Search This Blog

Monday, 19 December 2022

QUEEN MONICA (2) - 4

  






Simulizi : Queen Monica (2)
Sehemu Ya Nne (4)


na kusema “ Nilitegemea ungeniuliza swali kama hilo.Naomba nikuhakikishie kwamba usiku wa jana ni usiku wa kwanza kwangu kufanya mapenzi na

mwanamke ambaye si mke wangu.Toka nimefunga ndoa na Pauline sijawahi kujihusisha na mahusiano na mwanamke mwingine yoyote zaidi ya mke

wangu.Mimi na Pauline tunapendana sana na tunaaminiana mno” akasema David wakatazamana kwa muda kisha David akasema “ Monica ni wakati wa

kujiandaa kuna mgeni atakuja kuungana nasi hapa leo.Ukishaoga na kujiandaa pale ukutani kuna vitufe vitano,utabonyeza kitufe namba moja na watakuja

watumishi kukuhudumia kisha baada ya hapo tutaungana kwa mlo wa asubuhi akasema David na kutoka mle chumbani akampa nafasi Monica kujiandaa “ Tayari

maisha yangu yamebadilika.Monica wa jana si Monica wa leo.Ama kweli maisha yana maajabu makubwa.Sikuwahi kuota kama siku moja nitaishi maisha

makubwa kama haya” akawaza Monica na kuingia bafuni kuoga.Alipomaliza kuoga akafuata maelekezo aliyopewa na David akabonyeza kitufe namba moja na

haikumalizika dakika moja wakaingia wanawake zaidi ya sita kwa ajili ya kumuandaa Monica.Kila mmoja alikuwa na kazi yake. DAR ES SALAAM –

TANZANIA Zaidi ya dakika nne sasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest Mkasa alikuwa amesimama katika dirisha la chumba chake akitazama

nje.Agatha mke wake akamfuata taratibu “ Ernest darling” akasema na kumshika kiunoni. “ Kuna jambo gani linakusumbua? Nimekuona kwa siku mbili tatu

umebadilika sana na ninakufahamu vizuri lazima kuna kitu kinakisumbua akili yako.Niambie tafadhali kama kuna kitu kinakuumiza kichwa .” Ernest akageuka

na kumtazama mkewe akamshika mabegani na kusema “ hakuna tatizo lolote Agatha,niko kawaida.Kwa leo nina kikao cha dharura cha baraza la mawaziri,kuna

jambo la dharura la kujadili ndiyo maana unaniona katika hali hii.Kikao hakitakuwa chepesi” akasema Ernest na mke wake akaonekana kustuka “ Kuna mambo

gani ya dharura mnakwenda kujadili katika kikao hicho? Akauliza Agatha “ Siwezi kukueleza kwa sasa hadi hapo baadae” akasema Ernest na mke wake

akamtazama kwa macho makali.Hakuonyesha kufurahishwa na jibu lile “ Ernest toka lini umeanza kunificha mambo? Kila kinachoendelea katika ofisi yako

umekuwa unanitaarifu na kuniomba ushauri lakini nashangazwa leo umeamua kunificha mambo hayo ya dharura mnayokwenda kuyajadili.Au umepata mshauri

mwingine unayemuamini zaidi yangu? Akauliza Agatha

“ Agatha si hivyo unavyodhani.Nitaongea nawe baadae kwa kirefu lakini kwa sasa ngoja niwahi ofisini” akasema Ernest na kuchukua mkoba wake akatoka na

kumuacha mke wake akishangaa “ This is strange!!.Whats going on? Haijawahi kutokea hata mara moja Ernest akagoma kunieleza jambo.Kabla ya kikao

chochote anachokwenda lazima mimi na yeye tukae tujadili lakini leo amegoma kabisa .Kuna kitu kinaendelea ambacho nahitaji kukifahamu” akawaza Agatha na

kuchukua simu yake akazitafuta namba za makamu wa rais akampigia. “ hallo Madam first lady” akasema Muhsin “ Muhsin ,hukunipa mrejesho wowote kuhusu

lile jambo nililokuomba ulifuatilie jana” akasema Agatha “ Agatha sikuona sababu ya kukupa mrejesho kwa sababu vijana niliowatuma hawakuweza kugundua

jambo lolote.Katika ule muda uliosema kuna makabidhiano yatafanyika,kuna gari liliingia katika ubalozi wa Chia lakini ililikuwa ni gari la mizigo na

inaonekana kuna mzigo uliwasilishwa pale ubalozini.MUkasha naye aliwasili hapo ubalozini lakini alikuwa peke yake na baada ya muda akatoka akiwa peke

yake ” “ Are you sure Muhsin? Akauliza Agatha “ Ndiyo Agatha.Ninawamini vijana niliowatuma katika kazi hiyo” Agatha akafikiri kidogo kisha akasema “ Ok

Muhsin una taarifa ya kinachokwenda kujadiliwa katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri alichokiitisha rais leo? “ hapana Agatha,sina taarifa zozote

kuhusu yanayokwedna kujadiliwa katika kiako hicho.” Akasema Muhsin na ukimya mfupi ukapita,Agatha akasema “ Muhsin lakini jitahidi uwe mchunguzi wa

kila jambo Kwa sasa tuko katika hatua muhimu sana ya kufanikisha mambo makubwa kwa hiyo hatupaswi kulala.Kila mtu acheze nafasi yake vizuri.Utanieleza

kitakachojadiliwa katika hicho kikao kwani Ernest amegoma kabisa kunieleza chochote” “ sawa madam nitakujulisha usihofu “ akasema muhsin,Agatha akakata

simu. “Ninamfahamu vizuri Ernest kuliko mtu yeyote ,kuna jambo zito linalomsumbua na analifanya siri.Nitajua tu kinachoendelea “akasema Agatha. Ernest

mkasa aliingia ofisini kwake lakini alihisi kichwa chake kizito kufanya kazi yoyote. “ What I’m going to do today,i s very dangerous but I have to do it because

it’s the right thing .Nimechoshwa na kupelekwa pelekwa kama gari bovu.Maneno aliyoyaongea Austin jana yalinichoma sana na siwezi tena kuendelea kuwa

daraja la watu wachache kufanikisha mipango yao haramu.Lazima nisimame kama rais niwapiganie wananchi wangu wanyonge walionichagua.Kwa kuanzia

muswada wa haki za binadamu ninaufuta kuanzia leo.Nafahamu kitendo cha kuufuta muswada huo kutawastua sana hawa watu na wataanzisha mapambano na

mimi na kwa namna walivyo na nguvu ninaweza kuuawa kama alivyouawa rais aliyenitangulia .Alikataa kushiriki katika mipango yao na kilichofuata

wakamuua.I’m so scared.These people are monsters”akawaza Ernest na kufungua kompyuta yake akafungua sehemu alikohifadhi picha za Monica alizozitoa

mtandaoni akaanza kuzitazama moja baada ya nyingine akajikuta akitabasamu. “Ninaomba majibu yatoke na kunihakikishia kuwa Monica ni mwanangu kwa
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
sababu kile ninachokifanya sasa hivi ni kwa ajili yake.Kama atakuwa kweli ni mwanangu nitamlinda kwa kila namna nitakavyoweza kwani wabaya wangu

wakifahamu kuwa ni mwanangu basi watamtumia kama fimbo ya kunipigia.Lakini sina wasiwasi kwani Austine yupo na atakubali kubaki Tanzania kwani yale

yote aliyoyataka nimeyatekeleza.Nimetokea kumuamini sana Austine ni kijana mwenye akili nyingi na mwenye ujuzi wa hali ya juu.Alitaka kuuliwa kwa sababu

tayari alikwisha kuwa kikwazo kwa watu na hasa Alberto’s.Sifahamu aligundua nini hadi wakataka kumuua lakini naamini ni jambo zito.Austin amenikosha sana

kwa namna anavyojiamini” ******************* Austin aliwasili salama nyumbani kwake akifungua mlango wa gari akamshusha Dr Marcelo na kumsaidia

kutembea hadi sebuleni. “Damn ! you are so heavy !!”akasema Austin na kumsaidia Marcelo kuketi sofani .Akaenda jikoni na kurejea na chupa mbili za maji

moja akampatia Marcelo. “Thank you”akasema Marcelo. “You are welcome “akajibu Austin huku akifungua chupa na kunywa maji.Marcelo naye akanywa maji

halafu Austin akauliza , “How do you feel?unasikia maumivu yoyote?” “Ndiyo ninahisi maumivu katika zile sehemu zilizoshonwa”akasema Marcelo.Austin

akainuka akaenda chumbani na kurejea na paketi ya dawa. “Kunywa hizo zitakusaidia kupunguza maumivu wakati utaratibu wa kumpata daktari

ukiendelea”akasema Austin. Marcelo akamtazama Austin kwa makini na kuuliza , “Who are you? “I’m Austin” Marcelo akamtazama Austin kwa makini na

kusema, “Nafurahi kukufahamu Austin lakini nahitaji kufahamu kwanini niko hapa?” “Marcelo sina jibu la kukupa kwa swali lako.Kazi yangu niliyopewa

ilikuwa kukutoa hospitali na kukuleta hapa kwa hiyo sifahamu chochote kuhusu wewe.Nitafurahi endapo hutaniuliza swali lolote kama hilo bali usubiri mtu

aliyenituma kazi atakapofika naamini utakuwa na muda mzuri wa kuzungumza naye na kumuuliza maswali.Kwa sasa naomba nikupeleke ukapumzike nina kazi

za kufanya”akasema Austin akamsaidia Marcelo kunyanyuka akampeleka kupumzika. “Kazi ya kwanza nimemaliza,sasa nataka kutafuta namna nitavyo jenga

urafiki na Monica na kumfanya aniamini”akawaza Austin. “Kuna kitu kimoja ambacho kinaweza kuniweka karibu na Monica ambacho ni matindo.Nimesoma

taarifa zake jana usiku mtandaoni na kufahamu Monica anamiliki kampuni ya kubuni mitindo mavazi iliyojizolea umaarufu na soko kubwa afrika

mashariki.Kitu kingine nilichokifahamu kuhusu Monica ukiacha mitindo ni mtu anayependa sana kujitoa kwa jamii.Ana taasisi yake ya kusaidia watu wenye

matatizo hususani watoto na wazee wasiojiweza.

Hizo ni sehemu mbili pekee ambazo naweza kuzitumia kutengeneza urafiki na Monica. Aidha mitindo au kusaidia jamii” akachukua chupa yake ya maji

akamalizia maji yote yaliyokuwamo na kuendelea kutafakari “Sina utaalamu wowote na masuala ya mitindo inaweza ikanichukua muda kidogo kujifunza na

kuifahamu vyema fani hii.Sina muda huo wa kujifunza nadhani niachane na mitindo na niingie katika masuala ya kujitoa kwa jamii.Hata hivyo nikiamua niingie

kwa kutumia upande huo wa kusaidia jamii itanilazimu niwe na kiasi kikubwa cha pesa.Nitazungumza na rais atakapokuja leo usiku aniwezeshe kiasi cha

kutosha cha pesa .Kazi hiyo ya kujenga urafiki na Monica nitaianza rasmi kesho ila kwa siku ya leo nataka kwenda kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali

muhimu nitakavyovihitaji kama vile kompyuta zenye kasi na uwezo mkubwa,nahitaji mavazi mazuri ya gharama ili kujiweka nadhifu kila mara,nahitaji simu

kadhaa kwa mawasiliano.Kwa ujumla kuna vitu vingi vya lazima nitakavyovihitaji.” Akawaza Austin na kulikumbuka tukio lililotokea hospitali ya St Lucia. “

Naamini umakini ulikuwa mkubwa na sikuacha chochote kinachoweza kunitambulisha kama mhusika wa tukio lile.Naamini hata wakifanya uchunguzi

hawataweza kunipata” akawaza Austin KINSHASA – DRC “ Monica samahani kama nitakufuru lakini lazima nikiri kuwa Mungu ana upendeleo .Kuna watu

amewapendelea uzuri wa kipeke kabisa.Mmoja wa watu hao ni wewe .Una uzuri ambao hauelezeki kwa maneno.Itoshe tu kusema kwamba uzuri wako ni wa

kipekee.Nitamshukuru Mungu kwa siku zote kwa kunikutanisha nawe.” Akasema David “ Ahsante sana David lakini Mungu hana upendeleo .Kwake sote ni sawa

hakuna mzuri wala mbaya.” Akasema Monica .David akatabasamu akamshika mkono wakaelekea katika chumba cha chakula kwa ajili ya kupata kifungua

kinywa.Kabla hawajaanza kupata kifungua kinywa mlango ukagongwa wakaingia watu wanne walioonekana ni wana usalama na nyuma yao akafuata Pauline

mke wa David Zumo.Monica alihisi aibu lakini Pauline alionekana kuwa mchangamfu na uso wenye tabasamu.Akasalimiana kwanza na David Zumo halafu

akamfuata Monica wakasalimiana na wote wakajumuika kwa mlo ule wa asubuhi.Baada ya kupata kifungua kinywa wakatoka wakaelekea katika bustani nzuri

iliyokuwa pembeni ya ziwa dogo.Ulinzi ulikuwa mkali sana kulizunguka jumba lile la kifahari la David huku eneo lote likiwa na ukimya mkubwa sana.Ni sauti

za ndege ndizo zilisikika.Waliketi katika viti vya kifahari vyenye nakshi za dhahabu “ Monica napenda kutumia fursa hii kukukaribisha tena kwa mara nyingine

katika himaya hii ya kifalme.Ninasema ya kifalme kwani muda si mrefu sana nitatawazwa kuwa mfalme wa kwanza wa Congo.Nadhani tayari nimekwisha

kueleza kuhusu jambo hii.” Akasema David huku akitabasamu na kumgeukia mkewe Pauline “ Pauline leo ni siku ya furaha kubwa kwetu kwani hatimaye

maombi yetu yamejibiwa .Monica amekubali ombi la kuolewa nami.”akasema David na kwa furaha Pauline akainuka na kumkumbatia Monica kwa furaha

“ Ahsante Monica .Ahsante sana kwa uamuzi wako huu wa busara.Nakuhakikishia hautajutia uamuzi huu uloufanya.Binafsi nimetokea kukupenda sana na

nimeridhia kwa moyo mweupe uwe mke wa pili.Ninampenda David sana na ninataka awe na furaha katika maisha yake na mimi sina uwezo wa kukamilisha

furaha yake kama nilivyokueleza jana.Kuja kwako kutaifufua upya furaha yetu.Nakuahidi tutaishi kwa amani na upendo kwani jambo hili ni mimi ndiye

niliyekuwa nalihitaji sana” akasema Pauline huku machozi ya furaha yakimtoka “ Kwa niaba ya Pauline “ akasema Daniel “ Napenda nikushukuru sana Monica

kwa kukubali ombi letu.Kama alivyosema Pauline maisha yetu yatakuwa mazuri na yenye furaha zaidi na Mungu akijalia kupitia kwako tunaweza kumpata

mrithi wangu .Kwa hiyo Monica wewe ni mtu muhimu sana kwetu na kutokana na umuhimu huo hatuna tena haja ya kuendelea kuvuta muda zaidi.Taratibu za

ndoa hii zitaanza mara moja .Kesho nitakuwa na maongezi na baraza la wazee wa Congo na nitawafahamisha kuhusu suala hili.Baada ya hapo nitatuma rasmi

ujumbe Tanzania kwa wazazi wako kuja kuanza taratibu za uchumba na baada ya hapo tutatangaza ndoa.Sitaki jambo hili lichukue muda mrefu toka sasa.Nataka

nitakapotawazwa kuwa mfalme wa kwanza wa Congo tayari tuwe tumefunga ndoa.Kuhusiana na sherehe za ndoa hiyo nitamuachia Pauline kwani yeye ni

mtaalamu sana katika mambo hayo” akasema David.Uso wa Monica ulionyesha wasi wasi kidogo. “ Monica uso wako unaonyesha wasi wasi ,usiogope mpenzi

kila kitu kitakuwa kizuri.Hakuna kitakachoharibika” akasema Pauline “ Pauline kuna kitu kinanitatiza kidogo.Ninajiuliza je raia wa Congo watanipokea na

kunikubali? David akatabasamu na kusema “ Usihofu Monica.Watu wangu wananipenda na wanapenda ila ninachokipenda mkuu wo kwa hiyo hata wewe

watakupenda na kukuheshimu kama malkia wao” akasema David na wote watatu wakatabasamu wakaendelea na maongezi yaliyokuwa marefu yenye furaha

yaliyotawaliwa na vicheko DAR ES SALAAM – ANZANIA Agatha mkasa mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa ofisini kwake amejiegemeza

kitini huku mkono wake mmoja ukiwa shavuni,simu yake ikaita akaichukua haraka na kutazama mpigaji alikuwa ni makamu wa rais Muhsin

Abdulkareem.Haraka haraka akabonyeza kitufe cha kupokelea “ Hallow” akasema “ Agatha nimekupigia kukujulisha kuwa kikao kimemalizika muda si mrefu na

kilichotokea huwezi kuamini.Kila mtu hapa bado yuko katika mshangao ” “ Nini kimetokea Muhsin? Akauliza Agatha kwa wasi wasi “ Rais ameufuta ule

muswada wa haki za binadamu uliotarajiwa kuwasilishwa bungeni katika kikao kijacho” “ No ! that’s not true!! He cant do that !! Akasema Agatha “ It’s true

Agatha.Kulikuwa na mvutano mkali sana na kama ujuavyo karibu baraza lote la mawaziri tuliubariki muswada ule kwa hiyo tulijitahidi kwa kila namna

tuwezavyo kupinga maamuzi ya rais lakini yeye ndiye mwenye kauli ya mwisho na tukajikuta tukishindwa kumzuia asiufute.” akasema Muhsin “ Bado siamini

kama Ernest anaweza akafanya kitu kama hicho.Tafadhali Muhsin nieleze ukweli.Ernest ninayemfahamu mimi hawezi kufanya jambo hilo.” “ Ni vigumu
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuamini Agatha lakini huo ndio ukweli wa kilichotokea.Mpaka sasa hakuna anayeamini lakini hicho ndicho kilichotokea.Ernest wa leo siye Yule mwenzetu

tunayemfahamu.Amekuwa ni mtu mwingine tofauti kabisa.Tumepata pigo Agatha.Tumerudishwa nyuma hatua ishirini” akasema Muhsin.Uso wa Agatha

ulishindwa kuzuia kuonyesha mshangao na hasira alizopata kutokana na taarifa ile ya makamu wa rais. “ This is unbelievable.Why he did that? Nini kimemuingia

Ernest na kumfanya achukue maamuzi haya ? Nani kamshawishi afanye hivi? He betrayed us.!! Dah !! ni vigumu sana kuamini” akasema Agatha Agatha

nimekupigia kukupa taarifa hizo ili uwataarifu wakuu kilichotokea.” akasema Muhsin “ What am I going to tell them? Akauliza Agatha “ The truth..tell them

everything” akajibu Muhsin na kumfanya Agatha avute pumzi ndefu na kusema “ I think you know what happens to traitors” “ Yes I know.Ernest must die”

akajibu Muhsin. “ Na hii ina maana kwamba una nafasi kubwa ya kushika nafasi ya urais pindi Ernest akiondolewa” “ Yes I know that” akajibu Muhsin “ Ouh

Ernest ,Ernest nani amemshawishi akafanya jambo hili la kipuuzi wakati anajua kabisa kitakachotokea.? Akawaza Agatha na katika macho yake ikaonekana

michirizi ya machozi “ Muhsin ahsante kwa taarifa.Tutawasiliana baadae” akasema Agatha na kukata simu.Alihisi kuchanganyikiwa “ Whats going on? Kitu gani

au nani amembadilisha Ernest?

 Naamini lazima ipo sababu kubwa na lazima niijue.Kwa hiki alichokifanya Ernest kitaifanya nchi itikisike kwani amevunja kiapo chake na

ametusaliti.Ninampenda Ernest ,nimetoka naye mbali lakini kwa hili alilolifanya hata mimi sintakuwa na huruma naye.Hatuna huruma kwa wasaliti.Nguvu

kubwa imetumika katika kuhakikisha sheria ile inafika bungeni na kupitishwa na Ernest ameshiriki katika mchakato wake toka mwanzo,lakini kitendo cha

kutugeuka katika hatua za mwishoni ni sawa na uhaini na adhabu ya msaliti yeyote anayepatikana miongoni mwetu ni kifo.Ernest amekitafuta kifo chake

mwenyewe na hakuna namna ya kumsaidia,he must die.Nchi hii tayari tumewekeza nguvu kubwa na kufanikiwa kushika zile sehemu zote za muhimu na

muswada huu ulikuwa na umuhimu mkubwa sana kwetu lakini Ernest tayari ameonekana kuwa kikwazo .Hatuhitaji vikwazo vyovyote katika kutekeleza

malengo yetu kwa hiyo Ernest lazima aondoke” akawaza Agatha akiwa na hasira zisizoelezeka aada ya kumaliza kikao cha dharura cha baraza la mawaziri,rais wa

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest Mkasa akaendelea na ratiba yake ya siku ambapo alikutana na mabalozi wa mataifa mbaimbali pamoja na wageni

wengine waliomtembelea ikulu.Rais alimuagiza mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu asambaze taarifa katika vyombo vyote vya habari ili viwatangazie watanzania

kuwa atalihutubia taifa ifikapo saa mbili kamili za usiku. Ilipofika saa moja za jioni rais akarejea katika makazi yake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya hotuba

atakayoitoa kwa taifa usiku.Hakutaka mtu mwingine yeyote amuandalie hotuba kama ilivyozoelekea ,hakutaka jambo analotaka kulieleza livuje.Tayari mke wake

bi Agatha alikwisha rejea nyumbani kitambo na toka aliporudi alikuwa amejifungia chumbani .Ernest alipoingia chumbani alimkuta mkewe anaongea na simu na

mara tu alipomuona mumewe,akakatisha maongezi na kumtazama mumewe kwa hasira.Walitazamana kwa sekunde kadhaa bila kusemeshana halafu Ernest

akauvunja ukimya “ Natumai tayari umekwisha sikia kilichotokea” Agatha akainuka akamsogelea Ernest “ What have you done Ernest? Akauliza huku amekunja

sura kwa hasira.Ernest hakujibu kitu akabaki anamtazama “ What have you done you fool!! Akasema Agatha na ghafla sura ya Ernest ikabadiika.Akapandwa na

hasira “ Na iwe mwanzo na mwisho kunidharau kiasi hiki “ akasema Ernest kwa hasira “ yes you are a fool Ernest.Kwa nini umefanya jambo la kijinga kama

hili? Sikuwahi hata mara moja kufikiri kuwa unaweza kuwa mjinga kiasi hiki.Nini kimekubadilisha Ernest? Nani amekudanganya?

Nimetangaza vita lakini naamini nitashinda kwani ninafanya jambo sahihi kwa nchi na watu wake.Siko tayari tena kuona taifa likiangamia kwa kupitia mikono

yangu.I must stand up and fight .I’m doing this for Monica.Sitaki watoto wa mtoto wangu waje kuishi katika taifa ambalo nimeshiriki katika kuliharibu.It’s time

to make things right.Bado sijachelewa ninayo nafasi ya kufanya mabadiliko “ akawaza Ernest halafu akaanza kuandika hotuba yake. Aliandika machache

atakayoyazungumza ,akaipitia tena hotuba yake na alipohakikisha imekamilika akatoka mle katika chumba cha kusomea akaenda chumba cha kulala.Mke wake

hakuwepo chumbani.Juu ya meza kulikuwa na karatasi yenye ujumbe “ Stop what you are trying to do.You are going to turn the country upside down.Usithubutu

kuhutubia taifa usiku wa leo” Ulikuwa ni ujumbe toka kwa Agatha.Ernest akaichana chana karatasi ile na mara taratibu akasikia mlango ukifunguliwa.Akageuka

akajikuta akaitazamana na watu wawili waliovalia suti nyeusi na kila mmoja alikuwa na bastora mkononi iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti.Ernest

hakuwafahamu watu wale na hakuwahi kuwaona hata mara moja.Anawafahamu walinzi wake wote lakini jamaa hawa waliosimama mbele yake ilikuwa ni mara

ya kwanza kuwaona.Alihisi kutetemeka mwili akajikaza asionyeshe woga wa aina yoyote

“ Hey ! who are you?? Akauliza Ernest kwa ukali “ Huna haja ya kutufahamu mheshimiwa rais.Tumesimama hapa mbele yako kwa heshima kubwa kukutaarifu

kwamba usithubutu kulihutubia taifa usiku wa leo.Hii ni amri na hakuna kuipuuza.Endapo ukipuuzia basi unajua nini kitatokea.Hatuna maneno mengi kwa leo

kwani tayari ujumbe umefika na sisi tuaondoka” akasema mmoja wao na wote wakaingiza bastora zao katika makoti wakafungua mlango na kuondoka

wakimuacha Ernest akiwa bado amesimama akitetemeka .Alihisi miguu kuishiwa nguvu akakaa kitandani “ Vita imeanza.Nilitegemea mambo kama haya lazima

yajitokeze na kweli yameanza.Alberto’s tayari wamekwisha weka mizizi yao kila sehemu na wanaweza wakafanya jambo lolote muda wowote wautakao na ndiyo

maana watu wale wameweza kuuvuka ulinzi wote wa ikulu hadi wamefanikiwa kuingia katika chumba cha rais.Huu ni udhaifu mkubwa sana wa idara ya

usalama .Sintomueleza mtu juu ya hiki kilichotokea lakini lazima nichukue hatua za haraka.Watu wale wangeweza hata kuniua bila ya walinzi wangu kuwa na

habari.Nitamueleza Austin jambo hili ili kwa pamoja tujue namna ya kufanya.” Akawaza na kujifuta jasho jembamba la uoga lililomtoka “ Wamenitetemesha

kweli wale jamaa lakini pamoja na hayo usiku wa leo lazima nilihutubie taifa.Najua hawawezi kuniua kwa sasa kwani bado wanajiuliza sababu ya mimi
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuchukua maamuzi yale” Akawaza Ernest na kuwaita mkurugenzi wa idara ya mawasiliano ikulu na mlinzi wake mkuu akawapa maelekezo ya kuhakiki usalama

katika ukumbi wa habari ikulu. ufuatia agizo la rais waandishi wote wa habari wakatolewa nje ,ukumbi ukakaguliwa na wakaruhusiwa kuingia mmoja mmoja

huku wakikaguliwa .Baada ya kuhakikisha ukumbi uko salama ,rais akataarifiwa kuwa sasa anaweza kulihutubia taifa.Ernest mkasa akajitazama katika kioo

akarekebisha tai yake na kuvuta pumzi ndefu “ I must do this.Litakalotokea na litokee tu.” Akawaza Ernest akatoka mle chumbani na kabla ya kuingia katika

chumba habari akaandaliwa muonekano wake na alipokuwa tayari akaruhusiwa kuingia katika chumba cha habari “ Please help me God ! Help me do the right

thing for this country” akaomba kimya kimya huku akitembea kuingia katika chumba cha habari.karibu vituo vyote vikubwa vya redio na televisheni

vilisimamisha matangazo yao kupisha hotuba hii ya rais iliyokuwa inasubiriwa sana na wananchi Milango ya chumba cha habari kilichokuwa na ulinzi mkali

sana ikafunguliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akajitokea akaenda kuketi katika kiti alichoandaliwa.Tofauti na ilivyozoeleka kuwa hotuba ya

rais huwa imeandaliwa safari hii aliitoa karatasi mfukoni aliyoiandaa yeye mwenyewe na kuanza kuisoma “ habari za usiku huu ndugu watanzania wenzangu”


 “ Awali ya yote ninapenda nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuja mbele yenu na kuongea nanyi kuhusiana

na masuala kadhaa muhimu kwa taifa letu.Kuna mambo kadhaa makubwa kwa taifa letu ambayo yamenilazimu nije mbele yenu leo” akanyamaza halafu

akaendelea “ Kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja sasa tumekuwa katika mchakato wa kuandaa muswada wa haki za binadamu .Uandaaji wa muswada huo

umekuwa na changamoto nyingi na kubwa ni kupingwa kutoka kila kona na makundi mbali mbali ya wananchi,viongozi wa dini n.k.Ndani ya muswada huo kuna

vipengele kadhaa vinavyopigiwa kelele sana na wananchi ambavyo vinatambua haki za makundi ya watu wanaojihusisha na mapenzi na ndoa za jinsia moja.Vile

vile kuna haki ya kutoa mimba pamoja na mambo mengine kadhaa ambayo yanakwenda kinyume kabisa na tamaduni zetu na hata mafundisho ya dini zetu.”

Akanyamaza tena halafu akaendelea. “ Kumekuwa na shinikizo kubwa toka kwa nchi tajiri , zikizitaka nchi zote za afrika kuhakikisha kwamba zinapitisha sheria

za kutambua haki kadhaa za binadamu na hapa wanalenga makundi hayo niliyokwisha yaeleza.Nchi nyingi za Afrika tayari zimekwisha pitisha sheria hiyo na

chache ikiwemo Tanzania bado hatujafanya hivyo japokuwa sisi tulikuwa katika mchakato wa kuupeleka bungeni muswada wa sheria hiyo ili kutimiza matakwa

hayo ya nchi tajiri.Mchakato wa kuandaa muswada huo umekamilika na unategemewa kuwasilishwa katika kikao kijacho cha bunge lakini kumekuwa na

shinikizo kubwa toka kwa wanachi,wazee kwa vijana,wake kwa waume wakipinga muswada huo kupelekwa bungeni.Katika kila mkoa kumeanzishwa kampeni

kubwa za kupinga muswada huu na tayari makundi ya watu wameanza kujiandikisha kwa ajili ya kuelekea bungeni Dodoma kuupinga muswada huo”

akanyamaza kidogo na kuendelea “ Binafsi kama rais wenu nimekuwa kimya nikijaribu kulitafakari suala hili kwa kina na kusikiliza maoni ya watu mbali mbali

,viongozi wa dini n.k na leo hii nimefanya maamuzi yafuatayo 1. Nimeona muswada huo hauna tija kwa taifa letu bali lengo lake ni kuibomoa jamii yetu kwa

kutimiza matakwa ya mataifa makuwa ambayo yametutaka tufanye hivyo kwa kisingizio cha misaada.Taifa letu limejengwa katika misingi na tamaduni

zake.Waasisi wetu wametuachia taifa lenye harufu nzuri linalopendwa na kuheshimika lakini tunataka kulifanya linuke uvundo kwa mambo haya ya hovyo

tunayotaka kuyabariki.Mimi kama rais wenu siko tayari kuwa sehemu ya laana hiyo kwa hiyo natangaza kuwa nimeufuta muswaada huo na kuufunga kabisa

mjadala wake.Sitaki kusikia kuanzia sasa mtu au kikundi cha watu wakiendeleza mjadala huu.Badala yake serikali itapeleka bungeni muswada wa kutambua

vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au utoaji mimba au utumiaji wa madawa ya kulevya ni kosa la jinai na yeyote atakayekutwa akifanya mambo hayo afungwe

gerezani.Kwa hiyo ndugu zangu hakuna tena haja ya maandamano kwani sauti zenu tayari zimesikika.” Akanyamaza na kuendelea 2.

 Kulipa uzito suala la nililolizungumza hapo juu,nimeamua kutengua uteuzi wa waziri mkuu na kulivunja baraza la mawaziri .Sababu kubwa iliyonifaya nivunje

baraza la mawaziri ni utendaji kazi usioridhisha.Katika kikao kijacho cha bunge nitawasilisha jina la waziri mkuu mpya na wabunge watalipigia kura na baada ya

kuidhinishwa na bunge mimi na huyo waziri mkuu mpya tutaunda baraza jipya la mawaziri.Ninawaomba ndugu zangu watanzania tuendelee kuwa watulivu

katika kipindi hiki ambacho taifa linapitia katika majaribu makubwa.Tushikamane na tuliombee taifa letu lizidi kuwa imara na salama Mungu ibariki Afrika

Mungu ibariki Tanzania Ahsanteni kwa kunisikiliza Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya Muungano wa tanzania akamaliza hotuba yake akakunja karatasi zake

akaziweka katika mfuko wa koti akainuka na kuzungukwa na walinzi wake akaondoka.Alipotoka ndani ya chumba kile cha habari akamuelekeza mlinzi wake

mkuu Evansi aweke vijana tayari kwani anaondoka muda si mrefu kuelekea hotelini kwake Ernest akaingia chumbani kwake akakaa kitandani,akavuta pumzi

ndefu “ Oh thank you lord.” “ I did it.Nimefanikiwa kulihutubia taifa na ninaamini hotuba hii itafanikiwa kuleta utulivu nchini.Hotuba hii naichukulia kama

tamko la vita .Kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni pigo lingine kubwa kwa Alberto’s kwani karibu mawaziri wote ni watu wao.Nitaendelea kuwaondoa katika

kile sehemu walikootesha mzizi wao.Hii ni vita ngumu na ya hatari na ninapaswa kujilinda sana pamoja na kumlinda Monica.Kama kweli ni mwanangu

nitamlinda kwa nguvu zote.”akawaza wakati akibadili mavazi kwa ajili ya kuelekea hotelini kwake. Alipobadili mavazi akaondoka kuelekea hotelini.Kichwa

chake kilijaa mawazo mengio mno.Alipofika hoteini akaelekea katika chumba chake na kumuita Mukasha “ Mheshimiwa hotuba yako imekuwa gumzo kila

mahali.Nimekuwa nafuatilia mtandaoni watu wote hawaamini kilichotokea.Unastahili pongezi mheshimiwa kwa maamuzi haya ya kishujaa

uliyoyafanya.Unapongezwa na kila mwananchi.Kwa hiki ulichokifanya mheshimiwa rais kinakusafishia njia ya kupita kirahisi katika uchaguzi ujao.Hautakuwa

na haja ya kufanya kampenzi kubwa” akasema Mukasha.Ernest akatabasamu kwa mbali na kusema “ Mukasha sifikirii tena kuwania urais kwa kipindi kingine.” “
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mheshimiwa rais ni mapema mno kutoa tamko kama hilo.Wewe bado ni rais mwenye nguvu na wanachi wanakupena na kukukubali sana” akasema Mukasha “

Mukasha tayari nimekwisha fanya maamuzi kwamba sintogombea tena katika kipindi kingine.Nitakapomaliza kipindi changu sitaki tena” “ Kwa nini umechukua

maamuzi hayo mheshismiwa rais? Bado una nguvu sana kisiasa .Tafadhali nakushauri mheshimiwa rais usiwaze jambo kama hilo.Unategemewa sana kukivusha

chama katika uchaguzi ujao.Wewe ni ng........” “ Naomba nikukatishe Mukasha mimi si mwanasiasa na wala si chama kilichoniweka madarakani kwa hiyo chama

hakipaswi kunitegemea mimi nikivushe katika uchaguzi ujao” akasema “ Mheshimiwa rais najaribu sana kutaka kukuelewa lakini nashindwa” akasema MUkasha

“ Huwezi kunielewa Mukasha.Tuachane na hayo nimekuita hapa kukueleza jambo moja muhimu kuwa hotuba ile niliyoitoa leo ni tamko la vita “ “ Vita na nani

mheshimiwa rais? Akauliza Mukasha “ Siwezi kukueleza sasa hivi lakini nataka ufahamu kuwa kwa hivi sasa wewe ni mtu pekee kati ya watu wanaonizunguka

ninayekuamini.Please don’t evey betray me.I need you so much in this.Hata ikitokea kwa gharama ya uhai wako usimueleze mtu yeyote kuhusu Austin.Mukasha

kuna mambo makubwa yanaendelea hivi sasa na nitakufahamisha wakati mwingine”

“ Mheshimiwa unaniogopesha” akasema Mukasha hapana Mukasha,sikuogopeshi ila huo ndio ukweli.waandae vijana tunaenda kuonana na Austin” akasema

Ernest KINSHASA – DRC Wahudumu waliokuwa wanamremba Monica walimaliza kazi yao na kuondoka.Monica akasimama mbele ya kioo akajitazama namna

alivyopendeza akataasamu “ I hope I’m doing the right thing.Nimeshindwa kabisa kulishinda jaribu hili na kumpa David mwili wangu.Sikuwa nimepanga

kufanya mapenzi kabla ya ndoa lakini kwa David nimeshindwa kujizuia.Nahisi labda David kuna nguvu anatumia kunilainisha kwani I’m not the same Monica

anymore.Kila anachokisema David ninajikuta nakubali.Ninajishangaa kwa namna nilivyobadlika.” Akawaza Monica “ Kingne ni kwamba baada ya kufanya

mapenzi jana leo nahisi hamu kubwa ya kufanya tena.Naona kama vile David anaanza taratibu kuniingia akilini.Ngoja tu niolewe naye kwani anaonekana ni zaidi

ya mwanaume yule niliyekuwa namuhitaji katika maisha yangu.Siw.....” Monica akatolewa mawazoni na mlango uliofuguliwa akaingia David Zumo ambaye uso

wake ulikuwa na tabasamu kubwa baada ya kumuona Monica,akamfuata akamshika mkono akaubusu. “ Monica uzuri wako siwezi kuuelezea.Ninajiona ni

mwanaume mwenye bahati kubwa sana kukupata malaika kama wewe.Ninakupena sana Monica na sipati maneno mazuri ya kukueleza namna ninavyokupenda”

akasema David na kumshika Monica mkono akamketisha na kumbusu akaanza kumpapasa maungoni “ David una haraka sana.Huna sababu ya kuwa na haraka

.Mimi tayari ni wako ” Akasema Monica “ Nitashindwaje kuwa na haraka Monica mbele ya mwanamke mrembo kuliko wote duniani” Akasema David “ Monica

narudia kusema kuwa inawezekana sina hata kigezo kimoja cha mwanaume Yule umtakaye katika maisha yako lakini nakuahidi kuwa nitajitahidi kuwa

mwanaume bora kabisa kwako.Mimi si mkamilifu ni mdhaifu kama wengine lakini naomba unichukulie hivyo hivyo nilivyo pamoja na madhaifu yangu.Mimi ni

mtawala wa nchi hii lakini wewe ni mtawala wangu.Nataka unitawale.Niamuru chochote nitakutii.” Akasema David kwa sauti ya taratibu na kwa hisia

kubwa.Monica akabaki anamtazama bila kusema chochote “ Ama kweli huyu jamaa amebarikiwa sauti nzuri ya kushawishi.Haya maneno aliyoyaongea

yameniingia hadi moyoni na kunisisimua mno.Hapa nilipo nahisi kama vile ninavutwa na sumaku.Halafu mhh...” Monica akastuka kidogo na kuyaelekea macho

yake katika maeneo nyeti ya David ambayo yalionekana kukasirika .Ngozi ile aliyoivaa David haikuweza kuzuia kuonyesha namna ikulu kulivyochachamaa

Oh y gosh !! ..” akawaza Monica na kutabasamu.David akagundua kuwa tayari Monica ameona kilichotokea. “ Monica nilikueleza hapo awali kuwa naomba

unichukulie na madhaifu yangu na hili ni mojawapo ya udhaifu wangu kwako.Kila nikuonapo napatwa na msisimko wa ajabu sana na kushindwa kujizuia hali

hii kunitokea.Naamini sintakuwa kero kwako.Lakini naomba niweke wazi kwamba si kila wakati hali hii hunitoea bali ni pale tu ninapokuwaza au nikiwa karibu

yako kama hivi.Monica ni wazi umeiteka akili yangu na kwa sasa ninakuwaza wewe tu.Sikuwahi kutokewa na hali hii hapo kabla na hata mke wangu Pauline

hakuwahi kuipeleka mbio akili yangu kama ilivyotokea kwako.” Akasema David na kunyamaza akamtazama Monica.Walitazamana kwa zaidi ya sekunde kumi na

kila mmoja alionekana kama vile kuna kitu anataka kumueleza mwenzake.David akaushika mkono wa Monica na kusema “ Monica nahitaji kujua wewe

unajisikia vipi ukiwa karibu nami kama hivi? Unahisi chochote? Unahisi msisimko wowote ? Nieleze tafadhali nahitaji sana kujua” Monica akamtazama David

usoni kwa makini na kusema “ David nitakudanganya nikikwambia kwamba ninahisi chochote juu yako kwa sasa.Ni mapema mno kwa hilo.Tumekutana na

kufahamiana kwa muda mfupi kwa hiyo bado sina hisia zozote ila naomba jibu hili lisikukatishe tamaa kwani kadiri siku zinavyosonga na tunavyozidi kuwa

karibu zaidi kwa mbali naanza kuhisi mabadiliko,nahisi kama vile kuna sumaku inanivuta kwako zaidi.” Akasema Monica Uso wa David Zumo ukajenga

tabasamu kubwa “ Monica maneno yako yananisisimua mno na kuufanya mwili wangu wote utetemeke.Monica narudia tena kusema kwamba ninajiona ni

mwenye bahati kubwa kuliko wanaume wote kwa kukupata mwanamke kama wewe.Nataka suala la ndoa yetu liende haraka .Natak kila niamkapo asubuhi niwe
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
pembeni yako.oh Monica siwezi kuvumilia tena.Tafadhali ....” Akasema David na taratibu akambusu Monica busu ambalo lilionekana kuitibua akili ya

Monica,akapatwa na msisimko wa aina yake ,akajikuta akianza kuhema haraka haraka .David Zumo ambaye alionekana mjuvi sana wa mambo yale akaitumia

vyema nafasi ile kwa kuanza utundu wake.Monica ambaye bado alikuwa mgeni katika ulimwengu huu wa mapenzi alimuachia David nafasi ya kuutawala uwanja

.Alihisi raha ya ajabu ambayo hakuwahi kuipata hapo kabla David Zumo aliridhika na maandalizi aliyoyafanya na bila kupoteza muda filimbi ikapulizwa na

mtanange ukaanza.


DAR ES SALAAM - TANZANIA Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa katika staili yake ya kubadili muonekano ili asitambulike

kirahisi aliwasili katika nyumba anayoishi Austin.Kama ilivyokuwa kwa siku iliyotangulia Austin aliwataka wale wote waliokuwa wameongozana na Ernest

wabaki nje ,akaingia ndani na rais pekee “ Austin do you have anything to drink in here? Akauliza Ernest .Austin akamtazama na kuuliza “ Unahitaji kinywaji

gani? “ Anything strong” akasema Ernest .Austin akaenda jikoni ambako aliweka chupa kadhaa za pombe kali akachukua chupa moja kubwa ya pombe kali na

kurejea sebuleni “ Rickot !!! .akasema Ernest na kutabasamu baada ya kuiona pombe ile aliyopewa na Austin “ Mtengenezaji wa pombe hii anaitwa Pineck

Rickot raia wa ufaransa mwenye asili ya Urusi.Mvinyo huu umewahi kushinda tuzo kadhaa kubwa kama pombe bora kabisa duniani.Ahsante Austin kwa mvinyo

huu” akasema Ernest na kumimina katika glasi akanywa wote na kufumba macho “ It’s one of the strongest whysky in the world” akasema Ernest .Austin

hakujibu kitu “ Do you smoke ? akauliza Ernest “ No !! akajibu Austin Toka katika mfuko wa koti Ernest akatoa mkebe ambao ndani yake ulikuwa na sigara

akatoa moja akaiwasha na kupuliza moshi mwingi “ Hii inaita Gurkha Black dragon.Hii ni sigara ya bei ya juu zaidi duniani.You can try one” akasema Ernest “

No thank you “ akajibu Austin. Ernest akavuta mikupuo kadhaa kisha akasema “ How’re you Austin ? “ I’m ok “ Austin akajibu “ Umepata mahitaji yote? “

Usijali mzee nimepata kila kitu” “ Good.” Akajibu Ernest a kuvuta tena mkupuo mmoja akageuza shingo na kutazama sebule yote “ Natumai utakuwa

umetazama katika luninga hotuba niliyoitoa usiku huu” akasema Ernest “ Ndiyo mzee nimetazama.Hongera sana .Ni mwanzo mzuri.Umeingia katika historia ya

dunia kama rais shujaa.Kitendo hiki ulichokifanya leo kimefuta yale mabaya yoye uliyoyafanya kwa wananchi na kila raia huko aliko anakupongeza kwa ushujaa

huu.Hakuna aliyetegemea hata mimi sikutegea kama ungekuwa na ujasiri mkubwa wa namna hii.Ahsante mheshimiwa rais kwa kuyasikiliza mawazo yangu”

akasema Austin.Ernest akamimina whysky katika glasi na kugugumia yote akafumba macho kwa sekunde kadhaa na kuusiklizia ukali wa ile pombe halafu

akavuta mkupuo mmoja wa sigara na kusema “ It wasn’t easy my son”


“ I know “ akajibu Austin “ Austin tuna maongezi marefu usiku wa leo lakini kabla hatujaongea chochote nataka unipe ripoti kuhusu kazi zangu.Kuna

maendeleo yoyote? Halafu nilipewa taarifa kwamba kulitokea mlipuko katika hospitali ya Mt Lucia hebu nieleze una husiana nao? Akauliza Ernest.Bila

kupepesa macho Austin akajibu “ Mheshimiwa rais ninahusika na jambo hilo.Mimi ndiye niliyetega hicho kinachodaiwa ni mlipuko.” “How could you do that

Austin? Huoni kuwa unajenga mazingira ya kujulikana? Ni vipi kama ukifanyia uchunguzi na ukagundulika? Vipi kama ulichukuliwa na kamera za ulinzi ?

Akauliza Ernest “ mheshimiwa rais kwanza naomba nikueleweshe kuwa mlipuko ule haukuwa bomu bali ni fataki .Ni kama vile unavyoona milipuko katika

filamu huwa si mabomu halisi kama wengi wanavyodhani kwa hiyo ni kitu ambacho kisingeweza kuleta madhaa yoyote makubwa zaidi ya mstuko kwa baadhi ya

wagonjwa .Nililazimika kutumia njia hii ili kuleta taharuki pale hospitali kwani bila kufanya vile nisingeweza kuikamilisha kazi ile kwa ufanisi na kwa

wakati.Ulinieleza kwamba Marcelo alikuwa anataka kuuawa kwa hiyo ninaamini watu waliokuwa wanataka kumuua lazima walikuwepo hapo hapo hospitali

kwa hiyo kitendo nilichokifanya cha kusababisha taharuki pale hospitali kilinipa nafasi ya kumchukua Marcelo kirahisi kwani hakuna aliyekuwa na muda wa

kumfuatilia mwenzake .Kila mmoja alikuwa anahaha kuokoa maisha yake.Kingine ,nataka nikutoe wasi wasi,kabla ya kufanya kazi yagu tayari nilikwisha

chunguza mfumo mzima wa ulinzi ulivyo.Hakuna kamera yoyote iliyofungwa na kwa kifupi naweza kusema kwamba hakuna ulinzi pale hospitali .Mheshimiwa

rais kuwa na amani.I’m good at this”akasema Austin “ I believe you” akasema Ernest “ kwa hiyo mheshimiwa rais “ Austin akaendelea “ Nilifanikiwa kumpata

Marcelo akiwa mzima na kwa sasa amepumzika chumbani.” “ Thank you Austin,thank you so much” akasema Ernest na kuinuka “ I need to se him” akasema “

mheshimiwa rais kabla haujaenda kuonana na Marcelo kuna jambo nataka kulifahamu” akasema Austin “Uliza Austin” “ Unawafahamu wanaotaka kumuua

Marcelo?


 Kwa nini wanataka kumuua? Ernest mkasa aliyekuwa amesimama akaketi sofani na kujibu “ Austin kwa kuwa wewe ni kijana wangu nitakueleza
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ukweli.Marcelo simfahamu na wala hatujawahi kuonana na siwafahamu wanaotaka kumuua ni akina nani.Nilipigiwa simu na rais wa Congo mheshimiwa David

Zumo akaniomba nimsaidie kumuokoa Marcelo dhidhi ya watu wanaotaka kumuua.Nilimtaka David anipe taarifa za kina kuhusiana na Marcelo na anihakikishie

kama hahusiki katika mambo ya kihalifu ,akanihakikishia kwamba Marcelo hahusiki na genge lolote la uhalifu.Kwa kuwa ni rais mwenzangu nilikubali

kumsaidia kwani ni kawaida yetu sisi marais kusaidiana.Kwa hiyo Austin sifahamu chochote kuhusu Marcelo labda tukimuhitaji tunaweza kupata jibu ni akina

nani wanaotaka kumuua na kwa nini” akasema Ernest “ Mheshimiwa rais kutokana na maelezo hayo sidhani kama litakuwa jambo la busara kuanza

kumuhoji.Kwa vile tayari yuko katika mikono salama ni vyema kama tutasubiri maelekezo ya David Zumo aliyekuomba umsaidie na tusijiingize katika masuala

mengine yasiyotuhusu hasa katika wakati huu ambao kuna mambo mengi mazito yako mbele yetu” akasema Austin “ Wazo lako zuri Austin.Ngoja tuachane naye

na tujielekeze katika mambo yanayotuhusu lakini baadae nitakwenda kuonana naye tutakapomaliza maongezi yetu” akasema Ernest ukapita ukimya mfupi Ernest

akasema “ Austin leo nina furaha kubwa kwani nimefanya jambo ambalo sikutegemea kulifanya.Nimeuzuia muswada wa haki za binadamu usipelekwe bungeni

na kama haitoshi nimelivunja baraza la mawaziri.Nimefanya mambo haya mawili kutokana na ushauri wako ulionipa jana usiku.Ahsante sana kwa kunipa nguvu

na ujasiri wa kuweza kufanya haya niliyoyafaya.Kwa muda mrefu nilikwisha choshwa kuwa kibaraka wa Alberto’s lakini sikuwa na ujasiri wa kuweza

kupambana nao.Nimekuwa rais kivuli kwa muda mrefu na sitaki kuendelea tena kuwa kivuli huku nikiwaacha watu wengine wafanye maamuzi yote ya nchi

.Wananchi ambao ndio walionipigia kura wanateseka na mimi sina namna ya kuwasaidia kwani kila ninachokifanya lazima nipangiwe na

Alberto’s.Waliponichagua wananchi walikuwa na uhakika mkubwa wa maisha yao kuboreka lakini mpaka leo bado sijaitimiza ahadi hiyo.Nimeamua kutoka

kuwa kibaraka wa mashetani hawa na kuwa rais wa watanzania.” Ernest akanyamaza na kuendelea “ Kingine kilichonipelekea nikafanya maamuzi haya magumu

ni Monica.Ikitokea Monica akawa mwanangu naamini siku moja atakuwa na watoto na sitaki wajukuu zangu wafahamu kwamba babu yao alichangia kubomoa

nchi kwa kubariki matendo machafu ya mapenzi ya jinsia moja,utoaji mimba n.k.Austin niko tayari kwa mapambano.Nitapambana na watu hawa hadi mwisho

wangu.Najua mwisho wangu utakuwa ni kuuawa lakini kabla hawajaniua lazima nihakikishe nimeikata mizizi yote ya Alberto’s hapa nchini.Nataka niisafishe

nchi.Nataka niondoke madarakani taifa likiwa safi kama lilivyoachwa na waasisi wetu” akanyamaza na kumimina whysky katika glasi akanywa “ Mheshimiwa

rais hiki ulichokifanya umedhihirisha wazi kuwa wewe si Alberto’s.Nitakuwa nawe bega kwa bega na nitakulinda” akasema Austin “ Ahsante sana

Austin.Ninaamini ni kwa maongozi ya Mungu tumekutana ili uweze kupambana na genge hili lenye kutaka kuiharibu dunia.Karibu sehemu kubwa ya watu

wanaonizunguka ni Alberto’s.Makamu wa rais,waziri mkuu , mawaziri ,mkuu wa majeshi,wakuu wa vyombo mbali mbali vya usalama,wote hawa ni Albertos’

na nilipewa maelekezo ya kuwateua kwa hiyo utaona ni namna gani tulivyo na vita ngumu kwani tayari Alberto’s wamekwisha otesha mizizi imara hapa

nchini.Wanaiongoza nchi watakavyo na hii inaniumiza mno kwani wananchi hawajui kuhusu Alberto’s bali wananifahamu mimi.Nchi ikiyumba lawama zote

zitaniangukia mimi.Halafu kingine kibaya zaidi hata mke wangu Agatha naye ni mfuasi wa Alberto” “ Oh my God !! akasema Austin kwa mshangao “ Even your

wife? Akauliza “ Yes even my wife” akajibu Ernest na kimya kifupi kikapita Austin akauliza

“ Imekuaje hadi mkeo akaingia katika kundi hili? “ Austin swali lako linajibiwa kwa historia na historia yangu mimi ni ndefu lakini kwa kuwa tuko pamoja

katika mapambano haya nitakueleza japo kwa ufupi” akanyamaza kidogo halafu akaanza kumuhadhithis Austin Austin historia yake DAR ES SALAAM – 2001

Saa nne na dakika nane za usiku ndege aliyopanda bi Agatha ikatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam.Bi Agatha akiwa ameongozana na

waumini wenzake wanne pamoja na askofu wa kanisa lao wakitokea Italia katika safari ya kidini wakashuka ndegeni.Uwanjani hapo bilionea Ernest Mkasa tayari
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alikisha fika kumpokea mkewe.Baada ya kukamilisha taratibu za uwanjani hapo bi Agatha akatoka na kulakiwa na mumewe Ernest “ Pole sana kwa safari”

akasema Enest ,mizigo ya Agatha ikapakiwa garini wakaondoka kuelekea nyumbani “ Ernest nipe taarifa za maendeleo ya Yolanda” akasema Agatha wakiwa

garini wakielekea nyumbani “ Kwa sasa ana nafuu ya kutosha lakini bado hajaweza kutembea vizuri.Daktari anafika kila siku kumpa mazoezi” akajibu Ernest “

Ernest what real happened? Uliponigia simu kunitaarifu kuwa Yolanda ameanguka ghafla na kupoteza fahamu ulikuwa kwenye taharuki kubwa” Agatha akauliza

“ I don’t know exactly what happened .Nilipigiwa simu na mwalimu akanifahamisha kuwa Yolanda ameanguka ghafla na kupoteza fahamu.Alikimbizwa hospitali

akapatiwa huduma na alipozinduka madaktari wakamfanyia uchunguzi wa kina kufahamu kilichosababisha apoteze fahamu lakini hawakugundua chochote.Hata

hivyo wamemshauri apunguze uzito kwani alionao ni mkubwa kulingana na umri wake” akasema Ernest “ She’ll be fine” akajibu Agatha .Ernest akauliza “ Vipi

safari yenu ilikuaje? “ Safari yetu ilikuwa nzuri na yenye mafanikio makubwa.Tutaongea zaidi baadae lakini kwa sasa naomba uniache kidogo niingie katika

maombi mazito kwa ajili ya Yolanda” akasema Agatha na kufumba macho akajiegemeza kitini “ Bado ninajiuliza sana kuhusiana na kilichomfanya Agatha ahame

dhehebu lake la awali na kujiunga na dhehebu hili jipya.Kinachonishangaza zaidi ni kwamba toka amejiunga katika dhehebu hili jipya amekuwa mtu wa ibada

lakini matendo yake bado hayajabdilika hata kidogo.Kuna biashara zetu nyingi ambazo si halali na zinatuingizia fedha nyingi lakini sijawahi kusikia hata siku

moja akiongelea kuhusu biashara hizo na badala yake amekuwa akichukua pesa zinazotokana na biashara hizo na kuzipeleka kanisani.Ngoja nimuache na imani

yake” akawaza Ernest Walifika nyumbani na moja kwa moja baada ya kushuka garini wakaelekea katika chumba cha Yolanda mtoto wao ambaye anaumwa

ugonjwa usiojulikana. “ my baby !! akasema Agatha na kumkumbatia mwanae “ Unajisikiaje sasa ? “ Najisikia kidogo afadhali” “ Can you walk? Akauliza

Agatha wili mzito sana mama kama vile nimebeba gunia zito.Siwezi hata kunyanyua mguu.” Akasema Yolanda huku machozi yakimtoka “ Basi usijali

mwanangu .Ndani ya muda mfupi toka sasa utakuwa mzima tena.” Akasema Agatha akaikunja mikono yake kifuani na kufumba macho baada ya muda akasema “

Mio Dio beliee,si prega I mostrare il proprio patere e quarine questo poverto bambiko ” alikuwa anaoangea kwa kiitalinao akimaanisha “ Mungu wangu

nakuamini,tafadhali onyesha nguvu zako na umponye mtoto huyu” Agatha akamsogelea Yolanda na kumuwekea mkono wa kulia katika paji la uso akasema “

Svegliarsie Camminare.Mai male di nuovo ” akimaanisha “ Inuka na tembea na usiumwe kamwe”

Taratibu Yolanda akaanza kuhisi wepesi wa mwili akainuka na kusimama akatembea hatua mbili akaongeza nyingine mbili.Hakuyaamini macho yake .Ule uzito

wote aliokuwa akihisi kama vile amebeba gunia la mchanga ulitoweka.Alijiona mwepesi kama karatasi “ This is a miracle!! Akasema Ernest kwa mshangao

mkubwa.Agatha hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu .Ulikuwa ni mshangao kwa kila mtu.Akamuamuru Yolanda ajaribu kukimbia na akafanya hivyo.Akamuwekea

mkono kichwani na kusema. “ Gracie ll mio lord.I fara’ ris parmiare Voie solo per il rest o della mia vita” akimaanisha “ Ahsante Mungu wangu.Nitakutumikia

wewe pekee kwa maisha yangu yote yaliyobaki” “ Mama umepata wapi nguvu hii ya kuponya? Akauliza Yolanda “ Agatha akamtaka Yolanda aendelee kupumzika

akamshika mkono mume wake wakatoka mle chumbani.Bado Ernest alikuwa katika mshangao mkubwa kwa kile alichokifanya mke wake.Hata baada ya kuingia

chumbani kwao Ernest Mkasa aliendelea kumtazama Agatha kwa mshangao mkubwa “ What ?..mbona unanitazama hivyo Ernest? Akauliza Agatha “

Nimeshangazwa na kustushwa sana kwa jambo ulilolifanya kwa Yolanda” What was that? mazingaombwe? “ Si mazingaombwe Ernest.That was a real thing” “

real thing? Toka lini umekuwa na nguvu za kuponya? Akauliza Ernest “ Ernest mambo yamebadilika siku hizi.Vitu vidogo vidogo kama hivi mtu yeyote anaweza

akafanya.Si vitu vigumu tena kama tulivyokuwa tunafikiri.Kwa mfano naweza kufanya kitu kidogo tu sasa hivi ambacho unaweza kufikiri hakiwezekani”

akasema Agatha na kumsogelea Ernest akamshika machoni na kusema “ Tio ordino di essepe cieco” akimaanisha “ Ninakuamuru kuwa kipofu” “ Do you see

anything Ernest? Agatha akamuuliza mumewe “ No ! I cant see anything.It’s dark...what the hell are you doing Agatha? Please give me back my vision now !!

akasema Ernest kwa ukali.Agatha akacheka kidogo na kusema torno vostra vision indietro” Mara tu alipotamka maneno hayo Ernest akaanza kuona tena.Mwili

ulimtetemeka kwa woga “ Ernest tafadhali usiniogope.Hivi ni vitu vya kawaida sana ambavyo mtu yeyote anaweza akafanya na hata wewe unaweza kufanya

ukipewa nguvu.kwa hiyo usinishangae kuona ninafanya mambo kama haya” akasema Agatha “ Agatha umejiingiza katika imani gani hizo? Mambo haya

tumezoea kuyaona yakifanywa na hawa wanaojiita manabii .Are you one of them? “ I’m not one of them.Ernest kuna mambo mengi ambayo mimi na wewe

tunahitaji kuzungumza.Ni mambo yenye manufaa makubwa kwetu” akasema Agatha na kuingia bafuni kuoga akimuacha Ernest bado katika mshangao “ Ama

kweli hizi ndizo zile zama za mwisho zilizotabiriwa katika vitabu.Yaani Agatha naye amekuwa na nguvu ya kufanya mambo kama haya? Katoa wapi nguvu hiyo

ya kufanya viini macho? Huko alikotoka ndiko alikotoa nguvu hii.Nasikia wananunua nguvu ya kufanya miujiza ili kuwavuta waumini katika makanisa yao

lakini inasemekana pia nguvu hii waitumiayo katika kufanya matendo haya ya ajabu ajabu ili kuwahadaa watu ni nguvu za giza.Kama ni kweli hilo linalosemwa

basi Agatha naye atakuwa mfuasi wa imani hizo_Oh my God !! Amekosa nini huyu mwanamke hadi ameamua kujiingiza katika mambo hayo? Nakubali kuna

mambo mengi machafu tunayafanya lakini sikutegema kama siku moja Agatha angejiingiza katika imani hizi za kishetani.” Akawaza Ernest na kustuliwa

mawazoni na mkewe aliyetoka kuoga. Familia ilikutana mezani kwa chakula na kila mmoja alikuwa na mshangao juu ya kile kilichotokea kwa Yolanda.Baada ya

chakula kila mmoja akaenda chumbani kwake kulala. “ Agatha ni wakati sasa wa kunieleza ukweli wa yale uliyoyafanya.Umetoa wapi nguvu ya kufanya mambo

yale? Naomba nikuweke wazi uwa umeniogopesha mno na kama hunielezi ukweli I swear nitafanya jambo ambalo hukuwa umelifikiria kabisa” akasema Ernest
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ What will you do? Akauliza Agatha huku akitabasamu “ I’ll forget what me and you have ,what we’ve been through and I’ll leave you!! Akasema Ernest na sura

yake ikionyesha kutokuwa na masihara.Ghafla tabasamu likatoweka usoni pa Agatha “ Ok Ernest lets get serious now.Nitakueleza ukweli na tafadhali naomba

unisikilize kwa makini sana hadi nitakapomaliza.” Akasema Agatha “ Nilielekezwa na rafiki yangu mmoja anaishi afrika ya kusini kuhusiana na kanisa jipya

liitwalo Holy faith ministry.Maelezo niliyopewa na huyo rafiki yangu kuhusu kanisa hili yalinivutia ikanilazimu kumtafuta askofu Gidion Guchal.Nilifanikiwa

kuonana naye akaniombea na akanieleza mambo mengi ambayo sikuwahi kuelezwa na mtu yeyote hapo kabla.Alinieleza kila kitu kuhusu maisha yangu

nikashangaa mno.Akanieleza kuwa hata mimi ningeweza kuwa na uwezo kama ule endapo ningehitaji.Nilitamani sana kuwa na uwezo wa kufanya mambo

ambayo wengine hawawezi ,mambo makubwa kushinda uwezo wa mwanadamu kwa hiyo nikajiunga rasmi na kanisa hilo.Baba askofu Gidion alituchagua watu

watano kwa ajli ya kwenda hija katika makao makuu ya kanisa letu huko Italia.Tulipofika tukapokewa na mtu mmoja anaitwa Giovanni.Siku Iliyofuata ndipo

tulipoelezwa rasmi dhumuni la ziara yetu ile .Tulielezwa kwamba tumepelekwa pale ili kuingizwa rasmi katika jumuiya ya Alberto’s.Hakuna miongoni mwetu

aliyeelewa chochote kuhusiana na Alberto’s hivyo tukataka kufahamu na tukafahamishwa kwa kina.” Akanyamaza na baada ya muda akaendelea. “ Mwaka 1894

Kardinali Albert Mcrecks wa California alianzisha vugu vugu la uasi ndani ya kanisa kwa kuwashawishi wenzake waunge mkono mpango wake wa mageuzi

ndani ya kanisa mpango ambao alitarajia kuwasilisha kwa kiongozi wa kanisa hilo duniani.Mpango huo ulilenga kulishawishi kanisa katoliki likubali mabadiliko

na kuruhusu makasisi wake kuoa,kutambua makundi mbali mbali hasa ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja,kuruhu utoaji mimba n.k.Alberto

Alifanikiwa kupata uungwaji mkono mkubwa na vugu vugu la mabadiliko ndani ya kanisa likapamba moto.Aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo kwa wakati huo

alikasirishwa sana na jambo hilo na hivyo akamvua daraja Alberto pamoja na wenzake wote waliomuunga mkono.Baada ya kufukuzwa na kuvuliwa

daraja.Alberto bado aliendelea na msimamo wake wa mageuzi na sasa alitaka kufanya mageuzi makubwa duniani .Alipotea kwa meizi sita na aliporejea alidai

kuwa alikuwa katika maombi makubwa mahala pa siri na Mungu akamtuma aje afanye mabadiliko makubwa duniani na hapo ndipo jumuiya ya Albertos

ikaanzishwa.Alianza kwa kutengeneza mtandao wake uliopata nguvu kutokana na kuungwa mkono na viongozi hasa wa mataifa makubwa.


Alberto alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwa hiyo alifanikiwa kuwashawishi viongozi wengi wa mataifa makubwa wakamkubali na kujiunga naye.Katika

kujenga mtandao wake alianzia na mataifa ya Amerika na ulaya na baadae akafika hadi bara Asia na kuotesha mizizi .Alberto kwa kwanza alipofariki ,alifuata

Alberto wa pili na sasa yuko Alberto wa tatu ambaye ni kijana zaidi na mwenye nguvu kubwa.Baada ya kazi kubwa kufanyika katika mataifa ya Amerika na ulaya

Alberto wa tatu ameamua kuelekeza nguvu barani Afrika.Wanataka kuibadili Afrika na tayari wamekwisha ingia na kuotesha mizizi.Haikuwa kazi ngumu kwa

nchi za afrika kukubaliana nao kwani walitumia kigezo cha umasikini wa nchi hizi kuzishinikiza zifuate masharti yao.Kwa kutumia mataifa makubwa ambayo

yamekuwa yakitoa misaada mikubwa ,nchi zote za Afrika zimetakiwa kutunga sheria zao na kutambua haki za watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.Tayari

nchi nyingi za Afrika zimekubaliana na sharti hilo na zimetunga sheria kukubaliana na mambo hayo.Nchi pekee ambayo imewapa ugumu mkubwa kuingia ni

Tanzania kutokana na misingi imara iliyowekwa na waasisi wa taifa hili .Kwa sababu hiyo wameunda timu ya watu kumi ambayo itahakikisha Alberto’s

wanaingia Tanzania.Mimi ni miongoni mwa watu hao kumi” “ Oh my God !! akasema Ernest kwa mshangao “ Ernest naomba usiongee chochote kwanza hadi

nitakapomaliza.Naomba uendelee kunisikiliza.” Akasema Agatha “ Mimi na wenzangu tuliochaguliwa ,tumekula kiapo mbele ya mkuu Alberto wa tatu

kuhakikisha kuwa tunafanya kila tuwezalo kuondoa vizingiti vyote vinavyofanya Alberto’s washindwe kupenya na kufanya kazi zao nchini Tanzania.Tumepewa

nguvu ya kufanya mambo ambayo binadamu wengine hawawezi kuyafanya.Nimekuwa mtu mpya .Nimeweka agano mbele ya Alberto mkuu la kuwa mtiifu na

kufuata maelekezo yote anayoyatoa.Kwa hiyo basi tumepewa kazi kubwa ya kufanya na kazi ya kwanza ambayo tunatakiwa kuifanya ni kutengeneza

serikali.Tunataka rais ,makamu wa rais ,waziri mkuu na mawaziri wote wawe ni Alberto’s .Tukilifanikisha hilo basi tutakuwa tumeotesha mzizi na Tanzania

itabadilika.Tunataka Tanzania mpya.” Agatha akanyamaza akamtazama mumewe ambaye uso wake ulijikunja kqwa hasira .Agatha hakujali akaendelea “ Ernest

nafahamu jambo hili limekustua sana lakini ni suala ambalo lina manufaa makubwa si kwetu pekee bali kwa nchi na dunia kwa hiyo nakusihi usikasirike

mpendwa wangu kwani kuna jambo kubwa umeandaliwa na ambalo hukuwa umelitarajia kabisa” akanyamza kidogo akaendelea “ Baada ya kupewa jukumu la

kuhakikisha tunaandaa serikali ambayo itakuwa chini ya Alberto’s,nimekupendekeza wewe uwe rais mpya wa Tanzania.” “ Nini ?? Akauliza Ernest kwa

mshangao “ Nimekupendekeza uwe rais wa Tanzania.Utaongoza serikali itakayokuwa chini yetu.Wew................” “ Stop Agatha!!!..stop!!...!! akasema Ernest kwa

hasira “ Wewe na hao mashetani wenzako ni mataahira.Agatha kitu gani umekosa hadi ukaingia katika mambo haya ya kishetani? Please Agatha toka huko

ulikoingia haraka sana.I need back my old Agatha,the one I married and not you!! Akasema Ernest kwa ukali “ Ernest I’m still the same Agatha, your one and only

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog