Search This Blog

Monday, 19 December 2022

QUEEN MONICA (2) - 2

  




Simulizi : Queen Monica (2)
Sehemu Ya Pili (2)


unataka kutambua haki za wapenzi wa jinsia moja na utoaji mimba.Haya ni mambo ambayo yanalipeleka taifa hili katika laana na inaniumiza kwa sababu watu

waliopewa dhamana ya kuiongoza nchi hii wamewageuka wale waliowapa dhamana ya kuwaongoza.Nilikuwa kikwazo kwao na walitaka kunitoa uhai lakini

wakashindwa.Wao ndio sababu ya mdogo wangu Linda kujitumbukiza katika biashara haramu.Kama nisingeikimbia nchi kwa sababu yao mdogo wangu

angeendelea kuishi maisha mazuri .I’m back again and I must fight them with all the strength I have.Nahisi ni kama vile Mungu amenirudisha nyumbani ili nije

niiokoe nchi yangu.Safari hii watakimbia wao wakajifiche na si mimi tena.Nitawanyima usingizi na nitahaikisha ninawafagia mmoja baada ya mwingine.”

Akawaza Austin na kukumbuka kitu “ Nimemkumbuka mpenzi wangu Maria,alilia machozi mengi nilipomwambia kwamba ninakuja Tanzania.Maria ananipenda

kwa dhati na amekuwa nguzo kubwa katika maisha yangu.Natakiwa kuwasiliana naye kumjulisha kuwa tayari nimekwisha fika Dar es salaam.” Austin akaingia

ndani akafungua begi lake dogo akatoa kompyuta akawasha na kumpigia simu Maria mchumba wake kwa kupitia mtandao wa Skype “ Hallow Austin my love”

akasema Maria.Austin akatabasamu baada ya kuiona sura ya Maria “ Maria sijui umenipa nini mpenzi wangu kwani kila ninapoiona sura yako akili yangu

inahama.Unaendeleaje malaika wangu? “ Ninaendelea vizuri Austin.Muda si mrefu nimemaliza kikao na Alnoor na kesho au kesho kutwa tutasaini mkataba

.Nimechoka kukaa hapa Dubai.Wiki ya tatu sasa niko mbali nawe.Tukishasaini mkataba nitaondoka haraka sana” “ Good job Maria.Najua haikuwa kazi rahisi

kumshawishi Alnoor akubali kufanya biashara nasi.Mimi tayari nimekwisha wasili Dar es salaam muda si mrefu” “ Ahsante kama umefika salama mpenzi

wangu.Mimi nitakapomaliza mambo ya huku kesho au kesho kutwa nitakuja moja kwa moja Dar es salaam.Ni muda mrefu sijafika Dar “ akasema Maria huku

akitabasamu na kuzichezea nywele zake ndefu. “ Maria my love nakuomba sana malaika wangu usije Dar es salaam.Ukitoka Dubai nenda moja kwa moja

nyumbani Afrika kusini mimi nitakapomaliza tu kazi iliyonileta huku basi nitaondoka haraka sana kurejea huko.Narudia tena kukuomba Maria tafadhali usije

Dar es salaam.” Maria akacheka kidogo na kusema “ Mbona una wasiwasi hivyo? Austin wiki hizi tatu nilizoishi mbali nawe nimejihisi kama mfu.Nimejihisi

kama ....oh no!! Nashindwa hata kukueleza how I feel.Siwezi kuvumilia zaidi ya hapa.Kwa hiyo Austin nitakapomaliza tu mambo yangu huku Dubai nitapanda

ndege na kuja Tanzania and please don’t say

no.Hakuna mjadala katika hilo” akasema Maria. “ Maria tafadhali mpenzi wangu nakupenda sana zaidi ya kitu chochote duniani,nakuomba usije Dar .Kama

ujuavyo kwamba huku si sehemu salama kwangu lakini nimekuja tu kwa sababu ya lile suala la dada yangu kwa hiyo siwezi kuhatarisha maisha yako kwa

kukuruhusu uje huku Dar es salaam.Nisubiri Afrika kusini sintakawia kurudi” akasema Austin “ Austin hakuna kitu utakachonieleza kitakachonizuia nisije

Dar.Hapo ni nyumbani kwetu na ninaweza kuja muda wowote nikitaka lakini nijapo safari hii ni kwa ajili ya kukufuata wewe tu.Siogopi hayo masuala ya

usalama kwani najua utanilinda.Kwa hiyo Austin nitakuja Dar es salaam au labda kuna sababu nyingine iliyokupeleka huko tofauti na hilo suala la ndugu yako

na hautaki mimi nifahamu .Au umepata mwanamke huko? Au umerudia zile kazi zako? Akauliza Maria “ Maria ondoa mawazo hayo.Kilichonileta huku ni suala

la mdogo wangu ambaye amejiingiza katika madawa ya kulevya na hakuna jambo lingine.Siwezi kurudia zile kazi zangu tena.Nimekwisha achana nazo

kabisa.Kuhusu mwanamke mwingine ondoa wasi wasi katika hilo ,wewe ni pekee nikupendaye katika dunia hii.Thamani yako kwangu ni kubwa kuliko hata
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kontena lenye madini ya almasi.Kwa hiyo hakuna mwigine anayeweza kuwa na thamani ya juu kukushinda wewe” akasema Austin na kumfanya Maria atabasamu

“ Mungu amekujalia ulimi wenye kutamka maneno matamu ambayo hunifikisha mbingu ya saba.Basi ngoja nikuache upumzike kwani tayari nimekwisha hisi

kuanza kuchafuka huku chini kutokana na msisimko ninaoupata kwa kuongea nawe.Nitakutaarifu kesho kama tutakuwa tumesaini mkataba na Alnoor ili ujue

siku nitakayokuja Dar .One more thing kesho nataka unipe namba ya simu unayotumia ukiwa Dar.I love you baby” akasema Maria na kufunika kompyuta

yake.Austin akashika kichwa “ Maria anataka kuja Dar es salaam.Nilimdanganya kuwa ninakuja kushughuilikia suala la mdogo wangu anayetumia madawa ya

kulevya .Nisingeweza kumueleza kuwa nimeitwa na rais kuna kazi anataka nimfanyie kwani nilikwisha kula kiapo cha kuachana na kazi hizi na endapo atakuja

Dar lazima ataufahamu ukweli.What am I going to do? akajiuliza “ Akiufahamu ukweli ataumia sana kwani hii ni mara ya kwanza ninamdanganya hataniamini

tena.Maria nampenda sana na na sitaki kumuumiza lakini lazima nifanye kazi ya rais kwa ajili ya kumsaidia mdogo wangu.Mimi nadhani sina namna nyingine ya

kufanya zaidi ya kumueleza ukweli potelea mbali kama ataumia lakini sina namna nyingine ya kumsaidia mdogo wangu zaidi ya kufanya kazi ya rais.” akawaza

Austin

Simu iliyopigwa na balozi wa China nchni Tanzania ilimkuta rais Ernest Mkasa tayari amekwisha amka kitambo na alikuwa anajiandaa kwenda katika mazoezi ya

asubuhi kama kawaida yake.Ilipata saa kumi na mbili na dakika tatu za asubuhi. “ Hallow mheshimiwa balozi” akasema Ernest baada ya kupokea simu “ Habari

za asubuhi mheshimiwa rais” “ habari nzuri mheshimiwa balozi.Nadhani una habari nzuri za kunipa asubuhi hii” akasema Ernest “ Ndiyo meshimiwa rais.Ninazo

taarifa nzuri asubuhi ya leo.Nimetaarifiwa muda mfupi uliopita na msaidizi wa rais kuwa kutokana na urafiki mzuri baina ya China na Tnzania,rais amekubali

ombi lako kwa hiyo tutafanya mabadilishano ya wafungwa.Kwa hiyo mheshimiwa rais saa tano kamili leo kwa saa za hapa Tanzania mfungwa Linda

atakabidhiwa kwa ubalozi wa Tanzania nchini China na kwa taratibu za mabadilishano zilivyo muda huo huo wafungwa wa China watakabidhiwa kwa ubalozi

wa China hapa Tanzania.Natumai tumeelewana meshimiwa rais” “ Nashukuru sana mheshimiwa balozi.Siwezi elezea furaha yangu kwa jambo hili

kufanikiwa.Makabidhiano yatafanyika kama kawaida katika muda huo.Mheshimiwa balozi narudia kukushukuru tena.Ahante sana” akasema Ernest na kukata

simu. “Sasa kazi yangu inakwenda kufanyika kwani Austin hakuwa tayari kufanya chochote hadi pale atakapohakikisha mdogo wake ametoka gerezani.” Akawaza

Ernest huku akizitafuta namba za simu za Mukasha na kumpigia “ Habari zaa asubuhi mheshimiwa rais” akasema Mukasha baada ya kupokea simu “ Habari

nzuri Mukasha.Nimepokea simu muda si mrefu kutoka kwa balozi wa China anasema ule mpango umefanikiwa kwa hiyo saa tano kamili leo kwa saa za

Tanzania mabadilishano yatafanyika katika balozi zetu.Kwa hiyo lishghulikie suala hili” “ Hizo ni taarifa njema sana mheshimiwa rais.Nitamtaarifu mkuu wa

magereza suala hili ili mchakato uanze mara moja” akasema Mukasha . “ Sawa Mukasha,shughulikia suala hilo na tutawasiliana baadae’ akasema Ernest na

kukata simu akatoka mle chumbani akasalimiana na walinzi wake akaelekea katika mazoezi.Mara tu alipotoka mle chumbani,bi Agatha Mkasa mke wa Ernest

akaichukua simu na kupekua akaipata namba ya simu ya mtu aliyekuwa anaongea na rais muda mfupi uliopita “ Jing wang Zhu??...akajiuliza “ Balozi wa China

na Ernest wana mpango gani unaoendelea? Nimemsikia Ernest akiongelea kuhusu makabidhiano yatakayofanyika leo,wanakabidhiana kitu gani? Nahisi kuna

jambo Ernest ananificha kwani nimegundua kwa siku za karibuni amebadilika ghafla .Ni wazi kuna jambo linaloendelea chini kwa chini na hataki

kunitaarifu.Nimemuona hata usiku anakuwa macho muda mwingi ,lazima kuna kitu kinamsumbua” akawaza “ Ili nifahamu kinachoendelea lazima nimchunguze

Mukasha kwani ndiye aliyetumwa kuhakikisha makabidhiano hayo yanafanyika” i Agatha akairudisha simu mezani na haraka akaichukua simu yake akazitafuta

namba Fulani akapiga “ Hallow “ akasema Agatha baada ya simu yake kupokelewa upande wa pili.Baada ya salamu Agatha akasema “ Muhsin nimekupigia

asubuhi hii kuna jambo nataka nikueleze.Kwa siku kadhaa nimeona mabadiliko kwa Ernest nikahisi kuna kitu kinamsumbua.Leo asubuhi nimemsikia
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akizungumza na balozi wa China hapa nchini na walikuwa wanazungumiza kuhusu makabidhiano.Sifahamu ni makabidhiano gani hayo ila ninaamini kuna kitu

kinachoendelea kati ya Ernest na balozi wa China.Kuna chochote unachokifahamu kuhusu Ernest na balozi wa China? “ Mhh !! hapana sifahamu chochote .Rais

hajanieleza jambo lolote” akajibu Muhsin. “Damn you Muhsin,you are a vice president and its your job to know everything that’s going on.Tunakutegemea sana

wewe kujua kila kinachoendelea katika ofisi ya rais.Be smart Muhsin.Find out whats going on.Kwa kukusaidia kujua kinachoendelea ni kwamba tuma vijana

wamchunguze Mukasha kwani ndiye aliyekabidhiwa kazi hiyo aisimamie.Kupitia kwake kuna kitu tunaweza kukigundua” akasema Bi Agatha “ Agatha ahsante

kwa taarifa nitaifanyia kazi” akajibu Muhsin Abdulkareem masoud makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kukata simu


KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO Saa ya dhahabu iliyokuwa inaning’inia ukutani ilionyesha tayari imekwisha timu saa mbili na

dakika tisa za asubuhi.Taratibu Monica akatoka kitandani na kusimama katikati ya chumba kile kikubwa na kutabasamu .Alivutiwa mno na uzuri wa chumba

kile. “ Jana sikukichunguza vizuri chumba hiki ..mhh ni chumba chenye uzuri wa ajabu kabisa.” Akaenda dirishani akafunua pazia na kuchungulia nje ‘” Wow !!

akajikuta akitamka baada ya kuishuhudia mandhari ya aina yake kulizunguka jumba lile “ This house is amazing.Kuna uzuri wa kipekee kabisa mahala

hapa.Panavutia na unaweza kutamani uishi hapa maisha yako yote” akawaza na kuvaa nguo zake za mazoezi akatoka mle chumbani ,akasalimiana na wafanyakazi

wa ndani halafu akaelekea katika chumba cha mazoezi.Kisha maliza mazoezi akarejea chumbani akaoga na akiwa katika kujiandaa kengele ya mlangoni ikalia

akaenda kuufungua mlango akakutana na mwanadada mrembo aliyejitambulisha kama mpambaji wake mkuu,akamtaka waongozane hadi katika saluni

iliyokuwamo ndani ya hilo jengo ambako Monica akarembwa vilivyo. Kisha maliza kujiandaa akaenda katika chumba cha chakula akapata kifungua kinywa

halafu akarejea tena chumbani kumsubiri Pauline ambaye alimuahidi kuwa angefika kumchukua .Wakati akimsubiri Pauline Monica akatumia simu iliyokuwao

mle chumani kuwapigia simu wazazi wake akawahakikishia kwamba anaendelea vizuri na wasiwe na wasiwasi.Kisha maliza kuwasiliana na wazazi wake akapata

wazo “ Natamani nijue hali ya Dr Marcelo.Mtu pekee ambaye anaweza akanipa habari za Marcelo ni Daniel “ akawaza na haraka haraka akaziandika namba za

simu za Daniel kwani alizifahamu kwa kichwa akampigia. “ Hallow” ikasikika sauti ya Daniel upande wa pili wa simu “ Daniel its me Monica” “ Monica!! How

are you? Umenipigia kwa namba hi...” akasema Daniel lakini Monica akamkatisha kabla hajaendelea zaidi “Daniel nimekupigia kutaka kufahamu jambo moja

tu.Ni kuhusiana na Dr Marcelo.Anaendeleaje? “ Nimetoka kumtazama leo asubuhi anandelea vizuri lakini bado hajaanza kuzungumza.Bado anatumia maadishi

kuwasiliana.Amekuulizia nikamdanganya kuwa umepata dharura nje ya Dar es salaama na akasema nikukumbushe kuhusu ombi lake.Hizi ni namba za Congo


umekw......” akasema Daniel lakini kabla hajamaliza Monica akasema “ Niko Kinshasa.Kumbuka nilikueleza kwamba nimepata safari ya dharura kwa hiyo niko

hapa Kinshasa nitarejea kesho au kesho kutwa” akasema Monica akaagana na Daniel akakata simu “ Hili suala la Marcelo mbona linazidi kuniumiza kichwa ?

Kama ameendelea kukumbusha kuhusu ombi lake la kunitaka nimsaidie ,basi ni kweli kuna watu wanaotaka kumuua.How am I going to help him? Akajiuliza “ I

must find a way to hep him as quick as possible.Siwezi kuach.....” Monica akaondolewa mawazoni na mlio wa kengele ya mlangoni.Akaenda kuufungua na

kukutaa na sura inayong’aa yenye tabasamu ya Pauline Zumo “ Monica” akasema Pauline kwa furaha. “ Pauline karibu sana,nimestuka nikadhani ninatazamana

na malaika “ akasema Monica na wote wakacheka.Pauline alipendeza mno.Alivaa suti nzuri nyeupe iliyomkaa vyema na bila kusahau vito vya thamani .Baada ya

maongezi machache Pauline akamtaka Monica amfuate wakatoka nje ya jumba lile na kuelekea moja kwa moja sehemu kulikokuwa na helkopta ya rangi nyeupe

wakaingia na helkopta ikapaa.Walilitazama jiji la Kinshasa kutokea angani na kuufanya uso wa Monica usikaukiwe tabasamu.Helkopta ile ilitua katika uwanja

mzuri wenye nyasi za kijani za kuvutia uliokuwa pembeni ya hoteli moja kubwa.Mlango ukafunguliwa Monica na Pauline wakashuka Pauline akamuongoza
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Monica hadi katika meza iliyokuwa kandoni mwa mto mdogo uliopita pemeni ya hoteli hiyo kubwa.Bata wazuri weupe walikuwa majini wakiogeleza na

kuifanya mandhari ya eneo lile kuwa ya kuvutia mno.Haraka haraka wahudumu wakafika na kuanza kuwahudumia.Pauline akawataka walinzi wake wasogee

mbali na kuwaacha peke yao “ Monica mahala hapa panaitwa hoteli Patrice.Ni hoteli inayomilikiwa na rafiki yangu.Mimi hupenda sana kuja hapa mara moja kila

juma kupunga upepo .Hii ni hoteli inayosifika nchini Congo kwa kuwa na madhari nzuri ya kuvutia.” Akasema Pauline. “ Kweli Pauline hii ni sehemu nzuri na

hata mimi nimepapenda” akasema Monica.Pauline akainua glasi ya maji akanywa na kusema “ Monica nimekuleta hapa nje ya jiji kwa ajili ya maongezi ya

muhimu mno” akasema Pauline na kumfanya Monica ahisi baridi kwa ndani,alianza kuingiwa na woga. “ nahisi atakuwa amegundua kitu anachotaka kukifanya

mumewe na anataka kunikanya,nilifaya kosa kubwa kukubali ombi la David la kuja Congo.I’m so stupid! Akawaza Monica na macho yake yalionyesha wasiwasi

mkubwa alionao “ Kama nilivyojitambulisha kwako jana naitwa Pauline Zumo mke wa David Zumo rais wa Congo.Historia yangu na David ni ndefu na tuna

miaka 12 sasa katika ndoa yetu.Tulifunga ndoa tukiwa bado vijana sana.Baba yangu na baba yake David ni marafiki wakubwa na urafiki huo ndio uliopelekea

hata mimi na David tukawa marafiki wakubwa ,urafiki uliotupeleka hadi katika ndoa.Baba yake

David alikuwa mwanasiasa na mfanya biashara tajiri ambaye alimshawishi David aingie katika siasa na kwa bahati nzuri watu wa Congo wakavutiwa naye na

wakamchagua awe rais.Amefanya mambo mengi makubwa kiasi cha kuwafanya raia wa Congo wamtake awe kiongozi wao wa maisha.” Pauline akatabasamu

baada ya sekunde kadhaa akaendelea. “ Mimi na David tuna maisha mazuri ya furaha lakini kuna jambo moja ambalo kwa miaka mingi sasa limekuwa

linatunyima usingizi na kama tusingekuwa na mapenzi ya dhati toka mioyoni mwetu basi ndoa yetu ingekwisha sambarataika lakini penzi letu lina mizizi imara

na ndiyo maana kila uchao penzi letu linachanua “ Akanyamaza akainua glasi yake ya maji akanywa halafu akaendelea “ Mimi na David tunalo tatizo letu la ndani

ambalo hatujawahi kumueleza mtu yeyote na leo nitakueleza kwa mara ya kwanza.Toka tumeoana hadi leo hii hatujabahatika kupata mtoto na hatuna mategemeo

ya kupata mtoto kwani sina uwezo wa kubeba mimba.Kizazi changu kiliondolewa ili kunusuru maisha yangu” Pauline akainama na sura yake ikabadilika

akaonyesha namna jambo lile linavyomuumiza.Monica akamuonea huruma sana.Pauline akaendelea “ Jambo hili limekuwa linaniumiza mno japokuwa kila

dakika uso wangu unatabasamu na watu wananiona ni mwanamke mwenye furaha lakini ndani nina mauivu ambayo hakuna anayeweza kujua uchungu wake

zaidi ya Mungu pekee.Tuna mali nyingi mno,ni matajiri namba moja Afrika lakini huwezi kuamini kila usiku ninapopanda kitandani hufumba macho na

kumuomba Mungu anichukue ili nisiione kesho na kuzidi kuteseka.Sina hamu na kuishi tena .Nimekwisha kata tamaa” akasema na machozi

yakamtoka.Akachukua kitambaa akafuta machozi na kuendelea “ Yapata miaka mitatu sasa imepita nilifanya maamuzi .Nilimruhusu David aoe mke wa

pili.Nilimtaka afanye hivyo ili tuweze kupata mtoto,mrithi wa utajiri wetu huu mkubwa.David hakuwa tayari kwa hilo hadi hivi juzi baada ya kutoka katika

mkutano Dar es salaama aliponifuata na kunieleza kwamba amekubali ombi langu na tayari ameona mwanamke anayeweza kutufaa.Kwangu hizo zilikuwa ni

taarifa njema sana na nikataka kumfahamu mwanamke huyo ambaye amebadili msimamo wa David na ndipo aliponieleza kwamba ni wewe.Nilijikuta na mimi

nikivutiwa nawe sana na nikataka nikufahamu zaidi na David akakuomba uje kwa ajili ya kuhudhuria kongamano la vijana.Kwa ufupi utatusamehe sana Monica

kwani hakuna Kongamano hilo alilokueleza David bali hili lilikuwa ni wazo langu kwa lengo la kutaka kukuona.Kwa hiyo Monica karibu sana

Congo.Tunafurahi na tunaona fahari kubwa kuwa na mgeni kama wewe”. akanyamaza Pauline akamimina maji katika glass akanywa kidogo na kumgeukia

Monica. “Monica huna haja ya kunieleza wewe ni nani kwani tayari nimekwisha fanya uchunguzi wangu na kufahamu kila kitu kuhusu wewe na nimetokea

kukupenda sana.Sote tunakupenda.David alinieleza kuwa hakuweza kukutamkia wazi wazi kuhusu azma yake ya kutaka

CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuanzisha mahusiano nawe na hatimaye kufunga nawe ndoa lakini anadai aliongea na baba yako na nina hakika ujumbe wake ulifika”.Pauline akanyamaza Monica aliyekuwa anamsikiliza Pauline kwa makini akakohoa kidogo kurekebisha koo halafu akasema, “Pauline kabla sijasema chochote naomba nikupe pole sana kwa tatizo hili kubwa ulilonalo.Nimeguswa sana kama mwanamke kwa hali yako.Nafahamu mateso anayopitia mwanamke kwa kukosa mtoto”akanyamaza kidogo halafu akaendelea. “Nimeyasilikiza maelezo yako kwa makini na ninapenda nitumie nafasi hii kukupongezeni kwa upendo mkubwa mlio nao ambao umewawezesha muendelee kuisha kwa amani na kuzishinda changamoto hizi mnazokumbana nazo.David zumo ni mtu ambae ni maarufu sana duniani.Nilimfahamu kutokana na umaarufu wake huo.Anajulikana dunia nzima kwa namna alivyoweza kuibadili nchi ya Congo na sikuwai kuwa na ndoto ya siku moja kukutana na mtu mkubwa kama huyu”.akanyamaza halafu akaendelea “Ninamiliki kampuni ya mavazi na vile vile ninayo taasisi yangu ambayo inajishughulisha na kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji hususani wazee wasiojiweza na watoto.Mwaka huu mimi na taasisi yangu tuliazimia kuanzisha mradi mkubwa wa kujenga shule kubwa ya watoto wenye ulemavu wa kutokuona na kusikia,ili kupata fedha za kutuwezesha kuanza ujenzi wa shule hiyo ilitulazimu tuandae mambo Kadhaa ikiwemo kuandaa mbio za nusu marathon.Wakati wa mbio hizo ndipo nilipokutana na Jean pierre Muyeye ambaye alitumwa kumuwakilisha David na akanipa ujumbe aliopewa ulionitaka nikaonane na David kwani kuna msaada anahitaji kuutoa.Nilionana na David akanipa mchango wake mkubwa na akaniomba siku inayofuata akutane na wazazi wangu.Nilimkutanisha na wazazi wangu na tukiwa katikati ya maongezi nilipata taarifa kuwa rafiki yangu mmoja alipatwa na matatizo ikatulazimu mimi na mama kuondoka tukamuacha baba na David wakiendelea na maongezi.Niliporejea nyumbani baba akanielezea alichokiongea na David Zumo.Zilikua ni taarifa zilizonistua sana na sikuwa na jibu la kuwapa.Wakati bado nikiwa katika tafakari juu ya suala hilo David akanipigia simu na kuniambia nije Congo kwenye kongamano la vijana.kwa hiyo Pauline mpaka sasa bado sijafanya maamuzi yoyte kuhusiana na ombi la David .Nadhani nahitaji muda zaidi kulitafakari suala hili.Si suala ambalo ninaweza kulitolea maamuzi ya haraka” akasema Monica. “ Nimekuelewa Monica .Hata mimi kama ningekuwa katika nafasi yako ningekuwa na woga kama uliokupata.Ni jambo la kustusha Monica kwa mtu kuibuka na kutangaza kutaka kukuoa na hasa mtu mwenyewe akiwa mkubwa kama David.Nafahamu kila mtu ana malengo yake katika maisha na kila mtu ana aina ya mtu anaye muhitaji kama mwenzi wake kwa hiyo naamini kabisa yawezekana labda David akawa si mwanaume wa aina ile ambayo unaitaka lakini ninataka kukuhakikishia kwamba japokuwa ni

muda mfupi sana mmeonana na kufahamiana lakini tayari amekwisha kupenda na ninamfahamu David akipenda huwa amependa kweli.Ninakuthibitishia hilo kwa namna anavyonipenda na kunifanya nijione niko juu ya wanawake wengine wote wa dunia.David hapendi kumuumiza mwanamke na katika kipindi chote ambacho nimeishi naye hajawah kunitoa chozi hata mara moja.Ni mtu anayejali,anasikiliza na akikupenda chochote ukitakacho utakipata.NI mwanaume ambaye nikiamua kukueleza sifa zake naweza kutumia siku nzima.Kwa kifupi ni mwanaume ambaye kila mwanamke anaota kumpata.Wanaume wa aina hii ni wachache sana kupatikana katika dunia ya sasa.” Pauline akanyamaza wakatazamana kisha Monica akauliza “ Kwa nini unaniambia haya yote Paulie? “ Ni kwa sababu hauko tayari kulikubali ombi la David na ndiyo maana nimeamua kukuambia hata yale mambo ya ndani ya kumuhusu David ili ufahamu kwamba hana nia mbaya nawe ,ni mtu mwema na lengo lake au lengo letu kwako ni jema sana.Nadhani mimi ninaweza kuwa mwanamke wa kwanza katika hii dunia ya sasa kumshawishi mwanamke mwenzangu akubali kuolewa na mume wangu.Jambo kama hili ni nadra mno kutokea katika zama hizi lakini mimi ninalifanya tena kwa moyo mweupe kabisa.Monica nakuomba kubali kuolewa na David .Mimi sina tatizo lolote na suala hili na niko radhi David awe na mke wa pili .Nataka umzalie David watoto ambao watakuwa ni watoto wetu na ndio watakaokuwa warithi wa utajiri wetu.Tutakuwa na familia yenye furaha na upendo mkubwa.Nakuhakikishia kwamba hautajutia uamuzi wako kama utakubali kuolewa na David.Utaishi maisha mazuri na utakuwa kweli malkia wa Afrika .Dunia nzima itakufahamu na kukuheshimu.David atakufanya mwenye furaha ,sote tutakuwa na furaha.Maisha yetu yatakuwa ya furaha kubwa.Monica naamini unanishangaa sana kwa msisistizo huu lakini ninafanya hivi kwa sababu ya furaha ya mwanaume ninayempenda.Furaha ya David ni yangu pia na ni wewe pekee ambaye unaweza ukaifanya furaha ya David ikakamilika kwa kukubali ombi lake .Nakuhakikishia Monica mimi binafsi nitakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unaishi maisha mazuri na ya furaha.Narudia tena kukuomba Monica tafadhali kubali ombi la David” akasema Pauline.Monica akainamisha kichwa na kutafakari .Ukimya ukatanda.Baada ya kama dakika tatu Monica akasema “ Pauline umeniweka katika nafasi ngumu.Huu ni mtihani mgu....” Akasema Monica lakini Pauline akamzuia asiendelee “ Monica huu si mtihani.Yaamini maneno yangu na hautajutia maamuzi yako” akasema Pauline,Monica akabaki kimya “ Usiku wa leo” Pauline akaendelea “ Utakutana na David Zumo .Katika usiku wa leo atautumia kukueleza wazi yeye mwenyewe kuhusu jambo hili.Tafadhali Monica naomba atakapokutamkia kwamba anataka kukuoa sema ndiyo.Utauvunja moyo wake,na wangu pia kama ukisema hapana.Usiku wa leo ni muhimu mno kwako kwani ndiyo utakaoamua aina ya maisha unayotaka kuishi.Maisha yako yanaweza kubadilika kuanzia usiku wa leo kwa hiyo ulimi wako utafanya kazi kubwa ya maamuzi kwa kutaamka neno ndiyo au hapana.Siwezi kukulazimisha ukubali japo nimejitahidi sana kukushawishi ukubali ombi la David kwa hiyo wewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.Kwa sasa naomba tuachane na suala hilo na tuendelee na mamo mengine.” Akasema Pauline na kuagiza waletewe chakula wakaendelea na maongezi mengine.

DAR ES SALAAM – TANZANIA Saa tano na dakika kumi,simu ya Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ikaita.Alikuwa balozi wa China Jing wang Zhu.Hii ni simu ambayo Ernest alikuwa anaisubiri sana hivyo akaipokea haraka haraka “ Hallow Balozi.” Akasema Enest “ Mheshimiwa rais nimekupigia kukutaarifu kwamba makabidhiano yetu yamekwenda vizuri.Wafungwa raia wa China wamekabidhiwa kwangu saa tano kamili juu ya alama wakiwa na afya njema kabisa.Katika muda huo h uo mfungwa Linda January raia wa Tanzania aliyekuwa amefungwa nchini China amekabidhiwa kwa ubalozi wa Tanzania nchini China.Unaweza kuwasiliana na balozi wa Tanzania China kwa uhakika zaidi.Hongera mheshimiwa rais kwa kulifanikisha jambo hilo “ akasema Jing wang “ Ahsante sana mheshimiwa balozi kwa kulifanikisha suala hili.Nifikishie shukrani zangu nyingi kwa rais wa China” akasema Ernest akaagana na balozi .Alipokata simu haraka haraka akazitafuta namba za balozi wa Tazania nchini China akampigia. “ habari yako mheshimiwa balozi “ akasema Ernest baada ya Edger Chuswa balozi wa Tanzania nchini China kupokea simu. “ Habari nzuri mheshimiwa rais.Nilikuwa katika harakati za kutaka kukupigia simu na kukupa taarifa za suala lile ulilonieleza.Yule msichana tayari amekabidhiwa hapa ubalozini ,akiwa na afya njema.Nitamuhifadhi nyumbani kwangu wakati nikisubiri maelekezo toka kwako mheshimiwa rais” akasema balozi Edger “ Ahsante Edger.Nitakupa maelekezo nini cha kufanya .Kitu pekee ninachopenda kukukumbusha ni kwamba suala hili halipaswi kusambaa kwani ni suala la siri kubwa.” “ Nalifahamu hilo mheshimiwa rais nakuomba usihofu kabisa” “ Ahsante Edger ,naomba umpe uangalizi wa hali ya juu sana huyo msichana .Baadae mida ya saa tatu usiku kwa saa za afrika mashariki ambayo itakuwa ni saa nane usiku kwa saa za China nitakupigia nitataka kuongea na Linda.” “ Sawa mheshimiwa rais,nitajitahidi kuhakikisha anakuwa macho mida hiyo ili uweze kuzungumza naye” “ Ahsante sana balozi ,tutawasiliana hapo baadae” akasema Ernest na kukata simu “ Nimelazimika kutumia madaraka yangu kama rais kuweza kulifanikisha ombi la Austin.Hili ni suala zito na linaweza kuniletea matatizo likijulikana kwani ni kinyume na sheria za nchi na nimetumia vibaya ofisi yangu lakini sikuwa na nama nyingine ya kufanya .Nahitaji Austin anifanyie kazi yangu na asingeweza kuifanya bila ya sharti lake hilo kutimizwa.Hakukuwa na namna nyingine ya kuweza kumtoa Linda gerezani bila kubadilishana wafungwa.” Akawaza Ernest.

aa saba za mchana Daniel aliwasili hospitali kwa ajili ya kumjulia hali Dr Marcelo.Alishuka garini na kutembea taratibu kuingia katika wodi alikolazwa Marcelo.Kichwa alikiinamisha chini ilionyesha wazi alisongwa na mawazo. “ Sijui nitamjibu nini Marcelo endapo ataniuliza kuhusu Monica.” akawaza Daniel “ Ni wazi Monica amekwisha nitoa kabisa katika akili yake.Zamani kila akitaka kusafiri iwe ndani au nje ya nchi alikuwa ananijulisha lakini kwa sasa hana habari tena na mimi.Nini kimetokea na kumbadilisha Monica namna hii?Lakini haya yote yameanza ghafla tu baada ya Dr Marcelo kutokea.Anyway ngoja niachane na mawazo haya” akawaza wakati amekaribia wodi alimolazwa Marcelo.Ndani ya wodi walikuwemo watu kadhaa waliokuja kumjulia hali Marcelo na kwa kuwa chumba hakikuwa kikubwa sana iliwalazimu wengine kukaa nje kusubiri zamu yao ifike.Wakati akiwa nje akisubiri kuingia,akatokea Julieth dada wa Marcelo,wakasalimiana “ Nimefurahi umefika Daniel.Marcelo aliniuliza kama umekuja nikamjibu bado” akasema Julieth “ Nimefika muda si mrefu “ akajibu Daniel “ Where is Monica? Sijamuona jana na hata leo.Si kawaida yake kutoonekana hapa hospitali toka Marcelo alipopata matatizo” “ Monica amepata safari ya dharura lakini kesho atarejea” akasema Daniel na mara watu waliokuwa ndani ya chumba wakatoka Daniel hakutaka tena maongezi na Julieth akaingia ndani.Bado Marcelo alikuwa anawasiliana kwa ishara na hakuwa ameweza kuzungumza. “ Monica yuko wapi? Marcelo akauliza kwa njia ya maandishi “ Monica amepata dharura na ametoka nje ya Dar es salaam lakini muda si mrefu atarejea” Daniel akamjibu kwa maandishi “ Call and tell her to hurry” “ Sawa nitamueleza” akajibu akajibu Daniel kwa maandishi na kutoka mle chumbani “ Kuna kitu gani kati ya Monica na Marcelo?Toka jana Marcelo amekuwa ananisisitiza kuhusu Monica.Nadhani hakuna tena ulazima wa mimi kuja hapa tena kama Monica hayupo.Sitaki kuendelea kudanganya kila siku.Kingine kinachoniumiza zaidi ni kwamba Marcelo ameharibu mahusiano yangu na Monica.Nadhani itakuwa vyema nikiweka pembeni niwaache waendelee.” Akawaza Monic
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO Tayari ni saa moja kasorobo za jioni jijini Kinshasa.Kwa zaidi ya saa moja sasa Monica alikuwa katika saluni iliyokuwamo ndani ya jumba anamoishi na akina dada wapatao wanne wakifanya kazi ya kumremba kwa ajili ya usiku a kipekee ambao angekutana na David Zumo.Wakati akiendelea kurembwa bado mambo aliyozungumza na Pauline mchana yaliendelea kumjia kichwani.Bado aliendelea kuisikia sauti ya Pauline masikioni mwake ikimtaka akubali ombi la David Zumo.Kwa siku nzima jambo hili lilimuumiza sana kichwa. Baada ya kurembwa akarejea chumbani kwake kujiandaa na alipoingia chumbani akakuta kuna gauzi zuri sana limewekwa kitandani pamoja na vito vya thamani kwa ajili ya kuvaa usiku ule.Akatabasamu “ maisha haya ni mazuri mno.Unaishi kama malkia,unahudumiwa kwa kila kitu.Nimeanza kuyapenda maisha haya na endapo usiku wa leo nitamkubalia David Zumo ombi lake basi haya yatakuwa ndiyo maisha yangu ya kawaida.Hata hivyo bado moyo wangu haujafanya maamuzi kama nikubali au nikatae kuolewa na David Zumo .Natamani niombe ushauri kwa mtu lakini suala hili linahusu maisha yangu na siwezi kutegemea mtu anishauri.Wazazi wao tayari wamekwisha amua wanataka nikubali” akakaa kitandani na kukumbuka kitu “ Ngoja nimpigie Daniel nimuulize maendeleo ya Marcelo.Sijui atakuwa katika hali gani hivi sasa.Naomba Mungu aendelee kumlinda hadi hapo nitakaporejea ili nitafute namna ya kumsaidia.” Akawaza Monica huku akiziandika namba za Daniel katika simu akapiga.Baada ya muda Daniel akapokea. “ hallow “ akasema “ Hallow Daniel its me Monica” “ Monica,nafurahi kuisikia tena sauti yako.Lini unarudi? “ Nitarudi muda wowote Daniel.Nimekupigia kufahamu hali ya Dr Marcelo,anaendeleaje? “ Anaendelea vizuri .Nilikwenda kumtazama mchana wa leo.Bado hajaanza kuzungumza ila amenipa tena ujumbe nikufikishie anasema ufanye haraka.Hakutoa maelezo mengine zaidi ya hayo.Monica jitahidi umletee kitu anachokihitaji kwani nimechoka kumdanganya kila siku.Kama itakuchukua muda mrefu kurejea itakuwa vyema endapo tutamueleza ukweli kwamba haupo nchini ili awe akifahamu” akasema Daniel “ Daniel please naomba usimueleze chochote kama niko nje ya nchi.Usiache kwenda kumtembelea na tafuta namna ya kuendelea kumdanganya .Leo namalizia mambo yangu na kesho nitarejea.Tafadhali Daniel nakuomba fanya hivyo” akaomba Monica .Baada ya sekunde chache Daniel akajibu Sawa Monica nitafaya hivyo lakini usichelewe sana kurudi tafadhali’ akasema Daniel “ Ahsante Daniel.Nitakupigia tena asubuhi.” Akasema Monica na kukata simu,akavuta pumzi ndefu. “ What am I going to do to help him? Akajiuliza na kuinamisha kichwa

Kesho lazima nirejee Dar es salaam.Marcelo needs my help.Nisipomsaidia kwa haraka kama alivyoomba anaweza akauawa.” Akawaza Monica na kuinuka akaanza kuvaa Alimaliza kuvaa na kujitazama katika kioo akatabasamu “ Sipendi kujisifu lakini mimi ni mzuri.Naamini usiku huu David Zumo atapag.....” Monica akastuliwa toka mawazoni na kengele ya mlangoni.Akaenda kuufungua akakutana na mfanyakazi wa mle ndani akiwa na mwanamke mmoja mwenye umbo kubwa “ Mama Monica huyu ni mbunifu wa mavazi anaitwa Sheris.Alitakiwa kuwasili hapa kitambo lakini alipata tatizo njiani ndiyo maana amechelewa” “ Hallow Sheris” Monica akamsalimu Yule mwanamama. “ Hallow Monica.Nimefurahi sana kukuona.Nilitakiwa kufika hapa muda mrefu uliopita lakini niliharibikiwa na gari njiani.Nimepewa kazi ya kukuvalisha kwa usiku wa leo” akasema Sheris na kuingia chumbani akaanza kumkagua Monica kuanzia juu hadi chini akamfanyia marekebisho kadhaa “ Sasa uko tayari kukutana na mtukufu rais usiku wa leo” akasema Sheris baada ya kumaliza kumfanyia Monica marekebisho Saa mbili kamili juu ya alama kengele ya mlangoni ikalia,Monica akaufungua na kujikuta anatabasamu “ Pierre Muyeye” akasema kwa furaha “ Monica” akasema Muyeye wakasalimiana “ Monica umependeza sana kweli wewe ni malkia wa Afrka” akasema Muyeye na wopte wakacheka “ nadhani uko tayari” “ Niko tayari Muyeye” akasema Monica kisha Muyeye akamuongoza kushuka chini hadi katika gari zuri la kifahari akafunguliwa mlango akaingia na msafara wa magari zaidi ya kumi uliokuja kumchukua ukaondoka ukitanguliwa na piki piki za polisi.Magari yote katika barabara ulikopita msafara yakawekwa pembeni kuupisha msafara wa Monica upite.Monica hakutaka kuonyesha furaha yake usoni lakini moyoni alifurahi kupita maelezo.Hakuwahi kuota kama siku moja atapewa heshima kubwa namna ile kiasi cha magari barabarani kuwekwa pembeni kumruhusu apite.

DAR ES SALAAM - TANZANIA Inakariabia saa mbili na nusu jijini Dar es salaam rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest mkasa yupo katika chumba chake maalum ndani ya hoteli hii anayoimiliki . “Mukasha nadhani ni muda muafaka sasa wa kwenda kuonana na Austine”Ernest akamweleza Mukasha aliyekuwa naye mle chumbani wakijadiliana mambo kadhaa,akainuka na kurejea katika chumba cha kulala na kama alivyofanya siku iliyotangulia akabadili muonekano wake.akajitazama na kutabasamu. “ Austin amenifanya nikumbuke mbali sana enzi za ujana wangu.Nimepitia mambo mengi sana na siamini eti leo hii mimi ni rais a jamhuri ya muungano wa Tanzania.Kweli maisha yana maajabu .Najikubali kwa historia ya maisha yangu sikuwa na vigezo vya kuniwezesha kushika nafasi kubwa na nyeti kama hii .I’m a monster,lakini tazama nilipo sasa,niko katika ofisi kubwa kuliko zote nchini.Kweli hakuna kisichowezekana chini ya jua” akawaza Ernest na kutoka mle chumbani na kama ilivyokuwa usiku uliopita akaongozana na Mukasha na Evans mlinzi wake wakazunguka upande wa nyuma ambako kuna njia ya siri ya kupita wakaingia katika magari na kuondoka. Waliwasili katika nyumba anayoishi Austin.Evans akashuka na kubonyeza kengele ya getini baada ya dakika tatu geti likafunguliwa na gari zile mbili zikaingia ndani.Rais akafunguliwa mlango akashuka “ Hallow Austine” akasema Ernest “
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Karibu sana mheshimiwa rais” akasema Austin na kugeuka akaanza kupiga hatua kuelekea ndani.Mukasha ,Evans na wale walinzi wengine wawili wakaambatana nao.Mara Austin akageuka. “ Namuhitaji rais peke yake humu ndani.Wengine mtasubiri nje” “ Hilo halitawezekana kaka.Huyu ni rais wa nchi na jukumu letu ni kumlinda katika sehemu anayokwenda .Hatuwezi kumuacha peke yake hata sekunde moja.” Akasema Evans.Austin akamuelekezea macho Ernest “ You want to talk to me ? Waambie watu wako wabaki nje “ Austin akamwambia Ernets ambaye aliwataka walinzi wabaki nje akaingia ndani na Austin “ Karibu mheshimiwa rais” akasema Austin na kumkaribisha rais sofani “ Ahsante Austin lakini hukupaswa kufanya vile,wale ni walinzi wangu walioapa kuyatoa maisha yao kunilinda ,wanastahili heshima” “ I’m sorry mr President ,that’s how I work.I don’t trust people so easily.Ukitaka kufanya kazi na mimi lazima ukubali tabia zangu” “ Sawa hakuna tatizo.Umeshindaje leo?

Mr President lets go straight to the point.Why you are here? Umefanikiwa nilichokuomba? Ernest hakujibu kitu akachukua simu yake akazitafuta namba za
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
balozi wa Tanzania nchini China akapiga na simu ikapokelewa “ Habari za usiku huu mheshimiwa balozi.Samahani sana kwa kukuamsha mida hii ambayo huko

kwenu ni usiku mwingi” akasema Ernest “ Bado sijalala mheshimiwa rais kwani uliniahidi kunipigia usiku hivyo niko macho nikisubiri simu yako.” Akasema

balozi “ Nashukuru sana balozi.Sitaki nichukue muda wako mwingi.Naomba nizungumze na Linda kama yuko hapo karibu” akasema rais “ Ninaye hapa

mheshmiwa rais” akasema balozi na kumpa Linda simu ili azungumze na rais.Ernest akaweka sauti kubwa ili Austin aweze kusikia kila kitu “ Mheshimiwa rais

shikamoo baba” akasema Linda.Mara moja Austin akaitambua sauti ile na kutabsamu huku machozi yakimlenga. “ Marahaba hujambo Linda? “ Sijambo “

akajibu Linda “ Samahani Linda hebu nieleze historia yako kwa ufupi” akasema rais “ Naitwa Linda January,ninatokea Tanzania.Nilikamatwa hapa China na

kufungwa miaka kumi na tano kwa kosa la kujaribu kuingiza madawa ya kulevya.Ninashukuru mheshimiwa rais umenisaidia nimeweza kutoka

gerezani.Ninaomba mheshimiwa rais nitakaporejea nyumbani nisiendelee na kifungo.Nakuahidi sintajihusisha tena na biashara hii ya dawa za kulevya,nakuomba

sana baba” akasema Linda na kwa mbali akasikika akilia kwa kwikwi.Austin naye akashindwa kuyazuia machozi kumtoka. “ Linda nimekusikia na

ninakuhakikishia kwamba hautakwenda gerezani tena.Nitakuandalia mpango mzuri sana wa maisha yako mapya na kwa sasa utaendelea kukaa hapo hapo kwa

balozi wetu China.Utapata kila unachokihitaji.Naomba umpe simu balozi tafadhali” akasema Ernest na kuagana na balozi akamgeukia Austin “ Ahsante sana

mheshimiwa rais.Sina neno zuri la kukushukuru kwa hili ulilonifanyia ila nakuahidi kukufanyia kazi yako kwa ufanisi mkubwa.Now we can talk” akasema
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Austin “ Nilikwambia Austin kwamba nina nguvu ya kuweza kumtoa dada yako gerezani.Baada ya kulitimiza ombi lako ni nafasi yako sasa kunisikiliza

nikueleze kile ambacho nimekuitia hapa Tanzania” akasema Ernest “ Mheshimiwa rais kabla hujaendelea naomba nikuulize swali moja tu na ninaomba unipe

jibula kweli” “ Uliza Austin nitakujibu bila wasi wasi” Austin akamtazama Rais kisha kwa sauti ya taratibu akauliza “ Mr president are you one of them? “ One

of them? Unazungumzia akina nani? Rais naye akauliza “ The Alberto’s ´” akajbu Austin. Mstuko aliuopata Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa

Tanzania ulikuwa mkubwa na wa wazi.Haraka haraka akajifanya kama vile hajastuka na kuuliza lberto’s ? Who are they? Akauliza rais huku sauti yake

ikionyesha kitetemeshi kwa mbali “ Nijibu kama nawe ni mmoja wao au vipi? Akauliza Austin “ Sifahamu unazungumzia watu gani Austin .I don’t know those

people and I’m not one of them” akasema Ernest “ Show me your hands” akasema Austin na kumfanya rais ahamaki “ What are you trying to do Austin? Mimi

ndiye niliyekuita hapa na unapaswa kunisikiliza na si kuanza kuniuliza maswali hayo ya hovyo!! “ Mheshimiwa rais nimekuuliza swali rahisi sana na ninataka

unijibu ndiyo au hapana.Nina sababu zangu kukuuliza hivyo.Ukamilifu wa kazi yako unayotaka kunipa utategemea sana jibu la swali nililokuuliza” akasema

Austin .Ernest akamtazama Austin kwa makini “ Austin unanishangaza sana.I real don’t know what you are talking about.Naomba tusipoteze muda Austin

kujadili mambo yasiyokuwa na msingi wowote.Tayari nimekwisha fanya ulichotaka nikufanyie kwa hiyo ni zamu yangu kufanya kile ninachotaka uifanye !! “

Mheshimiwa rais sijakataa kuifanya kazi yako .Nitaifanya tena kwa ufanisi mkubwa lakini ufanisi wake utategemea jibu la swali nililokuliza.Kama unakiri kuwa

wewe si mmoja wao basi nionyeshe mkono wako wa kulia” akasema Austin “ Austin kwani hao Alberto’s ni akina nani? Umewafahamu vipi? Wanahusiana nini

na wewe? Akauliza Ernest “ Tuokoe muda mheshimiwa rais .Nonyeshe kiganja cha mkono wako wa kulia” akasema Austin.Ernest akamtazama kwa makini

akagundua kuwa Austin hakuwa akiongea kwa masihara hata kidogo bali alimaanisha alichokiongea. “ Mr President..” akasema Austin “ Kama hutaki

kunionyesha kiganja chako cha mkono wa kulia utanifanya niamini kuwa nawe pia ni mmoja wao na kama ni kweli basi kutakuwa na ugumu wa mimi kufanya

kazi yako” akasema Austin “ Austin what do you real want? Akauliza Ernest . “ Mheshimiwa rais nipe jibu moja ili twende sawa.Are you one of them? Austin

akauliza tena.Taratibu Ernest Mkasa akainua mkono wake wa kulia na kumuonyesha Austin kiganja chake.Austin akamsogelea na kukikagua kiganja kile kwa

umakini mkubwa kisha akasema “ Ok good.You are not one of them, but you know them right? Akauliza na rais akabaki kimya “ Mr President do you know

them? “ Austin let’s not talk about this.Hili si suala dogo kama unavyofikiria” akasema rais. “Sentensi hiyo mheshimiwa rais inanipa uhakika kuwa

unawafahamu watu hao ni akina nani.Naomba sasa unieleze kazi unayotaka nikufanyie” akasema Austin .kabla Ernest hajasema chochote simu yake

ikaita.Akatazama mpigaji alikuwa David Zumo rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. KINSHASA – JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Msafara uliombeba Monica uliwasili katika jumba la mapumziko la rais David Zumo lililokuwa nje kidogo ya jiji la Kinshasa.Lilikuwa ni jumba kubwa la

kupendeza na ulinzi ulikuwa mkali .Mlango wa gari alilopanda ukafunguliwa Monica akashuka “ Monica karibu sana katika kasri la mapumziko la mtukufu rais

David Zumo” akasema Jean Piere Muyeye kisha akamuongoza Monica kupita katika zuria jekundu kuelekea ndani.Walipanda hadi ghorofa ya nne ambako

kulikuwa na utulivu wa aina yake.Pierre Muyeye akamuongoza hadi katika mlango wenye nakshi za dhahabu akabonyeza kengele na mlango ukafunguka. “

Kutokea hapa ni watu wachache tu wanaoruhusiwa kufika.Mimi nitabaki hapa na wewe utaelekea ndani kuonana na rais.Tafadhali usiogope Monica” akasema

Muyeye. “ Ninaogopa Muyeye” akasema Monica “ Usiogope Monica.Hakuna tatizo lolote sehemu hii ni salama mno.Nenda tafadhali rais anakusubiri” akasema

Muyeye. Monica akalivuka lango lile zuri ambalo lilijifunga mara tu alipopita .Alipita katika milango kadhaa na kila alipokaribia mlango ulijifungua na

kujifunga alipopita .Mlango wa mwisho ulipofunguka alijikuta akiingia katika sebule kubwa na nzuri. “ Usiogope Monica niko hapa” Ikasikika sauti ya David

Zumo “ David !! akasema Monica kwa mstuko kidogo baada ya kumuona David Zumo akiwa amesimama katikati ya sebule ile akitabasamu.Usiku huu hakuwa

amevaa mavazi ya kawaida ambayo amezoeleka kuonekana nayo alivaa ngozi ya chui na kichwani alivaa kofia yenye manyoya ya Simba “ Karibu sana

Monica.Karibu katika kasri la kifalme la David Zumo.Hapa ndipo ninapokuja kupumzika kila ninapohitajika kupumzisha kichwa changu.Najua umestuka

kidogo kwa mavazi haya niliyovaa.Haya ndiyo mavazi nitakayokuwa nikivaa kama mfalme wa Congo pale nitakapotawazwa rasmi kuwa mfalme wa kwanza wa

Congo.Monica nadhani kuna jambo ambalo itakuwa vyema ukalifahamu toka kwangu mwenyewe ambalo nahisi umeshawahi kulisikia kwani linapigiwa kelele

nyingi na baadhi ya mataifa makubwa.Ninataka kuigeuza Congo kuwa nchi ya kifalme na utafiti umefanyika na unaonyesha asilimia themanini ya raia wa Congo

wanataka nchi yao iwe ya kifalme.Muswada unaandaliwa ili upelekwe bungeni na bunge likiridhia basi itafanyika kura ya maoni na wananchi wataamua kama

wanataka nchi ya kifalme au vipi.Endapo wataamua kuwa wanataka Congo iwe nchi ya kifalme basi nitatawazwa kuwa mfalme David wa kwanza na kama ilivyo

kawaida kwa nchi zenye utawala wa kifame uko mmoja ndio hutawala kwa hiyo basi familia yangu itatawala Congo kwa vizazi na vizazi.” Akasema David Zumo

huku akitabasamu “ Tuachane na hayo ,napenda nikushuru sana Monica kwa kukubali mwaliko wangu.Umeacha shughuli zako nyingi za muhimu na kuja

Congo.Ahsante sana” akasema David Hata mimi nashukuru sana David kwa makaribisho mazuri niliyoyapata.Sijawahi pewa heshima


kubwa kama uliyonipata wewe na mkeo Pauline.Ahsanteni sana” akasema Monica “ Monica wewe ni mgeni wetu wa heshima kwa hiyo ni jukumu letu

kuhakikisha kwamba unafurahi na nimefarijika kusikia umefurahi.Naomba uwe na amani na ujisikie uko nyumbani.Muda wowote kama kuna chochote unahitaji

usisite kutueleza.” Akasema David “ Ahsante David” akajibu Monica “ Leo asubuhi nimewasiliana na wazazi wako nikawafahamisha kwamba umefika salama na

kuwatoa hofu .Wazazi wako wanakupenda sana Monica” akasema David na Monica akatabasamu “ Vipi kuhusu Yule rafiki yako aliyepigwa risasi anaendeleaje?

“ Anaendelea vizuri lakini bado hajaanza kuzungumza “ akajibu Monica “ Pole sana.Waliofanya unyama huo tayari wamekamatwa? “ Hapana bado

hawajakamatwa mpaka leo” “ Ninahisi lazima atakuwa anawafahamu.Laiti kama angeweza kuzungumza basi angewataja ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua”

“ David suala hili lina utata mwingi.Jana mchana nilimtembelea Dr Marcelo hospitali na akaniandikia ujumbe wa kunitaka nimsaidie kumtorosha pale hospitali

kuna watu wanataka kumuua” “ Una hakika hajapatwa na tatizo lolote la kiakili? Watu wanaotamka maneno kama hayo mara nyingi huwa wana matatizo ya

akili”Akauliza David “ Hapana hana tatizo la akili.Anazo akili zake timamu na hata madaktari wamethibitsha hivyo” “ Kama anawafahamu watu wanaotaka

kumuua basi suala hili linatakiwa kuwasilishwa katika vyombo husika ili vilishughulikie” “ Ningeweza kufanya hivyo lakini katika ujumbe alioniandikia
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alinieleza kuwa suala hili ni la siri na hapaswi mtu mwingine yeyote kufahamu kwa hiyo siwezi kumueleza mtu yeyote hata polisi.Endapo angetaka niliwasilishe

jambo hili polisi basi angenielekeza hivyo lakini hakutaka nifanye hivyo.” akasema Monica “Monica nakushauri achana kabisa na suala hilo.Watu hao wanaotaka

kumuua huyo rafiki yako wakibaini kuwa unajihusisha na jambo hilo unaweza ukajikuta katika matatizo” “ Hapana David,siwezi kuacha kumsaidia Dr Marcelo

kwani ni rafiki yangu.Anahitaji mno msaada wangu na hana mwingine wa kumkimbilia.Nisipomsaidia anaweza akauawa” akasema Monica.David akamtazama

kwa makini kisha akasema “ Monica wewe ni mtu mwenye moyo wa aina yake.Uko tayari hata kuyaweka hatarini maisha yako kwa sababu ya rafiki yako.Pamoja

na hayo sitaki ujiingize katika suala hili la hatari.Naomba uniachie mimi jambo hili nilishughulikie .Rais wa Tanzania ni rafiki yangu na nitaongea naye

kumuomba alishughulikie suala hili.Yeye ana watu wengi wanaoweza kuifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.Nitajie jina la mgonjwa wako na mahala alipo ili

nimuombe rais wa Tanzania anisaidie kwenda kumuondoa.Niambie vile vile unahitaji huyo rafiki yako apelekwe wapi baada ya kutolewa hospitali? Akauliza

David “ Ahsante sana David na sijui nitakushukuruje kwa msaada huu mkubwa.Mgonjwa anaitwa Dr Marcelo na amelazwa hospitali ya mtakatifu Lucia wodi za

watu maalum chumba namba tatu.

Nataka akishatolewa hapo hospitali apelekwe sehemu salama hadi hapo nitakaporejea .Naomba umsisitize rais kwamba jambo hili ni la siri na watu

watakaotumwa kwenda kumtoa Marcelo hospitali wasithubutu kumuhoji chochote” “ sawa Monica nimekuelewa na maelekezo yako yatazingatiwa” akasema

David akachukua simu na kumpigia rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest Mkasa DAR ES SALAAM - TANZANIA Ernest Mkasa alistushwa na simu

toka kwa David Zumo.Hakuwa ametegemea kabisa kama David Zumo angeweza kumpigia usiku ule.Akabonyeza kitufe cha kupokelea “ Hallow David”

akasema “ hallow Ernest,habari za usiku huu? “ habari nzuri sana.habari za Kinshasa? “ Huku kwema kabisa” akasema David “ Mheshimiwa rais umenistua

kidogo kwa simu yako ya usiku huu “ akasema Ernest “ Samahani sana kwa hilo mheshimiwa rais lakini nimelazimika kukupigia kutokana na kuhitaji sana

msaada wako” “ Sawa David nakusikiliza” “ Mheshimiwa rais kuna kijana mmoja anaitwa Marcelo ni daktari alipigwa risasi hivi karibuni na watu wasiojulikana

amelazwa hospitali ya mtakatifu Lucia chumba namba tatu.Mtu huyu bado yuko katika hatari ya kuuawa.Ninaomba msaada wako mheshimiwa rais utume vijana

wako wamuondoe hapo hospitali kwa siri na kumuweka sehemu salama na baadae nitakupa maelekezo mengine.Ninaomba sana unisaidie kwa hilo mheshimiwa

rais” akasema David Baada ya sekunde kadhaa Ernest akasema “ Huyo kijana ni raia wa Congo? “ Hapana si raia wa Congo .Ni mtanzania ila ananihusu sana na

ndiyo maana ninaomba msaada wako katika suala hili.Tafadhali mheshimiwa rais naomba unisaidie” Ukapita ukimya mfupi kisha Ernest akasema “ Sawa David

nitakusaidia lakini naomba mtu huyo asiwe amejihusisha na jambo lolote la kihalifu” “ Ahsante sana mheshimiwa rais.Nakuhakikishia kijana huyo ni safi na

hana rekodi yoyote ya uhalifu” ‘” Vizuri.Nitakutaarifu suala hili likikamilika” akasema Ernest wakaagana na kukata simu KINSHASA – DRC Alipomaliza

kuzungumza na Ernest simuni,David Zumo akamgeukia Monica “ Monica usihofu tena.Suala hili limemalizika na rafiki yako atakuwa salama.Rais wa Tanzania

ameahidi kulishughulikia haraka iwezekanavyo.Kuwa na amani” akasema David “ Ahsante sana David.Mungu akubariki sana” akasema Monica “ Usijali

Monica.Kuna ule msemo unaosema kuwa ukikaa karibu na uaridi basi utanukia harufu ya uaridi kwa hiyo ukikaa karibu a watu wakubwa hata mambo yako

yatakuwa makubwa na rahisi.Simu moja tu na kila kitu kinakaa sawa” akasema David halafu akamuomba Monica waelekee katika chakula.Waliingia katika

chumba kikubwa cha chakula David akabonyeza kitufe chini ya meza wakaingia wahudumu sita wakiwa na nyuso zenye tabasamu na waliovalia nadhifu

sana.Wakaandaa meza na baada ya dakika kumi meza ikawa tayari wahudumu wakatoka wakamuacha David Zumo na Monica peke yao mle chumbani “ Monica

chakula hiki kimeandaliwa maalum kwa ajili yako” akaanzisha maongezi David wakiwa mezani wakipata chakula.Monica akatabasamu na kusema “ Ahsante

David nashukuru sana.Siwezi kuelezea furaha yangu kwa namna wewe na mkeo mlivyonipokea na kunijali” “ Monica ni kawaida yetu kuwapokea wageni wengi

wanaokuja kututembelea lakini nakuhakikishia kwamba katika wageni wote tuliowahi kuwapokea hakuna ambaye ana umuhimu mkubwa kwetu kama wewe.

Upekee wako ndio uliosababisha hadi muda huu uko humu ndani ya kasri hili ambalo si kawaida kwa mtu ambaye hana ukaribu na rais kuingia.” Akanyamaza

kwa muda kisha akasema “ Monica siku ile nilipowakaribisha wazazi wako kwa chakula na kufahamiana ,halafu ukaondoka baada ya kupata taarifa za rafiki yako

kupigwa risasi ,mimi na baba yako tuliongea mambo mengi makubwa na ya msingi sana” akanyamaza tena akamtazama Monica na kusema “ Nina imani mzee

Benard tayari amekwisha kueleza yale yote tuliyoyaongea” akasema David na Monica akatikisa kichwa ishara ya kukubali kile alichokisema David “ Vizuri.”

Akasema David na baada ya sekunde chache akaendelea. “ Nafahamu sikufanya vizuri kuongea suala kama lile na baba yako kabla ya kuzungumza nawe

kwanza.Nilikwenda nje ya utaratibu na ninaamini utakuwa umekwazika .Nisamehe sana kwa hilo lakini nilifanya vile kutokana na umuhimu wa suala lenyewe
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwangu.Nilitaka kupata msaada toka kwa wazazi wako .Kuna msemo usemao when it comes to love,smart people becomes idiots.Hicho ndicho kilichonitokea

mimi na kujikuta nikifanya mambo kinyume na taratibu na kuzungumza na baba yako badala ya w ewe.lakini nashukuru pamoja na mzunguko huo mrefu

nilioutumia ,ujumbe wangu umefika” akasema David na wote wakaangua kicheko.David akaendelea “ Monica nilichomueleza baba yako ni kitu cha kweli na

kinatoka hapa moyoni” akasema na kunyamaza akamtazama Monica aliyekuwa anamsikiliza kwa makini “ Kutwa nzima ya leo umekuwa na mke wangu

Pauline.Amekueleza mambo mengi na kubwa ni suala lile nililomueleza baba yako.Nilitaka upate kwanza nafasi ya kuonana na kuongea na Pauline na ninaamini

alikueleza kwa kirefu sana kuhusuana na suala hilo kwa hiyo sina haja ya kurudia tena.Monica nakiri kwako kwamba ninakupenda sana zaidi ya ninavyoweza

kukueleza.Nakiri sikuwahi kukufahamu hapo kabla hadi pale jarida la The Face lilipokutangaza kuwa ni mwanamke mrembo zaidi kuliko wote barani Afrika

lakini mara tu nilipoiona picha yako katika ukurasa wa mbele wa jarida lile nilisikia sauti ndani mwangu ikiniambia kwamba huyu ndiye.Naamini Pauline

alikueleza historia yetu na mambo gani tunayapitia katika ndoa yetu.Ni kutokana na changamoyo hizo ndipo Pauline kwa upendo aliponitaka nitafute mwanamke

mwingine nioe ili atuzalie watoto ambao watakuwa ni warithi wetu .Pauline ni mwanamke mwenye upendo wa kipekee kabisa .Sikuwa tayari kwa hilo na

hakuchoka kunisisitiza kuwa nitafute mwanamke nioe.Imepita miaka mitatu sasa toka aliponipa ruhusa hiyo na sikuwa tayari kwa sababu moyo wangu

ulimpenda yeye pekee.Nilipokuona kwa mara ya kwanza katika jarida ,nilihisi kama vile moyo wangu unataka kusimama.Nilipatwa na mstuko

mkubwa.Nilitokea kukupenda ghafla mno kabla hata ya kuonana nawe ana kwa ana.Japokuwa nilikuja Dar es salaam kikazi lakini lengo kuu la safari ile ya kuja

Dar ilikuwa kuonana nawe.

Ninashukuru sana Monica kwa uelewa wako na ukaitika wito pale nilipokuomba tuonane na ninashukuru kwa kuwa leo hii niko nawe hapa ana kwa ana kwa

uhuru zaidi kuliongelea suala hili ” akanyamaza tena halafu akaendelea “ Monica ninarudia tena kukuhakikishia kwamba toka katika sakafu ya moyo wangu

ninakupenda mno na nina nia ya dhati ya kutaka kukuoa uwe mke wangu wa pili.” Akanyamaza kwa sekunde kadhaa akaendelea “ Nafahamu kwako hili si suala

rahisi hata kidogo .Tumefahamiana katika kipindi kifupi ambacho hakijaziti hata wiki moja na tayari ninatanganza ndoa ,hili si jambo jepesi.Ndoa ni jambo

kubwa na ili ukubali kuingia katika ndoa na mtu Fulani inafaa uwe tayari unamfahamu vyema mtu huyo nje na ndani na umpende pia.Kwa upande wangu

japokuwa nimekufahamu katika kipindi kifupi nimejitafakari sana na ninaongea kwa ujasii mkubwa kuwa ninakupenda na niko tayari kuwa nawe.Nafahamu kila

mmoja katika maisha yake ana ndoto zake juu ya mwenzi amtakaye na ninafahamu yawezekana sina vigezo vya mwanaume Yule wa ndoto zako lakini nakuahidi

kufanya kila niwezalo kuwa mwanaume bora kwako.Sina wasi wasi nawe kwani naamini wewe ni mwanamke bora kabisa ambaye kila mwanaume anaota

kukupata kwa hiyo nakuomba Monica tafadhali kubali ombi langu .Nitakuweka juu zaidi ya wanawake wote wa dunia hii.” Akasema David Zumo.Ilimchukua

Monica zaidi ya dakika mbili kufungua mdomo wake na kutamka “ David ninaomba nikiri kwako kuwa toka nilipopata taarifa za suala hili toka kwa baba

nimekuwa silali nikilitafakari.Mkeo Pauline naye amenieleza kwa kirefu kabisa na nimemuelewa lakini moyo wangu unakuwa mzito kufanya maamuzi kwa

haraka.Nashindwa nikujibu nini David ila naomba ufahamu kuwa wewe ni mwanaume bora kabisa.Haihitaji nguvu kubwa kufahamu namna ulivyo mkarimu na

mwenye moyo wa huruma.Pauline amenieleza mambo mengi kuhusu wewe namna unavyompenda na kujali na nimemuamini alichonieleza.Pamoja na hayo yote


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog