Simulizi : Mzimu Umerudi Tena Kulipiza Kisasi
Sehemu Ya Tano (5)
Mpango wa kurudi tena Ismani ukafeli, yule boda boda alitumiwa mtu na kuambiwa kuwa yule mteja wake alikuwa amepata shughuli flani iliyom'bana pale hivyo asingetoka mda huo..
" Sasa sijalipwa ujira wangu kaka ''
Yule kijana alilalama..
" Nipatie namba yako nimpelekee. ''
Namba ikatolewa, japo boda boda huyo hakuwa na matumaini kama angepewa kweli pesa hiyo, ila tu alitoa namba na kisha kuondoka zake..
' Akinidhulumu potelea mbali '
Kijana alijisema huku akizidi kuvuta mafuta ili kuwahi kijiweni tena..
" Dada.. Kijana kasema hujamlipa hela yake ''
Tarishi aliludi na taarifa mpya!
" Ooh! Yuko wapi? ''
" Kaenda ila kanipa namba ya simu... ''
" Nitajie ''
" 0672****** ''
" Asante ''
Papo hapo Ashura hakutaka kuchelewa akamtumia boda boda huyo pesa yake..
*** MASAA YAKASONGA... HATIMAE MDA ULIOKUWA UKINGOJEWA UKAWADIA ***
Naam! Saa kumi na mbili na nusu ndiyo mda uliokuwa umepangwa lifanyike tukio kubwa la ajabu hapo sheli,
" Sasa mda ndiyo huu ''
" Ndiyo ''
" Malipo kwanza ''
" Hakuna shida naomba namba za akaunt ya benk ''
Walimtajia kisha muamala ukafanyika, baada ya hapo Ashura akatolewa mlango mwingine na kutoke sehemu nyingine, kumbuka mpaka hapo wanaoujua uwepo wa dada huyo hapo sheli ni watu wachache sana hata watano hawafiki..
Alikwenda kupewa Prado nyingine inayofanana na hiyo na kuambiwa aiendeshe mpaka eneo la kujaza mafuta baada ya hapo yeye atashuka na kuacha funguo ndani na kuelekea kule yanakowekwa mafuta, baada ya hapo kuna kijana atakuja kuikurupua!
Dooh! Lilikuwa ni bonge la sinema!
Ashura alifanya vile vile.. Aliendesha gari na kwenda kuipaki pale inapotakiwa kupaki gari yoyote inayohitaji kujazwa mafuta hapo sheli.
Kama kawaida Ashura aliteremka garini kama mtu yeyote anaehitaji huduma hapo. Akaongea na kijana anaesimamia suala zima la uuzaji mafuta ambae na pia alikuwa ameshatonywa kuhusu mpango huo
Wakati huo mlango wa gari upo wazi na ufunguo ulee! Pili haijazimwa iko on, inatokota pale!
Sasi ile wanatumbukiza paipu tu kwenye tank, kuna mhuni akatokea tena akiwa kaficha sura yake! Wakiwa bado wanashangaa akazama ndani ya gari..
" Uwiii.. ''
Ashura akajifanya kushtuka gari ikaondolewa na kuacha mpira unamwaga mafuta chini..
"Gariinaibiwaaa..... pyreeeeeeh!! ''
Yule kijana aliekuwa anamhudumia Ashura alipiga yowe kali ikifuatiwa na filimbi..
Boda boda zikajaa barabarani kumfukuzia mwizi huyo. Hata hivyo juhudi zao ziligonga mwamba mtu huyo alikuwa ni mtaalamu wa usukani baraa ndani ya dakika tano tu! Hakukuwa na hata dalili ya kwamba mtu alitoka na gari eneo hilo..
Ashura alijifanya kuangua yowe kali lililoambatana na machozi ya fulaha ambayo kwa watu weingine walijua analia, alijilegeza na kuanguka chini
Alibebwa na kupelekwa tena katika ofisi za wamiliki wa sheli hiyo..
" Hee! Dada vipi tena? ''
Walijifanya hawajui ili kuwapoteza wale waliomleta humo ndani..
" Niliacha funguo mimi aaaah! ''
" Heee! Pole yako na huo ni uzembe wako .. Kwanza inatakiwa unaposhuka garini bana mlango.. A'a ona sasa ''
Walijifanya kugomba.. Mpaka pale wale waliomleta kutoka nje ndipo story mpya zikazuka!
" Shukran sana! Kaka zangu mmenisaidia mno ''
" Usihofu kikubwa ibaki kuwa siri tu ''
" Mimi tena? Sisubutu kusema popote ''
" Ok! Sasa endelea kumpanga huyo bosi wako ''
Ashura alitoka mle ndani kwa mara nyingine, kwenda nje kwa Staili ya mtu aliechanganyikiwa na kutembea mpaka kina moja tulivu sana, kwaajili ya kumwarifu Patrick kile kilichotoke, wakati huo huku ndani wakaafikiana kuwa inatakiwa ile memory card inayohifadhi matukio yote yanayorekodiwa pale itolewe na kuharibiwa kabisa ili kufuta kila kitu kwa maana wanaamini hata kama camera zilizimwa mda ule lakini asubuhi wakati anafika hapo alirekodiwa hivyo kikubwa ni memory kuharibiwa,
Haraka memory hiyo ikaenda kutolewa na kuvunjwa vunjwa kisha ikabadili nyingine..
Ashura alikwenda mpaka mahali palipotulia na kuanza kuitafuta namba ya Patrick, hakupata shida kuipata..
Akapiga!!
'' Ngrrr!! Ngrrr!! Ngrrr!! Ngrrr!! ''
Alimnasa hewani...!!
" Halloo.. Mke wangu! ''
Simu ikapokelewa kwa mbwembwe nyingiii..
" Patrick.. Gari imebiwa!! ''
Ashura alizungumza kwa sauti kavu yenye kutilia mkazo kwelikweli,, roho ya Patrick ikapiga paah!!
" Nini?! ''
" Wahi.. Ni hapa kihesa sheli ''
" Imeibiwaje? ''
Patrick aliuliza huku akisimama kabisa sofani alipokuwa kajipumzisha..
" Nilikuwa najaza mafuta hapa sheli ndipo kuna mtu kaja gafla na kupanda garini na kuondoka nayo ''
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ashura alijibu..
" Sijakuelewa.. Kwani funguo uliacha garini? ''
Patrick aliuliza huku taharuki ikizidi kumpanda..
" Sikuwa hata nimelizima na mlango niliacha wazi kwa maana sikuwa na wasiwasi wowote ''
Ashura alitoa jibu ambalo kwa Patrick lilikuwa ni kama msumali wa moto ndani ya kidonda kibichi, gari ya bei ghari namna hii halafu eti imeibiwa?
" Shiiiit.. Nakuja sasa hivi.. ''
Patrick alijibu kisha akakata simu na kukimbilia chumbani kwake, moja kwa moja akalisogelea kabati la nguo na kuvuta track moja na sweta lake na kuviweka kitandani, akavua zile alizokuwa kazivaa, na kuzitupia huko, akachuku track ile na sweta lake akazitia mwilini..
Akachukua na bastola yake iliyokuwa na risasi za kutosha akaichomeka kwenye soksi, akabeba funguo za gari na kutoka nazo nje..
" Fungua geti hapo haraka.. ''
Patrick alimwambia mlinzi wake wa geti bwana Emanuel afungue geti wakati huo yeye akielekea uwani kuchukua gari..
Gari aliyokuwa amepanga kuondoka nayo Patrick ilikuwa ni Rand Rover moja hatari sana toleo la mwaka 2008 Aliyoinunua Japan mwaka 2012 Kwa Dola Elfu sitini za kimarekani..
Gari hiyo inauwezo wa kwenda Kiromita elfu tano kwa saa!, nae aliamini kwa kutumia gari hiyo angeweza kunusuru gari yake hiyo yenye thamani kubwa pia..
Alichomeka funguo na kuiwasha, gia namba moja ikapangwa na kuigeuza kwa nguvu mpaka ikalenga usawa wa geti la kutokea nje!
Hakulemba! Akaingiza gia ya pili na kukanyaga mafuta, gari ikachomoka kwa kasi na kupita getini kama upepo, Emanuel alibaki kumshangaa bosi wake tu!
' Nini kimempata tena na jioni hii? '
Emanuel alijiuliza pasi na kupata jibu, mwishowe akafunga geti na kurudi kibandani kwake..
***
Ni ndani ya dakika tano tu! Patrick alishatia timu ndani ya sheli hiyo ya kihesa, alikuta umati mkubwa wa watu mahali pale, kila mtu alikuwa akiguna kwa jinsi tukio kubwa lilivyotendeka kwa mda mfupi..
" Kwani ilikuwaje? ''
Patrick alimuuliza kijana yule anahusika na swala zima la kuwahudumia wale wote wanahitaji huduma ya kujaziwa mafuta gari zao..
" Huyo dada alikuja na gari yake na kuipaki hapa, akashuka na kuja kunipa maelekeza kiasi cha mafuta anayohitaji kuwekewa, sasa ndiyo tumetumbukiza mpira ndipo alitokea mwanaume alieziba sura yake na kuingia gari gafla gafla na gari ikaondoka ''
Kijana huyo alijibu, jibu ambalo kwa namna moja ama nyingine lilimfanya Patrick ajutie kumpatia gari yake mwanadada huyo yaani alijutia kweeli..
" Sasa huyo mtu kaelekea wapi? ''
Patrick aliuliza wakati huo jasho jingi likianza kumwagika pasipo na jua wala kazi yoyote anayifanya
" Ameenda na barabara hiyo ya Dodoma, japo vijana wa boda boda walijaribu kutoa msaada kwa kumfukuzia na pikipiki ila walishindwa.. ''
" Shiiiiiit... Huyo dada yupo wapi? ''
Patrick aliuliza akiwa na maana ya kumuulizia Ashura..
" Nipo hapa.... ''
" Panda kwenye gari tuondoke ''
Walipanda kwenye gari aliyokuja nayo Patrick na kuondoka katika eneo hilo kwa kasi kama kimbunga!
" Hakikisheni mnazuia gari zote ndogo kutoka Iringa mjini hapo getini kuna gari imeibiwa huku ''
" Tumekupata ''
Patrick aliwasiliana na walinzi wa geti la Iginglanyi.. Ili wazuie gari zote ndogo kutoka Iringa mjini, baada ya hapo akatupia simu pembeni na kukanyaga mafuta ipasavyo.
Brek ya kwanza ilikuwa getini.. Hapo alikutana na gari kadhaa zilizozuiliwa! Ila yake hakuiona..
" Vipi mzee hizi hapa ''
" Waruhusu hapo haipo.. Je? Kuna prado yoyote nyeupe ilipita kabla ya mimi kupiga simu?? ''
" Yaah! Kuna prado ya rangi hiyo ilipita dakika moja kabla ''
" Ok! Shukran ''
Patrick aliamini kwamba gari hiyo iliyopita hapo dakika moja kabla ya yeye kupiga simu ndiyo hiyo iliyokuwa imeibiwa, mzee akajitosa barabarani kuifukuzia..
Huyu bwana kwenye usukani ni shiiiidaaa! Unaambiwa alipanga gia zote mpaka zikaisha! Exreter alikanyaga mpaka ikagusa mwisho! Spidi nazo alihakikisha mshale unacheza kwenye namba nyekundu ambazo ni 260, aiseee! Mwendo huo sasa! Mashindano ya magari ya marason yaende shule!
Shida ikabaki kwa Ashura sasa! Hakuweza kutulia kwenye siti hasa sehemu za kona! Patrick alikuwa analala kwa fujo konani mpaka Ashura anakwenda kupiga kichwa kwenye kioo cha dirisha.. Naaam! Akikunja kushoto Ashura anahama siti na kwenda kupiga kichwa bega la Patrick!! Hahaha! Ilikuwa ni baraa!!
***
Saa 07:20 PM, waliweza kuwasiri Isimani, hiyo gari hawakuweza kuikuta, pia giza lilianza kutanda juhudi za Patrick kuikamata gari hiyo zikagonga mwamba,
Wenda yule msafiri alikuwa na gari hiyo alichepukia karibu tu.. wao wanakimbiakimbia ovyo tu!
Hata hivyo hakukata tamaa! Aliwasha taa na kuendelea kusonga! Aliifuatilia sana gari hiyo lakini wapi hakuweza kuikuta mpaka usiku mnene unaingi walikuwa makonani huko, ikabidi Patrick ageuze tu hakuwa na namna..
" Ngoja turudi tu.. Lakini hiyo gari nitaipata tu, nitapiga simu vituo vyote vya polisi na nitaweka msako nchi nzima! ''
Patrick alizungumza wakati huo wakiwa wanarudi sasa..
" Yaani.. Sijui huyu mtu alikuwa ananifuatilia? ''
Ashura aliongea kwa kuigiza sauti yenye masikitiko makubwa..
" Tulia mke wangu nitaipata tu! Ujue kwa sasa hivi nina maadui wengi sana kisa mafanikio na huyo wenda alikuwa anakufuatilia.. ''
" Daaah!! ''
" Lakini usiwaze tutaipata ''
" Lakini.. Ninaumia sana Patrick ''
" Ninatambua ya kwamba unaumia ila usihofu ni mambo ya kawaida ''
Story hizo zikawasindikiza mpaka nyang'oro ambapo walishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwa tayari ilishakuwa usiku mnene,
Walitafuta gesti na kwa bahati nzuri wakaipata na kuchukua chumba,
Hakika kwa siku hiyo Patrick hakuwa na amani kabisa, mara kadhaa alijaribu kufikiria ni nani aliemfanyia mchezo huo ila jibu hakulipata..
***
Asubuhi na mapema waliwahi kuamka, kwanza kiufupi Patrick hakulala usiku huo tumbo lilikuwa moto sana! Hali iliyompelekea awe macho mpaka majogoo,
Ashura alizidisha umakini sana kwa mwanaume huyo, kila alichokizungumza Patrick alikitafsiri kwa upande wa pili ili Kama Kuna mabadiliko atambue mapema..
Walitoka hapo gest na kwenda mgahawani kupata chai, wakiwa hapo mgahawani ndipo Patrick alipoanza kusambaza taarifa vituo vyote vya polisi nchi nzima pamoja na kambi kadhaa za jeshi alizokuwa anafahamiana nao.
Siyo hivyo tu! Taarifa zilisamaa mpaka vituo mbalimbali vya redio na akatangaza dau nono kwa yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa gari hiyo..
Baada ya hapo walipanda gari na kuanza kurudi kihesa..
" Lakini Ashuu.. Jana imekuwaje unakuja kimya kimya bila kuniarifu?? ''
Patrick aliuliza swali la kushtukiza wakati huo anavuta mkanda wa siti ajifunge kwaajili ya usalama barabarani..
" Simu haikuwa na chaji mume wangu nilikuwa nimeiweka chaji ndani ya gari, nilitoa pindi nashuka pale sheli ''
Kiufupi ninaweza kusema.. Dada huyu ana kipaji cha uwongo siyo makhara, yaani alidanganya kwa point ambayo licha ya Patrick ingekuwa ngumu hata kwa mtu yeyote kuweza kugundua kama ulikuwa ni uongo wa maangamizi..
" Daah! Kumbe ulizimiwa na simu? ''
" Ndiyo jamani.. Sasa ningeanzaje kuja pasipo kukupa taarifa? ''
" Hata mi nilitaka kushangaa! ''
" Ndiyo ivyo baby ''
" Basi usiwaze.. ''
Walifika mpaka kihesa.. Ambapo ndipo yalipo makazi ya Patrick ambapo kama kawaida mlinzi wa geti aliwafungulia..
Maisha yakaanza upya! Lakini kwa upande wa pili mlinzi wa geti bwana Emanuel alijawa na maswali lukuki kuhusu gari aliyoondoka nayo Ashura siku mbili zilizopita..
' Mmmh!! Jana katoka mkuku mkuku.. Leo anarudi na huyu mwanamke kampakia, Je, gari aliyotoka nayo majuzi iko wapi? '
Emanuel alijiuliza sana swali hilo pasipo kulipatia jibu..
Maisha yakaendelea kusonga, hatimae siku tatu zikakatika pasipo Patrick kupewa ripoti yoyote kuhusu gari yake..
' Aah! Ina maana gari yangu ndiyo imeenda hivi? '
Ndiyo swali alilojiuliza Patrick kila leo, Baadae wiki ikakatika! Hapo ndipo patrick alipojihakikishia kuwa walioiba gari yake walikuwa ni watu hatari sana na mpaka hapo asingeweza kuiona!
Daah!!
Hali ya Saida ilikuwa imeshatengemaa sasa tangu afanyiwe upasuaji kwa mara ya pili kiufupi ni kwamba ilibaki tu kufutika ile alama ya pale alipokuwa amefanyiwa upasuaji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Madaktari wa Hospitali ya IPAMBA Walimpa taarifa ya kwamba zilikuwa zimesalia siku mbili tu aweze kuruhusiwa Hospitalini hapo..
" Sasa mwanangu mimi ninaruhusiwa kesho kutwa hapa.. ''
Saida aliongea akimwambia Felister. Ilikuwa ni jioni moja tulivu sana!
" Unakwenda wapi?! ''
Felister aliuliza kwa tahamaki kubwa!
" Ndiyo ninaruhusiwa.. ''
" Sawa najua unaruhusiwa ila wapi unakwenda? ''
" Mjini narudi.. ''
" Kwa mumeo huyo au? ''
" Hapana nitaenda kupanga chumba sehemu nyingine.. ''
" Lakini mama.. Tulikubaliana nini siku za nyuma? ''
" Ninakumbuka ya kwamba tuliahidiana kuwa tutaenda kuishi kwako siyo? ''
" Ndiyo.. ''
" Asante.. Nashukuru sana kwa moyo wako narudia tena nashukuru kwa kunipigania uhai wangu kwa nguvu zako zote ninakiri sina cha kukulipa, ila nakukabidhi mikononi mwake bwana akupe maisha malefu ''
" Asante ninashukuru pia.. Lakini ni kipi kimekubadilisha mawazo na kutaka kukaa mbali nami? ''
" Nimependa mimi iwe hivyo na ninasikitika ya kwamba huwezi kuyabadili mawazo hayo.. ''
Felister alivuta pumzi ndefu na kuishusha, mawazo mengi yakaanza kuzunguka kichwani mwake, hakujua amshauri vipi mama huyo ambae alikuwa amemzoea kama mama yake mzazi aendelee kuwa nae,
" Kesho ninaondoka.. ''
Saida alihitimisha na kupanda kitandani kwake kwaajili ya safari nzima ya kuusaka usingizi..
Mawazo mengi sana yalikizonga kichwa cha Felister, wakati huo akiwa bado pale wodini kakaa mkekani walipokuwa wamekaa na Saida hapo awali, hakika alijikuta anatoa macho mwanadada huyo.
Lakini machozi hayo hayakuwa na maana yoyote kwake, hayakuweza kubadili msimamo wa mwanamama huyo alibaki kuushikilia kuwa siku ya pili yake kabla ya kuruhusiwa angeondoka hospitalini hapo..
Felister hakuwa na jinsi alibeba vyombo walivyokuwa wakilia chakula na kuondoka wodini hapo.
***
Sauti za majogoo kuwika mitaa ya jirani na Hospitali hiyo zilimtoa usingizini Saida..
Naam.. Kulikuwa kumekucha sasa! Ni siku ya pili,, siku ambayo Saida angeondoka IPAMBA Baada ya kusota kwa wiki kazaa, pia ni siku ambayo ingekuwa ni siku chungu kwa Felister kama matango pori..
" Ngo! Ngo! Ngo! Ngo! ''
Mlango wa wodi ya Saida ukagongwa..
" Ingia ''
Saida amkaruhusu mgongaji, ambapo mlango ulisukumwa, na Felister akaingia akiwa na chupa ya chai mikononi pamoja na vitafunwa vyake.
" Mama shikamoo ''
" Marhaba za kuamaka? ''
" Salama.. Za kuamka wewe? ''
" Njema kabisa. ''
" Tunashukuru.. Karibu kifungua kinywa.. ''
" Asante.. Kiweke hapo ''
Saida aliamka na kuelekea bafuni kunawa uso, hazikupita hata dakika tano akarudi, ambapo alimkuta Felister akimiminia chai nzito ya maziwa kwenye kikombe, pembeni kukiwa na chapati za kutosha.
Kumbuka.. Hayo yote alikuwa akiyafanya kwa gharama yake mwenyewe, maana hospitali iliweza kumsaidia matibabu kwa maana aliletwa na serikali..
Saida baada ya kunywa chai alimshukuru binti huyo na pia kumkumbusha ya kwamba siku hiyo ndiyo siku ya yeye kuondoka..
" Lakini.. Mama una tatizo gani? ''
" Sina tatizo binti yangu hayo ni maamuzi yangu binafsi ''
" Aaa..!! ''
Felister alishindwa kuyazuia machozi kwa mara ya pili, tayari alishamtabili mama huyo kuwa kiu yake kubwa ilikuwa ni mumewe tu hakuwa na jipya hapo..
' Hakika mapenzi ni upofu.. Hapa ndiyo naamini.. '
Aliwaza Felister wakati huo akiwa hana namna, na hana cha kufanya bali alikuwa akisubili kushuhudia mama huyo akibeba kifurushi cha nguo zake.
Na kweli..!!
Mnamo majira ya saa moja na dakika Isirini asubuhi Saida alionekana akishuka ngazi kutoka katika jengo la hospitali hiyo kubwa na sasa alikuwa akielekea getini..
" Wapi Mama? ''
" Mshindo.. ''
" Haya nipe buku tatu hapo ''
" Nina elfu mbili ''
" Lete iyo.. ''
Yalikuwa ni maongezi kati ya Saida na mwendesha boda boda pindi alipokuwa ametoka nje ya uzio wa hospital hiyo..
Saida alipanda boda boda iliyompeleka moja kwa moja mpaka sehemu moja wanaita mshindo, ni kabla ya kufika Iringa mjini ndani..
Huko alipanga chumba na kuanza maisha mapya!
Unajua bahati ya Saida ni kwamba siku ile anamfukuzia Patrick mpaka anapatwa na ajali, alikuwa na kadi zake za benk kwenye mkoba wake, hiyo ilikuwa ni maandalizi ya siku moja kabla ya mkasa huo aliziweka kadi hizo kwenye mkoba wake kwa lengo la kutaka kwenda kutoa pesa benk siku ya pili yake ambapo kwa bahati mbaya kukakucha na baraa!
Naam! Saida sasa alikuwa ameyaanza maisha mapya! Maisha ya kutokuwa na muume, tena aliapa kutokuja kuolewa tena mpaka anaingia kaburini. Saida alitokea kuwachukia wanaume wote duniani na kuwaona ni kama nyoka fulani wenye sumu kali..
***
Siku moja ikiwa ni mida ya mchana, mida ya pilikapilika, Saida alishuka sokoni kwenda kununua mahitaji, soko hilo lipo mashine tatu karibu sana na stand kuu ya mabasi Iringa. Lakini pia siku hiyo alitaka kuosha osha macho kwa maana alikuwa na mda mrefu sana hajatembea..
Wale wote waliokuwa wanamfahamu Saida hakika walimshanga kumuona akitembea barabarani, yaani Saida yule mke wa tajiri anaemiliki majengo na mahoteli ya kifahali, na ambae siku za nyuma alikuwa akitembele V8 ya nguvu kila mahali leo hii anatembea ya mguu?
" Hivi yule si mke wa Patrick? ''
" Ndiyo kama mwenyewe.. ''
" Mbona kapungua? ''
" Sijui.. Halafu ana makovu mfano wa mtu aliepataga ajali? ''
" Licha ya hilo, mbona leo yupo ya mguu? ''
" Hata mi nashangaa! ''
Popote alipopita Saida nyuma aliacha minong'ono na hata wengine wenye vinywa vya moto walidiriki kumcheka!
Ila yeye hakujali aliingia mpaka sokoni ndani na kupata mahitaji yake muhimu, na taratibu akaanza kurudi mahali anapoishi,
Mara gafla katika tembea yake macho yake yaligongana na uso wa mlinzi wake wa geti bwana Emanuel, nae pia alikuwa katika mizunguko zunguko ya hapo mjini ila haikujulikana alikuwa na mishe gani pale, Saida alitamani sana amsalimie mwanaume huyo aliekuwa na roho ya kibinadam isiyo na kinyongo, lakini kwa bahati mbaya haikuwa hivyo kwani Emanuel hakuwa amemwona Saida hivyo alipotelea kwenye umati wa watu..
Saida kumuona Emanuel kuliamsha kumbukumbu nyingi sana kichwani kwake. Kumbukumbu ambazo mwishowe ziliweza kumtoa machozi, hii ni baada ya kukumbuka mambo mengi sana ya nyuma!
Alifika mpaka pale alipopanga, kwanza hakuwa na hamu tena ya kupika mazaga zaga yale, hivyo aliyaweka tu na kwenda kupanda kitandani..
' Lazima nilipe kisasi kwa hiki alichonitendea huyu mwanaume sintokubali kushindwa kirahisi namna hii.. Felister nisamehe huko uliko nina imani nimekuacha katika lindi kubwa la mawazo yanayokuumiza na usijue sababu ya mimi kukuacha peke yako ingali ulitokea kunipenda na kunijali kama mama yako, ila sijaweza kwenda na matakwa yako kwa maana nina vita kubwa sana mbele yangu na sitaki kukushirikisha wenda ikakupoteza na nikakosa cha kujibu siku ya kiama '
Saida alijisemea kimoyomoyo wakati akiwa kitandani pale..
Naam! Hapa ndipo tunapata kujua sababu ya Saida kumchenjia gafla Felister mschana aliejitolea kwa hali na mali kumhudumia kule Hospitali, na kumwahidi kuwa angekuwa nae mda wote na pia akamwomba endapo ataruhusiwa waende kuishi pamoja kule anakoishi Felister, mwanzoni walikubaliana lakini baadae mama huyo alikuja kugeuka na kuondoka hali iliyomwacha njia panda Felister na kibaya zaidi hakumwambia sababu haswa iliyobadilisha uamuzi wa awali waliokuwa wameafikiana..
Kumbe Saida kapanga kulipiza kisasi dhidi ya Patrick na ndiyo sababu kubwa ya yeye kutengana na Felister kwa kuhofia usalama wa Binti huyo.
Ilikuwa imepita takribani wiki moja tangu Saida ahamie pale Mshindo, na leo ilikuwa ni siku nyingine tena, Saida aliamka mamepa sana yaani alfajiri mno, aliamka na kusali sara ndefu, sara ambayo ilichukua takribani nusu saa nzima kiasi cha kupelekea jasho jembamba kuanza kumshuka..
Hatimae alihitisha sara hiyo na baada ya hapo akaingia jikoni na kuanza kuandaa chai..
Nusu saa nyingine ilitosha maandalizi hayo chai, akainywa baada ya hapo aliingia bafuni na kuoga nako pia akatoka..
Alirudi ndani na kutupia viwalo vya uhakika na kutoka, kwa jinsi alivyoonekana ni dhahiri kabisa alikuwa na safari..
Baada ya maandalizi kukamilika alitoka na kufunga chumba chake na kuondoka safari ikaiva.
***
Safari ya Saida ilitia nanga nje ya jengo kubwa la mahakama inayoshughulika na mambo ya Jinsia, wazee na watoto..
Lengo la Saida kufika mahakamani lilikuwa ni kupinga taraka aliyokuwa amepewa na mumewe Patrick kinyume na taratibu za kisheria Wiki kadhaa zilizopita.
Naam! Alikuwa na uhakika wa kushinda kwa asilimia mia moja, na kama ingetokea akashinda basi Patrick angelazimika kupasua mali ile aliyokuwa anamiliki ili amgawie nusu Saida kwani ndiye mwanamke aliechuma nae..
' Ee mola nisimamie katika hili '
Alijisemea Saida wakati huo akiwa katika mabenchi akisubili zamu yake ya kwenda kuona na hakimu..
" Saida Yahya! ''
Askari aliekuwa katika mlango wa kuingilia ndani ya mahakama hiyo aliita, kumaanisha zamu ya Saida imewadia..
Kwanza tumbo lilimpasuka paa! Mwili mzima ukamsisimka, taratibu akanyanyuka kwenye benchi na kujiweka sawa moja mbili akawa anaingia ndani ya jengo hilo kubwa la mahakama hii ya pili kwa kubwa mkoani Iringa ukiachana na mahakama ya Ardhi..
Ndani ye jengo hilo kulikuwa na ukimya wa ajabu! Yaani hutosikia hata mlio wa nzi, maana ake hata mapigo yako ya moyo yanapodunda husikika!
Mara moja mahakama hii ilikaa tayari na kutega sikio kumsikiliza mwanamke huyo,
Nae bila hiana alieleza kile kilichompeleka pale, alieleza kwamba alifika mahakamani hapo kupinga taraka aliyokuwa amepewa na mumewe wiki kadhaa zilizopita, alidai kuwa taraka hiyo alipewa kinyume na sheria kwani hakushirikishwa mahakani wakati taraka hiyo inataolewa.
“” Bi.. Saida Yahya.. Mahakama inapokea shitaka lako la kupinga taraka uliyokuwa umepewa na mumeo kwa kudai kuwa siyo harali Mahakama hii inahitaji majibu ya maswali kadhaa utakayoulizwa kabla ya kupokea shitaka lako “”
Hakimu mkuu wa mahakama hii bwana Amani Jumbe alieleza huku akimtizama Saida usoni..
" Nipo tayari kuulizwa na nitayajibu. ''
Saida alijibu kwa kujiamini..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“” Shukrani.. Swali la kwanza ni hili.. Mahakama inauliza je? Ni sababu gani haswa ya kupewa taraka? Ambayo hata hukushirikishwa? ”
Hakimu aliuliza tena..
" Asante.. Ni hivi mnamo tarehe 15 ya mwezi huu nilipata ajali mbaya ya gari, ajali iliyopelekea gari hiyo kufa kabisa, sababu ni kwamba asubuhi ya siku hiyo tulipishana pale nyumbani na akaondoka kwa hasira pasipo kuniaga, wakati akiwa ameondoka huku nyuma ilitokea shida iliyohitaji uwepo wake, nilijaribu kumpigia simu hakuweza kupoke.. Ndipo nikajaribu kumfuatilia kwa gari
Ajabu nilipofika maeneo ya barabara kuu iendayo dodoma, nilishuhudia gari yake ikipita eneo hilo kwa Kasi ya ajabu kama upepo!
Nilishtuka! Kwa maana haikuwa kawaida yake kwenda kasi namna hiyo.. Ndipo nikajawa na wasiwasi kuwa wenda katekwa! Ndipo hapo nikajipa jukumu la kuifukuzia gari hiyo jambo lililopelekea nipate matatizo makubwa mpaka leo hii. ''
Saida alizungumza kwa urefu na kunyoosha sentesi kiasi cha hakimu kumwelewa vizuri kabisa..
" Hapo umeeleweka.. Lakini pia mahakama inaomba sababu maalumu ya wewe kupewa taraka i ipi? ''
Hakimu aliuliza Na kumwacha Saida akijiandaa kujibu..
" Asante.. Mheshiwa hakimu sababu ya mimi kupewa taraka ni ajali ile iliyopeleka gari hiyo kuharibika ''
" Na ulipomweleza kwamba ulikuwa ukimfuatilia yeye kwa kuhofia pengine hakuwa katika usalama alikujibuje? ''
" Alinijibu kuwa sikupaswa kumfuatilia kwani yeye yuko na mizunguko na miradi mingi sana na hapo kuna mradi alikuwa akiuwahi..''
" Je? Wewe ulikubaliana na kauli hiyo uliyopewa? ''
" Hapana sikukubaliana nayo hata kidogo.. ''
" Kwanini? ''
" Sababu siku za nyuma alikuwa akinishirikisha katika mizunguko yake yote, na hata alipoondoka nilikuwa najua anakwenda wapi? ''
" Hapo umeelewa Bi Saida.. Lakini mahakama ina swali moja tu kwako, nalo ni hili " Je? Una hisa kwenye mali za mumeo? ''
" Ndiyo nina hisa kwani wakati ananioa hakuwa na chochote, hivyo tumezichuma tukiwa pamoja..''
" Kipi ambacho unaiaminisha mahakama hii kuwa mlichuma pamoja na unahaki ya kudai nusu yake? ''
" Hotel zote za PATRICK HOTEL Pamoja na majumba yote yaliyandikwa jina hilo hapa mkoani Iringa pamoja na Gest zake.. ''
Jibu lile lilifanya hakimu pamoja na wajumabe wake kutizamana.. Jina la Patrick liliwashtua mnoo na hawakutaka kuamini kama ni kweli utajiri ule mkubwa aliokuwa akiumiliki mwanaume huyo aliusaka akiwa na mwanamke huyo. Kwani watu wengine waanamini utajiri huo huenda ulikuwa ni urithi wa kutoka kwa mababu na mababu ndiyo maana alipokuja kuumiliki Patrick ulikuwa umetanuka sana!
" Saida Yahya.. Ni ngumu sana kuiamisha mahakama kuwa mali hizo zinazomilikiwa na tajiri huyo mkubwa anaeshika nafasi ya pili Kati matajiri wakubwaa mkoani Iringa na nafasi ya tano kwa utajiri Tanzania, eti mali hizo alizisaka tu kipindi cha ujana? Hapana hebu tueleze mlizisaka vipi? ''
Dooh! Swali hilo lilikuwa ni kama kimbunga cha gafla kilicholeta kumbukumbu za gafla zilizompeleka moja kwa moja mpaka kipindi hicho wanaingia katika harakati za kuupiga vita umasikini na adha waliyokumbana nazo zilizopelekea hadi kizazi chake kupita hapo hakika alishindwa kuyazuia machozi yake mwizowe yalimdondoka mbele ya mahakama..
Wasaidizi wa mahakama hiyo walikwenda kumtoa pale na kumpeleka kwanza kwenye chumba cha mapumziko, ambapo alikaa kwa zaidi ya masaa matatu ndipo aliporajea tena kizimbani..
' Lazima tu niseme ukweli.. '
Alijisemea Saida wakati akikaa sawa tena kumsikiliza Hakimu..
" Bi Saida mahakama inakuuliza ni vipi mliweza kuzichuma mali hizo kwa haraka ikiwa unadai ulimkuta akiwa hana kitu? ''
" Baada ya kusumbuliwa kwa umasikini kwa mda mrefu ndipo mume wangu aliponishauri tukasake bahati kwa waganga. ''
Saida aliongea na kuweka kituo hapo.. Mahakama nzima ilitulia tuli kumsikiliza..
" Sikupinga kwa maana hali tuliyokuwa nayo mi mwenyewe nilikuwa ninaiona.. Hatimae tulifunga safari mpaka kwa mganga huyo ambapo baada ya kufika huko tulipewa shariti la mimi kutolewa kizazi.. ''
Kila mtu alitumbua macho yake! Na hata hakimu pia alishtushwa na maneno hayo..
" Ehee ikawaje? ''
Hakimu alimruhusu Saida aendelee ambapo mda huo leso yake ilikuwa mkononi maana macho yake yaligeuka chem chemi..
" Sikuweza kukataa! Kwani nilikuwa nampenda sana na alinisisitiza kufanya hivyo nami sikuwa na jinsi nilikitoa sadaka kizazi changu ndipo ukwa mwanzo wa utajiri.. ''
Saida alihitimisha na kuyaachia machozi yaliyomtoka kwa fujo kama bomba..
" Bi Saida.. Mahakama hii tukufu ya kutetea maswala ya jinsia, wazee na watoto imepoke shitaka lako na inakuomba ufike tena hapo mnamo tarehe 30 Mwezi huu ''
Hakimu alihitimisha na kugonga kirungu juu ya meza yake kufunga mjadala.
KIMENUKA…!!
Ilikuwa ni Asubuhi na mapema, kunako makazi ya tajiri Patrick ilikuwa ni asubuhi moja tulivu sana mke wa Patrick Ashura alikuwa akiandaa chai ya asubuhi hiyo wakati huo Patrick akizunguka zunguka katika mabustani yaliyoizunguka nyumba yake akipunga upepo mwanana ulichanganyika na harufu murua kutoka katika maua ya bustani hizo na kufanya aburudike sana..
Gafla…!
“ Bosi… Bosi ”
Haraka Patrick aligeuka na kutizama mahali alipoisikia sauti hiyo.. Alikutana na mlinzi wake Emanuel akija maeneo hayo…
“ Kuna nini? ”
Patrick aliuliza kwa mshangao.
“ Kuna watu wanakuhitaji… ”
“ Watu?! ”
“ Ndiyo bosi… ”
“ Kina nani? ”
“ Siwafahamu ”
“ Wapo wapi? ”
“ Hapo nje…”
“ Hebu twende…”
Walitoka pale huku Patrick akiwa na maswali lukuki kichwani, hakuwa anafahamu kama hao wanaweza kuwa ni kina nani?
‘ Kina nani hawa?! ’
Alikuwa akitembea huku akijiuliza njia nzima bila kupata majibu Patrick…
‘ A’ah nitawajua hapo hapo… ’
Aliamua kukata kauli namna hiyo baada ya kuona anachojaribu kukifikiria na hewa…
Baada ya kitambo kifupi hatimae walifika Getini.. Patrick alishituka baada ya kuona watu waliomtembelea walikuwa na gari iliyokuwa na namba za usajili wa serikali..
“ Karibuni jamani…”
Patrick aliwakaribisha wageni hao huku mara kadhaa akijalibu kukisia watu hao wamefika hapo kwa shida gani? Lakini bado hakupata jibu…
“ Asante… Lakini sisi hatukai tumekuja kwa shida ndogo tu ”
Aliongea mwanaume mmoja wakati huo akifungua begi lake na kutoa bahasha flani ya khaki na kumkabidhi Patrick..
Patrick aliipokea huku wimbi la maswali likizidi kumkumba kichwani..
Akifugua bahasha hiyo na kukutana na barua ndani, nayo aliichomoa na kuanza kuisoma kwa pupa!
“ Mmmmh!! Mahakamani kuna nini tena? ”
Patrick alijikuta akiponyokwa na swali hilo..
“ Kwa kweli hata sisi hatujui ila tumetumwa tu kuifikisha mikononi mwako… ”
Alijibu mwanaume mmoja kati ya wale waliokuwa wameileta barua hiyo..
“ Sawa nitafika bila kukosa.. ”
“ Tunashukuru.. ”
Watu hao wakapanda gari yao na kuondoka nyumbani hapo..
Patrick alibaki katika tafakari nzito mnoo! Mara kadhaa alijiuliza huko mahakamani kuna nini haswaa? Bado jibu hakulipata alirudia kuisoma tena na tena barua hiyo pasipo na mafanikio ya kujua wito wake zaidi ya kumtaka afike mahakama ya Haki Jinsia wazee na watoto..
‘ Ni tarehe 30 Mwezi huu.. Yaani kesho kutwa…. ’
Alihitimisha kuhifadhi kumbukumbu hiyo, akairudisha karatasi hiyo kwenye bahasha yake na kwenda kuihifadhi vizuri kisha akaendelea na majukumu mengine..
Hakutaka hata kumwambia Ashura kuhusu hilo lililomfikia hiyo ilikuwa ni siri yake na barua hiyo..
Kwa kipindi hiki Patrick hata unywaji wa pombe ulipungua kwani ulikuwa ni wakati m'baya sana kwake, V8 Imekufa, PRADO, Imeibiwa wakati huo huo bado ana Thamanzi ya kutakiwa kufika mahakamani daah!
Hatimae siku iliyokuwa ikingojewa ilikaribia..
“ Mke wangu? ”
“ Bee ”
" Kesho niandalie mapema nina kijisafari.. ''
" Wapi tena jamani? ''
" Nafika mbeya ila nitarudi ''
" Jamani mi waniacha? ''
" Nitarudi mke wangu ''
" Hivi Pati waniachaje mpweke jamami? ''
" Aaa.. Ashuu nitarudi mke wangu khaa ''
Ashura alijifanya kunununa! Lakini moyoni alifulahia mnoo! Alijua nafasi nyingine hiyo hapo..
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
' A'ah ili lizee mbona litaisoma namba? '
Alijisemea ashura wakati huo akiwa kajifanya kununa kweli kweli..
Patrick akajipa kazi ya kum'bembeleza wee! mpaka ule mdomo aliokuwa kashona mfano wa rasketi iliyojaa nguo ukakunjuruka! Kujifanya hasira zimeisha!
Kwa pamoja walipanda kitandani na kuianza safari ya usingizi, ambapo haikupita hata mda mrefu lifti saaafi ya usingizi iliwachukua na kuwasafirisha mpaka majogoo.
***
Siku hiyo Ashura aliamka mapema sana kwaajili ya kumuandalia mumewe huyo wa bandia safari yake ambayo pia ni ya bandia kwa maana Patrick alidanganya kuwa anakwenda mbeya lakini ukweli ni kwamba alikuwa akienda kuitika wito mahakamani..
Saa 07:45 mapema!
Patrick alikuwa akimaliziwa kufungwa tai yake na baada ya hapo waliagana kwa kiss kadhaa na Patrick kuondoka nyumbani hapo..
Ashura alikuwa akisimsindikiza kwa macho kupitia dirisani ililokuwa limesapotiwa kwa vioo vyeusi na kumfanya asionekane na yeyote aliekuwa nje..
Patrick alitokomea kabisaa! Na Emanuel kufunga geti..
' Wao.. '
Ashura alijawa na fulaha ya ajabu kwa siku hiyo kwani ilikuwa ni siku nyingine tena ya kuwasiliana na m'babe wake Dany ambae sasa zilikuwa zimepita wiki na ushee hawajawasiliana!
Haraka alijisachi kwenye nguo yake nyeti ya ndani ambayo imeshonewa kijimfuko maalumu kidogo sana! Ambacho siyo rahisi kwa mtu yeyote kukiona hata iweje!
Alitoa Laini ya private kabisa ambayo ni mahususi kwa kuwasiliana na Dany, kisha akatoa line moja kwenye simu yake kupachika iyo..
Akaiwasha!
Baada ya dakika moja mbele mtandao ukatulia na majina yote kusoma kwenye simu hiyo..
Cha kwanza alifunga laini moja na kubaki hewani ile aliyoikusudia.
Kwanza kabla ya yote alikwenda tena dilishani na kuchungulia kwa mara ya mwisho na kujirisha kuwa Patrick alikuwa amekwena jumla..
Alirudi mbio mbio kwenye simu yake, akaibeba na kuingia sehemu ya majina/contact, haraka akaanza kulipekua jina la Daniel Masumbwa!
Hakupata tabu kulipata.. Na bila kupoteza mda akapiga..
" Ngrrr!! Ngrrr!! Ngrrr!! Ngrrr!! ''
Alimfuma hewani na simu ikawa inaita! Wakati huo Ashura anahaha usipime! Anahisi kama hapokei mapema!!
" Hallo.. ''
Sauti safi ya kiujana ujana yenye kibesi kwa mbali ilisikika kwa upande wa pili..
" Oooh!! Dany?! ''
" Naam Asha.. ''
" Upo?! ''
" Nipo nimejaa tele.. ''
" Wacha wee! ''
" Yeeah!! Kwema huko? ''
" Yaani kwema kabisa.. ''
" Oky! Kwani siku ile ni kina nani walikufuma? ''
" A'ah! Ile ilikuwa ni kukamilisha kamilisha ule mpango tu wala hakukuwa na tatizo.. ''
" Sawa una mpya? ''
" Bila shaka! ''
" Ipi tena?! ''
Dany alizungumza safari hii kwa kwa kupunguza sauti na kuiweka katika mfumo wa kunong'ona!
" We subili na hii ndiyo itakuwa ya mwisho nahama na huku.. ''
" Halafu kweli tukifanikiwa safari hii iwe ndo misho kama ni pesa tayari tunayo.. ''
" Kweli kabisa Dany ''
" Sawa.. Naomba nikupe nafasi tena ukiwa na mda unanitafuta ''
" Shaka ondoa.. ''
Simu ikakata, Ashura akavuta pumzi ndefu na kuishusha, simu yake akaitupia pembeni..
************************
" Ndugu unaitwa nani? ''
" Patrick Chars.. ''
" Ndugu Patrick Chars huyo mama pale unamjua?? ''
Taratibu Patrick akageuza shingo yake na macho yake kuyaelekeza kule alikomwoneshea Hakimu!
Moyo ukapiga paaah!! Baada ya kukutanisha macho yake na macho ya Saida! Mwili mzima ukamwishia nguvu!
Naam! ilikuwa ni kortini, Patrick alikuwa amefika mahakamani hapo kuitikia wito, sasa hakuwa na hili wala lile, na hakutambua uwepo wa Saida mahali hapo mpaka pale Hakimu alipomwoneshea..
' Huyu mwehu bado yupo hai? '
Patrick alijiuliza kimoyo moyo wakati huo akisikilizia jinsi hasira pamoja na hofu vinavyopanda taratibu..
" Ndiyo ninamfahamu.. ''
Kukataa lilikuwa ni jambo gumu mnoo kwani wengi wanamjua kuwa ni mkewe ukitoa mahakamani hapo..
" Ni nani kwako? ''
Swali baab kubwa lilipenya taratibu katika masikio ya Patrick na kuzama moja kwa moja mpaka kwenye ubongo! Na kwenda kumwachia kigugumizi kikali kilichowakilishwa na mdomo..
Patrick alibaki kugugumia tu! Hakuna jibu la moja kwa moja alipata kulitoa..
" Patrick Chars.. Narudia tena ni nani yako? ''
" Alikuwa mke wangu.. ''
Hiyo ndiyo point iliyokuwa ikisakwa na mahakama, hapo ndipo mjadala mzito ukazuka! Kwanini waliachana? Je? Taratibu zote ya taraka zilifatwa?
Mjadala ulivuma takribani masaa matatu! Patrick alishindwa kwenye kipengele cha taraka, ilibainika kuwa taraka yake ilikuwa ni bandia na ilitakiwa itolewe upya kulingana na taratibu zote za utaratibu wa utolewaji wa taraka pindi wanandoa wanapoachana..
Kufikia hapo mjadala ukafungwa na kukatwa tarehe nyingine tena kufika mahakamani hapo..
' Lazima ukafilie mbali nguruwe wewe.. '
Alijisemea Patrick wakati huo wakiwa nje ya mahakama hiyo na alishuhudia Saida akichukua Bajaji na kuondoka.
Haraka sana akawasha gari yake na kuanza kuifukuzia bajaji hiyo nyuma nyuma mpaka sehemu moja wanaita mashine tatu, ni eneo lenye msongamano mkubwa wa watu Hali iliyopelekea ashindwe kuwahi vile alivyotaka na ile bajaji kwa kuwa ni ndogo ilikuwa inapenya kwa urahisi kwenye msongamano huo na kupeleka Patrick aanze kuachwa..
" Shiiiit.. ''
Patrick alikasirika kuona sasa anaanza kuachwa na hakutaka hilo litoke nae alishuka na kuchukua bajaji..
" Dogo hebu nifukuzie bajaji ilee ''
" Poa twende.. ''
" Sawa.. Ila usikimbize mpaka tuwakute nataka kuwafuatilia tu ''
" Kwema lakini? ''
" Ondoa shaka.. ''
Basi wakaingia barabarani na kuanza kuifuatili bajaji ile kwa mbali mpaka wanafika mshindo, Patrick alijitahidi sana kuyawekea kumbukumbu maeneo hayo ili isiwe rahisi siku nyingine kuyasahu.
Bajaji aliyokuwa amepanda Saida ilikwenda kupaki mbele ya mlango wa chumba alichokuwa amepangisha mwanamama huyo..
" Simamisha hapa.. ''
Patrick alimwamuru yule kijana aliemleta.
Patrick aliendele kulitizama kwa makini eneo hilo na kugundua ni moja kati ya maeneo yasiyo na watu wengi sana yaani ni ile mitaa tulivu sana!
Yule boda boda alilipwa ujira wake na taratibu kuanza kugeuza bajaji yake..
" Geuza turudi.. ''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Patrick aliludishwa tena mpaka kwenye gari yake kama alivyokuwa amemwamuru kijana huyo..
" Ngapi dogo? ''
" Buku mbili kaka.. ''
Patrick alitoa noti ya shilingi elfu tano na kumpatia kijana huyo bila hata kusubiki chenji akajitosa garini..
" Kaka..! Kaka umesahau chenji yako? ''
Yule kijana alimkumbushia mteja wake kwa kuzani wenda kasahau..
" Iyo baki nayo tu! ''
Patrick alijibu wakati huo kaweka gari yake sawa na kuondoka!
Njia nzima Patrick alikuwa na mawazo mengi mnoo hakuwa akiamini kama yule aliekuwa amesimama nae alikuwa ni Saida..
' A'ah! Yupo hai? Daah! Hili ni tatizo moja kubwa sana.. '
Patrick alijisemea wakati huo akiwa anaitafuta kihesa, kwa maana kutoka Iringa mjini mpaka kihesa ni sawa na pua na mdomo..
' Lakini nitahakikisha ninadili nae kabla mambo hayajaniwia ugumu '
Alizidi kujisemea wakati huo akichepuka na kuiacha barabara kuu iendayo Dodoma na kuchepuka na barabara iendayo kwake!
' Ooh! Hebu nipitie nikakague mjengo wangu kama umekamilika '
Gafla! Patrick alighairi kurudi nyumbani na kuamua kupitia kuukagua mjengo wake ambao mara ya mwisho kuwatembelea mafundi wake ilikuwa ni wiki moja iliyopita, na jengo hilo lilikuwa katika hatua za mwisho kukamilika!
Napo pia hapakuwa mbali, aliweza kufika...
" Aa.. Bosiiii ''
Vijana, mafundi waliokuwa wakimalizia kupaka paka rangi walimchangamkia bosi wao baada ya kumwona!
" Kazi nzuri vijana.. Daah! Hakika nyinyi ni mafundii.. ''
Alizungumza Patrick kwa fulaha huku akitoa simu yake na kuanza kupiga picha mfululizo za nyumba hiyo..
Ilikuwa ni nyumba nzuri sana na yenye kuvutia, naweza kusema nyumba hiyo inaweza kuwa moja kati ya nyumba kumi bora mkoani Iringa jambo linalokwenda kumpatia Patrick heshima nyingine ya hali ya hali ya juu!
" Basi mi nilikuwa napitia kuwapa hai vijana wangu kazi njema ''
" Aaah! Bosiii kwahiyo umekuja mpaka hapa unatuacha hivi hivi? Hebu tupatie ya kubadilisha mboga leo.. ''
Hilo halikuwa tatizo kwa mtu tajiri kama Patrick aliwagawia kila mmoja laki moja moja na kuondoka zake..
***
Ashura akiwa hana hili wala lile mara gafla!
" Pipiiiiip...!! ''
Honi kali ya gari ilipenya masikioni mwake..
' Alaaa! Huyo si Patrick? '
Alijiuliza Ashura kwa taharuki kubwa kwa maana mda huo hakutegemea kabisa kama Patrick angeludi, kwani kutoka Iringa mpaka mbeya siyo pa kitoto. Alitegemea Patrick angeludi usiku wa manane sasa iwaje saa saba hii arudi?
Alijiuliza maswali lukuki huku akisogelea dirisani ili achungulie nje!
Sasa kutizama.. Ayaaaaa!! Anamshuhudia mlinzi wa geti akifunga geti wakati huo Patrick yulee anaelekea uwani kupaki gari..
Moyo ukapiga paah! Ashura hakuwa na uhakika kama mda ule alipowasiliana na Dany alitoa line au laa!
Haraka akautumbukiza mkono mahali kilipo kijifuko anapoiwekaga siku zote, akakutana hewa..
Kudadadek! Halafu simu yenyewe haioni ilipo, na Patrick anaingia hapo ndani mda si mrefu..
Weeee!! Alitingwa mtoto wa kike alianza kuzunguka kwa kasi kama mwehu! Alitafuta huko na kule pasipo mafanikio..
' Chumbani? '
Mawazo yalimwelekeza huko na bila kupoteza mda akakimbilia huko ambako breck ya kwanza ilikuwa ni kitandani alianza kuchambua mashuka kwa kasi ya ajabu mwishowe..
" Pwakalaa! ''
Ulisikika mlio wa simu kuanguka chini, haraka akaiokota na kuizima kabisa kisha akaiweka chini ya godolo ikalalia chaga..
Halafu yeye akajifanya kuchambua chambua nguo sijui aende kuzifua?
Hazikupita hata sekunde kumi Patrick alingia chumbani hapo.. Daah! Nusura afumaniwe kama asingeiona mapema simu hiyo na Patrick akawahi kuikuta imezagaa ingekuwa shoo mpya tena! Kwa maana Patrick huwa anapenda sana kuikagua kagua sana simu hiyo..
Sasa ingekuwa maajabu anakutana laini ya mtandao mwingine ambapo hajawahi hata kuuona kwenye simu ya mwanadada huyo,
Na Patrick alivyo na wivu juu ya mwanadada huyo nafikiri pasingetosha!
" Sap..raizzz....! ''
Patrick alizungumza hivyo na kumshika Ashura akiamini ya kwamba alikuwa hajamuona mda wote..
" Uwiiii... ''
Ashura alijifanya kushtuka na kugeuka haraka!
" Khaaa! Patrick ndiyo nini utakuja kuniuwa mwenzio.. ''
Ashura alizunga kwa taharuki ya uwongo huku akiwa kashikilia kifua chake!
" Aaaah! Tulia wewe.. Ufee?! Halafu Patrick wamuacha na nani jamani we mwanamke?? ''
Patrick alizungumza huku akizidi kutalii, ni wazi kabisa alihitaji kunguza hasira za siku hiyo kunako uwanja wa sita kwa sita!
Naam! Kilichofata kuanzi hapo ni 18+ yaani ni weka mbali na watoto..
Ila siri ilikuwa ni kwamba kabla ya wawili hao kusafiri bahari ya huba ilikuwa ni lazima kuwe na kinga kati kati..
Yaani Ashura alikuwa macho sana jambo hilo hakutaka hata siku moja itokee wakasafiri bila ngao hata Patrick am'bembeleze vipi hakuweza kufanikiwa katika hilo Ashura alikuwa na visingizio kibao..
***
" Daah! Lakini Ashuu kwanini wataka hivi kila leo? ''
Ilikuwa ni tripu ya pili sasa Patrick akilalama kwa tabia hiyo ya Ashura kutaka kila siku safari ya huba inavyoanza kinga ihusike
Na hapo ilikuwa ni baada ya shoo!
" Subili mpaka mama apone ili tukajitambulishe tuwe huru na hapo nitakuwa tayari kukubebea ujauzito ''
Ashura alijibu kwa point moja kuntu sana! Iliyomkata makali mwanaume huyo!
" Sawa.. Harafu samahani hivi hali yaendaje? Maana mimi nina majukumu mengi mnoo hata sijakumbuka kukuliza tena tangu gari yangu iibiwe.. ''
" Aah wala usijali.. Sema mi mwenyewe niliwasiliana nao juzi wakasema ameshafanyiwa upasuaji.. Ila toka siku hiyo kaka yangu hajapatikana mpaka hivi sasa ''
" Tatizo ni nini?? ''
" Huenda tatizo ni mtandao ''
" Sawa ila usikate tamaa kuwatafuta ili tupate kujua hali yake mkwe jamani.. ''
" Nitamjaribu tena mida ngoja mda uende ende, maana nilitafuta mda si mrefu.. ''
" Sawa sawa ''
Maongezi yakaishia hapo na kila mmoja kuendelea na shughuli zinazom'bidi mpaka pale siku hiyo ilipofika tamati...
Siku zikaendelea kusonga, hakuna jambo liliokuwa linamuumiza kichwa Patrick kama Saida kuipinga taraka yake ambayo alipata kwa garama kubwa leo hii inatupiliwa mbali na kuahidiwa kutolewa taraka nyingine itakayokuwa halali kisheria..
Hapo aliamini kabisa ni lazima fungu kubwa la mali atatoka nalo Saida..
' Aiii nilichokikwepa ndo hicho kinarudi daah! '
Yalikuwa ni mawazo ya Patrick kila siku iliyokuja na kwenda yeye kwake ilikuwa mbaya! Aliiwazia sana siku hiyo ambayo nayo ilikuwa inakuja kwa kasi kama upepo wa kipupwe!
' Aishiiiiit.. Zimebaki siku mbili '
Patrick alikuwa akihesabu siku na kadili siku zilivyokuwa zinasonga ndipo alivyozidi kuchanganyikiwa! Mwishowe Ashura akamgundua!
" Kwani mume wangu una tatizo gani? ''
Ilikuwa ni jioni moja baada ya chakula cha jioni aliamua kumuliza Patrick baada ya kuona siku hiyo yupo tofauti kabisa!
" Sipo sawa kuna mradi hauendi sawa! ''
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Patrick alidanganya jibu..
" Mradi gani? ''
" Kuna maishe yangu ya kumwagilia nyanya huko Ilula imepata hitilafu na kazi zimesimama! ''
" Khaa! Pole mume wangu.. ''
" Asante.. Halafu kesho nataka nikaiangalie hivyo niandae mapema sana ''
" Sawa nitafanya hivyo.. ''
Naam! Siku ya pili yake ilikuwa ni tarehe ambayo ilipangwa na mahakama wafike wote wawili bila kukosa ili taraka hiyo ikafanyiwe marekebisho,
Na yeye kadanganya kwamba anakwenda ilula kuangalia mtambo wake wa kumwagilia nyanya, yaani hataki Ashura ajue kama ana matatizo..
***
" Kokoliko!!! Kokoliko!!! Kokolikoo!! ''
Sauti za majogoo kuwika zilipenya vizuri kunako ngoma za masikio ya Patrick na kumfanya afunue shuka!
Alikuta tayari Ashura keshaamka mda mrefu sana! Yupo jikoni..
Nae akainuka na kuingia bafuni, ambako alioga huku mara kadhaa alikuwa akifikiri kile atakachokutana nacho leo..
Dakika kumi zilimtosha kule bafuni, akarudi chumbani na kuvaa suti kali yeusi tiii iliyosanifiwa na tai ndogo ya kipepeo! Mguuni akamalizia na kiatu cha bei ghali..
Baada ya kujiridhisha kwa jinsi alivyokuwa ametoka kama raisi vile! Alichukua funguo ya gari na kujongea sebleni ambapo alikutana na chai ya uhakika..
Lakini chai hiyo hakuifaidi kwa maana tumbo lilikuwa moto, hakuwa na uhakika kama angetoka salama leo..
Aliinywa hivyo hivyo kwa kujilazima, baada ya hapo akachukua gari na kuondoka zake..
***
Saa 08:30 PM
Naam! Wote wawili walikuwa wamesharipoti mahakamani hapo na sasa kesi ilikuwa inaendelea kuunguruma..
Patrick alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kutoa taraka isiyo rasimi
Kumbuka toleo lililopita yalikuwa ni mashitaka ambapo Saida alishinda kesi hiyo na kuonekana Patrick ni mkosaji sasa leo kapandishwa kizimbani kujibia kosa hilo.
Mjadala ulikuwa ni mrefu sana Patrick alitoa sababu ambazo mahakama ilizitupilia mbali kwani alipokwama ni kwenye kipengele cha utafutaji mali hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli walizisaka pamoja!
" Mwanamke hata awe na kosa kubwa namna gani? Huwezi kumpunja haki yake pindi mnapoachana.. Hivyo mahakama hii tukufu ya kusimamia haki na sheria inakusomea kifungu cha sheria cha mwaka 2006 Kuhusu taraka, kifungu hicho kinasema iwapo ulimwoa mwanamke ingali huna chochote. Ikatokea mmeshindana na kupeana taraka.. Kile mlichokitafuta mnagawana kati kwaa kati ''
Hakimu alizungumza huku akimtizama Patrick ambae nusura atokwe na macho..
" Na kama ulimwoa akakuta nazo.. Wakati wa kuachana mahakama hungalia ni muda gani umedumu nae.. Na muda huo utakaokuwa umedumu nae kuna kitu katafuta pale ni lazima umugawie.. ''
Hakimu aliendelea kutoa maneno ambayo yalikuwa ni sumu kali au makaa ya moto kwenye kidonda kibichi kwa upande Patrick
" Mahakama inatambua una majumba sita hapa Iringa.. Hivyo basi Bi Saida Yahya ana haki ya kumiliki vibali vitatu vya umiliki wa nyumba tatu ikiwa kama ni haki yake baada ya wewe kumpa taraka na karatasi hizo ziletwe mahakamani hapa hapo kesho muda na wasaa kama huu ''
Hakimu alihitimisha mjadala huo na kugonga kilungu chake mezani kuashiria mjadala umefika tamati..
Saida alishikwa na fulaha ya ajabu, wakati huo Patrick akiungulia maumivu yasiyo na mfano..
Patrick alichukua gari yake na kurudi nyumbni wakati huo Saida nae akachukua boda boda na kurudi yaliko makazi yake.
***
Ilikuwa ni mida ya saa kumi na mbili jioni ambapo Patrick alionekana kuwa na safari mpya tena! Lakini safari hii kwa namna moja ama nyingine naweza kusema haikuwa nzuri kwa Patrick..
Kwanini nasema hivyo?
Kwa maana Patrick aliweza kuvaa nguo ambazo ziliweza kumbadilisha na kutofahamika kirahisi rahisi..
Akachukua na bastola yake iliyokuwa na risasi saba ndani akaichomeka kwenye soksi..
Wakati huo Ashura yupo jikoni na hajui chochote..
Huku Patrick akachukua na kofia kubwa ya kapero na kuivaa, aaah! Yaani hapo kama angepishana na mtu haraka haraka asingeweza kumtambua.
Akachukua na funguo za gari na kutoka zake,
Emanuel yeye hakuweza hata kumuuliza kama anakwenda wapi jioni hiyo kwani ilishakuwa kawaida yake kutoka toka jioni, hivyo alimfungulia tu geti mwanaume akapotelea nje wakati huo kajua kaleee! Kanalikaribisha giza la usiku huo.
Safari ya Patrick ilitia nanga palee Mshindo karibu kabisa na kanisa la roma, alipaki maeneo yale kwa sababu msongamano wa watu ulikuwa umepungua maeneo hayo kwa sababu tayari jua lilishatua na giza linaanza kuuteka ulimwengu taratibu..
Alifungua mlango wa gari yake na kushuka, kisha akaufunga tena alitoa bastora yake iliyokuwa kwenye soksi na kuiweka katika mfuko wa koti..
Kichwani Patrick alipanga kwenda kumtoa roho Saida yaani swala la kugawa kati mali aliyojimilikisha kwamba ni yake yeye kama yeye halafu leo nusu nzima yaani Majengo matatu makubwa yamilikiwe na Saida? Hapana aliona ni jambo gumu mnoo lisilowezekana hata kwa dawa!
Alianza kuzipiga hatua taratibu kuelekea eneo kilipo chumba cha mwanamama huyo wakati huo gari kaipaki mbali kabisa!
Hakupa tabu kufika maeneo hayo, ambapo alipoanza kuchunguza kwa makini kama kungekuwa na mtu yoyote zaidi, Alifanikiwa kumuona Saida mwenyewe akitokea msalani kuingia chumbani kwake, chumba ambacho kilikuwa na mlango wa kujitegemea..
' Hapa hapa.. '
Alijisemea Patrick wakati huo akisogea karibu kabisa kwenye pembe ya nyumba hiyo na kutoa bastola yake..
Alimwangalia Saida mpaka anasukuma mlango kuingia ndani ndipo haraka akafunga kiwambo cha kuzui sauti bastola yake na kuusogelea mlango huo haraka sana
Bahati mbaya ni kwamba Saida alikuwa hajafunga mlango kwani mda ulikuwa bado bado wa kuubana kabisa hivyo alikuwa kaurudishia tu!
Bila hodi wala kugonga, Patrick alisukuma na kujaa ndani kisha akuurudishia tena..
Saida alishtuka na kutaka kupiga kelele lakini akamzima!
" Tulia we malaya.. Ukifungua domo lako umekwisha.. ''
Patrick aliongea kwa sauti nzito ya kutisha, bastola akiwa kaielekeza kichwani kwa saida..
" Kwanini unisumbue? Kipi unachokitaka haswa? Gari uliua nilikuacha Na mali zangu unataka kunipora hivi we ni mnyama wa aina gani? ''
Patrick alizungumza kwa sauti ya chini ili asisikike na watu wa vyumba vya pili ambako kulikuwa na midundo ya miziki isingekuwa rahisi kwao kusikia chochote.. Hata hivyo Saida hakuwa na cha kujibu..
" Tangulia kuzimu malaya mkubwa weee! ''
Patrick alitokwa na maeno hayo kisha akashika triga na kuivuta nyuma kisha akaachia risasi tatu zikatoka kwa kasi na kwenda kuzama katika kichwa cha Saida na kumfumua kabisa, maisha yake
yakakomea hapo.
Patrick alipohakikisha ametimiza azimio lake alifungua mlango kwa makini asije kuonwa na yeyote kisha akaufunga tena kuondoka zake
Siku hiyo hakutaka kurudi mapema nyumbani alipitia kwanza bar na kubwia pombe ya uhakika ndipo akarudi nyumbani ikiwa ni usiku wa manane..
***
Siku ya pili asubuhi na mapema mmama moja aliekuwa na desturi ya kumtembelea Saida katika chumba chake alifika mahali hapo kumjulia hali na ilikuwa ni kawaida yao wawili hawa kutembeleana kwani kutokana na ukarimu mkubwa aliokuwa nao Saida ulimfanya kupata marafiki ndani ya mda mfupi na popote pale..
Mama huyo alishikwa na bumbuazi la gafla baada ya kuona michilizi ya Damu kupitia chini ya mlango kutoka ndani, alijaribu kuita mara kadhaa wito wake haukupokelewa
Ndipo alipopatwa na mashaka na kuondoka eneo hilo haraka kwenda kuita watu..
Dakika kadhaa mbele kengele ya mtaa huo iligongwa kwa mtindo wa tahadhari, watu wote walikusanyika kwa pamoja na kupewa taarifa ya kile kilichokuwa kimeelezwa na mama mmoja kuhusu chumba flani kilichokuwa na mgeni..
Wananchi wakamiminika mpaka kwenye nyumba hiyo ambapo hakukuwa na maelezo zaidi ya kufungua mlango na kukutana na maajabu!
Ni kweli Saida alikuwa amepoteza maisha kwa kupigwa risasi tatu za kichwa,,
Watu wote hawakujua chanzo ni nini? Nani aliehusika? Na hata walipojaribu kuwasaka ndugu wa mwanamama huyo hawakuweza kuwapata
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndipo uongozi wa eneo hilo ulipoamua kuikabidhi maiti hiyo manispaa ambapo baada ya siku tatu manispaa iliamua kumzika baada ya wao pia harakati za kuwasaka ndugu wa mwanamke huyo kugonga mwamba..
Saida alizikwa na manispaa katika makaburi yaliyopo eneo la makanyagio huko Iringa..
MWISHO
0 comments:
Post a Comment