake na kuanza kulipitia faili alilotumiwa lenye taarifa za MathewMulumbi.Kadiri alivyoendelea kusoma taarifa za MathewMulumbi ndivyo alivyoendelea kuhisi baridi.Alimaliza kulipitia faili lile akajiegemeza kitini.Kichwa kilibeba mzigo wa mawazo. “MathewMulumbi !! akasema “Taarifa zake zinatisha.Ni mmoja kati ya majasusi mahiri kabisa kuwahi kutokea nchini mwetu.Nimepitia misheni zote alizozifanya na zote amezikamilisha vyema kwa umahiri mkubwa sana.Mambo yaliyomo katika faili hili ni mazito kabisa” akawaza Dr Evans “Imeibuka vita mpya.Huyu mtu aliyejitokeza naweza kusema ni jeshi la mtu mmoja kutokana na uwezo wake mkubwa.Tunatakiwa kupambana naye kwa umakini mkubwa sana kwani huyu jamaa amekusudia kumtafuta Olivia na anaweza akampata kutokana na uwezo mkubwa alio nao” akawaza Dr Evans na kumpigia simu Devotha “Devotha zoezi linakwendaje?akauliza “Kwa sasa tunamuondoa Twiga hapa kitalu 7 kuelekea kitalu 2 na tayari timu P3 Unit wako njiani wanakuja hapa kuimarisha ulinzi kama ulivyoelekeza” akasema Devotha “Good.Naomba baada ya kutoka kitalu 2 njoo hapa ikulu moja kwa moja kuna masuala muhimu sana ya kuzungumza” akasema Dr Evans na kukata simu “Hili suala la Olivia linazidi kuwa kubwa.Kabla hatujapata majibu kutoka kwa Olivia kuhusiana na ukaribu wake na kikundi cha IS ambao ameibuka MathewMulumbi ambaye ni tatizo kubwa pia.Mathewamedhamiria kumkomboa Olivia kutoka katika mikono ya watekaji na tayari anafahamu mahala alipo.Je anafahamu kama ni serikali ndio tunaomshikilia Olivia?Anafahamu kama Olivia ana ukaribu na watu wa IS? Naye pia ni mmoja wao? Dr Evans akajiuliza maswali “Nashukuru kwa Agrey kunipa taarifa mapema kuhusiana na Mathewna baada ya kufahamu uwepo wake kinachofuata sasa ni kupambana naye.Hatampata Olivia tena kwani mahala alikopelekwa si rahisi kupafikia.Wakati tukiendelea na suala la Olivia tutaendelea pia kushughulika naye.Tutaelekeza nguvu kubwa kumsaka na kuhakikisha anapatikana.Hawezi kunishinda mtu mmoja” akawaza Dr Evans.
“Pamoja na kumueleza kwamba ninafahamu mahala alipo Olivia lakini Agrey bado hajaonekana kunikubali.Hakuniamini au kuna tatizo lingine? Hainiingii akilini kwa mtu ambaye mwanae ametekwa na anatokea mtu ambaye anajitolea maisha yake kumsaidia kumtafutamwanae lakini bado inakuwa na ukakasi kumkubali afanye hivyo.Hata mke wake amemshangaa sana kwa namna alivyokuwa anasita.Agekuwa si baba yake mzazi Olivia ningehisi labda anahusika katika suala hili kwa sababu nilitegemea angefurahi sana kupata taarifa za kufuruhisha kuhusu mwanae.Namshukuru mama yake Olivia kwa kutokuwa na mashaka yoyote nami na kunipa ruhusa nikamtafute mwanae.Niache kumuwaza yule mzee nijielekeze katika jukumu kubwa lililoko mbele yangu” akawaza Mathewbaada ya kuondoka nyumbani kwa wazazi wa Olivia “Watu ninaokwenda kukabiliana nao si watu wa kufanyia mchezo.Wamejiandaa kikamilifu na wana uwezo mkubwa sana hivyo basi natakiwa kujiandaa kwa silaha na zana mbali mbali za kunisaida kuikamilisha kazi yangu.Kwa muda mrefu sijashiriki purukushani zozote na sikuwa nimejiwekea akiba ya silaha.Kuna ulazima wa kuwa na silaha za kutosha ndani kwani sijui ni muda gani nitajikuta katika tukio” akawaza Mathew Kabla ya kwenda nyumbani kwake akaelekea eneo la Manziki katika nyumba ambayo ukuta wa kuizunguka ulikuwa unaendelea kujengwa.Akachukua simu akafungua sehemu ya kuhifadhi namba za simu akatafuta jina limeandikwa Tino akapiga “Mathew” akasema jamaa wa upande wa pili “Kaka vipi?akauliza Mathew “Mathewamani ipo mdogo wangu? Simu yako imenistua kidogo” akasema Yule jamaa “Samahani kwa kukustua.Niko hapa nje ya nyumba yako.Upo ndani? “Acha utani Mathew.Umefikaje bila kunipa taarifa?akauliza Tino “Nimelazimika kuja kimyakimya.Naomba tuonane tafadhali nina shida Tino”akasema Mathewna mlango ukafunguliwa akatoka jamaa mmoja aliyevaa kaptura na fulana iliyokatwa mikono.Alikuwa ni kipande cha mtu aliyejazia vyema.Mikono yake ilichorwa michoro mbali mbali.Mathewakawasha taa za gari na yule jamaa akamfuata wakasalimiana “Sipendezwi na ujio kama huu Mathew.Namba zangu unazo kwa nini hukunijulisha kama unakuja?akauliza Tino “I’m sorry brother,it won’t happen again” akasema Mathew.Tino akamuangalia kwa makini halafu akasema “Karibu ndani” Wakaelekea sebuleni “Tatizo gani limekuleta usiku huu Mathew?akauliza Tino “Tino ninahitaji silaha.Kuna kazi ya dharura imejitokeza” akasema Mathew “Hauweki akiba ya silaha siku hizi? “Hapana sina akiba zaidiya bastora chache na vifaa vingine vidogo vidogo” “Mathewninataka kuachana na biashara hii kwani hivi majuzi imetaka kuniletea matatizo makubwa.Kuna watu niliwapa silaha wakaenda kufanya kazi na kwa bahati mbaya mmoja wao akauawa na silaha ile ikapatikana.Kama nisingekuwa na mtandao mkubwa hivi sasa ningekuwa ndani.Ninafikiria kuachana na biashara hii ya ukodishaji na uuzaji wa silaha.Itaniletea matatizo siku moja.Nitakuja kwako nikuone tuzungumze unielekeze biashara nyingine ninayoweza kufanya ikanipatia fedha badala ya hii” akasema Tino “Usihofu Tino kama unataka kubadili biashara mimi niko tayari na nitakusaidia kimawazo na hata kifedha kama itahitajika.Tutazungumza hayo siku nyingine lakini kwa usiku wa leo nina haraka kidogo”akasema Mathew “Tatizo gani limetokea Mathew? Akauliza Tino “Umesikia kuhusu tukio lililotokea leo la kutekwa kwa yule daktari?akauliza Mathew “Ndiyo nimesikia kuna daktari ametekwa kwa namna yake” akasema Tino “Anaitwa Dr Olivia ni mtu wangu wa karibu sana.Nilipata taarifa hizo nikiwa Arusha ikanilazimu kuondoka mkutanoni kuja Dar es salaam kumtafuta.Tino najua wewe ni mtu mwenye kupata taarifa nyingi za mambo mengi yanayoendelea hapa jijini.Una tetesi zozote za watu waliofanya kitendo kile?akauliza Mathewna Tino akatikisa kichwa “Hapana sina taarifa zozote za kuhusiana na tukio hili.Kwa namna lilivyotokea lazima limefanywa na watu wataalamu sana.Waliofanya tukio lile lazima watakuwa ni watu wenye taaluma kama yako.Nilipigiwa simu na kamanda wa polisi Dar es salaam naye aliniuliza kama nina tetesi zozote kuhusiana na tukio lile.Hata polisi wenyewe linawaumiza vichwa sana namna tukio lile lilivyoratibiwa.Kuna taarifa gani mpaka sasa? Ameshapatikana?akauliza Tino “Mpaka sasa hakuna taarifa zozote na bado Olivia hajapatikana” akasema Mathewna Tino akamtaka amfuate wakaenda katika chumba kimoja kilichojificha ambacho ili kuingia ililazimu kupita katika mtambo maalum ambao ulimtambua Tino ndipo milango ilipofunguka. “Sijawahi kumuingiza mtu katika chumba hiki kwani nimehifadhi mzigo mzito ambao huuza nje kwa vikundi vya waasi nk.Silaha ipi unadhani inaweza kukufaa?akauliza Tino. “Wow ! akasema Mathewkwa mshangao baada ya kuingia katika chumba kile kilichosheheni silaha mbali mbali. “Nitachukua hii Uzi sub machine gun kwa sababu ya wepesi wake.Ziko ngapi hizi? Akauliza Mathew “Hizi ziko nne” “Basi nitachukua mbili” akasema Mathewna kuikagua bunduki ile na kuiweka pembeni. “Desert eagle Mark XIX pistol.Hii bastora ni hatari sana,hizi nitachukua tatu” akasema Mathewna kuziweka pembeni. “AS50 Snipe rifle.Nitachukua na hii pia” Mathewakakusanya silaha na vifaa ambavyo aliona vingemfaa kwa kazi yake akaelewana na Tino kuhusu malipo kisha wakapakia silaha zile katika gari akaondoka “Tino anawezaje kuingiza nchini silaha nzito kama hizi?Chumba kile kimejaa silaha nzito nzito.Ninaungana naye katika mpango wake wa kuachana na biashara hii ya kuuza silaha.Si biashara nzuri kwani silaha anazouza zinakwenda kuua watu wasio na hatia.Hata hivyo ninamshukuru kwa kunipatia silaha hizi nzito ambazo zitanisaidia mno.Watu ninaokwenda kukabiliana nao wamejiandaa kwa silaha nzito na mimi siwezi kwenda nikiwa na silaha nyepesi lazima niende nikiwa nimekamilika” akawaza Mathewbaada ya kuondoka kwa Tino Aliwasili nyumbani kwake akashusha mizigo yake ya silaha na kwenda kuzihifadhi katika chumba chake maalum cha kuhifadhia zana na silaha. “Sehemu moja ya maandalizi imekamilika kinachofuata sasa ni sehemu ya pili nayo ni kuifahamu vyema sehemu yenyewe alipo Olivia.Hatua hii lazima niwasiliane na Ruby ambaye atanisaidia kupafahamu mahala hapo” akawaza Mathewna kuchukua simu akampigia Ruby aliyeko nchini Uingereza.Simu ikapokelewa “Mathew” akasema Ruby “Ruby habari yako? Siku ya nne leo hatujawasiliana.Vipi maendeleo yako?akauliza Mathew “Ninaendelea vyema lakini nimetoka kidogo nje ya London nimekuja kuwapa pole familia ya mmoja wa marafiki zangu aliyefariki kwa ajali ya gari.Vipi wewe unaendeleaje?akauliza Ruby “Mimi ninaendelea vizuri.Ruby japokuwa uko mwenye majonzi ya kuondokewa na rafiki yako lakini nina tatizo ninahitaji msaada wako” akasema Mathew “Umeingia kwenye tatizo gani safari hii Mathew?Ruby akauliza “Unakumbuka ile program uliyonipa ya kupata taarifa kama mmoja wa watu wangu yuko katika hatari? “Ndiyo ninaikumbuka Mathew.Kuna mtu yuko kwenye hatari?akauliza Ruby “Ninaye mtu wangu wa karibu sana ni daktari anaitwa OIivia aliwahi kunidokeza kwamba yuko katika hatari nikampa namba apige pindi akiwa katika hatari.Leo nikiwa Arusha nikapokea ujumbe kutoka katika namba zile na baada ya kufuatilia nikapata taarifa kwamba ametekwa na watu wasiojulikana ikanilazimu kuondoka haraka kurejea Dar es salaam.Program inanionyesha kwamba ujumbe ule ulitumwa kutokea eneo Fulani Kigamboni.Ninajiandaa kuelekea huko ninataka unisaidie kulifahamu vyema eneo hilo kabla sijaenda huko usiku huu” akasema Mathew “Sijatembea na kompyuta yangu leo ndiyo maana sijaupata ujumbe huo kwani kwa namna nilivyotengeneza program ile ni kwamba namba utakayompa mtu ikipigwa wewe utapata ujumbe na mimi pia nitapata ujumbe.Kwa ufupi tu ni kwamba namba zile ni kirusi ambacho kitafanya kazi ya kuiba taarifa na kuzituma kwangu.Ninaamini katika kompyuta yangu kutakuwa na taarifa za kutosha kuhusiana na mahala hapo alipo huyo rafiki yako Olivia.Kwa kuwa niko mbali na nyumbani ngoja nijaribu kutafuta kompyuta yoyote hapa karibu ili nione namna ya kufanya” akasema Ruby na baada ya dakika sita akapiga “Mathewtayari nimepata kompyuta nitakuomba uwe karibu na kompyuta yako kuna vitu ninataka kuvifahamu kutoka katika ujumbe uliotumiwa” akasema Ruby na kuendelea kuwasiliana na Mathew.Baada ya kupata taarifa alizozihitaji Ruby akaomba apewe muda kidogo azifanyie kazi.Wakati Ruby akiendelea kuzifanyia kazi taarifa zile Mathewaliendelea kujiandaa.Zilipita dakika kumi na tatu Ruby akapiga simu “Mathewnimeshindwa kuona chochote mahala hapo it’s too dark.Satelaiti niliyoipata haina uwezo mkubwa sana.Kwa nini usisubiri hadi kesho niangalie namna ya kupata satelaiti nzuri ninayoweza kuitumia kupachunguza vyema mahala hapo?akauliza Ruby “Ruby ahsante sana kwa kujaribu lakini siwezi kusubiri hadi kesho_Olivia yuko katika hatari kubwa natakiwa kuhakikisha usiku huu wa leo anapatikana” akasema Mathew “Mathewsikushauri uende mahala hapo usiku huu bila kujua namna palivyo.Ingekuwa vyema uende ukiwa tayari umepata picha nzuri” “Usiogope Ruby.Lazima niende huko kumtafuta Olivia.Nitawasiliana nawe kesho au baadae nitakaporudi” akasema Mathew “Mathewsikushauri uende lakini kwa kuwa umedhamiria kwenda siwezi kukuzuia ila kuwa makini sana.Kama kutakuwa na tatizo lolote nijulishe tafadhali.Unakwenda na nani? Akauliza Ruby “Sintakuwa peke yangu nitakuwa na mbwa wangu Bravo” akasema Mathewna Ruby akapatwa na mshangao “A dog?akauliza “Yes.He’s a highly trained military dog.Ana mafunzo makubwa sana na anaweza kufanya mambo makubwa ambayo hata mwanadamu hawezi” akasema Mathewna Ruby akabaki kimya “Ruby ahsante sana,nitawasiliana nawe baadae” “Mathewkuna kitu kingine nimekigundua” “Nini Ruby? “Namba hizi zilipigwa katika simu iliyounganishwa na mfumo Fulani wa mawasiliano.Kwa sababu namba zile ni kirusi ninaamini taarifa zitakuwa zimetumwa katika kompyuta yangu.Ninaondoka sasa hivi kurejea nyumbani kwangu nikafuatilie kilichotumwa katika kompyuta yangu” “Sawa Ruby tutawasiliana baadae” akasema Mathewna kukata simu “Siwezi kulala ndani wakati Olivia hajulikani mahala alipo.Lazima nifanye kila niwezalo kuhakikisha ninafika mahala alipo” akawaza Mathewna kutoka akaenda katika nyumba iliyokuwa pembeni kidogo akafungua mlango na kuingia ndani akamtoa mbwa wake mkubwa. “Bravo tutakuwa pamoja usiku wa leo” akasema Mathewhuku akimkuna kuna Bravo shingoni.Akatoka naye na kwenda naye hadi chumbani kwake akamfunga mkanda shingoni.Mkanda ule ulikuwa na kifaa maalum kabisa kumuwezesha Mathewkumuona gizani. “Olivia alifanya jambo zuri kuweka baadhi ya nguo zake huku kwa ajili ya kubadilisha siku akiamua kulala huku kwangu” akawaza Mathewna kufungua kabati la nguo akatoa nguo chache za Olivia akaziweka katika begi dogo halafu akaingia katika chumba cha silaha akazibeba na kuzipeleka garini “Bravo it’s time.Let’s go to find Olivia” akasema Mathewna kumpakia Bravo ndani ya gari wakaondoka **************** Magari matatu yaliwasili katika nyumba alimokuwa amehifadhiwa Olivia ambayo ni moja ya nyumba ambayo hutumiwa na idara ya siri ya usalama wa taifa(SNSA)Watu wapatao kumi na nne wakashuka kutoka ndani ya magari yale wote wakiwa na bunduki nzito na mavazi meusi.Kaiza ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa idara hii akawapokea na kwenda nao sebuleni “Ahsanteni sana P3 Unit kwa kufika kwa haraka.Tumepokea taarifa usiku huu kwamba kuna hatari ya usalama mahala hapa hivyo tunataka kuhakikisha panakuwa salama ndiyo maana mkaitwa haraka.Jukumu lenu ni kuhakikisha kwamba mahala hapa panakuwa salama na yeyote atakayethubutu kutaka kujaribu kuingia mahala hapa hakikisheni mnamtia mikononi haraka sana.Mtaendelea kupokea maelekezo mengine kadiri muda unavyokwenda lakini kwa sasa maelekezo yaliyopo ni hayo” akasema Kaiza “Narudia tena kusisitiza kwamba hakikisheni hakuna mtu au watu watakaoingia humu ndani na yeyote atakayethubutu mtieni mikononi haraka sana.Hakuna kuua bali hakikisheni mnamtia mikononi”akasema Kaiza na kikundi kile cha walinzi wakatoka kwenda kuanza majukumu yao ya kulinda nyumba ile.Taa za nje za nyumba ile zote zikazimwa kukawa giza ili waweze kupata nafasi nzuri ya kujiicha.Kutokana na mavazi meuzi waliyoyavaa haikuwa rahisi kuonekana katika giza.Wakati nyumba ile ikiwa imezungukwa na P3 unit ndani ya nyumba vifaa vyote vilivyokuwamo viliendelea kupakiwa katika gari.Kompyuta zote na mitambo yote iliyokuwamo viliondolewa ndani ya muda mfupi na kupakiwa garini.Kaiza ambaye ndiye aliyesimamia zoezi lile alihakikisha kila kitu kimekwenda kama ilivyotakiwa akawataka vijana wote waingie katika magari na kuondoka “Jamani sisi tunaondoka.The house is all yours now” Kaiza akamwambia mkuu wa kikosi kile wakati wakitoka “Nini kimetokea hadi mambo yakabadilika ghafla namna hii?Kuna mtu tayari amekwisha gundua kinachoendelea hapa? Mpaka rais atoe taarifa ile ya haraka lazima kuna tatizo kubwa.Naamini Devotha atanieleza kila kitu” akawaza Kaiza baada ya kuondoka kitalu 7. ***************** Devotha Adolph aliwasili ikulu kama alivyotakiwa na rais.Alimkuta Dr Evans akiwa ni mwenye mawazo mengi. “Karibu sana Devotha.Kabla ya yote nataka kwanza nipate taarifa kila kitu kimekwenda kama nilivyoelekeza? Akauliza Dr Evans “Ndiyo mheshimiwa rais kila kitu kimekwenda kama ulivyoelekeza.Olivia tumemuhamisha kutoka kitalu 7 na kumpeleka kitalu 2.Muda mfupi uliopita nimewasiliana na Kaiza akaniambia kwamba kazi ya kuondoa vifaa kitalu 7 imekamilika na kila kitu kimeondolewa.P3 Unit tayari wamekwisha fika pale na ulinzi umeimarishwa” akasema Devotha na Dr Evans akashusha pumzi na kusema. “Ahsante sana kwa kutekeleza maelekezo kwa haraka” akasema Dr Evans “Kuna kitu gani kimetokea mheshimiwa rais? Kila mtu amebaki katika mshangao kwa maagizo yako ya ghafla” akasema Devotha.Dr Evans akamfungulia faili la MathewMulumbi katika kompyuta yake na kumtaka asome. “MathewMulumbi..who is he?akauliza Devotha akionyesha wasiwasi kidogo “Read” akasema Dr Evans. Wakati Devotha akiendelea kusoma faili lile la Mathew,DrEvans akatoka nje ya kile chumba na kumpigia simu Dr Mbeula “Mheshimiwa rais” akasema Dr Mbeula “Dr Mbeula nataka kujua zoezi linakwendaje?akauliza Dr Evans “Tunaendelea na zoezi la vipimo.Tutakapokamilisha nitakujulisha” “Coletha yuko wapi kwa sasa? “Anapumzika katika mojawapo ya chumba cha watu maalum.Usihofu mheshimiwa rais tunamuangalia vyema” “Ahsante sana Dr Mbeula.Naomba pindi mtakapokamilisha uchunguzi wenu unijulishe tafadhali” akasema Dr Evans “Nitakujulisha mheshimiwa rais”akasema Dr Mbeula wakaagana.Dr Evans akampigia simu mkuu wa jeshi la polisi “IGP nataka kujua zoezi la kumtafuta Olivia limefikia wapi?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais zoezi linaendelea.Vijana wangu wako kazini hakuna kulala”akasema mkuu wa jeshi la polisi “Kuna hatua yoyote imepigwa hadi sasa? Kuna viashiria vyovyote vya matumaini ya kumpata Olivia? “Mheshimiwa rais mpaka sasa bado hakuna viashiria vyovyote kutuonyesha mahala alipo Olivia lakini kwa mwendo tunaokwenda nao nina uhakika si muda mrefu sana tutafika mahala pazuri.Watu hawa waliofanya mchezo ule nao pia ni wataalamu wazuri na walifahamu kwamba nguvu kubwa itatumika kumtafuta Olivia na wakajiandaa kikamilifu lakini mheshimiwa rais tutahakikisha hadi kufikia kesho tunakuwa tayari na mwangaza mkubwa wa suala hili”akasema mkuu wa jeshi la polisi “Nafahamu juhudi zenu ninaomba muongeze nguvu zaidi ili Olivia aweze kupatikana.Nina imani kubwa sana na jeshi la polisi hata wananchi pia wana imani kubwa mno na jeshi lao na sote tunaamini kwamba mtafanikiwa kumpata Olivia akiwa salama.Endelea kuwasiliana nami kunijulisha kila hatua mtakayokuwa mnapiga” akasema Dr Evans na kuagana na mkuu wa jeshi la polisi akarejea ndani alikomuacha Devotha akipitia faili la MathewMulumbi “Umemaliza?akamuuliza “Nimemaliza kulisoma.Faili linaonyesha amewahi kufanya kazi katika idaraya ujasusi Tanzania na ni mmoja wa majasusi mahiri kabisa aliyewahi kutokea nchini.Kwa nini umenipa nisome taarifa hizi?akauliza Devotha “Mapema usiku huu nimepokea simu kutoka kwa Agrey Themba baba yake Olivia akinifahamisha kwamba amepata mgeni usiku huu nyumbani kwake ambaye amejitambulisha kama MathewMulumbi.Amedai kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa Olivia na alikwenda pale ili kuwaomba wamruhusu aweze kusaidia katika zoezi la kumtafuta Olivia kwani anafahamu mahala alipo” Sura ya Devotha ikaonyesha mstuko “Anajua mahala alipo Olivia?Amejuaje?akauliza “Yeye ndiye aliyempa Olivia zile namba ambazo aliwadanganya kwamba ni za Sayid Omar na ambazo zilifunga mifumo yetu” Devotha na Dr Evans wakabaki wanatazamana “is that true?akauliza Devotha “Yes it is true.Mathewndiye aliyempa Olivia zile namba maalum kwa lengo la kumjulisha pale atakapokuwa ameingia katika hatari hivyo basi mara tu baada ya kupiga namba zile Mathewalitambua mara moja kwamba Olivia yuko katika hatari na akalazimika kuondoka Arusha kurejea Dar es salaam haraka sana kumtafuta.Kibaya zaidi tayari anayo ramani inayoonyesha mahala alipo Olivia ambako ni kitalu 7 Kigamboni” akasema Dr Evans “This man.Where is he now?akauliza Devotha “Kwa sasa sifahamu yuko wapi lakini alipotoka nyumbani kwa Agrey alikuwa anajipanga kwenda kitalu 7 Kigamboni kumkomboa Olivia” “Nimestuka sana mheshimiwa rais.Unadhani huyu jamaa tayari anafahamu kuhusu sisi? “Kwa maelezo aliyonipa Agrey inaonekana bado hafahamu chochote kuhusu nani waliomteka Olivia na anajiandaa kuanza kufanya uchunguzi.Kama angekuwa anafahamu kwamba ni sisi ndio tuliomteka Olivia angekwisha mueleza Agrey” akasema Dr Evans na ukimya ukapita “Mathewamedhamiria kumtafuta Olivia na tayari anao mwongozo ukimuelekeza mahala alipo Olivia na ndiyo maana nikachukua hatua ile ya kumuhamisha kwanza Olivia kutoka mahala pale na kumpeleka sehemu nyingine pili kuweka kikosi maalum kwa ajili ya kumsubiri Mathewambaye naamini lazima atakwenda hapo kumfuata Olivia.Hajui kama tayari tumekwishapata taarifa zake hivyo atakwenda akijiamini kwamba hakuna anayemfahamu na hiyo ni nzuri kwetu kwani tutamchukua kwa kumstukiza.Sitaki auawe bali nataka achukuliwe akiwa mzima ahojiwe na kufahamu watu wengine wanaoshirikiana nao.Kumbuka Olivia ana mawasiliano na watu wa IS hivyo ninahisi hata huyu Mathewanaweza akawa ni mmoja wao.Taratibu ninaanza kupata picha kwamba IS tayari wameanza kujenga mtandao wao hapa nchini na watu hawa wawili Olivia na MathewMulumbi wote ni washirika wao.Juhudi za kuufungua mfumo wetu zimefikia wapi? Akauliza Dr Evans “Mpaka sasa wataalamu wanaendelea lakini bado hawajafanikiwa.Nilimuuliza Olivia akasema kwamba amekupa wewe namba za kufungulia mfumo ule.Nilitaka kukuuliza kama kweli amekupa lakini kwa hali uliyotoka nayo niliogopa kukuuliza” akasema Devotha “Alikwambia hivyo? “Ndiyo mheshimiwa rais.Nilimtaka atupe namba za kufungua kompyuta zetu akadai kwamba amekwisha kueleza kila kitu tukuulize wewe” akasema Devotha “Yule binti ana matatizo ya akili”akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais najua ukaribu ulio nao na familia ya Olivia lakini kwa namna nilivyomchunguza anaonekana tayari amejiunga na IS.Kitendo cha kwenda Congo kukutana na Seif Almuhsin na kukuta mawasiliano kati yake na Sayid Omar vinatuonyesha wazi kwamba kuna kitu kikubwa kinaendelea kati yao.Tunachohitaji kujua ni mipango yao kama kuna kitu wanapanga kukifanya hapa nchini na vile vile kuwafahamu watu wengine ambao wako katika mtandao wa IS hapa nchini”akasema Devotha “Devotha nitakueleza jambo lakini naomba libaki kati yetu asifahamu mtu mwingine yeyote” “Sawa mheshimiwa rais” “Nilipozungumza na Olivia alikiri kwa kinywa chake kwamba alikwenda Kinshasa kukutana na Seif almuhsin” “Alikueleza ni kwa nini alikwenda kuonana na Seif? Akauliza Devotha “Alisema atanieleza sababu ya kwenda kukutana na Seif lakini kabla ya kunieleza kuna kitu alitaka nikifanye” “Alitaka ufanye nini mheshimiwa rais? “Nadhani unamkumbuka Edger Kaka” “Ndiyo ninamkumbuka si yule mbunge aliyefariki katika ajali ya gari” “Ndiyo_Olivia anadai kwamba Edger hajafariki dunia” “Hajafariki dunia?! Devotha akashangaa “Anadai hivyo.Hata mimi amenishangaza sana kwani ni yeye ambaye aliutambua mwili wake hospitali.Olivia anadai kwamba Edger hakufariki dunia katika ile ajali na kwamba serikali tulifanya mchezo ili ionekane kwamba amekufa katika ajali ya gari.Amekwenda mbali zaidi na kunitaka nimrejeshe Edger.Ili kunishinikiza nimrejeshe Edger, Olivia adai kwamba ametengeneza virusi ambavyo vinaua na mwanangu Coletha amechomwa sindano yenye virusi hivyo na kama sintamejesha Edger Kaka ndani ya siku kumi basi mwanangu atakufa lakini nikimrejesha atamtibu mwanangu” “Are you serious mr President?akauliza Devotha “Hicho ndicho alichonieleza Olivia na ndiyo sababu ya kutoka pale kama kichaa kwani kichwa changu kilivurugika kabisa” “Yule mwanamke ana matatizo ya akili mheshimiwa rais si bure.Hakupaswa kutamka maneno kama hayo.Wewe utamrejesha vipi Edger? Akauliza Devotha “Mwanzoni hata mimi niliamini hivyo kwamba ana matatizo ya akili lakini baada ya kutafakari kwa kina nikaona nisimpuuze Olivia.Aliponieleza mambo haya alionekana kumaanisha kile anachokisema” “Do you believe her?akauliza Devotha “Nimempeleka Coletha hospitali usiku huu na madaktari wanaendelea kumfanyia vipimo ili kujua kama kweli ana virusi hivyo kama Olivia alivyosema.Nimewasiliana na daktari muda mfupi uliopita bado wanaendelea na uchunguzi na watakapokamilisha atanijulisha” “Mheshimiwa rais hebu tujiulize ni miaka mitatu sasa toka alipofariki Edger,Kwanza kwa nini Olivia aibuke sasa na kudai kwamba Edger hajafa na kwamba ni serikali ndio waliofanya mchezo ule ili ionekane Edger amefariki?Mheshimiwa rais tukubali Olivia ana matatizo ya akili” “No she is not sick.Olivia ni mzima kabisa.Baada ya kutafakari sana nimegundua kwamba kuna mchezo mbaya unataka kuchezwa hapa na ninaamini mpango huu utakuwa na ufadhili kutoka nje ya nchi kutaka kuvuruga amani yetu.Wanataka kuzusha kashfa kwamba Edger hajafa na kwamba serikali ilighushi kifo chake na tunamshikilia Edger sehemu Fulani na hapa wananilenga moja kwa moja mimi.Devotha hii ni kashfa kubwa sana wanataka kuianzisha ambayo wakiipandikiza kwa wananchi watawaamini haraka sana na vurugu kubwa itazuka nchini.Edger alikuwa na watu wengi sana waliokuwa wanamuunga mkono na kama wakiaminishwa yuko hai machafuko yataibuka.Olivia anatumika tu kama chambo lakini kuna watu wakubwa wako nyuma yake” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais unadhani IS watakuwa wanahusika katika mpango huu? Devotha akauliza “Ni wazi lazima IS wanahusika sana katika mpango huu.Kwa miaka ya karibuni IS wamekuwa wakitafuta kujitanua hasa katia nchi za afrika.Tumewasikia tayari wana kambio zao katika nchi majirani zetu lakini hapa Tanzania hawajafanikiwa kuweka mizizi yao na sasa wanatafuta namna ya kuingia nchini ndiyo maana wanataka kuleta machafuko ili wapate nafasi ya kupenda na kuingia.Olivia kwa nini amekubali kutumika kiasi hiki kuibomoa nchi yake?Ameshindwa kupima athari za kinachoweza kutokea endapo uongo huu utafika kwa wananchi? Olivia amekulia katika mikono yetu sikutegemea kama siku moja angeweza kugeuka na kuwa msaliti kwa taifa lake” akasema Dr Evans “IS wana fedha nyingi na wanazitumia katika kutengeneza mtandao wao hapa nchini.Wanawapa utajiri mkubwa wale watu ambao wanataka kuwatumia.Tazama Olivia ni tajiri sana amejenga kituo kile cha utafiti ambacho kimegharimu mabilioni ya fedha ambacho naamini atakuwa amepewa fedha nyingi na IS. Tazama pia Mathewni bilionea.Ninaamini wote hawa wawili utajiri wao umetoka kwa IS ili kuwasaidia katika mipango yao hapa Tanzania” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais maelezo yako yananipa picha kwamba mapambano haya yaliyoanza ni kati yetu na IS.Hayatakuwa mapambano rahisi kwani IS ni kikundi chenye nguvu kubwa kwa sasa na kinaendelea kujitanua sehemumbali mbali duniani.”akasema Devotha “Exactly,hii ni vita kati yetu na IS.Olivia na Mathewni watu wadogo naamini kuna watu wakubwa nyuma yao.Huu ni mtandao mkubwa wapo waliomo ndani ya nchi na wapo waliopo nje ya nchi.Kazi yetu kwa sasa ni kujipanga ili kuufahamu mtandao huo unawahusisha akina nani tukianza na hawa waliomo hapa nchini.Kwa kuwa tayari tunaye Olivia na tunatarajia kumpata Mathewusiku huu hawa wawili watatusaidia sana katika kuufahamu kwa kina mtandao huu mkubwa” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais tumeyafahamu haya yote baada ya kumteka Olivia kama tusingefanya hivyo haya yote yasingejulikana.Najiuliza nini hasa ilikuwa mipango yao?Walipanga wafanye nini kuanzisha suala ili la Edger?akauliza Devotha “Nadhani walipanga wamtumie Coletha kwani tayari walikwisha mchoma sindano yenye virusi kabla hata Olivia hajatekwa.Nina uhakika mkubwa kabisa kwamba Olivia ndiye aliyeratibu mipango yote hii.Hata kama tusingemteka Olivia lazima wangetafuta namna ya kunifikishia ujumbe kwamba mwanangu atakufa hivyo nitekeleze kile wanachokihitaji.Inaniumiza sana kwa Olivia kufanya jambo kama hili.Yeye na Coletha ni kama ndugu wamekuwa wakiishi kwa upendo mkubwa sana iweje leo amfanyie hivi mwenzake?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais usiwe na hofu yawezekana hakuna virusi hivyo anavyodai Olivia yawezekana ikawa ni moja ya njia zao za kutaka kukuogopesha tu.Tusubiri majibu ya daktari kama yataonyesha ni kweli amechomwa virusi hivyo” “Devotha suala hili hakuna anayelifahamu zaidi yako.Ninataka idara yako ilishughulikie kikamilifu na kuhakikisha wahusika wote wanatiwa nguvuni.Ni suala nyeti sana kwa usalama wa nchi.Kuna kila dalili kwamba IS wanataka kuvuruga amani yetu na katu siwezi kuruhusu hilo likatokea ndiyo maana idara hii ya siri ikaundwa ambayo majukumu yake ni kuhakikisha taifa linakuwa salama.Nataka mjipange wewe na watu wako muhakikishe kwamba mnawatafuta na kuwapata watu wote ambao hawalitakii mema taifa letu.Nataka mtandao wote wa IS hapa nchini ujulikane.” “Mheshimiwa rais idara yetu ina watu wenye ujuzi na uwezo mkubwa ninakuhakikishia kwamba tutafanikiwa kuwapata watu hao.Kitu kizuri ni kwamba tayari tunaye Olivia na Mathewtutampata si muda mrefu sana.watu hawa wawili watatusaidia kuufahamu mtandao wao wote ulio hapa nchini na nje ya nchi”akasema Devotha.Ukapita ukimya wa dakika mbili Dr Evans akasema “Sifa moja ya magaidi ni kutokutoa siri kuhusiana na mitandao yao na mipango yao mbalimbali ya kigaidi.Sina hakika kama Olivia atakuwa tayari kutoa siri za watu anaoshirikiana nao au kutaja mipango yao yote hivyo basi kuna kitu ninakifikiria kukifanya ambacho kitamlazimisha aweze kusema kila kitu”
“Unafikiria tufanye nini mheshimiwa rais?akauliza Devotha “Tunatakiwa kumpata Agrey Themba baba yake Olivia” “Mheshimiwa rais ! Devotha akashangaa “Tumchukue tena na Agrey Themba?Tayari tunaye mwanae tukimchukua na yeye huoni kama tutazidi kukoroga mambo? “Hiyo ndiyo njia pekee ya kumfanya Olivia azungumze.Bila kutishia kumuua baba yake basi Olivia hataweza kusema chochote.Hii ni vita na ili tupate ushindi lazima tutumie kila mbinu kupigana.Olivia anampenda mno baba yake hivyo kama tukifanikiwa kumpata na kutishia kumuua basi atatueleza kila kitu” “Ni vipi kama hata baada ya kutishia kumuua baba yake Olivia hatakuwa tayari kusema chochote?akauliza Devotha “Agrey ni rafiki yangu wa siku nyingi sana lakini hapa tunaweka mbele maslahi ya taifa hivyo kama ikilazimika kumkata pumzi tutafanya hivyo kwani tayari urafiki wetu umekwisha ingia dosari kwa suala hili la Olivia.Katu siwezi kuwa na huruma kwa Olivia kwani yeye amekubali kutumika na magaidi na sasa familia yangu yote iko mashakani.” akasema Dr Evans na ukimya mfupi ukapita “Agrey alikuwa na wasiwasi sana na Mathewndiyo maana akanipigia kunipa taarifa zake na kunitaka nimsaidie kufanya uchunguzi kama kweli Mathewamewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi Tanzania.Nitampigia simu na kumfahamisha kwamba Mathewni kweli amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na nitamshauri tumpe nafasi Mathewya kuchunguza suala hili la Olivia.Baada ya saa moja kutoka sasa mtu mmoja kutoka idara yako atampigia simu Agrey akijifanya ni Mathew.Atazungumza kama vile yuko katika sehemu ya kujificha na atamjulisha kwamba amefanikiwa kumpata Olivia ingawa hali yake si nzuri sana hivyo atamuelekeza sehemu ya kwenda.Mtu huyo amuonye Agrey asiwasiliane na mtu yeyote yule kumueleza kuhusu suala lile.Ninaamini Agrey atafuata maelekezo hayo na atakapofika mahala alipoelekzwa na Mathewatachukuliwa na vijana wetu na huo utakuwa ni mwisho wake” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais wazo lako ni zuri lakini ..” “Agrey Themba lazima apatikane Devotha. Hakuna mjadala katika suala hilo.Bila kumpata Agrey hatutapata chochote kutoka kwa Olivia ambaye anashirikiana na magaidi hivyo kama hatutatumia nguvu kubwa hatutaweza kupata chochote kutoka kwake.Nataka operesheni ya kumchukua Agrey Themba ifanyike usiku wa leo.Kabla ya mapambazuko ya kesho tuwe tayari tumeanza kupata taarifa muhimu.Umenielewa Devotha?” akauliza Dr Evans “Niumekuelewa mheshimiwa rais” “Good.Wekeni nguvu usiku huu katika mambo haya mawili kwanza kumpata Mathewna vile vile kumpata Agrey Themba.Hakikisha unanijulisha kila kinachoendelea” akasema Dr Evans akachukua simu na kumpigia Agrey “Dr Evans” akasema Agrey Themba “Agrey nimekupigia kukupa mrejesho kuhusiana na kinachoendelea.Nimewasiliana tena na mkuu wa jeshi la polisi nchini na amenihakikishia kwamba jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi na wamefikia hatua nzuri.Yawezekana hadi asubuhi ya kesho wakawa na taarifa nzuri za kutupa.Tuendelee kuwa wavumilivu na kuwaamini” akasema Dr Evans “Nashukuru sana Dr Evans.Imani yangu kwa jeshi la polisi ni kubwa na ninaamini watafanikiwa kumpata mwanangu” akasema Agrey Themba “Agrey suala la pili uliniomba nikusaidie kufanya uchunguzi kuhusiana na MathewMulumbi.Nimewasilian a na mkurugenzi wa idara ya ujasusi Tanzania na amenitumia faili la MathewMulimbi.Nimelipitia kwa umakini ni kweli alichokisema aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi na faili lake linaonyesha kwamba ni mmoja wa majasusi wa kiwango cha juu kabisa.Baada ya kupitia faili lake nimejiridhisha kwamba ni mtu anayeweza kuwa na msaada mkubwa.Ninashauri tumuache aendelee na uchunguzi wake lakini ahakikishe kwamba uchunguzi wake hauleti mkanganyiko kati yake na jeshi la polisi.Mpe muda na nafasi ya kufanya uchunguzi wake kwa uhuru ninaamini anaweza akasaidia sana”akasema Dr Evans “Dr Evans ahsante sana kwa taarifa hizo nzuri.Nitampa nafasi kama ulivyoshauri yawezekana akawa na msaada mkubwa”akasema Agrey “Sawa Agrey nitaendelea kukupa taarifa kila pale nitakapokuwa ninazipata.” Akasema Dr Evans na kukata simu akamgeukia Devotha “Tayari nimetengeneza njia.Pale atakapopokea simu kutoka kwa mtu atakayejifanya ni MathewMulumbi hatakuwa na wasiwasi wowote lazima atafuata maelekezo atakayopewa” Akasema Dr Evans akaagana na Devotha. RIYADH - SAUDI ARABIA Saa nne za usiku magari manne yaliwasili katika makazi ya Habiba Jawad.Kabla magari yale hayajasimama wakaruka watu na kulizingira gari moja na baada ya dakika chache mlango wa lile gari ukafunguliwa akashuka jamaa mmoja mwenye ndevu nyingi aliyejifunga kilemba kichwani .Moja kwa moja akaingia ndani ya jumba lile kubwa akaelekea ndani katika chumba kilichokuwa na meza ya duara na viti zaidi ya kumi.Ndani ya chumba kile kulikuwa na watu wapatao saba “Sayid karibu sana.” akasema Habiba Jawad “Samahani sana kwa kuchelewa.Nilipata dharura iliyonichelewesha.Tayari kikao kimeanza? Akauliza Sayid “Bado hatujaanza tulikuwa tunakusubiri wewe.Tunaweza kuanza sasa.Abu wakaribishe akina Khalid” Akasema Habiba.Mbele ya chumba kile kulikuwa na luninga mbili kubwa Abu dahir akabonyeza kitufe katika kifaa cha kuwashia na luninga zile zikawaka wakaonekana watu wawili.Yalikuwa ni mazungumzo ya moja kwa moja.Habiba akarekebisa koo na kusema “Karibuni sana Khalid Radwan na Rashid.Mtatusamehe kwa kuchelewa kuanza kwa kikao hiki muhimu ni kutokana na Sayid kuchelewa kufika lakini tayari yuko hapa tunaweza kuendelea.” “Hakuna tatizo tuendelee” akasema Khalid Radwan mmoja kati ya viongozi wa juu wa kundi la IS akiwa nchini Iraq “Ndugu zangu kikubwa katika kikao hiki ni kujadili kwa kina kile kilichotokea Tanzania siku ya leo na hatima ya mipango yetu ya kumpata Seif.Taarifa tulizozipata ni kwamba,Olivia Themba ambaye amekuwa akitusaidia katika mambo mengi hasa katika operesheni ya kumtafuta Seif ametekwa nyara na watu wasiojulikana.Huyu ndiye tulimtanguliza mbele hivyo kama ametekwa mipango yetu itatetereka sana ndiyo maana nimeitisha kikao hiki ili tujadili ni namna gani mipango yetu itakavyoendelea.Karibuni sana kwa michango ya mawazo” akasema Habiba Jawad “Kwa maelezo ambayo Habiba amenipa ni kwamba Olivia ametekwa wakati akitokea Kinshasa alikoenda kuonana na Seif al muhsin.Nataka kujua mpaka sasa kuna taarifa zozote mmekwisha zipata kutoka kwa watu wetu walioko Tanzania kuhusiana na tukio hilo? Akauliza Khalid “Tumekuwa na mawasiliano na watu wetu Tanzania na kwa taarifa za mpaka jioni hii bado Olivia hajapatikana na hajulikani alipo” akajibu Sayid Omar “Mnahisi nani anahusika katika tukio hili la kumteka Olivia? Akauliza Khalid “Mpaka sasa hatujui ni nani anahusika na tukio lile lakini kwa namna lilivyotokea ni tukio lililofanywa kitaalamu sana” akasema Sayid Omar na kuelekea upande mwingine kulikokuwa na luninga nyingine kubwa. “Tumejaribu kukusanya picha kadhaa kutoka eneo la tukio.Zinazoonekana hapa ni gari mbili moja ikiwa ya Olivia na nyingine ikiwa ni ya walinzi wake.Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mashuhuda ni kwamba magari haya yalipokaribia kufika nyumbani kwa Olivia ilitokea helkopta angani na kuanza kufanya mashambulizi.Walinzi wote wa Olivia waliuawa na mara yakatokea magari mawili yaliyofika kwa kasi kubwa na kumchukua Olivia wakaondoka naye na mpaka sasa hajulikani mahala alipo.Tunajaribu kulihusisha tukio hili na yale ambayo yamewahi kutokea sehemu nyingine Afrika ambapo watu matajiri au wanafamilia wao hutekwa na kisha watekaji hudai fedha nyingi.Tunahisi kwamba lengo la watekaji hao ni kujipatia fedha”akasema Sayid Omar.Ukimya ulitawala mle ndani ya chumba kila mmoja akiwa ameyaelekeza macho yake mbele katika luninga na baada ya muda Khalid akasema “Kwa mtazamo wangu,waliomteka Olivia walifahamu alikuwa nchini Congo na walikuwa wanamfuatilia kwa karibu kila anachokifanya.Ninafahamu mbinu mbali mbali za utekaji na kwa namna tukio hili lilivyotokea ninaamini watekaji hawajafanya hivi kwa ajili ya kujipatia fedha.Hili tukio ni la kitaalamu sana na limefanywa na watu wenye taaluma kubwa” Khalid akanyamaza kwa muda kisha akasema “Naomba mkubaliane nami kuwa tukio hili limefanywa na watu wa serikali” Watu wote mle ndani wakatazamana “Ninawahakikishia ndugu zangu,kwamba huu mchezo umechezwa na serikali.Nina uzoefu mkubwa na mambo kama haya ya utekaji na ninafahamu aina mbali mbali za utekaji na kwa utekaji huu wa Olivia ninashawishika kuamini kwa asilimia mia moja kwamba serikali ya Tanzania wanahusika” akasema Khalid “Serikali ya Tanzania wana sababu yoyote ya kumteka Olivia?akauliza Habiba “Olivia ni mtu mwenye jina kubwa Tanzania,baba yake ni bilionea ni rafiki mkubwa wa rais wa Tanzania.Inasemwa kwamba urafiki wao umeanza toka wakiwa vijana hadi leo.Iweje serikali wamteke mtu kama huyu mwenye ukaribu mkubwa na rais?akauliza Abu dahir “Jibu la swali hilo ni rahisi,tayari kuna kitu wamekigundua kwa Olivia ndiyo maana wamemteka.Olivia hana sababu yoyote ya kutekwa na serikali isipokuwa kwa sababu moja tu kubwa ambayo ni kugundulika kushirikiana nasi.Ninawaambia ukweli ndugu zangu kwamba hiyo ndiyo sababu pekee iliyompelekea Olivia akatekwa.Nina uhakika mkubwa wamekuwa wakifuatilia nyendo zake kwa muda mrefu na wakagundua kila kitu kuhusu Olivia na mtandao wetu.Mmekuwa makini kwa muda mrefu na kila kitu kikaenda vyema lakini kuna mahala mlijisahau na kuachia mwanya mkasababisha Olivia akajulikana” akanyamaza na wote walikuwa kimya wakimsikiliza “Jambo la pili” akaendelea “Yawezekana Olivia alikuwa anatumiwa na serikali kuchota siri zetu na baada ya kupata siri za kutosha kabisa wakaamua kucheza mchezo ionekane kwamba Olivia ametekwa na watu wasiojulikana lengo ni kumuhifadhi sehemu kwa muda ili kushughulikia kwanza taarifa zile walizozipata” akasema Khalid.Bado chumba kiliendelea kuwa kimya wote wakimsikiliza yeye “Katika hayo mawili niliyoyaelezea moja wapo linaweza kuwa ni sababu ya kupotea kwa Olivia hata hivyo kupotea kwa Olivia si sababu ya kuturudisha nyuma na kuvuruga mipango yetu.Tunawapoteza watu wetu kila uchao na wengine ni makamanda muhimu na bado mapambano yanaendelea hivyo mipango yetu yote itaendelea kama kawaida hadi tuhakikishe Seif anapatikana lakini kutakuwa na mabadiliko kidogo.Nataka kujua je kile kirusi alichotengeneza Olivia kimekwisha tumika kama tulivyokusudia?akauliza Khalid “Ndiyo.Tayari Coletha mtoto wa rais amechomwa sindano yenye virusi”akajibu Sayid “Baada ya kuchomwa mmefuatilia kujua maendeleo yake? akauliza Khalid “Toka alipochomwa sindano ile yenye virusi Coletha hajaweza kuingia darasani tayari ameanza kuumwa na amepewa mapumziko hadi pale hali yake itakapokuwa nzuri” akasema Sayid Omar “Vizuri sana kama tayari amekwisha chomwa sindano yenye virusi .Mpango wetu wa awali ulikuwa ni kumpigia simu rais kumjulisha kwamba mwanae amechomwa sindano yenye virusi na atakufa endapo hatatupa taarifa za Edger lakini baada ya hili lililotokea leo itatulazimu kubadili mpango.Tunatakiwa kumteka huyo mtoto wa rais na kisha tutawasiliana na rais moja kwa moja na tutamuonyesha maendeleo ya mtoto wake anavyopata taabu na hii itamfanya atekeleze kila tunachokitaka.Wasiliana na watu wetu Dar es salaam waandae mpango huo haraka sana ikiwezekana usiku huu huu mtoto huyo wa rais apatikane.Wapigie simu nizungumze nao sasa hivi niwape maelekezo” akasema Khalid. Kwa kutumia simu iliyokuwa mezani Sayid Omar akampigia Fahad mmoja wa watu wao aliyepo Tanzania. “Hallo Sayid” akasema Fahad “Fahad nini kinaendelea hapo Dar es salaam?akauliza Sayid “Huku bado mambo ni vile vile.Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kupatikana Olivia” “Sawa Fahad nataka uzungumze na Khalid Radwan” akasema Sayid “Fahad unazungumza na Khalid Radwan naomba nisikilize vizuri.Kufuatia tukio la kutekwa kwa Olivia mipango yetu imebadilika.Nataka mjipange usiku huu wa leo muweze kumpata mtoto wa rais wa Tanzania.Najua nimewastukiza lakini nawaombeni mfanye kila linalowezekana usiku wa leo aweze kuchukuliwa kutoka hapo chuoni hata kama ni kwa kufanya shambulio lakini lazima huyo mtoto wa rais apatikane”akasema Khalid “Khalid kuna tatizo kidogo katika mpango huo” akasema Fahad “Kuna tatizo gani?sura ya Khalid ikabadilika “Nimepewa taarifa na Karim mtu wangu ambaye anasoma katika chuo anachosoma Coletha,rais amefika usiku huu pale chuoni na kumchukua mwanae inasemekana amempeleka hospitali”akasema Fahad “Amempeleka hospitali?Khalid akauliza “Ndiyo amempeleka hospitali kuchunguzwa afya yake” “Una uhakika na taarifa hizo Fahad? “Ndiyo.Karim ana ukaribu mkubwa na marafiki zake Coletha ambao wamempa taarifa hizo.Wanadai kwamba Coletha amepelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi wa afya yake” “Kwa nini rais amchukue Coletha usiku huu na kumpeleka hospitali kumchunguza afya yake? Akauliza Sayid “Msiumize vichwa vyenu,tayari rais amefahamu mwanae amechomwa sindano yenye virusi.Niliwaambia kwamba Olivia yuko upande wa serikali na ndiye aliyempa rais siri hii na nyingine nyingi kuhusu sisi.Baada ya rais kupewa taarifa kwamba mwanae amechomwa sindano yenye virusi amemchukua haraka na kumpeleka hospitali na huko lazima atapona kwani Olivia ndiye aliyetengeneza virusi hivyo na anafahamu tiba yake”akasema Khalid chumba kikawa kimya.Baada ya muda Sayid akasema “Kuna swali ninajiuliza,Olivia ndiye aliyetengeneza kirusi kile na angeweza kumtibu mtoto wa rais kimya kimya kwa nini basi rais amempeleka mwanae hospitali kumchunguza afya yake? akauliza Sayid Omar “Swali zuri Sayid lakini hatuwezi kupata majibu yake kwa sasa.Ukweli ni kwamba tumerudi kwenye sifuri ndugu zangu.Mipango yetu yote ya muda mrefu imeshindikana kwa sababu ya kumuamini Olivia.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kutumia nguvu kumshinikiza rais ili atupe taarifa tunazozihitaji.Bila kutumia nguvu hatutafahamu mahala alipo Seif kwani Olivia tayari amekwisha tusaliti” akasema Khalid “Khalid unashauri nini kifanyike? akauliza sema Habiba. “Sikilizeni ndugu zangu mpango wetu bado unaendelea kama kawaida na hakuna kitakachosimama.Rashid Mombasa unanisikia? “Ninakusikiliza mkuu” akasema Rashid mmoja wa viongozi wa IS aliyeko Mombasa Kenya ambaye toka kikao kilipoanza amekuwa kimya “Kwako kuna kikosi kikubwa kuliko Tanzania.Nataka uandae watu kumi usiku huu kwa ajli ya safari ya kuelekea Tanzania ambako watakutana na timu ya Fahad wataungana katika kumteka mtoto wa rais wa Tanzania.Nataka kesho kwa namna yoyote ile mtoto wa rais akachukuliwe hospitali na tukishafanikisha hilo ndipo tutakuwa na uhakika wa mipango yetu kuendelea kama tunavyotaka. Katika mambo tutakayomtaka rais wa Tanzania ayafanye ni kutukabidhi Seif pamoja na Olivia ambaye tutamkata kichwa kama adhabu ya usaliti mkubwa aliotufanyia.Rashid na Fahad mmenielewa?akauliza Khalid “Nimekuelewa Khalid.Maelekezo yako yatafanyiwa kazi haraka sana” akasema Rashid “Nimekuelewa Khalid na maandalizi yanaanza usiku huu huu” akasema Fahad kutokea Dar es salaam “Safi sana.Kumbukeni hatupaswi kushindwa vita hii na yeyote ambaye atasababisha tushindwe hii vita adhabu yake ni kukatwa kichwa.Tanzania ni muhimu sana tuipate kwani tukiipata tutakuwa tumeipata Afrika nzima hivyo kila juhudi zifanyike kuhakikisha kwamba mipango yetu yote nchini Tanzania inakwenda vizuri.Nawatakia utekelezaji mzuri wa mipango yetu” akasema Khalid na kuzima kamera.Wote mle ndani wakatazamana kwa muda kisha Habiba akasema “Nadhani nyote mmesikia maelekezo yaliyotolewa.Mikakati ianze mara moja kuitekeleza.Lazima tuhakikishe Seif anapatikana” akasema Habiba “Mimi bado nina mashaka kidogo kuhusiana na kauli ya Khalid kwamba Olivia anatumiwa na serikali.Wote humu tulionana naye alipokuja na sote ni mashahidi namna alivyokuwa tayari kusaidia katika kupatikana kwa Edger.Ni kwa sababu yake Seif yuko hai mpaka leo,alipambana dhid yal wale walijaribu kumuua kwa kumuwekea sumu na kuokoa maisha yake.Tuna uhakika kwamba Edger yuko hai leo kwa sababu yake.Bila yeye kusingejengwa kituo kile cha utafiti nchjini Tanzania ambacho kitakuwa na manufaa makubwa kwetu.Iweje leo itolewe amri ya kumkata kichwa na wote humu tunakaa kimya?akauliza Sayid kwa ukali “Sayid yuko sahihi.Sina hakika Olivia anatumiwa na serikali.Tumekwisha shirikiana naye mambo mengi hadi sasa kama angekuwa anashirikiana na serikali tusingefika hatua hii tuliyofika.Ninaweza kukubaliana na ile sababu yake ya kwanza kwamba huenda serikali ya Tanzania wamemgundua kwamba anashirikiana nasi na ndiyo maana wakamteka nyara lakini Olivia kushirikiana na serikali ya Tanzania hilo ninalikataa”akasema Habiba “Jambo lingine kama Olivia angekuwa anashirikiana na serikali asingekubali mtoto wa rais achomwe sindano yenye virusi.Angemjulisha rais mapema na angemuondoa mtoto wake lakini inaonekana rais amefahamu leo hii kwamba mwanae amechomwa sindano yenye virusi na atakuwa ameambiwa na Olivia” akasema Abu dahir “Kama Olivia amemweleza rais kwamba mwanae amechomwa sindano yenye virusi tujiulize ni kwa nini alimwambia?Aliamua kutumia njia hiyo kumshinikiza rais amueleze kuhusu Edger?akauliza Habiba “Hata mimi ninaanza kuhisi hivyo lakini hatuwezi kuwa na jibu la uhakika hadi pale Olivia atakapopatikana hivyo basi tujitahidi kumtafuta Olivia na kumpata ili tufahamu sababu za kutekwa kwake.Binafsi siko tayari kumuona Olivia anakatwa kichwa labda hadi nitakapothibitisha kweli anashirikiana na serikali hivyo basi nitahakikisha ninasimama upande wake na kunusuru maisha yake” akasema Sayid Omar “Sayid sote hapa hakuna anayetaka au kutamani kumuona Olivia akikatwa kichwa.Lazima tufanye kila linalowezekana kumuokoa na tutamuokoa pale tutakapothibitisha kwamba hashirikiani na serikali ya Tanzania ” akasema Habiba wakaendelea na mjadala wa kina kuhusiana na suala lile DAR ES SALAAM – TANZANIA Mathewaliendesha gari taratibu akiifuata ramani iliyokuwa katika kompyuta yake aliyoiweka pembeni na kwa mujibu wa ramani yake alikaribia sana kufika eneo alilokuwa anakwenda “Nimekaribia kufika eneo la tukio ninatakiwa kuhakikisha eneo lote linakuwa giza ili kuniwezesha kuingia mahala aliko Olivia bila tatizo”akawaza Mathewakiendelea kutazama nje “Eneo liko kimya watu wote wamejifungia majumbani mwao” Mathewakasimamisha gari akafungua begi lake na kutoa kitu Fulani kilichofungwa nyaya kadhaa akashuka garini akatazama pande zote kama kuna mtu lakini barabara ilikuwa tupu,kwa haraka akaenda katika nguzo ya umeme iliyokuwa pembeni ya barabara akakipachika kifaa kile katika nguzo ya umeme akakifunga na gundi halafu akarejea haraka garini na kuondoka eneo lile.Baada ya umbali mfupi akachukua kifaa mithili ya simu ya mkononi akabonyeza namba Fulani na mlipuko ukatokea katika ile nguzo aliyoweka kile kifaa na eneo lote likawa giza umeme ulikatika. “Kazi inaanzia hapa” akasema Mathewbaada ya umeme kukatika Mathewaliendelea na safari yake akiifuata ramani ile akafika katika barabara ambayo ilikuwa inaelekea mahala ambako ramani ilionyesha ndiko aliko Olivia.Aliipita barabara ile akaendelea mbele zaidi akazima gari akageuka na kumtazama mbwa wake “Bravo it’s time” akasema huku akimkuna mbwa wake shingoni.Akachukua bunduki aina ya AS50 Snipe rifle na bastora mbili akaweka kichwani miwani ya kumuwezesha kuona vyema kwenye giza halafu akaweka begi lake lenye vifaa vingine mgongoni akashuka garini akiwa na Bravo wakaanza kutembea hadi walipoikuta ile barabara inayoelekea katika nyumba aliko Olivia.Kulikuwa na maua kandoni mwa barabara ile.Mathewakiwa na bunduki yake yenye uwezo mkubwa aliambaa ambaa kandoni mwa barabara ile akiwa na mbwa wake wakijinga na miti ya maua.Alikuwa katika tahadhari kubwa.Alikaribia sana kufika katika jumba lile akamkuna kuna mbwa wake shingoni akampa maelekezo “Bravo now go ! Mathewakamuelekeza mbwa wake ambaye alitoka mbio kuelekea katika ile nyumba.Mathewaliyevaa miwani ile maalum ya kuonea kizani akaendelea kunyata huku akimfuatilia Bravo aliyekuwa amemuwekea kitu Fulani katika mkanda wake ambacho kilimuwezesha kumuona kupitia ile miwani aliyovaa. Bravo alikwenda kimya kimya hadi katika geti la nyumba ile na taratibu bila kutoa ukelele akanusa harufu ya mtu eneo lile akamsogelea jamaa mmoja aliyekuwa amejibanza kandoni mwa geti akiwa amevaa mavazi meusi.Kwa macho ya kawaida haikuwa rahisi kumtambua.Yule jamaa alistuka baada ya kumuona mbwa karibu yake.Akawasha tochi ili aweze kumtazama vyema yule mbwa.MathewMulumbi kupitia miwani yake aliweza kumuona yule jamaa vizuri na kwa kutumia bunduki yake aliyoifunga kiwambo cha kuzuia sauti akampiga risasi kati kati ya paji la uso akaanguka chini.Baada ya yule jamaahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kuanguka Bravo akaambaa na ukuta akakutana na mtu wa pili aliyekuwa amejibanza nyuma ya mti.Mathewakamuona na kumdondosha kwa risasi moja ya kichwa.Kazi kubwa ya Bravo ilikuwa ni kuwatafuta walinzi waliojificha gizani na Mathewaliweza kuwaona kirahisi na kuwamaliza kwa kutumia bunduki yake kubwa iliyofungwa kiwambo cha sauti “Hawa walinzi mbona hawaishi?akajiuliza baada ya kumuona Bravo akiendelea kuzunguka ile nyumba akimfuata mwingine baada ya kuhisi harufu ya mtu.Tayari alikwisha wakata pumzi watu nane lakini bado ilionekana wapo zaidi.Akiendelea kumfuatilia Bravo akawaona watu watano wakiwa wamekaa katika matofali wakizungumza wote wakiwa na bunduki “Kuna ulinzi mkubwa kuzunguka hii nyumba.Nadhani ulinzi huu wote ni kwa ajili ya kumlinda Olivia.Naamini OIivia yuko ndani ya nyumba hii kama ramani inavyonionyesha?akawaza Mathewna kuielekeza bunduki yake kwa wale jamaa ambao mmoja wao alistuka na kuruka baada ya kuguswa na kitu.Wenzake walianza kumcheka mwenzao baada ya kumulika tochi na kugundua kilichomstua mwenzao ni mbwa.Yule jamaa tayari alikwisha iweka sawa bunduki yake tayari kwa shambulio. “Hey hey hey..ni mbwa usiogope! Yule jamaa ambaye aliruka alipoguswa na kitu akaambiwa na mwenzake ndipo alipotulia na kumuona mbwa mkubwa akiwa karibu yao akiwaangalia “Katokea wapi huyu mbwa?akauliza mmoja wao.Wakati wakiendelea kujiuliza mmoja wao akaanguka.Wakapatwa na mstuko na kila mmoja akashika silaha yake vyema mara akaanguka wa pili na watatu.Haikujulikana sababu yakuanguka kwao mmoja kati ya wawili waliobaki akainama ili kuwatazama wenzake walioanguka ajue sababu ya kuanguka kwao akajikuta akipigwa risasi ya bega akaanguka na kutoa mguno wa maumivu.Yule mwenzake aliyebaki akaiweka sawa bunduki yake akaanza kuangaza pande zote kumtafuta mtu aliyewapiga wenzake risasi lakini hakuona mtu yeyote akamfuata yule mwenzake aliyepigwa risasi ya bega.Alikuwa anavuja damu nyingi.Haraka haraka akachukua redio ya mawasiliano na kutaka kuwajulisha wenzake lakini alipobonyeza tu Mathewakampa tiketi ya kuzimu kwa risasi moja iliyotua katikati ya paji la uso.Alibaki yule jamaa mmoja aliyepigwa risasi ya bega ambaye alikuwa anagugumia kwa maumivu.Mathewakanyata kumsogelea lakini kabla hajamfikia akatokea mtu mmoja ambaye naye alikuwa na bunduki mkononi.Akamulika tochi na kuwaona wenzake wakiwa wamelala chini wakivuja damu hawakuwa na uhai.Kwa kasi ya umeme akaitupa bunduki yake na kutoka mbio.Mathewakaachia risasi mbili lakini alichelewa kwani jamaa alikwisha potea.Akanyata kumuendea yule jamaa aliyekuwa amepigwa risasi ya bega.Yule jamaa aliweza kusikia hatua za mtu akimsogelea haraka haraka akachomoa bastora iliyofungwa kiwambo cha sauti na kujipiga risasi ya kichwa akafa pale pale. “Oh no !! Huyu alikuwa muhimu sana kwani angeweza kunipa taarifa zote kuhusiana na watu hawa” akawaza Mathewmara Bravo akatokea. “Thank you Bravo ! akasema Mathewkwa sauti ndogo. “Bravo amerejea nadhani hakuna huku nje wamekwisha.Nimewaondoa watu kumi na tatu.Ni wengi sana.Walikuwa wamejizatiti mno kiulinzi kama ningekuja kichwa kichwa nisingetoka salama eneo hili.Ulinzi huu unanipa uhakika kuwa lazima Olivia yuko ndani ya nyumba hii.Lakini watu hawa ni wenye bunduki nzito kama hizi ni akina nani? Akajiuliza na kutazama pande zote lakini hakuona mtu akaanza kutembea kwa tahadhari kurejea getini.Mlango wa pembeni ya geti haukuwa umefungwa akausukuma ukafunguka. “Sasa ni zamu ya ndani.Kama nje kulikuwa na watu wengi kiasi hiki huku ndani wanaweza kuwa zaidi ya wale.Lakini hata wakiwa wangapi nitapambana nao.Ni heri nife wakati nikipambana kumuokoa Olivia kuliko kukata tamaa.Sijawahi kukata tamaa katika maisha yangu” akawaza Mathewna kujibanda katik aukuta wa geti akaangaza kila upande lakini hakumuona mtu yeyote. “Ndani kuko kimya kabisa kunaonekana hakuna mtu yeyote” akawaza halafu akampa Bravo maelekezo afanya kama alivyofanya kule nje.Bravo akatoka mbio huku Mathewakiendelea kumfuatilia nyuma kwa tahadhari.Waliizunguka nyumba ile na hakukuwa na mtu yeyote.Mathewakarejea katika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba,akakiminya kitasa ulikuwa umefungwa.Akatoa vitu Fulani katika begi lake na kuchokonoa kitasa mlango ukafunguka.Mathewakatoa nguo za Olivia katika begi lake na kumuwekea Bravo puani “Go find Olivia ! akasema Mathewna kumruhusu Bravo aingie ndani ya nyumba ile Mathewakimfuata kwa kunyata.Ndani Kulikuwa giza na hakukuwa na dalili zozote za mtu.Mathewaliendelea kumfuata Bravo aliyemuongoza kuelekea katika chumba Fulani ambacho mlango wake ulikuwa wazi.Bravo akaanza kunusa chini kisha akakwaruza sakafu “Olivia was here” akawaza Mathew “She was here.Where is she now?akajiuliza kisha akakikagua kile chumba kwa makini sana hakupata chochote cha kumsaidia akatoka na kuanza kuzunguka katika vyumba vingine.Nyumba ilikuwa tupu hakukuwa na kitu chochote ndani “Hakuna kitu chochote wala dalili zozote za kuishi mtu ndani ya nyumba hii lakini inaonekana kuna shughuli maalum inayofanyika humu ndani.Inaonekana kulikuwa na mitambo au kompyuta humu ila zimeondolewa tena inaonekna zimeondolewa haraka haraka kwani kwani kuna baadhi ya vitu vidogo vidogo wamevisahau.Who are these people? Olivia alikuwemo ndani ya nyumba hii wamempeleka wapi?akajiuliza akiendelea kuchunguza kile chumba kilichokuwa na nyaya nyingi zilizokatwa katwa. “Mmoja wa wale jamaa alifanikiwa kukimbia naamini tayari amewapa taarifa wenzake kwamba wamevamiwa na yawezekana wako njiani wanakuja kupambana nami.Ngoja niondoke haraka kwani hakuna kitu chochote humu ndani cha kunisaidia” akawaza Mathewna kumchukua Bravo wakatoka haraka sana ndani ya ile nyumba wakatembea kwa haraka kuelekea mahala walikoacha gari na kuondoka “Bado swali kubwa ninalojiuliza ni kuhusu watu hawa ni akina nani? Kwa nini wamemteka Olivia? Naamini kabisa Olivia alikuwemo ndani ya nyumba ile lakini ameondolewa,amepelekwa wapi? Hali niliyoikuta ndani ya ile nyumba inaonyesha kuna shughuli Fulani ilikuwa inafanyika mle ndani lakini wahusika wake waliondoka kwa haraka haraka. Kuna kila dalili za kunithibitishia watu wale waliondoka kwa haraka sana na kuna baadhi ya vitu wameviacha na vingine walishindwa kuvifungua ikawalazimu kuving’oa.Nini kiliwakimbiza? akajiuliza “Nje ya jumba lile nimeua walinzi kumi na tatu na wote wakiwa na silaha, namshukuru sana Bravo kwani ndiye aliyenisaidia kuweza kuwatambua na kuwaondoa wale jamaa.Swali ninalojiuliza ni kwamba ndani ya nyumba ile hakukuwa na mtu au kitu chochote cha maana kwa nini watu kumi na nne wenye silaha wazunguke kuilinda nyumba isiyokuwa na kitu chochote ndani yake? Mathewakaendelea kujiuliza maswali Alipita mahala alipoilipua nguo ya umeme na kuyakuta magari zaidi ya matano ya Tanesco na mawili ya polisi wakiwa wamelizunguka eneo lile wakifanya uchunguzi,hakusimama akaendelea na safari yake. “Zoezi la kumtafuta Olivia linazidi kuwa gumu lakini sikati tamaa nitahakikisha ninafanya kila linalowezekana hadi nipate mahala alikohamishiwa.Natakiwa pia kumjulisha mama yake ambaye naamini hivi sasa atakuwa hajalala anasubiri simu yangu.Mama yule aliniamini sana hivyo lazima nimpe mrejesho na kumpa moyo kwamba Olivia lazima apatikana ingawa zoezi la kumtafuta halitakuwa rahisi kwani watu waliomteka nyara ni watu wanaonekana wamejiandaa vya kutosha na baada ya wenzao kumi na tatu kuuawa itafanya mapambano ya kumpata Olivia yawe magumu zaidi” akawaza Mathewna kusimamisha gari pembeni ya barabara akawasha simu yake akazitafuta namba za Lucy Themba mama yake Olivia akampigia na simu ikapokelewa haraka haraka “Mathewnashukuru sana umepiga baba.Nimekutafuta sana katika namba uliyonipa lakini haikuwa ikipatikana.Nilitaka nikushukuru kwa kazi kubwa uliyoifanya mwanangu” akasema Lucy na Mathewakapatwa na mshangao “Nlikuwa nimezima simu mama nimeiwasha sasa hivi kwa ajili ya kukupa mrejesho wa ile kazi niliyokuja kuifanya”akasema Mathew “Pole sana baba.Mzee tayari amefika hapo? Akauliza Lucy na Mathewakastuka akaitoa simu sikioni akatazama jina la aliyempigia liliandikwa Lucy Themba.Alihisi amekosea namba “Mathew”akaita Lucy “Mama samahani,mzee yupi unamzungumzia? “Namzungumzia Agrey baba yake Olivia.Amekwisha fika mahala hapo ulipomuelekeza akufuate?akauliza Lucy “Mama sielewi.Nimemuelekeza Agrey anifuate wapi?akauliza Mathew “Mathewsi umempigia simu Agrey muda si mrefu na kumueleza kwamba umefanikiwa kumpata Olivia lakini hali yake si nzuri na wewe umejeruhiwa kwa risasi ukamuelekeza mahala ulipo ili akufuate?Nataka kujua kama tayari amekwisha fika mahala ulipomuelekeza akufuate” akasema Lucy. “Mama sielewi unazungumza jambo gani.Simu yangu niliizima na baada ya kuiwasha mtu wa kwanza kukupigia ni wewe.Nimekupigia kukujulisha kwamba nimetoka mahala ambako niliamini alikuwepo Olivia nimefanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo lakini Olivia sijamkuta ila kuna kila dalili kwamba Olivia alikuwemo ndani ya ile nyumba na akahamishwa.Mama kwa ufupi ni kwamba sijafanikiwa kumpata Olivia lakini si mwisho wa uchunguzi bado ninaendelea na operesheni hii hadi nihakikishe Olivia amepatikana” akasema Mathew “Mathewunasema hujampata Olivia?! Akauliza Lucy Themba huku akihema haraka haraka “Ndiyo mama sijafanikiwa kumpata lakini bado ninaendelea na uchunguzi wangu.Alikuwemo katika nyumba ile ambayo programu yangu ilinionyesha lakini ameondolewa na sijui amepelekwa wapi” “Mungu wangu ! akasema Lucy “Mama ulisema kuna mtu aliwapigia simu akijifanya ni mimi na kuwaeleza kwamba Olivia amepatikana?Mathewakauliza “Mathewumenichanganya. Ninahisi moyo wangu unataka kupasuka kwa mstuko” akasema Lucy “Mama nieleze tafadhali nini hasa kimetokea?akauliza Mathew “Kuna mtu amempigia simu Agrey usiku huu kwa kutumia namba nyingine tofauti na hii akajitambulisha kwamba yeye ni Mathewna akadai kwamba amefanikiwa kumpata Olivia lakini amejeruhiwa kwa risasi akamtaka Agrey amfuate mara moja mahala alipomuelekeza ili awapeleke hospitali.Hatukuwa na shaka yoyote kuwa ni wewe kwani mtu huyo alizungumza akiwa katika hali ya maumivu makali na tuliamini kwamba ni wewe umejeruhiwa.Agrey alitoka na kukufuata.Nimeishiwa nguvu kusikia kwamba si wewe uliyepiga simu” “My God ! akasema Mathew “Mimi sikupiga simu hiyo mama na wala sina namba za simu za mzee Agrey.Mama naomba usihamaki tunachotakiwa kufanya ni kumzuia haraka sana mzee asiende huko mahala anakoelekea kwani anakwenda katika hatari kubwa.Naomba umpigie simu na umtake ageuze haraka sana asiende huko alikoelekezwa” akasema Mathewna Lucy akaisubirisha simu yake akampigia simu Agrey lakini simu yake haikuwa ikipatikana “Mathewsimu yake haipatikani tena” akasema Lucy akianza kulia.Mathewakahisi miguu inamtetemeka akaegemea kiti na kuvuta pumzi ndefu. “Mambo yanazidi kuwa magumu” akawaza “Mathewnitafanya nini mimi?akauliza Lucy “Mama huyo jamaa alimuelekeza Agrey amkute wapi? “Alimuelekeza aende mtaa wa Msanzi mbele kidogo ya jengo la Zawama Saccos kuna jengo la ghorofa halijamaliziwa kujengwa akamtaka wakutane hapo” “Mama ninakwenda hapo sasa hivi.Ngoja nijaribu kumuwahi kabla hajafika hapo” akasema Mathewna kuwasha gari akaingia barabarani “Mathewtafadhali naomba uhakikishe unampata Agrey.Hakikisha haingii katika tatizo lolote” akasema Lucy huku akilia “Mama nitafanya kila niwezalo lakini nitakuomba suala hili usimueleze mtu yeyote hadi nitakapompata Agrey na kumfahamu mtu huyo aliyewapigia simu.Hata hivyo mama kuna kitu nataka kukifahamu.Kuna mtu yeyote ambaye mlimueleza kuhusu mimi kwenda kumtafuta Olivia? “Hakuna mtu tuliyemueleza baba ndiyo maana ulipopiga ile simu moja kwa moja tukaamini ni wewe” akajibu Lucy “Sawa mama nitawasiliana nawe baadae” akasema Mathewna kukata simu “Ni nani aliyempigia simu Agrey Themba akajifanya nini mimi? Lazima ni mtu aliyefahamu kuwa nimekwenda kumtafuta Olivia.Lucy anakataa kwamba hawajamueleza mtu yeyote kuhusu suala hili la mimi kwenda kumtafuta Olivia sasa mtu huyo amefahamu vipi kama nimekwenda kumtafuta Olivia?akajiuliza “Mtu pekee ambaye nilimueleza kuhusu mpango wangu ni Tino ambaye nilichukua silaha kwake.Tino ninamfahamu sana hawezi akafanya kitu kama hiki.Mwingine aliyefahamu kuhusu operesheni hii ni Ruby.Yule ni mwenzangu na hawezi akatoa siri zangu.Huyu mtu aliyepiga simu amefahamu vipi kama nimekwenda kumuokoa Olivia?Nini hasa lengo la kumpigia Agrey Themba na kumtaka amfuate mahala hapo alipomuelekeza? Mathewakajiuliza maswali ambayo alishindwa kuyapatia majibu “Lucy hataki kuniambia ukweli lakini lazima kuna mtu wamemueleza kuhusu mpango wangu wa kwenda kumuokoa Olivia.Ninaanza kupata picha kwamba kuna mtu wa karibu sana na familia ya Agrey Themba ambaye anahusika na tukio la kutekwa Olivia.Mtu huyo lazima atakuwa anawasiliana na watekaji na kuwapa taarifa zote anazozipata kutoka kwa akina Agrey.Ninahisi kwamba hata kitendo cha Olivia kuhamishwa mtu huyo n diye aliyewapa taarifa watekaji kwamba ninafahamu mahala alipo Olivia na ninakwenda kumuokoa hivyo ndiyo maana wakamuondoa haraka sana katika ile nyumba” akawaza na kuongeza mwendo wa gari “Sasa nimepata majibu kwa nini nyumba ile tupu ilikuwa inalindwa na watu kumi na nne wenye silaha.Ulikuwa ni mtego.Walijua lazima nitakwenda pale hivyo wakajipanga kunisubiri lakini kwa bahati mbaya kwao mimi ninazo mbinu nyingi zaidi yao.Hii ni hatua kubwa sana nimeipiga katika kufahamu mahala alipo Olivia na ninaamini nimekaribia sana kumpata.Nikimfahamu mtu ambaye walimueleza kuhusu mpango wangu wa kwenda kumuokoa Olivia tutakuwa tumempata Olivia.Ngoja kwanza nifike mahala ambapo wamemuelekeza Agrey aende.Naomba nimuwahi kabla hajafika mahala hapo kwani naamini lengo lao kumtaka aende hapo ni kumuua au kuteka.Watu hawa ni wataalamu sana wamejipanga vizuri na wanahakikisha hakuna kikwazo chochote kinajitokeza katika kukamilisha mipango
Swali ambalo mpaka sasa sijalipatia majibu nini sababu ya kumteka Olivia? Ni pesa au kuna sababu nyingine?akajiuliza Mathew “Majibu yatapatikana baada ya kumpata Olivia.Usiku huu lazima nikaonane na Lucy nikazungumze naye anieleze kama kuna mtu yeyote waliyempa taarifa zangu” akawaza Mathew *************** Kaiza akiwa na wataalamu wa kompyua wa idara yao wakiwa katika zoezi la kufunga mfumo mpya wa mawasiliano baada ya kuuondoa mfumo wa zamani ambao uliingiwa na kirusi hatari ukajifunga,alipigiwa simu.Mpigaji alikua ni Zakaria mmoja wa watu walio katika kikosi kilichokwenda kulinda kitalu 7 mahala ambako Olivia alihifadhiwa awali “Hallo Zakaria”akasema Kaiza “Kaiza..!! akasema yule jamaa akihema kwa kasi “Zakaria nini kimetokea?Hebu tulia nieleze nini kimetokea” akasema Kaiza “Kaiza tumevamiwa na watu wasiojulikana na wenzangu wameuawa” “Unasema?!! Akauliza Kaiza kwa mstuko “Tumevamiwa na watu wasiojulikana wenzangu wameuawa” Ukimya ukapita “Zakaria hebu nieleze taratibu nini hasa kimetokea?Nani wamewavamia? “Tulikuwa tumejipanga tukiendelea na ulinzi lakini ghafla nikasikia kama mwenzangu mmoja anagugumia maumivu nikatoka eneo langu na kwenda kujua kilichomsibu nikamulika tochi na kumkuta akiwa amepigwa risasi na wengine wanne wote wakiwa wamekufa tayari.Nikakimbia huku na mimi nikikoswa na risasi” “Zakaria wait…Nani..ah I mean…” Kaiza akababika.Alihisi mwili kumtetemeka “Kwa sasa uko wapi Zakaria?Kaiza akauliza “Nimekimbia nimejificha.Naomba msaada tafadhali”akasema Zakaria “Zakaria endelea kukaa mahala hapo hapo ulipo nitawasiliana nawe baada ya muda mfupi” akasema Kaiza na kukata simu akashusha pumzi Kaiza aliingiwa na hofu kubwa akampigia simu Devotha “Kaiza zoezi linakwendaje hapo?Muda gani mfumo mpya utakamilika?akauliza Devotha “Devotha kuna tatizo kubwa” “Tatizo gani Kaiza? “P3 Unit wamevamiwa” “Wamevamiwa? “Ndiyo wamevamiwa na watu wasiojulikana.Nimepigiwa simu na Zakaria muda mfupi uliopita akanipa taarifa hizo.kwa macho yake ameshuhudia watu watano wakiwa wameuawa” akasema Kaiza “MathewMulumbi” akasema Devotha “MathewMulumbi ni nani? Kaiza akauliza “Tutazungumza baadae Kaiza kwa sasa tujielekeze katika kusaidia watu wetu”akasema Devotha “Inaonekana wavamizi wamekwenda na nguvu kubwa ndiyo maana wakafanikiwa kuwavamia watu wetu na kuwazidi nguvu hivyo basi tunatakiwa kutuma nguvu kubwa kwenda kutoa msaada wa haraka sana” akasema Kaiza “Kaiza hatuwezi kutuma kikosi kingine kikubwa kwa haraka bila kujua kinachoendelea kitalu 7.Chukua watu watatu muende kitalu 7 mfanye uchunguzi ili tupate picha halisi ya nini kimetokea na tujue hatua zipi tuzichukue.Yawezekana huo aliyepiga simu ameshikiliwa mateka na wavamizi hivyo tukipeleka watu wetu wengine wanaweza wakavamiwa na kuuawa.Nataka ripoti ya kutoka kitalu 7 haraka hivyo achana na kila kitu unachokifanya sasa uende kitalu 7” akasema Devotha. Kaiza alihisi kuchanganyikiwa.Aliingiwa na woga mwingi. “Kwenda kitalu 7 ni kujipeleka katika hatari kubwa.Nimemsikia Devotha akitaja jina la MathewMulumbi ni nani?Yawezekana akawa ndiye mvamizi?akajiuliza Kaiza akachukua watu watatu kama alivyoelekezwa wakaondoka kuelekea kitalu 7. Devotha alipomaliza kuzungumza na Kaiza simuni akampigia Denis “Denis nipe ripoti.Mambo yanakwendaje huko? “Madam kazi imekamilika na hivi sasa tuko njiani tunarejea” “Hakukuwa na tatizo lolote?akauliza Devotha “Hakukuwa na tatizo lolote madam.Agrey alikuja peke yake kama tulivyomuelekeza” akajibu Denis “Good job Denis” akasema Devotha na kukata simu “Agrey Themba tayari tunaye mikononi mwetu.Nina hakika Olivia lazima atafunguka kila kitu atakapojua kwamba baba yake tunaye.Kwa sasa nguvu kubwa inaelekezwa kwa MathewMulumbi. Anaonekana ni mtu hatari sana.Anapaswa apatikane haraka vinginevyo ataharibu kila kitu.Ilikuwa vyema tuliwahi kumuondoa Olivia pale kitalu 7 kwani tusingefanya hivyo angeweza kumuokoa” akawaza Devotha ambaye naye macho yake yalionyesha woga kufuatia taarifa zile za watu wake kuvamiwa na kuuawa
Eneo lote la kuzunguka kitalu 7 kulikuwa na giza lililosababishwa na kukatika kwa umeme baada ya nguzo kulipuliwa na mlipuko.Kaiza na watu wake waliacha gari lao umbali wa mita mia mbili wakatembea kwa miguu wakiwa katika tahadhari kubwa.Kila alipojaribu kupiga simu kwa watu wake waliokuwa wakilinda nyumba ile hazikuwa zikipokelewa hii ikazidi kumpa hofu.Walifika katika geti la kuingilia ndani ya ile nyumba na kukuta mtu wa kwanza akiwa amelala chini amekwisha kufa.Wakamgeuza wakamtazama alikuwa amepigwa risasi katika paji la uso. “Damn !! Kaiza akasema kwa hasira Waliendelea kuzunguka ukuta uliozunguka ile nyumba na kukuta miili ya watu kumi na tatu. “Hii ni mara ya kwanza tukio kama hili linatokea katika idara yetu.Nani kawaua watu hawa wote? akajiuliza Kaiza na kumpigia simu Zakaria akamtaka afike pale kitalu 7 kwani wao tayati walikwisha fika.Haraka haraka akawaelekeza watu aliokwenda nao waingize miili yote ndani kisha akawasiliana na Devotha kumjulisha kile alichokikuta “Devotha ni hali ya kusikitisha sana iliyoko hapa.P3 Unit imekwisha.Watu kumi na tatu wote wameuawa isipokuwa Zakaria peke yake.Kitu cha kushangaza karibu wote wamepigwa risasi za kichwa.Inaonekana wauaji walikuwa wanawalenga vichwani bila wao kuwa na taarifa ndiyo maana wameweza kuua timu nzima”akasema Kaiza “Kaiza hili unaloniambia limenipa mstuko mkubwa.Haijawahi kutokea toka idara hii ianzishwe kupoteza watu wengi kiasi hicho.Haraka sana mili yote ya waliouawa iondolewe hapo na kuletwa hapa kitalu 2 tuihifadhi.Vipi hapo maeneo ya karibu hakuna taharuki yoyote?Hakuna wananchi wanaoishi maeneo ya karibu ambao wamefika eneo la tukio baada ya kusikia milio ya risasi? “Eneo liko kimya kabisa Devotha na inaonekana majirani wa eneo hili hawafahamu kilichotokea.Ninahisi wauaji walitumia bunduki zenye viwambo vya kuzuia sauti na kuua watu wetu kimya kimya”akajibu Kaiza “Sawa Kaiza hakikisha miili hiyo inaondolewa haraka sana eneo hilo” akasema Devotha na kukata simu “Haya ni majabu.Hadi nitakapoiona miili ya watu wetu ndipo nitakapoamini kama hii ninachoambiwa na Kaiza ni kitu cha kweli.P3 Unit ni kikosi tegemezi kabisa katika idara yetu na kina watu waliopata mafunzo ya hali ya juu nje ya nchi.Ni watu ambao tumekuwa tunawatumia katika operesheni mbalimbali na hawajawahi kushindwa au kuuawa hata mmoja wao.Imetokeaje leo wakauawa wengi kiasi hicho?.Huyu MathewMulumbi ni kiumbe wa aina gani anayeweza kuwaua watu wote hao kirahisi namna hii?akajiuliza Devotha “Nilitegemea suala hili lingekuwa dogo na kumalizika bila matatizo lakini sasa tayari limechukua sura mpya na limekuwa kubwa.Ameingia MathewMulumbi na kuharibu mchezo wote.Ngoja nimjulishe rais hiki kilichotokea” akawaza Devotha na kumpigia simu Dr Evans “Devotha habari za usiku huu.Mambo yanakwendaje hapo.Kila kitu kimekwenda vizuri?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais mambo yanakwenda vyema.Tumefanikiwa kumuhamisha Olivia na kumleta hapa kitalu 2 kama ulivyoelekeza.Vile vile tayari tumempata Agrey Themba na hivi tuongeavyo yuko njiani analetwa hapa kitalu 2” akasema Devotha “Very good.Vipi kuhusu MathewMulumbi?Uliweka kikosi cha kumsubiri pale kitalu 7?akauliza Dr Evans “Mheshimia rais tumepata mafanikio katika sehemu zote lakini kuna tatizo kidogo katika upande wa Mathew” “Kuna tatizo gani Devotha?Mmeshindwa kumpata Mathew?Hajafika kitalu 7?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais hivi sasa Kaiza na timu ndogo nimewatuma waende kitalu 7 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mmoja wa watu wetu aliye ndani ya P3 unit kwamba kumetokea wamavizi na wameua watu wetu.Kaiza amefika hapo na taarifa aliyonipa ni mbaya sana.Watu kumi na tatu wameuawa isipokuwa mmoja tu” akasema Devotha na kumstua Dr Evans “Kikosi kizima kimeuawa? Imewezekanaje wakauawa wote?akauliza “Amesalia mmoja tu mheshimiwa rais” “Kusalia mtu mmoja si hoja.Ninachotaka kufahamu ni namna hawa watu walivyouawa.P3 Unit ni kikosi maalum katika idara yetu chenye mafunzo ya hali ya juu na ndicho kikosi tegemeo.Wamefanya operesheni nyingi na hakuna opereseni hata moa waliyowahi kumpoteza mtu.Nini kimetokea hadi wauawe wote?Una hakika ulipeleka P3 unit kweli? “Ndiyo mheshimiwa rais kikosi kilichokwenda kulinda pale kitalu 7 ni P3 unit”akajibu Devotha “MathewMulumbi !!Mathew!!!..akasema Dr Evans huku akisikika akigonga meza kwa hasira “Ni kiumbe wa aina gani huyu?akauliza Dr Evans na ukapita ukimya “Devotha huyu mtu tayari amevuka mpaka na kama tusipokuwa waangalifu atavuruga kila kitu.Hiki alichokifanya leo ni tangazo la vita hivyo tunapaswa kumsaka kwa kila uwezo tulio nao na kuhakikisha anapatikana.Bila kumpata MathewMulumbi tumekwisha.Nataka mpaka kufikia kesho asubuhi nipate mikakati yako namna ya kumpata Mathew.Kama hauna mikakati au uwezo wa kumpata nieleze ukweli ili niweze kutumia vyombo vingine kumpata lakini nina imani na idara yako kuwa hamuwezi kushindwa kumpata Mathew.” akasema Dr Evans “Sawa mheshimiwa rais tutafanya hivyo.”akasema Devotha “Devotha kwa sasa baada ya kumpata Agrey Themba hakikisha unamfungua Olivia.Nina uhakika mkubwa kwamba kwa kumumia baba yake lazima atafunguka kila kitu.Hakikisha kabla ya mapambazuko uwe tayari umefahamu kila kitu kuhusu Olivia na IS” akasema Dr Evans na kukata simu
Mathewalipunguza mwendo wa gari alipoliona bango kubwa limeandikwa Zawama Saccos katika mtaa wa Msanzi na mbele kidogo akaliona jengo la ghorofa ambalo halijamaliziwa.Mbele ya jengo hilo kulikuwa na jengo lingine la ghorofa lililokuwa na maduka akasimamisha gari karibu na uzio wa jengo lile linaloendelea kujengwa akashuka.Aliangaza pande zote kuhakiki usalama wake,kulikuwa na magari machache yakipita barabarani.Kuzunguka jengo lile kulikuwa na uzio wa mabati akaingia ndani ya uzio akaliona gari moja likiwa limeegeshwa akalisogelea na kuchungulia ndani hakukuwa na mtu akaingia ndani ya lile jengo akaanza kuchunguza kama kuna mtu yeyote mle ndani.Alilikagua jengo lote lakini hakukuwa na mtu yeyote,akashuka na kwenda katika lile gari akakinyonga kitasa mlango ulikuwa umefungwa.Akatoa simu na kumpigia Lucy Themba mke wa Agrey “Mathewumekwisha fika mahala hapo?akauliza Lucy “Ndiyo mama nimekwisha fika” “Umempata Agrey?Amekwisha fika hapo?akauliza kwa wasi wasi “Mama nataka kufahamu mzee aliondoka nyumbani na gari ya aina gani? “Aliondoka na gari lake aina ya landcruiser V8 rangi nyeusi’ akasema Lucy na Mathewakabaki kimya “Mathew” akaita Lucy “Sawa mama ahsante.Nitakupigia simu muda si mrefu lakini kwa sasa naomba usimueleze mtu yeyote suala hili” akasema Mathewna kukata simu “Tayari wamemchukua Agrey.Hili suala linazidi kuwa gumu.Naamini watu hawa waliomchukua Olivia ndio hao hao waliomteka baba yake.Ni kikundi gani hiki? Nini hasa malengo ya kuwateka Olivia na baba yake?Ninaanza kupata picha kwamba suala hili ni zaidi ya fedha.Baada ya Olivia kutekwa tuliamini kwamba watekaji walifanya vile ili kujipatia fedha kutoka kwa familia yake lakini sasa baada ya baba yake pia kutekwa ninaanza kuhisi kwamba hili suala ni kubwa zaidi ya tunavyolichukulia.Ngoja niende kwa Lucy nitapata majibu yote” akawaza Mathewna kuingia katika gari lake akaondoka kuelekea nyumbani kwa Agrey Themba “Ninajaribu kuunganisha matukio yote yanayohusiana na kutekwa kwa Olivia lakini bado sipati picha nzuri ila ninachoweza kukipata mpaka hapa nilipofika ni kwamba kuna mtu au watu walio karibu na familia ya akina Olivia ambao wanahusika katika tukio hili.Ni Lucy pekee anayeweza kusaidia kupata ufumbuzi wa suala hili kama atakuwa tayari kunieleza ni nani waliyempa taarifa za mimi kwenda kumuokoa Olivia”akawaza Mathew Kabla hajafika nyumbani kwa bilionea Agrey Themba akampigia simu Lucy akamjulisha kwamba amekaribia kufika nyumbani kwake hivyo awataarifu walinzi wake.Alipofika getini tayari taarifa zake zilikuwa kwa walinzi wakamfungulia geti akaingia ndani na kumkuta Lucy Themba akiwa amesimama katika kibaraza akimsubiri.Alihisi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Mathewakishuka garini peke yake “Mathew,yuko wapi agrey?akauliza Lucy “Mama tunaweza kuzungumza ndani tafadhali? Mathewakaomba.Lucy akamuongoza wakaingia ndani “Mathewnaomba usiniambie umemkosa Agrey” akasema Lucy midomo ilikuwa inamtetemeka “Mama nimekosa Agrey.Samahani sana nilichelewa kufika mahala walikopanga wakutane.Nilichokikuta pale ni gari la Agrey ulilosema aliondoka nalo hapa nyumbani”akasema Mathew “Ouh Agrey…Agrey mume wangu .........akalia Lucy Mathewakamfuata “Mama usipige kelele tafadhali.Unatakiwa kuwa na nguvu hasa katika kipindi hiki kigumu” akasema Mathew. “Mathewmambo gani haya yanatutokea?Alianza Olivia na sasa amefuata baba yake.Nani hawa wanatuandama namna hii?akasema Lucy akiendelea kulia “Mama kuna jambo nataka kulifahamu kutoka kwako ambalo litatupa mwangaza kuhusiana na matukio haya yanayoendelea ndani ya familia yako.Nitakuomba unieleze ukweli bila kunificha” akasema Mathew “Kitu gani unataka kukifahamu Mathew?akauliza Lucy “Mama nimefika mahala ambako ninaamini Olivia alikuwa amefichwa,nimekuta nyumba ikiwa tupu ila kuna kila dalili kwamba Olivia alikuwepo pale lakini alihamishwa .Nikiwa bado natafakari kuhusu suala lile la Olivia likajitokeza suala la Agrey.Alipotekwa Olivia tulidhani kwamba watekaji wana lengo la kujipatia fedha lakini baada ya kutekwa baba yake pia nimetafakari na kuona suala hili ni zaidi ya fedha.Lengo la watekaji si kujipatia fedha kuna jambo lingine kubwa zaidi ya fedha.Kikubwa zaidi nilichokipata katika matukio haya mawili ni kwamba kuna watu au mtu ambaye yuko karibu yenu sana anashirikiana na watekaji.Ukiacha wewe na Agrey sikuwa nimemueleza mtu mwingine kama ninafahamu alipo Olivia na ninakwenda kumuokoa.NInajiuliza kama sikumweleza mtu mwingine juu ya jambo hili mtu aliyempigia simu Agrey na kujifanya ni mimi alipata wapi taarifa zangu?Jibu ninalolipata ni kwamba mtu huyo alipata taarifa hizo za mimi kwenda kumuokoa Olivia kutoka hapa kwenu.Endapo nikimfahamu huyo mtu tutakuwa tumepata mwanga mkubwa sana na itatusaidia katika kumpata Olivia na baba yake.Mama nimekuja hapa kuomba unieleze ukweli nani ambaye mlimueleza kuhusu mimi kufahamu mahala alipo Olivia? akauliza Mathew.Lucy Themba akafuta machozi na kusema “Hakuna mtu yeyote tuliyemueleza kuhusu suala la wewe kufahamu mahala alipo Olivia.Tunaofahamu ni mimi na Agrey hakuna mtu mwingine anayejua” akasema Lucy Themba “Mama hili ninalokuomba unieleze ni la muhimu sana na ninakuhakikishia kwamba kama tukimfahamu mtu huyo tutakuwa tumempata Olivia na baba yake.Ninaomba mama usinifiche kitu hata kama umemueleza mwanao au mtu wako wa karibu niambie usihofu.Nina uhakika mkubwa kwamba kuna mtu ambaye yuko karibu yenu anashirikiana na watekaji na ndiyo maana Olivia alihamishwa haraka mahala alipokuwa amefichwa baada ya kupata taarifa kwamba ninakwenda kumuokoa.Kama mtu huyo asingekuwa na taarifa hizo hivi sasa ningerejea na Olivia lakini nimemkosa baada ya kuhamishwa na taarifa za mimi kwenda kumfuata Olivia naamini wamezipata toka hapa.Mama kama kweli unataka tumpate Olivia na baba yake naomba uniambie nani ulimpa taarifa za kwamba ninakwenda kumfuata Olivia Kigamboni? “Mathewhakuna mtu yeyote tuliyemueleza.Ninakuhakikishia baba hakuna mtu yeyote ambaye tumemueleza.Kama kungekuwa na mtu yeyote ningekwisha kueleza” “Mama fikiria tena tafadhali ni muhmu sana.Kumbuka hata kama kulikuwa na mtu yeyote karibu yenu wakati mnazungumza wewe na Agrey” “Hakuna Mathew.Ulipoondoka tulikuwa na wageni wetu uliowaacha,wakaja tena wengine na walipoondoka mimi na Agrey tukaenda chumbani kwetu na hatukuzungumza kuhusu suala lako” akasema Lucy “Mama nisikilize vizuri.Wewe na familia yako tayari mko katika hatari na mtu ambaye anayaweka maisha yenu hatari yuko karibu yenu na kama tukiweza kumfahamu basi tutaweza kuwapata Olivia na Agrey.Kwa sasa wakati tukiendelea kumtafuta mtu huyo ni nani nitakuondoa hapa na kukupeleka sehemu salama ambako utakaa hadi hapo suala hili litakapopatiwa ufumbuzi” “Hapana Mathewsiendi kokote.Kama kuna mtu ambaye anaiandama familia yetu basi aje aniulie hapa hapa nyumbani kwangu,siendi kokote” akasema Lucy “Mama uko katika hatari kubwa.Ninataka kukusaidia uwe salama wakati tunaendelea kuwatafuta Olivia na baba yake” “Mathewnimekwambia siendi kokote.Kama yupo huyo ambaye anaiandama familia yetu anifuate hapa hapa sintamuogopa” “Mama ninataka nikupeleke sehemu sal…………” “Mathewstop! Nimesema siendi sehemu yoyote.Tafadhali kama una hakika yupo mtu ambaye anaiandama familia yetu basi mtafute na hakikisha unampata lakini mimi nitaendelea kukaa hapa hapa kwangu nikiwasubiri mume wangu na mwanangu kama watapatikana” akasema Lucy “Olivia na Agrey watapatikana mama lakini nitahitaji sana ushirikiano wako ndiyo maana ninataka uniambie kama kuna mtu ambaye umemueleza kuhusu mimi.Ni huyo pekee atakayelifumbua fumbo hili”akasema Mathew “Mathewnimekwambia hakuna mtu yeyote tuliyemwambia kuhusu wewe” “Sawa mama nimekuelewa.Nitatafuta namna nyingine ya kufanya kuweza kumfahamu mtu huyo na kwa kuwa umekataa wazo langu la kukuondoa hapa kukupeleka sehemu salama ninakushauri uimarishe ulinzi hapa nyumbani kwako usipokee simu ya mtu usiyemfahamu na usimueleze mtu yeyote jambo lolote kuhusiana na mimi.Ukipigiwa simu hata na simu ya mumeo au ya mwanao kwamba uende sehemu Fulani tafadhali usifanye hivyo nijulishe kwanza.Nitakupa namba ya simu ya siri ambayo mimi na wewe tutakuwa tunawasiliana”akasema Mathew “Mathewtafadhali watafute Agrey na Olivia.Nitakufa kama hawatapatikana” akasema Lucy “Usihofu mama ninakuahidi kuwatafuta Agrey na Olivia na ninakuhakikishia kwamba lazima watapatikana lakini ninaomba sana ushiriiano wako mkubwa hasa katika kumtafuta mtu huyu ambaye yuko karibu yenu ambaye ndiye anayeratibu matukio haya ya utekaji ndani ya familia yako” akasema Mathewna kumpa Lucy maelekezo kadhaa halafu akaondoka kurejea nyumbani kwake Baada ya Mathewkuondoka Lucy akachukua simu na kumpigia Dr Evans “Lucy habari za usiku huu?akauliza Dr Evans “Habari si nzuri Dr Evans” “Nafahamu Lucy,hata mimi mpaka sasa sijalala ninaendelea kuwasiliana na viongozi wa jeshi la polisi kila mara kupata ripoti za maendeleo ya uchunguzi.Usiwe na hofu yoyote ninakuhakikishia kwamba Olivia atapatikana” akasema Dr Evans “Dr Evans tatizo limezidi kuwa kubwa.Agrey naye ametekwa usiku huu” “Agrey ametekwa?akauliza Dr Evans kwa mshangao kana kwamba hajui chochote kilichotokea “Ndiyo ametekwa usiku huu” “Oh my God ! Ametekwa vipi?Wamekuja hapo nyumbani watekaji wakamchukua?Hebu nieleze mazingira ya kutekwa kwake Lucy” akasema Dr Evans “Mapema leo jioni alikuja kijana mmoja akajitambulisha kwetu kwamba anaitwa MathewMulumbi akadai kwamba yeye ni mpelelzi na anafahamu mahala alipo Olivia akatuomba tumpe ruhusa ya kwenda kumuokoa Olivia,Agrey alisita lakini mimi nikamuamini na kumtaka akafanye uchunguzi wake na amlete Olivia nyumbani.Saa kadhaa baada ya Mathewkuondoka,Agrey alipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni MathewMulumbi na akamueleza Agrey kwamba amefanikiwa kumpata Olivia lakini amejeruhiwa na anahitaji msaada hivyo akamtaka Agrey amfuate akamuelekeza sehemu ya kumkuta.Sote tuliamini kwamba ni MathewMulumbi lakini baadae baada ya Agrey kuondoka nikapigiwa simu na MathewMulumbi akaniambia kwamba amemkosa Olivia ndipo hapo nilipostuka.Mathewalikana kupiga simu yoyote nikamuelekeza aende mahala yule jamaa alikopanga akutane na Agrey akalikuta gari la Agrey lakini yeye mwenyewe hakuwepo na simu yake haipatikani tena.Tayari mume wangu ametekwa” akasema Lucy na kuanza kudondosha machozi “Lucy nyamaza kulia.Umefanya vyema kunipa taarifa hizi.Kwa maelezo uliyonipa ni wazi huyo MathewMulumbi anaonekana anahusika katika tukio hilo la kutekwa kwa Agrey.Huyo ndiye atakayekuwa mshukiwa wetu wa kwanza na anatakiwa afanyiwe uchunguzi mkubwa kujua uhusika wake katika sakata hili na nitaomba ushirikiano wako mkubwa Lucy ili tuweze kumpata.Kesho nitatuma timu ya wapelelezi hapo kwako na utampigia simu Mathewutamuomba muonane nyumbani kwako na akishafika atakamatwa atahojiwa na ataonyesha watu anaoshirikiana nao.Lucy nakuhakikishia kwamba tukimpata huyu jamaa tutakuwa tumewapata Olivia na baba yake.Huyo jamaa anafahamu kila kitu kinachoendelea” akasema Dr Evans “Hata mimi ninahisi huyu Mathewsi mtu mzuri.Agrey alinionya kuhusu kumuamini lakini sikutaka kumsikia niliamini tumepata mkombozi wa kutusaidia kumpata mwanetu.Yote haya ni makosa yangu. Ahsante sana Dr Evans kwa kunifumbua macho kuhusu huyu jamaa.Hata usiku huu amekuja hapa na akanitaka eti anipeleke sehemu salama nilikataa kata kata kwamba siwezi kutoka nyumbani kwangu.Sikujua kumbe alikuwa na malengo yake shetani yule” akasema Lucy Themba kwa hasira “Ulifanya vyema Lucy kumkatalia kwani kama ungekubali hata wewe nadhani ungeungana na akina Agrey” akasema Dr Evans “Lakini huyu jamaa anataka nini kwetu? “Mathewni mpelelezi kama alivyojitambulisha kwenu na ninaamini kuna watu ambao wanamtumia kufanya haya aliyoyafanya.Tukimpata atahojiwa na atawataja wale ambao wamemtuma afanye matukio haya mabaya.Lucy narudia tena kukuhakikishia tutawapata Olivia na Agrey” “Nashukuru sana Agrey tafadhali naomba ufanye kila uwezalo kuwapata Olivia na Agrey.Nitakufa kama wasipopatikana” akasema Lucy “Niamini mimi Lucy,watu hawa watapatikana” akasema DrEvans na kuagana na Lucy Themba
Mathewalipunguza mwendo wa gari alipoliona bango kubwa limeandikwa Zawama Saccos katika mtaa wa Msanzi na mbele kidogo akaliona jengo la ghorofa ambalo halijamaliziwa.Mbele ya jengo hilo kulikuwa na jengo lingine la ghorofa lililokuwa na maduka akasimamisha gari karibu na uzio wa jengo lile linaloendelea kujengwa akashuka.Aliangaza pande zote kuhakiki usalama wake,kulikuwa na magari machache yakipita barabarani.Kuzunguka jengo lile kulikuwa na uzio wa mabati akaingia ndani ya uzio akaliona gari moja likiwa limeegeshwa akalisogelea na kuchungulia ndani hakukuwa na mtu akaingia ndani ya lile jengo akaanza kuchunguza kama kuna mtu yeyote mle ndani.Alilikagua jengo lote lakini hakukuwa na mtu yeyote,akashuka na kwenda katika lile gari akakinyonga kitasa mlango ulikuwa umefungwa.Akatoa simu na kumpigia Lucy Themba mke wa Agrey “Mathewumekwisha fika mahala hapo?akauliza Lucy “Ndiyo mama nimekwisha fika” “Umempata Agrey?Amekwisha fika hapo?akauliza kwa wasi wasi “Mama nataka kufahamu mzee aliondoka nyumbani na gari ya aina gani? “Aliondoka na gari lake aina ya landcruiser V8 rangi nyeusi’ akasema Lucy na Mathewakabaki kimya “Mathew” akaita Lucy “Sawa mama ahsante.Nitakupigia simu muda si mrefu lakini kwa sasa naomba usimueleze mtu yeyote suala hili” akasema Mathewna kukata simu “Tayari wamemchukua Agrey.Hili suala linazidi kuwa gumu.Naamini watu hawa waliomchukua Olivia ndio hao hao waliomteka baba yake.Ni kikundi gani hiki? Nini hasa malengo ya kuwateka Olivia na baba yake?Ninaanza kupata picha kwamba suala hili ni zaidi ya fedha.Baada ya Olivia kutekwa tuliamini kwamba watekaji walifanya vile ili kujipatia fedha kutoka kwa familia yake lakini sasa baada ya baba yake pia kutekwa ninaanza kuhisi kwamba hili suala ni kubwa zaidi ya tunavyolichukulia.Ngoja niende kwa Lucy nitapata majibu yote” akawaza Mathewna kuingia katika gari lake akaondoka kuelekea nyumbani kwa Agrey Themba “Ninajaribu kuunganisha matukio yote yanayohusiana na kutekwa kwa Olivia lakini bado sipati picha nzuri ila ninachoweza kukipata mpaka hapa nilipofika ni kwamba kuna mtu au watu walio karibu na familia ya akina Olivia ambao wanahusika katika tukio hili.Ni Lucy pekee anayeweza kusaidia kupata ufumbuzi wa suala hili kama atakuwa tayari kunieleza ni nani waliyempa taarifa za mimi kwenda kumuokoa Olivia”akawaza Mathew Kabla hajafika nyumbani kwa bilionea Agrey Themba akampigia simu Lucy akamjulisha kwamba amekaribia kufika nyumbani kwake hivyo awataarifu walinzi wake.Alipofika getini tayari taarifa zake zilikuwa kwa walinzi wakamfungulia geti akaingia ndani na kumkuta Lucy Themba akiwa amesimama katika kibaraza akimsubiri.Alihisi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Mathewakishuka garini peke yake “Mathew,yuko wapi agrey?akauliza Lucy “Mama tunaweza kuzungumza ndani tafadhali? Mathewakaomba.Lucy akamuongoza wakaingia ndani “Mathewnaomba usiniambie umemkosa Agrey” akasema Lucy midomo ilikuwa inamtetemeka “Mama nimekosa Agrey.Samahani sana nilichelewa kufika mahala walikopanga wakutane.Nilichokikuta pale ni gari la Agrey ulilosema aliondoka nalo hapa nyumbani”akasema Mathew “Ouh Agrey…Agrey mume wangu .........akalia Lucy Mathewakamfuata “Mama usipige kelele tafadhali.Unatakiwa kuwa na nguvu hasa katika kipindi hiki kigumu” akasema Mathew. “Mathewmambo gani haya yanatutokea?Alianza Olivia na sasa amefuata baba yake.Nani hawa wanatuandama namna hii?akasema Lucy akiendelea kulia “Mama kuna jambo nataka kulifahamu kutoka kwako ambalo litatupa mwangaza kuhusiana na matukio haya yanayoendelea ndani ya familia yako.Nitakuomba unieleze ukweli bila kunificha” akasema Mathew “Kitu gani unataka kukifahamu Mathew?akauliza Lucy “Mama nimefika mahala ambako ninaamini Olivia alikuwa amefichwa,nimekuta nyumba ikiwa tupu ila kuna kila dalili kwamba Olivia alikuwepo pale lakini alihamishwa .Nikiwa bado natafakari kuhusu suala lile la Olivia likajitokeza suala la Agrey.Alipotekwa Olivia tulidhani kwamba watekaji wana lengo la kujipatia fedha lakini baada ya kutekwa baba yake pia nimetafakari na kuona suala hili ni zaidi ya fedha.Lengo la watekaji si kujipatia fedha kuna jambo lingine kubwa zaidi ya fedha.Kikubwa zaidi nilichokipata katika matukio haya mawili ni kwamba kuna watu au mtu ambaye yuko karibu yenu sana anashirikiana na watekaji.Ukiacha wewe na Agrey sikuwa nimemueleza mtu mwingine kama ninafahamu alipo Olivia na ninakwenda kumuokoa.NInajiuliza kama sikumweleza mtu mwingine juu ya jambo hili mtu aliyempigia simu Agrey na kujifanya ni mimi alipata wapi taarifa zangu?Jibu ninalolipata ni kwamba mtu huyo alipata taarifa hizo za mimi kwenda kumuokoa Olivia kutoka hapa kwenu.Endapo nikimfahamu huyo mtu tutakuwa tumepata mwanga mkubwa sana na itatusaidia katika kumpata Olivia na baba yake.Mama nimekuja hapa kuomba unieleze ukweli nani ambaye mlimueleza kuhusu mimi kufahamu mahala alipo Olivia? akauliza Mathew.Lucy Themba akafuta machozi na kusema “Hakuna mtu yeyote tuliyemueleza kuhusu suala la wewe kufahamu mahala alipo Olivia.Tunaofahamu ni mimi na Agrey hakuna mtu mwingine anayejua” akasema Lucy Themba “Mama hili ninalokuomba unieleze ni la muhimu sana na ninakuhakikishia kwamba kama tukimfahamu mtu huyo tutakuwa tumempata Olivia na baba yake.Ninaomba mama usinifiche kitu hata kama umemueleza mwanao au mtu wako wa karibu niambie usihofu.Nina uhakika mkubwa kwamba kuna mtu ambaye yuko karibu yenu anashirikiana na watekaji na ndiyo maana Olivia alihamishwa haraka mahala alipokuwa amefichwa baada ya kupata taarifa kwamba ninakwenda kumuokoa.Kama mtu huyo asingekuwa na taarifa hizo hivi sasa ningerejea na Olivia lakini nimemkosa baada ya kuhamishwa na taarifa za mimi kwenda kumfuata Olivia naamini wamezipata toka hapa.Mama kama kweli unataka tumpate Olivia na baba yake naomba uniambie nani ulimpa taarifa za kwamba ninakwenda kumfuata Olivia Kigamboni? “Mathewhakuna mtu yeyote tuliyemueleza.Ninakuhakikishia baba hakuna mtu yeyote ambaye tumemueleza.Kama kungekuwa na mtu yeyote ningekwisha kueleza” “Mama fikiria tena tafadhali ni muhmu sana.Kumbuka hata kama kulikuwa na mtu yeyote karibu yenu wakati mnazungumza wewe na Agrey” “Hakuna Mathew.Ulipoondoka tulikuwa na wageni wetu uliowaacha,wakaja tena wengine na walipoondoka mimi na Agrey tukaenda chumbani kwetu na hatukuzungumza kuhusu suala lako” akasema Lucy “Mama nisikilize vizuri.Wewe na familia yako tayari mko katika hatari na mtu ambaye anayaweka maisha yenu hatari yuko karibu yenu na kama tukiweza kumfahamu basi tutaweza kuwapata Olivia na Agrey.Kwa sasa wakati tukiendelea kumtafuta mtu huyo ni nani nitakuondoa hapa na kukupeleka sehemu salama ambako utakaa hadi hapo suala hili litakapopatiwa ufumbuzi” “Hapana Mathewsiendi kokote.Kama kuna mtu ambaye anaiandama familia yetu basi aje aniulie hapa hapa nyumbani kwangu,siendi kokote” akasema Lucy “Mama uko katika hatari kubwa.Ninataka kukusaidia uwe salama wakati tunaendelea kuwatafuta Olivia na baba yake” “Mathewnimekwambia siendi kokote.Kama yupo huyo ambaye anaiandama familia yetu anifuate hapa hapa sintamuogopa” “Mama ninataka nikupeleke sehemu sal…………” “Mathewstop! Nimesema siendi sehemu yoyote.Tafadhali kama una hakika yupo mtu ambaye anaiandama familia yetu basi mtafute na hakikisha unampata lakini mimi nitaendelea kukaa hapa hapa kwangu nikiwasubiri mume wangu na mwanangu kama watapatikana” akasema Lucy “Olivia na Agrey watapatikana mama lakini nitahitaji sana ushirikiano wako ndiyo maana ninataka uniambie kama kuna mtu ambaye umemueleza kuhusu mimi.Ni huyo pekee atakayelifumbua fumbo hili”akasema Mathew “Mathewnimekwambia hakuna mtu yeyote tuliyemwambia kuhusu wewe” “Sawa mama nimekuelewa.Nitatafuta namna nyingine ya kufanya kuweza kumfahamu mtu huyo na kwa kuwa umekataa wazo langu la kukuondoa hapa kukupeleka sehemu salama ninakushauri uimarishe ulinzi hapa nyumbani kwako usipokee simu ya mtu usiyemfahamu na usimueleze mtu yeyote jambo lolote kuhusiana na mimi.Ukipigiwa simu hata na simu ya mumeo au ya mwanao kwamba uende sehemu Fulani tafadhali usifanye hivyo nijulishe kwanza.Nitakupa namba ya simu ya siri ambayo mimi na wewe tutakuwa tunawasiliana”akasema Mathew “Mathewtafadhali watafute Agrey na Olivia.Nitakufa kama hawatapatikana” akasema Lucy “Usihofu mama ninakuahidi kuwatafuta Agrey na Olivia na ninakuhakikishia kwamba lazima watapatikana lakini ninaomba sana ushiriiano wako mkubwa hasa katika kumtafuta mtu huyu ambaye yuko karibu yenu ambaye ndiye anayeratibu matukio haya ya utekaji ndani ya familia yako” akasema Mathewna kumpa Lucy maelekezo kadhaa halafu akaondoka kurejea nyumbani kwake Baada ya Mathewkuondoka Lucy akachukua simu na kumpigia Dr Evans “Lucy habari za usiku huu?akauliza Dr Evans “Habari si nzuri Dr Evans” “Nafahamu Lucy,hata mimi mpaka sasa sijalala ninaendelea kuwasiliana na viongozi wa jeshi la polisi kila mara kupata ripoti za maendeleo ya uchunguzi.Usiwe na hofu yoyote ninakuhakikishia kwamba Olivia atapatikana” akasema Dr Evans “Dr Evans tatizo limezidi kuwa kubwa.Agrey naye ametekwa usiku huu” “Agrey ametekwa?akauliza Dr Evans kwa mshangao kana kwamba hajui chochote kilichotokea “Ndiyo ametekwa usiku huu” “Oh my God ! Ametekwa vipi?Wamekuja hapo nyumbani watekaji wakamchukua?Hebu nieleze mazingira ya kutekwa kwake Lucy” akasema Dr Evans “Mapema leo jioni alikuja kijana mmoja akajitambulisha kwetu kwamba anaitwa MathewMulumbi akadai kwamba yeye ni mpelelzi na anafahamu mahala alipo Olivia akatuomba tumpe ruhusa ya kwenda kumuokoa Olivia,Agrey alisita lakini mimi nikamuamini na kumtaka akafanye uchunguzi wake na amlete Olivia nyumbani.Saa kadhaa baada ya Mathewkuondoka,Agrey alipigiwa simu na mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni MathewMulumbi na akamueleza Agrey kwamba amefanikiwa kumpata Olivia lakini amejeruhiwa na anahitaji msaada hivyo akamtaka Agrey amfuate akamuelekeza sehemu ya kumkuta.Sote tuliamini kwamba ni MathewMulumbi lakini baadae baada ya Agrey kuondoka nikapigiwa simu na MathewMulumbi akaniambia kwamba amemkosa Olivia ndipo hapo nilipostuka.Mathewalikana kupiga simu yoyote nikamuelekeza aende mahala yule jamaa alikopanga akutane na Agrey akalikuta gari la Agrey lakini yeye mwenyewe hakuwepo na simu yake haipatikani tena.Tayari mume wangu ametekwa” akasema Lucy na kuanza kudondosha machozi “Lucy nyamaza kulia.Umefanya vyema kunipa taarifa hizi.Kwa maelezo uliyonipa ni wazi huyo MathewMulumbi anaonekana anahusika katika tukio hilo la kutekwa kwa Agrey.Huyo ndiye atakayekuwa mshukiwa wetu wa kwanza na anatakiwa afanyiwe uchunguzi mkubwa kujua uhusika wake katika sakata hili na nitaomba ushirikiano wako mkubwa Lucy ili tuweze kumpata.Kesho nitatuma timu ya wapelelezi hapo kwako na utampigia simu Mathewutamuomba muonane nyumbani kwako na akishafika atakamatwa atahojiwa na ataonyesha watu anaoshirikiana nao.Lucy nakuhakikishia kwamba tukimpata huyu jamaa tutakuwa tumewapata Olivia na baba yake.Huyo jamaa anafahamu kila kitu kinachoendelea” akasema Dr Evans “Hata mimi ninahisi huyu Mathewsi mtu mzuri.Agrey alinionya kuhusu kumuamini lakini sikutaka kumsikia niliamini tumepata mkombozi wa kutusaidia kumpata mwanetu.Yote haya ni makosa yangu. Ahsante sana Dr Evans kwa kunifumbua macho kuhusu huyu jamaa.Hata usiku huu amekuja hapa na akanitaka eti anipeleke sehemu salama nilikataa kata kata kwamba siwezi kutoka nyumbani kwangu.Sikujua kumbe alikuwa na malengo yake shetani yule” akasema Lucy Themba kwa hasira “Ulifanya vyema Lucy kumkatalia kwani kama ungekubali hata wewe nadhani ungeungana na akina Agrey” akasema Dr Evans “Lakini huyu jamaa anataka nini kwetu? “Mathewni mpelelezi kama alivyojitambulisha kwenu na ninaamini kuna watu ambao wanamtumia kufanya haya aliyoyafanya.Tukimpata atahojiwa na atawataja wale ambao wamemtuma afanye matukio haya mabaya.Lucy narudia tena kukuhakikishia tutawapata Olivia na Agrey” “Nashukuru sana Agrey tafadhali naomba ufanye kila uwezalo kuwapata Olivia na Agrey.Nitakufa kama wasipopatikana” akasema Lucy “Niamini mimi Lucy,watu hawa watapatikana” akasema DrEvans na kuagana na Lucy Themba
“Lucy amekana kabisa kumueleza mtu yeyote kuhusu mimi na mpango wa kwenda kumuokoa Olivia mahala alikofichwa.Japo anakakataa hawajamueleza mtu lakini naamini kabisa kwamba taarifa ile imevuja kutokea kwao na ndiyo maana watekaji wakawahi kumuhamisha Olivia toka sehemu walikkokuwa wamemficha.Kwa nini hataki kuwa muwazi ili niweze kuwasaidia yeye na familia yake? Hata hivyo bado sijakata tamaa nitaendelea kumsaka mtu huyo hadi nimfahamu kwani ndiye anayefahamu walipo Olivia na baba yake Agrey.Ngoja nikatulize akili nilitafakari jambo hili nijue namna ya kufanya” akawaza Mathew. Saa nane za usiku akafika nyumbani kwake akafungua mlango wa gari Bravo akashuka “Thank you Bravo.Umefanya kazi nzuri sana leo” akasema Mathewna kumrejesha Bravo katika nyumba yake,akaingiza ndani silaha zake “Wale jamaa walikuwa na bunduki kali nimezitazama zilikuwa ni M4 Cabin.Ni kampuni ya ulinzi au ni kikundi cha watu wamekodishwa kuifanya ile kazi?Kama ni kampuni ya ulinzi wanawezaje kuwa na silaha za namna ile?Serikali wanafah…….Mathewakatolewa mawazoni baada ya simu yake kuita alikuwa ni Ruby “Hallo Ruby” akasema Mathew “Mathewunaendeleaje?Nim ekuwa na wasiwasi sana nilikutafuta lakini simu yako haikuwa ikipatikana.Uko wapi mida hii? “Nimerejea nyumbani kwangu muda mfupi uliopita” “Umefanikiwa kumpata Olivia?akauliza Ruby “Hapana sikufanikiwa kumpata”akajibu Mathewna kumueleza Ruby kila kitu kilichotokea katika ile nyumba alimokuwa amefichwa Olivia. “Dah! Akasema Ruby “Kitu nilichokigundua kufuatia kilichotokea usiku huu,kuna mtu wa karibu sana na familia ya akina Olivia ambaye anashirikiana na watekaji na huyo ndiye aliyewapa watekaji taarifa kwamba ninakwenda kumuokoa Olivia wakamuondoa haraka sana kabla sijawasili.Ili kuwapata Olivia na baba yake lazima kumfahamu mtu huyo ambaye yuko karibu na familia yao na anafahamu kila kinachoendelea.Hapo ndipo nilipofikia kwa usiku huu Ruby” akasema Mathew “Pole sana Mathewjapokuwa haujampata Olivia lakini ulichokigundua kuhusu uwepo wa mtu mwenye ukaribu na familia ya Olivia ni kitu kikubwa.Mathewnimekupigia kukujulisha kuhusu jambo moja muhimu nililoligundua.Uliponipigia simu na kunipa taarifa za tukio hili nilirejea nyumbani mara moja kuangalia ujumbe uliotumwa katika kompyuta yangu.Kama nilivyotegemea kirusi chetu kimefanikiwa kuiba mafaili mengi na kuyatuma katika kompyuta yangu.Toka nimerudi nimekuwa nikiyapitia mafaili hayo na sijafanikiwa kuyamaliza ni mengi sana.Mathewsuala hili ni kubwa zaidi ya tunavyofikiri” akasema Ruby “Kwa nini unasema hivyo Ruby? Umegundua nini? akauliza Mathew. “Mafaili yaliyotumwa kwangu yanaonyesha kwamba yanatoka katika idara ya siri ya usalama wa ndani wa taifa” akasema Ruby “Ruby subiri kidogo unasema kuna kitu kinaitwa idara ya siri ya usalama wa ndani wa taifa?Sijawahi kusikia kitu kama hicho” “Hata mimi ni mara yangu ya kwanza kufahamu kwamba kuna idara ya siri ya usalama wa ndani wan chi.Inaonekana haina muda mrefu toka kuanzishwa kwake na inaendeshwa kwa siri bila kujulikana”akasema Ruby “Je Olivia ametekwa na idara hii ya serikali?Mathewakauliza “Nashawishika kuamini hivyo kwa sababu namba zile ulizompa Olivia zimepigwa kutoka idara hiyo ya serikali hivyo ni wazi wao ndio waliomteka Olivia.Hata kama si wao basi kuna kitu wanakifahamu kuhusu Olivia” akasema Ruby.Ukapita ukimya mfupi “Awali nilidhani watekaji walikuwa na shida na fedha lakini baada ya tukio la kutekwa Agrey Themba nilianza kuhisi suala hili ni zaidi ya kutaka fedha.Nilikuwa najiuliza maswali kuhusiana na silaha walizokuwa nazo wale watu niliowaua kule Kigamboni usiku huu sasa nimepata jibu kwa nini walikuwa na bunduki nzito kama zile.” akasema Mathew “Mathewswali linaloibuka hapa,nini sababu ya serikali kuwateka Olivia na baba yake?akauliza Ruby “Hilo ni swali zuri kwa kuanzia uchunguzi.Ninavyofahamu mimi serikali wanaweza wakateka mtu kama ni hatari pale anapoonekana ni hatari kwa usalama wa nchi” “Unadhani familia ya Olivia ni hatari kwa usalama wa nchi?akauliza Ruby “Nimekuwa na ukaribu na Olivia kwa miezi kadhaa sasa,mambo yake mengi ninayafahamu chumba chake ninaingia kama kwangu,sijawahi kuhisi hata mara Olivia anaweza kuwa hatari kwa usalama wa nchi.Hata kwa kumuangalia machoni Olivia hawezi kuwa hatari kwa usalama wan chi.Hata hivyo bado swali linabaki pale pale kwa nini idara hii nyeti ya serikali wamteke Olivia?Naamini ipo sababu kubwa”akasema Mathew “Mathewhili suala ni kubwa.Tunapaswa kulichimba kwa undani sana hadi tupate sababu ya Olivia na baba yake kutekwa na idara ya serikali ambayo inahusika na usalama wa ndani ya nchi.Ninakuja Dar es salaam” “Unasema Ruby?Mathewakauliza “Ninakuja Dar es salaam.Siwezi kukuacha ukaifanya kazi hii peke yako.You need help and I’m the one to help you so I’m coming to Dar es salaam” “Ruby ahsante sana kwa kujitolea kuja Dar es salaam lakini sidhani kama kuna ulazima wa kuja huku.Sitaki uingie katika hatari Ruby.Unaweza ukanisaidia hata ukiwa huko London” “Hapana Mathewlazima nije Dar es salaam.Wewe ni rafiki yangu na siogopi kuingia katika hatari kwa kukusaidia.Hili suala ni kubwa Mathewhivyo kubali au kataa unanihitaji sana.Unamuhitaji vile vile papii Gosu Gosu kwa ajili ya kusaidiana naye.Mathewwatu waliomteka Olivia ni taasisi ya serikali na tayari wameshakufahamu na hivi tuzungumzavyo watakuwa wanakutafuatilia sana hivyo unahitaji mtu kama Gosu Gosu kwa ajili ya kusaidiana naye.Tayari nimepata tiketi katika ndege ya shirika la ndege la Misri itakayoondoka kesho saa mbili za asubuhi hapa London kupitia Cairo na saa moja za jioni nitakuwa Dar es salaam jiandae kunipokea” akasema Ruby “Ahsante sana Ruby sijui nikushukuruje kwa kuamua kuja kunisaidia.Ni wazi ninakuhitaji sana katika suala hili.Nitawasiliana pia na Gosu gosu ambaye kwa sasa yuko Dubai.Atakuja na kwa pamoja tutatengeneza timu nzuri ya kulishughulikia suala hili” akasema Mathew “Mathewnakuhakikishia kwamba tutalimaliza suala hili.Nina imani kubwa sana na wewe na hatujawahi kushindwa chochote tukiwa pamoja.Najua Olivia ana umuhimu mkubwa kwako hivyo binafsi nitajitolea kila niwezalo kuhakikisha anapatikana akiwa hai yeye na baba yake” “Nakushukuru sana Ruby.Tafadhali naomba unitumie orodha ya vitu vyote unavyovihitaji ili kesho asubuhi nianze maandalizi” akasema Mathewna kuandika orodha ya vitu ambavyo Ruby angevihitaji halafu wakaagana “Ni mara ya kwanza ninasikia kuna idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Zipo taasisi mbali mbali za serikali zinazohusiana na masuala ya usalama wa nchi kama jeshi la polisi idara ya usalama wa taifa n.k.Nini hasa majukumu ya idara hii ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Ninapata ukakasi kuhusiana na malengo ya kuanzishwa kwake wakati zipo taasisi zenye kushughulikia masuala haya ya usalama wa nchi kwa ujumla wake.Kwa kuwa tayari Ruby anayo mafailli yaliyoibwa na kirusi kutoka katika idara hii tutachunguza na tujue kazi zake ni zipi hasa.”akawaza Mathewakachukua simu na kutafuta namba za Gosu Gosu akampigia “Hallo Mathewhabari za Dar es salaam?akauliza Gosu Gosu “Huku kwema kabisa Papii Gosu Gosu,mambo yanakwendaje hapo Dubai? “Kila kitu kinakwenda vizuri kabisa mkuu” “Gosu Gosu nimekupigia usiku huu ninakuomba kesho uje Dar es salaam kuna kazi imejitokeza” “Kazi gani mkuu wangu ya kibiashara? “Si kibiashara Gosu Gosu.Kuna mtu wangu wa karibu sana anaitwa Olivia Themba ametekwa jana na watu wasiojulikana hivyo nimejikuta sina namna zaidi ya kuingia katika opresheni ya kumtafuta.Ninahitaji sana msaada wako.Nimezungumza na Ruby atakuja kesho saa moja za joni hivyo nakuomba na wewe uje ili tuunde timu nzuri ya kuhakikisha tunamsaka Olivia na kumpata” “Usihofu Mathewnitakuja kesho.Kuna ndege ya Emirates itaondoka hapa Dubai kesho saa nne na robo kuja Dar es salaam nitakata tiketi niweze kuja na ndege hiyo.Nitakujulisha kila kitu kuhusiana na safari yangu kesho asubuhi” “Sawa Gosu Gosu.Nashukuru sana “ akasema Mathewna kukata simu “Kwa ukubwa wa suala hili ninawahitaji sana Ruby na Gosu Gosu.kwa upande wangu umakini mkubwa sana unatakiwa kuanzia sasa.Hawa jamaa tayari wamenifahamu na lazima watakuwa wananifuatilia kwani tayari nimekuwa mtu hatari kwao” akawaza Mathew
Agrey Themba alishushwa katika gari akiwa amefungwa pingu mikononi na kufunikwa mfuko mweusi kichwani.Hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia milango ikifunguliwa na kufungwa.Watu waliokuwa wamemshika mikono wakamkalisha katika kiti wakamfungua pingu alizokuwa amefungwa mkononi wakaifunga mikono yake katika pingu zilizokuwa zimeunganishwa na meza. “Jamani nimewakosea nini?akauliza Agrey lakini hakuna aliyemjali wala kumjibu “Kama kuna kuna mtu kawatuma mwambieni anisamehe asinitese kiasi hiki.Kama kuna mtu yeyote nim…………” akasema Agrey Themba na kunaswa kofi zito “Shut up !! akasema jamaa aliyemnasa kofi.Bado alikuwa na mfuko kichwani hakuweza kumuona mtu yeyote. “Mnanipiga nimewakosea nini jamani? Niambieni tafadhali kama kuna kitu nimewakosea.Niambieni kama mnahitaji fedha nitawapa kiasi chochote mnachokihitaji ili mradi mniache salama” akasema Agrey lakini hakuna aliyemjibu akasikia mlango ukifungwa na chumbani mle kukawa kimya. “Nilifanya ujinga mkubwa sana kumuamini mtu yule aliyepiga http://deusdeditmahunda.blogspot.com/simu akasema yeye ni Mathewna amempata Olivia.Nilitakiwa kuwasiliana kwanza na polisi lakini nikafuata maelekezo yake aliyoyatoa na ndiyo sababu ya kufika hapa nilipofika.Naamini hii yote ni michezo ya MathewMulumbi.Toka mwanzo sikuwa nimemuamini kabisa na ndiyo maana nilisita aliponiambia anataka kusaidia kumtafuta Olivia.Lucy ndiye ameyataka haya yote kwa kumuamini haraka haraka na kukubali kumpa ruhusa akamtafute Olivia.Naamini Mathewndiye anayehusika katika tukio la kutekwa kwa Olivia na sasa wameniteka mimi.Nini hasa anakihitaji kutoka kwetu?Shida yake ni fedha au kuna kitu kingine ? akajiuliza Agrey Themba “Lakini anajidanganya bure yule kijana kwani hatafika mbali na uhalifu huu anaoufanya.Jeshi la polisi wanaendesha operesheni kubwa ya kuhakikisha Olivia anapatikana na baada ya kupata taarifa kwamba na mimi pia nimetekwa nyara msako utaongezeka zaidi na lazima watamkamata.Mpaka kesho asubuhi nitakuwa tayari nimejulikana kuwa nimetekwa hivyo nguvu itakuwa kubwa zaidi ya kunitafuta mimi na Olivia” akawaza Agrey Themba Devotha Adolph akiwa ofisini kwake mlango ukafunguliwa akaingia Dennis “Karibu Dennis” akasema Devotha “Madam nimekuja kukupa taarifa kwamba kila kitu tayari na Agrey yuko katika chumba E1 kama ulivyoelekeza” “Ahsante Dennis.Kazi nzuri.Hakukuwa na tatizo lolote wakati wa kumchukua? “Kama nilivyokueleza simuni kwamba hakukuwa na tatizo lolote alikuja mwenyewe hadi eneo la tukio tukamchukua kwa wepesi bila purukushani zozote isipokuwa mlinzi anayelinda jengo lile tumelazimika kumkata pumzi na ametupwa baharini” “Good job Dennis.Unaweza kwenda sasa lakini muwe katika utayari kwani muda wowote kunaweza kujitokeza kazi ya kufanya” “Sawa Madam” akajibu Dennis na kuondoka.Devotha akayaelekza macho yake katika luninga kubwa ukutani iliyokuwa inaonyesha picha kutoka katika kamera zote zinazoizunguka nyumba ile.Katika kamera ya lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba ile ziliingia gari tatu “Kaiza anarejea na miili ya wenzetu.Sikutegemea kabisa kama suala hili lingebadilika na kuwa namna hii.Tayari limekuwa kubwa na maisha ya watu wetu yamekatishwa kikatili sana na huyu shetani MathewMulumbi.Bado najiuliza amewezaje kuua watu kumi na tatu?Alikuwa peke yake au kuna watu anashirikiana nao? Akajiuliza Mlango ukagongwa akaingia Kaiza akamtazama Devotha ambaye sura yake ilionyesha majonzi makubwa “Nimerejea Devotha” akasema Kaiza “Niambie hali mliyoikuta huko” akasema Devotha “Ni hali yakusikitisha sana.Karibu kikosi chote kimeteketea.Kwa inaonekana walikuwa wanauawa kimya kimya bila kuwa na taarifa.Karibu wote wamepigwa risasi kichwani.Baada ya kufanya mauaji hayo wauaji waliingia ndani ya nyumba kwani tumekuta mlango uko wazi.Ilikuwa vyema tuliwahi kumuondoa Olivia na kila kitu kilichokuwamo.Inaonekana lengo lao lilikuwa ni Olivia” akasema Kaiza. “Kaiza ni wakati wako wa kufahamu kuhusu suala hili.Mtu aliyefanya mauji haya anaitwa MathewMulumbi” “Unamfahamu?akauliza Kaiza “Nilipigiwa simu na rais akanitaka nimuhamishe Olivia pale kitalu 7 haraka na kuondoa kila kitu kwani kuna mtu tayari amekwisha fahamu mahala alipo Olivia. Baada ya kumuhamisha Olivia nilikwenda kuonana na rais” akasema Devotha na kumueleza Kaiza kila kitu alichozungumza na rais. “Nimestushwa sana kwa taarifa hii.Nina wasiwasi huyu jamaa anashirikiana na mtu katika idara yetu?akasema Kaiza “Kwa nini unahisi hivyo Kaiza? “Mpango huu ulikuwa ni wa siri kubwa.Devotha hainiingii akilini huyu jamaa agundue kuhusu mpango huu wa siri kama hana mtu anayeshirikiana naye ndani ya idara yetu” akasema Kaiza “Hicho unachokisema kinawezekana Kaiza hata mimi nimekuwa nina mawazo kama hayo.Lakini kwa mujibu wa maelezo ya rais ni kwamba Mathewaliweza kugundua mahala alipo Olivia kutokana na zile namba ambazo Olivia alitupa tuzipige na mifumo yetu yote ikajifunga.Mathewalimueleza Agrey kwamba namba zile alizompa Olivia ni programu maalum ambayo ingemuwezesha kujua mahala aliko Olivia pindi anapozipiga na sisi tulizipiga tu bila kuchuua tahadhari hivyo Mathewakagundua mahala namba zile zilikopigwa.Hayo ni maneno ya Mathewjapo siamini sana katika programu hiyo lakini tutafahamu kila kitu pale tutakapomtia mik………………” akanyamza Devotha simu yake ilipoita akaichukua na mpigaji alikuwa ni Dr Evans “Rais anapiga” akasema Devotha na kuipokea ile simu “Mheshimiwa rais” akasema Devotha “Devotha mnaendeleaje? “Tunaendelea vyema mheshimiwa rais.Miili ya P3 Unit imewasili muda si mrefu” akasema Devotha “Devotha nimezungumza na Lucy Themba muda mfupi uliopita akanipa taarifa kuwa Agrey ametekwa na watu wasiojulikana nikamuhakikishia kwamba lazima aliyefanya hivyo ni MathewMulumbi.Nimemuomba kesho asaidiane nasi katika mpango wetu wa kumpata Mathew.Andaa kikosi cha watu watano au zaidi waende nyumbani kwa Agrey kesho asubuhi,Lucy atampigia simu Mathewna kumtaka waonane na akifika pale nyumbani kwa Lucy hakikisheni mnamkamata Mathew.Nimewapeni njia rahisi ya kuweza kumpata Mathew.Baada ya kumkamata mpelekeni kitalu 1 hakikisheni anahojiwa na anaeleza kila kitu.Sitaki tena kusikia kwamba mmeshindwa kumkamata MathewMulumbi.Hii ni nafasi ya dhahabu imepatikana itumieni vyema” akasema Dr Evans. “Ahsante sana mheshimiwa rais kwa nafasi hii kubwa tuliyoipata ninakuahidi kwamba hakutafanyika kosa na lazima Mathewatapatikana” akasema Devotha “Vipi kuhusu Olivia mmekwisha anza kumfanyia mahojiano? “Tunajipanga ili tuanze kazi.Nitakupa mrejesho kila tutakachokuwa tunakipata” akasema Devotha “Devotha nasisitiza tena umakini mkubwa katika suala hili.Tulichokifanya kumteka Olivia na baba yake ni siri kubwa sana lakini tayari kuna mtu amekwisha ifahamu hivyo lazima kwa namna yoyote ile tumtie mikononi mwetu ili kuendelea kuhakikisha kwamba siri yetu inabaki salama.Endapo tutashindwa kumdhibiti Mathewtutajiweka katika mazingira magumu.Dhumuni la kuanzisha idara hii ni kushughulika na mambo ambayo idara nyingine za ulinzi na usalama wa nchi haziwezi kuyaona.Kwa sasa MathewMulumbi ni hatari sana kwa usalama wa nchi hivyo fanyeni kazi yenu kuhakikisha nchi inakuwa salama.Kilichotokea kitalu 7 sitaki kukisikia tena.Maelezo ya Mathewyanaonyesha kwamba ni mtu hatari hivyo mnapokwenda kukabiliana naye hakikisheni mnakuwa na kikosi kilichokamilika chenye watu wenye uwezo wa hali ya juu.P3 Unit ni kikosi kilichopata mafunzo ya hali ya juu sana lakini jana wameuawa kama kuku.Imeniumiza sana.Ni gharama kubwa imetumika kuwapatia mafunzo lakini wanakufa kifo ambacho naweza kusema kwamba ni kifo cha aibu.Inawezekanaje mtu mmoja akawashinda watu kumi na tatu na wote wana silaha kali?Sitaki jambo kama hilo lijitokeze tena” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais nimekuelewa na ninakuhakikishia kwamba hakutakuwa na uzembe wowote.Tunaipa uzito mkubwa sana operesheni hii” “Good.Nipeni taarifa baadae mtakachokipata kwa Olivia.Devotha nataka mpate taarifa zote tunazozihitaji kutoka kwa Olivia.Nilikupa idara hiyo uiongoze kwa sababu ninakuamini kwamba unao uwezo wa kuongoza idara kama hiyo.Nataka Olivia aongee na aseme kila kitu.Don’t be soft on her make her talk !’ akasema Dr Evans na kukata simu. Devotha akamueleza Kaiza kile alichoelekezwa na rais “Kwa mpango huu tayari ninaiona picha ya huyo Mathewmikononi mwetu.Nitaandaa kikosi kidogo lakini kizito na Mathewhataweza kufanya chochote.Hesabu hilo limekwisha Devotha” “Kaiza endapo tutamkosa Mathewsafari hii rais hataweza kutuvumilia tena.Kuna uwezekano mkubwa akatafuta watu wengine kuchukua nafasi zetu.Kaiza bado ninaihitaji hii kazi hivyo basi nakuomba ufanye kila lililo ndani ya uwezo wako kuhakikisha MathewMulumbi anapatikana kesho.Tukimpata Mathewhatutakuwa na kitu cha kuhofia tena lakini kama tukimkosa tutakuwa tumejiweka katika nafasi mbaya kwanza kama idara na pili rais hatatuamini tena” akasema Devotha “Nimekuelewa Devotha naomba nikutoe hofu kwamba MathewMulumbi ana muda mfupi sana kutoka sasa kabla ya kutua mikononi mwetu” akasema Kaiza “Good.Ni wakati sasa wa kumuhoji Olivia.Nitaifanya shughuli hiyo mimi mwenyewe.Agrey Themba tayari amekwishafikishwa hapa yuko E1.Kabla ya mapambazuko lazima tuwe tumepata kila taarifa tunayohitaji kutoka kwa Olivia.Tonight she must talk !! akasema Devotha. “Devotha kwa nini usinipe mimi nafasi hii nikamuhoji.Nakuhakikishia lazima atafunguka kila kitu” akasema Kaiza “Maneno aliyonieleza Dr Evans usiku huu yamenikumbusha mimi ni nani hadi akaniteua kuwa mkurugenzi wa idara hii muhimu kabisa.Alinichagua kutokana na uwezo wangu mkubwa nilio nao lakini katika sakata hili ninaonekana kupwaya hadi akaamua kunikumbusha majukumu yangu.Leo nitamuonyesha Olivia kwa nini niliaminiwa na rais akanichagua kuongoza idara hii” akawaza Devotha na kuchukua simu akapiga “Cindy shughulikia miili yote iliyoletwa ihifadhiwe katika kontena lile maalum lenye baridi hadi tutakapomaliza shughuli yetu” akasema Devotha akatoka mle katika ofisi yake akiwa na Kaiza wakaenda katika chumba kimoja kilichokuwa na kompyuta tatu.Olivia alionekana kupitia moja ya kompyuta akiwa amefungwa katika kiti.Devotha akamtazama kwa hasira halafu akasema “It’s time.Hakuna muda wa kupoteza” Akatoka ndani ya chumba kile akaenda katika chumba alimofungwa Olivia akapitisha kadi katika mlango ukafunguka akaingia ndani.Chumba kilikuwa cheupe na Olivia alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma katika kiti.Mbele yake kulikuwa na meza na viti viwili.Devotha akavuta kiti akaketi “Hallo Olivia” akasema Devotha na kwa mbali akatabasamu na vishimo vikaonekana katika mashavu yake.Olivia akamtazama hakusema kitu “Olivia I’m back again” akasema tena Devotha na kuendelea kumtazama Olivia “Mazungumzo yetu ya awali hayakumalizika vizuri na safari hii nimekuja kumaliza mazungumzo yetu.Sikuwa nimejitambulisha kwako pale awali.Ninaitwa Devotha Aldoph ni mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Kazi yetu ni kuhakikisha nchi inakuwa salama.Tunashughulika na mambo yale yaliyofichika kabisa ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi” akasema Devotha na kumtazama Olivia kwa sekunde kadhaa halafu akasema “Niliaminiwa na kupewa kuongoza idara nyeti kama hii nikiwa mwanamke wa kwanza kabisa kuongoza idara nyeti kama hii hapa nchini.Unadhani kwa nini niliaminiwa na kupewa idara hii niiongoze?akauliza lakini Olivia hakujibu kitu “Nitakupa jibu.They call me a female devil.Ninaitwa hivyo kutokana na ujasiri wangu wa kutoogopa kitu au mtu yeyote.Ninapokuwa katika kutekeleza majukumu yangu ya ulinzi wa nchi sisiti kutoa roho ya mtu na ndiyo maana nikaitwa shetani wa kike.Usione sura yangu ikitabasamu lakini mimi ni mkatili mno.Kwa kukupa mfano tu nilimuua kaka yangu ambaye ndiye ndugu yangu wa pekee aliyebaki baada ya kujiunga na makundi ya uhalifu.Sikusita kuondoa uhai wake.Nataka upate picha kama niliweza kuondoa uhai wa kaka yangu ambaye nimezaliwa naye tumbo moja nitashidwaje kukukata kichwa chako?Nitashindaje kuiteketeza familia yako? Devotha alipotaja familia Dr Olivia akamtazama kwa hasira “Nakuonya usithubutu kuigusa familia yangu” “Taratibu Olivia.Sijasema nitaiteketeza familia yako lakini endapo italazimu kufanya hivyo sintasita kuwateketeza mmoja baada ya mwingine huku ukishuhudia.Sitaki tufikie huko nataka tuzungumze tumalize haya mambo bila ya kufungua ukurasa mpya.Ninataka kuzungumza nawe kwa amani na ukinipa ushirikiano ninakuahidi Olivia nitakuacha huru” “Nini hasa mnachokitafuta kwangu?akauliza Dr Olivia “Rais amekwisha nieleza kila kitu ulichomueleza kuhusu mahusiano yako na IS na kila kitu ulichokifanya” “Sikumueleza chochote kuhusu mimi na IS.Nilichomweleza ni kwamba ni kweli nilikwenda Kinshasa kuonana na Seif Almuhsin lakini sikumueleza kwa nini” “Unafahamu kama Seif Almuhsin ni mmoja kati ya watu muhimu sana katika mtandao wa IS? “Ndiyo ninafahamu”akajibu Olivia “Kama ulifahamu yule ni mtu hatari kabisa kwa nini basi ukaenda kukutana naye Kinshasa?Are you one of them?akauliza Devotha “What if I’m one of them?akauliza Dr Olivia “IS ni kikundi cha kigaidi ambacho kimekuwa kikipigwa vita duniani kote.Wamekuwa wakifanya mashambulio ya kigaidi sehemu mbali mbali duniani na kuua watu wasio na hatia.Kwa sasa IS wameanza kujipenyeza barani Afrika na wanataka kuotesha mizizi yao Tanzania jambo ambalo katu hatuwezi kulikubali hivyo kama wewe ni mmoja wao basi jihesabu kwamba wewe ni adui yetu na utaeleza kila kitu kuhusiana na mikakati ya kikundi hicho.Nat…..”Kabla Devotha hajamaliza Dr Olivia akamkatisha “Hey ! Let’s make this short.Hauwezi kuniogopesha.Ulisema rais amekueleza kila kitu nilichozungumza naye hii inanipa picha kwamba wewe na rais ni watu wa karibu sana.Nataka kufahamu where is Edger Kaka? “Olivia nani kakuaminisha kwamba Edger kaka yuko hai?Nani wamekutuma uanzishe kashfa hii?Nini hasa malengo yenu?Ni moja ya mipango ya IS kutaka kuleta machafuko hapa nchini?akauliza Devotha “Nimekwisha muonya rais kwamba kama asiponieleza mahala alipo Edger kaka mwanae atakufa.Amechomwa sindano yenye virusi na mwenye dawa ya kumponya ni mimi mwenyewe ambaye nimevitengeneza virusi hivyo kwa hiyo msisitize kwamba ninamtaka Edger kaka ama sivyo atampoteza mwanae na hii itaendelea kwa familia yake yote hadi pale atakaponieleza wapi alio Edger Kaka” “Olivia kwa nini unafanya hivi kwa nchi yako?Wamekupa nini watu unaoshirikiana nao kiasi cha kukubali kutumika namna hii? Akauliza Devotha “Nieleze tafadhali watu unaoshirikiana nao ni akina nani? akasema Devotha “Devotha nimekwisha kwambia kwamba unapoteza muda wako bure siwezi kukueleza chochote.Mtu ninayeweza kuzungumza naye ni rais pekee.Ninaamini lazima atakuja kwangu akilia na atanieleza mahala alipo Edger Kaka” “Olivia ninasema kwa mara ya mwisho Edger amekwisha fariki dunia miaka mitatu ilopita.Hayupo tena duniani unachoweza kukipata ni mifupa yake tu.Ondoa ujinga huo kichwani mwako kwamba Edger yuko hai.Muda wa mzaha umekwisha sasa nataka unieleze nini hasa sababu ya wewe kwenda kukutana na Seif almuhsin jijini Kinshasa?Mazungumzo yetu rasmi yataanzia hapo”akasema Devotha “Devotha nimekwambia siwezi kuzungumza chochote na mtu kama wewe.Ninayeweza kuzungumza naye ni rais peke yake wewe ni mtu mdogo sana kuzungumza nami” akasema Dr Olivia “Olivia wewe ni mwanamke mwenzangu na sitaki nikufanyie ukatili.Sitaki kutumia nguvu kukulazimisha uongee lakini kwa kuwa umeonyesha kwamba hauko tayari kwa mazungumzo ya amani basi tutaufungua ukurasa mpya” akasema Devotha na kufungua moja ya kabati jeupe akatoa kisanduku cheupe akakiweka mezani akakifungua na kutoa vitu mbalimbali akaviweka mezani.Akachukua kisu kikali na kumsogelea Olivia “Olivia nilikwambia muda wa mzaha umekwisha na sasa nataka ufunguke kabla sijaanza kukuharibu.Umekwenda Kinshasa kukutana na Seif Almuhsin ambaye anatumiwa na IS kusajili vijana wanaokwenda kupatiwa mafunzo ya ugaidi na kupeleka katika sehemu mbali mbali duniani kupambana.Kama haitoshi tumekuta mawasiliano yako na Sayid Omar ambaye anatajwa kama mfadhili mkubwa wa kikundi cha IS.Ukaribu huu na watu wa IS unatufanya tuamini unashirikiana nao.Nataka unieleze mipango yenu yote mliyopanga kuitekekeleza hapa Tanzania ” akasema Devotha.Olivia hakumjibu chochote alikuwa kimya akimtazama “Olivia umesikia nilichokuuliza….” Akasema Devotha “Nimekwambia siwezi kuzung………..” kabla Olivia hajamaliza sentensi yake Devotha akakizamisha kisu katika paja la Olivia “Aaaagghhh !! Olivia akapiga ukelele mkubwa “Huo ni mwanzo tu Olivia kama hautafunguka nitaendelea kukuharibu” akasema Devotha na kuchukua kichupa kidogo akapuliza mahala alipochoma kisu na Olivia akapiga tena ukelele kwa maumivu makali aliyoyapata “Talk to me!! Akasema Devotha lakini Olivia aliendelea kulia “Olivia usipofunguka nitakuacha upoteze damu na ufariki dunia.Hebu pata picha mama yako atajisikiaje akipata taarifa kwamba umefariki dunia? Rafiki yako MathewMulumbi pia ataumia sana” akasema Devotha na Olivia akastuka baada ya kusikia jina la Mathewlikitajwa “Usistuke Olivia tunafahamu kila kitu kuhusu maisha yako.Utafunguka au tuendelee na huu mchezo?akauliza Devotha lakini Olivia hakumjibu kitu.Bado damu iliendelea kumwagika katika jeraha “Good.Tunaendelea na zoezi letu hadi pale utakaposema basi” akasema Devotha na kuchukua mkasi akamtazama Olivia halafu akachukua dawa katika sanduku akamuwekea katika jeraha lile lililokuwa linavuja damu.Devota akalishika sikio la Olivia na kujiandaa kulikata kwa mkasi mara akakumbuka kitu “Olivia u mwanamke mrembo na sitaki kuuharibu uzuri wako.Yupo mtu ambaye anapaswa abebe mzigo wako wa adhabu”akasema Devotha na kuielekea kamera “Nipe E1”akasema na katika moja ya kuta za chumba kile ikatokea picha kubwa ya mtu akiwa ndani ya chumba ameketi kitini akiwa amefungwa mikono na pinguu iliyo juu ya meza na kichwani alikuwa amevishwa mfuko mweusi “Huyu umuonaye pichani ndiye atakayebeba mateso yote badala yako hivyo ni jukumu lako kumuokoa na utamuokoa pale utakapofunguka kila kitu” akasema Devotha na kuamuru mtu yule ndani ya chumba avuliwe mfuko kichwani.Olivia akapatwa na mstuko mkubwa “Baba?! Akasema akiwa hayaamini macho yake “This is not true.Baba yangu hayupo hapa” akasema Olivia “Olivia unachokishuhudia ni kitu cha kweli kabisa na si picha ya kutengeneza.Yule ni baba yako Agrey Themba.Huyu ni mtu wa kwanza tumemleta hapa aje akusaidie kubeba mateso yako hivyo kama unampenda na unataka kumuokoa funguka na utueleze ukweli wote” akasema Devotha “Please don’t hurt him.Don’t touch my father.Don’t touch my family.Hangaikeni na mimi lakini familia yangu waacheni kabisa hawahusiki na chochote! “Olivia unaipenda sana familia yako nao wanakupenda pia na ndiyo maana tunawaleta hapa ili waweze kukuonyesha upendo wao na kukusaidia kubeba mateso yako”akasema Devotha na kuigeukia kamera “Guys he’s all yours” akasema Devotha na watu watatu waliojazia miili wakajitokeza na kuanza kumtandika makonde Agrey.Yalikuwa ni makonde mazito na damu nyingi ikaanza kumtoka.Olivia akafumba macho asione kilichokuwa kinaendelea kwa baba yake. “Stop ! akasema Devotha “Olivia umeona mateso anayoyapata baba yako.Kwa nini ukakubali baba yako ateseke kiasi hiki?Tell me everything and we’ll let your father go!! Akasema Devotha Olivia akafumbua macho na kumtazama baba yake ambaye uso wake ulikuwa umechafuka kwa damu akahisi kitu kama kisu kinaukata moyo wake.Akamtazama Devotha na kusema “Go ahead kill him ! “Unasemaje Olivia ?akauliza Devotha.Hakutegemea kusikia kauli kama ile “Umedhamiria kumpa mateso baba yangu huku niishuhudia ili kunilazimisha niweze kufunguka na kukueleza yale uyatakayo.Umekosea sana njia hiyo haitaweza kusaidia chochote kwani sintawaeleza chochote.Anzeni kumuua yeye,muendelee na watu wengine wa familia yangu na mwisho mnimalizie mimi.Go ahead kill him ! akasema Dr Olivia kwa ukali.Devotha akamuangalia kwa hasira “Olivia unajifanya shujaa sana? Akauliza Devotha “Kill him” akasema Dr Olivia. “You think this is a joke? Let me show you it’s not a joke” akasema Devotha na kutoka mle chumbani kwa hasira na baada ya dakika kama nne akaonekana katika chumba alimo Agrey Themba. “Olivia nimekuja kukuonyesha kwamba sisi hatutanii” akasema Devotha na Agrey aliposikia jina Olivia likitajwa akainua kichwa.Hakuweza kumuona aliyekuwa anaongea kutokana na damu nyingi kumtiririka usoni kufuatia kipigo kizito alichopigwa.Devotha akachukua bastora na kumlenga Agrey “Olivia I’ll count to three”akasema Devotha “Three” “Jamani naomba msiniue sina kosa lolote!! Akasema Agrey kwa taabu “Two! Devotha akaendelea kuhesabu huku akimtazama Olivia kupitia luninga iliyokuwamo ndani ya kile chumba “Please forgive me my father.I love you” akawaza Olivia na kufumba macho asishuhudie kifo cha baba yake. “One! Akasema Devotha na mlio wa risasi ukasikika.Baada ya sekunde kadhaa Olivia akafumbua macho na kumtazama baba yake akiwa bado amekaa kitini “Thank you God ! akasema kwa sauti ndogo.Devotha hakumpiga risasi Agrey alipiga pembeni “Olivia nilitaka kukuonyesha kwamba sisi hatuna utani.Next time I won’t miss.Uko tayari kufunguka ?akauliza Devotha.Olivia hakujibu kitu.Ukasikika mlio mwingine wa risasi.Devotha alimpiga Agrey Themba risasi katika paja.Agrey akapiga kelele kubwa “Are you ready to talk Olivia? Devotha akamuuliza Olivia kupitia kamera.Olivia alihisi maumivu makali kwa ndani kumuona baba yake akipata mateso makali namna ile “Bila Edger kupatikana sintakuwa huru.Ili niweze kujinasua kutoka katika mikono ya IS lazima nihakikishe Edger kaka anapatikana.Natakiwa kuendelea na msimamo wangu ili kujilinda na kuilinda familia yangu dhidi ya IS.Najua hawawezi kumuua baba ila watamtesa sana kunilazimisha nifunguke”akawaza Olivia “Olivia !! akauliza Devotha kwa ukali lakini Olivia hakujibu kitu aliendelea kumtazama.Mara ukasikika mlio mwingine wa risasi.Devotha alimpiga Agrey risasi katika paja la mguu mwingine. “My God please save my father” akaomba Olivia akiwa amefumba macho alihisi uchungu mkubwa lakini hakufumbaa kinywa chake kusema chochote.Devotha kwa hasira akaitupa chini bastora ile. “Mpelekeni mkamtibu haraka sana ! Devotha akawaelekeza wale jamaa waliokuwemo mle ndani akatoka kwa hasira na kwenda katika chumba walimo akina Kaiza “Huyu ni mwanamke wa aina gani ?Kwa nini imekuwa ngumu kumfungua? Akauliza Devotha akiwa amejishika kiuno “Devotha kwa namna nilivyomuona Olivia hatupaswi kutumia nguvu.Nashauri tumuendee taratibu tunaweza kufanikiwa kumfungua.Kumbuka huyu tayari ni mshirika wa IS hivyo amekwisha kula kiapo cha kutokusema chochote.Kama ameweza kushindwa kufunguka hata baada ya kushuhudia baba yake akipigwa risasi mbili hakuna tunachoweza kufanya kumfungua.Hata tukimpa mateso ya aina gani hataweza kufunguka”akasema Kaiza “Kaiza we must break her before sunrise.Kila kitu lazima kimalizike usiku wa leo kwa sababu kesho itaamshwa na taarifa mpya za kupotea kwa Agrey Themba na mambo yatazidi kuwa magumu.Hatuna muda wa kusubiri wala kubembeleza.Tutatumia kila njia hadi afunguke”akasema Devotha “Devotha tunatakiwa kukaa chini na kutafuta namna ya kumfungua Olivia.Kutumia nguvu hatutaweza kamwe.Nashauri tubadili mbinu” akasema Kaiza.Devotha akainamisha kichwa akafikiri “Unashauri nini?akauliza Devotha “Tusitumie nguvu hatutaweza kupata chochote.Nashauri kesho tumueleze Agrey kila kitu kuhusiana na Olivia na yeye ndiye atakayekwenda kuzungumza na mwanae kumtaka aeleze ukweli.Kwa njia hii naamini Olivia anaweza akafunguka lakini kwa kutumia nguvu hatutapata kitu” akasema Kaiza. “Hilo linaonekana ni wazo zuri.Lakini vipi kama rais akitaka kujua tumefikia wapi? “Mwambie bado tunaendelea na mahojiano” akasema Kaiza “Sawa nakubaliana na ushauri wako wa kumtumia Agrey.Tuma mtu akamtibu Olivia jeraha lake katika paja” akasema Devotha na kuelekea ofisini kwake “Sasa ninaamini kweli Olivia ni mshirika wa IS.Tayari amekwisha ingiwa na ile roho ya kikatili kama waliyo nayo.Hata baba yake alipotishiwa kuuawa hakuonyesha kujali.Hapa kuna kazi ngumu sana kumfungua.Hili suala litakwenda mbali zaidi. Halafu Olivia bado anaendelea kusisitiza kuhusu Edger Kaka kwamba yuko hai.Ukimtazama machoni anamaanisha kile anachokiongea.Kwa nini amlenge rais DrEvans kuhusiana na suala hili hadi kufikia hatua ya kumchoma mwanae sindano yenye virusi ili kumshinikiza aweze kumuonyesha mahala alipo Edger? Kuna kitu chochote Dr Evans anakifahamu kuhusu kifo cha Edger?Hainiingii akilini Olivia aweke msisitizo mkubwa namna hii na hata kuhatarisha maisha yake kwa jambo ambalo hana uhakika nalo.Yawezekana kweli kuna kitu kuhusiana na kifo cha Edger” akawaza Devotha “Niachane na mawazo hayo ya Edger nijielekeze katika jukumu langu kuhakikisha Olivia anafunguka kuhusu yeye na kikundi cha IS na mipango yao hapa Tanzania.Nilitegemea lingekuwa suala rahisi na ningeweza kupata kirahisi taarifa kutoka kwa Olivia lakini limegeuka na kuwa suala gumu na kadiri muda unavyokwenda ndivyo linavyozidi kuwa gumu.Ngoja nipumzishe kichwa changu kwanza hadi asubuhi yawezekana nikapata ufumbuzi” akawaza Devotha
Saa kumi moja za alfajiri Dr Evans akampigia simu Dr Stanslaus Mbeula “Mheshimiwa rais habari za asubuhi” akasema DrMbeula “Habari yako Dr Mbeula.Mnaendeleaje huko? “Mheshimiwa rais tumefanya kazi usiku kucha” akasema Dr Mbeula “Kuna chochote mmekigundua” akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais tumegundua virusi fulani katika damu ya Coletha lakini tunaendelea kuvichunguza zaidi.Baada ya kufanya kazi usiku kucha tumechukua mapumziko mafupi tutarejea tena baadae kuendelea kuchunguza zaidi” akasema Dr Mbeula “Dr Mbeula nakushukuru sana kwa kazi kubwa mliyoifanya.Vipi Coletha anaendeleaje? “Coletha anaendelea vyema japo usiku hali yake ilikuwa inabadilika badilika lakini hadi ninaondoka hospitali muda mfupi uliopita hali yake ilikuwa inaendelea vyema” “Dr Mbeula ninaomba tafadhali mfanye juu chini kutambua virusi hivyo ni vya aina gani ili kuokoa maisha ya mwanangu.Kama zoezi litakuwa gumu naomba unijulishe ili nimpeleke Coletha nje ya nchi” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais usiwe na shaka.Tutakaporejea tutaendelea na uchunguzi wetu kuhusiana na virusi hivyo nina hakika tutafanikiwa kupata dawa yake baada ya kuvitambua.Hata hivyo mheshimiwa rais nina swali nataka kuuliza” “Uliza Dr Mbeula” akasema Dr Evans “Ulifahamuje kama mwanao Coletha ana maambukizi ya virusi hivi? akauliza Dr Mbeula.Swali lile likamfanya Dr Evans akae kimya kwa muda halafu akasema “Dr Mbeula kwa sasa naomba nisiliongelee hilo suala..Naomba ujitahidi kwa kadiri uwezavyo kuhakikisha unapambana na virusi hao.Tafadhali naomba uokoe maisha ya mwanangu nakutegemea sana Dr Mbeula” “Nakutoa hofu mheshimiwa rais mimi na wenzangu tutafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunalipatia ufumbuzi suala hili lakini mheshimiwa rais nimeuliza swali hilo ili kujua asili ya virusi hivi” akasema Dr Mbeula “Dr Mbeula baadae nitakuita ikulu tutazungumza vizuri lakini kwa sasa endeleeni na jitihada za kupambana na vizuri hao” “Sawa mheshimiwa rais nitawasiliana nawe tena baadae kukujulisha maendelo yetu” akasema Dr Mbeula akaagana na rais. “Olivia ! Olivia ! kwa nini umemfanyia hivi Coletha? Sisi ni kama ndugu tumekukosea nini hadi ukatufanyia hivi? Akawaza Dr Evans akiwa amekaa kitandani akachukua simu na kumpigia Devotha.Simu iliita bila kupokelewa akapiga tena ikapokelewa.Devotha alizungmza kwa sauti ya uchovu. “Hallo mheshimiwa rais” “Devotha umelala? “Ndiyo nilikuwa nimejipumzisha mheshimiwa rais” “Samahani kwa kukuamsha.Nataka kujua zoezi limekwendaje?akauliza “Mheshimiwa rais zoezi lilikuwa gumu kidogo tofauti na tulivyotegemea.Olivia amegoma kabisa kufunguka hata baada ya kumpiga risasi baba yake” “Agrey amepigwa risasi?! Dr Evans akastuka “Nilimpiga risasi katika paja na haina madhara kwani haikugusa mfupa,lengo lilikuwa kumfanya Olivia aogope na afunguke.Pamoja na kitendo hicho bado Olivia aligoma kabisa kufunguka na alidiriki hata kutamka kwamba kama ninataka kumuua baba yake nifanye hivyo kwani hatanieleza chochote.Mheshimiwa rais,Olivia anashirikiana na magaidi hivyo haitakuwa rahisi kufunguka kwani magaidi hula kiapo cha kutokusema chochote.Tumefikiria kubadili mbinu na kumtumia baba yake Agrey.Tutamueleza kila kitu kuhusu mwanae na yeye ndiye atakayemshawishi afunguke” akasema Devotha “That’s a mistake Devotha.Mkiwakutanisha Olivia na baba yake lazima atamueleza kwamba mimi niko nyuma ya mpango huu jambo ambalo sitaki Agrey alifahamu.Agrey ni zaidi ya rafiki tumetoka mbali hivyo sitaki afahamu kabisa uhusika wangu katika suala hili hivyo nataka asikutanishwe na Olivia kabisa.Tafuteni mbinu nyingine za kuweza kumfungua Olivia na si mbinu hiyo ya kumkutanisha na baba yake.Devotha mnazo mbinu nyingi sana kwa nini mnashindwa kuzitumia?Hakikisha jua halizami leo bila kupata taarifa zote kutoka kwa Olivia.Jambo lingine nawasisitiza kuhusu kumpata MathewMulumbi” Akasema Dr Evans “Tumejipanga vizuri kwa ajili ya suala hilo mheshimiwa rais.Mara tu kutakapopambazuka kikosi kilichoandaliwa kitakwenda kuonana na Lucy Themba na kila kitu kitakwenda kama ulivyoelekeza.Mheshimiwa kuna jambo lingine ambalo nataka kulifahamu.Wakati ninamuhoji Olivia alirudia tena ile kauli yake kwamba unafahamu kuhusu Edger kaka kuwa hai.Kuna chochote unakifahamu kuhusu Edger mheshimiwa rais?Nimeuliza hivi kutokana na msisitizo mkubwa aliouweka Olivia katika suala hili kwani hata ukimtazama usoni wakati akizungumza haonekani kutania” akasema Devotha “Devotha hata mimi suala hili limenishangaza sana.Ni mara ya kwanza nimelisikia kwa Olivia.Edger Kaka amekwisha fariki miaka mitatu iliyopita na hakuna namna yoyote anayoweza kurudi.Sielewi hili suala la kwamba Edger yuko hai kalitoa wapi.Mimi ninachofahamu Edger alikwisha fariki dunia.Kingine cha ajabu ni yeye mwenyewe Olivia ndiye aliyeutambua mwili wa Edger hospitali iweje leo ageuke na kudai Edger hakufa? Hapo ndipo unapoweza kuamini kwamba hili ni jambo linalotengenezwa kunichafua mimi na serikali yangu.Olivia na mtandao wake kuna kitu wanakitafuta ndiyo maana wakaanzisha kitu kama hiki.Hii ni kashfa mbaya kabisa Devotha na inaweza kuleta machafuko makubwa kwa nchi ndiyo maana nataka kwa namna yoyote ile lazima Olivia ateswe hadi afunguke ni akina nani anaoshirikiana nao katika kutunga uongo huu” akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais nimekuelewa lakini ukijipa dakika chache kutafakari kile anachokisema Olivia utapata picha kwamba hajakurupuka kudai kwamba Edger Kaka yuko hai.Huu ni mpango ambao umekuwa na maandalizi makubwa hadi kuandaa kirusi hicho na unaonekana si mpango wa muda mfupi.Wamechukua muda mrefu kuuandaa.Ninachojiuliza kwa nini wakulenge wewe moja kwa moja?Mheshimiwa rais kama kuna kitu chochote unakifahamu kuhusu suala hili nieleze tafadhali inaweza ikasaidia kupata ufumbuzi wa hili jambo kwani Olivia amesisitiza kwamba atazungumza pale atakapopatikana Edger Kaka” akasema Devotha “Devotha narudia tena sifahamu chochote kuhusu jambo hili.Kama ningefahamu chochote ningekueleza” “Sawa mheshimiwa rais” “Nipigie simu mara kwa mara kunijulisha mnavyoendelea” akasema Dr Evans na kukata simu “Olivia amekosa nini katika maisha yake hadi akakubali kujiunga na magaidi ambao wamembadilisha na kumfanya amekuwa mkatili kiasi hiki?Hawa magaidi wanatumia mbinu gani kuwaharibu watu akili na kuwageuza kuwa wakatili kama walivyomfanya Olivia?Nimemshuhudia Olivia toka akiwa mtoto na sikuwahi hata mara moja kuhisi kama siku moja angegeuka na kuwa mtu katili namna hii.Ametengeneza virusi ambavyo vinaweza kumuua Coletha ambaye ni sawa na mdogo wake.Amemtumia mwanangu ninayempenda kunishinikiza eti nimrejeshe Edger Kaka.Kwa nini hili suala la Edger kaka amelikazania sana wakati anafahamu kabisa Edger Kaka amekwisha fariki na kuoza kabirini?Halafu kwa nini ananilenga mimi moja kwa moja kwamba ninafahamu mahala alipo Edger?Najilazimisha kuamini Olivia amechanganyikiwa lakini haonekani kama mgonjwa wa akili.Hapo ndipo linapokuja lile wazo langu kwamba lengo lake na watu anaoshirikiana nao ni kutaka kuleta machafuko hapa nchini kwa kuuaminisha umma kwamba Edger hajafa na mimi ninafahamu mahala alipo na kwa kuwa Edger alikuwa na watu wengi wanaompenda hasa vijana yataibuka machafuko na wao watapata nafasi ya kujipenyeza hapa nchini kufanya wanachokitaka.Huu ni mpango wa IS ili waweze kuingia hapa nchini na kuotesha mizizi.Olivia amelipwa shilingi ngapi hadi akubali kufanya kitu cha namna hii? Katu sintakubali watu hawa wafanikiwe lengo lao.Lazima kuwaondoa haraka sana nikianza na Olivia mwenyewe na kupitia kwake lazima atawataja wale wote anaoshirikiana nao” akawaza Dr Evans
Saa kumi na mbili na dakika nne simu ya Mathewikaita alikuwa ni Lucy Themba.Mathewakaipokea haraka haraka ile simu “Mama shikamoo” “Marahaba Mathewhujambo baba” “Sijambo kabisa mama.Unaendeleaje?akauliza “Hivyo hivyo mwanangu” “Kuna taarifa zozote zimepatikana toka wakati ule tulipoachana? “Hakuna taarifa zozote baba,nimelia hadi machozi yamekauka” “Pole sana mama” “Mathewnimekupigia kukuomba uje hapa nyumbani kwangu mapema asubuhi hii kuna suala la muhimu sana nataka kuzungumza nawe” “Jambo gani mama? “Ulisema kuna mtu wa karibu na familia yetu ambaye anashirikiana na watekaji? “Ndiyo mama ninahisi hivyo kuna mtu yuko karibu yenu ambaye anashirikiana na watekaji”Mathewakajibu “Nadhani tayari nimekwisha mfahamu”akasema Lucy na Mathewakashusha pumzi “Una hakika mama? “Ndiyo Mathewnadhani “Unaweza ukanitajia mtu huyo ni nani?akauliza Mathew “Naomba uje hapa nyumbani tuzungumze Mathew” “Sawa mama ninakuja hapo nyumbani muda si mrefu” “Nashukuru sana” akasema Lucy na kukata simu “Jana nimemuomba sana Lucy Themba anieleze kama kuna mtu walimpa taarifa zangu akakataa kata kata kwamba hakuna mtu yeyote.Inawezekana baada ya kukaa na kutafakari amenielewa na tayari kuna mtu amemuhisi.Ngoja nikamsikilize mara moja” akawaza Mathewna kuamka akaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na Lucy Themba. Hakuchukua muda mrefu kujiandaa kabla hajatoka akamuelekeza Derick msimamizi mkuu wa nyumba yake aandae vyumba viwili kwani kuna wageni watafika pale nyumbani jioni ya siku ile.Baada ya kutoa maelekezo yale akaondoka kuelekea kwa Lucy Themba.Akiwa njiani akampigia simu Ruby “Ruby nimepigiwa simu na Lucy Themba ameniambia kuna mtu anamuhisi kushirikiana na watekaji.Niko njiani ninakwenda kuonana naye” akasema Mathew “Mathewuliniambia kwamba ulimuomba sana akwambie kama kuna mtu aliyemweleza kuhusu wewe akakataa.Kitu gani kimemfanya abadili mawazo asubuhi hii? “Yawezekana baada ya kutafakari sana kuna kitu amekigundua na anataka kunieleza.Vipi mipango ya safari? Akauliza Mathew “Ninaondoka asubuhi hii kuja Dar es salaam kama nilivyokuahidi.Nipokee uwanja wa ndege saa moja za jioni” akasema Ruby “Usihofu Ruby nitakuwepo uwanjani kukupokea” akasema Mathewakaagana na Ruby Mathewaliwasili nyumbani kwa bilionea Agrey Themba akafunguliwa geti akaingia ndani akashuka garini na kwenda kugonga kengele ya mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni.Akatoka msichana wa kazi akamkaribisha ndani.Wakati akimsubiri Lucy akaletewa kikombe cha kahawa akaendelea kunywa taratibu.Akiwa ameyaelekeza macho yake luningani akitazama vipindi vya asubuhi mara ghafla wakajitokeza watu watano wote wakiwa na bunduki.Mathewalihisi kama yuko ndotoni lakini ile haikuwa ndoto bali ni kitu cha kweli kabisa alikuwa amezungukwa na watu wenye silaha. “MathewMulumbi uko chini ya ulinzi.Tafadhali piga magoti na inua mikono yako juu! Akasema jamaa mmoja kwa sauti kali.Mathewakawatazama wale jamaa kama vile anatafuta nafasi hata ndogo aweze kuitumia “Mathewhakuna utakachoweza kufanya kwa sasa.Piga magoti inua mikono yako juu tafadhali” akasema yule jamaa na vyuma vikasikika katika zile bunduki za wale jamaa.Mathewhakuwa na ujanja akapiga magoti na kuinua mikono juu.Kwa mzoefu wa mambo haya kama Mathewunaposikia vyuma vile vimelia huna budi kutii amri utakayopewa.Mmoja wa wale jamaa akamsogelea huku wenzake wakiwa katika tahadhari kubwa na akamshika MathewMikono na kumfunga pingu kisha akamsachi na kuichukua bastora yake na vifaa vingine kama simu ambayo ilizimwa haraka.Bila kupoteza muda Mathewakafunikwa mfuko kichwani akazungushwa upande wa nyuma kulikokuwa na magari matatu akaingizwa katika gari la kati kati kisha magari yale yakaondoka.Kaiza ambaye alikuwa amepanda gari la mbele kabisa akampigia simu Devotha baada ya kuyaacha makazi ya Agrey Themba. “Devotha kazi imekwisha.Tumempata MathewMulumbi” akasema Kaiza “Unasema kweli Kaiza? Akauliza Devotha “Ndiyo Devotha.Tunaye MathewMulumbi na hivi tuongeavyo tunayaacha makazi ya Agrey tunaelekea kitalu 1” “Nimekosa neno la kuongea Kaiza.Hakukutokea machafuko yoyote? “Hakukuwa na machafuko yoyote.Tulimstukiza kiasi kwamba alishindwa hata kunyoosha mkono kuishika bastora yake” “Good job Kaiza.Ninaelekea kitalu 1 kushuhudia MathewMulumbi akifikishwa pale.Huyu mtu ni hatari sana” akasema Devotha na kukata simu bila kupoteza muda akampigia simu rais Dr Evans “Devotha unasemaje?akauliza Dr Evans “Mheshimiwa rais nimekupigia kukujulisha kwamba tayari tumempata MathewMulumbi” “Mmempata MathewMulumbi? “Ndiyo mheshimiwa rais,tumempata Mathewhivi sasa anapelekwa kitalu 1” “Kazi nzuri sana Devotha.Huyo ndiye aliyekuwa anatunyima usingizi na baada ya kumpata sasa tunaweza kupumua.Devotha hakikisha unatumia vyema nafasi hii kumfungua Olivia.Naendelea kukumbusha tena kwamba MathewMulumbi ni mtu hatari hivyo kila aina ya tahadhari inapaswa kuchukuliwa” Dr Evans akamuelekeza Devotha mambo kadhaa wakaagana
Wakati suala la kutekwa kwa Dr Olivia Themba likiendelea kuchukua sura mpya baada ya baba yake Agrey Themba naye kutekwa,katika mpaka wa Namanga basi la Mkombozi luxury linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Nairobi lilifanikiwa kuvuka mpaka na kuingia Tanzania.Abiria walipewa dakika chache za kujisaidia na mmoja kati ya abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo akashuka na kuwasha simu yake akatafuta namba Fulani akapiga “Hallo” akasema mtu aliyepokea simu upande wa pili “Fahad nimekupigia kukujulisha kwamba tumekwisha vuka mpaka na tayari tumeingia Tanzania” akasema mtu yule aliyepiga simu “Karibuni sana Tanzania.Tunawasubiri Dar es salaam.Maandalizi yanaendelea kwani kila kitu kinatakiwa kumalizika usiku wa leo” akasema Fahad na kukata simu MPENZI MSOMAJI SIRI KUBWA BADO IMETANDA KATIKA SUALA LA KUTEKWA DR OLIVIA NA BABA YAKE AGREY THEMBA.USIKOSE SEHEMU IJAYO………………
Jumba la bilionea Agrey Themba lilikuwa na mfumo wa kisasa kabisa wa ulinzi.Kulikuwa na kamera za siri katika sehemu mbali mbali za jumba lile ambazo zilimuwezesha mtu aliyeko ndani ya chumba kikubwa kulala cha Agrey kufuatilia kila kinachoendelea kuzunguka jumba lake.Lucy Themba alikuwa ameketi kitini chumbani kwake akimfuatilia Mathew Mulumbi katika kamera toka alivyoingia sebuleni na hadi alipovamiwa ghafla na kuchukuliwa. “Nilifanya kosa kubwa sana kumuamini huyu kijana.Akili yangu haikuwa sawa ndiyo maana aliponiaminisha tu kuwa yeye ni mpelelezi na anafahamu mahala alipo Olivia nikamuamini haraka na kumtuma akamtafute mwanangu sikujua kumbe ninamtuma chui kwenda kuniletea kondoo wangu.Naamini baada ya kumkamata leo ufumbuzi wa wapi walipo mwanangu Olivia na mume wangu Agrey utapatikana.Huyu kijana anafahamu kila kitu na lazima ataeleza” akawaza Lucy Themba huku akishuhudia Mathew akivishwa mfuko kichwani na kutolewa sebuleni,akahamia katika kamera nyingine akashuhudia akipakiwa garini na magari yakaondoka. “Huyu kijana ni hatari sana.Alitumia akili sana kumteka mume wangu na hata mimi nimenusurika pale alipotaka kunihamisha kunipeleka sehemu anakodai ni sehemu salama.Nilifanya vyema kukataa kwani na mimi hivi sasa ningekwisha ungana na akina Olivia huko waliko.Kuna nini anakitafuta kwetu? Anahitaji fedha?Kama ni fedha kwa nini hataki kuwa wazi tumpatie kuliko kuendelea kututesa namna hii? Au kuna watu wanamtumia ili kututesa namna hii? Lakni leo kila kitu kitajulikana baada ya kuhojiwa” Akawaza Lucy na kuchukua simu akampigia Dr Evans “Lucy nipe mrejesho mambo yamekwendaje?akauliza Dr Evans “Dr Evans mambo yamekwenda vizuri kama tulivyopanga.Nimempigia simu Mathew na kumtaka afike hapa nyumbani na akafika bila kuchelewa.Wale watu uliowatuma walijipanga vyema na kumvamia akashindwa afanye nini wakamfunga pingu na hivi tunavyoongea wameondoka naye”akasema Lucy Dr Evans akashusha pumzi baada ya kupewa taarifa ile. “Lucy nakushukuru sana kwa kusaidia huyu jamaa amepatikana.Ni mtu muhimu sana ambaye ninaamini atatupa maelezo yote kuhusiana na kutekwa kwa Olivia na Agrey.Nina uhakika mkubwa kwamba huyu jamaa anashirikiana na watekaji na anazo taarifa zote za kinachoendelea hivyo atahojiwa na ataeleza kila kitu.Ninachokuomba Lucy endelea kuwa mvumilivu kwa wakati huu ambao tunaendelea kushughulikia suala hili.Nitawasiliana na mkuu wa jeshi la polisi na kumjulisha kuhusu kupotea kwa Agrey Themba.Watakuja hapo nyumbani askari polisi kukuhoji lakini usiwaeleze kitu chochote kuhusiana na Mathew Mulumbi.Waeleze kwamba Agrey alikuaga usiku wa jana kuwa anakwenda kuonana na mtu Fulani lakini hakukueleza ni wapi anakwenda na hakurejea nyumbani hadi kulipopambazuka na simu yake haipatikani ndipo uliponipigia mimi simu kunijulisha kupotea kwake.Narudia kukusisitiza Lucy usitamke lolote kuhusu Mathew Mulumbi.Kuna tatesi nimezipata ambazo ninazifanyia kazi kuwa watekaji wana watu wao ndani ya jeshi la polisi ndiyo maana sijataka kuwashirikisha suala hili la Mathew.Wale waliomchukua ni walinzi wangu na watamuhoji ataeleza kila kitu.Tukijua mahala alipo Olivia na baba yake ndipo tutawataarifu polisi wakawachukue lakini kwa hili la Mathew litaendelea kubaki siri.Nadhani umenielewa Lucy”akasema Dr Evans “Dr Evans nimekuelewa usiwe na wasiwasi.Nitatoa maelezo kama ulivyonielekeza.Nashukuru sana kwa namna ulivyojitolea kuisaidia familia yangu.Naomba ufanye kila linalowezekana leo hii Agrey na Olivia wapatikane” akasema Lucy Themba “Ninakuahisi Lucy,huyu jamaa lazima atahojiwa na ataeleza kila kitu.Nina uhakika mkubwa sana wa kuwapata Olivia na Agrey siku ya leo” “Jambo lingine Dr Evans naomba atakachowaeleza huyu jamaa na mimi nikifahamu.Naamini hayuko peke yake,kuna watu nyuma yake anaomtuma afanye haya anayoyafanya hivyo nataka kuwajua watu hao ni akina nani wanaotuandama kiasi hiki.” akasema Lucy “Hilo ni moja wapo ya mambo tutakayomuhoji huyu jamaa.Hata mimi naamini hayuko peke yake hivyo tutamtaka atueleze watu anaoshirikiana nao.Tutaufahamu mtandao wake wote na nitakujulisha.Lucy kwa mara ya mwisho ninarudia tena kukusisitiza kwamba usimweleze mtu yeyote yule kuhusu Mathew Mulumbi”akasisitiza Dr Evans “Usihofu Dr Evans siwezi kumweleza mtu yeyote” “Ahsante Lucy.Nitawasiliana nawe tena baadae kukupa mrejesho wa mahala tulikofikia” “Nitashukuru sana Dr Evans” akasema Lucy na kukata simu Wakati Lucy na Dr Evans wakiwa katika mazungumzo,gari lililomchukua Mathew lilikuwa katika mwendo mkali.Mathew alikuwa amelazwa chini amefungwa barabara na mitutu minne ya bunduki ikiwa imemuelekea.Wale jamaa hawakutaka kufanya kosa hata dogo kwani walikwisha onywa yule ni mtu hatari “Hiki kilichonitokea ni kweli au niko ndotoni? Siamini kama kweli nimetekwa” akawaza Mathew na kurudisha kumbu kumbu namna tukio lile lilivyotokea.Akauma meno kwa hasira “Sikuwa na mawazo yoyote kama tukio hili lingetokea.Ruby alikwisha hisi kitu Fulani kufuatia mwito ule wa Lucy Themba lakini mimi sikuwa na wasi wasi wowote.Nilimuamini Lucy na sikuwa na shaka naye hata kidogo ndiyo maana niliitika wito wake haraka sana aliponiita.Nilifanya makosa kutostuka kuwa ule ulikua ni mtego ule ambao naamini hata Lucy Themba ameshiriki kuuandaa.Niliwatazama hawa jamaa walioniteka naamini ni kikundi kimoja na wale niliowaua kule Kigamboni jana usiku ambao kwa mujibu wa Ruby ni idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Hawa ndio wamemteka Olivia na ninaamini hata Agrey Themba ametekwa na wao pia.Bado ninaendelea kuamini lazima yupo mtu ambaye ana mahusiano na idara hii ya siri na vile vile ana ukaribu mkubwa na familia ya akina Olivia kiasi kwamba anafahamu kila kinachoendelea.Naamini mtu huyo ndiye aliyesuka mpango huu wa mimi kukamatwa baada ya kupata taarifa zangu kuwa tayari ninafahamu mahala alipo Olivia.Ninachojiuliza kwa nini Lucy Themba akakubali kutumiwa na huyo mtu na kushiriki katika kuandaa mtego huu ili nikamatwe wakati nimejitolea kumtafuta mwanae na mume wake?Ninashindwa kuelewa je alifanya hivi kwa shinikizo? Je na yeye pia ametekwa na hawa watu wakamlazimisha anipigie simu? Mathew akaendelea kujiuliza maswali “Kadiri muda unavyokwenda suala hili nalo linaendelea kuwa kubwa.Ninajiuliza nini sababu ya hii inayoitwa idara ya siri ya usalama wa ndani ya nchi kuiandama familia ya Agrey Themba? Walianza kumteka Olivia,akafuata baba yake Agrey na sasa wamenipata mimi ambaye tayari ninafahamu nani waliomteka Olivia.Ninaanza kupata picha kwamba kuna siri kubwa imejificha katika suala hili.Si rahisi Olivia na baba yake wakatekwa na idara ya serikali kama hakuna jambo kubwa lazima ipo sababu ambayo natakiwa kuifahamu.Yawezekana labda Agrey Themba anajihusisha na mambo haramu na ndiyo maana wamemteka ili kumfanyia mahojiano.Kama si sababu hiyo basi ipo sababu nyingine kubwa iliyopelekea Agrey na mwanae Olivia watekwe.Ili kufahamu siri iliyojificha katika sakata hili lazima nitafute namna ya kujiokoa kutoka katika mikono ya hawa jamaa.Vile vile natakiwa kumuokoa Olivia na familia yake na hapo ndipo nitakapoupata ukweli.Hawa jamaa wamekwisha elezwa mimi ni mtu hatari ndiyo maana wananilinda namna hii na ninaamini huko wanakonipeleka watanihoji na kunitesa sana lakini nikipata nafasi hata ndogo lazima niitumie kikamilifu kujiokoa”akawaza Mathew
Jengo la ghorofa sita lililojengwa mita chache kutoka bahari ya Hindi limekuwa likizua maswali mengi kutoka kwa watu wakitaka kumfahamu mmiliki wake na wengi wakitaka kufahamu mmiliki wake alipataje kibali cha kujenga jengo sehemu ile.Mjadala kuhusiana na jengo lile ambalo kwa muonekano wake ni kama jengo la hoteli ya kifahari ulimalizika kimya kimya na ujenzi wa jengo lile ukaendelea hadi lilipomalizika.Kitu ambacho kiliendelea kuzusha maswali hata baada ya jengo lile kubwa na zuri sana kumalizika ni kutokuonekana shughuli yoyote ikiendelea zaidi ya watuna magari kuonekana wakiingia na kutoka pamoja na uwepo wa ulinzi mkali.Kitu ambacho wengi hawakukifahamu kuhusu jengo lile ni kwamba jengo lile halikuwa jengo la hoteli au ofisi bali jengo lile lilikuwa chini ya idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi na lilijulikana kama kitalu 1. Magari matatu ambayo mojawapo alikuwemo Mathew Mulumbi yalifunguliwa geti la jengo lile yakaingia ndani na kuvuka geti la pili hadi katika jengo,lango lingine likafunguliwa yakaingia chini katika maegesho.Mathew akafunguliwa pingu za miguu akashushwa ndani ya lile gari akaingizwa ndani ya jengo.Bado aliendelea kulindwa.Hawakutaka kumpa hata nafasi ndogo.Waliingia ndani ya lifti iliyowashusha chini umbali wa mita mia moja.Lango la chumba kimoja likafunguliwa akaingizwa ndani. Miguu yake ikafungwa na minyororo mizito halafu akasikia lango linafungwa watu wale wakaondoka.Bado aliendelea kufunikwa mfuko ule mweusi kichwani. “Hapa wamenileta wapi? Akajiuliza Mathew baada ya wale jamaa kuondoka na kumuacha mle ndani peke yake “Nisipofanya juhudi za kujiokoa kutoka katika mikono ya hawa jamaa ninaweza kujikuta katika matatizo makubwa.Nikipata hata nafasi ndogo tu lazima niitumie kikamilifu.Ili kuifahamu siri iliyojificha nyuma ya sakata hili lazima nihakikishe ninatoka humu na kuwaokoa Olivia na baba yake” akawaza Mathew Ndani ya chumba kimoja watu sita wakiongozwa na Kaiza walikuwa wanamuangalia Mathew kupitia kamera zilizomo ndani ya chumba alimowekwa. “Tunatakiwa kuanza kumtesa taratibu wakati tunamsubiri Devotha.Tuanze na baridi” akasema Kaiza aliyekuwa amevaa suti ya rangi ya kijivu. Mabomba ya maji yaliyokuwamo ndani ya chumba alimowekwa Mathew yakafunguka na kuanza kumwaga maji ya baridi sana.Mathew aliloa chapa chapa na kuanza kutetemeka kwa baridi kali.Baada ya dakika kadhaa maji yale yakaacha kutoka na ikatokea baridi kali sana.Mathew alihisi viungo vyake vyote vinaganda. “Imetosha tumpe muda wa mapumziko” akasema Kaiza na mashine ile yenye kupeleka ubaridi ndani ya kile chumba ikazimwa lakini bado Mathew aliendelea kutetemeka kwa baridi kali. “Atolewe mle apelekwe chumba cheupe” akasema Kaiza.Baada ya muda mfupi lango la chumba kile alimo Mathew likafunguliwa wakaingia watu sita watatu kati yao wakiwa na silaha.Mathew akatolewa ndani ya kile chumba akavuliwa ule mfuko mweusi kichwani akavuliwa mavazi yake akavishwa mavazi meupe akatolewa ndani ya kile chumba akapelekwa katika chumba chenye weupe mkali.Kila kitu kilichokuwamo mle ni cheupe.Akafungwa mikono katika meza wakamuacha mle ndani peke yake “Ninahisi baridi kali mno.Sijawahi kuhisi baridi ya namna hii toka kuzaliwa kwangu.Najua hizi ni mbinu zao za kunitesa lakini hawatafanikiwa.Nimepitiam ateso mengi zaidi ya haya,wanajisumbua bure” akawaza Mathew ***************** Jua lilipochomoza lilimkuta tayari Devotha Adolph amekwisha wasili kitalu 2 mahala alikohifadhiwa Olivia na baba yake Agrey.Bado wataalamu wa mawasiliano wa idara yake waliendelea na zoezi la kuhakikisha mtandao mpya wa mawasiliano unakamilika.Devotha akawasalimu na kuelezwa kile kilichokuwa kinaendelea akaelekea ofisini kwake.Mara tu alipoketi kitini akampigia simu Kaiza “Hallo Devotha” akasema Kaiza baada ya kupokea simu “Kaiza mnaendeleaje huko? “Huku tunaendelea vyema kabisa.Tayari tumeanza kumpa Mathew mateso taratibu.Tumeanza na baridi kali,tayari tumemtoa kwenye baridi na kumpeleka katika chumba cheupe.”akajibu Kaiza “Good.Mmefanya kazi nzuri sana Kaiza.Huyo ni mtu wa muhimu sana kwetu” “Unakuja saa ngapi huku Devotha?akauliza Kaiza “Niko hapa kitalu 2 nataka kuendelea na zoezi la kumfungua Olivia na vile vile nitazungumza na baba yake kama kuna kitu chochote anakifahamu kuhusu mwanae.Endeleeni kumpa mateso Mathew na nikitoka huku nitakuja huko mara moja.Kwa sasa hatuna tena hofu,aliyekuwa anatupa hofu ni huyo Mathew ambaye tayari tunaye mikononi mwetu” akasema Devotha “Sawa Devotha tunakusubiri” akasema Kaiza na Devotha akakata simu “Leo ninajihisi mwenye amani sana baada ya Mathew kukamatwa.Nitaifanya kazi yangu kwa Amani.Nataka kubadili namna ya kumuhoji Olivia.Kutumia nguvu hakutasaidia kumfungua” akawaza Devotha akachukua simu akapiga na kuomba kuunganishwa na chumba cha Olivia.Baada ya sekunde chache akaunganishwa na kamera zilizopo katika chumba alimolala Olivia. Olivia alikuwa amelala katika chumba kizuri na kitanda safi.Hakuwa amefungwa pingu mikononi wala miguuni.Alionekana mwingi wa mawazo_Olivia akampigia simu Jasmin na kumtaka afike oisini kwake haraka “Jasmin leo tunabadili mbinu za kumuhoji Olivia.Hatutaendelea na taratibu zetu za kutumia mabavu hivyo nataka tumuonyeshe kwa sisi si watu wabaya.Nataka tumfanye aamue mwenyewe kwa hiyari yake kufunguka na kushirikiana nasi.Nataka uende chumbani alimo mpelekee mavazi mazuri,hakikisha ameoga na kisha andaa kifungua kinywa kwa ajili yangu naye” akasema Devotha na Jasimn akaenda kutekeleza maagizo aliyopewa.Olivia alipelekwa bafuni kuoga,akatibiwa jeraha alilochomwa kisu pajani,kisha akapewa mavazi mazuri ya kuvaa.Wakati yote haya yanafanyika Devotha alikuwa akishuhudia kupitia kamera na kila kitu kilipokamilika akaelekea katika chumba cha chakula ambako kuliandaliwa kifungua kinywa maalum kwa ajili yake na Olivia.Akampigia simu Jasmin na kumtaka ampeleke Olivia katika chumba cha chakula.Olivia alistuka na kupandwa na hasira baada ya kumkuta Devotha akiwa amekaa katika chumba kile cha chakula akitabasamu “Hallo Olivia” akasema Devotha.Olivia akasimama na kumtazama Devotha kwa hasira.Devotha akasimama na kuvuta kiti “Karibu Olivia.Karibu tupate kifungua kinywa” akasema Devotha “I’m not hungry!! Akasema Olivia na kumgeukia Jasmin “Take me back to my room” “Olivia come and join me here, this is an order!! Akasema Devotha kwa ukali.Mmoja wa walinzi waliokuwa nyuma ya Olivia akamshika mkono na kumkalisha kitini “Please madam usifanye mambo yakawa magumu kwako.Fanya utakavyoelekezwa” akasema yule mlinzi na Olivia akaketi huku akiendelea kumtazama Devotha kwa macho yaliyojaa hasira.Dr Olivia na Devotha wakanywa chai kimya kimya na baada ya kumaliza Devotha akasema “Olivia let’s take a walk” Olivia akainuka na kuongozana na Devotha wakaenda katika bustani ndogo kulikokuwa na sehemu nzuri ya kukaa kupumzika.UKimya wa dakika mbili ukapita kisha Devotha akasema “Unaendeleaje Olivia?akauliza Devotha lakini Olivia hakumjibu kitu. “Olivia I’m sorry for what I did to you yesterday” akasema Devotha na Olivia akaonekana kupandisha hasira zaidi “You are sorry?akauliza “With my own two eyes I watched you shot my father twice .What kind of a woman are you?akauliza Olivia kwa ukali Devotha akamtazama kwa muda halafu akasimama “Niangalie vyema” akasema “I’m a very sexy woman.Najifahamu mimi ni mzuri kukushinda hata wewe lakini umejiuliza kwa nini mwanamke mwenye uzuri kama wangu nikawa mkatili?Ulichokishuhudia jana si kitu.Bado haujauona ukatili wangu.Nilikwambia kwamba wananiita shetani wa kike.Unadhani ni kwa nini nimefikia hapo nilipofika?akauliza Devotha lakini Olivia hakujibu kitu. “Uso wangu umejaa tabasamu kila wakati lakini si tabasamu la furaha.Do you think when I smile I’m happy?akauliza na kuendelea kumtazama Olivia ambaye bado alikuwa kimya “I’m not happy.I’ve never been happy in my life.Tabasamu hili ni uumbaji wa Mungu lakini ndani mwangu hakuna furaha hata chembe.Ninapata kila ninachokihitaji katika maisha yangu,I have money,jewels,expensive cars,houses, but I’m not happy.Umejiuliza kwa nini? Akauliza Devotha na kuvuta pumzi ndefu.Akatoa miwani aliyoivaa na kuiweka mezani “Nitazame vizuri macho yangu” akasema Devotha lakini Olivia hakusumbuka kuinua kichwa chake kumtazama “Olivia nitazame machoni tafadhali!! Akasema Devotha na Olivia akainua kichwa akamtazama Devotha “Kuna kitu umekigundua? akauliza Devotha lakini Olivia akabaki kimya “Umegundua kitu chochote kisicho cha kawaida?akauliza lakini Olivia akaendelea kuwa kimya “Kama umeshindwa kugundua nitakueleza” akasema Devotha “Nina jicho moja linalofanya kazi.Jicho la kushoto ni bandia na halina kazi yoyote.Ukinitazama ni vigumu kuamini kwamba ni natumia jicho moja” akasema Devotha na kuvaa miwani yake “Umewahi kujiuliza kwa nini kila unaponiona ninakuwa na glovu mkono wangu wa kushoto? Unadhani ni urembo? akauliza Devotha na kuvua glovu yake aliyovaa mkono wa kushoto “Unaona mkono wangu ulivyo?akauliza.Mkono wa kushoto wa Devotha ulikuwa na vidole vitatu pekee. “Nina vidole vitatu katika mkono wangu wa kushoto.Ninavaa hii glovu ambayo imetengenezwa maalum ili nionekane nina vidole timilifu lakini sina vidole viwili” akasema Devotha na kuvaa glovu yake halafu akafungua mkoba na kutoa albamu la picha akampa Olivia aangalie “Tazama hizo ni picha zangu za zamani” akasema Devotha. “Picha zako zitanisaidia nini? akauliza Olivia “Fungua tazama” akasema Devotha na Olivia akafungua ukurasa wa kwanza wa albamu lile akazitazama picha mbili kubwa na sura yake ikaonyesha mshangao kidogo akaendelea kufunua kurasa kwa kurasa na alipomaliza akalifunga lile albamu “This is stupid!! Akasema Olivia na kuiweka mezani ile albamu “Umegundua nini Olivia?akauliza Devotha “Stop wasting my time Devotha.Unanipima akili yangu?akauliza Olivia “Nieleze umeona nini katika hizo picha?Devotha akauliza.Olivia akamtazama kwa muda halafu akasema “Nimemuona msichana ambaye hafanani kabisa na wewe.Naomba usitake kucheza na akili yangu Devotha” akasema Olivia “Huyo unayemuona katika hizo picha ni mimi”akasema Devotha “Nimekwambia usitake kuijaribu akili yangu Devotha.Aliyeko katika picha hizi na wewe ni watu wawili tofauti kabisa”akasema Olivia “Uko sahihi Olivia.Kwa kutazama picha za kwenye albamu na kunitazama mimi ni watu wawili tofauti kabisa lakini ni mtu mmoja ambaye ni mimi” akasema Devotha na kunyamaza kimya kwa sekunde kadhaa halafu akasema “Olivia umejiuliza kwa nini nimekueleza haya yote?akauliza Devotha.Olivia hakujibu kitu alikuwa anachezea vidole vyake “Nisikilize vyema” akasema Devotha “Picha hizo ulizoziona ni wakati nikiwa msichana mdogo.Wazazi wangu walikuwa masikini.Hatukuwa na nyumba,tuliishi katika nyumba za kupanga.Katika harakati za kutafuta maisha baba alijikuta akifika hadi nchini Kenya na kupata kazi katika shamba moja kubwa la uzalishaji maua.Ililazimu familia yetu kuhamia Kenya kumfuata baba.Katika sehemu tuliyokuwa tukiishi nchini Kenya nilipata rafiki aliyeitwa Halima.Huyu alikuwa msomali.Wazazi wake walihama kutoka Somalia na kuishi Kenya.Familia yao na yetu tulikuwa na ukaribu mkubwa.Siku moja wakati tukitoka shule Halima aliniambia kwamba baba yake anamtengenezea chombo ambacho kitampeleka peponi.Nilikuwa mdogo bado lakini katika mafundisho niliyopewa na walimu wa dini nilifahamu wanaokwenda peponi pekee ni wale waliokufa.Nilimtaka akanionyeshe chombo hicho ambacho kitampeleka peponi.Kabla wazazi wake hawajarejea kutoka katika mihangaiko yao ya siku Halima akanipeleka katika chumba ambacho baba yake alikuwa anamtengenezea chombo cha kumpeleka peponi.Alinionyesha chombo chenyewe kilichokuwa juu ya meza.Lilikuwa ni bomu likitengenezwa la kujitoa mhanga.Toka nikiwa mdogo nilipenda sana kutazama filamu mbalimbali hasa za mapambano na magaidi na niligundua lile lilikuwa bomu ,niliogopa sana nikamdanganya kwamba ninakwenda kuwaita wazazi wangu ili waje waone kifaa kile na mimi wanitengenezee chombo kama kile cha kunipeleka peponi ili ikiwezekana tuende pamoja mimi na yeye.Nilikimbia nyumbani nikawachukua wazazi wangu tukaenda hadi katika chumba kile cha baba yake Halima na tukamkuta tayari Halima amekwisha livaa lile bomu na akasema anataka kuwaonyesha wazazi wangu namna kifaa kile kinavyofanya kazi.Baba alimsihialivue lakini Halima akagoma,baba akamfuata ili amvue lile bomu lakini alichelewa Halima alibonyeza kilipuzi na moto mkubwa ukatokea” akanyamaza Devotha na kuinamisha kichwa kwa muda “I’m sorry sipendi kulikumbuka tukio lile ni moja ya tukio linaloniumiza mno katika maisha yangu.Picha ya moto ule mkubwa haijawahi kunitoka katika akili yangu” akanyamaza tena “Pole sana” akasema Olivia akionekana kuguswa na taarifa ile ya Devotha “Wazazi wa Halima walikuwa ni wafuasi wa kikundi cha Alshabaab cha Somalia na walikuwa wanajiandaa kufanya shambulio kwa kumtumia Halima.Wazazi wangu wote wawili walipoteza maisha pale pale.Halima naye alifariki akiwa angali msichana mdogo.Mimi sikuwa natazamika,niliharibika vibaya sana.Serikali ya Marekani waliamua kunichukua na kugharamia matibabu yangu.Nilipelekwa Marekani kwa matibabu ambako nilifanyiwa operesheni thelathini na saba hadi kufikia hali hii niliyonayo leo ndiyo maana unaona muonekano wangu wa sasa na ule wa kwenye picha ni tofauti.Baada ya kupona niliendelea na masomo nchini Marekani na baadae nikasomea masuala ya kupambana na ugaidi.Nilisomeshwa na kufanya kazi katika idara ya kupambana na ugaidi ya Marekani.Nikiwa kule niliendelea kufuatilia taarifa za nyumbani Tanzania na nilisikia kuhusu kuanza kuchomoza kwa vikundi vyenya viashiria ya ugaidi nchini Tanzania.Niliwasiliana na Rais nikampa wazo la kuanzisha idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Rais Dr Evans alikubali wazo langu nikarejea nchini kuanzisha idara hii na japo imeanzishwa ndani ya muda mfupi lakini tayari kazi tuliyoifanya ni kubwa.Tumefanikiwa kufyekelea mbali vile vikundi vyote vyenye muelekeo wa kigaidi vilivyoanza kuchomoza na hadi sasa hujasikia tena tishio lolote la kuibuka kwa vikundi vya kigaidi.”akatulia tena na kumtazama Olivia “Olivia nimekueleza haya yote kwa sababu nataka utambue ni namna gani ninawachukia magaidi.Ni kwa sababu yao leo hii maisha yangu hayako sawa.Maisha yangu hayana furaha hata chembe.Ni kwa sababu ya magaidi leo hii niko peke yangu katika hii dunia sina baba ,mama wala ndugu yeyote I’m all alone.Nimeshuhudia unyama unaofanywa na magaidi toka nikiwa mdogo.Asubuhi ya Jumanne ya 11 September 2011 nilikuwepo jijini New York wakati kikundi cha kigaidi cha Alqaeda kiliposhambulia majengo pacha ya kituo cha kibiashara cha kimataifa na kusababisha watu wapatao elfu tatu kupoteza maisha na maelfu wengine kujeruhiwa.Yawezekana unafahamu kupitia mitandao na vyombo vingine vya habari lakini mimi nilikuwepo eneo la tukio na nilishuhudia unyama ule kwa macho yangu.Ukiacha tukio hilo nimeshuhudia matukio mengine mbali mbali ya kigaidi yanayofanywa na vikundi mbali mbali vya kigaidi duniani hivyo sina huruma hata kidogo na watu hawa” akasema Olivia “Baada ya jitihada za muda mrefu hatimaye serikali ya Marekani walifanikiwa kumuua kiongozi mkuu wa kikundi cha Alqaeda ambacho kilikuwa kinaongoza mashambilizi ya kigaidi na kuua watu wengi duniani.Kuuawa kwa kiongozi huyo na wengine kadhaaa kulilifanya kundi la Alqaeda likose nguvu na kufifia lakini kwa sasa limeibuka kundi la IS ambalo limekuwa likifanya mashambulio mengi sehemu mbali mbali duniani na kuua watu wengi wasio na hatia na wameapa kuendelea kufanya mashambulio na kuua watu hadi pale bendera yao itakapopepea kutoka mashariki hadi magharibi mwa dunia.Nilipogundua kuwa una mawasiliano na watu walio katika mtandao wa IS nilistuka sana na kupata hasira nyingi.Nilijuliza maswali mengi kuhusu ukaribu wako na hawa watu.Kama nilivyokueleza awali kwamba ninawachukia magaidi na wewe pia uliingia katika orodha ya maadui zangu lakini nikikutazama machoni Olivia hauonekani kama ni gaidi.Hauna sifa za kuwa gaidi.Nataka kufahamu kitu gani kinaendelea kati yako na hawa watu wa IS? Olivia wewe u mwanamke mwenye heshima kubwa hapa Tanzania kutokana na shughuli yako unayofanya ya kuokoa maisha ya watu na hata kesho ukitaka kugombea urais watanzania hawatakuwa na sababu ya kutokukuchagua kutokana na sifa yako iliyotukuka.Familia yako pia ina sifa nzuri lakini haya yote yanaharibiwa na jambo moja tu nalo ni ushirika wako na watu wa kikundi cha kigaid cha IS.Olivia nataka kuwa rafiki yako badala ya adui.Nataka nikusaidie sipendi kukutesa mtu kama wewe lakini nitakusaidia pale tu utakapokuwa tayari kunieleza ukweli wote kuhusu wewe na IS.Sipendi kuendelea kukushikilia hapa kukutesa,kumtesa baba yako nataka tulimalize suala hili kwa amani ili maisha yaendelee” akasema Devotha na kutulia akaangalia juu kundi la ndege lilikuwa linapita.Ulipita ukimya wa dakika mbili “Olivia please” akasema Devotha “Devotha umejitahidi sana kunishawishi nikueleze kila kitu lakini kabla sijakueleza chochote kuna kitu nakihitaji kujua kutoka kwako” akasema Olivia “Sema Olivia unahitaji nini?Ninakuahidi chochote ukitakacho kama kiko ndani ya uwezo wangu nitakupatia” akasema Devotha.Olivia akamtazama na kusema “Nataka kujua mahala aliko Edger Kaka.Ukinipa taarifa hizo na ukanisaidia kumpata ninakuahidi kukueleza kila kitu unachokitaka” akasema Olivia.Devotha akavuta pumzi ndefu na kusema “Olivia my dear,Edger Kaka hayuko hai.Amekwisha fariki miaka mitatu iliyopita na kilichobaki hivi sasa ni mifupa yake tu.Labda kama unataka nikupeleke mahala lilipo kaburi lake” akasema Devotha “Devotha ninayasoma mawazo yako,kila ninapowaeleza kuhusu suala hili unaamini nina matatizo ya akili.Naomba nikutoe wasiwasi kwamba mimi ni mzima sina tatizo lolote la kiakili.Ninachokisema nina uhakika nacho” akasema Olivia “Olivia kila atakayesikia suala hili ataamini una matatizo ya akili kwa sababu Edger amekwisha fariki na wewe mwenyewe ndiye uliyetambua mwili wake hospitali”akasema Devotha “Wote tuliaminishwa hivyo kwamba Edger amekufa lakini naomba ufahamu Devotha kwamba mwili ule uliozikwa haukuwa mwili wa Edger Kaka” “That’s not true Olivia” akasema Devotha “It’s true and I have proof” “What proof? “Nimefanya vipimo kwa kutumia masalia ya mwili ule ambao wote tunaamini ni wa Edger na majibu yamenionyesha kwamba mwili ule haukuwa wa Edger” “That’s a lie Olivia.That’s not true.Edger Kaka is dead” akasema Devotha “Sikudanganyi Devotha ninachokwambia ni ukweli mtupu.Wote tumeaminishwa hivyo kwamba Edger alifariki katika ile ajali lakini ukweli ni kwamba Edger yuko hai anashikiliwa sehemu Fulani” akasema Dr Olivia “Olivia do you think I can believe you?akauliza Devotha “Believe me or not but that’s the truth Edger is still alive.Kama unataka nikueleze yote unayohitaji kuyajua kuhusu IS nipe taarifa za alipo Edger” akasema Olivia na Devotha akaendelea kumuangalia “Najua huniamini Devotha lakini nitakupa maelekezo ambayo ukiyafuatilia utagundua hiki ninachokueleza ni kitu cha kweli.Katika kaburi la Edger upande wa kulia ukichunguza vizuri utagundua kumechimbwa na ukifukua eneo hilo utakuta kuna tobo kubwa lililotobolewa katika ukuta wa kaburi.Mimi ndiye niliyetoboa tobo hilo kwa ajili ya kuingia ndani na kuchukua sampuli za mabaki ya mwili ule nikaenda kufanya vipimo na kugundua mwili ule haukuwa wa Edger Kaka.Kama ukitaka unaweza ukachukua sampuli za mwili ule pia na kwenda kuufanyia uchunguzi na ninakuhakikishia majibu utakayoyapata ni kama haya ninayokwambia kwamba mwili ule haukuwa wa Edger Kaka.Devotha kuna siri kubwa hapa ambayo huifahamu na kama ukitaka kuifahamu nisaidie kujua mahala alipo Edger Kaka.Nakuhakikishia ni siri kubwa” akasema Olivia Baada yatafakari ya muda Devotha akasema “Olivia natamani sana nikuamini lakini nafsi yangu inasita kabisa” “C’mon Devotha.Unadhani ningeibuka tu na kudai Edger yuko hai kama sina uhakika? Ninao uhakika mkubwa kwamba yuko hai ndiyo maana mtoto wa Rais amechomwa sindano yenye virusi ili kumshinikiza Rais aweze kunipa maelezo ya mahala alipo Edger.Sijakurupuka Devotha” akasema Olivia “Kwa nini umemlenga Rais moja kwa moja katika suala hili?Kwa nini unataka kumchafua rais kwa jambo hili ambalo halina ukweli wowote?akauliza Devotha “Rais ninamuita baba.Amekuwa ni rafiki mkubwa wa baba yangu toka wakiwa wadogo lakini jiulize kwa nini nikatengeneza virusi ambavyo vinaweza kumuua mtoto wake Coletha ambaye ananiita dada?Nimefanya hivi kwa kuwa ninafahamu rais anazo taarifa za jambo hili na nimefanya hivi ili kumshinikiza anipe taarifa hizo” akasema Olivia “Olivia naomba tuachane na hilo la Edger.Nataka tuzungumze masuala mengine.Nataka unieleze kuhusu mahusiano yako na IS.Umeonekana ukiwa na Seif Almuhsin na vile vile umekuwa na mawasiliano na Sayid Omar.Nataka kuf…………..” “Hakuna haja ya kwenda mbali Devotha.Sintaweza kukueleza chochote.Kama nilivyokueleza kuwa nitazungumza nawe pale ambapo utanipa taarifa za mahala alipo Edger Kaka.Kama hakuna taarifa hizo hakuna nitakachoweza kukwambia.Mmekosea sana kumteka hata baba yangu ili kunilazimisha niongee lakini nawahakikishia hata kama mtatishia kuua familia yangu nzima mbele yangu sintafumbua mdomo wangu kutamka chochote.Muacheni baba aende zake muendelee kunishikilia mimi” akasema Olivia “One more thing.Fikisha salamu zangu kwa Rais kwamba muda unakwenda na asipofanya juhudi atampoteza mwanae.Mimi ndiye niliyetengeneza virusi hivyo alivyoambukizwa mwanae na ndiye mwenye uwezo wa kumtibu.Asisumbuke kutafuta tiba hospitali kwani atampoteza mwanae.Anachotakiwa kufanya ni kunionyesha mahala alipo Edger na mimi nitamponya mwanae.Devotha nadhani hatuna cha kuzungumza zaidi hapa nirejeshe chumbani nataka kupumzika mguu unaniuma” akasema Olivia.Devotha akawapa ishara walinzi watatu waliokuwa karibu akawataka wampeleke Olivia chumbani wakamfungie “Natamani sana kumpuuza Olivia na kuamini ana matatizo ya akili lakini kuna kitu kinanilazimisha intake kumuamini.Japo tunajaribu kuamini kwamba ana matatizo ya akili lakini Olivi ani mzima hana tatizo lolote.Alizungumza kwanza na Rais akamueleza jambo hilo la Edger,nilipozungumza naye akaendelea kusisitiza kuwa Edger yuko hai na leo tena ameendelea kusisitiza na amekwenda mbali zaidi akadai anao ushahidi wa kuthibitisha hicho anachokisema.Nadhani Olivia hajakurupuka katika suala hili.Ninachojiuliza kwa nini amlenge moja kwa moja Rais Dr Evans? Kuna kitu anakifahamu kuhusu jambo hili?akajiuliza Devotha “Maneno aliyoyatamka Olivia yamenishawishi kulitazama suala hili.Ngoja nitumie muda mfupi kulitazama suala hili.Nitaanza kwanza katika makaburi ya Midizini alikozikwa Edger.Nataka nikalichunguze hilo kaburi kama kweli limechimbwa” akawaza Devotha na kuelekea katika gari lake akaondoka.Moja kwa moja alielekea katika makaburi ya midizini alikozikwa Edger Kaka.Alilitafuta kaburi la Edger akalipata na kuangalia upande wa kulia mwa kaburi lile kama alivyoelekezwa na Olivia ni kweli kulionekana kama kumetitia kidogo.Akapiga picha za kutosha halafu akaondoka “Olivia anaweza kuwa sahihi.Alisema upande wa kulia mwa kaburi la Edger kumechimbwa na hata ukitazama panaonekana kweli pamechimbwa japo si hivi karibuni.Nashawishika kutaka kulifanyia suala hili uchunguzi wa kina.Yawezekasna lina ukweli ndani yake” akawaza Devotha akiwa garini “Devotha kuna siri kubwa hapa ambayo huifahamu na kama ukitaka kuifahamu nisaidie kujua mahala alipo Edger Kaka.Nakuhakikishia ni siri kubwa” akayakumbuka maneno ya Olivia “Msisitizo huu wa Olivia si wa bure.Hata mimi kuna kitu nimeanza kukiona katika maelezo yake.Michezo kama hii ya kutengeneza vifo ipo na inafanyika sana katika nchi za wenzetu zilizoendelea.Kama suala hili ni la kweli kwa nini watengeneze kifo cha Edger?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Na kama ni kweli nani waliofanya jambo hilo? Devotha akaendelea kujiuliza maswali “Najiuliza swali lingine suala hili la Edger lina maslahi gani kwa Olivia?Kwa nini alifuatilie namna hii? Je katika suala hili yuko peke yake au kuna watu wako nyuma yake? Kama wapo ni akina nani? Kweli hapa kuna siri kubwa kama alivyosema Olivia.Nitajipa zoezi la kuchunguza ili niupate ukweli wa jambo hili hata hivyo bado nitalazimika kumuhoji zaidi Olivia kuna mengi ninaweza kuyapata kwake zaidi ya hili suala la mahusiano yake na IS.Natakiwa kujenga naye urafiki badala ya kuwa adui yake.Hili halitamfurahisha Dr Evans lakini nitatafuta namna ya kufanya ili lisiweze kuleta mgongano.Dr Evans anataka majibu ya haraka kutoka kwa Olivia lakini ukimuangalia Olivia ana mambo mengi ambayo ili kuyapata hatupaswi kufanya haraka wala kutumia nguvu” akawaza Devotha
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment