Simulizi : Mzimu Umerudi Tena Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Nne (4)
Ilikuwa yapata saa kumi kasorobo! Gari aliyokuwa akiiendesha mwanadada Ashura sasa ilikuwa inaitafuta mkungugu! Mpaka hapo ismani hapakuwa mbali tena kwani mdada huyu kwenye usukani alikuwa hajambo watu wote aliopishana nao au kuwapita njiani hakuna hata aliefikiria kuwa mwendeshaji wa gari hii anaweza kuwa mwanamke maana mwendo aliokuwa nao ni kama vile wasindikizaji wa rais..!!
Ndani ya gari naonekana Ashura akipeleka simu yake sikioni huku mkono wake mmoja ukidili na usukani. Punde tu simu ikapokelewa..
" Hallow...? ''
Inasikika sauti ya kiume yenye kibesi kidogo! Bila shaka huyo ni DANIEL MASUBWA! Pande la kijana.
" Ndiyo uko wapi Dani?? ''
" Nipo hapa nyumbani tu! ''
" Tayari huku.. ''
" Oooh! Unasema kweli?? ''
" Nipo mkungugu saa hizi nakuja ''
" Weee!! ''
" Ndiyo we cha kufanya fungasha kila kilicho chako mkabidhi mwenye nyumba funguo yake na uondoke katika mazingira ambayo hakuna atakaekushtukiakama ndiyo unaiaga nyang'oro ''
" Daaah! Hapo ndipo ninapokupendeaga mimi huwa huniangushi mke wangu.. ''
" Ni maisha tu wala usihofu.. Maisha ni kutafuta.. ''
" Ni vizuri.. Je?? Ni mzigo gani huo?? Tex ama?? ''
" Tex??? We hata mlio huusikii?? Hii ni Prado moja ghari sana siyo chini ya milioni mia.. ''
" Ndiyo halafu kata simu nakaribia getini hapa kwenye mzani.. ''
" Nini?? Ushafika getini?? ''
" Hii ni kama BOENG nyepesi baraa.... ''
" Ok! Ok! Ok! Utanikuta kule kule si unapapata??? ''
" Nitaanzaje kupasahau sasa?? ''
" Poa ngoja nitangulie.. ''
" Sawa na zile plate number unazo?? ''
" Ndiyo ninazo.. ''
" Sawa ''
Mpango kabambe uliokuwa umesukwa na wawili hawa ulikuwa ni kuiba gari ambayo Ashura atakuja nayo kutoka mjini.. Wataibaje ibaje?? Tunaona huko mbeleni jinsi itakavyokuwa..
Labda kwa ufupi tupate kujua historia ya Ashura na Daniel.. Watu hawa ni wapenzi na walikuwa ni wanafunzi katika chuo kimoja maarufu huko Soweto Africa kusini, wawili hao walitokea Walikuwa ni watanzania waliokwenda nchini Africa kusini kusomea maswala ya IT, lakini walifukuzwa shule mwaka 2012 Kwa shutuma za kudukua kompyuta za walimu na kuharibu baadhi ya nyaraka za chuo zilizokuwa katika kompyuta hizo.
Daniel na Ashura walipanda ndege na kurudi Tanzania ambapo baada ya kurudi nchini vijana hawa walikuwa wamepoteza dira ya maisha kabisa! Hawakuwa na mbele wala nyuma, Mwanamo mwishoni mwa mwaka 2013 Daniel alifanikiwa kuipa Laptop moja katika moja kati ya maofisi ya watu binafsi alifanya hivyo kwa lengo flani kwani wao kompyuta zao walikataziwa kuondoka nazo Africa kusini.
Baada ya kufanya wizi Jijini Dar es Salaam Daniel alimchukua Ashura na kukimbilia Arusha kwa kukwepa kukamatwa na Askari polisi. Huko walipanga chumba na kuanza maisha mapya!
Hapo ndipo Daniel alipoanza kucheza na mitandao sasa.. Maana Africa kusini hakutoka bule! Tayari alishakuwa Hacker mzuri sana na hapo lengo lake lilikuwa ni kujaribu kudukua akaunt za watu katika mitandao ya kijamii kama Facebook n.k
Huko ali-harck sana akaunt za watu lakini hakuna alichokiambulia, ndipo alipoamua kurudi kwenye GPS Alikuwa akikusanya namba za watu huko mtandaoni na kuja kuziingiza katika GPS Lengo lake lilikuwa ni ku-track maongezi ya watu mbali mbali, na hapo alipania kunasa mazungumzo yoyote nyeti atrack na kuyalerecord ili apige kwa watu hao..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Juhudi zake zikazaa matunda, mwaka 2014 mwezi April tarehe tano alifanikiwa kunasa maongezi kati ya raia mmoja mwenye asili ya kijapan na mfanyabiashara mmoja kigogo kutoka Tanzania maongezi hayo yalikuwa yanahusu biashara ya unga (madawa ya kulevya)
Kulikuwa na takribani Kilo 10000 Za mihadarati zilizokuwa zimehifadhiwa katika mapango ya amboni, ambapo ndipo zilikuwa zikijadiliwa jinsi ya kuzitoa kule mpaka bandari ya Dar es salaam ili ziweze kusafirishwa kwenda Japan.
Hatimae mazungumzo ya wawili hao yakawa yamefika tamati, lengo waliokuwa wamelifikia kuhusu kuutoa mzigo huo kutoka Amboni Tanga mpaka Bandarini Dar es salaam ilikuwa ni kuwatafuta na kuongea na madaktari wakuu kutoka hospital ya muhimbili ili waweze kupewa AMBULACE (gari ya wagonjwa) itakayokwenda kuuchukua mzigo huo
Daniel akahifadhi record hiyo vizuri kisha akampigi uyo mwanaume, baada ya sekunde kadhaa simu ikapokelewa Sauti nzito ikasikika upande wa pili..
Alichokifanya bwana Dani ni kumtisha mtu huyo kwa kusema yeye ni mwana IT anaefanya kazi katika jeshi la wananchi, na amenasa maongezi kati yake na mjapani mmoja mda mfupi uliopita..
Mwanaume huyo alichanganyikiwa kwa kuhisi huenda ni kweli, alianza kujiuma uma, mwishowe Daniel akamwambia ikiwa anataka swala hilo lisifike mbali atoe kiasi cha Tsh 600,0000 (milioni sita) Taslimu za kitanzania na swala lingeishia pale.
Huyo mwanaume hakuamini kwani kiasi kilichotajwa ni kidogo mnoo tofauti na baadhi ya sehemu alizowahi kukamatwa na kuhonga zaidi ya milioni hamsini..
Miamala ikafanyika, pesa ikatumwa kwa njia kutuma mtu ambae alizifikisha pesa hizo ndani ya masaa 6.. Ina maana ya kwamba mfanya biashara huyo alikuwa na genge lingine la siri mkoani Arusha na pesa hiyo ilikwenda kutupwa jalalani. Watu hao waliweka pesa hizo jalalani na kutoweka kwani waliamini kuwa kweli mtu huyo aliempigia bosi wao alikuwa ni mtaalam wa kompyuta kutoka (JWTZ) Hivyo waliondoka mapema kuhofia kukamatwa.
Ashura na Dani walifika katika eneo hilo kisha Daniel akamtuma Ashura aende kubeba mfuko mweusi wenye maganda ya karanga ndani yeye akabaki kando kutizama usalama..
Walifanikiwa kuichukua pesa hiyo na kuanzia hapo wakawa ni watu hatari zaidi kwani magari mengi yalikuwa yakiibiwa na kubadilishwa plate number kisha kwenda kuuzwa sehemu nyingine..
Mwaka 2016 Daniel na mpenzi wake Ashura waliwasili mkoani Iringa kwaajili ya kufanya madili ya pesa, Walifikia nyang'oro na kuchukua chumba hapo,, machoni mwa watu hawakuonekana kuwa ni wachumba, wala hakuna aliegundua kuwa hao ni watu wenye akili ya hali ya juu! Bali Daniel alionekana ni kama mlevi mlevi tu asie na ishu yoyote..
Ashura nae alionekana kama ni mdada flani amaizing kwa starehe za kimwili, lakini licha ya kuonekana hivyo hakuna mwanaume aliekuwa akimgusa!, baadae alianza safari za kutoka nyang'oro na kuingia Iringa mjini huku akimwacha Daniel nyang'oro.
Mwishoni mwa mwaka 2018 walifanikisha kuiba tex moja ambapo haikuweza kukamatwa mpaka inapigwa bei na watu.. Ashura aliendelea kutengeneza mipango.. Mnamo tarehe 7 Mwezi December 2018 Aliweza kukutana na Patrick katika hotel moja ya kifahari sana iitwayo PATRICK HOTEL. Mwanaume huyo akadata na umbile la mwanadada huyu..
ILIKUWA NI HISTORIA FUPI YA VIJANA HAWA DANIEL NA ASHURA.
Mpaka hapo mmeshaelewa Daniel na Ashura ni watu wa namna gani?? Na wana mipango gani?? Pia mnafahamu baada ya Patrick kudata kwa Ashura nini kilitoke?? Hayo yote nimeshayazungumzia sehemu za nyuma hapa tunasonga mbele.....
***
Hatimae Ashura anafika Nyang'oro kitu cha muhimu ilikuwa ni kufika mahali walipoahidiana kukutana na Daniel, ilikuwa ni nje ya mji ambapo alimkuta Daniel akimsubili kwa hamu kubwa mno! Mara kwa mara alitamani Ashura atokee maana hapo alipo tayari ameshasuka mpango kuwa kuna Prado ya magendo inakuja na mteja ameshapata tayari..
Maraa breck chwiiii Prado kali inasimama karibu yake alishtuka na kutaka kukimbia akizani huenda ni polisi lakini mwishowe Daniel alipigwa na butwaa! Baada ya kuona mlango ukifunguliwa na Ashura kushuka hukuwa akiwa na funguo mkononi.
Daniel hakuamini macho yake kwa kile alichokuwa akikiona! Nywele zilimsisimka mnoo! Alihisi kuogopa kwani gari anayoiona mbele yake hata bei yake haijui japo ni mjanja mjanja, ila hapo kanywea!!
" Waooo!! Jamani mume wangu..!! ''
Ashura alimkimbilia na kumkumbatia kwa fulaha kubwa Daniel kakini kwa mda huo yeye alikuwa katika bumbuazi kubwa wala hakutoa ushirikiano wowote zaidi ya kutumbua macho tu!
" Dani..!! ''
" Aa'ah! Naam! ''
" Vipi mbona nakuchangamkia ila we upo kimya nini tatizo?? ''
Ashura aliuliza huku machoni akionekana kukumbwa na huzuni maana hakufurahishwa na hali ile..
" Samahani daaah!! Unajua ziliniruka kwa mda sikuwa najitambua mie.. ''
" Kwanini?? ''
" Bado siamini kama ni wewe Asha ninaekufahamu umesuka mpango mkubwa namna hii?? ''
" Hahaha... Amini hivyo ''
" Ok Hebu tusipoteze mda hapa twende na mda.. ''
" Yaah! Ndiyo hii gari nimeitorosha kwa hesabu kali sana na inatakiwa nawe ujitahidi itoke nje ya Iringa ndani ya nusu saa kuanzia hivi sasa.. ''
" Ila nakushauri twende wote tu! Hii gari nimeshasuka mpango kabambe na hivi inavyonekana umaskini bai bai na kazi hii tunaacha.. ''
Aliongea Daniel huku akizunguka upande wa pili kulikagua kagua gari hili, hakika gari hii ilionekana ni gari za mabosi maana hata tairi ni mpya zote! Vioo ni tin-ted kali ya gharama. Mda wote huo alikuwa akilikagua gari hilo huku masikio yake yakilingoja kwa hamu kubwa sana jibu la Asha..
" Hapana wewe tangulia kuna ng'ombe mmoja mshamba mshamba inatakiwa tumnyonye vilivyo.. ''
" Asha chunga sana usije ukanisaliti elewa tumetoka mbali?? ''
" Hakuna kitu kama hicho.. Kumbuka kama ningekuwa na lengo hilo ningeshakusaliti tangu zamani kule Africa kusini.. ''
" Sawa mimi nakutegemea na tambua kuwa mali hizi tunazozichuma pasipo wewe si kitu.. ''
" Hofu ondoa hapa tupo kikazi na ni kiapo ambacho tulishawekeana mimi na wewe siku ambayo tunaanza kazi hizi za hatari katika harakati za kusaka mafanikio.. ''
" Ni kweli Asha.. Mimi ninakuamini na ninaamini hata wewe pia waniamini.. ''
" Tena kwa asilimia zote! Na ili kuzihilisha hilo.. Siku ambayo tutatundika mikoba hii ya utaftaji na kuanza kujenga familia tutahakikisha tunakwenda kupima. Ili kila mmoja awe na amani juu ya mwenzake.. ''
Yalikuwa ni maneno matamu sana waliyokuwa wakiyazungumza wawili hao.. Taratibu walikumbatiana na kuagana kwa mabusu moto moto, kisha bila kupoteza mda kidume akingia garini na kufunga mkanda.. Sekunde chache mbele gari iliondolewa mahali pale kama kimbunga na kumwacha Ashura nywele zikipepea kwa kupigwa na upepo pindi Prado inaondolewa na mtaalam Mr DANI.
***
Patrick akafika mpaka nyumbani kwake ambapo alikuta geti limefungwa, alilisogelea taratibu na kubofya kitupe cha kengele! Haraka Emanuel akakurupuka na kwenda kulifungua huku akijiuliza ni nani huyu??
Alitahamaki baada ya kumkuta boss wake nje! Hana gari wala nini?? Hakika alishindwa kuyaelewa maisha ya boss wake kwa siku hizi.
Patrick baada ya kufunguliwa alianza kupiga hatua kuelekea ndani ya mjengo wake..
" Bosi samahani kidogo.. ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Emanuel aliita na bila hiana Patrick alimgeukia na kumtizama kwa ishara ya " NAKUSIKILIZA ''
Emanuel alimsogelea bosi wake mpaka pale..
" Samahani boss kidogo.. ''
" Nakusikiliza.. ''
" Asante.. Naomba kujua mbona Saida simwoni mahali hapa ni wiki mbili sasa?? ''
" Kwani gari yake si uliona tulikwenda kuchoma moto kule porini?? ''
" Ndiyo.. Ila sikuelewa chochote.. ''
" Kwa sasa hivi boss wako mwingine badili ya huyo malaya ni huyu dada unaemwona siku zote hapa.. ''
" Eee???! ''
" Hujasikia, hujaelewa au?? ''
" Nimesikia boss ila sijakuelewa.. ''
" Kwani we unachotaka hapa nini?? Zaidi ya mshahara?? ''
" Nisamehe bosi boss.. ''
" Siku nyingine usije kuuliza maswali ya kipumbavu kama hayo..''
Emanuel aliambiwa maneno ya kejeli na dharau kubwa na boss wake kisha akaachwa hapo akiwa kaduwaa asijue moja wala mbili.
' Daaah! Huyu jamaa vipi?? Sasa kwa staili hii nitaendelea na kazi kweli?? Duu hapana wacha nipokee mshahara wangu nisepea zangu.. '
Aliwaza hayo mlinzi wa geti bwana Emanuel kisha kwa hatua za taratibu akarudi kibandani chake na kutulia kimya..
*************************
Ilikuwa yapata mida ya saa kumi alasiri Saida na Felister walionekana wakitoka katika hospital hiyo kubwa ya IPAMBA Na kuelekea matembezini..
" Tunaelekea wapi?? ''
Saida alimuuliza Felister huku akijiweka sawa hususan nywele..
" Tuelekee zizi la ng'ombe.. ''
Felister nae alijibu huku akiweka sawa mkoba wake mdogo..
" Zizi la ng'ombe?? ''
" Ndiyo.. ''
" Sawa.. ''
Wakajitosa ndani ya Haisi zinazotoka IPAMBA Kuja Iringa mjini, kutoka IPAMBA HOSPITAL Mpaka zizi la ng'ombe siyo mbali sana, ni ndani ya dakika kadhaa tu! Konda alipayuka!!
" Hayaaaa!! Zizi la ng'ombe! Zizi la ng'ombee tushafikaaa!! ''
Basi Saida na Felister waliteremka mahali pale kisha Dala Dala hiyo ikasepa..
" Sasa hapa tunaelekea wapi?? ''
Saida alimuuliza mwenyeji wake Felister, maana yeye siyo mwenyeji sana kwa maeneo haya..
" Hapa itabidi tupande kule Over comer's power center ''
" Wapi??? ''
Saida aliuliza kana kwamba hajasikia vizuri..
" Kanisani kwa mchungaji Dk boaz sollo.. ''
Felister alijibu bila wasiwasi wowote! Japo kwa Saida uligeuka mtihani mkubwa sana! Kwani ana mda mrefu sana hajawahi kutia mguu katika nyumba za ibada sasa leo aende Mhuuu! hata nafsi inamsuta.
*************************
Ashura alimtizama Dani mpaka anapotelea tena kwa spidi ya ajabu! Akacheka kimoyomoyo na kujisemea kimoyomoyo..
' Ee mola linda penzi letu! Pia tusamehe kwa haya tunayoyatenda yote ni kwaajili ya kuupinga umaskini.. '
Alipokwisha kujisemea hayo taratibu alianza kurudi huku changanyikeni.. Ashura aliingia ndani ya Changanyikeni pasipo mtu yeyote kumshtukia kwani aliingia kienyeji mno!
Alitafuta mahali akatulia tuli.! Huku akiendelea kuyasoma mazingira katika eneo hili, aligundua hakukuwa na dalili yoyote! Aliendelea kukaa pale mara akatoke mmama mmoja ambae kimwonekano alionekana ni mtu wa kubangaiza maisha sana! Kwani hata yebo zake alizokuwa amevaa zilikuwa zimetoboka kwenye visigino! Ashura akapa wazo!
" Samahani mama.. ''
Ashura alimwita mama huyo kwa sauti ya chini huku akitizama eneo zima chinichini kuona kama kuna mtu yeyote alikuwa akimtizama! Akaona hakuna yeyote anaemtia jicho..
Yule mama hakukaidi alisogelea mpaka mahali alipokuwa Ashura, wakasalimiana, Kisha bila kupoteza mda Ashura akamueleza kuwa yeye alikuwa mgeni hivyo aliomba hifadhi ya usiku huo!
" Mmmh!! ''
Mama huyo aliguna kuonesha wasiwasi juu ya dada huyo ambae kimuonekano alionekana ni mtu wa hadhi anaestahili kulala gest kwa gharama yoyote ile iweje aombe hifadhi kwake??
Lakini Ashura alimtuliza mama huyo kwa manoti..
" Nitakupa Elfu hamsini tafadhari mama yangu nisaidie.. ''
Wasiwasi wote juu ya mwanadada huyo vikamtoweka mama huyo na kujikuta akimkubalia dada huyo ombi lake. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Ashura kwani anaona mipango yake kabambe inazidi kwenda sawia!
***
Kijana Msomi.. Kijana mwana IT.. Kijana mwizi/kibaka lakini anaeiba kwa teknolojia ya hali ya juu! Mr. Daniel masubwa sasa alikuwa anaanza kuitafuta Dodoma! Fanya mchezo na Prado wewe?? Halafu imekutana na kichaa wa usukani..!! Yaani kabla hata Patrick hajafikiria kama Ashura atakuwa ametimba Ismani kumbe gari inavuka Mtera bwawani..!!
Hahahaha....!! Hatari sanaa!!
" Ndiyo... Naitafuta Dodoma sasa hivi.. ''
" Ok sawa jitahidi usiku huu.. Huu uingize mwanza tuje kuifanyia maarifa.. ''
" Usihofu kaka nipe masaa matatu mbele.. ''
" Nakuaminia kamanda wangu.. ''
" Poa poa.. ''
Yes! Yalikuwa ni maongezi kati ya Daniel masubwa na washirika wake! Katika mpango mzima wa kuiba na kusafirisha magari na sasa walikuwa wakijadiliana kuhusu Prado hiyo..
Daniel masubwa. Aliweka simu kando baada ya kukatwa akashika vyema usukani na kuzidi kuipaiza gari ipasavyo! Hapo kilichosikika ni upepo ukipiga kwa nguvu kwenye vioo kwa nje!!
Yeaar!! Nimerudi tena namna hii.. Na kabla hatujaendelea mbele zaidi hebu tunanzie hapa...
Saida alijishauri mara kadhaa! Niende au nisiende?? Akili yake ikawa nzito kuchanganua jibu gani ni sahihi.. Hivyo akabaki katikati.
" Mi nafikiri twende huko au unasemaje? Mama?? ''
Felister aliuliza swali hilo huku akimtizama mama huyo usoni na tayari alishagundua kitu,
" Mmmh! ''
Mkanganyiko wa maamuzi uliokuwa ndani ya ubongo wa Saida ulimpelekea kuachia mguno pasipo yeye kujielewa.
" Mbona unaguna?? ''
Felister aliuliza swali ambalo pia liliacha taharuki ndani ya kichwa cha Saida!
" Ee?! ''
" Nimeona umeguna?? ''
" Mmmh! Hapana twende ila... ''
" Ila nini?? ''
" Nina mda sana sijawahi kukanyaga nyumba za ibada ''
" Hii ndiyo nafasi sasa.. ''
" Sawa twende ila nafsi inanisuta.. ''
" Hiyo nafsi inayokusuta ni nafsi ya kipepo yakufaa uikemee hebu twende.. ''
Kwanzi hapo ikawa mguu kwa mguu, hatu kwa hatua mpaka katika kanisa moja kubwa sana hapa Iringa na mikoa mingine lililo chini ya Askofu nabii dk Boaz sollo. Ibada mbali mbali zilikuwa zikifanyika, shuhuda mbali mbali zilikuwa zikitolewa na baadhi ya waumini waliofika mahali hapo kupata miuujiza yao,
Hakika mahali pale palianza kumvutia Saida, aliona pale ndiyo mahali sahihi na siyo kule alikokuwa, hata yeye alianza kujihisi tofauti kabisa.. Ule unyonge unyonge ulianza kumtoka! Alianza kuchangamka katika maombi. Kwani katika kanisa hili watu huomba wakiwa huru Hasa wakati wa kila mtu kuomba. Ukitaka kuruka rukaaa mpaka uchoke! Ukitaka kuliaa liaa mpaka majungu yako yaishe! Pia ukitaka kucheka kufurahi ni wewe tu!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maombezi yalifanyika takribani masaa mawili mpaka inatimu saa kumi na mbili kamili jioni Ibada ikafungwa na watu kuanza kutawanyika.
Saida na Felister walichukuana na kuanza kurudi kule hospital..
" Hii sehemu nimeipenda.. ''
Saida aliongea..
" Hahaha.. Hapa ndiyo mahali sahihi pa kuja kupumzisha ubongo na kutafakari ya dunia.. ''
" Hakika Na ninaapa nitakuwa nikihudhuria kila siku za ibada.. ''
" Nashukuru kusikia hivyo mama ''
Felister alijibu huku kwa mbali tabasamu la furaha likichanua usoni kwake.. Ilikuwa ni furaha iliyoje kwa dada huyo, alitaka maisha ya mama huyo yawe furaha na ya kumpendeza muumba wetu.
Wakafika mpaka katika stand ya zizi la ng'ombe, hapo hawakukawia kwani Daladala zinazotoka Posta kwenda IPAMBA Ni tele! Hazikupita hata dakika kadhaa Haisi ilitimba hapo wakapanda kisha haoo!
*************************
Unajua ni mpango gani mwingine alikuwa nao Ashura juu ya mwanamama huyo maskini??
Somaa hiyo..!!
Baada ya kukamilisha zoezi zima la kumkabidhi Dani gari, sasa kilichobaki hapo ni kumpumbaza Patrick ili aendelee kuamini kama huku aliko kweli kuna mgonjwa na baada ya hapo atafute njia ya kujitetea ili asikutwe na kosa lolote kuhusu kupotea kwa gari hiyo ya mamilioni..
Na wazo alilolipata ni kuweza kumpata mama yeyote ambae angeweza kuigiza sauti ya mgonjwa mahututi ili hatua ya kwanza ikamilike..
Ni kweli alifanikiwa kumpata kwa kujifanya yeye ni mgeni anaeomba hifadhi, mama huyo aliweza kukubali baada ya kupewa kitita cha Tsh elfu hamsini keshi za kitanzani. Na kukubali kumpeleka katika kijumba chake chakavu ambapo anaishi peke yake pasipo na muume wala watoto.
Ashura hakutaka kudadisi kujua kwanini mama yule yupo vile yeye moja kwa moja alikwenda kwenye pointi..
" Samahani mama.. ''
Ashura alianza kumpanga mama huyo mda huo ikiwa inasoma moja na nusu usiku giza likianza kuumeza ulimwengu..
" Bila samahani.. ''
Mama huyo alijibu huku akiweka sawa miguu yake na kuinyoosha ipasavyo katika kijimkeka chakavu walichokuwa wamekalia..
" Nina tatizo kidogo naomba unisaidie.. ''
" Ninaweza kukusaidia ikiwa litakuwa ndani ya uwezo wangu.. ''
" Nina imani utaweza mama.. ''
" Haya niambie sasa.. ''
Aliongea mama huyo huku akiweka utulivu wa hali ya juu kujua kipi ataambiwa.. Ashura nae alimeza funda ya mate na kuanza kumwaga wino.
" Kiukweli mama mimi ni mgeni natokea songea nilikuja hapa kuja kumuona rafiki yangu wa mda mrefu sana! Alikuwa ni rafiki yangu wa damu, rafiki yangu wa kusaidiana kwa shida na raha, urafiki wetu ni tangu chekea! Ila kwa bahati mbaya tukaja kupoteza wakati wa kuingia vyuo vikuu, mi nilipangiwa songea, yeye akapangia huku Iringa, ila wote tunatokea mkoa wa pwani..
Ashura alisitisha na kumeza mate huku akimsoma mama huyo usoni na kugundua tayari anaanza kuingia laini..
" Sasa ni miaka mingi tangu mwaka 2003! Mpaka leo! Nilikuwa binti sasa nimeolewa na bado sijaona nae! Na kila nikimwomba mume wangu nije nimsalimie huyo rafiki ananikatalia.. Sasa wiki hili nikaamua kumdanganya kuwa mama yangu yupo hoi bin taaban..!! Ndipo akaniruhusu kuja kumuona ila ukweli ni kwamba ninahitaji kumuona rafiki yangu kipenzi.. ''
Ashura alihitimisha ungwe ya kwanza hakika ulikuwa ni uongo wenye point ndani yake! Kwani aliongea mpaka machozi ya kinafiki yakaanza kumtiririka! Mama huyo akaanza kumwonea huruma japo hajajua dada huyo anahitaji msaada gani kwake??
Jamani mwanangu usilie sasa, mi nipo tayari kukusaidia japo sijajua unahitaji nikusaidiaje?? ''
Mama huyo aliongea tayari nae kwa mbaaali machozi yakianza kumlenga lenga, kwani maneno aliyoyaongea Ashura mda mfupi uliopita yanasabihiana kabisa na ukweli na si rahisi kwa mtu yeyote kuyashtukia kama ni uongo mkubwa usio na haya!
" Mama mimi nahitaji unisaidie kitu kidogo tu!! ''
Ashura aliongea kwa upole tena kwa kuigiza huzuni kubwa mno! Wakati huo machozi yakimwagika haswaa!
" Nipo tayari.. Usilie unanitonesha vidonda ndugu vilivyo ndani ya moyo wangu.. Niambie nitakusaidia.... ''
Ashura baada ya kusikia hivyo alivuta pumzi ndefu na kuishusha kisha akatoa simu yake! Kitu cha kwanza akaingia MAGIC SOUND Na kuseti sauti fulani ambayo mtu akiongea anakuwa kama anakoroma koroma vile yaani kwa tafsiri nyingine ni kwamba ukipigiwa na mtu alieseti sauti hiyo unaweza kusema mgonjwa ambae yupo hoi kitandani kumbe anaranda randa mtaani huko!
" Asante mama kwa kunipa nafasi hiyo... ''
Ashura aliongea hivyo kisha akaweka kituo kwanza! Akaingia sehemu ya " Majina '' akatafuta jina la Patrick baada ya kuliona akaliweka mkao wa kupiga. Baada ya hapo akaendelea...
" Mume wangu ni mkali na kanibana sana anapiga simu mara kwa mara kutaka kuongea na mgonjwa nami mgonjwa huku sina! Ninaomba unisaidie katika hili.. ''
Ashura aliongea maneno ambayo yalimwacha njia panda mwanamke huyo kwani bado hajajua mwanadada huyo anahitaji msaada gani kwake katika hilo.. ''
" Bado sijakuelewa japo nimekusikia ila sijaelewa unataka nikusaidiaje hapo??? ''
Mwanamama huyo alimtwanga swali hilo Ashura, wakati huo nae Ashura alikuwa akijiandaa kumjibu..
" Kazi ndogo sana ninaomba uongee na mume wangu huku ukiigiza kama mgonjwa alie mahututi, hapo utakuwa umenisaidia.. ''
Huo ulikuwa ni mtihani kwani ni ngumu sana kuigiza ni mngonjwa wakati mzima kabisaa tena wa afya!!
" Sasa hapo mwanangu huoni kama ni ngumu?? ''
" Ugumu upo wapi mama?? ''
" Unaelewa kuwa sauti ya mgonjwa mahututi na mtu mzima huwa sauti zinatofautiana?? ''
" Ndiyo ninaelewa lakini hilo linarekebishika simu hii hubadili sauti, unaweza kuwa unaongea na mtoto wa miaka kumi lakini ukasikia sauti ya mtu mzima mwenye umri wa miaka hata Sitini, pia kwa simu hiyo hiyo sauti ya mtu wa miaka hamsini yaweza kusikika kama ya mtoto wa miaka Kumi au mtu mzima akasikia kwa namna ambayo unaweza kuzani yupo muhimbili.. ''
Ashura alieleza kwa kirefu ili kumuondoa hofu mama huyu..
" Mmmh! ''
Mama aliguna...
" Usigune mama ni kazi rahisi sana na hakuna atakaejua.. ''
Ashura aliendelea kumwaga siasa mpaka mama huyo akaingia laini..
" Sawa nimekubali mpigie.. ''
Mama huyo aliongea, maneno yaliyoripua fulaha ya ajabu kwa Ashura kwani sasa kila kitu kinakwenda kukamilika....
Mda huo huo simu ikapigwa! Haikuita hata zaidi ya mara tatu ikapokelewa..
" Halow.. Mke wangu?.. ''
Sauti ya kiume yenye kibesi ilisikika upande wa pili, alikuwa ni Patrick..
" Ndiyo Baby za mda huu?? ''
Ashura aliongea kwa sauti yenye huzuni kubwa ya kuigiza!
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Njema umefika?? ''
" Ndiyo lakini mama hali ni mbaya Patrick sijui.. Sijui kama atapona.. ''
" Ooooh! Pole sanaaa vipi unaweza kumpatia simu japo nimfariji?? ''
Ashura alimkonyeza mama huyo ili akae sawa kisha yeye akamjibu Patrick..
" Ndiyo huyu hapa ongea nae.. ''
" Sawa.. ''
Wakati simu inakwenda kwa mama huyo Patrick alijikoholesha kuweka koo sawa kwajili ya kuzungumza na mkwe!!..
" Haloo.. ''
Tayari simu ilishakuwa kwa mama huyo na bila kupoteza mda akaita namna hiyo, sasa sauti aliyoitoa bwana!! Hata Ashura mwenyewe hakuamini kuwa mama huyo ana uwezo wa kuigiza sauti kiasi kile?
" Ndiyo mama pole sanaa.. Pole sana mama.. ''
" A..aa..aj..as.ant..ee.. ''
Mama huyu aliigiza sauti ambayo kwa Patrick ilisikika kama inatoka kwa mtu ambae ni mahututi mpaka anashindwa kuongea..
" Mama... Mama tatizo nini?? Mama??? ''
" N..aum..waa.. Ta..t..a....... ''
" Oooh!! Shit pole mama angu hebu mpe simu mwanao hapo.. ''
Simu ikarudi kwa Ashura, mda huo Ashura alikuwa amekaukia na kicheko cha kimoyomoyo.. Alipokea simu hiyo na kuiweka sikioni.. Wakati huo mama huyo akavunja haraka kipande cha kuti kutoka katika ule mkeka chakavu waliokuwa wameukalia pale kisha akasogeza mguu wake karibu na kibatari kisha kwa kutumia kile kipande cha kikuti akajiandika mguuni pale (TAIFODI)
Ashura alishaona kitambo na akatambua maana yake..
" Ndiyo mume wangu.. ''
" Jamani mama mkwe wangu anasumbuliwa na nini?? ''
Patrick aliongea huku akionekana kuhaha huko aliko..
" Anasumbuliwa na Taifodi mume wangu.. ''
" Heee!! Vipi upande wa huduma?? ''
" Kwa upande wa huduma aliambiwa aende BUGANDO Lakini tatizo ni hela.. ''
" Hela?? ''
" Ndiyo ''
" Shilingi ngapi inatakiwa?? ''
" Milioni sita.. ''
Ashura alijibu pasipo kubabaika wala nini?? Ingali kwa upande wa mama huyo macho yalikuwa yamemtoka pima mfano wa panya aliegundua uwepo wa paka katika makazi yake, maana pesa iliyotajwa mmmh! Hata Kuiona hajawahi..
" Hilo ndiyo tatizo?? ''
Patrick aliludia swali...
" Ndiyo ni tatizo tena tatizo kubwa hasa kwa familia masikini kama sisi... ''
" Na je?? Kama pesa hiyo ingekuwapo ilitakiwa aende lini?? ''
" Hata kesho angeenda mume wangu.. ''
" Vipi hapo kuna wakala anaetoa hiyo pesa?? ''
" Hapaaa mmmh! Hapana hayupo wa kutoa kiasi hicho.. ''
" Sasa nilitaka kujitolea kumsaidia mama mkwe wangu nitamsaidiaje sasa ''
" Ahaa sawa,, ila kwa sasa ni usiku ngoja nitakupigia kesho asubuhi na nitakuambia tufanyaje?? ''
" Sawa usiku mwema na poleni sana.. ''
" Asante sana kwa niaba ya wote na uwe na usiku mwema pia.. ''
" Inshallah ''
Simu zikakatwa! Ashura akavuta pumzi ndefu na kuishusha! Akilini akawaza kuwa Ungwe ya pili kaimaliza sasa hapa kilichobaki ni kutafuta njia sahihi ya kudanganya jinsi gari ilivyopotea potea!
Mama huyu nae alikuwa bado kaduwaa na mawazo! Tayari kuna kitu alianza kuhisi ila pia hakutaka kukipa kipaumbele saana, Ashura alimgeukia na kumtizama kwa macho yaliyojaa fulaha tele..
" Asante sana mama umefanya vyema mnoo! ''
" Asante pia lakini mbona umeenda mbali sana?? ''
" Sikiliza mama mimi nitakupatia milioni mbili cash, uondokane na umaskini huu ukajenge japo kibanda cha bati tano,, ila nawe hakikisha humwelezi mtu yeyote kuhusu haya iwe siri yako.. ''
" Sawa sitofanya hivyo. Lakini unaweza kunidodosea japo kidogo?? ''
" Ukweli nishakwambia au umesahau?? ''
" Nakumbuka lakini.... ''
" Sikiliza mama hebu tulale nimechoka baraa tutaongea kesho.... ''
Ashura ni mtu mjanja mjanja sana huwa haruhusu mtu amchukue hata nukta ya akili yake wala kupata hata upepo juu ya mipango yake na ndicho alichokifanya hapa! Akamzima mama huyu kiaina baada ya kuona anakoelekea siyo kwenyewe..
Mahali pa kulala palikuwa ni hapo hapo walipokuwa wamekaa hivyo basi walichokifanya ni kujilaza na kujifunika vitenge.. Usingizi ukawasafirisha mpaka majogoo!
Ilikuwa imeshatimu saa kumi na moja alfajiri tayari Ashura alikuwa macho akitafakari nini afanye? Au atumie njia gani kuzinasa milioni sita hizo pasipo Patrick kumshtukia?? Alitafakari kwa kina hatimae kuna wazo akalipata kuwa awasiliane na Daniel ili ipatikane line mpyaa ambayo baada ya miamala kufanyika ichomwe moto.
Akachuku simu yake na kutaka kumpgia muda huo ila akaona ni bado usiku wacha kukuche kabisa! Mwenye nyumba yeye bado alikuwa akiuchapa usingizi, sasa kwa kuwa Ashura alikuwa hana usingizi kwa mda huo alichokifanya ni kuwasha Data na kuingia mtandaoni kupoteza poteza mda ili kukuche,
Cha kwanza akafungua Facebook.. Hamadi anakutana na simulizi kali ya kijasusi iitwayo MPELELEZI WA KIKE Kutoka kwa mtunzi Andrea Stephano Jr. Kwa jinsi jina la simulizi na cover lake vilivyokuwa na mvuto vilimpelekea apate shaukuu ya kusoma kilicho ndani ya riwaya hiyo.. Hakika mda alioutumia kusoma riwaya hiyo haukwenda bure, alijifunza mengi ambayo pia yalikuwa na msaada mkubwa katika kazi yake hiyo aliyokuwa nayo..
' Daah! Huyu mtunzi ni lazima nimtafute tuongee japo mawili matatu! Na nitakuwa na zawadi yake spesho, siyo kwa story hii '
Aliwaza hayo Ashura huku akizima Data ili aamke na kuanza michakato maana kumekucha sasa..
*************************
" Sasa mzigo nimeuona bwana mdogo hapa nafikiri kilichobaki ni kufika muafaka.. ''
" Ni kweli bosi.. ''
Ilikuwa ni saa kumi na mbili Asubuhi Daniel alikuwa ameshatia timu mkoani mwanza na hapo alikuwa akiongea na bosi wake..
" Hebu nipatie ofa yako chap chap twende na mda.. ''
" Hapo bosi ukinipa kilo mia itakuwa poa ''
( Kilo mia kwa rugha nyepesi ni milioni mia.. )
" Labda nikuulize kitu kimoja bwana mdogo.. ''
" Ndiyo nakusikiliza boss ''
" Hii gari umeitoa katika mazingira gani?? ''
Ni swali aliloulizwa Daniel na boss wake huyo anaedili na vitu vya magendo. Swali ambalo kwa Daniel liligeuka mtihani mkubwa sana kwani nae alichobugi ni kwamba wakati anakabidhiwa gari hiyo na Ashura hakumuuliza ni wapi kaitoa jambo lililopelekea akose jibu kwa boss wake huyo.. ''
" Sikiliza bwana mdogo najua hii gari ni ya moja kati ya vigogo wenye mikwanja mirefu hapa nchini au siyo?? ''
" Ni kweli boss.. ''
Daniel alijibu ilimradi tu mada iishe lakini nafsini alijutia sana kwa uzembe mkubwa alioufanya..
" Sasa sikia nikupe siri.. ''
" Naam nakusikiliza.. ''
" Watu wanaomiliki gari kama hizi mara nyingi wanakuwaga ni watu wenye pesa sana, hawezi kushindwa kusambaza polisi nchi nzima kufanya msako wa nguvu ikiwa alimudu gharama ya kuinunua gari hii ya bei ghari sana kwa hapa Africa.. ''
" Sasa kwa hapo utanisaidiaje bosi wangu?? ''
" Hapaa nafikiri tufanye maarifa fulani hivi.. ''
" Yapi hayo?? ''
Daniel alianza kuhaha mfano wa mama mjamzito anapokaribia kujifungua. Maneno ya bosi wake kuwa mmiliki wa gari hii anaweza kusambaza polisi nchi nzima yalianza kumtisha alitamani kuichoma moto gari hiyo kabla mambo hayajaharibika zaidi..
" Hapa cha kukusaidia ni kwamba nikupe M80 Ili mi nifanye mchakato wa kuisafirisha nje ya nchi ndani ya masaa sita tu! ''
Daniel hakuwa na pingamizi juu ya bosi wake, alichokifanya ni kumpgia Ashura ili kumwarifu. Alijongea kando kidogo na kumpigia..
" Haloo! Dani.. ''
" Habari ya mda huu Asha?? ''
" Safi kwema?? ''
" Kwema kabisa.. Sasa nimeshafika mwanza.. ''
" Ndiyo.. ''
" Unajua jana nimesahau kukuuliza kwamba huu mzigo umeutoa katika mazingira gani?? ''
" Oooh! Mi pia nikasahu kukueleza ''
" Ndiyo yaani nimepatapa wakati mgumu hapa?? ''
" Pole.. Huu mzigo bwana unatoka kwa mtu mwenye mkwanja kidogo hivyo umakini unatakiwa juu ya hili.. ''
" Bosi wetu anasema atupatie milioni 80, ili yeye aisafirishe nje ya nchi kwa hapo wewe unasemaje? ''
" Kumbuka hizi ni dili za magendo haitakiwa kuwe na mabishano ni pesa ndefu sana iyo mume wangu...''
" Sawa kama na wewe kama umeridhia ni vizuri zaidi.. ''
" Yaaah! Malizana na hiyo kisha nitakupigia kuna mchongo mpya hapa ''
" Sawa ila kuwa makini sana ''
" Usihofu nipo makini na kila nikifanyacho.. ''
" Inshallah ''
Simu zikakatwa, Daniel akarudi ndani..
" Sasa bosi nami nilikuwa nazungumza na timu yangu hapa ''
" Ndiyo.. ''
" Kwa pamoja tumeridhia kiasi ulichokitaja ''
Mwanaume huyo baada ya kusikia hivyo alifulahi sana na bila kupoteza mda akanyanyua simu yake kwaajili ya kuwasiliana na washirika wake Ili gari hiyo isafirishwe mpema kwenda Rwanda.
Hazikupita hata dakika kumi tangu simu ipigwe, Gari moja makini sana aina ya TATA Ambayo tela lake lilikuwa katika mfumo wa contena iliwasiri mahali hapo huku nyuma ikifuatiwa na gari ndogo aina ya Hummer, watu kadhaa walishuka na kuingia katika ofisi hiyo walimokuwa Daniel na bosi wake huyo..
" Za saa hizi mr?? ''
Mwanaume mmoja alisalimia huku akirekebisha kofia yake..
" Salama vipi hali?? ''
" Safi kabisa.. ''
" Ok nimekuita hapa ''
" Ndiyo mkuu nimekuja kuitika.. ''
" Kuna gari hapa inatakiwa kufika Rwanda leo hii ''
" Ndiyo? ''
" Nilishaongea na Ibra hivyo kazi wewe ni kuifikisha tu!! ''
" Nimekupata.. ''
" Sawa ipo kule tunakopakiliaga siku zote. ''
" Sawa bosi.. Je?? Una la kuongeza?? ''
" Hapana.. ''
" Sawa ''
Yule mwanaume ambaye kimwonekano alionekana ni Dreva wa kijiroli hicho alitoka mle ndani moja kwa moja mpaka kwenye roli hilo na kuliwasha,
Kuna ngazi maalumu ya kupakizia magari kwenye makontena ambayo imejengwa ndani ya eneo hilo, basi ile Parado ilipandishwa juu ya ngazi hiyo ambayo mwishoni imeishia usawa wa gari yoyote yenye contena, TATA Ikasogezwa pale Parado ikaingizwa ndani na milango kufungwa!
Msafara ukaiva, gari ndogo aina ya Hummer ambayo ndani ilionekana kuwa na wanaume watano wa kushiba wenye silaha, ilitangulia huku nyuma likifuata roli hilo lililbobeba gari ya magendo ndani, kiukweli lilikuwa ni roli dogo sana ambalo isingekuwa rahisi kwa askari wa usalama barabarani kulishtukia kuwa ndani lilikuwa na gari nyingine ndogo, na kibaya zaidi contena lake kwa nje liliwekwa chapa ya COCA_COLA Kwa maana hiyo watu walijua ndani limebeba soda! Kumbe ni baraa tupu!!
***
Hapo sasa kilichokuwa kimebaki ni Daniel kukabidhiwa mpunga wake, walitoka mle ofisini na moja kwa moja wakaanza kutembea katika kordo moja ndefu sana ambayo pia haikuwa na mtu yeyote zaidi ya ukimya wa kutisha! Ile kordo ilikuwa ndefu sana! Kwani walitembea umbali mrefu ndipo wakafika mwisho!
Ajabu..!!
Hakukuwa na chumba chochote ambacho Daniel alidhani walikuwa wakienda kuingia hapana! Bali kordo ile nyembamba mwishowe ilishia kwenye ukuta!
' mmmh! '
Daniel aliguna kimoyomo huku moyoni akianza kujenga hofu nzito sana juu ya eneo hile lakini ghafla! Malumalu ikaachana chini ngazi ndefuu! Zikaonekana zikiteremka ardhini...!!
Alistaajabu!!
" Twende dogo.. ''
Ilibidi bosi wake huyo kumshtua kijana wake baada ya kuona kaduwaa! Tayari yeye alishaanza kushuka chini..! Bwana Dani nae hakusita akajitosa na kuanza kuteremka chini, Huku juu ule mlango ambao ulitengenezwa mfano wa malumalu nao ukajifunga na kusababisha kiza totoro!!
Daniel alishtuka na kusita kutembea lakini Gafla! Balbu za mwanga mkali zikawaka eneo lote lile ambalo njia hiyo ilikuwa ikielekea! Wakaendelea kushuka mwishowe wakafika katika chumba kimoja ambacho kilikuwa chini ya Ardhi, chumba hiki kina mwanga mkali halafu pia kimekarabatiwa ipasavyo na kuwekwa droo za ukutani, hakika kilikuwa ni chumba kizuri mnoo! Kama ofisi ya rais vile!!
Lakini Daniel alipochunguza kwa makini alibaini chumba hiki kilikuwa kimefungwa camera za CCTV Kila mahali,
Humo ndani hakukuwa na mjadala tena, yule mwanaume aliisogelea sehemu moja karibu na ukutani ambapo kulikuwa na BUTTON Akabonyeza batani hiyo Gafla Droo kubwa ikachomoka kutoka ukutani ndani ya droo hiyo kulikuwa na mashine ndogo ya kuhesabia pesa, akaitoa na kuiweka kando!
Mda wote huo Kijana Daniel Masubwa alikuwa kaduwaa tu! Asijue cha kufanya wala kuongea, alishia kumtiza bosi wake ambaye yeye alikuwa bize na ukuta!
Taratibu akasogea tena pembeni kidogo na kubofya battani zingine! Pia ilikuwa vile vile droo kubwa iliyosheheni vibunda vya pesa ikachomoka shwaaaa!! Daniel mate ya uchu yakaanza kumsumbua!!
Bila kupoteza mda yule mwanaume alianza kuchukua kibunda kimoja kimoja na kukitumbukiza ndani ya hicho kijimashine, kisha zinatokea upande wa pili..
" Tupo pamoja?? ''
" Ndiyo kaka ''
" Ngapi hizo?? ''
" Milioni 40!! ''
" Ok ''
Mzee akatoa kibunda kingine cha maana na kukitumbukiza humo! Milioni 80 Zikasoma!, haraka akazimwaga zile pesa sakafuni na kurudisha ile mashine kwenye droo yake! Kisha akaminya limote ndogo aliyoiunganisha na funguo zake droo zote zikajifunga kwa mara moja,
Alitoka pale na kwenda kwenye kabati moja dogo lililo ndani ya chumba hicho na kuvuta mfuko mmoja mweusi na kumkabidhi kijana huyo..
" Weka pesa hizo chap chap tuondoke huku.. ''
Daniel aliupokea mfuko huo na kuanza kuzoelea pesa hizo na kuzitia ndani ya mfuko huo tena bila hata mpangilio maalumu..
***
Ilikuwa yapata saa nne na nusu asubuhi, Gari zilizoondoka na Prado ya Patrick mkoani mwanza sasa zilikuwa zinavuka mpaka kuingia nchini Rwanda, Gari ya Parick ndiyo ikawa imeenda namna hiyo..
***
" Sasa unasikia kijana?? ''
" Naam nakusikia boss ''
" Usiwe na ulimi mwepesi sawa?? ''
" Una maana gani?? ''
" Maana yangu ni kwamba kile ulichokiona huruhusiwi kukitangaza kwa yeyote.. ''
" Hapana boss,, kusema ni sawa sawa na kuharibu je?? Nikiharibu kesho nitakimbilia wapi?? ''
" Safi kuwa na akili za kiutu uzima namna hiyo ili tupige pesa ''
" Yaaah! Naelewa hilo boss wangu...''
" Sawa safari njema na ukipata tena usisite kuniona.. ''
" Haina nyongo kamanda.. ''
Yalikuwa ni maongezi ya maagano kati ya kijana Dani na boss wake huyo,, kijana huyu baada ya kukabidhiwa kitita chake alipanga kusafiri siku hiyo hiyo mpaka Arusha..
Ili akatulize mawazo kwanza kabla ya kuendelea na harakati zake za kusaka shavu,
Baada ya kuagana na boss wake huyo alitoka katika ofisi hizo na moja kwa moja akafika katika duka moja la mabegi akanunua begi kubwa na kutumbukiza mfuko huo ndani, hakuna mtu aliezania kuwa mfuko ule ulikuwa na pesa ndani, baada ya hapo akajongea katika stand kuu ya mabasi, mabasi ya kwenda Arusha yalikuwa tele tu! Hivyo alikata tiketi katika moja ya mabasi yaendayo Arusha na kwenda kutulia ndani kwenye siti yake, mda wote alikuwa makini sana na watu wote waliokuwa wakikata tiketi na kuingia ndani ya basi hilo..
Mara simu yake ikaita.. Haraka akaitoa na kukuta mpigaji ni Ashura! Akaipokea tena kwa utulivu wa hali ya juu!
" Haloo.. ''
" Ndiyo vipi bado umetingwa?? ''
" Hapana nishamaliza kila kitu.. ''
" Ok.. Sasa kuna mpango mpya hapa hebu tuujadili kujua nini tufanye.. ''
Pale pale Daniel akili ikafunguka maana alikuwa kasahau jumla! Kwanza akazungusha macho chini chini kila upande kuona kama kuna mmoja atadukua mazungumzo yake,, akaona kupo salama, akapunguza sauti ya simu yake kisha akajibu..
" Samahani nilisahau kama uliniahidi mpango mpya hebu nidodosee.. ''
" Kuna mpango wa pesa huku kinachotakiwa hapo ni wewe kupata laini ya kutumia na kuiua papo hapo baada ya kazi.. ''
" Waweza niambia ni mpango gani huo?? ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ashura alisita kidogo kuongea, wakati huo akifikiria cha kumjibu mwanaume huyo maana alijua kumwambia ukweli ni kukata tiketi ya kuachana japo wapo kazini..
" Hapo hapo nilipoichomoa gari hiyo nimemraghai mtu huyo kuwa kuna jiwe kubwa la Dhahabu nimelifuma kwa mshamba mmoja na anasema anahitaji milioni sita,, sasa mzee huyo kadata anataka atume sasa hivi ili niondoke nalo.. ''
Ulikuwa ni uongo japo una point ndani yake,
" Kwahiyo..''
" Inatakiwa ichukuliwe hiyo.. ''
" Sawa subili nipe dakika tano.. ''
" Sawa.. ''
Simu zikakatwa, wakati huo basi alilopanda Daniel linaanza kuondoka mwanza, Siku zote huyu jamaa huwa hakubali dili la pesa limpite kizembe, haraka alianza kujisachi mifuko yake maana kumbu kumbu zake zinamwambia kuwa hapo alipo ana laini zaidi ya tano! Ambazo ikitokea michongo ya mpunga kama hivyo anatumia na kuziua papo hapo..
Tayari Ashura nae alianza kuitafuta namba ya Patrick, maana kuna mda Patrick alipiga akamwambia asubili kwanza yupo katika pilika pilika, lengo lake alitaka awasiliane na Dani kwanza! Na sasa walikuwa wameshawasiliana tayari.
Kilichobaki ni kumpanga Patrick atume pesa hiyo..
'' Ngrrr...!! Ngrrr....!! Ngrrr...!! Ngrrr...!!
Tayari alishamnasa hewani simu ilikuwa ikiita..
" Haloow...! ''
Hatimae ikapokelewa...
Patrick alipokea simu lakini cha ajabu kabisa Ashura hakuitikia zaidi yake aliachia kwikwi iliyoamatana na kuvuta kamasi nyepesi maana ake ni kwamba alisikika kwa Patrick kama mtu anaejizuia kulia!
" Ashura.. Ashura mke wangu nini tena??? Mbona waniweka roho jujuu mke wangu??? ''
" Ha..l.i. Yaa..a..a ma..m..ma, ni..n.iii ''
" Umesemaje?? Ongea nikusikia tafadhari.. ''
Patrick alianza kuhaha...
" Patrick.. Ma..m..maa ana..ana..ku..faaa.. ''
" Nini??? ''
Ashura alinyamza kidogo kana kwamba anakata kwikwi ili amueleze vizuri...
" Mume wangu.. Hali ya mama ni mbayaa sa... Sa... ''
" Sikuelewi Mke wangu... ''
" Tuma iyo pesaa ndiyo tunamsogeza barabarani mume wangu.. Hihi..hiii..hiii.. ''
" Ooh! Polee usilie usiliiiee natuma sasa hivi.. ''
Ashura akakata fasta na kumtafta Dani nae pia alikuwa hewani..
" Dani ushapata laini?? ''
" Yaah! kila kitu kipo sawa ''
" Sawa nipatie hiyo namba.. ''
" 0783****** ''
" Oky.. Sasa usikae mbali na simu yako.. ''
" Nipo nayo mkononi hapa.. ''
" Naa kuwa mwepesi kufanya miamala.. ''
" Usihofu we fanya mambo huko.. ''
" Sawa ''
Mda huo huo anakata simu meseji ikaingia kwenye simu ya Ashura alipoifungua...!!
Puuuuuph!! Milioni kumi hizi hapa!! Ashura hakuamini macho yake! Alihisi yupo katika ndoto moja ambayo ni adimu hata kuotwa! Mara akiwa katika taharuki hiyo simu ikaita..!
" Nashukuru mume wangu imeshafika.. ''
" Shilingi ngapi?? ''
" Sijaangalia kama ni kiasi gani maana hapa nina mawazo chungu nzima!! ''
" Milioni kumi nimetuma ''
" Waaoh!! Hakika sijutii kuolewa na wewe ''
" Yaah! Lazima nioneshe utofauti wa kuitwa mwanaume.. ''
" Shukuran sana! Natumai hata mama akipona atafurahi sana kukuona mkwe wake mwenye moyo wa kujitole kwa hali na mali..... ''
" Saana! Kikubwa tumuombee apone, aje kushuhudia matunda ya kukulea ''
" Inshallaah ''
" Vipi nawe utakwenda mwanza?? ''
" Hapana kuna kaka angu atashughulika na safari hiyo mi naludi baadae ''
" Sawa nimekuelewa.. ''
Simu zikakatwa, haraka sana Ashura akaitoa pesa hiyo kwenye simu yake na kuirusha kwa Daniel ambapo nae alipigwa na butwaa! Kuona kiasi kikubwa cha pesa namna hiyo tena kikiingia kwenye simu yake kizembe kizembe tu!
Nae pia hakutaka kuwa mzembe, alihamishia pesa hiyo katika laini yake Private kabisa ambayo namba yake hakuna alie nayo zaidi ya Ashura pekee..
Baada ya hapo akampigia na kumwarifu kuwa pesa hiyo tayari ilishaingia katika simu yake na tayari ameshaihamishia kwenye line yake ya siri, pia akamwaarifu kuwa alikuwa safarini kuelekea Arusha, Ashura akamtakia safari njema Daniel kisha simu zikakatwa..
Pumzi ndefu akaishusha Ashura, mawazo kem kem yakaanza kuzunguka kichwani kwake, alianza sasa kufikria mbinu atakayotumia kumwaninisha Patrick kuwa gari hiyo ilibiwa! Ashura aliumiza kichwa sana ili kupata uongo ambao ungekuwa na mantiki kiasi cha kumfanya Patrick asishtukie chochote!
Kwanza alitoa kitita cha shilingi laki moja na kumpatia mama mwenye nyumba maana nae ametoa mchango mkubwa sana katika mission hiyo.
" Mama leo twala nini?? ''
" Mmh! Ndiyo nafikiria kwenda vigengeni sasa hivi.. ''
" Ahaa! Sawa mi ngoja nijinyooshe maana najiskia uchovu! ''
Ashura aliongea hivyo ili aende kujipumzisha kuupa ubongo nafasi nzuri ya kufikiria mbinu ya kuweza kukabiliana na kazi nzito iliyopo mbele yake..
Mama mwenye nyumba nae aliaga kwenda kununua mahitaji ya chakula cha mchana huo vigengeni hivyo akamwacha Ashura akijinyoosha kwenye mkeka! Akatoka na kurudishia mlango na kwenda zake..
' Huyu mama lazima niondoke nae nikampangie nyumba Arusha.. '
Aliwaza Ashura wakati huo akiwa peke yake katika kijumba hicho chakavu.
Kingine pia alifikiria kuwa tukio la kudanganya kuhusu kuibiwa kwa gari la patrick lifanyike katika mazingira gani?? Alijiuliza na kufikiria kwa kina mwishowe akapata wazo...
*************************
Ikiwa ni jumatatu tulivu mida ya saa sita mchana, Saida alikuwa amejipumzisha kitandani katika wodi yake ya siku zote, ilikuwa ni siku ya kazi kwa Felister ni siku ambayo Saida alikuwa mpweke kwa kiasi fulani kwani hakukuwa na yule mfariji wake wa siku zote,
Taratibu mawazo yake ya kulipiza kisasi juu ya unyama aliotendewa na mwanaume ambae alimkabidhi moyo wake wote leo hii anakuja kumfanyia unyama ambao ni ngumu hata kusimulika, mara kwa mara Saida alifikiria kulipa kisasi juu ya ukatili huo.
' Ni lazima nikasimame kizimbani '
Alijisemea Saida kimoyomoyo huku akijigeuza kulalia upande wa pili baada ya kulalia ubavu mmoja kwa mda mrefu.
Masaa yakazidi kusonga, siku ikaisha! Hatimae jioni ikawadia Felister akaja baada ya sehemu kubwa ya kazi kuisha..
" Waoo! Mama jamani... ''
Saida alikurupuka kitandani kama chizi baada ya kuisikia sauti ya swahiba wake huyo!! Wakakumbatiana kwa mbwembwe nyiingii...!!
" Khaaa!! jamani leo umenifanya nishinde mpweeke! ''
" Oooh!! Ni maswala ya kusaka tonge mama.. ''
" Na kweli kazana maana hii dunia ni kizingumkuti, usipokuwa na chako umeumia.. ''
" Ni kweli kabisa mama.. ''
" Sawa.. Habari ya kazi.. ''
" Yaani njema kabisa ''
" Asante.. Nashukuru kwa kuja kuungana na mimi kwa mara nyingine! ''
" Usiwaze mama.. ''
Yalikuwa ni maongezi yenye faraja kati ya Saida na Felister ambapo kwa kipindi hiki kifupi walichokaa pamoja wametokea kupendana kama mapacha.
" Hivi Ferister! ''
" Bee! Mama.. ''
" Simu yako ina charge?? ''
" Ndiyo mama angu ''
" Ninaiomba mara moja ''
" Sawa.. ''
Felister alitoa simu yake katika mkoba na kumpatia mama huyo pasipokuja alikuwa na shida gani na simu yake..
" Naomba pia uniletee simu yangu ile ''
" Sawa.. ''
Pia Felister hakuchoka alikwenda kuichukua simu hiyo ambayo ilikuwa haitazamiki kwa jinsi ilivyoharibika kwa ajali aliyopatwa nayo Saida siku alipokuwa akimfukuzia Patrick..
" Hii hapa mama.. ''
Saida aliipokea na kutoa laini, kisha akaifungua na simu ya Mwanadada huyo nayo pia akatoa lini na kuweka zake, za Felister akampatia azihifadhi mwenyewe ili zisije kupotea..
" Unaweza kuendelea na kazi zinginea.. ''
Aliongea Saida wakati huo akiiwasha GALAXYS Hiyo ya Felister..
" Patern yake unachora "S" ''
" Ooh!! Asante kwa kunikumbusha yaani nilishasahau kuhusu Rock ''
" Sawa.. Naona unataka kuchati leo.. Hahaha ''
" Mmmmh!! We nae?! Mbona fujo sasa?? ''
" Mmh! Fujo tena? Hahaha! Ngoja nikuache.. ''
Ulikuwa ni utani mwiingi sana! Uliofanya kuwepo na furaha muda wote kati ya wawili hao, Felister aliondoka na kuelekea jikoni kwaajili ya kuandaa chakula cha usiku huo.
Kitu cha kwanza alichokifanya Saida ni kuingia mtandaoni, alianza na WhatsApp ambapo kama kawaida alimkuta Patrick yupo online!, uyo akaachana nae akawatafuta maswahiba zake wengine na kuwatupia jumbe fupi fupi za kuwa hai ambapo nao hawakusita kumjibu, wengine waliokuwa wanajua matatizo yake walimpatia pole, wale ambao walikuwa hawajui aliwajuza na pia walimpa pole zao..
Lakini kila mara macho yalikuwa yakipenda kumwangalia Patrick ambae nae mda wote huo alikuwa mtandaoni, mwishowe uvumilivu ukamshinda akajikuta amemtumia ujumbe..
,,, Hii..
Hazikupita hata sekunde kazaa ujumbe wa saida uliwekwa Tiki mbili za blue kumaanisha ujumbe umesomwa!,, Baada ya ujumbe huo kwenda Presha ikaanza kumsumbua sasa! Alikuwa akihofia jibu atakalopewa hilo!
Lakini tofauti kabisa na alivyofikiria ujumbe huo haukujibiwa na Patrick aliendelea kuwa Online, Maumivu ya wivu yalianza kumla Saida taratibu! Alihisi kabisa mwanaume huyo anachati na wanawake wengine mtandaoni,
Baada ya kusubili saana! Bila ujumbe huo kujibiwa mwishowe aliamua kutoka na kuingia Facebook, huko alikuta kumepooa wala hakukuwa na maana yoyote, na hakuendelea kupoteza mda huko, akatoka na kuingia tena WhatsApp ambapo kwa mshangao zaidi alikuta ujumbe wake umejibiwa! Alianza kuogopa hata kuufungua kwa kuhisi angekutana na tusi la ajabu...!!
Lakini alichokitegemea kilikuwa ni tofauti na alichokikuta! Kwani Patrick alituma emoj moja tu! Iliyoonekana ikitapika! Kisha ikafuata Brock!
Hali ile ilimuumiza Saida pasipo na mfano, yaani alijikuta machozi yakimwagika pasipo yeye kulia unajua siku zote hizi tangu Patrick amfanyie kitendo kile cha aibu kabisa bado hakuwa anaamini kama mwanaume huyo alikuwa amemwacha kweli, kuna mda mpaka alifikiria huenda zilikuwa ni hasira tu! Na alipitiwa
Mpaka pale alipompiga kufuli WhatsApp mbele ya macho yake tena aliona kumpiga ban pekee isingetosha ili kudhihilisha ni kwa namna gani alikuwa hamtaki, aliamua kumtumia Emoj inayotapika! Daah!!
' Patrick ananiona mimi kama matapishi.. Eee!! '
Saida alijisemea kimoyo moyo wakati huo mashavu yote yakiwa yameloa machozi, macho mekundu mfano wa mtu alieingiwa na pilipili machoni...
' Nitalipiza kisasi.. '
Saida alihitimisha kujisemea kimoyo moyo, akazima dada na kuweka pembeni simu hiyo, akajilaza kitandani usingizi ukampitiaa..
" Mama..!! Mama..!! Mamaaa!! ''
" Ee.. Ee? Kuna nini?? ''
Saida alikurupuka kitandani baada ya kuitwa kwa sauti na Felister..
" Mbona umelala bila kula?? ''
" Oooh! Nilipitiwa hee.. ''
" Twende ukanawe baasi mama unalala saa hizi khaa? ''
" Yaani hata sijui nimepitiwaje? ''
Waliongea wakati huo wakikokotana kuelekea bafuni,, unaambiwa kwa jinsi Felister alivyomjali mama huyo alianza kumnawisha usoni, wakati huo nae akinawa mikono..
Hatimae walirudi na kukuta chakula kipo pale pale wodini..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Mmmh!! Umenikumbusha mbali mwanangu?? ''
" Kwanini? ''
" Hili swala la kulia mikekani niliwahi japo ni mda sana.. ''
" Hehehe.. Kawaida hii mbona halafu ujue napenda sana?? ''
" Kweli? ''
" Kuliko hata mezani.. ''
" Hahaha.. Hongera na wachache saana! ''
Stori hizo zikawasindikiza katika mlo huo wa usiku mpaka pale matumbo yao yaliposema Stop!!
Vyombo vilitolewa wodini humo, na hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya Felister kumuaga mama huyo maana yeye haruhusiwi kulala humo, wodi ni kwaajili ya wagonjwa tu!
" Sasa.. Mamaa uwe na usiku mwema ee! ''
" Ahsante! Usiku mwema pia na barikiwa sana.. ''
" Ameen.. ''
Felister alitoka humo ndani, Saida akafunga mlango na kujirusha kitandani, lifti nzuri ya usingizi ikamchukua mpaka majogoo...
*************************
" kokolikooo!!!.. Kokolikooo!!! ''
Ilikuwa ni Sauti kali ya jogoo kuwika iliyopenya kwa usahihi kabisa katika ngoma za masikio ya Ashura na kupelekea usingizi kumtoka!
Naam! Kulikuwa kumekucha sasa! Siku ambayo inatakiwa Ashura acheze ipasavyo na akili ya Patrick kwa maana ndiyo siku ambayo Ashura anarudi mjini na gari hana inatakiwa akili ya hali ya juu aicheze hapo la sivyo gemu linamshinda!
Mama mwenye nyumba yeye alikuwa bado akiuchapa usingizi,
Ashura akili ilikuwa inachemka baraa! Nini atamweleza mpaka Patrick amwelewe?
' Yap!! Nimepata wazo.. '
Alijisemea kimoyomoyo huku akijigeuzia upande wa pili.
' Lakini katika wazo hili ni lazima pesa kubwa itumike.. Japo siyo mbayaa maana kwenye utafutaji imeandikwa tumia pesa upate pesa!! '
Alizidi kujisemea Ashura wakati huo mwanga mwekundu ukizidi kutanda katika anga la mashariki. Asubuhi mara nyingi haja ndogo huwa zinasumbua sana! Na hii ndivyo ilivyokuwa kwa Ashura alichukua simu yake na kutoka nayo nje..
Wakati anaelekea Chooni.. Bado aliendelea kuwaza ni vipi ataipata pesa ya kusawazisha msala huo?
' Nimpange Patrick au nimpigie Dany?? '
Bado aliendelea kuchemsha akili, mwishowe akaona si vyema kwa siku hiyo kumpigia pigia Patrick ni vizuri DANI Ndiyo akamtumia pesa hiyo ili akamilishe mpango, hakutaka kulaza damu papo hapo akampigia Dany ambapo simu iliita mara mbili tu! Na kupokelewa!
" Naam.. Asha ''
" Za asubuhi Dany ''
" Njema za kwako.. ''
" Salama aaa.. Samahani kwa kukukata stimu za usingizi ''
" Wala usihofu.. Nipo macho tangu saa kumi ''
" Ahaa.. Ok hebu ninaomba unitumia laki tano hapo.. ''
" Vipi.. Kuna tatizo? ''
" Hapana hakuna tatizo ni matumizi binafsi ''
" Ok! Ila kukiwa na tatizo usisite kunijuza.. ''
" Usihofu kuhusu hilo.. ''
" Sawa nipatie dakika tano ''
" Sawa.. ''
Simu ikakatwa na baada ya dakika kadhaa meseji iliingia kwenye simu ya Ashura ambapo baada ya kuifungua alikutana na meseji ya muamala uliothibitisha yeye kupokea laki tano kutoka kwa Daniel Masubwa!
Hakusita alimpigia na kumjulisha kuwa tayari alishaipokea pesa hiyo na baada ya hapo walitakiana Asubuhi njema kisha simu zikakatwa!
Ashura aliludi mpaka ndani ambako alimkuta mama huyo tayari yupo macho!
" Ooh! Mama umeamka?? ''
" Ndiyo mwanangu umeamkaje?? ''
" Nashukuru nipo mzima kabisa mama yangu sijui wewe?? ''
" Mimi pia niko salama! ''
" Inshallah ''
Basi wote kwa pamoja walianza kushughulika na mambo ya kifungua kinywa, wakati huo Ashura akiwa na mawazo ya kupandisha mjini Asubuhi hiyo.
Unaambiwa kwa siku hizo mbili ambazo Ashura alikuwa ndani ya nyumba ya mama huyu basi mama huyu alipata kuishi maisha anayostahili kuishi kila mmoja! Asubuhi alipata kifungua kinywa, mchana alipata mlo wa kutosha! Na jioni kama kawaida.. Eee! Hayo ndiyo maisha, lakini sasa tabu tupu! Ashura akitoka mambo yanarudi pale pale..
Saa 07:30 PM,
Tayari walishapata kifungua kinywa ambacho kilikuwa ni Chai kwa sambusa za kutosha!
Baada hapo Ashura aliaga kuwa alikuwa akienda mjini mara moja na angerudi mishare ya saa nne hivi..
" Mwanangu au ndiyo unaenda jumla? ''
" Hapana mama nitarudi usijali kuna mambo nafuatilia ila saa nne nitarudi.. ''
" Sawa mwanangu nikutakie safari njema ''
" Ameen.. Mama Shukrana sana ''
Walipokwisha kuagana hivyo Ashura aliondoka na kuelekea Stendi ya nyang'oro tayari kichwani alishapata wazo kabambe sana iwapo lingefanikiwa..
Akili yake sasa ilikuwa Sheli ya kihesa, alipanga kuonana na wafanya kazi wa sheli hiyo ili wapange mpango mmoja kabambe, ambao kama ungefanikiwa basi Patrick angekuwa ameshika makaa ya moto kwa mikono!
Cha kwanza alichokifanya ni kutoa pesa ile aliyokuwa ametumiwa na Dany ili aiweke mfukoni ili pale watakapokuwa wanazungumza na pesa iwepo. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio!
Mpango wake ulikwenda sawa, alifanikiwa kuitoa pesa hiyo na kuiweka kwenye mkoba kisha akatoka hapo kwenye kibanda cha wakala..
Breck ya kwanza ilikuwa ni kwenye kijiwe cha boda boda! Alitaka kutumia usafiri huo kwani aliamini ndiyo wa haraka zaidi..
" Mambo.. Mkaka ''
Ashura alisalimia kwa salamu ya kiujana ujana!
" Poa poa.. Karibu dada ''
" Asante.. Vipi waweza nikimbiza kihesa mara moja?? ''
" Bila shaka ''
" Utanichaji ngapi kaka ''
" Elfu ishirini ninakupeleka ''
" Kamata elfu thelathini tutaenda na kurudi.. ''
" Hapooo.. Hamna tatizo ngoja nijaze mafuta.. ''
" Sawa changamka ''
Mbele ya pesa watu huchangamka asikwambie mtu! Unaambiwa ndani ya dakika tatu! Wawili hao walikuwa juu ya pikipiki makini sana aina ya SKY MARK SM-150 Na tayari walishaanza kuzipunguza kilomita!
Kwa mda huo Ashura hakutaka tena usumbufu wa aina yoyote alichokifanya ni kuizima simu yake kabisa!
Saa 09:25
Naam! Walishatimba kihesa sheli, mahali alipokuwa amepakusudia Ashura, cha kwanza alitizama kila upande kuona kama kutakuwa na mtu yeyote anaemfahamu? Kwa bahati nzuri hakukuwa na yeyote aliemtilia Shaka..
" Nisubili ninakuja sasa hivi ''
" Sawa dada ila usikawie.. ''
" Usihofu ''
Ashura bila kupoteza mda aliingia ndani ya Sheli hiyo na kuonana na baadhi ya wafanya kazi, aliwaambia kuwa alihitaji kuonana na wamiliki wa sheli hiyo.
" Unataka kuonana na mabosi ili iweje?? ''
" Nina shida nao kaka angu nisaidie tafadhari.. ''
Kijana huyo alianza kujiuma uma ni wazi kabisa kuna kitu alikuwa akikihitaji, Ashura alitambua hilo akatoa noti ya Shlingi elfu tano na kumkabidhi kijana huyo..
Ndipo akakubali kumpeleka katika ofisi walipo wamiliki wa Sheli hiyo..
" Twende nikupeleke.. ''
" Sawa.. ''
' Hahaha.. Wabongo rushwa zitatuua '
Alicheka kimoyo moyo Ashura na kujisemea peke yake, wakati huo wanaelekea katika majengo zilipo ofisi za wamiliki wa sheli hiyo..
Hawakupata shida kufika, Ashura alifanikiwa kuonana na watu aliokuwa akiwahitaji kwa udi na uvumba, na bila kupoteza mda alieleza kile kilichompeleka pale..
Alidanganya kuwa alikuwa ameibiwa gari, na gari hiyo haikuwa yake ilikuwa ni gari ya bosi wake ambae alikuwa ni mkali kama mbogo na asingemwelewa kabisa kwani mahali gari hiyo ilipoibiwa kuna uzembe kidogo aliufanya hivyo alikuwa mahali pale kuhitaji msaada wao..
" Kwahiyo sisi tukusaidiaje hapo?? ''
Alikutana na Swali hilo...
" A'a nilitaka kifanyike kitu ionekane nilikuwa najaza mafuta hapa, ila kosa ni kwamba niliacha funguo ndani, akatokea mtu asiejulikana na kuivamia gari na kuondoka nayo. ''
Ashura aliongea kwa kujiamini kabisa pasipo kupepesa macho wala kujiumauma, hali iliyopelekea wamiliki wa sheli hiyo kumtizama kwa makini..
" Unataka kutuletea matatizo? ''
" Siyo matatizo kaka ''
" Ila ''
" Tutasaidiana na kuliandana ''
Tayari kwa mtu mwelewa ameshajua nini anamaanisha Ashura,
" Umejipanga? ''
" Ndiyo.. ''
" Umejipangaje? ''
" Ah! Hapo ninahitaji kuwasikia kwanza nyinyi.. ''
" Kama utakuwa umejipanga kwa kilo tatu, tunakusaidia ''
Kilo tatu kwa wale ambao hamjaelewa ilimaanishwa milioni tatu..
" Kaka zangu naomba mnisaidie kwa kilo mbili.. ''
" Hapana haitowezekana kwa sababu, inatakiwa gari ya bandia pamoja na mtu wa kujifanya kazua huo msala, pili inatakiwa mfanyakazi anaehusika na paipu ya mafuta ahusishwe na azibwe mdomo, haya tuna CCTV Inatakiwa tuzime kwa mda na tutafute la kujibu juu ya kutofanya kazi kwa camera hizo ndani ya mda ambao tukio linatakoe, hivyo kama unaweza jipange tumalize kazi.. ''
Mmoja kati ya wamiliki wa sheli hiyo alizungumza kwa urefu zaidi ili Ashura apate kumwelewa..
" Sawa nimewaelewa.. Ila kuna mawasiliano nahitaji kuyafanya ''
" Fanya hapa hapa ''
" Hapa? ''
" Yaah! Fanya twende na mda hutakiwi tena kutoka toka hivyo.. ''
" Sawa ''
Hakukuwa na jinsi Ashura alitoa simu yake na kumpigia Dany, simu ilita mara tatu na kupokelewa..
" Hallo.. ''
" Ndiyo.. Dany ''
" Safi hebu fanya kitu ''
" Nakusikiliza.. ''
" Bosi yupo hapo? ''
Daniel akaelewa kila kitu, kumbuka hawa ni watukutu wa mda mrefu hivyo basi tambua wanaweza kuzungumza kwa mafumbo au ishara zitakazokufanya usielewe chochote..
Neno ' Bosi ' likamfanya Dany kutambua ya kwamba Ashura yuko mahali anahitaji msaada fulani alichopaswa kukifanya hapo ni kuwa makini kumwelewa kila anachokizungumza..
" Bosiii.. Alikwepo vipi kuna tatizo? ''
" Kaenda wapi? ''
" Sijajua kwani watakaje? ''
" Nimekwama Bomba tatu pale ''
" Aha! Sawa nimekupata.. ''
Hahaha.. Hata wewe shabika hapo hujaelewa.
Hebu nikuchambulie kwa haraka haraka. Ni hivi..
- Neno " Boss ''
Tafsiri yake ni tatizo, hii ni kwa mujibu wa ishara zao za mazungumzo yaliyo ya siri ambayo haipaswi yeyote kutambua..
- Neno " Bomba ''
Tafsiri yake ni pesa, kwahiyo mmoja kati yao akisema nipo bombani maana yake anahitaji milioni moja haraka, eidha kakamatwa na polisi na anahitaji msaada wa pesa kwa mwenzie ili aweze kutoa hongo. Mafumbo hayo ndiyo hutumika ili hata polisi wasigundue chochote..
Nazani hapo umenipata japo kwa ufupi. Sasa tuendelee..
Mazungumzo hayo yalizua maswali kibao kwa wamiliki wa Sheli ile ndani ya ofisi yao kwani wao walichoambulia ni kusikia tu! Ila hawajelewa chochote!
" Je? Hii kazi tutaifanya muda gani? ''
Ashura aliuliza..
" Wowote utakao wewe hata saizi ''
" Mimi nafikiri......... ''
Kabla hajamalizia Sentesi yake mtetemo wa Vibration ya simu ukamkatisha, alipoitizama akagundua ni ujumbe mfupi yaani SMS, haraka akafungua na kukutana na sms ya muamala kuwa alipokea milioni tatu na laki tano kutoka kwa Daniel Masubwa..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
' Yes! safi sana '
Alijisemea Ashura kimoyomoyo wakati huo anainua kichwa chake taratibu na kuwatizama tena wanaume wale waliokuwa mbele yake..
" Mimi naona jioni ndiyo mda mzuri sana ''
" Sawa.. Ila hutotakiwa kutoka tena hapa mpaka kazi iishe.. ''
" Halafu sasa kuna mtu kanileta na boda boda ananingoja.. ''
" Huyo ataambiwa aende tu wewe hutakiwi kutoka hapa ''
" Sawa nimewaelewa ''
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment