Search This Blog

Monday, 19 December 2022

QUEEN MONICA (2) - 5

  




Simulizi : Queen Monica (2)
Sehemu Ya Tano (5)

wife.From now you are going to listen to me and do whatever I tell you to do.You here me? Akasema Agatha kwa ukali “ Mimi ndiye mwenye amri ya mwisho

ndani ya nyumba hii na utanisikiliza mimi pekee.Nataka uchukue simu na uwapigie hao mashetani wenzako uwaambie kwamba hutashiriki tena katika mambo

yao ya kishetani na baada ya hapo hautaruhisiwa tena kutoka nje ya nyumba hii.Umenisikia Agatha? Akasema Ernest huku mwili ukimtetemeka kwa hasira “ Una

dakika mbili za kuchukua simu na kuwapigia hao wenzako ama sivyo uchukue kila kilicho chako na uondoke katika nyumba hii.Nadhani umenielewa vizuri na

wala sitishwi na huo uchawi wako .Nitahakikisha kila mtu anafahamu ni mambo gani wewe na hao mashatani wenzako mnayafanya.” Akasema Ernest No Ernest

you dont have to do that and you cant do that.Kwa sasa maisha yako nimeyashika mimi na ndiyo maana nikakwambia kwamba utafuata kila nitakachokuamuru”

Ernest Mkasa akacheka kidogo na kusema “ Sikujua kama unaweza kuwa mjinga kiasi hiki .Ninakuambia huwezi kuniamuru chochote na ninarudia tena

kukuonya kuwa sikuogopi hata kama una nguvu zako za kishetani” akasema Ernest “ Sikiliza Ernest ,tayari nimekwisha weka agano na mkuu Alberto kwamba

wewe ndiye utakayekuwa rais wa Tanzania .Niliulizwa mara tatu kama ninaliweza jukumu hilo la kukushawishi ukubali kuwa rais nikasema ndiyo na hapo

likafanyika agano kati yangu na Alberto mkuu kwamba nitakaposhindwa kutimiza kile tulichokubaliana basi watoto wetu wote watapotea.Kwa ufupi tu ni

kwamba watoto wetu nimewaweka dhamana na endapo nitashindwa kufanya kile nilichokiahidi yaani kukushawishi ukubali kuwa rais wa Tanzania basi wote
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
watakufa”

 “ Oh my God !!! akasema Ernest akiwa amejishika kiuno akimtazama mkewe kwa hasira “ Suala hili halitaishia kwa watoto tu bali kama utaendelea na ukaidi

wako basi itafuata zamu yako na mimi nitakuwa wa mwisho.You will die Ernest.The whole family will die.Kwa nini tufike huko Ernest? Kwa nini tuwapoteze

watoto wetu wakati unao uwezo wa kuwaokoa.Just say yes and our family will be saved.Ernest kubali kuwa rais wa Tanzania ambayo ni nafasi ya juu

kabisa,ikubali heshima hii kubwa na utakuwa mtu mkubwa mwenye nguvu,utajulikana duniani kote,utajiri wako utaongezeka maradufu.Kukubali kwako kuwa

rais haimaanishi kwamba utakuwa mfuasi wa Alberto’s.Tutakuweka katika nafasi ya juu kwa ajili ya kutusaidia katika baadhi ya masuala yetu Fulani

Fulani.Tunataka Tanzania ipokee mabadiliko na tunatakuhitaji sana utusaidie mabadiliko haya yafanikiwe kwa hiyo basi unapaswa kuanza kulitafakari suala hili

kwa mapana kwa manufaa yetu na watoto wetu utakapokuwa tayari utanitaarifu. Ernest Mkasa akawasha sigara nyingine akavuta mikupuo kadhaa akamtazama

Austin "Hivyo ndivyo ilivyokuwa Austin .Thats how my wife became a devil” akasema Ernest “ This is going to be hard than I thought” akanong’ona Austin

.Ernest akamimina mvinyo katika glasi akanywa na kusema “ Nilimchukia sana Agatha na toka siku ile sikuweza hata kulala naye kitanda kimoja.Baada ya

mwaka mmoja akanikumbusha kama tayari nimefanya maamuzi kuhusu lile suala aliloniambia.Hapo ugomvi ukaibuka upya.Sikuwa tayari kwa jambo lile.Miezi

mitatu baadae watoto wetu wote watatu wakiwa katika gari wakitokea Dodoma katika sherehe ya mmoja wa marafiki zao walipata ajali mbaya ya gari na wawili

wakapoteza maisha papo hapo ,mmoja akawa mahututi akakimbizwa hospitali.Tukiwa hospitali kufuatilia hali ya mwanetu aliyekuwa mahututi ,Agatha akiwa na

uso mkavu kabisa akaniambia kwamba vifo vya watoto wetu nimevisababisha mimi kwa kiburi changu.Alinikumbusha agano alilolifanya na hao wenzake na

kwamba alishindwa kulitimiza na hiyo ndiyo adhabu yake.Aliniambia kwamba nina dakika ishirini tu kufanya maamuzi ili nimuokoe mtoto wetu

aliyebaki.Nilikuwa na hasira kali na wakati huo nilitamani nimkate shingo nimmalize kabisa” Ernest akanyamaza akainamisha kichwa na baada ya muda akainua

kichwa na kufuta machozi na kusema “ I’m sorry for this Austin.Nimekumbuka mbali sana.Napatwa na uchungu mkubwa nikiwambuka wanangu.Anyway

tuendelee na maongezi yeu” akavuta mikupuo miwili ya sigara na kuendelea “ Pamoja na kuwapoteza watoto wangu wawili lakini bado nilikuwa na moyo

mgumu sana kukubaliana na Agatha.Baada ya dakika ishirini kama alivyosema, mwanangu wa tatu akapoteza maisha.Agatha akanieleza kwamba nisipofanya

maamuzi ndani ya dakika thelathini itakuwa ni zamu yangu.Niliogopa sana na ikanilazimu kukubali wanachokitaka .Hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi nikawa

rais.Kuna mambo mengine mengi yalitokea ikiwemo kifo cha rais Ferdinand aliyefariki kwa ajali na yote hii ikiwa ni mipango ya Alberto’s na baada ya kifo

chake ukafanyika uchaguzi na mimi nikawa rais mpya.Austin hapa nilipo nina kisasi kikubwa sana kwa Alberto’s na muda mrefu nilipanga siku moja lazima

nilipize kisasi ila nilikosa mtu wa kuungana naye katika mapambano haya kwani wengi wa watu wanaonizunguka ni wafuasi wa Alberto’s.Kwa hiyo Austin

naamini tayari umekwisha pata picha halisi ya vita tunayokwenda kuipigana.It’s not an easy war.These people are very powerfull.Wameiteka sehemu kubwa ya

dunia na wamesimika utawala wao.Wanataka kuitawala dunia .Kwa sasa wamehamishia nguvu zao Afrika.Wanataka bara lote la Afrika lipepee bendera yao na

tayari wamekwisha anza kupata mafanikio kwani kati ya nchi 54 za bara la Afrika nchi 36 tayari tayari wamekwisha fanikiwa kuingia na zilizobaki aidha ziko

katika mchakato au ushawishi unaendelea.Austin hii ni jamii yenye kumuabudu shetani na ndiyo maana mambo yao yote ambayo wanataka kuyahalalisha duniani

ni yale yanayokwenda kinyume na matakwa ya Mungu.Kwa hiyo Austin vita tunayoipigana ni kubwa . As far as God is on our side we’ll win” akasema

Ernest.Austin akamtazama kwa muda kisha akasema “ Mheshimiwa rais,ninawafahamu Albertos.Ninafahamu nini wanakifanya hivi sasa duniani kwa hiyo

ninafahamu ugumu wa vita tunayokwenda kupigana” akasema Austin na kufumba macho kwa sekunde kadhaa na kusema “ Sijawahi kumueleza mtu yeyote

jambo hili na kwa mara ya kwanza leo ninaufungua mdomo wangu na kulitamka.” “ Jambo gani hilo? Akaulzia Ernest “ Niliugundua mpango wa siri wa kutaka

kumuua rais Ferdinand uliokuwa umesukwa na watu walioko ndani ya serikali ambao kama ulivyosema kuwa ulikuwa ni mpango wa Alberto’s.Baada ya

kuugundua mpango huo nilianza harakati za kutaka kuzuia jambo hilo lisifanikiwe na ndipo ulipofanyika mkakati wa kuniua.Nilitaka sana kumuokoa rais

Ferdinand lakini sikuweza kwani nilinusurika kufa Somalia na sikurejea tena Tanzania na baadae rais Ferdinand akafariki katika ajali.” Akanyamaza na

kumtazama Ernest “ Mheshimiwa rais nitakulinda kwa hiyo usihofu. walijaribu kuniua mara ya kwanza wakashindwa na sasa ni zamu yao kuishi kwa

uoga.Tukishirikiana pamoja tunaweza kabisa kuwashinda hawa mashetani .

Anyway tuweke kwanza pembeni suala hilo tuongelee kuhusiana na kazi ulizonikabidhi.Moja kati ya kazi ulizonituma nimeikamilisha ambayo ni kumtoa

hospitali Dr Marcelo .Kazi ya pili ni kuhusiana na Monica.Nimepanga kuanza kuifanya kazi hiyo kesho .Ili kujenga ukaribu na mazoea na Monica itanilazimu

nijihusishe katika mambo anayoyapenda .Monica ni mtu anayejitoa sana kwa jamii hasa kwa watoto na wazee wasiojiweza .Nimeamua nipitie upande huu ili

kujenga ukaribu na Monica.Kwa hiyo mheshimiwa rais I’m going to need money,lots of money.Nahitaji kujenga muonekano mzuri wenye hadhi ili Monica

anikubali kwa haraka” “ Usijali kuhusu fedha Austin,utapata kiasi chochote cha fedha unachokihitaji ili mradi kazi yangu ifanyike.Lakini kuna jambo moja

nahitaji kulifahamu toka kwako.Nikikutazama you are very handsome.Muonekano wako ukijumlisha na kiasi kikubwa cha fedha nitakachokupatia vinaweza

kumchanganya mwanamke yeyote .Nataka kufahamu aina ya ukaribu unaotaka kutengeneza na Monica.Are you going to make her fall for you? Austin

akatabasamu na kusema “ Usihofu mheshmiwa rais ,siwezi kufanya jambo kama hilo.Niwapo kazini huwa ninaielekeza akili yangu katika kazi tu na si mambo
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mengine.I’m always proffesional.Isitoshe tayari nina mchumba na tunapendana sana” “ Good.I’m glad to hear that.Austin kama kuna chochote ambacho

unakihitaji tafadhali usisite kunieleza” akasema Ernest “ Ahsante mheshimiwa rais ,nashukuru sana nitakupa orodha ya mahitaji yangu ila kuna jambo ambalo

nataka niliweke sawa kwako.Ni kuhusu usalama wako.Unawamini walinzi wako? “ Tena umenikumbusha Austin.Nilipanga kujadili nawe juu ya suala hilo hilo

la ulinzi wangu.Ninaweza kusema kwamba sina ulinzi wa uhakika.Ninasema hivyo kwa sababu kuna kitu kimetokea leo muda mfupi kabla ya kutoa hotuba

yangu watu wawili nisiowafahamu waliingia chumbani kwangu tena wakiwa na bastora zilizofungwa viwambo vya kuzuia sauti na wakanionya kwamba

nisithubutu kuhutubia.Najua watu wale walitumwa na Alberto’s ili kuniogopesha na kunithibitishia kwamba wana nguvu kubwa ya kuweza kufanya lolote muda

wowote wautakao.Tukio lile limeniogopesha sana na kunifanya nisiwaamini kabisa walinzi wangu ila kuna walinzi wawili au watatu hivi ambao ninaweza

kuwaamini wale ambao ninakuja nao hapa.Ukiacha hao mtu mwingine ninayemuamini ni mzee Mukasha msaidizi wangu” Maelezo yale ya Ernest yakamfanya

Austin atakafakari kwa muda halafu akasema “ Mheshimiwa rais You are not safe.Wewe ndiye mwanga wa mapambano haya kwa hiyo unahitaji ulinzi wa

uhakika .Kwa ulinzi huo ulio nao sasa hivi anything can happen.You need to be guarded by the people you trust ,the people I trust “ akasema Austin “ Unashauri

tufanye nini Austin? Akauliza Ernest “ Nitaunda kikosi cha kukulinda badala ya walinzi wako wa sasa” “ Hilo linaweza kuwa gumu sana Austin kwa sababu

ulinzi wa rais ni jambo ambalo lina taratibu zake ambazo siwezi kuzikiuka” “ Wewe ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa hiyo utalifanya hilo

liwezekane.Bila kufanya hivyo watakuua mheshimiwa rais.Watu nitakaowateua ni watu ninaowaamini na wenye mafunzo na uwezo wa hali ya juu mno na

endapo utawapa nafasi hiyo basi kwa pamoja tutashirikiana vizuri katika vita hii .Mheshimiwa rais hatutakuwa tunaonana mara kwa mara kwa hiyo lazima

tutafute namna ya kufanya mawasiliano baina yetu kuwa rahisi.Watu hao ambao nataka wakulinde ndio watakaokuwa kiungo muhimu kati yetu.Bila kufanya

hivyo mheshmiwa rais you are a dead man.Watakuua kama walivyomuua rais Ferdinand.Kitu kingine unachopaswa kukifanya kwa haraka ni kuhakisha

unaungwa mkono na jeshi kwa hiyo unapaswa haraka sana kutengua uteuzi wa mkuu wa majeshi na kuteua mkuu mpya wa majeshi.Napendekeza nafasi hiyo

apewe Luteni jenerali Lameck Msuba.Ninamfahamu vyema Lameck ni mtu mtiifu na mzalendo wa kweli.Jeshi likiwa chini yake basi hauna tena hofu ya

kufanyika uasi.Mheshimiwa rais nafahamu ugumu wa hiki ninachokueleza lakini ili tufanikiwe lazima hayo niliyokwambia yafanyike” akasema Austin. “ Austin

ninakubali ombi lako ila niachie nikatafakari namna nitakavyofanya ili kulitekeleza jambo hilo.” “ sawa mheshimiwa rais,kalitafakari na utakapokuwa tayari

utanijulisha” akasema Ernest.Austin akamchukua mheshimiwa rais wakaongozana kuelekea katika chumba alimo Dr Marcelo.Akaufungua mlango wa chumba

taratibu na Dr Marcelo ambaye tayari alikuwa usingizini akastuka na kufikicha macho “ Halow Marcelo.” Akasema Austin “ Austin” akasema Marcelo akainuka

kitandani na kuketi “ Marcelo samahani kwa kukuamsha lakini nimekuletea mgeni” “ hallow Macelo “ akasema Ernest na kuvua kofia na miwani yake na

kumfanya Dr Marcelo apigwe na butwaa

 “ Mr President !!! akasema Marcelo kwa mshangao “ Relax Marcelo.Unajisikiaje? akauliza Ernest “ Ninajisikia vizuri mheshimiwa rais.Nimestuka sana

kukuona hapa mzee” akasema Marcelo Marcelo nimekuja kujua maendeleo yako na kama uko salama.Mimi ndiye niliyemtuma Austin akutoe kule hospitali

baada ya kuombwa kufanya hivyo na rais wa Congo David Zumo” “ David Zumo?!!... Akauliza Marcelo kwa mshangao mkubwa. “ Ndiyo.David Zumo

aliniomba nifanye kila niwezao nikuondoe pale hospitali “ akajibu Ernest “ Nimestuka sana kwani sifahamiani na David Zumo na sijui amepataje taarifa zangu.”

Akasema Marcelo .Austin na Ernest wakatazamana. “ Imekuaje David akazifahamu taarifa zangu kwamba kuna watu wanataka kuniua? This is weird” akasema

Marcelo “ Swali hilo ni swali ambalo tunapaswa tukuulize wewe” akasema Ernest “ Mimi kama nilivyosema awali kwamba sifahamiani kabisa na David Zumo

.Wakati anakupa maelekezo ya kunitoa hospitali hakukueleza jambo lingine lolote? “ Hapana hakunieleza chochote.Yeye alichoniomba nikutoe hospitali kuna

watu wanataka kukuua na hakutoa maelekezo mengine.kwa hivi sasa tunasubiri maelekezo toka kwake” akasema Ernest. “ Ahsante sana mheshimiwa rais kwa

kufanikisha kunitoa pale hospitali ambako ni kweli kama alivyokueleza David ,maisha yangu yalikuwa hatarini” akasema Marcelo. “ Ni nani wanaotaka kukuua

Marcelo? Akauliza Austin “ Hii ni hadithi ndefu kidogo lakini kwa ufupi wanaotaa kuniua ni rafiki zake baba” “ Rafiki za baba yako? Kwa nini? Akauliza

Austin. Marcelo akatafakari kidogo na kusema “ Baba yangu Dr Richard alikuwa daktari wa saratani ya damu.Yeye ndiye aliyenishawishi na mimi nisomee

kuhusu saratani.Kabla ya kifo chake alinipa kitabu fulani nikihifadhi.Pamoja na kitabu hicho alinipa namba za simu za mtu ambaye nilitakiwa nimpigie ili nipate

maelekezo kuhusiana na kitabu hicho .Alinionya kuhusu rafiki zake Fulani watatu kwamba nisiwe karibu nao na kwamba ni watu hatari sana.Kitabu alichonipa
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baba nilikihifadhi katika kasiki na sikuwahi kukifungua na wala sijui kuna nini kiliandikwamo.Hivi majuzi nikiwa kazini watu waliingia chumbani kwangu

wakafungua kasiki na kuchukua kitabu hicho.Nikiwa bado natafakari aliyefanya kitendo kile nikazikumbuka namba za simu nilizopewa na baba kuwa nipige kwa

ajili ya maelekezo kuhusu kile kitabu.Nilipiga lakini simu ikapokelewa na kukatwa na jioni ya siku hiyo nikapigwa risasi na watu nisiowafahamu waliokuwa

katika pikipiki mbili.Nilikimbizwa hospitali wakafanikiwa kuokoa uhai wangu.Nikiwa pale hospitali nilimuona mmoja wa wale rafiki zake baba ambao

alinionya nikae nao mbali nikajua tayari maisha yangu yako hatarini”akasema Marcelo “ Unasema kuna mtu aliingia chumbani kwako akafungua kasiki na

kuchukua kitabu ulichopewa na baba yako ,unadhani kitabu hicho ni sababa ya wewe kupigwa risasi? Akauliza Austin Ninahisi hivyo kwani tukio hilo limetokea

baada tu ya kitabu hicho kutoweka” akajibu Marcelo “ Unamfahamu mtu mwenye hizo namba alizokupa baba yako ? akauliza tena Austin “ Hapana simfahamu”

Austin na Ernest wakatazamana kisha Austin akasema “ Suala hili linaonekana si suala dogo.Ninasita kujiingiza huko kwa sababu tayari kuna masuala mazito

yanayotukabili.Kwa kuwa tayari suala hili liko katika mikono ya polisi basi hatuna budi kuwaacha waendelee na uchunguzi” akasema Austin

“ Uko sahihi Austin.Nitaweka mkazo pia kwa jeshi la polisi wahakikishe wanawasaka na kuwapata watu hao waliotaka kukuua.Kwa sasa hadi hapo tutakapopata

maelekezo mengine toka kwa David Zumo utaendelea kukaa hapa pamoja na Austin.Hii ni sehemu salama sana kwako kwa sasa.Utafuata yale yote

utakayoelekezwa na Austin” “ Ahsante mheshimiwa rais.Mungu awabariki sana” akasema Marcelo.Ernest na Austin wakatoka mle chumbani “ Suala la Dr

Marcelo linaonekana ni suala tata sana.David zumo ameingiaje katika suala hili? Hicho kitabu alichopewa na baba yake kina nini ndani yake? Maswali haya

yanalifanya jambo hili kuwa gumu” akasema Ernest “ Ni kweli mheshimiwa rais.Suala hili linaoneana si suala jepesi.Ni suala pana .Lazima kuna kitu kimejificha

hapa na ndiyo maana Marcelo anataka kuuawa.Nahisi labda yawezekana ukawa ni mtandao wa mambo haramu kama vile madawa ya kulevya n.k Lakini hata

mimi uhusika wa David Zumo katika jambo hili unanila akili sana.Anamfahamu Marcelo lakini Marcelo hamfahamu David.Inakanganya kidogo.Mheshimiwa

rais naomba tusiumize vichwa vyetu kwa suala hili.Tuwaachie jeshi la polisi watafanya uchunguzi wao na kupata ukweli” akasema Austin wakaagana Ernest

akaondoka. ******************** Wakati rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ernest Mkasa akiondoka katika nyumba anayoishi Austin,ukumbi mmoja

mdogo wenye kuweza kuchukua watu zaidi ya hamsini uliopo ndani ya jumba moja kubwa la kifahari lililoko kandoni mwa bahari ,kikao kizito kilikuwa

kinafanyika kilichowakutanisha watu zaidi ya arobaini.Katika ukumbi huo kulikuwa na luninga nne kubwa ambazo kulikuwa na watu wakionekana waliokuwa

nje ya nchi wakiunganana wenzao wa hapa Tanzania katika kikao kile.Kikao kile kilihudhuriwa na makamu wa rais wa Tanzania,waziri mkuu aliyevuliwa

madaraka pamoja na baadhi ya viongozi na wafanya biashara wakubwa ambao ni wajumbe wa kamati kuu ya Alberto’s Tanzania. “ Kabla ya kiongozi wa kikao

kuwasili kulikuwa na minong’ono ya hapa na pale na wajumbe wakijadiliana hili na lile.Kiongozi wa kikao kile aliyevaa suti nyeusi mfanya biashara tajiri

mtanzania mwenye asili ya Ghana,Obi Ochukwu akatokea akiwa ameongozana na wajumbe

wengine sita wakaelekea meza kuu.Kabla ya kikao kuanza yakafanyika maombi halafu wimbo wa maalum wa kumtukuza Alberto mkuu ukaimbwa huku ubani ukifukizwa na baada ya hapo kikao kikaanza. “ Ndugu wajumbe ,tumekutana hapa kwa dharura ili tujadili kile ambacho kimetokea leo.Kilichotokea leo ni anguko kubwa ambalo halijawahi kutokea tangu Alberto mkuu wa kwanza .Mtu ambaye tulimuamini kwamba angeweza kutuvusha hapa Tanzania ,ametugeuka na kufanya jambo ambalo hakuna aliyetarajia.Nafikiri nyote mnafahamu ugumu tulioupata kuingia hapa Tanzania.Toka historia ya kuanzishwa jumuia hii ya Alberto’s hakujawahi kuwa na nchi ngumu kuingia kama Tanzania.Hii inatokana na waasisi wa taifa hili kujenga misingi imara na thabiti na hivyo kulifanya taifa hili kutopenyeka kirahisi.Ilitulazimu kutumia nguvu nyingi na muda mrefu kupenya na kuotesha mizizi hapa Tanzania.Mizizi imeota na mmea umechipua na mti umemea na kutoa maua yenye harufu nzuri lakini wakati unakaribia kuanza kutoa matunda ametokea mwenzetu mmoja akaukata.Tulimuamini sana Ernest Mkasa tukamuweka katika nafasi ya juu kabisa lakini baada ya kufanikisha yale aliyokuwa anayahitaji amechagua kutusaliti.Ndugu zangu kufutwa kwa muswada huu na kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni pigo kubwa kwetu.

Muswada huu ulikuwa ni mwanzo wa kuipeleka Tanzania kule tunakotaka na kufutwa kwake kumetufanya turudi nyuma hatua ishirini zaidi.Hili ni anguko kubwa ndugu zangu na si suala la kupuuzia.Ofisi ya rais ndiyo mzizi wetu mkuu kwa hiyo kama tukiikosa ofisi ile hata sisi hatutakuwa na nguvu tena na mambo yetu yatakwama.Kwingineko kote duniani ambako Jumuiya ya Alberto imeweka mizizi yake marais wa nchi ndio wenyeviti wa kamati kuu za Alberto za kila nchi lakini hapa Tanzania ilikuwa tofauti kidogo ,tulimpa urais mtu ambaye si Alberto’s japokuwa ni kwa makubaliano maalum lakini nataka nikiri kuwa tulifanya kosa kubwa.tulitakiwa kuchagua rais kutoka miongoni mwetu.Kosa tulilolifaya sasa linatugharimu.Kwa hiyo ndugu zangu tumekutana hapa kwa ajili ya kulijadili suala hili.Nakaribisha sasa maoni yenu lakini kabla ya yote napenda kwanza nimpe nafasi ya kwanza mwenzetu waziri mkuu mstaafu”akasema Obi.Waziri mkuu aliyevuliwa madaraka akasimama “ Ndugu zangu sidhani kama kuna haja ya kuendelea kulijadili suala hili wakati kinachotakiwa kifanyike kiko wazi.Ernest mkasa ametusaliti na kwa mujibu wa sheria zetu yeyote anayetusaliti au kushindwa kutimiza wajibu wake na kuhatarisha maslahi ya jumuia adhabu yake ni kifo.Rais Ferdinand alikufa kwa kukataa kushirikiana nasi na hivyo ndivyo tunatakiwa kufanya kwa Ernest Mkasa.He must die.Kama alivyosema mwenyekiti kwamba ofisi ya rais ndiyo mzizi wetu mkuu na hatutakiwi kuikosa basi tumuondoe Ernest haraka ,tunaye Mr Muhsini ambaye ni makamu wa rais atashika usukani kwa muda na mambo yetu yataendelea kama kawaida.Baadae utafanyika uchaguzi na mtu wetu mwingine ashike nafasi hiyo ili mipango yetu iendelee.Hatutaweza kufanya chochote bila kuwa na mtu wetu ambaye ni rais wa nchi.Kwa hiyo ndugu wajumbe pendekezo langu mimi ni kwamba hakuna chochote tunachoweza kukifanya kama hatutaitwaa tena ofisi ya rais.Tusipoteze muda mwingi kujadili jambo hili wakati suluhu ya jambo hili ni moja tu” akasema waziri mkuu aliyevuliwa wadhifa.Kabla mjumbe mwingine hajasimama Agatha mke wa Ernest Mkasa akasimama “ Ndugu mwenyekiti naungana na mjumbe aliyetangulia kwamba sheria zetu zinasema hivyo lakini suala hili si dogo kama tunavyodhani.Ernest ni mume wangu na ninamfahamu vizuri ,lazima kuna watu waliompa nguvu ya kuweza kufanya haya aliyoyafanya.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Peke yake naamini hawezi kuyafanya haya.Kwa hiyo basi tusiwe na haraka ya kutaka kumuua,tufanye kwanza uchunguzi wa kina tufahamu anashirikiana na akina nani .Kwa kulipanua zaidi suala hili ni kwamba kwa siku za hivi karibuni niligundua mabadiliko Fulani kwa Ernest .Niliamini lazima kuna jambo linalomsumbua.Siku ya jana asubuhi alipigiwa simu na mtu wakazungumza kuhusu kufanyika kwa makabidhiano.Nilimchunguza mtu aliyeongea naye na kugundua ni balozi wa China hapa nchini.Niliwasiliana na makamu wa rais nikamtaka achunguze nini kinaendelea kati ya Ernest na balozi wa China lakini hakuweza kupata chochote.Ninaamini kabisa kuna jambo linaloendelea kati yao na ndiyo maana nikasema kwamba tufanye uchunguzi wa kina kwani endapo tutamuondoa Ernest peke yake na kuwaacha watu anaoshirikiana nao bado hatutakuwa tumefanya kitu .Hatufahamu watu anaoshirikiana nao wanatufahamu kiasi gani kwa hiyo tulipe suala hili uzito unaostahili.Inawezekana tayari wanaufahamu mtandao wetu kiundani na ndiyo maana Ernest amekuwa na nguvu kubwa na haogopi.Tunapaswa kuwa waangalifu sana.Kwa ushauri kuna mtu mmoja ni msaidzi wa karibu sana wa rais anaitwa Mukasha huyu ndiye ambaye amekuwa akimshirikisha katika mambo yake mengi .Tuanze kwa kumchunguza kwanza huyu kuna kitu atakuwa anakifahamu.Huyu ndiye aliyebeba siri zote za Ernest” akasema Agatha “ Agatha wazo lako ni zuri na hata mimi nakubaliana nalo lakini tunapaswa kutafuta njia ya haraka ya kuhakikisha tunaurejesha bungeni muswada ule muhimu.Nahitaji mawazo zaidi” akasema Obi mwenyekiti wa kikao kile “ Mimi kwa maoni yangu endapo suala la kumuua Ernest litakuwa gumu basi tuwatumie wabunge kumuondoa.Asilimia karibu sabini ya wabunge ni watu wetu.Tumegharamia kampeni zao wakashinda na kila mwezi wanapokea fedha nyingi kutoka kwetu kwa hiyo tuwatumie hawa kuanzisha mchakato wa kura ya kutokuwa na imani na rais.Kwa kuwa tuna idadi kubwa ya wabunge walio wafuasi wetu basi itakapigwa hiyo kura lazima tutaibuka na ushindi.Kwa kutumia njia hiyo tunaweza kumuondoa rais madarakani kwa haraka wakati tukiendelea kufanya uchunguzi kuwabaini watu anaoshirikiana nao huku mambo yetu yakienda kama kawaida” akasema mmoja wa wajumbe Hilo nalo ni wazo zuri mno.Nitakaa na kamati ya uongozi tutalijadili hilo pia na kwa kuwa tunao mabingwa wa sheria tutawashirikisha na watatushauri nini cha kufanya kwani jambo hili ni la kisheria zaidi” akasema mwenyekiti Kilikuwa ni kikao kirefu ,mawazo mengi yakatolewa na kujadiliwa na hadi mwisho wakaafikia mambo kadhaa wanayotakiwa kuyafanya na kikao kikafungwa


yari ni saa tisa za usiku kwa saa za Dubai ambayo ni sawa na saa nane kwa saa za afrika mashariki ,katika chumba kimoja ndani ya hoteli kubwa ya kifahari msichana mmoja mrembo Maria alikuwa amejilaza kitandani akiwa na kompyuta yake ndogo.Mawazo mengi yalimsumbua “ Ni usiku mwingi sasa ,Austin hajapiga simu na mtandaoni hapatikani.What happened ? Kwa nini hajanipigia simu? Hii si kawaida yake.Hawezi kupitisha siku bila ya kuwasiliana nami.Amepatwa na tatizo gani? Au ni janja yake ya kutotaka mawasiliano nami kwa vile nilimwambia nataka kwenda Dar es salaam? Ninahisi bado hataki niende Tanzania kwa sababu hakuonyesha kupendezwa na wazo hilo.Kuna kitu gani anakificha? Ana mwanamke mwingine Dar es salaam na hataki nijue? Akajiuliza Maria akainuka na kuketi. “ Sitaki kuwaza mambo hayo ya Austin kuwa na mwanamke mwingine kwani sijui nini kitatokea kwa namna ninavyompenda .Sijawashi kumpenda mwanaume kama nimpendavyo Austin.Niliapa kufanya jambo lolote kwa ajili yake kwa hiyo lazima niende Dar .Lazima nijue maendeleo yake.Sintomweleza kama ninakwenda lakini atashangaa niko Dar es salaam.Anasema kuna hatari , mimi siogopi hatari yoyote.Ngoja niwasiliane kwanza na baba nimtaarifu kuwa kesho ninakwenda Dar es salaam na yeye ndiye atakayenipa maelekezo ya mahala ninakoweza kumpata Austin” akawaza Maria akazitafuta namba za simu za hoteli aliyofikia baba yake akapiga. “ hallow “ ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Maria akaitambua ilikuwa ya baba yake. “ Hallow baba.It’s me Maria” “Hello Maria hujalala bado? Najua ni usiku mwingi hapo Dubai “ “ Ndiyo baba ni saa tisa za usiku hapa Dubai.Nimekosa kabisa usingizi” “ Oh my princess pole sana” “ Ahsante baba” akasema Winnie halafu ukimya mfupi ukapita “ Baba nimekupigia kukutaarifu kuwa baada ya kumaliza majukumu yangu hapa Dubai kesho ninakwenda Dar es salaam.Nataka unielekeze mahala nitakapomuona Austin” “Unakwenda Dar es salaam? Akauliza Boaz “Ndiyo baba nakwenda Dar es salaam kesho kuonana na Austin” “Austin anafahamu kuwa unakwenda huko ?

“Ndiyo anafahamu ila sijamueleza lini ninakwenda.I want to surprise him” akasema Maria.Boaz akafikiri kidogo na kusema “Maria mimi pia nimepata dharura nahitajika Dar es salaam mara moja kwa hiyo kesho nitaondoka hapa Comoro kuelekea huko.Tutakutana Dar es salaam na halafu tutaonana na Austin “ “Ahsante baba tutaonana hiyo kesho” akasema Maria na kukata simu “Huu ndio wakati niliopanga Austin aanze kunifanyia kazi zangu.Nilimuokoa toka mikono ya Alshabaab nikamtunza na kwa kujua thamani yake na nilijua iko siku atanisaidia na wakati wenyewe ni sasa gatha aliwasili katika makazi yao akitokea katika kikao na kuelekea moja kwa moja chumbani .Tayari Ernest Mkasa alikwisha rejea muda mrefu alikuwa kitandani amejilaza akitafakari.Hakuwa na usingizi kutokana na mawazo mengi.Mara tu mke wake alipoingia chumbani akainuka na kukaa,wakatazamana kwa sekunde kadhaa halafu Ernest akasema “ Leo ni siku ya mwisho kurejea hapa nyumbani mida kama hiyo.Nitatoa amri ukichelewa kurudi zaidi ya saa tatu usiku usiruhusiwe kuingia na urudi ulikotoka” akasema Ernest kwa ukali “ Usinitishe Ernest ,si wewe au mtu yeyote anayeweza kunizuia nisiingie humu ndani muda wowote nitakao” akasema Agatha naye kwa ukali “ Tambo hizo zilikuwa zamani na kuanzia sasa utafuata amri zangu na kama utashindwa kufuata kile ninachokiamuru basi mlango uko wazi unaweza kuondoka zako lakini kama unataka kuendelea kuishi humu ndani utafuata sheria na taratibu na kwa hapa ikulu mimi ndiye mwenye kauli ya mwisho ninachokiamuru lazima kitekelezwe!!! Agatha akamtazama mumewe kwa hasira na kusema “ You are doing a very big mistake Ernest.You don’t know what you’ve done” akasema Agatha “ I know what I’m doing tena ninajilaumu kwani haya niliyoyafanya nimechelewa sana.Sikutakiwa kuwaacha wewe na hao wenzako mkaitawala nchi hii.Hilo ni kosa ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote hadi siku naingia kaburini” “ I trusted you Ernest.Sikutegemea kama siku moja ungeweza kutusaliti kiasi hiki.Uliaminiwa ukapewa nafasi ya urais lakini umechagua kutugeuka .Kwa hiki ulichokifanya umetengeneza uadui mkubwa kati yetu nawe na unafahamu utaratibu wetu kwa wale wanaotusaliti” “ Naomba kwanza nikuweke wazi kwamba sikuwahi kufikiria wala sikutaka kuwa rais.Mlinilazimisha nishike nafasi hii kwa maslahi yenu.Ulikubali kuwatoa kafara wanao wa kuwazaa mwenyewe.Jambo hilo linaniuma sana na leo nataka nikuweke wazi kwamba ninajua kukutana na mwanamke kama wewe.Kila usiku ninasikia sauti za wanangu uliowatoa kwa huyo shetani wako unayemuabudu.I swear I’ll never forgive you for that.Wewe na wenzako mliwaua wanangu ili kunishinikiza nikubali kuwa rais.Nilikubali wakati ule kwa kuwa nilikuwa na woga wa kufa lakini kwa sasa siogopi tena.Hata leo mkitaka kuniua fanyeni hivyo lakini mkae mkijua kwamba wakati wenu umefika na hamna nafasi tena ya kufanya ushenzi wenu hapa Tanzania.Kuanzia sasa mimi na wewe ni maadui na hautalala tena katika chumba hiki.Tayari kuna chumba kingine kimeandaliwa kwa ajili yako.Kwa ufupi tu ni kwamba me and you we’re over.We’re finished.Hakujawahi kuwa na mapenzi kati yetu,its all lies.One more thing kwa kukutunzia heshima yako nitakuacha uendelee kuishi hapa ikulu lakini baada tu ya kumaliza kipindi changu kila mmoja ataenda kuishi maisha yake.Nadhani umenielewa vizuri” akasema Ernest kwa ukali
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Ernest unajidanganya kwa kujifanya malaika wakati we’re both devils.Ulikunywa kikombe cha damu ya mwanadamu na kwa kitendo kile ulibatizwa kuwa mfuasi wetu kwa hiyo basi usijidanganye kuwa unaweza kupambana nasi.Wewe bado mdogo sana na utapeperushwa kama tiara inavyopeperushwa na upepo.Kufumba na kufumbua utapotea kama matone ya mvua yanavyopotea ardhini .Nakushauri Ernest muda bado unao jirudi ,utubu na utasamehewa.Bila kufanya hivyo sintakuwa na namna nyingine ya kukusadia.Mimi pekee ndiye mwokozi wako.Kwa taarifa yako nimetoka katika kikao cha kujadili hiki ulichokifanya na wajumbe waliamua uuawe kama sheria zinavyosema lakini mimi nikasimama na kukutetetea kwa hiyo bado unao muda Ernest jirudi” “ You are Idiot!!! Akasema Ernest “ Mwokozi wangu ni Yesu pekee ambaye alitufia msalabani.Nakubali nimemkosea sana lakini nimeamua kujirudi kwake na kumkiri kuwa ndiye bwana na mwokozi wa maisha yangu na nitamtumikia yeye peke yake.Naomba utoke chumbani kwangu haraka sana!! Akafoka Ernest na kumshika Agatha mkono akamtoa mle chumbani akampeleka katika chumba kingine “ Nani kambadilisha Ernest namna hii? Katoa wapi ujasiri huu? Anajiamini na haogopi chochote.” akawaza Agatha baada ya kuingia katika chumba alimohamishiwa.Mara akakumbuka kitu na kuinamisha kichwa “ Ernest amenikubumbusha kuhusu watoto wangu na kwa mara ya kwanza baada ya miaka kupita ninahisi kuumizwa na jambo nililolifanya” akafuta machozi “ Lakini sipaswi kujilaumu kwa hiki nilichokifanya .Nilifanya vile kwa ajili ya nchi hii.Tanzania lazima ibadilike.kwa ajili ya wanangu ambao ni mashujaa wa mabadiliko hayo sintorudi nyuma.Nitaendelea kupigania mabadiliko hadi nihakikishe Tanzania imebadilika.” Akawaza Agatha. Agatha alipotoka mle chumbani Ernest akapanda tena kitandani “ Agatha ni adui yangu mkubwa.Yeye ndiye aliyenifanya nikubaliane na mashetani wenzake.Najua Alberto’s watamtumia sana Agatha ili kukabiliana nami lakini hawataweza kwani nitahakikisha ninakuwa mbali naye na njia pekee ya kujiweka mbali naye ni kukata kabisa mawasiliano.Hakuna kinachotuunganisha tena ,kilichobaki ni ndoa iliyoko katika makaratasi.” Akawaza Ernest akamkumbuka Monica na kutabasamu “Toka Janet aliponieleza kuwa Monica ni mwanangu nimekuwa na hisia kubwa kuwa jambo hili ni la kweli.Endapo vipimo vitaonyesha kweli Monica ni mwanangu nitatumia gharama zozote kumlinda.” akawaza Ernest na kujilaza kitandani “ Siku ya kwanza ya mapambano imekwisha ngoja nilale nisubiri siku ya kesho.” Akawaza Ernest na kuanza kuutafuta usingizi KINSHASA – DRC Miale ya jua ilipenya dirishani na kukifanya chumba kiwe na nuru ya kuvutia asubuhi hii.Monica alifumbua macho na kujikuta akitazamana na sura yenye tabasamu ya David Zumo “ Hallow malaika wangu” akasema David huku akitabasamu “ hallow David,umeamkaje? “ Nimeamka salama malaika wangu.Usiku wako ulikuaje? “ Nilikuwa na usiku mzuri sana David” akajibu Monica.Bado David Zumo aliendelea kumtazama “ Mbona unanitazama hivyo David? Akauliza Monica huku naye akitabasamu “ Monica nashindwa nikueleze nini mpenzi wangu kwa namna ulivyoyafanya maisha yangu yakawa na furaha.Nakupenda mno Monica.Tafadhali naomba usibadilishe mawazo ya kuolewa na mimi ” Monica akatabasamu na kusema “ Usiogope David siwezi kubadilisha mawazo.Tayari nimekwisha fanya maamuzi na kukubali kuolewa nawe kwa hiyo mimi ni wako daima” akasema Monica.David akambusu akamtazama kwa makini na kusema “ Monica naomba nikuulize kwa mara nyingine tena .Japokuwa umekubali kuolewa nami lakini je ndani ya moyo wako ninayo nafasi au nitakuwa na nafasi? Monica huku akikichezea kifua cha David akasema “ kama nilivyokujibu uliponiuliza mara ya kwanza kwamba tulipe nafasi suala hili kwani tumefahamiana ndani ya kipindi kifupi na ndani ya muda huo mfupi mambo makubwa yamefanyika.Nimefanya mapenzi kwa mara ya kwanza,nimekubali kuolewa nawe .Hiyo ni ishara tosha kuwa unayo nafasi kwangu kwani kama usingekuwa na nafasi nisingekubali kuyafanya hayo mambo makubwa.Japokuwa bado nafasi yenyewe ni ndogo lakini kadiri tutakavyoendelea ndivyo utakavyozidi kujijenga ndani ya moyo wangu kwa hiyo basi usiwe na wasi wasi” “ Ahsante Monica kwa kuwa muwazi.U mwanamke wa pekee sana.Nakuahidi nitajitahidi kuwa mwanaume bora kwako na siku zote uso wako hautakauka tabasamu” Monica akatabasamu na kumbusu David “ Una maneno matamu sana.Ahsante kwa maneno hayo mazuri ambayo naamini yametoka moyoni.Halafu David nataka kufahamu kuhusu Yule rafiki yangu niliyekuomba unisaidie kama zoezi lile lilifanikiwa.Nina wasiwasi mwingi kuhusu maisha yake” “Oh ! samahani sana Monica nilisahau kabisa kumuuliza rais wa Tanzania kama suala lile lilifanikiwa.Ngoja nimpigie sasa hivi” akasema David na kuchukua simu akatafuta namba za Ernest Mkasa akampigia “ Hallow David “ akasema Ernest alipopokea simu “ Habari za asubuhi Ernest “


 “ habari nzuri David ,habari za Kinshasa? “ Huku kwema kabisa.Ernest nimekupigia ili kufahamu kuhusu ule msaada niliokuomba wa kumuondoa Yule kijana hospitali,je lile zoezi lilifanikiwa? “ Ndiyo David lile zoezi lilifanikiwa.Samahani sana sikukutaarifu mapema.Dr Marcelo ameondolewa pale hospitali na kwa sasa amehifadhiwa sehemu salama tukisuburi maelekezo yako” “ Ahsante sana Ernest.Ninaomba uendelee kumuhifadhi sehemu salama nitakupa maelekezo hivi karibuni.Naomba unijulishe kama kuna gharama zozote zinahitajika” “ usijali David hakuna gharama zozote kuwa na amani” “ Ahsante sana Ernest” akajibu David na kukata simu akamgeukia Monica “ Monica usiwe na wasi wasi tena malaika wangu lile zoezi limefanikiwa na rafiki yako yuko sehemu salama kwa sasa” Monica akamkumbatia David kwa furaha na kumbusu “ Ahsante sana David .Hiki ulichokifanya ni kitu kikubwa mno kwangu” akasema Monica “ Monica kwa ajili yako niko tayari kufanya jambo lolote .Hata hivyo rais anasubuiri maelekezo ya nini kitafuata baada ya kumuondoa Marcelo hospitali.Umepanga kumsaidiaje rafiki yako? “ Kitu kikubwa nilichokihitaji kwanza ni kumtoa hospitali na baada ya hapo nitajua nini kitafuata pale nitakaporejea Dar es salaam.” “ Ukihitaji msaada wa aina yoyote ile usisite kunitaarifu” “ Nitakutaarifu David kila pale nitakapohitaji msaada” akasema Monica DAR ES SALAAM – TANZANIA Habari kubwa iliyoliamsha taifa asubuhi hii ni hotuba ya rais aliyoitoa usiku .Maamuzi aliyoyafanya yaliendelea kuwa gumzo kila kona ya nchi.Wengi walipiga simu katika vituo vya redio na televisheni wakimpongeza rais Ernest Mkasa kwa maamuzi yake ya busara kuhusiana na muswada ule wa haki za binadamu pamoja na kulivunja baraza la mawaziri.Wakati mjadala wa maamuzi yale ya rais ukiendelea ,kurugenzi ya mawasiliano ikulu ikatoa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo ilizidi kuwashangaza wengi.Taarifa hiyo ilieleza kwamba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amemvua wadhifa mkuu wa majeshi na Jenerali Bonifasi Kandima na papo hapo amempandisha cheo Luteni jenerali Lameck Msuba kuwa jenerali na kumteua kuwa mkuu wa majeshi kushika nafasi iliyoachwa wazi na jenerali Bonifasi.Uteuzi huo unaanza mara moja.Taarifa hii ilizidi kuukoleza moto wa mjadala uliokuwa ukiendelea. Austin akiwa sebuleni akifuatilia habari zilizoliamsha taifa pamoja na uchambuzi wa magazeti ,mara mtangazaji aliyekuwa akichambua kurasa za magazeti akasitisha na kutangaza habari iliyowafikia pale muda huo kuhusiana na rais kutengua uteuzi wa mkuu wa majeshi na kumteua jenerali Lameck Msuba kuwa mkuu mpya wa majeshi.Austin akaruka kwa furaha “ Good !! Very good.Sasa vita imeanza rasmi” akaongea mwenyewe pale sebuleni “ Vita gani Austin? Akauliza Dr Marcelo baada ya kuingia pale sebuleni na kumkuta Austin akizungumza mwenyewe kuhusiana na vita.Austin akastuka na kugeuka akajikuta akitazamana na Marcelo “ Marcelo,vipi maendeleo yako? Akauliza “ Ninaendelea vizuri Austin.Nimekusikia unaongea mwenyewe kuhusu vita,ni vita ipi hiyo unaiongelea? “ Forget about that.Nilikuwa natazama taarifa ya habari rais ameteua mkuu mpya wa majeshi” “ Austin nini kinaendelea? Jana rais kaufuta muswada wa haki za binadamu pamoja na kulivunja baraza la mawaziri,leo kamvua wadhifa mkuu wa majeshi ,nini kinaendelea? Akauliza Dr Marcelo.Kabla Austin hajajibu Marcelo akauliza tena “ Who are you Austin? Kuna kitu gani kinaendelea kati yako na rais? “ Dr Marcelo itakuwa vyema endapo hutajihusisha na masuala yoyote yanayohusiana na mimi wala rais.Kikubwa unachopaswa kukitilia mkazo kwa sasa ni kupona na kuhakikisha wale wote wanaokuwinda wakuue wanapatikana.” Akasema Austin.Dr Marcelo akamtazama Austin kwa makini na kusema “ Austin kuna jambo ambalo limeninyima usingizi kabisa.Kama nilivyowaeleza jana kwamba nimestuka sana kusikia eti rais wa Congo ndiye aliyemuomba rais wetu anisaidie kunitoa pale hospitali.Sijapata usingizi usiku wa leo nikitafakari namna David Zumo alivyoingia katika hili suala langu.Sifahamiani naye na wala hatuna mahusiano yoyote ya kindugu.Kwa kuwa uko karibu na rais naomba unisaidie kumuomba amuulize David Zumo amezipata wapi taarifa zangu.Nahitaji sana kufahamu.Au kama kuna uwezekano niongee na David moja kwa moja kwa simu.Yawezekana kuna jambo limejificha hapa na silifahamu” “ Sawa Marcelo nitaongea na rais na kuufikisha ujumbe wako .

Halafu kuna jambo lingine ni kwamba leo nitatoka kuna sehemu ninakwenda.Utabaki peke yako hapa kwa hiyo usiogope.Hapa ni sehemu salama na hatari yoyote ikitokea nitajua na nitajua nini cha kufanya.Usijaribu kutoka nje kama humu humu ndani na usimfungulie mlango mtu yeyote Yule zaidi yangu.” Akasema Austin “ Nimekuelewa Austin.Nitakupa pia orodha ya dawa ninazozihitaji ukaninunulie ” akasema Marcelo na kuelekea chumbani kwake akimuacha Austin akiandaa stafstahi. “ Suala la David Zumo kufahamu kuwa ninataka kuuawa bado linanishangaza mno.Mtu pekee ambaye nilimuomba msaada ni Monica lakini toka nilipomueleza jambo hili sijamuona tena .Amepotelea wapi? Au yawezekana aliogopa kujiingiza katika masuala haya ya hatari .Naanza kuhisi kuwa tayari nimekwisha mpoteza Monica.Kwanza aligundua nina saratani ya damu na halafu nikapigwa risasi na nikamuomba anisaidie kunitorosha hospitali.Naweza kukiri kwamba nilimtwisha mzigo mkubwa tofauti na uwezo wake.Lakini nilifanya hivyo kwa kuwa sikuona mtu mwingine ninayeweza kumuamini katika jambo nyeti kama hili.Ninamlaumu sana baba kwani yeye ndiye chanzo cha haya yote.Ninaamini matatizo yote haya yamesababishwa na kile kitabu.Kitabu kile kilikuwa na nini ndani yake? Naanza kuhisi kuna jambo kubwa limejificha ambalo nahitaji kulifahamu.Ni nani aliingia chumbani kwangu akachukua kitabu kile?Mtu ambaye nilipewa namba nimpigie ni nani? Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza kunisaidia kupata majibu ya maswali haya ambaye ni Austin.Nitaongea naye nimueleze ukweli na nitamuomba anisaidie kuutafuta ukweli.Anaonekana ni mtu jasiri katika kazi yake na mwenye mbinu nyingi.Kwa mbinu aliyoitumia ili kunitoa pale hospitali inaonyesha ni jinsi gani alivyo mahiri “ akawaza Marcelo na kujikuta akizama zaidi mawazoni “ Austin na rais Ernest wana jambo gani la siri? Nilistuka sana kumuona rais hapa tena akiwa katika muonekano wa tofauti kabisa kiasi cha kumfanya iwe vigumu kutambulika.Ni wazi rais hataki kujulikana kama anakuja hapa usiku.Kama ni hivyo lazima kuna jambo linaloendelea kati yao.Austin ni nani? Anaweza kuwa mlinzi wa siri wa rais ? Akajiuliza “ Ngoja niachane na mambo yao nielekeze nguvu katika masuala yangu ila jioni ya leo nitazungumza na Austin na nitamueleza kwa kirefu suala langu na kumuomba anisaidie kwani sielewi hatima ya maisha yangu “ akaendelea kuwaza Marcelo Wakati Austin akifanya maandalizi kwa ajili ya kuanza kazi ya pili ya kutafuta ukaribu na Monica,katika ikulu ya Dar es salaam hali ilikuwa tofauti na siku nyingine.Maamuzi yaliyoendelea kufanywa na rais yaliwastua wengi.Wengi walijaribu kujiuliza sababu ya maamuzi yale makubwa lakini wengi hawakujua kwa nini rais alichukua maamuzi yale . Ernest Mkasa aliingia ofisini kwake mapema mno tofauti na kawaida yake.Alikuwa na mambo mengi ya kufanya siku hii “ Siku mpya na mapambano yanaendelea.Habari hii ya maamuzi niliyoyafanya imesambaa dunia nzima .Naamini hivi sasa maadui zangu watakuwa wanajipanga ili kukabiliana nami.Natakiwa kufanya mambo haraka haraka kuwadhibiti.Nitauzingatia ushauri wa Austin kubadilisha kikosi cha kumlinda rais kwani picha niliyoiona jana si nzuri kabisa. Alberto’s wanaweza wakaniua wakati wowote .Hata hivyo wapo walinzi wawili ambao wataendelea kuwa walinzi wangu Evans na Winnie.Siwezi kumuacha Winnie katika orodha ya walinzi wangu kwani licha ya kuwa ni mlinzi wangu lakini amekuwa ni mfariji wangu kwa muda mrefu sasa.” Akawaza Ernest na kutabasamu kwa mbali “ Ninashukuru kwa ujio wa Austin.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni kijana jasiri asiyeogopa na mwenye akili nyingi.kwa sababu yake nimepata ujasiri wa kuja kufanya haya niliyoyafanya.kwa muda mrefu nilikuwa nimefikiria kuanzisha mapambano na Alberto lakini sikuwa nimepata mtu sahihi wa kushirikiana naye.Kwa sasa baada ya kumpata Austin lazima niwafutilie mbali mashetani hawa” akawaza Ernest “ Kinachonila akili kwa sasa ni nani nimteue awe waziri mkuu? Nahitaji haraka sana kuunda serikali lakini bado mpaka sasa sijampata mtu ambaye anaweza kuwa waziri mkuu.Asilimia kubwa ya wabunge ni wafuasi wa Alberto’s na sitaki kurudia makosa. sitaki tena kuwa na Alberto katika serikali yangu.Nitaanza kwanza na waziri mkuu.Nataka awe ni mtu ninayemuamini .Kichwani kuna majina mawili tu ambayo yanazunguka.Austin na Mukasha.Austin angefaa sana kuwa waziri mkuu tena kijana mzalendo na mchapakazi lakini yeye ndiye ninayemtegemea asimame mstari wa mbele kuongoza mapambano haya.Nikimtoa Austin ninabaki na Mukasha.Huyu amefanya kazi ikulu kwa muda mrefu,ni mtu mzuri mwadilifu na muaminifu.Anafaa sana kuwa waziri mkuu.Nitaongea naye kuhusu jambo hili na kumuomba anisaidie.Endapo tutamaliza mapambano haya salama Austin nitamtafutia nafasi nyingine serikalini aidha uwaziri au nimteue awe mkuu wa usalama wa taifa” akawaza Ernest akamuita Evans mlinzi wake anayemuamini sana “ Evans wewe ni mmoja wa watu ninaowaamini mno” akasema Ernest “ Ahsante mheshimiwa rais” akajibu Evans “ I know at any second you are ready to take a bullet for me.” “ Yes Mr President “ akajibu Evans kwa adabu. “ Ahsante sana kwa hilo.Evans nimekuita hapa kukueleza kwamba kwa sasa ninapitia wakati mgumu sana katika uongozi wangu.Hiki ni kipindi ambacho nakuhitaji mno.Nahitaji ulinzi wa kutosha na wa uhakika kwa ajili hiyo basi kuna mabadiliko kidogo nitayafanya katika kikosi cha kumlinda rais.Nitaunda kikosi kidogo cha watu wachache ambacho utakiongoza wewe.Nitakufahamisha baadae kwa kina zaidi kuhusu jambo hili lakini kwa sasa kuna sehemu nataka nikutume.Nataka uende pale katika ofisi za Ernest group of campanies utakutana na mtu mmoja anaitwa Susan yombo kuna mzigo atakupatia nataka uupeleke kule hotelini ukauhifadhi katika chumba changu.” “ sawa mheshimiwa rais nitafanya hivyo ulivyoagiza” akasema Evans kwa ukakamavu “ Ahsante Evans .Nitakuwa na maongezi nawe marefu jioni ya leo.” Akasema Ernest na evans akatoka kuelekea mahala alikotumwa


saa tano kasoro dakika saba Austin aliwasili zilipo ofisi za kampuni ya kubuni mavazi inayomilikiwa na Monica mwamsole.Lilikuwa ni jengo zuri lenye madhari ya kuvutia mno.Alifunguliwa geti akaingia ndani na kuelekea sehemu ya maegesho.Katika bustani nzuri baadhi ya warembo walikuwa wanapiga picha za mitindo mbali mbali ya mavazi yaliyobuniwa na wabunifu mahiri wa kampuni hii. “ Wow ! what a paradise ! akasema Austin kwa sauti ndogo akiwa ndani ya gari “ Sehemu nzuri ,watoto wazuri yaani kila kitu hapa ni kizuri.” Akawaza Baadhi ya warembo waligeuza shingo zao kulitazama gari lile la kifahari alilokuwa nalo Austin.Alijitazama katika kioo cha gari akachukua uturi akajipulizia na kutabasamu “ Get ready Monica I’m coming for you” akawaza na kufungua mlango wa gari akashuka.Austin alikuwa amependeza kupita maelezo.Mara tu aliposhuka garini akaangaza angaza pande zote kisha taratibu akafuata kibao kilichoelekeza sehemu ya mapokezi.Kwa sekunde kadhaa zoezi la upigaji picha lililokuwa likiendelea bustanini lilionekana kusimama kwani kila mtu aligeuka kumtazama Austin.Hakuwajali akaendelea kupiga hatua kuelekea mapokezi ambako aliwakuta akina dada wawili warembo wenye nyuso changamfu.Akawasalimu wakamuitikia kwa ukarimu mkubwa na kumkaribisha ,akawaeleza shida iliyompeleka pale “ Samahani kaka,Monica amepata dharura amesafiri na hatuna uhakika atarudi lini lakini yupo msaidizi wake ambaye hufanya shughuli zote za Monica akiwa hayupo.Ukimuona huyo ni sawa na kuonana na Monica” akasema msichana Yule wa mapokezi Austin akapeleka kuonanana Linah msaidizi wa Monica. “ karibu sana kaka ,mimi naitwa Linah ni msaidizi wa Monica ” akasma Linah “ Nafurahi kukufahau Linah.Mimi naitwa Austin.Ni mkurugenzi wa utawala na fedha wa kampuni ya A.A Safaris.Hii ni kampuni ya utalii inayomilikiwa na mtanzania lakini makao yake makuu yako nchini Afrika kusini ila hivi karibuni tuna mpango wa kufungua ofisi hapa nyumbani Tanzania”akasema Austin “ Karibu sana Austin.Tunafurahi umetutembelea ofisini kwetu” akasema Linah “ Ahsante Linah.Kilichonileta hapa kwenu leo ni kwamba kampuni yetu imekuwa ikisaidia miradi mbali ya kijamii na tunalenga sana jamii masikini.Baada ya kufanya utafiti tumegundua kwamba mnayo taasisi ambayo inajishughulisha na miradi ya kijamii hivyo tukaona itakuwa vyema endapo tutaungana na taasisi yenu ili uweza kufikisha mchango wetu kwa jamii.Kwa hiyo dhumuni la kufika hapa leo ni kuonana nanyi ili tuzungumze suala hili na kuona namna tunavyoweza kufanya kwa pamoja miradi kadhaa ya kijamii” akasema Austin “ Austin kweli tunayo taasisi yetu inayojishughulisha kuwasaidia watoto na wazee wasiojiweza .lakini kwa bahati mbaya mimi sina mamlaka yoyote kwa upande huo.Itakuwa vyema sana endapo utalizingumza suala hilo na Monica mwenyewe.Kwa sasa Monica amepata dharura yuko nje ya nchi utaniachia mawasiliano yako ili atakapokuja nikujulishe muonane”


lini anatarajia kurejea nchini? “ Sina uhakika ni lini lakini hatachukua muda mrefu kwani kuna mradi wa ujenzi wa shule unatarajia kuanza na anayesubiriwa ni yeye pekee” “ sawa Linah basi nitakuwa nikifika hapa mara kwa mara kujua kama amerudi” “ Usisumbuke Austin nipe mawasiliano yako na nitakupigia simu kukufahamisha pindi Monica atakaporejea” “ Uhhm !! kwa bahati mbaya bado sina namba za simu ninayotumia kwa hapa Tanzania.Japokuwa mimi ni mtanzania lakini kwa sasa makazi yangu ni Afrika kusini na tayari nina uraia wa kule kwa hiyo hapa Tanzania nimekuja kama mgeni.Naomba unipatie wewe mawasiliano yako na nitakutafuta “ “ Kwani hapa dar es salaam umefikia hoteli gani? Akauliza Linah “ Sijafikia hotelini ,nimefikia kwa rafiki yangu” “ Hauna ndugu hapa dar ? “ Naweza sema kwamba sina ndugu.Wazazi wangu wamekwisha fariki kitambo na ndugu yangu niliyezaliwa naye tumbo moja anaishi nje ya nchi” “ Pole sana kwa kuwapoteza wazazi wako “ “ Ahsane sana Linah” Linah akampatia Austin kadi yake ya biashara yenye mawasiliano yake na halafu akaandika namba nyingine ya simu katika karatasi “ Hii ni namba yangu binafsi ambayo unaweza ukanipata muda wowote .Unaruhusiwa kupiga kwa saa ishirini na nne” “ sawa nitafaya hivyo Linah” Akasema Austin huku akiinuka “ By the way ,kabla hujaondoka hutajali endapo nitakuzungusha sehemu mbali mbali za kampuni yetu ili ufahamu namna kazi zinavyofanyika hapa? Akauliza Linah huku akitabasamu.Austin akakubali na Linah akamzungusha sehemu mbali mbali za kampuni yao halafu akamsindikiza hadi kaika maegesho ya magari “ Linah nashukuru sana kwa makaribisho mazuri .Watu wa hapa wote ni wakarimu sana.Nina imani tutaonana tena hivi karibuni” akasema Austin “ Uhhm ! Austin I know you are alone here so if you need someone to talk to ,someone to hang out with, just give me a call.I like to hang out with friends” akasema Linah huku akitabasamu

 “ Usijali Linah,nitakapokuwa na nafasi nitakutafuta .Thanks again” akajibu Austin na kuingia katika gari lake akaondoka “ Umekuwa ni mwanzo mzuri .Ama kweli kampuni hii imebahatika kuwa na warembo wasio hata na chembe ya kasoro.Japokuwa sijabahatika kuonana na Monica lakini naamini mambo yatakuwa mazuri kwani Linah ambaye ni mtu wa karibu na Monica amenionyesha kila dalili za mafanikio.Linah ni mwanamke mzuri ,amenipokea kwa uchangamfu kana kwamba tunafahamiana muda refu”akawaza Austin akiwa garini “ Sifahamu kama ndivyo alivyo au ni kwangu tu lakini uchangamfu wa Linah naona kama ulipitiliza .Anaonekana kama vile kavutiwa na mimi .Natakiwa kuwa makini sana nisije anguka katika vishawishi na kujikuta nikimsaliti mpenzi wangu Maria.”
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipomkumbuka mpenzi wake akastuka “ Jana sikuwasiliana na Maria, naamini alisubiri sana nimpigie ili anieleze kuhusu safari yake kama alivyoahidi kwamba baada tu ya kukamilisha mambo yake atakuja Tanzania.Maria hatanii katika hili na lazima atakuja.Siwezi kumruhusu akaja Tanzania na kuyaweka hatarini maisha yake.Huku niliko niko katika hatari kubwa na siko tayari kumuona mwanamke ninamyependa akiingia katika hatari.Njia pekee ya kumzuia asije Tanzania ni kwa kukata mawasiliano naye kwa sasa ili hata kama ataamua kuja basi hatajua anipate vipi.Inaniuma sana kumfanyia hivi Maria lakini sina namna” akawaza KINSHASA – DRC Msafara mrefu wa magari ukiwa chini ya ulinzi mkali uliwasli katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa.Huu ulikuwa ni msafara wa mke wa rais wa Congo bi Pauline Zumo.Ndani ya gari la kifahari la mke wa rais walikuwemo Pauline na Monica.Pauline alikuwa anamsindikiza Monica uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurejea Dar es salaam “ Monica sipati maneno mazuri ya kuelezea furaha niliyonayo kwa kuja kututembelea na kwa yale mambo yote mazuri tuliyoyafikia.Ahsante sana Monica.” Akasema Pauline wakati wakiiingia uwanja wa ndege.Huku akitabasamu Monica akasema “ Hata mimi nashukuru sana Pauline kwa ukarimu wenu mkubwa. Mioyo yenu imejaa upendo usioelezeka.Siku zote nitawaweka moyoni mwangu.Ahsanteni sana” akasema Monica.Pauline akainamisha kichwa kana kwamba kuna kitu anakifikiri halafu akasema “ Monica kabla hatujashuka garini kuna siri nataka nikupe” akasema Pauline na kutazama Monica kwa makini kwa sekunde kadhaa akasema

 “ Monica jambo nililolifanya la kumshawishi mwanamke mwenzangu akubali kuolewa na mume wangu si jambo rahisi kufanywa na mwanamke yeyote na nina imani japokuwa umekubali lakini una maswali mengi unajiuliza ni kwa nini nimefanya hivi.Pamoja na changamoto zile zote nilizokueleza awali lakini kuna sababu nyingine kubwa nyuma yake ambayo sikuwahi kukueleza” akasema Pauline na kunyamaza kimya akamtazama Monica kisha akaendelea “ Nitakufa hivi karibuni Monica” “ Nini?..!!! Monica akastuka sana “ Rudia ulichokisema Pauline” akasema Monica huku sura yake ikionyesha mstuko mkubwa “ Monica tafadhali naomba usistuke .Nimeona nikueleze ukweli wote uufahamu.Nitakufa hivi karibuni ,nina muda mfupi sana wa kuishi hapa duniani.Ninasumbuliwa na saratani ya ubongo na kwa mujibu wa madaktari ni kwamba sehemu kubwa ya ubongo wangu tayari imekwisha athirika na kwa hiyo hakuna matibabu yanayoweza kuniponya tena.Wiki ijayo ninakwenda nchini Ufaransa kufanyiwa upasuaji mwingine wa kichwa lakini kwa mujibu wa madaktari wanasema hawana uhakika kama nitaamka tena endapo nitafanyiwa upasuaji huo.Nimeamua tu nifanyiwe upasuaji huo kwani siwezi kukaa tu nikisubiri kifo changu,lazima niendelee kuyapigania maisha yangu.Hakuna ajuaye pengine unaweza ukatokea muujiza nikapona.”akasema Puline na kushindwa kujizuia machozi kumtoka.Monica naye machozi yakaanza kumporomoka “ Monica” Pauline akaendelea “ Monica inawezekana haya yakawa ni mazungumzo yetu ya mwisho kwani sina uhakika wa kutoka salama katika chumba cha upasuaji kwa hiyo endapo hatutaonana tena tafadhali yazingatie yale yote tuliyokubaliana.Wewe ni mwanamke wa pekee kabisa ambaye ninaamini hata nikifa leo nitakuwa na uhakika kwamba mwanaume nimpendaye atakuwa katika mikono salama na atakuwa na furaha.” “ Pauline...” Monica akataka kusema kitu lakini Pauline akamzuia “ Monica najua nimekushtua sana lakini lazima nikwambie ukweli ili ufahamu sababu kubwa ya kusisitiza uolewe na David.Hivyo nakuomba usibadili mawazo yako.David ni mtu mzuri anayejua kupenda na anayejali .Mimi ndiye niliyemtuma atafute mwanamke wa kuishi naye baada ya kugundua kwamba sintakuwa na maisha marefu.

Katika mamilioni ya wanawake wote duniani amekuona wewe pekee.Narudia tena kukuomba Monica kubali kuolea na David kwa moyo mmoja na utakuwa na furaha” akasema Pauline huku wote wawili wakitokwa na machozi “ Tafadhali usilie Pauline.Mambo hayatakuwa kama unavyohisi.Mungu yuko nawe na utapona.Endapo mambo yatakuwa tofauti basi mimi nitaolewa na David kama tulivyokubaliana lakini Pauline hupaswi kukata tamaa .Lazima tupambane kuhakikisha kwa namna yoyote ile unapona” Pauline akatabasamu kwa mbali na kusema “ Ahsante sana Monica kwa maneno hayo ya faraja lakini kuhusu kupona nimemuachia Mungu pekee yeye ndiye mwamuzi katika hili kwani uwezo wa wanadamu umefikia kikomo.” Akasema Pauline wakabaki wanatazamana “ Monica futa machozi na ujiandae kwa safari ndege inakusubiri” akasema Pauline.Wote wawili wakafuta machozi na kushuka garini.Pauline akamuongoza Monica wakaingia ndani ya jengo la uwanja na kuelekea moja kwa moja iliko ndege ya rais iliyokuwa tayari kwa ajili ya kumrejesha Monica Tanzania. “ Monica ni muda wa kuondoka sasa.Kwa mara nyingine ahsante sana kwa kuja nakutakia kila la heri.Ninachokuomba uzidi kuniombea ili ikimpendeza Mungu tuonane tena lakini endapo hatutaonana tena yazingatie yale yote tuliyoongea” akasema Pauline.Macho ya Monica yakalengwa na machozi “ Monica tafadhali usiangushe chozi hata moja.Jikaze na uendelee kutabasamu hadi utakapoingia ndegeni.Kitu cha mwisho mambo haya niliyokueleza ni siri kubwa na hatakiwi mtu yeyote kufahamu” akasema Pauline huku naye akijlazimisha kutabasamu.Monica akatoa miwani myeusi katika mkoba wake akavaa akakumbatiana na Pauline wakaagana halafu akaagana pia na watu kadhaa walioambatana na Pauline akiwemo Pierre Muyeye na taratibu akaanza kupanda ngazi kuelekea ndani ya dege hili kubwa.Alipofika mlangoni akageuka na kupunga mkono kisha akaingia ndegeni.Akapelekwa moja kwa moja katika chumba cha rais na haikuchukua muda mrefu dege likapaa na kuanza kuchana anga kuelekea Dar es salaam.Ilipata saa sita za mchana muda huo “ Toka mwanzo nilihisi lazima kuna sababu iliyomfanya Pauline anisisitize nikubali kuolewa na David .Kumbe ana tatizo kubwa namna hii.Nimeumia sana.” Akawaza Monica na machozi mengi yakamtoka

“ safari yangu ilikuwa nzuri lakini imekuja kutibuka mwishoni baada ya Pauline kunieleza ukweli.Oh my Lord please save her.She deserve to live.Please lord don’t let her die this soon” DAR ES SALAAM – TANZANIA Dege la rais wa Congo linalotajwa kuwa la kipekee kabisa kwa marais wa Africa ,lilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere saa nane na nusu za mchana.Wengi wa waliokuwepo uwanjani walidhani ni rais Davids Zumo amewasili lakini kwa mshangao wa wengi aliyeshuka ndani ya dege hilo alikuwa ni binti malaika mwenye uzuri wa kipekee anayatajwa kuwa mrembo kuliko wote Africa,Monica Benedict mwamsole.Kabla ya kushuka ndegeni,Monica aliwashukuru wahudumu wa ndege pamoja na marubani kwa kumfikisha salama akaagana nao akashuka . Kisha shuka ndegeni aliingia ndani ya jengo la uwanja kukamilisha taratibu halafu akatoka nje ya uwanja na kulakiwa na rafikiye kipenzi Linah.Wakakumbatiana kwa furaha , wakapakia mizigo ya Monica katika gari na kuondoka uwanjani hapo “Welcome home Monica” akasema LInah “ Thank you Linah” akajibu Monica “ By the way how are things here? “ Things are good but I’m so angry.Nina hasira sana nawe Monica.How could you do this to me? Unapata safari na huniagi hata mimi? Nimekukosea nini Monica? Akahoji Linah “ Linah najua nimekukosea sana lakini naomba unisamehe .Kilichotokea ni kwamaba nilipata safari ya dharura nikaondoka na hakuna aliyefahamu kuhusu safari hiyo zaidi ya baba na mama pekee.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halafu kutokana na unyeti wa safari yenyewe sikutaka mtu yeyote afahamu ninakwenda wapi ndiyo maana sikuwasiliana nawe.Nisamehe sana Linah” “ NImejiuliza maswali mengi sana nilipopata simu yako ukaniambia uko ndani ya ndege unarejea Dar.Monica mimi na wewe ni zaidi ya marafiki na hatujawahi kufichana jambo lolote ,imekuaje ukanitenga katika suala hili? Don’t you trust me anymore? “ Siyo hivyo Linah.I trust you with my life.Usijali nitakueleza kila kitu ,wapi niikwenda na kufanya nini.We have lots to talk today” akasema “ Good.I swear I wont forgive you till you tell me everything” akasema Linah Safari iliendelea hadi walipofika nyumbani kwa Monica.Kitu cha kwanza alichokifanya mara tu baada ya kuingia chumbani kwake ni kuwasiliana na Daniel. “ hallow Monica.Welcome home” akasema Daniel baada ya kupokea simu ya Monica “ Ahsante Daniel.Naomba unieleze anaendeleaje Dr Marcelo? Akauliza Monica “ Hujapata habari? Akauliza Daniel “ habari zipi Daniel? Akauliza Monica kana kwamba haelewi chochote kilichotokea. “ Kuna tatizo lilitokea ambalo hadi sasa linaumiza vichwa vya watu wengi” “ Nieleze Daniel ni tatizo gani? “ Ulitokea mlipuko ambao haukuwa na madhara katika hospitali aliyokuwa amelazwa Marcelo na baadae ikagundulika kwamba Marcelo ametoweka na hajulikani alipo.Jambo hili limetushangaza sana.Mpaka sasa hatuelewi ni wapi alipo Marcelo na kama ni mzima au amekufa


Mungu wangu !! akasema Monica kwa mshangao “ Polisi wametoa taarifa gani hadi hivi sasa? Akauliza “ Mpaka sasa jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi wao na bado hawajatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.Familia yake wako kimya nao wanasubiri taarifa toka polisi.Nimeongea na Julieth asubuhi ya leo na ameniambia kwamba mpaa sasa hawana taarifa zozote kuhusiana na Marcelo.Hilo ndilo jambo lililotokea wakati ukiwa safarini Monica.By the way nimefurahi umerudi salama Monica.Karibu tena nyumbani.” “ Ahsante Daniel.Nikipata nafasi nitakutafuta kuna mambo ambayo nahitaji kuzungumza nawe” akasema Monica akaagana na Daniel kisha akamgeukia Linah “ Kuna tatizo lolote Monica? Nimesikia unazungumzia ripoti ya jeshi la polisi” akauliza LInah “ Kuna rafiki yangu mmoja alipigwa risasi hivyo nilitaka kujua kuhusu ripoti ya uchunguzi ya jeshi la polisi kama wamefanikiwa kuwabaini waliofanya kitendo hicho .Tuachane na hayo ,mambo yamekwendaje kwa hizi siku mbili ambazo sikuwepo? Akauliza Monica “ Mambo yamekwenda vizuri hakuna tatizo lolote lililojitokeza.Hata hivyo kuna mgeni alikuja kukutafuta leo asubuhi.Gosh ! he’s super handsome.Kijana huyo ameacha gumzo pale ofisini kwani kila mtu anamzungumzia.” Akasema Linah huku akitabasamu “ Anaitwa nani huyo kijana mzuri ?Anahitaji nini? Akauliza Monica huku akitabasamu “ Anaitwa Austin .Ni mtanzania mwenye makazi yake afrika ya kusini .Monica huyo kijana ni mzuri mno.” “ Mhh ! leo Linah umemsifia mwanaume basi lazima atakuwa ni kijana mzuri haswa.Alikuwa na shida gani na mimi?

CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
 “ Monica lazima nimsifie naamini hata wewe ukimuona utakubaliana nami kwamba Austin ni kijana wa kipekee sana.Ana sura nzuri ya kuvutia,ana umbo zuri la kiuana mitindo.Ana sautio nzuri, ni mcheshi,mstaarabu,dah ! ana sifa nyingi Yule kijana itoshe tu kusema ni wa kipekee” akasema Linah na Monica akaangua kicheko kisha akasema “ Mhh ! Linah usiniambie tayari umekufa kwa huyo kijana kwa sababu namna unavyomsifia dah ! “ “ Monica wewe ni msiri wangu na sijawahi kukuficha jambo lolote.Nakuambia ukweli nilipomuona tu Austin nilihisi kama moyo wangu unataka kusimama.Nilihisi kama ninataka kupagawa kwa msisimko nilioupata.Monica usinione mjinga lakini naomba niwe wazi kwamba Yule kijana amenitikisa na nimetokea kumpenda.” Akasema LInah “ C’mon baby girl,give me a break usiseme tayari umempenda mtu ambaye umekutana naye kwa dakika kumi tu” akasema Monica “ It’s true Monica.Hata mimi mwenyewe najishangaa kwa hali hii iliyonitokea.” Monica akamtazama Linah kisha akatabasamu. “ Austin alikuwa anahitaji nini? “ Austin ni mkurugenzi wa kampuni ya utalii inaitwa AA safaris ambao wamekuwa wakifadhili miradi mbali mbali ya kijamii katika sehemu zile mbali mbali.Kwa sasa wana mpango wa kufungua ofisi nchini Tanzania kwa hiyo wanataka kushiriki pia katika kufadhili miradi kadhaa ya kijamii.AA safaris wanataka kushirikiana na sisi katika jambo hilo na hicho ndicho kilichomleta Austin ofisini kwetu” akasema Linah “ Ni jambo zuri sana.Mliafikiana mambo gani? “ Hatukuafikiana chochote kuhusu suala hilo nilimueleza kwamba mtaongea kwa kirefu utakaporejea.Aliahidi kufika ofisini kila siku kufahamu kama umerudi” “ Sawa Linah endapo mtafanikiwa kuwasiliana mueleze nimekwisha rejea na aje tuonane” “ It’s your turn now.Nieleze ulikuwa wapi na ikawaje ukarudi na ndege ya rais wa Congo? Akauliza Linah kama kawaida yae Monica akatabasamu na kusema “ Ni hadithi ndefu kidogo lakini kama nilivyokuahidi kwamba nitakueleza kila kitu ila kwa sasa nitakupa kwa kifupi tu” akasema Monica akanyamaza kidogo halafu akasema “ Nilikwenda Congo DRC.Nilialikwa na rais David Zumo kuhudhuria kongamano la umoja wa vijana wa Congo” “ Hebu subiri kwanza Monica.Wewe na David mmefahamiana kwa muda gani? Akauliza Linah “ Mimi na David tumefahamiana siku ya zile mbio.Kama unakumbuka wewe ndiye uliyempokea Jean Pierre Muyeye msaidizi wa David Zumo.Siku ile alitumwa na David kuniletea ujumbe kuwa David anahitaji kuonana nami kwa sababu amevutiwa na juhudi zangu za kusaidia jamii masikini.Nilikwenda kuonana naye hotelini kwake tukaongea mambo mengi na akanipa mchango wake mkubwa.Alipoondoka kurudi Congo akanialika niende kuhuduhuria kongamano la vijana wa Congo .Alituma ndege yake binafsi kuja kunichukua na kunipeleka Congo.Nilipokewa vizuri na mke wa rais wa Congo aitwaye Pauline Zumo.Nilipelekwa katika jumba kubwa la kifahari.Ndani ya jumba hilo hadi vijiko ni vya dhahabu.Nashindwa nikuelezeaje uzuri wa jumba hilo na maisha ya kifahari niliyoshi Congo.Linah katika dunia hii kuna watu wanaishi kama vile wako peponi.Kila nilipopita magari yaliwekwa pembeni .Sikuwahi kuota hata siku moja kama ningeweza kupewa heshima kubwa kiasi kile.Anyway tuachane na hayo maisha ya kifahari,kuna jambo kubwa ambalo David Zumo aliniitia Congo ukiacha hilo ” akasema Monica “ Jambo gani hilo Monica? Monica akamtazama Linah kwa sekunde kadhaa ,akatabasamu na kusema “ David Zumo anataka kunioa” “ What ?? akasema Linah kwa mstuko mkubwa na kusimama akajishika kiuno “ David Zumo anataka kufanya nini?!! “ David Zumo anataka kunioa “ Linah akamtazama Monica kwa macho makali na kusema “ Tafadhali Monica usifanye utani katika jambo kubwa kama hilo “ “Siwezi kuweka utani Linah katika suala kama hili.Ni kweli ninachokwambia” inah akashusha pumzi ndefu na kuendelea kumtazama Monica kisha akasema taratibu “ What a suprise” “ Ni kweli Linah jambo hili litawashangaza wengi “ “ Monica mimi sishangazwi na David kutangaza ndoa nawe bali nashangazwa na muda mfupi toka mlipofahamiana.” “ Uko sahihi Linah.Muda umekuwa mfupi sana ambao mimi na David tumekutana hadi kufikia hatua ya David kutangaza kutaka kunioa” “ kwa hiyo uelipokeaje ombi la david? Akaulzia Linah.Bila kupepesa macho Monica akasema “ I said yes!! Linah akainuka na kumkumbatia Monica “ Oh ! Monica thank you.You did good.Hata kama ningekuwa mimi nisingekubali kutamka hapana kwa mtu kama Yule tajiri namba moja Afrika.Monica una bahati ya kupata fursa nyingi na unajua kuzitumia .Hii ni fursa kubwa umeipata na umeitumia vyema.” Akasema LInah “ Linah hii si fursa kama unavyodhani.hya ni maamuzi ya kutoka moyoni.kwa hiari yangu nimekubali kuolewa na David na si kwa sababu ya utajiri wake.Ni kweli ni muda mfupi sana tumkutana na kufikia makubaliano ya kufunga ndoa lakini hicho si kigezo.hata masaa mawili yanatosha sana kutangaza ndoa.Ni kama wewe ulivyochanganyikiwa na Austin baada ya kuonana naye kwa muda usiozidi nusu saa.Tuachane na hilo suala tutaliongelea siku nyingine kwani nahitaji kupumzika “ akasema Monica wakaagana Linah akaondoka “ Suala la ndoa yangu na David litatengenza vichwa vya habari kwa muda mrefu pindi likiwekwa wazi lakini sintajali chochote.Nimekwisha amua kuolewa na David Zumo na hakuna wa kunibadilisha mawazo.Kwa sasa ninachotakiwa kufanya ni kujua mahala alipo Marcelo ili nikamjulie hali.Ngoja niwasiliane na David nimtaarifu kuwa nimefika salama na nimuulize mahala alipo Marcelo” Monica akachukua simu akaandika namba za David Zumo akapimpigia “ Hallow malaika wangu habari gani Monica? Natumai umefika salama Dar es salaam” “ Nimefika salama David.Nimekupigia kukushukuru mno wewe na mkeo Pauline kwa ukarimu wenu mkubwa.Mungu amewajalia mioyo iliyojaa upendo wa aina yake .Sipati neno zuri la kuwashukuru kwa namna mlivyonipokea.Nazidi kuwaombea kwa Mungu aendelee kuwaongoza na kuwapa mafanikio mengi” akasema Monica “ Ahsante sana Monica malkia mtarajiwa wa Congo.Halafu kuna kitu nilisahahu kukueleza .Ninafikiria kukuletea walinzi nane kutoka Israel kwa ajili ya kukulinda.Nataka uwe salama malkia wangu.” Akasema David “ David ahsante sana kwa kunijali na kuthamini usalama wangu lakini kwa wakati huu nadhani bado sihitaji ulinzi wowote. Huku kwetu amani imetawala na kingine ni kwamba mimi ni mtu wa watu kwa hiyo hata kama nina mahusiano na rais au mfalme sitaki kubadlika.Nataka niendelee kuwa mtu wa kawaida kwa hiyo David naomba usisumbuke kuhusu suala hilo la ulinzi” “ Monica mpenzi wangu,wewe ni malkia mtarajiwa wa Congo kwa hiyo unahitaji ulinzi wa hali ya juu lakini kama una uhakika uko salama hakuna tatizo” “ Ahsante David kwa kunielewa” “ Usijali Monica ,siku zote neno lako ni amri kwangu.Halafu kuna jambo lingine” akasema David na kunyamaza kidogo “ Jambo gani David? Monica akaulliza.David akasikika simuni akivuta pumzi ndefu kisha akasema “ Wakati akikusindikiza uwanja wa ndege ,Pauline kuna jambo alikueleza” “ Ndiyo David.Kuna jambo alinieleza limenistua na kunitoa machozi mengi” “ Ndiyo hivyo Monica.Hilo ni jambo ambalo tunajitahidi kukabiliana nalo.Si jambo jepesi kwangu lakini naamini utakuwa pamoja nami kwani nahitaji nguvu ya kulikabili suala hili.” “ David niko pamoja nawe katika jambo hili lakini nakuomba tusikate tamaa.Tunatakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Pauline anapona.Ni mapema mno kukata tamaa” “ Monica suala hili la Pauline ni suala ambalo tumeshughulika nalo kwa muda mrefu na tumejaribu kila tiba bila mafanikio.Laiti kama kuna mahali ningeweza kupata tiba kwa ajili ya Pauline,niko tayari kutumia utajiri wangu wote kupata tiba hiyo lakini hakuna tiba hiyo.Madaktari wamekwisha kata tamaa na wanaamini kuwa Monica hawezi kupona tena.Tumeliweka suala hili katika mikono ya Mungu .Ni yeye pekee atakaye amua hatima ya Pauline.Hata hivyo atafanyiwa upasuaji wa mwisho ingawa madaktari wana wasi wasi mkubwa kwamba yawezekana Pauline asiamke tena na huo ukawa ndio mwisho wake.Kwa hiyo Monica lazima tujiweke tayari kwa lolote litakalotokea.”akasema David “Nimekuelewa David,kitu cha muhimu kwa sasa ni kuzidisha maombi.Tukiachana na suala hilo David ninataka kushughulikia suala la Marcelo kwa hiyo nahitaji kufahamu mahala alipo ili nikamchukue na kumpeleka sehemu salama zaidi.unaweza kunisaidia kumuuliza rais Ernest mahala alipo Marcelo?”

 “Sawa Monica,nitaongea naye anielekeze mahala aliko hifadhiwa Marcelo halafu nitakujulisha”Akasema David,wakaongea kidogo kisha wakaagana. “Huyu Marcelo ni nani kwa monica ?anaonekana ni mtu mwenye umuhimu mkubwa sana kwake hadi akafikia hatua ya kutaka kuhatarisha maisha yake kumuokoa dhidi ya watu wanaotaka kumuua.Inawezekana wakawa na mahusiano ya kimapenzi?”akawaza David zumo baada ya kumaliza kuongea na Monica . “ Kuna uwezekano mkubwa Marcelo na Monica wakawa na mahusiano ya kimapenzi .Japokuwa nimemkuta Monica akiwa bado bikira lakini nashawishika kuamini kwamba lazima ana mahusiano na Marcelo.Hainingii akilini eti mwanamke mzuri kama Yule asiwe na mpenzi.Ninampenda sana Monica na kwa ajili yake niko tayari kufanya jambo lolote hata kama ni baya na kwa hiyo nitahakikisha Monica na Marcelo hawaonani tena.Nitaongea na rais wa Tanzania na kumsisitizia Marcelo aendelee kuhifadhiwa mahala salama na ikiwezekana nitafanya mpango wa kumuhamisha na kumleta Congo atahifadhiwa mahala ambako hatatoka hadi kifo chake au kama nitalazimika kumtoa uhai nitafanya hivyo.Kwa ajili ya Monica nitajifunza kuwa mkatili.Monica ni wangu peke yangu”akawaza David na kumpigia simu Ernest Mkasa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakaongea akamuomba Ernest eandelee kumuhifadhi Marcelo mahlala alikofichwa na asiruhusiwe kutoka hadi hapo atakapotoa maelekezo mengine.Alipomaliza kuzungumza na Ernest Mkasa akampigia Monica
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Monica nimezungumza na rais wa Tanzania amesema kwamba atanipa maelekezo baadae ya mahala alipo Marcelo ili umtembelee” “ Ahsante sana David kwa msaada wako huu mkubwa” akasema Monica wakaagana tena “ Ngoja nipumzike kidogo nahisi uchovu mwingi.Sintakwenda kuwatembela wazazi leo nataka nipumzike hadi kesho asubuhi ndipo nitawatembelea” akawaza Monica. ******************* Saa tisa na nusu za alasiri ndege ya shirika la ndege la Emirates iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere jijni Dar es salaam ikitokea Dubai na miongoni kwa abiria walioshuka katika ndege hiyo ni Maria mpenzi wa Austin Alikamilisha taratibu za uhamiaji hapo uwanjani kisha akatoka nje ya uwanja na kwa kuwa hakukuwa na mtu yeyote aliyekuja kumpokea uwanjani ikamlazimu akodishe teksi kuelekea hotelini “ Austin yuko ndani ya jiji hili na ndiye aliyepaswa kuja kunipokea hapa uwanjani leo lakini toka jana hakunitafuta kama tulivyokuwa tumekubaliana.Ameniumiza sana lakini kwa kuwa ninampenda sina budi kumtafuta.Inaonyesha wazi hataki nije Dar es salaam kwani toka nilipomueleza nia yangu ya kuja Dar amekuwa akitoa kisingizio cha usalama.Kuna kitu gani Austin hataki nikijue? Ninahisi lazima lazima atakuwa na mwanamke huku Dar.Nitajua tu kinachoendelea na ambacho hataki nikifahamu” akawaza Maria akiwa garini akipelekwa hotelini “ Dar es salaam imebadilika sana.Limekuwa jiji la kisasa na la kupendeza.Serikali ya Tanzania inastahili pongezi kwa kulifanya jiji kuu la kibiashara Tanzania kuwa zuri namna hii” akaendelea kuwaza Monica huku akitazama nje kushuhudia uzuri wa jiji la Dar es salaam.


kumtafuta.Inaonyesha wazi hataki nije Dar es salaam kwani toka nilipomueleza nia yangu ya kuja Dar amekuwa akitoa kisingizio cha usalama.Kuna kitu gani Austin hataki nikijue? Ninahisi lazima lazima atakuwa na mwanamke huku Dar.Nitajua tu kinachoendelea na ambacho hataki nikifahamu” akawaza Maria akiwa garini akipelekwa hotelini “ Dar es salaam imebadilika sana.Limekuwa jiji la kisasa na la kupendeza.Serikali ya Tanzania inastahili pongezi kwa kulifanya jiji kuu la kibiashara Tanzania kuwa zuri namna hii” akaendelea kuwaza Monica huku akitazama nje kushuhudia uzuri wa jiji la Dar es salaam. ********************* Tayari kiza kimeanza kutanda angani ,rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Ernest Mkasa alipowasili katika hoteli yake ya kifahari ya White Panda kama ilivyo ada yake kufika hapa kila jioni kwa ajili ya kupumzika, kupata kinywaji pamoja na kukutana na watu mbali mbali kwa faragha.Kwa siku nzima alikuwa amejifungia ofisini kwake na hakutaka kuonana na mtu yeyote.Alikuwa na kazi ngumu ya kuchambua baadhi ya watu anaodhani wanaweza kumfaa katika baraza lake jipya la mawaziri Alipofika hotelini akapitiliza hadi katika chumba chake na mtu wa kwanza kuwa na maongezi naye usiku huu alikuwa ni Mukasha. “ Mukasha nini kinaendelea huko mtaani? Watu wanasemaje kuhusu maamuzi niliyoyachukua? Akaanzisha maongezi Ernest “ Kuna mjadala mkali sana mheshimiwa rais.Kila mahala ukipita leo hii habari kubwa ni kuhusiana na maamuzi uliyoyafanya.Ni maamuzi makubwa ambayo hakuna aliyeyatarajia.Wengi wanapongeza kwa hiki ulichokifanya na wanakuunga mkono lakini wengi wanahoji kutaka kufahamu sababu ya wewe kufanya maamuzi yale.Hilo limekoleza mjadala na kila mmoja anaongea analolifahamu lakini ukweli wote unaujua wewe mheshimiwa rais” akasema Mukasha.Ernest akanywa mvinyo akakohoa kidogo na kusema “Ni kweli Mukasha.Wananchi hawajui sababu ya mimi kuchukua maamuzi yale makubwa.Kuvunja baraza la mawaziri si jambo dogo.Ni jambo zito lakini nililazimika kufanya hivyo .Mukasha wewe ni mmoja kati ya watu wachache ninaowaamini sana na ninataka nikiri kwako kwamba kuna jambo kubwa linaloendelea ndani ya serikali” akasema Ernest akanywa tena funda mbili za mvinyo na kuendelea “Kuna nguvu kubwa hivi sasa inayotaka kuibadili dunia” “ Nguvu kubwa? Ipi hiyo? Kubadili dunia kivipi mheshimiwa rais? Akauliza Mukasha
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
 “ Ni hadithi ndefu lakini nitakueleza kwa ufupi kwa kuwa wewe ni mtu wangu wa muhimu sana” akanyamaza akamtazama Mukasha halafu akaendelea Kuna kiongozi mmoja wa kanisa aliwahi kuasi kanisa lake kwa kuanzisha vuguvugu la kudai mabadiliko katika ndani ya kanisa, mabadliko ambayo hayaendani na imani ya kanisa hilo.Kiongozi mkuu wa kanisa hilo kwa wakati huo hakupendezwa na kitendo cha kiongozi Yule kutaka kuanzisha uasi ndani ya kanisa hivyo akamvua daraja na kumfukuza katika kanisa hilo.Baada ya kufukuzwa akaanzisha kundi la Alberto ambalo ndilo linataka kuibadili dunia na kuyafanya mataifa yote yafuate imani yao.Kundi hili lenye makao yake makuu nchini Italia limekuwa likipata nguvu kila uchao na kusambaa sehemu mbali mbali duniani.Kitu kimoja ambacho unapaswa kukifahamu ni kwamba kundi hili linaongozwa na nguvu za giza na mambo ambayo wanayashabikia na kutaka dunia nzima iyafuate ni yale ambayo yanakwenda kinyume na Mungu muumba wa mbingu na nchi.Baadhi ya mambo hayo ni mahusiano na ndoa za jinsia moja,kutoa mimba,uhuru wa ngono kwa vijana wadogo n.k.” Ernest akanyamaza na kumtazama Mukasha kisha akaendelea “ Ili kufanikisha mipango yao ,wamekuwa wakiwatumia wakuu wa nchi kuhalalisha mambo hayo katika nchi zao.Walianza kuotesha mizizi katika mataifa makubwa ya Amerika na Ulaya na wamefanikiwa kiasi kikubwa sana huko kwani tayari nchi nyingi zimeyapokea na kuyakubali mambo hayo na kuyashabikia sana.Kwa kuyatumia mataifa hayo makubwa wameweza kuyafikia mabara mengine na kwa sasa wamefika bara la Afrika.Walilifanya bara hili kuwa la mwisho kutokana na nchi zake nyingi kuwa masikini na kutegemea sana misaada na mikopo toka mataifa makubwa kwa hiyo kazi ya kuotesha mizizi katika nchi za Afrika si ngumu.Hadi hivi sasa sehemu kubwa ya nchi za Afrika wameyakubali mashari yaliyotolewa na nchi wafadhili ya kutunga sheria kukubaliana na mapenzi ya jinsia moja,utoaji mimba n.k.Nchi pekee ambayo wamepata ugumu kuingia ilikuwa Tanzania lakini baadae walifanikiwa kuingia na kuotesha mizizi na mimi ndiye mzizi mkuu” Kauli ile ya Ernest ikamfanya Mukasha ainuke na kumtazama Ernest kwa macho ya woga “ Mr President you are one of them?? Akauliza kwa mshangao.Ernest akavuta pumzi ndefu na kusema “ Mimi si mmoja wao lakini ni sehemu yao.They are using me.......” “ Oh my God !!! akasema Mukasha “ Alberto’s ....” Ernest akaendelea “ Ndio walioniweka mimi madarakani.Walitumia nguvu yao nikachaguliwa kugombea urais na kuibuka mshindi kwa kura nyingi.Walinipa nafasi hiyo kubwa kwa sharti moja kwamba wataitumia ofisi yangu katika kufanikisha mambo yao.Baada ya kuupata mzizi mkuu walianza kusambaza miziz midogo midogo katika sehemu mbali mbali ili kutengeneza mmea wenye afya.Walichokifanya kwanza ni kuliteka bunge.Asilimia kubwa ya wabunge ni wafuasi wao waligharamia kampeni zao na kuwasaidia kushinda na kila mwezi kuna kiasi kikubwa cha pesa wanakipokea kwa siri kutoka kwa Alberto’s.Lengo la kuliteka kwanza bunge ni kuweka urahisi wa kupitisha miswada mbali mbali itakayowasilishwa mbele yao.Nilimteua mgombea mwenza ambaye ni makamu wa rais kwa maelekezo yao,waziri mkuu pia walinipa maelekezo wao,na haijaishia hapo bali hata mawaziri wote nimewachagua kwa maelekezo yao.Kwa ufupi ni kwamba Alberto’s wameishika nchi hii na wanaipeleka namna watakavyo.Mimi niko kama kivuli tu lakini nchi inaongozwa na watu wengine kabisa.Kuna baraza dogo la vingozi wa juu wa Alberto hapa nchini ndio wanaofanya kazi ya kuongoza nchi na mimi ninatekeleza maagizo na maelekezo yao.Alberto’s wana nguvu na kwa sasa wanamiliki robo tatu ya dunia” akanyamaza akanywa funda la mvinyo na kuendelea

“ Uliandaliwa muswada wa sheria uliotazamiwa kupelekwa bungeni ambao unazitambua haki za wapenzi wa jinsia moja.Endapo ungefikishwa bungeni na kupitishwa basi mambo hayo yangehalalishwa hapa nchini lakini kabla hilo halijafanyika nimewahi na kuufutilia mbali muswada huo ,na kama haitoshi nikalivunja baraza la mawaziri,nikamteua pia mkuu mpya wa majeshi” akasema Ernest na ukimya ukatanda mle ndani baada ya muda Mukasha akauliza “ Nini hasa kilipelekea ukachukua maamuzi hayo ya kuwageuka watu hatari kama hawa ambao ndio waliokuweka madarakani?Huwaogopi? Ernest akatoa mkebe katika mfuko wa koti akatoa sigara kubwa akaiwasha akavuta mikupuo kadhaa na kusema “ Mke wangu Agatha ni mmoja wa viongozi wa Alberto’s hapa Tanzania” “ What ??!!..Mukasha akazidi kushangaa “ Even First lady??? Akauliza “ Yes.She’s one of them,” akajibu Ernest na kuvuta tena mkupuo mmoja akapuliza moshi na kusema “ yeye ndiye aliyenishawishi mimi nikubaliane nao niwe rais.Kama nilivyokueleza awali kwama hawa jamaa wanatumia nguvu za giza kufanya mambo yao kwa hiyo Agatha aliwatoa kafara watoto wetu watatu ili kunishikiniza nikubaliane nao . Baada ya kuwazika wanangu watatu kwa siku moja sikuweza tena kupata mtoto mwingine.” Akanyama na kuvuta tena sigara akanywa funda moja la mvinyo “ So sorry for that Mr president.Sikujua kama umepitia mambo magumu namna hiyo” akasema Mukasha “ Ni kweli Mukasha,nimepitia mambo mengi magumu latika kipindi hiki cha urais wangu.Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta upenyo wa kuniwezesha kuachana na watu hawa lakini nilishindwa .Hivi majuzi niligundua kwamba enzi za ujana wangu niliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke mmoja na katika mahusiano hayo tulibahatika kuwa na mtoto ingawa mwanamke huyo alinificha hadi hivi majuzi alipoamua kuja kunieleza ukweli.Nilifurah mno kwani niliamini ningekufa bila kuwa na mrithi wa utajiri wangu.Japokuwa hizi zilikuwa ni taarifa njema mno kwangu lakini sikutaka kuamini haraka haraka na ndiyo maana nikam tafuta Austin li aweze kunisaidia kupata sampuli toka kwa huyo mtoto kwa dhumuni la kufanya kipimo cha vinasaba kubaini kama kweli mtoto huyo


ni wangu .Baada ya kukutana na Austin ndipo nilipopata ujasiri wa kuachana na kupambana na Alberto’s.Nataka mwanangu na watoto wake waishi katika nchi yenye neema iliyobarikiwa na si katika nchi yenye laana.Kwa hiyo mimi na Austin tumeungana na tunapigana vita hii kwa pamoja.Tunataka kuwaondoa Alberto’s hapa nchini na kuiondoa kabisa mizizi yake yote.Nilipopokea uongozi ,taifa hili lilikuwa imara kama lilivyoachwa na waasisi wetu kwa hiyo sitaki kulibomoa kwa mikono yangu kwa hiyo nitapambana kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa ile ile iliyoachwa na wazee wetu.Mukasha hili si jambo jepesi.Ni jambo la hatari kubwa kwani hawa jamaa ni watu hatari kama nilivyokueleza na wanaweza wakanitoa uhai sekunde yoyote lakini pamoja na hatari hiyo iliyopo nimeamua kupambana nao.” Akanyamaza.Mukasha akahisi joto akavua koti.Ernest akaendelea “ Mukasha nimekueleza haya yote wa sababu wewe ni mmoja wa watu wachache ninaowamini .Pili ninataa uwe mshirika wangu katika mapambano kwani ninafikiria kukuteua kuwa waziri mkuu mpya wa jamhuri ya muungano wa Tanzania” Kauli ile ya Ernest ikamstua sana Mukasha akasimama na kumtazama rais kwa macho ya woga “ hapana mheshimiwa rais !! akasema Mukasha “ Mheshimiwa rais mimi sistahili nafasi hiyo.Ahsante kwa kuniamini na kunipa heshima hii kubwa lakini nakuomba utafute mtu mwingine anayefaa .Mimi naomba uniache katika nafasi hii niliyo nayo sasa “ akasema Mukasha .Ernest akavuta sehemu ya mwisho ya sigara akapuliza moshi hewani na kumtazama Mukasha “ Mukasha hakuna mtu mwingine ambaye ninamuamini kwa sasa kumpa nafasi hiyo ya uwaziri mkuu zaidi yako.Nahitaji mtu wa kufanya naye kazi ,nahitaji mtu wa kusaidiana naye kuisafisha nchi hii,na mtu huyo ni wewe.Endapo utakataa nafasi hii utanifanya niwe na mashaka labda pengine nawe unashirikiana nao kwa siri” “ mheshimiwa rais naomba usinifikirie hivyo tafadhali.Watu hao siwafahamu na leo ni mara ya kwanza kuwasikia toka kwako.Kinachonifanya nikatae ni kwamba nafasi hii ni kubwa mno kwangu.Sitaki kukuangusha mheshimiwa rais.Niko tayari kukuunga mkono katika mapambano haya hata kuyaweka rehani maisha yangu lakini si kwa nafasi ya uwaziri mkuu.Naomba unielewe kwa hilo mheshimiwa rais” akasema Mukasha “ Ninakuelewa Mukasha na ninaelewa kinachokupa wasiwasi kuikubali nafasi hii.Unawaogopa Alberto’s ,unaogopa kufa” “ Hapana mheshimiwa rais japokuwa ni watu hatari lakini nakuhakikishia siwaogopi hata kidogo.” Akasema Mukasha.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ If you ‘re not scared of them then join me in this war.Nikiwa nawe kama waziri mkuu itakuwa rahisi sana kuendehsa mapambano haya na tutatengeneza baraza dogo la mawaziri la watu tunaowaamini na tutahakikisha tunawang’oa kabisa Alberto’s hapa nchini.Mzizi wao mkuu ulikuwa ni ofisi ya rais lakini kwa sasa tayari mzizi huo umetetereka na ninaamini hivi tuongeavyo lazima watakuwa katika mikakati mizito ya kuhakikisha haraka wawezavyo wananiondoa mimi ambaye tayari nimekuwa kikwazo kwao ili mipango yao ifanikiwe.Uwezo huo wanao kwani wamenizunguka kila kona.Kwa hiyo nataka muda huu mfupi nilio nao niutumie vizuri kuhakikisha kama si kuingoa kabisa mizizi yote ya Alberto’s nchini basi ninawadhoofisha kabisa.Siwezi kufanya jambo hili peke yangu bali nahitaji nguvu za ziada toka kwa watu wachache ninaowaamini na wewe ukiwa mmoja wao.Kwa hiyo Mukasha nakuomba uikubali nafasi hii kwa manufaa ya nchi.” Akasema Ernest.Mukasha akainamisha kichwa akatafakari halafu akasema “ Mheshimwia rais ,kama nilivyokueleza awali kuwa mimi nitapambana pamoja nawe bega kwa bega lakini si kwa nafasi hii ya uwaziri mkuu.Niko tayari kushirikiana nawe kumtafuta mtu ambaye anafaa kwa nafasi hiyo” Ernest akainamisha kichwa akafikiri kwa muda akainua kichwa na kusema Mukasha you have two daughters ,right? “ Yes Mr president.Wote wako chuo kikuu” “ ‘Good.Hebu pata taswira unatazama picha mtandaoni ya wanawake wakishiriki mapenzi ya jinsia moja au wanafunga ndoa na unagundua mmoja wa wanaoonekana pichani ni mwano ,utajisikiaje? Sura ya Mukasha ikabadilika “ Mungu atanisamehe kwa hicho nitakachokifanya .Naapa nitaondoa shingo ya mtu !! “ It hurt ,right? Akaulizi Ernest “ So badly.Mtoto ambaye unamtegemea akuzalie wajukuu halafu anaolewa na mwanamke mwenzake!!!! Inaumiza sana.Ni laana kubwa hiyo” “ Unavyohisi kuumizwa na jambo hilo ndivyo wengi wa wazazi watakavyoumia pindi Alberto’s wakifanikiwa mipango yao kwani lengo lao kubwa ni hilo la kuruhusu mapenzi ya jinsia moja.Tunatakiwa kuungana pamoja kuzuia jambo hili lisitokee hapa nchini kwetu na kuwaathiri watoto wetu.Nakubali nimefanya kosa kuwapa mwanya mashetani hawa wa kupenya lakini naamini pia bado ninayo nafasi ya kuwazuia wasiendelee na mipango yao miovu na ndiyo maana nakuomba uwe waziri mkuu ili tutengeneza baraza la mawaziri la watu watiifu na wazalendo na kwa pamoja tuisaifisha nchi hii” akasema Ernest.Mukasha akafikiri kwa muda na kusema “ Mheshimiwa rais,ninakubali nafasi hiyo ya uwaziri mkuu .Nataka tuisafishe nchi.Nataka wanangu na wajukuu zangu waishi katika nchi yenye neema na si nchi yenye laana” akasema Mukasha .Ernest akainuka na kumpa mkono wa pongezi “ Ahsante sana Mukasha kwa uamuzi huo. Usihofu Mungu anaiona nia yetu njema na atatutangulia katika vita hii na tutashinda.” “ Nashukuru Mheshimwa rais kwa kuniamini lakini kuna jambo moja nataka nikuombe” “ Jambo gani? Omba chochote Mukasha” “ Promise me that my family will be safe.My wife and my two daughters will all be safe”

“ I promise you Mukasha.I’ll do whatever I can to protect you and your family.I give you my word” “ Thank you mr Prsident” akasema Mukasha “ Nitakuteua kwanza kuwa mbunge halafu nitalipeleka jina lako katika kikao kitakachofuata cha bunge kwa ajili ya kuidhinishwa na wabunge. Na baada ya hapo tutaunda serikali” “ Mheshimwia rais uliniambia kwamba Alberto’s wana wafuasi wengi pia bungeni ,unadhani ukipeleka bungeni jina la mtu ambaye si mfuasi wao wataliidhinisha ? Nina hofu tunaweza kushindwa” Ernest akafikiri kidogo na kusema “Uko sahihi Mukasha .Alberto’s wana wafuasi wengi bungeni lakini nitawatumia wabunge wa vyama pinzani ambao wakiungana na wale wachache ambao si wafuasi wa Alberto’s basi tutakuwa na uhakika wa kufikisha idadi ya kura zinazohitajika.Nitajitahdi sana kuzungumza na wabunge mmoja mmoja kutafuta uungwaji mkono katika hili.Usihofu Mukasha,utapita tu na utakuwa waziri mkuu mpya wa Tanzania.Nitateua pia wabunge wapya kumi kwa mujibu wa mamlaka niliyonayo na hawa wote watakuwa mawaziri.Tunatakiwa kuwa makini sana katika kufanya uteuzi wa watu hawa “ Ernest akanyamaza kidogo na kusema “ Mukasha nadhani tumelimaliza suala hili kwa hiyo ni wakati wa kwenda kuonana na Austin.Kuna mzigo ninampelekea.Vipi kuhusu zile laini za simu umefanikiwa kuzipata? Yanahitajika mawasiliano ya karibu kwani sitaki kwenda kwa Austin kila siku ili watu wasigundue na kuanza kumfuatilia Austin.” “ Ndiyo mheshimiwa rais ,ninazo hapa” “ Good.Lakini kabla hatujakwenda huko kuna jambo nataka kulifanya “ akasema Ernest akainuka akaelekea katika chumba kidogo kunamohifadhiwa vyombo vya chakula akachukua kisu halafu akachukua kisanduku cha huduma ya kwanza akamtaka Mukasha waelekee bafuni.Walipoingia bafuni Ernest akavua shati na kupasua sehemu Fulani katika mkono wake wa kushoto akaingiza vidole viwili na kutoa kitu Fulani kidogo “ Mukasha zuia damu tafadhali isiendele kutoka” akasema Ernest akiwa na maumivu makali.Haraka haraka Mukasha akachukua dawa na kumtibu Ernest jeraha lake.Baada ya hapo Ernest akajisafisha damu na kukisafisha kile kifaa alichokitoa mkononi na kumuonyesha Mukasha “ Hiki ni kifaa ambacho rais huwekewa mkononi na ambacho huwawezesha walinzi wa rais kufahamu kila mahala aliko .Kuanzia sasa nitakuwa nakiweka kifaa hiki mfukoni na nitakapokuwa nakwenda sehemu muhimu kama kwa Austin nitakuwa nakiacha hapa kifaa hiki ili wasinifuatilie” akasema Ernest
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kiwa chumbani kwake amejipumzisha baada ya mizunguko aliyofanya,saa yake ya mkononi ikatoa mlio akainuka haraka na kuibonyeza ikamuonysha sababu ya mlio ule.Kulikuwa na mtu getini.Akafutika bastora yake kiunoni akatoka kuelekea getini. Akafungua mlango mdogo wa geti kwa tahadhati kubwa na kukutana na Evans akiwa ameongozana na mheshimwa rais kama kawaida yao.Akawakaribisha ndani na kabla hawajangia sebuleni Ernest akasema “ Austin leo nataka Mukasha na Evans nao pia washiriki maongezi kwani tutakayoyazungumza yanawahusu pia wao” “ Hakuna tatizo mheshimiwa rais.” Akasema Austin wakaingia sebuleni.Kabla ya maongezi kuanza Ernest akampatia Austin begi lililojaa fedha.Austin akalifungua na kutabasamu “ Wow ! It’s cash” akasema na kulichomoa bunda moja akalitazama na kufunga begi. “Ahsante mheshimiwa rais kwa mzigo huu ,utanisaidia sana” akasema Austin. “ Usijali Austin.Muda wowote utakapohitaji kitu chochote usisite kunitaarifu na utakipata .By the way Mukasha amefanikisha kupata laini za simu ambazo utazitumia kwa mawasiliano baina yetu.” “ Ahsante mheshimiwa rais” akasema Ernest na baada ya muda akaendelea. “ Austin nadhani tayari umekwisha sikia kuhusu mabadiliko mengine niliyoyafanya leo.Nimemteua mkuu mpya wa majeshi .Kwa kufanya hivyo nimezidi kuikata mizizi ya Alberto’s.

Nitaendelea kukata mzizi moja mmoja hadi nihaikishe wamekosa nguvu na kufa.Nimempandisha cheo Luten jenerali Lameck Msuba kuwa jenerali na kumteua kuwa mkuu mpya wa majeshi Tanzania.Hili lilikuwa pendekezo lako na nina hakika Jenereali msuba ni mtu mzalendo na ambaye tutashirikiana naye katika vita hii” akasema Ernest .Mukasha na Evans wakatazamana Austin akasema “ Ahsante mheshimiwa rais kwa kulikubali pendekezo langu.Lameck Msuba ni mtu muadilifu na mtiifu.Ninamfahamu vyema na hautajutia uteuzi huo” “ Tukiachana na hilo la mkuu wa majeshi ,nimefanya pia uteuzi wa waziri mkuu japokuwa bado sijautangaza lakini nimeona niwajulishe kwa kuwa ninyi ni wenzangu katika mapambano haya.Nahitaji kuunda baraza la mawaziri lenye watu ambao hawatakuwa na mafungamano na Alberto’s.Wengi wa wabunge waliomo katika bunge letu tayari ni wafuasi wa Alberto’s kwa hiyo nimeamua kuteua wabunge kumi kwa mujibu wa mamlaka ya kikatiba niliyonayo na hao wote kumi watakuwa mawaziri.Miongoni mwa hao kumi atatoka waziri mkuu mpya ambaye atakuwa ni Mr Mukasha” “ Mukasha !!! Evans akasema kwa mshangao.Ni yeye pekee aliyeonekana kustushwa sana na kauli ile ya rais kwamba amemteua Mukasha kuwa waziri mkuu.Ernest akamtazama Evans na alionyesha wazi kutofurahishwa na mshangao ule wa Evans “ Evans ninaamini sikukosea kukukaribisha katika kikao hiki cha kujadili mambo mazito ya nchi.Kwa ufupi tu ni kwamba kuna mambo makubwa yanaendelea hapa chini kwa sasa na watu hawa unaowaona humu ndani ni pekee wanaopambana kuiokoa nchi hii isitumbukie katika laana.Nimeamua na wewe pia ushiriki katiaka kikao hiki kwa kuwa nawe ni mmoja wa watu wachache ninaowamini wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika mapambano haya kwa hiyo nakuomba utulie na usubiri wakati wako ukifika utafahamishwa kila kitu juu ya mambo yanayoendelea.Kwa sasa naomba usichangie jambo lolote uwe msikilizaji tu” akasema Ernest na kumgeukia Austin “Kwa hiyo Austin nimemteua Mukasha awe waziri mkuu mpya.Ni mtu ambaye ninamuamini sana,ni mzalendo wa kweli.Nimeongea naye na amekubali kwa hiyo nitatangaza uteuzi wake kama mbunge yeye pamoja na wenzake kumi na baada ya hapo nitaliwasilisha bungeni jina lake ili likapigiwe kura na wabunge na hatimaye kuidhinishwa.Ninafahamu haitakuwa kazi nyepesi lakini nitajitahidi kwa kadiri niwezavyo ili Mukasha apite na kuwa waziri mkuu” “ Ni uteuzi mzuri mheshimiwa rais na sina mashaka naye ila Mukasha anapaswa afahamu kinachoendelea hivi sasa na awe tayari kwa lolote hata ikibidi kuifia nchi yake.Hatuhitaji msaliti katika mapambano haya kwani yeyote ambaye atathubutu kwenda kinyume na sisi basi atakumbana na mkono wangu na ninakuhakishia mheshimiwa rais na wote mlioko humu kwamba ninapokwua kazinihuwa sina urafiki kwa hiyo atakayediriki kutusaliti ataufahamu unyama wangu” akasema Austin “ Usihofu Austin.Tayari nimekwisha mueleza kila kitu na amekubali kwa moyo mmoja kushirikiana nasi katika mapambano haya.Kuhusu usaliti ,sahau kabisa hilo jambo kwani watu hawa wawili ninawamini mno”akasema Ernest “ Good!! Akasema Austin

“ Baada ya kumpata waziri mkuu,kinachofuata ni kufanya mabadiliko katika kikosi cha kumlinda rais kama ulivyopendekeza.Nimekuachia wewe suala hili ulishughulikie nataka hadi kesho uwe tayari na majina ya watu unaowapendekeza watakaounda kikosi cha kumlinda rais.Pamoja na kufanya mabadiliko hayo lakini kikosi hicho kitakuwa chini ya Evans.Naomba uchague watu mahiri sana ambao wataimudu kazi hii na zaidi ya yote wawe tayari kuyaweka maisha yao hatarini kunilinda” akasema Ernest .Austin akamtazama rais na kusema “ Ahsante mheshimiwa rais kwa kuona umuhimu wa pendekezo langu na kulikubali.Mimi ni mzoefu katika mambo haya kwa hiyo nitaunda kikosi kidogo lakini chenye watu mahiri sana na ninakuhakikishia mheshimiwa rais utapata ulinzi wenye uhakika toka kwa watu hao.” “ Nafurahi kusikia hilo.Naomba sasa Mukasha na Evans mnisubiri hapo nje nina maongezi binafsi na Austin” akasema Ernest na Evans wakatoka kama walivyotakiwa na rais “ Austin nipe taarifa za maendeleo ya kazi yetu.Umefanikiwa kuonana na Monica? Akauliza Ernest “ Sijafanikiwa bado kuonana naye ,nilitaarifiwa yuko nje ya nchi lakini atarejea hivi karibuni .Nitakwenda tena kesho ofisini kwake kupata uhakika zaidi ni lini atarejea” “ Naomba ujitahidi sana Austin,ufanye kila uwezalo kupata sampuli kwa ajili ya kipimo cha vinasaba.Ninataka jambo hili lifanyike haraka ili nifahamu kama Monica ni mwanangu au siyo nijue namna ya kumlinda.Japokuwa nafsi yangu inaniambia kweli Monica ni mwanangu lakini lazima niwe na uhakika na uhakika utapatikana pale tu nitakapofanya kipimo cha vinasaba” “ Usihofu mheshimiwa rais,nakuhakikishia jambo hili lazima litafanikiwa tu.Naomba unipe siku kadhaa” “ Nakuamini Austin ila nilitaka tu kukupa msisitizo kwani haya yote ninayafanya kwa sababu ya Monica.Tuachane na hayo,vipi kuhusu Marcelo anaendeleaje? “ Anaendelea vizuri.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yuko chumbani amejipumzisha .Kuna taarifa yoyote toka kwa David Zumo? “ Ndiyo.Nimeongea naye mchana wa leo na akaniambia kwamba niendelee kumuhifadhi Marcelo mahala pa siri na asiruhusiwe kuonana na mtu yoyote hadi hapo atakapotoa maelekezo mengine.Kwa hiyo Marcelo ataendelea kukaa hapa hadi hapo tutakapopata maelekezo mengine toka kwake” “ Suala hili la Marcelo linaonekana ni suala pana ” akasema Austin “ Kuna mambo ambayo yananipa ugumu kuyaelewa lakini sitaki kujihusisha na suala hili wakati huu ambao kuna mambo mazito yanatukabili” “Uko sahihi Austin.Suala hili la Marcelo linaonekana ni gumu.Tusishughulike nalo kwa sasa.Tukiachana na hayo kuna jambo lingine ambalo sikuwanimekueleza hapo awali ambalo ni la muhimu sana ukilifahamu” “ Nakusikiliza mheshimiwa rais” akasema Austin.Ernest akafikiri kidogo na kusema Kuna kundi kubwa la vijana limeathirika na dawa za kulevya.Kwa tathmini iliyofanywa ,katika kila vijana kumi wanne ni waathirika wa dawa hizo .Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana hivi sasa na nguvu kazi kubwa ya vijana inapotea.Hii yote ni mipango ya Alberto’s ya kuharibu nguvu kazi ya taifa ili hapo baadae iwe rahis kwao kuingia na kutawala Afrika.Mpango huu ni wa siri na wa muda mrefu na tayari athari zake zimekwisha anza kuonekana na kama hali ikiendelea hivi ndani ya miaka kumi ijayo basi hatutakuwa na nguvu kazi kabisa , vijana wengi tayari watakuwa wamejitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Albertos’a wana mtandao mkubwa sana wa kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya duniani na hiki ni chanzo chao kikubwa cha mapato.Kwa mwaka wanakusanya trilioni nyingi ambazo ndizo zinazowasaidia katika kuendesha mambo yao.Rais wa nchi unapokubali kushirikiana na Alberto’s kuna masharti unapewa na mojawapo ya masharti hayo ni kuhakikisha kwamba unafungua njia kwa biashara ya dawa za kulevya kuingia nchini kwako na kuwalinda wale wote wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo.Toka nilipoingia madarakani vita dhidi ya dawa za kulevya imelega lega sana na Tanzania imekuwa ni kama ghala na njia kuu ya kupitisha dawa za kulevya kwa ukanda huu wa Afrika mashariki.Bandari ,viwanja vya ndege ,vinatumika katika kuingiza na kusafirishia dawa za kulevya.Austin.


Ninajiona kama nimekalia kiti cha damu kwani mimi ndiye chanzo cha haya yote” akasema Ernest na kukawa kimya .Ernest akachukua sigara katika mkebe akaiwasha na kuvuta “ Austin nimekueleza haya ili ufahamu kwamba tunapoingia katika vita dhidi ya Alberto’s tunaingia vile vile katika vita dhidi ya mtandao wao mkubwa wa wauzaji wa dawa za kulevya.Watu hawa ni hatari na wanaroho za kikatili mno.Wengi wao ni matajiri na walipa kodi wakubwa.wanamiliki biashara kubwa kubwa na wametengeneza ajira nyingi.Ni watu ambao huwezi kuwagusa kwani wameushika uchumi wa nchi.Ukiwagusa watu hao lazima uchumi wa nchi utetereke.I have to be honest with you Austin,these people are very very dangerous but we must stop them !! akasema Ernest.Austin akavuta pumzi ndefu na kusema “ This war is bigger than I though” “ Yes ! It’s a big war.Austin najua nimeiharibu nchi hii ila ninataka kuitengeneza tena.Katika hilo nakutegemea sana wewe.Please help me to rebuild the country and make it great again” akasema Ernest na ukimya ukatanda.Baada ya kimya cha dakika mbili Austin akasema “ Mheshimiwa rais,naomba nikuhakikishie kwamba nimejitoa mhanga kwa hiari yangu mwenyewe kupambana na watu hawa na ninakuahidi kupambana hadi tone la mwisho la damu .Japokuwa ni watu hatari lakini siwaogoi.Mheshimiwa rais nina swali moja tu kwako ,do you know them? Do you have a list? “ Ninawafahamu wachache ambao nilipewa maelekezo ya kuwalinda na kuwasaidia kila pale wanapokwama lakini kuna sehemu ninaweza kupata orodha yao.Nitakupa orodha hiyo pindi nikiipata”
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa mheshimiwa rais” akasema Austin wakaendelea na maongezi mengine na baadae wakaagana rais akaondoka “ Kama isingekuwa ni kwa ajili ya mdogo wangu ,katu nisingekubali kuingia katika vita hii ambayo ni mbaya na ngumu kuliko nilivyotegemea.Hata hivyo sina namna nyingine ya kufanya lazima nipambane na Alberto’s.Ili nifanikiwe lazima nitafute msaada” akawaza Austin baada ya rais kuondoka Austin aliwahi sana kuamka akafanya mazoezi na alipomaliza akachukua kisinia chenye dawa akaenda kugonga katika mlango wa chumba cha Dr Marcelo “ Austin habari za asubuhi? “ Habari nzuri ,unaendeleaje? “ Nashukuru naendelea vizuri .Maendeleo yangu mazuri.Dawa ulizoniletea jana zimenisaidia sana nikalala usingizi mnono.Nilisikia sauti za watu jana ,alikuwa ni rais? “ Ndiyo alikuwa ni rais” akajibu Austin “ Alisemaje kuhusu ombi langu? Alifanikiwa kuwasiliana na David Zumo? “ Hapana hakufanikiwa kuongea naye jana ila amesema atajaribu leo kama ataweza kufanikiwa kuzungumza naye” akasema Austin Kauli ile ikaonekana kumnyong’onyeza sana Marcelo.Austin hakumjali akamsogelea na kumsafisha vidonda “ Austin umesomea pia mambo haya ya utabibu? Unaonekana unayafahamu vyema” akasema Austin “ Ndiyo nimesomea.Kazi zetu hizi zinakulazimu ufahamu mambo mengi ikiwamo mambo kama haya” akasema Austin “ Unanifurahisha sana namna unavyofanya mambo yako.By the way kuna mambo Fulani ambayo nataka kuzungumza nawe na pengine unaweza ukanisaidia kupata ufumbuzi.”

 “ Ni mambo gani hayo “ akauliza Austin “Ni kuhusu hili suala langu.Kuna mambo ambayo bado watu hawayafahamu na sijayaweka wazi bado kwa mtu yeyote .Naamini nikikueleza unaweza ukanisaidia kupata ufumbuzi wa hili suala langu.” Akasema Marcelo.Austin hakujibu kitu akabaki anamtazama Marcelo “ Marcelo anaonekana ana jambo kubwa .Nataka nimsikilize na nione kama ninaweza kumsaidia” “ Austin saa ngapi utakuwa na muda wa kutosha tuzungumze ? akauliza Dr Marcelo “ Nitatoka asubuhi kuna mahala ninakwenda na nitakaporejea tunaweza kuongea” “ Ahsante Austin” akasema Marcelo,Austin akatoka akaelekea jikoni kuandaa kifungua kinywa.Ilipotimu saa nne za asubuhi tayari alikwishamaliza kujiandaa akaondoka tayari kwa kukutana na Monica.Siku hii alipendeza mno kupita hata siku iliyotangulia ******************* Saa tatu na dakika ishirini Maria akiwa tayari ameamka akijiandaa kupata stafstahi alipigiwa simu na mtu wa mapokezi akamtaarifu kwamba alikuwa na mgeni wake na akaomba apelekwe chumbani moja kwa moja “ Huyu lazima atakuwa ni baba ambaye niliwasiliana aye jana usiku nikamuelekeza hoteli niliyofikia.Hakuna mtu mwingine anayefahamu kama niko hapa” akawaza Maria baada ya dakika nne mlango ukagongwa akaufungua na kukutana na baba yake wakasalimiana “ Oh ! dady I missed you so much” akasema Maria na kumkaribisha baba yake “ Umekuja saa ngapi baba? “ Nimetua na ndege muda si mrefu na toka uwanja wa ndege nimekuja moja kwa moja hapa kukuona.How’s everything ? Are you comfortable here? “ I’m ok dady.This place is good.Sikutaka kwenda katika nyumba yetu kwa sababu sitaki mtu yeyote afahamu kama niko hapa.Dady please help me find Austin” akasema Maria “ Nitakusaidia Maria kwani hata mimi nimekuja kwa sababu yake.Kuna masuala ya kibiashara nataka nizungumze naye .Tutakwenda sote kuonana naye”

 “ Una fahamu mahala anakoishi? Akauliza Maria “ Sifahamu amefikia wapi hapa Dar es salaam lakini kuna mtu anayefahamu atanielekeza” akasema Boaz na kulifungua sanduku lake dogo akatoa simu na kuweka laini ya simu ambayo huitumia akiwa Tanzania akazitafuta namba za simu za rais Ernest Mkasa kabla ya kupiga akamtazama Maria aliyekuwa akimtazma kwa makini “Excuse me ,I need to make a phone call” akasema Boaz na kutoka akampigia rais. “ Hallow” akasema rais baada ya kupokea simu ya Boaz “ Mr president it’s me Boaz” “ Boaz? Ernest akashangaa kidogo “ Ndiyo mheshimiwa rais “ Nilijua uko nje ya nchi.Umekuja lini Tanzania? “ Nimekuja leo asubuhi mheshimiwa rais” karibu sana Boaz.Nitafurahi sana kabla haujaondoa tukipata nafasi ya kuonana” “ Ahsante kwa heshima hiyo mheshimiwa rais,nitajitahidi kabla sijaondoka tuonane.” Akasema Boaz na kimya cha sekunde kadhaa kikapita kisha Boaz akasema “ Mheshimiwa rais samahani kwa kukusumbua mapema hivi nina shida ndogo naomba unisaidie” “ Shida gani Mr Boaz? “ Nahitaji kuonana na Austin.Kuna masuala Fulani ya kibiashra nahitaji kuzungumza naye lakini sijui namna ya kumpata .Nielekeze tafadhali mahala ninakoweza kumpata au kama una mawasiliano yake unipe ili niwasiliane naye” akasema Boaz na Ernest akafikiri kidogo kisha akasema “ Nielekeze mahala ulipo na saa ngapi unataka kumuona Austin ili nimtume kijana aje akuchukue akupeleke mahala aliko Austin” akasema Ernest na Boaz akampa maelekezo mahala anakopatikana wakaagana Boaz akarejea chumbani “ Jioni ya leo tunakwenda kuonana na Austin kwa hiyo itanilazimu nichukue chumba hapa hapa katika hoteli hii ” akasema Boaz na kufanya taratibu za kupata chumba katika hoteli ile kwani hakutaka kwenda katika jumba lake la kifahari lililoko ufukweni mwa bahari *******************
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Monica alidamka asubuhi na mapema akafanya mazoezi kama ilivyo kawaida yake halafu akajiandaa tayari kwa shughuli za siku.Baada ya kutoka nyumbani kwake alielekea moja kwa moja nyumbani kwa wazazi wake.Siku hii alivaa suti nyeupe iliyomkaa vyema na kila aliyemuona alikiri kwamba kweli huyu anastahili kuwa malkia wa urembo Afrika.Magari yalikuwa mengi asubuhi hii hivyo akajikuta akilazimika kukaa katika foleni “ Nitaachana na adha hii ya kukaa katika foleni muda si mrefu sana toka sasa.Nimeanza kuyakumbuka maisha yale niliyoishi Congo.Sikuwahi kukaa katika foleni.Kila nilikokwenda niliongozwa na gari lenye king’ora na magari yote barabarani yakakaa pembeni kupisha nipite.Nimeyapenda maisha yale” akawaza Monica na mara akanyong’onyea baada ya kumkumbuka Pauline mke wa David Zumo “Masikini Pauline ,amenisikitisha sana.Kila nimkumbukapo na kuyakumbuka maneno aliyonieleza nahisi uchungu mwingi.Moyo unaniuma sana.Why her? Akawaza na kwa mbali macho yake yakalengwa na machozi “ She’s so pretty.Ukimtazama ni kama vile hana matatizo but she’s dying” akashindwa kuyazuia machozi kumtoka .

Tayari magari yalianza kwenda “ Anyway there is nothing I can do to help her.Kitu pekee ninachoweza kufanya ni kulitimiza ombi lake aliloniomba yaani kuolewa na mume wake David Zumo.Pamoja na kulikubali ombi lake lakini lazima niendelee kumuombea ili kama ikimpendeza Mungu afanye miujiza yake na Pauline apone.Ana roho nzuri sana” akawaza Monica na mara akakumbuka kitu Dr Marcelo ni bingwa wa saratani ya damu,hawezi kufanya kitu chochote kuhusu Pauline? Nina uhakika anaweza akawa na mchango fulani hata kama ni mdogo.Tatizo ni kujua mahala alipo.Nitazungumza na David baadae ili anielekeze mahala aliko Marcelo” akaendelea kuwaza Monica Aliwasili nyumbani kwa wazazi wake wakasalimiana kwa furaha na kujumuika wote mezani kupata kifungua kinywa na baadae wakaelekea bustanini kwa ajili ya maongezi “ Pole na safari Monica.Ni siku mbili tu lakini umebadilika ,umezidi kupendeza” akasema mzee Ben ambaye alionekana kuwa na furaha iliyopitiliza “ C’mon dady,niko vile vile sijabadilika chochote” akasema Monica “ Haya tueleze safari yako ilikuaje? Mambo yamekwendaje huko Congo? Anasemaje David Zumo? Akauliza mzee Ben .Monica akatabasamu na kusema “ Kwa ujuml safari yangu ilikuwa nzuri mno zaidi ya nilivyotegemea .Nilipokewa vizuri na mke wa rais nikapelekwa katika jumba kubwa la kifahari nikalala hapo.Asubuhi nikaja kuchukuliwa na mke wa rais aitwaye Pauline,tukapanda helkopta hadi katika hoteli moja kubwa nje ya jiji tukawa na maongezi marefu.Jioni ya siku hiyo nikapelekwa katika jumba la mapumziko la David Zumo.Ni jumba ambalo sipati namna ya kulielezea lilivyo.” Akasema Monica na kutabasamu

“ Usiku huo nikawa na maongezi marefu na David Zumo .Kikubwa ambacho kilitawala mazungumzo yote kuanzia mchana nilipokutana na Pauline ni kuhusiana na ombi la David la kutaka kunioa.Wote walijaribu kunishawishi nikubali kuolewa na David.” Monica akanyamaza na kuwatazama wazazi wake waliooneka kuwa na shauku kubwa ya kutaka kufahamu kilichojiri huko Congo “ Ulifikia maamuzi gani? Akauliza Janet ambaye muda mwingi alikuwa kimya .Huku akiona aibu kwa mbali Monica akasema “ Nimekubali kuolewa na Dav.................” Kabla hajamaliza mzee Ben akaruka kwa furaha na kwenda kumkumbatia “Thank you Monica.Thank you so much.Umefanya jambo kubwa sana .I’m proud of you my queen” akasema Ben.Alikuwa na furaha isiyoelezeka “ Hongera Monica kwa maamuzi hayo lakini nahitaji kufahamu jambo moja ,maamuzi hayo yametoka moyoni? Umekubali kwa moyo mmoja bila ya shinikizo? Akauliza Janet na Ben akamtazama kwa macho makali ,akataka kusema kitu lakini Monica akamuwahi “ Kusema kweli wazazi wangu,David simfahamu vyema ni mwanaume wa namna gani kwani tumefahamiana kwa muda mfupi .Kwa tamaduni zetu zilivyo ili ukubali kuolewa na mtu Fulani basi lazima mtu huyo muwe mnafahamiana vyema na mmekaa katika uchumba kwa muda wa kutosha.Kwa mimi na David imekuwa tofauti, hatujapitia hatua hizo lakini nimekubali kuolewa naye baada ya kumuona ni mtu mwenye mapenzi ya kweli nami.I don’t know how much he loves me but the little he loves me I’m sure its true and I value that” “ Are yu sure Monica? Akauliza Janet “ David speaks from heart.
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
When he says he loves me, he mean it.He’s a good person ,loving and caring.Hata mke wake Pauline amenihakikishia hilo kuwa David ni mtu mzuri.Mama sikutaka kuipoteza nafasi hiyo kama nawe ulivyonishauri.Nisingeweza kukataa kuolewa na mtu kama David ambaye ana karibu sifa nyingi za mwanaume wa ndoto zangu.Hata kama bado moyo wangu haujafunguka kwa sasa but I know someday I’ll fall in love with him” akasema Monica “ Monica binafsi nakupongeza mno kwa kukubali kolewa na David Zumo .Ni uamuzi wa busara na wenye manufaa makubwa kwako,kwetu na kwa nchi zetu pia.David Zumo ni mtu mkubwa,yuko kwenye orodha ya matajiri wa dunia.Kukubali kwako kuolewa naye kutakuingiza katika orodha ya watu maarufu duniani.Hongera sana Monica” akasema Ben “ Mtazame huyu mjinga anachowaza yeye ni mali tu hajui kuwa tunampeleka mtoto kwenye matatizo makubwa.Nililipinga jambo hili hadi kufikia hatua ya kutoa siri kubwa niliyokuwa nayo lakini bado haijasaidia na sasa Monica amekubali kuolewa na David.Inaniuma mno ila sina cha kufanya” akawaza bi janet huku akijlazimisha kutabasamu “ Monica” akaita Janet “ Tell me abut this wife of David.Is she happy? “ Kuna jambo moja nataka kuwafahamisha ambalo hata mimi nimelifahamu jana wakati nikijiandaa kuondoka” akanyamaza kidogo akawatazama wazazi wake na kusema “ Pauline is sick”

“ Sick ?? Ben na Janet wakauliza kwa pamoja “ yes ! She’s sick.Ana saratani ya ubongo na kwa mujibu wa madaktari wanaomtibu wanadai hakuna uwezekano wa kupona.She’s going to die” akashindwa kuyazuia machozi kumtoka. “ Pole sana Monica.Jipe moyo” akasema Janet.Monica akafuta machozi na kusema “ Pauline alifahamu kwamba hataweza kupona ndiyo maana akamtaka David Zumo atafute mwanamke mwingine afunge naye ndoa ndipo David aliponichaga mimi.Suala hili linaumiza sana,Pauline ana roho nzuri.She’s so nice and young to die” akasema na kufuta machozi yaliyondelea kumtiririka “ Sikuwa nikilifahamu jambo hili hadi jana aliponieleza wakati nikijiandaa kuondoka Congo.Amenisisitiza sana nisibadili uamuzi wangu wa kuolewa na David.Nimemkubalia na kumuhakikishia kuwa sintobadili uamuzi wangu” akasema Monica na wote wakabaki kimya. “ Hivyo ndivyo ilivyokuwa huko nilikokwenda.David atatuma ujumbe wake muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kuanza taratibu za awali za ndoa yetu.Hataki suala hili lichukue muda mrefu” “ Ahsante Mungu.Safari ya kuelekea katika orodha ya matajiri 100 wa dunia imewadia.Hii ilikuwa ni ahadi ya David Zumo endapo Monica angekubali kuolewa naye.Nitakapoingia katika orodha hiyo nitakuwa na nguvu na sauti na huo utakuwa ni wakati wangu mzuri wa kulipa kisasi kwa Ernest Mkasa.Jambo alilonifanyia siwezi kuliacha likaisha hivi hivi.I must destroy him.Kama ikiwezekana nitawashughulikia wote wawili Ernest na mke wangu Janet ili siri ya kuwa Monica si mwanangu isivuje na Monica ataendelea kuwa mwanangu daima” akawaza Ben Maongezi yalionekana kukolea na ndipo Monica alipoamua kuwaaga wazazi wake ili aelekee kazini kwa ahadi ya kurejea tena jioni kwa maongezi zaidi. “ Wameonekana kulifurahia jambo hili hasa baba lakini mama mhhh !!!.. akawaza Monica akiwa garini akielekea ofisini kwake baada ya kutoka nyumbani kwa wazazi wake “ Yawezekana labda hakuamka vizuri siku ya leo ndiyo maana alionekana kutokuwa na furaha na hata maswali yeye ndiye alikuwa muulizaji mkubwa.Anyway apende asipende tayari nimekwisha fanya maamuzi ya kuolewa na David na hivyo ndivyo walivyotaka.Kikubwa ninachopaswa kuwaza kwa sasa ni mabadiliko ya ghafla katika maisha yangu.Kutoka Monica Yule wa kawaida hadi Queen Monica.Ama kweli maisha yana maajabu sana.Sikutegemea kama ningepata bahati ya kuolewa na tajiri namba moja Afrika.Ninapaswa kumshukuru Mungu sana kwa jambo hili.”

 Monica aliwasili ofisini kwake akasalimiana wafanyakazi wake waliofurahi mno kumuona tena .Baada ya salamu akaelekea ofisini kwake Linah akamfuata “ Austin amenipigia simu muda mfupi uliopita nikamjulisha kuwa umekwisha rejea na hivi tunavyoongea yuko njiani anakuja “ akasema LInah na Monica akatabasamu. “Huyo kijana anaonekana kumchanganya sana Linah.Sijawahi kumuona Linah akimsifia mwanaume kiasi hiki.Safari hii ameshikwa barabara.” Akawaza Monica na kuendelea na kazi zake. “David amenipigia simu asubuhi lakini hakuongea chochote kuhusu Dr Marcelo.Nahitaji kujua maendeleo ya Marcelo.Nahitaji sana kuonana naye.Jioni ya leo nitamuomba tena anielekeze mahala aliko Dr Marcelo nikamtaz...” Monica akatolewa mawazoni na Linah aliyeingia kwa kasi mle ofisini onica “ akaita “He’s here.Austin tayari amekuja.Ngoja nikamchukue yupo mapokezi “ akasema Linah na kutoka .Baada ya dakika tano akarejea akiwa ameongozana na kijana mmoja mtanashati sana mwenye sura iliyojaa tabasamu “Wow! What a handsome guy” akawaza Monica baada ya kumuona Austin.Alikuwa ni kama mtu aliyepigwa na butwa kwa kitu alichokuwa anakitazama mbele yake. “Monica “ akaita Linah na kumstua Monica “Huyu anaitwa Austin January.Ndiye mgeni Yule niliyekueleza alikuwa anakutafuta” “Austin huyu ndiye Monica Benedict mwamsole,mkuu wa kampuni hii” LInah akafanya utambulisho.Monica akasimama na kumpa Austin mkono. “karibu sana Austin.Nimefurahi kukutana nawe” “Hata mimi nimefurahi sana kuonana nawe Monica” akasema Austin na kuketi katika sofa.Linah akatoka na kuwaacha Monica na Austin pale ofisini.


MWISHO WA SEASON 2

MPENZI MSOMAJI MAMBO YANAZIDI KUKOLEA......USIKOSE SEASON 3 YA SIMULIZI HII....

*************
*********************
CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog