haraka.Nashindwa
nikujibu nini David ila naomba ufahamu kuwa wewe ni mwanaume bora
kabisa.Haihitaji nguvu kubwa kufahamu namna ulivyo mkarimu na mwenye moyo wa
huruma.Pauline amenieleza mambo mengi kuhusu wewe namna unavyompenda na kujali
na nimemuamini alichonieleza.Pamoja na hayo yote lakini nasikitika kukueleza
David kuwa bado sina hisia zozote za mapenzi nawe.Sitaki nikudanganye David
labda unipe muda zaidi wa kulitafakari jambo hili” akasema Monica David akaivua
kofia yake yenye manyoya ya Simba na kujifuta jasho kichwani “ Monica sina
maneno mazuri na matamu ya kuulainisha moyo wako au laiti ningekuwa na uwezo wa
kuyawezesha macho yako yaweze kuona namna moyo wangu unavyoteseka juu yako
ungenionea huruma na kulikubali ombi langu.Monica sihitaji
unipende.Ninachohitaji mimi ni kuwa nawe tu.Nipe nafasi Monica nikuonyeshe
namna ninavyokujali na kukupenda.Najua hauna mchumba bado kwa hiyo tafadhali
naomba usininyime nafasi hii.Yawezekana labda unaogopa kuwa mke wa pili lakini
naomba usiogope.Tutafunga ndoa halali serikalini na utakuwa mke wangu wa
halali.Hakuna tatizo kwa upande wa Pauline na tayari amekwisha kuthibitishia
hilo.” Akasema David akainuka na kumshika mkono Monica wakatoka katika chumba
cha chakula wakaelekea sebuleni wakaketi sofani.Mapigo ya moyo wa Monica
yalikuwa yanakwenda kwa kasi ya ajabu “ Monica ninapokutazama machoni najiona
mimi.Ninaiona kesho yangu.Ninaiona kesho ya Congo.Kesho yangu iko juu yako
Monica kwa hiyo naomba usininyime nafasi ya kuiona kesho yangu.Nikubali nikuoe
Monica nikuonyeshe namna ulivyo muhimu kwangu,namna ulivyo muhimu kwa Congo
.Nchi yote ya Congo itakusujudu kama malkia wao.Niruhusu nikupe nafasi hii ya
kuwa malkia wa Congo kwani naamini kutokea kwako atazaliwa mtawala mpya wa
Congo baada yangu kwa hiyo wewe ni mtu muhimu sana kwa nchi hii.Ufungue moyo
wako Monica na niruhusu niingie kama niivyoufungua wa kwangu na kukuruhusu
uingie na utawale.” David Zumo akatamka maneno yale kwa hisia kubwa akiwa
ameishika mikono ya Monica.Walikuwa wamekaribiana sana na maneno yale ya David
yakaonekana kumuingia . “ Kuna sauti kubwa ninaisikia ndani mwangu inaniambia
nimkubali David.Tayari nimekwisha pata picha ya maisha nitakayoishi
nitakapokubali kuolewa na David.Ni maisha ya kifahari mno.Hakuna mwanamke
katika dunia hii ambaye hataki kuishi kama malkia.Nitapoteza kitu gani
nikimkubali David hata kama bado hajaniingia moyoni mwangu? Akajiuliza Monica “
Hakuna chochote nitakachopoteza nikikubali kuolewa na David Zumo.Ngoja tu
nikubali kwani nafasi kama hizi hutokea mara chache sana duniani.Imekuwa ni
kama bahati imeniangukia mimi,sipaswi kufanya mzaha katika jambo
hi.................” Mara Monica akaondolewa mawazoni baada ya kuhisi kitu kama
mkono ukipapasa na kuyatomasa matiti yake.Alistuka sana.Hakuwahi kutomaswa
matiti yake na mwanaume yeyote “ David !!! akasema na kutaka kumsukuma lakini
mikono yeye nguvu ya David ikamshika bara bara “ Monica tafadhali naomba
usihamaki.Nimeshindwa kuvumilia.Najua umekwisha fahamu ninachokihitaji kwako na
ninafahamu hata wewe unahitaji pia jambo hili kwa hiyo naomba Monica unipe
heshima hii” akasema David kwa sauti ya kubembeleza huku akihema haraka
haraka.Monica akashindwa afanye nini kwani tayari David alikwisha onyesha
dhamira ya wazi ya kutaka kufanya ngono.David aliendelea na kuyapapsa maungo ya
Monica na kumfanya ahisi msisimko wa aina yake “ Ni mara ya kwanza ninachezewa
hivi na mwanaume.Nahisi raha ya aina yake.David ananigusa katika sehemu zile
ambazo zinanifanya nipagawe.oh my gosh !!.Leo nimepatikana sina ujanja tena.I
have to do it.Ngoja tu nimuachie afanye kile anachokitaka lakini ukweli utabaki
pale pale kuwa I’m so weak and stupid.Nimejitunza kwa kipindi kirefu lakini leo
nimenasa kwenye mtego kama kinda na siwezi kujinasua.” Akawaza Monica wakati
David akiendelea kumfanyia utundu wa kila aina na kumfanya atoe migumo kwa raha
aliyokuwa anaipata.Alihisi kuhamishwa dunia.Alilainika na hakuweza kufumbua
hata ukope. SEHEMU YA 42 DAR ES SALAAM – TANZANIA Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Ernest Mkasa alipomaliza kuzungumza na David Zumo katika simu
akamgeukia Austin “Austin sasa naomba unisikilize vizuri.” Akasema
Ernest.Akatulia kidogo akamtazama Austin kwa makini na kusema “ Nina kazi mbili
ambazo nataka unifanyie.Kazi ya kwanza kuna mtu Fulani anaitwa Dr Marcelo
amelazwa hospitali ya mtakatifu Lucia.Nataka ukamtoe hapo hospitali kwani kuna
watu wanataka kumuua.Nataka atolewe kimya kimya bila ya mtu yeyote kufahamu na
baada ya kumtoa utamleta hapa kwako atakaa hapa hadi hapo nitakapokupa
maelekezo mengine.” Akasema Ernest na kunyamaza “ Ni nani huyo Marcelo? Nani
wanataka kumuua? Akauliza Austin “ Austin umepewa kazi ya kufanya tafadhali
naomba uifanye.Sihitaji maswali katika jambo hili.” Akasema Ernest “ Mheshimiwa
rais ,nimekuuliza maswali hayo kwa lengo la kutaka kufahamu kwa kina kuhusu
jambo hili.Nataka kufahamu ni akina nani wanaotaka kumuua na kwa nini ili
ninapokwenda huko niwe tayari ninafahamu nguvu ya hao wanaotaka kumuua
Marcelo.Hata hivyo unataka lini kazi hiyo ifanyike? “ Soon as possible” akajibu
Ernest kwa haraka “ kama kungekuwa na uwezekano hata usiku wa leo ungeifanya
kazi hiyo lakini naomba uifanye kesho.Kama kuna chochote utakachohitaji
utanitaarifu” akasema Ernest “ kazi ya pili ambayo ni kubwa” akaendelea “ Kuna
msichana mmoja anaitwa Monica benedict mwamsole ambaye hivi majuzi ametajwa na jarida
moja kubwa la mitindo la The Face kuwa ndiye mrembo kuliko wote Afrika.Enzi za
ujana wangu niliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke mmoja ambaye ni mke wa
rafiki yangu na hivi karibuni mwanamke huyo amekuja kwangu akanieleza kwamba
wakati ule tukiwa katika mahusiano aliwahi kupata mimba yangu ila
akanificha.Mwanamke huyo akadai kwamba Monica ni mwanangu.Hapa nilipo sina
mtoto hata mmoja kwani watoto wangu wote wamekwisha tangulia mbele za haki na
nilipopewa taarifa hizi nilistuka sana na sijataka kuziamini moja kwa moja kwa
hiyo nataka nifanya uchunguzi wangu wa siri kubaini kama kweli Monica ni
mwanangu.Ninataka kufanya kipimo cha vinasaba ambacho kitanipa jibu kama kweli
Monica ni mwanangu .Jambo hili ni la siri kubwa na sitaki mtu mwingine yeyote
alifahamu zaidi yako.Nimekuamini na ndiyo maana nikafanya kila lililo ndani ya
uwezo wangu kuhakikisha ninatimiza masharti yako ili unifanyie kazi hii”
akanyamza na baada ya muda akaendelea. “ Nataka kupata sampuli kwa siri toka
kwa Monica kwa hiyo basi nataka ujenge urafiki wa karibu naye .Nataka kuutumia
ukaribu huo wako na yeye kumfahamu vizuri Monica ili hata kama ikitokea akawa
kweli ni mwanangu iwe rahisi kujenga mahusiano mazuri naye.” Akanyamaza tena
kidogo, akaendelea “ Tukisha ipata sampuli hiyo ,kipimo kitakwenda kufanyika
nje ya nchi.Sitaki kipimo kifanyike hapa nchini kwa kuogopa udanganyifu.Austin
nimekukabidhi jukumu hili lote ulisimimamie wewe mwenyewe na mwisho unipatie
majibu .Nakuomba ufanye kila linalowezekana kufanikisha jambo hili.Chochote utakachokihitaji
katika saula hili niambie nitakupatia.Kama nimeweza kumtoa ndugu yako kifungoni
China siwezi kushindwa jambo lingine lolote.kwa hiyo Austion kaa na utafakari
namna utakavyoweza kulifanikisha suala hili.Narudia tena chochote
utakachokihitaji katika jambo hili utakipata na yale yote niliyokuahidi kuhusu
dada yako yatatekelezwa.Natumai umenielewa Austin” Ukimya ukatanda wa takribani
dakika mbili kisha Austin akasema “ Nimekuelewa mheshimiwa rais.Nitakufanyia
kazi yako ila nina mambo mawili ya kukwambia kabla sijafanya kazi zako”
akanyamaza kidogo na kusema “ Kwanza nataka kukuweka wazi kwamba baada ya
kumaliza kazi zako mbili mkataba wangu na wewe utakuwa umemalizika na
sintapokea tena kazi nyingine yoyote kwa hiyo kama una mawazo ya kunipa kazi
nyingine baada ya hizi yafute kabisa mawazo hayo.” Akanyamaza kidogo halafu
akaendelea “ Jambo la pili nilikuuliza kuhusu Alberto’s ukakiri kuwafahamu japo
wewe si mmoja wao.Nimefurahi kusikia hivyo kwani kuna jambo nataka ulifanye.”
Akanyamaza akameza mate na kuendelea “ Nimekuwa nikifuatilia habari za
Tanzania.Ni siku ya tatu leo katika kila mkoa hapa Tanzania kuna makundi ya
watu wake kwa waume ,wazee kwa vijana wanajiandikisha kwa ajili ya kufanya
maandamano makubwa kuelekea bungeni mjini Dodoma ambako kunatarajiwa
kuwasilishwa muswada wa kutetea haki za binadamu katika kikao kijacho cha bunge
kitakachoanza hivi karibuni.Katika muswaada huo kuna vipengele ambavyo vinataja
kutambua haki za baadhi ya makundi kadhaa ya watu wakiwamo watu wanaoshiriki
mapenzi ya jinsia moja.Muswada huu unazitambua pia ndoa za jinsia moja na kama
haitoshi musaada huu pia unatambua haki ya mwanamke kutoa mimba.Miswada ya aina
hii tayari imekwisha pitishwa kuwa sheria katika nchi zaidi ya ishirini barani
afrika.Lengo ni kuhakikisha nchi zote za Afrika zinakubaliana na mambo hayo
.Imetumika nguvu kubwa kuufikisha muswada huu hapa ulipofika na toka maandalizi
ya muswaada huu yalipoanza kumekuwa na kelele nyingi toka kwa wananchi
wakiupinga lakini viongozi na wewe ukiwemo ,mmeziba masikio na mmeendelea na
mchakato wake kwa kigezo cha manufaa kwa nchi.Mheshimiwa rais ninakueleza haya
yote lakini unafahamu kila kitu kwani umeshiriki pia katika kuubariki muswada
huu uende kujadiliwa bungeni na nina hakika uko tayari kuweka saini yako ili
uwe sheria pindi utakapofikishwa katika ofisi yako baada ya kujadiliwa na
bunge.Mheshimiwa rais wewe na wenzako hamuwezi mkawa sababu ya Tanzania
kulaaniwa kwa mambo mnayotaka kuyafanya kwa hiyo utaitisha mkutano wa dharura
wa watendaji wako kesho na utatangaza kuufutilia mbali muswada huo ,usipelekwe
bungeni na wala usijadiliwe sehemu yoyote ile.” “ Austin.....!!! Ernest akataka
kusema kitu Austin akamzuia “ Naomba usubiri nimalize mheshimiwa rais.” Akasema
Austin “ Kesho hiyo hiyo baada ya kuufuta muswada huo wa haki za binadamu
,jioni utalihutuba taifa na kuwataarifu wananchi kuwa hakutakuwa tena na
muswada huo na utaitumia nafasi hiyo kuitangazia dunia kuwa Tanzania haiko na
haitakuwa tayari kukubaliana na masharti toka kwa taifa lolote kubwa au dogo na
utamke wazi wazi kuwa mapenzi au ndoa ya jinsia moja ni marufuku nchini
Tanzania.Mr president are you readuy for that? Akauliza Austin.Bila kukawia
Ernest akasema “ Austin that’s impossible.Hilo ni jambo lisilowezekana na
ninaomba tusiliongelee hilo kabisa !! akasema Ernest kwa hamaki “ Mheshimiwa
rais naomba nikuweke wazi kwamba utimilifu wa kazo zako utategemea sana na wewe
utakavyolipokea suala hili.Endapo utafanya kama nilivyokueleza nitakufanyia
kazi yako tena kwa muda mfupi sana lakini endapo hautakuwa tayari kutekeleza
hayo maagizo yangu basi sintoifanya kazi yako na nitaamini wewe ni mfuasi wa
Alberto’s ambao ni maadui zangu kwa hiyo na wewe utakuwa mmoja wa maadui
zangu.” Akasema Austin.Ernest akamtazama kwa macho makali na kusema “ Austin
ninakuamini sana na ndiyo maana niko tayari kufanya kila lililo ndani ya uwezo
wangu ili unifanyie kazi yangu vizuri.Nitafanya lolote utakaloniamuru nifanye
lakini hili unalotaka nilifanye kesho ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wangu
na sina mamlaka nalo kwa hiyo siwezi kulifanya” Akanyamaza akamtazama Austin
halafu akasema “ Austin ninaamini mpaka hapa tayari unawafahamu Alberto’s ni
watu wa namna gani.” “ Ndiyo mheshimiwa rais ninawafahamu” “ Basi naomba
nikuweke wazi kuwa wao ndio walioniweka madarakani.” Sura ya Austin ikabadilika
akapandwa na hasira . “ You lied to me.You are one of them!! Akasema Austin kwa
hasira “I’m not one of them,ila walinisaidia nikaingia madarakani kwa
makubaliano ya kuwasaidia katika mambo yao Fulani Fulani.Sikutegemea kama siku
moja wangeweza kuja na muswada kama huu.Siwezi kuufuta muswada huu kwa sababu
tayari nimekwisha weka makubaliano nao kuitumia ofisi yangu kufanikisha mambo
yao na moja ya mambo hayo ni huu muswada unaotarajia kuwasilishwa bungeni hivi
karibuni.Nitakapokwenda kinyume nao I’m dead.These people are powerfull and
mosters.I can’t betray them.Naomba mambo haya tuyaache kama yalivyo na
tuongelee kuhusu yale yanayohusiana na kazi yetu” akasema Ernest “ Hata hili
linanihusu pia.” Akasema Austin na kumkazia macho Ernest kisha akasema “
Alberto’s are my enemies mr President.If you want me to do your job then they
should be your enemies too.” Macho ya Ernest Mkasa yalionyesha woga mkubwa “
Austin hutakiwi kuweka uadui na hawa watu.Kama nilivyokueleza they are
powerfull and monsters.Wako kila sehemu .Wamekita mizizi katika sehemu zote za
muhimu za serikali na hivyo ni vigumu sana kupambana nao.Nakushauri Austin
tafadhali achana kabisa na watu hawa kijana wangu” akasema Ernest “Mzee naomba
nikuweke wazi kitu kimoja .Mimi kutaka kuuawa kule Somalia ulikuwa ni mpango
wao na walitaka kuniua baada ya kuifahamu mipango yao miovu hapa
Tanzania.Niliponusurika kifo niliamua kuachana kabisa na kazi hizi na sikutaka
kujishughulisha nao.Nilichukizwa mno na kitendo kile na ndiyo maana nikaichukia
Tanzania na sikutaka tena kurejea nikaamua kuchukua uraia wa Afrika kusini
ambako ninaishi kwa amani.Uliponimbia nije Tanzania nilikubali kwa sababu ya
mambo mawili kwanza kumkomboa dada yangu na pili niliamua kuja kuwakomboa
watanzania wenzangu dhidi ya mambo machafu wanayofanyiwa na Alberto’s kupitia
viongozi walioweka maslahi yao mbele na kusahau kuwahudumia wananchi.Mheshimiwa
rais nimekuja kupambana na Alberto’s na ninaomba uniunge mkono.Macho yako
yanaonyesha wazi kwamba hufurahishwi na mambo yanayofanywa na Alberto’s lakini
huna namna ya kuweza kuwakatalia kwa sababu ya makubaliano yenu.Mheshimiwa rais
imetosha sasa na umefika wakati wa kuachana nao.Wakati wako ni huu wa kufanya
maamuzi yenye kufaa kwa mustakabali wa taifa letu.Nakuhakikishia mheshimiwa
rais ukishindwa kufanya maamuzi leo na ukakubali taifa likatumbukia katika
laana hii kubwa,siku ukifa kaburi lako litapigwa mawe .Liokoe taifa hili
lisilaaniwe” akasema Austin .Ernest akainamisha kichwa akafikiri kwa sekunde
kadhaa akasema “ Austi sina la kusema zaidi ya kurudia ushauri wangu kuwa
achana na mambo hayo.Kama hutaki ushauri wangu na ukaamua kuendelea na hicho
unachokiita mapambano dhidi ya Alberto’s naomba usinishirikishe tafadhali na
nina wasiwasi sintakuwa na namna nyingine ya kukusaidia.Ninakushauri tena kama
kijana wangu,fanya kazi zangu nilizokuagiza halafu urejee zako afrika ya kusini
ukaendelee na maisha yako ya amani .Usitake kuyaharibu maisha yako kwa kutafuta
ushujaa.” Akasema Ernest .Austin akamtazama kwa makini sana na kusema “
Mheshimiwa rais ,utajisikiaje iwapo ungekuwa na mtoto wa kiume ambaye umemlea
kwa mapenzi makubwa na ukiwa na mategemeo kuwa atakuletea wajukuu lakini badala
yake akageuzwa mke na mwanaume mwenzake? Au utajisikiaje iwapo ikatokea Monica
akawa kweli ni mwanao halafu ukagundua kwamba ameolewa na mwanamke mwenzake?
Ernest akainamisha kichwa akafikiri na kusema “ Ni wazi nitajisikia vibaya na
ninaomba usiku na mchana laana hiyo ipite mbali na familia yangu.Siwezi
kuvumilia upuuzi kama huo!!! Akasema Ernest “ Jinsi utakavyojisikia ndivyo
watakavyojisikia vibaya wazazi ambao watoto wao watafanywa wenzi na wenzao wa
jinsia moja pale tu utakaporuhusu muswada huo ukaingia bungeni na baadae ukatia
saini kuufanya sheria.Tafadhali mheshimiwa rais usikubali jambo hili.Unazo
nguvu za kuhakikisha muswada huu haupelekwi bungeni .Tumia madaraka yako kama
rais” akasema Austin.Ernest akatumia zaidi ya dakika saba kutafakari kisha
akasema “ Austin maneno uliyoyasema ni mazitoi na yameniingia barabara.Ninakiri
kwako kuwa nilifanya kosa kubwa sana kukubali kutumiwa na watu hawa .Ni tamaa
ya urais iliniponza.Kuna mambo mengi mabaya yamefanywa na watu hawa kwa
wananchi ambao niliapa kuwatumikia na ninaumia sana kila ninapoona taarifa za
habari na kusikia kasi ya saratani ya kizazi inaongezeka kila uchao kwa
wanawake kutokana na madawa mengi yanayoingizwa kwa makusudi yanayosababisha
saratani ya kizazi.Lengo hapa ni kupunguza idadi ya watu barani Afrika ili
baadae kusiwe na nguvu kazi na wazungu waje waitawale tena Afrika.Kundi kubwa
la vijana nguvu kazi ya taifa limeathirika na dawa za kulevya.Ninatamani
nifanye kitu lakini mikono yangu tayari imefungwa .Nimekuwa rais kivuli ambaye
ninatumiwa na watu wengine.I cant fight these people so do you.” Akasema Ernest
kwa unyonge “ Mr President nimefarijika kuona kuwa una umizwa na mambo
haya.Naomba usiogope tafadhali.Kuwa jasiri na ufanye leo maamuzi makubwa ambayo
yatakufaya ukumbukwe na vizazi vingi vijavyo.Kuwa rais wa mfano na ufanye nchi
hii iwe nzuri na salama kuishi kwa watoto wa watoto wetu” akasema
Austin.Ilimchukua dakika zaidi ya tatu Ernest kuongea “Austin narudia tena
kusema kuwa mambo uliyoyaongea ni mazito na yenye manufaa makubwa.Nimekuelewa
kijana wangu na niko tayari kufanya maamuzi makubwa na magumu lakini ukae ukijua
kuwa nitakapofanya hivyo unavyotaka nifanye basi tayari mimi na wewe tutakuwa
katika hatari kubwa.Sitaki kukuingiza katika matatizo.Sitaki niwe chanzo cha
maisha yako kuharibika tena” akasema Ernest “ Mheshimiwa rais umesoma faili
langu na tayari umefahamu mambo mengi kuhusu mimi.Siogopi kuingia katika
matatizo na wala maisha yangu kuvurugika.Kwa hiyo usihofu kuhusu usalama wangu
na wako” akasema Austin.Ernest akafikiri tena kwa muda kidogo na kusema “
Austin nitafanya hivyo unavyotaka nifanye lakini kwa sharti moja” “ Sharti gani
mheshimiwa rais? Akauliza Austin “ Nataka unihakikishie kwamba hautarejea tena
Afrika kusini bali utabaki hapa hapa nchini.Austin I need you here to protect
me” Mheshimiwa rais unao ulinzi wa kutosha kwa hiyo sioni sababu ya mimi kubaki
Tanzania” “ Ni kweli Austin ninao ulinzi mkubwa lakini hakuna kati ya walinzi
wangu mwenye uwezo mkubwa kama wewe.Umepata mafunzo ya hali ya juu katika nchi
tofauti tofauti .Ni mtanzania pekee kati ya 10 uliyemaliza na kuhitimu mafunzo
ya operesheni maalum katika chuo cha Navy seal nchini Marekani.”akasema Ernest
“ Mheshimiwa rais nipe muda wa kulitafakari suala hili kwani siwezi kukupa jibu
la haraka haraka kama ninaweza kulikubali ombi lako ama vipi” “ Austin ni wewe
ambaye umenishawishi kuingia katika hii vita kwa hiyo lazima tupambane wote
wawili.You are going to stay here for good.Nitakupatia kila unachokihitaji na
utakuwa mlinzi wangu wa siri.Austin kazi hii huwezi kuikimbia ,haya ndiyo
maisha yako.Yakubali na uyaishi.Mimi kesho nitafanya kama tulivyokubaliana na
nina imani na wewe utatekeleza kwa upande wako” akasema Ernest “ Mheshimiwa
rais ,ahsante kwa kunisikiliza na kunielewa.Kesho nitaanza kufanya kazi
zako.Nitakupa orodha ya vitu nitakavyovihitaji kwa ajili ya kuikamilisha kazi
hizo.Natumai tutakuwa tena na kikao kingine cha kuzungumzia kwa undani kuhusu
vita hii tunayokwenda kuianza.Kwa sasa naomba uende ukapumzike na mimi uniache
nitafakari namna nitakavyofanya kazi zako” akasema Austin akaagana na Ernest
akaondoka “ hatimaye ninarejea tena rasmi katika kazi ambayo sikuwa ninataka
kuifanya katika kipindi cha maisha yangu yote yaliyobakia lakini kama
alivyosema rais kuwa this is my life ,this is my job,this is where I belong.Ni
muda muafaka sasa umefika wa kupambana na Albertos na kuung’oa kabisa mzizi
wake hapa Tanzania.Watu hawa walinifanya nikaichukia nchi yangu na hata kuapa
kutokurudi tena,ninasema safari hii ni ama zao ama zangu.Siwaogopi
tena.Nitapambana nao hadi mwisho wangu.Nashukuru kwa rais kuamua kuniunga mkono
.Endapo kesho atafanya kama nilivyomuelekeza basi litakuwa ni pigo kubwa kwa
Alberto’s.Hawataamini kilichotokea.Wakati wakiwa katika mshangao wakijiuliza
juu ya kilichotokea nitawaondoa mmoja baada ya mwingine.Si kazi nyepesi hii
lakini nitajitahidi kwa nguvu zangu zote na pale itakapobidi nitaomba
msaada.Lazima nipambane nao ,lazima waondoke Tanzania.Hii ni nchi pekee ambayo
wamehangaika kwa miaka mingi kuotesha mizizi yao na walifanikiwa baada ya
kumsaidia Ernest Mkasa kuingia madarakani.Toka hapo nchi imebadilika sana na wamekuwa
wakifanya yale ambayo wameyafanya katika nchi nyingine za afrika na dunia.
Lakini ngoja kwanza niachane na mawazo hayo kuhusu vita na Alberto’s kwa sasa
na nielekeze akili yangu katika kutafuta namna ya kuweza kumtoa Marcelo
hospitali na namna nitakavyojenga ukaribu na Monica” akawaza Austine na mara
akamkumbuka mpenzi wake Maria “ Natakiwa kuwasiliana na Maria nijue maendeleo
yake.Nimekuwa namuwaza kutwa nzima ya leo.Ninampenda sana na moyo unaiuma kwa
kitendo nilichokifanya cha kumdanganya kuhusu kazi iliyonileta Dar es
salaam.Itanilazimu nimueleze ukweli wa kila kitu ili asije huku kwani mambo
yanayokwenda kutokea siku si nyingi ni ya hatari sana kwa usalama wake na siko
tayari kuyaweka maisha yake hatarini.” Akawaza Austin na kwenda kuchukua kompyuta
yake akamtafuta Maria mtandaoni akampigia.Maria akapokea simu “ How’re you my
love.Huwezi jua ni kwa namna gani nimeisubiri simu hii leo.Sijui kama ningeweza
kulala bila kuisikia sauti yako nzuri.Nakupenda sana Austin na ndiyo maana
ninakuwaza mno kuliko kitu kingine chochote.” Akasema Maria na kumfanya Austin
atabasamu “ Hello malaika wangu, umeshindaje leo? Nisingeweza kulala bila kujua
hali yako “ “ Nimeshinda salama mpenzi wangu na hali yangu ni njema sana.Leo
nimeshindwa kusaini ule mkataba ,wanasheria wa Alnoor wanaweka sawa baadhi ya
vipengele ila kesho nina uhakika tutasaini mkataba na baada ya hapo sintopoteza
hata dakika moja ,nitapanda ndege kuja Dar es salaama kukutana nawe mfalme
wangu” Akasema Maria na Austin akajikuta akikosa neno la kusema “ Mbona umekuwa
kimya ghafla Austin? Hutaki nije Dar es salaam? Akauliza Maria.Austin akakohoa
kidogo na kusema “ Uhhmm ! Maria bado unasisitiza kutaka kuja Dar es salaam? “
Ndiyo ninasisitiza Austin.Mbona unaonekana hujapendezwa na mimi kutaka kuja Dar
es salaam?Kuna nini unanificha Austin? Tafadhali kuwa muwazi” akasema
Maria.Austin akatabasamu na kusema “ Hakuna chochote ninachokificha Maria ila
nina wasi wasi na usalama” “ Kama huna unachokificha basi hupaswi kuwa na wasi
wasi.Nitakuja Dar es salaam mara tu baada ya kumalizana na Alnoor.Austin
siogopi hatari yoyote kama kuna lolote baya basi litufike sote kwa hiyo
ujiandae kunipokea kesho kutwa.Nitakutaarifu kesho ni ndege gani nitapanda ili
unipokee uwanja wa ndege” akasema Maria wakaendelea na maongezi mengine na
baada ya saa nzima wakaagana “ Nimeshindwa kumueleza Maria ukweli na hii ina
maana lazima aje Dar es salaam.What can I do? Nifanye nini kumzuia asije? Ulimi
umekuwa mzito kumueleza ukweli na endapo atakuja Dar lazima atagundua
nimemdanganya na ataumia sana kwani mimi ni mtu anayeniamini kuliko hata baba
yake mzazi.Nitaongea na baba yake pengine anaweza akanisaidia kwa namna yoyote
ile kumfanya Maria asije Dar es salaam” akawaza Austin na kuanza kuwaza tena
juu ya majukumu yaliyoko mbele yake “ Monica Benedict Mwamsole ,who is this
woman? Kwa bahati mbaya mimi si mfuatiliaji sana wa habari za mambo haya ya
urembo ndiyo maana simfahamu huyo Monca ni nani hadi kutangazwa kuwa mwanamke
mrembo kuliko wote Afika.Haiwezekani atokee mwanamke mmoja awe mzuri kuliko
mamilioni ya wanawake wa Afrika,awe mzuri kumshinda hata mpenzi wangu
Maria.Mimi naamini Maria ni mwanamke mzuri kuliko wote Afrika na dunia “
akawaza Austin na kuanza kupekua mtandaoni kutafuta t aarifa za Monica. Alipata
picha nyingi za Monica alizoweka mtandaoni na akabaki mdomo wazi “ What a
beautiful woman.!!! She’s an angel..I was wrong,huyu anastahili kabisa kuwa
mrembo kuliko wote afrika.” Austin akajikuta akiongea mwenyewe kwa sauti ndogo
na kuendelea kupitia picha za Monica moja baada ya nyingine halafu akajiegemeza
kitini “ Monica Benedict !!..akasema kwa suti ndogo “ Nilidhani labda ni
mwanamke mwenye uzuri wa kawaida tu lakini kumbe ni mwanamke mwenye uzuri
usioweza kuelezeka kwa maneno.Nawapongeza watu wa jarida la The Face walifanya
kazi kubwa ya kusakanya na kumpata mtu sahihi kuwa malkia wa urembo Afrika.”
Akawaza Austin huku akiendelea kuzitazama picha za Monica “ Mpenzi wangu Maria
ni mzuri sana lakini nakiri hawezi kufikia uzuri wa Monica” Bado picha za
Monica zilionekana kumsisimua mno “ Japokuwa kazi nimekubali kuifanya lakini
nathubutu kukiri ina majaribu makubwa .Mara nyingi huwa sipendi kufanya kazi
ambazo ndani yake kunakuwa na wanawake warembo kama Monica.Binadamu siku zote
ni dhaifu na unaweza ukajikuta umeanguka kishawishini na kushindwa kuitekeleza
kazi yako ipasavyo.Nitajitahidi sana hilo lisitokee.Nakumbuka nliwahi kutumwa
kazi na rais aliyetangulia kabla ya Ernest kuwasaka watu waliotaka kumuua Boaz
na nikajikuta nimezama mapenzini na mtoto wake Maria.Sitaki kilichotokea wakati
ule kinitokee sasa na kusababisha kutetereka kwa mahusiano yangu na
Maria.Ninampenda sana na sitaki kumuumiza.Yeye ndiye sababu ya mimi kuendelea
kuwa hai hadi sasa.Yeye ndiye aliyemshawishi baba yake akalipa kiasi kikubwa
cha pesa walichokitaka wanamgambo wa Alshabaab wakaniachia huru.Ninamuheshimu
sana Maria na siku zote atabaki kuwa mwanamke wa pekee kabisa katika maisha
yangu” akawaza Austin akainuka na kuelekea chumba cha kulaa.tayari umekwisha
kuw ausiku mwingi wa sekunde kadhaa sasa David Zumo alikuwa amepiga magoti
pembeni ya mwanamke mrembo kuliko wote Afrika Monica Benedict Mwamsole
aliyekuwa amelala kifudi fudi huku wote wakiwa watupu sebuleni .David alikuwa
anahema kwa kasi kubwa na jasho jingi likimtiririka.Macho yake aliyaelekeza kwa
mwanamke aliyelala pembeni yake ambaye alikuwa analia kwa kwikwi “ Ni vigumu
kuamini lakini ni kweli.Monica hajawahi kumjua mwanaume na mimi ndiye mwanaume
wake wa kwanza.Huyu ni mwanamke wa kipekee kabisa .Wanawake wanaotunza bikira
zao hadi umri kama huu wa Monica ni wachache mno katika ulimwengu wa sasa.Laiti
ningejua Monica bado ni bikira ningesubiri hadi tutakapofunga ndoa kwani
naamini kabisa hawezi kukataa” akawaza David “ Najisikia fahari kubwa kuwa
mwanaume wa kwanza kumjua Monica.Hii ni heshima kubwa kwangu na lazima
niitunze.Nitamuweka Monica katika nafasi ya juu mno.Nitampa heshima ya kipekee
kabisa mwanamke huyu wa pekee ambaye sikuwahi kuota kama nitaweza kumpata
katika maisha yangu.” Akawaza David huku akiendelea kumtazama Monica aliyekuwa
amejilaza kitandani akilia kwa kwikwi.Akamuinua na kumfuta machozi “ Pole
Monica.Tafadhali nyamaza kulia” akasema David akimfuta Monica machozi “ Najua
umeumia Monica lakini nakuomba usiendelee kulia malaika wangu.” Akasema David
Zumo.Monica akamtazama na kusema “ Umenishawishi tukafanya mapenzi na
umeniondolea bikira yangu ambayo ilikuwa ni zawadi kwa mwanaume wa maisha
yangu” akasema Monica na kuendelea kumwaga machozi “ Monica malaika wangu
usilie tafadhali.Hata mimi ninajilaumu sana kwa hiki kilichotokea.Laiti kama
ningejua mapema ningejitahidi kujizuia lakini tayari imeshatokea kwa hiyo
nakuomba unifanye mimi niwe mwanaume wako wa kwanza.Nifanye mimi niwe mfalme
wako.Monica wewe ni mwanamke wa pekee kabisa kuwahi kukutana nawe.Ni nadra sana
kwa zama hizi kukutana na mwanamke aliyetunza usichana wake hadi kufikia umri
kama wa kwako.Unastahili pongezi na heshima ya kipekee kabisa.Mimi kama
mwanaume wako wa kwanza ninaomba unipe nafasi Monica ili nikupe heshima
unayostahili mwanamke kama wewe.Naomba nikuonyeshe namna ninavyokupenda .Nipe
ruhusa nikuinue juu ya wanawake wote wa dunia hii.Kubali kuolewa nami Monica “
akasema David Monica akaupeleka mkono sirini akautazama, ulikuwa na
damu,akamtazama David na kusema “ Umenitoa bikira yangu ambayo nimeitunza kwa
miaka hii yote kwa ajili ya mwanaume Yule ambaye atakuwa wa pekee
kwangu,mwanaume ambaye nitamkabidhi moyo wangu autunze zaidi ya mboni ya jicho
lake.Bikira hiyo imekuwa ikinipa ujasiri na subira ya kumsubiri mwanaume wa
ndoto zangu .Ni kitu nilichojivunia na kukithamini mno lakini kwa sasa baada ya
kuiondoa nimekua mtu wa kawaida nisiye na thamani tena.Kwa kuwa wewe ndiye
uliyenitoa usichana wangu siwezi kulikataa tena ombi lako la kutaka
kunioa.Ninakubali kuolewa nawe ila nomba yale yote uliyoniahidi yawe ya kweli.”
Akasema Monica.David hakumpa nafasi ya kuendelea zaidi akapagawa kwa jibu lile
la Monica akajikuta amemkumbatia kwa nguvu na kuanza kumporomoshea mabusu
katika sehemu mbali mbali za mwili “ Ahsante Monica.Ahsante malaika wangu kwa
kukubali ombi langu.Sijui nikwambie nini Monica kuhusu furaha niliyonayo kwa
kulikubali ombi langu.Nakuahidi hautajutia uamuzi wako .Nakuahidi nitakupenda
zaidi ya upendo wenyewe.” Akasema David na kumbusu Monica “ Sasa twende
chumbani ukapumzike malaika wangu,siku yetu imekuwa nzuri na njema sana .Kesho
tutakuwa na maongezi mengi zaidi kuhusiana na maisha yetu.” akasema David
akambusu Monica na kumshika mkono akamuinua wakaelekea katika chumba cha
kulala. “ Hiki ni chumba chako cha kulala malkia wa Congo.Panda kitandani
upumzike ewe mzuri wa wazuri” akasema David Zumo akambusu Monica na kutoka mle
chumbani.Monica akaingia bafuni kuoga.Kwa dakika kadhaa alikuwa amesimama
bafuni akitafakari “ Sielewi nini kimenitokea hadi nikajikuta kwa hiari yangu
nikimvulia nguo David.Nahisi huyu jamaa anatumia uchawi kwani mimi ni mtu
mwenye msimamo mkali linapokuja suala la haya ya mapenzi lakini najishangaa
kwani leo nimejikuta mwenyewe nikichojoa nguo na kufanya mapenzi.I’m so weak
and stupid...” akawaza Monica huku akijipiga vibao shavuni “ So this is
it.Bikira yagu imeondolewa na sina tena cha kujivunia.Imenilazimu nikubali
kuolewa na David Zumo .Hata hivyo nikimtazama David anaonekana ananipenda kwa
dhati ya moyo wake na hata mke wake pia amenikubali .Ngoja tu niolewe na David
japokuwa nitakuwa mke wa pili lakini hakuna tatizo kwani Pauline mke wa David
ameridhia jambo hilo “ akaendelea kuwaza Monica huku akioga “ David anaonekana
kuchanganyikiwa kabisa na mimi .Sijui amechanganyikiwa na nini lakini nahisi
lengo lake kubwa yeye na mke wake ni kupata mtoto kutoka kwangu.Sipati picha
hiyo harusi yetu itakuaje.Mhh ..!! mwili wote unanisisimka.Halafu kuna jambo
ambalo bado sijapata muafaka wake.Nikiolewa na David najua atanitaka niishi
hapa Congo karibu naye lakini kama nitakubali kuishi hapa nitaendeshaje program
zangu? Hapana sitaki kuishi Kinshasa ,nitaishi Tanzania” akawaza Monica.Picha
nyingi za haraka haraka zikamjia kuhusiana na maisha atakayoyaishi baada ya
kuolewa na David Zumo.Akatabasamu DAR ES SALAAM – TANZANIA Kijua tayari
kimekwisha chomoza kuashiria mwanzo wa siku nyingine .Austin tayari alikuwa
katika chumba cha mazoezi akiweka mwili sawa kuikabili siku.Alipomaliza kufanya
mazoezi akatoka akaelekea jikoni akafungua mojawapo ya kabati akatoa kitu
Fulani alichokitengeneza mara tu alipoamka asubuhi akakichunguza kwa makini
halafu akakiweka katika boksi na kuliingiza boksi lile katika begi la mgongoni
“ I’m back to work again.Sikutegemea kabisa kama nitarejea tena katika mambo
haya” akawaza na kutoka mle jikoni akaenda bafuni akaoga halafu akarejea tena
jikoni akaandaa stafstahi.Alikunywa chai kwa haraka akiwa amesimama na
alipomaliza akachukua begi lake la mgongoni alimoweka lile boksi lenye kifaa
Fulani ndani yake .Akaenda tena chumbani akafungua sanduku kubwa na ndani yake akatoka
sanduku lingine la kadiri akalifungua.Lilikuwa limesheheni silaha ndogo
ndogo.Akachukua bastora mbili pamoja na vifaa vingine vichache ambavyo
vingeweza kumsaidia.Kabla hajatoka alihakikisha kamera tatu za ulinzi
alizofunga zinafanya kazi vizuri.Kamera zile ndogo lakini zenye uwezo mkubwa
ziliunganishwa na mfumo wa kompyuta ambao uliweza kutuma picha za kila
kilichokuwa kinaendelea moja kwa moja katika miwani maalum aliyoivaa.Mara tu
anapoivaa miwani hiyo na kugusa sehemu Fulani yenye kitu mfano wa doa jeusi
sehemu moja ya miwani hiyo hubadilika na kuanza kupokea picha toka katika
kamera zilizoko nyumbani kwa hiyo kumuwezesha kujua kinachoendelea .Hii ilikuwa
teknolojia ya hali ya juu sana “ It’s perfect.” Akasema na kutoka akafunga
nyumba na kuelekea katika maegesho zilikoegeshwa gari tatu mpya .Akachagua moja
ambalo aliona lingemfaa kwa shughuli anayokwenda kuifanya kisha akaondoka “
Filimbi tayari imepulizwa sasa kinachofuata ni kuingia vitani.” Akawaza akiwa
garini na mara akamkumbuka mpenzi wake Maria. “ Leo atasaini mkataba na Alnoor
na kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba mara tu atakapomaliza masuala
yaliyompelekea Dubai ,moja kwa moja atapanda ndege kuja Tanzania.Ni wiki ya
tatu sasa hatujaonana na imekuwa ni kama miezi mitatu kwetu .She loves me a lot
na hata mimi ninampenda mno zaidi ya ninavyoweza kueleza lakini suala la yeye
kuja dar es salaam bado siliafiki kabisa kwani ni hatari mno kwake.mambo
yatakayotokea ndani ya siku chache zijazo ni mambo ya hatari na sitaki mwanamke
nimpendaye kuliko wote aingie katika hatari.Nasikitika kwamba sina cha kufanya
kumzuia asije Tanzania.Nilishindwa kumueleza ukweli kwa hiyo lazima atakuja dar
es slaam” akaendelea kutafakari akiwa amesimama katika taa za kuongozea magari.
“ Kuna kitu kimoja ninachoweza kufanya ili kumzuia Monica asije dar .Ni kuacha
kuwasiliana naye.Nikifanya hivyo hata kama akija Dar hatajua namna ya kunipata
na ataondoka kurejea afrika ya kusini.Ni bora nikafanya hivyo kwa ajili ya
usalama wake yeye mwenyewe ingawa najua ataumia na atanichukia sana lakini sina
ujanja.Nitamuelewesha huko mbele ya safari naamini atanielewa.” Akaendelea
kuwaza Austin na sura ya Monica ikamjia Sura ya binti malaika huyu inanijia
kichwani kila mara.Ngoja kwanza nishughulikie kazi ya kwanza ya kumuondoa hospitali
Marcelo na baada ya hapo nitajipanga wa ajili ya Monica.” Lango la kuingilia
hospitali ya Mt Lucia lilikuwa wazi,watu na magari walikuwa wakipita bila
kikwazo chochote.Hakukuwa na ukaguzi wowote japokuwa walikuwepo walinzi
waliovalia sare za kampuni binafsi ya ulinzi .Kulikuwa na magari mawili mbele
ya Austin yakiingia mle hospitali .Austin kwa haraka haraka akachunguza ulinzi
ulivyo pale getini akatabasamu “ Hakuna ulinzi wowote wa maana hapa getini.Hawa
walinzi wako hapa kutangaza kampuni yao tu” akawaza wakati akivuka geti na
kukutana na kibao kilichomuelekeza sehemu ya kuegesha gari.Ilipata saa tatu na
dakika ishirini na tayari eneo la maegesho lilisheheni magari .Austin akachukua
kofia nyeusi akavaa pamoja na miwani ile ya kielektroniki yenye kuweza kufanya
mambo kadhaa kwa wakati mmoja.Akahakikisha bastora zake zimekaa vizuri kisha
akachukua begi akashuka.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika katika hospitali
hii kubwa iliyokuwa na bango kubwa lenye ramani ya hospitali ikielekeza namna
ya kufika katika sehemu mbali mbali za hospitali ile .Taratibu huku akiyasoma
mazingira Austin akakamata njia iliyoelekea ziliko wodi za kulaza wagongwa.. “
Hospitali ya kisasa sana hii.Ina miundo mbinu mizuri lakini kuna kasoro moja tu
kubwa,hakuna usalama” akawaza Austin akiwa amezifikia wodi . akakutana na bango
lingine lililoelekeza namna mpangilio wa wodi ulivyo ukianzia na zile wodi za
watu maalum.Kwa kufuata maelekezo ya lile bango akafika katika wodi za watu
maalum.Kulikuwa na pilika pilika nyingi eneo hili hivyo hakuna yeyote aliyekuwa
na muda wa kumfuatilia Austin.Alichunguza eneo la chumba alimolazwa Dr Marcelo
na kuondoka akaelekea katika jengo la mapokezi.Lilikuwa ni jengo kubwa la
ghorofa nne.Watu walikuwa wengi katika jengo hilo na Austin akajumuika nao huku
akiyasoma mazingira ya mle ndani yalivyo.Alitoka mle ndani akaelekea katika
bustani nzuri iliyokuwa karibu na jengo la mapokezi.Begi lake akaliweka pembeni
na alioneka kama mtu aliyekuwa akisubiria huduma.Akapita kijana muuza magazeti
akanunua gazeti moja akaanza kusoma huku akichunguza mazingira
yalivyokaa.Alipohakikisha hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa anamtilia shaka
akalifungua begi lake na katika lile boksi lililokuwa na kifaa ndani yake
akabonyeza kidude Fulani kilichokuwa mithili ya saa kikaanza kuandika namba kwa
haraka haraka,akalifunga begi na kuliweka pembeni na kwa kutumia mguu wake
akalisogeza katika maua halafu akaangaza tena pande zote lakini hakukuwa na mtu
yeyote aliyekuwa anamfuatilia.Taratibu akainuka akaingia tena katika jengo la
mapokezi halafu akatoka na kuanza kuelekea ziliko wodi.Alipokaribia chumba cha
Marcelo akatoa kitu Fulani mithili ya simu akabonyeza namba kadhaa na mara
ukatokea mlipuko mkubwa karibu na jengo la mapokezi.Kizaa zaa kikubwa kikaibuka
hapo hospitali watu wakaanza kukimbia hovyo kunusuru maisha yao. Taharuki ile
ndiyo aliyokuwa anaihitaji Austin ili afanikishe kazi yake.Akachomoka kama
mshale hadi katika chumba cha Marcelo.Hakukuwa na daktari yeyote mle chumbani
,alikuwemo Dr Marcelo pekee akiwa hajui afanye nini.Marcelo akastuka sana kwa
namna Austin alivyoingia mle chumbani “ Are you Marcelo? Akauliza Austin “ yes
“ akajibu Marcelo kwa wasiwasi “ Good.My name is Austin and I’m here to take
you out of here.Naomba ufuate maelekezo yangu” akasema Austin “ Wewe ni nani?
Umetumwa na nani? “ Marcelo ninao muda mchache sana wa kufanikisha zoezi la
kukutoa hapa kwa hiyo nahitaji ushirikiano wako.” Akajibu Austin huku akimshika
mkono Marcelo na kumtaka ainuke “ Siendi kokote bila kufahamu ni nani
aliyekutuma” Marcelo akagoma “ What ??..akauliza Austin “ Najua umetumwa uje
unichukue ukaniue.Naomba uniulie hapa hapa ila huko unakotaka kunipeleka
siendi” akasema Marcelo. Austin akavua kofia na kumtazama Marcelo “ Nisikilze
kaka.Kazi yangu ni kukuondoa hapa na kukupeleka sehemu salama kwa hiyo sina
muda wa mabishano na wewe.Kuna mambo mawili ya kuchagua ,aidha ufuate maelekezo
yangu nikutoa hapa au nikutoe humu kwa nguvu” akasema Austin kwa sauti ya ukali
wakaendelea kutazamana “ Are we going or you want me to use force? Akauliza
Austin.Marcelo akatikisa kichwa ishara ya kukubaliana na Austin Haraka haraka
Austin akamuinua Marcelo akamuweka begani na kuchungulia nje ambako bado
taharuki ilikuwa imetanda na watu wakikimbia hovyo kunusuru maisha
yao.Akaangaza pande zote kuhakiki usalama “ It’s clear” akasema taratibu na
kuingia katika gari lake akaondoka eneo lile akipishana na magari mawili ya
zima moto yaliyofika kwa haraka sana huku magari matatu ya polisi yaliyosheheni
askari yakifika kwa haraka “ Nini kimetokea hapa? Nimesikia kishindo kikubwa
kama mlipuko na watu wakaanza kukimbia huku wakipiga makelele na ghafla
ukatokea chumbani kwangu.Who are you? Nani kakutuma uje unitoe hapa hospitali?
Unahusika na kilichotokea hapa? Akauliza Marcelo lakini Austin hakumjibu kitu
akaendelea kuendesha gari kwa umahiri kuhakikisha hakuna mtu anayemfuatilia “
C’mon brother I deserve to know who are you? Who sent you and where are you
taking me? Akauliza Dr Marcelo .Bado Austin hakumjibu chochote “ Huyu mtu ni
nani? Ametumwa na nani aje anitoe pale hospitali?Ananipeleka wapi? Maswali haya
yalimuumiza sana Kichwa Dr Marcelo “ Kuna mtu mmoja tu ambaye nilimueleza
tatizo langu na nikamuomba anisaidie ambaye ni Monica.Inawezekana huyu jamaa
ametumwa na Monica au ametumwa na wale jaama wanaotaka kuniua? Lakini
nikimtazama kwa makini haonyeshi kama ana lengo la kuniua.Kama ni Monica ndiye
aliyemtuma sijui nitamshukuruje kwani nisingemaliza siku mbili bila
kuuawa.Asubuhi ya leo niliwaona watu wao wawili wakiongea na daktari na baada
ya hapo daktari akaja akanipima na kuondoka.Kilichoniweka hai hadi sasa ni kwa
sababu nilijifanya siwezi tena kuongea.Natakiwa niikimbie nchi kwani endapo
nitaendelea kukaa humu nchini lazima watanisaka na kuniua.” Akawaza Dr Marcelo
wakati gari likikata mitaa ya jiji huku akiwa hajui ni wapi alipokuwa
anapelekwa. “ Nimewastua na mlipuko ule wa fataki wamechanganyikiwa
kabisa.Kimetokea kizaa zaa cha kutisha pale hospitali” akawaza Austin huku
akitabasamu kwa mbali “ Kazi ya kwanza kati ya mbili za rais
nimeimaliza.Imekuwa ni kazi nyepesi mno zaidi ya nilivyotazamia japokuwa
nimetumia nguvu kubwa kidogo lakini nimefanya vile ili kuwapoteza lengo watu
waliokuwa na nia ya kumuua Marcelo.Ninaamini kabisa kama kweli huyu jamaa
alikuwa anataka kuuawa basi lazima kuna watu waliowekwa pale hospitali
kumfuatilia na nisingeweza kumtoa pale kirahisi bila ya kuonekana lakini kwa
njia hii niliyoitumia naamini hata wao kama walikuwepo lazima walikimbia
kunusuru maisha yao.Nasikitika kishindo kile cha mlipuko kinaweza kuwa
kimesababisha madhara kwa baadhi ya wagonjwa hasa wenye matatizo ya moyo lakini
sikuwa na namna nyingineya kufanya ili kumuokoa Marcelo.”akawaza Austin
KINSHASA – DRC Muziki wa ala uliosikika kwa sauti ya chini ulimfanya Monica
aote ndoto nzuri .Alikuwa katika uwanda mpana wenye nyasi nzuri za
kijani.Vijito vya maji vikitiririka katika kila kona ya uwanda huu wa kuvutia
mno.Ndege wa rangi mbali mbali wakubwa wa wadogo walikuwa wanaruka .Upande wa
juu watu waliovalia nadhifu walikuwa wamejipanga katika mstari wakiimba na
wengine walikuwa pembeni wakipiga vyombo vya muziki.Ulikuwa ni muziki mtamu
ulioburudisha.Pembeni na pale alipokuwa amekaa kulikuwa na wanawake zaidi ya
sita wakiwa tayari kumuhudumia kwa chochote akitakacho.Tabasamu halikukauka
.Alikuwa amevaa taji la dhahabu pamoja na vito vingi vyenye kung’aa vya thamani
kubwa.Alikuwa anameremeta .Ghafla akastushwa na kengele iliyolia akakurupuka
toka usingizini.Kulikuwa na mtu mlangoni.Haraka haraka akajifunga taulo na
kwenda kuufungua mlango akakutana na sura yenye tabasamu ya mwanamama mmoja wa
makamo akamsalimiana kujitambulisha. “ naitwa Anna.Ni muhudumu mkuu wa rais
katika jumba hili.Nimefurahi kukuona malkia wa wangu.Kuna chochote unahitaji
asubuhi hii? “ hata mimi nimefurahi kukufahamu Anna.Nitakujulisha baadae endapo
nitahitaji chochote” akajibu Monica na Anna akaondoka kwenda kuendelea na
shughuli zake.Monica Akakaa kitandani na kuanza kutafakari kilichotokea usiku
uliopita.” “Nilifanya ujinga mkubwa sana jana.Nilimkubalia David kirahisi
kufanya mapenzi bila hata kutumia kinga.Oh my gosh ni vipi kama ana magonjwa?
Akawaza na kushika kichwa “ Lakini hapana David ni mtu muungwana asingeweza
kukubali kufanya nami mapenzi bila kinga hali akifahamu kuwa ana matatizo.”
Akajipa moyo na kutabasamu baada ya kuikumbuka ndoto ile nzuri aliyoiota. “
Ilikuwa ndoto nzuri ajabu.Sijawahi kuota ndoto nzuri kama ile katika maisha
yangu.Je ndoto ile inaashiria maisha yangu yatakavyokuwa huko mbeleni? Kama
nilichokiota katika ndoto ndivyo maisha yangu yatakavyokuwa basi sikufanya
makosa kukubali kuolewa na David Zumo.” Akawaza Monica halafu akamkumbuka
Marcelo “ Marcelo..Hali yake ikoje sasa hivi?Jana David aliongea na rais wa
Tanzania na akamuahidi kumsaidia kumtoa pale hospitali.Natamani kujua kama
zoezi hilo limekwisha fanyika au vipi.Nikionana na David nitamuuliza kuhusu
jambo hili” Akiwa bado amekaa kitandani huku akiwaza mambo mengi kengele ya
mlango ikalia akaenda kufungua na kukutana na David Zumo “U hali gani Monica?
Akauliza David Zumo aliyekuwa amesimama mlangoni akiwa amevaa mavazi yale
aliyokuwa ameyavaa usiku yaani ngozi ya chui na kofia ya manyoya ya Simba. “
Hallow David” akasema Monica huku akitabasamau na kuona aibu kwa mbali.David
akaingia ndani “ Umeamkaje malaika wangu? Akauliza “ Nimeamka salama kabisa
,sijui wewe” “ Hata mimi nimeamka salama kabisa.Vipi maendeleo yako?Una hali
yoyote ya maumivu nimuite daktari? “ Ninahisi maumivu kwa mbali lakini
nitatumia dawa za kutuliza maumivu tu na nitapona.” Akasema Monica “ Samahani
sana Monica.” “ Usiogope David.Jambo hili limeshatokea na limepita kwani hata
kama isingekuwa ni wewe basi angefanya mwanaume mwingine.Kwa sasa tuachane na
suala hilo tuangalie mengine ya msingi lakini awali ya yote kuna kitu nataka
kuuliza” “ Uliza Monica” “ jana tulipofanya mapenzi hukutumia kinga.Una hakika
uko salama? David Zumo akatabasamu na kusema “ Nilitegemea ungeniuliza swali
kama hilo.Naomba nikuhakikishie kwamba usiku wa jana ni usiku wa kwanza kwangu
kufanya mapenzi na mwanamke ambaye si mke wangu.Toka nimefunga ndoa na Pauline
sijawahi kujihusisha na mahusiano na mwanamke mwingine yoyote zaidi ya mke
wangu.Mimi na Pauline tunapendana sana na tunaaminiana mno” akasema David
wakatazamana kwa muda kisha David akasema “ Monica ni wakati wa kujiandaa kuna
mgeni atakuja kuungana nasi hapa leo.Ukishaoga na kujiandaa pale ukutani kuna
vitufe vitano,utabonyeza kitufe namba moja na watakuja watumishi kukuhudumia
kisha baada ya hapo tutaungana kwa mlo wa asubuhi akasema David na kutoka mle
chumbani akampa nafasi Monica kujiandaa “ Tayari maisha yangu yamebadilika.Monica
wa jana si Monica wa leo.Ama kweli maisha yana maajabu makubwa.Sikuwahi kuota
kama siku moja nitaishi maisha makubwa kama haya” akawaza Monica na kuingia
bafuni kuoga.Alipomaliza kuoga akafuata maelekezo aliyopewa na David akabonyeza
kitufe namba moja na haikumalizika dakika moja wakaingia wanawake zaidi ya sita
kwa ajili ya kumuandaa Monica.Kila mmoja alikuwa na kazi yake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment